funguo za wajibu wa kumlinda david mifumo ya ... za kumlinda david dhidi ya ukatili wajibu wa mifumo...

13
FUNGUO ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia dawa za kulevya, na mama yangu akiwa hayupo, alikuwa akinipapasa na kunigusa sehemu zangu za siri. Sikufahamu kilichokuwa kinaendelea. Nilikuwa mtoto tu, mwenye umri wa miaka sita. Alikuwa akiniambia kwamba jambo hili liwe siri kati yetu sisi wawili na kwamba nisimwambie mtu yeyote. Wakati mwingine alikuwa akinifanyia vitendo ambavyo vilikuwa vinaumiza. Nilisikia aibu na sikupenda watu wengine wanione, kwahiyo nilijificha. - David Zifuatazo ni funguo za mfumo wa kitaifa wa ulinzi wa watoto Mifumo ya ulinzi wa watoto ni muhimu ili kuzuia na kushughulikia aina zote za uonevu dhidi ya watoto, ukiwemo unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji, kutojali, utandikwaji wa viboko, watoto wanaofanya kazi za hatari, ajia ya watoto katika vikundi vya kivita, ndoa za mapema na vitendo vingine vya kimila vyenye madhara.

Upload: lamnga

Post on 18-Apr-2018

295 views

Category:

Documents


14 download

TRANSCRIPT

Page 1: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

FUNGUO ZA

KUMLINDA DAVID

DHIDI YA UKATILI

Wajibu wa

Mifumo ya Kitaifa

ya Ulinzi watoto

“ Nilipokuwa mtoto,baba yangu wa kambo

alikuwa akitumia dawa za kulevya, na mama yangu

akiwa hayupo,alikuwa akinipapasa na kunigusa

sehemu zangu za siri. Sikufahamu kilichokuwa

kinaendelea. Nilikuwa mtoto tu, mwenye umri wa

miaka sita.

Alikuwa akiniambia kwamba jambo hili liwe siri kati yetu

sisi wawili na kwamba nisimwambie mtu yeyote. Wakati mwingine alikuwa

akinifanyia vitendo ambavyo vilikuwa vinaumiza.

Nilisikia aibu na sikupenda watu wengine wanione,

kwahiyo nilijificha.

”- David –

Zifuatazo ni funguo za

mfumo wa kitaifa wa

ulinzi wa watoto

Mifumo ya ulinzi wa watoto ni muhimu ili kuzuia na kushughulikia aina zote za uonevu dhidi ya watoto, ukiwemo unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji, kutojali, utandikwaji wa viboko, watoto wanaofanya kazi za hatari, ajia ya watoto katika vikundi vya kivita, ndoa za mapema na vitendo vingine vya kimila vyenye madhara.

Page 2: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

Mkakati wa kitaifa unahakikisha

kwamba mpango tendaji wa kuzuia hali kama

iliyomtokea David unakuwepo.

Mkakati wa

Kitaifa

Mkakati wa kitaifa,

sera au mpango

tendaji wa kuzuia

ukatili dhidi ya

watoto wenye

makusudi halisi na

ya muda maalum na

mkakati wa

utekelezaji ni lazima

uandaliwe.

Mkakati wa kitaifa unahakikisha kwamba mpango tendaji wa

kuzuia hali kama iliyomtokea David upo.

Mkakati wa kitaifa, sera au mpangotendaji wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto, wenyemakusudi halisi na wa muda maalum, pamoja na mkakati wa utekelezaji ni lazima viandaliwe.

MKAKATI

WA KITAIFA

Page 3: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“ Hatimaye nilimwambia rafiki yangu yaliyonitokea

na akanishawishi nimweleze mwalimu

wangu. Mwalimu wangu alikuwa na wakati mgumu kuniamini mwanzoni lakini

pia alinieleza kwamba kitendo alichonifanyia

baba yangu si sawa na ni kinyume na sheria.

MFUMO WA

KISHERIA

Sheria za kitaifa ni lazima zizuie aina zote za ukatili dhidi ya watoto katika mazingira yote ikiwemo majumbani, na ni lazima zitekelezwe na kufuatiliwa kwa namna inayoleta matokeo.

Page 4: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Mwishoni walimu wangu walinisindikiza kituo cha Polisi

kutoa taarifa kuhusu yale yaliyotokea. Polisi walimwita

mwanaume mmoja kutoka katika idara ya huduma za jamii,

Bob, ambaye ndiye aliyekuwa mtu niliyekuwa nawasiliana nae.

Alinisindikiza kwa daktari na alizungumza na mama yangu.

Mama yangu alipata mshtuko mwanzoni, lakini baadae

alikasirika sana na baba yangu wa kambo. Aliamua tukakae na

bibi kwa muda. Bob alikubaliana na uamuzi huu.

SHIRIKA

LINALORATIBU

Shirika linahusika na uratibu ngazi ya taifalinawajibika katika utekelezaji wa mkakati wa kitaifa na inabidi liwe na uwezo wa kuzihusisha na kuziratibu sekta za serikali (ustawi wa jamii, afya, elimu, haki, n.k..) na kuzihusisha asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa, familia na watoto kwa njiailiyo salama.

Page 5: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Katika miezi iliyofuata nilipata msaada mkubwa kutoka kwa Bob na wengine, ikiwemo kwenda kumwona

daktari mara kwa mara. Mnasihi wangu aliniomba nisimulie yale

yaliyonitokea kwa kuchora picha. Wakati mwingine nilikuwa nalia na

kupiga makelele na sikuona raha yoyote ya kuishi.

Mwanzoni sikutaka baba yangu wa kambo aadhibiwe kwani nilihisi kuwa

mimi ndiye niliyesababisha yaliyotokea. Lakini baada ya

kuzungumza na Bob, nilielewa na kukubali kwamba baba yangu wa

kambo anahitaji kuadhibiwa na pia kusaidiwa kutambua kwamba

kitendo alichonifanyia kilikuwa ni kosa.

HUDUMA ZA KUZUIA

NA KUSHUGHULIKIA

MASUALA ZA MAHALI

HUSIKA

Ngazi ya serikali ya mahali inayo wajibu wa kwanza wa kuhakikisha kuwepo kwa huduma zinazofikika, zenye kujali watoto, zinazozuia kutokea kwa hali fulani, zenye mwitikio ambazo zinajumuisha utoaji wa taarifa, pamoja na taratibu za kutoa rufaa na programu za uponyaji, urekebishaji na kuingizwa upya katika kundi.

Page 6: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Baada ya muda fulani baba yangu wa kambo alipelekwa mahakamani.

Sikutaka kukutana naye mahakamani kwahiyo Bob

alihakikisha kwamba niliweza kuwaeleza majaji kile kilichotokea

kwa kutumia kinasa sauti cha video. Nilielezwa kwamba baba

yangu wa kambo atafungwa hela kwa miaka 5.

Sikuona tena aibu, lakini nilimkumbuka baba yangu wa

kambo na mambo mazuri tuliyofanya pamoja, kama kwenda

kuona wanyama nilipokuwa mdogo.

MFUMO WA

SHERIA WENYE

KUJALI WATOTO

Serikali inaanzishamfumo maalum wa kisheria wenye kulengawatoto ambaounahakikisha kwamba watoto wanaweza kutoa taarifa kuhusu ukatiliwanaofanyiwa na kwamba wakosajiwanachukuliwa hatua za kisheria.

Page 7: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Baada ya miezi kadhaa, nilianza kujisikia vizuri,

kwa msaada wa Mnasihi wangu, Bob aliniuliza

ningependa kufanya nini na ni kwa njia gani

angeweza kunisaidia. Nilitaka kurudi shule na

pia nilitaka kwaeleza watoto wengine kuhusu

uonevu wa kijinsia. Nilianzisha klabu ya

watoto.

Inabidi Serikali iwasikilize wasichana na wavulana na kuwahusisha watoto moja kwa moja katika uundaji na utekelezaji wa sera (na programu) zinazoshughulikia ukatili ambao watoto wanafanyiwa. Vitendo vya watoto wenyewe vya kushughulikia ukatili inabidi viungwe mkono.

USHIRIKI WA

WATOTO

Acha ukatili

dhidi ya watoto

Page 8: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Klabu yangu ya watoto ilianza kuwahamasisha watoto na watu wazima

kuchukua hatua dhidi ya uonevu wa watoto, na kuishawishi Serikali ifanye

mambo mengi zaidi. Kwa kuwa mara nyingi watu hawapendi kuzungumzia uonevu wa

kijinsia, Serikali ya mitaa haikuwa tayari kabisa kulikubali wazo hilo.

Lakini baada ya muda, Serikali iliamua kuanza kampeni ya kutoa taarifa. Magazeti

ya mahali yalitoa makala ili kuwapa taarifa walimu na wazazi wengine kuhusu uonevu

wa kijinsia.

Umma wenye uelewa na unaounga mkono jitihada husika unatakiwa uhusishwe katika jitihada za kuzuia madhara kwa watoto na kushughulikia masuala ya ulinzi wa watoto katika jamii zao, maeneo wanakoishi na katika jamii nzima.

UMMA WENYE

UELEWA NA

UNAOUNGA

MKONO JITIHADA

MABADILIKO

YANAHITAJI

UJASIRI

Page 9: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Kutokana na shinikizo kutoka asasi za kiraia , baadhi ya shule

zilianza kuingiza suala la uonevu wa kijinsia katika mitaala ya

mafunzo ya walimu, na shule na taasisi nyingine zinazoshughulikia

watoto zilianzisha vifungu vya ulinzi wa watoto. Wataalamu wote wanaoshuhgulikia watoto walipata

taarifa na mafunzo kuhusu uonevu wa kijinsia ili waweze

kutambua mtoto ambaye yuko hatarini.

Kama walimu wangelikuwa wamepata mafunzo wangelitambua

kwamba kuna jambo ambalo halikuwa sawa katika maisha yangu. Kwa mfano, mwalimu

wangu shuleni angegundua kwamba wakati mwingine nilikuwa

najificha na kulia na angeweza kutambua tatizo ni nini.

Wataalamu wote wanaofanya kazi na au wanaowashughulikia watoto kama vile polisi, walimu, wafanyakazi wa serikali, walezi, maafisa wa mahakama, wataalamu wa afya na wafanyakazi wa jamii, ni lazima wapatiwe mafunzo kuhusu jinsi ya kutambua ukatili, kutoa rufaa na kuhakikisha matunzo na usiri.

Hatua za kuzuia ukatili kama vile kutoa taarifa, kampeni na mafunzo kuhusu haki za watoto na ulinzi na msaada kwa wazazi na walezi vinapaswa kutolewa.

WAFANYAKAZI

WANAOJITOA

KWA MOYO

Page 10: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Rasilimali zaidi zilihitajika kuhakikisha kwamba watoto wote nchini wanalindwa zaidi kutokana

na aina zote za ukatili.

Miaka michache baadae, kutokana na ushawishi wa asasi za kiraia,

Serikali iliongeza bajeti ili kuzisaidia familia kwa ukamilifu

kutoa malezi bora zaidi kwa watoto wao na kuzuia uonevu wa

aina zote.

Rasilimali za kutosha na zinazostahili zinapaswa kutolewa ili kukomesha aina zote za ukatili dhidi ya watoto.

RASILIMALI ZA

KUTOSHA

Page 11: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Serikali iliamua pia kuweka viwango kwa ajili ya malezi

mbadala ya watoto na kuanzisha mfumo wa

ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba wataalamu

wanaowashughulikia watoto na wnaofanya kazi na watoto

wanafuata taratibu sahihi.

Serikali inawajibika kuhakikisha kwamba huduma na jitihada vinasimamiwa kisheria na kufuatiliwa kwa ufanisi.

VIWANGO, SHERIA,

UFUATILIAJI NA

USIMAMIZI

Page 12: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

“Jambo ambalo bado linakosekana ni mfumo

unaofahya kazi wa kukusanya data ambao unaisaidia

Serikali kufanya makadirio ya ukubwa wa tatizo, idadi ya

watoto waliopata msaada na idaadi ya watoato

waliosaidiwa kurudia hali ya kawaida. Serikali imejitoa

kutekeleza suala hili na kwa msaada wa baadhi ya

wafadhili tunatarajia mfumo huu utaanzishwa mapema.

Hivi sasa nina umri wa miaka 20 na mambo mengi

yamebadilika katika nchi yangu. Licha ya mambo yote ambayo Serikali na wengine wamefanya, wapo baadhi ya

watoto ambao bado wanaonewa kijinsia. Hivyo ni

lazima tuendelee kupigania haki ya watoto ya ulinzi.

Kila nchi inapaswa kuanzisha mfumo wa ukusanyaji data unaoratibiwa mahali pamoja, ambao unahakikisha upatikanaji wa taarifa za kila wakati kuhusu ukubwa wa tatizo pamoja na uelewa kuhusu masuala ya ulinzi wa watoto na njia zinazofaa za kushughulikia suala hilo.

MIFUMO YA

UKUSANYAJI DATA

Page 13: FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo ya Kitaifa ya Ulinzi watoto “ Nilipokuwa mtoto, baba yangu wa kambo alikuwa akitumia

Funguo zinazohakikisha

kuwepo kwa mfumo wenye

ufanisi wa ulinzi wa watoto

Hadithi ya David ni ya kutunga. Inaeleza hali za watoto wengiduniani kote. Kwa bahati mbaya, katika nchi nyingi, si mara zotekunakuwa na mwitikio na huduma zenye ufanisi, kama ilivyo katika kisa cha David. Hadithi hiiilitungwa kuonyesha jinsi ambavyomifumo ya ulinzi wa watoto inaweza kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili dhidi ya watoto.

Maandishi yameandikwa na Catherine Kates,

Roberta Cechetti na Lena Carlsson.

Usimamizi wa Mradi na Catherina Kates na

Roberta Cechetti.

Mpango wa Ulinzi wa Watoto

Shirika la Save the Children

Mei 2011

Kwa taarifa zaidi:

Tovuti: resourcecentre.savethechildren.se

Barua pepe: [email protected]

Imechapishwa na Pazzini Stampatore Editore

Verucchio (RN) Italia

Imechapishwa kwenye karatasi

zilizorejeleshwa

DIRA NA DHIMA YA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN

SISI NI shirika la watoto linalojitegemealinaloongoza duniani .

DIRA yetu ni dunia ambamo kila mtotoanapata haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa na kushiriki.

DHIMA yetu ni kuhamasisha mafanikiokatika namna dunia inavyoawatendeawatoto, na kufanikisha mabadiliko ya mara moja na ya kudumu katika maisha yao.

Mfumo wa Sheria