taarifa ya utekelezaji wa serikali hadi mei, 2019 · mifumo ya kisasa na mapato ya serikali; na...

25
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 Imetolewa na: Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Alhamisi, Mei 30, 2019.

Upload: others

Post on 25-Sep-2020

10 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019

Imetolewa na: Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO naMsemaji Mkuu wa Serikali, Alhamisi, Mei 30,

2019.

Page 2: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MUHTASARI WA TAARIFA

• Taarifa ya Mwezi Mei, 2019 Itajikita Katika:

• 1. Masuala Mbalimbali ya Utangulizi;

• 2. Ziara za Rais Nje ya Nchi:

• 2. Mageuzi Sekta ya Madini;

• 3. Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na

• 4. Maswali na Majibu [Q & A].

Page 3: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

UTANGULIZI • Ndugu wanahabari;

• Nianze kwa kuwashukuru tena kwa kufika hapa nakuwapongeza kwa kuendelea kutekeleza majukumu yenuipasavyo katika kutimiza wajibu mkuu wa vyombo vyahabari ambao ni KUCHAGIZA MAENDELEO;

• Kuhusu sekta ya Habari, mtakumbuka kuwa Mei 3, 2019tuliadhimisha kwa pamoja Siku ya Uhuru wa HabariDuniani na tulipata fursa ya kujadiliana masualambalimbali na tulikubaliana kuunda Kamati ambayoitachambua changamoto za kisekta. Kazi ya kuunda Kamatihiyo na kuiwezesha ianze Kazi inaendelea na itatangazwawakati wowote kuanzia sasa.

Page 4: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

UTANGULIZI…SEKTA YA HABARI• Aidha, nitumie fursa hii kwa mara nyingine

kuwakumbusha wamiliki wa magazeti kuwa tunaendeleakuweka hadharani [angalia www.maelezo.go.tz] majina yamagazeti yote ambayo hayajahuisha leseni na hivyokukiuka Sheria ya Huduma za Habari Na. 12, 2016. Kilammiliki husika asisubiri hatua kali za Serikali, achukuehatua sasa;

• Kwa upande wa wanahabari, niwasisitize tena hii ni kaziadhimu hivyo mnapaswa kuendelea kuitekeleza kwakufuata maadili ya taaluma na zaidi mfanye kazi mkiwawanataaluma kamili ikiwemo kuhakikisha mnakata “presscard” ili ziwasaidie kutekeleza vyema majukumu yenu.Kuanzia Julai mosi, 2019 tutaanza kuchukua hatua dhidi yawaandishi wasio na “press card.” kushiriki shughulimbalimbali rasmi.

Page 5: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

UTANGULIZI…WAANDISHI NA TTCL• Kuna masuala kadhaa pia yamekuwa yakijitokeza kwenye

mijadala kuhusu uamuzi mbalimbali wa Serikali au baadhiya taasisi za Serikali:

• Waandishi kutakiwa kukata vitambulisho vya ujasiriamaliIringa: Mkuu wa Mkoa ameshafafanua kuwa si waandishini wapigapicha za mitaani;

• Suala kwamba Serikali imeagiza watumishi wote waumma wawe na line ya TTCL si sahihi, Rais alikuwa wazikuwa kwa viongozi wanaohudumiwa stahili ya simuwatapewa vocha za TTCL lakini hakuna agizo la ulazimakwa wafanyakazi wengine, TTCL ni Shirika bora nalitaendelea kupata wateja wengi kwa sababu ya uborawake.

Page 6: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

UTANGULIZI…KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

• Ndugu wanahabari;• Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla ya

kufika Juni Mosi, 2019, nisisitize kwa Watanzania nawadau wote kuwa katazo la kuingiza, kusafirisha nje,kutengeneza hapa nchini, kutumia na kuingiza nchinimifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku liko pale palena usisubiri saa ifike, chukua hatua sasa;

• Baada ya bashrafu hii, kama nilivyosema leo ninamambo makuu matatu ya kuwaeleza kuhusuyanayoendelea na yanayotokea Serikalini katikautekelezaji wa ahadi, mipango na mikakati ya Serikalikama ifuatavyo:

Page 7: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

1. ZIARA ZA RAIS NJE YA NCHI • Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya

Muungano, kwa takribani wiki moja sasa amekuwaziarani katika nchi kadhaa za Afrika akianzia AfrikaKusini, Namibia na sasa amekamilisha ziara nchiniZimbabwe;

• Ziara katika nchi hizi wanachama wa SADC ilikuwamuhimu kwa sababu pamoja na uhusiano wakipekee na kihistoria wa Tanzania na nchi hizo,mfahamu kwamba baada ya miaka 16, kuanzia Julaimwaka huu, Tanzania itashika Uenyekiti wa SADC naitakuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa SADCAgosti, 2019

Page 8: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

ZIARA YA RAIS NJE YA NCHI…• Pamoja na kuimarisha Ushirikiano na urafiki uliopo

kati ya Tanzania, Afrika Kusini, Namibia naZimbabwe, ziara hii pia imekuwa na mafanikioyafuatayo katika Diplomasia ya Uchumi:

• 1. Uwekezaji, masoko na biashara: Kupitia ziara hii,Tanzania imefikia makubaliano kadhaayatakayoiwezesha nchi yetu kuongeza kiwango chabiashara na uwekezaji na mataifa yote matatu.Aidha, Tanzania imepata soko la mahindi tani700,000 nchini Zimbabwe na maeneo mengine yaushirikiano katika kilimo, utalii, usafiri wa anga,miundombinu pia yamefikiwa na/au yatajadiliwazaidi kupitia Tume za Ushirikiano wa Pamoja (JPCs).

Page 9: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MANUFAA ZIARA YA RAIS… • 2. Fursa kwa lugha ya Kiswahili: Akiwa ziarani, Mhe. Rais

ametumia fursa ya uhitaji uliopo hasa nchini Afrika Kusinina Namibia wa walimu wa lugha ya Kiswahili, kwa kufikiamazungumzo ya awali ili baadaye walimu wa Tanzaniaambao ndio manju, galacha na nguli wa asili wa lughaadhimu ya Kiswahili wapate fursa ya ajira katika nchi hizo;

• Niseme tu kufuatia kazi kubwa aliyoifanya Rais, niwatoewasiwasi, ukiacha ubauji wetu katika lugha hii aushi yaKiswahili, tayari kama Taifa tumeanza kufanya Ithibati yaWataalamu bingwa wa kufundisha Kiswahili. Hadi sasa,BAKITA imewathibitisha wataalamu 708 ambao ni walimuna wakalimani wa Kiswahili na wako kwenye Kanzidata yaKitaifa ya Watalaamu wa Kiswahili. Kujisajili ingiawww.lugha.bakita.go.tz au www.bakita.go.tz

Page 10: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

2. MAGEUZI SEKTA YA MADINI YAANZA KUWA BARAKA

• Ndugu waandishi wa habari;• Eneo la pili la muhimu leo wananchi kujua kwa kina

kinachoendelea ni mageuzi ambayo wengiwamekuwa wakiyasikia kuwa yanatokea katika sektamuhimu ya madini. Swali kuu ni Je, vita hiitunashinda au tunaanguka?;

• TUNASHINDA: Katika sekta ya Madini Serikali yaAwamu ya Tano imefanya mageuzi mbalimbaliikiwemo kutunga Sheria Mpya za Madini,kurekebisha za zamani ikiwemo marekebishomakubwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017ambapo iliundwa taasisi mpya ya Tume ya Madini.

Page 11: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

SEKTA TA MADINI…TUNASHINDA• 1.Sifa kwa Taifa: Mabadiliko haya yameanza kuleta faida

kwa Nchi ambapo kwa sasa Tanzania inasifika duniani kamanchi ambayo inageuza “laana” ya madini kuwa “Baraka” yaMadini na nchi nyingi za Afrika zimeanza kuiga mageuzitunayoyafanya ikiwemo kupitia upya mikataba nawawekezaji na pia watafiti mbalimbali wanairejea Tanzaniakatika hili;

• 2. Masoko ya Madini Yaanza: Baada ya takribani miaka 10ya tamko katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 lakuanzisha masoko ya madini kukwama, hatimaye Januarimwaka huu, Rais Magufuli alitoa agizo na sasalimetekelezwa. Masoko haya ni vituo vya kuthibiti ubora,thamani na takwimu za madini. Mpaka Mei 29, 2019masoko 24 yalishafunguliwa na kuanza kazi.

Page 12: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MASOKO 24 YA MADINI YAANZA…

Page 13: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

i.MASOKO NI CHACHU YA MAPATO

• Mfano wa Mkoa wa Geita: Soko hili la kwanza nchinililianza rasmi Machi 17, 2019:

• Takwimu za jumla ya uzalishaji wa miezi miwili kabla yakuanza Soko la Geita, zinaonesha kuwa uzalishaji wadhahabu uliorekodiwa ulikuwa ni jumla ya kilogramu259.12;

• Takwimu za jumla ya uzalishaji wa dhahbu kwa miezi miwilibaada ya kuanza Soko la Madini Geita, zinaoneshauzalishaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikiakilogramu 312.65 za dhahabu huku mwezi April, 2019pekee ukiweka rekodi ya Geita kwa kuzalisha kilogramu200 ambazo hazijapata kufikiwa mkoani humo kwawachimbaji wadogo na wa kati.

Page 14: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MAPATO ZAIDI YAMIMINIKA….• 3. Mapato Sekta ya Madini Yanamiminika:

Tunaweza kujinasibu kwa yote katika mageuzi yasekta ya madini; sheria mpya, masoko na udhibiti wautoroshaji, lakini nafahamu watanzania wengiwanataka kuona ni kwa kiwango gani tumeanzakufaidika na madini kutoka “laana” hadi “baraka”?

• Takwimu za mpaka Mei, 2019 zinazidi kuthibitishakuwa Watanzania wanapaswa kuendeleakumuombea na kumuunga mkono Rais Magufulikwani mawazo, nia yake na miongozo yake katikasekta hii ni ushahidi mwingine kuwa FALSAFA za RaisMagufuli zisizo na mawaa zinailetea mafanikiomakubwa. Makusanyo ya miezi 11 mwaka huuyameshazidi ya mwaka jana kama ifuatavyo:

Page 15: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MAPATO YA JUMLA YAONGEZEKA

Page 16: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MFANO WA TANZANITE MIRERANI…

• Uzalishaji na Mapato ya Tanzanite Vyaongezeka:

• Tangu Serikali ilipoamua kujenga ukutakuzunguka eneo la wachimbaji na kisha kuwekamifumo ya masoko na ukaguzi humo humo ndani,uzalishaji na mapato ya Serikali kutoka kwawachimbaji wadogo vimeongezeka kwa kiwangocha kuridhisha kama ifuatavyo:

Page 17: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

UZALISHAJI, MAPATO VYAONGEZEKA MIRERANI

Page 18: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

SOKO LA DHAHABU CHUNYA

• Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Mhe. Raisalipokuwa ziarani Mbeya na alipofika Chunya aliagizaharaka soko la madini lianze, kwanza niwajulishekuwa soko hilo limeanza rasmi tangu Mei 2, 2019 natayari limeanza kuonesha mafanikio kama ifuatavyo:

• Mwezi Machi kabla ya soko uzalishaji ulikuwatakribani kilogramu 29.02 na Serikali ilikuwa ikipatamapato ya TZS milioni 173.53. Siku 28 tangu sokolianze uzalishaji umepanda kilogramu 100.22 namapato yameongezeka hadi kufikia TZS milioni588.91 .

Page 19: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MIFUMO YA KIDIGITALI YA MAPATO YALETA MAFANIKIO MAKUBWA

• Ndugu Waandishi wa Habari;

• Mnafahamu kuwa Serikali ya Awamu ya Tanoimewekeza sana msisitizo katika kukusanyamapato lakini na si tu kukusanya mapato bali piakutumia mifumo ya kisasa itakayoongeza Ufanisi;

• Tayari Serikali ilishazindua mifumo kama ule wakufuatilia miamala ya simu (TTMS), Mfumo Mkuuwa Mapato ya Serikali (GePG) na mingine mingi.

Page 20: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MFUMO WA TTMS

• “Telecommunications Traffic Monitoring System”(TTMS) ni Mfumo wenye uwezo wa kubainitakwimu mbalimbali zinazopita katika mitandaoya mawasiliano. Mfumo huu baada ya mwekezajikuusimamia kwa miaka mitano Januari, 2019 Raisaliupokea rasmi na sasa uko chini ya Serikali;

• Mfumo huu unasaidia Serikali kujua mapato yakampuni za simu na mapato yanayotokana namifumo ya kutuma na kupokea fedha.

Page 21: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MAFANIKIO YA TTMS • Kabla ya Mfumo wa TTMS Serikali ilikuwa haipati kitu kabisa

katika miito ya simu za nje wala kuwa na uwezo wa kuhakikimapato ya simu za ndani katika kuapata mapato stahikikatika miamala ya fedha kwa njiia ya simu za mkononi;

• Tangu mfumo wa TTMS ulipofungwa kwa eneo la mapato yasimu za nje tu, Serikali imekwishakusanya TZS. Bilioni 97.16 ikiwa ni malipo ya kodi zitokanazo na mapato ya kampuni zasimu kwa simu za kimataifa zinazoingia na kuishia hapanchini.

• Aidha, kwa idadi ya miamala ya fedha kwa njia ya simu katiya Julai, 2018 na Machi, 2019, uhakiki wa TTMS umeoneshakuongezeka kwa miaka kutoka miamala bilioni 1.94 hadimiamala bilioni 2.26 na hii inamaanisha Serikali inapata kodizaidi, jambo ambalo kabla ya mfumo ilikuwa ngumu kujua.

Page 22: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MFUMO WA MAKUSANYO YA MAPATO YA SERIKALI GePG

• GePG ni kifupi cha “Government e-Payment GatewaySystem”. Huu ni Mfumo wa kielektroniki unaowezeshaukusanyaji wa fedha za umma kielektroniki Serikalini.;

• Mfumo huu umebuniwa na kutengenezwa na wataalamuwa ndani wa Serikali. Mfumo wa GePG unasimamiwa naWizara ya Fedha na Mipango kiufundi na kiundeshaji.

• Miundombinu ya mfumo huuimesimikwa kwenye kituo cha kuhifadhi DATA cha Serikali(Government Data Center) na inasimamiwa na wataalamuwa Kitanzania.

Page 23: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

TAASISI ZILIZOUNGANISHWA GePG

Taasisi mbalimbali za umma zimeendeleakuunganishwa na Mfumo wa GePG ili kukidhimatakwa ya Sheria ya Fedha za Umma lakini piakuongeza ufanisi.

Mpaka tarehe 29 Mei, 2019, idadi ya taasisizilizounganishwa na kutumia Mfumo kukusanyaFedha za Umma ni 430. Taasisi zilizounganishwani pamoja na Halmashauri zote nchini ambazo ni185.

Page 24: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

GePG YAONGEZA MAPATO YA TAASISI

Page 25: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI HADI MEI, 2019 · Mifumo ya Kisasa na Mapato ya Serikali; na •4. Maswali na Majibu [Q & A]. ... •Kwa kuwa leo zimebaki chini ya saa 48 kabla

MWISHO• Mwisho niendelee kuwasisitizia Watanzania

kuungana na Serikali katika safari hii yamabadiliko, mabadiliko ya kweli katika kilakona;

• Mwezi huu niliona tu mpate mwelekeo wamakusanyo na mageuzi katika sekta muhimu,katika taarifa ijayo tutaangalia zaidi utekelezajiwa miradi zaidi ya maendeleo, maanakukusanya fedha linaweza kuwa jambo tofautina kuwaletea wananchi maendeleo. Tutajikitahuko zaidi;

• Niko tayari sasa kupokea maswali yenu.