mwongozo wa mwezeshaji utangulizi wa mikutano ya elimu ya ... · mpango wa kuinua ubora wa elimu...
TRANSCRIPT
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
2
Yaliyomo
Mwongozo wa Mwezeshaji ....................................................................................................... 3
Siku ya 1 Mkutano wa Elimu wa Wilaya ........................... Error! Bookmark not defined.
Kipindi cha 1 Utangulizi wa mafunzo na Mkutano wa Elimu wa Wilaya ........................... 6
Kipindi cha 2 Malengo ya Mkutano wa Elimu wa Wilaya ................................................ 10
Kipindi cha 3 Kupanga na kuandaa Mkutano wa Elimu wa Wilaya ................................. 13
Kipindi cha 4 Umuhimu wa Mada za majadiliano na Mwongozo wa mada za mwaka ... 16
Siku ya 2 Kuandaa na Kuendesha mikutano ya MEW ...................................................... 20
Kipindi cha 5 Matarajio ya Maafisa Elimu Kata na kujenga uwezo wao wa kitaaluma .. 21
Kipindi cha 6 Ufuatiliaj, Msaada na Mapitio ya Mkutano wa Elimu wa Wilaya ............. 25
Kipindi cha 7 Kupanga Mkutano wa Elimu wa Wilaya ..................................................... 30
Kipindi cha 8 Kukutokea nini baada ya mafunzo? ........................................................... 32
Viambatisho
Kiambatisho A Majukumu ya Kamati ya Maandalizi naWajibu wa Mwakilishi wa MEW..35
Kiambatisho B Kiolezo cha Mikutano ya MEW .................................................................... 36
Kiambatisho C Kipindi cha 1 Manufaa ya MEW ................................................................... 37
Kiambatisho D Kipindi cha 2 Mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Shule ........................ 41
Kiambatisho E Kipindi cha 3 Ziara za Afisa Elimu Kata na Uandishi mzuri wa ripoti........... 44
Kiambatisho F Mfano wa Mwongozo wa mada za Mwaka .................................................. 47
Kiambatisho G Ufafanuzi wa Kazi ya Afisa Elimu Kata ........................................................ 49
Kiambatisho H Waraka juu ya namna ya kuandika taarifa nzuri ........................................ 50
Kiambatisho I Mpangokazi kwa ajili ya mikutano ya MEW ....................................................... 53
Kiambatisho J Mjukumuna Taratibu za utoaji taarifa za mkutanoa wa Elimu was Mkoa na
Wilaya...................................................................................................................54.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
3
Mwongozo wa Wawezeshaji Wawezeshaji wanaandaaje semina zao.
Wagawanye washiriki katika makundi ili kila Mwezeshaji apewe jukumu la kuwezesha kundi moja (kwa mfano, ikiwa kuna Wawezeshaji wa 3 na jumla ya washiriki ni 60, kila Mwezeshaji atafanya kazi na kundi la Washiriki 20).
Maandalizi ya Wawezeshaji kabla ya Semina kuanza: • Kusoma mwongozo huu wa mwezeshaji kwa kila kipindi • Kuandaa kila kipindi mapema na kuhakikisha kuwa una nakala za kutosha za:
Kitini cha mshiriki Miongozo ya mikutano ya MEW Karatasi za bango kitita zenye maelezo, vielelezo, n.k zilizoandaliwa mapema Mabangokitita yasiyoandikwa, kalamu rashasha, madaftari ya kuandikia kumbukumbu,
na kalamu Kompyuta, projekta-mashine ya kurusha picha/maandishi ukutani, kisitiri na waya wa
kuunganishia umeme kwa siku ya kwanza.
Wawezeshaji wanaandaaje kazi za vikundi: Hakikisha kwamba washiriki wanaelewa vyema kazi yao, Muda na jinsi ya kutoa Mrejesho kabla ya kuanza kufanya kazi katika vikundi:
Kazi: Hakikisha washiriki wanaelewa vyema kile wanachopaswa kufanya (hii ni "LAZIMA" wakati washiriki wanafanya kazi ya kikundi);
Muda: Hakikisha washiriki wanajua wazi wana muda gani. Hakikisha kila kikundi kinateua mtunza muda ili kuhakikisha vikundi vinazingatia muda;
Mrejesho: Hakikisha kila kikundi kinateua mwandishi/mtoa taarifa. Hakikisha washiriki wanajua ni mambo gani wanapaswa kuyatolea taarifa kwa ujumla. Waambie kwamba kuna ukomo wa muda kwa kila mrejesho.
Vidokezo na mbinu za Mwezeshaji: Tumia ujuzi na uzoefu wa washiriki kama hatua ya kuanzia:
Waalimu wakuu na Maafisa Elimu Kata tayari wanayajua haya kwa kiwango kikubwa, na changamoto yako wewe kama Mwezeshaji ni kuyachota haya kutoka kwao na kuwaongezea dhana na mawazo mapya ambayo hawana.
Hakikisha washiriki wote wanashiriki kikamilifu muda wote wa Semina: kuanzia wakati wa utangulizi, vipindi vya pamoja, wakati wa kazi za vikundi, na wakati washiriki wanafanya kazi katika jozi kwa kutumia:
o Vipindi vya majadiliano katikati ya maelezo ya pamoja. Waombe washiriki wageukiane na wenza wao na wajadili uzoefu au uelewa wao katika suala fulani. Majadiliano haya ni mafupi, na mrejesho unafanywa katika majadiliano mafupi ya pamoja yanayoongozwa na Mwezeshaji.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
4
o Vipindi vya bungua bongo hivi ni vipindi ambavyo makundi makubwa ya washiriki hufikiria juu ya mada au suala fulani na kujaribu kuibua masuala kadhaa au uzoefu wao kuhusiana na suala hilo.
Tazamana na washiriki mara kwa mara na jaribu kujifunza na kutumia majina yao
Washiriki wanapokuwa wanafanya kazi katika vikundi, tembelea kila kikundi. Ingilia majadiliano yao ikiwa tu utagundua kwamba wanakikundi husika hawaelewi wanachofanya au kama wamekwama na hawajui jinsi ya kuendelea.
Wakati mwingine washiriki huomba kupewa tafsiri au ufafanuzi zaidi (kwa mfano, maana ya "kusikiliza vizuri au vibaya", au maana ya "lengo" na "kusudi") kabla ya zoezi hilo kuanza. Usiwape ufafanuzi bali waambie washiriki kuwa watapata majibu ya maswali yao kwa kufanya zoezi lao na wakati wa majumuisho.
Wakati wa kutoa majumuisho, usielezee wala kufundisha. Badala yake, tumia "pointi kusisitiza" na kuuliza maswali zaidi (kudadisi) ili kuwafanya washiriki wafikiri wenyewe.
Usiogope unapoona hali ya ukimya baada ya kuuliza swali. Wapatie washiriki muda wa kufikiria na kutoa majibu ("hesabu hadi kumi").
Kiti cha Kusikilizia: Wakati washiriki wanafanya kazi katika vikundi, ikiwa samani za kutosha zinapatikana, weka kiti cha ziada kwenye kikundi na ungana nao kusikiliza bila kuvuruga sana majadiliano yao. Njia hii ni ya kiungwana zaidi kuliko kusimama karibu na kikundi.
Usisahau kuwapatia washiriki karatasi ya tathimini ili waweze kujaza/kuandika kwa namna gani mafunzo yalivyo fanyika.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
5
Siku ya 1: Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Muda Shughuli Mbinu na maudhui Rasilimali
01:30-02:00 Usajili wa Washiriki
02:00-03:45 Kipindi cha 1 Ukaribisho, Utangulizi Kuchangamkiana/ vunja ukimya Mkutano wa Elimu wa Wilaya
1. Ukaribisho na Utangulizi Maneno ya kufungua Afsa Elimu wa Mkoa na Kiongozi wa EQUIP mkoa(RTL). 2. Kuchangamshana 3. Hali ya sasa kwa ajili ya Maboresho ya shule (kazi ya kikundi) 4. Mreojesho wote
Nakala za kutosha za vitabu vya mshiriki Karatasi za Bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe Karatasi ya A4, kalamu
03:45-04:15
04:15-06:00 Kipindi cha 2 Malengo ya Mkutano wa Elimu wa Wilaya
5. Habari za MEW mpaka sasa – ‘PowerPoint’ 6 Manufaa za MEW 7. Mreojesho wote 8. Kipindi cha Majumuisho
Nakala za kutosha za Kiambatisho A. Bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe Karatasi ya A4, kalamu Projekta, kisitiri, kompyuta
06:00-07:00
07:00-08:45 Kipindi cha 3
Kupanga na kuandaa Mkutano wa Elimu wa Wilaya
9.Kamati ya maandalizi na Wajibu wa Mwakilishi wa MEW 10. Mfano wa MEW na kupanga Mkutano 11. Mfano wa mipango ya Mikutano ya mwazo 12. Uwezeshaji na mbinu shirikishi 13. Majumuisho ya wote na majadiliano
Nakala za kutosha za Mipango ya Mkutano zilizoandaliwa (Kiambatisho B, C, D na E) Karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe Karatasi ya A4, na kalamu
08:45-09:15
09:15-11:00 Kipindi cha 4 Umuhimu wa Mada za majadiliano na Mwongozo wa mada za mwaka
14. Mada zipi zinafaa 15. Tengeneza orodha ya Mada 16. Mrejesho wa wote 17. Tafakuri juu ya umuhimu wa kuchagua mada 18. Kupiga kura ili kuchagua Mada 10 bora zaidi 19.Kushirikishana mwongozo wa Mada za mwaka 20 Kuhitimisha siku
Karatasi za bango kitita zilizoandikwa kwa ajili ya kazi ya 17 Mfano wa Mwongozo –Kiambatisho F Karatasi ya ukubwa wa bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
6
Kipindi cha 1
Utangulizi wa mafunzo na Mkutano wa Elimu wa Wilaya (MEW) Kama ‘Jamil
Inayojifunza”
Muda: Saa 1 na dakika 45 (dakika 105) Lengo la Kipindi:
Kukuza uelewa wa washiriki juu ya Mikutano ya Elimu ya Wilaya na malengo yake ya kusaidia uboreshaji wa shule.
Kuelewa ni kwa jinsi gani Mikutano ya Elimu ya Wilaya (MEW) inaendana na jamii nyingine inayojifunza.
Matokeo ya kujifunza: Mwishoni mwa kipindi washiriki wataweza kuelezea: Jinsi Mkutano wa Elimu wa Wilaya unavyohusika na “Jamii inayojifunza” Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni nini, na tofuati yake na mikutano inayofanyika sasa Wawezeshaji watakiwa kuwa wameandaa:
Mpangilio wa namna ya kukaa ukumbini: hakikisha washiriki wote wanaweza kumuona Mkufunzi
Nakala za kutosha za vitabu vya washiriki
Karatasi ya bango kitita kama inavyoonekana katika kielelezo hapa chini.
_____________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi
1. Kukaribisha washiriki na kutoa utangulizi (dakika 20)
Pitia kijitabu na ueleze kuw:
Wakaribishe washiriki kwenye warsha na ueleze kwa ufupi malengo ya warsha. Eleza kuwa utaongoza na kuwezesha mchakato na kwamba washiriki watashiriki ipasavyo wakati wa vipindi vya semina (kama vile katika mafunzo ya Usimamizi wa Utendaji wa shule (SPMM). Tangaza na weka wazi taratibu zote za ndani ya ukumbi ikiwa ni pamoja na muda wa vipindi na uandike hayo kwenye karatasi ya bango kitita:
Muda gani tunaanza (2:00 asubuhi), kupumzika, kupata chakula cha mchana, na mwisho (11:00 jioni)
Mbinu, kufanya kazi katika jozi, na katika vikundi
Umuhimu wa kuteua mwandishi wa taarifa kwa ajili ya vipindi vya mrejesho Waulize washiriki ni kanuni gani au taratibu zipi za ndani ya ukumbi wangependa ziwepo na uziandike kwenye bango kitita. Hakikisha kuwa karatasi ya bango kitita itabaki imebandikwa ukutani kwa muda wote wa semina.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
7
Elezea Nii kwa jinsi gani mafunzo haya kuhusu MEW ni Jamii nyingine Inayojifunza na inavyohusiana na Mikutano ya Kila wiki ya Shule na Mikutano kati ya Waalimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata inayojadili kuhusu Usimamizi wa Utendaji wa Shule.
English Swahili
Communities of learning Jamii zinazojifunza
PTP+School Committee+Village Government UWW+Kamati ya Shule+Kamati ya Kijiji
District Education Meeting Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Zonal Kikanda
Region-District-Ward-School Mkoa-Wilaya-Kata-Shule
Community Jamii
Score card IdadiAlama
QA Mthibiti wa Ubora SIS Mfumo wa Taarifa za Shule
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
8
Afisa Elimu Kata anahusika katika kila mafunzo ya jamii inayojifunza. Hii inamfanya yeye kuwa muhimu sana katika mambo yote ya uboreshaji wa shule.
1. Mikutano mipya ya kila wiki ngazi ya shule ni kwa ajili ya Mwalimu mkuu na Walimu yenye lengo la kuboresha kiwango cha ufaulu shuleni
2. Mikutano ya jamii inahusisha wazazi na jamii katika kuleta maendeleo ya shule na kuwasaidia wanafunzi 3. Mkutano wa kata wa Walimu wakuu ni kwa ajili ya kushirikishana uzoefu na kuwajengea uwezo walimu wakuu,
kujadili changamoto na mambo yanayohusu maendeleo ya shule 4. MEW ni jukwaa la Wathibiti Ubora wa Shule, Maafisa Elimu Wilaya na Waratibu Elimu Kata linalotoa fursa ya
kushirikishana masuala mbalimbali yanayohusu elimu katika wilaya ili kuboresha shule. Unatoa msaada maalumu kwa Maafisa Elimu Kata kwenye kutekeleza kazi zao
Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni Mkutano wa kila mwezi unaowahusisha Maafisa Elimu wa Wilaya, Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu Kata. MEW unawezesha kutenga muda ili;
Kushughulikia masuala yanayohusu ufundishaji na ujifunzaji yanapoibuka --> ni lengo la MEW
Kushirikishana na kuimarisha jitihada za uboreshaji elimu katika wilaya
Kuwezesha mawasiliano kuwa mazuri zaidi.
MEW ni mkutano rasmi wa Wilaya unaotambulika na wizara i, kama vile Ofisi ya ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Elimu, wenye lengo la kuteta mawazo ya pamoja, katika kusaidia kuboresha maendeleo ya shule.
2. Kuvunja ukimya, zoezi la kuchangamsha mwili (dakika 25)
Wagawanye washiriki katika makundi matatu; Kundi la 1 litajifanya kuwa Maafisa Elimu Kata, kundi la 2 litajifanya kuwa la Wadhibiti Ubora na kundi la 3 litakuwa la Maafisa Elimu. Wapatie kila kundi karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha.
Waambie kila kundi wajadili ni kwa jinsi gani wanachangia katika kuboresha shule, na waandike mawazo yao kwenye bango kitita. Kundi la kwanza kumaliza litaita kwa sauti "BINGO". Kundi hili litabandika bango kitita ukutani. Endelea kufanya hivyo hivyo hadi makundi yote 3 yakamilishe.
Ni mambo gani muhumu mliyo yakuta katika majadiliano?
Tutayaangalia/jadili mambo hayo katika siku hizi mbili za mafunzo. 3. Kazi ya kikundi: Wajibu wa sasa katika kuboresha shule katika Wilaya (dakika 35) Hakikisha kila kundi lina bango kitita na kalamu rashasha. Yakumbushe makundi kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye atachukua maelezo na kuwasilisha wakati wa majumuisho.
Waambie washiriki wajadili ni kwa namna gani shule zinasimamiwa kwa sasa. Lengo la zoezi hili ni kupata maoni ya washiriki juu ya wajibu wao wa kuboresha shule Wilayani. 4. Majumuisho ya Mrejesho (dakika 25) Kila kundi libandike bango kitita ukutani. Waambie washiriki wasome orodha ya majukumu ya kila kikundi.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
9
Mwezeshaji sasa anaongoza mjadala wa majumuisho ya mrejesho kwa kutumia maswali yafuatayo:
• Ni zipi kati ya kazi zenu zinasaidia sana kuboresha shule? • Je, mnatumia muda mwingi zaidi kwenye kazi zipi ? • Ni majukumu gani na kazi zipi vinawasaidia kutekeleza uboreshaji wa shule yenu?
Mambo muhimu ya kusisitiza:
Kupitia mafunzo haya ya jamii inayojifunza Wilaya zinahakikisha kwamba:
Ufundishaji na ujifunzaji unaboreshwa
Viwango vya ufaulu wa wanafunzi vinaboreshwa
Shule zinawajibika
Ubunifu mpya unatolewa kwa wengine na unafanyiwa majaribio
Jamii zinashiriki na kujishughulisha na masuala ya shule zao
Taarifa zinapokelewa na kusambazwa
Masuala ya fedha yanajadiliwa, kama vile ruzuku ya IGA
Hili ni jukumu la pamoja!
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
10
Kipindi cha 2 Lengo la Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Muda: Saa 1 na dakika 45 (dakika 105)
Malengo ya Kipindi:
Kuelezea malengo ya siku ya 2 ya mafunzo kuhushu MEW
Kuwawezesha washiriki kuelewa madhumuni ya Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Kuonesha kuwa Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni chombo muhimu cha kusaidia kuboresha maendeleo ya shule>
Kuhusianisha MEW na fursa nyingine za kujifunza
Matokeo ya mafunzo: Hadi kufikia mwisho wa kipindi washiriki wa kipindi hiki wataweza:
• Kuelezea ni kwa jinsi gani Mkutano wa Elimu wa Wilaya unasaidia kuboresha shule • Kuelewa tofauti iliyopo kati ya mikutano ya Wilaya ya sasa na MEW
Wawezeshaji wameandaa:
Mahali pa kuweka kompyuta, projekta na skrini, na zana za kuunganishia umeme
Mpangilio mzuri wa ukumbi wa mafunzo ili washiriki wote waweze kuona vyema kwenye skrini
Karatasi za bango kitita za kutosha, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu
_________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi 5. Uwasilishaji kwa kutumia “PowerPoint” (dakika 40) Kushirikishana malengo ya mafunzo na taarifa za mkutano wa majaribio wa MEW uliofanyika Mkoa wa Tabora. Tumia maswali na majibu kutoka kwa washiriki. 6. Kazi ya kikundi: Faida za Mkutano (dakika 20) Hakikisha kila kikundi kina karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha. Wakumbushe washiriki kuwa wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye atachukua maelezo na kuwasilisha waliyojadili wakati wa majumuisho.
Kuna manufaa gani kwa Wathibiti Ubora, Maafisa Elimu Kata na Maafisa wa Wilaya kukutana kila mwezi kujadili mbinu za kuinua ubora wa elimu katika Wilaya?
Kwa jinsi gani MEW unatofautiana na mikutano ya sasa?
7. Mrejesho wa wote (Uwasilishaji) (dakika 30)
Waombe washiriki wa kila kikundi wakwambie majibu yao (yasizidi majibu 2). Kisha endelea kwa mzunguuko huohuo mpaka wametoa majibu yao yote. Yaombe makundi yasirudie ambacho kimesemwa na kundi kingine.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
11
Andika mambo muhimu (siyo neno kwa neno) kutoka kwa washiriki kwenye bango kitita.
Faida za mikutano ya MEW: Mambo muhimu ya kusisitiza:
Uelewa wa pamoja kuhusu mchango wa kila mmoja na kushirikishana mawazo
Kufikia makubaliano ya kuchukua hatua za pamoja za kuboresha shule wilayani
Kuthamini na kujenga uwezo wa washiriki wote kwenye mkutano, hasa Maafisa Elimu Kata
Kushirikishana mafanikio na mawazo mapya
Kuboresha utendaji wa shule ni jukumu la pamoja!
Kipi cha tofauti kuhusu Mikutano ya Elimu ya Wilaya (MEW)? Mikutano ya Maafisa Elimu wa Wilaya na Maafisa Elimu Kata imelenga mambo mengi, yakiwemo yafuatayo:
Kazi za kiutawala kwa kuzingatia miongozo ya Wizara
Kuwataarifu wafanyakazi kuhusu nyaraka na maagizo ya Wizara
Kujadili kuhusu ufaulu wa wanafunzi
MEW ni chombo cha kusaidia kuboresha utendaji wa shule:
Mijadala inalenga njia za kuboresha elimu wilayani
Maamuzi yanatolewa kwa pamoja kama ‘jamii inayojifunza’
Ufumbuzi unapatikana, licha ya changamoto, kwa ushirikiano wa Maafisa Elimu Kata, Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu kwa kufanya kazi pamoja
Jitihada na wajibu wa kuboresha shule vinafanywa kwa kushirikishana na kukubaliana, pamoja na ufuatiliaji
Ni fursa kwa Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma Maafisa Elimu Kata.
Maafisa Elimu Kata wanabeba jukumu la kuhakikisha ufumbuzi unapatikana
8. Majumuisho ya Kipindi (dakika 15) Elezea kwa ufupi jinsi tunavyoiona mikutano ya MEW:
Kujenga uelewa wa pamoja na njia za kuinua viwango na ubora wa elimu katika wilaya:
o Kwa Wathibiti ubora wa Shule waweze kuchangia utaalamu wao, na Maafisa Elimu
Kata waweze kuwapa taarifa muhimu za shule katika wilaya zao.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
12
o Kwa Halmashauri kuweza kupokea taarifa za kuiwezesha kuandaa mipango yao kwa
ajili ya kusaidia, kufundisha na kuhamasisha shule kufanya vizuri, vile vile kuweka
vipaumbele kwenye mipango yao ya kuboresha na kugharamia elimu.
o Kwa kusaidia upatikanaji wa taarifa kati ya Wathibiti Ubora wa Shule, Maafisa Elimu wa
Wilaya na Maafisa Elimu Kata kuhusu shughuli zao za mwezi uliopita na na za mwezi
unaofuata.
Kufanya mapitio ya mikakati ya wilaya na kupata mrejesho kuhusu progamu mbalimbali
Kujikita kwenye masuala muhimu yanayoinua ubora wa elimu wilayani, kupanga shughuli
za mafunzo na kusaidia maendeeo ya shule kwa ujumla.
Kutoa fursa kwa Maafisa Elimu Kata, Wathibiti Ubora wa Shule na Maafisa Elimu
wengine ngazi ya wilaya kuwa na Mikutano “Jamii inayojifunza” ya kila mwezi, ili kupata
mawazo mapya na kutafuta njia za kutatua changamoto za uboreshaji wa maendeleo ya
shule.
MEW ni tofauti na mikutano mingine ya sasa:
• Katika ,MEW masuala pekee yanayojadiliwa yanayohusiana moja kwa moja na Uboreshaji
wa shule.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
13
Kipindi cha 3 Maandalizi na Kupanga Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Muda: saa 1 na dakika 45 (dakika 105) Lengo la kipindi: Lengo la kipindi ni kuwapatia washiriki fursa ya kuelewa umuhimu wa kupanga na kuandaa Mkutano wa Elimu wa Wilaya. Matokeo ya kujifunza: Hadi mwisho wa kipindi hiki washiriki watakuwa na uwezo mkubwa wa:
Kujua kuhusu umuhimu wa kupanga na kuandaa Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Kuelewa wajibu wa Kamati ya Maandalizi na jukumu la Mwakilishi wa Mkutano wa Elimu wa Wilaya
Kuelewa umuhimu wa kuwezesha na mbinu shirikishi
Kuangalia mipango mitatu iliyoandaliwa kwa ajili ya mikutano ya awali ya huko Tabora
Kubuni muundo wa Mkutano wa Elimu wa Wilaya Wawezeshaji waandae:
Nakala za viambatisho A, B, C, D na E kwa ajili ya washiriki wote
Idadi ya kutosha ya karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu
______________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi 9. Majukumu ya Timu ya Maandalizi na Wajibu wa Mwakilishi wa MEW (dakika 20) Soma na kupitia Majukumu ya Kamati ya Maandalizi na Wajibu wa Mwakilishi wa MEW Kiambatisho A: Elezea jukumu la Mwakilishi wa MEW kuwa ni mtu anayeratibu mkutano na mwenendo wa Kamati ya MEW. Mwakilishi wa MEW mara nyingi ni Afisa Elimu Taaluma / Afisa Elimu Vifaa na Takwimu na Afisa wa EQUIP-T kwa kuwa majadiliano mara nyingi hurejea mafunzo yaliyopita. Angalia ajenda na vifaa Soma na kupitia malengo makuu ya Mkutano
Hakikisha washiriki wanaelewa kuwa malengo makuu ya Kuandaa na Kupanga Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni:
Wathibiti bora, Maafisa Elimu Kata na Maafisa Elimu kwa pamoja ni timu ya kuandaa mkutano
Kutazama mafanikio ya mkutano wa mwisho wa MEW na kushirikishana mawazo ambayo yaliyofanikiwa vizuri
Kuamua kwa pamoja ni hatua gani ambazo watachukua ili kuboresha
Kuangalia ni nini kinapaswa kufuatiliwa kutokana na mikutano ya awali
Kuandaa ajenda na mada kuu kwa ajili ya mkutano ujao
Kutafuta wawezeshaji na kuandaa mbinu shirikishi Kukutana kila mwezi
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
14
10. Kiolezo cha mkutano wa MEW kilichotumika Tabora (dakika 15) Soma na kushirikishana Kiolezo cha MEW kwa pamoja. Kiambatisho B Muda Tarehe na muda wa MEW unapangwa kulingana na ratiba ya wilaya husika. Katika baadhi ya wilaya tarehe za mwaka mzima zimekwishapangwa kabisa. Chakula/Chai Eleza kuwa chai inaweza inaweza kuwepo au kutokuwepo kulingana na bajeti ya wilaya husika na utoe mifano halisi kutoka mkoa wa Tabora. Wengine wanapata chai, wengine chakula cha mchana, kwa wengine ni soda na biskuti, na wengine hawapati kitu chochote. Kila Wilaya inapaswa kuzingatia na kuamua kuhusu chakula kulingana na bajeti yake. Hata hivyo, muda wa mkutano utategemea mipangilio na upatikanaji wa viburudisho. Uwezeshaji na Mbinu Shirikishi Uwezeshaji na Mbinu Shirikishi ni muhimu kwa jinsi MEW unavyofanya kazi. Ili majadiliano yafanikiwe tunahitaji kutumia masomo tuliyojifunza kutoka kwenye Mafunzo kuhusu Usimamizi wa Utendaji wa Shule (SPMM) kuhusu mawasiliano bora - kuwa ni mawasiliano shirikishi yanayozingatia tabia ya 'Twiga'. Taratibu nyingine Mpango unapaswa kuonesha nani atakayewezesha wakati wa kipindi na vifaa vinavyotakiwa. 11. Elezea kwa ufupi kupitia mipango ya sampuli ya MEW 1, 2 na 3 ya huko Tabora (dakika 10) Mpango wa 1 ni mkutano wa kwanza: Kutambulisha MEW na kuangalia faida zake Kiambatisho C Mpango wa 2 ni mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Shule Kiambatisho D Mpango wa 3 unaangalia taarifaza Maafisa Elimu Kata na Ziara za Shule Kiambatisho E & H
12. Kazi kubwa ya kikundi: Uwezeshaji wa Mkutano (dakika 30) Wagawanye washiriki katika makundi matatu: kundi la1 wafanye mapitio ya Mpango wa 1, kundi la 2 mapitio ya Mpango wa 2 na kundi la 3 mapitio ya Mpango wa 3. Hakikisha kila kundi lina karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha. Yakumbushe makundi kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye atachukua maelezo na kuwasilisha wakati wa majumuisho. Waambie washiriki wajadili kuhusu mkutano:
Njia gani zimetumika kuwezesha mkutano huu?
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
15
Ni nani anayehusika na kuongoza mkutano?
Ni faida gani kuu za mkutano huu? 13. Mrejesho wa wote na Mjadala (dakika 30) Kila kikundi kibandike bango kitita ukutani. Kisha waambie wasome.
Nini maoni yako?
Kuna kitu gani kingine cha ziada ambacho umekiona? Mwezeshaji sasa anaongoza majumuisho ya mrejesho kwa kusisitiza vipengele vifuatavyo
Vipengele muhimu vya kusisitiza: Mbinu za Uwezeshaji zilizotumika ni: Majadiliano, bungua bongo ya kikundi, mrejesho, igizo dhima, uchambuzi wa Mpango wa Maendeleo ya Shule, kwa kutumia vigezo vya pamoja Wajibu wa kuongoza mkutano Ni jukumu la pamoja. Katika mikutano ya baadaye Maafisa Elimu Kata watachukua nafasi ya utendaji katika mikutano. Faida za Mkutano
Uelewa wa pamoja wa michango kutoka kwa kila mtu na kushirikishana mawazo.
Kufikia makubaliano ya kuchukua hatua za pamoja za kuboresha shule wilayani
Kuthamini na kujenga uwezo wa washiriki wote katika mkutano hasa Maafisa Elimu Kata.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
16
Kipindi cha 4 Umuhimu wa Kujadalii mada na Mwongozo wa Mada za MEW kwa Mwaka Muda: saa 1 na dakika 45 (dakika 105) Malengo ya kipindi:
Kukuza uelewa wa wawashiriki kuhusu wigo na upana wa mikutano ya MEW kwa kuangalia mada za mwaka
Kukuza uelewa wa washiriki kuhusu changamoto zinazoweza kujitokeza kwenye kufikia elimu bora
Matokeo ya kujifunza: Mwisho wa kipindi washiriki wataweza:
Kuelewa umuhimu wa mada kwa kila MEW
kutoa orodha ya mada zitakazo endesha mikutano ya .MEW
Kupanga mpango wa kuwezesha mada moja
Wawezeshaji waandae:
Karatasi za bango kitita za kutosha, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu
Karatasi za bango kitita zilizo na maswali yaliyoandikwa kwa ajili ya kutafakari mada katika Kazi ya 17.
watu wa 2 wa kuhesabu kura wakati wa kupiga kura katika Kazi ya 18.
Nakala za Mwongozo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Kiambatisho F
Mambo muhimu ya kusisitiza:
Mkutano una lengo la kuboresha maendeleo ya shule na kuinua viwango vya wanafunzi
Mkutano ni kwa ajili ya kuboresha uelewa wa maswala muhimu au mada ambazo zinahitaji ufafanuzi
Mkutano ni kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi na kujua nini cha kufanya
Mkutano unapaswa kusababisha maboresho ya kazi ya wadau wote Mada zilizochaguliwa inapaswa kuwa ni zile ambazo MEW unaweza kuzitekeleza na kupata matokeo chanya, hasa mada zinazolenga katika ufundishaji na ujifunzaji Jaribu kupata urari wa mada za mwaka ikiwa ni pamoja na: Jamii, Kufundisha na Kujifunza, Usimamizi wa Shule, Ufuatiliaji na Tathmini Mada zinaweza kurudiwa mara kadhaa katika miaka mingine. Mkutano sio kwa ajili ya kujadili masuala ya utawala au kuwafundisha Maafisa Elimu Kata. Majadiliano kuhusu piki piki, posho, miundombinu au ukosefu wa walimu sio mambo ambayo mkutano huu unaweza kuyabadilisha hivyo masuala haya inapaswa yasipewe nafasi ya kujadiliwa sana.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
17
14. Ni mada gani ambazo zinaweza kuingizwa katika MEW ? (Dakika 5)
Mwezeshaji anaanzisha somo kwa kugawana baadhi ya mada zilizochaguliwa kwenye mkutano wa MEW Mkoani Tabora:
• Kufanya kazi na walimu wakuu wenye changamoto • Kuelewa Mtaala Mpya • Kuboresha Mahudhurio ya Mwalimu Darasani • Uchambuzi wa ubora wa Mipango ya Maendeleo ya Shule • Uchambuzi wa ubora wa taarifa za Maafisa Elimu Kata na ziara za kutembelea shule
Mada zinapaswa:
Kupelekea maboresho kwa maendeleo bora ya shule na kuinua viwango vya wanafunzi
Kusaidia kupata ufumbuzi na kujua nini cha kufanya Mada hazipaswi:
Kuwa za masuala ya utawala na kutoa maelekezo kwa Maafisa Elimu Kata
Kuwa za kuhusu piki piki, posho, miundombinu au ukosefu wa walimu
15. Kazi ya vikundi: Andaa orodha ya Mada (dakika 15) Wagawe washiriki katika makundi 6 Hakikisha kila kundi lina karatasi za bango kitita na kalamu rashasha. Wakumbushe kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye ataandika maelezo na kutoa mrejesho wakati wa majumuisho. Waambie washiriki waorodheshe mada ambazo zinaweza kufanyiwa kazi kwenye MEW Bandika mara moja orodha hizo ukutani na omba kila kikundi wasimame karibu na karatasi yao wakiwa na kalamu.
16. Mrejesgo wa wote kuhusu orodha ya mada (dakika 15)
Kikundi cha 1 watoe mrejesho na kama mada tajwa imerudiwa na vikundi vingine wanapaswa kuifuta. Kisha vikundi vingine watoe mrejesho wao pia.
17. Kazi ya mtu mmoja mmoja na vikundi vidogo; Kutafakari juu ya mada zilizotajwa (Dakika 30)
Mwezeshaji anasoma swali na kuelezea umuhimu wa kila mada katika kuchagua mada za MEW
Ni mada gani zinafaa zaidi?
Ni mada zipi zitaleta matokeo chanya zaidi katika ufundishaji na ujifunzaji?
Ni mada gani zina changamoto zaidi katika kuleta mabadiliko?
Ni mada zipi ambazo zitasababisha kupanda kwa viwango vya ufaulu shuleni?
Ni mada gani zinaweza kuchaguliwa ili kupata mada bora zaidi za mwaka?
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
18
Kila mtu anafikiria juu ya maswali haya na kuandika sababu za majibu yao (dakika 5) Kisha kujadili katika vikundi maoni yao na maelezo ya uchaguzi wao. (dakika 15) Mwezeshaji anaongoza majadiliano ya kundi zima (dakika 10):
Je, kuna kikundi chochote kilikubaliana juu ya maswali yoyote / majibu? Haishangazi kwa kikundi kutokubaliana maana hakuna majibu sahihi na wote tutakuwa na machaguo tofauti tofauti.
Je, kuna mtu yeyote amepata shida kuelewa au kujibu maswali yoyote?
Vipengele muhimu vya kusisitiza: Mkutano una lengo la kuboresha maendeleo ya shule na kuinua viwango vya wanafunzi Mkutano ni kwa ajili ya kuboresha uelewa wa masuala muhimu au mada ambazo zinahitaji ufafanuzi Mkutano ni kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi na kujua nini cha kufanya Mkutano unapaswa kusaidia maboresho ya kazi ya wadau wote Mada zilizochaguliwa inapaswa kuwa ambazo MEW inaweza kuzitekeleza na kupata matokeo chanya, hasa mada zinazolenga katika ufundishaji na ujifunzaji Jaribu kupata mada kwenye masuala tofuati tofauti za mwaka ikiwa ni pamoja na: Jamii, Kufundisha na Kujifunza, Usimamizi wa Shule, Ufuatiliaji na Tathmini Mada zinaweza kurudiwa mara kadhaa katika miaka mingine. Mkutano siyo kwa ajili ya kujadili masuala ya utawala au kuwafundisha Maafisa Elimu Kata. Majadiliano kuhusu piki piki, posho, miundombinu au ukosefu wa walimu sio mambo ambayo mkutano huu unaweza kuyabadilisha hivyo masuala haya inapaswa yasipewe nafasi ya kujadiliwa sana.
18. Kupiga kura kuchagua Mada 10 bora zaidi (dakika 20) Mwezeshaji anaelezea kuwa sasa tunakwenda kuchagua mada 10. Kila mtu anaweza kupiga kura mara 3 tu. "Unaweza kuchagua mada tatu tu za kupigia kura. Unaruhusiwa kupiga kura mara tatu tu. Nitasoma orodha ya mada. Katika kila mada wale wanaotaka kuipigia kura mada hiyo wanaweza kuinua mikono yao juu na wenzangu watahesabu jumla ya kura hizo." Soma orodha na kuwaomba washiriki wanaochagua wainue mikono kila wakati na uandike kwa kila mada jumla ya kura zilizohesabiwa kwa mada hiyo. Endelea kufanya hivyo kwa haraka ili zoezi hili lisichoshe.
Baada ya kupiga kura, weka alama ya nyota kwenye mada 10 zenye kura nyingi zaidi. Mwezeshaji anawauliza washiriki "je zoezi hili limetupa orodha nzuri ya mada za mwaka mmoja? Je, kuna mada zinazohusu: • Jamii • Kufundisha na Kujifunza • Uongozi na Usimamizi • Ufuatiliaji na Tathmini? "
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
19
19. Kushirikishana Mwongozo wa Mwaka (dakika 10) Kazi ya kupiga kura kuchagua mada ilikamilishwa katika DEM nyingi huko Tabora. Maafisa Elimu Kata, Maafisa Elimu na Wathibiti Ubora walipiga kura na kuamua mada za mwaka nzima. Mada hizo ndizo zilizoandikwa kwenye Mwongozo. Mwongozo huu ni mojawapo kati ya miongozo ya kutumia. Kusoma na kushirikishana Mwongozo wa Wilaya ya Nzega. Kiambatisho F Je, kuna usawa mada za mwaka?
Jamii
Kufundisha na Kujifunza
Uongozi na Usimamizi
Mafunzo Mada zitarudiwa mara kadhaa kwa miaka mingi ijayo ili kuimarisha, kuboresha na ili kuwasaidia wadau wapya. 20. Majumuisho ya huhitimisha Siku (dakika 5) "Leo tumeangalia kuhusu MEW, malengo ya Mkutano na upangaji mipango kwa ajili ya MEWna Kuandaa Mwongozo wa Mada za mwaka. Kesho tunatakiwa kufika hapa saa 1.30 asubuhi kujisajili na saa 02.00 tutaanza kipindi. Tutaangalia juu ya kuendeleza utaalamu wa Maafisa Elimu Kata na kufanya maandalizi kwa ajili ya MEW katika Mkoa huu." Maliza kwa Wimbo Kabla ya kuondoka hakikisha endapo kila Wilaya imeleta mifano 5 ya ripoti za Maafisa Elimu Kata kutoka katika Wilaya yao.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
20
Siku ya 2: Kuandaa na kutekeleza mkutano wa MEW
Muda Kazi Mbinu na Maudhui Zana
02:00-3:45
Kipindi cha 5 Matarajio ya Maafisa Elimu Kata na kujenga uwezo wao wa kitaaluma
21. Utangulizi na ufupisho wa mada za siku ya 1 22. Wajibu wa Maafisa Elimu Kata 23. Kujenga uwezo wa Maafisa Elimu Kata 24. Matembezi kuona majibu na Mrejesho 25. Uhusiano wa kazi za Maafisa Elimu Kata na Wathibiti Ubora wa shule
Karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu Mpira Yaliyoandikwa kwa ajili ya Kazi ya 23 Ufafanuzi wa Kazi ya Afisa Elimu Kata-Kiambatisho G
03:45-04:15
04:15-06:00
Kipindi cha 6 Ufuatiliaji, Msaada, na Mapitio ya Mkutano wa Elimu wa Wilaya
26. Kuchangamshana na tafakari 27. Ufuatiliaji, Msaada na mrejesho wa MEW 28. Mjadala wa wote 29. Taarifa za Maafisa Elimu Kata 30. Kushirikishana taarifa bora zaidi za Maafisa Elimu Kata.
Karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu Kadi kubwa yenye namba 0, 5 & 10. Ripoti ya 5 za Maafisa Elimu Kata kutoka kila Wilaya Nakala iliyoandikwa kwa vikundi 3 kwa ajili ya Kazi ya 27 Nakala za Kiambatisho E & H Orodha ya Machaguo ya lazima
06:00-07:00
07:00-08:45
Kipindi cha7 Kupanga Mkutano wa Elimu wa Wilaya
31. Utangulizi 32. Kupanga na kuandaa Mkutano wa MEW 33. Mjadala wa wote 34. Maswali na Majibu, hitimisho
Karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu Nakala za kiolezo cha MEW Kiambatisho A Orodha ya Mada kutoka Kipindi cha 4
08:45-09:15
09:15-11:00
Kipindi cha 8 Kutatokea nini baada ya mafunzo? Kuhitimisha
35. Ufupisho wa mada za MEW 36. Maswali na Majibu, Hitimisho 37. Nini cha kufanya baada ya mafunzo? 38. Muhtasari wa siku 2 za mafunzo 39. Maneno ya kuhitimisha na kuagana
Miongozo ya mikutano ya kila wiki ya Walimu wakuu, nakala moja kwa kila mshiriki Fomu za Tathmini Nakala na Chati ya Kazi ya 37
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
21
Kipindi cha 5 Matarajio ya Maafisa Elimu Kata na kujenga uwezo wao wa kitaaluma
Muda: saa 1 na dakika 45 (dakika 105)
Malengo ya kipindi:
Kuinua uelewa na umuhimu wa MEW wa kuongeza uwezo wa kitaaluma wa Maafisa Elimu Kata
Kuamsha ujuzi wa washiriki kuhusu Wajibu wa Maafisa Elimu Kata
Kuonyesha uhusiano uliopo kati ya kazi za Maafisa Elimu Kata na Wathibi Ubora
Matokeo ya kujifunza: Hadi mwisho wa kipindi hiki washiriki wataweza:
Kueleza matokeo chanya ambayo Maafisa Elimu Kata wanaweza kuchangia katika kuinua viwango vya shule
Kueleza jinsi MEW unaweza kuwasaidia Maafisa Elimu Kata kuboresha utendaji wao
Kueleza uhusiano na mwingiliano uliopo kati ya kazi ya Maafisa Elimu Kata na Wathibiti Ubora
Wawezeshaji waandae: Mpira wa kutumia kuchangamsha mwili
Swali kuhusu kazi ya Maafisa Elimu Kata katika Kazi ya 23 litakuwa tayari limeandikwa kwenye karatasi ya bango kitita
Nakala za kutosha za Maelezo ya majukumu ya Maafisa Elimu Kata - Kiambatisho G
Mabango kitita na kalamu rashasha
_____________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi 21. Utangulizi na Muhtasari wa Siku ya 1 (dakika 10) Anza siku na wimbo kwa kuwaomba washiriki wasimame kwa jinsi ya mduara. Rusha mpira kwenye mduara ili warushiane wao kwa wao. Kila anayedaka mpira anajitambulisha na kusema anachokumbuka kuhusu mafunzo ya jana. 22. Majukumu ya Maafisa Elimu Kata (dakika 15) Waombe washiriki waketi katika vikundi. Waambie washiriki kuwa asubuhi hii watatazama kuhusu majukumu ya Mafisa Elimu Kata na jinsi mkutano wa MEW unaweza kujenga uwezo wao wa kitaaluma. Maafisa Elimu Kata ni wasaidizi kwanza wa shule, na hivyo wanaweza kuleta matokeo muhimu sana kwenye maendeleo ya shule. Kwa haraka soma maelezo ya kazi ya Maafisa Elimu Kata Kiambatisho G
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
22
23. Kujenga uwezo wa Maafisa Elimu Kata (dakika 25)
Hakikisha kila kikundi kina karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha. Wakumbushe kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye atachukua maelezo ya majadiliano yao na kutoa mrejesho wakati wa majumuisho.
Ni uboreshaji gani wa kitaaluma tunaotaka kuboresha utendaji wa Maafisa Elimu Kata?
Ni kwa jinsi gani Maafisa Elimu Kata wanaweza kuinua viwango vya shule?
Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia Maafisa Elimu Kata kuboresha utendaji wao?
Toa mifano ya Maafisa Elimu Kata wanaofanya kazi vizuri ambao wanaweza kushirikishana uzoefu wao na wengine 24. Kuzunguka kuona kazi na mrejesho (dakika 40) Waombe washiriki wabandike karatasi zao ukutani. Wapatie dakika kumi za kila mshiriki kutembea tembea ili kusoma kazi za vikundi vingine. Wahimize washiriki kuandika maoni / maswali yoyote waliyo nayo, au nyongeza yoyote wanayopenda kuongeza.
Baada ya dakika kumi, endesha mjadala wa majumuisho juu ya masuala ambayo wameibua kwa ajili ya MEW na kwa nini hayo. Wapeni washiriki fursa ya kuuliza maswali yao nk. Andika mambo muhimu kwenye bango kitita. Sisitiza kuwa kwa mikutano ya MEW, masuala yanayoibuliwa yanapaswa kuwa yanahusiana na yale ambayo Maafisa Elimu Kata wanaweza kufanya ili kuboresha utendaji wao au masuala ambayo Maafisa Elimu Kata wanaweza kushawishi kwa namna isiyo ya moja kwa moja.
25. Uhusiano uliopo kati ya kazi ya Maafisa Elimu Kata na Wathibiti Ubora (dakika 15) Elezea Imezoeleka Wathibiti wa Ubora wamekuwa wakifahamika kama Wakaguzi wa Shule na jukumu lao kuu ilikuwa ni kufanya ukaguzi wa shule, jukumu ambalo kimsingi linabeba dhana ya kuhukumu au kukosoa. Hili lilifuatiwa na utoaji wa mrejesho wa papo kwa papo na taarifa ya maandishi. Hata hivyo, kutokana na mabadiliko yanayoendelea katika Idara ya Ukaguzi, kwa sasa Wakaguzi wanafahamika kama Wathibiti Ubora wa shule. Wakaguzi wa Shule sasa ni Wasimamizi wa Shule wa nje. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaandaa mwongozo mpya wa Uthibiti Ubora wa Shule unaompa majukumu mengi zaidi Afisa Elimu Kata kama Afisa kwenye ngazi ya kata. Majukumu makuu ya Maafisa Elimu kata ni: - (i) Kumshauri Afisa Mthibiti Ubora wa elimu wa Wilaya kuhusu ubora wa elimu katika kata (ii) Kusaidia na kufanya mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Shule, na mchakato wa Tathmini ya ndani ya Shule na utekelezaji wake (iii) Kumwezesha mwalimu mkuu kama msimamizi wa ndani katika shule husika Uthibiti Ubora wa Ndani Mwalimu Mkuu anatarajiwa kuwa msimamizi wa ndani wa shule. Mwalimu mkuu anawajibika kuandaa Tathmini ya ndani ya Shule inayo tazama kwa kina masuala ya shule ili kuboresha zaidi hali ya utendaji wa
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
23
shule. Imekuwa ni jambo muhimu sana kwa sasa kukubali na kuhamasisha kufanyika kwa Tathmini ya ndani ya Shule kama njia muhimu ya kuinua viwango vya mafanikio shuleni. Jambo hili linaenda sambamba na mchakato wa Mpango wa Maendeleo ya Shule na Kikao cha Jamii inayojifunza cha kila wiki. Afisa Elimu Kata atahakikisha haya yote yanatekelezwa.
English Swahili QA led with support from WEO Mthibiti Ubora anaongoza akisaidiwa na Afisa Elimu Kata Follow up WEO and School Community Ufuatiliaji wa Afisa Elimu Kata na Jumuiya ya Shule Input from WEO and School Community
Mchango kutoka kwa Afisa Elimu Kata na Jumuiya ya Shule
Periodic Quality Assurance inspection of school
Uthibiti ubora wa mara kwa mara wa ukaguzi wa shule
Monthly review of progress against plan and amendments
Mapitio ya kila mwezi kuangalia maendeleo dhidi ya mpango na kufanya marekebisho
Implementation of plan Utekelezaji wa Mpango School Development Plan-based on self assessment and previous QA reports
Mpango wa Maendeleo ya Shule – Kutokana na tathmini ya ndani ya shule na ripoti za nyuma za Uthibiti Ubora
School self assessment Tathmini ya ndani ya shule Mchakato wa Nje wa Uthibiti Ubora Afisa Elimu Kata anatoa usimamizi wa nje wa mara kwa mara karibu mara mbili au zaidi kwa mwezi. Afisa Elimu Kata humsaidia mwalimu mkuu katika kufanya mapitio ya ndani, na anaweza kumsaidia kufanya maandalizi ya taarifa ya maandishi kwa ajili ya maandalizi ya ukaguzi. Afisa Elimu Kata pia anajukumu la kumsaidia Afisa Mthibiti Ubora wa Wilaya anayehusika na masuala ya Uthibiti Ubora wa shule kwenye kata yake.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
24
English Swahili Report to region/zone/national Taarifa kwenda mkoani/kanda/Taifa QA able to prioritise follow up on the most necessary cases
Mthibiti Ubora anaweza kuweka vipaumbele kufuatilia masuala ambayo ni ya muhimu zaidi
Annual/biannual Quality Assurance Visit to School and report
Ziara za kutembelea shule kwa mwaka/kila nusu mwaka za Uthibiti Ubora na kuandaa taarifa
Monthly WEO/QA (LGA) discussion of progress
Majadiliano ya maendeleo ya kila mwezi ya Afisa Elimu Kata/Mthibiti Ubora/ Afisa Elimu
Monthly WEO follow up at school level-support implementation of improvements
Ufuatiliaji wa kila mwezi wa Afisa Elimu Kata katika ngazi ya Shule-Kusaidia utekelezaji wa maboresho
Mfano wa mabadiliko ambayo yanatokea sasa Waratibu Elimu Kata wawili hadi watatu wamekuwa wakiungana na kushirikiana kutembelea shule zao na kukusanya taaarifa katika mambo muhimu yanayohusu uboreshaji wa shule. Wamekusanya matokeo ya ziara zao zote na kuyawasilisha kwenye mkutano wa Elimu wa wilaya(MEW), wakionesha maeneo mbalimbali yanayohitaji maboresho. Maeneo haya yaliunda mwongozo wa mada kwa ajili ya mikutano yao ya MEW ya miezi ijayo, kwa msaada maalum uliotolewa na Wathibiti Ubora.
Mambo yatakayoathiri majukumu na utendaji wa Mratibu Elimu Kata siku zijazo: Mfumo wa ukaguzi unabadilika na kuwa wa kimaendeleo zaidi
Shule zinatakiwa kukamilisha tathmini ya ndani ya maendeleo ya shule na hatua zinazochukuliwa kwa ajili ya maboresho ya shule.
Maafisa Elimu Kata wanatakiwa kumsaidia Mwalimu Mkuu kujitathmini na kuisaidia shule kujiandaa na ukaguzi.
Maafisa Elimu Kata na Wathibiti Ubora wanatakiwa kufanya kazi kwa ukaribu ili kujiridhisha na mchakato wa tathmini ya ndani na namna inavyoendana na ukaguzi.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
25
Kipindi cha 6 Msaada wa Ufuatiliaji na Mapitio ya mikutano ya MEW
Muda saa 1 na dakika 45 (dakika 105)
Malengo ya kipindi:
Kukuza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa kufuatilia na kuunga mkono MEW.
Kukuza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa kuchunguza na kufuatilia matokeo ya mikutano hii.
Ili kukubaliana juu ya mifumo ya kufanya hili.
Kufahamu umuhimu wa ripoti ya Maafisa Elimu Kata. Matokeo ya kujifunza: Hadi mwisho wa kipindi washiriki wataweza:
Kueleza jinsi ya kuunga mkono MEW
Kueleza mfumo wa kufuatilia mikutano
Kuhimiza maboresho ya ripoti ya Afisa Elimu Kata
Wawezeshaji waandae: Namba O, 5 na 10 kwa ajili ya zoezi la Machaguo ya lazima. Weka 0 na 10 mwisho wa
chumba na 5 katikati. Unataka watu wasikie maoni na maelezo ya wengine, hivyo ruhusu hii kwa umbali kati ya 0 hadi 10.
Orodha ya Machaguo ya lazima kwa ajili ya kazi ya 26
Hakikisha Maafisa wote wa Wilaya wanakuwa na ripoti zao 5 za Maafisa Elimu Kata.
Kadi 3 zilizoandaliwa hapo awali kwa ajili ya makundi 3 kwenye kazi ya 27
Nakala za Kiambatisho E-Mpango wa MEW na Kiambatisho H-Ziara za Maafisa Elimu Kata na Uandishi wa Ripoti.
Nakala of Annex J Majukumu na Taratibu za utoaji taarifa mkutano wa Elimu wa Mkoa na Wilaya
Mambo muhimu ya kusisitiza: Kwamba msaada utahitajika mwanzoni hasa kutoka EQUIP -T na kwa Afisa Elimu Wilaya Kwamba ripoti ya Afisa Elimu Kata ni muhimu. Rejea kwenye Kiambatisho E-Mpango wa MEW na Kiambatisho H-Ziara za Maafisa Elimu Kata na Uandishi wa Ripoti Washiriki wanajua nini cha kufanya baada ya mkutano kwa ajili ya kusaidia na kufuatilia MEW
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
26
26. Zoezi la Machaguo ya Lazima (dakika 15)
Sifuri upande mmoja hadi 10 upande mwingine, 5 iwe katikati. Eleza kwamba utasoma sentensi/kauli na wanapaswa wajiweka kwenye mstari kutoka 0 hadi 10 kulingana na jinsi wanavyokubaliana au hawakubaliana na sentensi/kauli hiyo. 10 ina maana ya kukubaliana kabisa 0 inamaanisha hawakubaliani kabisa Basi utaisoma sentensi/kauli ya kwanza na baada ya washiriki kuwa wamesimama kwenye nafasi zao waombe baadhi yao waeleze sababu yao ya kuchagua nafasi hiyo katika chumba. Wakati mwingine unaweza kuwauliza ikiwa wanataka kubadilisha msimamo wao kwa sasa baada ya kuwa wamesikia maelezo kutoka kwa wengine. Baada ya majadiliano mafupi, endelea na sentensi/kauli inayofuata. Sentensi/Kauli • Tanzania inatoa elimu bure • Elimu katika mkoa imeboreshwa kwa wanafunzi wengi zaidi • Nadhani MEW itakuwa muhimu • Nadhani MEW inapaswa kuwa ya lazima • Nadhani MEW inapaswa kufanyika kila mwezi, bila kujali chochote kinachoendelea • Nadhani MEW inapaswa kuingizwa inapofaa kufanya hivyo • Nadhani kuna manufaa yatokanayo na MEW kwa kila mtu • Nadhani Maafisa Elimu Kata watafaidika na MEW • Nadhani Wilaya inaweza kutoa fedha kugharamia vifaa vya MEW • Nadhani Wilaya inaweza kutoa fedha kwa ajili ya chakula wakati wa MEW
27. Msaada wa Ufuatiliaji na Mrejesho (dakika 25)
Utangulizi Mwezeshaji anaelezea haja ya kupata msaada kiasi fulani. Kutokana na uzoefu wetu huko Tabora, MEW, kama ilivyo katika programu nyingine nyingi, inahitaji msaada.
Mikutano bora ya MEW ni ile ambayo Afisa Elimu wa Wilaya anahuhudhuria baadhi au sehemu ya mikutano hiyo
Kutoa msaada kwa Kamati ya Mipango
Kuhamasisha mikutano ifanyike
Kusaidia na kushirikisha taarifa
Kuchukua malalamiko kama vile mabadiliko ya mjumbe muhimu wa Kamati ya Mipango ya MEW
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
27
Mwezeshaji ataelezea haja ya kupata Mrejesho kutoka MEW
Kuna haja ya kushirikishana maswala mbalimbali na maamuzi yaliyotolewa katika Mkutano wa MEW
Kuna haja ya kujua ya mafanikio na changamoto za MEW
Kuna haja kwa wengine kuelewa na kuchangia kikamilifu kwenye MEW.
Kazi ya Kikundi Wagawe washiriki katika vikundi 3. Hakikisha makundi yana idadi sawa ya washiriki, lakini
Kikundi cha 1 ni cha wafanyakazi wote wa Mkoa na Kanda pamoja na washiriki wengine
Kikundi cha 2 ni Afisa Elimu Wilaya na ADQA na washiriki wengine
Kikundi cha 3 ni wafanyakazi wote wa EQUIP-T na washiriki wengine Hakikisha kila kikundi kina karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha. Wakumbushe kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye ataandika maelezo na kutoa mrejesho wakati wa majumuisho. Kila kikundi kina orodha yake ya maswali kulingana na uhusika wao.
Kundi la 1 Wote ni wafanyakazi wa Kanda na Mkoa pamoja na washiriki wengine.
Ni taarifa gani Afisa Elimu wa Mkoa na Wafanyakazi wa kanda wanahitaji kutoka MEW?
Ni mabadiliko gani Afisa Elimu wa Mkoa na Wafanyakazi wa kanda wanatarajia kutokana
na mikutano hii?
Watajuaje kuhusu maendeleo na majadiliano ya Maafisa Elimu Kata?
Watajuaje kuhusu mafanikio na changamoto?
Wanaisaidiaje Halmashauri kuwajibika kwenye mikutano na mrejesho wa taarifa ya
Maafisa Elimu Kata?
Ni msaada gani Wathibiti Ubora na Halmashauri wanahitaji kutoka kwa Maafisa wa mkoa
na kanda ili kuendeleza mikutano hii?
Ni msaada gani unaweza kutolewa ili kufanikisha mikutano hii?
Kundi la 2 Linajumuisha Maafisa Elimu, na Wadhibiti Ubora wa Wilaya pamoja na washiriki wengine.
Ni taarifa zipi Afisa Elimu Wilaya na Mthibiti Ubora wanahitaji kutoka kwenye mikutano
hii?
Ni mabadiliko gani Afisa Elimu Wilaya na Mthibiti Ubora wanatarajia kutokana na
mikutano hii?
Watajuaje kuhusu maendeleo na majadiliano ya Elimu Kata?
Watajuaje kuhusu mafanikio na changamoto?
Wanasaidiaje kuhakikisha kuna ushiriki mzuri kwenye mikutano na kutoa mrejesho wa
taarifa za Maafisa Elimu Kata?
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
28
Ni msaada gani Wafanyakazi wa Mkoa na Kanda wanahitaji kutoka kwa Wathibiti Ubora
na Halmashauri ili kuendeleza mikutano hii?
Ni msaada gani unaweza kutolewa ili kufanikisha mikutano hii?
Kundi la 3 Linajumuisha wafanyakazi wa EQUIP-T na washiriki wengine
Ni taarifa zipi EQUIP-T inazihitaji kutoka kwenye mikutano hii?
Ni mabadiliko gani wafanyakazi wa EQUIP-T wanatarajia kutokana na mikutano hii?
Watajuaje kuhusu maendeleo na majadiliano ya Maafisa Elimu Kata?
Watajuaje kuhusu mafanikio na changamoto?
Wanaisaidiaje kupata mrejesho wa ripoti za mikutano ya MEW na ya Maafisa Elimu Kata?
Ni msaada gani unaweza kutolewa ili kuendeleza mikutano hii?
28. Majumuisho (dakika 30) Vikundi vitatu vinatoa mrejesho kimoja kimoja na kufafanua pointi zilizopatikana. Mwendeshaji anapaswa kuuliza mwishoni:
Je, kuna uwiano kati ya vikundi hivi 3 kwa taarifa na mrejesho?
Ikiwa jibu ni hapana, je, tofauti zilizopo zinaweza kutatuliwa?
Je, kuna masuala mengine zaidi ya kuzingatiwa?
Fafanua ili kwamba washiriki wote wajue nini cha kufanya baada ya mkutano kwa ajili kusaidia na kufuatilia MEW.
Afisa Elimu Mkoa, Kanda, Afisa Mthibiti Ubora na Afisa Elimu wa Wilaya wanatakiwa
kuonesha dhamira na utayari wao kwenye MEW:
Kuwaonesha Maafisa Elimu Kata na Wawezeshaji kwamba MEW inathaminiwa
Kuwapa msaada Kamati ya Mipango
Kuhamasisha mikutano ifanyike
Kuunga mkono na kushirikishana taarifa mbalimbali
Kuchukua na kuyafanyia kazi mambo yaliyoibuliwa kwenye mkutano
Kusaidia mabadiliko ya kubadili mjumbe muhimu wa Kamati ya Mipango ya MEW
Kuweka wazi mambo mbalimbali na maamuzi yaliyofanyika wakati wa MEW kwa maendeleo ya Wilaya
Kujua mafanikio na changamo za MEW
Kushiriki mara kwa mara na kutoa mchango stahiki kwenye MEW
Kwa kusoma taarifa ya Afisa Elimu Kata, kuielewa na kutoa msaada kwa Maafisa Elimu Kata na Kata zao
Kusoma yatokanayo na MEW Kutoa mrejesho na taarifa muhimu
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
29
29. Ripoti za Afisa Elimu Kata (dakika 20) Mwezeshaji awaombe washiriki waketi katika vikundi vya Kiwilaya.
"Mtakuwa katika makundi haya kwa siku nzima ya leo, hivyo jipangeni ili mkae vizuri."
Utangulizi
Mwezeshaji anafafanua kuwa, Ripoti ya Afisa Elimu Kata ni muhimu sana kwa sababu inatoa
mrejesho kuhusu shule.
Kila wilaya imeleta ripoti 5 za mfano ambazo tutakwenda kuzipitia na mwishoni tutachukua
ripoti iliyo bora zaidi.
30. Kushirikishana Ripoti bora zaidi ya Afisa Elimu Kata (dakika 15)
Kwa ufupi kila kikundi kinashirikisha ripoti bora zaidi waliyoichagua na kuelezea kwa nini wameichagua. Mwezeshaji anaweka pamoja mawazo ya jumla.
Taarifa nzuri itaeleza yafuatayo Ni sababu zipi zimekufanya kutembelea hilo eneo Ni maamuzi gani mmeyafanya kutokana na mabadiliko Katika ufuatiliaji wenu ni vitu gani vinahitajika ili kuweza kuboreshaji
Onyesha kwamba wanaweza kutumia Kiambatisho E - Mpango wa MEW kwa ajili ya Kuboresha
Ziara za kutembelea Shule za Afisa Elimu Kata na Taarifa za Maandishi kwa msaada wa
Kiambatisho H.
Washukuru maafisa kwa kuleta ripoti za Maafisa Elimu Kata kwa ajili ya kipindi hiki.
Maafisa Elimu Kata wanapaswa kupata mrejesho mwezi kuhusu ubora a wa ripoti zao na juu ya ufuatiliaji wa maendeleo ya maboresho ya shule yaliyofikiwa tangu ripoti ya itolewe.
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
30
Kipindi cha 7 Uandaaji wa Mkutano wa Elimu wa Wilaya Muda: saa 1 na dakika 45 (dakika 105) Lengo la kipindi: Kutoa fursa kwa washiriki ya kujizoeza kuandaa mpango na kuandaa MEW. Matokeo ya kujifunza: Hadi mwisho wa kipindi washiriki watakuwa na uwezo wa: • Kuthamini kamba wanafanya kazi kama timu ya kuandaa na kupanga mpango wa MEW • Kutengeneza mpango wao wenyewe Wawezeshaji wameandaa: • Karatasi za bango kitita zenye orodha ya mada kutoka Siku ya kwanza • Kiolezo cha Mpango wa MEW (Kiambatisho C) • Idadi ya kutosha ya karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu
____________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi 31. Utangulizi (dakika 15) Anza na wimbo au changamsha mwili Mwezeshaji anafafanua kwamba watakwenda kubungua bongo kwa kuhusu ajenda za Mkutano wa Maandalizi ya MEW. Kamati ya Mipango Kamati ya mipango inakutana kupanga mikutano ya MEW
Afisa Mwakilishi wa MEW-ndiyo Mwenyekiti. Wajumbe ni: Afisa Elimu Wilaya, Afisa Elimu Watu wazima / Afisa Elimu Takwimu wanaohusika na EQUIP-T au Maafisa wengine. Wawakilishi wawili wa Wathibiti Ubora Maafisa Elimu Kata 2
Agenda
Kuamua na kupitisha mada
Kufuatilia jambo lolote muhimu lililojitokeza katika mkutano uliopita
Kuhakikisha uwezeshaji wa mada utakaohusisha njia shirikishi unaandaliwa
Kukubaliana nani atakuwa Mwezeshaji kwa kila sehemu ya mkutano
Kupanga vifaa vitakavyotumika
Kupanga na kuandaa ukumbi
Kuandaa mpangilio wa ukaaji
Kupanga kuhusu chai/chakula cha mchana kama bajeti inaruhusu
Kuweka wazi majukumu ya kila mhusika kwa ajili ya MEW ijao
Kuchagua mtu atakayeandika yatokanayo na mkutano na kuwasambazia wengine
Kuchagua mtu atakaye wataarifu Maafisa Elimu Kata, Wathibiti Ubora, na Maafisa wengine kuhusu tarehe na muda wa mkutano
nye karatasi nyingine tofauti bungua bongo kuhusu mbinu za uwezeshaji: Tafakuri
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
31
Bungua bongo
Igizo dhima
Fikiri, jozisha, shirikisha
Mijadala ya vikundi na mrejesho
Maswali na Majibu
Mambo muhimu Kupanga tarehe na muda wa mkutano. Ikiwezekana pangeni haya mwanzoni mwa kila mwaka. Kwa mfano, Ijumaa ya kwanza ya mwezi Kuwepo ukumbini kuwakaribisha wengine wanapofika
32. Maandalizi na Kupanga Mipango ya MEW (dakika 40)
Washiriki watafanya kazi katika vikundi vya Wilaya. Waombe washiriki kuchagua watu watakaoshika nafasi hizi:
• Afisa Mwakilishi wa MEW ambaye atakuwa Mwenyekiti • Afisa Elimu Taaluma / Afisa Elimu Vifaa na Takwimu anayehusika na EQUIP-T • Wathibiti Ubora • Maafisa Elimu Kata 2
Eleza kuwa sasa wana Mkutano wa Mipango na Maandalizi ya MEW.
Kwa hiyo watapanga MEW wa mwezi ujao.
Watahitaji kuchagua mada kutoka kwenye orodha ya mada zilizochaguliwa jana.
Wanahitaji kuhakikisha kwamba wanatumia mbinu shirikishi za uwezeshaji
Watahitaji kuhakikisha wamekamilisha vipengele vyote vilivyoorodheshwa kwenye ajenda
Kiolezo cha MEW Kiambatisho B kinaweza kuwa cha msaada
33. Majumuisho ya majadiliano (dakika 40) Waombe washiriki kushirikishana mipango yao, hasa maelezo ya kina ya uwezeshaji wa mada, kundi moja baada ya jingine. 34.Maswali na majibu, kuhitimisha (dakika 10) Waulize washiriki wana maswali gani au wasiwasi wao kuhusu kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa .
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
32
Kipindi cha 8 Nini kitafuata baada ya mafunzo?
Muda: Saa 1 na dakika 45 (dakika 105) Malengo ya kipindi.
Kutoa fursa kwa washiriki kufikiri, kushirikishana na kutoa mawazo yao juu ya jinsi ya kuanzisha mikutano ya MEW kwenye Wilaya zao.
Kukubaliana mpangokazi kwa ajili ya kuanzisha MEW watakaporudi kwenye Wilaya zao. Matokeo ya kujifunza: Hadi mwishoni mwa kipindi washiriki watakuwa na mpango unaoonyesha nini cha kufanya baada ya mafunzo na ambao unaweza kuwasaidia kupata msaada inapobidi.
Wawezeshaji waandae: • Fomu ya tathmini, fomu moja kwa kila mshiriki • Idadi ya kutosha ya karatasi za bango kitita, kalamu rashasha, gundi utepe, karatasi za A4, na kalamu ______________________________________________________________________________ Maelezo ya Kipindi 35. Muhtasari wa Majumuisho ya MEW; kazi ya kikundi (dakika 25) Waombe washiriki kujadili katika vikundi yale waliyojifunza kuhusu "lini", "kwa muda gani", "madhumuni ya MEW", "jukumu la timu", "taratibu za MEW", "umuhimu wa Mada na uwezeshaji wake "na" jukumu la mwakilishi wa MEW" kuhusiana na MEW. 36. Maswali na Majibu, Kufunga (dakika 15) Washiriki wana nafasi ya kuuliza maswali mengine zaidi 37. Kupanga "nini cha kufanya baada ya mafunzo" Kimabatisho I (dakika 45) Waambie washiriki kwamba wataanza kuandaa MEW baada ya kurudi katika Wilaya zao. Wataanza pia kufuatilia kuhusu MEW. Wakiwa katika vikundi vya Wilaya wajadili: • Tunakwenda kufanya nini sasa, baada ya mafunzo haya? • Je, ni ujuzi gani na zana zipi tutakazotumia? • Tukiwa na shida yoyote katika kuandaa au kuwezesha MEW, ni nani tunaweza kumuomba msaada? • Tutaanza lini MEW katika Wilaya yetu? • Tukiwa na matatizo katika kufuatilia MEW, ni nani tunaweza kumuomba msaada?
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
33
Baada ya
mafunzo haya
nini tunapaswa
kufanya?
Tutafanya nini
na wakati gani?
Tutajiandaaje na
kuendeshaje
MEW? Zana zipi
tutatumia?
Tunatakiwa
kufanya nini
baada ya MEW,
kusaidia na
kufuatilia?
Nani
atatusaidia?
Wataarifu
Maafisa Elimu
Kata kuhusu
MEW
Mkubaliane
tarehe na muda
38. Muhtasari wa mada za siku 2 (dakika 15) Jumuisha kwa ufupi siku 2 za mafunzo, sisitiza kuwa mikutano ya MEW ni zana za usimamizi wa Wilaya za kuboresha shule. Waulize washiriki wanajisikiaje kwa sasa ikilinganishwa na siku ya kwanza? Hitimisha kwa kupokea maswali yoyote ambayo washiriki wanaweza kuwa nayo. Waulize kama kuna maswali yoyote, ufafanuzi, malalamiko, au changamoto nyingine ambazo wangependa kuuliza au kushirikishana. Washukuru washiriki wote kwa michango yao na kuwatakia kila la heri katika kuanzisha na kuwezesha mikutano ya MEW na ufuatiliaji, na mawasiliano yenye ufanisi. Usisahau kuwapa washiriki fomu ya tathmini ili wajaze 39. Maneno ya kuhitimisha na kuagana (dakika 10)
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
34
VIAMBATISHO
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
35
KIAMBATISHO A Majukumu ya Kamati ya Maandalizi na Wajibu wa Mwakilishi wa MEW Mwakilishi wa MEW anawajibu kwa kuhakikisha kuwa mikutano ya MEW inafanyika na vigezo vyote vya mkutano vinatekelezwa. Hata hivyo, jukumu hili wamepewa Wathibiti Ubora, Maafisa Elimu na Maafisa Elimu Kata wanaohudhuria Kamati ya mipango. Hili ni jukumu la pamoja. Mwakilishi wa MEW Ataitisha mkutano wa Kamati na kuuongoza mkutano wa maandalizi kama mwenyekiti kila mkutano wa mwezi wa MEW. Mkutano wa maandalizi au MEW usifanyike bila uwepo wa watajwa hapo juu isipokuwa kwasababu maalumu. Atamwalika Afisa Elimu Wilaya kuhudhuria MEW angalau mara 4 kwa mwaka. Atatoa taarifa muhimu zote kuhusu mikutano ya MEW kila inapotakiwa kufanya hivyo kwa wafanyakazi wote, Maafisa Elimu, Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu Kata. Atawakaribisha na kuwashirikisha wafanyakazi wapya kwenye mikutano. Kwa pamoja Kamati itafanya yafuatayo Itaandaa agenda kwa ajili ya MEW ujao
Itafanya mapitio ya Mafanikio ya MEW iliyopita na kushirikishana mambo yaliyofanikiwa vizuri
Itathibitisha kwa pamoja hatua zilizochukuliwa kuboresha Itaangalia mambo gani yanapaswa kufuatiliwa kutokana na mkutano uliopita Itafafanua Mada za Mkutano Itapanga Uwezeshaji wa mada kwa kutumia mbinu shirikishi Itakubaliana kuhusu wawezeshaji wa vipengele vya mkutano Itaandaa upatikanaji wa zana mbalimbali Itapanga tarehe na muda wa mkutano Itapanga na kuandaa ukumbi Itapanga jinsi ya kukaa katika makundi au duara ukutani wakitazamana Itakuwepo ukumbini mapema ili kuwakaribisha Waratibu Elimu Kata wanapofika
Itaandaa utaratibu wa kupata chai / chakula cha mchana kama inavyotakiwa kulingana na bajeti
Itaweka wazi majukumu ya nani atafanya nini wakati wa MEW ujao Mwakilishi wa MEW atakuwa na jukumu la kupokea na kushughulikia jambo lolote litakalojitokeza baada ya mkutano. Wanakamati wanapaswa kumtaarifu mwawakilishi jambo lolote ambalo linaweza kuathiri mkutano ujao Mwishoni mwa mwaka kamati itafanya yafuatayo Itafanya tathimini ya mwaka ya mada zilizofanyiwa kazi Itabainisha mafanikio na changamoto zilizojitokeza Itaandaa mwongozo wa mada kwa ajili ya mwaka ujao
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
36
KIAMBATISHO B
MKUTANO WA MAAFISA ELIMU, WATHIBITI UBORA NA WARATIBU ELIMU KATA
MWONGOZO WA RATIBA ULIOPENDEKEZWA
Vifaa: Matumizi ya bango kitita na kalamu rashasha
MUDA SHUGHULI MWEZESHAJI
2.30 Kuwasili na kujisajili
3.00 Kufungua Mkutano na kuelezea malengo ya mkutano Afisa Elimu (W)
3.30
Kuelezea/Kuwezesha mada inayohusu mkutano husika
Mthibiti Ubora
5.00 Chai
5.30
Kujadili utekelezaji wa shughuli fulani kutokana na maazimio ya
mkutano au mikutano iliyopita
Afisa Elimu /
Mthibiti Ubora
6.30 Mrejesho kutoka kwa Maafisa Elimu na Wathibiti Ubora kuhusu
taarifa mbalimbali za Waratibu Elimu Kata
Maafisa Elimu na
Wathibiti Ubora
7. 30
Maandalizi kwa ajili ya mkutano ujao
Maafisa Elimu na
Wathibiti Ubora
7.45 Matangazo mbalimbali
Afisa Elimu (W)
8.00 Kuagana
Afisa Elimu (W)
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
37
KIAMBATISHO C MKUTANO WA KWANZA WA MWEZI WA MAAFISA ELIMU, WARATIBU ELIMU KATA NA WATHIBITI UBORA-MANUFAA YA MKUTANO KATI YA AFISA ELIMU, WARATIBU ELIMU KATA NA WATHIBITI UBORA
Vifaa: Karatasi kubwa ya bango kitita na kalamu rashasha
MUDA SHUGHULI MWEZESHAJI
2.30 - Kuwasili na kujisajili
3.00
Kipindi cha Ufunguzi: Maneno ya ufunguzi ya Afisa Elimu na Utangulizi
Kuwasilisha malengo
Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni mkutano mpya
unaowakutanisha Maafisa Elimu wa wilaya, Wathibiti Ubora, na
Waratibu Elimu Kata.
Hauhusiki na masuala ya fedha, Pikipiki au posho
Mkutano huu unahusu uboreshaji wa Elimu kwa wanafunzi
madarasani katika Wilaya zetu na kwenye jamii
Malengo ya Mkutano huu ni kuangalia faida kwa kila mshiriki wa
mkutano
AFISA ELIMU
WILAYA
4.00
Kipingi cha 1: Wagawanye washiriki katika makundi 3
Kundi la 1, Watasimama kama Waratibu Elimu Kata
Kundi la 2. Watasimama kama Wathibiti Ubora
Kundi la 3. Watakuwa Maafisa Elimu
Wapatie kila kundi Karatasi ya bango kitita na Kalamu
rashasha. Waambie kila kundi wajadili yafuatayo
Wanachangiaje katika kuboresha shule?
Wanaonaje umuhimu wa mkutano huu kwenye kazi zao
kama Halmashauri, Wathibiti Ubora, na Waratibu Elimu
Kata?
Andika mawazo yao kwenye karatasi ya bango kitita. Kundi
litakalokuwa la kwanza kumaliza litasema kwa sauti "BINGO". Kundi
hilo waambie wabandike bango kitita lao ukutani. Fanya hivyo hadi
makundi yote 3 yamalize. Zipi ni hoja muhimu?
Mjadala wa wote
Hoja muhimu ni zipi?
Ni zipi kati ya kazi zao zinasaidia zaidi katika kuboresha shule?
ADQA
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
38
Ni kwenye kazi gani hasa mnatumia muda wenu mwingi?
Kazi na jukumu gani vinawasaidia kutekeleza uboreshaji wa shule?
Mambo ya msingi ya kusisitiza
Kwa kupitia Jamii inayojifunza Wilaya ihakikishe kwamba;
Ufundishaji na Ujifunzaji unaboreshwa
Viwango vya wanafunzi vinaboreshwa
Shule zinawajibika
Changamoto za fedha zinajadiliwa kama vile ruzuku za IGA
Jamii zinawajibika na kushiriki kwenye masuala yanayohusu shule zao
Taarifa zinapokelewa na kusambazwa kwa kupitia ripoti
Hili ni jukumu la pamoja
Ili kufanya kazi pamoja lazima pawepo muda maalumu uliotengwa,
unaitwa mkutano wa MEW ili:
Kushughulikia masuala yanayohusu ufundishaji na ujifunzaji yanapotokea
Kushirikishana na kuimarisha uboreshaji wa elimu katika wilaya
Kuwezesha mawasiliano yawe imara zaidi
5.00 Chai
5.30
Kipindi cha 2 : Katika vikundi 6 vyenye watu saba saba
Faida za MEW ni nini? Dakika 20
Hakikisha kila kikundi kina bango kitita na kalamu rashasha.
Wakumbushe wanakikundi wachague mtu mmoja kati yao
atakayekuwa anaandika wanayoyajadili na atatoa mrejesho wakati wa
majumuisho.
Kuna manufaa gani kwa Wathibiti Ubora, Waratibu Elimu Kata, na Maafisa Elimu kukutana kila mwezi kujadili namna ya kuboresha elimu katika wilaya?
Kuna kipi cha tofauti kuhusu MEW?
Mrejesho wa wote Dakika 40
Omba kila kundi liwasilishe majibu ya vipengele walivyojadili (yasizidi
majibu 2 kwa kila kipengele). Kisha rudia kwa mzunguko uleule mpaka
Afisa Vifaa na
takwimu/Afisa
Taaluma
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
39
majibu ya vipengele vyote yakamilike. Waombe washiriki wasirudie
majibu ambayo yamekwishatolewa na kikundi kingine.
Mambo ya kusisitiza
Uelewa wa pamoja wa michango ya kila mshiriki na kushirikishana mawazo mbalimbali
Makubaliano ya hatua za kuchukua kwa ajili ya kuboresha shule Wilayani
Kuthamini na kuwajengea uwezo washiriki wote kwenye mkutano, hasa Waratibu Elimu Kata
Mafanikio ya pamoja na mawazo mapya
Umuhimu wa mahusiano ya MEW na ‘Jamii nyingine zinazojifunzaji’
Umuhimu wa kushirikishana taarifa za mikutano ya “Jamii inayojifunza”
Uboreshaji wa utendaji wa shule ni jukumu la pamoja!
Mkutamno wa MEW Una tofauti gani na program nyingine?
Mikutano ya Afisa Elimu wa Wilaya na Waratibu Elimu Kata inalenga mambo mengi ikiwa ni pamoja na yafuatayo:
Kazi za kiutawala kwa kuzingatia muongozo wa wizara
Kuwataarifu wafanyakazi kuhusiana na nyaraka na maelekezo ya wizara
Kujadili kuhusu ufaulu wa wanafunzi
6.30
Majumuisho kwa ufupi
Kwa ufupi elezea juu ya mkutano wa MEW:
Kujenga uelewana wa pamoja na mbinu za kuinua viwango na ubora wa elimu katika Wilaya
o Ili Wathibiti Ubora waweze kushirikisha utaalamu wao na
Waratibu Elimu Kata waweze kutoa taarifa juu ya shule
zao katika wilaya
o Ili Halmashauri iweze kupokea taarifa za kuiwezesha
kuandaa mipango yao kwa ajili ya kusaidia, kufundisha na
kuhamasisha na pia kuweka kipaumbele cha mipango
yake kwa ajili ya kuboresha na kugharamia elimu
o Ili kusaidia upatikanaji wa taarifa kati ya Wathibiti Ubora
, Maafisa Elimu wa Wilaya, na Waratibu Elimu Kata
kuhusu shughuli zao za mwezi uliopita na kazi za mwezi
unaofuata
ADQA
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
40
Kufanya mapitio ya miradi ya wilaya na kupata mrejesho
Kuangalia masuala muhimu kwa ajili ya kuinua ubora wa elimu
katika wilaya; kupanga shughuli za mafunzo na kusaidia
maendeleo ya shule kwa ujumla
Kutoa fursa kwa Waratibu Elimu Kata,Wathibiti Ubora na
Maafisa Elimu kuwa na Mkutano “Jamii Inayojifunzaji” wa kila
mwezi, ili kupata mawazo mapya na kutafuta njia za kutatua
changamoto za uboreshaji wa maendeleo ya shule
7. 00
Maandalizi ya Mkutano ujao
Kamati ya mipango: Afisa Elimu Wilaya, 2 Afisa Elimu , 2 Maafisa Elimu
Kata wa 2, na Wathibiti Ubora wa
Wafanyakazi wa EQUIP-T
Watakutana kupeana taarifa na tarehe
Chagua Maafisa Elimu Kata 2 watakaoungana na Kamati ya mipango
7.20 KUPANGA MADA ZA MKUTANO UJAO
Mpango wa Maendeleo ya Shule ni moja ya nyaraka muhimu sana za
shule
Maafisa Elimu Kata waje na nakala za Mipango ya Maendeleo ya Shule
kutoka katika Kata zao
Watafanya mapitio ya Mwongozo wa Mafunzo ya Mpango wa
Maendeleo ya Shule hasa zana za uchambuzi. SWOC, Mti wa matatizo,
Kuhusisha Wadau na uwekaji vipaumbele.
7.30 Matangazo kuhusu matukio ya kazi nyingine
Maoni na kuhitimisha
8.00 Kuagana
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
41
KIAMBATISHO D MKUTANO WA PILI WA MAAFISA ELIMU WILAYA, WARATIBU ELIMU KATA NA WATHIBITI
UBORA -KUCHAMBUA NA KUBORESHA MPANGO WA MAENDELEO YA SHULE
Vifaa: Karatasi ya bango kitita na kalamu rashasha
Maafisa Elimu Kata waliombwa kuja na nakala za Mpango wa Maendeleo ya shule
MUDA SHUGHULI MWEZESHAJI
2.30 Kuwasili na Kujisajili Wote
3.00 Kufungua kipindi cha 1
Maneno ya ukaribisho na utangulizi toka kwa Afisa Elimu Wilaya
Kujikumbusha malengo ya Mkutano
Malengo ya Mkutano wetu wa leo
1 Kushirikishana mambo yanayofanya ziara ya kutembelea shule
iwe yenye mafanikio
2 Kushirikishana changamoto zinazoweza kufanya ziara ya
kutembelea shule isifanikiwe
3 Kutaja mada tunazoweza kuzijadili kwenye mkutano yetu
4 Kufanya mapitio juu ya mafaniko ya Mpango wa Maendeleo ya
Shule
5 Kufanya mapitio ya taarifa za Waratibu Elimu Kata
Afisa Elimu
Wilaya
3.15
Kipindi cha 2
Unda makundi 6 mchanganyiko, angalau awepo Mthibiti Ubora 1,
na Afisa Elimu 1 katika kila kikundi
Dakika 5 katika jozi
Sisi sote huwa tunatembelea shule. Tushirikishane mifano ya ziara
zenye mafanikio ambazo unajua mchango wako umechangia katika
kuboresha shule uliyotembelea.
Je, ulifanya nini kuongeza ubora?
Kipindi cha 2 kinaendelea
Dakika 20 za kushirikishana katika vikundi
Je, kuna mafanikio yanayojirudia?
Je, una uhakika ni juhudi zako zilizoleta mafanikio hayo?
Tumia bango kitita na kalamu rashasha
Dakika 20 Kufanya majumuisho ya pamoja ya mkutano
ADQA
4.00
Kipindi cha 3: katika vikundi vilevile
Dakika 30
Mambo gani yanakwamisha jitihada za kuboresha ziara zako
shuleni?
DAO/DSLO
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
42
Unafanya nini kutatua changamoto hizo?
Mambo gani yanakuwepo shuleni yanayosaidia ziara ifanikiwe?
Tumia bango kitita na kalamu rashasha
Dakika 20 za majumuisho ya awali ya mkutano
5.10 Chai WOTE
5.45
Kipindi cha 4: Kufanya mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Shule
Vikundi vyenye watu 6, Wathibiti Ubora na Waratibu Elimu Kata
waungane na Maafisa Elimu katika vikundi
Katika mkutano uliopita Waratibu Elimu Kata waliombwa waleta
nakala za Mpango wa Maendeleo ya shule kutoka katani kwao, na
kila mmoja aliambiwa kufanya mapitio ya Mwongozo wa Mafunzo
ya Mpango wa Maendeleo ya Shule.
Kazi ya vikundi Dakika 40
Pitia Mpango wa Maendeleo ya Shule kwa kuzingatia yafuatayo
Je, malengo yote matano yapo?
Rasilimali za shule na fedha
Ufundishaji na Ujifunzaji
Mazingira Chanya yanayozingatia jinsia
Maboresho ya shule
Ushiriki wa jamii
Je, kila lengo angalau limeonekana kuwa na shabaha 2 zenye
uhalisia?
Je, kila lengo limepata angalau mambo 3 ya kufanyia kazi?
Je, malengo, shabaha, na kazi zake vinaendana?
Je, muda wa utekelezaji una uhalisia?
Je, imewekwa bayana ni nani atawajibika kwa kila kazi?
Je, kuna ushahidi unaothibitisha kwamba zana za uchambuzi
zilitumika?
SWOC, Mti wa matatizo, Kuhusisha Wadau na uwekaji vipaumbele.
Je, kuna ushahidi kwamba wadau wote walishirikishwa?
Chagua Mpango wa Maendeleo ya Shule ulio bora zaidi
Dakika 30: Mjadala wa wote
ADQA
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
43
7.00 -
7.45
Kipindi cha 5. Mada za Mkutano Ujao
Mkutano ujao utahusisha kushirikishana ripoti za utekelezaji wa
Mratibu Elimu Kata.
Waratibu Elimu Kata watatakiwa waje na nakala za mifano ya ripoti
kwenye mkutano ujao
Wazingatie mambo yanayofanya ripoti iwe nzuri
DAO/DSLO
7.45 -
8.00
Taarifa kuhusu matukio ya kazi nyingine
Mkutano mwingine wa mipango utafanyika.......
Mkutano kamili ujao utafanyika........
Maoni na kuhitimisha
Mambo mengine ya kufanya
Kikao cha maandalizi kitakuwa ………………..
Kikao kitakuwa ……..
Mengineyo
Afisa Elimu
Wilaya
8.00 Kuagana WOTE
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
44
KIAMBATISHO E
MKUTANO WA TATU WA KILA MWEZI WA MAAFISA WA WILAYA, WARATIBU ELIMU KATA, NA
WATHIBITI UBORA – NINI KINAFANYA TAARIFA YA AFISA ELIMU KATA IWE BORA?
Zana
Bango kitita na Kalamu rashasha
Waratibu Elimu Kata waliombwa kuleta nakala za Ripoti zao kwa Afisa Elimu Wilaya
Nakala moja kwa kila mshiriki ya Kiambatisho H “NINI HUFANYA RIPOTI YA MRATIBU ELIMU
KATA IWE BORA” KIAMBATISHO H
MUDA SHUGHULI MWEZESHAJI
2.30 - Kuwasili na kujisajili Wote
3.00
1 Kufungua kipindi – Maneno ya ukaribisho na Utambulisho
Lengo la Mkutano -
2 Kuangalia na kujadili mambo yanayofanya uandishi mzuri wa
ripoti
Afisa Elimu
3.30
Tumia
bango kitita
na kalamu
rashasha
Kipindi cha 1. Kupitia matarajio ya ripoti za Maafisa Elimu Kata
Dakika 30
Mpatie kila mtu na upitie kusoma Kiambatisho H “NINI
KINAFANYA RIPOTI YA MRATIBU ELIMU KATA IWE BORA”
1. Kuna maelezo na ripoti zilizoandaliwa kwa kila ziara ya
kutembelea shule
1. 2. Mratibu Elimu Kata huandika kwenye Kitabu Cha Wageni (log book)kila anapotembelea shule
2. 3. Kuna ripoti ya kila mwezi ya Mratibu Elimu Kata kwa Afisa Elimu wa Wilaya imbayo;
Inabainisha masuala kadha wa kadha ya shule husika Inalinganisha masuala ya shule Inalenga maeneo muhimu yanayohitaji msaada
4 Halmashauri hupokea ripoti hizo na kufuatilia ubora wa taarifa
za Mratibu Elimu Kata
Huhakikisha mambo muhimu yanayoibuliwa katika ripoti
yanajadiliwa
Hufanya uchambuzi na kuchukua hatua dhidi ya utendaji wa
shule
Hatua zilizoafikiwa hutekelezwa kwa kutengewa muda
maalum
Dakika 30
ADQA Kwa
kutumia
maelezo ya
Kiambatisho
H
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
45
Majadiliano ya wazi na maswali
4.30 Chai
5.00
Kipindi cha 2- Katika vikundi mchanganyiko
Kila igizo dhima la kikundi ni mahojiano kati ya Mratibu Elimu Kata
na mwalimu mkuu, fanya igizo dhima moja moja. Baada ya kila
igizo dhima waulize washiriki wamegundua nini na mjadiliane kwa
pamoja ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizoibuliwa. Ni
mahojiano gani mazuri unapokutana na mwalimu mkuu?
Igizo dhima 1
1 Mwalimu mkuu hasikilizi na amevurugwa. Mwalimu mkuu anaongea na simu, na kushughulika na kazi za kuandika kwenye makaratasi, mtoto yuko mlangoni. Je, MEK atalishughulikiaje hili?
Igizo dhima 2
2 MEK anatoa taarifa ambazo ni siri juu ya shule nyingine na Mwalimu mkuu? Igizo dhima 3
3 MEK anazungumza muda wote na Mwalimu Mkuu mwenye wasiwasi hana nafasi ya kuzungumza kuhusu matokeo ya hivi karibuni ya mitihani ya shule ambayo yanaonesha shule imeboresha sana.
Igizo dhima 4
4 Mahojiano hayana malengo ya wazi kuhusu shule. Yamejikita kuongelea kuhusu Magufuli na matatizo yao binafsi.
Igizo dhima 5
5 MEK anazungumza na Mwalimu mkuu kuhusu mafunzo ya walimu ngazi ya shule(INSET). Hajui majibu lakini anajaribu, hata hivyo majibu yake hayaeleweki kabisa kama alivyoelekezwa kwenye kozi aliyohudhuria. MEK atafanya nini?
Igizodhima 6
6 MEK anataka taarifa kuhusu UWW ya shule na wadau. Mwalimu mkuu anatoa ushirikiano mdogo kwao. Je, MEK anawezaje kumshauri na kumsaidia Mwalimu mkuu kujenga mahusiano m azuri na wadau?
Mjadala wa wote – Je, mkutano mzuri una sifa zipi?
DAO/DSLO
6.00
Kipindi cha 3. Kushirikishana RIPOTI ZA MRATIBU ELIMU KATA
katika vikundi.
Dakika 30
ADQA
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
46
Kushirikishana katika vikundi ripoti ya Mratibu Elimu Kata na
kuichunguza kwa kuangalia vigezo vifuatavyo.
Tumia bango kitita na Kalamu rashasha kuandika jambo lolote
linaloibuliwa kwenye majadaliano
Je, sentensi zinaeleweka bayana?
Je, unajua mambo ambayo Mratibu alifuatilia tangu mkutano wa
mwisho, wiki 2 kabla?
Je, unajua mambo gani muhimu yaliyopo shuleni?
Je, unajua Mratibu alisema alifanya nini wakati wa ziara yake?
Je, unajua majukumu waliyokubaliana kufanya ili kuboresha
shule?
Dakika 30
Majumuisho
7. 00
Maandalizi ya Mkutano ujao wa 4
Kwenye mkutano ujao tunatarajia kuangalia kazi za Afisa Elimu
Kata na Jamii /UWW na Kamati ya shule.
1. Zingatia hali ya wadau katika shule yako
2. Tafadhali kumbuka kuleta jambo lolote linalohusu miradi ya
IGA
7.45 Taarifa kuhusu matukio ya kazi nyingine
Maoni na Hitimisho
8.00 Kuangana
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
47
KIAMBATISHO F Mfano wa Mwongozo wa mada wa MEW kwa mwaka 2017
MEW- 2017
Mapitio/Ufuatiliaji
MADA/LENGO Mwezeshaji
JAN Hakuna
FEB 14
Mwongozo wa mada 2017 Mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Shule wa mwaka 2017 Mipango na taarifa za hivi karibuni Taarifa
ADQA DAO/MEW REP
MACH 17
Angalia 25% ya MMS iliyobora zaidi ya 2017
Mapitio ya Uandishi wa Taarifa ya Mratibu Elimu Kata kwa kutumia mwongozo wa mwaka 2016 Simulizi za mabadiliko Klabu za Juu IGA
DEO ADQA DAO/MEW REP RES
APR 21
Uboreshaji wa ushiriki wa jamii katika masuala ya Elimu shuleni.
ADQA DAO/MEW REP
MEI 19
Kuwasaidia walimu wakuu kutathmini maandalio ya masomo ya walimu
DAO/MEW REP ADQA na VSO
JUNI 16
Mtaala mpya
ADQA DAO/MEW REP
JULAI 21
Kuboresha mahudhurio ya walimu shuleni na darasani
DAO/MEW REP ADQA
AGOS Kuzisaidia shule kupata zana za kufundishia na kutumia vyema zilizopo
DAO/MEWREP
SEPT Kushirikishana vigezo vya ukaguzi? & Jinsi Waratibu Elimu Kata wanavyoweza kusaidia?
ADQA
OKT 20
Kuzisaidia shule zenye uhitaji wa miundombinu bora zaidi ya vyumba vya madarasa, vyoo, vyumba vya madarasa ya walimu
DEO & DSLO
NOV 17
Mapitio ya Mipango ya Mpango wa
Kufuatilia uhamisho wa wanafunzi wa Vituo vya Utayari(SRP) kwa ajili ya kuendelea na maboresho wanavyoingia shuleni
Mwakilishi wa SRP
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
48
Maendeleo ya Shule 2017
Mapitio ya Mwongozo wa mada za MEW 2017 Kuamua na kupitisha Mwongozo wa mada wa mwaka 2018
DES 15
Mapitio ya malengo ya utendaji wa shule na kupanga malengo mengine kwa ajili ya mwaka ujao
DAO
Mada nyingine zilizochaguliwa kwa ajili ya mwaka 2018 Ufundishaji wa madarasa makubwa Kufanya kazi na walimu wakuu wenye matatizo Kusaidia Elimu jumuishi kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum Changamoto na mafanikio ya kufanya kazi na shule shikizi Masuala ya mipaka ya shule Mipango ya uzalishaji mali na utekelezaji wake Kusaidia Elimu ya watoto wa kike Kuwezesha Mikutano ya shule kwa kutoa dondoo za mbinu za uwezeshaji
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
49
KIAMBATISHO G Ufafanuzi wa kazi ya Afisa Elimu Kata
Kutoka chuo cha ADEM
Atawajibika na masuala ya elimu ndani ya kata yake
Kusimamia elimu ya awali, shule za msingi, sekondari na elimu ya watu wazima katika kata yake
Kuhakikisha kuwa sera na nyaraka za mtaala zinapatikana na kuzingatiwa pamoja marekebisho
ya sera za nyaraka za serikali
Kufanya usimamizi wa mara kwa mara wa elimu katika shule za kata yake
Kufanya tathmini ya walimu ili kuhakikisha wanafundisha vizuri
Kutoa ushauri kwa walimu
Kuandaa Mafunzo ya Walimu – Mafunzo ya Walimu ngazi ya Shule (INSET), Kufanya uchunguzi
wa vipindi vya masomo darasani, semina na warsha za mafunzo
Kuanzisha jamii zinazojifunza ili walimu waweze kujiendeleza wenyewe
Kuwa daraja kati ya walimu na jamii
Kutoa taarifa za shule katika kata yake kwa wadau wote kama vile kwa Afisa Elimu Wilaya,
Wathibiti Ubora, Wazazi na Jamii.
Mada za Ziada kutoka EQUIP-T
Kufuatilia na kusaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni katika mitihani yao na majaribio
Kufuatilia ustawi wa watoto, watoto wenye ulemavu, ulinzi wa Mtoto, vilabu vya shule.
Kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi na walimu – watoto wasioandikishwa shule, walioacha
shule, walimu n.k
Kufuatilia upangaji mipango kimkakati katika shule- Mpango wa Maendeleo ya Shule - MMS
Kusaidia utunzaji na usimamizi wa fedha na rasilimali za shule – ruzuku na zana za darasani,
Kuhakikisha kuna utawala bora shuleni-kamati za shule
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
50
KIAMBATISHO H
MAMBO GANI YANAFANYA RIPOTI YA MRATIBU ELIMU KATA IWE NZURI?
RIPOTI ZIPI NA MATARAJIO
1. Ripoti ya WEO ya mikutano ya Shule
Hii ni ripoti inayoandikwa baada ya kila ziara ya shughuli za shule kufuatilia Utendaji wa Shule.
Ripoti hii itaandikwa baada ya kila ziara ya kutembelea shule. Maelezo ya kila ziara pia
huandikwa kwenye batli (logbook) ya shule.
Kila ziara zinapaswa kuwa na lengo mahususi na ijikite kwenye suala fulani. Ripoti inahitaji
kurekodi lengo hili na sual lilifuatiliwa na matokeo yake. Inarekodi ushauri wa pamoja na mambo
ya kufanya waliyokubaliana ili yaweze kukaguliwa wakati wa ziara zinazofuata.
Mfano wa suala la kujikita
Ukusanyaji wa data za mfumo wa taarifa za shule (SIS). Kusaidia uboreshaji na usimamizi wa
Shule.
Takwimu tofauti tofauti hukusanywa na kuripotiwa kwa mzunguko tofauti kulingana na sababu
ya ziara ya kutembelea shule na taarifa zozote zinazotakiwa na Halmashauri.
Fuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mambo waliyokubaliana wakati wa ziara ya mwisho
Fuatilia utekelezaji wa MMS.
Kuna matokeo gani yaliyoonekana kutokana na mafunzo ya walimu ngazi ya shule na mikutano
ya walimu (Pata ushahidi).
Fuatilia na pitia mafunzo au kozi yoyote ilifanyika nje ya shule. Kama vile kozi/mafunzo ya EQUIP-
Tanzania
Chunguza kwa kina uandaaji mipango, kazi za wanafunzi, maandalio ya kazi na ushauri
uliotolewa
Tunashauri huu uwe utaratibu endelevu wa kutoa taarifa utakaojazwa kwa kila shule
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
51
RIPOTI YA MIKUTANO YA SHULE
Tarehe ya 1
Ripoti iliyoandikwa ……….………………………………………
………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
Tarehe ya 2
Ripoti iliyoandikwa ……..………………………………………
………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
2. Ripoti ya Mwezi ya MEK ya kata iliyounganishwa
Hii ni ripoti iliyounganisha taarifa za Mkutano ya kila shule na kuunda ripoti ya kila mwezi ya
WEO. Ripoti inapaswa:
Ibainishe masuala ya kata nzima yanayotokana na taarifa za mikutano ya kila shule
Ioneshe kwa kina takwimu za shule
Ifanye ulinganisho kati ya shule na shule. Ichambue maendeleo ya shule tofauti
Ibainishe maeneo ya shule yanayohitaji msaada na hatua za kushughulikia
o Itoe taarifa juu ya matokeo ya mafunzo na mafunzo ya walimu ngazi ya shule
o Itoe taarifa juu shughuli zilizofanyika kama vile kukagua kazi, yaliyoonekana
Fomu ya kuomba fedha za ruzuku ya mwezi
Ripoti ya fedha za ruzuku ya mwezi/robo mwaka
Shughuli za Ruzuku ya UWW na fedha kama vile za Miradi ya kuingizia shule kipato (IGA)
3 Halmashauri inawajibu wa kupokea Ripoti za Mratibu Elimu Kata na kufuatilia ubora wa
Ripoti zake
Huweka takwimu hizo kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa wa Halmashauri
Huhakikisha masuala muhimu yaliyoibuliwa katika ripoti yanajadiliwa
Huchambua na kuchukua hatua juu ya maendeleo ya shule
Hatua zilizoafikiwa zinatekelezwa kwa wakati
RIPOTI NZURI NI IPI?
Mrejesho wa ana kwa ana unaofuatiwa na ripoti ya maandishi
Haifuati muundo maalum lakini inagusa maeneo muhimu ya ziara
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
52
Rahisi kusoma, ina lugha rahisi, maelezo mafupi
Maudhui yake yanabeba picha halisi ya masuala yaliyochunguzwa wakati wa ziara
Inarekodi maendeleo yaliyofikiwa tangu ziara ya mwisho
Mawazo yanapangwa kwa mtiririko mzuri, kwa ufupi na kwa ufasaha
Pointi za msingi sana na zile dhaifu zinaelezwa kwa uwazi na kwa kifupi
Hakuna utata
Inaonesha ushauri na mapendekezo ya kusaidia masuala yaliyoibuliwa
Imeandikwa katika muundo wa aya na kila aya ina taarifa kamili
Ina uwazi
Inaangalia uboreshaji wa taaluma
Inarekodi maendeleo ya ujifunzaji wa wanafunzi tangu ziara ya mwisho ilipofanyika
Inarekodi maendeleo ya ubora wa ufundishaji tangu ziara ya mwisho
Inarekodi maendeleo ya UWW na Kamati za shule tangu ziara ya mwisho
Inarekodi ushauri na msaada uliotolewa
Inarekodi hatua zinazopaswa kuchukuliwa, na nani wa kuchukua hatua
KUFANYA ZIARA NZURI ZA SHULE Ripoti nzuri inatokana na ziara iliyoandaliwa vizuri na yenye
malengo maalum
Weka wazi malengo ya ziara ya kutembelea shule, kama vile;
Kukusanya takwimu za shule
Kusaidia shule kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya mtaala na mbinu mpya
za ufundiji
Kuhakikisha kuna utekelezaji wa sera za Elimu
Kusaidia kuainisha mahitaji na kutoa msaada kwa wanafunzi, walimu, walimu wakuu na
wafanyakazi wengine
Kutoa ushauri juu ya jinsi ya kuboresha usimamizi wa shule kwa ujumla
Kupitia na kusaidia katika masuala ya Mpango wa Maendeleo ya Shule na Utekelezaji wake
Kufuatilia na kuangalia maendeleo ya shule tangu ilivyotembelewa mara ya mwisho
Mwenendo mzuri wenye maadili ya kitaaluma
Dumisha mahusiano ya kikazi na kitaaluma
Onesha mfano
Heshimu wengine
Uwe mwaminifu na muwazi katika kutekeleza majukumu
Linda usiri
Baki kwenye lengo
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
53
KIAMBATISHO I NINI CHA KUFANYA BAADA YA MAFUNZO
Baada ya
mafunzo haya
nini tunapaswa
kufanya?
Tutafanya nini
na wakati gani?
Tutaandaaje na
kuwezesha
MEW? Vifaa vipi
tutatumia?
Tunatakiwa
kufanya nini
baada ya
mkutano wa
MEW, kusaidia
na kufuatilia?
Nani
atatusaidia?
Wa taarifu
Waratibu Elimu
Kata kuhusu
MEW
Mkubaliane
tarehe na muda
KIAMBATISHO J
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
54
MAJUKUMU NA TARATIBU ZA UTOAJI TAARIFA ZA MKUTANO WA ELIMU WA MKOA NA
WILAYA
AFISA ELIMU MKOA NA KANDA
Majukumu
Afisa Elimu Mkoa atagawa majukumu kati ya ofisi ya elimu ya kanda na mkoa
Kufuatilia kuhakikisha kwamba mikutano ya Halmashauri inafanyika na kuendeshwa vizuri na kutoa msaada kwa kupiga simu mara kwa mara
• Kuhudhuria MEW mara kwa mara na kuwasaidia maafisa elimu wa Halmashauri na Wathibiti Ubora
• Kupokea Mwongozo wa mada za mwaka kutoka Halmashauri mwezi Januari kila mwaka • Kujaza idadi ya mikutano na mada zilifanyiwa kazi • Kujaza mahudhurio ya maafisa elimu wa Halmashauri na Wadhibiti Ubora • Kuchangia kuendesha mada na kuzitawanya kwenye Halmashauri nyingine • Kutunza na kuboresha orodha ya namba za mawasiliano
Kutoa taarifa
• Kupokea Mwongozo wa mada za mwaka mwezi Januari kila mwaka • Kudai taarifa za MEW kama sehemu ya ripoti ya Afisa Elimu Wilaya • Kumbukumbu za mikutano ya MEW • Kutoa mrejesho kwa Halmashauri
Halmashauri
Majukumu
• Afisa Elimu Wilaya atateua Mwakilishi/Mratibu wa MEW • Halmashauri kuonesha nia na uwajibikaji wa kusimamia mikutano ya MEW na Jamii
inayojifunza • Kushirikishana na kuisaidia Kamati ya Maandalizi ya MEW • Wilaya zote kuboresha mrejesho unaotolewa kwa Waratibu Elimu Kata kuhusu ripoti zao • Kufuata na kutekeleza mambo yaliyopitishwa wakati wa MEW • Wilaya kutenga bajeti na kuhakikisha mikutano ya MEW inaendelea kufanyika
Utoaji wa taarifa
• Afisa Elimu Wilaya atatoa taarifa kuhusu MEW kwenye ripoti yake ya maendeleo ya kila mwezi kwa Afisa Elimu Mkoa, kada na EQUIP-Tanzania
• Kumbukumbu za mikutano ya MEW zitasambazwa kwenda EQUIP-T, kwa Afisa Elimu Mkoa na Mthibiti Ubora wa Kanda
• Kupokea Mrejesho na taarifa za kufuatiliaji kutoka mkoani kuhusu kupokea yatokanayo na MEW na ripoti ya maendeleo ya Afisa Elimu Wilaya
WARATIBU ELIMU KATA
Majukumu
• Afisa Elimu Kata kuonesha nia na uwajibikaji wa kusimamia mikutano ya MEW na Jamii inayojifunza
• Kufuata na kutekeleza makubaliano yaliyopitishwa wakati wa MEW • Kushirikishana na kuisaidia Kamati ya Maandalizi ya MEW
Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania)
Uongozi na Usimamizi wa Shule
55
Kutoa wa taarifa
• Kuandika na kusambaza taarifa za mkutano wa MEW kwa ADQA, Afisa Elimu wa Wilaya, Afisa Elimu Mkoa, Mthibiti Ubora wa Kanda, na EQUIP-T
• Kuboresha taarifa za kila mwezi ya Afisa Elimu kata • Kupokea mrejesho na kufuatiliaji kutoka Halmashauri baada ya kupokea ripoti za Afisa
Elimu Kata