katiba ya umoja wa wapare kimara king'ongo 2

13
KATIBA YA UMOJA WA WAPARE KIMARA KING’ONGO (UPAKIKI) Imetayarishwa na: Kamati ya Katiba Ndugu: Elisante,Mduma,Mfinanga,Karani na Majaliwa

Upload: donasian-mbonea-elisante-mjema

Post on 22-Feb-2015

168 views

Category:

Documents


17 download

TRANSCRIPT

Page 1: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

KATIBA

YA

UMOJA WA WAPARE KIMARA KING’ONGO (UPAKIKI)

Imetayarishwa na: Kamati ya KatibaNdugu: Elisante,Mduma,Mfinanga,Karani na Majaliwa

Page 2: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

YALIYOMO1.0 Kifungu cha 1. Utangulizi------------------------------------------------------------32.0 Kifungu cha 2. Jina na Anwani ya Umoja-------------------------------------33.0 Kifungu cha 3.Akaunti ya Benki--------------------------------------------------34.0 Kifungu cha 4. Malengo---------------------------------------------------------------35.0 Kifungu cha 5. Uwanachama-------------------------------------------------------36.0 Kifungu cha 6. Aina za Uanachama----------------------------------------------47.0 Kifungu cha 7. Haki za Mwanachama------------------------------------------48.0 Kifungu cha 8.Kusitishwa Uanachama-----------------------------------------49.0 Kifungu cha 9. Uongozi,Utendaji na Utawala-------------------------------410.0 Kifungu cha 10. Wajibu na Madaraka ya Viongozi wa Umoja------611.0 Kifungu cha 11. Vikao vya Umoja-----------------------------------------------612.0 Kifungu cha 12. Mapato ya Umoja-------------------------------------------713.0 Kifungu cha 13. Matumizi ya Fedha za Umoja---------------------------714.0 Kifungu cha 14. Marekebisho ya Katiba------------------------------------715.0 Kifungu cha 15. Kiingilio-----------------------------------------------------------716.0 Kifungu cha 16. Michango ya Kila Mwezi-----------------------------------817.0 Kifungu cha 17. Watakao changiwa na chama ni hawa wafuatao:---------------------------------------------------------------------------------------------------------818.0 Kifungu cha 18. Mkutano Mkuu-------------------------------------------------919.0 Kifungu cha 19. Uwajibikaji------------------------------------------------------920.0 Kifungu cha 20. Kuvunjika kwa Umoja wa wapare----------------------921.0 HITIMISHO------------------------------------------------------------------------------9

2

Page 3: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

KATIBA YA UMOJA WA WAPARE WA KIMARA KINGO’NGO PAMOJA NA WAUME WALIOA DADA ZETU.

1.0 Kifungu cha 1. UtanguliziKatiba hii ya Umoja wa wapare Kimara King’ongo imetengenezwa na wanachama waanzilishi wa Umoja tarehe 16.04.2011 na itawahusu wanachama wote wa umoja huu pamoja na wale wote watakaojiunga baadaye kwa utaratibu uliowekwa kwenye katiba hii.

2.0 Kifungu cha 2. Jina na Anwani ya UmojaSehemu ya 01 Jina la Umoja huu ni: Umoja WA Wapare wa Kimara King’ongo - UPAKIKISehemu ya 02 Makao Makuu: King’ongo – Dar es Salaam.Sehemu ya 03 tarehe ya kuanzishwa 12.03.2011

3.0 Kifungu cha 3.Akaunti ya Benki Sehemu ya 01 Akaunti ya benki itafunguliwa katika benki ambayo mkutano mkuu

wa umoja utaridhia. Sehemu ya 02 Watia saini: Sehemu ya 03 Kutakuwa na watia saini wanne; wawili kutoka kundi “A” ambao ni

Mwenyekiti na Katibu wake.Kundi “B” watakuwa wajumbe wawili wasio na madaraka yeyote katika Umoja huu.

Sehemu ya 04 Kutoa fedha benki: Sehemu ya 05 Saini mbili kati ya nne zitakuwa na uwezo wa kutoa fedha benki

kwa utaratibu wa saini moja kutoka kundi “A” na saini moja kutoka kundi “B”

4.0 Kifungu cha 4. Malengo Malengo ya umoja wa Wapare wa Kimara Kingo’ngo ni kuwaunganisha wapare

wa Kimara King’ongo kuanzia Michungwani hadi mto Mbezi. Kushirikiana katika kutatua matatizo yanayowahusu: Malengo hayo ya msingi ni:

i. Misibaii. Ugonjwa

iii. Harusiiv. Kutoa Mikopo midogo midogo kwa wanachama yenye riba nafuu

5.0 Kifungu cha 5. Uwanachama Sehemu ya 01 Mpare yeyote mwenye umri usiopungua miaka 18; mwenye akili

timamu; mwenye kufanya kazi halali kisheria;bila kujali dini,rangi au jinsia,aliyelipa kiingilio kilichoidhinishwa na Umoja.

Sehemu ya 02 Umoja huu niwa Hiari kwa Mpare yeyote,anayekaa eneo husika. Sehemu ya 03 Umoja utawapokea wanaume waliooa dada zetu,wanahiari ya

kujiunga.

3

Page 4: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

6.0 Kifungu cha 6. Aina za Uanachama Sehemu ya 01 Umoja huu utakuwa na aina moja ya Uanachama.Mwanachama

wa umoja huu ni yule ambaye jina lake lipo katika orodha ya wanachama,na ambaye amelipa kiingilio na ada ya kila mwezi.

7.0 Kifungu cha 7. Haki za Mwanachama Sehemu ya 01 Kushiriki katika mijadala na maamuzi katika masuala yote

yanayohusu umoja. Sehemu ya 02 Kuchagua na Kuchaguliwa kushika nafasi za uongozi Sehemu ya 03 Kupata ushirikiano wa wanachama itokeapo haja inayotambuliwa na

Umoja. Sehemu ya 04 Kusaidiwa na umoja katika masuala yanayotambulika na umoja huu.

8.0 Kifungu cha 8.Kusitishwa Uanachama Sehemu ya 01 Kujiuzulu Mwanachama. Sehemu ya 02 Kufariki mwanachama Sehemu ya 03 Kusitishwa Uanachama na mkutano mkuu halali.Uamuzi huo

utapitishwa kwa kura ambapo theluthi mbili(2/3) za wajumbe wote waliohudhuria zitahitajika.

Sehemu ya 04 Kutohudhuria vikao bila taarifa wala sababu za msingi vikao vinne(4) vya umoja mfululizo.

Sehemu ya 05 Kutolipa mchango wa kila mwezi kwa muda wa miezi sita(6) Sehemu ya 06 Kuchukua mikopo na kutorudisha kwa wakati Sehemu ya 07 Kueneza nje taarifa za siri za umoja kwa nia ya kuchafua umoja Sehemu ya 08 Mwanachama akilazimika kusitisha uanachama,ina maana

asipofukuzwa au kufariki(kwa mfano kuhama King’ongo) hatarudishiwa kitu chochote.

9.0 Kifungu cha 9. Uongozi,Utendaji na Utawala Sehemu ya 01 Muda wa Uongozi kukaa Madarakani Kipengele cha 1. Muda wa uongozi kukaa madarakani ni miaka miwili,baada ya

hapo uchaguzi utaitishwa ili kuchagua viongozi wapya wa umoja.

Sehemu ya 02 Mkutano Mkuu wa Wanachama wote Kipengele cha 1.Hiki ndicho kikao chenye mamlaka ya juu kabisa kuhusu maamuzi

ya Umoja. Kipengele cha 2. Utafanyika angalau mara mbili kwa mwaka Kipengele cha 3 . Koram ni theluthi (2/3) au zaidi ya wajumbe wenye haki ya

kuhudhuria itafanya mkutano mkuu kuwa halali. Kipengele cha 4 Wanachama watapewa taarifa ya mkutano wa kawaida siku 30

kabla ya mkutano mkuu. Kipengele cha 5 Theluthi moja (1/3) au zaidi ya wajumbe wenye haki ya

kuhudhuria mkutano wanaweza kuitisha mkutano wa dharura.

4

Page 5: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

Sehemu ya 03 Kamati ya Utendaji Kipengele cha 1.Shughuli zote za kila siku za Umoja zitaendeshwa chini ya

usimamizi wa kamati ya utendaji yenye wajumbe waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Umoja kila baada ya miaka miwili (2)

Kipengele cha 2 . Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni wafuatao:i. Mwenyekiti

ii. Makamu Mwenyekitiiii. Katibu Mkuu/Katibu Msaidiziiv. Mtunza Hazina Mkuu na Msaidizi wakev. Kamati ya kuratibu mikopo na kujadiliana

Kipengele cha 3 .Kamati ya Utendaji itakuwa na jukumu ya kuwajulisha wanachama tukio lolote lile linapotokea.Kamati hii itaratibu masuala yote ya kujadiliana.

Sehemu ya 04 Kamati ya Kuratibu Mikopo na Kujadiliana Kipengele cha 1.Wajumbe wa kamati hii watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa

Umoja kila baada ya miaka miwili(2) Kipengele cha 2. Kamati hii itapokea maombi ya mwanachama.Itajadili maombi

haya na kuyawasilisha katika kamati ya Utendaji itakayotoa uamuzi wa mwisho .

Kipengele cha 3. Kamati hii itamshirikisha Mweka Hazina Mkuu wa Umoja katika masuala yahusuyo mfuko wa mikopo.

Kipengele cha 4. Kamati hii itaratibu masuala yote ya mikopo Kipengele cha 5. Wajumbe wa kamati hii ni:

i. Mwenyekiti wa mikopoii. Afisa mikopo

iii. Wajumbe wawili wa kuratibu na kuimarisha umoja huuKipengele cha 6.Mjumbe wa kamati hii atasimamishwa ujumbe na Mkutano mkuu kutokana na mwendo mbovu kwa kura ya theluthi mbili(2/3) ya wajumbe waliohudhuria.Kipengele cha 7. Kamati ya mikopo itatoa mikopo pale tu,chama kitakapokuwa na zaidi ya shilingi milioni moja benki na sio chini ya hapo.

Sehemu ya 05 Kamati ndogo ndogo Kipengele cha 1. Kamati ya utendaji itaunda kamati mbalimbali za kushughulikia

uratibu wa shughuli za umoja kama itakavyohitajika.Kutakuwa na kamati ya mikopo,kamati ya misiba,kamati ya magonjwa na kamati ya Harusi.

Sehemu ya 06 Sifa za Uongozi wa Umoja wetu. Kipengele cha 1. Awe amelipa mchango wa kiingilio na mchango wa mwezi. Kipengele cha 2.Awe amejishughulisha kikamilifu na mipango ya umoja hasa

kuhudhuria mikutano ya wanachama. Kipengele cha 3. Awe mkazi wa Kimara King’ongo

5

Page 6: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

Kipengele cha 4.Kiongozi atakayeachishwa uongozi kwa mazingira ya uwajibikaji hawezi kugombea nafasi nyingine kabla ya miaka mitano kupita tangu aachishwe uongozi

Kipengele cha 5. Mgombea wa nafasi yeyote katika umoja huu sharti awe ametimiza angalau mwaka mmoja wa uwanachama.Kifungu hiki hakitawahusu waanzilishi wa umoja huu.

10.0 Kifungu cha 10. Wajibu na Madaraka ya Viongozi wa Umoja Kipengele cha 1.Mwenyekiti

i. Ndiye msimamizi na msemaji mkuu wa masuala yote ya umoja huu.ii. Ndiye mwenyekiti wa Kamati ya utendaji na Mkutano mkuu wa umoja

iii. Endapo Mwenyekiti ana udhuru,kazi zake zitafanywa na Makamu Mwenyekiti.

Kipengele cha 2.Katibu Mkuui. Ni mtendaji mkuu wa shughuli zote za kila siku za umoja

ii. Ataitisha mikutano na vikao vya umojaiii. Atatoa taarifa ya kazi za Umoja katika Mkutano Mkuu wa Umoja.iv. Ni mtunza kumbukumbu za umoja

Kipengele cha 3.Mtunza Hazina Mkuu na Msaidizi wakeKutokana na unyeti wa nafasi hii,Mweka Hazina atakuwa na msaidizi wake ambaye atawajibika moja kwa moja kwa Mweka Hazina Mkuu.Majukumu yao yatakuwa kama ifuatavyo:-

i. Watakusanya na kutunza mapato ya umojaii. Watatoa ripoti ya fedha katika kila kikao cha wanachama wote au

wakati wowot e inapohitajikaiii. Watawajibika kuonyesha taarifa ya benki yaani “bank statement”katika

kila kikao cha kamati ya utendaji na mkutano mkuu.Kipengele cha 4.Wajumbe wa Kamati mbalimbaliHawa ni Wenyeviti na Makatibu wa Kamati ndogo ndogo

i. Mwenyekiti atakuwa ni msemaji mkuu wa kamati husika na atasimamia vikao

ii. Katibu atakuwa ni mtendaji mkuu wa kamati husika;atatoa taarifa kwa Kamati ya Utendaji au katika Mkutano Mkuu.

11.0 Kifungu cha 11. Vikao vya Umoja Kipengele cha 1. Mkutano Mkuu wa wanachama wote utafanyika mara mbili kwa

mwaka Kipengele cha 2. Wanachama wote watakutana mara moja kwa mwezi

ilikuwasilisha michango yao ya mwezi Kipengele cha 3.Kamati ya utendaji itafanya vikao vyake angalau mara moja kila

baada ya miezi mitatu na wakati wa dharura

6

Page 7: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

Kipengele cha 4. Kamati ya Uratibu wa Mikopo itafanya vikao vyake kila mara wakati wa kujadili mikopo na angalau wiki moja kabla ya hafla maalum ya umoja.

12.0 Kifungu cha 12. Mapato ya Umoja Mapato ya Umoja yatatokana na:-

i. Viingilio vya wanachamaii. Mchango wa mwezi wa shilingi elfu mbili na mia tano(2,500)

iii. Michango itakayoidhinishwa na wanachama woteiv. Riba itokanayo na mikopo midogo midogov. Harambee ya umoja

vi. Adhabu kwa mwanachama kuchelewa vikao/kutofika bila taarifa.

13.0 Kifungu cha 13. Matumizi ya Fedha za Umojai. Fedha za umoja zitatumika kwa ajili ya malengo makuu ya umoja huu kama

yalivyo ainishwa kwenye kifungu cha 4 cha katiba hii.ii. Fedha za umoja zitatumika kwa mujibu wa maelekezo na kanuni za katiba

hii,au kama itakavyoelekezwa na mkutano mkuu wa umoja vinginevyo utaratibu wa maamuzi ya Mkutano Mkuu ambapo zaidi ya robo tatu (3/4) ya wanachama wataafiki matumizi husika utafuatwa.

iii. Fedha zitachukuliwa benki na Mtunza Hazina Mkuu kwa kufuata taratibu za kutia saini kama ilivyoinishwa kwenye katibu hii kifungu cha 3.Ikiwa mwanachama yeyote atapatiwa huduma ya fedha,italazimika kusaini ili kudhibitisha kuwa amepokea fedha hizo.

iv. Watunza hazina hawaruhusiwi kukaa na pesa ya umoja majumbani mwao kwa zaidi ya masaa 72 isipokuwa kwa ruhusa maalum toka kwa Kamati ya Utendaji.

v. Kamati ya Utendaji inaweza kutoa idhini ya kutumia fedha kwa jambo la muhimu la umoja baada ya kupata ridhaa ya wanachama wasiopungua asilimia hamsini(50%) wasiokuwa wajumbe wa kamati ya utendaji na taarifa itatolewa kwenye mkutano wa wanachama wote wa mwezi.

14.0 Kifungu cha 14. Marekebisho ya Katiba Sehemu ya 01 Kipengele chochote cha katiba hii kitabadilishwa au kurekebishwa

na mkutano mkuu wa umoja huu.

15.0 Kifungu cha 15. Kiingilioi. Kila mwanachama atalipa kiingilio cha Tshs.10,000/= Ikumbukwe kuwa

mwanachama mpya atakayeomba kujiunga na umoja huu atalazimika kuongeza katika kiingilio hiki jumla ya michango yote ambayo wanachama waanzilishi washatoa hadi hapo anapojiunga na umoja huu.

ii. Mwanachama mpya yaani mhamiaji ataanzia kulipa wakati huo huo anaojiunga.Lakini yule anayefahamu umoja huu kuwa upo utamlazimu kulipa michango yote.

7

Page 8: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

16.0 Kifungu cha 16. Michango ya Kila Mwezi Sehemu ya 01 Kila mwanachama atatoa mchango wa kila mwezi wa shilingi elfu

mbili na mia tano(2,500/=) kuanzia Aprili,2011 na kuendelea, Kiwango hiki kinaweza kubadilishwa na Mkutano mkuu wa mwaka tu.

Sehemu ya 02 Mwanachama asipotoa mchango wake wa mwezi kwa muda wa miezi sita(6) atakuwa amejifukuza mwenyewe uwanachama.

17.0 Kifungu cha 17. Watakao changiwa na chama ni hawa

wafuatao:- Kipengele cha 1. Misiba

i. Mwanachama akifa yeye mwenyeweii. Mwanachama akifiwa na Mkewe/Mumewe

iii. Mwanachama akifiwa na mtoto/watoto wake wa kuzaa mwenyeweiv. Mwanachama akifiwa na Baba/Mama mzazi halisiv. Mwanachama akifiwa na Baba/mama mkwe halisi

vi. Mfanyakazi wa nyumbani ilimradi msiba upo katika kaya yakevii. Mwanachama akifiwa na ndugu wa karibu ambaye ameishi naye

nyumba moja si zaidi ya miezi mitatu mpaka mauti yanamfika na msiba upo nyumbani kwa mwanachama.

Mwanachama akifiwa na mmoja wa ndugu waliotajwa hapo juu na anasafirishwa kila mwanachama atatoa shilingi 5,000/=

Mwanachama akifiwa umoja utamchangia Tshs.100,000/= kutoka kwenye mfuko wa chama.

Kipengele cha 2. KuuguaSehemu ya 01 Ikiwa mwanachama ataugua na kulazwa hospitali au kuuguza mme/mke/mtoto halisi hospitali kwa muda wa wiki moja,kamati ya utendaji itajulishwa ili iidhinishe malipo ya shillingi 50,000/= kutoka mfuko wa Umoja.Sehemu ya 02 Kila mwanachama atalazimika kumjulia hali mgonjwa akipata wasaa wa kufanya hivyo.Kamati inayohusika itapaswa kutoa taarifa kwa wanachama wa umoja.

Kipengele cha 3. Sherehe

Sehemu ya 01 Kuhusu sherehe kama vile kuoza na kuoa ni wajibu wa mwanacha kutoa taarifa kwa wanachama wote ndani ya miezi mitatu(3),ili kamati ya utendaji ifanye maamuzi juu ya namna ya kushiriki,na Kamati ya Utendaji itateua uwakilishi wa wanachama wawili.

Sehemu ya 02 Umoja utahusika pale tu shughuli inapomhusu mwanachama kama vile kuoa/kumuoza mtoto halisi wa mwanachama(maana ya mtoto halisi ni mtoto wa kuzaa mwenyewe) au Mwanachama akioa au kuolewa kwa mara ya kwanza.Mfuko utachangia shilingi 50,000/= ili zitumike kumpunguzia makali.

8

Page 9: Katiba Ya Umoja Wa Wapare Kimara King'Ongo 2

Sehemu ya 03 Mara moja kwa mwaka kutakuwepo kujipongeza katika kufungua au kufunga mwaka.Familia za wanachama zitaalikwa katika sherehe hiyo.Kamati ya utendaji itasimamia suala hilo.

Kipengele cha 4. Mikopo midogo midogo Sehemu ya 01 Ili kuboresha kipato cha wanachama wa umoja huu, Kamati ya mikopo itatoa mikopo midogo midogo kuanzia elfu hamsini na kuendelea.Riba ya asilimia 10% ya mkopo itarejeshwa kwa mwezi.Kamati ya mikopo itaweka utaratibu mzuri zaidi.

18.0 Kifungu cha 18. Mkutano Mkuu Sehemu ya 01 Katika Kila kikao cha Mkutano Mkuu kila mwanachama atatakiwa

kuchangia shilingi 1,000/= kutoka mfukoni mwake ikiwa ni gharama za kikao hicho.

19.0 Kifungu cha 19. Uwajibikaji Sehemu ya 01 Ili kuhakikisha kwamba wanachama wanatimiza wajibu wao na

kuweka hali ya amani na upendo katika umoja adhabu na fani zitatolewa kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu wa umoja.Kamati ya utendaji ina madaraka ya kutoza faini kwa mujibu wa kanuni hizi; isipokuwa adhabu ya kufukuza mwanachama itatolewa na mkutano mkuu. Msingi na viwango vya adhabu ni kama ifuatavyo:-

Kipengele cha 1. Mwanachama atakayechelewa katika vikao/mikutano bila taarifa ya awali atalipa faini ya shilingi mia tano(shs.500/=)

Kipengele cha 2. Mwanachama atakayeshindwa kuhudhuria vikao/mikutano kama hana udhuru au maelezo yatakayokubaliwa na kamati ya utendaji atalipa shilingi elfu moja(1,000/=)

20.0 Kifungu cha 20. Kuvunjika kwa Umoja wa wapare Sehemu ya 01 Sio lengo la Katiba hii wala wanachama wa Umoja wa Wapare

kuvunja umoja huu,lakini ikitokea Umoja huu umevunjika kwa sababu moja au nyingine, kila mwanachama atarudishiwa kiingilio chake,na kamati ya utendaji itafanya mahesabu ya michango ya mwezi na kila mwanachama atarudishiwa kiasi kilichopo kulingana na alivyochangia kila mwezi.

21.0 HITIMISHO Sehemu ya 01 Hii ndiyo Katiba halali ya Umoja wa Wapare Kimara King’ongo na

sisi tuliojiorodhesha majina yetu na kutia saini ndio wanachama waanzilishi wa umoja huu.

9