kukusanya sala mbili

107
Mfululizi wa Masuala ya Kifikihi al-Jam’ Baina ‘s-Salaatayn KUKUSANYA SALA MBILI Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Kimeandikwa na: Sheikh Jafar Subhani Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page A

Upload: alitrah-foundation

Post on 29-Mar-2016

344 views

Category:

Documents


12 download

DESCRIPTION

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "Al-Jam’u Bayna Salaatayn" Sisi tumekiita: "Kukusanya Sala mbili." Kitabu hiki, "Kusanya Sala mbili" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sheikh Jafar Subhani. Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake.

TRANSCRIPT

Mfululizi wa Masuala ya Kifikihi

al-Jam’ Baina ‘s-Salaatayn

KUKUSANYA SALA MBILIKwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Kimeandikwa na:Sheikh Jafar Subhani

Kimetarjumiwa na:Hemedi Lubumba Selemani

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page A

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 - 427 - 41 -3 Kimeandikwa na:

Sheikh Jafar Subhani

Kimetafsiriwa na:Hemedi Lubumba Selemani

P.O. Box 19701, Dar es Salaam. Tanzania.

Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed

Kupangwa katika Kompyuta na:Ukhti Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai 2007Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

P.O. Box 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2110640Fax: +255 22 2131036Email: [email protected]

Website: www.alitrah.org

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page B

YALIYOMO

Kukusanya sala mbili.....................................................2

Kukusanya sala mbili Muzdalifa na Arafa...................3

Kukusanya kati ya sala mbili safarini...................... ....5

Kukusanya sala mbili bila udhuru pasipo safari..........19

Mgawanyo wa nyakati ndani ya Fiqhi ya Kisuni..........26

Anayeafikiana na Imamiyya katika baadhi ya

nukta...............................................................................27

Masunni wanaoafikiana na Imamiyya katika kila kitu

kuhusu suala hili.............................................................29

Kukusanya sala mbili bila udhuru usipokuwa safarini kwa

mujibu wa Sunna............................................................35

Wanazuoni wengi wa Kisuni wameacha kuifanyia kazi.50

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page C

Hadithi haielezi kukusanya kwa kutanguliza au kwa

kuchelewesha................................................................. 55

Alikusanya sala mbili kimuonekano......................... 58

Dalili za As-Shaukaniy za kuthibitisha kuwa kukusanya

kulikuwa kwa kimuonekano ..........................................62

Alikusanya kwa sababu ya udhuru usiyo julikana ........74

Maswali na majibu..........................................................79

(a) Ya kwanza: Mgongano wa Hadithi ya kuku

sanya na ile ya hanashu..............................79

(b) Ya pili: Mgongano wa Hadithi ya kukusanya

na ile ya usiku wa harusi............................81

(c) Ya tatu: Hadithi ya Habib bin Thabit si

hoja.............................................................83

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page D

Neno la mchapishajiKitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabucha Kiarabu kwa jina la: "Al-Jam’u Bayna Salaatayn"Sisi tumekiita: "Kukusanya Sala mbili."

Kitabu hiki, "Kusanya Sala mbili" ni matokea ya utafitiwa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu,Sheikh Jafar Subhani.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika nakila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanay-ompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake.

Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamuwamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katikamatendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo katiya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofautina kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayowanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingiya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilingan-isha na yale tunayokubaliana nayo.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page E

Kukusanya Sala mbili ni suala ambalo wanachuo wetuwamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati yamadhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, balini hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafi-ana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamuwengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyokuongelea katika dhana na kusababisha mizozoisiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu,Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili nakuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia mso-maji mwenyewe kutoa uamuzi.

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huuwa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote.Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-ItrahFoundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha yaKiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudu-mia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ilikuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemanikwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabuhiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwanjia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page F

kitabu hiki.

Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page i

KUKUSANYA SALA MBILIKwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola waulimwengu. Rehma na Amani zimfikie mbora wa viumbena hitimisho la mitume Wake, pia kizazi chake kitakatifuambacho ndio kasha la elimu yake na hazina ya mafunzoyake.

Hakika Uislamu ni imani na sheria. Imani ni kuaminiMwenyezi Mungu, mitume Wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni hukumu za Mwenyezi Mungu ambazo zinajukumu la kumpa mwanadamu maIsha bora na kumhakik-ishia wema wa dunia na akhera.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika nakila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanay-ompata mwanadamu katika sekta zote za maIsha yake,hivyo Mwenyezi Mungu akasema:

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page ii

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizienineema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe diniyenu.” (5:3).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayowanazuoni wa sheria wametofautiana kwa sababu yakuhitilafiana kwao kuhusu riwaya zitokanazo kwa Mtume(s.a.w.w.). Jambo ambalo limepelekea kutofautianakuhusu masuala madogo madogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti, basi hakika katikamtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka suala hilijuu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia yakuunganIsha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanjahuu, kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dinihata ipelekee kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyoponi kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo nijambo dogo ukilinganIsha na mambo mengi ambayotunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu.

Na muongozo wetu katika njia hii ni kauli ya MwenyeziMungu (s.w.t):

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page iii

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungunyote wala msifarikiane. Na kumbukeni neema yaMwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maaduina akaziunganIsha nyoyo zenu, hivyo kwa neema zakemkawa ndugu." (3:103).

Jafar SubhanyTaasisi ya Imam Sadiq (a.s.)Qum

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page iv

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 1

Kukusanya Sala mbili

2

KUKUSANYA SALA MBILI

Kukusanya kati ya Sala mbili kuna sura tofauti:

Kukusanya Sala mbili Muzdalifa na Arafa.

Kukusanya Sala mbili safarini.

Kukusanya Sala mbili pasipokuwa safarini kwa udhurukama vile mvua na tope.

Kukusanya Sala mbili pasipokuwa safarini bila ya kuwe-po udhuru wowote.

Hivyo sura mbili za kwanza ndizo zinazoingia katikahukumu ya safari na si sura mbili za mwisho. Wanazuoniwa sheria ya Kiislamu wamekubaliana kuhusu kukusanyaSala hapo Muzdalifa na Arafa lakini wametofautianakuhusu kukusanya Sala eneo lingine lisilokuwa kaati yahayo mawili. Hivyo sisi hapa tutazungumzia kwa ufupisura moja baada ya nyingine huku tukitaja kauli zinazo-husu suala hili na vyanzo vya kauli hizo.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 2

Kukusanya Sala mbili

3

1. Kukusanya Sala mbili Muzdalifa na Arafa

Wanazuoni wa sheria ya Kiislamu wamekubaliana kuhusukupendelea kukusanya Sala Muzdalifa na Arafa na walahakuna tofauti katika hilo.

Al-Qurtuby amesema: “Wamekubaliana kuwa ni sunnakukusanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr wakati waAdhuhuri uwapo Arafa, na kati ya Magharibi na Ishawakati wa Isha uwapo Muzdalifa, huku wakitofautianakuhusu kukusanya sehemu nyingine zisizo hizo mbili. 1

Ibnu Quddama amesema: “Al-Hasan na Ibnu Sirin nawatu wa rai wote wamesema: “Hairuhusiwi kukusanyaisipokuwa siku ya Arafa uwapo Arafa, na usiku waMuzdalifa uwapo Muzdalifa."2

Amepokea Muslim toka kwa Jabir bin Abdillah kuwaMtume wa Mwenyezi Mungu alikaa miaka tisa bila kuhi-ji, kisha akawatangazia watu mwaka wa kumi kuwa1 Bidayatul-Mujtahid Juz. 1 / Uk. 170 chini ya anuani: sehemu yapili kuhusu kukusanya Sala.2 Al-Mughny: Juz. 2, Uk. 112.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 3

Kukusanya Sala mbili

4

Mtume (s.a.w.w.) atahiji, hivyo watu wengi wakaendaMadina huku wote wakitaka waongozwe na Mtume nawafanye kama atakavyofanya. - Akaendelea mpakaakasema - mpaka alipofika Arafa akakuta quba limepamb-wa kwa madoa, akashuka hapo mpaka jua lilipopinduka,akaamrIsha aletewe ngamia, akaondoka mpaka alipofikandani ya bonde akatoa hotuba - akaendelea mpaka akase-ma - kisha akaadhini na akakimu, akaswali Sala yaAdhuhuri, kisha akakimu akaswali Sala ya Al-Asr walahakuswali chochote baina ya hizo mbili, - akaendeleampaka akasema - akaenda mpaka akafika Muzdalifa,hapo akaswali Sala ya Magharibi na Isha kwa adhanamoja na iqama mbili wala hakufanya tasbihi yoyote bainaya Sala hizo mbili. 3

Kwa kuwa suala hili ni jambo linalokubalika kwaWaislamu wote basi tutafupIsha kwa kiasi hiki.

3 Sahih Muslim: Juz. 4, uk. 39 - 42 mlango: Hija ya Mtume.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 4

Kukusanya Sala mbili

5

Kukusanya kati ya Sala mbili safarini

Wanazuoni wengi wa Kiislamu wamekubaliana kuhusukukusanya Sala mbili safarini isipokuwa Al-Hasan, An-Nakhai, Abu Hanifa na jamaa zake wawili. Hivyoinaruhusiwa kukusanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr kwakutanguliza kwa kuziswali wakati wa Sala ya mwanzo, nakwa kuchelewesha kwa kuziswali wakati wa Sala ya pili,hii ni kwa wote isipokuwa kwa hao tu.

Na Magharibi na Isha wakati mmoja kwa kuzitanguliza nakuzichelewesha.

Sala zinazokusanywa ni: Adhuhuri na Al-Asr, Magharibina Isha katika wakati wa mojawapo ya hizo, huitwa kuku-sanywa hizo Sala za mwanzo Jam’u taqdiim, (kwa kutan-guliza), na katika nyakati za Sala za pili huitwa Jam’utaakhiri (kukusanya kwa kuchelewesha).

As-Shaukani ametaja kauli mbali mbali kuhusiana nasuala hili kwa namna ifuatayo:Wanazuoni wengi wa sheria wameruhusu kukusanya

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 5

Kukusanya Sala mbili

safarini kwa hali yoyote kwa kutanguliza na kuchelewe-sha, na kauli hii ndio ya maswahaba wengi na wanafunziwa maswahaba na wanazuoni wa sheria huku miongonimwao ni: At-Thaury, As-Shafy, Ahmad, Is’haqa na As-Shahaby.

Wengine wakasema: “Hairuhusiwi kukusanya kwa haliyoyote ile isipokuwa Arafa na Muzdalifa. Na hii ndiyokauli ya Al-Hasan, An-Nakhai, Abu Hanifa na wenzakewawili.

Al-Laythu amesema: “Na kauli hii ni mashuhuri tokakwa Malik kuwa kukusanya kunamuhusu yule tu mwenyeharaka na safari."

Ibnu Habibu amesema: “Kunamhusu mwenye kutembea."

Al-Awzay amesema: “Hakika kukusanya safarinikunamhusu mwenye udhuru.”

Ahmad amesema: Inaruhusiwa kukusanya kwakuchelewesha (taakhiri) na wala si kwa kutanguliza(taqdiim). Kauli hii ndio chaguo la Ibnu Hazm nayo ime-

6

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 6

Kukusanya Sala mbili

7

pokewa toka kwa Malik.

Hizi ndizo kauli sita: Hivyo ikiwa suala kwa ufupiwamekubaliana wote isipokuwa wachache kama ulivy-owaona, basi ni lazima tujadili suala hili sehemu mbili:

Je? Kukusanya kunamhusu tu yule mwenye haraka nasafari.

Je? Inaruhusiwa kukusanya kwa kuchelewesha tu walahakujumuishi kukusanya kwa kutanguliza?

Ama sehemu ya kwanza tunasema, habari zinazoonyeshakitendo cha Mtume (s.a.w.w) ziko katika makundi maw-ili: Kundi moja linaweka wazi kuwa alikuwa akikusanyaawapo na haraka na safari, au aharakishwapo na safari:

Ameandika Muslim toka kwa Nafiu toka kwa Ibnu Umarkuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akikusanyakati ya Magharibi na Isha awapo na haraka na safari.4

4 Sahih Muslim, Juz. 2, uk. 150 Kitabu cha Sala. Mlango: Ruhusa yakukusanya Sala mbili safarini. Mlango wa Sala.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 7

Kukusanya Sala mbili

8

Ametoa Muslim toka kwa Salim, toka kwa baba yake:“Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akikusanyakati ya Magharibi na Isha awapo na haraka na safari."

Ametoa Muslim toka kwa Salim bin Abdallah kuwa babayake alisema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Munguanapokuwa na haraka ya safari, akichelewesha Sala yaMagharibi mpaka anapokuja kuikusanya na Sala ya Isha.”5

Ametoa Muslim toka kwa Anas toka kwa Mtume kuwaaharakishwapo na safari huchelewesha Adhuhuri mpakamwanzo mwa wakati wa Al-Asr hivyo huzikusanyapamoja, na huchelewesha Magharibi mpaka anapokujakuikusanya na Isha pindi mawingu mekundu yanapoza-ma.6

Kundi la pili linaonyesha kitendo cha Mtume waMwenyezi Mungu bila sharti lolote (iwapo ana haraka nasafari).5 Sahih Muslim, Juz. 2, uk. 150 Kitabu cha Sala. Mlango: Ruhusa yakukusanya Sala mbili safarini. Mlango wa Sala.6 Sahih Muslim Juz. 2 Uk. 151 Kitabu cha Sala. Mlango: Ruhusa yakukusanya Sala mbili safarini. Mlango wa Sala

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 8

Kukusanya Sala mbili

9

Ametoa Muslim toka kwa Anas bin Malik amesema:“Iwapo Mtume akianza safari kabla ya kupinduka juaalikuwa akichelewesha Adhuhuri mpaka wakati wa Al-Asr, kisha hushuka na kuzikusanya pamoja. Na iwapo jualitapinduka kabla ya safari, basi huswali Adhuhuri kishahupanda kipando. 7

Ametoa Muslim toka kwa Anas amesema: “IlikuwaMtume akitaka kukusanya kati ya Sala mbili safarini basihuchelewesha Adhuhuri mpaka mwanzoni mwa wakatiwa Al-Asr kisha huzikusanya pamoja. 8

Abu Daud na Tirmidhy wamepokea toka kwa Maadh binJabal kuwa: “Mtume alikuwa katika vita vya Tabukanapotaka kusafiri kabla ya kupinduka kwa juaakachelewesha Adhuhuri mpaka akaja kuikusanya na Al-Asr pamoja, na anapotaka kusafiri baada ya kupindukajua, huswali Adhuhuri na Al-Asr pamoja kisha huondoka,na ilikuwa akitaka kuondoka kabla ya Magharibi,7 Sahih Muslim, Juz. 2, Uk. 151 Kitabu cha Sala. Mlango: Ruhusa yakukusanya Sala mbili safarini. Mlango wa Sala

8 Sahih Muslim, Juz. 2 Uk. 151 Kitabu cha Sala. Mlango: Ruhusa yakukusanya Sala mbili safarini. Mlango wa Sala

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 9

Kukusanya Sala mbili

10

huichelewesha Magharibi mpaka aiswali na Isha pamoja,na ilikuwa akitaka kuondoka baada ya Magharibi huitan-guliza Isha na kuiswali na Magharibi pamoja. 9

Ahmad amepokea ndani ya Musnad yake toka kwaAbbas` (r.a.) toka kwa Mtume kuwa Mtume akiwa nasafari alikuwa kabla ya kupanda kipando hukusanya Salaza Adhuhuri na Al-Asr iwapo jua limepinduka akiwanyumbani kwake.

Na iwapo halijapinduka akiwa nyumbani kwake, basihuondoka mpaka unapofika wakati wa Al-Asr ndipohushuka kisha hukusanya Adhuhuri na Al-Asr. Na iwapoMagharibi itaingia akiwa nyumbani kwake basi huku-sanya Magharibi na Isha pamoja, na iwapo Magharibi hai-jaingia akiwa nyumbani kwake huondoka mpaka Ishainapoingia ndipo hushuka na kuzikusanya pamoja.10

9 Sunan Abi Daud: Juz. 2, uk. 8 Kitabu cha Sala mlango: KukusanyaSala mbili. Hadithi ya 1220

10 Musnad Ahmad bin Hambal: Juz 5 Uk. 241, Sunan Abi Daud: Juz.2, uk. 2 kitabu cha Sala mlango: Kukusanya kati ya Hadithi mbili1220

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 10

Kukusanya Sala mbili

11

Baada ya As-Shaukany kunukuu riwaya hii akasema:Shafy amepokea riwaya hii katika Musnad yake kwanamna yake akasema: “Na akiondoka kabla jua halijapin-duka huchelewesha Adhuhuri mpaka aje aikusanye na Al-Asr wakati wa Al-Asr.”11

Nasema: Kanuni ni kuchukuwa chenye sharti maalumu nakukitanguliza kabla ya kisicho na sharti maalumu, hivyokuziwekea riwaya zisizo na sharti maalum lile shartimaalum lililomo kwenye riwaya zenye sharti maalumu,ndio maana hata Anas kanukuu kitendo cha Mtume bilaya kuwa na sharti maalumu na mara nyingine kikiwa nasharti maalumu. 12

Naongeza kuwa riwaya zinazoonyesha kitendo chaMtume ni dalili ya ufahamu si tamko la Mtume, na sualalinapokuwa hivi linakuwa halina sifa ya kuwa aukutokuwa sharti, kwa sababu hali hii ya kuwa aukutokuwa sharti ni hali ya tamko si ya kitendo, na wala

11 Naylul-Awtwar: Juz. 3, Uk. 21312 Bidayatul-Mujtahid: Juz. 1, Uk. 173 Chapa nyingine iliyohakiki-wa: Juz. 2, Uk. 374.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 11

Kukusanya Sala mbili

12

katika suala hili hakuna tamko lolote lililopokewa tokakwa Mtume bali ni kitendo alichokinukuu mpokezi, nahuenda kitendo chake hiki kilikuwa kimekutana na hali yakuwa na haraka na safari, na ikawa mpokezi hakutaja halihii kwa kutegemea kuwa haihusiki na hukumu.

Kutokana na haya maelezo hakusanyi isipokuwaanapokuwa na haraka na safari. Na inawezekana ndiloaliloliashiria Ibnu Rushdi aliposema: “Kukusanyakumenukuliwa kwa kitendo tu.” 13

Na kinachoweza kuipa nguvu kauli ya pili (bila shartimaalum) ni kuwa sharti lililopo katika riwaya hizi (iwapoana haraka na safari) ni miongoni mwa mashartiyatokanayo na hali ya mara kwa mara, masharti ambayohuwa hayafahamiki kama sharti, hiyo ni mfano wa kauliya Mwenyezi Mungu: “Na binti zenu wa kambo waliokatika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenumliowaingilia”14 Hakika binti wa kambo ameharamish-

13 Bidayatul-Mujtahid: Juz. 1, Uk. 173 Chapa nyingine iliyohakiki-wa: Juz.2 Uk. 37414 Nisaa; 4: 23

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 12

Kukusanya Sala mbili

13

wa, sawa awe katika ulinzi wa mwanaume au hapana,lakini mara nyingi mwanamke anapoolewa huenda nabinti yake kwa mume wa pili. Kwa ajili hiyo binti yeyotewa kambo ni haramu bila sharti lolote sawa awe katikaulinzi wa mwanaume au hapana.

Kukusanya Sala mbili pasipo na safari kwaajili ya udhuru

Jambo lililo mashuhuri ni kuwa inaruhusiwa kukusanyakati ya Magharibi na Isha kwa ajili ya udhuru kinyume naHanafiyya ambao hawajaruhusu kukusanya kwa hali yoy-ote ile isipokuwa msimu wa Hijja uwapo Arafa auMuzdalifa.

Ama wanaoruhusu kukusanya nao wametofautiana kwanamna zifuatazo:

Je ruhusa inahusu mvua tu au inajumuisha udhurumwingine?

Je ruhusa inahusu Magharibi na Isha au inajumuishaAdhuhuri na Al-Asr?

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 13

Kukusanya Sala mbili

14

Je ruhusa inahusu kukusanya kwa kutanguliza tu au ina-jumuisha kukusanya kwa kuchelewesha?15

Yafuatayo ni maneno yao kuhusu sura hizo tatu:Ya kwanza: Dhahiri toka kwa Shafy ni kuwa ruhusainahusu mvua tu.

As-Shiraziy amesema: “Inaruhusiwa kukusanya Salambili katika hali ya mvua. Hairuhusiwi kukusanya kwaajili ya hali ya upepo mkali, tope, ugonjwa na giza."16

(1). Ibnu Rushdi amesema: “Shafi ameruhusu kukusanyausipokuwa safarini kwa ajili ya mvua, - mpaka aliposema- ama kukusanya kwa ajili ya ugonjwa usipokuwa safari-ni ni kuwa Malik ameruhusu iwapo atahofia kuzimia auana ugonjwa wa tumbo, lakini Shafy kakataza hilo.17

(2). Akasema ndani ya kitabu As-Sharhul-Kabiru kuwa:Na je ni ruhusa hilo - kinyume na mvua - kwa ajili ya tope15 Tuliyoyataja ni vichwa vya tofauti zao, lakini matawi yake nimengi hatuna haja ya kuyaingilia16 Al-Majmuu: Juz. 4, Uk. 258, Kifungu cha matni17 Bidayatul-Mujtahid: Juz. 1, Uk. 173-174 mahali pawili

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 14

Kukusanya Sala mbili

15

na upepo mkali wenye baridi, au kwa mwenye kuswalianyumbani au msikitini huku njiani kuna mvua nyingi.18

Ya pili: Yaani je ruhusa inahusu Magharibi na Isha tu auinajumuisha Adhuhuri na Al-Asr? Ibnu Rushdi amesema:“Shafy ameruhusu kukusanya usipokuwa safarini kwaudhuru wa mvua usiku au mchana, ama Malik yeyeameruhusu usiku akakataza mchana.19

An-Nawawy amesema: “Shafy na jamaa wamesemainaruhusiwa kukusanya Adhuhuri na Al-Asr, Magharibina Isha katika hali ya mvua. Imam wa haramaini akaelezakuwa inaruhusiwa kukusanya Magharibi na Isha wakatiwa Magharibi, wala hairuhusiwi kati ya Adhuhuri na Al-Asr, na haya ndio madhehebu ya Malik.

Al-Mazny amesema: “Hairuhusiwi kwa hali yoyote.Madhehebu ya kwanza ndiyo yanayotokana na maelezoya Shafy, ya zamani hadi mapya.”20

18 Al-Mughni, Juz. 2, Uk. 11819 Bidayatul-Mujtahid, Juz. 1, Uk. 17320 Al-Majmuu: Juz. 4, Uk. 260

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 15

Kukusanya Sala mbili

16

Ya tatu: Yaani ruhusa inahusu kukusanya kwa kutangulizabila kujumuisha kukusanya kwa kuchelewesha.

A-Shirazy amesema: “Ni ruhusa kukusanya Sala mbilikatika hali ya mvua katika wakati wa Sala za kwanza, naje inaruhusiwa kuzikusanya katika wakati wa Sala zapili?" Hapa kuna kauli mbili: Shafy amesema ndani yaAl-Imlau: “Inaruhusiwa kwa sababu ni udhuruunaoruhusu kukusanya katika wakati wa Sala ya mwanzohivyo ikaruhusiwa kukusanya katika wakati wa Sala yapili kama kukusanya kwa safarini.

Akasema katika Al-ummu: “Hairuhusiwi kwa sababuiwapo akichelewesha huenda mvua ikakatika hivyoakawa kakusanya bila udhuru."21

Huu ni ufupi wa kauli katika nukta hizi tatu. Pia wao wanatofauti katika sehemu nyingine ambazo hakuna haja yakuzitaja.

Baada ya kutambua hilo la muhimu ni kuwepo dalili juuya ruhusa ya kukusanya kwa udhuru usipokuwa safarini. 21 Al-Majmuu: Juz, 4. Uk. 258

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 16

Kukusanya Sala mbili

17

Wamethibitisha hilo kwa Hadithi mbili: Inayoonyesha kuwa inaruhusiwa kukusanya usipokuwasafarini katika hali yoyote ile, hivyo wakaichukulia katikahali ya mvua au udhuru wowote ule. Bukhari ametoa tokakwa Ibnu Abbas` (r.a.) kuwa Mtume aliswali Madinarakaa saba na rakaa nane, yaana Adhuhuri na Al-Asr,Magharibi na Isha.22 Ibnu Rushdi amesema: “Amakuhusu kukusanya usipokuwa safarini bila udhuruwowote ni kuwa Malik na wanazuoni wengi hawaruhusu,lakini hilo limeruhusiwa na wengi kati ya kundi la dhahirina Ash’habu ambaye ni kati ya wafuasi wa Malik. Sababukubwa ya kutofautiana kwao ni tofauti yao kuhusu ufa-hamu wa Hadithi ya Ibnu Abbas`, hivyo wapo waliy-oitafsiri kuwa ilikuwa ni katika hali ya mvua kamaalivyosema Malik, na wapo walioichukulia kuwa ni haliyoyote.

Aliyoipokea Ibnu Abbas` kuwa Mtume alikusanyaAdhuhuri na Al-Asr na kati ya Magharibi na Isha Madinabila ya hofu, safari wala mvua. Akaulizwa Ibnu Abbas:Alitaka nini katika hilo? Akasema: “Alitaka asiutaabishe22 Katika sura ya nne utaona vyanzo vya riwaya hizi.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 17

Kukusanya Sala mbili

18

umma wake.”23

Dhahiri inaonyesha kuwa kukusanya wakati wa hali yamvua ni jambo lililokuwa linajulikana kabla, ndio maanaIbnu Abbas` alijaribu kubainisha kuwa kukusanya hukuhakukuwa ni kwa lengo la mvua au nyudhuru nyinginebali ilikuwa ni msamaha kwa lengo la kutokuutaabishaumma wake. Hivyo ikiruhusiwa kukusanya katika haliisiyo ya safari kwa udhuru wowote, basi kukusanyasafarini bila udhuru wowote itakuwa ni hiyari kati yahukumu za safari. Kwa sababu msafiri atakusanya Salambili safarini bila udhuru.

Ama yule asiye safarini yeye atakusanya kwa ajili yaudhuru au kwa lengo lingine. Ama tukisema kuwainaruhusiwa kukusanya bila udhuru wowote usipokuwasafarini, basi haitakuwa kukusanya kati ya Sala mbili nikati ya hukumu za safari.

Mpaka hapa maneno yametimia kuhusu sura ya tatu,hivyo imebakia sura ya nne.

23 Katika sura ya nne utaona vyanzo vya riwaya hizi.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 18

Kukusanya Sala mbili

19

Kukusanya Sala mbili bila udhuru pasipo safari

Imamiyya wameafikiana kuwa inaruhusiwa kukusanyaSala mbili bila ya udhuru wowote pasipo safarini,japokuwa kutenganisha ni bora.

Sheikh Tusi amesema: “Inaruhusiwa kukusanya Salambili kati ya Adhuhuri na Al-Asr na kati ya Magharibi naIsha, uwapo safarini au usipokuwa safarini na katika haliyoyote ile. Wala hakuna tofauti kati ya kukusanya wakatiwa Sala ya mwanzo au wakati wa Sala ya pili. Kwasababu wakati wa baada ya kupinduka jua ni wakati wakushirikiana, na wakati wa baada ya Magharibi ni wakatiwa kushirikiana pia kama tulivyobainisha.24

Hakika upande wa madhehebu ya Imamiyya haina maanakuwa kukusanya Sala mbili ni kuiswali Sala nje ya wakatiwake wa kisheria, bali muradi wake ni kuiswali katikamuda usiyo wa ubora. Hivyo ufuatao ni ufafanuzi wa

24 Al-Khilafu: Juz. 1 Uk. 588 mas'ala ya 351 Huko mbele utaona jinsiwakati ulivyobainishwa

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 19

Kukusanya Sala mbili

20

madhehebu yenyewe: Kutokana na maelezo toka kwa Maimamu wa Ahlul-BaytImamiyya wamesema kuwa jua likipinduka basi umeingiawakati wa Sala mbili, yaani wakati wa Adhuhuri na Al-Asr, isipokuwa Sala ya Adhuhuri huswaliwa kabla ya Al-Asr, hivyo wakati uliyopo kati ya kupinduka jua na kuza-ma kwake ni wakati wa kushirikiana kati ya Sala mbilihizo.

Isipokuwa muda wa kutosha rakaa nne kabla ya kuzamakwa jua ni muda mahususi kwa ajili ya Sala ya Adhuhuri,na muda wa kutosha rakaa nne mwishoni mwa wakati niwakati mahususi kwa ajili ya Sala ya Al-Asr, na mudauliyopo kati ya nyakati hizo mbili ni wakati wakushirikiana kati ya Sala mbili.

Hivyo akiswali Sala ya Adhuhuri na Al-Asr katika mudawowote kati ya kupinduka jua na kuzama kwake atakuwakaswali Sala hizi ndani ya wakati wake, kwa sababu niwakati wa kushirikiana kati ya Sala mbili hizo.

Isipokuwa muda wa kutosha kuswali rakaa nne tokamwanzo wa wakati ni mahususi kwa ajili ya Adhuhurihivyo haisihi kuswali Al-Asr humo.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 20

Kukusanya Sala mbili

21

Na muda wa kutosha kuswali rakaa nne mwishoni mwawakati ni mahususi kwa ajili ya Al-Asr hivyo haisihikuswali Adhuhuri humo.

Hii ndio hali halisi ya madhehebu, kwa ajili hiyo mwenyekukusanya Sala mbili nje ya wakati mahususi ame-tekeleza faradhi ndani ya wakati wake, hivyo Sala yakeinakuwa ni kutekeleza (ndani ya wakati) na wala si kuli-pa.

Hivyo ni kuwa kila Sala ukiachilia mbali wakati wake wakusihi bado ina wakati wake wa ubora. Hivyo wakati waubora wa Sala ya Adhuhuri ni kuanzia kupinduka kwa juampaka kivuli cha kitu kilichosimama kufikia urefu wakipimo cha kitu chenyewe, baada ya kile kivuli chamwanzo cha kabla ya kupinduka jua kuwa kimeondoka aukimetoweka.

Na mashuhuri ni kuwa wakati wa ubora wa Al-Asr nikuanzia pale kivuli kinapolingana na kipimo mpaka palekinapokuwa mara mbili ya kipimo husika.

Kwa wakati wa Magharibi na Isha hujulikana kuwa lik-izama jua zimeingia nyakati mbili mpaka nusu ya usiku.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 21

Kukusanya Sala mbili

22

Wakati wa mwanzo ni mahususi kwa ajili ya Magharibikwa muda wa kutimiza Sala nzima, na wakati wa mwishoni mahususi kwa Isha kwa muda wa kutimiza Sala nzima,na wakati uliyopo kati ya muda huo ni wakati wakushirikiana.

Hivyo kila Sala kati ya Sala mbili hizi ina wakati waubora. Wakati wa ubora wa Magharibi ni kuanzia kuzamakwa jua mpaka kuondoka kwa wekundu wa Magharibi, nawakati wa ubora wa Isha ni kuanzia kuondoka kwawekundu wa Magharibi mpaka theluthi ya usiku.25

Mara nyingi anayewashangaa Imamiyya kukusanya katiya Sala mbili hudhani kuwa mwenye kukusanya huswalimoja ya Sala mbili nje ya wakati wake, lakini amesahaukuwa mwenye kuswali huwa ameiswali nje ya wakati waubora lakini huwa ameiswali ndani ya wakati wa kusihi,na wala si ajabu Sala kuwa na nyakati tatu.

Ya kwanza: Wakati mahususi ni ule wa kutosha rakaa nnemwanzoni mwa kuingia wakati, na wakati wa mwisho ni

25 Angalia Al-Ur'watul-Wuthqa: Uk. 171. Kipengele cha nyakati zaSala

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 22

Kukusanya Sala mbili

23

pale unapokaribia kwisha wakati. Au rakaa tatu baada tuya kuzama jua na rakaa nne kabla kidogo ya nusu yausiku.

Ya pili: Wakati wa ubora ambao tayari maelezo yakeyameshatangulia kuhusu Adhuhuri na Al-Asr, Magharibina Isha.

Ya tatu: Wakati wa kusihi ambao ni wakati wote uliyopokati ya vipimo viwili isipokuwa ule tu uliyo mahususikwa moja ya Sala mbili, hivyo wakati wa kusihi unaju-muisha wakati wa ubora na ule wa baada ya ubora.

As-Swaduq amepokea kwa isnadi yake toka kwa Zararatutoka kwa Abu Jafar (a.s.) alisema: “Jua likipindukaumeingia wakati wa Sala mbili: Adhuhuri na Al-Asr. Najua likizama umeingia wakati wa Sala mbili: Magharibina Isha ya mwisho.”26

Shekhe Tusi amepokea toka kwa Ubaydu bin Zararatualisema: “Nilimuuliza Aba Abdillah kuhusu wakati wa

26 Al-Faqihi: Juz. 1 Uk. 140. Pia inapatikana kwenye Hadithi ya 1mlango wa 17

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 23

Kukusanya Sala mbili

24

Adhuhuri na Al-Asr. Akajibu: “Jua likipinduka umeingiawakati wa Adhuhuri na Al-Asr isipokuwa hii inakuwakabla ya hii, kisha wewe unakuwa katika wakati ambao niwa sala zote mbili mpaka jua lizame.”27

Riwaya zenye maana hii ni nyingi lakini sisi tunaishiahapa. Hivyo ikiwa Sala zina nyakati tatu kama tulivy-obainisha basi inatubainikia kuwa kukusanya si jambobaya isipokuwa kinachokupita ni wakati wa ubora wala siwakati asili wa Sala, kwa ajili hiyo imepokewa toka kwaMaimamu wa Ahlul-Bayt kuwa kutenganisha ni borakuliko kukusanya, hivyo hapa tutataja baadhi ya riwayazinazoruhusu kukusanya ili tupate baraka tu kwani sualahili kwenye fiqhi ya shia Imamiyya ni suala la wazi sana.

Amepokea As-Saduqu toka kwa Abdallah bin Sanani tokakwa Swadiq (a.s.) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungualikusanya Adhuhuri na Al-Asr kwa adhana moja naiqama mbili, na akakusanya Magharibi na Isha kwaadhana moja na ikama mbili, bila ya kuwa safarini na bilaya udhuru wowote.28

27 At-Tahadhibu: Juz. 2, uk. 2628 Al-Faqihi: Juz. 1, Uk. 186 namba 886

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 24

Kukusanya Sala mbili

25

Pia amepokea toka kwa Is'haqa bin Ammar toka kwa AbaAbdillah alisema: “Hakika Mtume aliswali Adhuhuri naAl-Asr sehemu moja bila ya udhuru wala sababu yoyote.Umar akauliza: “Je kuna kitu kimezuka ndani ya Sala?”Akajibu: “Hapana isipokuwa nimetaka kuupa nafuuumma wangu.”29

Kulayny ametoa toka kwa Zararatu toka kwa AbaAbdillah amesema: “Mtume aliwaswalisha watu jamaaAdhuhuri na Al-Asr baada ya kupinduka jua bila ya udhu-ru wowote, na aliwaswalisha jamaa Magharibi na Ishakabla ya kuondoka wekundu wa Magharibi bila ya udhu-ru wowote, hakika alifanya hivyo ili aupe umma wakenafuu ya wakati.30

Na kuna riwaya nyingi ambazo amezikusanya shekhe Al-Hurru AlAamily ndani ya kitabu chake Wasailul-Shia. 31

Mpaka hapa umebainika mtazamo wa Shia Imamiyyakuhusu kukusanya Sala mbili.29 Ilalul-Sharaiu: 321 mlango wa 1130 Al-Kafiy: Juz. 3 Uk. 286 Hadithi ya 131 Al-Wasailu: Juz.4 Uk. 220-223 mlango wa 32 kati ya milango yanyakati.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 25

Kukusanya Sala mbili

26

Mgawanyo wa nyakati ndani ya Fiqhi yaKisunni

Huenda mtu asiyejua akadhani kuwa mgawanyo huu wanyakati unahusu fiqhi ya Imamiyya tu, bali ni kuwamgawanyo huu wa nyakati katika aina tatu unahusu fiqhizote mbili japokuwa kunatofauti kuhusu muda wa wakati. Ndani ya Sharhul-Muhadhabu An-Nawawiy amesema:“Tawi: Adhuhuri ina nyakati tatu: Wakati wa ubora,wakati wa hiyari na wakati wa udhuru, hivyo wakati waubora ni mwanzoni mwa wakati, na wakati wa hiyari nibaada ya wakati wa ubora mpaka mwisho wa wakati, nawakati wa udhuru ni wakati wa Al-Asr kwa mwenye hakiya kukusanya kwa ajili ya safari au mvua.”

Kisha akasema: Al-kadhi Huseini amesema: “Adhuhuriina nyakati nne: Wakati wa ubora, wakati wa hiyari,wakati wa ruhusa, na wakati wa udhuru. Hivyo wakati waubora ni pale kivuli cha kitu kilichosimama kitakapofikiarobo ya kipimo cha kitu hicho, na wakati wa hiyari nikitakapofikia nusu yake, na wakati wa ruhusa nikitakapolingana kivuli na hicho kitu na hapo ndio mwisho

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 26

Kukusanya Sala mbili

27

wa wakati. Na udhuru ni wakati wa Al-Asr kwa mwenyekukusanya kwa ajili ya safari au mvua. 32

Anayeafikiana na Imamiyya katika baadhi ya nukta

Pia wapo wanaoafikiana na Imamiyya katika baadhi yanukta za suala hili.

An-Nawawy amenukuu kwa kusema: Atwau na Tausiwamesema: “Kivuli cha kitu kikilingana na kituchenyewe hapo umeingia wakati wa Al-Asr na ufuatao niwakati wa Adhuhuri na Al-Asr kwa kushirikiana mpakajua litakapozama.

Kauli hii inahusu Adhuhuri kwa kivuli cha kitu kulinganana kitu husika, kisha inafanya wakati uliobaki ni wakushirikiana Adhuhuri na Al-Asr mpaka jua litakapoza-ma. Kauli hii inakaribiana na ile ya Imamiyya.

32 Al-Majmuu Juz.3 Uk. 27

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 27

Kukusanya Sala mbili

28

Malik amesema: “Kivuli kikilingana na kipimo cha kitukilichosimama ndio mwisho wa wakati wa Adhuhuri namwanzo wa wakati wa Al-Asr kwa kushirikiana. Hivyokivuli kikizidi kipimo ziada ya wazi basi wakati waAdhuhuri umekwisha.33

Kauli hii inafanya sehemu ya wakati kuwa wakati wakushirikiana kati ya Adhuhuri na Al-Asr nao ni - baada yakivuli kulingana na kipimo cha kitu kilichosimama -mpaka kivuli kinapokizidi kipimo hicho kwa ziada yawazi, ni wakati wa kushirikiana kati ya Adhuhuri na Al-Asr.

Pia imenukuliwa toka kwake kuwa, wakati wa Adhuhuriunaendelea mpaka kuzama kwa jua.34

Na kuna kauli nyingine ambazo zina namna fulani yamuafaka na fiqhi ya Imamiyya.

33 Al-Majmuu, Juz. 3, Uk. 2434 Al-Majmuu, Juz. 3, Uk. 27

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 28

Kukusanya Sala mbili

29

Masunni wanaoafikiana na Imamiyya katikakila kitu kuhusu suala hili

Japokuwa kukusanya Sala bila udhuru ni kati ya mamboya wazi katika fiqhi ya Imamiyya lakini suala hili simahususi kwa Imamiyya peke yao bali kuna baadhi yawanazuoni wa sheria wa kisunni wameafikiana nao kati-ka suala hili.

Ibnu Rushdi amesema: “Ama kukusanya bila udhuruusipokuwa safarini hakika Malik na wanazuoni wengi washeria hawaruhusu, lakini wameruhusu hilo baadhi yajamaa katika watu wa Dhahir na Ash'habu katika wafuasiwa Malik. Na sababu ya kutofautiana kwao ni tofauti yaokuhusu kuifahamu hadith ya Ibnu Abbas, hivyo wapowalioifafanua kuwa ilikuwa kwa sababu ya safari, nawapo walioichukulia katika hali yoyote ile.

Muslim katika Hadithi yake ameondoa kauli: ‘Bila yahofu wala safari wala mvua.’ Hili ndilo waliloshikiliawatu wa Dhahir.35

35 Bidayatul-Mujtahid, Juz. 2, Uk. 374 chapa iliyohakikiwa

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 29

Kukusanya Sala mbili

30

An-Nawawy amesema: Tawi: “Kuhusu madhehebu yaokuna kukusanya bila hofu, safari, mvua, wala ugonjwa.Madhehebu yetu (ya Shafy) na madhehebu ya AbuHanifa, Malik, Ahmad, na jamuhuri ni kuwa hairuhusiwi. Ibnu Al-Mundhir ameelezea kuhusu kundi linaloruhusubila udhuru wowote. Akasema: Ibnu Sirin ameruhusu kwaajili ya haja maalum au asipochukulia kama mazoea.36

Kwa namna yoyote ile la muhimu ni dalili si kauli, hivyoiwapo kauli zitaafikiana na dalili basi ni vizuri, na kamasi hivyo basi marejeo ya mwisho ni dalili.

Kukusanya Sala mbili kwa mujibu wa Kitabu(Qur’an)

Mwenyezi Mungu amesema: “Simamisha Sala jualinapopinduka, mpaka giza la usiku na Qur'ani yaalfajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa” 37

Aya imebeba jukumu la kubainisha nyakati za Sala tano,hivyo iwapo tukisema makusudio ya giza la usiku ni nusu

36 Al-Majumuu, Juz. 4, Uk. 26437 Israa; 17:78

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 30

Kukusanya Sala mbili

31

ya usiku basi wakati uliyopo kati ya kupinduka kwa jua nagiza la usiku utakuwa wa Sala nne, isipokuwa dalili ime-onyesha kuwa wakati wa Adhuhuri na Al-Asr unakomeakwa kuzama jua, hivyo wakati uliopo kati ya kupindukajua na kuzama jua ni wakati wa kushirikiana kati yaAdhuhuri na Al-Asr. Kama inavyokuwa wakati uliyopokati ya kuzama kwa jua mpaka kuingia giza la usiku niwakati wa kushirikiana kati ya Magharibi na Isha. Na huenda mtu akafasiri giza la usiku kwa maana yakuzama jua, hivyo Aya itakuwa imebeba jukumu lakubainisha wakati wa Adhuhuri, Al-Asr na Sala ya alfajiribila kubainisha Magharibi na Isha. Na maarufu ni tafsiriya mwanzo.

At-Tabarasiy amesema: “Katika Aya hii kuna dalili ionye-shayo kuwa wakati wa Sala ya Adhuhuri umerefushwampaka mwisho wa mchana, kwa sababu MwenyeziMungu alifanya wakati wa kuanzia kupinduka kwa juaambako ndio kugeuka mpaka giza la usiku ni wakati waSala nne, isipokuwa Adhuhuri na Al-Asr zinashirikianakatika wakati mmoja nao ni kuanzia kugeuka kwa juampaka kuzama kwake.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 31

Kukusanya Sala mbili

32

Na Magharibi na Isha zinashirikiana katika wakati mmojanao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka giza la usiku. NaSala ya alfajiri ameitenganisha kwa kusema: ‘Na Qur'aniya alfajiri’, hivyo Aya inabainisha wajibu wa Sala tanohuku ikibainisha nyakati zake.38

Tuliyoyataja ndio maelezo aliyoyatoa Imam Al-Baqir(a.s.) aliposema: “Mwenyezi Mungu alimwambia Mtumewake: ‘Simamisha Sala jua linapopinduka mpaka giza lausiku.’ Hizi ni Sala nne alizozipa majina MwenyeziMungu, akazibainisha na kuziwekea nyakati. Na giza lausiku ni nusu ya usiku. Kisha Mwenyezi Mungu akasema:‘Na Qur'ani ya alfajiri, hakika Qur'ani ya alfajiriinashuhudiwa,’ hii ni Sala ya tano.”39

As-Sadiq (a.s.) amesema: “Ndani ya Aya hiyo kuna Salambili mwanzo wa wakati wake ni kupinduka kwa juaisipokuwa hii ni kabla ya hii. Na kuna Sala mbili mwan-zo wa wakati wake ni kuzama kwa jua mpaka nusu yausiku isipokuwa hii ni kabla ya hii.”

38 Maj'maul-Bayan, Juz. 3, Uk. 43439 Nuru-Thaqalain, Juz. 3, Uk. 202 Hadith ya 377

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 32

Kukusanya Sala mbili

33

Al-Qurtuby amesema: “Kuna watu wameona kuwawakati wa Sala ya Adhuhuri unaanzia kupinduka kwa juampaka kuzama kwake, kwa sababu Mwenyezi Munguameuweka wajibu wake kutegemeana na kupinduka kwajua na wakati wote huu ni kupinduka kwa jua. Kauli hiikaisema kwa upana Al-Awzay na Abu Hanifa. Ama Malikna Shafy wenyewe wameashiria kauli hii wakati wadharura.40

Ar-Raziy amesema: “Laiti tukitafsiri giza la usiku kwamaana ya kuingia kwa giza la mwanzo, basi ibara giza lausiku itamaanisha mwanzo wa Magharibi, kwa maana hiinyakati zilizotajwa na Aya zitakuwa tatu: Wakati wakupinduka kwa jua, wakati wa kuanza Magharibi nawakati wa alfajiri.”

Akasema: “Hili linapelekea kupinduka kwa jua kuwe niwakati wa Adhuhuri na Al-Asr hivyo wakati huu unakuwani wa kushirikiana kati ya hizi Sala mbili.

Na mwanzo wa Magharibi uwe ni wakati wa Magharibina Isha, hivyo uwe ni wakati wa kushirikiana kati ya hizi40 Al-Jamiu-liah'kamil-Qur'ani, Juz. 1, Uk. 304

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 33

Kukusanya Sala mbili

34

Sala mbili. Hii inapelekea kuruhusiwa kukusanya katikahali yoyote ile kati ya Adhuhuri na Al-Asr Magharibi naIsha, isipokuwa dalili inaonyesha kuwa kukusanya bilaudhuru pasipo na safari hairuhusiwi, hivyo ikalazimikairuhusiwe kukusanya kwa ajili ya udhuru wa safari, mvuana udhuru mwingine.”41

Aliyoyahakiki Ar-Razi katika mada hii ni ukweli mtupu,lakini kuiacha kwake haki kwa hoja ya: ‘Hakika kuku-sanya bila udhuru wowote pasopo na safari hairuhusiwikwa kuwa kuna dalili juu ya hilo,’ ni dhana tu.

Ni dalili ipi iliyopo inayokataza kukusanya bila udhuruwowote, je, dalili ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu? HukuKitabu kwa mujibu wa uhakiki wake kinaruhusu kuku-sanya. Au ni Sunna? Baada ya muda utaona jinsi maelezoya Sunna yanavyoruhusu.

Lakini pia umeshajua jinsi Masunni walivyosema kuwainaruhusiwa, zaidi ya hapo ni kuwa Maimamu wa Ahlul-Bayt nao wameruhusu. Hivyo baada ya Kitabu, Sunna naijmai hakuna hoja nyingine kama ilivyo ‘baada ya Abadan41 Tafsirul-Kabir, Juz. 12, Uk. 27

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 34

Kukusanya Sala mbili

35

hakuna kijiji kingine.’42

Kukusanya Sala mbili bila udhuru usipokuwasafarini kwa mujibu wa Sunna

Kuna riwaya nyingi zinazodhihirisha haki kuhusu ruhusaya kukusanya Sala mbili bila udhuru pasipokuwa safarini,riwaya hizo zimepokewa na waandishi wa Sahih sita,Sunan na Masanidi. Hivyo tuanze aliyopokea Muslimkwa sanadi na tamko kisha twende kwenye yale waliy-onukuu wengine.

1. Ametuhadithia Yahya mwana wa Yahya amesema:Nilisoma kwa Malik toka kwa Zuberi toka kwa Said binJubair toka kwa Ibnu Abbas alisema: ‘Mtume aliswaliAdhuhuri na Al-Asr pamoja, Magharibi na Isha pamojabila ya hofu wala safari.”42 Mara ngapi Imam Ar-Razi amehakiki na kuongea lile lililo hakiambalo yeye mwenyewe anastahiki kulifuata lakini huliacha kwahoja ya kipuuzi. Angalia aliyoyahakiki kuhusu kupaka miguu miwilikatika tafsiri ya: “Na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpakavifundoni.” Na yale aliyozungumza kuhusu makusudio ya “Wenyemamlaka katika ninyi” katika tafsiri ya Aya: “Mtiini MwenyeziMungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi". Na sehe-mu nyingine kama hizi.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 35

Kukusanya Sala mbili

36

2. Ametusimulia Ahmad bin Yunus na Aun bin Salamwote toka kwa Zuhayri, Ibnu Yunus alisema:“Ametusimulia Zuhayri, ametusimulia baba Zuberi tokakwa Saidi bin Jubair toka kwa Ibnu Abbas` alisema:‘Mtume aliswali Adhuhuri na Al-Asr pamoja Madina pasina hofu wala safari.’ Baba Zuberi akasema: ‘NikamuulizaSaid, kwa nini alifanya hivyo? Akajibu: Nilimuuliza IbnuAbbas kama ulivyoniuliza akasema: ‘Alitaka asimpetaabu yeyote katika umma wake.'”

3. Ametusimulia Abu Bakr bin Abi Shaybat na AbuKuraybi wamesema: Ametusimulia Abu Muawiya naametusimulia Abu Kuraybi na Abu Said Al-Ashaju(tamko ni la Abu Kuraybi) walisema: ‘Alitusimulia Wakiuwote kutoka kwa Al-A’amash toka kwa Habibu bin AbiThabit, toka kwa Said bin Jubairi toka kwa Ibnu Abbasalisema: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu alikusanyaAdhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha Madina pasi nahofu wala mvua.’

Katika hadith ya Wakiu amesema: Nikamwambia IbnuAbbas: Kwanini alifanya hivyo? Akasema: Ili asiupetaabu umma wake. Katika Hadithi ya Abu Muawiya nikuwa Ibnu Abbas` aliambiwa: Alitaka nini katika hilo?

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 36

Kukusanya Sala mbili

37

Akasema: Ili asiupe taabu umma wake.

Ametusimulia Abu Bakr bin Shaybat, ametusimuliaSufiani bin Uyayna toka kwa Amru toka kwa Jabiri binZaidi toka kwa Ibnu Abbas alisema: “Niliswali na Mtumewa Mwenyezi Mungu rakaa nane pamoja na saba pamoja.Nikasema: Ewe baba As-sha’shau, nadhani alicheleweshaAdhuhuri na akaharakisha Al-Asr, akacheleweshaMagharibi akaharakisha Isha. Akasema: “Na mimi nad-hani hivyo.”43

Kama atakusudia kukusanya kwa kimuonekano basidhana yake si kitu haisaidii haki chochote. Muda si mrefuutakufikia ufafanuzi kuhusu kukusanya kimuonekano.

Ametusimulia Abu Rabiu Az-Zaharany, ametusimuliaHamadi bin Zaid toka kwa Amru bin Dinari toka kwaJabiri bin Zaid toka kwa Ibnu Abbas kuwa, Mtumealiswali Madina rakaa saba na nane,44 Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha.

43 Kwa alama ya hadith ya tano ni kuwa Mtume alifanya hivyoalipokuwa Madina.44 Kutaja bila kufuata mpangilio kwani mpangilio ni nane na saba

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 37

Kukusanya Sala mbili

38

Amenisimulia Abu Rabiu Az-Zaharany. AmetusimuliaHamadi toka kwa Zuberi bin Al-Khariti toka kwaAbdallah bin Shaqiqi alisema: “Siku moja Ibnu Abbas ali-tutolea muhadhara baada ya Al-Asr mpaka lilipokuchwajua na nyota zikaanza kuonekana. Watu wakawa wanase-ma: Sala! Sala! Mara akaja mtu mmoja wa koo ya BaniTamim huku akisisitiza: Sala! Sala! Ndipo aliposema IbnuAbbas: “Je unanifundIsha Sunna? Usiye na mama wee!Kisha akasema: ‘Nilimuona Mtume amekusanya Sala yaAdhuhuri na Al-Asr, na Magharibi na Isha.’ Abdallah binShaqiqi anasema: ‘Hilo likanitia shaka moyoni mwangu,mara moja nikaenda kwa Abu Huraira nikamuuliza, nayeakathibitisha habari ya Ibnu Abbas kuwa ni kweli.”

Ametusimulia Ibnu Abi Omar. Ametusimulia Wakiu.Ametusimulia Amrani bin Hudayri toka kwa Abdallah binShaqiq Al-Uqayliy amesema: Mtu mmoja alimwambiaIbnu Abbas: “Sala!” Akanyamaza. Kisha akasema:“Sala!” Akanyamaza. Kisha akasema: “Sala!”Akanyamaza. Kisha akasema: “Ee usiye na mama we!”Unatufunza Sala ilhali tulikuwa tukikusanya kati ya Salambili zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu.45

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 38

Kukusanya Sala mbili

39

Haya ndiyo aliyoyanukuu Muslim ndani ya Sahih yake.Yafuatayo ni waliyonukuu wengine.

Ametoa Bukhari toka kwa Ibnu Abbas kuwa: “Mtumealiswali Madina saba na nane pamoja, Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha. Ayubu akasema: ‘Huenda alikuwandani ya usiku wa mvua.’ Akasema, huenda.”46

Ametoa Bukhari toka kwa Jabiri bin Zaidi toka kwa IbnuAbbas amesema: “Mtume aliswali saba pamoja na nanepamoja.”47

Ametoa Bukhari kwa kuivusha toka kwa Ibnu Omar na45 Sherhe ya Sahih Muslim ya An-Nawawiy Juz. 5 Uk. 213-218.Mlango wa kukusanya Sala usipokuwa safarini. Japokuwa huu nimlango mahususi kwa ajili ya riwaya za kukusanya usipokuwa safari-ni lakini kanukuu riwaya tatu zinazoonyesha kukusanya Sala mbilisafarini hivyo hatujazinukuu. Inawezekana aliziweka riwaya hizikatika mlango huu ili kuonyesha kuwa kukusanya katika hali isiyo yasafari ni vilevile kama unavyokusanya safarini46 Sahih Bukhari, Juz. 1, Uk. 110 Kitabu cha Sala mlango wakuchelewesha Sahih Bukhari: Juz.1 Uk. 113, Kitabu cha Sala mlan-go wa wakati wa Magharibi.47 Sahih Bukhari: Juz.1 Uk. 113 Kitabu cha Sala mlango wa wakatiwa Magharibi.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 39

Kukusanya Sala mbili

40

Abi Ayyub na Ibnu Abbas kuwa: Mtume aliswaliMagharibi na Isha.48

Ametoa Tirmidhiy toka kwa Saidi bin Jubairy toka kwaIbnu Abbas alisema: Mtume alikusanya kati ya Adhuhurina Al-Asr na kati ya Magharibi na Isha Madina pasi nahofu yoyote wala mvua. Akasema: Akaambiwa IbnuAbbas: ‘Alitaka nini katika hilo?’ Akasema: ‘Alitaka asi-upe taabu umma wake.' Baada ya kunukuu Hadithi hiiTirmidhy akasema: Hadithi ya Ibnu Abbas imepokewatoka kwake na watu zaidi ya mmoja, kaipokea Jabir binZaidi, Saidi bin Jubayri, na Abdallah bin Shaqiqi Al-Uqayliy. 49

48 Sahih Bukhari: Juz.1 Uk. 113 mlango wa Isha

49 Sunanut-Tirmidhy: Juz.1, Uk. 354 Hadithi namba 187 mlango wayanayozungumzia kukusanya usipokuwa safarini. Kisha angaliakuwa muhakiki kwenye ufafanuzi kataja njia za upokezi zilizopokeaHadithi hii toka kwa Ibnu Abbas. Pia At-Tirmidhy ana tafsiriisiyokubalika kuhusu Hadithi hii. Utaiona muda wake ukifika.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 40

Kukusanya Sala mbili

41

Imam Ahmad ameitoa toka kwa Qatada amesema:“Nilimsikia Jabir bin Zaidi toka kwa Ibnu Abbas akisema:Mtume wa Mwenyezi Mungu alikusanya kati yaAdhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha Madina pasipo nahofu wala mvua.’ Ibnu Abbas akaulizwa: ‘Alitaka ninikinyume na hayo?’Akasema: ‘Alitaka asiupe taabu ummawake.’50

Imam Ahmad ametoa toka kwa Sufiyani amesema Umar:Amenipa habari Jabir bin Zaidi kuwa alimsikia IbnuAbbas akisema: Niliswali na Mtume wa MwenyeziMungu nane pamoja na saba pamoja. Nikamwambia:‘Ewe Abu Shauthau, nadhani alichelewesha Adhuhuri naakaharakisha Al-Asr, Akachelewesha Magharibi aka-harakisha Isha. Akasema: Nami nadhania hivyo.”51

14. Imamu Ahmad ametoa toka kwa Abdallah bin Shaqiqialisema: “Siku moja Ibnu Abbas alitutolea muhadharabaada ya Al-Asr mpaka lilipokuchwa jua na nyota zikaan-50 Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 22351 Musanad Ahmad Juz.1, Uk. 221 alidhania kuwa alikusudia kuku-sanya kimuonekano. Dhana hii si hoja hata kwa yeye mwenyewemdhaniaji. Dhana haisaidii haki chochote

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 41

Kukusanya Sala mbili

42

za kuonekana. Watu wakawa wanasema: “Sala! Sala!Alikuwepo mtu mmoja wa ukoo wa Bani Tamimu akaan-za kusema: Sala Sala! Ibn Abbas akaghadhibika akasema:Je unanifundisha Sunna? Nilimuona Mtume amekusanyabaina ya Adhuhuri na Al-Asr, na Magharibi na Isha.Abdallah anasema: Hilo likanitia shaka moyoni mwangu,mara moja nikaenda kwa Abu Huraira nikamuuliza, aka-likubali.52 (1)

Ametoa Malik toka kwa Saidi bin Jubairy toka kwaAbdallah bin Abbas kuwa alisema: “Mtume waMwenyezi Mungu aliswali Adhuhuri na Al-Asr zotepamoja, Magharibi na Isha zote pamoja pasipo na hofuwala safari.”53

Ametoa Abu Daudi toka kwa Saidi bin Jubairy toka kwaAbdallah bin Abbas` amesema: Mtume wa MwenyeziMungu aliswali Adhuhuri na Al-Asr zote pamoja,Magharibi na Isha zote pamoja pasipo na hofu wala safari.52 Musnad ya Ahmad Juz. 1, Uk. 151 53 Muwatta ya Malik Juz.1, Uk. 144 Hadithi ya 4 mlango wa kuku-sanya Sala safarini na pasipo safari.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 42

Kukusanya Sala mbili

43

Malik akasema: Mimi naona alifanya hivyo wakati wamvua.(3)

Abu Daudi ameitoa toka kwa Jabiri bin Zaidi toka kwaIbnu Abbas alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ali-tuswalisha Madina nane na saba, Adhuhuri na Al-Asr,Magharibi na Isha. Abu Daudi akasema: Ameipokea piaSwaleh bwana wa At-Tauamah toka kwa Ibnu Abbasakasema: ‘Pasipo na mvua.”54

Ametoa An-Nasai toka kwa Saidi bin Jubair toka kwaIbnu Abbas kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliswaliAdhuhuri na Al-Asr zote pamoja, Magharibi na Isha zotepamoja pasipo na hofu wala safari.”55

Ametoa An-Nasai toka kwa Saidi bin Jubair toka kwaIbnu Abbas kuwa: Mtume alikuwa akiswali Madinaakikusanya kati ya Sala mbili kati ya Adhuhuri na Al-Asr,Magharibi na Isha bila ya hofu wala safari. Akaambiwa:

54 Rejea iliyopita, Hadith Na, 1214 55 Sunanun-Nasai, Juz. 1 Uk. 290 mlango wa kukusanya Sala mbiliusipokuwa safarini.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 43

Kukusanya Sala mbili

44

Kwa nini? Akasema: Ili asiupe taabu umma wake.” (3)Ametoa An-Nasai toka kwa Abi Shauthau toka kwa IbnuAbbas amesema: “Niliswali nyumma ya Mtume waMwenyezi Mungu nane zote pamoja na saba zote pamo-ja."56

Ametoa An-Nasai toka kwa Jabir bin Zaidi toka kwa IbnuAbbas kuwa aliswali huko Basra Sala ya mwanzo na Al-Asr bila ya kitu kati yake, na Magharibi na Isha bila yakitu kati yake. Alifanya hivyo kutokana na shughuli. NaIbnu Abbas akadai kuwa Aliswali na Mtume waMwenyezi Mungu Madina Sala ya mwanzo na Al-Asrsijida nane bila ya kitu kati yake.57

Hafidh Abdu Razaqi toka kwa Daudi bin Qaysi toka kwaSwaleh bwana wa At-Tauamah kuwa alimsikia IbnuAbbas akisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliku-sanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha56 Sunanun-Nasai, Juz.1 Uk. 290 mlango wa kukusanya Sala mbiliusipokuwa safarini.57 Sunanun-Nasai, Juz.1 Uk. 286 mlango: Wakati ambao asiyesafarini hukusanya Sala, na makusudio ya sijida

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 44

Kukusanya Sala mbili

45

Madina pasipo na safari wala mvua.” Akasema:‘Nikamwambia Ibnu Abbas: Unadhani kwa nini alifanyahivyo?’ Akasema: ‘Ninaona ili aupe nafuu ummawake.”58

Ametoa Abdu Razaqi toka kwa Ibnu Abbas amesema:“Mtume wa Mwenyezi Mungu alikusanya kati yaAdhuhuri na Al-Asr Madina pasipo na safari wala hofu.Akasema: ‘Nikamwambia Ibnu Abbas, unaona ni kwanini alifanya hivyo? Akasema: ‘Alitaka asimpe yeyotetaabu katika umma wake.”59

Ametoa Abdu Razaqi toka kwa Amru bin Dinari kuwaAba As-Shauthau alimpa habari kuwa Ibnu Abbas`alimueleza akasema: ‘Niliswali nyuma ya Mtume nanezote pamoja na saba zote pamoja Madina. Ibnu Jarihuakasema: ‘Nikamwambia Abu Shauthau mimi nadhaniMtume alichelewesha Adhuhuri kidogo akatanguliza Al-Asr kidogo. Abu Shaathau akasema: “Na mimi nadhania58 1-2- Muswanafu Abdu-Razaqi, Juz. 2 Uk. 555-556 Hadithi ya4434, 4435.59 1-2- Muswanafu Abdu-Razaqi, Juz. 2 Uk. 555-556 Hadithi ya4434, 4435.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 45

Kukusanya Sala mbili

46

hivyo.”60

Nasema: Dhana ya Ibnu Jarihu si chochote japo AbuShauthau ameiafiki, dhana haisaidii haki chochote.Matokeo yake ni kuwa kukusanya kulikuwa ni kimfano sikihalisi, hivyo tutakubainishia udhaifu wa maana hii yakukusanya kimuonekano, na kuwa kukusanyakimuonekano kunawajibisha taabu zaidi kuliko kutengan-isha, kwani kujua mwisho wa wakati wa Sala ya mwanzona mwanzo wa Sala ya pili ni taabu zaidi kuliko kuku-sanya.

Abdu Razaqi ametoa toka kwa Amru bin Shuaybu tokakwa Abdallah bin Omar amesema: “Mtume wa MwenyeziMungu alitukusanyia bila ya kuwa safarini akakusanyaAdhuhuri na Al-Asr.” Mtu mmoja akamwambia IbnuOmar: “Unaona ni kwa nini Mtume alifanya hivyo.”Akajibu: “Ili umma wake usipate taabu iwapo mtu akiku-sanya.”61

60 Muswanafu Abdu-Razaqi: Juz. 2, Uk. 556 Hadithi ya 4436 61 Muswanafu Abdu-Razaqi, Juz. 2 Uk. 556 Hadithi ya 4437

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 46

Kukusanya Sala mbili

47

At-Twahawiy ndani ya kitabu Maanil-athari amesematoka kwa Jabir bin Abdallah: “Mtume wa MwenyeziMungu alikusanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr, Magharibina Isha Madina kwa hiyari bila ya hofu wala ila.” 62

Al-Hafidh Abu Naiimu Ahmad bin Abdallah Al-Isfihaniy(aliyefariki mwaka 430 A.H.) ametoa toka kwa Jabir binZaidi kuwa Ibnu Abbas alikusanya kati ya Adhuhuri naAl-Asr, na akadai kuwa yeye aliswali na Mtume MadinaAdhuhuri na Isha.63

Abu Naiimiy ametoa toka kwa Amru bin Dinari amesema:“Nilimsikia Abu Shauthau akisema: “Ibnu Abbas` amese-ma: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliswali rakaa nanezote pamoja, na rakaa saba zote pamoja bila ya ugonjwawala udhuru."64

Ametoa Al-Bazari ndani ya Musnadi yake toka kwa AbuHurayra kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu

62 Maanil-Athari, Juz.1, Uk. 16163 Hil-yatul-Awliyai, Juz. 3, Uk. 90 mlango wa Jabir bin Zaid64 Hulyatul-Awliya, Juz. 3, Uk. 90 mlango wa Jabir bin Zaid

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 47

alikusanya kati ya Sala mbili Madina bila ya hofu.”65

At-Tabaraniy ametoa ndani ya kitabu Al-Awsatu na Al-Kabiri toka kwa Abdallah bin Zaid kuwa Mtume waMwenyezi Mungu alikusanya Adhuhuri na Al-Asr,Magharibi na Isha. Akaulizwa kuhusu hilo akajibu:“Nimefanya hivyo ili nisiupe taabu umma wangu.” 66

Hizi ni Hadithi thelathini tumezikusanya toka kwenyeSahih Sita, Masnadi na Sunnani.

Tumefupisha maneno kwa kutoa riwaya hizi tu ili mso-maji ajue kuwa ni Hadithi ambazo wanazuoni wa Hadithina wakubwa wao wamezitilia umuhimu hivyo wakazihi-fadhi, na wala mtu hawezi kuzikataa na kuzikanusha. Nakuna riwaya nyingize zaidi ya hizi hatujazitaja kwa ajiliya kufupisha.67

Mtiririko huu wa wapokezi unakomea kwa watu wafu-

Kukusanya Sala mbili

48

65 Musnadul-Bazari, Juz. 1, Uk. 283 Hadithi namba 41266 Al-Muujamul-Kabiri Juz.10, Uk. 269 Hadithi ya 10525

67 Angalia Al-Maujamul-Awsatu, Juz. 2, Uk. 94. Kanzul-Ummal,Juz.8 Uk.246-251 namba 22764, 22767, 22771, 22774, 22777,22778.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 48

Kukusanya Sala mbili

49

atao:Abdallah bin AbbasAbdallah bin OmarAbu Ayubu Al-Annswariy mwenyeji wa Mtume MadinaAbu Hurayra Ad-DuusiyJabiri bin Abdillah Al-AnswariyAbdallah bin Mas'udi.

Riwaya zinaeleza wazi kuwa Mtume wa MwenyeziMungu alikusanya Madina kati ya Sala mbili pasipo nahofu, mvua wala sababu yoyote. Alikusanya ili kubainisharuhusa ya kukusanya na kuwa kufanya hivyo ni sheria. Piaili mtu asije akadhani kuwa kutenganisha ni lazimakutokana na yeye Mtume kuendelea kuswali ndani yawakati wa ubora. Hivyo kwa kitendo chake cha kuku-sanya kimethibitisha kuwa kukusanya ni ruhusa japokuwakutenganisha ni bora.

Kwa kuwa madhumuni ya riwaya yanapingana na madhe-hebu za kifiqhi zilizozoweleka hivyo baadhi ya watu waHadithi na wanazuoni wa fiqhi wamejaribu kuzilazimishariwaya zifuate fat'wa za maimamu zao na kufanya fat'wahizo ndio kipimo cha haki na batili.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 49

Kukusanya Sala mbili

50

Hivyo wengi wao wakaacha kuzitumia riwaya hiziisipokuwa wachache tu ndio waliozitumia wakatoa fat'wakulingana na madhumuni ya riwaya, hao wametajwamajina yao na Ibnu Rushdi ndani ya kitabu chakeBidayatul-Mujtahidu. Na Wametajwa na An-Nawawiyndani ya Al-Maj'muu kama ilivyotangulia.

Na kifuatacho ni sababu na nyudhuru walizozitoawaliokhalifu riwaya, nazo ni sababu na nyudhuru dhaifukuliko nyumba ya buibui.

Wanazuoni wengi wa kisunni wameachakuifanyia kazi

Hakika kati ya mambo yanayozisibu riwaya hizi niwanazuoni wengi wa kisunni kuacha kuzitumia, jamboambalo linawajibIsha zisiwe na hoja.

Baada ya kutaja Hadithi za kukusanya, Tirmidhiy anase-ma: Kuzifanyia kazi hizi riwaya kwa masunni nikutokukusanya kati ya Sala mbili isipokuwa safarini auArafa. 68

68 Sunanut-Tirmidhiy, Juz.1, Uk. 354

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 50

Kukusanya Sala mbili

51

Watafiti wengi wa dini wameijibu kauli hii:a). An-Nawawiy anasema: “Riwaya hizi zimethibiti ndaniya Muslim kama unavyoziona. Na wanazuoni wana tafsirina madhehebu mbalimbali kuhusu riwaya hizi, naTirmidhiy mwisho wa kitabu chake amesema: Ndani yakitabu changu hakuna Hadithi ambayo ummaumeafikiana juu ya kuiacha na kutokuifanyia kaziisipokuwa Hadithi ya Ibnu Abbas inayohusu kukusanyaMadina bila ya hofu wala mvua, na Hadithi ya kumuuamnywaji wa pombe mara ya nne.”69

Hili alilolisema Tirmidhiy kuhusu Hadithi ya mnywaji wapombe ndivyo lilivyo, yenyewe ni Hadithi iliyofutwakwani ijmai imethibitisha hilo. Ama kuhusu Hadithi yaIbnu Abbas hakuna ijmai inayothibitIsha kuachakuifanyia kazi, isipokuwa kuna baadhi ya tafsiri ambazotutaziashiria.70 (1)

b). As-Shaukaniy amemjibu At-Tirmidhiy kwa kusema:“Haijifichi kuwa Hadithi ni Sahih, na wala kitendo cha

69 Taz. Al-Ilali, Juz. 2, Uk. 331 na Juz. 4, Uk. 38470 Sharh ya Sahih Muslim ya An-Nawawiy Juz. 5 Uk. 224

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 51

Kukusanya Sala mbili

52

masunni wengi kuacha kuifanyia kazi hakitii dosariusahih wake, na wala hakiwajibishi kuporomoka hojayake. Baadhi ya wanazuoni wameifanyia kazi kama ilivy-otangulia. Japokuwa dhahiri ya maneno ya Tirmidhiy nikuwa yeye haifanyii kazi lakini wengine wamethibitishakuifanyia kazi, na kilichothibitishwa hutangulizwa.71

c). Al-Alusiy amesema: “Madhehebu ya kundi la maima-mu linaruhusu kukusanya usipokuwa safarini kwamwenye haja asiyefanya kuwa ni mazowea. Kauli hiindiyo ya Ibnu Sirini, na Ash'habu mfuasi wa Malik.

Al-Khatabiy Ameinukuu toka kwa Al-Qufali As-ShashiyAl-Kabiru mfuasi wa Imam Shafy, na kutoka kwa AbiIs'haqa Al-Marwaziy na toka kwa jamaa kati ya watu waHadithi.

Ibnu Al-Mundhiru amechagua kauli hii, na inaungwamkono na dhahiri iliyosihi toka kwa Ibnu Abbas` na iliy-opokewa na Muslim kuwa alisema: Mtume wa MwenyeziMungu alikusanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi71 Naylul-Awtwari ya As-Shawkaniy Juz. 3, Uk. 218 mlango wakukusanya kwa asiye msafiri kwenye mvua au kingine.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 52

Kukusanya Sala mbili

53

na Isha Madina pasipo na hofu wala mvua. Akaambiwa:Kwa nini amefanya hivyo? Akasema: “Hakutaka yeyoteapate taabu katika umma wake.”

Inatokana na taabu kwa maana ya uzito hivyo hajatoasababu ya ugonjwa wala ya kitu kingine.

Kutokana na tuliyoyataja inafahamika kuwa kauli ya At-Tirmidhiy mwishoni mwa kitabu chake: Ndani ya kitabuchangu hakuna Hadithi ambayo umma umeafikiana juu yakuiacha na kutokuifanyia kazi isipokuwa Hadithi ya IbnuAbbas inayohusu kukusanya Madina bila ya hofu walamvua, na Hadithi ya kumuua mnywaji wa pombe mara yanne. Inatokana na kutokufanya utafiti .

Ndio! Aliyoyasema kuhusu Hadithi ya pili ni sahih kwaniwameeleza wazi kuwa Hadithi hiyo imefutwa na ijmaiimethibitisha kufutwa kwake.72 (1)

d). Kwa ukosoaji huu imedhihirika kuwa hakuna hali yakususa kuifanyia kazi Hadithi hii, na huenda masunni72 Ruhul-Maaniy, Juz. 15 Uk. 133-134 katka tafsiri ya Aya:“Simamisha Sala jua linapopinduka”

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 53

Kukusanya Sala mbili

54

wengi hawajatoa fat'wa kulingana na makusudio yaHadithi hizi kwa sababu ya ubora wa kutenganisha nakuzigawa kwa nyakati.

Lakini ubora huu unapingana na ubora mwingine, nao nikuwa katika zama zetu hizi kitendo cha kutenganishakinapelekea watu wengi wenye shughuli kuacha kuswali(kama tunavyoshuhudia kwa macho). Kinyume na kuku-sanya kwenyewe ambako kunarahisisha kuhifadhi Salakwa kuziswali, kwa ajili hiyo ubora umegeukia upandewa pili, hivyo ni bora wanazuoni wa sheria wakatoafat'wa ya kukusanya, na watie wepesi badala ya kutiauzito.

Allah (s.w.t.) anasema: “Mwenyezi Mungu huwatakieniyaliyo mepesi wala hawatakieni yaliyo mazito.”73 “Walahakuweka juu yenu uzito katika dini.”74

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani zipo dalili zina-zoruhusu kukusanya katika hali yoyote, tena ni dalili

73 Al-Baqara: 18574 Al-Hajji: 78

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 54

Kukusanya Sala mbili

55

sahih na za wazi kama ulivyoona, bali ni Kitabu chenyehekima ndio kimebainisha hivyo.75

2. Hadithi haielezi kukusanya kwa kutanguliza au kwakuchalewesha.

Al-Qadhiy Sharafudini Al-Husein bin Muhammad Al-Maghribiy amesema ndani ya kitabu chake Al-Badru At-Tamamu fi sharhu Bulughul-Marami kuwa: “HakikaHadithi ya Ibnu Abbas haisihi kuwa hoja kwa sababuhaiainishi ni kukusanya kwa kutanguliza au ni kwakuchelewesha, hiyo ni kama ilivyo dhahiri katika riwayaya Muslim na kuainisha moja kati ya hizo ni kulazimisha.Hivyo inawajibika kuhama kwenda kwenye lile la wajibukwa kubakia katika Hadithi za nyakati zinazomjumuishamwenye udhuru na asiye na udhuru kisha kumuainishamsafiri tu kwa kuthibiti kiainishi.76

Anajibiwa kuwa: Ibnu Abbas hakunukuu namna ya kuku-sanya kwa kuwa jambo lenyewe liko wazi, kwani kuku-75 Masailul-Fiqihiya ya Imam Sharaful-dini: 976 Ameelezea As-Sayyid Muhammad bin Ismail As-Swanaaniy aju-likanae kwa jina la Al-Amiru ndani ya kitabu chake Subulus-Salami:Juz. 2, Uk. 43

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 55

Kukusanya Sala mbili

56

sanya katika hali isiyo ya safari ni sawa na kukusanyakatika hali ya safari, hivyo kama inavyoruhusiwa kuku-sanya kwa namna zote mbili uwapo safarini yaani kuku-sanya kwa kutanguliza na kwa kuchelewesha kamamaelezo yalivyotangulia ndivyo hivyo hivyo hatausipokuwa safarini.

Kunyamaza kwa Ibnu Abbas na kitendo cha wapokezikutokumuuliza kuhusu namna ya kukusanya ni dalilikuwa kutokana na maneno yake walifahamu kukusanya simahususi kwa namna moja tu kati ya namna mbili, kwanilaiti isingekuwa hivyo ingewalazimu kuuliza tena: Je,Mtume alikusanya kwa namna ya kutanguliza aukuchelewesha?

Linalounga mkono hilo ni umoja wa sababu iliyopokwenye maneno ya Ibnu Abbas kwani inapatikana katikanamna zote mbili.

Ametoa Muslim toka kwa Ibnu Abbas kuwa Mtume waMwenyezi Mungu alikusanya Sala mbili katika safarialiyosafiri katika vita vya Tabuk, hivyo akakusanya katiya Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Isha. Said akasema:

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 56

Kukusanya Sala mbili

57

‘Nikamwambia Ibnu Abbas kitu gani kilimpelekeakufanya hivyo, akasema: “Alitaka asiupe taabu ummawake.”77

Hivyo kinachoupa nguvu uhusikaji wa namna zote mbilibila tofauti kati ya namna hizo ni kule kuenea kwa sababunayo ni kuuondolea taabu umma wake, kwani kwa hakikataabu inayopatikana kwa kutenganisha Sala mbili inaon-doka kwa kukusanya kwa namna yoyote ile kati ya namnambili. Sawa iwe kwa kutanguliza au kuchelewesha.

Zaidi ya hapo ni kuwa Ibnu Abbas aliifanyia kazi Hadithikwa sura ya kukusanya kwa kuchelewesha.Imeshatangulia kuwa Ibnu Abbas siku moja alihutubiabaada ya Al-Asr mpaka jua likazama na nyota zika-chomoza; watu wakaanza kusema: ‘Sala! Sala!’ Akajamtu toka ukoo wa Bani Tamimu akaanza kusisitiza kwakusema: ‘Sala! Sala!’ Ibnu Abbas akasema: “JeunanifundIsha sunna? Ee usiye na mama we!" Mpakamwisho wa Hadithi kama ilivyotangulia.Kwa hakika ndugu msomaji ni kuwa mpinzani alipofika77 Sharhu ya Sahih Muslim ya An-Nawawiy, Juz. 5, Uk. 224 mlangowa kukusanya Sala mbili Hadithi ya 51

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 57

Kukusanya Sala mbili

58

mbele ya riwaya hizi nyingi zinazoruhusu kukusanyadhidi ya kutenganiha, kisha akaona wanazuoni wengiwako kinyume basi kwa makusudi akaanza kushakia, nakwa ajili hiyo akaleta utata huu ambao unafanana na swalila Bani Israeli kwa Nabii Musa bin Imran kuhusu miakana rangi ya ng'ombe jike.78

Alikusanya sala mbili kimuonekano

Wengi wanaojaribu kutatua suala hili hukimbilia kudaikuwa haikuwa ni kukusanya kwa halisi kama kukusanyakwa safarini, bali ilikuwa ni kukusanya kwakimuonekano, yaani Mtume alichelewesha Adhuhurimpaka ulipobakia muda wa rakaa nne ndipo akaswaliAdhuhuri na baada ya kumaliza tu ukawa umeingiawakati wa Al-Asr akaswali Al-Asr, hivyo akawa kaku-sanya Sala mbili huku akiwa kaswali kila moja ndani yawakati wake.

Hili ndilo linalodhihirika toka kwa wengi wanaofafanuaHadithi; na yafuatayo ni maelezo yao:An-Nawawiy amesema: “Wapo waliofasiri kuwa ni

78 Al-Baqarat; 2: 67-71

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 58

Kukusanya Sala mbili

59

kuchelewesha ya mwanzo mpaka mwisho wa wakatiwake kisha aiswali ndani ya wakati wake, hivyo baada yakumaliza ukawa umeingia wakati wa Sala ya piliakaiswali, hivyo Sala yake ikawa katika muonekano wakukusanya.”

Kisha akapinga akasema: “Kauli hii nayo ni dhaifu aubatili kwa sababu inapingana na dhahiri kwa namna isiy-otegemewa. Kwa sababu kitendo cha Ibnu Abbas tuli-chokitaja katika hotuba kisha kutoa kwake Hadithi kamahoja ya usahihi wa kitendo chake, kisha kuthibitishakwake Abu Huraira bila kukanusha ni hoja tosha katikakupinga tafsiri hii.79

An-Nawawiy alipasa amjibu kwa hoja tuliyoitaja nayo nikuwa: Mtume alikusanya Sala mbili kwa lengo la kuuon-dolea umma wake taabu, na kukusanya kwa namna hiyoiliyotajwa kunataabisha zaidi kuliko kutenganisha.

Ibnu Quddama amesema: “Kukusanya ni hiyari, hivyoingekuwa kukusanya ni kwa namna waliyoielezea basiingekuwa ni taabu zaidi kuliko kuiswali kila Sala wakati

79 Sharhu ya Sahih Muslim, Juz. 5, Uk. 225

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 59

Kukusanya Sala mbili

60

wake. Kwa sababu kuiswali kila Sala wakati wake niwepesi zaidi kuliko kulinda mwisho wa wakati, mwishoambao unalingana na muda wa kuswali Sala ya mwanzotu bila wakati kubaki.

Pia laiti kukusanya kungekuwa ni kwa namna hiyo basiingeruhusiwa kukusanya kati ya Al-Asr na Magharibi naIsha na Asubuhi. Ilihali hakuna tofauti kati ya ummakuwa kufanya hivyo ni haramu. Hivyo kuzifanyia kaziriwaya kwa ufahamu uliyo karibu ni bora zaidi kulikokulazimisha maana hiyo.80 (1)

Pia Al-Muqaddasiy ndani ya kitabu As-Sharhu Al-Kabiru81 amejibu tafsiri hii kama alivyojibu Ibnu Quddama,tamko ni moja katika vitabu vyote viwili hivyo ndiomaana tumetosheka na tamko la Ibnu Quddama.

Ndio, Kulingana na tuliyonukuu toka kwao ni kuwa waowamemjibu yule aliyefasiri ruhusa ya kukusanya Sala80 Al-Mughni, Juz. 2, Uk. 113-114 ameitaja alipokuwa akikosoamaneno ya yule aliyefasiri maana hii katika kukusanya kwa safarini.Hivyo kwa kuwa jambo ni moja ndio maana tumeitaja hapa.81 As-Sharhul-Kabiru fi Dhaylil-Mughniyi, Juz. 2, Uk. 115

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 60

Kukusanya Sala mbili

61

mbili kwa msafiri kwa tafsiri ya kukusanya kimuonekano.

Hivyo kwa kuwa sababu ya kukusanya katika hali zotembili (Msafiri na asiye msafiri) ni moja, nayo ni kuuon-dolea umma wake taabu na uzito huku kukusanya kwamuonekano kukiwa ni taabu na uzito zaidi kuliko kuten-ganisha basi tunathibitisha maneno yao katika mada hii.(Kukusanya bila udhuru katika hali isiyo ya safari).

Dhahiri ni kuwa jina kukusanya, kijamii halimlengi mtualiyechelewesha Adhuhuri akaja kuiswali mwisho wawakati wake na akaiharakisha Al-Asr akaiswali mwanzowa wakati wake, kwa sababu huyu kaswali kila Sala ndaniya wakati mahususi kwa Sala husika.

Amesema: “Hakika kukusanya kunakojulikana ni kuswaliSala zote mbili pamoja ndani ya wakati wa mojawapo,hivi huoni kukusanya Sala mbili Arafa na Muzdalifa ndi-vyo kulivyo?"82

82 Maalimus-Sunan, Juz. 2 Uk. 53 Hadithi ya 1163, Aunul-Maabudu,Juz. 1, uk. 468.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 61

Kukusanya Sala mbili

62

Dalili za As-Shaukaniy za kuthibitisha kuwakukusanya kulikuwa kwa kimuonekano

Kisha As-Shaukaniy ni kati ya watu wanaounga mkonokuwa kukusanya kulikuwa ni kwa kimuonekano.Ameunga mkono hilo kwa hoja tatu:

Ya kwanza: Riwaya aliyoitoa Malik katika Al-Muwatwauna Bukhari, Abu Daud na An-Nasaiy toka kwa IbnuMas'udi kuwa alisema: “Sikumuona Mtume akiswali Salanje ya wakati wake isipokuwa Sala mbili alikusanyaMagharibi na Isha Muzdalifa na siku hiyo akaswali alfa-jiri kabla ya wakati wake.”

As-Shaukaniy akasema: Ibnu Mas'ud kakataa namna yoy-ote ya kukusanya na akaihusisha na kukusanya Muzdalifatu, japokuwa yeye mwenyewe ni kati ya watu waliy-opokea kukusanya kwa Madina kama ilivyotangulia.

Hivyo inaonyesha kuwa kukusanya kulikofanyikaMadina ni kukusanya kwa kimuonekano, kwani laitiingekuwa ni kukusanya kwa halisi basi riwaya zake

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 62

Kukusanya Sala mbili

63

zingepingana, na ni lazima tukusanye riwaya hizi kwanamna itakayowezekana. 83

Anajibiwa: Kwanza: Ibnu Mas'udi si hoja kwa sababu amehusishakukusanya na Muzdalifa tu ilihali kuna riwaya nyingizinazoonyesha kuwa Mtume alikusanya Muzdalifa naArafa, hivyo dhahiri ya Hadithi hii inaachwa walahaitegemewi, wala haisihi kuwa alama ya kuainishamakusudio ya kukusanya katika riwaya za mada hii.

Pili: Ibnu Mas'udi mwenyewe amepokea kukusanya kwaMtume Sala mbili Madina, na akasema: “AlikusanyaMtume wa Mwenyezi Mungu Adhuhuri na Al-Asr,Magharibi na Isha.” Akaulizwa kuhusu hilo akasema:“Nimefanya hivyo ili umma wangu usitaabike.” 84

Umeshafahamu kuwa kukusanya kwa kimuonekanokunataabisha zaidi kuliko kukusanya kwa halisi, kwanikufahamu mwisho wa nyakati na mwanzo wake bila83 Naylul-Awtari min ahadithi Sayidul-Akhbari, Juz. 3, Uk. 21784 Angalia riwaya namba 30

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 63

Kukusanya Sala mbili

64

kukosea ilikuwa ni tatizo kwa zama zilizopita hivyo haku-na njia isipokuwa ni kutafsiri kukusanya kwa maana yakukusanya kwa uhalisia. Hii ni dalili kuwa riwaya inay-ohusisha kukusanya kwa Muzdalifa tu imeachwa na walasi hoja.

Ya pili: Aliyopokea Ibnu Jariri toka kwa Ibnu Umar ame-sema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alitujia akawaakichelewesha Adhuhuri na kuharakisha Al-Asr hivyoanazikusanya pamoja. Anachelewesha Magharibi na ana-harakisha Isha hivyo anazikusanya pamoja na huku ndiokukusanya kwa kimuonekano.”85

Anajibiwa kuwa Hadithi hii japokuwa inahusIsha kuku-sanya kwa kimuonekano lakini haichukuliwi kwa sababumuradi wake hauko wazi, kwani laiti akimaanIsha kuwaMtume alifanya hivyo safarini basi imeshatangulia kuwaukusanyaji wa Mtume safarini ulikuwa ni halisi.

Amepokea Muslim toka kwa Anas bin Malik kuwa alise-ma: “Ilikuwa Mtume akisafiri kabla ya kugeuka juahuchelewesha Adhuhuri mpaka wakati wa Al-Asr kisha85 Naylul-Awtari, Juz. 3, Uk. 217

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 64

Kukusanya Sala mbili

65

anashuka na kuzikusanya pamoja.”86

Na katika riwaya nyingine toka kwake: “Hakika Mtumealikuwa aharakishwapo na safari huchelewesha Adhuhurimpaka mwanzo wa wakati wa Al-Asr kisha anazikusanyapamoja, na anachelewesha Magharibi mpaka aje aiku-sanye na Isha mpaka wekundu wa Magharibi unapoondo-ka.” 87

Kama makusudio yake ni kuwa Mtume alikusanya kati yaSala mbili kukusanya kwa kimuonekano ilihali hayuposafarini basi nadhani umeshajua jinsi riwaya zinazoonye-sha ukusanyaji halisi zilivyonyingi, kiasi kwamba Hadithiya Ibnu Abbas` na nyingine zimeweka wazi na ni alamatosha ya kutafsiri riwaya kwa maana ya ukusanyaji halisi,hivyo hatuwezi kuitupa Hadithi na kitendo cha IbnuAbbas` eti kwa ajili ya Hadithi isiyokuwa wazi ya IbnuOmar.

86 Sharhu Sahih Muslim, Juz. 5 mlango: Ruhusa ya kukusanya Salambili safarini. Namba 46 na 48

87 Sharhu Sahih Muslim, Juz. 5 mlango: Ruhusa ya kukusanya Salambili safarini. Namba 46 na 48

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 65

Kukusanya Sala mbili

66

Ya tatu: Ameipokea An-Nasai toka kwa ibnu Abbas kuwa:Niliswali na Mtume Adhuhuri na Al-Asr pamoja, naMagharibi na Isha pamoja. Alichelewesha Adhuhuri aka-harakisha Al-Asr, na akachelewesha Magharibi akaharak-isha Isha. Na huyu ni Ibnu Abbas mpokezi wa Hadithi zamlango huu ametamka wazi kuwa aliyopokea kuhusukukusanya ni kukusanya kwa kimuonekano.88

Anajibiwa kuwa: Tafsiri hii, yaani kauli: AlicheleweshaAdhuhuri akaharakisha Al-Asr, na akacheleweshaMagharibi akaharakisha Isha, si ya Ibnu Abbas bali ni yaJabir bin Zaid, hiyo ni kwa alama ya Hadithi aliyoitoaImam Ahmad toka kwa Jabir bin Zaid kuwa alimsikiaIbnu Abbas akisema: “Niliswali na Mtume wa MwenyeziMungu nane pamoja na saba pamoja. Nikamwambia, eweAba As-Shauthau nadhania alichelewesha Adhuhuri akai-harakisha Al-Asr na akachelewesha Magharibi akaiharak-isha Isha. Akasema: ‘Na mimi nadhani hivyo.’89

Hii ni dalili ya wazi kuwa tafsiri iliyotoka kwa Abu As-

88 Naylul-Awtari, Juz. 3, Uk. 21789 Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 221

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 66

Kukusanya Sala mbili

67

Shauthau na wenzake, inatokana na wao kuzoea kuten-ganisha Sala na kuipa kila Sala wakati wake, hivyowakadai kuipa kila Sala wakati wake ni faradhi isiyoach-wa. Hivyo walipojikuta mbele ya riwaya hizi nyingiwakashindwa kujua makusudio ya riwaya, hivyo kilammoja akakimbilia njia yake na Abu As-Shaathauakatafasiri kukusanya kwa kimuonekano.

4. Alikusanya kwa sababu ya udhuru wa mvua

Hii ndio tafsiri ya tatu ambayo amekimbilia kwayo yuleasiyeruhusu kukusanya Sala mbili katika hali isiyo yasafari.

An-Nawawiy amesema: “Kati yao yupo aliyetafsiri kuwakukusanya ni kwa ajili ya mvua. Kauli hii ndio mashuhuritoka kwa wanazuoni wakubwa waliotangulia.”

Kisha akaijibu akasema: “Ni dhaifu kutokana na riwayanyingine za pasipo na hofu wala mvua.” 90

Sababu kubwa ya kupatikana aina hii ya tafsiri ni kujaribu90 Sharhu ya Sahih Muslim ya An-Nawawiy, Juz, 5. Uk. 225

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 67

Kukusanya Sala mbili

68

kulinganisha riwaya na fat'wa za wanazuoni wengi, kamasi hivyo basi riwaya ziko wazi kuwa kukusanya ilikuwabila udhuru wowote. Iwapo utafuatilia maelezo ya riwayatulizonukuu toka kwa Ibnu Abbas utaishia kusema kuwakukusanya haikuwa kwa udhuru fulani bali kwa ajili yakuuondolea taabu umma wake.

Hivyo katika baadhi ya Hadithi utakuta kipengele: Pasipona hofu wala safari (Angalia riwaya namba 1, 2, 15, 16,18 na 23).

Katika nyingine. Pasipo na hofu wala mvua. (Angaliariwaya namba 3, 4, 11, 12, na 19).

Katika nyingine: Pasipo na safari wala mvua (Angaliariwaya ya 22). Katika nyingine: Pasi na hofu wala sababu.(Angalia riwaya ya 26).

Katika nyingine: Bila ugonjwa wala sababu (Angaliariwaya ya 28).

Zaidi ya hapo ni kuwa, ila iliyopokewa ndani ya riwayaambayo ndio inapinga uwezekano huo iko wazi sana, na

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 68

Kukusanya Sala mbili

69

yafuatayo ni maelezo yake: Katika baadhi ya riwaya ila nikauli yake: Alitka asimsumbue yeyote kati ya watu waumma wake (Angalia riwaya namba: 2, 3, 11, 12, na 23.) Katika baadhi ya riwaya nyingine: Ili umma wake usiwena taabu. (Angalia riwaya ya 19).

Katika baadhi ila ni: Kuurahisishia umma wake. (Angaliariwaya ya 22)

Katika baadhi ya riwaya nyingine: Asiutaabishe ummawake iwapo mtu akikusanya. (Angalia riwaya ya 25).

Katika baadhi ya riwaya nyingine: Ili umma wangu usi-taabike. (Angalia riwaya ya 30).

Hivyo mwenye kuzichunguza hizi riwaya anaamini kuwakukusanya haikuwa kwa udhuru wa mvua wala safari,hofu wala ila nyingine, hivyo Mtume alikusanya Salambili Madina bila ya udhuru wowote, ikiwa ni amri tokakwa Mwenyezi Mungu ili aurahisishie umma wake, na iliasidhani mwenye kudhani kuwa kuipa kila Sala wakatiwake ni faradhi ambayo hairuihusiwi kuikhalifu bali niubora usiyokatalika.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 69

Kukusanya Sala mbili

70

Hivyo kila mmoja ndani ya umma huu ana haki ya kuku-sanya bila kuipa kila Sala wakati wake.

5. Alikusanya kwa sababu ya mawingu mbinguni

Miongoni mwao yupo aliyetafsiri kuwa kulikuwa namawingu hivyo akaswali Adhuhuri. Kisha mawinguyakaondoka na ikabainika kuwa wakati wa Al-Asr ume-shaingia basi akaswali Al-Asr. Dhana hii ni dhaifu sana,hivyo aliyoyataja An-Nawawiy yanatosha kuonyeshaudhaifu wake amesema: Japokuwa kuna mategemeofulani ya dhana hii katika Adhuhuri na Al-Asr lakinihamna kabisa mategeneo ya dhana hii katika Magharibina Isha. Tena kukusanya hakukuwa mahususi kwa ajili yaAdhuhuri na Al-Asr bali alikusanya Magharibi na Ishampaka Ibnu Abbas akachelewesha Magharibi mpakawakati wa Isha.91

Zaidi ya hapo ni kuwa laiti kukusanya kungekuwa ni kwahali hiyo basi wapokezi wangeelezea wazi wazi. Hivitunaweza kusema Ibnu Abbas alisahau sharti, au alikum-buka lakini hakulinukuu. Pia wenzake mfano wa AbuHuraira, Abdallah bin Omar na Abdallah bin Masudi.91 Sharhu ya Sahih Muslim: Juz. 5, Uk. 225

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 70

Kukusanya Sala mbili

71

6. Alikusanya kwa sababu ya ugonjwa

Baadhi ya wale wasiyopendezeshwa na kukusanya Salambili wametafsiri riwaya wakasema riwaya inamaanishaalikusanya kwa sababu ya udhuru wa ugonjwa au mfanowake.

Mtazamo huu kaunukuu An-Nawawiy toka kwa Ahmadbin Hambali, Al-Qadhi Huseini mfuasi wa Shafi. Pia ameuchagua Al-Khatabiy, At-Tawaliy, na Al-Rawiyaniy wafuasi wa mad-hehebu ya Shafi.

An-Nawawiy ameuchagua akasema: Ndio mtazamo auch-aguao katika tafsiri yake kutokana na dhahiri ya Hadithina kitendo cha Ibnu Abbas` na uthibitisho wa Abu Hurairana kwa sababu ndani ya ugonjwa kuna taabu zaidi kulikokwenye mvua. 92

Anajibiwa kuwa: Tafsiri hii ni dhaifu na haifai kamatafsiri nyingine kwani ndani ya riwaya hizo kuna: Bilahofu wala ila. Na katika nyingine kuna: Bila ugonjwawala ila. Na linalozidi kubatilisha hoja hiyo ni kuwa Ibnu92 Sharhu ya Sahih Muslim ya An-Nawawiy Juz. 5, Uk. 226

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 71

Kukusanya Sala mbili

72

Abbas alikusanya kati ya Magharibi na Isha huku akiwa simgonjwa wala hakuna ugonjwa. Bali alikuwa akihutubiawatu na maneno yake yakarefuka mpaka muda wa uborawa Magharibi ukapita hivyo akaswali Magharibi na Ishandani ya wakati mmoja.

Pia ni kuwa, laiti ingekuwa kuchelewesha ni kwa ajili yaugonjwa basi ingesihi kwa mgonjwa mweyewe binafsi sikwa yule asiye mgonjwa, lakini Mtume alikusanya yeyena swahaba zake wote, hivyo kudhania kuwa wotewalikuwa ni wagonjwa ni dhana iliyo mbali na ukweli. 93

Kutokana na tuliyoyataja ndio maana Al-Hafidhu IbnuHajari Al-Asqalaniy amesema: “Laiti angekusanya kwasababu ya ugonjwa basi asingeswali na yoyote isipokuwana yule mwenye udhuru kama wake. Na dhahiri ni kuwaaliswali na maswahaba zake. Hilo kalitamka wazi IbnuAbbas katika riwaya yake.” 94

Huyu hapa Al-Khatabiy anaelezea ndani ya (Maalimu)toka kwa Ibnul-Mundhir kuwa alisema: “Wala hakunamaana yoyote ya kulinasibisha jambo hili na udhuru93 Angalia Naylul-Awtari ya As-Shaukaniy Juz. 3, Uk. 21694 Fathul-Baariy, uk. 24

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 72

Kukusanya Sala mbili

73

wowote kwa sababu Ibnu Abbas ameelezea ila yakeakasema: “Alitaka asiutaabishe umma wake.”

Na imeelezwa toka kwa Ibnu Sirin kuwa alikuwa haoniubaya kukusanya Sala mbili kwa sababu ya haja fulani aukitu fulani iwapo tu hafanyi mazowea.95

Muhakiki wa Sunanut-Tirmidhi baada ya kunukuumaneno ya Al-Khatabiy amesema: Na hili ndio sahihiinayopatikana ndani ya Hadithi. Ama tafsiri ya ugonjwaau udhuru au jambo lingine ni kulazimisha jambo walahalina dalili. Kwa kuchukua sahihi hii watu wengi wame-ondolewa taabu kwani kazi zao na mazingira yao magu-mu yanaweza kuwalazimisha kukusanya Sala mbili hivyowakajikuta wanapata dhambi au wanataabika katika hilo,hivyo katika kukusanya kuna raha kwao na msaada wakumtii Mwenyezi Mungu iwapo tu hawatofanya kuwa nimazoea kama alivyosema Ibnu Sirin. 96

95 Maalimus-Sunnani, Juz. 1, Uk. 6596 Sunanut-Tirmidhiy, Juz. 1, Uk. 358 Upande wa nyongeza kwakalamu ya Ahmad Muhammad Shakir

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 73

Kukusanya Sala mbili

74

Aliyoyasema ni haki lakini (Ibnu Sirin) kabana kile ali-chokipanua Mtume kwani kahusisha kukusanya kwamwenye haja tu. Ilihali Mtume amepanua kwa watu wotekwa amri toka kwa Mwenyezi Mungu kwa yule mwenyeila au asiye na ila.

Ndio hakuna shaka kuwa kuipa kila Sala wakati wake waubora ni bora kuliko kuiswali ndani ya wakati wakushirikiana, kwa hiyo kwa mujibu wa sheria ni kuwamuda wa kutekeleza Sala ni mpana.

Alikusanya kwa sababu ya udhuru usiyo-julikana

Kwa kuwa kuainisha udhuru unaoruhusu kukusanyaimekuwa ni jambo gumu hivyo baadhi yao wamepita njiaya kutokujulikana na kutokuwa wazi, hivyo wakadaikuwa alikusanya kwa sababu ya udhuru unaoruhusu hilolakini bila kuuainisha.

Kati ya watu waliounga mkono dhana hii ni Mufti wazamani wa Saudia Abdul-Azizi bin Bazi katika ufafanuzi

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 74

Kukusanya Sala mbili

75

wake mfupi wa Kitabu Fat-hul-Bari fi sharhi Sahihl-Bukhari Baada ya kudhoofIsha mtazamo wa Ibnu Hajarkuhusu maana ya kukusanya (kukusanya kimuonekano)kwa kusema: Kukusanya kwa namna hii ni dhaifu.

Akasema: Sahihi ni kuitafsiri Hadithi iliyotajwa kuwaalikusanya Sala zilizotajwa kwa sababu ya taabu iliy-opatikana siku hiyo kutokana na ugonjwa uliozidi au bari-di kali au matope na mfano wa hayo. Na dalili juu ya hiloni kauli ya Ibnu Abbas alipoulizwa kuhusu ila ya kuku-sanya huku, akasema: “Ili asiutaabishe umma wake.”

Kisha (Ibnu Bazi) akapendekeza kukusanya huku akase-ma: Nako ni jawabu kubwa sahihi lenye kutibu.”97

Anajibiwa kuwa: Kukusanya huku na kule alikokud-hoofisha kote ni dhaifu, kwa sababu kunapingana nariwaya na kitendo cha Ibnu Abbas, kwani yeye alikusanyaSala mbili huko Basra bila ya kuwa na ugonjwa mkali aubaridi kali au matope.

97 Fathul-Bari fi Sharhu Sahihl- Bukhari, Juz. 2, Uk. 24 maelezo yaAbdul-Azizi bin Bazi

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 75

Kukusanya Sala mbili

76

Zaidi ya hapo ni kule kuenea kwa ila. Yaani kuuondoleataabu umma, kwani taabu haihusu hali za udhuru tu baliinajumuisha hata kuwalazimisha watu kutenganisha Salakwa namna ya wajibu ndani ya maisha yao.

Hapa si vibaya kunukuu maneno ya Ibnu As-Siddiq yaliy-omo ndani ya kitabu chake kiitwacho Izalatul-Hadhariaman jamaa bayna salatayni fil-hadhar, amesema:“Hakika Mtume (s.a.w.w.) elieleza wazi kuwa alifanyahivyo kwa lengo la kuuondolea umma wake taabu.

Akawabainishia kuwa inaruhusiwa iwapo wakihitajiakufanya. Hivyo kusema kuwa ila ni mvua baada ya kuwatayari Mtume na maswahaba wapokezi wameshabainishaila yake ni nini, itakuwa ni kuzuwa dhahiri isiyokuwepobali itakuwa ni kuwapinga maswahaba na kumkosoaMwenyezi Mungu na Mtume Wake.

Kwa sababu laiti angefanya hivyo kwa ajili ya mvua basiMtume asingeeleza kinyume, wala wapokeziwasingeacha ila husika na kushikilia ila ya kuondoataabu.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 76

Kukusanya Sala mbili

77

Pia imepokewa toka kwa Mtume kuwa katika usikuwenye mvua alikuwa akimwamrisha mtu anadi: "Salienimajumbani kwenu”. Wala hawakutaja hili katika kuku-sanya, ndio itakuwaje wataje ilihali wameshakanushamvua?

Akaongeza kwa kusema: “Hakika Ibnu Abbas mpokeziwa Hadithi hii alichelewesha Sala akakusanya kwa ajili yakujishughulisha na hotuba, kisha akatumia hoja ya kiten-do cha Mtume kukusanya. Hairuhusiwi kutumia hoja yakitendo cha Mtume kukusanya kwa ajili ya mvuakuthibitisha kitendo cha kukusanya kwa ajili ya hotuba ausomo. Ilihali (Ibnu Abbas) alikuwa anaweza kusitishakwa ajili ya Sala kisha baadae aendelee au amalize somoau hotuba uingiapo wakati wa Sala na wala asipate mad-hara yoyote wala taabu yoyote kama taabu na madharayampatayo mtu atokapo wakati wa mvua na matope. 98

Matokeo: Sheria hii toka kwa Mtume aliyopewa naMwenyezi Mungu ni sheria ya raha inayoweza kutumikazama zote na katika hali zote za maisha ya kisasa vyovy-

98 Izalatul-Hadhari aman jamaa bayna salatayni fil-hadhari, 116-120

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 77

Kukusanya Sala mbili

78

ote yatakavyokuwa.

Atakayechunguza kwa undani maisha ya kisasa ya ki-Magharibi ya biashara na viwanda ataona kuwa kuten-ganisha kati ya Sala mbili hasa Adhuhuri na Al-Asr nijambo gumu na taabu kwa Waisilamu hasa wafanyakazina watumishi. Kiasi kwamba inafikia ima akubali taabuau aache Sala, na inawezekana ikampelekea kukataafaradhi.

Wanazuoni wa sharia wa kisunni wenye mwamkowachukulie umuhimu ndani ya ijtihadi na hesabu zaomsamaha huu uliyotolewa na Uislamu, na wepesi uliolet-wa na riwaya. Wawatangazie watu waziwazi kuwa kuku-sanya Sala mbili Adhuhuri na Al-Asr, Magharibi na Ishani jambo lililoruhusiwa kisheria japokuwa kutenganishani bora.

Hivyo atakaetenganisha atapata ubora wa kutenganisha naatakayekusanya atakuwa katekeleza faradhi ndani yawakati wake.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 78

Kukusanya Sala mbili

79

Maswali na Majibu

Kisha yule asiyeruhusu kukusanya Sala mbili amepingakwa hoja mbali mbali huku akitumia Hadithi ya IbnuAbbas na za wengine kama hoja katika suala hili.Zifuatazo ni hoja zake na majibu yake:

Ya kwanza: Mgongano wa Hadithi ya kukusanya naile ya hanashu:

Habari za kukusanya zinapingana na habari aliyoitoa At-Tirmidhiy toka kwa Hanash toka kwa Ikrima toka kwaIbnu Abbas toka kwa Mtume alisema kuwa:“Atakayekusanya kati ya Sala mbili bila udhuru wowoteatakuwa kaja kwenye mlango kati ya milango ya mad-hambi makubwa.” 99

Nasema: kuwepo Hanash katika mapokezi yake ni dalilitosha juu ya udhaifu wa riwaya hii, na Hanashi ni lakabu99 Sunanut-Tirmidhiy: Juz. 1, Uk. 356

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 79

Kukusanya Sala mbili

80

ya Huseini bin Qaysi Ar-Rahbiy Al-Wasitwiy na yeye nidhaifu mkubwa!

Ahmad amesema: “Huachwa.”

Bukhari amesema: “Hadithi zake hukanushwa walahaiandikwi Hadithi yake.”Abu Zar'ati na Ibnu Mu'ini wamesema: “Ni dhaifu.” An-Nasaiy amesema: “Si mkweli.”

Marat amesema: “Huachwa.” As-Saadiy amesema:"Hadithi zake hukanushwa sana.” Ad-Daruqutniy amese-ma: “Huachwa.” Na Al-Dhahabiy ameiweka Hadithi hiikatika fungu la Hadithi zinazokanushwa. 100

Al-Uqayly amezungumzia Hadithi yake:“Atakayekusanya kati ya Sala mbili bila udhuru wowoteatakuwa kaja kwenye mlango kati ya milango ya mad-hambi makubwa.” Akasema: “Haifuatwi wala haijulikaniisipokuwa kupitia yeye, wala haina chanzo. Imesihi tokakwa Ibnu Abbas kuwa Mtume alikusanya kati yaAdhuhuri na Al-Asr.” 101

100 Mizanul-Itidali, Juz. 1, Uk. 546 maelezo namba 2043101 Tahdhibut-Tahadhibu, Juz. 1, Uk. 538

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 80

Kukusanya Sala mbili

81

Ninaongeza kuwa katika mapokezi yake yumo Ikrimaambaye naye ni dhaifu, Hadithi zake haziwi hoja.

Ya pili: Mgongano wa Hadithi ya kukusanya na ile yausiku wa harusi

Huenda mtu akadhani kuwa riwaya zinazoruhusu kuku-sanya Sala mbili kwa halisi zinapingana na Hadithi yausiku wa harusi aliyoipokea Muslim.

Al-Alusiy ameinukuu ndani ya tafsiri yake toka kwaIbnul-Hamam kwa kusema: “Ibnul-Hamam amesema:‘Hakika Hadithi ya Ibnu Abbas inapingana na aliyoy-apokea Muslim katika Hadithi ya usiku wa harusi kuwaMtume alisema: Usingizini hakuna uzembe bali uzembeni katika hali isiyo ya usingizi kwa mtu kucheleweshaSala mpaka uingie wakati wa Sala nyingine.”

Al-Alusiy baada ya kunukuu maneno haya ya Ibnul-Hamam alisema: Kuna nukta nyingi za kuhoji.102

102 Ruhunil-Maani, Juz. 15 Uk. 134 tafsiri ya Aya: "Simamisha Salalipindukapo jua"

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 81

Kukusanya Sala mbili

82

Katika mdahalo huu kuna nukta nyingi za kuhoji bali zakujibu.

Kwanza: Hadithi ya harusi haijumuishi kukusanya kwakutanguliza bali inahusika na kukusanya kwa kuchelewe-sha tu kwani alisema: “Kuchelelewesha Sala mpakauingie wakati wa Sala nyingine.”

Pili: Kitendo cha Ibnu Abbas kinaonyesha kuwa kuku-sanya kwa Mtume kulikuwa kwa kuchelewesha kwamujibu wa riwaya aliyopokea Muslim kama ilivyotangu-lia kuwa: Siku moja Ibnu Abbas alitutolea muhadharabaada ya Al-Asr mpaka lilipokuchwa jua na nyota zikaan-za kuonekana. Watu wakawa wanasema: ‘Sala! Sala!Mara akaja mtu mmoja wa koo ya Bani Tamim huku aki-sisitiza: Sala! Sala! Ndipo aliposema Ibnu Abbas: ‘Jeunanifundisha Sunna? Eee usiye na mama we!’ Kishaakasema: ‘Nilimuona Mtume amekusanya baina yaAdhuhuri na Al-Asr, na Magharibi na Isha.’ Abdallah binShaqiqi anasema: ‘Hilo likanitia shaka moyoni mwangu,mara moja nikaenda kwa Abu Huraira nikamuuliza,akathibitisha habari ya Ibnu Abbas kuwa ni kweli.”103

103 Angalia riwaya namba 6

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 82

Kukusanya Sala mbili

83

Ni Hadithi ipi kati ya hizo mbili inafaa kuchukuliwa?Hadithi inamaanisha kuchelewesha Sala ya Isha mpakaunaingia wakati wa Sala ya alfajiri, linalounga mkonomaana hii ni kupatikana riwaya katika usiku wa harusi,usiku ambao mtu anajishughulisha na mambo mpakawakati wa alfajiri unaingia.

Ya tatu: Hadithi ya Habib bin Thabiti si hoja

Riwaya ya tatu aliyoitoa Muslim ndani ya upokezi wakeyumo Habib bin Abi Thabiti.

Al-Khatabi ndani ya Maalimu yake ameizungumziaakasema: “Hadithi hii hawaisemi wanazuoni wengi zaidiwa sheria, upokezi wake ni safi isipokuwahawakuzungumza kuhusu Habib.” 104

Anajibiwa kuwa: Kusema kuwa wanazuoni wengi washeria hawaisemi ni kweli, lakini wapo wanaoisema nakuitolea fat'wa, majina yao yameshatangulia. Ama kuhusuwanazuoni wengi sababu ya kutokuichukua ima ni kwakuwa kutenganisha ndio kunakubaliana na ubora

104 Maalimus-Sunan, Juz. 2, Uk. 55, Hadith Na. 1167

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 83

Kukusanya Sala mbili

84

(Ihtiyati), au kwa kuwa inatofautiana na hali aliyoendeleanayo Mtume.

Ama kuhusu ubora ni kuwa imeshatangulia kuwa katikamazingira yetu haya kutoa fat'wa ya kutenganisha nikinyume na ubora, kwa sababu fat'wa hiyo inapelekeawatu kuacha Sala.

Ama kuhusu kitendo cha Mtume ni kuwa yeyemwenyewe alikusanya ili aufahamishe umma wake kuwakuendelea kwake kutenganisha ni Sunna wala si faradhi.

Ama aliyoyasema kuhusu dosari walizozungumza juu yaHabib bin Thabit ni kinyume na aliyoyataja Ad-Dhahabiyndani ya kitabu Mizanul-iitidal kwani amesema: “Watuwote wa Sahih Sita wametoa hoja kutumia Hadithi hii bilakusita. Akasema: Yahya bin Mu'ini: na jamaa wame-thibitisha ukweli wake.” 105

Zaidi ya hapo ni kuwa riwaya hii inapatikana ndani yamoja kati ya Sahih mbili ambazo masunni wameafikianajuu ya usahihi wa Hadithi zake na juu ya kufanyia kaziyaliyomo humo.

105 Mizanul-Itidal, Juz. 10, Uk. 1690

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 84

Kukusanya Sala mbili

85

Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru MwenyeziMungu Bwana wa ulimwengu wote.

Imetarjumiwa na:Hemedi Lubumba Selemani 0773- 0171780715- 0171780754- 017178Dar es Salaam.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 85

Kukusanya Sala mbili

86

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL-ITRAH FOUNDATION:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanzampaka kumi na sita

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Sala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 86

Kukusanya Sala mbili

87

20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua kwa mujibu wa Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mtazamo wa Qur’an na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa

Mtazamo wa Qur’ani na Sunna43. Kupaka juu ya khofu

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 87

Kukusanya Sala mbili

88

BACK COVER

KUKUSANYA SALA MBILI

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kilajambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompatamwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyoMwenyezi Mungu akasema:

"Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neemaYangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoniwa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwaokuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jamboambalo limesababisha kutofautiana kuhusu masuala madodomadogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katikamtiririko wa masomo haya mwandishi amejaribu kuliweka salahili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia yakuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu.

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 88

Kukusanya Sala mbili

89

Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hataisababishe kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo nikuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogoukilinganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati yamadhehebu za Kiislamu. Na mwongozo wetu katika njia hii nikauli ya Mwenyezi Mungu:

"Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyotewala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Munguiliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyozenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu." (3:103)

Kimetolewa na kuchapishwa na:Al-Itrah Foundation P.O. Box 19701,Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Fax: +255 22 2131036Email: [email protected]

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 89

Kukusanya Sala mbili

90

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 90

Kukusanya Sala mbili

91

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 91

Kukusanya Sala mbili

92

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 92

Kukusanya Sala mbili

93

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 93

Kukusanya Sala mbili

94

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 94

Kukusanya Sala mbili

95

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 95

Kukusanya Sala mbili

96

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 96

Kukusanya Sala mbili

97

kukusanya swala mbili.qxd 7/2/2011 10:44 AM Page 97