kwa nini niwe mkristo? - mwokozi.commwokozi.com/downloads/kwa_nini_niwe_mkristo.pdf · hati safi ya...

42
Kwa Nini Niwe Mkristo? Na Weldemar Sardaczuk Roce Publisher P.O.Box 7812, Dar es Salaam, Tanzania

Upload: lamdiep

Post on 24-Jun-2018

606 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

1

Kwa Nini Niwe Mkristo?

NaWeldemar Sardaczuk

Roce PublisherP.O.Box 7812,

Dar es Salaam, Tanzania

2 3

Printed by Jamana Printers Ltd, Dar es Salaam, Tanzania

Kwa Nini Niwe Mkristo?

Published by ROCE PUBLISHER,P.O.Box 7812, Dar es Salaam, Tanzania

Toleo la kwanza 2011Nakala 10,000

ISBN 978-9987-711-03-2

Kwa mawasilianoMaranatha Reconciliation Church,P.O.Box 7812 Dar es Salaam,TanzaniaBarua pepe: [email protected]: www.maranatha-upendo.org

Kilichapwa kwa mara ya kwanza kwa Kijerumani Julai, 1988Kilitafsiriwa kwenda Kingereza na Dorothy LeekKilitafsiriwa kwenda Kiswahili na Marehemu Joel Ludovick Eugene Marchi, 1993Kimehaririwa na kuwa kama kilivyo na Askofu Rodrick Mbwambo Desemba, 2011

ONYOHairuhusiwi kuchapisha au kuhamisha sehemu ya kitabu hiki kwa njia yoyote ile kwa lengo la kuuza. Kama umebarikiwa na kitabu hiki wasiliana nasi katika anwani iliyotolewa hapo juu.

Yaliyomo1. Wanaokumbukwa katika kitabu hiki.........................4

2. Dibaji..........................................................................7

3. Mkristo ni nani?.........................................................8

4. Kwa nini niwe Mkristo?............................................13

5. Jinsi ya kuwa Mkristo...............................................18

6. Ukristo ulio imara....................................................23

7. Hatua za wokovu.....................................................29

8. Kushinda hofu za kimaisha......................................39

9. Mapumziko yanayomfurahisha Mungu...................45

10. Uanafunzi na mashua inayoitwa kanisa..................51

11. Kuomba katika Roho................................................59

12. Hati safi ya afya nzuri.............................................63

13. Hukumu ya mwisho.................................................70

14. Tamati......................................................................78

4 5

Kwa heshima ya:

KaTIKa kipindi hiki cha machafuko na uovu wa kiroho na kimwili, kitabu hiki cha ndugu Weldemar Sardaczuk kinatarajiwa kuonyesha maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu. Kutokana na kweli za kibiblia zinazopatikana katika kitabu hiki, mwandishi ameona vema kutoa tafsiri hii ya Kiswahili, kwa kumbukumbu ya upendo kwa watu wanne walioingia utukufuni kama mashujaa wa Injili. Wakati wa uhai wao, maisha yao yaling’ara na kuwa kielelezo kizuri cha maisha yasiyo na ubinafsi, yenye kumpendeza Mungu na baraka kwa wengine.

Ndugu Hans Gjuka, ni wa kwanza katika kikundi hiki cha mashujaa wa upendo na moyo wa kuwasaidia wengine. Mjerumani huyu mwe-nye moyo wa upendo na huruma kwa yatima, alikuja Tanzania akiwa na umri wa miaka 69, kwa lengo la kusaidia yatima. Mungu alimpa-tia eneo la kujenga kijiji cha yatima katika mji mdogo wa Kemondo, mkoani Kagera. Hata hivyo baada tu ya kuweka msingi wa jengo la kwanza, aliingia utukufuni mwaka 1991 Februari.

Mwinjilisti David Gabriel Maeda

Mwingine katika kundi hili, ni kijana mdogo wa Kitanzania aliye-ungana na Bwana akiwa na umri wa miaka 32. Huyu alipigwa hadi kufa, alipokuwa akigawa maandiko na misaada ya kibinadamu, kwa wakimbizi wa Rwanda. Wakimbizi hawa waliokuwa wamewe-

ka kambi yao katika eneo la Benako, wilayani Ngara -Tanzania.

Ingawa mambo yalionekana kwenda sawa katika ulimwengu wa kimwili asubuhi ya tarehe 1 Novemba, mwaka 1994, katika ulim-wengu wa roho, Shetani alikuwa wamekamilisha mpango wa kum-wangamiza kijana huyu. akiwa hajui hili wala lile, Marehemu David Maeda alianza kugawa maandiko huku akitoa tabasamu lisilo na unafiki. Katikati ya huduma hii ya kimisheni, watu waovu wasio na upendo wa Kristo, walimvamia na kumteka nyara. Walioshuhudia kuuawa kwake, walisimulia tukio hilo kwa machozi, huku wakifa-nanisha kifo chake na kile cha Stefano wa agano jipya!

Baada ya kupigwa pigo la kwanza kwa kutumia chuma kizito, shujaa huyu aliwaambia watesi wake, “Njooni kwa Yesu!” Ingawa pigo la pili tayari lilikuwa limepasua kichwa chake, bado aliendelea kuwashuhudia watesi wake kwa kuwaambia, “Yesu anawapenda!” Pigo la tatu liliposhuka kichwani mwake, aliwaleta watesi wake madhabahuni kwa kuwaambia, “Mwaminini Yesu!” Pigo la mwisho lilimaliza nguvu zake, na hapo akaanguka chini huku akisema “amen!”

Mchungaji E. Masatu

Kama kumaliza mwendo kwa Hans na Maeda, kumeanza kuten-geneza machozi ndani ya kope za macho yako, nakuomba ujikaze ili tukamilishe safari ya mashujaa waliosalia.

Mchungaji E. Masatu ni mtumishi aliyekuwa na msimamo wa aina yake katika kumpenda Mungu na kuwasaidia wengine. Katika mi-aka hii ambayo watu wengi wanataabikia matumbo na maisha yao, yeye alikuwa na kiu moja tu katika maisha yake, kuuona ufalme wa Mungu ukikua na kuimarika. Mara tu baada ya kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wake, shauku kubwa iliumbika ndani yake ya kuona kanisa la Kibiblia likichipua katika kila kona ya taifa la Tanzania. La kusikitisha ni kuwa, ingawa miguu yake ilikuwa tayari kwenda kila mahali, alifanikiwa tu kupandikiza kanisa moja katika rasi ya Kigamboni, Dar es Salaam.

Huyu naye akafikwa na mauti wa ghafla, pale lori la mchanga lili-pokutana uso kwa uso na pikipiki yake. Tukio hili lililoacha baadhi

6 7

ya viungo vyake vikiwa vimetapakaa barabarani, lilimaliza mwendo wa mtumishi huyu, tarehe 17 mwezi wa Machi, mwaka 2000!

Mmishenari Dieter Basson

Mpaka kufika hapa unaweza kuona wazi kuwa, mbingu imefurika watu walio na shuhuda za kushangaza za watu waliompenda Yesu zaidi ya vile walivyoyapenda mapigo ya mioyo yao!

Ndugu Dieter Basson, ni wa mwisho katika orodha ya mashujaa wa injili wanaokumbukwa katika kitabu hiki. Huyu naye baada ya sa-fari nyingi za kimishenari juu ya milima na mabonde ya Tanzania, mauti ilimtenganisha na huduma ya kuipeleka Tanzania kwa Yesu. alifikwa na mauti katika ajali ya gari tarehe 19 agosti, mwaka 2000, katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma.

Mengi yanaweza kuzungumzwa juu ya kijana huyu, ila niyaungan-ishe tu kwa kusema kuwa, alimpenda Yesu kwa dhati. Kutokana na utii na upendo wake, kila wakati alikuwa tayari kwenda mwendo wa ziada ili kugusa mahitaji ya kiroho na kimwili ya watu wa mari-ka yote. Hata safari iliyosababisha kifo chake, ilikuwa ni ya kuwa-sumbukia wahitaji. alikuwa anakwenda kununua mahindi kwa ajili ya maskini wasiokuwa na chakula!

DibajiUkiangalia umri ambao Ukristo umekaa duniani, na idadi ya Wakristo waliopo, unaweza kudhania kuwa kila mtu anajua maana ya kuwa Mkristo. Hata hivyo, idadi kubwa ya watu duniani, hawafahamu maana ya kuwa Mkristo. Kutokana na mkanganyiko huu kuhusu Ukristo wa kweli, naomba ujiulize swali lifuatalo: “Je, hivi Mkristo ni mtu wa namna gani?” Sanjari na swali hili, jiulize kibinafsi, ikiwa u Mkristo au la. Kama una uhakika na Ukristo wako, ilitokeaje hata ukawa Mkristo?

Hali kadhalika, hebu jiulize ikiwa kuna tofauti yoyote iliyo wazi, kati yako na watu wengine wasio Wakristo. Je, unaweza kuwaelezea wengine kwa kina kuhusu Ukristo wako? Kama unaweza kufanya hivyo, ninakupongeza licha ya kuwa sijawahi kukutana nawe. Hata hivyo, watu wengi niliowauliza kuhusu swali hili, walinijibu kwa hu-zuni na kusema, “samahani, sielewi!”

Mwandishi

8 9

Mkristo ni nani?

Majibu kutoka Ulaya

Kile ninachoenda kukueleza kinaweza kuonekana kama utani, ila ni jambo la kweli lililotokea katika mji mmoja huko Ujerumani wakati nilipowauliza watu kadhaa ikiwa wanafahamu maana ya Ukristo. Vijana wawili walionekana kutekewa huku kila mmoja akimtegea mwenzake ajibu. Ingawa walikuwa wameingia rika la watu wazima kulingana na taratibu za dhehebu lao, walikiri kuwa walikuwa ha-wajui.

Nilipomwuliza mwanamke mmoja ikiwa anaelewa maana ya kuwa Mkristo, alijibu kwa kusema: “Ingawa ninahudhuria kanisani kila Ju-mapili na kuimba kwaya, nikiri wazi kuwa sina jibu sahihi la swali hilo!” Nikiwa nimeshikwa na mshangao nilimuuliza ikiwa hajawahi kufafanuliwa na mchungaji wake kuhusu swali hili. Jibu lake lili-kuwa, “Hapana, mchungaji wangu hajawahi kufanya hivyo!”

Kutokana na jibu lake, nilipata mpenyo wa kuingia ndani zaidi ka-tika maongezi yangu na yeye. Nilipomwuliza ikiwa yeye ni Mkristo, alisema hapana. Katika kile kilichoonekana kutotaka kunivunja moyo, aliongeza kwa kusema, “nadhani Ukristo ni jambo linalohusu maombi.” Hapo tena nikataka anieleze ikiwa maombi yake yalikuwa yanajibiwa. “Wakati mwingine ndiyo na wakati mwingine hapana.” Hayo tu ndiyo mwanamke huyu aliyofahamu kuhusu swali letu la

Mkristo ni nani?

Kwa wengine nikiri wazi kuwa nimepata majibu yasiyo na kichwa wala miguu. Kwa mfano, yuko mmoja aliyejibu kwa kusema, “kuwa Mkristo ni kuishi sawasawa na hotuba ya Yesu aliyoitoa mlimani!” Wengine wakasema, “ni kushika amri kumi” au “kutenda matendo mema.”

Majibu nje ya Ulaya

Nilipokuwa afrika nilikutana na majibu ya kutia moyo kuhusiana na swali hili. Wakati fulani baada ya kumaliza kugawa misaada ya kibinadamu nchini Uganda, mimi na rafiki yangu tuliingia hotelini upande wa Kenya, ili kupata chakula. Hapo tulikutana na kijana wa Kiafrika aliyetuhudumia vizuri. Tulipokaribia kuondoka, nilimwuliza ikiwa yeye ni Mkristo. “Ndiyo, mimi ni Mkristo”, alijibu huku ma-cho yake yakiwa yamejaa nuru yenye matumaini. Kisha akaongeza kusema, “Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yangu!”

Huku nikiwa nimeguswa na jibu lake, nilimuuliza ikiwa yeye ni mshirika wa kanisa lolote. Hapo tena bila kusita jibu lake lilikuwa ni Ndiyo, kisha akataja dhehebu linalomlea kiroho. alibatizwa katika dhehebu hilo na baadaye akaamua kuwa mshirika mwaminifu ka-tika dhehebu hilo. Hapo tukafurahi pamoja na mwamini mwenzetu mpya katika Bwana.

Nimekutana na visa vya kutia moyo vinavyofanana na hiki karibu kila mahali nilipokwenda. Siku moja nilipokuwa angani ndani ya ndege kati ya Kanada na amerika, nilimuuliza mhudumu mmoja wa ndege ikiwa ni Mkristo. Bila kusita alijibu na kusema, “Nilikuwa Mka-toliki ila kwa sasa nimeokoka, na nimejazwa Roho Mtakatifu.” Kwa sauti ya furaha, alimwita mhudumu mwingine aliyekuwa ameokoka ili aje kunisalimia.

Baada ya kutambulishana alitamka maneno yafuatayo; “Nasikiti-ka kuwa ndani ya ndege hii, hakuna mahali tunapoweza kufanya faragha ya maombi!” alinitambulisha pia kwa mhudumu mwingine ambaye licha ya kuwa ameokoka, bado alikuwa hajabatizwa kwa

Sura ya 1

10 11

Roho Mtakatifu na ishara ya kunena kwa lugha mpya. alituomba tumwombee huku akifanya utani kwa kusema, “kwa kuwa tuko mawinguni huenda tuko karibu zaidi na mbingu!”

Hebu nikueleze jambo lililonitokea nilipokuwa katika mji wa Berlin nchini Ujerumani. Nilikuwa hapo na kikundi cha vijana waliookoka tukifanya uinjilisti mitaani. Baadhi ya watu walisimama kutusikiliza na wengine walitucheka na kuondoka. Wakati nilipokuwa nikizun-gumza habari za Yesu, alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa akiingilia mara kwa mara mazungumzo yangu kwa kusema. “ Nyamaza, acha kutueleza habari za Mungu wako aliyepitwa na wakati. Huyo Mun-gu wako hata hayupo!”

Mojawapo ya mambo nisiyoyapenda ni pale watu wawili wanapos-hindana kuzungumza kwa wakati mmoja. Kutokana na kukerwa na maneno yake nilimshika mkono, kisha nikamwambia, “Nimefurahi kukutana na Kafiri, katikati ya jiji kubwa hili la Berlin.” Huku akiwa amekasirika, alinijibu kwa ukali kwa kusema, “Kwa nini unanidhal-ilisha namna hii? Ninaamini mimi ni Mkristo mzuri kuliko wewe!”

Ndugu mbona unanishangaza, nilimjibu. Muda mfupi uliopita ulise-ma kuwa hakuna Mungu na hata Yesu hajawahi kuishi duniani. Tena umesema Biblia ni kitabu chenye hadithi za kutunga na hata habari za watu wanaotajwa huko ni za uzushi. Hiyo ndiyo imani yako, iweje tena uniambie kuwa wewe ni Mkristo, tena mzuri kuliko mimi? Mtu huyu ni mfano wa watu wanaojiona kuwa wanajua mengi kuhusu Ukristo, kumbe ni mbumbumbu wasiojua kitu.

MAMBO YASiYOMfANYA MtU KUwA MKRiStOIngawa mambo yafuatayo ni mazuri pale yanapofanyika ndani ya wokovu, kamwe siyo yanayomfanya mtu kuwa Mkristo.

Matendo mema

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (waefeso 2:8). Kama nilivyotangulia kusema, matendo mazuri ni kitu chema pale yanapofanyika ndani ya wokovu. Hata hivyo kulingana na andiko hili, matendo haya siyo yanayomfanya mtu awe Mkristo. Wokovu hupatikana bure kwa neema, kupitia damu ya Yesu.

Kuzungumza na Mungu katika maombi

Maombi ni moja ya taratibu za ibada zinazofanywa na watu wa dini mbalimbali duniani. Baadhi ya watu hujitesa kwa kutokula na kunywa ili maombi yao yajibiwe na wako wanaojikata kwa visu na kuomba wakiwa juu ya vitanda vya misumari ili miungu ijibu maombi yao. Hata katika ulimwengu wa Wakristo, kuna mamilioni ya watu wanaomwomba Mungu usiku na mchana. Ingawa neno la Mungu limewaagiza watu wamwombe Mungu bila kukoma, bado maombi, siyo yanayomfanya mtu awe Mkristo.

Kuhudhuria misa kanisani

“wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na des-turi ya kukutana, tuhimizane sisi kwa sisi kadri tuonavyo siku ile inakaribia” (waebrania 10:24). Kukusanyika pamoja katika ibada takatifu, ni jambo jema lililoagizwa na Mungu mwenyewe. Ingawa misa hizi zinaweza kumwongoza mtu kupata wokovu, bado kuhud-huria ibadani, siko kunakomfanya mtu akubalike mbele za Mungu kama Mkristo. Ubatizo wa maji

“Ndugu zetu, tufanye nini?” Petro akawajibu, “tubuni, mkabatiz-we kila mmoja wenu akabatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate

12 13

kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38). Petro alipoulizwa mambo ya msingi yanayofuata baada ya mtu kutubu dhambi zake, alitaja ubatizo wa maji kama mojawapo ya mambo hayo. Hakusema batizweni mka-tubu, bali, tubuni mkabatizwe. Kwa kuwa toba ya kweli ndiyo in-ayozaa wokovu, jibu la Petro linaonyesha wazi kuwa, ubatizo wa maji sio unaoleta wokovu.

Ubatizo wa maji uwe wa kibiblia au wa mapokeo ya kidini, haum-fanyi mtu kuwa Mkristo. Katika hili ni vema tutambue kuwa ubatizo usiotanguliwa na wokovu, hauna faida yoyote.

Sakramenti ya kipaimara.

Ingawa madhehebu mengi yanatukuza sakramenti mbalimbali iki-wemo hii ya kipaimara, sakramenti hizi haziwezi kumwingiza mtu ndani ya moyo wa Mungu. Zinaweza kuwa taratibu nzuri za kimad-hehebu, ila hazimfanyi mtu kuwa Mkristo. Wakati mwingine hata wachungaji wanaozitoa sakramenti hizi, ni watu wasio na uhu-siano na Mungu. Kwa kuongezea niseme wazi kuwa hata kushiriki kikamilifu katika sikukuu za Kibiblia na kuamini juu ya kuwepo kwa Mungu, navyo havimfanyi mtu kuwa Mkristo.

KiNACHOMfANYA MtU KUwA MKRiStO

Kama mambo haya yote tuliyoyataja hayamfanyi mtu kuwa Mkris-to, ni kitu gani cha msingi kinachomfanya mtu awe Mkristo? Ingawa swali hili ni kubwa, Biblia inatupatia jibu. Jambo la kwanza, ni vema utambue kuwa heshima ya kuitwa Mkristo, ni jambo linalohusiana na Yesu Kristo. Neno ‘Mkristo’, linalotokana na neno Kristo. Biblia inasema wazi kuwa wanafunzi wa Yesu waliitwa Wakristo, kwa mara ya kwanza huko antiokia (Matendo 11:26).

Kupitia andiko hili, Mkristo anaweza kuelezewa kama mtu anayem-wamini Yesu na kuishi maisha yanayofanana na yale Kristo aliyoyai-shi alipokuwa duniani. Hali kadhalika, Wakristo tunaweza kuwael-ezea kama watu waliokaribisha utawala wa Mungu katika maisha yao. Ni watu walio tayari kumwishia Yesu katika kipindi chote cha maisha yao na wako tayari kufa ikibidi, kwa ajili ya kulinda ushirika wao na Yesu.

Kwa nini niwe Mkristo?

Je, hili ni swali ambalo na wewe unajiuliza? Ikiwa kuwa Mkristo ni jambo litakalonichosha na kunifanya nipoteze uhuru wangu, kuna haja gani ya kuwa Mkristo? Ni kwa nini niwe Mkristo ikiwa kwa ku-fanya hivyo, itanilazimu kumuuliza Mungu kila siku, lile ninalotaki-wa kufanya na lile nisilotakiwa kufanya? Kuna sababu gani katika ulimwengu huu wa uhuru na utandawazi, mtu atake kumtegemea mwingine? Ili kulijibu swali hili, fuatana nami katika kisa hiki kili-chotokea katika mkutano wa injili mjini Berlin.

Siku moja tulipokuwa katika hema la mkutano, mtu mmoja alitujia na kutuuliza kile kilichokuwa kikiendelea katika hema hilo. “Je, hili ni hema la kuuzia pombe au ni la michezo ya sarakasi?”, aliuliza. “Hapana”, nilimjibu, “hili ni hema la mkutano wa injili na huwa tu-nakuwa na ibada kila siku jioni.” Kwa dharau alitikisa kichwa na kucheka kwa sauti kubwa, kisha akasema, “Unasema nini? Hakuna mtu anayemwamini Mungu huyo aliyepitwa na wakati!” Bila ku-kawia nilijibu kwa kumwambia, “mimi ni miongoni mwa wale wa-naomwamini huyo Mungu unayemwona kuwa amepitwa na waka-ti.”

Huku akionekana kukerwa na jibu langu, alijibu kwa hasira na kuse-ma, “Nyamaza! sitaki kusikia habari za huyo Mungu wako, Mungu

Sura ya 2

14 15

huyo hayupo na hata kama yupo, sina haja naye!” Nilimtizama kwa upendo kisha nikamwuliza ikiwa angependa nimsimulie hadithi moja inayoendana na mazungumzo yetu. utisho wa Mungu ulimkamata na akakubali kunisikiliza.

Rafiki, hebu piga picha kuwa unatembea kando ya ziwa, na ghafla unasikia kelele ndani ya maji za mtu anayetaka msaada. Hapo kwa kusukumwa na upendo, unahatarisha maisha yako kwa kuruka ndani ya maji, kwa lengo la kumwokoa. La kushangaza ni kuwa, baada ya kumwokoa, mtu huyu anaonekana kutojali wema na msaada uliom-patia. Kitu pekee alichofanya, ni kukung’uta uchafu mwilini mwake na kwenda zake bila kusema neno lolote la shukrani! Je, ungemlin-ganisha mtu huyo na kitu gani? “Ndugu, mtu huyu ni kama ngu-ruwe”, alijibu kwa sauti kubwa. Basi, wewe ndiwe, huyo nguruwe! nilimjibu kwa upole na nashukuru kuwa hakunitia kabali.

Ukimya aliouonyesha baada ya kumpatia jibu hilo, ulinipa ujasiri wa kuendelea kusema naye. Ndugu, jibu lako ni sahihi, yeyote anayem-fanyia hivyo mtu aliyeokoa maisha yake, ni mbaya kuliko nguru-we. Lakini wewe umesema nini muda mfupi uliopita kuhusu Yesu? Yeye alitoa maisha yake ili kutuokoa na mauti ya milele. alikufa kifo cha aibu kilichojaa mateso mengi ili mimi na wewe tusipotee katika Jehanamu ya moto. Mgongo wake ulijaa majeraha kutokana na kuchapwa mijeledi na askari wa Kirumi. Tena nyama ya kichwa chake ilitobolewa na miiba iliyosokotwa kama taji, na kusukumizwa kichwani mwake! Hakika alikutana na maumivu makali, yasiyo na mfano.

Baada ya mateso haya yanayotia simanzi katika kuyasimulia, wal-imtemea mate usoni, na kumbebesha msalaba mzito, hadi Golgotha. Walipofika mahali hapo paitwapo Fuvu la kichwa, walirarua mavazi yake, kisha wakapigilia mikono na miguu yake juu ya mti uliolaani-wa. Ni vigumu kuelewa ukali wa maumivu yaliyompata, wakati walipouinua ule mti (msalaba) na kuukita ardhini! Yeye hakuwa na hatia yoyote, hata maadui zake hawakupata neno lolote la kumtia hatiani. alichukua adhabu iliyotustahili, ili atuokoe dhambini kupi-tia mauti yake.

Mpaka kufikia hatua hii, bado rafiki yangu alikuwa amesimama

kimya huku akiwa amefadhaika. Mtu ambaye mwanzoni alione-kana kuzungumza bila mpangilio, aligeuka kuwa msikilizaji mzuri mwenye shauku ya kujua ukweli. Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana zinaelezea kwa undani mateso ya Yesu na kusulubishwa kwake. Mateso na kifo chake, ndivyo vilivyonifanya niwe Mkristo. Nimefanya uamuzi huo kama shukrani yangu kutokana na kukubali kwake kuteseka na kuangikwa mtini kwa lengo la kuyaokoa maisha yangu. Hakika alikufa na kufufuka kwa ajili yangu!

Umuhimu wa kufufuka kwa Yesu

Kitendo cha mtu kufa kamwe sio cha ajabu kutokana na ukweli kuwa, watu wasiopungua milioni moja hufa kila siku, duniani kote. Muujiza tunaokutana nao katika kifo cha Yesu, uko katika kufufu-ka kwake na kuendelea kuishi, bila kurudia kaburi. Ufufuo wake ni mhimili mkubwa unaoshikilia Ukristo wangu. Kufufuka kwake ku-nathibitisha kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu aliye hai.

Baada ya kufufuka, maandiko yanasema kuwa aliwatokea watu 500 wakiwa mahali pamoja. “Na kwamba alimtokea Kefa, kisha aka-watokea wale kumi na wawili. Baadaye akawatokea wale ndugu waamini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala (1 wakorintho 15:5-6). Ni kweli Yesu amefufuka na yu hai! Biblia inaonyesha wazi jinsi alivyowatokea wanafunzi wake wakiwa ndani ya nyumba, huku milango ikiwa im-efungwa. alizungumza nao, na hata akawaonyesha alama za mis-umari katika mikono yake. Naye Tomaso aliyekuwa na mashaka, alipewa nafasi ya kuweka vidole vyake katika kovu lililokuwa uba-vuni mwake. Ili kuthibitisha kuwa ni yeye na sio mzimu, alikula mi-kate na samaki, akiwa na wanafunzi wake.

Uamuzi wangu wa kuwa Mkristo

Sababu ya kwanza iliyonifanya niwe Mkristo, ni ili niungane na Yesu katika mauti na kufufuka kwake. Kuungana naye katika mauti na kufufuka kwake, kunaniwezesha kuishi maisha aliyoyaishi waka-ti alipokuwa hapa duniani. atanirithisha tabia yake ya kumpenda Mungu na kuichukia dhambi. Hali kadhalika, kwa kuwa Yesu ame-

16 17

pewa mamlaka yote mbinguni na duniani, atatumia mamlaka hiyo kunilinda, kunibariki na kunitia moyo. Kuwa Mkristo ni zaidi ya kuwa na urafiki na Yesu. Ni kuwa na mtu aliyeshinda mauti na Kuz-imu anayekuwakilisha na kukutetea mbele za Mungu.

Inakupasa kuwa Mkristo ili uokoke dhidi ya hukumu ya Mungu na maangamizi ya milele. Huu ndio ukweli ambao kila mtu anatakiwa aujue. Mara zote tunapowapenda wengine, ni lazima tuwaeleze uk-weli kuhusu kupotea milele, kunakowangojea waliokataa Ukristo wa kweli. Biblia inasema wazi kuwa, “Yeyote anayemwamini Mwana anao uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake” (Yohana 3:36).

Kamwe Jehanamu sio mahali palipobuniwa ili kuwaogopesha watu, kama baadhi ya watu wanavyofikiria. Ingawa watu wengi wanad-hania kuwa Mungu wa upendo hawezi kuwatupa watu Jehanamu, dhana hii ni potofu. Ukweli ni kuwa Mungu anaichukia dhambi, na ataiadhibu hata pale inapokuwa kwa watu aliowaumba kwa sura na mfano wake. Hivyo ndivyo alivyofanya kwa watu wa Sodoma na wale wa kizazi cha Nuhu.

Kushiriki baraka zinazotokana na mabadiliko makubwa yanayotokea pale mtu anapompokea Yesu, ni sababu nyingine iliyonifanya niwe Mkristo. Ndani ya Biblia na katika maisha ya kila siku kuna mifano mingi ya watu wabaya, waliobadilishwa na kuwa watu wema baa-da ya kufanya uamuzi wa kuwa Wakristo wa kweli. Sauli, alibadil-ishwa kutoka kwenye uuaji wa watu wa Mungu, na kuwa Mkristo aliyekuwa tayari kuifia imani yake.

Katika kitabu cha Matendo, tunasoma habari za kuokolewa kwa mchawi maarufu aliyejulikana kama Simoni. alipoamua kuwa Mkristo wa kweli, nguvu ya Mungu ilimtenganisha na uchawi na kumfanya awe mwanafunzi wa Yesu. “Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kuwa yeye ni mtu mkuu...naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona” (Ma-tendo 8:9-13).

Jambo la kujifunza hapa ni kuwa, kamwe haiwezekani mtu awe Mkristo na wakati huohuo awe mchawi au mshirikina. Kuwaendea waganga kwa lengo la kutafuta zindiko la biashara, nyumba, kazi, ulinzi, mafanikio kwenye masomo au kupanda cheo, ni uthibitisho wa kutokuwa na Yesu moyoni. Kitendo cha watu wabaya kubadi-lika na kuwa wema, ni ishara nyingine ya wazi inayoonyesha ukuu na uweza wa Yesu. Watu ambao hapo mwanzo walikuwa walevi, majambazi, malaya, wachawi, wezi, mafisadi na kadhalika, wame-badilishwa na nguvu za Yesu kuwa watu wa kufaa katika jamii.

Sababu ya tatu iliyochangia kunifanya niwe Mkristo, inatokana na matendo ya kushangaza yanayotokana na udhihirisho wa nguvu za Yesu. Miujiza na ishara zinazofanywa na Wakristo wa kweli, ni nguzo imara inayoshikilia maisha yangu ya Ukristo. Kupitia injili na maombezi yao, wagonjwa hupona, vipofu huona, viwete hutem-bea, viziwi husikia, pepo wabaya hufukuzwa, ndoa zinakuwa na amani, wafu hufufuliwa pamoja na miujiza mingi inayofanana na hii. Mambo haya yalitendeka katika siku za Biblia na yanaendelea kutendeka katika siku zetu. “Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona” (Marko 16:17).

Ingawa ulimwengu una imani na dini nyingi, kamwe sijawahi kuona mambo haya yakitendeka katika imani zingine nje ya Ukristo. Badala yake nimeona maelfu ya watu wa imani na dini mbalimbali wakilet-wa kwa Yesu, ili akutane na matatizo yao. Miujiza inayotokea pale Wakristo wa kweli wanapohubiri na kufanya maombezi, inaonyesha wazi kuwa Ukristo peke yake ndiyo njia sahihi inayowapeleka wan-adamu kwa Mungu. “wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).

18 19

Jinsi ya kuwa Mkristo

Baada ya kuangalia kwa undani sababu zinazotufanya tuwe Wakristo katika sura iliyopita, sasa tuangalie jinsi mtu anavyoweza kuwa Mkristo. Kama tulivyotangulia kuona katika sura iliyopita, watu wabaya kupindukia waliposikia injili na kuiamini, injili iliwa-badilisha na kuwa watu wa baraka na wa kutegemewa katika jamii. Ili upate picha kamili vile mtu anavyoweza kuwa Mkristo, naomba tuangalie kile kilichotokea mjini Yerusalemu, wakati wa siku kuu ya Pentekoste.

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya pili tunasoma kuhusu maelfu ya watu waliokusanyika mjini Yerusalemu, ili kusherehekea siku kuu ya Pentekoste. Ni katika sherehe hii, ndipo waliposhuhudia mmwagiko mkubwa wa kihistoria wa Roho Mtakatifu. Watu hawa waliwasikia wanafunzi 120 wa Yesu, wakimsifu Mungu kwa lugha mbalimbali, baada ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Watu hawa waliowakilisha mataifa kumi na tano, walishangaa walipowasikia wanafunzi hawa wasio na elimu, wakiomba na kumsifu Mungu kwa lugha za mataifa ya kigeni!

Katikati ya mshangao huu, Petro alisimama na kuhubiri ujumbe we-nye nguvu za Mungu, kuhusu kufufuka kwa Yesu. aliwathibitishia kuwa Yesu yu hai na ndiye aliyesababisha tendo hilo la kushangaza.

Baadhi ya watu waliousikia ujumbe wake walidharau na kuondoka kwa kiburi, ila wengi, waliuona kama nafasi ya kipekee ya kuujua ukweli. Huku wakiwa wamefadhaika waliwaendea mitume na ku-wauliza wakisema, “Ndugu zetu, tufanye nini?” Petro akawajibu, “tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38).

Kulingana na ujumbe wa Petro, ziko hatua tatu ambazo mtu anataki-wa kuzichukua ili neema ya Mungu iweze kutenda kazi katika maisha yake. Hatua ya kwanza ni kutubu au kubadilisha mwelekeo. Kutubu hutokea pale mtu anapokuwa na huzuni ya dhati, kuhusu maisha yake ya dhambi. Katika hili, wako wanaoweza kujificha ndani ya matendo yao mema, na kujiona kama watu wasio na dhambi. Hata hivyo Biblia inaikosoa dhana hii, kupitia maneno yafuatayo: “Kwa sababu wote wametenda dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (warumi 3:23).

Baada ya mtu kuchukia maisha ya dhambi aliyokuwa akiyaishi, anatakiwa kuomba msamaha mbele za Mungu kwa kumaanisha.

Hatua ya pili inahusu imani. Hapa ni kuamini vile neno la Mungu linavyosema kuhusu kujidhabihu kwa Yesu na jinsi wokovu unavyo-patikana. Biblia inasema wazi kuwa, Yesu Kristo aliteseka na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. alizichukua dhambi zetu katika mauti yake. Hali kadhalika, katika waraka wa Paulo kwa Warumi tunasoma maneno yafuatayo: “Kwa kuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka” (warumi 10:13). Hatua ya tatu, ni kubatizwa kwa maji kama ishara ya kuingia katika agano la uaminifu na Mungu. Hatua hizi tatu zinaonekana katika andiko lifuatalo: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa” (Marko 16:16).

Sanjari na hatua hizi, baada ya kuokoka, mwamini anatakiwa aba-tizwe kwa Roho Mtakatifu. Tendo hili litamwimarisha na kumfanya kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu. Ukiangalia katika kitabu cha Matendo ya Mitume, utaona kuwa kila mahali injili ilipohubiriwa, mambo haya manne yaliweza kufanyika. Watu walitubu, waliamini na walibatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu. Wakati fulani,

Sura ya 3

20 21

Petro alishangaa kuona mambo haya yakitendeka kwa watu wasio Wayahudi. aliporudi Yerusalemu, aliwasimulia wenzake jinsi watu wa mataifa walivyokutana na Mungu kama ilivyotukia kwao. “iki-wa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyo-tushukia sisi mwanzo” (Matendo 11:15).

Ujumbe wa Petro kwa watu wa Kaisaria unapatikana kwa kina ka-tika Matendo 10:34-48. Baadaye Mtume Paulo alihubiri ujumbe un-aofanana na huu, akiwaagiza watu wote watubu. “Zamani za wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu” (Matendo 17:30). Kama nilivyotan-gulia kusema, toba ni kugeuka. Ni kuacha kutembea katika baraba-ra pana na kutembea katika barabara nyembamba.

Uamuzi wenye busara

Baada ya kusikia kuhusu hatua zinazomwezesha mtu kuwa Mkristo wa kweli, sasa unayo hiari ya kuchagua. Je, bado kipo kikwazo ki-nachokuzuia kuwa Mkristo wa kweli? Nakuuliza swali hili, huku ni-kielewa kuwa huenda wewe ni Mkristo, ila bado hujaokoka (hujawa Mkristo wa kweli) au huenda wewe ni mfuasi wa imani nyingine nje ya Ukristo. Kama huna kikwazo cha kukuzuia, Je, uko tayari kuokoka sasa? Kumbuka kuwa wokovu ni jambo la baraka sana lisilotakiwa kungojea au kuomba ruhusa kwa mtu mwingine. Neno la Mungu linasema wazi kuwa saa ya kuwa Mkristo wa kweli ni sasa. “Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia; Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa” (ii wakorintho 6:2).

Kama uko tayari kuachana na imani zilizokufa na kuingia katika Ukristo wa kweli, maelezo yanayofuata yatakusaidia kufanya hivyo. Jambo la kwanza, soma kifungu cha maneno yafuatayo na kuy-aamini. “tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:19). Yatendee kazi maneno ya andiko hili kwa kutafuta mahali pa utulivu utakapokaa peke yako. Baada ya kupata eneo la jinsi hii, anza kuzungumza na Mungu anayependa kubadilisha moyo na maisha yako. Neno la Mungu linasema kuwa, ataondoa moyo wa

kijiwe ndani yako na kukupa moyo wa nyama (Ezekieli 11:19).

Katika kuongea naye, tubu dhambi zako kwa kumaanisha huku uki-kumbuka kuwa, Yesu Kristo amepewa mamlaka yote na Baba yake (Mathayo 28:19). Katika maombi haya ya kujikabidhi kwa Yesu un-aweza kusema sala hii kwa kumaanisha. “Mungu Baba nimechoka kuishi chini ya vifungo vya dhambi. Naomba unisamehe dhambi nilizofanya na ninaomba unitenge na laana za dhambi hizo. Ni-nampokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Najiweka chini ya uongozi wako na ninaahidi kukutumikia kwa moyo wangu wote. Naamini umenisamehe na kunifanya mmoja wa watoto katika familia yako. Amen”

Kwa kuwa umeungama dhambi zako kwa kumaanisha, amini kuwa umesamehewa na kupatanishwa na Mungu. Moyo wako uliokuwa maskani ya wanyama wabaya wanaowakilisha dhambi, unaoone-kana katika mchoro unaofuata, umesafishwa na damu ya Yesu.

22 23

Badala ya kuwa maskani ya wanyama wabaya, sasa moyo wako umekuwa maskani ya Roho Mtakatifu, kama unavyoonekana katika picha ya pili.

Kumbuka kuwa neno la Mungu linasema wazi kuwa, “Mungu hu-wasamehe wote wanaoziungama dhambi zao kwa kumaanisha...” (1 Yohana 1:5-9). Kutokana na msamaha ulioupokea, wewe sasa u mtoto katika familia ya Mungu. Unaweza kujiita Mkristo wa kweli, kwa kuwa u mali ya Kristo. Maandiko yafuatayo yanaweza kuku-thibitishia kuhusu maisha mapya uliyoyapokea. Yohana 1:11-14; 1 Petro 1:23; 1 Yohana 3:1-2).

Ukristo ulio imaraKwanza nakupongeza kutokana na uamuzi wa busara ulioufanya wa kuwa Mkristo wa kweli. Naomba tu nikutahadharishe kuwa Shet-ani atakufuatilia ili akurudishe katika gereza la dhambi. atajaribu kuwarejesha ndani ya moyo wako wale wanyama wanaowakilisha dhambi, waliofukuzwa siku ile ulipoamua kuokoka. Jitihada zitaka-zofanywa na Ibilisi kukurudisha katika maisha ya dhambi, zinaone-kana katika mchoro unaofuata. Katika mchoro huu, Shetani ana-jaribu kuingiza wanyama ndani ya moyo wa mtu aliyeamua kuwa Mkristo wa kweli.

Sura ya 4

24 25

wasimulie wengine kuhusu maisha mapya uliyoyapokea. Unataki-wa kufanya hivyo pasipo kukawia na bila aibu. Kwa kuwa umepata dawa ya tatizo kubwa kuliko yote duniani, unatakiwa uwaeleze wengine kuhusu dawa hii. Huu ndio wakati muafaka kwako, kuten-geneza na watu uliokwaruzana nao. Zoezi hili liendane na kuomba msamaha, kwa wale uliowakosea. Hali kadhalika, kama ulikuwa unadaiwa na mtu yeyote, huu ndio wakati mzuri wa kuzungumza na mtu huyo kuhusu deni hilo.

Batizwa katika maji

Kwa baadhi ya watu hatua hii inaweza kuwa ngumu kuliko hat-ua zingine, katika somo hili la kuukulia wokovu. Petro alipohubiri wakati wa siku kuu ya Pentekoste, aliwaambia wasikilizaji wake kuwa, wanatakiwa kutubu na kubatizwa. “tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu akabatizwe kwa jina la Yesu Kristo...” (Matendo 2:38). Ubatizo wa kibiblia ni ule unaofanyika kwa njia ya kuzamishwa ma-jini, baada ya kuokoka. Ni ishara ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Yesu. “Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo ka-tika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima” (warumi 6:4).

Ubatizo ni mojawapo ya mambo ya msingi yaliyotamkwa na Yesu katika agizo kuu alilowaachia wanafunzi wake. “Enendeni ulim-wenguni mwote mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wan-gu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru...” (Mathayo 28:19-20). Mtu anapoamua kuwa Mkristo wa kweli, anatakiwa atii mane-no yote ya Mungu bila kuchagua. Yeye aliyesema “tubuni”, ndiye aliyeagiza kubatizwa kwa maji. Kama baada ya kuokoka bado hu-jabatizwa majini, tafuta kanisa linalofundisha Biblia kwa usahihi na uueleze uongozi wa kanisa hilo, kuwa unahitaji kubatizwa katika maji.

Soma neno la Mungu

Ni jambo la ajabu na kufurahisha, pale mtoto mchanga wa kimwili

Ili kumzuia Shetani asiingize wanyama hawa ndani ya moyo wako, unatakiwa umpinge kwa nguvu zako zote. Biblia inasema wazi kuwa, “Mpingeni Shetani naye atakimbia” (Yakobo 4:7). Mambo yatakayokuimarisha na kukuwezesha kumpinga Shetani, ni pamoja na haya yafuatayo:

tangaza maisha yako mapya

Baada ya kusamehewa dhambi zako na kuwa Mkristo wa kweli,

26 27

anapozaliwa. Jambo hili linapotokea, watu hupongezana na hata kupelekeana zawadi. Hivi ndivyo inavyotokea na kuzidi pale mtoto wa kiroho anapozaliwa katika ufalme wa Mungu. Biblia inasema wazi kuwa, kunakuwa na furaha mbinguni, pale mwenye dhambi mmoja anapotubu (Luka 15:7). Pamoja na furaha hii, watoto wa-changa huwa wanakabiliwa na hatari nyingi. Kutokana na wingi wa hatari zinazowakabili, wanahitaji kulishwa na kutunzwa.

Kama vile mtoto wa kimwili anavyohitaji chakula chenye lishe, neno la Mungu ni lishe nzuri itakayomwezesha mwamini kukua na kuwa imara. Kutokana na ukweli huu, mwamini mchanga anataki-wa asome neno la Mungu kila siku. Biblia kama barua ya Mungu kwa wanadamu, imejaa maneno ya kutuelekeza, kutuonya, kututia moyo, kutufariji na kuturekebisha. Kuonyesha kuwa ni barua ya Mungu kwa wanadamu, Biblia imetafsiriwa kwa lugha nyingi ku-liko vitabu vyote duniani na ndicho kinachonunuliwa kuliko vitabu vyote. Ingawa imeandikwa kwa ulimwengu mzima, utakapoisoma kwa kumaanisha, utashangaa jinsi Mungu atakavyoitumia kuongea nawe kibinafsi.

Kwa kuwa Biblia ni kitabu kikubwa chenye vitabu 66, nakushauri usome sura tatu za injili ya Yohana kila siku. Hakikisha kuwa un-akisoma kwa uaminifu, huku ukiandika yale Mungu atakayoongea nawe. Ukimaliza injili ya Yohana, endelea kusoma kitabu cha Ma-tendo ya mitume kisha nyaraka na Ufunuo wa Yohana. Ukimaliza kusoma vitabu 27 vya agano jipya, anza vile vya agano la kale, kuanzia Mwanzo hadi Malaki.

Jenga tabia ya kuomba

“Ombeni pasipo kukoma” (1 wathesalonike 5:17). Jambo lingine linalochangia kumfanya mtu kuwa Mkristo mwenye ushindi, ni mao-mbi. Katika andiko letu hapo juu, neno la Mungu linatuagiza kudu-mu katika maombi. Maombi tunayoyazungumzia hapa, ni ile hali ya kuzungumza na Mungu. Mara zote maombi ya kibiblia yanahusisha mwamini kusema na Mungu, na Mungu kusema naye. Jenga tabia ya kusema na Mungu wakati wowote kwa lengo la kuimarisha ushiri-ka naye. Unaweza kutumia nafasi hii ya maombi kuumimina moyo

wako mbele zake, kumsifu, kumweleza mahitaji yako, kuwaombea wengine, kumshukuru Mungu na kumngojea. Ni vema pia ujifunze kuisikiliza sauti yake moyoni mwako. Muda mzuri wa kuomba ni alfajiri kabla watu hawajaamka na jioni kabla ya kwenda kulala.

Shikamana na watakatifu wengine

Neno la Mungu katika kitabu cha Waebrania linawahimiza waamini kujumuika pamoja katika ibada na ushirika. “wala tusiache kuku-tana pamoja, kama wengine walivyo na desturi ya kukutana, tuhi-mizane sisi kwa sisi kadri tuonavyo siku ile inakaribia” (waebrania 10:24). Kwa kuwa sasa umeokoka (umekuwa Mkristo wa kweli), un-atakiwa kutafuta kanisa linaloamini wokovu na linalofundisha injili sahihi ya Yesu Kristo. Kamwe usikubali kuabudu katika kanisa lenye mafundisho yanayopingana na imani yako mpya. Kama hujui jinsi ya kupata kanisa sahihi, unaweza kuomba ushauri kwa kutumia anwani inayopatikana mwanzoni mwa kitabu hiki. Ukipata kanisa sahihi, litakulinda dhidi ya hila zote za yule mwovu na kukusaidia kuwa imara kiroho.

Ukielewa faida zinazopatikana katika kushirikiana na waamini wengine, kamwe kwenda kanisani halitakuwa jambo la usumbufu kwako. Badala yake utahamasika kufanya hivyo, huku ukijua kuwa ni fursa nzuri kwako kukutana na Mungu na familia yake. Wakristo wa kweli wanaposhirikiana na Mungu kumwabudu na kumtumikia, hupokea ujuzi wa kweli kuhusu ushirika na kuhudumiana kupitia huduma zinazopatikana kanisani.

Jitolee kumtumikia Mungu

Kwa kuwa sasa u Mkristo wa kweli, tumia karama na uwezo uli-opewa na kumtumikia Mungu. Unaweza kufanya hivyo kwa kuishi maisha ya ushuhuda pale unapoishi, kazini, shuleni, ofisini, kiwan-dani, chuoni na ndani ya kanisa. Hali kadhalika, unaweza kufanya hivyo kwa kuwashirikisha wenzako kuhusu yale unayoyafahamu. Ruhusu nyumba yako na vyote ulivyo navyo, vitumike kuujenga ufalme wa Mungu. Kwa kuwa Ukristo ni zaidi ya maneno, unataki-wa uwapelekee wengine habari njema za Kristo na kukutana na ma-

28 29

hitaji yao. Kila Mkristo mwenye afya ya kiroho atakuwa na shauku kubwa ya kuwaleta wengine kwa Yesu. Inakuwa rahisi kuwaleta wengine kwa Yesu pale unaporuhusu wayaone mabadiliko yaliyo-tokea ndani yako. Hakikisha kuwa unawaambia rafiki zako kuhusu uzuri wa maisha mapya uliyo nayo katika Kristo Yesu.

Kama utayatendea kazi maelezo haya, ninakuhakikishia kuwa utakuwa na Ukristo ulio na furaha na uliojaa mafanikio. Hali kadha-lika, kweli ulizojifunza katika sura hii, zitakuwezesha kukua haraka na kuzaa matunda. Neno la Mungu linasema wazi kuwa, “Si ninyi mlionichagua, Bali Mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awape” (Yohana 15:16).

Hatua za wokovu

Kabla ya kuangalia yaliyotokea katika mfano huu unaopatikana katika injili ya Luka 10:25-37, uko mlinganisho ninaotaka kuu-fanya kuhusu watu, vitu au miji iliyotajwa katika mfano huu. Mtu wa kwanza tunayekutana naye katika mfano huu ni Mwanasheria, anayewakilisha watu wanaotetea dini na mji wa Yerusalemu tu-naoweza kuulinganisha na maskani ya Mungu. Mambo mengine yal-iyotajwa katika hadithi hii, ni mji wa Yeriko, unaowakilisha mji ulio-laaniwa. Naye msafiri aliyeangukia mikononi mwa wanyang’anyi, ni mfano mzuri wa mwanadamu. Kuhani anawakilisha Torati ya Musa huku Mlawi, akiwakilisha dini.

Katika mfano huu Yesu anawakilishwa na Msamaria na nyumba ya wageni inaliwakilisha kanisa la kweli la Yesu Kristo. Mwenye nyumba ya wageni ni kama mchungaji wa kanisa, dinari ya kwanza tunaweza kuifananisha na neno la Mungu. Nayo dinari ya pili, ni mfano wa Roho Mtakatifu, huku matunzo ya msafiri yakifananish-wa na utakaso. Kitu cha mwisho kutajwa ni kurudi kwa Msamaria kunakowakilisha kurudi kwa Yesu kunyakua kanisa lake.

Ingawa mfano huu umekusudiwa kuongea na mtu kibinafsi, wengi huusoma bila kujiona kuwa sehemu ya mfano huu. Ukiangalia mfano huu kwa kumaanisha, utagundua kuwa unakuhusu. Jambo lingine la

Sura ya 5

30 31

kushangaza katika mfano huu, ni ule uhodari wa Yesu katika kusim-ulia mifano. Hakika hakuna mtu anayeweza kusimulia mifano kwa ufundi unaofanana na wake. Mifano yake ilivutia, ilifurahisha na ilikuwa na mafundisho ya kustaajabisha. Mara zote alifundisha kwa mifano, ili kuweka wazi ukweli fulani wa kiroho. Kwa kutumia vitu halisi vya kawaida au vya kubuni, alitoa mafundisho yaliyobeba ukweli wa kiroho, kuhusu maisha ya watu ya umilele.

Baada ya kusema haya, naomba tuungane na Luka yule tabibu, aliyetafuta kwa usahihi kuhusu maelezo ya mfano huu. Kabla ya kutolewa kwa mfano huu, Mwanasheria mmoja ambaye siku hizi tungelimwita mtaalamu wa elimu ya Mungu, alijadiliana na Yesu kuhusu jambo fulani. alianza kwa kuuliza kile anachotakiwa ku-fanya ili aurithi uzima wa milele. Naye Yesu akamjibu kwa kusema, “imeandikwa nini katika torati? wasomaje?” (Luka 10:25). Yule mwanasheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako”(Luka 10:27). Yesu akamjibu akisema, “ Umejibu vyema, fanya hivi nawe utaishi” (Luka 10:28).

Baada ya kupokea jibu kutoka kwa Yesu, yule mwana sheria alitaka kujionyesha kuwa ni mwenye haki kwa kuuliza swali lingine akise-ma, “Na jirani yangu ni nani?” (Luka 10:29). Kulingana na mtiririko wa mazungumzo yao, nadhani angekuwa sahihi kama angeliuliza maana ya upendo. Swali la mtaalam huyu wa Sheria, ndilo lililozaa mfano tunaouzungumzia katika sura hii.

Kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko

Mtu mmoja alishuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Neno ‘shu-ka’ limetumika kisahihi kutokana na ukweli kuwa, mtu anapotoka Yerusalemu kwenda Yeriko inampasa kushuka. Mji wa Yerusalemu uko mita 760 kutoka usawa wa bahari, huku mji wa Yeriko ukiwa mita 250 chini ya usawa wa bahari! Mji huu ulioko karibu na bahari ya chumvi, uko kwenye eneo la ardhi lililoko chini ya usawa wa ba-hari kuliko maeneo yote duniani. akiwa njiani, msafiri katika mfano wetu, alishambuliwa na majambazi.

Yerusalemu ni eneo lililochaguliwa na Mungu kuwa maskani yake. Ndani yake kulikuwa na hekalu lililojengwa kwa ustadi wa ajabu na kwa maelekezo ya Mungu. Baada ya ujenzi wa hekalu hili kukami-lika, Mungu aliweka masharti ambayo wanadamu walitakiwa kuy-ashika, ili kumfanya Mungu aendelee kuishi ndani ya hekalu hilo. Kwa kuwa jina la Mungu lilikuwa ndani ya Yerusalemu, lilikuwa jambo la heshima na kujivunia, kuwa raia wa mji huu au kuhudhuria ibada katika hekalu la Yerusalemu.

Mbali na heshima na uzuri wa mji huu, kitu fulani kilimsukuma msa-firi huyu kwenda mbali na uwepo wa Mungu, na kutoka katika eneo lililobarikiwa. Naomba utulie na kufikiria hiki ninachoenda kukise-ma. Lengo la mtu huyu lilikuwa kufika Yeriko, mji uliolaaniwa! Mji huu uliharibiwa na majeshi ya Israeli wakati wa Yoshua na watu wengi walipoteza maisha yao, wakati wa kuujenga upya. Kwa kuwa baadaye mji huu ulikaliwa na watu, ilikuwa rahisi watu kufanya biashara ndani yake. Ndani ya mji huu, watu waliendelea kuishi maisha ya anasa, starehe na kumkataa Mungu wa kweli.

Maelezo kuhusu miji hii miwili na huyu mtu aliyeamua kusafiri kuto-ka Yerusalemu kwenda Yeriko, ndio ufunguo wa mfano huu. Inasikit-isha kuona kuwa wanadamu wameondoka Yerusalemu mji ambao Mungu hukaa ndani yake, na kuwa na ushirika na watu wake! Wakiisha kuondoka katika mji huu uliobarikiwa, hushuka kuelekea Yeriko mahali pa anasa, starehe na uharibifu. Kila mtu anayemwa-cha Mungu na kuacha kushirikiana naye, anasafiri kuelekea chini.

Mambo mengi maovu yanayojulikana kwa wengi kama kwenda na wakati, ni uchafu unaowapeleka wanadamu upotevuni, mbali na uwepo wa Mungu. Na yeyote anayeamua kukimbizana na mambo haya, siku moja ataangukia mikononi mwa wanyang’anyi. Watam-wibia bidhaa zake (afya, uwezo), nguo (heshima), chakula cha safa-rini (tumaini) na uhai wake. Hiki ndicho kilichomtokea msafiri katika mfano wetu, alipigwa akaachwa ili afe kando ya njia, huku akivuja damu!

Mtu anayekufa kwa kutokuwa na damu, hufa taratibu hatua kwa hatua, kutokana na mateso na maumivu makali. Hiki ndicho kinach-

32 33

otokea kwa watu wengi wanaotuzunguka. Wengi wao wako kando ya njia, wakitokwa na damu na wakiwa karibu ya kufa. Wengi wao ni vijana wanaoishi bila kuwa na uzima wala furaha ya kweli ndani yao. Muziki wa kidunia, ngono, kamari, ulevi wa pombe na madawa ya kulevya na ujambazi vinaendelea kumaliza nguvu za ujana wao. Ukiwaangalia kwa macho ya rohoni, utagundua kuwa ni watu am-bao mioyo yao inavunjika, kila inapodunda!

Mitaa na mabarabara zetu zimefurika watu wa jinsi hii wanaohi-taji msaada wa kiroho na kimwili. Watu hawa wasio na mbele wala nyuma, hawana furaha wala amani ya kweli katika maisha yao. Zaidi ya yote, hatima ya maisha yao ya umilele iko katika giza nene. Ni ukweli usiopingika kuwa, kila familia ina mtu au watu wa jinsi hii, wanaozaliwa na hatimaye kufa pasipo kuwa na matumaini.

Kuhani na Mlawi

Sasa hadithi yetu inafikia mahali pazuri. Watu wawili ambao walid-haniwa kuwa watatoa msaada pale tendo la uhalifu linapotokea, walipita na kumkuta yule mtu aliyepigwa na wanyang’anyi. Watu hawa ni Kuhani ambaye ni mwakilishi wa Torati, na Mlawi anayewak-ilisha kiongozi mkubwa wa dini. Wote wawili walimwangalia kwa mbali, kisha wakaendelea na safari zao. Hawakuwa tayari kum-saidia. Je, watu hawa walikuwa na shughuli nyingi? Yawezekana ni hivyo. Huenda walikuwa wanawahi ibada au kikao fulani cha kidini. Kwao mapokeo ya dini zao, yalikuwa ni ya thamani kuliko kuokoa roho na uhai wa mtu.

Je, hii siyo hali halisi inayoukabili ulimwengu kwa sasa? Tunayo mashirika mengi ya kimataifa na jumuiya nyingi zilizo na uwezo wa kuwasaidia wengine, ila bado maelfu kama sio mamilioni ya wen-zetu, wanaishi maisha yasiyo na matumaini. Hata makanisa mengi yaliyo na uwezo wa kutoa misaada, yameshindwa kutoa msaada unaohitajika wa kiroho na kimwili. Kutokana na kushindwa huku, mitaa yetu imefurika watu waliotelekezwa kando ya njia, waki-vunja damu. Wengi kati ya watu hawa, wameharibiwa na ulevi, zi-naa, madawa ya kulevya, ushirikina, ufisadi, uchawi, wizi na maovu mengine yanayofanana na haya. Dhambi ndiyo chimbuko la taabu

na aibu zote zinazompata mwanadamu.

Ni ukweli usiopingika kuwa torati na dini, haziwezi kumwokoa mtu aliyepotea dhambini. Mashirika mengi ya kibinadamu yanashughu-likia miili na maisha ya duniani peke yake, lakini hayatoi msaada wa kiroho au kupambana na dhambi.

Msamaria anatoa msaada

Baada ya Mlawi na Kuhani kupita bila kutoa msaada, mtu wa tatu alifika katika eneo la tukio. Huyu alikuwa mtu aliyedharauliwa wa taifa la Kisamaria. Ingawa hakuna mtu aliyemtarajia kuwa atatoa msaada, mtu huyu asiyejulikana na aliyedharauliwa, ndiye aliyetoa msaada! akiongozwa na huruma na upendo, alishuka juu ya punda wake na bila kusema neno lolote, alisafisha majeraha ya yule msa-firi na kumpaka dawa ya kupunguza maumivu. Yawezekana baada ya kufunga majeraha yake, alimpa kinywaji cha kumburudisha.

Baadaye alifanya nini? Je, alimfariji tu na kumpa ushauri mzuri kisha akapanda punda wake na kwenda zake, huku akimpungia mkono wa urafiki? Hapana, sanjari na kumpatia huduma ya kwanza, al-imwinua na kumpandisha juu ya punda wake. Kisha akampeleka ilikokuwa nyumba ya wageni, huku yeye mwenyewe akitembea kwa miguu!

Je, ni fundisho gani la kiroho tunalokutana nalo katika kipengele hiki? Msamaria huyu aliyetoa msaada, ni mfano wa Yesu. Ni wach-ache sana wanaomtegemea Yesu na kuamini kuwa anaweza kuin-gilia kati na kutatua matatizo wanayopitia. Ukweli ni kuwa, Yesu anaweza na anataka kufanya hivyo. Jambo la kwanza, anataka ku-tuondoa katika eneo la hatari kando ya njia, na kutupeleka katika eneo la usalama. Wako watu wengi wanaotangatanga mitaani bila kuwa na nyumba na mahali pa kuishi. Lakini wote watakaoruhusu nguvu za Yesu ziguse maisha yao, atawainua na kuwatoa mitaani. atazuia damu isivuje katika majeraha yao, atatuliza maumivu yao na kuwapa kinywaji kitakachowaburudisha.

Yesu peke yake, ndiye anayeweza kutusaidia na kututoa katika hali hii ngumu ya taabu na dhiki. Mwite sasa! Naye atakuja na kuku-

34 35

safisha kutoka dhambini na kukuokoa dhidi ya mauti ya milele. Msamaha wa dhambi uletao wokovu ni huduma ya kwanza atakay-okupatia. Huduma hii itakufanya uwe raia katika ufalme wa Mun-gu. Sanjari na msaada huu wa huduma ya kwanza, Yesu atafanya zaidi kwa:

Kukupeleka kwenye nyumba ya wageni

Kama ilivyokuwa kwa mtu yule aliyeangukia mikononi mwa wanyang’anyi, wewe pia unahitaji huduma ya nyumba ya wageni. Nyumba hii ni mahali pa usalama kwa ajili ya roho yako, ambayo ni ya thamani kuliko vitu vyote. Nyumba ya wageni ni mfano wa kanisa la mahali la Yesu. Baada ya yule ndugu aliyejeruhiwa kupata huduma ya kwanza, alipelekwa katika nyumba ya wageni. Ndani ya nyumba hii ndipo huduma kamili ya kumtunza ilipoanza.

Kutokana na mfano huu, tunaweza kusema kuwa baada ya kum-pokea Yesu kama Bwana na Mwokozi, Wakristo wachanga wa-nahitaji kanisa litakalowalea. Kuwa Mkristo bila kuwa na kanisa linalokulea, ni jambo la kigeni na lisilo la kibiblia. Ndani ya kanisa ndipo waamini wanapofundishwa jinsi ya kushinda malango ya Kuzimu. Yesu alisema, “...juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya Kuzimu haitalishinda” (Mathayo 16:18).

Wote tunafahamu hasira na chuki za Shetani dhidi ya mtu yeyo-te aliyeamua kuwa Mkristo. Wakati wa mateso hutumia mateso kuharibu Wakristo wa kweli na wakati wa amani na uhuru wa kuabudu, hutumia mbinu nyingine kuwazuia wasikutanike kuabudu na kuhudumiana. Kamwe Wakristo wa kweli ambao ndilo kanisa la kweli la Kristo, sio jengo au mahali pa kukutania panapoonekana. Badala yake, kanisa ni ushirika unawaunganisha watu walio na uhusiano na Mungu wa kweli. Watu hawa hukutana chini ya uwepo wa Yesu, aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yao ili kulisha roho zao, na kujifunza jinsi ya kufanya mapenzi ya Mungu.

Yesu mwenyewe anatufundisha kupitia huduma ya Msamaria mwe-ma umuhimu wa kuwepo kwa nyumba zitakazowahudumia watu wake. Hali kadhalika, mfano huu unaonyesha aina ya matunzo

yanayotakiwa kutolewa kwa Wakristo wachanga. Baada ya yule Msamaria kumaliza kumpatia yule msafiri huduma ya kwanza, alimpeleka kwenye nyumba ya wageni na kuweka huduma za ma-tunzo chini ya uangalizi wa mwenye nyumba. Hata hivyo, kabla ya kupokea majukumu ya kumhudumia yule msafiri, mwenye nyumba ya wageni alipokea vifaa vya huduma. Kwanza tunamwona Msa-maria akimkabidhi mtunza nyumba ya wageni dinari mbili, kisha anamwagiza kuzitumia kumtunza mgeni hadi atakapopata afya.

Dinari hizi mbili zinawakilisha ukweli fulani wa kiroho. Dinari ya kwanza ni neno la Mungu. Kamwe mwenye nyumba ya wageni hat-akiwi kuifungia kabatini, au kuitumia vibaya. Dinari yote ilitakiwa itumike kumtunza msafiri. Katika makanisa yetu tunahitaji wahubiri wanaohubiri Biblia yote huku wakitaja miiko yote na ahadi zote. Wakristo wenye afya hutokana na mlo kamili wa neno la Mungu. Mhubiri anayehubiri sehemu tu ya Biblia, anafanya makosa. Ma-tokeo ya Injili ya jinsi hii ni kuzaa Wakristo dhaifu, wagonjwa na wa-sio na uwezo wa kumzalia Mungu matunda. Kama tunahitaji kuwa na kanisa lenye afya, ni lazima tuhubiri Biblia yote.

Waamini watakapokosa kulishwa neno la Mungu, Wataishia kuchan-ganyikiwa na kuchukuliwa na upepo wa mafundisho ya uongo, ku-tokana na kukosa mwongozo sahihi wa neno la Mungu. Madhehebu mengi yameishia kuwa mawakala wa mapokeo ya kidini badala ya kuwa mawakili wa siri za Mungu, kutokana kutolipa neno la Mungu nafasi ya kwanza. Badala ya wokovu kuwa tiketi ya kujiunga na madhehebu hayo, watu hujiunga ili kukamilisha ratiba za kidini. Wakati mwingine hufanya hivyo, ili wakifa wazikwe Kikristo!

Dinari ya neno la Mungu, inawakilisha kweli nyingi na za kustaaja-bisha. Neno la Mungu ni mkate wa uzima, ni maji matamu ya kuny-wa na kuoga, maziwa yaliyo na virutubisho vyake ambayo ni lishe bora ya kiroho. Tena, neno la Mungu ni asali tamu wakati wa hu-zuni, chakula kigumu kwa kazi nzito na dawa inayoponya na kutu-liza maumivu. Ni vazi la haki, ngao ya ulinzi, nuru kwa walio gizani, ramani ya mjenzi, nyundo ya mfinyanzi, wimbo wa mwimbaji, kazi ya msanii na maneno ya mtunzi. Biblia inahusisha torati, historia, zaburi tamu, unabii, upatanisho, hukumu na uhuru.

36 37

Dinari ya pili, ni Roho Mtakatifu ambaye ni nafsi ya tatu ya Mungu. Roho huyu ni zawadi ya Mungu kwa kanisa. Yesu alipoondoka duni-ani kurudi kwa Baba yake, alimtuma Roho Mtakatifu kama mwak-ilishi wake na msaidizi mkuu wa kanisa. Kwa kuwa Roho Mtakatifu ndiye mwakilishi wa Biblia, peke yake ndiye anayeweza kuwapatia waamini tafsiri sahihi. Sanjari na kutoa tafsiri sahihi ya maandiko, ubatizo wa Roho Mtakatifu unawapatia waamini nguvu za kiroho zinazowawezesha kuishi kama mashahidi wa udhihirisho wa nguvu za Mungu, na kuwapatia ushindi usio na mwisho.

Hali kadhalika, mwamini anapompokea Roho Mtakatifu, kwa imani hupokea karama za roho. Kupitia udhihirisho wa karama hizi na bi-dii ya kujifunza kutoka kwa Yesu, tunda la Roho huzaliwa ndani ya maisha ya mwamini. Mtume Paulo ameielezea mionjo ya tunda la Roho kama, upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, upole, kiasi, uaminifu na fadhili (wagalatia 5:22-23).

Waamini wote wanayo haki ya kupokea dinari hizi mbili. Hata hivyo, Roho Mtakatifu atakuwa wa manufaa tu pale waamini watakapom-ruhusu atende kazi ndani ya mioyo yao, na ndani ya makanisa yao. Karama za roho ambazo Mungu anataka zitende kazi ndani yetu, ni zile za ufunuo zinazojumuisha karama ya neno la hekima, neno la maarifa na karama ya kupambanua roho. Karama zingine ni za ngu-vu zinazojumuisha karama ya imani, matendo ya miujiza na karama za kuponya. Mwisho ni karama za unenaji zinazojumuisha karama za unabii, tafsiri ya lugha na karama ya aina za lugha (1 wako-rintho 12:8-12). Karama zote hizi tisa ni za muhimu sana pale kanisa linapotaka kufanya yale yaliyofanywa na Yesu alipokuwa duniani.

Kama mwenye nyumba ya wageni anahubiri neno lote la Mungu na kumruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi ndani ya kanisa, kamwe nyumba ya wageni haitaishia kuwa hospitali, na mahali wagonjwa wanapofia. Badala yake itakuwa bandari ya afya njema, chemchem ya uzima, nyumba ya furaha na amani, na mahali pa masaidiano. Katika nyumba hii majeraha na maumivu yataponywa. Tena mi-gawanyiko kati ya waamini na makwazo yaliyoko moyoni vita-toweka. Katikati ya baraka hizi, waamini watakaza macho mbele kwa furaha, wakitarajia kurudi kwa Msamaria ambaye ni Yesu.

Ushauri kwa waamini wachanga

Waamini wachanga hawatakiwi kuyafanya maisha ya watunza nyumba za wageni kuwa magumu. Neno la Mungu linawaonya kutofanya jambo lolote litakalowahuzunisha. “watiini wenye ku-waongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi” (waebrania 13:17).

Sanjari na kuwa mwanana kwa watunzaji wa nyumba za wageni, Wakristo wachanga wanatakiwa kukaa ndani ya nyumba za wageni hata pale wanapokuwa sio wagonjwa. Wanatakiwa kujibidisha ndani ya kanisa ili wawe na afya itakayowawezesha kusimama na kuwatunza waliojeruhiwa. afya njema itawawezesha waamini wa-changa kuhudumia vizuri, huku wakingojea kwa hamu kurudi kwa Yesu. Ni jambo litakalopendeza kama wakati akirudi, atawakuta wakitenda kazi katika nyumba ya wageni!

Kama tulivyotangulia kujifunza, nyumba ya wageni ni kanisa. Kanisa la kibiblia ni kama mama mtunzaji au mlezi anayenyonye-sha. Kama vile mama aliyekufa asivyoweza kunyonyesha kichanga chake, kanisa lililokufa kiroho, haliwezi kuwalea watoto wa kiroho. Kama wewe umeokolewa, nenda kaabudu katika kanisa linalohubiri wokovu kamili, badala ya kung’ang’ana na mama aliyekufa!

Mwisho wa mfano

Sasa tumefikia mwisho wa mfano wetu, ninaoamini kuwa ume-kuwa wa baraka na msaada maishani mwako. Baada ya kumka-bidhi msafiri kwa mtunzaji wa nyumba ya wageni, yule Msamaria alisema kuwa atarudi tena. Ndugu yangu, Yesu atarudi tena kama alivyoahidi. Yeye alisema, “Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo” (Yohana 14:3). atakaporudi mambo mengi ya baraka yatatokea, yule mtu aliyelala kando ya njia akiwa ameumiz-wa vibaya, hatachechemea kwa magongo wakati wa kumwendea Mwokozi wake. Badala yake, atamkimbilia Bwana wake kwa furaha

38 39

na kupiga kelele za sifa akisema, “Asante Bwana, mimi ni mzima na nitaishi pamoja nawe milele.”

Huu ndio wajibu wa kanisa, kuwaongoza watu kupata afya njema na kuwatayarisha kwa ujio wa Yesu. Tunapofikia mwisho wa mfano huu, naomba nirudie yale tuliyokwisha kujifunza. Baada ya kupokea wokovu, mwamini anatakiwa kuwa na kanisa litakalomtunza na kumwezesha kuwahudumia wengine. Hivi ndivyo inavyofanyika mahospitalini. Wagonjwa wenye nafuu, huwasaidia wenzao wal-iozidiwa, kwa hiari bila kuwaachia waganga jukumu hilo. Ingawa mfano wetu hauzungumzii aina hii ya masaidiano, bado Wakristo wanapojifunza neno la Mungu katika kanisa la mahali, watajifun-za kuwahudumia wengine. Watazitumia karama zao ili nao wawe Wasamaria wema kwa wenzao walio na mahitaji.

Kushinda hofu katika maisha

Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa nikisisimka kwa hofu wakati wa kucheza mchezo wa mbwa mwitu. Je, ulishawahi kucheza mchezo huu ulipokuwa mdogo? Katika mchezo huu, mkamataji anakaa upande mmoja wa mstari na kisha anaiuliza timu wanayoshindana nayo akisema, “Nani asiyemwogopa mbwa mwitu?” Timu ya pili wanajibu kwa pamoja kwa kusema, “Hakuna!” Kisha kila mmoja anaanza ku-kimbia huku mkamataji akijitahidi kumkamata mtu mmoja au zaidi. Jambo hili lilikuwa likiniogopesha na kuniletea hofu kubwa.

Yule anayekamatwa, anakuwa upande wa mkamataji na kisha mch-ezo unaendelea hadi pale wote wasioogopa wanapokuwa wameka-matwa na mbwa mwitu na wasaidizi wake. Leo hii hofu imeone-kana kuwa shujaa anayewashinda watu wengi wakiwemo wale wanaoonekana kuwa na sifa za kuwa majasiri. Swali kubwa la ku-jiuliza ni hili, “hofu hii ni ya kitu gani?”

Ujuzi wangu kuhusu hofu

Hofu ni kitu gani? Ni kuhisi vitisho visivyojulikana. Wakati mwingine bila sababu yoyote unahisi kuwa kitu fulani kibaya cha hatari, na

Sura ya 6

40 41

pengine cha kuhatarisha maisha yako kitakutokea. Swali lingine la kujiuliza hapa ni hili, “hivi hisia hizi zinatoka wapi?”

Siku moja niliendesha gari langu kwa kasi isiyotakiwa katika ba-rabara kuu. Ghafla mwanga wa kamera ya askari wa barabarani ulimulika kuonyesha kuwa nilikuwa nimefanya kosa. Mara tu baa-da ya kitendo hiki kutokea, nilikamatwa na hofu kubwa huku niki-jiuliza maswali yasiyo na idadi. Je, niliendesha kwa kasi ya kiwango gani? Faini itakuwa kiasi gani? Ina maanisha jina langu litaingia kwenye orodha ya wavunja sheria za usalama barabarani? Haya ndiyo maswali yaliyokuwa yakinikabili katika kipindi hiki cha kun-gojea barua itakayoelezea kosa langu na kiwango cha faini nitakay-otakiwa kulipa. Kama angelitokea askari wa barabarani wakati wa tukio na kunitaka nilipe faini wakati uleule, hilo lingekuwa jambo la heri kwangu.

Kosa nililolifanya ndilo lililokuwa chimbuko la hofu yangu. Nilikuwa ninangojewa na adhabu, kwa kuwa nilikuwa nimevunja sheria za usalama barabarani. Yeyote anayevunja sheria za barabarani mara zote hujikuta katika hali hii iliyokuwa ikinikabili. Jambo kama hili hutendeka pia pale mtu anapokwenda kinyume na sheria za vyaku-la na kula chakula kisichostahili. Mtu huyu ataishia kuugua, kud-hoofika na hata kufa kabla ya wakati wake.

Hivi ndivyo sheria za Mungu zilivyo. Yeyote anaye vunja amri na sheria za Mungu kwa kuchagua kuishi maisha ya zinaa, upagani, uchawi, kuabudu sanamu, ulevi, udanganyifu, uchoyo na kadha-lika, ataishia kuwa na maisha yaliyojaa hofu. Hata hivyo, Mungu anaweza kuzitumia hofu hizi, kutupeleka kwenye toba na Ukristo wa kweli.

Hofu ya giza

Mara zote giza linapoingia, hofu ya aina fulani hutunyemelea. Giza linatuletea sitofahamu na kutufanya tuwe na mipaka katika yale tunayotakiwa kuyafahamu kuhusu mazingira ya njia tunayopitia. Giza linapokuwa mbele zetu, hatujui kitakachotokea au mahali miguu yetu itakapokanyaga. Hata pale kunapokuwa na jiwe kubwa

njiani, uchafu, au watu wabaya waliojiandaa kutudhuru au kutu-chukua mateka, hatuwezi kuelewa. Kutokana na hofu, wako watu wanaoogopa hata kuzima taa wakati wa kulala.

Ni jambo la kusikitisha kuwa hata watu walioelimika katika nyakati hizi za maendeleo na mapinduzi ya habari, nao wanaendelea ku-papasa katika giza. Hawajui jinsi wanavyoweza kukabiliana na migogoro ya kiuchumi, gharama za matibabu, gharama za kuso-mesha, kukosekana kwa ajira na taabu za maisha ya uzeeni. Wasi-wasi mwingine unatokana na kupanda kwa gharama za vyakula na bidhaa, mabadiliko ya kisiasa, ugaidi, ufisadi, vita, magonjwa ya milipuko, mabadiliko ya tabia nchi na matatizo mengine yanayofa-nana na haya.

Japo watu wana nyumba, magari, vyombo vya thamani, luninga, tovuti, video, mashine za aina mbalimbali za kuchezea muziki na kuonyeshea picha, simu za mikononi na maburudisho ya kila aina, bado wanaendelea kuishi katika hofu. Cha kushangaza ni kuwa jinsi starehe na utajiri vinavyozidi kuongezeka, ndivyo hofu za kimaisha zinavyozidi kuongezeka.

Hofu ya upweke

Jambo lingine linalosababisha hofu ni upweke unaowakabili watu katika maeneo mbalimbali ya maisha. Watu wanajihisi kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya kimaisha, pia hawajui iki-wa watapata mtu wa kuwasaidia pale watakapokutana na tatizo lililo juu ya uwezo wao. Pasipo shaka yoyote, upweke unaonekana kuwa tishio dhidi ya muda wetu maendeleo yetu, uvumbuzi wetu na tekinolojia tuliyo nayo. Ingawa tunaishi karibukaribu mijini na vijijini kiasi cha kutukosesha hewa ya kutosha, bado watu wanaji-hisi kuwa wapweke na waliotelekezwa. Hapo zamani hali kama hii, ilikuwa haipo.

Katika miaka ya hivi karibuni mzee mmoja alifariki peke yake akiwa amekaa juu ya kiti, chumbani mwake. Nyumba aliyofia ilikuwa na wapangaji wawili tu, yeye na mganga mmoja wa kike aliyepanga jirani na chumba chake. Huyu mganga hakutaka kusumbuka kumju-

42 43

lia hali huyu mzee na kuangalia ikiwa alikuwa mzima au la. Moyo wake ulijiona kutokuwa na sehemu katika maisha ya mzee huyu! Siku inakuja ambapo mbegu ya ubinafsi, inayowatumikisha watu wengi itapokea ijara yake. Kipindi hicho kitakapofika watu watase-ma, “Nilitumia viwiko vya mikono yangu kupandia ngazi kwenda juu, kujipatia uhuru na ufanisi, lakini hayo yote yamenifikisha wapi? Bado niko mpweke!” Je, hakuna ufumbuzi wa tatizo hili la hofu? Ndio ufumbuzi utakuwepo pale chimbuko litakapoondolewa.

Hakuna sababu ya kuogopa

Hebu nikupe hadithi ya mtu kutoka Romania aliyegundua majibu ya Mungu dhidi ya hofu aliyokuwa nayo. Yafuatayo ni maelezo yake. “Nilikuwa nikisoma Biblia katika kitabu cha Yoshua na ghafla nilis-hangazwa kuona jinsi neno ‘usiogope’ lilivyorudiwa rudiwa katika kitabu hicho. Hapo moyo wangu ulianza kusumbuka kutokana na ukweli kuwa, Yesu alituambia kuwa tusirudierudie maneno, wakati wa kuomba. Baada ya kupekua Biblia yote, niligundua kuwa Mun-gu alikuwa amelinena neno hili mara 366. Je, kurudiwa kwa neno hili kulitokea kwa bahati? Hapana, naamini Mungu aliruhusu iwe hivyo, ili kila siku liwepo neno kutoka kwa Mungu kwenda kwa wa-toto wake, linalosema, ‘usiogope.’

Nilifurahi sana kutokana na ugunduzi huu ninaoamini kuwa hau-kutokea kwa kubahatisha. Ni wazi Yoshua hakujadiliana na Pet-ro kuwa neno hili aliandike mara ngapi katika nyaraka zake. Hali kadhalika, Daudi hakujua ni mara ngapi, Mathayo atalitumia neno hili katika injili yake. Kile tunachojua ni kuwa, Biblia imeandikwa na mwandishi mmoja ambaye ni Roho Mtakatifu. alitambua kuwa kila siku mwanadamu anahitaji neno hili, pamoja na neno moja la ziada!

Ndugu huyu alinisimulia kisa kingine kilichochangia kuipeleka hofu mbali nami. Hivi ndivyo alivyoanza ushuhuda wake. “Jumapili moja nilipokuwa njiani kuelekea kanisani, ghafla gari moja lilisimama kando yangu na nikajikuta nikiwa mikononi mwa watu wanne. Watu hawa walitoka katika kikosi cha siri cha jeshi la askari wa Romania ya zamani, wakati wa siasa za Kikomunisti. Nilianza kuta-basamu baada ya kutupwa ndani ya gari lao, pale nilipokumbuka

kuwa neno ‘usiogope’ limetajwa mara 366 katika Biblia!

Mmoja wa maofisa hao aliniangalia na kuniuliza kwa ukali akise-ma, “una jambo gani?” Kwa kawaida mtu anapokamatwa na polisi hawezi kutabasamu. Nikamjibu nikisema, nilichoahidiwa ni kweli. Huenda walidhania kuwa nimepatwa na mshtuko na kupoteza ‘net-work.’ “ahadi gani?”, wakaniuliza kwa haraka. 366, nikawaambia. Hatimaye niliwafahamisha maana ya tarakimu hizo ili wasiendelee kuchanganyikiwa. Leo ni tarehe 29 Februari na iko katika maneno 366 ya Mungu yasemayo, usiogope. Hilo ndilo jibu langu kutoka mbinguni. Kwa uhakika huu kutoka kwa Mungu nilikuwa na uwezo wa kukabiliana na jambo lolote litakalotokea ikiwa ni mahojiano na polisi, kupelekwa mahakamani au kufungwa gerezani.”

Kama kuna mtu anayeona taabu kuamini hadithi hii ya kimiujiza, ngoja nikupatie ushuhuda mwingine unaofanana na huu wa ndu-gu wa Romania. Ushuhuda huu nao ulitokea katika mojawapo ya maeneo yaliyokuwa yakitesa Wakristo. Mkristo mmoja alikamatwa kutokana na bidii yake katika kuwapelekea wengine Injili kinyume cha sheria za nchi yake. Katika kutaka kuizimisha kiu yake, polisi walimtisha kwa kumwambia maneno yafuatayo, “shughuli zako za Kikristo hazipatani na sheria za jamii yetu. Kama hutakubali ku-tutajia wale unaoshirikiana nao na kuacha kuhubiri Injili, leo ndiyo mwisho wa Mathayo kwako!”

Mara nyingi kinachofuatia baada ya vitisho vya jinsi hii, ni mate-so makali na hata kuuawa. Baada ya mshtuko wa sekunde chache uliotokana na kukamatwa kwake, ndugu huyu alianza kutabasamu huku akisema, “hiyo ni ajabu, ahsante, ahsante!” Yule aliyemka-mata akawaduwaa na kusema, “una nini?” Huku akiendelea kuta-basamu alijibu akisema, “sasa hivi umenikumbusha sura ya mwisho ya kitabu cha Mathayo, yaani, Mathayo 28:20.” Katika andiko hili Yesu alitamka maneno yafuatayo, “Hakika mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.”

Huyu naye aliendelea kuwa thabiti na kwa uaminifu alivumilia mateso kwa ajili ya Kristo. Shuhuda za watu hawa ni uthibitisho mwingine kuwa katika kujaribiwa kwa imani yetu, Mungu husi-mama na kutuokoa dhidi ya hofu na vitisho.

44 45

Mapumziko yanayo-mfurahisha Mungu

Katika ulimwengu huu wa kuheshimu na kuokoa muda, watu wen-gi wanapenda kutumia mashine katika shughuli zao, kwa lengo la kurahisisha kazi na kupunguza uchovu unaotokana na kazi nyingi. Neno ‘Jihurumie!’, linatamkwa na watu wengi pale wanapomwona mtu akiendelea kujishughulisha na kazi, licha ya kuonekana kuwa amechoka. Mara zote mtu anapotuambia neno hili tunatambua jinsi alivyoguswa na bidii tuliyoionyesha katika kutumika kwetu. Kwa ujumla tunajisikia vizuri, pale watu wanapotambua kuwa tumefan-ya kazi ya kuchosha na hivyo tunahitaji kupumzika. Je, tukubaliane na watu pale wanapotuhurumia na kututaka tupumzike? Je, Yesu angeliitikiaje kama wangejitokeza watu na kumpa ushauri huo?

Ukiangalia ratiba ya huduma yake, utaona kuwa siku zote alikuwa anakwenda huku na huko, bila kupumzika. Wakati fulani, rafiki yake wa karibu sana alimchukua pembeni na kumpa ushauri am-bao kibinadamu, haukuwa mbaya. Ushauri huo uliotolewa na Petro ulikuwa umebeba maneno yafuatayo; “Bwana, pumzika!” alitoa ushauri huu huku akifahamu shughuli za Yesu na mwenendo mzima wa huduma yake. Kama mtenda kazi na msafiri pamoja na Yesu,

Sura ya 7

46 47

alishuhudia yale Mathayo yaliyoandika katika injili yake akisema, “Naye Yesu alikuwa akizunguka zunguka katika miji yote na vi-jiji akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa na udhaifu wa kila aina” (Mathayo 9:35.

Wakati alipokuwa duniani, Yesu na wanafunzi wake hawakusa-firi kwenye magari yaliyo na viyoyozi au kulala kwenye mahoteli makubwa ya kitalii. Badala yake, walisafiri kwa miguu, kwenye jua kali na katika barabara zilizojaa vumbi. Walihubiri sehemu ze-nye watu wengi kama vile kwenye minada, masokoni na kadhalika. Hata watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi waliotapakaa majasho, walipata nafasi ya kumkaribia. Hali kadhalika, watu wa-liokuwa na magonjwa sugu na ya hatari, walimwomba awawekee mikono ili wapate kuponywa. Nao wenye pepo walipata nafasi ya kumkaribia huku wakilia na kupiga makelele ya kutaka kufungu-liwa. Safari zake zilikuwa ngumu kutokana na joto kali na wingi wa watu waliohitaji kufunguliwa.

Kituo cha kudumu cha huduma

Siku moja Yesu alipewa kituo maalum cha huduma, nyumba ya ku-lala na mshahara. Hiki ndicho kilichotakiwa kufanyika pale kundi kubwa la watu lilipojaribu kumshikilia ili asiondoke katika mji wao. Je, shinikizo hili halikuwa jaribu kubwa kwa Yesu? Kama ange-likubaliana na shinikizo hilo, angekuwa na kundi kubwa la watu wa kumsikiliza mara kwa mara, tofauti na hali aliyokutana nayo kule Nazareti. Katika mji huo wa nyumbani kwake, watu walitaka kumpiga kwa mawe na kumtupa chini ya korongo kubwa.

Je, ukarimu huu haukuwa mpango wa Mungu kumpatia sehemu ambayo angekubalika na kutambuliwa na kutunzwa? Pangekuwa mahali pa starehe zaidi kuliko kuwa mhubiri anayesafiri kila mahali pasipo kupumzika. Yawezekana hata wanafunzi na wafuasi wake walitamani wawe na kituo maalum cha huduma na mahali wataka-popumzika kwa muda mrefu. Wakati wafuasi wengine walipokuwa wakifikiria kumjengea hekalu ili awe na makazi maalum, yeye alitoa tangazo lenye maneno yafuatayo: “Yanibidi nitembelee miji

mingine, kutangaza ufalme wa Mungu.”

Kukatizwa usingizi wa mchana

Katika mazingira ya kazi, wafanyakazi wanapenda kupumzika mchana kabla ya kuanza awamu ya mwisho ya uwajibikaji wao wa kutwa. Katika nchi za Ulaya, watu hutumia mapumziko haya ku-pumzisha miili yao kwa usingizi mfupi unaojulikana kama ‘siesta.’ Kwa watu walio na utaratibu huu, huwa ni jambo lisilopendeza pale mtu anapokatiza ‘siesta’ ya mtu mwingine.

Jambo kubwa la kujifunza ni kuwa Yesu hakuwa hata na nafasi ya kupumzisha mwili wake kwa usingizi wa mchana. Watu wengine walipata nafasi na kwenda kujiburudisha mjini, ila yeye alibakia nyuma akiwa ameketi katika kisima cha Yakobo. alifanya hivyo kwa lengo la kumhubiria mwanamke aliyekuja kuteka maji. Wanafunzi wake walirudi na walipompatia chakula ili ale, yeye alikataa na kusema, “Chakula changu ni kuyatenda mapenzi ya Baba yangu” (Yohana 4:34).

Kinachoonekana hapa ni kuwa, badala ya kutumia muda wake wa mchana kujiburudisha, aliutumia kumwonyesha mwanamke wa Kisamaria mwenye mateso, njia ya wokovu. Njia itakayomaliza kiu yake ya zinaa na kumpatia amani, msamaha wa dhambi. Kwake kumhudumia mwanamke huyu lilikuwa jambo muhimu kuliko kula chakula cha mchana.

Katika injili ya Luka tunakutana na kisa kingine kinachofanana na hiki. Siku moja Yesu alikuwa amechoka sana na akaamua kupumzi-ka. Ghafla akaamshwa usingizini na kelele za watu wazima na za watoto waliokuwa wakilia. alipoamka, macho yake yalikutana na wanawake waliokuwa wakitetemeka na wanaume walioonyesha kutotendewa haki. alipotaka kujua chanzo cha mkanganyiko huo, wanafunzi wake walimjibu kwa kujigamba wakisema, “kundi hili la watu lilitaka kukusumbua, na sisi tulikuwa tukiwatawanya ili wa-ondoke. Samahani tumekatiza usingizi wako, hata hivyo tulishindwa kuwaondoa kimyakimya!”

Kamwe Yesu hakukubaliana na wanafunzi wake katika wazo lao,

48 49

badala yake aliwaambia maneno yafuatayo: “waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie kwa maana watoto kama hawa, ufalme wa Mungu ni wao” (Luka 18:16). Baada ya kuzung-umza maneno haya, aliwachukua watoto hao mikononi mwake na kuwakumbatia. Pengine aliwafuta makamasi na machozi kwenye nyuso zao. Kisha akaweka mikono juu yao, akawabarikia. Sanjari na kuwabarikia, aliwapa salaam maalum kutoka mbinguni akise-ma, “kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wa watoto wadogo kama hawa!” Huu ni mfano halisi wa maisha ya Yesu ya kila siku, pa-sipo kulegea mchana kutwa alifanya kazi ili kujenga na kuimarisha ufalme wa Mungu.

Muda wa Yesu wa usiku

Nyakati za usiku watu wote walipokuwa usingizini, Yesu alikuwa ak-ienda peke yake mlimani au nyikani kuomba. Hali kadhalika wakati wa usiku, ndipo watu waoga walipomwendea, kwa lengo la kuzun-gumza naye. Yohana amemwelezea mmoja wa watu hawa katika injili yake. Basi palikuwa na mtu mmoja farisayo, jina lake Niko-demo, mmoja wa baraza la wayahudi lililotawala. Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye” (Yohana 3:1-2).

Yesu hakuwa na muda wa Mapumziko

Katika injili ya Marko tunasoma jinsi Yesu na wanafunzi wake walivyoamua kupumzika baada ya kuwahudumia watu. Huduma ili-kuwa nzito kiasi kilichowafanya wakose hata muda wa kula chaku-la. Kutokana na hali hii, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Njooni ninyi mahali pa faragha pasipo na watu tupate kupumzika” (Marko 6:31). Yawezekana wanafunzi wake walimwangalia kwa mshangao na kuulizana wakisema, je, itawezekana zamu hii kupata muda wa kupumzika tukiwa na Yesu? Hata hivyo walipanda mashua kuelekea upande wa pili wa bahari, ili kutafuata mahali panapofaa kwa ma-pumziko.

La kushangaza ni kuwa, walipofika upande wa pili, walikutana na makelele ya watu kuashiria kuwa hata huko, hapakuwa na nafasi ya mapumziko. Kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyi-ka kumlaki Yesu na wanafunzi wake! Watu hawa walitembea kwa miguu kutoka vijijini wakiwaleta wagonjwa na watu waliokuwa na mahitaji mengine. Yesu alipoona hivyo alifanya nini? Je, aliwawekea bango linalosema, “hakuna huduma leo, kwa kuwa nataka ku-pumzika?” Hapana isingeliwezekana kwake kufanya hivyo, wala hakuamua kufanya huduma ya kuhubiri na kuombea kwa kulipua, ili hatimaye awaruhusu watu waende zao. Badala yake, aliamua kuwahudumia kwa muda mrefu!

Ukiendelea na habari hii, utaona kuwa baadaye wanafunzi wake walianza kumsumbua wakisema, “Bwana wajua tumekuja hapa kwa lengo la kupumzika na siku ya kwanza imekwisha tukihudumia watu. Waage watu waende zao, nasi tupate muda wa kupumzika.” Lakini Yesu alikuwa na wazo tofauti. aliwaeleza kuwa hawezi ku-waruhusu waondoke wakiwa na njaa. Hapo akafanya muujiza wa kulisha watu 5,000 kwa mikate mitano na samaki wawili!

Tukiendelea na habari hii, tunakutana na Yesu katika mstari wa 45 wa sura ya 6 ya injili ya Marko, akiwalazimisha wanafunzi wake kupanda chomboni, kurudi kule walikotoka. “tumekuwa na ma-pumziko mazuri!” Yawezekana ndivyo wanafunzi walivyosemezana wao kwao. Kwa upande mmoja walikuwa sahihi kutokana na uk-weli kuwa, katika kukaa kwao huko, waliweza kuhudumia maelfu ya watu kiroho na kimwili. Haya ndiyo mapumziko ya kweli, yanay-oupendeza moyo wa Mungu.

Liko jambo la msingi tunaloweza kujifunza kutokana na habari hii. Badala ya kujiburudisha tu wakati wa likizo na mapumziko yetu, mapumziko hayo yanaweza kuwa ya baraka zaidi, pale tutakapo-tenga muda kufanya uinjilisti na umisheni. Baadhi ya vijana wal-iotendea kazi ushauri huu, walinijia baada ya likizo zao na kusema, “Tulikuwa na mapumziko ya baraka ambayo kamwe hatutakaa tuy-asahau!” Likizo au mapumziko yanayojumuisha kufanya shughuli za uinjilisti na umisheni, zinaweza kutuzalia mambo mengi ya baraka. Zitatuwezesha kuwa na ushirika na Wakristo wa maeneo mengine

50 51

na kutupatia muda wa kutosha kujifunza Biblia na kuomba. Kama haya hayatoshi, kutumia mapumziko kwa ajili ya ufalme wa Mungu, kutatupatia muda wa kutosha na Roho Mtakatifu.

Miongoni mwa shughuli za uinjilisti zinazoweza kufanywa na waamini wakati wa likizo au mapumziko, ni pamoja na uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, mikutano ya nje, maigizo, kugawa maandiko, ujenzi wa majengo ya ibada na kushiriki huduma mbalimbali ma-kanisani. Hebu fikiria furaha inayobubujika moyoni pale mtu binafsi anapoleta mwingine kwa Bwana. Waamini watapokea baraka zisizo na kifani, pale watakapotumia likizo au mapumziko yao kama vile Yesu alivyofanya. Kama unataka kutumia sehemu ya muda wako kwa ajili ya uinjilisti na umisheni ila hujui pa kuanzia, tuandikie kwa anwani inayopatikana mwanzoni mwa kitabu hiki. Uanafunzi na mashua

inayoitwa kanisa

Tunapoendelea kujifunza kuhusu mambo ya msingi Mkristo anay-otakiwa kuyafanya ili aimarike, naomba tushirikiane kuangalia funzo hili la uanafunzi na mtumbwi unaoitwa kanisa. Funzo hili tu-nalipata katika Injili ya Mathayo 14:21-36. Maandiko haya yanat-uonyesha wazi kuwa ufalme wa Mungu sio kula na kunywa kama baadhi ya waamini wanavyofikiria.

Wazo lingine tunalokutana nalo katika andiko hili, ni ule ukweli kuwa wanaume elfu tano, pamoja na wanawake na watoto, wote walikula mkate wa Bwana. Walikula mkate ulioongezwa kimiujiza na uliobarikiwa na wote wakashiba. Walishangaa na kusisimka na bila shaka walikuwa na shukrani kwa tendo hilo. Hata hivyo baada ya kumaliza kula, walimwacha Yesu pale Yesu alipowaruhusu ku-rudi makwao. Waliondoka huku kila mmoja akiwa na mawazo na hisia zake kuhusu muujiza uliofanyika. Naamini kuwa wewe hufa-nani na watu kama hawa. Wanaokuja ibadani ili tu Mungu akutane na mahitaji yao ya kiroho na kimwili.

Sura ya 8

52 53

wanaokula lazima wafanye kazi

Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kupanda ndani ya mashua na ku-tangulia kurudi kule walikotoka. Wanafunzi wa kweli wa Yesu, ni wale wanaozitii amri zake. Wanaongozwa na Roho Mtakatifu, huku wakiwa tayari kufanya mapenzi ya Mungu na kutii maagizo yake. Katika waraka wa Warumi tunasoma maneno yafuatayo, “kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (warumi 8:14).

Mpendwa, unaijua sauti ya Yesu? Unatambua kuwa anaweza kusema nawe, kuyaelekeza mawazo yako katika kitu fulani na ku-pandikizia wito maalum ndani maisha yako? Yesu alisema, “kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua nao wanifuata” (Yo-hana 10:27). Mfuasi mwaminifu wa Yesu hatakiwi kuishia tu katika kubarikiwa na Mungu na kula mkate wa kiroho. Tukumbuke kuwa hata wana wa Israeli walikula mikate kutoka mbinguni walipokuwa jangwani, ila wengi walifia jangwani. Kwa nini walishindwa kuit-waa nchi ya ahadi licha ya kula chakula kizuri kilichowatia nguvu? Bila shaka, tatizo lao linafanana na la wale wanaume 5,000 waliol-ishwa mkate na Yesu.

Pamoja na kuwapa mkate kwa ajili ya miili yao, Yesu aliwapa-tia neno la uzima. Je, waliomsikiliza walikuwa tayari kutii? Hili ni swali ambalo hata wewe unaweza kujiuliza. Je, uko tayari kufanya yote yanayokuhusu yaliyoandikwa katika Biblia na kuingia ndani ya mashua kwa lengo la kufanya kazi ya Mungu? Kiko chombo au mashua inayoitwa kanisa. Katika habari hii, tunasoma kuwa watu walipoondoka, Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kupanda ndani ya mashua kwenda upande wa pili wa bahari.

Kama tulivyotangulia kusema, mwanafunzi wa kweli wa Yesu ni yule anayethibitisha uanafunzi wake, kwa kutii maagizo ya Yesu. Wana wa Israeli waliangamia jangwani licha ya kula mikate kutoka mbinguni, kutokana na kutokutii! Katika habari yetu, wanafunzi wa Yesu wao walifanya tofauti. Wao walipoagizwa kuingia chomboni, walifanya hivyo huku wakitarajia kuvuka ng’ambo ya pili ya bahari. Mara zote Yesu anataka kuwaona watoto wake wakikaa pamoja na

kusonga mbele kwa pamoja. adui peke yake, ndiye asiyetaka kuona jambo hilo likifanyika. Yeye anataka kuwaangamiza. Ile mashua ambayo Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake kuingia ndani yake ni kanisa. Yesu anataka kuona watu wote wanaomwamini wakiingia ndani ya mashua, kisha watumikie ule wito uliowekwa na Mungu ndani yao. Kama vile ile mashua ilivyoelea majini bila kuzama, ndi-vyo kanisa la Mungu hapa ulimwenguni linavyotakiwa liwe.

Maji katika habari hii, yanafananishwa na ulimwengu. Kanisa ni lazima lielee ulimwenguni bila kukubali kuzamishwa na ulimwen-gu. Kwa kuwa watu waliojikabidhi kwa Yesu ni raia wa ufalme wa Mungu, ni lazima wao kama wanafunzi wa Yesu, watafute nafasi zao chomboni na kuanza kukiendesha. Mpendwa, Mungu ameweka nafasi maalum kwa ajili yako ndani ya kanisa la kweli lililo karibu nawe. Kama hakuna kanisa linaloamini na kuhubiri wokovu karibu na eneo unapoishi, Mungu anakutaka ushiriki kupandikiza kanisa la jinsi hiyo.

Utii unaweza kusababisha matatizo

Mara nyingi watu wanafikiria kuwa wakimtii Mungu, kamwe ha-watakutana na matatizo. Ukweli ni kuwa, yako matatizo yanay-otokana na kutii sauti ya Mungu. Hivi ndivyo ilivyotukia pale wa-nafunzi wa Yesu walipoingia chomboni, na kuanza safari kwenda upande wa pili wa bahari. Tufani kubwa ya upepo ilianza ghafla na kuipiga mashua yao. Kile walichofanya baada ya kukumbwa na tu-fani hii, kinatufundisha ukweli fulani kuhusiana na kiwango cha utii wao. Wangeweza kutia nanga ili kungojea dhoruba ipite, ila sivyo walivyofanya. Wala hawakuamua kurahisisha mambo kwa ku-geuza mashua ili ielekee kule upepo unapokuwa ukielekea. Badala yake, waliendelea kupiga makasia bila kukata tamaa. Waliagizwa na Bwana wao kwenda upande wa pili wa bahari, nao hawakutaka kwenda kinyume na amri hiyo.

Kanisa la Yesu katika kipindi hiki linasongwa na taabu nyingi zisizo na mfano. Kuna mawimbi makubwa ya kupenda vitu, utumwa wa mafanikio ya kimwili, kujipenda, dini za Mashariki, ukatili, maisha machafu, vitendo vya kishirikina ndani ya kanisa na kadhalika. Yote

54 55

haya yanataka kusambaratisha ushirika wa watoto wa Mungu na moyo wa kusaidiana ndani ya kanisa. Mawimbi haya yanalipiga kanisa bila huruma, huku yakijaribu kujenga makao ya kudumu ndani ya kanisa.

Makanisa mengi yamemezwa na yanaonekana kutojua jinsi ya ku-jinasua dhidi ya mawimbi haya. Makanisa haya yameacha kusonga mbele na kupambana na maovu. Wengi wanataka kuugeuza ulim-wengu ufanane na Ukristo, ila wameshindwa kuona jinsi wao we-nyewe wanavyofanana na ulimwengu, kutokana na kutawaliwa na tamaa za kimwili. Madhehebu mengine yameishia kung’ang’ania misimamo ya kidini isiyo na wokovu ndani yake. Kwa kufanya hivi, madhehebu haya yameshindwa kulitumikia kusudi la Mungu. Dhe-hebu lolote la Kikristo linatakiwa kutumikia kusudi la Mungu la kuutayarisha ulimwengu kwa harusi ya Mwanakondoo. Ieleweke wazi kuwa, Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu (warumi 14:17).

Tukirejea katika habari yetu inayotawala sura hii, tunakutana na matukio makubwa matatu. Jambo la kwanza, watu waliolishwa na Bwana walikuwa wamerudi majumbani mwao. Pili, wanafunzi wa Yesu wao walikuwa ndani ya mashua wakipambana na tufani. Tatu, Yesu alikuwa mlimani akiomba. Kanisa linapokuwa vitani, kamwe waamini hawatakiwi kutegemea elimu na uwezo wao wa kibina-damu. Mara zote nguvu za asili za kibinadamu, haziwezi kushinda nguvu za Kuzimu na zile za pepo wabaya. Kile kanisa au waamini wanachohitaji, ni nguvu za Mungu.

Tunaambiwa katika habari hii kuwa Yesu alipokuwa mlimani aki-omba, aliwaona wanafunzi wake wakipambana na upepo mkali. alivutiwa sana na juhudi na bidii yao, na ile hali yao ya kutoka-ta tamaa. Ni jambo la faraja mno pale tunapotambua kuwa, Yesu Bwana wa kanisa, anaona yale tunayoyapitia na kutujali. Wakati mwingine tufani za kimaisha zinapiga maisha yetu na hata tunaku-tana na misukosuko inayozidi uwezo wetu katika kupigana nayo. Kama tulivyosema, tamaa za vitu, anasa za dunia, mapokeo maba-ya na malezi yaliyopotoka na nguvu za pepo wabaya, vinavuma kwa kasi kubwa kwa lengo la kutuangamiza. Hata hivyo, Yesu ndiye

faraja na tumaini letu.

Neno la Mungu limetamka bayana kuwa tunaye kuhani mkuu anayeketi mkono wa kuume wa Mungu, anayetuhurumia na kuchu-kuliana na udhaifu wetu. Huyu hutuombea mara zote ili imani yetu isishindwe na nguvu za yule Mwovu (waebrania 4:15; Luka 22:31-32; warumi 8:32). Kamwe mtu wa Mungu hatakiwi kukata tamaa anapopambana na Ibilisi. Hata kama wewe ni mwalimu wa watoto, mhubiri, mzee, shemasi, kiongozi wa vijana, kiongozi wa kina mama au kiongozi wa kwaya, endelea kupambana na roho za uovu ndani na nje ya kanisa. Omba kwa bidii bila kukoma, huku ukishuhudia kila mahali kuhusu nguvu za Yesu. Ukifanya hivyo, Mungu naye ataruhusu uweza wake ukusaidie na kukuwezesha kushinda mata-tizo yatakayoinuka mbele yako.

Ukaribu wa Yesu wakati wa shida

Wakati wanafunzi wa Yesu walipokuwa wakipambana na dhoruba, tunasoma kuwa Yesu aliwaendea ila wao walishikwa na hofu kuu. Uwezo aliouonyesha wa kutembea juu ya mawimbi makali ya tufani, lilikuwa jambo geni kwao. Yesu anaweza kutumia njia mbalimbali pale anapotaka kutuonyesha uwezo wa Baba yake. aliwajia wana-funzi wake akitembea juu ya maji, ili kukutana na hitaji lao. Uweza wake wa Kiungu ulishinda nguvu ya asili iliyoinuka dhidi yao.

Mara kwa mara Mungu hutenda kazi kimiujiza ili kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni Bwana. Hufanya hivi ili kulilinda kanisa lake na kulivusha salama upande wa pili wa bahari. Neno la Mungu linatueleza wazi kuwa, katika siku hizi za mwisho za kanisa, Roho Mtakatifu atamiminwa kwa watu wote. Wanaume kwa wanawake watatabiri, vijana wataona maono na wazee wataota ndoto (Yoeli 2:28). Mpendwa, ahadi hizi zimetimizwa katika siku zetu na zipo kwa ajili yako na mimi. Sisi kama wafuasi wa Yesu tunatakiwa kupokea nguvu hizi zisizo za kibinadamu, kutoka kwa Mungu. Hali kadha-lika, ni lazima makanisa yetu yawe na waamini waliompokea Roho Mtakatifu kwa kipimo cha tele.

Nguvu za Roho Mtakatifu ndizo zitakazoiwezesha mashua yetu, kusa-

56 57

firi salama na kutumikia kusudi la Mungu, bila kuvunjwa vunjwa na dhoruba. Lengo na kusudi la safari yetu ni lipi? Wengi miongoni mwa watu wanaotuzunguka ni wagonjwa na waliofungwa na dhambi na mateso mengine ya kimwili. Maisha yao ni ya kufukuza upepo, yasiyo na nuru wala matumaini. Ni wajibu wa kanisa, kuwapelekea watu hawa neno la uzima na kulitambulisha kanisa kwao, kama mahali salama pa kukimbilia. Kanisa ndilo litakalowawezesha ku-fikia kilele la lengo la maisha yao, ambalo ni kuwa na ushirika wa milele na Yesu.

walidhania wanaona mzimu

Unaweza kushangaa kuona jinsi tunavyozungumza waziwazi kuhusu karama za roho, na jinsi ambavyo hatuogopi kutaja kuhusu maono na kuzungumza kwa lugha mpya. Huenda hujawahi kusikia kuhusu habari hizi au kushuhudia udhihirisho wa mambo haya. Yawezeka-na hata umeonywa kujihadhari na watu wanaozungumzia mambo haya, eti kwa vile ni uzushi wa Wapentekoste!

Katika habari yetu tumeona udhihirisho mkubwa wa karama za Mungu, pale Yesu alipotembea juu ya maji. Wanafunzi walidhania kuwa ni mzimu pale walipomwona akitembea juu ya maji. Tendo hilo lilikuwa geni kwao, kutokana na ukweli kuwa, alikuwa hajawa-hi kujidhihirisha kwao kwa njia hiyo. Neno la Mungu linasema wazi kuwa walipomwona walilia kwa hofu, wakidhania kuwa wanaona mzimu. Je, ni vigumu kutofautisha njia za Mungu na zile zisizo za Kimungu? Inawezekanaje mtu amfananishe Bwana wake mpendwa na mzimu? Jambo hili linaweza kutokea pale tu kunapokuwa na hali ya kutomfahamu vizuri. Hata hivyo, Yesu aliiona hofu yao, hivyo akawaita katikati ya mvumo wa mawimbi na kusema. “Msiogope, msiwe na hofu, ni mimi!”

Katika miaka tuliyo nayo, Ukristo wa kibinafsi na ule wa kijumuia katika kanisa la mahali umepoteza ladha yake. Waamini wengi ha-waishi maisha ya kumpendeza Mungu na ibada za makanisa mengi zimegeuka kuwa za kidini na kimapokeo. Watu wanapoteza kwa kasi hamu ya kwenda makanisani kutokana na kuelewa kuwa, hakuna kitu kisicho cha kawaida kitakachotokea katika ibada makanisani

mwao. Yesu Kristo anataka kujifunua katikati ya ubaridi huu wa kiroho.

Je, umewahi kuona mgonjwa akiponywa kimiujiza na Mungu? Je, shangwe, nderemo na furaha vilikuwaje kwa wale walioshuhudia muujiza huo? Je, ulishawahi kumwona mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu na ishara ya kunena kwa lugha mpya? Yawezekana iliku-wa kero kwa watu wasioelewa, ila kwa wale wanaofahamu, ulikuwa wakati wa furaha na shangwe. Walitambua kuwa hiyo ni mojawapo ya njia zinazotumiwa na Yesu kujidhihirisha kwa watu wake.

Shuka ndani ya mashua

Tunapoendelea na habari hii, yako mambo mengi ya kiroho ya kuji-funza. Mchukue Petro, amekaa ndani ya Mashua huku akishuhudia jinsi Yesu alivyokuwa akitembea juu ya maji. Ndani yake iliumbika shauku kubwa ya kutaka kufanya kile kilichokuwa kikifanywa na Yesu. “Bwana kama ni wewe, niruhusu nije kwako nikitembea juu ya maji.” Hii ni imani. Petro alijua kuwa alitakiwa kutegemea maneno ya Yesu. alitambua kuwa imani itambeba na kumpatia ujuzi mpya. Naye Yesu akamwambia, “njoo.” Petro akaiweka imani yake katika matendo, akatembea juu ya maji jambo ambalo kibinadamu hali-wezekani.

Lilikuwa jambo la kufurahisha kumwona Petro akishuka katika mashua na kuanza kumwendea Yesu. Hapo Petro naye akashinda nguvu za asili, kwa vile tu alikuwa njiani kumwendea Yesu. alikuwa amedumu katika ushirika na Yesu na kukubali wito kutoka juu, wa kuwa shahidi wa nguvu za Yesu. Ni mapenzi ya Mungu kutufanya tuwe kama Yesu. anataka tumwangalie Yeye kama kielelezo kwa, kumpenda, kumtumikia, kumtii na kisha kuishi naye milele. Tutaka-poishi maisha ya aina hii, tutashiriki ushindi wake usio na mwisho.

Mfano wa kutokuamini

Naamini ulishawahi kuona michoro katika madirisha ya majengo mengi ya makanisa inayoonyesha Petro akiwa amezama ndani ya maji. Naamini huku ni kupotosha ukweli. Kama wachoraji wanat-

58 59

aka kuwa na mchoro unaoonyesha mwanafunzi aliyezama majini, wangemchora Mkristo yeyote yule, au wanaweza hata kujichora wao wenyewe! Ukweli kuwa Petro alizama ni jambo la kawaida, linalot-okea kila siku lakini kuwezeshwa kwake kutembea juu ya maji, hilo ndilo jambo muhimu linalotakiwa kukumbukwa katika habari hii. Sanjari na ukweli huu, ni vema tukumbuke kuwa Petro alianza ku-zama, pale tu alipoondoa macho yake kwa Yesu. Hata hivyo Bwana alinyosha mikono yake na kumwinua.

Uwe na moyo mkuu

Tunapofikia tamati ya habari hii, nakusihi uchukue hatua ya kum-wendea Yesu siku ya leo. Mwombe ili ajifunue kwako. Tunapoomba mambo makubwa kutoka kwa Mungu pasipo kuongozwa na ubinaf-si na kiburi, kamwe Mungu hatayachukia maombi haya. Yeye atati-miza ahadi zake maishani mwetu, kamwe hatutakiwi kuogopa! Neno la Mungu linasema, “ ...walakini alipo Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru” (2 wakorintho 3:17; Marko 9:23). Nguvu, karama na tunda la Roho Mtakatifu, uponyaji na matendo ya miujiza vyote vinawezekana katika jina la Yesu na kwa mamlaka yake na katika kushirikiana naye (wagalatia 5:22, Yohana 15), Marko 16:17).

Kuomba katika roho

Tukaabudu wapi? Lipi ni kanisa sahihi? Tutapata wapi kanisa zuri, ambalo ndani yake ibada ya kweli inafanyika? Kila mara watu hu-jiuliza maswali haya na wataendelea kufanya hivyo. Hata hivyo, Yesu alitoa majibu ya maswali haya wakati alipokuwa akizungum-za na mama Msamaria katika kisima cha Yakobo (Yohana 4:19-24). Kila mtu anayejiuliza maswali haya, anatakiwa amwendee Yesu kwa majibu.

Kuabudu katika roho na kweli

Ni jambo linalofurahisha tunapokutana na watu wasio wabishi pale unapofikia wakati wa kuzungumzia kuhusu mahali pazuri pa kuabudia. Ieleweke wazi kuwa, Mungu anatafuta ibada ya kweli in-ayotoka moyoni. Yesu alisema, “saa inakuja nayo sasa ipo ambayo wamwabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yo-hana 4:32).

aliendelea zaidi kusema kuwa, kwa kuwa Mungu ni roho, basi, wamwabuduo halisi yawapasa kumwabudu katika roho na kweli. Huu ni ukweli unaojidhihirisha katika agano jipya. Katika waraka wake kwa Waefeso, Mtume Paulo anamaliza mjadala wake juu ya

Sura ya 9

60 61

silaha za Mungu kwa maneno yafuatayo: “Kwa sala zote na mao-mbi kila wakati mkisali katika Roho” (waefeso 6:18). Yuda naye ameandika katika waraka wake akisema: “Lakini ninyi wapenzi, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu” (Yuda 20). Maandiko haya yanatuhimiza kuomba kila wakati na katika Roho Mtakatifu.

Kuomba katika Roho

Wakristo wengi wanaamini kuwa kuomba katika Roho ni kuomba kimoyomoyo au kuwa na mawasiliano na Mungu, yasiyohusisha mawazo. Hata mimi niliwahi kuamini hivyo siku za nyuma kabla ya kufunuliwa undani wa jambo hili. Ufunuo huu niliupata katika nyaraka zilizoandikwa na Mtume Paulo. Katika waraka wake kwa Wakorintho Paulo anawaulizwa wasomaji wake swali lifuatalo; “itakuaje?” (1 wakorintho 14:15). Kisha anatoa jibu mwenyewe kwa kusema, “Nitaomba kwa roho tena nitaomba kwa akili pia” (1 wakorintho 14:15). Katika mstari wa 14 anasema waziwazi kuwa, kuomba kwa roho ni kuomba kwa lugha. “Nikiomba kwa lugha roho yangu huomba” (1 wakorintho 14:14).

Katika mstari wa 2 mtume Paulo anatumia maneno yafuatayo ku-fafanua tendo hili la kunena kwa lugha: “Yeye anenaye kwa lugha huzungumza na Mungu mambo ya siri katika roho yake” (1 wako-rintho 14:2). Kwa hiyo mtu anaponena kwa lugha hunena kutoka ndani ya roho yake. Kumbuka, sio kwa akili zake ambazo wakati mwingine, hazisadiki mambo ya Mungu. aombaye kwa lugha ana-zungumza kutoka katika kilindi cha mtu wake wa ndani na kwa kuwezeshwa na uhusiano wake wa ndani na Mungu. Kwa upande mwingine kuomba kwa akili, kunaweza kugeuka kuwa hotuba, ku-rudia rudia maneno au kuwakilisha orodha ya mahitaji mbele za Mungu.

Mtu anayeomba kwa kumaanisha, atakubaliana na maneno ambayo mtume Paulo alizungumza katika waraka wake kwa Warumi akise-ma; “Kwa maana hatujui yale tunayotakiwa kuyaomba” (warumi 8:26). Kama wewe unadhania kuwa unajua kuomba, mwisho wa mstari huu Mtume Paulo anaeleza waziwazi kuwa, hatujui jinsi ya

kuomba! Kutokana na maneno haya, waamini wanatakiwa kuto-ishia tu kuomba kwa akili, bali, waombe pia katika roho. Huu ndio msisitizo tunaokutana nao katika maandiko yafuatayo; Na Roho Mtakatifu hutusaidia udhaifu wetu. Kwani hatujui yale tunay-otakiwa kuyaomba na wala hatujui jinsi ya kuomba. Lakini Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea, kwa kuugua kusikotamkika. Na Baba aijuaye mioyo yetu, anajua kile Roho anachosema. Kwa kuwa Roho huwaombea waamini, kama Mungu apendavyo (warumi 8:26-28)NLt.

Yeyote anayeomba kwa lugha mpya, kila wakati ataomba sawasa-wa na mapenzi ya Mungu. Kulingana na maandiko haya, nimefikia mahali pa kuamini kuwa, yeyote anayeomba katika Roho, anaom-bwa kwa njia inayompendeza Mungu. Kama unataka Mungu apen-dezwe na maisha yako, omba katika Roho. Kama bado hujapokea ubatizo wa Roho Mtakatifu na ishara ya kunena kwa lugha, anwani mwanzoni mwa kitabu hiki, inaweza kukusaidia kufikia kilele cha hitaji lako. Kamwe usipuuzie jambo hili. Mtume Paulo anatuonyesha umuhimu wa kuomba kwa Roho kupitia maandiko yafuatayo: “Na-taka ninyi nyote mnene kwa lugha” kisha anaendelea kwa kusema, “Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote” (1 wakorintho 14:5,18).

Je, ni muhimu kunena kwa lugha? Tunapaswa kupokea zawadi hii ya kuzungumza kwa lugha mpya? Nitayajibu maswali haya kwa kuuliza maswali yafuatalo; Je, maombi ni muhimu? Hivi inatupasa kuomba? Kamwe Mungu hatoi kitu chochote kisicho na faida kwa watoto wake. alimleta Roho Mtakatifu duniani, huku akitambua kuwa waamini watamhitaji katika mapambano yao dhidi ya Ibilisi. aliwabatiza kwa Roho Mtakatifu wale 120 wakati wa siku kuu ya Pentekoste na angali akifanya hivyo. Watu wanaendelea kubatiz-wa kwa Roho Mtakatifu na kumsifu Mungu kwa lugha mpya kama ilivyotokea katika Biblia. Mahali popote pale waamini wanapom-pokea Roho Mtakatifu, huomba kwa kumaanisha kadri Roho ana-vyowaongoza. Yuda alisema, “kwa sala zote na maombi mkiisali kila wakati katika Roho...” (Yuda 20). Na jinsi Paulo alivyomwagiza Timotheo akisema, “nakukumbusha uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako” (2 timotheo 1:6).

62 63

Ombi letu kwa waamini wote vijana na wazee ni hili: Ombeni ka-tika Roho, ombeni kwa lugha mpya! Mungu ametupa kipawa hiki ili kitujenge, kituimarishe, kituinue, kutuburudisha na kutuweze-sha kudumu katika uwepo wake (1wakorintho 14:4). Wakristo wa-napoimarika hapo kanisa litakuwa na waamini imara. Je, ubora wa kanisa hautegemei uimara wa waamini wake? Mungu ni roho na wamwabuduo halisi, ni lazima wamwabudu katika roho na kweli.

Hati safi ya afya nzuri

Kutokana na yale niliyoyapitia katika maisha yangu, najua fika vile magonjwa yalivyo. Mke wangu alitakiwa kupasuliwa baada ya ku-gunduliwa kuwa ana ugonjwa wa saratani. Mimi mwenyewe nili-teseka kutokana na muwasho mkali ndani ya mishipa ya ufahamu. Tatizo hili liligunduliwa katika hospitali moja huko Ujerumani. Mad-aktari walijaribu kunisaidia ila hakuna tiba iliyofanikiwa kumaliza tatizo hilo. Ingawa baadaye nilitoka Hospitalini na kurudi nyumba-ni, bado hali yangu iliendelea kuwa mbaya kwa majuma mengi. Ka-tika hali hii ya maumivu makali na kuteseka, nilipata wafariji kama wale ayubu! Kwa kuwa nilikuwa mhitaji, nililazimika kutendea kazi kile kinachojulikana kama, mafundisho ya imani.

Kutubu dhambi

Ushauri wa kwanza nilioupata ni ule uliohusisha tatizo nililokuwa nalo na na dhambi. Niliambiwa kuwa ugonjwa unaweza kujitokeza kwa mwamini pale tu anapokuwa amefanya dhambi. Nilitakiwa ku-likubali hilo na kutubu mbele za Mungu. Ni rahisi kumpatia mwenye mateso ushauri wa jinsi hii, hasa pale wewe mwenyewe unapokuwa huna tatizo.

Sura ya 10

64 65

Kukiri ushindi kwa imani

Mtu mmoja alinijia na kunishauri nikiri imani yangu kwa kujiambia na kuwaambia watu wengine, vile ninavyoamini kuhusu uponyaji wa kimiujiza. Niliambiwa kuwa nikifanya hivyo, kila kitu kitakuwa sawa. Nilifanya hivyo kwa uaminifu, ila mlima wa udhaifu uliende-lea kusimama.

Dharau ugonjwa unaokukabili

Wafariji wengine walikuja na ushauri wa kushangaza, “wewe udha-rau tu ugonjwa unaokukabili”, haya ndiyo maneno yaliyotoka viny-wani mwao. Ushauri huu nao haukuweza kunisaidia.

Mkemee Shetani

Wengine walinishauri niendelee tu kumkemee Shetani, naye ataon-doka pamoja na ugonjwa aliouweka ndani yangu. Hili nalo nilili-fanya ila hali yangu ya kuumwa, ilizidi kuwa mbaya.

Sifu mbele za Mungu

“Kumtukuza Mungu kwafaa sana, wewe imba tu na umtukuze Bwa-na kwa bidii, na hapo ugonjwa ulio nao utatoweka.” Ushauri huu nao nilioutendea kazi, nilisifu kwa bidii ila sikupata muujiza nilioku-wa nikiuhitaji.

Ombewa kisha jione umepona

Mtu mmoja alipendekeza niombewe na kisha niyatupe magongo yaliyokuwa yakinisaidia kutembelea. “Mwamini Bwana amekwisha kukuponya na ya kwamba unaweza kutembea bila magongo!” Mara zote waombeaji wa imani, huamini kuhusu matokeo ya haraka, hata pale maumivu ya mgonjwa yanapoonekana kuongezeka. Wakati mwingine wanaweza kukukatisha tamaa zaidi pale wanapokuam-bia kuwa, hujapona kutokana na kutokuwa na imani. Wanaamini kuwa ukiwa na imani, lazima utapata kila unachokihitaji!

Kiri maandiko mara kwa mara

Ushauri mwingine nilioupata ni huu wa kurudia kutamka mistari ka-

tika Biblia inayohusu uponyaji, hadi pale itakapoumba muujiza wa uponyaji. Utawasikia wakikuambia, mtu mmoja aliponywa homa kali baada ya kutamka andiko hili mara mia moja!

Kamwe usikate tamaa

Kama uliwahi kutendea kazi mafundisho haya bila kufanikiwa, nataka nikuhakikishie kuwa mimi pia nimewahi kuyatendea kazi pamoja na mengine mengi yanayofanana na haya. Nililia, nilim-cheka Shetani, nilimtukuza Mungu, niliomba, kukiri ushindi na ku-funga, lakini maumivu hayakuondoka. Hata vidonge vya usingizi vyenye nguvu sana vilinipa usingizi wa masaa mawili tu! Nilikuwa mzito kukubali matibabu yanayotolewa hospitalini. Nilisherehekea mwaka wangu wa 50 nikiwa na mke wangu huko afrika ya Kusini, nikiwa na maumivu makali.

Mbali na kulazwa muda mrefu hospitalini nilipokuwa mtoto, sikum-buki kama nilishawahi kuugua katika maisha yangu. Hata hivyo katika kipindi hiki cha kuugua, niliona ni heri liendelee kudhoofika kiafya, kuliko kunywa vidonge! Kusema ukweli, mara kadhaa nime-shuhudia miujiza ya ulinzi dhidi ya magonjwa, wakati nilipotembe-lea maeneo yaliyokubuhi kwa magonjwa. La kushangaza ni kuwa, katika kipindi hiki, mawingu mazito ya wakati wa hari yalinipiga mimi na familia yangu.

Wakati wa kiangazi mwaka 1985 ilinilazimu niandamane na mke wangu katika safari za kimisheni nje ya Ujerumani. Mpango huu uli-kuja wakati akiwa amelazwa hospitalini tayari kwa upasuaji! Siku moja kabla ya upasuaji nilipokuwa kitandani kando yake, mtaalam wa kike wa dawa ya ganzi alikuja kumpatia maelezo kuhusu mata-yarisho yanayohusu upasuaji, kisha akaondoka. Baada ya dakika kadhaa, alirudi huku akitetemeka. “Bibi Sardaczuk, hapa nina ma-jibu ya vipimo vya mwenendo wa mwili wako. Ninaweza kukupa dawa ya usingizi kesho, ila sina uhakika kuwa nitafanikiwa kuku-amsha! Vile afya ya mwili wako ilivyo, haitawezekana kukupasua.”

Baada ya kuwauliza kile tunachotakiwa kufanya, walinitaka nirudi naye nyumbani. Tuliruhusiwa huku wakituomba turudi hospitalini

66 67

kwa upasuaji, pale mwenendo wa mwili wa mke wangu utakuwa sawa. Nilimtia mke wangu moyo, na kumwomba tuandamane pamoja katika safari ya umisheni nje ya Ujerumani, huku tukimwa-mini Mungu kuhusiana na kuugua kwake. Mke wangu akaacha ku-endelea na matibabu na tukaenda pamoja kuwahudumia wahitaji katika bara la afrika.

Tuliporudi baada ya safari yetu, mke wangu alienda tena kumwona daktari na kumfahamisha kuwa Mungu amemponya na sasa hatumii tena dawa. Huku akionekana kusumbuka moyoni, yule daktari alisema; “kama hutaki kufuata ushauri wangu unaweza kumwen-dea daktari mwingine. Lakini kama hutaendelea na dawa, ugon-jwa utaongezeka na hali yako itakuwa mbaya zaidi.” Jibu la mke wangu lilikuwa, “Mungu anapoponya, huponya kabisa.” Naye dak-tari akamjibu kwa kumwambia “kwa Mungu yote yanawezekana.” Ingawa matokeo ya vipimo yalionyesha kuwepo kwa tatizo, tenzi katika koo lake ilipona na hadi leo ni mzima. Tunamrudishia Mungu utukufu na shukrani kwa muujiza huu. Yeye ni Tabibu mkuu, jana leo na hata milele! Baadaye mke wangu aliponywa pia kimiujiza kutokana na maumivu makali ya goti.

Oktoba mwaka 1985 mke wangu alipatwa na uvimbe uliosababisha afanyiwe upasuaji hospitalini. Baada ya ganzi kumalizika mwilini mwake, alitambua kuwa uvimbe uliokuwa ukimtesa ulikuwa um-eondolewa. Hata hivyo, kutokana na kuenea kwa saratani, ilimbidi mpasuaji auondoe pamoja na majimaji kwenye viungo vyake. Jam-bo hili linaweza kukufanya ushikwe na butwaa. Huko nyuma mke wangu aliponywa mara mbili kimiujiza bila madaktari kuhusika, je, ni kwa nini zamu hii ilibidi afanyiwe upasuaji?

Kama unatatizika kutokana na jambo hili, naomba nikueleze kuwa, nilipomtembelea mke wangu baada ya upasuaji, niliruka kwa fura-ha ndani ya chumba chake. Tulimsifu Mungu pamoja kwa kuwa tuliusikia uwepo wake katika chumba kile. Tulitambua kuwa Yeye ndiye aliyeruhusu upasuaji ufanyike ili kunusuru maisha ya mke wangu. Tofauti tu ni kuwa, zamu hii amemponya kwa kushirikiana na madaktari!

Ujuzi wangu kuhusu magonjwa

Baada ya kuelezea yale mke wangu aliyoyapitia kiafya, naona ni vema nikamilishe mazungumzo niliyoyaanza kuhusu afya yangu. Kama nilivyotangulia kuelezea, kitendo cha kutembea kwa msaada wa magongo, kiliniweka katika hatari ya kuanguka na kilinihuzu-nisha sana. Niliombewa mara nyingi ila sikupokea uponyaji. Siku moja tulitembelewa na wageni nyumbani kwetu mmojawao akiwa mtumishi wa Mungu kutoka Uholanzi. Kwa heshima nilimtambul-isha ndugu huyu kwa wenzake kwa kutumia maneno yafuatayo; “Ndugu wapendwa, sasa muujiza unaenda kutokea kutokana na ukweli kuwa ndugu huyu, alitumiwa kueneza injili katika nchi ya Indonesia na katika huduma yake, aliwahi kushuhudia watu waki-fufuliwa!” Baada ya kutamka maneno haya, yule ndugu alinigeukia na kusema, “hiyo ni kweli kabisa. Lakini pia niliwahi kuwaombea watu kama mia hivi, bila kushuhudia matokeo yoyote!”

Jibu la ndugu huyu la kuwa mkweli bila kujivuna au kuongeza chumvi, lilinifanya nilijisikie kuwa huru. Watumishi wengi katika kipindi tulicho nacho wanapenda kukuza mambo. Wanafikiri kuwa wakielezea mambo yaliyoshindikana kufanyika katika huduma zao, watampunguzia Mungu utukufu wake! Mashujaa wengi wa sasa wa imani, wanapenda kusimulia upande wa mafanikio peke yake! Ndu-gu huyu kutoka Uholanzi, alitutia moyo na kutuomba tumshukuru Mungu, hata kwa ajili ya magongo yangu, kwa kuwa yalinisaidia kutembea.

Ingawa bado nilikuwa nasikia maumivu makali mwilini mwangu, mtizamo mpya wa ushindi ulikuwa umejengeka ndani yangu. Pa-sipokujali maumivu makali niliyokuwa nayo, nilianza safari zangu za kimisheni, ingawa baadhi ya watu walikuwa hawajisikii vizuri pale walipoona madhabahu ikihudumiwa na mtumishi anayetem-belea magongo! Mara nyingi nililazimika kutoa hadithi za kuchek-esha kuhusiana na afya yangu kabla ya kuhubiri, ili kutuliza nyoyo za wasikilizaji wangu. Kwa kiwango fulani, hadithi hizi zilichangia kurefusha mahubiri na mafundisho yangu.

Siku moja mimi na mke wangu tulikuwa tukihubiri katika mji mmoja

68 69

na baada ya ibada tulilazimika kupakia mizigo ndani ya gari letu tayari kwa safari ya kurudi nyumbani. Ilikuwa kazi ya kuchosha na ilinilazimu kusaidia kubeba masanduku ya nguo licha ya maumivu makali niliyokuwa nayo. Ghafla nikasikia kupokea mabadiliko fu-lani katika mwilini wangu. Nilimwita mke wangu na kumwambia, “mpenzi, kitu fulani kimenitokea, najisikia nafuu!” Kuanzia wakati huo na kuendelea afya yangu iliendelea kuimarika. Jumapili ya Pa-saka mwaka 1986, wakati nilipokuwa katika juma la mafundisho ya Biblia nchini Uswisi, niliweza kuhubiri nikiwa nimesimama bila msaada wa magongo! Mungu amenigusa na kuniponya kabisa! Ni-namsifu Yesu kwa muujiza huu.

Mara nyingi afya yangu inapotetereka, huwa ninafanya mazoezi na kutumia dawa zinazopatikana katika matunda na vyakula. Mwan-zoni mwa mwezi Desemba mwaka 1987, nilipatwa na jaribu lingine. asubuhi nilikuwa ofisini kama kawaida, ila jioni nilijikuta nikiwa hospitalini, tayari nikiwa nimefanyiwa upasuaji! Hata hivyo kuto-kana na kosa lililofanywa na madaktari katika vipimo vyao, hali yangu ilizidi kuwa mbaya kutokana na kupokea matibabu yasiyo sahihi. Baadaye ilibidi nifanyiwe uchunguzi mwingine, uliogundua tatizo lililokuwa likinikabili. Hata hivyo madaktari walimweleza mke wangu kuwa, walikuwa hawana uhakika ikiwa watafaulu ku-maliza tatizo hilo. Baada ya kupata fununu kuhusu wasiwasi huu wa madaktari, nilitulia kwa Bwana bila kuwa na hofu yoyote ya kifo. Kisha niliwaita wazee wa kanisa ili waniombee na kunipa-ka mafuta sawasawa na neno la Mungu. “Mtu wa kwenu akiwa hawezi awaite wazee wa kanisa nao wampake mafuta katika jina la Bwana...”(Yakobo 8:14-16).

Baada ya maombi, Mungu alinithibitishia moyoni kuwa nilikuwa nimekwisha kuponywa. Kwa bahati mbaya madaktari wao wali-kuwa hawana tumaini hilo, kutokana na hali halisi ya matokeo ya vipimo vyao. Kutokana wasiwasi wao, walinilaza katika chumba cha wagonjwa mahututi, kwa majuma saba. Namshukuru Mungu pia kwa ujuzi nilioupata kutokana na tukio hili, natambua kuwa wema wake ndio ulioniokoa.

Kwa nini nimeamua kutoa maelezo marefu namna hii kuhusu kuu-

gua kwangu? Sababu kubwa ni ili uelewe kuwa ninalielewa somo hili. Katika kipindi cha kuugua kwangu na kupitia maumivu makali, nilijifunza kuhusiana na ukweli wa neno la Mungu. Kulingana na Biblia, nilikuwa na hati safi ya afya nzuri!

70 71

Hukumu ya mwisho

Nataka nianze sura hii kwa kusimulia habari ya kweli katika Bib-lia inayoweza kukusaidia kufanya uamuzi wa kumchagua Mungu na kuendelea kumtumikia. Kutokana na urefu wa maandiko haya, naomba uyasome mwenyewe katika Luka 19:11-27.

wahusika wakuu

Wahusika wakuu katika habari hii ni mfalme tunayeweza kumlin-ganisha na Yesu. Safari ya mfalme huyu, inalinganishwa na kupaa kwa Yesu kurudi kwa Baba yake. Wahusika wengine ni watumwa watatu wanaowakilisha waamini wa kweli wa kanisa la Yesu. Kisha wametajwa raia wa nchi wanaowakilisha watu wanaoishi dhambini. amana au talanta iliyokabidhiwa, ni mfano wa uzima mpya kutoka kwa Mungu. Katika habari hii kumetajwa pia kurudi kwa mfalme ambako ni sawa na kuja kwa Yesu mara ya pili. Nayo hukumu ya mwisho ni mfano wa kiti cha hukumu cha Yesu.

Mfano huu unaelezea hali halisi vile mambo yanavyotendeka ulim-wenguni. Leo hii watu wengi hawataki kukaa chini ya utawala wa Yesu. Hata wale wanaotamka kuwa ni Wakristo, wanaishi maisha yasiyofanana na yale Kristo aliyoyaishi. Ieleweke wazi kuwa tu-napoamua kuwa Wakristo, tutakabiliwa na upinzani mkubwa, hivyo

hatutakiwi kuishi kwa kupapasa papasa. Kila wakati tunapomkiri Yesu na kuhudumu katika ufalme wake, vita kubwa itainuka mbele yetu. Vita hii hutokea kutokana na ukweli kuwa, tunazungukwa na mamlaka ya giza na watu wasioamini, wanaoishi kama maadui wa Yesu Kristo.

Katikati ya upinzani huu, Yesu anataka kuutumia mfano huu kutu-tia moyo na kutuondolea hofu dhidi ya upinzani tunaokutana nao. anataka tuuone upinzani huu kama rafiki. Lakini swali kubwa tu-naloweza kujiuliza ni ile hali ambayo Yesu akirudi atatukuta nayo. Je, atatukuta tukiwa na hali gani? Je, tutakuwa Wakristo waliojitoa, wanaoishi katika upendo na kuuzalia ufalme wake matunda? Siku hiyo ya hukumu ya mwisho itakuwaje kwetu?

Maandiko yanayotawala sura hii yanatabiri kuhusu kurudi kwa Yesu, tukio ambalo maadui zake hawataweza kulizuia. atakuja ku-shika uongozi wa serikali na hapo watumishi wake (Watu waliooko-ka) wataitwa kutoa hesabu ya maisha yao, na jinsi walivyotumia mafungu ya fedha waliyokabidhiwa. Kila mmoja atasimama mbele za Bwana kutoa hesabu ya maisha na utumishi wake. Wako wat-akaosimama mbele za Bwana wakiwa wamejaa furaha huku kila mmoja akisema, “Bwana tazama fedha uliyonipa, nimeizalisha.” Naye Bwana atawalipa na kuwasifu bila kujali ikiwa wameleta fai-da kubwa au ndogo.

Mwisho wa mfano huu, tunaona akija mbele za Bwana wake yule mtumwa aliyepewa fungu moja. anamkaribia Bwana huku akiwa amejawa na hofu kubwa moyoni. Kisha kwa heshima anafungua kikasha kilicho mkononi mwake na kumkabidhi Bwana wake kitu fulani huku akisema, “hii ndiyo talanta yako uliyonipa. Nilipata wakati mgumu kuitunza na kuilinda, kwa kuwa nilikuwa ninaishi kwenye maeneo hatari na pia maisha yalikuwa magumu sana. Hata hivyo nimefanikiwa kuitunza na kuilinda isipotee au kuharibika. Hii hapa talanta yako!” Kisha kwa huzuni Bwana wake anamaliza kwa kusema, “Wewe mtumwa mwovu.” akawaamuru wale watumwa wenzake waliosimama kando, wamfunge na kumtupa nje!

Kwa nini Bwana anafanya hivi kwa mtumwa wake? Si yule mtumwa

Sura ya 11

72 73

amelitunza fungu lake na kulirudisha kama lilivyokuwa? Tena haku-ruhusu ulimwengu na watu waovu kumnyang’anya fungu lake. Kwa uaminifu alilishikilia fungu hilo akingojea kurudi kwa Bwana wake, lakini sasa, Bwana wake anamnyang’anya kile wezi walichoshind-wa kukichukua na kumpa mtu mwingine. Baadaye, mtumwa huyu anapotea! Kwa nini Bwana amfanyie jambo zito kama hili?

Kwa kuwa mfano huu unaonyesha hali halisi ya mambo ilivyo ndani ya kanisa, ni wazi umebeba funzo kubwa kwa kila mmoja wetu. Hebu anza wewe mwenyewe kwa kujiuliza maswali yafuatalo: “Hivi unataka upate nini kutokana na maisha yako ya Ukristo? Lengo kuu la wewe kuwa Mkristo, ni lipi? Je, unataka uishie tu katika kuhifa-dhi kile ulichokabidhiwa na Mungu? Je, inatosha pale tu unapohifa-dhi amana uliyokabidhiwa au unatakiwa kufanya jambo la ziada ili siku moja usimame mbele za Mungu ukiwa salama? Kitu kimoja ni dhahiri katika kuyajibu maswali haya. Mtumwa huyu alitunza vema fungu alilopewa, lakini siku ya mwisho ilipofika, alipoteza kila kitu pamoja na nafsi yake. Kupitia mfano wa mtumwa huyu, tunajifunza kweli zifuatazo:

Uhusiano na Bwana wake

Imani yake ilikuwa hivi, Bwana najua kuwa wewe ni mtu mgumu, waondoa usichoweka na wavuna usichopanda. Kwa maneno men-gine alimfananisha Bwana wake na mtawala dhalimu. Kusema kweli, hakuna mtu anayaweza kumpenda na kumtumikia mtawala aliye dhalimu. Hivi ndivyo baadhi ya watu wanavyomfikiria Mungu, humfikiria kama Kadhi anayetoa adhabu na kufurahia kuwaona watu wakipotea na kuingia jehanamu. Badala ya kumwona kama Mfalme aliyejaa upendo, tumaini na furaha moyoni mwake, wan-amwona kama mtawala asiye na upendo na kama anao, basi, ni kidogo sana. Tena humwona kama mtawala anayetumia mamlaka yake vibaya.

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa, watumishi wengi wa Mungu nao wa-menasa katika mtego huu mbaya wa Shetani. Badala ya kumtumikia Mungu kwa furaha, huishia kujiuliza maswali. “Kwa nini nimezaliwa katika familia ya Kikristo? Kwa nini niishi maisha ya Kikristo? Kwa

nini nishirikiane na watu wanaoamini? Kwa nini nimtumikie Mungu wakati watu wengine wanastarehe? Kutokana na mtizamo wao usio sahihi dhidi ya Mungu, hujikuta wakiwa na Ukristo uliojaa huzuni na misononeko. Kwao Mungu ni mlipiza kisasi kutoka mlima wa Hore-bu, mwenye neno lililochongwa juu ya mbao za mawe. Neno lililojaa amri, sheria na adhabu kali kwa yule atakayekosea hata nukta moja ya yale yaliyoandikwa humo! Wamesahau kuwa ule moto wa hu-kumu wa Sinai, ulizimwa na Yesu pale msalabani. Moto, ngurumo, na mawingu ya moshi, vyote hivi vilimgusa Yesu, rafiki wa wenye dhambi, alipokuwa pale Kalvari. Yeye anataka kuona watu wote wakiokolewa.

Watu hawa wa Mungu wanadhania kuwa kazi yao ni kulinda tal-anta waliyopewa na Mungu. Hawajui kuwa talanta hiyo inaweza kujitunza na kujizalisha yenyewe. Injili maana yake ni habari njema, hivyo tuhakikishe kuwa tunaipeleka kwa wengine. Tufanye hivyo huku tukiacha kuhubiri jumbe zinazovunja moyo na zinazotisha, kana kwamba zinatoka kwa Mungu mlipiza kisasi.

Watumwa wengine katika mfano huu walitoka na kushirikiana na wengine talanta walizokabidhiwa. Walifanya hivyo kwa furaha huku wakitambua kuwa, watu walikuwa wakizihitaji. Walifahamu kuwa Mungu aliwapa uwezo wa kuzalisha talanta zao na kwamba walitakiwa kuwa chanzo cha furaha na msamaha kwa jirani zao. Walipowashirikisha wengine karama zao, zilifanyika uzima, chaku-la, mavazi na uhuru kwa wote waliofanikiwa kukutana nao. Sanjari na kuwa baraka kwa wengine, nao walibarikiwa sana.

Yule mtumwa mpumbavu kwa upande mwingine, alijishughulisha tu na shughuli za kuitunza ile talanta. Kila wakati mashaka yake yalikuwa, “nitaitunzaje ili isije ikaangukia mikononi mwa watu waovu?” Ukweli ni kuwa talanta hii hakuna anayeweza kuifanyia mzaha au kuidharau. alifanya hivyo huku akiwaona wale watumwa wenzake kama maadui na wafujaji wa talanta. Kutokana na mtiza-mo huu usiofaa, aliishia kufanya kama vile akili yake ilivyomtuma, yaani, kuitunza talanta kwa uangalifu. Kwake, ile talanta ilikuwa ya thamani kuliko watu walioihitaji. Kwa maneno mengine, mtum-wa huyu, alikuwa na uhusiano mbaya na Bwana wake. Hakumfa-

74 75

hamu kwa kina, licha ya kukiri kuwa ni Bwana wake. Hakutambua kuwa ingawa alitakiwa kuisimamia, haikutakiwa kufukiwa ardhini. Ilikuwa kwa ajili ya watu wengine, na kujizalisha kwake, ni pale inaposhirikishwa kwa wengine.

Hofu yake na amri ya upendo

Uhusiano mbaya na Bwana wake ulimfanya aingie kwenye kosa la pili, la kutoelewa kuwa amri ya Mungu ni kumpenda Mungu. Badala ya kutambua kuwa hakuna vitisho au hofu katika amri hii, yeye al-imwogopa Bwana wake na kuacha kumtumikia. Inawezekana alia-mua kutofanya jambo lolote, ili asionekane kuwa mkosaji. Huenda alifanya hivyo huku akiongozwa na ile mithali isemayo, “Yeye ali-yelala hatendi dhambi”, au pengine alifikiria moyoni mwake kuwa, “mimi sistahili, sijaandaliwa vya kutosha na wala sio mkamilifu. Hivi kweli Mungu anaweza kutumia mtu kama mimi? Kwanza inanipasa nitakaswe zaidi, kabla sijamtumikia Mungu. Mimi ni dhaifu sana na mtu duni, wala sina hadhi yoyote. Naogopa!”

Hivi ndivyo baadhi yetu tunavyofikiria, pale tunapotakiwa ku-wapelekea wengine neno la Mungu. Dhana za jinsi hii hazina ukweli wowote na hazifai ndani ya kanisa la Mungu. Mara zote baada ya Shetani kufaulu kutufanya kuwa duni, ataharibu pia uhusiano kati yetu na watu wengine. Hofu ni nguvu inayoondoa uhai na kama tutamwogopa Mungu, tutaishia kuwa watazamaji badala ya kuwa watendaji! Tukiendelea kuogopa kamwe hatutakuwa baraka kwa wengine. acha kungojea kile Mungu atakachokuambia, anza kuten-dea kazi zile talanta ambazo tayari amekupatia.

Mungu amekupa kitu fulani maalum ambacho ni uzima mpya, hiki peke yake ni heshima kubwa inayoonyesha jinsi Mungu anavyoku-furahia na kukuthamini. anakuamini! U wa thamani mbele zake, unastahili na anakupenda. Nawe mpende, mshukuru na mtumikie kwa furaha. Kumbuka kwamba kwa njia ya Yesu, tunapendwa, tumehesabiwa kuwa haki na tumeitwa kuwa watu wa milki yake na watumishi wake. Sisi ni watumishi tuliojaliwa na kuvikwa vipawa vya kila aina.

Kutafuta usalama

Kutafuta usalama wa kile alichokabidhiwa, ni kosa la tatu lililo-fanywa na huyu mtumwa aliyeshindwa kuzalisha fedha aliyokabi-dhiwa. Baada ya kutafuta na kupata sehemu ya usalama, aliificha ardhini ile talanta aliyokabidhiwa. alitaka kutunza kile alichonacho na kamwe hakutaka mtu yeyote, aichukue kutoka kwake. Lengo lake lilikuwa kumrudishia Mungu talanta hiyo kama ilivyokuwa. alikuwa amenasa katika mtego wa usalama. Wote tunaelewa ile mithali isemayo, “akiba haiozi”, au “heri kenda shika, kuliko kumi nenda njoo kesho. Kile ulicho nacho sasa ndicho chako, hujui utaka-chopata kesho.” Tena, “ndege mmoja aliye mkononi ni bora kuliko mia wanaoruka angani.”

Ndugu huyu aliufuatilia mwenendo wa maisha yake kwa juhudi sana. Tumesoma kuwa aliilinda na kuitunza talanta hiyo kwa uw-ezo wake wote. Lakini ijulikane kuwa alikabidhiwa talanta hiyo ili aizalisha badala ya kuitunza. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa, apandacho mtu, ndicho atakachovuna (wagalatia 6:7).

76 77

wOKOVU NA KUfiKiA wASiOfiKiwABwana ametuita ili tuwalete wanadamu wote kwake. ametupa wito wa kupeleka injili ulimwenguni pote, soma Mathayo 28:19-20.

Wakati fulani huko nyuma niliwahi kusikia habari za kiwanda fulani cha viatu huko Sweden, kilichotuma wajumbe afrika kutafuta soko la viatu. Baada ya kutembelea maeneo mbalimbali, mjumbe mmoja aliutumia uongozi wa kiwanda taarifa yenye maneno yafuatayo; “simamisheni maandalizi ya kupeleka viatu afrika, watu wa huku wanatembea na kukimbia huku na huko, bila viatu. Ni wazi hakuna sababu ya kuwaletea viatu!” Mjumbe wa pili kwa furaha alituma ujumbe kwa njia ya simu na kusema: “Hapa pana soko kubwa sana la viatu, watu wote wanatembea bila viatu, ni wazi wanahitaji viatu vyetu!”

Je, wewe unapoutazama ulimwengu, huwa unapata picha gani? Je, unauona ukiwa tu na watu waovu wenye dini na mila zao, wasiohi-taji kumjua Mungu? au unawaona kama makinda ya ndege yenye njaa na kiu ya neno la Mungu? Je, unayo shauku ya kuwashirikisha wengine imani yako?

Inahuzunisha kuwaona jinsi Wakristo wengi wanavyoishi maisha ya kuhofia kunyang’anywa walicho nacho na watu wa dunia, badala ya kukizalisha. Unapofika wakati wa kuwapelekea wengine habari njema au kuwalea waamini wachanga, utawasikia wakitoa visin-gizio visivyohesabika. Utawasikia wakisema, “sina muda, sina wa kunisaidia watoto, nina wageni, sijisikii vizuri, nauguliwa, nina kikao cha harusi, nimealikwa kwenye sherehe na kadhalika. Wakati mwingine wanajihisi kutokuwa na ujuzi wa kuwawezesha kufanya hivyo. Mara zote waamini wa jinsi hii, hufurahia kukaa kwa usala-ma katika eneo moja.

Kuna makanisa au vikundi vya nyumbani vingapi, vinavyokaa hali ya kutoongezeka licha ya kuwa na miaka mingi tangia vianzishwe? Badala ya kutoka kwa lengo la kuzalisha waamini wapya au vi-kundi vipya, wanaishia tu kuweka bidii kulinda kile walicho nacho! Makundi haya yanaishia kujiburudisha kupitia taratibu mbalimba-

li za ibada na kuimbiana ule wimbo wa ‘happy birthday’, pale in-apofikia siku ya kuzaliwa kwa mmoja wao! Wakati umefika kwa Wakristo wote kutambua kuwa tunaishi katika kipindi cha utume mkuu, yaani, kutumia injili ya Kristo kuvuta mataifa yote kwake.

Katika Injili, Yesu alitupatia dondoo zifuatayo ili zituongoze ka-tika maombi. alisema, “ ombeni kuwa ufalme wako uje.” Kauli hii inatufundisha kuomba na kujibidisha kuifanya kazi yake hadi pale atakaporudi. Kama tutachoka au kuingia katika shida na mateso, Roho Mtakatifu atatupatia nguvu ya kuendelea mbele. Katika hili ninao mfano wa mhubiri aliyejitolea kutumika, hata pale wenzake walipokataa kushiriki. Yeye na familia yake walilazimika kubeba gharama zote za mkutano wa Injili. Waamini wenzake walifikia mahali hata pa kukwazika, kutokana na utayari wake. Hata hivyo, mkutano ulipofikia mwisho, madeni yote yalikuwa yamelipwa. Na huo ukawa ni mwanzo wa ongezeko katika kikundi chake. awali kilikuwa kikundi kidogo kilichokuwa kikikutana nyumbani chenye waamini kati 30 na 40, ila baada ya mkutano, kiliongezeka na kuwa kanisa la waamini 300!

Inapendeza pale tunapojaribu mambo kwa ajili ya Mungu, badala ya kutafuta usalama usio wa kibiblia. Tunatakiwa tutumie muda na nguvu zetu kukamilisha utume mkuu wa kuuleta ulimwengu kwa Yesu, huku tukimwangalia yeye peke yake kwa ushindi. Huu ndio wakati wako wa kuinuka na kuwa Mkristo wa kweli, mwe-nye kiu ya kuwapelekea wengine Injili ya Ufalme. Yesu ametamka waziwazi kuwa, “injili ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14).

78 79

tamatiTunapokaribia mwisho wa kitabu hiki, naamini sasa unaweza kuu-tambua undani wa imani yako ikiwa u Mkristo au la. Hali kadhalika, unaweza aina ya talanta uliyokabidhiwa na Mungu ili uizalishe. Ili umtumikie Mungu vizuri, unatakiwa kuyafahamu mambo haya kwa upana.

Kwangu talanta ninayoiona mbele zangu, ni ule muujiza ulionitokea wa kuzaliwa mara ya pili. Kamwe hakuna talanta inayozidi muu-jiza huu. Kupitia muujiza huu nimefanyika kuwa kiumbe kipya. Kitu chochote kinapokuwa kipya kinajitangaza chenyewe. Kwa mfano, unaponunua vazi au gari jipya, hakuna sababu ya kupiga panda, ili watu watambue kuwa una kitu kipya. Unapolivaa kama ni vazi, rafiki zako watatambua kuwa umevaa vazi jipya. Kupitia mfano huu wa vazi au gari jipya, unapozaliwa mara ya pili, ni lazima wengine waone upya wa maisha yako na matunda ya kuwa na uzima wa Mungu ndani yako.

Unapokuwa na vazi jipya, unaweza kufanya mojawapo ya mambo haya mawili. Waweza kulivaa na kuwapa wengine fursa ya ku-liona au unaweza kulihifadhi sandukuni. Hali kadhalika, kama ni gari jipya unaweza kuliendesha na kuwawezesha wengine kufura-hia uzuri wake au unaweza kuliegesha mahali pa usalama ili watu wasije wakaliona na kukuonea wivu!

Kamwe Mungu hataki kutuona tukiweka sandukuni uzima mpya tulioupokea kutoka kwake. anataka tuutembeze kila mahali kama taa ili walioko gizani, waone nuru yake. Kwa kuwa unayo talanta ya maisha mapya ndani yako, hakikisha kuwa unaishi maisha safi

yatakayokuwa ukombozi kwa wengine. Usiache kuwaeleza wengine kuwa uzuri wote wanaouona ndani yako, ni matokeo ya utawala wa Yesu ndani yako. Katika kuwasimulia wengine kuhusu maisha yako mapya, wako watakaobeza na kukudharau, lakini wako wataka-oonyesha shauku kubwa ya kupokea kile ulicho nacho.

Utakapotumia vipawa ulivyo navyo kuifanya kazi ya Mungu, wako watakaovutwa na kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale wataka-okataa kumpatia Mungu maisha yao, watapotea katika Jehanamu ya moto, ila wewe hutakuwa na hatia juu ya damu yao. Kama kuna kitu chochote unachoweza kukifanya kitakachobadilisha maisha ya mwingine ni vema uharakishe ukifanye. Hakikisha kuwa Ukristo wako wa kweli unaangaza kila mahali, ili wengine wauone wema wako. Kamwe usiogope maneno ya watu, wala usionee aibu injili ya Yesu Kristo. Paulo alisema, “Mimi siionei haya injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye...” (warumi 1:16).

Katika hili namkumbuka binti mmoja aliyekuwa ameajiriwa na mama mmoja mstaarabu. Muda mfupi baada ya kuajiriwa, mwa-jiri wake alimchukua pembeni na kumwambia maneno yafuatayo; “Ninatambua kuwa huu ni wakati wako wa kufanya kazi, ila kwa vile mimi ndiye mwajiri wako, nimeona vema kuutumia muda huu kuzungumza nawe. Hebu nisimulie undani wa maisha yako. Nimea-jiri watumishi wengine kabla yako, ila wewe nimekuona kuwa wa tofauti. Lazima una kitu fulani, ni kitu gani hicho?”

Ingawa msichana huyu alikuwa na aibu kuzungumza mbele za watu, alijikakamua na kusema, “Mimi nimeokoka. Nimeyatoa maisha yangu kwa Mungu naye amenifanya kuwa kiumbe kipya.” akiwa bado na aibu, aliendelea kueleza yale Yesu aliyomtendea. Maneno yalipomwishia alimwambia mwajiri wake maneno yafuatayo; “Uki-niruhusu naweza kumwomba baba yangu aongee na wewe. Yeye anaweza kukueleza vizuri zaidi!” Ingawa msichana huyu hakuwa mwongeaji, uzima wa Mungu ndani yake, ulipasua njia na kuone-kana kwa kila mtu. alikuwa tayari kushirikiana na wengine kuhusu maisha mpya aliyoyapokea, na ushuhuda wake ukazaa matunda.

80 81

Naamini kuwa kutakuwa na watu wengi mbinguni watakaookole-wa kupitia njia hii iliyoonekana kwa huyu msichana. Kwa upande mwingine, wale waliojaliwa kuwa hodari wa kusema, wanaweza kutumia kipawa hicho, kuwaongoza wengine kwa Bwana. Hawa wanafananishwa na mtumwa yule aliyepewa talanta kumi. Hata hivyo, hatutapewa thawabu kutokana na mafungu tuliyopewa, kilicho cha muhimu ni jinsi tulivyoyatumia kuwaleta wengine kwa Yesu. Na wale watakaojaribu kuyasalimisha maisha yao kwa kufi-cha talanta zao, ndiyo watakaoaibika!

Ni jambo la kutia moyo kuona jinsi baadhi ya waamini wanavyoji-bidisha kuwaleta wengine kwa Bwana. Bwana wa mavuno anataka kumwona kila mtu akijishughulisha katika kukusanya mavuno. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, kila aliye tayari atazaa matunda tele. Roho Mtakatifu ndiye mtaji tuliopatiwa na Mungu tulipozaliwa mara ya pili. Utumie mtaji huu, kwenda kila mahali, kumletea Bwana ma-vuno ya siku za mwisho. Umeokolewa ili ufanye kazi ya kujenga na kuimarisha ufalme wa Mungu. Ukiifanya kazi hii kwa bidii, siku moja utapumzika na kuingia utukufuni. Hapo malaika atakupeleka mbinguni na kwa heshima Yesu atakupatia taji ya uzima. Amen.

82