mchungaji afanyaye watu kuwa wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila mkristo anapaswa...

28
www.shepherdserve.org Unaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza haya kwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukata chochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Haki zote zimehifadhiwa 2006 David Servant Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi David Servant Sura Ya Nane Mahubiri Ya Yesu Mlimani Kwa sababu ya shauku yake ya kutaka kufanya watu kuwa wanafunzi na kuwafundisha kuyashika yote ambayo Kristo aliagiza, mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi atavutiwa sana na Mahubiri ya Yesu pale Mlimani. Hakuna ujumbe mwingine mrefu wa Yesu ulioandikwa, nao umejaa maagizo au amri Zake. Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi atataka kutii mahubiri hayo na kuwafundisha wanafunzi wake kila kitu alichoamuru Yesu katika mahubiri hayo. Kwa kuwa ni hivyo, nitakushirikisha ninayoelewa kuhusu mahubiri hayo, yapatikanayo katika Mathayo sura ya 5 hadi 7. Ninawatia moyo watumishi kuwafundisha wanafunzi wao Mahubiri ya Yesu ya Mlimani mstari kwa mstari. Natumaini kwamba niliyoandika yatasaidia kufanikisha jambo hilo. Ufuatao ni ufupisho au muhtasari wa Mahubiri ya Yesu Mlimani, ili kutusaidia kuyaona kwa mtazamo wa jumla pamojana kuonyesha mada kuu. I) Yesu akusanya wasikilizaji Wake (5:1-2) II) Utangulizi (5:3-20) A) Sifa na baraka za wenye heri (au waliobarikiwa) (5:3-12) B) Wito wa kuendelea kuwa chumvi na nuru (5:13-16) C) Uhusiano kati ya Torati na wafuasi wa Kristo (5:17-20) III) Mahubiri Yenyewe: Kuwa na haki kuliko waandishi na Mafarisayo (5:21 – 7:12) A) Pendaneni, si kama waandishi na Mafarisayo (5:21-26) B) Usafi katika maadili ya kimwili. Msiwe kama waandishi na Mafarisayo (5:27-32) C) Uwe mkweli, si kama waandishi na Mafarisayo (5:33-37) D) Msilipe kisasi, kama wanavyofanya waandishi na Mafarisayo (5:38-42) E) Msiwachukie adui zenu, kama wanavyofanya waandishi na Mafarisayo (5:43-48) F) Tenda mema kwa nia njema, si kama waandishi na Mafarisayo (6:1-18) 1) Wape maskini kwa nia njema (6:2-4) 2) Omba kwa nia njema (6:5-6) 3) Maelezo kidogo kuhusu maombi na msamaha (6:7-15) a) Mafundisho kuhusu maombi (6:7-13) b) Umuhimu wa kusameheana (6:8-15) 4) Funga kwa nia njema (6:16-18) G) Usitumikie fedha, kama waandishi na Mafarisayo (6:19-34) H) Usitafute makosa madogo madogo kwa ndugu yako (7:1-5) I) Usipoteze wakati kuwapa ukweli watu wasio na shukrani (7:6)

Upload: others

Post on 12-Oct-2019

17 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

www.shepherdserve.orgUnaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza hayakwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukatachochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Hakizote zimehifadhiwa 2006 David Servant

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziDavid Servant

Sura Ya NaneMahubiri Ya Yesu Mlimani

Kwa sababu ya shauku yake ya kutaka kufanya watu kuwa wanafunzi nakuwafundisha kuyashika yote ambayo Kristo aliagiza, mtumishi anayefanya watu kuwawanafunzi atavutiwa sana na Mahubiri ya Yesu pale Mlimani. Hakuna ujumbe mwinginemrefu wa Yesu ulioandikwa, nao umejaa maagizo au amri Zake. Mtumishi anayefanyawatu kuwa wanafunzi atataka kutii mahubiri hayo na kuwafundisha wanafunzi wake kilakitu alichoamuru Yesu katika mahubiri hayo.

Kwa kuwa ni hivyo, nitakushirikisha ninayoelewa kuhusu mahubiri hayo,yapatikanayo katika Mathayo sura ya 5 hadi 7. Ninawatia moyo watumishi kuwafundishawanafunzi wao Mahubiri ya Yesu ya Mlimani mstari kwa mstari. Natumaini kwambaniliyoandika yatasaidia kufanikisha jambo hilo.

Ufuatao ni ufupisho au muhtasari wa Mahubiri ya Yesu Mlimani, ili kutusaidiakuyaona kwa mtazamo wa jumla pamojana kuonyesha mada kuu.

I) Yesu akusanya wasikilizaji Wake (5:1-2)II) Utangulizi (5:3-20)

A) Sifa na baraka za wenye heri (au waliobarikiwa) (5:3-12)B) Wito wa kuendelea kuwa chumvi na nuru (5:13-16)C) Uhusiano kati ya Torati na wafuasi wa Kristo (5:17-20)

III) Mahubiri Yenyewe: Kuwa na haki kuliko waandishi na Mafarisayo (5:21 – 7:12)A) Pendaneni, si kama waandishi na Mafarisayo (5:21-26)B) Usafi katika maadili ya kimwili. Msiwe kama waandishi na Mafarisayo (5:27-32)C) Uwe mkweli, si kama waandishi na Mafarisayo (5:33-37)D) Msilipe kisasi, kama wanavyofanya waandishi na Mafarisayo (5:38-42)E) Msiwachukie adui zenu, kama wanavyofanya waandishi na Mafarisayo (5:43-48)F) Tenda mema kwa nia njema, si kama waandishi na Mafarisayo (6:1-18)

1) Wape maskini kwa nia njema (6:2-4)2) Omba kwa nia njema (6:5-6)3) Maelezo kidogo kuhusu maombi na msamaha (6:7-15)

a) Mafundisho kuhusu maombi (6:7-13)b) Umuhimu wa kusameheana (6:8-15)

4) Funga kwa nia njema (6:16-18)G) Usitumikie fedha, kama waandishi na Mafarisayo (6:19-34)H) Usitafute makosa madogo madogo kwa ndugu yako (7:1-5)I) Usipoteze wakati kuwapa ukweli watu wasio na shukrani (7:6)

Page 2: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

J) Himizo kuhusu kuomba (7:7-11)IV) Hitimisho: Ufupisho wa Mahubiri Yenyewe

A) Maneno ya ufupisho (7:12)B) Ushauri kuhusu kutii (7:13-14)C) Jinsi ya kutambua manabii na waamini wa uongo (7:15-23)D) Onyo la mwisho kuhusu kutokutii, na ufupisho (7:24-27)

Yesu Akusanya Wasikilizaji Wake

Naye alipowaona makutano alipanda mlimani; na baada ya kuketi,wanafunzi Wake walimjia. Naye, akifunua kinywa Chake alianzakuwafundisha (Mathayo 5:1-2, TLR).

Inaonekana kwamba Yesu alipunguza ukubwa wa wasikilizaji Wake kwa makusudi,maana aliondoka kuwaacha “makundi”, akapanda mlimani. Tunaambiwa “wanafunziWake wakamwendea,” kama ishara kwamba ni wale tu waliokuwa na njaa ya kumsikilizandiyo walikuwa radhi kupambana na kilima mpaka kufikia mahali alipopumzikia. Bilashaka walikuwa wengi maana katika 7:28 wanaitwa “makutano”.

Yesu akaanza mahubiri Yake akizungumza na wanafunzi Wake, na tangu mwanzotunapata kidokezo kuhusu mada Yake kuu. Anawaambia wamebarikiwa (au wana heri)kama watakuwa na tabia fulani, kwa sababu tabia hizo ni za wanaokwenda mbinguni.Hiyo ndiyo mada itakayotawala mahubiri haya – Watakatifu tu ndiyo watakaorithi ufalmewa Mungu. Kiini hicho kinatawala sehemu ya mahubiri hayo yenye kuzungumza kuhusu“Heri”, katika 5:3-12.

Yesu aliorodhesha vitu mbalimbali vinavyoonyesha watu waliobarikiwa (au wenyeheri), na akaahidi baraka nyingi mbalimbali kwao. Wasomaji wa juu juu mara nyingihufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila– wasomaji waangalifu wanatambua kwamba Yesu hakuwa anapanga orodha ya waaminiwa aina tofauti watakaopokea baraka mbalimbali, bali alizungumza juu ya waamini wotewa kweli watakaopokea baraka moja tu ya jumla katika siku za baadaye: kuurithi ufalmewa mbinguni. Hakuna njia nyingine inayofaa ya kutafsiri maneno yake, yafuatayo:

Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.Heri wenye huzuni; maana hao watafarijika.Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi.Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibirishwa.Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu.Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu.Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao.Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno bayakwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabuyenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabiiwaliokuwa kabla yenu (Mathayo 5:3-12).

Baraka Zenyewe, Na Tabia

Kwanza, hebu tutazame zile baraka zote zilizoahidiwa. Yesu alisema hivi: Hao wenyeheri – (1) wataurithi ufalme wa mbinguni, (2) watafarijiwa, (3) watairithi nchi, (4)

Page 3: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

watashibishwa, (5) watapata rehema, (6) watamwona Mungu, (7) wataitwa wana waMungu, na (8) wataurithi ufalme wa mbinguni (marudio ya namba 1).

Je, Yesu anataka tudhani kwamba ni walio maskini wa roho na ambao wameteswakwa ajili ya haki ndiyo tu watakaorithi ufalme wa Mungu? Je, ni wale walio safi moyonitu ndiyo watakaomwona Mungu, na ni wale wapatanishi tu ndiyo watakaoitwa watoto waMungu, lakini hakuna atakayerithi ufalme wa Mungu? Tukifikiri hivyo tutakuwatunakosea. Basi, ni salama kusema kwamba zile baraka nyingi zilizoahidiwa ni barakambalimbali zilizomo katika baraka moja kuu – kuurithi ufalme wa Mungu.

Sasa, hebu tufikiri zile tabia mbalimbali ambazo Yesu alitaja: (1) maskini wa roho,(2) wenye huzuni, (3) wapole, (4) wenye njaa na kiu ya haki, (5) wenye rehema, (6)wenye moyo safi, (7) wapatanishi, na (8) wenye kushutumiwa na kuudhiwa.

Je, Yesu anataka tufikiri kwmaba mtu anaweza kuwa na moyo safi lakini akakosarehema? Je, mtu anaweza kushutumiwa na kuudhiwa kwa ajili ya haki na asiwe mwenyenjaa na kiu ya haki? Hapo tena tunasema haiwezekani. Zile tabia au sifa nyingi za waliona heri ni tabia mbalimbali ambazo, kwa pamoja – kwa kiwango fulani – zinapatikanakatika wote wenye heri.

Ni dhahiri basi kwamba Maandiko hayo yanaeleza tabia au sifa za wafuasi wa kweliwa Yesu. Kwa kuorodhesha sifa hizo kwa wanafunzi Wake, aliwahakikishia kwamba waowana heri na wameokoka, na ndiyo wangefurahia mbingu siku moja. Kwa wakati huowanaweza wasijisikie kuwa ni heri kwa sababu ya mateso yao, na dunia inayowatazamainaweza ikawaona si heri, lakini machoni pa Mungu wao ni heri.

Ni hivi: Watu wasiolingana na maelezo ya Yesu si heri, na hawataurithi ufalme wambinguni. Kila mchungaji anayefanya watu kuwa wanafunzi anawajibika kuhakikishakwamba watu katika kundi lake wanajua hayo.

Tabia Za Walio Heri

Hizo sifa au tabia nane za walio heri zinatakiwa kutafsiriwa kiasi fulani. Kwa mfano:Nini cha kujisifia ukiwa “maskini wa roho”? Mimi nadhani kwamba Yesu alikuwaanaeleza sifa ya kwanza muhimu ambayo mtu lazima awe nayo kama ataokolewa –lazima atambue umaskini wake kiroho. Mtu lazima kwanza aone kwamba anamhitajiMwokozi ndipo aokolewe, na walikuwepo watu aina hiyo katika wasikilizaji wa Yesuwaliokuwa ametambua hali yao mbaya. Kweli, wao walikuwa na heri, ukiwalinganishana Israeli wenye kiburi, waliokuwa hawaona dhambi zao!

Hiyo sifa ya kwanza inaondoa hali yoyote ya kujitegemea au kujitosheleza, na wazololote kwamba mtu anastahili wokovu. Mtu mwenye heri kweli kweli ni yuleanayetambua kwamba hana chochote cha kumpa Mungu, na kwamba haki yake binafsi nisawa na “matambara machafu” (Isaya 64:6, TLR).

Yesu hakutaka mtu yeyote afikiri kwamba kwa juhudi zake mwenyewe anawezakujipatia sifa za kuwa heri. Hapana. Watu wana heri – yaani, kubarikiwa na Mungu –kama watakuwa na tabia au sifa za wenye heri. Hayo yote yanatoka katika neema yaMungu. Watu wenye heri ambao Yesu alizungumza juu yao walikuwa heri, si kwasababu ya kilichokuwa kinawangojea mbinguni, bali kwa sababu ya kazi Mungualiyokuwa amefanya katika maisha yao duniani. Ninapoona sifa za mwenye herimaishani mwangu zinatakiwa kunikumbusha juu ya kile ambacho Mungu amefanyandani yangu kwa neema Yake, si kunikumbusha kile nilichofanya mimi.

Page 4: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Wenye Huzuni

Kama sifa ya kwanza kutajwa imetajwa kwa sababu ndiyo sifa ya kwanzainayotakiwa kwa wanaokwenda mbinguni, pengine ya pili nayo imetajwa ya pili kwasababu maalum. “Heri wenye huzuni” (Mathayo 5:4). Je, Yesu alikuwa anazungumzakuhusu toba kutoka moyoni pamoja na kujisikia vibaya? Yawezekana. Maana, Maandikoyako wazi kabisa kwamba huzuni ya kiMungu huzaa toba ambayo ni ya lazima kwawokovu (ona 2Wakor. 7:10). Yule mtoza ushuru aliyekuwa na huzuni, ambaye Yesualimtaja katika mfano, ni mtu wa aina hiyo mwenye heri. Yeye aliinamisha kichwa chakeHekaluni kwa unyenyekevu sana, akipiga-piga kifua chake na kuomba rehema za Mungu.Farisayo jirani yake ambaye, alipoomba, alimkumbusha Mungu – tena kwa kiburi –kwamba yeye alitoa fungu la kumi na kufunga mara mbili kwa juma. Yule mtoza ushurualiondoka hapo akiwa amesamehewa dhambi zake. Katika kisa hicho, mtoza ushurualikuwa heri; Farisayo hakuwa (ona Luka 18:9-14). Mimi nadhani kwamba, katikawasikilizaji wa Yesu walikuwepo wengine ambao kwa kusukumwa na Roho Mtakatifu,walikuwa wana huzuni. Faraja ya Roho Mtakatifu ingewafikia!

Kama Yesu hakuwa anazungumza juu ya ile huzuni ya mwanzo, ya mwenye dhambianayetubu na kumjia Kristo, basi pengine alikuwa anazungumza juu ya huzuni ambayowaamini wote huipata wanapokabiliana kila siku na dunia inayomwasi Mungu,anayewapenda. Paulo alieleza hilo kuwa “huzuni kubwa na uchungu usiokoma moyoni”(Warumi 9:2).

Wenye Upole

Sifa ya tatu – upole – inatajwa pia katika Maandiko kwamba ni tunda mojawapo laRoho (tazama Wagalatia 5:22-23). Upole si tabia itokanayo na mtu binafsi. Wale ambaowamepokea neema ya Mungu na Roho anakaa ndani yao wamebarikiwa pia kufanyikawapole. Siku moja watairithi nchi, maana ni wenye haki tu watakaoishi kwenye duniampya ambayo Mungu anaiumba. Wanaojiita Wakristo ambao ni wakali na wenye fujowajiangalie. Wao si heri.

Njaa Na Kiu Ya Haki

Sifa ya nne – kuwa na njaa na kiu ya haki – hueleza ile shauku ya ndani, itokayo kwaMungu, ambayo kila mtu aliyezaliwa mara ya pili anayo. Yeye anahuzunishwa na maovuyote duniani, na sehemu inayobaki ndani yake. Anachukia dhambi (ona Zaburi 97:10;119:128, 163), na anapenda haki.

Mara nyingi tunaposoma neno haki katika Maandiko, tunatafsiri upesi kwamba ni“kuhesabiwa kuwa wenye haki na Kristo”. Lakini, neno hilo halimaanishi hivyo wakatiwote. Mara nyingi maana yake ni: “Hali ya kuishi kwa haki kulingana na viwango vyaMungu”. Bila shaka hiyo ndiyo maana aliyokusudia Yesu hapa, maana hakuna sababukwa Mkristo kuwa na njaa na kitu alicho nacho tayari. Wale waliozaliwa na Rohohutamani kuishi kwa haki, na uhakikisho ni kwamba “watashibishwa” (Mathayo 5:6). Nihakika kwamba Mungu kwa neema Yake atakamilisha kazi aliyoianza ndani yao (onaWafilipi 1:6).

Maneno ya Yesu hapa ni kama utabiri wa wakati wa dunia mpya – dunia ambayo“haki yakaa ndani yake” (2Petro 3:13). Hiyo haitakuwa na dhambi. Kila mtu atampendaMungu kwa moyo wote na kumpenda jirani yake kama nafsi yake. Wale ambao sasawana njaa na kiu ya haki watashibishwa wakati huo. Hatimaye, sala yetu ya dhati kabisa

Page 5: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

kutoka moyoni itajibiwa kikamilifu: “Mapenzi Yako yatimizwe hapa duniani, kama hukombinguni” (Mathayo 6:10).

Wenye Rehema

Sifa ya tano – rehama – nayo inapatikana na kila mtu aliyezaliwa mara ya pili kwasababu ya Mungu mwenye rehema kuishi ndani yake. Wale wasiokuwa na rehemahawana heri ya Mungu, nao wanadhihirisha kwamba si washiriki wa neema Yake.Mtume Yakobo anakubali – “Hukumu haitakuwa na rehema kwa asiyekuwa na rehema”(Yakobo 2:13, TLR). Unaonaje – mtu akisimama mbele za Mungu na kuhukumiwapasipo rehema, ataingia mbinguni au jehanamu?1 Nadhani jibu ni dhahiri kabisa.

Yesu alisimulia kisa fulani, cha mtumishi aliyepata rehema kutoka kwa bwana wake,ambaye hakuweza kumwonyesha mtumwa mwenzake rehema hata kidogo. Bwana wakealipogundua kilichokuwa kimetokea, alimpeleka “kwa watesaji mpaka atakapolipa kilaalichokuwa anadaiwa” (Mathayo 18:34). Deni lake la zamani alilokuwa amesamehewalikarudi pale pale. Kisha Yesu akawaonya wanafunzi wake hivi: “Baba yangu wambinguni atafanya hivyo hivyo kwenu, kama ninyi hamtawasamehe ndugu zenu kutokamoyoni” (Mathayo 18:35). Kwa hiyo, kukataa kumsamehe ndugu au dada katika Kristoanayeomba msamaha husababisha dhambi zetu za zamani kurudishwa. Matokeo ni sisikukabidhiwa kwa watesaji mpaka tulipe kitu ambacho hatuwezi kulipa. Na hapo simbinguni. Narudia tena – wasio na rehema hawatapokea rehema kutoka kwa Mungu.Wao si heri.

Wenye Moyo Safi

Tabia au sifa ya sita ya wanaokwenda mbinguni ni usafi wa moyo. Tofauti na wengiwanaokiri Ukristo, wafuasi a kweli wa Kristo si watakatifu kwa nje tu. Mioyo yaoimefanywa kuwa safi kwa neema ya Mungu. Wanampenda Mungu kweli kutoka ndani yamioyo yao, na hali hiyo inaathiri tafakari zao na makusudi yao ya moyo. Yesu aliahidikwamba watamwona Mungu.

Naomba niulize tena: Je, tuamini kwamba kuna waamini wa kweli Wakristo ambao sisafi moyoni, na kwamba hawatamwona Mungu? Je, Mungu atawaambia, “Mnawezakuingia mbinguni, lakini hamtaniona kamwe?” Hapana. Bila shaka, kila mwamini wakweli aendaye mbinguni ana moyo safi.

Wapatanishi

Wapatanishi ndiyo wanaofuata. Wataitwa wana wa Mungu. Hapo tena ni kwambaYesu anazungumza juu ya kila mfuasi wa kweli wa Kristo, maana kila amwaminiyeKristo ni mtoto wa Mungu (ona Wagalatia 3:26).

Wale waliozaliwa na Roho ni wapatanishi kwa namna tatu:Kwanza – Wamefanya mapatano na Mungu, ambaye hapo kwanza alikuwa adui yao

(ona Warumi 5:10).Pili – Wanaishi kwa amani na watu wengine, kwa kiasi kinachowezekana. Si watu

wenye tabia za vurugu na magomvi. Paulo aliandika kwamba wale wenye kutendavurugu, fujo, wenye wivu, wenye ghadhabu, wenye mafarakano, wenye magomvi nakuleta mafarakano hawataurithi ufalme wa Mungu (ona Wagalatia 5:19-21). Waaini wa

1 Cha kuvutia ni kwamba, mstari unaofuata katika kitabu cha Yakobo unasema hivi: “Ndugu zangu, inafaanini mtu akisema anayo imani, pasipo matendo? Je, imani hiyo yaweza kumwokoa?” (Yakobo 2:14).

Page 6: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

kweli watakwenda maili ya pili ili kuepuka ugomvi na kuhifadhi amani katika mahusianoyao. Hawadai kuwa na amani na Mungu na huku hawawapendi ndugu zao (ona Mathayo5:23-24; 1Yohana 4:20).

Tatu – Kwa kuwaambia wengine Habari Njema (Injili), wafuasi wa kweli wa Kristohuwasaidia wengine nao kuwa na amani na Mungu, na wanadamu wenzao. PengineYakobo alikuwa anaunganisha hoja yake na Mahubiri ya Mlimani alipoandika hivi: “Nambegu ile ambayo mazao yake ni haki, hupandwa katika amani na wale wafanyao amani”(Yakobo 3:8, TLR).

Wenye Kushutumiwa Na Kuudhiwa

Mwisho – Yesu alisema wale wanaoshutumiwa na kuteswa kwa ajili ya haki wanaheri. Ni dhahiri kwamba alikuwa anazungumza na watu wenye kuishi maisha ya haki, siwale ambao wanafikiri tu kwamba haki ya Kristo imehesabiwa kwao. Watu wenye kutiiamri za Kristo ndiyo wanaoshutumiwa au kuudhiwa na wasioamini. Hao wataurithiufalme wa Mungu.

Sasa – Yesu alikuwa anazungumza juu ya kuudhiwa au shutuma za aina gani? Matesokimwili? Kuteswa mpaka kufa? Hapana. Alichotaja hasa ni kutukanwa na kunenewamabaya kwa ajili Yake. Hili tena linaonyesha kwamba wakati mtu anapokuwa Mkristowa kweli, ni kitu kinachoonekana kwa wasioamini. Vinginevyo, wasioaminiwasingejaribu kusema maovu kinyume chake. Je, ni wangapi wanaoitwa Wakristowasioweza hata kutofautishwa na wasioamini kiasi cha kwamba wasioamini hawana lakusema vibaya juu yao? Ukweli ni kwamba hao si Wakristo wa kweli. Yesu alisema hivi:“Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabiiwa uongo mambo kama hayo” (Luka 6:26). Watu wote wanapowasema vizuri, ni isharakwamba wewe ni mwamini bandia. Dunia inawachukia Wakristo wa kweli (ona piaYohana 15:18-21; Wagalatia 4:29; 2Timo. 3:12; 1Yohana 3:13-14).

Chumvi Na Nuru

Baada ya Yesu kuwahakikishia wanafunzi Wake watiifu kwamba walikuwa miongonimwa waliobadilishwa na watu wenye heri, watakaourithi ufalme wa mbinguni, anatoaonyo. Yesu aliwapenda kweli kweli wanafunzi Wake halisi kiasi cha kuwaonya kwambawangejiondoa katika fungu la wenye heri. Hii ni tofauti na wahubiri wengi wa siku hiziambao wanawatia moyo tu mbuzi wa kiroho kwamba hawawezi kupoteza wokovuwanaodhani wanao.

Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini, chumvi ikiwa imeharibika itatiwanini hata ikolee? Haifai tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa nawatu. Ninyi ni nuru yaulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu yamlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pichi, bali juu yakiango, nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo, nuruyenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema,wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni (Mathayo 5:13-16).

Ona kwamba Yesu hakuwashauri wanafunzi Wake kufanyika chumvi au kufanyikanuru. Alisema (kimfano) kwamba wao ni chumvi tayari, na akawashauri wadumu kuwachumvi. Alisema (kimfano) kwamba wao ni nuru tayari, na akawashauri wasiache nuruyao isifichike bali iendelee kung’aa. Hiyo ni tofauti sana na yale mahubiriwanayoambiwa wanaojiita Wakristo, kwamba kuna haja kwao kufanyika chumvi na nuru.

Page 7: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Kama watu si chumvi na nuru tayari, si wanafunzi wa Kristo hao. Hawako miongonimwa walio na heri. Hawaendi mbinguni hao.

Katika siku za Yesu, chumvi ilitumiwa kimsingi kama kihifadhi nyama. Sisi kamawafuasi watiifu wa Kristo ndiyo tunaohifadhi dunia hii yenye dhambi isioze kabisa nakupotoka. Lakini, tukiwa kama dunia kwa tabia, kweli “hatufai kwa chochote” (ms. 13).Yesu aliwaonya walio heri kudumu kuwa chumvi, yaani, wahifadhi tabia zao za kipekee.Ni lazima wawe tofauti na dunia inayowazunguka, wasije wakapoteza ladha yao,wakastahili “kutupwa nje na kukanyagwa na watu.” Hili ni onyo mojawapo kati ya mengiya wazi kabisa kuhusu kurudi nyuma, yapatikanayo katika Agano Jipya, lenyekuelekezwa kwa waamini wa kweli. Kama chumvi ni chumvi kweli, itakuwa na ladha yachumvi. Vivyo hivyo, wafuasi wa Yesu hutenda kama wafuasi wa Yesu. Vinginevyo,wao si wafuasi wa Yesu hata kama waliwahi kuwa hapo zamani.

Pia, wafuasi wa kweli wa Kristo ni nuru ya dunia. Nuru hung’aa kila wakati. Kamahaing’ai, hiyo si nuru. Kwa mfano huu, nuru inafananishwa na matendo yetu mema (onaMathayo 5:16). Yesu hakuwa anawashauri wale wasio na matendo mema wafanye bidiiwapate. Aliwashauri wale wenye matendo mema wasifiche wema wao kwa watu. Kwakufanya hivyo, wangemtukuza Baba yao wa mbinguni kwa sababu kazi Yake ndani yaondiyo asili ya wema wao. Hapo tunaona mlingano mzuri sana kati ya kazi ya Mungu yaneema na ushirikiano wetu sisi – pande zote mbili hizo zinahitajiana ili mtu awemtakatifu.

Uhusiano Wa Torati Na Wafuasi Wa Kristo

Tumefikia mahali muhimu katika mafundisho haya. Ni sehemu ya msingi na yenyemaana sana – ni kama utangulizi wa mengi ambayo Kristo atasema katika sehemuinayosalia ya mahubiri Yake.

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii. La! Sikujakutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbinguna nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka,hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizizilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katikaufalme wa mbinguni. Bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyoataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia yakwamba, haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo,hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:17-20).

Ikiwa Yesu aliwaonya wasikilizaji Wake wasifikiri kwamba alikuwa anaitanguaTorati au manabii, tunaweza kuamua kwamba bila shaka walikuwepo wachache katikakundi lililomsikiliza waliodhani hivyo. Kilichosababisha wafikiri hivyo hatukijui.Pengine ni kwa sababu Yesu aliwakemea vikali sana waandishi na Mafarisayowalioshika sana sheria.

Vyovyote vile ni kwamba, Yesu alitaka wanafunzi Wake watambue wazi wazi kosala kufikiri hivyo. Yeye ndiye alivuvia Agano la Kale lote. Basi, asingeweza kutangua kilakitu alichosema kupitia kwa Musa na Manabii. Kinyume chake – angetimiliza Torati naManabii, kama alivyosema.

Angetimilizaje Torati na Manabii? Kuna wanaofikiri kwamba Yesu alimaanishakutimizwa kwa unabii uliomhusu Masiya. Ingawa kweli Yesu alitimiza (na badoatatimiza) kila unabii uliomhusu Masiya, hiyo haikuwa maana yake tu. Ni wazi kwambamantiki ya mistari hiyo inaonyesha kwamba alikuwa anazungumza kuhusu yote

Page 8: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

yaliyoandikwa katika Torati na Manabii, mpaka “yodi ndogo kabisa” (ms. 18) ya Torati,na mpaka amri “iliyo ndogo kabisa” (ms. 19).

Kuna wengine wanaodhani kwmaba Yesu alimaanisha atatimiza Torati kwa kutimizamatakwa yake kwa niaba yetu, kwa maisha Yake ya kumtii Mungu na kifo Chake chakujitoa (ona Warumi 8:4). Lakini ukitazama mantiki ya mistari husika, utaona kwambahiyo haikuwa maana yake. Katika mistari inayofuata, yesu hasemi chochote kuhusumaisha Yake au kufa Kwake kwamba ni kitu kitakachotimiza Torati. Badala yake utaonakwamba katika mstari uliofuata alisema kwamba Torati itadumu mpaka “mbingu na nchizitakapopita” na “kila kitu kitimizwe”. Hiyo inasema juu ya kipindi kirefu baada ya kifoChake msalabani. Kisha akatangaza kwamba hali za moyo za watu kuhusu Toratizingeamua hata nafasi zao mbinguni (ms. 19), na kwamba watu lazima waitii Torativizuri zaidi kuliko waandishi na Mafarisayo, la sivyo hawataingia mbinguni (ms. 20).

Basi, ni wazi kwamba, zaidi ya kutimiza tu unabii kuhusu Masiya na mifano yake yaTorati, pamoja na kutimiza matakwa ya Torati kwa niaba yetu, Yesu pia alikuwa anafikirijuu ya wasikilizaji Wake kuzishika amri za Torati na kufanya yaliyosemwa na Manabii.Kwa sehemu moja, Yesu angeitimiza Torati kwa kufunua kusudi la kweli la Mungu ndaniyake, kwa kulifafanua na kuiunga mkono, na kukamilisha kilichokuwa kimepunguakatika ufahamu wa wasikilizaje Wake.2 Neno la Kiyunani linalotafsiriwa kutimiza katikamstari wa 17 ndilo linalotafsiriwa kukamilisha, kumaliza, kujaza na kutekeleza kikamilifukatika Agano Jipya. Hayo ndiyo Yesu aliyokuwa anataka kufanya, kamaitakavyoonekana hapo baadaye.

Hapana. Yesu hakuja kutangua Torati wala Manabii. Alikuja kutimiliza – yaani –“kujazia.” Ninapofundisha fungu hili la Mahubiri ya Mlimani, mara nyingininawaonyesha watu bilauri ya maji ambayo iko nusu, ili kuwa mfano wa ufunuo waMungu aliotoa katika Torati na Manabii. Yesu hakuja kutangua Torati na Manabii (naninaposema hivyo, ninajifanya kama anayetaka kumwaga yale maji). Kinyume chake,angetimiliza Torati na Manabii (na hapo, ninachukua chupa ya maji na kuijaza ile bilaurimpaka juu). Hilo huwasaidia watu kuelewa maana ya Yesu.

Umuhimu Wa Kushika Torati

Kuhusu kushika zile amri zipatikanazo katika Torati na Manabii, Yesu alisemamambo waziwazi kabisa. Aliwatazamia wanafunzi Wake kuziti. Zilikuwa za maana kamanini! Ukweli ni kwamba: Jinsi walivyothamini amri zile ingeamua nafasi yao mbinguni.“Basi, mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watuhivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Bali mtu atakayezitenda nakuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni” (5:19).

2 Hii ingekuwa kweli kwa habari ya kinachoitwa “sehemu za kuabudu katika Torati” pamoja na zilesehemu za “kiadili za Torati”, japo sehemu kubwa ya maelezo Yake kamili kuhusu Yeye kutimiza ilesehemu ya Torati ya kuabudu ingetolewa na Roho Wake Mtakatifu kwa mitume, baada ya kufufukaKwake. Sasa tunaelewa ni kwanini hakuna haja ya kutoa dhabihu ya wanyama katika agano jipya. Ni kwasababu Yesu alikuwa Mwanakondoo wa Mungu. Wala hatufuati zile sheria za vyakula zha agano la zamanikwa sababu Yesu alisema vyakula vyote vimetakaswa (ona Marko 7:19). Hatuna haja ya kuombewa nakuhani mkuu mwanadamu kwa sababu sasa Yesu ni Kuhani wetu Mkuu, n.k. Lakini – tofauti na sheria zakuabudu – hakuna sehemu yoyote ya sheria za maadili iliyobadilishwa na chochote alichosema au kutendaBw2ana Yesu, kabla au baada ya kufa na kufufuka Kwake. Badala yake, Yesu alifafanua na kuunga mkonosheria ya Mungu ya maadili, kama walivyofanya wanafunzi kwa uvuvio wa Roho, baada ya kufufukaKwake. Sehemu za maadili katika Torati ya Musa ziko kwa ukamilifu kabisa katika Sheria ya Kristo –sheria ya agano jipya. Kumbuka pia kwamba Yesu alikuwa anazungumza na Wayahudi waliokuwa chini yaTorati ya Musa. Basi maneno Yake katika Mathayo 5:17-20 yanapaswa kutafsiriwa katika mwangaza wamafunuo Yake yanayoendelea yapatikanayo katika Agano Jipya.

Page 9: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Ndipo tunafikia mstari wa 20 sasa – “Maana nawaambia ya kwamba haki yenuisipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wambinguni.”

Ona kwamba hilo si wazo jipya, bali wazo la kumalizia mistari ile mingine yoteiliyotangulia. Imeunganishwa na neno maana. Je, ni muhimu kiasi gani kuzishika amri?Ni muhimu sana. Mtu anapaswa azishike vizuri zaidi kuliko waandishi na Mafarisayo iliaweze kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hapo tena tunamwona Yesu akibakia kwenyemada Yake kuu – Ni watakatifu tu watakaorithi ufalme wa Mungu.

Ili asipingane na Kristo, yule mtumishi mwenye kufanya watu kuwa wanafunzihawezi kumhakikishia mtu yeyote kwamba wokovu wake uko salama kama haki yakehaizidi ya waandishi na Mafarisayo.

Je, Yesu Alikuwa Anazungumzia Haki Ya Namna Gani?

Je, Yesu alipotamka kwamba haki yetu lazima izidi ile ya waandishi na Mafarisayo,hakumaanisha ule msimamo kisheria wa haki ambao tungehesabiwa baada ya wokovukama zawadi? Hapana, na ni kwa sababu nzuri tu. Kwanza: Mantiki yenyewe hailinganina tafsiri hiyo. Kabla na baada ya kusema hivyo (na katika mahubiri yote), Yesu alikuwaanazungumza juu ya kushika amri – yaani, kuishi maisha ya haki. Tafsiri ya karibu kabisaya maneno Yake ni kwamba lazima tuishi kwa haki zaidi ya waandishi na Mafarisayo.Na ni upuuzi kufikiri kwamba Yesu aliwabana waandishi na Mafarisayo washikekiwango ambacho hakutaka wanafunzi Wake washike. Itakuwa ni upuuzi kabisa kufikirikwamba Yesu angewahukukumu waandhsi na Mafarisayo kwa ajili ya kufanya dhambiambazo asingewahukumia wanafunzi Wake kwa kuwa waliomba “sala ya wokovu” tu.3

Tatizo letu ni kwamba hatutaki kukubali maana halisi ya mstari huo, kwa sababutunaona ni kukazia ushikaji wa sheria. Lakini, tatizo letu hasa ni kwamba hatuelewiumoja ulioko kati ya haki inayohesabiwa na haki halisi ya vitendo. Mtume Yohanaalielewa, na akaandika hivi: “Watoto wadogo! Mtu yeyote asiwadangaye. Yeye atendayehaki ni mwenye haki” (1Yohana 3:7, TLR). Tena, hatuelewi umoja ulipo kati ya kuzaliwaupya na haki halisi ya vitendo. Yohana alielewa, na anasema hivi: “Kila atendaye hakiamezaliwa na Yeye” (1Yohana 2:29, TLR).

Yesu angeweza kuongezea maneno, katika yale aliyosema katika 5:20. Angewezakusema hivi: “Mkitubu, na kuzaliwa mara ya pili kweli, na kupokea zawadi yangu yahaki kw anjia ya imani hai, haki yenu ya vitendo itazidi ile ya waandishi na Mafarisayomtakaposhirikiana na nguvu za Roho Wangu, akaaye ndani yenu.”

Jinsi Ya Kuwa Mtakatifu Kuliko Waandishi Na Mafarisayo

Bila shaka swali linalojitokeza hapo kama itikio la maneno ya Yesu katika 5:20 nihili: Hao waandishi na Mafarisayo walikuwa na haki kiasi gani? Jibu ni hili: HaikuwaNyingi.

Wakati fulani Yesu aliwaita “makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa njeyanapendeza, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote” (Mathayo 23:27,TLR). Yaani, walionekana kuwa wenye haki kwa nje, lakini ndani walikuwa waovu.

3 Tena, kama Yesu alikuwa anazungumza juu ya ile haki ya kisheria tunayohesabiwa na kuipokea kamazawadi kwa sababu ya kumwamini, mbona hakusema hivyo? Mbona akasema kitu ambacho kingekuwarahisi kueleweka vibaya na wale watu waliokuwa wanamsikiliza, wasiosoma, ambao wasingeweza hatakukisia tu kwamba alikuwa anazungumza juu ya kuhesabiwa haki?

Page 10: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Walijitahidi sana kushika andiko la Torati, lakini walipuuzia maana yake, na mara nyingiwalijihesabia haki kwa kupindisha au hata kubadili amri za Mungu.

Hili tatizo la ndani la waandishi na Mafarisayo ndilo Yesu alikazia zaidi katikasehemu inayosalia ya Mahubiri Yake pale Mlimani. Tunakuta kwamba alitaja baadhi yaamri zinazojulikana sana za Mungu, na baada ya kutaja kila moja, alionyesha tofauti katiya kushika andiko na maana ya kila sheria. Kwa kufanya hivyo, alifunua tena na tenamafundisho ya uongo na unafiki wa waandishi na Mafarisayo, na kudhihirisha matazamiohalisi ambayo Yeye alikuwa nayo kwa wanafunzi Wake.

Yesu alianza kila mfano kwa kusema hivi: “Mmesikia”. Alikuwa anazungumza nawatu ambao hawakuwahi kusoma magombo ya Agano la Kale bali walisikia yakisomwakatika masinagogi na waandishi na Mafarisayo. Ni sawa kusema kwamba wasikilizajiWake walikuwa wameketi chini ya mafundisho ya uongo maisha yao yote, wakisikilizamaelezo na mafafanuzi potofu ya waandishi na Mafarisayo kuhusu Neno la Mungu, nakuona jinsi walivyoishi maisha yasiyokuwa matakatifu.

Mafarisayo kuhusu Neno la Mungu, na kuona jinsi walivyoishi maisha yasiyokuwamatakatifu.

Mafarisayo kuhusu Neno la Mungu, na kuyaona maisha waliyoishi, ambayohayakuwa matakatifu.

Pendaneni. Si Kama Waandishi Na Mafarisayo

Kwa kutumia amri ya sita kama kianzio, Yesu alianza kufundisha wanafunzi Wakematazamio ya Mungu kwao, na hapo hapo akifunua unafiki wa waandishi na Mafarisayo.

Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, ‘Usiue’, na mtu akiua,itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yakehasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake itampasa baraza;na mtu akimwapiza, itampasa jehanamu ya moto (Mathayo 5:21-22).

Kwanza: Ona kwamba Yesu alikuwa anaonya kuhusu kitu kinachowezakumsababisha mtu kwenda jehanamu. Hiyo ndiyo iliyokuwa mada Yake kuu –Watakatifu tu ndiyo watakaorithi ufalme wa Mungu.

Waandishi na Mafarisayo walihubiri na kukataza kuua, wakitumia amri ya sita, japoinaonekana wao walisema kuua kungemfikisha mtu mahakamani.

Yesu alitaka wanafunzi Wake wajue kitu ambacho ni kama waandishi na Mafarisayohawakukitambua – yalikuwepo makosa mengine “madogo” ambayo yangemfikisha mtumahakamani – mahakama ya Mungu. Kwa sababu ni muhimu sana sisi kwa sisitupendane (ni amri ya pili iliyo kuu), tunapomkasirikia ndugu tunapaswa kujihesabukwamba tayari tumepatikana na hatia katika mahakama ya Mungu. Kama tutaitamkahasira yetu kwa kusema maneno mabaya, kosa letu ni kubwa zaidi, na tunatakiwakujihesabu kuwa na hatia katika mahakama ya juu sana ya Mungu. Na kama tutazidihapo – na kumwaga chuki yetu dhidi ya ndugu kwa maneno mengine mabaya, tuna hatiambele za Mungu ya kutosha kutupwa jehanamu!4 Hiyo si mchezo!

Uhusiano wetu na Mungu unapimwa na mahusiano yetu na ndugu zetu. Tukimchukiandugu inadhihirisha kwamba hatuna uzima wa milele. Yohana aliandika hivi:

4 Hilo linahusika katika mahusiano yetu na ndugu na dada zetu katika Kristo. Yesu aliwaita viongozi fulaniwa kidini wapumbavu (tazama Mathayo 23:17), na utaona Maandiko mengine yakifanya hivyo kwa ujumla(ona Mithali 1:7; 13:20).

Page 11: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji, nanyi mwajua kwambahakuna mwuaji aliye na uzima wa milele ndani yake (1Yohana 3:15,TLR).

Mtu akisema, ‘Nampenda Mungu’ naye amchukia ndugu yake, nimwongo huyo. Kwa maana, mtu asiyempenda ndugu yake ambayeamemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona (1Yohana4:20, TLR).

Ni muhimu sana tupendane, na kama Yesu alivyoamuru, tujitahidi kutafutaupatanisho wakati tunapokwazana (ona Mathayo 18:15-17). Yesu aliendelea hivi:

Basi, kama unatoa sadaka yako madhabahuni, na hapo ukumbukekwamba ndugu yako ana jambo nawe, iache sadaka yako hapo mbele yamadhabahu uende zako. Patana kwanza na ndugu yako, kisha rudi na uitoesadaka yako (Mathayo 5:23-24, TLR).

Maana ya hayo yote ni kwamba, kama mahusiano yetu na ndugu si mazuri, hatamahusiano yetu na Mungu si mazuri. Mafarisayo walikuwa na hatia ya kutilia mkazo vituvilivyokuwa na umuhimu mdogo na kupuuzia vitu vilivyokuwa na umuhimu mkubwa,“wakichuja mbu na kumeza ngamia” kama Yesu alivyosema juu yao (Mathayo 23:23-24). Wao walikazia umuhimu wa kutoa zaka na sadaka, lakini walipuuza yaliyokuwa yamuhimu zaidi sana, yaani ile amri ya pili iliyo kuu ya kupendana. Ni unafiki ulioje,kuleta sadaka ambayo inadhanishia kuonyesha upendo wa mtu kwa Mungu, hukuakihalifu ile amri kuu ya pili! Yesu alikuwa anaonya dhidi ya hayo. Kuhusu msimamomkali wa mahakama ya Mungu, Yesu anaendelea kusema hivi:

Patana na mshitaki wako upesi wakati uwapo pamoja naye njiani; yulemshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari,ukatupwa gerezani. Amin nakuambia, hutoki humo kamwe hata uishekulipa senti ya mwisho (Mathayo 5:25-26).

Ni vizuri kuepuka kuingia mahakama ya Mungu kabisa kwa kuishi kwa amani nandugu zetu kiasi inachowezekana. Kama ndugu au dada atatukasirikia, nasi kwa kujivunatukatae kutafuta upatanisho “njiani kuelekea mahakamani”, yaani, katika safari yetumaishani kwenda kusimama mbele za Mungu, tutajutia jambo hilo. Alichosema Yesuhapa ni sawa na maonyo Yake kuhusu sisi kumwiga yule mtumwa ambaye hakumsamehemwenzake katika Mathayo 18:23-35. Yule mtumwa aliyekuwa amesamehewa lakini yeyeakakataa kusamehe alirudishiwa deni lake, akakabidhiwa kwa watesaji “mpakaatakapolipa yote aliyodaiwa” (Mathayo 18:34). Hapa, Yesu anaonya dhidi ya matokeomabaya ya milele ya sisi kutowapenda ndugu zetu kama Mungu anavyotazamia.

Usafi Katika Maadili ya Kimwili. Msiwe Kama Waandhsi Na Mafarisayo

Amri ya saba ikatumiwa na Yesu kama mfano wa pili kuonyesha jinsi waandishi naMafarisayo walivyoshika andiko la Torati huku wakipuuza maana yake. Yesualiwatazamia wanafunzi Wake kuwa safi zaidi katika maadili ya kimwili kulikowaandishi na Mafarisayo.

Page 12: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini. Lakini mimi nawaambia, Kilamtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini nayemoyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbalinawe. Kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wakomzima usitupwe katika jehanamu. Na mkono wako wa kuumeukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe. Kwa maana yakufaa kiungochako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanamu(Mathayo 5:27-30).

Ona tena kwamba Yesu alikuwa bado kwenye mada Yake kuu – Watakatifu tu ndiyowatakaorithi ufalme wa Mungu. Alionya tena kuhusu jehanamu na kile kinachotakiwakufanywa na mtu ili asiende huko.

Waandishi na Mafarisayo wasingeweza kuipuuza amri ya saba. Basi, waliitii kwa njena kusalia waaminifu kwa wake zao. Lakini walikuwa wanafanya mapenzi na wanawakekatika mawazo yao. Walipokuwa sokoni au barabarani, waliwavua nguo kimawazowanawake waliokuwa wanawaona. Moyoni walikuwa wazinzi, na kwa njia hiyowalikuwa wanavunja maana ya amri ya saba. Je, ni wangapi siku hizi kanisani ambaohawana tofauti na hao?

Mungu alikusudia watu wawe safi kabisa kimaadili katika mahusiano ya kimwili. Niwazi kwamba kama ni kosa kuwa na mahusiano kimapenzi na mke wa jirani yako, nimakosa pia kufikiri au kuwaza hayo hayo. Si kwamba Yesu aliongezea sheria kali zaidikwenye ile iliyokuwepo katika Torati ya Musa. Amri ya kumi ilikuwa na maneno haya yakukataza tamaa mbaya: “Usimtamani mke wa jirani yako” (Kutoka 20:17).

Je, kati ya wasikilizaji wa Yesu kuna aliyejisikia hatia? Bila shaka walikuwepo. Je,wafanye nini? Wangetubu mara moja, kama Yesu alivyoagiza. Wale wenye tamaa mbayawalitakiwa kuiacha – kwa gharama yoyote – maana, watu aina hiyo wanakwendajehanamu.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayedhani kwamba Yesu alimaanisha kwambawatu wenye tamaa mbaya wang’oe jicho kweli au kukata mkono. Mtu mwenye tamaaanayeng’oa jicho anakuwa mwenye tamaa chongo tu! Yesu alikuwa anakazia tuumuhimu wa kutii maana ya amri ya saba – kwamba, umilele wa mtu ulitegemeana najinsi anavyoitii.

Basi – akifuata mfano wa Kristo, mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunziatawashauri wanafunzi wake “kukatilia mbali” chochote kinachowafanya kujikwaa.Kama ni televisheni ya kulipia, iache kulipiwa. Kama ni ya kawaida, iondolewe. Kama nigazeti linalolipiwa, liache kulipiwa. Kama ni mtandao, achana nao. Kama ni dirishalisilofungwa, lifungwe. Hakuna hata kimoja katika vitu hivyo kinachostahili kumfanyamtu aende jehanamu milele, na kwa sababu mtumishi anayewafanya watu kuwawanafunzi anawapenda kondoo wake, atawaambia ukweli na kuwaonya, sawa na jinsiYesu alivyofanya.

Njia Nyingine Ya Kuzini

Mfano unaofuata wa Yesu unafanana na huo tuliomaliza. Pengine ndiyo sababuunatajwa sasa. Unatakiwa kuonekana kama ufafanuzi wa zaidi badala ya kuonekanakwamba ni mada mpya. Mada ni hii: “Kitu kingine Mafarisayo wafanyachokinacholingana na uzinzi”.

Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya talaka. Lakinimimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe isipokuwa kwa habari ya

Page 13: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini(Mathayo 31-32).

Ufuatao ni mfano tu, jinsi waandishi na Mafarisayo walivyopindisha sheria ya Munguili kutosheleza maisha yao ya dhambi.

Hebu tujiundie Farisayo wa kufikirika, aliyeishi siku za Yesu. Kuna mwanamkemzuri tu anayemtamani sana, anayeishi ng’ambo ya barabara. Wanataniana kila wanapo-onana. Inaonekana huyo mwanamke amevutiwa naye, na tamaa ya Farisayo inazidikuongezeka. Angependa kumwona akiwa hana nguo, naye humfikiria sana kila wakati,kimapenzi. Laiti ingewezekana akampata!

Lakini ana tatizo. Yeye ana ndoa, na dini yake inakataza uzinzi. Hataki kuivunja amriya saba (ingawa amekwisha ivunja kila wakati anapotamani). Sasa, afanye nini?

Lipo jibu! Akiachana na mwenzake, anaweza kumwoa huyo mwanamkeanayemtamani! Lakini, talaka inaruhusiwa? Farisayo mwenzake anamwambia, Ndiyo!Tena hata andiko lipo! Kumbukumbu 24:1 inasema kitu juu ya kumpa mke wako cheticha talaka unapomwacha. Basi, talaka bila shaka ni halali kwa mazingira fulani! Sasa –ni mazingira gani hayo? Anasoma kwa makini maneno ya Mungu, kwamba:

Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machonimwake kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati yakumwacha, akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake(Kumbu. 24:1).

Loo! Kumbe inawezekana kumwacha mke wake akipata hitilafu kwake! Naamekwisha ipata! Havutii kama yule mwanamke anayekaa ng’ambo ya barabara! (Nahuu si mfano usiowezekana. Kulingana na Rabbi Hillel, ambaye alikuwa na mafundishokuhusu talaka yaliyopendwa sana katika siku za Yesu, mtu angeweza kumwacha mkewake kihalali kabisa kama angempata mwingine aliyekuwa wa kupendeza zaidi, maanatendo hilo lilimfanye mke wake “kutokuwa na kibali” machoni pake. Vile vile RabbiHillel alifundisha kwamba mwanamume angeweza kumwacha mke wake kamaakizidisha chumvi katika chakula, au kama angezungumza na mwanamume mwingine, aukama asingezaa mtoto wa kiume).

Basi, Farisayo wetu mwenye tamaa anaachana na mke wake kihalali kabisa kwakumpa hati ya talaka, na haraka sana anamwoa yule mwanamke anayemtamani. Tena,hayo yote yanafanyika bila yeye kujisikia hatia hata kidogo kwa sababu Torati ya Munguimefuatwa!

Mtazamo Tofauti

Mungu anaona mambo kwa njia tofauti. Yeye hakutaja kwamba “kutokuwa na kibali”ni kitu gani katika Kumbukumbu 24:1. Wala haisemi kwamba sababu halali ya kuachanana mke ni nini. Maandiko hayo hayasemi chochote kuhusu wakati ambapo kuachanakunaruhusiwa au hakuruhusiwi. Hapo tunaambiwa tu juu ya katazo kuhusu mwanamkealiyeachwa mara mbili au mara moja, au hata aliyefiwa, kuolewa tena na mume wake wakwanza. Kusema kwamba kuna hali ya “kutokuwa na kibali” mbele za Mungu, yenyekuhalalisha kuachana katika mistari hii ni kulazimisha maana nyingine kabisa.

Tena – mbele za Mungu, huyo mwanamume wa kufikirika ambaye nimesimuliahabari zake hana tofauti na mzinzi. Amekwisha vunja ile amri ya saba. Tena ana hatiakuliko hata mzinzi wa kawaida, maana yeye ana kosa la uzinzi “mara mbili”. Utasema,kivipi? Kwanza: Amefanya uzinzi mwenyewe. Baadaye Yesu alisema hivi: “Kila mtu

Page 14: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, akaoa mwanamke mwingine,anazini” (Mathayo 19:9, TLR).

Pili: Kwa sababu, huyo mkewe ambaye ameachika lazima atafute mwanamumemwingine ili aendelee kuishi. Machoni pa Mungu, huyo Farisayo amekwisha fanyakitendo kinacholingana na kumlazimisha mke wake kushirikiana kimwili namwanamume mwingine. Basi, anakuwa na hatia kwa “uzinzi” wa huyo mwanamke.5

Yesu alisema hivi: “Yeyote amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati,amfanya azini” (Mathayo 5:32, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Yawezekana Yesu alikuwa anamhukumu hata huyo Farisayo wetu mwenye tamaakwa kosa la “kuzini mara tatu” ikiwa maneno Yake yaliyofuata, kwamba “yeyoteamwoaye mwanamke aliyeachwa azini” (Mathayo 5:32, TLR) yanamaanisha kwambaMungu anamhesabia Farisayo huyo hatia kwa sababu ya “zinaa” ya mume mpya wa mkewake wa zamani. 6

Hili lilikuwa jambo moto katika siku za Yesu, maana tunasoma mahali pengineMafarisayo walipomwuliza hivi: “Je, ni halali kwa mtu kumwacha mkewe kwa sababuyoyote?” (Mathayo 19:3). Swali lao linadhihirisha mioyo yao. Bila shaka kuna waliotakakuamini kwamba kuachana au talaka ni halali kwa sababu yoyote.

Ila, naomba niseme kwamba ni aibu sana kwa Wakristo kuchukua mistari hii kuhusutalaka, na kuitafsiri vibaya, kisha kuweka mizigo mizito juu ya watoto wa Mungu. Yesuhakuwa anazungumza juu ya Mkristo ambaye alikuwa na talaka wakati hajaokoka, naambaye akiisha kumpata mwenzake mzuri tu anayempenda Kristo pia, wanaamuakuoana. Hiyo si uasherati. Kama Yesu alimaanisha hivyo, itabidi tubadilishe Injili maanahaitoi nafasi ya msamaha kwa dhambi zote za wenye dhambi. Itabidi tangu sasa tuhubirihivi: “Yesu alikufa kwa ajili yako, nawe ukitubu na kumwamini, utasamehewa dhambizako zote. Lakini, kama umeachana na mwenzake, hakikisha kwamba huingii katika ndoanyingine maana hapo utaishi katika uasherati, na Biblia inasema waasherati watakwendajehanamu. Pia, kama umeachika na kuingia tena katika ndoa, unahitaji kufanya dhambinyingine moja kabla ya kumjia Kristo – achana na mwenzako. La sivyo, utaendeleakatika uasherati, na watu aina hiyo hawajaokoka.”7 Je, hiyo ni injili?8

Uwe Mkweli. Si Kama Waandishi Na Mafarisayo

Mfano wa tatu wa Yesu kuhusu mwenendo usio wa haki na matumizi mabaya yaMaandiko ya waandishi na Mafarisayo unahusiana na amri ya Mungu kuhusu kusemaukweli. Waandishi na Mafarisayo walikuwa wabunifu sana kwa habari ya kudanganya.Tunajifunza kutoka Mathayo 23:16-22 kwamba wao hawakujihesabu kuwa na wajibu wakutunza nadhiri zao kama wangeapa kwa hekalu, madhabahu au mbingu. Lakini, kamawangeapa kwa dhahabu ya hekalu, au sadaka iliyoko juu ya madhabahu, au kwa Mungualiyeko mbinguni, basi walikuwa na wajibu wa kutunza nadhiri au viapo vyao! Hayo nimawazo ya mtu mzima akifikiri kitoto kwamba ana haki ya kutosema ukweli mradi

5 Mungu hamhesabii hatia akiolewa tena, maana alinaswa katika dhambi ya mumewe. Maneno ya Yesuhayana maana yoyote kama hataolewa, maana kwa hali hiyo hawezi kuhesabiwa kuwa mzinzi.6 Hapa tena ni kwamba, Mungu hamhesabii hatia ya uasherati yule mume mpya. Yeye anafanya kitu chakiungwana, kumwoa na kumtunza mwanamke aliyeachwa. Lakini, kama mwanamume atamtia mwanamkemoyo amwache mume wake ili waoane, hapo ana hatia ya uzinzi, na yawezekana hiyo ndiyo maana yamaneno ya Yesu hapa.7 Kuna mazingira mengine ambayo lazima yashughulikiwe. Kwa mfano: Mwanamke aliyeokokaanayeachwa na mume wake asiyeokoka hana hatia ya uasherati kama ataolewa na mwanamumealiyeokoka.8 Huko mbele katika sura nyingine kuhusu talaka na ndoa tena, ninashughulikia swala hili kwa upana zaidi.

Page 15: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

vidole vyake vimeshikana kwa nyuma. Yesu anatazamia wanafunzi Wake wasemeukweli.

Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, ‘Usiape uongo, ilamtimizie Bwana nyapo zako.’ Lakini mimi nawaambia, ‘Usiape kabisa;hat a kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwanchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu,kwa maana ndio mji wa Mfalme mmuu. Wala usiape kwa kichwa chako,maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Balimaneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayoyatoka kwa yule mwovu’ (Mathayo 5:33-37).

Amri ya Mungu kuhusu viapo na nadhiri haikusema chochote juuya kufanya kiapokwa kuapa na kitu kingine. Mungu alikusudia watu Wake waseme kweli wakati wote.Basi, isingekuwepo haja ya kuapa kamwe.

Hakuna kosa kuapa, kwa sababu kiapo si kitu zaidi ya nadhiri au ahadi. Kwa kweli,viapo vya kumtii Mungu ni vizuri sana. Wokovu huanza kwa kiapo cha kumfuata Yesu.Lakini watu wanapotakiwa kuapa kwa kitu kingine ili kuwafanya wengine waaminiwanachosema, ni ukiri wa moja kwa moja kwamba kwa kawaida wao husema uongo.Watu wanaosema kweli sikuzote hawana haja ya kuapa hata siku moja. Lakini makanisamengi siku hizi yamejaa waongo, na watumishi mara nyingi ndio viongozi katikaudanganyifu na hila.

Mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi huonyesha mfano wa kusema kwelina kuwafundisha wanafunzi wake kusema kweli sikuzote. Anajua Yohana alionyakwamba waongo wote watatupwa katika ziwa liwakalo moto na kibiriti (ona Ufunuo21:8).

Msilipe Kisasi, Kama Wanavyofanya Waandishi Na Mafarisayo

Kinachofuata katika orodha ya malalamiko ya Yesu ni kupotoshwa kwa Kifarisayokwa andiko maarufu sana katika Agano la Kale. Tumekwisha kutazama maandiko hayokatika sura kuhusu kutafsiri maandiko.

Mmesikia kwamba imenenwa, ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.’Lakini mimi nawaambia, ‘Msishindane na mtu mwovu; lakini mtuakupigaye shavu la kuume mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitakina kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimishamwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye mpe; naye atakayekukopa kwako, usimpe kisogo’ (Mathayo 5:33-37).

Torati ya Musa ilitamka kwamba mahakama ikimpata mtu na hatia ya kumjeruhimwingine, adhabu yake italingana na madhara aliyoleta. Kama alimtoa mtu jino, kwahaki na uhalali kabisa jino lake na yeye litang’olewa. Amri hii ilitolea ili kuhaikishakwamba haki ingetendeka katika mashauri ya mahakamani kwa makosa makubwa.Mungu alianzisha utaratibu wa mahakama na mahakimu katika Torati ili kupinga uhalifu,kuhakikisha haki na kuzuia visasi. Na Mungu aliwaamuru mahakimu kutokuwa naupendeleo, na kuwa wenye haki katika hukumu zao. Walitakiwa kuhukumu “jicho kwajicho na jino kwa jino”. Lakini, maneno hayo pamoja na amri hiyo hupatikana katikamaandiko yanayohusiana na haki katika mahakama.

Page 16: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Lakini tena, waandishi na Mafarisayo walikuwa wamebadilisha amri yenyewe nakuifanya kuwa amri ya kulipiza kisasi kuwa wajibu mtakatifu. Walikuwa wamekubalikutokuwa na uvumilivu, wakitafuta kulipiza kisasi hata kwa makosa madogo madogokabisa.

Mungu daima ametazamia viwango vya juu zaidi kutoka kwa watu Wake. Kisasi nikitu alichokataza Yeye (ona Kumbu. 32:35). Agano la Kale lilifundisha kwamba watu waMungu wanatakiwa kuwaonyesha adui zao wema (ona Kutoka 23:4, 5; Mithali 25:21-22). Yesu aliunga mkono kweli hii kwa kuwaambia wanafunzi Wake wageuze shavu lapili na kwenda maili nyingine zaidi katika kushughulika na watu waovu. Tunapokosewa,Mungu anataka tuwe na rehema, tukilipa jema kwa ovu tulilotendewa.

Lakini je! Yesu anatazamia kwamba tutawaachia watu watutumie vibaya tu,wakiharibu maisha yetu kama wapendavyo? Je, ni makosa kumpeleka asiyeaminimahakamani na kutafuta haki kwa uovu tunaotendewa? Hapana. Yesu hakuwaanazungumza juu ya kupata haki tunayuostahili kwa makosa makubwa mahakamani.Alikuwa anazungumzia juu ya kutafuta kulipa kisasi kwa mambo madogo madogo.Onakwamba Yesu hakusema tutoe shingo yetu ili tunyongwe na mtu ambaye ametuchomakisu mgongoni. Hakusema tutoe nyumba kwa mtu anayetaka gari. Alichokuwaanatuambia ni jinsi ya kuonyesha uvumilivu na rehema kwa kiwango cha juu sana,tunapokutana na vikwazo vidogo vidogo kila siku, na zile changamoto za kawaidazinazotokana na kushughulika kwetu na watu wenye kujipenda, au ubinafsi. Anatakatuwe wakarimu kuliko watu wenye ubinafsi wanavyotazamia. Waandishi na Mafarisayohawakukaribia kufikia kiwango hicho.

Mbona Wakristo wengi wanakwazika kirahisi? Mbona ni wepesi sana kukasirishwana vikwazo vidogo ambavyo ni vidogo mara kumi kuliko kupigwa kofi? Je, hao watuwameokoka kweli? Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi huonyesha mfano wakumgeuzia mtu shavu la pili, naye anawafundisha wanafunzi wake kufanya hivyo hivyo.

Msiwachukie Adui Zenu, Kama Wanavyofanya Waandishi Na Mafarisayo

Kwa kumalizia, Yesu anaorodhesha amri nyingine iliyotolewa na Mungu ambayowaandishi na Mafarisayo waliibadili ili kutosheleza mioyo yao yenye chuki.

Mmesikia kwamba imenenwa, ‘Umpende jirani yako na umchukieadui yako’. Lakini mimi nawaambia, ‘Wapendeni adui zenu, waombeeniwanaowaudhi ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. MaanaYeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshe amvua wenyehaki na wasio haki. Maana, mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapatathawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tenamkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wamataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu,kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu’ (Mathayo 5:43-48).

Katika Agano la Kale Mungua likuwa amesema hivi: “Mpende jirani yako kamaunavyojipenda mwenyewe” (Walawi 19:18, TLR). Waandishi na Mafarisayo wakatafsirijirani kuw ani wale watu waliowapenda tu. Kila mwingine yeyote alikuwa adui, na kwakuwa Mungu alisema kuwapenda jirani zetu tu, bila shaka ni sawa kuwachukia adui zetu.Lakini, kulingana na mafundisho ya Yesu, Mungu hakuwa amekusudia hayo.

Page 17: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Yesu baadaye angefundisha katika habari za Msamaria Mwema kwamba, tunatakiwakumhesabu kila mtu kuwa jirani yetu.9 Mungu anataka tumpende kila mtu, mpaka aduizetu. Hicho ndicho kiwango cha Mungu kwa ajili ya watoto Wake – na ni kiwangoambacho Yeye Mwenyewe anakitumia. Anatuma jua na mvua kwa ajili ya kuoteshamimea, kwa watu wote – wema na wabaya. Tunatakiwa kufuata mfano Wake,tukonyesha wema kwa watu wasiostahili. Tunapofanya hivyo, inaonyesha kwamba sisi ni“wana wa Baba [yetu] aliye mbinguni” (Mathayo 5:45). Watu waliozaliwa upya kwelikweli hutenda kama Baba yao.

Upendo ambao Mungu anatazamia tuuonyeshe kwa adui zetu si hisia au kukubalianana uovu wao. Mungu hatutaki tuendelee kujisikia vizuri juu ya wale wanaotupinga.Hatuambii tuseme kisichokuwa kweli – kwamba adui zetu ni watu wazuri sana. Lakini,anatazamia kwamba tutawahurumia na kuchukua hatua ya makusudi kuonyesha jambohilo – haidhuru hata kwa kuwasalimu tu na kuwaombea.

Ona tena kwamba Yesu anatilia mkazo mada Yake kuu – Ni watakatifu tuwatakaorithi ufalme wa Mungu. Aliwaambia wanafunzi wake kwamba, kamawatawapenda wale wawapendao tu, hawana tofauti na wapagani na watoza ushuru – ainambili za watu ambao kila Myahudi alikubali kwamba wanakwenda jehanamu. Ilikuwa ninjia nyingine ya kusema kwamba watu wanaowapenda wale wanaowapenda tuwanakwenda jehanamu.

Tenda Mema Kwa Nia Njema, Si Kama Waandishi Na Mafarisayo

Yesu hatazamii wafuasi Wake kuwa watakatifu tu. Anawatazamia wawe watakatifukwa sababu sahihi. Inawezekana kabisa kutii amri za Mungu na bado usimpendeze ikiwautii wa mtu unatokana na nia mbaya. Yesu aliwahukumu waandishi na Mafarisayo kwasababu walitenda matendo yao mema yote ili wasifiwe na watu (ona Mathayo 23:5).Yesu anatazamia wanafunzi Wake wawe tofauti.

Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu kusudi mtazamwena wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Babayenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yakokama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe nawatu. Amin nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali weweutoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wakowa kuume. Sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye siriniatakujazi (Mathayo 6:1-4).

Yesu alitazamia kwamba wafuasi Wake watawapa maskini sadaka. Torati iliagizahivyo (Kutoka 23:11; Walawi 19:10; 23:22; 25:35; Kumbu. 15:7-11), lakini waandishi naMafarisayo walifanya hivyo huku tarumbeta zikipigwa, bila shaka ili kuwaita masiniwaje kupokea sadaka zao za ukarimu. Pamoja na hayo, ni Wakristo wangapi wanaotoachochote kwa maskini? Hawajawahi kufikia hata mahali pa kuchunguza tu nia yao yakutoa sadaka. Kama ubinafsi uliwasukuma waandishi na Mafarisayo kutangaza kutoakwao, ni kitu gani kinachowasukuma Wakristo kupuuza matatizo ya maskini? Kwa halihiyo, haki yao inazidi ile ya waandishi na Mafarisayo?

9 Myahudi mmoja aliyekuwa mwalimu wa Torati alimwuliza Yesu swali hili: “Jirani yangu ni nani?” ilikujihesabia haki. Naomba ujue kwamba alikuwa anajua jibu sahihi. Bwana Yesu alimjibu kwa kusimuliahabari ya Msamaria, mtu kutoka kabila lililochukiwa sana na Wayahudi, aliyejionyesha kuwa jirani kwaMyahudi aliyekuwa ametendewa vibaya. Jisomee Luka 10:25-37.

Page 18: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Kama Paulo atakavyorudia katika 1Wakorintho 3:10-15, tunaweza kufanya memakwa nia mbaya. Kama nia yetu si safi, matendo yetu mema hayatapata thawabu. Pauloaliandika kwamba inawezekana hata kuhubiri Injili kwa nia isiyo safi (ona Wafilipi 1:15-17). Kulingana na maneno ya Yesu, njia nzuri yakuhakikisha kwamba utoaji wetu ni kwania safi ni kutoa kwa siri kiasi iwezekanavyo – bila ya kuruhusu mkono wa kushoto kujuakinachofanywa na mkono wa kuume. Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzihuwafundisha wanafunzi wake kuwapa vitu maskini (kama wanaweza), naye anatendakama mahubiri yake, kimya kimya tu.

Kufunga Na Kuomba Kwa Sababu Zilizo Sahihi

Yesu pia alitazamia kwamba wafuasi Wake wataomba na kufunga, na kwambawangefanya mambo hayo ili kumpendeza Baba yao, si ili kuonekana na watu.Vinginevyo wasingekuwa tofauti na wale waandishi na Mafarisayo wanaokwendajehanamu, waliokuwa wanafunga na kuomba ili wasifiwe na watu. Hiyo ni thawabu yamuda sana. Yesu aliwashauri hivi wafuasi Wake:

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki. Kwa maana wao wapenda kusalihali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia iliwaonekane na watu. Amin nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.Bali wewe usalipo ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiishakufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Babayako aonaye sirini atakujazi.

Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana;maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga.Amin nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapojipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwaunafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye siriniatakujazi (Mathayo 6:5-6, 16-18).

Je, ni Wakristo wangapi wenye kuishi maisha yasiyo na maombi, na ambao hatahawajawahi kufunga?10 Sasa, haki yao inalinganishwaje na ile ya waandishi naMafarisayo, waliofanya yote mawili – japo ni kwa sababu mbaya?

Machache Kuhusu Maombi Na Msamaha

Akiendelea na somo la maombi, Yesu alifoa mafundisho ya ziada kwa wanafunziWake kuhusu jinsi wanavyotakiwa kuomba. Yesu anataka sisi tuombe kwa njia ambayohaimtukani Baba Yake kwa kukana yale aliyofunua juu Yake Mwenyewe. Kwa mfano:Kwa kuwa Mungu anajua tunachohitaji kabla ya kumwomba (maana anafahamu mamboyote), hakuna sababu ya kurudia-rudia maneno tunapoomba.

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke kama watu wa mataifa;maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yaokuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitajikabla ninyi hamjamwomba (Mathayo 6:7-8).

10 Katika kitabu hiki huko mbele kuna sura nzima kuhusu hilo somo la kufunga.

Page 19: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Kweli – maombi yetu hudhihirisha jinsi tunavyomjua Mungu vizuri. Walewanaomjua kama alivyojidhihirisha katika Neno Lake huomba ili mapenzi Yake Yeyeyafanyike, na Yeye atukuzwe. Shauku yao kuu ni kuwa watakatifu – wenye kumpendezaYeye kabisa. Hili linaonekana katika sala ya Yesu ya mfano, ambayo sisi tunaiita Sala yaBwana. Imo katika sehemu inayofuata ya mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi Wake.Inadhihirisha matazamio Yake kwa habari ya mambo tunayotanguliza, na upendo wetu.11

Basi ninyi salini hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama hukombinguni. Utupe leo riziki yetu’ (Mathayo 6:9-11).

Basi, inatakiwa wajibu wa kwanza kabisa wa wanafunzi wa Kristo uwe jina la Mungukutukuzwa – kwamba liheshimiwe, listahiwe na kutakatifuzwa.

Wale wanaoomba kwamba jina la Mungu litakaswe wanatakiwa kuwa watakatifuwao wenyewe – watu wenye kulitakasa jina la Mungu. Vinginevyo ni unafiki tu. Kwahiyo, sala hii huonyesha shauku tuliyo nayo kwamba wengine wajinyenyekeze mbele zaMungu kama ambavyo sisi tumekwisha fanya.

Ombi la pili katika sala hiyo mfano linafanana: “Ufalme wako uje”. Wazo la ufalmelinamaanisha kuwepo kwa Mfalme mwenye kutawala ufalme Wake. Mfuasi Mkristoanatamani kumwona Mfalme wake – yule anayetawala maisha yake – atawale dunianzima. Laiti kila mmoja angepiga goti lake kwa Mfalme Yesu – katika imani tiifu!

Ombi la tatu katika sala hiyo linarudia la kwanza na la pili, hivi: “Mapenzi yakoyatendeke hapa duniani kama huko mbinguni”. Hapa tena – tunawezaje kuomba kwadhati sala kama hiyo bila sisi wenyewe kuwa tumekubali kukaa chini ya mapenzi yaMungu maishani mwetu? Mwanafunzi wa kweli huwa na shauku kwamba mapenzi yaMungu yafanyike duniani kama yafanyikavyo huko mbinguni – kikamilifu na kabisa.

Yanayotakiwa kuwa muhimu zaidi kwetu kuliko hata chakula – “riziki yetu” – ni jinala Mungu litakaswe, mapenzi Yake yafanyike, na ufalme Wake uje. Hili ombi la nnelinawekwa la nne kwa kusudi. Hata kwa mtazamo huo tu inaonyesha mpangilio unaofaawa mambo muhimu maishani mwetu, na hakuna dalili ya uchoyo au ubinafsi hapa.Wanafunzi wa Kristo wanamtumikia Mungu, sio mali. Lengo lao si kujiwekea hazinaduniani.

Hebu niongeze pia kwamba ombi hili la nne linaonyesha kwamba sala hii mfanoinapaswa kuombwa kila siku – mwanzo wa kila siku.

Sala Mfano Inaendelea

Je, wanafunzi wa Kristo hutenda dhambi? Wakati mwingine wanatenda, maana Yesualiwafundisha kuomba msamaha wa dhambi zao.

“Utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Nausitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme niwako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] Kwa maanamkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasameheninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenuhatawasamehe ninyi makosa yenu” (Mathayo 6:12-15).

11 Kwa bahati mbaya, kuna wengine wanaosema haya si maombi yanayopaswa kutumiwa na Wakristo kwasababu si “katika jina la Yesu”. Tukishika hoja hiyo, itabidi tuseme pia kwamba sala nyingi za mitumezinazopatikana katika Matendo na nyaraka mbalimbali hazikuwa “za Kikristo”.

Page 20: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Wanafunzi wa Yesu hutambua kwamba kutokutii kwao humkwaza Mungu, nawanapotenda dhambi, wanajisikia aibu. Wanataka doa hilo liondolewe, na Baba yao wambinguni, kwa neema sana, yuko tayari kuwasamehe. Lakini lazima waombe msamaha,ambalo ndilo ombi la tano lipatikanalo katika Sala ya Bwana.

Ila – kusamehewa kwao kunategemea sana wao kuwasamehe wengine. Kwa sababuwamesamehewa vingi, wanawajibika kumsamehe kila mtu anayewaomba msamaha (nakumpenda na kutafuta upatanisho na wale wasioomba msamaha). Wakikataa kusamehe,Mungu hatawasamehe.

Ombi la sita na la mwisho pia linaonyesha shauku ya mwanafunzi wa kweli kuwamtaka tifu: “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu [au, ‘maovuni’].”Mwanafunzi wa kweli ana shauku na utakatifu kiasi cha kwamba anamwomba Munguasimwongoze katika hali anayoweza kujaribiwa, asije akashindwa. Tena, anamwombaMungu amwokoe na maovu yoyote yanayoweza kumnasa. Hakika hii ni sala kubwa sanaya kuomba mwanzoni mwa kila siku, kabla hatujaingia katika dunia yenye maovu namajaribu. Na hakika tunaweza kumtazamia Mungu kujibu sala hii aliyotuambia tuiombe!

Wale wamjuao Mungu wanaelewa ni kwa nini maombi yote sita katika sala hiiyanafaa. Sababu inafunuliwa katika mstari wa mwisho wa sala: “Kwa kuwa [au kwasababu] ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele” (Mathayo 6:13). Mungu niMfalme mkuu anayetawala ufalme Wake ambao ndani yake sisi ni watumishi. Yeyendiye mwenye nguvu zote, na hakuna anayethubutu kupingana na mapenzi Yake.Utukufu wote ni Wake milele. Anastahili watu wamtii.

Je, somo kubwa katika Sala ya Bwana ni nini? Utakatifu. Wanafunzi wa Kristowanatamani jina la Mungu litukuzwe, utawala Wake uimarishwe duniani kote, namapenzi Yake yafanyike kikamilifu kila mahali. Hii ni muhimu sana kwao kuliko hatariziki yao ya kila siku. Wanataka kumpendeza, na wanaposhindwa, wanataka msamahaWake. Kama watu waliosamehewa, wanawasamehe wengine. Wanatamani kuwawatakatifu kabisa mpaka wanataka kuepuka majaribu kwa sababu majaribu huongezanafasi zao za kutenda dhambi. Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi hufundishamambo hayo kwa wanafunzi wake.

Mwanafunzi Na Vitu Alivyo Navyo

Somo linalofuata katika Mahubiri ya Mlimani linaweza kuwakorofisha Wakristoambao lengo lao kubwa maishani ni kuzidi kujipatia vitu.

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo na wevi huvunjana kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondowala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi. Kwa kuwa hazina yakoilipo ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Taa ya mwili ni jicho. Basijicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicholako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi, ile nuruiliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! Hakuna mtu awezayekutumikia mabwana wawili. Kwa maana atamchukia huyu na kumpendahuyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezikumtumikia Mungu na mali (Mathayo 6:19-24).

Yesu aliagiza kwamba tusijiwekee hazina hapa duniani. Sasa – “hazina” ni kitu gani?Hazina halisi huwekwa katika masanduku ya hazina, na kuhifadhiwa mahali. Hazitumikikwa kitu chochote kinachofaa. Yesu alifafanua hizo kuwa ni vitu vinavyovutia kutu,

Page 21: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

nondo na wezi. Yaani ni kusema kwamba “si vya muhimu”. Nondo hula vilivyo ndanikabisa ya makabati yetu – hawali vile tunavyotumia kila siku. Kutu hula vtu tusivyotumiasana. Katika nchi zilizoendelea sana, kwa kawaida wevi huiba vitu ambavyo watuhawavihitaji sana: picha, lulu, vitu vya thamani, na kitu kinachoweza kuuzwa haraka.

Wanafunzi wa kweli wamekwisha “toa mali zao zote” (ona Luka 14:33). Wao niwasimamizi tu wa fedha za Mungu. Basi, kila uamuzi wa kutumia fedha ni wa kiroho.Tunachofanya na fedha yetu huonyesha nani anayetawala maisha yetu. Tunapokusanya“hazina” na kwa njia hiyo kulundika fedha na kununua visivyo muhimu, tunadhihirishakwamba Yesu si anayetawala maishani mwetu. Maana, kama angekuw andiye mtawala,tungefanya vitu bora zaidi na zile fedha alizotukabidhi.

Hivyo vitu bora zaidi ni kama nini? Yesu anatuagiza tujiwekee hazina mbinguni.Inawezekanaje kufanya hivyo? Anatuambia katika Injili ya Luka: “Viuzeni mlivyo navyomtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahalipasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu” (Luka 12:33).

Kwa kutoa fedha kuwasaidia maskini na kueneza Injili, tunajiwekea hazina mbinguni.Yesu anatuambia tuchukue kile kitakachopungua thamani mpaka kufikia kutokuwa nayo,tukitie katika kitu kingine ambacho hakipotezi thamani kamwe. Hayo ndiyo afanyayomtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi, naye anawafundisha wanafunzi wakekufanya hivyo hivyo.

Jicho Bovu

Je, Yesu alimaanisha nini alipozungumza juu ya watu wenye macho mazuri ambaomiili yao imejaa nuru, na watu wenye macho mabovu, ambao miili yao imejaa giza? Bilashaka maneno Yake yalihusu mambo ya fedha na vitu, kwa sababu kabla ya kusema hayoalikuwa anazungumzia vitu hivyo, na baada ya kusema hivyo alizungumzia vitu hivyo.

Neno la Kiyunani lililotafsiriwa “bovu” katika 6:23 ndiyo limetafsiriwa “ovu” katikaMathayo 20:15. Hapo tunasoma kuhusu mwajiri aliyemwambia mfanya kazi wake hivi:“Je, jicho lako limekuwa ovu kwa kuwa mimi ni mkarimu?” (TLR) Ni wazi kwambajicho haliwezi kuwa ovu. Sasa – “jicho ovu (au bovu)” maana yake mtu mwenye choyo.Hii inatusaidia sisi kuelewa vizuri zaidi maana ya Kristo katika Mathayo 6:22-23.

Mtu mwenye jicho safi ni mfano wa yule mwenye moyo safi, anayeruhusu mwangazawa kweli kuingia ndani yake. Basi, anamtumikia Mungu na kujiwekea hazina – si duniani– bali mbinguni, mahali ambapo moyo wake upo. Mtu mwenye jicho bovu hufungia njemwanza wa kweli usiingie, kwa sababu yeye hudhani tayari ana ukweli. Basi amejaagiza, akiaini uongo. Anajiwekea hazina duniani mahali moyo wake ulipo. Yeye anaaminikwamba kusudi la maisha yake ni kujitosheleza. Fedha ni mungu wake. Haendimbinguni.

Nini maana ya fedha kuwa mungu wako? Maana yake ni kwamba fedha ina nafasiambayo Mungu anapaswa kuwa nayo maishani mwako. Fedha inatawala maisha yako.Ndiyo inayochukua nguvu zako, mawazo yako na muda wako. Ndiyo chanzo kikuu chafuraha yako. Unazipenda.12 Ndiyo maana Paulo alifananisha tamaa (au choyo) nakuabudu sanamu, akisema kwamba hakuna yeyote mwenye tamaa atakayeurithi ufalmewa Mungu (ona Waefeso 5:5; Wakolosai 3:5-6).

12 Wakati mwingine tena Yesu alisema haiwezekani kumtumikia Mungu na mali. Luka anatuambia hivi:“Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki” (Luka16:14). Basi – hapa tena katika Mahubiri ya Mlimani, Yesu alikuwa anafunua wazi kawaida na mafundishoya Mafarisayo.

Page 22: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Mungu na fedha hutaka kutawala maisha yetu, na Yesu alisema hatuwezikuwatumikia wote wawili. Hapo tena tunaona Yesu alibakia kwenye somo Lake kuu – Niwatakatifu tu watakaorithi ufalme wa Mungu. Aliweka wazi kabisa kwamba watuwaliojaa giza, ambao mungu wao ni fedha, ambao mioyo yao ipo duniani na wenyekujiwekea hazina za kidunia hawako kwenye ile njia nyembamba iongozayo watukwenda uzimani.

Maskini Mwenye Kutamani

Kutaka sana kupata vitu si kosa wakati vitu hivyo ni vya anasa. Mtu anaweza kukoseana kuwaza sana kuhusu vitu hata kama hivyo vitu ni mahitaji ya msingi. Yesu aliendeleakufundisha hivi:

Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle niniau mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakulana mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani ya kwambahawapandi wala hawavuni wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wambinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenuambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?Na mavazi ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba jinsiyameavyo; hayafanyi kazi wala hayasokoti, nami nawaambia ya kwambahata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapola hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leona kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi waimani hapa? Msisumbuke basi mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? AuTuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta. Kwa sababu Babayenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafutenikwanza ufalme wake na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basimsisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatoshakwa siku maovu yake (Mathayo 6:25-34).

Wasomaji wengi wa kitabu hiki hawataweza kujilinganisha hata kidogo na watuambao Yesu alikuwa anazungumza nao. Je, wewe ulipata wasiwasi lini mara ya mwishokuhusu chakula, kinywaji au mavazi?

Maneno ya Yesu kwa hakika yanatuhusu sisi wote. Ikiwa ni makosa kuwaza sana nakuchukuliwa na upatikanaji wa mambo muhimu maishani, vipi kuhusu yasiyokuwamuhimu? Yesu anawatazamia wanafunzi Wake kuhusika zaidi na kutafuta mambomawili: Ufalme Wake na haki Yake. Mkristo anaposhindwa kutoa zaka – fungu la kumi –(na hiyo ni amri ya agano la kale) lakini aweze kujipatia vitu vingi tu visivyo muhimu, je,anaishi kulingana na kanuni ya Kristo ya kutafuta kwanza ufalme na haki Yake? Jibu niwazi kabisa!

Usiwe Mtafuta Makosa

Maagizo ya Yesu yanayofuata kwa wafuasi Wake yanahusu dhambi za kuhukumu nakutafuta makosa kwa wengine.

Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ilemhukumuyo ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kila mpimiacho ndichomtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho

Page 23: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; nakumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe. Itoekwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vemakukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako (Mathayo 7:1-5).

Ingawa Yesu hakuwashtaki waandishi na Mafarisayo moja kwa moja au vinginevyokatika fungu hili, wao walikuwa na hatia ya dhambi hii. Walimkosoa Yeye!

Je, Yesu alimaanisha nini hasa katika onyo hili la kuwahukumu wengine?Kwanza: Hebu tufikiri hakumaanisha nini. Yeye hakumaanisha kwamba tusiwe

wenye uwezo wa kupambanua na kufanya maamuzi ya msingi kuhusu tabia za watu kwakuwatazama matendo. Hilo ni wazi kabisa. Mara tu baada ya sehemu hii, Yesualiwaagiza wanafunzi Wake wasitupe lulu zao mbele ya nguruwe na wasiwape mbwakilicho kitakatifu (ona 7:6). Bila shaka alikuwa anazungumza kwa mifano juu ya watufulani, akiwaita nguruwe na mbwa – watu ambao hawakuthamini thamani ya vituvitakatifu – “lulu” – walivyokuwa wanapewa. Bila shaka hawajaokoka hao. Kwa kweli nilazima kupima kama watu ni nguruwe na mbwa ikiwa tutatii agizo hili.

Tena, Yesu akawaambia wafuasi Wake baadaye kidogo jinsi ya kupima waalimu wauongo – “mbwa mwitu waliovaa mavazi ya kondoo” (7:15) – kwa kukagua matunda yao.Basi, ni dhahiri kwamba ili tuweze kutii maagizo ya Yesu lazima tutazame jinsi watuwanavyoishi na kutoa hukumu.

Paulo vile vile aliwaambia waamini Wakorintho hivi:

Lakini mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane namtu aitwaye ndugu akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenyekuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namnahii msikubali hata kula naye (1Wakor. 5:11).

Ili kutii agizo hili inatakiwa tuchunguze maisha ya watu na kufanya maamuzi juu yao– kuhukumu – kutokana na kile tunachokiona.

Hata mtume Yohana pia alituambia tunaweza kutambua kirahisi tu nani ni wa Munguna nani ni wa Shetani. Kwa kutazama maisha ya watu, ni dhahiri kwetu nani ameokokana nani hajaokoka (ona 1Yohana 3:10).

Kama mambo ni hayo, Kristo hasemi kwamba ni dhambi kutambua tabia za watukwa kuyatazama maisha yao na kuhukumu kama wao ni wa Mungu au wa Shetani. Sasa,alimaanisha nini basi?

Hebu gundua kwamba Yesu alikuwa anazungumza juu ya kutafuta makosa madogo –vibanzi katika ndugu – tafadhali ona kwamba Yesu anatumia neno ndugu mara tatukatika fungu hili. Yesu hakuwa anatuonya dhidi ya kuwahukumu watu kwamba niwasioamini kwa kutazama makmosa yao makubwa sana (kama tutakavyoona punde tukatika mahubiri haya). Kinyume chake – haya ni mafundisho kuhusu jinsi Wakristowanavyopaswa kuwatendea Wakristo wengine. Hawapaswi kuwa watafutaji makosamadogo madogo miongoni mwao – hasa kama wao wenyewe hawaoni makosa yaomakubwa sana. Ikifikia hapo wanakuwa wanafiki. Yesu aliwahi kuwaambia watuwengine waliokuwa wanafiki, hivi: “Yeyote asiyekuwa na dhambi miongoni mwenu, naawe wa kwanza kutupa jiwe” (Yohana 8:7, TLR).

Mtume Yakobo, ambaye barua yake inafanana na Mahubiri ya Mlimani sehemusehemu, aliandika hivi, “Ndugu! Msinung’unikiane msije mkahukumiwa. Angalieni,mwamuzi amesimama mbele ya milango” (Yakobo 5:9). Pengine hili nalo litatusaidiakuelewa kidogo kuhusu kitu Yesu alichokuwa anaonya – kutafuta makosa katika

Page 24: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

waaminio kisha kutangaza tulichopata – kunung’unikiana. Hii ni dhambi moja kubwasana katika kanisa, na wale wenye hatia ya dhambi hiyo wanajiweka katika nafasi hatarisana ya kuhukumiwa. Tunapomsema mwamini mwenzsetu, tukionyesha makosa yakekwa wengine, tunahalifu Amri Kuu, kwa sababu sisi hatupendi watu waseme ubaya wetuwakati hatupo.

Tunaweza kwa upendo kabisa kumwendea mwamini ambaye ana tatizo, lakini wakatitunapoweza kufanya hivyo bila ya unafiki, tukiwa na uhakika kwamba hatuna hatia (auhatia zaidi) ya dhambi hiyo hiyo kama mtu tunayembana. Ila, ni kupoteza wakati kabisakufanya hivyo na asiyeamini, na hicho ndicho kisemwacho katika mstari unaofuata. Yesualisema hivi:

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu wala msitupe lulu zenu mbele yanguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka nakuwararua (Mathayo 7:6).

Vivyo hivyo kuna mithali inayosema hivi: “Usimkaripie mwenye dharau asijeakakuchukia. Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda” (Mithali 9:8). Mahali pengineYesu aliwaambia wanafunzi Wake kukung’uta mavumbi ya miguu yao kama kulalamikakinyume cha wanaokataa injili yao. “Mbwa” wakiisha tambuliwa kwa kutokufurahia nakupenda kweli, Mungu hataki watumishi Wake wapoteze muda wao kujaribu kuwafikia,huku kuna wengine ambao hawajapata nafasi hata moja.

Himizo Kuomba

Hatimaye tunafikia sehemu ya mwisho ya mahubiri ya Yesu. Inaanza kwa ahadi zakutia moyo sana kuhusu maombi, kama ifuatavyo:

Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyimtafunguliwa. Kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona;naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu ambaye,mwanamwe akimwomba mkate atampa jiwe? Au akiomba samaki atampanyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawavyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema waowamwombao? (Mathayo 7:7-11).

Msomaji mmoja anaweza kusema, “Aha! Nimepata sehemu ya Mahubiri ya Mlimaniambayo hayahusiani na utakatifu.”

Inategemeana na tunachokomba, na kwamba tunabisha na kutafuta nini katika sala.Kama wenye kuwa na “njaa na kiu ya haki”, tunatamani kutii yote ambayo Yesuameamuru katika mahubiri Yake, na hiyo shauku inaonekana katika sala zetu. Ukweli nikwamba ile sala mfano ambayo Yesu amefundisha hapo nyuma katika Mahubiri haya nionyesho la shauku kwamba mapenzi ya Mungu yafanyike, na utakatifu upatikane.

Tena, tafsiri ya Luka ya ahadi hizo hizo za sala tunazotazama humalizika kwamaneno yafuatayo: “Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawavyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu haowamwombao?” (Luka 11:13). Yesu hakuwa anafikiria vituv ya starehe alipotuahidi“mema”. Katika akili Yake, Roho Mtakatifu ni “kipawa chema” kwa sababu hutufanyasisi kuwa watakatifu na kutusaidia kueneza Injili inayowafanya wengine kuwa watakatifupia. Na watakatifu ndiyo wanaokwenda mbinguni.

Page 25: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Zawadi zingine nzuri ni chochote kilicho katika mapenzi ya Mungu. Ni wazi kwambaMungu anashughulika zaidi na mapenzi Yake na ufalme Wake. Basi na sisi tutazamiekwamba sala zetu kuhusu chochote kitakachoongeza faida yetu katika ufalme wa Munguzitajibiwa kila wakati.

Maneno Ya Kuhitimisha

Sasa tunafikia mstari ambao unapaswa kuhesabiwa kuwa ni hitimisho la kila kituambacho Yesu amesema kufikia hapa. Waandishi wengi wa mafafanuzi ya Bibliahushindwa kuona hilo, lakini ni muhimu sisi tusikosee. Mstari huu ni wa kumaliziamaana unaanza kwa neno hili: Basi. Kwa hali hiyo umeunganika na mafundishoyaliyopita, na swali ni hili: Je, ni muhtasari kiasi gani wa yale ambayo Yesu amesema?Hebu tuusome na kufikiri kidogo juu yake.

Basi, yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyohivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii (Mathayo 7:12).

Maneno hayo hayawezi kuwa muhtasari wa ile mistari michache inayosema kuhusumaombi. Ingekuwa hivyo, haileti maana yoyote.

Kumbuka kwamba mapema kabisa katika mahubiri yake, Yesu alikuwa ameonyakuhusu kosa la kudhani kwamba amekuja kuitangua Torati na Manabii (ona Mathayo5:17). Kuanzia hapo na kuendelea, mpaka mstari huu tunaotazama sasa, hakufanya kitukingine isipokuwa kuunga mkono na kufafanua amri za Mungu katika Agano la Kale.Kwa hiyo sasa anahitimisha kila kitu kilichoagizwa – yote yaliyotoka katika Torati naManabii – “Basi, yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo;maana hiyo ndiyo Torati na Manabii” (7:12). Maneno “Torati na Manabii” huunganishakila kitu alichosema Yesu kati ya Mathayo 5:17 na 7:12.

Sasa, anapoanza kuhitimisha mahubiri Yake, anakariri tena fundisho Lake kuu – Niwatakatifu tu ndiyo watakaorithi ufalme wa Mungu.

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba. Maana mlango nimpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwamlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayouzimani, nao waionao ni wachache (Mathayo 7:13-14).

Bila shaka huo mlango mwembamba na njia endayo uzimani ambayo wachachewanaiona, ni mfano wa wokovu. Ule mlango mpana na njia pana iendayo upotevuniambayo ndiyo inafuatwa na wengi, ni mfano wa kupotea. Kama kila kitu alichosemaYesu kabla ya maneno haya kinamaanisha chochote – kama mahubiri haya yanakwendakwa mpangilio unaofaa – kama Yesu alikuwa msemaji fundi mwenye ufahamu kuhusukuwasiliana na watu, basi tafsiri halisi kabisa ni kwamba njia nyembamba ni njia yakumfuata Yesu na kutii mafundisho Yake. Ile pana ni kinyume chake. Je, ni Wakristowangapi walio kwenye njia hiyo nyembamba yenye kuelezwa katika mahubiri haya?Mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi yuko kwenye ile njia nyembamba, nayeanawaongoza wanafunzi wake kuipitia.

Inawashangaza Wakristo wengine kwamba Yesu hakusema chochote kuhusu imaniau kumwamini katika mahubiri haya ambayo kwa sehemu kubwa sana alizungumzia juuya wokovu na kupotea. Kwa wale wanaoelewa kiungo kilichoko kati ya kuamini namwenendo, mahubiri haya hayana matatizo yoyote. Watu wanaomtii Yesu huonyeshaimani yao kwa matendo yao. Wale wasiomtii hawaamini kwamba ni Mwana wa Mungu.

Page 26: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

Wokovu wetu si onyesho tu la neema ya Mungu kwetu, bali hata lile badiliko lililotokeamaishani mwetu ni onyesho pia. Kihalisi ni kwamba utakatifu wetu ni utakatifu Wake.

Jinsi Ya Kutambua Viongozi Waongo Wa Dini

Yesu alipoendelea kumalizia mahubiri Yake, alitoa onyo kwa wanafunzi Wakekuhusu manabii wa uongo ambao wanawaongoza wasioweza kuwatambua kuelekeaupotevuni kwa njia ile pana. Hao si wa Mungu kweli, lakini wamejigeuza na kuonekanahivyo. Waalimu wote wa uongo na viongozi wa aina hiyo wako katika fungu hili.Wanawezaje kutambuliwa?

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavaziya kondoo walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwamatunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katikamibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mtimwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matundamabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tundazuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.Si kila aniambiaye ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wambinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jinalako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujizamingi?’ Ndipo nitawaambia dhahiri, ‘Sikuwajua ninyi kamwe; ondokenikwangu, ninyi mtendao maovu’ (Mathayo 7:15-23).

Yesu alionyesha waziwazi kwamba waalimu wa uongo ni wadanganyifu sana.Wanaonekana kwa nje kuwa ni halisi. Wanaweza kumwita Yesu Bwana wao, wakatabiri,wakatoa pepo na kutenda miujiza. Lakini yale “mavazi ya kondoo” huficha “mbwamwitu wakali”. Wao si kondoo wa kweli. Itajulikanaje kwamba ni wa kweli au wauongo? Tabia yao ya kweli inaweza kutambulika kwa kuchunguza “matunda” yao.

Nini matunda anayozungumzia Yesu? Bila shaka si matunda ya miujiza. Ila, nimatunda ya kutii yote ambayto Yesu alifundisha. Wale walio kondoo wa kweli hufanyamapenzi ya Baba. Wale walio wa uongo ni “watenda maovu” (7:23). Wajibu wetu basi nikulinganisha maisha yao na yale ambayo Yesu alifundisha na kuamuru.

Siku hizi waalimu wa uongo ni wengi sana makanisani, na hilo lisitushangaze kwasababu Yesu na Paulo walituonya kwamba, kadiri mwisho unavyokaribia, tutazamiehivyo (ona Mathayo 24:11; 2Timo. 4:3-4). Manabii wa uongo walio wengi siku hizi niwale wanaofundisha kwamba mbinguni wataingia wasiokuwa watakatifu. Haowanawajibika kwa kupotea kwa mamilioni ya watu. John Wesley – mhubiri maarufu wasiku za nyuma – aliandika hivi juu yao:

Kitu hiki ni kibaya sana! – wakati wawakilishi wa Munguwanapofanyika watendaji wa Shet ani! – wakati wale ambao wameagizwakuwafundisha watu njia ya kufika mbinguni wanapowafundisha njia yakwenda jehanamu … Kama mtu akiuliza, “Nani amewahi kufanya hviyo?”… Ninajibu hivi: Watu elfu kumi, wenye hekima na wanaoheshimiwasana. Naam, wale wote, wa dhehebu lolote lile, wanaowatia moyo watuwenye kiburi, wenye kuchukulia mambo kirahisi-rahisi tu, wenye tamaa,wanaopenda dunia, wanaopenda starehe, wasiotenda haki au wema, waturahisi kudanganyika, wasiojali, wasiodhuru chochote, wasiofaa,

Page 27: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

wasiokuwa tayari kuteseka kwa ajili ya haki, kwamba hao watakwendambinguni. Hao ni manabii wa uongo wa hali ya juu sana. Hao ni wasalitiwa Mungu na mwanadamu … Daima wanawaongoza watu kuelekeakatika nchi za giza; na watakapowafuata hao maskini waliowapoteza,“kuzimu chini itataharuki ili kuwapokea!”13

Maneno hayo aliyasema katika kufafanua juu ya waalimu wa uongo ambao Yesualionya juu yake katika Mathayo 7:15-23.

Ona tena kwamba Yesu alisema wazi kabisa – kinyume na tunavyoambiwa nawaalimu wengi wa uongo siku hizi – wale wasiozaa matunda mema watatupwa jehanamu(7:19). Tena, hilo si kwa ajili ya waalimu na manabii tu, bali ni kwa wote. Yesu alisemahivi: “Si kila mtu aniitaye ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; balini wale watendao mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21, TLR).Kinachohusu manabii kinawahusu wote. Hiyo ndiyo mada kuu ya Yesu – Waliowatakatifu tu ndiyo wataurithi ufalme wa Mungu. Watu wasiomtii Yesu wanakwendajehanamu.

Ona pia jinsi Yesu anavyounganisha hali ya mtu ndani na jinsi alivyo nje. Miti“mizuri” huzaa matunda mazuri. Miti “mibaya” haiwezi kuzaa matunda mazuri. Chanzocha matunda mazuri yanayoonekana kwa nje ni ile asili ya mtu. Mungu kwa neema Yakeamebadilisha asili ya watu ambao wamemwamini Yesu kweli.14

Onyo La Mwisho Na Hitimisho

Yesu alimalizia mahubiri Yake kwa onyo la mwisho pamoja na hitimisho kwa njia yamfano. Kama unavyotazamia, ni mfano kuhusu kweli kuu aliyozungumzia – Watakatifundiyo watakaorithi ufalme wa Mungu.

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya, atafananishwa namtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvuaikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ileisianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kilaasikiaye hayo maneno yangu asiyafanye atafananishwa na mtu mpumbavualiyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mafurikoyakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo angukolake likawa kubwa (Mathayo 7:24-27).

Mfano wa mwisho wa Yesu sio ufunguo wa “mafanikio maishani” kama wenginewanavyosema. Mantiki inaonyesha kwamba hakuwa anatoa ushauri kuhusu jinsi yakufanikiwa kifedha katika nyakati ngumu kwa kuwa na imani katika ahadi Zake. Huu nimuhtasari wa yote ambayo yesu alisema katika Mahubiri Yake ya Mlimani. Wale 13 Hayo yametoka katika kitabu cha John Wesley kiitwacho The Works of John Wesley (Baker: GrandRapids, 1996). Kimechapishwa upya kutoka toleo la 1872 la Wesleyan Methodist Book Room, London.Ukurasa wa 441, 416.14 Sitaacha kusema hapa kuhusu msemo wa kawaida watu wanaotumia, wanapojaribu kutetea dhambi ndaniya wengine. Wansema hivi: “Hatujui yaliyomo moyoni mwake.” Kinyume cha maneno hayo, Yesuanasema hapa kwamba mambo ya nje hudhihirisha mambo ya ndani. Mahali pengine alisema hivi:“Kinywa hunena yaujazayo moyo” (Mathayo 12:34). Mtu anapozungumza maneno ya chuki, inaonyeshachuki imejaa moyoni mwake. Yesu pia alituambia hivi: “Kutoka ndani – moyoni mwa mtu – hutokeamawazo maovu, uasherati, wizi, mauaji, uzinzi, tamaa na uovu, pamoja na udanganyifu, ashiki, wivu,matukano, kiburi na upumbavu” (Marko 7:21-22). Mtu anapozini, tunajua kilicho moyoni mwake: niuzinzi.

Page 28: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com · hufkiri kwamba kila Mkristo anapaswa kujitafuta katika “Heri” mojawapo – moja tu. Ila – wasomaji waangalifu wanatambua

wanaofanya anayosema ni wenye hekima na watadumu. Hawahitaji kuogopa hasira yaMungu itakapokuja. Wasiomtii ni wapumbavu nao watateseka sana. Watalipa gharama ya“adhabu ya kuangamizwa milele” (2Wathes. 1:9).

Jibu La Swali

Je, haiwezekani kwamba Mahubiri ya Yesu Mlimani yalikuwa ni kwa ajili ya wafuasiWake tu, walioishi kabla ya kifo na kufufuka Kwake? Si wao walikuwa chini ya Toratikama njia ya muda tu ya wokovu, na baada ya Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zao ndipowaliokolewa kwa imani na kutangua kweli kuu inayotawala mahubiri haya?

Wazo hilo ni baya sana. Hakuna yeyote aliyewahi kuokolewa kwa matendo yake.Kila wakati imekuwa ni kwa imani – kabla na katika kipindi cha agano la kale. Pauloanatoa hoja katika Warumi 4 kwamba Ibrahimu (kabla ya agano la kale) na Daudi(wakati wa agano la kale) walihesabiw ahaki kwa imani, si kwa matendo.

Tena, ilikuwa ni vigumu kwa yeyote katika wasikilizaji wa Yesu kuokolewa kwamatendo, maana wote walikuwa wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu waMungu (ona Warumi 3:23). Neema ya Mungu tu ndiyo ingewaokoa, na imani tu ndiyoingepokea neema hiyo ya Mungu.

Kwa bahati mbaya sana – wengi katika kanisa siku hizi wanaona amri za Yesu kuwahazina kusudi lingine isipokuwa kutufanya tujisikie hatia ili tuone jinsi isivyowezekanakupata wokovu kwa matendo. Kwa kuwa sasa “tumepata ujumbe” na kuokolewa kwaimani, tunaweza kupuuza amri Zake. Ila, kama tunataka wengine “waokolewe” basituzifuate. Tuzichomoe na kuwaonyesha watu jinsi walivyo na dhambi, ili waokolewekwa “imani” isiyo na matendo.

Pamoja na hayo, Yesu hakuwaambia wanafunzi Wake hivi: “Enendeni ulimwengunimwote mkawafanye watu kuwa wanafunzi, na mhakikishe kwamba, wakiisha tambuahatia yao na kuokolewa kwa imani, amri zangu zimemaliza kusudi lake katika maishayao.” Badala yake alisema hivi: “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi …na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” (Mathayo 28:19-20. Manenomepesi kukazia). Watumishi wanaofanya watu kuwa wanafunzi wanafanya hayo hayo.