lishe na ulaji bora kwa wagonjwa wa kifua kikuucounsenuth-tz.org/sites/default/files/lishe na ulaji...
TRANSCRIPT
Lishe na Ulaji Bora kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu
COUNSENUTHInformation Series No.15December, 2008
GLOBAL FUNDROUND 4 PROGRAM
Kitabu hiki kimetayarishwa na:Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)
S.L.P. 8218, Dar es SalaamSimu/ Nukushi: +255 222 152 705
Barua pepe: [email protected]
Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo ya kibiashara ili mradi ionyeshwe kwamba maelezo hayo yametolewa toka kwenye kitabu hiki.
ISBN 978-9987-9017-8-4
© COUNSENUTH, 2008
Lishe na Ulaji Bora kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu
Wahariri:Dr. Lunna KyunguRestituta Shirima
Tuzie Edwin
Kimefadhiliwa na:Global Fund Round 4 Program
ii
YALIYOMO
VIFUPISHO ............................................................................................ .. iv
SHUKRANI ............................................................................................ .. vi
FARAHASA ............................................................................................ .. vii
1.0 UTANGULIZI ............................................................................................... 1
2.0 KIFUA KIKUU NI NINI? ....................................................................... ..... 2
2.1 Utangulizi ................................................................................................. ..... 2
2.2 Jinsi maambukizi ya kifua kikuu yanavyotokea
2.3 Dalili za kifua kikuu ................................................................................ ...... 2
2.4 Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata kifua kikuu ..................... ...... 3
3.0 UHUSIANO KATI YA KIFUA KIKUU NA UKIMWI .......................... .... 4
4. 0 UHUSIANO KATI YA LISHE NA KIFUA KIKUU ................................... 4
4.1 Utangulizi ................................................................................................. ..... 4
4.2 Athari za kifua kikuu kwenye lishe .......................................................... ..... 4
4.3 Athari za lishe kwenye kifua kikuu .......................................................... ..... 4
5.0 LISHE NA ULAJI UNAOTAKIWA KWA MGONJWA WA
KIFUA KIKUU ....................................................................................... ...... 5
5.1 Utangulizi ..................................................................................... ..... 5
5.2 Ulaji unaoshauriwa kwa mgonjwa wa kifua kikuu ....................... ..... 5
5.3 Jinsi ya kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayompata ..................
mgonjwa wa kifua kikuu ............................................................... ................ 7
5.3.1 Kukosa hamu ya kula ......................................................... . 8
5.3.2 Kichefuchefu na kutapika .................................................. .. 9
5.3.3 Kupungua uzito ............................................................................ ...... 9
5.3.4 Upungufu wa wekundu wa damu ................................................. ..... 10
5.3.5 Homa ............................................................................................. ..... 10
5.3.6 Kuharisha ...................................................................................... ..... 11
5.3.7 Matatizo ya ngozi .......................................................................... .... 12
6.0 MATUMIZI YA DAWA NA CHAKULA................................................. ... 13
6.1 Utangulizi ...................................................................................... .... 13
6.2 Ushauri wa matumizi sahihi ya chakula na dawa ......................... ..... 14
7.0 MAMBO YA KUZINGATIA KWA MGONJWA WA
KIFUA KIKUU......................................................................................... ..... 14
8.0 BIBLIOGRAFIA ...................................................................................... ..... 15
9.0 KIAMBATANISHO: Baadhi ya virutubishi, umuhimu na vyanzo vyake .. 16
iii
VIFUPISHO
COUNSENUTH - Centre for Counselling, Nutrition and Health Care
MoHSW - Ministry of Health and Social Welfare
VVU - Virusi Vya UKIMWI
UKIMWI - Upungufu wa Kinga Mwilini
ORS - Oral Rehydration Solution
NACP - National AIDS Control Program
TB - Tuberculosis
TFNC - Tanzania Food and Nutrition Centre
SUA - Sokoine University of Agriculture
GFR4 - Global Fund Round Four
iv
SHUKRANI
Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) kinatoa shukrani
za dhati kwa Programu ya Global Fund Round Four (GFR4) kwa ufadhili wake
ambao umewezesha kitabu hiki kutayarishwa na kutolewa.
COUNSENUTH inapenda kuwatambua wafuatao ambao walishiriki kutoa
msaada wa kitaalam wakati wa kutayarisha kitabu hiki: Dr. Grace Magembe
(Manispaa ya Ilala), Dr. Saul Nkya (TFNC), Toligwe Kaisi (SUA), Justine
Kiondo (St. Augustine University), Restituta Shirima (COUNSENUTH), Dr.
Lunna Kyungu (COUNSENUTH), Mary Materu (COUNSENUTH) na Tuzie
Edwin (COUNSENUTH). Shukrani pia kwa mashirika mbalimbali na watu
wote walioshiriki kutoa maoni yao katika kutayarisha na kukamilisha kitabu
hiki. Shukrani za dhati kwa Donald Navetta kwa kuhariri kitabu hiki.
v
FARAHASA
Asusa: Kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bila matayarisho makubwa. Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na mwingine.
Chakula: Kitu chochote kinacholiwa na kuupatia mwili virutubishi.
Kafeini: Kiini kilichoko kwenye vinywaji kama vile chai, kahawa na soda ambavyo huchangamsha mwili; lakini huweza kuathiri ufanisi wa baadhi ya virutubishi mwilini.
Lishe: Sayansi ya jinsi mwili unavyokitumia chakula. Lishe inahusisha jinsi mwili unavyosaga, unavyoyeyusha chakula na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini.
Mlo kamili: Mlo unaotokana na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi mbalimbali ya vyakula.
Nishati-lishe: Nguvu inayouwezesha mwili kufanya kazi mbalimbali.
Nyuzi-nyuzi: Aina ya kabohaidreti ambayo mwili hauwezi kuyeyusha. Hupatikana kwenye matunda, mboga-mboga na nafaka
zisizokobolewa. Nyuzi-nyuzi pia hujulikana kama makapi-mlo.
Ulaji bora: Hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha. Ikiwa ni pamoja na kutumia mafuta, chumvi na sukari kwa
kiasi.
Utapiamlo: Hali ya kupungua au kuzidi kwa virutubisho mwilini.
Vimelea: Vijidudu au viumbe vidogo sana ambavyo havionekani kwa macho.
Virutubishi: Viini vilivyoko kwenye vyakula ambavyo mwili hutumia kufanya kazi mbalimbali.
1
1.0 UTANGULIZI
Katika Afrika ugonjwa wa kifua kikuu ndio chanzo cha vifo vingi zaidi vinavyotokea kutokana na maambukizi yanayoweza kutibika. Inakadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya watu duniani wameambukizwa vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kifua kikuu. Katika Tanzania inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 50,000 wanaugua kifua kikuu kila mwaka; kati ya hao, zaidi ya asilimia 25 wapo mkoa wa Dar es Salaam.
Utapiamlo ni tatizo kubwa kwa wagonjwa wa kifua kikuu. Pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, hakuna taarifa za kutosha kuhusu jinsi ya kumhudumia na kukabiliana na matatizo yanayompata mgonjwa wa kifua kikuu kilishe. Hali nzuri ya lishe husaidia dawa kufanya kazi kwa ufanisi na kuboresha kinga ya mwili.
Madhumuni ya kitabu hiki ni kutoa maelezo muhimu kuhusu lishe na ulaji bora kwa mgonjwa wa kifua kikuu.
Kitabu hiki kinajumuisha taarifa kuhusu uhusiano kati ya ugonjwa wa kifua kikuu na lishe, lishe na ulaji unaoshauriwa kwa mgonjwa wa kifua kikuu na jinsi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayompata mgonjwa wa kifua kikuu.
Walengwa wa kitabu hiki ni watoa huduma za afya, watoa huduma katika ngazi ya jamii ikijumuisha watoa huduma majumbani; wagonjwa wa kifua kikuu na jamii kwa ujumla.
Ni matumaini yetu kuwa taarifa zilizomo katika kitabu hiki zitakuwa ni msaada mkubwa katika kuboresha matunzo na huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu.
2
2.0 KIFUA KIKUU NI NINI?
2.1 UtanguliziKifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea vya bakteria ajulikanae kama Mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, lakini huweza kuathiri pia sehemu nyingine za mwili kama uti wa mgongo, mifupa, moyo, ubongo na figo.
2.2 Kifua kikuu kinavyoambukizaKifua kikuu huambukizwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye uambukizo wa kifua kikuu ambaye bado hajaanza matibabu akikohoa, kupiga chafya, kuongea, kuimba au hata kucheka, vimelea vya kifua kikuu husambaa hewani na huweza kumuathiri mtu aliye karibu naye anapovuta hewa yenye vimelea hivyo. Baada ya vimelea vya kifua kikuu kuingia mwilini, mambo matatu huweza kutokea ambayo ni:
i. Uambukizo ambao hauonyeshi daliliMara nyingi vimelea vya kifua kikuu vikiingia katika mwili wa mtu aliye na hali nzuri ya lishe na afya, kinga ya mwili huweza kuviangamiza au kuvizuia vimelea hivyo kuzaliana. Hali hii ya uambukizo huweza kuonyesha dalili kidogo za muda mfupi au kutoonyesha dalili zozote kwani uambukizo unakuwa umezuiwa. Hali hii ya uambukizo ndio hutokea kwa watu wengi.
ii. Uambukizo unaoendelea na kusababisha kifua kikuuUambukizo wa aina hii hutokea pale ambapo kinga ya mwili hushindwa kupambana na vimelea vya kifua kikuu vilivyoingia mwilini. Vimelea hivyo huzaliana na kuenea sehemu mbalimbali za mwili. Dalili huanza kujionyesha katika kipindi cha wiki sita hadi nane baada ya uambukizo.
Mara nyingi uambukizo wa aina hii hutokea kwa watu ambao hali zao za lishe na afya ni duni; kwa mfano watoto wachanga, watoto au watu wazima wenye utapiamlo na watu ambao kinga yao ya mwili imepungua.
iii. Uambukizo unaojitokeza baadaye Uambukizo wa aina hii hutokea baada ya miezi au miaka michache baada ya kupata uambukizo ambao haukuonyesha dalili. Vimelea vya kifua kikuu huweza kuendelea kuishi bila ya kuzaliana na bila athari yoyote mwilini kwa muda mrefu. Kinga ya mwili inapodhoofika kwa sababu mbalimbali, vimelea huanza kuzaliana na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.
3
Walio katika uwezekano mkubwa wa kupata aina hii ya uambukizo ni watu:
• walioambukizwavirusivyaUKIMWI(VVU);• wenyeutapiamlo;• wazee;• dhaifu;• wenyeugonjwawakisukari;• wenyematatizoyafigo;• wenyesaratanikamavilesarataniyadamu;• wanaotumia dawa za kuongeza nguvu (steroid) au dawa zinazo
punguza kinga ya mwili;• wanaovutasigara;na• walevi.
2.3 Dalili za kifua kikuuDalili za kifua kikuu hutegemea vimelea hivyo vimeathiri sehemu gani za mwili. Dalili kuu za kifua kikuu ni pamoja na:
• Kukohoamfululizozaidiyawikimbili;• Kukohoamakohoziyenyemchanganyikonadamu;• Kupunguauzito/kukonda;• Maumivuyakifuanakupumuakwashida;• Homazajionizaidiyawikimbilizinazoambatananakutokwana
jasho jingi usiku;• Kujisikiauchovumarakwamara;• Kukosahamuyakula;na• Uvimbe au maumivu katika kiungo kilichoathirika iwapo kifua
kikuu si cha mapafu.
2.4 Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata kifua kikuu• Utapiamlo;• UpungufuwavitaminiD;• MaambukiziyaVVU;• Kuishinamgonjwawakifuakikuuambayehajaanzamatibabu;
KUMBUKA:Mtu mwenye kifua kikuu anaweza kuwa na dalili kama za maradhi mengine.
4
• Kuwanakisukariambachohakidhibitiwisawasawa;• Kupunguakwakingayamwili;• Kuvutahewayamoshiausigara;na• Baadhiyasarataninamatibabuyake.
3.0 UHUSIANO KATI YA KIFUA KIKUU NA VVU
Kifua kikuu ndio ugonjwa nyemelezi unaojitokeza zaidi kwa watu walioambukizwa VVU. Maambukizi ya VVU hupunguza kinga ya mwili na hivyo kufanya mwili uwe katika hatari zaidi ya kushambuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo kifua kikuu.
Kuwepo kwa maambukizi ya VVU kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa wagonjwa wa kifua kikuu kwani idadi ya watu waliopata maambukizi ya VVU pia wameambukizwa kifua kikuu.
Ugonjwa wa kifua kikuu na UKIMWI vinapojitokeza kwa pamoja, huathiri afya kwa kiasi kikubwa. Iwapo maradhi hayo hayatakabiliwa kikamilifu, mgonjwa huweza kupoteza maisha.
4. 0 UHUSIANO KATI YA LISHE NA KIFUA KIKUU
4.1 UtanguliziHali ya lishe ya mtu huchangia kwa kiasi kikubwa uwezo wa mwili kupambana na maambukizi mbalimbali. Hali duni ya lishe huweza kusababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo kuongeza uwezekano wa mtu kupata maradhi ikiwemo kifua kikuu.
KUMBUKA:• Dalili za kifua kikuu na zile za maambukizi ya VVU huweza
kufanana, hivyo ni muhimu kuchunguza afya katika kituo cha tiba.
• KumbukasiokilamgonjwawakifuakikuuanamaambukiziyaVVU
5
4.2 Athari za ugonjwa wa kifua kikuu kwenye lisheVimelea vya kifua kikuu vinapoanza kuzaliana mwilini, mahitaji ya virutubishi huongezeka na hivyo huweza kusababisha uzito wa mwili kupungua hata kabla ya mtu kugundua kama ana ugonjwa wa kifua kikuu. Wakati huo huo, dalili zinazojitokeza kwa mgonjwa wa kifua kikuu kama vile kukosa hamu ya kula, kutapika, homa na kukohoa huchangia mtu huyu kushindwa kukidhi ongezeko la mahitaji ya virutubishi mwilini. Vilevile, kutokana na mabadiliko yanayotokea mwilini, ufanisi wa matumizi ya virutubishi kama vile protini huweza kupungua. Ulaji duni, ongezeko la mahitaji ya virutubishi na kupungua kwa ufanisi wa utumikaji wa virutubishi huweza kusababisha utapiamlo.
4.3 Athari za lishe duni kwenye kifua kikuuMtu mwenye utapiamlo yupo katika hatari zaidi ya kupata uambukizo wa kifua kikuu kwani kinga yake ya mwili ni dhaifu. Endapo mtu alipata uambukizo ule ambao haonyeshi dalili, wakati hali yake ya lishe na afya ni thabiti, akipata utapiamlo vimelea hivyo huanza kuzaliana na hivyo huweza kusababisha kuugua kifua kikuu.
Utapiamlo kwa mgonjwa wa kifua kikuu husababisha kurefusha kipindi cha kuugua, mwili hudhoofika zaidi, kushindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayoambatana na ugonjwa wa kifua kikuu na pia ufanisi wa matibabu huweza kupungua.
5.0 LISHE NA ULAJI UNAOSHAURIWA KWA MGONJWA WA KIFUA KIKUU
5.1 UtanguliziMatibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu yazingatie ulaji bora ambao unaojumuisha kula vyakula mbalimbali. Mgonjwa wa kifua kikuu anahitaji msaada wa jinsi ya kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayojitokeza ambayo yanachangia kuwa na ulaji duni. Matatizo yanayoweza kujitokeza ni kama vile kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito, homa, kuharisha, upungufu wa wekundu wa damu na matatizo ya ngozi. Matatizo
6
hayo huweza kuingilia ulaji na uyeyushwaji wa chakula na pia ufyonzwaji wa virutubishi.
5.2 Ulaji unaoshauriwa kwa mgonjwa wa kifua kikuuUshauri wa lishe hutolewa ili kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza wakati wa ugonjwa wa kifua kikuu. Mgonjwa yeyote wa kifua kikuu anashauriwa kufanya yafuatayo:
• Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku. Mlo kamilihutayarishwa kutokana na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi ya chakula yafuatayo:• Nafaka,mizizinandizi;• Jamiiyakundenaasiliyawanyama;• Mboga-mboga;• Matunda;na• Mafutanasukari.
• Kulavyakulavinavyoupatiamwilinguvu(nishati-lishe)kwawingiili kuzuia kupungua uzito, kuongeza nguvu na kusaidia kupona haraka. Vyakula vyenye nishati-lishe kwa wingi ni pamoja na mahindi, mtama, uwele, mchele, ngano, viazi aina zote, mihogo, magimbi na ndizi za kupikwa. Vyakula vingine ni mafuta ya alizeti, mawese, mbegu zitoazo mafuta, siagi, majarini, maziwa, jibini, asali na sukari.
• Kula vyakula vyenye protini kwa wingi ili kusaidia kujenga
misuli, kukarabati mwili na kuimarisha mfumo wa kinga. Vyakula vyenye protini kwa wingi ni kama maharagwe, choroko, njegere, kunde, dengu, njugu mawe, karanga, korosho, aina zote za nyama, samaki, mayai na maziwa.
• Kulamatundanamboga-mbogakwawingiilikupatavitamininamadini kwa ajili ya kuwezesha kupona haraka na kuboresha kinga ya mwili.
KUMBUKA:Ni muhimu kujenga tabia ya kula mlo kamili ikiwa ni pamoja na kula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha katika kila mlo.
7
• Kula vyakula vyenye Vitamini B6 kwa wingi kama vile viazivitamu, maharagwe, mahindi yasiyokobolewa, parachichi, nyama na samaki kwani baadhi ya dawa za kutibu kifua kikuu huingilia matumizi ya vitamini hiyo mwilini.
• Kulavyakulavyenyemadinichumakwawingiilikuzuiaupungufuwa wekundu wa damu. Vyakula vyenye madini chuma kwa wingi ni kama maini, dagaa, figo, nyama, samaki, mbaazi, maharagwe, korosho, choya (rozela), kisamvu, majani ya kunde, matembele na mchicha.
• KulavyakulavyenyeVitaminiAkwawingi ili kuboresha mfumo wa kinga na kuzuia matatizo ya ngozi. Vyakula vyenye Vitamini A kwa wingi ni kama vile maini, mawese, samaki wenye mafuta, kisamvu, matembele, majani ya kunde, maboga, karoti, papai, embe na viazi vitamu vyenye rangi ya manjano.
• KulavyakulavyenyeVitaminiDkwawingikamavilenyama,samaki, mafuta ya samaki na maziwa. Vilevile, Vitamini D hupatikana kwenye jua. Upungufu wa vitamini hii huweza kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.
5.3 Jinsi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayompata mgonjwa wa kifua kikuu
Matatizo mbalimbali ya kiafya yanayompata mgonjwa wa kifua kikuu huweza kukabiliwa kilishe. Kufuata ulaji unaoshauriwa kutaimarisha kinga ya mwili na kuepusha mwili kudhoofika. Matatizo ya kiafya yanayoweza kumpata mgonjwa wa kifua kikuu ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, homa, kuharisha, upungufu wa wekundu wa damu na matatizo ya ngozi.
8
5.3.1 Kichefuchefu na kutapikaKichefuchefu hupunguza hamu ya kula na huweza kusababisha kutapika. Ili kupunguza kichefuchefu na kutapika, mgonjwa wa kifua kikuu anashauriwa kufanya yafuatayo:
- Kuepuka kula vyakula vyenye viungo vingi, mafuta mengi au sukari nyingi kwani vyakula hivyo huongeza kichefuchefu.
- Kula vyakula vikavu na vyenye chumvi kidogo kama mkate, muhogo, ndizi au kiazi cha kuchoma au kuchemsha.
- Kunywa maji mengi na vinywaji vingine kama vile maziwa, togwa, juisi ya matunda halisi, madafu na supu ili kuongeza kiasi cha maji mwilini.
- Kunywa juisi ya limau au ndimu iliyochanganywa na maji ya moto.
- Kula vyakula vilivyochachushwa kama mtindi na togwa.
- Kula milo midogo midogo mara kwa mara yaani si chini ya mara tano kwa siku.
- Kula taratibu.- Kula akiwa amekaa wima au amejiegemeza
kidogo kwenye mto. Aepuke kujilaza mara tu baada ya kula.
- Kuepuka kukaa muda mrefu bila kula au kunywa chochote.
5.3.2 Kukosa hamu ya kulaMgonjwa wa kifua kikuu anapokosa hamu ya kula anashauriwa kufanya yafuatayo:
- Kuongeza viungo kidogo, kama kitunguu saumu, tangawizi, limau, ndimu, mdalasini, kotimiri au iliki kwenye vinywaji au vyakula mbalimbali. Mara nyingi viungo husaidia kuongeza ladha ya chakula na hivyo kuongeza hamu ya kula.
9
- Kuepuka kutayarisha vyakula mwenyewe au kukaa jikoni au karibu na jiko, kwani harufu ya vyakula huweza kupunguza hamu ya kula.
- Kuepuka kunywa maji au vinywaji vingine wakati wa kula kwani hii itasababisha tumbo kujaa haraka.
- Kuongeza vyakula kama vile karanga, maziwa au mafuta kwenye vyakula mbalimbali ili kuviboresha na kuvifanya viwe rahisi kumeza. Vyakula hivi viongezwe kwa kiasi kidogo, kwani vikitumika kwa kiasi kikubwa huweza kusababisha kuharisha.
- Kubadili ladha na aina ya vyakula, kwani mtu anapokula vyakula vya aina mbalimbali na vyenye ladha tofauti hamu ya kula huongezeka. Mbinu mbalimbali za kupika kama kuchemsha, kupika kwa mvuke kutokosa, kuchoma na kubanika zikitumika huweza pia kusaidia.
- Kunywa vinywaji vilivyo bora na kula vyakula anavyovipenda. Pale inapowezekana mgonjwa asile peke yake, ale pamoja na familia au marafiki.
- Kufanya mazoezi mbalimbali kwani husaidia kuongeza hamu ya kula na uyeyushwaji wa chakula tumboni. Hata hivyo aina ya mazoezi hutegemea hali ya mgonjwa.
- Kula milo midogo midogo mara nyingi kwa siku.- Iwapo njia zote zilizoshauriwa hazitasaidia, inabidi mgonjwa
ajilazimishe kula kwani chakula ni muhimu sana.
5.3.3 Kupungua uzito Ili kukabiliana na tatizo la kupungua uzito inashauriwa ifuatavyo:
- Kuongeza kiasi cha chakula, idadi ya milo kwa siku pamoja na kula vyakula vya aina mbalimbali.
- Kuboresha chakula kwa kuongeza vyakula kama karanga, mafuta, siagi, maziwa, sukari au asali, kwani vyakula hivi vina nishati-lishe kwa wingi.
- Kutumia asusa mara kwa mara kati ya mlo na mlo. Asusa zinazoweza kutumika ni kama karanga, matunda, mtindi, uji ulioboreshwa, andazi, sambusa, chapati, kitumbua, muhogo, kiazi au ndizi.
- Kuongeza kiasi kidogo cha viungo katika chakula ili kuongeza hamu ya kula na kusaidia uyeyushwaji wa chakula.
10
- Kutumia vyakula vilivyochachushwa kama maziwa ya mgando na togwa kwani vyakula hivyo huyeyushwa kwa urahisi na husaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine na ufyonzwaji wa virutubishi mwilini.
- Kuepuka kunywa maji mengi kabla tu au wakati wa kula kwani huweza kujaza tumbo na hivyo kumfanya mgonjwa kushindwa kula chakula cha kutosha.
- Kufanya mazoezi kwani husaidia kuongeza hamu ya kula na kujenga misuli. Aina ya mazoezi hutegemea hali ya mgonjwa.
5.3.4 Upungufu wa wekundu wa damuUpungufu wa wekundu wa damu huweza kukabiliwa kwa kufanya yafuatayo:
- Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi, kama vile maini, samaki, dagaa, figo, nyama, kisamvu, matembele, majani ya kunde, mchicha, choya, maharagwe, choroko, njegere, kunde, dengu, njugu mawe, na korosho.
- Kula matunda kwa wingi pamoja na mlo, hasa yale yenye Vitamini C kwa wingi kama vile mapera, machungwa, machenza, mapesheni, mananasi, mabungo, ubuyu na ukwaju. Vitamini C husaidia ufyonzwaji na utumikaji wa madini chuma yaliyoko kwenye vyakula vyenye asili ya mimea.
- Kuepuka vinywaji kama chai, kahawa au soda wakati wa mlo, kwani vina kemikali iitwayo kafeini ambayo huzuia upatikanaji wa madini chuma yaliyoko kwenye vyakula vyenye asili ya mimea. Iwapo italazimu kutumia vinywaji hivyo ni vema kuvitumia saa moja kabla au saa moja baada ya kula chakula na si wakati wa kula.
- Kutibu maradhi kama vile malaria na minyoo mapema
KUMBUKA:Mtu mwenye kifua kikuu anashauriwa kupima uzito mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo yake na kuchukua hatua inayofaa.
11
kwani huchangia kuleta upungufu wa wekundu wa damu.- Kumuona daktari kwa ushauri zaidi ikiwa ni pamoja na kupewa
vidonge vya madini chuma na foliki asidi ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa wekundu wa damu.
5.3.5 HomaMtu anapokuwa na homa anashauriwa yafuatayo:
- Kunywa maji safi na salama na vinywaji vilivyo bora kwa wingi mara kwa mara ili kusaidia kupunguza joto la mwili na kurudishia maji yanayopotea.
- Kula milo midogo midogo mara nyingi ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya virutubishi mwilini linalosababishwa na homa.
- Kuoga maji ya uvuguvugu na kupunguza nguo nzito mwilini.- Kumuona daktari kwani homa huashiria kuwepo kwa tatizo fulani
mwilini.
5.3.6 KuharishaIli kukabiliana na tatizo la kuharisha, mgonjwa anashauriwa kufanya yafuatayo:
- Kunywa maji safi na salama kwa wingi (zaidi ya lita moja na nusu) ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.
- Kunywa vinywaji kama, madafu, togwa, supu, maji ya matunda na supu ya mchele.
- Kutumia mchanganyiko maalum wa maji, sukari na chumvi yaani “Oral Rehydration Solution” (ORS).
- Kuongeza vitunguu saumu kiasi kwenye vinywaji vya moto kama vile supu na vinginevyo.
- Kula matunda kama ndizi mbivu, tikiti maji na mboga-mboga zilizopikwa ambazo hazina nyuzi-nyuzi nyingi kama karoti na maboga ili kurudisha madini na vitamini zinazopotea kutokana na kuharisha.
- Kula milo midogo midogo mara nyingi kwa siku ili kurudisha virutubishi vinavyopotea na kumwezesha kukidhi mahitaji ya mwili kilishe.
- Kutafuna chakula mpaka kilainike au kula vyakula laini ili kurahisisha uyeyushwaji na hivyo upatikanaji wa virutubishi.
12
- Kutumia maziwa ya mgando au togwa kwani huyeyushwa kwa urahisi na huweza kupunguza kuharisha.
- Kuzingatia kanuni bora za afya ikiwa ni pamoja na usafi na usalama wa chakula na maji.
Vyakula ambavyo mtu anapaswa kuviepuka wakati wa tatizo la kuharisha ni:
- Vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vingi au pilipili nyingi kwani vimeonekana kuzidisha tatizo la kuharisha
- Matunda yasiyoiva vizuri au yenye uchachu mkali kama embe, nyanya, chungwa, chenza, au limau kwani wakati mwingine huweza kuongeza kuharisha.
- Chai, kahawa na soda, kwani vina kafeini ambayo husababisha upotevu zaidi wa maji.
- Pombe kwani huzuia uyeyushwaji na ufyonzwaji wa baadhi ya virutubishi na huongeza upotevu wa maji mwilini.
- Vyakula vyenye nyuzi-nyuzi kwa wingi, kama nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, matunda kama vile papai, embe, parachichi; na mboga-mboga kama vile kabichi, mchicha na matembele. Vyakula hivi huweza kuzidisha tatizo la kuharisha.
5.3.7 Matatizo ya ngoziBaadhi ya matatizo ya ngozi huweza kusababishwa na upungufu wa baadhi ya vitamini hasa Vitamini A na Vitamini B6. Ulaji wa vyakula vyenye Vitamini A au Vitamini B6 kwa wingi huweza kupunguza au kuzuia maradhi hayo, hata hivyo matibabu huweza kuhitajika.
KUMBUKA:Tatizo la kuharisha linapoisha mgonjwa anashauriwa kuendelea kula kama kawaida.
13
Mgonjwa mwenye matatizo ya ngozi anashauriwa kufanya yafuatayo:• KulavyakulavyenyeVitaminiAkwawingikamavilemawese,
maini, kisamvu, matembele, mayai, maziwa, papai, embe na karoti.
Kumbuka kuongeza mafuta wakati wa utayarishaji wa vyakula ili kusaidia ufyonzwaji na upatikanaji wa Vitamini A mwilini.
• Kula vyakula vyenye Vitamini B6 kwa wingi kama vilemaharagwe, mboga za kijani, karanga, mahindi yasiyokobolewa, nyama, samaki, viazi vitamu na parachichi.
5.3.8 Kupumua kwa shidaMgonjwa anashauriwa kufanya yafuatayo:
• Kuongezatangawizinavitunguusaumukatikachakulanavinywajimbalimbali vya moto.
• Kutumiavitunguusaumuvilivyopondwatembetanohadisitakwasiku.
• Kujikanda kifuani kwa kutumia maji yaliyochemshwa natangawizi. Usimkande mtu ambaye ni dhaifu sana au mwenye homa kali.
6.0 MATUMIZI YA DAWA NA CHAKULA
6.1 UtanguliziChakula na dawa huweza kuwa na mwingiliano ambao huwa na faida au hasara. Chakula huweza kuingilia usharabu wa dawa tumboni, usambazwaji wake na pia utoaji wa mabaki ya dawa mwilini. Baadhi ya vyakula huweza kuboresha usharabu na namna dawa inavyofanya kazi na vingine huweza kupunguza.
Kwa upande mwingine, baadhi ya dawa huweza kuingilia usharabu wa virutubishi, matumizi ya virutubishi mwilini na utoaji mabaki mwilini. Tatizo hili linaweza kukabiliwa kwa kuepuka au kupunguza aina ya chakula kinachoingiliana na dawa
14
hiyo mwilini, kuongeza kiasi cha chakula au kutumia virutubishi vya nyongeza ili kuongeza kiwango cha aina ya virutubishi vinavyoathiriwa na dawa hiyo.
Baadhi ya athari zitokanazo na dawa huweza kumfanya mgonjwa ashindwe kula chakula cha kutosha, pia kudhoofisha usharabu wa virutubishi mwilini. Kwa mfano, baadhi ya dawa husababisha kichefuchefu, mabadiliko ya ladha, kukosa hamu ya kula, kutapika n.k.
6.2 Ushauri wa matumizi sahihi ya chakula na dawaMgonjwa anapaswa kuzingatia yafuatayo:
• Kupanga utaratibu wa kumeza dawa na kula chakula kwakuzingatia maelekezo yaliyotolewa na mtaalamu wa afya kuhusu matumizi ya dawa na chakula ili kuepuka kuathiri matibabu na hali ya lishe ya mgonjwa.
• Kuendeleakumezadawakamaalivyoelekezwanamtaalamuwaafya, hata kama amepata nafuu.
• Kutumiamajikumezeadawanasikutumiavinywajikamajuisi,soda, chai au kahawa.
• Kuepukakutumiachaiaukahawamudamfupibaadayakumezadawa.
• Kunywamajisafinasalamakwawingiangalauglasi8kwasikuili kuondoa mabaki yatokanayo na dawa mwilini.
• Kukabiliananaatharizinazowezakusababishwanamatumiziyadawa kama vile kichefuchefu, kutapika, kuharisha, n.k. Rejea kipengele cha Tano ya kitabu hiki kuhusu jinsi ya kukabiliana na athari hizo.
KUMBUKA:• Dawailiyoelekezwakumezwakablayakulachakulaimezwesaa
moja kabla ya kula au saa mbili baada ya kula.• Mudawakumezadawaugawanywekatikasikunzimaambayoni
saa 24. Kwa mfano, dawa iliyoelekezwa kumezwa mara tatu kwa siku, imezwe kila baada ya saa 8; na ile iliyoelekezwa kumezwa mara mbili kwa siku, imezwe -kila baada ya saa 12. Hali kadhalika, dawa iliyoelekezwa kumezwa mara nne kwa siku, imezwe kila baada ya saa 6.
15
• Kuepukamatumiziyapombe,tumbakunabidhaazakenamadawaya kulevya.
• Kumuonamtaalamuwaafyaiwapoatharizitokanazonamatumiziya dawa zitazidi.
7.0 MAMBO YA KUZINGATIA KWA MGONJWA WA KIFUA KIKUU
• Kupatamatibabusahihikutokakatikakituochatibanakutimizamasharti yote aliyopewa na mtaalam wa afya;
• Kulamlokamili;• Kufuata ulaji unaoshauriwa wakati wa matatizo mbalimbali ya
kiafya;• Kupatamudawakupumzika;• Kujenga tabia ya kutafuta taarifa kuhusu afya kwa kusoma
vijarida, kusikiliza redio na kuhudhuria vipindi vya elimu ya afya katika kituo cha huduma au katika jamii; na
• Kuepukamatumiziyapombenasigara.
8.0 BIBLIOGRAFIA
COUNSENUTH; Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI; Kitabu cha Mafunzo na Rejea, 2004
COUNSENUTH and APHFTA; Ulaji na Mtindo Bora wa Maisha: Kitabu cha Wanafunzi wa Shule za Msingi , 2008
Ministry of Health and Social Welfare; Manual of the National Tuberculosis and Leprosy Programme in Tanzania, 2006
NACP; Kifua Kikuu na UKIMWI: Ujumbe Muhimu kwa Jamii, Dar –es-Salaam 2008
PATH TB/HIV Project; Kifua Kikuu/UKIMWI Mahali Po Pote Pale ni Kifua Kikuu/UKIMWI Kila Mahali
Ramakrishna Mission Tuberculosis Sanatorium; The Role of Nutrition in Tuberculosis, 2007
USAID –Africa’s Health in 2010; Nutrition and Tuberculosis: A Review of the Literature and Considerations for TB Control Programs, USAID, Washington 2008
Wizara ya Afya; Mwongozo wa Matibabu ya Wagonjwa wa Kifua Kikuu Majumbani, 2005
Wizara ya Afya; Kifua Kikuu (TB) ni Ugonjwa Hatari: Fahamu Ukweli Kuhusu Kifua Kikuu
16
Ain
aU
muh
imu
BA
AD
HI
YA
VIR
UT
UB
ISH
I, U
MU
HIM
U N
A V
YA
NZ
O V
YA
KE
9.0
VIA
MB
AT
AN
ISH
O
Hup
atik
ana
kwa
win
gi k
wen
ye:
Kab
ohai
dret
i
Vita
min
i B2
Vita
min
i B1
Prot
ini
Maf
uta
Vita
min
i A
Mah
indi
, mch
ele,
nga
no, u
wel
e, m
tam
a,
ulez
i, ai
na z
ote
za v
iazi
, mih
ogo,
mag
imbi
, nd
izi,
asal
i, su
kari
Maz
iwa,
nya
ma,
mbo
ga z
a ki
jani
, naf
aka
zi-
sizo
kobo
lew
a, s
amak
i, m
ahar
agw
e, k
aran
ga,
koro
sho
Naf
aka,
mah
arag
we,
nya
ma,
sam
aki,
kuku
, m
ayai
, kar
anga
, kor
osho
Ain
a zo
te z
a ny
ama,
ain
a zo
te z
a m
ikun
de,
sam
aki,
daga
a, w
adud
u, m
aziw
a, ji
bini
, may
ai
Siag
i, m
afut
a ya
sam
aki,
sam
li, m
afut
a ya
ny
ama,
mbe
gu z
itoaz
o m
afut
a ka
ma
kara
nga,
al
izet
i, m
awes
e, u
futa
, kw
eme,
kor
osho
, m
begu
za
mab
oga
Mai
ni, m
boga
za
kija
ni, f
igo,
may
ai, s
amak
i, jib
ini,
siag
i, vi
azi v
itam
u (h
asa
vya
man
jano
),
mab
oga,
kar
oti,
maw
ese
na m
atun
da h
asa
yeny
e ra
ngi y
a m
anja
no a
u ny
ekun
du k
ama
papa
i na
embe
Huu
pa m
wili
ngu
vu z
a ku
fany
a ka
zi n
a jo
to
linal
otak
iwa
Hus
aidi
aum
etab
oli w
a ni
shat
i-lis
he, h
usai
dia
mac
ho k
uona
viz
uri n
a hu
bore
sha
ngoz
i
Hus
aidi
a um
etab
oli w
a ni
shat
i-lis
he m
wili
ni, h
uong
eza
ham
u ya
kul
a na
hus
aidi
a m
fum
o w
a fa
ham
u
Uku
aji w
a m
wili
na
kute
ngen
eza
vim
eng’
enyo
, vi
choc
heo
na s
eli z
a m
wili
Huu
pa m
wili
ngu
vu, j
oto
na k
usai
dia
uyey
ushw
aji n
a us
hara
bu w
a ba
adhi
ya
viru
tubi
shi
Uku
aji w
a ak
ili n
a m
wili
, hui
mar
isha
che
mbe
ch
embe
za
king
a ya
mw
ili n
a hu
said
ia m
acho
ku
ona
vizu
ri
17
Vita
min
i B3
Vita
min
i D
Vita
min
i E
Mad
ini C
hum
a
Vita
min
i B6
Vita
min
i B12
Vita
min
i C
Maz
iwa,
may
ai, n
yam
a, k
uku,
kar
anga
, sa
mak
i, m
ahar
agw
e, n
afak
a zi
sizo
kobo
lew
a
Kiin
i cha
yai
, sam
aki h
asa
wen
ye m
afut
a,
maz
iwa,
sia
gi n
a m
ionz
i ya
jua
Mbo
ga z
a ki
jani
, maf
uta
yato
kana
yo n
a m
imea
, mai
ni, k
iini c
ha y
ai n
a ai
na n
ying
ine
za m
boga
-mbo
ga
Nya
ma
nyek
undu
, sam
aki,
may
ai, a
ina
za
mik
unde
kam
a ka
rang
a, m
ahar
agw
e, b
aadh
i ya
mat
unda
yal
iyok
aush
wa,
mbo
ga z
a m
ajan
i za
kija
ni n
a ba
adhi
ya
nafa
ka
Via
zi v
itam
u, m
ahar
agw
e, m
ahin
di,
para
chic
hi, n
yam
a, s
amak
i, ka
bich
i
Nya
ma,
sam
aki,
kuku
, jib
ini,
may
ai, m
aziw
a,
vyak
ula
viliv
yoch
achu
shw
a (f
erm
ente
d)
kam
a m
tindi
na
togw
a
Map
era,
mac
hung
wa,
nya
nya,
ukw
aju,
m
alim
au, n
dim
u, m
ache
nza,
mad
alan
si,
ubuy
u, k
arak
ara
(pes
heni
), m
abun
go, n
a ai
na
nyin
gine
za
mat
unda
Hub
ores
ha n
gozi
, hus
aidi
a ka
tika
umet
abol
i wa
nish
ati-
lishe
, mfu
mo
wa
chak
ula
na f
aham
u
Huw
ezes
ha u
fyon
zwaj
i wa
mad
ini y
a ch
okaa
na
fosf
oras
i. H
utum
ika
katik
a ku
teng
enez
a m
ifup
a na
men
o. H
uim
aris
ha m
fum
o w
a fa
ham
u na
hu
wez
esha
moy
o ku
fany
a ka
zi v
izur
i.M
uhim
u ka
tika
king
a ya
mw
ili n
a ka
tika
kute
ngen
eza
na u
kuaj
i wa
seli
za m
wili
Huz
uia
chem
bech
embe
za
dam
u zi
siha
ribi
we,
hu
zuia
mw
ili u
sipa
twe
na m
agon
jwa
Hus
afir
isha
hew
a ya
oks
ijeni
kw
enye
dam
u,
huon
doa
chem
bech
embe
nye
kund
u za
dam
u zi
lizoc
haka
a au
kuh
arib
ika
na k
uten
gene
za
nyin
gine
Hus
aidi
a us
hara
bu n
a ut
umik
aji w
a m
afut
a na
pr
otin
i, hu
said
ia k
uten
gene
za c
hem
bech
embe
ny
ekun
du z
a da
mu
Hut
enge
neza
che
mbe
chem
be z
a da
mu
na s
eli z
a ne
va
Muh
imu
kwa
king
a ya
mw
ili n
a hu
said
ia u
sh-
arab
u w
a m
adin
i ya
chum
a
18
Mad
ini y
a C
hoka
a
Mag
nesi
a
Sele
niam
Zin
ki
Mad
ini J
oto
Maz
iwa,
may
ai, n
yam
a, k
uku,
kar
anga
, sa
mak
i, m
ahar
agw
e, n
afak
a zi
sizo
kobo
lew
a
Naf
aka,
mbo
ga z
a ki
jani
, vya
kula
vya
ba
hari
ni, j
amii
ya m
ikun
de, k
aran
ga
Cha
nzo:
Im
ebor
eshw
a na
kut
afsi
riw
a ku
toka
Net
wor
k of
Afr
ican
Peo
ple
Liv
ing
wit
h H
IV/A
IDS,
200
9
Nya
ma,
sam
aki,
kuku
, jib
ini,
may
ai, m
aziw
a,
vyak
ula
viliv
yoch
achu
shw
a (f
erm
ente
d)
kam
a m
tindi
na
togw
a
Nya
ma,
kuk
u, s
amak
i, na
faka
na
mbo
ga-
mbo
ga
Sam
aki,
vyak
ula
ving
ine
vya
baha
rini
, ch
umvi
iliy
owek
wa
mad
ini y
a jo
to
Hub
ores
ha n
gozi
, hus
aidi
a ka
tika
umet
abol
i wa
nish
ati-
lishe
, mfu
mo
wa
chak
ula
na f
aham
u
Hui
mar
isha
mis
uli,
muh
imu
katik
a m
fum
o w
a fa
ham
u, u
kuaj
i na
huim
aris
ha m
ifup
a na
men
o
Huz
uia
kuha
ribi
ka k
wa
mis
uli y
a m
oyo
Hus
aidi
a ki
nga
ya m
wili
, hus
aidi
a uy
eyus
hwaj
i w
a ch
akul
a na
usa
firi
shw
aji w
a V
itam
ini A
Uku
aji,
husa
idia
ubo
ngo
na m
fum
o w
a fa
ham
u ku
fany
a ka
zi v
izur
i
Kijarida hiki kimetayarishwa na:
The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care (COUNSENUTH)
United Nations Rd./Kilombero Str.Plot No. 432, Flat No. 3
P.O Box 8218, Dar es Salaam, Tanzania.Tel/Fax: +255 22 2152705, Cell: +255 755 165112
Email: [email protected]
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:Mkurugenzi Mtendaji
The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care (COUNSENUTH)
ISBN 978-9987-9017-8-4
© COUNSENUTH, 2008
Kimefadhiliwa na:
GLOBAL FUND ROUND 4 PROGRAM
Designed &Printed by:DeskTop Productions Limited
P.O Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania.