lishe na ulaji bora kwa watu wanaoishi na virusi vya...

18
COUNSENUTH Information series No. 6 Toleo la Kwanza, March, 2004 Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upload: others

Post on 14-Jan-2020

34 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

C O U N S E N U T H

I n f o rmation series No. 6Toleo la Kwanza, March, 2004

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi naVirusi vya UKIMWI

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page i

Page 2: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

1

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na

Virusi vya UKIMWI

ISBN 9987-8936-7-8

© C O U N S E N U T H , 2004

MATUMIZI YA VIUNGO VYA VYAKULAKATIKA KUBORESHA LISHE NA AFYA

K i m e t aya ri s h wa na:Center for Councelling,N u t rition and Health Care

(COUNSENUTH) n a

Ku fa d h i l i wa na: M p a n go wa Ta i fa wa kudhibitiUKIMWI ( NACP) - Wi z a ra ya A f ya

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 1

Page 3: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

ShukraniKituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) kinatoa

shukrani za pekee kwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP)

kwa kufadhili utayarishaji na uchapishaji wa kijitabu hiki.

Shukrani za dhati kwa WAMATA, TAHEA, SHDEPHA+, NACP na watu

binafsi walioshiriki katika kutayarisha na kuboresha kijitabu hiki.

Asanteni sana.

2

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 2

Page 4: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

3

UTANGULIZIHali bora ya lishe huchangia katika kuongeza ubora wa afya na maishaya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI. Pamoja na ulaji wa chakulamchanganyiko na cha kutosha, viungo mbalimbali vimeonekana piakusaidia kuboresha lishe na afya. Hata kabla ya ugonjwa wa UKIMWI,viungo vimekuwa vikitumika katika mapishi mbalimbali ili kuongezaubora wa chakula na hivyo kuchangia katika kuboresha lishe na afya yamtu yeyote.

Viungo hutokana na sehemu fulani ya mmea kama majani, mizizi,maua, mbegu au magome. Viungo huweza kuongezwa katika chakula ilikukipa ladha nzuri hivyo kuongeza hamu ya kula. Viungo huweza piakusaidia uyeyushwaji wa chakula na usharabu (ufyonzwaji) wavirutubishi mbalimbali. Baadhi ya viungo huweza kutumika kuhifadhibaadhi ya vyakula ili visiharibike mapema. Wakati mwingine viungohuweza kutumika katika kutuliza au kutibu baadhi ya matatizo madogomadogo ya afya kama kichefuchefu, fangasi, kutapika, kuharisha, mafuaau flu.

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI hukabiliwa na matatizombalimbali yakiwemo kukosa hamu ya kula, uyeyushwaji duni wachakula na usharabu (ufyonzwaji) duni wa virutubishi. Matumizi yaviungo mbalimbali kwa kiasi yameonekana kupunguza baadhi yamatatizo hayo.

Kijarida hiki kimeweka pamoja taarifa zilizopo hivyo kumpa mtuchaguo kubwa ili aweze kutumia vile viungo anavyovipata kwa urahisi.Kijarida hiki kinazungumzia matumizi ya kawaida ya viungo kamasehemu ya mlo na katika kupunguza makali ya baadhi ya matatizo.

Baadhi ya watu baada ya kusikia kwamba viungo vinasaidia, wamekuwawakivitumia kwa kiasi kikubwa mno na wakati mwingine kuwaleteamatatizo. Ni muhimu kutumia viungo kwa kiasi, katika mapishi yakawaida au katika vinywaji kama inavyoshauriwa.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 3

Page 5: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

4

MSAMIATI

• Kinywaji cha viungo:

Hiki ni kinywaji chochote ambacho kimetengenezwa kwa kuwekwaviungo. Kinywaji hiki kinaweza kuwa cha moto au cha baridi. Kinywajicha baridi kinapotengenezwa, yatumike maji yaliyochemshwa.

• Chai:

Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto namajani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa.

Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita“chai” hata kama havina majani ya chai. Ukweli ni kwamba chai ni yalemajani ya chai. Katika kijitabu hiki vinywaji vya viungo havikuitwa chai.

BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDAZAKE

Kitunguu saumu (Garlic)

Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizimbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo maranyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenyerangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogona nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.

Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengikama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayona bakteria, baadhi ya virusi na fangasi hasakatika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni.Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula,kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani,maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 4

Page 6: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

5

Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai aukinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguusaumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sitakwa siku hasa kama vitatumika vibichi .

Tangawizi (Ginger)

Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea watangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa

kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z iinaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa.Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au

kwenye chakula.

Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula,kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha,

maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidiauyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa

matatizo ya mafua au flu.

Iliki (Cardamom)

Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazohutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwaau kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula aukatika vinywaji.

Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu,kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwajiwa chakula na huongeza hamu ya kula.

Mdalasini (Cinnamon)

Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome yammea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwaau kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini

h u weza kuongezwa kwe n ye chakula au katikavinywaji vilivyochemshwa au baridi.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 5

Page 7: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

6

Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu,vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hikihuongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizokatika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha.

Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini natangawizi kinaweza kutuliza kikohozi.

Giligilani (Coriander)

Giligilani ni aina ya kiungo ambachomajani na mbegu zake huwez akutumika kama kiungo katika mapishiya vyakula mbalimbali kama nyama,supu au mchuzi.

Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula nakupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi

ya bakteria na fangasi.

Kotimiri (Parsley)

Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbeguzake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula.Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto watumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha.Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng’ e n yotumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa.

Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji yaziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwakatika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.

Karafuu (Cloves)

Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungohiki huweza kutumika peke yake au kwakuchanganya na viungo vingine. Kiungo hikihusaidia kuleta hamu ya kula na kubore s h a

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 6

Page 8: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

7

uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguzakichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenyeuvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa.

Binzari (Turmeric/Yellow Root)

Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzarimanjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi yabinzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza

unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kamakiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi

inaweza kutwangwa na kutumika kwenyemapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katikachakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano.Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au

vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi aumaharagwe.

Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwiliusiharibiwe na kemikali mbaya.

Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwaniwakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi.Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina zaunga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano nabinzari kidogo.

Limau (Lemon)

Limau linaweza kutumika kama kiungo katikachakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine.

Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa waprotini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidondavya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 7

Page 9: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

8

Binzari nyembamba (Cumin seeds)

Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu zagiligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga

ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbalimfano; supu, mchuzi, wali, n.k.

Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguzamaumivu ya tumbo na hata kuharisha.

Mrehani (Basil)

Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwakuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia

kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwajiwa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. Kwa

vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumikakwa kusukutua.

“Calendula”

Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuiakukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na piakupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatoryfunction). Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizimbalimbali katika mfumo wa chakula.

‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inawez akutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwajiwa chakula tumboni.

Pilipili (Cayenne)

“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamiiijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na

nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina ranginyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa nakusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwana rangi nyekundu.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:34 PM Page 8

Page 10: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

9

“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inawezaikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupikaau wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au majiya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi.

Shamari (Fennel)

Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzarinyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na

kupunguza gesi tumboni.

Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenyechakula. Mbegu za shamari zinawez a

kutumika kuandaa chai au kinywaji chochotecha moto.

Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.

Nanaa (Mint)

Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo.Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto

tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika nakuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo namkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika

uyeyushwaji wa chakula tumboni.

Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inawez akutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji chamoto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani.

Meti (Methi)

Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza“Fenugreek”. Hii ni aina ya kiungo ambachohuchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaaniumetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwana kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa

mabichi. Vilevile mbegu za “Fenugreek” huweza

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 9

Page 11: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

10

kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungoyaani “curry powders”. Meti inaweza kutumika kama kiungo katikavyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevilekatika mapishi mbalimbali ya samaki.

“Thyme”

‘‘T h y m e’’ inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa nabakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguzakikohozi na kulainisha koo. Zaidi ya hayo “thyme” husaidiaukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wachakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto aukusukutua.

JINSI YA KUTAYARISHA BAADHI YAVINYWAJI VYA VIUNGO

Kinywaji cha mdalasini

Mahitaji:• Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini;• Kikombe kimoja cha maji safi.

Matayarisho:• Chemsha maji vizuri, na kisha ongeza unga

wa mdalasini;• Baada ya hapo unaweza kuongeza asali au sukari

kidogo ili kuongeza ladha;• Na hapo kinywaji ni tayari; kinaweza kunywewa muda wowote.

Kinywaji cha tangawizi

Mahitaji:• Kikombe kimoja cha maji;• Kijiko kimoja cha tangawizi mbichi

iliyopondwa;• Sukari kidogo.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 10

Page 12: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

11

Matayarisho:• Osha tangawizi na ponda ponda;• Changanya tangawizi na kikombe kimoja cha maji safi;• Chemsha mchanganyiko huo ukiwa umefunikwa;• Acha kwenye moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10;• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda);• Kinywaji ni tayari.

Kinywaji cha kitunguu saumu

Mahitaji:• Tumba 3 hadi 4 za kitunguu saumu

kilichopondwa au kukatwa vipande vidogovidogo;

• Kikombe kimoja cha maji safi;• Asali au sukari kidogo.

Matayarisho:• Chemsha maji vizuri;• Ongeza kitunguu saumu kilichopondwa au kukatwa vipande vidogo

vidogo, kwe n ye maji yanayochemka, funika na kisha achamchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 10;

• Ipua na acha mchanganyiko huo upoe;• Unaweza kuongeza asali au sukari ili kuongeza ladha;• Kinywaji ni tayari.

Kinywaji cha tangawizi na mdalasini

Mahitaji:• Nusu ( ) kijiko cha chai cha tangawizi mbichi

iliyopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo;• Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini;• Kikombe kimoja cha maji safi.

Matayarisho:

• Chemsha maji kisha ongeza tangawizi, funika na achavichemke kwa dakika 10;

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 11

Page 13: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

12

• Baada ya hapo ongeza unga wa mdalasini na acha mchanganyikohuo uchemke kwa muda wa dakika 5 zaidi;

• Ipua na kisha chuja kinywaji hicho. Sasa kinywaji ni tayari kwakutumia;

• Unaweza kuongeza sukari kidogo ili kuongeza ladha.

Kinywaji cha Limau

Mahitaji:• Limau moja;• Nusu ( ) kikombe cha maji safi;• Sukari kidogo.

Matayarisho:• Osha limau kwa maji safi kisha kamua ili kupata maji ya limau;• Chemsha maji vizuri;• Ongeza maji ya limau kwenye maji hayo;• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda);• Ni vizuri kunywa kinywaji hiki kingali cha moto.

Kinywaji cha Nanaa (Mint)

Mahitaji:

• Majani ya nanaa;• Kikombe kimoja cha maji safi;• Sukari kidogo (kama unapenda).

Matayarisho:• Osha nanaa vizuri na kisha katakata vipande

vidogo vidogo;• Weka vipande hivyo kwenye kikombe;• Chemsha maji vizuri na ongeza maji hayo kwenye kikombe chenye

nanaa;• Funika vizuri na acha kwa dakika 5.• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda) na sasa kinywaji ni tayari.

Kumbuka kutumia vyombo safi na maji safi na salama wakati wote.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 12

Page 14: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

13

HITIMISHOInashauriwa kutumia viungo mbalimbali kwa kiasi ili kuepuka madharayanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi yaliyozidi kiasi. Hatahivyo bado hakuna ushahidi wa kitaalamu wa kutosha kuonyesha ni jinsigani viungo vinaweza kutibu baadhi ya matatizo yanayoambatana nakuishi na virusi vya UKIMWI. Taarifa nyingi kuhusu namna viungovinavyoweza kupunguza matatizo mbalimbali zimetokana na ripotiz i l i zo t o l ewa na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambaowamejaribu kutumia viungo hivyo na kuona vinasaidia. Mtu anayeishina virusi vya UKIMWI anapoamua kutumia viungo kama tibaanashauriwa kujaribu na kuona kama vinamsaidia.

Baadhi ya viungo kama vile nanaa, kitunguu saumu, tangawizi, binzarimanjano na vinginevyo vinaweza kuoteshwa nyumbani katika bustanindogondogo au vyombo kama makopo, madebe au vyungu na hivyokurahisisha upatikanaji wake.

Ikumbukwe kuwa viungo vitachangia kuboresha afya na lishe ya mtuyeyote kwa kuboresha uyeyushwaji wa chakula na usharabu (ufyonzwaji)wa virutubishi mbalimbali vilivyomo kwenye chakula. Zaidi ya hayoviungo huongeza ladha nzuri kwenye chakula na hivyo kumwezesha mtuale chakula cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya mwili.

Viungo vingi vinaweza kuoteshwa katika bustani za nyumbani.Baadhi ya vungo ambavyo mimea yake ni midogo huweza

kuoteshwa katika vyombo kama makopo, madebe au vyungu.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 13

Page 15: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

14

VYANZO1. Bijlsma, M., Living Positively: Nutrition guide for People with

HIV/AIDS, Muntare City Health Department, Zimbabwe, SecondEdition, 1997.

2. COUNSENUTH, Nutritional Care for PLHA: Training andReference Manual (DRAFT), September, 2003.

3. Davidson S., Passmore R., Brock J.F., Truswell A. S,. HumanNutrition and Dietetics; Seventh Edition. Wilture Enterprises,(International) Ltd. 1979.

4. FAO, Living Well With HIV/AIDS, A manual on nutritional careand support for people living with HIV, 2002.

5. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), HIV/AIDS: AGuide for Nutrition, Care and Support. Academy for EducationalDevelopment, Washington DC, 2001.

6. http://webhost.sun.ac.za/nicus/Factsheets/HIV_alternative_diet_therapy.htm

7. Ministry of Health, The United Republic of Tanzania. A NationalGuide on Nutrition Care and Support for People Living withHIV/AIDS, TFNC (DRAFT), May, 2003.

8. Morris, S. and Macklley, L. The Spice Ingredients cookbook. LorenzBooks. 1997.

9. The Netwok of African people living with HIV/AIDS (NAP+).Food for people living with HIV/AIDS, July, 1996.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 14

Page 16: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

15

VIJITABU VINGINE KUHUSU LISHE NA ULAJI BORAKWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

VILIVYOTOLEWA NA COUNSENUTH

1. Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI:“Vidokezo muhimu”, COUNSENUTH Information series No.2, Toleo la Pili, January, 2004.

2. Lishe na Ulaji bora kwa Watu Wanaoishi na Vi rusi vyaUKIMWI: “Maswali yanayoulizwa mara kwa mara” ,COUNSENUTH Information series No. 3, Toleo la Pi l i ,January, 2004.

3. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Vi rusi vyaUKIMWI: “Vyakula vinavyoboresha uyeyushwaji wa chakula nau f yonzwaji wa virutubishi mwilini”, COUNSENUTHInformation series No. 4, March, 2003.

4. Ulishaji wa Mtoto Mchanga kwa Mama mwenye Virusi vyaUKIMWI: “Vi d o k ezo Muhimu kwa Washauri Na s a h a” ,COUNSENUTH Information series No. 1, Toleo la Pi l i ,January, 2004.

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 15

Page 17: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

16

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 16

Page 18: Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWIcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na-Ulaji-Bora-kwa-Watu-wanaoishi-na...C O U N S E N U T H I n f o r mation

17

ISBN 9987-8936-7-8

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:M k u r u g e n z i

Kituo cha Ushauri Nasaha,Lishe na A f ya( C O U N S E N U T H )

S . L . P. 8218, Dar es Salaam,Ta n z a n i a

Simu: (22) 2152705 au 0744 279145Fax: (22) 2152705

Kijarida hiki kimetayarishwa na kutolewa na:

The Centre for Counselling, N u t rition and Health Care( C O U N S E N U T H )

United Nations Rd./ Kilombero Str.Plot No. 432, Flat No.3

P.O. Box 8218, Dar es Salaam Ta n z a n i a .

Kimefadhiliwa na:

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI

S. L. P 11857

Dar es Salaam, Ta n z a n i a .

Designed & printed by:

Desktop Productions LimitedP.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania

matumizi ya viungo a5.qxd 1/7/05 2:35 PM Page 17