maelezo mafupi kuhusu halmashauri...4 (ii) afya manispaa ya temeke ina vituo 117 vya kutolea huduma...
TRANSCRIPT
1
SURA YA 1
1.0 MAELEZO MAFUPI KUHUSU HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
1.1 ENEO
Temeke ni mojawapo ya Halmashauri tano zinazounda Jiji la Dar es
Salaam. Manispaa nyingine ni Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni.
Manispaa ya Temeke ina eneo la kilometa za mraba 240 na ukanda wa
Pwani wa kilometa 5. Aidha ipo katika nyuzi 39012’ – 39033’ Mashariki na
nyuzi 6048 – 7033 Kusini. Temeke ipo upande wa kusini mwa Jiji la Dar es
Salaam ambapo kwa upande wa Mashariki inapakana na Bahari ya
Hindi, Kusini inapakana na Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani na
upande wa Kaskazini na Magharibi inapakana na Manispaa ya Ilala.
1.2 HALI YA HEWA
Kwa ujumla Manispaa ya Temeke ina joto sana katika miezi ya Januari,
joto hufikia nyuzi joto 350 C na miezi ya Juni hadi Agosti hufikia wastani wa
nyuzi joto 250C Halmashauri ya Manispaa ya Temeke hupata misimu miwili
ya mvua. Mvua za vuli ambazo hunyesha miezi ya Oktoba hadi Novemba
na mvua za Masika ambazo hunyesha miezi ya Februari hadi Mei.
1.3 IDADI YA WATU
Kulingana na sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya
Temeke ilikuwa na jumla ya watu 1,205,949 na Kaya 307,760. Kati yao
wanaume walikuwa 587,857 na wanawake walikuwa 618,092. Hadi kufikia
mwaka huu 2016, Manispa ya Temeke inakisiwa kuwa na watu wapatoa
1,443,629 na Kaya 368,416. Kati yao wanaume ni 703,718 na wanawake ni
739,912
1.4 UTAWALA
MUUNDO WA KIUTAWALA
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina jumla ya Idara kumi na tatu (13)
na vitengo sita (6).
Kiutawala Manispaa ya Temeke imegawanyika kama ifuatavyo:
Tarafa Kata Mitaa Majimbo ya uchaguzi
2 23 142 2
1.5 HALI YA UKUSANYAJI WA MAPATO
Makusanyo ya Mapato yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka
kutokana na mikakati na malengo ya Halmashauri iliyojiwekea. Hii ni
pamoja na kutoa elimu kwa walipa Kodi, ada na ushuru mbalimbali na
matumizi ya mfumo wa GIS kwa ajili ya kukusanya takwimu za kodi za
mabango na huduma za jiji.
2
Makusanyo halisi kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2005 – Desemba 2016 ni
kama inavyoonekana hapo chini:-
MWAKA
LENGO LA
UKUSANYAJI UKUSANYAJI HALISI ASILIMIA
2005/2006 3,642,725,473.00 3,891,025,346.00 106.8
2006/2007 4,826,572,438.00 5,139,541,243.93 106.5
2007/2008 6,500,000,000.00 6,355,969,906.50 97.8
2008/2009 8,287,570,000.00 8,014,437,464.00 96.7
2009/2010 10,171,334,000.00 9,010,647,663.00 88.6
2010/2011 13,430,142,228.00 12,059,617,942.00 89.8
2011/2012 19,021,938,341.00 14,339,934,927.00 75.4
2012/2013 22,437,551,883.00 25,175,053,009.00 112.2
2013/2014 25,243,405,600.00 27,441,013,080.00 108.7
2014/2015 31,721,802,500.00 32,073,794,332.00 101.1
2015/2016 38,553,189,000.00 31,967,414,712.00 82.9
2016/2017 42,227,364,000.00 11,133,739,556.29 26.4
Makusanyo ya mwaka 2016/2017 hadi Disemba 2016.
1.6 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA HALMASHAURI
1.6.1 HUDUMA ZA JAMII
(i) ELIMU
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina jukumu la kutoa elimu kuanzia shule
za awali, msingi, Sekondari na Elimu ya watu Wazima. Aidha utoaji wa Elimu
kwa ujumla ni jukumu la Halmashauri, chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Katika utekelezaji wa majukumu yake Halmashauri inao watendaji 17 katika
Idara ya Elimu ya Msingi (Makao makuu) 12 walimu na 9 wasio walimu.
(a) ELIMU YA AWALI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina shule/vituo vya awali 132 kati ya
hivyo 83 ni vya Serikali na 49 visivyo vya Serikali. Vituo vyote hivi vina jumla ya
wanafunzi 9601, kati yao wavulana ni 4346 na wasichana 5255, vituo vya
serikali vina jumla ya wanafunzi 7326 wakiwemo wavulana 3217 na
wasichana 4109 na vituo visivyo vya serikali vina jumla ya watoto 2275 kati yao
wavulana ni 1129 na wasichana 1146. Jumla ya walimu katika shule za awali ni
132 wanaume 26 na wanawake 106.
3
(b) ELIMU YA MSINGI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina shule za Msingi zipatazo 127, kati ya
hizo 83 ni za Serikali, na 44 zisizo za Serikali. Ikiwa na jumla ya wanafunzi
172,002, wakiwemo wavulana ni 84,229, na wasichana ni 87,773. Idadi ya
Walimu ni 3,357 kati ya yao Wanaume ni 576 na Wanawake ni 2,781.
Jumla ya Walimu 126 wanajiendeleza katika hatua mbalimbali za Elimu ili
kuweza kuinua kiwango cha taaluma na kupanua uwezo wao kitaaluma.
Aidha kupitia mpango wa MWAKEM unaofadhiliwa na Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Chuo cha Ualimu Vikindu pamoja na Unicef walimu 520
kutoka katika shule 20 wameweza kusoma Moduli za masomo ya ujuzi,
Hisabati na English na kufaulu vizuri katika masomo hayo. Walimu wamepata
ujuzi mpya wa kufundisha kupitia mhamo wa Luwaza.
(c) ELIMU YA WATU WAZIMA
Halmashauri ya Manispaa inafanya juhudi ya kupunguza ujinga wa kutojua
kusoma na kuandika kwa watu wazima, Vijana na watoto waliokosa Elimu ya
Msingi kwa sababu moja au nyingine na pia kuwapatia stadi
zitakazowawezesha kuinua kiwango cha mapato ili waweze kujitegemea na
kujiajiri kupitia vikundi vya uzalishaji mali. Wapo jumla ya wanakisomo 67
walimu 17 na madarasa 10 ya kisomo chenye manufaa. Aidha kuna
madarasa ya MEMKWA yenye jumla ya wanafunzi 1301 walimu 50 na vituo
vipo 15.Utaratibu huu unawasaidia watu wazima na wale watoto waliokosa
elimu ya msingi MEMKWA kufuta ujinga kwa wasio jua kusoma, kuhesabu na
kuandika, kuwajengea uwezo wananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji
mali na kutambua haki zao za msingi katika jamii anamoishi na kuwajengea
uwezo wa kukaa pamoja kubuni miradi kulingana na mazingira yao.
(d) ELIMU YA SEKONDARI
Halmashauri ina jumla ya shule za Sekondari 26 za serikali na 35 zisizo za
serikali, zenye jumla ya wanafunzi 34,459 wakiwemo wavulana 16,124 na
wasichana 18,335 wanasoma katika shule za serikali na Wanafunzi 11,531
wanaosoma shule zisizo za Serikali, kati yao wavulana 6,286 na wasichana
5,245.
Ina jumla ya walimu 1285 katika shule za serikali wakiwemo Wanaume 440 na
wanawake 845 na Walimu wasio serikali 789 kati yao Wanaume 621
wanawake 168. Walimu wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari za
serikali wapo 239 na wa masomo mengine wapo 1,046. Upo upungufu wa
walimu wa biashara 84 na masomo ya sayansi 274. Upungufu wa nyumba
za walimu 1,274, vyumba vya madarasa 290, na majengo ya utawala 18.
4
(ii) AFYA
Manispaa ya Temeke ina vituo 117 vya kutolea huduma za afya kati ya hivi
23 ni vya Serikali na 94 ni vya binafsi. Kuna hospitali 5 ambapo 3 ni za Serikali
nazo ni Temeke, Rangitatu na Police barracks na Hospitali 2 ni za binafsi
nazo ni TOH na Walter Hospital, vituo vya afya 12, ambapo 2 ni vya Serikali
navyo ni Round table na Yombo vituka, na vilivyobaki 10 ni vya binafsi na
mashirika.
(iii) UKIMWI
Mapambano dhidi ya UKIMWI yameendelea kupewa kipaumbele ambapo
jumla ya vituo 66 vinatoa ushauri Nasaha (VCT), Aidha kuna Vituo 36
vinavyotoa huduma ya kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka
kwa Mama kwenda kwa Mtoto.
(iv) MAJI
Wakazi wa Manispaa ya Temeke wanapata huduma ya maji kutoka katika
vyanzo vya Maji ya visima na Mtandao wa mabomba ya DAWASA, visima
virefu 232 na maji mengine kutoka katika chanzo cha Mto Kizinga kilichopo
Mtoni. Kati ya kata 23, kata 10 zina mitandao ya mabomba ya DAWASCO
na visima virefu(Tandika, Sandali, Azimio, Temeke, Keko,Chang’ombe,
Kurasini, Miburani, Mtoni na sehemu kidogo ya kata ya kijichi).
Aidha Kata 13 zinamahitaji halisi ya maji ni kiasi cha lita za ujazo 115.5
milioni kwa siku wakati kiasi halisi kinachopatikana ni lita za ujazo 75.2 milioni
kwa siku sawa na asilimia 65.28% tu ya mahitaji ya wakazi wa Manispaa ya
Temeke kwa matumizi ya aina zote, wakazi, Viwanda na shughuli nyingine
za kiuchumi na kijamii.
(v) USAFISHAJI
Kata zote 23 zinakadiriwa kuzalisha wastani wa tani 1,344 kwa siku, kwenye
makazi ya watu na tani 150 huzalishwa kila siku kwenye masoko, ambapo,
taka hizo huondolewa na magari ya Manispaa na magari ya kukodi ya
wakandarasi. Uwezo wa kuzoa taka wa magari ya halmashauri kwa
kushirikiana na wakandarasi na taasisi binafsi ni wastani wa tani 659 kwa
siku ambazo ni sawa asilimia 49% ya taka zinazozalishwa kila siku. Hivyo
bado kuna wastani wa tani 685 ambazo ni sawa na asilimia 51% ya taka
zinazozalishwa kwa siku hazikupata udhibiti rasmi.
1.6.2 HUDUMA ZA KIUCHUMI
(i) KILIMO
Halmashauri ya manispaa ya Temeke , sekta ya kilimo imekuwa ndio
msingi mkubwa wa kukuza kipato na chakula kwa familia na jamii kwa
ujumla, zaidi ya kaya 6118 zenye wakulima 11270 wanajishughulisha na
kilimo kwenye eneo la hekta 1000. Mazao yanayolimwa ni mpunga, hekta
5
250, mhogo hekta 20, mboga na matunda 450.hivyo asilimia kubwa ya
chakula katika maeneo ya mjini kinaingizwa kutoka nje ya mkoa.
Uzalishaji wa mboga unachangia zaidi ya asilimia 75 ya mboga zote
zinazoliwa katika halmashauri yetu. Huduma za ugani zinafanyika kwa
kutoa ushauri kwa wakulima na mashine za kusaga, masoko na maghala
ya chakula
(ii) MIFUGO
Manispaa ya Temeke ina jumla ya Ng’ombe wa maziwa 3281, Ng’ombe
wa kienyeji 592, mbuzi wa maziwa 104 mbuzi wa kienyeji 5,205 na kondoo
402 na aina zingine za Mifugo kama vile kuku wa mayai 127,298 na kuku
wa nyama 186,796. Huduma za ugani zinazotolewa ni pamoja na ushauri
kuhusu ufugaji bora, uzuiaji na matibabu dhidi ya magonjwa mbalimbali
ya mifugo.
(iii) MISITU
Halmashauri inalo jukumu la Kutoa elimu ya hifadhi ya Mali asili na
upandaji miti wa aina mbalimbali, ikiwemo Miti ya kiasili, Mbao,
Mapambo, Uvuvi na Maua. Aidha Serikali iliweka Lengo la kupanda miti
1,500,000 kwa mwaka. Hivyo miti hiyo hupandwa kwa kushirikiana na
Wadau wa mazingira katika Shule, Polisi, Jeshi, katika vyanzo vya maji,
mabondeni, mashambani, maeneo ya wazi, kandokando ya barabara
kuu, makazi, NGO’s na wananchi.
(iv) UVUVI
Eneo la bahari la Manispaa ya Temeke liko katika kata za Kurasini, Mtoni
na Kijichi. Shughuli zinazofanyika hasa kwenye eneo lenye Mikoko ni
ukusanyaji na fugaji wa Kaa, Kamba na mazao mengine ya baharini
kama Simbi.
Aidha ufugaji wa Samaki aina ya Perege na Kambare hufanyika katika
kata zote za Temeke ambapo kuna jumla ya mabwawa 22 yanayotumika
kwa ufugaji huu.
(v) NYUKI
Halmashauri ina majukumu ya kutoa elimu, ushauri na kuhamasisha
wananchi katika zao la ufugaji nyuki kwa njia bora na ya kisasa kulingana
na ubora wa maeneo. Aidha Halmashauri inalo jukumu la kuhamasisha
uhifadhi wa Misitu ambayo ni chanzo cha upatikanaji wa mazao ya
Nyuki.
(vi) WANYAMAPORI
Halmashauri inalo majukumu ya kuwalinda wananchi dhidi ya wanyama
wakali na waharibifu wa mazao pamoja na mali zingine zinazotumika
kwaajili ya kulinda Wanyama pori.
6
(vii) BARABARA NA MIFEREJI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina mtandao wa barabara zenye
urefu wa km. 409.92 Kati ya hizo km.98.42 ni za lami, km. 221.25 ni za
changarawe na km 349.9 ni za udongo. Barabara zilizopo chini ya
Halmashauri ni km. 847.3 na zilizo chini ya Mkoa ni km. 259.
Mgawanyo wa barabara hizo ni kama ilivyo kwenye jedwali.
Na Kiwango Aina ya Barabara (km)
Lami Changarawe Udongo Jumla
1 Barabara kuu 32 - - 32
2 Barabara za Mkoa 57 100 70 227
3 Barabara za Wilaya 80.3 387.1 197.9 665.3
4 Barabara za Vijiji - 100 82 182
Jumla 169.3 587.1 349.9 1106.3
(viii) MIPANGO MIJI
Halmashauri inalojukumu la kuboresha makazi kwa kupima viwanja vipya
na kumalizia upimaji wa viwanja 4,806 kati ya viwanja 5,000
vilivyokusudiwa kupimwa.
Kuendelea kuandaa Michoro ya Mipangomiji ili kuongeza upimaji wa
viwanja na kuboresha maeneo ya makazi. Kwa upande wa maeneo ya
umma, Idara inaendelea kupima maeneo hayo ambapo jumla ya
maeneo 31 yamepimwa. Zoezi la uthamini wa maeneo mbalimbali
umefanyika ili kuwezesha ulipaji wa fidia za maeneo mbalimbali.
(ix) USHIRIKA
Halmashauri ya Manispaa inalojukumu la kuhakikisha Ushirika wa aina
mbalimbali unakua na kuongezeka kama inavyoonyeshwa katika
jedwali hapa chini:
Na. Aina ya Vyama Idadi ya Vyama
2009/10 2010/11 2011/12 2012/13 2013/14 2014/15 2015/16
1 Vyama vya mazao 23 24 24 24 25 25 20
2 Vyama vya akiba na
Mikopo
138 150 167 200 209 212 212
3 Vyama vya Viwanda 6 6 6 6 9 9 6
4 Vyama vya Ushirika
wa Nyumba
3 3 5 4 6 6 5
5 Vyama vya Ushirika
wa Wafugaji
2 2 2 2 2 2
6 Vyama vya Ushirika
wa Huduma
24 25 34 2 40 40
7 Vyama vya Uvuvi 2 2 2 2 2 2
7
Pia kuhakisha kuwa Vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS)
vinaongezeka mwaka hadi mwaka. Aidha mitaji ya wanachama pia
inaongezeka sambamba na ukuaji wa ongezeko la vyama vya ushirika
wa Akiba na Mikopo.
(x) USTAWI WA JAMII
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa kupitia kitengo cha ustawi wa
Jamii inalojukumu la;
Kutoa huduma ya matunzo kutoka kwa wazazi wao
Kusimamia Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na
kuhakikisha vinapatiwa usajilil
Kuhakikisha Watoto wanaokinzana na sheria wanafanyiwa
marekebisho ya tabia katika kituo cha marekebisho ya tabia
makangarawe
Kuhakikisha Kesi za watoto wahanga wa ukatili zinasikilizwa
na hukumu kutolewa
Kuhakikisha Wazee na watu wenye ulemavu wanasaidiwa na
kupatiwa huduma za kujikimu na kutambua watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi wametambuliwa na
kupatiwa huduma.
(xi) SEKTA ISIYO RASMI
Halmashauri inakadiriwa kuwa na wafanyabiashara ndogo ndogo katika
Sekta Isiyo Rasmi. Hivyo shughuli zao huziendesha katika maeneo
yasiyokubalika.
Halmashauri ya Manispaa inalo jukumu la kuboresha maisha yao ili
kuongeza kipato na waondokane na umaskini kwa kufanya yafuatayo;
i. Kuboresha maeneo rasmi ya kufanya biashara ya TAZARA, Rangi
Tatu Kata ya Charambe, Tandika karibu na Kituo kidogo cha
Polisi Kata ya Tandika, Masoko ya Temeke Stereo, Madenge,
Mtoni kijichi, Yombo vituka na Toa ngoma
ii. Kutoa elimu ya biashara kwa machinga na kuwaelimisha
walengwa ambao sio rasmi kurasimisha biashara zao.
iii. Kuendelea kuboresha masoko ya Temeke Stereo, Tandika,
Mangaya, Mbagala Rangitatu, Toa ngoma, Yombo vituka na
Mtoni kijichi. ili kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara
wadogo wadogo.
iv. Kuanzisha eneo jipya la soko la Malela - Toangoma.
1.7 MAENEO MTAMBUKA
(i) MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Halmashauri inalo jukumu la kusimamia Mkakati wa Mapambano dhidi ya
Rushwa.
8
Shughuli zifuatazo zinafanyika katika mkakati huo;
1. Kutekeleza mpango wa mapambano dhidi ya rushwa, Halmashauri
inalojukumu la kusimamia uwazi na uwajibikaji kuanzia ngazi ya mitaa
hadi Halmashauri.
2. Kutoa elimu kuhusu sheria mpya ya rushwa imetolewa kwa maafisa
watendaji wa kata 23 na wa mitaa 142.
3. Watumishi waendelee kuelimishwa kuhusu uvaaji wa vitambulisho
wakati wote wawapo kazini.
4. Kuendelea kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Idara ya Afya,
maafisa watendaji kata na mitaa, madiwani ,idara za halmashauri
kama idara za fedha,uhandisi mitambo , ujenzi, wahudumu na askari.
5. Kuendelea kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa mkakati wa
mapambano ya rushwa kwenye maeneo yote ya Halmashauri
6. Kufanya vikao vya kutatua kero za wananchi kila robo mwaka.
(ii) HALI YA UMASKINI
Umaskini unaweza kutafsiriwa kuwa ni hali inayomzuia mtu kuishi maisha
yanayoridhisha. Hali hii inatokana na ukosefu wa nyenzo na uwezo wa
kumudu maisha na inajidhihirisha kwa vigezo mbalimbali kama vile
utapiamlo, ujinga, maradhi, mazingira machafu, vifo vya watoto na
wanawake wajawazito, mavazi na makazi duni, matumizi ya teknolojia
duni uharibifu wa mazingira, ukosefu wa ajira, elimu duni, uhamiaji mjini
kiholela na mawasiliano duni.
Umaskini katika Manispaa ya Temeke unatokana na mambo yafuatayo:
Ongezeko kubwa la watu ambalo ni wastani wa asilimia 4.6 kwa
mwaka, kwa sehemu kubwa likichangiwa na uhamiaji mkubwa
kutoka mikoani.
Mtandao hafifu wa barabara.
Uhaba wa miundombinu imara wa kibiashara
Halmashauri itatumia vipaumbele vilivyoainishwa hapo juu kama mkakati
wa kufikia malengo ya kuondoa umaskini.
(iii) MASUALA YA KIJINSIA
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeweka viashiria katika kuyapatia
ufumbuzi matatizo ya wanawake na wanaume na haki zao katika
huduma za Afya, Elimu, Maji na ajira. Wanawake wengi wamekuwa
wanaishi katika mazingira magumu na umaskini uliokithiri ukilinganisha na
wanaume. Mchakato wa bajeti hii katika ngazi mbalimbali umechambua
utoaji wa huduma na mipango ya maendeleo kwa kuainisha suala la
usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu kwa wanawake.
Suala la jinsia ni la mtambuka lenye malengo mahsusi ya usawa wa
kijinsia ambayo yameainishwa katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Sekta
isiyorasmi na ajira ambapo mambo muhimu yanayozingatiwa katika
Bajeti ni pamoja na :
9
Kuimarisha huduma za maji kwa kuchimba visima
Kuongeza idadi ya zahanati na huduma ya mama na mtoto ili
kupunguza vifo vya wajawazito vinavyotokana na kutopata
huduma kwa karibu
Kuboresha Masoko na kutengeneza maeneo maalum ili kuongeza
nafasi za kufanyia biashara hasa kwa akina mama na vyama
Taasisi za utoaji wa mikopo uweke riba nafuu ili wakina
mama,vyama na wazee waweze kunifaika na mikopo hiyo
10
SURA YA 2
2.0 UPEMBUZI WA MWELEKEO WA HALMASHAURI
2.1 SERA NA MIONGOZO
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeandaa Bajeti yake ya mwaka
2017/2018 ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya
mwaka 2025. Uandaaji wa mpango na bajeti ya matumizi ya mwaka
2017/2018 umezingatia sera mbalimbali za Serikali ikiwemo mkakati wa
Taifa wa kuondoa umaskini na kukuza uchumi (MKUKUTA II), Malengo ya
Maendeleo endelevu (SDGs), Ilani ya chama Tawala ya 2015 – 2020,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa awamu ya pili miaka mitano 2016/2017
– 2020/2021 na Mpango Mkakati wa Halmashauri 2016/2017 – 2020/2021
kama nyenzo muhimu za kiutekelezaji katika kufikia maendeleo.
Mchakato wa maandalizi ya Bajeti na Mpango wa Maendeleo
umeshirikisha ngazi zote za Halmashauri ikiwa ni pamoja na kupokea
mapendekezo ya mipango iliyoibuliwa katika ngazi za Mitaa na kujadiliwa
na Kamati za Maendeleo za Kata zote 23 za Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke. Miradi ya Fursa na Vikwazo katika Maendeleo kutoka katika
Kamati za Maendeleo ya Kata imejumuishwa baada ya kuchambuliwa
na kuainishwa kulingana na vipaumbele kisekta na kiidara kwa kuzingatia
uwezo wa kifedha Kitaifa wa Halmashauri yenyewe.
Miradi ya jamii
Mpango wa mwaka 2017/2018 umeshirikisha ngazi zote za chini za Serikali
za Mitaa kwa kutumia mfumo na taratibu za fursa na vikwazo kwa
Maendeleo (O & OD).
Mchakato wa O & OD katika jamii huanza kwa kuzipatia mamlaka za
Serikali za Mitaa ngazi ya chini (LLGAS) takwimu za upangaji mipango
(IPFs) na miongozo ya uandaaji mipango ya maendeleo na Bajeti ya
mwaka. Zoezi hili hufanyika baada ya timu ya Menejimenti ya
Halmashauri kuzijadili IPFs na miongozo husika na baadaye kuzituma kwa
LLGAs.
Ili kufanikisha mchakato wa O & OD Halmashauri hutuma wawezeshaji wa
Kata (WF) kila kata ambako hujumuika na Kamati za Maendeleo ya Kata
katika kuchambua mapendekezo ya Miradi na mipango ya Jamii
(Community Development Plans - CDPs) hatua hii hufanyika kati ya mwezi
Desemba na Januari. Mipango kata yenye Miradi ya Mipango ya Jamii
(CDPs) huwasilishwa Manispaa na kujadiliwa na Timu ya Menejimenti ya
Halmashauri. Katika kikao hiki wakuu wa Idara huchangia kwa kuzingatia
taaluma husika, sera za kisekta na miongozo ya kitaifa.
11
Kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 jumla ya Miradi 230 iliyoibuliwa na
jamii iliwasilishwa kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya chini
(LLGA).
2.1.1 SERA NA MIONGOZO ILIVYOZINGATIWA KATIKA BAJETI YA MWAKA
2017/2018
Mpango wa maendeleo na Bajeti ya mwaka 2017/2018 umeandaliwa
kwa kuzingatia mwongozo wa uandaaji wa Bajeti kutoka Serikali Kuu, Sera
na Malengo yaliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015 - 2020, Dira ya maendeleo ya Taifa – 2025 na maagizo ya viongozi
wa kitaifa. Sera hizi zimezingatiwa katika mpango huu kama ifuatavyo:
Mwongozo wa uandaaji mipango na bajeti
Uandaaji wa bajeti hii umezingatia Mwongozo wa kuandaa Mpango na
Bajeti wa 2016/2017 katika utekelezaji wa mpango wa Maendeleo wa
Taifa awamu ya pili wa miaka mitano 2016/2017 – 2020/2021 kutoka
Wizara ya fedha (HAZINA) toleo la Novemba, 2016. Mambo muhimu
yalijitokeza katika mwongozo huu ni:
Mabadiliko ya mfumo wa bajeti kutoka bajeti inayozingatia
rasilimali na kuwa bajeti inayo zingatia fursa zilizopo
Mpango unaozingatia viashiria vya MKUKUTA II
Muundo wa taasisi zinazosimamia mfumo wa bajeti zikiwa na
majukumu mbalimbali zimeainishwa kama ifuatavyo:
Wizara ya Fedha na uchumi
Wizara,Wakala wa serikali kuu,sekretarieti za mikoa na serikali za
mitaa
MKUKUTA II
Katika eneo hili bajeti imezingatia Mpango wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) – ukiwa na maeneo makuu matatu
kama yanavyoainishwa hapa chini:
1.Kujenga Uchumi ulio imara na kupunguza umaskini katika jamii,
2.Kuboresha na kuimarisha huduma za jamii na kuinua hali za maisha ya jamii na
3. Utawala bora na Uwajibikaji.
12
Katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Halmashauri imezingatia maelekezo
mbalimbali ya viongozi wa Kitaifa yaliyomo katika hotuba ya Rais, Mh.
John Pombe Magufulii inayohusisha kubana matumizi yasiyo ya lazima,
kuinua mapato ya Serikali ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa
Tanzania.
2.1.2 WADAU WA MANISPAA YA TEMEKE NA MATARAJIO YAO
Manispaa ya Temeke inalo jukumu kubwa la msingi la kutoa huduma za
kiuchumi na kijamii kwa wakazi wake, ili kutekeleza jukumu hilo Manispaa
inashirikiana na wadau mbalimbali ambao hutoa mchango wao ili
kuboresha huduma zinazotolewa kwa wakazi wa Temeke. Aidha wadau
hawa wanayo matarajio yao kutokana na huduma zitolewazo na
Manispaa kama inavyoainishwa hapa chini.
JINA LA
MDAU
MATARAJIO YA MDAU TOKA
MANISPAA
MATOKEO YA KUTOTIMIZA
MATARAJIO YAKE
KIPAUMBELE
Serikali Kuu 1. Kuzingatia taratibu na sheria
zinazotolewa na Serikali.
2. Mahusiano mazuri na wadau
wengine.
3. Utawala Bora na uwajibikaji
mzuri
4. Mipango mizuri
inayotekelezeka
1. kuchelewa kufika kwa
fedha kama
inavyopangwa
2. Kutopata msaada
toka kwa wadau
waliopo
Juu
Sekretarieti
ya Mkoa
1. Kuzingatia na kutekeleza
ushauri unaotolewa
2. Uwajibikaji na utawala bora
3. Utoaji huduma bora kwa jamii
1. Upungufu wa rasilimali
fedha
juu
Wafadhili 1. Kuzingatia makubaliano
yaliyopo kwenye mkataba
2. Mahusiano mazuri kiutendaji
3. Misaada kuwafikia walengwa
4. Mazingira mazuri ya kuvutia
wafadhili
1. Kuhamisha ufadhili wao
2. Kutofikia malengo
yaliyowekwa
3. Kusitisha misaada
4. Kuhamisha misaada
Kati
CBO/NGO’s 1. Mazingira mazuri yanayofaa
kufanyia kazi
2. Kupewa msaada pale
inapohitajika
1. Kushindwa kukamilisha
malengo
2. Kuacha kuwekeza
3. Kupunguza misaada
Kati
13
JINA LA
MDAU
MATARAJIO YA MDAU TOKA
MANISPAA
MATOKEO YA KUTOTIMIZA
MATARAJIO YAKE
KIPAUMBELE
3. Mahusiano mazuri katika
kutoa huduma
4. Tatatibu za uwazi na ukweli
katika kazi
5. Kutimiza makubaliano
kwenye mikataba
kwa walengwa
4. Kutokuwa wazi katika
utendaji wao
Watumishi 6. kuwepo kwa mazingira
mazuri ya kufanyia kazi
7. Stahili za watumishi
kuboreshwa
1.Kuchelewa kupatiwa
stahili zao kwa wakati
2. kutotimiza malengo
ipasavyo
juu
Wananchi 1. Huduma Bora
2. Utawala Bora na Uwazi
3. Kiwango cha Kodi/Ushuru
kinachowiana na kipato
chao
4. Sheria zinazolinda maslahi
yao
5. Ushirikishwaji katika mipango
na maamuzi yanayowahusu
6. Uwiano katika huduma
zitolewazo na Manispaa
1. Malalamiko mengi
2. Kushindwa kuchangia
maendeleo
3. Kukwepa kulipa kodi
4. Uvunjaji wa Sheria wa
makusudi
5. Kutotimiza wajibu wao
katika kuleta
maendeleo
Kati
2.1.3 FURSA NA VIKWAZO KWA MAENDELEO
Manispaa ya Temeke inao uwezo na fursa mbalimbali ambazo zikitumika
vizuri zitasaidia kuinua kiwango cha maisha ya wakazi wake. Uchambuzi
wa hali halisi umebainisha kuwepo kwa Fursa na Vikwazo vifuatavyo:
(i) FURSA
1. Miundo mbinu bora ya majengo na Ofisi za Watendaji wa
makao Makuu na Kata
2. Mtandao mzuri wa mawasiliano ya barabara na makampuni
ya simu
3. Nguvu kazi ya kutosha kuweza kufanya kazi za maendeleo
4. Uongozi unaozingatia uwazi na uwajibikaji
5. Ardhi ya kutosha kwa ajili ya uendelezaji wa Kilimo,uwekezaji
na makazi
6. Kuwepo kwa makampuni, taasisi na NGO’s nyingi zinazosaidia
kutoa huduma kwa wananchi
7. Mahusiano mazuri na wadau wanaochangia maendeleo ya
wakazi kwa ujumla wake
14
8. Fukwe za bahari kwa ajili ya kuendeleza utalii.
(ii) VIKWAZO
Pamoja na uwezo na fursa zilizopo kwenye Manispaa ya Temeke,
bado kiwango cha kufikia malengo yanayowekwa si cha kuridhisha
kutokana na changamoto na vikwazo vifuatavyo:
1. Kutofikiwa kwa malengo ya ukusanyaji mapato kwenye baadhi
ya vyanzo vya Manispaa unaosababisha upungufu wa rasilimali
fedha, wataalam, zana za kitaalam
2. Ongezeko kubwa la watu ambalo halilingani na huduma zilizopo
3. Uharibifu wa mazingira
4. Kutofikia malengo ya utendaji kazi kutokana na bajeti finyu
5. Milipuko ya magonjwa ya Kipindupindu, kuhara na kuenea kwa
ugonjwa wa UKIMWI
6. Hali ya umaskini katika jamii na kupanda kwa gharama za bei za
huduma kwa wakazi
Uchambuzi wa hali halisi ya utoaji huduma na utekelezaji wa majukumu
mbalimbali umebaini masuala muhimu na changamoto mbalimbali
zinazohitaji ufumbuzi kwa kuchukua hatua muafaka zitakazisaidia kuleta tija
na maendeleo endelevu kwa wananchi wa Temeke, ikiwemo:
i. Kuimarisha utawala bora kwa kuhimiza uwazi wa uwajibikaji
ii. Kuongeza na kukarabati miundombinu ya huduma za jamii, Elimu,
maji na Afya
iii. Kuimarisha ukusanyaji wa mapato
iv. Kuongeza na kuinua kiwango cha mtandao wa biashara
v. Kuimarisha shughuli za Mipango miji, kusimamia makazi na
upatikanaji wa viwanja
vi. Kuimarisha huduma za ugavi za kilimo/mifugo na upatikanaji wa
zana za kilimo, mbolea, madawa na mbegu bora kwa wakati
vii. Kuimarisha sekta isiyorasmi na kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa
vijana na wanawake.
15
SURA YA 3 3.0 DIRA (VISION)
“Wakazi wa Manispaa ya Temeke kuwa na maisha bora.”
3.1 DHAMIRI (MISSION)
“Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inachukua jukumu la kufanikisha
maisha bora kwa wakazi wote kwa kutoa huduma bora za kijamii na
kiuchumi.”
3.2 MALENGO (OBJECTIVES)
A. Huduma ya Ukimwi imeboreka na maambukizi mapya yamepungua
B. Uboreshaji, uendelezaji na utekelezaji kikamilifu mpango wa Taifa
kupambana na rushwa kuimarika.
C. Upatikanaji na ubora wa huduma endelevu za jamii umeimarika.
D. Idadi na ubora wa huduma za kiuchumi na miundombinu zimeimarika.
E. Utawala bora na huduma za kiutawala katika ngazi zote umeimarika.
F. Usimamizi na hifadhi ya maliasili na mazingira umeboreka
G. Huduma ya dharura na usimamizi wa majanga umeboreka
Vipaumbele vya Halmashauri Kwa mwaka 2017/2018
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka wa Fedha wa 2017/2018
imedhamiria kutekeleza majukumu yake kwa kuweka vipaumbele katika
maeneo yafuatayo:
Elimu
Kuboresha utoaji huduma ya elimu ya msingi na sekondari katika ngazi
zote kwa kuongeza maabara, vyumba vya madarasa, madawati,
shule mpya, jengo la kidato cha V na VI na matundu ya vyoo
Kuboresha mazingira ya watumishi wa elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa makazi bora ya walimu.
Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Kuboresha mfumo wa upatikanaji wa masoko ya mazao ya
kilimo,mifugo, uvuvi na usindikaji wa mazao hayo
Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na upatikanaji wa huduma za
ugani na pembejeo.
16
Barabara
Kuboresha miundombinu na mtandao wa usafiri kwa kujenga na
kukarabati barabara, madaraja na vivuko.
Afya
Kuboresha huduma za kinga na tiba kwa kujenga/kukarabati
miundombinu na kutoa nyezo za kutolea huduma za afya katika ngazi
zote.
Kuwajengea uwezo kwa kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya.
Kuhahakikisha dawa na vitendanishi vinapatikana wakati wote katika
vituo vya kutolea huduma
USAFI NA MAZINGIRA
Kuongeza uwezo wa uzoaji taka kutoka tani 193,851 hadi tani 288,715
Kuimarisha udhibiti wa taka ngumu katika mitaa 97
Kuimarisha programu ya elimu jamii kuhusu usafi wa mazingira
Maji
Kuboresha uwezo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Mipango miji, Ardhi na maliasili
Kusimamia kikamilifu na Kuboresha matumizi ya maliasili.
kuboresha makazi bora kwa kupima na kuendeleza viwanja
Fedha
Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na uimarishaji na udhibiti
wa matumizi ya fedha za umma na utoaji wa elimu kwa walipa kodi
Kubuni, kusimamia na kuimarisha vyanzo vya Mapato ya Halmashauri
Kusimamia ipasavyo mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya
kielectroniki pamoja na mfumo wa uhasibu wa IFMS na epicor
Kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia viwango vya
kiuhasibu vya kimataifa (IPSAS)
Uwekezaji
Kuimarisha programu ya uwekezaji katika maeneo yaliyoainishwa na
kuendelezwa.
Biashara
Kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa kuboresha
miundombinu.
Kuimarisha programu ya uwekezaji na kuweka mazingira rafiki kwa
sekta binafsi katika uwekezaji.
17
Raslimali watu na utawala
Kuimarisha programu ya mafunzo kwa watumishi
Kuimarisha utawala bora na uwajibikaji
Maeneo mtambuka
Kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa kutoa elimu
Kuboresha asasi zilizo katika mapambano dhidi ya maambukizi ya
virusi vya UKIMWI
Kuendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa katika ngazi
zote katika Halmashauri
Kuimarisha masuala ya usafi na uboreshaji wa Mazingira
Kuimarisha huduma za dawati la jinsia.
Uhusiano
Kuendelea kutoa matangazo katika vyombo vya habari na vipaza
sauti mitaani
Kuandaa na kuchapisha jarida la Mafanikio ya utekelezaji wa Miradi na
vipeperushi
Kutoa matangazo juu ya ukusanyaji wa kodi na mapato mbalimbali.
Kurekodi nakala (documentaries) za miradi na kodi za mapato
mbalimbali.
Tehama
Kusimika mtandao wa internet katika majengo matatu ya Manispaa
(jengo la ujenzi, Elimu na ugavi)
Kuimarisha na kuboresha taarifa za kijeografia (Geodata) kwa shughuli
za GIS
Kufanya matengenezo pamoja na maboresho ya vifaa vyote vya
TEHAMA
Kuimarisha mifumo tisa (9) ya manispaa, LGRCIS, MOLIS, LAWSON,
EHMIS, EPICOR, PLANREP, PSSN AND GIS
Kuwajengea uwezo watumishi wa TEHAMA pamoja na watumiaji wa
kompyuta na mifumo
GIS
Kuboresha GIS katika utendaji kazi wake
Kuanisha anuani za makazi(post code) katika kata mbili
Kutambua vituo vya shule, barabara na zahanati kwa kutumia mfumo
wa Ramani
Kuwatambua walipa kodi wa leseni za biashara kwa kutumia mfumo wa
ramani
18
3.3 SHABAHA
500A UTAWALA
Mpango wa mapambano dhidi ya rushwa katika kata 23 umewezeshwa na
kuimarishwa ifikapo 2020
Mazingira ya kazi yameboreshwa kwa watumishi 194 ifikapo 2020
Ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi umeongezeka kutoka 60%
mpaka 80% ifikapo 2020
Maadhimisho 12 ya kitaifa yamefanyika ifikapo 2020
Halmashauri imetekeleza michango ya kisheria ifikapo 2020
500B UTUMISHI
Watumishi 398 watawezeshwa ifikapo 2020
Watumishi wenye sifa katika Halmashauri wameongezeka kutoka 7,850
mpaka 8,563 ifikapo 2020
500C OFISI YA MEYA
Mazingira ya kazi yameboreshwa kwa madiwani 49 ifikapo 2020
501A MAZINGIRA NA USAFISHAJI
Uwezo wa kukusanya taka kuongezeka kutoka tani 193,815 kufikia tani
288,815 kwa mwaka ifikapo 2020
Udhibiti wa Taka kuimarishwa katika mitaa 142 ifikapo 2020
Kuongeza uwezo wa kukusanya na kuhifadhi maji taka kwa Mita za ujazo
2100 ifikapo 2020
Kuongeza uwezo wa kuzoa taka toka 47% mpaka 75% kutokana na
kuboresha miundombinu ifikapo 2020
Kuwezesha watumishi wa idara ya usafi na mazingira kumudu maisha yao ya
kila siku ifikapo 2020
Elimu ya kitaaluma ya udhibiti wa mazingira imeimarika ifikapo 2020
Kuhakikikisha Taratibu na kanuni za kimazingira za Manspaa zinazingatiwa
ifikapo 2020
501B AFYA KINGA
Uboreshaji wa usimamizi wa usafi na afya ya mazingira kuimarika kutoka
68% hadi 75% ifikapo 2020
502A FEDHA NA BIASHARA
Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi 98 ifikapo 2020
Kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni za fedha za Umma zinazingatiwa na
kufuatwa ifikapo 2020
Makusanyo ya Mapato ya ndani ya Halmashauri yanaongezeka kutoka
19
Bilioni 40 mpaka Bilioni 50 ifikapo 2020
Kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara ifikapo 2020
Kuboresha mazingira ya biashara katika masoko ya Temeke ifikapo 2020
Kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi 18 ifikapo 2020
503A MIPANGO, SERA NA UFUATILIAJI
Bajeti na mipango bora ya maendeleo ya Halmashauri kuandaliwa ifikapo
2020
Kuwezesha miradi 10 ya maendeleo inayotekelezwa kwa kushiriana na
wafadhili ifikapo 2020
Maeneo 25 ya uwekezaji kutambuliwa katika kata 23 ifikapo 2020
Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Idara ya Mipango,
Takwimu na ufuatiliaji ifikapo 2020
upembuzi na kuwasilishwa kwaajili ya kuhuisha hali ya kiuchumi ya Manispaa
ifikapo 2020
Takwimu za kiuchumi zitakusanywa katika Kata 23, zitafanyiwa upembuzi na
kuwasilishwa kwaajili ya kuhuisha hali ya kiuchumi ya Manispaa ifikapo 2020
505A MIFUGO
Mazingira ya kazi kwa watumishi 41 wa Mifugo na Uvuvi kuimarika ifikapo
2020
Taaluma kwa watumishi 41 kuimarika ifikapo 2020
Huduma za ugani kwa wafugaji 2000 kuimarika ifikapo 2020
Kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wazalishaji wa ngozi ifikapo
2020
Miundombinu ya mifugo katika kata 4 kuimarika ifikapo 2020
Huduma za ugani kuboreshwa kwa wafugaji 200 ifikapo 2020
505D UVUVI
Matumizi endelevu ya raslimali za uvuvi kuimarika ifikapo 2020
Huduma za ugani za uvuvi kuimarika ifikapo 2020
506A KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi 42 wa idara ya kilimo kuboreshwa
ifikapo 2020
Kuwajengea uwezo wa kufanya kazi watumishi 42 wa idara ya kilimo ifikapo
Wakulima 26000 kutembelewa na maofisa ugani ifikapo 2020
Mafunzo ya kitaalamu kutolewa kwa wakulima 3000 yahusuyo uzalishaji wa
mazao ya bustani na mazao ya shambani ifikapo 2020
Miundo mbinu ya kilimo katika kata tano (5) kuboreshwa na kukarabatiwa
ifikapo 2020
Mafunzo ya kitaalamu kutolewa kwa wakulima 3000 yahusuyo uzalishaji wa
20
mazao ya bustani na mazao ya shambani ifikapo 2020
Mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi 42 wa idara ya kilimo kuboreshwa
ifikapo 2020
Tahadhari ya majanga na magonjwa kutolewa katika kata 23 ifikapo 2020
506D USHIRIKA
Kutoa elimu ya biashara na menejimenti ya ushirika kwa vyama 60 vya
ushirika ifikapo 2020
Mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi 6 kwenye kitengo cha ushirika
ifikapo 2020
507A ELIMU MSINGI
Shule 83 za Msingi kusimamiwa ifikapo 2020
Madarasa 15 ya Elimu ya watu wazima kuimarishwa ifikapo 2020
"Mpango wa ndiyo ninaweza' katika Kata 23 Kuimarishwa ifikapo 2020
Mazingira ya kutendea kazi kwa watumishi 63 Kuimarishwa ifikapo 2020
Majengo ya Shule za Msingi kuongezeka kutoka 10642 hadi 10742 ifikapo
2020
Vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa shule 83 kutolewa ifikapo 2020
Samani katika shule za Msingi kuongezeka kutoka 40161 hadi 48141 ifikapo
2020
Haki za kiutumishi kwa Walimu 3548 kutolewa k wa shule za Msingi ifikapo
2020
Shule inayomjali mtoto katika kata 23 kuimarishwa ifikapo 2020
508A AFYA
Kupunguza maabukizi ya Ukimwi kutoka 5% hadi 3% ifikapo 2020
Maambukizi ya ugonjwa wa macho kupunguzwa kutoka 6% hadi 3% ifikapo
2020
Vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu kupungua kutoka 15.5% hadi 7%
ifikapo 2020
Magonjwa ya akili kupunguzwa kutoka 2% hadi 1% ifikapo 2020
Vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano kupungua toka13 hadi
7/1000 ifikapo 2020
Magonjwa ya minyoo kupunguzwa kutoka 7.5% hadi 5% ifikapo 2020
Uwezo wa usimamizi wa afya ya mazingira katika jamii kudhibitiwa na
kuimarishwa kutoka 48% hadi 68% ifikapo 2020
Uelewa wa jamii kuhusu ustawi wa jamii kuongezeka kutoka 20% hadi 75%
ifikapo 2020
Vifo vya akina mama wajawazito kupungua kutoka 175/100000 hadi
150/100000 ifikapo 2020
Ufahamu kuhusu afya na ustawi wa jamii kwenye ngazi ya jamii
unaongezeka kutoka 50% hadi 75% ifikapo 2020
21
508A AFYA UTAWALA
Kiwango cha watoto wanaofariki mara baada ya kuzaliwa )Nepnatal
mortality rate) kimepungua kutoka 13/1000 mpaka 8/1000 ifikapo 2020
Kiwango cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 vimepungua kutoka
13 mpaka 7/1000 ifikapo 2020
Uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya dharula unaongezeka kutoka 50%
hadi 70% ifikapo 2020.
Kupunguza kazi ya maambukizi ya Ukimwi kutoka 5% hadi 3 ifikapo 2020
Kupungua kwa uhaba wa vifaa Tiba, uchunguzi , madawa, chanjo na
vitendanishi katika vituo vya vyote vya kutolea huduma za Afya kutoka 15%
hadi 35% ifikapo 2020
Kupungua kwa vifo vya akinamama wajawazito kutoka 134 hadi
125/100,000 ifikapo 2020
Kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 7% hadi 6%
ifikapo 2020
Kuongezeka kwa uwezo wa kutoa huduma za majeruhi kutoka 30% hadi
55% ifikapo 2020
508B AFYA HOSPITALI
Kuboresha utoaji huduma katika kitengo cha kinywa na meno kutoka 60%
hadi 75% ifikapo 2020
Kupungua kwa idadi ya magonjwa ya macho kutoka 5% hadi 3% ifikapo
2020
Kuboreshwa kwa na uwezo wa kusimamia usafi wa mazingira katika vituo
vyote vya kutolea huduma za afya kutoka 60% hadi 75% ifikapo 2020
Kupungua kwa tatizo la miundo mbinu ya kutolea huduma za afya kutoka
30% hadi 25% ifikapo 2020
Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za afya na jamii kwa walioko
kwenye mazingira magumu kutoka 35% hadi 38% ifikapo 2020
Kuongezeka kwa uwezo wa kutoa huduma za dharura kwa ngazi ya
hospitali kutoka 50% hadi 55% ifikapo 2020
Maambukizi ya UKIMWI kupunguzwa toka 5% hadi 3% ifikapo 2020
Upungufu wa madawa , vifaa na tiba katika vituo vya kutolea huduma ya
afya upunguzwe toka 35% hadi 15% ifikapo 2020
Vifo vinavyotokana na ujauzito vipunguzwe toka 134 kati ya wamama
100,000 hadi 125 kati ya wamama 100,000 ifikapo 2020
uwezo wa kutoa huduma ya magonjwa ya kisukari uongezwe kutoka 20%
mpaka 25% ifikapo 2020
kupunguzwa idadi ya wagonjwa wapya wa akili toka 1.5% mpaka1% ifikapo
2020
Upungufu wa miuondombinu upunguzwe toka 60% hadi 30% ifikapo 2020
Uwepo wa usafiri na usafirishaji uongezwe kutoka 10% hadi 100% ifikapo
2020
22
508E AFYA ZAHANATI
Maambukizi ya virusi vya ukimwi kupungua kutoka 5% hadi 3% ifikapo 2020
Upungufu wa dawa muhimu,vitendanishi,vifaa tiba na chanjo kwa kiwango
cha kutoka 35% hadi 15% ifikapo 2020
Vifo vya wajawazito kupungua kutoka 134/100,000 hadi 125/100,000 ifikapo
2020
Vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kupungua kutoka 7 mpaka
6/1000 ifikapo 2020
Maambukizi dhidi ya malaria kupungua kutoka 4% hadi 1% ifikapo 2020
Vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo kupungua kutoka 18% hadi 16%
ifikapo 2020
Usafi wa mazingira katika vituo vya kutolea huduma kuimarika kutoka 25%
hadi 20% ifikapo 2020
Upungufu wa majengo ya kutolea huduma za afya kupungua kutoka 30%
hadi 25%) ifikapo 2020
Uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko katika vituo vya tiba kuimarika
kutoka 50% hadi 55% ifikapo 2020
509A ELIMU SEKONDARI
Kuongeza uelewa wa mkakati wa kupambana na rushwa katika shule 26 za
sekondari za serikali ifikapo 2020
Kutoa stahili za utumishi kwa walimu 1285 wa shule za sekondari za serikali
ifikapo 2020
Kuweka mazingira vutivu ya kazi kwa watumishi 16 wa idara ya elimu
sekondari ifikapo 2020
Kuwezesha shule 61 za sekondari kutekeleza shughuli zake ifikapo 2020
Majengo ya shule za sekondari za serkali kuongezeka kutoka 1082 hadi 1164
ifikapo 2020
510A MAJI VIJIJINI
Miradi ya maji 40 kujengwa na kukarabatiwa katika Kata ifikapo 2020
Kuboresha usambazaji wa maji katika Kata 23 ifikapo 2020
Mazingira mazuri kwa watumishi 12 wa Idara ya maji kuboreshwa
ifikapo 2020
511A UJENZI UTAWALA
Kuwapatia stahiki watumishi 30 ifikapo 2020
Kuwapatia vitendea kazi na vifaa vya kazi watumishi 30 ifikapao 2020
511B BARABARA
Kufanya matengenezo ya kawaida ya barabara zenye urefu wa km 100
ifikapo 2020
Uboreshaji na matengenezo ya barabara zenye urefu wa km 109 ifikapo
2020
23
511E MAJENGO
Uboreshaji wa majengo 3 ya Manispaa ifikapo 2020
512A ARDHI
Mazingira bora kwa watumishi 70 wa idara ya Mipangomiji kuimarika ifikapo
Maeneo yaliyopimwa ya umma na binafsi kuongezeka ifikapo 2020
Hati 15,000 na Leseni za Makazi 10,000 kuandaliwa ifikapo 2020
Uthamini wa mali na majengo kwa maeneo ya umma 400 na ya wananchi
100000 kufanyika ifikapo 2020
upimaji wa maeneo ya Makazi kwa maeneo ya pembezoni na mjini
kuboreka ifikapo 2020
Kusimamia uthibiti wa ukuaji wa mji katika manispaa ifikapo 2020
512F MALIASILI
Mazingira bora ya utendaji kazi yameimarishwa kwa watumishi 14 ifikapo
2020
Usimamizi na hifadhi ya maliasili na mazingira umeimarishwa katika kata 23
ifikapo 2020
Wanyama pori hatari kwa maisha na mali za binadamu wanadhibitiwa
katika kata 23 ifikapo 2020
514A SHERIA
Kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi 33 ifikapo 2020
515A UKAGUZI WA NDANI
Kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi 9 ifikapo 2020
Kuhakikisha sharia, kanuni na taratibu za fedha zinafuatwa ifikapo 2020
Upatikanaji wa huduma kwa jamii unaboreshwa katika kata 23 ifikapo 2020
Kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi 9 wa kitengo cha ukaguzi wa
ndani ifikapo 2020
Kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana katika miradi
inayotekelezwa na Halmashauri ifikapo 2020
Kuwezesha Idara kutambua na kuorodhesha viashiria vya hatari na kuweka
njia za kupunguza athari zake katika utekelezaji wa mradi ifikapo 2020
516A UGAVI
Kuboreshwa mazingira ya kazi kwa watumishi 15 ifikapo 2020
517A UCHAGUZI
Ushiriki wa jamii katika uchaguzi kuongezeka kutoka 70% hadi 85% ifikapo
2020
518A TEKNOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)
Mazingira bora ya utendaji kazi kwa watumishi wa TEHAMA Kuboreshwa
ifikapo 2020
24
Uwezo wa kitaaluma ya kazi kwa watumishi wa TEHAMA Kuimarishwa ifikapo
2020
Kuhakikisha miundombinu na mifumo ya mawasiliano katika idara 13 na
vitengo 6 inapatikana ifikapo 2020
Huduma ya ICT na Miundombinu kuboreshwa ifikapo 2020
Mifumo ya Taarifa na Mawasiliano kuimarishwa ifikapo 2020
Kuboresha GIS na kuhakikisha upatikanaji wa Takwimu za Kigeografia ifikapo
2020
Matangazo 5850 kutolewa kutoka idara 13 na vitengo 6 ifikapo 2020
519A NYUKI
Mazingira bora ya utendaji kazi yameimarishwa kwa watumishi 3 ifikapo 2020
Usimamizi na hifadhi ya maliasili na mazingira umeimarishwa katika kata 23
ifikapo 2020
Segimenti MKUKUTA
527A MAENDELEO YA JAMII
Ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo kuimarishwa ifikapo 2020
Mipango ya UKIMWI ya Wilaya na Jamii kuimarika ifikapo 2020
Maambukizi ya HIV/AIDs kupunguzwa kutoka 5% hadi 3% ifikapo 2020
Miradi ya TASAF katika kata 23 kuimarishwa ifikapo 2020
Kuwezesha mazingira mazuri ya kufanyakazi kwa watumishi 50 wa
Maendeleo ya Jamii ifikapo 2020
Ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo kuimarishwa ifikapo 2020
Wanawake na vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo kutoka katika
mitaa 142 ifikapo 2020
Usimamizi wa shughuli za maafa kuimarishwa katika mitaa 142 ifikapo 2020
Uelewa wa maswala ya afya na ustawi wa jamii kuimarika kwa kuongezeka
kutoka 60% mpaka 85% ifikapo 2020
527C USTAWI WA JAMII
Migogoro ya ndoa 500 kusuluhishwa na watoto kupata stahiki zao ifikapo
2020
mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi 20 kuboreshwa ifikapo 2020
Marekebisho ya tabia za watoto 200 walio katika hatari ya kukinzana na
kukutana na sheria ifikapo 2020
Msaada wa kiuchumi na uangalizi kwa watoto 300 wanaoishi katika
mazingira hatarishi na familia zao ifikapo 2020
Msaada wa kiuchumi ,matibabu kutolewa kwa wazee 50 na watu wenye
ulemavu 50 ifikapo 2020
Omba omba 200 na watoto 100 wanaotumikishwa mtaani kuondolewa na
watoto kuwaunganisha na familia zao ifikapo 2020
Mfumo wa ulinzi na usalama kuimarishwa ifikapo 2020
Mfumo wa ulinzi na usalama wa mtoto kuboreka ifikapo 2020
25
SURA YA 4
4.0 MAPITIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/2016 NA 2016/2017
(JULAI – DESEMBA 2016)
4.1 MAPATO
Halmashauri ilikisia kukusanya jumla ya Tshs. 191,278,229,307.00 ikiwa ni
makisio kwa mwaka 2016/2017. Kati ya makisio hayo vyanzo vya nje
vilikadiriwa kuingiza Tshs. 149,050,865,307.00 na vyanzo vya ndani vilikadiria
kuingiza Tshs. 42,227,364,000.00. Hadi kufikia mwezi Desemba 2016
Halmashauri ilikuwa imepokea jumla ya Tshs. 63,184,245,286.35 ikiwa ni asilimia
33.03% ya lengo la mapato kwa mwaka. Kati ya mapato hayo vyanzo vya
nje viliingizia Halmashauri yetu jumla ya Tshs. 52,050,505,730.06 sawa na
asilimia 34.92% ya lengo la mapato ya nje.Vyanzo vya ndani viliingiza Tshs.
11,133,739,556.29 ikiwa ni asilimia 26.37% ya lengo la mapato ya ndani kwa
mwaka.
MAPITIO YA MAKISIO YA MAPATO NA MAPATO HALISI YA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA
2014/2015 NA 2015/2016 ( JULAI - JANUARI 2016)
CHANZO CHA MAPATO
2015/2016 2016/2017
MAKISIO MAPATO HALISI
JUAIL. 2015 - JUNI 2016
MAKISIO MAPATO
HALISI JULAI – DESEMBA 2016
A. VYANZO VYA NDANI 38,553,189,000.00 31,967,411,712.00 42,227,364,000.00 11,133,739,556.29
B. VIANZIO VYA NJE:
RUZUKU:
Mishahara 75,596,716,815 73,175,620,071.00 52,890,445,047.00 44,159,207,404.70
Matumizi Mengineyo -(OC) 5,679,308,000 6,093,117,809.00 6,739,778,145.00 3,084,870,785.00
LGCDG –CAPITAL 3,337,574,000 0.00 3,001,144,123.00 0.00
Road Fund 6,674,475,000 1,689,661,389.28 5,782,580,000.00 1,561,988,397.92
SEDEP 88,627,000 0.00 200,000,000.00 0.00
RUZUKU YA MAJI (RWSSP ) 900,000,000 952,208,922.00 337,284,853.00 338,882,694.00
BASKET FUND 1,508,187,000 1,519,653,000.00 2,732,231,000.00 1,112,552,643.68
UNICEF 397,654,000 231,912,000.00 663,366,000.00 169,995,000.00
HIV/AIDS ( TACAID) 56,634,000 0.00 226,535,100.00
DMDP 3,229,126,165 0.00 72,909,132,167.00 0.00
WORLD BANK 636,536,087.00 636,536,087.00 0.00 0.00
MMAM 359,000,000.00 115,342,300.00 431,960,000.00 0.00
CDCF 130,885,000.00 130,885,000.00 142,943,972.00 185,435,000.00
DADPS 10,415,000.00 0.00 40,000,000.00 0.00
JUMLA VYANZO VYA NJE 97,968,601,980 88,252,622,896.28 149,050,865,307.00 52,050,505,730.06
JUMLA KUU YA MAPATO: 136,521,790,980 120,220,034,608.28 191,278,229,307.00 63,184,245,286.35
26
TATHMINI YA MATUMIZI
Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2016 hadi mwezi Desemba 2016 Manispaa
ilitumia jumla ya Tshs 63,184,245,286.35 Kati ya fedha hizo Tshs. 44,159,207,404.70 ni
kwa ajili ya malipo ya Mishahara (P.E), Tshs. 3,084,870,785.00 matumizi mengineyo
(O.C) na Tshs. 2,256,845,022.92 zimetumika katika kutekeleza miradi ya Maendeleo
ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali kuu na Wafadhili. Vyanzo vya ndani (Own Source)
Manispaa imekusanya na kutumia jumla ya Tshs. 11,133,739,556.29. Kati ya hizo Tshs.
5,492,920,508.88 zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo, Tshs. 4,996,910,000.00
zimetumika kwa ajili ya matumizi mengineyo na Tshs. 643,909,047.41 kwa ajili ya
mishahara.
Changamoto katika ukusanyaji wa mapato yametokana na:
Baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kwa makusudi kulipa kodi, ada na
ushuru mbalimbali.
Hamasa ndogo kwa wananchi ya kutochangia ama kulipa ada ya usafishaji
hivyo kusababisha halmashauri kubeba mzigo mkubwa wa gharama hizi.
Baadhi ya wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara katika maeneo
yasiyo rasmi na kusababisha halmashauri kukosa mapato.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokurejesha 30% ya
makusanyo yatokanayo na kodi ya pango la ardhi kwa wakati. Hivyo
kuisababishia Halmashauri kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Serikali kuu kuchelewa kutoa ruzuku upande wa miradi ya maendeleo. Hivyo
kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati.
(i) Mkakati wa Ukusanyaji mapato:-
Halmashauri imejizatiti kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa kufanya yafuatayo:-
Kuendelea kutumia mkondo wa kisheria pale uhiari wa kulipa kodi na ada
mbalimbali unapokosekana.
Halmashauri inaendelea kuhakikisha kila mfanyabiashara wa kila chanzo
anatambulika na kuingizwa kwenye mfumo wa Mapato (mrecom) ili
afuatiliwe na kulipa kodi /Ada /stahiki na kwa wakati.
Inapendekezwa kila kikao cha WDC kuwepo “Agenda” ya ushafishaji na
ulipaji Ada ya usafi na iwe ya kudumu na viongozi wa kuchaguliwa na
27
watendaji kwenye maeneo yao ya utawala wahakikishe wanashiriki
kikamilifu kutoa hamasa kwa wananchi ili washiriki katika usafirishaji.
Halmashauri itaendelea kufuatilia urejeshwaji wa 30% kutoka wizara ya Ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi.
Kuendelea kuingiza takwimu za walipa kodi wapya na kuboresha takwimu za
walipa kodi waliopo kwenye mfumo wa GIS na MRECOM.
Kufanya ukaguzi wa walipa ushuru wa huduma (service levy) ili kubaini kama
wanalipa kiasi stahili.
Kuendelea kutumia mfumo wa kielotronik kwa kukusanya mapato katika
hospitali zetu za Halmashauri ya Temeke ili kuepuka uvujaji wa mapato ya
uchangiaji kwenye huduma za afya
4.2 MAPITIO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA KUANZIA
JULAI 2016 DESEMBA 2016
Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
ilipanga kutumia TShs. 113,088,888,173.00 kutekeleza Miradi ya Maendeleo.
Kati ya fedha hizo TShs 26,480,247,290.00 zinatokana na mchango wa
Halmashauri, TShs. 666,366,000.00 ni mchango wa Wafadhili na Tshs.
85,942,274,883.00 ni fedha za mifuko maalum.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo
hapa chini:
NA. CHANZO CHA FEDHA KIASI CHA FEDHA ASILIMIA
1 Halmashauri 26,400,477,057.00 62.2
2 Ruzuku ya maendeleo (LGCDG) 3,001,144,123.00 7.97
3
Ruzuku ya Maendeleo ya Mifugo
(LDF) 40,000,000.00
0.02
4 Ruzuku ya maji 337,284,853.00 2.15
5 Mfuko wa barabara 5,782,580,000.00 15.95
6 Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo 142,943,972.00 0.31
7 SEDP 200,000,000.00 0.21
28
8 TASAF 3,180,000,000.00 0.14
9 Wafadhili (UNICEF) 663,366,000.00 0.95
10 MMAM - LOCAL 431,960,000.00 0.86
11 DMDP 72,909,132,168.00 7.72
12 Ruzuku ya Elimu (WORLD BANK) 0.00 1.52
Jumla 113,088,888,173.00 100.00
FEDHA ZILIZOPATIKANA NA KUTUMIKA HADI DESEMBA, 2016
Hadi kufikia Desemba, 2016, Kiasi cha Tshs. 10,771,700,246.88 sawa na asilimia 9.5
kimepatikana kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo. Kati ya
fedha hizo Halmashauri imechangia Tshs. 5,492,920,508.88 mifuko maalum
imechangia jumla ya Tshs. 5,278,779,738.00 na wafadhili 40,000,000.00.
Mchanganuo wa uchangiaji ni kama ifuatavyo:-
Fedha zilizopatikana hadi Desemba 2016
NA. MCHANGIAJI JULAI 2016 – DESEMBA 2016
1 Mchango wa Manispaa 5,492,920,508.88
2 Road Fund 1,888,325,178.00
3 BASKET FUND 683,057,750.00
4 UNICEF 40,000,000.00
5 RUZUKU YA MAJI 399,543,332.00
6 TASAF 1,223,811,000.00
7 LGCDG 2,222,807,000.00
8 CDCF 142,943,972.00
JUMLA 10,771,700,246.88
4.3 UTEKELEZAJI
Hali halisi ya utekelezaji wa malengo kwa kila sekta ni kama ifuatavyo;
(I) SEKTA YA ELIMU:
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina jukumu la kutoa elimu kuanzia shule za
awali, msingi, Sekondari na Elimu ya watu Wazima. Aidha utoaji wa Elimu kwa
ujumla ni jukumu la Halmashauri, chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
29
Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katika utekelezaji
wa majukumu yake Halmashauri inao watendaji 17 katika Idara ya Elimu ya Msingi
(Makao makuu) 12 walimu na 9 wasio walimu.
(a) ELIMU YA AWALI
Katika sekta hii manispaa ya Temeke imepata mafanikio makubwa kwa upande wa
elimu ya awali na elimu ya msingi. Madarasa ya elimu ya awali yapo 49 hadi kufikia
desemba 2016, wakati idadi ya wanafunzi wa awali wameongezeka kutoka 1543
mwaka 2005 hadi 9601 mwaka 2016.
(b) ELIMU YA MSINGI
Sekta ya Elimu Msingi Katika kipindi cha 2016/2017 imefanikiwa kutengeneza
madawati 22,112 kwa gharama ya Tshs. 1,706,454,792.00, Ujenzi wa vyumba 54 vya
madarasa katika shule za Msingi za maji matitu, mbande, msufini, chamazi,Rufu,
mbagala annex na Rangi tatu, kwa gharama ya Tshs. 434,000,000.00, Umaliziaji wa
chumba 1 na Ukarabati wa vyumba 60 katika shule za msingi za maji matitu,
chamazi, mbande, chemchem, Mbagala kuu, msufini, upendo na kibasila, kwa
gharama ya Tshs. 68,1920,000.00. Hadi kufikia Desemba 2016 shule zipo 83
Aidha ina wanafunzi 138,809 hadi Desemba mwaka 2016. Nyumba za Walimu zipo
210, Walimu wa shule za Msingi 3548 hadi Desemba 2016.
Mafanikio haya yametokana na utekelezaji mzuri wa mpango wa MMEM. Aidha
vituo vya Elimu ya awali katika shule zisizo za Serikali vipo 49 hadi Desemba 2016,
Madarasa ya awali katika shule za Msingi za Serikali yapo 77 hadi Desemba 2016.
Jumla ya Walimu 126 wanajiendeleza katika hatua mbalimbali za Elimu ili kuweza
kuinua kiwango cha taaluma na kupanua uwezo wao kitaaluma. Aidha kupitia
mpango wa MWAKEM unaofadhiliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Chuo cha Ualimu Vikindu pamoja na Unicef walimu 520 kutoka katika shule 20
wameweza kusoma Moduli za masomo ya ujuzi, Hisabati na Kiingereza na kufaulu
vizuri katika masomo hayo. Walimu wamepata ujuzi mpya wa kufundisha kupitia
mhamo wa Luwaza.
Wanafunzi wanaofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanakuwa
wakichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa asilimia 100, Kwa kushirikiana na
Unicef pamoja na wananchi, Halmashauri imeweza kujenga matundu ya vyoo 27
pamoja na visima 11 katika shule za msingi 14
(c) ELIMU YA WATU WAZIMA
Halmashauri ya Manispaa inafanya juhudi ya kupunguza ujinga wa kutojua kusoma
na kuandika kwa watu wazima, Vijana na watoto waliokosa Elimu ya Msingi kwa
sababu moja au nyingine na pia kuwapatia stadi zitakazowawezesha kuinua
30
kiwango cha mapato ili waweze kujitegemea na kujiajiri kupitia vikundi vya uzalishaji
mali. Wapo jumla ya wanakisomo 67 walimu 17 na madarasa 10 ya kisomo chenye
manufaa. Aidha kuna madarasa ya MEMKWA yenye jumla ya wanafunzi 1301
walimu 50 na vituo vipo 15.Utaratibu huu unawasaidia watu wazima na wale
watoto waliokosa elimu ya msingi MEMKWA kufuta ujinga kwa wasio jua kusoma,
kuhesabu na kuandika, kuwajengea uwezo wananchi kushiriki katika shughuli za
uzalishaji mali na kutambua haki zao za msingi katika jamii anamoishi na
kuwajengea uwezo wa kukaa pamoja kubuni miradi kulingana na mazingira yao.
(ii) ELIMU YA SEKONDARI
Sekta ya Elimu ina lengo la kuongeza nafasi za wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya
Sekondari kufikia 100%. Pia Halmashauri imeendelea na ukarabati wa vyumba vya
madarasa 13 kwa gharama ya Tsh. 144,813,064.00 na ujenzi wa vyumba vya
madarasa 40 kwa gharama ya Tshs. 220,000,000.00 ambapo ni malipo ya awamu
ya kwanza.
Aidha Halmashauri imenunua madawati 3000 kwa gharama ya Tshs. 380,000,000.00
na tayari yamesambazwa katika shule za Sekondari.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina jumla ya shule za Sekondari 61, ikiwa shule
za Serikali 26 na zisizo za serikali 135.Jumla ya Wanafunzi 34,459 wakiwemo
wavulana 16,124 na wasichana 18,335 wanasoma katika shule za Serikali.
Wanafunzi wanaosoma shule zisizo za serikali ni 11,531 wakiwemo wavulana 6,286
na wasichana 5245. Wapo walimu 1285 katika shule hizo, wakiwemo wanaume 437
na wanawake 848. Walimu wa sayansi katika shule za sekondari ni 239 na wa
masomo mengine wapo 1046. Upo uoungufu wa walimu 358 kati yao wa masomo
ya sayansi ni 274 na masomo mengine ni 84. Pamoja na upungufu wa walimu pia
kuna upungufu wa nyumba za walimu 1274, vyumba vya madarasa 290 na
majengo ya utawala 18.
(iii) SEKTA YA MAJI
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri iliweka lengo la kupanua na
kuboresha huduma za maji katika kata 23 Hadi Desemba 2016
. Kazi zifuatazo zimefanyika:
Kuchimba visima virefu 15 katika kata za Kilakala, Chang’ombe, Mtoni,
Toangoma, Miburani, Azimio, Sandali, Tandika, Mbagala kuu, Mianzini,
Mbagala,Yombo Vituka (2) na Temeke (2).
Ujenzi wa miundombinu ya maji umefanyika katika kata 5 Toangoma,
Mianzini, Buza, Kurasini, Chang’ombe.
(iv) SEKTA YA AFYA:
Huduma za afya zimeendelea kuimarishwa na kuboreshwa, kwa mwaka
2016/2017 Halmashauri ilipanga kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma
pamoja na kuongeza upatikanaji wa madawa na vifaa tiba ili kuboresha
huduma za afya. Hadi Desemba 2016 shughuli zifuatazo zimefanyika.
31
Madawa na vifaa tiba vimeweza kupatikana katika vituo vyetu vya
kutolea huduma.
Idara ya afya iliweza kuweka dawa za kibailojia za kuangamiza mbu katika
kata 19 zenye mazalia ya mbu 2,542.
Katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu elimu emeendelea
kutolewa kwa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Huduma za afya mazingira katika jamii pia zimeendelea kutolewa.
Ujenzi wa zahanati ya Charambe umefanyika na unaendelea.
Ujenzi wa uzio katika zahanati ya Mbande umefanyika na kukamilika.
Umaliziaji wa uzio katika zahanati ya yombo Vituka umefanyika na
kukamilika.
Halmashauri imejenga gorofa moja kuongezea jengo la huduma za
Wazazi lenye uwezo wa vitanda 32 na wodi ya watoto wachanga.
Ukarabati sehemu ya malipo ya uanzishwaji wa huduma ya malipo kwa
njia ya mfumo wa kielektroniki (kwa kadi) umefanyika.
(v) SEKTA YA USAFI NA MAZINGIRA:
Katika kuinua kiwango cha usafi wa mji idara ya usafi na mazingira imelenga kwa
kipindi cha 2017/2018 kuongeza kiwango cha uzoaji na utupaji taka kutoka tai
193,815 sawa na 47% mpaka tani 211,632 sawa 75% ifikapo 2020
Kushirikisha jamii katika shughuli za usafi wa mazingira, kutoa elimu ya udhibiti
wa usafi wa mazingira, usafi wa barabara(kufyeka majani na kusafisha
mifereji ya wazi)
Kuhakikisha mitaa 142 inakuwa safi wakati wote
Kuondoa maji taka kwenye majengo ya Halmashauri
Kuandaa vikundi vya jamii vyakufanya usafi
Kuvihamasisha vikundi vya jamii kujua majukumu yao
Uondoshaji wa marundo ya taka kwa baadhi ya mitaa na vizimba,
Kusimamia shughuli za usafi wa mazingira,
Kuratibu shughuli za udhibiti wa athari za mazingira viwandani, maeneo
yenye vyanzo vya maji na maeneo ya wazi,
Ukarabati wa magari mabovu ya kubebea taka,
Kufanya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wananchi mara moja kwa
mwezi
(vi) SEKTA YA KILIMO
Halmashauri ya manispaa ya Temeke katika katika sekta ya kilimo kazi zilizofanyika
kuanzia julai hadi Desemba 2016
Kuandaa na kushiriki maonesho ya wakulima nanenane ya kanda ya mashariki
ambapo wakulima na wasindikaji 60,watumishi 28 pamoja na wadau wengine wa
32
Halmashauri walishiriki. Aidha wakulima 365 walipata ushauri wa kitaalam. Maghala
138 na mashine za kukoboa na kusaga131 zimekaguliwa, wakulima na wadau 250
walipata mafunzo mbalimbali ya uzalishai na usindikaji wa mazao
(vii) MIFUGO
Juma ya watumishi 20, wafugaji na wavuvi 40 waliwezeshwa kuhudhuria maonesho
ya nanenane.
Jumla ya wafugaji na wavuvi 735 walipata mafunzo ya ufugaji bora wa wanyama
na samaki kwenye mabwawa. Jumla ya mbwa 3321, na paka 499 walipata chanjo
dhidi ya kichaa cha mbwa.
(viii) SEKTA YA UJENZI:
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri imepanga kutunza barabara
zenye urefu wa km 418. Hadi kufikia Desemba 2016 barabara zifuatazo zimefanyiwa
matengenezo:-
Ujenzi wa barabara ya Kijichi – Nasaco yenye urefu wa km 1,2, kazi zilizofanyika ,
Kuondoa udongo usiofaa m318799.8, kutifua na kushindilia (Scarification) m28100
Kuweka changarawe na kushindilia m34078.43, kuweka kokoto ( Crushed
aggregate) m31040, kuchimba m33635.5 kujenga mifereji ya maji ya mvua
m3358.7, kuweka waya (BRC mesh) kwa ajili ya ubora wa mfereji m2 2082 na
kujenga makalavati (600mm) m 126, (900mm) 9.9m, kumwaga lami nyepesi
m27127 uwekaji wa tabaka jipya la lami m3300.6, kujenga matuta kupunguza
mwendo kasi 4Nr, uwekaji wa alama za barabarani.
Matengenezo ya Barabara ya Rufu yenye urefu wa Km 1.3, kazi zilizofanyika ,
Kuchonga 1.3km, kuweka kifusi (Fill) m3481,kuweka changarawe na kushindilia
m3139, kujenga makalavati 6m (600mm) 13.8m (900mm), kuchimba M3100,
kutaka na kuondoa udongo usiofaa , kujenga mifereji ya maji ya mvua M2237
na kupanga mawe m3231.
Ujenzi wa mfereji wa Tambani kazi zilizofanyika Kuchimba m3238.2, kumwaga
zege m3282.85, kuweka nyavu za chuma kuimarisha zege la mfereji (BRC mesh)
m2558.
Matengenezo ya barabara za Ndunguru & Toangoma Masaki zenye urefu wa
km 2,kazi zilizofanyika, kwa kuchonga 1.73km, kuweka changarawe na
kushindilia m31959
Matengenezo ya barabara za Pazi, Nzasa Secondary na eneo la maegesho
soko Nzasa kazi zilizofanyika, kusafisha eneo m23575 kwa kuchonga 1.15km,
33
kuweka kifusi (Fill) m3847.8, kuweka changarawe na kushindilia m3997.6, kujenga
makalavati 600mm m32, kuchimba (common Excavation) M3446 na kujenga
mifereji ya maji ya mvua M21309 na kujenga kivuko (drift) m3131.
Ujenzi wa Mfereji Evareth (Chang'ombe Barracks) , ukarabati wa kalavati la
Mwanamtoti kazi zilizofanyika Kujenga mfereji wa maji ya mvua kwa kuchimba ,
kufunga waya ,kuweka changarawe, kujenga mfereji, kusuka vikapu vya mawe,
kujenga kalavati
Matengenezo ya barabara za Lumo - Sigara, Kwa Limboa , Mwanagati na
Kidagaa zenye urefu wa km 5, ujenzi kalavati (Box) Buza kanisani (Sepeku) wa
mfereji Limboa kazi zilizofanyika, kuchonga, 3.3km, kuweka changarawe
m32137,42, kujenga mifereji m2 1596,07, kujenga kalavati Lm 65, kuchimba
m3884.1 , kupanga mawe m329.5 kumwaga zege m390.9, na kusuka chuma kg
5904
Mataengenezo ya barabara za Charambe post, Mangaya , Round table ,
Uzomboko – Kigugi, Machinjioni na Chamazi sekondari zenye urefu wa km 10.5
kuchonga 7.7km, kuweka changarawe m33284.8, kujenga mifereji m21230.60 na
kujenga kalavati (600mm) m12.
Matengenezo ya barabara za Mission - Mwanamtoti , Jeshi la wokovu , Kibonde
maji Tasafu dinspesary 9.5km kazi zilizofanyika, kuchonga 2.15km, changarawe
m3578, kujenga mifereji m21130, kujenga kalavati (600mm) M12 na kujenga
kivuko (drift) 2.
matengenezo ya barabara za Keko maendeleo, Lushoto , Kisiwani (sandali) ,
Mindu , Sandali CIUP zenye urefu wa km 7.2 kazi zilizofanyika, kuchonga 2.55km,
kuweka changarawe m31820.7 na kumwaga zegem3 63.75.
matengenezo ya barabara za Toangoma plot, Kibada , Kigamboni TBA Estate
na ungindoni 12km, kuchonga 8km, kuweka changarawe m31108, kujenga
mifereji m21139.81, kujenga kalavati 116m na kujenga vivuko 2
Matengenezo ya kawaida barabara za Dr Omary 4km, Temeke -Mbagala 3.5km,
Mgulani 1.5km, Chang'ombe 3km, Mbozi 2.1km, Taifa 1.5km, Mandela - Wailes
2km, Kurasini 2km,Mision - Kijichi- Zakhem 6.5km, Kichangani 3km,Mwembe
Madafu 2km, Mahunda 2.8km, Yombo 1.5km, Veternary 2km,Hospitali 0.5km,
Stereo roads 3km, Copper road, Evareth 0.8km, Bububu/Ruvuma 1km na Saza
1.5km kwa kuziba mashimo kwa lami m2 2540, kujenga matuta ya kupunguza
mwendo kasi na kuweka alama za tahadhari.
34
(ix) UHUSIANO
Katika kipindi cha Julai 2016 mpaka Desemba 2016 kitengo cha Tehama – Sehemu
ya uhusiano kimeweza kufanya yafuatayo;
Mchapisho; Vipeperushi 2,500 vya Idara ya Mifugo, Kilimo, fedha na Uvuvi
vilichapishwa na kusambazwa.
Jarida la mafanikio ya awamu ya nne nakala 500
Mabango 5 ya nane nane na 2 ya Dira na dharura yalichapishwa
Makala; (Documentary) 3 moja yam bio za mwenge na mafanikio ya
kipindi cha Uongozi wa awamu ya nne, vilevile utekelezaji wa mradi wa
DMDP Mikutano ngazi za Mitaa
Matangazo: Matangazo 100, yalitolewa kupitia magazeti na Radio.
Matangazo 300 yalitolewa kupitia vipaza Sauti Mitaani kuhusu Afya, Maafa,
kodi na Sikukuu za kitaifa
Manunuzi
Manunuzi yaliyofanyika ni ununuzi wa Ipad 3, Computer 4 (Laptop) na
desktop 1 na printer 1
(x) TEHAMA
Kuongoza / upanuzi wa mifumo wa MRECOM kuwezesha utumike na Idara
ya Biashara
Kutoa mafunzo kwa maafisa Biashara juu ya utumiaji wa mfumo –
MRECOM
Kuongeza wigo wa mtandao wa mawasiliano (LAN & WAN) kuwezesha
upatikanaji wakati wote
Kuboresha na kusimamia mtandao wa simu (PBAX) kwa ajili ya
mawasiliano ya ndani ya Halmashauri na ya nje pamoja na FAX
Kusimika mtandao wa ndani wa mawasiliano (LAN) katika jengo la ardhi
Kuandaa usimikaji wa mtandao wa mapato “Lipa kwa kadi” Hospitali ya
Temeke
GIS
Upatikanaji wa Satelite image upya ya mwaka 2016
Uwekaji namba – Post code katika nyumba na Mitaa 17 ya Jimbo la
Temeke
Kuboresha kodi ya Majengo kwa kutumia ramani ili kuweza kuwatambua
na kuwafikia walipa kodi kwa urahisi
(xi) IDARA YA MAENDELEO YA JAMII, USTAWI WA JAMII NA VIJANA
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Manispaa Temeke kupitia
Idara hii huhakikisha wananchi wake wanajiletea maendeleo na kustawisha familia
35
zao. Ili kutimiza azma hii, idara kwa niaba ya Halmashauri huhamasisha wananchi
kuanzisha Vikundi vya kiuchumi vya Vijana, wanawake na vikundi mchanganyiko
kwa nia ya kuinua vipato vyao ili kujiletea maendeleo, hadi Desemba 2016
Halmashauri ina jumla ya vikundi 3,486 vyenye wanachama 24,495 vikundi 2,280
vya wanawake na vikundi 1,206 ni vya Mchanganyiko wa vijana na wanawake.
Pia makundi maalum kama wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na wazee
hujengewa uwezo na kuwasaidia kwa kuwapa mitaji/mikopo.
(xii) UDHIBITI UKIMWI (TACAIDS)
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ilikuwa na lengo la kupunguza
maambukizi mapya ya VVU na kutoa huduma kwa wagonjwa na kutoa huduma
na tiba kwa watu wanaoishi na VVU/Ukimwi. Katika kufika lengo hili shughuli
zifuatazo zimefanyika:
Mapambano dhidi ya UKIMWI yameendelea kupewa kipaumbele ambapo
jumla ya vituo 66 vinatoa ushauri Nasaha (VCT). Aidha kuna vituo 36 vinavyotoa
huduma ya kupunguza maambukizi yaVirusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto.
Vituo vinavyotoa dawa za kupunguza makali ya VVU vimeongezeka kutoka
vituo 2 mwaka 2006 hadi 53 mwaka 2016. Jitihada bado zinafanyika kuongeza
vituo zaidi ili kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika vituo
vinavyotoa huduma hii.
(xiii) MIRADI MAALUM YA WAFADHILI
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ilitekeleza Programu Maalum
ambazo ni Programu ya UNICEF, SAVE THE CHILDREN na mradi wa uboreshaji wa
miundo mbinu katika maeneo yasiyopimwa (CIUP) na TASAF.
Idara ya Maendeleo ya Jamii imejikita katika:
Kuondoa umaskini na kuinua viwango vya maisha kwa kutoa mikopo ya
wanawake na vijana
Kuhamasisha jamii ili kuziwezesha kujiletea maendeleo
Kupunguza vifo kwa kuelimisha na kutoa misaada katika kupambana na janga
la ukimwi
Kutoa ushauri na kusaidia watu wanaopatwa na maafa
(xiv) MPANGO WA UHAI ULINZI NA MAENDELEO YA MAMA NA MTOTO (CSPD)
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali
inayopata fedha kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya watoto
36
UNICEF. Miradi mbalimbali imekuwa ikitekelezwa katika Idara/ Sekta za Mipango na
Takwimu, Elimu, Afya na Mazingira, Maji na Ustawi wa Jamii.
Hadi Desemba 2016 Halmashauri imetekeleza huduma zifuatazo katika sekta
mbalimbali ambazo zinashiriki katika mpango huu.
(xv) MIPANGO NA TAKWIMU
Katika eneo hili kumefanyika ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
kuwashirikisha Maafisa na wadau husika. Jumla ya miradi ya maendeleo 187
imekaguliwa na Kamati ya Ushauri ya Wilaya – DCC na timu ya uandaaji wa Bajeti
ya Halmashauri wamepatiwa mafunzo juu ya MTEF, Kuahinisha vigezo vya ufuatiliaji
na tathmini pamoja na kutembelea miradi mbalimbali.
(xvi) AFYA MAZINGIRA
Katika eneo hili Halmashauri imetoa mafunzo mbalimbali kuhakikisha maeneo ya
Manispaa ya Temeke yanakuwa safi. Jumla ya waelimisha jamii (CORPS) 485,
wamepata mafunzo ya Afya na jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.
Maafisa Afya 75 wamepatiwa mafunzo juu ya usimamizi wa Afya na sheria ya usafi
wa mazingira na jinsi ya kuhimiza wanajamii kuitambua. Pamoja na kuwafundisha
maafisa Afya pia jumla ya mafundi waashi 135 kutoka Kata zote 30 wamepewa
mafunzo kuhusu ujenzi wa vyoo kwa gharama nafuu, wamefundishwa baba/mama
Lishe 195 juu ya uandaaji wa vyakula na usafi binafsi.
Walimu wa Afya mashuleni 120 walipatiwa mafunzo juu ya Afya na usafi wa
mazingira na kuunda vikundi vya wanafunzi 20 kwa ajili ya kufundishana wao kwa
wao.
(xvii) USTAWI WA JAMII
Wajumbe 153 ngazi ya Wilaya wamefundishwa sheria ya mtoto, timu ya ulinzi na
usalama ngazi ya kata na mtaa wajumbe 200 wamefundishwa juu ya kutoa
msaada wa kisaikolojia kwa watoto walioathirika na ukatili.
Vikao vya robo mwaka vimefanyika ngazi ya Wilaya kwa wajumbe 25 na kata
wajumbe 400
Uhamasishaji juu ya ulinzi na usalama kwa kutumia ngoma, maigizo umefanyika
kwa kata 4
Watoto 40 wamepata huduma ya matibabu na nauli.
Wazee na walemavu 10 walipewa fedha za kujikimu na vifaa vya viungo
Mama mmoja aliyejifungua watoto 3 alipewa fedha za kujikimu
(xviii) MIPANGO MIJI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuanzia tarehe 25/7/2016 ilichukua wathamini
wanafunzi wapatao 105 ili kusaidia kufanya uthamini wa majengo ili kutoza kodi ya
37
majengo kwakuwa majengo mengi yalionekana kutozwa viwango mlingano ( flat
rate)
Wanafunzi hao waliweza kukagua majengo 93,000 ambayo Halmashauri itaweza
kukusanya zaidi ya Tshs. 3,000,000,000 kama kodi ya majengo kwa mwaka wa
fedha 2016/17
Maeneo yaliyotembelewa katika zoezi hili ni kata za chamazi yenye mitaa 10, kata
ya mianzini yenye mitaa 4, kata ya mbagala kuu yenye mitaa 10, kata ya mbagala
yenye mitaa 6, kata ya kilungule yenye mitaa 5, Kata ya kibonde maji yenye mitaa
5, kata ya Toa ngoma yenye mitaa 14 na kata ya charambe yenye mitaa 8.
MAENEO YA UMMA YALIYOFANYIWA UTHAMINI NA KULIPWA FIDIA
-Zahanati ya Buza
-S/msingi mbagala
- Ofisi ya kata kijichi
- Barabara ya Yombo vituka
Kulipa watumishi 6 wa kitengo cha leseni za makazi kama ushauri wa kitaalam
wa kuandaa leseni za makazi, kutoa nakala za kadi za ardhi, kupokea nyaraka za
mikopo, kuongeza muda wa umiliki,kuhamasisha umiliki, na kupokea maombi
mapya ya leseni.
(xix) UWEKEZAJI
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ilipanga kuendeleza
maeneo 10 ya uwekezaji hadi Desemba 2016, shughuli zifuatazo zimefanyika:
Kufanya ziara katika maeneo ya uwekezaji
Umilikishaji maeneo ya uwekezaji
Kukamilisha mchakato wa zabuni katika maeneo ya uwekezaji
Mafunzo ya kamati ya uwekezaji
Upembuzi yakinifu (Feasibility study)
Kuandaa Sera ya uwekezaji na Sera ya mradi wa upimaji wa Viwanja
4.4 CHANGAMOTO
Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kupata mafanikio makubwa
katika utoaji wa huduma kwa wananchi bado kumekuwepo na matatizo
mbalimbali yaliyojitokeza na hivyo kuathiri utendaji wa baadhi ya majukumu yake.
Baadhi ya matatizo hayo ni:
38
Kuchelewa kupokelewa kwa fedha za ruzuku za Miradi ya Maendeleo na
matumizi ya kawaida kwa wakati au kutokupatikana kabisa kwa fedha hizo
kama zilivyoidhinishwa katika bajeti ya mwaka husika.
Ongezeko kubwa la idadi ya watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke
ambalo huletea ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kijamii na
kiuchumi.
Kuongezeka kwa idadi kubwa ya watoto wanaojiunga na elimu ya
msingi/kuandikishwa darasa la kwanza.
Kutokurudishwa kwa kodi ya Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi na makazi ambayo
inakusanywa na Halmashauri kwa niaba ya Wizara.
Uhaba wa maeneo ya upanuzi kwa ajili ya kutolea huduma ikiwemo maeneo
ya zahanati, elimu msingi na sekondari.
Upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi katika shule za sekondari
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke kutopatiwa ruzuku kulingana na
mahitaji hivyo kuendelea kuhudumiwa na Fedha za Halmashauri.
Mwitikio mdogo wa wananchi katika ulipaji wa Ushuru na kodi mbalimbali.
4.5 MIKAKATI
Kuweka msukumo mkubwa zaidi katika kuimarisha ushirikiano wa
wadau wote katika kupambana na umasikini hususani katika kutoa
elimu na mikopo mingi zaidi kwa sekta inayojiajiri ambayo ina uwezo
wa kutoa ajira kwa vijana wengi wa jinsia zote.
Kuhamasisha matumizi endelevu ya maliasili ikijumuisha matumizi
endelevu ya ardhi hasa uratibu wa maendeleo ya makazi
yasiyopimwa.
Kuboresha mbinu za ukusanyaji wa mapato na kodi mbalimbali zilizopo
kwa mujibu wa sheria.
Kusimamia na kuendeleza vikundi vya vijana wanawake, uratibu na
utekelezaji wa mikakati ya kupambana na vita dhidi ya UKIMWI, rushwa
na umaskini.
Uhamasishaji na uundaji wa vyama vya kuweka na kukopa makazini,
maofisini na viwandani kama silaha muhimu dhidi ya umaskini.
39
Kuboresha mbinu za kushughulikia kero za wananchi kwa kuanzisha
dawati la upokeaji kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi.
Kuendeleza jitihada za kuhamasisha wananchi kushiriki katika
kutekeleza miradi ya maendeleo hasa ujenzi shule za Sekondari.
Kuendelea kuhamasisha wananchi ulipaji wa kodi na kuboresha
vyanzo vya mapato ya Halmashauri.
Kuhamasisha wananchi kutumia uzazi wa mpango.
Kuboresha makazi.
Kuongeza na kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi .
Kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeo.
40
SURA YA 5
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA KAWAIDA PAMOJA NA MIRADI YA
MAENDELEO KWA MWAKA 2017/2018
5.0 MAPATO:
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2017/2018 imekadiria
kukusanya na kupokea jumla ya TShs. 236,746,512,167.00 kutoka katika vyanzo
mbalimbali vya mapato ambapo jumla ya Tshs. 197,590,436,667.00 ni Ruzuku
kutoka Serikali Kuu, Jumla ya Tshs. 38,907,388,000.00 mapato yake yenyewe na
Wahisani wanatarajiwa kuchangia Tshs.248,687,500.00 kama inavyoonyesha katika
jedwali na. 1.
Jedwali Na. 1: Makadirio ya Mapato ya Halmashauri kwa mwaka 2017/2018
NA. CHANZO KIASI (TSHS) ASILIMIA
1 Mapato ya Manispaa (own source) 38,907,388,000 16.43
Jumla ndogo 38,907,388,000
Vyanzo vya nje:
2 Ruzuku - Mishahara na matumizi
mengineyo
103,090,104,500 43.54
3 Fedha za maendeleo - Mifuko
maalum
18,124,175,000 7.66
4 DMDP 76,376,157,167 32.26
Jumla Ndogo 197,590,436,667
5 Wahisani (UNICEF) 248,687,500 0.11
Jumla kuu 236,746,512,167 100
RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2017/2018 inategemea kupata
Ruzuku kutoka Serikali Kuu jumla ya T.shs. 197,590,436,667.00 ambazo zitatumika
katika maeneo ya mishahara na utoaji wa huduma. Jedwali 2 lifuatalo
linaonyesha mchanganuo wa Ruzuku kutoka Serikali Kuu.
41
Jedwali Na. 2: Ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa mwaka 2017/2018:
Mishahara 100,939,169,000
Matumizi Mengineyo 2,150,935,500
Ruzuku ya Mifuko Maalum
Ruzuku ya Maendeleo (LGCDG) 2,160,610,000
Elimu bure shule za msingi 1,227,314,000
Elimu bure shule za sekondari 1,035,320,000
Mfuko wa maendeleo ya Jimbo 174,687,000
Mfuko wa barabara 6,431,400,000
Livestock Fund 10,415,000
Mfuko wa pamoja wa Afya 2,804,429,000
DMDP 76,376,157,167
Ada ya TASAF 3,180,000,000
Ruzuku ya maji 1,100,000,000
Jumla Mifuko Maalum 94,500,332,167
Jumla Ruzuku ya Serikali kuu 197,590,436,667
Wahisani (UNICEF) 248,687,500
Jumla kuu 197,839,124,167
WAHISANI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2017/2018 inategemea kupata
fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali jumla ya TShs. 248,687,500.00 ambazo
zitatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Wafadhili hao ni kama
inavyoonekana katika jedwali namba 3.
Jedwali Na. 3: Orodha ya Wahisani:
Na. Jina Kiasi
1 UNICEF 248,687,500.00
Jumla kuu 248,687,500.00
5.1 MATUMIZI:
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2017/2018 imekadiria
kutumia jumla ya Tshs. 236,746,512,167.00 katika maeneo ya Mishahara,
Matumizi mengineyo na Miradi ya maendeleo.
RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU:
Kwa mwaka 2017/2018 Halmashauri itatumia jumla ya TShs. 197,590,436,667.00
kutekeleza vipaumbele vya maendeleo na maeneo ya utoaji wa huduma, Kati ya
fedha hizo, TShs. 100,939,169,000.00 ni Mishahara ya watumishi na Kiasi cha TShs.
42
2,150,935,500.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Halmashauri pia itatumia TShs.
94,500,332,167.00 ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu kupitia Mifuko Maalum.
Jumla ya matumizi kwa maeneo yakijumuisha matumizi ya kawaida, mifuko
maalum, Miradi ya Maendeleo ni kama yanavyoonekana katika Jedwali Na.4
lifuatalo.
Jedwali Na. 4: Mgawanyo wa Matumizi maeneo ya Ruzuku:
Na. Eneo la matumizi Kiasi (Tshs)
1 Mishahara ya Watumishi 100,939,169,000.00
2 Matumizi Mengineyo 2,150,935,500.00
3
Matumizi ya fedha za mifuko
maalum 94,500,332,167.00
JUMLA 197,590,436,667.00
MATUMIZI FEDHA ZA NDANI-(OWN SOURCE)
Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 itatumia
Tshs. 38,907,388,000.00 kwa matumizi mengineyo, mishahara, miradi ya maendeleo
na uchangiaji(Cost sharing). Kati ya fedha hizo Tshs. 23,344,433,000.00 zitatumika
kutekeleza miradi ya maendeleo na Tshs 14,824,228,972.00 zitatumika katika
maeneo ya uendeshaji wa shughuli za ofisi na Tshs. 738,726,028.00 zitatumika katika
kulipa mishahara ya watumishi.
Jedwali Na. 5 Matumizi Fedha za Halmashauri(Own Source)
NA. MAELEZO KIASI (TSHS)
1 Matumizi mengineyo 14,824,228,972.00
2
Kuchangia Miradi ya
Maendeleo
23,344,433,000.00
3 Mishahara ya Watumishi 738,726,028.00
Jumla kuu: 38,907,388,000.00
MATUMIZI (WAHISANI)
Halmashauri kwa mwaka 2017/2018 itatumia jumla ya Tshs.248,687,500.00
kutoka kwa Wahisani wa UNICEF.