masiha - messiah...kitabu kinahusu neno la mungu aliye hai. kupitia kwa neno hili, kwa uongozo wa...

412
www.boazmultimedia.nl 2018 Masiha aliyeonyeshwa kwenye Maandiko Matakatifu MWONGOZO WA KUSOMA BIBLIA Hendrik Schipper

Upload: others

Post on 05-Dec-2020

13 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

Page 1: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

www.boazmultimedia.nl

2018

Masiha

aliyeonyeshwa kwenye Maandiko Matakatifu

MWONGOZO WA KUSOMA BIBLIA

Hendrik Schipper

Page 2: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

2

Ninawashukuru sana watu, waliotajwa hapa chini, ambao kwa njia moja au nyingine,

walinisaidia kukamilisha kuandika kitabu hiki.

Dkt. Ir. Henk Post

Dkt. Willem H. Velema

Mke wangu Kenna

Nukuu zote kutoka kwa Maandiko zinawasilishwa kwa Biblia ya Kiswahili

Nunua kwenye mtandao kupitia: www.themessiahrevealed.com

ISBN/EAN 978-94-91382-30-7

Kimechapishwa na: Boaz Multi Media - Veenendaal – Uholanzi.

This book is the Swahili translation of “The Messiah revealed in the Holy Scriptures”

akimiliki: Hakimiliki ©2016 ya Hendrik Schipper/Boaz Multi Media.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu za chapisho hili zinaweza kutolewa upya,

kuhifadhiwa kwenye mfumo wa upatikanaji tena, au kusambazwa kwa muundo au mbinu yoyote

- ya kielektroniki, kimitambo, fotokopi, kurekodiwa, au nyingine yoyote - isipokuwa nukuu fupi

za kuchapishwa kwenye uhakiki, bila idhini ya awali ya mchapishaji.

Page 3: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

3

MAUDHUI

Maudhui mafupi ya kitabu

Utangulizi 5

Majina wa vitabu vya Biblia 7

Mwongozo wa masomo haya ya Biblia

Orodha ya Mafungu ya Biblia yaliyoangaziwa 9

Mada 17

Ufalme wa Masiha wa siku zijazo 27

MWANZO – MALAKI - uangaziaji wa mafungu ya Biblia 30-393

Marejeleo ya Biblia ya Kiebrania (Agano la Kale) 395

-Nukuu na vionyeshi vya Biblia ya Kiebrania kwenye

Vitabu vya Matendo ya Mitume

-Nukuu na vionyeshi vya Biblia ya Kiebrania kwenye

nyaraka za Paulo 403

Bibliografia 409

Page 4: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

4

MUKHTASARI MFUPI WA KITABU

Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai.Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu,unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani.

Nabii Hosea anasema kwenye Hosea 4:6:

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.”

Na Masiha anasema katika Yohana 5:39:

“Mnayasoma Maandiko kwa bidii; kwa sababu mnadhani kwamba humo mtapata uzima wa milele;

na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia Mimi.”

Masiha anasema haya kuhusu mistari iliyo kwenye Biblia ya Kiebrania.Hivyo, ni muhimu kiasi gani, kufahamu ni mafungu yapi ya Maandiko

ambayo Masiha alimaanisha.

Katika kitabu hiki utapatana na mafungu zaidi ya 300 kutoka kwa Biblia ya Kiebrania ambayo yanarejelea moja kwa moja au kwa njia isiyo ya

moja kwa moja Masiha aliyeahidiwa.Mafungu haya yanazingatiwa na kuelezwa kwa mujibu wa mafungu

kwenye Agano Jipya ambayo yanahusiana nayo.

Kitabu hiki ni somo la Biblia na mwongozo wa kipekee.Kitabu hiki ni tofauti kwa sababu ni vitabu vichache, iwapo vipo, kwa

sasavinaonyesha umoja wa Biblia kwa njia hii.

Kitabu hiki kinaweza kutumiwa kusomea Biblia au kama marejeleo.

Page 5: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

5

Kitabu hiki kinahusu Masiha wa Biblia ya Kiebrania. Kwenye kiini cha Torati, Manabii na Maan-

diko Matakatifu ni kuja kwa Masiha na huduma yake. Masiha atakuwa Mtu Myahudi Atakayekuja

duniani kwanza kabisa kuokoa na kuweka huru watu wake ambao ni taifa la Kiyahudi. Lakini, ku-

lingana na ahadi zilizopewa Abrahamu, mataifa yale mengine yote pia yatabarikiwa kupitia kwake.

Na taifa la Kiyahudi litahusika katika mchakato huo.

Wakati wake alipokuwa duniani, Masiha Yeshua alisema kuwa Maandiko yanamshuhudia. Kwa

hivyo kila kitu kilichofanyika wakati wa kuishi Kwake duniani, kilitabiriwa kwenye Biblia ye Kie-

brania. Hii ina maana kuwa tunaweza kuthibitisha kwenye Maandiko iwapo Yeshua ndiye au siye

Masiha wa kweli. Masiha alikuja duniani kuleta upatanisho wa deni la dhambi, lakini Alitumia

sehemu kubwa ya miaka Yake duniani kufafanua Maandiko kuhusu kuja kwa Masiha na huduma

Yake. Kitu pekee ambacho wanafunzi na wafusai wake Wayahudi walifanya ni kufafanua Maan-

diko na kuita watu wamgeukie Mungu na wawe na imani kwa Masiha Yeshua.

Ni wazi kwamba bado kuna umuhimu mkubwa wa kujua kile kinachofundishwa na Biblia ya Kie-

brania kuhusu Masiha, na ni wapi inafundisha.

Kitabu hiki kitakupa mafungu ya Biblia zaidi ya 300 yanavyohusu kuja kwa Masiha na huduma

Yake. Kitataja pia jinsi mafungu hayo yanavyohusiana na matukio na matangazo yaliyorekodiwa

kwenye Agano Jipya kamilishi.

Kuna aina mbili ya mafungu yanayohusu Masiha. Kwanza, kuna mafungu ambayo moja kwa

moja yanaweza kutambuliwa kuwa yanayohusu Masiha - haya yanaitwa mafungu ya “moja kwa

moja”. Pili, mafungu mengine yanaweza kutambuliwa tu kuwa yanamhusu Masiha na wasomaji

ambao wanafahamu Agano Jipya - haya yanaitwa mafungu yasiyo ya “moja kwa moja”. Kitabu

hiki kinatumia maandishi ya mlazo (kiitaliki) au yaliyokolezwa kwa mafungu ya moja kwa moja.

Mafungu yote yanayohusu Masiaha yamechapishwa kwenye mandhari nyuma ya rangi ya kijivu.

Ili kupunguza ukubwa wa kitabu hiki, mafungu mengi hayajachapishwa ila yametajwa tu kama

mafungu ya marejeleo.

Mafungu yanayohusu Masiha yanarejelea pia kuja Kwake duniani kwa mara ya pili ili kuanzisha

ufalme Wake. Taifa nzima la Kiyahudi litarejea tena kwa ardhi ya babu zao, watamjua Bwana, na

Masiha atakuwa Mfalme wao. Mataifa yote yatakuwa chini Yake. Mafungu yanayorejelea haya ya-

metajwa kwenye sura iliyo kando na kuonyeshwa kwa alama ya #1 - #7.

Kwenye Biblia ya Kiebrania tunapata pia ahadi nyingi zinazohusiana na watu wasio Wayahudi.

Ahadi hizi zinahusiana na wakati uliopo, na Ufalme wa wakati ujao.

Kitabu hiki kimetokana na kuomba bila kukoma ili kupewa hekima na kuongozwa na Roho

UTANGULIZI

Page 6: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

6

Mtakatifu. Ni ombi langu kuwa kusoma mafungu haya kutakuwa kwenye baraka; kwamba kwa

kusoma maneno ya Mungu pazia itaondolewa, giza litatokomea na mwangaza wa Roho wa Mungu

utakuwepo na kufanya kazi.

Hendrik Schipper

Julai 2018

UTANGULIZI

Page 7: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

7

Agano la Kale

Mwanzo

Kutoka

Mambo ya Walawi

Hesabu

Kumbukumbu la Torati

Yoshua

Waamuzi

Ruthu

1 Samweli

2 Samweli

1 Wafalme

2 Wafalme

1 Mambo ya Nyakati

2 Mambo ya Nyakati

Ezra

Nehemia

Esta

Ayubu

Zaburien

Mithali

Mhubiri

Wimbo Ulio Bora

Isaya

Yeremia

Maombolezo

Ezekieli

Danieli

Hosea

Yoeli

Amosi

Obadia

Yona

Mika

Nahumu

Habakuki

Sefania

Hagai

Zekaria

Malaki

Agano Jipya

Mathayo

Marko

Luka

Yohana

Matendo ya Mitume

Warumi

1 Wakorintho

2 Wakorintho

Wagalatia

Waefeso

Wafilipi

Wakolosai

1 Wathesalonike

2 Wathesalonike

1 Timotheo

2 Timotheo

Tito

Filemoni

Waebrania

Yakobo

1 Petro

2 Petro

1 Yohana

2 Yohana

3 Yohana

Yuda

Ufunuo wa Yohana

MAJINA NA MPANGILIO WA VITABU VYA BIBLIA

Page 8: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

8

Kwa kufuata mtindo wa Petro, Stefano na Paulo, ambao walitangaza Masiha kutoka kwa Biblia ya

Kiebrania (kwa utaratibu wa mfululizo), kitabu hiki kinanuia kuwa mwongozo sawia.

Kitabu hiki kinaweza pia kutumiwa kama:

a. Mwongozo wa jumla kwa nyakati zako tulivu;

b. Somo linalofuata mada;

c. Nyenzo ya marejeleo. Hivyo, kwa mfano, utapata mwishoni mwa kitabu mukhtasari wa

mafungu mengi ya Agano Jipya ambayo yanahusiana moja kwa moja na Biblia ya Kiebrania.

Aidha, kimeangazia kwa makini mada ambazo kwa kawaida hazijasisitizwa sana kama:

- Uhusiano kati ya sadaka, sherehe na Masiha;

- Kubadilishwa kwa jamii ya Wayahudi;

- Kurudi kwa Masiha;

- Kurejea kwenye ardhi iliyoahidiwa;

- Agano Jipya

Muombe Bwana akupe mwongozo wa Roho Mtakatifu unaposoma na kutafakari Neno lake.

H.S.

MIONGOZO YA SOMO HILI

Page 9: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

9

Mwanzo3:15

3:21

9:26,27

12:3

14:18

17:7,8,19,21

21:12

22:8

22:17,18

26:3-5

28:14

49:8-12

Kutoka3:6

3:14

12:5-14,22-24

12:46

15:1,2

17:6

23:20-21

25:8-9,22

28:12

28:29,36

28:37,38

29:45,46.

33:19

Mambo ya Walawi1:5,13

2:1,2

3:1-5,16

4:3-12, 27-29

7:16

16:1-31

17:11

Mambo ya Walawi22:17-21

23:6-8

23:9-14

23:15-21

23:33-43

26:11,12

HESABU

19:2,3,9

21:9

24:7,8,15-19

28:3-10

Kumbukumbu la Torati11:18-20

18:15-19

21:23

33:3

Ruthu4:13,14,17,21,22

1 Samweli2:10

2 Samweli7:12-16

22:20-25

23:1-4

2 Wafalme1:6,11,12

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

31

32

32

33

33

33,34

34

34

34

35

36

36

38

38

38,39

40

40

40

41

41

42

43

43

43

44

46

46

46,47

48,49

51

52,53

53

UKURASA UKURASA

55

57

57,58

59

60

62

64

64

65

66,67

69

70

72

72

74

75

76

77

78

80

Page 10: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

10

1 Mambo ya Nyakati17:11

17:12

17:13

17:14

Ayubu17:3

19:25-27

Zaburien1:1-6

2:1

2:2,3

2:4-6

2:7

2:8

2:9

2:10-12

8:1,2,3

8:7

16:8-11

17:15

18:5-7

18:22-25

20:5-7

21:5

21:6

21:7,8

22:1-3

22:6

22:7

22:8

22:9,10

22:11

22:12,13

22:14

Zaburien22:15

22:16

22:17

22:18

22:22

22:23-31

23:1-6

24:3

24:7-10

27:2

27:12

28:8

30:3

31:4,5

31:11,15

33:6,9

34:20

35:4-6

35:11,12

35:19

38:12,13,20

40:2,3

40:6

40:7

40:8

40:9,10

40:14

41:5-9

42:7

43:3

45:1,2

45:3,4

45:5

45:6,7

45:9,13-15

45:16,17

46:4-11

47:1-9

49:15

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

81

81

81

82

83

83

84

84

85

85

86

87

87

88

88,89

89

89

90

91

92

92

93

94

94

95

95

96

96

97

97

97,98

98

99

99

100

100

100

101

102

103

103

104

104

104

105

105

105

106

106

106

107

107

108

108

109

109

110

110

110

111

111,112

112

113

114

114

116

117

118

119

120

120

UKURASA UKURASA

Page 11: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

11

Zaburien50:2-6

51:17

53:6

55:4,5,12-14

61:6,7

62:3,4

65:2

67:1-7

68:1-4

68:18

69:4

69:7-9

69:19-21

69:26

71:20

72:7-19

75:7,8

78:2

80:14,15,17

85:9

85:10-13

86:9

86:12-13

86:15

88:14-18

89:3,4

89:19

89:20,21

89:22

89:23

89:24

89:25

89:26

89:27-29

89:35-37

90:2

91:11, 12

91:13

Zaburien91:14-16

93:1,2

95:1-3

95:7-11

96:1-3

96:7-13

97:1-6

98:1-3

98:4-9

99:1-5

102:1-12

102:13-22

102:25-27

103:3,12

103:4

103:5

103:13

103:11,17

103:22

107:1-16

107:25-29

109:1-5

109:8

109:25

110:1,2

110:3

110:4

110:5,6

110:7

112:4

118:22-24

118:26, 27

119:97-103

129:3

130:7,8

132:11,12

132:13

132:14

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

122

123

124

125

126

126

127

127

128

129

130

130

131

132

132

133

134

135

135

136

136

137

138

138

138

139

139

140

141

141

142

142

142

143

144

144

144

144

145

145

146

146

148

149

150

151

15151,152

152

153

154

155

155

156

156

157

157

158

158

159

159

160

160

160

161

162

163

163

163

164

164

164

165

166

166

167

167

UKURASA UKURASA

Page 12: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

12

Zaburien132:15

132:16

132:17,18

138:4,5

139:1-4

139:7-10

145:10-13

146:8

147:3,6

147:2,13-14,20

149:1-5

149:6-9

Mithali1:23

8:22-29

8:9,31

30:4

Wimbo Ulio Bora 5:16

Isaya2:2,3

2:4

2:5

4:2

4:3

4:4-6

5:1,2

6:1-4

6:9,10

7:14-16

8:13-15

9:1

Isaya9:2-4

9:6,7

10:20-22

11:1-3

11:4,5

11:6-9

11:10-12

12:1-6

14:1-3

16:5

17:7

19:23-25

22:22

24:13-16

24:18-23

25:6-12

26:1-4

26:19-21

27:1-3,6,12,13

28:15,16

29:10,13,14

29:18

29:19

29:22-24

30:18-33

32:1-4

32:15-18

33:17-24

35:1-10

40:1-5

40:9-11

41:8-20

41:25

41:26,27

42:1

42:2-4

42:6,7,16

42:21

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

169

1169

169

170

171

172

172

173

174

174

175

176

177

177

178

179

180

181

182

183

184

185

186

188

188,189

189

190

191

191

192

193

195

196,197

198

198,199

199,200

201

202

203

203

204

205

206

207

208

210

211

212

213

214

215

216

219

219

220

220

221

223

224

225

227

228

228,229

229

230

231

232

UKURASA UKURASA

Page 13: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

13

Isaya43:1-21

44:1,2

44:3-8

44:21-26

45:17-18

45:21-25

46:3-4,13

47:4

48:15-17

49:1

49:2

49:3

49:4

49:5

49:6

49:7

49:8-26

50:3

50:4

50:5,6

50:7-9

51:1-23

52:1-12

52:13

52:14

52:15

53:1,2

53:3

53:4-6

53:7,8

53:9

53:10,11

53:12

54:1-17

55:1

55:2

55:3

55:4

Isaya55:5

55:6

55:7

55:10,11

55:12,13

56:6-8

57:15-18

57:19

59:16

59:17

59:18-20

59:21

60:1-5

60:6-21

61:1-3

61:4-9

61:10,11

62:1-3

62:4-9

62:10-12

63:1-6

63:7-9

65:1,2

65:8-10

65:17-25

66:1

66:2

66:10-14

66:15-24

Yeremia3:14-19

4:2

10:7

12:15

16:14,15,19

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

233

234

235

236

237

238

238,239

239

239,240

240

241

241

242

242

243

244

244,245

246

246

247

247

248

249

251

251

252

253,254

254

255

256

257

257

258

259

260

261

262

263

262

263

264

264

265

266

267,268

269

269

270

271

271

272

273,274

275

276,277

277

277,278

280

281

282

282,283

284

284

285,286

286

287

287,288

288,289

291

292

293

293

294

UKURASA UKURASA

Page 14: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

14

Yeremia17:10

23:3,4,7,8

23:5,6

28:9

30:3-20,23,24

30:21-22

31:1-9

31:15

31:22

31:31-34

32:37-41

33:6-13

33:14-18,22

50:4-7,19,20

Maombolezo3:25,26

3:30

Ezekieli1:26

11:17-20

16:60-63

17:22-24

20:34-44

21:26,27

33:32,33

34:11-15,22-31

36:8-15,24-38

37:1-14

37:21-28

38:16

38:18

38:19

38:20

38:21

Ezekieli38:22

38:23

39:6-8,21-29

47:6-23

Danieli2:34,35,44,45

7:13,14,18,22,27

9:24

9:25

9:26

9:27

10:5,6

12:1

12:2

12:3

Hosea1:10,11

2:15-23

3:4

3:5

6:1-2

6:3

11:1

13:14

14:4-8

Yoeli2:1-17

2:18-27

2:28,29

2:30-32

3:1-21

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

295

296

297

297

298

299

300

301

302

302

304

305

306

307

309

309

310

310

311

312

313

313

314

315

317

318

319,320

321

321

321

322

322

322

322

324

325,326

327

328

330

331

331,332

332

333

333,334

334

335

336

337

338

339

339

340

340

340

341

343

343

344

346

347

UKURASA UKURASA

Page 15: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

15

Amosi8:9

8:11

9:11-15

Obadia1:17-21

Yona1:17

2:2-7

Mika2:12,13

4:1-4,7

5:1

5:2

5:3,4

5:5

7:15-20

Habakuki2:3

2:4

2:14

Sefania3:9-20

Hagai2:7-10

2:24

Zekaria1:16,17

2:1-13

3:1-10

6:12,13,15

8:3-23

9:9

9:10-12

10:3-12

11:4-6

11:7

11:8

11:9

11:10-11

11:12,13

12:1-14

13:1,2

13:7

13:8,9

14:1-21

Malaki1:11

3:1

3:2-5,16-18

4:1-4

4:5,6

ORODHA YA MAFUNGU YA BIBLIA YALIYOANGAZIWA

349

349

349,350

351

352

352

353

354

355

355

356

356

357

359

359

360

361

363

363

364

364,365

366,367

368

370

372

372

374

375

376

377

377

378,379

380

381

382

383

383

384,385

388

388

389,390

391

392

UKURASA UKURASA

Page 16: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema
Page 17: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

17

A. Masiha kama Mtu.

01. Masiha ni wa ukoo wa Abrahamu.

Mwanzo 9:26,27; Mwanzo 17:7,8,19,21;

Mwanzo 21:12; Mwanzo 22:17,18;

Mwanzo 28:14.

02. Masiha ni wa ukoo wa Yuda.

Mwanzo 49:8-12.

03. Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

Ruthu 4:13,14,17,21,22; 2 Samweli 7:12-16;

1 Mambo ya Nyakati 17:11; Isaya 11:1-3;

Isaya 16:5; Yeremia 30:3-24.

04. Masiha amekuwepo tangu milele.

Zaburi 21:5; Zaburi 89:28-30; Zaburi 90:2;

Zaburi 93:1,2; Mithali 8:22-29; Mika 5:1.

05. Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

Kutoka 23:20,21; 1 Mambo ya Nyakati 17:13;

Zaburi 16:8-11; Zaburi 20:5-7; Zaburi 28:8;

Zaburi 89:27; Mithali 8:30-31;

Isaya 42:21; Isaya 49:5; Yeremia 30:21,22.

06. Masiha ndiye Muumbaji.

Zaburi 33:6,9; Zaburi 102:26-28; Isaya 44:1-

8,21-24,26; Yohana 1:1-3.

07. Atakuwa Masiha wa Israeli.

Isaya 4:2; Isaya 49:6; Danieli 9:25.

08. Majina na vyeo vya Masiha.

Kutoka 17:6; Zaburi 95:1-3; Isaya 5:1-2;

Isaya 9:5,6.

B. Asili ya Masiha.

01. Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

2 Samweli 7:12-16; Zaburi 2:7;

Mithali 30:4; Isaya 43:1-13,18-21;

Zaburi 89:4,27,28.

02. Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

Mwanzo 22:8; Kutoka 12:5-14,22-24; Mambo

ya Walawi 4:3-12; Mambo ya Walawi 4:27-29;

Mambo ya Walawi 16:1-31; Mambo ya

Walawi 22:17-21;

Hesabu 28:3,4; Isaya 53:7.

03. Masiha ndiye Mwana wa mtu.

Zaburi 80:15,16,18; Isaya 7:14; Isaya 9:5,6;

Ezekieli 1:26; Danieli 7:13.

04. Sifa za Uungu za Masiha.

Zaburi 2:7; Zaburi 24:7,10; Isaya 11:2;

Yeremia 23:5,6; Mika 5:4.

05. Masiha amejawa na Roho na Mtakatifu.

Zaburi 45:8; Zaburi 89:21,22; Isaya 11:1-3;

Isaya 42:1.

06. Masiha ndiye Mchungaji mwema.

Zaburi 95:7; Isaya 40:9-11;

Ezekieli 34:11-15,22-24; Mika 2:12,13;

Zekaria 11:4-6,7.

07. Uweza wa Yote wa Masiha.

Zaburi 8:7; Zaburi 107:25-29; Zaburi 110:3;

Isaya 22:22; Isaya 40:10;

08. Ujuzi wa Yote wa Masiha.

Zaburi 139:1-4; Yeremia 17:10.

09. Uwezo wa Masiha wa kuwa Kila Mahali.

Zaburi 139:7-10.

MADA

Page 18: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

18

10. Unyenyekevu na umaskini wa Masiha.

Isaya 42:2-4.

11. Utiifu wa Masiha.

Zaburi 1:1-6; Zaburi 18:22-25; Zaburi 40:8,9;

Isaya 53:7,8.

12. Ukamilifu wa Masiha.

Zaburi 45:3; Isaya 53:9; Mika 5:3.

13. Mamlaka ya Masiha.

Kutoka 3:6; Kumbukumbu la Torati 18:18,19;

2 Samweli 23:1-4; Zaburi 98:9;

Zaburi 110:1,2; Zekaria 9:10.

14. Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

Zaburi 21:6; Zaburi 45:4,5; Isaya 4:2;

Isaya 12:1-6; Isaya 49:3; Isaya 60:1-5.

15. Masiha atajawa na rehema.

Zaburi 103:13; Zaburi 112:4; Isaya 66:2;

Zekaria 11:7.

16. Uweza na nguvu ya Masiha.

Kutoka 17:6; Zaburi 45:6; Isaya 40:9-11; Isaya

49:2,7; Mika 2:12,13.

17. Upole na udhaifu wa Masiha.

Zaburi 45:4,5; Isaya 29:19.

18. Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

Zaburi 17:15; Zaburi 21:6; Zaburi 45:2,3;

Zaburi 99:1-5; Wimbo Ulio Bora 5:16;

Isaya 33:17-24; Isaya 42:21; Danieli 10:5,6.

19. Fumbo la Masiha.

Kutoka 3:14; Zaburi 78:2.

20. Upendo wa Mfalme kwa watu Wake.

Isaya 62:4-9; Hosea 2:15-23.

21. Masiha ndiye Nuru.

2 Samweli 23:1-4; Zaburi 43:3; Isaya 2:5;

Isaya 9:1-3; Isaya 42:6,7,16;

Isaya 60:19,20.

22. Uzuri wa Mungu na Masiha.

Kutoka 15:1,2; Zaburi 86:15; Zaburi

103:11,17; Yeremia 31:1-9.

23. Neema ya Mungu na Masiha.

Mwanzo 28:14; Kutoka 33:19; Zaburi 45:3;

Zaburi 86:15; Isaya 62:4-9;

Maombolezo 3:25,26.

24. Mungu na Masiha hupeana furaha na faraja

kwa wenye haki na waumini.

Isaya 29:19.

C. Kuonekana kwa Masiha.

01. Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

Mwanzo 3:15; Zaburi 132:11,12; Isaya 9:5,6;

Isaya 11:1-3; Isaya 49:1;

Isaya 60:1-3; Yeremia 23:5,6; Yeremia 31:22;

Yeremia 33:14-15,22; Habakuki 2:3;

Hagai 2:24; Zekaria 3:8.

02. Mtangulizi wa Masiha anatangazwa.

Isaya 40:1-5; Malaki 3:1; Malaki 4:5,6.

03. Mahali pa kuzaliwa kwa Masiha.

Mika 5:1.

04. Maisha ya Masiha hadi kuonekana Kwake

kwa mara ya kwanza.

Isaya 7:14-16.

MADA

Page 19: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

19

05. Unabii wa kuuliwa kwa watoto Bethlehemu.

Yeremia 31:15.

D. Kazi za Masiha.

01. Kupakwa kwa mafuta kwa Masiha.

Zaburi 89:21; Mithali 8:22-29; Isaya 61:1.

02. Kazi ya Masiha kama Nabii.

Kumbukumbu la Torati 18:15-19; Isaya 50:4;

Yeremia 28:9; Ezekieli 33:32,33;

Malaki 4:5,6.

03. Kazi ya Masiha kama Kuhani.

Mwanzo 14:18; Kutoka 28:12,29,36-38;

Zaburi 110:4; Yeremia 33:14-18,22;

Zekaria 6:12,13,15.

04. Kazi ya Masiha kama Mfalme.

Mwanzo 49:8-12; Hesabu 24:7,8,15-19;

2 Samweli 7:12-16; 1 Mambo ya Nyakati

17:11;

Zaburi 45:10,14-18; Zaburi 47:2-10;

Zaburi 72:7-19; Zaburi 93:1,2;

Zaburi 132:17,18; Zekaria 9:9.

05. Masiha atakuwa Mkombozi.

Ayubu 19:25-27; Isaya 41:8-20;

Isaya 44:1-8,21,24-26; Isaya 45:17;

Isaya 47:4; Isaya 52:7-12; Isaya 59:18-20;

Isaya 63:1-6; Yeremia 30:3-24;

Yeremia 33:14-18,22; Sefania 3:9-20; Zekaria

3:1-10; Zekaria 10:3-12.

06. Masiha atakuwa Mshauri.

Isaya 59:16.

07. Masiha atakuwa Mpatanishi.

Kumbukumbu la Torati 18:15-19; Isaya

59:16.

08. Masiha atakuwa Dhamana.

Ayubu 17:3; Yeremia 30:21,22.

09. Masiha atakuwa Mwokozi.

Zaburi 130:7,8; Isaya 43:1-13,18-21;

Isaya 25:9; Isaya 30:18; Isaya 45:21,22; Isaya

49:6; Yeremia 23:6; Yeremia 33:16.

10. Masiha atakuwa Hakimu.

Zekaria 3:1-10.

E. Kazi na huduma ya Masiha.

01. Aina ya huduma ya Masiha.

2 Wafalme 1:6,11,12; Isaya 28:15,16;

Isaya 42:6,7,16; Isaya 48:15-17.

02. Mahali pa huduma ya Masiha.

Isaya 8:23; Isaya 41:25; Hosea 11:1.

03. Kujaribiwa kwa Masiha.

Zaburi 91:11,12.

04. Ushindi wa Masiha dhidi ya dhambi.

Hosea 13:14; Zekaria 13:1,2.

05. Miujiza ya Masiha.

Zaburi 146:8; Isaya 35:5-10; Isaya 29:18.

06. Kazi na mwito wa Masiha.

Isaya 61:1-3.

07. Wokovu unaotolewa na Masiha.

Zaburi 85:10; Isaya 55:1,2,6.

08. Haki ya Masiha.

Mwanzo 3:21; Zaburi 40:10,11; Zaburi

MADA

Page 20: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

20

45:7,8; Zaburi 85:11-14; Isaya 32:1,2; Isaya

46:13; Isaya 59:16,17; Yeremia 33:14-18,22.

09. Uadilifu wa Masiha.

2 Samweli 23:1-4; Zaburi 45:4,5;

Zaburi 112:4; Isaya 16:5.

10. Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

Mwanzo 12:3; Mwanzo 26:3-5;

Kumbukumbu la Torati 33:3;

Zaburi 2:8; Zaburi 22:24-32; Zaburi 46:11;

Zaburi 72:7-19; Zaburi 98:1-3;

Zaburi 102:14-23;

Isaya 11:10-12; Isaya 19:23-25;

Isaya 24:13-16; Isaya 42:2-4;

Isaya 45:22-25; Isaya 49:6; Isaya 51:1-23;

Isaya 52:15; Isaya 55:4,5; Isaya 56:6-8; Isaya

60:1-5; Isaya 61:10,11;

Isaya 62:1-3,10-12; Isaya 65:1,2;

Isaya 66:10-13,15-24; Yeremia 4:2;

Yeremia 10:7; Yeremia 16:19;

Amosi 9:11-15; Mika 4:1-4; Hagai 2:7-10;

Zekaria 2:1-13; Zekaria 8:1-23;

Zekaria 14:1-21; Malaki 1:11.

11. Masiha atapeana uzima wa milele.

Ayubu 19:25; Zaburi 103:4; Isaya 25:8;

Isaya 55:3; Hosea 13:14;

Ezekieli 37:11-14; Zekaria 2:1-13.

12. Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

Kumbukumbu la Torati 11:18-20;

2 Samweli 22:20-25; Zaburi 1:1-6;

Zaburi 40:7; Zaburi 119:97-103; Isaya 42:2-4.

13. Mungu anathibitisha huduma ya Masiha.

Zaburi 20:5-7; Zaburi 89:23,28-30;

Isaya 42:1.

14. Masiha atashinda kifo na giza.

Zaburi 49:16; Zaburi 86:12,13; Zaburi 110:1;

Hosea 13:14.

15. Masiha ataleta habari njema.

Zaburi 96:1-3; Isaya 9:1-3; Isaya 41:26,27;

Isaya 52:7-12; Isaya 61:1-3; Ezekieli 33:32,33.

16. Masiha atabariki watu Wake.

Zaburi 21:7,8; Zaburi 45:10,14-16;

Zaburi 132:13-16; Isaya 4:2; Yoeli 2:18-27.

17. Masiha atajenga hekalu la Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 17:12; Zaburi 118:22-

24;

Isaya 66:1; Yeremia 31:1-9;

Ezekieli 37:26-28; Zekaria 1:16,17;

Zekaria 6:12,13,15.

18. Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

Kutoka 25:8,9; Kutoka 29:45,46;

Mambo ya Walawi 26:11,12; Zaburi 46:5-12;

Isaya 12:1-6; Ezekieli 37:21-28;

Sefania 3:9-20; Zekaria 2:1-13.

19. Masiha atafariji.

Isaya 51:3; Isaya 52:9; Isaya 66:10-13; Zekaria

1:16,17.

20. Masiha ataweka agano jipya.

Isaya 49:8-26; Isaya 55:3; Isaya 59:21; Isaya

61:4-9; Isaya 62:4-9;

Yeremia 31:31-34; Yeremia 32:37-41;

Yeremia 50:4-7,19,20; Ezekieli 16:60-63;

Ezekieli 37:21-28; Hosea 2:15-23;

Amosi 9:11-15.

21. Masiha atasamehe dhambi.

Zaburi 103:3,12; Isaya 55:7; Yeremia 33:6-13;

Yoeli 3:21; Mika 7:15-20.

MADA

Page 21: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

21

22. Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

Mwanzo 22:17,18; Mwanzo 28:14;

Zaburi 89:25; Isaya 40:9-11; Isaya 49:4;

Isaya 53:10-12; Isaya 55:10,11;

Isaya 62:10-12; Ezekieli 17:22-24;

Amosi 8:11.

23. Masiha atawabadilisha watu Wake.

Zaburi 51:19; Isaya 57:15-19;

Ezekieli 11:17-20; Hosea 2:15-23; Hosea 3:4;

Hosea 6:1,2; Malaki 4:5,6.

24. Masiha ataleta amani.

Isaya 54:10-13; Isaya 57:15-19;

Isaya 66:10-13; Yeremia 28:9;

Yeremia 33:6-13; Mika 5:4;

Zekaria 9:10-12.

25. asiha ataaminiwa na kusifiwa.

Zaburi 8:2-3; Zaburi 22:23; Zaburi 45:17,18;

Zaburi 103:22; Isaya 8:13-15; Habakuki 2:4;

Zekaria 11:10,11.

26. Kazi ya ukombozi ya Masiha.

Hesabu 21:9; Zaburi 53:7; Zaburi 89:20;

Zaburi 95:7-11; Zaburi 103:4;

Zaburi 107:1-3; Zaburi 130:7,8;

Zaburi 147:3,6; Isaya 40:1-5; Isaya 49:6; Isaya

63:7-9; Ezekieli 34:11-15,22-31;

Danieli 9:24.

27. Kutoa moyo mpya na roho mpya.

Zaburi 51:19; Zaburi 103:5; Ezekieli 11:17-

20; Ezekieli 36:26,27; Ezekieli 37:9,10,14;

Ezekieli 39:29; Yoeli 2:28,29.

F. Mateso na kifo cha Masiha.

01. Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

Zaburi 16:8-11; Zaburi 22:1,2;

Zaburi 91:14-16; Danieli 9:25-26;

Zekaria 13:7.

02. Kuingia kwa Masiha Yerusalemu

kunatabiriwa.

Zaburi 118:26,27; Zekaria 9:9.

03. Masiha atakataliwa.

Zaburi 62:4,5; Zaburi 118:22-24;

Isaya 5:1,2; Isaya 8:13-15;

Isaya 29:10,13,14; Isaya 49:4,5,7;

Isaya 53:3; Isaya 65:1,2;

Zekaria 11:8; Zekaria 12:1-14.

04. Matokeo ya kukataliwa kwa Masiha.

Danieli 9:25-27; Zekaria 11:10,11.

05. Masiha atasalitiwa.

Zaburi 41:6-10; Zaburi 55:5,6,13-15; Zaburi

109:8; Isaya 29:18; Zekaria 11:12,13.

06. Masiha ataachwa pweke.

Zaburi 88:15-19; Zekaria 13:7.

07. Masihtaka na majaribu ya Masiha.

Zaburi 27:12; Zaburi 35:11,12;

Zaburi 41:6-10; Zaburi 109:1-5.

08. Maelezo ya kifo cha Masiha.

Zaburi 22:2,3,7-19; Zaburi 34:21;

Isaya 53:9; Amosi 8:9; Zekaria 12:1-14.

09. Dhabihu na kulipiwa makosa na Masiha.

Isaya 53:4-6,10-12.

10. Utayari wa Masiha kwa ajili ya kifo.

Zaburi 31:5,6; Zaburi 40:8.

11. Mateso ya Masiha.

MADA

Page 22: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

22

Kumbukumbu la Torati 21:23; Zaburi 18:5-7;

Zaburi 27:2; Zaburi 31:12-16; Zaburi 35:19;

Zaburi 38:13,14,21; Zaburi 40:15; Zaburi

42:8; Zaburi 55:5,6,13-15; Zaburi 69:5,9-10;

Zaburi 102:1-12; Zaburi 109:25; Zaburi

110:7; Isaya 50:3; Isaya 53:1,2; Isaya 63:1-6;

Maombolezo 3:30; Zekaria 11:8.

12. Masiha atapingwa.

Zaburi 2:1-3; Zaburi 35:4-6;

Zaburi 41:6-10; Zaburi 69:5.

13. Maelezo ya mateso ya Masiha.

Kutoka 12:46; Zaburi 69:20-22,27;

Zaburi 88:15-19; Zaburi 129:3; Isaya 50:7-9;

Isaya 52:14; Isaya 53:1-8; Mika 4:14.

14. Masiha hataaminiwa.

Isaya 6:9,10; Isaya 53:1,2.

G. Kufufuka na kupaa mbinguni kwa Masiha.

01. Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

Ayubu 19:25-27; Zaburi 16:8-11; Zaburi 30:4;

Zaburi 40:3,4; Zaburi 49:16; Zaburi 71:20;

Zaburi 91:14-16; Isaya 53:10,11;

Yona 1;17; Yona 2:2-7.

02. Kupaa mbinguni kwa Masiha kunatabiriwa.

Zaburi 24:3,7-10; Zaburi 47:2-10;

Zaburi 68:19.

03. Kuinuliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

Zaburi 91:14-16; Zaburi 110:7; Isaya 52:13;

Ezekieli 21:26,27.

04. Masiha atatoa Roho Wake.

Zaburi 68:19; Mithali 1:23;

Isaya 32:15-18; Isaya 44:3-4;

Ezekieli 36:8-38; Ezekieli 39:29;

Yoeli 2:28,29; Zekaria 12:10.

05. Masiha atapata matunda mengi.

Zaburi 1:3; Isaya 60:21;

Isaya 61:11; Hosea 14:4-8.

06. Makao ya Roho Mtakatifu.

Isaya 57:15-19; Yeremia 31:33;

Ezekieli 11:19; Ezekieli 36:26,27;

Ezekieli 37:9,10.

H. Mstakabali wa Masiha.

01. Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

Zaburi 50:3-6; Zaburi 96:13; Isaya 25:6-12;

Isaya 65:17-25; Isaya 66:15,16;

Danieli 7:13,14,18,22,27; Habakuki 2:3;

Zekaria 12:1-14; Zekaria 14:1-21.

02. Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

1 Samweli 2:10; Zaburi 2:4-6,9-12;

Zaburi 50:2-6; Zaburi 68:1-5;

Zaburi 75:8,9; Zaburi 96:7-13; Zaburi 97:1-6;

Zaburi 98:4-9; Zaburi 110:1,2,5,6;

Zaburi 149:6-9; Isaya 2:4; Isaya 11:4,5;

Isaya 24:18-23; Isaya 26:19-21;

Isaya 27:1-3,6,12,13; Isaya 51:5,6;

Isaya 59:18-20; Isaya 63:1-6;

Isaya 66:15-24; Ezekieli 38:16-23;

Danieli 12:1,2; Yoeli 2:1-17,30-32;

Yoeli 3:1-21; Zekaria 11:9; Zekaria 13:8,9;

Malaki 3:2-5,16-18; Malaki 4:1-4.

03. Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

Mwanzo 49:8-12; Hesabu 24:7,8,15-19;

1 Samweli 2:10; 2 Samweli 7:12-16;

1 Mambo ya Nyakati 17:14; Zaburi 2:4-6,8-12;

MADA

Page 23: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

23

Zaburi 22:24-32; Zaburi 45:8,9,17,18;

Zaburi 46:5-12; Zaburi 47:2-9; Zaburi 50:2-6;

Zaburi 53:7; Zaburi 65:3.

Zaburi 67:2-7; Zaburi 68:1-5; Zaburi 72:7-19;

Zaburi 85:11-14; Zaburi 86:9;

Zaburi 89:4,5,24,25,26,28-30,36-38;

Zaburi 96:7-13; Zaburi 97:1-6;

Zaburi 98:4-9; Zaburi 99:1-5;

Zaburi 102:14-23; Zaburi 107:1-3;

Zaburi 110:1-3,5,6; Zaburi 130:7,8;

Zaburi 132:11-18; Zaburi 138:4,5;

Zaburi 145:10-13; Zaburi 147:2,13,14,20;

Zaburi 149:1-5; Isaya 2:2-5; Isaya 4:2,6; Isaya

6:1-4; Isaya 10:20-22; Isaya 11:4-12; Isaya

12:1-6; Isaya 14:1-3; Isaya 16:5;

Isaya 17:7; Isaya 19:23-25;

Isaya 24:13-16,18-23; Isaya 25:6-12;

Isaya 26:1-4; Isaya 27:1-3,6,12,13;

Isaya 29:22-24; Isaya 30:18-33;

Isaya 32:1,2,15-18; Isaya 33:17-24;

Isaya 35:5-10; Isaya 40:1-5,9-11;

Isaya 41:8-20; Isaya 42:2-4,6,7,16;

Isaya 43:1-13,18-21; Isaya 44:1-8,21-24,26;

Isaya 45:17,18,22-25; Isaya 46:3,4,13;

Isaya 49:6-26; Isaya 51:1-23; Isaya 52:7-12;

Isaya 54:1-17; Isaya 55:12,13; Isaya 56:6-8;

Isaya 59:18-21; Isaya 60:1-21;

Isaya 61:4-11; Isaya 62:1-12;

Isaya 63:7-9; Isaya 65:17-25;

Isaya 66:15-24; Yeremia 3:14-19;

Yeremia 12:15; Yeremia 15:19-21;

Yeremia 16:14,15,19; Yeremia 23:3-8;

Yeremia 24:6,7; Yeremia 29:14;

Yeremia 30:3-24; Yeremia 31:1-9,31-34;

Yeremia 32:37-41; Yeremia 33:6-13;

Yeremia 50:4-7,19,20; Ezekieli 11:17-20;

Ezekieli 20:34-42; Ezekieli 34:11-31;

Ezekieli 36:8-38; Ezekieli 37:1-14,21-28;

Ezekieli 38:23; Ezekieli 39:6-8,21-29; Ezekieli

47:6-23; Danieli 2:34,35,44,45;

Danieli 7:13,14,18,22,27; Danieli 12:1,3;

Hosea 1:10,11; Hosea 2:15-23; Hosea 3:5;

Hosea 6:1-3; Hosea 13:14; Hosea 14:4-8;

Yoeli 2:18-27; Yoeli 3:1-21; Amosi 9:11-15;

Obadia 1:17-21; Mika 2:12,13;

Mika 4:1-4,7; Mika 5:2,3; Mika 7:15-20;

Habakuki 2:14; Sefania 3:9-20;

Haggaí 2:7-10; Zekaria 1:16,17;

Zekaria 2:1-13; Zekaria 3:1-10;

Zekaria 6:12,13,15; Zekaria 8:1-23; Zekaria

9:10-12; Zekaria 10:3-12;

Zekaria 12:1-14; Zekaria 13:1-2,8,9;

Zekaria 14:1-21; Malaki 1:11;

Malaki 3:2-5,16-18; Malaki 4:1-4.

04. Kiti cha enzi cha Masiha.

Zaburi 45:7; Isaya 9:5,6.

05. Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

Zaburi 46:5-12; Zaburi 61:7,8;

Zaburi 72:7-19; Zaburi 95:1-3;

Zaburi 102:14-23; Isaya 25:6-12;

Isaya 60:8-21; Isaya 65:17-25.

06. Kazi ya uombezi ya Masiha.

Isaya 53:12,; Isaya 59:16.

07. Masiha ataketi kwenye mkono wa kulia wa

Mungu.

Zaburi 80:15,16,18; Zaburi 110:1-2.

08. Masiha atakuwa na maisha ya milele.

Zaburi 61:7,8.

09. Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

Zaburi 91:13; Isaya 4:3; Isaya 10:20-22; Isaya

14:1-3; Isaya 17:7; Isaya 27:1-3,6,12,13;

Isaya 33:17-24; Isaya 35:5-10;

Isaya 41:8-20; Isaya 43:1-13,18-21;

Isaya 45:22-25; Isaya 46:3,4,13;

MADA

Page 24: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

24

Isaya 49:8-26; Isaya 52:7-12; Isaya 54:1-17;

Isaya 56:6-8; Isaya 57:15-18; Isaya 59:21;

Isaya 60:6-21; Isaya 61;4-9,10,11;

Isaya 62:1-12; Isaya 65:8-10;

Isaya 66:15-24; Yeremia 3:14-19;

Yeremia 12:15; Yeremia 15:19-21;

Yeremia 16:14,15,19; Yeremia 23:3,4,7,8;

Yeremia 24:6,7; Yeremia 29:14;

Yeremia 30:3-24; Yeremia 32:37-41;

Yeremia 33:6-18,22; Ezekieli 20:34-42;

Ezekieli 34:11-31; Ezekieli 36:8-38;

Ezekieli 37:1-14; Ezekieli 39:6-8,21-29;

Danieli 9:27; Hosea 1:10,11; Hosea 2:15-23;

Hosea 3:4; Amosi 9:11-15; Obadia 1:17-21;

Mika 2:12,13; Mika 4:1-4,7;

Mika 7:15-20; Sefania 3:9-20; Hagai 2:7-10;

Zekaria 1:16,17; Zekaria 2:1-13;

Zekaria 3:1-10; Zekaria 8:1-23;

Zekaria 9:10-12; Zekaria 10:3-12;

Zekaria 12:1-14; Zekaria 13:8,9;

Zekaria 14:1-21; Malaki 4:1-4.

10. Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

Isaya 9:6; Isaya 11:6-9;

Ezekieli 37:1-14,21-28; Danieli 2:34,35,44,45;

Danieli 7:13,14,18,22,27; Hosea 2:15-23;

Yoeli 3:1-21.

11. Masiha atatukuzwa.

Isaya 4:2; Isaya 43:21; Isaya 44:23;

Isaya 49:3; Isaya 60:21; Isaya 61:3;

Danieli 7:13,14.

I. Masiha kwenye dhabihu na sherehe.

01. Sadaka ya kuteketeza - na nyama

inawakilisha kazi ya Masiha - ladha nzuri.

Mambo ya Walawi 1:5,13; Mambo ya Walawi

2:1,2.

02. Sadaka ya kuteketeza inaonyesha kazi ya

Masiha - sadaka ya kujitolea kwa hiari.

Mambo ya Walawi 7:16.

03. Sadaka ya kuteketeza inawakilisha kazi ya

Masiha - sadaka isiyo na

dosari - sadaka ya kudumu ya kuteketeza

.

Mambo ya Walawi 22:17-21; Hesabu 28:3,4.

04. Sadaka ya amaini na dhabihu ya kutoa

shukrani inawakilisha kazi ya Masiha.

Mambo ya Walawi 3:1-5,16; Zaburi 51:17.

05. Sadaka ya kuchomwa inarejelea kazi ya

Masiha.

Mambo ya Walawi 4:3-12; Mambo ya Walawi

4:27-29.

06. Siku ya sherehe ya upatanisho inarejelea

kazi ya Masiha.

Mambo ya Walawi 16:1-31; Mambo ya

Walawi 17:11.

07. Sadaka ya ndama wa kike mwekundu

inarejelea kazi ya Masiha.

Hesabu 19:2,3,9.

08. Sherehe ya Pasaka inarejelea kazi ya Masiha.

Kutoka 12:5-14, 22-24.

09. Sherehe ya mkate usiotiwa chachu inarejelea

kazi ya Masiha.

Mambo ya Walawi 23:6-8.

10. Kupungia kwa mgada wa mazao ya kwanza

ya nafaka kunarejelea kufufuka kwa Masiha.

Mambo ya Walawi 23:9-14.

MADA

Page 25: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

25

11. Sherehe ya matunda ya kwanza, siku 50

baada ya Pasaka, inarejelea kutolewa kwa

Roho Mtakatifu.

Mambo ya Walawi 23:15-21.

12. Sherehe ya tabenakulo kuhusiana na kazi ya

Masiha.

Mambo ya Walawi 23:33-43.

Page 26: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema
Page 27: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

27

Mistari mingine kwenye Maandiko Matakatifu

inahusiana na kuja kwa Ufalme wa Masiha.

Baada ya kuja kwa Masiha kwa mara ya

kwanza Ufalme umekaribia, lakini Ufalme

utatimia kikamilifu wakati wa kuja Kwake kwa

mara ya pili.

Mistari iliyotajwa hapa chini inarejelea Ufalme.

Ili kuokoa nafasi hatukutaja mistari yote

inayohusika lakini kwa kutumia msimbo

wa nambari tunarejelea vikundi vya mistari

iliyotajwa hapa chini.

Misimbo hii ni #1, #2, #3, #4, #5, #6, #7.

Ufalme wa Masiha wa hapo baadaye siku hiyo:

#1 Nguvu, ukuu na utukufu wa Ufalme wa

Masiha.

Mwanzo 49:10; Hesabu 24:17-19;

1 Samweli 2:10; 2 Samweli 7:12-16;

Zaburi 2:6-12; Zaburi 8:2-3;

Zaburi 21:5; Zaburi 45; Zaburi 46:6-12;

Zaburi 47:3,4,8-10; Zaburi 48:2-4,9-15;

Zaburi 50:2-6; Zaburi 61:7,8;

Zaburi 66:1-5; Zaburi 67:2-8;

Zaburi 68:1-5; Zaburi 72:6-20;

Zaburi 85:2-4,10-14; Zaburi 86:9;

Zaburi 89:1-5,26-29,36,37; Zaburi 93:1;

Zaburi 95:3-7; Zaburi 96:1-13;

Zaburi 97:1,6; Zaburi 98:1-9;

Zaburi 99:1-4; Zaburi 110:1-6;

Zaburi 130:7,8; Zaburi 132:11-14;

Zaburi 138:4,5; Zaburi 145:10-13;

Zaburi 149:1-9; Isaya 2:10-22; Isaya 9:5,6;

Isaya 11:2-10; Isaya 16:5; Isaya 24:19-23;

Isaya 26:1-4; Isaya 32:1-5,13-20;

Isaya 33:17-24; Isaya 35:1-10;

Isaya 40:5,9-11; Isaya 41:18-20;

Isaya 42:4,13,16; Isaya 49:7;

Isaya 52:1-3,10,13; Isaya 63:1-6; Isaya

65:13-25; Isaya 66:10-17,22-24; Yeremia 23:5;

Ezekieli 40-48; Danieli 2:35,44;

Danieli 4:3; Danieli 7:13,14,18,27;

Danieli 12:1-3; Yoeli 2;

Yoeli 3; Obadia 1:17-21; Mika 4:13;

Habakuki 2:14; Sefania 2:11;

Zekaria 6:12,13; Zekaria 9:9-12;

Zekaria 10:11,12; Zekaria 14:9;

Malaki 4:1-6; Mathayo 6:10;

Mathayo 19:28; Mathayo 28:18;

Luka 1:32,33; Luka 22:29; Yohana 17:24;

Yohana 18:36; Matendo ya Mitume 1:6,7;

Warumi 8:19-23; Warumi 14:17; 1

Wakorintho 15:24,25; Waefeso 1:10,20;

Wafilipi 2:9; 1 Wathesalonike 2:12;

1 Timotheo 6:15; Waebrania 1:8;

Waebrania 2:5-9; 1 Petro 1:3-5;

Ufunuo wa Yohana 6:2;

Ufunuo wa Yohana 11:15;

Ufunuo wa Yohana 12:10;

Ufunuo wa Yohana 19:15,16;

Ufunuo wa Yohana 20:1-6.

#2 Kubadilishwa na kuteuliwa kwa Israeli.

Mambo ya Walawi 26:40-45;

Kumbukumbu la Torati 4:29-31;

Kumbukumbu la Torati 30:1-10;

Kumbukumbu la Torati 33:28,29;

Zaburi 47:5;

Zaburi 69:36,37; Zaburi 85:9-14;

Zaburi 102:14,17,18,22; Zaburi 106:5;

Zaburi 121; Zaburi 126; Zaburi 130:7,8;

Isaya 4:2-6; Isaya 12:1-6; Isaya 14:1-3;

Isaya 26:1-4; Isaya 27:6; Isaya 29:18-24;

Isaya 30:18-26; Isaya 40:1,2;

Isaya 41:8-20; Isaya 44:1-8,21-24,26;

Isaya 45:17,18,22-25; Isaya 46:13;

Isaya 49:6-26; Isaya 51;

Isaya 54:1-14,17; Isaya 55:1-3;

Isaya 59:16-21; Isaya 60:10,15-18,21,22;

UFALME WA MASIHA WA SIKU ZIJAZO

Page 28: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

28

Isaya 61:1-11; Isaya 62;

Isaya 65:8-10; Yeremia 3:14-16, 18,19;

Yeremia 23:4-6; Yeremia 30:18-24;

Yeremia 31:1-7,16-40; Yeremia 32:38-44;

Yeremia 33:6-22,26; Yeremia 50:4-7,20;

Ezekieli 16:60-63; Ezekieli 34:20-31;

Ezekieli 36:8-15,26-38; Ezekieli 37:1-28;

Hosea 1:7,11; Hosea 2:14-23; Hosea 3:5;

Hosea 14:5,6; Amosi 9:11-15; Mika 4:7;

Mika 5:2-15; Mika 7:14-20;

Sefania 3:11-19; Zekaria 1:12-17;

Zekaria 2:1-5,10,12,13;

Zekaria 3:10; Zekaria 8:3-7,9-19;

Zekaria 9:10-17; Zekaria 10:3-7;

Zekaria 12:1-14; Zekaria 13:1,2,8,9;

Zekaria 14:1-21; Malaki 3:1-6,11,12,16-18;

Matendo ya Mitume 15:16-18;

Warumi 9:27,28; Warumi 11:1-36;

Wagalatia 3:17;

Waebrania 8:6-12; Waebrania 10:16,17;

#3 Kurudi kwa Israeli.

Kumbukumbu la Torati 30:3-5;

Zaburi 14:7;

Zaburi 53:7; Zaburi 106:47;

Zaburi 107:2,3; Zaburi 147:2;

Isaya 10:20-22; Isaya 11:11-16;

Isaya 27:12,13; Isaya 35:8-10; Isaya 43:5,6;

Isaya 49:6,12,22; Isaya 51:11;

Isaya 52:8-10; Isaya 54:7; Isaya 56:8;

Isaya 60:3-11; Isaya 66:20-21;

Yeremia 3:18,19; Yeremia 12:15;

Yeremia 15:19-21; Yeremia 16:14,15;

Yeremia 23:3,7,8; Yeremia 30:3,10,11,17;

Yeremia 31:8-14,17; Yeremia 32:37;

Yeremia 46:27-28; Yeremia 50:19;

Ezekieli 11:17-20; Ezekieli 20:34-44;

Ezekieli 28:24-26; Ezekieli 34:11-14;

Ezekieli 36:24-27; Ezekieli 37:21;

Ezekieli 39:25-29; Hosea 1:11;

Hosea 14:7-8; Mika 2:12,13; Mika 4:6;

Sefania 3:18-20; Zekaria 1:17;

Zekaria 8:7,8; Zekaria 10:8-10;

Yohana 11:52; Waefeso 1:10.

#4 Wayunani watakuja pia.

Mwanzo 26:4;

Kumbukumbu la Torati 32:43;

Zaburi 22:28-32; Zaburi 72:11,17;

Zaburi 86:9; Zaburi 96:10;

Zaburi 102:16-23;

Zaburi 117:1; Isaya 2:2-6; Isaya 5:26;

Isaya 11:10,12;

Isaya 19:16-25; Isaya 25:6-12; Isaya 26:2;

Isaya 43:9; Isaya 51:5; Isaya 55:5;

Isaya 56:6-7; Isaya 60:3-7, 10-14;

Isaya 62:10; Isaya 66:18-23; Yeremia 3:17;

Yeremia 4:2; Yeremia 10:6,7;

Yeremia 16:19; Danieli 7:18,25-27;

Mika 4:1-4; Hagai 2:6,7; Zekaria 2:11;

Sefania 3:8-10;

Zekaria 8:3,20-23; Zekaria 14:16-19;

Maleach 1:11; Marko 11:17; Yohana 10:16;

Warumi 3:29; Warumi 15:9-12;

Wagalatia 3:8; Waefeso 2:11-13;

Waebrania 2:11-13;

Waebrania 12:23;

Ufunuo wa Yohana 7:9-12;

Ufunuo wa Yohana 15:4;

Ufunuo wa Yohana 21:24-26;

Ufunuo wa Yohana 22:2.

#5 Kurudi kwa Masiha na kufufuka kutoka

kwa kifo.

Zaburi 68:22,23; Zaburi 71:20;

Zaburi 126:5,6; Isaya 25:8; Isaya 26:19;

Hosea 13:14; Danieli 12:13;

Mathayo 22:32;

Mathayo 24:27-51; Mathayo 26:64;

Marko 13:24-37; Luka 12:37;

UFALME WA MASIHA WA SIKU ZIJAZO

Page 29: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

29

Luka 14:13-15; Luka 20:34-37;

Luka 21:22-36; Luka 22:29; Luka 23:43;

Yohana 3:21; Yohana 5:28,29;

Yohana 6:39,40; Yohana 8:51;

Yohana 11:25,26; Yohana 12:25,26;

Yohana 14:2,3; Yohana 17:24;

Matendo ya Mitume 2:6-8;

Matendo ya Mitume 23:6-8;

Matendo ya Mitume 26:6-8;

Warumi 8:17,24;

1 Wakorintho 6:14; 1 Wakorintho 15:1-58;

2 Wakorintho 4:14,17; Waefeso 1:10;

Wafilipi 2:10,11; Wafilipi 3:20,21;

Wakolosai 3:4; 1 Wathesalonike 1:10;

1 Wathesalonike 4:14-17;

2 Wathesalonike 1:7-10;

2 Wathesalonike 2:7,8;

2 Timotheo 2:11,12,18; 2 Timotheo 4:8;

Waebrania 1:13; Waebrania 11:13,35;

1 Petro 1:4-9; 1 Petro 4:13; 1 Petro 5:4;

2 Petro 1:11; 1 Yohana 3:2; Yuda 1:14;

Ufunuo wa Yohana 1:6,7;

Ufunuo wa Yohana 2:26,27;

Ufunuo wa Yohana 3:21;

Ufunuo wa Yohana 5:1-14;

Ufunuo wa Yohana 7:3,4;

Ufunuo wa Yohana 10:7;

Ufunuo wa Yohana 11:15;

Ufunuo wa Yohana 12:10;

Ufunuo wa Yohana 15:3,4;

Ufunuo wa Yohana 20:1-6.

#6 Siku ya hukumu.

Mwanzo 18:25; Zaburi 1:4; Zaburi 9:8;

Zaburi 68:1-5; Zaburi 73:20;

Zaburi 96:11-13; Zaburi 98:9;

Zaburi 122:5; Mhubiri 12:14;

Isaya 5:30; Isaya 13:1-22; Isaya 30:8,27-30;

Isaya 34:1-4; Isaya 66:15,16;

Danieli 7:9,10;

Danieli 12:1,2; Yoeli 2:1,10,11,30-32;

Yoeli 3:12-16; Mika 1:3,4; Nahumu 1:5,6;

Sefania 1:14-18; Malaki 3:5,16-18;

Mathayo 8:11,12; Mathayo 10:28;

Mathayo 11:21-24; Mathayo 12:36,41,42;

Mathayo 13:40-43; Mathayo 19:28;

Mathayo 24:50,51;

Mathayo 25:21,23,31-46;

Marko 9:43-48; Luka 10:12-14; Luka 19:27;

Luka 20:35,36; Luka 22:30;

Yohana 5:24-29; Yohana 12:31,32;

Matendo ya Mitume 10:42;

Matendo ya Mitume 17:31;

Matendo ya Mitume 24:15;

Warumi 2:5-16; Warumi 14:10-12; 1

Wakorintho 3:12-15;

1 Wakorintho 4:5; 1 Wakorintho 6:1-3;

2 Wakorintho 5:10; Wakolosai 3:6;

2 Timotheo 4:1; Waebrania 6:2;

2 Petro 2:9; 2 Petro 3:7; 1 Yohana 4:17;

Yuda 1:6,13-15; Ufunuo wa Yohana 2:11;

Ufunuo wa Yohana 3:4,5;

Ufunuo wa Yohana 6:12-17;

Ufunuo wa Yohana 11:18,19;

Ufunuo wa Yohana 14:1-11;

Ufunuo wa Yohana 17:14-16;

Ufunuo wa Yohana 19;

Ufunuo wa Yohana 20:10-15;

#7 Mbingu mpya na dunia mpya.

Zaburi 48:8; Isaya 60:18-20;

Isaya 65:17-19; Isaya 66:22-24;

Mathayo 8:11; Mathayo 24:35;

1 Wakorintho 15:24,25; Wagalatia 4:26;

Waebrania 10:12,13; Waebrania 11:10;

Waebrania 12:22-28; 2 Petro 3:7-13;

Ufunuo wa Yohana 3:12,21;

Ufunuo wa Yohana 16:20;

Ufunuo wa Yohana 21, 22.

UFALME WA MASIHA WA SIKU ZIJAZO

Page 30: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema
Page 31: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

31

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

MWANZO 3:15 nami nitaweka uadui kati

yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao

wako na uzao wake; huo utakuponda

kichwa, na wewe utamponda kisigino.

HESABU 21:8 Bwana akamwambia Musa,

Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu

ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa,

aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu

ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu,

alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

MATHAYO 27:50 Naye Yesu akiisha kupaza

sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka

vipande viwili toka juu hata chini; nchi

ikatetemeka; miamba ikapasuka;

MATHAYO 28:5 Malaika akajibu, akawaambia

wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa

maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu

aliyesulibiwa.

6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama

alivyosema. Njoni, mpatazame mahali

alipolazwa.

LUKA 2:10 Malaika akawaambia,

Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea

habari njema ya furaha kuu itakayokuwa

kwa watu wote;

11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa,

kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo

Bwana.

YOHANA 3:14 Na kama vile Musa

alivyomwinua yule nyoka jangwani,

vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi

kuinuliwa;

WAGALATIA 3:19 Torati ni nini basi? Iliingizwa

kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao

aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi

wa malaika kwa mkono wa mjumbe.

WAGALATIA 4:4 Hata ulipowadia utimilifu wa

wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye

amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini

ya sheria,

5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya

sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa

wana.

WAEBRANIA 2:14 Basi, kwa kuwa watoto

wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo

hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya

mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za

mauti, yaani, Ibilisi,

UFUNUO WA YOHANA 12:9 Yule joka

akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,

aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye

ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na

malaika zake wakatupwa pamoja naye.

UFUNUO WA YOHANA 20:10 Na yule

Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa

katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule

mnyama na yule nabii wa uongo. Nao

watateswa mchana na usiku hata milele na

milele.

MWANZO

Page 32: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

32

Ona pia: Hesabu 21:6,7; Marko 16:18; Luka 10:19; Matendo ya Mitume 28:3-6.

E09 Uadilifu wa Masiha.

MWANZO 3:21 Bwana Mungu akawafanyia

Adamu na mkewe mavazi ya ngozi,

akawavika.

MWANZO 3:7 Wakafumbuliwa macho wote

wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona

majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

ISAYA 61:10 Nitafurahi sana katika

Bwana, nafsi yangu itashangilia katika

Mungu wangu; maana amenivika mavazi

ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama

bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha

maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa

vyombo vya dhahabu.

UFUNUO WA YOHANA 4:4 Na viti

ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha

enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini

na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi

meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na

taji za dhahabu.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu

una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi,

na Mwana-Kondoo.

11 Na malaika wote walikuwa wakisimama

pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao

wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao

wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha

enzi, wakamsujudu Mungu,

12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na

hekima na shukrani na heshima na uweza

na nguvu zina Mungu wetu hata milele na

milele. Amina.

13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia,

Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni

akina nani? Na wametoka wapi?

14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.

Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika

dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,

na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-

Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 21:2 Nami

nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu

mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa

Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi

aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

Ona pia: Zaburi 132:9,16; Isaya 52:1; Ezekieli 16:8-18.

A01 Masiha ni wa ukoo wa Abrahamu.

MWANZO 9:26 Akasema,Na atukuzwe

Bwana,Mungu wa Shemu;Na kaanani awe

mtumwa wake.

27 Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika

hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa

wake.

LUKA 3:23 Na Yesu mwenyewe,

alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri

wake kama miaka thelathini, akidhaniwa

kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,

LUKA 3:24-33

MWANZO

Page 33: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

33

LUKA 3:34 wa Yakobo, wa Isaka, wa

Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori,

35 wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi,

wa Sala,

36 wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa

Nuhu, wa Lameki,

Ona pia: Isaya 11:10; Warumi 9:5; Warumi 15:12; Waefeso 2:19;

Waefeso 3:6.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

MWANZO 12:3 nami nitawabariki

wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani;

na katika wewe jamaa zote za dunia

watabarikiwa.

MATENDO YA MITUME 3:25 Ninyi

mmekuwa watoto wa manabii na wa

maagano yale, ambayo Mungu aliagana

na baba zenu, akimwambia Ibrahimu,

Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu

zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

wenu na maovu yake.

Ona pia: Zaburi 72:17; Warumi 4:11; Wagalatia 3:8,16,28; Wakolosai 3:11; Ufunuo wa Yohana 7:9.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

MWANZO 14:18 Na Melkizedeki mfalme wa

Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa

kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

MATHAYO 26:26 Nao walipokuwa wakila

Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega,

akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni,

mle; huu ndio mwili wangu

27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa,

akisema, Nyweni nyote katika hiki;

28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano,

imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo

la dhambi.

29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa

tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku

ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi

katika ufalme wa Baba yangu.

WAEBRANIA 6:20 alimoingia Yesu kwa

ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa

kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa

Melkizedeki.

WAEBRANIA 7:1 Kwa maana Melkizedeki

huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa

Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu

alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao

wafalme, akambariki;

2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya

kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake

kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa

Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

Ona pia: Zaburi 110:4; Waebrania 5:6,10; Waebrania 7:1-3.

A01 Masiha ni wa ukoo wa Abrahamu.

MWANZO 17:7 Agano langu nitalifanya

imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako

baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la

milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na

kwa uzao wako baada yako.

8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada

MWANZO

Page 34: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

34

yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote

ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami

nitakuwa Mungu wao.

19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo

atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita

jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu

imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili

ya uzao wake baada yake.

21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa

Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama

haya mwaka ujao.

MWANZO 21:12 Mungu akamwambia

Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni

pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo

mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza

sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao

wako utaitwa.

WARUMI 9:6 Si kana kwamba neno la

Mungu limetanguka. Maana hawawi wote

Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao

wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako

wataitwa;

8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto

wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi

wanahesabiwa kuwa wazao.

9 Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo

wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na

mwana.

Ona pia: Mwanzo 21:2,3,6; Wagalatia 4:28-31.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

MWANZO 22:8 Ibrahimu akasema, Mungu

atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka,

mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili

pamoja.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

Ona pia: Yohana 1:36; 1 Petro 1:19,20; Ufunuo wa Yohana 5:6,12; Ufunuo wa Yohana 7:9,13,14.

A01 Masiha ni wa ukoo wa Abrahamu.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

MWANZO 22:17 katika kubariki nitakubariki,

na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako

kama nyota za mbinguni, na kama mchanga

ulioko pwani; na uzao wako utamiliki

mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia

watajibarikia; kwa sababu umetii sauti

yangu.

YOHANA 8:56 Ibrahimu, baba yenu,

alishangilia kwa vile atakavyoiona siku

yangu; naye akaiona, akafurahi.

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu

asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na

kutengwa na watu wake.

24 Naam, na manabii wote tangu Samweli na

wale waliokuja baada yake, wote walionena,

walihubiri habari za siku hizi.

MWANZO

Page 35: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

35

25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa

maagano yale, ambayo Mungu aliagana

na baba zenu, akimwambia Ibrahimu,

Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu

zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

wenu na maovu yake.

WARUMI 4:17 (kama ilivyoandikwa,

Nimekuweka kuwa baba wa mataifa

mengi); mbele zake yeye aliyemwamini,

yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu,

ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba

yamekuwako.

18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza

kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa

mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo

utakavyokuwa uzao wako.

2 WAKORINTHO 1:20 Maana ahadi zote

za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena

kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate

kutukuzwa kwa sisi.

WAGALATIA 3:16 Basi ahadi zilinenwa kwa

Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa

wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana

kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani,

Kristo.

17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa

kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka

mia nne na thelathini baadaye hailitangui,

hata kuibatilisha ile ahadi.

18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi

tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia

Ibrahimu kwa njia ya ahadi.

WAGALATIA 3:29 Na kama ninyi ni wa Kristo,

basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na

warithi sawasawa na ahadi.

Ona pia: Mwanzo 12:2,3; Mwanzo 13:16; Mwanzo 15:1,5,6; Mwanzo 17:1,6,7; Mwanzo 18:18; Mwanzo 22:3,10; Mwanzo

26:4,5; Mwanzo 27:28,29; Mwanzo 28:3,14; Mwanzo 49:25,26; Kumbukumbu la Torati 1:10; Kumbukumbu la Torati 28:2; Zaburi 2:8; Zaburi 72:8,9,17; Yeremia 7:23; Yeremia 33:22;

Danieli 2:44,45; Luka 1:68-75; Waefeso 1:3; Ufunuo wa Yohana 11:15.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

MWANZO 26:3 Kaa ugenini katika nchi hiyo,

nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki,

maana nitakupa wewe na uzao wako nchi

hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo

nilichomwapia Ibrahimu baba yako.

4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za

mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi

hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote

ya dunia watajibarikia.

WAEBRANIA 6:17 Katika neno hilo Mungu,

akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio

ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza

kubadilika, alitia kiapo katikati;

WAEBRANIA 11:9 Kwa imani alikaa ugenini

katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi

isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na

Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa

ahadi ile ile.

WAEBRANIA 11:13 Hawa wote wakafa

katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali

wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na

kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri

juu ya nchi.

14 Maana hao wasemao maneno kama hayo

waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi

yao wenyewe.

MWANZO

Page 36: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

36

15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile

waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora,

yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu

haoni haya kuitwa Mungu wao; maana

amewatengenezea mji.

Ona pia: Mwanzo 12:1-3; Mwanzo 13:15-17; Mwanzo 15:18; Mwanzo 17:8; Mwanzo 22:16-18; Zaburi 32:8; Zaburi 39:12;

Isaya 43:2,5.

A01 Masiha ni wa ukoo wa Abrahamu.

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

MWANZO 28:14 Na uzao wako utakuwa kama

mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa

magharibi, na mashariki, na kaskazini, na

kusini; na katika wewe, na katika uzao wako,

jamaa zote za dunia watabarikiwa.

MATENDO YA MITUME 3:25 Ninyi

mmekuwa watoto wa manabii na wa

maagano yale, ambayo Mungu aliagana

na baba zenu, akimwambia Ibrahimu,

Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu

zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

wenu na maovu yake.

WAGALATIA 3:8 Na andiko, kwa vile

lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu

atawahesabia haki Mataifa kwa imani,

lilimhubiri Ibrahimu habari njema

zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote

watabarikiwa.

WAGALATIA 3:16 Basi ahadi zilinenwa kwa

Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa

wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana

kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani,

Kristo.

Ona pia: Mwanzo 12:3; Mwanzo 18:17,18; Mwanzo 22:18; Mwanzo 26:4; Zaburi 72:17.

A02 Masiha ni wa ukoo wa Yuda.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

MWANZO 49:8 Yuda, ndugu zako

watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni

mwa adui zako. Wana wa baba yako

watakuinamia.

9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika

mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama

akajilaza kama simba, Na kama simba mke;

ni nani atakaye mwamsha?

10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,

Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata

atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye

mataifa watamtii.

11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na

mwana-punda wake katika mzabibu mzuri.

Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi

yake kwa damu ya zabibu.

12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa

mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa

maziwa.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

MWANZO

Page 37: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

37

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

MATHAYO 1:1 Kitabu cha ukoo wa Yesu

Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa

Ibrahimu.

2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa

Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu

zake;

3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari;

Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa

Aramu;

4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu

akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa

Salmoni;

5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi

akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa

Yese;

6 Yese akamzaa mfalme Daudi.

7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu

akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati

akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa

Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;

10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa

Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake,

wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli,

Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli

akamzaa Zerubabeli;

13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi

akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa

Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;

15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa

Matani; Matani akamzaa Yakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu

aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi

ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi

hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi

na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli

hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.

WAEBRANIA 7:14 Maana ni dhahiri kwamba

Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila

ambayo Musa hakunena neno lo lote juu

yake katika mambo ya ukuhani.

UFUNUO WA YOHANA 5:5 Na

mmojawapo wa wale wazee akaniambia,

Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya

Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate

kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake

saba.

Ona pia: Mwanzo 29:35; Hesabu 24:17; Kumbukumbu la Torati 33:7; 2 Samweli 22:41; 1 Mambo ya Nyakati 5:2; Zaburi

60:6; Zaburi 72:8-11; Isaya 9:6; Isaya 11:1-5; Isaya 42:1-4; Isaya 49:6,7,22,23; Isaya 55:4,5; Isaya 60:1-5; Isaya 63:1-3;

Yeremia 23:5,6; Yeremia 30:21; Hosea 5:14; Hosea 11:12; Hagai 2:7; Mathayo 17:5; Mathayo 21:9; Luka 2:30-32; Warumi 15:12; 1 Wakorintho 15:24,25; Ufunuo wa Yohana 11:15; Ufunuo wa

Yohana 20.

MWANZO

Page 38: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

38

B13 Mamlaka ya Masiha.

KUTOKA 3:6 Tena akasema, Mimi ni

Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu,

Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.

Musa akaficha uso wake; kwa maana

aliogopa kumwangalia Mungu.

MATHAYO 22:31 Tena kwa habari ya kiyama

ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na

Mungu, akisema,

32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu

wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si

Mungu wa wafu, bali wa walio hai.

33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa

mafunzo yake.

LUKA 20:37 Lakini, ya kuwa wafu

hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika

sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa

ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa

Isaka, na Mungu wa Yakobo.

38 Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai;

kwa kuwa wote huishi kwake.

Ona pia: Mwanzo 17:7,8; Mwanzo 28:13; Mwanzo 32:9; Kutoka 3:14,15; Kutoka 4:5; 1 Wafalme 18:36; Marko 12:26; Matendo ya

Mitume 7:32; Waebrania 12:21; Ufunuo wa Yohana 1:17.

B19 Fumbo la Masiha.

KUTOKA 3:14 Mungu akamwambia

Musa, MIMI NIKO AMBAYE

NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia

wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma

kwenu.

MATHAYO 22:32 Mimi ni Mungu wa

Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu

wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali

wa walio hai.

LUKA 9:20 Akawaambia, Nanyi

mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro

akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu.

YOHANA 6:35 Yesu akawaambia, Mimi

ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu

hataona njaa kabisa, naye aniaminiye

hataona kiu kamwe.

YOHANA 8:58 Yesu akawaambia,

Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu

asijakuwako, mimi niko.

YOHANA 11:25 Yesu akamwambia,

Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye

aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa

anaishi;

WAEBRANIA 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana

na leo na hata milele.

UFUNUO WA YOHANA 1:8 Mimi ni

Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema

Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na

atakayekuja, Mwenyezi.

Ona pia: Zaburi 90:2; Mithali 30:4; Isaya 44:6; Mathayo 13:11; Yohana 8:12; Yohana 10:9,14; Yohana 14:6; Yohana 15:1; Ufunuo

wa Yohana 1:4,17; Ufunuo wa Yohana 4:8.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

I08 Sherehe ya Pasaka inarejelea kazi ya

Masiha.

KUTOKA 12:5 Mwana-kondoo wenu

atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja;

mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na

KUTOKA

Page 39: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

39

nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la

mkutano wa Israeli watamchinja jioni.

7 Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia

katika miimo miwili na katika kizingiti cha

juu, katika zile nyumba watakazomla.

8 Watakula nyama yake usiku ule ule,

imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa

chachu; tena pamoja na mboga zenye

uchungu.

9 Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini,

bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja

na miguu yake, na nyama zake za ndani.

10 Wala msisaze kitu chake cho chote hata

asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata

asubuhi mtakichoma kwa moto.

11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa

viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni,

na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi

mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.

12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku

huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza

wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu

na wa mnyama; nami nitafanya hukumu

juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi

Bwana.

13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika

zile nyumba mtakazokuwamo; nami

nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu,

lisiwapate pigo lo lote likawaharibu,

nitakapoipiga nchi ya Misri.

14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu,

nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana;

mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu

vyote, kwa amri ya milele

22 Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye

katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga

kizingiti cha juu, na miimo miwili ya

mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli;

tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke

mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.

23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao

Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu

katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo

miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala

hatamwacha mwenye kuharibu aingie

nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.

24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri

kwako na kwa wanao milele.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

1 WAKORINTHO 5:7 Basi, jisafisheni,

mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa

donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa

chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha

kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

WAEFESO 1:7 Katika yeye huyo, kwa damu

yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya

dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.

WAEBRANIA 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja,

aliye kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na

kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono,

maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na

mafahali na majivu ya ndama ya ng›ombe

waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa

hata kuusafisha mwili;

14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye

kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi

KUTOKA

Page 40: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

40

yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na

mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na

matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu

aliye hai?

WAEBRANIA 10:29 Mwaonaje?

Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu

yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu,

na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa

kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri

Roho wa neema?

WAEBRANIA 11:28 Kwa imani

akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu,

ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa

kwanza asiwaguse wao.

1 PETRO 1:18 Nanyi mfahamu kwamba

mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,

kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika

mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa

baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-

kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya

Kristo.

Ona pia: Kutoka 12:7; Mambo ya Walawi 23:4,5; Hesabu 19:18; Zaburi 51:5; Mathayo 26:17-19,30; Marko 14:12-16; Yohana 1:36; Waebrania 9:7,19; Waebrania 10:14; Waebrania 12:24; Ufunuo

wa Yohana 5:6-13; Ufunuo wa Yohana 21:22,23.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

KUTOKA 12:46 Na aliwe ndani ya nyumba

moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yo

yote; wala msivunje mfupa wake uwao wote.

YOHANA 19:36 Kwa maana hayo yalitukia

ili andiko litimie, Hapana mfupa wake

utakaovunjwa.

Ona pia: Hesabu 9:12; Zaburi 34:20; Yohana 19:33.

B22 Uzuri wa Mungu na Masiha.

KUTOKA 15:1 Ndipo Musa na wana wa

Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu

wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana,

kwa maana ametukuka sana; Farasi na

mpanda farasi amewatupa baharini.

2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu;

Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni

Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu

wa baba yangu, nami nitamtukuza.

UFUNUO WA YOHANA 15:3 Nao

wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa

Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

Ona pia: Zaburi 22:3; Zaburi 132:5; Isaya 66:1; Matendo ya Mitume 4:12; Waefeso 2:21,22; Ufunuo wa Yohana 5:9-14; Ufunuo

wa Yohana 19:1.

A08 Majina na vyeo vya Masiha.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

KUTOKA 17:6 Tazama, nitasimama mbele

yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu;

nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu

wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele

ya wazee wa Israeli.

1 WAKORINTHO 10:1 Kwa maana, ndugu

zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa

baba zetu walikuwa wote chini ya wingu;

wote wakapita kati ya bahari;

KUTOKA

Page 41: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

41

2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika

wingu na katika bahari;

3 wote wakala chakula kile kile cha roho;

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho;

kwa maana waliunywea mwamba wa roho

uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni

Kristo.

Ona pia: Yohana 4:10,14; Yohana 7:37; Ufunuo wa Yohana 22:17.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

KUTOKA 23:20 Tazama, mimi namtuma

malaika aende mbele yako, ili akulinde

njiani na kukupeleka mpaka mahali pale

nilipokutengezea.

21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti

yake; wala msimtie kasirani; maana,

hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina

langu limo ndani yake.

MALAKI 3:1 Angalieni, namtuma

mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia

mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta

atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule

mjumbe wa agano mnayemfurahia,

angalieni, anakuja, asema Bwana wa

majeshi.

MATHAYO 17:5 Alipokuwa katika kusema,

tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na

tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,

ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, ninayependezwa naye; msikieni

yeye.

YOHANA 10:30 Mimi na Baba tu umoja.

YOHANA 10:36 je! Yeye ambaye Baba

alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi

mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu

nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

37 Kama sizitendi kazi za Baba yangu,

msiniamini;

38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini

mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na

kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu,

nami ni ndani ya Baba.

YOHANA 17:6 Jina lako nimewadhihirishia

watu wale ulionipa katika ulimwengu;

walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako

wamelishika.

YOHANA 17:26 Nami naliwajulisha jina

lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile

ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami

niwe ndani yao.

Ona pia: Mwanzo 48:16; Kutoka 3:2-6; Kutoka 14:19; Kutoka 32:34; Kutoka 33:2,14,15; Hesabu 20:16; Yoshua 5:13,14; Zaburi

2:12; Isaya 9:6; Isaya 42:8; Isaya 63:9; Yohana 10:30,38; Yohana 12:28; Yohana 14:9,10; Wakolosai 2:9; Waebrania 3:10,11,16;

Waebrania 10:26-29; Waebrania 12:25; Ufunuo wa Yohana 1:8.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

KUTOKA 25:8 Nao na wanifanyie

patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.

9 Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo,

mfano wa maskani, na mfano wa vyombo

vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.

22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza

nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema,

katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu

ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote

nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.

LUKA 7:16 Hofu ikawashika wote,

KUTOKA

Page 42: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

42

wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii

mkuu ametokea kwetu; na, Mungu

amewaangalia watu wake.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

MATENDO YA MITUME 7:44 Ile hema

ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu

jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema

na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na

mfano ule aliouona;

45 ambayo baba zetu, kwa kupokezana,

wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki

ya Mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza

mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi;

46 aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye

aliomba ampatie Mungu wa Yakobo

maskani.

47 Lakini Sulemani alimjengea nyumba.

48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba

zilizofanywa kwa mikono, kama vile

asemavyo nabii,

49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni

pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani

mtakayonijengea? Asema Bwana,

WAEBRANIA 9:2 Maana hema ilitengenezwa,

ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha

taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo

palipoitwa, Patakatifu.

3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo

Patakatifu pa patakatifu,

4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku

la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande

zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu

lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni

iliyochipuka, na vile vibao vya agano;

5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia

kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi

sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja

kimoja.

WAEBRANIA 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja,

aliye kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na

kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono,

maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: Mwanzo 18:33; Kutoka 15:2; Kutoka 20:24; Kutoka 29:42,43; Kutoka 30:6; Kutoka 31:18; Kutoka 36:2; Mambo

ya Walawi 4:6; Mambo ya Walawi 16:2; Hesabu 7:89; Kumbukumbu la Torati 5:26-31; Zaburi 80:1; Isaya 12:6; Isaya

37:16; Zekaria 2:10; Zekaria 8:3; 2 Wakorintho 6:16; Waebrania 8:5; Waebrania 9:9.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

KUTOKA 28:12 Nawe utavitia vile vito viwili

juu ya vipande vya mabegani vya hiyo

naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili

ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua

majina yao mbele za Bwana juu ya mabega

yake mawili ili kuwa ukumbusho.

WAEBRANIA 7:24 bali yeye, kwa kuwa akaa

milele, anao ukuhani wake usioondoka.

KUTOKA

Page 43: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

43

25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa

kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye;

maana yu hai sikuzote ili awaombee.

26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu

wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na

uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa

na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

27 ambaye hana haja kila siku, mfano wa

wale makuhani wakuu wengine, kwanza

kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake

mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao

watu; maana yeye alifanya hivi mara moja,

alipojitoa nafsi yake.

28 Maana torati yawaweka wanadamu walio na

unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo

neno la kiapo kilichokuja baada ya torati

limemweka Mwana, aliyekamilika hata

milele.

Ona pia: Zekaria 6:13; Luka 1:54,72.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

KUTOKA 28:29 Na Haruni atayachukua

majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko

cha kifuani cha hukumu juu ya moyo

wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali

patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya

Bwana daima.

WAEBRANIA 8:6 Lakini sasa amepata huduma

iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe

wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya

ahadi zilizo bora.

WAEBRANIA 9:24 Kwa sababu Kristo hakuingia

katika patakatifu palipofanyika kwa mikono,

ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia

mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa

Mungu kwa ajili yetu;

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

KUTOKA 28:36 Nawe fanya bamba la

dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano

wa machoro ya muhuri, MTAKATIFU KWA

Bwana.

WAEFESO 5:27 apate kujiletea Kanisa

tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo

lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na

mawaa.

Ona pia: Kutoka 39:30; Mambo ya Walawi 8:9; Mambo ya Walawi 10:3; Zekaria 14:20.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

KUTOKA 28:37 Nawe ulitie hilo bamba

katika ukanda wa rangi ya samawi, nalo

litakuwa katika kile kilemba; litakuwa

upande wa mbele wa kile kilemba.

38 Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha

Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile

vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana

wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu,

nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso

sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa

mbele za Bwana.

WAEBRANIA 4:14 Basi, iwapo tunaye kuhani

mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu,

Mwana wa Mungu, na tuyashike sana

maungamo yetu.

Ona pia: Mambo ya Walawi 1:4; Mambo ya Walawi 22:27; Mambo ya Walawi 23:11; Isaya 53:6,11,12; Zekaria 3:1-5; Zekaria

KUTOKA

Page 44: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

44

14:20; Yohana 1:29; 2 Wakorintho 5:21; Waebrania 9:28; 1 Petro 2:5,24; 1 Petro 3:18.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

KUTOKA 29:45 Na mimi nitakaa kati ya

wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao.

46 Nao watanijua kuwa mimi ndimi Bwana,

Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi

ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi

Bwana Mungu wao.

KUTOKA 25:8 Nao na wanifanyie

patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.

KUTOKA 40:34 Ndipo lile wingu

likaifunikiza hema ya kukutania, na huo

utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.

ZEKARIA 2:10 Imba, ufurahi, Ee binti

Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami

nitakaa kati yako, asema Bwana.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 14:17 ndiye Roho wa kweli;

ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea,

kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali

ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu,

naye atakuwa ndani yenu.

20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni

ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu,

nami ndani yenu.

23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda,

atalishika neno langu; na Baba yangu

atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya

makao kwake.

2 WAKORINTHO 6:16 Tena pana

mapatano gani kati ya hekalu la Mungu

na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la

Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema,

ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao

nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao

watakuwa watu wangu.

WAEFESO 2:22 Katika yeye ninyi nanyi

mnajengwa pamoja kuwa maskani ya

Mungu katika Roho.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: Mambo ya Walawi 26:12; Hesabu 9:15; Kumbukumbu la Torati 18:15; 1 Wafalme 8:10,11; 2 Mambo ya Nyakati 7:1-3.

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

KUTOKA 33:19 Akasema, Nitapitisha wema

wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza

jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili

yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye

nitakayemrehemu.

WARUMI 9:15 Maana amwambia Musa,

Nitamrehemu yeye nimrehemuye,

nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule

atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa

KUTOKA

Page 45: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

45

yule arehemuye, yaani, Mungu.

17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao,

ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi

hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina

langu likatangazwe katika nchi yote.

18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu

humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu

humfanya mgumu.

WARUMI 9:23 tena, ili audhihirishe wingi

wa utukufu wake katika vile vyombo vya

rehema, alivyovitengeneza tangu zamani

vipate utukufu;

KUTOKA

Page 46: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

46

I01 Sadaka ya kuteketeza - na nyama

inawakilisha kazi ya Masiha - ladha nzuri.

MAMBO YA WALAWI 1:5 Naye atamchinja

huyo ng›ombe mbele ya Bwana; kisha wana

wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu

hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake

kando-kando katika madhabahu iliyo hapo

mlangoni pa hema ya kukutania

13 lakini matumbo yake, na miguu yake,

ataosha kwa maji; na huyo kuhani

atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya

madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa,

dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya

harufu ya kupendeza kwa Bwana.

MAMBO YA WALAWI 2:1 Na mtu

atakapomtolea Bwana matoleo ya sadaka

ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga

mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na

kutia na ubani juu yake;

2 kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao

makuhani; naye atatwaa konzi moja katika

huo unga mwembamba, na katika mafuta

yake, na huo ubani wote; kisha kuhani

atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake

juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa

kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza

kwa Bwana;

ZABURI 141:2 Sala yangu ipae mbele zako

kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu

kama dhabihu ya jioni.

HOSEA 6:6 Maana nataka fadhili wala si

sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za

kuteketezwa.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WAEBRANIA 9:14 basi si zaidi damu yake

Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele

alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka

isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu

na matendo mafu, mpate kumwabudu

Mungu aliye hai?

Ona pia: Mwanzo 8:21; Kutoka 29:18,25,41; Mambo ya Walawi 2:2,9,12; Mambo ya Walawi 3:5,16; Mambo ya Walawi

4:31; Mambo ya Walawi 6:15,21; Mambo ya Walawi 8:21,28; Mambo ya Walawi 17:6; Mambo ya Walawi 23:13,18; Hesabu

15:3,7,10,13,14,24; Hesabu 18:17; Hesabu 28:2,6,8,13,36; Hesabu 29:2,6,8,13,36; Isaya 1:13; Mathayo 12:7; Marko 12:33; Yohana

4:34; Yohana 6:38; Ufunuo wa Yohana 5:8; Ufunuo wa Yohana 8:3,4.

I04 Sadaka ya amaini na dhabihu ya kutoa

shukrani inawakilisha kazi ya Masiha.

MAMBO YA WALAWI 3:1 Na matoleo yake

kwamba ni sadaka za amani; kwamba

asongeza katika ng›ombe, mume au mke,

atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya

Bwana.

MAMBO YA WALAWI

Page 47: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

47

2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake

huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa

hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao

makuhani, watainyunyiza damu yake katika

madhabahu pande zote.

3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya

amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa

kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo

matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya

matumbo,

4 na figo zake mbili, na mafuta

yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na

kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini,

pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.

5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa

moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya

kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya

moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya

moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana.

16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu

ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya

kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya

kupendeza; mafuta yote ni ya Bwana.

MAMBO YA WALAWI 7:11 Na sheria ya

matoleo ya sadaka za amani, atakazosongeza

mtu kwa Bwana, ni hii.

12 Kwamba aitoa kwa ajili ya shukrani, ndipo

atakaposongeza pamoja na hiyo sadaka

ya shukrani mikate isiyotiwa chachu,

iliyoandaliwa na mafuta, na mikate ya kaki

isiyochachwa iliyopakwa mafuta, na mikate

ya unga mwembamba uliolowama mafuta.

KUMBUKUMBU LA TORATI 27:7 ufanye na

sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi

mbele za Bwana, Mungu wako.

LUKA 22:15 Akawaambia, Nimetamani

sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya

kuteswa kwangu;

LUKA 22:19 Akatwaa mkate, akashukuru,

akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio

mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu;

fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

YOHANA 4:32 Akawaambia, Mimi ninacho

chakula msichokijua ninyi.

33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je!

Mtu amemletea chakula?

34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho

hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka,

nikaimalize kazi yake.

YOHANA 6:51 Mimi ndimi chakula chenye

uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu

akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula

nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili

ya uzima wa ulimwengu.

52-57

58 Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka

mbinguni; si kama mababa walivyokula,

wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi

milele.

1 WAKORINTHO 10:16 Kikombe kile cha

baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa

damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si

ushirika wa mwili wa Kristo?

1 WAKORINTHO 11:23 Kwa maana mimi

nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi,

ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa

alitwaa mkate,

24 naye akiisha kushukuru akaumega,

akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa

ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho

MAMBO YA WALAWI

Page 48: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

48

wangu.

25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa

kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano

jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila

mnywapo, kwa ukumbusho wangu.

26 Maana kila mwulapo mkate huu na

kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza

mauti ya Bwana hata ajapo.

27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea

kikombe hicho cha Bwana isivyostahili,

atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu

ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule

mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alaye na kunywa, hula na

kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa

kutokuupambanua ule mwili.

WAEBRANIA 13:15 Basi, kwa njia

yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa

daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo

jina lake.

1 PETRO 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe

yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za

roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya

Yesu Kristo.

Ona pia: Kutoka 24:11; Mambo ya Walawi 7:18-21; 1 Samweli 9:12; 1 Samweli 16:3; 1 Wafalme 8:62; Zaburi 27:6; Zaburi 50:14; Zaburi 96:8; Zaburi 107:22; Zaburi 116:17; Ezekieli 43:27; Luka 11:41; Warumi 14:14,17; Waefeso 5:20; Wagalatia 5:22; Wafilipi

4:18; Tito 1:15; Waebrania 13:16; Yohana 1:6-9.

B

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

I05 Sadaka ya kuchomwa inarejelea kazi ya

Masiha.

Dhambi ya kuhani:

MAMBO YA WALAWI 4:3 kama kuhani

aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata

analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe

kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na

kumsongeza kwa Bwana ng’ombe mume

mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya

dhambi.

4 Naye atamleta huyo ng’ombe na kumweka

mlangoni pa hiyo hema ya kukutania,

mbele za Bwana; naye ataweka mkono wake

kichwani mwake ng’ombe, na kumchinja

huyo ng’ombe mbele za Bwana.

5 Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa

baadhi ya damu ya huyo ng’ombe, na kuileta

ndani ya hiyo hema ya kukutania;

6 kisha kuhani atatia kidole chake katika

hiyo damu na kuinyunyiza damu mbele ya

Bwana mara saba, mbele ya pazia la mahali

patakatifu.

7 Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu

juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia

uvumba mzuri mbele ya Bwana iliyo ndani

ya hema ya kukutania; kisha damu yote

ya huyo ng’ombe ataimwaga hapo chini

ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa,

iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.

MAMBO YA WALAWI 4:8-11

MAMBO YA WALAWI 4:12 maana, huyo

ng’ombe mzima atamchukua nje ya

marago hata mahali safi, hapo wamwagapo

majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni;

atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.

Dhambi ya mwanadamu - ujinga:

MAMBO YA WALAWI

Page 49: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

49

MAMBO YA WALAWI 4:27 Na mtu awaye yote

katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo

kukusudia, kwa kufanya neno lo lote katika

hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe,

naye akapata hatia;

28 akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya,

ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu,

awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake

aliyoifanya.

29 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake

hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja

sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya

kuteketezwa.

ISAYA 53:6 Sisi sote kama kondoo

tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia

yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu

yake Maovu yetu sisi sote.

7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala

hakufunua kinywa chake; Kama mwana-

kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama

vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao

manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa

chake.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na

kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi

wangu mwenye haki Atawafanya wengi

kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu

yao.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

YOHANA 1:36 Akamtazama Yesu

akitembea, akasema, Tazama, Mwana-

kondoo wa Mungu!

MATENDO YA MITUME 8:32 Na

fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni

hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama

kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo

kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo

hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

WAEBRANIA 9:12 wala si kwa damu ya mbuzi

na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe

aliingia mara moja tu katika Patakatifu,

akiisha kupata ukombozi wa milele.

13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na

mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe

waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa

hata kuusafisha mwili;

14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye

kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi

yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na

mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na

matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu

aliye hai?

WAEBRANIA 9:21 Na ile hema nayo na vyombo

vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo

hivyo.

22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa

kwa damu, na pasipo kumwaga damu

hakuna ondoleo.

MAMBO YA WALAWI

Page 50: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

50

23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo

mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini

mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe

kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.

24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika

patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio

mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia

mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa

Mungu kwa ajili yetu;

25 wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama

vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu

kila mwaka kwa damu isiyo yake;

WAEBRANIA 10:4 Maana haiwezekani damu ya

mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili

uliniwekea tayari;

6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika

gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye

mapenzi yako, Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na

sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi

hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo

(zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja

niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza,

ili kusudi alisimamishe la pili.

10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa

kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja

tu.

11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya

ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara

nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa

dhambi.

12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya

dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele,

aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

13 tangu hapo akingojea hata adui zake

wawekwe kuwa chini ya miguu yake.

14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata

milele hao wanaotakaswa.

WAEBRANIA 13:11 Maana wanyama

wale ambao damu yao huletwa ndani ya

patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya

dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya

kambi.

12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu

kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya

lango.

13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi,

tukichukua shutumu lake.

1 PETRO 1:18 Nanyi mfahamu kwamba

mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,

kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika

mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa

baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-

kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya

Kristo.

20 Naye amejulikana kweli tangu zamani,

kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini

alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili

yenu;

UFUNUO WA YOHANA 5:6 Nikaona

katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye

uhai wanne, na katikati ya wale wazee,

Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana

kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba

na macho saba, ambazo ni Roho saba za

Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono

wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti

cha enzi.

8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai

MAMBO YA WALAWI

Page 51: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

51

wanne na wale wazee ishirini na wanne

wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo,

kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya

dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni

maombi ya watakatifu.

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema,

Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu

na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa

ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu

yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa

na taifa,

Ona pia: Mathayo 18:21,22; Warumi 3:24-26; Warumi 8:1-4; Wagalatia 4:4; Waebrania 1:3; Waebrania 10:29; 1 Petro 2:22-24; 1

Petro 3:18; Yohana 1:7-9; Ufunuo wa Yohana 7:9,10.

I02 Sadaka ya kuteketeza inaonyesha kazi ya

Masiha - sadaka ya kujitolea kwa hiari.

MAMBO YA WALAWI 7:16 Lakini kwamba hii

sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka

ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka

yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia

kitaliwa;

KUTOKA 35:21 Wakaja kila mtu ambaye

moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye

roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao

wakaleta sadaka za kumpa Bwana, kwa kazi

ya hema ya kukutania, na kwa utumishi

wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.

22 Nao wakaja, waume kwa wake, wote

waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta

vipini, na hazama, na pete za muhuri, na

vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila

mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa

Bwana.

MAMBO YA WALAWI 22:21 Na mtu

awaye yote atakayemtolea Bwana dhabihu

katika sadaka za amani, ili kuondoa

nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda,

katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa

mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na

kilema ndani yake cho chote.

ZABURI 40:7 Ndipo niliposema,

Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo

nimeandikiwa,)

ZABURI 66:13 Nitaingia nyumbani mwako

na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu;

ISAYA 53:7 Alionewa, lakini

alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa

chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye

machinjoni, Na kama vile kondoo

anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya

yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

LUKA 3:22 Roho Mtakatifu akashuka

juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama

hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe

ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu;

nimependezwa nawe.

YOHANA 2:17 Wanafunzi wake

wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu

wa nyumba yako utanila.

YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu

aliupenda ulimwengu, hata akamtoa

Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye

asipotee, bali awe na uzima wa milele.

YOHANA 10:17 Ndiposa Baba anipenda, kwa

sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.

18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa

mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa,

ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo

MAMBO YA WALAWI

Page 52: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

52

nalilipokea kwa Baba yangu.

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

2 WAKORINTHO 8:9 Maana mmejua

neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi

alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa

alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa

matajiri kwa umaskini wake.

WAFILIPI 2:7 bali alijifanya kuwa hana

utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa

ana mfano wa wanadamu;

Ona pia: Kutoka 25:39; Kutoka 35:29; Kutoka 36:3; Hesabu 15:3; Kumbukumbu la Torati 12:6; Kumbukumbu la Torati 23:23;

Zaburi 69:9; Zaburi 116:14,18; 1 Mambo ya Nyakati 29:3,9; 2 Mambo ya Nyakati 35:8; Ezekieli 46:12; Mathayo 3:17; Mathayo

17:5; Marko 1:11; Marko 9:7; Luka 9:35; Matendo ya Mitume 2:44; Warumi 12:1; 2 Wakorintho 9:7; Waefeso 5:2; 2 Petro 1:17.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

I06 Siku ya sherehe ya upatanisho inarejelea

kaziya Masiha

.

Kulipia kuhani makosa:

MAMBO YA WALAWI 16:1 Bwana akasema na

Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili

wa Haruni, walipokaribia mbele za Bwana,

wakafa;

2 Bwana akamwambia Musa, Sema na Haruni

ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo

wote katika mahali patakatifu ndani ya

pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho

juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi

nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha

rehema.

MAMBO YA WALAWI 16:3,4,6

Kulipia watoto wa Israeli makosa kwa kuua mbuzi:

MAMBO YA WALAWI 16:5 Kisha atatwaa

mikononi mwa mkutano wa Waisraeli

mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya

dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya

kuteketezwa.

7 Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na

kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa

hema ya kukutania.

8 Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi

wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na

kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.

9 Na Haruni atamleta yule mbuzi

aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana,

na kumtoa awe sadaka ya dhambi.

MAMBO YA WALAWI 16:11-14

MAMBO YA WALAWI 16:15 Kisha

atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya

dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta

damu yake ndani ya pazia, na kwa damu

hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa

damu ya ng’ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti

cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,

16 naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali

patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu

ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya

makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao

zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema

ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya

machafu yao.

MAMBO YA WALAWI 16:17-19

Kulipia watoto wa Israeli makosa kwa kumfukuza

mbuzi:

MAMBO YA WALAWI 16:10 Bali

yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili

MAMBO YA WALAWI

Page 53: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

53

ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana

ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka

jangwani kwa ajili ya Azazeli.

20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya

mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na

madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.

21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili

juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na

kuungama juu yake uovu wote wa wana

wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi

zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa

chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende

jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.

22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu

wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye

atamwacha mbuzi jangwani.

23 Na Haruni ataingia katika hema ya

kukutania, naye atavua mavazi yake

ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika

patakatifu, atayaacha humo;

MAMBO YA WALAWI 16:24-28

MAMBO YA WALAWI 16:29 Amri

hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika

mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi,

mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya

namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati

yenu.

30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa

kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi

mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za

Bwana.

31 Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi

mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele.

MAMBO YA WALAWI 17:11 Kwa

kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu;

nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya

madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili

ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo

upatanisho kwa sababu ya nafsi.

ISAYA 53:4 Hakika ameyachukua

masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu;

Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,

Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,

Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu

ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa

kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea;

Kila mmoja wetu amegeukia njia yake

mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake

Maovu yetu sisi sote.

MATHAYO 27:51 Na tazama, pazia la hekalu

likapasuka vipande viwili toka juu hata chini;

nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

LUKA 23:46 Yesu akalia kwa sauti kuu,

akasema, Ee Baba, mikononi mwako

naiweka roho yangu.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

WARUMI 4:24 bali na kwa ajili yetu

sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi

tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu

Bwana wetu katika wafu;

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,

na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

WAEBRANIA 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu

amekuwa mdhamini wa agano lililo bora

zaidi.

WAEBRANIA 8:1 Basi, katika hayo

tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili:

MAMBO YA WALAWI

Page 54: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

54

Tunaye kuhani mkuu wa namna hii,

aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi

cha Ukuu mbinguni,

2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema

ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si

mwanadamu.

WAEBRANIA 9:7 Lakini katika hema hiyo ya

pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara

moja kila mwaka; wala si pasipo damu,

atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi

za kutokujua za hao watu.

8 Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya

kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa

haijadhihirishwa bado, hapo hema ya

kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;

9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu

uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu

zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi

kumkamilisha mtu aabuduye,

10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu,

vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine

kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa

matengenezo mapya.

11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani

mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo,

kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi,

isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo

ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na

mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe

waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa

hata kuusafisha mwili;

14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye

kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi

yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na

mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na

matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu

aliye hai?

15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano

jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa

kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya

agano la kwanza, hao walioitwa waipokee

ahadi ya urithi wa milele.

16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo

mauti yake aliyelifanya.

17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu

palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina

nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.

18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa

pasipo damu.

19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na

Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru

sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya

mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu

na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe,

na watu wote,

20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa

na Mungu.

21 Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada

alivinyunyizia damu vivyo hivyo.

22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa

kwa damu, na pasipo kumwaga damu

hakuna ondoleo.

23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo

mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini

mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe

kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.

24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika

patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio

mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia

mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa

Mungu kwa ajili yetu;

25 wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama

vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu

kila mwaka kwa damu isiyo yake;

MAMBO YA WALAWI

Page 55: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

55

26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa

mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa

ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu,

katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa,

azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi

yake.

27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa

mara moja, na baada ya kufa hukumu;

28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa

sadaka mara moja azichukue dhambi za

watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo

dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa

wokovu.

WAEBRANIA 10:4 Maana haiwezekani damu ya

mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

WAEBRANIA 10:14 Maana kwa toleo

moja amewakamilisha hata milele hao

wanaotakaswa.

1 YOHANA 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa

dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu,

bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Ona pia: Mwanzo 32:30; Kutoka 28:2,30; Kutoka 30:10; Kutoka 33:20; Mambo ya Walawi 16:4; Mambo ya Walawi

23:26-32; Mambo ya Walawi 25:9; Hesabu 27:21; Hesabu 29:7; Kumbukumbu la Torati 5:24; Waamuzi 6:22; Zaburi 51:15,17;

Zaburi 103:12; Isaya 38:17; Isaya 43:25; Isaya 44:22; Isaya 53:12; Ezekieli 10:18,19; Danieli 10:5; Hosea 6:2,3; Yona 1-3; Mika 7:19; Mathayo 28:30; Marko 15:38; Luka 23:41,45; Yohana 1:14; Yohana 2:11,19; Yohana 19:23; Matendo ya Mitume 13:39; Warumi 5:9; 2

Wakorintho 5:19,21; Waefeso 2:6; 1 Timotheo 2:5; Waebrania 7:26-28; Waebrania 8:5; Waebrania 10:19-22; Waebrania 12:24; 2 Petro

3:9; Ufunuo wa Yohana 19:7,8.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

I03 Sadaka ya kuteketeza inawakilisha kazi ya

Masiha - sadaka isiyo na

dosari - sadaka ya kudumu ya kuteketeza

.

MAMBO YA WALAWI 22:17 Kisha

Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

18 Nena na Haruni na wanawe, na wana wa

israeli wote, uwaambie, Mtu ye yote wa

nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika

Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni

nadhiri zao mojawapo, au kama ni sadaka yo

yote ya hiari, watakayomtolea Bwana kuwa

sadaka ya kuteketezwa;

19 ili mpate kukubaliwa, mtaleta mume

mkamilifu, katika ng’ombe, au katika

kondoo, au katika mbuzi.

20 Lakini mnyama ye yote aliye na kilema

msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili

yenu.

21 Na mtu awaye yote atakayemtolea Bwana

dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa

nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda,

katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa

mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na

kilema ndani yake cho chote.

MAMBO YA WALAWI 17:11 Kwa

kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu;

nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya

madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili

ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo

upatanisho kwa sababu ya nafsi.

HESABU 28:3 Nawe utawaambia, Hii

ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto

mtakayomsongezea Bwana; wana-

kondoo waume wa mwaka wa kwanza

wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya

MAMBO YA WALAWI

Page 56: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

56

kuteketezwa ya sikuzote.

4 Mwana-kondoo mmoja utamsongeza

asubuhi, na mwana-kondoo wa pili

utamsongeza jioni;

ZABURI 40:6 Dhabihu na matoleo

hukupendezwa nazo, Masikio yangu

umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi

hukuzitaka.

ISAYA 53:8 Kwa kuonewa na

kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake

ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa

mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa

sababu ya makosa ya watu wangu.

MATHAYO 20:28 kama vile Mwana wa Adamu

asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na

kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

MATHAYO 26:28 kwa maana hii ndiyo damu

yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya

wengi kwa ondoleo la dhambi.

MATHAYO 27:19 Na alipokuwa ameketi juu

ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea

mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na

yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa

mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.

LUKA 23:4 Pilato akawaambia wakuu

wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo

ovu katika mtu huyu.

LUKA 23:47 Alipokwisha kusema hayo

alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia,

alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake,

mtu huyu alikuwa mwenye haki.

1 WAKORINTHO 1:30 Bali kwa yeye

ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu,

aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa

Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

WAEFESO 5:2 mkaenende katika upendo,

kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena

akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu

kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

WAEBRANIA 10:4 Maana haiwezekani damu ya

mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili

uliniwekea tayari;

6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika

gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye

mapenzi yako, Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na

sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi

hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo

(zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja

niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza,

ili kusudi alisimamishe la pili.

10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa

kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja

tu.

1 PETRO 1:18 Nanyi mfahamu kwamba

mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,

kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika

mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa

MAMBO YA WALAWI

Page 57: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

57

baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-

kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya

Kristo.

20 Naye amejulikana kweli tangu zamani,

kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini

alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;

21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye

kumwamini Mungu, aliyemfufua katika

wafu akampa utukufu; hata imani yenu na

tumaini lenu liwe kwa Mungu.

Ona pia: Kutoka 12:5; Mambo ya Walawi 1:1-4,10; Mambo ya Walawi 3:1,6; Mambo ya Walawi 4:32; Mambo ya Walawi 7:11; Mambo ya Walawi 21:16-24; Mambo ya Walawi 22:27; Hesabu 16:40; Kumbukumbu la Torati 14:6; Kumbukumbu la Torati

15:21; Kumbukumbu la Torati 17:1; Ezra 6:8-10; Zaburi 50:8-12; Zaburi 51:16; Isaya 1:11-15; Malaki 1:8,13,14; Mathayo 3:15;

Mathayo 27:19,24,54; Marko 10:45; Marko 14:24; Luka 4:3; Luka 9:56; Luka 23:41; Yohana 4:34; Yohana 5:30; Yohana 6:38; 2

Wakorintho 5:21; Wagalatia 4:4; Waefeso 5:26; 1 Wathesalonike 2:10; Tito 1:7,10; Tito 2:14; Waebrania 9:22; Waebrania 10:19-21;

Waebrania 13:12; Yohana 1:7; Yohana 2:1.

I09 Sherehe ya mkate usiotiwa chachu

inarejelea kazi ya Masiha.

MAMBO YA WALAWI 23:6 Na siku ya kumi

na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa

Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila

mikate isiyochachwa muda wa siku saba.

7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko

takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi.

8 Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana

kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni

kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya

utumishi.

KUMBUKUMBU LA TORATI 16:3 Usimle

pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku

saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu,

nayo ni mikate ya mateso; kwa maana

ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate

kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri,

siku zote za maisha yako.

MATHAYO 26:17 Hata siku ya kwanza ya

mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake

wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni

wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?

MARKO 14:1 Baada ya siku mbili ilikuwa

sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa;

wakuu wa makuhani na waandishi

wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na

kumwua.

1 WAKORINTHO 5:7 Basi, jisafisheni,

mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa

donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa

chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha

kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

WAEFESO 5:2 mkaenende katika upendo,

kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena

akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu

kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.

Ona pia: Kutoka 12:15-20,39; Kutoka 13:6,7; Kutoka 23:15; Kutoka 34:18; Hesabu 28:17-25; Kumbukumbu la Torati 16:8,16; Waamuzi 6:12-24; 2 Mambo ya Nyakati 30:13,21; 2 Mambo ya

Nyakati 35:17; Ezra 6:22; Marko 14:12; Luka 22:1,7.

I10 Kupungia kwa mgada wa mazao ya kwanza

ya nafaka kunarejelea kufufuka kwa

Masiha.

MAMBO YA WALAWI 23:9 Kisha Bwana

MAMBO YA WALAWI

Page 58: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

58

akanena na Musa, na kumwambia,

10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo

mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi

niwapayo, na kuyavuna mavuno yake,

ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa

malimbuko ya mavuno yenu;

11 naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili

kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya

pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.

12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda,

mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume

mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe

sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.

13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu

za kumi mbili za efa za unga mwembamba

uliochanganywa na mafuta, ni kafara

iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa

harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya

kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.

14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke

machanga, hata siku iyo hiyo, hata

mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya

Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika

vizazi vyenu katika makao yenu yote.

MATHAYO 28:5 Malaika akajibu, akawaambia

wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa

maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu

aliyesulibiwa.

6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama

alivyosema. Njoni, mpatazame mahali

alipolazwa.

7 Nanyi nendeni upesi, mkawaambie

wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu.

Tazama, awatangulia kwenda Galilaya;

ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha

waambia.

WARUMI 8:29 Maana wale aliowajua tangu

asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe

na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe

mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu

wengi.

1 WAKORINTHO 15:20 Lakini sasa

Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao

waliolala.

21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu,

kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote

wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote

watahuishwa.

23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko

ni Kristo; baadaye walio wake Kristo,

atakapokuja.

WAKOLOSAI 1:18 Naye ndiye kichwa cha

mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni

mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba

awe mtangulizi katika yote.

WAEBRANIA 10:10 Katika mapenzi

hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili

wa Yesu Kristo mara moja tu.

11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya

ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara

nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa

dhambi.

12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya

dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele,

aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

1 PETRO 1:18 Nanyi mfahamu kwamba

mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,

kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika

mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa

baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-

kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya

Kristo.

MAMBO YA WALAWI

Page 59: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

59

UFUNUO WA YOHANA 1:17 Nami

nilipomwona, nalianguka miguuni pake

kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake

wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope,

Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na

tazama, ni hai hata milele na milele. Nami

ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Ona pia: Mwanzo 4:4,5; Mambo ya Walawi 1:10; Yoshua 5:11,12.

I11 Sherehe ya matunda ya kwanza, siku 50

baada ya Pasaka, inarejelea kutolewa kwa

Roho Mtakatifu.

MAMBO YA WALAWI 23:15 Nanyi

mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya

Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda

wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato

saba;

16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya

saba mtahesabu siku hamsini; nanyi

mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya.

17 Mtatoa katika makao yenu mikate miwili

ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi

mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba,

itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa

Bwana.

18 Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza

wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa

mwaka wa kwanza, na ng›ombe mume

mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa

sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, pamoja

na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za

kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza

iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

19 Nanyi mtasongeza mbuzi mume mmoja

kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo

wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa

dhabihu ya sadaka za amani.

20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo

mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya

kutikiswa mbele za Bwana, pamoja na wale

wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu

kwa Bwana, wawe wa huyo kuhani.

21 Nanyi mtapiga mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa

na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi

yo yote ya utumishi; ni amri ya milele katika

makao yenu yote, katika vizazi vyenu.

YOHANA 15:26 Lakini ajapo huyo Msaidizi,

nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo

Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye

atanishuhudia.

MATENDO YA MITUME 2:1 Hata

ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako

wote mahali pamoja.

2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama

uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi,

ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana,

kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja

wao.

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza

kusema kwa lugha nyingine, kama Roho

alivyowajalia kutamka.

MATENDO YA MITUME 2:32 Yesu huyo

Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi

wake.

33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono

wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba

ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga

kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

WARUMI 8:23 Wala si hivyo tu; ila na

sisi wenyewe tulio na malimbuko ya

MAMBO YA WALAWI

Page 60: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

60

Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu,

tukikutazamia kufanywa wana, yaani,

ukombozi wa mwili wetu.

1 WAKORINTHO 12:13 Kwa maana katika

Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa

mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au

kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au

ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho

mmoja.

WAEBRANIA 10:15 Na Roho Mtakatifu

naye amshuhudia; kwa maana, baada ya

kusema,

16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada

ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria

zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao

nitaziandika; ndipo anenapo,

YAKOBO 1:18 Kwa kupenda kwake

mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli,

tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

UFUNUO WA YOHANA 14:4 Hawa

ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake,

kwa maana ni bikira. Hawa ndio

wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako.

Hawa wamenunuliwa katika wanadamu,

malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-

Kondoo.

Ona pia: Kutoka 19-20; Kutoka 34:22; Mambo ya Walawi 23:10; Hesabu 28:26-31; Kumbukumbu la Torati 16:9-11; Yeremia 31:31-34; Ezekieli 36:24-30; Malaki 1:13,14; Warumi 8:3; 2 Wakorintho

5:21.

I12 Sherehe ya tabenakulo kuhusiana na kazi

ya Masiha.

MAMBO YA WALAWI 23:33 Kisha

Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku

ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni

sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa

Bwana.

MAMBO YA WALAWI 23:35-38

MAMBO YA WALAWI 23:39 Lakini

siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba,

hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma

mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya

Bwana muda wa siku saba; siku ya kwanza

kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya

nane kutakuwa na kustarehe kabisa.

40 Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda

ya miti mizuri, na makuti ya mitende,

na matawi ya miti minene, na mierebi ya

vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za Bwana,

Mungu wenu, muda wa siku saba.

41 Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa Bwana

muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya

milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika

mwezi wa saba.

42 Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba;

wazalia wote wa Israeli watakaa katika

vibanda;

43 ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa

niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda,

hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri;

mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

ISAYA 12:3 Basi, kwa furaha mtateka

maji katika visima vya wokovu.

ISAYA 55:1 Haya, kila aonaye kiu, njoni

majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni

mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,

Bila fedha na bila thamani.

ZEKARIA 14:16 Hata itakuwa, ya kwamba

kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja

MAMBO YA WALAWI

Page 61: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

61

kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka

baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme,

Bwana wa majeshi, na kuishika sikukuu ya

Vibanda.

17 Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote

wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea

kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme,

Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.

YOHANA 4:13 Yesu akajibu, akamwambia,

Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale

nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali

yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

WAEBRANIA 11:9 Kwa imani alikaa ugenini

katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi

isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na

Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa

ahadi ile ile.

10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye

misingi, ambao mwenye kuubuni na

kuujenga ni Mungu.

11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea

uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa

amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu

yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu

mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu

wengi kama nyota za mbinguni wingi wao,

na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza

kuhesabika.

13 Hawa wote wakafa katika imani,

wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona

tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri

kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya

nchi.

14 Maana hao wasemao maneno kama hayo

waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi

yao wenyewe.

15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile

waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora,

yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu

haoni haya kuitwa Mungu wao; maana

amewatengenezea mji.

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na

upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa

uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,

wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na

majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: Kutoka 13:14; Hesabu 29:12-38; Kumbukumbu la Torati 16:13-15; Kumbukumbu la Torati 31:10-13; 1 Wafalme 8:65,66; 2 Mambo ya Nyakati 7:8-10; Ezra 3:4; Nehemia 8:13-17; Zaburi

36:8; Zaburi 42:1,2; Isaya 35:10; Isaya 41:17,18; Isaya 44:3; Isaya 49:10; Yeremia 2:3; Ezekieli 45:25; Yoeli 3:18; Zekaria 3:10; Zekaria 14:18,19; Yohana 4:10-12; Yohana 16:22; 1 Wakorintho

10:4; 2 Wakorintho 5:1; Waebrania 13:13,14; Ufunuo wa Yohana 7:17; Ufunuo wa Yohana 21:6; Ufunuo wa Yohana 22:1,17.

MAMBO YA WALAWI

Page 62: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

62

Kulingana na mila ya Kiyahudi sadaka ya

kinywaji ilisherehekewa kama ifuatavyo.

Mwanzoni mwa siku ya saba, siku hiyo huitwa

Hoshana Raba kwa lugha ya Kiebrania, kuhani

alitembelea kidimbwi cha Shiloamu. Alichota

maji kutoka kwa kidimbwi na kuyabeba

kwenye mtungi wa dhahabu hadi kwa hekalu.

Alipofika hapo maji yalimwagwa kama sadaka

kwenye mnyama anayetolewa dhabihu. Wakati

wa sherehe ya sadaka ya maji fungu lifuatalo

lilisomewa watu:

Isaya 12:3 Mtachota maji kwa furaha kwa

visima vya wokovu.

Kitabu cha zamani sana cha Kiyahudi

kinasema: «Yule ambaye hajaona furaha

ikionyeshwa wakati wa kuchota maji hajawahi

kamwe kuona furaha maishani mwake

(Mishna Sukka, 5:1). Hivyo kula na kunywa

kwa furaha kubwa wakati wa sherehe ya

tabenakulo kuliamrishwa na Mungu.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

MAMBO YA WALAWI 26:11 Nami

nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala

roho yangu haitawachukia.

12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa

Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.

EZEKIELI 37:27 Tena maskani yangu itakuwa

pamoja nao; nami nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 1:49 Nathanaeli akamjibu, Rabi,

wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme

wa Israeli.

YOHANA 5:46 Kwa maana kama

mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi;

kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

MATENDO YA MITUME 15:16 Baada ya

mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena

nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga

tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

WAEBRANIA 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja,

aliye kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na

kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono,

maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

WAEBRANIA 9:22 Na katika Torati karibu vitu

vyote husafishwa kwa damu, na pasipo

kumwaga damu hakuna ondoleo.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

MAMBO YA WALAWI

Page 63: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

63

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: Kutoka 29:45,46; Kumbukumbu la Torati 18:15; Yoshua 22:19; 2 Mambo ya Nyakati 29:6; Zaburi 78:59,60; Amosi 9:11,12;

Waebrania 8:5,6; Waebrania 13:10-13.

MAMBO YA WALAWI

Page 64: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

64

I07 Sadaka ya ndama wa kike mwekundu

inarejelea kazi ya Masiha.

HESABU 19:2 Hii ndiyo amri ya sheria

Bwana aliyoagiza, akisema, Waambie

wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke

mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu,

ambaye hajatiwa nira bado;

3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye

atakwenda naye nje ya kambi, na mtu

mmoja atamchinja mbele yake;

9 Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu

ya huyo ng’ombe, na kuyaweka yawe akiba

katika mahali safi nje ya kambi, nayo

yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana

wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni

sadaka ya dhambi.

YOHANA 15:3 Ninyi mmekwisha kuwa safi

kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

WAGALATIA 3:13 Kristo alitukomboa katika

laana ya torati, kwa kuwa alifanywa

laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

WAEFESO 5:26 ili makusudi alitakase na

kulisafisha kwa maji katika neno;

WAEBRANIA 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao

wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,

akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake,

akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi

mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

WAEBRANIA 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja,

aliye kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na

kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono,

maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na

mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe

waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa

hata kuusafisha mwili;

14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye

kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi

yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na

mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na

matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu

aliye hai?

WAEBRANIA 10:14 Maana kwa toleo

moja amewakamilisha hata milele hao

wanaotakaswa.

WAEBRANIA 13:11 Maana wanyama

wale ambao damu yao huletwa ndani ya

patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya

dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya

kambi.

12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu

kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya

lango.

13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi,

tukichukua shutumu lake.

Ona pia: Waebrania 10:19-22,29.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

HESABU 21:9 Musa akafanya nyoka ya

shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka

amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya

shaba, akaishi.

HESABU

Page 65: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

65

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

YOHANA 3:14 Na kama vile Musa

alivyomwinua yule nyoka jangwani,

vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi

kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa

milele katika yeye.

YOHANA 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake

Baba yangu ni haya, ya kwamba kila

amtazamaye Mwana na kumwamini yeye,

awe na uzima wa milele; nami nitamfufua

siku ya mwisho.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

Ona pia: 2 Wafalme 18:4.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HESABU 24:7 Maji yatafurika katika ndoo

zake, Na mbegu zake zitakuwa katika maji

mengi. Na mfalme wake ataadhimishwa

kuliko Agagi, Na ufalme wake utatukuzwa.

8 Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu

mfano wa nguvu za nyati; Atawameza

mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa

yao vipande vipande. Atawachoma kwa

mishale yake.

15 Akatunga mithali yake akasema, Balaamu

mwana wa Beori asema, Yule mtu

aliyefumbwa macho asema,

16 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na

kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye

maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi,

amefumbuliwa macho,

17 Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini

si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo

Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli;

Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na

kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.

18 Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa

milki, waliokuwa adui zake; Israeli

watakapotenda kwa ushujaa.

19 Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo,

Atawaangamiza watakaobaki mjini.

MWANZO 49:10 Fimbo ya enzi haitaondoka

katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya

miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye

milki, Ambaye mataifa watamtii.

ZABURI 110:2 Bwana atainyosha toka

Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi

kati ya adui zako;

DANIELI 2:44 Na katika siku za wafalme

hao Mungu wa mbinguni atausimamisha

ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala

watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali

utavunja falme hizi zote vipande vipande na

kuziharibu, nao utasimama milele na milele.

MATHAYO 2:1 Yesu alipozaliwa katika

Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme

Herode, tazama, mamajusi wa mashariki

walifika Yerusalemu, wakisema,

2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa

Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake

HESABU

Page 66: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

66

mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

1 WAKORINTHO 15:24 Hapo ndipo

mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme

wake; atakapobatilisha utawala wote, na

mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke

maadui wake wote chini ya miguu yake.

WAFILIPI 2:10 ili kwa jina la Yesu kila

goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi;

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa

hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia

mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

UFUNUO WA YOHANA 19:16 Naye ana

jina limeandikwa katika vazi lake na paja

lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana

WA MABwana.

UFUNUO WA YOHANA

22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika

wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo

katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina

na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa

ya asubuhi.

Ona pia: #1; Hesabu 24:4; Zaburi 18:43; Yohana 1:49; Yuda 1:11; 2 Petro 1:19; Ufunuo wa Yohana 2:14; Ufunuo wa Yohana 20.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

I03 Sadaka ya kuteketeza inawakilisha kazi ya

Masiha - sadaka isiyo na

dosari - sadaka ya kudumu ya kuteketeza

.

HESABU 28:3 Nawe utawaambia, Hii

ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto

mtakayomsongezea Bwana; wana-

kondoo waume wa mwaka wa kwanza

wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya

kuteketezwa ya sikuzote.

4 Mwana-kondoo mmoja utamsongeza

asubuhi, na mwana-kondoo wa pili

utamsongeza jioni;

5 pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya

unga mwembamba kuwa sadaka ya unga,

uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta

ya kupondwa.

6 Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote,

iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe

harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa

kwa Bwana kwa moto.

7 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo

ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo

sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia

Bwana katika mahali hapo patakatifu.

8 Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza

wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga

iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake

ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni

sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu

ya kupendeza kwa Bwana.

9 Tena katika siku ya Sabato watasongezwa

wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa

kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya

kumi mbili za efa za unga mwembamba

kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na

mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;

10 hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila

HESABU

Page 67: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

67

Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa

ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya

kinywaji.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

MATHAYO 27:51 Na tazama, pazia la hekalu

likapasuka vipande viwili toka juu hata chini;

nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

LUKA 23:45 jua limepungua nuru yake;

pazia la hekalu likapasuka katikati.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

WAEBRANIA 7:25 Naye, kwa sababu hii, aweza

kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa

yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu

wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na

uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa

na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

27 ambaye hana haja kila siku, mfano wa

wale makuhani wakuu wengine, kwanza

kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake

mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao

watu; maana yeye alifanya hivi mara moja,

alipojitoa nafsi yake.

28 Maana torati yawaweka wanadamu walio na

unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo

neno la kiapo kilichokuja baada ya torati

limemweka Mwana, aliyekamilika hata

milele.

WAEBRANIA 9:26 kama ni hivyo, ingalimpasa

kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi

wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu,

katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa,

azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi

yake.

WAEBRANIA 10:1 Basi torati, kwa kuwa ni

kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura

yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile

zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi

wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.

2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma

kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha

kusafishwa mara moja, wasingejiona tena

kuwa na dhambi?

3 Lakini katika dhabihu hizo liko

kumbukumbu la dhambi kila mwaka.

4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na

mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili

uliniwekea tayari;

6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika

gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye

mapenzi yako, Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na

sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi

hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo

(zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja

HESABU

Page 68: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

68

niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza,

ili kusudi alisimamishe la pili.

10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa

kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja

tu.

1 PETRO 1:19 bali kwa damu ya thamani,

kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na

waa, yaani, ya Kristo.

20 Naye amejulikana kweli tangu zamani,

kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini

alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili

yenu;

Ona pia: Kutoka 29:41,42; Mambo ya Walawi 6:9,12; Mambo ya Walawi 9:3; Mambo ya Walawi 12:6; Mambo ya Walawi 14:12,13,21,24,25; Mambo ya Walawi 17:3; Mambo ya Walawi 23:12; Hesabu 6:12,14; Hesabu 29:6,41-43; Waamuzi 13:33; 2

Mambo ya Nyakati 2:4; Ezra 3:4,5; Nehemia 10:33; Zaburi 50:8; Zaburi 51:16-19; Isaya 56:7; Ezekieli 43:27; Ezekieli 46:13-15; Yoeli 2:14; Marko 15:38; Yohana 4:34; Warumi 12:1; Waebrania 10:14;

1 Petro 2:5.

HESABU

Page 69: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

69

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

KUMBUKUMBU LA TORATI 11:18 Kwa hiyo

yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu

na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu

ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe

katikati ya macho yenu.

19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa

kuyazungumza uketipo katika nyumba

yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na

uondokapo.

20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba

yako, na juu ya malango yako;

YOSHUA 1:8 Kitabu hiki cha torati

kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari

maneno yake mchana na usiku, upate

kuangalia kutenda sawasawa na maneno

yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo

utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo

utakapositawi sana.

ZABURI 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki; Wala

hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala

hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na

sheria yake huitafakari mchana na usiku.

ZABURI 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka

neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

ZABURI 119:97 Sheria yako naipenda mno

ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana

kutwa.

98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui

zangu, Kwa maana ninayo sikuzote.

99 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,

Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.

ISAYA 34:16 Tafuteni katika kitabu

cha Bwana mkasome; hapana katika hao

wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja

atakayemkosa mwenzake; kwa maana

kinywa changu kimeamuru, na roho yake

imewakusanya.

YEREMIA 8:9 Wenye hekima

wametahayari, wamefadhaika na kushikwa;

tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana

akili gani ndani yao?

MATHAYO 22:29 Yesu akajibu, akawaambia,

Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko

wala uweza wa Mungu.

LUKA 16:29 Ibrahimu akasema, Wanao

Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini

kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu,

watatubu.

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na

manabii, hawatashawishwa hata mtu

akifufuka katika wafu.

YOHANA 5:39 Mwayachunguza maandiko,

kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna

uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo

yanayonishuhudia.

MATENDO YA MITUME 17:11 Watu

hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa

Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno

kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza

maandiko kila siku, waone kwamba mambo

hayo ndivyo yalivyo.

WARUMI 3:2 Kwafaa sana kwa kila njia.

Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia

ya Mungu.

KUMBUKUMBU LA TORATI

Page 70: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

70

2 PETRO 1:19 Nasi tuna lile neno

la unabii lililo imara zaidi, ambalo,

mkiliangalia, kama taa ing›aayo mahali

penye giza, mwafanya vyema, mpaka

kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi

kuzuka mioyoni mwenu.

20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba

hakuna unabii katika maandiko upatao

kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.

21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa

mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu

walinena yaliyotoka kwa Mungu,

wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

UFUNUO WA YOHANA 1:3 Heri

asomaye na wao wayasikiao maneno ya

unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa

humo; kwa maana wakati u karibu.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 6:6-8; Zaburi 19:7-10; Waefeso 6:17; Wakolosai 3:16; 1 Wathesalonike 5:27; 1 Petro 2:2.

B13 Mamlaka ya Masiha.

D02 Kazi ya Masiha kama Nabii.

D07 Masiha atakuwa Mpatanishi.

KUMBUKUMBU LA TORATI 18:15 Bwana,

Mungu wako, atakuondokeshea nabii

miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo

mimi; msikilizeni yeye.

16 Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu

wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko,

ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana,

Mungu wangu, wala nisiuone tena moto

huu mkubwa, nisije nikafa.

17 Bwana akaniambia, Wametenda vema

kusema walivyosema.

18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni

mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami

nitatia maneno yangu kinywani mwake,

naye atawaambia yote nitakayomwamuru.

19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno

yangu atakayosema yule kwa jina langu,

nitalitaka kwake.

MATHAYO 17:5 Alipokuwa katika kusema,

tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na

tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,

ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, ninayependezwa naye; msikieni

yeye.

MATHAYO 21:10 Hata alipoingia Yerusalemu,

mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni

nani huyu?

11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii,

Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

MARKO 16:16 Aaminiye na kubatizwa

ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

LUKA 7:13 Bwana alipomwona

alimwonea huruma, akamwambia, Usilie.

14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale

waliokuwa wakilichukua wakasimama.

Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.

15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza

kusema. Akampa mama yake.

16 Hofu ikawashika wote, wakamtukuza

Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea

kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.

LUKA 9:18 Ikawa alipokuwa akisali

kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo

pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao

wanasema ya kuwa mimi ni nani?

19 Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji;

lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba

mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.

KUMBUKUMBU LA TORATI

Page 71: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

71

20 Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba

mimi ni nani? Petro akamjibu akasema,

Ndiwe Kristo wa Mungu.

LUKA 9:35 Sauti ikatoka katika wingu,

ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule

wangu, msikieni yeye.

LUKA 24:17 Akawaambia, Ni

maneno gani haya mnayosemezana hivi

mnapotembea? Wakasimama wamekunja

nyuso zao.

18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa,

akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni

katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia

humo siku hizi?

19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia,

Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu

nabii, mwenye uwezo katika kutenda na

kunena mbele za Mungu na watu wote;

20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa

wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa,

wakamsulibisha.

YOHANA 1:45 Filipo akamwona

Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona

yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na

manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa

Nazareti.

YOHANA 4:19 Yule mwanamke

akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u

nabii!

YOHANA 4:25 Yule mwanamke

akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi,

(aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye

atatufunulia mambo yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe,

ndiye.

YOHANA 6:14 Basi watu wale, walipoiona

ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni

nabii yule ajaye ulimwenguni.

YOHANA 7:40 Basi wengine katika

mkutano walipoyasikia maneno hayo,

walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.

41 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo.

Wengine wakasema, Je! Kristo atoka

Galilaya?

42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo

atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka

Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu

asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na

kutengwa na watu wake.

24 Naam, na manabii wote tangu Samweli na

wale waliokuja baada yake, wote walionena,

walihubiri habari za siku hizi.

25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa

maagano yale, ambayo Mungu aliagana

na baba zenu, akimwambia Ibrahimu,

Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu

zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

wenu na maovu yake.

MATENDO YA MITUME 7:37 Musa

huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana

Mungu wenu atawainulieni nabii, katika

ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye.

KUMBUKUMBU LA TORATI

Page 72: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

72

WAEBRANIA 2:3 sisi je! Tutapataje kupona,

tusipojali wokovu mkuu namna hii?

Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha

ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

WAEBRANIA 3:7 Kwa hiyo, kama anenavyo

Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti

yake,

8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati

wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika

jangwa,

Ona pia: Waebrania 1:1,2; Waebrania 3:2-8; Waebrania 10:26; Waebrania 12:25,26.

F11 Mateso ya Masiha.

KUMBUKUMBU LA TORATI 21:23 mzoga

wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima

utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa

amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi

katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu

wako, iwe urithi wako.

WAGALATIA 3:13 Kristo alitukomboa katika

laana ya torati, kwa kuwa alifanywa

laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

KUMBUKUMBU LA TORATI 33:3

Hakika awapenda hayo makabila ya watu;

Watakatifu wake wote wamo mkononi

mwako; Nao waliketi miguuni pako;

Watapokea kila mmoja katika maneno yako.

YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu

aliupenda ulimwengu, hata akamtoa

Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye

asipotee, bali awe na uzima wa milele.

YOHANA 10:28 Nami nawapa uzima wa

milele; wala hawatapotea kamwe; wala

hakuna mtu atakayewapokonya katika

mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

YOHANA 17:24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate

na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa

maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

1 WATHESALONIKE 1: 6 Nanyi mkawa

wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha

kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja

na furaha ya Roho Mtakatifu.

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 1:20 Siri ya

zile nyota saba ulizoziona katika mkono

wangu wa kuume, na ya vile vinara saba

vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa

KUMBUKUMBU LA TORATI

Page 73: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

73

yale makanisa saba; na vile vinara saba ni

makanisa saba.

Ona pia: Kutoka 19:5,6; Kumbukumbu la Torati 7:7-10; 1 Samweli 2:9; Zaburi 31:23; Yeremia 31:3; Malaki 1:2; Luka 10:39; Yohana 17:11-15; Warumi 8:35-39; Warumi 9:11-13; Waefeso 2:4,5;

Yohana 4:19; Yuda 1:1.

KUMBUKUMBU LA TORATI

Page 74: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

74

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

RUTHU 4:13 Basi Boazi akamtwaa

Ruthuu, naye akawa mke wake; naye

akaingia kwake, na Bwana akamjalia

kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa

kiume.

14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi,

Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali

huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu

na liwe kuu katika Israeli.

17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake

wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa

mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye

ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

21 na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi

akamzaa Obedi;

22 na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa

Daudi.

MATHAYO 1:5 Salmoni akamzaa Boazi kwa

Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu;

Obedi akamzaa Yese;

6 Yese akamzaa mfalme Daudi.

MATHAYO 1:15 Eliudi akamzaa Eleazari;

Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa

Yakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu

aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi

ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi

hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi

na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli

hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

Ona pia: Mambo ya Walawi 25:25-29; Mambo ya Walawi 27:13-31; Ayubu 19:25; Zaburi 19:14; Zaburi 78:35; Isaya 41:14; Isaya

44:6,24; Isaya 48:17; Isaya 49:7; Isaya 54:5,8; Isaya 59:20; Isaya 60:16; Mathayo 1:1-17; Luka 3:23-38.

RUTHU

Page 75: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

75

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

1 SAMWELI 2:10 Washindanao na Bwana

watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye

atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho

ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu,

Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

ZABURI 96:13 Mbele za Bwana, kwa maana

anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu

nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na

mataifa kwa uaminifu wake.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake;

naye atawabagua kama vile mchungaji

abaguavyo kondoo na mbuzi;

WARUMI 14:10 Lakini wewe je! Mbona

wamhukumu ndugu yako? Au wewe je!

Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa

maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti

cha hukumu cha Mungu.

11 Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo,

anena Bwana, kila goti litapigwa mbele

zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.

12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu

atatoa habari zake mwenyewe mbele za

Mungu.

2 WAKORINTHO 5:10 Kwa maana

imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele

ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu

apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa

mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema

au mabaya.

UFUNUO WA YOHANA 20:11 Kisha

nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe,

na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na

mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao

hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo,

wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi;

na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine

kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na

hao wafu wakahukumiwa katika mambo

hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,

sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani

yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu

waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa

kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa

la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo

ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana

ameandikwa katika kitabu cha uzima,

alitupwa katika lile ziwa la moto.

Ona pia: #1; #6; Zaburi 2:2; Zaburi 20:6; Zaburi 45:7; Zaburi 89:17,24; Zaburi 92:9; Mathayo 28:18; Luka 1:69; Matendo ya

Mitume 4:27; Matendo ya Mitume 10:38.

1 SAMWELI

Page 76: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

76

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

2 SAMWELI 7:12 Nawe siku zako

zitakapotimia, ukalala na baba zako,

nitainua mzao wako nyuma yako,

atakayetoka viunoni mwako, nami

nitaufanya imara ufalme wake.

13 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina

langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake

nitakifanya imara milele.

14 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa

mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu

kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya

wanadamu;

15 lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama

vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa

mbele yako.

16 Na nyumba yako, na ufalme wako,

vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti

chako kitafanywa imara milele.

ZABURI 89:26 Yeye ataniita, Wewe baba

yangu, Mungu wangu na mwamba wa

wokovu wangu.

27 Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa

kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa

dunia.

28 Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na

agano langu litafanyika amini kwake.

29 Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na

kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.

MATHAYO 3:17 na tazama, sauti kutoka

mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo

wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua

cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao wa utukufu wake

na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote

kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa

kuume wa Ukuu huko juu;

4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri

jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.

5 Kwa maana alimwambia malaika yupi

wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo

nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake

baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza

ulimwenguni, asema, Na wamsujudu

malaika wote wa Mungu.

7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye

2 SAMWELI

Page 77: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

77

malaika zake kuwa pepo, Na watumishi

wake kuwa miali ya moto.

8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti

chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na

milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya

adili.

1 YOHANA 4:9 Katika hili pendo la Mungu

lilionekana kwetu, kwamba Mungu

amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni,

ili tupate uzima kwa yeye.

10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda

Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi,

akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa

dhambi zetu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; 1 Wafalme 5:5; 1 Wafalme 8:19; 1 Mambo ya Nyakati 17:11; Zaburi 72:17-19; Zaburi 89:36,37; Isaya 9:7;

Yeremia 23:5,6; Danieli 2:44; Danieli 7:14; Zekaria 6:13; Mathayo 16:18; Yohana 12:34; Matendo ya Mitume 13:34-37; 1 Petro 2:5;

Ufunuo wa Yohana 20.

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

2 SAMWELI 22:20 Akanitoa akanipeleka panapo

nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa

nami.

21 Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu;

Sawasawa na usafi wa mikono yangu

akanilipa.

22 Maana nimezishika njia za Bwana, Wala

sikumwasi Mungu wangu.

23 Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele

yangu; Na kwa habari za amri zake,

sikuziacha.

24 Nami nalikuwa mkamilifu kwake,

Nikajilinda na uovu wangu.

25 Basi Bwana amenilipa sawasawa na haki

yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu

mbele zake.

ZABURI 1:2 Bali sheria ya Bwana ndiyo

impendezayo, Na sheria yake huitafakari

mchana na usiku.

ZABURI 22:8 Husema, Umtegemee

Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa,

maana apendezwa naye.

ZABURI 40:8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee

Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam,

sheria yako imo moyoni mwangu.

ISAYA 42:1 Tazama mtumishi wangu

nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye

nafsi yangu imependezwa naye; nimetia

roho yangu juu yake; naye atawatolea

mataifa hukumu.

MATHAYO 3:17 na tazama, sauti kutoka

mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

MATHAYO 17:5 Alipokuwa katika kusema,

tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na

tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,

ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, ninayependezwa naye; msikieni

yeye.

YOHANA 15:10 Mkizishika amri zangu,

mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi

nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa

katika pendo lake.

2 SAMWELI

Page 78: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

78

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WARUMI 10:4 Kwa maana Kristo ni

mwisho wa sheria, ili kila aaminiye

ahesabiwe haki.

Ona pia: Zaburi 18:19-24; Zaburi 37:31; Zaburi 119:13,30,102; Yohana 8:29; Yohana 13:31,32; Warumi 3:31; Warumi 7:12;

Warumi 8:3,4; Wagalatia 3:13,21; Wagalatia 5:22,23.

B13 Mamlaka ya Masiha.

B21 Masiha ndiye Nuru.

E09 Uadilifu wa Masiha.

2 SAMWELI 23:1 Basi haya ndiyo maneno

ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa

Yese, anena, anena huyo mtu aliyeinuliwa

juu, Yeye, masihi wake Mungu wa

Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli

mwenye kupendeza;

2 Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na

neno lake likawa ulimini mwangu.

3 Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa

Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu

kwa haki, Akitawala katika kicho cha

Mungu,

4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,

Asubuhi isiyo na mawingu.

ZABURI 72:6 Atashuka kama mvua juu

ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu

yainyweshayo nchi.

7 Siku zake yeye, mtu mwenye haki

atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi

utakapokoma.

8 Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka

Mto hata miisho ya dunia.

MIKA 5:2 Bali wewe, Bethlehemu

Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa

elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea

mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;

ambaye matokeo yake yamekuwa tangu

zamani za kale, tangu milele.

LUKA 1:76 Nawe, mtoto, utaitwa nabii

wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia

mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia

zake;

77 Uwajulishe watu wake wokovu, Katika

kusamehewa dhambi zao.

78 Kwa njia ya rehema za Mungu wetu,

Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu

umetufikia,

79 Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa

mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye

njia ya amani.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

YOHANA 12:35 Basi Yesu akawaambia,

Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo.

Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza

lisije likawaweza; maana aendaye gizani

hajui aendako.

36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo

aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha

wasimwone.

UFUNUO WA YOHANA 21:23 Na mji

ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,

2 SAMWELI

Page 79: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

79

kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru,

na taa yake ni Mwana-Kondoo.

Ona pia: #1; Kumbukumbu la Torati 32:4,30,31; Zaburi 2:6-8; Zaburi 72:6; Zaburi 89:35; Isaya 4:2; Isaya 60:1-3,19,20; Hosea

6:3; Mika 5:8; Yohana 1:6,7.

2 SAMWELI

Page 80: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

80

E01 Aina ya huduma ya Masiha.

2 WAFALME 1:6 Wakamwambia, Mtu

alitokea, akaonana nasi, akatuambia,

Enendeni, rudini kwa mfalme yule

aliyewatuma, mkamwambie, Bwana asema

hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu

katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa

Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa

ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda

ulichokipanda, bali hakika utakufa.

11 Akatuma tena akida wa hamsini mwingine

pamoja na hamsini wake, wamwendee.

Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu,

mfalme asema, Shuka upesi.

12 Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni

mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka

mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini

wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka

mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini

wake.

LUKA 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake

zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso

wake kwenda Yerusalemu;

52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso

wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha

Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa

vile alivyouelekeza uso wake kwenda

Yerusalemu.

54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana

walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka

tuagize moto ushuke kutoka mbinguni,

uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?

55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema,

Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]

56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja

kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.

Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

YOHANA 3:17 Maana Mungu hakumtuma

Mwana ulimwenguni ili auhukumu

ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe

katika yeye.

YOHANA 12:47 Na mtu akiyasikia maneno

yangu, asiyashike, mimi simhukumu;

maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila

niuokoe ulimwengu.

MATENDO YA MITUME 1:8 Lakini

mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu

Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi

wangu katika Yerusalemu, na katika

Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho

wa nchi.

MATENDO YA MITUME

8:14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu,

waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali

neno la Mungu, wakawapelekea Petro na

Yohana;

Ona pia: Mithali 9:8; Yeremia 23:13; Mika 1:5; Mathayo 18:11; Mathayo 20:28; Luka 19:10; Yohana 4:4,9,40-42; Matendo ya

Mitume 9:31; 1 Timotheo 1:15.

2 WAFALME

Page 81: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

81

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

1 MAMBO YA NYAKATI 17:11 Hata

itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende

na babazo, nitainua mzao wako nyuma

yako, atakayekuwa wa wana wako; nami

nitaufanya imara ufalme wake.

MATHAYO 2:1 Yesu alipozaliwa katika

Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme

Herode, tazama, mamajusi wa mashariki

walifika Yerusalemu, wakisema,

2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa

Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake

mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

MATENDO YA MITUME 13:36 Kwa

maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri

la Mungu katika kizazi chake, alilala,

akawekwa pamoja na baba zake, akaona

uharibifu.

37 Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona

uharibifu.

WARUMI 1:3 yaani, habari za Mwanawe,

aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi

ya mwili,

Ona pia: #1.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

1 MAMBO YA NYAKATI 17:12 Yeye ndiye

atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya

imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele.

YOHANA 2:19 Yesu akajibu, akawaambia,

Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu

nitalisimamisha.

20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili

lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na

sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili

wake.

MATENDO YA MITUME 7:47 Lakini

Sulemani alimjengea nyumba.

48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba

zilizofanywa kwa mikono, kama vile

asemavyo nabii,

49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni

pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani

mtakayonijengea? Asema Bwana,

WAKOLOSAI 2:9 Maana katika yeye unakaa

utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya

kimwili.

Ona pia: #1; Zekaria 6:12,13.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

1 MAMBO YA NYAKATI 17:13 Nitakuwa

baba yake, naye atakuwa mwanangu;

wala sitamwondolea fadhili zangu, kama

nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako;

LUKA 9:35 Sauti ikatoka katika wingu,

ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule

wangu, msikieni yeye.

YOHANA 3:3 Yesu akajibu, akamwambia,

Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa

mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa

Mungu.

WAEBRANIA 1:5 Kwa maana alimwambia

1 MAMBO YA NYAKATI

Page 82: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

82

malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe

mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na

tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye

atakuwa kwangu mwana?

Ona pia: #1; Zaburi 2:7,12.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

1 MAMBO YA NYAKATI 17:14 ila

nitamstarehesha katika nyumba yangu na

katika ufalme wangu milele; na kiti chake

cha enzi kitathibitishwa milele.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Ona pia: #1; Waebrania 3:6.

1 MAMBO YA NYAKATI

Page 83: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

83

D08 Masiha atakuwa Dhamana.

AYUBU 17:3 Nipe rehani basi, uwe

dhamana kwa ajili yangu kwako wewe

mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea

dhamana?

MITHALI 11:15 Amdhaminiye mgeni hakosi

ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu

salama.

MITHALI 17:18 Aliyepungukiwa na akili

hupana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini

mbele ya mwenzake.

MITHALI 22:26 Usiwe mmoja wao wawekao

rehani; Au walio wadhamini kwa deni za

watu;

WAEBRANIA 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu

amekuwa mdhamini wa agano lililo bora

zaidi.

Ona pia: Isaya 38:14; Yeremia 30:21,22.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

E11 Masiha atapeana uzima wa milele.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

AYUBU 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa

Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye

atasimama juu ya nchi.

26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa

hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu

nitamwona Mungu;

27 Nami nitamwona mimi nafsi yangu,

Na macho yangu yatamtazama, wala si

mwingine. Mtima wangu unazimia ndani

yangu.

ISAYA 26:19 Wafu wako wataishi, maiti

zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi

mnaokaa mavumbini, kwa maana umande

wako ni kama umande wa mimea, nayo

ardhi itawatoa waliokufa.

DANIELI 12:2 Tena, wengi wa hao walalao

katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine

wapate uzima wa milele, wengine aibu na

kudharauliwa milele.

YOHANA 5:28 Msistaajabie maneno hayo;

kwa maana saa yaja, ambayo watu wote

waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

WARUMI 8:13 kwa maana kama tukiishi

kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka

kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya

mwili kwa Roho, mtaishi.

1 WAKORINTHO 15:22 Kwa kuwa kama

katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na

katika Kristo wote watahuishwa.

23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko

ni Kristo; baadaye walio wake Kristo,

atakapokuja.

UFUNUO WA YOHANA 1:18 na aliye

hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama,

ni hai hata milele na milele. Nami ninazo

funguo za mauti, na za kuzimu.

Ona pia: Ayubu 33:23,24; Zaburi 19:14; Isaya 54:5; Isaya 59:20,21; Ezekieli 37:7-10; Waefeso 1:7; 2 Timotheo 4:8.

AYUBU

Page 84: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

84

B11 Utiifu wa Masiha.

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

G05 Masiha atapata matunda mengi.

ZABURI 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki; Wala

hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala

hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na

sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa

Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao

matunda yake kwa majira yake, Wala

jani lake halinyauki; Na kila alitendalo

litafanikiwa.

4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama

makapi yapeperushwayo na upepo.

5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama

hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko

la wenye haki.

6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,

Bali njia ya wasio haki itapotea.

ZABURI 40:8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee

Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam,

sheria yako imo moyoni mwangu.

ISAYA 53:11 Ataona mazao ya taabu ya

nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake

mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya

wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua

maovu yao.

YEREMIA 17:7 Amebarikiwa mtu yule

anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni

tumaini lake.

8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando

ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto;

Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali

jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika

mwaka wa uchache wa mvua, Wala

hautaacha kuzaa matunda.

YOHANA 4:34 Yesu akawaambia, Chakula

changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake

aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

WARUMI 3:12 Wote wamepotoka, wameoza

wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata

mmoja.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

UFUNUO WA YOHANA 22:2 katikati

ya njia kuu yake. Na upande huu na upande

huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima,

uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye

kutoa matunda yake kila mwezi; na majani

ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: Mwanzo 2:9; Kumbukumbu la Torati 11:18-20; Yoshua 1:8; Zaburi 37:30,31; Zaburi 104:34; Zaburi 112:1; Zaburi

119:11,15,16,24,47,97-99; Yeremia 31:33; Malaki 3:17,18; Warumi 7:22; Waebrania 8:10; Yohana 5:3.

F12 Masiha atapingwa.

ZABURI 2:1 Mbona mataifa wanafanya

ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?

LUKA 18:32 Kwa kuwa atatiwa mikononi

mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa

jeuri, na kutemewa mate;

MATENDO YA MITUME 4:24 Nao

waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao

ZABURIEN

Page 85: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

85

kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe

ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na

nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;

25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa

kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako,

Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na

makabila wametafakari ubatili?

26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu

wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na

juu ya Kristo wake.

27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato

pamoja na Mataifa na watu wa Israeli,

walikusanyika katika mji huu juu ya

Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia

mafuta,

28 ili wafanye yote ambayo mkono wako na

mashauri yako yamekusudia tangu zamani

yatokee.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #1; Zaburi 83:2-5; Mathayo 21:38; Yohana 11:50; Matendo ya Mitume 5:33; Matendo ya Mitume 16:22.

F12 Masiha atapingwa.

ZABURI 2:2 Wafalme wa dunia

wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri

pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi

wake.

3 Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia

mbali nasi kamba zao.

LUKA 13:31 Saa ile ile Mafarisayo kadha

wa kadha walimwendea, wakamwambia,

Toka hapa, uende mahali pengine, kwa

sababu Herode anataka kukuua.

LUKA 19:14 Lakini watu wa mji wake

walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata

na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

LUKA 23:11 Basi Herode akamfanya

duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki,

na kumvika mavazi mazuri; kisha

akamrudisha kwa Pilato.

12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana

kwa urafiki kwa maana hapo kwanza

walikuwa na uadui wao kwa wao.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #1; Mathayo 2:16; Mathayo 25:59; Mathayo 27:1; Yohana 1:41; Yohana 15:23; Matendo ya Mitume 4:5-8; Matendo ya Mitume 10:38; Matendo ya Mitume 12:1-6; Waebrania 1:9; 1

Petro 2:7,8.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 2:4 Yeye aketiye mbinguni

anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

5 Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na

kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.

6 Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya

Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

MATHAYO 23:33 Enyi nyoka, wana wa majoka,

mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

ZABURIEN

Page 86: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

86

34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma

kwenu manabii na wenye hekima na

waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua

na kuwasulibisha, na wengine wao

mtawapiga katika masinagogi yenu, na

kuwafukuza mji kwa mji;

35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki

iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya

Habili, yule mwenye haki, hata damu ya

Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya

patakatifu na madhabahu.

36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote

yatakuja juu ya kizazi hiki.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

WAEFESO 1:22 akavitia vitu vyote chini ya

miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya

vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 14:1 Kisha

nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo

amesimama juu ya mlima Sayuni, na

watu mia na arobaini na nne elfu pamoja

naye, wenye jina lake na jina la Baba yake

limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

UFUNUO WA YOHANA 19:15 Na

upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

Ona pia: #1; Zaburi 11:4; Zaburi 37:13; Zaburi 50:16-22; Zaburi 59:8; Zaburi 115:3; Mithali 1:26; Isaya 40:22; Zekaria 1:15; Luka 19:27,43,44; Matendo ya Mitume 2:34-36; Matendo ya Mitume

5:30,31; Waebrania 12:22-25; Ufunuo wa Yohana 14:1; Ufunuo wa Yohana 19:15.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

B04 Sifa za Uungu za Masiha.

ZABURI 2:7 Nitaihubiri amri; Bwana

aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo

nimekuzaa.

MATHAYO 3:17 na tazama, sauti kutoka

mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

MATENDO YA MITUME 13:32 Na sisi

tunawahubiri habari njema ya ahadi ile

waliyopewa mababa,

33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto

wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama

ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe

ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.

WARUMI 1:1 Paulo, mtumwa wa Kristo

Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa

aihubiri Injili ya Mungu;

2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa

kinywa cha manabii wake katika maandiko

matakatifu;

3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika

ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,

ZABURIEN

Page 87: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

87

4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana

wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu,

kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana

wetu;

WAEBRANIA 5:5 Vivyo hivyo Kristo naye

hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani

mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe

mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

6 kama asemavyo mahali pengine,

Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa

Melkizedeki.

Ona pia: Mathayo 16:16; Mathayo 17:5; Yohana 1:14,18; Warumi 1:1-4; Waebrania 1:5,6.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 2:8 Uniombe, nami nitakupa

mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya

dunia kuwa milki yako.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali

nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WAFILIPI 2:9 Kwa hiyo tena Mungu

alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile

lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ona pia: #1; #2; #4; Zaburi 22:17; Matendo ya Mitume 20:21; Matendo ya Mitume 26:18-20; Warumi 16:26; 1 Wathesalonike

1:9; Ufunuo wa Yohana 7:9-12; Ufunuo wa Yohana 15:4.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 2:9 Utawaponda kwa fimbo ya

chuma, Na kuwavunja kama chombo cha

mfinyanzi.

UFUNUO WA YOHANA 2:26 Na yeye

ashindaye, na kuyatunza matendo yangu

hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya

mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma,

kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo,

kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba

yangu.

UFUNUO WA YOHANA

12:5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye

atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya

chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata

kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.

Ona pia: #1; Zaburi 21:8,9; Zaburi 89:22; Isaya 30:14; Isaya 60:12; Danieli 2:44.

ZABURIEN

Page 88: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

88

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 2:10 Na sasa, enyi wafalme,

fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia,

mwadibiwe.

11 Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni

kwa kutetemeka.

12 Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira,

Nanyi mkapotea njiani,Kwa kuwa

hasira yake itawaka upesi,Heri wote

wanaomkimbilia.

ISAYA 60:1 Ondoka, uangaze; kwa kuwa

nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana

umekuzukia.

2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na

giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali

Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake

utaonekana juu yako.

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme

kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4 Inua macho yako, utazame pande zote; Wote

wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana

wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako

watabebwa nyongani.

5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo

wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa

wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri

wa mataifa utakuwasilia.

YOHANA 5:23 ili watu wote wamheshimu

Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.

Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba

aliyempeleka.

2 WATHESALONIKE 1:8 katika mwali

wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao

wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya

Bwana wetu Yesu;

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele,

kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa

nguvu zake;

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa

moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi;

naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila

yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika

damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,

wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani

nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake

na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA

Bwana WA MABwana.

Ona pia: #1; #2; Zaburi 40:4; Zaburi 84:12; Zaburi 146:3-5; Mithali 16:20; Yeremia 17:7; Warumi 10:11; Waebrania 1:5;

Waebrania 12:22-25,28,29; 1 Petro 2:6; 1 Petro 1:21.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

ZABURI 8:1 Wewe, MUNGU, Bwana

wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani

mwote! Wewe umeuweka utukufu wako

mbinguni;

2 Vinywani mwa watoto wachanga na

wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu;

Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;

ZABURIEN

Page 89: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

89

Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.

MATHAYO 11:25 Wakati ule Yesu akajibu,

akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana

wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo

haya uliwaficha wenye hekima na akili,

ukawafunulia watoto wachanga.

MATHAYO 21:15 Lakini wakuu wa makuhani

na waandishi walipoyaona maajabu

aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao

hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa

Daudi! Walikasirika,

16 wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo?

Yesu akawaambia, Naam; hamkupata

kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga

na wanyonyao umekamilisha sifa?

Ona pia: Luka 10:21; 1 Wakorintho 1:27.

B07 Uweza wa Yote wa Masiha.

ZABURI 8:6 Umemtawaza juu ya kazi za

mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya

miguu yake.

WAEFESO 1:22 akavitia vitu vyote chini ya

miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya

vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

Ona pia: Mathayo 28:18; Waebrania 1:2; Waebrania 2:8.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 16:8 Nimemweka Bwana mbele

yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni

kwangu, sitaondoshwa.

9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao

utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili

wangu nao utakaa kwa kutumaini.

10 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,

Wala hutamtoa mtakatifu wako aone

uharibifu.

11 Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso

wako ziko furaha tele; Na katika mkono

wako wa kuume Mna mema ya milele.

ZABURI 49:15 Bali Mungu atanikomboa

nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa

kuzimu, maana atanikaribisha.

ZABURI 71:20 Wewe, uliyetuonyesha

mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena.

Utatupandisha juu tena Tokea pande za

chini ya nchi.

ISAYA 25:8 Amemeza mauti hata milele;

na Bwana MUNGU atafuta machozi katika

nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa

katika ulimwengu wote; maana Bwana

amenena hayo.

MATENDO YA MITUME 2:25 Maana

Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana

mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko

upande wa mkono wangu wa kuume,

nisitikisike.

26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi

wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao

utakaa katika matumaini.

ZABURIEN

Page 90: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

90

27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika

kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako

aone uharibifu.

28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza

furaha kwa uso wako.

29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi,

niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za

baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki

akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa

Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba

katika uzao wa viuno vyake atamketisha

mmoja katika kiti chake cha enzi;

31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya,

alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya

kwamba roho yake haikuachwa kuzimu,

wala mwili wake haukuona uharibifu.

MATENDO YA MITUME 13:33 ya

kwamba Mungu amewatimizia watoto

wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama

ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe

ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.

34 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate

kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitawapa

ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo

amini.

35 Kwa hiyo anena na pengine, Hutamwachia

Mtakatifu wako kuona uharibifu,

36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia

shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala,

akawekwa pamoja na baba zake, akaona

uharibifu.

37 Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona

uharibifu.

UFUNUO WA YOHANA 1:18 na aliye

hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama,

ni hai hata milele na milele. Nami ninazo

funguo za mauti, na za kuzimu.

Ona pia: Zaburi 30:3; Zaburi 86:13; Isaya 26:19; Hosea 6:2; Hosea 13:14; Mathayo 27:52,53; Yohana 8:51-55; Matendo ya

Mitume 3:14,15; 1 Wakorintho 15:20,26,42,54,55.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

ZABURI 17:15 Bali mimi nikutazame uso

wako katika haki, Niamkapo nishibishwe

kwa sura yako.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

LUKA 9:26 Kwa sababu kila

atakayenionea haya mimi na maneno yangu,

Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu

huyo, atakapokuja katika utukufu wake na

wa Baba na wa malaika watakatifu.

LUKA 9:32 Petro na wale waliokuwa

pamoja naye walikuwa wamelemewa na

usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona

utukufu wake, na wale wawili waliosimama

pamoja naye.

33 Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye,

Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni

vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda

vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja

cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui

asemalo.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 11:40 Yesu akamwambia, Mimi

sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona

ZABURIEN

Page 91: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

91

utukufu wa Mungu?

YOHANA 17:22 Nami utukufu ule ulionipa

nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi

tulivyo umoja.

23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe

wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu

ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma,

ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

24 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja

nami po pote nilipo, wapate na kuutazama

utukufu wangu ulionipa; kwa maana

ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

MATENDO YA MITUME 7:55 Lakini

yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho

yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu

wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa

mkono wa kuume wa Mungu.

WARUMI 8:18 Kwa maana nayahesabu

mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu

kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.

1 WAKORINTHO 13:12 Maana wakati wa

sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo;

wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa

sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule

nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa

sana.

2 WAKORINTHO 3:18 Lakini sisi sote,

kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha

utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo,

tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo,

toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa

utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

1 YOHANA 3:2 Wapenzi, sasa tu wana

wa Mungu, wala haijadhihirika bado

tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa

atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa

maana tutamwona kama alivyo.

Ona pia: Zaburi 104:31; Zaburi 138:5; Isaya 6:1-5; Isaya 24:14; Isaya 35:2; Isaya 40:5; Isaya 60:1; Isaya 61:6; Ezekieli 3:23;

Ezekieli 10:4; Habakuki 2:14; Mathayo 8:38; Mathayo 19:28; Marko 8:38; Marko 13:26; Luka 19:38; Yohana 12:41.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 18:4 Kamba za mauti

zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia

hofu.

5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya

mauti ikanikabili.

6 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na

kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia

sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu

kikaingia masikioni mwake.

ZABURI 88:6 Mimi umenilaza katika

shimo la chini, Katika mahali penye giza

vilindini.

7 Ghadhabu yako imenilemea, Umenitesa kwa

mawimbi yako yote.

ZABURI 116:3 Kamba za mauti

zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata.

Naliona taabu na huzuni;

MARKO 14:33 Akamtwaa Petro na Yakobo

na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika

sana na kuhangaika.

34 Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi

kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.

35 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka

kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana,

saa hiyo imwepuke.

ZABURIEN

Page 92: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

92

36 Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana

kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini,

si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.

LUKA 22:44 Naye kwa vile alivyokuwa

katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake

ikawa kama matone ya damu yakidondoka

nchini.]

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

B11 Utiifu wa Masiha.

ZABURI 18:21 Maana nimezishika njia za

Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu.

22 Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu,

Wala amri zake sikujiepusha nazo.

23 Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake,

Nikajilinda na uovu wangu.

24 Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki

yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu

mbele zake.

LUKA 23:4 Pilato akawaambia wakuu

wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo

ovu katika mtu huyu.

LUKA 23:14 akawaambia, Mtu huyu

mmemleta kwangu kana kwamba

anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua

mambo yake mbele yenu, ila sikuona

kwake kosa lo lote katika mambo hayo

mliyomshitaki;

LUKA 23:22 Akawaambia mara ya tatu,

Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu

gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo

kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

Ona pia: Kutoka 23:21; Zaburi 1:2; Zaburi 37:31; Zaburi 40:8; Zaburi 119:1,44,51,97,102; Yeremia 31:33; Ezekieli 36:27; Yohana

18:38; Yohana 19:4,6.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

E13 Mungu anathibitisha huduma ya Masiha.

ZABURI 20:4 Akujalie kwa kadiri ya haja

ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako

yote.

5 Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la

Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana

akutimizie matakwa yako yote.

6 Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi

wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.

ZABURI 132:17 Hapo nitamchipushia Daudi

pembe, Na taa nimemtengenezea masihi

wangu.

18 Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji

yake itasitawi.

YOHANA 11:42 Nami nalijua ya kuwa

wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili

ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema

haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe

uliyenituma.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

ZABURIEN

Page 93: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

93

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali

nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

MATENDO YA MITUME 2:36 Basi

nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya

kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo

mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

MATENDO YA MITUME 5:31 Mtu huyo

Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa

kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape

Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

Ona pia: Zaburi 13:5; Zaburi 18:35,50; Zaburi 28:8; Isaya 57:15; Mathayo 6:9; Yohana 9:31; Matendo ya Mitume 2:33.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

ZABURI 21:4 Alikuomba uhai, ukampa,

Muda mrefu wa siku nyingi, milele na

milele.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

MATHAYO 28:5 Malaika akajibu, akawaambia

wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa

maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu

aliyesulibiwa.

6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama

alivyosema. Njoni, mpatazame mahali

alipolazwa.

YOHANA 11:25 Yesu akamwambia,

Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye

aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa

anaishi;

UFUNUO WA YOHANA 1:18 na aliye

hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama,

ni hai hata milele na milele. Nami ninazo

funguo za mauti, na za kuzimu.

Ona pia: Zaburi 16:10,11; Zaburi 91:16.

ZABURIEN

Page 94: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

94

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

ZABURI 21:5 Utukufu wake ni mkuu kwa

wokovu wako, Heshima na adhama waweka

juu yake.

YOHANA 13:31 Basi huyo alipokwisha

kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa

Mwana wa Adamu, naye Mungu

ametukuzwa ndani yake.

32 Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi

yake; naye atamtukuza mara.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali

nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WAFILIPI 2:9 Kwa hiyo tena Mungu

alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile

lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

WAEBRANIA 8:1 Basi, katika hayo

tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili:

Tunaye kuhani mkuu wa namna hii,

aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi

cha Ukuu mbinguni,

UFUNUO WA YOHANA 5:13 Na kila

kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi

na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu

vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

Ona pia: #2; Mathayo 28:18; Yohana 17:22; Waefeso 1:20-22; 1 Petro 3:22.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

ZABURI 21:6 Maana umemfanya kuwa

baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha

ya uso wako.

7 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na

kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.

MATENDO YA MITUME 3:26

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

wenu na maovu yake.

WAGALATIA 3:9 Basi hao walio wa imani

hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa

mwenye imani.

WAGALATIA 3:14 ili kwamba baraka ya

Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu

Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa

ZABURIEN

Page 95: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

95

njia ya imani.

WAEFESO 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa

Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa

baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa

roho, ndani yake Kristo;

WAEBRANIA 2:13 Na tena, Nitakuwa

nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi

nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.

Ona pia: #1; Mwanzo 12:2; Zaburi 16:8,11; Zaburi 18:2; Zaburi 63:2-5; Zaburi 91:2,9.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:1 Mungu wangu, Mungu

wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali

na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua

kwangu?

2 Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini

hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha.

MATHAYO 27:45 Basi tangu saa sita palikuwa

na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.

46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti

yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama

sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu

wangu, mbona umeniacha?

LUKA 22:41 Mwenyewe akajitenga nao

kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti

akaomba,

42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako,

uniondolee kikombe hiki; walakini si

mapenzi yangu, bali yako yatendeke.

43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea

akamtia nguvu.

44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki,

akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama

matone ya damu yakidondoka nchini.]

45 Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia

wanafunzi wake, akawakuta wamelala

usingizi kwa huzuni.

46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi?

Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia

majaribuni.

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

Ona pia: Zaburi 22:11; Zaburi 32:3,4; Zaburi 38:8; Mathayo 26:39; Marko 15:34; Luka 24:44.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:6 Lakini mimi ni mdudu wala

si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa

watu.

ISAYA 53:3 Alidharauliwa na kukataliwa

na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye

sikitiko; Na kama mtu ambaye watu

humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala

hatukumhesabu kuwa kitu.

MATHAYO 12:24 Lakini Mafarisayo

waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila

kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

MATHAYO 27:28 Wakamvua nguo, wakamvika

vazi jekundu.

ZABURIEN

Page 96: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

96

MARKO 9:12 Akajibu akawaambia, Ni

kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya

yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje

Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa

mengi na kudharauliwa?

LUKA 23:38 Na juu yake palikuwa na

anwani; HUYU NDIYE MFALME WA

WAYAHUDI.

39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa

alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo?

Jiokoe nafsi yako na sisi.

YOHANA 7:20 Mkutano wakajibu, Ama!

Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua?

YOHANA 7:47 Basi Mafarisayo wakawajibu,

Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?

48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au

katika Mafarisayo?

49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati

wamelaaniwa.

Ona pia: Zaburi 31:11; Zaburi 44:13; Zaburi 69:7-12,19,20; Zaburi 88:8; Zaburi 89:41; Zaburi 109:25; Isaya 37:22; Isaya

49:7; Maombolezo 3:30; Waebrania 13:12.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:7 Wote wanionao hunicheka

sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;

MATHAYO 27:29 Wakasokota taji ya miiba,

wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi

katika mkono wake wa kuume; wakapiga

magoti mbele yake, wakamdhihaki,

wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

MATHAYO 27:39 Nao waliokuwa wakipita

njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa

vichwa vyao, wakisema,

40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga

kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe

Mwana wa Mungu, shuka msalabani.

LUKA 16:14 Basi Mafarisayo, ambao

wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo

yote, wakamdhihaki.

LUKA 23:11 Basi Herode akamfanya

duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki,

na kumvika mavazi mazuri; kisha

akamrudisha kwa Pilato.

LUKA 23:35 Watu wakasimama

wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa

wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa

wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye

Kristo wa Mungu, mteule wake.

36 Wale askari nao wakamfanyia dhihaka,

wakimwendea na kumletea siki,

Ona pia: Zaburi 109:25; Isaya 37:22,23; Isaya 57:4; Marko 15:20,29; Luka 23:21-23.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:8 Husema, Umtegemee

Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa,

maana apendezwa naye.

MATHAYO 27:41 Kadhalika na wale wakuu

wa makuhani wakamdhihaki pamoja na

waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa

wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.

42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa

msalabani, nasi tutamwamini.

43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa,

kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi

ZABURIEN

Page 97: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

97

ni Mwana wa Mungu.

2 WAKORINTHO 13:4 Maana, alisulibiwa

katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu

za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika

yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza

wa Mungu ulio kwenu.

Ona pia: Zaburi 42:10; Marko 15:30-32; Luka 23:35.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:9 Naam, Wewe ndiwe

uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha

matitini mwa mama yangu.

10 Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka

tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu

wangu.

LUKA 2:40 Yule mtoto akakua,

akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na

neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

UFUNUO WA YOHANA 12:4 Na

mkia wake wakokota theluthi ya nyota za

mbinguni, na kuziangusha katika nchi.

Na yule joka akasimama mbele ya yule

mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo,

amle mtoto wake.

5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye

atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya

chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata

kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.

Ona pia: Zaburi 71:6,17; Isaya 7:14,15; Isaya 49:1,2; Luka 1:30-33; Luka 2:52.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:11 Usiwe mbali nami maana

taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.

MATHAYO 26:31 Ndipo Yesu akawaambia,

Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili

yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa,

Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi

watatawanyika.

MATHAYO 26:56 Lakini haya yote yamekuwa,

ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo

wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

MATHAYO 26:72 Akakana tena kwa kiapo,

Simjui mtu huyu.

73 Punde kidogo, wale waliohudhuria

wakamwendea, wakamwambia Petro,

Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa

sababu hata usemi wako wakutambulisha.

74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema,

Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.

YOHANA 16:32 Tazama, saa yaja, naam,

imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila

mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke

yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa

kuwa Baba yupo pamoja nami.

Ona pia: Zaburi 10:1; Zaburi 38:21; Zaburi 59:1,2; Zaburi 71:12; Mathayo 26:31-56.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:12 Mafahali wengi

wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani

wamenisonga;

13 Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba

ZABURIEN

Page 98: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

98

apapuraye na kunguruma.

MATHAYO 26:3 Wakati ule wakuu

wa makuhani, na wazee wa watu,

wakakusanyika katika behewa ya Kuhani

Mkuu, jina lake Kayafa;

4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate

Yesu kwa hila na kumwua.

MATHAYO 26:59 Basi wakuu wa makuhani na

baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo

juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa

uongo wengi.

61 Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema,

Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la

Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama

akamwambia, Hujibu neno? Hawa

wanakushuhudia nini?

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu

akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye

hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo,

Mwana wa Mungu.

64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini

nawaambieni, Tangu sasa mtamwona

Mwana wa Adamu ameketi mkono wa

kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya

mbinguni.

65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake,

akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya

mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo

kufuru yake;

MATHAYO 27:1 Na ilipokuwa asubuhi,

wakuu wa makuhani wote na wazee wa

watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate

kumwua;

MATENDO YA MITUME 4:27 Maana ni

kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na

Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika

katika mji huu juu ya Mtumishi wako

mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:14 Nimemwagika kama maji,

Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu

umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya

mtima wangu.

MATHAYO 26:38 Ndipo akawaambia, Roho

yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa;

kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.

LUKA 22:44 Naye kwa vile alivyokuwa

katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake

ikawa kama matone ya damu yakidondoka

nchini.]

YOHANA 12:27 Sasa roho yangu

imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe

katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo

nilivyoifikia saa hii.

YOHANA 19:32 Basi askari wakaenda,

wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili,

aliyesulibiwa pamoja naye.

33 Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa

amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;

34 lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu

kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.

35 Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda

wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema

kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki.

36 Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie,

Hapana mfupa wake utakaovunjwa.

ZABURIEN

Page 99: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

99

37 Na tena andiko lingine lanena,

Watamtazama yeye waliyemchoma.

Ona pia: Marko 14:33,34.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:15 Nguvu zangu zimekauka

kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya

zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti

MATHAYO 27:50 Naye Yesu akiisha kupaza

sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

YOHANA 19:28 Baada ya hayo Yesu, hali

akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika

ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi

wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa

hisopo, wakampelekea kinywani.

30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki,

alisema, Imekwisha. Akainama kichwa,

akaisalimu roho yake.

1 WAKORINTHO 15:3 Kwa maana

naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale

niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa

Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama

yanenavyo maandiko;

Ona pia: Zaburi 32:3,4; Zaburi 69:3,21; Isaya 53:12; Waebrania 2:14; Waebrania 9:14.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:16 Kwa maana mbwa

wamenizunguka; Kusanyiko la waovu

wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu.

MARKO 15:16 Nao askari wakamchukua

ndani ya behewa, ndiyo Praitorio (yaani,

nyumba ya uliwali), wakakusanya pamoja

kikosi kizima.

17 Wakamvika vazi la rangi ya zambarau,

wakasokota taji ya miiba, wakamtia

kichwani;

18 wakaanza kumsalimu, Salamu, Mfalme wa

Wayahudi!

19 Wakampiga mwanzi wa kichwa,

wakamtemea mate, wakapiga magoti,

wakamsujudia.

20 Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua

lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika

mavazi yake mwenyewe; wakamchukua nje

ili wamsulibishe.

LUKA 11:53 Alipotoka humo, waandishi

na Mafarisayo walianza kumsonga vibaya, na

kumchokoza kwa maswali mengi,

54 wakimvizia, ili wapate neno litokalo

kinywani mwake.

LUKA 23:10 Wakuu wa makuhani na

waandishi wakasimama wakamshitaki kwa

nguvu sana.

11 Basi Herode akamfanya duni, pamoja na

askari zake, akamdhihaki, na kumvika

mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa

Pilato.

LUKA 23:23 Lakini wakatoa sauti zao kwa

nguvu sana, wakitaka asulibiwe. Sauti zao

zikashinda.

YOHANA 19:37 Na tena andiko lingine

lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.

YOHANA 20:25 Basi wanafunzi wengine

wakamwambia, Tumemwona Bwana.

ZABURIEN

Page 100: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

100

Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi

mwake kovu za misumari, na kutia kidole

changu katika mahali pa misumari, na kutia

mkono wangu katika ubavu wake, mimi

sisadiki hata kidogo.

YOHANA 20:27 Kisha akamwambia Tomaso,

Lete hapa kidole chako; uitazame mikono

yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni

mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali

aaminiye.

Ona pia: Zaburi 40:6; Zaburi 86:14; Zekaria 12:10; Mathayo 27:41-43; Marko 15:29-32; Luka 23:35; Ufunuo wa Yohana 22:15.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:17 Naweza kuihesabu mifupa

yangu yote; Wao wananitazama na

kunikodolea macho.

MARKO 15:29 Nao waliokuwa wakipita

njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa

vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenye

kulivunja hekalu na kulijenga katika siku

tatu,

30 jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.

31 Kadhalika na wakuu wa makuhani

wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na

waandishi, wakisema, Aliponya wengine;

hawezi kujiponya mwenyewe.

32 Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa

msalabani tupate kuona na kuamini.

Hata wale waliosulibiwa pamoja naye

wakamfyolea.

LUKA 23:27 Mkutano mkubwa wa watu

wakamfuata, na wanawake waliokuwa

wakijipiga vifua na kumwombolezea.

YOHANA 19:32 Basi askari wakaenda,

wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili,

aliyesulibiwa pamoja naye.

Ona pia: Zaburi 102:3-5; Isaya 52:14; Mathayo 27:39-41.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 22:18 Wanagawanya nguo zangu,

Na vazi langu wanalipigia kura.

YOHANA 19:23 Nao askari walipomsulibisha

Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya

mafungu manne, kwa kila askari fungu lake;

na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa,

ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.

24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini

tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko

lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na

vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo

walivyofanya wale askari.

Ona pia: Mathayo 27:35; Marko 15:24; Luka 23:34.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

ZABURI 22:22 Nitalihubiri jina lako

kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko

nitakusifu.

WAEBRANIA 2:11 Maana yeye atakasaye na hao

wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja.

Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;

12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu

zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.

Ona pia: Zaburi 40:9,10; Mathayo 28:10; Yohana 20:17; Warumi 8:29.

ZABURIEN

Page 101: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

101

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 22:23 Ninyi mnaomcha Bwana,

msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo,

mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao

wa Israeli.

ZABURI 22:25-27

ZABURI 22:27 Miisho yote ya dunia

itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana;

Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

28 Maana ufalme una Bwana, Naye ndiye

awatawalaye mataifa.

29 Wakwasi wote wa dunia watakula na

kusujudu, Humwinamia wote washukao

mavumbini; Naam, yeye asiyeweza

kujihuisha nafsi yake,

30 Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa

habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja,

31 Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake,

Ya kwamba ndiye aliyeyafanya.

MATHAYO 3:9 wala msiwaze mioyoni

mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye

Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya

kwamba Mungu aweza katika mawe haya

kumwinulia Ibrahimu watoto.

YOHANA 10:16 Na kondoo wengine ninao,

ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa

kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha

kutakuwako kundi moja na mchungaji

mmoja.

YOHANA 11:25 Yesu akamwambia,

Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye

aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa

anaishi;

26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa

kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

WARUMI 1:17 Kwa maana haki ya Mungu

inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata

imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki

ataishi kwa imani.

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

WAGALATIA 3:26 Kwa kuwa ninyi nyote

mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya

imani katika Kristo Yesu.

27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo

mmemvaa Kristo.

28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana

mtumwa wala huru. Hapana mtu mume

wala mtu mke. Maana ninyi nyote

mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa

uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na

ahadi.

WAFILIPI 2:10 ili kwa jina la Yesu kila

goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi;

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa

hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia

mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

WAEBRANIA 2:10 Kwa kuwa ilimpasa yeye,

ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake

vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi

waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi

mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.

ZABURIEN

Page 102: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

102

11 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa

wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii

haoni haya kuwaita ndugu zake;

12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu

zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.

13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na

tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto

niliopewa na Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #4; Zaburi 49:6-8; Isaya 45:23; Isaya 53:10; Yohana 3:36; Warumi 3:21-25; Warumi 5:19-21; Warumi 14:10-12;

1 Petro 2:9.

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

ZABURI 23:1 Bwana ndiye mchungaji

wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,

Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza

Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa

mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe

upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo

yako vyanifariji.

5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa

watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani

pangu, Na kikombe changu kinafurika.

6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote

za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani

mwa Bwana milele.

YOHANA 10:11 Mimi ndimi mchungaji

mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai

wake kwa ajili ya kondoo.

YOHANA 10:14 Mimi ndimi mchungaji

mwema; nao walio wangu nawajua; nao

walio wangu wanijua mimi;

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

28 Nami nawapa uzima wa milele; wala

hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu

atakayewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

30 Mimi na Baba tu umoja.

WAEBRANIA 13:20 Basi, Mungu wa

amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu

Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya

agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,

1 PETRO 2:25 Kwa maana mlikuwa

mnapotea kama kondoo; lakini sasa

mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa

roho zenu.

1 PETRO 5:4 Na Mchungaji mkuu

atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya

utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 7:17 Kwa

maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati

ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

Ona pia: Zaburi 80:1; Isaya 40:11; Isaya 53:11; Ezekieli 34:11,12,23,24; Ezekieli 37:24; Mika 5:5; Zekaria 13:7.

ZABURIEN

Page 103: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

103

G02 Kupaa mbinguni kwa Masiha

kunatabiriwa.

ZABURI 24:3 Ni nani atakayepanda katika

mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama

katika patakatifu pake?

MATENDO YA MITUME 1:10

Walipokuwa wakikaza macho mbinguni,

yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu

wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo

nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona

mmesimama mkitazama mbinguni?

Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu

kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo

mlivyomwona akienda zake mbinguni.

12 Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka

mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na

Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.

Ona pia: Zaburi 15:1; Zaburi 68:18; Yohana 20:17.

B04 Sifa za Uungu za Masiha.

G02 Kupaa mbinguni kwa Masiha

kunatabiriwa.

ZABURI 24:7 Inueni vichwa vyenu, enyi

malango, Inukeni, enyi malango ya milele,

Mfalme wa utukufu apate kuingia.

8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana

mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa

vita.

9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam,

viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa

utukufu apate kuingia.

10 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana

wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

MARKO 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya

kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni,

akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

LUKA 24:51 Ikawa katika kuwabariki,

alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.

MATENDO YA MITUME 1:10

Walipokuwa wakikaza macho mbinguni,

yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu

wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo

nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona

mmesimama mkitazama mbinguni?

Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu

kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo

mlivyomwona akienda zake mbinguni.

MATENDO YA MITUME 7:55 Lakini

yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho

yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu

wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa

mkono wa kuume wa Mungu.

WAEFESO 1:20 aliotenda katika Kristo

alipomfufua katika wafu, akamweka mkono

wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

WAEBRANIA 9:24 Kwa sababu Kristo hakuingia

katika patakatifu palipofanyika kwa mikono,

ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia

mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa

Mungu kwa ajili yetu;

1 PETRO 3:22 Naye yupo mkono wa kuume

wa Mungu, amekwenda zake mbinguni,

malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa

chini yake.

UFUNUO WA YOHANA 22:14 Heri

ZABURIEN

Page 104: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

104

wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea

huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa

milango yake.

Ona pia: #1; Zaburi 18:19; Zaburi 118:19,20; Isaya 26:2; Yeremia 17:25; Danieli 7:13,14; Zaburi 45:2-5; Isaya 9:7; Isaya 63:1-6; Wakolosai 2:15; Ufunuo wa Yohana 6:2; Ufunuo wa Yohana

19:11-21; Isaya 6:3; Isaya 54:5.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 27:2 Watenda mabaya

waliponikaribia, Wanile nyama yangu,

Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa

wakaanguka.

YOHANA 18:3 Basi Yuda, akiisha kupokea

kikosi cha askari na watumishi waliotoka

kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo,

akaenda huko na taa na mienge na silaha.

4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata,

akatokea, akawaambia, Ni nani

mnayemtafuta?

5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti.

Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye

aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja

nao.

6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi

nyuma, wakaanguka chini.

F07 Masihtaka na majaribu ya Masiha.

ZABURI 27:12 Usinitie katika nia ya

watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo

wameniondokea, Nao watoao jeuri kama

pumzi.

MATHAYO 26:59 Basi wakuu wa makuhani na

baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo

juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa

uongo wengi.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

ZABURI 28:8 Bwana ni nguvu za watu

wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi

wake.

ZABURI 80:17 Mkono wako na uwe juu

yake Mtu wa mkono wako wa kuume; Juu ya

mwanadamu uliyemfanya Kuwa imara kwa

nafsi yako;

ZABURI 89:20 Nimemwona Daudi,

mtumishi wangu, Nimempaka mafuta

yangu matakatifu.

21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti

kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

22 Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu

hatamtesa.

LUKA 22:41 Mwenyewe akajitenga nao

kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti

akaomba,

42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako,

uniondolee kikombe hiki; walakini si

mapenzi yangu, bali yako yatendeke.

43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea

akamtia nguvu.

YOHANA 8:28 Basi Yesu akawaambia,

Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua

Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu

ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi

ZABURIEN

Page 105: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

105

neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba

alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.

29 Naye aliyenipeleka yu pamoja nami,

hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya

sikuzote yale yampendezayo.

YOHANA 10:38 lakini nikizitenda, ijapokuwa

hamniamini mimi, ziaminini zile kazi;

mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu

ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.

Ona pia: Zaburi 2:2; Zaburi 20:6; Zaburi 68:28; Isaya 61:1.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 30:3 Umeniinua nafsi yangu, Ee

Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na

kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.

MATHAYO 28:6 Hayupo hapa; kwani

amefufuka kama alivyosema. Njoni,

mpatazame mahali alipolazwa.

7 Nanyi nendeni upesi, mkawaambie

wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu.

Tazama, awatangulia kwenda Galilaya;

ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha

waambia.

MATENDO YA MITUME 2:27 Kwa

maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;

Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone

uharibifu.

MATENDO YA MITUME 13:35 Kwa hiyo

anena na pengine, Hutamwachia Mtakatifu

wako kuona uharibifu,

Ona pia: Zaburi 16:10; Zaburi 49:15; Zaburi 71:20; Zaburi 86:13; Yona 2:4-6.

F10 Utayari wa Masiha kwa ajili ya kifo.

ZABURI 31:4 Utanitoa katika wavu

walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe

ngome yangu.

5 Mikononi mwako naiweka roho yangu;

Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.

LUKA 23:46 Yesu akalia kwa sauti kuu,

akasema, Ee Baba, mikononi mwako

naiweka roho yangu.

Ona pia: Zaburi 22:13,17; Zaburi 25:15; Zaburi 35:7; Zaburi 57:6; Zaburi 140:5; Mathayo 27:50; Marko 15:37; Yohana 17:17; Yohana

19:30.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 31:11 Kwa sababu ya watesi wangu

nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani

zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;

Walioniona njiani walinikimbia.

12 Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa;

Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.

13 Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu

ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu,

Walifanya hila wauondoe uhai wangu.

14 Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana,

Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

15 Nyakati zangu zimo mikononi mwako;

Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.

MATHAYO 27:39 Nao waliokuwa wakipita

njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa

vichwa vyao, wakisema,

40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga

kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe

Mwana wa Mungu, shuka msalabani.

41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani

wakamdhihaki pamoja na waandishi na

ZABURIEN

Page 106: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

106

wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi

kujiokoa mwenyewe.

42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa

msalabani, nasi tutamwamini.

43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa,

kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi

ni Mwana wa Mungu.

44 Pia wale wanyang›anyi waliosulibiwa pamoja

naye walimshutumu vile vile.

Ona pia: Mathayo 26:3,4,59; Mathayo 27:1; Yohana 11:53.

A06 Masiha ndiye Muumbaji.

ZABURI 33:6 Kwa neno la Bwana mbingu

zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya

kinywa chake.

9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye

aliamuru, ikasimama.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye

hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ZABURI 34:20 Huihifadhi mifupa yake yote,

Haukuvunjika hata mmoja.

YOHANA 19:32 Basi askari wakaenda,

wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili,

aliyesulibiwa pamoja naye.

33 Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa

amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;

34 lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu

kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.

35 Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda

wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema

kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki.

36 Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie,

Hapana mfupa wake utakaovunjwa.

37 Na tena andiko lingine lanena,

Watamtazama yeye waliyemchoma.

Ona pia: Kutoka 12:46; Hesabu 9:12; Zaburi 22:16,17; Zekaria 12:10; Ufunuo wa Yohana 1:7.

F12 Masiha atapingwa.

ZABURI 35:4 Waaibishwe,

wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu.

Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,

Wanaonizulia mabaya.

5 Wawe kama makapi mbele ya upepo,

Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.

6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa

Bwana akiwafuatia.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

YOHANA 18:4 Basi Yesu, hali akijua yote

yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni

nani mnayemtafuta?

5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti.

Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye

aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja

nao.

6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi

nyuma, wakaanguka chini.

ZABURIEN

Page 107: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

107

7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani?

Wakasema, Yesu Mnazareti.

8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya

kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta

mimi, waacheni hawa waende zao.

9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale

ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.

Ona pia: Ayubu 21:17,18; Zaburi 31:17,18; Zaburi 35:26; Zaburi 40:14,15; Zaburi 70:2,3; Zaburi 71:24; Hosea 13:3,4.

F07 Masihtaka na majaribu ya Masiha.

ZABURI 35:11 Mashahidi wa udhalimu

wanasimama, Wananiuliza mambo

nisiyoyajua.

12 Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata

nafsi yangu ikaingia ukiwa.

MATHAYO 23:29 Ole wenu, waandishi na

Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga

makaburi ya manabii, na kuyapamba

maziara ya wenye haki,

30 na kusema, Kama sisi tungalikuwako

zamani za baba zetu, hatungalishirikiana

nao katika damu ya manabii.

31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba

ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

MATHAYO 26:59 Basi wakuu wa makuhani na

baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo

juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa

uongo wengi.

61 Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema,

Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la

Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama

akamwambia, Hujibu neno? Hawa

wanakushuhudia nini?

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu

akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye

hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo,

Mwana wa Mungu.

64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini

nawaambieni, Tangu sasa mtamwona

Mwana wa Adamu ameketi mkono wa

kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya

mbinguni.

YOHANA 7:19 Je! Musa hakuwapa torati?

Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati.

Mbona mnatafuta kuniua?

YOHANA 8:37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao

wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa

sababu neno langu halimo ndani yenu.

MATENDO YA MITUME 7:52 Ni

yupi katika manabii ambaye baba zenu

hawakumwudhi? Nao waliwaua wale

waliotabiri habari za kuja kwake yule

Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa

wasaliti wake, mkamwua;

Ona pia: Zaburi 27:12; Marko 14:55-62; Matendo ya Mitume 6:13; Matendo ya Mitume 24:12,13.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 35:19 Walio adui zangu bure

wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu

wasining›ong›e.

YOHANA 15:25 Lakini litimie lile neno

lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia

bure.

ZABURIEN

Page 108: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

108

Ona pia: Zaburi 38:19; Zaburi 69:4; Zaburi 109:3.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 38:12 Nao wanaoutafuta uhai

wangu hutega mitego; Nao wanaotaka

kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila

mchana kutwa.

13 Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama

bubu asiyefumbua kinywa chake.

20 Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa

adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.

ZABURI 109:3 Naam, kwa maneno ya chuki

wamenizunguka, Wamepigana nami bure.

4 Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,

Ijapokuwa naliwaombea.

5 Wamenichukuza mabaya badala ya mema,

Na chuki badala ya upendo wangu.

LUKA 20:19 Nao waandishi na wakuu

wa makuhani walitafuta kumkamata saa iyo

hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua

ya kwamba mfano huu amewanenea wao.

20 Wakamvizia-vizia, wakatuma wapelelezi

waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase

katika maneno yake, wapate kumtia katika

enzi na mamlaka ya liwali.

1 PETRO 2:23 Yeye alipotukanwa,

hakurudisha matukano; alipoteswa,

hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye

ahukumuye kwa haki.

Ona pia: Zaburi 35:12; Zaburi 39:9; Zaburi 119:10; Zaburi 140:5; Isaya 53:7; Yeremia 18:20.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 40:2 Akanipandisha toka shimo

la uharibifu, Toka udongo wa utelezi;

Akaisimamisha miguu yangu mwambani,

Akaziimarisha hatua zangu.

3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu,

Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona

na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana

MATENDO YA MITUME 2:24 ambaye

Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa

mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe

nao.

MATENDO YA MITUME 2:27 Kwa

maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;

Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone

uharibifu.

28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza

furaha kwa uso wako.

29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi,

niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za

baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki

akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa

Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba

katika uzao wa viuno vyake atamketisha

mmoja katika kiti chake cha enzi;

31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya,

alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya

kwamba roho yake haikuachwa kuzimu,

wala mwili wake haukuona uharibifu.

Ona pia: Zaburi 103:1-5; Isaya 12:1-4; Matendo ya Mitume 2:32-41; Matendo ya Mitume 4:4.

ZABURIEN

Page 109: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

109

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

ZABURI 40:6 Dhabihu na matoleo

hukupendezwa nazo, Masikio yangu

umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi

hukuzitaka.

ISAYA 50:5 Bwana MUNGU amenizibua

sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala

sikurudi nyuma.

MATHAYO 9:13 Lakini nendeni, mkajifunze

maana yake maneno haya, Nataka rehema,

wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita

wenye haki, bali wenye dhambi.

WAEBRANIA 10:4 Maana haiwezekani damu ya

mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,

Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili

uliniwekea tayari;

6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika

gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye

mapenzi yako, Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na

sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi

hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo

(zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja

niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza,

ili kusudi alisimamishe la pili.

10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa

kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja

tu.

11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya

ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara

nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa

dhambi.

12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya

dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele,

aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

Ona pia: Kutoka 21:6; Zaburi 51:16; Isaya 1:11; Yeremia 7:21-23; Hosea 6:6.

B11 Utiifu wa Masiha.

F10 Utayari wa Masiha kwa ajili ya kifo.

ZABURI 40:7 Ndipo niliposema,

Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo

nimeandikiwa,)

LUKA 24:27 Akaanza kutoka Musa na

manabii wote, akawaeleza katika maandiko

yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

LUKA 24:44 Kisha akawaambia, Hayo

ndiyo maneno yangu niliyowaambia

nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba

ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa

katika Torati ya Musa, na katika Manabii na

Zaburi.

WAEBRANIA 10:7 Ndipo niliposema,

Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo

nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako,

Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na

sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi

hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo

(zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja

niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza,

ili kusudi alisimamishe la pili.

UFUNUO WA YOHANA 19:10 Nami

nikaanguka mbele ya miguu yake, ili

ZABURIEN

Page 110: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

110

nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye

hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako

walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie

Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio

roho ya unabii.

Ona pia: Yohana 5:39; 1 Wakorintho 15:3,4; 1 Petro 1:10,11.

B11 Utiifu wa Masiha.

ZABURI 40:8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee

Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam,

sheria yako imo moyoni mwangu.

YOHANA 4:34 Yesu akawaambia, Chakula

changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake

aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

WAEBRANIA 5:8 na, ingawa ni Mwana,

alijifunza kutii kwa mateso hayo

yaliyompata;

Ona pia: Zaburi 37:30,31; Zaburi 119:16,24,47; Yeremia 31:33; Warumi 7:22.

E08 Haki ya Masiha.

ZABURI 40:9 Nimehubiri habari za haki

katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo

yangu; Ee Bwana, unajua.

10 Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;

Nimetangaza uaminifu wako na wokovu

wako. Sikuficha fadhili zako wala kweli yako

Katika kusanyiko kubwa.

MARKO 16:15 Akawaambia, Enendeni

ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa

kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka;

asiyeamini, atahukumiwa.

LUKA 3:6 Na wote wenye mwili

watauona wokovu wa Mungu.

WARUMI 1:16 Kwa maana siionei haya

Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu

uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa

Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa

ndani yake, toka imani hata imani; kama

ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa

imani.

WAFILIPI 3:9 tena nionekane katika yeye,

nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo

kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani

iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa

Mungu, kwa imani;

WAEBRANIA 2:12 akisema, Nitalihubiri jina

lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa

nitakuimbia sifa.

Ona pia: Zaburi 22:22,25; Zaburi 35:18; Zaburi 71:15-18; Zaburi 119:13; Luka 2:30-32; Luka 4:16-22; Yohana 1:17; Yohana 3:16,17; Matendo ya Mitume 20:20,21; Warumi 3:22-26; Warumi 10:9,10;

1 Timotheo 1:15.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 40:14 Waaibike, wafedheheke

pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu

waiangamize. Warudishwe nyuma,

watahayarishwe, Wapendezwao na shari

yangu.

ZABURIEN

Page 111: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

111

YOHANA 18:6 Basi alipowaambia, Ni mimi,

walirudi nyuma, wakaanguka chini.

F03 Masiha atakataliwa.

F07 Masihtaka na majaribu ya Masiha.

F12 Masiha atapingwa.

ZABURI 41:5 Adui zangu wananitaja kwa

maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake

likapotea?

6 Na mmoja wao akija kunitazama asema

uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu,

Naye atokapo nje huyanena.

7 Wote wanaonichukia wananinong›ona,

Wananiwazia mabaya.

8 Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo

amelala hatasimama tena.

9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula

chakula changu, Ameniinulia kisigino

chake.

MATHAYO 26:20 Basi kulipokuwa jioni aliketi

chakulani pamoja na wale Thenashara.

21 Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin,

nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti.

22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza

mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana?

23 Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono

wake pamoja nami katika kombe, ndiye

atakayenisaliti.

24 Mwana wa Adamu aenda zake, kama

alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule

ambaye amsaliti Mwana wa Adamu!

Ingekuwa heri kwake mtu yule kama

asingalizaliwa.

25 Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu,

akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia,

Wewe umesema.

LUKA 11:53 Alipotoka humo, waandishi

na Mafarisayo walianza kumsonga vibaya, na

kumchokoza kwa maswali mengi,

54 wakimvizia, ili wapate neno litokalo

kinywani mwake.

LUKA 20:20 Wakamvizia-vizia, wakatuma

wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki,

ili wamnase katika maneno yake, wapate

kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali.

LUKA 22:47 Basi alipokuwa katika

kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule

aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale

Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia

Yesu ili kumbusu.

48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana

wa Adamu kwa kumbusu?

YOHANA 13:18 Sisemi habari za ninyi nyote;

nawajua wale niliowachagua; lakini andiko

lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu

Ameniinulia kisigino chake.

19 Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili

yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi

ndiye.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

Ona pia: Zaburi 12:2; Zaburi 22:6-8; Zaburi 102:8.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 42:7 Kilindi chapigia kelele kilindi

kwa sauti ya maboromoko ya maji yako,

ZABURIEN

Page 112: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

112

Gharika zako zote na mawimbi yako yote

yamepita juu yangu.

ISAYA 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa

yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu

ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa

kupigwa kwake sisi tumepona.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

MATHAYO 27:46 Na kama saa tisa, Yesu

akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi,

Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu,

Mungu wangu, mbona umeniacha?

LUKA 22:44 Naye kwa vile alivyokuwa

katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake

ikawa kama matone ya damu yakidondoka

nchini.]

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

Ona pia: Zaburi 22:1-10; Zaburi 88:7,15-17; Yona 2:3; Nahumu 1:6; Marko 15:34.

B21 Masiha ndiye Nuru.

ZABURI 43:3 Niletewe nuru yako na kweli

yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima

wako mtakatifu na hata maskani yako.

ISAYA 9:2 Watu wale waliokwenda

katika giza Wameona nuru kuu; Wale

waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru

imewaangaza.

ISAYA 49:6 naam, asema hivi, Ni neno

dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili

kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza

watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo

nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa

wokovu wangu hata miisho ya dunia.

YOHANA 1:4 Ndani yake ndimo

ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa

nuru ya watu.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 1:17 Kwa kuwa torati ilitolewa

kwa mkono wa Musa; neema na kweli

zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

YOHANA 9:5 Muda nilipo ulimwenguni,

mimi ni nuru ya ulimwengu.

YOHANA 12:35 Basi Yesu akawaambia,

ZABURIEN

Page 113: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

113

Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo.

Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza

lisije likawaweza; maana aendaye gizani

hajui aendako.

36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo

aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha

wasimwone.

YOHANA 12:46 Mimi nimekuja ili niwe nuru

ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi

asikae gizani.

YOHANA 14:6 Yesu akamwambia, Mimi

ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa

Baba, ila kwa njia ya mimi.

YOHANA 16:13 Lakini yeye atakapokuja,

huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie

kwenye kweli yote; kwa maana hatanena

kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote

atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo

atawapasha habari yake.

1 YOHANA 1:5 Na hii ndiyo habari

tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya

kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote

hamna ndani yake.

Ona pia: Zaburi 36:9; Isaya 60:1,3,19,20; Yohana 15:26; Yohana 2:7-10.

B12 Ukamilifu wa Masiha.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

ZABURI 45:1 Moyo wangu umefurika kwa

neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia

mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya

mwandishi mstadi.

2 Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;

Neema imemiminiwa midomoni mwako,

Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

LUKA 2:40 Yule mtoto akakua,

akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na

neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

LUKA 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea

katika hekima na kimo, akimpendeza

Mungu na wanadamu.

LUKA 4:21 Akaanza kuwaambia,

Leo maandiko haya yametimia masikioni

mwenu.

22 Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia

maneno ya neema yaliyotoka kinywani

mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa

Yusufu?

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 1:16 Kwa kuwa katika utimilifu

wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya

neema.

17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa

Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono

wa Yesu Kristo.

MATENDO YA MITUME 15:11 Bali

twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya

Bwana Yesu vile vile kama wao.

WARUMI 3:24 wanahesabiwa haki bure

kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio

katika Kristo Yesu;

ZABURIEN

Page 114: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

114

WARUMI 5:15 Lakini karama ile haikuwa

kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa

kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi

sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho

katika neema yake mwanadamu mmoja

Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.

1 WAKORINTHO 15:10 Lakini kwa neema

ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema

yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali

nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote;

wala si mimi, bali ni neema ya Mungu

pamoja nami.

2 WAKORINTHO 1:15 Nami nikiwa na

tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo

kwanza, ili mpate karama ya pili;

2 WAKORINTHO 12:9 Naye akaniambia,

Neema yangu yakutosha; maana uweza

wangu hutimilika katika udhaifu. Basi

nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi,

ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

WAEFESO 2:8 Kwa maana mmeokolewa

kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo

haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha

Mungu;

TITO 2:11 Maana neema ya Mungu

iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

WAEBRANIA 2:9 ila twamwona yeye

aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika,

yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu

ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na

heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje

mauti kwa ajili ya kila mtu.

YAKOBO 4:6 Lakini hutujalia sisi

neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu

huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema

wanyenyekevu.

UFUNUO WA YOHANA 22:21 Neema

ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote.

Amina.

Ona pia: Wimbo Ulio Bora 2:3; Wimbo Ulio Bora 5:10-16; Isaya 63:9; Zekaria 9:16; Mathayo 17:2; Warumi 5:17,21;

Warumi 6:1,14,15; Warumi 11:5,6; Warumi 12:3,6; Warumi 16:20; 1 Wakorintho 3:4; 2 Wakorintho 4:15; 2 Wakorintho 8:9; 2 Wakorintho 9:8; 2 Wakorintho 13:14; Wagalatia 1:6; Wagalatia

5:4; Waefeso 1:7; Waefeso 2:5,7; Waefeso 4:7; Wafilipi 1:29; Wakolosai 1:15-18; 1 Timotheo 1:14; 2 Timotheo 2:6; Tito 3:7;

Waebrania 1:3; Waebrania 4:16; Waebrania 7:26; Waebrania 10:29; Waebrania 12:15,28; Waebrania 13:9; 1 Petro 1:10,13; 1 Petro 2:19,20; 1 Petro 5:10,12; 2 Petro 3:18; Ufunuo wa Yohana 1:13-18.

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

B17 Upole na udhaifu wa Masiha.

E09 Uadilifu wa Masiha.

ZABURI 45:3 Jifungie upanga wako pajani,

wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na

fahari ni yako.

4 Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa

ajili ya kweli na upole na haki Na mkono

wako wa kuume Utakufundisha mambo ya

kutisha.

SEFANIA 2:3 Mtafuteni Bwana, enyi

nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi

mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki,

utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa

katika siku ya hasira ya Bwana.

MATHAYO 11:29 Jitieni nira yangu, mjifunze

kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na

mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha

nafsini mwenu;

MATHAYO 21:5 Mwambieni binti Sayuni

ZABURIEN

Page 115: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

115

Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-

punda, mtoto wa punda.

YOHANA 17:17 Uwatakase kwa ile kweli;

neno lako ndiyo kweli.

2 WAKORINTHO 10:1 Basi, mimi Paulo

mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu

wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu

nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo

ni mwenye ujasiri kwenu;

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

WAEFESO 4:2 kwa unyenyekevu wote na

upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika

upendo;

WAKOLOSAI 3:12 Basi, kwa kuwa mmekuwa

wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao,

jivikeni moyo wa rehema, utu wema,

unyenyekevu, upole, uvumilivu,

1 TIMOTHEO 6:11 Bali wewe, mtu wa

Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate

haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.

WAEBRANIA 4:12 Maana Neno la Mungu li

hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko

upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na

viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi

ya moyo.

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa

moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi;

naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila

yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika

damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,

wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani

nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

UFUNUO WA YOHANA 19:21 na wale

waliosalia waliuawa kwa upanga wake

yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga

utokao katika kinywa chake. Na ndege wote

wakashiba kwa nyama zao.

Ona pia: Hesabu 12:3; Zaburi 18:35; Isaya 49:2,3; Isaya 63:1-6; 1 Wakorintho 4:21; 2 Wakorintho 6:4-7; Wagalatia 6:1; 2 Timotheo

2:25; Tito 3:2; Yakobo 1:21; 1 Petro 3:15.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

ZABURI 45:5 Mishale yako ni mikali, watu

huanguka chini yako; Imo mioyoni mwa

adui za mfalme.

ZABURIEN

Page 116: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

116

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

MATENDO YA MITUME 4:4 Lakini

wengi katika hao waliosikia lile neno

waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa

kama elfu tano.

2 WAKORINTHO 10:3 Maana ingawa

tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa

jinsi ya mwili;

4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali

zina uwezo katika Mungu hata kuangusha

ngome;)

5 tukiangusha mawazo na kila kitu

kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya

Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate

kumtii Kristo;

WAEBRANIA 4:12 Maana Neno la Mungu li

hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko

upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na

viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi

ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi

mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na

kufunuliwa machoni pake yeye aliye na

mambo yetu.

Ona pia: #1; Zaburi 22:27,28; Zaburi 66:3,4; Matendo ya Mitume 5:14; Matendo ya Mitume 6:7.

B05 Masiha amejawa na Roho na Mtakatifu.

E08 Haki ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H04 Kiti cha enzi cha Masiha.

ZABURI 45:6 Kiti chako cha enzi, Mungu,

ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme

wako ni fimbo ya adili.

7 Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma.

Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako,

amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko

wenzako.

MATHAYO 3:15 Yesu akajibu akamwambia,

Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo

kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

MATENDO YA MITUME 10:37 jambo lile

ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi

wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo

aliouhubiri Yohana;

38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu

alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na

nguvu naye akazunguka huko na huko,

akitenda kazi njema na kuponya wote

walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu

alikuwa pamoja naye.

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

ZABURIEN

Page 117: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

117

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa

hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia

mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

Ona pia: #1; Zaburi 33:5; Zaburi 89:29,36,37; Zaburi 93:2; Zaburi 145:13.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

ZABURI 45:9 Binti za wafalme wamo

Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki.

Mkono wako wa kuume amesimama malkia

Amevaa dhahabu ya Ofiri.

13 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,

Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.

14 Atapelekwa kwa mfalme Na mavazi

yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake

wanaomfuata, Watapelekwa kwako.

15 Watapelekwa kwa furaha na shangwe, Na

kuingia katika nyumba ya mfalme.

WIMBO ULIO BORA 1:4 Nivute nyuma

yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza

vyumbani mwake. Tutafurahi na

kukushangilia; Tutazinena pambaja zako

kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.

WIMBO ULIO BORA 2:10 Mpendwa wangu

alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi

wangu, mzuri wangu, uje zako,

WIMBO ULIO BORA 6:2 Mpendwa wangu

ameshukia bustani yake, Kwenye matuta

ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili

kuchuma nyinyoro.

3 Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni

wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.

ISAYA 61:10 Nitafurahi sana katika

Bwana, nafsi yangu itashangilia katika

Mungu wangu; maana amenivika mavazi

ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama

bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha

maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa

vyombo vya dhahabu.

YOHANA 17:24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate

na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa

maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

2 WAKORINTHO 11:2 Maana nawaonea

wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa

naliwaposea mume mmoja, ili nimletee

Kristo bikira safi.

1 WATHESALONIKE 4:17 Kisha sisi tulio hai,

tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika

mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na

hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

2 WATHESALONIKE 1:10 yeye atakapokuja

ili kutukuzwa katika watakatifu wake,

na kustaajabiwa katika wote waliosadiki

katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu

ulisadikiwa kwenu).

ZABURIEN

Page 118: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

118

1 YOHANA 3:2 Wapenzi, sasa tu wana

wa Mungu, wala haijadhihirika bado

tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa

atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa

maana tutamwona kama alivyo.

UFUNUO WA YOHANA 3:5 Yeye

ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe,

wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu

cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za

Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

UFUNUO WA YOHANA 7:15 Kwa hiyo

wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,

nao wanamtumikia mchana na usiku katika

hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha

enzi atatanda hema yake juu yao.

16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 19:7 Na

tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri,

ing›arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo

ni matendo ya haki ya watakatifu.

Ona pia: Isaya 35:10; Isaya 51:11; Isaya 55:12,13; Isaya 60:19,20; Waefeso 2:4-6.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 45:16 Badala ya baba zako

watakuwapo watoto wako, Utawafanya kuwa

wakuu katika nchi zote.

17 Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu

Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa

watakushukuru Milele na milele.

MATHAYO 19:28 Yesu akawaambia, Amin,

nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata

mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi

Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu

wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi

na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na

mbili za Israeli.

29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu

wa kiume au wa kike, au baba, au mama,

au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina

langu, atapokea mara mia, na kuurithi

uzima wa milele.

MATHAYO 26:13 Amin, nawaambieni,

Kila patakapohubiriwa Injili hii katika

ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda

huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

ZABURIEN

Page 119: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

119

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

Ona pia: #1; #2; #4.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ZABURI 46:4 Kuna mto, vijito vyake

vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa

maskani zake Aliye juu.

5 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa;

Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

6 Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki;

Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.

7 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu

wa Yakobo ni ngome yetu.

8 Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi

alivyofanya ukiwa katika nchi.

9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;

Avunja uta, akata mkuki, achoma moto

magari.

10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,

Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika

nchi.

11 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu

wa Yakobo ni ngome yetu.

ISAYA 2:4 Naye atafanya hukumu

katika mataifa mengi, atawakemea watu wa

kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe

majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa

halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala

hawatajifunza vita tena kamwe.

MIKA 4:3 Naye atafanya hukumu kati

ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea

mataifa wenye nguvu walio mbali; nao

watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki

yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu

ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena

kamwe.

4 Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu

wake, na chini ya mtini wake; wala hapana

mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa

cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.

ZEKARIA 2:10 Imba, ufurahi, Ee binti

Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami

nitakaa kati yako, asema Bwana.

YOHANA 3:14 Na kama vile Musa

alivyomwinua yule nyoka jangwani,

vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi

kuinuliwa;

YOHANA 12:32 Nami nikiinuliwa juu ya

nchi, nitawavuta wote kwangu.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali

ZABURIEN

Page 120: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

120

nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

MATENDO YA MITUME 5:31 Mtu huyo

Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa

kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape

Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

UFUNUO WA YOHANA 15:3 Nao

wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa

Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #2, #5; Zaburi 66:7; Zaburi 83:2-4; Isaya 5:16; Isaya 8:9; Yeremia 16:19; Habakuki 2:20; Yohana 8:28; Matendo ya

Mitume 2:33; Wafilipi 2:9.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

G02 Kupaa mbinguni kwa Masiha

kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 47:1 Enyi watu wote, pigeni

makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya

shangwe.

2 Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye

kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia

yote.

3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na

mataifa chini ya miguu yetu.

4 Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo

ambaye alimpenda.

5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

Bwana kwa sauti ya baragumu.

6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;

Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.

7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa akili.

8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi

katika kiti chake kitakatifu.

9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe

watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao

za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.

LUKA 24:50 Akawaongoza mpaka

Bethania, akainua mikono yake akawabariki.

51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao;

akachukuliwa juu mbinguni.

52 Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu

wenye furaha kuu.

53 Nao walikuwa daima ndani ya hekalu,

wakimsifu Mungu.

MATENDO YA MITUME 1:6 Basi

walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je!

Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia

Israeli ufalme?

7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati

wala majira, Baba aliyoyaweka katika

mamlaka yake mwenyewe.

8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia

juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa

mashahidi wangu katika Yerusalemu, na

katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata

mwisho wa nchi.

9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa

wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea

kutoka machoni pao.

10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni,

ZABURIEN

Page 121: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

121

yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu

wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo

nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona

mmesimama mkitazama mbinguni?

Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu

kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo

mlivyomwona akienda zake mbinguni.

WAEFESO 4:8 Hivyo husema, Alipopaa juu

aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.

9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini

kama siyo kusema kwamba yeye naye

alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana

kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.

1 TIMOTHEO 3:16 Na bila shaka siri

ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa

katika mwili, Akajulika kuwa na haki

katika roho, Akaonekana na malaika,

Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa

katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika

utukufu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #4; #5; Kumbukumbu la Torati 33:29; Yoshua 21:44; Zaburi 18:47; Zaburi 24:7-10; Zaburi 68:17,18,24,25,33;

Ufunuo wa Yohana 20.

E14 Masiha atashinda kifo na giza.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 49:15 Bali Mungu atanikomboa

nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa

kuzimu, maana atanikaribisha.

YOHANA 20:11 Lakini Mariamu alikuwa

akisimama karibu na kaburi, nje yake,

analia. Basi akilia hivi, aliinama na

kuchungulia ndani ya kaburi.

12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi

meupe, wameketi, mmoja kichwani na

mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili

wake Yesu.

YOHANA 20:15 Yesu akamwambia, Mama,

unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye,

huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani,

akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua

wewe, uniambie ulipomweka, nami

nitamwondoa.

16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye

akageuka, akamwambia kwa Kiebrania,

Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).

17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana

sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda

kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa

kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu,

kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

MATENDO YA MITUME 2:27 Kwa

maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;

Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone

uharibifu.

MATENDO YA MITUME 13:35 Kwa hiyo

anena na pengine, Hutamwachia Mtakatifu

wako kuona uharibifu,

ZABURIEN

Page 122: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

122

MATENDO YA MITUME 26:23 ya

kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya

kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika

wafu atatangaza habari za nuru kwa watu

wake na kwa watu wa Mataifa.

Ona pia: Zaburi 16:10; Zaburi 30:3; Zaburi 71:20; Zaburi 86:13; Yona 2:4-6.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 50:2 Tokea Sayuni, ukamilifu wa

uzuri, Mungu amemulika.

3 Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza,

Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma

sana ikimzunguka pande zote.

4 Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia

awahukumu watu wake.

5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu

Waliofanya agano nami kwa dhabihu.

6 Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa

maana Mungu ndiye aliye hakimu.

ZABURI 97:6 Mbingu zimetangaza haki

yake, Na watu wote wameuona utukufu

wake.

ISAYA 12:6 Paza sauti, piga kelele,

mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa

Israeli ni mkuu kati yako.

ISAYA 33:22 Kwa maana Bwana ndiye

mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria

wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye

atakayetuokoa.

MATHAYO 24:31 Naye atawatuma malaika

zake pamoja na sauti kuu ya parapanda,

nao watawakusanya wateule wake toka pepo

nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka

mwisho huu.

YOHANA 12:48 Yeye anikataaye mimi,

asiyeyakubali maneno yangu, anaye

amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo

litakalomhukumu siku ya mwisho.

MATENDO YA MITUME 17:31 Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu

walimwengu kwa haki, kwa mtu yule

aliyemchagua; naye amewapa watu wote

uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua

katika wafu.

WARUMI 2:5 Bali kwa kadiri ya ugumu

wako, na kwa moyo wako usio na toba,

wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya

hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya

Mungu,

WARUMI 2:16 katika siku ile Mungu

atakapozihukumu siri za wanadamu,

sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

1 WATHESALONIKE 4:16 Kwa sababu

Bwana mwenyewe atashuka kutoka

mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya

malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;

nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa

kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa

pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki

Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja

na Bwana milele.

2 TIMOTHEO 4:1 Nakuagiza mbele za Mungu,

na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu

ZABURIEN

Page 123: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

123

walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa

kwake na kwa ufalme wake;

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu

ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya

Habili.

25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana

ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa

yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana

hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye

atuonyaye kutoka mbinguni;

26 ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati

ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara

moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na

mbingu pia.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 16:5 Nami

nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe

u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako,

Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;

6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na

ya manabii, nawe umewapa damu wainywe;

nao wamestahili.

7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam,

Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za

haki, hukumu zako.

UFUNUO WA YOHANA 19:2 kwa

kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki;

maana amemhukumu yule kahaba mkuu

aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake,

na kuipatiliza damu ya watumwa wake

mkononi mwake.

UFUNUO WA YOHANA 22:20 Yeye

mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam;

naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.

Ona pia: #1; #6; Mwanzo 18:25; Zaburi 7:11; Zaburi 94:2; 1 Wakorintho 6:2,3; Yakobo 5:9; 1 Petro 4:5; Ufunuo wa Yohana

11:15; Ufunuo wa Yohana 16:7; Ufunuo wa Yohana 19:2; Ufunuo wa Yohana 20.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

I04 Sadaka ya amaini na dhabihu ya kutoa

shukrani inawakilisha kazi ya Masiha.

ZABURI 51:17 Dhabihu za Mungu ni

roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na

kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

ISAYA 57:15 Maana yeye aliye juu,

aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina

lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi

mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena

pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu

na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za

wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao

waliotubu.

MATHAYO 5:3 Heri walio maskini wa roho;

Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

ZABURIEN

Page 124: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

124

MARKO 12:33 na kumpenda yeye kwa

moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa

nguvu zote, na kumpenda jirani kama

nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za

kuteketezwa na dhahibu zote pia.

LUKA 15:10 Nawaambia, Vivyo hivyo

kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu

kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja

atubuye.

LUKA 18:11 Yule Farisayo akasimama

akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu,

nakushukuru kwa kuwa mimi si kama

watu wengine, wanyang›anyi, wadhalimu,

wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.

12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa

zaka katika mapato yangu yote.

13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali,

wala hakuthubutu hata kuinua macho yake

mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema,

Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye

dhambi.

14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda

nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko

yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa,

naye ajidhiliye atakwezwa.

WARUMI 12:1 Basi, ndugu zangu,

nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni

miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu,

ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu

yenye maana.

1 PETRO 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe

yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za

roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya

Yesu Kristo.

Ona pia: Zaburi 22:24; Zaburi 34:18; Zaburi 102:17; Zaburi 147:3; Isaya 61:1-3; Isaya 66:2; Luka 15:2-7,21-32; Wafilipi 4:18;

Waebrania 3:16.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 53:6 Laiti wokovu wa Israeli

utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo

wafungwa wa watu wake; Yakobo

atashangilia, Israeli atafurahi.

ISAYA 59:20 Na Mkombozi atakuja

Sayuni, kwao waachao maasi yao katika

Yakobo, asema Bwana.

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

LUKA 1:68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa

Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na

kuwakomboa.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

LUKA 21:28 Basi mambo hayo yaanzapo

kutokea, changamkeni, mkaviinue

vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu

umekaribia.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

ZABURIEN

Page 125: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

125

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEBRANIA 9:12 wala si kwa damu ya mbuzi

na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe

aliingia mara moja tu katika Patakatifu,

akiisha kupata ukombozi wa milele.

Ona pia: #1; # 2; #3; Zaburi 14:7; Zaburi 42:11; Zaburi 43:5; Zaburi 44:4; Zaburi 74:12; Zaburi 78:35; Zaburi 111:9; Habakuki

3:13; Luka 1:71; Luka 2:38; Waefeso 1:7; Wakolosai 1:14.

F05 Masiha atasalitiwa.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 55:4 Moyo wangu unaumia ndani

yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia.

5 Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa

imenifunikiza.

12 Kwa maana aliyetukana si adui; Kama

ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu

yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo,

ningejificha asinione.

13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki

yangu, niliyejuana nawe sana.

14 Tulipeana shauri tamu; na kutembea

Nyumbani mwa Mungu pamoja na

mkutano.

MATHAYO 26:31 Ndipo Yesu akawaambia,

Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili

yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa,

Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi

watatawanyika.

32 Lakini baada ya kufufuka kwangu,

nitawatangulia kwenda Galilaya.

33 Petro akajibu, akamwambia,

Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi

sitachukizwa kamwe.

34 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe,

usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana

mara tatu.

35 Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe,

sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote

wakasema vivyo hivyo.

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka

bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia

wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende

kule nikaombe.

37 Akamchukua Petro na wale wana wawili

wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na

kusononeka.

38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni

nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe

pamoja nami.

YOHANA 13:21 Naye alipokwisha kusema

hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia

akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja

wenu atanisaliti.

YOHANA 13:27 Na baada ya hilo tonge

Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia,

Uyatendayo yatende upesi.

YOHANA 13:37 Petro akamwambia, Bwana,

kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa?

Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako.

38 Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako

kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia,

Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa

umenikana mara tatu.

Ona pia: Zaburi 6:3; Zaburi 69:20,21; Zaburi 102:3-5; Marko 14:33,34.

ZABURIEN

Page 126: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

126

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

H08 Masiha atakuwa na maisha ya milele.

ZABURI 61:6 Utaziongeza siku za mfalme,

Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.

7 Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize

fadhili na kweli zimhifadhi.

2 SAMWELI 7:16 Na nyumba yako, na ufalme

wako, vitathibitishwa milele mbele yako.

Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

WAEBRANIA 9:24 Kwa sababu Kristo hakuingia

katika patakatifu palipofanyika kwa mikono,

ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia

mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa

Mungu kwa ajili yetu;

Ona pia: #1; Zaburi 41:12; Waebrania 7:21-25.

F03 Masiha atakataliwa.

ZABURI 62:3 Hata lini mtamshambulia

mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?

Kama ukuta unaoinama, Kama kitalu kilicho

tayari kuanguka,

4 Hufanya shauri kumwangusha tu katika

cheo chake; Huufurahia uongo. Kwa kinywa

chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.

ZABURI 2:1 Mbona mataifa wanafanya

ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?

2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu

wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na

juu ya masihi wake.

3 Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia

mbali nasi kamba zao.

MATHAYO 26:3 Wakati ule wakuu

wa makuhani, na wazee wa watu,

wakakusanyika katika behewa ya Kuhani

Mkuu, jina lake Kayafa;

4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate

Yesu kwa hila na kumwua.

MATHAYO 27:1 Na ilipokuwa asubuhi,

wakuu wa makuhani wote na wazee wa

watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate

kumwua;

YOHANA 11:49 Mtu mmoja miongoni

mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu

mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno

lo lote;

50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja

afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa

zima.

51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi

yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu

mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa

kwa ajili ya taifa hilo.

MATENDO YA MITUME 4:25 nawe

ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa

cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona

mataifa wamefanya ghasia, Na makabila

wametafakari ubatili?

26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu

ZABURIEN

Page 127: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

127

wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na

juu ya Kristo wake.

27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato

pamoja na Mataifa na watu wa Israeli,

walikusanyika katika mji huu juu ya

Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia

mafuta,

28 ili wafanye yote ambayo mkono wako na

mashauri yako yamekusudia tangu zamani

yatokee.

Ona pia: Mathayo 2:14-16.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 65:2 Wewe usikiaye kuomba,

Wote wenye mwili watakujia.

ZABURI 22:27 Miisho yote ya dunia

itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana;

Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

ZABURI 86:9 Mataifa yote uliowafanya

watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana,

Watalitukuza jina lako;

ISAYA 66:23 Na itakuwa, mwezi mpya

hata mwezi mpya, na sabato hata sabato,

wanadamu wote watakuja kuabudu mbele

zangu, asema Bwana.

LUKA 11:9 Nami nawaambia, Ombeni,

nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona;

bisheni, nanyi mtafunguliwa.

10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea;

naye atafutaye huona; naye abishaye

atafunguliwa.

YOHANA 12:32 Nami nikiinuliwa juu ya

nchi, nitawavuta wote kwangu.

1 YOHANA 5:14 Na huu ndio ujasiri tulio nao

kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na

mapenzi yake, atusikia.

15 Na kama tukijua kwamba atusikia,

tuombacho chote, twajua kwamba tunazo

zile haja tulizomwomba.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; Zaburi 66:4; Zaburi 145:18,19; Isaya 49:6; Isaya 65:24; Yeremia 29:12,13.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 67:1 Mungu na atufadhili na

kutubariki, Na kutuangazia uso wake.

2 Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake

katikati ya mataifa yote.

3 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu

wote na wakushukuru.

4 Mataifa na washangilie, Naam, waimbe

kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu

watu, Na kuwaongoza mataifa walioko

duniani.

5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu

wote na wakushukuru.

6 Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu

wetu, ametubariki.

7 Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia

itamcha Yeye.

ISAYA 2:2 Na itakuwa katika siku

ZABURIEN

Page 128: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

128

za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote

watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake maana katika Sayuni

itatoka sheria, na neno la Bwana katika

Yerusalemu.

4 Naye atafanya hukumu katika mataifa

mengi, atawakemea watu wa kabila

nyingi; nao watafua panga zao ziwe

majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa

halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala

hawatajifunza vita tena kamwe.

DANIELI 7:14 Naye akapewa mamlaka, na

utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote,

na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie;

mamlaka yake ni mamlaka ya milele,

ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake

ni ufalme usioweza kuangamizwa.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #2; #4; #5; Yeremia 10:10.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 68:1 Mungu huondoka, adui

zake wakatawanyika, Nao wamchukiao

huukimbia uso wake.

2 Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo

uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo

mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo

usoni pa Mungu.

3 Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia

uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa

furaha.

4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,

Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye

majangwani kama mpanda farasi; Jina lake

ni YAHU; shangilieni mbele zake.

2 WATHESALONIKE 1:8 katika mwali

wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao

wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya

Bwana wetu Yesu;

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele,

kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa

nguvu zake;

UFUNUO WA YOHANA 18:20 Furahini

juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na

mitume na manabii; kwa maana Mungu

amehukumu hukumu yenu juu yake.

UFUNUO WA YOHANA 19:7 Na

tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Ona pia: #1; Kutoka 3:14; Isaya 12:4-6; 1 Wathesalonike 5:16; 1 Petro 1:8; Ufunuo wa Yohana 6:16,17.

ZABURIEN

Page 129: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

129

G02 Kupaa mbinguni kwa Masiha

kunatabiriwa.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

ZABURI 68:18 Wewe umepaa juu, umeteka

mateka, Umepewa vipawa katikati ya

wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana

Mungu akae nao.

MARKO 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya

kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni,

akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

LUKA 24:51 Ikawa katika kuwabariki,

alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.

YOHANA 7:39 Na neno hilo alilisema katika

habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

MATENDO YA MITUME 1:2 hata

siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa

amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu

wale mitume aliowachagua;

MATENDO YA MITUME 1:8 Lakini

mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu

Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi

wangu katika Yerusalemu, na katika

Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho

wa nchi.

9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa

wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea

kutoka machoni pao.

MATENDO YA MITUME 2:17

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu, na

wana wenu na binti zenu watatabiri; na

vijana wenu wataona maono; na wazee wenu

wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi

wangu wanaume na wanawake Roho yangu,

nao watatabiri.

WARUMI 12:6 Basi kwa kuwa tuna karama

zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema

mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa

kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu;

mwenye kufundisha, katika kufundisha

kwake;

WAEFESO 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa

Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa

baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa

roho, ndani yake Kristo;

WAEFESO 4:8 Hivyo husema, Alipopaa juu

aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.

9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini

kama siyo kusema kwamba yeye naye

alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

WAEBRANIA 4:14 Basi, iwapo tunaye kuhani

mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu,

Mwana wa Mungu, na tuyashike sana

maungamo yetu.

WAEBRANIA 6:20 alimoingia Yesu kwa

ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa

kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa

Melkizedeki.

WAEBRANIA 8:1 Basi, katika hayo

tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili:

Tunaye kuhani mkuu wa namna hii,

aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi

ZABURIEN

Page 130: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

130

cha Ukuu mbinguni,

Ona pia: Zaburi 24:3,7-10; Zaburi 47:5; Zaburi 72:17-19; Zaburi 104:3; Zaburi 110:1; 1 Wakorintho 12:4-10; 1 Petro 3:22.

F11 Mateso ya Masiha.

F12 Masiha atapingwa.

ZABURI 69:4 Wanaonichukia bure ni

wengi Kuliko nywele za kichwa changu.

Watakao kunikatilia mbali wamekuwa

hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.

Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu

nisivyovichukua.

YOHANA 15:25 Lakini litimie lile neno

lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia

bure.

YOHANA 19:4 Kisha Pilato akatokea tena

nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje

kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi

sioni hatia yo yote kwake.

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

1 PETRO 2:22 Yeye hakutenda dhambi,

wala hila haikuonekana kinywani mwake.

1 PETRO 2:24 Yeye mwenyewe alizichukua

dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti,

tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe

hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa

kwake mliponywa.

1 PETRO 3:18 Kwa maana Kristo naye

aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi,

mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili

atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa,

bali roho yake akahuishwa,

Ona pia: Zaburi 35:19; Zaburi 109:3; Isaya 53:4-7; Mathayo 26:59.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 69:7 Maana kwa ajili yako

nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika

uso wangu.

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na

msikwao kwa wana wa mama yangu.

9 Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na

laumu zao wanaokulaumu zimenipata.

MATHAYO 26:48 Na yule mwenye kumsaliti

alikuwa amewapa ishara, akisema,

Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu,

Rabi, akambusu.

50 Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia.

Wakaenda, wakanyosha mikono yao

wakamkamata Yesu.

MATHAYO 26:56 Lakini haya yote yamekuwa,

ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo

wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

MATHAYO 26:74 Ndipo akaanza kulaani na

kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara

akawika jogoo.

YOHANA 1:10 Alikuwako ulimwenguni,

hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako,

wala ulimwengu haukumtambua.

11 Alikuja kwake, wala walio wake

ZABURIEN

Page 131: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

131

hawakumpokea.

YOHANA 2:16 akawaambia wale waliokuwa

wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye

nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya

biashara.

17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa

imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

YOHANA 7:5 Maana hata nduguze

hawakumwamini.

YOHANA 15:21 Lakini haya yote

watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa

kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.

22 Kama nisingalikuja na kusema nao,

wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa

hawana udhuru kwa dhambi yao.

23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba

yangu.

24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda

mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi;

lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu,

na kutuchukia.

WARUMI 15:8 Kwa maana nasema, ya

kwamba Kristo amefanyika mhudumu

wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli

ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi

walizopewa baba zetu;

Ona pia: Zaburi 22:6-8; Zaburi 31:11; Zaburi 119:139; Mathayo 26:70-74; Marko 11:15-17.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ZABURI 69:19 Wewe umejua kulaumiwa

kwangu, Na kuaibika na kufedheheka

kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi

wangu wote.

20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua

sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala

hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona

mtu.

21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;

Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha

siki.

MATHAYO 27:34 wakampa kunywa divai

iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye

alipoionja hakutaka kunywa.

MATHAYO 27:39 Nao waliokuwa wakipita

njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa

vichwa vyao, wakisema,

40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga

kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe

Mwana wa Mungu, shuka msalabani.

41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani

wakamdhihaki pamoja na waandishi na

wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi

kujiokoa mwenyewe.

42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa

msalabani, nasi tutamwamini.

43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa,

kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi

ni Mwana wa Mungu.

44 Pia wale wanyang›anyi waliosulibiwa pamoja

naye walimshutumu vile vile.

45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya

nchi yote hata saa tisa.

46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti

yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama

sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu

wangu, mbona umeniacha?

47 Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia,

walisema, Huyu anamwita Eliya.

48 Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa

sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi,

ZABURIEN

Page 132: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

132

akamnywesha.

MARKO 15:23 Wakampa mvinyo iliyotiwa

manemane, asiipokee.

YOHANA 19:28 Baada ya hayo Yesu, hali

akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika

ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi

wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa

hisopo, wakampelekea kinywani.

30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki,

alisema, Imekwisha. Akainama kichwa,

akaisalimu roho yake.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

1 PETRO 2:23 Yeye alipotukanwa,

hakurudisha matukano; alipoteswa,

hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye

ahukumuye kwa haki.

24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu

katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu

kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa

mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake

mliponywa.

Ona pia: Zaburi 22:6,7; Isaya 53:3-5.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ZABURI 69:26 Maana wanamwudhi mtu

uliyempiga Wewe, Wanasimulia maumivu

ya hao uliowatia jeraha.

MARKO 15:28 Basi andiko likatimizwa

linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.]

29 Nao waliokuwa wakipita njiani

wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa,

wakisema, Ahaa! Wewe mwenye kulivunja

hekalu na kulijenga katika siku tatu,

30 jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.

31 Kadhalika na wakuu wa makuhani

wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na

waandishi, wakisema, Aliponya wengine;

hawezi kujiponya mwenyewe.

32 Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa

msalabani tupate kuona na kuamini.

Hata wale waliosulibiwa pamoja naye

wakamfyolea.

Ona pia: Isaya 53:4,10; Zekaria 13:7.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 71:20 Wewe, uliyetuonyesha

mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena.

Utatupandisha juu tena Tokea pande za

chini ya nchi.

LUKA 24:6 Hayupo hapa, amefufuka.

Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa

akaliko Galilaya,

LUKA 24:34 wakisema, Bwana amefufuka

kweli kweli, naye amemtokea Simoni.

WARUMI 14:9 Maana Kristo alikufa akawa

hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa

na walio hai pia.

MATENDO YA MITUME 2:27 Kwa

maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;

Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone

ZABURIEN

Page 133: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

133

uharibifu.

Ona pia: Zaburi 16:10; Zaburi 30:3; Zaburi 49:15; Zaburi 86:13; Yona 2:4-6; Matendo ya Mitume 13:35.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ZABURI 72:7 Siku zake yeye, mtu mwenye

haki atasitawi, Na wingi wa amani hata

mwezi utakapokoma.

8 Na awe na enzi toka bahari hata bahari,

Toka Mto hata miisho ya dunia.

9 Wakaao jangwani na wainame mbele zake;

Adui zake na warambe mavumbi.

10 Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete

kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe

vipawa.

11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na

mataifa yote wamtumikie.

12 Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na

mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.

13 Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na

nafsi za wahitaji ataziokoa.

14 Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na

udhalimu, Na damu yao ina thamani

machoni pake.

15 Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba;

Na wamwombee daima; Na kumbariki

mchana kutwa.

16 Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu

ya milima; Matunda yake na yawaye-waye

kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi

kama majani ya nchi.

17 Jina lake na lidumu milele, Pindi ling›aapo

jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na

wajibariki katika yeye, Na kumwita heri.

18 Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Mungu wa

Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake;

19 Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia

yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.

MATHAYO 2:11 Wakaingia nyumbani,

wakamwona mtoto pamoja na Mariamu

mamaye, wakaanguka wakamsujudia;

nao walipokwisha kufungua hazina zao,

wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na

manemane.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

MARKO 16:15 Akawaambia, Enendeni

ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa

kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka;

asiyeamini, atahukumiwa.

WAFILIPI 2:10 ili kwa jina la Yesu kila

goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi;

WAEBRANIA 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana

na leo na hata milele.

UFUNUO WA YOHANA 1:18 na aliye

hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama,

ni hai hata milele na milele. Nami ninazo

funguo za mauti, na za kuzimu.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

ZABURIEN

Page 134: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

134

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #1; #2; #5; Mwanzo 22:18; Zaburi 21:4.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ZABURI 75:7 Bali Mungu ndiye

ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua

huyu.

8 Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe,

Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa

machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira

zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na

kuzinywa.

LUKA 1:52 Amewaangusha wakuu

katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge

amewakweza.

MATENDO YA MITUME 17:31 Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu

walimwengu kwa haki, kwa mtu yule

aliyemchagua; naye amewapa watu wote

uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua

katika wafu.

WARUMI 2:16 katika siku ile Mungu

atakapozihukumu siri za wanadamu,

sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

2 TIMOTHEO 4:1 Nakuagiza mbele za Mungu,

na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu

walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa

kwake na kwa ufalme wake;

UFUNUO WA YOHANA 14:9 Na

mwingine, malaika wa tatu, akawafuata,

akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote

akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake,

na kuipokea chapa katika kipaji cha uso

wake, au katika mkono wake,

10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya

ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo

kuchanganywa na maji, katika kikombe

cha hasira yake; naye atateswa kwa moto

na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na

mbele za Mwana-Kondoo.

11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu

hata milele na milele, wala hawana raha

mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo

mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye

chapa ya jina lake.

UFUNUO WA YOHANA 16:19 Na mji

ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu,

na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule

mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu,

kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu

ya hasira yake.

Ona pia: #1; #6; 1 Samweli 2:7,8; Isaya 51:17-22; Yeremia 25:15-17.

ZABURIEN

Page 135: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

135

B19 Fumbo la Masiha.

ZABURI 78:2 Na nifunue kinywa changu

kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale.

MATHAYO 13:10 Wakaja wanafunzi,

wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa

mifano?

11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa

kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali

wao hawakujaliwa.

12 Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa,

naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na

kitu, hata kile alicho nacho atanyang›anywa.

13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano;

kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia

hawasikii, wala kuelewa.

MATHAYO 13:34 Hayo yote Yesu aliwaambia

makutano kwa mifano; wala pasipo mfano

hakuwaambia neno;

35 ili litimie neno lililonenwa na nabii,

akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa

mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu

awali.

MARKO 4:11 Akawaambia, Ninyi

mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu,

bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa

mifano,

YOHANA 16:25 Hayo nimesema nanyi kwa

mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi

tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi

habari ya Baba.

1 WAKORINTHO 4:1 Mtu na atuhesabu

hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na

mawakili wa siri za Mungu.

Ona pia: Zaburi 49:4; Hosea 12:9; Mathayo 21:45; Marko 3:23; Marko 4:2,13,33; Marko 12:1; Luka 8:10; 1 Wakorintho 13:2; 1

Wakorintho 14:2.

B03 Masiha ndiye Mwana wa mtu.

H07 Masiha ataketi kwenye mkono wa kulia

wa Mungu.

ZABURI 80:14 Ee Mungu wa majeshi,

tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone,

uujilie mzabibu huu.

15 Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako

wa kuume; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa

imara kwa nafsi yako.

17 Mkono wako na uwe juu yake Mtu wa

mkono wako wa kuume; Juu ya mwanadamu

uliyemfanya Kuwa imara kwa nafsi yako;

ISAYA 11:1 Basi litatoka chipukizi katika

shina la Yese, na tawi litakalotoka katika

mizizi yake litazaa matunda.

ZEKARIA 3:8 Sikiliza sasa, Ee Yoshua,

kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio

mbele yako; maana hao ni watu walio ishara;

kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi

wangu, aitwaye Chipukizi.

YOHANA 15:1 Mimi ndimi mzabibu wa

kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

MATENDO YA MITUME 10:38 habari za

Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia

mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye

akazunguka huko na huko, akitenda kazi

njema na kuponya wote walioonewa na

Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja

naye.

MATENDO YA MITUME 15:15 Na

ZABURIEN

Page 136: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

136

maneno ya manabii yapatana na hayo, kama

ilivyoandikwa,

16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami

nitaijenga tena nyumba ya Daudi

iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake,

Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

WAKOLOSAI 1:15 naye ni mfano wa Mungu

asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa

viumbe vyote.

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,

vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,

vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa

ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au

mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia

yake, na kwa ajili yake.

17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu

vyote hushikana katika yeye.

18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha

kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa

wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe

mtangulizi katika yote.

19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu

wote ukae;

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao wa utukufu wake

na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote

kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa

kuume wa Ukuu huko juu;

Ona pia: #2; Zaburi 7:7; Zaburi 80:8; Zaburi 90:13; Isaya 63:15,17; Yeremia 2:21; Yeremia 23:5,6; Ezekieli 17:22-24; Danieli

9:16-19; Zekaria 6:12; Marko 12:1-9.

E07 Wokovu unaotolewa na Masiha.

ZABURI 85:9 Hakika wokovu wake u

karibu na wamchao, Utukufu ukae katika

nchi yetu.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

MATENDO YA MITUME 13:26 Ndugu

zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao

miongoni mwenu wanaomcha Mungu,

kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.

Ona pia: #2; Zaburi 24:4,5; Zaburi 50:23; Marko 12:32-34; Matendo ya Mitume 10:2-4; Matendo ya Mitume 13:14-16.

E08 Haki ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 85:10 Fadhili na kweli zimekutana,

Haki na amani zimehusiana.

11 Kweli imechipuka katika nchi, Haki

imechungulia kutoka mbinguni.

12 Naam, Bwana atatoa kilicho chema, Na nchi

yetu itatoa mazao yake.

13 Haki itakwenda mbele zake, Nayo itazifanya

hatua zake kuwa njia.

MATHAYO 3:15 Yesu akajibu akamwambia,

Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo

kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

ZABURIEN

Page 137: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

137

MATHAYO 21:32 Kwa sababu Yohana alikuja

kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini;

lakini watoza ushuru na makahaba

walimwamini, nanyi hata mlipoona,

hamkutubu baadaye, ili kumwamini.

YOHANA 14:6 Yesu akamwambia, Mimi

ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa

Baba, ila kwa njia ya mimi.

WARUMI 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa

haki itokayo katika imani, na mwe na amani

kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu

Kristo,

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

WAFILIPI 1:10 mpate kuyakubali yaliyo

mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila

kosa, mpaka siku ya Kristo;

11 hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya

Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.

2 PETRO 3:13 Lakini, kama ilivyo ahadi

yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi

mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

1 YOHANA 2:6 Yeye asemaye ya kuwa

anakaa ndani yake, imempasa kuenenda

mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

Ona pia: #1; #2; Yohana 13:14-16,34; Warumi 3:25,26; Waefeso 5:1,2; Wafilipi 2:5-8; Waebrania 12:1,2; 1 Petro 2:18-24.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 86:9 Mataifa yote uliowafanya

watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana,

Watalitukuza jina lako;

ISAYA 66:23 Na itakuwa, mwezi mpya

hata mwezi mpya, na sabato hata sabato,

wanadamu wote watakuja kuabudu mbele

zangu, asema Bwana.

ZEKARIA 14:9 Naye Bwana atakuwa

Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana

atakuwa mmoja, na jina lake moja.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #4.

ZABURIEN

Page 138: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

138

E14 Masiha atashinda kifo na giza.

ZABURI 86:12 Nitakusifu Wewe, Bwana,

Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote,

Nitalitukuza jina lako milele.

13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;

Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

1 WATHESALONIKE 1:10 na kumngojea

Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye

alimfufua katika wafu, naye ni Yesu,

mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.

Ona pia: Zaburi 16:10; Zaburi 56:13; Yona 2:3-6.

B22 Uzuri wa Mungu na Masiha.

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

ZABURI 86:15 Lakini Wewe, Bwana, U

Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu,

mwingi wa fadhili na kweli.

YOHANA 1:17 Kwa kuwa torati ilitolewa

kwa mkono wa Musa; neema na kweli

zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

WARUMI 5:20 Lakini sheria iliingia ili kosa

lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi,

neema ilikuwa nyingi zaidi;

21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala

katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki

neema itawale hata uzima wa milele kwa

Yesu Kristo Bwana wetu.

WAEFESO 1:9 akiisha kutujulisha siri ya

mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake,

alioukusudia katika yeye huyo.

WAEFESO 2:4 Lakini Mungu, kwa kuwa

ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake

makuu aliyotupenda;

5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu

ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na

Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha

pamoja naye katika ulimwengu wa roho,

katika Kristo Yesu;

7 ili katika zamani zinazokuja audhihirishe

wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema

wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

Ona pia: Zaburi 86:5; Zaburi 103:8; Zaburi 111:4; Zaburi 130:4,7; Zaburi 145:8; Yoeli 2:13; Mika 7:18.

F06 Masiha ataachwa pweke.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ZABURI 88:14 Bwana, kwa nini kuitupa

nafsi yangu, Na kunificha uso wako?

15 Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana,

Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.

16 Hasira zako kali zimepita juu yangu,

Maogofyo yako yameniangamiza.

17 Yamenizunguka kama maji mchana kutwa,

Yamenisonga yote pamoja.

18 Mpenzi na rafiki umewatenga nami, Nao

wanijuao wamo gizani.

MATHAYO 26:37 Akamchukua Petro na

wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza

kuhuzunika na kusononeka.

38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni

nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe

pamoja nami.

39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka

kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu,

ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke;

walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama

ZABURIEN

Page 139: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

139

utakavyo wewe.

40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta

wamelala, akamwambia Petro, Je!

Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa

moja?

MATHAYO 26:56 Lakini haya yote yamekuwa,

ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo

wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

MATHAYO 27:28 Wakamvua nguo, wakamvika

vazi jekundu.

29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu

ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono

wake wa kuume; wakapiga magoti mbele

yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu,

Mfalme wa Wayahudi!

30 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule

mwanzi, wakampiga-piga kichwani.

31 Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile

vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua

kumsulibisha.

MATHAYO 27:46 Na kama saa tisa, Yesu

akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi,

Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu,

Mungu wangu, mbona umeniacha?

Ona pia: Zaburi 22:11-21; Zaburi 31:11; Zaburi 38:10,11; Zaburi 69:17-21; Zaburi 88:8; Zaburi 143:3,4; Isaya 53:4-6,8,10,11; Isaya

63:3; Danieli 9:26; Zekaria 13:7; Mathayo 27:39-44; Marko 14:33,34; Luka 22:44; Warumi 8:32; Wagalatia 3:13; 1 Petro 2:24.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:3 Nimefanya agano na mteule

wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi

wangu.

4 Wazao wako nitawafanya imara milele,

Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

MATHAYO 12:18 Tazama, mtumishi wangu

niliyemteua; Mpendwa wangu, moyo wangu

uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu

yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

19 Hatateta wala hatapaza sauti yake; Wala mtu

hatasikia sauti yake njiani.

20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala

utambi utokao moshi hatauzima, Hata

ailetapo hukumu ikashinda.

21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

MATENDO YA MITUME 2:29 Waume,

ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa

ujasiri mbele yenu habari za baba yetu

mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na

kaburi lake liko kwetu hata leo.

30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa

Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba

katika uzao wa viuno vyake atamketisha

mmoja katika kiti chake cha enzi;

Ona pia: Zaburi 89:28-34; Yeremia 30:9; Ezekieli 34:23,24; Hosea 3:5; Mathayo 3:17; Waebrania 7:21.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

ZABURI 89:19 Ndipo ulipowaambia

watakatifu wako kwa njozi, Ukasema,

nimempa aliye hodari msaada;

Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni

mwa watu.

ZABURIEN

Page 140: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

140

KUMBUKUMBU LA TORATI 18:18 Mimi

nitawaondokeshea nabii miongoni mwa

ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia

maneno yangu kinywani mwake, naye

atawaambia yote nitakayomwamuru.

19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno

yangu atakayosema yule kwa jina langu,

nitalitaka kwake.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 7:16 Hofu ikawashika wote,

wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii

mkuu ametokea kwetu; na, Mungu

amewaangalia watu wake.

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

WAFILIPI 2:6 ambaye yeye mwanzo

alikuwa yuna namna ya Mungu, naye

hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni

kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa

namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa

wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama

mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii

hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha

mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

UFUNUO WA YOHANA 3:7 Na

kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia

andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye

mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo

wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala

hapana afungaye, naye afunga wala hapana

afunguaye.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 33:29; Marko 1:24; Waebrania 2:9-17.

B05 Masiha amejawa na Roho na Mtakatifu.

D01 Kupakwa kwa mafuta kwa Masiha.

ZABURI 89:20 Nimemwona Daudi,

mtumishi wangu, Nimempaka mafuta

yangu matakatifu.

21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti

kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

YOHANA 3:34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa

na Mungu huyanena maneno ya Mungu;

kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

YOHANA 12:3 Basi Mariamu akatwaa ratli

ya marhamu ya nardo safi yenye thamani

nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta

miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia

ZABURIEN

Page 141: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

141

ikajaa harufu ya marhamu.

YOHANA 12:7 Basi Yesu alisema, Mwache

aiweke kwa siku ya maziko yangu.

MATENDO YA MITUME 10:38 habari za

Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia

mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye

akazunguka huko na huko, akitenda kazi

njema na kuponya wote walioonewa na

Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja

naye.

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa

hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia

mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Ona pia: #2; Zaburi 89:13; Isaya 41:10; Isaya 42:1; Zekaria 10:12; Mathayo 26:12.

E13 Mungu anathibitisha huduma ya Masiha.

ZABURI 89:22 Adui hatamwonea, Wala

mwana wa uovu hatamtesa.

MATHAYO 4:1 Kisha Yesu alipandishwa na

Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.

2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku,

mwisho akaona njaa.

3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe

Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe

haya yawe mikate.

4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu

hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno

litokalo katika kinywa cha Mungu.

5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji

mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha

hekalu,

6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana

wa Mungu jitupe chini; kwa maana

imeandikwa, Atakuagizia malaika zake;

Na mikononi mwao watakuchukua; Usije

ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa,

Usimjaribu Bwana Mungu wako.

8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima

mrefu mno, akamwonyesha milki zote za

ulimwengu, na fahari yake,

9 akamwambia, Haya yote nitakupa,

ukianguka kunisujudia.

10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako,

Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie

Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke

yake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:23 Bali nitawaponda

watesi wake mbele yake, Nitawapiga

wanaomchukia.

YOHANA 15:23 Yeye anichukiaye mimi

humchukia na Baba yangu.

LUKA 19:27 Tena, wale adui zangu,

wasiotaka niwatawale, waleteni hapa

mwachinje mbele yangu.

Ona pia: #1; Zaburi 2:1-6; Zaburi 21:8,9; Zaburi 110:1; Zaburi 132:8.

ZABURIEN

Page 142: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

142

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:24 Uaminifu wangu na fadhili

zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu

pembe yake itatukuka.

YOHANA 17:6 Jina lako nimewadhihirishia

watu wale ulionipa katika ulimwengu;

walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako

wamelishika.

YOHANA 17:11 Wala mimi simo tena

ulimwenguni, lakini hawa wamo

ulimwenguni, nami naja kwako. Baba

mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde

hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

YOHANA 17:25 Baba mwenye haki,

ulimwengu haukukujua; lakini mimi

nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe

uliyenituma.

Ona pia: #1; Zaburi 89:16,17,28,33; Zaburi 91:14.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:25 Nitaweka mkono wake juu

ya bahari, Na mkono wake wa kuume juu ya

mito.

KUTOKA 23:21 Jitunzeni mbele yake,

mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani;

maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa

kuwa jina langu limo ndani yake.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

ZABURI 89:26 Yeye ataniita, Wewe baba

yangu, Mungu wangu na mwamba wa

wokovu wangu.

MATHAYO 11:27 Akasema, Nimekabidhiwa

vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye

Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye

Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana

apenda kumfunulia.

LUKA 23:46 Yesu akalia kwa sauti kuu,

akasema, Ee Baba, mikononi mwako

naiweka roho yangu.

YOHANA 14:7 Kama mngalinijua mimi,

mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua,

tena mmemwona.

YOHANA 14:23 Yesu akajibu, akamwambia,

Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na

Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake,

na kufanya makao kwake.

YOHANA 20:17 Yesu akamwambia.

Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda

kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu

ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba

yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu

wangu naye ni Mungu wenu.

ZABURIEN

Page 143: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

143

2 WAKORINTHO 6:18 Nitakuwa Baba

kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu

wa kiume na wa kike,

WAEBRANIA 1:5 Kwa maana alimwambia

malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe

mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na

tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye

atakuwa kwangu mwana?

UFUNUO WA YOHANA 3:21 Yeye

ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami

katika kiti changu cha enzi, kama mimi

nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba

yangu katika kiti chake cha enzi.

Ona pia: 2 Samweli 22:47; 1 Mambo ya Nyakati 22:10; Zaburi 18:46; Zaburi 62:2,6,7; Zaburi 95:1; Mathayo 10:32,33; Mathayo

26:39,42; Yohana 8:54; Yohana 11:41; Wagalatia 4:6.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

E13 Mungu anathibitisha huduma ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:27 Nami nitamjalia kuwa

mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana

kuliko wafalme wa dunia.

28 Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na

agano langu litafanyika amini kwake.

29 Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na

kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.

MATENDO YA MITUME 13:32 Na sisi

tunawahubiri habari njema ya ahadi ile

waliyopewa mababa,

33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto

wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama

ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe

ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.

34 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate

kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitawapa

ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo

amini.

WAEBRANIA 1:5 Kwa maana alimwambia

malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe

mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na

tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye

atakuwa kwangu mwana?

6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza

ulimwenguni, asema, Na wamsujudu

malaika wote wa Mungu.

7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye

malaika zake kuwa pepo, Na watumishi

wake kuwa miali ya moto.

8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti

chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na

milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya

adili.

WAKOLOSAI 1:15 naye ni mfano wa Mungu

asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa

viumbe vyote.

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,

vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,

vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa

ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au

mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia

yake, na kwa ajili yake.

17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu

vyote hushikana katika yeye.

18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha

kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa

wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe

mtangulizi katika yote.

19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu

wote ukae;

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

ZABURIEN

Page 144: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

144

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #4; Warumi 8:20.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 89:35 Neno moja nimeliapa kwa

utakatifu wangu, Hakika sitamwambia

Daudi uongo,

36 Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake

kitakuwa kama jua mbele zangu.

37 Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi

aliye mbinguni mwaminifu.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Ona pia: Isaya 9:8; Ufunuo wa Yohana 1:5.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

ZABURI 90:2 Kabla haijazaliwa milima,

wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata

milele ndiwe Mungu.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

Ona pia: Mithali 8:22-26; Isaya 44:6; Waebrania 1:10-12; Waebrania 13:8; Ufunuo wa Yohana 1:8.

E03 Kujaribiwa kwa Masiha.

ZABURI 91:11 Kwa kuwa atakuagizia

malaika zake Wakulinde katika njia zako

zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije

ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

LUKA 4:9 Akamwongoza mpaka

Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha

hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana

wa Mungu, jitupe chini;

10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia

malaika zake wakulinde;

11 na ya kwamba,mikononi mwao

watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako

katika jiwe.

12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa,

Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Ona pia: Mathayo 4:6; Waebrania 1:14.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZABURI 91:13 Utawakanyaga simba na

nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa

miguu.

MARKO 16:18 watashika nyoka; hata

wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru

kabisa; wataweka mikono yao juu ya

wagonjwa, nao watapata afya.

MATENDO YA MITUME 28:3 Paulo

alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na

kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya

ule moto akamzonga-zonga mkononi.

4 Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-

lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi

ZABURIEN

Page 145: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

145

mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa

ameokoka katika bahari haki haimwachi

kuishi.

5 Lakini yeye akamtukusia motoni asipate

madhara.

2 TIMOTHEO 4:17 Lakini Bwana

alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili

kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa

utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami

nikaokolewa katika kinywa cha simba.

Ona pia: Isaya 1:6-8; Isaya 35:9; Isaya 65:25; Danieli 6:21; Ufunuo wa Yohana 5:5.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

G03 Kuinuliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 91:14 Kwa kuwa amekaza

kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo

juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa

pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na

kumtukuza;

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami

nitamwonyesha wokovu wangu.

YOHANA 12:28 Baba, ulitukuze jina

lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni,

Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

YOHANA 13:32 Mungu naye atamtukuza

ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.

YOHANA 14:23 Yesu akajibu, akamwambia,

Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na

Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake,

na kufanya makao kwake.

YOHANA 16:14 Yeye atanitukuza mimi,

kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na

kuwapasha habari.

YOHANA 16:27 kwa maana Baba mwenyewe

awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda

mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka

kwa Baba.

YOHANA 21:19 Akasema neno hilo

kwa kuonyesha ni kwa mauti gani

atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha

kusema hayo akamwambia, Nifuate.

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa

mateso hayo yaliyompata;

Ona pia: Warumi 8:28; Zaburi 18:3,4; Zaburi 16:10; Zaburi 21:4; Zaburi 61:5,6.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

ZABURI 93:1 Bwana ametamalaki,

amejivika adhama, Bwana amejivika,

na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu

umethibitika usitikisike;

2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;

Wewe ndiwe uliye tangu milele.

MITHALI 8:22 Bwana alikuwa nami katika

mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo

yake ya kale.

ZABURIEN

Page 146: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

146

23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla

haijawako dunia.

WAEBRANIA 1:2 mwisho wa siku hizi

amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka

kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya

ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao wa utukufu wake

na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote

kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa

kuume wa Ukuu huko juu;

UFUNUO WA YOHANA 19:6 Nikasikia

sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama

sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi

yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa

Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Ona pia: #1; #2; Mika 5:2; Waebrania 1:10-12; Waebrania 13:8; Ufunuo wa Yohana 1:8,17,18.

A08 Majina na vyeo vya Masiha.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ZABURI 95:1 Njoni, tumwimbie Bwana,

Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu

wetu.

2 Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie

shangwe kwa zaburi.

3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na

Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

2 SAMWELI 22:2 akasema, Bwana ndiye jabali

langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,

naam, wangu;

2 SAMWELI 22:32 Maana ni nani aliye Mungu,

ila Bwana? Ni nani aliye mwamba, ila

Mungu wetu?

2 SAMWELI 22:47 Bwana ndiye aliye hai; Na

ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe

Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;

2 SAMWELI 23:3 Mungu wa Israeli alisema,

Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye

wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho

cha Mungu,

1 WAKORINTHO 10:4 wote wakanywa

kinywaji kile kile cha roho; kwa maana

waliunywea mwamba wa roho uliowafuata;

na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

Ona pia: #1; #4; Kumbukumbu la Torati 32:4,15,18; Zaburi 18:1,2,31,46; Zaburi 19:14; Zaburi 31:2,3; Zaburi 62:2,6,7; Zaburi

71:3; Zaburi 73:26; Zaburi 78:35; Zaburi 89:26; Zaburi 92:15; Zaburi 94:22; Zaburi 144:1; Isaya 26:4; Isaya 30:29; Isaya 44:8.

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

ZABURI 95:7 Kwa maana ndiye Mungu

wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na

kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo

msikie sauti yake!

8 Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile

huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani.

9 Hapo waliponijaribu baba zenu,

Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

10 Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,

Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,

Hawakuzijua njia zangu.

11 Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani

mwangu.

ZABURIEN

Page 147: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

147

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa

kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa

moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

YOHANA 10:14 Mimi ndimi mchungaji

mwema; nao walio wangu nawajua; nao

walio wangu wanijua mimi;

15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo

Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya

kondoo.

16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi

hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti

yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi

moja na mchungaji mmoja.

WAEBRANIA 3:7 Kwa hiyo, kama anenavyo

Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti

yake,

8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati

wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika

jangwa,

9 Hapo baba zenu waliponijaribu,

wakanipima, Wakaona matendo yangu

miaka arobaini.

10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,

Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka

mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;

11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,

Hawataingia rahani mwangu.

12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika

mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini,

kwa kujitenga na Mungu aliye hai.

13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu

iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe

mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo,

kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti

wetu kwa nguvu mpaka mwisho;

15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti

yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama

wakati wa kukasirisha.

16 Maana ni akina nani waliokasirisha,

waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri

wakiongozwa na Musa?

17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka

arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga

yao ilianguka katika jangwa?

18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba

hawataingia katika raha yake, ila wale

walioasi?

19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia

kwa sababu ya kutokuamini kwao.

WAEBRANIA 4:1 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya

kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja

wenu asije akaonekana ameikosa.

2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa

habari njema vile vile kama hao. Lakini neno

lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu

halikuchanganyika na imani ndani yao

waliosikia.

3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha

ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa

kwa hasira yangu, Hawataingia rahani

mwangu:

4 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali

fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba,

akaziacha kazi zake zote;

5 na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu.

6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba

wako watu watakaoingia humo, na wale

waliohubiriwa habari ile zamani walikosa

kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

7 aweka tena siku fulani, akisema katika

Daudi baada ya muda mwingi namna hii,

Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani,

Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye

ZABURIEN

Page 148: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

148

migumu mioyo yenu.

8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha,

asingaliinena siku nyingine baadaye.

9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa

Mungu.

10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake

amestarehe mwenyewe katika kazi yake,

kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi

zake.

11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile,

ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa

mfano uo huo wa kuasi.

1 PETRO 2:25 Kwa maana mlikuwa

mnapotea kama kondoo; lakini sasa

mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa

roho zenu.

YUDA 1:5 Tena napenda

kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha

kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha

kuwaokoa watu katika nchi ya Misri,

aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.

Ona pia: Mwanzo 2:2,3; Kutoka 17:2-7; Hesabu 14:11-30; Kumbukumbu la Torati 1:34,35; Kumbukumbu la Torati 2:14-

16; Zaburi 78:17,18,40,41,56; Matendo ya Mitume 20:28; 1 Wakorintho 10:9; Waebrania 11:16; Waebrania 12:25; Ufunuo wa

Yohana 14:13.

E15 Masiha ataleta habari njema.

ZABURI 96:1 Mwimbieni Bwana wimbo

mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.

2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake,

Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,

Na watu wote habari za maajabu yake.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

WAEFESO 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa

Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa

baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa

roho, ndani yake Kristo;

UFUNUO WA YOHANA 5:13 Na kila

kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi

na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu

vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

UFUNUO WA YOHANA 14:6 Kisha

nikaona malaika mwingine, akiruka

katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele,

awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila

taifa na kabila na lugha na jamaa,

7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu,

na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu

yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya

mbingu na nchi na bahari na chemchemi za

maji.

ZABURIEN

Page 149: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

149

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 96:7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za

watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.

8 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, Leteni

sadaka mkaziingie nyua zake.

9 Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu,

Tetemekeni mbele zake, nchi yote.

10 Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki;

Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,

Atawahukumu watu kwa adili.

11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,

Bahari na ivume na vyote viijazavyo,

12 Mashamba na yashangilie, na vyote

vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe

kwa furaha;

13 Mbele za Bwana, kwa maana anakuja,

Kwa maana anakuja aihukumu nchi.

Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na

mataifa kwa uaminifu wake.

WAGALATIA 1:16 alipoona vema

kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu,

ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara

sikufanya shauri na watu wenye mwili na

damu;

1 WATHESALONIKE 4:16 Kwa sababu

Bwana mwenyewe atashuka kutoka

mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya

malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;

nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa

kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa

pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki

Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja

na Bwana milele.

18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

2 WATHESALONIKE 1:10 yeye atakapokuja

ili kutukuzwa katika watakatifu wake,

na kustaajabiwa katika wote waliosadiki

katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu

ulisadikiwa kwenu).

2 TIMOTHEO 4:8 baada ya hayo nimewekewa

taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu

mwenye haki, atanipa siku ile; wala si

mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda

kufunuliwa kwake.

TITO 2:13 tukilitazamia tumaini lenye

baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo

Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

2 PETRO 3:12 mkitazamia hata ije siku ile

ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo

mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe

vya asili vitateketea na kuyeyuka?

UFUNUO WA YOHANA 11:18 Na

mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja,

na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa,

na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako

manabii na watakatifu, na hao walichao

jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa

kuwaharibu hao waiharibuo nchi.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

Ona pia: #1; #2; #6.

ZABURIEN

Page 150: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

150

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 97:1 Bwana ametamalaki, nchi na

ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.

2 Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na

hukumu ndio msingi wa kiti chake.

3 Moto hutangulia mbele zake, Nao

huwateketeza watesi wake pande zote.

4 Umeme wake uliuangaza ulimwengu, Nchi

ikaona ikatetemeka.

5 Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,

Mbele za Bwana wa dunia yote.

6 Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu

wote wameuona utukufu wake.

2 WATHESALONIKE 1:8 katika mwali

wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao

wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya

Bwana wetu Yesu;

WAEBRANIA 12:29 maana Mungu

wetu ni moto ulao.

2 PETRO 3:10 Lakini siku ya Bwana itakuja

kama mwivi; katika siku hiyo mbingu

zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe

vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na

nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa

hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia

gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na

kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu

zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili

vitateketea na kuyeyuka?

UFUNUO WA YOHANA 1:7 Tazama,

yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona,

na hao waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.

Amina.

UFUNUO WA YOHANA 5:13 Na kila

kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi

na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu

vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

UFUNUO WA YOHANA 6:16

wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni,

tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya

kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao,

imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 19:2 kwa

kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki;

maana amemhukumu yule kahaba mkuu

aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake,

na kuipatiliza damu ya watumwa wake

mkononi mwake.

Ona pia: #1; #6; #7.

ZABURIEN

Page 151: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

151

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

ZABURI 98:1 Mwimbieni Bwana wimbo

mpya, Kwa maana ametenda mambo ya

ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe,

Mkono wake mtakatifu umemtendea

wokovu.

2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni

pa mataifa ameidhihirisha haki yake.

3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu

wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya

dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.

ISAYA 52:10 Bwana ameweka wazi

mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa

yote; Na ncha zote za dunia Zitauona

wokovu wa Mungu wetu.

ISAYA 52:15 ndivyo atakavyowasitusha

mataifa mengi; wafalme watamfumbia

vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa

watayaona; na mambo wasiyoyasikia

watayafahamu.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote

kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la

Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

MARKO 16:15 Akawaambia, Enendeni

ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa

kila kiumbe.

LUKA 1:70 Kama alivyosema tangu

mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake

watakatifu;

71 Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao

wote wanaotuchukia;

72 Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na

kulikumbuka agano lake takatifu;

73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,

74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi

mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,

75 Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku

zetu zote.

LUKA 2:30 Kwa kuwa macho yangu

yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na

kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

WARUMI 10:18 Lakini nasema, Je! Wao

hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao

imeenea duniani mwote, Na maneno yao

hata miisho ya ulimwengu.

WARUMI 15:8 Kwa maana nasema, ya

kwamba Kristo amefanyika mhudumu

wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli

ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi

walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili

ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa

hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami

nitaliimbia jina lako.

Ona pia: Mambo ya Walawi 26:14-45; Zaburi 106:45; Isaya 45:21-23; Isaya 49:6; Mika 7:20; Luka 3:6.

B13 Mamlaka ya Masiha.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 98:4 Mshangilieni Bwana, nchi

yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha,

imbeni zaburi.

ZABURIEN

Page 152: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

152

5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa

kinubi na sauti ya zaburi.

6 Kwa panda na sauti ya baragumu.

Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.

7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo,

Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.

8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe

pamoja kwa furaha.

9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja

aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu

kwa haki, Na mataifa kwa adili.

MATHAYO 24:30 ndipo itakapoonekana

ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni;

ndipo mataifa yote ya ulimwengu

watakapoomboleza, nao watamwona

Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu

ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu

mwingi.

MATHAYO 26:64 Yesu akamwambia, Wewe

umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa

mtamwona Mwana wa Adamu ameketi

mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya

mawingu ya mbinguni.

UFUNUO WA YOHANA 1:7 Tazama,

yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona,

na hao waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.

Amina.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 14:14 Kisha

nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu

ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa

Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu

ya kichwa chake, na katika mkono wake

mundu mkali.

15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu,

akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa

ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako,

ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja;

kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.

16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa

mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa.

Ona pia: #5; #6; Matendo ya Mitume 1:9-11.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 99:1 Bwana ametamalaki, mataifa

wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi,

nchi inatikisika.

2 Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye

ametukuka juu ya mataifa yote.

3 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa;

Ndiye mtakatifu.

4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu;

Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya

hukumu na haki katika Yakobo.

5 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni

penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu.

ISAYA 14:32 Wajumbe wa taifa hilo

waletewe jibu gani? Ya kuwa Bwana

ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake

wale walioonewa katika watu wake wataona

kimbilio.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

ZABURIEN

Page 153: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

153

mbinguni na duniani.

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu

ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya

Habili.

1 YOHANA 3:3 Na kila mwenye matumaini

haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo

mtakatifu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 14:1 Kisha

nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo

amesimama juu ya mlima Sayuni, na

watu mia na arobaini na nne elfu pamoja

naye, wenye jina lake na jina la Baba yake

limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

UFUNUO WA YOHANA 19:16 Naye ana

jina limeandikwa katika vazi lake na paja

lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana

WA MABwana.

Ona pia: #1; #2.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 102:1 Ee Bwana, usikie kuomba

kwangu, Kilio changu kikufikie.

2 Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,

Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu

upesi.

3 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi,

Na mifupa yangu inateketea kama kinga.

4 Moyo wangu umepigwa kama majani na

kukauka, Naam, ninasahau kula chakula

changu.

5 Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa

yangu imegandamana na nyama yangu.

6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

Na kufanana na bundi wa mahameni.

7 Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro

Aliye peke yake juu ya nyumba.

8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa;

Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu

Huapa kwa kunitaja mimi.

9 Maana nimekula majivu kama chakula, Na

kukichanganya kinywaji changu na machozi.

10 Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira

yako; Maana umeniinua na kunitupilia

mbali.

11 Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa,

Nami ninanyauka kama majani.

MARKO 14:33 Akamtwaa Petro na Yakobo

na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika

sana na kuhangaika.

34 Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi

kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.

ZABURIEN

Page 154: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

154

LUKA 22:44 Naye kwa vile alivyokuwa

katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake

ikawa kama matone ya damu yakidondoka

nchini.]

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ZABURI 102:13 Wewe mwenyewe

utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa

maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam,

majira yaliyoamriwa yamewadia.

14 Maana watumishi wako wameyaridhia mawe

yake, Na kuyaonea huruma mavumbi yake.

15 Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana, Na

wafalme wote wa dunia utukufu wako;

16 Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,

Atakapoonekana katika utukufu wake,

17 Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,

Asiyadharau maombi yao.

18 Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na

watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.

19 Maana ametazama toka patakatifu pake pa

juu, Toka mbinguni Bwana ameiangalia

nchi,

20 Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na

kuwafungua walioandikiwa kufa.

21 Watu walitangaze jina la Bwana katika

Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu,

22 Pindi mataifa watapokusanyika pamoja,

Falme nazo ili kumtumikia Bwana.

ZEKARIA 2:10 Imba, ufurahi, Ee binti

Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami

nitakaa kati yako, asema Bwana.

11 Na mataifa mengi watajiunga na Bwana

katika siku ile, nao watakuwa watu wangu;

nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa

Bwana wa majeshi amenituma kwako.

12 Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu

yake katika nchi takatifu, naye atachagua

Yerusalemu tena.

LUKA 2:32 Nuru ya kuwa mwangaza

wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako

Israeli.

MATENDO YA MITUME 13:46

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa

wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu

linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa

mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi

zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele,

angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi,

wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa

wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

ZABURIEN

Page 155: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

155

Nitakapowaondolea dhambi zao.

UFUNUO WA YOHANA 21:24 Na

mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; Zaburi 51:18; Matendo ya Mitume 10:45; Matendo ya Mitume 11:1,18; Matendo ya Mitume 13:42.

A06 Masiha ndiye Muumbaji.

ZABURI 102:25 Hapo mwanzo uliutia msingi

wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako.

26 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu

Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama

mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika.

27 Lakini Wewe U Yeye yule; Na miaka yako

haitakoma.

LUKA 21:33 Mbingu na nchi zitapita,

lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

WAEBRANIA 1:10 Na tena, Wewe,Bwana,hapo

mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu

ni kazi za mikono yako;

11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;

Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12 Na kama mavazi utazizinga, nazo

zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na

miaka yako haitakoma.

WAEBRANIA 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana

na leo na hata milele.

Ona pia: 2 Petro 3:7-12; Ufunuo wa Yohana 20:11; Ufunuo wa Yohana 21:1.

E21 Masiha atasamehe dhambi.

ZABURI 103:3 Akusamehe maovu yako

yote, Akuponya magonjwa yako yote,

12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

ZABURI 147:3 Huwaponya waliopondeka

moyo, Na kuziganga jeraha zao.

ISAYA 33:24 Wala hapana mwenyeji

atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao

humo watasamehewa uovu wao.

ISAYA 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi

niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu

mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi

zako.

ISAYA 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa

yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu

ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa

kupigwa kwake sisi tumepona.

MARKO 2:5 Naye Yesu, alipoiona imani

yao, akamwambia yule mwenye kupooza,

Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

MARKO 2:10 Lakini mpate kujua ya

kwamba Mwana wa Adamu anayo amri

duniani ya kusamehe dhambi, (hapo

amwambia yule mwenye kupooza),

ZABURIEN

Page 156: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

156

11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako

uende nyumbani kwako.

YAKOBO 5:15 Na kule kuomba kwa imani

kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana

atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi,

atasamehewa.

1 YOHANA 1:7 bali tukienenda nuruni,

kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana

sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana

wake, yatusafisha dhambi yote.

E11 Masiha atapeana uzima wa milele.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

ZABURI 103:4 Aukomboa uhai wako na

kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,

1 WAKORINTHO 9:25 Na kila

ashindanaye katika michezo hujizuia

katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi

wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee

taji isiyoharibika.

2 WAKORINTHO 1:10 aliyetuokoa sisi

katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa;

ambaye tumemtumaini kwamba atazidi

kutuokoa;

WAGALATIA 3:13 Kristo alitukomboa katika

laana ya torati, kwa kuwa alifanywa

laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

2 TIMOTHEO 4:8 baada ya hayo nimewekewa

taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu

mwenye haki, atanipa siku ile; wala si

mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda

kufunuliwa kwake.

YAKOBO 1:12 Heri mtu astahimiliye

majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa

ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia

wampendao.

1 PETRO 5:4 Na Mchungaji mkuu

atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya

utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 2:10 Usiogope

mambo yatakayokupata; tazama, huyo

Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili

mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku

kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami

nitakupa taji ya uzima.

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

ZABURI 103:5 Aushibisha mema uzee

wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;

2 WAKORINTHO 4:16 Kwa hiyo hatulegei;

bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa,

lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya

siku kwa siku.

1 TIMOTHEO 6:17 Walio matajiri wa

ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune,

ZABURIEN

Page 157: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

157

wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali

wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa

wingi ili tuvitumie kwa furaha.

B15 Masiha atajawa na rehema.

ZABURI 103:13 Kama vile baba

awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana

anavyowahurumia wamchao.

MATENDO YA MITUME 13:26 Ndugu

zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao

miongoni mwenu wanaomcha Mungu,

kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.

Ona pia: Isaya 63:15; Yeremia 31:9,20; Malaki 3:16,17.

B22 Uzuri wa Mungu na Masiha.

ZABURI 103:11 Maana mbingu zilivyoinuka

juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu

kwa wamchao.

17 Bali fadhili za Bwana zina wamchao Tangu

milele hata milele, Na haki yake ina wana wa

wana;

ISAYA 54:8 Kwa ghadhabu ifurikayo

nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini

kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema

Bwana, Mkombozi wako.

YEREMIA 31:3 Bwana alinitokea zamani,

akisema, Naam nimekupenda kwa upendo

wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa

fadhili zangu.

HOSEA 2:20 Nami nitakuposa kwa

uaminifu; nawe utamjua Bwana.

WARUMI 2:4 Au waudharau wingi

wa wema wake na ustahimili wake na

uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa

Mungu wakuvuta upate kutubu?

WARUMI 11:22 Tazama, basi, wema na ukali

wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali,

bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa

katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe

utakatiliwa mbali.

2 WAKORINTHO 6:6 katika kuwa safi,

katika elimu, katika uvumilivu, katika utu

wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo

usio unafiki;

2 WAKORINTHO 10:1 Basi, mimi Paulo

mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu

wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu

nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo

ni mwenye ujasiri kwenu;

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

WAEFESO 2:7 ili katika zamani zinazokuja

audhihirishe wingi wa neema yake upitao

kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika

Kristo Yesu.

WAKOLOSAI 3:12 Basi, kwa kuwa mmekuwa

wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao,

jivikeni moyo wa rehema, utu wema,

unyenyekevu, upole, uvumilivu,

TITO 3:4 Lakini wema wake Mwokozi wetu

ZABURIEN

Page 158: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

158

Mungu, na upendo wake kwa wanadamu,

ulipofunuliwa, alituokoa;

5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Ona pia: Hesabu 14:19; 2 Samweli 7:15; 2 Samweli 22:51; 1 Mambo ya Nyakati 16:34,41; 1 Mambo ya Nyakati 17:13; 2

Mambo ya Nyakati 20:21; Nehemia 1:5; Nehemia 13:22; Zaburi 5:7; 6:4; 13:5; 18:50; 21:7; 25:6,7,10; 26:3; 31:7,16,21; 32:10;

33:5,18,22; 36:5,7,10; 42:7; 44:26; 51:1; 52:2,7; 57:3,10; 59:10,16,17; 61:7; 62:12; 63:3; 66:20; 69:13,16; 77:8; 85:7,10; 86:5,13,15;

88:11; 89:2,14,24,28,33,49; 90:14; 92:2; 94:18; 98:3; 100:5; 101:1; 103:4,8,11; 106:1,7,45; 107:1,8,15,21,31,43; 108:4; 109:21,26; 115:1; 117:1; 118:1-4,29; 119:41,64,76,88,90,124,149,159; 130:7; 136:(26

x); 138:2,8; 143:8,12; 144:2; 145:8; 147:11; Mithali 3:3; Mithali 16:6; Isaya 16:5; Isaya 54:10; Isaya 63:7; Yeremia 3:12; Yeremia

16:5; Yeremia 32:18; Yeremia 33:11; Maombolezo 3:22,32; Yoeli 2:13; Yona 4:2; Mika 7:18,20; Zekaria 7:9; Yohana 3:16; Waefeso 2:3-5.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

ZABURI 103:22 Mhimidini Bwana, enyi

matendo yake yote, Mahali pote pa milki

yake. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

UFUNUO WA YOHANA 5:12 wakisema

kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo

aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na

hekima na nguvu na heshima na utukufu na

baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu

ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na

vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

14 Na wale wenye uhai wanne wakasema,

Amina. Na wale wazee wakaanguka,

wakasujudu.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 107:1 Mshukuruni Bwana kwa

kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni

za milele.

2 Na waseme hivi waliokombolewa na Bwana,

Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.

3 Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki

na magharibi, kaskazini na kusini.

ZABURI 107:4-16

YEREMIA 23:6 Katika siku zake Yuda

ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina

lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

LUKA 1:68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa

Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na

kuwakomboa.

LUKA 1:74 Ya kwamba atatujalia sisi,

Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na

kumwabudu pasipo hofu,

LUKA 24:21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya

kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli.

Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu

yalipotendeka mambo hayo;

WAGALATIA 3:13 Kristo alitukomboa katika

laana ya torati, kwa kuwa alifanywa

laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

1 WATHESALONIKE 1:10 na kumngojea

Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye

alimfufua katika wafu, naye ni Yesu,

mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.

TITO 2:14 ambaye alijitoa nafsi yake

ZABURIEN

Page 159: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

159

kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi

yote, na kujisafishia watu wawe milki yake

mwenyewe, wale walio na juhudi katika

matendo mema.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 31:5; Isaya 43:1; 2 Wakorintho 1:10; 1 Petro 1:18; Yuda 1:5.

B07 Uweza wa Yote wa Masiha.

ZABURI 107:25 Maana husema, akavumisha

upepo wa dhoruba, Ukayainua juu mawimbi

yake.

26 Wapanda mbinguni, watelemka vilindini,

Nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya.

27 Wayumba-yumba, wapepesuka kama mlevi,

Akili zao zote zawapotea.

28 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao,

Akawaponya na shida zao.

29 Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi

yake yakanyamaza.

MATHAYO 8:24 Kukawa msukosuko mkuu

baharini, hata chombo kikafunikizwa na

mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.

25 Wanafunzi wake wakamwendea,

wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe,

tunaangamia.

26 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga,

enyi wa imani haba? Mara akaondoka,

akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari

kuu.

Ona pia: Yona 1:4; Marko 4:39-41; Luka 8:23-25.

F07 Masihtaka na majaribu ya Masiha.

ZABURI 109:1 Ee Mungu wa sifa zangu,

usinyamaze,

2 Kwa maana wamenifumbulia kinywa;

Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila,

Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.

3 Naam, kwa maneno ya chuki

wamenizunguka, Wamepigana nami bure.

4 Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,

Ijapokuwa naliwaombea.

5 Wamenichukuza mabaya badala ya mema,

Na chuki badala ya upendo wangu.

MATHAYO 26:59 Basi wakuu wa makuhani na

baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo

juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa

uongo wengi.

61 Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema,

Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la

Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama

akamwambia, Hujibu neno? Hawa

wanakushuhudia nini?

YOHANA 10:32 Yesu akawajibu, Kazi njema

nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba;

kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga

kwa mawe?

YOHANA 15:25 Lakini litimie lile neno

lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia

bure.

Ona pia: Zaburi 22:12; Zaburi 31:13; Zaburi 35:7,12; Zaburi 38:20; Zaburi 64:3,4; Zaburi 69:5; Zaburi 88:17,18; Zaburi 140:3.

ZABURIEN

Page 160: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

160

F05 Masiha atasalitiwa.

ZABURI 109:8 Siku zake na ziwe chache,

Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

MATENDO YA MITUME 1:20 Kwa

maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi,

Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo

mtu mwenye kukaa humo;

Ona pia: Mathayo 25:41; Luka 9:54-56; 13:27; 1 Wakorintho 16:22; Wagalatia 1:8; Ufunuo wa Yohana 6:10-17; Ufunuo wa Yohana

19:1-6.

F11 Mateso ya Masiha.

ZABURI 109:25 Nami nalikuwa laumu kwao,

Wanionapo hutikisa vichwa vyao.

MATHAYO 27:39 Nao waliokuwa wakipita

njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa

vichwa vyao, wakisema,

40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga

kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe

Mwana wa Mungu, shuka msalabani.

WARUMI 15:3 Kwa maana Kristo naye

hakujipendeza mwenyewe; bali kama

ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu

wewe yalinipata mimi.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

Ona pia: Zaburi 22:6,7; Zaburi 69:9-12,19-21; Waebrania 13:13.

B13 Mamlaka ya Masiha.

E14 Masiha atashinda kifo na giza.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H07 Masiha ataketi kwenye mkono wa kulia

wa Mungu.

ZABURI 110:1 Neno la Bwana kwa Bwana

wangu, Uketi mkono wangu wa kuume,

Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya

miguu yako.

2 Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya

nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako;

MATHAYO 22:41 Na Mafarisayo

walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema,

Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa

Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika

Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi

mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo

adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni

mwanawe?

46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala

hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile

kumwuliza neno tena.

MATENDO YA MITUME 2:33 Basi yeye,

akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume

wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi

ZABURIEN

Page 161: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

161

ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki

mnachokiona sasa na kukisikia.

34 Maana Daudi hakupanda mbinguni;

bali yeye mwenyewe anasema, Bwana

alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa

mkono wangu wa kuume.

35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya

miguu yako.

1 WAKORINTHO 15:24 Hapo ndipo

mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme

wake; atakapobatilisha utawala wote, na

mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke

maadui wake wote chini ya miguu yake.

26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya

miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote

vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye

aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake,

ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa

chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili

kwamba Mungu awe yote katika wote.

WAEFESO 1:20 aliotenda katika Kristo

alipomfufua katika wafu, akamweka mkono

wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka,

na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo,

wala si ulimwenguni humu tu, bali katika

ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,

akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa

ajili ya kanisa; ambalo

23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake

anayekamilika kwa vyote katika vyote.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao wa utukufu wake

na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote

kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa

kuume wa Ukuu huko juu;

WAEBRANIA 1:13 Je! Yuko malaika

aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono

wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui

zako chini ya nyayo zako?

WAEBRANIA 10:13 tangu hapo

akingojea hata adui zake wawekwe kuwa

chini ya miguu yake.

14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata

milele hao wanaotakaswa.

Ona pia: #1; Marko 12:35-37; Marko 16:19; Luka 20:41-44; Matendo ya Mitume 2:34-37; Waebrania 12:2; 1 Petro 3:22.

B07 Uweza wa Yote wa Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 110:3 Watu wako wanajitoa kwa

hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa

utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao

umande wa ujana wako.

MATENDO YA MITUME 2:41 Nao

waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku

ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

MATENDO YA MITUME 19:20 Hivyo

ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na

kushinda kwa nguvu.

ZABURIEN

Page 162: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

162

MATENDO YA MITUME

21:20 Nao waliposikia wakamtukuza

Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu,

unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo

elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa

ajili ya torati.

WAEFESO 1:4 kama vile alivyotuchagua

katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya

ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio

na hatia mbele zake katika pendo.

WAFILIPI 2:13 Kwa maana ndiye Mungu

atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na

kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake

jema.

WAEBRANIA 13:21 awafanye ninyi

kuwa wakamilifu katika kila tendo jema,

mpate kuyafanya mapenzi yake, naye

akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake,

kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na

milele. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

Ona pia: #1; #2; #4; Matendo ya Mitume 1:8; Matendo ya Mitume 4:4,30-35; 2 Wakorintho 8:3; 2 Wakorintho 13:4; 1

Wathesalonike 4:7; Tito 2:14.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

ZABURI 110:4 Bwana ameapa, Wala

hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa

mfano wa Melkizedeki.

WAEBRANIA 5:5 Vivyo hivyo Kristo naye

hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani

mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe

mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

6 kama asemavyo mahali pengine,

Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa

Melkizedeki.

WAEBRANIA 6:20 alimoingia Yesu kwa

ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa

kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa

Melkizedeki.

WAEBRANIA 7:21 (maana wale walifanywa

makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja

na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana

ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani wa

milele;)

22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini

wa agano lililo bora zaidi.

WAEBRANIA 7:28 Maana torati yawaweka

wanadamu walio na unyonge kuwa

makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo

kilichokuja baada ya torati limemweka

Mwana, aliyekamilika hata milele.

Ona pia: Mwanzo 14:18; Zekaria 6:13; Waebrania 5:7-10; Waebrania 7:1-28; Waebrania 10:1-11.

ZABURIEN

Page 163: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

163

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 110:5 Bwana yu mkono wako wa

kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu

yake.

6 Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi

mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi.

MARKO 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya

kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni,

akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

YOHANA 5:22 Tena Baba hamhukumu mtu

ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;

MATENDO YA MITUME 2:34 Maana

Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye

mwenyewe anasema, Bwana alimwambia

Bwana wangu, Keti upande wa mkono

wangu wa kuume.

35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya

miguu yako.

36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini

ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo

mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

WAEBRANIA 10:12 Lakini huyu,

alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi

dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi

mkono wa kuume wa Mungu;

13 tangu hapo akingojea hata adui zake

wawekwe kuwa chini ya miguu yake.

14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata

milele hao wanaotakaswa.

Ona pia: #1; #4; #6; Zaburi 16:8; Isaya 2:4; Isaya 42:1; Isaya 51:5; Matendo ya Mitume 7:56.

F11 Mateso ya Masiha.

G03 Kuinuliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

ZABURI 110:7 Atakunywa maji ya mto

njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.

ZABURI 27:6 Na sasa kichwa

changu kitainuka Juu ya adui zangu

wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za

shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam,

nitamhimidi Bwana.

MATHAYO 20:22 Yesu akajibu akasema,

Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza

kunywea kikombe nitakachonywea mimi?

Wakamwambia, Twaweza.

MATHAYO 26:42 Akaenda tena mara ya pili,

akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa

haiwezekani kikombe hiki kiniepuke

nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.

LUKA 24:26 Je! Haikumpasa Kristo

kupata mateso haya na kuingia katika

utukufu wake?

Ona pia: Zaburi 3:3; Zaburi 102:9; Isaya 53:11,12; Yohana 18:11; Wafilipi 2:7-11; Waebrania 2:9,10; 1 Petro 1:11.

B15 Masiha atajawa na rehema.

E09 Uadilifu wa Masiha.

ZABURI 112:4 Nuru huwazukia wenye adili

gizani; Ana fadhili na huruma na haki.

LUKA 6:36 Basi, iweni na huruma,

kama Baba yenu alivyo na huruma.

YOHANA 12:46 Mimi nimekuja ili niwe nuru

ZABURIEN

Page 164: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

164

ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi

asikae gizani.

2 WAKORINTHO 8:8 Sineni ili

kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine

nijaribu unyofu wa upendo wenu.

9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu

Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili

yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi

mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

1 YOHANA 2:29 Kama mkijua ya kuwa yeye

ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye

haki amezaliwa na yeye.

Ona pia: Wakolosai 1:12,13; Yohana 3:7,10.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

F03 Masiha atakataliwa.

ZABURI 118:22 Jiwe walilolikataa waashi

Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

23 Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu

machoni petu.

24 Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,

Tutashangilia na kuifurahia.

ISAYA 28:16 kwa ajili ya hayo Bwana,

MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka

jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe

lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani,

msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya

haraka.

MATHAYO 21:42 Yesu akawaambia,

Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe

walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe

kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa

Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

LUKA 20:17 Akawakazia macho akasema,

Maana yake nini basi neno hili lililoandikwa,

Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa

jiwe kuu la pembeni?

MATENDO YA MITUME 2:23 mtu

huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu

lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu

zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono

ya watu wabaya, mkamwua;

MATENDO YA MITUME 3:13 Mungu

wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo,

Mungu wa baba zetu, amemtukuza

mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi

mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato,

alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

MATENDO YA MITUME 4:10 jueni

ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa

kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye

ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua

katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu

anasimama ali mzima mbele yenu.

11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi

waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la

pembeni.

WARUMI 9:33 kama ilivyoandikwa, Tazama,

naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na

mwamba uangushao; Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

WAEFESO 2:20 Mmejengwa juu ya msingi

wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu

mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja

ZABURIEN

Page 165: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

165

kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

1 PETRO 2:6 Kwa kuwa imeandikwa

katika maandiko Tazama, naweka katika

Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule,

lenye heshima, Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

Ona pia: Danieli 2:34; Zekaria 3:9; Zekaria 4:7; Zekaria 12:3; Mathayo 28:1-8; Marko 12:10,11; Matendo ya Mitume 5:31,32; 1

Wakorintho 3:11; Waefeso 1:19-22; 1 Petro 2:4-8.

F02 Kuingia kwa Masiha Yerusalemu

kunatabiriwa.

ZABURI 118:26 Na abarikiwe yeye ajaye

kwa jina la Bwana; Tumewabarikia toka

nyumbani mwa Bwana.

27 Bwana ndiye aliye Mungu, Naye ndiye

aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa

kamba Pembeni mwa madhabahu.

MATHAYO 21:9 Na makutano waliotangulia,

na wale waliofuata, wakapaza sauti,

wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye

mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana;

Hosana juu mbinguni.

10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote

ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?

11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii,

Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

MATHAYO 23:39 Kwa maana nawaambia,

Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata

mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina

la Bwana.

LUKA 19:36 Na alipokuwa akienda

walitandaza nguo zao njiani.

37 Hata alipokuwa amekaribia matelemko

ya mlima wa Mizeituni, kundi zima la

wanafunzi wake walianza kufurahi na

kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya

matendo yote ya uwezo waliyoyaona,

38 wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye

kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na

utukufu huko juu.

YOHANA 12:13 wakatwaa matawi ya

mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki,

wakapiga makelele, Hosana! Ndiye

mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme

wa Israeli!

WAEFESO 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa

Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa

baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa

roho, ndani yake Kristo;

Ona pia: Marko 11:9,10.

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

ZABURI 119:97 Sheria yako naipenda mno

ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana

kutwa.

98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui

zangu, Kwa maana ninayo sikuzote.

99 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,

Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.

100 Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa

nimeyashika mausia yako.

101 Nimeiepusha miguu yangu na kila njia

mbaya, Ili nilitii neno lako.

102 Sikujiepusha na hukumu zako, Maana

Wewe mwenyewe umenifundisha.

103 Mausia yako ni matamu sana kwangu,

Kupita asali kinywani mwangu.

ZABURIEN

Page 166: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

166

MATHAYO 11:25 Wakati ule Yesu akajibu,

akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana

wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo

haya uliwaficha wenye hekima na akili,

ukawafunulia watoto wachanga.

LUKA 2:46 Ikawa baada ya siku tatu

wakamwona hekaluni, ameketi katikati

ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza

maswali.

47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu

zake na majibu yake.

YOHANA 3:2 Huyo alimjia usiku,

akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u

mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana

hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi

uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu

pamoja naye.

YOHANA 4:34 Yesu akawaambia, Chakula

changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake

aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

YOHANA 15:10 Mkizishika amri zangu,

mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi

nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa

katika pendo lake.

WARUMI 13:10 Pendo halimfanyii jirani

neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa

sheria.

1 YOHANA 2:5 Lakini yeye alishikaye

neno lake, katika huyo upendo wa Mungu

umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua

ya kuwa tumo ndani yake.

1 YOHANA 5:3 Kwa maana huku ndiko

kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri

zake; wala amri zake si nzito.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 4:6-8; Yeremia 2:8; Yeremia 8:9; Yoeli 2:23; Mathayo 13:11; Mathayo 15:6-9,14; Waebrania

5:12.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ZABURI 129:3 Wakulima wamelima

mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu

mifuo yao.

ISAYA 50:6 Naliwatolea wapigao mgongo

wangu, na wang›oao ndevu mashavu yangu;

sikuficha uso wangu usipate fedheha na

kutemewa mate.

ISAYA 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa

yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu

ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa

kupigwa kwake sisi tumepona.

MATHAYO 20:19 kisha watampeleka kwa

Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga

mijeledi, na kumsulibisha; na siku ya tatu

atafufuka.

MATHAYO 27:26 Ndipo akawafungulia

Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi,

akamtoa ili asulibiwe.

Ona pia: Isaya 51:23; Marko 10:34; Marko 15:15; Luka 18:33.

ZABURIEN

Page 167: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

167

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 130:7 Ee Israeli, umtarajie Bwana;

Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake

kuna ukombozi mwingi.

8 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake

yote.

ZABURI 103:3 Akusamehe maovu yako

yote, Akuponya magonjwa yako yote,

4 Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji

ya fadhili na rehema,

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

LUKA 1:68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa

Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na

kuwakomboa.

WARUMI 3:24 wanahesabiwa haki bure

kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio

katika Kristo Yesu;

WARUMI 6:14 Kwa maana dhambi

haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi

chini ya sheria, bali chini ya neema.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

WAEFESO 1:7 Katika yeye huyo, kwa damu

yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya

dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.

TITO 2:14 ambaye alijitoa nafsi yake

kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi

yote, na kujisafishia watu wawe milki yake

mwenyewe, wale walio na juhudi katika

matendo mema.

WAEBRANIA 9:12 wala si kwa damu ya mbuzi

na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe

aliingia mara moja tu katika Patakatifu,

akiisha kupata ukombozi wa milele.

1 YOHANA 3:5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye

alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na

dhambi haimo ndani yake.

6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila

atendaye dhambi hakumwona yeye, wala

hakumtambua.

7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye;

atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo

na haki;

8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa

Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.

Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu

alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

Ona pia: #2; #3; Marko 15:31; Luka 2:38; Luka 21:28; Luka 24:21; 1 Wakorintho 1:30; Waefeso 1:14; Wakolosai 1:14.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 132:11 Bwana amemwapia Daudi

neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu,

Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka

katika kiti chako cha enzi.

12 Wanao wakiyashika maagano yangu, Na

shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao

nao wataketi Katika kiti chako cha enzi

milele.

ZABURIEN

Page 168: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

168

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 1:69 Ametusimamishia pembe ya

wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi

wake.

70 Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa

kinywa cha manabii wake watakatifu;

MATENDO YA MITUME 2:30 Basi

kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu

amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika

uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja

katika kiti chake cha enzi;

Ona pia: #1; #2; Zaburi 102:28; Isaya 59:21.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 132:13 Kwa kuwa Bwana

ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani

yake.

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu

ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya

Habili.

Ona pia: #1; Zaburi 68:16; Zaburi 78:68,69; Zaburi 87:2; Isaya 14:32.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

ZABURI 132:14 Hapo ndipo mahali pangu

pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana

nimepatamani.

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa

kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa

moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

YOHANA 14:23 Yesu akajibu, akamwambia,

Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na

Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake,

na kufanya makao kwake.

WAEBRANIA 4:3 Maana sisi tulioamini

tunaingia katika raha ile; kama vile

alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira

yangu, Hawataingia rahani mwangu:

Ona pia: #1; #2; Zaburi 68:16; Zaburi 76:1,2; Zaburi 132:8,9; Zaburi 135:21; Isaya 57:15; Isaya 66:1; Ezekieli 38:8; 43:7,9; 2

Wakorintho 6:16; Waebrania 4:1-11.

ZABURIEN

Page 169: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

169

E16 Masiha atabariki watu Wake.

ZABURI 132:15 Hakika nitavibariki vyakula

vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula.

MATHAYO 5:6 Heri wenye njaa na kiu ya

haki; Maana hao watashibishwa.

MATHAYO 6:32 Kwa maana hayo yote

Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu

wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo

yote.

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki

yake; na hayo yote mtazidishiwa.

MARKO 8:6 Akawaagiza mkutano waketi

chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru,

akaimega, akawapa wanafunzi wake

wawaandikie; wakawaandikia mkutano.

7 Walikuwa na visamaki vichache;

akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo

pia.

8 Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya

vipande vya mikate makanda saba.

9 Na watu waliokula wapata elfu nne.

Akawaaga.

LUKA 1:53 Wenye njaa amewashibisha

mema, Na wenye mali amewaondoa mikono

mitupu.

YOHANA 6:35 Yesu akawaambia, Mimi

ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu

hataona njaa kabisa, naye aniaminiye

hataona kiu kamwe.

MATENDO YA MITUME 2:44 Na wote

walioamini walikuwa mahali pamoja, na

kuwa na vitu vyote shirika,

45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa

navyo, na kuwagawia watu wote kama kila

mtu alivyokuwa na haja.

46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu

ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba

kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa

furaha na kwa moyo mweupe,

Ona pia: Zaburi 34:9,10; Isaya 33:16; Yeremia 31:14; Mathayo 14:19-21.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

ZABURI 132:16 Na makuhani wake

nitawavika wokovu, Na watauwa wake

watashangilia.

WAGALATIA 3:27 Maana ninyi nyote

mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

UFUNUO WA YOHANA 1:6 na

kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa

Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu

una Yeye hata milele na milele. Amina.

Ona pia: #1; #2; 2 Mambo ya Nyakati 6:41; Zaburi 132:9; Isaya 61:10; Ufunuo wa Yohana 3:5; Ufunuo wa Yohana 4:4; Ufunuo

wa Yohana 7:9-14; Ufunuo wa Yohana 20:6.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 132:17 Hapo nitamchipushia Daudi

pembe, Na taa nimemtengenezea masihi

wangu.

18 Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji

yake itasitawi.

LUKA 1:67 Na Zakaria, baba yake,

akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri,

ZABURIEN

Page 170: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

170

akisema,

68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa

kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.

69 Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika

mlango wa Daudi, mtumishi wake.

70 Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa

kinywa cha manabii wake watakatifu;

71 Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao

wote wanaotuchukia;

LUKA 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu

palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni

mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia

faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa

juu yake.

26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu

ya kwamba hataona mauti kabla ya

kumwona Kristo wa Bwana.

27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho;

na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu

ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa

desturi ya sheria,

28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi

mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako,

Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu

wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na

kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

LUKA 20:42 Maana, Daudi mwenyewe

asema katika chuo cha Zaburi, Bwana

alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono

wangu wa kuume,

43 Hata niwaweke adui zako Kuwa kiti cha

kuwekea miguu yako.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #5; Zaburi 21:8,9; Zaburi 109:29; Zaburi 148:14; Ezekieli 29:21.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 138:4 Ee Bwana, wafalme wote

wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia

maneno ya kinywa chako.

5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa

maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

ISAYA 49:22 Bwana MUNGU asema

hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono

wangu, na kuwatwekea kabila za watu

bendera yangu; nao wataleta wana wako

vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa

mabegani mwao.

23 Na wafalme watakuwa baba zako za

kulea, na malkia zao mama zako za kulea;

watainama mbele yako kifudifudi, na

kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe

utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena

waningojeao hawatatahayarika.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #5.

ZABURIEN

Page 171: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

171

B08 Ujuzi wa Yote wa Masiha.

ZABURI 139:1 Ee Bwana, umenichunguza

na kunijua.

2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka

kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea

mbali.

3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala

kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.

4 Maana hamna neno ulimini mwangu

Usilolijua kabisa, Bwana.

MATHAYO 9:4 Naye Yesu, hali akijua

mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza

maovu mioyoni mwenu?

MATHAYO 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno

lisilo maana, watakalolinena wanadamu,

watatoa hesabu ya neno hilo siku ya

hukumu.

37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa

haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

LUKA 9:47 Naye Yesu alipotambua

mawazo ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo

akamweka karibu naye,

LUKA 10:22 Akasema, Nimekabidhiwa

vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye

Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye

Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana

apenda kumfunulia.

YOHANA 2:24 Lakini Yesu hakujiaminisha

kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;

25 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu

kushuhudia habari za mwanadamu; kwa

maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo

ndani ya mwanadamu.

YOHANA 13:21 Naye alipokwisha kusema

hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia

akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja

wenu atanisaliti.

YOHANA 16:30 Sasa tumejua ya kuwa wewe

wafahamu mambo yote, wala huna haja

ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya

kwamba ulitoka kwa Mungu.

YOHANA 21:17 Akamwambia mara ya

tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro

alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara

ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana,

wewe wajua yote; wewe umetambua ya

kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha

kondoo zangu.

1 WAKORINTHO 4:5 Basi ninyi

msihukumu neno kabla ya wakati wake,

hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha

yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha

mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu

atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

WAEBRANIA 4:13 Wala hakuna kiumbe

kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu

vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake

yeye aliye na mambo yetu.

UFUNUO WA YOHANA 3:8 Nayajua

matendo yako. Tazama, nimekupa mlango

uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana

awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu

kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala

hukulikana jina langu.

Ona pia: Zaburi 17:3; Zaburi 44:21; Zaburi 94:11; Zaburi 121:3-8; Zaburi 139:23; Mithali 5:21; Mhubiri 12:14; Isaya 29:15; Isaya

37:28; Yeremia 12:3; Yeremia 17:9,10; Yeremia 23:24; Danieli 2:22; Malaki 3:16; Yohana 4:16-19,28.

ZABURIEN

Page 172: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

172

B09 Uwezo wa Masiha wa kuwa Kila Mahali.

ZABURI 139:7 Niende wapi nijiepushe

na roho yako? Niende wapi niukimbie uso

wako?

8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;

Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe

uko.

9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa

pande za mwisho za bahari;

10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na

mkono wako wa kuume utanishika.

MATHAYO 18:20 Kwa kuwa walipo wawili

watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami

nipo papo hapo katikati yao.

MATHAYO 28:20 na kuwafundisha kuyashika

yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi

nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu

wa dahari.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

YOHANA 14:20 Siku ile ninyi mtatambua ya

kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi

ndani yangu, nami ndani yenu.

WAKOLOSAI 1:17 Naye amekuwako kabla ya

vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika

yeye.

Ona pia: Yeremia 23:23,24; Mika 5:2; Ufunuo wa Yohana 21:2,3,10,22,23.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 145:10 Ee Bwana, kazi zako zote

zitakushukuru, Na wacha Mungu wako

watakuhimidi.

11 Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na

kuuhadithia uweza wako.

12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,

Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.

13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na

mamlaka yako ni ya vizazi vyote.

WAEFESO 3:7 Injili hiyo ambayo

nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya

kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa

kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.

8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo

wa watakatifu wote, nalipewa neema hii

ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo

usiopimika;

1 TIMOTHEO 1:17 Sasa kwa Mfalme

wa milele, asiyeweza kuona uharibifu,

asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe

heshima na utukufu milele na milele.

Amina.

WAEBRANIA 13:15 Basi, kwa njia

yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa

daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo

jina lake.

UFUNUO WA YOHANA 5:12 wakisema

kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo

aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na

hekima na nguvu na heshima na utukufu na

baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu

ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na

vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

ZABURIEN

Page 173: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

173

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu

una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi,

na Mwana-Kondoo.

11 Na malaika wote walikuwa wakisimama

pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao

wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao

wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha

enzi, wakamsujudu Mungu,

12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na

hekima na shukrani na heshima na uweza

na nguvu zina Mungu wetu hata milele na

milele. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

16 Na wale wazee ishirini na wanne waketio

mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao

wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia

Mungu

17 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana

Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako,

kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio

mkuu, na kumiliki.

UFUNUO WA YOHANA 12:10

Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa

kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme

wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo

wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki

wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za

Mungu wetu, mchana na usiku.

UFUNUO WA YOHANA 19:5 Sauti

ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema,

Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake

wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.

6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano

mengi, na kama sauti ya maji mengi, na

kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema,

Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu,

Mwenyezi, amemiliki.

Ona pia: #1; #2; 1 Wakorintho 15:21-28.

E05 Miujiza ya Masiha.

ZABURI 146:8 Bwana huwafumbua macho

waliopofuka; Bwana huwainua walioinama;

Bwana huwapenda wenye haki;

ISAYA 35:5 Ndipo macho ya vipofu

yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi

yatazibuliwa.

MATHAYO 9:30 Macho yao yakafumbuka.

Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema,

Angalieni hata mtu mmoja asijue.

MATHAYO 11:5 vipofu wanapata kuona,

viwete wanakwenda, wenye ukoma

wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu

wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa

ZABURIEN

Page 174: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

174

habari njema.

LUKA 18:42 Yesu akamwambia, Upewe

kuona; imani yako imekuponya.

YOHANA 9:10 Basi wakamwambia, Macho

yako yalifumbuliwaje?

11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya

tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda

Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa,

nikapata kuona.

MATENDO YA MITUME

26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza

waiache giza na kuielekea nuru, waziache na

nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu;

kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na

urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa

imani iliyo kwangu mimi.

WAEFESO 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe

nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi

lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake

katika watakatifu jinsi ulivyo;

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

Ona pia: Isaya 42:16,18.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

ZABURI 147:3 Huwaponya waliopondeka

moyo, Na kuziganga jeraha zao.

6 Bwana huwategemeza wenye upole,

Huwaangusha chini wenye jeuri.

MATHAYO 5:5 Heri wenye upole; Maana

hao watairithi nchi.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

Ona pia: 1 Petro 5:6.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 147:2 Bwana ndiye aijengaye

Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika

wa Israeli.

13 Maana ameyakaza mapingo ya malango

yako, Amewabariki wanao ndani yako.

14 Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,

Akushibishaye kwa unono wa ngano.

20 Hakulitendea taifa lo lote mambo kama

hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua.

Haleluya.

ISAYA 11:12 Naye atawatwekea mataifa

bendera, atawakutanisha watu wa Israeli

waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda

waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.

ZEKARIA 8:3 Bwana asema hivi, Mimi

nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya

Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji

wa kweli; na Mlima wa Bwana wa majeshi

utaitwa, Mlima mtakatifu.

ZABURIEN

Page 175: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

175

WARUMI 3:1 Basi Myahudi ana ziada

gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?

2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa

wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 102:13-16; Mathayo 16:18; Mathayo 19:13,14; Waefeso 1:10; Waefeso 2:17-19; Warumi 11:25.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZABURI 149:1 Haleluya. Mwimbieni Bwana

wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la

watauwa.

2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana

wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa

matari na kinubi wamwimbie.

4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake,

Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe

kwa sauti kuu vitandani mwao.

MATHAYO 21:5 Mwambieni binti Sayuni

Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-

punda, mtoto wa punda.

LUKA 19:38 wakasema, Ndiye mbarikiwa

Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani

mbinguni, na utukufu huko juu.

WAEBRANIA 2:12 akisema, Nitalihubiri jina

lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa

nitakuimbia sifa.

1 PETRO 1:8 Naye mwampenda,

ijapokuwa hamkumwona; ambaye

ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini;

na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka,

yenye utukufu,

1 PETRO 3:4 bali kuwe utu wa

moyoni usioonekana, katika mapambo

yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na

utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za

Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

UFUNUO WA YOHANA 19:6 Nikasikia

sauti kama sauti ya makutano mengi, na

kama sauti ya maji mengi, na kama sauti

ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya;

kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi,

amemiliki.

Ona pia: #1; #2; Kumbukumbu la Torati 7:6,7; 1 Samweli 12:22; Zaburi 22:22,25; Zaburi 33:2,3; Zaburi 96:1; Zaburi 98:1; Zaburi 100:1-3; Zaburi 111:1; Zaburi 116:18; Zaburi 135:3,4; Zaburi 144:9;

Zaburi 150:4; Isaya 42:10; Isaya 54:5; Isaya 62:4,5; 1 Petro 5:5.

ZABURIEN

Page 176: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

176

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ZABURI 149:6 Sifa kuu za Mungu na ziwe

vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili

mikononi mwao.

7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu

juu ya kabila za watu.

8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

Na wakuu wao kwa pingu za chuma.

9 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo

ndiyo heshima ya watauwa wake wote.

Haleluya.

ZEKARIA 14:17 Tena itakuwa, ya kwamba

mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo

duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili

kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi,

mvua haitanyesha kwao.

18 Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala

hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako

tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa,

wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.

19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya

mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu

ya Vibanda.

1 WAKORINTHO 6:2 Au hamjui

ya kwamba watakatifu watauhukumu

ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu

utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili

kukata hukumu zilizo ndogo?

3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika,

basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?

WAEBRANIA 4:12 Maana Neno la Mungu li

hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko

upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na

viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi

ya moyo.

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 3:21 Yeye

ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami

katika kiti changu cha enzi, kama mimi

nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba

yangu katika kiti chake cha enzi.

Ona pia: #1; #6; Zaburi 96:14; Zaburi 145:3-5; Zaburi 148:14; Danieli 7:18,22; Luka 2:14; Ufunuo wa Yohana 19:11-21.

ZABURIEN

Page 177: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

177

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

MITHALI 1:23 Geukeni kwa ajili ya maonyo

yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu,

Na kuwajulisheni maneno yangu.

YOELI 2:28 Hata itakuwa, baada ya hayo,

ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya

wote wenye mwili; na wana wenu, waume

kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota

ndoto, na vijana wenu wataona maono;

ZEKARIA 12:10 Nami nitawamwagia watu

wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa

Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao

watamtazama yeye ambaye walimchoma;

nao watamwombolezea, kama vile mtu

amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao

wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile

mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa

wake wa kwanza.

MATENDO YA MITUME 2:4 Wote

wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza

kusema kwa lugha nyingine, kama Roho

alivyowajalia kutamka.

MATENDO YA MITUME 2:38 Petro

akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila

mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate

ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea

kipawa cha Roho Mtakatifu.

Ona pia: Isaya 32:15.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

D01 Kupakwa kwa mafuta kwa Masiha.

MITHALI 8:22 Bwana alikuwa nami katika

mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo

yake ya kale.

23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla

haijawako dunia.

24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,

Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa

maji.

25 Kabla milima haijawekwa imara, Kabla ya

vilima nalizaliwa.

26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde

Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;

27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;

Alipopiga duara katika uso wa bahari;

28 Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;

Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;

29 Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji

yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi

ya nchi;

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye

hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao

ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

YOHANA 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze

mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule

niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya

ulimwengu kuwako.

YOHANA 17:24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate

na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa

MITHALI

Page 178: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

178

maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

WAKOLOSAI 1:15 naye ni mfano wa Mungu

asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa

viumbe vyote.

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,

vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,

vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa

ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au

mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia

yake, na kwa ajili yake.

17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu

vyote hushikana katika yeye.

18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha

kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa

wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe

mtangulizi katika yote.

19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu

wote ukae;

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao wa utukufu wake

na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote

kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa

kuume wa Ukuu huko juu;

4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri

jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.

5 Kwa maana alimwambia malaika yupi

wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo

nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake

baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Ona pia: Mwanzo 1:26; Zaburi 2:6; Mika 5:2; Waefeso 1:10,11; Yohana 1:1,2.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

MITHALI 8:29 Alipoipa bahari mpaka

wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake;

Alipoiagiza misingi ya nchi;

30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi

wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku;

Nikifurahi daima mbele zake;

31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu; Na

furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.

MATHAYO 3:16 Naye Yesu alipokwisha

kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na

tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona

Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija

juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema,

Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,

ninayependezwa naye.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye

hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

YOHANA 1:18 Hakuna mtu aliyemwona

Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana

pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu

ndiye aliyemfunua.

YOHANA 4:34 Yesu akawaambia, Chakula

changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake

aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

YOHANA 5:19 Mwana hawezi kutenda neno

mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba

analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye,

ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.

MITHALI

Page 179: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

179

20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye

humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe;

hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo

atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.

Ona pia: Zaburi 40:6-8; Isaya 42:1; Mathayo 17:5; Yohana 12:28; Yohana 13:1; Yohana 16:28; 2 Wakorintho 8:9.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

MITHALI 30:4 Ni nani aliyepanda

mbinguni na kushuka chini? Ni nani

aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni

nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake?

Ni nani aliyefanya imara ncha zote za

nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la

mwanawe, kama wajua?

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

YEREMIA 23:6 Katika siku zake Yuda

ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina

lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

YOHANA 1:18 Hakuna mtu aliyemwona

Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana

pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu

ndiye aliyemfunua.

YOHANA 3:13 Wala hakuna mtu aliyepaa

mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka

mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

WAEFESO 4:9 Basi neno hilo, Alipaa,

maana yake nini kama siyo kusema kwamba

yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini

za nchi?

10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana

kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 30:3; Waamuzi 13:18; Ayubu 38:4; Zaburi 2:7; Yeremia 7:14; Mathayo 1:21-23; Yohana 6:46;

Warumi 10:6,7.

MITHALI

Page 180: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

180

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

WIMBO ULIO BORA 5:16 Kinywa chake

kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana

pia pia. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu

rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu.

ZABURI 45:1 Moyo wangu umefurika kwa

neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia

mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya

mwandishi mstadi.

YOHANA 3:29 Aliye naye bibi arusi ndiye

bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi,

yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia

sana sauti yake bwana arusi.

WAGALATIA 2:20 Nimesulibiwa pamoja na

Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali

Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio

nao sasa katika mwili, ninao katika imani

ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda,

akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

1 YOHANA 4:16 Nasi tumelifahamu pendo

alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini.

Mungu ni upendo, naye akaaye katika

pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu

hukaa ndani yake.

Ona pia: Wimbo Ulio Bora 1:2; Wimbo Ulio Bora 2:16; Wimbo Ulio Bora 6:3; Mathayo 11:19; Mathayo 26:50; Luka 7:34; Yakobo

2:23.

WIMBO ULIO BORA

Page 181: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

181

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 2:2 Na itakuwa katika siku

za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote

watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake maana katika Sayuni

itatoka sheria, na neno la Bwana katika

Yerusalemu.

ZABURI 22:27 Miisho yote ya dunia

itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana;

Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

28 Maana ufalme una Bwana, Naye ndiye

awatawalaye mataifa.

ISAYA 49:22 Bwana MUNGU asema

hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono

wangu, na kuwatwekea kabila za watu

bendera yangu; nao wataleta wana wako

vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa

mabegani mwao.

23 Na wafalme watakuwa baba zako za

kulea, na malkia zao mama zako za kulea;

watainama mbele yako kifudifudi, na

kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe

utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena

waningojeao hawatatahayarika.

YEREMIA 3:17 Wakati ule watauita

Yerusalemu kiti cha enzi cha Bwana;

na mataifa yote watakusanyika huko

Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana; wala

hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo

wao mbaya.

ZEKARIA 8:20 Bwana wa majeshi asema

hivi, Itatokea halafu ya kwamba watakuja

mataifa na wenyeji wa miji mingi;

21 wenyeji wa mji huu watauendea mji huu,

wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka

tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta

Bwana wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.

22 Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa

hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta

Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za

Bwana.

23 Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo

watu kumi, wa lugha zote za mataifa,

wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye

Myahudi; naam, wataushika wakisema,

Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana

tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.

YOHANA 6:45 Imeandikwa katika manabii,

Na wote watakuwa wamefundishwa na

Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa

Baba huja kwangu.

MATENDO YA MITUME 1:8 Lakini

mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu

Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi

wangu katika Yerusalemu, na katika

Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho

wa nchi.

WARUMI 15:18 Maana sitathubutu kutaja

neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu,

Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa

tendo,

1 YOHANA 2:27 Nanyi, mafuta yale

mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu,

wala hamna haja ya mtu kuwafundisha;

ISAYA

Page 182: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

182

lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha

habari za mambo yote, tena ni kweli wala si

uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni

ndani yake.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 12:10

Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa

kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme

wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo

wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki

wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za

Mungu wetu, mchana na usiku.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

UFUNUO WA YOHANA 21:10

Akanichukua katika Roho mpaka mlima

mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji

mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka

mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

Ona pia: Zaburi 2:8; Zaburi 72:8,11,17-19; Zaburi 86:9; Zaburi 89:15-17; Zaburi 110:2; Isaya 2:2,3; Isaya 11:10; Isaya 27:15; Isaya 30:29; Isaya 49:6,7; Isaya 50:4,5; Isaya 51:4,5; Isaya 54:13; Isaya 55:5; Isaya 60:3-14; Yeremia 16:19; Yeremia 31:6; Yeremia 50:4,5; Danieli 2:44,45; Danieli 7:14,18,22,27; Hosea 2:23; Amosi 9:11,12;

Mika 4:1-3; Sefania 3:9,10; Zekaria 2:11; Zekaria 8:3; Zekaria 14:9; Malaki 1:11; Malaki 3:12; Matendo ya Mitume 13:46-48;

Warumi 10:18; Ufunuo wa Yohana 20.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 2:4 Naye atafanya hukumu

katika mataifa mengi, atawakemea watu wa

kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe

majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa

halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala

hawatajifunza vita tena kamwe.

ISAYA 60:18 Jeuri haitasikiwa tena katika

nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa

mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako,

Wokovu, Na malango yako, Sifa.

ZEKARIA 9:10 Na gari la vita nitaliondoa

liwe mbali na Efraimu, na farasi awe

mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita

utaondolewa mbali; naye atawahubiri

mataifa yote habari za amani; na mamlaka

yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na

toka Mto hata miisho ya dunia.

YOHANA 5:22 Tena Baba hamhukumu mtu

ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;

23 ili watu wote wamheshimu Mwana

kama vile wanavyomheshimu Baba.

Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba

aliyempeleka.

MATENDO YA MITUME 17:31 Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu

walimwengu kwa haki, kwa mtu yule

ISAYA

Page 183: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

183

aliyemchagua; naye amewapa watu wote

uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua

katika wafu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

Ona pia: 1 Samweli 2:10; Zaburi 46:9; Zaburi 72:3-7; Zaburi 82:8; Zaburi 96:13; Zaburi 110:6; Isaya 9:7; Isaya 11:3-9; Isaya 60:17; Hosea 2:19; Yoeli 3:10; Mika 4:3; Ufunuo wa Yohana 20.

B21 Masiha ndiye Nuru.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 2:5 Enyi wa nyumba ya Israeli,

njoni, twende katika nuru ya Bwana.

ISAYA 30:26 Na tena nuru ya mwezi

itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua

itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku

saba, katika siku ile Bwana atakapofunga

mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la

jeraha yao.

ISAYA 49:6 naam, asema hivi, Ni neno

dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili

kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza

watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo

nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa

wokovu wangu hata miisho ya dunia.

LUKA 1:79 Kuwaangaza wakaao katika

giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu

yetu kwenye njia ya amani.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

YOHANA 12:35 Basi Yesu akawaambia,

Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo.

Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza

lisije likawaweza; maana aendaye gizani

hajui aendako.

36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo

aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha

wasimwone.

WARUMI 13:12 Usiku umeendelea sana,

mchana umekaribia, basi na tuyavue

matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.

WAEFESO 5:8 Kwa maana zamani ninyi

mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru

katika Bwana; enendeni kama watoto wa

nuru,

9 kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema

wote na haki na kweli;

1 WATHESALONIKE 5:5 Kwa kuwa ninyi

nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa

mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali

tukeshe, na kuwa na kiasi.

1 YOHANA 1:7 bali tukienenda nuruni,

kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana

sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana

wake, yatusafisha dhambi yote.

ISAYA

Page 184: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

184

UFUNUO WA YOHANA 21:23 Na mji

ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,

kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru,

na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

Ona pia: Zaburi 18:29; Zaburi 89:15; Isaya 2:3; Isaya 42:6,16; Isaya 50:10; Isaya 51:4; Isaya 60:1,3,19,20; Zekaria 14:6,7.

A07 Atakuwa Masiha wa Israeli.

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

E16 Masiha atabariki watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 4:2 Siku hiyo chipukizi la Bwana

litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya

nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza,

kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.

YEREMIA 23:5 Tazama siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi

Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme,

atatenda kwa hekima, naye atafanya

hukumu na haki katika nchi.

6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli

atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni

hili, Bwana ni haki yetu.

YOELI 3:18 Tena itakuwa siku ile, ya

kwamba milima itadondoza divai tamu, na

vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote

vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi

itatokea katika nyumba ya Bwana, na

kulinywesha bonde la Shitimu.

ZEKARIA 6:12 ukamwambie, ukisema,

Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba,

Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni

Chipukizi; naye atakua katika mahali pake,

naye atalijenga hekalu la Bwana.

13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye

atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki

katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na

kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri

la amani litakuwa kati ya hao wawili.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 15:5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni

matawi, akaaye ndani yangu nami ndani

yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi

ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

UFUNUO WA YOHANA 22:2 katikati

ya njia kuu yake. Na upande huu na upande

huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima,

uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye

kutoa matunda yake kila mwezi; na majani

ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: #1; #2; #3; Mathayo 24:22; Yohana 1:14; Yohana 15:2-4,8,16; 2 Wakorintho 4:6; Wakolosai 1:10; 2 Petro 1:16; Ufunuo

wa Yohana 7:9-14.

ISAYA

Page 185: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

185

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 4:3 Tena itakuwa ya kwamba

yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye

aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa

mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa

miongoni mwa hao walio hai ndani ya

Yerusalemu;

YOELI 3:16 Naye Bwana atanguruma

toka Sayuni, atatoa sauti yake toka

Yerusalemu; na mbingu na nchi

zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio

la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.

17 Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi

ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni,

mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu

utakapokuwa mtakatifu, wala wageni

hawatapita tena ndani yake kamwe.

ZEKARIA 14:20 Siku hiyo katika njuga

za farasi yataandikwa maneno haya,

WATAKATIFU KWA Bwana; navyo vyombo

vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana

vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya

madhabahu.

21 Naam, kila chombo katika Yerusalemu,

na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa

Bwana wa majeshi; nao wote watoao

dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na

kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo

hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya

nyumba ya Bwana wa majeshi.

WARUMI 11:16 Tena malimbuko yakiwa

matakatifu, kadhalika na donge lote; na

shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEFESO 1:4 kama vile alivyotuchagua

katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya

ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio

na hatia mbele zake katika pendo.

WAEFESO 5:26 ili makusudi alitakase na

kulisafisha kwa maji katika neno;

27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila

wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali

liwe takatifu lisilo na mawaa.

WAEBRANIA 12:14 Tafuteni kwa

bidii kuwa na amani na watu wote, na huo

utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona

Bwana asipokuwa nao;

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

UFUNUO WA YOHANA 3:5 Yeye

ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe,

wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu

cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za

Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

UFUNUO WA YOHANA 13:8 Na watu

wote wakaao juu ya nchi watamsujudu,

kila ambaye jina lake halikuandikwa katika

kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo,

aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya

dunia.

ISAYA

Page 186: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

186

UFUNUO WA YOHANA 17:8 Yule

mnyama uliyemwona alikuwako, naye

hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka

kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na

hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa

majina yao katika kitabu cha uzima

tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu,

watastaajabu wamwonapo yule mnyama,

ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye

atakuwako.

UFUNUO WA YOHANA 20:15 Na iwapo

mtu ye yote hakuonekana ameandikwa

katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile

ziwa la moto.

UFUNUO WA YOHANA 21:27 Na ndani

yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho

kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na

uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu

cha uzima cha Mwana-Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 22:15 Huko

nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na

wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila

mtu apendaye uongo na kuufanya.

Ona pia: #1; #2; Kutoka 32:32,33; Kumbukumbu la Torati 12:7,12; Ezekieli 13:9; Ezekieli 43:12; Ezekieli 44:9; Zekaria 1:17; Mathayo 21:12,13; Luka 10:20; Yohana 17:17; Matendo ya Mitume 13:48; 1 Wakorintho 3:16; 1 Wakorintho 6:9-11; Waefeso 2:19-22; Wafilipi

4:3; Wakolosai 3:12; 1 Petro 2:9; Ufunuo wa Yohana 18:11-15.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 4:4 hapo Bwana atakapokuwa

ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni

na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati

yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya

kuteketeza.

5 Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na

juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba

wingu na moshi wakati wa mchana, na

mwangaza wa miali ya moto wakati wa

usiku; kwa maana juu ya utukufu wote

itatandazwa sitara.

6 Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati

wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa

mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa

tufani na mvua.

ZABURI 87:2 Bwana ayapenda malango ya

Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo.

3 Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa

Mungu.

ISAYA 31:5 Kama ndege warukao,

Bwana wa majeshi ataulinda Yerusalemu;

ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na

kuuhifadhi.

ISAYA 33:20 Angalia Sayuni, mji wa

sikukuu zetu; macho yako yatauona

Yerusalemu umekuwa kao la raha;

hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake

havitang›olewa, wala kamba zake

hazitakatika.

EZEKIELI 36:25 Nami nitawanyunyizia maji

safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na

uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami

nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa

moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu,

nami nitawapa moyo wa nyama.

27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na

kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi

mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

28 Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba

zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami

nitakuwa Mungu wenu.

ISAYA

Page 187: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

187

29 Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote;

nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka

njaa juu yenu tena.

ZEKARIA 12:8 Katika siku hiyo Bwana

atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye

aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama

Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi

itakuwa kama Mungu, kama malaika wa

Bwana mbele yao.

ZEKARIA 13:1 Katika siku hiyo watu

wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa

Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa

dhambi na kwa unajisi.

2 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema

Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina

ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe

tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya

uchafu, watoke katika nchi.

MATHAYO 3:11 Kweli mimi nawabatiza

kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye

nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala

sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye

atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa

moto.

12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake,

naye atausafisha sana uwanda wake; na

kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi

atayateketeza kwa moto usiozimika.

YOHANA 16:8 Naye akiisha kuja, huyo

atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya

dhambi, na haki, na hukumu.

9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu

hawaniamini mimi;

10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi

naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni

tena;

11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule

mkuu wa ulimwengu huu amekwisha

kuhukumiwa.

1 WAKORINTHO 6:11 Na baadhi yenu

mlikuwa watu wa namna hii; lakini

mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini

mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu

Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

UFUNUO WA YOHANA 7:14

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.

Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika

dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,

na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-

Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 14:1 Kisha

nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo

amesimama juu ya mlima Sayuni, na

watu mia na arobaini na nne elfu pamoja

naye, wenye jina lake na jina la Baba yake

limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

Ona pia: #1; #2; #5; Kutoka 13:21,22; Zaburi 27:5; Zaburi 78:14; Zaburi 91:1; Mithali 18:10; Isaya 25:4; Isaya 26:20; Isaya 37:35;

Yeremia 16:19; Ezekieli 11:16; Ezekieli 16:6-9; Ezekieli 22:15,18-22; Ezekieli 24:7-14; Yoeli 3:16-21; Zekaria 2:5-10; Mathayo 18:20; Mathayo 23:37; Mathayo 28:20; Ufunuo wa Yohana 7:15,16;

Ufunuo wa Yohana 11:15; Ufunuo wa Yohana 20.

ISAYA

Page 188: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

188

A08 Majina na vyeo vya Masiha.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 5:1 Na nimwimbie mpenzi

wangu wimbo wa mpenzi wangu katika

habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi

wangu alikuwa na shamba la mizabibu,

Kilimani penye kuzaa sana;

2 Akafanya handaki kulizunguka pande

zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani

yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara

katikati yake, Akachimba shinikizo ndani

yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu,

Nao ukazaa zabibu-mwitu.

ZABURI 80:14 Ee Mungu wa majeshi,

tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone,

uujilie mzabibu huu.

15 Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako

wa kuume; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa

imara kwa nafsi yako.

YEREMIA 2:21 Nami nalikuwa

nimekupanda, mzabibu mwema sana,

mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi,

kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu

machoni pangu?

MATHAYO 21:33 Sikilizeni mfano mwingine.

Kulikuwa na mtu mwenye nyumba,

naye alipanda shamba la mizabibu,

akalizungusha ugo, akachimba shimo la

shinikizo ndani yake, akajenga mnara,

akapangisha wakulima, akasafiri.

34 Wakati wa matunda ulipokuwa karibu,

akawatuma watumwa wake kwa wale

wakulima, wapokee matunda yake.

35 Wale wakulima wakawakamata watumwa

wake, huyu wakampiga, na huyu

wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.

36 Akawatuma tena watumwa wengine wengi

kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile.

37 Mwishowe akamtuma mwanawe kwao,

akisema, Watamstahi mwanangu.

38 Lakini wale wakulima walipomwona yule

mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu

ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi

wake.

39 Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la

mizabibu, wakamwua.

YOHANA 3:29 Aliye naye bibi arusi ndiye

bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi,

yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia

sana sauti yake bwana arusi.

YOHANA 15:1 Mimi ndimi mzabibu wa

kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 32:32,33; Zaburi 80:7; Wimbo Ulio Bora 2:8,16; Wimbo Ulio Bora 5:2,16; Wimbo Ulio Bora

6:3; Isaya 5:7; Isaya 27:2,3; Hosea 10:1; Marko 12:1-9; Luka 13:7; Yohana 2:1-11; Warumi 9:4,5.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 6:1 Katika mwaka ule aliokufa

mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi

katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na

kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake

zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja

alikuwa na mabawa sita; kwa mawili

alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika

miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake,

wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,

ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa

utukufu wake.

4 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa

ISAYA

Page 189: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

189

sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba

ikajaa moshi.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

UFUNUO WA YOHANA 4:11

Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu

wetu, kuupokea utukufu na heshima na

uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba

vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako

vilikuwako, navyo vikaumbwa.

UFUNUO WA YOHANA 15:3 Nao

wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa

Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; Kutoka 24:10,11; Hesabu 12:8; 1 Wafalme 8:10,11; Zaburi 24:7-10; Ezekieli 1:25-28; Danieli 7:9; Yohana 1:18; 1

Timotheo 6:16; Ufunuo wa Yohana 4:1-11; Ufunuo wa Yohana 5:1,7; Ufunuo wa Yohana 6:16; Ufunuo wa Yohana 7:11,12.

F14 Masiha hataaminiwa.

ISAYA 6:9 Naye akaniambia, Enenda,

ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia,

lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini

msione.

10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie

uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao;

wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia

kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo

yao, na kurejea na kuponywa.

YOHANA 12:39 Ndiyo sababu wao

hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya

alisema tena,

40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito

mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao,

Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka,

nikawaponya.

41 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa

aliuona utukufu wake, akataja habari zake.

MATENDO YA MITUME 28:24 Wengine

waliamini yale yaliyonenwa, wengine

hawakuyaamini.

25 Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao,

wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema

neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu

alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha

nabii Isaya,

26 akisema, Enenda kwa watu hawa,

ukawaambie, Kusikia, mtasikia wala

hamtafahamu; Na kuona, mtaona wala

hamtatambua;

27 Kwa maana mioyo ya watu hawa

imepumbaa, Na masikio yao ni mazito

ya kusikia, Na macho yao wameyafumba;

Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia

kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo

yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 2:30; Isaya 6:5; Isaya 29:10,13; Isaya 30:8-11; Isaya 63:17; Ezekieli 3:6-11; Hosea 1:9; Mathayo 13:14,15; Marko 4:12; Luka 8:10; Matendo ya Mitume 28:26,27;

Warumi 11:8; 2 Wakorintho 2:16.

ISAYA

Page 190: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

190

B03 Masiha ndiye Mwana wa mtu.

C04 Maisha ya Masiha hadi kuonekana Kwake

kwa mara ya kwanza.

ISAYA 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe

atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua

mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye

atamwita jina lake Imanueli.

15 Siagi na asali atakula, wakati ajuapo

kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.

16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua

kuyakataa mabaya na kuyachagua mema,

nchi ile, ambayo wewe unawachukia

wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa.

MATHAYO 1:20 Basi alipokuwa akifikiri

hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea

katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa

Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo,

maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho

Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina

lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa

watu wake na dhambi zao.

22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno

lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii

akisema,

23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye

atazaa mwana; Nao watamwita jina lake

Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.

MATHAYO 16:15 Akawaambia, Nanyi

mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe

Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

MATHAYO 18:20 Kwa kuwa walipo wawili

watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami

nipo papo hapo katikati yao.

MATHAYO 28:20 na kuwafundisha kuyashika

yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi

nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu

wa dahari.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje

neno hili, maana sijui mume?

35 Malaika akajibu akamwambia, Roho

Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake

Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa

sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa

kitakatifu, Mwana wa Mungu.

YOHANA 1:15 Yohana alimshuhudia,

akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye

niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye

nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa

maana alikuwa kabla yangu.

YOHANA 14:15 Mkinipenda, mtazishika

amri zangu.

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa

Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata

milele;

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu

hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni

wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua,

maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani

yenu.

ISAYA

Page 191: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

191

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: Mwanzo 3:15; Isaya 9:6; Luka 2:40-52; Yohana 1:1,2,14; 1 Timotheo 3:16.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 8:13 Bwana wa majeshi ndiye

mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na

awe yeye utisho wenu.

14 Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni

jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa

kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego

na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.

15 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka

na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.

MATHAYO 11:6 Naye heri awaye yote

asiyechukizwa nami.

MATHAYO 13:57 Wakachukizwa naye. Yesu

akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima,

isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani

mwake mwenyewe.

LUKA 2:34 Simeoni akawabariki,

akamwambia Mariamu mama yake, Tazama,

huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka

wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara

itakayonenewa.

LUKA 20:17 Akawakazia macho akasema,

Maana yake nini basi neno hili lililoandikwa,

Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa

jiwe kuu la pembeni?

18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo

atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye

litamwangukia litamsaga kabisa.

LUKA 21:35 kwa kuwa ndivyo

itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso

wa dunia nzima.

WARUMI 9:31 bali Israeli wakiifuata sheria

ya haki hawakuifikilia ile sheria.

32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata

kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa

njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile

likwazalo,

33 kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka

katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba

uangushao; Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

1 PETRO 2:7 Basi, heshima hii ni kwenu

ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,

Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe

kuu la pembeni.

Ona pia: Ezekieli 11:16; Mathayo 15:14; Mathayo 21:43-45; 1 Wakorintho 1:23,24.

E02 Mahali pa huduma ya Masiha.

ISAYA 9:1 Lakini yeye aliyekuwa katika

dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza

aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali

katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za

mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na

njia ya bahari; ng›ambo ya Yordani, Galilaya

ya mataifa.

ISAYA

Page 192: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

192

MATHAYO 2:22 Lakini aliposikia ya kwamba

Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali

pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko;

naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri

pande za Galilaya,

23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti;

ili litimie neno lililonenwa na manabii,

Ataitwa Mnazorayo.

MATHAYO 4:12 Basi Yesu aliposikia ya

kwamba Yohana amefungwa, alikwenda

zake mpaka Galilaya;

13 akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu,

mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni

na Naftali;

14 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya,

akisema,

15 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia

ya bahari, ng›ambo ya Yordani, Galilaya ya

mataifa,

YOHANA 1:45 Filipo akamwona

Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona

yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na

manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa

Nazareti.

46 Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema

kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo

uone.

B21 Masiha ndiye Nuru.

E15 Masiha ataleta habari njema.

ISAYA 9:2 Watu wale waliokwenda

katika giza Wameona nuru kuu; Wale

waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru

imewaangaza.

3 Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao;

Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya

wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo

wagawanyapo nyara.

4 Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake,

na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye

aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.

MATHAYO 4:16 Watu wale waliokaa katika

giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa

katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga

umewazukia.

LUKA 1:76 Nawe, mtoto, utaitwa nabii

wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia

mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia

zake;

77 Uwajulishe watu wake wokovu, Katika

kusamehewa dhambi zao.

78 Kwa njia ya rehema za Mungu wetu,

Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu

umetufikia,

79 Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa

mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye

njia ya amani.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye

hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao

ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

5 Nayo nuru yang›aa gizani, wala giza

halikuiweza.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

ISAYA

Page 193: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

193

YOHANA 12:35 Basi Yesu akawaambia,

Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo.

Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza

lisije likawaweza; maana aendaye gizani

hajui aendako.

36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo

aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha

wasimwone.

46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu,

ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

WAEFESO 5:8 Kwa maana zamani ninyi

mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika

Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,

Ona pia: Isaya 50:10; Isaya 60:1-3,19; Luka 2:32; 1 Petro 2:9; Yohana 1:5-7.

A08 Majina na vyeo vya Masiha.

B03 Masiha ndiye Mwana wa mtu.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

H04 Kiti cha enzi cha Masiha.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani

Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika

kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;

Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa

hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata

milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio

utakaotenda hayo.

MATHAYO 1:23 Tazama, bikira atachukua

mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita

jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja

nasi.

MATHAYO 9:15 Yesu akawaambia,

Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza,

muda bwana arusi akiwapo pamoja nao?

Lakini siku zitakuja watakapoondolewa

bwana arusi; ndipo watakapofunga.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

MARKO 10:33 akisema, Angalieni,

tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana

wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa

makuhani na waandishi, nao watamhukumu

afe, watamtia mikononi mwa Mataifa,

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 1:35 Malaika akajibu

akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu

yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika

kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho

kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana

wa Mungu.

LUKA 2:10 Malaika akawaambia,

Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea

habari njema ya furaha kuu itakayokuwa

kwa watu wote;

11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa,

kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo

ISAYA

Page 194: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

194

Bwana.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

YOHANA 1:18 Hakuna mtu aliyemwona

Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana

pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu

ndiye aliyemfunua.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

YOHANA 4:25 Yule mwanamke

akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi,

(aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye

atatufunulia mambo yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe,

ndiye.

YOHANA 10:11 Mimi ndimi mchungaji

mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai

wake kwa ajili ya kondoo.

MATENDO YA MITUME 4:26

Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu

wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na

juu ya Kristo wake.

1 WAKORINTHO 15:45 Ndivyo

ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu,

akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni

roho yenye kuhuisha.

2 WAKORINTHO 4:4 ambao ndani yao

mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao

wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya

utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

WAEFESO 1:20 aliotenda katika Kristo

alipomfufua katika wafu, akamweka mkono

wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka,

na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo,

wala si ulimwenguni humu tu, bali katika

ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,

akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa

ajili ya kanisa; ambalo

WAEFESO 2:14 Kwa maana yeye ndiye

amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa

wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza

cha kati kilichotutenga.

WAFILIPI 2:7 bali alijifanya kuwa hana

utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa

ana mfano wa wanadamu;

2 WATHESALONIKE 3:16 Sasa, Bwana wa

amani mwenyewe na awape amani daima

kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi

nyote.

1 TIMOTHEO 2:5 Kwa sababu Mungu ni

mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na

wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo

Yesu;

2 TIMOTHEO 4:8 baada ya hayo nimewekewa

taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu

mwenye haki, atanipa siku ile; wala si

mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda

kufunuliwa kwake.

WAEBRANIA 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao

wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,

ISAYA

Page 195: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

195

akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake,

akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi

mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

WAEBRANIA 4:14 Basi, iwapo tunaye kuhani

mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu,

Mwana wa Mungu, na tuyashike sana

maungamo yetu.

WAEBRANIA 5:6 kama asemavyo mahali

pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa

mfano wa Melkizedeki.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

1 PETRO 2:6 Kwa kuwa imeandikwa

katika maandiko Tazama, naweka katika

Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule,

lenye heshima, Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

UFUNUO WA YOHANA 1:8 Mimi ni

Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema

Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na

atakayekuja, Mwenyezi.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

UFUNUO WA YOHANA 19:16 Naye ana

jina limeandikwa katika vazi lake na paja

lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana

WA MABwana.

UFUNUO WA YOHANA

22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika

wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo

katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina

na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung›aa

ya asubuhi.

Ona pia: Waamuzi 13:18; 1 Samweli 7:16; Zaburi 2:8; Zaburi 72:8-11; Zaburi 89:35-37; Isaya 7:14; Yeremia 33:15-17; Danieli

2:44; Danieli 7:14,27; Yohana 18:37; 1 Wakorintho 15:24-28; Waefeso 1:20-22.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 10:20 Tena itakuwa katika siku

hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa

nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena

yeye aliyewapiga, bali watamtegemea Bwana,

Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.

21 Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo,

watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu.

22 Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa

wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki

tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa,

kunakofurika kwa haki.

ZABURI 53:6 Laiti wokovu wa Israeli

utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo

wafungwa wa watu wake; Yakobo

atashangilia, Israeli atafurahi.

ISAYA

Page 196: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

196

ISAYA 1:9 Kama Bwana wa majeshi

asingalituachia mabaki machache sana,

tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana

na Gomora.

ISAYA 12:6 Paza sauti, piga kelele,

mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa

Israeli ni mkuu kati yako.

HOSEA 1:9 Bwana akasema, Mwite

jina lake Lo-ami kwa maana ninyi si watu

wangu,wala mimi sitakuwa MUNGU wenu.

10 Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana

wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari,

usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena

itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu

wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa

Mungu aliye hai.

ZEKARIA 10:9 Nami nitawapanda kama

mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka

katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja

na watoto wao; tena watarudi.

WARUMI 9:25 Ni kama vile alivyosema

katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale

wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu

yeye asiyekuwa mpenzi wangu.

26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa,

Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana

wa Mungu aliye hai.

27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya

Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa

Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake

juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena,

Kama Bwana wa majeshi asingalituachia

uzao, Tungalikuwa kama Sodoma,

tungalifananishwa na Gomora.

WARUMI 11:5 Basi ni vivi hivi wakati huu

wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa

neema.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

2 WAKORINTHO 3:14 ila fikira zao

zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi,

wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo

huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba

huondolewa katika Kristo;

15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji

huikalia mioyo yao.

16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia

Bwana, ule utaji huondolewa.

Ona pia: #1; #2; #3; #4.

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

B04 Sifa za Uungu za Masiha.

B05 Masiha amejawa na Roho na Mtakatifu.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

ISAYA 11:1 Basi litatoka chipukizi katika

shina la Yese, na tawi litakalotoka katika

mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho

ya hekima na ufahamu, roho ya shauri

ISAYA

Page 197: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

197

na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha

Bwana;

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha

Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata

ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya

kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

MATHAYO 3:16 Naye Yesu alipokwisha

kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na

tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona

Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija

juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema,

Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,

ninayependezwa naye.

LUKA 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea

katika hekima na kimo, akimpendeza

Mungu na wanadamu.

YOHANA 3:34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa

na Mungu huyanena maneno ya Mungu;

kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote

mkononi mwake.

36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele;

asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali

ghadhabu ya Mungu inamkalia.

YOHANA 16:13 Lakini yeye atakapokuja,

huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie

kwenye kweli yote; kwa maana hatanena

kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote

atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo

atawapasha habari yake.

MATENDO YA MITUME 10:37 jambo lile

ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi

wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo

aliouhubiri Yohana;

38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu

alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na

nguvu naye akazunguka huko na huko,

akitenda kazi njema na kuponya wote

walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu

alikuwa pamoja naye.

MATENDO YA MITUME 13:21 Hatimaye

wakaomba kupewa mfalme; Mungu

akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa

kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka

arobaini.

22 Na alipokwisha kumwondoa huyo,

akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye

alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi,

mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo

wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.

23 Katika uzao wake mtu huyo Mungu

amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu,

kama alivyoahidi;

1 WAKORINTHO 1:30 Bali kwa yeye

ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu,

aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa

Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

UFUNUO WA YOHANA 4:5 Na katika

kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti

na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka

mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba

za Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 5:6 Nikaona

katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye

uhai wanne, na katikati ya wale wazee,

Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana

kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba

na macho saba, ambazo ni Roho saba za

Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

ISAYA

Page 198: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

198

Ona pia: Isaya 42:1; Isaya 59:21; Isaya 61:1; Mathayo 12:25; Mathayo 13:54; Luka 2:40,52; Luka 3:21,22; Yohana 1:32,33;

Waefeso 1:17,18; 2 Timotheo 1:7; Ufunuo wa Yohana 3:1.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 11:4 bali kwa haki atawahukumu

maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa

dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa

fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya

midomo yake atawaua wabaya.

5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na

uaminifu mshipi wa kujifungia.

YEREMIA 23:5 Tazama siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi

Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme,

atatenda kwa hekima, naye atafanya

hukumu na haki katika nchi.

6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli

atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni

hili, Bwana ni haki yetu.

2 WAKORINTHO 6:7 katika neno la

kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za

haki za mkono wa kuume na za mkono wa

kushoto;

WAEFESO 6:14 Basi simameni, hali

mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya

haki kifuani,

2 WATHESALONIKE 2:8 Hapo ndipo

atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana

Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake,

na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo

kwake;

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

UFUNUO WA YOHANA 19:15 Na

upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

UFUNUO WA YOHANA 20:11 Kisha

nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe,

na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na

mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao

hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo,

wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi;

na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine

kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na

hao wafu wakahukumiwa katika mambo

hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,

sawasawa na matendo yao.

Ona pia: #1; #2; #5; 1 Petro 4:1; Ufunuo wa Yohana 1:13.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

ISAYA 11:6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja

na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja

na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba

ISAYA

Page 199: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

199

na kinono watakuwa pamoja, na mtoto

mdogo atawaongoza.

7 Ng›ombe na dubu watalisha pamoja; watoto

wao watalala pamoja; na simba atakula

majani kama ng›ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la

nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono

wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika

mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia

itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji

yanavyoifunika bahari.

HABAKUKI 2:14 Kwa maana dunia itajazwa

maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji

yaifunikavyo bahari.

ZEKARIA 14:8 Tena itakuwa siku hiyo,

ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika

Yerusalemu; nusu yake itakwenda upande

wa bahari ya mashariki, na nusu yake

upande wa bahari ya magharibi; wakati wa

hari na wakati wa baridi itakuwa hivi.

9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi

yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na

jina lake moja.

MATHAYO 5:44 lakini mimi nawaambia,

Wapendeni adui zenu, waombeeni

wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye

mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake

waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye

haki na wasio haki.

MATENDO YA MITUME 2:44 Na wote

walioamini walikuwa mahali pamoja, na

kuwa na vitu vyote shirika,

45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa

navyo, na kuwagawia watu wote kama kila

mtu alivyokuwa na haja.

46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu

ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba

kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa

furaha na kwa moyo mweupe,

47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu

wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku

kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

WARUMI 14:17 Maana ufalme wa Mungu si

kula wala kunywa, bali ni haki na amani na

furaha katika Roho Mtakatifu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #5; #6; #7; Ayubu 5:23; 1 Wakorintho 6:9-11; 1 Wathesalonike 5:15; Ufunuo wa Yohana 5:9,10; Ufunuo wa

Yohana 20:2-6.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 11:10 Na itakuwa katika siku hiyo,

shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa

kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa

watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia

patakuwa na utukufu.

11 Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana

atapeleka mkono wake mara ya pili, ili

ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka

Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka

Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu,

na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na

kutoka visiwa vya bahari.

12 Naye atawatwekea mataifa bendera,

ISAYA

Page 200: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

200

atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa,

atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika,

kutoka ncha nne za dunia.

WIMBO ULIO BORA 5:10 Mpendwa wangu

ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri

miongoni mwa elfu kumi;

ISAYA 59:19 Basi, wataliogopa jina

la Bwana toka magharibi, na utukufu

wake toka maawio ya jua; maana yeye

atakuja kama mkondo wa mto ufurikao,

uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.

YOHANA 11:51 Na neno hilo yeye

hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa

alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri

ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa

hilo.

52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini

pamoja na hayo awakusanye watoto wa

Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.

WARUMI 11:15 Maana ikiwa kutupwa kwao

kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je!

Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si

uhai baada ya kufa?

WARUMI 11:22 Tazama, basi, wema na ukali

wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali,

bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa

katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe

utakatiliwa mbali.

23 Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini

kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu

aweza kuwapandikiza tena.

24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa

katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu

kwa asili yake, kisha ukapandikizwa,

kinyume cha asili, katika mzeituni ulio

mwema, si zaidi sana wale walio wa asili

kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao

wenyewe?

25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue

siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya

kwamba kwa sehemu ugumu umewapata

Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

WARUMI 15:9 tena ili Mataifa wamtukuze

Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama

ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati

ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na

watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana;

Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la

Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

2 WAKORINTHO 3:16 Lakini wakati wo

wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji

huondolewa.

WAEBRANIA 4:9 Basi, imesalia raha ya sabato

kwa watu wa Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

UFUNUO WA YOHANA

ISAYA

Page 201: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

201

22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika

wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo

katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina

na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung›aa

ya asubuhi.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 12:1 Na katika siku hiyo utasema,

Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa

kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako

imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.

2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;

Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana

YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;

Naye amekuwa wokovu wangu.

3 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima

vya wokovu.

4 Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni

Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni

matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina

lake kuwa limetukuka.

5 Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda

makuu; Na yajulikane haya katika dunia

yote.

6 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;

Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati

yako.

ZABURI 132:13 Kwa kuwa Bwana

ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani

yake.

14 Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele,

Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.

ISAYA 66:13 Mfano wa mtu

ambaye mama yake amfariji, ndivyo

nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa

katika Yerusalemu.

YEREMIA 23:6 Katika siku zake Yuda

ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina

lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

SEFANIA 3:15 Bwana ameziondoa hukumu

zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa

Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako;

Hutaogopa uovu tena.

16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,

Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.

17 Bwana, Mungu wako, yu katikati yako

shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa

furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake,

Atakufurahia kwa kuimba.

ZEKARIA 2:5 Kwa maana mimi,

asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto

kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo

utukufu ndani yake.

YOHANA 4:14 walakini ye yote

atakayekunywa maji yale nitakayompa

mimi hataona kiu milele; bali yale maji

nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ISAYA

Page 202: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

202

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

UFUNUO WA YOHANA 7:17 Kwa

maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati

ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 21:6

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa

na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi

nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya

maji ya uzima, bure.

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung›aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

UFUNUO WA YOHANA 22:17 Na Roho

na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye

na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na

yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

Ona pia: #1; #2; #3; #4.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 14:1 Maana Bwana atamhurumia

Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye

atawaweka katika nchi yao wenyewe; na

mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na

nyumba ya Yakobo.

2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta

mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba

ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya

watumishi na wajakazi katika nchi

ya Bwana; nao watawachukua hali ya

kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao

watawamiliki watu wale waliowaonea.

3 Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana

atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada

ya taabu yako, na baada ya utumishi ule

mgumu uliotumikishwa;

ZABURI 102:13 Wewe mwenyewe

utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa

maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam,

majira yaliyoamriwa yamewadia.

ISAYA 61:5 Na wageni watasimama na

kulisha makundi yenu, na watu wa kabila

nyingine watakuwa wakulima wenu, na

watunzaji wa mizabibu yenu.

EZEKIELI 28:24 Wala hautakuwapo

mchongoma uchomao kwa nyumba ya

Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa

wote wamzungukao, waliowatenda mambo

ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi

Bwana MUNGU.

ZEKARIA 1:17 Piga kelele tena, na kusema,

Bwana wa majeshi asema hivi, Miji yangu

kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko

ISAYA

Page 203: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

203

tena; naye Bwana ataufariji Sayuni tena,

atauchagua Yerusalemu tena.

LUKA 1:72 Ili kuwatendea rehema baba

zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;

73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,

74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi

mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,

LUKA 2:32 Nuru ya kuwa mwangaza

wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako

Israeli.

WARUMI 15:27 Naam, imewapendeza, tena

wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa

Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho,

imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya

mwili.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #2; #3; #4; Isaya 14:4-18; Matendo ya Mitume 15:14-17; Waefeso 2:12-19.

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

E09 Uadilifu wa Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 16:5 Na kiti cha enzi kitafanywa

imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu

yake katika kweli, katika hema ya Daudi;

akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki,

mwepesi wa kutenda haki.

LUKA 1:33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo

hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna

mwisho.

LUKA 1:69 Ametusimamishia pembe ya

wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi

wake.

70 Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa

kinywa cha manabii wake watakatifu;

YOHANA 12:48 Yeye anikataaye mimi,

asiyeyakubali maneno yangu, anaye

amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo

litakalomhukumu siku ya mwisho.

MATENDO YA MITUME 15:16 Baada ya

mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena

nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga

tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

Ona pia: #1; Zaburi 89:14.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 17:7 Katika siku hiyo

mwanadamu atamwangalia Muumba wake,

na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa

Israeli.

ISAYA 10:20 Tena itakuwa katika siku

hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa

nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena

yeye aliyewapiga, bali watamtegemea Bwana,

Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.

21 Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo,

ISAYA

Page 204: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

204

watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu.

22 Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa

wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki

tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa,

kunakofurika kwa haki.

HOSEA 3:5 baada ya hayo wana wa

Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana,

Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao

watamwendea Bwana na wema wake kwa

kicho siku za mwisho.

MIKA 7:7 Lakini mimi, nitamtazamia

Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu

wangu; Mungu wangu atanisikia.

8 Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu;

niangukapo, nitasimama tena; nikaapo

gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu.

MATENDO YA MITUME 15:16 Baada ya

mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena

nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga

tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

1 YOHANA 3:2 Wapenzi, sasa tu wana

wa Mungu, wala haijadhihirika bado

tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa

atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa

maana tutamwona kama alivyo.

UFUNUO WA YOHANA 1:7 Tazama,

yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona,

na hao waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.

Amina.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 19:23 Katika siku hiyo itakuwako

njia kuu itokayo Misri na kufika hata

Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri

atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu

pamoja na Waashuri.

24 Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu

pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa

baraka kati ya dunia;

25 kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki,

akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri;

na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na

wewe Israeli, urithi wangu.

ISAYA 66:12 Maana Bwana asema

hivi, Tazama, nitamwelekezea amani

kama mto, na utukufu wa mataifa

kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata

kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti

mtabembelezwa.

ZEKARIA 2:11 Na mataifa mengi

watajiunga na Bwana katika siku ile, nao

watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati

yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa

majeshi amenituma kwako.

ZEKARIA 10:11 Naye atapita kati ya bahari ya

mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na

vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na

kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya

enzi ya Misri itatoweka.

ZEKARIA 14:18 Na kama jamaa ya Misri

hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha

kwao; itakuwako tauni, ambayo Bwana

atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika

sikukuu ya Vibanda.

ISAYA

Page 205: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

205

LUKA 2:32 Nuru ya kuwa mwangaza

wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako

Israeli.

WARUMI 3:29 Au je! Mungu ni Mungu wa

Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia?

Naam, ni Mungu wa Mataifa pia;

WARUMI 9:24 ndio sisi aliotuita, si watu wa

Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?

25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea,

Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu

wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa

mpenzi wangu.

WARUMI 10:11 Kwa maana andiko lanena,

Kila amwaminiye hatatahayarika.

12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na

Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa

wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;

13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana

ataokoka.

WAEFESO 2:18 Kwa maana kwa yeye sisi

sote tumepata njia ya kumkaribia Baba

katika Roho mmoja.

19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala

wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na

watakatifu, watu wa nyumbani mwake

Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na

manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni

jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja

kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Ona pia: #1; #4; #5; Kumbukumbu la Torati 32:43; Isaya 19:16-22; Isaya 49:6; Warumi 15:9; Waefeso 3:6-8; 1 Petro 2:10.

B07 Uweza wa Yote wa Masiha.

ISAYA 22:22 Na ufunguo wa nyumba

ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye

atafungua wala hapana atakayefunga; naye

atafunga wala hapana atakayefungua.

MATHAYO 16:18 Nami nakuambia, Wewe

ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu

nitalijenga kanisa langu; wala milango ya

kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme

wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga

duniani, litakuwa limefungwa mbinguni;

na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa

limefunguliwa mbinguni.

MATHAYO 18:18 Amin, nawaambieni, yo

yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa

yamefungwa mbinguni; na yo yote

mtakayoyafungua duniani yatakuwa

yamefunguliwa mbinguni.

19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu

watakapopatana duniani katika jambo lo lote

watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu

aliye mbinguni.

UFUNUO WA YOHANA 1:18 na aliye

hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama,

ni hai hata milele na milele. Nami ninazo

funguo za mauti, na za kuzimu.

UFUNUO WA YOHANA 3:7 Na

kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia

andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye

mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo

wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala

hapana afungaye, naye afunga wala hapana

afunguaye.

ISAYA

Page 206: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

206

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 24:13 Maana katikati ya dunia,

katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama

wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati

waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.

14 Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele;

kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga

kelele toka baharini.

15 Basi, mtukuzeni Bwana katika mashariki,

litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa Israeli,

katika visiwa vya bahari.

16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia

nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo

niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda

kwangu! Ole wangu! Watenda hila

wametenda hila, naam, watendao hila

wametenda hila sana.

ISAYA 12:5 Mwimbieni Bwana; kwa

kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya

katika dunia yote.

6 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;

Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati

yako.

ISAYA 42:10 Mwimbieni Bwana wimbo

mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia;

Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo,

Na visiwa, nao wakaao humo.

11 Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,

Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe

wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele

vya milima.

12 Na wamtukuze Bwana, Na kutangaza sifa

zake visiwani.

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

1 PETRO 1:7 ili kwamba kujaribiwa

kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu

kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo

hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa

kwenye sifa na utukufu na heshima, katika

kufunuliwa kwake Yesu Kristo.

1 PETRO 4:12 Wapenzi, msione kuwa ni

ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata

kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni

kitu kigeni kiwapatacho.

13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya

Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa

utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri

yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa

Mungu anawakalia.

UFUNUO WA YOHANA 15:2 Tena

nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo

iliyochangamana na moto, na wale wenye

kushinda, watokao kwa yule mnyama, na

sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake,

walikuwa wamesimama kando-kando

ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya

Mungu.

3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa

wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

ISAYA

Page 207: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

207

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #2; #3; #4.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 24:18 Itakuwa kila akimbiaye

sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na

kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa

na mtego; kwa maana madirisha yaliyo

juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia

inatikisika.

19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia

kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika,

imetikisika sana.

20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo

inawaya-waya kama machela; na mzigo wa

dhambi zake utailemea; nayo itaanguka,

wala haitainuka tena.

21 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana

ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika

mahali palipo juu, na wafalme wa dunia

katika dunia;

22 nao watakusanywa pamoja kama vile

wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao

watafungwa katika gereza; na baada ya muda

wa siku nyingi watajiliwa.

23 Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona

haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi

atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika

Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa

utukufu.

ZEKARIA 14:4 Na siku hiyo miguu yake

itasimama juu ya mlima wa Mizeituni,

unaoelekea Yerusalemu upande wa

mashariki, nao mlima wa Mizeituni

utapasuka katikati yake, upande wa

mashariki na upande wa magharibi;

litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu

ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa

kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda

upande wa kusini.

MATHAYO 24:29 Lakini mara, baada ya dhiki

ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi

hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka

mbinguni, na nguvu za mbinguni

zitatikisika;

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu

ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya

Habili.

UFUNUO WA YOHANA 6:12 Nami

nikaona, alipoifungua muhuri ya sita,

palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa

jeusi kama gunia la singa, mwezi wote

ukawa kama damu,

UFUNUO WA YOHANA 6:14 Mbingu

zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa,

na kila mlima na kisiwa kikahamishwa

kutoka mahali pake.

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na

majemadari, na matajiri, na wenye

nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana,

wakajificha katika pango na chini ya miamba

ya milima,

16 wakiiambia milima na miamba,

ISAYA

Page 208: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

208

Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake

yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya

Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao,

imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

Ona pia: #1; #2; #5; #6; Zaburi 149:6-9; Isaya 4:1,2; Isaya 5:30; Isaya 13:9-11; Marko 13:24-37; Luka 21:25-36; Ufunuo wa Yohana

18:9.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

E11 Masiha atapeana uzima wa milele.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ISAYA 25:6 Na katika mlima huu Bwana

wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu

ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa

juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono

vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa

juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

7 Naye katika mlima huu atauharibu uso wa

sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji

ule uliotandwa juu ya mataifa yote.

8 Amemeza mauti hata milele; na Bwana

MUNGU atafuta machozi katika nyuso

zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika

ulimwengu wote; maana Bwana amenena

hayo.

9 Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu

ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja

atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja,

Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.

10 Kwa maana mkono wa Bwana utatulia

katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa

chini huko aliko, kama vile majani makavu

yakanyagwavyo katika maji ya jaa.

11 Naye atanyosha mikono yake katikati yake,

kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono

yake ili aogelee, naye atashusha kiburi

chake, pamoja na hila za mikono yake.

12 Na boma la ngome ya kuta zako

ameliinamisha, na kulilaza chini, na

kulitupa chini hata mavumbini.

YEREMIA 33:10 Bwana asema hivi, katika

mahali hapo ambapo mnasema kwamba ni

ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama,

naam, katika miji ya Yuda na katika njia

za Yerusalemu, zilizo ukiwa, hazina

mwanadamu wala mwenyeji wala mnyama,

11 itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya

shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya

bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni

Bwana wa majeshi, maana Bwana ni

mwema, rehema zake ni za milele; na sauti

zao waletao sadaka za shukrani nyumbani

kwa Bwana. Kwa kuwa nitawarudisha

wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema

Bwana.

MATHAYO 8:11 Nami nawaambieni, ya

kwamba wengi watakuja kutoka mashariki

na magharibi, nao wataketi pamoja na

Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme

wa mbinguni;

MATHAYO 26:29 Lakini nawaambieni,

Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu

wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa

mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba

yangu.

MATHAYO 28:5 Malaika akajibu, akawaambia

wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa

maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu

aliyesulibiwa.

6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama

ISAYA

Page 209: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

209

alivyosema. Njoni, mpatazame mahali

alipolazwa.

1 WAKORINTHO 15:26 Adui wa mwisho

atakayebatilishwa ni mauti.

1 WAKORINTHO 15:54 Basi huu

uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na

huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo

ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa,

Mauti imemezwa kwa kushinda.

55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U

wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za

dhambi ni torati.

57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye

kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

2 WAKORINTHO 3:13 nasi si kama Musa

alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba

Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile

iliyokuwa ikibatilika;

14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata

leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale,

utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa

kwamba huondolewa katika Kristo;

15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji

huikalia mioyo yao.

16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia

Bwana, ule utaji huondolewa.

17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo

Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji,

tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile

katika kioo, tunabadilishwa tufanane na

mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu,

kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana,

aliye Roho.

2 TIMOTHEO 1:10 na sasa

inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake

Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti,

na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa

ile Injili;

WAEBRANIA 2:14 Basi, kwa kuwa watoto

wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo

hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya

mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za

mauti, yaani, Ibilisi,

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha

yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika

hali ya utumwa.

UFUNUO WA YOHANA 7:15 Kwa hiyo

wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,

nao wanamtumikia mchana na usiku katika

hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha

enzi atatanda hema yake juu yao.

16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 19:7 Na

tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri,

ing›arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo

ni matendo ya haki ya watakatifu.

9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa

karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo.

Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya

kweli ya Mungu.

ISAYA

Page 210: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

210

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho

yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala

maombolezo, wala kilio, wala maumivu

hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya

kwanza yamekwisha kupita.

Ona pia: #1; #2; #5; Isaya 61:10,11; Yeremia 25:10; Yoeli 2:16; Mathayo 22:1-14; Mathayo 25:1-13; Mathayo 27:51,52; Yohana

3:29; Yohana 11:25,26; Waefeso 3:5,6; Waebrania 12:22-26; Ufunuo wa Yohana 1:7,17,18; Ufunuo wa Yohana 20:14.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 26:1 Siku ile wimbo huu

utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao

mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa

kuta na maboma.

2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki,

lishikalo kweli, liingie.

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake

umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa

kuwa anakutumaini.

4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana

YEHOVA ni mwamba wa milele.

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa

na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha

Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na

kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki,

Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana

wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

ISAYA 57:19 Mimi nayaumba matunda

ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye

mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema

Bwana; nami nitamponya.

20 Bali wabaya wanafanana na bahari

iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji

yake hutoa tope na takataka.

21 Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu

wangu.

YOHANA 14:27 Amani nawaachieni; amani

yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama

ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni

mwenu, wala msiwe na woga.

MATENDO YA MITUME 2:47

wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu

wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku

kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

WARUMI 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa

haki itokayo katika imani, na mwe na amani

kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu

Kristo,

WAEFESO 2:14 Kwa maana yeye ndiye

amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa

wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza

cha kati kilichotutenga.

15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili

wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika

maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu

mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya

amani.

16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu

ISAYA

Page 211: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

211

katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba,

akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.

Ona pia: #1; #2; #4; #7; Kumbukumbu la Torati 32:4,15; 1 Samweli 2:2; Zaburi 18:1; Zaburi 106:5; Isaya 50:10; Yeremia

17:7,8; Wafilipi 4:7; 1 Petro 2:9.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ISAYA 26:19 Wafu wako wataishi, maiti

zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi

mnaokaa mavumbini, kwa maana umande

wako ni kama umande wa mimea, nayo

ardhi itawatoa waliokufa.

20 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya

vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma

yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka

ghadhabu hii itakapopita.

21 Kwa maana, tazama, Bwana anakuja

kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu

wakaao duniani, kwa sababu ya uovu

wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala

haitawafunika tena watu wake waliouawa.

ZABURI 71:20 Wewe, uliyetuonyesha

mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena.

Utatupandisha juu tena Tokea pande za

chini ya nchi.

ISAYA 25:8 Amemeza mauti hata milele;

na Bwana MUNGU atafuta machozi katika

nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa

katika ulimwengu wote; maana Bwana

amenena hayo.

DANIELI 12:2 Tena, wengi wa hao walalao

katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine

wapate uzima wa milele, wengine aibu na

kudharauliwa milele.

YOHANA 5:28 Msistaajabie maneno hayo;

kwa maana saa yaja, ambayo watu wote

waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

29 Nao watatoka; wale waliofanya mema

kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda

mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

YOHANA 11:25 Yesu akamwambia,

Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye

aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa

anaishi;

26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa

kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

MATENDO YA MITUME 24:15 Nina

tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao

wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na

ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki

pia.

1 WATHESALONIKE 4:14 Maana, ikiwa

twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka,

vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu,

Mungu atawaleta pamoja naye.

15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la

Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia

hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika

hatutawatangulia wao waliokwisha kulala

mauti.

UFUNUO WA YOHANA 20:5 Hao wafu

waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile

miaka elfu.

6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na

mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika

ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili

haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa

Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja

naye hiyo miaka elfu.

ISAYA

Page 212: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

212

UFUNUO WA YOHANA 20:12

Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo,

wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi;

na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine

kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na

hao wafu wakahukumiwa katika mambo

hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,

sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani

yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu

waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa

kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Ona pia: #5; #6; Ezekieli 37:1-14.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 27:1 Katika siku hiyo Bwana, kwa

upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio

na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka

yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule

mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule

joka aliye baharini.

2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la

mvinyo, liimbieni.

3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila

dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na

mchana nitalilinda.

6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli

atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso

wa ulimwengu matunda.

12 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana

atayapiga-piga matunda yake toka gharika

ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi

mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa

Israeli.

13 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta

kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na

kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja;

na hao waliotupwa katika nchi ya Misri;

nao watamsujudu Bwana katika mlima

mtakatifu huko Yerusalemu.

ISAYA 4:2 Siku hiyo chipukizi la Bwana

litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya

nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza,

kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.

LUKA 3:8 Basi, toeni matunda

yapatanayo na toba; wala msianze kusema

mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye

Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya

kwamba katika mawe haya Mungu aweza

kumwinulia Ibrahimu watoto.

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

28 Nami nawapa uzima wa milele; wala

hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu

atakayewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

30 Mimi na Baba tu umoja.

YOHANA 15:5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni

matawi, akaaye ndani yangu nami ndani

yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi

ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

YOHANA 15:8 Hivyo hutukuzwa Baba

yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi

mtakuwa wanafunzi wangu.

YOHANA 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi,

ISAYA

Page 213: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

213

bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami

nikawaweka mwende mkazae matunda; na

matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba

lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu

awapeni.

UFUNUO WA YOHANA 20:2

Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani,

ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga

miaka elfu;

UFUNUO WA YOHANA 20:7 Na

hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani

atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;

UFUNUO WA YOHANA 20:10 Na yule

Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa

katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule

mnyama na yule nabii wa uongo. Nao

watateswa mchana na usiku hata milele na

milele.

UFUNUO WA YOHANA 22:2 katikati

ya njia kuu yake. Na upande huu na upande

huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima,

uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye

kutoa matunda yake kila mwezi; na majani

ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: #1; #2; #3; Isaya 5:1-7; Isaya 26:1; Isaya 46:4; Mathayo 21:28-46; Wakolosai 1:5,6.

E01 Aina ya huduma ya Masiha.

ISAYA 28:15 Kwa sababu mmesema,

Tumefanya agano na mauti, tumepatana

na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita,

halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya

maneno ya uongo kuwa kimbilio letu,

tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

16 kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema

hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni,

liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la

pembeni lenye thamani, msingi ulio imara;

yeye aaminiye hatafanya haraka.

ZABURI 118:22 Jiwe walilolikataa waashi

Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

MATHAYO 21:42 Yesu akawaambia,

Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe

walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe

kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa

Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

MATENDO YA MITUME 4:11 Yeye

ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi

waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la

pembeni.

12 Wala hakuna wokovu katika mwingine

awaye yote, kwa maana hapana jina jingine

chini ya mbingu walilopewa wanadamu

litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

WARUMI 9:31 bali Israeli wakiifuata sheria

ya haki hawakuifikilia ile sheria.

32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata

kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa

njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile

likwazalo,

33 kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka

katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba

uangushao; Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

1 WAKORINTHO 3:11 Maana msingi

mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka,

isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani,

Yesu Kristo.

ISAYA

Page 214: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

214

WAEFESO 2:17 Akaja akahubiri amani

kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani

kwao wale waliokuwa karibu.

18 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia

ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.

19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala

wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na

watakatifu, watu wa nyumbani mwake

Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na

manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni

jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja

kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

1 PETRO 2:4 Mmwendee yeye, jiwe lililo

hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa

Mungu ni teule, lenye heshima.

5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai,

mmejengwa mwe nyumba ya Roho,

ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho,

zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu

Kristo.

6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko

Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu

la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila

amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi

mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe

walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la

pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba

wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa

neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi

wapate hayo.

Ona pia: Mwanzo 49:24; Isaya 8:14; Hosea 2:19-21; Zekaria 3:9; Marko 12:10; Luka 20:17,18.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 29:10 Kwa maana Bwana

amewamwagieni roho ya usingizi,

amefumba macho yenu, yaani, manabii;

amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji.

13 Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa

hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa

vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami,

na kicho chao walicho nacho kwangu ni

maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;

14 kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi

ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na

mwujiza; na akili za watu wao wenye akili

zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao

utafichwa.

ZABURI 69:22 Meza yao mbele yao na iwe

mtego; Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.

EZEKIELI 33:32 Na tazama, wewe umekuwa

kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu

mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga

kinanda vizuri; maana, wasikia maneno

yako, lakini hawayatendi.

33 Na hayo yatakapokuwapo (tazama,

yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa nabii

amekuwapo kati yao.

MATHAYO 15:7 Enyi wanafiki, ni vema

alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,

8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila

mioyo yao iko mbali nami.

9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha

mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

MARKO 4:11 Akawaambia, Ninyi

mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu,

bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa

ISAYA

Page 215: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

215

mifano,

12 ili wakitazama watazame, wasione; Na

wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije

wakaongoka, na kusamehewa.

MARKO 7:6 Akawaambia, Isaya alitabiri

vema juu yenu ninyi wanafiki, kama

ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa

midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;

7 Nao waniabudu bure, Wakifundisha

mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,

8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na

kuyashika mapokeo ya wanadamu.

MATENDO YA MITUME 28:26 akisema,

Enenda kwa watu hawa, ukawaambie,

Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na

kuona, mtaona wala hamtatambua;

27 Kwa maana mioyo ya watu hawa

imepumbaa, Na masikio yao ni mazito

ya kusikia, Na macho yao wameyafumba;

Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia

kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo

yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.

WARUMI 11:7 Imekuwaje basi? Kitu

kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta

hakukipata; lakini wale waliochaguliwa

walikipata, na wengine walitiwa uzito.

8 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho

ya usingizi, macho hata wasione, na masikio

hata wasisikie, hata siku hii ya leo.

9 Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na

mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo

kwao;

10 Macho yao yatiwe giza ili wasione,

Ukawainamishe mgongo wao siku zote.

Ona pia: Isaya 6:9,10; Isaya 30:10; Isaya 35:5; Isaya 44:18; Yeremia 12:2; Ezekieli 33:31; Mika 3:6; Mathayo 15:2-6; Marko

7:1,2; 2 Wakorintho 4:4; 2 Wathesalonike 2:9-12.

E05 Miujiza ya Masiha.

ISAYA 29:18 Na katika siku hiyo viziwi

watasikia maneno ya hicho chuo, na macho

ya vipofu yataona katika upofu na katika

giza.

MATHAYO 11:5 vipofu wanapata kuona,

viwete wanakwenda, wenye ukoma

wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu

wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa

habari njema.

MATHAYO 13:14 Na neno la nabii Isaya

linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia,

wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama,

wala hamtaona.

15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,

Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na

macho yao wameyafumba; Wasije wakaona

kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao,

Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka,

nikawaponya.

16 Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona;

na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

LUKA 7:22 Ndipo alipojibu,

akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana

hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu

wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye

ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu

ISAYA

Page 216: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

216

wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari

njema.

MATENDO YA MITUME

26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza

waiache giza na kuielekea nuru, waziache na

nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu;

kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na

urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa

imani iliyo kwangu mimi.

2 WAKORINTHO 3:14 ila fikira zao

zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi,

wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo

huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba

huondolewa katika Kristo;

15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji

huikalia mioyo yao.

16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia

Bwana, ule utaji huondolewa.

17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo

Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji,

tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile

katika kioo, tunabadilishwa tufanane na

mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu,

kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana,

aliye Roho.

WAEFESO 1:17 Mungu wa Bwana wetu Yesu

Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho

ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue

tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri

wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu

jinsi ulivyo;

YAKOBO 1:21 Kwa hiyo wekeeni mbali

uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea

kwa upole neno lile lililopandwa ndani,

liwezalo kuziokoa roho zenu.

UFUNUO WA YOHANA 3:18

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu

iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri,

na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi

wako isionekane, na dawa ya macho ya

kujipaka macho yako, upate kuona.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 29:4; Zaburi 12:5; Isaya 29:10-12,16; Isaya 42:16-19; Marko 7:37; 2 Wakorintho 4:2-6; 1 Petro 2:9.

B17 Upole na udhaifu wa Masiha.

B24 Mungu na Masiha hupeana furaha na

faraja kwa wenye haki na waumini.

ISAYA 29:19 Wanyenyekevu nao

wataongeza furaha yao katika Bwana, na

maskini katika wanadamu watafurahi katika

Mtakatifu wa Israeli.

MAMBO YA WALAWI 23:40 Nanyi

siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti

mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya

miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi

mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu,

muda wa siku saba.

KUMBUKUMBU LA TORATI 16:11 nawe

utafurahi mbele ya Bwana, Mungu wako,

wewe na mwana wako na binti yako,

na mtumwa wako na mjakazi wako, na

Mlawi aliye ndani ya malango yako, na

mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa

na mumewe, walio katikati yako, katika

mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako,

apakalishe jina lake.

ZABURI 5:11 Nao wote wanaokukimbilia

ISAYA

Page 217: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

217

watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha.

Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao

jina lako watakufurahia.

ZABURI 32:11 Mfurahieni Bwana;

Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni

vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio

wanyofu wa moyo.

ZABURI 64:10 Mwenye haki atamfurahia

Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye

moyo wa adili watajisifu.

ZABURI 68:3 Bali wenye haki hufurahi, Na

kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga

kelele kwa furaha.

ZABURI 107:30 Ndipo walipofurahi kwa

kuwa yametulia Naye huwaleta mpaka

bandari waliyoitamani.

ZABURI 118:24 Siku hii ndiyo aliyoifanya

Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.

ZABURI 149:2 Israeli na amfurahie

Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na

wamshangilie mfalme wao.

WIMBO ULIO BORA 1:4 Nivute nyuma

yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza

vyumbani mwake. Tutafurahi na

kukushangilia; Tutazinena pambaja zako

kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.

ISAYA 9:3 Umeliongeza taifa,

umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele

zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno,

Kama watu wafurahivyo wagawanyapo

nyara.

ISAYA 25:9 Katika siku hiyo watasema,

Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye

tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana

tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia

wokovu wake.

YEREMIA 31:12 Nao watakuja, na kuimba

katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema

wa Bwana, nafaka, na divai, na mafuta, na

wachanga wa kondoo na wa ng›ombe; na

roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa

maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.

13 Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na

vijana na wazee pamoja; maana nitageuza

masikitiko yao kuwa furaha, nami

nitawafariji, na kuwafurahisha waache

huzuni zao.

HABAKUKI 3:18 Walakini nitamfurahia

Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu

wangu.

ZEKARIA 2:10 Imba, ufurahi, Ee binti

Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami

nitakaa kati yako, asema Bwana.

MATHAYO 5:3 Heri walio maskini wa roho;

Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

MATHAYO 5:5 Heri wenye upole; Maana

hao watairithi nchi.

MATHAYO 11:29 Jitieni nira yangu, mjifunze

kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na

mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha

nafsini mwenu;

LUKA 1:14 Nawe utakuwa na furaha

na shangwe, na watu wengi watakufurahia

kuzaliwa kwake.

ISAYA

Page 218: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

218

LUKA 2:10 Malaika akawaambia,

Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea

habari njema ya furaha kuu itakayokuwa

kwa watu wote;

YOHANA 3:29 Aliye naye bibi arusi ndiye

bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi,

yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia

sana sauti yake bwana arusi.

YOHANA 16:22 Basi ninyi hivi sasa mna

huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na

mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu

hakuna awaondoleaye.

YOHANA 20:20 Naye akiisha kusema hayo,

akawaonyesha mikono yake na ubavu

wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi

walipomwona Bwana.

MATENDO YA MITUME 5:41 Nao

wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa

sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili

kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo.

MATENDO YA MITUME 13:48 Mataifa

waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza

neno la Bwana, nao waliokuwa

wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

MATENDO YA MITUME 13:52 Na

wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.

WAFILIPI 2:17 Naam, hata nikimiminwa

juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu,

nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.

18 Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini

pamoja nami.

WAFILIPI 4:4 Furahini katika Bwana

sikuzote; tena nasema, Furahini.

1 WATHESALONIKE 3:9 Maana ni shukrani

gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili

yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia,

kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;

1 PETRO 4:13 Lakini kama mnavyoyashiriki

mateso ya Kristo, furahini; ili na katika

ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa

shangwe.

1 YOHANA 1:4 Na haya twayaandika, ili

furaha yetu itimizwe.

Ona pia: Hesabu 10:10; Kumbukumbu la Torati 12:7,12,18; Kumbukumbu la Torati 14:26; Kumbukumbu la Torati 16:14; Kumbukumbu la Torati 26:11; Kumbukumbu la Torati 27:7; 1 Samweli 2:1; 1 Wafalme 1:39,40; 1 Mambo ya Nyakati 15:16; 2 Mambo ya Nyakati 29:30; 2 Mambo ya Nyakati 30:23,26;

Nehemia 8:9,11,16; Nehemia 12:43,44; Esta 9:22; Zaburi 2:11; Zaburi 9:2,14; Zaburi 13:5; Zaburi 14:7; Zaburi 16:9,11; Zaburi

28:7; Zaburi 31:7; Zaburi 32:7; Zaburi 33:1,3,21; Zaburi 34:2; Zaburi 35:9,27; Zaburi 40:16; Zaburi 43:4; Zaburi 45:8,15; Zaburi 48:11; Zaburi 51:8,12,14; Zaburi 53:6; Zaburi 59:16; Zaburi 63:5,7,11; Zaburi 66:6; Zaburi 67:4; Zaburi 69:32;

Zaburi 70:4; Zaburi 81:1; Zaburi 89:16; Zaburi 90:14,15; Zaburi 92:4; Zaburi 95:1; Zaburi 96:11,12; Zaburi 97:1,8,11,12; Zaburi

98:4; Zaburi 100:2; Zaburi 104:34; Zaburi 105:3,43; Zaburi 106:5; Zaburi 107:42; Zaburi 119:14,62,74,111; Zaburi 122:1;

Zaburi 126:3; Zaburi 149:5; Mithali 10:28; Mithali 15:15; Isaya 9:3; Isaya 12:3,6; Isaya 24:14; Isaya 30:29; Isaya 35:1,2,10; Isaya 41:16; Isaya 44:23; Isaya 51:5,13; Isaya 54:1; Isaya 55:12; Isaya 56:7; Isaya 60:15; Isaya 61:3,7,10; Isaya 62:5; Isaya 65:18,19;

Isaya 66:2,10,14; Yeremia 15:16; Yeremia 33:9,11; Yeremia 49:25; Yoeli 2:21,23; Sefania 3:14,17; Zekaria 8:19; Zekaria 9:9;

Zekaria 10:7; Mathayo 2:10; Mathayo 5:12; Mathayo 13:44; Luka 1:47,58; Luka 6:23; Luka 10:17,20; Luka 15:7,23,32; Luka

19:6,37; Luka 24:41,52; Yohana 4:36; Yohana 8:56; Yohana 14:28; Yohana 15:11; Yohana 16:20,24; Yohana 17:13; Matendo ya Mitume 2:26,28,46,47; Matendo ya Mitume 8:8,39; Matendo ya Mitume 11:23; Matendo ya Mitume 14:17; Matendo ya Mitume 15:3,31; Matendo ya Mitume 16:34; Matendo ya Mitume 20:24;

Warumi 12:12,15; Warumi 14:17; Warumi 15:10,13; 1 Wakorintho 12:26; 2 Wakorintho 1:24; 2 Wakorintho 2:3; 2 Wakorintho 7:4; 2 Wakorintho 8:2; Wagalatia 5:22; Wafilipi 1:4,18,25; Wafilipi

2:2,29; Wafilipi 3:1; Wafilipi 4:1; Wakolosai 1:11; 1 Wathesalonike 1:6; 1 Wathesalonike 2:20; 1 Wathesalonike 3:9; 2 Timotheo

1:4; Waebrania 10:34; 1 Petro 1:6,8; Yohana 1:12,4; Ufunuo wa Yohana 14:3; Ufunuo wa Yohana 19:7.

ISAYA

Page 219: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

219

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 29:22 Basi, Bwana aliyemkomboa

Ibrahimu asema hivi, katika habari za

nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika

sasa, wala uso wake hautabadilika rangi

yake.

23 Bali atakapowaona watoto wake, walio

kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao

watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa

Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu

wa Israeli.

24 Hao nao wakosao rohoni mwao watapata

kufahamu, na hao wanung›unikao

watajifunza elimu.

MATENDO YA MITUME 2:37

Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao,

wakamwambia Petro na mitume wengine,

Tutendeje, ndugu zetu?

WAEFESO 2:10 Maana tu kazi yake,

tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende

matendo mema, ambayo tokea awali Mungu

aliyatengeneza ili tuenende nayo.

1 TIMOTHEO 1:13 ingawa hapo

kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye

kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata

rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa

ujinga, na kwa kutokuwa na imani.

Ona pia: #1; #2; #4; Isaya 5:16; Isaya 8:13; Mathayo 5:9; Luka 15:17-19; Yohana 6:45; 2 Wakorintho 4:2-6; Wagalatia 5:22,23; 1

Petro 2:9.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 30:18 Kwa ajili ya hayo Bwana

atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya

hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana

Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote

wamngojao.

19 Kwa maana watu watakaa katika Sayuni

huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika

yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya

kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.

20 Na ingawa Bwana atawapeni chakula cha

shida na maji ya msiba, lakini waalimu

wako hawatafichwa tena, ila macho yako

yatawaona waalimu wako;

ISAYA 30:21-25

ISAYA 30:26 Na tena nuru ya mwezi

itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua

itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku

saba, katika siku ile Bwana atakapofunga

mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la

jeraha yao.

ISAYA 30:27-28

ISAYA 30:29 Mtakuwa na wimbo kama

vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu

takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo kama

vile mtu aendapo na filimbi katika mlima wa

Bwana, aliye Mwamba wa Israeli.

ISAYA 30:30-33

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

ISAYA

Page 220: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

220

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEBRANIA 8:10 Maana hili ndilo agano

nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada

ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria

zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao,

Nao watakuwa watu wangu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #5.

E08 Haki ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 32:1 Tazama, mfalme atamiliki

kwa haki, na wakuu watatawala kwa

hukumu.

2 Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa

kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na

dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu,

kama kivuli cha mwamba mkubwa katika

nchi yenye uchovu.

ISAYA 32:3,4

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa

na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha

Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na

kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki,

Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana

wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

MATHAYO 5:6 Heri wenye njaa na kiu ya

haki; Maana hao watashibishwa.

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

YOHANA 4:14 walakini ye yote

atakayekunywa maji yale nitakayompa

mimi hataona kiu milele; bali yale maji

nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

Ona pia: #1; #2; Isaya 7:14; Mika 5:4,5.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 32:15 hata roho itakapomwagwa

juu yetu kutoka juu; hata jangwa

litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo

shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa

msitu.

16 Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki

itakaa katika shamba lizaalo sana.

17 Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao

ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini

daima.

18 Na watu wangu watakaa katika kao la amani;

na katika maskani zilizo salama, na katika

mahali pa kupumzikia penye utulivu.

ISAYA 44:3 Kwa maana nitamimina maji

ISAYA

Page 221: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

221

juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu

ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu

juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao

utakaowazaa;

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

MATENDO YA MITUME 2:17

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu, na

wana wenu na binti zenu watatabiri; na

vijana wenu wataona maono; na wazee wenu

wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi

wangu wanaume na wanawake Roho yangu,

nao watatabiri.

MATENDO YA MITUME 2:33 Basi yeye,

akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume

wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi

ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki

mnachokiona sasa na kukisikia.

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

2 WAKORINTHO 3:8 je! Huduma ya

roho haitazidi kuwa katika utukufu?

TITO 3:5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya

Yesu Kristo Mwokozi wetu;

Ona pia: #1; #2; #5; Mithali 1:23; Zaburi 104:30; Luka 24:49.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 33:17 Macho yako yatamwona

mfalme katika uzuri wake, yataona nchi

iliyoenea sana.

ISAYA 33:18-19

ISAYA 33:20 Angalia Sayuni, mji wa

sikukuu zetu; macho yako yatauona

Yerusalemu umekuwa kao la raha;

hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake

havitang›olewa, wala kamba zake

hazitakatika.

21 Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi,

mwenye adhama; mahali penye mito

mipana na vijito, pasipopita mashua na

makasia yake; wala hapana merikebu ya vita

itakayopita hapo.

22 Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu;

Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana

ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.

23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza

sana shina la mlingoti wao; hawakuweza

kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka

yaligawanywa, hata wachechemeao walipata

mateka.

24 Wala hapana mwenyeji atakayesema,

Mimi mgonjwa; watu wakaao humo

watasamehewa uovu wao.

ISAYA

Page 222: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

222

YEREMIA 31:33 Bali agano hili ndilo

nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya

siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu

ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika;

nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa

watu wangu.

MATHAYO 17:2 akageuka sura yake mbele

yao; uso wake ukang›aa kama jua, mavazi

yake yakawa meupe kama nuru.

MATHAYO 21:5 Mwambieni binti Sayuni

Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-

punda, mtoto wa punda.

LUKA 1:33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo

hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna

mwisho.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

YOHANA 17:24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate

na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa

maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

YOHANA 18:37 Basi Pilato akamwambia,

Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe

wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi

nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili

ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili

niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli

hunisikia sauti yangu.

MATENDO YA MITUME 10:42

Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia

ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu

awe Mhukumu wa walio hai na wafu.

1 WAKORINTHO 15:24 Hapo ndipo

mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme

wake; atakapobatilisha utawala wote, na

mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke

maadui wake wote chini ya miguu yake.

1 TIMOTHEO 6:13 Nakuagiza mbele

za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote,

na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama

maungamo mazuri yale mbele ya Pontio

Pilato,

14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa,

pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake

Bwana wetu Yesu Kristo;

15 ambako yeye kwa majira yake

atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa,

Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa

wafalme, Bwana wa mabwana;

1 YOHANA 3:2 Wapenzi, sasa tu wana

wa Mungu, wala haijadhihirika bado

tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa

atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa

maana tutamwona kama alivyo.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:3 Nao

wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa

Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

ISAYA

Page 223: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

223

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #1; #2; #5; #6; #7; Zaburi 45:2; Wimbo Ulio Bora 5:10; Isaya 32:1,2; Zekaria 9:17.

E05 Miujiza ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 35:1 Nyika na mahali palipo

ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na

kuchanua maua kama waridi.

2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam,

kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa

Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni;

watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa

Mungu wetu.

3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni

imara magoti yaliyolegea.

4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni

moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu

atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu;

atakuja na kuwaokoa ninyi.

5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na

masikio ya viziwi yatazibuliwa.

6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama

kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba;

maana katika nyika maji yatabubujika; na

vijito jangwani.

7 Na mchanga ung›aao mfano wa maji

utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye

kiu itakuwa chemchemi za maji; katika

makao ya mbweha, walipokuwa wamelala,

patakuwa na majani, pamoja na mianzi na

manyasi.

8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia,

nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi

hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili

ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga,

hawatapotea katika njia hiyo.

9 Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama

mkali hatapanda juu yake; hawataonekana

hapo; bali waliokombolewa watakwenda

katika njia hiyo.

10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi,

watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya

milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao

watapata kicheko na furaha, huzuni na

kuugua zitakimbia.

MATHAYO 11:4 Yesu akajibu akawaambia,

Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia

na kuyaona;

5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda,

wenye ukoma wanatakaswa, viziwi

wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini

wanahubiriwa habari njema.

6 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.

MATHAYO 12:22 Wakati ule akaletewa

mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu;

akamponya, hata yule bubu akanena na

kuona.

23 Makutano wote wakashangaa, wakasema,

Huyu siye mwana wa Daudi?

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

ISAYA

Page 224: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

224

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

YOHANA 9:39 Yesu akasema, Mimi

nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu,

ili wao wasioona waone, nao wanaoona

wawe vipofu.

YOHANA 10:28 Nami nawapa uzima wa

milele; wala hawatapotea kamwe; wala

hakuna mtu atakayewapokonya katika

mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

30 Mimi na Baba tu umoja.

YOHANA 14:6 Yesu akamwambia, Mimi

ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa

Baba, ila kwa njia ya mimi.

UFUNUO WA YOHANA 21:4 Naye

atafuta kila chozi katika macho yao, wala

mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo,

wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo

tena; kwa kuwa mambo ya kwanza

yamekwisha kupita.

UFUNUO WA YOHANA 22:14 Heri

wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea

huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa

milango yake.

Ona pia: #1; #2; #5; #7; Zaburi 146:8; Isaya 29:18; Isaya 32:3,4; Isaya 42:7,16; Isaya 43:8; Isaya 44:3,4; Mathayo 9:27-33; Mathayo

15:29-31; Mathayo 20:30-34; Mathayo 21:14; Marko 7:32-35; Marko 8:22-25; Yohana 4:14; Yohana 5:2-9; Yohana 7:38; Yohana 9:1-7; Matendo ya Mitume 9:17,18; Matendo ya Mitume 14:8-10;

Matendo ya Mitume 26:18.

C02 Mtangulizi wa Masiha anatangazwa.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 40:1 Watulizeni mioyo, watulizeni

mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.

2 Semeni na moyo wa Yerusalemu,

kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita

vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa;

kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana

adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.

3 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni

nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani

njia kuu kwa Mungu wetu.

4 Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima

na kilima kitashushwa; Palipopotoka

patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza

patasawazishwa;

5 Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote

wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa

kinywa cha Bwana kimenena haya.

MATHAYO 3:1 Siku zile aliondokea Yohana

Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi,

na kusema,

2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni

umekaribia.

3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii

Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani,

Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni

mapito yake.

MARKO 1:1 Mwanzo wa Injili ya Yesu

Kristo, Mwana wa Mungu.

2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya,

Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya

uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.

3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni

njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na

ISAYA

Page 225: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

225

kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la

dhambi.

LUKA 1:52 Amewaangusha wakuu

katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge

amewakweza.

53 Wenye njaa amewashibisha mema, Na

wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

LUKA 3:2 wakati wa ukuhani mkuu wa

Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia

Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.

3 Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani,

akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la

dhambi,

4 kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno

ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani,

Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni

mapito yake.

5 Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na

kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa

pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;

6 Na wote wenye mwili watauona wokovu wa

Mungu.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

2 WAKORINTHO 3:18 Lakini sisi sote,

kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha

utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo,

tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo,

toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa

utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

WAEBRANIA 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao

wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,

akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake,

akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi

mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

UFUNUO WA YOHANA 21:23 Na mji

ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,

kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru,

na taa yake ni Mwana-Kondoo.

Ona pia: #1; #2; #5; #7; Isaya 42:11-16; Isaya 57:15-19; Ezekieli 17:24; Hosea 2:15; Luka 18:14; 2 Wakorintho 1:4; 1 Wathesalonike

4:15-18.

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

B07 Uweza wa Yote wa Masiha.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 40:9 Wewe uuhubiriye Sayuni

habari njema, Panda juu ya mlima mrefu;

Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema,

Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako,

usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni,

Mungu wenu.

10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja

kama shujaa, Na mkono wake ndio

utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i

pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.

11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji,

Atawakusanya wana-kondoo mikononi

mwake; Na kuwachukua kifuani mwake,

Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

ISAYA 62:11 Tazama, Bwana ametangaza

habari mpaka mwisho wa dunia,

Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu

wako unakuja; Tazama, thawabu yake i

pamoja naye, Na malipo yake yako mbele

zake.

ISAYA

Page 226: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

226

EZEKIELI 34:23 Nami nitaweka mchungaji

mmoja juu yao, naye atawalisha, naam,

mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha,

naye atakuwa mchungaji wao.

24 Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na

mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati

yao; mimi, Bwana, nimesema haya.

MIKA 4:1 Lakini itakuwa katika siku za

mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya

Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa

watauendea makundi makundi.

2 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake; kwa maana katika

Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana

litatoka Yerusalemu.

MATHAYO 9:36 Na alipowaona makutano,

aliwahurumia, kwa sababu walikuwa

wamechoka na kutawanyika kama kondoo

wasio na mchungaji.

YOHANA 10:11 Mimi ndimi mchungaji

mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai

wake kwa ajili ya kondoo.

12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji,

ambaye kondoo si mali yake, humwona

mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na

kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na

kuwatawanya.

13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara;

wala mambo ya kondoo si kitu kwake.

14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio

wangu nawajua; nao walio wangu wanijua

mimi;

15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo

Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya

kondoo.

16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi

hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti

yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi

moja na mchungaji mmoja.

WARUMI 10:18 Lakini nasema, Je! Wao

hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao

imeenea duniani mwote, Na maneno yao

hata miisho ya ulimwengu.

WAEFESO 1:20 aliotenda katika Kristo

alipomfufua katika wafu, akamweka mkono

wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka,

na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo,

wala si ulimwenguni humu tu, bali katika

ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,

akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa

ajili ya kanisa; ambalo

23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake

anayekamilika kwa vyote katika vyote.

WAEBRANIA 2:14 Basi, kwa kuwa watoto

wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo

hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya

mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za

mauti, yaani, Ibilisi,

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha

yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika

hali ya utumwa.

1 PETRO 5:4 Na Mchungaji mkuu

atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya

utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 7:17 Kwa

maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati

ISAYA

Page 227: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

227

ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 23:1; Zaburi 78:71,72; Zaburi 80:1; Isaya 9:6,7; Isaya 41:27; Isaya 49:9,10; Isaya 52:7; Yohana 12:13-

15; Matendo ya Mitume 2:7-11; Waebrania 13:20; 1 Petro 2:25.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 41:8 Nawe, Israeli, mtumishi

wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa

Ibrahimu, rafiki yangu;

9 wewe niliyekushika toka miisho ya dunia,

na kukuita toka pembe zake, nikikuambia,

Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua

wala sikukutupa;

10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu

wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia,

naam, nitakushika kwa mkono wa kuume

wa haki yangu.

ISAYA 41:11-13

ISAYA 41:14 Usiogope, Yakobo uliye

mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi

nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi

wako ni Mtakatifu wa Israeli.

15 Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali

kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha

milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima

kuwa kama makapi.

16 Utawapepeta, na upepo utawapeperusha;

upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe

utamfurahia Bwana, utajitukuza katika

Mtakatifu wa Israeli.

17 Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala

hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu;

mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa

Israeli, sitawaacha.

18 Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na

chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza

jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu

kuwa vijito vya maji.

19 Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita,

mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika

mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja;

20 ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu

pamoja, ya kuwa mkono wa Bwana ndio

uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli

ndiye aliyeliumba.

ISAYA 10:17 Na mwanga wa Israeli

utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake

atakuwa mwali wa moto; nao utateketeza na

kula mbigili zake na miiba yake katika siku

moja.

ISAYA 10:20 Tena itakuwa katika siku

hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa

nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena

yeye aliyewapiga, bali watamtegemea Bwana,

Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.

ISAYA 43:15 Mimi ni Bwana, Mtakatifu

wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.

ISAYA 47:4 Mkombozi wetu, Bwana wa

majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.

ISAYA 49:7 Bwana, mkombozi wa

Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi

yeye anayedharauliwa na wanadamu;

yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye

mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona,

watasimama; wakuu nao watasujudu;

ISAYA

Page 228: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

228

kwa sababu ya Bwana aliye mwaminifu,

Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua

MARKO 1:24 akisema, Tuna nini

nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja

kutuangamiza?

YOHANA 4:14 walakini ye yote

atakayekunywa maji yale nitakayompa

mimi hataona kiu milele; bali yale maji

nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

YOHANA 6:35 Yesu akawaambia, Mimi

ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu

hataona njaa kabisa, naye aniaminiye

hataona kiu kamwe.

UFUNUO WA YOHANA 3:7 Na

kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia

andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye

mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo

wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala

hapana afungaye, naye afunga wala hapana

afunguaye.

UFUNUO WA YOHANA 7:16

Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung›aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Isaya 17:7,13; Isaya 21:10.

E02 Mahali pa huduma ya Masiha.

ISAYA 41:25 Nimemwinua mtu toka

kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua

amekuja anitajaye jina langu; naye atawajilia

maliwali kama akanyagaye matope, na kama

mfinyanzi afinyangaye udongo.

ISAYA 9:1 Lakini yeye aliyekuwa katika

dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza

aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali

katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za

mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na

njia ya bahari; ng›ambo ya Yordani, Galilaya

ya mataifa.

MATHAYO 4:13 akatoka Nazareti, akaja

akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani,

mipakani mwa Zabuloni na Naftali;

14 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya,

akisema,

15 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia

ya bahari, ng›ambo ya Yordani, Galilaya ya

mataifa,

E15 Masiha ataleta habari njema.

ISAYA 41:26 Ni nani aliyeihubiri

habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na

tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni

mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja

aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja

aliyetuonyesha; naam, hapana hata mmoja

ISAYA

Page 229: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

229

aliyesikia maneno yenu.

27 Mimi kwanza nitauambia Sayuni, Tazama;

hawa ndio; nami nitampa Yerusalemu

mletaji wa habari njema.

ISAYA 61:1 Roho ya Bwana MUNGU

i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia

mafuta niwahubiri wanyenyekevu

habari njema; amenituma ili kuwaganga

waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka

uhuru wao, na hao waliofungwa habari za

kufunguliwa kwao.

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 2:10 Malaika akawaambia,

Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea

habari njema ya furaha kuu itakayokuwa

kwa watu wote;

11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa,

kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo

Bwana.

WARUMI 10:15 Tena wahubirije,

wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni

mizuri kama nini miguu yao wahubirio

habari ya mema!

UFUNUO WA YOHANA 2:8 Na kwa

malaika wa kanisa lililoko Smirna andika;

Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na

wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa

hai.

Ona pia: Isaya 40:9; Isaya 43:9,10; Isaya 44:6,7; Isaya 48:12; Isaya 52:9.

B05 Masiha amejawa na Roho na Mtakatifu.

E13 Mungu anathibitisha huduma ya Masiha.

ISAYA 42:1 Tazama mtumishi wangu

nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi

yangu imependezwa naye; nimetia roho

yangu juu yake; naye atawatolea mataifa

hukumu.

MATHAYO 3:16 Naye Yesu alipokwisha

kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na

tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona

Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija

juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema,

Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,

ninayependezwa naye.

MATHAYO 12:16 akawakataza

wasimdhihirishe;

17 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya,

akisema,

18 Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;

Mpendwa wangu, moyo wangu

uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu

yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

MATHAYO 17:5 Alipokuwa katika kusema,

tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na

tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,

ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, ninayependezwa naye; msikieni

yeye.

ISAYA

Page 230: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

230

YOHANA 3:34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa

na Mungu huyanena maneno ya Mungu;

kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

WAEFESO 1:4 kama vile alivyotuchagua

katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya

ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio

na hatia mbele zake katika pendo.

WAFILIPI 2:7 bali alijifanya kuwa hana

utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa

ana mfano wa wanadamu;

Ona pia: Zaburi 89:19,20; Isaya 11:2-5; Isaya 43:10; Isaya 49:3-8; Isaya 50:4-9; Isaya 52:13; Isaya 61:1; Malaki 1:11; Marko 1:10,11; Luka 3:22; Yohana 1:32-34; Yohana 6:27; Matendo ya Mitume 9:15; Matendo ya Mitume 10:38; Matendo ya Mitume 11:18;

Matendo ya Mitume 26:17,18,28; Warumi 15:8-16; Waefeso 3:8; Wakolosai 1:13; 2 Petro 1:17.

B10 Unyenyekevu na umaskini wa Masiha.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E12 Masiha anatimiza sheria ya Mungu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 42:2 Hatalia, wala hatapaza sauti

yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu.

3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala

utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza

hukumu kwa kweli.

4 Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata

atakapoweka hukumu duniani; na visiwa

vitaingojea sheria yake.

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa

kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa

moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo

wangu ni mwepesi.

MATHAYO 12:19 Hatateta wala hatapaza sauti

yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.

20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala

utambi utokao moshi hatauzima, Hata

ailetapo hukumu ikashinda.

21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WAEBRANIA 2:17 Hivyo ilimpasa

kufananishwa na ndugu zake katika mambo

yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye

rehema, mwaminifu katika mambo ya

Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za

watu wake.

18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa

alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao

wanaojaribiwa.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye

aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna

hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao,

msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

1 PETRO 2:22 Yeye hakutenda dhambi,

wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano;

ISAYA

Page 231: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

231

alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi

kwake yeye ahukumuye kwa haki.

Ona pia: #1; #4; Zaburi 147:3; Isaya 53:2-12; Isaya 57:15; Isaya 61:1-3; Isaya 66:2; Yeremia 31:25; Ezekieli 34:16; Mathayo 18:11-14.

B21 Masiha ndiye Nuru.

E01 Aina ya huduma ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 42:6 Mimi, Bwana, nimekuita

katika haki, nami nitakushika mkono, na

kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu,

na nuru ya mataifa;

7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa

gerezani waliofungwa, kuwatoa wale

walioketi gizani katika nyumba ya

kufungwa.

16 Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua;

katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza;

nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na

mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya

nitayatenda, wala sitawaacha.

ISAYA 29:18 Na katika siku hiyo viziwi

watasikia maneno ya hicho chuo, na macho

ya vipofu yataona katika upofu na katika

giza.

MATHAYO 11:5 vipofu wanapata kuona,

viwete wanakwenda, wenye ukoma

wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu

wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa

habari njema.

LUKA 2:28 yeye mwenyewe alimpokea

mikononi mwake, akamshukuru Mungu,

akisema,

29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako,

Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu

wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na

kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

LUKA 3:5 Kila bonde litajazwa, Na kila

mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka

patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza

patalainishwa;

LUKA 4:17 Akapewa chuo cha nabii

Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali

palipoandikwa,

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana

amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari

njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi,

akaketi; na watu wote waliokuwamo katika

sinagogi wakamkazia macho.

21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya

yametimia masikioni mwenu.

LUKA 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao

wapate kuelewa na maandiko.

YOHANA 9:39 Yesu akasema, Mimi

nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu,

ili wao wasioona waone, nao wanaoona

wawe vipofu.

MATENDO YA MITUME 13:46

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa

wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu

ISAYA

Page 232: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

232

linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa

mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi

zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele,

angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

MATENDO YA MITUME

26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza

waiache giza na kuielekea nuru, waziache na

nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu;

kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na

urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa

imani iliyo kwangu mimi.

2 WAKORINTHO 4:6 Kwa kuwa Mungu,

aliyesema, Nuru itang›aa toka gizani, ndiye

aliyeng›aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya

elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa

Yesu Kristo.

UFUNUO WA YOHANA 3:18

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu

iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri,

na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi

wako isionekane, na dawa ya macho ya

kujipaka macho yako, upate kuona.

Ona pia: #1; #2; Zaburi 107:10-16; Zaburi 146:7,8; Isaya 9:2; Isaya 29:18; Isaya 32:3; Isaya 35:5,8; Isaya 40:4; Isaya 42:1; Isaya 45:13; Isaya 48:17; Isaya 49:6,8,9; Isaya 51:4,5; Isaya 60:1-3; Isaya 61:1; Yeremia 31:8; Yeremia 32:39,41; Luka 1:69-72,78,79; Yohana 8:12; Matendo ya Mitume 26:23; Warumi 3:25,26; Warumi 15:8,9; Wagalatia 3:15-17; Waefeso 1:17,18; Waefeso 5:8; 2 Timotheo 2:26; Waebrania 1:8,9; Waebrania 8:6; Waebrania 9:15; Waebrania

12:24; Waebrania 13:5,20; 1 Petro 2:9.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

ISAYA 42:21 Bwana akapendezwa, kwa

ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na

kuiadhimisha.

MATHAYO 3:17 na tazama, sauti kutoka

mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

MATHAYO 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja

kuitangua torati au manabii; la, sikuja

kutangua, bali kutimiliza.

YOHANA 8:29 Naye aliyenipeleka yu

pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa

sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

YOHANA 13:31 Basi huyo alipokwisha

kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa

Mwana wa Adamu, naye Mungu

ametukuzwa ndani yake.

YOHANA 15:10 Mkizishika amri zangu,

mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi

nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa

katika pendo lake.

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WARUMI 10:4 Kwa maana Kristo ni

mwisho wa sheria, ili kila aaminiye

ahesabiwe haki.

ISAYA

Page 233: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

233

Ona pia: Zaburi 40:8; Mathayo 5:18-20; Mathayo 17:5; Warumi 3:26,31; Warumi 7:12; Warumi 8:3; Wagalatia 3:13,21; Wagalatia

5:22,23; Wafilipi 3:9; Waebrania 8:10.

B01 Masiha ndiye Mwana wa Mungu.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 43:1 Lakini sasa, Bwana

aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye

aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi,

Usiogope, maana nimekukomboa;

nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja

nawe; na katika mito, haitakugharikisha;

uendapo katika moto, hutateketea; wala

mwali wa moto hautakuunguza.

ISAYA 43:3-4

ISAYA 43:5 Usiogope; maana mimi

ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka

mashariki, nitakukusanya toka magharibi;

6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie;

waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti

zangu kutoka miisho ya dunia.

7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu,

niliyemwumba kwa ajili ya utukufu

wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi

nimemfanya.

ISAYA 43:8-9

ISAYA 43:10 Ninyi ni mashahidi wangu,

asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua;

mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya

kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa

Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi

hatakuwapo mwingine.

11 Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu

mimi hapana mwokozi.

12 Nimetangaza habari, nimeokoa,

nimeonyesha, na hapakuwa mungu wa

kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni

mashahidi wangu, asema Bwana, nami ni

Mungu.

ISAYA 43:13-17

ISAYA 43:18 Msiyakumbuke mambo

ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya

zamani.

19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa

litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya

njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.

20 Wanyama wa kondeni wataniheshimu,

mbweha pia na mbuni; kwa sababu

nimewapa maji jangwani, na mito nyikani,

ili kuwanywesha watu wangu, wateule

wangu;

21 watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili

wazitangaze sifa zangu.

MATHAYO 12:18 Tazama, mtumishi wangu

niliyemteua; Mpendwa wangu, moyo wangu

uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu

yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

MATHAYO 16:16 Simoni Petro akajibu

akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa

Mungu aliye hai.

LUKA 1:47 Na roho yangu imemfurahia

Mungu, Mwokozi wangu;

LUKA 2:11 maana leo katika mji wa

Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi,

ndiye Kristo Bwana.

YOHANA 1:7 Huyo alikuja kwa ushuhuda,

ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini

kwa yeye.

8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili

aishuhudie ile nuru.

ISAYA

Page 234: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

234

YOHANA 6:69 Nasi tumesadiki, tena

tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa

Mungu.

YOHANA 15:27 Nanyi pia mnashuhudia, kwa

kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja

nami.

MATENDO YA MITUME 1:8 Lakini

mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu

Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi

wangu katika Yerusalemu, na katika

Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho

wa nchi.

MATENDO YA MITUME 4:12 Wala

hakuna wokovu katika mwingine awaye

yote, kwa maana hapana jina jingine chini

ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo

sisi kuokolewa kwalo.

1 YOHANA 4:14 Na sisi tumeona na

kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma

Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

Ona pia: #1; #2; Isaya 12:2; Isaya 44:7,8; Isaya 45:21,22; Isaya 46:10; Hosea 13:4; Luka 4:41; Yohana 11:27; Yohana 16:14; Tito

3:4-6; 2 Petro 3:18.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

ISAYA 44:1 Lakini sikia sasa, Ee Yakobo,

mtumishi wangu; na Israeli, niliyekuchagua;

2 Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka

tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi;

Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na

wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.

ZABURI 105:6 Enyi wazao wa Ibrahimu,

mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo,

wateule wake.

ZABURI 105:43 Akawatoa watu wake kwa

shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za

furaha.

MATHAYO 24:31 Naye atawatuma malaika

zake pamoja na sauti kuu ya parapanda,

nao watawakusanya wateule wake toka pepo

nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka

mwisho huu.

WARUMI 2:28 Maana yeye si Myahudi aliye

Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya

nje tu katika mwili;

29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa

ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si

katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa

wanadamu bali kwa Mungu.

WARUMI 11:7 Imekuwaje basi? Kitu

kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta

hakukipata; lakini wale waliochaguliwa

walikipata, na wengine walitiwa uzito.

WARUMI 11:28 Basi kwa habari ya Injili

wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa

habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa

wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

29 Kwa sababu karama za Mungu hazina

majuto, wala mwito wake.

WAKOLOSAI 3:12 Basi, kwa kuwa mmekuwa

wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao,

jivikeni moyo wa rehema, utu wema,

unyenyekevu, upole, uvumilivu,

1 WATHESALONIKE 1:4 Kwa maana, ndugu

mnaopendwa na Mungu, twajua uteule

wenu;

ISAYA

Page 235: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

235

2 WATHESALONIKE 2:13 Lakini imetupasa

sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili

yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa

kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo

mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho,

na kuiamini kweli;

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

2 PETRO 1:10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini

zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule

wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa

kamwe.

Ona pia: Zaburi 106:5; Isaya 41:8,9; Isaya 45:4; Yeremia 31:3; Amosi 3:1,2; Marko 13:27; Warumi 8:33.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 44:3 Kwa maana nitamimina maji

juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu

ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu

juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao

utakaowazaa;

4 nao watatokea katika manyasi, kama mierebi

karibu na mifereji ya maji.

5 Mmoja atasema, Mimi ni wa Bwana; na

mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na

mwingine ataandika juu ya mkono wake,

Kwa Bwana, na kujiita kwa jina la Israeli.

6 Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako,

Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa

kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu

mimi hapana Mungu.

ISAYA 44:7-8

ISAYA 41:4 Ni nani aliyetenda na

kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu

mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa

mwisho, mimi ndiye.

ISAYA 49:10 Hawataona njaa, wala

hawataona kiu; hari haitawapiga, wala

jua; kwa maana yeye aliyewarehemu

atawatangulia, naam, karibu na chemchemi

za maji atawaongoza.

EZEKIELI 39:29 wala sitawaficha uso wangu

tena; kwa maana nimemwaga roho yangu

juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana

MUNGU.

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

MATENDO YA MITUME 2:17

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu, na

wana wenu na binti zenu watatabiri; na

vijana wenu wataona maono; na wazee wenu

wataota ndoto.

MATENDO YA MITUME 2:33 Basi yeye,

akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume

ISAYA

Page 236: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

236

wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi

ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki

mnachokiona sasa na kukisikia.

MATENDO YA MITUME

5:14 walioamini wakazidi kuongezeka kwa

Bwana, wengi, wanaume na wanawake;

UFUNUO WA YOHANA 21:6

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa

na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi

nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya

maji ya uzima, bure.

Ona pia: #1; #2; Isaya 32:15; Isaya 35:6,7; Isaya 41:17; Isaya 43:10,11,19,20; Isaya 48:12; Isaya 59:20,21; Ezekieli 34:26;

Yoeli 2:28; Yoeli 3:18; Mika 4:2; Zekaria 8:20-23; Zekaria 12:10; Mathayo 25:34; Mathayo 27:37; Matendo ya Mitume 2:41-47;

Matendo ya Mitume 4:4; Matendo ya Mitume 10:45; 1 Timotheo 3:16; Tito 3:5,6; Ufunuo wa Yohana 1:8,11,17; Ufunuo wa Yohana

2:8; Ufunuo wa Yohana 22:13,17.

A06 Masiha ndiye Muumbaji.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 44:21 Kumbuka haya, Ee Yakobo;

nawe Israeli, maana wewe u mtumishi

wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu;

Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.

22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito,

na dhambi zako kama wingu; unirudie;

maana nimekukomboa.

23 Imbeni, enyi mbingu, maana Bwana

ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde

ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe,

msitu, na kila mti ndani yake. Maana Bwana

amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza

katika Israeli.

24 Bwana, mkombozi wako, yeye aliyekuumba

tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana,

nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu

peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye

pamoja nami?

25 Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia

waganga wazimu; niwarudishaye nyuma

wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao

kuwa ujinga;

26 nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na

kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu;

niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na

watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami

nitapainua mahali pake palipobomoka;

AMOSI 9:14 Nami nitawarejeza tena

watu wangu Israeli waliohamishwa, nao

wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na

kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu

katika mashamba, na kunywa divai yake; nao

watafanyiza bustani, na kula matunda yake.

YOHANA 1:3 Vyote vilifanyika kwa huyo;

wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote

kilichofanyika.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

1 WAKORINTHO 8:6 lakini kwetu sisi

Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu

vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake;

yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye

kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa

yeye huyo.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

ISAYA

Page 237: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

237

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

1 PETRO 1:18 Nanyi mfahamu kwamba

mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,

kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika

mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa

baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-

kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya

Kristo.

1 PETRO 4:11 Mtu akisema, na aseme

kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu,

na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na

Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo

yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una

yeye hata milele na milele. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 5:11 Nikaona

nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote

za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai,

na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu

kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-

Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na

utajiri na hekima na nguvu na heshima na

utukufu na baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu

ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na

vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

Ona pia: #1; #2; Zaburi 103:12; Isaya 1:18; Isaya 40:22; Isaya 43:25; Isaya 45:12,13; Isaya 49:13; Isaya 51:13; Isaya 61:4; Yeremia 3:12-14; Yeremia 33:8; Ezekieli 36:10; Matendo ya Mitume 3:19; Warumi 11:28,29; Waefeso 3:9; Wakolosai 1:12-18; Waebrania 1:10-12; Ufunuo wa Yohana 12:12; Ufunuo wa Yohana 18:20;

Ufunuo wa Yohana 19:1-6.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 45:17 Bali Israeli wataokolewa

na Bwana kwa wokovu wa milele; ninyi

hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na

milele.

18 Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema

hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba

dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara;

hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe

na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana

mwingine.

MATENDO YA MITUME 13:39 na

kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa

haki katika mambo yale yote asiyoweza

kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.

WARUMI 2:28 Maana yeye si Myahudi aliye

Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya

nje tu katika mwili;

29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa

ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si

katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa

wanadamu bali kwa Mungu.

WARUMI 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu

ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

ISAYA

Page 238: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

238

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

Ona pia: #1; #2; Isaya 26:4; Warumi 3:24,25; Warumi 5:1,18,19; 1 Wakorintho 1:30,31; 1 Wakorintho 6:11; Wafilipi 3:8,9; Yohana

4:15.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 45:21 Hubirini, toeni habari;

naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani

aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni

nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi,

Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi;

Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana

mwingine zaidi ya mimi.

22 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha

zote za dunia; maana mimi ni Mungu;

hapana mwingine.

23 Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili

limetoka kinywani mwangu katika haki,

wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila

goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

24 Mmoja ataniambia, Kwa Bwana, peke

yake, iko haki na nguvu; naam, watu

watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia

watatahayarika.

25 Katika Bwana wazao wote wa Israeli

watapewa haki, na kutukuka.

YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu

aliupenda ulimwengu, hata akamtoa

Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye

asipotee, bali awe na uzima wa milele.

YOHANA 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake

Baba yangu ni haya, ya kwamba kila

amtazamaye Mwana na kumwamini yeye,

awe na uzima wa milele; nami nitamfufua

siku ya mwisho.

WARUMI 9:33 kama ilivyoandikwa, Tazama,

naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na

mwamba uangushao; Na kila amwaminiye

hatatahayarika.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

WARUMI 14:10 Lakini wewe je! Mbona

wamhukumu ndugu yako? Au wewe je!

Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa

maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti

cha hukumu cha Mungu.

11 Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo,

anena Bwana, kila goti litapigwa mbele

zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.

12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu

atatoa habari zake mwenyewe mbele za

Mungu.

Ona pia: #1; #2; Mwanzo 22:15-18; Zaburi 65:5; Zekaria 12:10; Waebrania 12:2.

E08 Haki ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 46:3 Nisikilizeni, enyi wa nyumba

ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya

Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni,

mlioinuliwa tangu mimbani;

4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata

ISAYA

Page 239: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

239

wakati wenu wa mvi nitawachukueni;

nimefanya, nami nitachukua; naam,

nitachukua na kuokoa.

13 Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa

mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami

nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya

Israeli, utukufu wangu.

WARUMI 1:17 Kwa maana haki ya Mungu

inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata

imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki

ataishi kwa imani.

WARUMI 3:21 Lakini sasa, haki ya Mungu

imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa

na torati na manabii;

22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani

katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.

Maana hakuna tofauti;

WARUMI 10:3 Kwa maana, wakiwa hawaijui

haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha

haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki

ya Mungu.

4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili

kila aaminiye ahesabiwe haki.

5 Kwa maana Musa aliandika juu ya haki

itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye

hiyo ataishi kwa hiyo.

6 Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena

hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani

atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni

kumleta Kristo chini),

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

Ona pia: #1; #2.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

ISAYA 47:4 Mkombozi wetu, Bwana wa

majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.

ISAYA 44:6 Bwana, Mfalme wa Israeli,

Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema

hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa

mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

UFUNUO WA YOHANA 1:8 Mimi ni

Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema

Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na

atakayekuja, Mwenyezi.

Ona pia: Mwanzo 32:24-31; 2 Samweli 22:3; Ayubu 19:25; Zaburi 19:14; Zaburi 78:35; Isaya 41:14; Isaya 44:24; Isaya 48:17; Isaya

49:7,26; Isaya 54:5,8; Isaya 59:20; Isaya 60:16; Isaya 63:16; Ufunuo wa Yohana 1:11; Ufunuo wa Yohana 21:6; Ufunuo wa

Yohana 22:13.

E01 Aina ya huduma ya Masiha.

ISAYA 48:15 Mimi, naam, mimi,

nimenena; naam, nimemwita; nimemleta,

naye ataifanikisha njia yake.

16 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo

sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo,

mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU

amenituma, na roho yake.

17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa

Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu

wako, nikufundishaye ili upate faida,

ISAYA

Page 240: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

240

nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

YOHANA 3:34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa

na Mungu huyanena maneno ya Mungu;

kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

YOHANA 6:45 Imeandikwa katika manabii,

Na wote watakuwa wamefundishwa na

Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa

Baba huja kwangu.

YOHANA 18:20 Yesu akamjibu, Mimi

nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote

nalifundisha katika sinagogi na katika

hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala

kwa siri mimi sikusema neno lo lote.

YOHANA 20:21 Basi Yesu akawaambia tena,

Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma

mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.

22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia,

akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

WAEFESO 4:21 ikiwa mlimsikia

mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo

katika Yesu,

Ona pia: Zaburi 32:8; Isaya 49:9,10.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

ISAYA 49:1 Nisikilizeni, enyi visiwa;

tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu

mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu

tumboni; toka tumbo la mama yangu

amenitaja jina langu.

MATHAYO 1:20 Basi alipokuwa akifikiri

hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea

katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa

Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo,

maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho

Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina

lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa

watu wake na dhambi zao.

YOHANA 10:36 je! Yeye ambaye Baba

alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi

mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu

nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

WAEFESO 2:17 Akaja akahubiri amani

kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani

kwao wale waliokuwa karibu.

WAEBRANIA 12:25 Angalieni

msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa

hawakuokoka wale waliomkataa yeye

aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana

hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye

atuonyaye kutoka mbinguni;

1 PETRO 1:19 bali kwa damu ya thamani,

kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na

waa, yaani, ya Kristo.

20 Naye amejulikana kweli tangu zamani,

kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini

alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili

ISAYA

Page 241: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

241

yenu;

Ona pia: Zaburi 71:5,6; Isaya 42:1-4,12; Isaya 45:22; Isaya 49:5; Isaya 51:5; Isaya 55:3; Sefania 2:11; Luka 1:15,31; Luka 2:10,11.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

ISAYA 49:2 Naye anifanya kinywa

changu kuwa kama upanga mkali; katika

kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye

amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa;

katika podo lake amenificha;

ZABURI 27:5 Mradi atanisitiri bandani

mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika

sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya

mwamba.

ZABURI 45:5 Mishale yako ni mikali, watu

huanguka chini yako; Imo mioyoni mwa

adui za mfalme.

ZABURI 91:15 Ataniita nami nitamwitikia;

Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa

na kumtukuza;

WAEBRANIA 4:12 Maana Neno la Mungu li

hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko

upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na

viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi

ya moyo.

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

UFUNUO WA YOHANA 2:12 Na kwa

malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika;

Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo

upanga mkali, wenye makali kuwili.

UFUNUO WA YOHANA 19:15 Na

upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

Ona pia: Zaburi 45:2-5; Zaburi 91:11; Isaya 50:4; Isaya 51:16; Isaya 61:1-3; Isaya 66:19.

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 49:3 akaniambia; Wewe u

mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika

wewe nitatukuzwa.

YOHANA 12:28 Baba, ulitukuze jina

lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni,

Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

Ona pia: Yohana 13:31,32; Wafilipi 2:6-11.

ISAYA

Page 242: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

242

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 49:4 Lakini nikasema,

Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu

zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu

yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina

Mungu wangu.

MATHAYO 17:17 Yesu akajibu, akasema, Enyi

kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa

pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana

nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.

MATHAYO 23:37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu,

uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe

wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi

nimetaka kuwakusanya pamoja watoto

wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja

vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini

hamkutaka!

YOHANA 1:11 Alikuja kwake, wala walio

wake hawakumpokea.

YOHANA 17:4 Mimi nimekutukuza

duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa

niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja

nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao

pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

WARUMI 10:21 Lakini kwa Israeli asema,

Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu

wasiotii na wakaidi.

2 WAKORINTHO 12:15 Nami kwa furaha

nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa

kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo

kuwapenda sana, ninapungukiwa

kupendwa?

WAGALATIA 4:11 Nawachelea, isiwe labda

nimejitaabisha bure kwa ajili yenu.

WAFILIPI 2:9 Kwa hiyo tena Mungu

alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile

lipitalo kila jina;

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

Ona pia: Zaburi 22:22-31; Isaya 40:10; Isaya 53:10-12; Isaya 62:11; Isaya 65:2.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 49:5 Na sasa Bwana asema

hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe

mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na

Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana

mimi nimepata heshima mbele ya macho ya

Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu

zangu);

MATHAYO 15:24 Akajibu, akasema,

Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa

nyumba ya Israeli.

MATHAYO 23:37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu,

uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe

wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi

nimetaka kuwakusanya pamoja watoto

wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja

ISAYA

Page 243: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

243

vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini

hamkutaka!

YOHANA 1:11 Alikuja kwake, wala walio

wake hawakumpokea.

12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa

kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale

waliaminio jina lake;

YOHANA 3:35 Baba ampenda Mwana, naye

amempa vyote mkononi mwake.

YOHANA 13:31 Basi huyo alipokwisha

kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa

Mwana wa Adamu, naye Mungu

ametukuzwa ndani yake.

32 Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi

yake; naye atamtukuza mara.

MATENDO YA MITUME 10:36 Neno lile

alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri

habari njema ya amani kwa Yesu Kristo

(ndiye Bwana wa wote),

UFUNUO WA YOHANA 5:12 wakisema

kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo

aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na

hekima na nguvu na heshima na utukufu na

baraka.

Ona pia: Zaburi 110:1-3; Isaya 49:1; Mathayo 3:17; Mathayo 11:27; Mathayo 17:5; Mathayo 21:37-41; Mathayo 28:18; Luka 19:42; Warumi 15:8; Waefeso 1:20-22; 1 Wathesalonike 2:15,16;

Yakobo 5:20-27; 1 Petro 3:22.

A07 Atakuwa Masiha wa Israeli.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 49:6 naam, asema hivi, Ni neno

dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili

kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza

watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya

hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate

kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.

LUKA 2:32 Nuru ya kuwa mwangaza

wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako

Israeli.

LUKA 24:46 Akawaambia, Ndivyo

ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na

kufufuka siku ya tatu;

47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa

kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la

dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

MATENDO YA MITUME 13:46

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa

wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu

linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa

mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi

zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele,

angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi,

wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa

wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

WAEBRANIA 8:10 Maana hili ndilo agano

nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada

ISAYA

Page 244: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

244

ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria

zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao,

Nao watakuwa watu wangu.

Ona pia: #1; #2; Isaya 42:6; Yohana 1:4-9; Matendo ya Mitume 26:18,32.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

F03 Masiha atakataliwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 49:7 Bwana, mkombozi wa

Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi

yeye anayedharauliwa na wanadamu;

yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye

aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme

wataona, watasimama; wakuu nao

watasujudu; kwa sababu ya Bwana

aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli

aliyekuchagua

ZABURI 35:19 Walio adui zangu bure

wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu

wasining›ong›e.

MATHAYO 27:22 Pilato akawaambia, Basi,

nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema

wote, Asulibiwe.

23 Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda?

Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na

asulibiwe.

YOHANA 7:47 Basi Mafarisayo wakawajibu,

Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?

48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au

katika Mafarisayo?

49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati

wamelaaniwa.

YOHANA 15:22 Kama nisingalikuja na

kusema nao, wasingalikuwa na dhambi;

lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.

23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba

yangu.

24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda

mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi;

lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu,

na kutuchukia.

25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika

torati yao, Walinichukia bure.

WARUMI 14:11 Kwa kuwa imeandikwa,

Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti

litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi

utamkiri Mungu.

WAFILIPI 2:10 ili kwa jina la Yesu kila

goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ona pia: #1; #2; #4; Zaburi 22:6-8; Zaburi 69:7-9; Zaburi 109:3; Isaya 42:1; Isaya 52:15; Isaya 53:13; Mathayo 20:28; Mathayo

26:67; Mathayo 27:38-44; Luka 22:27; Luka 23:18,23,35; Yohana 18:40; Yohana 19:6,15; 1 Petro 2:4.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 49:8 Bwana asema hivi, Wakati

uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu

nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa

uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi

hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa;

9 kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni;

na hao walio katika giza, Jionyesheni.

Watajilisha katika njia, na juu ya majabali

ISAYA

Page 245: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

245

watapata malisho.

10 Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari

haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye

aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu

na chemchemi za maji atawaongoza.

11 Nami nitafanya milima yangu yote kuwa

njia, na njia kuu zangu zitatukuzwa zote.

12 Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na

tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka

magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.

13 Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi;

Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa

kuwa Bwana amewafariji watu wake, Naye

atawahurumia watu wake walioteswa.

ISAYA 49:14-15

ISAYA 49:16 Tazama, nimekuchora katika

vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko

mbele zangu daima.

ISAYA 49:17-21

ISAYA 49:22 Bwana MUNGU asema

hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono

wangu, na kuwatwekea kabila za watu

bendera yangu; nao wataleta wana wako

vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa

mabegani mwao.

ISAYA 49:23-26

MIKA 7:19 Atarejea na kutuhurumia;

atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa

dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.

MATHAYO 5:6 Heri wenye njaa na kiu ya

haki; Maana hao watashibishwa.

MATHAYO 12:18 Tazama, mtumishi wangu

niliyemteua; Mpendwa wangu, moyo wangu

uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu

yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

LUKA 2:13 Mara walikuwapo pamoja na

huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni,

wakimsifu Mungu, na kusema,

14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani

iwe amani kwa watu aliowaridhia.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

LUKA 12:32 Msiogope, enyi kundi dogo;

kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa

ule ufalme.

YOHANA 6:35 Yesu akawaambia, Mimi

ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu

hataona njaa kabisa, naye aniaminiye

hataona kiu kamwe.

YOHANA 10:14 Mimi ndimi mchungaji

mwema; nao walio wangu nawajua; nao

walio wangu wanijua mimi;

2 WAKORINTHO 6:2 (Kwa maana

asema, Wakati uliokubalika nalikusikia,

Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati

uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya

wokovu ni sasa)

WAEBRANIA 5:7 Yeye, siku hizo za mwili

wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa

na kumtoa katika mauti, maombi na

dua pamoja na kulia sana na machozi,

akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha

Mungu;

8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa

mateso hayo yaliyompata;

9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa

ISAYA

Page 246: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

246

sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote

wanaomtii;

UFUNUO WA YOHANA 7:15 Kwa hiyo

wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,

nao wanamtumikia mchana na usiku katika

hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha

enzi atatanda hema yake juu yao.

16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 23:1-6; Zaburi 102:13; Zaburi 107:10-14; Zaburi 146:7; Isaya 42:7; Yohana 10:1-16; Wakolosai 1:13; 1

Petro 2:9.

F11 Mateso ya Masiha.

ISAYA 50:3 Mimi nazivika mbingu

weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa

kifuniko chao.

MATHAYO 27:45 Basi tangu saa sita palikuwa

na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.

Ona pia: Luka 23:44,45; Ufunuo wa Yohana 6:12.

D02 Kazi ya Masiha kama Nabii.

ISAYA 50:4 Bwana MUNGU amenipa

ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua

jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye

aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya

asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate

kusikia kama watu wafundishwao.

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

MATHAYO 13:54 Na alipofika nchi yake,

akawafundisha katika sinagogi lao, hata

wakashangaa, wakasema, Huyu amepata

wapi hekima hii na miujiza hii?

LUKA 4:22 Wakamshuhudia wote,

wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka

kinywani mwake, wakasema, Huyu siye

mwana wa Yusufu?

LUKA 21:15 kwa sababu mimi nitawapa

kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote

hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

YOHANA 5:19 Mwana hawezi kutenda neno

mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba

analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye,

ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.

YOHANA 7:15 Wayahudi wakastaajabu

wakisema, Amepataje huyu kujua elimu,

ambaye hakusoma?

16 Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo

yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye

aliyenipeleka.

17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake,

atajua habari ya yale mafunzo, kwamba

yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi

nanena kwa nafsi yangu tu.

YOHANA 7:46 Wale watumishi wakajibu.

Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu

anavyonena.

ISAYA

Page 247: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

247

Ona pia: Kutoka 4:11,12; Zaburi 45:2; Yeremia 1:9.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 50:5 Bwana MUNGU amenizibua

sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala

sikurudi nyuma.

6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na

wang›oao ndevu mashavu yangu; sikuficha

uso wangu usipate fedheha na kutemewa

mate.

MATHAYO 26:39 Akaendelea mbele kidogo,

akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema,

Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki

kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi,

bali kama utakavyo wewe.

MARKO 14:65 Wengine wakaanza

kumtemea mate, wakamfunika uso, na

kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri.

Hata watumishi nao wakampiga makofi.

YOHANA 8:29 Naye aliyenipeleka yu

pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa

sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

YOHANA 14:31 Lakini ulimwengu ujue

ya kuwa nampenda Baba; na kama vile

Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo.

Ondokeni, twendeni zetu.

YOHANA 19:1 Basi ndipo Pilato alipomtwaa

Yesu, akampiga mijeledi.

2 Nao askari wakasokota taji ya miiba,

wakamtia kichwani, wakamvika vazi la

zambarau.

3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu!

Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.

WAFILIPI 2:7 bali alijifanya kuwa hana

utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa

ana mfano wa wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama

mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii

hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha

mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

Ona pia: Zaburi 40:6-8; Maombolezo 3:30; Mika 5:1; Mathayo 5:39; Mathayo 26:67,68; Marko 15:19; Luka 22:63; Waebrania

5:8; Waebrania 10:5-9.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 50:7 Maana Bwana MUNGU

atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari,

kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama

gumegume, nami najua ya kuwa sitaona

haya.

8 Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni

nani atakayeshindana nami? Na tusimame

pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na

anikaribie basi.

9 Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia;

ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa?

Tazama hao wote watachakaa kama vazi;

nondo atawala.

MATHAYO 27:19 Na alipokuwa ameketi juu

ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea

mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na

yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa

mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.

LUKA 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake

zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso

wake kwenda Yerusalemu;

LUKA 23:4 Pilato akawaambia wakuu

ISAYA

Page 248: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

248

wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo

ovu katika mtu huyu.

LUKA 23:14 akawaambia, Mtu huyu

mmemleta kwangu kana kwamba

anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua

mambo yake mbele yenu, ila sikuona

kwake kosa lo lote katika mambo hayo

mliyomshitaki;

YOHANA 8:46 Ni nani miongoni mwenu

anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami

nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?

WARUMI 8:33 Ni nani atakayewashitaki

wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye

kuwahesabia haki.

WAEBRANIA 1:11 Hizo zitaharibika, bali wewe

unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12 Na kama mavazi utazizinga, nazo

zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na

miaka yako haitakoma.

Ona pia: Ayubu 13:28; Zaburi 89:21-27; Zaburi 102:26; Isaya 41:1,21; Isaya 51:6-8; Ezekieli 3:8,9; Zekaria 3:1; Mathayo 5:25;

Ufunuo wa Yohana 12:10.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E19 Masiha atafariji.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 51:1-2

ISAYA 51:3 Maana Bwana ameufariji

Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa

ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama

bustani ya Edeni, na nyika yake kama

bustani ya Bwana; furaha na kicheko

zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti

ya kuimba.

4 Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu;

nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka

kwangu, nami nitaistarehesha hukumu

yangu iwe nuru ya mataifa.

5 Haki yangu i karibu, wokovu wangu

umekuwa wazi, na mikono yangu

itawahukumu kabila za watu; visiwa

vitaningoja, navyo vitautumainia mkono

wangu.

6 Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame

nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama

moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao

wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali

wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki

yangu haitatanguka.

ISAYA 51:7-10

ISAYA 51:11 Nao waliokombolewa

na Bwana watarejea, Watafika Sayuni,

wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya

vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha;

Huzuni na kuugua zitakimbia.

ISAYA 51:12-23

ISAYA 2:3 Na mataifa mengi

watakwenda na kusema, Njoni, twende juu

mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu

wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake,

nasi tutakwenda katika mapito yake maana

katika Sayuni itatoka sheria, na neno la

Bwana katika Yerusalemu.

ISAYA 34:4 Na jeshi lote la mbinguni

litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa

kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka

kama vile jani la mzabibu linyaukavyo

na kupukutika, na kama jani la mtini

linyaukavyo na kupukutika.

MATHAYO 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja

kuitangua torati au manabii; la, sikuja

ISAYA

Page 249: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

249

kutangua, bali kutimiliza.

LUKA 2:30 Kwa kuwa macho yangu

yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na

kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

MATENDO YA MITUME 26:23 ya

kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya

kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika

wafu atatangaza habari za nuru kwa watu

wake na kwa watu wa Mataifa.

2 WAKORINTHO 1:3 Na ahimidiwe

Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,

Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;

4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi

tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za

namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa

na Mungu.

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

UFUNUO WA YOHANA 6:12 Nami

nikaona, alipoifungua muhuri ya sita,

palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa

jeusi kama gunia la singa, mwezi wote

ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama

vile mtini upukutishavyo mapooza yake,

utikiswapo na upepo mwingi.

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa

ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa

kikahamishwa kutoka mahali pake.

Ona pia: #1; #2; #3:#5; #6; #7.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

E15 Masiha ataleta habari njema.

E19 Masiha atafariji.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 52:1-6

ISAYA 52:7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya

milima Miguu yake aletaye habari njema,

Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari

njema ya mambo mema, Yeye autangazaye

wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako

anamiliki!

8 Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao,

wanaimba pamoja; Maana wataona jicho

kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.

9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi

mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;

Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake,

Ameukomboa Yerusalemu.

10 Bwana ameweka wazi mkono wake

mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha

zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu

wetu.

ISAYA 52:11-12

ZABURI 22:27 Miisho yote ya dunia

itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana;

Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

ZABURI 98:1 Mwimbieni Bwana wimbo

mpya, Kwa maana ametenda mambo ya

ISAYA

Page 250: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

250

ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe,

Mkono wake mtakatifu umemtendea

wokovu.

2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni

pa mataifa ameidhihirisha haki yake.

3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu

wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya

dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.

ISAYA 66:13 Mfano wa mtu

ambaye mama yake amfariji, ndivyo

nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa

katika Yerusalemu.

ISAYA 66:18 Nami nayajua matendo

yao na mawazo yao; wakati unakuja

nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote;

nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.

MATHAYO 5:4 Heri wenye huzuni; Maana

hao watafarijika.

LUKA 1:74 Ya kwamba atatujalia sisi,

Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na

kumwabudu pasipo hofu,

LUKA 2:38 Huyu alitokea saa ile ile

akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa

wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu

akawatolea habari zake.

LUKA 3:6 Na wote wenye mwili

watauona wokovu wa Mungu.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

WARUMI 10:15 Tena wahubirije,

wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni

mizuri kama nini miguu yao wahubirio

habari ya mema!

2 WAKORINTHO 1:10 aliyetuokoa sisi

katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa;

ambaye tumemtumaini kwamba atazidi

kutuokoa;

WAEBRANIA 2:3 sisi je! Tutapataje kupona,

tusipojali wokovu mkuu namna hii?

Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha

ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 14:6 Kisha

nikaona malaika mwingine, akiruka

katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele,

awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila

taifa na kabila na lugha na jamaa,

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

ISAYA

Page 251: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

251

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Isaya 42:10-13; Isaya 48:20; Isaya 49:6; Isaya 55:12; Mathayo 24:30,31; Matendo ya Mitume 2:5-11; 2

Wakorintho 1:3-5; Wakolosai 2:2,3; Ufunuo wa Yohana 1:7.

G03 Kuinuliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

ISAYA 52:13 Tazama, mtumishi wangu

atatenda kwa busara, atatukuzwa, na

kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.

ISAYA 9:7 Maongeo ya enzi yake na

amani Hayatakuwa na mwisho kamwe,

Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme

wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa

hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata

milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio

utakaotenda hayo.

YOHANA 5:22 Tena Baba hamhukumu mtu

ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;

23 ili watu wote wamheshimu Mwana

kama vile wanavyomheshimu Baba.

Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba

aliyempeleka.

MATENDO YA MITUME 2:31 yeye

mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja

habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba

roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili

wake haukuona uharibifu.

33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono

wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba

ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga

kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

34 Maana Daudi hakupanda mbinguni;

bali yeye mwenyewe anasema, Bwana

alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa

mkono wangu wa kuume.

35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya

miguu yako.

36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini

ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo

mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

WAFILIPI 2:9 Kwa hiyo tena Mungu

alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile

lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

UFUNUO WA YOHANA 5:13 Na kila

kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi

na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu

vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

Ona pia: #1; Isaya 9:6; Isaya 49:6; Mathayo 28:18; Waefeso 1:20-23; Waebrania 1:3; Ufunuo wa Yohana 5:6-12.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 52:14 Kama vile wengi

walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa

umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na

umbo lake zaidi ya wanadamu),

ZABURI 22:6 Lakini mimi ni mdudu wala

si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa

watu.

MATHAYO 27:29 Wakasokota taji ya miiba,

wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi

katika mkono wake wa kuume; wakapiga

ISAYA

Page 252: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

252

magoti mbele yake, wakamdhihaki,

wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

30 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule

mwanzi, wakampiga-piga kichwani.

WAFILIPI 2:5 Iweni na nia iyo hiyo ndani

yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo

Yesu;

6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna

ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa

na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana

nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa

namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa

wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama

mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii

hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Ona pia: Zaburi 71:7; Mathayo 7:28; Mathayo 26:67; Marko 5:42; Marko 6:51; Luka 2:47.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

ISAYA 52:15 ndivyo atakavyowasitusha

mataifa mengi; wafalme watamfumbia

vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa

watayaona; na mambo wasiyoyasikia

watayafahamu.

MATHAYO 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote

msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,

nami nitawapumzisha.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu

aliupenda ulimwengu, hata akamtoa

Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye

asipotee, bali awe na uzima wa milele.

17 Maana Mungu hakumtuma Mwana

ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali

ulimwengu uokolewe katika yeye.

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

MATENDO YA MITUME 2:21 Na

itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana

ataokolewa.

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

MATENDO YA MITUME 17:30 Basi,

zamani zile za ujinga Mungu alijifanya

kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu

ISAYA

Page 253: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

253

wote wa kila mahali watubu.

31 Kwa maana ameweka siku

atakayowahukumu walimwengu kwa haki,

kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa

watu wote uthabiti wa mambo haya kwa

kumfufua katika wafu.

WARUMI 15:20 kadhalika nikijitahidi

kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo

jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije

nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;

21 bali kama ilivyoandikwa, Wale

wasiohubiriwa habari zake wataona, Na wale

wasiojasikia watafahamu.

WARUMI 16:25 Sasa na atukuzwe yeye

awezaye kuwafanya imara, sawasawa na

injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu

Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri

iliyositirika tangu zamani za milele,

26 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya

manabii, ikajulikana na mataifa yote kama

alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii

Imani.

2 WAKORINTHO 5:19 yaani, Mungu

alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha

ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie

makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la

upatanisho.

WAEFESO 3:8 Mimi, niliye mdogo kuliko

yeye aliye mdogo wa watakatifu wote,

nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa

utajiri wake Kristo usiopimika;

9 na kuwaangaza watu wote wajue habari za

madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani

zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba

vitu vyote;

1 TIMOTHEO 2:3 Hili ni zuri, nalo lakubalika

mbele za Mungu Mwokozi wetu;

4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na

kupata kujua yaliyo kweli.

TITO 2:11 Maana neema ya Mungu

iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

2 PETRO 3:9 Bwana hakawii kuitimiza

ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani

kukawia, bali huvumilia kwenu, maana

hapendi mtu ye yote apotee, bali wote

wafikilie toba.

1 YOHANA 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa

dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu,

bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

1 YOHANA 4:14 Na sisi tumeona na

kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma

Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

1 YOHANA 5:11 Na huu ndio ushuhuda, ya

kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na

uzima huu umo katika Mwanawe.

12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima;

asiye naye Mwana wa Mungu hana huo

uzima.

Ona pia: Mathayo 11:29; Yohana 4:42; 2 Wakorintho 5:14; 1 Timotheo 2:6; Waebrania 2:3,4,9; 1 Petro 3:18; Ufunuo wa

Yohana 22:17.

F11 Mateso ya Masiha.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

F14 Masiha hataaminiwa.

ISAYA 53:1 Ni nani aliyesadiki

habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana

amefunuliwa nani?

ISAYA

Page 254: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

254

2 Maana alikua mbele zake kama mche

mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu;

Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo

hana uzuri hata tumtamani.

MARKO 6:3 Huyu si yule seremala,

mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo,

na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu

yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.

YOHANA 12:37 Walakini ajapokuwa

amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele

yao, hawakumwamini;

38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema,

Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na

mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki;

kwa maana Isaya alisema tena,

40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito

mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao,

Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka,

nikawaponya.

WARUMI 8:3 Maana yale yasiyowezekana

kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa

sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma

Mwanawe mwenyewe katika mfano wa

mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya

dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

WARUMI 10:16 Lakini si wote walioitii ile

habari njema. Kwa maana Isaya asema,

Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu?

17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na

kusikia huja kwa neno la Kristo.

WAFILIPI 2:6 ambaye yeye mwanzo

alikuwa yuna namna ya Mungu, naye

hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni

kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa

namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa

wanadamu;

Ona pia: Isaya 11:1,2; Yeremia 23:5; Ezekieli 17:22-24; Zekaria 6:12; Luka 2:7,40,52.

F03 Masiha atakataliwa.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 53:3 Alidharauliwa na kukataliwa

na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye

sikitiko; Na kama mtu ambaye watu

humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala

hatukumhesabu kuwa kitu.

ZABURI 22:7 Wote wanionao hunicheka

sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;

8 Husema, Umtegemee Bwana; na amponye;

Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.

MATHAYO 26:65 Ndipo Kuhani Mkuu

akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru;

mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni,

sasa mmesikia hiyo kufuru yake;

66 mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema,

Imempasa kuuawa.

67 Ndipo wakamtemea mate ya uso,

wakampiga makonde; wengine wakampiga

makofi,

68 wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani

aliyekupiga?

MARKO 9:11 Wakamwuliza, wakisema,

Mbona waandishi hunena ya kwamba

imempasa Eliya kuja kwanza?

12 Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja

kwanza, na kurejeza upya yote; lakini,

pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana

ISAYA

Page 255: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

255

wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na

kudharauliwa?

13 Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja,

nao wakamtenda yote waliyoyataka kama

alivyoandikiwa.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye

aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna

hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao,

msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

Ona pia: Zaburi 69:10-12,19,20; Isaya 50:6; Mika 5:1; Zekaria 11:8-13; Mathayo 27:39-44; Marko 15:19; Luka 9:22; Luka 16:14;

Yohana 8:48.

F09 Dhabihu na kulipiwa makosa na Masiha.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 53:4 Hakika ameyachukua

masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu;

Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,

Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,

Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu

ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa

kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila

mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;

Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu

sisi sote.

MATHAYO 8:16 Hata kulipokuwa jioni,

wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa

pepo kwa neno lake, akawaponya wote

waliokuwa hawawezi,

17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii

Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu

wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

WARUMI 4:24 bali na kwa ajili yetu

sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi

tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu

Bwana wetu katika wafu;

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,

na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

2 WAKORINTHO 5:21 Yeye asiyejua

dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili

yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu

katika Yeye.

WAGALATIA 3:13 Kristo alitukomboa katika

laana ya torati, kwa kuwa alifanywa

laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

1 PETRO 2:21 Kwa sababu ndio mlioitiwa;

maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu,

akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila

haikuonekana kinywani mwake.

23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano;

alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi

kwake yeye ahukumuye kwa haki.

24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu

katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu

kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa

mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake

mliponywa.

25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama

kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji

na Mwangalizi wa roho zenu.

1 YOHANA 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa

ISAYA

Page 256: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

256

dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu,

bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Ona pia: Danieli 9:24; Mathayo 20:28; Luka 15:3-7; Warumi 5:6-10; 1 Wakorintho 15:3; Waefeso 5:2; Waebrania 9:12-15,28;

Waebrania 10:14; 1 Petro 3:18.

B02 Masiha ndiye Mwanakondoo wa Mungu.

B11 Utiifu wa Masiha.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

ISAYA 53:7 Alionewa, lakini

alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa

chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye

machinjoni, Na kama vile kondoo

anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya

yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;

Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?

Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio

hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya

watu wangu.

MATHAYO 26:62 Kisha Kuhani Mkuu

akasimama akamwambia, Hujibu neno?

Hawa wanakushuhudia nini?

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu

akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye

hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo,

Mwana wa Mungu.

64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini

nawaambieni, Tangu sasa mtamwona

Mwana wa Adamu ameketi mkono wa

kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya

mbinguni.

MATHAYO 27:12 Lakini aliposhitakiwa na

wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu

hata neno.

13 Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni

mambo mangapi wanayokushuhudia?

14 Asimjibu hata neno moja, hata liwali

akastaajabu sana.

MARKO 15:3 Nao wakuu wa makuhani

walikuwa wakimshitaki mambo mengi.

4 Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu

neno? Tazama ni mambo mangapi

wanayokushitaki!

5 Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato

akastaajabu.

LUKA 23:9 Akamwuliza maneno mengi,

yeye asimjibu lo lote.

LUKA 23:33 Na walipofika mahali

paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo

walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu,

mmoja upande wa kuume, na mmoja

upande wa kushoto.

MATENDO YA MITUME 8:30 Basi

Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma

chuo cha nabii Isaya; akanena, Je!

Yamekuelea haya unayosoma?

31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu

asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na

kuketi pamoja naye.

32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma

ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni

kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo

alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya,

Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

33 Katika kujidhili kwake hukumu yake

iliondolewa. Ni nani atakayeeleza

kizazi chake? Kwa maana uzima wake

umeondolewa katika nchi.

Ona pia: Zaburi 22:12-21; Zaburi 69:12; Mathayo 26:66-68; Yohana 19:7-9; 1 Petro 2:23.

ISAYA

Page 257: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

257

B12 Ukamilifu wa Masiha.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

ISAYA 53:9 Wakamfanyia kaburi pamoja

na wabaya; Na pamoja na matajiri katika

kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala

hapakuwa na hila kinywani mwake.

MATHAYO 27:57 Hata ilipokuwa jioni akafika

mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu,

naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa

Yesu;

58 mtu huyu alimwendea Pilato akauomba

mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru

apewe.

59 Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga

katika sanda ya kitani safi,

60 akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa

amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe

kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda

zake.

MARKO 15:27 Na pamoja naye

walisulibisha wanyang›anyi wawili, mmoja

mkono wake wa kuume na mmoja mkono

wake wa kushoto. [

28 Basi andiko likatimizwa linenalo,

Alihesabiwa pamoja na waasi.]

WAEBRANIA 5:9 naye alipokwisha

kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa

milele kwa watu wote wanaomtii;

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

Ona pia: Marko 15:43-46; Luka 23:41,50-53; Yohana 19:38-42; Matendo ya Mitume 13:28; 1 Wakorintho 15:4; Yohana 3:5.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

F09 Dhabihu na kulipiwa makosa na Masiha.

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

ISAYA 53:10 Lakini Bwana aliridhika

kumchubua; Amemhuzunisha;

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa

dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku

nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa

mkononi mwake;

11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na

kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi

wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa

wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.

ZABURI 110:3 Watu wako wanajitoa kwa

hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa

utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao

umande wa ujana wako.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote

kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la

Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote

niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo

pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa

dahari.

LUKA 22:44 Naye kwa vile alivyokuwa

katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake

ikawa kama matone ya damu yakidondoka

nchini.]

YOHANA 12:24 Amin, amin, nawaambia,

Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi,

ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali

ikifa, hutoa mazao mengi.

ISAYA

Page 258: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

258

WARUMI 3:21 Lakini sasa, haki ya Mungu

imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa

na torati na manabii;

22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani

katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.

Maana hakuna tofauti;

23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na

kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake,

kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo

Yesu;

1 WAKORINTHO 6:11 Na baadhi yenu

mlikuwa watu wa namna hii; lakini

mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini

mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu

Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

2 WAKORINTHO 5:20 Basi tu wajumbe

kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu

anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi

kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.

21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa

dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa

haki ya Mungu katika Yeye.

WAEFESO 4:11 Naye alitoa wengine kuwa

mitume, na wengine kuwa manabii; na

wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa

wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,

hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili

wa Kristo ujengwe;

WAEBRANIA 9:22 Na katika Torati karibu vitu

vyote husafishwa kwa damu, na pasipo

kumwaga damu hakuna ondoleo.

WAEBRANIA 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye

kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;

ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele

yake aliustahimili msalaba na kuidharau

aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti

cha enzi cha Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

Ona pia: Isaya 42:1; Mathayo 17:5; Yohana 12:27-32; Warumi 5:1,9,18,19; Wagalatia 4:19; Tito 3:6,7; 1 Petro 2:24; 1 Petro 3:18;

Ufunuo wa Yohana 7:9-17.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

F09 Dhabihu na kulipiwa makosa na Masiha.

H06 Kazi ya uombezi ya Masiha.

ISAYA 53:12 Kwa hiyo nitamgawia

sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya

nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu

alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa

pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua

dhambi za watu wengi, Na kuwaombea

wakosaji.

MARKO 15:28 Basi andiko likatimizwa

linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.]

LUKA 22:37 Kwa kuwa nawaambia,

hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa

kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na

wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao

mwisho wake.

LUKA 23:34 Yesu akasema, Baba,

ISAYA

Page 259: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

259

uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.

Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.

WAFILIPI 2:8 tena, alipoonekana ana

umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza

akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya

msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha

mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ona pia: Zaburi 2:8; Isaya 49:24,25; Isaya 52:15; Mathayo 12:28,29; Wakolosai 2:15; Waebrania 2:14,15.

E24 Masiha ataleta amani.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 54:1-4

ISAYA 54:5 Kwa sababu Muumba wako

ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo

jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye

Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa

dunia yote.

ISAYA 54:6-9

ISAYA 54:10 Maana milima itaondoka,

na vilima vitaondolewa; bali wema wangu

hautaondoka kwako, wala agano langu

la amani halitaondolewa; asema Bwana

akurehemuye.

11 Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani,

usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako

kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa

yakuti samawi.

12 Nami nitaifanya minara yako ya akiki

nyekundu, na malango yako ya almasi, na

mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.

13 Na watoto wako wote watafundishwa na

Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa

nyingi.

ISAYA 54:14-17

LUKA 10:21 Saa ile ile alishangilia kwa

Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru,

Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa

kuwa mambo haya umewaficha wenye

hekima na akili; umewafunulia watoto

wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo

ilivyokupendeza.

LUKA 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao

wapate kuelewa na maandiko.

YOHANA 6:45 Imeandikwa katika manabii,

Na wote watakuwa wamefundishwa na

Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa

Baba huja kwangu.

YOHANA 6:65 Akasema, Kwa sababu hiyo

nimewaambia ya kwamba hakuna mtu

awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa

na Baba yangu.

YOHANA 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo

Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka

kwa jina langu, atawafundisha yote, na

kuwakumbusha yote niliyowaambia.

MATENDO YA MITUME 14:22 wakifanya

imara roho za wanafunzi na kuwaonya

wakae katika ile Imani, na ya kwamba

imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu

kwa njia ya dhiki nyingi.

ISAYA

Page 260: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

260

WAEFESO 4:21 ikiwa mlimsikia

mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo

katika Yesu,

1 WATHESALONIKE 4:9 Katika habari ya

upendano, hamna haja niwaandikie; maana

ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu

kupendana.

WAEBRANIA 8:10 Maana hili ndilo agano

nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada

ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria

zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao,

Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

UFUNUO WA YOHANA 21:18 Na

majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi,

na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano

wa kioo safi.

19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa

imepambwa kwa vito vya thamani vya kila

namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi;

wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa

nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba

krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda

yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa

kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili

amethisto.

21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi

na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia

ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Zaburi 25:8-12; Zaburi 34:19; Zaburi 71:17; Isaya 2:3; Isaya 11:9; Isaya 51:6; Yeremia 31:34; Mathayo

11:27; Warumi 11:29; Yohana 2:20,27.

E07 Wokovu unaotolewa na Masiha.

ISAYA 55:1 Haya, kila aonaye kiu, njoni

majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni

mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,

Bila fedha na bila thamani.

YOHANA 4:13 Yesu akajibu, akamwambia,

Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

1 PETRO 2:2 Kama watoto wachanga

waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili

yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia

wokovu;

UFUNUO WA YOHANA 21:6

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa

na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi

nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya

maji ya uzima, bure.

UFUNUO WA YOHANA 22:17 Na Roho

na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye

na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na

yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

Ona pia: Isaya 41:18; Isaya 52:3; Isaya 63:1; Yoeli 3:18; Mathayo 13:44; Mathayo 26:29; Warumi 3:24; 1 Wakorintho 3:2; Waefeso

2:8.

ISAYA

Page 261: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

261

E07 Wokovu unaotolewa na Masiha.

ISAYA 55:2 Kwani kutoa fedha kwa ajili

ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu

kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa

bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha

nafsi zenu kwa unono.

MATHAYO 15:9 Nao waniabudu bure,

Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya

wanadamu.

MATHAYO 22:4 Akatuma tena watu kwa

wengine, akisema, Waambieni wale

walioalikwa, Tazameni, nimeandaa

karamu yangu; ng›ombe zangu na vinono

vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa

tayari, njoni arusini.

MARKO 7:14 Akawaita makutano tena,

akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu.

WARUMI 10:2 Kwa maana nawashuhudia

kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu,

lakini si katika maarifa.

3 Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya

Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki

yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya

Mungu.

WARUMI 10:17 Basi imani, chanzo chake ni

kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

WAFILIPI 3:7 Lakini mambo yale

yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu

kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.

Ona pia: Zaburi 34:11; Mithali 8:32; Isaya 46:6; Isaya 51:1,4,7; Yeremia 2:13; Yeremia 31:14; Habakuki 2:13; Luka 15:23; Yohana

6:48-58.

E11 Masiha atapeana uzima wa milele.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

ISAYA 55:3 Tegeni masikio yenu, na

kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami

nitafanya nanyi agano la milele, Naam,

rehema za Daudi zilizo imara.

MATHAYO 13:16 Lakini, heri macho yenu,

kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa

kuwa yanasikia.

MATHAYO 17:5 Alipokuwa katika kusema,

tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na

tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,

ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, ninayependezwa naye; msikieni

yeye.

YOHANA 5:24 Amin, amin, nawaambia,

Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini

yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele;

wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka

mautini kuingia uzimani.

25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja,

na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti

ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao

watakuwa hai.

YOHANA 6:37 Wote anipao Baba watakuja

kwangu; wala ye yote ajaye kwangu

sitamtupa nje kamwe.

YOHANA 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja

kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka;

nami nitamfufua siku ya mwisho.

45 Imeandikwa katika manabii, Na wote

watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi

kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja

kwangu.

ISAYA

Page 262: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

262

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

YOHANA 8:47 Yeye aliye wa Mungu

huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi

hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

MATENDO YA MITUME 13:34 Tena ya

kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia

uharibifu, amenena hivi, Nitawapa ninyi

mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.

Ona pia: Mwanzo 17:7; Zaburi 78:1; Zaburi 89:35-37; Mithali 4:20; Isaya 61:8; Yeremia 32:40; Yeremia 50:5; Ezekieli 37:24,25;

Mathayo 11:28; Waebrania 13:20.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

ISAYA 55:4 Angalieni, nimemweka kuwa

shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi

na jemadari kwa kabila za watu.

YOHANA 10:3 Bawabu humfungulia

huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye

huwaita kondoo wake kwa majina yao, na

kuwapeleka nje.

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

YOHANA 13:13 Ninyi mwaniita, Mwalimu,

na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana

ndivyo nilivyo.

YOHANA 18:37 Basi Pilato akamwambia,

Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe

wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi

nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili

ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili

niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli

hunisikia sauti yangu.

1 TIMOTHEO 6:13 Nakuagiza mbele

za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote,

na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama

maungamo mazuri yale mbele ya Pontio

Pilato,

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

UFUNUO WA YOHANA 3:14 Na kwa

malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika;

Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina,

Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli,

mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

Ona pia: Ezekieli 34:23,24; Danieli 9:25; Hosea 3:5; Mika 5:2-4; Mathayo 2:6; Yohana 3:16; Yohana 12:26; Waebrania 2:10;

Waebrania 5:9.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

ISAYA 55:5 Tazama, utaita taifa

usilolijua, na taifa lisilokujua wewe

litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana,

Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa

Israeli; maana amekutukuza.

YOHANA 10:16 Na kondoo wengine ninao,

ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa

ISAYA

Page 263: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

263

kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha

kutakuwako kundi moja na mchungaji

mmoja.

YOHANA 13:31 Basi huyo alipokwisha

kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa

Mwana wa Adamu, naye Mungu

ametukuzwa ndani yake.

32 Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi

yake; naye atamtukuza mara.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

WARUMI 15:21 bali kama ilivyoandikwa,

Wale wasiohubiriwa habari zake wataona, Na

wale wasiojasikia watafahamu.

1 PETRO 1:11 Wakatafuta ni wakati

upi, na wakati wa namna gani ulioonywa

na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani

yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia

mateso yatakayompata Kristo, na utukufu

utakaokuwako baada ya hayo.

Ona pia: Mwanzo 49:10; Zaburi 18:43; Zaburi 110:1-3; Isaya 11:10; Isaya 52:15; Isaya 60:5,9; Hosea 1:10; Matendo ya Mitume

3:13; Matendo ya Mitume 5:31; Waebrania 5:5.

E07 Wokovu unaotolewa na Masiha.

ISAYA 55:6 Mtafuteni Bwana, maadamu

anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

MATHAYO 6:33 Bali utafuteni kwanza

ufalme wake, na haki yake; na hayo yote

mtazidishiwa.

MATHAYO 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa;

tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi

mtafunguliwa;

8 kwa maana kila aombaye hupokea;

naye atafutaye huona; naye abishaye

atafunguliwa.

LUKA 11:9 Nami nawaambia, Ombeni,

nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona;

bisheni, nanyi mtafunguliwa.

10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea;

naye atafutaye huona; naye abishaye

atafunguliwa.

YOHANA 12:35 Basi Yesu akawaambia,

Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo.

Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza

lisije likawaweza; maana aendaye gizani

hajui aendako.

36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo

aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha

wasimwone.

WARUMI 11:7 Imekuwaje basi? Kitu

kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta

hakukipata; lakini wale waliochaguliwa

walikipata, na wengine walitiwa uzito.

WAEBRANIA 2:3 sisi je! Tutapataje kupona,

tusipojali wokovu mkuu namna hii?

Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha

ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

Ona pia: Zaburi 27:8; Zaburi 69:32; Zaburi 105:4; Zaburi 145:18; Zaburi 148:14; Isaya 12:6; Isaya 45:19; Isaya 46:13; Yeremia 29:12-14; Maombolezo 3:25; Amosi 5:4; Sefania 2:3; Malaki 3:1; Mathayo

7:7,8; Luka 12:31; Luka 13:25; Yohana 6:26; Yohana 7:33,34; 2 Wakorintho 6:1,2.

ISAYA

Page 264: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

264

E21 Masiha atasamehe dhambi.

ISAYA 55:7 Mtu mbaya na aache njia

yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake;

Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na

arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe

kabisa.

MATHAYO 7:21 Si kila mtu aniambiaye,

Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme

wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi

ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana,

hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa

jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako

kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi

kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao

maovu.

MATHAYO 9:13 Lakini nendeni, mkajifunze

maana yake maneno haya, Nataka rehema,

wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita

wenye haki, bali wenye dhambi.

LUKA 7:47 Kwa ajili ya hayo nakuambia,

Amesamehewa dhambi zake ambazo ni

nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini

asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.

LUKA 15:10 Nawaambia, Vivyo hivyo

kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu

kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja

atubuye.

LUKA 15:24 kwa kuwa huyu mwanangu

alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa

amepotea, naye ameonekana. Wakaanza

kushangilia.

MATENDO YA MITUME 3:19 Tubuni

basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate

kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako

kwake Bwana;

1 TIMOTHEO 1:15 Ni neno la

kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa,

ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni

awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza

wao ni mimi.

16 Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika

mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe

uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa

wale watakaomwamini baadaye, wapate

uzima wa milele.

Ona pia: Kutoka 34:6,7; Zaburi 130:7; Isaya 1:16-18; Isaya 43:25; Isaya 44:22; Yeremia 3:12; Ezekieli 3:18,19; Ezekieli 18:21-23,27-32; Ezekieli 33:11,14-16; Hosea 13:16; Hosea 14:1; Yona 3:10; Mathayo

23:25,26; Warumi 5:16-21; 1 Wakorintho 6:9-11; Waefeso 1:6-8; Yakobo 4:8-10.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

ISAYA 55:10 Maana kama vile mvua

ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni,

wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi,

na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu

apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;

11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo

katika kinywa changu; halitanirudia

bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo

litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

MATHAYO 24:35 Mbingu na nchi zitapita;

lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

YOHANA 6:63 Roho ndiyo itiayo

uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo

niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

ISAYA

Page 265: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

265

WARUMI 10:17 Basi imani, chanzo chake ni

kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

1 WATHESALONIKE 2:13 Kwa sababu hiyo

sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma,

kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe

la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea

si kama neno la wanadamu, bali kama

neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli

kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi

mnaoamini.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

WAEBRANIA 2:3 sisi je! Tutapataje kupona,

tusipojali wokovu mkuu namna hii?

Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha

ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

YAKOBO 1:18 Kwa kupenda kwake

mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli,

tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

1 PETRO 1:23 Kwa kuwa mmezaliwa mara

ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa

ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye

uzima, lidumulo hata milele.

Ona pia: Isaya 45:23; Isaya 46:10; Luka 8:11-16.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 55:12 Maana mtatoka kwa furaha,

Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu

milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti

yote ya kondeni itapiga makofi.

13 Badala ya michongoma utamea msunobari,

Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili

litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa

ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

WARUMI 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa

haki itokayo katika imani, na mwe na amani

kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu

Kristo,

WARUMI 15:13 Basi Mungu wa tumaini

na awajaze ninyi furaha yote na amani

katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na

tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

1 WAKORINTHO 6:9 Au hamjui ya kuwa

wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?

Msidanganyike; waasherati hawataurithi

ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu,

wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi,

wala watukanaji, wala wanyang›anyi.

11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna

hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa,

lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana

Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

2 WAKORINTHO 5:17 Hata imekuwa,

mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe

kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa

mapya.

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

WAKOLOSAI 1:11 mkiwezeshwa kwa uwezo

wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake,

mpate kuwa na saburi ya kila namna na

uvumilivu pamoja na furaha;

ISAYA

Page 266: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

266

UFUNUO WA YOHANA 2:7 Yeye

aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo

Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye,

nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio

katika bustani ya Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 22:2 katikati

ya njia kuu yake. Na upande huu na upande

huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima,

uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye

kutoa matunda yake kila mwezi; na majani

ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: #1; #2; #5.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 56:6 Na wageni, walioandamana

na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda

jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila

aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana

agano langu;

7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu

mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba

yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao

zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa

maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya

sala kwa mataifa yote.

8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa

katika Israeli asema, Pamoja na hayo

nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao

walio wake waliokusanywa.

ISAYA 43:6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo

kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka

mbali, na binti zangu kutoka miisho ya

dunia.

ISAYA 49:22 Bwana MUNGU asema

hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono

wangu, na kuwatwekea kabila za watu

bendera yangu; nao wataleta wana wako

vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa

mabegani mwao.

MARKO 11:17 Akafundisha, akasema,

Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa

nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi

mmeifanya kuwa pango la wanyang›anyi.

YOHANA 10:16 Na kondoo wengine ninao,

ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa

kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha

kutakuwako kundi moja na mchungaji

mmoja.

YOHANA 11:51 Na neno hilo yeye

hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa

alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri

ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa

hilo.

52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini

pamoja na hayo awakusanye watoto wa

Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.

MATENDO YA MITUME 2:41 Nao

waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku

ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

MATENDO YA MITUME 10:34 Petro

akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika

natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;

35 bali katika kila taifa mtu amchaye na

kutenda haki hukubaliwa na yeye.

WAEFESO 1:10 Yaani, kuleta madaraka ya

wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote

katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya

ISAYA

Page 267: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

267

duniani pia. Naam, katika yeye huyo;

WAEFESO 2:11 Kwa ajili ya hayo kumbukeni

ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa

Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa

Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa

Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini

iliyofanyika kwa mikono;

12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo,

mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni

wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa

hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi

mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa

karibu kwa damu yake Kristo.

WAEFESO 2:18 Kwa maana kwa yeye sisi

sote tumepata njia ya kumkaribia Baba

katika Roho mmoja.

19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala

wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na

watakatifu, watu wa nyumbani mwake

Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na

manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni

jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu

ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya

Habili.

WAEBRANIA 13:15 Basi, kwa njia

yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa

daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo

jina lake.

1 PETRO 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe

yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za

roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya

Yesu Kristo.

UFUNUO WA YOHANA 14:1 Kisha

nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo

amesimama juu ya mlima Sayuni, na

watu mia na arobaini na nne elfu pamoja

naye, wenye jina lake na jina la Baba yake

limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

Ona pia: #1; #3; #4; Isaya 56:3; Matendo ya Mitume 11:23; 2 Wakorintho 8:5; Waebrania 10:19-22; 1 Petro 1:1,2.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

G06 Makao ya Roho Mtakatifu.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 57:15 Maana yeye aliye juu,

aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina

lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi

mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena

pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu

na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za

wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao

waliotubu.

16 Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote,

wala sitakuwa na hasira siku zote; maana

roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi

nilizozifanya.

ISAYA

Page 268: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

268

17 Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake

naliona hasira, nikampiga; nalificha uso

wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea

kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake

mwenyewe.

18 Nimeziona njia zake; nami nitamponya;

nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja

zake, yeye na hao wanaomlilia.

MATHAYO 19:28 Yesu akawaambia, Amin,

nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata

mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi

Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu

wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi

na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na

mbili za Israeli.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

YOHANA 1:12 Bali wote waliompokea

aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa

Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa

mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya

mtu, bali kwa Mungu.

YOHANA 3:3 Yesu akajibu, akamwambia,

Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa

mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa

Mungu.

4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu

kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia

tumboni mwa mamaye mara ya pili

akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu

asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi

kuuingia ufalme wa Mungu.

6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na

kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna

budi kuzaliwa mara ya pili.

8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake

waisikia, lakini hujui unakotoka wala

unakokwenda; kadhalika na hali yake kila

mtu aliyezaliwa kwa Roho.

WAGALATIA 6:15 Kwa sababu kutahiriwa si

kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.

WAEFESO 2:1 Nanyi mlikuwa wafu kwa

sababu ya makosa na dhambi zenu;

WAKOLOSAI 3:9 Msiambiane uongo, kwa

kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja

na matendo yake;

10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate

ufahamu sawasawa na mfano wake yeye

aliyeuumba.

TITO 3:5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

YAKOBO 1:18 Kwa kupenda kwake

mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli,

tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

1 PETRO 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba

wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa

rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili

tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka

kwake Yesu Kristo katika wafu;

1 PETRO 1:23 Kwa kuwa mmezaliwa mara

ISAYA

Page 269: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

269

ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa

ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye

uzima, lidumulo hata milele.

1 PETRO 2:2 Kama watoto wachanga

waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili

yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia

wokovu;

1 YOHANA 2:29 Kama mkijua ya kuwa yeye

ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye

haki amezaliwa na yeye.

1 YOHANA 3:9 Kila mtu aliyezaliwa na

Mungu hatendi dhambi, kwa sababu

uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi

kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa

kutokana na Mungu.

1 YOHANA 5:1 Kila mtu aaminiye kwamba

Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila

mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda

hata yeye aliyezaliwa na yeye.

1 YOHANA 5:4 Kwa maana kila kitu

kilichozaliwa na Mungu huushinda

ulimwengu; na huku ndiko kushinda

kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

1 YOHANA 5:18 Twajua ya kuwa kila mtu

aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali

yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala

yule mwovu hamgusi.

Ona pia: #2; Zaburi 51:10; Zaburi 103:9-16; Zaburi 138:6; Zaburi 147:3; Isaya 66:2; Yeremia 31:33; Yeremia 32:40; Ezekieli 11:19; Ezekieli 18:31; Ezekieli 36:26,27; Mathayo 5:3; Luka 15:20-24;

Yohana 14:23; Warumi 5:21; 2 Wakorintho 5:17; Waefeso 2:5,8,10; Wafilipi 2:13; Wakolosai 1:13; Wakolosai 2:13; Yakobo 4:6.

E24 Masiha ataleta amani.

ISAYA 57:19 Mimi nayaumba matunda

ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye

mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema

Bwana; nami nitamponya.

LUKA 2:14 Atukuzwe Mungu juu

mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu

aliowaridhia.

WAEFESO 2:14 Kwa maana yeye ndiye

amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa

wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza

cha kati kilichotutenga.

15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili

wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika

maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu

mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya

amani.

16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu

katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba,

akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.

17 Akaja akahubiri amani kwenu ninyi

mliokuwa mbali, na amani kwao wale

waliokuwa karibu.

D06 Masiha atakuwa Mshauri.

D07 Masiha atakuwa Mpatanishi.

E08 Haki ya Masiha.

H06 Kazi ya uombezi ya Masiha.

ISAYA 59:16 Akaona ya kuwa hapana

mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana

mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe

ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo

iliyomsaidia.

ISAYA

Page 270: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

270

ZABURI 20:6 Sasa najua kuwa Bwana

amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka

mbingu zake takatifu.

ZABURI 80:17 Mkono wako na uwe juu

yake Mtu wa mkono wako wa kuume; Juu ya

mwanadamu uliyemfanya Kuwa imara kwa

nafsi yako;

1 TIMOTHEO 2:5 Kwa sababu Mungu ni

mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na

wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo

Yesu;

WAEBRANIA 9:15 Na kwa sababu hii ni

mjumbe wa agano jipya, ili, mauti

ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa

yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao

walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa

milele.

WAEBRANIA 10:7 Ndipo niliposema,

Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo

nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako,

Mungu.

1 YOHANA 2:1 Watoto wangu wadogo,

nawaandikia haya ili kwamba msitende

dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi

tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo

mwenye haki,

Ona pia: Mwanzo 18:23-32; Zaburi 40:7; Zaburi 98:1,2; Zaburi 106:23; Zaburi 108:6; Zaburi 138:7; Isaya 63:5; Yeremia 5:1;

Ezekieli 22:30.

E08 Haki ya Masiha.

ISAYA 59:17 Akajivika haki kama deraya

kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani

pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi

yake, naye alivikwa wivu kama joho.

ISAYA 11:5 Na haki itakuwa mshipi

wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa

kujifungia.

WARUMI 13:12 Usiku umeendelea sana,

mchana umekaribia, basi na tuyavue

matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.

2 WAKORINTHO 6:7 katika neno la

kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za

haki za mkono wa kuume na za mkono wa

kushoto;

WAEFESO 6:14 Basi simameni, hali

mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya

haki kifuani,

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa

Injili ya amani;

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani,

ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale

yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga

wa Roho ambao ni neno la Mungu;

1 WATHESALONIKE 5:8 Lakini sisi tulio

wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika

kifuani imani na upendo, na chapeo yetu

iwe tumaini la wokovu.

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

ISAYA

Page 271: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

271

haki ahukumu na kufanya vita.

Ona pia: Isaya 51:9.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 59:18 Kadiri ya matendo yao,

kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao

wampingao, malipo kwa adui zake; naye

atavirudishia visiwa malipo.

19 Basi, wataliogopa jina la Bwana toka

magharibi, na utukufu wake toka maawio ya

jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa

mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya

Bwana.

20 Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwao

waachao maasi yao katika Yakobo, asema

Bwana.

ISAYA 11:10 Na itakuwa katika siku hiyo,

shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa

kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa

watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia

patakuwa na utukufu.

MALAKI 1:11 Kwa maana tokea maawio

ya jua hata machweo yake jina langu ni

kuu katika Mataifa; na katika kila mahali

unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa

jina langu; maana jina langu ni kuu katika

Mataifa, asema Bwana wa majeshi.

MATHAYO 16:27 Kwa sababu Mwana wa

Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake

pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa

kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #4; #5; Mambo ya Walawi 25:25,26; Ruthu 4:1-22; Isaya 41:14; Isaya 44:6,24; Isaya 48:17; Isaya 49:7; Isaya

54:5,8; Isaya 60:16; Isaya 63:16; Yeremia 14:8; 2 Wakorintho 1:10; Wagalatia 4:5; 2 Timotheo 4:18; Tito 2:14; Waebrania 2:15;

2 Petro 2:9.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 59:21 Tena katika habari zangu,

hili ndilo agano langu nao, asema Bwana;

roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu

niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka

kinywani mwako, wala kinywani mwa wana

wako, wala kinywani mwa wajukuu wako,

asema Bwana, tangu leo na hata milele.

YEREMIA 31:31 Angalia, siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na

nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya

na baba zao, katika siku ile nilipowashika

ISAYA

Page 272: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

272

mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri;

ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa

nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na

nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na

katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa

Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake,

na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue

Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu

mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye

mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;

maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi

yao sitaikumbuka tena.

LUKA 11:13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu

mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,

je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana

kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

WARUMI 9:6 Si kana kwamba neno la

Mungu limetanguka. Maana hawawi wote

Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao

wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako

wataitwa;

8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto

wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi

wanahesabiwa kuwa wazao.

WAEBRANIA 8:8 Maana, awalaumupo, asema

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami

nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba

ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

Ona pia: #1; #2; Mathayo 26:26-29.

B14 Masiha anatambulisha utukufu wa Mungu

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 60:1 Ondoka, uangaze; kwa kuwa

nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana

umekuzukia.

2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na

giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali

Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake

utaonekana juu yako.

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme

kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4 Inua macho yako, utazame pande zote; Wote

wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana

wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako

watabebwa nyongani.

5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo

wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa

wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri

wa mataifa utakuwasilia.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

LUKA 2:30 Kwa kuwa macho yangu

yameuona wokovu wako,

ISAYA

Page 273: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

273

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na

kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

YOHANA 1:9 Kulikuwako Nuru halisi,

amtiaye nuru kila mtu, akija katika

ulimwengu.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

MATENDO YA MITUME

26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza

waiache giza na kuielekea nuru, waziache na

nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu;

kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na

urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa

imani iliyo kwangu mimi.

WARUMI 11:11 Basi nasema, Je!

Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha!

Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia

Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.

12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa

ulimwengu, na upungufu wao umekuwa

utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu

wao?

13 Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa

Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa

watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo

yangu,

14 nipate kuwatia wivu walio damu moja na

mimi na kuwaokoa baadhi yao.

15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta

upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa

kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya

kufa?

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Mathayo 15:14; Mathayo 23:19,24; Matendo ya Mitume 14:16; Matendo ya Mitume 17:30,31;

Warumi 15:9-12; Waefeso 5:14.

B21 Masiha ndiye Nuru.

G05 Masiha atapata matunda mengi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 60:6-7

ISAYA 60:8 Ni nani hawa warukao kama

wingu, Na kama njiwa waendao madirishani

kwao?

9 Hakika yake visiwa vitaningojea, Na

merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta

wana wako kutoka mbali, Na fedha yao

na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili

ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili

yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa

amekutukuza wewe.

10 Na wageni watajenga kuta zako, Na

wafalme wao watakuhudumu; Maana katika

ghadhabu yangu nalikupiga, Lakini katika

upendeleo wangu nimekurehemu.

11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima;

Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu

wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na

wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

ISAYA

Page 274: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

274

ISAYA 60:12-15

ISAYA 60:16 Utanyonya maziwa ya

mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe

utajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi

wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa

Yakobo.

17 Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala;

ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti,

shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena

nitawafanya wasimamizi wako wawe amani,

Na hao wakutozao fedha kuwa haki.

18 Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako,

Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani

mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na

malango yako, Sifa.

19 Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa

mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa

mwangaza wake; Bali Bwana atakuwa nuru

ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa

utukufu wako.

20 Jua lako halitashuka tena, Wala mwezi wako

hautajitenga; Kwa kuwa Bwana mwenyewe

atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za

kuomboleza kwako zitakoma.

21 Watu wako nao watakuwa wenye haki wote,

Nao watairithi nchi milele;

ZABURI 37:29 Wenye haki watairithi nchi,

Nao watakaa humo milele.

ZABURI 72:11 Naam, wafalme wote na

wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.

ISAYA 26:1 Siku ile wimbo huu

utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao

mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa

kuta na maboma.

2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki,

lishikalo kweli, liingie.

ISAYA 49:23 Na wafalme watakuwa baba

zako za kulea, na malkia zao mama zako

za kulea; watainama mbele yako kifudifudi,

na kuramba mavumbi ya miguu yako;

nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena

waningojeao hawatatahayarika.

YOHANA 9:5 Muda nilipo ulimwenguni,

mimi ni nuru ya ulimwengu.

YOHANA 12:28 Baba, ulitukuze jina

lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni,

Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

YOHANA 15:1 Mimi ndimi mzabibu wa

kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na

kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

YOHANA 15:8 Hivyo hutukuzwa Baba

yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi

mtakuwa wanafunzi wangu.

WARUMI 1:17 Kwa maana haki ya Mungu

inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata

imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki

ataishi kwa imani.

WARUMI 5:19 Kwa sababu kama kwa kuasi

kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa

katika hali ya wenye dhambi, kadhalika

kwa kutii kwake mmoja watu wengi

wameingizwa katika hali ya wenye haki.

WAEFESO 2:10 Maana tu kazi yake,

tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende

matendo mema, ambayo tokea awali Mungu

aliyatengeneza ili tuenende nayo.

2 PETRO 3:13 Lakini, kama ilivyo ahadi

ISAYA

Page 275: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

275

yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi

mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

UFUNUO WA YOHANA 21:12 ulikuwa

na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango

kumi na miwili, na katika ile milango

malaika kumi na wawili; na majina

yameandikwa ambayo ni majina ya kabila

kumi na mbili za Waisraeli.

13 Upande wa mashariki milango mitatu;

na upande wa kaskazini milango mitatu;

na upande wa kusini milango mitatu; na

upande wa magharibi milango mitatu.

14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi

na miwili, na katika ile misingi majina kumi

na mawili ya wale mitume kumi na wawili

wa Mwana-Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 21:23 Na mji

ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,

kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru,

na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe

mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa

ndani yake.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe

cho chote kilicho kinyonge, wala yeye

afanyaye machukizo na uongo, bali wale

walioandikwa katika kitabu cha uzima cha

Mwana-Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 22:5 Wala

hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja

ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana

Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Zaburi 1:5; Zaburi 112:1-6; Isaya 57:13.

D01 Kupakwa kwa mafuta kwa Masiha.

E06 Kazi na mwito wa Masiha.

E15 Masiha ataleta habari njema.

H11 Masiha atatukuzwa.

ISAYA 61:1 Roho ya Bwana MUNGU

i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia

mafuta niwahubiri wanyenyekevu

habari njema; amenituma ili kuwaganga

waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka

uhuru wao, na hao waliofungwa habari za

kufunguliwa kwao.

2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,

na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji

wote waliao;

3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni,

wapewe taji ya maua badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate

kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana,

ili atukuzwe.

ISAYA 57:15 Maana yeye aliye juu,

aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina

lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi

mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena

pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu

na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za

wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao

waliotubu.

MATHAYO 3:16 Naye Yesu alipokwisha

kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na

tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona

Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija

juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema,

ISAYA

Page 276: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

276

Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,

ninayependezwa naye.

MATHAYO 5:4 Heri wenye huzuni; Maana

hao watafarijika.

5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi

nchi.

LUKA 4:17 Akapewa chuo cha nabii

Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali

palipoandikwa,

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana

amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari

njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi,

akaketi; na watu wote waliokuwamo katika

sinagogi wakamkazia macho.

21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya

yametimia masikioni mwenu.

YOHANA 1:32 Tena Yohana akashuhudia

akisema, Nimemwona Roho akishuka kama

hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.

33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye

aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo

aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho

akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye

abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa

huyu ni Mwana wa Mungu.

YOHANA 15:11 Hayo nimewaambia, ili

furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha

yenu itimizwe.

2 WAKORINTHO 6:2 (Kwa maana

asema, Wakati uliokubalika nalikusikia,

Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati

uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya

wokovu ni sasa)

2 WAKORINTHO 7:9 Sasa nafurahi, si

kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali

kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu.

Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu,

ili msipate hasara kwa tendo letu katika

neno lo lote.

10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu

hufanya toba liletalo wokovu lisilo na

majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

Ona pia: #1; Zaburi 30:11; Isaya 12:1; Ezekieli 16:8-13; Yohana 14:14-26; Tito 3:4-6.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 61:4 Nao watajenga mahali pa

kale palipoharibiwa, watapainua mahali

palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza

miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa

kizazi baada ya kizazi.

5 Na wageni watasimama na kulisha makundi

yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa

wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu

yenu.

6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana;

watu watawaiteni wahudumu wa Mungu

wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia

utukufu wao.

7 Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na

badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao;

basi katika nchi yao watamiliki maradufu;

furaha yao itakuwa ya milele.

ISAYA

Page 277: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

277

8 Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu

ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami

nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana

nao agano la milele.

9 Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa,

na uzao wao katika kabila za watu; wote

wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi

kilichobarikiwa na Bwana.

MATENDO YA MITUME 20:28 Jitunzeni

nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo

Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa

waangalizi ndani yake, mpate kulilisha

kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu

yake mwenyewe.

WAEBRANIA 8:8 Maana, awalaumupo, asema

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami

nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba

ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na

dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya

lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu

kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki

karibu na kutoweka.

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

1 PETRO 5:1 Nawasihi wazee walio

kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na

shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa

utukufu utakaofunuliwa baadaye;

2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na

kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa

hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka

fedha ya aibu, bali kwa moyo.

3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya

mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa

lile kundi.

4 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa,

mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 1:6 na

kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa

Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu

una Yeye hata milele na milele. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 5:10

ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

UFUNUO WA YOHANA 20:6 Huo

ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu,

ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa

kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina

nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu

na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye

hiyo miaka elfu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

ISAYA

Page 278: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

278

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

G05 Masiha atapata matunda mengi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 61:10 Nitafurahi sana katika

Bwana, nafsi yangu itashangilia katika

Mungu wangu; maana amenivika mavazi

ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama

bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha

maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa

vyombo vya dhahabu.

11 Maana kama nchi itoavyo machipuko

yake, na kama bustani ioteshavyo vitu

vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana

MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele

ya mataifa yote.

MWANZO 3:11 Akasema, Ni nani

aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula

wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

LUKA 1:46 Mariamu akasema, Moyo

wangu wamwadhimisha Bwana,

47 Na roho yangu imemfurahia Mungu,

Mwokozi wangu;

2 WAKORINTHO 5:2 Maana katika

nyumba hii twaugua, tukitamani sana

kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;

3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu

uchi.

UFUNUO WA YOHANA 3:5 Yeye

ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe,

wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu

cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za

Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

UFUNUO WA YOHANA 3:18

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu

iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri,

na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi

wako isionekane, na dawa ya macho ya

kujipaka macho yako, upate kuona.

UFUNUO WA YOHANA 7:14

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.

Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika

dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,

na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-

Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 19:7 Na

tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri,

ing›arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo

ni matendo ya haki ya watakatifu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Mwanzo 2:25; Mwanzo 3:7-15; Wafilipi 4:4; 1 Petro 1:3-9; 1 Petro 2:9.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 62:1 Kwa ajili ya Sayuni

sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu

sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama

mwangaza, na wokovu wake kama taa

iwakayo.

2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme

wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa

jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha

Bwana.

3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono

wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi

ISAYA

Page 279: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

279

mwa Mungu wako.

MATENDO YA MITUME 9:15 Lakini

Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana

huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue

Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na

wana wa Israeli.

1 WAKORINTHO 9:25 Na kila

ashindanaye katika michezo hujizuia

katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi

wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee

taji isiyoharibika.

WAFILIPI 4:1 Basi, ndugu zangu,

wapendwa wangu, ninaowaonea shauku,

furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni

imara katika Bwana, wapenzi wangu.

2 TIMOTHEO 4:8 baada ya hayo nimewekewa

taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu

mwenye haki, atanipa siku ile; wala si

mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda

kufunuliwa kwake.

YAKOBO 1:12 Heri mtu astahimiliye

majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa

ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia

wampendao.

1 PETRO 5:4 Na Mchungaji mkuu

atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya

utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 2:10 Usiogope

mambo yatakayokupata; tazama, huyo

Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili

mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku

kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami

nitakupa taji ya uzima.

UFUNUO WA YOHANA 2:17 Yeye

aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo

Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye

nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa,

nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo

limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye

anayelipokea.

UFUNUO WA YOHANA 3:11 Naja

upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu

akaitwaa taji yako.

UFUNUO WA YOHANA 4:4 Na viti

ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha

enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini

na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi

meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na

taji za dhahabu.

UFUNUO WA YOHANA 4:10 ndipo hao

wazee ishirini na wanne huanguka mbele

zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi,

nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na

milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile

kiti cha enzi, wakisema,

11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu

wetu, kuupokea utukufu na heshima na

uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba

vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako

vilikuwako, navyo vikaumbwa.

UFUNUO WA YOHANA 12:1 Na ishara

kuu ilionekana mbinguni; mwanamke

aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya

miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya

nyota kumi na mbili.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Mathayo 27:29; 1 Wathesalonike 2:19; Ufunuo wa Yohana 6:2; Ufunuo wa Yohana 14:14.

ISAYA

Page 280: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

280

B20 Upendo wa Mfalme kwa watu Wake.

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 62:4 Hutaitwa tena Aliyeachwa,

wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali

utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa

kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako

itaolewa.

5 Maana kama vile kijana amwoavyo

mwanamwali, ndivyo wana wako

watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana

arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo

Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee

Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala

usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana,

msiwe na kimya;

7 wala msimwache akae kimya, mpaka

atakapoufanya imara Yerusalemu, na

kuufanya kuwa sifa duniani.

8 Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume,

na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika

sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa

chakula chao; wala wageni hawatakunywa

divai yako, uliyoifanyia kazi.

9 Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na

kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio

watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu

pangu.

HOSEA 2:20 Nami nitakuposa kwa

uaminifu; nawe utamjua Bwana.

21 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika,

asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo

zitaiitikia nchi;

ISAYA 54:6 Maana Bwana amekuita

kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa

rohoni, kama mke wakati wa ujana,

atupwapo, asema Mungu wako.

7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa

rehema nyingi nitakukusanya.

SEFANIA 3:17 Bwana, Mungu wako,

yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;

Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza

katika upendo wake, Atakufurahia kwa

kuimba.

LUKA 12:32 Msiogope, enyi kundi dogo;

kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa

ule ufalme.

LUKA 15:7 Nawaambia, Vivyo hivyo

kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya

mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa

ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao

hawana haja ya kutubu.

YOHANA 3:29 Aliye naye bibi arusi ndiye

bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi,

yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia

sana sauti yake bwana arusi.

YOHANA 15:11 Hayo nimewaambia, ili

furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha

yenu itimizwe.

WARUMI 9:27 Isaya naye atoa sauti yake

juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana

wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

UFUNUO WA YOHANA 19:7 Na

tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu

wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo

ISAYA

Page 281: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

281

imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

UFUNUO WA YOHANA 21:9 Akaja

mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na

vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya

mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo

huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi,

mke wa Mwana-Kondoo.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Kumbukumbu la Torati 4:31; Kumbukumbu la Torati 30:9; Kumbukumbu la Torati 31:6,8,16-18; Yoshua 1:5; 1 Samweli 12:22; 1 Wafalme 19:10; 1 Mambo ya

Nyakati 16:31; Zaburi 16:11; Zaburi 94:14; Isaya 49:14-16; Isaya 53:10; Isaya 54:1,6,7; Isaya 60:10; Isaya 62:12; Yeremia 32:41;

Ezekieli 20:41; Hosea 1:7-11; Yohana 17:13; Warumi 14:17; Wafilipi 2:2; Ufunuo wa Yohana 21:2.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 62:10 Piteni, piteni, katika

malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni,

tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni

bendera kwa ajili ya kabila za watu.

11 Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka

mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni,

Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama,

thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake

yako mbele zake.

12 Nao watawaita, Watu watakatifu,

Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa,

Aliyetafutwa, Mji usioachwa.

KUTOKA 17:15 Musa akajenga madhabahu,

akaiita jina lake Yehova-nisi;

ISAYA 11:10 Na itakuwa katika siku hiyo,

shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa

kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa

watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia

patakuwa na utukufu.

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

MATHAYO 3:3 Kwa sababu huyo ndiye

aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti

ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya

Bwana, Yanyosheni mapito yake.

MATHAYO 21:5 Mwambieni binti Sayuni

Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-

punda, mtoto wa punda.

LUKA 1:17 Naye atatangulia mbele

zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake,

ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee

watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye

haki, na kumwekea Bwana tayari watu

waliotengenezwa.

YOHANA 3:14 Na kama vile Musa

alivyomwinua yule nyoka jangwani,

vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi

kuinuliwa;

WARUMI 10:18 Lakini nasema, Je! Wao

hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao

imeenea duniani mwote, Na maneno yao

hata miisho ya ulimwengu.

UFUNUO WA YOHANA 22:12 Tazama,

naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami,

kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Kumbukumbu la Torati 7:6; Kumbukumbu la Torati 26:19; Kumbukumbu la Torati 28:9;

Zaburi 98:1-3; Wimbo Ulio Bora 5:10; Isaya 18:3; Isaya 49:22; Isaya 57:14; Isaya 59:19; Marko 16:15; Warumi 10:11-18.

ISAYA

Page 282: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

282

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

D06 Masiha atakuwa Mshauri.

F11 Mateso ya Masiha.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ISAYA 63:1 Ni nani huyu atokaye

Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu

kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari,

Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?

2 Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na

nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?

3 Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala

katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;

Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu,

Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na

mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu

yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.

4 Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni

mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa

umewadia.

5 Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia;

Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye

kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe

uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo

iliyonitegemeza.

6 Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira

yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu,

Nami nikaimwaga damu yao chini.

LUKA 12:50 Lakini nina ubatizo unipasao

kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata

utimizwe!

YOHANA 16:32 Tazama, saa yaja, naam,

imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila

mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke

yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa

kuwa Baba yupo pamoja nami.

WAEBRANIA 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng›ao

wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,

akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake,

akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi

mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

UFUNUO WA YOHANA 14:19 Malaika

yule akautupa mundu wake hata nchi,

akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa

zabibu katika shinikizo hilo kubwa la

ghadhabu ya Mungu.

20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu

ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye

hatamu za farasi, kama mwendo wa maili

mia mbili.

UFUNUO WA YOHANA 19:13 Naye

amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na

jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,

wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani

nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

Ona pia: #1; #5; Isaya 59:16,17; Ufunuo wa Yohana 6:9-17; Ufunuo wa Yohana 18:20.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ISAYA 63:7 Nitautaja wema wa Bwana,

sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia

Bwana; na wingi wa wema wake kwa

nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa

rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.

8 Maana alisema, Hakika ndio watu wangu

ISAYA

Page 283: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

283

hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi

wao.

9 Katika mateso yao yote yeye aliteswa,

na malaika wa uso wake akawaokoa;

kwa mapenzi yake, na huruma zake,

aliwakomboa mwenyewe; akawainua,

akawachukua siku zote za kale.

MATHAYO 14:14 Yesu akatoka, akaona

mkutano mkuu, akawahurumia,

akawaponya wagonjwa wao.

WARUMI 11:1 Basi, nauliza, Je! Mungu

aliwasukumia mbali watu wake? Hasha!

Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja

wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya

Benyamini.

2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake

aliowajua tokea awali. Au hamjui yale

yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi

anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,

WARUMI 11:28 Basi kwa habari ya Injili

wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa

habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa

wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

TITO 3:4 Lakini wema wake Mwokozi wetu

Mungu, na upendo wake kwa wanadamu,

ulipofunuliwa, alituokoa;

5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya

Yesu Kristo Mwokozi wetu;

7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake,

tupate kufanywa warithi wa uzima wa

milele, kama lilivyo tumaini letu.

WAEBRANIA 2:17 Hivyo ilimpasa

kufananishwa na ndugu zake katika mambo

yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye

rehema, mwaminifu katika mambo ya

Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za

watu wake.

18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa

alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao

wanaojaribiwa.

WAEBRANIA 4:15 Kwa kuwa hamna kuhani

mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika

mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa

sawasawa na sisi katika mambo yote, bila

kufanya dhambi.

WAEBRANIA 5:8 na, ingawa ni Mwana,

alijifunza kutii kwa mateso hayo

yaliyompata;

1 YOHANA 4:9 Katika hili pendo la Mungu

lilionekana kwetu, kwamba Mungu

amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni,

ili tupate uzima kwa yeye.

10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda

Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi,

akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa

dhambi zetu.

1 YOHANA 4:14 Na sisi tumeona na

kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma

Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

ISAYA

Page 284: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

284

Ona pia: #1; #2; Mwanzo 22:11-17; Mwanzo 48:16; Isaya 41:8; Isaya 43:11; Isaya 46:3,4; Yeremia 14:8; Hosea 13:4; Malaki 3:1.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

F03 Masiha atakataliwa.

ISAYA 65:1 Watu wasionitaka wanauliza

habari zangu; nimeonekana na hao

wasionitafuta; naliliambia taifa lisiloitwa kwa

jina langu,

2 Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa

nimewanyoshea mikono yangu watu

walioasi, watu waendao katika njia isiyo

njema, wakifuata mawazo yao wenyewe;

KUMBUKUMBU LA TORATI

32:21 Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu;

Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami

nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami

nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.

MATHAYO 23:37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu,

uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe

wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi

nimetaka kuwakusanya pamoja watoto

wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja

vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini

hamkutaka!

MATENDO YA MITUME 13:40 Angalieni,

basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika

manabii.

41 Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni,

mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi

siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki

kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.

WARUMI 9:24 ndio sisi aliotuita, si watu wa

Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?

25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea,

Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu

wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa

mpenzi wangu.

26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa,

Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana

wa Mungu aliye hai.

WARUMI 10:20 Na Isaya anao ujasiri

mwingi, asema, Nalipatikana nao

wasionitafuta, Nalidhihirika kwao

wasioniulizia.

21 Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa

naliwanyoshea mikono watu wasiotii na

wakaidi.

Ona pia: Mithali 1:24; Luka 13:34; Luka 19:41,42.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 65:8 Bwana asema hivi, Kama

vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala,

na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa

maana mna baraka ndani yake; ndivyo

nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi

wangu, ili nisiwaharibu wote.

9 Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi

wa milima yangu toka Yuda, na mteule

wangu atairithi, na watumishi wangu

watakaa huko.

10 Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya

kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala

makundi ya ng›ombe, kwa ajili ya watu

wangu walionitafuta.

MWANZO 49:10 Fimbo ya enzi haitaondoka

katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya

miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye

milki, Ambaye mataifa watamtii.

ISAYA

Page 285: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

285

ISAYA 35:2 Litachanua maua mengi, na

kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba;

litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa

Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa

Bwana, ukuu wa Mungu wetu.

HOSEA 2:16 Tena siku hiyo itakuwa,

asema Bwana, utaniita Ishi

WARUMI 9:27 Isaya naye atoa sauti yake

juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana

wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake

juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena,

Kama Bwana wa majeshi asingalituachia

uzao, Tungalikuwa kama Sodoma,

tungalifananishwa na Gomora.

WARUMI 11:5 Basi ni vivi hivi wakati huu

wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa

neema.

WARUMI 11:24 Kwa maana ikiwa wewe

ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio

mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha

ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika

mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale

walio wa asili kuweza kupandikizwa katika

mzeituni wao wenyewe?

25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue

siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya

kwamba kwa sehemu ugumu umewapata

Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

WAGALATIA 3:29 Na kama ninyi ni wa Kristo,

basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na

warithi sawasawa na ahadi.

WAGALATIA 4:7 Kama ni hivyo, wewe si

mtumwa tena bali u mwana; na kama u

mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

Ona pia: #1; #2; #3; Mathayo 24:21; Marko 13:20; Warumi 11.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H05 Utukufu na nguvu za Masiha zinazokuja.

ISAYA 65:17 Maana, tazama, mimi

naumba mbingu mpya na nchi mpya, na

mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala

hayataingia moyoni.

18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa

ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama,

naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu

wake wawe furaha.

ISAYA 65:19-22

ISAYA 65:23 Hawatajitaabisha kwa kazi

bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu

wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na

Bwana, na watoto wao pamoja nao.

ISAYA

Page 286: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

286

24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba,

nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.

25 Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha

pamoja, na simba atakula majani kama

ng›ombe; na mavumbi yatakuwa chakula

cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu

katika mlima wangu mtakatifu wote, asema

Bwana.

ISAYA 61:9 Na kizazi chao kitajulikana

katika mataifa, na uzao wao katika kabila za

watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao

ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana.

2 PETRO 3:12 mkitazamia hata ije siku ile

ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo

mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe

vya asili vitateketea na kuyeyuka?

13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia

mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki

yakaa ndani yake.

UFUNUO WA YOHANA 7:16

Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 21:1 Kisha

nikaona mbingu mpya na nchi mpya;

kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya

kwanza zimekwisha kupita, wala hapana

bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu,

Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka

mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari,

kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa

mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile

kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani

ya Mungu ni pamoja na wanadamu,

naye atafanya maskani yake pamoja nao,

nao watakuwa watu wake. Naye Mungu

mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho

yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala

maombolezo, wala kilio, wala maumivu

hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya

kwanza yamekwisha kupita.

Ona pia: #1; #2; #3; #5.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

ISAYA 66:1 Bwana asema hivi, Mbingu

ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali

pa kuweka miguu yangu; mtanijengea

nyumba ya namna gani? Na mahali pangu

pa kupumzikia ni mahali gani?

MATHAYO 24:2 Naye akajibu akawaambia,

Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni,

Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.

MARKO 14:58 Sisi tulimsikia akisema,

Mimi nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa

mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine

lisilofanyika kwa mikono.

MATENDO YA MITUME 7:47 Lakini

Sulemani alimjengea nyumba.

48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba

zilizofanywa kwa mikono, kama vile

asemavyo nabii,

ISAYA

Page 287: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

287

49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni

pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani

mtakayonijengea? Asema Bwana,

MATENDO YA MITUME 17:24 Mungu

aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote

vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa

mbingu na nchi, hakai katika hekalu

zilizojengwa kwa mikono;

UFUNUO WA YOHANA 21:22 Nami

sikuona hekalu ndani yake; kwa maana

Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-

Kondoo, ndio hekalu lake.

Ona pia: 1 Wakorintho 3:16-19; 2 Wakorintho 6:16; Waefeso 2:21; Ufunuo wa Yohana 15:5-8.

B15 Masiha atajawa na rehema.

ISAYA 66:2 Maana mkono wangu

ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote

vikapata kutokea, asema Bwana; lakini

mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu

aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka,

atetemekaye asikiapo neno langu.

MATHAYO 5:3 Heri walio maskini wa roho;

Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

MATENDO YA MITUME 9:6 Lakini

simama, uingie mjini, nawe utaambiwa

yakupasayo kutenda.

MATENDO YA MITUME 16:29 Akataka

taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa

hofu, akawaangukia Paulo na Sila;

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu,

yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

1 WAKORINTHO 1:18 Kwa sababu neno

la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi,

bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya

Mungu.

19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima

yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili

nitazikataa.

WAFILIPI 2:12 Basi, wapendwa wangu,

kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi

nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi

nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu

wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.

WAEBRANIA 1:2 mwisho wa siku hizi

amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka

kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya

ulimwengu.

1 PETRO 3:4 bali kuwe utu wa

moyoni usioonekana, katika mapambo

yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na

utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za

Mungu.

Ona pia: Isaya 40:26; Wakolosai 1:17.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E19 Masiha atafariji.

E24 Masiha ataleta amani.

ISAYA 66:10 Furahini pamoja na

Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi

nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa

furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake;

11 mpate kunyonya, na kushibishwa kwa

maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na

kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.

12 Maana Bwana asema hivi, Tazama,

nitamwelekezea amani kama mto, na

ISAYA

Page 288: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

288

utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho,

nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu

ya magoti mtabembelezwa.

13 Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji,

ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi

mtafarijiwa katika Yerusalemu.

ISAYA 66:14-17

ISAYA 60:16 Utanyonya maziwa ya

mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe

utajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi

wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa

Yakobo.

ZEKARIA 14:11 Na watu watakaa ndani

yake, wala hakutakuwako laana tena; lakini

Yerusalemu utakaa salama.

YOHANA 14:27 Amani nawaachieni; amani

yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama

ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni

mwenu, wala msiwe na woga.

WARUMI 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa

haki itokayo katika imani, na mwe na amani

kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu

Kristo,

1 PETRO 2:2 Kama watoto wachanga

waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili

yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia

wokovu;

UFUNUO WA YOHANA 21:24 Na

mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe

mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa

ndani yake.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ISAYA 66:15 Maana Bwana atakuja na

moto, na magari yake ya vita kama upepo

wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu

yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa

miali ya moto.

ISAYA 66:16-17

ISAYA 66:18 Nami nayajua matendo

yao na mawazo yao; wakati unakuja

nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote;

nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.

19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami

nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa,

Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde,

kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali;

watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona

utukufu wangu; nao watahubiri utukufu

wangu katika mataifa.

ISAYA 66:20-21

ISAYA 66:22 Kama vile mbingu mpya

na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa

mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao

wenu na jina lenu litakavyokaa.

23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya,

na sabato hata sabato, wanadamu wote

watakuja kuabudu mbele zangu, asema

Bwana.

24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya

watu walioniasi; maana funza wao hatakufa,

wala moto wao hautazimika nao watakuwa

ISAYA

Page 289: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

289

chukizo machoni pa wote wenye mwili.

ISAYA 2:2 Na itakuwa katika siku

za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote

watauendea makundi makundi.

YOHANA 17:2 kama vile ulivyompa

mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili

kwamba wote uliompa awape uzima wa

milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali

nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

WARUMI 15:8 Kwa maana nasema, ya

kwamba Kristo amefanyika mhudumu

wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli

ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi

walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili

ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa

hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami

nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na

watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana;

Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la

Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

2 WAKORINTHO 5:17 Hata imekuwa,

mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe

kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa

mapya.

2 WATHESALONIKE 1:6 Kwa kuwa ni haki

mbele za Mungu kuwalipa mateso wale

wawatesao ninyi;

7 na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na

sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana

Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika

wa uweza wake

8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza

kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao

wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele,

kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa

nguvu zake;

WAEBRANIA 8:13 Kwa kule kusema, Agano

jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa

kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa

kikuukuu na kuchakaa ki karibu na

kutoweka.

2 PETRO 3:10 Lakini siku ya Bwana itakuja

kama mwivi; katika siku hiyo mbingu

zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe

vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na

nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa

hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia

gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na

kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu

zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili

vitateketea na kuyeyuka?

13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia

mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki

yakaa ndani yake.

UFUNUO WA YOHANA 19:15 Na

upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

ISAYA

Page 290: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

290

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

UFUNUO WA YOHANA 21:1 Kisha

nikaona mbingu mpya na nchi mpya;

kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya

kwanza zimekwisha kupita, wala hapana

bahari tena.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Matendo ya Mitume 11:25,26.

ISAYA

Page 291: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

291

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 3:14 Rudini, enyi watoto wenye

kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume

wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji

mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami

nitawaleta hata Sayuni;

15 nami nitawapa ninyi wachungaji

wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha

kwa maarifa na fahamu.

16 Kisha itakuwa, mtakapoongezeka na kuwa

wengi katika nchi hiyo, asema Bwana, siku

zile hawatasema tena, Sanduku la agano

la Bwana; wala halitaingia moyoni; wala

hawatalikumbuka, wala hawatalizuru, wala

hayatafanyika hayo tena.

17 Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi

cha Bwana; na mataifa yote watakusanyika

huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana;

wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa

moyo wao mbaya.

18 Siku zile nyumba ya Yuda watakwenda

pamoja na nyumba ya Israeli, nao watakuja

pamoja, kutoka nchi ya kaskazini, mpaka

nchi ile niliyowapa baba zenu iwe urithi

wao.

19 Lakini mimi nalisema, Nitawezaje kukuweka

pamoja na watoto, na kukupa nchi

ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa?

Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala

hamtageuka na kuacha kunifuata.

ISAYA 17:6 Lakini kilichosazwa na

mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile

wakati wa kupiga mizeituni, matunda

mawili matatu yaliyo juu sana; matunda

manne matano katika matawi, matawi ya

mti wa matunda, asema Bwana, Mungu wa

Israeli.

EZEKIELI 34:11 Maana, Bwana MUNGU

asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe,

naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na

kuwaulizia.

12 Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo

zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake

waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta

kondoo zangu; nami nitawaokoa katika

mahali pote walipotawanyika, katika siku ya

mawingu na giza.

ZEKARIA 13:7 Amka, Ee upanga, juu

ya mchungaji wangu, na juu ya mtu

aliye mwenzangu, asema Bwana wa

majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo

watatawanyika; nami nitaugeuza mkono

wangu juu ya wadogo.

YOHANA 4:21 Yesu akamwambia,

Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo

hamtamwabudu Baba katika mlima huu,

wala kule Yerusalemu.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi

tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu

watoka kwa Wayahudi.

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo

waabuduo halisi watamwabudu Baba katika

roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta

watu kama hao wamwabudu.

YOHANA 10:1 Yesu aliwaambia, Amin,

amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia

mlangoni katika zizi la kondoo, lakini

akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni

mnyang›anyi.

2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa

kondoo.

3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo

humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo

wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.

YEREMIA

Page 292: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

292

4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote,

huwatangulia; na wale kondoo humfuata,

kwa maana waijua sauti yake.

5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali

watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za

wageni.

YOHANA 21:15 Basi walipokwisha kula,

Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni

wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?

Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua

kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha

wana-kondoo wangu.

16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa

Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo,

Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.

Akamwambia, Chunga kondoo zangu.

17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa

Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika

kwa vile alivyomwambia mara ya tatu,

Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe

wajua yote; wewe umetambua ya kuwa

nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha

kondoo zangu.

WARUMI 9:27 Isaya naye atoa sauti yake

juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana

wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEBRANIA 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja,

aliye kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na

kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono,

maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Ezekieli 34:13,14; Hosea 2:20,21; Zekaria 13:8,9; Luka 15:11-32; Matendo ya Mitume 20:28; Warumi 11:4-6;

Waefeso 4:11,12; 1 Petro 5:1-4.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

YEREMIA 4:1 Kama ukitaka kurudi, Ee

Israeli, asema Bwana, utanirudia mimi;

na kama ukitaka kuyaondoa machukizo

yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo

hutaondolewa;

2 nawe utaapa hivi, Kama Bwana aishivyo,

katika kweli, na katika hukumu, na katika

haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye,

nao watajitukuza katika yeye.

MATENDO YA MITUME 11:1 Basi

mitume na ndugu waliokuwako katika

Uyahudi wakapata habari ya kwamba

watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la

Mungu.

MATENDO YA MITUME 11:18

Waliposikia maneno haya wakanyamaza,

wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi,

Mungu amewajalia hata mataifa nao toba

liletalo uzima.

MATENDO YA MITUME 13:46

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa

wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu

linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa

mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi

YEREMIA

Page 293: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

293

zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele,

angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi,

wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa

wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.

MATENDO YA MITUME 14:27

Hata walipofika wakalikutanisha kanisa,

wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya

Mungu pamoja nao, na ya kwamba

amewafungulia Mataifa mlango wa imani.

WAGALATIA 3:8 Na andiko, kwa vile

lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu

atawahesabia haki Mataifa kwa imani,

lilimhubiri Ibrahimu habari njema

zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote

watabarikiwa.

Ona pia: Mwanzo 22:18; Zaburi 72:17.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

YEREMIA 10:7 Ni nani asiyekucha wewe,

Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa

yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye

hekima wote wa mataifa, na katika hali yao

ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama

wewe.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

LUKA 12:5 Lakini nitawaonya

mtakayemwogopa; mwogopeni yule

ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza

wa kumtupa katika Jehanum; naam,

nawaambia, Mwogopeni huyo.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #4; Zaburi 22:28; Isaya 2:4; Yeremia 10:6; 1 Wakorintho 1:19,20.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 12:15 Tena itakuwa, baada ya

kuwang›oa, nitarudi na kuwahurumia; nami

nitawaleta tena, kila mtu aingie katika urithi

wake, na kila mtu aingie katika nchi yake.

YEREMIA 15:19 Kwa sababu hiyo Bwana

asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi

nitakapokurejeza, upate kusimama mbele

zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani

katika kilicho kibovu, utakuwa kama

kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali

YEREMIA

Page 294: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

294

hutawarudia wao.

20 Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa

boma la shaba juu ya watu hawa; nao

watapigana nawe; lakini hawatakushinda;

maana mimi nipo pamoja nawe, ili

nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.

21 Nami nitakuokoa na mkono wa watu

wabaya, nami nitakukomboa katika mkono

wao wenye kutisha.

YEREMIA 24:6 Kwa maana nitawatulizia

macho yangu, wapate mema, nami

nitawaingiza katika nchi hii tena;

nami nitawajenga, wala sitawabomoa;

nitawapanda wala sitawang›oa.

7 Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa

mimi ni Bwana; nao watakuwa watu wangu,

nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana

watanirudia kwa moyo wao wote.

YEREMIA 29:14 Nami nitaonekana kwenu,

asema Bwana, nami nitawarudisha watu

wenu waliofungwa, nami nitawakusanya

ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote,

na katika mahali pote, nilikowafukuza,

asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata

mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya

mchukuliwe mateka.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEBRANIA 8:8 Maana, awalaumupo, asema

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami

nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba

ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 16:14 Kwa hiyo, angalia,

siku zinakuja, asema Bwana, ambapo

hawatasema tena, Aishivyo Bwana,

aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya

Misri;

15 lakini, Aishivyo Bwana, aliyewaleta wana wa

Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi

zote alikowafukuza; nami nitawarudisha

katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba

zao.

19 Ee Bwana, nguvu zangu, ngome yangu, na

kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe

watakuja mataifa yote toka ncha za dunia,

wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila

uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.

YEREMIA

Page 295: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

295

ZABURI 22:27 Miisho yote ya dunia

itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana;

Jamaa zote za mataifa watamsujudia.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

MATENDO YA MITUME 9:15 Lakini

Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana

huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue

Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na

wana wa Israeli.

MATENDO YA MITUME 10:45 Na wale

waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa,

watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa

sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa

cha Roho Mtakatifu.

MATENDO YA MITUME 13:47 Kwa

sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

WAGALATIA 3:14 ili kwamba baraka ya

Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu

Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa

njia ya imani.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Matendo ya Mitume 14:27; Matendo ya Mitume 28:28; Warumi 10:18; 1 Wathesalonike 2:16.

B08 Ujuzi wa Yote wa Masiha.

YEREMIA 17:10 Mimi, Bwana, nauchunguza

moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila

mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda

ya matendo yake.

YOHANA 2:25 na kwa sababu hakuwa

na haja ya mtu kushuhudia habari za

mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe

alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

WARUMI 8:27 Na yeye aichunguzaye

mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa

huwaombea watakatifu kama apendavyo

Mungu.

WAEBRANIA 4:12 Maana Neno la Mungu li

hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko

upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na

viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena

li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi

YEREMIA

Page 296: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

296

ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi

mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na

kufunuliwa machoni pake yeye aliye na

mambo yetu.

UFUNUO WA YOHANA 2:23 nami

nitawaua watoto wake kwa mauti. Na

makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye

achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa

kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo

yake.

Ona pia: Zaburi 7:9; Zaburi 139:1,2,23,24; Mithali 17:3; Yeremia 11:20; Yeremia 20:12; Yeremia 32:19.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 23:3 Nami nitakusanya mabaki

ya kundi langu, katika nchi zile zote

nilizowafukuza, nami nitawaleta tena

mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.

4 Nami nitaweka juu yao wachungaji

watakaowalisha; wala hawataona hofu tena,

wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja

wao, asema Bwana.

7 Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema

Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo

Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika

nchi ya Misri;

8 lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na

kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli

kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi

zote nilikowafukuza; nao watakaa katika

nchi yao wenyewe.

YOHANA 6:39 Na mapenzi yake

aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika

wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali

nimfufue siku ya mwisho.

40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni

haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana

na kumwamini yeye, awe na uzima wa

milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

28 Nami nawapa uzima wa milele; wala

hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu

atakayewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

30 Mimi na Baba tu umoja.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

YOHANA 18:9 Ili litimizwe lile neno

alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata

mmoja wao.

1 PETRO 1:5 Nanyi mnalindwa na nguvu

za Mungu kwa njia ya imani hata mpate

wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa

mwisho.

Ona pia: #1; #2; #3; Mika 2:12,13; Yohana 21:15-17; Matendo ya Mitume 20:28,29; 1 Petro 5:1-5.

YEREMIA

Page 297: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

297

B04 Sifa za Uungu za Masiha.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

YEREMIA 23:5 Tazama siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi

Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme,

atatenda kwa hekima, naye atafanya

hukumu na haki katika nchi.

6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli

atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni

hili, Bwana ni haki yetu.

MATHAYO 1:1 Kitabu cha ukoo wa Yesu

Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa

Ibrahimu.

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 1:71 Tuokolewe na adui zetu Na

mikononi mwao wote wanaotuchukia;

72 Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na

kulikumbuka agano lake takatifu;

73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,

74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi

mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,

LUKA 19:9 Yesu akamwambia, Leo

wokovu umefika nyumbani humu, kwa

sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.

10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja

kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

YOHANA 1:45 Filipo akamwona

Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona

yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na

manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa

Nazareti.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

1 WAKORINTHO 1:30 Bali kwa yeye

ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu,

aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa

Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

UFUNUO WA YOHANA 19:11 Kisha

nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama,

farasi mweupe, na yeye aliyempanda,

aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa

haki ahukumu na kufanya vita.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 72:2; Isaya 7:14; Isaya 53:10; Yeremia 33:15; Zekaria 3:8; Warumi 3:22; 2 Wakorintho 5:21; Wafilipi 3:9.

D02 Kazi ya Masiha kama Nabii.

E24 Masiha ataleta amani.

YEREMIA 28:9 Nabii atabiriye habari za

amani, neno la nabii yule litakapotokea,

ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa

Bwana amemtuma kweli kweli.

MATHAYO 3:17 na tazama, sauti kutoka

mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,

YEREMIA

Page 298: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

298

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

LUKA 2:14 Atukuzwe Mungu juu

mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu

aliowaridhia.

LUKA 24:36 Na walipokuwa katika

kusema habari hiyo, yeye mwenyewe

alisimama katikati yao, akawaambia, Amani

iwe kwenu.

YOHANA 14:27 Amani nawaachieni; amani

yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama

ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni

mwenu, wala msiwe na woga.

MATENDO YA MITUME 10:36 Neno lile

alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri

habari njema ya amani kwa Yesu Kristo

(ndiye Bwana wa wote),

WARUMI 10:15 Tena wahubirije,

wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni

mizuri kama nini miguu yao wahubirio

habari ya mema!

Ona pia: Isaya 52:7; Yeremia 6:14; Ezekieli 13:10-16; Nahumu 1:15; Zekaria 9:10; Mathayo 17:5; Luka 7:50; Luka 19:42; Yohana

20:19,21; Matendo ya Mitume 9:31; Warumi 5:1; Warumi 8:6; Warumi 14:17; 1 Wakorintho 14:33; Waefeso 2:14,15,17; Wakolosai

3:15; 2 Wathesalonike 3:16; Waebrania 12:14; 2 Petro 1:2,17; Ufunuo wa Yohana 1:4.

A03 Masiha ni wa ukoo wa Daudi.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 30:3 Kwa maana, tazama, siku

zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza

watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa,

asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi

niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.

YEREMIA 30:4-8

YEREMIA 30:9 bali watamtumikia Bwana,

Mungu wao, na Daudi, mfalme wao,

nitakayemwinua kwa ajili yao.

10 Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo,

mtumishi wangu, asema Bwana; wala

usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama,

nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka

nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi,

naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu

atakayemtia hofu.

11 Maana mimi ni pamoja nawe, asema

Bwana, nikuokoe; maana nitawakomesha

kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya,

bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini

nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha

bila adhabu.

YEREMIA 30:12-15

YEREMIA 30:16 Basi, watu wote wakulao

wataliwa; na adui zako wote watakwenda

kufungwa; kila mmoja wao; na hao

waliokuteka nyara watatekwa; na wote

waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo.

YEREMIA 30:17,18

YEREMIA 30:19 Tena kwao itasikiwa

shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami

nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache;

tena nitawatukuza, wala hawatakuwa

wanyonge.

20 Watoto wao nao watakuwa kama zamani,

na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu,

nami nitawaadhibu wote wawaoneao.

YEREMIA 30:23,24

2 SAMWELI 22:51 Ampa mfalme wake wokovu

mkuu; Amfanyia fadhili masihi wake Daudi

na mzao wake ,hata milele.

YEREMIA

Page 299: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

299

LUKA 1:30 Malaika akamwambia,

Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata

neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto

mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 1:69 Ametusimamishia pembe ya

wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi

wake.

YOHANA 12:15 Usiogope, binti Sayuni;

tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda

mwana-punda.

MATENDO YA MITUME 2:30 Basi

kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu

amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika

uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja

katika kiti chake cha enzi;

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui

kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule

kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili

ya baba zetu.

UFUNUO WA YOHANA 19:15 Na

upanga mkali hutoka kinywani mwake ili

awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga

kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga

shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira

ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake

na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA

Bwana WA MABwana.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

A05 Uhusiano kati ya Masiha na Baba Yake.

D08 Masiha atakuwa Dhamana.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 30:21 Na mkuu wao atakuwa

mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye

kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao;

nami nitamkaribisha, naye atanikaribia;

maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu

kunikaribia? Asema Bwana.

22 Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa

Mungu wenu.

YEREMIA 24:7 Nami nitawapa moyo,

wanijue ya kuwa mimi ni Bwana; nao

watakuwa watu wangu, nami nitakuwa

Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa

moyo wao wote.

WAEBRANIA 4:15 Kwa kuwa hamna kuhani

mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika

mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa

sawasawa na sisi katika mambo yote, bila

kufanya dhambi.

16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa

ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema

ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

YEREMIA

Page 300: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

300

WAEBRANIA 5:4 Na hapana mtu ajitwaliaye

mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na

Mungu, kama vile Haruni.

5 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi

yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye

aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo

nimekuzaa.

6 kama asemavyo mahali pengine,

Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa

Melkizedeki.

WAEBRANIA 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu

amekuwa mdhamini wa agano lililo bora

zaidi.

23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa

sababu wazuiliwa na mauti wasikae;

24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao

ukuhani wake usioondoka.

25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa

kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye;

maana yu hai sikuzote ili awaombee.

WAEBRANIA 8:10 Maana hili ndilo agano

nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada

ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria

zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao,

Nao watakuwa watu wangu.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: Mwanzo 49:10; Kumbukumbu la Torati 26:17-19; Yeremia 24:7; Yeremia 31:1,33; Ezekieli 11:20; Ezekieli 36:28;

Ezekieli 37:27; Hosea 2:23; Zekaria 13:9; Waebrania 9:14,15,24.

B22 Uzuri wa Mungu na Masiha.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

YEREMIA 31:1 Wakati huo, asema Bwana,

nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli,

nao watakuwa watu wangu.

2 Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa

na upanga walipata neema jangwani; yaani,

Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.

3 Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam

nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo

maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

4 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa,

Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa

kwa matari yako, nawe utatokea katika

michezo yao wanaofurahi.

5 Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya

milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao

watayafurahia matunda yake.

6 Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi

watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni,

tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.

7 Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni

Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu

wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme,

Ee Bwana, uwaokoe watu wako, mabaki ya

Israeli.

8 Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini,

na kuwakusanya katika miisho ya dunia,

na pamoja nao watakuja walio vipofu, na

hao wachechemeao, mwanamke mwenye

mimba, na yeye pia aliye na utungu wa

kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.

9 Watakuja kwa kulia, na kwa maombi

nitawaongoza; nitawaendesha penye mito

ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia

hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa

Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza

wangu.

YEREMIA

Page 301: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

301

MWANZO 45:7 Mungu alinipeleka mbele

yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na

kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.

AMOSI 9:11 Siku hiyo nitaiinua tena

maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba

mahali palipobomoka; nami nitayainua

magofu yake, na kuyajenga kama siku za

kale;

MATENDO YA MITUME 15:16 Baada ya

mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena

nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga

tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;

WARUMI 9:27 Isaya naye atoa sauti yake

juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana

wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

WARUMI 11:5 Basi ni vivi hivi wakati huu

wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa

neema.

WAEFESO 2:20 Mmejengwa juu ya msingi

wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu

mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja

kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

1 PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule,

ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa

milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili

zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie

katika nuru yake ya ajabu;

UFUNUO WA YOHANA 5:10

ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

UFUNUO WA YOHANA 21:10

Akanichukua katika Roho mpaka mlima

mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji

mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka

mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Yeremia 31:10-14,27-30,38-40.

C05 Unabii wa kuuliwa kwa watoto

Bethlehemu.

YEREMIA 31:15 Bwana asema hivi, Sauti

imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo

mengi, Raheli akiwalilia watoto wake;

asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa

kuwa hawako,

MWANZO 35:16 Wakasafiri kutoka Betheli,

hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika

Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa

kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.

17 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu,

mzalisha akamwambia, Usiogope, maana

sasa utamzaa mwanamume mwingine.

18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana

alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini

babaye alimwita Benyamini.

19 Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi,

ndio Bethlehemu.

20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi

lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata

leo.

MATHAYO 2:16 Ndipo Herode, alipoona ya

kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi,

alighadhabika sana, akatuma watu akawaua

YEREMIA

Page 302: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

302

watoto wote wanaume waliokuwako huko

Bethlehemu na viungani mwake mwote,

tangu wenye miaka miwili na waliopungua,

kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale

mamajusi.

17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii

Yeremia, akisema,

18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo

mengi, Raheli akiwalilia watoto wake,

Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

YEREMIA 31:22 Hata lini utatanga-tanga,

Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana

ameumba jambo jipya duniani; mwanamke

atamlinda mwanamume.

MATHAYO 1:18 Kuzaliwa kwake Yesu

Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake

alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla

hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa

uweza wa Roho Mtakatifu.

19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa

mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu

kumwacha kwa siri.

20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama,

malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto,

akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu

kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba

yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina

lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa

watu wake na dhambi zao.

WAGALATIA 4:4 Hata ulipowadia utimilifu wa

wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye

amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini

ya sheria,

Ona pia: Mwanzo 3:15; Zaburi 2:7,8; Isaya 7:14; Luka 1:34,35.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

G06 Makao ya Roho Mtakatifu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

YEREMIA 31:31 Angalia, siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na

nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya

na baba zao, katika siku ile nilipowashika

mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri;

ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa

nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na

nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na

katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa

Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake,

na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue

Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu

mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye

mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;

maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi

yao sitaikumbuka tena.

MATHAYO 26:27 Akakitwaa kikombe,

akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni

nyote katika hiki;

28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano,

imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo

la dhambi.

29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa

tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku

ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi

katika ufalme wa Baba yangu.

YEREMIA

Page 303: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

303

YOHANA 1:15 Yohana alimshuhudia,

akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye

niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye

nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa

maana alikuwa kabla yangu.

16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote

tulipokea, na neema juu ya neema.

17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa

Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono

wa Yesu Kristo.

YOHANA 6:45 Imeandikwa katika manabii,

Na wote watakuwa wamefundishwa na

Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa

Baba huja kwangu.

2 WAKORINTHO 3:2 Ninyi ndinyi

barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu,

inajulikana na kusomwa na watu wote;

3 mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua

ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa

wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai;

si katika vibao vya mawe, ila katika vibao

ambavyo ni mioyo ya nyama.

4 Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa

njia ya Kristo.

5 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri

neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali

utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.

6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa

wahudumu wa agano jipya; si wa andiko,

bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali

roho huhuisha.

WAGALATIA 3:17 Nisemalo ni hili; agano

lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati

iliyotokea miaka mia nne na thelathini

baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile

ahadi.

WAEBRANIA 8:6 Lakini sasa amepata huduma

iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe

wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya

ahadi zilizo bora.

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa

halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa

lile la pili.

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku

zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia

nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano

jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na

dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya

lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu

kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki

karibu na kutoweka.

1 YOHANA 2:27 Nanyi, mafuta yale

mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu,

wala hamna haja ya mtu kuwafundisha;

lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha

habari za mambo yote, tena ni kweli wala si

uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni

ndani yake.

YEREMIA

Page 304: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

304

Ona pia: #1; #2; Kutoka 19-20; Matendo ya Mitume 2:14-47.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 32:37 Tazama, nitawakusanya, na

kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza,

katika hasira yangu, na uchungu wangu, na

ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta

tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha

salama salimini;

38 nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa

Mungu wao;

39 nami nitawapa moyo mmoja na njia moja,

wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na

ya watoto wao baada yao;

40 nami nitafanya agano la milele pamoja

nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha,

ili niwatendee mema; nami nitatia kicho

changu mioyoni mwao, ili wasiniache.

41 Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema,

nami nitawapanda katika nchi hii kweli

kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho

yangu yote.

EZEKIELI 11:19 Nami nitawapa moyo

mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao;

nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika

miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

20 ili waende katika amri zangu, na kuyashika

maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa

watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

LUKA 1:72 Ili kuwatendea rehema baba

zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;

73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,

74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi

mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,

75 Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku

zetu zote.

YOHANA 17:21 Wote wawe na umoja; kama

wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami

ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili

ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe

ndiwe uliyenituma.

MATENDO YA MITUME 4:32 Na

jamii ya watu walioamini walikuwa na

moyo mmoja na roho moja; wala hapana

mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote

alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali

walikuwa na vitu vyote shirika.

WAEBRANIA 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu

amekuwa mdhamini wa agano lililo bora

zaidi.

1 YOHANA 3:8 atendaye dhambi ni wa

Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi

tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa

Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za

Ibilisi.

9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi

dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani

yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa

sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na

watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda

haki hatokani na Mungu, wala yeye

asiyempenda ndugu yake.

1 YOHANA 5:18 Twajua ya kuwa kila mtu

aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali

yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala

yule mwovu hamgusi.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Mwanzo 17:7; Kumbukumbu la Torati 26:17-19; Isaya 55:3; 2 Wakorintho 13:11; Wagalatia 3:14-17;

YEREMIA

Page 305: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

305

Waebrania 6:13-18; Waebrania 8:9-11.

E21 Masiha atasamehe dhambi.

E24 Masiha ataleta amani.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 33:6 Tazama, nitauletea afya

na kupona, nami nitawaponya; nami

nitawafunulia wingi wa amani na kweli.

7 Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na

wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama

kwanza.

8 Nami nitawasafisha na uovu wao wote,

ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami

nitawasamehe maovu yao yote, ambayo

kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu

yangu.

9 Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha,

na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote

ya dunia, watakaosikia habari ya mema

yote niwatendeayo, nao wataogopa na

kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na

amani nitakaoupatia mji huo.

YEREMIA 33:10-13

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote

kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la

Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote

niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo

pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa

dahari.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi,

akaketi; na watu wote waliokuwamo katika

sinagogi wakamkazia macho.

21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya

yametimia masikioni mwenu.

YOHANA 1:17 Kwa kuwa torati ilitolewa

kwa mkono wa Musa; neema na kweli

zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

WAEBRANIA 8:10 Maana hili ndilo agano

nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada

ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria

zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao,

Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na

dhambi zao sitazikumbuka tena.

1 PETRO 2:24 Yeye mwenyewe alizichukua

dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti,

tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe

hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa

kwake mliponywa.

1 YOHANA 1:7 bali tukienenda nuruni,

kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana

sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana

wake, yatusafisha dhambi yote.

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi,

YEREMIA

Page 306: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

306

twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo

mwetu.

9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni

mwaminifu na wa haki hata atuondolee

dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu

wote.

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Zaburi 65:3; Yohana 18:37; Waebrania 9:11-14.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

D09 Masiha atakuwa Mwokozi.

E08 Haki ya Masiha.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

YEREMIA 33:14 Tazama, siku zinakuja,

asema Bwana, nitakapolitimiza neno lile

jema nililolinena, katika habari za nyumba

ya Israeli, na katika habari za nyumba ya

Yuda.

15 Katika siku zile, na wakati ule,

nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki;

naye atafanya hukumu na haki katika nchi

hii.

16 Katika siku zile Yuda ataokolewa, na

Yerusalemu utakaa salama, na jina lake

atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

17 Maana Bwana asema hivi, Daudi hatakosa

kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi

cha nyumba ya Israeli;

18 wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na

mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa

sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo,

na kufanya dhabihu daima.

22 Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi

kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari

kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao

wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi

wanaonihudumia.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

WAEBRANIA 7:17 maana ameshuhudiwa

kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano

wa Melkizedeki.

18 Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri

iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake,

na kutokufaa kwake;

19 (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno);

na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini

yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo

twamkaribia Mungu.

20 Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,

21 (maana wale walifanywa makuhani pasipo

kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa

yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala

hataghairi, Wewe u kuhani wa milele;)

22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini

wa agano lililo bora zaidi.

YEREMIA

Page 307: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

307

1 PETRO 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe

yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za

roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya

Yesu Kristo.

UFUNUO WA YOHANA 1:4 Yohana,

kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia;

Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo

kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na

atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba

walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi

aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani

kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na

ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 5:10

ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

Ona pia: #1; #2; #5; Isaya 4:2; Isaya 11:1-5; Isaya 53:2; 2 Wakorintho 1:20; 1 Petro 2:9.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

YEREMIA 50:4 Katika siku hizo, na wakati

huo, asema Bwana, wana wa Israeli

watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja;

Wataendelea njiani mwao wakilia, nao

watamtafuta Bwana, Mungu wao.

5 Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao

zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi,

mjiunge na Bwana, kwa agano la milele

ambalo halitasahauliwa.

6 Watu wangu wamekuwa kondoo

waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza;

wamewapotosha milimani; wamekwenda

toka mlima hata kilima, wamesahau mahali

pao pa kupumzika.

7 Watu wote waliowaona wamewala; na adui

zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa

hao wametenda dhambi juu ya Bwana, aliye

kao la haki, yaani, Bwana, tumaini la baba

zao.

19 Nami nitamleta Israeli tena malishoni

kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na

Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya

milima ya Efraimu, na katika Gileadi.

20 Katika siku hizo na wakati huo, asema

Bwana, uovu wa Israeli utatafutwa,

wala uovu hapana; na dhambi za Yuda

zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana

nitawasamehe wale niwaachao kuwa

mabaki.

ISAYA 44:22 Nimeyafuta makosa yako

kama wingu zito, na dhambi zako kama

wingu; unirudie; maana nimekukomboa.

MIKA 7:19 Atarejea na kutuhurumia;

atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa

dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.

MATENDO YA MITUME 3:19 Tubuni

basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate

kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako

kwake Bwana;

MATENDO YA MITUME 3:26

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake

Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili

kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja

YEREMIA

Page 308: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

308

wenu na maovu yake.

WARUMI 8:33 Ni nani atakayewashitaki

wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye

kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo

Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya

hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko

mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye

anayetuombea.

WARUMI 11:16 Tena malimbuko yakiwa

matakatifu, kadhalika na donge lote; na

shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAEBRANIA 10:16 Hili ni agano

nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena

Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,

Na katika nia zao nitaziandika; ndipo

anenapo,

17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena

kabisa.

18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo

tena kwa ajili ya dhambi.

Ona pia: #2; #3.

YEREMIA

Page 309: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

309

B23 Neema ya Mungu na Masiha.

MAOMBOLEZO 3:25 Bwana ni mwema

kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi

imtafutayo.

26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na

kumngojea kwa utulivu.

ISAYA 25:9 Katika siku hiyo watasema,

Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye

tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana

tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia

wokovu wake.

LUKA 2:38 Huyu alitokea saa ile ile

akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa

wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu

akawatolea habari zake.

1 WATHESALONIKE 1:10 na kumngojea

Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye

alimfufua katika wafu, naye ni Yesu,

mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.

WAEBRANIA 9:28 kadhalika Kristo naye,

akiisha kutolewa sadaka mara moja

azichukue dhambi za watu wengi; atatokea

mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao

wamtazamiao kwa wokovu.

WAEBRANIA 10:37 Kwa kuwa bado

kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja,

wala hatakawia.

1 PETRO 1:13 Kwa hiyo vifungeni viuno vya

nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia

kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa

katika ufunuo wake Yesu Kristo.

Ona pia: Zaburi 22:26; Zaburi 27:14; Zaburi 33:20; Zaburi 39:7; Zaburi 130:5; Isaya 8:17; Isaya 26:8; Isaya 33:2; Isaya 64:4; Mika

7:7; Habakuki 2:3.

F11 Mateso ya Masiha.

MAOMBOLEZO 3:30 Na amwelekezee

yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe

mashutumu.

ISAYA 50:6 Naliwatolea wapigao mgongo

wangu, na wang›oao ndevu mashavu yangu;

sikuficha uso wangu usipate fedheha na

kutemewa mate.

MIKA 5:1 Sasa utajikusanya vikosi

vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru;

watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni

mwake kwa fimbo.

MATHAYO 26:67 Ndipo wakamtemea mate

ya uso, wakampiga makonde; wengine

wakampiga makofi,

MAOMBOLEZO

Page 310: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

310

B03 Masiha ndiye Mwana wa mtu.

EZEKIELI 1:26 Na juu ya anga, lililokuwa

juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa

kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti

samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha

enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana

kwa mfano wa mwanadamu juu yake.

DANIELI 7:13 Nikaona katika njozi za

usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa

mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya

mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku,

wakamleta karibu naye.

14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na

ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote,

na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake

ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita

kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza

kuangamizwa.

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

WAEBRANIA 8:1 Basi, katika hayo

tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili:

Tunaye kuhani mkuu wa namna hii,

aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi

cha Ukuu mbinguni,

UFUNUO WA YOHANA 5:13 Na kila

kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi

na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu

vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia,

vikisema, Baraka na heshima na utukufu

na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha

enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na

milele.

Ona pia: Isaya 6:1; Danieli 7:9,10; Zekaria 6:13; Waebrania 12:2; Ufunuo wa Yohana 4:2,3; Ufunuo wa Yohana 20:11.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

G06 Makao ya Roho Mtakatifu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

EZEKIELI 11:17 Basi nena, Bwana MUNGU

asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya

kabila za watu, na kuwakutanisha toka nchi

zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi

ya Israeli.

18 Nao watafika huko, nao wataondolea mbali

vitu vyake vyote vichukizavyo, na machukizo

yake yote.

19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia

roho mpya ndani yao; nami nitauondoa

moyo wa kijiwe katika miili yao, nami

nitawapa moyo wa nyama;

20 ili waende katika amri zangu, na kuyashika

maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa

watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

EZEKIELI 36:25 Nami nitawanyunyizia maji

safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na

uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami

nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa

moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu,

nami nitawapa moyo wa nyama.

27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na

kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi

mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

MATHAYO 3:11 Kweli mimi nawabatiza

kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye

nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala

sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye

atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa

EZEKIELI

Page 311: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

311

moto.

YOHANA 3:3 Yesu akajibu, akamwambia,

Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa

mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa

Mungu.

MATENDO YA MITUME 2:38 Petro

akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila

mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate

ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea

kipawa cha Roho Mtakatifu.

TITO 3:5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

1 PETRO 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba

wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa

rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili

tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka

kwake Yesu Kristo katika wafu;

Ona pia: #1; #2; #3; Yohana 1:13; 1 Petro 1:23; 1 Petro 2:2; Yohana 2:29; Yohana 3:9; Yohana 4:7; Yohana 5:1,4,18.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

EZEKIELI 16:60 Walakini nitalikumbuka

agano langu nililolifanya pamoja nawe,

katika siku za ujana wako, nami nitaweka

imara agano la milele pamoja nawe.

61 Hapo ndipo utakapozikumbuka njia zako,

na kutahayarika, hapo utakapowakaribisha

maumbu yako, walio wakubwa wako na

wadogo wako; nami nitakupa hao wawe binti

zako, lakini si kwa agano lako.

62 Nami nitaweka imara agano langu nawe;

nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana;

63 upate kukumbuka, na kufadhaika,

usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu

ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote

uliyoyatenda, asema Bwana MUNGU.

MATHAYO 26:28 kwa maana hii ndiyo damu

yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya

wengi kwa ondoleo la dhambi.

WAEBRANIA 8:6 Lakini sasa amepata huduma

iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe

wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya

ahadi zilizo bora.

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa

halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa

lile la pili.

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku

zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia

nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano

jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na

dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya

lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu

EZEKIELI

Page 312: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

312

kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki

karibu na kutoweka.

Ona pia: #1; #2; #5; Luka 22:14-20; Yohana 6:45; 2 Wakorintho 3:2-6,14-16; Waebrania 10:15-17; Waebrania 12:24; Waebrania

13:20.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

EZEKIELI 17:22 Bwana MUNGU asema

hivi; Mimi nami nitakitwaa kilele kirefu cha

mwerezi, na kukipandikiza mahali; na katika

vitawi vyake vilivyo juu nitatwaa kitawi

kimoja kilicho chororo, nami nitakipanda

juu ya mlima mrefu ulioinuka sana;

23 juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa

Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi,

na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi

mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila

namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi

yake watakaa.

24 Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa

mimi, Bwana, nimeushusha chini mti

mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha

mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu;

mimi, Bwana, nimenena, nami nimelitenda

jambo hili.

MATHAYO 7:17 Vivyo hivyo kila mti mwema

huzaa matunda mazuri; na mti mwovu

huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda

mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda

mazuri.

19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa

ukatupwa motoni.

20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

YOHANA 12:24 Amin, amin, nawaambia,

Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi,

ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali

ikifa, hutoa mazao mengi.

YOHANA 15:4 Kaeni ndani yangu, nami

ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza

kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya

mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani

yangu.

5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye

ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa

sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi

kufanya neno lo lote.

6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje

kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya

na kuyatupa motoni yakateketea.

7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno

yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo

lote nanyi mtatendewa.

8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile

mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi

wangu.

WAFILIPI 2:9 Kwa hiyo tena Mungu

alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile

lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu

vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini

ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO

NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ona pia: Zaburi 80:15; Zaburi 92:12; Zaburi 96:11-13; Isaya 4:2; Isaya 11:1; Isaya 27:6; Isaya 55:12,13; Yeremia 23:5; Yeremia

33:15,16; Zekaria 4:12-14; Zekaria 6:12,13.

EZEKIELI

Page 313: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

313

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

EZEKIELI 20:34 nami nitawatoa katika

mataifa, na kuwakusanya, na kuwatoa katika

nchi mlizotawanyika ndani yake, kwa mkono

hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa

ghadhabu iliyomwagika;

35 nami nitawaingiza katika jangwa la mataifa,

na huko ndiko nitakakoteta nanyi uso kwa

uso.

EZEKIELI 20:36-39

EZEKIELI 20:40 Kwa maana katika mlima

wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana

wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko

watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli,

wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali

huko, na huko nitataka matoleo yenu, na

malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu

vyenu vitakatifu vyote.

41 Nitawatakabali kama harufu ipendezayo,

nitakapowatoa katika mataifa, na

kuwakusanya toka nchi zile mlizotawanyika;

nami nitatakaswa kwenu machoni pa

mataifa.

42 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana,

nitakapowaingiza katika nchi ya Israeli,

katika nchi ile ambayo niliuinua mkono

wangu kwamba nitawapa baba zenu.

EZEKIELI 20:43-44

WARUMI 9:6 Si kana kwamba neno la

Mungu limetanguka. Maana hawawi wote

Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao

wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako

wataitwa;

8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto

wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi

wanahesabiwa kuwa wazao.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WAGALATIA 6:15 Kwa sababu kutahiriwa si

kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.

16 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo,

amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa

Israeli wa Mungu.

WAEFESO 1:5 Kwa kuwa alitangulia

kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia

ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa

mapenzi yake.

6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo

ametuneemesha katika huyo Mpendwa.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Ezekieli 28:24-26.

G03 Kuinuliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

EZEKIELI 21:26 Bwana MUNGU asema hivi;

Kiondoe kilemba, ivue taji; haya hayatakuwa

tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini,

kakishushe kilichoinuka.

27 Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua;

hiki nacho hakitakuwa tena, hata

atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami

nitampa.

WAEBRANIA 2:7 Umemfanya mdogo punde

kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu

na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za

mikono yako;

8 Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake.

Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini

EZEKIELI

Page 314: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

314

yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake.

Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa

chini yake.

9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo

punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa

sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji

ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya

Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.

UFUNUO WA YOHANA 4:4 Na viti

ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha

enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini

na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi

meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na

taji za dhahabu.

UFUNUO WA YOHANA 4:10 ndipo hao

wazee ishirini na wanne huanguka mbele

zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi,

nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na

milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile

kiti cha enzi, wakisema,

11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu

wetu, kuupokea utukufu na heshima na

uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba

vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako

vilikuwako, navyo vikaumbwa.

E15 Masiha ataleta habari njema.

D02 Kazi ya Masiha kama Nabii.

EZEKIELI 33:32 Na tazama, wewe umekuwa

kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu

mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga

kinanda vizuri; maana, wasikia maneno

yako, lakini hawayatendi.

33 Na hayo yatakapokuwapo (tazama,

yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa nabii

amekuwapo kati yao.

MATHAYO 21:46 Nao walipotafuta

kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa

maana wao walimwona kuwa nabii.

LUKA 7:16 Hofu ikawashika wote,

wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii

mkuu ametokea kwetu; na, Mungu

amewaangalia watu wake.

LUKA 7:31 Bwana akasema,

Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki?

Nao wamefanana na nini?

32 Wamefanana na watoto walioketi sokoni na

kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala

hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

33 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali

mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema,

Ana pepo.

34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na

kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi

huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao

watoza ushuru na wenye dhambi.

35 Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa

watoto wake wote.

YOHANA 6:14 Basi watu wale, walipoiona

ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni

nabii yule ajaye ulimwenguni.

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu

asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na

kutengwa na watu wake.

EZEKIELI

Page 315: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

315

Ona pia: Yeremia 28:9.

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

EZEKIELI 34:11 Maana, Bwana MUNGU

asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe,

naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na

kuwaulizia.

12 Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo

zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake

waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta

kondoo zangu; nami nitawaokoa katika

mahali pote walipotawanyika, katika siku ya

mawingu na giza.

13 Nami nitawatoa katika watu wa mataifa,

na kuwakusanya katika nchi zote, nami

nitawarudisha katika nchi yao wenyewe;

nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli,

kando ya mifereji ya maji; na katika mahali

pote pa nchi panapokaliwa na watu.

14 Nami nitawalisha malisho mema, pa juu

ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli

litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi

jema; nao watakula malisho mema, juu ya

milima ya Israeli.

15 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu,

nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU.

22 basi mimi nitaliokoa kundi langu, wala

hawatakuwa mateka tena; nami nitahukumu

kati ya mnyama na mnyama.

23 Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao,

naye atawalisha, naam, mtumishi wangu,

Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa

mchungaji wao.

24 Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na

mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati

yao; mimi, Bwana, nimesema haya.

EZEKIELI 34:25-31

EZEKIELI 20:41 Nitawatakabali kama

harufu ipendezayo, nitakapowatoa katika

mataifa, na kuwakusanya toka nchi zile

mlizotawanyika; nami nitatakaswa kwenu

machoni pa mataifa.

EZEKIELI 28:25 Bwana MUNGU asema hivi;

Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba

ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao

wametawanyika kati yao, na kutakasika kati

yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa

katika nchi yao wenyewe, niliyompa

mtumishi wangu, Yakobo.

26 Nao watakaa humo salama; naam, watajenga

nyumba, na kupanda mashamba ya

mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa

nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu

wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande

zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi

Bwana, Mungu wao.

EZEKIELI 30:3 Kwa maana siku ile i karibu,

siku ile ya Bwana i karibu, siku ya mawingu;

itakuwa wakati wa mataifa.

LUKA 15:4 Ni nani kwenu, mwenye

kondoo mia, akipotewa na mmojawapo,

asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani,

aende akamtafute yule aliyepotea hata

amwone?

5 Naye akiisha kumwona, humweka mabegani

pake akifurahi.

6 Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki

zake na jirani zake, akawaambia, Furahini

pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha

kumpata kondoo wangu aliyepotea.

EZEKIELI

Page 316: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

316

YOHANA 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu

akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na

kutoka, naye atapata malisho.

10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;

mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha

wawe nao tele.

11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji

mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya

kondoo.

12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji,

ambaye kondoo si mali yake, humwona

mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na

kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na

kuwatawanya.

13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa

mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu

kwake.

14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio

wangu nawajua; nao walio wangu wanijua

mimi;

15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo

Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya

kondoo.

16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi

hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti

yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi

moja na mchungaji mmoja.

YOHANA 21:15 Basi walipokwisha kula,

Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni

wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?

Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua

kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha

wana-kondoo wangu.

WAEBRANIA 13:20 Basi, Mungu wa

amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu

Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya

agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,

21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila

tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake,

naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele

zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye

milele na milele. Amina.

1 PETRO 2:25 Kwa maana mlikuwa

mnapotea kama kondoo; lakini sasa

mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa

roho zenu.

1 PETRO 5:4 Na Mchungaji mkuu

atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya

utukufu, ile isiyokauka.

UFUNUO WA YOHANA 7:16

Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu

tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo

yote.

17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye

katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Sefania 1:15.

EZEKIELI

Page 317: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

317

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

G06 Makao ya Roho Mtakatifu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

EZEKIELI 36:8 Lakini ninyi, enyi milima ya

Israeli, mtachipuza matawi yenu na kuwapa

watu wangu Israeli matunda yenu; maana

wa karibu kuja.

EZEKIELI 36:9-14

EZEKIELI 36:15 wala sitakusikizisha tena

aibu yao wasioamini, wala hutachukua

matukano ya watu tena; wala hutalikwaza

taifa lako tena, asema Bwana MUNGU.

EZEKIELI 36:24 Maana nitawatwaa kati ya

mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa

katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi

yenu wenyewe.

25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi

mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu

wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami

nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa

moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu,

nami nitawapa moyo wa nyama.

27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na

kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi

mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

28 Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba

zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami

nitakuwa Mungu wenu.

EZEKIELI 36:32- 38

EZEKIELI 11:19 Nami nitawapa moyo

mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao;

nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika

miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

EZEKIELI 36:31 Ndipo mtazikumbuka njia

zenu mbaya, na matendo yenu yasiyokuwa

mema, nanyi mtajichukia nafsi zenu kwa

macho yenu, kwa sababu ya maovu yenu na

machukizo yenu.

WARUMI 6:21 Ni faida gani basi

mliyopata siku zile kwa mambo hayo

mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana

mwisho wa mambo hayo ni mauti.

22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa

mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa

Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa,

na mwisho wake ni uzima wa milele.

WARUMI 8:14 Kwa kuwa wote

wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao

ndio wana wa Mungu.

15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa

utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya

kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia,

Aba, yaani, Baba.

16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na

roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

2 WAKORINTHO 3:7 Basi, ikiwa huduma

ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika

mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli

hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa,

kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni

utukufu uliokuwa ukibatilika;

EZEKIELI

Page 318: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

318

8 je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika

utukufu?

2 WAKORINTHO 5:17 Hata imekuwa,

mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe

kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa

mapya.

WAGALATIA 5:22 Lakini tunda la Roho ni

upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu

wema, fadhili, uaminifu,

WAGALATIA 6:15 Kwa sababu kutahiriwa si

kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Kutoka 19-20; Luka 11:13; Matendo ya Mitume 2:14-47; 1 Wakorintho 3:16; Waefeso 1:13,14; Waefeso

2:10; Tito 3:5,6; Waebrania 10:22; 1 Petro 1:18,19,22; Yohana 3:24; Yohana 5:5.

E11 Masiha atapeana uzima wa milele.

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

G06 Makao ya Roho Mtakatifu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

EZEKIELI 37:1-8

EZEKIELI 37:9 Ndipo akaniambia, Tabiri,

utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie

upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo,

kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi,

ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.

10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi

ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa

miguu yao, jeshi kubwa mno.

11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa

hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao

husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini

yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali

kabisa.

12 Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU

asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi

yenu, na kuwapandisha kutoka katika

makaburi yenu, enyi watu wangu, nami

nitawaingizeni katika nchi ya Israeli.

13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana,

nitakapoyafunua makaburi yenu, na

kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi

watu wangu.

14 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi

mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi

yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana,

nimesema hayo, na kuyatimiza, asema

Bwana.

ISAYA 66:14 Nanyi mtaona, na mioyo

yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi

kama majani mabichi; na mkono wa Bwana

utajulikana, uwaelekeao watumishi wake,

naye atawaonea adui zake ghadhabu.

EZEKIELI 28:25 Bwana MUNGU asema hivi;

Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba

ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao

wametawanyika kati yao, na kutakasika kati

yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa

katika nchi yao wenyewe, niliyompa

mtumishi wangu, Yakobo.

HOSEA 6:2 Baada ya siku mbili

atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi

tutaishi mbele zake.

AMOSI 9:14 Nami nitawarejeza tena

watu wangu Israeli waliohamishwa, nao

wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na

kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu

katika mashamba, na kunywa divai yake; nao

watafanyiza bustani, na kula matunda yake.

EZEKIELI

Page 319: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

319

15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala

hawatang›olewa tena watoke katika nchi yao

niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako.

WARUMI 8:11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye

aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani

yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika

wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika

hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani

yenu.

WARUMI 11:1 Basi, nauliza, Je! Mungu

aliwasukumia mbali watu wake? Hasha!

Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja

wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya

Benyamini.

2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake

aliowajua tokea awali. Au hamjui yale

yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi

anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,

3 Bwana, wamewaua manabii wako,

wamezibomoa madhabahu zako, nami

nimesalia peke yangu, nao wananitafuta

roho yangu.

4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje?

Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti

mbele ya Baali.

5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako

mabaki waliochaguliwa kwa neema.

WARUMI 11:24 Kwa maana ikiwa wewe

ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio

mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha

ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika

mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale

walio wa asili kuweza kupandikizwa katika

mzeituni wao wenyewe?

25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue

siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya

kwamba kwa sehemu ugumu umewapata

Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

WARUMI 11:32 Maana Mungu amewafunga

wote pamoja katika kuasi ili awarehemu

wote.

Ona pia: #1; #2; #5; Zaburi 126:2,3; Isaya 32:15; Yeremia 33:24-26; Ezekieli 11:19; Ezekieli 16:62,63; Ezekieli 36:24-31; Ezekieli

37:21,25; Ezekieli 39:29; Yoeli 2:28.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

EZEKIELI 37:21 Ukawaambie, Bwana

MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa

wana wa Israeli toka kati ya mataifa

walikokwenda, nami nitawakusanya pande

zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;

22 nami nitawafanya kuwa taifa moja katika

nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na

mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote;

wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala

hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena,

hata milele.

23 Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago

vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo,

wala kwa makosa yao mojawapo; lakini

nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao

yote, ambayo wamefanya dhambi ndani

yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa

watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

24 Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa

EZEKIELI

Page 320: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

320

mfalme juu yao, nao wote watakuwa na

mchungaji mmoja; nao wataenenda katika

hukumu zangu, na kuzishika amri zangu,

na kuzitenda.

25 Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo,

mtumishi wangu, walimokaa baba zenu;

nao watakaa humo, wao na watoto wao, na

watoto wa watoto wao, milele; na Daudi,

mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao

milele.

26 Tena nitafanya agano la amani pamoja nao;

litakuwa agano la milele pamoja nao; nami

nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu

pangu nitapaweka katikati yao milele.

27 Tena maskani yangu itakuwa pamoja nao;

nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa

watu wangu.

28 Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi

Bwana, mimi niwatakasaye Israeli,

patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao

milele.

EZEKIELI 11:19 Nami nitawapa moyo

mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao;

nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika

miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

20 ili waende katika amri zangu, na kuyashika

maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa

watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 10:14 Mimi ndimi mchungaji

mwema; nao walio wangu nawajua; nao

walio wangu wanijua mimi;

15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo

Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya

kondoo.

16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi

hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti

yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi

moja na mchungaji mmoja.

17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa

uhai wangu ili niutwae tena.

WARUMI 11:15 Maana ikiwa kutupwa kwao

kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je!

Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si

uhai baada ya kufa?

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

2 WAKORINTHO 6:16 Tena pana

mapatano gani kati ya hekalu la Mungu

na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la

Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema,

ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao

nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao

watakuwa watu wangu.

WAKOLOSAI 2:9 Maana katika yeye unakaa

utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya

kimwili.

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa

EZEKIELI

Page 321: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

321

kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu

mwamuzi wa watu wote, na roho za watu

wenye haki waliokamilika,

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

UFUNUO WA YOHANA 21:22 Nami

sikuona hekalu ndani yake; kwa maana

Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-

Kondoo, ndio hekalu lake.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Mwanzo 17:7; Kutoka 31:13; Kumbukumbu la Torati 30:1-10; 2 Samweli 23:5; Zaburi 126:1-6;

Isaya 9:6,7; Isaya 27:6,12,13; Isaya 40:11; Isaya 43:5,6; Isaya 49:8-26; Isaya 55:3,4; Isaya 59:20,21; Isaya 60:21,22; Yeremia

16:14-17; Yeremia 23:3-8; Yeremia 30:3,8-11,17-22; Yeremia 31:8-10,27,32-40; Yeremia 32:37-44; Yeremia 33:7-26; Yeremia

50:4,5; Ezekieli 11:11-16; Ezekieli 14:11; Ezekieli 20:12,43; Ezekieli 28:25,26; Ezekieli 34:13,23-25; Ezekieli 36:23-31,36-38; Ezekieli 38:23; Ezekieli 39:7; Ezekieli 43:7-9; Danieli 2:44,45; Hosea

1:11; Hosea 2:19-23; Hosea 3:4,5; Hosea 14:4-7; Amosi 9:14,15; Obadia 1:17-21; Mika 5:2-4,8,12,13; Yoeli 3:20; Zekaria 2:2-6;

Zekaria 6:12,13; Zekaria 8:4,5; Zekaria 13:1,2; Zekaria 14:11,21; 1 Wakorintho 1:30; 1 Wathesalonike 5:23; Waefeso 5:25,26.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

EZEKIELI 38:16 nawe utapanda juu uwajilie

watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika

nchi; itakuwa katika siku za mwisho,

nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa

wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu,

mbele ya macho yao.

ZEKARIA 12:9 Hata itakuwa siku hiyo, ya

kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa

yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.

2 TIMOTHEO 3:1 Lakini ufahamu neno hili, ya

kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za

hatari.

Ona pia: #1; #4; Isaya 2:2; Ezekieli 36:23; Ezekieli 38:8,23; Ezekieli 39:21; Danieli 10:14; Mika 4:1; 7:15-17.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

EZEKIELI 38:18 Itakuwa katika siku hiyo,

Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya

Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu

yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu.

WAEBRANIA 12:29 maana Mungu

wetu ni moto ulao.

Ona pia: Ezekieli 36:5,6; Zaburi 18:7,8; Zaburi 89:46.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

EZEKIELI 38:19 Kwa maana katika wivu

wangu, na katika moto wa ghadhabu

yangu, nimenena, Hakika katika siku ile

kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya

Israeli;

WAEBRANIA 12:26 ambaye sauti

yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini

sasa ameahidi akisema, Mara moja tena

nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

UFUNUO WA YOHANA 11:13 Na katika

saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi,

na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka;

wanadamu elfu saba wakauawa katika

tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na

hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.

EZEKIELI

Page 322: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

322

Ona pia: Isaya 42:13; Ezekieli 39:25; Yoeli 2:18; Yoeli 3:16; Hagai 2:6,7,21,22; Zekaria 1:14; Zekaria 14:3-5; Ufunuo wa Yohana

16:10.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

EZEKIELI 38:20 hata samaki wa baharini, na

ndege wa angani, na wanyama wa kondeni,

na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi,

na wanadamu wote walio juu ya uso wa

nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu;

nayo milima itatupwa chini, na magenge

yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.

UFUNUO WA YOHANA 6:12 Nami

nikaona, alipoifungua muhuri ya sita,

palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa

jeusi kama gunia la singa, mwezi wote

ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama

vile mtini upukutishavyo mapooza yake,

utikiswapo na upepo mwingi.

Ona pia: #6; Isaya 30:25; Yeremia 4:23-26; Hosea 4:3; Zekaria 14:3-5.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

EZEKIELI 38:21 Nami nitaita upanga, uje

juu yake katika milima yangu yote, asema

Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu

utakuwa juu ya ndugu yake.

22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa

damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na

mvua ya mawe makubwa sana, na moto na

kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa

kabila nyingi walio pamoja naye.

HAGAI 2:22 nami nitakipindua kiti cha

enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za

falme za mataifa; nami nitayapindua magari,

na hao wapandao ndani yake; farasi na hao

wawapandao wataanguka chini; kila mtu

kwa upanga wa ndugu yake.

23 Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi,

nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi

wangu, mwana wa Shealtieli, asema Bwana,

nami nitakufanya kuwa kama pete yenye

muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema

Bwana wa majeshi.

UFUNUO WA YOHANA 11:19 Kisha

Hekalu la Mungu lililoko mbinguni

likafunguliwa, na sanduku la agano lake

likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa

na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la

nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.

UFUNUO WA YOHANA 16:21 Na mvua

ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama

talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu

ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana

Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya

mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

Ona pia: #6; Zaburi 11:6; Isaya 28:17; Isaya 29:6; Isaya 54:17; Yeremia 25:31; Ezekieli 13:11; Zekaria 12:2,9.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

EZEKIELI 38:23 Nami nitajitukuza, na

kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya

macho ya mataifa mengi; nao watajua ya

kuwa mimi ndimi Bwana.

MATHAYO 24:35 Mbingu na nchi zitapita;

lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

EZEKIELI

Page 323: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

323

2 WATHESALONIKE 1:7 na kuwalipa ninyi

mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa

kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka

mbinguni pamoja na malaika wa uweza

wake

8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza

kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao

wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;

WAEBRANIA 12:26 ambaye sauti

yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini

sasa ameahidi akisema, Mara moja tena

nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

27 Lakini neno lile, Mara moja tena,

ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo

kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu

visivyoweza kutetemeshwa vikae.

28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza

kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo

kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya

kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na

kicho;

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:3 Nao

wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa

Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo,

wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo

yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za

haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa

mataifa.

4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 19:1 Baada ya

hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano

mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema,

Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina

BWANA MUNGU wetu.

2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za

haki; maana amemhukumu yule kahaba

mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake,

na kuipatiliza damu ya watumwa wake

mkononi mwake.

3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi

wake hupaa juu hata milele na milele.

4 Na wale wazee ishirini na wanne, na

wale wenye uhai wanne, wakasujudu na

kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti

cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.

5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi

ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi

watumwa wake wote, ninyi mnaomcha,

wadogo kwa wakuu.

6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano

mengi, na kama sauti ya maji mengi, na

kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema,

Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu,

Mwenyezi, amemiliki.

UFUNUO WA YOHANA 21:1 Kisha

nikaona mbingu mpya na nchi mpya;

kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya

kwanza zimekwisha kupita, wala hapana

bahari tena.

Ona pia: #1; #5; #6; Ezekieli 36:23; Ezekieli 37:28; 2 Petro 3:10,11.

EZEKIELI

Page 324: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

324

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

EZEKIELI 39:6 Nami nitapeleka moto juu ya

Magogu; na juu ya watu wote wakaao salama

katika visiwa; nao watajua ya kuwa mimi

ndimi Bwana.

7 Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa

limejulika kati ya watu wangu Israeli; wala

sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi

tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi

ndimi Bwana, na Aliye Mtakatifu katika

Israeli.

8 Tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema

Bwana MUNGU; hii ndiyo siku ile

niliyoinena.

21 Nami nitauweka utukufu wangu kati ya

mataifa, na mataifa wote wataiona hukumu

yangu niliyoitekeleza, na mkono wangu

niliouweka juu yao.

22 Basi, nyumba ya Israeli watajua ya kuwa

mimi ndimi Bwana, Mungu wao, tangu siku

hiyo na baadaye.

23 Nao mataifa watajua ya kuwa nyumba ya

Israeli walihamishwa, na kwenda kifungoni,

kwa sababu ya uovu wao; kwa sababu

waliniasi, nami nikawaficha uso wangu; basi

nikawatia katika mikono ya adui zao, nao

wakaanguka kwa upanga, wote pia.

24 Kwa kadiri ya uchafu wao, kwa kadiri ya

makosa yao, ndivyo nilivyowatenda, nami

nikawaficha uso wangu.

25 Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema

hivi, Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo

waliohamishwa, nitawahurumia nyumba

yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina

langu takatifu.

26 Nao watachukua aibu yao, na makosa

yao yote waliyoniasi, watakapokaa salama

katika nchi yao wenyewe, wala hapana mtu

atakayewatia hofu;

27 nitakapokuwa nimewaleta tena kutoka kabila

za watu, na kuwakusanya kwa kuwatoa

katika nchi za adui zao, na kutakaswa kati

yao mbele ya macho ya mataifa mengi.

28 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana,

Mungu wao, kwa kuwa naliwahamisha,

waende utumwani kati ya mataifa, na mimi

nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi

yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko

kamwe, hata mmojawapo;

29 wala sitawaficha uso wangu tena; kwa maana

nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya

Israeli, asema Bwana MUNGU.

YOELI 2:28 Hata itakuwa, baada ya hayo,

ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya

wote wenye mwili; na wana wenu, waume

kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota

ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa

wanawake, katika siku zile, nitamimina roho

yangu.

YOHANA 17:3 Na uzima wa milele ndio

huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa

kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

MATENDO YA MITUME 2:33 Basi yeye,

akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume

wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi

ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki

mnachokiona sasa na kukisikia.

WARUMI 9:6 Si kana kwamba neno la

Mungu limetanguka. Maana hawawi wote

Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

EZEKIELI

Page 325: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

325

7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao

wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako

wataitwa;

8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto

wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi

wanahesabiwa kuwa wazao.

WARUMI 11:1 Basi, nauliza, Je! Mungu

aliwasukumia mbali watu wake? Hasha!

Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja

wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya

Benyamini.

2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake

aliowajua tokea awali. Au hamjui yale

yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi

anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,

3 Bwana, wamewaua manabii wako,

wamezibomoa madhabahu zako, nami

nimesalia peke yangu, nao wananitafuta

roho yangu.

4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje?

Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti

mbele ya Baali.

5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako

mabaki waliochaguliwa kwa neema.

6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa

matendo tena, au hapo neema isingekuwa

neema.

7 Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli

alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale

waliochaguliwa walikipata, na wengine

walitiwa uzito.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui

kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule

kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili

ya baba zetu.

29 Kwa sababu karama za Mungu hazina

majuto, wala mwito wake.

30 Kwa maana kama ninyi zamani

mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata

rehema kwa kuasi kwao;

31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa

kupata rehema kwenu wao nao wapate

rehema.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Ezekieli 40-48; Matendo ya Mitume 2:14-18; Yohana 3:24.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

EZEKIELI 47:6 Akaniambia, Mwanadamu,

je! Umeona haya? Kisha akanichukua

akanirudisha mpaka ukingo wa mto.

7 Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya

ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana,

upande huu na upande huu.

8 Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka

kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo

yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika

bahari maji yatokezwayo yataingia baharini

,na maji yake yataponyeka.

9 Tena itakuwa, kila kiumbe hai

kisongamanacho, kila mahali itakapofika

mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi

mkubwa wa samaki, kwa sababu maji

haya yamefika huko maana maji yale

yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote

utakapofikilia mto huo.

10 Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu

nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu,

patakuwa ni mahali pa kutandazia

nyavu; samaki wao watakuwa namna zao

EZEKIELI

Page 326: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

326

mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa,

wengi sana.

11 Bali mahali penye matope, na maziwa yake,

hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi.

12 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake,

upande huu na upande huu, utamea

kila mti wa chakula, ambao majani

yake hayatanyauka, wala matunda yake

hayatatindika kamwe; utatoa matunda

mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake

yanatoka mahali patakatifu; na matunda

yake yatakuwa ni chakula; na majani yake

yatakuwa ni dawa.

EZEKIELI 47:13-23

MATHAYO 4:18 Naye alipokuwa akitembea

kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu

wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea

nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa

maana walikuwa wavuvi.

19 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya

kuwa wavuvi wa watu.

20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

MATHAYO 13:47 Tena ufalme wa mbinguni

umefanana na juya, lililotupwa baharini,

likakusanya samaki wa kila namna;

48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi,

wakakusanya walio wema vyomboni, bali

walio wabaya wakawatupa.

49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa

dunia; malaika watatokea, watawatenga

waovu mbali na wenye haki,

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung›aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na

upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa

uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,

wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na

majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Ona pia: #1; #2; #5; Mwanzo 2:10; Hesabu 34:1-12; Zaburi 65:9; Isaya 43:19,20.

EZEKIELI

Page 327: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

327

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

DANIELI 2:34 Nawe ukatazama hata jiwe

likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe

hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa

ya chuma na udongo, likaivunja vipande

vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na

ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu,

vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa

kama makapi ya viwanja vya kupepetea

wakati wa hari; upepo ukavipeperusha

hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe

lililoipiga hiyo sanamu likawa milima

mikubwa, likaijaza dunia yote.

44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa

mbinguni atausimamisha ufalme ambao

hautaangamizwa milele, wala watu wengine

hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme

hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao

utasimama milele na milele.

45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe

lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono,

na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma,

na ile shaba na ule udongo, na ile fedha,

na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu

amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa

baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri

yake ni thabiti.

2 SAMWELI 7:16 Na nyumba yako, na ufalme

wako, vitathibitishwa milele mbele yako.

Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa

na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha

Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na

kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki,

Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana

wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

MATHAYO 26:29 Lakini nawaambieni,

Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu

wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa

mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba

yangu.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 18:36 Yesu akajibu, Ufalme wangu

sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu

ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi

wangu wangenipigania, nisije nikatiwa

mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme

wangu sio wa hapa.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 12:10

Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa

kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme

wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo

wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki

DANIELI

Page 328: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

328

wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za

Mungu wetu, mchana na usiku.

Ona pia: #1.

B03 Masiha ndiye Mwana wa mtu.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

H11 Masiha atatukuzwa.

DANIELI 7:13 Nikaona katika njozi za

usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa

mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya

mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku,

wakamleta karibu naye.

14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na

ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote,

na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake

ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita

kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza

kuangamizwa.

18 Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea

ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele,

naam hata milele na milele.

22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao

watakatifu wake Aliye juu wakapewa

hukumu; na majira yakawadia watakatifu

waumiliki ufalme.

27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa

ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa

watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme

wake ni ufalme wa milele, na wote wenye

mamlaka watamtumikia na kumtii.

MATHAYO 11:27 Akasema, Nimekabidhiwa

vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye

Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye

Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana

apenda kumfunulia.

MATHAYO 24:30 ndipo itakapoonekana

ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni;

ndipo mataifa yote ya ulimwengu

watakapoomboleza, nao watamwona

Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu

ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu

mwingi.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

MATHAYO 26:64 Yesu akamwambia, Wewe

umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa

mtamwona Mwana wa Adamu ameketi

mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya

mawingu ya mbinguni.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote

kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la

Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote

niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo

pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa

dahari.

LUKA 10:22 Akasema, Nimekabidhiwa

vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye

Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye

Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana

apenda kumfunulia.

DANIELI

Page 329: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

329

LUKA 21:27 Hapo ndipo watakapomwona

Mwana wa Adamu akija katika wingu

pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

YOHANA 3:35 Baba ampenda Mwana, naye

amempa vyote mkononi mwake.

YOHANA 5:22 Tena Baba hamhukumu mtu

ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;

23 ili watu wote wamheshimu Mwana

kama vile wanavyomheshimu Baba.

Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba

aliyempeleka.

YOHANA 5:27 Naye akampa amri ya

kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa

Adamu.

WAEFESO 1:19 na ubora wa ukuu wa uweza

wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa

kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;

20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika

wafu, akamweka mkono wake wa kuume

katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka,

na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo,

wala si ulimwenguni humu tu, bali katika

ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,

akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa

ajili ya kanisa; ambalo

2 TIMOTHEO 2:12 Kama tukistahimili,

tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana

yeye, yeye naye atatukana sisi;

WAEBRANIA 12:28 Basi kwa kuwa

tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa,

na mwe na neema, ambayo kwa hiyo

tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza,

pamoja na unyenyekevu na kicho;

UFUNUO WA YOHANA 1:7 Tazama,

yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona,

na hao waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.

Amina.

UFUNUO WA YOHANA 2:26 Na yeye

ashindaye, na kuyatunza matendo yangu

hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya

mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma,

kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo,

kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba

yangu.

UFUNUO WA YOHANA 5:9 Nao

waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili

wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua

muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa,

ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu

wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa

Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

UFUNUO WA YOHANA 20:6 Huo

ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu,

ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa

kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina

nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu

na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye

hiyo miaka elfu.

UFUNUO WA YOHANA 22:5 Wala

hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja

ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana

Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata

milele na milele.

DANIELI

Page 330: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

330

Ona pia: #1; #5; Zaburi 8:6; Ezekieli 1:26; Mathayo 13:41; Marko 14:61,62; Yohana 3:13; Yohana 12:34; Matendo ya Mitume 2:33-36;

1 Petro 3:22; Ufunuo wa Yohana 14:14.

E26 Kazi ya ukombozi ya Masiha.

DANIELI 9:24 Muda wa majuma sabini

umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji

wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na

kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho

kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele,

na kutia muhuri maono na unabii, na

kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

MATHAYO 11:13 Kwa maana manabii wote na

torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi,

akaketi; na watu wote waliokuwamo katika

sinagogi wakamkazia macho.

21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya

yametimia masikioni mwenu.

LUKA 24:25 Akawaambia, Enyi

msiofahamu, wenye mioyo mizito ya

kuamini yote waliyoyasema manabii!

26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya

na kuingia katika utukufu wake?

27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote,

akawaeleza katika maandiko yote mambo

yaliyomhusu yeye mwenyewe.

YOHANA 1:41 Huyo akamwona

kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe,

akamwambia, Tumemwona Masihi (maana

yake, Kristo).

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

WARUMI 5:10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa

adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti

ya Mwana wake; zaidi sana baada ya

kupatanishwa tutaokolewa katika uzima

wake.

2 WAKORINTHO 5:18 Lakini vyote pia

vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha

sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa

huduma ya upatanisho;

19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo,

akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake,

asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani

yetu neno la upatanisho.

20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana

kwamba Mungu anasihi kwa vinywa

vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo

mpatanishwe na Mungu.

21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa

dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa

haki ya Mungu katika Yeye.

WAFILIPI 3:9 tena nionekane katika yeye,

nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo

kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani

DANIELI

Page 331: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

331

iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa

Mungu, kwa imani;

WAKOLOSAI 2:14 akiisha kuifuta ile hati

iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu

zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa

isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

WAEBRANIA 1:8 Lakini kwa habari za Mwana

asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha

milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako

ni fimbo ya adili.

WAEBRANIA 7:26 Maana ilitupasa sisi tuwe na

kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu,

asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo

lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu

kuliko mbingu;

WAEBRANIA 10:14 Maana kwa toleo

moja amewakamilisha hata milele hao

wanaotakaswa.

1 YOHANA 3:8 atendaye dhambi ni wa

Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi

tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa

Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za

Ibilisi.

Ona pia: Mambo ya Walawi 25:8; Hesabu 14:35; Zaburi 45:7; Isaya 53:10,11; Isaya 56:1; Isaya 61:1; Yeremia 23:5,6; Ezekieli 4:6; Luka 24:44,45; 1 Wakorintho 1:30; 2 Wakorintho 5:21; Wakolosai 1:20; Waebrania 2:17; Waebrania 9:11-14,26; Ufunuo wa Yohana

14:6.

A07 Atakuwa Masiha wa Israeli.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

F04 Matokeo ya kukataliwa kwa Masiha.

DANIELI 9:25 Basi ujue na kufahamu, ya

kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza

na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani

zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na

majuma saba; na katika majuma sitini na

mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu

zake na handaki, naam, katika nyakati za

taabu.

ISAYA 55:4 Angalieni, nimemweka kuwa

shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi

na jemadari kwa kabila za watu.

MARKO 13:14 Lakini mlionapo chukizo la

uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye

na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na

wakimbilie milimani;

YOHANA 1:41 Huyo akamwona

kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe,

akamwambia, Tumemwona Masihi (maana

yake, Kristo).

MATENDO YA MITUME 3:15

mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye

Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu

mashahidi wake.

MATENDO YA MITUME 5:31 Mtu huyo

Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa

kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape

Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

Ona pia: Isaya 9:6; Mika 5:2; Mathayo 24:15; Yohana 4:25.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

DANIELI 9:26 Na baada ya yale majuma

sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali,

naye atakuwa hana kitu; na watu wa

mkuu atakayekuja watauangamiza mji,

na patakatifu; na mwisho wake utakuwa

DANIELI

Page 332: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

332

pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita

vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.

ISAYA 53:8 Kwa kuonewa na

kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake

ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa

mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa

sababu ya makosa ya watu wangu.

MATHAYO 24:2 Naye akajibu akawaambia,

Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni,

Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.

MARKO 9:12 Akajibu akawaambia, Ni

kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya

yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje

Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa

mengi na kudharauliwa?

MARKO 13:2 Yesu akajibu, akamwambia,

Wayaona majengo haya makubwa?

Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomolewa.

LUKA 21:24 Wataanguka kwa ukali

wa upanga, nao watatekwa nyara na

kuchukuliwa katika mataifa yote; na

Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata

majira ya Mataifa yatakapotimia.

LUKA 24:26 Je! Haikumpasa Kristo

kupata mateso haya na kuingia katika

utukufu wake?

LUKA 24:46 Akawaambia, Ndivyo

ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na

kufufuka siku ya tatu;

YOHANA 11:51 Na neno hilo yeye

hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa

alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri

ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa

hilo.

52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini

pamoja na hayo awakusanye watoto wa

Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.

YOHANA 12:32 Nami nikiinuliwa juu ya

nchi, nitawavuta wote kwangu.

33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani

atakayokufa.

34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia

katika torati ya kwamba Kristo adumu

hata milele; nawe wasemaje ya kwamba

imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa?

Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

Ona pia: Luka 19:43,44; Luka 21:6; 1 Petro 2:24; 1 Petro 3:18.

F04 Matokeo ya kukataliwa kwa Masiha.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

DANIELI 9:27 Naye atafanya agano thabiti

na watu wengi kwa muda wa juma moja; na

kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka

na dhabihu; na mahali pake litasimama

chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo,

na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu

yake mwenye kuharibu.

MATHAYO 24:14 Tena habari njema ya ufalme

itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa

ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule

mwisho utakapokuja.

15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la

uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli,

limesimama katika patakatifu (asomaye na

afahamu),

DANIELI

Page 333: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

333

MARKO 13:14 Lakini mlionapo chukizo la

uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye

na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na

wakimbilie milimani;

LUKA 21:20 Lakini, hapo mtakapoona mji

wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi,

ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake

umekaribia.

21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie

milimani, na walio katikati yake wakimbilie

nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili

yatimizwe yote yaliyoandikwa.

23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha

katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na

shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya

taifa hili.

24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao

watatekwa nyara na kuchukuliwa katika

mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa

na Mataifa, hata majira ya Mataifa

yatakapotimia.

Ona pia: Kumbukumbu la Torati 4:26-28; Kumbukumbu la Torati 28:15; Kumbukumbu la Torati 31:28,29; Isaya 10:22,23;

Isaya 28:22; Danieli 8:13; Danieli 11:36; Danieli 12:11; 1 Wathesalonike 2:14-16.

B18 Utakatifu, uzuri na utukufu wa Masiha.

DANIELI 10:5 naliinua macho yangu,

nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo

za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu

safi ya Ufazi;

6 mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi

safi, na uso wake mfano wa umeme, na

macho yake kama taa za moto, na mikono

yake na miguu yake rangi yake kama shaba

iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake

kama sauti ya umati wa watu.

UFUNUO WA YOHANA 1:13 na

katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano

wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika

miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu

matitini.

14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa

nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na

macho yake kama mwali wa moto;

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa

sana, kana kwamba imesafishwa katika

tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji

mengi.

16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono

wake wa kuume; na upanga mkali, wenye

makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake;

na uso wake kama jua liking›aa kwa nguvu

zake.

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni

pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono

wake wa kuume juu yangu, akisema,

Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa

mwisho,

Ona pia: Mathayo 17:2; Luka 9:29; Ufunuo wa Yohana 19:12.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

DANIELI 12:1 Wakati huo Mikaeli

atasimama, jemadari mkuu, asimamaye

upande wa wana wa watu wako; na

kutakuwa na wakati wa taabu, mfano

wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo

taifa hata wakati uo huo; na wakati huo

watu wako wataokolewa; kila mmoja

atakayeonekana ameandikwa katika kitabu

DANIELI

Page 334: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

334

kile.

ISAYA 4:3 Tena itakuwa ya kwamba

yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye

aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa

mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa

miongoni mwa hao walio hai ndani ya

Yerusalemu;

MATHAYO 24:21 Kwa kuwa wakati huo

kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea

namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu

hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

LUKA 10:20 Lakini, msifurahi kwa vile

pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu

majina yenu yameandikwa mbinguni.

UFUNUO WA YOHANA 3:5 Yeye

ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe,

wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu

cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za

Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #2; Zaburi 69:28; Isaya 9:7; Isaya 26:20,21; Yeremia 30:7; Ezekieli 34:24; Danieli 9:25; Danieli 10:21; Marko 13:19;

Luka 21:23,24; Wafilipi 4:3; Ufunuo wa Yohana 13:8; Ufunuo wa Yohana 16:17-21; Ufunuo wa Yohana 19:11-16.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

DANIELI 12:2 Tena, wengi wa hao walalao

katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine

wapate uzima wa milele, wengine aibu na

kudharauliwa milele.

MATHAYO 25:31 Hapo atakapokuja Mwana

wa Adamu katika utukufu wake, na malaika

watakatifu wote pamoja naye, ndipo

atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake;

naye atawabagua kama vile mchungaji

abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume,

na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko

mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa

na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa

tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

MATENDO YA MITUME 17:31 Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu

walimwengu kwa haki, kwa mtu yule

aliyemchagua; naye amewapa watu wote

uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua

katika wafu.

WARUMI 2:16 katika siku ile Mungu

atakapozihukumu siri za wanadamu,

sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

1 WATHESALONIKE 4:14 Maana, ikiwa

twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka,

vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu,

Mungu atawaleta pamoja naye.

UFUNUO WA YOHANA 20:12

Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo,

wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi;

na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine

kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na

hao wafu wakahukumiwa katika mambo

hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,

DANIELI

Page 335: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

335

sawasawa na matendo yao.

Ona pia: #5; #6; Ayubu 19:25-27; Mathayo 22:32; Warumi 9:21.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

DANIELI 12:3 Na walio na hekima

watang›aa kama mwangaza wa anga; na hao

waongozao wengi kutenda haki watang›aa

kama nyota milele na milele.

MATHAYO 13:43 Ndipo wenye haki

watakapong›aa kama jua katika ufalme wa

Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

MATHAYO 19:28 Yesu akawaambia, Amin,

nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata

mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi

Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu

wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi

na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na

mbili za Israeli.

WAFILIPI 2:16 mkishika neno la uzima;

nipate sababu ya kuona fahari katika siku

ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala

sikujitaabisha bure.

17 Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na

ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi

pamoja nanyi nyote.

1 WATHESALONIKE 2:19 Maana tumaini

letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea

fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana

wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?

20 Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha

yetu.

Ona pia: #1; Danieli 11:33,35; Luka 1:16,17; 1 Wakorintho 3:10; Waefeso 4:11.

DANIELI

Page 336: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

336

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

HOSEA 1:10 Tena itakuwa ya kwamba

hesabu ya wana wa Israeli itafanana na

mchanga wa bahari, usioweza kupimwa

wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala

ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu,

wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu

aliye hai.

11 Na wana wa Yuda na wana wa Israeli

watakusanyika pamoja, nao watajiwekea

kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika

nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa

kuu sana.

MWANZO 13:16 Na uzao wako nitaufanya

uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu

akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao

wako nao utahesabika.

YOHANA 11:52 Wala si kwa ajili ya taifa

hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye

watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe

wamoja.

MATENDO YA MITUME 2:47

wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu

wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku

kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

WARUMI 9:26 Tena itakuwa mahali pale

walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo

wataitwa wana wa Mungu aliye hai.

27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya

Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa

Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa

bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

WAGALATIA 3:27 Maana ninyi nyote

mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana

mtumwa wala huru. Hapana mtu mume

wala mtu mke. Maana ninyi nyote

mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa

uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na

ahadi.

WAGALATIA 6:15 Kwa sababu kutahiriwa si

kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.

16 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo,

amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa

Israeli wa Mungu.

WAEFESO 1:10 Yaani, kuleta madaraka ya

wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote

katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya

duniani pia. Naam, katika yeye huyo;

WAEBRANIA 11:12 Na kwa ajili ya hayo

wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa

kama mfu, watu wengi kama nyota za

mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio

ufuoni, usioweza kuhesabika.

13 Hawa wote wakafa katika imani,

wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona

tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri

kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya

nchi.

UFUNUO WA YOHANA 7:4 Nikasikia

hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila

kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na

nne elfu.

Ona pia: #1; #2; #3; Mwanzo 32:12; Isaya 43:5,6; Isaya 49:17-26; Isaya 54:1-3; Isaya 60:4-22; Isaya 66:20-22; Hosea 2:23.

HOSEA

Page 337: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

337

B20 Upendo wa Mfalme kwa watu Wake.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

HOSEA 2:15 Nami nitampa mashamba

yake ya mizabibu toka huko, na bonde

la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye

ataniitikia huko, kama siku zile za ujana

wake, na kama siku ile alipopanda kutoka

nchi ya Misri.

16 Tena siku hiyo itakuwa, asema Bwana,

utaniita Ishi

17 Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali

kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa

majina yao.

18 Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama

wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege

wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami

nitavivunja upinde na upanga na silaha

vitoke katika nchi, nami nitawalalisha

salama salimini.

19 Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele;

naam, nitakuposa kwa haki, na kwa

hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.

20 Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe

utamjua Bwana.

21 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika,

asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo

zitaiitikia nchi;

22 nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na

mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli.

23 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili

yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye

asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale

wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu

wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu

wangu.

ISAYA 11:6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja

na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja

na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba

na kinono watakuwa pamoja, na mtoto

mdogo atawaongoza.

7 Ng›ombe na dubu watalisha pamoja; watoto

wao watalala pamoja; na simba atakula

majani kama ng›ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la

nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono

wake katika pango la fira.

ISAYA 54:5 Kwa sababu Muumba wako

ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo

jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye

Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa

dunia yote.

HABAKUKI 2:4 Tazama, roho yake hujivuna,

haina unyofu ndani yake; lakini mwenye

haki ataishi kwa imani yake.

MATHAYO 11:27 Akasema, Nimekabidhiwa

vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye

Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye

Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana

apenda kumfunulia.

YOHANA 17:3 Na uzima wa milele ndio

huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa

kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

WARUMI 1:17 Kwa maana haki ya Mungu

inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata

imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki

ataishi kwa imani.

WARUMI 9:24 ndio sisi aliotuita, si watu wa

Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?

25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea,

HOSEA

Page 338: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

338

Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu

wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa

mpenzi wangu.

26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa,

Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana

wa Mungu aliye hai.

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

2 WAKORINTHO 11:2 Maana nawaonea

wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa

naliwaposea mume mmoja, ili nimletee

Kristo bikira safi.

WAEBRANIA 8:11 Nao hawatafundishana kila

mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu

yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana

wote watanijua, Tangu mdogo wao hata

mkubwa wao.

1 YOHANA 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana

wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa

akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,

nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli,

yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.

Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa

milele.

UFUNUO WA YOHANA 12:6 Yule

mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo

ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili

wamlishe huko muda wa siku elfu na mia

mbili na sitini.

UFUNUO WA YOHANA 12:14

Mwanamke yule akapewa mabawa mawili

ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake

nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo

kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati,

mbali na nyoka huyo.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: #1; #2; #5; Mambo ya Walawi 26:40-45; Kumbukumbu la Torati 26:17-19; Kumbukumbu la Torati 30:3-5; Isaya 49:13-26; Isaya 51:3; Yeremia 2:2; Yeremia 3:12-24; Yeremia 24:7; Yeremia 30:18-22; Yeremia 31:1-37; Yeremia 32:36-41; Yeremia 33:6-26;

Ezekieli 34:22-31; Ezekieli 36:8-15; Ezekieli 37:11-28; Ezekieli 39:25-29; Hosea 1:11; Amosi 9:11-15; Mika 7:14-20; Sefania 3:12-20;

Zekaria 1:16,17; Zekaria 8:12-15; Zekaria 10:9-12; Zekaria 13:9.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

HOSEA 3:4 Kwa maana wana wa Israeli

watakaa siku nyingi bila mfalme, wala

mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala

naivera, wala kinyago;

MATHAYO 24:1 Yesu akaenda zake, akatoka

hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili

kumwonyesha majengo ya hekalu.

2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya

yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa

jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.

LUKA 21:24 Wataanguka kwa ukali

wa upanga, nao watatekwa nyara na

kuchukuliwa katika mataifa yote; na

Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata

majira ya Mataifa yatakapotimia.

HOSEA

Page 339: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

339

YOHANA 19:15 Basi wale wakapiga kelele,

Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe!

Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme

wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi

hatuna mfalme ila Kaisari.

Ona pia: Mwanzo 49:10; Ezekieli 34:23,24; Danieli 8:11-13; Danieli 9:27; Danieli 12:11; Mika 5:2-5; Zekaria 13:2; Waebrania

10:26.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HOSEA 3:5 baada ya hayo wana wa

Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana,

Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao

watamwendea Bwana na wema wake kwa

kicho siku za mwisho.

MATENDO YA MITUME 15:16 Baada ya

mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena

nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga

tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

WAEBRANIA 1:1 Mungu, ambaye alisema

zamani na baba zetu katika manabii kwa

sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika

Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote,

tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

Ona pia: #2; Yeremia 3:22,23; Hosea 5:15; Hosea 10:3.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HOSEA 6:1 Njoni, tumrudie Bwana;

maana yeye amerarua, na yeye atatuponya;

yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha

zetu.

2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu

atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.

WARUMI 11:15 Maana ikiwa kutupwa kwao

kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je!

Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si

uhai baada ya kufa?

WARUMI 11:26 Hivyo Israeli wote

wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi

atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na

maasia yake.

1 WAKORINTHO 15:4 na ya kuwa

alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu,

kama yanenavyo maandiko;

Ona pia: #1; #2; Mwanzo 1:9-13; Hesabu 17:8; Isaya 26:19; Isaya 55:7; Yeremia 3:22; Maombolezo 3:22,40,41; Hosea 5:15; Hosea

13:16; Luka 24:21; Yohana 2:1; Warumi 14:8; Ufunuo wa Yohana 11:14,15.

HOSEA

Page 340: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

340

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HOSEA 6:3 Nasi na tujue, naam,

tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake

ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama

mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.

2 SAMWELI 23:3 Mungu wa Israeli alisema,

Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye

wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho

cha Mungu,

4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,

Asubuhi isiyo na mawingu.

LUKA 1:78 Kwa njia ya rehema za

Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza

utokao juu umetufikia,

YOHANA 17:3 Na uzima wa milele ndio

huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa

kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

UFUNUO WA YOHANA

22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika

wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo

katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina

na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung›aa

ya asubuhi.

Ona pia: #1; #2; Hosea 10:12; 2 Petro 1:19.

E02 Mahali pa huduma ya Masiha.

HOSEA 11:1 Israeli alipokuwa mtoto,

nalikuwa nikimpenda, nikamwita

mwanangu atoke Misri.

MATHAYO 2:13 Na hao walipokwisha

kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana

alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema,

Ondoka, umchukue mtoto na mama yake,

ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie;

kwa maana Herode anataka kumtafuta

mtoto amwangamize.

14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama

yake usiku, akaenda zake Misri;

15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili

litimie neno lililonenwa na Bwana kwa

ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri

nalimwita mwanangu.

E04 Ushindi wa Masiha dhidi ya dhambi.

E11 Kazi na huduma ya Masiha.

E14 Masiha atashinda kifo na giza.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HOSEA 13:14 Nitawakomboa na nguvu za

kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti,

ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi

kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na

macho yangu.

1 WAKORINTHO 15:52 kwa dakika

moja, kufumba na kufumbua, wakati wa

parapanda ya mwisho; maana parapanda

italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na

uharibifu, nasi tutabadilika.

53 Maana sharti huu uharibikao uvae

kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae

kutokufa.

54 Basi huu uharibikao utakapovaa

kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa

kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile

neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa

kushinda.

55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U

wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

HOSEA

Page 341: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

341

56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za

dhambi ni torati.

57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye

kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ona pia: Isaya 26:19; 1 Wakorintho 15:21,22; 2 Wakorintho 5:4; Ufunuo wa Yohana 20:13; Ufunuo wa Yohana 21:14.

G05 Masiha atapata matunda mengi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HOSEA 14:4 Mimi nitawaponya kurudi

nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa

moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.

5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli;

naye atachanua maua kama nyinyoro, na

kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.

6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake

utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu

yake kama Lebanoni.

7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake

watarejea; watafufuka kama ngano, na

kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake

itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.

8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena

na sanamu? Mimi nimeitika, nami

nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi

wenye majani mabichi. Kwangu mimi

yamepatikana matunda yako.

ISAYA 44:3 Kwa maana nitamimina maji

juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu

ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu

juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao

utakaowazaa;

4 nao watatokea katika manyasi, kama mierebi

karibu na mifereji ya maji.

WIMBO ULIO BORA 2:3 Kama mpera kati ya

miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu

kati ya vijana. Naliketi kivulini mwake kwa

furaha, Na matunda yake naliyaonja kuwa

matamu.

MIKA 4:4 Bali wataketi kila mtu

chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini

wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu;

kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi

kimesema hivi.

MIKA 5:7 Na hayo mabaki ya Yakobo

yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa

umande utokao kwa Bwana, mfano wa

manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea

mtu, wala kuwakawilia wanadamu.

ZEKARIA 3:10 Katika siku ile, asema Bwana

wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu

jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya

mtini.

LUKA 3:8 Basi, toeni matunda

yapatanayo na toba; wala msianze kusema

mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye

Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya

kwamba katika mawe haya Mungu aweza

kumwinulia Ibrahimu watoto.

9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa

penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa

matunda mazuri hukatwa na kutupwa

motoni.

LUKA 6:43 Kwa maana hakuna mti

mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti

mbaya uzaao matunda mazuri;

44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa

matunda yake; maana, katika miiba

hawachumi tini, wala katika michongoma

hawachumi zabibu.

HOSEA

Page 342: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

342

YOHANA 15:2 Kila tawi ndani yangu

lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo

hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya

lile neno nililowaambia.

4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu.

Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake,

lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi,

msipokaa ndani yangu.

5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye

ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa

sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi

kufanya neno lo lote.

6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje

kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya

na kuyatupa motoni yakateketea.

7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno

yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo

lote nanyi mtatendewa.

8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile

mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi

wangu.

Ona pia: #1; #2; Zaburi 72:16; Isaya 27:6; Isaya 35:2; Isaya 57:18; Yeremia 2:21; Yeremia 3:22; Yeremia 33:6; Ezekieli 17:8,22-

24; Hosea 2:12; Hosea 10:1; Yoeli 2:22; Habakuki 3:17,18.

HOSEA

Page 343: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

343

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

YOELI 2:1 Pigeni tarumbeta katika

Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima

wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi

na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana

inakuja. Kwa sababu inakaribia;

YOELI 2:2-12

YOELI 2:13 rarueni mioyo yenu, wala si

mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu

wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye

neema, amejaa huruma; si mwepesi wa

hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi

mabaya.

14 N›nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka,

na kutuachia baraka nyuma yake, naam,

sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa

Bwana, Mungu wenu?

YOELI 2:15-17

WARUMI 2:4 Au waudharau wingi

wa wema wake na ustahimili wake na

uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa

Mungu wakuvuta upate kutubu?

1 WATHESALONIKE 5:2 Maana ninyi

wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya

Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

1 PETRO 4:7 Lakini mwisho wa mambo

yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe

katika sala.

Ona pia: #5; Zaburi 103:8; Isaya 57:15; 66:2; Amosi 3:6; Mika 7:18; Sefania 2:3; 3:11; Zekaria 8:3; Malaki 4:2.

E16 Masiha atabariki watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

YOELI 2:18 Hapo ndipo Bwana alipoona

wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia

watu wake.

19 Bwana akajibu, akawaambia watu wake;

Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na

mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala

sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa;

YOELI 2:20-22

23 Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni,

mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa

kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika,

kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea

mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli,

kama kwanza.

YOELI 2:24-25

YOELI 2:26 Nanyi mtakula chakula tele

na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana,

Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya

ajabu; na watu wangu hawatatahayari

kamwe.

27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya

Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana,

Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na

watu wangu hawatatahayari kamwe.

WARUMI 9:23 tena, ili audhihirishe wingi

wa utukufu wake katika vile vyombo vya

rehema, alivyovitengeneza tangu zamani

vipate utukufu;

YAKOBO 5:11 Angalieni, twawaita heri

wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira

yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana

ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema,

mwenye huruma.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

YOELI

Page 344: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

344

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

Ona pia: #1; #2; #3; Zaburi 72:6,7.

E27 Kutoa moyo mpya na roho mpya.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

YOELI 2:28 Hata itakuwa, baada ya hayo,

ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya

wote wenye mwili; na wana wenu, waume

kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota

ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa

wanawake, katika siku zile, nitamimina roho

yangu.

ISAYA 44:3 Kwa maana nitamimina maji

juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu

ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu

juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao

utakaowazaa;

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

LUKA 11:13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu

mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,

je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana

kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

YOHANA 3:5 Yesu akajibu, Amin, amin,

nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na

kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa

Mungu.

YOHANA 7:38 Aniaminiye mimi, kama vile

maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo

hai itatoka ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

YOHANA 14:16 Nami nitamwomba Baba,

naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae

nanyi hata milele;

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu

hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni

wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua,

maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani

yenu.

YOHANA 15:26 Lakini ajapo huyo Msaidizi,

nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo

Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye

atanishuhudia.

YOHANA 16:7 Lakini mimi nawaambia iliyo

kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa

maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi

hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,

nitampeleka kwenu.

8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha

ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki,

na hukumu.

9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu

hawaniamini mimi;

10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi

naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni

tena;

11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule

YOELI

Page 345: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

345

mkuu wa ulimwengu huu amekwisha

kuhukumiwa.

12 Hata bado nikali ninayo mengi ya

kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili

hivi sasa.

13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa

kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli

yote; kwa maana hatanena kwa shauri

lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia

atayanena, na mambo yajayo atawapasha

habari yake.

14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa

katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.

MATENDO YA MITUME 2:16 lakini

jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha

nabii Yoeli,

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu, na

wana wenu na binti zenu watatabiri; na

vijana wenu wataona maono; na wazee wenu

wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi

wangu wanaume na wanawake Roho yangu,

nao watatabiri.

MATENDO YA MITUME 10:44 Petro

alipokuwa akisema maneno hayo Roho

Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile

neno.

45 Na wale waliotahiriwa, walioamini,

wakashangaa, watu wote waliokuja

pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao

wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.

MATENDO YA MITUME 13:2 Basi

hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana

ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema,

Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile

niliyowaitia.

WARUMI 5:5 na tumaini halitahayarishi;

kwa maana pendo la Mungu limekwisha

kumiminwa katika mioyo yetu na Roho

Mtakatifu tuliyepewa sisi.

WARUMI 8:13 kwa maana kama tukiishi

kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka

kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya

mwili kwa Roho, mtaishi.

14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa

Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa

utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya

kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia,

Aba, yaani, Baba.

16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na

roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

1 WAKORINTHO 2:12 Lakini sisi

hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho

atokaye kwa Mungu, makusudi tupate

kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

13 Nayo twayanena, si kwa maneno

yanayofundishwa kwa hekima ya

kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho,

tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno

ya rohoni.

1 WAKORINTHO 6:19 Au hamjui ya kuwa

mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu

aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?

Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

Ona pia: Mithali 1:23; Mathayo 12:32; Warumi 8:9-12; 1 Wakorintho 12:4,8,11,13; 1 Wakorintho 15:45; 2 Wakorintho 3:6;

Wagalatia 4:6; 2 Wathesalonike 2:13; 1 Petro 1:11,12.

YOELI

Page 346: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

346

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

YOELI 2:30 Nami nitaonyesha mambo ya

ajabu katika mbingu na katika dunia, damu,

na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa

damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo

kuu na itishayo.

32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote

atakayeliita jina la Bwana ataponywa;

kwa kuwa katika mlima Sayuni na

katika Yerusalemu watakuwako watu

watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na

katika mabaki, hao awaitao Bwana.

MATHAYO 24:29 Lakini mara, baada ya dhiki

ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi

hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka

mbinguni, na nguvu za mbinguni

zitatikisika;

30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana

wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote

ya ulimwengu watakapoomboleza, nao

watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya

mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na

utukufu mwingi.

31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na

sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya

wateule wake toka pepo nne, toka mwisho

huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

MATHAYO 27:45 Basi tangu saa sita palikuwa

na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.

MARKO 13:24 Lakini siku zile, baada

ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi

hatautoa mwanga wake.

25 na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka,

na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.

LUKA 21:11 kutakuwa na matetemeko

makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali

mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu

kutoka mbinguni.

LUKA 21:25 Tena, kutakuwa na ishara

katika jua, na mwezi, na nyota; na katika

nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa

uvumi wa bahari na msukosuko wake;

26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na

kwa kutazamia mambo yatakayoupata

ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni

zitatikisika.

MATENDO YA MITUME 2:19 Nami

nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara

katika nchi chini, damu na moto, na mvuke

wa moshi.

20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa

damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo

kuu na iliyo dhahiri.

21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana

ataokolewa.

UFUNUO WA YOHANA 6:12 Nami

nikaona, alipoifungua muhuri ya sita,

palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa

jeusi kama gunia la singa, mwezi wote

ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama

vile mtini upukutishavyo mapooza yake,

utikiswapo na upepo mwingi.

Ona pia: #5; #6; #7; Zaburi 50:15; Isaya 13:9,10; Isaya 34:4,5; Yoeli 2:10; Yoeli 3:15; Zekaria 13:9; Warumi 10:11-14; 1 Wakorintho

1:2.

YOELI

Page 347: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

347

E21 Masiha atasamehe dhambi.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H10 Unabii wa Ufalme wa milele wa amani.

YOELI 3:1 Kwa maana, angalieni,

siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha

mateka wa Yuda na Yerusalemu,

YOELI 3:2-16

YOELI 3:17 Hivyo ndivyo mtakavyojua

ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu,

nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu;

ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu,

wala wageni hawatapita tena ndani yake

kamwe.

18 Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima

itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka

maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji

tele; na chemchemi itatokea katika nyumba

ya Bwana, na kulinywesha bonde la Shitimu.

19 Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa

jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma

waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu

wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi

yao.

20 Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu

tangu kizazi hata kizazi.

21 Nami nitaitakasa damu yao ambayo

sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye

Sayuni.

DANIELI 12:1 Wakati huo Mikaeli

atasimama, jemadari mkuu, asimamaye

upande wa wana wa watu wako; na

kutakuwa na wakati wa taabu, mfano

wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo

taifa hata wakati uo huo; na wakati huo

watu wako wataokolewa; kila mmoja

atakayeonekana ameandikwa katika kitabu

kile.

MIKA 4:7 Nami nitamfanya yeye

aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye

aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu,

na Bwana atawamiliki katika mlima Sayuni

tangu sasa na hata milele.

ZEKARIA 13:1 Katika siku hiyo watu

wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa

Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa

dhambi na kwa unajisi.

YOHANA 4:13 Yesu akajibu, akamwambia,

Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale

nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali

yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

UFUNUO WA YOHANA 21:6

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa

na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi

nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya

maji ya uzima, bure.

UFUNUO WA YOHANA 21:27 Na ndani

yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho

kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na

uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu

cha uzima cha Mwana-Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

YOELI

Page 348: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

348

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung›aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na

upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa

uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,

wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na

majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na

kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-

Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na

watumwa wake watamtumikia;

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Kumbukumbu la Torati 30:3; 2 Mambo ya Nyakati 6:36-39; Isaya 4:3-6; Isaya 11:11-16; Isaya 19:1-15;

Isaya 33:20-22; Isaya 41:17-20; Isaya 52:1; Isaya 55:12,13; Yeremia 16:15,16; Yeremia 23:3-8; Yeremia 30:3,18; Yeremia 31:23-25;

Yeremia 49:17; Maombolezo 4:21,22; Ezekieli 35:1-15; Ezekieli 36:25-38; Ezekieli 37:21-28; Ezekieli 39:25-29; Ezekieli 43:12; Ezekieli 47:1-12; Yoeli 2:27; Amosi 9:13-15; Sefania 3:14-20;

Zekaria 8:3; Zekaria 10:10-12; Zekaria 14:8,9,18-21; Malaki 1:3,4.

YOELI

Page 349: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

349

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

AMOSI 8:9 Tena itakuwa siku hiyo,

asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue

wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza

wakati wa nuru ya mchana.

MATHAYO 27:45 Basi tangu saa sita palikuwa

na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.

Ona pia: Amosi 4:13; Amosi 5:8.

E22 Kazi ya Masiha itakuwa imebarikiwa.

AMOSI 8:11 Angalia, siku zinakuja,

asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta

njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula,

wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa

kuyasikia maneno ya Bwana.

MATHAYO 4:25 Na makutano mengi

wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli,

na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng›ambo ya

Yordani

MATHAYO 7:28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza

maneno hayo, makutano walishangaa mno

kwa mafundisho yake;

MATHAYO 8:1 Naye aliposhuka mlimani,

makutano mengi walimfuata.

MATHAYO 9:36 Na alipowaona makutano,

aliwahurumia, kwa sababu walikuwa

wamechoka na kutawanyika kama kondoo

wasio na mchungaji.

MATHAYO 12:23 Makutano wote

wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana

wa Daudi?

MATHAYO 13:34 Hayo yote Yesu aliwaambia

makutano kwa mifano; wala pasipo mfano

hakuwaambia neno;

MATHAYO 21:11 Makutano wakasema, Huyu

ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

MATHAYO 22:33 Na makutano waliposikia,

walishangaa kwa mafunzo yake.

Ona pia: Mathayo 9:33; Mathayo 12:15; Mathayo 13:2; Mathayo 14:13; Mathayo 15:30,31; Marko 10:1; Luka 4:42; Luka 5:15; Luka

9:11.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E20 Masiha ataweka agano jipya.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

AMOSI 9:11 Siku hiyo nitaiinua tena

maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba

mahali palipobomoka; nami nitayainua

magofu yake, na kuyajenga kama siku za

kale;

12 wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na

mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema

Bwana, afanyaye hayo.

13 Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana,

ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye,

na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia

apandaye mbegu; nayo milima itadondoza

divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.

14 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli

waliohamishwa, nao wataijenga miji

iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake;

nao watapanda mizabibu katika mashamba,

na kunywa divai yake; nao watafanyiza

bustani, na kula matunda yake.

AMOSI

Page 350: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

350

15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala

hawatang›olewa tena watoke katika nchi yao

niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako.

MATENDO YA MITUME 15:14 Simeoni

ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza

alivyowaangalia Mataifa ili achague watu

katika hao kwa ajili ya jina lake.

15 Na maneno ya manabii yapatana na hayo,

kama ilivyoandikwa,

16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami

nitaijenga tena nyumba ya Daudi

iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake,

Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

Ona pia: #1; #2; #3; #4; Isaya 11:14; Isaya 14:1,2; Obadia 1:8.

AMOSI

Page 351: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

351

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

OBADIA 1:17 Bali katika mlima Sayuni

watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa

mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki

milki zao.

18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na

nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto,

na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu,

nao watawaka kati yao, na kuwateketeza;

wala hatasalia mtu awaye yote katika

nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema

hayo.

19 Na watu wa Negebu wataumiliki mlima

wa Esau; na watu wa Shefela watawamiliki

Wafilisti; nao watalimiliki konde la Efraimu,

na konde la Samaria, na Benyamini atamiliki

Gileadi.

20 Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli

waliotekwa, walio kati ya Wakanaani,

watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa

Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi,

wataimiliki miji ya Negebu.

21 Tena waokozi watakwea juu ya mlima

Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na

huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana.

ZABURI 2:6 Nami nimemweka mfalme

wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu

mtakatifu.

ZABURI 102:15 Kisha mataifa wataliogopa

jina la Bwana, Na wafalme wote wa dunia

utukufu wako;

ISAYA 24:23 Ndipo mwezi utatahayari,

na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa

majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni,

na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee

wake kwa utukufu.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

WAEBRANIA 12:22 Bali ninyi

mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa

Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,

na majeshi ya malaika elfu nyingi,

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 14:1 Kisha

nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo

amesimama juu ya mlima Sayuni, na

watu mia na arobaini na nne elfu pamoja

naye, wenye jina lake na jina la Baba yake

limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

UFUNUO WA YOHANA 21:27 Na ndani

yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho

kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na

uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu

cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

OBADIA

Page 352: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

352

G01 Kufufuka kwa Masiha kunatabiriwa.

YONA 1:17 Bwana akaweka tayari

samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye

Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule

muda wa siku tatu, mchana na usiku.

YONA 2:2 Akasema, Nalimlilia Bwana

kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia;

Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe

ukasikia sauti yangu.

3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo

wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka

pande zote; Mawimbi yako yote na gharika

zako zote zimepita juu yangu.

4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na

macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili

hekalu lako takatifu.

5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;

Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga

kichwa changu;

6 Nalishuka hata pande za chini za milima;

Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata

milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu

kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,

7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,

Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu

yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

MATHAYO 12:39 Akajibu, akawaambia, Kizazi

kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala

hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku

tatu mchana na usiku katika tumbo la

nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu

atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku

katika moyo wa nchi.

41 Watu wa Ninawi watasimama siku ya

hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki,

nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa

sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona;

na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

MATHAYO 16:4 Kizazi kibaya na cha zinaa

chataka ishara; wala hakitapewa ishara,

isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha,

akaenda zake.

Ona pia: Mwanzo 22:4; 2 Wafalme 20:8; Zaburi 27:13; Zaburi 42:7; Zaburi 66:11,12; Zaburi 68:20; Zaburi 69:1,2.

YONA

Page 353: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

353

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

B16 Uweza na nguvu ya Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

MIKA 2:12 Hakika nitakukusanya, Ee

Yakobo, nyote pia; Bila shaka nitawakusanya

waliobaki wa Israeli; Nitawaweka pamoja

kama kondoo wa Bozra; Kama kundi la

kondoo kati ya malisho yao; Watafanya

mvumo kwa wingi wa watu;

13 Avunjaye amekwea juu mbele yao;

Wamebomoa mahali, wakapita mpaka

langoni, Wakatoka nje huko; Mfalme wao

naye amepita akiwatangulia, Naye Bwana

ametangulia mbele yao.

ISAYA 42:13 Bwana atatokea kama shujaa;

Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia,

naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake

mambo makuu.

ISAYA 55:4 Angalieni, nimemweka kuwa

shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi

na jemadari kwa kabila za watu.

1 WAKORINTHO 15:25 Maana sharti

amiliki yeye, hata awaweke maadui wake

wote chini ya miguu yake.

WAEBRANIA 2:9 ila twamwona yeye

aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika,

yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu

ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na

heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje

mauti kwa ajili ya kila mtu.

10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa

ajili yake na kwa njia yake vitu vyote

vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie

utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa

wokovu wao kwa njia ya mateso.

WAEBRANIA 2:14 Basi, kwa kuwa watoto

wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo

hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya

mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za

mauti, yaani, Ibilisi,

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha

yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika

hali ya utumwa.

WAEBRANIA 6:20 alimoingia Yesu kwa

ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa

kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa

Melkizedeki.

UFUNUO WA YOHANA 6:2

Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye

aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye

akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

UFUNUO WA YOHANA 7:17 Kwa

maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati

ya kiti cha enzi, atawachunga, naye

atawaongoza kwenye chemchemi za maji

yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi

yote katika macho yao.

UFUNUO WA YOHANA 17:14 Hawa

watafanya vita na Mwana-Kondoo, na

Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana

Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa

Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio

walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Yohana 10:27-30; Ufunuo wa Yohana 19:13-17.

MIKA

Page 354: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

354

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

MIKA 4:1 Lakini itakuwa katika siku za

mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya

Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa

watauendea makundi makundi.

2 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake; kwa maana katika

Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana

litatoka Yerusalemu.

3 Naye atafanya hukumu kati ya watu wa

kabila nyingi, naye atawakemea mataifa

wenye nguvu walio mbali; nao watafua

panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe

miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa

lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.

4 Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu

wake, na chini ya mtini wake; wala hapana

mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa

cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.

7 Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa

mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa

lenye nguvu, na Bwana atawamiliki katika

mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.

ISAYA 2:2 Na itakuwa katika siku

za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote

watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake maana katika Sayuni

itatoka sheria, na neno la Bwana katika

Yerusalemu.

4 Naye atafanya hukumu katika mataifa

mengi, atawakemea watu wa kabila

nyingi; nao watafua panga zao ziwe

majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa

halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala

hawatajifunza vita tena kamwe.

5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende

katika nuru ya Bwana.

LUKA 1:33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo

hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna

mwisho.

MATENDO YA MITUME 17:31 Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu

walimwengu kwa haki, kwa mtu yule

aliyemchagua; naye amewapa watu wote

uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua

katika wafu.

WARUMI 11:5 Basi ni vivi hivi wakati huu

wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa

neema.

6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa

matendo tena, au hapo neema isingekuwa

neema.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

MIKA

Page 355: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

355

Nitakapowaondolea dhambi zao.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Mathayo 25:31,32; Yohana 5:22-29; Matendo ya Mitume 4:32-35.

F13 Maelezo ya mateso ya Masiha.

MIKA 5:1 Sasa utajikusanya vikosi

vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru;

watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni

mwake kwa fimbo.

MATHAYO 26:67 Ndipo wakamtemea mate

ya uso, wakampiga makonde; wengine

wakampiga makofi,

68 wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani

aliyekupiga?

Ona pia: Isaya 33:22; Maombolezo 3:30; Mathayo 27:30; Yohana 18:22; Yohana 19:3.

A04 Masiha amekuwepo tangu milele.

C03 Mahali pa kuzaliwa kwa Masiha.

MIKA 5:2 Bali wewe, Bethlehemu

Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa

elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea

mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;

ambaye matokeo yake yamekuwa tangu

zamani za kale, tangu milele.

MATHAYO 2:4 Akakusanya wakuu wa

makuhani wote na waandishi wa watu,

akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya

Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa

na nabii,

6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,

Hu mdogo kamwe katika majumbe wa

Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala

Atakayewachunga watu wangu Israeli.

LUKA 1:31 Tazama, utachukua mimba

na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake

utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

LUKA 2:4 Yusufu naye aliondoka

Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda

kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi,

uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa

mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe,

ambaye amemposa, naye ana mimba.

6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za

kuzaa zikatimia,

7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba,

akamvika nguo za kitoto, akamlaza

katika hori ya kulia ng›ombe, kwa sababu

hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

YOHANA 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako

Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,

naye Neno alikuwa Mungu.

YOHANA 7:41 Wengine walisema, Huyu

ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo

MIKA

Page 356: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

356

atoka Galilaya?

42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo

atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka

Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?

1 PETRO 1:20 Naye amejulikana kweli

tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya

dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani

kwa ajili yenu;

21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye

kumwamini Mungu, aliyemfufua katika

wafu akampa utukufu; hata imani yenu na

tumaini lenu liwe kwa Mungu.

Ona pia: Ruthu 4:11; 1 Mambo ya Nyakati 4:4; Zaburi 102:25-27; Zaburi 132:6; Mithali 8:22-31; Isaya 9:6,7; Isaya 11:1; Isaya 53:2;

Ezekieli 17:22-24; Ezekieli 34:23,24; Ezekieli 37:22-25; Amosi 9:11; Zekaria 9:9; Luka 23:38; Yohana 1:1-3; Yohana 19:14-22;

Waebrania 13:8; Yohana 1:1; Ufunuo wa Yohana 1:11-18; Ufunuo wa Yohana 19:16; Ufunuo wa Yohana 21:6.

B12 Ukamilifu wa Masiha.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

MIKA 5:3 Kwa sababu hiyo atawatoa,

hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu;

ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia

wana wa Israeli.

4 Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa

nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana,

Mungu wake; nao watakaa; maana sasa

atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.

MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe

utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye

atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

YOHANA 10:16 Na kondoo wengine ninao,

ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa

kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha

kutakuwako kundi moja na mchungaji

mmoja.

YOHANA 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti

yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

28 Nami nawapa uzima wa milele; wala

hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu

atakayewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu

kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye

kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

Ona pia: #1; #2; #3; Mathayo 25:31; Yohana 14:9-11; 2 Wakorintho 6:16; Ufunuo wa Yohana 1:13-18; Ufunuo wa Yohana

12:1,2.

B04 Sifa za Uungu za Masiha.

E24 Masiha ataleta amani.

MIKA 5:5 Na mtu huyu atakuwa amani

yetu;

YOHANA 14:27 Amani nawaachieni; amani

yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama

ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni

mwenu, wala msiwe na woga.

WARUMI 16:20 Naye Mungu wa amani

atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe

MIKA

Page 357: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

357

pamoja nanyi. [Amina.]

WAEFESO 2:14 Kwa maana yeye ndiye

amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa

wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza

cha kati kilichotutenga.

WAKOLOSAI 1:20 na kwa yeye kuvipatanisha

vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya

amani kwa damu ya msalaba wake; kwa

yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au

vilivyo mbinguni.

WAEBRANIA 13:20 Basi, Mungu wa

amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu

Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya

agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,

Ona pia: Zaburi 72:7; Isaya 9:6,7; Luka 2:14; Yohana 14:27; Yohana 16:33; Warumi 3:17; 2 Wakorintho 13:11; Waefeso 2:14-17; Wafilipi 4:9; 1 Wathesalonike 5:23; 2 Wathesalonike 3:16;

Waebrania 7:2.

E21 Masiha atasamehe dhambi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

MIKA 7:15 Kama katika siku zile

za kutoka kwako katika nchi ya Misri

nitamwonyesha mambo ya ajabu.

16 Mataifa wataona, na kuzitahayarikia nguvu

zao zote; wataweka mikono yao juu ya

vinywa vyao, masikio yao yatakuwa na uziwi.

17 Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama

vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka

katika mahali walimojificha, wakitetemeka;

watakuja kwa Bwana, Mungu wetu, kwa

hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.

18 Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye

kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu

wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira

yake milele, kwa maana yeye hufurahia

rehema.

19 Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga

maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao

zote katika vilindi vya bahari.

20 Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na

Ibrahimu rehema zako, ulizowaapia baba

zetu tangu siku za kale.

2 MAMBO YA NYAKATI 7:14 ikiwa

watu wangu, walioitwa kwa jina langu,

watajinyenyekesha, na kuomba, na

kunitafuta uso, na kuziacha njia zao

mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na

kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi

yao.

ISAYA 55:7 Mtu mbaya na aache njia

yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake;

Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na

arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe

kabisa.

MAOMBOLEZO 3:32 Maana

ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri

ya wingi wa huruma zake.

HOSEA 3:5 baada ya hayo wana wa

Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana,

Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao

watamwendea Bwana na wema wake kwa

kicho siku za mwisho.

ZEKARIA 10:6 Nami nitaitia nguvu nyumba

ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu,

nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea

rehema; nao watakuwa kana kwamba

sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana,

Mungu wao, nami nitawasikia.

MIKA

Page 358: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

358

MATHAYO 18:21 Kisha Petro akamwendea

akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose

mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara

saba?

22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara

saba, bali hata saba mara sabini.

LUKA 7:49 Ndipo wale walioketi

chakulani pamoja naye walianza kusema

mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe

dhambi?

WAEBRANIA 10:16 Hili ni agano

nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena

Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,

Na katika nia zao nitaziandika; ndipo

anenapo,

17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena

kabisa.

1 PETRO 2:10 ninyi mliokuwa kwanza si

taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa

hamkupata rehema, bali sasa mmepata

rehema.

Ona pia: #1; #2; #3; #5; Zaburi 103:3.

MIKA

Page 359: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

359

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

HABAKUKI 2:3 Maana njozi hii bado ni

kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili

kuufikilia mwisho wake, wala haitasema

uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina

budi kuja, haitakawia.

ZABURI 130:5 Nimemngoja Bwana,

roho yangu imengoja, Na neno lake

nimelitumainia.

6 Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko

walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi

waingojao asubuhi.

ISAYA 8:17 Nami nitamngojea Bwana,

awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo,

nami nitamtazamia.

ISAYA 46:13 Mimi ninaleta karibu haki

yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu

hautakawia; nami nitaweka wokovu katika

Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.

LUKA 18:7 Na Mungu, je! Hatawapatia

haki wateule wake wanaomlilia mchana na

usiku, naye ni mvumilivu kwao?

8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini,

atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona

imani duniani?

WAEBRANIA 10:37 Kwa kuwa bado

kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja,

wala hatakawia.

2 PETRO 3:9 Bwana hakawii kuitimiza

ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani

kukawia, bali huvumilia kwenu, maana

hapendi mtu ye yote apotee, bali wote

wafikilie toba.

Ona pia: Zaburi 27:14; Isaya 30:18; Maombolezo 3:25,26; Mika 7:7; Luka 2:25; 2 Wathesalonike 2:6-8; Yakobo 5:7,8.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

HABAKUKI 2:4 Tazama, roho yake hujivuna,

haina unyofu ndani yake; lakini mwenye

haki ataishi kwa imani yake.

WARUMI 1:17 Kwa maana haki ya Mungu

inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata

imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki

ataishi kwa imani.

WAGALATIA 2:16 hali tukijua ya kuwa

mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo

ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi

tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki

kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo

ya sheria; maana kwa matendo ya sheria

hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa

haki.

WAGALATIA 3:11 Ni dhahiri ya kwamba

hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za

Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye

haki ataishi kwa imani.

12 Na torati haikuja kwa imani, bali,

Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.

WAEBRANIA 10:38 Lakini mwenye

haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-

sita, roho yangu haina furaha naye.

Ona pia: Isaya 53:11; Yeremia 23:5; Mathayo 27:19; Matendo ya Mitume 3:14; Matendo ya Mitume 22:14; Yohana 2:1; Yohana

5:10-12.

HABAKUKI

Page 360: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

360

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

HABAKUKI 2:14 Kwa maana dunia itajazwa

maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji

yaifunikavyo bahari.

ISAYA 11:9 Hawatadhuru wala

hawataharibu katika mlima wangu wote

mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua

Bwana, kama vile maji yanavyoifunika

bahari.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; Zaburi 67:1-7; Zaburi 72:19; Zaburi 86:9; Zaburi 98:1-8; Isaya 6:3.

HABAKUKI

Page 361: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

361

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

SEFANIA 3:9 Maana hapo ndipo

nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi,

wapate kuliitia jina la Bwana, wamtumikie

kwa nia moja.

SEFANIA 3:10-11

SEFANIA 3:12 Lakini nitasaza ndani

yako watu walioonewa na maskini, nao

watalitumainia jina la Bwana.

13 Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala

kusema uongo; wala ulimi wa hadaa

hautaonekana kinywani mwao; kwa maana

watakula na kulala, wala hapana mtu

atakayewaogofya.

14 Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli;

Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,

Ee binti Yerusalemu.

15 Bwana ameziondoa hukumu zako,

Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa

Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako;

Hutaogopa uovu tena.

16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,

Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.

17 Bwana, Mungu wako, yu katikati yako

shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa

furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake,

Atakufurahia kwa kuimba.

SEFANIA 3:18-19

SEFANIA 3:20 Wakati huo nitawaingizeni,

na wakati huo nitawakusanya; kwa

maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na

jina, miongoni mwa watu wote wa dunia,

nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele

ya macho yenu, asema Bwana.

EZEKIELI 37:24 Na mtumishi wangu,

Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote

watakuwa na mchungaji mmoja; nao

wataenenda katika hukumu zangu, na

kuzishika amri zangu, na kuzitenda.

25 Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo,

mtumishi wangu, walimokaa baba zenu;

nao watakaa humo, wao na watoto wao, na

watoto wa watoto wao, milele; na Daudi,

mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao

milele.

MATHAYO 21:9 Na makutano waliotangulia,

na wale waliofuata, wakapaza sauti,

wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye

mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana;

Hosana juu mbinguni.

MATHAYO 26:61 Hata baadaye wawili

wakatokea, wakasema, Huyu alisema,

Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na

kulijenga kwa siku tatu.

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama

akamwambia, Hujibu neno? Hawa

wanakushuhudia nini?

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu

akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye

hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo,

Mwana wa Mungu.

MATHAYO 27:12 Lakini aliposhitakiwa na

wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu

hata neno.

13 Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni

mambo mangapi wanayokushuhudia?

14 Asimjibu hata neno moja, hata liwali

akastaajabu sana.

LUKA 4:18 Roho wa Bwana yu juu

yangu, Kwa maana amenitia mafuta

SEFANIA

Page 362: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

362

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona

tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana

uliokubaliwa.

LUKA 24:47 na kwamba mataifa yote

watahubiriwa kwa jina lake habari ya

toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu

Yerusalemu.

YOHANA 13:1 Basi, kabla ya sikukuu ya

Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake

imefika, atakayotoka katika ulimwengu

kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda

watu wake katika ulimwengu, aliwapenda

upeo.

YOHANA 15:11 Hayo nimewaambia, ili

furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha

yenu itimizwe.

12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama

nilivyowapenda ninyi.

13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu,

wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki

zake.

WARUMI 8:37 Lakini katika mambo hayo

yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa

yeye aliyetupenda.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 19:1 Baada ya

hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano

mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema,

Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina

BWANA MUNGU wetu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Isaya 62:1-7; Isaya 65:19; Yeremia 32:41; Mathayo 28:18,19; Matendo ya Mitume 6:7; Matendo ya

Mitume 9:15; Ufunuo wa Yohana 19:7.

SEFANIA

Page 363: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

363

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

HAGAI 2:6 Kwa maana Bwana wa

majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni

kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo

mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi

kavu;

7 nami nitatikisa mataifa yote, na vitu

vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja;

nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema

Bwana wa majeshi.

8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali

yangu, asema Bwana wa majeshi.

9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii

utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa

kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika

mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana

wa majeshi.

MWANZO 49:10 Fimbo ya enzi haitaondoka

katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya

miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye

milki, Ambaye mataifa watamtii.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

WARUMI 14:17 Maana ufalme wa Mungu si

kula wala kunywa, bali ni haki na amani na

furaha katika Roho Mtakatifu.

2 WAKORINTHO 3:9 Kwa maana ikiwa

huduma ya adhabu ina utukufu, siuze

huduma ya haki ina utukufu unaozidi.

10 Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na

utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio

sana.

UFUNUO WA YOHANA 21:2 Nami

nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu

mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa

Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi

aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile

kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani

ya Mungu ni pamoja na wanadamu,

naye atafanya maskani yake pamoja nao,

nao watakuwa watu wake. Naye Mungu

mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Luka 21:10,11.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

HAGAI 2:23 Katika siku ile, asema

Bwana wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee

Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa

Shealtieli, asema Bwana, nami nitakufanya

kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa

nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi.

LUKA 3:23 Na Yesu mwenyewe,

alipoanza kufundisha, alikuwa amepata

umri wake kama miaka thelathini,

akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa

Eli,

24 wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa

Yusufu,

25 wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa

Esli, wa Nagai,

26 wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa

Yusufu, wa Yuda,

27 wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa

Shealtieli, wa Neri,

HAGAI

Page 364: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

364

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

E19 Masiha atafariji.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

.

ZEKARIA 1:16 Kwa sababu hiyo Bwana

asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa

rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa

ndani yake, asema Bwana wa majeshi, na

kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.

17 Piga kelele tena, na kusema, Bwana wa

majeshi asema hivi, Miji yangu kwa

kufanikiwa itaenezwa huko na huko

tena; naye Bwana ataufariji Sayuni tena,

atauchagua Yerusalemu tena.

ISAYA 40:1 Watulizeni mioyo, watulizeni

mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.

2 Semeni na moyo wa Yerusalemu,

kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita

vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa;

kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana

adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.

ISAYA 40:9 Wewe uuhubiriye Sayuni

habari njema, Panda juu ya mlima mrefu;

Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema,

Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako,

usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni,

Mungu wenu.

ISAYA 66:13 Mfano wa mtu

ambaye mama yake amfariji, ndivyo

nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa

katika Yerusalemu.

MATHAYO 9:35 Naye Yesu alikuwa

akizunguka katika miji yote na vijiji,

akifundisha katika masinagogi yao, na

kuihubiri habari njema ya ufalme, na

kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila

aina.

LUKA 4:43 Akawaambia, Imenipasa

kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu

katika miji mingine pia; maana kwa sababu

hiyo nalitumwa.

MATENDO YA MITUME 1:8 Lakini

mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu

Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi

wangu katika Yerusalemu, na katika

Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho

wa nchi.

MATENDO YA MITUME 5:16 Nayo

makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando

ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta

wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu;

nao wote wakaponywa.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

E18 Mungu ataishi miongoni mwa watu Wake.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 2:1-2

ZEKARIA 2:3 Na tazama, yule malaika

aliyesema nami akasimama karibu, na

malaika mwingine akatoka ili kuonana naye;

4 naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie

kijana huyu, na kusema, Yerusalemu

utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na

kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na

mifugo iliyomo ndani yake.

5 Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa

ukuta wa moto kuuzunguka pande zote,

ZEKARIA

Page 365: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

365

nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.

ZEKARIA 2:6-9

ZEKARIA 2:10 Imba, ufurahi, Ee binti

Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami

nitakaa kati yako, asema Bwana.

11 Na mataifa mengi watajiunga na Bwana

katika siku ile, nao watakuwa watu wangu;

nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa

Bwana wa majeshi amenituma kwako.

12 Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu

yake katika nchi takatifu, naye atachagua

Yerusalemu tena.

13 Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele

za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka

katika maskani yake takatifu.

ZABURI 40:7 Ndipo niliposema,

Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo

nimeandikiwa,)

LUKA 2:32 Nuru ya kuwa mwangaza

wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako

Israeli.

YOHANA 8:14 Yesu akajibu, akawaambia,

Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe,

ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu

najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi

hamjui nilikotoka wala niendako.

YOHANA 8:42 Yesu akawaambia, Kama

Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda

mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu,

nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu,

bali yeye ndiye aliyenituma.

YOHANA 14:28 Mlisikia ya kwamba mimi

naliwaambia, Naenda zangu, tena naja

kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi

kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana

Baba ni mkuu kuliko mimi.

MATENDO YA MITUME 9:15 Lakini

Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana

huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue

Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na

wana wa Israeli.

WARUMI 3:29 Au je! Mungu ni Mungu wa

Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia?

Naam, ni Mungu wa Mataifa pia;

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

WARUMI 15:8 Kwa maana nasema, ya

kwamba Kristo amefanyika mhudumu

wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli

ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi

walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili

ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa

hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami

nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na

watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana;

Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la

Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

WAEBRANIA 9:27 Na kama vile watu

wanavyowekewa kufa mara moja, na baada

ya kufa hukumu;

28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa

sadaka mara moja azichukue dhambi za

ZEKARIA

Page 366: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

366

watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo

dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa

wokovu.

WAEBRANIA 10:7 Ndipo niliposema,

Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo

nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako,

Mungu.

UFUNUO WA YOHANA 3:11 Naja

upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu

akaitwaa taji yako.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 16:15 (Tazama,

naja kama mwivi. Heri akeshaye, na

kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata

watu wakaione aibu yake.)

UFUNUO WA YOHANA 22:7 Na

tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye

maneno ya unabii wa kitabu hiki.

UFUNUO WA YOHANA 22:12 Tazama,

naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami,

kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

UFUNUO WA YOHANA 22:17 Na Roho

na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye

na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na

yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

UFUNUO WA YOHANA 22:20 Yeye

mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam;

naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Yohana 17:13; Matendo ya Mitume 10:45; Matendo ya Mitume 11:1,18; Waebrania 10:9; 1 Petro 5:4.

C01 Kuzaliwa kwa Masiha kunatabiriwa.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

D10 Masiha atakuwa Hakimu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 3:1 Kisha akanionyesha Yoshua,

kuhani mkuu, amesimama mbele ya

malaika wa Bwana, na Shetani amesimama

mkono wake wa kuume ili kushindana naye.

2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na

akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana,

aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je!

Hiki si kinga kilichotolewa motoni?

3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu

sana, naye alikuwa akisimama mbele ya

malaika.

4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale

waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni

nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia

yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako,

nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.

5 Nikasema, Na wampige kilemba kizuri

kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba

kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi;

naye malaika wa Bwana akasimama karibu.

ZEKARIA 3:6-7

ZEKARIA 3:8 Sikiliza sasa, Ee Yoshua,

kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio

mbele yako; maana hao ni watu walio ishara;

kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi

wangu, aitwaye Chipukizi.

9 Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele

ya Yoshua; katika jiwe moja yako macho

ZEKARIA

Page 367: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

367

saba; tazama, nitachora machoro yake,

asema Bwana wa majeshi, nami nitauondoa

uovu wa nchi ile katika siku moja.

10 Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi,

ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini

ya mzabibu, na chini ya mtini.

MATHAYO 22:11 Lakini alipoingia yule

mfalme ili kuwatazama wageni wake,

akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la

arusi.

12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe

huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

LUKA 1:32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa

Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu

atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

WARUMI 16:20 Naye Mungu wa amani

atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe

pamoja nanyi. [Amina.]

WAEFESO 6:11 Vaeni silaha zote za Mungu,

mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu

ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na

mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya

majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu

wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za

Mungu, mpate kuweza kushindana siku

ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote,

kusimama.

1 YOHANA 3:8 atendaye dhambi ni wa

Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi

tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa

Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za

Ibilisi.

UFUNUO WA YOHANA 4:4 Na viti

ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha

enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini

na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi

meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na

taji za dhahabu.

UFUNUO WA YOHANA 4:10 ndipo hao

wazee ishirini na wanne huanguka mbele

zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi,

nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na

milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile

kiti cha enzi, wakisema,

11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu

wetu, kuupokea utukufu na heshima na

uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba

vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako

vilikuwako, navyo vikaumbwa.

UFUNUO WA YOHANA 7:9 Baada

ya hayo nikaona, na tazama, mkutano

mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye

kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na

jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile

kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,

wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya

mitende mikononi mwao;

10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu

una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi,

na Mwana-Kondoo.

11 Na malaika wote walikuwa wakisimama

pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao

wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao

wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha

enzi, wakamsujudu Mungu,

12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na

hekima na shukrani na heshima na uweza

ZEKARIA

Page 368: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

368

na nguvu zina Mungu wetu hata milele na

milele. Amina.

13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia,

Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni

akina nani? Na wametoka wapi?

14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.

Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika

dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,

na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-

Kondoo.

UFUNUO WA YOHANA 19:8 Naye

amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing›arayo,

safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni

matendo ya haki ya watakatifu.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Isaya 6:2,3; Isaya 64:6; Zekaria 6:11-13.

D03 Kazi ya Masiha kama Kuhani.

E17 Masiha atajenga hekalu la Mungu.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZEKARIA 6:12 ukamwambie, ukisema,

Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba,

Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake

ni Chipukizi; naye atakua katika mahali

pake, naye atalijenga hekalu la Bwana.

13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana;

naye atauchukua huo utukufu; ataketi

akimiliki katika kiti chake cha enzi; na

kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha

enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya

hao wawili.

15 Nao walio mbali watakuja na kujenga katika

hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa

Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Na

haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti

ya Bwana, Mungu wenu.

MATHAYO 12:6 Lakini nawaambieni,

kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko

hekalu.

MATHAYO 26:61 Hata baadaye wawili

wakatokea, wakasema, Huyu alisema,

Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na

kulijenga kwa siku tatu.

LUKA 1:31 Tazama, utachukua mimba

na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake

utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa

Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha

enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na

ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

YOHANA 2:19 Yesu akajibu, akawaambia,

Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu

nitalisimamisha.

20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili

lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na

sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili

wake.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue

wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu

Kristo uliyemtuma.

ZEKARIA

Page 369: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

369

MATENDO YA MITUME 2:39 Kwa kuwa

ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto

wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa

wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu

wamjie.

MATENDO YA MITUME 15:14 Simeoni

ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza

alivyowaangalia Mataifa ili achague watu

katika hao kwa ajili ya jina lake.

15 Na maneno ya manabii yapatana na hayo,

kama ilivyoandikwa,

16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami

nitaijenga tena nyumba ya Daudi

iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake,

Nami nitaisimamisha;

17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,

Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa

kwao;

2 WAKORINTHO 6:16 Tena pana

mapatano gani kati ya hekalu la Mungu

na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la

Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema,

ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao

nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao

watakuwa watu wangu.

WAEFESO 2:19 Basi tangu sasa ninyi si

wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji

pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani

mwake Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na

manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni

jiwe kuu la pembeni.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa

vema na kukua hata liwe hekalu takatifu

katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja

kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

WAEBRANIA 3:3 Kwa maana huyo

amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi

kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye

nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo

nyumba.

4 Maana kila nyumba imetengenezwa na

mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni

Mungu.

5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika

nyumba yote ya Mungu kama mtumishi,

awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa

baadaye;

6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba

ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi,

kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na

fahari ya taraja letu mpaka mwisho.

WAEBRANIA 7:24 bali yeye, kwa kuwa akaa

milele, anao ukuhani wake usioondoka.

WAEBRANIA 10:12 Lakini huyu,

alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi

dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi

mkono wa kuume wa Mungu;

1 PETRO 3:22 Naye yupo mkono wa kuume

wa Mungu, amekwenda zake mbinguni,

malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa

chini yake.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

UFUNUO WA YOHANA 21:22 Nami

sikuona hekalu ndani yake; kwa maana

ZEKARIA

Page 370: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

370

Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-

Kondoo, ndio hekalu lake.

Ona pia: #1; #3; Isaya 9:7; Zekaria 4:1-6; Matendo ya Mitume 2:1-4,16-18,37-42; 17:31; 19:4-6; Waefeso 1:20-23; Wafilipi 2:7-11;

Waebrania 2:7-9.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 8:1-2

ZEKARIA 8:3 Bwana asema hivi, Mimi

nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya

Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji

wa kweli; na Mlima wa Bwana wa majeshi

utaitwa, Mlima mtakatifu.

4 Bwana wa majeshi asema hivi, Wazee

wanaume na wazee wanawake watakaa

tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu

ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni

mzee sana.

5 Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na

wasichana, wakicheza katika njia zake.

6 Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili

ni neno lililo gumu mbele ya macho ya

mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je!

Liwe neno gumu mbele ya macho yangu?

Asema Bwana wa majeshi.

7 Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama,

nitawaokoa watu wangu toka nchi ya

mashariki, na toka nchi ya magharibi;

8 nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya

Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu,

nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na

katika haki.

ZEKARIA 8:9-11

ZEKARIA 8:12 Kwa maana itakuwako

mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda

yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na

hizo mbingu zitatoa umande wake; nami

nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu

hivi vyote.

13 Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana

katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na

nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa,

nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini

mikono yenu na iwe hodari.

ZEKARIA 8:14-19

ZEKARIA 8:20 Bwana wa majeshi asema

hivi, Itatokea halafu ya kwamba watakuja

mataifa na wenyeji wa miji mingi;

21 wenyeji wa mji huu watauendea mji huu,

wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka

tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta

Bwana wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.

22 Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa

hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta

Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za

Bwana.

23 Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo

watu kumi, wa lugha zote za mataifa,

wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye

Myahudi; naam, wataushika wakisema,

Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana

tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.

LUKA 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao

wapate kuelewa na maandiko.

46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba

Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa

kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la

dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

WARUMI 11:25 Kwa maana, ndugu zangu,

sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa

wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu

umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa

Mataifa uwasili.

ZEKARIA

Page 371: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

371

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama

ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka

Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao,

Nitakapowaondolea dhambi zao.

28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui

kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule

kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili

ya baba zetu.

29 Kwa sababu karama za Mungu hazina

majuto, wala mwito wake.

30 Kwa maana kama ninyi zamani

mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata

rehema kwa kuasi kwao;

31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa

kupata rehema kwenu wao nao wapate

rehema.

32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja

katika kuasi ili awarehemu wote.

WARUMI 15:8 Kwa maana nasema, ya

kwamba Kristo amefanyika mhudumu

wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli

ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi

walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili

ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa

hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami

nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na

watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana;

Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la

Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

WARUMI 16:25 Sasa na atukuzwe yeye

awezaye kuwafanya imara, sawasawa na

injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu

Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri

iliyositirika tangu zamani za milele,

26 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya

manabii, ikajulikana na mataifa yote kama

alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii

Imani.

2 WAKORINTHO 6:16 Tena pana

mapatano gani kati ya hekalu la Mungu

na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la

Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema,

ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao

nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao

watakuwa watu wangu.

WAGALATIA 3:8 Na andiko, kwa vile

lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu

atawahesabia haki Mataifa kwa imani,

lilimhubiri Ibrahimu habari njema

zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote

watabarikiwa.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

UFUNUO WA YOHANA 21:3 Nikasikia

sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha

enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu

ZEKARIA

Page 372: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

372

ni pamoja na wanadamu, naye atafanya

maskani yake pamoja nao, nao watakuwa

watu wake. Naye Mungu mwenyewe

atakuwa pamoja nao.

UFUNUO WA YOHANA 21:24 Na

mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Luka 8:43,44; Yohana 12:20,21; Ufunuo wa Yohana 7:9.

D04 Kazi ya Masiha kama Mfalme.

F02 Kuingia kwa Masiha Yerusalemu

kunatabiriwa.

ZEKARIA 9:9 Furahi sana, Ee binti Sayuni;

Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama,

mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye

haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu,

amepanda punda, Naam, mwana-punda,

mtoto wa punda.

MWANZO 49:10 Fimbo ya enzi haitaondoka

katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya

miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye

milki, Ambaye mataifa watamtii.

11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na

mwana-punda wake katika mzabibu mzuri.

Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi

yake kwa damu ya zabibu.

ISAYA 62:11 Tazama, Bwana ametangaza

habari mpaka mwisho wa dunia,

Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu

wako unakuja; Tazama, thawabu yake i

pamoja naye, Na malipo yake yako mbele

zake.

MATHAYO 21:4 Haya yote yamekuwa, ili

litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,

5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme

wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda

punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.

YOHANA 12:12 Nayo siku ya pili yake watu

wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba

Yesu anakuja Yerusalemu;

13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka

nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele,

Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la

Bwana, Mfalme wa Israeli!

14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda,

akampanda, kama vile iliyoandikwa,

15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme

wako anakuja, amepanda mwana-punda.

16 Mambo hayo wanafunzi wake

hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu

alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya

kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba

walimtendea hayo.

Ona pia: Isaya 12:6; Isaya 40:9; Isaya 52:9,10; Sefania 3:14,15; Zekaria 2:10; Marko 11:7-10; Luka 19:29-38.

B13 Mamlaka ya Masiha.

E24 Masiha ataleta amani.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 9:10 Na gari la vita nitaliondoa

liwe mbali na Efraimu, na farasi awe

mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita

utaondolewa mbali; naye atawahubiri

mataifa yote habari za amani; na mamlaka

yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na

toka Mto hata miisho ya dunia.

ZEKARIA 9:11-12

ZEKARIA

Page 373: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

373

ZABURI 72:7 Siku zake yeye, mtu mwenye

haki atasitawi, Na wingi wa amani hata

mwezi utakapokoma.

ISAYA 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;

Na uweza wa kifalme utakuwa begani

mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa

milele, Mfalme wa amani.

7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa

na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha

Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na

kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki,

Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana

wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

MATHAYO 8:27 Wale watu wakamaka

wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata

pepo na bahari zamtii?

MATHAYO 9:6 Lakini mpate kujua ya

kwamba Mwana wa Adamu anayo amri

duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia

yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike

kitanda chako, uende nyumbani kwako.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

MARKO 1:27 Wakashangaa wote, hata

wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu

mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata

pepo wachafu, nao wamtii!

LUKA 2:14 Atukuzwe Mungu juu

mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu

aliowaridhia.

LUKA 4:32 wakashangaa mno kwa

mafundisho yake, kwa kuwa neno lake

lilikuwa na uwezo.

YOHANA 5:22 Tena Baba hamhukumu mtu

ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;

YOHANA 5:27 Naye akampa amri ya

kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa

Adamu.

YOHANA 10:17 Ndiposa Baba anipenda, kwa

sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.

18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa

mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa,

ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo

nalilipokea kwa Baba yangu.

YOHANA 14:27 Amani nawaachieni; amani

yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama

ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni

mwenu, wala msiwe na woga.

YOHANA 16:33 Hayo nimewaambieni mpate

kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni

mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi

nimeushinda ulimwengu.

YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema

Yesu; akainua macho yake kuelekea

mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha

kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako

naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote

wenye mwili, ili kwamba wote uliompa

awape uzima wa milele.

MATENDO YA MITUME 9:31 Basi

kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na

Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea

ZEKARIA

Page 374: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

374

na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na

faraja ya Roho Mtakatifu.

MATENDO YA MITUME 10:36 Neno lile

alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri

habari njema ya amani kwa Yesu Kristo

(ndiye Bwana wa wote),

WARUMI 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa

haki itokayo katika imani, na mwe na amani

kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu

Kristo,

WAEFESO 2:17 Akaja akahubiri amani

kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani

kwao wale waliokuwa karibu.

2 WATHESALONIKE 3:16 Sasa, Bwana wa

amani mwenyewe na awape amani daima

kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi

nyote.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; 1 Samweli 2:10; Zaburi 2:8; Zaburi 22:27; Zaburi 37:11; Zaburi 67:7; Zaburi 72:8; Zaburi 85:8-10; Zaburi 98:3; Zaburi 122:6-8; Zaburi 147:14; Isaya 26:12; Isaya

45:22; Isaya 48:18; Isaya 52:7; Isaya 53:5; Isaya 55:12; Isaya 57:19; Isaya 62:11; Isaya 66:12; Yeremia 8:11; Yeremia 16:19-21; Yeremia 28:9; Yeremia 33:9; Hosea 1:7; Hosea 2:19; Mika 5:4,10,11; Hagai

2:32; Danieli 4:17; Danieli 7:13,14,27; Marko 1:27; Luka 4:32; Luka 10:19; Luka 11:31; Luka 12:15; Yohana 10:17,18; Yohana

20:19,21,26; Warumi 10:15,17,18; Warumi 14:17; 1 Wakorintho 15:24; 2 Wakorintho 10:4,5; Waefeso 2:14,15; Wakolosai 1:20;

Wakolosai 3:15; 2 Petro 3:14.

D05 Masiha atakuwa Mkombozi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 10:3-5

ZEKARIA 10:6 Nami nitaitia nguvu nyumba

ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu,

nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea

rehema; nao watakuwa kana kwamba

sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana,

Mungu wao, nami nitawasikia.

7 Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa,

na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa

divai; naam, watoto wao wataona mambo

haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia

Bwana.

8 Nitawapigia kelele, na kuwakusanya

pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao

wataongezeka kama walivyoongezeka.

9 Nami nitawapanda kama mbegu kati ya

mataifa; nao watanikumbuka katika nchi

zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto

wao; tena watarudi.

10 Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri,

nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru;

nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi

na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha

haitaonekana.

11 Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na

kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi

vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi

cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi

ya Misri itatoweka.

12 Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao

watatembea huko na huko katika jina lake,

asema Bwana.

MATHAYO 24:14 Tena habari njema ya ufalme

itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa

ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule

mwisho utakapokuja.

MATHAYO 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye

mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho

Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote

niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo

pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa

ZEKARIA

Page 375: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

375

dahari.

LUKA 21:24 Wataanguka kwa ukali

wa upanga, nao watatekwa nyara na

kuchukuliwa katika mataifa yote; na

Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata

majira ya Mataifa yatakapotimia.

WARUMI 11:11 Basi nasema, Je!

Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha!

Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia

Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.

12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa

ulimwengu, na upungufu wao umekuwa

utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu

wao?

13 Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa

Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa

watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo

yangu,

14 nipate kuwatia wivu walio damu moja na

mimi na kuwaokoa baadhi yao.

15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta

upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa

kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya

kufa?

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Matendo ya Mitume 2:5-11; 1 Petro 1:1,2; Ufunuo wa Yohana 8:7-11.

F04 Matokeo ya kukataliwa kwa Masiha.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ZEKARIA 11:4 Bwana, Mungu wangu,

alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,

5 ambalo wenye kundi hilo huwachinja,

kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao

wawauzao husema, Na ahimidiwe Bwana,

kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji

wao wenyewe hawawahurumii.

6 Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji

wa nchi hii, asema Bwana; bali, tazama,

nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa

mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao

wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa

mikononi mwao.

EZEKIELI 34:23 Nami nitaweka mchungaji

mmoja juu yao, naye atawalisha, naam,

mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha,

naye atakuwa mchungaji wao.

MIKA 5:4 Naye atasimama, na kulisha

kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi

ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa;

maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya

dunia.

MATHAYO 15:24 Akajibu, akasema,

Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa

nyumba ya Israeli.

MATHAYO 23:1 Kisha Yesu akawaambia

makutano na wanafunzi wake, akasema,

2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika

kiti cha Musa;

3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na

kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo

yao, msitende; maana wao hunena lakini

hawatendi.

4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika

watu mabegani mwao; wasitake wenyewe

kuigusa kwa kidole chao.

LUKA 19:41 Alipofika karibu aliuona mji,

akaulilia,

42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika

siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa

yamefichwa machoni pako.

ZEKARIA

Page 376: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

376

43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako

watakapokujengea boma, likuzunguke;

watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

44 watakuangusha chini wewe na watoto wako

ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe,

kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa

kwako.

YOHANA 19:13 Basi Pilato, aliposikia

maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu

ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu

ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.

14 Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata

saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama,

Mfalme wenu!

15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe!

Mwondoshe! Msulibishe! Pilato

akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme

wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi

hatuna mfalme ila Kaisari.

YOHANA 21:15 Basi walipokwisha kula,

Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni

wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?

Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua

kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha

wana-kondoo wangu.

16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa

Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo,

Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.

Akamwambia, Chunga kondoo zangu.

17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa

Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika

kwa vile alivyomwambia mara ya tatu,

Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe

wajua yote; wewe umetambua ya kuwa

nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha

kondoo zangu.

Ona pia: Isaya 40:9-11; Mathayo 23:14,37; Mathayo 24:10; Luka 12:52,53; Luka 21:16,17; Yohana 12:13; Waebrania 2:3; Waebrania

10:26,27.

B06 Masiha ndiye Mchungaji mwema.

B15 Masiha atajawa na rehema.

ZEKARIA 11:7 Basi nikalilisha kundi

la machinjo, kweli kondoo waliokuwa

wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo

mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na

ya pili nikaiita, Vifungo; nikalilisha kundi

lile

MATHAYO 9:35 Naye Yesu alikuwa

akizunguka katika miji yote na vijiji,

akifundisha katika masinagogi yao, na

kuihubiri habari njema ya ufalme, na

kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila

aina.

36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia,

kwa sababu walikuwa wamechoka na

kutawanyika kama kondoo wasio na

mchungaji.

MATHAYO 11:5 vipofu wanapata kuona,

viwete wanakwenda, wenye ukoma

wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu

wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa

habari njema.

YOHANA 10:16 Na kondoo wengine ninao,

ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa

kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha

kutakuwako kundi moja na mchungaji

mmoja.

YOHANA 17:21 Wote wawe na umoja; kama

wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami

ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili

ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe

ZEKARIA

Page 377: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

377

ndiwe uliyenituma.

22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao;

ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe

wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu

ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma,

ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

Ona pia: Isaya 61:1; Yeremia 5:4; Ezekieli 37:16-23; Sefania 3:12; Zekaria 11:4,10,11,14.

F03 Masiha atakataliwa.

F11 Mateso ya Masiha.

ZEKARIA 11:8 Nami nikawakatilia mbali

wachungaji watatu katika mwezi mmoja;

maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa

ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.

MATHAYO 23:34 Kwa sababu hiyo, angalieni,

mimi natuma kwenu manabii na wenye

hekima na waandishi; na wengine wao ninyi

mtawaua na kuwasulibisha, na wengine

wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na

kuwafukuza mji kwa mji;

35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki

iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya

Habili, yule mwenye haki, hata damu ya

Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya

patakatifu na madhabahu.

36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote

yatakuja juu ya kizazi hiki.

MATHAYO 27:20 Nao wakuu wa makuhani

na wazee wakawashawishi makutano ili

wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.

LUKA 12:50 Lakini nina ubatizo unipasao

kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata

utimizwe!

LUKA 19:14 Lakini watu wa mji wake

walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata

na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

YOHANA 7:7 Ulimwengu hauwezi

kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi,

kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi

zake ni mbovu.

YOHANA 15:18 Iwapo ulimwengu

ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia

mimi kabla ya kuwachukia ninyi.

YOHANA 15:23 Yeye anichukiaye mimi

humchukia na Baba yangu.

24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda

mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi;

lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu,

na kutuchukia.

25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika

torati yao, Walinichukia bure.

Ona pia: Zaburi 106:40; Isaya 49:7; Yeremia 12:8; Hosea 9:15.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

ZEKARIA 11:9 Ndipo nikasema,

Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa

mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia,

kila mmoja na ale nyama ya mwili wa

mwenziwe.

YEREMIA 23:33 Na watu hawa, au nabii au

kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa

Bwana ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo

gani? Bwana asema, Nitawatupilia mbali.

ZEKARIA

Page 378: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

378

YEREMIA 23:39 basi, kwa hiyo angalieni,

nitawasahau ninyi kabisa, nami

nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu

niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele

za uso wangu;

MATHAYO 15:14 Waacheni; hao ni viongozi

vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza

kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni

wote wawili.

MATHAYO 21:19 Akaona mtini mmoja kando

ya njia, akauendea, asione kitu juu yake

ila majani tu; akauambia, Yasipatikane

matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini

ukanyauka mara.

MATHAYO 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia,

Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao

watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda

yake.

MATHAYO 23:38 Angalieni, nyumba yenu

mmeachiwa hali ya ukiwa.

39 Kwa maana nawaambia, Hamtaniona

kamwe tangu sasa, hata mtakaposema,

Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.

YOHANA 8:21 Basi akawaambia tena, Mimi

naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa

katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi

hamwezi kuja.

YOHANA 8:24 Kwa hiyo naliwaambieni ya

kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa

sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye,

mtakufa katika dhambi zenu.

MATENDO YA MITUME 13:46

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa

wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu

linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa

mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi

zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele,

angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,

Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate

kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

MATENDO YA MITUME 28:26 akisema,

Enenda kwa watu hawa, ukawaambie,

Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na

kuona, mtaona wala hamtatambua;

27 Kwa maana mioyo ya watu hawa

imepumbaa, Na masikio yao ni mazito

ya kusikia, Na macho yao wameyafumba;

Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia

kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo

yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.

28 Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu

huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa,

nao watasikia!

UFUNUO WA YOHANA 22:11 Mwenye

kudhulumu na azidi kudhulumu; na

mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu;

na mwenye haki na azidi kufanya haki; na

mtakatifu na azidi kutakaswa.

Ona pia: Isaya 9:20,21; Yeremia 19:9; Ezekieli 5:10.

E25 asiha ataaminiwa na kusifiwa.

F04 Matokeo ya kukataliwa kwa Masiha.

ZEKARIA 11:10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu,

iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili

nipate kulivunja agano langu nililolifanya na

watu wa kabila zote.

11 Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale

ZEKARIA

Page 379: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

379

kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya

kuwa neno hili ndilo neno la Bwana.

LUKA 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu

palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni

mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia

faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa

juu yake.

LUKA 2:38 Huyu alitokea saa ile ile

akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa

wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu

akawatolea habari zake.

LUKA 21:5 Na watu kadha wa kadha

walipokuwa wakiongea habari za hekalu,

jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na

sadaka za watu, alisema,

6 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja

ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.

LUKA 21:32 Amin, nawaambieni, Kizazi

hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

LUKA 23:51 (wala hakulikubali shauri

na tendo lao), naye ni mtu wa Arimathaya,

mji mmoja wa Wayahudi, tena anautazamia

ufalme wa Mungu;

LUKA 24:49 Na tazama, nawaletea juu

yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni

humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao

juu.

WARUMI 9:3 Kwa maana ningeweza

kuomba mimi mwenyewe niharimishwe

na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu

zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;

4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa

wana, na ule utukufu, na maagano, na

kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi

zake;

5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka

Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya

mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa

milele. Amina.

WARUMI 11:7 Imekuwaje basi? Kitu

kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta

hakukipata; lakini wale waliochaguliwa

walikipata, na wengine walitiwa uzito.

8 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho

ya usingizi, macho hata wasione, na masikio

hata wasisikie, hata siku hii ya leo.

9 Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na

mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo

kwao;

10 Macho yao yatiwe giza ili wasione,

Ukawainamishe mgongo wao siku zote.

11 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata

waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa

lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao

wenyewe watiwe wivu.

12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa

ulimwengu, na upungufu wao umekuwa

utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu

wao?

WAGALATIA 3:16 Basi ahadi zilinenwa kwa

Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa

wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana

kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani,

Kristo.

17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa

kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka

mia nne na thelathini baadaye hailitangui,

hata kuibatilisha ile ahadi.

18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi

tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia

ZEKARIA

Page 380: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

380

Ibrahimu kwa njia ya ahadi.

WAEBRANIA 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu

amekuwa mdhamini wa agano lililo bora

zaidi.

WAEBRANIA 8:8 Maana, awalaumupo, asema

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami

nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba

ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana

na baba zao, Katika siku ile nilipowashika

mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.

Kwa sababu hawakudumu katika agano

langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na

nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema

Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia

zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami

nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu

wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani

yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua,

Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na

dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya

lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu

kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki

karibu na kutoweka.

Ona pia: Zaburi 89:39; Isaya 8:17; Isaya 26:8,9; Yeremia 14:21; Yeremia 31:31,32; Ezekieli 7:20-22; Ezekieli 16:59-61; Ezekieli

24:21; Danieli 9:26; Mika 7:7; Luka 24:49-53.

F05 Masiha atasalitiwa.

ZEKARIA 11:12 Nikawaambia, Mkiona vema,

nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe.

Basi wakanipimia vipande thelathini vya

fedha, kuwa ndio ujira wangu.

13 Kisha Bwana akaniambia, Mtupie mfinyanzi

kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu

hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini

vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani

ya nyumba ya Bwana.

MATHAYO 26:14 Wakati huo mmoja wa

wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote,

aliwaendea wakuu wa makuhani,

15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami

nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande

thelathini vya fedha.

16 Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi

apate kumsaliti.

MATHAYO 27:3 Kisha Yuda, yule mwenye

kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha

kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia

wakuu wa makuhani na wazee vile vipande

thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa

nilipoisaliti damu isiyo na hatia.

4 Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi?

Yaangalie haya wewe mwenyewe.

5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika

hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

6 Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile

vipande vya fedha, wakasema, Si halali

kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa

kuwa ni kima cha damu.

7 Wakafanya shauri, wakavitumia kwa

kununua konde la mfinyanzi liwe mahali pa

kuzika wageni.

8 Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu

hata leo.

9 Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii

Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande

thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa

kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia

ZEKARIA

Page 381: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

381

kima; 1)

10 wakavitumia kwa kununua konde la

mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.

1) Maneno yaliyonukuliwa hapa hayapatikani

kwenye kitabu cha Yeremia, lakini kwenye

kitabu cha Zekaria; na makisio mbalimbali

yameundwa, ili kupatanisha utofauti

huu. Maoni yenye uwezekano mkubwa

zaidi yanaonekana kuwa, jina la nabii

halikujumuishwa awali na Mwinjilisti, na

kwamba jina la Yeremia liliongezwa na mtu

fulani aliyenakili baada yake. Watu wa zamani

wenye hekima walikuwa wanasema: “Roho wa

Yeremia anaishi ndani ya Zekaria”.

F03 Masiha atakataliwa.

F08 Maelezo ya kifo cha Masiha.

G04 Masiha atatoa Roho Wake.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 12:1-2

ZEKARIA 12:3 Tena itakuwa siku

hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe

la kuwalemea watu wa kabila zote;

wote watakaojitwika jiwe hilo watapata

jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia

watakusanyika pamoja juu yake.

ZEKARIA 12:4-7

ZEKARIA 12:8 Katika siku hiyo Bwana

atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye

aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama

Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi

itakuwa kama Mungu, kama malaika wa

Bwana mbele yao.

9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba

nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote

watakaokuja kupigana na Yerusalemu.

10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba

ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu,

roho ya neema na kuomba; nao

watamtazama yeye ambaye walimchoma;

nao watamwombolezea, kama vile mtu

amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao

wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile

mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa

wake wa kwanza.

ZEKARIA 12:11-14

YOHANA 19:34 lakini askari mmojawapo

alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara

ikatoka damu na maji.

35 Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda

wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema

kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki.

36 Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie,

Hapana mfupa wake utakaovunjwa.

37 Na tena andiko lingine lanena,

Watamtazama yeye waliyemchoma.

MATENDO YA MITUME 2:17

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu, na

wana wenu na binti zenu watatabiri; na

vijana wenu wataona maono; na wazee wenu

wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi

wangu wanaume na wanawake Roho yangu,

nao watatabiri.

MATENDO YA MITUME 2:23 mtu

huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu

lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu

zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono

ya watu wabaya, mkamwua;

24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua

ZEKARIA

Page 382: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

382

uchungu wa mauti, kwa sababu

haikuwezekana ashikwe nao.

MATENDO YA MITUME 2:33 Basi yeye,

akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume

wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi

ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki

mnachokiona sasa na kukisikia.

MATENDO YA MITUME 2:36 Basi

nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya

kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo

mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao,

wakamwambia Petro na mitume wengine,

Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila

mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate

ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea

kipawa cha Roho Mtakatifu.

UFUNUO WA YOHANA 1:7 Tazama,

yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona,

na hao waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.

Amina.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Matendo ya Mitume 10:45; Matendo ya Mitume 11:15; Tito 3:5,6.

E04 Ushindi wa Masiha dhidi ya dhambi.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

ZEKARIA 13:1 Katika siku hiyo watu

wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa

Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa

dhambi na kwa unajisi.

2 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema

Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina

ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe

tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya

uchafu, watoke katika nchi.

EZEKIELI 36:25 Nami nitawanyunyizia maji

safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na

uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

YOHANA 1:29 Siku ya pili yake amwona

Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye

dhambi ya ulimwengu!

1 WAKORINTHO 6:11 Na baadhi yenu

mlikuwa watu wa namna hii; lakini

mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini

mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu

Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

TITO 3:5 si kwa sababu ya matendo ya haki

tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,

kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na

kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya

Yesu Kristo Mwokozi wetu;

1 YOHANA 1:7 bali tukienenda nuruni,

kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana

sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana

wake, yatusafisha dhambi yote.

UFUNUO WA YOHANA 1:5 tena

zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye

mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa

waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu

katika damu yake,

UFUNUO WA YOHANA 7:13 Akajibu

mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu

ZEKARIA

Page 383: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

383

hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina

nani? Na wametoka wapi?

14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.

Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika

dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,

na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-

Kondoo.

Ona pia: #1; #2; #5; Ezekieli 37:23-26; Hosea 2:18; Hosea 14:7; Sefania 1:3,4; Waefeso 5:25-27; Waebrania 9:13,14; Yohana 5:6.

F01 Kifo cha Masiha kinatabiriwa.

F06 Masiha ataachwa pweke.

ZEKARIA 13:7 Amka, Ee upanga, juu

ya mchungaji wangu, na juu ya mtu

aliye mwenzangu, asema Bwana wa

majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo

watatawanyika; nami nitaugeuza mkono

wangu juu ya wadogo.

MATHAYO 26:31 Ndipo Yesu akawaambia,

Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili

yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa,

Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi

watatawanyika.

MATHAYO 26:56 Lakini haya yote yamekuwa,

ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo

wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

MARKO 14:27 Yesu akawaambia,

Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili

yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa,

Nitampiga mchungaji, na kondoo

watatawanyika.

MARKO 14:50 Ndipo wakamwacha,

wakakimbia wote.

YOHANA 16:32 Tazama, saa yaja, naam,

imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila

mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke

yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa

kuwa Baba yupo pamoja nami.

YOHANA 17:12 Nilipokuwapo pamoja nao,

mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa,

nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao

aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili

andiko litimie.

YOHANA 18:7 Basi akawauliza tena,

Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu

Mnazareti.

8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya

kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta

mimi, waacheni hawa waende zao.

9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale

ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.

Ona pia: Isaya 5:1-5; Isaya 27:1,2; Mathayo 18:10-14; Matendo ya Mitume 2:23.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

ZEKARIA 13:8 Hata itakuwa, ya kwamba

katika nchi yote mafungu mawili

yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema

Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo.

9 Nami nitalileta fungu lile la tatu na

kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha

kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu

kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina

langu, nami nitawasikia; mimi nitasema,

Watu hawa ndio wangu; nao watasema,

Bwana ndiye Mungu wangu.

ZEKARIA

Page 384: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

384

MATHAYO 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia,

Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao

watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda

yake.

44 Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-

vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia,

litamsaga tikitiki.

MATHAYO 24:2 Naye akajibu akawaambia,

Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni,

Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.

MATHAYO 24:21 Kwa kuwa wakati huo

kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea

namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu

hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa,

asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya

wateule zitafupizwa siku hizo.

LUKA 21:24 Wataanguka kwa ukali

wa upanga, nao watatekwa nyara na

kuchukuliwa katika mataifa yote; na

Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata

majira ya Mataifa yatakapotimia.

UFUNUO WA YOHANA 8:7 Malaika

wa kwanza akapiga baragumu, kukawa

mvua ya mawe na moto vilivyotangamana

na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi

ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti

ikateketea, na majani mabichi yote

yakateketea.

8 Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu,

mfano wa mlima mkubwa uwakao moto,

kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari

ikawa damu.

9 Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo

baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu

zikaharibiwa.

10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota

kubwa ikaanguka kutoka mbinguni,

iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu

ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za

maji.

11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga;

theluthi ya maji ikawa pakanga, na

wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo,

kwa kuwa yalitiwa uchungu.

12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi

ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na

theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi

itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake,

wala usiku vivyo hivyo.

UFUNUO WA YOHANA 16:19 Na mji

ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu,

na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule

mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu,

kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu

ya hasira yake.

Ona pia: #1; #2; #5; Zaburi 66:10-12; Mathayo 23:35-37; Luka 19:41-44; Luka 21:20-24; Luka 23:28-30; 1 Wakorintho 3:11-13; 1

Wathesalonike 2:15,16; 1 Petro 1:6-8; 1 Petro 4:12,13.

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H01 Kurudi kwa Masiha kunatabiriwa.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

.

ZEKARIA 14:1-2

ZEKARIA 14:3 Hapo ndipo atakapotokea

Bwana, naye atapigana na mataifa hayo,

kama vile alipopigana zamani siku ya vita.

4 Na siku hiyo miguu yake itasimama

juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea

Yerusalemu upande wa mashariki, nao

mlima wa Mizeituni utapasuka katikati

ZEKARIA

Page 385: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

385

yake, upande wa mashariki na upande wa

magharibi; litakuwako huko bonde kubwa

sana; na nusu ya mlima ule utaondoka

kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake

itaondoka kwenda upande wa kusini.

5 Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la

milima yangu; kwa maana bonde lile

la milima litaenea hata Aseli; naam,

mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele

ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme

wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja,

na watakatifu wote pamoja naye.

6 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru

yake haitakuwa na mwangaza na kiwi;

7 lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na

Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini

itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni

kutakuwako nuru.

8 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji

yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu;

nusu yake itakwenda upande wa bahari ya

mashariki, na nusu yake upande wa bahari

ya magharibi; wakati wa hari na wakati wa

baridi itakuwa hivi.

9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi

yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na

jina lake moja.

ZEKARIA 14:10-15

ZEKARIA 14:16 Hata itakuwa, ya kwamba

kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja

kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka

baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme,

Bwana wa majeshi, na kuishika sikukuu ya

Vibanda.

17 Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote

wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea

kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme,

Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.

18 Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala

hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako

tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa,

wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.

19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya

mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu

ya Vibanda.

20 Siku hiyo katika njuga za farasi yataandikwa

maneno haya, WATAKATIFU KWA Bwana;

navyo vyombo vilivyomo ndani ya nyumba

ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko

mbele ya madhabahu.

21 Naam, kila chombo katika Yerusalemu,

na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa

Bwana wa majeshi; nao wote watoao

dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na

kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo

hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya

nyumba ya Bwana wa majeshi.

ISAYA 2:2 Na itakuwa katika siku

za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana

utawekwa imara juu ya milima, nao

utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote

watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema,

Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,

nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye

atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda

katika mapito yake maana katika Sayuni

itatoka sheria, na neno la Bwana katika

Yerusalemu.

4 Naye atafanya hukumu katika mataifa

mengi, atawakemea watu wa kabila

nyingi; nao watafua panga zao ziwe

majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa

halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala

hawatajifunza vita tena kamwe.

MATHAYO 16:27 Kwa sababu Mwana wa

Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake

pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa

ZEKARIA

Page 386: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

386

kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

MATHAYO 24:35 Mbingu na nchi zitapita;

lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna

aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala

Mwana, ila Baba peke yake.

37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za

Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake

Mwana wa Adamu.

MATHAYO 28:18 Yesu akaja kwao, akasema

nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote

mbinguni na duniani.

YOHANA 4:10 Yesu akajibu, akamwambia,

Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye

ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe,

ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji

yaliyo hai.

YOHANA 4:14 walakini ye yote

atakayekunywa maji yale nitakayompa

mimi hataona kiu milele; bali yale maji

nitakayompa yatakuwa ndani yake

chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa

milele.

YOHANA 7:37 Hata siku ya mwisho, siku

ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama,

akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu,

na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko

yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka

ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari

ya Roho, ambaye wale wamwaminio

watampokea baadaye; kwa maana Roho

alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa

hajatukuzwa.

MATENDO YA MITUME 1:10

Walipokuwa wakikaza macho mbinguni,

yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu

wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo

nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona

mmesimama mkitazama mbinguni?

Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu

kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo

mlivyomwona akienda zake mbinguni.

12 Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka

mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na

Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.

UFUNUO WA YOHANA 11:13 Na katika

saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi,

na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka;

wanadamu elfu saba wakauawa katika

tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na

hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 16:18 Pakawa

na umeme na sauti na radi; na palikuwa

na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu

wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa

namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko

hilo.

19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu

matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na

Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za

Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya

ghadhabu ya hasira yake.

20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima

ZEKARIA

Page 387: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

387

haikuonekana tena.

21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe

mazito kama talanta, ikashuka kutoka

mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu

wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile

pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake

ni kubwa mno.

UFUNUO WA YOHANA 21:23 Na mji

ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,

kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru,

na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na

wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani

yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe

mchana; kwa maana humo hamna usiku.

UFUNUO WA YOHANA 22:1 Kisha

akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye

kung›aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha

enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na

upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa

uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,

wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na

majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

UFUNUO WA YOHANA 22:5 Wala

hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja

ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana

Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 22:17 Na Roho

na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye

na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na

yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

Ona pia: #1; #2; #3; #4; #5; Ufunuo wa Yohana 21:1-3.

ZEKARIA

Page 388: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

388

E10 Masiha atakuwa pia Masiha wa Wayanuni.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

MALAKI 1:11 Kwa maana tokea maawio

ya jua hata machweo yake jina langu ni

kuu katika Mataifa; na katika kila mahali

unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa

jina langu; maana jina langu ni kuu katika

Mataifa, asema Bwana wa majeshi.

ISAYA 66:20 Nao watawaleta ndugu zenu

wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa

Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na

katika machela, na juu ya nyumbu, na juu

ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu

mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama

vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao

nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.

WARUMI 14:11 Kwa kuwa imeandikwa,

Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti

litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi

utamkiri Mungu.

WAFILIPI 2:10 ili kwa jina la Yesu kila

goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi;

WAEBRANIA 9:9 ambayo ndiyo mfano wa

wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka

na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi

ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,

10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu,

vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine

kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa

matengenezo mapya.

11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani

mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo,

kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi,

isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo

ya ulimwengu huu,

12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali

kwa damu yake mwenyewe aliingia mara

moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele.

UFUNUO WA YOHANA 8:3 Na

malaika mwingine akaja akasimama mbele

ya madhabahu, mwenye chetezo cha

dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie

pamoja na maombi ya watakatifu wote juu

ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya

kiti cha enzi.

4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele

za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu,

kutoka mkononi mwa malaika.

Ona pia: #1; #4; #5; Zaburi 113:3,4; Isaya 45:6; Isaya 59:19.

C02 Mtangulizi wa Masiha anatangazwa.

MALAKI 3:1 Angalieni, namtuma mjumbe

wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu;

naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu

lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano

mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema

Bwana wa majeshi.

ISAYA 40:3 Sikiliza, ni sauti ya mtu

aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana;

Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu

wetu.

MATHAYO 3:3 Kwa sababu huyo ndiye

aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti

ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya

Bwana, Yanyosheni mapito yake.

MATHAYO 11:10 Huyo ndiye aliyeandikiwa

MALAKI

Page 389: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

389

haya, Tazama, mimi namtuma

mjumbe wangu Mbele ya uso wako,

Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu

katika wazao wa wanawake aliye mkuu

kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye

mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu

kuliko yeye.

MARKO 1:2 Kama ilivyoandikwa

katika nabii Isaya, Tazama, namtuma

mjumbe wangu Mbele ya uso wako,

Atakayeitengeneza njia yako.

3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni

njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na

kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la

dhambi.

LUKA 1:76 Nawe, mtoto, utaitwa nabii

wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia

mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia

zake;

77 Uwajulishe watu wake wokovu, Katika

kusamehewa dhambi zao.

78 Kwa njia ya rehema za Mungu wetu,

Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu

umetufikia,

79 Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa

mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye

njia ya amani.

LUKA 7:26 Lakini, mlitoka kwenda

kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na

aliye zaidi ya nabii.

27 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama,

namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso

wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele

yako.

28 Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa

na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko

Yohana; lakini aliye mdogo katika ufalme wa

Mungu ni mkuu kuliko yeye.

LUKA 10:24 Kwa kuwa nawaambia

ya kwamba manabii wengi na wafalme

walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi

wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi

wasiyasikie.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

MALAKI 3:2 Lakini ni nani

atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni

nani atakayesimama atakapoonekana yeye?

Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu

asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu

afuaye nguo;

3 naye ataketi kama asafishaye fedha na

kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi,

atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao

watamtolea Bwana dhabihu katika haki.

4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na

Yerusalemu zitakapopendeza mbele za

Bwana, kama katika siku za kale, na kama

katika miaka ya zamani.

5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu;

nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya

wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao

waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao

mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara

wake, wamwoneao mjane na yatima, na

kumpotosha mgeni asipate haki yake,

wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa

majeshi.

16 Ndipo wale waliomcha Bwana

MALAKI

Page 390: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

390

waliposemezana wao kwa wao. Naye

Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha

ukumbusho kikaandikwa mbele zake,

kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na

kulitafakari jina lake.

17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana

wa majeshi, katika siku ile niifanyayo;

naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami

nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo

mwanawe mwenyewe amtumikiaye.

18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua

kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye

amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

DANIELI 7:10 Mto kama wa moto

ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu

wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu

kumi wakasimama mbele zake; hukumu

ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.

MATHAYO 3:10 Na shoka limekwisha

kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila

mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na

kutupwa motoni.

11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya

toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu

kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua

viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho

Mtakatifu na kwa moto.

12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake,

naye atausafisha sana uwanda wake; na

kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi

atayateketeza kwa moto usiozimika.

MATHAYO 12:35 Mtu mwema katika akiba

njema hutoa mema; na mtu mbaya katika

akiba mbaya hutoa mabaya.

36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana,

watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu

ya neno hilo siku ya hukumu.

37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa

haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

YOHANA 12:48 Yeye anikataaye mimi,

asiyeyakubali maneno yangu, anaye

amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo

litakalomhukumu siku ya mwisho.

YOHANA 17:24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate

na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa

maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi

ulimwengu.

WAEFESO 5:26 ili makusudi alitakase na

kulisafisha kwa maji katika neno;

2 WATHESALONIKE 1:7 na kuwalipa ninyi

mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa

kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka

mbinguni pamoja na malaika wa uweza

wake

8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza

kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao

wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;

TITO 2:14 ambaye alijitoa nafsi yake

kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi

yote, na kujisafishia watu wawe milki yake

mwenyewe, wale walio na juhudi katika

matendo mema.

1 PETRO 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe

yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za

roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya

Yesu Kristo.

UFUNUO WA YOHANA 1:6 na

kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa

MALAKI

Page 391: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

391

Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu

una Yeye hata milele na milele. Amina.

7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho

litamwona, na hao waliomchoma; na kabila

zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake.

Naam. Amina.

UFUNUO WA YOHANA 6:17 Kwa

maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja;

naye ni nani awezaye kusimama?

UFUNUO WA YOHANA 15:4 Ni

nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza

jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako

u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote

watakuja na kusujudu mbele zako; kwa

kuwa matendo yako ya haki yamekwisha

kufunuliwa.

Ona pia: #1; #2; #5; Malaki 4:1; Amosi 5:18-20; Mathayo 23:13-35; Luka 3:9,17; Luka 12:49; Yohana 4:23,24; Warumi 11:5-10;

Waebrania 10:28-30; Waebrania 12:25,26.

H02 Hukumu ya Masiha ya siku zijazo.

H03 Ufalme wa Masiha wa siku zijazo.

H09 Unabii wa mustakabali wa watu Wake.

MALAKI 4:1 Kwa maana, angalieni, siku

ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu

wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu,

watakuwa makapi; na siku ile inayokuja

itawateketeza, asema Bwana wa majeshi;

hata haitawaachia shina wala tawi.

2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu,

jua la haki litawazukia, lenye kuponya

katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na

kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.

3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana

watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu

yenu; katika siku ile niifanyayo, asema

Bwana wa majeshi.

4 Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi

wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa

ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.

MATHAYO 3:12 Ambaye pepeto lake li

mkononi mwake, naye atausafisha sana

uwanda wake; na kuikusanya ngano yake

ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto

usiozimika.

LUKA 1:50 Na rehema zake hudumu

vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

YOHANA 1:4 Ndani yake ndimo

ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa

nuru ya watu.

5 Nayo nuru yang›aa gizani, wala giza

halikuiweza.

YOHANA 3:19 Na hii ndiyo hukumu; ya

kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu

wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana

matendo yao yalikuwa maovu.

YOHANA 8:12 Basi Yesu akawaambia tena

akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,

yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,

bali atakuwa na nuru ya uzima.

MATENDO YA MITUME 13:26 Ndugu

zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao

miongoni mwenu wanaomcha Mungu,

kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.

WARUMI 16:20 Naye Mungu wa amani

atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe

pamoja nanyi. [Amina.]

MALAKI

Page 392: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

392

2 WATHESALONIKE 1:8 katika mwali

wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao

wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya

Bwana wetu Yesu;

UFUNUO WA YOHANA 11:15 Malaika

wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti

kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa

dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana

wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata

milele na milele.

UFUNUO WA YOHANA 11:18 Na

mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja,

na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa,

na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako

manabii na watakatifu, na hao walichao

jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa

kuwaharibu hao waiharibuo nchi.

Ona pia: #1; #2; #5; Isaya 50:10; Isaya 66:1,2; 2 Petro 3:7.

C02 Mtangulizi wa Masiha anatangazwa.

D02 Kazi ya Masiha kama Nabii.

E23 Masiha atawabadilisha watu Wake.

MALAKI 4:5 Angalieni, nitawapelekea

Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana,

iliyo kuu na kuogofya.

6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee

watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee

baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa

laana.

MATHAYO 11:13 Kwa maana manabii wote na

torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya

atakayekuja.

MATHAYO 17:11 Naye akajibu, akawaambia,

Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza

yote,

12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha

kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote

waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu

naye yuaenda kuteswa kwao.

13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya

kuwa amesema nao habari za Yohana

Mbatizaji.

LUKA 1:16 Na wengi katika Waisraeli

atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.

17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya

Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya

baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi

akili za wenye haki, na kumwekea Bwana

tayari watu waliotengenezwa.

YOHANA 1:14 Naye Neno alifanyika mwili,

akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,

utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa

Baba; amejaa neema na kweli.

15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake

akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake

ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa

mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla

yangu.

16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote

tulipokea, na neema juu ya neema.

17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa

Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono

wa Yesu Kristo.

MATENDO YA MITUME 3:22 Kwa

maana Musa kweli alisema ya kwamba,

Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii,

katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni

yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.

23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu

MALAKI

Page 393: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

393

asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na

kutengwa na watu wake.

UFUNUO WA YOHANA 1:16 Naye

alikuwa na nyota saba katika mkono wake

wa kuume; na upanga mkali, wenye makali

kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso

wake kama jua liking›aa kwa nguvu zake.

Ona pia: #5; Isaya 40:3; Malaki 3:1; Mathayo 13:14-26; Mathayo 23:35-38; Mathayo 24:27-30; Mathayo 27:47-49; Marko 9:11-13; Luka 1:76; Luka 7:26-28; Luka 19:41-44; Luka 21:22-27; Yohana

1:21,25.

MALAKI

Page 394: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

394

Page 395: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

395

Nukuu na vionyeshi vya Biblia ya Kiebrania

kwenye Vitabu vya Matendo ya Mitume.

MATHAYO

1:23 Isaya 7:14

2:6 Mika 5:1

2:15 Hosea 11:1

2:18 Yeremia 31:15

2:23 Hesabu 6:13; Zaburi 69:9,10;

Isaya 53:2

3:3 Isaya 40:3

4:4 Kumbukumbu la Torati 8:3

4:6 Zaburi 91:11,12

4:10 Kumbukumbu la Torati 6:13,14;

Kumbukumbu la Torati 10:20

4:15,16 Isaya 9:1,2

4:7 Kumbukumbu la Torati 6:16

5:3 Isaya 57:15

5:4 Isaya 61:2,3

5:5 Isaya 29:19; Isaya 61:1

5:6 Isaya 41:17; Isaya 49:10;

Isaya 55:1-3

5:7 Zaburi 112:4; Mika 6:8

5:8 Zaburi 73:1; Mithali 22:11;

Ezekieli 36:25

5:11 Isaya 66:5

5:12 Isaya 3:10

5:13 Mambo ya Walawi 2:13; Ayubu 6:6;

5:14 Mithali 4:18

5:15 Kutoka 25:37

5:16 Isaya 60:1-3; Isaya 61:3

5:17 Zaburi 40:7-9; Isaya 42:21

5:18 Isaya 40:8; Isaya 51:6; Zaburi 119:89

5:19 Kumbukumbu la Torati 12:32;

Kumbukumbu la Torati 27:26;

Danieli 12:3

5:21 Mwanzo 9:5,6; Kutoka 20:13;

Kumbukumbu la Torati 5:17

5:23-24 Kumbukumbu la Torati 16:16,17;

Isaya 1:10-17

MATHAYO

5:25 Mithali 25:8

5:27 Kutoka 20:14;

Kumbukumbu la Torati 5:18

5:31 Kumbukumbu la Torati 24:1

5:33 Mambo ya Walawi 19:12; Hesabu 30:2

5:34,35 Hosea 4:15; Zekaria 5:3

5:38 Kutoka 21:24

5:42 Kumbukumbu la Torati 15:7-14

5:43 Mambo ya Walawi 19:18;

Zaburi 139:21

5:44 Kutoka 23:45

5:48 Mambo ya Walawi 19:2;

Mambo ya Walawi 20:26

6:2 Zaburi 37:21; Mithali 20:6

6:4 Isaya 58:10-12

6:5,6 2 Wafalme 4:33; Danieli 6:10

6:7 Mhubiri 5:2

6:8 Zaburi 38:10

6:9 Isaya 63:16; Isaya 64:8

6:10 Danieli 2:44; Danieli 7:27

6:11 Kutoka 16:16-35

6:12 Kutoka 34:7; Isaya 1:18

6:13 Kumbukumbu la Torati 8:2

6:16 Isaya 58:3-5

6:17 Mhubiri 9:8; Danieli 10:3

6:19 Zaburi 62:11; Mhubiri 5:10-14

6:24 Kutoka 20:39

6:25 Zaburi 55:23

6:26 Mwanzo 1:29-30

6:31 Mambo ya Walawi 25:20-22;

Zaburi 55:23

6:33 1 Wafalme 3:11-13; Mithali 3:9,10

6:34 Kutoka 16:18-20; Maombolezo 3:23

7:3 2 Samweli 12:5; Zaburi 50:16-21

7:7 Isaya 55:6,7; Yeremia 29:12,13

7:11 Mwanzo 8:5; Zaburi 103:11-13

7:12 Amosi 5:14,15; Zekaria 8:16,17

7:14 Isaya 35:8

7:15 Kumbukumbu la Torati 13:1-3

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 396: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

396

MATHAYO

7:17 Zaburi 92:14,15

7:18 Yeremia 17:8

7:19 Ezekieli 15:2-7

7:21 Isaya 29:13; Hosea 8:2,3

7:23 Zaburi 6:9

7:26,27 Ezekieli 13:10-16

7:29 Kumbukumbu la Torati 18:18,19

8:17 Isaya 53:4

9:13 Mithali 21:3; Hosea 6:6;

Mika 6:6-8

10:35,36 Mwanzo 3:15; Yeremia 12:6

10:37 Kumbukumbu la Torati 33:9

10:41 Mwanzo 20:7

11:5 Isaya 29:18; Isaya 35:4-6;

Isaya 42:6-7

11:10 Malaki 3:1

11:14 Malaki 4:5

11:23 Isaya 14:13,15

11:24 Maombolezo 4:6

11:25 Zaburi 8:3; Yeremia 1:5-8

11:26 Isaya 45:10

11:28 Isaya 11:10; Isaya 55:1-3;

Yeremia 6:16

11:29 Isaya 42:1-4; Zekaria 9:9;

Yeremia 6:16

12:1 Kumbukumbu la Torati 23:25

12:2 Kutoka 23:12; Hesabu 15:32-36

12:3 1 Samweli 21:3-6

12:4 Kutoka 25:30; Kutoka 29:33;

Mambo ya Walawi 24:8-9

12:5 Hesabu 28:19,20; Nehemia 13:17

12:6 Malaki 3:1

12:7 Isaya 1:11-17; Hosea 6:6;

Mika 6:6-8

12:11 Kutoka 23:4,5

12:17,21 Isaya 11:2,10; Isaya 42:14;

Isaya 49:6

12:35 Zaburi 37:30,31

12:36 Mhubiri 12:14

MATHAYO

12:37 Mithali 13:3

12:40 Yona 1:17

12:41,42 1 Wafalme 10:110

13:3 Ezekieli 17:2; Ezekieli 24:3

13:11 Zaburi 25:8,9,14; Isaya 29:10

13:13 Isaya 44:15; Ezekieli 12:2

13:14,15 Isaya 6:9,10; Isaya 29:10,12

13:35 Zaburi 78:2

13:43 Danieli 12:3

15:4 Kutoka 20:12; Mambo ya Walawi 20:9;

Kumbukumbu la Torati 5:16

15:8 Isaya 29:3

15:13 Zaburi 92:14; Isaya 60:21

15:14 Isaya 9:16

15:18 Mithali 10:32

15:19 Mwanzo 6:5; Yeremia 17:9

16:4 Yona 1:17

16:27 Zaburi 62:13; Danieli 7:10

17:11 Malaki 4:5,6

18:10 Zaburi 34:8; Zaburi 91:11;

Zekaria 13:7

18:14 Isaya 40:11; Zekaria 13:7

18:15 Mambo ya Walawi 19:17

18:16 Kumbukumbu la Torati 19:15

18:22 Isaya 55:7

19:4 Mwanzo 1:27

19:5,6 Mwanzo 2:24

19:7 Kumbukumbu la Torati 24:1

19:9 Yeremia 3:1

19:18 Kutoka 20:12-17;

Kumbukumbu la Torati 5:16-21

19:19 Mambo ya Walawi 19:3

19:23 Kumbukumbu la Torati 8:10-18

19:26 Yeremia 32:27; Zekaria 8:6

19:28 Isaya 66:22; Danieli 7:22

21:4,5 Zekaria 9:9

21:9 Zaburi 118:26

21:12 Malaki 3:1,2

21:13 Isaya 56:7

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 397: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

397

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

MATHAYO

21:16 Zaburi 8:4

21:42 Zaburi 118:22,23

21:43 Kutoka 32:10; Isaya 26:2; Isaya 55:5

21:44 Isaya 8:14; Zekaria 12:3

22:32 Kutoka 3:6

22:37 Kumbukumbu la Torati 6:5;

Kumbukumbu la Torati 10:12;

Kumbukumbu la Torati 30:6

22:39 Mambo ya Walawi 19:18

22:44 Zaburi 110:1

23:12 Mithali 29:23; Isaya 57:15

23:35 Mwanzo 4:28;

2 Mambo ya Nyakati 24:20-22

23:38 Yeremia 22:5

23:39 Zaburi 118:26

24:15 Danieli 9:27

24:21 Danieli 12:1

24:29 Isaya 13:10; Ezekieli 32:7,8; Yoeli 2:31

24:30 Danieli 7:10,13; Zekaria 12:10

24:31 Isaya 11:12; Isaya 27:13

24:35 Zaburi 102:27; Isaya 51:6

25:31 Danieli 7:13,14

25:32 Ezekieli 34:17-22

25:35 Mwanzo 18:2-8; Mithali 25:21

25:36 Ayubu 31:19,20

25:46 Danieli 12:2

26:15 Zekaria 11:12,13

26:23 Zaburi 41:10

26:31 Zekaria 13:7

26:52 Mwanzo 9:6

26:54 Zaburi 22:1-32; Isaya 53:1-12

26:56 Zekaria 13:7

26:64 Zaburi 110:1; Danieli 7:13

27:9-10 Zekaria 11:12,13

27:35 Zaburi 22:19

28:18 Zaburi 2:6-9; Zaburi 8:7; Danieli 7:14

MARKO

1:11 Zaburi 2:7; Isaya 42:1

1:2,3 Isaya 40:3; Malaki 3:1

1:15 Danieli 2:44

1:17 Ezekieli 47:10

1:24 Zaburi 89:19,20

2:25 1 Samweli 21:3-6

2:26 Mambo ya Walawi 24:9

2:27 Kutoka 31:14;

Kumbukumbu la Torati 5:12-15

4:2 Zaburi 78:2

4:3-9 Isaya 55:10,11

4:12 Isaya 6:9,10

4:22 Zaburi 78:2-4; Zaburi 90:9,10

4:27 Mhubiri 8:17

4:29 Yoeli 3:13

4:30-32 Ezekieli 31:5,6; Danieli 4:10-12

4:39 Zaburi 107:29; Zaburi 93:4

6:34 Yeremia 50:6; Zekaria 10:2

6:45-52 Zaburi 107:2332

7:6 Isaya 29:13; Ezekieli 33:31

7:10 Kutoka 20:12;

Kumbukumbu la Torati 5:16

7:21-23 Mwanzo 6:5; Zaburi 14:1,3

7:24 Isaya 42:2

8:18 Zaburi 115:5-7; Yeremia 5:21

8:31 Hosea 6:2; Yona 1:17

8:37 Zaburi 49:8,9

9:2 Isaya 33:17

9:3 Danieli 7:9

9:7 Danieli 7:13

9:11 Malaki 3:1; Malaki 4:5

9:12 Zaburi 22:1-32; Isaya 40:3-5;

Isaya 53:1-12

9:13 Malaki 4:5,6

9:44-48 Isaya 66:24

9:49 Mambo ya Walawi 2:13

10:6 Mwanzo 1:27; Mwanzo 5:2

10:7,8 Mwanzo 2:24

Page 398: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

398

MARKO

10:18 1 Samweli 2:12; Zaburi 86:5

10:19 Kutoka 20:1217;

Kumbukumbu la Torati 5:1620

10:34 Zaburi 16:10; Zaburi 22:7-9,14

10:34 Isaya 53:10; Hosea 6:2

10:44 Isaya 53:10-12; Danieli 9:24,26

11:7 Zekaria 9:9

11:9 Zaburi 118:26

11:10 Ezekieli 34:24; Ezekieli 37:24

11:17 Isaya 56:7; Yeremia 7:11

12:10,11 Zaburi 118:22,23

12:19 Mwanzo 38:8;

Kumbukumbu la Torati 25:5-10

12:26 Kutoka 3:6,16

12:29,30 Kumbukumbu la Torati 6:4,5;

Kumbukumbu la Torati 10:12;

Mambo ya Walawi 19:18

12:36 Zaburi 110:1

13:8 Hagai 2:22; Zekaria 14:13

13:14 Danieli 11:31; Danieli 12:11

13:19 Danieli 9:12; Danieli 12:1

13:24,25 Isaya 13:10; Isaya 24:20-23; Yoeli 2:31

13:26 Danieli 7:13-14

13:27 Kumbukumbu la Torati 30:4;

Danieli 7:13

13:31 Zaburi 102:26-28; Isaya 40:8;

Isaya 51:6

14:18 Zaburi 41:10

14:21 Isaya 53:1-12; Danieli 9:26

14:27 Zekaria 13:7

14:50 Zaburi 38:12; Zaburi 88:9; Isaya 63:3

14:62 Zaburi 110: 1; Danieli 7:13

14:65 Isaya 50:6; Mika 4:14

15:24 Zaburi 22:19

15:28 Isaya 53:12

15:29 Zaburi 22:8,9; Zaburi 109:25;

Maombolezo 1:12

15:34 Zaburi 22:2

15:36 Zaburi 69:22

LUKA

1:17 Malaki 4:5,6

1:48 Zaburi 113:7,8; Zaburi 136:23;

Malaki 3:12

1:50 Mwanzo 17:7; Zaburi 103:17

1:51 Zaburi 98:1; Isaya 21:10

1:52 Zaburi 107:40,41; Amosi 9:11

1:53 Zaburi 107:9

1:54 Zaburi 98:3

1:55 Mwanzo 12:3; Mwanzo 22:18;

Mwanzo 28:14

1:69 1 Samweli 2:10; Zaburi 132:17,18;

Ezekieli 29:21

1:70 Mwanzo 3:15;

Kumbukumbu la Torati 18:15-19;

Danieli 9:24-27

1:71 Kumbukumbu la Torati 33:29;

Zaburi 106:10;

Isaya 14:1-3

1:72 Mwanzo 12:3; Mwanzo 28:14;

Zaburi 98:3

1:73 Mwanzo 22:16,17

1:74 Sefania 3:15; Zekaria 9:8-10

1:75 Yeremia 31:33,34

1:76 Malaki 3:1; Malaki 4:5

1:78 Hesabu 24:17; Malaki 4:2

1:79 Isaya 9:1; Isaya 60:1-3

2:21 Mwanzo 17:12;

Mambo ya Walawi 12:3

2:23 Kutoka 13:2,12,15

2:24 Mambo ya Walawi 12:6-8

2:31 Zaburi 96:13; Zaburi 98:2,3

2:32 Isaya 49:6

2:34 Isaya 8:14,15

3:46 Isaya 40:35

4:4 Kumbukumbu la Torati 8:3

4:8 Kumbukumbu la Torati 6:13;

Kumbukumbu la Torati 10:20;

Zaburi 83:18

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 399: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

399

LUKA

4:10,11 Zaburi 91:11,12

4:12 Kumbukumbu la Torati 6:16

4:17-19 Isaya 61:1,2

4:25,26 1 Wafalme 17:116

4:27 2 Wafalme 5:1-14

5:14 Mambo ya Walawi 13:2

5:21 Kutoka 34:7;

Mambo ya Walawi 24:16

6:2 Kutoka 31:15; Kutoka 35:2

6:3,4 Mambo ya Walawi 24:5-9;

1 Samweli 21:3-6

6:21 Zaburi 126:5,6; Isaya 55:1,2

7:21-22 Zaburi 146:8; Isaya 28:18,19

7:27 Yeremia 4:3; Malaki 4:5

8:21 Kumbukumbu la Torati 29:4;

Zaburi 25:14

9:16,17 2 Wafalme 4:42-44

9:54 2 Wafalme 1:10-14

9:61,62 1 Wafalme 19:1922

10:42 Zaburi 27:4; Zaburi 62:13

11:31,32 1 Wafalme 10:1,2;

2 Mambo ya Nyakati 9:1;

Isaya 9:5,6

13:14 Kutoka 20:9; Kutoka 23:12;

Mambo ya Walawi 23:3

14:11 Isaya 57:15

14:16 Isaya 25:6

15:11-32 Kumbukumbu la Torati 21:1521

16:8 Zaburi 27:4; Zaburi 49:11-20

17:25 Isaya 53:3

17:26,27 Mwanzo 7:7-23

17:28 Mwanzo 19:4-15

17:29 Mwanzo 19:16-25

17:32 Mwanzo 19:26

18:7 Zaburi 55:18; Zaburi 86:3;

Yeremia 20:11-13

18:11 Yeremia 2:35

18:19 Ayubu 14:4

18:20 Kutoka 20:12-17

LUKA

18:22 Zaburi 27:4

18:31 Zaburi 22:1-32; Zaburi 69:1-37;

Isaya 53:1-12

18:32 Isaya 50:6; Isaya 52:14; Isaya 53:3

18:33 Zaburi 71:20; Hosea 6:2

19:38 Zekaria 9:9

19:41 Yeremia 17:16; Hosea 11:8

19:42 Kumbukumbu la Torati 5:29;

Isaya 6:9,10;

Isaya 29:10-14

19:43 Kumbukumbu la Torati 28:49-58;

Danieli 9:26,27

19:44 Isaya 29:3; Yeremia 6:6; Danieli 9:24;

Mika 3:12

20:17 Zaburi 118:22

20:18 Isaya 8:14,15

20:42,43 Zaburi 2:1-9; Zaburi 110:1

20:44 Zaburi 2:7; Zaburi 89:28; Zaburi 110:1

21:6 Isaya 64:10,11; Mika 3:12;

Zekaria 14:2

21:10 Zekaria 14:2,3,13

21:20 Danieli 9:27

21:22 Mhubiri 9:12; Danieli 9:26,27

21:25 Isaya 13:10,13; Ezekieli 32:7,8;

Yoeli 2:30,31

21:26 Kumbukumbu la Torati 28:32-34,65-67

21:27 Danieli 7:13

21:33 Zaburi 102:27; Isaya 51:6

21:34,35 Isaya 24:17

22:2 Zaburi 2:1-5

22:3 Zaburi 41:10; Zaburi 55:13-15

22:21 Zaburi 41:10

22:22 Zaburi 22:1-32; Zaburi 55:13-16;

Zaburi 109:6-8

22:30 Zaburi 49:15

22:37 Isaya 53:12

22:63 Isaya 50:6; Mika 4:14

22:69 Zaburi 110:1; Danieli 7:14

23:30 Yeremia 2:19; Hosea 10:8

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 400: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

400

LUKA

23:34 Zaburi 22:19

23:36 Zaburi 69:22

23:46 Zaburi 31:6

23:53 Isaya 53:9

24:36 Mambo ya Walawi 16:28

24:46,47 Mwanzo 49:10; Hesabu 21:6-9;

Kumbukumbu la Torati 18:15;

24:46,47 Zaburi 22:1-32; Isaya 53:1-12;

Mika 5:1-3;

YOHANA

1:1 Mwanzo 1:1; Mithali 8:22-31

1:3 Isaya 45:12,18

1:10 Mwanzo 11:6-7

1:14 Zaburi 45:3; Isaya 7:14; Isaya 60:1,2

1:15 Mithali 8:22; Isaya 9:5

1:18 Kutoka 33:20-23; Yoshua 5:13-15;

Mithali 8:30

1:19 Mambo ya Walawi 16:21,22;

Isaya 53:11

1:23 Isaya 40:3

1:45 Kumbukumbu la Torati 18:1518;

Isaya 4:2;

Mika 5:1; Zekaria 6:12

1:51 Danieli 7:9-14

2:17 Zaburi 69:10

3:14 Hesabu 21:9

3:17 Isaya 53:10-12

3:35 Mithali 8:30; Isaya 42:1

3:36 Zaburi 2:12; Habakuk 2;4

4:23 Isaya 58:9,10

4:24 Isaya 57:15; Isaya 58:9,10

5:10 Isaya 58:13; Yeremia 17:21,27

5:19 Mwanzo 1:26

5:20 Mithali 8:22-31

5:37 Kutoka 20:19;

Kumbukumbu la Torati 4:12

5:46 Kumbukumbu la Torati 18:15,18,19

6:14 Kumbukumbu la Torati 18:15-18

YOHANA

6:31,35 Zaburi 78:24,25; Kutoka 16:4,8,15;

Hesabu 11:69

6:39 Hesabu 26:65

6:45 Isaya 54:13; Yeremia 31:33,34

7:2 Kumbukumbu la Torati 16:13-16;

Zekaria 14:16-19

7:3 Yeremia 12:6

7:6 Zaburi 102:14; Mhubiri 3:1

7:7 Mithali 8:36; Isaya 49:7; Zekaria 11:8

7:10 Zaburi 40:9; Isaya 42:2,3

7:15 Amosi 7:15

7:17 Zaburi 25:8,9,12

7:22 Mwanzo 17:10-14

7:24 Kumbukumbu la Torati 1:16,17,19

7:38 Kumbukumbu la Torati 18:15

7:41,42 Mika 5:1

7:51 Kumbukumbu la Torati 17:8-11;

Kumbukumbu la Torati 19:15-19

8:5 Mambo ya Walawi 20:10

8:7 Kumbukumbu la Torati 17:6;

Zaburi 50:16-20; Yeremia 17:13

8:12 Isaya 9:1; Isaya 49:6; Isaya 60:1-3

8:16 Zaburi 98:9; Yeremia 23:5,6

8:17 Kumbukumbu la Torati 19:15

8:28 Kumbukumbu la Torati 18:18

8:42 Kumbukumbu la Torati 18:18

8:44 Mwanzo 3:3-7

8:56 Mwanzo 22:18

9:5 Isaya 42:6,7; Isaya 49:6

10:9 Zaburi 23:1-6; Ezekieli 34:12-16

10:11 Isaya 40:11; Ezekieli 37:24;

Mika 5:3

10:12 Isaya 56:10-12; Ezekieli 34:2-6

10:16 Mwanzo 49:10; Zekaria 8:20-23

10:30 Zekaria 14:9

10:34 Zaburi 82:6

12:13 Zaburi 118:25,26; Sefania 3:15

12:15 Isaya 62:11; Sefania 3:16,17;

Zekaria 2:9-11

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 401: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

401

YOHANA

12:37,38 Isaya 53:1

12:40 Isaya 6:10; Isaya 29:10

12:46 Isaya 42:6,7; Malaki 4:2

12:49 Kumbukumbu la Torati 18:18

13:18 Zaburi 41:10

13:21,26 Zaburi 41:10

14:21 Kumbukumbu la Torati 30:6-8;

Yeremia 31:31-34

14:31 Zaburi 40:9

15:25 Zaburi 35:19; Zaburi 69:5;

Zaburi 109:3

16:32 Zekaria 13:7

16:33 Zaburi 68:19; Zaburi 85:9-12;

Isaya 9:5,6

17:12 Zaburi 109:6-8

18:22 Isaya 50:6; Mika 4:14

19:23,24 Zaburi 22:19

19:28,29 Zaburi 22:16; Zaburi 69:22

19:36 Kutoka 12:46; Zaburi 34:21

19:37 Zekaria 12:10

20:19 Mambo ya Walawi 16:28

MATENDO YA MITUME

1:5 Yoeli 2:28,29; Isaya 44:3

1:8 Zaburi 22:28; Isaya 2:3

1:16 Zaburi 41:10; Zaburi 55:13-15

1:20 Zaburi 69:26; Zaburi 109:8

2:17-21 Yoeli 2:28-32

2:25-28 Zaburi 16:8-11

MATENDO YA MITUME

2:31 Zaburi 16:10

2:34,35 Zaburi 110:1

2:39 Yoeli 2:28

3:18 Isaya 50:6; Isaya 53:1-12

3:22,23 Kumbukumbu la Torati 18:1519

3:25 Mwanzo 22:18

4:11 Zaburi 118:22; Isaya 28:16

4:25,26 Zaburi 2:1,2

MATENDO YA MITUME

5:38 Mithali 21:30; Maombolezo 3:37

6:3 Kumbukumbu la Torati 1:13

7:2,3 Mwanzo 12:1

7:5 Mwanzo 12:7; Mwanzo 13:15

7:6 Mwanzo 15:13,16

7:7 Mwanzo 15:14-16; Kutoka 7:1-14

7:8 Mwanzo 17:9-14; Mwanzo 21:2;

Mwanzo 25:24

7:9 Mwanzo 37:4-11,18-29;

Mwanzo 39:21-23

7:10 Mwanzo 41:12-46

7:11 Mwanzo 41:54-57

7:12 Mwanzo 42:1

7:13 Mwanzo 45:4

7:14 Mwanzo 45:9-11

7:15 Mwanzo 46:3-7; Mwanzo 49:33

7:16 Mwanzo 49:29-32; Kutoka 13:19;

Yoshua 24:32

7:17-45 Kutoka 1-40

7:44 Kutoka 38:21

7:45 Yoshua 3:11-14

7:46 1 Wafalme 8:17-19; Zaburi 132:1-5

7:47 1 Wafalme 6:1;

2 Mambo ya Nyakati 2:1-4:22

7:48 1 Wafalme 8:27

7:49 Isaya 66:1; Yeremia 7:4-11

7:50 Mwanzo 1:4; Kutoka 20:11

7:51 Kutoka 32:9;

Kumbukumbu la Torati 10:16;

Isaya 63:10

7:53 Kumbukumbu la Torati 33:2;

Kutoka 19:3

8:32,33 Isaya 53:7,8

10:14 Mambo ya Walawi 11:1-17;

Mambo ya Walawi 20:25

10:35 Isaya 56:3-8

13:17 Mwanzo 12:1-3; Kutoka 1:7-9;

Kutoka 6:1

13:18 Kutoka 16:35; Zaburi 78:17-42

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 402: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

402

MATENDO YA MITUME

13:19 Kumbukumbu la Torati 7:1; Y

oshua 24:11; Zaburi 78:55

13:20 Waamuzi 2:16; Waamuzi 3:9,10;

1 Samweli 3:20

13:21 1 Samweli 8:5,6; 1 Samweli 10:1

13:22 1 Samweli 15:11; 1 Samweli 16:12,13

13:32 Mwanzo 3:15; Danieli 9:24,25

13:33 Zaburi 2:7

13:34 Zaburi 89:3-5,20-38; Isaya 55:3

13:35 1 Mambo ya Nyakati 17:11;

Zaburi 16:10

13:41 Isaya 28:14; Habakuki 1:5

13:47 Isaya 42:6; Isaya 49:6

14:15 Mwanzo 1:1; Zaburi 33:6;

Zaburi 124:8

14:16 Zaburi 81:13

14:17 Zaburi 65:10-14; Yeremia 5:24;

Yeremia 14:22

15:15,16 Amosi 9:11,12

15:17 Zaburi 22:27,28; Isaya 65:1

15:18 Isaya 46:9,10

15:29 Mambo ya Walawi 17:14

17:24 Isaya 45:18; Isaya 66:1; Danieli 4:25

17:25 Mwanzo 2:7; Isaya 42:5;

Zaburi 50:8-13

17:26 Mwanzo 3:20;

Kumbukumbu la Torati 32:8

17:27 Yeremia 23:23,24

17:28 Ayubu 12:10; Zaburi 79:13

17:29 Isaya 44:9-20; Habakuki 2:19,20

17:31 Zaburi 96:13

23:5 Kutoka 22:28

26:6 Mwanzo 3:15; Malaki 4:2

28:26 Isaya 6:9,10; Ezekieli 12:2

28:27 Isaya 29:10; Isaya 66:4

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 403: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

403

Nukuu na vionyeshi vya Biblia ya Kiebrania

kwenye nyaraka za Paulo.

WARUMI

1:17 Habakuki 2:4

2:6 Zaburi 62:13

2:11 Kumbukumbu la Torati 10:17

2:13 Kumbukumbu la Torati 6:3

2:16 Zaburi 96:13

2:18 Nehemia 9:14

2:24 Isaya 52:5

2:28,29 Kumbukumbu la Torati 30:6

3:4 Zaburi 51:6

3:10-12 Zaburi 14:1-3; 53:1-4

3:13A Zaburi 5:10

3:13B Zaburi 140:3; Zaburi 5:10

3:14 Zaburi 10:7

3:15-17 Isaya 59:7-8

3:18 Zaburi 36:2

4:3 Mwanzo 15:6

4:7-8 Zaburi 32:1-2

4:17 Mwanzo 17:5

4:18 Mwanzo 15:5

7:7 Kutoka 20:17;

Kumbukumbu la Torati 5:21

8:36 Zaburi 44:23

9:7 Mwanzo 21:12

9:9 Mwanzo 18:10,14

9:12 Mwanzo 25:23

9:13 Malaki 1:2,3

9:15 Kutoka 33:19

9:17 Kutoka 9:16

9:25 Hosea 2:23

9:26 Hosea 1:10; 2:1

9:27-28 Isaya 10:22; Hosea 1:10

9:29 Isaya 1:9

9:33 Isaya 8:14; 28:16

10:5 Mambo ya Walawi 18:5

10:6-8 Kumbukumbu la Torati 30:12-14

10:11 Isaya 49:23

WARUMI

10:13 Yoeli 2:32; 3:5

10:15 Isaya 52:7

10:16 Isaya 53:1

10:18 Zaburi 19:5

10:19 Kumbukumbu la Torati 32:21

10:20-21 Isaya 65:1-2

11:3 1 Wafalme 19:10

11:4 1 Wafalme 19:18

11:8 Kumbukumbu la Torati 29:4

11:9-10 Zaburi 69:23-24

11:26-27 Isaya 59:20,21

11:27B Yeremia 31:31-34

11:34 Isaya 40:13

11:35 Ayubu 41:11

12:19 Kumbukumbu la Torati 32:35

12:20 Mithali 25:21-22

13:9A Kumbukumbu la Torati 5:17-21

13:9B Mambo ya Walawi 19:18

14:11 Isaya 45:23

15:3 Zaburi 69:10

15:9 Zaburi 18:50

15:10 Kumbukumbu la Torati 32:43

15:11 Zaburi 117:1

15:12 Isaya 11:10

15:21 Isaya 52:15

1 WAKORINTHO

1:19 Isaya 29:14

1:31 Yeremia 9:23,24

2:16 Isaya 40:13

3:19 Ayubu 5:13

3:20 Zaburi 94:11

5:13 Kumbukumbu la Torati 17:7

6:16 Mwanzo 2:24

9:9 Kumbukumbu la Torati 25:4

10:7 Kutoka 32:6

10:26 Zaburi 24:1; 50:12

14:21 Isaya 28:11-12

15:27 Zaburi 8:7

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 404: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

404

1 WAKORINTHO

5:32 Isaya 22:13

15:45 Mwanzo 2:7

15:54 Isaya 25:8

15:55 Hosea 13:14

2 WAKORINTHO

3:16 Hosea 3:4,5

4:13 Zaburi 116:10

6:2 Isaya 49:8

6:16 Mambo ya Walawi 26:12

6:17 Isaya 52:11

6:18 2 Samweli 7:14

8:15 Kutoka 16:18

9:7 Kumbukumbu la Torati 15:4

9:9 Zaburi 112:9

10:17 Yeremia 9:24

13:1 Kumbukumbu la Torati 19:15

WAGALATIA

3:6 Mwanzo 15:6

3:8 Mwanzo 12:3; 18:18

3:10 Kumbukumbu la Torati 27:26

3:11 Habakuki 2:4

3:12 Mambo ya Walawi 18:5

3:13 Kumbukumbu la Torati 21:23

3:16 Mwanzo 13:15; 17:7; 22:18

4:27 Isaya 54:1

4:30 Mwanzo 21:10

5:14 Mambo ya Walawi 19:18

WAEFESO

4:8 Zaburi 68:19

5:31 Mwanzo 2:24

6:2,3 Kutoka 20:12;

Kumbukumbu la Torati 5:16

1 WATHESALONIKE

4:16,17 Isaya 57:1,2

1 TIMOTHEO

5:18 Kumbukumbu la Torati 24:14,15; 25:4

2 TIMOTHEO

2:19 Zaburi 1:6; Nahumu 1:7

2:19 Zaburi 34:15

WAEBRANIA

1:1 Kumbukumbu la Torati 18:15;

Hesabu 12:6-8

1:2 Zaburi 2:6-9;

Mithali 8:22-31

1:4 Zaburi 2:7,8; Isaya 9:6

1:5 Zaburi 2:7; Zaburi 89:27,28

1:6 Zaburi 97:7; Mithali 8:24,25

1:7 Zaburi 104:4

1:8 Zaburi 45:7,8; Zaburi 145:13;

Isaya 9:6

1:9 Zaburi 45:8; Zaburi 89:21;

Isaya 61:1

1:10 Zaburi 102:26-28

1:11 Isaya 50:9; Isaya 51:6,8

1:12 Zaburi 102:27,28

1:13 Zaburi 110:1

1:14 Zaburi 103:20,21; Danieli 7:10

2:2 Mambo ya Walawi 24:14-16

2:6 Zaburi 8:6,7; Ayubu 7:17,18

2:8 Zaburi 8:7; Danieli 7:14

2:12 Zaburi 22:23,26

2:13 Zaburi 16:1; Isaya 8:18;

Isaya 12:2

2:14 Isaya 25:8; Hosea 13:14

2:15 Zaburi 56:14

2:16 Mwanzo 22:18

3:2 Hesabu 12:7

3:3 Zekaria 6:13

3:5 Kumbukumbu la Torati 18:15-19

3:8 Kutoka 17:7; Zaburi 106:14

3:9 Kumbukumbu la Torati 4:9;

Hesabu 14:33; Yoshua 23:3;

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 405: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

405

WAEBRANIA

3:10 2 Wafalme 21:9; Isaya 63:17

3:11 Kumbukumbu la Torati 1:34,35;

Hesabu 32:10-13

3:15 Kumbukumbu la Torati 10:16

3:17 Hesabu 26:64,65

3:18 Kumbukumbu la Torati 1:34,35

4:3 Zaburi 95:11

4:4 Mwanzo 2:2

4:5 Zaburi 95:11

4:7 Zaburi 95:7,8

4:9 Isaya 11:10

4:12 Mhubiri 12:11; Isaya 49:2;

Yeremia 17:10

4:13 Zaburi 33:13-15; Zaburi 90:8

5:3 Mambo ya Walawi 9:7;

Mambo ya Walawi 16:6

5:4 Kutoka 28:1

5:5 Zaburi 2:7

5:6 Zaburi 110:4

6:13 Mwanzo 22:15-18

6:14 Mwanzo 12:3; Mwanzo 22:17

6:15 Mwanzo 15:2-6

6:16 Kutoka 22:11

6:17 Mithali 19:21; Zaburi 33:11

7:1 Mwanzo 14:18-20

7:2 Mwanzo 28:22;

Mambo ya Walawi 27:32

7:3 Mwanzo 14:18-20; Zaburi 110:4

7:4 Mwanzo 14:20

7:5 Hesabu 18:21-26

7:6 Mwanzo 14:19,20

7:9 Mwanzo 14:20

7:12 Yeremia 31:31-34

7:14 Mwanzo 49:10; Isaya 11:1

7:17 Zaburi 110:4

7:21 Zaburi 110:4

8:5 Kutoka 25:40; Kutoka 26:30

8:8 Yeremia 31:31-34; Ezekieli 37:26

8:9 Kutoka 34:10,28; Isaya 63:11-13;

WAEBRANIA

Yeremia 31:32

8:10 Yeremia 31:33; Ezekieli 36:26,27

8:11 Yeremia 31:34

8:12 Yeremia 33:8; Yeremia 50:20;

Mika 7:19

9:2 Kutoka 25:23,30; Kutoka 40:4;

Mambo ya Walawi 24:5,6

9:3 Kutoka 26:31-33;

1 Wafalme 8:6

9:4 Kutoka 16:33; Hesabu 17:8-10;

Kumbukumbu la Torati 10:2-5;

9:5 Kutoka 25:17-22

9:6 Kutoka 27:21; Kutoka 30:7,8

9:7 Kutoka 30:10;

Mambo ya Walawi 16:2-20,34

9:8 Isaya 63:11

9:9 Zaburi 40:7,8; Zaburi 51:18-21

9:10 Kutoka 30:19-21;

Mambo ya Walawi 11:2;

Kumbukumbu la Torati 14:3-21;

9:13 Mambo ya Walawi 16:14-16;

Hesabu 19:2-21

9:19 Kutoka 12:22; Kutoka 24:8;

Mambo ya Walawi 16:14-18

9:20 Kumbukumbu la Torati 29:12

9:21 Kutoka 29:12,20,36

9:22 Mambo ya Walawi 4:20,26,35;

Mambo ya Walawi 5:10,12,18;

Mambo ya Walawi 17:11

9:25 Kutoka 30:10;

Mambo ya Walawi 16:2-34

10:4 Zaburi 51:18; Isaya 1:11-15;

Hosea 6:6

10:5 Zaburi 40:7-9; Yeremia 6:20;

Amosi 5:21,22

10:6 Malaki 1:10

10:7 Mwanzo 3:15; Zaburi 40:8

10:9 Zaburi 40:8; Malaki 1:10

10:11 Zaburi 50:8-13; Isaya 1:11

10:12,13 Zaburi 110:1

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 406: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

406

WAEBRANIA

10:16 Yeremia 31:33,34

10:22 Ezekieli 36:25

10:26 Hesabu 15:28-31

10:27 Zaburi 21:10; Yeremia 4:4

10:28 Hesabu 15:30,31,36;

Kumbukumbu la Torati 13:6-10

10:29 Kumbukumbu la Torati 32:35,36;

Zaburi 98:9

10:31 Zaburi 90:11; Isaya 33:14

10:37 Habakuki 2:3; Ezekieli 18:24

10:38 Habakuki 2:4

11:3 Mwanzo 1:1; Zaburi 33:6

11:4 Mwanzo 4:3-5

11:5 Mwanzo 5:22-24

11:6 Isaya 55:3

11:7 Mwanzo 6:13,22; Mwanzo 7:1,5

11:8 Mwanzo 12:1-4; Mwanzo 15:5;

Mwanzo 22:18

11:9 Mwanzo 13:8; Mwanzo 17:8;

Mwanzo 26:3

11:11 Mwanzo 17:17-19; Mwanzo 18:11-14;

Mwanzo 21:1,2

11:12 Mwanzo 22:17

11:13 Mwanzo 23:4; Mwanzo 49:10;

Zaburi 39:12

11:15 Mwanzo 11:31; Mwanzo 24:6-8

11:16 Mwanzo 17:7,8; Isaya 41:8-10

11:17 Mwanzo 22:1-12

11:18 Mwanzo 17:19; Mwanzo 22:12

11:20 Mwanzo 27:27-40

11:21 Mwanzo 47:31; Mwanzo 48:5-22

11:22 Mwanzo 50:24,25; Kutoka 13:19

11:23 Kutoka 2:2

11:24-27 Kutoka 2:10-15

11:28 Kutoka 12:3-14; Kutoka 12:21-30

11:29 Kutoka 14:13-31

11:30 Yoshua 6:3-20

11:31 Yoshua 2:1-22; Yoshua 6:22-25

11:32 Waamuzi 4:6; Waamuzi 6:11;

WAEBRANIA

Waamuzi 11:1; Waamuzi 12:7

11:33 Zaburi 44:3-7

11:34 1 Samweli 17:51:52;

2 Samweli 21:16,17;

2 Wafalme 6:16-18;

11:34 Waamuzi 8:4-10;

Waamuzi 15:14-20;

Ayubu 42:10;

11:35 1 Wafalme 17:22-24;

2 Wafalme 4:27-37

11:36 Waamuzi 16:25; Yeremia 20:7

11:37 1 Samweli 22:17-19; 2 Wafalme 1:8;

Yeremia 2:30

11:38 1 Samweli 23:15; 1 Wafalme 17:3

12:5 Ayubu 5:17; Mithali 3:11

12:6 Kumbukumbu la Torati 8:5;

Mithali 3:12

12:12 Isaya 35:3

12:13 Mithali 4:26,27; Isaya 35:6

12:16 Mwanzo 25:31-34

12:17 Mwanzo 27:31-41

12:18 Kutoka 19:10-19; Kutoka 20:18;

Kutoka 24:17;

Kumbukumbu la Torati 5:22-26

12:19 Kutoka 19:16-19; Kutoka 20:18,19;

Kumbukumbu la Torati 5:24-27;

Kumbukumbu la Torati 18:16

12:20 Kutoka 19:13,16

12:21 Kutoka 19:16,19; Isaya 6:3-5

12:24 Mwanzo 4:10

12:26 Kutoka 19:18; Isaya 2:19;

Isaya 13:13

12:29 Kutoka 24:17;

Kumbukumbu la Torati 4:24

13:5 Mwanzo 28:15;

Kumbukumbu la Torati 31:6,8;

Zaburi 119:36

13:6 Zaburi 56:12; Zaburi 118:6

13:10 Hesabu 7:5

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 407: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

407

13:11 Kutoka 29:14;

Mambo ya Walawi 4:16-21

13:15 Zaburi 116:17-19; Hosea 14:2

13:20 Isaya 40:11; Ezekieli 34:23

MAREJELEO YA BIBLIA YA KIEBRANIA (AGANO LA KALE)

Page 408: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

408

Page 409: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

409

Lugha ya Kiingereza

Abram Kenneth Abraham, Promises of the

Messiah, New Testament Fulfilment of Old

Testament Prophecies, 1987 Barbour and

Company, USA.

Bibleworks, 2001, LLC. Hermeneutika

Computer Bible Research Software,

Bigfork,USA.

Briggs, Charles A., Messianic prophecy, 1988,

Hendrickson Publishers, Peabody, MA.

Delitzsch, Franz, Messianic prophecies in

historical succession, 1998, WIPP & Stock

Publishers, Eugene, OH.

Dewart, Edwart Hartley, Jesus the Messiah in

prophecy and fulfilment, 1891, Cranston &

Stowe, Cincinnati, OH.

Fruchtenbaum, Arnold G., Messianic

Christology, 1998, Manna Books, UK.

Fruchtenbaum, Arnold G., The Feasts of

Israel, 1993 Ariel Ministries, Manna Books,

UK.

Fryland, Rachmiel, What the Rabbies know

about the Messiah, 1993, Messianic

Publishing Company, Columbus, MD.

Henry, Matthew, Commentary of the whole

Bible, 1991, Henrickson Publishers,

Peabody, MA.

Hengstenberg, W.E., Christology of the Old

Testament, 1970, Kregel Publications,

Grand Rapids, MI.

Kaiser, Walter C., The Messiah in the Old

Testament, 1995, Zondervan Publishing

House, Grand Rapids, MI.

Klingerman, Aaron J., Messianic prophecy

in the Old Testament, 1957, Zondervan

Publishing House, Grand Rapids, MI.

Locklyer, Herbert, All the Messianic

Prophesies of the Bible, 1973, Zondervan

Publishing House, Grand Rapids, MI.

Meldau, Fred John, The Messiah in Both

Testaments, 1967, The Christian Victory

Publishing Company, Denver, USA

Payne, Barton J., Encyclopedia of Biblical

Prophecy, 1973, Baker Books, Grand

Rapids, MI.

Reich, Max I. The Messianic Hope of

Israel, 1940, W.M. Eerdmans Publishing

Company, Grand Rapids, MI.

Santala, Risto, The Messiah in the Old

Testament, 1992, Keren Ahvat Meshhit,

Jerusalem.

Smith, James, What the Bible teaches about

the promised Messiah, 1993, Thomas

Nelson Publishers, Nashville, TN.

Spurgeon, C.H., Christ in the Old Testament,

1994, AMG Publishers, Chattanooga, TN.

Stern, David H. Jewish New Testament

Commentary, 1992, Jewish New Testament

Publications, Clarksville, MD.

BIBLIOGRAFIA

Page 410: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

410

Lugha ya Kiholanzi

Ambrosius, Isaäc, Het zien op Jezus, 1984,

Den Hertog, Houten

à Brakel, Wilhelmus, Redelijke Godsdienst, 7e

druk, De Banier, Utrecht.

Bunyan, John, Al de werken, deel I, 1967,

Den Hertog B.V.

Calvijn, J., Institutie of onderwijzing in de

christelijke godsdienst, Uit het Latijn

vertaald door A. Sizoo.

Calvijn, J., Uitlegging op de Profetieën van de

Profeten Isaya en Jeremia, deel I, 1900,

Ten Bokkel Huinink, Utrecht.

van Campen, M., Leven uit Gods beloften,

1988

De Groot Goudriaan,Kampen

van Campen, M., “Brede aandacht voor de

Joden in Nederland tijdens de zeventiende

en achttiende eeuw", 2007, in Profetisch

Perspectief.

Edelkoort, A.H., De Christus-verwachting in

het Oude Testament, 1941, H. Veenman &

Zn.

Klein Haneveld, Jb., God’s feestkalender

voor Israël, 1975, Brochure Morgenrood,

Bodegraven

Klein Haneveld, Jb., De Messias in het oude

en nieuwe testament, vrije bewerking naar

Fred John Meldau, St. Israël en de Bijbel,

Harmelen.

Haverkamp, B., De tent onder de wolk, 1963,

De Banier, Utrecht.

De Heer, Joh., Het duizend jarig Vrederijk,

1939, Zoeklicht Boekhandel, Rotterdam.

Hoek, J., Hoop op God: Eschatologische

verwachting, 2004, Boekencentrum

Zoetermeer.

van Kooten, R., Verzoend door Christus, 1996,

Uitg. J. J. Groen en Zn., Leiden

van Kooten, R., Meer kennis van Christus,

1995, Uitg. J. J. Groen en Zn., Leiden

Koekoek, H. G., De geheimen van de Offers,

Uitg. Het Licht des Levens, Alphen a/d

Rijn.

Mackintosh, C.H., Aantekeningen op Mambo

ya Walawi,

Uit het Woord der Waarheid, Winschoten.

van Nieuwpoort, A., Tenach opnieuw, 2006,

Van Gennep, Amsterdam.

Spurgeon, C.H., De Zaburien Davids, 5e

druk, D.Los, Amsterdam

Stier, A.B., Warumi IX-XI.

Verduin, M., Canticum Canticorum: Het Lied

der liederen.

Vreekamp, H., Zonder Israël niet volgroeid,

1988, J.H. Kok, Kampen.

de Vries, P., Het Lam overwint, 2003, Groen,

Heerenveen.

van de Weerd, Gert A., De Profeet Ezekieli,

Bijbelverklaring, deel 1, 2006, PMI,

Veenendaal.

van de Weerd, Gert A., De Profeet Danieli,

Bijbelverklaring, deel 1 & 2, 2000, PMI,

Veenendaal.

van de Weerd, Gert A., De Profeet Mika,

Bijbelverklaring, 2001, PMI, Veenendaal.

van de Weerd, Gert A., De Profeet Hosea,

Bijbelverklaring, 2007, PMI, Veenendaal.

van de Weerd, Gert A., De Profeet Zacharia,

Bijbelverklaring, 1999, PMI, Veenendaal.

BIBLIOGRAFIA

Page 411: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

411

Page 412: Masiha - Messiah...Kitabu kinahusu Neno la Mungu aliye hai. Kupitia kwa Neno hili, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu, unaweza kujifunza Mungu ni Nani na Mwanawe ni Nani. Nabii Hosea anasema

412