yesu upendo unyenyekevu kujishusha kujitoa upendo neno la kiyunani ágape linatumika katika agano la...

8

Upload: others

Post on 17-May-2020

23 views

Category:

Documents


5 download

TRANSCRIPT

Yesu Upendo Unyenyekevu Kujishusha Kujitoa

Kudumisha umoja katika familia kunahitaji juhudi za kila mwanafamilia.

Familia itakuwa na umoja imara kama kila mwanafamilia atakuwa na funguo zifuatazo:

“Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.” (Wagalatia 3:28)

Kuishi katika Kristo huleta mabadiliko ya kimwili katika maisha yetu (Warumi 6:22; 2 Wakorintho 5:17).

Msalaba wa Kristo huondoa mipaka yote inayotenga watu.

YESU

Kwa kadri tunavyoishi karibu na Yesu, ndivyo tunavyokuwa karibu na wengine.

Hii ni kweli pia kwa ngazi ya familia.

Yesu anapokuwa kiini cha kila moyo wa mwanafamilia, kuna kuwa umoja kati ya mume na mke, kati ya wazazi na Watoto, kati ya kaka na dada…

UPENDO

Neno la kiyunani ágape linatumika katika agano la jipya kwa ajili ya upendo wa Mungu na upendo tunaopaswa kuonesha.

Aina hii ya upendo ni Zaidi ya upendo wa kimili. Ni kipawa cha Roho Mtakatifu. (Warumi 5:5).

• Huvumilia na hufadhili ____ • hauhusudu ____ • hautakabari ____ • haujivuni ____ • haukosi kuwa na adabu ____ • hautafuti mambo yake ____ • hauoni uchungu ____ • hauhesabu mabaya ____ • haufurahii udhalimu ____ • bali hufurahi a kweli ____ • huvumilia yote ____ • huamini yote ____ • hutumaini yote ____ • hustahimili yote ____

Andika jina lako

pembeni ya sentensi

zinazofanana na ukweli maishani

mwako leo:

Hebu linganisha tabia yako na maana ya upendo wa ágape katika 1 Wakorintho 13:4-7. Je; Ni mabadiliko gani unaweza kufanya maishani?

UNYENYEKEVU

Kwa sababu ya Dhambi, ubinafsi umekuwa sehemu inayorithiwa ya ubinadamu.

“Kama majivuno na ubinafsi vingewekwa

kando, dakika tano zingeondoa hata

yaliyo magumu zaidi.”

(Ellen G. White, Early Writings, p. 119)

Paulo anatuhimiza kuiga mfano wa unyenyekevu wa Kristo (fg. 4-8).

Tunaweza kuufikia unyenyekevu wa kweli tu kama tutapiga magoti miguuni pa msalaba.

KUJISHUSHA Wale wanaompenda Mungu wameitwa kujishusha kila mmoja kwa mwenzake. Paulo anatoa mifano mitatu ya kujishusha:

Kwanza, kujishusha katika Kristo kuna pande mbili. Pili, kuna masharti katika mifano ya awali ya kujishusha:

Mambo haya tayari yalikuwa yakitegemewa katika jamii. sasa, kwa nini ushauri wa Paulo uwe mpya? Tunawezaje kuubeba katika jamii yetu leo?

Waume wajishushe kwa Kristo

• Waefeso 5:25-33

Wazazi wasiwachokoze watoto

• Waefeso 6:4

Mabwana wasiogofye

• Waefeso 6:9

Wake wajishushe kwa waume zao

• Waefeso 5:22

Watoto wajishushe kwa wazazi wao

• Waefeso 6:1 Watumwa wajishushe kwa Mabwana zao

• Waefeso 6:5

KUJITOA “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.” (Mwanzo 2:24)

Kila familia ilianza kwa kujitoa.

Kujitoa huku huenea kwa familia yote:

Kukosa kujitoa husababisha matatizo na mgawanyiko (Tazama kisa na Yusufu na ndugu zake).

Kujitoa kuliko imara hujenga muunganiko wa familia ulio imara na wakudumu (Tazama kisa cha Naomi na Ruthu).