mct yatahadharisha kuhusu rushwa uchaguzi mkuu · licha ya maadili ya taaluma ya uandishi wa...

18
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 155, Julai, 2020 ISSN 0856-874X Runinga ya Kwanza yafungiwa JOWUTA yakubaliwa uanachama wa IFJ Tido Mhando mwanahabari nguli Uk 7 Uk 11 Uk 9 MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu

Upload: others

Post on 16-Sep-2020

31 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 155, Julai, 2020ISSN 0856-874X

Runinga ya Kwanza yafungiwa

JOWUTA yakubaliwa uanachama wa IFJ

Tido Mhando mwanahabari nguli

Uk 7 Uk 11Uk 9

MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu

Page 2: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Vyombo vya habari vikatae rushwa katakata katika Uchaguzi MkuuNi wakati wa uchaguzi. Tume ya taifa ya

Uchaguzi imetangaza Oktoba 28 kuwa siku ya kupiga kura kumchagua Rais, wabunge na madiwani.

Kati ya sasa na siku ya kupiga kura, vyombo vya habari vitakuwa na kazi kubwa ya kuripoti kuhusu kampeni za wagombea na vyama mbalimbali vinavyowania nyadhifa hizo za uwakilishi na uongozi.

Ni jukumu hili muhimu la vyombo vya habari ambalo linabidi lifuatiliwe na kuangaliwa kwa umakini bila ya kuwa na upendeleo hata chembe.

Uchaguzi Mkuu nchini mwetu hufanyika kila baada ya miaka mitano. Hili ni zoezi muhimu la kidemokrasia linalowapa raia fursa ya kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua wawakilishi ambao watasimamia maslahi yao ya maendeleo binafsi na hata ya nchi kwa jumla.

Wajibu wa vyombo vya habari ni muhimu kuhakikisha watu wanapewa taarifa za kutosha kuhusu wagombea wa vyama mbalimbali na ahadi wanazotoa wakati wa kampeni.

Ni muhimu vyombo vya habari vikaandika na kuchambua masuala yanayoibuliwa wakati wa kampeni na kuanagalia kama yamo kwenye ilani za vyama vya uchaguzi vinavyoshiriki uchaguz huo.

Umakini ni muhimu kwa vyombo vya habari, kuhakikisha kuwa wapiga kura hawadanganywi na wagombea watakaotoa ahadi nzuri lakini hazitekelezeki.

Rushwa katika aina mbalimbali – iwe fedha, zawadi na upendeleo isikikubalike wakati wa kampeni na siku ya kupiga kura kwa kuwa inaathiri umakini na kushawishi kuwepo upendeleo.

Vyombo vya habari vijitahidi kutoa nafasi sawa kwa vyama na wagombea wote katika uchaguzi.

Dhamira na lengo kuu iwe kuhakikisha uchaguzi unakamilika kwa mafanikio na kwamba vyama vyote na wagombea wataridhika na matokeo.

Hali hiyo itawezekana tu ikiwa rushwa itapigwa vita kikamilifu na wanahabari wakatae kutumiwa. Wawe makini na macho dhidi ya vichocheo na vishawishi vyovyote vya rushwa.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Waandishi wa habari wakiwa kazini katika chumba cha habari

Page 3: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 155, Julai, 2020

Na Mwandishi wa Barazani

Wakati mchakato wa Ucha-guzi Mkuu nchini una-shika kasi, Baraza la Habari Tanzania lime-

tahadharisha wanahabari na vyombo vya habari kuwa makini na rushwa.

Uchaguzi Mkuu wa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani utafanyika Oktoba.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa imetangaza kuwa uchaguzi utafanyika Oktoba 28, uteuzi wa

wagombea utafanyika Agosti 25 na kampeni zitaaanza Agosti 26 hadi Oktoba 27, 2020.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga, alizungumzia kifungu 1.6 cha Maadili ya Wanahabari ambacho kinahusu kukabiliana na rushwa, zawadi na fadhila ama viburudisho.

Kifungu hicho kinahimiza wakuu wa vyombo vya habari kwamba iwapo zawadi zitatolewa, wapokeaji lazima wawaarifu wakuu wao wa kazi kuhusu zawadi na upendeleo wa aina yoyote watakaopewa.

Kuhusu fadhila, wakuu wa vyombo vya habari na wahariri wanazuiwa

kupokea upendeleo aina yoyote ambao unaweza kuathiri maamuzi yao ya uhariri. Pia wasitumie nyadhifa zao ama fursa kujinufaisha.

Kifungu hicho pia kinawatadharisha wakuu wa vyombo vya habari dhidi ya kununua habari ama kulipa vyanzo vya habari kutoa taarifa, kikionyesha kwamba hiyo ni sawa na kufanya habari kuwa bidhaa ya biashara jambo lisilokubalika.

Pia wakuu wa vyombo vya habari na wahariri wasipokee fedha ama aina yoyote ya malipo kuwachagiza kuchapisha au kutangaza habari.

Baraza pia limewataka wakuu wa vyombo vya habari, wahariri na waandishi kuhakikisha wanazingatia maadili ya taaluma ambazo wanahabari wamejiwekea wenyewe.

Baraza limetoa taarifa hiyo kufuatia kukamatwa kwa mhariri mmoja wa gazeti la Serikali la Kiswahili kwa madai ya rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Baraza limesema limepokea taarifa hizo kwa mshangao hasa kwa kuzingatia kuwa mtuhumiwa ni viongozi wakuu wa vyumba vya habari ambao wanatakiwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Kama tukio hilo ni la kweli, Baraza linalaani vikali, taarifa imeeleza na kuwataka wahariri wa vyombo vya habari kuzingatia

MCT yatahadharisha vyombo vya habari kuhusu rushwa katika Uchaguzi Mkuu

Endelea Ukurasa wa 4

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Page 4: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

maadili ya taaluma ya habari. Mhariri ni kiongozi wa chombo cha

habari ambaye anatakiwa kuzingatia maadili ya Uandishi. Inasikitisha kama mhariri hazingatii maadili na fedheha kwa tasnia. Baraza linatumaini kwamba mhariri huyo ataonekana kutohusika na tuhuma hizo na kuendelea na majukumu yake.

Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi.

Jaribio kubwa la kiitaaluma na maadili kwa vyombo vya habari, kanuni za uandishi wa habari za uchaguzi zimeeleza katika dibaji yake, ni jinsi vilivyoshughulikia mabadiliko ya kisiasa kama

yanavyotakiwa na uchaguzi. Kanuni hizo, imeelezwa

zimeandaliwa kuhakikisha vyombo vya habari havichukui upande wowote na kutoa habari za uhakika wakati wa uchaguzi kwa kuegemea ukweli, usahihi, na haki.

Zinalenga kuwapa taarifa na uwezo wa kuhoji kuthibitisha habari zao na pia kutoa nafasi kwa wapiga kura kutoa maoni yao.

Baraza linahimiza kanuni za maadili zisomwe pamoja na Kanuni za Maadili za Taaluma ya Unadishi wa habari.

Imeelezwa kwenye utangulizi kwamba uchaguzi mara nyingi huibua wanasiasa na wanahabari wabaya – maoni mabaya, ahadi zisizotekelezeka na hotuba za ubabaishaji na kwamba wanahabari na waandishi lazima wawe makini na

hotuba za kuhamasisha chuki, ghasia na maoni makali katika uandishi wao.

“Kulinda amani ni kazi ya polisi, lakini waandishi wasifanye jambo lolote kuchochea kutokuwepo uvumilivu na chuki ”, kanuni hizo zimeonya.

Kanuni za uandishi wa uchaguzi pia zinahimiza vyama vya siasa na taasisi zingine kuheshimu haki za waandishi kuripoti uchaguzi na kuhakikisha usalama wao.

Waandishi wasinyanyaswe kwa mdomo na hata kimwili na makundi na watu wasihamasishwe kufanya hivyo. Kanuni hizo pia zinaeleza waandishi waruhusiwe kufanyakazi zao kwa uhuru sehemu yoyote nchini na visiyumbishwe kwa kupewa fadhila, zawadi upendeleo au viburudisho.

MCT yatahadharisha vyombo vya habari kuhusu rushwa katika Uchaguzi MkuuInatoka Ukurasa wa 3

Wanahabari wakiwa katika tukio mojawapo la habari.

Page 5: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeendesha mafunzo maalum kwa wahadhiri wa vyuo vya uandishi wa habari

na wanahabari waandamizi Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mfulu-lizo wa mafunzo ya aina hiyo kwa mikoa mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo kwa wahadhiri wa vyuo vya uandishi wa habari yalifanyika Juni 25 na 26, 2020 wakati mafunzo kwa wanahabari waandamizi yalifanyika Juni 29 na

30,2020.Waandishi habari waandamizi 25

na wahadhiri 14 kutoka vyuo vya uandishi wa habari walihudhuria mafunzo hayo kuhusu sheria zinazohusu habari na hukumu za kesi za mahakamani.

Waandishi walitoka mikoa ya Zanzibar, Lindi, Mtwara, Pwani na Dar e s Salaam wakati wahadhiri walitoka mikoa ya Pwani, Zanzibar na Dar es Salaam.

Kufungua mashtaka ya kimkakati kama njia ya uragbishi na kuwasilisha ujumbe ndiyo mwelekeo mkubwa wa mafunzo hayo

yaliyojielekeza zaidi katika masuala mawili muhimu ya kwanini njia ya kufungua mashtaka inapendekezwa na nani anaweza kuhususika (na kama kuna nafasi ya wadau zaidi kushirikishwa).

Washiriki wa mafunzo hayo mawili waligawiwa katika makundi kuweza kubaini nguvu na udhaifuwa sheria ikiwamo sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya 2016, Kanuni za mitadanoni za mwaka 2018 za sheria ya EPOCA na Sheria ya makosa ya Mitandaoni ya

5

Habari

Toleo la 155, Julai, 2020

Endelea Ukurasa wa 6

MCT yaendesha mafunzo maalumu kwa wanahabari na wahadhiri

Wahadhiri wa vyuo vya uandishi wa habari waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga (wapili kushoto walioketi.

Page 6: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Wanahabari waandamizi waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakiwa katika majadiliano ya kikundi.

2015. Walipewa nakala za kesi,

muongozo wa wa majadiliano na kupewa majukumu.Walifanya majadiliano na wakakabiliwa na changamoto za kubainisha masuala katika kila kesi – mambo muhimu na uamuzi wa kesi.

Katika mafunzo hayo washiriki walieleweshwa kuhusu hukumu zilizotolewa na mahakama za hapa nchini za kanda na za kimataifa ikiwa pamoja na hukumu ya kesi ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 iliyotolewa na

Mahakama ya Afrika Mashariki iliyowapa ushindi wadau wa habari waliyoipinga sheria hiyo kuwa mbaya na inakiuka uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, utawala bora, utawala wa sheria na inakiuka mkataba wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hukumu hiyo ilitolewa na EACJ Machi 28, 2019 na jaribio la serikali kutaka kukata rufani lilishindikana baada ya Kitengo cha Rufani cha Mahakama hiyo kutupilia mbali notisi ya serikali ya kukata rufani Juni 9, 2020.

Washiriki wa mafunzo hayo pia walieleweshwa kuhusu uamuzi

uliofikiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Mjini Mwanza kuhusu kesi iliyofunguliwa na wadau kupinga Sheria ya Huduma ya Vyombo vya habari na maendeleo ya rufani dhidi ya uamuzi huo.

Hukumu zingine za mahakama zilizoelezewa katika mafunzo hayo ni pamoja na za Halihalisi na magazeti ya Mseto, Mawio, naTanzania Daima ambayo yalifungiwa na mahakama kuona hatua hiyo haikuwa sahihi na kuamuru yafunguliwe.

Mafunzo aina hiyo yameshafanyika kikanda katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya na Mwanza.

MCT yaendesha mafunzo maalumu kwa wanahabari na wahadhiriInatoka Ukurasa wa 5

Page 7: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Runinga ya Mtandaoni ya Kwanza imekuwa chombo cha pili kuzimwa na wenye mamlaka ndani ya wiki mbili kufuatia ua-

muzi wa Kamati ya Maudhui ya Mam-laka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuisimamisha kwa miezi 11 kwa madai ya kutangaza habari ambayo kamati hiyo imeziona kuwa za kupotosha.

Leseni ya gazeti la Tanzania Daima ilifutwa na Msajili wa Magazeti kwa madai ya ukiukaji wa maadili ya taaluma ya habari.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Joseph Mapunda aliwaambia waandishi wa habari kuwa Julai mosi, 2020 Kwanza TV katika mtandao wa kijamii ilirusha habari kuhusu ugonjwa wa Covid 19 nchini ambazo hazikuwa na mizania.

Alisema kuwa habari hiyo ililenga kusababisha hofu na wasiwasi na kuathiri uchumi wa taifa kwa kushusha kasi ya biashara mbalimbali na kuwa tishio kwa watalii.

"Hivyo kamati ya maadili imefunga Runinga hiyo kutoa huduma kwa miezi 11 kutokana na kutoa huduma kinyume cha sheria. Hii itawapa muda wa kusahihisha makosa yao”, alisema Mapunda.

Aliongeza kuwa bila kuzingatia maelekezo ya kitaaluma, runinga ya Kwanza katika siku hiyo ilitangza habari potofu zilizotolewa na ubalosi wa Marekani kwa raia wake kuhusu hali ya virusi vya corona nchini kinyume na Kanuni za mtandaoni za mwaka 2018 za sheria ya Mawasialaino ya kieletroniki na posta.

Runinga ya Kwanza imeamua kukata rufani dhidi ya hatua hiyo ya kufungiwa kwa Tume ya Ushindani.

“Tutaendelea kupigania haki yetu kuhusu suala hili, kabla ya kiwenda mahakamani. Mwisho wa siku kila kitu kiko mikononi mwa Mungu,” amsema Maria Sarungi-Tsehai, mmiliki wa runinga hiyo na Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications Media, alikaririwa kwenye Facebook.

Tangu 2016, serikali imekuwa ikitumia m ara kadhaa kanuni za mtandaoni kulazimisha wandesha

majukwaa mtandaoni, blogi na huduma za kurusha matangazo mtandaoni kulipa faini kubwa, na kuzuia uendeshaji bila kusajiliwa , kutekeleza sera kali ama kushitakiwa.

Ikizungumzia kusimamishwa kwa Runinga ya Kwanza, Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kwa nchi ya Zimbabwe (MISA- Zimbabwe)imeeleza ingawa ni muhimu kudhibiti habari zisizo sahihi, msimamo wetu ni kwamba kutumia kanuni na kukimbilia kusimamisha vyombo vya habari si hatua sahihi.

Tunahimiza mamlaka Tanzania kuweka mkazo zaidi kuhimiza uhuru wa kujieleza na kuachana na kutunga sheria zinazokwaza.

Taasisi imewataka wenye mamlaka nchini Tanzania kwa kushirikiana na vyama vya kiraia na umma kuwa na njia za kukabiliana na habari ziziso sahihi, bila kutumia kanuni zinazobana.

Hii itawezekana kwa kuwezesha kuwepo masafa zaidi, kuwepo magazeti na vyombo zaidi vya mtandaoni badala ya hatua za kukwaza tasnia ya habari, MISA Zimbabwe imesema .

Kwa upande wake , Kamati ya Kutetea Waandishi (CPJ) imeitaka mamlaka inayosimamia utangazaji Tanzania kuondoa amri ya kusimamisha Runinga ya Kwanza na kuacha kutumia kanuni dhidi ya vyombo vinavyokosoa. “Kutangaza habari kuhusu virusi vya corona kunachukuliwa kuwa ni kukosa uzalendo kutokana na serikali ya Rais John Magufuli kuzidi kubana vyombo

huru vya habari,” amesema Mwakilishi wa CPJ wa Afrika kuisni mwa Sahara, Muthoki Mumo amesema.

“Tanzania iondoe amri ya kufungia Runinga ya Mtandaoni ya Kwanza mara moja na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya habari vinafanyakazi kwa uhuru .

Runinga ya Kwanza ilifungiwa kwa miezi sita Septemba 2019 kwa kuchapisha habari zizilizodaiwa na wenye mamlaka kuwa ni za kupotosha. Kusimimaisha huko kulimalizika mwezi Machi mwaka huu. Kituo hicho kimeeleza kuwa kinaendelea na rufani yake mahakamani dhidi ya kusimamishwa huko.

Kufutwa kwa leseni ya gazeti la Tanzania Daima kuliibua upinzani mkali kutoka vyombo na taasisi za kutetea habari na haki na kuhoji busara ya wenye mamlaka kuchukua hatua hiyo wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao unahitaji kuwepo vyombo zaidi vya habari ili kuwa na maoni zaidi na kuwezesha wananchi kutoa uamuzi makini. Hatua hiyo imechukuliwa na wengi kuwa imelenga kubana vyombo vya habari huru.

Taarifa zinaeleza kuwa gazeti hilo limeomba upya kupewa leseni ya kuendelea na shughuli zake hatua ambayo ni mojawapo ya fursa ambazo gazeti hilo lilikuwa nazo ambapo nyingine ni kukata rufani kwa Waziri wa habari. Hata hivyo inahofiwa kuwa gazeti hilo ambalo linaonekana kuwa sumbufu kisiasa litabaki liemfungiwa mpaka baada ya uchaguzi.

7

Habari

Toleo la 155, Julai, 2020

Chombo kingine cha habari chanyamazishwa

Page 8: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania(MCT) limeshiriki ka-tika mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa na Chama cha

Waandishi wa Habari wa China (ACJA) ambao uliwakutanisha wana-habari wa China na Afrika.

Licha ya Tanzania nchi zingine zilizo shiriki mkutano huo uliofanyika Julai 16, 2020 ambao kauli mbiu yake ilikuwa “Mshikamano dhidi ya COVID 19 na Jamii ya China-Afrika kwa mtazamo wa baadae wa pamoja ni Nigeria, Kenya, Rwanda, Ivory Coast na China.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema vyombo vya habari Tanzania vimeathirika sana

na waandishi wanafanyakazi kwa shida na kuona kazi yao kuwa ya hatari.

Alisema wanakabiliwa na matumainio makubwa na shinikizo kutoka kwa jamii na wakati huo huo taarifa hazipatikani kwa urahisi kutoka kwa wenye mamlaka kwa kuwa imeelezwa taarifa kuhusu COVID 19 nchini Tanzania zitatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Msemaji Mkuu wa serikali.

Alisema kuchapisha taarifa nyingine yoyote kumewaingiza wanahabari

katika matatizo, amesema Mukajanga na kuongeza

kuwa wanahabari na vyombo vya habari wanajikuta katika hali ngumu.

Alisema awali taarifa zilikuwa zikitolewa kila mara

baada ya mgonjwa wa kwanza nchini humo kutangazwa Machi 16 katika mji wa Kaskazini wa Arusha unaojulikana kama kitovu cha utalii na kituo cha mikutano ya kimataifa, na takwimu za wagonjwa wapya na waliofariki kuelezwa kwa vyombo vya habari.

Hata hivyo Aprili 29, 2020 utaratibu huo wa kutoa taarifa ulisimamishwa kufuatia shaka kuhusu uwezo wa vitio vya kupima kutoa majibu yasiyo sahihi baada ya Rais John Magufuli kuiponda Maabara ya Taifa kwa matokeo yake kwa sampuli zisizo za binadamu, Mukajanga alisema.

Mara baada ya kutangazwa mtu wa kwanza kuumwa ugonjwa huo Machi 16, Baraza lilitoa muongozo kuhusu usalama na maadili ya kuandika COVID 19 na kusambaza kwa vyombo vya habari.

Pia alisema kuna taarifa zisizo sahihi za nchini, eneo na kimataifa na kwamba kuchambua habari zisizo sahihi za COVID 19 ni changamoto kwa waandishi Tanzania katika kuboresha na muktadha wa habari zao.

Wengi hawajafunzwa jinsi ya kuchuja na kuacha habari zisizo kweli zilizotapakaa kwenye mitandao na nje yake, Mukajanga alisema, na kuongeza kwamba muongozo uliotolewa na MCT unasaidia, lakini bado kuna kazi kubwa kuhakikisha waandishi hawaathiriki wala kuwa wasambazaji wa taarifa potofu.

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo wa mtandaoni kuwa changamoto wanayoweza kujadili ni kupambana na taarifa potofu mtandaoni zenye kauli za chuki za kibaguzi na kuongeza kuwa jamii zetu lazima zielimishwe kuhusu madai haya yanayolenga kueleza kuwa ugonjwa huo umesababishwa na watu fulani.

Wakati waandishi wetu na vyombo vya habari vinakabiliwa na jukumu la kuthibitisha na kurekebisha taarifa zisizo sahihi, amesema jamii lazima zihusishwe kuepuka mtazamo hasi wa kibaguzi kukuzwa na kuota mizizi.

Amesema majadiliano mengi zaidi yanaweza kufanywa mitandaoni ili kubadilishana uzoefu na mikakati na kutoa mfano wa mjadala uliofanyika wa mabaraza ya habari uliojumuisha Kenya, Uganda, Rwanda, Algeria, Zimbabwe, Afrika Kusini na Tanzania ambayo miongoni mwa mambo mbalimbali ulijadili suala la vyombo vya habari na COVID 19.

“Mkutano huu wa sasa ni dalili tosha kwamba tunaweza kuufanya mara kwa mara na kuhakikisha vyombo vya habari siyo tu viko salama, lakini pia vinaandika kwa ukamilifu na ufanisi habari za janga hili”, alisisitiza.

MCT yashiriki mkutano wa mtandaoni wa Afrika, China kuhusu COVID -19

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari, Kajubi Mukajanga.

Page 9: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

9

Toleo la 155, Julai, 2020

Habari

Na Mwandishi wa Barazani

Chama cha Wafanyakazi kwenye Vyombo vya Habari (JOWUTA) kimekubaliwa kuwa mwanachama wa

Shirikisho la Kimataifa la vyama vya waandishi wa Habari (IFJ).

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa JOWUTA, Said Mmaanga imeelza kuwa kuwa Maombi ya chama hicho yalikubaliwa na IFJ katika kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Julai 9, 2020, Brussels, Ubelgiji.

IFJ inawakilisha waandishi wa Habari wapatao 600,000 katika nchi 140 duniani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwenyekiti wa JOWUTA, Claud Gwandu, amesema chama hicho kiliwasilisha rasmi maombi ya kujiunga na IFJ mwishoni mwa Juni, 2020.

JOWUTA inaamini katika mshikamano wa pamoja baina ya mwandishi wa habari mmoja, vyama vya waandishi wa habari na hata kampuni za habari kwa kuwa ndiyo njia sahihi ya kutatua changamoto zinazowakabili waandishi wa habari nchini na duniani kote.

Gwandu ameeleza kuwepo kwa faida kubwa kwa JOWUTA kujiunga IFJ kama taasisi na kwa mwanachama mmoja mmoja hasa kipindi hiki ambacho sekta ya habari duniani inakabiliwa na matatizo ambayo baadhi yake yanazuia waandishi wa habari kutimiza majukumu yao.

Baadhi ya faida za JOWUTA kuwa mwanachama wa IFJ alisema ni pamoja na wanachama wake kupata fursa za kushiriki katika mafunzo, semina na mikutano mbalimbali inayoandaliwa na shirikisho hilo moja kwa moja au kupitia ofisi yake ya Afrika yenye makao yake makuu Dakar, Senegal.

“Katika kipindi hiki tunahitaji sana kuwajengea uwezo waandishi wanachama wetu na waandishi wa habari kwa ujumla katika maeneo mbalimbali, kama kuandika habari za uchaguzi kwa ufasaha, habari za

maendeleo, sayansi na teknolojia na kama inavyofahamika kuwa elimu ni ghali, hivyo nafasi hii itasaidia kuongeza kasi ya kuwajengea uwezo wanachama wetu,” alisema Gwandu.

Katika barua yake, Katibu Mkuu wa IFJ Anthony Bellanger amesema shirikisho hilo linafurahi kuona JOWUTA inajiunga katika umoja wa vyama vya wafanyakazi vya waandishi wa habari na vyama vya habari duniani.

JOWUTA ilisajiliwa rasmi Julai 26, 2018, ambapo Novemba 30, 2019 ilifanikiwa kupata viongozi katika

mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma. Uchaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2006.

Kwa sasa JOWUTA ina wanachama zaidi ya 300 waliopo katika mikoa mbalimbali nchini, lakini pia tangu kusajiliwa kwake imefanikiwa kuendesha mafunzo ya Usalama na Usawa wa Kijinsia kwa waandishi wa habari wanawake 204 katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Arusha, Mwanza, Tabora na Tanga.

JOWUTA yakubaliwa uanachama wa IFJ

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Claud Gwandu.

Page 10: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Salim Said Salim

Rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Benjamin William Mkapa (1995- 2005), aliyefariki Alhamisi, usiku

wa tarehe 23 Julai akiwa na miaka 82 alikuwa mwandishi habari makini, msemaji mzuri wa lugha ya Kiingereza na mwana diplomasia mahiri.

Nilifurahia kufanya kazi naye kwa karibu alipokuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Daily na Sunday News kutoka 1972 hadi 1974 na baadaye katikati ya miaka ya 1980 alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Wakati huo nilikuwa mwandishi wa habari wa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mkapa amekuwa akitambulika na wtu wengi, hasa wale waliofanya naye kazi kwa karibu kama mwandishi anayechambua mambo kwa uweledi na mwana siasa mwenye kupenda ujamaa.

Lakini alipochukua uongozi wa nchi kutoka kwa Rais wa pili wa Tanzania, Sheikh Ali Hassan Mwinyi alifungua milango ya biashara huru, Mkapa alizingatia hali halisi ya uchumi na kuweza kuongeza kukua kutoka asilimia 3.6 katika mwaka 1995 na kufikia asilimia mwaka 2004, mwaka mmoja kabla ya kumaliza muda wake kama kiongozi mkuu wa nchi.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanafikiria uzoefu alioupata wa kufanya kazi mbalimbali, zikiwemo za kuongoza wizara tafauti na kufanya kazi nchi mbalimbali pamoja na kuhudhuria mikutano mingi ya mataifa ndani na nje ya nchi kumemsaidia utendaji wake wa kazi kama Rais.

Marehemu

Rais Mkapa alifanya juhudi kubwa kuifufua tena Jumuiya ya Afrika Mshariki iliyovunjika mwaka 1977 na kuimarisha Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Nimejifunza mengi kwa kufanya naye kazi kwa karibu ijapokuwa zipo nyakati tulitofautiana na kubishana, lakini wakati wote aliendelea kuniangalia kama rafiki na mwana habari mwenzake ambaye upo waki tuliishi majirani na kutembeleana. Wakati tukiwa Daily News, wafanyakazi waandamizi, kama mimi wakati huo nilipokuwa Mhariri wa Michezo wakati yeye akiwa Mhariri Mtendaji tulikuwa tunamwita kwa jina lake la kwanza Ben.

Mkapa naye pia aliwaita wafanyakazi wa chumba cha habari kwa majina yao ya kwanza, isipokuwa mtu aliyekuwa na umri mkubwa kuliko watu wote chumba cha habari, mzee Shaabani ambaye alikuwa tarishi.

Sote tulikuwa tunamwita mzee Shaabani au kumtania na kumwita dogo.

Mkapa alikuwa Mhariri Mtendaji ambaye hakufanya

kazi ya utawala tu na

kusimamia sera ya

gazeti, mfumo wake, kutia

saini

hundi na barua za kuruhusu mfanyakazi kwenda safari au kupata likizo au mkopo. Alikuwa na kawaida ya kila asubuhi kuhudhuria mkutano wa kupitia gazeti la siku ile kwa kufanya tathmini na kupanga gazeti la siku ya pili liwe na habari na makala gani.

Mara nyingi alichangia na wakati mwengine katika mjadala alibishana na waandishi waliotofautiana naye.

Nakumbuka zipo siku aliondoka katikati ya mjadala kwa hasira, lakini siku ya pili akahudhuria kama kawaida na kushiriki katika mjadala.

Alitoa maelekezo ya kutaka kila mhariri na anayesanifu gazeti kuandika angalau habari moja na makala mbili kila mwezi na sio kungojea zile zinazoandikwa na waandishi chipukizi na kuziandikia vichwa vya habari

Katika kuonyesha njia sahihi Mkapa alikuwa anaandika uchambuzi wa masula mbalimbali kila wiki baadhi yao zikiwaakosoa viongozi wa serikali na mashirika ya umma. Katika makala hizi alitumia jina la Mwana wa Matonya.

Kama alivyofanya Mkapa akiwa kiongozi mkuu wa gazeti wahariri na waandishi waandamizi nao waliandika makala za wiki. Wapo waliotumia majina yao na wengine ya bandia.

Miongoni mwa ushauri aliokuwa akipenda kuutoa mara kwa mara anapofanya mikutano ya waandishi ambayo huchukua kati ya nusu saa hadi dakika 40 ni kusisitiza juu ya umuhimu wa mwandishi kukumbuka wakati wote kuwa anayo dhamana kwa jamii na ambayo haifai kuichezea.

Pia aliweka utaratibu wa wataalamu na maofisa wa wizara na mashirika kufika katika chumba cha habari na kuelezea maswala mbalimbali kuhusu taasisi zao na kazi zao na waandishi hupata fursa kuuliza maswali.

Kwa njia hii Mkapa alisaidia kuongeza ufahamu wa wanahabari katika masuala mbalimbali.

Mkapa licha ya kuwa Mhariri Mtendaji Daily News aliwahi pia kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Nationalist na Uhuru, Mwandishi wa Habari wa Rais na Mkurugenzi Mwanzislishi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA).

Rais wetu wa tatu Benjamin William Mkapa hatunaye tena. Kila binaaadamu hufanya makosa. Wakati mtu akitangulia mbele ya haki huwa tunapaswa kumsamehe makosa yake tunao wajibu wa kuthamini

kazi nzuri aliyoifanya katka nyadhifa mbali mbali za kulitumikia taifa lake kwa

unyenyekevu na uadilifu. Kwaheri mpenzi wetu rais mstaafu

Benjamin William Mkapa. Mungu

ailaze pema roho yake.

10

Tanzia

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Benjamin Mkapa: Mwandishi na mwanasaful Alitumia jina la Mwana wa Matonya katika

makala za uchambuzi

Hayati Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa

Page 11: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

11

Wasifu

Toleo la 155, Julai, 2020

Na Saidi Nguba.

Hakuna abishaye kwa dhati kabisa kuwa Tido Dunstan Mhando ndiye aliyejitokeza kuwa mtangazaji mahiri

anayegombewa katika Afrika Mashariki, Kati na Kusini, kwa muda wote. Ni mtu wa kupigiwa mfano, mwenye bidii na anayeheshimika sana.

Alianzia Radio Tanzania mwaka 1969 akiwa Mtangazaji Msaidizi baada ya kumaliza elimu yake katika Shule ya Sekondari ya Minaki.

Tido, ambaye anapenda kuitwa kwa jina hilo lake la kwanza, miaka 10 baadaye akaenda kufanyakazi Kenya, ambako nako alikuwa anagombewa na makampuni mbalimbali ya matangazo na habari.

Baadaye katika miaka ya mwanzo ya 1990, aijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mjini London na huko

baadaye akafanikiwa kuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza Idhaa ya Kiswahili iliyoanzishwa miaka ya nyuma sana.

Mwaka 2006, wakati serikali ya awamu ya nne ikiwa madarakani, aliitwa nyumbani kuja kuifufua Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT) , iliyokuwa ya kawaida sana, iliyochusha na kutokuwa na mvuto.

Ingawa waliomtangulia walijitaidi, kwa kadri walivyoweza, wakiwa na rasilimali chache, kuweka misingi ya chombo cha umma cha utangazaji, Tido aliichukua na kupenyeza uhodari, ubunifu na weledi na kuibadilisha jina kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (Tanzania Broadcasting Corporation –TBC) na kuleta Televisheni na Redio ya Taifa vikiwa ni vyombo vipya kabisa, vilivyojipambanua na vya kuaminika, katika muda usiozidi miaka mitatu tu.

Haishangazi basi kuwa watafiti, Kampuni ya Synovate, waliochunguza ni chombo gani cha habari cha kielektroniki kilichokuwa kinaongoza nchini Tanzania, waliitaja TBC kuwa ni nambari moja, mwaka 1999.

TBC, wakati huo, ilikuwa inapendwa na watu

wengi nchini na

kuwaambukiza hata watu wa nchi jirani kutazama Televisheni TBC na kusikiliza Redio hiyo.

Baada ya mkataba wa miaka minne na serikali kupitia TBC, Tido alidakwa na wamiliki wa kampuni ya vyombo vya habari ya Nation Media Group (NMG) kuwa angefaa kuongoza kampuni yake tanzu ya Mwananchi Communications Ltd. (MCL) inayochapisha Magazeti ya Kiswahili, Mwananchi na Kiingereza, The Citizen nchini Tanzania.

Hivi sasa, tangu mwaka 2014, Tido, baada ya kukaa miaka miwili na nusu kama bosi wa MCL, amekuwa akiiongoza Kampuni ya matangazo ya televisheni na redio ya Azam Media.

Amekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Star Media tangu mwaka 2008; mjumbe wa bodi ya Umoja wa Utangazaji wa Afrika Kusini (South African Broadcasting Association – SABA, mwaka 2006 - 2010) na mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika ya Umma ya Utangazaji ya Afrika Mashariki (East African Public Broadcasters Association, mwaka 2007 -2010). Ni uhodari usiomithilika.

“Utangazaji ndiyo kazi iliyokuwa katika ndoto yangu…” Tido aliniambia katika mahojiano hivi karibuni kwa ajili ya kuandika Makala hii huku akisema kwamba walimu wake wa sekodari walimsihi sana aendelee na masomo ya juu kulingana na uwezo wake. Wakati

RTD inatafuta vijana wenye vipaji ili kuingia katika kazi ya

utangazaji, Tido alikuwa miongoni mwa vijana

watatu waliochaguliwa kutokana na kundi la

200 waliosailiwa. Baada vya

miaka takriban 10 RTD, Tido alikwenda kufanyakazi

Tido Dunstan Mhando: Mwanahabari nguli anayependa kuchapa kazi

Endelea Ukurasa wa 12Mtangazaji nguli. Tido Mhando.

Page 12: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Kenya. Aliajiriwa kwanza na kampuni ya kutengeneza matangazo kwa ajili ya redio na televisheni, High Fidelity Company, akiwa Meneja Biashara Uzalishaji. Jukumu lake lilikuwa kutengeneza vipindi vya matangazo kwa ajili ya redio na televisheni vilivyokuwa vinatangazwa na kuonyesha na Sauti ya Kenya ambayo wakati huo ndiyo ilikuwa kituo cha kitaifa cha utangazaji.

Lakini baadaye kampuni ya High Fidelity Production ilipoangukia kwa mmiliki mwingine, alianza kuwa mtangazaji na mwandishi wa kujitegemea.

Katika mafanikio mengine, akiwa mwandishi wa kujitegemea, alichukuliwa kwa kuaminika kwake, kwa wakati mmoja kuwa mwakilishi wa BBC, Sauti ya Amerika (VOA), na Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle –DW), yakiwa mashirika matatu makubwa kati ya mashirika ya utangazaji ya kimataifa. Akiwa na makao yake makuu Nairobi, alikuwa akipeleka habari zilizotoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan na Ethiopia.

“Huu ndio wakati wa mabadiliko makubwa ya kisiasa duniani, mwishoni mwa ‘Vita Baridi’ na kwa vile nchi hizi zote nazo zilihusika na mabadiliko hayo,” Tido anasema” nilikuwa mwandishi niliyejulikana

sana lakini mwenye shughuli nyingi nikituma habari kuhusu matukio mbalimbali ambayo sasa yanatambulika kuwa ni makubwa ya kihistoria.”

Miongoni mwa matukio hayo ni vita ya wenyewe kwa wenyewe Sudan; ukame Ethiopia vita vya kikabila Rwanda na Burundi na jitihada za upatanishi; vita ya wenyewe kwa wenyewe Zaire ambayo sasa ni Congo DRC, Somalia na Uganda na jitihada za upatanishi na ujio wa serikali mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya Rais Museveni; kung’atuka kwa Rais wa kwanza wa Tanzania mwaka 1985 Mwalimu Julius Nyerere na mabadiliko ya kurejesha mfumo wa vyama vingi na vurugu za kisiasa Zanzibar na Kenya.

Tido ndiye alikuwa mwanahabari wa kwanza kutoa habari za kutoweka kimiujiza na hatimaye kuuawa kwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi wa Kenya, Dk. Robert Ouko, Januari 1990. Tido ilikuwa kidogo aingie katika matatizo na wakuu wa Kenya wakati huo kuhusu habari hiyo, na muda mfupi baadaye, akaalikwa aende London na kuagana na Nairobi.

Ndani ya BBC. Alialikwa kwa miezi mitatu, baadaye ikaongezwa hadi sita, halafu ikawa miaka mitano na mwishowe moja kwa moja akapewa kazi ya kudumu. “Hiki ndiyo kilikuwa kipindi muhimu katika taaluma yangu ya utangazaji…ni mafanikio adhimu sana kwa sababu wakati huo sera ilikuwa kwamba huwezi kupata kazi ya kudumu BBC mpaka kwanza ukamilishe mkataba wa miaka mitatu,” Tido anasema.

Mwaka 1993 alipandishwa cheo na kuwa Mtangazaji Mwandamizi akiwa ni kiongozi wa watangazaji na ripota na alipewa jukumu la kufanya mahojiano muhimu na kuandika habari za matukio makubwa.

Mwaka 1999, baada ya usaili mkali wa BBC, akapandishwa cheo kuwa Mwafrika wa kwanza kuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili “na kuwaongoza kwa unyenyekevu mkubwa na weledi wafanyakazi wenzangu walionipokea na kunikaribisha London nilipofika kwa mara ya kwanza. Miaka yake saba akiwa kiongozi wa Idhaa ya Kiswahili aliacha hiba kubwa.

Kipindi hicho ndicho kile kilicholeta mabadiliko makubwa ya namna ya utayarishaji vipindi, uzuri wa vipindi vyenyewe na maendeleo ya teknolojia na Idhaa hiyo ikawa ya kuaminika na ni ya lazima

Wasifu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Endelea Ukurasa wa 14

Mhando: Mwanahabari nguli anayependa kuchapa kaziInatoka Ukurasa wa 11

Tido Mhando akibadilishana mawazo na mtangazaji veteran, Edda Sanga.

Page 13: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

13

Toleo la 155, Julai, 2020

Uchambuzi

Na Gervas Moshiro

Hongera Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kumaliza robo karne ya maisha ya kuongoza taaluma

ya habari nchini. Ni ushindi stahiki kwani lilipambana dhidi ya nguvu kinzani nyingi zilizonuia kudhoofisha jitihada za baraza za kufanya wananchi wafurahie haki yao ya kuzaliwa ya habari.

Nimeshawishika kutoa salamu hizo baada ya kusoma mafanikio ya Baraza yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 25 ya kwanza ya uhai wake yaliyochapishwa katika jarida dada la Media Watch toleo la Juni, 2020. Ni salamu zilizochelewa kidogo, lakini hata hivyo hongera tena kwani, kama wasemavyo wahenga, heri kuchelewa kuliko kutofika kabisa.

Katika makala hayo yametajwa mafanikio muhimu na ambayo kusema kweli ni ya kupigiwa mfano ukichukulia mazingira magumu yaliyozingira vyombo vya habari na jamii wakati wa kuanzishwa Baraza katikati ya miaka ya 90. Jamii ilikuwa ndio kwanza inaingia katika mageuzi ya uliberali na umiliki binafsi na uendeshaji wa vyombo vya habari ulikuwa ndio kwanza unafanywa kwa mara ya kwanza tangu nchi iwe huru mwanzoni mwa miaka ya 60.

Vyombo vya habari vilikuwa vinaibuka kila mahali nchini pamoja na changamoto zilizokuweko – ukosefu wa nguvukazi yenye ujuzi, sheria zilizopitwa na wakati, viongozi wa serikali waliokuwa wanang’ang’ania mfumo wa milikihodhi licha ya mabadiliko, kutoeleweka kwa falsafa ya habari kuwa huduma ya jamii, serikali ikichukulia habari kuwa zana ya kufanikisha utawala tu, chombo cha usuluhishi kukosekana ndani ya tasnia ya habari na kubwa zaidi ni kule kutokuweko kwa viwango vya taaluma. Baraza la Habari lilikusudiwa liwe ndio mwarobaini wa mapungufu yote hayo na mengine.

Baada ya miaka 25, imethibitika kuwa Baraza la Habari ndio taasisi ya suluhisho la yote licha ya changamoto zilizopo. Katika makala haya nitatoa mawazo yangu ninavyoiona MCT kutokana na uzoefu wangu kama mmoja wa viongozi waanzilishi, mwanazuoni mkereketwa na mjuzi wa mwenendo wa Baraza kama yanavyobainishwa katika vyombo vyake vya mawasiliano kwa jamii, rika

moja baada ya kuasisiwa. Chimbuko la Baraza la Habari

Tanzania limeelezwa vizuri sana katika kitabu kwa lugha ya kiingereza: Self Regulate or Perish: The History of the Media Council of Tanzania, kilichochapishwa na Baraza mwaka 2010. Katika kitabu hicho mimi natajwa kama Makamu wa

Mwenyekiti na pia mtu niliyelea Baraza kwa kulipa maskani ya kuanzia ofisini kwangu nikiwa Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania pale Sharrif Shamba Ilala, Dar es Salaam na ambacho sasa ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na

MCT ni muhimu zaidi sasa

Endelea Ukurasa wa 15

WANAHARAKATI WA WANAHABARI

KUJISIMAMIA WENYEWE

Salva Rweyemamu

Lawrence Kilimwiko

Ndimara Tegambwage

Kajubi Mukajanga

Page 14: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

kuisikiliza kwa wazungumzaji wa Kiswahili katika Afrika Mashariki na Kati.

“Nilipochukua uongozi mwaka 1999, Idhaa hiyo ilikuwa inasikilizwa na watu miioni 7, lakini wakati naondoka, BBC ikawa ni kituo cha utangazaji wa redio cha kuaminika na kinachopendwa sana katika eneo la Afrika Mashariki na Kati,” ameongeza.

Ingawa alisomea Utangazaji wa Biashara, kwenye Chuo cha Kibiashara cha Kenya, ustadi wa uandishi wa habari alioupata akiwa kazini, anavyopenda kutafuta habari, uwezo wake wa kunusanusa na uchangamfu alionao, umemuwezesha kuifungua milango mingi iliyofungwa.

Ana sifa ya kuwa mwanahabari pekee katika eneo hili la dunia kumudu kufanya mahojiano binafsi, bila vikwazo, na wakuu wa nchi na serikali karibu wote, waliopo hai sasa na wale ambao wametaangulia mbele ya haki, katika Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

Orodha ni ndefu, lakini wamo Marais wa Tanzania - Rais wa kwanza hayati Mwalimu Nyerere, wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa, wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete; Marais waliopita wa Zanzibar - Dk. Salmin Amour na Amani Abeid Karume na wa sasa, Dk. Ali Mohammed Shein; Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na wa zamani, Iddi Amin; Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano; Rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda; Marais wa DRC, Joseph Kabila na hayati Laurent Kabila; Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa zamani wa Burundi, hayati Pierre Nkurunzinza.

Miongoni mwa watu wengine mashuhuri ambao Tido alifanyanao mahojiano ni Dk. Asha Rose Migiro akiwa Naibu Katibu Muku wa Umoja wa Mataifa; Makamu wa Rais wa Kenya wa zamani, Kalonzo Musyoka na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga.

Miongoni mwa matukio muhimu

Mhando: Mwanahabari nguli anayependa kuchapa kazi

14

Wasifu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Inatoka Ukurasa wa 12

Tido Mhando akimhoji hayati Rais Daniel arap Moi wa Kenya.Endelea Ukurasa wa 17

Page 15: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

15

Toleo la 155, Julai, 2020

Uchambuzi

Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia niliongoza jitihada za kupata fedha kianzio cha uendeshaji wa Baraza.

Historia hujirudia, tunaambiwa. Ilikuwa serikali, kupitia Waziri Dk. William Shija (RIP) aliyeanzisha utaratibu wa kuwa na baraza la habari la serikali kudhibiti sekta ya habari na alifikia hatua ya kuandaa mswada wa kupeleka bungeni, japo hakumalizia azma yake. Mswada huo ulikataliwa katakata na tasnia ya habari. Nakumbuka maneno ya kichwa cha habari katika moja ya gazeti yaliyokolezwa na kukuzwa kujaza nusu kurasa yakisema: “Acha Shija, Acha: Mswada wa Kishetani”. Hii inaashiria kuwa wanahabari walikuwa tayari kwa mapambano makali na serikali. Baada ya kusoma alama za nyakati, serikali ilikubali kuondoa mswada huo lakini ikitishia kuwa itaurejesha ikiwa tasnia itashindwa kuanzisha Baraza lenye uwezo wa kusimamia taaluma ya habari nchini.

Hii iliamsha hisia na mori za wanaharakati kama Kajubi Mukajanga, Ndimara Tegambwage,, Lawrence Kilimwiko, Salva Rweyemamu, Gideon Shoo na wengine kufanya kazi usiku na mchana ili kuanzisha baraza. Historia ile inasisimua sana kusoma – vikao vyao vingi katika vijiwe vyao, kufukuzana na waziri wa habari, njama kutaka kukipindua chama cha waandishi wa habari cha kiserikali, uragbishi mwingi kwa wanasiasa na viongozi serikalini na utafutaji wa ufadhili kutoka balozi za nchi za nje.

Nilijifunza somo kubwa hapa. Wakereketwa wale hawakuchukua nafasi za uongozi katika baraza baada ya kuanzishwa. Nia ilikuwa kupata baraza huru, kitu ambacho walifanikiwa. Ilikuwa ni mapenzi yao tu kwa taaluma ya habari yaliyohalalisha masaibu waliyopata kwa kujitolea kwa hali na mali. Nikakumbuka usemi mmoja unaosema kuwa hakuna maendeleo bila kujitolea. Tunawiwa deni kubwa kwa wanaharakati hawa, ambao kwa namna moja ama nyingine walitufunza diplomasia ya kijamii inavyofanya kazi.

Tokea mwanzo, serikali ilihakikishiwa kuwa isiwe na hofu kuhusu baraza huru la kusimamia tasnia. Habari ni sekta mtambuka, iko katika sekta zote - iwe kilimo, afya,

ujenzi, usafiri na nyingine, ikiwemo hata ofisi ya rais. Ukweli huu ulifanya waanzilishi kubuni mkakati wa usimamizi unaozingatia hali hiyo, ambapo japo baraza linalenga tasnia ya habari, kuishi kwake kunaingia ndani ya maisha ya jamii kwa jumla.

Chombo kilichoainisha muundo wa usimamizi kilitoa nafasi kubwa kwa msimamizi, ambayo ni Bodi, kwamba ijumuishe watu mushuhuri walio na uadilifu usio na mashaka. Ilianza kwa kishindo – wajumbe mashuhuri na wanaofahamika kwa utendaji wao uliotukuka, walichaguliwa katika bodi ya kwanza: mwanataaluma Prof. Geoffrey Mmari, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba, mawakili wa Mahakama Kuu Dk. Masumbuko Lamwai na Dk. Seng’ondo Mvungi, wanasiasa, wabunge na wanaharakati wa jinsia Edith Lucina na Naila M. Jidawi kuwakilisha jamii. Kwa pamoja na wanataaluma saba waliochaguliwa na mkutano mkuu, waliunda bodi ya kwanza ya usimamizi.

Mkakati ulikuwa kuaminisha serikali na wananchi kwa jumla waelewe kuwa baraza lilikuwa ni taasisi ya jamii inayopigania maslahi ya wananchi wote, kama ambavyo chombo cha habari makini kingefanya.

Kukuza taaluma kwa haraka ndilo lililokuwa na bado ndilo lengo kuu la Baraza, ikihusisha uboreshaji na ukuaji wa ujuzi, mwenendo sahihi wa kitaaluma na kukumbatiwa na jamii. Katika jitihada za kukuza ujuzi na maarifa ilikuwa kupitia mafunzo, semina, warsha, kongamano, mikutano, kutengeneza kanuni kwa matumizi ya fani zote za tasnia na usuluhishaji wa migogoro mbalimbali kuhakikisha kuna amani, utulivu na kuelewana kati ya wanahabari wenyewe na kati ya wanahabari na jamii. Zaidi ya yote ni kuhakikisha mazingira ya sheria yanakuwa rafiki kwa utendaji wa wanahabari. Majukumu hayo yalitekelezwa kwa ufanisi mkubwa kama ilivyoelezwa kwenye makala ile ya Media Watch, na bado kazi inaendelea ambapo kwa mazingira ya sasa inahitajika nguvu zaidi, kasi zaidi na ari zaidi.

Namna ya kuvuka robo karne nyingine, ndilo linalopaswa kushughulisha tasnia zaidi. Mazingira ni ya wasiwasi sana kisiasa na kiteknolojia yanateleza sana kwa maana ya mabadiliko ya haraka, hivyo inahitaji kuwa makini na ubunifu mwingi katika kuyakabili. Kwa kweli

huenda Baraza likawa na mazingira magumu zaidi kuliko huko lilikotoka. Kizuizi kikubwa cha baraza huru la wanahabari ni sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016 ambayo inakusudia kuchukua baadhi ya majukumu yanayotekelezwa na Baraza na ambayo ndiyo muhimu na bendera ya MCT.

Uzuri ni kwamba sheria bado inatambua uwepo wa taasisi za binafsi za habari, na hivyo itakuwa muhimu kutafuta mbinu za ushindani, labda iwe kwamba serikali haitaki kujali kuwa wakati wa uanzishwaji wa baraza lake, tayari lilikuweko baraza lililoandikishwa kisheria na ambalo lina majukumu yaliyobainishwa mahususi na sera ya habari na utangazaji nchini. Ni chombo rasmi na hakiwezi kufutwa kienyeji. Kwa kweli kinastahili kupongezwa kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa robo karne chini ya usimamizi wake kikiwa sasa kinasubiri kuja kwa baraza jipya tayari kwa maisha ya ushindani kwenda mbele.

Mabaraza haya yanatofautiana sana katika mambo ya msingi. Baraza la serikali linasajili waandishi mmoja mmoja kuwa wanachama wake ambapo baraza la tasnia lina wamiliki wa vyombo vya habari kama wanachama. Suala muhimu la fedha nalo halishirikishwi kwani vyanzo vya mapato vitakuwa vinatofautiana. Mabaraza haya yanaweza kuishi yakisaidiana kwa manufaa ya taaluma. Ni namna nzuri ila itahitaji kumshawishi waziri ili aone kuwa sekta itatajirika na kuchangamka zaidi ikiwa mabaraza hayo yatasaidiana majukumu kwa kushindana.

Changamoto nyingine iliyopo mbele ni ile ya viongozi wa siasa na serikali kutoelewa dhima na falsafa ya vyombo vya habari katika jamii, kitu ambacho kimejijenga kwa muda mrefu toka wakati wa siasa za ujamaa ambapo vyombo vyote vya habari vilitumiwa na watawala kutangaza mazuri waliyofanya na kuonesha tabia zao nzuri ili waweze kushinda tena uchaguzi unaofuata. Udanganyifu mwingi ulishamiri kwa kuwa hakuna chombo cha habari kilichosaili mienendo yao.

Serikali ingependa vyombo vya habari vitangaze mafanikio yake, jambo ambalo ni jema, lakini ikikataa yasitangazwe mapungufu yake. Ni majanga kuwa vyombo ambavyo vimekubali kuchukua mkondo huo wa

MCT ni muhimu zaidi sasaInatoka Ukurasa wa 13

Endelea Ukurasa wa 16

Page 16: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

kutangaza mazuri tu na kukwepa mapungufu vimekuwa kipenzi cha serikali. Kufanya hivyo wanakuwa hawafanyi kazi ya uandishi wa habari bali ya uhusiano mwema.

Vyombo vya habari, na hapa nina maana ya vyombo ambavyo vina wajibu kwa jamii kama dhima yao kuu, haviwezi kuwa ni vyombo vya uhusiano mwema tu. Inatokea vikafanya kazi ya uhusiano mwema kama jambo linahusu jamii kwa jumla kwa manufaa ya wengi. Mafanikio ni upande mmoja wa sarafu. Ni mapungufu yanayoleta changamoto na kusukuma jamii kujituma zaidi kuondoa vipingamizi vya maendeleo yake. Hiki ndicho jamii inatakiwa kukifahamu ili itafute ufumbuzi. Mchakato wake ndio huleta maendeleo. Jambo hili litahitaji kutiliwa mkazo sana wakati wa vikao vya kubadilisha fikra za viongozi wetu.

Mimi sipendi kumsifu mtu aliyefanikisha jukumu alilopewa na jamii na ambao ni wajibu halali anaotakiwa kutekeleza. Mtu aliyetenda vema majukumu yake hawezi kuwa habari kwa vigezo vya habari, bali yule aliyeshindwa kwani jamii itahitaji kuchukua hatua kwa vile itakuwa imeathirika kwa namna moja au nyingine. Ndio maana kushindwa huwa ni habari kwani sio tegemeo la jamii. Aliyepewa shilingi milioni akanunue dawa za zahanati kijijini na akafanya hivyo, hawezi kutangazwa kuwa kafanikwa kununua dawa kama ni jambo jipya, lakini angezifuja inakuwa habari kubwa kijijini kwani athari ni kubwa na ni kitu kisichotarajiwa na itahitaji kijji kuchukua hatua kwa mtu yule. Waandishi wa habari wanafundishwa kutafuta jambo ambalo si la kawaida - liwe zuri au baya. Kutotimiza majukumu inavyotarajiwa na jamii, kutaleta kutangazwa, mtu apende, asipende.

Vyombo vya habari vina jukumu la kuifanya jamii ijijue iko wapi – mafanikio iliyopata na pia mapungufu yaliyopo. Ningeshauri MCT ije na jitihada ambazo zitabadili mtazamo wa viongozi wetu wakubali kuwa maovu wakati wote yanawindwa na wanahabari kama yanaathiri maisha ya jamii. Hii ipo katika katiba ya nchi kifungu cha 18(d) kinachoeleza kuwa kila mtu “anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na

shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa wananchi”. Hii inaeleza pia kwa nini vyombo vya habari hujishughulisha na habari za uchunguzi. Kuvinyima kufanya uchunguzi ni kuvunja katiba kwani ni kinyume na matakwa yaliyobainishwa katika kifungu hicho cha 18(d). Vyombo vya habari ni wapashaji habari tu wakisaidia jamii kufanya wananchi wake wawajibike.

Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alilielezea vizuri jukumu hilo mwaka 1970 wakati analipa majukumu gazeti laThe Standard, ambalo sasa ni Daily News: (tafsiri isiyo rasmi) “The Standard mpya itakuwa huru kudadisi uzuri au ubaya wa vitendo vya viongozi wa TANU na serikali na kutangaza mapungufu yaliyo katika jamii, ya yeyote atakeyekuwa ameyatenda. Litakuwa huru kukosoa utekelezaji wa sera zilizokubaliwa , ama kwa juhudi zake peke au kufuatia malalamiko na ushauri kutoka kwa wasomaji”. Tunahitaji kusema zaidi?

Licha ya Baraza kufanya kazi kwa miaka mingi bila hitilafu, Serikali bado inataka kuanzisha baraza lake kama ilivyobainishwa katika sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016. Kubwa la kuhalalisha hatua hiyo ni kwamba MCT inakosa nguvu ya kulazimisha utekelezaji wa maamuzi yake kwenye vikao vya usuluhishi. Ukweli uliodhahiri kutoka kwenye kumbukumbu za kesi zote zilizosuluhishwa, ni kwamba utekelezaji umekuwa zaidi ya 98%. Walalamikaji wamekuwa wakieleza kuridhika na jinsi kesi zinavyoendeshwa na kuamuliwa. Wanufaika wa utaratibu huo ni wengi, kutoka makamu wa rais, waziri mkuu mstaafu,mawaziri, majaji, wakuu wa mikoa, wilaya, viongozi wa taasisi kubwa nchini na wengine wengi. Kwa nini tutilie shaka ushuhuda wao kama lengo lilikuwa ni kuhakikisha haki inatendeka? Lazima kuna ajenda iliyojificha ambayo naweza kusema kuwa ni kuhakikisha vyombo vya habari vinakosa uhuru wa kitaaluma na kujitegemea, hivyo kufanywa kutekeleza zipendavyo mamlaka za siasa. Kuna mabadiliko makubwa yametokea kuhusu tabia za watu kwenye kutumia vyombo vya babari, utendaji kwenye vyombo vya habari na teknolojia ya kidijiti. Kuweza kutumia fursha ya mabadiliko haya vyombo vya habari vyahitaji uongozi wa pamoja na wenye mtazamo wa maendeleo, kitu ambacho MCT inaweza kufanya kwa

wepesi. Halafu kuna hili la uongezekaji wa

tv za mtandaoni. Imekuwa mtindo kupata leseni na kuweka mtandaoni video za maudhui mbalimbali. Maudhui haya mara nyingi ni matukio mbalimbali ya kuokoteza hapa na pale na hayana mpangilio maalum na sifa za kuwa ni uandishi wa habari tulivyozea kwa chombo kujiita tv. Kwa maoni yangu naona maudhui mengi ni propaganda tupu kutokana na uteuzi na mrengo wa maudhui. Hii ipo pia kwenye mitandao ya kijamii ambapo, ukiondoa matangazo ya tv za kawaida, wengine hutumia kutolea video za matukio moja moja hapa na pale, sawa na wale wa tv za mtandaoni. Maudhui ya tv za mtandaoni nionavyo sio linganifu, ni ya upande mmoja na hayaoneshi juhudi za kuthibitisha usahihi na ukweli wa taarifa. Wanaotazama na kusikiliza video hizo huenda wakachukulia kuwa ndio ukweli wote na kuchukua hatua nyingine kufuatia taarifa hizo ambazo ni za upande mmoja, kitu ambacho ni usaliti wa chombo cha habari kumpotosha mwananchi.

Baraza yabidi libuni jitihada za kusaidia watoa taarifa mbalimbali kupitia mitandao kuelewa wajibu wao mitandaoni kuliko kusubiri serikali iwastue kwa kutumia rungu la sheria, nyingine ambazo tayari zinatumika kama ile ya Mawasliano ya Posta 2010 ikiimarishwa na kanuni zake. Elimu nyingi inahitajika na chombo chenye kuweza kutoa elimu hiyo ni baraza huru pekee la tasnia.

Kazi za MCT tuendako, kama ilivyojadiliwa katika makala haya ni nyingi na kubwa. Kuendelea na juhudi za kutafuta mazingira rafiki kisheria yabidi iwe ni ajenda ya kudumu. Kuongeza ujuzi na maarifa kuhusu taaluma pia ni jukumu la MCT. Usuluhishi, japo pia umetajwa katika baraza la serikali, inatakiwa ubaki sambamba na huo wa kisheria. Ni juu ya mlalamikaji kuamua wapi aende kutegemea mazingira ya suala husika. Inatakiwa ifahamike kwa serikali na wananchi kuwa vyombo vya habari havichukulii makosa ya kimaadili kuwa ni jinai, falsafa ambayo inatofautiana na ile ya serikali. Kwa hiyo chombo cha usuluhishi cha MCT ni mbadala unaopendelewa zaidi, hivyo una uhai wa kudumu katika mazingira ya kidemokrasia. Kwani, kama isemwavyo, ushindani ni afya.

Kaa salama, ONDOA CORONA

MCT ni muhimu zaidi sasaInatoka Ukurasa wa 15

Page 17: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

17

Wasifu

Toleo la 155, Julai, 2020

ambayo Tido aliandika habari zake ni mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, ambayo BBC walikuwa ndio wa kwanza kuyaibua hadharani. Pia alitoa habari za kifo cha Mwalimu Nyerere, London, mwaka 1999 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kwaka 1995. Mengine ni uchaguzi mkuu wa kwanza wa Kenya wa vyama vingi, mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa mwaka 1997; uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka 1996; mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, mwaka 2001; mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola, Edinburg, Scotland, mwaka 1997; kifo cha Princess Diana wa England, mwaka 1998; mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Dakar, Senegal, mwaka 1992 na mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA, Ufaransa, mwaka 1998.

Mtangazaji mkongwe na nguli nchini Tanzania, Hamza Kassongo, alisema kuhusu Tido: “kwetu sisi ni kijana lakini kwa wengine ni mzee…Tido ni mwandishi jabari. Anajituma na kujiingiza pale wenzake wanasita na kuogopa. Kutokana na hilo, Tido amewahoji wakuu wa nchi au watu wengi wenye madaraka kuliko waandishi wengi wa kisasa.”

Salva Rweyemamu aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Msemaji wa Rais na Mwandishi wa Habari wa Rais wakati wa Rais Kikwete na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBC anasema: “Nguvu ya Tido ipo katika kufanyakazi kwake kwa juhudi na uwezo wake mkubwa wa kutoa matunda. Ni mtu makini sana...” Mtangazaji mwingine mahiri, Ahmed Kipozi aliongeza: “ Nilipojiunga na RTD nikiwa mtangazaji mwanafunzi, kina Tido ndio walikuwa kaka zetu. Siku moja alinishika mkono na kuniweka kwenye taipureta na kunikaripia kuwa nisiaandike tena taarifa zangu kwa mkono.

Mimi nilidhani zile taipureta wakati huo, kabla ya kompyuta, ni kwa ajili ya watu maalum wenye ustadi mkubwa na hivyo mimi nilikuwa naandika kwa kalamu tu…”.

Mimi binafsi, nilikutana na Tido

mara ya kwanza mwaka 1971 nilipojiunga na Chumba cha Habari RTD kuanza taaluma ya uandishi wa habari. Tangu wakati huo, nimekuwa nikimuheshimu sana Tido.

Tido anasema wakati wake mgumu sana katika taaluma yake, ni jinsi mkataba wake wa miaka minne na serikali ulipokatishwa kwa ghafla “saa 24 kabla ya wakati”.

Anasema alikuwa akiambiwa kwa kauli kuwa mkataba wake utaongezwa kwa vile amekuwa akifanyakazi nzuri. “Lakini siku moja, mwezi Desemba mwaka 2010, mara baada ya uchaguzi mkuu, nikaonyeshwa mlango wa kutokea. Nilivunjika moyo siyo kwa kukosa kazi, bali nilikuwa na mambo ya kutosha mkononi niliyoyaandaa ya kuendelea kuisuka upya TBC…Iibidi nirudi London, kupumzika na kupata nguvu upya.

Lakini alipokuwa London, akapata mawasiliano kutoka kwa wakuu wa kampuni ya Nation Media Group (NMG) ya Kenya wakimwomba awe Mtendaji Mkuu wa kampuni yao tanzu ya Mwananchi Communications Ltd. (MCL) nchini Tanzania inayochapisha Magazeti ya Mwananchi, Kiswahili na Kiingereza, The Citizen. “Bado kidogo nikatae kwa sababu nilibaini kuwa sina ujuzi wowote wa kazi ya Magazeti. Lakini hatimaye nikakubali na kwa kweli kukaa kwangu MCL kumeniongezea kitu

kikubwa katika taaluma yangu…”. Mwaka 2014, aliondoka MCL

kujiunga na kampuni ya Azam Media Ltd, inayojihusisha na matangazo, redio na televisheni na kwa maneno ya Tido mwenyewe “ilikuwa ni kama kumpiga teke chura kuingia kwenye dimbwi”. Wakati wake mzuri, anasema, ni pale alipotangazwa kuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili BBC.

Huyu ndiye Tido Dunstan Mhando, ambaye amekuwa akizungumzwa sana kwa umahiri wake. Kikazi ni mwenye adabu lakini pia hana ustahamilivu katika kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri na kijamii na kibinafsi, ni mtu muungwana sana, Kwa wanahabari vijana chipukizi anasema lazima wawe na weledi, wawe wabunifu zaidi, watulivu na wastahamilivu. Pia wajiepushe na tamaa na wasiwe wepesi wa kuigaiga tu mambo ya ovyoovyo na kupenda sana fedha.

Tido siyo tu wa kiongozi kwa kukaa kitini, hadi sasa akiwa Mtendaji Mkuu,huonekana kila inapobidi akifanya vipindi muhimu na vya maana katika televisheni ya Azam.

Mwandishi ni mwanahabari na mhariri mkongwe nchini.

Anapatikana kupitia Simu/WhatsApp: 0754-388418 na

Barua-pepe: [email protected]

Mhando: Mwanahabari nguli anayependa kuchapa kazi

Tido Mhando akimhoji hayati Rais Laurent Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Inatoka Ukurasa wa 14

Page 18: MCT yatahadharisha kuhusu rushwa Uchaguzi Mkuu · Licha ya Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, Baraza pia lina Maadili ya uandishi wa Habari za Uchaguzi. Jaribio kubwa la kiitaaluma

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

Na Mwandishi wa Barazani Pemba

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesambaza Sera ya jinsia na vyombo vya habari kwa vyombo vya

habari vya Pemba.Ofisa Programu Mwandamizi wa

Baraza, Shifaa Hassan Said kutoka ofisi ya Baraza iliyopo Zanzibar alikabidhi sera hiyo ya jinsia katika vyombo mbali mbali vya habari Pemba.

Akikabidhi sera hiyo alisema kuwa sera hiyo ni muhimu kutumika ili kuweka mazingira bora ambayo yatazingatia haki na usawa wa wanawake na wanaume katika utendaji wao wa kazi.

“Sera ya jinsia ni muongozo muhimu katika kufanikisha dhana ya usawa wa jinsia katika vyombo vya habari kwani inatoa maelekezo mbali mbali ambapo yakifanyiwa kazi yataleta ufanisi katika vyombo

vya habari”, shifaa alifafanua.Mapema akikibidhi sera hiyo kwa

Redio Jamii Mkoani alisema kuwa kuna haja ya sera hiyo itumike kwa ukamilifu ili wafanyakazi wa redio jamii mkoani waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia mahitaji ya jinsia zote.

Alisisitiza kuwa ingawa vyombo vyetu vya habari vya Tanzania vimekuwa na pengo kubwa katika kuimarisha dhana ya jinsia na vyombo vya habari hivyo sera hiyo itakuwa dira ya kuonyesha mapungufu yaliyojitokeza na hatua za kuchukuliwa.

“Kuwepo kwa sera ni hatua moja hata hivyo sera hiyo itakuwa na maana zaidi ikiweza kutumika katika vyumba vya habari na kamwe isibaki katika majalada”, alisisitiza

Akipokea sera hiyo Mwenyektii wa Bodi ya Wadhamini ya Redio Jamii Mkoani Hamdu Hassan alisema kuwa wamepokea sera hiyo

na kuahidi kuifanyia kazi ili kuweza kuleta maendeleo ya jinsia katika redio hiyo.

Alisema kuwa bado kuna mapungufu ya utendaji katika kuimarisha haki na usawa wa jinsia katika vyombo vya habari na kuongeza kwamba sera hiyo itakuwa dira kuondoa mapungufu hayo.

“Nina amini kuwa yaliyomo katika sera ya jinsia na vyombo vya habari tutayafanyia kazi na Baraza la Habari liendelee kusaidia redio jamii kwa kadri inavyowezekana hususan katika masuala ya jinsia na vyombo vya habari”, alifafanua.

Msaidizi Meneja wa Redio Jamii Micheweni, Shaaban Ali Abeid, alisema kuwa kuwepo kwa sera ya jinsia na vyombo vya habari kutasaidia katika kuweza kupata haki za wanawake na wanaume katika vyombo vya habari.

Shaaban alisema kuwa bado kuna changamoto kadhaa za wanawake waandishi wa habari ambazo zinataka zijadiliwe kwa kina hata hivyo sera itawapa mwanga wa kuweza kupunguza changamoto hizo.

“Ni lazima tukiri kuwa kuna changamoto nyingi wa waandishi wanawake katika vyombo vya habari na sera hii itasaidia kuleta mabadiliko chanya ili wanawake na wanaume waweze kufanya kazi zao kwa weledi bila ya kubughudhiwa”, alifafanua.

Naibu Katibu Mkuu wa klabu ya waandishi ya Pemba Mchanga Haroub alisema kuwa klabu ya waandishi imepokea sera hiyo na hivyo wanachama wake wataipeleka katika vyombo vyao mbali mbali vya habari.

Wanawake tumekuwa na changamoto nyingi hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna wanawake wengi zaidi katika vyombo vya habari hivyo sera itakuwa muongozo wa kuwasaidia wanawake kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Alishukuru MCT kwa kuweza kuandaa na kuisambaza sera hiyo na klabu ya waandsihi wa habari Pemba itaitumia sera hiyo katika shughuli zao za kila siku.

Baraza limeandaa sera hiyo maalum ya jinsia na vyombo vya habari ikiwa ni njia moja muhimu ya kuendeleza haki na usawa wa wanawake na wanaume katika vyombo vya habari.

Sera hiyo imeandaliwa chini ya mradi maalum wa wanawake na vyombo vya habari unaofadhiliwa na shirika la VIKES kutoka finland.

MCT yasambaza sera ya jinsia kwa wanahabari Pemba

Msaidizi Meneja wa Redio Jamii Micheweni Shaaban Ali Abeid akipokea nakala za Sera ya Jinsia katika Vyombo vya Habari kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa MCT ofisi ya Zanzibar, Shifaa Said Hassan katika redio hiyo Julai 13, 2020.