misingi na utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/uongozi.pdf · uongozi...

16
Uongozi Misingi na Utendaji Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT) Yameandaliwa na Joseph & Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, ©2016

Upload: trinhque

Post on 24-Feb-2018

365 views

Category:

Documents


24 download

TRANSCRIPT

Page 1: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi

Misingi na Utendaji

Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT)

Yameandaliwa na

Joseph & Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, ©2016

Page 2: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Yaliyomo

Somo Uk.

Utangulizi 2

1 Nehemia – Kiongozi wa Matengenezo 3

2 Sauli, Mfalme Asiye Mwaminifu 5

3 Roho ya Mhudumu – Shina na Msingi 7

4 Huduma ya Kutoa Taarifa 8

5 Huduma ya Kuhubiri na Kufundisha 9

6 Huduma ya Kuongoza Ibada 10

7 Huduma ya Kuchunga Kondoo wa Mungu 11

8 Huduma ya Usuluhisho na Kupatanisha 12

9 Majaribu na Mitego katika Uongozi 14

10 Maono, Mikakati, Utekelezaji 15

Utangulizi

Kazi ya uongozi ni huduma na utumishi. Yesu alisema hakuja kutumikiwa, bali kutumika (Mathayo 20:28). Kama mti ulivyo na mizizi na matawi, ndivyo huduma yetu kwa nje inalishwa na hali ya roho yetu ya ndani. Msingi wa huduma ni tabia, na msingi wa tabia ni roho.

Kusudi ya somo hili ni kuelewa maana ya uongozi (somo la 1), tabia ya kiongozi (somo la 2), hali ya kiroho ya kiongozi (somo la 3), na utendaji wa uongozi (masomo 4-10). Masomo yanatumia mifano ya viongozi katika Biblia na mafundisho ya Biblia kuhusu uongozi.

Naomba masomo haya yataongeza maarifa na uwezo wa kuongoza, na kanisa litazidi kuwa imara.

Mch. Joseph Bontrager, Mwandishi Morogogo, Tanzania, 2016

Page 3: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.3

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 1. Nehemia – Kiongozi wa Matengenezo

1) Wito. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita…. (Warumi 8:30)

Nehemia hakusikia sauti ya Mungu (kama Musa alivyosikia – Kutoka 3:4-10) wala kumwona Mungu (kama Isaya alivyomwona – Isaya 6:1)

Nehemia alisikia wito kwa kutambua hali ya watu wake Yerusalemu. Hali yao ilikuwaje? (1:3)

Wito wake ulithibitishwa na mfalme na alimpeleka (2:6)

Waumini wote wanaitwa kuamini na katika huduma ya Mungu. Watumishi wanaitwa kwa kazi fulani ya utumishi. Wito kwa utumishi kwa kawaida unaunganisha uwezo wa mtu na haja zilizopo, kuthibitishwa na wenzako na kusikia rohoni kuthibitishwa na Mungu.

Je, wito wako kwa utumishi ulikuwaje?

2) Imani. Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo.… (Waebrania 11:1)

Nehemia alitambua sababu ya shida ni dhambi. Je, alitubu dhambi gani? (Nehemia 1:6)

Eleza ahadi za Mungu kuhusu kutawanya au kukusanya watu wake. (Nehemia 1:8-9)

Nehemia alikuwa na imani gani kuhusu Waisraeli kukusanyika? (Nehemia 1:9)

Uongozi unaofanikiwa unatokana na imani kwamba Mungu atafanya. Imani hiyo wakati mwingine inaitwa maono, yaani, kutazama mbele kwa hali inayoweza kutokea.

Je, una imani (au maono) gani kwa huduma unayofanya?

3) Utendaji. Utimizeni wokovu wenu …. Kwa ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. (Wafilipi 2:12-13)

Nehemia alifanya nini aliposikia hali ya watu wa Yerusalemu? Mkuu (Nehemia 1:4)

Nehemia alishauriana na nani kuhusu shida aliyoona? (Nehemia 2:4-6)

Tazama hatua za mipango yake ili kutimiza wito wake: o Alikadiria muda (Nehemia 2:6) o Aliomba vibali vya safari (Nehemia 2:7) o Alikusanya vifaa vya kujenga malango na nyumba (Nehemia 2:8) o Alichunguza hali ya ukuta wa Yerusalemu (Nehemia 2:11-17)

Alikusanya timu ya viongozi wa Wayahudi o Aliwafahamisha mpango wake wa kujenga nini? (Nehemia 2:17-18) o Walipanga wafanyakazi wa kujenga nini? (Nehemia 3:1-32) o Alichukua hatua gani walipotishwa na adui? (Nehemia 4:9) o Alisema maneno gani kwa kuwatia moyo wakuu wao? (Nehemia 4:14)

Utendaji ni kutekeleza maono. Pasipo mpango utekelezaji ni dhaifu. Utendaji ni kuchunguza mahitaji, kushauriana na wanaohusika, kukadiri na kukusanya vifaa, kujenga na kuwezesha timu ya wahudumu.

Je, katika maono yako kwa huduma unayoifanya, hatua ya kwanza ya utekelezaji ni nini?

4) Upinzani. Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;… Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu. (Waefeso 6:12-13

Nehemia alitambua hila za adui. Katika mistari inayotajwa hapo chini, adui alitumia mbinu gani kuzuia kazi ya Nehemia? Nehemia 2:19; 4:1; 4:11; 6:13; 13:4-5.

Page 4: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.4

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Nehemia alijua wito wake na kumtegemea Mungu; alitekeleza na kumaliza kazi aliyoitwa kuifanya wala hakutishwa na adui.

Ni kawaida kukabiliana na upinzani katika kazi yo yote ya kujenga watu, au kuleta mabadiliko. Wataalum wanasema wakati wa kuleta mabadiliko, ni kawaida mtu 1 kwa 5 atajiunga, 1 kwa 5 atapinga, na 3 wengine watasubiri mafanikio.

Uongozi imara:

Uhakika wa wito – kujua umetumwa

Maono unaotokana na imani – kuona mwisho unaotakiwa

Utendaji kwa mpango na hatua za ushirikiano na utekelezaji

Kutambua na kujibu upinzani na hila za maadui bila kuacha utendaji

Kwa majadiliano:

1. Eleza njia mbalimbali jinsi Mungu anavyowaita watumishi.

2. Kama mtu atakuambia, Kazi hii ni ya Mungu, kwa hiyo mpango si lazima, Mungu atatuongoza. Utakubali? Utamjibuje?

3. Kati ya maneno hayo 4, wito, imani, utendaji, na upinzani, je, ni ipi kuna shida kubwa katika uongozi wa makanisa yetu? Ni lipi wewe binafsi unasikia udhaifu zaidi?

4. Umekuta upinzani gani katika huduma yako? Uliitikia vipi?

Page 5: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.5

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 2. Sauli, Mfalme Asiye Mwaminifu

Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi kama ukafiri na vinyango. (1 Samweli 15:22-23)

1. Sauli alianza utawala kwa wito na uwezo wa Mungu. Soma 1 Samweli 10:1, 6-9

Taja dalili zinazoonyesha Mungu alimchagua Sauli kuwa mfalme. (6-7)

Eleza maana ya Mungu akambadilisha moyo. (9)

Katika 1 Samweli 11, Sauli aliwashinda Waamoni wa nguvu gani? (1 Samweli 11:6)

Mungu akiita, ndipo anawezesha. Sauli alipewa Roho Mtakatifu, alibadilishwa moyo, na aliweza kushinda Waamori.

Uongozi unaofanikiwa ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kwa moyo uliobadilishwa.

2. Alitoa dhabihu ingawa aliagizwa kumsubiri nabii Samweli. Soma 1 Samweli 13:5-14

Kwa nini Sauli alitoa sadaka mwenyewe, badala ya kumsubiri Samweli? (11-12)

Matokeo ya haraka ya Sauli yalikuwa nini? (14)

Hofu husababisha haraka. Sauli alipoona adui alikuwa na hofu. Aliamini uwezo wa tendo la dhabihu unazidi uwezo wa moyo wa utii. Alivunja Agano la Mungu, hivyo aliondolewa ufalme.

Uongozi unaofanikiwa unathamini na kuimarisha Agano na Mungu. Sadaka bila utii haina nguvu.

Je, tunawezaje kuimarisha agano kati yetu na Mungu? Je, sababu ya kuwa na hofu katika kazi zetu ni nini?

3. Aliapisha watu wake kipumbavu na kuweka laana. Soma 1 Samweli 14:24-30, 43-46

Sauli aliwaapisha Waisraeli kwa kiapo gani? (24)

Kwa sababu gani watu wa Israeli walisumbuka sana siku ile? (24, 30)

Kwa nini Yonathani alivunja kiapo cha Sauli? (25-27)

Kwa nini Waisraeli walianza kupinga uongozi wa Sauli? (45)

Agizo bila kushauriana hudhoofisha uongozi. Badala ya kutia nguvu, agizo la Sauli liliwadhoofisha kimwili. Halafua watu walipinga uamuzi wake juu ya Jonathan. Sauli alipouliza Mungu ushauri hakupata jibu (1 Samweli 14:37).

Laana haitoki kwa Mungu, na inatia hofu. Neno la Mungu ni ukombozi na imani.

Uongozi unaofanikiwa hushauriana na wenzao ili kutambua hekima ya Mungu.

Je? Faida kwa viongozi za kushauriana ni zipi?

4. Hakutii agizo la Mungu kuwaangamiza Waamaleki. Soma 1 Samweli 15:1-3, 7-9, 19-26

Mungu alitoa agizo gani kwa Sauli? (3)

Sauli alifanya nini alipowashinda Waamaleki? (8-9)

Sauli alitoa udhuru gani kuhusu kutoangamiza mfalme na mifugo? (20-21)

Kwa nini Mungu alimkataa Sauli kuwa mfalme wa Israeli? (26)

Mungu ni Mtakatifu, anadai watu wake kuondoa uovu kati yao. Katika Biblia, Waamaleki ni mfano wa uovu. Uasi ni kama uchawi (1 Samweli 15:22). Kawaida wafalme wa kipagani walikuwa washirikina. Sauli alitaka kuongeza nguvu za kimila katika utawala wake. Lakini

Page 6: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.6

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

ushirikina haipatani na nguvu za Mungu, ni chukizo kwa Mungu. Sauli hakujali agano la Mungu, alidhani atashinda kwa nguvu za kimila.

Uongozi unaofanikiwa unaimarisha agano na Mungu kwa kutii maagizo yake. Ushindi ni kuondoa uovu na kutegemea uwezo wa Mungu, wala si kuchanganya na mila.

5. Roho wa Mungu alimwacha Sauli. Soma 1 Samweli 15:26, 16:14, 21-23

Elezo: Katika lugha ya asili, kusema “roho mbaya kutoka kwa Bwana” inaweza kumaanisha “Bwana ameruhusu roho mbaya.” Roho ya Mungu si roho mbaya, ila roho mbaya anapewa ruhusa kufuatana na uamuzi wa mtu kumkataa Mungu.

Kwa nini Roho ya Bwana ilimwacha Sauli? (15:26)

Roho mbaya iliyomsumbua Sauli ilimfanya kuwa na tabia gani? (18:8, 9, 12; 19:1)

Kumkataa Mungu ni kuruhusu roho ya mwovu kuingia na kubadilisha moyo. Kufuatana na uasi wa Sauli, Roho wa Mungu alimwacha na ibilisi alipewa nafasi (Waefeso 4:26-27).

Uongozi unaofanikiwa umeacha matendo ya mwili (Wagalatia 5:19-21), na kuimarisha tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23). Tuwe na nia iliyokuwemo ndani ya Yesu Kristo, nia ya msamaha, unyenyekevu, na utumishi, kwa mfano wa Yesu (Wafilipi 2:1-8).

Je? Tunawezaje kulinda roho zetu, ili tuwe na Roho ya Mungu wala si roho mbaya?

6. Alimwendea mwenye pepo wa utambuzi. Soma 1 Samweli 28:5-7, 10, 15-18

Kwa nini Mungu alikataa ushirikina? (Kumbukumbu 18:10-13)

Kwa nini Sauli alimtafuta mwenye pepo wa utambuzi? (5,6,15)

Matokeo ya ushirikina wa Sauli yalikuwaje? (17-19)

Mwisho wa Sauli ulikuwaje? (1 Samweli 31:4)

Ushirikina ni chukizo kwa Mungu na alikataza Waisraeli wasifanye. Lakini badala ya kumrudia Mungu, Sauli alitafuta mwenye pepo wa utambuzi. Sauli alivunja Agano, alitafuta ushindi kwa njia ya ushirikina, Waisraeli walishindwa, na Sauli alijiua.

Uongozi unaofanikiwa unashika agano la Mungu. Hekima inatoka kwa Mungu, kwa kujilinda nafsi zetu, na kukua katika neema na kumjua Yesu (2 Petro 3:17-18).

Je? Kwa nini ushirikina unazidi kati ya Wakristo?

Kwa mazungumzo:

1. Taja makosa katika tabia wa Sauli unavyoyaona.

2. Unavyofikiri, chanzo cha matatizo ya Sauli kilikuwa nini?

3. Katika uongozi wako, je, utaimarisha tabia gani ili kuwa na uongozi unaofanikiwa?

4. Taja jinsi uongozi wa Sauli ni tofauti na uongozi wa Nehemia.

Page 7: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.7

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 3. Roho ya Mhudumu – Shina na Msingi

Jitahidini kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu, hamtajikwaa kamwe. 2 Petro 1:10

Tabia ni msingi wa uongozi. Msingi wa tabia ni hali ya kiroho. Yaani, imani yake, utii wake, na jinsi anavyotembea na Yesu na kufanana naye. Tabia imara ni kuwa na shina na msingi.

Mafundisho ya Biblia kuhusu tabia imara

Kumjua Kristo. Wafilipi 3:8-11

Kukaa ndani ya Yesu. Yohana 15:1-5

Kuwa na shina na msingi katika upendo. Waefeso 3:14-19

Kuishi kwa msalaba wa Yesu Kristo. Wagalatia 6”14

Msingi wa imani na maisha yetu ni Yesu Kristo (1 Wakorintho 3:11) – kumjua, kukaa naye, kuteswa naye, kufuata mfano wa tabia yake.

Je, kufuatana na maelezo hayo, tabia muhimu kwa mtumishi wa Mungu ni zipi?

Kujifanya imara

Tabia zinazotakiwa (2 Petro 1:5-7). Taja tabia hizo.

Matokeo ya kuongeza tabia hizo (2 Petro 1:10). Eleza matokeo ni nini?

Watu waovu tunaokutana nao (2 Petro 2:1). Ni watu gani?

Tabia na tumaini zinazotulinda na uongo. (2 Petro 3:11-13). Ni tabia na tumaini gani?

Kujilinda na kukua kiroho. (2 Petro 3:17-18). Eleza neno hilo.

Mtumishi wa Mungu anapaswa kufanya bidi kuimarisha tabia yake. Kwa njia hiyo, anajilinda na maovu na kutoa mfano wa maadili ya kikristo.

Je, ni kwa njia gani mtumishi atajilinda na kukua kiroho?

Tunda la Roho na tamaa za mwili

Kutotimiza tamaa za mwili (Wagalatia 5:16). Nguvu za kushinda tamaa za mwili ni nini?

Tamaa za mwili (Wagalatia 5:19-21). Soma tabia hizo.

Tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23). Soma tabia hizo.

Kipimo cha tabia ya kikristo ni tunda la Roho. Tunda la Roho linatokana na uhusiano wetu na Yesu. Linatupatia nguvu tusitimize tamaa za mwili.

Je, ni nini maana ya kusulubisha mwili pamaja na mawazo yake? (Wagalatia 5:24)

Kwa mazungumzo:

1. Yesu alifundisha tuwe na uhusiano gani naye? (Yohana 15:5)

2. Mwenendo mtakatifu (2 Petro 3:11) ni mwenendo gani?

3. Eleza maana ya kukua katika neema (2 Petro 3:18).

4. Je, shina na msingi (Waefeso 3:17) ni hali gani kwa mtumishi?

5. Unavyoona, mtumishi wa Mungu atafanya nini ili kuimarisha tunda la Roho katika maisha yake?

Page 8: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.8

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 4. Huduma ya Kutoa Taarifa

Mtafakarini sana Mtume wa Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu (Waebrania 3:2).

Kila mtumishi anapaswa kuwa mwaminifu kwa yule aliyemtuma, kama Yesu na Musa walivyokuwa waaminifu. Kufuata taratibu na kuwajibika ni kawaida katika Biblia, na inampasa mtumishi kuwajibika hivyo. Katika uaminifu huo, mtumishi anatoa taarifa ya huduma yake kwa kiongozi wake. Uaminifu ni tunda la roho (Wagalatia 5:22).

Kanisa na miradi yake ni ya waumini wote, wanastahili kupewa taarifa.

Soma mifano ifuatayo ya utaratibu katika Biblia na ufafanuzi wake:

Biblia: Ufafanuzi:

Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu. 1 Wakorintho 14:40

Paulo alishauri utaratibu katika ibada

Imempasa msimamizi awe mwenye kusumamia nyumba yake vyema… 1 Timotheo 3:4-5

Msimamizi katika kanisa anapaswa awe mtu wa utaratibu

Uwe na kiasi katika mambo yote, …timiliza huduma yako. 2 Timotheo 4:5

Paulo anamshauri Timotheo kufanya huduma kwa uaminifu

Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Mathayo 25:19

Bwana alidai taarifa jinsi watumwa walivyotumia mali yake

Walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote…. Mdo 14:27

Paulo alipomaliza ziara ya unjilisti alirudi kwa kanisa na kutoa taarifa

Namna za taarifa katika kanisa: (kupewa kwa anayehusika katika tawi, jimbo, au dayosisi)

Taarifa ya Ibada ya Jumapili – mahudhurio, sadaka, viongozi wa ibada, n.k.

Taarifa ya fedha – mapato, matumizi, makisio

Taarifa ya kikao cha kanisa – mahudhurio, ajenda ya kikao, uamuzi

Taarifa ya miradi ya kanisa – makisio, mafanikio, mahitaji

Ni taarifa gani zaidi? Ongeza hapa.

Faida za kutoa taarifa:

Kuonyesha maendeleo katika kutekeleza mipango

Kuweka wazi jinsi Mungu anavyobariki kazi yake na watu wake

Kuhakikisha uwajibikaji wa watumishi

Kuweza kuhakikisha uamuzi wa zamani na kupima utekelezaji

Kujenga imani na kuondoa mashaka juu ya matumizi ya pesa na uongozi kwa jumla

Kanisa ni mwili wa Kristo. Kwa hiyo, unapotoa taarifa kwa kanisa, unatoa kwa Yesu.

Vifaa vya taarifa:

Kitabu cha Ibada au daftari.

Faili ya kutunza taarifa za vikao, za fedha, n.k.

Mahali pa kutunzi taarifa kwa usalama.

Kwa mazungumzo:

1. Eleza kwa nini ni muhimu kutoa taarifa za huduma zako kanisani.

2. Eleza taarifa zinazotakiwa katika dayosisi, jimbo, na tawi.

3. Je, kwa huduma unayofanya, unawajibika kwa nani? Anastahili kupokea taarifa gani?

Page 9: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.9

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 5. Huduma ya kufundisha na kuhubiri

Yesu … alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Mathayo 11:1

Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Warumi 10:14

Tumepewa huduma muhimu ya kutangaza na kufundisha injili ya Yesu Kristo.

Kufundisha ni kueleza, kutoa maarifa, ili wasikilizaji wataelewa na kufahamu.

Kuhubiri ni kutangaza, kushuhudia, kunena neno la Mungu na matendo yake.

Kuhusu mahubiri and mafundisho: 1. Kiini na msingu wa mahubiri yetu ni Yesu Kristo. 1 Wakorintho 1:23; 3:11 2. Mahubiri na mafundisho yetu yanasimama juu ya Biblia. 2 Timotheo 3:14-17 3. Mafundisho na mahubiri yetu yanashuhudiwa na mwenendo wetu. 1 Timotheo 4:12,16 4. Kiongozi awe na uwezo wa kufundisha. 1 Timotheo 3:2; 2 Timotheo 2:24 5. Kusudu ya mafundisho yetu ni kuimarisha katika imani. 2 Timotheo 3:16-17 6. Mafundisho na mahubiri yanahitaji mtumishi kujiandaa. 1 Timotheo 4:13-15 7. Kufundisha na kuhubiri ni karama za Roho. Warumi 12:8; Waefeso 4:11

Unabii katika Biblia, sawa na kuhubiri, ni kutoa ujumbe kwa kufunuliwa na Mungu. Mara ni utabiri wa yaliyo mbele, na wakati mwingine ni neno la ushauri. Manabii na wahubiri wote wanasema neno waliopokea kwa kufunuliwa na Mungu.

Kujiandaa:

Sheria ya kwanza ya kuhubiri na kufundisha ni kujiandaa – kiroho, kimaisha, na kiakili.

1. Kujiandaa kiroho – tulia mbele ya Mungu; kutubu, kushukuru, kuomba uongozi katika maandalizi.

2. Kujiandaa kimaisha – kutembea katika nuru na ukweli na unyenyekevu kwa watu wote; kubali practice what you preach, yaani kutenda mwenyewe yale unayohubiri.

3. Kujiandaa kiakili a. Chagua somo la mafundisho au mahubiri – mistari au somo fulani. b. Jifahamisha na mistari au somo utakayoeleza. c. Soma maandishi ya wengine juu ya somo hilo ili kupanua mawazo yako. d. Panga somo katika vichwa vyake kuu – si kuzidi vichwa 3 au 4 tu. e. Tafuta mistari mingine inayohusu somo. f. Chagua mifano au hadithi inayofafanua somo. g. Andika muhtasari ya mafundisho au mahubiri jinsi utakavyotoa. h. Kama ni mafundisho, tunga maswali yanayoelekeza wanafunzi kugundua

ukweli wa somo. i. Maswali ya maarifa (nini? lini? nani?)

ii. Maswali ya ufafanuzi (kwa nini? maana?) iii. Maswali ya utekelizaji (utafanyaje?)

4. Kuomba Baraka ya Mungu juu ya mafundisho na mahubiri yako, na kutoa kwa ujasiri na unyenyekevu, katika nia ya utumishi na upendo.

Mazoezi: Utaanzaje kujiandaa kwa masomo hayo: Yoshua 1:1-9; Wafilipi 3:7-11; Upendo wa Mungu kwa watu wote; Ushindi wa Yesu Kristo

Page 10: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.10

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 6. Huduma ya kuongoza ibada

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zote. Kumbukumbu la Torati 6:4-5

Kusudi ya ibada:

Kumshukuru na kusifu Mungu.

Kukumbuka matendo ya Mungu.

Kusogea karibu na Mungu, kumjua na moyo wake zaidi.

Kupokea maonyo na ushauri.

Wakristo wa kwanza walikutana kwa ibada ya mafundisho, ushirika, sala, na kumsifu Mungu. Matendo 2:42-47.

Taratibu ya Ibada – inavyopendekezwa na Kanisa la Mennonite 1) Kuimba nyimbo chache au kwaya 2) Kukaribisha mkutano 3) Maombi ya kimya ya kumaliza na sala ya kiongozi 4) Somo la kwanza 5) Wimbo namba 6 Tenzi na kukiri Imani ya Mitume 6) Somo la pili 7) Sala kwa kupiga magoti kisha Sala ya Bwana 8) Matangazo 9) Wimbo kwaya au wimbo maalum

10) Mahubiri 11) Kukazia mahubiri 12) Nafasi fupi ya kushukuri, kuamini,, au kutubu 13) Wimbo wa kutoa sadaka 14) Sala ya shukrani kwa sadaka 15) Kufunga ibada na kumalizia na Neema ya Bwana…

Uongozi wa ibada unahitaji maandalizi 1) Chagua wahudumu:

a. Kuongoza ibada b. Kusoma masomo - wanaohusika wasome somo kabla ya kuingia katika ibada

2) Kuongoza nyimbo za pamoja - wanaohusika wachague nyimbo kabla ya kuingia katika ibada

3) Kuongoza maombi 4) Kuhubiri 5) Kumbusha wahudumu

Kuhusu utendaji

Tangaza somo na wimbo kwa kusikika na kueleweka

Soma masomo ya pamoja bila haraka, ili wote wasome pamoja

Kwaya wanasoma kwa kumsifu Mungu, si kuonekana kwa binadamu

Kupaza sauti kwa kiasi; kupaza sana kunachafua sauti na pengine kuharibu masikio

Kwa mazungumzo

1. Kwa mawazo yako, ni nini inafanya ibada kuwa ya maana?

2. Ni nini inachafua ibada?

3. Je, kuna jambo lo lote mnaweza kubadilisha ili kuboresha ibada katika kanisa lenu?

Page 11: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.11

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 7. Huduma ya Uchungaji

Lichungeni kundi la Mungu, lililo kwenu. 1 Petro 5:2 Tuangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri. Waebrania 10:24

Bwana Mchungaji wetu – Zaburi 23:1-6 Kuna kazi gani za uchungaji zinatajwa katika Zaburi 23?

Utendaji katika kanisa – Waefeso 4:12-16 Kuna kazi gani za uchungaji zinatajwa katika Waefeso 4:12-16?

Mfano mkuu wa uchungaji ni Yesu Kristo

Yesu alifundisha uzima wa ufalme wa Mungu. Mathayo 4:23

Yesu aliwahurumia mkutano, aliwaponya. Mathayo 14:14

Yesu aliponya mtu mzima, mwili, nafsi, na roho. Marko 1:32-34

Yesu alipata nguvu kwa njia ya maombi na kufunga. Marko 1:35

Yesu hakumhukumu mwenye shida. Yohana 8:11

Yesu aliwapatanisha wagonjwa na watu na desturi zao. Mathayo 8:4

Huduma za uchungaji

Uchungaji ni kujenga kanisa, mwili wa Kristo, katika imani, umoja, na upendo.

Uchungaji ni huduma ya kiroho ya rehema, kuleta faraja, ushauri, na uponyaji kwa mtu aliye na mashaka, hofu, au kuumizwa na hali ya maisha yake.

Viongozi wanaitwa kujenga waumini kwa kufarijiana na kushauriana.

Waumini wote wanaweza huduma za kutunzana, kushauriana, na kufarijiana.

Shida kali zinaweza kuwashinda waumini wengi, zishughulikiwe na viongozi wenye mafunzo na uzoefu.

Anayeponya ni Mungu tu, tunaelekeza watu kwa Mungu mwenye rehema.

Tabia muhimu katika huduma za kichungaji

Huruma – kutambua shida za watu na kuwatakia uzima na amani

Usikivu – kusikiliza ili kuwaelewa kabla ya kutoa ushauri

Ushauri – hekima ya kujenga uzima na kuwashauri wenye shida

Usiri – kulinda yale uliyosikia, wala si kuyasambaza kwa wasiohusika

Maombi –huduma hizo ziwe kwa maombi kabla ya, wakati wa, na baada ya huduma.

Huduma za namna mbalimbali huhitaji msaada mbalimbali. Inabidi tujue ipi tunaweza, na ipi inazidi uwezo wetu. Matatizo yanatofautiana kama vifuatavyo:

Matatizo mengi, misongo ya kazi au familia au maisha kwa jumla, waumini husaidiana, kufarijiana, na kuombeana – tuchukuliane mizigo. Wagalatia 6:2

Matukio makubwa, kama kufiwa, talaka, magonjwa makali, mapepo, au maswali makuu ya kiroho, huenda itazidi uzoefu wa kila mshiriki, na kuhitaji mshauri mwenye mafunzo na uzoefu, pamoja na maombi – wanafunzi …wasiweze. Mark 9:18; Yakobo 5:14-16.

Ugonjwa wa akili na mwili huenda huhitaji maombi pamoja na madawa na huduma ya wataalamu – tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako. 1 Timotheo 5:23

Kwa mazungumzo:

1. Kwa maneno yako, eleza kusudi kuu ya huduma ya uchungaji.

2. Kwa njia gani viongozi wanaweza kujenga waumini wawe imara na kuchukuliana?

3. Unavyoona, shida zinazotokea mara kwa mara katika maisha ya waumini ni zipi?

Page 12: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.12

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 8. Huduma ya Upatanisho

Tunda la Roho ni …amani. Wagalatia 5:22 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu. Wakolosai 3:15

Naye alitupa huduma ya upatanisho. 2 Wakorintho 5:18

Watu wa Mungu in watu wa amani

Isaiah 26:3. Mungu aliahidi amani kwa watu wanaofanyaje?

Yohana 14:27. Je, kwa nini tusifadhaike moyoni?

Wafilipi 4:7. Je, amani ya Mungu itafanyaje mioyo yetu?

Watu wa Mungu wanaleta amani

Mathayo 5:9. Wapatanishi ni watu gani?

Warumi 12:18; 14:19. Tunashauriwa kufuata hali gani kati mwetu?

Sababu za mapigano

Yakobo 4:1-3. Katika mistari hiyo, je, mapigano yanatoka wapi?

Wagalatia 5:19-21. Taja maneno kati ya hayo yanayoeleza hali ya mapigano.

Mathayo 20:24-28. Kwa nini wanafunzi 10 waliwakasirikia ndugu wao wawili?

Huduma ya Upatanisho Hali ya dunia in mashindano na vita, kati ya watu na kati ya mataifa.

2 Wakorintho 5:18. Je, Mungu ametupatia huduma gani?

Mathayo 5:23-24. Yesu aliagiza tufanye nine, tukiwa madhabahuni na kukumbuka jinsi tulivyomkwaza ndugu?

Mathayo 18:15-17. Eleza hatua 3 za kufanya suluhu na ndugu aliyetukosea.

Ngazi za Mapambano

Ngazi ya 1. Tofauti za mazoea, desturi, taratibu

Tunavumiliana na tunaendelea kufanya pamoja

Suluhu ni kupatana juu ya faida ya desturi tofauti na kuiheshimu

Tusipopatana tofauti, zinaweza kuwa mvutano Ngazi ya 2. Mvutano

Tunadai kufanya tunavyopendelea na kupinga mawazo ya mwenzetu

Suluhu ni kupatana namna ya kuendelea kwa kuheshimiana

Tusiposuluhisha mvutana, unaweza kuwa mashindano Ngazi ya 3. Mashindano

Tunataka kumshinda mwenzetu na kumwondoa, tunaanza kumwona ni adui

Suluhu inahitaji mpatanishi kusaidia kupata njia inayokubaliwa na wote

Tusiposulihisha mashindano, yanweza kuwa mapigano Ngazi ya 4. Mapigano au Vita

Tunataka kumwumiza kama adui asiwe na nguvu

Suluhu inahitaji mpatanishi, lakini ni vigumu au kushindwa

Kuhusu mapambano

Mambo kuwa tofauti ni kawaida katika maisha. Yasitutenge, bali kupanua mawazo na maono yetu. Tofauti zetu ni nafasi ya kuimarisha uelewano.

Shida ya kimsingi si tofauti wala mapambano; shida ni kutojua hatua za usuluhishi.

Jambo muhimu ni kulinda uhusiano wetu. Msingi wa suluhu ni kuaminiana.

Page 13: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.13

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Hatua za kusululisha

1. Kubali umuhimu wa kulinda uhusiano na kuonyesha heshima kwa wote.

2. Ongea kuhusu tofauti zilizopo, au shida iliyopo. Kila mmoja apewe nafasi kueleza jinsi anavyoona tatizo. Jaribu kuelewa jinsi mwingine anavyoona na anavyohisi.

3. Hapo ambapo mtu amemkwaza mwenzake, ombeana msamaha.

4. Tambua malengo ya kimsingi mnayoshiriki. Ingawa kuna tofauti kati yenu, pia kuna maneno mnayokubali. Hayo ni msingi wa suluhu.

5. Tafuta suluhu inayolinda heshima ya wanaohusika na kufikia malengo yetu.

6. Agana kuheshimiana na kufuata maelekezo mliyokubali.

Kwa mazungumzo:

1) Usuluhishi wa kimila ulikuwaje? Kwa vipi unalingana na mafundisho ya Biblia, na kwa vipi ni tofauti?

2) Je, unaelewa mapambano yaliyotokea katika jamaa, au kanisa? Suluhu ulifanywaje? Matokeo yake yalikuwaje?

3) Katika maisha yako, je, umejifunza nini kuhusu kukaa na watu wa kabila na desturi tofauti?

Page 14: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.14

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 9. Majaribu na Mitego katika Uongozi

Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi…. Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. 1 Timotheo 4:12,16

Maisha ya kiongozi ni mfano kwa waumini. Akitegwa na tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima (1 Yohana 2:16), mfano wake mbaya utaharibu uongozi wake.

Mitego katika maisha ya kiongozi

1. Ulegevu wa kazi

Yohana 9:4. Kwa nini imetupasa kuzifanya kazi zake Mungu?

1 Timotheo 4:13-16. Paulo anatoa ushauri gani kwa Timotheo?

Kiongozi awe na bidii na uaminifu katika huduma zake.

Kwa nini viongozi wengine wanalegea katika shughuli zao?

2. Kutafuta ukubwa

1 Petro 5:6. Kwa nini tunashauriwa kujinyenyekea?

Mathayo 20:25-28. Kiongozi awe na nia gani?

Kiongozi awe na nia ya unyenyekevu na utumishi.

Kiongozi anawezaje kukwepa kiburi cha ukubwa?

3. Kupenda mali

1 Timotheo 6:6-10. Inatupasa kuridhika na vitu gani?

1 Petro 5:2. Kiongozi asifanye kwa kutaka nini?.

Kiongozi awe na nia ya kuridhika na ukarimu.

Kiongozi anawezaje kukwepa tamaa za mali?

4. Upendeleo na ubaguzi

Yakobo 2:1-9. Upendeleo unatoka kwa mawazo gani? (mst. 4)

Kiongozi awe mtu wa heshima na haki kwa watu wote.

Msingi wa ubaguzi ni nini? Ni ukabila? Au uchumi? Au elimu? Au nini?

5. Uzinzi

1 Wakorintho 6:18-20. Kwa sababu zipi tunaambiwa kukimbilia zinaa?

Wagalatia 5:19. Kati ya matendo ya mwili, ni matendo gani ni ya uzinzi?

Kiongozi awe na maisha safi jinsi inavyostahili mwakilishi wa Yesu Kristo.

Kwa nini majaribu kwa uzinzi yana nguvu sana, hata kwa viongozi?

6. Ushirikina

Kumbukumbu 18:10-13. Mshirikina ni nini kwa Bwana? (mst. 12)

1 Wakorintho 10:18-21. Kwa nini mtu wa Mungu asishirikiane na mashetani?

Kiongozi amwabudu na kumtegemea Mungu tu atoaye uzima.

Je, ushirikina unaleta hasara gani katika kanisa?

Kwa mazungumzo:

1) Je, unavyoona, ni mitego gani ni hatari zaidi kwa viongozi wa kanisa leo?

2) Katika maisha ya Yesu, je, unaona mifano gani jinsi alivyoshinda majaribio haya?

3) Je, unaweza kutaja majaribu mengine yanayoshika viongozi wa kanisa?

Page 15: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.15

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Somo la 10. Maono, Mikakati, Utekelezaji

Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Luka 14:28

Mungu anafanya kwa kusudi. Kusudi ya Mungu ni ukombozi; maono ni uzima wa ufalme wa Mungu; mikakati na utekelezaji ni kwa hatua za kufanya taifa Israeli na kuandaa kuja kwa Mkombozi Yesu, na mwisho kutukusanya katika Yerusalemu mpya.

Miradi yetu inajengwa juu ya maono, kwa hatua za mikakati na utekelezaji, vifuatavyo.

Kila hatua inabidi ifanywe kwanza kwa maombi, kwa sababu inahusu kazi ya kiroho; na pili kwa mazungumzo, kwa kuongeza ushauri. Je, Mithali 15:22 inasemaje kuhusu mashauri?

Hatua ya 1. Kusudi (mission statement)

Shabaha yetu, imani yetu, na masharti yetu ya kimsingi (core values)

Wito wa Mungu kwetu

Kwa mawazo yako, eleza kusudi ya kanisa lako.

Uchambuzi wa SWOT – ni vizuri kupima hali mara kwa mara kwa yafuatayo: Strengths: Uwezo (kutuwezesha kufikia kusudi yetu) Weaknesses: Udhaifu (kuimarisha tunapokosa uwezo) Opportunities: Fursa (tunapoweza kuongeza huduma) Threats: Vitisho (vinavyozuia au kupunguza maendeleo)

Hatua ya 2. Maono (vision statement)

Lengo, hapo tunapotarajia kufikia, hali na huduma za kanisa baada ya miaka 5 au 10

Kwa mawazo yako, eleza maono ya kanisa lako.

Hatua ya 3. Mikakati (strategies)

Mikakati ni mipango inayoelekea Maono na kutekeleza Kusudi

Mikakati inapatana na Uwezo na Fursa, na kuzingatia Udhaifu na Vitisho

Pima malengo kama ni SMART

Eleza mpango mmoja unaoweza kusaidia kanisa kufikia kusudi yake.

SMART Goals – Malengo yawe: Specific – lengo ni wazi, linahusu jambo au kitu kilicho wazi Measurable – maendeleo na matokeo yanaweza kupimwa Achievable – lengo linaweza kufikiwa Reasonable – lengo linahusu kusudi na maono, na halizidi uwezo wetu Time-limited – kuweka muda au wakati wa kumaliza au kufikia lengo

Hatua ya 4. Utekelezaji (implemention)

Kupanga nani ni mtekelezaji wa hatua fulani, na muda anaopewa

Kila mtekelezaji anawajibika kufanya na kutoa taarifa

Hatua ya 5. Tathmini (evaluation)

Baada ya muda kupokea taarifa na kupima utekelezaji

Kurudia uchambuzi wa SMART kutambua hali zilizobadilika

Kupanga hatua kwa kipindi zinazofuata

Kwa mazungumzo:

1. Faida ya kupanga hivyo ni nini?

2. Faida ya tathmini ni nini?

Page 16: Misingi na Utendaji - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level3/Uongozi.pdf · Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.2 Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, ... yanatumia

Uongozi – Misingi na Utendaji, uk.16

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2016 Joseph Bontrager

Mifano:

Pendekezo: Makanisa mengine yanaweka Neno Kuu ya mwaka, ili kuongoza mipango na mikakati, hata mahubiri na mafundisho, kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kwa mfano:

Tangaza Neno Kuu kwa kanisa.

Chora bendera ya Neno Kuu na kuweka mbele ya kanisa kuwakumbusha.

Panga mahubiri kufuatana na vipengele vya Neno Kuu.

Idara zote zieleze jinsi watakavyofuata Neno Kuu katika miradi yao.

Mwisho wa mwaka kila idara watoa taarifa jinsi walivyofuata Neno Kuu.

Kwa mwaka mpya chagua Neno Kuu jipya.

Uchambuzi wa SWOT – andika maelezo katika kila eneo: (mifano)

Strength/Uwezo: (nguvu, rasilimali, ujuzi zinazojenga uwezo)

Jengo

Uongozi imara

Weakness/Udhaifu: (tunapokosa uweza na nguvu)

Wachache wana elimu ya Biblia

Washiriki wanakaa mbali

Opportunities/Fursa: (nafasi za kuingia na kuongeza huduma)

Majirani karibu

Vijana

Threats/Vitisho: (yanayopunguza au kuzuia maendeleo yetu)

Kulegea kiroho

Mvuto wa dunia

Utekelezaji – andika kwa kila lengo: (mfano)

Lengo

Hatua Anayehusika Tarehe ya kumaliza Imekamilika

1.

2.

3.