asili ya ushia na misingi yake - home - shia maktab

200

Upload: others

Post on 04-Oct-2021

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab
Page 2: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

asili ya ushia na misingi yake

(aslu’sh-shia wa usuluha)

Mwandishi : A M H A KG

Mfasiri : S M S M

Kimetolewa na Kimechapishwa na :BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM

Page 3: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

Haki za kunakili zimehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 42 6

Mwandishi : A M H A KG

Mfasiri : S M S M

Kimepangwa Katika Kompyuta na : B M M T

Mchapaji : A P N D

Toleo la Kwanza : D 2005 N: 5000

Kimetolewa na Kimechapishwa na :BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM

Page 4: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

YALIYOMO

Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11. Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 32. Utangulizi wa chapa ya saba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 163. Sababu zilizonifanya niandike kitabu hiki . . . . . . . . . . . . 244. Majadiliano na Ahmad Amin kuhusu uzushi wake . . . . 275. Mchango wa Shia katika maendeleo ya Uislamu . . . . . 316. Shia ndiyo waasisi wa elimu za Kiislamu . . . . . . . . . . . . 377. Ushairi na Washairi Bora Kabisa wa Kiislamu . . . . . . 40

Kundi la Kwanza: Masahaba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 40Kundi la Pili katika Zama za Tabiin . . . . . . . . . . . . . . . . . 41Kundi la Tatu lililowafuatia Tabiin . . . . . . . . . . . . . . . . . 41Kundi la Nne lililokuwepo kuanzia Karne ya Nne na kuendelea . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 41

8. Wafalme na Mawaziri wa Kiislamu . . . . . . . . . . . . . . . . . 439. Masingizio yasiyo na Msingi juu ya Ushia . . . . . . . . . . . 47

10. Tuhuma ya Kushangaza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 4911. Chimbuko hasa la misiba hii . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5212. Ushia na Abdallah ibn Sabaa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5313. Sehemu ya Kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5614. Kina nani walikuwa wakiitwa Shia . . . . . . . . . . . . . . . . . 5915. Sababu za kuenea Ushia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6216. Sababu ya Imam Ali (a.s.) kukaa kimya na kutodai

haki yake . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6317. Imam Ali (a.s.) kama Khalifa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6318. Muawiyah na jinsi alivyoichezea Dini ya Kiislamu . . . . 6419. Makhalifa wa Kidunia na Uchaji Mungu wa Ahlul-Bayt 6420. Uhalifu wa kizazi cha Umayyah na kizazi cha Marwan 6721. Utawala wa Bani Abbasi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6922. Wana wa Imam Ali (a.s.) wasimamizi wa Uislamu . . . . 7023. Zama za heri, wakati wa Imamu Ja’far As-Sadiq (a.s.) . . 71

Page 5: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

24. Mashia wa awali walivyojitoa muhanga . . . . . . . . . . . . . 7325. Sehemu ya Pili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7726. Misingi ya dini ya Kiislamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7727. Tofauti baina ya Mashia na Waislamu wengine . . . . . . 7828. Maasumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7929. Tofauti kati ya Mu’min na Mwislamu . . . . . . . . . . . . . . . 8030. Imamiyyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8131. Maimamu Kumi na Wawili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8132. Hao Kumi na Wawili ni kina Nani . . . . . . . . . . . . . . . . . 8233. Mambo Muhimu juu ya Itikadi na Amali za Kishia . . . . 8334. Tawhid . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8335. Utume (Huu ni mzizi wa pili wa itikadi) . . . . . . . . . . . . . 8436. Itikadi ya Shia Imamiyyah juu ya Qur’an Tukufu . . . . . 8537. Uimamu (Huu ni Mzizi wa Tatu wa Itikadi) . . . . . . . . . . 8638. Tangazo la kumtangaza Ali (a.s.) kuwa ni Imam . . . . . 8639. Imam Ali (a.s.) alipingwa baada tu ya kufariki Mtume

(s.a.w.w.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8740. Kumbukumbu za vitabu juu ya Uimamu . . . . . . . . . . . . 8941. Al-Imam Mahdi (a.s.) na umri wake mrefu . . . . . . . . . . 9142. Maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima ya

kubaliwe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9443. Uadilifu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9544. Jabr Wal-Ikhtiyaar: Kutenzwa nguvu na kuwa na

Hiyari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9745. Al-Ma’ad Siku ya Qiyama . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9846. Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9947. Mwanzo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9948. Mujtahid . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10349. Sala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10550. Masharti kabla ya Sala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10751. Nguzo za Sala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10852. Saumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 109

Page 6: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

53. Saumu zilizo Faradhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10954. Saumu za Sunna . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10955. Saumu zilizo Haramu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10956. Saumu zilizo Makruhu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10957. Sharti za Saumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11058. Zaka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11059. Zakatul – Fitra . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11160. Khums . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11161. Wanaostahiki kupewa Khums . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11262. Hija . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11463. Sharti za Hija . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11464. Jihad (Vita vya Dini) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11565. Namna za Jihadi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11666. Kanuni Mbili Kubwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11667. Shughuli na Biashara kwa nadhari ya Shia . . . . . . . . . . . 11868. Ndoa ya Muda kwa mtazamo wa Shia . . . . . . . . . . . . . . . 12069. Kisa cha Mtanguo wa Aya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12170. Mke anayeolewa katika Ndoa kama hii ni Mke Halali 12271. Upambanuzi na kuondosha utata kuhusu ndoa ya

Mut’a’ . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12972. Masahaba ambao wakiamini uhalali wa Mut’a’ . . . . . . . 13573. Maelezo kwa Ufupi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14574. Talaka Wanavyoona Shia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14775. Namna mbalimbali ya kuvunja Ndoa . . . . . . . . . . . . . . . 14876. Al-Khul-a’h na Mubārāt . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15877. Dhi-haar, Iilaa na Liaa’n . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15978. Urithi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16079. Wakfu, Hiba, na Sadaka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16380. Uqadhi na Hukumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16581. Kuwinda na kuchinja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16882. Hadithi ya Kuvutia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 170

Page 7: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

83. Vyakula na vinywaji viliyohalalishwa na vilivyoharamishwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 171

84. Alama za kumtambua ndege aliye halali . . . . . . . . . . . . . 17285. Vitu vingine ambavyo ni halali au haramu kula au

kunywa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17286. Uharamu wa mkojo na mvinyo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17387. Orodha ya adhabu kwa wanaokwenda kinyume cha

sharia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17488. Adhabu ya kosa la uzinifu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17489. Adhabu ya kulawiti na kusagana (Sahq) . . . . . . . . . . . . . 17590. Adhabu ya Al-Qazf (Masingizio) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17691. Adhabu ya Mlevi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17792. Adhabu ya Wizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17793. Adhabu ya Muhaarib . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17894. Adhabu Mbalimbali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17995. Kisasi na Malipo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18096. Mwisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18597. Sharti za Taqiyyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 189

Page 8: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

1

DIBAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

Katika uandishi uliojaa utata, mara nyingi hudaiwa kwamba Madhehebu ya Sunni ni “Imani Sahihi” ya Kiislamu na kwamba madhehebu ya Shia ni “Madhehebu iliyozushwa”, na ni madhehebu iliyoanzishwa kwa lengo la kufanya mapinduzi ndani ya Uislamu. Wazo hili wakati mwingine huelezwa kwamba “Ushia” ulianza kama harakati za kisiasa na baadaye kupata nguvu ya kidini.

Huu upinzani dhidi ya Ushia, haukomi tu kwa Waandishi wa karne zilizopita, bali hata Wanazuoni wa Kisunni wa karne hii wanakubaliana na mawazo haya. Wanazuoni kama Abul Hassan Ali Nadwi, Manzur Ahmad Nu’mani (wote wawili wa India), Ihsa’n Illahi Zahir (wa Pakistan), Muhibbu ‘d-Din al-Khatib na Mussa Ja’r Allah (wa Mashariki ya Kati); wanaunga mkono mawazo haya. Nadharia hii inakubaliwa pia na kikundi cha Wanazuoni waliohitimu kutoka Seminari za Kidini na ambao hawakusoma kabisa Elimu Dunia. Fazlur Rahman (wa Pakistan) na Ahmad Amin (wa Misri) wamo katika kundi hili.

Kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha kiliandikwa ili kujibu maandishi ya Ahmad Amin aliyoyaandika katika kitabu chake Fajru’l-Islam. Mwandishi mashuhuri wa kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha ni al-‘Allamah ash-Sheikh Muhammad al-Husayn Al-e Kashiful-Ghita (alifariki 1373 A.H.) ambaye alikuwa mmoja wa Mujtahid mashuhuri wa karne iliyopita, kwa mukhtasari ameelezea Imani na matendo ya ibada ya madhehebu ya Shia na halikadhalika michango ya Shia (miongoni mwa masahaba na tabi’in) katika nyanja mbali mbali za Sayansi ya Dini katika Uislamu. Katika kitabu hiki amejadili pia mada kama vile raj’at, ‘Abdulla’h bin Saba’, bada’a, na taqiya.

Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ya Aslu’sh-Shia wa Usuluha ilitafsiriwa na Sheikh Muhammad Nasser (aliyeukubali Ushia hivi karibuni) katika mwaka wa sitini na nane. Marehemu baba yangu Allamah

Page 9: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

2

Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alipelekea Mswa’da wa Tafsiri hiyo kwa Bw. Ibrahim Qassim wa Zanzibar na Agha Sayyid Muhammad Mahdi Shushtari kwa ajili ya kuhaririwa. Wote wawili kwa pamoja walihariri nusu ya Mswa’da huu, na nusu iliyobakia ilihaririwa baadaye na Agha Sayyid Mahdi. Marehemu Agha Mahdi alipohamia Tehran, alianza kutafsiri upya Aslu’sh-Shia wa Usuluha na ilichapishwa kwa mtiririko katika matoleo ya Gazeti la Sauti ya Umma chini ya jina “Asili ya Shi’a” iliyotafsiriwa na Agha Mahdi. Hata hivyo, hiyo haikuwa tafsiri ya kitabu kamili.

Marehemu baba yangu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alipotembelea Iran mwaka 2000, kwa ajili ya matibabu ya moyo, katika kikao chake na Ayatullah Sayyid Ali al-Khamenai, Kiongozi huyu mtukufu alionyesha shauku yake ya kuona kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha katika lugha ya Kiswahili.

Baada ya kuipitia sehemu ya tafsiri iliyokuwa tayari wakati huo, Marehemu Baba alimwambia Sheikh Musabbah Shaban kufasiri upya kwa lugha ya Kiswahili kutoka kwenye toleo la lugha ya Kiarabu kilichochapishwa na “Imam Ali Foundation (Qum)”, yenye rejea fasaha kilichoandikwa na Bw. Alla Al-e-Ja’far, mwaka 1415 A. H. Unayoiona mikononi mwako ni ile tafsiri mpya.

Tunamuomba Allah (s.w.t.) ateremshe Rehema Zake juu ya Roho za Mwandishi, Wafasiri wa mwanzo na Wahariri wote. Pia tunamuomba Allah (s.w.t.) amlipe Sheikh Musabbah kwa kazi hii na amzidishie Tawfeeq aweze kutangaza na kueneza mafundisho ya Uislamu wa kweli miongoni mwa Jamii zizungumzao lugha ya Kiswahili.

Muharram 1426 / Machi 2005 Sayyid Muhammad RizviToronto, Canada.

Page 10: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

3

UTANGULIZI

Vipi Waislamu wanaweza kuwa na umoja?Au tamko la pamoja juu ya kuleta usuluhishi (baina ya Waislamu) hapana budi litamkwe.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

Shikamaneni nyote kwenye kamba ya Mwenyezi Mungu na wala msifarakiane.1

Sasa hivi hakuna mtu mwenye akili au busara ulimwenguni kote aliyebakia hali ya kuwa hatambui kuhusu umuhimu wa muungano na umoja, na madhara ya utengano na kutokuwa na umoja. Siku hizi jambo hilo limekuwa ni jambo linalotambulikana kwa kila Muislamu kama vile anavyoweza kuyahisi matatizo yake binafsi kutokana uzima wake na ugonjwa wake au njaa yake na kiu yake. Bila shaka yote haya ni kutokana na juhudi walizozisimamia wanachuoni wengi wanaotaka mafanikio katika zama hizi za mwisho.

Wanachuoni hao ambao wameilingania jamii ya Waislamu na kuiita kwa sauti kama ile ya mwalimu mahiri, na wakajifananisha na daktari stadi aliyeugundua ugonjwa na dawa yake, kisha lengo lililokusudiwa akalipatia kwa kile alichokibainisha na kukieleza. Si hivyo tu bali wameweza kuziamsha nyoyo (za Waislamu) na kuzihimiza juu ya utumiaji wa dawa hiyo ili kuuondosha ugonjwa huo mbaya na maradhi mengine yanayoangamiza, kabla maradhi hayo hayaja uteketeza mwili huu (Uislamu) uliyohai na kuuweka katika hesabu ya waliokufa.

Viongozi hao walipaza sauti na Waislamu wote wakazisikia sauti zao ya kwamba, “Ugonjwa wa Waislamu leo hii ni huko kutawanyika na kutopatana, na dawa ya kuwaletea uhai si nyingine bali ni kupatana na kuwa na umoja na kutiana nguvu wao kwa wao.” Ni dawa ambayo watakaokuja mwishoni hawataweza kufanikiwa isipokuwa kwa dawa 1 Al-Imraan aya 103

Page 11: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

4

hiyo, Kama ambavyo waliopita nao hawakuwa na mafanikio isipokuwa kwa kutumia dawa hiyo, na kisha kuyatupa chini ya nyayo zao mambo yanayosababisha bughdha, chuki na mafundo ya moyo (baina yao). Mpaka sasa juhudi zinaendelea kufanywa na watu wema (ambao tunamuomba Mwenyezi Mungu awape mwangaza wa mafanikio) ili kulifikia lengo hili tukufu. Isitoshe bado wanaimarisha azma zao na kuwasha mwenge wa utakaso wa moyo kwa ajili ya kuleta upatanishi katika umma huu kutokana vifuniko vilivyofunika nyoyo zao.

Wao daima hawajaacha kuwalingania Waislamu na kuwaita kwenye umoja mtakatifu ambao ni umoja wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja na kuwakusanya Waislamu wote chini ya kivuli cha bendera ya fahari ya Lailaha-illa-llaah Muhammad Rasuulullah bila ya kutofautisha asili zao, mataifa yao wala madhehebu yao.

Wao wanawaita watu kwenye mkusanyiko huu mkuu, na mashiko imara na kamba madhubuti hali ambayo Mwenyezi Mungu ameamuru iimarishwe. Wanawaita watu waelekee huko, kwani huko ndiko uliko uhai na ndiko kwenye uokovu wa umma wa Kiislamu, na kinyume cha hivyo ni maangamio na mauti ya milele. Hao ni walinganiaji wa umoja na ndiyo waliobeba mwenge wa umoja na ndiyo wanaolingania (watu) kwenye haki na ni wajumbe wa ukweli ambao wametumwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wa zama hizi. Kwa hakika wanayakumbusha mafunzo ya Kiislamu yaliyokwisha toweka. Wanainua upya minara ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambayo imekwishafutwa. Na kutokana na bidii na juhudi zinazoendelea za watu hao ambao ni wachache, hapana shaka bishara za wema na kudhihiri kwa mafanikio vimekwishaanza kuonekana. Isitoshe hali hiyo, bali juhudi hizo tukufu zinatambaa na kuenea ndani ya nafsi za Waislamu kiasi kwamba, baadhi yao wameanza kushirikiana kwa ushirikiano wa karibu na kundi moja linajitokeza ili kuhusiana na kundi jingine. Mwanzo wakujitokeza kwa ukweli huu na kukua kwa mbegu na fikra hii, ni lile tukio lililotokea baina ya Waislamu kabla ya miaka michache ilyopita katika mkutano wa mwaka wa Kiislamu uliyofanyika kwenye Msikiti Mtukufu wa Baitul-muqaddas pale walipokusanyika kwa wingi Wanachuoni wakubwa wa Kiislamu na wakabadilishana

Page 12: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

5

mawazo kuhusu mambo ya Kiislamu na kuonyesha kuaminiana na udugu uliyopo baina yao pamoja na kuwepo kwa tofauti katika madhehebu, uraia, umbali wa miji na nchi wanazotoka. Huo ulikuwa ni mkutano wa mwanzo na wa aina yake na ni wa kipekee katika ufunguzi. Ni mkutano ambao Waislamu waliyafunga matumaini yao makubwa kwenye mkutano huo, ukawa ndicho kiliwazo chao kama ambavyo mkutano huo ukawa ni mwiba wa macho kwa wakoloni, bali waliutilia dhana chungu nzima na wakajitahidi kuuuzuwia usifanyike kwa kadri walivyoweza.

Lakini pamoja na maandalizi yaliyofanywa na wanataaluma hao (wa Kiislamu), juhudi na muhanga wote walioutoa wakuu hawa ili wafikie lengo lao la kupanda mbegu hiyo (ya umoja), kisha kuitunza na kuiangalia mpaka itoe matunda yaliyowiva, na yachukuwe nafasi yake ya kuimarika na kuwa na nguvu. Sisi Waislamu kwa mujibu wa mtazamo wa wengi hatujaacha kuwa tunaning’inia kwenye kamba ya matumaini na tunatosheka kwa maneno bila vitendo. Isitoshe tunazunguka kwenye mzunguko wa matarajio bila kuufikia uhakika wenyewe. Tunazunguka juu ya gamba na wala hatufahamu ni jinsi gani tutafika kwenye kiini jambo ambalo ni kinyume kabisa na namna walivyokuwa wazee wetu waliotutangulia. Wao walikuwa ni watu wenye bidii na hamasa, wakweli katika matendo (yao) kabla ya kusema lolote na katika maazimio kabla ya kuongea kitu. Yote hayo ni sifa za wazee wetu ambazo wale wenye ghera wasiokuwa sisi wamezichukuwa kutoka kwa wazee wetu na wakatutangulia. Na hapo zamani sisi tulikuwa ndiyo wenye kutangulia na tulikuwa na nguvu dhidi yao, lakini leo wao wako juu yetu. Huo ndiyo utaratibu wa Mwenyezi Mungu, na wala huwezi kukuta mabadiliko katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu. Qur’an; 33:62

Sisi tunadhani kwamba, tutakaposema kuwa, Tunao umoja na tunayo maafikiano na kwa maneno hayo yakatutia majivuno, kisha magazeti yetu na makala zetu nazo tukazisheheneza maneno kama hayo. Hivi kweli kwa vitu kama hivi na mfano wa haya tunadhani kwamba lile lengo muhimu linalotokana na umoja linaweza kupatikana na kukifikia kile kiwango kinachotakiwa? Na kwa ajili hii ndiyo maana hakuna kinachozidi kwetu isipokuwa kutetereka na kuharibikiwa, kwani huwezi kuyakuta maneno yetu na vitendo vyetu

Page 13: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

6

vina athari yoyote. Hapana shaka kwamba sisi huwa tunaliwazika kwa maneno hayo kwa muda tu baada ya kuyasikia lakini hatimaye huwa yanabakia bila utekelezaji wa aina yoyote ile.2

Ikiwa mambo kama haya yataendelea ni muhali kwa Waislamu kuweza kuimarika au kukubaliana na kusimama kiongozi katika jamii ya watu hata kama magazeti na majarida yatajaa na kuisheheni mbingu na ardhi kwa makelele ya mshikamano na umoja na kila kinachotokana na hayo. Bali hata kama zitazungumzwa hotuba zenye ufasaha mkubwa kwa kutumia mifumo ya fasihi na wakapanga maweko na misingi bora (ya uzungumzaji), yote hayo hayasaidii kitu iwapo hawatajituma kufanya kazi kwa bidii na kuitakasa mienendo yao na undani wa nafsi zao. Si hivyo tu bali wazuwie hasira zao zinazotokana na matamanio yao na nafsi zao kwa kutumia kamba ya akili na mazingatio na hekima. Inapasa kila Muislamu ayaone maslahi ya Muislamu mwenzake kuwa ni maslahi ya nafsi yake, kwa hiyo aweze kuyashughulikia kama vile anavyoshughulikia mambo yake binafsi. Hilo linawezekana tu iwapo kila Muislamu ataondosha kutoka moyoni mwake khiyana na chuki, na kila Muislamu akamuangalia ndugu yake kwa mtazamo wa kidugu na siyo mtazamo wa kiadui. Pia amtazame kwa jicho la kumridhia na siyo kwa jicho la chuki, kadhalika amwangalie kwa jicho la huruma vyovyote alivyo na siyo kwa jicho la hasira.

Hali hiyo inawezekana tu pale (Muislamu) atakapokuwa na ile hisiya ya utu wake na akaona umuhimu wa hisiya yake kiasi kwamba heshima yake ikawa ndiyo heshima anayostahiki ndugu yake na nguvu zake ni nguvu za wasaidizi wake, na kwamba kila mmoja miongoni mwao ni msaidizi wa mwenzake. Hivi kweli kwa hali kama hii kuna atakayeona kuwa ni vigumu kumuimarisha mwenzake na kumsaidia? Kwa nini jambo hili lisiwezekane? Isitoshe ikiwa kujipamba kwa mwenendo huu mwema ni jambo zito lisilowezekana na lengo lililoko kwenye ngazi ya juu isiyowezekana 2 Katika makosa yanayofanywa na viongozi wa nchi za Kiarabu ambazo ni zenye Waislamu wengi ni kule kujali na kuthamini utaifa wao zaidi kuliko Uislamu. Kwao wao dini inakuja baada ya utaifa, yaani Uarabu kwanza kisha Uislamu kama wasemavyo wenyewe, “Ummatuna Ummatul-Arabiyyatul-Islamiyyah.” Yaani taifa letu ni taifa la Kiarabu na ni la Kiislamu.

Page 14: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

7

kuifikia na kwamba Muislamu hawezi kumkunjulia kifua nduguye wala kumpendelea kile akipendacho katika nafsi yake, na akawa haoni kuwa mafanikio yake yanatokana na mafanikio ya umma wa Kiislaamu, basi kwa uchache angalau amfanyie uadilifu na rai nzuri na wala asimpige vita nduguye kwa kumnyima haki yake. Bali pawepo na usawa miongoni mwetu.

Walakini (lengo) hili halitatekelezwa isipokuwa sifa mbaya tulizonazo za tamaa, uhasidi, uchoyo, ubinafsi na kupenda mamlaka zing’olewe kutoka ndani ya nyoyo zetu. Maovu haya ya tabia ndiyo chimbuko la misiba, maangamizo, balaa na msiba. Yote haya yanaposhikamana na kila moja kumtia nguvu mwingine, matokeo yake ni kuangamia kwa umma ambao leo hii unatapatapa na hatimaye utatumbukia ndani ya uovu usio kipimo na maangamio makubwa.

Mbegu ya mabaya yote hayo ni ile sifa mbaya ya kutaka mamlaka, kwani inasemwa kwamba, “Kutaka mamlaka ndiyo chimbuko la uhasidi, na uhasidi ni chanzo cha uadui, na uadui ndiyo sababu ya kuhitilafiana, na kuhitilafiana husababisha kugawanyika na mgawanyiko husababisha kushindwa, na kushindwa ni chanzo cha udhalili na unyonge, na udhalili na unyonge huangamiza madola na hatimaye umma wote huangamia.”

Historia inashuhudia na pia kama tuonavyo kwa macho yetu kuwa popote yalipo maovu na machafu hayo, hapana shaka umma na kila taifa linalohusika huangamia kutokana na kushindwa kwa kila maazimo na kudhoofika kwa misingi yake. Matokeo ya hali kama hiyo ni kujikuta wanakuwa watumwa na wakoloni na mataifa ya kigeni kuwatawala.

Walakini taifa lenye fikara na mawazo yenye kuungana na nyoyo zao zikashikamana na wakashikana mkono kwa mkono na katika shida wakasaidiana na wala hakuna chuki kati ya Taifa, kama hilo hupata heshima na utukufu, huwa ni taifa lenye ushindi na ni imara. Isitoshe taifa kama hilo huwa ni taifa tajirin, na Mwenyezi Mungu hulipa faraja mafanikio na kulipa utukufu na hulipa amani badala ya khofu kila hulifanya kuwa ni taifa linaloongoza.

Page 15: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

8

Waislamu wa zama hizi inawapasa wawakumbuke vizuri wazee wao waliokuwa kabla ya kuja Uislamu. Hawakuwa na makao, walikuwa wanyonge, masikini wa maisha. Hawakuwa na kiongozi wapate kutegemea fikra zake wala hawakuwa na umoja ulinganifu ili waishi salama. Kila aina ya balaa ziliwazonga, ujahili na ujinga iliwavaa, vita zilikuwa nyingi, vita moja baada ya nyingine zilikuwa zikipiganwa. Walikuwa wakinyang’anyana mali kikatili na wakiteketea na wakiwazika watoto wao wa kike bila ya kuwa na huruma wakiwa hai. Si hivyo bali walikuwa wakiabudia sanamu, kukata udugu na kumwaga damu bila sababu. Lakini hebu oneni ni kwa kiasi gani walibadilika baada ya Mwenyezi Mungu kuwaunganisha chini ya kivuli cha Uislamu na wakawa wenye umoja kwenye dini ya tauheed, na rehma ya Mwenyezi Mungu ikawafunika. Matokeo ya yote hayo ni kuwa na maendeleo mazuri chini ya serikali moja yenye nguvu na uwezo iliyotawala, ikawalinda na kuwahifadhi na mambo yao yote yakatengenezeka. Hao ndiyo wale ambao kabla ya hapo walikuwa wanyonge na dhalili, hatimaye wakawa ni watawala juu ya walimwengu ambao hapo kabla walikuwa wakiwatawala. Yote hayo yalipatikana kwa kuwa Waislamu walikuwa na umoja wenye nguvu na udgu wa kweli. Masilahi ya Uislamu yalikuwa yakirishikishwa kwa kila mmoja, kwani Muislamu alikuwa hawezi kuliona tatizo la Muislamu mwenziwe isipokuwa atakuwa tayari kumsaidia na kumlinda. Kisha baada ya miaka mingi kupita, sasa hivi Muislamu hawezi tena kupata (lolote la wema) kutoka kwa nduguye wa karibu licha ya yule wa mbali isipokuwa shutuma na kutengana, hakuna anachokisubiri ila ni vitisho tu kutoka kwa nduguye huyo. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa sasa hivi Muislamu anamtahadhari mno Muislamu mwenziwe kuliko adui yake asiyekuwa Muislamu. Basi ni vipi tutatarajia mafanikio na uongozi imara iwapo hali yetu iko kama hivi? Ni muhali kabisa kuupata umoja au mafanikio, kamwe kabisa Waislamu hawawezi kushikamana iwapo hawatasaidiana wenyewe kwa wenyewe. Basi je, ni vipi katika hali kama hiyo tutakuwa na matumaini ya ushindi na utukufu?

Enyi Waislamu yawapasa mjue kwamba, hamutaweza kuufikia umoja waliokuwa nao wazee wenu kwa kuwa na maneno matamu ya kupeana matumaini, wala kwa kuandika maandiko yanayovutia nyoyo, au kusambaza makala na hotuba za kupendeza na pengine

Page 16: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

9

kwa kutumia makelele ya magazetini. Sivyo kabisa; umoja hauji kwa maneno matupu bali utakuja kwa kuzisafisha niya zetu na kufanya juhudi za kuondokana na kila jambo ambalo limekuwa ndiyo sababu ya Waislamu kuwa katika hali waliyonayo leo. Umoja utaletwa na tabia njema pamoja na sifa adhimu, pia kuweko na maandalizi na nafsi zenye kushikamana pamoja. Umoja ni utungo wa kanuni ya mema, nia njema na upendo. Umoja ni pale Waislamu watakaposhirikiana katika mambo yanayowanufaisha, na wawe waadilifu. Kwa mfano ikiwa katika nchi za Waislamu kama vile Syria au Iraq, kuna makundi mawili ya Waislamu au zaidi, basi ni wajibu wao kufahamu na kujilazimisha kuishi kama ndugu wawili halisi kwa baba na mama waliorithi shamba kutoka kwa baba yao. Hivyo basi mali ile wataigawa kwa uadilifu na wala kundi moja lisijipendelee zaidi kuliko kundi jingine. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema, “Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndiyo wenye kufanikiwa.”3

Maana ya umoja katika umma siyo kundi moja kupokonya haki ya mwenzake au kumkandamiza kisha yule aliyepokonywa haki hiyo au kukandamizwa akanyamaza. Pia siyo uadilifu pale yule aliyedhulumiwa atakapodai haki yake au akawalingania Waislamu juu ya uadilifu aambiwe kwamba analeta vurugu na utengano ndani ya Umma. Bali kinachotakiwa kwa wengine ni kuyachunguza madai yake, kama yatakuwa ni madai ya haki basi ni lazima wamsaidie, na kama madai hayo ni ya kuleta fitina basi wamungoze na kumtosheleza, kama haikuwezekana wajadiliane naye kwa njia iliyo nzuri na pia yawe ni majadiliano mfano wa majadiliano ya ndugu mwema kwa nduguye, wala siyo kwa njia ya matusi na mshambulizi na kuitana majina mabaya ambayo matokeo yake itakuwa ni kuwasha moto wa uadui kati yao, moto ule ambao pande zote mbili zitageuka kuwa kuni za moto huo na wataangamia na mwishowe watakuwa ni chakula cha wageni watakaowameza na hatimaye watamiliki bila ya tabu yoyote.

Leo Waislamu wote hata viziwi na bubu wanajua vema kwamba, kila mahali walipo Waislamu kuna joka la ukoloni wa magharibi

3 Qur’an 59:9.

Page 17: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

10

limefunua mdomo wake ili lipate kumeza kila kilichomo katika nchi za Kiislamu. Je jambo hilo pekee halitoshi kuwafanya Waislamu washikamane? Je hali hiyo pekee haitoshi kuwasha moto wa ghera na hamasa katika nyoyo za Waislamu? Je maumivu hayo makali ya ukoloni hayatoshi kuwa ni yenye kuwaamsha na kuwafanya wawe na umoja na kuua kabisa chuki na husda zilizojengeka miongoni mwao? Kuna usemi usemao kuwa “Wakati wa matatizo ndiyo wakati wa kuondoa chuki.” Inakuwaje basi Muislamu leo hii anakuwa na tamaa ya kumdhulumu Muislamu mwenzake au kumfanya mtumwa wakati huyo ndiye mshirika wake katika nchi toka zama za mababu waliopita hapo kale? Hivi kweli mitihani na mashaka inayowakumba Waislamu leo hii kutoka kwa wasiokuwa wao haitoshi kuwa ndiyo mambo yatakayowalazimisha kufanyiana uadilifu na wema miongoni mwao ili tu iwezekane kupatikana usawa baina yao?

Kwa hakika sisi tunakaribia kukata tamaa juu ya kupatikana matokeo mazuri yatakayoweza kujenga umoja wenye manufaa. Na hali hii inatokana na kukosekana athari na heshima inayostahiki kupewa maneno na juhudi za watu wema wenye dhamira ya kuleta maafikiano kati ya Waislamu.

Yeyote kati yetu lau atayatazama kwa makini yale yanayochapishwa na kusambazwa miongoni mwa khutba zetu zilizojaa semi zenye ufasaha mkubwa zinazohimiza umoja na mshikamano, kisha akaiangalia hali ya Waislamu wa leo namna walivyo, na kwamba hakuna kinachozidi isipokuwa ni kubaguana na kutengana, basi ataona kama kwamba kazi tuifanyayo ni ya kuwalingania Waislamu waongeze migogoro na mashambulizi baina yao, na tunauchochea moto uzidi kuwaka.

Naam, iwapo mtu yeyote atasoma kwa makini maandiko yaliyotawanywa na bwana mmoja aitwaye Nashaa-shibi katika kitabu alichokiita Uislamu Sahihi.4 Kwa ufupi wa kitabu hicho maana ya Uislamu sahihi kwa mujibu wa fikara za Nashaa-shibi si kitu isipokuwa ufidhuli, ujinga na utovu wa adabu dhidi ya Watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w) ambao ni Sayyidna Ali, Bibi Fatima, Hasan na Husain (a.s.). Si hivyo tu bali amekanusha kila fadhila, utukufu

4 Mara nyingi majina hupotosha, kwani anuani na yaliyomo huwa haviafikiani.

Page 18: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

11

na heshima iliyokuja ndani ya Qur’an na Riwaya sahihi zilizowatajwa kwa sifa njema.

Kwa mfano aya ya Tat-heer (utakaso). Isemayo kuwa, “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na kukutakaseni mno enyi watu wa nyumba (ya Mtume).”5 Kwa mujibu wa itikadi ya Nashaa-shibi yeye anasema kuwa, “Aya hiyo inahusikana na wake za Mtume (s.a.w.w.) na hasa mama Aisha”, bali kwa itikadi yake Ahlul-Bait hapana mwingine isipokuwa mama Aisha tu! Na amma Fatima (a.s.) ambaye ni sehemu ya kiwiliwili cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anamtoa kabisa katika Ahlul-Bait.6

5 Qur’an, 33: 336 Hakika jambo la kuhuzunisha ni kukuta kwamba, baada ya yote yaliyoandikwa, kusemwa na kuthibitishwa ya kwamba aya ya utakaso iliteremshwa kuhusu watu wa kishali (shuka) ambao mjumbe wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. aliwakusanya wao tu (na kuwafunika kwa kishali hicho na watu hao walikuwa) ni Ali, Fatmah, Hasan na Hussein (a.s.), (cha ajabu ni kuwa) utawakuta baadhi ya watu bado wanang’ang’ania tena mno kuugeuza ukweli huo na kuupotosha na wanajitahidi kuvutia upande wa madai yao batili. Kwa hakika yeyote atakayefuatilia uzushi wao huu usiyotegemea msingi wowote wa kielimu, hapana budi atalazimika kuuona uzushi huu kuwa ni dhaifu kwa kila namna japokuwa baadhi yake unaweza kujidhihirisha kuwa unao ukweli na umesihi, bali wengine utawalazimisha kuwapelekea kuonesha sababu za ubinafsi na chuki za kimadh-hebu na bughdha inayoudhuru Uislamu na Waislamu.

Pia (chuki hiyo na bughdha hiyo) inapelekea kuleta mfarakano na ugomvi na wala haijengi udugu na umoja (kati ya Waislamu) jambo ambalo tumekuwa tukililingania na bado tunalihimiza, na tutabakia katika msimamo huo (siku zote) kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Naam, haya ni baadhi ya mambo tunayotaka kuyasema, na tumeyakariri mara nyingi bila kubabaika wala kukata tamaa.

Na katika kipindi hiki ambacho tunachambua kurasa za kitabu hiki, sisi hatuna makusudio ya kuurudi ubatili na uongo mbaya, kwani jambo hilo linachukua nafasi kubwa kitu ambacho siyo lengo letu, na pia kutokana na wanachuoni wetu wengi na wanafikra wa madh-hebu yetu kulishughulikia hilo tangu zamani mpaka siku hizi. Maudhui hiyo wameijadili na kuyaweka wazi makusudio na mipaka yake, lakini hali hii haituzuwii kutokuashiria baadhi ya riwaya zilizotajwa ndani ya vitabu vya wenzetu, riwaya ambazo zimeeleza kwamba aya hii iliteremka kwa ajili ya haki inayowahusu watu hawa watano na si wengine. Basi (kwa kulithibitisha hilo) rejea: Sahih Muslim J. 4 uk. 1883/2424, Sunan Tirmidhi J. 5 uk. 663/3787 na 699/3871, Musnad Ahmad J. 4 uk 107 na J. 6 uk 292, Sunan Baihaqi J. 2 ⇒

Page 19: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

12

Bila shaka si Nashaa-shibi peke yake mwenye mawazo na itikadi kama hiyo bali kabla yake walikuweko kina Nasuuli na Al-Hisan na wengine kama wao.

Kwa hali hiyo ndugu msomaji unatarajia kwamba hali ya Waislamu inaweza ikatengenea na kuondosha mtawanyiko na kutopatana badala yake ukaja umoja, uaminifu na ukweli? Je kwa mambo yalivyo huoni kwamba ninayo haki ya kuvunjika moyo na nikate tamaa?

Je Nashaa-shibi na wenziwe ambao wanawashutumu Mashia na Maimamu wao (a.s.) hawafahamu kwamba kitendo hicho kinaweza kumfanya mmoja katika waandishi wa Kishia naye akafanya vivyo hivyo na kuwahujumu vibaya Makhulafaa Rashideena wa Kisunni? Kuna msemo maarufu ya Waarabu usemao kuwa, “Hakika watoto wa ami zako pia wanayo mikuki.” Kwa hali kama hii yawezekana kabisa kuutumia msemo kama huu. Na iwapo hali hii ikiachwa ikaendelea itafanya kila upande kumshambulia mwenzake. Je unadhani ni faida gani itakayopatikana?

Kuna haja kwa Wanachuoni na wataalamu wenye fikra njema wa pande zote mbili kufikiria na kutazama ni nini itakuwa hatima ya Waislamu ambao sasa hivi wamefikia kwenye pango la hatari, na pia wachunguze kwa makini juu ya hali hii na je kuna faida gani watakayoipata kwa kuyaachia mambo hayo yaendelee?

Kwa hakika hakuna kosa lolote alilonalo Shia isipokuwa ni kwa sababu tu ya kuwatawalisha Watu wa ndani ya nyumba ya Mtume wao (s.a.w.w.).

Pamoja na yote hayo hapaswi kuvunjika moyo na kukata tamaa kutokana na Rehema ya Mwenyezi Mungu na kwa fadhili makhsusi ambayo Mola anayo juu ya dini na sheria yake.

⇐ uk 149, J. 5 uk. 152, Tarikh Baghdad J. 10 uk. 278, Tafsir Tabari J. 22 uk. 5, 6 na 7, Riyadh an-Nadhrah J. 3 uk. 152, Usudul-Ghabah J. 1 uk. 490 na J. 3 uk. 543 na 607, Mustad-rak al-Hakim J. 2 uk. 416 na J. 3 uk 147, Maj-mauz-Zawaid J. 9 uk. 121 na 167, Al-Fusul-Muhimmah uk. 25, Dhakhair-ul-Uqba uk. 21, Faraidus-Simtain J. 1 uk. 25, Durul-Manthoor J. 5 uk 198, Kifayatut-Talib uk. 371, As-Sawaiqul-Muhriqah uk. 187 na 238.

Page 20: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

13

Matarajio yetu ni kwamba Mwenyezi Mungu atawaongoza watu wenye ghera na uchungu juu ya Uislamu kutoka pande zote mbili waidhibiti ile mikono inayosambaza na kueneza maandiko mabaya yenye sumu yanayolenga kuuangamiza Uislamu. Kutokana na mtumaini hayo, hiyo imekuwa ndiyo sababu iliyotufanya tutoe idhini ya kuchapisha upya kitabu hiki kwa mara ya pili na kuusambaza muongozo uliyomo miongoni mwa maelekezo yetu na mafunzo yetu ili kumhimiza kila Muislamu kuusimamia wajibu huu na jambo hili muhimu (la kurejesha udugu na umoja miongoni mwa Waislamu wote) kila mmoja awajibike kwa kiasi cha uwezo wake na nafasi yake. Na sharti yake ya mwanzo, ni kuufunga kikamilifu mlango wa majadiliano ya kimadh-hebu kwani iwapo mmoja wetu atataka kuyakosoa madh-hebu yake basi iwe ni kwa sharti ya kuingilia madh-hebu ya wengine kwa ubaya wala kwa njia ya kushutumu.

Na sharti ya pili ambayo ni ya mwanzo kutokana na umuhimu iliyonao ni juu ya kila Muislamu kuufunga moyo wake kwa nduguye Muislamu, na ampendelee yale ayapendayo kwa nafsi yake na pia ajiepushe na chuki na husda dhidi ya nduguye kikweli kabisa. Yote haya asiyafanye hali ya kuwa anamhadaa mwenzake ulimini tu kutokana na maslahi yake binafsi kama hali ilivyo leo hii kwa wote.

Hapana shaka kwamba umoja wa kweli na udugu sahihi ambao Uislamu umekuja nao na ambao mataifa mengine yanafanikiwa kwa kuutumia umoja huo na pia yameweza kuheshimika na kuwa na nguvu, ni pale tu kila mmoja ndani ya Umma atakapoona kwamba maslahi binafsi ndiyo hayo maslahi ya Umma, bali awe na mtazamo zaidi ya huo.

Sifa hii ni nyepesi kuitamka kwenye ulimi lakini ni ngumu mno kitekelezaji, na inakaribia kuwa ni jambo lisilowezekana kwetu sisi Waislamu, hasa kutokana na kila kikundi kinapokitazama kikundi kingine kwa mtazamo wa uadui mkubwa na uhasama mkali. Na iwapo itatokezea kimojawapo kujionesha kwa wema katika maneno, au kudhihirisha mapenzi, basi huyu mwingine hawezi kuonesha wema kama huo zaidi ya kujitahidi kumuepuka mwenzake na au kumhadaa pengine tu apate kuchukua mali yake au kumdhulumu

Page 21: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

14

haki yake. Kwa hakika wote wamezama ndani ya giza na wala hakuna kelele yoyote ya mwenye kuwapigia na wala hakuna makemeo yoyote wala mawaidha yatakayowazuwia kuyatenda hayo wayatendayo.

Wote wamemsahau adui yao au wanajifanya kumsahau adui huyo wakati yeye anawafuatilia kwa makini nyendo zao hali ya kuwa hamu yake kubwa ni kuwaangamiza na kuwafuta wote kabisa. Hakuna njia anayoitumia isipokuwa kusambaza mbegu ya utengano miongoni mwao aili wapigane wao kwa wao na amewawekea chungu nzima ya mitego ili apate kuwanasa. Kwa hakika Waislamu hawawezi kusalimika kutokana na mitego hiyo iliyosambazwa katika kila njia waipitayo ispokuwa kwa kuurudisha umoja wao kwa vitendo na wala siyo kwa maneno, kwa juhudi zote na wala siyo katika hali ya uzembe na ugoigoi.

Fikra pekee niionayo inayoweza kuwasaidia Waislamu kuimarisha umoja miongoni mao, ni kuitisha mkutano wa Wanataaluma na Wanachuoni wa Kiislamu kila mwaka au kila baada ya miaka miwili ili kwanza wafahamiane na pili wapate nafasi ya kubadilishana mawazo baina yao kuhusu mambo ya Uislamu. Bali jambo la wajibu zaidi kuliko hilo ni kuitisha mkutano wa viongozi wa nchi za Kiislamu (iwapo tu Waislamu wanao viongozi wa haki) wawe kitu kimoja, bali wawe sawa na mikono miwili ndani ya kiwiliwili kimoja. Viongozi hawa wazuie kila aina ya hatari iliyowazunguka Waislamu kila upande. Ili kuitambua hatari hiyo hakuna shaka kwamba matukio yaliyotokea baada ya vita kuu yanatosha kuwa ni somo, na ni mawaidha tosha kabisa ikiwa wao ni wenye kufanya mazingatio.

Ni juu yao kukumbuka ni jinsi gani Wataliano walivyoifanya nchi ya Ethiopia pale tu walipoikalia kwa muda wa miezi michache jambo ambalo lilipelekea kuharibu makazi ya wananchi wa nchi hiyo na kuwafanya kutokupata usingizi. Inawapasa waiangalie hali yao ya baadaye kwa kila namna ya tahadhari vinginevyo (yatakayowapata ni madhila makubwa ambayo mimi nina hakika) kwamba wao wanafahamu mno ni jambo gani litakalotokea.7

7 Jaribio la kwanza la Wataliano kutaka kuishambulia Nchi ya Uhabeshi (Ethiopia) lilifanyika mwishoni mwa karne ya kumi na tisa A.D., lakini Wataliano walishindwa vibaya mwaka huo wa 1896 na walipata hasara kubwa mno toka ⇒

Page 22: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

15

Kiasi hiki cha maelezo kinatosha kuwa ni maonyo na mawaidha na kufanya uzindushi kwa Waislamu, nasi katika kuikamlisha faida katika chapa hii tumejitahidi kufanya masahihisho kuondosha mapungufu yaliyojitokeza katika baadhi ya uchunguzi na uchambuzi wa kitabu hiki na kufikia hali ya uchunguzi mpana zaidi na kuyapa maudhui yaliyomo haki yake inayostahiki ikiwa ni pamoja na hamu yetu ya kuyafanya maelezo yaliyomo kuwa ni yenye muhtasari ili lengo muhimu lililokusudiwa lipate kutimia na pia kuwaweza watu wa namna zote kuweza kukisoma kwa wepesi.

Jambo muhimu katika zama hizi tulizonazo na hizo zijazo hapo baadaye, ikiwa wao watapendenda kukikunjuwa zaidi kitabu hiki (hakuna kizuwizi) sisi tumewafungulia mlango wa kulifanya jambo hilo na tumewawekea njia isiyokuwa na mashaka wala taabu, njia ambayo iko karibu mno na mazingira ya wakati tulionao na elimu za wakati huu.

Tunasema hivyo kwa sababu ndani ya kitabu hiki tumetumia njia yenye manufaa na wala hatukuyapanda madhehebu yoyote yale wala kuigusa heshima ya mtu fulani kwa ubaya. Pamoja na hali hiyo hatukuacha kutaja baadhi ya dalili na hoja (kuhusu uhaki wa Madhehebu ya Shia) na tumetaja rejea mbalimbali kwa ujumla.

Kuwafiqishwa kunatoka kwa Mwenyezi Mungu, nami kwake ndiko ninakotegemea na kwake ndiko nitakako rejeshwa.

Muhammad Husein Aalu Kashiful-GhitaUtangulizi huu umeandikwa katika mwezi wa

mfungo saba mwaka 1355 Hijria.

⇐ kwa jeshi tiifu la Wahabeshi.

Hata hivyo Wataliano walijaribu tena katika kipindi cha Musolini, na huo ulikuwa mwaka 1935 A.D, pale majeshi yao yalipoivamia ardhi ya Uhabeshi na wakafaulu kuiteka mwaka 1936 A.D. na kuiingiza ndani ya makoloni yao wakifuata nyayo za washirika wenzao miongoni mwa wakoloni wa zama hizo kama Uingereza, Ufaransa na Ureno. Uhabeshi ilibakia chini ya ukoloni wa Italia hadi mwaka 1941 walipofukuzwa na jeshi la Waingereza.

Page 23: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

16

UTANGULIZI WA CHAPA YA SABA ULIOANDIKWA NA MTUNZI WA KITABU HIKI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

(Ewe mola kikunjuwe kifua changu, na uyafanye mambo yangu kuwa mepesi, na uniondoshee fundo ulimini mwangu

ili kauli yangu ipate kufahamika.)8

Jambo lililo wazi na lisilohitaji kubainishwa, ni ile hali waliyoifikia Waislamu hasa katika karne hizi za mwisho kutokana na unyonge, udhalili, kuporomoka na hatimaye kutawaliwa na wageni kutoka nje na kufanywa watumwa. Si hivyo tu bali wageni hao wamemiliki ardhi yao na miji yao na wana tumiwa kama wanavyotumiwa wanyama. Wageni hao wanafanya hivyo kwa maslahi yao, na wanawanyonya mno Waislamu na kuwatendea maovu mengi yatakayowaingiza katika hasara kubwa na unyonge usio na kifani. Yote hayo yako wazi kama ambavyo sababu zilizosababisha hali nazo ziko wazi bila kificho. Lakini sababu ya pekee ni kule kutengana, kufarakana, kugombana na uadui ulioko baina ya Waislamu, na kisha kila kikundi miongoni mwao kuwakufurisha wenzake.

Kutokana na mazingira ya kutokuwepo maafikiano baina ya Waislamu kiasi cha wao kukufurishana wenyewe kwa wenyewe, imefikia kiasi cha kikundi kimoja kinapowakufurisha Waislamu wengine, basi hapo ndipo pasipokuwa na muhali katika kuwashambulia na kuwaangamiza waislamu wenzao. Hakika yote hayo hayfanyiki ispokuwa ni kutokana na ujinga ulioenezwa miongoni mwao, ujinga ambao umewapofua macho na uanawavuta kuwaelekeza kwenye hali ya kuvuka mipaka. Kwa hakika vitimbi vya wageni kutoka nje ndivyo vinavyowadanganya. Hapana shaka kwamba, kalamu za waandishi mbali mbali na hotuba za wazungumzaji wengi, zimejaa ndani ya magazeti na vitabu vingi kuhusu maudhui hii inayohusu suala la kuhimiza umoja na 8 Qur’an, 20: 25-28.

Page 24: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

17

maelewano miongoni mwa Waislamu. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kukuta kwamba masikio ya Waislamu yanapuuza kila kilichomo ndani ya nasaha hizo ambazo wachapishaji nao hawakufanya ajizi kuzichapisha.

Ndani ya utangulizi wa chapa ya pili ya kitabu hiki tuliweka anuani isemayo, “Vipi Waislamu wanaweza kuwa na umoja? Au tamko la pamoja juu ya kuleta usuluhishi (baina ya Waislamu) hapana budi litamkwe.”

Makusudio ya kuweka bayana katika tamko hilo ilikuwa kama ifutavyo. Kwa hakika sisi tulipoikuta hali ya Waislamu iko kama hivyo tulivuyoielezea hapo kabla, na tukawaona Waislamu wako katika makundi mawili makubwa ambayo ni Shia na Sunni na kwamba makundi mengine yaliyobakia yanarejea katika kundi la mwanzo au la pili kiasi ambacho inafaa kabisa kuitwa kuwa ni kundi la Kiislamu. Baada ya kuichunguza hali hiyo tumeona kwamba Mashia na hasa Wanachuoni wao wanayaelewa vizuri madhehebu ya ndugu zao Masunni kama wanavyoyaelewa madhehebu yao kiasi ambacho wameandika na kutunga vitabu vingi juu ya hilo. Kwa mfano kitabu kiitwacho Al-Intisari kilichoandikwa na Sayyid Murtadha, Al-Khilafu cha Sheikh Tusi, At-Tadhkiratu kilichoandikwa na Allamah Hilli na vingi vinginevyo vilivyoandikwa na Wanachuoni wengine wasokuwa hawa.

Amma ndugu zao Masunni ukiachilia mbali watu wa kawaida bali Wanachuoni wao hawana wakijuacho kuhusu uhakika na ukweli wa madhehebu ya Shia, zaidi ya hapo Wanachuoni wa Kisunni wanawaona Mashia kuwa ni watu walio nje kabisa ya dini hii ya Kiislamu na kwamba wao Mashia ni watu wanaovunja Uislamu. Isitoshe hali hiyo bali wanawanasibisha na kila aina ya ubaya. Kutokana na hali hiyo pindi Mashia nao wanapokuta mashambulizi dhidi yao ndani ya vitabu vya wenzao, nao kutokana na chuki na hasira za mashambulizi, huwakabili wenzao kwa hali ile ile waliyoikuta ndani ya vitabu vya Kisunni au zaidi ya hapo.

Hali kama hii na mazingira kama haya ndiyo yaliyopelekea kuvunjika

Page 25: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

18

kwa umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu, na hilo limekuwa ni kiliwazo kizuri kwa wakoloni na ndiyo maana wameweza kutimiza malengo na matarajio yao.

Kwa matokeo hayo ndipo mimi nilipoona kuwa kuna umuhimu mkubwa na ni dharura kwangu mimi kuandika kitabu japo kwa ufupi ili niwabainishie Waislamu Misingi na Matawi ya itikadi zilizomo ndani ya Madhehebu ya Shia, na ni vipi madhehebu haya yalivyoanza, nani aliyeyaanzisha na ni sababu zipi zilizopelekea kukua kwake. Ndipo nilipotunga kitabu hiki kiitwacho Aslu’sh-Shia wa Usuluha.

Nimetumia njia nyepesi kwa sababu kitabu chenyewe hakikuwa ni kitabu kinacholenga kufanya malumbano na majadiliano kiasi cha kuwepo ulazima wa kusimamisha dalili na hoja, bali ni kueleza misingi tu ya mas-ala yanayohusika ili watu wapate kufahamu daraja na nafasi ya Ushia ndani ya Uislamu, na ni namna gani Ushia unavyoshikamana na dini na kanuni za Uislamu.

Kwa hakika hatukutarajia kabisa kwamba kitabu hiki kingeweza kupata hadhi kwa haraka namna hivyo, na kwamba kitakubalika mno, kwani mpaka sasa hivi kimekwisha kufasiriwa katika lugha nyingi na kuchapishwa karibu mara tano. Lakini jambo la kusikitisha mno ni kuwa hali ya Waislamu bado iko vile vile na wala kitabu hiki hakikuweza kupunguza chuki za watu, na wala hakikuweza kukata makali yao, bali kalamu za Mashekhe wa Kimisri bado ziaendelea kuwashambulia Mashia katika kila minasaba na kuwahukumu kwamba wao wamepotea.

Mashambulizi kama haya yalikuwa yakinasibishwa kwa Mashia katika zile zama za giza na ndani ya karne za kipindi cha kati ambacho ni kipindi walichoishi kina Ibn Al-Khaldoun, Ibn Hajar na wengineo mfano wa hao. Cha ajabu ni kwamba kitabu hiki Aslu’sh-Shia wa Usuluha chapa yake ya tatu kimechapishwa nchini Misri na nakala zake zote zikagawiwa huko.

Hivi kweli bado haujafika wakati unaofaa, au tuseme kuwa ni

Page 26: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

19

wajibu kwa wanachuoni hao na wengine kupunguza mashambulizi yao dhidi ya Mashia? Wapi bwana, bali bado wanaendelea kudai kwamba Mashia ni kikundi cha watu wa Bida’ na chenye mtazamo potofu!! Chuki zao na mashambulizi yao yanaendelea hadi kurudi nyuma kwenye zama za utawala wa dola ya Fatimiyyah. Kwa nini kurudi mpaka kipindi hicho? Hakuna sababu isipokuwa ni kwa kuwa watawala wa dola ya Fatimiyyah walikuwa ni Mashia, na wakapachikwa jina la Marafidhi na eti nasaba yao inaanzia kwa Myahudi kama wasemavyo baadhi yao. Wanaendelea kusema kuwa, “Itikadi ya watawala hao wa dola ya Fatimiyyiha ilikuwa ni itikadi ya Walahidi.”

Yote haya yanasemwa bila kukumbuka kwamba watawala wa dola ya Fatimiyyah walitoa mchango mkubwa sana kwa Uislamu kwa jumla na hasa hasa kwa nchi ya Misri. Watawala wa dola hiyo walieneza elimu na ustaarabu katika nchi ya Misri kwa kujenga vyuo na misikiti mingi. Walitengeneza merikebu za kivita ili kujilinda kutokana na mashambulizi ya maadui wa Uislamu. Ndugu msomaji hivi kweli hushangazwi na mashambulizi na shutuma za Wamisri dhidi ya dola hiyo ya Fatimiyyaha, wakati wewe na wao mnafahamu wazi kwamba ile fahari kubwa na ya kipekee nchini Misri ambayo ni miongoni mwa urithi ulioachwa na watawala wa dola ya Fatimiyyah, nayo si nyingine bali ni kile chuo kikuu cha Misri kiitwacho Al-azhar?9

9 Chuo Kikuu cha Az-har kinahesabiwa kuwa ni miongoni mwa athari kongwe za Kiislamu (na hili ni jambo lisilo na ukinzani). Ni Chuo ambacho licha ya kuwa ni cha muda mrefu uliopita, kimebakia kuwa ni kielelezo madhubuti kinachowakilisha athari za kale zinazoshuhudia kuchomoza kwa nuru ya Uislamu mbele ya baadhi ya madola na miji japokuwa dini hii tukufu imezungukwa na vitimbi na vita.

Kadhalika Chuo hiki cha Az-har kimekuwa ni mojawapo ya hayo matunda matukufu tena yenye baraka, kwani kilianzishwa katika zama za dola ya Fatimiyyah na kiliitwa Az-har ili kutabaruku kwa jina la Bibi Fatimah Az-Zahra ambaye ni mwanamke bora kuliko wote ulimwenguni, Rehma nyingi na Amani zimshukie.

Msikiti huu ulijengwa na Jauhar As-Siqli kiongozi wa jeshi la Abu-Taim Ma’ad. Ujenzi huo ulifanyika baada ya mwaka mmoja tangu Fatimiyyiina walipoiteka Misri na kusimamisha dola yao nchini humo katika mwaka 359 A.H. Jengo lake lilipokamilika ilisaliwa rasmi Ijumaa ya kwanza tarehe saba ya mwezi wa Ramadhani mwaka wa 361 A.H. sawa na 972 A.D. Kabla ya hapo sala ya ⇒

Page 27: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

20

Hapana shaka kwamba, zama hizo za dola hiyo zilikuwa ni zama tukufu zenye mafanikio yaliyokuwa yakiongoza ulimwengu, kutokana na chuo hicho ambacho kimetoa mamia ya Wasomi miongoni mwa Wanachuoni wakubwa na viongozi wa kisiasa wa Kimisri kama vile Sheikh Muhammad Abdoh na Saad Zaghloul na wengineo katika watu walioitumikia nchi ya Misri na Uislamu kwa jumla.

Kuendelea kubakia kwa taasisi hii ya Kiislamu kwa zaidi ya miaka elfu moja na heshima na mafanikio iliyokwisha kujipatia na inayoendelea kujipatia kila mwaka, ni ushahidi tosha kabisa juu ya kuonesha ni namna gani aliyeiasisi na kuijenga alikuwa na utakaso wa moyo.10 ⇐ Ijumaa ilikuwa ikisaliwa katika msikiti wa Amri na wakati mwingine ikisaliwa katika msikiti wa At-Tooloni.

Msikiti huo ulibakia kuwa ni kituo cha wenye kusali na ziyara nyinginezo hadi ilipopita miaka michache Qadhi Mkuu Abul-Hasan Ali Ibn Nuuman Al-Qairawani alipoanzisha masomo ambapo aliusoma (na kuusomesha) mukhtasari wa baba yake juu ya Fiqhi ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na huo ulikuwa ni mwezi wa mfungo tano mwaka 365 A.H. sawa na mwaka 975 A.D.

Msikiti huu uliendelea kutunzwa na watawala wa dola ya Fatimiyyah ambapo baadaye Mustansir na Hakim walipoliongeza jengo lake na kulipanua, na walikuwa wakipokea makundi ya wanafunzi wanaotafuta elimu nyingi iliyo bora toka kwa Waalimu wa hapo.

Msikiti huo ulibakia hivyo kwa muda mrefu mpaka pale dola ya Fatimiyyah ilipomalizika na hatimaye alikuja Salahud-Din Al-Ayyubi akalinyoosha panga lake ili kuwapiga vita Mashia na kuwauwa popote pale alipowakuta na kufuta athari zao na waliyoyafanya. Pia akazuwia kusomwa khutba ndani ya msikiti kisha akayapuuza mambo mengi aliyokuwa ameyasimamisha Hakim hapo msikitini.

Vita hivi viliendelea kwa muda unaokaribia karne moja, mpaka pale Mfalme Ad-Dhahir Baibris alipoamuru khutba irejeshwe msikitini hapo na akahimiza masomo katika misingi bora, si hivyo tu bali aliongeza baadhi ya majengo.

Basi hivi ndivyo Az-har ilivyoshuhudia misukosuko mingi ya kila aina (ikawa ni baina ya) kuendelea na kuanguka ambako kulitokana na athari za matukio tofauti yaliyouzunguka ulimwengu wa Kiislamu. Pamoja na yote hayo Chuo cha Az-har kimebakia kuwa ni athari ya kudumu inayozishuhudia hizo zama zilizopita ambazo dola ya Fatimiyyah ilitawala Misri na kuyaongoza mambo yake.10 Utakaso wa moyo: Maana yake ni kulifanya jambo fulani la wema kwa nia njema na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Page 28: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

21

Jambo la kusikitisha ni kwamba, waanzilishi wa taasisi hiyo ambao ni watawala wa dola ya Fatimiyyah, mbele ya Wamisri wanaonekana ni watu ambao nasaba yao siyo ya halali, wanaambiwa kuwa ni Walahidi katika dini, bali wanaitwa kuwa ni Marafidhi, kwa sababu tu walikuwa ni Mashia.

Lakini ni vema ikafahamika kwamba pamoja na yote hayo wanayotupiwa, taasisi hiyo inaendelea na bado iko chini ya uangalizi na msaada mkubwa wa Mwenyezi Mungu.

Si hayo tu bali yako mengi yanayohusu shutma dhidi ya Mashia ikiwemo ile isemayo kuwa, “Eti Mashia husimama kila siku usiku baada ya sala ya magharibi kwenye Sardaab11 huko Samarra nchini Iraq na kuanza kumpigia makelele Imam wao kwa kusema, Toka Toka….” Basi na mengi mengineyo miongoni mwa uzushi alioueleza Muheshimiwa Mwanachuoni wa Kisunni ndani ya kitabu chake kiitwacho Al-harakatul-fikriyyah ambacho kimechapishwa hivi karibuni.12 Tuhuma hii ni sawa na kichekesho ambacho baadhi ya washupavu na wapuuzi wa tangu karne nyngi zilizopita wamekuwa wakiwatuhumu Mashia kuhusu jambo hilo, ni mambo yanayokaririwa mara kwa mara bila ya kuhakikisha ukweli au uwongo wa maneno hayo.

Lakini jambo linalostaajabisha mno ni kuwa Samarraa ni mji wanaoishi Masunni na zuri zaidi ni kuwa, Msikiti ambamo imo hiyo Sardaab uko mikononi mwa Masunni na wanaswali humo Msikitini sala zao za Ijumaa na zile za jamaa katika nyakati zote tano, na kamwe Mashia hawana mamlaka yoyote katika Msikiti huo isipokuwa kupita njia na kuingia humo kwa ajili ya kufanya ziyara, kusali na kusoma dua. Na wanafanya hivyo kwa sababu ndani ya Msikiti huo wamezikwa Maimamu wao watatu ambao walikuwa wakisali humo sala za tahajjudi na wakifanya faragha humo kwa ajili ya ibada za Mwenyezi Mungu usiku na mchana. Maisha ya Maimamu hao (a.s.) yalikuwa ni maisha ya uchaji Mungu, usiku kwao ilikuwa ni wakati wa kusali tahajjudi na ibada zinginezo, na mchana waliutumia kwa 11 Nyumba ambayo hujengwa chini ya ardhi na mara nyingi hutumika katika kipindi cha baridi huko Mashariki ya Kati.12 Mwandishi wa kitabu hicho anaitwa Doctor Abdul-latif Hamzah.

Page 29: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

22

ajili ya kutoa mafunzo ya dini. Kwa hakika usiku na mchana katika mji huo wa Samarra, wao walivitumia kwa ajili ya tahajjudi na ibada mbalimbali, na wakati huo huo Mutwakkil alikuwa ndiyo Khalifa wa Waislamu, lakini yeye aliutumia mchana na usiku kwa ajili ya ulevi na vinywaji vinginevyo. Si hivyo tu bali alikuwa akikusanya wanawake wakimuimbia na kucheza mbele yake na pia walikuwepo wachekeshaji mbalimbali akiwemo Ubbadah Al-mukhannath na wengineo. Kiongozi huyu alizama katika machafu hayo mpaka akajisahau kiasi cha kwamba, Waturuki walipomshambulia yeye na waziri wake aliyekuwa akiitwa Al-fathu ibn Khaqaan, walikatwakatwa kwa mapanga hali ya kuwa ulevi umewatopea hawajitambui na hakuna kilichowazindua isipokuwa ule ukali na maumivu ya mapanga yale. Kutokana na mashambulizi hayo mabaya Mutawakkil na waziri wake walivurugwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulikana huyu ni nani na huyu ni nani.

Ewe ndugu msomaji, hivi kweli Mashia wanalaumiwa eti tu kwa sababu ya kuzitukuza nyumba za Maimamu wao, nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu jina lake litajwe humo na kutukuzwa?

Hebu basi na turudi kwenye makusudio yetu na tuyabainishe, makusudio ambayo sisi kwa upande wetu baada ya kukisambaza kitabu hicho kidogo tulikuwa tunatarajia kuwa kitaleta athari na nguvu ikiwa ni pamoja na kuleta uadilifu (miongoni mwa makundi ya Kiislamu) kiasi cha angalau kupunguza maneno makali baina ya Waislamu na pia kuwafanya wakaribiane. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna tulichokipata isipokuwa kukatishwa tamaa na matumaini kututoka, na imetufahamisha hali kwamba itikadi hizo zilizoko kati ya waislamu ni itikadi mbambazo zimekuwa ni urithi na ni tabia za watu hawawezi tena kuziondosha.

Kwa hakika watu wa kawaida miongoni mwa makundi haya mawili ya Kiislamu (Shia na Sunni) hawana lawama yoyote kutokana na dhana mbaya iliyoko kati yao kila mmoja kumdhania vibaya na kumfanyia uadui mwenzake. Lakini wenye lawama ni Wanachuoni na Wanataaluma wa makundi haya mawili ambao wao ndiyo wanaouchochea moto wa uadui na chuki, wakati ambapo Mwenyezi

Page 30: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

23

Mungu amewafanya Waislamu kuwa ni ndugu, na dini yao ni dini ya Tauhidi na Umoja.

Pamoja na hali iliyopo ya kukata tamaa na huzuni zenye kutia uchungu, kuna watu na hasa mwanangu Muhammad Kadhim Alkutubi ambao wameniomba kukichapisha tena kitabu hiki kwa mara ya saba, na wameniomba pia niongeze baadhi ya nyongeza muhimu na niweke istilahi mbali mbali na kukikunjua zaidi. Hapana shaka kwamba jambo hilo tumelikubali lakini katika mazingira ya kutokuwa na matumaini ya kupatikana udugu baina ya Waislamu.

Katika baadhi ya milango tumeongeza nyongeza ambayo haitakifanya kitabu hiki kutoka kwenye lengo lake la kuwa ni muhtasari, kwani katika zama tulizonazo kufanya kitu kwa muhtasari ni jambo rahisi kukubalika.

Ewe Mola wetu, kwako wewe ndiko kwenye mategemeo na kwako ndiko tutakako rejea.

Page 31: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

24

SABABU ZILIZONIFANYA NIANDIKE KITABU HIKI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Kwa Mwenyezi ndiko ninakotegemea na ndiko ninakoomba msaada. Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kutoa salamu kwa waja wake wateule, Mimi Muhammad Husain Kashiful-Ghita kutoka Najaf mwandishi wa kijitabu hiki ambacho nimekiandika mwanzoni mwa mwezi wa mfungo nane, baada ya kupita miaka ipatayo elfu moja mia tatu tangu Bwana Mtume kuhama Makka kwenda Madina. Sababu zilizonifanya kuandika kijitabu hiki ni kwamba, kiasi miaka miwili iliyopita nilipata barua kutoka kwa kijana mmoja mwanafunzi wa Kiiraqi ambaye alipelekwa pamoja na ujumbe wa elimu wa serikali ya Iraq kwenda kusoma katika Chuo cha masomo ya ngazi ya juu nchini Misri. Barua yenyewe ilikuwa ndefu mno. Kwa ufupi barua hiyo inasema hivi:“Mimi ninabadilishana mawazo na baadhi ya wanavyuoni wakubwa wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na wakati mwingine tunazungumzia habari za Najaf na wanavyuoni wa huko, namna wanavyofundisha na wanafunzi wanaokwenda huko kutoka kila mahali kujifunza elimu katika makao makuu ya dini mjini Najaf.

Hakuna shaka kwamba jamii ya wanavyuoni wa al-Azhar wanawatukuza na kuwasifu wanavyuoni wa Najaf, na wanatia maanani busara, ujuzi na maendeleo ya wanavyuoni wa hapo, lakini juu ya hayo yote hawaachi kusema: ‘Ni wazuri lakini kwa bahati mbaya wao ni Mashia!’”

Kijana huyo anaendelea kusema katika barua yake: “Niliona ajabu mno kwa msemo wao huo, basi mimi nikawatolea hoja nikasema: ‘Kwani Shia si madhehebu moja miongoni mwa madhehebu za Kiislamu? Kwani Mashia si katika jamii ya Waislamu!?’

Page 32: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

25

Lakini wao wakajibu kwa ubaya, wakiwa na maana hasa kuwa: ‘Mashia si Waislamu wala Shia si katika madhehebu za Kiislamu; tena ni kosa kuwahesabu Mashia na madhehebu yao kuwa ni madhehebu au dini miongoni mwa madhehebu na dini za duniani. Hii ilikuwa ni mbinu iliyobuniwa na Mairani, na lilikuwa ni jambo la kisiasa la kupindua utawala wa Bani Umayyah na kuleta utawala wa Bani Abbasi tu, wala haina uhusiano wowote ule na dini zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu.’”

Baada ya hayo, kijana huyo anaendelea kuandika:“Muheshimiwa, kama unavyojua kwamba mimi ni kijana mwenye umri mdogo, sijui wala sina elimu ya dini wala sijui madhehebu hizi zilianza vipi, zikakuwa na kuenea vipi. Kwa sababu hiyo, nikawa na shaka. Na kwa nini nisiwe na shaka hali nakutana na kupambana na wanavyuoni wakubwa wa Kisunni? Kwa kweli, nilikaribia kuwa na shaka juu ya Uislamu wao licha ya kuwa madhehebu hiyo ni ya haki na sahihi!”

Baadaye, kijana huyo akaniomba nimfunulie ukweli na uhakika ili nimtoe katika mashaka yaliyomkuta.

Vile vile ameandika: “Ikiwa hutoniondolea mashaka hayo na nikapotea, basi jukumu litakuwa juu yako.”

Kwa hivyo, nikaona kwamba ilikuwa lazima nimjibu kwa njia ya barua kwa kiasi inavyoyumkinika, na kwa kuiangalia fikra ya kijana huyo nikaandika hoja ambazo kwazo zitamtoa shaka moyoni mwake na kumweka imara. Lakini mshangao wangu ulikuwa zaidi kuliko shaka ya kijana huyo. Kwani mimi bado sikuweza kusadiki jambo hilo!

Nikafikiri ni vipi inawezekana kwa wanavyuoni na wataalamu wa nchi ya elimu kama Misri wawe katika hali ya kutojua hayo!? Ikiwa Misri ni chimbuko la ustaarabu wa ulimwengu wa Kiislamu, mahali pa kushindania elimu ya Kiislamu, kitovu cha Waarabu, mahali ambapo uhakika na uhalisi huangazishwa na kutatuliwa

Page 33: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

26

mapazia ya uwongo ambayo aghlabu hutokana na matamanio au makusudio ya kibinafsi au kutokana na kutegemea maneno yaliyozuliwa na watu wasio na elimu, na wanavyuoni wao wako katika hali hiyo, basi wakoje watu wengine?

Mimi sikuweza kabisa kusadiki maneno ya kijana huyo, na kwa bahati katika siku zilezile nilipata kitabu kimoja kiitwacho Fajrul- Islam kilichoandikwa na mwandishi mashuhuri aitwaye Ahmad Amin.

Nikaanza kukisoma kitabu hicho, na nilipofika mahali anapozungumzia habari za Shia, nikaona kwamba mtungaji si kuwa tu alikuwa ameandika shelabela, lakini kwa hakika alikuwa hatungi kitabu ila alikuwa akiwazulia mambo yasiyo na uhakika. Iwapo mtu katika zama hizi ataandika mambo kama haya kuhusu Shia, hatasamehewa japo awe anaishi katika nchi za mbali kama vile Uchina, seuze aliyeko katika nchi ya Misri? Kwa vyovyote vile, niliona kwamba yote yaliyoandikwa na kijana wa Kiiraq yalikuwa kweli na sahihi.

Nikafikiri kwamba, ikiwa mwandishi maarufu kama huyo Ahmad Amin, ambaye anaandika kwa ajili ya umati ambao kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu kila mmoja anaitwa ndugu wa mwenziwe, ameandika kitabu ambacho ndani yake anasingizia na kuzusha uwongo juu ya madhehebu ya Shia, basi wakoje watu wajinga na wasio na maarifa ikiwa wanavyuoni kama hawa wanazua uwongo kama huo?

Kila mwenye akili na busara anafahamu na kujua jinsi siku hizi sisi Waislamu tunavyohitaji kufungamana, kuungana, kupendana na kuwa na umoja kati yetu. Waislamu wa ulimwengu huu hawawezi kuishi bila ya kuwa na umoja na upendano kati yao. Kama si hivyo, hakuna maisha ya heshima wala kifo cha staha.

Kusema kweli, lau ndugu zetu Waislamu watatambua ukweli na uhakika wa madhehebu ya Shia na kwa insafu watawatambua ndugu zao hao, basi wataviteketeza vitabu kama hivyo vyenye sumu na vyenye kutia mbegu ya uadui, fitina na ugomvi kati ya Waislamu na

Page 34: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

27

kulifanya jambo hilo kuwa silaha kwa wakoloni na wapingao dini zote.

Maneno yaliyomo ndani ya Fajrul-Islam yasemayo kuwa, “Kwa kweli Ushia ulikuwa ni kimbilio kwa wale wanaotaka kuuangamiza Uislamu.” (uk.33). Hivi kweli maneno kama haya hayawezi kuzusha hasira na kuwasha moto wa chuki katika nyoyo za Mashia?

Mwandishi si mjinga kiasi hicho. Yeye anajua kwamba anaandika maneno kama hayo yasiyokuwa na msingi ambayo yatapingwa. Pia anajua kuwa tabia hii ya uchokozi itayaumiza mawazo ya mamilioni ya watu ambao wanaunda taifa hilo kubwa la Kiislamu.

MAJADILIANO NA AHMAD AMIN KUHUSU UZUSHI WAKE

Naam, kwa bahati isiyotarajiwa, bwana huyo Ahmad Amin ambaye mwaka uliopita (1349 Hijriyah) baada ya kukitawanya kitabu chake hicho na wanachuoni wengi wa Najaf wakasimama kukipinga, (bila matarajio), aliuzuru mji wa elimu akiwa miongoni mwa wajumbe 32, kati yao wakiwemo wanafunzi na waalimu. Wajumbe hao walipitisha muda mrefu pamoja nasi katika usiku mmoja wa mwezi mtukufu wa Ramadhani uliohudhuriwa na watu wengi.

Mimi kwa upole nikamlaumu Ahmad Amin, lakini sikutaka kusema yote niliyokuwa nikitaka kuyasema kwa sababu ya kuyafuata maamrisho ya Qur’ani Tukufu yanayosema: “Na wanapopita penye upuzi, hupita kwa heshima” (25:72), na: “Wajinga wakisema nao husema, amani” (25:63)

Yeye alitoa udhuru wake wa mwisho, akasema, “Sikuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kuhusu Shia.” Mimi nikasema kwamba, “Maneno hayo si sahihi kwani mtu yeyote anapotaka kuandika kitabu juu ya jambo lolote lile, ni lazima kwanza kabisa atayarishe habari na mambo yote yanayohusu jambo hilo na baada ya kuyachunguza ndipo aanze kuandika. Kama si hivyo, haitakuwa sahihi wala busara kwa mtu huyo kuandika juu ya jambo ambalo hana habari zake kamili.”

Page 35: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

28

Niliendelea kusema, “Hebu angalia maktaba za Kishia jinsi zilivyoratibiwa vizuri. Chukua kwa mfano maktaba yangu ambayo ina kiasi cha vitabu elfu tano, vingi vyao vikiwa vimetungwa na wanavyuoni wa Kisunni. Mji mdogo kama huu wa Najaf usiokuwa na utajiri wala chochote ila elimu na utukufu una maktaba nyingi ukifananishwa na mji mkubwa wa Cairo ambao licha ya kuwa na maktaba nyingi, inahuzunisha mno kuona kwamba vitabu vya Kishia mjini humo ni vichache sana vikilinganishwa na vitabu vyao!”

Naam, ingawa watu hao hawana ujuzi kuhusu Shia, lakini pamoja na hayo hawasiti kabisa kuandika wayatakavyo dhidi ya Shia.

Ajabu kuliko hiyo ni kuwa baadhi ya vijana wa Kisunni wa Iraq ambao ni jirani zetu wa karibu sana, nao pia hawajui kuhusu Shia. Wao wanawahesabu Mashia kuwa ni kikundi cha washenzi wa jangwani tu!

Miezi michache iliyopita, kijana mmoja wa Baghdad mwenye tabia njema aliniandikia barua kuhusu safari yake ya karibuni iliyomfikisha hadi Dulaimi13 (mkoa ulio karibu na Baghdad). Wenyeji wengi wa hapo ni Masunni. Kijana huyo kwa kushirikiana na watu wa hapo alikuwa akihudhuria mikutano yao. Wao walifurahi mno kuona tabia nzuri na adabu alizokuwa nazo kijana huyo. Lakini walipofahamu kuwa alikuwa Shia, wakastaajabu mno kwa kusema: “Sisi hatukudhani kuwa miongoni mwa kikundi hiki (cha Mashia) kuna wenye tabia njema na hulka nzuri mbali na kuwa na maarifa, elimu na dini! Sisi tulikuwa tukiwahesabu kuwa ni washenzi wa jangwani tu!” Hilo ndilo lililokuwa wazo na makisio yao juu ya Shia.

Kijana huyu alikuwa akinipandisha mori kutokana na maneno hayo yanayoumiza, pia hakuacha kunihimiza mara kwa mara kuhusu maombi yake ya kunitaka kutunga kijitabu kuhusu Ushia kwa muhtasari kwa ajili ya kuwagawia watu kama hao wasiojua kitu ijapokuwa wachache watajua na kufahamu itikadi za Kishia.

Baada ya muda kupita, kijana huyu akafika Syria kwa matembezi ya

13 Sasa hivi unajulikana kwa jina la Mkoa wa Ambar

Page 36: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

29

kiangazi, na kutoka huko akaenda Misri. Baada ya kufika hapo na kuwaelewa watu wa hapo walivyo, akaniandikia tena hivi: “Mawazo na uamuzi wa watu wa Misri ni kama ule wa watu wa mkoa wa Dulaimi kama nilivyokuelezea hapo awali.”

Tena, akaongeza kusema: “Je, bado haukufika wakati wa kuitimiza ahadi yenu na kulisimamia jukumu mlilokuwanalo mabegani mwenu?”

Watu hao walikuwa wakiwafikiria Mashia kwa mifano mibaya sana. Vilevile aliniandikia mambo mengi mengine kama hayo ijapokuwa yalikuwa kwa kirefu lakini yote yalikuwa na uhakika na ukweli.

Mambo haya na matukio mengi mengine dhidi ya Shia tunayaona katika magazeti ya Misri, Syria n.k., yakiandika makala za sumu mara kwa mara na yakisingizia kila aina ya tuhuma juu ya Mashia, tuhuma ambazo zinafanana na kisa cha Nabii Yusuf (a.s.) na nduguze kuhusu wizi. Lakini kwa bahati mbaya, maradhi ya ujinga na ushupavu dhidi ya dini ni maradhi yasiyo na dawa hata madaktari wanashindwa kuyatibu.

Naam, baada ya matukio hayo yote, nikafikiri kwamba kukaa kimya huko ni sawa na kudhulumu, na nikaona kwamba wajibu wangu haukuwa tu wa kuwalinda na kuwasimamia Mashia mbele ya mafuriko ya tuhuma na dhuluma, bali ulikuwa na lengo kubwa kabisa la kuondoa vizuizi vya ujinga mbele ya macho ya Waislamu wote duniani, ili watu waadilifu katika fikra zao wachunguze na kuangalia upya na washike njia nyoofu, na wale wakaidi na wachochezi iwe hoja kwao, na kusibaki lawama yoyote juu ya wanavyuoni wa Kishia ambao hawakushindwa kuwadhihihirishia na kuwajulisha watu madhehebu hiyo.

Muhimu zaidi kuliko hilo ni matumaini ya kuimarisha umoja wa mapenzi kati ya Waislamu, upatikane umoja madhubuti zaidi na uadui utoweke kati yao, kwani kila binadamu hasa katika zama zetu hizi anafahamu kuwa kuungana na kuondoa hitilafu ni moja katika mambo muhimu kabisa ambayo viumbe wanayahitajia katika maisha ya kijamii.

Page 37: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

30

Labda tena, mwandishi wa kitabu cha Fajrul-Islam ambaye amezungukwa na mawingu ya dhuluma na kiza kutoka kila upande, sasa hataandika tena dhidi ya Shia.

Mtungaji wa Fajrul-Islam anaandika hivi: “Hakika ni hii kwamba, madhehebu ya Shia ni kimbilio kwa kila mwenye kutaka kuufanyia Uislamu uadui au kubomoa msingi wake, na vilevile ni kimbilio kwa wale wanaotaka kutia mafundisho ya mababu zao Wayahudi, Wakristo na Wazartoshi (Maparisi) katika dini ya Kiislamu na kutimiza matilaba yao chini ya kivuli cha Ushia.”

Anaendelea kuandika hivi: “Asili ya itikadi ya Raj’ah (ufufuo mdogo) ambayo Mashia wanaitakidi inatokana na Uyahudi. Vilevile, Mashia wanaitakidi kuwa moto wa Jahannam ni haramu kwao isipokuwa kwa wachache tu. Wayahudi nao pia wanadai kwamba moto hautawagusa, kama Qur’ani Tukufu inavyoeleza itikadi yao hii waliposema: “Moto hautatugusa kabisa isipokuwa kwa siku chache tu” Qur’an 2:80. Hizi ni itikadi za Kiyahudi ambazo zinaaminiwa na Mashia pia. Ama Ukristo uliomo katika Ushia ni kule kusema kwa baadhi ya Mashia kwamba, Uhusiano wa Imam na Mwenyezi Mungu ni kama uhusiano wa Masihi Yesu na Mwenyezi Mungu. Nao pia wanasema kuwa Imam ni kiungo kati ya Lahut (ulimwengu wa kiroho) na Nasut (ulimwengu wa kimaumbile).”

“Pia wanaamini kwamba uhusiano wa Uimamu na Utume unaendelea na hautakatika kamwe. Na mwenye kuunganika na Lahut (Uungu) ni Mtume. Juu ya hayo, wanaitikadi Hulul (roho ya mtu kuingia katika mwili wa mtu mwingine [au kitu kingine] afapo. Vile vile, itikadi ya zamani ya kuwa Mungu ana umbo iliyoitikidiwa na Wahindu, (Wabrahmani), wanafalsafa na Wamajusi kabla ya Uislamu. Itikadi hizo zimetokeza katika Uislamu kwa jina la Ushia.”14

Hapana shaka, ingelikuwa si kwa sababu ya kuhifadhi umoja wa Waislamu, kuogopa kuharibika mapenzi, kuogopa kuchochea moto wa uadui, na kwa kufuata msemo wa kihekima usemao: “Usimkataze mwenzio jambo ambalo wewe mwenyewe walitenda.”

14 Fajrul-Islam, uk.230.

Page 38: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

31

basi tungelimthibitishia Ahmad Amin kuwa ni watu wepi wanaotaka hasa kubomoa msingi wa Uislamu na kuvunja umoja wa Waislamu kwa kutumia njia ya kuleta mfarakano na unafiki!

MCHANGO WA SHIA KATIKA MAENDELEO YA UISLAMU

Lakini sisi tunataka kumwuliza huyo mwandishi: “Je, ni kikundi kipi cha Kishia kilichotaka kuubomoa Uislamu? Je, kikundi hicho kilikuwa ni kile cha kwanza cha Mashia ambao walikuwa ni miongoni mwa Masahaba watukufu, watiifu na mashuhuri wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) kama akina Salman Al-Farisi, Abu Dharr, Miqdad, Ammar, Khuzaymah Dhush-Shahadatain, Abu Taihan, Hudhaifah Al-Yamani, Zubair, Fadhl ibn Abbas na nduguye, Abdullah ibn Abbas, Hashim ibn ‘Utbah Al-Marqal, Abu Ayyub Al-Ansari, Aban ibn Sa’id, Ubayyu ibn Ka’b Bwana wa wasomaji wa Qur’an na Anas ibn Harth ibn Nabih.

Sahaba huyu (Anas) ndiye aliyemsikia Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) akisema: “Mwanangu Husain atauawa katika ardhi iitwayo Karbala, na atakayekuwepo miongoni mwenu wakati huo amsaidie.” Anas ibn Harth akafika Karbala, akajiunga na Imam Husain (a.s.) na akauawa shahidi. Ukitaka kujua zaidi soma vitabu viitwavyo, Al-Isabah na Al-Istiia’b, ambavyo ni miongoni mwa vitabu vinavyotegemewa na vilivyotungwa na wanavyuoni wa Kisunni juu ya maisha ya Masahaba wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.).

Ningelitaka kuwataja Masahaba wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) waliokuwa Mashia na kuthibitisha Ushia wao katika vitabu vya Kisunni ingenibidi kutunga kitabu kikubwa, lakini kwa bahati nzuri wanavyuoni wa Kishia wameniondolea jukumu hili kwa kutunga vitabu bora kabisa kuhusu maudhui hiyo, kama kitabu Ad-Darajaatur-Rafia’h Fii Tabaqatish-Shi’ah,15 kilichotungwa na 15 Kitabu kiitwacho Ad-Darajaatur-Rafia’h Fii Tabaqatish-Shi’ah, mwandishi wake (Mwenyezi Mungu amrehemu) amekusanya humo mkusanyiko mkubwa wa Tar-juma na khabari za watu mashuhuri wa Kishia tangu mwanzoni mwa dola Tukufu ya Kiislamu, kimepangwa katika tabaka kumi na mbili kama mtunzi mwenyewe alivyoeleza ndani ya utangulizi wa kitabu chake.

Kimeanza kwa Masahaba na kumalizia wanawake mashuhuri, isipokuwa ⇒

Page 39: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

32

mwanachuoni marehemu Sayyid Ali Khan mtungaji wa kitabu kiitwacho As-Sulafah16 na vitabu vingine vya thamani kama vile Tirazul-Lughah ambacho ni miongoni mwa vitabu vizuri sana kuhusu lugha ya Kiarabu.17

Baada ya kuwataja Masahaba mashuhuri wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) katika kitabu hicho, Tabaqatish-Shiah, ambao walikuwa Mashia wa ukoo wa Bani Hashim, kama vile Hamza, Ja’far, A’qil na wengine kama hao, Sayyid Ali Khan amewataja pia wale ambao sisi tumekwishawataja kabla, na akaongeza Masahaba wafuatao: Uthman ibn Hunaif, Sahl ibn Hunaif, Abu Sa’id al-Khudri, Qais ibn Sa’d ibn Ubbadah (ambaye babake alikuwa mkuu wa kundi la Ansar), Buraid, Barraa ibn Malik, Khubbab ibn Al-Art, Rifa’a ibn Malik al-Ansari, Abu Tufail Amir ibn Wathilah, Hind ibn Abi Halah, Ju’dah ibn Hubayrah Al-Makhzumi na mamake Ummu Hani binti Abi Talib na Bilal ibn Rabbaah (mwadhini wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.)).

Kiasi cha majina miatatu ya Masahaba wa Kishia niliyoyakumbuka nimeyakusanya na kuyaandika kutoka katika vitabu vilivyoandikwa juu ya maisha ya Masahaba kama vile Al-Isabah, Usudul-Ghābah na Al-Istia’b. Wote hao walikuwa Masahaba wa Mtume Mtukufu

⇐ kitabu kilichoko mkononi mwangu hakina mkusanyiko (mwingine) ila ile tabaka ya kwanza na kidogo tabaka ya nne na ile ya kumi na moja tu, unaweza kurejea.16 Sulafatul-Asri fii Mahasinis-Shuarai Bikulli Misrin, Mwandishi wake Mwenyezi Mungu Amrehemu, amekipanga kitabu hiki baada ya kuzitembelea nchi nyingi na miji mingi, kiasi kwamba amekusanya kiasi kikubwa cha tarjuma ya washairi mashuhuri wa zama zake na wanafasihi wa zama zake, na akaleta sehemu ya qasida zao na upambanuzi wa maneno yao, hali ya kuwa akieleza sera zao, tungo zao na miaka ya kufariki kwao. Kama ambavyo mtunzi huyo, Mwenyezi Mungu amrehemu, amekipanga kitabu chake kama alivyofanya Ath-Thaalabi ndani ya “Yatimatud-Dahri” na Al-Bakhirzi katika “Dimyatul-Qasri.”17 At-Tirazul-Awwal Wal-Kunaazu lima Alaihi min Lughatil-Arabil-Muawwal, Sheikh At-Tahrani Mwenyezi Mungu amrehemu amesema kuhusu kitabu hiki ndani ya Ad-Dhariah J. 15 uk. 157 na 1035 kwamba, “Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu bora vya lugha ya Kiarabu,” lakini yeye hakuvuka herufi ya Sad bali ameishia kwenye neno “Qamisa”, Mtunzi huyo Mwenyezi Mungu amrehemu, amelizungumzia kila tamko kwa kila maana liliyonayo na istilahi yake, na akataja matumizi yake ya hakika na yale ya majazi ndani ya Qur’an na Sunna, pia mifano na mengineyo.

Page 40: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

33

(s.a.w.w.), Mashia na ni wafuasi wa Ali (a.s.). Inayumkinika kupata majina zaidi ya Masahaba ikiwa utachunguza na kutafuta zaidi.

Hakika mimi sifahamu, hivi ni kweli kwamba, kikundi hicho cha Masahaba watukufu wa Mtume (s.a.w.w.) eti ndio waliotaka kuubomoa msingi wa Uislamu? Au Imam wa Shia, Ali ibn Abu Talib (a.s.), eti naye alitaka kuubomoa Uislamu? Mtu ambaye ulimwengu mzima unashuhudia kwamba lau asingelikuwa yeye na upanga wake katika vita vya Badr, Uhud, Hunain, Ahzab, n.k., mti wa Uislamu usingelistawi, usingeota na wala usingezaa matunda yote hayo tunayoyaona. Abdul Hamid Al-Mu’tazili amevuka mpaka katika kusifu kujitolea kwa Ali (a.s.) kwa kusema: “Msingi wa dini umewekwa na jengo likajengwa, na lau si kuwepo pigo lake la upanga, jengo lisingesimama.”

Naam, kama isingelikuwa kujitolea kwake kabla na baada ya kuhajiri Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), na kama baba yake, Abu Talib, asingeihami na kuisaidia kwa ukamilifu dini ya Uislamu kabla ya Hijira, basi kabila la Quraishi na mbwa wa mwitu wa Uarabuni wangeliukomesha Uislamu tangu mwanzoni wakati ulipokuwa bado mchanga.

Ingawa Abu Talib alijitolea na kutoa huduma zote kwa ajili ya dini ya Kiislamu, lakini Waislamu walimlipa malipo ya ajabu kwa kusema kwamba, “Abu Talib hakusilimu kamwe, bali alikufa akiwa kafiri”!!!18

18 Naam, huenda baadhi yao wakaitakidi hivyo, lakini hali halisi na mtazamo wa kiakili uliosalimika vinapingana na itikadi hiyo. Pamoja na hali hiyo mpaka leo utasikia uzushi na uongo mwingi ulio nje kabisa ya maarifa na mantiki, kwani yanasemwa maneno machafu kutoka kwa wafuasi wa Masultani na watu wanaoitafuta dunia.

Hakika waliopita hapo kabla miongoni mwa wanachuoni wa hadithi, waandishi na watoa mawaidha wa Msultani, ni katika jumla ya watu ambao nafsi zao hutetemeka na mate ya uchu kuwadondoka wanapouona utajiri na vyeo vya Usultani. Watu hao siku zote wamekuwa na malengo yanayotatanisha, kwani huwezi kuwakuta wanasita kusema uongo dhidi ya dini na watu wake, hata kama ni kwa thamani ndogo waipatayo.

Bila shaka watu hao walioko kwenye soko la watumwa ndiyo chimbuko la mitihani na fitna inayovuruga maeneo mengi ya jamii kubwa ya Waislamu. ⇒

Page 41: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

34

⇐ Wamepotosha na kuyakuza mambo mengi (ya dini) yaliyothibiti, mambo ambayo yanamafungamano madhubuti na muhimu miongoni mwa itikadi za Waislamu. Matokeo ya uzushi huo ni kuzusha vurugu kubwa ambayo siyo ya kufumbia macho wala kuipuuza. Na ili kuiepuka hali hiyo inapasa kutuliza fikra na kumcha Mungu, nasi ndilo jambo tunalolilingania. Ukweli na usemwe: Kwa hakika watu wa mwanzo kuweka mwenendo huu mbaya na wakafanya kila juhudi kuwanunua watu hao wenye uchu wa fedha na dhahabu, ni wale wakorofi wa dola ya Banu Umayyah na watawala wao na shahidi mzuri wa Qadhia hii ni historia, bali ukweli huu uko wazi hatuhitaji dalili kuuthibitisha.

Hapana shaka kwamba mas-ala ya kuituhumu imani ya Abu Talib, Mwenyezi Mungu amrehemu, ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo watawala wa Kibanu Umayyah walifanya kila juhudi kujaribu kuyaimarisha ndani ya akili za Waislamu kwa kutumia kila aina ya mbinu, kwani mambo hayo ni nguzo muhimu ambazo Banu Umayyah kamwe hawawezi kuyafumbia macho. Na sababu kubwa zilizowapelekea kufanya hivyo ni hizi zifuatazo: -Ya Kwanza: Uadui wao wa kurithiana uliothibiti dhidi ya Uislamu, ambao uliwashinda wakubwa zao na Usultani wao waliokuwa wameusimamisha katika nchi (ya bara Arabu) ukiwemo ukandamizaji, dhulma na utajiri wao, kiasi kwamba (Uislamu ulipokuja) ulizisambaratisha ndoto zao za kuitawala nchi zikawa zinapeperuka kama yanavyopeperuka majani ya mti katika kipindi cha kipupwe pindi mvumo wa ulingano wa Uislamu ulipokuwa ukivuma. Na Abu Talib, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa na mchango mkubwa katika kuthibitisha na kubakia kwa ulingano huo. Kwa hiyo siyo ajabu kuzikuta nyoyo za Banu Umayyah zimejaa chuki na bughdha juu ya mtu huyu.

Ya Pili: Hapana shaka kwamba jambo hili ndiyo mhimili mkubwa ambao uadui huu ulikuwa unafukuta ndani ya nyoyo za Banu Umayyah dhidi ya mtu huyu; na hapana sababu nyingine isipokuwa ni kwa sababu (Abu Talib) ni baba yake Ali (a.s.) nai zaidi ya hapo mimi nasema kwa uaminifu kabisa kwamba, “Hakika Abu Talib lau angekuwa ni baba wa mtu mwingine kutoka ndani ya Waislamu wa kawaida tu au hata akawa mtu huyo ni miongoni mwa watu waovu na akawa na sehemu moja ya kumi katika huduma hii tukufu ya Uislamu, basi wangemmiminia sifa nyingi na wala wasingemuangusha. Wangelimuombea rehema katika vikao vyao na kwenye mikusanyiko yao na hafla zao, pia wangelimsifu mno kiasi cha kuyachosha masikio.

Lakini kwa kuwa yeye ni baba wa Ali (a.s.) jambo ambalo ndilo la msingi (wa wao kutomsifia Abu Talib) kutokana na kushindwa kwa mababu zao na wazee wao kupambana na (Ali a.s.) katika nyanja ya ushujaa na uhodari kwenye vita, na hapo ndipo walipojificha mapangoni mwao mfano wa watoto wa sungura waliompoteza mama yao. Wamebaki wanafanya kila namna ya njama na kujificha mno wasitambulikane (uadui wao dhidi ya Uislamu) na kuwanunua watu wadhaifu wa imani kwa thamani ndogo, na watu kama hao hawakosekani katika kila zama na kila mahali wapo. Hivyo basi wamewasheheneza mali chungu ⇒

Page 42: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

35

⇐ nzima, ili wafanye vitimbi vyao na kutoa picha mbaya dhidi yake.

Wengi katika wajinga hao walionunuliwa ni miongoni mwa watu waongo na wazushi tena wamechagua kuzusha mambo ambayo wao wanadhani kuwa yatakuwa na athari kubwa kwa jamii ya Waislamu dhidi ya heshima na utukufu wa Imam Ali (a.s.). Isitoshe hali hiyo bali wakautuhumu hata Uimamu wake. Hali hii imeafikiana kabisa na ile chuki yao dhidi ya Abu Talib, Mwenyezi Mungu amrehemu, (baba wa Ali a.s.) chuki ambayo ni matokeo ya yeye Abu Talib kusimama upande wa Mtume (s.a.w.w.) (na kuwaacha Maquraish) wakayakumbatia matokeo hayo kama mtu akumbatiapo mpira (baada ya kuudaka). Hivi ndivyo Bwana huyu alivyotolewa muhanga kutokana na njama za Banu Umayyah zilizoandaliwa, na ni miongoni mwa njama na vitimbi vingi vya Banu Umayyah dhidi ya Uislamu na Waislamu. Riwaya kama hizo ambazo ni za uongo zimeendelea kuwepo ndani ya rejea nyingi za historia na sehemu nyinginezo na zinaeneza sumu kali ndani ya mwili wenye maradhi, bila hata baadhi ya watu kujilazimisha nafsi zao kupata taabu ya kufanya uhakiki na kurejea ili kuthibitisha usahihi wa hicho wanachokinukuu. Hali hii imepelekea watu waliopo leo hii warithi maovu ya watu waliopita na wamewafuata mfano wa kipofu anavyofuata bila utafiti wala uchunguzi.

Wallahi namuapa Mwenyezi Mungu kuwa huo msingi uliofaulisha vitimbi (dhidi ya Uislamu) ni msiba mkubwa mno.

Ukweli lazima usemwe – hapana shaka kwamba ukifuatilia kwa haraka haraka tu jumla ya ukweli ambao baadhi ya watu wameghafilika (kuuona) inadhihirisha wazi dhulma aliyofanyiwa mtu huyu. Huwezi kuamini ususuavu aliofanyiwa Abu Talib kutoka kwa wataalamu na wachunguzi wengi wa umma wa Kiislamu katika historia. Upande wa wenzetu, licha ya mambo mengi niliyoyasoma kutoka katika baadhi ya utafiti unaotegemewa ambao umetolewa katika hali ya kufuata bila kutafakari kitu ambacho ni mwenendo wa watu wengi hapo zamani na mpaka leo bado inafanyika hivyo.

Kwa upande wangu mimi japokuwa mahala hapa hapatoshelezi kutoa maelezo juu ya ushahidi, dalili na ukweli halisi (wa hali ya Abu Talib) bali ninachoweza kukifanya ni kumuelekeza msomaji mtukufu asome na kujifunza kilichoandikwa na wanachuoni wa Kishia na wanafikra wake kuhusu maudhui hii (asome) kilichoandikwa hapo zamani na kilichoandikwa katika zama hizi, kisha baada ya hapo ninamtaka atoe maamuzi juu ya usahihi wa msimamo wetu ambao hauna upendeleo isipokuwa kueleza kilicho cha haki tu.

Miongoni mwa vitabu atakavyo visoma ni hivi vifuatavyo:-1. Imani ya Abu Talib – cha Sheikh Mufid Muhammad ibn Muhammad ibn

Nuuman Al-Baghdadi.2. Imani ya Abu Talib – cha Sayyid Ahmad Musa ibn Tauus Al-hilli. ⇒

Page 43: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

36

Lakini kinyume chake, Waislamu haohao wanamwita Abu Sufian kuwa ni Mwislamu, hali ya kuwa yeye ndiye aliyeleta fitna, akasababisha vita dhidi ya harakati za Kiislamu, na alisilimu bila ya kupenda, na katika hali hii pia hakuacha kabisa kuonesha uadui wake dhidi ya dini ya Kiislamu, kwani wakati Uthman aliposhika Ukhalifa, Abu Sufian alisema: “Enyi Bani Umayyah! Nyakueni ukhalifa kama mpira; naapa kwa yule ambaye Abu Sufiyan anamwapia,19 kwamba hakuna Pepo wala Moto.”!

Naam, mtu huyu Abu Sufian, ambaye anajulikana kwa vitendo vyake vya zamani na vya baadaye, ndiye ambaye kwa itikadi ya Waislamu hao, eti alikufa akiwa Mwislamu, lakini yule aliyeutetea Uislamu, yaani Abu Talib, hakuwa Mwislamu, bali kafiri!!

Abu Talib alionesha imani yake kwa usemi mfupi huu: “Bila shaka nimetambua kwamba dini ya Muhammad ni dini iliyo bora kabisa duniani kuliko dini zote.” Lakini pamoja na yote hayo Waislamu hao bado wanamsingizia kuwa Abu Talib alikuwa kafiri! Je, yawezekana kuwa Abu Talib alikuwa mtu dhaifu na bozibozi hata asiweze kufuata dini ya Muhammad, au alikuwa anawaogopa watu baada ya kujua dhahiri kwamba Uislamu ndiyo dini bora kabisa kuliko dini zote? Kwani yeye hakuwa “Sayyidul-Bat-ha” yaani mkuu wa watu wa Makka?

Na tuache suala la imani ya Abu Talib na turejee kwenye msingi wa mjadala wetu kuhusu wale waliotaka kuubomoa msingi wa Uislamu!

3. Imani ya Abu Talib, ambacho ni mashuhuri kuwa ni kitabu cha hoja dhidi ya wale wanaomkufurisha Abu Talib – kimeandikwa na Sayyid Abu Ali Fakhar ibn Saad Al-Musawi.

4. Sheikh Al-Abtah, au Abu Talib – cha Sayyid Muhammad Ali Alus- Sharafiddin Al-Musawi.

5. As-Shihabut-Thaqif Lirajmi Mukafiri Abi Talib – cha Sheikh Mir-za Muhammad At-Tahrani.

6. Dhiyaul-Alamina Fi Fadhail-Aim-Matil-mustafina – cha Sheikh Abul-Hasan Al-futuni An-Najafi.

7. Mawahibul-Wahib Fi Fadhail Abi Talib – cha Sheikh Jaafar An-Naqdi.8. Abu Talib Muuminu Quraish – cha Sheikh Abdullah Al-Khunaizi.

19 Anakusudia Lata na Uzza, Miungu ya washirikina wa Makkah.

Page 44: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

37

Eti Masahaba watukufu wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) waliotaka kuubomoa msingi wa Uislamu ni wale tuliokwishawataja, au ni kikundi kingine waliokuja baada yao ambao wanaitwa Tabi’in, na miongoni mwao walikuwa watu wenye imani na vyeo vikubwa kama hawa wafuatao: Ahnaf ibn Qais, Suwaid ibn Ghuflah, ‘Atiyyah Al-Awf, Hakam ibn ‘Utaybah, Salim ibn Abu Ju’d, Ali ibn Abi Ju’d, Hasan ibn Salih, Sa’id ibn Mussayyab, Asbagh ibn Nubaatah, Sulaiman ibn Mahran Al-A’mash, Yahya ibn Ya’mar Al-‘Adawani (aliyeishi zama moja na Hajjaj), n.k. Tukitaka kuwataja wote na kuthibitisha Ushia wao, basi mjadala utakuwa mrefu.

Je, kikundi hiki cha Tabi’ina waliokuwa mashuhuri na ambao wote walikuwa Mashia ndio waliotaka kuubomoa msingi wa Uislamu? Au kikundi hiki cha watu waliokuja baada yao ambao walikuwa watu wakubwa walioasisi na kuendeleza kwa juhudi elimu mbalimbali za Kiislamu?

SHIA NDIYO WAASISI WA ELIMU ZA KIISLAMU

Mfano wa hao ni Abu As-wad Ad-Duali, mwasisi wa elimu ya Nahau, Khalil ibn Ahmad, mwasisi wa elimu ya Lugha na Ushairi, Abu Muslim Ma’adh ibn Muslim Al-Harra’, mwasisi wa elimu ya Sarufi. Suyuti katika kitabu chake kiitwacho Al-Muzhir, juz. 2, na waandishi wengineo wamekiri juu ya Ushia wake. Na mwingine ni Ya’qub ibn Is-haq As-Sukait huyu alikuwa kiongozi na shaha wa fasihi ya Kiarabu.

Mashia walioweka msingi wa elimu ya Tafsiri ya Qur’an walikuwa: Abdullah ibn Abbas (mwanachuoni mashuhuri wa Kiislamu na Bwana wa wafasiri ambaye Ushia wake unajulikana vyema); Jabir ibn Abdullah al-Ansari, Ubayyu ibn Ka’b, Sa’id ibn Jubair, Sa’id ibn Mussayyab, na Muhammad ibn Umar al-Waqidi ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu zote za Qur’ani, na tafsiri yake inaitwa Ar-Raghib. Ibn Nadim na wengineo wanakubali kuwa alikuwa Shia.20

Mashia walioweka msingi wa elimu ya hadithi (hadith) walikuwa:

20 Taz: Fahrasat Ibn An-Nadim uk: 194.

Page 45: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

38

Abu Rafi’, (mtumwa aliyekombolewa na Mtume), mtungaji wa Al-Ahkam wa S-sunan wa Al-qadhaya, ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshikamana vyema na Amirul Muuminin Ali ibn Abi Talib (a.s.) na pia alikuwa mtunza hazina wa dola ya Kiislamu katika mji wa Kufah.

Baada ya Abu Rafi’, alifuatia mwanawe aliyekuwa akiitwa Ali ibn Abi Rafi’,21 ambaye alikuwa katibu wa Imam Ali (a.s.), huyu alikuwa ni mtunzi wa kwanza wa Fiq-hi, (elimu inayohusu sheria za dini). Kisha alifuatia nduguye aliyekuwa akiitwa Ubaidullah ibn Abi Rafi’, yeye alikuwa wa kwanza miongoni mwa Waislamu kuandika kuhusu historia na kudhibiti matukio na kumbukumbu.22

Mtu wa kwanza aliyeasisi elimu ya Itikadi na akatunga kitabu kizuri sana kuhusu elimu hiyo alikuwa Abu Hashim ibn Muhammad, mwana wa Muhammad ibn Hanafiyyah.

Mwingine ni katika Tabi’in aliyekuwa akiitwa Issa ibn Rawdha ambaye aliishi hadi zama za Imam Muhammad AlBaqir (a.s.). Mashia wawili hawa walikuwepo kabla ya Wasil ibn ‘Ataa na Abu Hanifa, ambao Suyuti amedai kwamba walikuwa ndiyo waanzilishi wa elimu hiyo.

Baada ya mabwana wawili hawa, wanavyuoni mashuhuri wa Kishia waliendeleza elimu hiyo, nao ni Qais Al-Masir; na Muhammad ibn Ali Al-Ahwal ambaye ni maarufu kwetu kwa jina la Muuminut-Taq anayetokana na kizazi cha Naubakht23 lakini wapinzani wetu wanamwita Shaitanut-Taq.

21 Taz: Taasisus-Shia’ uk: 283 na 298, Rijalun-Najjashi uk: 216 n.k.22 Taz: Taasisus-Shia’ uk: 283 na 298; Tanqihul-maqal juz: 2 uk: 237 n.k.23 Huu ni ukoo wenye heshima kubwa katika masuala ya kielimu na maarifa, na asili yao ni kutoka Iran. Mtu wa kwanza Kusilimu miongoni mwao alikuwa babu yao aliyekuwa akiitwa Naubakht. Neno hili Naubakht ni la Kiiran ambalo limefungamana na maneno mawili Nau kwa maana ya mpya na Bakht kwa maana ya Hadhi. Kwa hiyo maana yake kwa ukamilifu ni: Hadhi mpya. Kutokana na ukoo huu wamepatikana wanachuoni wengi, Wanafalsafa, Wanahistoria, Waandishi, Washairi na Mawaziri. Taz: A’yaanus-Shia’ kilichoandikwa na Sayyid Muhsin Al-Amin juz: 2 uk: 93.

Page 46: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

39

Ukoo wa Naubakht wametunga vitabu vingi vyenye thamani na manufaa, kama vile Fassu ‘l-Yaqut na vinginevyo. Ulikuwa ni ukoo mtukufu uliotoa wanavyuoni mahashumu na ukaendelea zaidi ya miaka mia kuwaangazia watu wa zama zao kwa nuru ya elimu waliyokuwa nayo.

Na miongoni mwa wanachuoni wa Kishia ni kama akina Hisham ibn Hakam, Muhammad ibn Al-Ahwal, Qais al-Masir, na pia wanafunzi wao kama vile Abu Ja’far Al-Baghadadi As-Sakkak, Abu Malik Adh-Dhahhak Al-Hadhrami, Hisham ibn Salim, Yunus ibn Ya’qub, na wengine kadha wa kadha, waliwatawala wanachuoni wa madhehebu mengine ya Kiislamu na wengineo miongoni mwa walahidi katika fani za mijadala na mahojiano, na waliwabana mno kuhusu masuala yanayohusiana na Upweke wa Mwenyezi Mungu (Tawhidi) na Uimam na mengineyo.

Ikiwa mtu atakusanya mazungumzo na majadiliano ya watukufu hao, hasa kama yale ya Hisham ibn Hakam, ambayo yanapatikana katika vitabu mbalimbali, ataweza kutunga kitabu kimoja kizuri chenye manufaa makubwa.

Vivyo hivyo, tukitaka kukusanya majina na maneno ya wanavyuoni, wanaitikadi na wanafalsafa wote wa Kishia na kueleza habari zao, basi tutahitaji kutunga vitabu vingi.

Sasa tuambie ewe mwandishi wa Fajrul-Islam: “Je, watu hao walitaka kubomoa msingi wa Uislamu (kama unavyowatuhumu) ambao ndio walioasisi elimu ya historia ya Kiislamu na wakakusanya na kutunga vitabu kuhusu elimu ya sira na matukio, na wakaandika kuhusu maisha, tabia, mwenendo na miujiza ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na vita vya kidini vilivyopiganwa naye?”

Mtu wa kwanza kutunga kitabu kama hicho miongoni mwa wanavyuoni wa Kiislamu alikuwa Tabi’in Aban ibn Uthman al-Ahmar (aliyefariki mwaka 140 a.h.) ambaye alikuwa Sahaba wa Imam Ja’far As-Sadiq (a.s.). Baada yake walikuwa Hisham ibn Muhammad ibn As-Saib al-Kalbi, Muhammad ibn Is-haq al-Matlabi,

Page 47: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

40

na Abu Makhnaf Al-Azdi. Na baada yao kila aliyeandika kitabu katika fani hiyo alitegemea kwao.

Wanavyuoni wote hao waliweka msingi wa elimu ya historia ya Kiislamu na sira ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), na wote wanakubaliana kwamba walikuwa wanavyuoni wakubwa wa Kishia.

Kisha walifuatiwa na wanahistoria wakubwa wa Kiislamu, na wote walikuwa Mashia. Kwa mfano, Ahmad ibn Muhammad ibn Khalid Al-Barqi, mwandishi wa kitabu kiitwacho Kitabul-Mahasin, Nasr ibn Mazahim al-Manqari, Ibrahim ibn Muhammad ibn Sa’d Ath-Thaqafi, Abdul Aziz Al-Jaaludi Al-Basri Al-Imami, Ahmad ibn Ya’qub, maarufu kwa jina la Al-Ya’qubi, ambaye kitabu chake cha historia kimechapishwa Ulaya na Iraq, Muhammad ibn Zakariya, Abu Abdillah Hakim (mashuhuri kwa jina la Ibn Al-Baii’), Masu’di (mtungaji wa kitabu maarufu kiitwacho Muruujudh-Dhahab), Muhammad ibn Ali ibn Tabatabai (mwandishi wa kitabu kiitwacho Al-Adabus-Sultaniyyah) na mamia ya wanavyuoni wengine ambao hatuwezi kuwataja wote hapa.

USHAIRI NA WASHAIRI BORA KABISA WA KIISLAMU

Sasa tuwachunguze washairi bora kabisa wa Kiislamu. Hapa pia utaona kuwa washairi bora kabisa na mashuhuri kuliko wote walikuwa Mashia, na mashairi yao yanahesabiwa kuwa ni hazina ya thamani ya Kiislamu. Kwa hakika, washairi Waislamu wamegawanywa katika makundi kadha tofauti:

Kundi la Kwanza: Masahaba:Viongozi wa kundi hili wote walikuwa Mashia. Shaha wa malenga wa kundi hili alikuwa Nabigha Al-Ju’di ambaye alishiriki pamoja na Imam Ali (a.s.) katika vita vya Siffin, na wakati wa kupigana alitunga mashairi.

‘Urwa ibn Zaid al-Khail, alikuwa pamoja na Imam Ali (a.s.) katika vita vya Siffin, (soma kitabu kiitwacho Al-Aghani.)

Page 48: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

41

Lubaid ibn Rabi’a Al-’Amiri. Kikundi cha wanavyuoni wamekiri na kukubali kuwa alikuwa Shia.

Abut-Tufail A’mir ibn Al-Wathilah aliyekuwa mashuhuri kwa jina la Abul-As-wad Ad-Duali, na Ka’b ibn Zuhair, mtungaji wa Qasida maarufu iitwayo Banat Sua’d na wengine wengi kama hao.

Kundi la Pili katika Zama za Tabi’in: Kama vile Farazdaq, Kumait, Kathir ‘Izza, Sayyid Himyari, Qais ibn Dhuraih, n.k.

Kundi la Tatu lililowafuatia Tabi’in:Walikuwa wakiishi katika karne ya pili Hijria, nao ni Da’bil al-Khuza’i, Abu Nawwas (Abu Nuwasi), Abu Tammam, Buhturi, Abdus-Salam Dikul-jinni, Abu Ash-Shais, Husain ibn Dhahhak, Ibn Ar-Rumi, Mansur An-Namri, Ashja’ Al-Aslami, Muhammad ibn Wahib, na Sari’ul Ghawani.

Kwa ufupi, aghlabu washairi wote walioishi katika zama za Bani Abbasi katika karne ya pili na ya tatu walikuwa Mashia, isipokuwa Mar-wan ibn Abi Hafsah na wanawe.

Kundi la Nne lililokuwepo kuanzia Karne ya Nne na kuendelea:Washairi waliokuwepo katika kundi hili walikuwa Mutanabbi Al-Gharbi, Ibn Hani Al-Andalusi, Ibn At-Ta’awidhi, Husain ibn Hajjaj (mtungaji wa Al-Mujuun), Mahyar ad-Daylami, shaha wa malenga Abu Firas Al-Hamdani (ambaye anatajwa kuwa ushairi umenzia na kumalizikia kwake), Kushajim, Nashiu As-Saghir, Nashiu Al-Kabir, Abu Bakr Al-Khawarzami, Badi’ Al-Hamdani, At-Tagharai’, Ja’far Shamsul-Khilafah, As-Saryi Ar-Riffa’. A’mmara Al-Yamani, Al-Wada’i, Al-Khubz Al-Arazzi, Az-Zahi, Ibn Bassam Al-Baghdadi, Sibt ibn at-Ta’awidhi, As-Salami na An-Nami.

Kwa jumla, aghalabu washairi ambao majina yao yametajwa katika kitabu cha majalada manne kiitwacho, Yatiymatuth-Tha‘labi walikuwa Mashia.

Page 49: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

42

Hakuna shaka umaarufu na umahiri wa washairi wa Kishia umemefikia hadi hii kwamba wanafalsafa walikuwa wakiulizana: “Je, yupo mwanafafasihi (na mshairi) hodari zaidi kuliko Shia?” Vivyo hivyo, walipokuwa wakitaka kuusifu uzuri na ufasaha wa mashairi, walikuwa wakisema: “Fulani anaonesha Ushia katika mashairi yake!”

Baadhi ya wanavyuoni wanawahesabu Al-Mutanabbi na Abul-alai kuwa ni Mashia, labda ni kwa sababu baadhi ya mashairi yao yanagusia itikadi za Kishia. Rejea kitabu kiitwacho Al-Muraja’tur-Raihaniyyah juz. 2 na uzingatie.

Isitoshe, miongoni mwa washairi wa Kishia, pia kuna kikundi kinachotokana na ukoo wa Kiquraishi, kama vile Fadhl ibn Abbas ibn Utbah ibn Abi Lahab (ambaye maelezo ya maisha yake yameelezwa katika kitabu kiitwacho Al-Aghani), Abu Dahbal Al-Jamhi Wahab ibn Rabi’a na wengineo.

Pia, wako wanaotokana na ukoo wa Imam ali (a.s.) kama vile Sharif Ar-Radhii na Sharif Al-Murtadha. Pia Sharif Abul-Hasan Ali al-Hamani mwana wa Sharif Muhammad ibn Ja’afar ibn Muhammad Sharif ibn Zaid ibn Ali ibn Husain (a.s.) ambaye ukoo wake mzima ulikuwa wa washairi.

Sharif Al-Hamani alikuwa akisema: “Mimi ni mshairi, baba yangu alikuwa mshairi, na babu yangu pia alikuwa mshairi.” Vile vile, maelezo ya maisha ya Muhammad ibn Saleh Al-Alawi na baadhi ya mashairi yake ya kuvutia yametajwa katika Al-Aghani.

Vile vile walikuwepo Ibn Ash-Shajari na washairi wengine wengi waliokuwa Mashia na Masharifu na wengi wengineo. Ukitaka kujua zaidi soma kitabu kiitwacho Nasmatus-Sahar Mimman Tashayya’ wa Shi’r kilichotungwa na Sharif al-Yamani.

Jambo ambalo linafaa kuangaliwa ni kuwa miongoni mwa washairi wa ukoo wa Bani Umayyah, walikuwepo pia Mashia, kama vile Abdul Rahman ibn Hakam, nduguye Marwan ibn Hakam, Khalid

Page 50: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

43

ibn Sa’id ibn Al-a’s, na Marwan ibn Muhammad As-Saruji Amawi Shii’. Ninakumbuka kuwa Zamakhshari katika kitabu chake kiitwacho Rabiu‘l-Abrar amemtaja huyu Marwan ibn Muhammad kwamba alikuwa Shia, na miongoni mwa mashairi aliyonukulu mojawapo lilikuwa hili:

Enyi wana wa Hashim ibn Abdi Manafi,Popote mlipo mimi ni pamoja nanyi,Ninyi mmeteuliwa na Mwenyezi Mungu,Na Ja’far At-Tayyar Dhuljanahi atokana nanyi,Na Ali na Hamza, Simba wa Mungu,Na binti wa Mtume na Hasan na Husaini,Japokuwa natokana na ukoo wa Umayyah,Lakini najitenga nao mbele ya Rahmani.

Washairi wengine waliokuwa Mashia ni Abul-faraj Al-Isfahani (mtungaji maarufu wa kitabu kiitwacho Al-Aghani na Maqatilut- Talibin), Abi Wardi Al-Amawi (mshairi mashuhuri na mtungaji wa kitabu kiitwacho An-Najdiyyat wa ‘l-Iraqiyyat) na wengine ambao kwa sasa sikumbuki majina yao.

Sijasahau, hapo zamani wakati nilipokuwa nikisoma kwa uangalifu vitabu vya Kiislamu, niliwahi kuyaona majina mengi ya Mashia katika ukoo wa Umayyah, lakini ilivyokuwa wakati huu wa kuandika kitabu hiki sivirudii vitabu nilivyovisoma, hivyo siwezi kuyakumbuka majina yote hayo.

WAFALME NA MAWAZIRI WA KIISLAMU

Tukiangalia historia ya wafalme na watawala wakubwa, mawaziri na makatibu mashuhuri, tutakuta wengi wao walikuwa Mashia. Kwa mfano, madola ya Fatimiyyah, Al-Buawaihiyyah, Al-Hamdaniyyin, Bani Mazid ibn Sadaqah, Bani Dubais, Imran ibn Shahin Amirul- Bataih, Muqalid ibn Musayyab Al-Uqaili na Qarwash ibn Musayyab.

Vilevile baadhi ya makhalifa mashuhuri wa Bani Abbasi walijigamba kuwa ni Mashia, kama vile Ma’mun, Al-Muntasir, Al-Mu’tadhid, Ahmad An Muwaffaq, na Nasir Ahmad ibn

Page 51: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

44

Mustadhia ambaye aliwashinda wote katika kujionesha Ushia wake, Mashairi yake na uhusiano mzuri aliokuwa nao na mtawala mashuhuri, Ali ibn Yusuf Salahuddin Ayyubi ni ushahidi dhahiri na maarufu wa madai yao.

Vile vile Al-Muntasir, Dhil-Qarnain At-Taghlabi Wajihud-Dawlah Abi Mutaa’, Tamim ibn Mu’iz ibn Badis (aliyekuwa mfalme wa Afrika kaskazini na Morocco) na wengi kama hao walikuwa Mashia ambao kuyataja majina yao tu kutatoa kitabu kikubwa seuze kueleza maisha yao!

Tukiangalia orodha ifuatayo ya mawaziri wakuu wa Kiislamu, tutaona kwamba wote au wengi wao walikuwa Mashia: Is’haq Al-Katib, ambaye labda yeye alikuwa ni mtu wa kwanza kuitwa rasmi waziri katika dini ya Kiislamu kabla ya kuja dola la Bani Abbasi.

Abu Salma Al-Khilal Al-Kufi alikuwa waziri wa kwanza wa khalifa wa kwanza wa utawala wa Bani Abbasi. Kutokana na ustadi wake wa kuendesha mambo ya utawala, khalifa Siffah alimkabidhi mambo yote ya kiserikali na akampa jina la “Waziru Aali Muhammad” (Waziri wa Ukoo wa Muhammad), lakini akaamrisha auawe alipotambua mapenzi yake juu ya ukoo wa Imam Ali (a.s.).

Abu Abdillah Ya’qub ibn Dawud alikuwa waziri wa khalifa Al-Mahdi (wa Bani Abbasi) ambaye alimkabidhi kazi ya uendeshaji wa mambo yote ya kiserikali. Baadhi ya washairi wametunga mashairi kuhusu waziri huyo. Kwa mfano, shairi hili lisemalo, “Enyi Bani Umayyah! Ondokeni kwenye usingizi wenu mrefu, Angalieni sasa Ya’qub bin Dawud ni Khalifa”.

Mwishowe, Khalifa alipoona waziri anaelekea kwenye Ushia, alimfunga na akaendelea kubaki katika jela yenye kiza kinene mno iliyokuwa chini ya ardhi mpaka Harun Rashid alipokuwa Khalifa ndipo akamtoa. Katika koo maarufu za Kishia zilizopata cheo cha uwaziri ni koo za Naubakht na Bani Sahl. Fadhl ibn Sahl na Hassan ibn Sahl walikuwa mawaziri wa Ma’mun, vilevile katika wazawa wa

Page 52: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

45

Furat, Hasan ibn Ali alifanywa waziri wa Khalifa Muqtadir mara tatu.

Abul Fadhl ibn Ja’far, Abul Fat’h Fadhl ibn Ja’far, wana wa Amid ibn Muhammad ibn Husain ibn Al-Amid, na mwanawe Abu Fat’h Ali ibn Muhammad (anayejulikana kwa jina la Dhul-Kifayatain) wote hao walikuwa mawaziri wa Rukn Ad-Dawlah.

Vile vile wazawa wa Tahir Al-Khuzai walikuwa mawaziri wa Ma’mun na makhalifa wengine wa Bani Abbasi. Mawaziri wengine walikuwa Hasan ibn Harun Al-Mahlabi, Abu Dalf Al-Ajali, Sahib ibn Ubbaad, Abul Qasim Al-Maghribi (mwanasiasa mwerevu), na Abu Abdillahi ibn Husain ibn Zakariya, mashuhuri kwa jina la Ash-Shii’ ambaye ndiye aliyeanzisha dola ya Fatimiyyah katika Misri.

Zaidi ya hao, wapo pia wengine kama vile Ibrahim ibn Abbas As-Suli (aliyekuwa katibu mashuhuri wa dola la Mutawakkil), Talai’ ibn Razik (aliyekuwa miongoni mwa mawaziri mashuhuri wa Fatimiyyah), Afdhal (aliyekuwa amiri jeshi wa Misri) na wanawe. Abu Hasan Ja’far ibn Muhammad ibn Fatir na Abul Ma’ali Hibatullah ibn Muhammad ibn Abdul Muttalib (waziri wa Mustadhhir), Muayyiduddin Muhammad ibn Abdul Karim Al-Qummi aliyetokana na ukoo wa Miqdad (ambaye alikuwa waziri wa makhalifa wa An-Nasir, Adh-Dhahir na Al-Mustansir wa Bani Abbasi). Vile vile Hasan ibn Sulaiman aliyekuwa katibu mmoja miongoni mwa makatibu wa dola la Baramika, na alijulikana sana kwa jina hilohilo la Ash-Shi’i, kama alivyoandika As-Suli katika Al-Awraq. Miongoni mwa makatibu wa Ma’mun Rashid walikuwepo Yahya ibn Salama Al-Hasfaki, Ibn Nadim (mtungaji wa Al-Fihrist), Abu Ja’far Ahmad ibn Yusuf na ndugu yake Abu Muhammad Al-Qasim. (Soma qasida fasihi za Al-Qasim zenye kuwasifu Ahlul Bait katika kitabu cha As-Suli kiitwacho Al-Awraq.)

Mashia wakubwa wengine walikuwa Ibrahim ibn Yusuf na wanawe, na bingwa wa fasihi ya Kiarabu, Abu Abdillah ibn Muhammad Imran Al-Mu’rzabani, mtungaji wa kitabu kiitwacho Al-Mu’jam ambaye Sam’ani na wengineo wemetaja kuwa yeye ni Shia na pia ni

Page 53: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

46

Mu’tazilah24, na wengi wengineo ambao nafasi haitoshi kuwaandika wote.

Lau tungetaka kurekodi majina ya wafalme, watawala, mawaziri na viongozi wote wa Kishia ambao walifikia daraja za juu kutokana na elimu, utungaji wa vitabu na huduma zao kubwa kwa ajili ya dini ya Kiislamu, itabidi tutunge vitabu vingi vikubwa.

Kwa bahati nzuri, marehemu mwanachuoni mzee wangu (Mungu amrehemu) ametunga kitabu chenye majalada25 kumi kiitwacho Al-Husunul-Mani’a Fi Tabaqatish-Shi’a.

Lakini inasikitisha kuwa majalada hayo hayakumalizika kuchapishwa. Amekusanya maelezo ya maisha ya Mashia hao na kuyagawa katika vikundi thelathini kufuatana na utaratibu wa alfabeti. Humo yamo maelezo ya Mashia waliokuwa wanavyuoni, wanasayansi, wafalme, watawala, mawaziri, matabibu, watabiri n.k.

Tunapenda kumwambia mtungaji wa Fajrul-Islam, kwamba: “Ikiwa watu hao mashuhuri tuliowataja na wale tusiowataja, unawatuhumu kuwa ni watu waliotaka kuuangamiza Uislamu, hali kwa hakika wao ndio waliotia msingi wa elimu za Kiislamu wakasimamisha nguzo na kuimarisha elimu hizo, basi je, wewe mwalimu wako na marafiki zenu ndio mlioitia umadhubuti misingi ya Uislamu? Ikiwa ni hivyo, itatubidi tuusomee fatiha Uislamu huo, tuuage na kuupa buriani!”

Mwenyezi Mungu amrehemu mwanafalsafa Al-Ma’arra kwa shairi lake linaloanza na kumalizika hivi:Ikiwa Marid (bakhili mashuhuri) humtangaza Hatim Tai (mkarimu mashuhuri) kuwa ni bahili; [Na ikiwa Baqil (ambaye ujinga wake 24 Ushia kwa maana yake hasa unatofautiana na madhehebu ya Mu’tazilah. Ili kufahamu uhakika wake inatosha kusema kwamba Mashia wanaamini na kuitakidi kuwa Uimamu na Ukhalifa baada ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) huthibitika na kukubaliwa kwa njia ya maneno na uteuzi dhahiri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kinyume chake, Mu’tazilah wanaitakidi kwamba Mtume (s.a.w.w.) alifariki bila ya kumteua mshika makamu wake! Hata hivyo katika zama hizo Mashia wengi walijidhihirisha kama Mu’tazilah kutegemeana na mazingira ya wakati huo. Miongoni mwao alikuwa ni Yahya ibn Zaid Al-Alawi.25 Volumes.

Page 54: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

47

na uzuzu wake umepigiwa mfano) humtangaza Quss ibn Sa’ida Al-Ayadi (mwanafalsafa na khatibu mahiri wa Kiarabu) kuwa ni mjinga na si msemaji hodari;] Basi ewe mauti! Njoo kwetu kwani kuishi katika mazingira hayo ni mashaka!

Mimi sikukusudia kuandika na kusema haya yote, lakini kalamu yangu inaendelea kuandika bila ya kutaka. Natumai waandishi wa zama hizi na watakaofuatia, watakapotaka kuandika wafikirie wanasema nini na wanaandika nini. Amiru ‘l-Muuminin Ali (a.s.) amesema: “Ulimi wa mwenye akili upo nyuma ya moyo wake, na moyo wa mpumbavu upo nyuma ya ulimi wake.” [Yaani mwerevu kwanza hufikiri kisha husema, lakini mpumbavu kwanza husema ki-sha hufikiri.]

MASINGIZIO YASIYO NA MSINGI JUU YA USHIA ITIKADI YA RAJ’AH

Sasa tuchunguze sehemu nyingine ya maneno ya Ahmad Amin anaposema: “Itikadi ya Kiyahudi juu ya Raj’ah (ufufuo wa muda) imetokeza pia katika Ushia.”

Ni jambo la kusikitisha mno. Lau wangelijua kwamba itikadi hii ya Raj’ah kuwa si miongoni mwa misingi ya madhehebu ya Shia, wasingekuwa na haja ya kuipinga madhehebu hii na kusema kwamba itikadi ya Raj’ah ina asili ya Kiyahudi. Je, ikiwa elimu ya mtu juu ya madhehebu fulani ni ndogo, si bora kwake anyamaze kimya? Kwani jambo usiloliweza kulifanya basi liache.

Tuseme wazi zaidi, ijapokuwa kuikubali Raj’ah kunahesabiwa kuwa ni lazima, lakini kuitakidi kwake si lazima wala kuikana haileti madhara, yaani hakuna tofauti yoyote katika imani yako ikiwa utaitakidi au la.26

26 Mtungaji anakusudia kusema kwamba ingawa itikadi ya Raj’ah ni moja katika itikadi zinazokubaliwa katika Ushia, lakini pia si miongoni mwa misingi ya itikadi za madhehebu ya Shia, kama ilivyo katika itikadi za Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, Utume na Uimamu ambazo kuzikana itikadi hizo humtoa mtu katika Ushia. (Mtarjumi).

Page 55: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

48

Kwa hakika, tukio la Raj’ah ni sawasawa kama baadhi ya matukio mengine ambayo yametabiriwa na viongozi wa Kiislamu kama vile kuteremka kwa Nabii Isa (a.s.) kutoka mbinguni, kudhihiri kwa Dajjali, kutokeza kwa Sufyani, n.k. ambayo ni maarufu katika madhehebu yote ya Kiislamu. Mambo haya si sehemu ya misingi na nguzo za Kiislamu wala kuyakana hayo hakutamtoa Mwislamu katika Uislamu. Vile vile kuitakidi matukio hayo tu si dalili ya kuikubali dini ya Kiislamu. Hebu tuchukulie, kwa mfano, kwamba Uyahudi umetokeza katika Ushia! Kusema maneno kama haya ni sawa na kusema kuwa Uyahudi umedhihiri pia katika dini ya Kiislamu, kwa sababu Mayahudi wanaitakidi kuwepo kwa Mungu Mmoja kama tunavyoitakidi sisi Waislamu. Je, upo usemi usio na msingi na wazo lisilo na maana kuliko hilo?

Laiti watu hao ambao tangu zamani na hata sasa wamerukwa na akili juu ya itikadi ya Kishia ya Raj’ah wangelijua maana halisi ya Raj’ah, basi isingelikuwepo haja ya kututuhumu kwa itikadi hiyo.

Je, ni muhali kwa Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo kuwapa uhai mwingine kikundi cha watu baada ya kufa kwao? Yupo Mwislamu yeyote anayeweza kukana uwezo huo wa Mwenyezi Mungu hali Qur’ani Tukufu imetaja waziwazi mfano wake? Je, hao wenye kushutumu na kuhoji hawakusoma katika Qur’ani kisa cha Bani Israili kinachosema:“Je! Hukuwaona wale waliotoka katika majumba yao wakiogopa mauti, nao walikuwa maelfu? Allah akawaambia: “Kufeni! Kisha akawahuisha.” (2:243).27

Je, hao wapingaji hawakusoma aya tukufu inayosema: “Siku tutakapofufua katika kila umma kundi moja...” (27:83).

Je, siku hiyo ni Siku ya Qiyama? Siyo kabisa, kwa sababu Siku ya 27 Aya hii imeteremshwa kuhusu kikundi cha Bani Israil ambao walikuwa wakiishi katika mji wa Dawurdan katika nchi ya Iraq. Wakati walipoamrishwa kupigana jihadi, na jeshi lao likawa tayari kupigana na adui, wakatoa kisingizio eti kwamba katika mji wa maadui upo ugonjwa wa kipindupindu, na wakakimbia na hawakwenda kupigana. Hapo tena kwa amri ya Mwenyezi Mungu wakafa na baadaye Mwenyezi Mungu akawafufua. Huu ni uthibitisho na ushahidi mmoja miongoni mwa ushahidi kadhaa juu ya Raj’ah. (Mtarjumi).

Page 56: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

49

Qiyama umma wote tangu mwanzo wa dunia hadi mwisho watafufuliwa, si kundi moja tu kutoka kila umma.

Suala la Raj’ah lilitumiwa na wanavyuoni wa Kisunni tangu zamani hadi zama hizi kama ni silaha yao kutushambulia sisi. Kwa hivyo, utaona kwamba waandishi wao wanapoandika juu ya maisha ya baadhi ya wanavyuoni na wapokeaji hadithi wa Kishia huwa hawana hoja yoyote ya kuweza kumponda, kumsingizia au kumharibia heshima mwanachuoni au mpokeaji hadithi huyo wa Kishia isipokuwa husema, “Yeye alikuwa akiitakidi Raj’ah!”, kana kwamba wanayemshutumu alikuwa mshirikina au mwenye kuabudu masanamu! Kisa cha Muumin wa Taaq na Abu Hanifa kuhusu jambo hili ni maarufu.

Ninavyoona mimi, suala hili halina umuhimu wa kutaka kuthibitisha, bali nilitaka tu nioneshe msimamo na maoni potofu ya mtungaji wa Fajrul-Islam.

TUHUMA YA KUSHANGAZA

Miongoni mwa masingizio yasiyo na msingi ambayo mwandishi huyo anawasingizia Mashia, mojawapo ni hili: “Mashia wanaitakidi kwamba moto wa Jahannamu ni haramu kwao isipokuwa (utawagusa) kidogo tu!”

Sijui ameiona hadithi hii katika kitabu kipi cha Kishia? Je, inafaa mtu ambaye amenuia kushindana, kutoa maoni juu ya itikadi ya madhehebu moja kwa kuwasingizia mambo yasiyo na msingi bila ya kuwa na dalili na uthibitisho?

Je, mwendo huu usiofaa unaweza kukubaliwa na mtafiti yeyote?

Vitabu vya Kishia vinasema kinagaubaga kwamba: “Mwenyezi Mungu ameiumba Pepo kwa ajili ya (malipo ya) watiifu hata akiwa mtumwa wa Kihabeshi, na ameumba Jahannamu kwa kila mwenye kumwasi hata akiwa Mtukufu wa Kiquraishi.” Hadithi kama hizi kutoka kwa Maimamu Maasum (a.s.) zimenukuliwa kwa wingi sana.

Page 57: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

50

Ikiwa kusudio la mtungaji ni shifaa (maombezi) ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na Maimamu (a.s.) kwa ajili ya baadhi ya walioasi, basi hilo ni jambo jingine ambalo Waislamu wote kwa jumla wanaliamini, na labda ni moja katika mambo ya lazima katika dini ya Kiislamu.28

Juu ya hayo, tunarejea kusema yale tuliyoyasema kabla, kwamba tuchukulie kuwa Mashia wanaitakidi jambo hili kama wanavyoitakidi Mayahudi. Je, hii ina maana kusema kwamba kufanana kwa itikadi za Kiyahudi na Kishia kunamaanisha kuwa Ushia una asili ya Kiyahudi au mafundisho ya Kiyahudi yameathiri madhehebu ya Kishia? Je, inaelekea kwa mwenye akili kusema kwamba, Fiqihi (sheria za dini) kwa mujibu wa Abu Hanifa ina asili ya Kimajusi kwa sababu baadhi ya fatwa zake kuhusu ndoa zinaafikiana nayo, na hasa kuwa yeye mwenyewe ana asili ya Kiajemi? Je, maneno kama haya yasiyo na msingi yanaleta faida gani isipokuwa kuwasha moto na uadui kati ya makundi ya Kiislamu?

Isitoshe, mwandishi wa Fajrul-Islam anaongeza kusema: “Dini ya Ukristo pia imedhihiri katika Ushia, kwa sababu baadhi ya Mashia wanaitakidi kwamba uhusiano wa Imam ni kama uhusiano wa Masihi Isa (a.s.) na Mwenyezi Mungu.”

Kama Ahmad Amin angetaka kuonesha uaminifu wake, angedhihirisha lengo lake, sio kwenda mwendo usiofaa na kusema maneno bila kufikiri. Kwa kweli, angesema waziwazi Shia yupi ana itikadi kama hiyo juu ya Imam na katika kitabu kipi itikadi hiyo imetajwa?

Ikiwa makusudio yake ni vikundi viitwavyo “Ghulatu ‘sh-Shi’a” kama Khitabiyyah, Gharabiyyah, ‘Alawiyyah, Mukhammasah, Bazi’iyya, na vingine kama hivyo, basi kwa bahati nzuri vyote hivyo haviko katika madhehebu ya Kishia wala havina uhusiano wowote na Ushia. Kuwafikiria na kuwadhania wafuasi wa vikundi hivyo kuwa ni Mashia ni dhuluma iliyo dhahiri, kwa sababu hao wote ni Walahidi, kama wale wafuasi wa Qaramitah ambao hawana dini. Lakini Shia

28 Taz: Sahih Bukhari juz: 1 uk:90 Kitabut-Tayammam; Sahih Muslim juz: 1 uk:188 Kitabul-Iman; Sunan Ibn Majah ju: 2 uk: 144 Kitabuz-Zuhd n.k.

Page 58: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

51

Imamia Ithnaashariyyah na Maimamu wao watukufu wako mbali na vikundi hivyo.

Hata hivyo, vikundi hivi pia hawaitakidi hivyo juu ya Imam, bali upotofu wa itikadi yao kwa ufupi ni huu: Wao wanasema kwamba Imam ni Mungu, na Mungu amejitokeza katika sura ya Imam, au wameungana, au Mungu ameingia katika kiwiliwili cha Imam, na maneno mengine kama haya.

Lakini Mashia Imamiyyah ambao wengi wao wako katika nchi za Iran na Iraq, na mamilioni wako katika Pakistan, India, na maelfu yao wako katika Syria na Afghanistan, wako mbali kabisa na fikra na itikadi kama hizi na wanazihesabu itikadi kama hizi kuwa ni ukafiri mbaya kabisa na upotofu dhahiri.

Mashia wanaamini Upweke wa Mwenyezi Mungu ambaye hafanani na kiumbe yeyote. Hawampi Mwenyezi Mungu sifa yoyote ambayo inafanana na sifa ya viumbe, kama vile kuweko mabadiliko katika Uungu Wake, kutodumu Kwake milele na kuwa na aibu na upungufu fulani. Wametunga vitabu vingi kuhusu Uungu, hasa vile vya itikadi na falsafa, kidogo kabisa kinaitwa At-Tajrid na kikubwa kabisa kinaitwa Al-Asfar na maelfu vinginevyo ambavyo kwa bahati nzuri vingi vyao vimechapishwa. Vitabu hivyo vinatoa dalili na thibitisho wa ubatilififu wa itikadi batili, kama vile kusema kwamba Mwenyezi Mungu hubadilisha maumbo Yake (Tanasukh), huungana na vitu (Ittihada), roho Yake huingia katika kiwiliwili kingine (Hulul), kujifanyia umbo fulani (Tajsim) n.k.

Ikiwa itikadi za Kishia zitaangaliwa kwa insafu na haki, itaonekana wazi kuwa masingizio yote hayo juu ya Tanasukh, Hulul na Tajsim hayana msingi wowote ila tu ni mawimbi ya fitina yanayotuelemea sisi katika zama hizi.

Kwa ufupi, ikiwa makusudio ya Ahmad Amin juu ya Ushia ni vile vikundi vilivyotoweka zamani na vilivyo vigeni katika Uislamu ambavyo huenda hakuna wafuasi wake waliobaki sasa duniani, basi tunakubaliana naye kuwa watu hao walikuwa na itikadi kama

Page 59: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

52

hizo zilizo potofu. Je, wafuasi hao na wafuasi wa Shia Imamiyyah wana uhusiano gani? Je, si dhuluma na kosa kubwa kututuhumu masingizio hayo? Lakini ikiwa kweli Ahmad Amin, kwa tuhuma hizo anatukusudia sisi Mashia ambao ni kundi kubwa na maarufu la mamilioni ya watu miongoni mwa mamilioni ya Waislamu wa duniani, basi amefanya kosa kubwa sana lisilosameheka, na tunamtaka atuletee dalili ya kuthibitisha madai yake kutoka katika kitabu chochote cha Kishia kilichoandikwa na wanavyuoni wa zamani na wa sasa.

Kwa jumla maneno yote yaliyoandikwa katika Fajrul-Islam kuhusu Ushia, hayana msingi wala dalili ila tu ni upuuzi mtupu.

Sisi hatuna haja ya kukijibu kitabu hicho kwa hoja moja baada ya nyingine na kueleza fikra za chuki zisizo za ukweli na za udanganyifu za mwandishi wake, bali haja yetu ni kutaja baadhi ya fikra za waandishi wa zama hizi zetu na za wale ambao wanahesabika kuwa ni wanavyuoni. Ikiwa waandishi na eti wanavyuoni wa umma huu mkubwa wanatufikiria hivyo sisi Mashia na kutuhukumu namna hii, basi ikoje hali ya watu wasiosoma na wasio na maarifa?

CHIMBUKO HASA LA MISIBA HII

Tukitafakari chanzo cha misiba hii, tutaona kuwa watu kama hao, aghlabu, kwa sababu ya kutojua madhehebu ya Shia wanategemea maneno ya Ibn Abd Rabbih Al-Andalusi au Ibn Khaldun Al-Barbari kama ndivyo hoja yao. Sasa mtu kama Ibn Khaldun alikuwa akiishi Morocco mahali palipo mbali kabisa katika Afrika, na akaandika kuhusu Ushia ndani ya Iraq, nchi iliyo mbali naye katika mashariki. Ili kuonesha maendeleo yao katika uchunguzi wao kuhusu Ushia, waandishi wa sasa wanaangalia na kutegemea maandishi ya wataalamu wa Magharibi kama Profesa Welthausen, Profesa Dozy, n.k., kuthibitisha hoja zao!

Jambo ambalo kamwe hawalizingatii ni kutafiti vitabu vyenyewe vya Kishia, ambapo kuna haja kwamba unapotaka kuzungumzia kuhusu Ushia inabidi kuvirejea vitabu vyao wenyewe.

Page 60: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

53

Lakini Mashia ambao wameziweka nguzo za itikadi zao juu ya msingi imara na wa kudumu, wanapoona maneno kama haya ya waandishi wa siku hizi kuhusu madhehebu yao ya Kishia, wanakumbuka kisa kifuatacho cha ajabu kilichonukuliwa na Raghib Al-Isfahan katika kitabu chake maarufu kiitwacho Al-Muhadharaat: “Mtu mmoja alikwenda katika baraza la Ja’far ibn Sulaiman kutoa ushahidi juu ya ukafiri wa mtu fulani, akasema: ‘Huyo ni kafiri.’ Akaulizwa kwa hoja gani, na akajibu: ‘Yeye ni mfuasi wa madhehebu za Khariji, Mu’tazalah, Nasibi, Haruri, Jabri na Rafidhi! Anamtukana Ali ibn Khattab, Umar ibn Qahafa, na Uthman ibn Abi Talib, na Abu Bakr ibn ‘Affan. Pia anamtukana Hajjaj ambaye alikuwa liwali wa Abu Sufian katika Kufah na akapigana na Husain ibn Muawiyah siku ya Qataif (alikusudia siku ya Taff au Taif)!’

“Baada ya kusikia ushuhuda huo ambao ulijaa makosa matupu, Ja’far akamwambia: ‘Mungu akulaani na akuue! Sijui nikuhusudu juu ya kitu gani, juu ya elimu yako ya nasaba, dini au madhehebu!’”29

USHIA NA ABDALLAH IBN SABAA

Abdallah ibn Sabaa ni mtu wanayemhusisha na Ushia au Ushia unahusishwa naye na anatambulishwa kama ni mwanzilishi wa Ushia. Tukiangalia kitabu chochote cha Kishia tutaona kuwa hakuna hata kimoja kinachozungumzia habari zake ila tu kinamlaani na kujiweka mbali naye. Katika vitabu vya Ilmur-rijali (inayohusu maisha ya wapokezi wa hadithi) chini ya alfabeti ya a’in, ametajwa kwa maneno machache hivi: “Abdallah ibn Sabaa amelaaniwa zaidi hata haifai kumzungumzia.” (Tazama Rijal cha Abu Ali na wengineo.)

Huenda Abdallah ibn Sabaa, Majnun Bani Amir, Abi Hilal na wengineo kama hawa ni watu wa kubuniwa tu katika ngano. Watungaji wa hadithi za kubuniwa wamewaumba watu hao katika dhana zao bila ya kuwepo uhakika wowote.

Uchunguzi wa historia ya Bani Umayyah na Bani Abbasi unaonesha kwamba katikati ya zama zao watu walikuwa wakiishi katika

29 Taz: Muhadharatul-Udabaa juz: 4 uk: 418.

Page 61: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

54

neema na raha iliyotia fora. Kwa desturi, kila starehe inapozidi na maisha yanapozidi kuwa mazuri, biashara ya udanganyifu, uzushi na utungaji wa visa vya uwongo huzidi ili walioshiba raha wajishughulishe navyo.

Sisi tunafikiri kwamba yale maneno matamu tunayoambiwa na akina Dakta Taha Husain na wenzake kuhusu Qur’ani na Uislamu hayafai katika zama hizi ambazo ni zama ya utafiti na uchunguzi wa ukweli kufuatana na kanuni ya uaminifu. Umekwisha ule wakati wa ujinga ambapo walikuwa wakipachika jina la ukweli na uhakika kwenye maneno yao ya tuhuma.

Kwa vyovyote, azma yetu si kuzungumzia mambo haya, bali hayo yalikuwa utangulizi. Lengo letu hasa ni hili, kwamba baada ya kuangalia sababu tofauti za uhasama, matatizo na tuhuma zisizofaa zinazotolewa na waandishi wa Misri na wengineo juu ya Ushia, imetubidi kuandika mjadala mfupi wenye nia njema kuhusu itikadi na asili ya madhehebu ya Kishia, na pia mambo mengi ya kidini ambayo yanakubaliwa na wanavyuoni wote wa Kishia kwa sauti moja.

Ni wazi kwamba katika mambo haya hatuwezi kutegemea rai ya mtu mmoja au watu kadhaa, kwani huwezi kuyatambulisha maoni hayo kwa jina la “Madhehebu ya Kishia”, hasa kwa kuwa katika Ushia mlango wa ijtihadi (uwezo wa kutoa fatwa) ulikuwa wazi na bado uko wazi, na kila mwanachuoni anaweza kutoa fatwa yake kufuatana na hoja na dalili madhali haiendi kinyume na rai za wanavyuoni wote kwa jumla (Ijmai’), Nassi ya Qur’ani na hadithi, au mahitaji ya kiakili. Fatwa kama hiyo itaheshimiwa, na ikiwa si hivyo, basi kwa mujibu na kanuni maalumu, itahesabiwa kuwa ni kinyume na madhehebu ya Kishia.

Kwa ufupi, shabaha yetu ya mwisho ni kueleza mambo muhimu yanayosimamisha misingi ya madhehebu ya Kishia ambayo kwayo hujenga itikadi za Kishia na kuitikadiwa na kufuatwa na watu wa kawaida na mahsusi, bila ya kuwepo hitilafu yoyote. [Hivyo, kitabu hiki tunakiita, Asili ya Ushia na Misingi Yake (Aslu ‘sh-Shia wa Usuluha)].

Page 62: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

55

Tunaeleza humu mas-ala hayo bila ya kushughulika kutoa hoja na marejeo yake. Ikiwa mtu anataka maelezo zaidi anaweza kuangalia vitabu vikubwa vilivyoandikwa kwa kusudio hilo.

Lengo letu kuu ni kutoa maelezo na utambulisho wa itikadi na fikra za Kishia kwa vikundi vyote vya Kiislamu, wanavyuoni na maamuma ili wafahamu kuwa Mashia ni Waislamu kama wao; na wasijidhulumu nafsi zao kwa kuwasingizia ndugu zao wa dini mambo batili na yasiyokuwa na msingi, na wasiwalinganishe na maafriti, mazimwi na mashetani, au kama washenzi wa porini na walawatu.

Wajue kuwa, Mashia kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, wamelelewa katika mfumo wa Kiislamu na ni wafuasi wa mafundisho matukufu ya Qur’ani. Mchango wao katika imani na maadili mema ni mkubwa mno. Hawategemei kitu isipokuwa Qur’ani, Sunna za Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na hoja madhubuti za kiakili.

Huu ndio msingi wao, hivyo basi wale wasiojua wajue, walioko katika mghafala wazinduke, wadadisi na wenye akili chache waache fitina zao, waungane kuondoa pazia la upinzani wa dini, na wawe kitu kimoja kuwaona kuwa ni ndugu zao wa kidini.

Huenda kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu kufuatia mzinduko huu na ukuruba wetu, Mwenyezi Mungu ataifanya kamba ya umoja kati ya Waislamu iwe madhubuti, akatupa nguvu ya kuwakabili maadui, na akatufanya tuwe na sauti moja katika kujitahidi kuutukuza Uislamu. Na Uwezo wa Mwenyezi Mungu hauko mbali kutekeleza matumaini yetu.

Katika kitabu hiki kwanza tutaanza kuzungumzia juu ya asili ya Ushia na vipi ulivyoendelea na kukua. Baadaye, tutaeleza misingi na itikadi za Kishia. Kwa hivyo, kitabu hiki kitakuwa na sehemu mbili: Kwanza, Asili ya Ushia na kuenea kwake, na pili, Itikadi na fikra za Kishia katika misingi na matendo ya dini.

Page 63: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

56

SEHEMU YA KWANZA

Ushia ulichipuka na kuanzishwa wapi na lini? Nani aliyeipanda na kuipalilia mbegu yake ya mwanzo na akauweka msingi wake? Vipi mche wake ulikua, ukastawi, ukanyanyuka na kuendelea kutoa maua na matunda? Vipi ulistawi na kufuatwa na hata baadhi ya watawala wakuu wa Kiislamu, makhalifa kadha wa kadha katika Bani Abbasi, kama Maamun na Nasiru-lidinillahi, na pia mawaziri wakubwa wa dola la Bani Abbasi na wengineo?

Sisi tunasema hali ya kuwa tunataraji msaada wa Mwenyezi Mungu kwamba, “Hakika mtu wa kwanza kuipanda mbegu ya Ushia katika konde la Uislamu si mwingine isipokuwa ni yule yule aliyekuja na sheria ya Kiislamu ambaye ni Mtume Muhammad (s.a.w.w.).” Hii ina maana kwamba, mbegu ya Ushia ilipandwa sambamba na mbegu ya Uislamu mahali pamoja na wakati mmoja, na aliendelea kuipalilia, kuihifadhi na kuitilia maji hadi mti wake ukakua na matawi yake yakatoa maua katika zama za uhai wake mwenyewe, kisha, (mti huo wa Ushia) ukatoa matunda baada ya kufariki kwake.

Uthibitisho wa maelezo haya umo katika hadithi za Mtume Mtukufu (s.a.w.w.). Hadithi hizo hazikupokewa kwa njia ya Kishia wala wapokezi wake hawakuwa Mashia hata isemwe kwamba hadithi hizo haziwezi kutiliwa maanani kwa kisingizio kwamba Mashia huitakidi Raj’ah (kurejea duniani kabla Qiyama hakijasimama) au isemwe kuwa wapokezi hao wa Kishia wanataka kujipendelea. Kwa hakika hadithi zenyewe zimepokewa na wanavyuoni na wakuu wa Kisunni na kwa njia zenye kutegemewa ambazo hazina shaka yoyote. Kamwe haziwezi kukataliwa, wala hakuna (mtu mwenye akili) anayeweza kusema kwamba zimetungwa na zimebuniwa.

Hapa ninazitaja baadhi tu ya hadithi ninazozikumbuka na ambazo niliziona nilipokuwa nikijisomea mas-ala mengine yasiyohusu jambo hili:1. (Mwanachuoni mashuhuri wa Kisunni, Jalalud-din ibn Abdul

Rahman As-Suyuti katika tafsiri yake ya Qur’ani iitwayo

Page 64: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

57

Ad-Durrul-Manthur fi Tafsiri Kitabil-Lahi bil-Ma-athur, amenukuu hadithi ifuatayo inayofasiri maneno ya Mwenyezi Mungu yanayosema: “Hao ndio viumbe bora.”30 kwamba, Ibn ‘Asakir amepokea hadithi kutoka kwa Jabir ibn Abdullah akisema hivi: “Sisi tulikuwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), alipokuja Ali (a.s.) Mtume akasema: ‘Naapa kwa Yule (Mola) ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, kwamba hakika huyu (Ali) na Mashia (wafuasi) wake ni (watu) wenye kufuzu siku ya Qiyama.’ Hapo ndipo ikateremka aya hii: ‘Hakika wale walioamini na wakatenda mema, basi hao ndio viumbe bora’.” (Qur’an 98:7)

2. Ibn ‘Adiyyi amepokea hadithi kutoka kwa Ibn Abbas akisema: “Ilipoteremka aya: “Hakika wale walioamini na wakatenda mema….”, Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Aya hii inakuhusu wewe na Mashia wako ambapo katika Siku ya Qiyama mtakuwa radhi na Mwenyezi Mungu, naye pia atakuwa radhi nanyi.”

3. Ibn Mardawaih amepokea hadithi kutoka kwa Ali akisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ameniambia: Je, hujasikia maneno haya ya Mwenyezi Mungu yanayosema: “Hakika wale walioamini na wakatenda mema, basi hao ndio viumbe bora”? Hao ni wewe na Mashia wako, na makutano yangu na wao yatakuwa kwenye Hodhi (la Kawthar) ambapo umma wote utakusanyika, na wafuasi wako wataitwa hali vipaji vyao viking’aa (kwa sababu ya amali njema walizozifanya).”

4. Vile vile baadhi ya hadithi hizo zimepokewa na Ibn Hajar katika kitabu chake kiitwacho As-Sawa’iqu ‘l-Muhriqa kutoka kwa Daruqutni. Vile vile amememnukuu Ummu Salama ambaye ni mke wa Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: Ewe Ali! Wewe na Masahaba wako (Mashia wako) mtakuwa Peponi.”

5. Ibn Athir amenukuu hadithi ifuatayo katika Al-Bidayah wa An-Nihayah chini ya neno qamh: “Ali (a.s.) amehadithia

30 Qur’an 98:7

Page 65: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

58

kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amemwambia: ‘Karibuni wewe na Mashia wako mtafika mbele ya Mwenyezi Mungu katika hali ya kuwa mmeridhika na Yeye amekuridhieni; na maadui zako watafika mbele Yake hali yakuwa wameghadhibika huku vichwa vyao vikiwa vinakokotwa. Kisha (Mtume) alifunganisha mikono yake shingoni mwake kuwaonesha namna vichwa vitakavyokokotwa!” Hadithi hii imepokewa pia na Ibn Hajar katika As-Sawaiq, na wanavyuoni wengine wameipokea kwa njia nyingine. Hadithi hii inaonesha kuwa ni moja katika hadithi maarufu kwa wataalamu wa hadithi.31

6. Katika kitabu kiitwacho Rabi’ul-Abrari cha Zamakhshari amepokea hadithi kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) akisema: “Ewe Ali! Nitakaposhikamana mimi na Mwenyezi Mungu katika Siku ya Qiyama, nawe utakaposhikamana nami, na wana wako watashikamana nawe, na Mashia wa wana wako watakaposhikamana nao, basi hapo utaona wapi tutakapoambiwa pa kwenda.”

Kama mtafiti atataka kufuatilia ndani ya vitabu vya hadithi kama vile Musnad cha Ahmad ibn Hambal na Khasa’is cha Abu Abdur- Rahman Ahmad ibn Ali An-nasai na vinginevyo, atakuta kwa urahisi hadithi nyingi zinazothibitisha yote hayo.

Kwa hivyo, ikiwa Bwana Mtume Muammad (s.a.w.w.) ambaye ndiye mwenye sheria za Kiislamu, mara kwa mara alikuwa akiwataja Shia wa Ali na akiwakusudia wao kuwa ndio wenye kupata amani siku ya Qiyama, wenye kufuzu na wenye kuridhika na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu, basi hapana shaka yoyote kwamba kila mwenye kuukubali Utume wa Muhammad (s.a.w.w.) lazima aamini na kuyakubali aliyoyasema, kwa sababu yeye “Hasemi (maneno) kwa matamanio yake mwenyewe isipokuwa hayo ni wahyi ulifunuliwa.” (Qur’an 53:3-4).

31 Rejea kitabu Fadhailil-khamsah minas-Sihahis-ittah cha Sayyid Murtadha Al-Husaini; Ihqaqul-haqqi wa Iz-haqul-batil cha As-Sayyid Nurullah Sustari na vinginevyo.

Page 66: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

59

KINA NANI WALIKUWA WAKIITWA SHIA?

Kutokana na hadithi tulizozitaja, tumefahamu kwamba jina la Shia walipewa kikundi makhususi cha masahaba wa Mtume tu wala si masahaba wote; na hadithi hizo zote zinathibitisha hivyo. Kwa hivyo, wale wanaoiacha maana yake halisi wakatafsiri kwamba masahaba wote wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) wanahusika, huwa hawakuielewa maana ya ndani ya hadithi hiyo.

Ijapokuwa masahaba wote wa Mtume hawakuwa Shia (yaani wafuasi wa Imam Ali), lakini bila shaka inawezekana kuwa baadhi yao walivutika kwa kufikiria maneno ya Mtume. Wao ni wale ambao walikuwa wamekwishazipata zile sifa alizozitaja Mtume (s.a.w.w.), si kwa kujidai na kujipendekeza tu, bali kwa kumfuata kidhati Imam Ali (a.s.).

Katika wakati wa uhai wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), idadi si ndogo ya masahaba waliokuwa karibu na Ali (a.s.), walishikamana naye, na walimtambua kuwa ni Imam wao, Wasii na mwenye kufikishia ujumbe unaotokana na Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Pia walimtambua Ali (a.s.) kama mfasiri wa mafundisho na elimu ya Mtume, na msiri wa hekima na hukumu zake. Walikuwa wakijuliakana tangu zama hizo kuwa ni Shia wa Ali (a.s.) na wakawa mashuhuri kwa jina hilo la Shia, kama walivyolieleza hilo wataalamu wa lugha ya Kiarabu ndani ya vitabu vyao, kama vile An-Nihayah32 cha Ibn Athir na Lisanu ‘l-Arab33 na vinginevyo.34 Vitabu hivyo vimeandika waziwazi kuwa neno ‘Shia’ lilitumika kama jina rasmi kwa wafuasi wa Ali (a.s.), wanawe na wanaowatawalisha mpaka likawa ni jina lao mahsusi.

Ikiwa makusudio ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) juu ya ibara ya “Shia wa Ali” ni wale waliokuwa wakimpenda Ali (a.s.) au kwa uchache hawakuwa na uadui naye, basi karibu Waislamu wengi au wote wangekuwa Shia wa Ali (a.s.) (kama wanavyodhania baadhi ya watu wenye maarifa madogo), na kwa matumizi hayo, neno Shia lisingeleta maana iliyokusudiwa.

32 An-Nihayah 2:51933 Lisanul-Arab 8:18934 Al-Qamusul-Muhit 3:47; Aqrabul-mawarid 1:627; Majmaul-Bahrain 4:356.

Page 67: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

60

Kuwa na mapenzi au kutokuwa na uadui na mtu fulani peke yake hakutoshi kumfanya mtu kupewa jina la Shia, bali neno hili lina maana yake makhsusi. Shia maana yake ni ufuasi, lakini kufuata peke yake hakutoshi, kwani maana yake hasa ni ufuasi na uambatanaji wa kudumu.

Kila mwenye elimu hata ndogo ya lugha ya Kiarabu na namna maneno yanavyotumika katika hali mbalimbali, anajua kwamba neno Shia, iwapo litatumika kwa maana nyingine, basi ni lazima lifuatane na maelezo ya kisarufi.

Kwa ufupi, sidhani mtu mwenye insafu (muadilifu) ataweza kukanusha hadithi hizo (za Mtume Mtukufu s.a.w.w) zenye kutoa maana hii kwamba makusudio ya ‘Shia’ ni kikundi mahususi cha Waislamu ambao walikuwa na uhusiano maalum na Ali (a.s.) na ambao walitofautiana kwa sifa maalum na Waislamu wengine wa siku hizo, na miongoni mwa hao hakukuwepo hata mmoja asiyempenda Ali (a.s.) seuze kumchukia.

Sikukusudia kusema kwamba masahaba wengine ambao hawakuwa katika kikundi hicho na ambao walikuwa wengi walimpinga Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), walikwenda kinyume na maneno yake au hawakufuata mafundisho yake - la hasha! Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kudhaniwa ndani yao jambo kama hilo, kwani masahaba wa Mtume katika zama hizo walikuwa ni watu walio bora kabisa katika dunia.

Hapa yanakuja maswali: Basi ni kwa nini masahaba hao hawakuwa miongoni mwa wafuasi wa Ali (a.s.)? Na ni kwa nini walipuuza masisitizo hayo yote kuhusu kuwa kwao wafuasi wa Ali (a.s.)?

Majibu ya maswali hayo yanajulikana. Huenda masahaba wote hawakuzisikia hadithi hizo; na huenda baadhi yao ambao walizisikia hadithi hawakuzifahamu makusudio yake halisi.

Kwa vyovyote vile, masahaba watukufu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) walikuwa na hadhi kubwa kwa kadiri ya kutoweza kufikiwa na wale wenye fikra finyu.

Page 68: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

61

Isitoshe hali hiyo, Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) hakuacha kuutilia maji ule mche (wa Ushia). Aliutilia maji matamu yatokanayo na maneno yake na ishara zake. Wakati mwingine alikuwa akisema waziwazi na wakati mwingine alikuwa akitoa ishara zenye maana kubwa kusisistiza ukweli huo. Hadithi zilizopokewa kuhusiana na suala hilo na wanavyuoni wakubwa wa Kisunni na hadithi ni maarufu, seuze zilizopokewa na wanavyuoni wa Kishia. Hadithi nyingi kati ya hizo zimenukuliwa katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim. Baadhi ya hadithi hizo ni kama hizi zifuatazo: 1. Hadithi maarufu iitwayo “Hadithul-manzilah”. Mtume Mtukufu

(s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali! Daraja yako kwangu mimi ni sawa na daraja ya Harun kwa Musa isipokuwa hakuna Mtume baada yangu.”35

2. Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema (kumwambia Imam Ali a.s.): “Hatakupenda mtu yeyote ila muumini, na hatakuchukia ila mnafiki.”36

3. Hadithi maarufu iijulikanayo kama “Hadithut-tair”. “Ewe Mola! Mlete kwangu mja aliye kipenzi kabisa kwako.” (Na Imam Ali a.s. akafika kwake.)37

4. Usiku mmoja wakati wa vita vya Khaibar, Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alisema: “Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda mtu huyo.”38 (Na Imam Ali a.s. ndiye aliyepewa bendera hiyo.)

5. Hadithi maarufu iitwayo “Hadithut-thaqalain”. Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: “Mimi ninakuachieni (vitu) vizito viwili: Kitabu cha Allah na watu wa ndani ya nyumba yangu.”39

35 Sahih Bukhari juz 5 uk 24; Sunan Ibn Majah juz 1 uk 42/115 na vingine vingi.36 Sahih Muslim juz 1 uk 86/131; Tarikh Baghdad juz 2 uk 255 na vinginevyo.37 Sunan Tirmidhi juz 5 uk 636/3721; Usudul-ghabah juz 4 uk 30 na zaidi ya hivyo. 38 Tarikh Dimishq juz 2 uk 105-151; Tadhkiratul-Khawwas uk 44.39 Sunan Tirmidhi juz 5 uk 662; Musnad Ahmad juz 3 uk 17 na juz 5 uk 181; Mustadrak Al-Hakim juz uk 109 na148.

Page 69: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

62

6. Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: “Ali yuko pamoja na haki, na haki iko pamoja na Ali”.40

Kuna hadithi nyingi nyingine kama hizi ambazo hakuna haja ya kuzitaja mojamoja na kuthibitisha sanadi zake. Kwa bahati nzuri, kuna vitabu vingi vilivyoandikwa na wanavyuoni wa Kishia Ithna- asharia katika uwanja huu ambavyo vimetupunguzia mzigo wetu. Miongoni mwa vitabu hivyo, kuna kimoja kiitwacho ‘Abaqaatul- Anwaar kilichoandikwa na mwanachuoni aliyebobea aitwaye Sayyid Hamid Husain wa Lucknow (India). Kitabu hiki kina zaidi ya juzuu kumi ambazo ukubwa wa kila juzuu moja karibu ni sawa na ukubwa wa Sahih Bukhari nzima. Sayyid Hamid Husain amezitaja sanadi za hadithi hizo kwa njia inayotegemewa na wanavyuoni wa Kisunni na akazitaja kwa hoja za makusudio yake. Mtungaji huyo ni mmoja tu kati ya maelfu ya watungaji waliomtangulia au waliomfuatia ambao waliandika kuhusu maadhui hiyo.

SABABU ZA KUENEA USHIA

Baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kufariki dunia, kundi moja la masahaba walipinga Imam Ali kupewa Ukhalifa, kwa sababu ya umri wake mdogo au kwa kuwa Maqureshi walitaka Utume na Ukhalifa usikusanyike na kuendelea katika ukoo wa Bani Hashim. Utafikiri kwamba kuchagua Utume na Ukhalifa kupo mikononi mwao, na kama wanavyotaka wao kumpa mtu fulani Ukhalifa humpa. Kundi hilo walitoa visingizio kuwa Ukhalifa unawahusu wao, au kwamba wao wana haki ya kuchagua kama wanavyotaka wao, au kwa sababu fulanifulani ambazo hatuna haja kuzichunguza hapa.

Madhehebu mbili za Kishia na Kisunni wanakubaliana kuwa Imam Ali (a.s.) hakumbai (hakumkubali na kumtii) khalifa wa kwanza aliyechaguliwa na watu. Pia, katika Sahih Bukhari mlango wa Vita vya Khaybar, imeandikwa kuwa Imam Ali (a.s.) hakumbayi ila baada ya miezi sita. Siyo Ali (a.s.) peke yake bali na kundi la masahaba wakubwa, kama mabwana Zubair, Ammar, Mikdad, Salman na wengi wengineo walimfuata Imam Ali (a.s.) vivyo hivyo.41 40 Tarikh Baghdad juz 14 uk 321; Mustadrak Al-Hakim juz 3 uk124. 41 Madai ya kuwa Imam Ali (a.s.) alimpa baia Khalifa wa kwanza baada ya miezi sita hayakuthibiti kwa upande wa Wanachuoni wa Kishia.

Page 70: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

63

Lakini Imam Ali (a.s.) alipoona kuwa kujitenga kwake kutaleta mtengano usioungika katika Uislamu, na kwa upande mwingine kila mmoja alijua kwa hakika kuwa Imam Ali (a.s.) hakuwa na tamaa ya kutaka Ukhalifa wala hakutaka ufalme na ushindi, bali alitaka kwa hamu Uislamu uwe na nguvu, uenee, utapakae, usimamishe haki na uangamize ubatilifu, alikubali kushirikiana naye. Hakika hayo yote yanathibitika katika mazungumzo yaliyo maarufu baina ya Imam Ali na Bwana IbnAbbas, katika mahali paitwapo Dhiiqar.42

SABABU YA IMAM ALI (A.S.) KUKAA KIMYA NA KUTODAI HAKI YAKE

Imam Ali (a.s.) alipoona makhalifa wawili wa kwanza walikuwa wakijitahidi kueneza jina la Mwenyezi Mungu Mmoja kwa kutayarisha majeshi yenye kuweza kuwaletea ushindi; bila ya kuonesha inadi au dhulma, hakujali madai yake ya haki, alishirikiana nao ili Uislamu uhifadhike na baadhi ya Waislamu wasirejee ukafirini. Wafuasi wa Imamu Ali (a.s.) walijiweka chini ya amri yake wakasoma kwake na kupata nuru ya elimu yake. Wakati ule hapakuwepo uwanja wa kuchomoza Ushia, kwani Uislamu ulikuwa ukiendelea vizuri kwa kadiri ya kupambanua haki na batili.

IMAM ALI (A.S.) KAMA KHALIFA

Imam Ali (a.s.) alipochaguliwa kuwa Khalifa, Muawiyah ibn Abu Sufyan hakukubali kumtii, bali alisimamisha majeshi yake na kupigana naye katika vita maarufu ya Siffin. Ushia ndipo ukachomoza wakati huu, na haki na batili vikadhihirika. Masahaba wakubwa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) waliobaki waliungana na kumfuata Imam Ali (a.s.) na wengi wao waliuawa katika vita hivi chini ya ya bendera yake. Masahaba wakubwa wapatao themanini hivi walikuwa pamoja na Imamu Ali (a.s.), kama vile mabwana Ammar ibn Yasir, Khuzamah maaarufu kwa jina la Dhish-Shahadatain, Abu Ayyub Ansari, na baadhi ya

42 Ibn Abbas anasema siku moja niliingia kwa Amirul-Muuminina (a.s.) alipokuwa mahala paitwapo Dhiiqar; nikamkuta anasafisha kiatu chake akasema, “Namuapa Mwenyezi Mungu, kiatu changu hiki ni bora mno kwangu kuliko huo utawala wenu (mnaoniitia) isipokuwa tu nikisimamisha haki na kuondoa batili”

Page 71: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

64

walioshirikiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika vita ya ‘Badr’ na katika makubaliano ya (Bay’ah) ‘Aqaba’.

MUAWIYAH NA JINSI ALIVYOICHEZEA DINI YA KIISLAMU

Imam Ali (a.s.) alipouawa, Ukhalifa wa ‘Rashidiyn’ ukamalizika. Baada yake, Muawiyah alipata fursa ya kuchukua utawala mikononi mwake, na kwa kwenda mwendo wa ukandamizaji na kutoa amri ya nguvu juu ya Waislamu, na alitenda mambo mengi kinyume cha sheria ya Kiislamu ambayo hatuna nafasi ya kueleza hapa. Waislamu wote wanakubaliana kuwa Muawiyah alikwenda kinyume cha Makhalifa waliomtangulia, na akatumia hukumu zake kwa nguvu juu ya Waislamu.

MAKHALIFA WA KIDUNIA NAUCHAJI MUNGU WA AHLUL-BAYT (A.S.)

Katika wakati wake wa Ukhalifa, Amirul-Mu’minina Ali (a.s.) aliishi maisha ya ibada, ucha Mungu, umasikini, kutokudanganya na kutokujipendekeza kwa watu kwa maneno na vitendo vyake. Muawiyah alikuwa akiishi maisha kinyume kabisa na maisha ya Imamu Ali (a.s.) tulivyoelezea hapa. Alikuwa hamsikilizi mtu yeyote; hutenda jambo kama anavyotaka na anavyopenda yeye mwenyewe. Nayo Qadhiya maarufu ya Muwaiyah kumkabidhi Amri ibn Al-Aas madaraka ya nchi ya Misri ni mfano mmoja wa kitendo chake cha udanganyifu na hiana.43 Mifano mingine wa hiana yake ni kule kuwalazimisha kwa nguvu Waislamu kula kiapo cha utii kwa mwanawe Yazid44, na kumwagizia Ziyad ibn Abih amfanye 43 Muawiyah alimwita Amri na kumshawishi washirikiane kumpiga Imam Ali (a.s.), na iwapo watashinda basi yeye Muawiyah atampa Amri nchi ya Misri aitawale.44 Namuapa Mwenyezi Mungu, hilo peke yake ni dhambi kubwa mno lenye kuangamiza na kumuingiza Muawiyah kwenye tabaka la chini kabisa la moto wa Jahannam, kwani yeye alimtawalisha juu ya Umma wa Kiislamu mtu aliyekuwa na kila aina ya sifa mbaya, bali alikuwa ni adui wa wazi kabisa dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na alikuwa ni mwenye chuki kubwa kwa Watu wa ndani ya nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) kiasi ambacho alifanya maovu mengi na miongoni mwa aliyoyafanya yalizitetemesha mbingu na ardhi. Katika hayo ni kule kumuuwa mwana wa binti ya Mjumbe waMwenyezi Mungu, Imam Husein (a.s.).

Page 72: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

65

mwana wa baba yake.45

Mali ya umma (Baytul-Maali au Hazina ya Serikali) ambayo makhalifa wa kwanza na wa pili46 walikuwa wakiitumia katika kuimarisha majeshi ya Kiislamu kwa kununulia zana za vita ili kulinda dini ya Uislamu, ilitumiwa na Muawiyah, kinyume cha madhumuni yake, kwa kujiandalia starehe na vyakula vizuri vya kila aina kwa ajili yake na wasaidizi wake.

Bwana Abu Said Mansur ibn Husain Al-abii aliyekufa mwaka 422 A.H anaeleza katika kitabu chake kiitwacho Nathrud-Durar Juzuu ya kwanza ukurasa 305 hivi: -“Ahnaf ibn Qais anasema: ‘Siku moja nilikwenda kwa Muawiyah, yeye akaniandalia kila aina ya vyakula. Mimi nikaona ajabu mno, kwani sijapata kuona vyakula namna hiyo. Kisha akaamrisha iletwe namna nyingine ya chakula. Mimi nikakichunguza sana lakini sikuweza kutambua chakula hicho. Nikamwuliza hicho kilikuwa chakula cha aina gani? Akanijibu kwamba ni matumbo ya bata yaliyotiwa ubongo na kukaangwa na mafuta ya karanga na kurashiwa sukari!

“Mimi nikalia, naye akaniuliza sababu ya kulia kwangu. Nikamjibu, “Nimemkumbuka Ali ibn Abi Talib, sitamsahau kamwe. Siku moja nilipokuwa kwake na wakati wa kufuturu ulipofika, akanitaka nisiondoke, kisha akaletewa mfuko wa ngozi uliofungwa. Nikamwuliza, “Mna nini katika mfuko huu?” Akanijibu, “Mna unga wa shairi.” Nikasema, “Kwa nini umeufunga? Kwani unaogopa usichukuliwe? Au hupendi mtu ale kilichomo humo?” Akanijibu, “Yote hayo siyo, bali naogopa wanangu Hasan na Husain wasichanganye unga pamoja na samli au mafuta ya alizeti!” 45 Naam Muawiyyah alimfanya Ziyad kuwa ni mtoto wa Abu Sufian kwa madai kwamba Abu Sufian alizini na mwanamke aliyekuwa akiitwa Sumayyah akazaliwa Ziyad. Ajabu iliyoje kwa Umma wa Kiislamu ambao bado unawaheshimu na kuwatukuza viongozi walioipotosha Dini wakapoteza hukmu zake, wakahalalisha yaliyoharamishwa, wakamwaga damu ya Waislamu na hawakuacha chochote miongoni mwa mambo maovu ila waliyafanya. Taz: Tarikh Tabari juz 5 uk 214; Tarikh Al-Kamil juz 3 uk 441; Muruj Ad-Dhahabi juz; 3 uk 193 n.k. 46 Huenda Sheikh Muhammad Kashiful-Ghita anawakusudia Abu Bakr na Umar, lakini mimi sijakuta wajihi wowote wa kuwahusisha na jambo hilo, yafaa ufanye mazingatio…… (Alau Alu Jaafar, Mhakiki).

Page 73: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

66

Nikasema, “Kwani ni haramu, ewe Amirul-Mu’minin?” akanijibu, “La! si haramu, lakini viongozi wa dini inawabidi wajiweke katika hali ya chini ili maskini wasivunjike moyo na kuudhika kwa umaskini wao.” Muwiyah akasema, “Umemtaja mtu ambaye hakuna mtu anayeweza kupinga Utukufu na mema yake.”

Katika kitabu cha Rabiul Abrar cha Bwana Zamakhshari na vitabu vingine kama hivyo, utaona visa vya ajabu vingi kama hiki, vyote vinashuhudia kuyakiri madai hayo ya Muawiyah.

Mambo hayo yote ya fedheha yaliyotendwa na Muawiyah, yalitokea wakati ambapo watu walikuwa bado wanakumbuka zama za Mtume (s.a.w.w.) na Makhalifa namna walivyokuwa wakiepukana na mapambo na matamanio ya dunia. Hali hii ya kuchukiza iliendelea hadi wakati Muawiyah alipovunja ahadi na makubaliano ya usuluhisho baina yake na Imamu Hasan (a.s.)47 na hatimaye akamtilia sumu na kumfanya Imam Hasan (a.s.) kuwa shahidi. Baadaye, Muawiyah alipata fursa ya kuendeleza maovu yake, na akawalazimisha watu wamtii mwanawe Yazid, hali ya kuwa Waislamu wa zama hizo walikuwa wakifahamu vizuri maovu yake kuliko tunavyomfahamu sisi.

Kwa sababu ya hali ya mambo hayo maovu, Waislamu wakajawa na chuki na bughudha moyoni mwao dhidi ya Muawiyah, na wakatambua kwamba hakuwa mtu wa dini hali alishughulika na dunia tu. Angalia vipi Muawiyah, kwa maneno yake mwenyewe anakiri na kutambua uovu wake, kwa kusema:- “Hakika Abu Bakr alisalimika na dunia, na dunia ikasalimika naye. Ama Umar aliipenda dunia, nayo ikampenda. Ama Uthman aliipata dunia na dunia ikampata yeye. Lakini mimi nimeipata dunia na kushikamana na kuungana nayo barabara, na dunia imeshikamana nami vivyo hivyo.” Habari hizi zimenukuliwa kutoka kitabu kiitwacho Rabiul Abrar cha Bwana Zamakhshari juz 1, uk 90.47 Walikubaliana kwamba Muawiyah atakapokufa basi ukhalifa urejeshwe kwa Imam Hassan (a.s), na kama Imam Hassan atatangulia kufa ukhalifa atachukua Imam Husein (a.s) baada ya Muawiyah kufariki, lakini kinyume chake kabla ya yeye Muawiyah kufariki alifanya njama za kumuuwa Imam Hassan kwa kumtilia sumu ndani ya chakula, na hatimaye akafanya maandalizi ya kumtawalisha mwanawe muovu Yazid.

Page 74: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

67

Kuanzia za Muawiyah na Yazid, dini na utawala vilitengana, si kama ilivyokuwa katika zama za makhalifa (wanne wa kwanza) waliotangulia ambao waliikusanya dini na utawala pamoja na kuwa ni kitu kimoja. Lakini kutoka zama za Muawiyah watu wakatambua kwamba yeye hakushikamana na dini bali amejishughulisha na siasa na kutafuta matilaba yake tu. Ndipo wakafahamu kwamba dini hasa ina waongozi wake mahsusi ambao ndio wanaohusika na dini yenyewe, na wenye sifa maalum za kuongoza. Na hakuna aliyekuwa na sifa za kuongoza, kama vile elimu, ucha-Mungu, ushujaa na utukufu kama walizokuwanazo Imam Ali (a.s.) na wanawe. Isitoshe, hadithi za Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), zilizopokelewa na masahaba zilithibitisha utukufu na daraja zao na kusababisha kutoa matunda kwa mche wa Ushia, na kuupa umma wa Kiislamu roho mpya.

Ufuasi kwa Imam Ali (a.s.) na wanawe uliendelea kukua na kuimarika polepole miongoni mwa Waislamu wote, kama mfano wa mgonjwa kupona na kupata siha pole pole. Kuteswa na kuuawa kishahidi Imamu Husain (a.s.) na wanawe katika ardhi ya Karbala kuliwazindua na kutia jeraha kubwa katika nyoyo za Mashia na masahaba waliobakia, kama vile Bwana Zaidi ibn Arqam, Jabir ibn Abdillahi Al-Ansari, Sahal ibn Sa’ad As-saidi na Anas ibn Malik. Kwa nini wasiwe hivyo, hali ya kuwa masahaba hao waliona na kushuhudia mapenzi ya Mtume kwa Imam Husain na nduguye Hasan (a.s.) na namna gani alivyokuwa akiwabeba mabegani mwake huku akisema “Kipando kizuri kilioje! na wapandaji wazuri walioje! Wao ni Mabwana wa vijana wa Peponi;”48 na maneno mengine aliyoyasema juu yao! Naam, masahaba hao walikuwa bado wahai, na wakauelezea umma yote waliyoyaona na kuyasikia kuhusu Imamu Husain (a.s.) na kaka yake. Wakaendelea kwa shauku kuzitangaza zile hadithi zenye kuwatukuza Imamu Ali (a.s.) na wanawe.

UHALIFU WA KIZAZI CHA UMAYYAH NA KIZAZI CHA MARWAN

Bani Umayyah waliendelea na dhulma yao ya kuwaua wazao wa

48 Unaweza kurejea vitabu mbalimbali vinavyohusu ubora na daraja ya Imam Hassan na Husein (a.s) ambavyo vimeandika riwaya nyingi mno sahihi kuwahusu wao.

Page 75: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

68

Mtume kwa kuwapa sumu, kuwachinja kwa upanga na kuwafunga magerezani kwa muda mrefu. Ni dhahiri kwamba dhulma hizo zilizotendwa na hao madhalimu hazikusaidia kitu ila tu ziliharakisha kuenea kwa Ushia na kutapakaa duniani; na utukufu wa Imamu Ali (a.s.) na wanawe ukajaa katika nyoyo za watu, na maonevu waliyoyapata yalizidisha mapenzi ya watu kwao. Kadiri Bani Umayyyah walivyotumia nguvu juu ya wafuasi wa Imamu Ali na wanawe kwa kuwatesa na kuwakandamiza mara kwa mara, na kwa kuwalazimisha wawatukane Imam Ali (a.s.) na wanawe, na kuficha sifa na utukufu wao, ili utawala wao uimarike hali hiyo ilileta matokeo kinyume chake, na ndivyo watu walivyozidi kuwapenda na kuwafuata.

Je, hukuyasikia maneno ya Bwana Sha’bi aliyomwambia mwanawe, “Ewe mwanangu, kila kilichojengwa na dini na wenye imani, hakitaweza kuvunjwa na dunia; na kila kilichojengwa na dunia na wapenda dunia kitabomolewa na dini. Huoni kwamba kitendo cha Bani Umayyah cha kujitahidi kuficha sifa na utukufu wa Imam Ali (a.s.) na wanawe kulikuwa kana kwamba ni kuwakamata na kuwachukua mbinguni. Lakini kujaribu kwao kwa jitahada kubwa kutangaza sifa za wazee wao (akina Abu Sufian na Muawiyah) kulikuwa kana kwamba ni kutandaza mizoga?”

Maneno haya ya Bwana Sha’bi aliyomwambia mwanawe yanadhihirisha sifa na utukufu wa Imamu Ali (a.s.) na wanawe, ingawa Bwana Sha’bi alituhumiwa kuwa ni mmoja kati ya wale waliokuwa wakiwabughudhi na kuwachukia Imam Ali na wanawe (a.s.). Bwana Zamakhshari, katika kitabu chake kiitwacho Rabiul Abrar anasema kuwa Sha’bi alisema, “Mambo gani haya yaliyotupata kwa ajili ya Imam Ali (a.s.), Tukimpenda tunauawa, na tukimchukia tutaangamia?”

Baada ya kumalizika utawala wa kizazi cha Sufiani, ukaanza uta-wala wa kizazi cha Mar-wani49 na mtawala wao wa kwanza alikuwa 49 Banu Umayyah wanagawika katika matumbo mawili makubwa ambayo ni, Al-Anabisah na Al-A’yaas. Hawa Al-Anabisah nasaba yao inatokana na A’mbasah ambaye ni ami yake Abu Sufian ibn Harb, na kutokana na huyu Abu Sufiyan ndiyo wakaitwa As-Suf-yaniyyiina. Amma hawa Al-A’yaas nasaba yao inatokana na mtu aliyekuwa akiitwa Al-A’is au Al-Uwais au Al-A’s au Abul-A’s ambaye miongoni ⇒

Page 76: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

69

Abdul Malik. Je, unajua maovu yepi aliyoyafanya huyu Abdul Malik? Kwa amri yake, liwali wake Hajjaj, alifunga majukwaa kwenye jumba la Ka’aba tukufu, akalibomoa na kulitia moto, kisha akawaua wenyeji wa Makka, na akamchinja Bwana Abdallah ibn Zubair katika Masjidul-Haram baina ya Ka’aba na Maqaam Ibrahim. Akauvunja utukufu na heshima ya msikiti wa Haram ambao ulikuwa ukiheshimiwa na makafiri (kabla ya kuja Mtume) hata walikuwa wakiogopa kumwaga damu ya mnyama seuze ya binadamu. Mfano mwingine wa ukatili na unyama alioufanya huyu Abdul Malik ni kule kumpa amani binamu yake Amr ibn Said Al-Ashdaq kwa kumwahidi na kumwapia Mwenyezi Mungu, kisha akageuka na kumwua kwa hila na ujanja; kitendo ambacho kilimfanya Abdulrahman ibn Hakam kutunga shairi lisemalo:-

“Mmemkhini Amr ibn Said, enyi wana wahaini waovu;Ahadi zenu mnazijenga juu ya msingi wa uhaini.”

Je, mwenye kutenda vitendo kama hivi inakubalika kuwa ni Muislamu seuze kuwa Khalifa wa Waislamu na Bwana wa walioamini!!”?

UTAWALA WA BANI ABBASI

Watawala wote wa dola ya Mar-wani walikuwa na vitendo viovu kama au kuliko hivyo, isipokuwa kijana mmoja tu, Umar ibn Abdul Aziz ambaye alikuwa mwema.

Baada ya utawala wa kizazi cha Mar-wani ukaja utawala wa kizazi cha Banu Abbas ambacho kilikuwa na udhalimu na uovu wa ulio vuka mpaka, hata kwamba uliimbiwa nyimbo na mwimbaji mmoja aliyeishi katika zama za tawala zote mbili, (za Mar-wani na Abbas) ikisema hivi:-

“Laiti dhulma ya Bani Mar-wani ingedumu kwetu,na uadilifu wa Bani Abbasi ungeangamia motoni.”

Kwa dhulma zao juu ya wana wa Ammi yao Bani Hashim au Alawiyyiin (wazao wa Imam Ali a.s.), Bani Abbasi walikuwa ⇐ mwa wanawe ni yule Al-Hakam ambaye yeye na mwanawe Mar-wan walifukuzwa na Mtume (s.a.w.w.) kutoka mjini Madina, na watu wawili hawa wanao utajo mbaya (katika historia ya Uislamu).

Page 77: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

70

wakiwasaka kila pembe na kuwaua hata wakipatikana chini ya jiwe, na walikuwa wakibomoa majumba yao wanayokaa na kuyafuta hata alama zao.

Mshairi mmoja katika wakati wa utawala wa dhalimu mkubwa wa Bani Abbasi aitwaye Mutawakkil, alisema hivi:-

“Naapa, kwa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa Bani Umayyah wamemwua kwa dhulma mtoto wa Binti wa Mtume, basi binamu zake (Bani Abbasi) wamefanya kama haya kwa kuwaua wajukuu zake na kujaribu kufuta alama ya kaburi la Imamu Husain;Bani Abbasi walijuta kwa kusema kwamba hawakushiriki kumwua Husain, bali wao wametenda uasi kuliko haya kwa kujaribu kumdhulumu baada ya kufariki kwake dunia.”50

Ikiwa msomaji utazingatia tabia njema walizokuwa nazo wana wa Imamu Ali (a.s.) na tabia mbaya walizokuwa nazo Bani Ummayyah, Bani Mar-wani na Bani Abbasi; hakika itadhihirikia ni kwa nini na kwa sababu gani Ushia ulienea.

Kwa bahati nzuri, kwa msaada wa habari za maisha yao zilizorikodiwa, ukweli umebainika kwamba, madhehebu ya Shia haina asili ya Kiajemi au Abdallah ibn Saba, n.k., bali ulikuwa ni Uislamu wa asili uliyoasisiwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

WANA WA IMAM ALI (A.S.) WASIMAMIZI WA UISLAMU

Ili kupata uhakika na ukweli, hebu tuangalie historia ya maisha ya 50 Suyuti ameeleza ndani ya kitabu chake cha historia uk. 277 kwamba, Mnamo mwaka wa 36 A.H. Mutawakkil aliyelaaniwa aliamuru kaburi la Imam Husain (a.s.) libomolewe, pia alizibomoa nyumba zilizokuwa zinalizunguka kaburi hilo na akaamuru eneo hilo lifanywe kuwa mashamba. Si hivyo tu bali aliwazuia watu kulizuru kaburi la Imam Husain (a.s.) kisha mahala hapo akapaharibu kabisa pakabakia patupu. Huyu Mutawakkil alikuwa mashuhuri kwa kuwachukia watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.), hali hiyo iliwatia uchungu sana Waislamu kiasi kwamba walilazimika kuonesha machungu yao na hasira zao kwa kuandika shutma zao dhidi ya Mutawakkil kwenye kuta za Miskiti na majumba. Washairi wa zama hizo nao hawakubaki nyuma bali walitunga mashairi kumshutumu.

Page 78: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

71

wana wa Ali (a.s.), wakiongozwa na Imam Ali ibn Husain (a.s.).

Kuna watu wanatuhumu kuwa Mashia wana asili ya Kimajusi au Kisabii (dini za kale), lakini hakika si hivyo, kwani hakuna shaka yoyote kwamba Mashia wanatokana na Waislamu na wanamfuata Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) tu. Tukiangalia maisha, tabia na mwenendo mwema wa wana wa Imamu Ali (a.s.), na hasa maisha ya Imam Ali ibn Husain (a.s.) mashuhuri kwa jina la Zainul Abidin (yaani Pambo la Wacha Mungu) utauona Uislamu wao kuwa ni wa kidhati. Baada ya kuuawa baba yake (Imamu Husain a.s.), Imam Zainul Abidin (a.s.) alipata masaibu mengi, akajitenga kabisa na dunia, akawa wakati wote katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, kujisafisha moyo kwa ajili Yake na na kujilinda na mambo yasiyofaa ya kidunia (kama ufalme na mali). Yeye ndiye aliyefungua mlango wa utawa kwa kikundi cha Tabi-ina kama vile Hassan Basri, Taus Yamani, Ibn Sirin, Umar ibn Abeid, na kadhalika.

Itakumbukwa kwamba katika wakati wa Imamu Zainul Abidin (a.s.), Waislamu walipata wakati wa kufaa na msaada mkubwa kutokana na vitendo vizuri vya mtukufu huyo, baada ya kuwa wao walipotoka mbali na njia ya haki.

Baada yake, wakafuatia mwanawe, Imamu Muhammad ibn Ali al-Baqir (a.s.) na mjukuu wake, Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) ambao wakatilia nguvu misingi ya Kiislamu.

ZAMA ZA HERI WAKATI WA IMAMU JA’FAR AS-SADIQ (A.S.)

Kwa bahati nzuri, katika wakati wa Imam Ja’far Sadiq (a.s.) tawala mbili za Bani Umayyah na Bani Abbasi walikuwa wakipigana. Bani Umayyah walikuwa wanaanguka na ikawa mwisho wa utawala wao. Na kwa kuwa Bani Abbasi walikuwa bado hawakupata nguvu kamili, Imam Sadiq (a.s.) alipata fursa nzuri ya kuimarisha dini ya babu yake (Mtukufu Mtume s.a.w.) na kuitangaza vyema. Hofu ya kudhulumiwa ikaondoka na watu wakapata uhakika wa hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.w.) moja kwa moja kutoka katika mdomo

Page 79: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

72

wa Imam Sadiq (a.s.). Katika wakati huo ndio Ushia ukadhihirika na ukapata nguvu isiyo na kifani ambayo haujapata katika zama za Maimamu waliomtangulia.

Katika wakati wa Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) watu wengi sana walipata elimu na wakapokea hadithi za Mtume kutoka kwake, hata kwamba Abul Hassan al-Washai aliwaambia watu kadhaa wa Kufa (Iraq) kuwa, “Aliwahi kuwaona wanavyuoni elfu nne katika msikiti wa Kufa ambao wote walikuwa wenye dini kamili na wacha Mungu, na kila mmoja katika hao alikuwa akisema, ‘Nimehadithiwa hadithi hizi za Mtume na Imam Ja’far Sadiq (a.s.)’.”

Hatuna haja kuendelea kuthibitisha juu ya mambo haya kwani tutatoka katika makusudio yetu. Mambo haya ni dhahiri kwa watu wote kama mwangaza wa jua katika siku za kaskazi.

Watawala wa Bani Umayyah na Bani Abbasi wote walikuwa wakijishughulisha katika kuimarisha tawala zao, kupigana na wapinzani wao na kujistarehesha na raha za dunia (kama ulevi, wanawake na muziki), wakati wana wa Imamu Ali (a.s.) walikuwa wakijishughulisha katika elimu, ibada, uchamungu na kujitenga na raha za dunia na matamanio yake. Hawakushughulika wala kuingia katika mambo ya kisiasa kwa kuwa siasa ya Bani Umayyah na Bani Abbasi ilikuwa ni kutumia uongo, hiana na hadaa.

Ni dhahiri kwamba tofauti katika makusudio mawili haya ilisababisha kuenea madhehebu ya Kishia na kukivuta kikundi kikubwa cha watu kuelekea kwenye madhehebu hiyo. Vile vile ni dhahiri kwamba hapana shaka kuwa nyoyo za watu wa zama hizo kama zama zozote zile, zilimilikiwa na matamanio ya mali na raha za dunia, lakini juu ya hayo yote, kwa wakati huo huo, nyoyo zao zilijawa zaidi na elimu na dini, kwani haukuwa muda mrefu tangu Mtume kufariki dunia, na mafundisho yake na hadithi zake zilikuwa bado nyoyoni mawao. Na dini ya Uislamu haikukataza kabisa mtu kuwa na mali au kujistarehesha duniani kwa njia za halali.

Na kwa upande mwingine, Waislamu wakaona wazi wazi na kujua

Page 80: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

73

kwamba dini ya Uislamu, ndiyo iliyowaneemesha kwa neema kubwa, na kuzidhoofisha tawala kubwa kubwa za makafiri (kama tawala za Kaisari na Kisra) na hatimaye kuzitia mikononi mwao hazina za Mashariki na Magharibi.

Kwa ufupi, haya yote yalikuwa ni sehemu tu ya heri waliyoipata Waislamu na Waarabu wa siku hizo mambo ambayo hawakutazamia. Je, hayo ndiyo yaliyowatia shauku ya kupanda dini na kujifunza hukumu (sheria) zake. Naam, ni dhahiri kwamba walitaka kwa hamu kubwa kujua mafundisho hasa ya Kiislamu, wajibu wa wanadamu na mambo ya kijamii, kwa mfano vipi kuishi kwa wema pamoja na wazee, watoto na watu wengineo, vipi kukuza ukoo wa kihalali, na mengineyo.

Je, walijifunza hayo kutoka kwa wale ambao walijitangaza kuwa wao ni Amirul-Mu’minin (Mabwana wa Walioamini) na Khalifatul Muslimin (Khalifa wa Waislamu)? Hasha!! Bali baada ya kuhakikisha wakakuta kwa ukamilifu mfano ulio bora wa kufuatwa kutoka kwa Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Hapo ndipo Waislamu walipokubali kuwafuata na kuwafanya Maimamu na makhalifa wa haki baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na watumishi wa sheria za Mtume na wafikishaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu.

Hii ni sababu moja katika sababu za kuenea madhehebu ya Ushia na kuitwa Mashia wafuasi wa Maimamu hawa. Inafaa hapa tuangalie maisha ya kikundi cha Mashia hao waliojitolea ambao walikuwa na itikadi na imani madhubuti ya dini yao nyoyoni mwao, mfano wa moto mkali uwakao nyoyoni mwao, hata wakawa tayari kujitia hatarini na kutoa roho zao ili kuhifadhi haki na dini.

MASHIA WA AWALI WALIVYOJITOA MUHANGA

Mashia kama vile Mabwana Hujr ibn Adiyyi Al-Kindi, Amr ibn al-Hamaq Al-khuzai, Rashid Ahijri, Maitham Tammar, Abdallah ibn Afif Al-Azdi na maelfu kama hawa walitoa roho zao kwa ajili ya dini na wakawafedhehi waliopinga dini kwa kusimama mbele yao kwa

Page 81: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

74

ushujaa mpaka wakawa mashahidi. Je, mashujaa hawa waliihami dini na wakajitoa mhanga kwa ajili ya kitu gani? Kupata mali? Kutaka daraja kutoka kwa Ahlul-Bait? Au walikuwa wakiwaogopa Maimamu wao? Hali ya kuwa wakati huo Ahlul-Bait wenyewe walikuwa na hofu na hawakuwa na mahali pa kwenda!! Hapana sababu nyingine bali walizitoa roho zao kwa ajili ya umadhubuti wa imani yao, na ukweli wa dini yao.

Tuangalie tena maisha ya watungaji wakubwa wa mashairi walioishi katika karne ya kwanza na ya pili. Kwa kweli, malenga hawa walihitajia sana msaada wa mali kwa watawala ambao walikuwa wakiwaogopa; kwani walikuwa wakichunguzwa sana. Lakini juu ya haya yote, hofu, mali na panga zilizofutwa vichwani mwao hazijawazuia kudhihirisha ukweli, kupigana na batili na kuifedhehi.

Kwa mfano, watazame mabwana hawa, tangu Farazdaq, Kumait, Sayyid al-Himyari, Debil, Dikul-Jinni, Abi Tamaam, Buhturi mpaka Al-Amir Abu Firaas Al-Hamdani ambaye shairi lake lasema: “Dini imefishwa na haki imemezwa, na sehemu ya Ahlul-Bait (a.s.) imenyakuliwa na kugawanywa kwa wengine.”51 Malenga wa zama hizo walitunga mashairi yaliyowasifu Maimamu wa haki na kuonesha mapenzi yao, na kuwalaumu na kuwachukia wafalme wa zama zao kwa ujeuri na udhalimu wao.

Mmoja katika mashaha wa malenga, Debil anatuambia hivi, katika shairi lake:

“Kwa muda wa miaka arobaini ninabeba mti wa kunyongea, lakini bado sijampata mtu wa kunitia kitanzi.”

Katika mashairi yake mengi, Debil aliwadhalilisha na kuwafedhehi kwa maneno makali wafalme wa zama zake, kina Harun Rashid na wanawe Amin na Ma’mun, na mfalme Mu’taasim, kwa sababu ya vitendo vyao viovu. Vile vile, katika mashairi yake aliwasifu Maimamu Ja’far Sadiq, Musa Kadhim na Ali Ridha (a.s.). Mashairi hayo ni maarufu na yameandikwa katika vitabu vya mashairi na historia.51 Shairi hili limechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho Ashafiyah cha Bwana Abu Firaas.

Page 82: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

75

Tusisahau kwamba haya yote waliyatenda bila ya kuogopa matokeo mabaya kutoka kwa wafalme wa Bani Umayyah na Bani Abbasi. Kwa ushujaa na ujasiri wao na kwa kuhatarisha nafsi zao walidhihirisha haki katika mashairi yao. Ikiwa tutaeleza habari za malenga wengine kama hawa basi maelezo yatakuwa marefu kinyume cha makusudio yetu ambayo ni kueleza vipi mbegu ya Ushia ilianza kupandwa katika bustani ya Uislamu, na nani mpandaji wake; na vpi iliota, ikakua, ikatoa maua na matunda.

Nimeeleza haya yote si kwa kupendelea, au kuvutia upande wa madhehebu yangu au kuwa na chuki, bali kwa kufuatana na uhakika, ukweli, ushahidi wa historia na utafiti wa kiakili. Namshukuru Mola wangu Mwenyezi Mungu kwa kunipa mafanikio ya kueleza haki kama inavyotakikana kuelezwa. Hivyo, anayependa na akubali na asiyependa basi na akatae.

Yafaa ieleweke kwamba, hapa isifikiriwe kwamba makusuido yetu tuliyoeleza ni kuyakanusha mema waliyoyatenda makhalifa wa kwanza waliotumikia dini ya Uislamu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa sisi hatuko pamoja na watu wanaopendelea upande mmoja, wanaotukana na walio na chuki. Sisi Mashia ni katika wale watu wanaoshukuru kwa mema na wanaochukia maovu. Tunasema kwamba hao ni umma uliokwisha pita na ndio wenye majukumu ya mema na maovu waliyoyatenda, na Mwenyezi Mungu Ndiye atakayewahukumu - ikiwa atawasamehe basi itakuwa ni kwa Fadhila Yake na ikiwa atawaadhibu basi itakuwa ni kwa uadilifu Wake. Naona ni lazima kukufahamisheni jambo hili kwamba sisi tusingeandika kitabu hiki kama isingelikuwa kule kututuhumu vibaya kwa baadhi ya waandishi wa zama hizi katika vitabu vyao, jambo ambalo lilituvunja nyoyo zetu na kutulazimu kuwajibu.

Kwa vyovyote vile, lengo letu hasa ni kufahamisha kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ndiye aliyeweka msingi hasa wa Ushia. Na hivyo ndivyo tulivyodhihirisha katika maelezo yetu kwamba hakuna aliyefanya kazi hiyo isipokuwa yeye.

Ukweli umebainika pia kwamba, usimamizi hasa wa kukua na

Page 83: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

76

kuenea kwa madhehebu ya Ushia unatokana na mfululizo wa sababu na matokeo ya namna mbali mbali yaliyofungamana na sababu nyingine ambazo kwa njia isiyoepukika ikaleta matunda hayo.

Twataraji kuwa kwa utangulizi huu imetosha kueleza yanayotakiwa, na sasa tunaingia Sura ya Pili juu ya imani na itikadi za Kishia.

Page 84: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

77

SEHEMU YA PILI

MISINGI YA DINI YA KIISLAMU

Kusudio la sura ya pili ni kueleza itikadi za Kishia juu ya misingi (Usul) na matawi (Furuu’) zake. Kwa ufupi, hapa tunaeleza zile kanuni na sheria muhimu zinazohusu misingi na matawi ya itikadi ya Kishia. Mfahamu na kuhakikisha kwamba hizi ni itikadi za madhehebu ya Kishia (Uislamu wa Asili) ambazo haziitakidiwi na mtu mmoja au watu wachache tu, bali ndizo itikadi za Mashia wote duniani. Ushia umesimama juu ya misingi mitano ya imani, nayo ni:

1. Kumjua Muumba (Mwenyezi Mungu).2. Kuwajua Mitume wa Mwenyezi Mungu na washika makamo

wao.3. Kujua maamrisho na kanuni za dini na kuzifuata kwa vitendo.4. Kutenda mema na kuacha maovu; na5. Kuamini siku ya Qiyama.

Kwa ujumla dini ni maarifa (Elimu), na vitendo (Amali). Mwenyezi Mungu anasema: “Bila shaka dini hasa mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.” (Qur’an, 3:19)

Kwa hiyo, “Uislamu” na “Imani” zina maana moja inayotegemea misingi mitatu:

1. Tawhid (Upweke wa Mwenyezi Mungu). 2. Nubuwwah (Utume).3. Ma’aad (siku ya Qiyama, Hesabu na Malipo).

Mtu yeyote mwenye kukanusha mojawapo katika misingi mitatu hii, huwa si Mwislamu wala si mwenye imani, na mwenye kukubali na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu, na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) Bwana wa Mitume ni Mjumbe wake, na Qiyama ni siku ya hesabu na malipo, basi huyo ndiye Mwislamu halisi na wa kweli. Kwa hivyo, kila Mwislamu humpasa kuhifadhi na kulinda damu, mali na watoto wa Mwislamu mwenzake.

Kwa upande wa pili, Uislamu na Imani zina maana makhususi katika

Page 85: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

78

kufuata msingi wa nne ambao ni - kutenda maamrisho matano haya:1. Sala2. Saumu3. Zaka4. Hija na5. Jihadi.

Kufuatana na msingi huu, wanavyuoni wanasema, “Imani ni kuitakidi moyoni, kutamka, kukaririri kwa ulimi, na kutenda maamrisho hayo.”52 Kama ilivyo kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: “Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na siku ya Qiyama.....”

Kila mahali ndani ya Qur’an palipotaja juu ya kumuamini Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Siku ya mwisho tu, basi hapo hukusudiwa Uislamu na Imani kwa ile maana ya kwanza; na kila inapoongezwa utajo wa kutenda mema basi hapo hukusudiwa ile maana ya pili. Mwenyezi Mungu anasema: “Mabedui walimwambia Mtume, ‘Tumeamini.’ Waambie, ‘Hamjaamini, lakini semeni, “Tumesilimu,” maana imani haijaingia nyoyoni mwenu bado.’” (Qur’an, 49:14)

Mwenyezi Mungu Mtukufu anazidi kubainisha maneno yake akisema: “Hakika waaminio ni wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kisha wakawa si wenye shaka na wakapigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kweli.” (Qur’an, 49:15)

Kwa hivyo, imani iko juu ya msingi wa kukiri, yaqini (kutokuwa na shaka) na vitendo (vyema); na misingi minne hii ya imani ndiyo shina la Uislamu kwa mujibu wa ile maana maalum kama invyokubalika kwa Waislamu wote.

TOFAUTI BAINA YA MASHIA NA WAISLAMU WENGINE

Ushia wa Imamiyyah, au Shia Ithna-Ashariyyah umeongeza msingi 52 Nahjul-Balaghah juz. 3 uk. 203/227; Sunan Ibn Majah juz. 1 uk. 25/651.

Page 86: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

79

wa tano wa imani ambao ni itikadi inayohusu ‘Uimamu’ ambacho ni cheo kinachotokana kwa Mwenyezi Mungu kama kilivyo cheo cha Mtume Mtukufu. Hii ina maana kwamba, kama ambavyo Mwenyezi Mungu anavyochagua katika viumbe vyake amtakaye kumpa Unabii na Utume na kuthibitisha Unabii na Utume kwa kumpa uwezo wa kufanya miujiza, vivyo hivyo, huchagua katika viumbe vyake amtakaye kumpa Uimamu, na humwamrisha Mtume Wake amtambulishe kwa Umma wake kuwa huyo ndiye atakayekuwa Imam baada yake.

Imamu hudhaminiwa kazi zote alizonazo Mtume ili kuendeleza kazi zake isipokuwa tu Imamu hashushiwi wahyi. Hukumu zote za Mwenyezi Mungu huzipata kwa Mtume na kwa msaada ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: “Na Mola wako huumba atakavyo na huchagua (walio wema); wao hawana hiari (ya kuchagua).” (Qur’an, 28:68)

Tofauti baina ya Utume na Uimamu ni kuwa Mtume huteremshewa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu; na Imamu huendelea kutumia sheria alizoachiliwa na Mtume akiwa anaongozwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, tunaona kwamba Mtume hueleza yale yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Imamu hueleza yale yanayotoka kwa Mtume.

Na Uimam umeendelea kwa Maimamu kumi na wawili baada ya Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.), na kila Imam aliyetangulia alimbainisha Imam atakayefuata baada yake.

MAASUMU

Mashia wanaamini kwamba Imamu Mtukufu, kama ilivyo kwa Mtume Mtukufu lazima awe ‘Maa’sum’, yaani hana dhambi wala kosa, hafanyi dhambi wala hakosei. Kama Imamu asingekuwa maasumu, watu wasingemwamini wala wasingemsadiki kwa kuwa vitendo vya maasumu ni mfano ambao watu hufuata. Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika Mimi nitakufanya Imamu (Kiongozi) wa watu. Akasema (Nabii Ibrahim), ‘Je, na katika wazawa wangu pia?’ Mwenyezi Mungu akasema, ‘Ahadi yangu haitawafikia watendao makosa (madhalimu).”

Page 87: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

80

(Qur’an, 2:124) Maneno haya ya Mwenyezi Mungu yanathibitisha kwamba Imamu lazima asifanye kosa wala dhambi yoyote. Haitoshi Imamu kuwa na sifa hii tu, bali lazima pia awe bora kwa kila sifa kuliko watu wote wa zama zake. Kwa mfano, awe na elimu zaidi kuliko watu wote.

Maimamu wameletwa na Mwenyezi Mungu wakiwa na sifa zote hizi ili wazisafishe nyoyo za wanadamu na wawaongoze katika njia ya haki kwa elimu na vitendo vizuri, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Yeye Ndiye aliyemwinua Mtume katika watu wasiojua kusoma, atokanaye miongoni mwao, anawasomea aya Zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na Hekima.” (Qur’an, 62:2)

Ni dhahiri kwamba asiyekamilika hataweza kuwakamilisha wengine, na asiyekuwa na kitu vipi ataweza kuwapa wengine? Kwa hivyo, Imamu kakamilika kwa kila jambo, na katika daraja ni chini ya Mtume lakini ni juu ya watu wote.

TOFAUTI KATI YA MU’MIN NA MWISLAMU

Mwenye kuitakidi Uimamu kama tulivyoeleza juu, basi mtu huyo huhisabiwa na Mashia kuwa ni Muumini kwa ile maana makhsus. Na mwenye kujitosheleza kwa kuitakidi misingi minne tu, basi mtu huyo ni Mwislamu na pia ni Mu’min kwa maana ile ya jumla. Mwislamu huyo atakuwa na haki kamili katika sheria ya Kiislamu, mathalan, atakuwa na haki ya kuhifadhiwa nafsi yake, watoto wake na mali yake na mengineyo.

Hatusemi abadan kwamba asiyeitakidi Uimamu si Mwislamu. (Nasi tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na tuhuma hiyo). Hakika faida ya kuitakidi Uimamu itadhihirika Siku ya Qiyama kwa kupata daraja la kumkaribia Mwenyezi Mungu. Ama kwa hapa duniani, Waislamu wote ni wamoja, na kila mmoja ni sawa mbele ya mwenzake. Hapana shaka, huko akhera Waislamu watatofautiana kwa daraja na vyeo mbele ya Mola wao kwa kufuatana na dhamiri zao na vitendo vyao; na Mwenyezi Mungu tu Ndiye Mwenye kujua mambo haya, wala hakuna njia kwa mtu yeyote kuyatolea maamuzi ya mkato.

Page 88: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

81

IMAMIYYAH

Tofauti iliyo dhahiri baina ya madhehebu ya Kishia na madhehebu mengine ya Kiislamu ni kule kuitakidi kwa Mashia juu ya Uimamu wa Maimamu kumi na wawili. Na ndiyo maana Mashia wanaitwa kwa jina la “Imamiyyah” - yaani waaminio Maimamu kumi na wawili.53 Ni muhimu ifahamike kwamba siyo kila aitwaye Shia basi anaamini Maimamu kumi na wawili hapana, (tunalibainisha hili) kwa sababu jina Shia pia linatumika kwa madhehebu ya Zaidiyyah,54 Ismailiyah,55 Waqafiyyah,56 Fat-hiyyah57 na wengineo.

Kwa kifupi tumetaja vikundi vilivyomo ndani ya jumuiya ya Kiislamu, pia vipo vikundi vingine ambavyo vimetoka nje ya mipaka ya dini ya Kiislamu, kama Khitabiyyah na wengineo. Kulikuwepo zaidi ya makundi mia moja katika madhehebu ya Kishia ambayo mengi katika hayo yameshaangamia, na yamebaki majina na kumbukumbu zao tu.

MAIMAMU KUMI NA WAWILI

Katika zama hizi, neno Shia linatumika makhususi kwa madhehebu ya Imamiyyah ambayo ni kikundi kikubwa katika Waislamu baada 53 Katika Afrika ya Mashariki wanajulikana zaidi kwa jina la Shia Ithna-Ashari.54 Madhehebu haya yalijitokeza zama za utawala mbaya wa dola ya Banu Umayyah. Kipindi hicho kilikuwa kigumu mno kwa Mashia kutokana na mateso waliyokuwa wakiyapata toka kwa watawala hao. Kutokana na hali hiyo Zaid ibn Ali ibn Husain alitoka dhidi ya watawala hao kuwapinga, lakini aliuawa. Baada ya kifo chake wako baadhi ya watu waliodai kwamba yeye ndiye aliyestahiki Uimamu baada ya Baba yake, na baada yake ni mwanawe aliyekuwa akiitwa Yahya. Madai yote haya hayakufanywa na Zaid. Taz: Al-Milal wan-Nihal juz: 1 uk: 154; Tarikh Madhahab Al-Islamiyyah uk: 44. 55 Tofauti kati ya kikundi hiki na Shia Imamiyyah ni kwamba, Ismailiyyah wanadai kuwa Uimam baada ya Imam Ja’far unakwenda kwa mwanawe Ismail, na Shia Imamiyyah wanaamini kuwa Imam baada ya Imam Ja’far ni mwanawe Musa ibn Ja’far na siyo Ismail kwani huyu alifariki katika zama za uhai wa baba yake. Taz: Firaqus-shia uk: 54, 81; Al-Milal wan-Nihal juz: 1 uk: 167.56 Jina hili linatumika kwa baadhi ya vikundi potofu ambavyo vinadai kuwa hakuna wajibu wa kuendelea kwa Uimamu kama ilvyobainishwa. 57 Kikundi hiki kinadai kwamba, Uimam baada ya Imam Ja’far unakwenda kwa mwanawe Abdillah. Taz: Firaqus-shia uk: 78; Tanqihul-maqaal juz: 1 uk: 198.

Page 89: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

82

ya Masunni. Neno la ‘Ithna-ashari’ maana yake ni kumi na mbili. Neno hilo si jipya wala geni katika historia ya Kiislamu, bali ni neno maarufu na limetajwa katika vitabu vya Sihah na wanavyuoni mashuhuri wa Kisunni. Bukhari katika Sahih Bukhari amenukuu hadithi nyingi juu ya Makhalifa kumi na wawili. Hapa tunanukuu baadhi ya hadithi hizo maarufu:1. Jabir ibn Samrah amesema: “Siku moja nilipokwenda kwa Mtume

Mtukufu pamoja na baba yangu, Mtume Mtukufu alisema, ‘Usimamizi (wa dunia) hautamalizika hadi makhalifa thenashara watawale.’ Baadaye Mtume Mtukufu akasema neno ambalo mimi sijalisikia. Nikamwuliza baba yangu alilosema Mtume Mtukufu. Akasema, “Mtume Mtukufu amesema kwamba wote hao watakuwa Maqureshi.”

2. Hadithi nyingine: “Mambo ya Watu yataendelea vema kwa muda ambao wamiliki kumi na wawili watatawalia mambo yao.”

3. Mtume Mtukufu amesema: “Kwa muda ambao Makhalifa kumi na wawili watakuwepo, watawaongoza watu duniani, na Uislamu utaheshimiwa na kuwa na nguvu.”

HAO KUMI NA WAWILI NI KINA NANI?

Kuna hadithi nyingi za Kisunni zinazoeleza, mojawapo inamdondoa Mtume Mtukufu akisema: “Baada yangu Ukhalifa utaendelea kwa muda wa miaka thelathini, baadaye utafuatia utawala wa kimabavu.”58

Natuyaache haya, kwani hakuna hoja ya kuleta zaidi ya kuthibitisha juu ya uhakika wa Maimamu au Makhalifa Kumi na wawili kwa kuwa kuna vitabu vingi, tena kwa maelfu, vinavyoeleza na kuthibitisha juu ya jambo hilo.59 Sasa tunakusudia hasa kueleza kwa ufupi itikadi za Kishia, na mambo muhimu yanayohusiana na Sheria za Kishia 58 Fat-hul-Bari juz: 8. Uk: 77; Al-jamiu’ liahkamil-Qur’an cha Qurtubi juz: 12 uk: 297; Al-Bidayatu wa An-Nihayah juz: 3 uk: 319.59 Kumekuwepo majaribio ya kuzitafsiri hadithi za Makhalifa Kumi na wawili kuonesha kwamba waliokusudiwa ni wasiyokuwa Maimamu kumi na wawili wa Ahlul-Bait. Lakini tafsiri hizo potofu hazina msingi wowote kwa kuwa Makhalifa wa Banu Umayyah walikuwa 14, na Banu Abbasi 36. (Mtarjumi)

Page 90: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

83

ambayo yanakubaliwa na kufuatwa nao. Kwa maelezo zaidi unaweza kupata katika vitabu vinavyohusika.

MAMBO MUHIMU JUU YA ITIKADI NA AMALI ZA KISHIA

Sasa tunarejea tena kwa kusema: “Dini ni Elimu na Vitendo.” Tunaanza na mambo yanayohusu kutumia akili.

TAWHID (UPWEKE WA MWENYEZI MUNGU)

Mashia (Imamiyyah) wanaitakidi kwamba, kila mwenye akili lazima ajifunze na awe na hakika na maarifa ya kumfahamu Mwenyezi Mungu kwa kadiri ya uwezo wa akili yake. Jambo muhimu ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu asiye na mwenziwe wala mshirika katika Uungu Wake. Awe na hakika kwamba Mwenyezi Mungu hamtegemei yeyote katika kuumba, kuruzuku, kufisha na kuhuisha kwa kuwa Yeye Peke Ndiye Mwenye mamlaka juu ya amri zote.

Kwa hivyo, mtu akiitakidi kwamba kuna mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye huumba, huruzuku, hufisha na kuhuisha, mtu huyo huwa ni kafiri na mushrikina, na hutoka katika Umma wa Kiislamu.

Imamiyyah pia wanaamini kwamba hakuna mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye anastahiki kuabudiwa. Basi yeyote anayemshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada zake kwa kumwabudu mtu au kukiabudu kitu kingine hata kama ikiwa kuabudu huko ni chombo cha kumpendekeza na kumkurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mungu ni kafiri pia.

Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa. Mitume na Maimamu lazima watiiwe kwa sababu kuwatii wao kwa hakika ni sawa na kumtii Mwenyezi Mungu, kwani wao ni

Page 91: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

84

wafikishaji wa maamrisho Yake na hukumu za sheria Zake. Lakini haijuzu kuwaabudu hao kwa kufikiria kwamba kuwaabudu wao ni sawa na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Huu ni ujanja wa kishetani, na ni hila na hadaa za kiiblisi.

Naam, inaruhusiwa kutaka baraka zao kwa jaha ya vyeo na sifa zao njema kwa kutawasuli kwao kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya utukufu waliokuwa nao mbele ya Mwenyezi Mungu. Inajuzu pia kusali pahali walipozikwa Mitume na Maimamu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kuelekea Qibla. Sifikiri kwamba kuna mtu yeyote mwenye akili atachukulia kwamba kusali huko kuwa ni sawa na kuwasalia wao. Bali mtu husali hapo akiwa na nia ya kusali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kama anavyosema: “Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu zitukuzwe, na humo litajwe jina lake.” (Qur’an, 24:30)

Kwa ufupi, hii ni itikadi ya Imamiyyah juu ya msingi wa Tawhid kama inavyokubaliwa na wote. Inawezekana kwamba msingi wa Tawhid umetiliwa nguvu zaidi kuliko ulivyotajwa hapa, kwani msingi huu una madaraja na maelezo yake kama vile Tawhidi ya Dhati, Tawhidi ya Zifa, Tawhidi ya Vitendo na kadhalika, ambapo hakuna dharura ya kutaja hapa kwa kirefu.

UTUME(HUU NI MZIZI WA PILI WA ITIKADI

YA IMAMIYYAH)

Shia Imamiyyah wanawaamini Mitume wote waliotajwa na kuelezwa katika Qur’ani Tukufu kuwa ni Mitume wa Mwenyezi Mungu na waja watukufu, wameletwa kuwaongoza viumbe kwenye njia ya haki.

Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ni mwisho wa Mitume, na Bwana wa Mitume, na yeye ni Maa’sum asiyefanya kosa wala dhambi, na yeye katika umri wake wote hakufanya kosa wala dhambi kabisa, na hakutenda lolote ila kwa amri ya Mwenyezi Mungu, mpaka aliporejea kwake (Mwenyezi Mungu).

Page 92: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

85

Shia (Imamiyyah) wanaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu, amemtukuza Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) kwa kumwita mbinguni usiku wa Mi’raj, kutoka Masjidul-haram (Makka) mpaka kufika Masjidul-Aqsa (Baytul-Muqadas) kisha, kwa kiwiliwili chake kitukufu akampandisha mbinguni juu zaidi ya ‘Arshi’ na Kursiyyi na akampitisha nyuma ya mapazia, kisha akakaribia na akateremka, akawa kama baina ya pinde mbili, au karibu zaidi.

ITIKADI YA SHIA IMAMIYYAH JUU YA QUR’AN TUKUFU

Shia (Imamiyyah) wanaitakidi kuwa kitabu kilichokuwa mikononi mwa Waislamu, ni kile kitabu alichoteremshiwa Mtume wetu, Muhammad (s.a.w.w.) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. (Qur’an) hii ni moja katika Miujiza ya Mtume, na kwa ajili ya kufundisha sharia na hukumu za Mola wetu, na kupambanua baina ya halali na haramu, na kitabu hiki hakikupunguzwa, hakikuongezwa wala hakikubadilishwa. Yote haya yamekubaliwa na Imamiyyah wote. Na ikiwa mtu yeyote katika Madhehebu za Kiislamu ataitakidi kuwa Qur’an imepunguzwa, imeongezwa au imebadilishwa, basi yeye yumo katika makosa, na Qur’ani inamhadharisha juu ya haya na kumrudi, kama inavyoeleza: Hakika sisi ndio tumeteremsha mauidha haya (yaani Qur’an) na hakika sisi ndio tutakaoyalinda. (Qur’an, 15:9).

Pia ikiwa katika baadhi ya hadithi zilizopokewa na Imamiyyah na zilizopokewa na Sunni kuonesha mabadiliko au upungufu wa Qur’an, kwanza hazina nguvu (dhaifu) na ni chache kabisa na hadithi hizo ni miongoni mwa zile hadithi ziitazwo ‘Akh-Baar Aahad’ hazifidishi maarifa wala amali yoyote kwa kuzijua au kuzifuata, na hadithi hizo hazina itibari yoyote na zipigwe ukutani (zisikubaliwe).

Imamiyyah wanaitakidi kuwa, yeyote atakayeitakidi au kudai Utume baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) au akadai kuteremshiwa wahyi, au kitabu, basi huyo ni kafiri na ni lazima auawe (kwani hapana Mtume baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.)). Yeye ni Mtume wa mwisho.

Page 93: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

86

UIMAMU(HUU NI MZIZI WA TATU WA ITIKADI

YA IMAMIYYAH)

Kama tulivyoeleza mbele kuwa mzizi huu ndio kitu muhimu chenye kupambanua na kutofautisha baina ya Imamiyyah na vikundi vingine vyote vya Kiislamu. Mzizi huu (wa Uimamu) ndio asili muhimu iliyoleta kufarikiana huku; lakini katika sharia ya matawi (Furuu’) tumetofautiana na makundi mengine ya Kiislamu kama wanavyotofautiana wenyewe kwa wenyewe, kwa mfano kama wanavyotofautiana wanavyuoni wao wa ijtihad Shafi, Hanafi na wengineo.

Umekwisha fahamu kuwa, maelezo ya Uimamu kwa (Imamiyyah), ni cheo kinachotokana kwa Mwenyezi Mungu, kama Utume, na Yeye Mwenyezi Mungu kwa elimu Yake ya tangu ndiye anayemchagua Imamu, kama anavyomchagua Mtume, na humuamrisha Mtume wake amtambulishe Imam kwa umma wote na wafuate amri zake, kama wanavyofuata amri za Mtume.

TANGAZO LA KUMTANGAZA ALI (A.S.) KUWA NI IMAM

Imamiyyah wanaitakidi kuwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwamrisha Mtume Muhammad (s.a.w.w.) atangaze, kwa kumweka Imam Ali (a.s.) awe wasii wake na kiongozi wa umma wote baada yake. Kwa upande mwingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua kuwa jambo hilo litakuwa zito kwa baadhi ya watu na watamtuhuhumu kuwa anafanya upendeleo kumchagua mwana wa ammi yake na mkwewe. Ni jambo linaloeleweka kwamba watu siku hizo na mpaka leo hawako namna moja katika imani na yaqini juu ya utakatifu wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kuhifadhika kwake kutokana na kuwa na matamanio binafsi. Hata hivyo hali hiyo haimkuzuwia Mwenyezi Mungu Kumwamrisha Mtume wake kuufikisha ujumbe huo wazi wazi kwa mujibu wa aya ifuatayo akamwamrisha amtangaze Ali kuwa ni Khalifa na mshika makamo wake baada yake pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya

Page 94: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

87

hivyo basi hukufikisha ujumbe Wake, na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu. (Qur’an, 5:67)

Baada ya kuhadharishwa kwa ukali namna hii ilimbidi sasa kufikisha amri hiyo ya Mola wake. Kwa hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwahutubia watu njiani mahali paitwapo ‘Ghadir-khum’ alipokuwa anarejea kutoka kuhiji hija yake ya mwisho. Alitangaza kwa sauti kubwa ya kusikia wote, na hali wakubwa wa makabila yote walikuwa wakisikia akisema hivi: “Je, Mimi siye bora zaidi juu ya walioamini kuliko nafsi zao?” Wakamjibu, “Naam, wewe ni bora kuliko nafsi zetu.” Mtume akasema tena: “Anayenikubali mimi kuwa ni kiongozi wake basi Ali vile vile ni kiongozi wake.....” Akaendelea kueleza zaidi mpaka mwisho wa maneno yake.60

Baadaye kwa ajili ya kutilia nguvu jambo hilo mahala na wakati mbalimbali akaeleza pengi dhahiri wazi wazi na pengine kwa ishara kuthibitisha cheo cha Imam Ali (a.s.) mpaka akatekeleza amri aliyopewa na Mola wake.

IMAM ALI (A.S.) ALIPINGWA BAADA TU YA KUFARIKI MTUME (S.A.W.W.)

Lakini kikundi cha wazee wa Ki-Islamu baada ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.), maagizo yote ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) waliyabadilisha kwa mujibu wa fikra zao, kwa sababu ya maslahi waliyoyaona wao kwa kufuata ijtihadi zao wakaona eti hali hiyo italeta maslaha juu ya Waislamu. Kwa hiyo waliyemtaka wao wakamtanguliza, na aliyestahiki wakamweka nyuma, na baada ya kufanya haya walisema hivi: “Mambo huzuka baada ya mambo.”

Mwanzo Imam Ali (a.s.) na kikundi cha masahaba wakubwa wa Mtume walijizuia kumbai Khalifa aliyechaguliwa na watu hao. Imam Ali (a.s.) baadaye baada ya muda walipoona kujuzia na Bai’a na

60 Rejea nyigi za hadithi na nyinginezo zimelisimulia tukio la Ghdir na tamko la Bwana Mtume (s.a.w.w.) kwa Sanad nyingi ambazo ni vigumu kuzidhibiti lakini rejea Sunan ibn Majah juz: 1 uk: 43/116 na 45/121; Sunan Tirmidhi juz: 5 uk: 633/3763 n.k.

Page 95: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

88

kukaa kwa utulivu kutaleta madhara makubwa juu ya dini ya Kiislamu pengine kuleta kupinga mafundisho yake na hali wakati huo, Uislamu ulikuwa mchanga unaanza kukua na kuenea, kwa hivyo waliinyamzia hali hiyo.61 na haikuwa ni jambo la kustaajabisha kwa sababu kwa upande mwingine Uislamu katika nadhari ya Amirul Muuminin ni kitu kitukufu na ni bora mno, na alikuwa na hamu nao na alitoa juhudi kubwa, hata alikuwa tayari kutoa roho yake na vyote alivyokuwa navyo mikononi mwake. Historia ya Uislamu haitasahau kujitolea kwake na mara nyingi aliwahi kujitosa nafsi yake katika midomo ya mauti, na alikuwa wakati wote tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya dini ya Kiislamu.

Kwa upande mwingine aliona kuwa aliyetawalishwa na watu kuwa mwongozi na Khalifa wa Waislamu, akitilia nguvu na kusaidia Uislamu, na kuueneza na kusimamisha bendera ya Uislamu Ulimwenguni. Na yote haya ndio ilikuwa lengo lake. Pamoja na hali hiyo, Imam Ali (a.s.) alibakia na cheo chake alichopewa na Mwenyezi Mungu kuwa ni Imam, ijapokuwa yeye kwa ajili ya maslaha alinyamaza na aliwaachia wengine wawe waongozi wa Waislamu.

Amma alipotawala Muawiyah ibn Abi Sufian, Imam Ali (a.s.) hakunyamaza kwa sababu aliona kumfuata na kupatana naye na kumuacha awe mtawala juu ya Waislamu kutaleta hasara kubwa na mgawanyiko mkubwa juu ya Waislamu hata usiweze kuunganika baadae, hapo Imam Ali (a.s.) akaona hana budi kumpinga na kumpiga vita.

Kwa ufupi, Imamiyyah wanasema hivi: “Sisi Shia na wafuasi wa Imam Ali (a.s.), tunafuata amri zake, tunapatana na kuridhika na kila anayepatana na kuridhika na Imam Ali (a.s.). Tunampiga vita na kufanya uadui na kila mwenye kumpiga vita na kumfanyia uadui Imam Ali (a.s.). Tunampenda mwenye kumpenda na tunamchukia mwenye kumchukia.” Imani hii na itikadi hiyo yatokana na kufuata 61 Imam Ali (a.s.) Aliinyamazia tu hali hiyo kwa maslahi ya Uislamu, lakini siyo kwamba aliridhika nayo kutokana ushahidi wa maneno yake mbali mbali aliyokuwa akiyasema kuonesha kutoridhika kwake Taz: Khutba Shaqshaqiyyah ndani ya Nahjul-Balaghah.

Page 96: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

89

na kuitikia maombi ya Mtume, Muhammad (s.a.w.w.), kama alivyosema: “Ewe Mola, mpende na umsaidie, anayempenda na mfanye adui yako anayemfanyia uadui.” Mapenzi yetu na kumtii kwetu Imam Ali (a.s.), na wanawe, ni mapenzi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kutii amri yake.

Mtungaji mashairi anasema: “Namuapa Mwenyezi Mungu, siyo kwamba watu hawakufahamu cheo chake (Imam Ali (a.s.)); lakini wao wameficha dhati ya mambo waliyokuwa wakiyafahamu kuhusu sifa zake.”

Tumetoka nje ya makusudio yetu, sasa na turejee, kwa kuendelea kukamilisha maelezo (kuhusu itikadi yetu) ya Imamiyyah na tunasema kuwa, “Sisi tunasema na tunaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hakuuacha kamwe ulimwengu kuwa tupu bila kuweka viongozi juu ya viumbe vyake, kwa kila mara kuwapelekea Mtume au Mawasii wa Mtume, waliodhahiri (wanaoonekana) na wasiodhahiri.”

Kwa hivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w.) wazi wazi alimteua Imam Ali (a.s.) kuwa mwongozi baada yake, na Imam Ali (a.s.) alimuusia mwanawe mkubwa, Imam Hasan (a.s.) na yeye alimusia nduguye Imam Husayn (a.s.) na hivyo hivyo wasiya uliendelea mpaka Imam wa kumi na mbili, Imam Muhammad Mahdi (a.s.) anayengojewa.

Jambo hili si jambo jipya, hii ni sharia iliyotokana na Mwenyezi Mungu kuwafanya Mitume wote, tokea Mtume Adam (a.s.) mpaka Mtume wetu wa mwisho, Muhammad (s.a.w.w.) wausiane pamoja na mawasii wao.

KUMBUKUMBU ZA VITABU JUU YA UIMAMU

Idadi kubwa ya wanavyuoni wa dini wametunga vitabu vingi, kuthibitisha huo wasia. Mimi hapa nakuletea majina ya baadhi ya hao watungaji wa mwanzo wa karne ya kwanza ya Al-Hijra, mpaka mwanzo wa karne ya nne:

1. Kitabul-Wasiyyah cha Bwana Hishaam ibn Hakam

Page 97: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

90

2. Al-Wasiyyah cha Bw. Husain ibn Saeed.3. Al-Wasiyyah cha Bw. Hakam ibn Miskeen.4. Al-Wasiyyah cha Bw. Ali ibn Mughirah.5. Al-Wasiyyah cha Bw. Ali ibn Husain ibn Fadhil.6. Kitabul-Wasiyyah cha Bw. Ibrahim ibn Muhammad ibn

Saeed ibn Hilal.7. Kitabul-Wasiyya cha Bw. Muhammad ibn Ali ibn Fadhil.8. Al-Wasiyyah cha Bw. Ahmad ibn Muhammad ibn Khalid

Al-Barqi, ambaye vile vile ni mtungaji wa kitabu kiitwacho Al-Mahasin.

9. Al-Wasiyyah cha Bw. Abdul-Aziz ibn Yahya Al-Jaludi mwandishi maarufu wa Historia.

Hawa wote tuliowataja ni waandishi maarufu walioishi karne ya kwanza na ya pili. Ama wale walioishi katika karne ya tatu ni wengi, lakini tutawataja baadhi ya wao kama hawa wafuatao: -

1. Al-Wasiyyah cha Bw. Ali ibn Riab.2. Al-Wasiyyah cha Bw. Isa ibn Al-Mustafaad.3. Al-Wasiyyah cha Bw. Muhammad bin Ahmad Saabuni.4. Al-Wasiyyah cha Bw. Muhammad ibn Hasan ibn Farukh.5. Kitabul-Wasiyyah Wal-Imamah cha Mwandishi mkubwa wa

Historia Bw. Ali ibn Husain Al-Mas-Udi. Mtungaji wa kitabu kiitwacho Muruju-dh-Dhahabb.

6. Al-Wasiyyah cha As-shakhut-taifah Bw. Muhammad ibn Hasan Al-Tusi.

7. Al-Wasiyyah cha Bw. Muhammad ibn Ali Shalmaghani.8. Al-Wasiyyah cha Bw. Musa ibn Hasan ibn Amur.

Ama wale vilivyotunga baada ya karne ya nne, ni vingi sana hata ni vigumu kujua idadi yake

Bw. Al-Mas-u’di katika kitabu chake kilicho maarufu kiitwacho Ithbatul-Wasiyah ameeeleza hivi: “Kila Mtume alikuwa na Mawasii kumi na wawili baada yake, naye kawataja wote kwa majina yao na vile vile kueleza kwa ufupi maisha ya kila mmoja katika hao, au kueleza zaidi kidogo juu ya maisha ya Mawasii kumi na wawili baada ya Mtume wetu, Muhammad (s.a.w.w.)” na kitabu hiki kimechapishwa nchini Iraq na Iran.

Page 98: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

91

Watungaji wote hawa tuliokwisha wataja hapo, walitunga vitabu hivyo vyote, ili kuhakikisha, na kuwathibitisha Maimamu kumi na wawili kwa hadithi na hoja zinazoingia akilini, lakini tulivyoashiria ni kwamba, lengo letu halikuwa kuthibitisha jambo hilo kwa dalili za kiakili na hadithi, bali tunataka kueleza misingi ya itikadi ya Shia bila kuzitaja hoja na mathibitisho, ili ijulikane sisi twasema nini. Na nini thamani ya masinginzio yasiyohalali yasiyo na kiasi tunaosingiziwa.

AL-IMAM MAHDI (A.S.) NA UMRI WAKE MREFU

Naam jambo ambalo makundi ya Waislamu wengi, na wasiokuwa Waislamu pia wanakinzana na kukanusha kabisa itikadi ya Imamiyyah kuwa Imam wa kumi na mbili yuko kwenye ghaibu (kafichikana machoni pa watu) kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Makundi hayo yanaona kuwa itikadi hiyo haina msingi na ni batili, na makelele mengi wanapiga juu ya jambo hilo, lakini upinzani wao unarudi kwenye mambo mawili.

Jambo la Kwanza: Kuhusu udumifu wa umri wa Imam Al-Mahdi (a.s.) vipi inaweza kusadikika mtu kuishi zaidi ya miaka elfu?

Lakini hoja hiyo hasa kwa Mwislamu ni jambo la ajabu mno. Wao wamesahau au wamesahaulishwa hadithi ya umri wa Nabii Nuh (a.s.) aliishi duniani kwa uchache umri wa miaka elfu moja na mia sita, na wengine wanasema zaidi mpaka miaka elfu tatu62.

Aliishi na Umma wake tu, kwa miaka elfu moja kasoro khamsini, kama inavyothibitisha wazi wazi Qur’ani Tukfu. Wanavyuoni wanasema kuwa Nabii Nuh (a.s.) aliishi duniani kwa uchache umri wa miaka elfu moja na mia sita, na wengine wanasema zaidi mpaka miaka elfu tatu.

Kikundi cha wanavyuoni wa hadithi wa Kisunni wamesema hivi: “Licha ya maisha ya Nabii Nuh (a.s.) hata wengine wameishi zaidi kuliko umri huu.”

62 Taz: Tafsirul-Kash-shaf ya Az-Zamakhshari juz: 3 uk: 200; Tafsirul-Qur’an-il-Adhiim ya Ibn Kathir juz: 3 uk: 418; Zaadul-Masiir cha Ibn Al-Jauzi juz: 6 uk: 261.

Page 99: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

92

Miongoni mwao ni mwanachuoni, Bw. Nawawi ambaye ni mmoja katika wanachuoni wa Ki-Sunni maarufu, na mwandishi wa hadithi katika kitabu chake Tah-Dhiibul-Asmaa ameandika hivi: “Wanavyuoni wametafautiana juu ya uhai wa Nabii Khidhr (a.s.), na juu ya utume wake. Wengi wamesema kuwa yeye ni hai, na yupo miongoni mwetu. Kundi la Masufi, na watu wema, na mabingwa wa maarifa wanawafikiana na kukubali maneno hayo. Hadithi za Masufi zinazohusu kumuona na kukutana na kumuliza masuala ya dini, na yeye (Khidhr a.s.) kuwajibu, na kuonekana kwake mahala pa kheri na patukufu, ni nyingi zisizo na hesabu, na ni mash-huri hata hatuna haja ya kuzitaja.”

Sheikh Abu-Amr ibn Salah, mmoja katika wanavyuoni wakubwa wa Kisunni ameandika katika fatwa zake amesema hivi: “Nabii Kh-idhr (a.s.) yu hai, na makundi ya wanavyuoni na watu wema, hawa wote wanakubali maneno haya na wanayokanusha ni wachache sana, miongoni mwa wanavyuoni wa hadithi.”63

Ninakumbuka kwamba yeye na pia Bw. Zamakhshari katika kitabu chake kinachoitwa Rabiul Abraar ameandika hivi: “Hakika Waislamu wote wanawafikiana kuwa Mitume wanne wako hai, wawili wako mbinguni nao ni Mtume Idris (a.s.) na Mtume Isa (a.s.), na wawili wapo juu ya ardhi, nao ni Mtume Ilyas (a.s.), na Mtume Khidhr (a.s.). Na Mtume Khidhr (a.s.) alizaliwa katika zama za Mtume Ibrahim (a.s.) ambaye ni baba wa Mitume.”64

Wanaoishi dunia zaidi kuliko umri wa desturi, ni wengi umri wao hupindukia mamia. Sayyid Murtadha (a.r.), mwanachuoni mkubwa wa Imamiyah, katika kitabu chake Amaali65 amewataja kwa majina jumla ya hao, na wengine miongoni mwao ni Sheikh Saddoq (a.r.) katika kitabu chake Ikmaalud-din66 vile vile amewataja zaidi kuliko alivyotaja Sharif.

Wangapi tunawaona katika ulimwengu huu wenye kupindukia 63 Taz: Tahdhibul-Asmaa Wal-lughaat juz: 1 uk: 176.64 Taz: Tahdhibul-Asmaa Wal-lughaat juz: 1 uk: 177; Rabiul Abraar juz: 1 uk: 397.65 Aamaalil-Murtadha juz: I uk: 232-272.66 Ikmaalud-din uk: 555-575.

Page 100: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

93

umri zaidi ya miaka mia na ishirini wengine hukaribia umri huu na wengine huzidi?

Juu ya hayo tukitazama haki na ukweli, ikiwa yupo mwenye uwezo wa kuhifadhi uhai wa Binadamu kwa muda wa siku moja; basi anaweza kuhifadhi uhai wake kwa elfu ya miaka; basi ni ajabu gani kwetu kuona Mitume na Mawalii wa Mwenyezi Mungu kuishi miaka kwa maelfu, ambayo si umri wa kawaida. Basi kuna ajabu gani kwa Mitume na Mawalii kuishi sana kinyume cha kawaida?

Angalia katika magombo (volumes) ya Al-Muqtataf ya zamani, utaona ndani mna makala mengi, na ushahidi wazi wa kuingia akilini, kutokana na walimu wa (Philosophy) wakubwa wa Magharibi wamethibitisha kuwa inawezekana binadamu kuishi ulimwenguni kwa muda mrefu.

Baadhi ya wanavyuoni wa Ulaya wamesema hivi: “Lau usingekuliwa upanga wa Ibnu Muljam, Seyyidna Ali ibn Abi Talib (a.s.) angekuwa katika wenye kuishi muda mrefu ulimwenguni, kwani yeye amekusanya sifa zote za ukamilifu na uadilifu.”

Juu ya maelezo haya tunahakika kuwa Mitume na Mawalii wanaweza kuishi kwa muda mrefu, lakini hapa hatuna nafasi ya kueleza zaidi.

Jambo la Pili: Kuhusu Imam (a.s.) kuwa katika Ghaibu wanauliza hivi: Kuwepo kwa Imam ambaye haonekani kunaleta faida gani? Kuwepo na kutokuwepo kwake kunatofauti gani?

Hivi hao wanaouliza hivyo wanataka kujua hekima na elimu ya Mwenyezi Mungu, na kutaka kujua maslaha aliyoyaweka Mwenyezi Mungu; Je wanaelewa siri zote za Mwenyezi Mungu katika kuiumba dunia na yote yaliomo humo na kuleta sharia? Mpaka leo hivi, tunayo mambo ya Mwenyezi Mungu aliyoyaleta duniani, hayakufahamika siri yake, na inatulazimu kuamini tu, kama kuhusu Hajar-al-As-wad (Jiwe jeusi lililowekwa katika pembe moja ya Qaaba) ijapokuwa jiwe hilo halina madhara wala faida; Je tunajua kwa nini tunasali sala ya magharibi rakaa tatu, isha nne, na asubuhi mbili? Na yapo mambo

Page 101: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

94

mengi zaidi kama haya. Mwenyezi Mungu amejiwekea elimu za jumla ya vitu na mambo, na wala hakuwajulisha Mitume wala Malaika watukufu, kwa mfano kujua Qiyama lini na saa gani kitakuja.

Qur’an inasema: Kwa hakika elimu ya Qiyama iko kwa Mwenyezi Mungu, na ndiye yeye huteremsha mvua. (Qur’an, 31:34).

Kwa vyovyote jambo la kuwako na kujificha Imam (a.s.) si jambo jipya kwa sababu katika Uislamu kuna mambo mengi ya siri ambayo hekima ya kuificha haikujulikana kwa ukamilifu, kama “Ismul-a-ad-ham” (Jina Kubwa Tukufu), na “Lai-latul-qadr” (Usiku wa Mtukufu), na saa au wakati wa kukubaliwa dua (anayoomba kiumbe).

MANENO YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) LAZIMA YAKUBALIWE

Kwa ufupi si jambo la ajabu kwa Mwenyezi Mungu kufanya jambo au kutoa hukumu fulani ambayo sisi tutakuwa hatujui hekima yake. Lililopo hapa ni kuhusu kuwepo kwa jambo hilo na uhakika wake, pindi itakaposihi khabari inayohusu jambo hilo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Mawasii wake (a.s.), hapana shaka itatulazimu kukubali na kutenda na wala haitulazimu kuchunguza hekima yake na sababu yake.

Mara nyingi tumeashiria kwamba lengo letu katika kitabu kidogo hiki ni kueleza itikadi za Shia juu ya Misingi na Matawi ya dini tu, si kutoa dalili. Wale wanaotaka wapate maelezo kwa kirefu juu ya mambo hayo basi waangalie vitabu vinavyohusika.

Ama hadithi za Imam Al-Mahdi (a.s.), zipo hadithi nyingi sana kwa pande zote mbili, Sunni na Shia zinazoeleza mambo haya.

Ama kuhusu sababu na siri ya Imam Mahdi (a.s.) kukaa katika Ghaiba Waislamu wengi na hata katika Mashia wasiofahamu dini sawa sawa huuliza suala hilo, nasi huwa tunawajibu kiasi waelewe tu. Lakini inatubidi kusema kwamba, kuna dalili nyingi za kutosheleza moyo kufahamu kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu, (tokea Nabii

Page 102: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

95

Adam (a.s.) mpaka mwisho wa dunia), siyo kuuacha ulimwengu tupu bila ya kuwa na Hoja (kiongozi, Nabii au Imam) wa kuongoza na kulinda Uislamu; basi kuwepo kwao duniani na vitendo vyao ni Rehema ya Mwenyezi Mungu (juu yetu). Utapotaka kujua zaidi juu ya mambo haya unaweza kuona katika vitabu vingi, kwa hivyo kiasi hicho cha maelezo yetu kwa makusudio tuliyoyakusudia kinatosha Insha-allah.

UADILIFU

Uadilifu, ni kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta-ala) hamdhulumu yeyote, wala hafanyi jambo lililo kinyume cha akili; kwa hakika sifa hii si yenye kujitenga mbali naye, bali sifa hii ni katika sifa za Wajibul-wujuud.67

Kwa Shia jambo hili ni moja katika mambo yanayohusu Tauhid, lakini Al-Ashaai’rah (wafuasi wa Abul Hasan Al-Ash-a’ri,) ambao ni kundi moja katika makundi ya madhehebu ya Kisunni, kikundi hiki kilikwenda kinyume cha itikadi ya ‘Al-adiliyyah’ (Wanaoamini Uadilifu wa Mwenyezi Mungu) ambao ni Muu’tazilah na Imamiyyah. Wao Al-Ashaai’rah walikanusha mchanganuo wa mema na maovu (unaokubalika kuwepo kwake) kiakili na walisema, “Hapana jambo zuri, ila lile lililoonekana kuwa ni zuri katika sharia, na hapana jambo baya ila lile lililoonekana kuwa ni baya katika sharia.” Kwa hiyo (wao wanasema kuwa) hata kama Mwenyezi Mungu, lau angemweka milele motoni mwenye kutii amri Zake, na akamweka peponi mwenye kumuasi basi jambo hili lisingekuwa baya, kwani Mwenyezi Mungu anatumia ufalme wake. Wala haulizwi kwa chochote anachokitenda, bali viumbe ndio watakaoulizwa. (Qur’an, 21:23)

Hawa Al-Ashaai’rah wanaitakidi kuwa wajibu wa kumjua Muumba na wajibu wa kuuchunguza muujiza ili kumtambua Nabii, vyote vinapatikana kwa njia ya kusikia na (kuainishwa) na sharia na siyo kwa njia ya kutumia akili. Na kwa sababu hii basi wamejikuta kuwa wamejichanganya waziwazi (wakajikuta hawawezi kutumia akili zao).

67 Kuwepo kwa sifa hiyo kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la tangu.

Page 103: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

96

Amma Al-Adaliyyah (ambao ni Muu’tazilah na Imamiyyah) wanasema kuwa, “Hakika hakimu (muamuzi) katika nadharia hizi ni akili peke yake, wala hapana nafasi ya hukumu ya sharia ndani yake isipokuwa (itakuja) kutilia nguvu na kuongoza.”

Vivyo hivyo akili inajitegemea kuhusu ubora wa baadhi ya mambo na ubaya wa baadhi ya mambo na (inatoa hukumu kuonesha kuwa hiki ni kitendo kizuri au hiki ni kitendo kibaya). Kama tulivyosema kuwa akili ni hakimu, na kwa maana hiyo basi, haiwezekani akili ikahukumu kuwa kitendo kinachotendwa na Mwenyezi Mungu ni kibaya; kwani Yeye Mwenyezi Mungu ni mwenye hekima, na kwa Mwenyezi Mungu kutenda ubaya ni kinyume na hekima Yake, na kumuadhibu mwenye kumtii ni dhulma, na dhulma ni kitendo kibaya ambacho hakiwezi kutokana na Mwenyezi Mungu.

Kwa utaratibu huo, wa Adaliyyah (wanaoamini uadilifu wa Mwenyezi Mungu) wameithibitisha sifa ya Uadilifu kwa Mwenyezi Mungu, na wakaitengea maelezo maalum kinyume na sifa nyingine (za Mwenyezi Mungu) ili kuonesha tofauti na ikhtilafu baina ya Adaliyyah na Ashaai’rah;

Lakini kwa hakika Ashaai’rah, hawakanushi kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwadilifu, isipokuwa kwa itikadi yao, kila jambo atendalo Mwenyezi Mungu, ni Uadilifu. Lakini maana ya uadilifu kwao wao ni kwamba kila jambo alitendalo Mwenyezi Mungu ni uadilifu, na kila akitendacho Mwenyezi Mungu ni kizuri.68 Kwa maana hii basi wamepinga ile maana iliyothibitishwa na Muu’tazilah na Imamiyyah juu ya kuwepo utawala wa akili na kutambua kwake zuri na baya, kwa madai kwamba akili haina maamuzi kwani kila jema na ovu yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa wenye kuamini ‘Uadilifu’ juu ya msingi wa itikadi ya kufahamu mema na maovu kitu ambacho kinakubalika kiakili, wamethibitisha mambo mengi yanayohusu elimu ya Aqida, kama vile ‘Kanuni ya Lutf’, wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha, na 68 Pamoja na hali hiyo, inasikitisha mno wao kumnasibishia Mwenyezi Mungu kutenda jambo baya pale wanaposema kuwa, “Kheri na shari zote zinatoka kwa Mwenyezi Mungu.”

Page 104: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

97

uwajibu wa kuchunguza na kufikiri madai ya mwenye kudai Utume (siyo kukubali kiupofupofu).69

JABR WAL-IKHTIYAAR :KUTENZWA NGUVU NA KUWA NA HIYARI

Miongoni mwa mas’ala yanayohusika na ‘Uadilifu’, ni suala la “Jabr wal Ikh-tiyaar” ambalo ni muhimu kabisa na lenye utata kuliko mas’ala mengine tunayozungumzia.

Ashaa’irah wanatakidi ‘Jabr’ yaani kutenzwa nguvu na kutokuwa na uhuru wa kuamua. Lakini Adaliyyah wanaitakidi kuwepo kwa Hiyari ya matakwa, na binadamu yuko huru katika kazi zake kuchagua ni kazi ipi aifanye, pia Mwenyezi Mungu Ameumba ndani mwake tabia ya hiari. Mwenyezi Mungu hamlazimishi yeyote kutenda au kutokutenda, ni waja ambao huchagua katika hayo mawili.

Kwa Adaliyyah zuri na baya yategemea juu ya akili tu, ambayo ndiyo itakayohukumu, lakini Ashaai’rah wanapinga haya, kama tulivyoeleza mbele, wanasema kuwa si lazima kutumia akili juu ya lolote linalotokana na Mwenyezi Mungu. Maelezo haya ni vigumu kufahamu, anayetaka kujua zaidi bora aulize wanavyuoni wao.

Kwa hivyo wenye akili humsifu yeyote anayetenda mema na humlaumu anayetenda mabaya, kwani katenda baya kwa khiari yake. Anayetenda mema hupata thawabu, na anayetenda maovu hupa-ta madhambi (na kuadhibiwa), na kama si hivyo, basi ingekuwa haina haja ya thawabu na adhabu; na ingekuwa haina haja vile vile kwa Mwenyezi Mungu kuwapeleka Mitume wote hawa duniani ili

69 Maana ya kanuni ya Lutf ni kwamba, Mwenyezi Mungu, ameweka uwezekano wote na chombo cha lazima cha kumwelekeza binadamu kwenye muongozo na fanaka (kwa ufupi chochote kitakachomfanya atii amri ya Mwenyezi Mungu na kupata Ukaribu naye, na kitakachomfanya awe mbali na maasi, na kumpa uhuru wa kuamua). Mwenyezi Mungu Anataka viumbe waongoke, kwa hivyo inambidi kumtayarishia njia za kuongoka, na haya yako wazi, na ndiyo maana ilimlazimu kuwapeleka Mitume, na kuteua washika makamo yao, na mambo yote kama haya yanatokana katika kanuni ya ‘Lutf.’ (Mtarjumi).

Page 105: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

98

kuwaongoza viumbe watende mema na waache maovu (mabaya) na kuwapa viumbe ahadi njema, na vitisho vya adhabu kwa waovu.

Hatuna nafasi ya kueleza zaidi juu ya jambo hilo hapa, atakayekujua zaidi atazame mwishoni mwa Juzuu ya kwanza ya kitabu kiitwacho Addiin Wal-islaam kilichoandikwa nami,70 humo tumeyafafanua zaidi kwa njia ambayo ni nyepesi inayoweza kufahamika kwa watu wa kawaida seuze wanavyuoni. Lengo letu hapa ni kueleza kwamba miongoni mwa itikadi na misingi ya Shia Imamiyah ni kuwa, Mwenyezi Mungu ni muadilifu na kwamba mtu yuko huru na mwenye hiyari katika matendo yake.

AL-MA-AAD - SIKU YA QIYAMA

Huu ni mzizi watano, katika itikadi ya Imamiyyah. Wao wanaitakidi Ma-aad kama wanavyoitakidi Waislamu wote, kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Atawarejesha siku ya Qiyama viumbe na kuwapa uhai baada ya kufa kwao; kwa ajili ya kutoa hesabu, na kuwalipa kheri waliotenda mema duniani, na kuwaadhibu waliotenda maovu duniani.

Marejesho ya viumbe siku ya Qiyama itakuwa ni roho pamoja na viwiliwili vyao, namna hii hata yeyote atayemuona amjuaye atamtambua na atasema huyu ni fulani. Wala si lazima kujua kurejeshwa huko kutakuwa kwa aina gani. Je ni kurejeshwa kiwiliwili kilichokufa au kutengenezwa upya au namna nyingine.

Imamiyyah wanaamini yote yaliyoelezwa katika Qur’an, na Sunnah (hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.w.)), kuhusu Pepo, Moto, neema za Barzakh (kipindi kilichopo baada ya kufa na Qiyama). Vile vile wanaamini adhabu za Barzakh, Mizani, Siraat, A-araaf, na Kitabu cha amali (kila kiumbe atakuwa na kitabu chake kilichoandikwa vitendo vyake vizuri na vibaya), hakikuacha dogo wala kubwa ila limedhibitiwa humo na kwamba watu watalipwa kufuatana na matendo yao.71 Basi atayefanya wema sawa na chembe

70 Al-Allamah Sheikh Muhammad Husain Kaashiful-Ghita, (a.r.)71 Haya ni mambo ambayo kama mtu hakuyajua habari zake kwa undani ⇒

Page 106: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

99

ndogo atauona, na atayefanya uovu sawa na chembe ndogo atauona. (Qur’an, 99:7-8). Na mambo mengi mengine aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na aliyoyaeleza yote yatakuwa.

Hapa tumekwisha kamilisha maelezo ya sehemu ya kwanza ya mzizi wa imani, maelezo haya yote yalitegemea juu ya kazi ya akili, moyo wa elimu na itikadi. Sasa tutaanza kueleza mambo yanayohusu wadhifa wa moyo na kiwiliwili, ambayo makusudio yake ni vitendo kwa mujibu wa nguzo za Imani na matendo ya kiwiliwili.

UTANGULIZI

Imamiyyah wanaitakidi kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu, kuwa, Mwenyezi Mungu kaweka hukumu yake juu ya kila jambo linalotakikana na linalotendwa na Binadamu hadi Qiyama, kubwa au dogo hata kama mtu akimkwaruza mwenziwe kuna kutozwa faini. Hapana tendo lolote miongoni mwa matendo ya mtu Mukallaf72 isipokuwa Mwenyezi Mungu ameliwekea hukumu jambo hilo katika zile hukumu tano ambazo ni: Wajibu, Haramu, Sunna, Makruhu na Mubaha.73

Hapana shughuli yeyote kuhusu mali, au ndoa na mengineyo kama hayo isipokuwa sheria (ya Kiislamu) inayohukumu katika jambo hilo juu kufaa kutendwa au kutokufaa.

MWANZO

Hakika Mwenyezi Mungu hukumu zake zote amemkabidhi Mtume wa mwisho, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), na kazipokea hukumu hizo kwa kuteremshiwa wahyi au ilhaam.

⇐ haitaleta madhara juu ya itikadi yote kuhusu Ma-aad (Qiyama) baada ya yeye kuitakidi asili (ya Qiyama). (Mtarjumi).72 Ni hali ya kutoka utotoni kuingia katika ujana, ambapo mtu huanza kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. 73 Wajibu: Ni jambo analolazimika muumini kulifanya; Haramu: Ni jambo lililokatazwa kulifanya; Sunna: Ni jambo linalofaa kufanywa na mara nyingi linakuwa ni miongoni mwa matendo ya Mtume au Imam (a.s.); Karaha: Ni jambo lisilofaa kutendwa; Mubaha: Ni jambo la halali.

Page 107: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

100

Mtume wetu (s.a.w.w.) alizibainisha hukumu hizo kwa watu khususan Masahaba wake waliokuwa wakimzunguka na kukaa nae usiku na mchana ili nao wawafikishie Waislamu wengine ulimwenguni. Mwenyezi Mungu anasema: “Ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu.” (2:143) Mtume (s.a.w.w.) alizibainisha hukmu hizo kwa mujibu wa wakati wake au kutegemeana na matukio mbali mbali.

Kuna hukmu nyingine zilibakia bila kubainishwa katika kipindi cha Utume, kwa sababu ya kutokuwepo mambo ambayo yangepelekea kubainishwa kwake au kutokuwepo maslahi ya kuzibainisha hukumu hizo ndani ya kipindi hicho. Hapana shaka kwamba kuna hekima fulani ya kubainisha hukmu kadhaa miongoni mwa hukmu za sheria na kutokuzibainisha nyingine. Pamoja na hali hiyo Bwana Mtume (s.a.w) aliwakabidhi hukmu hizo Mawasii wake ili nao wazieneze ulimwenguni kutegemeana na wakati muafaka, na kila Wasii baada yake alimkabidhi Wasii mwingine.

Hapana shaka kwamba hadithi alizozisimulia Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake huenda ikatokea tofauti kati ya Msahaba katika kuzifahamu maana zake kutokana tofauti zao kiuwezo wa kufahamu na uhodari wa kuzingatia. Mwenyezi Mungu anasema: “Ameteremsha maji kutoka mawinguni, na mbuga zikapita maji kwa kadiri yake” (13:17).

Mshairi mmoja anasema: Walakini akili (za watu) huchukua kutoka humo kwa kiasi cha uhodari na kufahamu.

Hutokea Sahaba mmoja kuhusu jambo fulani amesikia hukumu yake kwa Mtume (s.a.w.w.), na Sahaba mwingine katika tukio jingine lililoshabihiana alisikia hukumu kinyume ya mwenziwe, hukumu hizi mbili kwa nje (outwardly) huonekana zapingana, lakini kwa hakika tofauti iko katika matukio na ndiko kwenye chimbuko la hitilafu ya hukumu mbili hizi. Kwa vyovyote yule mtu aliyeeleza na kuhadithia hadithi hiyo hakuangalia tofauti hiyo, na kama alitanabahi, basi wakati wa kuhadithia hakueleza, kwa hivyo leo tunaona kwamba zapingana, lakini kwa hakika sivyo hivyo kwani kila moja katika hizo zahusiana na kadhia mahususi.

Page 108: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

101

Kwa sababu hii na sababu zinginezo, Waislamu wote na hata Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) ambao wamepata utukufu wa kuonana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walihitajia juhudi ya kufahamu hukumu za Uislamu, kwa kuzichunguza hadithi na baadaye kuziunga na kuzilinganisha na maneno mengine yanayodhihirisha maana yake.

Mara nyingi maneno ya hadithi (fulani) hufahamisha jambo fulani, lakini ukichungua na kulinganisha na hali ilivyo na sababu zake utaona limekusudiwa jambo jingine kutegemeana na Qarina inayohusika. Hivyo basi inawezekana hadithi ikanukuliwa na isinukuliwe Qarina husika.

Ni dhahiri kila mmoja miongoni mwa Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa na utambuzi na uwezo wa kusimulia hadithi za Mtume (s.a.w.w.) (kwani siyo kila Sahaba alikuwa na sifa hiyo) wakati mwingine aliisimulia hadithi kumsimulia mwingine kwa mujibu wa tamko lilelile alilotamka Mtume kwa muda mrefu au karibuni basi huyo anahesabika kuwa ni msimulizi na mtu wa hadithi. Na kuna wakati mwigine huieleza hukmu aliyoifahamu kutokana na riwaya au riwaya nyingi kwa mujibu wa uoni wake na jitihada yake, basi huyo katika hali kama hiyo huwa ni Mufti na ni Mtu mwenye rai. Kwa hiyo watu wenye uwezo kama huu ndiyo waitwao kuwa ni Mujtahid na Waislamu wengine ambao hawakufikia daraja hiyo, pindi watakapotumia rai za yule wa kwanza hao huitwa Muqallid (wanaofuata).

Mambo haya yalitendeka katika zama za Mtume (s.a.w.w.) na mbele ya macho yake, bali baadhi ya Masahaba waliwarejea wenzao na hii ni kwa sababu hapana shaka kwamba watu wote hawako sawa.

Ukiangalia kwa undani katika maelezo yaliyotangulia utaona wazi kwamba mlango wa Ijtihadi ulikuwa uko wazi katika zama za uhai wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) licha ya zama zingine zilizokuja baada yake. Pamoja na hali hiyo ni kwamba, siku hizo ulikuwa hauna uzito sana kutokana na kuwa karibu mno na zama za Utume na kuwepo kwa Qarina zinazotosheleza na pia uwezekano wa kufahamu maana

Page 109: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

102

ya hadithi ulikuwa mkubwa. Na juu ya hayo ikiwa kuna mabadiliko ya vipengile waliweza kumwuliza Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe na kupata yakini.

Lakini kila tunapozidi kuwa mbali na zama za Utume, na rai kuwa nyingi, na pia kuwepo maingiliano ya Waarabu na wasiokuwa Waarabu, na kubadilika kwa lugha na ugumu wa kuyafahamu maneno ya lugha ya Kiarabu, na pia kwa kupanuka uwanja wa hadithi na hasa walipoingia baadhi ya watu wenye nia mbaya wakaanza kuchafua baadhi ya hizo hadithi na kuzusha na kubuni hadithi za uwongo dhidi ya Bwana Mtume (s.a.w.w.), hapo ndipo Ijtihadi na kuzifahamu hukmu za sheria yakawa ni mambo magumu yanayohitajia mazingatio na juhudi.

Si hivyo tu bali inahitajika faragha na nafasi kizikusanya hadithi pamoja na kuzifanyia uchunguzi ili kupambanua kati ya hadithi sahihi na batili na pia kuzitilia nguvu baadhi yake juu ya zingine. Kwa hivyo kila ikizidi umbali na zama za Mtume (s.a.w.w.) na Uislamu kuzidi kupanuka na kupatikana wanavyuoni wengi na watu wanaosimulia, basi mambo huzidi kuwa magumu. Lakini vyovyote itakavyokuwa mlango wa ijtihadi ulikuwa wazi tangu zama za Mtume (s.a.w.w.) bali ni jambo la lazima kuendelea kuwa wazi, na mlango huo bado uko wazi mpaka leo kwa upande wa madhehebu ya Shia Imamiyyah, na kutokana na dharura ya hali tuliyonayo watu bado wako mchanganyiko baina ya wenye Elimu na wasiokuwa na elimu. Na kwa mujibu wa maumbile yalivyo na hukmu isiyopingika ni kwamba, asiyejua amrejee anayejua.

Kwa maana hiyo basi, ndani ya hukmu za sheria wako wasiyojuwa na wanaojuwa, na yule asiyejua ni wajibu wake katika kuyapambanua mambo yanayomuhusu kisheria kumrejea mmoja miongoni mwa wale Mujtahid. Waislamu wote wanakubaliana kwamba dalili za hukmu za kisheria zimefungika ndani ya Kitabu (Qur’an) na Sunna, na kisha Akili na Ijmai. Hakuna tofauti katika jambo hili baina ya Imamiyyah na wengine miongoni mwa makundi ya Waislamu, isipokuwa Imamiyyah wanahitilafiana na wasiokuwa wao katika mambo yafuatayo:

Page 110: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

103

1. Imamiyyah hawatumii Qiyas, na zimekuja riwaya nyingi kutoka kwa Maimamu wao zisemazo kuwa “Dini itakapofanyiwa qiyas basi itaangamia.” Na kubainisha ubaya wa kutumia qiyas ni jambo linalohitajia wasaa.

2. Imamiyyah hawaitilii maanani Sunna kwa maana ya hadithi za Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa ile tu ambayo imesihi kupitia mapokezi ya Ahlu-Bait (a.s.), waliyoipokea toka kwa babu yao Mtume (s.a.w.w.), yaani iliyopokewa na Imam Jaafar As-sadiq ku-toka kwa Al-Baqir, naye kutoka kwa baba yake Zainul-Abidin naye kutoka kwa Husein naye toka kwa Amiril-Muuminin naye toka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, amani ya Mwenyezi Mungu iwashukie wote. Amma riwaya inayopokelewa kutoka kwa Abu Hurairah, Samrah ibn Jundub, Mar’wan ibn Al-Hakam, Imran ibn Hittan Al-Khariji na Amr ibn Al-A’s na mfano wa watu kama hao kwa Imamiyyah riwaya kama hiyo haizingatiwi kwa lolote. Watu hao hali zao zinaeleweka hakuna haja ya kueleza, kwa nini isiwe hivyo wakati Wanachuoni wengi wa Kisunni wameziweka wazi tuhuma dhidi ya watu hao na wakabainisha juu uovu wao.

3. Kama ulivyokwishafahamu hapo kabla kwamba mlango wa ijtihadi kwa Imamiyyah bado uko wazi kinyume na Waislamu wengine, kwani wao mlango huu umefungwa, na umefungwa ili wenye akili wasitumie akili zao. Mimi sifahamu ulifungwa lini na kwa dalili ipi na ilikuwaje hiyo namna ya ufungaji. Kwa hakika sijamkuta mtu wa kuweza kutosheleza kueleza juu ya maudhui hii miongoni mwa Wanachuoni wa Kisunni, na hayo ni masuali ambayo sina nikijuacho katika majibu yake na wala simjui ni nani mwenye jukumu la kuyaweka wazi. Na mambo mengine yasiyokuwa hayo Imamiyyah na Waislamu wengine wanaafikiana, hawahitilafiani isipokuwa katika Furuu’ kama wanavyohitilafiana Wanachuoni wa Imamiyyah na Wanachuoni wa Kisunni katika kufahamu na kuchambua.

MUJTAHID

Makusudio ya neno Mujtahid ni yule mtu aliyezishughulikia na

Page 111: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

104

kuzifanyia kazi dalili za sheria, na akatumia muda wake mpaka ukapatikana uwezo na nguvu itakayomuwezesha kutoa hukumu za kisheria kutokana na dalili hizo. Hali hii haijuzishi kumfuata bali ziko sharti zingine, na muhimu zaidi ni Uadilifu, na huo uadilifu ni Uwezo ambao mtu kwa kupitia uwezo huo anaweza kujizuwia kutokana na maasi na akaweza kusimamia wajibu kama anavyoweza shujaa kuikabili vita kwa wepesi bila ya woga. Na upeo wake ni kwamba, hiyo ni hali ya kumkhofu Mwenyezi Mungu inayomlazimu mtu kuwa nayo katika hali zake zote na inazo daraja kadhaa, na ya juu kabisa ni Ismah ambayo hiyo ni sharti kwa Imam.

Kisha ni lazima ifahamike kuwa hapana Taqlid wala Ijtihad katika mambo ya Dharuriyyaat74 kama vile wajibu wa Sala, Saum na mfano wa mambo kama hayo ambayo amehukumiwa kuyatenda mtu mukallaf, na yeyote mwenye kuyapinga atakuwa amepinga Dharuriyyatid-din. Vile vile hapana Taqlid juu ya kuamini mizizi ya dini, kama Tauhid, Nubuwwah, Ma’aad na mingineyo ambayo inampasa kila aliyebalahe kuijua kwa dalili ya akili ijapokuwa kwa ujumla kwani hii ni kazi ya maarifa, na kuitaqidi kwake hakutegemei kudhani tu.

Kuhusu kuwa na maarifa ya matawi ya dini (furuu’) lazima ipatikane kwa Ijitihad au taqlid. Mwenye kubalehe ni lazima juu yake atende kwa kufuata sharia kwa njia ya Ijitihad au Taqlid. Atapata adhabu mwenye kuacha kujua sharia kutokana na moja katika njia hizi mbili.

Anayebalehe kwa sharia, vitendo vyake vina namna mbili. Ya kwanza ni baina yake na Mola wake (Mwenyezi Mungu) na cha pili ni baina yake na kiumbe mwenziwe. Kwa hivyo usahihi na ukamilifu hupatikana baina yake na Mwenyezi Mungu, kila kitendo kiwe kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Qurbatan Ila-llaahi). Ibada ina sehemu mbili, Ibada inayohusu kiwiliwli, kwa mfano, kusali na kufunga na inayohusu mali ni kutoa Zaka, Khums na Kafara.

74 Mambo ambayo mwenye kuyakanusha huwa kakanusha misingi ya dini k.m. Sala, Hijja, Saumu, Zaka n.k. Na anayekanusha misingi ya dini huwa ametoka katika Uislamu.

Page 112: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

105

Au ziko ibada ambazo ni za muamala kati yake na kiumbe mwenziwe, hufanyika kwa pande mbili au moja, ama kwa pande mbili mfano wake ni kama biashara, kuozeshana, n.k., na kwa upande mmoja mfano wake kama talaka, kuacha mtumwa huru n.k. Yapo mambo mengine yanayomhusu yeye binafsi yake, kwa mfano, kula, kunywa, kuvaa nguo na mengineyo.

Elimu ya (Fiqh) ni elimu inayojadili juu ya mambo yote ya dini, na imegawika milango minne: -

1. Ibada (Al-Ibaadaat)2. Matendo na shughuli ya kila namna (Al-Muaamalaat)3. Mapatano (Al-Iyqaa-aat)4. Hukumu (Al-Ahkaam).

Al-Ibaadaat: Imegawika sehemu sita, mbili katika hizi, huhusu kiwiliwili tu, nazo ni Sala na Saumu. Na mbili kuhusu mali tu nazo ni Zaka na Khums. Na mbili zimechanganyika, mali na kiwiliwili, nazo ni Haj na Jihad. Mwenyezi Mungu anasema: “Fanyeni juhudi kwa mali zenu, na nafsi zenu…” (9:40).

Kaffaarraat: (Fidio) Ni adhabu na fidio maalum kwa madhambi mahsusi.

SALA

Kwa Imamiyyah na kwa Waislamu wote Sala ni nguzo ya dini, na ni muungano baina ya kiumbe na Mola wake, na ni sababu ya kutukuka kiumbe, na kumkaribia Bwana wake yaani Mwenyezi Mungu.

Anaeacha Sala (asiyesali), hukatika muungano na uhusiano baina yake na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hizi, yamepokewa maelezo na hadithi nyingi zilizotokana na (Ahlul-Bayt). Ukilinganisha Uislamu na Ukafiri ni kwamba Mwislamu yeyote atayeacha Sala za faradhi moja au mbili atakufuru na kugeuka kafiri.

Sharia ya Islamu, imeiweka Sala kuwa ni ibada ya awali kuliko ibada

Page 113: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

106

zote, kwani Sala imetiliwa mkazo na kwamba ni bora kabisa kuliko ibada zote.75 Kwa itikadi ya wanavyuoni wa Imamiyyah wote wameafikiana kuwa, “Mwenye kuacha Sala ni muovu, hana heshima katika sharia, hifadhi yake kwa Uislamu itakatika, na atakuwa hana uaminifu, na inajuzu kwa mtu huyo kusengenywa.” Na hapana shaka kwamba kwa mujibu wa maafikiano ya Wanachuoni wa Imamiyyah, Sala ni jambo muhimu sana (haifai kuipuuza hata kidogo).

Katika Imamiyyah, Sala imetiliwa mkazo sana na kusisitizwa mno. Kwa muujibu wa sharia, zipo namna tano za sala za wajibu:-

1. Sala tano za kila siku (Raka 17)2. Sala ya Ijumaa3. Sala za Idi mbili (Eid-el-Fitr na Eid-El-Adh-haa)4. Sala za Aayaat (kupatwa mwezi au jua au tetemeko la ardhi)5. Sala ya kutufu (kuzunguka) Qaaba.

Sala inaweza kuwa faradhi juu ya yeyote anayeweka nadhiri, au ajifunge kuwa atasali raka fulani kwa kula yamini, au kusali kwa malipo ya pesa (Ijara), na zote zilizobakia ni Sunna.

Kwa Imamiyyah, Sala za Sunna zilizotiliwa nguvu ni Sala za Rawaatib,76 nazo ni rakaa 34. Kwa Mashia Imamiyyah, Juu ya Sala za fardhi rakaa 17, huongeza kusali Sala za Rawaatib raka 34 za usiku na mchana ambazo jumla yake inakuwa rakaa 51 kila siku. Hapa nakikumbuka kisa kimoja ambacho ni vema kukisimulia, kisa ambacho amekisimulia Ar-Raaghib Al-Isfahani ndani ya kitabu kiitwacho Al-Muhadharaat, nacho ni miongoni mwa vitabu madhubuti tena kizuri amesema: “Katika zama za Ahmad ibn Abdil-Aziz huko Isfahaan alikuweko mtu mmoja akiitwa Alkinaani. Huyu Ahmad alikuwa akisoma kwa mtu yule mambo yanayohusu Uimamu. Siku moja ikatokezea mama yake Ahmad akamuona mwanawe anasoma kwa huyo Alkinaani akasema, “Ewe mtu muovu, tayari umekwishamfanya mwanangu awe Rafidha” Alkinaani akamjibu akasema, “Ewe mwenye akili finyu, huyo umwitaye 75 Mtume (s.a.w.w.) anasema kwamba, “Ikiwa Sala itakubaliwa, ibada zingine zitakubaliwa, na ikikataliwa Sala, basi ibada zote zitakataliwa” 76 Sala za Sunna za kila siku, usiku na mchana yaani Qabliyyah, Baadiyyah na Tahajjud n.k

Page 114: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

107

Rafidha yeye anasali kila siku rakaa khamsini na moja, na huyu mwanao hasali japokuwa rakaa moja katika hizo rakaa khamsini na moja, basi iko vipi daraja yake mbele ya huyo umwitaye kuwa ni Rafidha?”77

Baada ya Sala za Rawaatib ambazo husaliwa siku zote, Sala zilizotiliwa nguvu zaidi, na zenye fadhila zaidi, ni Sala za Sunna za Mwezi Mtukufu wa Ramadhaan, nazo ni Rakaa elfu moja, juu ya zile Sunna za siku zote, sala zote hizi na kama zilivyokuwa kwa ndugu zetu Sunni, tafauti ilioko baina ya Imamiyyah na Sunni ni kuwa kwa Imamiyyah sala zote za Sunna hazijuzu kusaliwa Jamaa, (kwani hakuna kusali kwa jamaa) ila sala za faradhi tu, na ndugu zetu Sunni wanasali hizo sala za Sunna kwa Jamaa, na sala maarufu kwao ni sala za Sunna zinazojulikana kwa jina la sala za Taraawih.

Hakika hatuna haja ya kutoa maelezo kwa urefu juu ya sala za fardhi na za sunna ambazo zote zimekwisha elezwa katika vitabu zaidi kuliko elfu kumi, na yeyote anayetaka kujua zaidi atazame katika vitabu hivyo vya Imamiyyah. Na vipo vitabu vingine vingi bila ya hesabu, vilivyoandikwa juu ya Nyiradi na Dua za kabla na baada ya Sala, na vile vile adabu za Sala.

Kwa Imamiyyah, Sala zote hazisihiki wala hazikamiliki bila ya kufuata sharia tatu zifuatazo: -

MASHARTI KABLA YA SALA

1. Sharti za Sala zilizoshikamana na kanuni za kabla ya Sala na katika Sala, na muhimu katika hizo ni sita, ikiwa moja katika hizo haikupatikana, Sala hubatilika nazo ni hizi: -(a) Tahara (b) Kuingia wakati, (c) Kuelekea Qibla, (d) Kujisitiri (e) Kutia niya na (f) Mahala unaposalia, na kwa hakika mahala pa kusalia si katika nguzo japokuwa ni suala muhimu na ni sharti pawe ni mahali pa halali na pale unaposujudia ni lazima pawe na tahara.

77 Rafidha maana yake ni mpinzani: Maadui wa Shia wanawaita Mashia jina hilo kwa kuwa wao wameupinga Ukhalifa wa Abu Bakr na wenzake, na wakamtawalisha Imam Ali (a.s.), na baada yake ni watoto wake kama alivyousia Bwana Mtume (s.a.w.w.).

Page 115: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

108

NGUZO ZA SALA

2. Sehemu zinazokamilisha Sala ni mbili.Sehemu ya kwanza: ni Nguzo ambazo bila hizi (ikiwa mojawapo imeachwa makusudi au kwa kusahau) Sala hubatilika nazo ni nne, (a) Takbiratul-Ihram, (b) Qiyaam, (c) Rukuu, (d) Sujuud.Sehemu ya pili: isiyokuwa Rukn (ambazo kwa makusudi ikiwachwa sala hubatilika) nazo ni tano: (a) Qiraat (Kisomo cha Al-Hamdu na sura kamili) (b) Dhikri, (c) Tashahhud, (e) Salaam, na katika yote hayo (d) Tuma’niinah (utulivu wa mwili) lazima upatikane katika Sala nzima.

Adhana (Kuadhini) na Iqaamah (Kuqimu) ni katika Sunna zilizotiliwa nguvu sana na khasa ya pili (Iqaamah) imetiliwa nguvu zaidi ikiwa upo wakati wa kutosha kuitekeleza.

3. Vitendo vinavyobatilisha (vinavyovunja) Sala, vina namna mbili. Namna ya kwanza: ni vitendo vile ambavyo kwa vyovyote vimetendeka (ikiwa makusudi au si makusudi) hubatilisha Sala navyo ni vitatu:- (a) Hadathi kila kinachobatilisha Wudhu, (b) kuipa mgongo Qibla na (c) kutenda kitendo hata kikaondoa sura ya Sala. Kwa mfano kurukaruka au kupiga makofi katika hali ya sala. Namna ya pili: vitendo vitavyotendeka katika Sala ikiwa kwa makusudi basi hubatilisha (huvunja) Sala navyo ni hivi:- (a) Kuzungumza (b) Kucheka au kulia kwa sauti (c) Kugeuka kulia au kushoto (d) Kula na kunywa.

Amma Tahara ambayo ni udhu na kukoga ni sehemu katika shuruti za kabla ya sala tulizozitaja na kila moja wapo katika hizi mbili huwa na sababu ambayo kwayo huwa faradhi kuitenda. Na ikiwa haitawezekana kutawadha au kuoga kwa sababu fulani fulani, au kutokuwa na maji ya kutosha, au kwa sababu ya ugonjwa au baridi kali, au kuwa wakati hatoshi kwa kutawadha yaani jua litachomoza au kuzama, na asiweze kutawadha, basi badala yake ata tayamamu, kama inavyoeleza Qur’an tukufu, “Basi tayamamuni kwa udongo safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu.” (4:43)

Page 116: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

109

Wamehitilafiana wanavyuoni na mabingwa wa lugha juu ya neno la ‘Saeed’ lililotajwa katika aya ya nyuma: baadhi yao wanatakidi kwamba (Saeed) ni kwa maana ya udongo tu, lakini kikundi kingine maana ya neno hilo wamelitanua na kusema, chochote kilicho funika ardhi ikiwa udongo, changarawe, mchanga, jiwe, kokoto n.k. yote hayo yanakuja chini ya neno la Saeed hata mawe ya chokaa kabla ya kuchomwa pia yanaingia chini ya neno hilo.

Hayo yalikuwa muhtasari kuhusu Sala kwa mujibu wa itikadi ya Shia Imamiyah, na bila shaka kama tulivyoeleza huko nyuma kwamba sehemu ya mambo hayo kuhusu sala yameelezwa katika vitabu kwa kirefu mno na atakaye arejee kuviangalia.

SAUMU

Saumu wanavyoiona Shia Imamiyah ni moja katika nguzo za ibada ya Ki-Islamu, na hukumu zake zagawika sehemu tatu.

Saumu zilizo FaradhiSaumu zilizo faradhi hugawika namna mbili; ya kwanza ni saumu ile ambayo ni faradhi kwa asili ya sheria, kama vile saumu ya mwezi wa Ramadhani, na kuna wajibu wa saumu kwa sababu fulani kama vile saumu ya Kaffara kwa maana ya malipo na faini, au saumu badala ya kuchinja mbuzi katika Hija kwa udhuru fulani ulioruhusiwa, na saumu ya ‘Niyaba’ badala ya maiti fulani asiyefunga, au saumu ya Nadhiri n.k.

Saumu za SunnaSaumu za Sunna kama kufunga mwezi wa Rajabu na Shabani, na saumu za sunna nyinginezo ambazo ni nyingi sana.

Saumu zilizo HaramuSaumu za haramu (zilizokatazwa kufunga) ni Saumu ya sikukuu mbili Idul Fitri na Idul-Adh-haa.

Saumu zilizo Makruhu(a) Saumu ya siku ya Ashura (mwezi kumi Muharram, Mfungo nne).78

78 Zimepokewa hadithi nyingi zilizosemwa na Ahlul-Bait (a.s.) kulaumu ⇒

Page 117: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

110

(b) Kufunga siku ya Arafa (mwezi tisa Dhil-Haj-ji mfungo tatu)

Sharti za SaumuSaumu ina shuruti, na pingamizi adabu mahsusi, na Dua nyingi sana ambazo wanachuoni wa Ki-Shia wameandika vitabu vingi sana maelfu kwa maelfu kuhusu jambo hili.

Kwa vyovyote mshikamano wa Mashia na saumu ya Ramadhani uko katika kiwango cha juu mno kiasi kwamba watu wengi miongoni mwao hukurubia kufa kutokana na maradhi au kiu lakini hawawi tayari kufuturu bali wanavumilia ile taabu. Kwa kifupi Sala na Saumu ni ibada halisi zinazohusika na kiwiliwili.

ZAKA

Zaka kwa Shia Imamiyahh, ni muhimu sana na ni ya pili baada ya Sala, bali katika baadhi za hadithi za Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) zilizopokewa zinasema kuwa “Asiyetoa zaka sala yake haikubaliwi.”79 Shia kama Waislamu wengine wanaitakidi kwamba, ni faradhi kutoa Zaka juu ya vitu tisa. Mifugo ya aina tatu yenye miguu minne ambayo ni Kondoo na mbuzi,80 ng’ombe na ngamia. Nafaka zina namna nne Ngano, shairi, tende na Zabibu. Na Dhahabu, na fedha81. Ni Sunna kutoa Zaka katika mali ya biashara, farasi na kwa kila kinachoota ardhini miongoni mwa nafaka.

Bila shaka kufaradhika Zaka juu ya vitu hivyo tisa kuna sharti na kiasi cha kufikia ukomo fulani ndipo humlazimu mtu kutoa Zaka, na yote hayo katika vitabu vinavyohusika yameelezwa.

Ni muhimu kuonesha kwamba sharti zote na mazingira ambayo Shia

⇐ kufunga siku mbili za mwezi tisa na kumi ya Muharram na hasa siku ya Ashura, siku ambayo Banu Umay-yah walikuwa wakifurahia na kufunga kuonesha furaha yao kwa kumwua Imam Husain (a.s.) Bwana wa Vijana wa Peponi kwa kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). (Mtarjumi).79 Taz: Al-Kaafi juz: 3 uk. 497; Al-Faqiih juz: 2 uk. 8/2680 Katika lugha ya Kiarabu Kondoo na Mbuzi wamewekwa katika fungu moja na wote wawili huitwa Al-ghanam.81 Ni lazima iwe sarafu zenye chapa ya sarkali. (Mtarjumi).

Page 118: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

111

wanayaamini kuhusu Zaka, kwa vyovyote moja katika madhehebu manne mashuhuri ya Ki-Sunni ambayo ni Hanafi, Shafii, Malik na Hambal yanaafikiana na hayo.

Matumizi ya Zaka kwa Shia Imamiya ni yale yale yanayohusika kwa watu wa aina nane ambao Qur’an tukufu imeeleza wapewe: Mwenyezi Mungu aliposema “Hakika Sadaka ni kwa mafakiri tu, na maskini na wanaozitumikia na wenye kutiwa nguvu nyoyo zao (katika dini) na (kwa kuwakomboa) wafungwa na wenye madeni na katika njia ya Mwenyezi Mungu na msafiri....” (9:60)

ZAKATUL - FITRA

Ni namna moja katika namna za Zaka. Nifaradhi kutoa kwa kila Mwislamu aliyekuwa balehe, mwenye akili, mwenye mali siku ya Id-dul Fitri, atoe kwa nafsi yake, na kwa kila aliyekuwa ahali (jamaa) wa-naokula kwake au wanaishi kwa pesa zake, mdogo au mkubwa aliye-huru au mtumwa. Na kiasi cha Fitri, kwa kila mtu ni sa’a moja ambayo ni sawa na kilo tatu na gram mia mbili (31/5 kg) ambazo ni ratli sita na nusu kiasi. Aina ya vitu vya kutolea Zakatul-Fitri ni chakula kin-acholiwa sana katika nchi, kwa mfano, ngano, mchele, shairi, tende n.k.Hakuna tofauti yoyote juu ya jambo hili kati ya Shia na madhehebu za Ki-Sunni.

KHUMS

Shia wanaamini kwamba, ni faradhi kutoa Khums juu ya vitu saba. (a) Nyara za vita, (b) Vitu vinavyopatikana baharini kwa kuzamia baharini (kwenda mbizi), (c) Hazina na mali inayopatikana kwa kuchimba ardhini, (d) Madini, (e) Faida ya kila aina ya pato la halali, (f) Mali ya halali iliyochanganyika na haramu, (g) Ardhi ya Mwislamu ikinunuliwa na mtu anayeishi katika dola ya Kiislamu lakini yeye si Muislamu, mtu huyo inamlazimu atoe Khums.

Mwenyezi Mungu Anasema katika Qur’an tukufu hivi: “Na jueni ya kwamba, chochote mnachokichuma (mnachokipata) basi sehemu yake

Page 119: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

112

ya tano (1/5) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume na kwa jamaa zake, na yatima na maskini na msafiri.” (8:41)

Neno Ghanima kwa mujibu ya lugha ya Kiarabu lina maana nyingi ambazo kila pato analopata binadamu huingia katika neno hilo, na si kwa maana ya nyara tu. Zimepokewa hadithi nyingi za Ahlul-Bait (a.s.) ambazo zote zinafasiri maana hiyo hiyo, na kwa utaratibu huo huo (Khums) hupasika kwa kila pato analolipata binadamu. Kwa hakika hii ni namna moja ya kodi ya mapato ya Ki-Islamu, ambayo baada ya kutoa gharama zote za maisha katika mwaka moja, baadaye yatayozidi ndio hulazimu kutoa 1/5 katika yaliobakia.

WANAOSTAHIKI KUPEWA KHUMS

Sisi tunaitakidi kwamba, Mwenyezi Mungu Ameiweka Khums kwa ajili ya Kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w.) badala ya Zaka na sadaka ambazo amezifanya kuwa ni haramu kwao. Khums hugawika sehemu sita, sehemu tatu katika hizo: ni za Mwenyezi Mungu, Mtume wake na jamaa zake Mtume (kama ilivyoeleza Qur’an tukufu) na sehemu tatu za mwisho, anapokuwepo Imam (a.s.) lazima apewe yeye na yeye atazitumia kwa mujibu wa maslahi anayoyaona. Na wakati Imam (a.s.) yupo Ghaibu, ni faradhi kupewa Mujtahid mwadilifu ambaye (ni Naibu wa Imam) yeye hutumia katika mambo ya kulinda sharia, na miji ya Waislamu, na kueneza mambo ya dini na mambo muhimu ya Ki-Islam kama kuwasaidia wasiojiweza, maskini na wahitaji, na kama aonavyoona inafaa kutumika, na wala siyo kama alivyosema kwa kusimanga na mzaha Mahmod Al-Aloosi katika tafsiri yake eti kwamba, “Kwa Shia inafaa katika wakati huu (zama za kughibu kwa Imam) sehemu hizo (za Khums) waziweke katika Sardab!”82

Kusudi lake la kusema hivyo ni singizio na uwongo wanaosingiziwa Shia mara nyingi, na wanasema kwamba Shia wanaitakidi kuwa Imam Mahdi (a.s.) amejificha katika Sardab iliyoko katika Samarrah (Iraq).83

82 Ruhul-Maa’ni juz: 10 uk. 583 Sardab ni chumba kilichotengenezwa chini ya ardhi. (Mtarjumi).

Page 120: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

113

Sisi mara nyingi tumesoma kwamba singizio hili ni moja katika masingizio yasiofaa ambayo yanasikitisha tangu zamani hadi sasa. Masunni wanatusingizia, na katika vitabu vyao vingi wameandika kwamba “Shia wanaitakidi kuwa, Imam amejificha katika Sardab.” Hali hiyo Sardab haina uhusiano hata kidogo na suala la Imam kuwa katika ghaiba. Kwa hakika haijulikani singizio hili lisilofaa na uwongo kama huu vinatokana na kitabu kipi au mwandishhi yupi wa Ki-Shia.

Labda chanzo cha kosa hilo ni kuwa wanatuona sisi huenda kuzuru hiyo Sardab, lakini sisi tunapazuru ilikuwa mahala hapo kwa sababu Imam wetu Al-Mahdi na baba zake Imam Al-Hasan Al-Askari, na Imam Al-Hadi (a.s.) siku zote katika maisha yao mahala hapo walipafanya kuwa ni mahala pa kumwabudu na kumsujudia Mwenyezi Mungu.

Ama sehemu tatu zingine, ni haki ya wahitaji wa Kisharifu badala ya Zaka ambayo wameharamishiwa kupokea na wamewekewa sehemu hizi.

Hii ilikuwa hukumu ya sehemu sita za Khums kwa Shia ambayo tangu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi leo ipo, lakini Sunni baada ya kufariki dunia Mtume (s.a.w.w.) haki ya Khums ya Bani Hashim (masharifu) wameikata kabisa (na kuwanyima) na wakatia sehemu hizo katika Baitul Mali. Matokeo yake imekuwa wahitaji na masikini wa Ki-sharifu (Bani Hashim) wamenyimwa Zaka na Khums! (huku na huku!)

Labda kwa sababu hiyo Imam Shafii katika kitabu chake maarufu kiitwacho Al-Ummu uk. 69 ameashiria jambo hili kwa kusema hivi: “Ama watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) ambao wamewekewa Khums badala ya sadaka, wao hawapewi chochote kutoka katika sadaka zilizofaradhishwa, na wala si halali kwao kuchukua sadaka hizo. Na kama mtu akiwapa katika hizi (Zaka au Sadaka) basi itakuwa haina faida wala hakutekeleza faradhi (itambidi alipe tena).” Na akaendelea kusema, “Kutokupewa haki yao katika Khums, haitawajuzia (hakutoi nafasi kwao) kupokea katika Zaka au Sadaka ambayo ni haramu juu yao”.

Page 121: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

114

Kwa hivyo wanachuoni wa Ki-Sunni pia wameuondowa mlango wa Khums katika vitabu vyao, na katika tungo zao wala hawakuzungumzia jambo hili kabisa, kinyume chake wanachuoni wa Ki-Shia katika kila kitabu chao cha Fiqhi kidogo au kikubwa wamezungumzia katika mlango mahsusi kama walivyouzungumzia mlango wa Zaka na mingineyo.84

Haya yalikuwa maelezo kwa ufupi kuhusu itikadi ya Shia juu ya Ibada mbili za Ki-Islam zinazohusika na mali, yaani Zaka na Khums, na ama zile ibada zenye kuhusika na kiwiliwili na mali ni mbili pia, nazo ni Hija na Jihadi.

HIJA

Kwa Shia Hija ni moja katika nguzo kubwa ya Islam, kwa mujibu ya hadithi zilizopokewa katika vitabu vyetu kwamba mwenye kuacha kwenda kuhiji, wakati wa kufa atahiyarishwa achague kufa katika dini ya Uyahudi au Ukristo, mtu huyo huwa kafiri kama inavyosema Qur’ani tukufu hivi: Aliyekufuru (asende kuhiji) basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. (3:97)

Kwa hakika Hija ni aina moja ya Jihadi ya mwili na pesa, bali Hija ni jihadi yenye maana sana, vivyo hivyo Jihadi ni Hija halisi, kwa kuangalia kwa uangalifu utaona zote mbili hizo zaonesha umoja, upatano, wa moyo mmoja.

SHARTI ZA HIJA

Baada ya kutimia masharti ya jumla kwa mtu, kama kubalehe, akili, uhuru, na shuruti mahsusi kama vile kuwa na uwezo wa kiwiliwili, mali, usalama katika safari na gharama ya kwenda na kurejea, zote

84 Hapana shaka kwamba (Mwanachuoni mmoja shujaa wa Kisunni) aitwaye Abu Ubaid Al-Qasim ibn Salaam aliyefariki mwaka 224 A.H. ndani ya kitabu chake kiitwacho Kitabul-Amuwali, kitabu hiki ni miongoni mwa kumbukumbu nzuri ya vitabu, yeye ameueleza mlango wa Khums kwa ufafanuzi pia namna ya vitu vinavyopasa kuvitolea Khums na namna ya kuigawa na hukmu zake nyingine. Kwa hakika mengi aliyoyaeleza humo yanaafikiana na mambo mashuhuri kwa Imamiyyah. Mwenye kutaka na arejee kutoka ukurasa wa 303 hadi 349.

Page 122: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

115

hizo zikikusanyika basi Hija huwa ni faradhi mara moja tu katika umri (wa mtu) na aitekeleze haraka mara baada ya kutimia sharti zake.

Namna za Hija: Hija ina namna tatu, nazo ni hizi;1. Ifrād; ambayo Qur’an tukufu inasema hivi: “Na kwa ajili ya

Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu kuhiji kwenye nyumba hiyo.”

2. Qirān; ambayo Qur’an inaeleza hivi: “Timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” (2:196)

3. Tamat-Tuu kama ilivyo katika aya hii isemayo kuwa: “Basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndiyo akahiji.” (2:196)

Kila moja katika namna hizo, zina maelezo mengi sana ambayo yameelezwa katika vitabu mahsusi. Nimeangalia sana katika vitabu vya wanachuoni wa Ki-Sunni, nimeona aghlabu mambo ya Hija yanaafikiana na vitabu vya wanavyuoni wa Ki-Shia, isipokuwa mambo machache tu yanahitalifiana.

Ukiangalia tarehe ya Shia hapo zamani na sasa utaona Shia wanasisitiza sana watu kwenda kuhiji, na kwao ni jambo muhimu sana, na kila mwaka maelfu ya Shia wanaipata heshima ya kujaaliwa kwenda kuhiji, ijapokuwa wakipata taabu na mashaka ya kupambana na hatari kutokana na wale ambao walikuwa wanaichukulia mali na hata damu ya Mashia kuwa ni halali kwao kuimwaga. Lakini yote hayo hayakuwazuwia kutekeleza faradhi muhimu ya Hija. Katika njia hii wengi walijitoa muhanga, na kupoteza roho na mali. Ni ajabu mno juu ya yote hayo, bado wanasema ati Shia wanataka kuvunja nguzo za Uislamu!!

JIHAD (VITA VYA DINI)

Jihadi ni msingi muhimu katika kujenga majengo ya Uislamu, na ni mhimili wa hema hili. Jihadi ndiyo imesimamisha na kueneza dini ya Kiislamu! Isingalikuwa Jihadi, Uislamu usingelikuwa ni dini ya rehema na baraka kwa ajili ya watu wote ulimwenguni.

Page 123: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

116

Jihadi ni kumkabili adui na kupinga dhulma na ufisadi duniani, kwa roho na mali na kujitolea kwa ajili ya kusimamisha haki.

Namna za Jihadi: Kwa Shia jihadi ina namna mbili, Jihadi kubwa na Jihadi ndogo.

Jihadi kubwa: Ni kumpinga adui wa ndani, yaani nafsi, (kutokana na tamaa za mwili) na kupambana na sifa mbaya kama vile upotovu, ujinga, woga, udhalimu, kiburi, kujipenda, ubakhili, husuda n.k. Kwani adui yako mkubwa na wa hatari sana ni nafsi yako mwenyewe.

Jihadi ndogo: Ni kumpinga adui wa nje, ambaye ni adui bayana, adui wa uadilifu, adui wa wema, na adui wa dini.

Na kwa kuwa kupigana na tabia mbaya, na sifa mbaya ambayo imeota mizizi katika mwili na roho ya binadamu, vita hivyo vimekuwa vigumu sana, ndiyo maana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika baadhi ya maneno yake akaiita jihadi hiyo kuwa ni Jihadi kubwa.

Yeye na Masahaba wake (r.a.) katika uhai wao walishughulika na Jihadi mbili hizi, hata Uislamu ukafikia kilele cha utukufu na fahari hii.

Lakini hapa kimebakia kitu moja, lau tukitaka kwa kalamu yetu kuieleza Jihadi ya Waislamu waliopita na vipi walijitolea mhanga kwa ajili ya kusimamisha na kuinua utukufu wa Islam, na kuangalia tunayoyaona hivi sasa, machozi ya majuto na masikitiko yangechururika kutoka machoni mwetu, na nyoyo kwa huzuni nyingi zingepasuka.

Je! Mnajua kwa nini kalamu nimeizuwia kuandika? Hali muwako wa huzuni katika moyo wangu unawaka sana na kunisonga moyo hata siwezi kueleza kisa hicho!!

KANUNI MBILI KUBWA

Kwa itikadi ya Shia, Kuamrisha mema na kukataza maovu ni

Page 124: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

117

miongoni mwa mambo muhimu ya wajibu kisheria na yanakubalika kiakili, na ni miongoni mwa misingi katika misingi ya dini ya Kiislamu.

Wajibu mbili hizi kubwa ambazo zinahisabika kuwa ni misingi madhubuti ya Uislamu, na ni katika ibada na utiifu bora kabisa wa dini na pia ni moja katika namna za Jihadi.

Watu watakaosahau na kuacha misingi miwili hii Mwenyezi Mungu bila shaka Atawatia katika mazingira ya udhalili na unyonge, na kuwavisha maafa na masaibu; watu kama hawa watakuwa chambo kwa wadhalimu na wajeuri.

Kwa sababu hiyo Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu (a.s.) wote wamesisitiza mno kutekeleza wajibu mbili hizo, na kuhadharisha na matokeo mabaya kwa jamii ya binadamu kwa kuacha wajibu mbili hizi.85

Kwa bahati mbaya hivi sasa sisi tunaona na kushuhudia waziwazi hasara ya maovu kutokana na uzembe wa kutotekeleza wajibu mbili hizi, wala hatuhitajii dalili wala ushuhuda kuithibitisha hali hiyo.

Laiti mambo yangemalizikia hapa! kwa kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu basi, na hali yetu isivuke zaidi ya hapo kiasi ambacho sasa imefikia uovu unaonekana ni wema, na wema unaonekana ni uovu, na waamrishaji mema wao wenyewe wameyapiga teke hayo mema hawayatendi, na wenye kukataza maovu, wao ndiyo wanayatenda hayo. Innaa lillahi wa Innaa ilaihi Rajiu’na. Uovu umeeenea nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyotendwa na mikono ya watu.... (30:41).

Mwenyezi Mungu amewalaani wale ambao wanaawamrisha watu kutenda mema, na wao wenyewe hawatendi, na wale wanaokataza watu wasitende maovu hali wao wenyewe wanatenda maovu.86

85 (1) Kuamrisha mema. (2) Kuataza maovu.86 Dini ya Kiislamu ina wingi wa hukumu zenye uwezo wa kufahamu mambo mengi, kwa sababu chochote anachohitajia binadamu katika mambo ya dini na dunia na ya kumpeleka mbele kwenye maendeleo na mafanikio imeshampangia. ⇒

Page 125: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

118

Hii ilikuwa ni misingi ya Ibada ya Kiislamu katika nadhariya ya Shia Imamiyah, nasi tumetoshelezwa kwa muhtasari, maelezo na ufafanuzi zaidi ya hayo tumeuacha katika maelfu ya vitabu vilivyotungwa na wanachuoni wa mwanzo wa Kiislam hadi sasa atakaye arejee huko.

SHUGHULI NA BIASHARA KWA NADHARI YA SHIA

Kama tulivyoashiria hapo mwanzo kwamba shughuli zimegawika sehemu kadha wa kadha.

Shughuli kati ya pande mbili: Shughuli kama hii ni mfungamano wenye kuhitajia kuweko pande mbili, upande mmoja huitwa ‘Muujib’ na upande wa pili huitwa ‘Qaabil’ kwa mfano yule asemaye nimeuza kitu hichi ni ‘Muujib’ na yule asemaye nimekubali kununua ni ‘Qaabil’.

Wakati mwingine makusudio yanakuwa ni mali, basi hapo huitwa ‘Muawadhah’ (Badilisho), na katika mabadilisho pia kuna namna mbili:Ya kwanza:- (Uquud, al-lāzimah) mapatano na maafikiano ya lazima kufuata kama kununua, kuuza, kukodisha, masikilizano, rahani kupeana zawadi, bahshishi kwa malipo, n.k. Shughuli kama hizo, pengine pia huitwa ‘Al-mughābināt’

Ya pili:- Mapatano na maafikiano yenye kujuzu kuvunja. Yaani mapatano ambayo pande mbili au upande mmoja inawezekana kuvunja na kutangua, kama kukopesha, zawadi na bahshishi lakini bila malipo, na ‘Al-jā’la’ na mfano wake. Maana ya Jā’la ni kwamba mtu aseme: “Yeyote akinifanyia kazi fulani nitampa kadha wa kadha au kiasi fulani.”⇐ Mtukufu (s.a.w.w.) alipoweka sheria na kanuni za dini kwa ajili ya Umma, kwa hakika ilikuwa mamlaka na nguvu ya mfanya sharia. Ni dhahiri nguvu ya mfanya sharia bila ya kuweko nguvu ya utendaji ya kutosha haitaleta matunda. Kwa hivyo idhini na udhamini wa daraja ya kwanza ya utendaji kawapa Waislamu wote, na Amefaradhisha juu ya kila Mwislamu kuamrisha mema na kukataza maovu. Kila mmoja awe mwangalizi wa mwenziwe, na kila mmoja mbele ya mwenziwe ni mchunga, na kila mmoja anawajibika.

Page 126: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

119

Hukumu na shuruti za mapatano hayo zote mbili za lazima kufuata au za kujuzu kuvunja, zote hizo zimeelezwa katika vitabu vya Fiqhi, vikubwa na vidogo katika matni na sherhe zake.

Jambo ambalo ni muhimu na lazima kulitaja ni hili: Kwamba wanachuoni wa Ki-Shia, ikiwa kuhusu mambo ya mapatano na shughuli au mambo ya Ibada, hawaruhusu kitu chochote japo kidogo kwa kiasi cha unywele kwenda upande kwa kinyume cha Qur’an na Sunna ya Mtume (s.a.w), pia kanuni au utaratibu wa Istis-hāb. Sisi hatumruhusu kamwe mtu yeyote kuchuma mali isipokuwa kwa njia za halali za kisharia, kama vile kufanya biashara, kulima, sanaa, ufundi n.k., na mali yoyote ipatikanayo kwa kunyang’anya, riba, hiana, hadaa, kwetu yote hayo ni haramu.

Sisi hatumruhusu yeyote hata kwa wasio Waislamu kuwafanyia yote hayo ili kujipatia mali, kwetu sisi uaminifu ni jambo muhimu tena ni katika mambo ya faradhi, na kufanya hiana na kafiri licha ya Waislamu ni haramu.

Hii ilikuwa shughuli na mapatano ya mali, lakini fungu lingine la shughuli na mapatano kati ya pande mbili ambalo halihusiki na mali, ijapokuwa inawezekana kuwa enye mali kama kuozeshana ambalo lengo lake hasa ni kuwa na watoto na kutengeneza familia na ndiyo kudumu kwa binadamu.

Kwa Shia katika ndoa kuna namna mbili, (a) Ndoa ya daima (Dāim) kama Qur’an tukufu inavyosema: “Na waozeni wajane miongoni mwenu, na waliowema katika watumwa wenu, na wajakazi wenu.” (24:32).

Na namna ya pili, Ndoa ya muda utaowekwa kati ya wanaoowana kwa masikilizano, na pia ndoa hiyo huitwa ‘Mut’a’, au ‘Nikahul-Muaqqat’, na Qur’an tukufu ni ushahidi wa uhalali wake nayo ni hii “Na kwa wale ambao mmefanya nao (ndoa ya Muta’), basi wapeni mahari zao kama mlivyoaninisha, wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana (mkibadilisha) baada ya kuainisha hiyo mahari.....” (4:24).

Page 127: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

120

Namna ya kwanza ya ndoa Waislamu wote wanafikiana, lakini namna ya pili, ni jambo mahsusi kwa Shia.

Shia wanasema na kuamini kwamba, kama ilivyokuwa hapo mwanzo wa dini ya Kiislamu ndoa mbili hizi zilikuwa halali na kutumika, sasa pia vivyo hivyo na hadi Qiyama ni halali tu.

Siku zote yamekuwepo mapambano makubwa kati yetu na wengineo juu ya jambo hilo, na historia ya ugomvi huu imeanzia zama za Masahaba baada ya Mtume (s.a.w.w.). Kwa hivyo jambo hilo lina umuhimu kwa upande wake hivyo basi si vibaya tulieleze kwa kirefu, tena kwa uhakika na jinsi lilivyothibiti kwa ajili ya kuwafahamisha ndugu zetu wa Ki-Islamu na Inshallah tutalizungumzia zaidi, ili haki na ukweli ujulikane.

NDOA YA MUDA KWA MTAZAMO WA SHIA

Moja katika mambo muhimu yasiyokanushika ambayo hata kwa kila mwenye kuwa na ujuzi mdogo kabisa wa hukumu na kanuni, hatasita kulikubali jambo la ndoa ya Mut’a’ yaani ndoa ambayo huainishwa muda kati ya wenye kuoana, na hiyo ndoa imeletwa na kuhalalishiwa na mwenyewe Mtukufu Mtume wa Uslamu (s.a.w.w.). Hapana shaka kwamba kikundi cha Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake Mtukufu na baada ya kufariki kwake wakifaidika na kanuni hii.

Wafasiri (wa Qur’an) wa Ki-Islam juu ya jambo hili wamewafikiana kwamba kikundi cha Masahaba wakubwa wa Mtume (s.a.w.w.) kama Abdallah ibn Abbas, Jabir ibn Abdillahi, Imran ibn Haseen, Abdallah ibn Mas’ud, Ubayyi ibn Kaa’b na kama hao, walikuwa wakitoa Fatwa ya kuruhusu na kujuzu Mut’a’ (ndoa ya muda) na ile aya iliotangulia wakiisoma hivi: “Na wale ambao mmefanya nao (ndoa ya) Mut’a’ kwa muda maalum…”87

Hapana shaka fikra yao haikuwa kwamba Qur’an imepungua au kugeuzwa la, sivyo hivyo kabisa bali lengo lao ni kueleza tafsiri inayotokana na mwenyewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyeshushiwa 87 Angalia tafsiri ya Fakhr Razi juz. 3, uk. 201; na Tafsiri ya Tabari juz. 5, uk. 9; Tafsirul-adhim ya Ibn Kathir juz. 1 uk.474; Tafsirul-Kash-shaf ya Zamakhshari juz: 1 uk. 519.

Page 128: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

121

Kitabu hicho ambacho hakina shaka ndani yake, na ambayo wao waliisikia kwake, ijapokuwa kwa kadiri ionekanavyo katika hadithi alizopokea Ibn Jarir Tabari katika tafsiri yake kubwa inafahamika kuwa fungu hilo lilikuwa katika asili ya Qur’an, kama anavyoeleza Abu Naseerah kuwa aya hii nilimsomea Ibn Abbas, akaniambia soma, “Ilā ajalin Musammā”. Nikasema, “Mimi, sintasoma hivyo”. Akasema, “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (aya hii) imeshushwa vivyo hivyo.” Akakariri mara tatu.

Walakini hakika daraja ya Ibn Abbas, Sahaba mtukufu mashuhuri wa Uislamu ambaye alipewa jina la heshima kuitwa Hibrul-Ummah, haiwezekani kwa mtu kama huyu kudhania Qur’ani imegeuzwa, (kama ikiwa hadithi hii ni sahihi) bila shaka kusudio lake kusema hivyo ni kwamba tafsiri na maana imekuja hivyo.

KISA CHA MTANGUO WA AYA:Kwa vyovyote wanavyuoni wa Kiislamu wote wanaafikiana, bali ni katika mambo ya lazima katika dini kuitakidi kwamba, Mut’a’ hapo mwanzoni mwa dini ya Islam ilikuwa ni sharia na halali, na Waislamu wakilitenda na kulifuata jambo hilo, isipokuwa wapinzani wa hukumu hiyo ati wanadai kuwa hukumu hiyo baadaye ilifutwa na kupigwa marufuku, lakini kuhusu shauri ya kufutwa kwa amri hiyo kuna hitilafu nyingi, na hadithi wanazosimamishia madai yao zinapingana.

Ni dhahiri kwamba hadithi kama hizo si tu kwamba haziaminiki, bali hazifidishi dhana licha ya hukmu ya mkato, lakini kwa mujibu ya kanuni ya elimu inatuambia, hukumu ilio thabiti na halisi haitenguki isipokuwa kwa dalili thabiti vilevile.

Basi hao wanaodai kuwa hukmu ya ndoa hiyo ilitenguliwa, wakati mwingine utawaona wanamsingizia Mtume (s.a.w.w.) kuwa yeye mwanzoni aliruhusu na kuhalalisha na baadaye ati akaipiga marufuku, kwa hivyo imekuwa haramu kwa Sunna ya Mtume.88

88 Kauli za jamaa hawa zinapingana zenyewe tena mno. Wapo miongoni mwao wanaodai kwamba, Kwanza ndoa hiyo ilikuwa halali kisha ikaharamishwa siku ya Khaibar. Na kuna wengine wanadai kuwa, hapo zamani ilkuwa halali lakini ikaharamishwa katika mwaka wa Fat-hi Makkah. Na kauli ya tatu inasema ⇒

Page 129: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

122

Na pengine wanasema mtanguo wake ni kwa aya za Qur’an tukufu, na hapa pia wamehitalifiana ni kwa aya ipi imetenguka? Wengine wanasema kwa aya ya Talaka isemayo, “Mtakapotoa talaka kwa wanawake, basi toeni talaka katika wakati wa eda zao......................”89 (65:1) yaani, wakati ambapo wameshasafika na unajisi wa ujusi na hawakuingiliana nao.

Wengine wanasema aya ya urithi kati ya mume na mke ndio imetengua, “Nanyi mtapata nusu ya (mali) zilizoachwa na wake zenu, kama wao hawana mtoto....................” (4:12)

MKE ANAYEOLEWA KATIKA NDOA KAMA HII NI MKE HALALI

Tunafahamu kwamba madai yao yote kwa jinsi yalivyo dhaifu hayana ulazima na msingi wala haja ya kuyajibu, kwa sababu aya hizo (za talaka na urithi) kamwe hazilingani hata kidogo wala hazipingi aya ya Mut’a’ na hata tuseme kuwa zinatangua hukmu hii. Inshallah huko mbele tutaeleza zaidi jambo hilo kwamba ndoa ya muda ni moja miongoni mwa ndoa sahihi, na mwanamke anayeolewa kwa ndoa namna hii ni mke halisi wa mumewe na hukumu zote za sharia zinawahusu mume na mke huyo.

Lakini wapinzani, wengi wao wanadai kwamba aya ya Mut’a’ imetenguliwa na aya hii isemayo, “Isipokuwa kwa wake zao au kwa wanawake wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume.....” (23:6) Eti kwa sababu aya hii imeruhusu kuingiliana mume na mke chini ya anwani ya mambo mawili ambayo ni Mke na Wale ilyowamiliki mikono ya kuume.90

⇐ kuwa, Ilikuwa halali lakini ikaharamishwa katika Hijja ya mwisho.

Iko pia kauli ya nne isemayo kuwa, “Ilihalalishwa mwaka wa Autas kisha baadaye ikaharamishwa.” Ziko pia kauli nyingine nyingi unaweza kuzirejea. Taz: Sahih Muslim Babu nikahil-Mut’a’; Majmauz-zawaid juz: 4 uk. 264; Sunan Ibn Majah juz:2 uk.227; Tabaqat Ibn Sa’ad juz: 4 uk.348 n.k.89 Taz: Al-jamiu liahkamil Qur’ani ya Qurtubi juz: 5 uk. 130; Sunanul-Baihaqi juz: 7 uk.207. 90 Taz: Sunan Tirmidhi juz: 5 uk.50; Sunan Al-Baihaqi juz: 7 uk.206; Al-jamiu liahkamil Qur’ani ya Qurtubi juz: 5 uk.130.

Page 130: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

123

Al-Aloosi mwanachuoni maarufu wa Kisunni katika tafsiri yake anasema hivi, “Shia hawawezi kudai kuwa mke wa Mut’a’ anaingia katika anwani ya mjakazi, kwa sababu ni jambo batili (halimo) na pia hawawezi kudai kuwa anaingia katika anwani ya mume na mke wa kawaida, kwani hukumu za mke kama kurithi, eda, kulisha, na talaka yote hayo kwa mke wa Mut’a’ hayapo!”91

Kwa kweli hoja hii ya Aloosi ni ya kustaajabisha sana. Shia wanasema kuwa mke wa Mut’a’ ni mke halisi na wa hakika, na Aloosi anaposema kuwa ndoa hii haina kanuni ya mke na mume, bila shaka haina msingi na si sahihi kwa sababu zifuatazo:

Ya Kwanza: Sharti alizozitaja kama kurithi, kulisha n.k. ikiwa kusudio lake ni hili kwamba namna zote za ndoa zinazo sharti hizo, madai hayo bila shaka hayakubaliki. Katika jumla ya ushahidi wenye kuonesha kwamba sharti hizo hazimo katika ndoa zote. Tunaona mahala pengi mke harithi na kwa hali yeye ni mke kwa mfano, mke akiwa kafiri harithi kwa mumewe, vile vile mke aliyemuua mumewe hana haki ya kurithi, na pia mtu akimuoa mwanamke katika ugonjwa wake wa mwisho aliokufia naye kabla ya kuingiliana naye akafa, mke harithi (ingawa ndoa katika kadhia yote hiyo ilikuwa mke wa ndoa wa daima).

Na kinyume chake tunaona mahala pengine mke kwa kupewa talaka lakini haki ya urithi ipo bado, kwa mfano, mtu akimpa talaka mke wake katika ugonjwa wake aliofia, eda ya talaka ikaisha, baadaye mume kabla ya kupita mwaka mmoja akafa, mke atarithi.

Ya Pili: Lau tutakubali juu ya kuwepo kulazimiana lakini kutokurithi kwa mke wa ndoa ya Mut’a’ liwe ni jambo lisilowezekana. Kuna kikundi cha wanavyuoni wa Kishia wanasema kwamba, “Huyu mke kama mke wa ndoa ya daima hurithi.” Na kikundi kingine wanasema kuwa “Kwa kawaida mke huyu harithi lakini anaweza kuwekeana sharti wakati wa ndoa kama awe au wawe na haki ya kurithiana, hapo mke huyu kama mke wa daima atarithi.” Na baadhi ya wanavyuoni wetu wanasema kuwa, “Kwa hali yoyote atarithi isipokuwa tangu hapo mwanzo wakiwekeana sharti wasirithiane hapo mke hatarithi.”91 Taz: Ruuhul-Maani juz: 5 uk. 7.

Page 131: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

124

Kwa hali hii vipi inawezekana ukosefu wake katika urithi kufahamika ni thabiti? Kwa vyovyote kwa mujibu ya kanuni ya Fiqhi ilioko mikononi na kwa hali ilivyo tukiangalia (aya ya Mut’a’ na aya ya kuozana (funga ndoa) katika sura ya Mu’minun), hakika mke wa ndoa ya muda ni mke tu na hukumu zote za uke anazo isipokuwa yale mambo ambayo kwa dalili thabiti yamemtoa!

Ama kuhusu Eda wanavyuoni wote kwa pamoja wanaitakidi kwamba, hakika katika ndoa ya muda imethibiti kuwepo eda, na hatatokea mtu yeyote asithibitishe kuwepo eda.

Ama kuhusu posho kwa mke, hilo si jambo la lazima kwa mke, kwa dalili kwamba mke asiyemtii mumewe (anaokataa kuingiliana na mumewe) hana haki ya posho ijapokuwa yeye ni mke.

Na ama kuhusu Talaka ni lazima tukumbuke kwamba katika ndoa ya muda kuna jambo ambalo huwa badala ya talaka, nalo ni kusamehe muda wa ndoa, kwa sababu mume anaweza kumwachia mkewe muda uliobakia na kuwa mbali naye kwa hivyo hakuna tena haja ya talaka.

Ya Tatu: Kitanguo cha aya ya Mut’a’ kwa aya ya kuozana (aya ya 6 Sura Mu’minun) toka mwanzo wake ni muhali wala haielekei kabisa kwa sababu aya ya Mut’a’ ipo katika sura ya An-Nisaa na sura hii ni miongoni mwa sura zile zilizoteremshwa Madina,92 na juu ya hayo aya ya kuozana ipo katika sura ya Mu’minun na sura ya Ma’arij, sura zote hizo ni miongoni mwa sura zilizoshushwa Makka,93 kwa hivyo kwa mujibu ya tarehe, aya ya kwanza (yaani aya ya Mut’a’) imekuja nyuma, na haimkiniki kabisa kitu cha mbele kutengua cha nyuma (ambacho bado hakijateremshwa).

Ya Nne: Kikundi cha wanavyuoni wakuu wa Ki-Sunni wamenakili hadithi ambazo kwa mujibu ya hadithi hizo yaonesha kuwa aya ya Mut’a’ haikutenguliwa kamwe, katika jumla ya wanavyuoni hao ni 92 Taz: Al-kashfu an wujuhil-Qiraatis-sabi’ juz: 1 uk.375; Al-jamiu liahkamil Qur’ani juz: uk. 1; Al-Kash-shaf ya Az-Zamkhshari juz: 1 uk.140.93 Taz: Al-kashfu an wujuhil-Qiraatis-sabi’ juz: 2 uk.125 na 334; Al-jamiu liahkamil Qur’ani juz: 12 uk.102 na juz: 18 uk. 278; Al-Kash-shaf ya Az-Zamkhshari juz: 3 uk.24 na juz: 4 uk. 456.

Page 132: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

125

Zamakhshari katika tafsiri yake ndani ya tafsiri yake iitwayo al-Kash- shaf yeye amenakili kutoka kwa Ibn Abbas kwamba aya ya Mut’a’ ni miongoni mwa aya zile zisizoweza kufanyiwa taawili (kupewa tafsiri nje ya ile maana inayoonekana dhahiri) ni Muh-Kamaat.94 Baadhi ya wengine wamenukuu kwamba, Al-Hakam ibn Al-Uyainah alipoulizwa kuwa je, aya ya Mut’a’ imetanguliwa? Akajibu La!95

Kwa ufupi wapinzani wetu baada ya kukiri na kukubali kwamba ndoa ya muda ni ndoa halali na kuna wakati wanadai kuwa kutenguka kwa hukumu hiyo ni kutokana na aya ya Qur’an lakini dai hilo tayari umekwishaiona hali yake.

Na kuna wakati mwingine wanadai tanguo lake ni kwa hadithi, na wamelifanyia ushahidi kwa hadithi ilyosimuliwa na Bukhari na Muslim kwamba Mtume (s.a.w.w.) amepiga marufuku Mut’a’ na kula nyama ya punda wa mjini katika siku ya ushindi wa Makka, au Khaibar au katika vita vya Autas.96

Kama mnavyoangalia hadithi hii inahitilafu, machafuko na tawanyiko la namna kwa namna. Imesimuliwa kuwa Qadhi Ayadh amesema kuwa, “Baadhi yao wanasema kuwa hakika jambo hili ni miongoni mwa mambo yaliyobadilika badilika mno, kwani mara liliharamishwa na mara likahalalishwa na likafutwa mara mbili.”97

Lakini ikiwa tutatalii vema na kupanua mawazo na kuangalia vitabu mbalimbali vilivyoandikwa juu ya jambo hilo, tutaona ukinzani wa wenyewe.

Katika baadhi ya vitabu hivyo utaona tanguo ya hukumu hii ilikuwa katika Hijjatul Widaa98 yaani Hija ya mwisho ya Mtume (s.a.w.w.)

94 Al-Kash-shaf juz: 1 uk. 519.95 Ad-durul- manthoor ya Suyuti juz: 2 uk. 140.96 Taz: Sahih Bukhari juz: 7 uk.16; Sahih Muslim juz: 2, na hapo kabla tumetangulia kuashiria unaweza kurejea huko.97 Sharhi Sahih Muslim ya Nawawi juz: 9 uk. 181; Tafsirul Adhim ya Ibn Kathir juz: uk.474.98 Sunan Abi Dawood juz: 2 uk. 227; Sunan Al-Baihaqi juz: 4 uk. 348; Tabaqat ya Ibn Sa’ad juz: uk. 348.

Page 133: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

126

katika mwaka wa kumi wa Hijra, na kwa mujibu wa walivyonakili baadhi yao ilijiri katika vita vya Tabook mwaka wa tisa (a.s.)99

Na kwa hadithi nyingine inasemwa kuwa ilikuwa katika vita vya Aw-taas au vita vya ‘Hunain’ ambavyo vilikuwa katika mwaka wa nane mwezi wa mfungo mosi.100 Kuna hadithi nyingine siku ya ushindi wa Makka mwaka wa nane mwezi wa Ramadhan.101

Baadhi yao wanasema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku za ushindi wa Makka aliruhusu na baada ya siku chache aliiharamisha.102

Lakini kauli iliyomaarufu kwao na ndiyo msimamo wa wengi wao kwamba, tanguo la hukumu hii lilikuwa katika vita vya Khaibar mwaka wa saba au katika vita vya Umratu-Qadhaa katika mwaka huo huo mwezi wa Zilhaj. Ikiwa mazungumzo yote hayo tukiyachukulia kama ni hadithi basi itatubidi tukubali kwamba jambo hilo (ndoa ya muda) mara tano au sita lilihalalishwa na baadaye kuharimishwa, si mara mbili au tatu, si kama alivyosema mwanachuoni wa Ki-Sunni aitwaye Nawawi na wengineo katika kitabu cha Sharh ya Sahih Muslim.103 Enyi wanavyuoni wa Kiislamu! Mchezo gani huo mlioleta katika mambo ya dini? Je akili ipi itakubali na kupenda mashauri haya?

Ni dhahiri kwa namna tulivyoeleza haitaaminika hata kidogo maneno yaliyozungumziwa kuhusu tanguo la aya ya Mut’a’ kwa kutegemea habari zinazogongana zenyewe kwa zenyewe. Pili, Qur’an haifutwi kwa hadithi ya Ahaad isiyokuwa Mutawatir, na tatu, ni kwamba madai hayo yanapingwa na hadithi nyingi ambazo zimekuja kwa njia zao Masunni katika vitabu vyao tena ziko wazi na zinajulisha kwamba hukmu hiyo haikufutwa.

99 Al-jamiu liahkamil Qur’ani ya Qurtubi juz: 5 uk. 130; Sunan Al-Baihaqi juz:7 uk.207; Majmauz-zawaid juz: 4 uk. 264, Fat-hul bari juz: 11 uk. 73100 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1023.101 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1025; Sunan Al-Baihaqi juz:7 uk.202; Sunan Ad-darami juz: 2 uk. 140; Majmauz-zawaid juz:4 uk 264; Musannif Abi Shaibah juz: 4 uk292.102 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1025; Sunan Al-Baihaqi juz: 7 uk. 202.103 Sharhi Sahih Muslim juz: 9 uk. 180.

Page 134: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

127

Miongoni mwa vitabu hivyo ni Sahih Bukhari ameandika hivi:- Abu Raja’ amenakili kutoka kwa Imran ibn Haseen (r.a.) kwamba aya ya Mut’a’ imeshushwa katika Qur’an tukufu, nasi pamoja na Mtume (s.a.w.w.) tukatenda na wala haikushushwa aya yoyote kuitengua na mwenyewe Mtume (s.a.w.w.) hakuipiga marufuku katika uhai wake mpaka akafariki dunia, baadaye mtu mmoja kwa maoni yake akasema alivyotaka kuhusu jambo hilo.” Inasemekana mtu huyo alikuwa Umar. (Mwisho wa maelezo ya Bukhari).104

‘Muslim’ kwa sanadi yake kutokana kwa Ataa’ amenakili kwamba, “Jabir ibn Abdillahi Al-Ansari (r.a.) alifika Makka kwa ajili ya kufanya Umrah, sisi tukamfuata nyumbani kwake kuonana naye, watu waliohudhuria hapo wakamwuliza maswali, na hatimaye wakauliza kuhusu Mut’a’ akasema, katika zama za Mtume (s.a.w.w.) tulifanya Mut’a’, na katika zama za Abu Bakr na Umar pia tukitenda hayo.”105

Tena katika Sahih Muslim, kuna hadithi nyingine kutoka kwa Jabir ameinakili hivi: “Katika zama za Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tukioa Mut’a’ kwa Mahari ya fungu kidogo tu la tende na unga...... kwa ajili ya siku kidogo, tukioa Mut’a’, hiyo katika zama za Mtume (s.a.w.w.) na katika zama za Abu Bakr pia vivyo hivyo hata katika zama za Umar, baadaye Umar akapiga marafuku kutokana na mambo fulani kuhusu Amri ibn Hureith.”106 Pia katika kitabu hicho hicho, kuto kwa Abu Nadh-rah amesema, “Nilikuwa kwa Jabir ibn Abdallah, mara alimjia mtu fulani akamwambia kwamba, Abdallah ibn Abbas na Abdallah ibn Zubeir wanahitalifiana kuhusu Mut’a’ na Hija ya Tamat-tu’ Jabir akasema, “Sisi mambo yote mawili hayo tumetenda pamoja na Mtume (s.a.w.w.) baadae Umar yote mawili haya akayapiga marufuku nasi hatukuyarudia tena tukayawacha.”107

Hakika bila ya kusema kitu ni dhahiri yaonesha kwamba, Jabir

104 Sahih Bukhari juz: 6 uk. 33; pia taz: Sahih Muslim juz: 2 uk 900; Tafsirul-kabir ya Razi juz: 10 uk.49; Tafsir Albahr Almuhit ya Ibn Hayyan juz: 3 uk. 218; Sunan Alkubra ya Baihaqi juz: 5 uk. 20.105 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1023.106 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1023.107 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1023.

Page 135: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

128

akaacha kutumia Mut’a’ kwa kumuogopa Khalifa, kwani Umar akitumia hukumu za kuzini juu ya kila mwenye kufanya ndoa hiyo, na watendao Mut’a’ akiwapiga mawe hadi kufa!

Naam ikiwa tutalii kwa uangalifu kitabu hicho hicho cha Sahih Muslim tutaona mambo ya ajabu, hadithi kadha wa kadha kuhusu hukumu hiyo ya ndoa ya muda zenye kuthibitisha na pia zenye kukana zimenakiliwa humo.

Aljuhani anasema, “Mtume (s.a.w.w.) katika mwaka wa ushindi wa Makka tulipoingia Makka akatupa amri ya kuoa Mut’a’, lakini kabla hatukutoka Makka akatukataza.”108

Mara nyingine wanasema, Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe aliipiga marufuku hukumu hiyo, wakati mwingine wanasema, hukumu hiyo ilikuwapo zama za Mtume (s.a.w.w.) na za Khalifa wa kwanza ilikuwepo na Umar akaipiga marukufu, wakati mwingine wanamsingizia Imam Ali (a.s.) kuwa ameipiga marufuku na wanasema kuwa yeye Imam Ali (a.s.) mahala pengi alimkataza Ibn Abbas kuizungumzia Mut’a’ na akamkataza kufanya Mut’a’, na dakizo hilo limkafanya Ibn Abbas abadili itikadi yake kuhusu Mut’a’ na kuacha kabisa!109

Wakati huo huo wao wamenakili kwa Abdalla ibn Zubair kwamba, siku moja katika Makka alinyanyuka na kusema, “Wapo watu ambao Mwenyezi Mungu Amewapofua nyoyo zao kama alivyowapofua macho yao (akimkusudia Abdallah ibn Abbas) watu hao wanatoa fatwa kuruhusu Mut’a’! Ibn Abbas akasikia maneno hayo, akapiga ukelele akasema, “Wewe mpumbavu usiyekuwa na adabu, naapa hakika Mut’a’ ilikuwa ikitumika katika zama za kiongozi wa wacha Mungu wa dunia hii….”110

Kwa hadithi hii inafahamika vizuri kuwa, Ibn Abbas hadi mwisho wa uhai wake hata katika zama za utawala wa Ibn Zubair pia alikuwa na itikadi hiyo hiyo na fatwa yake hakuibadili.108 Sahih Muslim juz: 2 uk. 1025.109 Almusannif cha Abdur-razzaq juz: 7 uk: 501; al-Kash-shaf ya Zamakhshari juz; uk. 519.110 Sahih Muslim juz: uk. 102; Sunan Baihaqi juz: 7 uk. 205.

Page 136: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

129

Na kinachostaajabisha zaidi ni kumsingizia Ameerul Mumineen Ali (a.s.) kuwa aliipiga marufuku ndoa hiyo! Kwani ruhusa ya kujuzu hukumu hiyo inahisabiwa ni moja katika alama, mithali na sifa yao Ahlul-Bait (a.s.) na hapa kuna hadithi nyingi zilizonakiliwa kutoka kwa Ameerul Mumineen Ali (a.s.) zinazokanusha kupigwa marufuku kwa Mut’a’.

Moja katika maneno mashuhuri ya Ameerul Mumineen Ali (a.s.) ambayo ni ya kupigiwa mfano ni haya: “Lau Umar hakuipiga marufuku Mut’a’, asingezini mtu yoyote ispokuwa mhasharati au mfasiki!”111 Katika kitabu kikubwa cha tafsiri cha ‘Tabari’ amenakili kwamba Ali (a.s.) amesema: “Lau Umar hakuipiga marufuku Mut’a’, asingezini mtu yeyote ispokuwa mhasharati au watu wachache”112 Katika hadithi zetu sahihi zilizosimuliwa kutoka kwa Imam Ja‘far As-Sadiq (a.s.) Anasema, “Katika mambo matatu sitamchelea yeyote, Hijja ya Tamat-tu’, Mut’a’ (ndoa ya muda) na (ubatili wa) kupaka juu ya viatu (badala ya kapaka juu ya miguu katika udhu).”

Baada ya yote hayo, sasa hakuna shaka yoyote kufuatana na kanuni inayokubaliwa katika elimu ya ‘Usulul-fiqh’ kwamba, “Ikiwa habari za hadithi juu ya jambo fulani zinapingana, basi hadithi kama hizo huwa zinaanguka na si za kutegemea tena kutolea ushahidi, pia hapana budi kuzikanusha.” Kwa hiyo basi baada ya kuthibitika uhalali wa ndoa ya Mut’a’ kutokana na maafikiano ya Waislamu na kuonekana wazi kuwa ndoa hiyo haikufutwa, bali kinachoonekana bayana ni ile kauli inayoruhusu ndoa hiyo na kwamba ni halali hadi leo.

UPAMBANUZI NA KUONDOSHAUTATA KUHUSU NDOA YA MUT’A’

Tukitaka kupata mwangaza juu ya uhakika au matokeo, na kulipa unyoofu jambo hilo na kufahamu siri ya vurugu hiyo pia chanzo chake kilichozaa hali hiyo, hatuwezi kupata ufumbuzi isipokuwa tu ni

111 Yaani wasingezini isipokuwa watu wachache. Taz: As-sihah juz: 6 uk.2393; Lisanul Arabi juz: 14 uk.437.112 Jamiul-bayan ya Tabari juz: 5 uk. 9; pia taz: Tafsirul-kabir ya Razi juz: 10 uk. 50

Page 137: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

130

kwamba, Khalifa wa pili Umar kwa rai yake mwenyewe na kwa ajili ya maslahi fulani ambayo kwa mtazamo wake juu ya Waislamu na hali ya mazingira ya zama zake akaamua kuipiga marufuku hukumu hiyo, basi akapiga marufuku ndoa ya Mut’a’. Kuharimisha huko ilikuwa ni haramisho la ki-serikali si haramisho la sheria ya dini. Ndiyo maana mara nyingi amenukuliwa akisema, “Katika zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) palikuwa na Mut’a’ mbili, Hajj tamat-tu’ na Mut’a’ ya wanawake, mimi sasa ninaharimisha na kupiga marufuku na nitatoa adhabu dhidi ya mwenye kuzitenda.”

Kama inavyofahamika Khalifa wa pili hakusema kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameharimisha bali kasema, “Mimi ninaharimisha na mwenye kuzitenda nitamuadhibu” na wala hakusema kuwa, “Mwenyezi Mungu Atamuadhibu.”

Kwa nini iwe hivyo? Kwa kuwa mtu kama Khalifa wa pili ambaye akionesha kusisitiza kwake kutekeleza maamrisho ya dini, ilikuwaje halali aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu yeye aiharimishe? Au jambo ambalo halikuwemo katika hukumu na sharia ya Kiislamu yeye alitie? Hebu tuseme kweli, hivi ni kweli kwamba yeye alikuwa hajui kwamba, Halali aliyoihalalisha Mtume wa Uislamu ni halali hadi siku ya Qiyama? Na kwamba haramu aliyoiharamisha Mtume (s.a.w.w.) pia ni haramu hadi siku ya Qiyama kamwe haviwezi kubadilika?

Yeye alikuwa anajua vema nini Mwenyezi Mungu Alimtahadharisha Mtume Wake (s.a.w.w.) pale aliposema katika Qur’ani Tukufu kwamba: “Lau (Mtume) angelituzulia baadhi ya maneno, bila shaka tungelimshika kwa mkono wa kuume, kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo…” (69:44 hadi 47).

Kwa hali hiyo vipi tunaweza kulisadikisha azimio lake la kuharimisha halali ya Mwenyezi Mungu? Kwa hivyo hakika makusudi yake ilikuwa kuharimisha kwa kikanuni ya kiserikali kwa wakati ule.

Kwa bahati mbaya baadhi ya waliokuwa katika zama zake na wenziao waliokuja baada yake ambao walikuwa wajinga wepesi wa kuamini, walighafilika na lile fumbo lake dogo kabisa, ajabu kwa mtu kama

Page 138: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

131

Umar ambaye jukumu lake lilikuwa kulinda hukumu ya sharia za Kiislamu, lakini wao walikifikiria kuwa haielekei halali ya Mwenyezi Mungu aiharimishe, na avunje mipaka ya sharia, kwa hivyo basi wakawa wametafuta hoja ya kuepuka, na hawakuona njia isipokuwa kumsingizia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba jambo hilo kwanza aliruhusu na kuhalalisha na baadaye akaharimisha, na kwa vile madai hayo hayapatani na uhakika basi wakaanza kuleta maelezo ndio wakapambana na mabishano na hitilafu ya bila kiasi. Lau ingalikuwa kwa maana kama vile tulivyoeleza sisi waziwazi kuhusu kitendo cha Khalifa (kuharamisha Mut’a’) nao wangelieleza vivyo hivyo, basi wasingelazimika kamwe kusingizia wengine au kusema yasiyo ya kweli!!

Ushahidi wa neno hilo ni ile hadithi tuliyotaja nyuma kutoka katika Sahih Muslim ambaye amenakili kutoka kwa Jabir ibn Abdillah akisema, “Katika zama za Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tunaoa ndoa ya Mut’a’ kwa mahari ndogo kwa muda wa siku chache, hata ilipokuja zama za Umar alipiga marufuku kutokana na kadhia ya Amr ibn Hureith.”113

Ijapokuwa maelezo kamili kuhusu kisa cha (Amr ibn Huraith) hatukuyafuatilia kwa undani, lakini itoshe tu kuwa hali na mwenendo wa Khalifa wa pili ulikuwa unaeleweka. Kwa hakika yeye katika kila jambo alikuwa ni mwenye ghadhabu tena mkali na msusuavu, kwani ni mara nyingi linapotokea jambo ambalo yeye binafsi halikumpendeza, basi jambo hilo huwa ndiyo kichocheo

113 Ndani ya Sharh ya Sahih Muslim inayoitwa Ikmaalul-Mua’llim ya Mwanachuoni wa Ki-Sunni aitwaye ‘Washtani Al-Abi ameandika hivi: Baadhi wanasema kuwa kuharimishwa huko kulikuwa katika siku za mwisho wa Ukhalifa wa Umar, na baadhi ya wengine wamesema ilikuwa ndani ya kipindi cha Ukhalifa wake, Umar alisema: “Kila mwenye mke akifanya Mut’a’ na akiletwa kwangu basi nitampiga mawe hadi kufa, na mwanaume asiyeoa akiletwa kwangu kuwa amefanya Mut’a’ nitampiga viboko.” Na hiki kisa cha Amr ibn Huraith kilikuwa hivi: Katika zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bwana huyo alifanya Mut’a’, na akaendelea nayo mpaka katika zama za Khalifa Umar. Habari za mambo haya akazipata Umar, akaamrisha huyo mke wa Mut’a’ aletwe mbele yake na akamuliza, “Je ni kweli umeolewa kwa Mut’a’?” Akajibu “Ndiyo,” Akauliza, “Nani shahidi?” Akawaleta baba na mama yake kuwa ni mashahidi, Umar akasema, “Hakuna wengine?” Baadaye akapiga marufuku Mut’a’.

Page 139: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

132

cha hasira zake na anakuwa mkali mno na hayo ndiyo matokeo ya kuzuwia jambo hilo lisifanywe tena na pia kupiga marafuku kwa rai iliyojengeka katika mawazo yake na ijitihadi yake. Vinginevyo ni kwamba suala la Mut’a’ na uhalali wake baada tamko la Qur’an na kutendwa na Mtume (s.a.w.w.) na Masahaba katika muda wote wa uhai wake, na pia katika kipindi cha Ukhalifa wa Abu Bakr na sehemu fulani ya zama za Ukhalifa wa Umar, suala hili liko wazi mno wala halihitajii uchunguzi wa kina wala mabishano na mazungumzo marefu kama hayo.

Kwa nini ndoa hii isiwe halali wakati katika tarehe ya Kiislamu tunakuta kwamba, ndoa ya muda (Mut’a’) ilikuwepo zama za Mtume (s.a.w.w.) na ilifanyika kwa Masahaba wakubwa, na hata ikaleta matunda ya kupatikana vizazi na watoto wengi tena wenye daraja kubwa katika dini waliozaliwa ndani ya Mut’a’.

Mfano wake mmoja ni ule aliounakili mwanachuoni mkubwa tena mashuhuri wa Ki-Sunni aitwaye, Raghib Al-Isfahani’ ambaye wanamuamini mno anasema hivi: “Abdallah ibn Zubair, akimulaumu sana Ibn Abbas kwamba kwa nini yeye anaihalalisha Mut’a’, Ibn Abbas alimjibu akamwambia, Kamuulize mama yako ni namna gani vyetezo vyenye kueneza harufu nzuri vilifuka kati ya baba na mama yako,” (Ni fumbo la kuoana) Abdallah ibn Zubair akamuuliza mama yake, mama yake akamjibu akasema, “Naapa kuwa wewe nimekuzaa katika ndoa ya Mut’a’.”114

Hili ni tukio alilonakili Raghib Isfahani mwanachuoni maarufu wa Ki-Sunni. Je! Mnajua mama yake Abdallah ibn Zubeir ni nani? Ni Asmaa binti Abu Bakr, dada yake Aisha Ummul Mumineen. Na mumewe Asmaa ni Zubeir ambaye alikuwa miongoni mwa masahaba watiifu wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya hayo yote, yeye akamuoa Asmaa kwa ndoa ya Mut’a’. Sasa basi baada ya kuwa na ushahidi wote huo kuhusu jambo hilo, je wasemaje tena ewe mtu uliye mkaidi tena mshupavu?

Raghib baada ya kunakili kisa hicho, amenakili kisa kingine,

114 Muhadharatul-Udabai juz: 3 uk. 214.

Page 140: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

133

anasema, “Yahya ibn Aktham alimwuliza mmoja katika wazee wa Basra akasema, “Wewe unamfuata nani kuhusu uhalali wa Mut’a’?” Akamjibu, “Namfuata Umar ibn Khattab.” Yahya akamwuliza, “Kwa vipi, Mbona Umar alikuwa ni mmoja katika wapingaji wakubwa wa Mut’a’?” Akajibu, “Ndiyo, lakini hadithi sahihi zilizopokewa zasema kwamba Umar alipanda mimbari na akasema, “Enye watu, Mut’a’ mbili ambazo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walikuhalalishieni, mimi ninaziharamisha, na mtendaji wa mambo hayo mawili nitamtia adabu,” kwa hiyo sisi tunakubali ushahidi wake (juu ya kuwa hayo ni mambo halali ya Mungu na Mtume). Lakini uharamisho wake hatuukubali!”115

Kisa kama hicho kimenakiliwa pia kutoka kwa Abdallah ibn Umar. Lakini inafaa tujue kwamba fungu la maneno alilotumia yule mzee wa Basra katika hadithi yake akimnukuu Umar aliposema, “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Wamekuhalalishieni, na mimi ninaharamisha” kwa hakika haya ni maneno yaliyovuka mpaka tena ni yenye kuchukiza ambayo kamwe Muislamu hawezi kuyaridhia.

Tulipofika hapa baada ya kueleza mambo yote hayo, tulisimama ili kuyaangalia maneno ya mmoja miongoni mwa wanavyuoni wetu mashuhuri wa zamani walioishi katika karne ya tano Al-Muhaqqiq Muhammad ibn Idris Al-Hilli, nimeona maneno yake yanaafikiana na mengi tuliyoyaeleza, ndiyo maana nikapenda kuyaleta hapa ili yapate kutilia nguvu maneno yetu yaliyopita.

Yeye katika kitabu chake ‘As-sara-ir’ ambacho ni miongoni mwa vitabu vizuri kabisa vya Fiqh na Hadithi, katika mlango wa ndoa, anasema hivi: “Ndoa ya muda ni halali katika sharia ya Kiislamu, Waislamu wote wanaitakidi kwamba, katika Qur’an Tukufu na hadithi za mfululizo za Mtume (s.a.w.w.) zaruhusu ndoa hiyo, isipokuwa baadhi ya watu wanadai kuwa hukumu hiyo imefutwa, na ili waweze kuthibitisha madai yao inawalazimu walete dalili, lakini wataipata wapi dalili kama hiyo?”

Baada ya hayo, kwa mujibu wa ushahidi sahihi tuliokuwa nao

115 Muhadharatul-Udabai juz: 3 uk. 214.

Page 141: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

134

mikononi mwetu ni kuwa, kila kazi ambayo inafaida na haina hasara ya duniani wala ya akhera, kwa hukumu ya akili jambo hilo inajuzu na halali, na katika ndoa ya muda jambo hilo lipo na thabiti (yaani inafaida na haina hasara ya duniani wala ya akhera) kwa hivyo lazima tuhukumu kuwa inajuzu. Ikiwa mtu atahoji kwa vipi mnadai kwamba kazi hiyo haina hasara ya akhera hali Waislamu wanahitalifiana kuhusu kujuzu kwake?

Tutamjibu hivi:-Kwanza: Mwenye kudai kuwa ni haramu lazima alete dalili na kama hakuna dalili, akili inahukumu uhalali wake.

Pili: Kama tulivyoashiria kwamba bila ya shaka yoyote kuwa ndoa kama hiyo katika zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa halali isipokuwa wanadai hukumu hiyo ilifutwa, hali hawana ushahidi wa kufutwa kwake, kwa hivyo uhalali wake ni thabiti, walakini kufutwa kwake hakuna uthabiti, kwa hiyo ni dhahiri madhali haikuthibiti hukumu ya kufutwa, basi hatuwezi kuiacha.

Wakisema zimenakiliwa habari kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) zinazoeleza juu kufutwa na kuharamishwa kwake, basi majibu ya maneno haya yako wazi, kwani hadithi zote hizo, ikiwa (sanad) mtungo wa wapokezi ni salama, pia ni (khabar Aahaad) yaani haikufikia kupokewa kwa mfululizo yaani ‘ghairu Mutawatir’ habari kama hizo hazileti uhakika wala hatuwezi kwa sharia kuzitegemea, hatuwezi kuacha kilicho na uhakika na ukweli kwa habari kama hizo.

Juu ya hayo yote hayo Qur’an Tukufu baada ya kuwataja wanawake walioharamu kuwaoa imesema hivi: Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) wasiokuwa hao, kwamba muwatafute kwa mali zenu kwa kuwaoa bila ya kufanya zinaa. Na mkiwaoa kwa Mut’a’, wapeni mahari yao, (hiyo) ni faradhi wala hakuna dhambi juu yenu, ndoa ya Mu’tah kwa kuongeza muda na mahari zaidi mkafanya upya mara ya pili. (4:24)

Fungu la neno (Na mkiwaoa kwa Mut’a’) lililokuja katika aya hii, lina moja kati ya maana mbili: (a) maana ile ile ya kilugha (yaani kutumia

Page 142: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

135

kwa jinsi ya kupata faida yoyote iwezekanavyo kama kustarehe (b) au kusudio ni ile ndoa ya muda Mut’a’. Na kwa kanuni ya kisharia limekuja kwa maana hiyo hiyo ya ndoa ya muda.

Bila shaka kusudio si kwa maana ya kwanza (ya kilugha) tunathibitisha kwa dalili mbili:

1. Jambo hilo kati ya wanavyuoni wa elimu ya ‘Usuul’ hawahitilafiani kwamba, kama kuna neno katika Qur’ani Tukufu lenye kuchukua maana mbili (a) maana ya kilugha (b) na maana ya kisharia, lazima neno hilo kuchukuliwa kwa maana ya kisharia, kwa hivyo neno la Sala, Saum, Zaka na Hajj yaliyotajwa katika Qur’an hayakuchukuliwi kwa maana ya kilugha bali wamechukulia kwa maana ya kisharia.

Idadi kubwa ya Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na Taabii’n (wale waliokuja baada ya Masahaba) wote hao walikiri na kukubali Mut’a’, miongoni mwao ni Amirul Muminin Ali (a.s.), na Ibn Abbas. Na hadithi ya majadiliano kati yake na Abdallah ibn Zuber ni maarufu na wote wameinakili, hata washairi katika mashairi nao wameleta kisa hicho, mmoja katika wao anasema: “Namwambia huyu mzee pindi yaliporefuka mazungumzo yake (kuhusu Mut’a’), mimi ninamwambia, je unayo hoja dhidi ya fat-wa ya Ibn Abbas.”

MASAHABA AMBAO WAKIAMINI UHALALI WA MUT’A’

Vivyo hivyo Masababa na Tabi’in wafuatao: Abdallah ibn Masu’d, Mujahid, A’taa, Jabir ibn Abdillah Al-Ansari, Salmah ibn Al-Akuu’, Abu Saeed Al-Khudri, Mughira ibn Shu’bah, Saeed ibn Jubair, na Ibn Jareeh; wote hawa wanatoa fatwa ya kujuzu Mut’a’, na huo pia ni uthibitisho wa maana ya pili. Kwa hivyo chochote wanachodai wapinzani kuwa kuna maafikiano katika uharimisho wa ndoa ya muda, ni madai yasio na msingi (mwisho wa maneno ya Ibn Idris).116

Kwa kila mtu mwenye busara anaweza kabisa kufahamu uimara, 116 As-sarair juz: 2 uk. 618-620.

Page 143: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

136

uthabiti na nguvu ya hoja na ushindani unaopatikana ndani ya maelezo ya mwanachuoni huyu.

Mpaka sasa yote yaliyosemwa kuhusu jambo hilo yalikuwa yanahusu upande wa dini, historia na ushuhuda wa kisharia vinavyotokana na kanuni za msingi. Ama kwa upande wa wema wa tabia na jamii lazima tuangalie jambo moja kwamba: Hakuna shaka kwamba Uislamu ni agizo kutoka mbinguni na ni sauti ya Mwenyezi Mungu ambayo hufuatana na upepo wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu wa binadamu, na ikaipa pua ya maisha harufu nzuri yenye baraka.

Uislamu umekuja kwa ajili ya kuleta heri na fanaka kwa binadamu, si kuwaletea mateso. Uislamu ni neema kubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu wala si balaa na msiba. Uislamu unakwenda sambamba na wakati katika mambo yote ya maisha, na unatembea pamoja na msafara wa maendeleo. Uislamu ni maongozi ya Mwenyezi Mungu kwenye mafanikio na mahitajio yote ya binadamu kwa upande wa kiwiliwili na roho. Uislamu unawatakia binadamu hali ya ustawi, na unapambana na ufisadi na uharibifu. Kamwe Uislamu haukuja kuwazidishia watu shida na kuwatia katika janga na mashaka, sivyo kabisa. Bali Uislamu ni asili ya rehema na baraka kwa walimwengu, umewanyashoea barabara ya kukaa kwa raha na mafanikio na njia zote za neema.

Kwa kuwa dini ya Kiislamu ni dini iliyokamilika kuliko dini zote, na imani bora kabisa, na sharia na ni (dini) ya mwisho, na kwa sababu hii basi haikuacha jambo lolote lenye kumfikisha binadamu kwenye fanaka eti jambo hilo lije kukamilishwa dini nyingine, bali katika mambo yote ya maisha hakuna kitu au neno lililopungua au dhaifu hata dini nyingine ije kurekebisha haya.

Kwa upande mwingine, tangu siku ambayo binadamu kajijua, mambo ya kusafiri na kuwa mbali na mji wake ni moja miongoni mwa mambo ya lazima katika maisha yake. Usafiri ambao hutendeka mara kwa mara kwa ajili ya biashara na pengine kwa ajili ya kupata mafunzo na pengine kwa ajili ya ulinzi au matembezi na tafrija n.k.,

Page 144: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

137

je kulazimika kufanya safari kama hizo ni jambo linalopingika? Je si wengi wa wasafiri hao si vijana wazima wenye nguvu na siha?

Tena kwa upande mwingine, je Mwenyezi Mungu kwa hekima hakumwekea binadamu silika ya shauku kwa wanawake kwa ajili ya kuhifadhi uzazi na kuendelea kwa wanadamu? Je ikiwa silika hiyo ikidhoofika au kupotea kabisa, leo ungaliwakuta binadamu hapa duniani? Majibu ya maswali yote yako wazi na dhahiri.

Hii pia bila ya kusema ni dhahiri kwamba wasafiri aghlabu wanapokwenda safari mbali mbali hawawezi kuwachukuwa wake na watoto au kule waendako waowe ndoa ya daima, kwa sababu kuoa kwa daima kuna mambo yanahitajika ambayo kwa msafiri hawezi kutimiza masharti yake.

Sasa nadhani shauku binadamu kaumbwa nayo basi katika safari zake ndefu anazozifanya kwa ajili ya kutafuta elimu au biashara au mambo ya kiaskari kama kulinda mipaka ya mji au miji basi kwa ajili ya watu kama hawa lazima tuwe na jawabu lisilo na shaka.

Na hasa kwa wale ambao kwa ajili ya makusudio ya kila namna wanafanya safari (hasa zile safari ndefu) na aghlabu ni wale ambao bado ni vijana wabichi na wanapigana na mafuriko ya shauku ya ngono, vijana kama hawa wanajitolea kusafiri, na wao ndio wamo katika mapigano na silika hiyo. Hakuna ufumbuzi wa tatizo hili isipokuwa katika mambo mawili; Imma wavumilie na kupambana na nafsi kitu ambacho hupelekea mashaka ambayo hatimaye huwatumbukiza katika maradhi na matatizo ya kuangamiza. Zaidi ya hapo hali inaweza kusababisha kuua kizazi kisha kupoteza nasaba zilizowekwa ndani yao. Kwa matokeo haya itakuwa ni kutengua hekima ya kuumbwa kwao, na ni kupoteza lengo lililokusudiwa na kisha kuwatumbukiza ndani ya mazingira mazito, na mashaka makubwa ambayo sheria ya Uislamu inayapinga. Sheria tukufu ya Kiislamu ni nyepesi, Anasema Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’an, “Mwenyezi Mungu huwatakieni yaliyo mepesi wala Hawatakieni yaliyo mazito” (2:185), “Wala Hakuweka juu yenu udhia katika dini” (22:78)

Page 145: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

138

Njia ya pili, watu kama hawa ikiwa watakosa uvumilivu na subira, na watajitumbukiza katika shimo la Uhasharati kitendo kile kile cha kufedhehesha ambacho huandamana na ufasiki na mateso yaliojaa hivi sasa duniani.

Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu na cheo cha haki, ikiwa Waislamu wa ulimwengu wanashikamana na kufuata sharia na kanuni tukufu za Uislamu na wakarudi kwenye muongozo wa dini yao na sheria yao sahihi, “Bila shaka, tungalifuwangulia juu yao baraka nyingi za ardhini na mbinguni” (7:96) Na hapana shaka utukufu na heshima yao ingelirudi baada ya kupotea.

Moja katika kanuni adhimu, ni kanuni hii ya ndoa ya muda, lau Waislamu wangelikuwa wanaitumia kanuni hii kwa njia sahihi - ikiwemo kusoma khutba ya ndoa na kukaa eda na kulinda uzazi, basi milango ya club za ufisadi na makao ya uzinifu na uasharati ingelifungwa. Pasipo shaka uchafu na madhambi yangepungua, na wanawake wengi walioingia katika ufisadi uliopo wangesalimika, na uzazi wa halali ungeongezeka. Si hivyo tu bali watu wangepumzika kutokana na jinai la kutupwa watoto wachanga wasiokuwa na dhambi wanaotupwa majiani, na hali ya tabia nzuri katika jamii ingerejea. Na kwa kuitekeleza kanuni kwa njia ya halali na sahihi huleta faida kubwa kwa jamii ya wanadamu.

Mwanachuoni na Sahaba mashuhuri Bw. Abdallah ibn Abbas katika fungu la maneno machache ya milele yake ambayo Ibn Atheer katika kitabu chake ‘An-Nihaya’ na Zamakhshari katika ‘Faaiq’ na wengineo katika vitabu vyao wamenakili maneno hayo ambayo ni mazuri ya ajabu mno, yeye anasema:- “Mut’a’ ni jambo ambalo limewekwa ili iwe ni rehema tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya Umati wa Muhammad (s.a.w.w.), na lau Khalifa wa pili asingeipga marafuku, basi wasingalizini isipokuwa watu wachache tu!”117

Kwa hakika maneno haya Ibn Abbas ameyachota kwenye chemchem safi ya mwalimu wake ambaye ni Amirul Mu’minin Ali (a.s.), na kwa kweli kanuni hii ya Uislamu ni neema na baraka kuu kwa Waislamu.

117 An-nihayah juz: 2 uk.288; Al-faaiq juz: 2 uk. 255.

Page 146: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

139

Lakini nasikitika kusema kwamba, “Waislamu wenyewe wenye neema hiyo wameiangamiza kwa mikono yao, na wamejinyima matokeo na matunda ya thamani hiyo. Masheikh wengi wao wamezama katika matope ya ufisadi, uasharati na fedheha! Mwenyezi Mungu Anasema: “Je mnabadili vitu hafifu kwa vile vilivyo bora?” 2:61. Lahaula wala Quwwata illa Billah.

Lakini juu ya yote hayo je! Yanashangaza mazungumzo aliyoyanakili mwandishi wa gazeti la Al-I’tidal katika gombo la kwanza nambari 161 chini ya kichwa cha maneno kisemacho, “Hakuna hila isipokuwa badala ya kutumia kalamu sasa tutumie shindano kuyatia mambo ubongoni mwa watu”! Bwana huyu ameieleza humo barua kutoka Baghdad iliyoandikwa na mtu aliyejiita Khadimul-Ulamaa, yaani mtumishi wa Wanachuoni, inahusu jawabu juu ya misingi ya nuskha hii tuliyotangulia kuieleza ambayo iliandikwa na Ibn Mais-Samai, ambapo kwa hakika amekariri maelezo yanayodai kwamba, “Ndoa hii inalo tatizo la kuvuruga nasaba ya watoto, kutokana na mwanamke kuolewa na kila mwenye kupita njia na asiyejulikana.” Baadaye mwandishi huyo asiyejulikana ameongeza kusema kuwa, “Ibn Mais-Samai hakulipinga jambo moja ambalo lisilofahamika na lenye matatizo.” Akaendelea hata anasema: “Kuhusu ndoa ya vipindi Bwana huyo anasemaje? Je ikiwa watu watatu au wanne au kumi wakamuoa mwanamke mmoja, na kila saa moja mmoja akaingiliana naye! Sasa akizaliwa mtoto kwa huyo mwanamke utaweza vipi kuubainisha ukoo wake? Huyu mtoto ni mtoto wa nani? Na yupi miongoni mwa hao atatambuliwa kuwa ni baba wa mtoto huyo?”

Naam ni jambo linalofahamika wazi kwamba, kwa Shia namna zote za Mut’a’ zinakubalika kuwa ni halali, lakini (cha ajabu) ni kwamba, Viongozi na watu wenye hadhi miongoni mwa Mashia wanalionea ukakasi kulitekeleza jambo hili la Mut’a’ miongoni mwao, kwani haijasikika kwa mtu yeyote akisema kwa mfano, “Leo tumehudhuria ndoa ya Mut’a’ kati ya Sayyid118 au Mheshimiwa Fulani na Sayyidah Fulani binti Sayyid Fulani, ukilinganisha na

118 Sayyid au Sayyidah ni majina ya heshima maalum yanayotumiwa na Masharifu ambao wanatokana na kizazi cha Bwana Mtume (s.a.w.w.) kama kitambulisho chao.

Page 147: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

140

mazowea yaliyopo ambapo watu husema, leo tumehudhuria harusi ya kati ya Sayyid au Mheshimiwa Fulani na Binti Fulani.” Bali kilichopo ni kwamba mara nyigi linafanyika miongoni mwa watu wa kawaida tu. Je, hali hiyo siyo miongoni mwa aina za uhasharati tu ijapokuwa iwe iwavyo mtoto atapatikana, sasa kama si hivyo basi ni nini? Ingefaa Allamah Kashiful-Ghita ambaye amesimamia kuwafunza watu asili ya Ushia na misingi yake, azirekebishe tabia za wafuasi wa madhehebu hayo! na kuwafikisha kwenye ustaarabu wajitakase! sisi tunamuombea kwa Mola afanikiwe katika njia hii. Khadimul Ulama: Baghdad.119

Barua hiyo ilijibiwa na kusambazwa kama ifuatavyo: Imetufikia kwenye ofisi za jarida la ‘Al-Ii’tidal’ barua inayotoka kwa mwandishi asiyejulikana ambaye anasema kwamba, “Yeye amesoma katika toleo la tatu la gazeti, majibu yatokayo kwa mtu aitwaye Ibnu Mais-Samai, na akakuta kwamba jawabu hilo haliafikiani na swali lenyewe wala kilichosemwa humo.” Kisha huyu mwandishi alikariri kile kilichoelezwa na Sayyid Ar-Rawi kuhusiana na ndoa ya muda na kusema kuwa, “Ndoa kama hiyo huvuruga ukoo na kukipoteza kizazi.” Majibu ya madai haya yalikwishajibiwa na Ibnu Mais-Samai kwa hoja yenye nguvu tena kwa uwazi mno, na kwa hakika alimbainishia kwa kusema kwamba, “Hekima ya kuwekwa sheria ya kukaa eda kwa mwanamke maana yake ni kuhifadhi kizazi na kuzuwia kuchanganyikana maji ya mwanaume huyu na yule. Suala la eda kama ilivyo lazima katika ndoa ya daima wakati mwanamke anapopewa talaka vivyo hivyo ni lazima katika ndoa ya muda (Mut’a’). Mtu yeyote hana haki kumuoa ndoa ya Mut’a’ mwanamke aliyekuwa kaolewa ndoa ya muda na mtu mwingine kabla ya kumalizika muda wa eda yake. Yeyote atakayetenda kinyume chake basi mtu huyo atahukumiwa kuwa anafanya uzinifu.

Kwa kufuatana na mazingatio yaliyomo katika eda, basi katika hali kama hiyo hakuna kuchanganyikana ukoo na wala kizazi kupotea.

Baadaye mwandishi huyo anasema kwamba, “Ibnu Mais-Samai

119 Ibnu Mais-Samai na Khadimul Ulamaa, yote majina mawili hayo ni majina ya kubuni, na majina hasa ya waandishi hao hayajulikani. (Mtarjumi).

Page 148: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

141

hakupinga jambo hili lisilojulikana ambalo ndilo suala muhimu kwamba, Ikiwa mpita njia na mtu asiyejulikana kafunga ndoa ya Mut’a’ na mwanamke, na baada ya muda huyo mwanamke akazaa, kwa mujibu wa kauli ya Ibn Mais-Samaa ni kwamba mtoto huyo atamfuata baba yake, lakini mtoto huyo atampata wapi baba huyo ambaye hajulikani?”

Lakini yaonesha huyo Khadimul Ulamaa maneno yote na hoja zote alizozijibu Ibnu Mais-Samai hakuzisoma kwa mazingatio, na kama amezisoma kwa mazingatio basi hakufahamu maana na makusudio yake, kama si hivyo basi ni ubainisho gani utakaoweza kumuondolea tatizo hili? Hasa pale aliposema ndani ya ukurasa wa 112 kwamba “Ni wajibu kwa mume amtambue vyema yule mwanamke na yeye ajitambulishe vyema kwa mwanamke yule ili atakapozaa mtoto aweze kukutanishwa na naye kusudi nasaba hiyo isije ikapotea. Vile vile muda utapomalizika ni wajibu kwa mwanamke yule kukaa eda, ili ipate kujulikana kama ameshika mimba au la, na nia ni kumfahamu na kumjua sawa sawa mumewe hata kama akipata mtoto baada ya muda wa kunyonyesha amrejeshe kwa mtoto baba yake.

Ni lazima juu ya mwanamume atakaye kumuoa mwanamke fulani kwa ndoa ya Mut’a’, amfahamu na kumjua kwa ukamilifu hata akija kuzaa mtoto amuuganishe naye, na nasaba ihifadhike, vivyo hivyo kwa mwanamke ni lazima baada ya kwisha muda wa ndoa akae eda.” Baada ya hayo yote lilibakia jambo gani lisolojulikana alilodai mwandishi huyo?

Kwa hivyo ikiwa wewe mwandishi usiyejulikana hukuweza kufahamu ukweli uliowazi kama huo, basi hakuna njia isipokuwa badala ya kalamu tutumie sindano na kuyatia mambo katika bongo lako, huenda angalau ukazindukana na kufahamu!

Ama kuhusu usemi wako uliposema kwamba, “Mwasemaji enyi Mashia juu ya ndoa ya muda ambayo watabadilishana kwa zamu kiasi watu watatu, wanne, bali watu kumi kwa muda wa saa kadhaa kwa mwanamke mmoja!! Basi je mtoto huyo atakuwa ni wa nani?”

Kwanza ni lazima utuoneshe na kutaja hata kitabu kimoja tu

Page 149: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

142

ambacho kimeandikwa na licha ya wanavyuoni wa Ki-Shia hata mtu mmoja mjinga mpumbavu wa Ki-Shia, ambaye ameruhusu aina hii ya Mut’a’, na ikiwa hukuweza kutuonesha kitabu kama hicho au maandiko yatokanayo na Mashia, basi itabidi wewe utiwe adabu ya kisharia ya kusema uwongo na kuwasingizia watu.

Je! Kwani wewe hujui kwamba kwa Shia Imamiyah wote bila tofauti, mwanamke kukaa eda kwa katika ndoa ya Mut’a’ ambayo uchache wake ni siku arobaini na tano (45) ni lazima? Baada ya hayo kwa hali hii je, uko wapi utaratibu wa kwenda kwa zamu (kwa mwanamke mmoja) kwa muda wa saa kadhaa kama ulivyodai?

Na ikiwa makusudio yako ni kuhusu baadhi ya watu wajinga na wasioweza kujizuia, wazembe na wasiojali kutenda dhambi ambao jambo kama hilo linawezekana likatendeka miongoni mwao, hali kama hiyo haitawahusu wajinga waliomo katika jamii ya Kishia peke yake tu, bali huenda kwa wasiokuwa Mashia ndiyo zaidi kuliko hayo. Basi kwa maana hiyo kitendo kama hicho watendacho waasi, haipasi kukihalalisha kwa njia hiyo, kwani uhalali wa jambo hutegemezewa kwenye fatwa za wanachuoni wa Madhehebu husika na siyo kwa kutegemea waovu na waasi wa Madhehebu fulani. Na Mut’a’ kama hiyo uliyoieleza (yaani Mut’a’ ya masaa kadhaa) kitendo kama hicho kwa nadhariya ya wanavyuoni wa Kishia, jambo hilo halina tofauti kabisa na kuzini, kwa hivyo hukumu (adabu) ya zinaa lazima wapewe watu watendao hivyo, na mtoto atakayezaliwa ni haramu na hahusiani na yeyote katika hao. Na kama alivyosema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Al-waladu lilfiraash walil-a’hiril-hajar.” 120 Yaani Mtoto huunganishwa kutokana na mume na mke, na mtu mzinifu hana kitu isipokuwa jiwe!121

Ama kuhusu kujiepusha kwa Masharifu wa Ki-Shia wanaume wao na wanawake wao kutokana na ndoa ya Mut’a’, hali hiyo si kwa sababu ya ubaya na kuwa ati Mut’a’ si jambo jema, bali tabia hii ni namna moja ya unyoofu na kujitawala (kimaumbile) na kuridhika kwa wake wa ndoa ya daima, na juu ya yote hayo Uislamu umeruhusu kuwa 120 Kwa lugha na tafsiri ya Qur’ani, neno Firaash lina maana ya mume na mke na kila mmoja wao huitwa Firaash (Kifaa cha kulalia k.m. kitanda n.k.) (Mtarjumi).121 Sahih Bukhari juz: 5 uk. 192; Sunan Abi Dawuud juz: 2 uk. 282/2273; Sunan Ibn Majah juz: 2 uk. 647/2006 na 2007; Sunan Tirmidhi juz: 3 uk.463/1157.

Page 150: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

143

na wake zaidi ya mmoja, yaani wawili, watatu au wanne. Na kama wakitaka kufanya Mut’a’ ni jambo linalofaa kwao, kama ambavyo baadhi ya wenye mali na uwezo miongoni mwa viongozi wa makabila na wengineo wanalifanya jambo hilo. Kwa vyovyote vile kujizuwia kwa Masharifu kufanya Mut’a’, hiyo haiwezi kuwa ndiyo dalili ya kulifanya jambo hilo liwe ni lenye kuchukiza kisheria, licha ya kuwa haramu. Je, huoni kwamba Masahaba na Tabi’in walikuwa wakiwaowa Wajakazi na pia wakitamattui (wakiwaowa kwa ndoa ya Mut’a’) wanawake ambao imewamiliki mikono yao ya kuume, na kisha wakawazalia watoto wema? Na amma leo hii Masharifu hawapendelei tu kufanya jambo hilo pamoja na kwamba ni halali kwa mujibu wa maandiko ya Qur’an, kama ambavyo Mashrifu hao hao wanaonekana wazi kabisa kuwa ni watu wanaojiepusha mbali na tabia ya kutoa talaka kwa wake zao, kwani hatujapata kusikia kuwa Sharifu fulani kamuacha mkewe, lakini hali hiyo pia haiwezi kuwa ni dalili inayojulisha kwamba katika Uislamu ni haramu kutoa talaka.122

122 Hapa kuna jambo moja muhimu nalo ni kwamba, kwa masikitiko makubwa sana kikundi cha waovu na waasharati kwa kutokujua na kutojizuia, wanaitumia vibaya kanuni hii ya Kiislamu, kanuni ambayo imejengwa juu ya msingi na hukumu ya maumbile na mahitaji ya watu na jamii. Kanuni hii ikitumika kwa matumizi yake sahihi inaweza kuwa kama ni silaha ya kufaa yenye nguvu kwa ajili ya kupambana na uasharati na mambo mengi ya ufisadi ndani ya jamii. Naam, kanuni hii bora kama kanuni nyingi nyinginezo wanazitumia vibaya na kuzifanya kuwa ni njia za kutekeleza nia zao mbaya za uasharati na kutokujali bila ya kufuata sharia na kanuni zake. Mpaka sasa kila namna ya uovu na ukahaba unatendeka nyuma ya pazia hili la Mut’a’. Mambo yamefikia kiasi cha kuharibu maana halisi ya ndoa ya muda pamoja na sharti na kanuni zake zote. Imefikia pindi mwanamume mmoja mwasharati anapokutana na mwanamke muovu kwa kutamka sentensi moja bila kufahamu maana na kusudio lake na masharti yake hudhania wamefunga ndoa ya muda. Hapana shaka kwamba vitendo vya kinyaa na uchafu vya namna zote za kuaibisha huwa halali kwao kutokana na ujinga wa kutofahamu maana halisi ya ndoa hii. Vitendo hivyo vilivyopotoka vinavyotokana na kosa la kutokuzifahamu ipasavyo hukumu zinazohusu ndoa hii, vimekuwa ni ushahidi ulioko mikononi mwa watu wenye malengo na nia mbaya dhidi ya Uislamu, ili tu waendelee kutangaza na kueneza sumu. Kwa bahati mbaya sana hii imekuwa ndiyo sababu ya watu kuichukia ndoa ya muda au kwa jina lingine Mut’a’, kiasi kwamba Waislamu wenyewe hasa wale wasiofahamu kanuni za Kiislamu wanawake na wanaume wanaichukia ndoa hii na kuiangalia kwa jicho la dharau na pia kuiona kuwa ni kanuni inayomdhalilisha mwanamke.

Lakini sisi tunaosikitishwa sana na matumizi mabaya haya tunalo swali moja ⇒

Page 151: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

144

Amma kauli yako uliposema kwamba, “Ilikuwa inafaa sana kwa huyu Mwanachuoni Mkubwa Kashiful-Ghita ambaye amesimama kidete kutoa mafunzo yanayohusu Asili na Misingi ya Ushia, kwanza asimamie kurekabisha tabia ya wafuasi wa madhehebu hiyo na kuwafikisha wafuasi wake kwenye daraja ya utakatifu.” Hapana shaka kwamba, usemalo ni neno la haki, na neno la haki halina mabishano. Lakini inakupasa ufahamu kwamba, Mwanachuoni huyo mkubwa (Mwenyezi Mungu amzidishie baraka) siku zote na muda wote hajaacha kusimamia wajibu wake katika kutoa mafunzo na kuongoza, na si kuwaongoza Mashia peke yao tu, bali Waislamu wote ulimwenguni na wote hao mbele yake wako sawa. Lakini wajibu huu siyo kwake peke yake, bali ni wajibu pia kwa Wanavyuoni wengine wa Kiislamu. Na huenda wajibu huu ukawa na mkazo zaidi kwa Wanachuoni wa miji mikuu ya Kiislamu ambayo, ufisadi na utendwaji wa madhambi makubwa unafanyika hadharani tena kwa wingi mno. Kutokana na hali hii jukumu na wajibu wa Wanachuoni ni mambo ya lazima na muhimu sana. Sisi hatuna haja ya kuingia katika malumbano na gazeti hili la Al-Ii’tidal, vinginevyo tungenakili na kuweka wazi hali na mazingira ya makundi mengine ya Kiislamu hali ambayo ingesababisha kila mtu aone na afahamu kwamba, Mashia wa kwaida ukiachilia mbali Wanachuoni wao, ni watu wenye tabia ya kujiepusha na uovu, na ni Wachamungu tena wenye kujitakasa. Lakini kwa sababu ya muongozo anaotufunza Mwalimu wetu Allamah Kashiful-Ghita tumeepukana na tumejitenga na kila mabishano yenye kupelekea ubaguzi na machafuko makali ya ⇐ nalo ni hili: Je, tuseme kwa mfano kama kuna mtawala mmoja ambaye kutokana na madaraka aliyonayo kisheria akayatumia vibaya kwa kuujaza mfuko wake au akafanya maafikiano na watu fulani kuhusu mambo yake binafsi lakini kwa kutumia cheo chake, je suala la utawala liondolewe kabisa, au matumizi mabaya ya utawala ndiyo yakomeshwe? Au mhariri mmoja kwa ajili ya kujaza mfuko wake akatumia vibaya cheo chake cha uhariri na akawashawishi vibaya watu kuhusu mambo ya ndoa na kuleta ghasia za uwongo na mengineyo, je, maandishi yote ndani ya gazeti, na uenezaji wa habari nzuri zenye faida na za kuamsha fikara za watu yote haya yafutwe? Au jambo la lazima ni kumzuwia yule mwenye kufanya hivyo? Akili ipi, na ni hoja gani gani inayoruhusu kuzuwia kanuni na sharia zenye faida kwa sababu tu ya matumizi mabaya ya kanuni hizo? Je ni kwa ajili ya mtu mmoja tu asiyesali au watu mia wasiosali Msikiti hufungwa? Kwa ufupi makosa kama hayo kwa vyovyote hayataharibu hata kidogo uhalisi na matokeo yenye faida ya kanuni hizi za Kiislamu, kanuni hizo lazima zitumike na kutekelezwa kwa kuzuwia matumizi mabaya ya kanuni. (Mtarjumi).

Page 152: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

145

Kimadhehebu. Juhudi zetu ni kufuata maongozi yake katika njia ya kuleta umoja na kuziba mwanya ulioko kati ya umati wa Waislamu.

Kiongozi huyu mkubwa siku zote anatufundisha na kutufahamisha kwamba, Uislamu ni dini ya umoja, upendano na maelewano na siyo dini ya utengano na kuwa mbali mbali, kwani yeye anasema, “Maslahi ya Waislamu wa ulimwengu huu, yanategemea sana maelewano baina yao na kuondoa na kuing’oa kabisa mizizi ya ugomvi kati yao.” Hajaacha kutuusia pale aliposema, “Enyi Waislamu zitakaseni nyoyo zenu kutokana na kila aina ya nia mbaya, na ndimi zenu mzitakase kutokana na kauli za matusi, ugomvi, kubezana, makaripio na makinzano. Na kalamu zenu mziepushe kuandika maaandiko ya kusutana na kulaumiana ninyi kwa ninyi. Mkifanya hivyo mtafanikiwa na kuishi maisha ya Waislamu wa kweli, na hivyo ndivyo walivyoishi Wazee wenu waliokutangulieni, kwani wao walikuwa ni wakweli katika kauli zao, na ni wenye utakaso wa moyo katika matendo yao.

Ewe Khadimul Ulamaa! Hizi ndizo daraja za utakatifu, na wala siyo yale uliyotuletea wewe leo hii, kwani sisi tulidhani ya kwamba, mabishano na malumbano kuhusu ndoa ya Mut’a’ yamekwisha, na utata wa qadhia hiyo umekwishamalizika kutokana na majibu aliyoyatoa Ibn Mais-Samai. Cha ajabu ni kuwa, huyu aliyejiita Khadimul Ulamaa, iwe ni yeye binafsi anataka, au kutokujuwa kwake kunamshawishi, kwa mara nyingine tena anataka kulitimua vumbi la malumbano hayo na kuirejesha upya shari yake, na hatimaye aufunike ukweli kwa pazia. Lakini yampasa afahamu kwamba, ukweli siku zote ni nuru ambayo huchomoza katikati ya mapazia na vizuizi vinginevyo, na haikubali isipokuwa kuchomoza na kung’ara hata kama ni mbele ya mwalimu wa wajinga.”

MAELEZO KWA UFUPI

Kwa mukhtasari ni kwamba, ndoa ambayo ndiyo kiunganishi baina ya mwanaume na mwanamke, inazo athari maalum ambazo kupatikana kwake kunatokana na maafikiano makhsusi

Page 153: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

146

yanayotokana na matamko ya Iijāb na Qabul123 kwa kutekeleza sharti maalum. Ikiwa ndoa imetendeka bila ya kuainisha muda basi ndoa hiyo huwa ni ndoa ya daima, na haivunjiki isipokuwa kwa kupeana talaka na mfano wake. Lakini ukiainishwa muda k.m. siku moja, mwezi mmoja, mwaka mmoja, au zaidi, itakuwa ndoa ya muda tu si ya daima, walakini ifahamike kuwa, kwa maana ya mazingira ya mke na mume hakuna tofauti yoyote kati ya ndoa mbili hizi, tofauti iliyoko ni katika muda, ambapo moja ni ya kudumu na nyingine siyo ya kudumu. Wakati huo huo ni kwamba, ndoa mbili hizi zinashirikiana katika mambo mengi isipokuwa katika mambo machache tu, lakini tofauti hiyo si tofauti halisi bali ni kama tofauti ya jinsi au ya kuainisha, kama ilivyo tofauti kati ya taifa la watu weusi na weupe katika mambo mengi lakini asili yao ni moja.

Enyi Wanachuoni wa Kiislamu na enyi Waandishi, yana maana gani basi makelele mnayoyapiga, na ugomvi huu na kuitana majina mabaya na ususuavu mnaoufanya dhidi ya Shia kuhusu ndoa ya Mut’a’? Ndani ya maelezo haya pamoja na kuwa tumeyaleta kwa mukhtasari, je, yatakutoshelezeni ili muache uhasama na matokeo yake yapatikane maafikiano na kisha msalimu amri na kuifuata haki?

Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa heshima ya ukweli, yote niliyoyaandika sikuyaandika kwa chuki wala upendeleo, isipokuwa nimeyaandika kwa ajili ya haki na ukweli tu, na wala sikuwa mkali isipokuwa ni kwa ajili ya kupinga batili. Mwenyezi Mungu pekee Anatutosha na tunamtegemea yeye na tunageukia kwake na kwake ndiko kwenye marejeo.

Hebu na tutosheke na uchambuzi wa mambo yanayohusu mafungamano ya ndoa kwa kiasi hiki. Amma kuhusu ndoa inayowahusu Wajakazi na hukmu za Watoto watakaozaliwa, posho na namna za eda, unashiza na mengineyo, mambo hayo yamo ndani ya vitabu vya Wanachuoni wa Imamiyyah ambao katika vitabu hivyo wametoa maelezo kwa undani zaidi. Miongoni mwa vitabu hivyo, vipo ambavyo ni muhtasari tu uliokusanya ukamilifu wa somo la 123 Iijaab na Qabul ni matamko yanayotamkwa wakati wa maafikiano, k.m. katika ndoa, Namuozesha Fulani binti Fulani kwa mahari maalum, hii ni Iijab. Amma kusema, “Nimekubali kumuoa Fulani binti Fulani” hii ni Qabul.

Page 154: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

147

Fiqhi kuanzia mlango unaohusu Tahara hadi milango inayohusu hukumu za adhabu na fidia, kiasi cha vitabu hivyo kukusanya karatasi khamsini tu. Na kuna vitabu vingine ambavyo ni vikubwa, kama vile Al-jawahir na Al-hadaiq ambacho kimekusanya somo la Fiqhi kikiwa na Mijalladi ishirini (na kila Mjalladi mmoja) mfano wake ni sawa na Sahih Bukhari na Sahih Muslim. Si hivyo tu bali viko vingine kwa kiwango cha kati na kati, navyo ni vingi mno bila ya hesabu.

TALAKA WANAVYOONA SHIA

Hapana shaka kutokana na mazungumzo yetu yaliyopita hivi punde imekubainikia kuwa, hakika kuoana ni tamko linalobainisha kupatikana kwa mahusiano maalum yanayopatikana baina ya mke na mume, jambo ambalo humfanya kila mmoja kati ya wawili hawa awe ni sehemu ya mwenzake kutoana na maungamano hayo na mshikamano huo uliowabadilisha na kuwafanya kuwa ni watu wenye ushirikiano wa pamoja mfano wa ushirikiano wa macho mawili na mikono miwili pia masikio mawili. Yote haya hupatikana baada ya wawili hawa kuwa, hapo kabla walikuwa ni watu tofauti wasiyokuwa na maungamano kama hayo, lakini kule kuoana ndiko kuliko sababisha kupatikana kwa mvaano huo ambao hakuna tena mvaano zaidi kuliko huo. Kwa hakika haiingii akilini, bali hakuna namna nyingine inayoweza kufafanua ukweli na undani wa uhusiano huo wa mke na mume kuliko kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, “Wao wanawake ni nguo kwenu, nanyi ni nguo kwao.” (2:187). Kauli hii ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa dalili za kuonesha ufasaha na ushindi, bali ni namna ya pekee na ni uvumbuzi uliyomo ndani ya Qur’an. Nafasi hairuhusu kuorodhesha maana, siri za ubainishaji na maajabu yaliyomo katika Qur’an.

Pia neno hili limeshabainika kwamba wakati wa kuozeshwa kama hawakuweka sharti au muda, basi inajulikana kuwa ndoa hiyo ni ya daima hadi kufa, bali hata baada ya kufa isipokuwa itokee mambo yatakayosababisha kuuvunja uhusiano huo. Na kwa kuwa kuna mambo na mazingira ambayo husababisha kuvunja mahusiano hayo na hiyo ikawa ndiyo suluhisho baina ya pande mbili hizo au mmoja wao, kwa sababu hiyo basi sheria tukufu imeweka sababu na mambo

Page 155: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

148

kadhaa ambayo yakitokea itakuwa ndiyo njia ya kukata kamba iliyowaunganisha na kisha kuutenganisha mshikamano huo.

NAMNA MBALIMBALI YA KUVUNJA NDOA

Mara nyingi hutokea mambo yasioepukika, na kwa hali yalivyo hulazimika kuvunjika kwa ndoa hiyo. Kuna namna nyingi za Talaka: -

(a) Pande zote mbili (mume na mke) wanataka kuachana.(b) Upande mmoja tu unashikilia kuvunja ndoa.

Kwa hivyo katika kanuni za Kiislamu zimewekwa njia kwa ajili ya mambo haya, kutokana na njia hizo munaweza kuachana na kuvunja ndoa.

Ikiwa chuki ya kutoendelea na ndoa inatokana na mume tu, basi mamlaka ya kutoa Talaka yamo mikononi mwake. Na ikiwa chuki inatokana na mke tu, basi naye anayo mamlaka ya kujitoa katika ndoa, na ikiwa chuki inatokana na pande zote mbili basi wao ndiyo wenye mamlaka ya kuachana. Na kila moja katika hali hizo za talaka inazo hukmu zake na maeneo ambayo mipaka yake haivukwi na wala hakisimami kitu kingine mahala pake.

Kwa kuwa dini ya Islamu ni dini ya jamii na imewekwa juu ya misingi ya umoja na upatanishaji, na lengo lake muhimu kabisa ni kuleta upendano na upatano kati ya watu, bali si hivyo tu, ni lazima ieleweke wazi kuwa Uislamu unachukia mno mambo yanayosababisha ugomvi na utengano. Kwa ajili hiyo basi zimekuja riwaya nyingi zinazojulisha juu ya ubaya wa kutengana na kukata mawasiliano, pia zinajulisha juu ya kulizuwia jambo hilo lisitokee. Ndani ya baadhi ya riwaya hizo ziko zinazosema kwamba, “Hakuna halali yoyote ile ambayo ni yenye kuchukiza mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko Talaka.”124

Kutokana na ubaya wa tendo hilo la kuachana, hapo ndipo ilipokuwepo haja kwa waja wa Mwenyezi Mungu kupewa mwan-ya na njia ya kutafakari (kabla ya kuamua kuachana) kwa mujibu

124 Taz: Al-Kafi juz: 6 uk. 54.

Page 156: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

149

unaokubalika katika namna ya sheria za ndoa, ikiwemo hekima zake pia huruma (baina ya wawili hao). Yote hayo ni katika kuwaongoza waja wa Mwenyezi Mungu na kuwaonesha ni jinsi gani hawafahamu matokeo ya maamuzi yao pale Mwenyezi Mungu aliposema, “Basi huenda mkakichukia kitu na kumbe Mwenyezi Mungu ametia heri nyingi ndani yake.” (4:18). Maneno yote haya ya Mwenyezi Mungu lengo lake ni kutoa tahadhari na kuzuwia tendo la talaka, na yanawaamrisha watu kuwa na mazingatio katika suala zima la kuachana.

Kwa kulizingatia lengo hilo, Mola Mtukufu ameweka sharti nyingi kuhusu Talaka, ambazo nia yake na madhumuni yake ni kupunguza Talaka, kwani kila jambo lenye sharti na mipaka mingi jambo hilo huadimika likawa si lenye kupatikana mara kwa mara.

Miongoni mwa sharti muhimu kwa upande wa Shia ni kupatikana na kuhudhuria mashahidi wawili waadilifu wakati wa kuisoma Talaka hiyo, kama inavyoamrisha Qur’ani Tukufu: “Na muwashuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.” (65:2).

Kwa hivyo ikiwa imetangazwa Talaka bila kuwapo mashahidi wawili, talaka hiyo kwetu si sahihi ni batili. Sharti hiyo kwa hakika ni njia ya kuondoa kabisa chuki ya wao kwa wao na kuleta mapatano, kwa sababu ni dhahiri waadilifu juu ya kuwa maneno yao yana nguvu na kuathiri (kuleta matunda) kwa watu, wao vile vile wanatambua kwamba wanajukumu la kupatanisha kati ya watu wawili na kuwanasihi mke na mume ambao wanaachana na kuwafanya warudiane.

Naam, si lazima kuwa katika kila tukio juhudi zao zitaleta matunda, lakini kwa kiasi hicho lazima tukubaliane kwamba kwa njia hii jambo hilo la Talaka kwa kiasi cha kutosha litapungua.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona ndugu zetu wa Ki-Sunni wamenyimwa faida hiyo kubwa kwa sababu wanavyuoni wao hawakuweka sharti ya kuwapo mashahidi wawili waadilifu wakati wa

Page 157: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

150

kutoa talaka. Hii ina maana kwamba kwa upande wao hekima hii na falsafa hii ya kisheria kwao wao vimepotea, kwani hawakuweka sharti ya kuwepo mashahidi wawili waadilifu wakati wa kutolewa Talaka. Na kwa sababu hiyo kwa Masunni Talaka ni nyingi mno na umekuwa ni msiba mkubwa mno kwao.

Kwa bahati mbaya watu wengi miongoni mwetu na wao Masunni wameghafilika kutokana na kanuni za Kiislamu na hekima zake, na lau ingalikuwa tumefanya bidii na kuzifuata tungelikuwa tumefaidika kwa kila upande, na tusingalitumbukia katika maisha ya taabu na kupatikana na kila namna ya mateso, kiasi cha kuharibika kwa nidhamu ya ukoo ndani ya majumba mengi. Moja katika sharti muhimu kabisa za Talaka ni kuwa mume kwa kushurutishwa na kukalifishwa au katika hali ya ghadhabu na machafuko ambayo fikra zake sawa zimemtoka, hajifahamu, basi asifanye jambo hilo (asitoe talaka), na vivyo hivyo mwanamke anayeaachwa asiwe katika hali ya hedhi awe ameshasafika, na baada ya kusafika asiwe ameingiliwa na mumewe. Ni dhahiri kabisa mipaka kama hiyo itasaidia katika kupunguza Talaka.

Wanavyuoni wa Kishia wote wanaafikiana kwamba, Talaka tatu (kutangaza talaka tatu katika kikao kimoja) ni sawa na talaka moja, kwa hivyo mke hawi haramu kwa mumewe, bali anaweza kumrejea wala hakuna haja ya Muhal-lil.125 Lakini lau atamrejea kisha akamtaliki namna hiyo mara tatu hapo mke huyo si halali tena, isipokuwa aolewe na mume mwingine (ambaye kisharia huitwa Muhal-lil) na akitalikiwa na huyu mume ndiyo yule mume wa kwanza ataweza kumuoa baada ya kwisha eda.

Ikiwa mambo ya kupeana talaka yataendelea mara tisa na kila baada ya talaka tatu akaolewa na mume mwingine hapo tena mke huyo huwa haramu moja kwa moja kwa mumewe huyo wa kwanza kwa njia yoyote hawi halali tena.

125 Muhal-lil ni yule atayemuoa mke yule baada ya kuwa alikwisha kuwa ni haramu kuolewa na yule mume wa kwanza aliyemuacha talaka tatu, yaani huyu mume wa pili naye akimuacha mke huyu, basi huwa amesababisha imhalalikie yule mume wa kwanza amuoe tena mke huyo.

Page 158: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

151

Wanavyuoni wa Kisunni wengi wao wanahitilafiana nasi katika hukumu hii, wao talaka tatu katika kikao kimoja wanaruhusu kuwa ni talaka tatu, kwa hivyo mume akimwambia mkewe, “Wewe ninakupa talaka tatu.” Mke huyo kwa itikadi yao anakuwa haramu na bila Muhal-lil hawezi kumuoa tena, ijapokuwa katika vitabu vyao vyenye kutegemewa kama Sahih Bukhari imeelezwa kwa sanadi kutoka kwa Ibn Abbas wazi wazi kuwa, talaka tatu katika kikao kimoja ni moja tu na hadithi yenyewe ni hii: Katika zama za Mtume (s.a.w.w.) na Abu Bakr na miaka miwili katika zama za Umar, talaka tatu (katika kikao kimoja) ikihesabika moja tu, lakini Umar akasema, “Hakika watu wamekuwa na pupa ya kufanya jambo ambalo hapo kabla walikuwa na subira, basi lau tutalipitishia hukmu juu yao, kisha akapitisha hukmu juu yao.”126 Yaani watangaze kuwa talaka tatu katika kikao kimoja ni tatu.127

Tukiangalia Qur’ani Tukufu tutaona jambo hilo liko wazi kwa mtu anayefanya mazingatio (kuwa talaka tatu katika kikao kimoja ni jambo lisilowezekana). Mwenyezi Mungu anasema, “Talaka ni mara mbili, basi imma kukaa kwa wema au kuachana kwa wema.” Aya inaendelea hadi pale Mwenyezi Mungu anaposema, “Na kama amempa talaka (ya tatu), basi (mwanamke huyo) si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwingine.” (2:229/30).128

Kwa ujumla hizi ni miongoni mwa sababu za kutengana (mume na mke), lakini ufafanuzi zaidi unapatikana katika maeneo yanayohusika. Kuna sababu nyinginezo zinazosababisha mume

126 Hadithi hii sikuiona ndani ya Sahih Bukhari, bali nimeikuta ndani ya Sahih Muslim juz: 2 uk. 1099/15, na katika Musnad ya Imam Ahmad ibn Hambal juz; 1 uk. 314.127 Labda kwa sababu hiyo ndiyo maana Mufti mkubwa wa zamani wa Al-Azhar na mwanachuoni mashuhuri wa Ki-Sunni Sheikh Mahmood Shal-Toot alikubaliana na itikadi ya Shia kuwa talaka tatu katika kikao kimoja ni batili. (Mtarjumi).128 Mwanzo wa aya inabainisha waziwazi kwamba talaka ambayo baadaye waweza kumrjea mke wako ni talaka mbili, baada ya moja wapo ya kila talaka hizo mume anaweza kumrejea mkewe akitaka. Na mwisho wa aya yaonesha kuwa, baada ya talaka ya tatu hairuhusiwi tena kumrejea, kwa hivyo jumla za aya hizo za mwanzo na za mwisho zinafahamisha kwamba, Talaka tatu hutendeka katika vikao vitatu kati ya kuacha na kurejea na si kimoja. (Mtarjumi).

Page 159: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

152

na mke kutengana, k.m. aibu fulani itokanayo kwa mume inayolazimisha kuvunja ndoa, kama vile; wazimu, uhanisi, ukoma n.k. Na kwa mke kama Ritq na Qirn129 na mengine kama hayo.130 Pia ‘Zihaar’ na Iilaa’ ambazo maelezo yake yanapatikana katika vitabu vya Fiqhi humo utapata ufafanuzi wa eda zenyewe na vigawanyo vyake, ikiwemo eda ya talaka, eda ya kufiwa na mume, eda ya Wat’ush-Shubha na Milkul-yamini131. Kwa mujibu wa Shia, Eda ya kufiwa na mume ni faradhi kwa mke kukaa eda hiyo hata kama atakuwa ni Yaaisah au Saghiirah au Ghair Mad-Khoolumbihaa.132

Ama eda ya talaka eda hiyo huwa ni lazima isipokuwa kwa hawa watatu.133 Kufa kwa mume na kumwingilia mwanamke asiyekuwa mkewe kwa kudhania kuwa ni mkewe pia eda ni faradhi isipokuwa kwa Yaaisah, na Saghiirah. Ama tendo la uzinifu hilo halimuwajibishii mwanamke huyo kukaa eda kwa sababu maji ya mtu mzinifu hayana thamani wala heshima yoyote katika sheria ya Kiislamu. Eda ya mwenye kufiwa na mume ni miezi minne na siku kumi kama mke huyo hana uja uzito, na akiwa mjamzito eda yake itamalizika kwa kujifungua.134

Eda ya talaka kwa mwanamke asiyepata siku zake, (lakini yuko kwenye umri wa kupata siku zake) ni miezi mitatu kamili, na yule mwenye kupata siku zake, ni lazima baada ya talaka aone hedhi mara tatu na kusafika. Na eda ya mke mwenye mimba baada ya talaka, akizaa tu eda humalizika (Ikiwa muda ni mrefu au mfupi).129 Ni aina fulani ya maradhi yanayowahusu wanawake.130 Kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kila mmoja kati ya pande hizi mbili akigundua moja wapo miongoni mwa maradhi hayo kwa mwenziwe anayo haki ya kuivunja ndoa. (Mtarjumi).131 Mjakazi132 Yaaisah ni mwanamke ambaye amefikia umri wa kutokuzaa, na kwa mujibu wa Shia ni miaka hamsini, isipokuwa mwanamke huyo awe anatokana na ukoo wa Bani Hashim ambao ukomo wao wa kuzaa ni miaka sitini. Saghiirah ni mtoto wa kike asiyefikia miaka tisa, na Ghair Mad-Khoolumbihaa ni mwanamke ambaye ameolewa lakini bado mume hakumwingilia. (Mtarjumi).133 Anakusudia hawa wafuatao: Yaaisah, Saghiirah na Ghair Mad-Khoolumbihaa. 134 Ikiwa atajifungua ndani ya kipindi cha miezi minne na siku kumi, basi eda yake itamalizika baada tu ya kujifungua ndani ya kipindi hicho, na kama atajifungua baada ya kipindi cha miezi minne na siku kumi, basi eda yake itamalizika wakati atakapojifungua. (Mtarjumi).

Page 160: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

153

Ikiwa talaka haikutokea mara tatu, na pia hakupewa talaka ya Khula, basi katika muda wa eda anaruhusiwa kumrejea mkewe, lakini ikiwa muda wa eda umekwisha na hakumrejea, basi hapo tena hana haki ya kumrejea kwa kuwa maamuzi yote hubakia katika mamlaka yake huyo mwanamke, na ikiwa atapenda awe mkewe tena kwa mara nyingine, hakuna njia nyingine isipokuwa afunge naye ndoa upya (kwa makukubaliano ya pande zote mbili).

Kwetu sisi Shia, kuwepo mashahidi wawili wakati wa kurejeana mume na mke si faradhi kama ilivyo faradhi wakati wa kutoa talaka, ijapokuwa ni Sunna.135 Vile vile si faradhi kutamka maneno mahsusi

135 Mwaka huu wa 1355 A.H, Mwanachuoni aitwaye Al-Ustaadh Ahmad Muhammad Shakir Qadhi wa Sharia wa Misri alinizawadia kitabu chake chenye thamani kiitwacho, Nidhamut-Talaqi Fil-Islam. Kitabu hicho kilinipendeza mno na nikaona kuwa ni kitabu kimoja miongoni mwa vitabu bora katika zama hizi. Mimi nilimwandikia barua mtungaji wa kitubu hicho, na yeye akaichapisha barua hiyo niliyomuandikia ndani ya gazeti la Ar-risaalah katika toleo la 157 baada ya utangulizi ameandika hivi kuhusu barua yangu: “Miongoni mwa barua tukufu na zenye heshima kubwa, ni hii barua niliyoipata kutoka kwa Sahibu Mtukufu na Mwalimu wangu mkubwa ambaye ni kiongozi wa Mujtahadiin (Wanavyuoni) wa Ki-Shia katika mji wa Najaf nchini Iraq, aitwaye Al-Allamah Sheikh Muhammad Husain Aalu Kashiful-Ghitaa. Yeye ameyajadili maoni yangu katika moja ya Mas’ala miongoni mwa Mas’ala yaliyomo ndani ya kitabu hicho (Nidhamut-Talaqi Fil-Islam). Mas’ala hayo yanahusu Sharti la kuwepo mashahidi wakati mume anataka kumrejea mkewe aliyemtaliki ili kurejea huko kuwe ni sahihi. Mimi kwa upande wangu nimeona kuwa, ni sharti wawepo mashahidi wawili wakati wa kutolewa talaka na kama talaka itatolewa bila ya kuwepo mashahidi wawili, basi talaka hiyo haitakubalika na wala haitazingatiwa. Kwa hakika kauli hii (Niliyoisema mimi) japokuwa iko kinyume kabisa na ilivyo kwa upande wa madh-hebu manne, lakini inaungwa mkono na dalili za kisharia zilizopo na pia inaafikiana na Madh-hebu ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na Mashia Imamiyyah. Juu ya hayo mimi nimeona pia kwamba, ni sharti mashahidi wawili wawepo wakati mume anapotaka kumrejea mkewe aliyemtaliki, kwani mtazamo huu unaafikiana na moja kati ya kauli mbili za Imam Shafii lakini iko kinyume na Madh-hebu ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na Mashia Imamiyyah.

Mimi nilishangazwa mno na kauli ya Mashia kuhusu mambo haya kwa kuwa wao wanatenganisha baina ya mambo hayo mawili wakati dalili ya mambo yote mawili ni moja.

Kwa hivyo Ustadh Kashiful-Ghitaa aliona ni jambo jema kunifafanulia mtazamo wa Shia juu ya kuyatofautisha mambo haya mawili na katika barua yake ⇒

Page 161: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

154

⇐ aliniandikia kama ifuatavyo:-Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Utukufu ni wake Mwenyezi Mungu na sifa zote njema ni zake.

Barua ya tarehe 8 mwezi wa mfunguo tano mwaka 1355 kutoka Mji Mtukufu wa Najaf kwenda Misri.

Kwako Mheshimiwa Al-Ustadh Al-Allamah Sheikh Ahmad Muhammad Shakir, Mwenyezi Mungu akuimarishe. Nakuombea amani ya Mwenyezi Mungu ikushukie. Zawadi yako yenye thamani kubwa ambayo ni Kitabu ulichonitunukia kiitwacho Risalatu Nidhaamit-talaaq fil-Islam nimekipata. Nimekisoma mara mbili tena kwa mazingatio na kupendezewa mno kutokana na maana na fikara nyoofu zilizomo zilizofanyiwa utafiti wa kina. Si hivyo tu bali, umeonesha uhuru wa mawazo unaopelekea kwenye lengo na haki.

Hapana shaka kwamba, katika kitabu hiki umebainisha kiini na uhakika wa hadithi tukufu, na umeziondoa pazia za mawazo ya kudhania kwenye uwanja mtukufu wa sheria. Kwa kutumia dalili mkato na hoja nzito, umeikata minyororo ya kuiga kubaya, na kuyabomoa mapango ya fikra zilizogandamana. Nakupa heko, na ninazipongeza fikara zako zenye kung’ara na mema yako mengi. Katika kitabu chako umezungumzia mambo matatu (1) Talaka tatu (2) Al-hilfu bit-talaaq wal- Itaaq na (3) Mashahidi wa kushuhudia Talaka.

Kila moja katika mambo hayo matatu umelizungumzia vizuri mno kwa kulitimizia haki yake kutokana na uchunguzi ulioufanya. Kwa hakika umefungua mlango wa Ijtihaad sahihi kwa mujibu wa kanuni za elimu na ufahamu wa uchambuzi kutokana na Kitabu (Qur’an) na Sunna. Hali hiyo imekufikisha kwenye muongozo imara wenye mafanikio na asili ya hukumu ya Mola na maamrisho ya dini ya Kiislamu. Maoni yako mazuri katika Mambo haya matatu, hapana shaka kwamba yanakubaliana na kile ambacho Mashia Imamiyyah wanakubaliana kwa pamoja tangu hapo mwanzo wa Uislamu hadi leo, na hawatofautiani wawili miongoni mwao juu hayo, kiasi kwamba kwao wao hayo ni miongoni mwa mambo ya Dharuriyyaat. (Mambo ambayo mwenye kuyakanusha huwa kakanusha misingi ya dini k.m. Sala, Hijja, Saumu Zakka n.k.)

Vile vile Mashia wanakubaliana juu ya kuwa, siyo lazima kuwepo mashahidi wakati wa kurejeana mume na mke, wakati ambapo wanakubaliana juu ya ulazima wa kuwepo mashahidi wakati wa kutoa talaka, bali kwao wao talaka isiyokuwa na mashahidi (wawili waadilifu) ni batili haitambuliwi. Lakini kwako wewe umetilia mkazo juu ya ulazima wa mahudhurio ya mashahidi katika sehemu zote mbili (yaani wakati wa kutoa talaka na wakati wa kurejeana) na katika uk. 120 umesema hivi, na ninakunukuu: “Mashia wanaona kuwa ni lazima wawepo mashahidi katika Talaka na kwamba hilo ni nguzo mojawapo katika nguzo za Talaka kama ilivyoandikwa katika kitabu (chao) kiitwacho, Sharaiul-Islami na wala ⇒

Page 162: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

155

⇐ hawakulifanya jambo hilo kuwa ni lazima wakati wa kurejeana. Lakini kuitofautisha hukmu hii kati ya mambo haya mawili ni jambo la ajabu na wala hakuna dalili inayoruhusu kutofautisha.” Mwisho wa kunukuu.

Mimi nakuombea Mwenyezi Mungu akubariki, lakini kuhusu maneno yako haya kuna haja ya kuyafanyia uchunguzi na ninakuomba radhi na kukutaka idhini nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo; Katika mambo ya ajabu na ya kushangaza mno kwa mujibu wa misingi ya elimu, ni kumtaka mkanushaji alete ushahidi wakati yeye tayari kisha shika msingi, bali kilichopo ni juu ya yule anayethibitisha (mdai) kuleta dalili na uthibitisho wa madai yake.

Huenda wewe ukasema kwamba, “Tayari imekwisha simama dalili dhidi yake (yaani mdaiwa) nayo ni dhahiri ya aya.” Kama ulivyoeleza katika uk.118 uliposema kuwa, “Kinachoonekana wazi katika mfumo wa aya hiyo ni kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.” (65:2). Basi kauli hiyo ya Mwenyezi Mungu inarejea kwenye mambo yote mawili, yaani Talaka na Kurejea. (Kwa hivyo mahudhurio ya mashahidi wawili katika mambo yote mawili ni lazima.)”

Lakini yaonesha kuhusu jambo hili wewe hukufanya uchunguzi wa kina katika aya hizo, kama ilivyo kawaida yako katika mambo mengine ulivyoyachunguza kwa undani, vinginevyo jambo kama hili lisingefichikana kwako, kwa sababu sura tukufu hiyo yote (mwanzo hadi mwisho) inazungumzia hukumu za talaka na kwa sababu hiyo pia ikapewa jina la: Suratut-Talaq, (yaani Sura inayozungumzia mambo yanayohusu Talaka). Mwanzo wa maneno katika sura hiyo yameaanzwa na aya isemayo: Idhaa Tallaqtumun-Nisaa, (yaani Mtakapotoa talaka kwa wanawake). Baadaye inazungumzia kuhusu kanuni ya talaka na imeanzia na eda, maana yake talaka isitolewe wakati mwanamke yupo katika hali ya hedhi wala anapokuwa amesafika na hedhi (katika muda wa usafi huo) isiwe mume alimwingilia (iwe baada ya kusafika kwa mke na kabla ya kuingiliana). Baadaye (sura hiyo) yazungumzia ulazima wa kuweka hisabu ya eda na kutomtoa mwanamke nyumbani katika pindi ya eda.

Baada ya kueleza hukumu hizo, imeashiriwa kuhusu jambo la marejeo, lakini pasipo shaka ishara hiyo si lengo hasa la aya bali ndani ya maongezi ya talaka jambo la marejeo limekuja, ikasema hivi: Wanapofikia muda wao, basi wawekeni kwa wema. Maana yake ni kwamba, wanapokaribia kumaliza eda, ni juu yenu mnaweza kuwa rejea, au kuachana nao kwa wema pindi eda yao itakapomalizika. Kisha Qur’an inarudia kukamilisha hukmu za talaka kwa kusema hivi: “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.” Yaani kuhusu talaka ambayo ni kiini cha mazungumzo si kwa (marejeo) kwa sababu (marejeo) yameandamana tu na hukmu ya talaka. Kwa mfano, ikiwa umeambiwa, “Akikujia Mwanachuoni ni lazima juu yako kumheshimu, kumkirimu na kumpokea, awe amekuja peke yake au kafuatana na mtumishi au rafiki yake, na ⇒

Page 163: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

156

⇐ inakubidi pia umshindikize na kumuaga kwa heshima.” Hapana shaka kwamba, kutokana na maneno haya wewe hutafahamu isipokuwa kuwajibika kwako kumshindikiza na kumuaga yule Mwanachuoni tu na wala siyo mtumishi wake na rafiki yake.

Kwa vyovyote vile, jambo hili kwa mujibu wa kanuni za lugha ya Kiarabu na ufasaha wake sahihi ambao uko bayana sana, halikuwa ni jambo la kufichikana kwa mtu kama wewe ambaye ni bingwa wa lugha na ufasaha wa Kiarabu, isipokuwa yamekutokea hayo kwa sababu ya kughafilika tu wala hakuna ajabu kwa sababu pengine mghafla hupata ukamshika mwanachuoni pia. Maelezo hayo ni kwa mujibu wa dalili ya matamko yaliyomo ndani ya aya na mfumo wa aya tukufu ulivyo. Pamoja na hali hiyo, kuna mambo mengine yenye maana ya ndani zaidi na yanastahiki kufanyiwa mazingatio, hasa kutokana na hekima za sharia na falsafa ya Uislamu iliyomo katika mambo yake kama ifuatavyo: Hakuna shaka kwamba, katika mambo ya halali, talaka ni kitendo chenye kuchukiza mno mbele ya Mwenyezi Mungu, na dini ya Kiislamu kama tujuavyo ni dini kamili ya kijamii ambayo kwa vyovyote hairidhii na kupendelea namna yoyote ya utengano na mfarakano katika ya jamii ya Kiislamu, na hasa kwa watu wa nyumba moja au familia moja, na zaidi hasa baina ya mke na mume. Kwa hivyo basi, makusudio ya Mwenyezi Mungu na Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) kwa mujibu wa hekima ya hali ya juu, ni kuzipunguza talaka na mifarakano kwa kiwango kikubwa. Na ili kulikamilisha lengo hili, zimewekwa sharti na vikwazo vingi ili kuwe na uzito na ugumu katika kulitenda, ili yote hayo yaweze kupatikana, kwa kupitia kanuni maarufu isemayo kwamba, “Vikwazo vinapokuwa vingi kuhusu jambo fulani, basi jambo hilo huwa gumu kutendeka.”

Kutokana na hali hiyo, yamewekwa mazingatio makubwa juu ya mashahidi wawili waadilifu ili kwanza kuidhibiti hali ya mazingira ya talaka, pili upatikane ucheleweshaji wa kutoa talaka. Na kutokana na mambo hayo mawili itapatikana nafasi ya kuhudhuria mashahidi hao wawili, pia mke na mume au mmoja kati yao (na baada ya mashauriano) huenda wakajutia maamuzi yao ya kutaka kuachana, kisha watarudia uhusiano wao wa mapenzi baina yao kama inavyosema kauli ya Mwenyezi Mungu, “Hujuwi ya kwamba, labda Mwenyezi Mungu atatoa jambo jingine baada ya haya.” Hekima hii ya kuwazingatia mashahidi wawili (katika talaka) ni ya hali ya juu mno, na hapana shaka Mwenyezi Mungu ameiweka kwa lengo lililokwisha tajwa hapo kabla na kwa faida nyinginezo nyingi.

Ndiyo maana basi, suala la talaka haliko sawa na suala la kurejea, kwa kuwa Mwenyezi Mungu (katika suala la kurejea) anataka lifanyike haraka, kwani kulichelewesha kunaweza kusababisha maafa, na kwa ajili hiyo hakuweka ulazima wa sharti yoyote ile katika kumrejea mke. Kwetu sisi Mashia inafaa (na inatosha) kufanya jambo lolote lile litakalojulisha maana ya kumrejea, ikiwa ni kauli, kitendo au ishara. Hapana sharti yoyote ile ya kuwepo matamko maalum katika kurejea kama ilivyoshartiwa kwenye talaka. Wawili (katika talaka) ni ya hali ya juu mno, ⇒

Page 164: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

157

⇐ na hapana shaka Mwenyezi Mungu ameiweka kwa lengo lililokwisha tajwa hapo kabla na kwa faida nyinginezo nyingi. Yote hayo yamefanywa hivyo kutokana na Mwenyezi Mungu ambaye ni mwenye huruma kwa waja wake kupenda kulifanyia jambo hilo wepesi wa kutimia kwake, kadhalika upendo wake wa kuwaunganisha (mume na mke) ili wasitengane.

Sasa basi, ni kwa nini ishara na kumgusa mke (aliyeachwa talaka rejea) na kuweka mkono juu ya mwili wake kwa nia ya kumrejea isitosheleze kuwa ni dalili ya kumrejea? Kwetu sisi Mashia, mke (aliyepewa talaka rejea) huhesabiwa kuwa bado ni mke halali mpaka atakapotoka ndani ya eda, na kwa ajili hiyo anakuwa na haki ya kumrithi mume, kama ambavyo mume naye anakuwa na haki ya kumrithi mke, pia kumkosha mumewe na mume kumkosha mke (iwapo mmoja kati yao atafariki), istoshe mume hubakia na wajibu wa kumlisha mke huyo, na mume haruhusiwi kumuowa dada wa mwanamke huyo, na wala hawezi kuowa mke wa nne (kuziba pengo la huyu aliyeko katika eda), na hukmu nyinginezo zinazohusu mambo ya mke na mume.

Je! kutokana na haya tuliyoyaeleza umetosheka na itikadi ya Shia kwamba hakuna lazima ya kuwepo mashahidi katika kumrejea mke, na kuwa sharti hilo ni faradhi wakati wa kutoa talaka?

Ikiwa hizo dalili umekubaliana nazo, basi twamshukuru Mwenyezi Mungu na wewe pia, na kama si hivyo basi kwa furaha kuu tupo tayari kuyatalii (kuangalia) maoni yako juu ya mazungumzo hayo na hatuna nia isipokuwa kupata ukweli na kufuata haki popote ilipo na kwa kuyatupilia mbali maigo ya wapumbavu, nasi hatuna ushupavu wa dini wa kijinga, bali tunamuomba Mwenyezi Mungu Atulinde sisi na nyinyi kwa hayo na Atuhifadhi tusiende kwenye njia ya uptovu na Atuweke kwenye njia ya ukweli.

Na tunamuomba Mola Akupe mafanikio kwa ajili ya kazi kama hizi zitakazodumu daima na ziwe makumbusho baada yako: Anasema Mwenyezi Mungu, “Na vitendo vizuri vibakiavyo ni bora mbele ya Mola wako kwa malipo na matumaini mema.” (18:46)

Kwa kumalizia pokea salamu kutoka kwa nduguyo:Muhammad Husain Aalu Kashiful-Ghitaa.

Maelezo: Miongoni mwa mambo uliyoyafanyia uchunguzi na uchambuzi mzuri, ni hili suala la kutokusihi talaka kwa mwanamke mwenye hedhi. Kwa hakika nimeichekecha kwa uzuri hadithi ya Abdallah ibn Umar. Wanavyuoni wote wa Imaamiyah wamekubaliana kuhusu fatwa hii ya kwamba, mwanamke mwenye hedhi (katika kipindi cha hedhi) akipewa talaka basi talaka hiyo ni batili, isipokuwa katika baadhi ya maeneo maalum (ndiyo huruhusiwa). Hii ilikuwa ni barua halisi ya Mwanachuoni bingwa wa sheria, mimi sikuondoa chochote (katika maandiko yake) isipokuwa neno moja tu ambalo halina uhusiano na maudhui hii bali ⇒

Page 165: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

158

wakati wa kurejeana, bali neno au kitendo au ishara yenye kuonesha upendo wa mume kuendelea na mke yule inatosha na kwa kufanya hivyo peke yake huwa ni sababu ya kurejesha uhusiano wa mume na mke.

AL-KHUL-A’H NA MUBĀRĀT

Hakuna shaka fungamano kati ya mume na mke halitenguki isipokuwa pande zote mbili au mmojawapo aoneshe chuki kwa mwenziwe. Kwa kawaida hii ndio huwa sababu ya wawili hawa kuachana.

Ikiwa chuki yatokana na mume tu, basi talaka ipo mikononi mwake, anaweza kujiepusha na mke kama akitaka kufanya hivyo, na ikiwa chuki inatoka kwa mke dhidi ya mume, basi itampasa mke kutoa kiasi cha mali ya kujikomboa nafsi yake, ni sawa iwapo kiwango hicho kitalingana na kile alichotoa mume kumpa mke (mahari) au zaidi. Baada ya hapo mke huachika kutokana na thamani ya kile alichokitoa na tendo hili huitwa Al-khala’, na litatimia hilo kwa yule mume kusema “Fulani (ataje jina la mke) ameachika kwa kile alichokitoa kwani yeye ni Mukh-taliah.” Yaani amejikomboa.

Ni sharti zipatikane zile sharti zote zinazohusu Talaka, ukiongezea na hii sharti ya mke kwamba ile chuki (ya kutopendelea kuendelea ⇐ linahusu tunzo la vitabu alivyonitunukia. Mimi nitajaribu kubainisha mtazamo wangu hapo baadaye na nitamjadili Mwalimu wangu kuhusu yale aliyoyaona na kuyateua kwa kiwango cha juhudi zangu zitakapofikia katika toleo lijalo Mwenyezi Mungu akipenda. Ahmad Muhammad Shakir, Kadhi wa Sharia.

Huu ndiyo ukamilifu wa kile alichokichapisha Mheshimiwa Kadhi Ahmad Muhammad Shakir katika lile toleo la gazeti, kisha alifuatishia katika toleo la 159 na toleo la 160 kuendeleza mazungumzo yaliyopita katika matoleo hayo mawili. Yeye katika matoleo yote mawili alijaribu mno kutia nguvu nadharia yake kwa kila namna nasi kwa upande wetu tukayajibu, na kwa vile sisi tangu hapo mwanzoni tuliazimia kitabu hichi kiwe kwa muhtasari, basi tumeacha kunakili hoja zake na majibu yetu.

Wanaotaka kuayaangalia wanaweza kufanya hivyo kwa kuyapata matoleo yote ya gazeti hilo. Humo watapata faida nyingi kutokana na mazungumzo yaliyomo, kwa vyovyote sisi lengo letu la mwisho ni kuudhihirisha ukweli.

Page 166: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

159

na ndoa) iwe imetoka kwake. Zaidi ya hayo, inatakiwa ile chuki ya mke huyu iwe ni ya hali ya juu mno kama inavyoeleza Qur’ani Tukufu: “Na kama mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi si vibaya kwao kupokea ajikomboleacho mwanamke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiiruke.” (2:229).

Tafsiri ya aya hiyo katika ufafanuzi uliosimuliwa kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s.) imeelezwa kuwa, (Ifikie hatua ya mke kumwambia mumewe, “Sintasadiki kiapo chako, sintaiweka mipaka ya Mwenyezi Mungu kwako, wala sintakuruhusu uniingilie, nitamlaza kitandani kwako mtu mwingine, na nitawaingiza nyumbani mwako watu usiowapenda.”136

Ni dhahiri kuwa makusudio ya maneno kama haya ni kuonesha chuki hali ya juu sana, na pia yaonesha hakuna tamaa ya kurudiana kabisa kati yao.

Na ikiwa chuki inatokana na pande zote mbili, basi talaka kama hiyo kwa sharia huitwa Al-Mubārāt. Katika talaka kama hii pia sharti zote za talaka lazima zifuatwe, lakini hapa mume hana haki kuchukua zaidi ya mahari aliyompa mkewe wakati wa kuoana. Na namna ya kutoa talaka kama hii, mume humwambia mkewe hivi: “Nimejitenga nawe kwa kiasi kadhaa.” Na badala ya neno ‘kadhaa’ (ataje kiasi alichotoa mke). Talaka ya Al-khula’h na Al-mubārāt huitwa “Bāin” na hakuna marejeo kwa mume, lakini ikiwa mke akiomba arejeshewe malipo aliyolipa hapo mume anaweza kumrejea ikiwa mke yule bado yumo ndani ya eda.

DHI-HAAR, IILAA NA LIAA’N

Kwa itikadi ya Shia mambo haya matatu pia ni miongoni mwa sababu za mke kuwa haramu kwa mume. Maelezo ya mambo hayo na kwa masharti yake maalum yameelezwa katika vitabu vya Fiqhi, na hatutayazungumzia kwa kuwa ni mambo yanayotokea kwa uchache.

136 Taz. Tafsirul-I’yaashi, juz. 1 uk. 117/367; Tafsirul-Qummi juz. 1 uk.75, Majmaul-Bayaan fii Tafsiril-Quran juz. 1 uk. 329.

Page 167: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

160

URITHI

Urithi maana yake ni kuhamisha mali au haki fulani kutoka kwa mwenye kuimiliki anapofariki, kwenda kwa mtu mwingine kutokana na uhusiano wa damu (ukoo) au sababu (inayoweka maungamano baina ya wawili hao).

Jamaa aliyehai huitwa Wārith (Mrithi) na maiti (marehemu) huitwa Maw-rūth (Mwenye kurithiwa) na ile mali au haki huitwa Irth (Urith). Amma nasaba, ni kule kuzalikana mtu kutokana na mwingine au wote wawili wawe wamezaliwa na mtu wa tatu. Hiyo ndiyo Nasab.

Ikiwa Mwenyezi Mungu amekwishaibainisha sehemu ya mrithi katika Qur’ani Tukufu, basi huyo huwa miongoni mwa wanaorithi kwa Fardhi, kama si hivyo atarithi kwa njia ya ujamaa, Bil-Qarābah.

Sehemu za faradhi zilizotajwa katika Qur’an tukufu ni sita. Maelezo ya sehemu sita na warithi ni kama ifuatavyo:1. Nusu (½), na hili ni fungu analopata,

(a) Mume: Kwa mkewe kama mke hana mtoto.(b) Mtoto mmoja wa kike: Kama hakuna mtoto mwingine.(c) Dada mmoja tu: (dada halisi au wakambo kwa baba tu).

2. Robo (1/4)(a) Ni sehemu ya mume kama yupo mtoto wa mke.(b) Mke: Kwa mumewe ikiwa mume hakuacha mtoto.

3. Thumni (1/8) Ni sehemu ya mke kwa mumewe kama kuna mtoto wa huyo mume.

4. Theluthi (1/3) Ni sehemu ya mama kama hakuna mtoto wa maiti. Na pia ni sehemu wanayopata dada wawili na ndugu wawili au zaidi (lakini dada na ndugu wakambo kwa upande wa mama).

5. Theluthi mbili (2/3) Ni sehemu ya watoto wa kike wawili au zaidi ikiwa maiti hakuacha mtoto wa kiume, na pia ni sehemu ya dada wawili halisi au wa kambo kwa baba ikiwa hakuna ndugu wakiume kama hao.

6. Sudus (1/6) Ni sehemu ya kila mojawapo kati ya baba na mama ikiwa kuna mtoto, pia na ni sehemu mahusi ya mama pamoja na kuwapo Haajib yaani ndugu wa kiume wa maiti, na ni sehemu ya ndugu wa kambo wa kiume au wa kike kwa upande wa mama.

Page 168: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

161

Hao tuliowataja wanapata sehemu zao kwa mpango wa ‘faradhi’ ilivyoelezwa katika Qur’an Tukufu. Amma wasiokuwa hawa, wao watapata urithi kwa tegemeo la ujamaa, Mwanamume atapata mara mbili zaidi kuliko mwanamke, katika tabaka zote za urithi ambazo ni tatu.

Tabaka la Kwanza: Mama na baba, watoto na kushuka chini.Tabaka la Pili: Babu, bibi na kwenda juu, na ndugu wa kiume na wakike na kushuka chini.Tabaka la Tatu: Ammi (ndugu wa baba), Wajomba, shangazi wa upande wowote (wa baba au mama). Katika tabaka hili hakuna kabisa mwenye kurithi kwa faradhi.

Hapana shaka kwamba, wale wanaorithi kwa faradhi imma faradhi zao zinaweza zikalingana na mali iliyopo, kama vile baba na mama na mabinti wawili ambayo ni theluthi moja na theluthi mbili, au huenda faradhi ikazidi kuliko kile kilichoachwa kwa robo moja kama pale wanapokutana baba, mama, mabinti wawili na mume wa marehemu. Huenda pia Faradhi ikapungua kwa robo moja, au ikapungua kama watakutana dada na mke wa marehemu, kwani kilichozidi baada ya faradhi ni robo. Kwa hiyo basi ile ya kwanza inaitwa Mas-ala ya Aul, na ile ya pili inaitwa Mas-ala ya Taasiib.

Hakuna tofauti ya kuzingatiwa kati ya Shia na kongamano la wanachuoni wa Kisunni kuhusu mambo ya urithi isipokuwa katika Mas-ala haya mawili ya Aul na Taasiib. Kwa mujibu wa madhehebu ya Shia Imaamiyyah, imethibitika kufuatana na mfululizo wa hadithi kutokana na watukufu Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) kwamba, katika mambo ya urithi hakuna Aul wala Taasiib.137 Yaani sehemu halisi za urithi, hakuna upungufu wala kuzidi kutokana na jumla ya mali. Madh-hebu haya ndiyo yalikuwa yakifuatwa na kikundi cha Masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani ni jambo lilokuwa mashuhuri kwa Ibn Abbas (r.a) alipokuwa akisema kuwa, “Mwenyezi Mungu yule Ajuwaye hesabu ya mchanga jangwani, Anajua sehemu za urithi hazizidi.” Na iwapo imezidi (yaani sehemu

137 Taz: Ilalus-Sharai’ 568/2; U’yunu Akhbar Al-Imam Ar-Ridhaa (a.s.) juz. 2 uk. 125.

Page 169: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

162

ikiwa kasoro kuliko mali) ni lazima kilichozidi watapewa wenye kurithi kwa faradhi kufuatana na sehemu zao, na A’saba hapati kitu.138

Kwa mfano ikiwa maiti ameacha mtoto mmoja wa kike, na mama na baba wa maiti pia wapo, na juu ya hao ndugu mwanamume na Ami wa maiti pia wapo, bila shaka mtoto wa kike na wazee ambao wote hao wamo katika tabaka ya kwanza basi hao ndio warithi. Amma ndugu yeye yuko katika tabaka ya pili na ami yuko katika tabaka la tatu wanahisabiwa kua ni Asaba hawatapata chochote.

Na kwa itikadi ya Shia katika kisa hiki, nusu ya mali atapata mtoto wa kike, na sudusi (1/6) atapewa baba, na sudusi (1/6) nyingine mama, na sudusi moja itakayobakia watagawiwa hao watu watatu (mtoto wa kike, na wazee wawili kwa mujibu wa sehemu zao.

Amma wasiokuwa sisi Shia miongoni mwa Wanachuoni wa Kiislamu, wao huwarithisha ndugu na ami ambao ni Maa’saba. Naam, kwetu sisi Shia, mume na mke hawarudishiwi, kwani kwao hakuna upungufu. Iwapo faradhi itazidi kuliko mali kama ilivyo katika mfano uliotangulia, basi upungufu utaingia kwa binti au mabinti, pia kwa dada au madada na wala upungufu huo hauwezi kwenda kwa mume au mke na wengineo.

Sisi Mashia tunao ushahidi wa kutosha kutoka ndani ya Qur’ani na Sunna kupinga Aul na Taasiib, maelezo yake yameelezwa mahala panapohusika katika vitabu vikubwa.

Itikadi nyingine waliyohusika nayo Mashia peke yao miongoni mwa hukmu za mirathi ni hii iitwayo Al-hub-wah ambayo inamuhusu mtoto mkubwa wa kiume tu. Shia wanaitakidi kuwa, nguo na mavazi ya baba, Msahafu wake na pete, vyote hivi vinamuhusu mtoto huyo mkubwa wa kiume katika mirathi. Hukumu hii ina masharti na ufafanuzi ambao umeelezwa katika vitabu vya Fiqh ndani ya mlango husika. 138 Maana ya Asaba, au Taasiib ni wale wenye ujamaa (uhusiano) na maiti kwa upande wa baba na mtoto, hawa hawapewi sehemu iliyozidi katika mali, bali sehemu hiyo itagawanywa kwa warithi wale wale kwa mujibu wa utaratibu wa sehemu zao.

Page 170: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

163

Pia Shia Imamiyah wanayo hukumu ambayo iko kwao tu katika mambo ya urithi ambayo ni urithi wa ardhi, mashamba na majumba. Mke kwa vyovyote harithi (asili wala kima chake) na pia asili ya mti na nyumba pia harithi lakini kima chake atarithi. Thibitisho la fata-wa hizi ni zile habari zitokazo kwa Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) zilizopokelewa, na Maimamu wamepokea kwa babu yao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hayo ni mambo muhimu ambayo Shia wanahitalifiana na wengine katika mirathi, na yasiokuwa hayo kuna hitilafu ndogo sana kama zilivyo hitilafu kati ya wanavyuoni wa Ki-Sunni wao wao, na wale wa Kishia wenyewe kwa wenyewe.

WAKFU, HIBA, NA SADAKA

Mali ambayo ni milki yako halisi na unataka kuitoa kutoka kwenye mamlaka yako, imma itakuwa kwamba hukusudii kuitoa ndani ya mamlaka yako tu, bali kuitoa huko kutakuwa ni kwa moja kwa moja, kwa maana uitoe kabisa iwe huru na isifae asilani kuwa ni mali yako. Kwa mfano, kumuacha huru Mtumwa, Nyumba au Ardhi unaitoa isiwe milki yako na uifanye kuwa ni Mahala pa kufanyia Ibada, au Mahala pa Maziyara. Aina kama hii ya utoaji kamwe haimpi haki mwenye kutoa kukirudisha alichokitoa ndani ya mamlaka yake kwa namna yoyote ile itakayojitokeza na au mazingira yoyote yale.

Na imma kuwe huko kuitoa mali hiyo, siyo kuiondosha kabisa ndani ya mamlaka yako, bali ni kuitoa ndani ya umiliki wako tu na kumpa mwingine. Hapo imma litafanyika hilo kwa mabadilishano pamoja na maridhiano (ya pande zote mbili) katika mapatano yatakayofanyika kwa mdomo au namna nyingine inayoweza kubeba uzito kama huo. Mapatano kama haya ni mabadilishano kama vile, kuuza na kununua na (Sulh) na biashara kama hizo.

Na au unaweza kuwa ni utoaji usiyohusisha mabadilishano ya mali, basi kama itakuwa ni kwa makusudio ya kutaka thawabu na jazaa njema na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hiyo itakuwa ni sadaka kwa maana ya ujumla. Na ikiwa mali ile itakuwa ni yenye kubakia

Page 171: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

164

kwa muda ulioandaliwa kwa ajili yake, kisha yule mtoaji akawa amekusudia kubakia kile alichokitoa (yaani) ile dhati ya kile kitu ikabakia kwake lakini manufaa ya kitu hicho akayatoa, basi hii huitwa ni Waqfu.

Na ikiwa mali ile ni kitu ambacho hakiwezi kubakia, yule mwenye kutoa sadaka ile akawa hakuweka sharti ya kubakia kitu hicho, basi hiyo itakuwa ni sadaka kwa maana makhsusi.

Na kama kumilikisha kutakuwa siyo kwa makusdio ya kupata thawabu na malipo mema, bali kukawa ni kumilikisha bure kabisa, basi hiyo huitwa ni Hiba.139 Amma ikiwa itawekwa sharti mkabala wa Hiba, basi hiyo itakuwa ni Al-hibatul- Muawwadhah. Mfano wa Hiba hiyo ni kama vile mtu akisema, “Ninakupa nguo hii kwa sharti na wewe unipe kitabu.” Na yule anayepewa naye akasema, “Nimekubali.” Katika hali kama hiyo, itakuwa ni lazima (kutekeleza makubaliano hayo) na hairuhusiwi kwa mmoja wao kukirudisha kile alichopewa isipokuwa kama wote wawili watakubaliana kuvunja mapatano. Kinyume cha hivyo itakuwa ni Al-hibatul-Jaizah. Na wala hakiwezi kusihi chochote katika aina za Hiba isipokuwa kwa kuimiliki, na iatajuzu kurudisha Hibatul-Jaizah hata baada ya kuimiliki isipokuwa kama hiba hiyo ni ya ndugu, mume au mke na au baada ya kuharibika. Haifai kurudisha chochote katika sadaka baada ya kuimiliki, na vilevile haiwezi kusihi sadaka hiyo isipokuwa kwa kuimliki.

Iwapo mtu anayekiweka kitu chake katika wakfu, atatamka matamko ya kukiingiza kitu hicho ndani ya wakfu, kwa mfano akasema, “Nimeiweka nyumba hii ndani ya wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Kisha akamkabidhi mwenye kuisimamia au wale waliowekewa wakfu huo, au akakichukua kitu hicho yeye mwenyewe kwa nia ya kukiweka wakfu, katika hali hiyo ikiwa mamlaka ya kukisimamia atakuwa nayo yeye mwenyewe basi haitafaa kwake kukirejea kitu hicho asilani. Si hivyo tu bali haruhusiwi kukiuza wala kukigawa, sawasawa ikiwa ni wakfu kwa ajili ya watu maalum au wakfu wa matumizi ya jumla, k.m. kwa ajili ya Mafaqiri, Wageni, Shule na mfano wa vitu kama hivyo.

139 Hiba maana yake ni Tunzo au Zawadi.

Page 172: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

165

Naam, huenda ikafaa kuuza mali ya wakfu katika baadhi ya maeneo maalum ambayo yanahesabika kuwa ni ya dharura muhimu. Miongoni mwa dharura hizo ni kuhofia uharibifu wa wakfu kiasi cha kusababisha kukosekana manufaa yaliyokusudiwa, au kama itahofiwa kutokea uharibifu utakaofikia daraja tuliyoitaja hapo kabla, na au kuzuka kutokuelewana kati ya wamiliki wake, kutokuelewana ambako kutapelekea kuharibika kwa mali au nafsi na au kuvunjika kwa heshima za watu.

Pamoja na yote hayo, haifai kabisa kuuza wakfu kwa hali yoyote ile iwayo, wala kuigawa mpaka kwanza jambo hilo lifikishwe kwa Hakimu anayetambulikana kwa mujibu wa sheria (ya Kiislamu) na yeye alifanyie uchunguzi wa kina katika maeneo yote yanayohusika, hapo Hakimu huyo anaweza kutoa maamuzi ya kuuzwa kwa wakfu au kugawiwa.

Hapana shaka kwamba watu wengi wamelifanyia wepesi mno jambo la wakfu kiasi kwamba wanauza mali za wakfu na kulitoa nje kabisa ya mipaka inayohusu wakfu, hali ambayo imewatoa kwenye mizani ya kisheria na kanuni zinazostahiki kulindwa. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kufuatilia makusudio yoyote yale naye ni mpole tena mjuzi.

Yote hayo ni kwa mujibu wa njia iliyo mashuhuri, japokuwa sisi tunao uhakiki na uchambuzi zaidi kuhusu wakfu lakini kwa hapa nafasi haitoshi kuelezea.

UQADHI NA HUKUMU

Cheo na heshima ya Uqadhi katika usimamizi wa mambo na kuhukumu baina ya watu ni cheo kikubwa mno na ni wajibu muhimu. Kwa Shia Imamiyah ni tawi la mti unaotokana na Utume (wa Mtume Muhammad s.a.w. na Uimamu wa Maimamu wetu a.s., pia) na ni moja katika daraja za Uongozi wa utawala wa mambo yote na ndiyo Ukhalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi kama asemavyo katika Qur’ani hivi: “Ewe Daudi, hakika tumekujaalia kuwa Khalifa ardhini, basi uwahukumu watu kwa haki.....” Qur’an, (38:26).

Page 173: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

166

Na pia Anasema: “Naapa kwa haki ya Mola wako, wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye wewe kuwa hakimu katika yale waliyoihitilafiana kati yao, kisha wasione uzito mioyoni mwao juu ya hukumu uliyoitoa na wanyenyekee kabisa.” Qur’an, (4:65).

Kwa nini isiwe hivyo, hali ya kuwa Maqadhi na Mahakimu ni watu ambao wamepewa na Mwenyezi Mungu dhamana ya ulinzi wa mambo matatu matakatifu ambayo ni: 1. Kulinda Nafsi za watu.2. Kulinda Heshima za watu.3. Kulinda Mali za watu.

Kwa sababu hiyo kuna hatari kubwa katika cheo hiki na madhambi yake hayasemeki (ikiwa kadhi huyo atajikwaa asihukumu kwa haki, bali akafuata matamanio yake kinyume cha sharia)!

Kuhusu hatari hio zapatikana hadithi nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bait (a.s.) ambazo ukizisoma mwili hutetemeka na nywele kusimama!! Kwa mfano kauli ya Imam Ali (a.s.) aliposema, “Kadhi (hakimu) yuko ukingoni mwa shimo la moto, na ulimi wa Qadhi uko kati ya vinga viwili vya moto.”140

Katika hadithi nyingine Amirul-Muminina Ali (a.s.) anamwambia Qadhi Shuraih hivi: “Ewe Shuraih umekaa mahala ambapo hapakai isipokuwa Mtume au Wasii wa Mtume (mshika makamo yake) au mtu muovu.”141

Hadithi nyingine imenakiliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema hivi: “Ikiwa mtu amewekwa kuwa Kadhi ina maana kuwa mtu huyo amechinjwa bila ya kisu.”142 Hadithi kama hizo zipo nyingi.

Hukumu anayoitoa Mwanachuoni bingwa wa maarifa ya dini ambayo huipata kutokana na uchambuzi unaopatikana kutoka ndani ya dalili za Qur’an na Sunna ya Mtume (s.a.w.w.) ikiwa inahusu maudhui 140 At-tahdhib Juz 6 uk 292/808.141 Alkafi juz 7 uk 407.142 Almuqniah uk 721; Sunan Abi Dawud juz 3 uk 298; Sunan At-tirmidhi juz 3 uk 618; Sunan Ibn Majah juz 2 uk 774; Musnad Ahmad ibn Hambal juz 2 uk 230.

Page 174: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

167

ya ujumla juu ya mambo ya kijamii huitwa ‘Fatwa’ (ni amri) kwa mfano aseme, “Mtu kwa vyovyote vile hana haki kutumia mali ya mwenziwe bila ruhusa ya mwenye kuimiliki mali hiyo.” Au asema, “Mke wa Mume ni halali kwa mumewe, na asiyekuwa mkewe ni haramu.”

Lakini ikiwa hakumu inahusu mtu au jambo mahususi, huitwa Al-kadhaa wal hukuuma kwa mfano ahukumu “Huyu ni mke wa fulani, na yule mwanamke si mke wa fulani, au mali hii ni ya Zaid.”

Hukumu zote mbili hizo Fatwa na Al-Kadhaa Wal-Hukuma, ni miongoni mwa kazi za Mujtahid Mwadilifu ambaye anayo mamlaka ya cheo cha unaibu wa ujumla kutoka kwa Imam, isipokuwa Qadhaa ni ibara inayoelezea namna ya ufumbuzi wa maudhui mbalimbali na kutatua matatizo au mengineyo kama vile hukumu ya kuthibiti kuonekana mwezi, au kuwa mali fulani ni wakfu, au kuhusu hati ya nasaba n.k. Yote hayo huhitajia maarifa na akili pevu isiyo ya kawaida na busara ya utambuzi zaidi kuliko vile inavyohitajika katika kutoa Fatwa na uchambuzi wa hukumu za ujumla.

Sasa ikiwa mtu mmoja hana sifa zote hizo, anashika shughuli hii, bila shaka ataleta hasara kuliko faida na atakosea mno kuliko atakavyopatia.

Kwa sababu hiyo kwetu Shia Imamiyah ni dhambi kubwa sana mtu yeyote asiyekuwa na sifa zote hizo kushika au kukubali makamo haya bali jambo hilo linampelekea mtu katika kufru, isipokuwa inatakiwa awe ni Mujtahid Mwadilifu. Ndiyo maana siku zote tumeshuhudia wanavyuoni wakubwa wa Kishia, na kiasi iwezekanavyo wakijiepusha na kutotoa maamuzi na hukumu na aghalbu wakijitahidi kumaliza mambo ya ugomvi na madai kwa njia ya suluhisho, nasi kufuatana na mwendo huo mzuri wao tunawafuata babu zetu wachamungu.

Jambo jingine ambalo ni lazima kutajwa ni kuwa chanzo cha maamuzi ambayo Qadhi kwa msingi ule anatoa hukumu ni mambo matatu:1. Tendo la kukiri au kukubali. Iqrar.2. Ushahidi wa wazi.3. Kiapo.

Page 175: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

168

Katika Ushahidi wa wazi, mashahidi wawili waadilifu wanatakiwa, na ikiwa mashahidi ni wawili watapingana (yaani wawili wanatoa ushahidi juu ya jambo fulani na wawili wengine wanatoa ushahidi kinyume chao) hapa pana tofauti kubwa juu ya shahidi yupi kati yao atangulizwe kusikilizwa; je ni shahidi wa ndani au yule wa nje au yarejewe mambo yatakayotia nguvu ushahidi.

Kwa bahati nzuri wengi katika wanavyuoni wetu wametunga vitabu mahsusi vyenye kuhusika na mambo ya Uqadhi kwa upana zaidi ukiachilia mbali tunzi zao zilizokusanya milango ya Fiqh kwa ukamilifu. Kwa hapa nafasi haitoshi kuileta milango hiyo japo kwa uchache seuze kwa wingi. Sisi tumeeleza kiasi cha kutosha kinachohusu uchambuzi wa mas-ala haya ndani ya juzuu la nne la Tahrirul- Majallah, mwenye kutaka anaweza kurejea huko. Nasi pia tumeeleza kwa kirefu juu ya jambo hilo katika ‘Tahree-Rul-Majallah’.

Jambo la mwisho kuhusu mazungumzo yetu ambayo ni dharura na ni lazima kulieleza ni hili. Ikiwa Qadhi au hakimu mwenye kukamilisha sharti zote tulizozieleza hapo kabla atatoa hukumu, kisha mtu yeyote yule akampinga au kutokufuata hukmu yake, kwa hakika mtu huyo atakuwa amepinga amri ya Mwenyezi Mungu, wala haijuzu kwa mtu mwingine kuyachunguza tena malalamiko hayo baada ya kuyatolea maamuzi. Naam kwake yeye inajuzu kuyaangalia tena, na ikiwa itambainikia dosari atatengua maamuzi yake ya mwanzo kwa dharura.

KUWINDA NA KUCHINJA

Kwa Shia Imamiyah kila mnyama mwenye damu ya kuruka (anapochinjwa) akifa kwa kawaida (bila ya kuchinjwa) huwa najisi na kula nyama yake ni haramu.

Kuna aina mbili za wanyama: Kwanza, ni wanyama ambao toka asili ni najisi, (maana yake kwa vyovyote hawawezi kutahirika, kama mbwa na nguruwe huitwa Najisul-Ain) na, Pili: ni wanyama wengine ambao toka asili wao ni tohara, k.m. wanyama wangine wasiokuwa hao wawili tuliowataja na hawa huitwa Taahirul-Ain.

Page 176: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

169

Najisul-Ain: Aina ya kwanza ni najisi na nyama yao ni haramu, na wakati wowote wakiwa hai, baada ya kufa, kwa kuchinjwa au kwa vyovyote vile hawawi tohara wala halali.

Aina ya pili ya wanyama, iwapo hakuchinjwa kwa mujibu wa sharia akafa, ni najisi na ni haramu kumla, akiwa ni ndege au mwinginewe wa porini au afugwaye. Amma akichinjwa ni tohara kama alivyokuwa hai, kisha ni lazima ifahamike kwamba, nyama yake huwa ni halali ikiwa si katika wanyama wanaokula nyama na wa mwitu, ijapokuwa ni tahara, kinyume cha hivyo basi atakuwa halali kuliwa.

Njia za kuifanya nyama ya mnyama kuwa halali kula ni mbili:1. Kuwinda: Lakini mnyama wa halali tu. Na kuwinda pia kuna namna mbili:

(a) Kwa njia ya mbwa mkubwa wa kuwindia ambaye amefundishwa na awe anafuata amri ya bwana wake hana tabia ya kula mawindo.

Na yule mwenye kumtuma mbwa lazima awe Mwislamu, na anapomwachia lazima asome (atamke) Bismillahi na pia asitoweke machoni pa mwindaji. Mawindo anayoyakamata mbwa kama huyo kwa sharti hizo basi ni halali kuliwa.

(b) Kwa kutumia silaha kama, mshale, upanga na mkuki, na kila aina ya silaha yenye kupasua mwili, hata risasi za bunduki ikiwa itapasua mwili wa mnyama, risasi za bunduki ikiwa zitapasua mwili wa mnyama, na zikiwa ni za chuma au kitu kingine, kwa sharti mwenye kutumia silaha mojawapo wakati wa kuwinda awe ni Mwislamu na lazima atamke Bismillah.

Kwa njia mbili hizi, ikiwa mnyama kawindwa na huyo mbwa mwindaji, au silaha na akafa basi nyama yake ni halali, lakini ikiwa mwindaji kakuta windo lake bado liko hai hapo lazima amchinje kwa njia itakayoelezwa katika namna ya kuchinja.

Windo litalopatikana kinyume cha njia mbili hizo tulizozitaja si halali kabisa, kama kumwinda kwa mtego na mfano wake, au kumwinda kwa msaada wa mnyama mwingine kinyume cha

Page 177: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

170

yule (mbwa mwindaji) lakini ikiwa kwa njia hizo amewindwa na akapatikana yu hai, hapo baada ya kuchinjwa kwa mujibu wa sharia huwa halali kula nyama yake.

2. Kanuni ya Kuchinja: Kumchinja mnyama wa kumla lazima zipatikane sharti zifuatazo:

(a) Mchinjaji lazima awe Mwislamu, au yule alioko katika hukumu ya Islamu kama mtoto wa Kiislamu asiye balehe, au mtoto aliokotwa na Mwislamu.(b) Mnyama lazima achinjwe kwa ala (chombo) cha chuma ikiwezekana, ikiwa haiwezekani basi kwa kila kitu kinachokata mishipa minne mikubwa ambayo ni hii: Koo, wa kidaka tonge, mishipa miwili mikubwa ya shingo.(c) Na pia ni lazima wakati wa kuchinja (mchinjaji) atamke Bismillahi.(d) Yule mnyama alazwe uso wake uelekee Qibla.

Ama kumchinja ngamia badala ya kumkata kichwa ni kuchoma kisu au mkuki kwenye koo lake na uchinjaji kama huu huitwa Nahr, pamoja na sharti zingine zote.

Ikiwa kuchinja haiwezekani; kama mnyama ametumbukia kisimani au mnyama mghaghari sana unaweza kumpiga kwa upanga na mfano kama huo miongoni mwa vitu vinavyoua. Basi akifa itakuwa halali kula, na ikiwa bado yu hai lakini amevunjika nguvu basi lazima achinjwe kama desturi.

Wanyama wote wasiokuwa na damu ya kuruka (wakati wa kuchinja) wote ni haramu isipokuwa Samaki tena wale wenye magamba tu.

Hadithi ya Kuvutia:Bw. Muhammad ibn No’maan Ahwal ambaye jina lake mashuhuri anaitwa Mu’uminut-taaq143 anasimulia hivi: “Siku moja nilikwenda kwa Abu Hanifa, nikakuta vitabu vingi vipo mbele yake, kwa wingi vimetuziba kati yangu na yeye. Abu Hanifa akaniambia, “Vitabu vyote hivi vinahusu hukumu za Talaka.” Mimi nikamjibu, “Mwenyezi

143 Ni mmoja katika wanafunzi mashuhuri na hodari wa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.)

Page 178: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

171

Mungu katika aya moja tu ya Qur’an ametutosheleza kutokana na vitabu vyako hivyo vyote nayo ni hii: “Ewe Nabii! Mtakapotoa talaka kwa wanawake, basi toeni talaka katika wakati wa eda zao, na fanyeni hesabu ya siku za eda.” Qur’an, (65:1)

Abu Hanifa akasema: “Je ulipata kumwuliza rafiki yako Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) yeye anasema nini ikiwa ngombe katokeza baharini nyama yake ni halali kula”?

Nikamjibu, Naam, Yeye ametuambia kila chenye magamba kula, akiwa ngamia au ngombe, na asiye na magamba ni haramu tu.144

VYAKULA NA VINYWAJI VILIYOHALALISHWA NA VILIVYOHARAMISHWA

Kuna namna tatu za wanyama,(a) Wanyama wa nchi kavu.(b) Wanyama waliyomo katika maji.(c) Wenye kuruka; na kila mmoja anahukumu yake.

Kama tulivyokwishaeleza kwamba, wanyama wote wa baharini kwa jumla ni haramu isipokuwa samaki wenye magamba, mayai ya samaki hawa ni halali pia, yaani samaki alio halali kuliwa basi mayai pia ni halali, na wale samaki wasio na magamba ni haramu na mayai yao pia haramu.

Ama wanyama wa nchi kavu walio halali kuliwa ni namna chache tu nao ni hawa: Kondoo, mbuzi wa kila aina, ng’ombe, nyati, ngamia, paa kila aina, Punda milia. Farasi, nyumbu. Amma punda kula nyama yao makuruhu. Na mnyama wa halali akiwa anakula kinyesi cha binadamu ni haramu kuliwa, na mnyama mwenye tabia hii huitwa na Al-Jal-Laal. Mnyama huyo anaweza kuliwa tu baada ya 144 Yaonesha kwamba Abu Hanifa kwa kuleta swali la ajabu kama hilo alikusudia kumtia makosa kwa msemo wake Mu’uminut-taaq akisema, “Sisi tunayo kanuni (general rule) ya mambo yote kutokana na Qur’an tukufu na hadithi za Ahlul-Bait (a.s.) ambazo zinajibu mambo yote ya kidini yanapotokea. Lakini wapi!! Akamjibu kwa kanuni ya jumla yenye kuhusu wanyama wa baharini aliosikia kwa Imam, Jafar as-Sadiq (a.s.) akamjibu kwa kumfunga mdomo. (Mtarjumi).

Page 179: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

172

kufanyiwa ‘Istibraa’, (njia mahususi ya kumtakasisha ili awe halali kumla).

Wanyama wote wanaokula nyama ni haramu kuwala, pia sungura, mbweha, badgers, (gunguru), nguchiro, na wengineo miongoni mwa wanyama wa msituni, na pia wadudu, funza, nyoka, nge na wenye mfano kama hawa.

Amma wanyama wanaoruka (ndege) wanaokula wanyama wenzi-wao wote hawa ni haramu k.m. kengewe, tai, na kama hawa, wote ni haramu.

ALAMA ZA KUMTAMBUA NDEGE ALIYE HALALI

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameamuru kwa kueleza alama tatu ambazo ndege akiwa anazo huwa ni halali kumla, nazo ni hizi:(a) Ikiwa huyo ndege wakati wa kuruka hupiga mbawa zake zaidi kuliko kujitandaa basi ni halali kama si hivyo ni haramu.(b) Na ikiwa yupo ardhini lazima awe na kidole cha nyuma ya miguu ya ndege kama kuku na jogoo.(c) Ikiwa ameshachinjwa hatuwezi kumtambua kwa alama hizo mbili tulizozitaja kwa hivyo alama ya tatu ni hii, awe na kibofu cha kooni (ghala) ndio halali kula, kama si hivyo ni haramu.

Kwa hivyo tausi, popo, nyuki, wa kila aina wote ni haramu, ama kunguru anayekula mizoga ni haramu na anayekula majani ni halali.

VITU VINGINE AMBAVYO NI HALALI AU HARAMU KULA AU KUNYWA

Juu ya wanyama kuna vitu vingine pia ambavyo si halali kula au kunywa, vitu hivyo vimepangwa kwa namna nne:1. Chochote kilichopatikana kwa njia ya kunyang’anya ni haramu

kula au kunywa.2. Chochote kilicho najisi ni haramu.3. Chochote chenye madhara ni haramu.4. Chochote kibaya kinacho karihisha ni haramu.

Page 180: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

173

UHARAMU WA MKOJO NA MVINYO

Miongoni mwa vitu vya majimaji vya uchafu na vibaya na ni haramu kabisa, ni mkojo lakini kuliko hiyo baya zaidi ni ulevi (pombe, tembo, akari, gimbi) na kila kinacholewesha. Na pia maji ya zabibu yakichemka na theluthi mbili haikukaukaa (na kuwa mvuke) ni haramu na ni najisi.

Kwa Shia Imamiyah: Kuhusu uharamu wa ulevi kwa mujibu wa hadithi za Ahlul-Bayt (a.s.) zinapinga vikali sana na kuuchukia ulevi kuliko madhehebu zingine za Kiislamu.

Kuna hadithi zinazotokana na Ahlul-Bayt (a.s.) zenye kutikisa na kutia hofu, kugombeza kunakotisha kiasi cha kuzifanya nywele kugeuka na kuwa nyeupe, na humtetemesha mjasiri zaidi kuliko madhambi yote.

Wakamuaji wa zaibibu (kwa ajili ya kutengeneza ulevi), waletaji, wauzaji, wanywaji na wasaidizi wa aina yoyote kwa ajili ya kutayarisha ulevi, wote hao wamelaaniwa si mara moja bali mara nyingi. Na katika sharia yetu ulevi hujulikana kwa jina la ‘Ummul Khabaaith’ (mama wa maovu).145

Zipo baadhi ya hadithi za Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) zenye kuonesha kuwa, kukaa kwenye meza yenye ulevi ni haramu. Huenda siri ya mkatazo huo kuwa mvuke wa ulevi unaweza kugusana na vyakula vilivyoko mezani, au chembechembe ndogo za ulevi zikawaingia mdomoni au puani mwa watu walikaa mezani.146

Walingwa wa Sayansi wa siku hizi baada ya majaribio ya kitaalamu, wamekiri juu ya kuwepo madhara makubwa ya ulevi, madhara

145 Taz, Kitabul-wasail juz 25 uk 296, mlango unaoharamisha ulevi.146 Lazima tufahamu kwamba si kwa kushiriki mahala palipowekwa mvinyo peke yake (kuwa ni haramu tu), bali kushiriki popote panapotendeka maasi pia ni haramu. Kwa hivyo mikutano kama hiyo ni mfano wa kikwazo au genge linalomtupa binadamu kwenye upotevu, kwa kushiriki hata kwa wale wasiokuwemo pia huwavutia kwenye dhambi, ndio maana sharia inapiga marufuku kushriki humo. (Mtarjumi).

Page 181: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

174

ambayo uislamu umeyaeleza tangu hapo zamani kiasi karne kumi na tatu zilizopita bila kuwepo na taklifu wala taabu yoyote katika kulibainisha jambo hilo. Basi mabingwa hao wamejiharamishia matumizi ya ulevi ambao umeharamishwa na dini yao na pia sheria yao inalizuwia jambo hilo.

Heko kwa dini takatifu, nyoofu aliyoileta Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) namna gani imechunga kwa makini ubaya na uovu na kuupiga marufuku. Wamepata hasara kubwa wale Waislamu ambao hayawafuati hayo na wamejitumbukiza katika uharibifu na kuyapuuza makatazo hayo.

Tunatumai Insha-Allah mambo yatatengenea na Mwenyezi Mungu atawaongoza Waislamu wapotevu. Amina.

Huu ulikuwa muhtasari kuhusu vyakula na vinywaji vya halali na haramu. Bila shaka maelezo kamili anayetaka atayapata katika vitabu vikubwa.

ORODHA YA ADHABU KWA WANAOKWENDAKINYUME CHA SHARIA

Kuna adhabu (katika sheria ya Kiislamu) ambazo inapaswa zitekelezwe mara moja juu ya makosa maalum kwa lengo la kuilinda nidhamu ya jamii, na kukata mizizi ya maovu kutoka kwa wanadamu.

1) Adhabu ya kosa la Uzinifu:Kila mtu ambaye amekwisha kubalehe na anazo akili timamu, iwapo atamuingilia mwanamke ambaye siyo halali kwake kumuingilia kwa mujibu wa sheria, kisha akawa anafahamu (kuwa tendo hilo ni haramu) lakini akalifanya kwa makusudi, itamuwajibikia hakimu kumuadhibu mtu huyo kwa kumpiga mijeledi mia moja, kisha atapigwa kwa mawe kama mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa wenye kuhifadhika (yaani anaye mke anayemtimizia haja yake). Na kama atakuwa hana hifadhi basi atapigwa mijeledi peke yake na kichwa chake kitanyolewa na atafukuzwa hapo mjini kwa muda wa mwaka mmoja. Vile vile iwapo mke yule naye alikuwa ameridhia juu

Page 182: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

175

ya tendo hilo naye pia ataadhibiwa kwa adhabu hizo mbili iwapo tu mwenye kuhifadhika, na kama hana hifadhi basi atapigwa mijeledi tu.

Na kama atazini na mmoja wa wanawake ambao ni maharimu wake kwa njia ya nasaba au kunyonya, na au akazini na mke wa baba yake, au akazini na mwanamke wa Kiislamu wakati yeye ni Dhimmi,147 au akamlazimisha mwanamke yeyote azini naye, basi mtu huyu adhabu yake ni kuuwawa.

Kosa la uzinifu linathibiti kwa yule mzinifu mwenyewe kukiri mara nne, au wawepo mashahidi wanne waadilifu walioshuhudia, na au mashahidi watatu wanaume na wanawake wawili walioshuhudia.

Lau watashuhudia wanaume wawili na wanawake wanne kitakachothibiti hapo ni mijeledi mia moja tu na wala hatopig-wa mawe, na hauwezi kuthibiti ushahidi chini ya idadi hiyo. Na lau watashuhudia mashahidi watatu au wawili watapigwa haddi ya kuzusha. Pia ni sharti ushahidi wao uafikiane katika maeneo yote, na wawe wameona tendo hilo likitendeka wazi wazi.

Lau atakiri kufanya uzinifu utakaopelekea kupigwa mawe kisha baadaye akakanusha, basi adhabu hiyo itaondolewa, na lau atakiri kosa na baadaye akatubia, Hakimu wa sharia ana hiari ya kusamehe au kumtia adabu.

Lakini ikiwa baada ya mashahidi kutoa ushuhuda akatubia, toba yake haitaleta nguvu na lazima ahukumiwe.

Ikiwa mtu amezini mara mbili, na kila mara amepewa adabu yake, tena kwa mara ya tatu akatenda basi huyo lazima auwawe.

Mwanamke mwenye mimba haadhibiwi mpka azae, na pia mgonjwa naye haadhibiwi mpaka kwanza apone.

2) Adhabu ya kulawiti na Kusagana (Sahq):Hakuna adhabu kali mno katika maasi yote kuliko adhabu ya kitendo

147 Raia asiyekuwa Muislamu, lakini anaishi katika dola ya Kiislamu.

Page 183: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

176

kichafu cha kulawitiana ambayo adhabu yake ni mhalifu kuchomwa moto hadi kufa na hakuna kosa jingine lenye adhabu kali kama hii.

Hakimu wa Kiislamu anayo hiari kumpa adhabu mwenye kulawiti mojawapo katika adhabu hizi nne:

1. Kukatwa kichwa2. Kupigwa mawe hadi kufa3. Kutupwa kutoka mahala palipo juu hadi chini mpaka mifupa

yake ivunjike na au4. Kuchomwa moto.

Na yule mwenye kutendewa, ikiwa ni balahe, mwenye akili na mwenye hiari, basi yeye pia atakatwa kichwa. Na kama ni mtoto asiye balehe atapata adhabu iitwayo: ‘Taazeer’ Huthibiti kulawiti kwa njia zile zile za kuthibitisha zinaa.

Hukumu ya kusagana (wanawake kwa wanawake) uthibitisho wake ni kama ule wa zinaa, ikithibiti wote wawili (mtenda na mtendwa) hupigwa viboko mia kila mmoja, na kama wote wawili wanao waume basi hukumu ya kupigwa mawe inaweza ikatolewa.

Kuwadi: Mtu anayemtongoza mwanamke kwa ajili ya mwanamume mwingine, au mwanamume kwa mwanamume mwingine au mwanamke kwa mwanamke mwingine, wote hao ikithibiti hupigwa viboko sabini na tano na baadaye kunyolewa kipara kisha akatangazwa na kutolewa mjini. Huthibiti jambo hilo kwa kushughudia watu wawili waadilifu au kukiri mwenye (kwa kitendo hicho) mara mbili.

3) Adhabu ya Al-Qazf (Masingizio): Ikiwa mtu anamsingizia Mwislamu aliyebalehe tena aliyehuru kwa masingizio ya uhalifu (ya kisharia) ambayo uhalifu ule una adhabu maalum, kama vile kumsingizia uzinzi, ulawiti, kunywa ulevi, na huyo mingiziaji asiweze kuthibitisha, basi atapigwa viboko thamanini, lakini akithibitisha kwa uthibitisho unaokubalika au yule aliesingiziwa akakiri na kukubali basi adhabu hiyo hatapewa mchongezi.

Page 184: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

177

Na hilo huthibiti kwa mashahidi wawili waadilifu, au akikiri mara mbili kuwa alitenda.

Na lau kuna mtu kampa mwenziwe majina yasiyofaa, kwa mfano mtu kumwita, Ewe! fasiki au muovu, au mwenye ukoma! au mwenye mbaranga kisha aliyeambiwa hivyo akawa hana sifa hiyo, ni lazima mtu huyo apate adabu ya kuaziriwa.

Vivyo hivyo mtu akidai kuwa ni Mtume, au kumtukana Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) adhabu yake ni kukatwa kichwa.

4) Adhabu ya Mlevi:Ikiwa mtu balehe, mwenye akili akilewa kwa kunywa ulevi wa aina yoyote ya kizamani au ya kisasa, hata divai kabla ya kuwa mvuke thuluthi mbili, akinywa kwa kujua au makusudi, lazima avuliwe nguo (si kuwekwa uchi) na kupigwa viboko thamanini mgongoni na begani mwake. Ikiwa mtu huyo mara tatu keshatiwa adhabu ya Kisharia kwa kulewa, akitenda kwa mara ya nne, hukumu yake ni kuuwawa tu. Ikiwa kalewa kwa kuihalalisha basi huyo ni huwa ametoka katika dini na hukumu yake ni kuuawa tu.

Muuzaji wa ulevi hutakiwa kutubia kwanza, akitubia na kuacha hayo ni sawa hana adhabu ya kupewa, lakini akiendelea na kazi mbaya hiyo, hukumu yake ni kuuwawa.

5) Adhabu ya Wizi:Ikiwa mtu mzima mwenye akili aliyebalehe akiiba kutoka mahala palipofungwa (kwa aina zote za kufungia, kufuli, komeo n.k.) na mali aliyoiba thamani yake ni robo katika uzito wa dhahabu safi (au zaidi) atapelekwa mbele ya hakimu wa sharia baada ya kuthibiti dhambi hiyo, na kukiri mara mbili yule mwizi, au kwa ushahidi wa wanaume waadilifu wawili ikathibiti, hapa adhabu yake ni kukatwa vidole vyake vinne vya mkono wa kulia. Na kama baada ya kupata adhabu hiyo akaiba tena, mara hii atakatwa mguu wake wa kushoto katikati ya unyayo, na akirudia kuiba kwa mara ya tatu hukumu yake afungwe kifungo cha maisha, na akiiba tena humo humo katika jela basi hukumu yake ni kuuwawa.

Page 185: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

178

Na ikiwa amekwisha iba mara nyingi kabla ya kupata adhabu basi atapata adhabu mara moja tu kwa yote hayo.

Mtoto asiyebalehe au mwendawazimu wakiiba wao huaziriwa.

Kama mwizi amepoteza mali aliyoiba ni lazima alipe badala yake. Kuhusu malipo inatakiwa akiri mara moja na shahidi mwadilifu mmoja na kuapa yule shahidi inatosha.

Ikiwa baba kaibaba mali ya mwanawe hana hukumu ya kutiwa adabu, lakini mtoto akiiba mali ya baba yake atapewa adhabu ya kukatwa vidole.

6) Adhabu ya Muhaarib:148

Ikiwa mtu mmoja katika mji, jangwani, au baharini amekamata silaha na kuwatisha watu kwa ajili ya kunyang’anya mali zao, hakimu wa sharia (serikali ya Kiislamu) inambidi kumpa adhabu mojawapo katika hizi:

(a) Kumuua(b) Kumtundika (kumsulubu)(c) Kumkata mkono wa kulia na mguu wa kushoto(d) Kumtoa nje ya mji.

Kama isemavyo Qur’ani Tukufu: “Hakika malipo ya wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wafanyao fujo katika nchi, ni kuuawa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa kubadilishwa au kuhamishwa katika nchi.” (5:33).

Hakimu wa sharia akitoa amri ya kuhamishwa, itambidi kuwaandikia watu wa ule mji alikohamishiwa yule mhalifu kuwakataza wasiwe na mahusiano naye, kumpa uwakala ngilie naye, kukaa naye na kufanya naye biashara hadi yule mhalifu atubie.

Mwizi mwenye kuvamia nyumba ya watu hukumu yake ni sawa na Muhaarib, akiuwawa wakati wa mashambulio damu yake imepotea bure.148 Muhaarib anaweza akafasiriwa kama mnyang’anyi au jambazi na wenye sifa kama hizo.

Page 186: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

179

Mtu akimshambulia mwanamke na kuvunja stara yake, au mtoto wa kiume kutaka kutenda mabaya, wote hao wanayo haki kwa njia yoyote kujihami na kujilinda, na mshambuliaji akiuwawa katika mashambulio damu yake imepotea bure. Matapeli na watu wenye hadaa na wale wanaotoa ushahidi wa uwongo wote hawa hakimu wa sharia kwa kiasi cha hatia yao atawapa adhabu.

8) Adhabu Mbalimbali:Ikiwa mtu ametenda mambo machafu k.m. kumuingilia mnyama lazima apigwe viboko, na ikiwa mtu balehe akiendelea kutenda hayo, kwa mara ya nne atahukumiwa kuuwawa.

Ikiwa yule mnyama aliotendewa ni miongoni mwa wanyama wa halali (kama ng’ombe na mbuzi) baada ya kutendewa kitendo hicho kibaya nyama yake huwa haramu kuila, na baada ya kutendewa machafu hayo akizaa watoto wake pia nyama yao huwa haramu, kwa hivyo mnyama yule lazima kwanza achinjwe, na baada ya kuchinjwa mwili wake utiwe moto na kufanywa jivu. Yule mtu aliemtenda mabaya lazima alipe thamani ya mnyama huyo kwa mwenyewe.

Ikiwa huyo mnyama amechanganyika na wanyama wenziwe hajulikani hana alichotendewa basi huainishwa kwa njia ya kura.

Na ikiwa huyo mnyama aliotendwa, si mnyama ambaye kwa kawaida huliwa kama farasi na mfano wake, mnyama huyo achukuliwe mji mwingine huko auzwe na pesa zake zitolewe sadaka, na yule mtenda amlipe mwenye farasi kima chake.

Njia ya kuthibiti kitendo hicho kibaya ni mbili:-(a) Mtendaji mwenyewe akiri mara mbili au(b) Mashahidi waadilifu wawili watoe ushahidi.

Ikiwa mtu amezini na maiti ni kama amezini na mtu aliye hai na hukumu yake ni sawa, lakini katika kesi kama hii adhabu huwa kali zaidi. Na ikiwa ametenda hayo na maiti ya mkewe au mjakazi, hakimu wa sharia atampa adhabuya kumuadhiri.

Page 187: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

180

Njia ya kuthibitisha kitendo hicho ni ile ile, kwani wanatakiwa mashahidi wanne waadilifu kama uzinzi wa mtu hai, na pia hukumu ni hiyo hiyo kuhusu kulawiti.

Na ikiwa mtu anapiga punyeto, hakimu wa sharia atampa adhabu ya ‘Taazeer’ viboko kiasi atavyoona hakimu.

Kila mtu anayo haki kiasi awezavyo kulinda roho yake, mali, watoto na heshima ya watu wake wa nyumbani, lakini kwanza atumie njia rahisi, na kama haikufaa pole pole atumiye nguvu zaidi hata mshambuliaji amwondowe.

Ikiwa mtu bila ya ruhusa kwa kuparamia akachungulia ndani ya nyumba ya watu akatazwe, lakini akiendelea kufanya hivyo, wenye nyumba wanayo haki kwa kumtupia mawe au njia nyingine, wamwondowe na kwa kufanya hivyo, akiumia au kufa hakuna lawama, damu yake imekwenda bure.

Kisasi na Malipo: Kuua kwa kusudi kumekatazwa na sharia na ni dhambi kubwa kabisa na ni uharibifu mkuu. Mwenyezi Mungu katika Qur’an Tukufu kuhusu jambo hili baya Anasema:“Na mwenye kumwua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu, atakaa humo milele.” (4:93).

Vivyo hivyo kosa la kumkata (mtu) au kumlemaza kiungo katika viungo vya mwili, ni katika maasi makubwa.

Kwa vyovyote kuhalifu peke yake (ikiwa Kuuwa, kukata au kulemaza viungo) yote hayo yanakuja katika namna tatu hizi:

1) Kuuwa kwa makusudi2) Shabihi ya makusudi3) Lisilokusudiwa.

Kuuwa makusudi ni kosa dhahiri lisilohitajia maelezo. Ama shabihi ya makusudi (amekusudia jambo lingine na limekuwa lingine) kwa mfano mtu anampiga mwenziwe kwa kiasi cha kumtia adabu si kwa

Page 188: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

181

nia ya kumuuwa, lakini kwa bahati mbaya yule mtu akafa, au mfano mwingine ni kama vile umempa dawa mwenziyo ya kumponesha (kuondoa maumivu) na kwa bahati mbaya kwa kutumia dawa ile akafa, yote hayo ni mifano ya kufahamisha ‘Shabihi ya maksudi’.

Ama kitendo kisichokusudiwa, maana yake kamwe hakuwa na kusudio hilo, kwa mfano mtu amekamata bunduki kumwinda ndege na kwa bahati mbaya ikampiga mtu, au mtu amekamata bunduki na mara ikafyatuka risasi na kumuuwa mtu.

Moja katika mifano iliyodhahiri ya tendo lisilokusudiwa ni kosa analolifanya mtu aliyelala usingizi, au kufanya neno kwa kusahau, au bila kufahamu.

Vitendo afanyavyo mwendawazimu au mtoto asiyefahamu akafanya jambo la kitoto, na pia mtoto mwenye kufahamu madhali anaitwa mtoto kitendo chake hata kama kakusudia pia katika sharia inaingia katika hukumu ya namna ya tatu.

Ikiwa mtu amekusudia kumuuwa mtu fulani asiye na hatia, na kwa bahati akampiga mtu wa tatu akafa, na wote hao wawili ni miongoni mwa wale ambao damu zao lazima zilindwe, basi kwa hivyo atahukumiwa kosa la makusudi. Lakini ikiwa alikusudia kumuua mtu mwenye hatia ya kuuwawa kwa bahati ikampiga mwingine, kitendo hicho kwa sharia kinahukumiwa katika namna ya pili.

Jambo hili ni lazima likumbushwe kwamba, katika visa vyote tulivyovitaja hakuna tofauti yoyote kati ya mtu mwenyewe kutenda kosa, na kusababisha kwa kupanga mpango ya kuuwawa yule mtu (kitendo kiwe namna ile hata isemekane kuwa fulani amemtendea) na pia hakuna tofauti dhambi (kosa) hiyo aitende mtu mmoja peke yake au kwa kushirikiana na watu au mtu mwingine, zote hizo ni haramu, na mtenda au watenda watapewa adhabu ya Kisharia.

Ama kwa shauri ya hukumu, kisasi hutumika katika kitendo cha makusudi tu, lakini kwa kutokusudia kosa au kwa shabihi ya makusudi adabu yake ni ‘Diyah’ tu.

Page 189: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

182

Na katika kisasi mhalifu lazima awe ameshabalehe mwenye akili, kwa hivyo mtoto asiye balehe hata kama amefika umri wa miaka kumi hana kisasi, kama jinsi hiyo amefanyiwa mtoto au mtu mzima, na pia mwendawazimu hana kisasi, kama wazimu wake wa daima au wa kipindi, wakati wa kumjia uwazimu akitenda jinai, ikiwa mtendwa ni mwenye akili, au majununi kama yeye kwa vyovyote hana kisasi. Kwa sababu kusudio lake kwa sharia ni kosa tu (anaingia namna ya tatu) atatoa Malipo, (na malipo hiyo watalipa jamaa zake upande wa baba kama ndugu, ami na binamu.) Hizo zilikuwa sharti za kisasi kuhusu jinai (mtenda uhalifu).

Ama kuhusu mtendwa (mtu aliyetendewa kosa) na yeye pia lazima awe balehe na mwenye akili, kwa hivyo ikiwa mtendwa ni mtoto hana kisasi bali ‘Diyah’ (malipo) tu. Lakini baadhi ya Wanachuoni wanasema hapa pia kuna kisasi, na pia kuhusu mwendawazimu hukumu ni hiyo hiyo.

Sharti nyingine katika sharti za kisasi ni kuwa jinai asiwe amelazimishwa kutenda jinai hiyo, lakini sharti hii inahusu jinaya isiyokuwa ya kuuwa; ama kuhusu kuuwa kwa kulazimishwa hakuibadili hukumu, maana yake mtu hawezi kwa udhuru wa kuwa alilazimishwa alikuwa hana njia (majuburu), kwa hivyo kwa kumuuwa mtu asie na hatia hakuna ‘taqiyah’ na itabidi kutolewa kisasi na kuuwawa, na yule aliyemlazimisha atafungwa maisha.

Sharti nyingine ni kuwa mtendwa asiwe na hatia na pia asiwe miongoni mwa wale ambao sharia imeruhusu kuuwawa.

Ikiwa jinai imetendwa na baba au babu (na kwenda juu au chini wote) wa mtendwa (aliouwawa) hana kisasi lakini kuna malipo, na malipo haya watapewa warithi wote na alietenda hana sehemu humo. Na pia kisasi kipo kwa Mwislamu akimuuwa Mwislamu mwenziwe, vile vile mwanamume huru kwa mwanamume huru, au mwanamke huru kwa mwanamke huru.

Ikiwa mwanamume huru kwa kumuuwa mwanamke huru (akalipizwa kisasi) na akauwawa, inabidi msimamizi wa yule

Page 190: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

183

mwanamke alipe nusu ya ‘Diyah’ awalipe jamaa za yule mwanamume, kwa sababu ‘Diyah’ ya mwanamume ni mara mbili zaidi.

Lakini ikiwa kinyume chake, yaani ikiwa mwanamke huru kamuuwa mwanamume huru na akalipizwa kisasi kwa kuuwawa, basi si lazima kulipwa ‘Diyah’ jamaa za mwanamume huyo kwa sababu mwenye kutenda jinai hana jinai zaidi ya nafsi yake.

Faini ya Mwislamu huru ni ngamia mia, au ng’ombe mia mbili, au kondoo elfu moja, au visua mia mbili, (kila kisua kimoja moja kina nguo mbili) au Dinar elfu moja.

Kama tulivyoeleza nyuma kuwa, mtu akiuwawa makusudi wazee (walinzi) wa mtu aliouawa wanayo haki ya kuchukuwa kisasi (kamuuwa mwuaji) lakini wakiridhika kupokea faini, tena hakuna kisasi, na faini hiyo isichelewe kulipwa mwisho muda wake ni mwaka mmoja.

Lakini kwa kosa la shabihi ya makusudi, ni fidiya (dia) tu, na dia hiyo lazima kuitowa kati ya miaka miwili, vivyo hivyo kosa lisilokusudiwa ni kulipa dia tu na muda wa kulipa ni kati ya miaka mitatu, kwa uchache kila mwaka kiasi thuluthi ya malipo alipe.

Amma kosa ambalo husabisha upungufu wa mojawapo ya viungo vya kiwiliwili kama kukata mkono, au kupofowa jicho n.k. ikiwa kitendo hicho kilikuwa cha makusudi inawezekana kuchukuliwa kisasi, kama inavyoeleza Qur’ani Tukufu: “Jicho kwa jicho, pua kwa pua, sikio kwa sikio, na jino kwa jino, pia kisasi kitakuwa katika majeraha.” (6:45).

Ikiwa kosa hilo lisilokusudiwa, au shabihi ya makusudi kwa kila kiungo kuna dia mahsusi, baadhi ya dia ni kiasi cha dia ya bianadamu (Dinar elfu na kama hizo) na baadhi ni nusu dia tu, na baadhi kasoro kuliko nusu. Kwa jumla viungo ambavyo viko kimoja kimoja tu kama pua au k.m. uume hivyo hulipwa kwa dia kamili, na vile viungo ambavyo viko viwili viwili kama jicho, sikio, mikono, miguu, ikiwa kimoja kimepotea dia yake ni nusu, na kama vyote viwili vimepotea dia itakuwa ni kamili. Diya ya kitendo cha makusudi na

Page 191: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

184

shabihi ya makusudi ni juu ya mwenye kutenda jinai ile alipe, lakini dia kwa kosa lisilokusudiwa ni juu ya jamaa zake upande wa baba walipe.

Huu ulikuwa muhtasari wa itikadi ya Shia kuhusu kisasi na dia, maelezo zaidi kuhusu hayo hupatikana katika vitabu vikubwa vilivyotajwa juu ya mambo hayo, kama ambavyo hatukutaja vitabu vingi vya fiqhi na milango ya fiqhi kufutana na itikadi za Shia, k.m. milango ya kununua na kuuza inayohusisha manunuzi ya kutoa pesa mbele na mali iliyonunuliwa kukabidhiwa baada ya muda, saraf na uuzaji wa matunda, uuzaji wa wanyama, na pia kukodisha, kuweka kitu rehani, kuazima, kuweka amana, kilimo, kumwagilia, mashindano, kuweka dhamana, hawala,149 kafara, na milango mingi ya Fiqhi ambayo hatukuitaja. Kama tulivyosema mwanzoni kwamba lengo letu ni kuonesha na kufahamisha kwa muhtasari tu, kwa hivyo katika kitabu hichi tumewapeni faharasa na anwani za itikadi za Shia Imamiyah, na huu ni mfano mdogo kabisa ambao mtu anaweza kuzijua itikadi za Shia kwa ujumla, na kufahamu mizizi na matawi ya dini kwa dalili na thibitisho za kiakili, na pia kujua uwezo wa elimu ya dini na namna ya kufikiri na kufahamu kwao Shia.

Enyi wanavyuoni wa Kiislamu, enyi viongozi wa dini, je haya yote tuliyoyaeleza kuhusu itikadi za Shia, kuna jambo gani katika hayo lenye kuvunja dini ya Kiislamu? Je katika hayo yote ni kipi kinachotokana na Uyahudi, Ukristo, Umajusi au Uzardoshti?

Je ni kipi kimojawapo katika uchambuzi tulioufanya ambacho kiko kinyume na kanuni na sharia ya Uislamu au hakikubaliani na Qur’ani na hadithi na Sunna za Mtume (s.a.w.w.)?

Je! Haujafika wakati ambapo watu waadilifu wenye elimu na wenye kujua waamuwe wazi wazi na kutoa hukumu kuhusu jambo hilo, na waaache uzushi wao na masingizio yao ya kijinga?

149 Hawala: Maana yake, ni mtu kuwa na pesa zake au mali iliyoko kwa mtu fulani, kisha kukawa na mtu mwingine mwenye shida, basi huyu mwenye pesa au mali ile akaitatua shida ya huyu kwa kumwambia kuwa aende kuchukua mali au pesa hiyo kwa yule aliyewekezewa.

Page 192: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

185

Bila kwa kufanya hivyo huenda Mwenyezi Mungu atatufanya tuwe kitu kimoja na kuyaunganisha mambo yetu, kisha atatuondolea utengano, na Waislamu wote wawe chini ya benderea ya Qur’ani Tukufu ili tu heshima yao na utukufu wao urejee kama ulivyokuwa hapo zamani.

Lazima tufahamu matamanio yetu haya makubwa kamwe hayatatimia, na wala heshima ya Waislamu haitarudi isipokuwa wenyewe waondoe ushupavu wa kimadhehebu na kikabila usiohalali uliyoko kati yao.

Mimi maneno yangu haya nayakariri sana kwamba ni lazima sisi tuyaheshimu madhehebu yote ya Kiislamu na zaidi ya hapo hatuna budi tulilinde lile lengo la uhai wa Umma ambalo ni upendano kati ya ndugu Waislamu na kushirikiana katika mema, ili Muislamu huyu amfaidishe yule na huyu naye afaidike kwa mwingine. Isitoshe kila mmoja ampendelee ndugu yake kile akipendacho na wala wasifanyiane kiburi na ujeuri na kutaka ukubwa juu ya wenziwao, bali chochote wakipendacho wao, kwa imani na uhalisi wawapendelee wenziwao.

Hakika inawezekana baadhi ya watu wakajiuliza kwamba, baada ya kuweko hitilafu na ubishano kati ya Waislamu, vipi inawezekana kuwepo mahaba na upendano kati yao? Hii ni kama ndoto na jambo lisilowezekana. Lakini kwetu sisi Waislamu haifai kutokuzitumainia rehema za Mwenyezi Mungu, na tusikate tamaa katika rehema zake Mwenyezi Mungu. Kutia roho mpya katika kiwiliwili cha Umma kilichokufa na kuupa maisha mapya, na kuona baada ya kupofoka, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu inawezekana Insha-allah.

MWISHO

Kuna mambo mawili ambayo ni miongoni mwa mambo ambayo watu wanawashutumu na kuwadharau Shia kutokana na mambo hayo.

1) Itikadi ya Badaa – Wako baadhi ya watu wanawaza kwamba, Shia wanaamini kuwa, Badaa maana yake ni kuwa, inawezekana

Page 193: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

186

likawepo jambo ambalo hudhihiri kwa Mwenyezi Mungu ambapo hapo kabla hakulijua, na baada ya muda akalijua. Lakini je! yupo japo mtu mmoja mwenye akili na maarifa inawezekana akafikiri namna hii juu ya Mwenyezi Mungu? Je maneno kama haya si kufuru tupu tena ya kufadhaisha? Kwa sababu (kwa kuamini hivyo) inapasa awe kamsingizia Mwenyezi Mungu Mtukufu ujinga na kutokuwa na maarifa na kumdhania kwamba Yeye (Mola) yupo katika hali ya kupatikanwa na mabadiliko (yaani siku moja hakujua kitu na siku ya pili akakijua). Kwa hali ya namna hii vipi itawezekana Yeye (Mwenyezi Mungu) Awe asiye na mwisho wala mwanzo?

Mwenyezi Mungu apishembali, sivyo kabisa kwa Shia Imamiyah, bali hata vikundi vingine vya Waislamu hawaitakidi itikadi mbovu kama hii!! Itikadi ambayo ni ujinga na upotevu halisi.

Naam itikadi za kiupuzi na za kuchekesha kama hizi wanadhaniwa kuwa nazo kundi la “Mujas-Samah” wale ambao wanaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu Anacho kiwliwili. Mojawapo katika itikadi zao za kuchekesha kuhusu Mwenyezi Mungu, wanasema hivi kuhusu kiwiliwili cha Mwenyezi Mungu: “Nisameheni kuhusu ndevu na utupu tu, lakini mengine niulizeni mnachotaka.”!

Amma maana halisi ya Badaa ambayo Shia ndiyo wanavyoitakidi, na kuwa hizo ni miongoni mwa siri na elimu walizopewa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) kiasi kwamba imepokewa katika mapokeo (ya hadithi) zao kuelezwa hivi: “Hakuna njia yeyote ambayo kwayo wajibu upasavyo wa kumuabudu Mwenyezi Mungu umetekelezwa kwa uzuri kabisa kuliko Badaa, na asiyeitakidi ‘Badaa’ hakumfahamu na kumjua Mola wake.”150 Na mifano mingi kama hiyo.

Hii ‘Badaa’ ni ibara inayo maanisha kuwa, Mwenyezi Mungu kulidhihirisha jambo lililoko kwenye ubao wa kutangua na kuthibitisha (The tablet of erasure and subtitution) “Al-mahw wal ithbaat” kwa njia ya mojawapo katika Malaika kutoka kwenye ubao huo “Al-mahw wal-Ithbaat” na huyo Malaika kumpasha Mtume, na Mtume huwapasha habari hiyo umma wake kuwa kutajiri tukio

150 Kitabul-kafii juz 1 uk 113 mlango wa Albadaa.

Page 194: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

187

fulani, lakini baadaye jambo hilo halijiri, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amelifuta jambo hilo na badala yake tukio jingine likawekwa badala yake, na hapana yeyote ulimwenguni ajuaye uhakika huu isipokuwa Yeye Mwenyewe Mola. Kwa sababu hiyo ni daraja ya elimu iliyofichwa na Mwenyezi Mungu, wala hakuna Mtume au Malaika yeyote kuweza kujua wala Walii. Na hii ndiyo ile ngazi ya elimu inayosemwa katika Qurani kuwa ndiyo msingi wa kitabu, ‘Ummul-Kitaab’ kama inavyobainisha juu ya maana ya Badaa na juu ya Msingi wa Kitabu kwa kusema, Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo na kuthibitisha, na asili ya hukumu iko kwake. (13:39)

Lakini Mitume na Malaika wanapata kujua kutoka kibao cha ‘Al-Mahw Wal-Ithbaat’ na elimu zao haipindukii haya na katika Qur’ani imefafanua hivi:Inamkinika baadhi ya watu wasiokuwa na maarifa ya kutosha wakadhani kwamba kuficha uhakika na kujulisha kingine ni kama kueleza kinyume cha tukio na itakuwa ni kisukumizo kinachopelekea kwenye ujinga. Lakini lazima tufahamu kwamba mambo kama haya bila shaka ziko faida na masilahi na kuna hekima na siri ambazo akili za kawaida haziwezi kuzifahamu.

Kwa sababu ya kufahamika vizuri uhakika huo lazima tulinganishe kati ya ‘An-Naskh na Al-Badaa’. Twajua kwamba kufutwa kwa sharia na hukumu kwa Waislamu wote wanajuzisha. Kama ambavyo kufuta hukumu na kuibadilisha kwa kuleta hukumu nyingine kuna siri nyingi na maslahi mengi, baadhi ya siri na maslahi hayo yako dhahiri na mengine hayako dhahiri. Hali ni kama hiyo hiyo katika ulimwengu juu ya baadhi ya mambo kufichikana na mengine kudhihirika. Kwa hiyo sehemu fulani ya Badaa inapatikana kutokana na baadhi ya nafsi zenye maungamano na ulimwengu wa kiroho kuyaona mambo fulani bila kufahamu sharti zake wala vizuizi vyake. Kwa mfano, Nabii Isa (a.s.) aliona kwamba bwana harusi atafariki usiku ule wa harusi yake, lakini hakuona kuwa kulikuwa na sharti ya kuwa hilo litatimia tu iwapo jamaa zake hawatatoa sadaka. Lakini kwa bahati mama wa bwana harusi akamtolea sadaka bwana yule. Wakati huo Nabii Isa (a.s.) tayari alikwisha eleza kuwa bwana yule atafariki usiku wa harusi yake, lakini ikawa hakufariki. Alipoulizwa

Page 195: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

188

akasema, “Bila shaka ninyi mumemtolea sadaka, na sadaka inaweza kuondosha jambo ambalo limekwisha kupitishwa.”151

Pengine faida ya matukio kama haya huwa ni majaribio kwa watu ni vipi wanajiandaa kutii amri za Mwenyezi Mungu, kama vile kisa cha Mtume Ibrahim (a.s.) alipoamrishwa kumchinja mwanawe mpenzi Ismail (a.s.).

Kwa hakika isingelikuwepo ‘Badaa’ basi mambo, upaji wa sadaka, mateteo, upendano, kulia kwa Mitume na wapenzi wa Mungu, na hofu kubwa waliyokuwa nayo Mitume mbele ya Mwenyezi Mungu ijapokuwa walikuwa watiifu bila kiasi kwa Mola wao, yote hayo yangalikuwa hayana maana.

Ni dhahiri sababu ya kuogopa na kutetemeka kwao ilikuwa ile hazina ya elimu iliofichwa ambayo kiumbe mwingine haijui na ile ndio shina na asili ya Badaa.

Yeyote atakayekujua zaidi kwa kirefu kuhusu Badaa, Qazaa, na Qadar, na Lawh Al-Mahw-Wal-Ithbaat, na aangalie kitabu changu Ad-Deen wal Islam, Juzuu ya kwanza humo atayakuta yote.

Jambo la pili ambalo Shia wanashutumiwa na kulaumiwa ni Taqiyyah, na inahisabiwa kuwa ni moja katika aibu ya wafuasi wa madhehebu ya Shia.

Chanzo cha makinzano kuhusu jambo hili ni kuwa wao makusudio na uhakika wa jambo hilo hawaufahamu, na inasikitisha kusema kuwa hata hawakufanya uchunguzi kulifahamu jambo hilo! Iwapo kuhusu jambo hilo wangelihakikisha na kuchungua na kuwa na subira na kuvumilia, kwa upesi wangelijua hakika na ukweli wake kuwa Shia pekee tu ndiyo wanaoitakidi jambo hilo, bali jambo la Taqiyyah kwa upande wake ni jambo lenye hoja za kiakili na linakubaliana na kanuni na matakwa ya maumbile.

Na hii pia tunajua kwamba amri na sharia zote za Kiislamu zafuatana

151 Al-Aamaali cha Shaikh Sadouq.

Page 196: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

189

bega kwa bega na akili na elimu na hata kiasi cha ncha ya unywele haziachani na vitu viwili hivi (yaani akili na elimu).

Tukihisabia tabia ya kibinadamu utakubali kwamba ni faradhi isiyobudi, kwa kila mtu kulinda roho yake na uhai ni kitu cha thamani sana.

Naam ikiwa heshima ipo hatarini, au wajibu wa kulinda ukweli, hapo maisha hukosa thamani kwa sababu tu ya kulinda heshima au ukweli na kupigana na batili, mtu huitumia roho bila ya kuithamini.

Je, mwenye akili yupi anayeweza kusema kwamba kinyume cha mambo tuliyoyataja, na bila ya lengo takatifu la kidini, mtu anaruhusiwa kuiweka roho yake hatarinini? Ni dhahiri akili wala sharia haitampa ruhusa mtu yeyote kujiingiza hatarini. Basi lengo na maana ya Taqiyyah hakuna isipokuwa hili.

Uislamu wazi wazi umeruhusu kwamba binadamu ikiwa roho, mali, au heshima yake iko hatarini asidhihirishe itikadi yake wakati huo, bali kwa kwa kificho afuate itikadi yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani Tukufu: “Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya waumini. Na na yefanya hivyo, basi hatakuwachochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni, na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.” (3:28.) “Isipokuwa yule aliyeshurutishwa hali moyo wake umetulia kwa imani.” (16:106)

Na kisa cha Ammar na wazazi wake wawili pamoja na baadhi ya Masahaba ni kisa mashuhuri pale walipokuwa wakiadhibiwa na washirikina kwa kuwalazimisha wafanye ushirikina, nao walidhihirisha kufru na wakaficha imani.

SHARTI ZA TAQIYYAH

Jambo ambalo ni muhimu sana na yafaa kuangaliwa vema ni kwamba Taqiyyah kila mahala inahukumu mbali mbali. Pengine huwa faradhi, pengine ni haramu na pengine pia huwa halali.

Page 197: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

190

Kuna hukumu tatu za kufanya Taqiyyah:1. Wakati ambapo roho itapotea bila ya faida yoyote, basi Taqiyyah

hapo ni faradhi.2. Ikiwa kwa kudhihirisha neno la kweli itasaidia na kuleta faida

hapo ni hiari (si lazima) kufanya au kutofanya Taqiyyah ni halali. 3. Ikiwa kufanya Taqiyyah kutasababisha au kuipa nguvu batili na

dhuluma basi hapa Taqiyyah ni haramu na imekatazwa, lazima katika mambo kama haya mtu ajitolee na kukabili yatakayomfika.

Hebu sasa wacha tutoe mwanga juu ya mambo haya ili mtu mwaminifu na mwenye bidii apate kujua tena kwa urahisi ili aamue je, Shia wanastahiki kulaumiwa kwa kufuata Taqiyyah (iwapo lawama hiyo itathibitishwa kuwa ni kweli)? Au kwamba lawama hiyo yafaa kulaumiwa wale watu ambao wamewanyang’anya Shia uhuru wa kutekeleza imani yao na kuwalazimisha wafanye Taqiyyah? Kama ni hivyo, basi wakulaumiwa si Shia, bali hao waliowalazimisha Mashia kuingia ndani ya Taqiyyah ndio wakulaumiwa.

Sisi tunasoma katika historia kwamba, Muawiyah alinyakuwa utawala wa Islamu bila ridhaa ya Waislamu, akaichezea sharia na akawatwanga na kuwauwa Mashia wa Ali (a.s.), popote anapowapata licha ya hao hata wale ambao wakitiliwa shaka au kudhaniwa kuwa ni Mashia hakuwaachia. Damu ya Shia aliifanya kuwa ni kitu kisicho na thamani kuliko maji. Kizazi chote cha Umayyah na kizazi cha Mar-wan pia walifuata mtindo huo kwa kuwaadhibu na kuwauwa Mashia.

Ilipofika wakati wa enzi ya kizazi cha Bani Abbas, licha ya kuwafuata Bani Umayyah katika maovu yao, wao walifanya mambo ambayo waliopita kabla yao hawakupata kuyafanya.

Wakati ule unadhani Mashia wangaliweza kufanya nini? Hakuna kingine bali iliwabidi kuficha imani yao na kufanya Taqiyyah, na wakati mwingine kufuatana na hali iliyokuweko wakidhirisha imani yao kupigana na ubatili na upotovu, ili kuudhihirisha ukweli usije ukapotea miongoni mwa watu.

Page 198: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

191

Na kwa sababu hiyo watu wengi miongoni mwa viongozi wakubwa wa Kishia wao waliitupilia mbali Taqiyyah na wakajitolea kunyongwa au kuuwawa.

Je, wewe unayo kumbukumbu ya Mashahidi wa ‘Marj Adhra’?152 Wao walikuwa watu kumi na nne miongoni mwa viongozi wakubwa na mashuhuri wa Kishia, wakiongozwa na Sahaba Mtukufu Hujr ibn Adiyyi Al-Kindi.

Hujr ibn Adiyyi alikuwa kiongozi wa jeshi la Waislamu walipouteka mji wa Sham, lakini Muawiya aliwauwa watukufu wote hao kumi na wanne kwa ukatili, na baadaye huyo Muawiyah akasema, “Kila niliyemuuwa nilikuwa nafahamu ni kwa sababu gani nimemuuwa isipokuwa Hujr ibn Adiyyi, sikujua kosa lake lilikuwa nini.”

Mimi ninamwambia Muawiyah kuwa, “Kosa la Hujr lilikuwa ni kuacha kutumia Taqiyyah, kwa sababu lengo lake lilikuwa kuutangaza uovu wa Bani Umayyah na kuonesha ni kwa kiasi gani walikuwa hawana uhusiano na dini ya Kiislamu.”

Je unakifahmu kisa cha Sahaba Mtukufu Amr ibn Hamaq Al-Khuzai na Abdur-rahman ibn Hisaan Al-Anzi ambao Ziyad aliwazika wakiwa hai huko Qas-An-Naatif? Je, jambo kama hili ni la kusahaulika?

Je makumbusho ya kuuwawa Bw. May-Tham At-Tammaar, Rashid Al-Hajari, na Abdallah ibn Yaqtar ambao walisulibiwa katika uwanja wa mjini Kufa yatasahaulika?

Hawa na mamia kama hawa ambao roho zao tukufu waliziona hazina thamani, wakazitoa katika njia ya kutetea haki, hawakukubali mpaka wakauliwa na wala hawakuona kuwa kuna haja ya kufanya Taqiyyah. Hii ina maana kwamba, lau wangefanya Taqiyyah na wakanyamaza, basi haki isingetambulikana na watu wengine wasingeliitambua tena, na dini ya Kiislamu ingalikuja katika sura ya Muawiya, Yazid, Ziyad na Ibn Ziyad. Yaani ingalikuwa dini ya hadaa, uhaini na unafiki na

152 Kijiji kilichoko katika mji wa Sham.

Page 199: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

192

ingalikuwa dini yenye kila aina ya ubaya na uchafu. Hivyo basi dini hiyo ingelikuwa mbali mno na mafunzo ya Uislamu ambayo ni mafunzo yanayoelekeza kwenye wema. Naam hawa walikuwa ni mihanga ya Uslamu na mashahidi wa njia ya haki na wema.

Usikisahau kisa cha mashahidi wa Karbala ambao ni Hussein na wasaidizi wake wapenzi (a.s.) ni jambo linalojulikana kwa watu wote. Hao walikuwa ni viongozi wa mashahidi wa njia ya haki na mabwana wa mashahidi.

Naam hao kwa mambo yaliyowakabili waliona kuwa kufanya Taqiyyah kwao ni haramu na ni lazima wadhihirishe haki. Pamoja na hayo kuna wengine ambao wanaweza kuona kuwa kufanya Taqiyyah ni jambo la wajibu, na huenda wengine wakaona kuwa ni jambo linalojuzu kutegemeana na mazingira na maeneo yanayohusika. Ninakumbuka naliona katika baadhi ya habari kwamba Musailimatul-Kadhdhaab aliwakamata Waislamu wawili, akawalazimisha wakiri kwamba yeye ati ni mjumbe wa Mungu na Muhammad (s.a.w.w.) si Mtume. Mmoja kati yao akasema, “Nashuhudia kuwa Muhammad (s.a.w.w.) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nawe Musailimatul-Kadhdhaab ni mwongo”, Musailimah akatoa amri yule mtu akauwawa. Ama yule mtu wa pili akakiri alichokitaka Musailimatul-Kadhdhaab akamwachilia huru.

Habari hii ilipomfikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, “Mtu wa kwanza alifanya haraka kwenda peponi, na wapili pia akangojea amri, na kila mojawao atapata malipo yake.”

Enyi Waislamu! Msifanye mambo yatakayowalazimisha ndugu zenu kufanya Taqiyyah, na baadaye mkawalaumu wao kuwa kwa nini wanafanya Taqiyyah!

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Ajaaliye hatima yetu iwe njema na Waislamu wote wawe kitu kimoja kuelekea kwenye haki.

Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakātuh

Page 200: Asili ya Ushia na Misingi Yake - Home - Shia Maktab

ISBN 9987 620 42 6

أصل الشيعة وأصولها

محمد الحسين آل كاشف الغطا

B I L A L M U S L I M M I S S I O N O F TA N Z A N I A

S.L.P: 20033, dar es salaam, tanzania