moduli ya mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/moduli ya mwalimu-misingi ya kuandika.pdf · mafunzo ya...

24
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI YA KUANDIKA Moduli ya Mwalimu

Upload: hoangque

Post on 10-Sep-2018

465 views

Category:

Documents


15 download

TRANSCRIPT

Page 1: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III

Moduli ya Kumi: MISINGI YA KUANDIKA

Moduli ya Mwalimu

Page 2: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI
Page 3: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

1Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiOfisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu TanzaniaChuo Kikuu cha Dodoma

Chuo cha Ualimu MorogoroChuo Kikuu cha Dar Es SalaamChuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu MkwawaEQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U ButimbaC.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.U Ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga C.C.U BundaC.C.U Tarime

C.C.U ShinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 4: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

2 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Namna ya kutumia moduli ya mwalimuModuli hii ina vipengele vifuatavyo katika kuifanya iwe rafiki kwa mwalimu: 1) Maudhui ya Moduli; 2) Dhana Kuu; 3) Malengo ya Moduli; 4) Maelekezo Muhimu kuhusu Moduli; 5) Taratibu za kujifunza kwa kila kipindi cha mafunzo.

Moduli hii imekusudiwa kutoa fursa kwa mwalimu kusoma na kujifunza kwa vitendo kwa kushirikiana na walimu wenzake pamoja na Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule. Baada ya kila kipindi cha mafunzo, mwalimu anategemewa kutumia mikakati ya ufundishaji na kujifunza darasani kwa lengo la kujenga umahiri wa mwanafunzi wa kusoma. Aidha, moduli hii inatoa maelekezo yaliyo ya wazi na yenye kufuata hatua kwa hatua katika uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia stadi za kusoma na kuandika.

Moduli hii ina kipengele cha ufuatiliaji na tathmini ambacho hutoa nafasi kwa mwalimu kutoa mrejesho kuhusu dhana na maudhui ya moduli, uwasilishaji wa Mratibu wa Mafunzo ya Mwalimu Kazini na ushiriki wa walimu wakati wa mafunzo kwa lengo la kuboresha mafunzo ya walimu kazini ngazi ya shule.

Page 5: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

3Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO NA TASWIRA KATIKA MODULI

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Zifuatazo ni mifano ya taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu mwalimu anafanya kazi na mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya KUFUNDISHA wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.

Page 6: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

4 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MODULI YA 10: MISINGI YA KUANDIKA

MAUDHUI YA MODULIModuli ya 5 – 8 inahusu dhana na mbinu za KUFUNDISHA kusoma ambazo zinaendana na mabadiliko yaliyo kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Moduli hii pia inahusu baadhi ya dhana na shughuli kama zilivyoanishwa kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Moduli hii inahusu misingi ya kuandika. Ujuzi wa kuandika siyo tu unawasaidia wanafunzi kuwasilisha mawazo na taarifa, pia kuwa na uwezo wa kuandika vizuri kunakoendana na uwezo wa mwanafunzi kusoma na kuelewa matini. Kwenye moduli hii, utajifunza mbinu za kuwafundisha wanafunzi namna ya kuandika, herufi za alfabeti, namna ya kutumia ujuzi wao wa foniki na herufi kuandika maneno. Somo la kuandika litaendelea kwenye moduli ya 13, ambapo utajifunza zaidi kuhusu kuandika na kusoma vinavyofanya kazi pamoja ili kumsaidia mwanafunzi aweze kusoma na kuandika.

DHANA KUU1. Kuandika herufi moja moja – tumia mistari na vitanzi kutengeneza kila herufi moja moja ya alfabeti2. Kuandika maneno au ‘Kuficha’– Kinyume cha ‘kuhusianisha’ ambapo wanafunzi wanabainisha

neno ambalo wanataka kuandika, wanaligawa kwenye sauti moja moja, na halafu wanaandika herufi inayoendana na kila sauti.

3. Vitamkwa Vumbuliwa – ni pale ambapo wanafunzi wanajaribu kuficha maandishi lakini wakapata kitamkwa kisicho sahihi kwa sababu baadhi ya maneno hayatamkwi kama inavyotakiwa. Hivyo wanafunzi wanapaswa wafanye mazoezi ya ujuzi wao wa foniki na watajifunza utamkaji sahihi baada ya kuona neno mara nyingi.

4. Waandishi wanaotumia mkono wa kushoto – wanafunzi ambao kwa asili wanaandikia mkono wa kushoto. Hawa hawapaswi kulazimishwa kuandikia mkono wa kulia kwa sababu uamuzi huo utaharibu uwezo wao wa kujifunza na kuwa makini.

MALENGO YA MODULIMwisho wa moduli hii, walimu watakuwa na uwezo wa:

1. Kuwajengea wanafunzi umahiri wa kuandika wakiwemo wanafunzi wanaoandikia mkono wa kushoto.2. Kuelewa namna na kwa nini kuficha maandishi kupitia uandishi kunasaidia katika kusoma3. Kutumia shughuli na mbinu za kuimarisha ujuzi wa mwanafunzi katika kuandika na kuficha maandishi4. Tengeneza chati za mifukoni kusaidia mbinu za herufi/alama za uandishi

MAELEKEZO MUHIMU Njoo na vitu vifuatavyo:

1. Moduli ya mafunzo ya walimu kazini na kalamu

TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama

inavyoonekana katika picha2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki

wote waonane na kuongea kwa pamoja3. Waeleze walimu wawe huru kuuliza maswali

kama hawajaelewa4. Waeleze walimu kuwa msaada kwa wenzao5. Waeleze walimu kuwa wabunifu na kufikiria

dhana watakazojifunza na jinsi zitavyohusiana na darasa lao

6. Waeleze walimu waweke simu zao katika hali ya mtetemo

Page 7: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

5Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

Katika kipindi cha mwisho tulisoma kuhusu kutenganisha na kuunganisha fonimu. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa KUFUNDISHA maudhui ya moduli hiyo darasani kwako.

ANDIKA PEKE YAKO (DAKIKA 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.

JADILIANA KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)1. Shirikisha wenzako kwenye kundi mojawapo kuhusu uzoefu huo. 2. Kwa kila changamoto, pendekeza namna ya kukabiliana nayo.3. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.

Mafanikio(Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)

Changamoto (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)

Njia Muhimu za Ufumbuzi(Mawazo muhimu na mahususi kwa wenzetu)

Page 8: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

6 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

ZOEZI LA KUCHANGAMSHA (DAKIKA 10) Leo tutaanza na shughuli za kuandika. Anza kwa kujaza herufi zinazokosekana kwenye chati iliyoko hapa chini.

Sasa, jaza herufi za alfabeti zilizobakia, lakini safari hii, tafadhali tumia mkono wako mwingine kuandika. Kwa watu wengi, itawapasa kutumia mkono wao wa kushoto.

FIKIRI – JOZISHA – SHIRIKISHANA (DAKIKA 5) Jadili maswali yafuatayo hapa chini pamoja na mwenzako na kisha wasilisha majibu kwenye kundi zima:

1. Ni ujuzi gani umeufanyia mazoezi kwenye shughuli hizi?2. Kulikuwa na changamoto zipi katika shughuli hizi?3. Unadhani kulikuwa na kusudio gani katika shughuli ya pili?

Page 9: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

7Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Kuandika ni uwezo kuweka mawazo au dhana katika maandishi kwa ajili ya kusoma. Hata hivyo, kabla wanafunzi hawajafikisha mawazo na taarifa kupitia kuandika, lazima wafahamu namna ya kuumbaandika herufi kwenye kurasa.

Kuandika herufi moja moja

Ili kuwasiliana kupitia matini, wanafunzi lazima wawe na uwezo wa kuumba herufi ambazo zinaundwa kwa usahihi, uthabiti na kwa uwazi. Kujifunza kuandika herufi moja moja lazima kuanze kwenye mizania kubwa na polepole ikijielekeza mahali kunakolengwa. Kwa mfano, wafundishe wanafunzi wako kufanya mambo yafuatayo:

1. Kwanza kuandika herufi moja moja kwa kutumia vidole vyao hewani2. Halafu kuandika herufi moja moja kwa kutumia vidole vyao kwenye dawati, ardhini, au kwenye

mchanga3. Tena, kuandika herufi kwa kutumia penseli kwenye karatasi yoyote4. Mwisho, kuandika herufi kwa kutumia penseli kwenye mistari (mistari miwili miwili kama ipo)

KUFUNDISHA kuandika kwa njia hii kunaruhusu wanafunzi kukuza uwezo wao wa kudhibiti mikono yao na vidole.

Wanafunzi pia watajifunza kuumba herufi kwa kukuangalia ukiandika ubaoni. Wakati unaandika neno kwenye ubao, fanya uwezavyo kuandika kwa unadhifu katika ukubwa ambao wanafunzi wanaweza kuona vizuri (kwa kukadiria ukubwa wa mkono wako). Mara zote chapisha maneno – usiyaandike kwa kuyaviringisha. Hapa chini kuna mfano unaoweza kuufuata (siyo muhimu kwa walimu wa Darasa la 1 KUFUNDISHA herufi kubwa na ndogo kwa wakati mmoja).

Kumbuka, unaweza kuanza na herufi zinazofahamika sana: irabu a, e, i, o, u na kisha konsonati b, m, k, d, n. Hata hivyo, kuwa makini na baadhi ya herufi ambazo zinachanganywa kirahisi na wengine kwa sababu zinakaribia kufanana kwa maumbo, kama vile m-n, b-d, n-u na a-o. Jaribu kutofundisha herufi hizi kwa pamoja na ruhusu muda wa kutosha kwa wanafunzi kujifunza herufi moja kabla ya kuwaanzishia herufi nyingine.

Konsonati zinazofuata na ambazo hazifahamiki sana ni: l, t, p, s, f, j. Kundi la mwisho la herufi ni: g, y, z, h, r, w, v, ch. Kuwa makini na w-v kwa sababu zinafanana na zinaweza kuwachanganya wanafunzi.

MISINGI YA KUANDIKA (DAKIKA 25)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha sehemu (kwa mfano, aya au maelezo) amwite mwalimu mwingine kwa jina asome sehemu inayofuata.

2. Wakati unaposoma zingatia alama zifuatazo: • Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu.• Weka alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo.• Weka mduara katika (o) maneno ambayo ni mapya.

Page 10: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

8 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Mchakato huu unafanana sana kwa wanafunzi ambao wanajifunza kusoma:

Kama ilivyojadliwa kwenye moduli ya 8, chagua herufi ya kujielekeza kwa ajili ya somo. Baada ya kutumia mbinu ya Jina-Neno Kuu-Sauti KUFUNDISHA jina la herufi na sauti, unaweza tena kuwaonesha wanafunzi namna ya kuandika neno kwanza hewani, halafu kwenye dawati, halafu kwa penseli au katika karatasi isiyo na mistari, na mwisho kwenye karatasi yenye mistari

Wanafunzi wanaoandikia Mkono wa Kushoto

Kwa kukadiria, asilimia 25 ya watu walioko duniani kwa asili wanaandika kwa kutumia mkono wa kushoto. Wanasayansi wengi wanaamini kuwa uwezo wa mtu kuandikia mkono wa kulia au wa kushoto unabainishwa kabla hajazaliwa. Inapaswa kueleweka kuwa utumiaji wa mkono wa kushoto siyo upungufu – wanafunzi ambao huandikia mkono wa kushoto wanaweza kufanya shughuli zilezile ambazo watoto wanaoandikia mkono wa kulia wanaweza kuzifanya, hatahivyo katika muktadha mbalimbali, kuandika kwa kutumia mkono wa kushoto hakushauriwi sana.

Kumlazimisha mwanafunzi ambaye kwa asili anaandikia mkono wa kushoto, aanze kutumia mkono wa kulia, siyo tu ni kinyume cha asili na kumkosesha utulivu mwanafunzi, bali linaweza kuwa na athari mbaya kwenye kujifunza kwake. Mwanafunzi atatumia nguvu kubwa ya akili kujaribu kudhibiti mkono wake anaouandikia kwa kulazimishwa kuliko kutumia akili hiyo kujifunza ujuzi wa awali wa kuandika (hii inaweza kuwa namna ulivyojisikia wakati wa zoezi la kuchangamsha).

Page 11: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

9Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Kama walimu, lazima tutambue na kuwakubali wanafunzi wetu wanaotumia mkono wa kushoto kwa asili (na kuwaeleza wazazi wao kuwa hali hiyo ni ya asili). Kuna mbinu nyingine ambazo tunaweza kuzitumia kuwasaidia wanafunzi wa aina hii:

Namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoandikia kwa mikono ya kushoto:

1. Waeleze wanafunzi wakae upande wa kushoto wa madawati yao ili wasiwagonge wenzao kwa mikono

2. Wakalishe wanafunzi upande wa kushoto wa darasa ili wewe unapokuwa ubaoni wasilazimike kukuangalia kupitia mikono yao ya kushoto ambayo wanaiandikia.

3. Zungusha madaftari yao au karatasi za kuandikia ili sehemu ya juu kushoto iwe juu zaidi ya sehemu ya juu kulia. Hii inawasaidia wanafunzi kuona vizuri kile wanachoandika.

4. Hamasisha wanafunzi wanaoandikia mikono ya kushoto waweke mikono na vifundo vya mikono yao moja kwa moja na chini ya mstari wa kuandikia. Wanafunzi wengi wana tabia ya kugeuza vifundo vyao ili waandike kutokea juu ya mstari. Hatahivyo, hii inawafanya waandike kwa shida na inaweza kusababisha matatizo na vifundo vyao. Kuzungusha dafatari kunasaidia jambo hili.

Kuandika Maneno

Mara wanafunzi wanapokuwa na uwezo wa kuandika herufi moja moja, watatumia ujuzi wa foniki kuandika maneno. Sasa tufanye shughuli ifuatayo kuonesha. Kwanza, Mratibu wa Mafunzo Kazini atasema neno kwa sauti. Halafu tumia alama katika jedwali ufuatao kuandika neno kwa siri. Usitumie herufi za alfabeti isipokuwa kuandika irabu A au I.

1. ________________________________________________________________________________

2. ________________________________________________________________________________

3. ________________________________________________________________________________

Page 12: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

10 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Kuandika maneno kwa kutumia sauti za herufi

Kama ulivyopata uzoefu, kuandika maneno kwenye karatasi kunajumuisha kutambua neno ambalo unataka kuandika, kutenganisha sauti za herufi katika neno, halafu kuandika herufi zinazoendana na sauti hizo. Mchakato huu wa kuandika maneno unaitwa “Kufi cha Maandishi”, ambao unatumia ujuzi wa wanafunzi wa ‘kuhusianisha’, lakini kwa kinyume.

Kuhusianisha (kama tulivyojifunza kwenye Moduli ya 9)

Andika maneno kupitia sauti za herufi (Kufi cha)

Kuangalia uandishi kwa namna hii, tunaweza kuona kwamba kuandika na kusoma ni njia zinazotumia ujuzi wa foniki wa wanafunzi. Mara tu wanafunzi wanapokuwa na weledi na kila sauti ya herufi ya alfabeti, pamoja na namna ya kuandika kila herufi . Watakuwa na uwezo wa kuandika neno kwenye karatasi. Unapaswa kuwapa wanafunzi fursa nyingi kufanya mazoezi ya kufi cha maneno kwa kutumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya- Unafanya’. Kwa mfano:

1. Chukua neno linalotumia sauti za herufi ambazo wanafunzi wanazifahamu vizuri kama vile ‘paka’. Tamka neno kwa sauti.

2. Anza na ‘Ninafanya’: Waoneshe wanafunzi kwamba wanaweza kutumia mbinu kama Binya Vidole kutenganisha sauti za herufi katika neno.

3. Kwa kila sauti herufi iliyotambuliwa, waulize wanafunzi wakwambie ni herufi zipi zinakwenda na kila sauti

4. Mwanafunzi anapotambua herufi kwa usahihi, mweleze aje mbele ya darasa na umpe kadi ya herufi ashikilie ili kila mmoja aione. (Kama hauna kadi ya herufi , unaweza kuandika herufi kwenye ubao wakati wanafunzi wanazitambua)

5. Fanya hivi kwa kila herufi ili kuwe na kundi la wanafunzi lililosimama mbele ya darasa, likishikilia kila herufi ambayo inaunda neno ‘paka’

6. Endelea na ‘Tunafanya’: Waeleze wanafunzi wafanye zoezi la Binya Vidole pamoja na wewe. Mueleze kila mmoja aseme herufi inayoendana kwa kila sauti na waombe wanaojitolea washikilie kadi herufi . Ukishakuwa na wanafunzi walioshikilia kadi herufi , elekeza darasa zima liandike kila herufi kuunda neno (kwenye madaftari yao)

7. Malizia na ‘Unafanya’: Sema neno “paka” na waeleze wanafunzi kwa kujitegemea kila mmoja wao, watenganishe sauti herufi , watambue herufi zinazoendana na sauti, na kisha waandike maneno kwenye madaftari yao.

Angalia neno

TenganishaSauti / Silabi

UnganishaSauti / Silabi

Tamka neno

Sema neno

Tenganishasauti

Andika herufi kwa kila sauti

Page 13: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

11Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Andika maneno kwa kutumia silabi

Wanafunzi wanaweza pia kuvunjavunja maneno kuwa silabi wanazozijua, na kisha wakaandika kila silabi kuunda neno lililoandikwa:

Kuandika neno kutokanana na sauti ya silabi

Wakati mwingine, wanafunzi wangependa kuandika neno ambalo linajumuisha silabi zinazoungwa kwa herufi mwambatano na irabu. Hii inapotokea, wanafunzi wanaweza kutenganisha silabi zinazoungwa herufi mwambatano na kuwa sauti/herufi moja moja.

Kuandika neno kupitia matumizi ya sauti za herufi na silabi

Fanya mazoezi ya kuandika maneno

Wakati wanafunzi wanaandika, ni muhimu uwashauri waandike herufi zinazoendana na sauti au silabi wanazosikia. Hatahivyo, wakati mwingine wanafunzi wanaandika neno likiwa na matamshi yaliyokosewa kwa sababu baadhi ya maneno hayatamkwi kama yanavyosemwa. Hii ni sawa! Hii inaitwa vitamkwa vumbuliwa. Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kuandika neno “ng’ombe” kama hivi: gombe. Hii ni kwa sababu mwanafunzi bado hajajifunza sauti ya “ng” ( hii inaweza kutokea pamoja na herufi mwambatano zingine) kama “dh”, “ny” na “gh”.

Badala ya kusahihisha utamkaji wa wanafunzi hapo hapo, waruhusu watumie ujuzi wao wa foniki kutamka maneno kama wanavyoyasikia. Kadri muda utakavyokuwa unakwenda, kupitia mazoezi endelevu ya kusoma na maelekezo ya msamiati, wanafunzi watajifunza na kukumbuka matamshi sahihi.

MAJADILIANO KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)

1. Maudhui gani umewekea alama ya mshangao (!)?2. Maudhui gani umewekea alama ya kuuliza (?)?3. Maudhui gani umezungushia alama ya mduara?4. Ni namna gani ujuzi wa kuhusianisha unajenga uwezo wa wanafunzi kuandika?

Sema neno:“paka”

TenganishaSilabi:pa ka

Andika herufi kwa kila silabi:

paka

Sema neno:“mwalimu”

TenganishaSilabi:

mwa li mu

Tenganisha silabi ngumu kuwa sauti

herufi :“mwa” = /mw/ + /a/

Andika herufi kwa kila silabi / sauti:

mwalimu

Page 14: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

12 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

IGIZO (DAKIKA 20) Wakati unapotambulisha herufi mpya kuna njia nyingi za KUFUNDISHA uundaji herufi sahihi. Shughuli hii hapa chini inakupitisha kwenye uandikaji wa hewani, kuandika kwenye dawati na halafu kuandika kwenye karatasi. Kwa kutumia mbinu hizi, wanafunzi wanatumia misuli yote ya mabega na mikono. Hii inaifanya misuli iendane na uumbaji wa kila herufi na kusaidia kuhakikisha kwamba, pamoja na mazoezi endelevu, mwanafunzi anaandika herufi kwa usahihi zaidi kila wakati. Mratibu wa Mafunzo Kazini atafanya Igizo hili wakati mwalimu na kila mtu aliyebakia wakijifanya kuwa wanafunzi.

1. Mratibu wako wa Mafunzo Kazini ataandika herufi kubwa kwenye ubao

2. Simama na shikilia kidole kimoja kwa kutumia mkono wako wa kulia. Kidole hiki kitakuwa kama ‘penseli’ yako wakati unaandika hewani.

3. Nyoosha mkono wako na onesha “kidole penseli” chako kuelekea mahali ambapo herufi inaanzia kwenye ubao. Mratibu wa Mafunzo Kazini atakwambia kutafuta herufi kama vile ulikuwa unaandika herufi hewani kwa kutumia “kidole penseli” vyako. Hakikisha unaweka kidole chako na mkono kwa uimara. Tembeza mkono wako wote kutoka begani kwako, siyo kiwiko chako au kifundo.

4. Nyoosha mkono wako, na rudia kuandika ‘n’ hewani. Halafu, fanya hatua zile zile ukiwa umefumba macho yako.

Page 15: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

13Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

6. Baada ya kuandika ‘n’ hewani, tumia kidole cha shahada na cha kati “kidole penseli” kuandika herufi ile ile kwenye dawati. Mara hii unaweza kupindisha mkono wako ili uwe kama unaadika. Andika herufi kubwa ‘n’ kwenye dawati lako. Fanya hivi tena ukiwa umefumba macho yako. Kama wanafunzi wakiona ni rahisi kutumia njia hii kwa mikono yao ya kushoto, wanapaswa kutumia mikono ya kushoto kuandika.

Baada ya kuandika herufi kwenye dawati lako, jiandae kuandika herufi kwa kutumia kalamu yako. Kama wanafunzi wako bado hawajui kushikilia penseli sawasawa, tumia mbinu ya ‘kibanio na kishtuzi’ kuweka mikono yao kwenye sehemu sahihi kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapa chini.

HATUA YA 1: Shikilia kalamu ili ncha iwe katikati ya kidole gumba na kidole cha shahada.

HATUA YA 2: Tumia mkono wako wa pili kuzungusha kalamu ili ncha iangalie chini.

HATUA YA 3: Endelea kuzungusha kalamu hadi itulie kwenye mkono wako na ncha ikiangalia mbali na wewe.

HATUA YA 4: Leta mbele vidole vyako vitatu vilivyobakia ili kalamu ikae kwenye kidole chako cha katikati.

5. Rudia hatua ya 2 – 4 kwa mkono wako wa kushoto. Hii ni njia moja ya kuwasaidia wanafunzi kubaini kama wanajiona wako katika hali nzuri kuandika kwa kutumia mikono yao ya kushoto. Kama wanafunzi wakiona kuandika hewani ni rahisi kwa kutumia mkono wa kushoto, washauri wajaribu kutumia mikono yao ya kushoto kuandika.

Page 16: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

14 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

7. Baada ya kuwaonesha wanafunzi mbinu ya‘kibanio na kishtuzi’, tembea kuzunguka darasa kuhakikisha kuwa kila mmoja anafanya kwa usahihi. Halafu tumia mikupuo uliyotumia pamoja na ‘vidole kalamu’ vyako kuandika herufi ‘n’ kwa kutumia kalamu yako. Andika herufi kubwa kwenye karatasi isiyo na mistari. Kama huna karatasi isiyo na mistari, chora herufi kubwa ‘n’ kwenye karatasi ilinyooshwa halafu chora herufi kwa muendelezo huo huo lakini ikiwa ndogo.

Mbinu kama hizi zinasaidia wanafunzi wanaotumia mikono ya kushoto na mikono ya kulia kuandika kwa sababu wanaanza na eneo kubwa sana (hewani) na wanaendelea kuandika kuja kwenye eneo dogo (dawati) hadi kwenye sehemu yote ya karatasi, kwenye mistari ya karatasi). Taratibu huu unaifanya misuli kwenye mikono izoee na hivyo kuwezesha wanafunzi waweze kuandika kwenye karatasi kwa usahihi tena kwa ukubwa unaohitajika.

Kuandika hewani kunaweza kutumika kufanyia mazoezi mbinu nyingine pia! Kufanya mazoezi ya Foniki: Kufanya mazoezi ya maneno yaliyounganishwa kwenye sauti za herufi, taja sauti za herufi (usiiandike kwenye ubao) na waulize wanafunzi ‘kuandika’ hewani herufi ambayo imetokana na sauti hiyo. Kuandika Silabi, maneno yanayoonekana na maneno msamiati: Badala ya kuandika herufi moja tu kwenye ubao, andika silabi, maneno yanayoonekana, au maneno ya msamiati ambayo wanafunzi wanajifunza. Waeleze wanafunzi “waandike” hewani neno lililoko ubaoni.

JADILI PAMOJA NA KIKUNDI (DAKIKA 5)

Baada ya kufanyia mazoezi shughuli hii, jadili swali pamoja na kundi:

1. Ni namna gani hivi sasa unawafundisha wanafunzi kushikilia kalamu zao na kuumba herufi?

2. Ni namna gani kuandika hewani na kwenye dawati kunasaidia ujuzi wa wanafunzi katika uandishi?

3. Ni hatua gani nyingine ambazo unaweza kutumia mbinu hizi katika mazingira ya darasani kwako?

4. Ni namna gani utaweza kutumia mbinu hii kwenye masomo yako?

Page 17: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

15Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

KUAANDAA KIPINDI CHA “KUSOMA NA KUANDIKA” (DAKIKA 25)

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

UTANGULIZI

1. Waambie wanafunzi kwamba watafanya mazoezi ya kuandika herufi ‘m’. Unaweza kutumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’, kuonesha namna ya kuandika herufi.

2. Anza na ‘Ninafanya’: Simama na shikilia vidole viwili kwa kutumia mkono wako wa kulia. Vidole hivi vitakuwa kama ‘penseli’ yako ukiwa unaandika hewani.

3. Nyoosha mkono wako na geuka ili uelekeze “vidole penseli” vyako kuelekea mahali ambapo herufi zinaanzia kwenye ubao. Hakikisha wanafunzi wanaona na kuelewa kile unachofanya.

4. Tafuta herufi kama vile ulikuwa unaandika herufi hewani kwa kutumia “vidole penseli” vyako. Hakikisha vidole na mkono wako vinakuwa imara, tembeza mkono wako wote kutoka begani kwako, siyo kiwiko chako au kifundo.

5. Endelea na ‘Tunafanya’: Waeleze wanafunzi wasimame, watumie kidole kama ‘penseli’ yao, elekeza penseli yao kwenye herufi iliyoko ubaoni na waandike herufi hewani. Fanya hivi pamoja nao ili waweze kufuata vitendo vyako.

6. Malizia na ‘Mnafanya’: Waeleze wanafunzi waandike herufi hewani kwa kujitegemea. Zunguka darasani na hakikisha wanafunzi wanaandika herufi kwa usahihi.

7. Rudia kwa kutumia mkono wa kushoto. Hii ni njia ya kusaidia wanafunzi kutambua ikiwa wanakuwa huru zaidi kuandika kwa kutumia mkono wa kushoto.

MAPYA

1. Baada ya kuandika herufi ya siku hewani, waeleze wanafunzi wakae chini na watumie vidole vyao vya shahada na vya kati ‘vidole penseli’ kuandika herufi ile ile kwenye madawati yao.

2. Waambie kwamba wanaweza kupindisha mikono yao kuonesha kama vile wanaandika. Waambie watumie ‘vidole penseli’ vyao kuandika toleo kubwa la herufi ya siku kwenye madawati yao mara nyingi

3. Unaweza pia kuwaeleza wanafunzi wakae wawiliwawili na waeleze waandike herufi katika mgongo wa kila mmoja. Tena, tembea darasani kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaandika herufi kwa usahihi.

MWONGOZO WA MASOMO 1: Andika herufi za alfabeti HATUA ZA KUFUNDISHA

Ili kukuza uwezo wa wanafunzi kusoma, ni muhimu sana kwamba aweze kufanya mazoezi juu ya mbinu mpya za kusoma na kuandika alizosoma kutoka kwenye Mafunzo ya Walimu Kazini. Kurasa zifuatazo zinajumuisha masomo ya jumla yanayoelekeza shughuli ambazo unaweza kujaribu wakati wa kipindi chako cha kusoma na kuandika (au unaweza pia kujaribu wakati wa kipindi chako cha kawaida cha Kiswahili). Pamoja na mwenzako:

1. Soma kwenye mpango wa masomo.2. Jaza nafasi zilizo wazi mahali panapohitaji hivyo.3. Jaribu masomo wakati wa kipindi cha kusoma na kuandika.

Angalia maelezo yaliyotolewa katika moduli ya 9 kuhusu mwongozo wa somo.

Page 18: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

16 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

IMARISHA 1. Ikiwa wanafunzi wako ndiyo wanajifunza kutumia penseli, tumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’ kuonesha namna ya kushikilia penseli.

2. Anza na ‘ Ninafanya’: Shikilia penseli na kuhakikisha kuwa ncha iko kati ya dole gumba na kidole cha shahada (angalia picha kwenye sehemu ya shughuli katika moduli hii).

3. Tumia mkono wako mwingine kuzungusha penseli ili ncha iangalie chini4. Endelea kuzungusha penseli hadi ikae mkononi mwako na ncha ikiangalia mbali na

wewe5. Leta mbele vidole vyako vitatu vilivyobakia ili penseli ikae kwenye kidole chako cha

katikati6. Endelea na ‘Tunafanya’: Rudia hatua ya 2 – 5 wakati ukifanya pamoja na wanafunzi7. Malizia na ‘Mnafanya’: Waambie wanafunzi warudie hatua ya 2 – 5 peke yao. Tembea

kuzunguka darasani na saidia wanafunzi wenye matatizo.8. Mara tu kila mmoja akishikilia penseli kwa usahihi, waeleze wanafunzi watumie

mikupuo waliyotumia kwenye “vidole penseli” vyao kuandika herufi ya siku pamoja na penseli yao.

FANYIA MAZOEZI

9. Kama una nmuida wa ziada fanya mazoezi ya kutosha kwa herufi zingine

KUPIMA 1. Kwa herufi ambazo umekwishazifundisha, sema jina la herufi au sauti (usiandike herufi hizi ubaoni) na waelekeze wanafunzi waandike herufi hewani kwa kutumia vidole vyao.

2. Kisha waambie waandike herufi kwenye madawati yao na kwenye karatasi.3. Tembea kuzunguka darasani na rekodi kwenye kumbukumbu zako ikiwa wanafunzi

wanaandika herufi kwa usahihi.4. Weka rekodi ya herufi zinazotatiza na rudia KUFUNDISHA namna ya kuandika herufi

hizi katika kundi dogo. Unaweza pia kuwaweka wanafunzi wawiliwawili katika makun-di yenye wanafunzi werevu ambao wanaweza kuwasaidia hawa wenye matatizo

Tathmini:

Maoni:

Angalia maelezo yaliyotolewa katika moduli ya 9 kuhusu mwongozo wa somo

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MAAN-DALIZI

1. Kabla ya somo, andaa orodha ya maneno ambayo wanafunzi wanajifunza au tumia orodha hii hapa chini ambayo imechukuliwa kutoka kwenye mtaala wa Kiswahili kwa kila darasa.

2. Kuwa huru kuja na orodha yako mwenyewe na hakikisha unatumia maneno ambayo yana sauti za herufi na silabi ambazo wanafunzi wanazifahamu.

3. Chagua walau maneno 2 – 3 ambayo yana silabi ambazo wanafunzi wako wanaweza kuwa hawazifahamu. Kwa mfano, ‘shamba’, ‘mwalimu’ na ‘nyumbani’.

MWONGOZO WA SOMO LA PILI: Andika herufi kupitia Kuficha Maandishi HATUA ZA KUFUNDISHA

Page 19: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

17Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MAANDALIZI

UTANGULIZI1. Waambie wanafunzi kwamba wanakwenda kufanya mazoezi ya kaundika maneno

kulingana na sauti zao za herufi.2. Chagua neno kutoka kwenye orodha yako ya maneno na litamke kwa sauti. Halafu tumia

mbinu ya ‘ Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’ kuwasaidia wanafunzi wafanye mazoezi ya kuficha neno.

KUJENGA UMAHIRI

1. Chagua neno kutoka kwenye orodha yako ambalo linatumia sauti za herufi ambazo wanafunzi wanazifahamu vizuri, kama “jina”. Sema neno kwa sauti. Anza na ‘Ninafanya’: Onesha wanafunzi kwamba wanaweza kutumia mbinu ya Binya Vidole kutenganisha sauti za herufi katika neno. Kwa kila sauti ya herufi ambayo imetambuliwa, waambie wanafunzi wakwambie herufi gani inakwenda na kila sauti. Mwanafunzi akitambua herufi kwa usahihi, muombe aje mbele ya darasa na mpe kadi ya herufi ya kushikilia ili kila mtu aione. (Kama hauna kadi ya herufi, unaweza kuandika herufi kwenye ubao wakati wanafunzi wakizitambua). Fanya hivi kwa kila herufi ili kuwe na kundi la wanafunzi waliosimama mbele ya darasa, wameshikilia kila herufi ambayo inaunda neno “jina”. Endelea na ‘Tunafanya’: Waambie wanafunzi wafanye zoezi la Binya Vidole pamoja na wewe. Elekeza kila mmoja aseme herufi ambayo inaendana na kila sauti na omba anayejitolea ashikilie kadi ya herufi. Ukishakuwa na wanafunzi walioshikilia kadi za herufi, waambie wanafunzi wote darasani waandike kila herufi inayounda neno (kwenye madaftari yao)

2. Malizia na ‘Mnafanya’: sema neno “jina” na waambie wanafunzi kila mmoja akiwa peke yake atenganishe sauti za herufi, atambue herufi ambazo zinaambatana na sauti, na kisha aandike maneno kwenye daftari lake.

IMARISHA1. Chagua neno kutoka kwenye orodha yako ya maneno na litamke kwa sauti, kama “kitabu”. 2. Anza na ‘Ninafanya’: Waoneshe wanafunzi kwamba wanaweza kutumia mbinu kama vile

Kupiga Makofi kwa silabi (kutoka moduli ya 7) hadi kutenganisha silabi katika neno3. Waoneshe namna ‘kupiga makofi’ katika silabi za neno kunafanya usikie kila silabi peke yake4. Waulize wanafunzi herufi zipi zinatengeneza silabi. Mwanafunzi anapojibu kwa

usahihi (“ki”), mwambie aje mbele ya darasa na mpe kadi za herufi ashikilie na kila mmoja aone. (Kama huna kadi za herufi, unaweza kuandika herufi ubaoni wakati wanafunzi wanazitambua).

5. Fanya hivi kwa kila silabi hadi kuwe na wanafunzi watatu wamesimama mbele ya darasa, wakishikilia silabi: “ki” “ta” “bu”

6. Endelea na ‘Tunafanya’: Watake wanafunzi wapige makofi kwa silabi pamoja na wewe. Elekeza kila mmoja aseme herufi inayoendana na kila silabi na uliza wanaojitolea kushikilia kadi herufi. Mtake kila mwanafunzi aandike kila silabi kuunda neno (kwenye madaftari yao). Malizia na ‘Mnafanya’: sema neno “kitabu” na waeleze wanafunzi kila mmoja na kwa kujitegemea watenganishe silabi, watambue herufi ambazo zinaendana na silabi, na kisha waandike maneno kwenye madaftari yao.

Maneno kwa ajili ya darasa la 1

Maneno kwa ajili ya darasa la 2

Maneno kwa ajili yadarasa la 3

MamaBabaMimiJina

KitabuKalamu

MezaVikombeShamba

KofiaKoti

ViatuVijiko

WanyamaWadudu

BaridiMrefu

Mwalimu

SokoniSingiziaJengaKatili

UlimboHurumaKalendaMizani

Nyumbani

Page 20: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

18 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

UFUATILIAJI Baada ya kumaliza moduli hii, Mratibu Elimu wa Kata, Ofisa Elimu wa Wilaya na Mkaguzi Elimu wa Wilaya watafuatilia kuona namna unavyotumia mbinu za moduli hii darasani kwako. Wakati wa ufuatiliaji huu, ni vema ukawa na uwezo wa kuone sha mambo yafuatao:

a) Eleza mbinu za kuwasaidia wanafunzi kushikilia penseli na anza kuandika herufi moja moja

b) Eleza mchakato wa ‘kuficha maandishi’ na namna wanafunzi wanavyoweza kutumia ujuzi wao wa foniki kuandika maneno

c) Onesha namna ulivyotumia miongozo ya masomo kutoka katika moduli hii kwenye darasa lako.

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

KUTUMIA UMAHIRI

1. Waambie wanafunzi kwamba wanakwenda kufanya zoezi la kuandika maneno kutokana na sauti za herufi pamoja na silabi zao.

2. Chagua neno kutoka kwenye orodha yako ya maneno ambayo ina silabi ambazo wanafunzi wanaweza kuwa hawazifahamu. Kwa mfano ‘mwalimu’..

3. Anza na ‘Ninafanya’: Onesha wanafunzi kwamba wanaweza kutumia mbinu kama Kupiga Makofi kwa Silabi ili kutenganisha silani katika neno: /mwa/ /li/ /mu/

4. Mara tu ukishapiga makofi kwa silabi zote, tumia Binya Vidole kutenganisha sauti za herufi katika silabi hiyo.

5. Gusa kila sauti herufi na waambie wanafunzi watambue herufi zinazoenda na kila sauti ya herufi: /m/ /w/ /a/

6. Mwanafunzi anapojibu kwa uhakika, mwambie aje mbele ya darasa na mpe kadi herufi kushikilia kiasi cha kila mmoja kuiona.

7. Fanya hivi kwa kila sauti herufi na silabi ili kuwe na wanafunzi 6 waliosimama mbele ya darasa: watatu wakiwa wameshikilia herufi “m” “w” “a” na wawili wakiwa wameshikilia silabi: “li” “mu”

8. Endelea na ‘Tunafanya’: Waambie wanafunzi wabinye vidole na kupiga makofi kwa silabi pamoja na wewe. Elekeza kila mmoja aseme herufi ambazo zinaendana na kila silabi na omba wanaojitolea washikilie kadi herufi. Elekeza wanafunzi wote kuandika herufi ili kuunda neno (kwenye madaftari yao).

9. Malizia na ‘Mnafanya’: sema neno “mwalimu” na waeleze wanafunzi kila mmoja kwa kujitegemea, watenganishe sauti za herufi a silabi, watambue herufi ambazo zinaendana na sauti na silabi na kisha waandike neno kwenye madaftari yao.

KUPIMA1. Wanafunzi wakishakuwa na uwezo wa kuficha maandishi peke yao, soma maneno

mengine matatu kutoka kwenye orodha yako ya maneno. Waeleze wanafunzi waandike maneno kwenye madaftari yao.

Tathmini ya Ufundishaji:

Tathmini ya Ujifunzaji:

Maoni:

Page 21: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

19Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

MWISHO (DAKIKA 10)Binafsi jaza fomu ifuatayo kuweka rekodi ya tathmini ya moduli ya leo. Baada ya kukamilisha, chomoa ukurasa huu na umpe Mratibu wako. Tafadhali uwe mkweli kwa vile mrejesho wako utasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule hapo baadaye.

JEDWALI LA KUTATHMINI Alama 0:

Sikubaliani kabisa na usemi huu

Alama 1: Kwa kiasi Sikubaliani

na usemi huu

Alama 2:Nakubaliana kwa kiasi na usemi huu

Alama 3: Nakubaliana Kabisa

na usemi huu

FOMU YA TATHMINI

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:_____________________

Tathmini ya Moduli: ________ Mada ya Moduli: ______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki: ________ Mwalimu Mkuu alishiriki: Ndiyo/Hapana

Mratibu alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Soma semi zifuatazo kisha weka alama ya vema katika kisanduku husika kuonesha jibu lako:

0 1 2 3

1. Dhana kuu ya moduli ya leo ilikuwa inaeleweka.

2. Moduli hii ina mikakati mingi mizuri na yenye manufaa ambayo nitaitumia darasani kwangu.

3. Muda uliotumika kukamilisha moduli hii unafaa. Sikuhisi kwamba ni muda mrefu sana.

4. Moduli hii iliibua mjadala wa kufurahisha na tafakuri ya hali ya juu sana.

5. Violezo vya kipindi cha kusoma na kuandika vilisaidia sana. Natarajia vitakuwa rahisi kuvitumia ndani ya darasa langu.

6. Zana tulizotengeneza leo zitakuwa za manufaa sana (kama inahusika).

7. Mratibu amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia.

8. Mratibu anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu.

9. Mratibu anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika.

10. Mratibu anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini Mafunzo ya Walimu Kazini ni muhimu kwetu.

Page 22: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI
Page 23: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI
Page 24: Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-MISINGI YA KUANDIKA.pdf · MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi: MISINGI

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule