-module - mwalimuwakiswahili.co.tz · stashahada ya elimu ya watu wazima na mafunzo endelevu kwa...
TRANSCRIPT
-MODULE
Taasisi ya Elimu ya Watu WazimaIdara ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo EndelevuStashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu – Kwa Masafa
Kuchambua Sintaksia na Semantiki ya Kiswahili
KIT 0610
MODULI
Kuchambua Sintaksia na Semantiki ya Kiswahili
KIT 0610
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu kwa Masafa
Hakimiliki
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuzalisha, kunakili, wala kusambaza sehemu yoyote
ya kazi hii kwa namna yoyote isipokuwa kwa kunukuu matini fupifupi zinazoweza kutumika
kwa ajili ya utafiti na mapitio ya maandiko, bila kibali cha maandishi kutoka Taasisi ya
Elimu ya Watu Wazima.
© Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, 2014
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu kwa Masafa
S. L. B. 20679 Dar es Salaam,
Mtaa wa Bibi Titi Mohamed Tanzania
Nukushi: +255 22 2150836 Barua-pepe: [email protected]
Tovuti: www. iae.ac.tz
Shukrani
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Fidelis M. S. Mafumiko anapenda
kutoa shukurani za dhati kwa watu mbalimbali ambao wamechangia kwa namna moja au
nyingine katika kukamilisha kazi hii. Wafuatao ambao ni wafanyakazi wa TEWW wanastahili
kutajwa kipekee kwa kuongoza mchakato huu hadi kukamilika kwake.
A. Lekule: Mkuu, Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzi
Endelevu
T. Mamba: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mratibu)
A. Mashaka: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mwandishi)
S. Kileo: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mpitiaji)
E. Samba: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mhariri)
ii Yaliyomo
Yaliyomo
Kuhusu moduli hii 1
Muundo wa moduli hii ...................................................................................................... 1
Maelezo ya jumla kuhusu moduli 3
Karibu katika moduli hii ................................................................................................... 3 Umahiri wa Jumla ............................................................................................................. 4 Mbinu za usomaji .............................................................................................................. 4 Je, unahitaji msaada? ........................................................................................................ 5 Mazoezi ............................................................................................................................. 6
Namna ya kutumia moduli hii 7
Ishara za pambizo ............................................................................................................. 7
Somo la Kwanza 9
Kuchambua Mikabala ya Sarufi Mapokeo na Sarufi Miundo Virai ................................. 9 Utangulizi ................................................................................................................ 9 Matokeo ................................................................................................................... 9 Kufafanu Dhana ya Mkabala na Mkabala wa Kisarufi ........................................... 9 Kufafanua Misingi ya Mkabala wa Sarufi Mapokeo ............................................ 10
Mkabala wa Sarufi Mapokeo ....................................................................... 10 Misingi ya Sarufi Mapokeo ......................................................................... 10 Zoezi ............................................................................................................ 11
Kufafanua Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai ...................................... 12 Mkabala wa Sarufi Miundo Virai ................................................................ 12 Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai .............................................. 13
Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 14 Zoezi la Somo ................................................................................................................. 14
Somo la Pili 15
Kuchambua Kategoria za Kisintaksia ............................................................................. 15 Utangulizi .............................................................................................................. 15 Matokeo ................................................................................................................. 15 Ufafanuzi Dhana za Msingi za Kisintaksia ........................................................... 15
Sintaksia ....................................................................................................... 15 Kategoria ...................................................................................................... 16 Tungo ........................................................................................................... 16 Neno ............................................................................................................. 17 Kirai ............................................................................................................. 17 Kishazi ......................................................................................................... 17 Sentensi ........................................................................................................ 18
Kubainisha Kategoria ya Neno .............................................................................. 18 Nomino ........................................................................................................ 19
Aina za Nomino ................................................................................... 19 Dhima/ Kazi za Nomino ...................................................................... 20
Kiwakilishi ................................................................................................... 21 Kivumishi ..................................................................................................... 22 Kitenzi .......................................................................................................... 23 Kielezi .......................................................................................................... 24 Kihusishi ...................................................................................................... 26 Viunganishi .................................................................................................. 27
Dhima za Kiunganishi ......................................................................... 28 Zoezi .................................................................................................... 28
Kubainisha Kategoria ya Virai .............................................................................. 29 Aina za Virai ................................................................................................ 29
Kirai Nomino ....................................................................................... 30 Kirai Kitenzi ........................................................................................ 31 Kirai Kivumishi ................................................................................... 32 Kirai Kielezi ........................................................................................ 33 Kirai Kihusishi ..................................................................................... 34 Zoezi .................................................................................................... 34
Kubainisha Vishazi vya Kiswahili ........................................................................ 35 Aina za Vishazi ............................................................................................ 35
Kishazi Huru ........................................................................................ 35 Kishazi Tegemezi ................................................................................ 35 Zoezi .................................................................................................... 37
Kubainisha Sentensi za Kiswahili ......................................................................... 38 Aina za Sentensi kwa Kigezo cha Maana/ amilifu (kisemantiki) ................ 38 Aina za Sentensi kwa Kigezo cha Kimuundo (kisintaksia) ......................... 39
Zoezi .................................................................................................... 41 Uchanganuzi wa Tungo ......................................................................................... 41
Uchanganuzi wa Tungo kwa Mkabala wa Kimapokeo ............................... 42 Uchanganuzi wa Tungo kwa Mkabala wa Kimuundo ................................. 45
Zoezi .................................................... Error! Bookmark not defined. Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 48 Zoezi la Somo ................................................................................................................. 48
Somo la Tatu 50
Kufafanua Semantiki ya Kiswahili ................................................................................. 50 Utangulizi .............................................................................................................. 50 Matokeo ................................................................................................................. 50 Kufafanua Dhana ya Semantiki na Maana ............................................................ 50 Kuchambua Mikabala ya Semantiki ...................................................................... 51
Viwango vya Maana .................................................................................... 53 Dhana ya Maana .......................................................................................... 54
Kufafanua Aina za Maana ..................................................................................... 56 Aina za Maana ............................................................................................. 56 Uhusiano wa Kifahiwa katika Semantiki ..................................................... 58
Sinonimia ............................................................................................. 59 Hiponimia ............................................................................................ 59 Homonimia .......................................................................................... 60 Polisemia ............................................................................................. 60
iv Yaliyomo
Antonimia ............................................................................................ 61 Kufafanua Nadharia ya Maana Kimuktadha ya Ludwig Wittgenstain ................. 61
Kufafanua dhana ya nadharia....................................................................... 62 Nadharia ya Maana Kimukutadha ............................................................... 62
Kufafanua Ubora na Udhaifu wa Nadharia ya Maana Kimuktadha ..................... 63 Zoezi .................................................... Error! Bookmark not defined.
Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 64 Zoezi la Somo ................................................................................................................. 65
Marejeleo 66
1
Kuhusu moduli hii Moduli hii imetayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Moduli zote zilizotayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
zina muundo sawa, kama ilivyoelezwa hapa chini.
Muundo wa moduli hii
Maelezo ya jumla kuhusu moduli
Maelezo ya jumla kuhusu moduli hutoa utangulizi wa jumla wa moduli. Habari zinazopatikana katika maelezo ya jumla kuhusu moduli zitakusaidia kuamua:
Kama moduli hii inakufaa.
Kitu gani unatarajia kujifunza?
Muda utakaohitaji ili kukamilisha moduli.
Maelezo haya ya jumla pia hutoa mwongozo juu ya:
Mbinu za usomaji.
Mahali pa kupata msaada.
Mazoezi ya nyumbani na tathmini.
Ishara za vitendo mbalimbali.
Masomo.
Tunatilia mkazo ushauri kwamba usome maelezo ya jumla kuhusu moduli kwa makini kabla ya kuanza masomo yako.
Yaliyomo kwenye moduli
Moduli hii imegawanywa katika masomo. Kila somo lina:
Utangulizi wa yaliyomo kwenye moduli.
Matokeo ya somo.
Istilahi mpya.
Maudhui ya kimsingi ya somo pamoja na mazoezi mbalimbali ya kusoma.
Mazoezi ya nyumbani na/au tathmini, kama inavyohitajika.
Kuhusu moduli hii Error! No text of specified style in document.
2
Marejeleo
Kwa wale wanaopenda kujifunza mengi juu ya mada hii, tunawapa
orodha ya marejeleo ya ziada mwishoni mwa Moduli hii; haya
yanaweza kuwa vitabu, makala au tovuti.
Maoni yako
Baada ya kukamilisha Moduli ya Kiswahili Ufahamu na Utumizi
wa Lugha tutashukuru ikiwa utatenga muda mfupi kutupa maoni
yako kuhusu kipengele cho chote cha moduli hii. Maoni yako
yanaweza kuhusu:
Yaliyomo kwenye moduli na muundo wake.
Makala za kusoma kwa moduli na marejeleo mengine.
Mazoezi ya nyumbani ya moduli.
Tathmini za moduli.
Muda wa moduli.
Usaidizi katika moduli (wahadhiri waliosimamia moduli, usaidizi wa kiufundi, n.k.)
Ukitoa maoni mwafaka utatusaidia kuboresha moduli hii.
3
Maelezo ya jumla kuhusu moduli
Karibu katika moduli hii
Lengo kuu la Moduli hii kumwezesha mwanafunzi kutumia stadi
za sintaksia na semantiki ya Kiswahili sanifu katika mawasiliano.
Moduli hii inalenga kuwapatia wanafunzi maarifa ya awali ya
msingi katika uchambuzi wa taaluma ya sintaksia (miundo) na
Semantiki (maana). Kwa upande wa sintaksia kumekuwa na
mkanganyo mkubwa juuu ya suala nzima la vipashio vinavyounda
taaluma hii ikiwemo neno, kirai, kishazi, na sentensi. Hivyo,
moduli hii inatanzua uvuliuvuli (mkanganyo) huo kwa kufafanua
kwa ufasaha juu ya vipashio hivyo ambapo ndio uti wa mgongo
katika uchanganuzi wa tungo mbalimbali. Halikadhalika kwa
upande wa uchanganuzi wa tungo kumekuwa na uholela wa hali
ya juu kiasi ambacho kimewachanganya sana wanafunzi katika
suala hilo. Uholela huo umetokana na baadhi ya wanaisimu
kuchanganya istlahi za sarufi mapokeo na sarufi miundo katika
uchanganuzi. Hata hivyo, moduli hii imeondoa utata huo kwa
kuchambua misingi ya mikabala yote miwili kisha moduli
imechanganua tungo mbalimbali kwa kutumia kila mkabala yaani
pasipo kuchanganya istilahi za mikabala hiyo (kimapokeo na
kimuundo). Aidha, moduli hii inakupa maarifa yahusuyo semantiki
ambapo yatakujengea msingi katika taaluma hii. Tunakutakia
masomo mema!
Moduli hii imeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa Stashahada kwa
Njia ya Masafa katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Moduli
hii inahusu Uchambuzi wa Sintaksia na Semantiki ya Kiswahili.
Maelezo ya jumla kuhusu moduli Error! No text of specified style in document.
4
Umahiri wa Jumla
Baada ya kukamilisha moduli hii tunakusudia kila mwanafunzi aweze:
Kutofautisha baina ya mkabala wa sarufi mapokeo na sarufi miundo virai;
Kufafanua kwa ufasaha kategoria ya neno, kirai, kishazi na sentensi;
Kubainisha kategoria za neno, kirai, kishazi na sentensi katika tungo mbalimbali;
Kuchanganua tungo mbalimbali kwa kutumia mikabala ya sarufi mapokeo na sarufi miundo virai;
Kufafanua aina mbalimbali za maana; and
Kueleza kwa ufasaha nadharia ya maana kimuktadha
Mbinu za usomaji
Kwa kuwa wewe ni mwanafunzi wa Elimu Masafa na Ana kwa
Ana, utaratibu wako wa kusoma utakuwa tofauti na ule ulioutumia
ulipokuwa bado shuleni: utachagua unachotaka kusoma, utakuwa
na motisha ya kitaalamu na/au ya kibinafsi inayokusukuma, na bila
shaka utakuwa ukiratibu shughuli zako za kiusomaji huku
ukizingatia majukumu yako mengine ya kitaalamu au kinyumbani.
Kimsingi, utakuwa unayadhibiti mazingira yako ya masomo. Kwa
hivyo, utahitajika kufikiria juu ya maswala ya utendaji
yanayohusiana na udhibiti wa wakati, kuweka malengo, udhibiti wa
shinikizo, n.k. Pengine utahitaji kujizoesha tena katika maeneo
kama upangaji wa insha, namna ya kuimudu mitihani, na kutumia
mtandao kama marejeleo ya ujifunzaji.
Mambo utakayozingatia sana ni muda na nafasi, yaani muda
unaotenga kwa masomo yako na mazingira unamosomea.
Tunapendekeza kwamba uchukue nafasi hii – kabla ya kuanza
kujisomea kibinafsi – kujifahamisha mambo haya. Kuna marejeleo
mengi mazuri kwenye mtandao. Viungo vichache
vinavyopendekezwa ni:
5
http://www.how-to-study.com/
Tovuti ya “How to study” yaani “Jinsi ya kusoma” imetengwa mahsusi kwa ajili ya marejeleo ya mbinu za usomaji. Utapata viungo kuhusu kujitayarisha kusoma (orodha ya mambo tisa muhimu kuhusu mahali pazuri pa kusomea), kuandika kumbukumbu, mikakati ya kusoma vitabu vya kiada, kutumia vyanzo vya kumbukumbu, dukuduku la mitihani.
http://www.ucc.vt.edu/stdysk/stdyhlp.html
Hii ni tovuti ya Kitengo cha Maswala ya Wanafunzi, Virginia Tech. Utapata viungo vya namna ya kupanga muda wako (ikiwa ni pamoja na kiungo cha “wakati huenda wapi?”), orodha-kaguzi ya mbinu za usomaji, mbinu za kimsingi za kumakinikia jambo, udhibiti wa mazingira ya kusomea, kuandika kumbukumbu, namna ya kusoma insha kwa kusudi la kuchanganua, mbinu za kukumbuka.
http://www.howtostudy.org/resources.php
Hii ni tovuti nyingine ya “jinsi ya kusoma” iliyo na viungo muhimu kuhusu udhibiti wa wakati, kusoma kwa ufanisi, mbinu za kusaili/kusikiliza/kuchunguza, kufaidi kutokana na kutenda (ujifunzaji wa kiutendaji), kukuza kukumbuka, vidokezo vya namna ya kudumisha motisha, kukuza mpango wa ujifunzaji.
Viungo vilivyo hapo juu ni mapendekezo yetu ya kukuwezesha kuanza. Wakati tulipoandika, viungo vya tovuti hizi vilikuwa vinatumika. Ikiwa unataka kupata tovuti zaidi, nenda kwa www.google.com kisha upige taipu na kutafuata “self-study basics” (misingi ya usomi wa kibinafsi), “self-study tips” (vidokezo vya usomi wa kibinafsi), “self-study skills” (mbinu za usomi wa kibinafsi) au tovuti nyingine zenye mada kama hizo.
Je, unahitaji msaada?
Ndugu mwanafunzi, katika mchakato wako wa kujifunza, unaweza
kuhitaji msaada kuhusu mambo mbalimbali, kwa mfano, mahali
unapoweza kupata msaada na namna ya kupata msaada huo.
Pamoja na hayo, unaweza kuhitaji ufafanuzi kuhusu moduli
unazosoma. Hivyo basi, unashauriwa kuomba ufafanuzi wa yote
hayo kwa mratibu wa kituo chako au mwezeshaji wako. Pia,
unaweza kufungua tovuti ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
yenye anwani hii: www.iae.ac.tz au piga simu hii +255 22
2150836.
Maelezo ya jumla kuhusu moduli Error! No text of specified style in document.
6
Mazoezi
Baada ya kila somo, unahitajika kujibu maswali ya zoezi la somo.
Majibu ya zoezi hili la kila somo hautayawasilisha kwa mwezeshaji
wako, ni kwa ajili ya kufanya tafakuri ya ulichojifunza. Pia,
utapewa majaribio na mazoezi ambayo utayafanya na
kuyawasilisha kama utakavyoongozwa na mwezeshaji wako.
Pamoja na hayo, utatakiwa kufanya mitihani ya dhihaki/utamirifu
kwa ajili ya upimaji wa maendeleo yako ya kitaaluma.
7
Namna ya kutumia moduli hii
Ishara za pambizo Wakati ukijifunza moduli hii utagundua kwamba kuna matumizi
mengi ya ishara za pambizo. Ishara hizi zina jukumu la kushiria
aina fulani ya matini, kazi mpya au kubadilika kwa zoezi.
Zimetumiwa ili kukuongoza ujue namna ya kuitumia moduli hii.
Seti nzima ya ishara imetolewa hapa chini. Tunapendekeza kuwa
ujizoeze ishara hizi na maana yaka kabla ya kuanza masomo yako.
Zoezi Tathmini Zoezi la Mada Kisa Mafunzo
Mjadala Zoezi la Kikundi Usaidizi Kumbuka!
Matokeo Kusoma Tafakari Mbinu za
Usomaji
Muhtasari Istilahi Muda Kidokezi
9
Somo la Kwanza
Kuchambua Mikabala ya Sarufi Mapokeo na Sarufi Miundo Virai
Utangulizi
Katika sura hii tunakusudia kuchambua mikabala ya sarufi
mapokeo na sarufi miundo virai ambapo mambo yafuatayo
yatashughulikiwa. Mosi, sura inalenga kufafanua dhana ya mkabala
na chimbuko lake. Pili, tutafafanua misingi ya sarufi mapokeo
ambapo usuli wa sarufi mapokeo utafafanuliwa, kisha tutachambua
misingi ya sarufi mapokeo. Vilevile, katika sura hii tutafafanua
dhana ya sarufi miundo virai sambamba na misingi yake. Mwisho
sura imefumbata maswali/ mazoezi kwa ajili ya kujima.
Matokeo
Baada ya kukamilisha somo hili utaweza:
Kufafanua na Kufasili dhana ya mkabala wa kisarufi;
Kueleza chanzo cha kuibuka kwa mikabala ya kisarufi;
Kufafanua dhana na misingi ya sarufi mapokeo;
Kufafanua dhana na misingi ya sarufi miundo virai;
Kutofautisha baina ya sarufi mapokeo na sarufi miundo;
Kueleza maana ya dhana za misingi zifuatazo (kategoria, tungo, kirai, kishazi na sentensi);
Kubainisha virai vya lugha ya Kiswahili;
Kubainisha vishazi vya lugha ya Kiswahili;
Kubainisha sentensi za lugha ya Kiswahili; na
Kuchanganua sentensi kwa njia mbalimbali.
Kufafanu Dhana ya Mkabala na Mkabala wa Kisarufi
Kwa mujibu wa TUKI (2004) Mkabala ni utaratibu unaofuatwa ili
kukabili jambo. Kwa hiyo mkabala ni mtazamo wa namna ya
kufanya jambo fulani. Mkabala wa kisarufi unaweza kufafauliwa
kuwa ni mtazamo au utaratibu maalumu unaofuatwa katika
Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.
10
kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala lugha
fulani. Asili ya neno sarufi ni ugiriki ambapo kwa kigiriki inamana
ya “gramamantike”. Taaluma ya sarufi iliasisiwa na wanafalsafa
wa Ugiriki wakiwemo Plato na Aristotle. Katika harakati za
kuchimbua taaluma ya sarufi ndiko kulikozua mikabala mbalimbali
ya kisarufi.
Ndugu mwanafunzi, sasa tupitie aina za mikabala mbalimbali
ya sarufi na ufafanuzi wake kama ilivyojadiliwa hapa chini:
Taaluma ya sarufi imefafanuliwa katika mikabala mbalimbali ila
katika kiwango chetu tutatazama mikabala miwili ambayo ni:
a) Mkabala wa sarufi Mapokeo; na
b) Mkabala wa sarufi Miundo Virai
Kufafanua Misingi ya Mkabala wa Sarufi Mapokeo
Ndugu wanafunzi kipindi kilichopita tulijifunza kuhusu dhana ya
mkabala ambapo tulipitia kuhusu maana, chimbuko na aina ya
mikabala. Katika kipindi hicho tulitaja kuwa kuna aina mbili za
mkabala yaani: sarufi mapokeo na mkabala wasarufi miundo. Kwa
hiyo katika kipindi hiki tutajadili kwa undani aina hizo za mikabala
kwa kuangalia maana, chimbuko, misingi yake. Tuanze na mkabala
wa sarufi mapokeo:
Mkabala wa Sarufi Mapokeo
Huu ni mkabala wa awali/ kale ulioshughulikia sarufi ya lugha.
Mkabala huu ulizuka kuanzia karne ya 5 K.K (kabla ya Kuzaliwa
Kristo). Waasisi wake ni Plato, Aristotle, Protagoras, Thrax na
wengineo. Mkabala huu ulishughulikia sarufi kwa mtazamo wa
falsafa, dini, fasihi n.k. Katika sarufi mapokeo vipashio vya
uchanganuzi wa sarufi vilikuwa ni neno na sentesi.
Misingi ya Sarufi Mapokeo
Saufi mapokeo imejengwa na misingi mbalimbali kama ifuatavyo:
a) Mkabala wa sarufi mapokeo ulitumia lugha ya kilatini kama
msingi wa uchambuzi wa sarufi za lugha zote. Kwa wakati huo
lugha ya kilatini ilikuwa ipo katika maandishi. Kwa hiyo
11
kanuni na sheria za sarufi ya kilatini ndizo zilizotumika katika
kuchambua sarufi za lugha nyingine.
b) Wanasarufi mapokeo walichukulia kuwa lugha ya maandishi
ni bora zaidi kuliko lugha ya maadishi. Hii ndiyo sababu ya
kutumia kilatini kwani lugha ambazo hazikuwa katika
maandishi zilichukuliwa kuwa hazina sarufi.
c) Wanasarufi mapokeo walipendekeza kanuni za matumizi ya
lugha. Hivyo lugha ilipaswa iandikwe na kutamkwa kama
kanuni zinavyoelekeza kinyume chake lugha hiyo ilionekana
ni batili. Baadhi ya kanuni hizo ni kama vile:
Sentensi hapaswi kuanza na kiunganishi wala kuishia na
kihusishi, na
Vikanushi viwili au zaidi havipaswi kuambatana.
d) Mkabala wa sarufi mapokeo ulibainisha muundo wa sentensi
kuwa sentensi inaundwa na sehemu kuu mbili yaani kiima na
kiarifu. Plato ndiye aliyebaini kuwa sentensi imekitwa katika
kiima na kiarifu. Kiima huashiria mtenda na kiarifu huashiria
mtendwa.
e) Wanasarufi mapokeo pia waliainisha aina za maneno.
Dionysious thrax aliyebaini kuwa lugha ina aina nane za
maneno kama vile: Nomimo, Kitenzi, Kibainishi, Kihusishi,
Kibadala, Kielezi, Kiungo, Faridi pekee –mofimu huru.
f) Wanamkabala wa sarufi mapokeo walihusisha lugha na
taaluma ya sanaa, mantiki na falsafa. Hivyo lugha ilitumika
katika kazi hizo na lugha iliyotumika katika uchunguzi wa
sarufi ni ile iyotumiwa na wasomi, wanasiasa wakubwa na
watu maarufu tu, wale watu tabaka la chini walichukuliwa
hawajui lugha.
g) Aidha, wanamkabala wa kimapokeo waliainisha kategoria za
kisarufi kuwa ni nafsi, njeo kauli, dhamira uhusika na hali.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia kwa undani dhana ya
sarufi mapokeo, chimbuko na misingi yake sasa hebu chukua
kalamu na daftari tufanye zoezi lifuatalo:
Zoezi
1. Mkabala wa sarufi mapokeo ulizuka mnamo ...........................
Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.
12
2. Taja waasisi wawili wa mkabala wa sarufi mapokeo:
a) ...........................................................................................
b) ............................................................................................
3. Katika mkabala wa sarufi mapokeo sentesi iligawanywa
katika sehemu mbili ambazo ni:
a) ...........................................................................................
b) ...........................................................................................
4. .................... ni mwanamapokeo aliyeainisha aina za maneno.
5. Taja aina nane za maneno zilizoainishwa na wanasarufi
mapokeo.
6. Kila taaluma huwa na misingi yake. Jadili misingi ya
mkabala wa sarufi mapokeo.
Kufafanua Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai
Mkabala wa Sarufi Miundo Virai
TUKI (2004) wanafasili dhana ya muundo kuwa ni mpangilio wa
vipashio mbalimbali katika lugha.
Sarufi miundo virai ni utanzu unaojishughulisha na uchanganuzi
wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio
vyake (Massamba na wenzake, 2001).
Naye, Besha (2007) ameiita sarufi miundo virai kama “kanuni
vikundi” ambapo anafasiri kuwa ni sarufi inayoonyesha uhusiano
wa maneno na vipashio vingine vinavyojenga sentensi za lugha.
Hivyo, kutokana na fasili za wanaisimu hapo juu tunaweza kusema
kuwa mkabala wa sarufi miundo virai ni mkabala wa kisarufi
unaochunguza namna vipashio vidogo vinavyoungana ili kuunda
vipashio vikubwa zaidi. Hii ina maana kuwa namna neno na neno
linavyoungana ili kuunda kirai na kirai na kirai vinavyungana
kuuda kishazi na kishazi na kishazi vinavyoungana kuunda
sentensi. Mkabala huu unasisitiza kuwa vipashio katika tungo ni
sharti vichanganuliwe katika makundi (virai). Mkabala huu ulizuka
baada ya mkabala wa kimapokeo kushindwa kuchanganua miundo
13
ya lugha mbalimbali. Mkabala huu ni wa kisasa kwani huchunguza
lugha kisayansi. Mwasisi wa mkabala huu ni Noam Chomsky
(1957) katika kitabu chake cha “Syntactic Structure”.
Baada ya kufafanua dhana na chimbuko la mkabala wa sarufi
miundo virai sasa tutazame misingi ya mkabala huu.
Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai
Misingi ya sarufi miundo virai inafafanuliwa kama ifuatavyo:
a) Mkabala huu unatilia mkazo upekee wa lugha kuwa kila
lugha inaupekee wake. Hivyo lazima ichunguzwe kwa
misingi ya muundo wake wa vipashio kama vile maneno,
virai, vishazi na sentensi.
b) Mkabala wa sarufi miundo virai unasisitiza umuhimu wa
kuwa na kanuni zinazozalisha tungo au sentensi kutoka
darajia ya juu kabisa hadi ya chini
c) Mtazamo wa sarufi miundo virai unagawa sentensi katika
sehemu kuu mbili yaani Kirai Nomimo (KN) na Kirai Kitenzi
(KT).
d) Mtazamo huu unasisitiza kuwa kila kipashio katika sentensi
kipo katika kategoria fulani. Mfano kategoria ya neno, kirai,
kishazi ua sentensi.
e) Miundo Virai inaona kuwa kanuni za vipashio ni sharti
zifafanuliwe kwa kutumia msimbo mfano: N, KV nk.
f) Mkabala wa sarufi miundo virai unachanganua vipashio
mbalimbali katika tungo kwa kuonyesha uhusiano wake.
Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.
14
Muhtasari wa Somo
Katika somo hili tumejifunza sehemu kuu mbili katika muundo wa
sentensi ambazo ni Kirai Nomino (KN) na Kirai Kitenzi (KT).
Katika somo hili mwanafunzi amepitia mada ndogo zifuatazo:
Misingi ya Mkabala wa Sarufi Mapokeo, Misingi ya Mkabala wa
Sarufi Mapokeo na Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai,
Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai. Katika mada hizi
vipengele vifutavyo vilipitiwa: kategoria ya neno au virai
vinavyounda kirai nomino (KN), au virai vinavyounda kirai kitenzi
(KT) na maneno yanayounda virai vilivyoainishwa na kufafanua
dhana za kisintaksia lugha na sarufi na kuonyesha uhusiano uliopo
katika tanzu za sarufi.
Pia tumejifunza sifa mbalimbali za lugha pamoja na uhusiano
uliopo kati ya tanzu mbalimbali za fasihi. Sasa basi hebu chukua
kalamu yako na daftari ufanye zoezi fupi ili kupima uelewa wako
katika yale yaliyojadiliwaa hapo juu mambo muhimu ya
uchanganuzi wa tungo kwa mkabala wa sarufi miundo virai.
Zoezi la Somo
1. Mkabala wa sarufi miundo virai uliasisiwa na mwanaisimu
.....................mwaka...............
2. Eleza kwa kifupi chanzo cha kuibuka kwa mkabala wa sarufi
miundo virai.
3. Mkabala wa sarufi miundo virai unagawa sentensi katika
sehemu mbili ambazo ni ................................................. na
...........................................
4. Fafanua 4 hatua mbalimbali utakazofuata katika uchanganuzi
wa sentensi kwa mkabala wa sarufi miundo virai.
5. Tofautisha baina ya mkabala wa sarufi mapokeo na sarufi
miundo virai.
15
Somo la Pili
Kuchambua Kategoria za Kisintaksia
Utangulizi
Lengo la sura hii ni kuchambua kategoria za kisintaksia kwa
kuamisha kategoria mbalimbali za kisintaksia. Kwanza kabisa
tutafasili dhana za msingi kama sintaksia. Pili, kuchambua
kategoria za kisintaksia kama vile neno, kirai, kishazi na sentensi.
Katika uchambuzi huo wa kategoria tutajikita kwenye aina na
miundo yake. Tatu, tutachambua tungo na sentensi kwa njia ya
maelezo, mshale, matawi na jedwali. Aidha katika uchanganuzi wa
tungo na sentensi tutatumia mikabala yote miwili yaani mkabala
wa kimapokeo na ule mkabala wa kimuudo (sarufi miundo virai).
Matokeo
Baada ya kukamilisha somo hili utaweza:
Kufafanua dhana za msingi za Kisintaskia
Kubainisha kategoria ya neno
Kubainisha kategoria ya Virai
Ufafanuzi Dhana za Msingi za Kisintaksia
Sintaksia
Kwa mujibu wa Harper (2001-2010) Online Etymology Dictionary,
neno sintaksia liliibuka takribani miaka ya 1600 na linatokana na
neno la Kifaransa syntaxé au la Kilatini au Kigiriki syntaxis ambalo
maana yake ni kupanga au kuweka vitu pamoja katika mpango.
Hata hivyo, wataalamu wengi wa masuala ya sintaksia
wanakubaliana kuwa neno hili lina asili ya Kigiriki kwa kuwa
Wagiriki ndio wakongwe katika taaluma mbalimbali hapa duniani,
ikiwa ni pamoja na taaluma ya lugha. Hata hivyo historia ya isimu
inaonesha kuwa, uchunguzi wa kwanza wa lugha ulianza na
Wamisri mnamo karne ya 5 Kabla ya Kuzaliwa Kristo (KK),
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
16
Wagiriki ndio walioweka msingi wa taaluma ya lugha tuijuavyo
hivi leo (Khamis & Kiango, 2002: 1).
Kwa hiyo, sintaksia ni nini katika taaluma ya isimu?
Besha (1994: 84) anafasili sintaksia kama taaluma inayojihusisha
na uchambuzi na ufafanuzi wa muundo wa sentensi za lugha Kwa
mujibu wa O’Grady (1996: 181), sintaksia ni taaluma
inayochunguza jinsi maneno yanavyounganishwa ili kuunda
sentensi. Sintaksia kwa mujibu wa Massamba na wenzake (2009:
34) wanafasili sintaksia kama ni utanzu wa sarufi
unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika
sentensi na uhusiano wa vipashio vyake.” Wanaendelea kusema
kuwa katika utanzu huu kinachochunguzwa ni zile sheria au kanuni
ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha
katika mfuatano (neno moja baada ya jingine) kwa namna ambayo
itayafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika na kueleweka
katika lugha husika.
Kwa hiyo, sintaksia inaweza kufasiliwa kuwa ni taaluma
inayochunguza miundo ya tungo na kanuni mbalimbali za lugha
zinazotawala miundo hiyo. Katika uchunguzi huo, sintaksia
huhusika na mpangilio wa maneno katika miundo mitatu
iliyopangwa kidarajia, yaani jinsi maneno yanavyopangwa ili
kuunda virai, vishazi na sentensi.
Kategoria
Hamisi na Kiango (2009) wanafasili dhana ya kategoria kama
jamii, seti, kundi au makundi ya maneno yanayofanya kazi ya
kufanana. Kwa mantiki hiyo tunaweza kusema kuwa kategoria ni
darajia yoyote ya vipashio inayotumika katika uchambuzi wa lugha
fulani.
Tungo
Massamba na wenzake (2001) wanafasili dhana ya tungo kama
neno au maneno yanayotoa taarifa fulani ambayo inaweza kuwa
kamili au isiwe kamili. Anaendelea kufafanua zaidi kwa kutaja aina
za tungo kuwa ni neno, kirai, kishazi na sentensi. Hivyo, tungo
inaweza ikadokeza maana kamili na isiyo kamili.
17
Neno
Dhana ya neno inautata katika kuifasili hii ni kutokana na
mitazamo mbalimbali inayotumiwa katika somo letu tutatizama
dhana ya neno kisarufii ambapo inaelezwa kama ifuatavyo: Tungo
Mdee (1988) anafasili dhana ya neno kisarufi kuwa ni kipashio cha
kiisimu ambacho kipo kati ya mofimu na kifungu cha maneno.
Kirai
Dhana ya kirai imefafanuliwa na wataalamu kama ifuatavyo:
Matei (2008) anafasili kirai kama fungu la maneno ambalo hufanya
kazi kama neno moja. Kirai hudokeza maana lakini maana hiyo si
kamili...na hakina muundo wa kiima-kiarifu.
Massamba na wenzake (2009) wanafasili dhana ya kirai kama
kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho
hakina uhusiano wa kiima kiarifu
Kutokana na fasili za wataalamu hao tunabaini kuwa kirai
kinaweza kuwa sehemu ya kiima au kiarifu. Hivyo, tunaweza
kuhitimisha kwa kufasili dhana ya kirai kuwa ni kipashio cha
kimuundo kinachoanzia neno moja na kuendelea ambacho hakina
muudo kamili wa kiima na kiarifu.
Kishazi
Kishazi ni tungo ndogo yenye uoanifu ambayo nikubwa kuliko
neno au kirai lakini iliyo sehemu ya sentensi kubwa (Massamba na
wenzake, 2001).
Matei (2008) anafasili dhana ya Kishazi kama kundi la maneno
ambalo lina kiima kimoja na kiarifu kimoja.
Naye, Matinde (2012) anafasili dhana ya kishazi kuwa ni neno au
kifungu cha maneno chenye kiima na kiarifu au kiarifu pekee
ambacho ni sehemu ya sentensi kuu.
Hivyo, kwa ujumla tunaweza kuwa kishazi ni tungo ambayo ina
kiima na kiarifu na inaweza kusimama pekee na kukamilisha
maana au inaweza isisimame pekee na kukamilisha maana.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
18
Sentensi
Sentensi ni tungo iliyokamili kisarufi ambayo inajitegemea
kimaana (Wahiga, 1999)
Besha (2007) anadai kuwa sentensi ni tungo iliyo kamilifu kisarufi
isiyotegemea mazingira ya mwasiliano ili kueleweka.
Kwa hiyo, kutokana na fasili za wataalamu hao tunaweza kufasili
dhana ya sentensi kuwa ni tungo yenye kifungu cha maneno chenye
muundo wa kiima na kiarifu inayojitosheleza kiimaana.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kufafanua dhana tangulizi za
msingi katika sura hii, sasa tunajikita katika kubainisha tungo/
kategoria mbalimbali za kisintaksia ambapo tutaangalia
maana, aina, muundo na uamilifu wa tungo hiyo katika lugha
ya Kiswahili kama ifuatavyo:
Kubainisha Kategoria ya Neno
Lugha imeundwa na maneno mbalimbali, na maneno hayo
hugawanywa katika makundi kulingana na kazi zake. Hata hivyo
kategoria za maneno hazijafungika bali ziko wazi ili kupokea
maneno mapya kwa kadri yanavyozaliwa/ kujitokeza. Kila
kategoria ya maneno ina maneno mengi yenye mpangilio wake
wenye kanuni fulanifulani. Aidha, watalaamu mbalimbali
wanatofautiana katika kuainisha idadi ya maneno na istlahi
wanazotumia. Wapo wanaotaja kategoria saba (tazama Nkwera,
1978; Kapinga, 1983, Massamba na wenzake 2009). Kwa uapnde
wa wataalamu walioanisha kategoria nane (tazama Kihore, 1996).
Katika mjadala wetu wa leo tutajadili kategoria/ aina saba za
maneno kama zinavyoainishwa hapa chini:
i) Nomino,
ii) Kitenzi,
iii) Kivumishi,
iv) Kielezi,
v) Kihusishi,
vi) Kiwakilishi, na
19
vii) Kiunganishi.
ANGALIZO: Ndugu mwanafunzi, mbali na kwamba
wanasarufi wanakubaliana kuhusiana na aina hizo saba za maneno
zilizoanishwa hapo juu, bado kuna haja ya kuifahamu aina ya nane
ya neo kmama ilivyoanishwa na (Kihore, 1996) anaongezea aina ya
nane katika kategoria za maneno yaani “Vihisishi”. Haya ni
maneno ambayo yanaonyesha hisia, kwa mfano, Aaah! Mungu
wangu! Jamani!
Ndugu mwanafunzi, hebu sasa tuanze kufafanua na kudadavua
kategoria za maneno katika upekee wake ili kuzielewa
kategoria hizi kwa undani zaidi. Hebu sasa tupitie kategoria
hizo kama ifatavyo:
Nomino
Khamisi (2002) anafasili dhana ya nomino kuwa ni maneno
ambayo huwakilisha majina ya watu, vitu na mahali nk.
Nomino ni neno linalotaja mtu, kitu, hali au mahali (Wahiga,
1999). Mwanasarufi huyu anafafanua zaidi kwa kusema kuwa
nomino ni muhimu sana katika lugha kwa sababu kila sentensi ni
lazima iwe na nomino au kiwakilishi chake. Hivyo, nomino ni
maneno yanayodokeza/ kutaja majina ya watu, mahali, vitu, hali
n.k. Wataalamu mbalimbali wameainisha aina za nomino kama
ifuatavyo:
Ndugu mwanafunzi zipo aina mbalimbali za nomino kutokana
na mitazamo mbalimbali ya wanasarufi lakini kuu ambazo
zinajulikana na kutumiwa na wataalamu mbalimbali ni kama
ifauatavyo:
Aina za Nomino
1) Nomino za pekee: Hizi ni nomino ambazo hutaja vitu
mahususi / vya asilia mf: mahali, mito, bahari, viungo vya
mwili n.k mfano: mlima, Dodoma, Pasfiki nk
2) Nomino za kawaida: Ni aina ya nomino ambazo hutaja majina
ya watu mfano: Eliya, Hasssani, Amina nk.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
20
3) Nomino za dhahania: Hizi ni nomino ambazo huwakilisha/
hutaja vitu vya kufikirika au hisi mf: Mungu, wema upendo,
malaika, uzuri, uchoyo n.k
4) Nomino za familia/ kikundi: hizi huwakilisha/ hutaja majina
yenye vitu vingi ndani yake mf: kikosi, kamati, bunge , baraza,
kundi n.k
5) Nomino za kitenzi jina: hizi hueleza vitu vinavyotokana na
matendo mbalimbali aghalabu nomino hizi hufungamana na -
ku mwanzoni mf: kuimba, kucheza, kufurahi n.k.
Dhima/ Kazi za Nomino
Nomino huweza kutofautishwa na maneno ya kategoria nyingine
kutokana na kazi zake ndani ya miundo ya tungo. Haya
yanadhihirishwa kama ifuatavyo:
i) Nomino hufanya kazi kama kiima mf:
Mtoto/ anacheza
K
Ndugu wanafunzi kabla ya kuendelea zaidi ni vema tuangalie
dhana ya kiima. Kiima ni sehemu ya mwanzo katika tungo ambayo
hueleza/ hubeba mtenda wa jambo. Kiima chaweza kuundwa na
neno moja au zaidi.
ii) Nomino hufanya kazi kazi kama yambwa. Mf:
Mwalimu/ amenunua / kitabu
K y
Ndugu mwanafunzi, hebu sasa tuone maana ya dhana hii ya
yambwa.
Yambwa ni neno au kikundi cha maneno ambacho hueleza
mtendwa wa jambo au kitu au mtu ambaye huathiriwa moja kwa
moja na kitendo kutoka kuwa mtenda. Kwa mfano, katika tungo
hiyo hapo juu neno kitabu ndiyo linaathiriwa na tendo.
iii) Vilevile nomino hufanya kazi kama yambiwa. Mf:
Mwalimu amemnunulia mwanafunzi kitabu
Yambiwa
21
Ndugu mwanafunzi, kutokana na mfano huo hapo juusasa kuna
umuhimu pia ya kujua maana ya dhana ya yambiwa ili tuweze
kuelewa zaidi dhana ya hii.
Yambiwa ni neno ambalo linadokeza mtendewa wa jambo na pia ni
mtendwa ambaye haathiriwi moja kwa moja na tendo kutoka kwa
mtenda. Hivyo katika sentensi hiyo hapo juu neno mwanafunzi
linatendewa kitendo husika lakini kitendo hakimuathiriri moja kwa
moja bali huonyesha hali ya kutendewa.
Angalizo: Ndugu mwanafunzi, sentensi inaweza kuwa na
yambwa tu. Wakati mwingine inaweza kuwa na vyote, yaani
yambwa na yambiwa. Katika hali hii kuna kitu kimoja wapo
ambacho kinapokea tendo moja kwa moja na kingine hupokea
tendo lile sio moja kwa moja. Hali hii ndiyo huleta yambwa na
yambiwa
iv) Nomino huweza kuwa kijalizo yaani katika kukamilisha tu
maana ya sentensi na mara nyingi nomino ya namna hii hutokea
mwishoni mwa sentensi. Kwa mfano:
Mwalimu amenunua kitabu (Neno kitabu hapa limetumika kama
kijalizo)
Kiwakilishi
Ni maneno ambayo husimama badala ya nomino katika tungo/
sentensi kwa maana ya kuwakilisha nomino au kikundi nomino.
Aina za Viwakilishi
i) Viwakilishi vya nafsi: mimi,wewe, yeye, sisi, ninyi, wao
—Mimi ni mwalimu
—Yeye ni mwalimu
ii) Viwakilishi Vionyeshi: huyu/Yule, hiki/kile, hili/lile, hii/ ile
huu/ule hapa/pale
— Huyu ni mwalimu
— Kile ni kitabu
iii) Viwakilishi Viulizi: gani, lini, nini nk
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
22
— Nani ni mwalimu
— Yapi yameiva
iv) Viwakilishi vimilikishi: wangu/wetu, wako/wenu,
wake/wao, yangu/yetu, lake/lao, n.k
— Kwake sikujui
— Lao limepotea
v) Viwakilishi vya sifa. Hivi ni viwakilishi ambavyo
huwakilisha nomino kwa kutaja sifa zake. Kwa mfano:
warefu, wadogo, wafupi n.k.
_ Wakubwa kwa wadogo wanasoma
_Wafupi wasimame
vi) Viwakilishi vya idadi: wote, kimoja, michache, mengi,
kumi nk.
— Mmoja ni mwalimu
— Vyote ni vitabu
Dhima za viwakilishi
Kiwakilishi hufanya kazi kama kiima cha tungo
Aidha , kiwakilishi kinadhima ya kuwakilisha nomino
Kivumishi
Ni neno/ maneno ambayo hufafanua au kueleza zaidi juu ya
nomino. Hivyo kivumishi hutoa sifa juu ya nomino yaani jinsi
nomino ilivyo, inavyoonekana, inavyofikiriwa, tabia na idadi yake.
Aina za vivumishi
Vivumishi vinaweza kugawanywa kama ifuatavyo:
i) Vivumishi vya Sifa: -ema, -dogo, -chafu, nyenyekevu n.k. Kwa
mfano:
23
Mtoto mwema amekuja
Nguo chafu zimefuliwa
ii) Vivumishi vya Idadi: -chache, -ingi, -kubwa n.k
Idadi kubwa ya watanzania ni wakulima
Wanafunzi wengi wamefaulu mitihani
iii) Vivumishi vya umiliki: -ake, -anu, -etu n.k
Mwalimu wetu amesafiri
Kitabu chenu kimechanika
iv) Vivumishi viulizi: -ngapi, -gani, -ipi
Nyuzi ngapi zimekatika
Tunda lipi limeoza
v) Vivumishi vya pekee: -ingine, -ote (wote) n.k
Kucheza kwingine ni hatari
Mwanafunzi yeyote asipite hapa
Dhima za Kivumishi Kisarufi
Kivumishi hukumusha nomino; yaani hutoa taarifa juu ya nomino
au kiwakilishi chake.
. Kivumishi hutumika kama kijalizo. Angalia mfano ufauatao:
Juma ni mzuri
Hivyo, katika tungo hiyo hapo juu neno mzuri linakamilisha kitenzi
ni.
Kitenzi
Ni kategoria ya maneno yanayoeleza tendo linalofanywa na
nomino. Kisarufi huwa na sehemu kuu mbili yaani: kiima na
kiarifu. Pia ifahamike kuwa kitenzi ndiyo msingi wa sentensi kwa
maana bila kitenzi kwa hakika sentensi husika haiwezi kueleweka.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
24
Aina za Kitenzi
Aina za vitenzi zimejadiliwa na wanaisimu mbalimbali kwa namna
tofauti tofauti. Wataalamu hawa wameanisha aina mbili (2) za
vitenzi nazo zinafafanuliwa hapa chini:
i) Vitenzi Halisi
ii) Vitenzi Vishirikishi
i) Vitenzi halisi ni aina ya vitenzi vinavyoarifu tendo
linaliofanywa na mtu, mnyama, mdudu nk. Mfano:
analima, alikuwa anacheza n.k.
Aidha vitenzi hivi vimegawanyika katika makundi mawili yaani
vitenzi vikuu na visaidizi.
Vitenzi vikuu hubeba ujumbe unaorejelewa na kiima
Kwa mfano: analima, anacheza nk.
Vitenzi visaidizi husaidia vitenzi vikuu kuleta maana
kamili katika tungo kwa mfano: alikuwa, anataka nk.
h) Vitenzi vishirikishi nia aina ya vitenzi ambavyo hueleza
hali, tabia, sifa na mazingira ya wahusika. Kwa mfano: ni,
ndiye, u, angali, yu, si nk.
— Musa ni mkulima
— John ndiye fisadi
— Wewe u mwanafunzi mzuri
Ifahamike kuwa umbo la msingi la vitenzi ni lile ambalo
halijanyambulishwa mfano: -l-a, pig-a, fung-a, f-a, som-a, nyw-a,
som- nk.
Dhima za Vitenzi
Vitenzi hufanya kazi kama kiarifu kwa maana hutoa taarifa kile
kinachofanywa na nomino husika.
Kielezi
Kielezi ni aina ya maneno yanayofafanua juu ya kitenzi, kivumishi
na kielezi chenyewe. Kielezi kinapoeleza juu ya kitenzi ni dhahiri
25
kwamba hudokeza jinsi, wakati, kwanini na kwa kiwango gani
tendo hilo linatendeka. kwa mfano:
Mwizi alipigwa sana = kielezi cha kitenzi
Mtoto ni mweupe sana = kielezi cha kivumishi
Mwalimu anaongea upesi mno = kielezi cha kielezi
Aina za Vielezi
Vielezi vimegawanywa na watalaamu katika makundi mbalimbali.
Hatahivyo hapa tutagawa kielezi katika makundi makuu manne
kama ifuatavyo:
i) Vielezi vya namna: haraka, chubwi, fofofo, kifudifudi,
mno, n.k
Mtoto anatembea haraka mno
Kikongwe amelala fofofo
ii) Vielezi vya kiasi: mara nyingi, daima, mwaka huu, mara
tano n.k
Mvua hunyesha maranyingi
Asha ni mwigizaji daima
iii) Vielezi vya mahali: ndani, juu, shimoni, nyuma n.k
Panya ameingia shimoni
Mtoto anacheza nyuma ya nyumba
iv) Vielezi vya wakati: asubuhi, mapema, siku, wiki, mwaka
n.k
Mgeni anakuja jioni
Sherehe itafanyika wiki ijayo.
Dhima/ kazi ya Kielezi
Kazi kubwa ya kielezi ni kufafanua/ kutoa taarifa juu ya vitenzi,
vivumishi na vielezi vingine
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
26
Kihusishi
Ni maneno yanayoonyesha uhusiano wa vitu, watu, matukio, hali
na muda. Mathalani maneno hayo huonyesha uhusiano baina ya
sehemu mbili au zaidi. Haya ni maneno ambayo yana kazi ya
kisarufi ya huhusianisha maneno katika tungo au sentensi. Zipo
aina mbalimbali za vihusishi kama vile vihusishi vya wakati,
mahali, jinsi, kiasi n.k.
Aina za Vihusishi
Kimuundo vihusishi huweza kugawanywa katika makundi 2
i) Vihusishi vya a- unganifu yaani a- hupachikwa katika nafasi
iliyowazi. Kwa mfano: wa,ya,cha,la, za, vya, na, pa, mwa,
kwa nk. Hata hivyo maneno hayo hutumika pamoja na
maneno mengine kama vile: mbele ya, kwa kalamu, wakati
wa, na mwlimu, mahali pa, juu ya nk. Zingatia sentensi
zifuatazo:
a) Mtoto anacheza nyuma ya mlango
b) Musa anatembea kwa miguu
c) Kuna tofauti kati ya mwalimu na mwanafunzi
NB: Ikumbukwe kwamba a-unganifu pia hutumika kuunda
vivumishi na vielezi
ii) Aina ya pili ya vihusishi ni vile vya mkopo kwa maana
kwamba maneno hayo yametokana na kategoria nyingine za
maneno ya Kiswahili ama toka lugha za Kigeni. Aina
nyingine za maneno zinazoweza kujitokeza katika vihusishi
ni Nomino, Vitenzi na Vielezi kwa mfano: hadi, katika, tena,
kuliko, hata, lakini, bila, pasipo, ama, au, tangu, kwamba,
ingawa nk. Kama inavyodhihirika katika mifano ifuatayo:
a) Juma amenipiga tena amevunja mkono
b) Anakimbia toka shuleni hadi nyumbani
Maneno tena na hadi katika sentensi hapo juu ni vielezi lakini
katika sentensi hizo yametumika kuhusisha maneno mbalimbali.
Kwa maneno mengine katika tungo hizo yanafanya kazi ya
uhusishi pasi na uelezi, kwa mfano:
27
c) Raia wameuawa pasipo makosa
d) Jino linauma sana kuliko jicho
Halikadhalika maneno pasipo na kuliko kwa uhalisia ni vitenzi
lakini katika sentensi hizo yametumika kuhusianiasha maneno
husika. Hapa pia ni vema kukumbuka kwamba sintaksia haijikiti na
dhana za maneno bali huchunguza namna vipashio vinavyofanya
kazi katika tungo kwa kuangalia mpangilio na uhusiano wake.
Dhima za Kihusishi
• Kihusishi hufanya kazi ya kuhusisha na kueleza
Viunganishi
Viunganishi ni maneno yanayounganisha maneno au mafungu ya
maneno ama sentensi. Viunganishi ni lazima viunganishe maneno
au kategoria za hadhi sawa. Kwa mfano:
Baba na mama.
Kaka analima lakini dada anasuka mkeka.
Katika mifano hiyo utaona kuwa kiunganishi na kimeunganisha
neno na neno pia kiunganishi lakini kimeunganisha sentensi na
sentensi. Aidha ni vema ikumbukwe kuwa viunganishi na vihusishi
vinashabihiana kwa sababu wakati mwingine maneno yaleyale
hutumika katika kategoria zote. Cha msingi ni kuzingatia namna
yanavyojitokeza katika tungo na kazi inayobebwa na neno hilo.
Zingatia mifano ifuatayo:
1) Baba analima na mama anapika.
2) Mwizi amepigwa na askari.
Sentensi zote hapo juu zimetumia neno na. Hatahivyo neno hilo
limebeba dhima tofauti ambapo katika sentensi ya 1 na limetumika
kama kiunganishi kwa maana kwamba kinaunganisha sentensi
mbili yaani “baba analima na mama anapika”. Katika sentensi ya
2 neno na limetumika kama kihusishi kwa mantiki kwamba
linahusisha tendo la kupigwa na askari.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
28
Dhima za Kiunganishi
Kiunganishi kazi yake ni kuunganisha maneno, tungo hadi sentensi.
Ndugu wanafunzi baada ya kubainisha aina za maneno na
kutazama mifano kuntu sasa tufanye zoezi lifuatalo:
Zoezi
1. Bainisha nomino katika sentensi zifuatazo na ueleze ni aina gani
ya nomino:
i) Maradhi hayo yamefutiwa chanjo
ii) Kuiga mitindo ya kigeni kumemletea madhara makubwa
iii) Darasa lile linafanya vizuri katika mitihani
iv) Utandawazi umerahisisha maisha
v) Kipungu huruka juu kwa madaha.
2. Taja dhima 4 za nomino
3. Taja aina 5 za vivumishi kisha kwa kila kivumishi tunga sentensi
mbilimbili
4. Bainisha vitenzi katika sentensi zifuatazo kisha eleza ni aina gani
ya kitenzi
i) Mbiu ya mgambo ingali inalia
ii) Kikombe ki mezani
iii) Mwalimu alikuwa anataka kupumzika
iv) Sahani zimo kabatini
v) Yule ni mhariri
vi) Babu angali analima
vii) Sisi tu wachezaji hodari
5. (a) Eleza maana ya kielezi
(b) Pigia mstari vielezi katika sentensi zifuatazo
29
i) Minazi imepandwa Mombasa
ii) Mgonjwa alimeza vidonge mara mbili kwa kutwa
iii) (iii) Amina anatembea kilimbwende
iv) (iv) Daudi anazungumzwa haraka sana
v) Mwalimu anawapenda wanafunzi kwa dhati
6. Tofautisha baina ya kategoria ya kiunganishi na kivumishi
7. Tunga sentensi mbilimbili ukitumia vihusishi katika
a) Kulinganisha
b) Wakati
c) Mahali
d) Sababu
e) Mtenda
Baada kujadili kina na kufanya zoezi fupi kuhusiana kategoria
ya neno sasa tuingie katika kuangalia kategoria ya virai.
Katika mada hii ndogo tutajikita katika kubainisha kategoria
ya kirai (kikundi) ambapo tutajikita zaidi katika kubainisha aina
za virai, muundo na dhima za virai kwa ujumla. Sasa tuanze moja
kwa moja na kubainisha aina za virai vya Kiswahili kama
ifuatavyo:
Kubainisha Kategoria ya Virai
Aina za Virai
Wanaisimu mbalimbali wamebainisha aina tofautitofauti za virai
lakini kimsingi tuna aina tano za virai kama zinavyoainishwa hapa
chini:
a) Kirai Nomino (KN)
b) Kirai Kivumishi (KV)
c) Kirai Kitenzi (KT)
d) Kirai Kielezi (KE)
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
30
e) Kirai Kihusishi (KH)
Kirai Nomino
Massamba na wenzake (2001) wanafasiri dhana ya kirai nomino
kuwa ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino na
mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno. Kirai
nomino hujengwa kwa nomino moja au zaidi au kiwakilishi cha
nomino (Matinde, 2012). Hivyo kwa ujumla, tunaweza kufasili
kirai nomino kama aina ya kirai ambacho neno kuu ni nomino au
kiwakilishi cha nomino.
Muundo wa Kirai Nomino
Kirai Nomino kinaweza kuundwa na maneno yafuatayo:
(i) Nomino pekee, kwa mfano:
Baba anakula
(ii) Kiwakilishi pekee, kwa mfano:
Wewe unapenda Kiswahili?
(iii) Nomino zaidi ya moja, kwa mfano:
Walimu na wazazi walihudhuria mkutano.
(iv) Nomino na kivumishi kimoja au zaidi
Mtoto mdogo analia.
Kijana mweusi mfupi mkorofi ameumia
(v) Kiwakilishi na kivumishi
Ile nyeupe inauzwa.
(vi) Nomino na kishazi tegemezi (sentensi) kwa mfano:
Kitabu kilichonunuliwa kimepotea.
(vii) Nomino, kivumishi na kishazi tegemezi kwa, mfano:
Meza kubwa niliyopewa imevunjika.
31
(viii) Nomino ya kitenzi jina kwa, mfano:
Kutembea kumenichosha.
(ix) Nomino ya kitenzi jina na kivumishi
Kucheza kwake kunahatarisha.
(x) Nomino na kihusishi/ vihusishi
Mtoto wa jirani
Askari wa jeshi la anga la Kibaha
Dhima ya Kirai Nomino
Kirai Nomino kina dhima kama kiima, yambwa na yambiwa katika
sentensi.
Kwa mfano;
Walimu wakuu waliwapa wanafunzi wao wote vyeti vyao
Kiima yambiwa yambwa
Kirai Kitenzi
Massamba na wenzake (2001) wanaeleza kirai kitenzi kama kirai
ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya kitenzi
na neno au mafungu ya maneno.
Kirai kitenzi huundwa kwa kitenzi na maneno mengine
yanayohusiana kitenzi hicho (Matinde, 2012)
Hivyo, Kirai kitenzi ni aina ya kirai ambacho neno kuu lake ni
kitenzi. Kirai hiki kina miundo ifuatayo:
Muundo wa Kirai cha Kitenzi
(i) Kitenzi kikuu pekee, kwa mfano:
Amekuja.
(ii) Kitenzi kikuu na nomino moja au zaidi, kwa mfano:
Wamenunua vitabu.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
32
Amempa mwanafunzi zawadi.
(iii) Kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi na kitenzi kikuu, kwa
mfano:
Alikuwa anakula
Alikuwa anataka kununua gari
(iv) Kitenzi kikuu na kielezi
Mtoto analia sana
(v) Kitenzi kishirikishi na nomino
Juma ni mgonjwa
(vi) Kitenzi kikuu na kihusishi
Anapigwa na askari
Dhima za Kirai kitenzi
Kidhima, kirai kitenzi kinafanya kazi ya kiarifu.
Kirai Kivumishi
Matinde (2012) anafafanua kirai kivumishi kuwa ni kirai ambacho
kimekitwa kwenye kivumishi.
Kwa hiyo, kirai kivumishi ni aina ya kirai ambapo neno kuu lake ni
kivumishi. Miundo ya kirai kivumishi inaweza kuchanganuliwa
kama ifuatavyo:
Miundo ya Kirai Kivumishi
(i) Kivumishi kimoja au zaidi, kwa mfano:
Mtoto mzuri
Kijana mrefu mweusi mtanashati
(ii) Kivumishi na nomino moja au zaidi, kwa mfano:
Mti wenye matunda
33
(iii) Kivumishi na kihusishi, kwa mfano:
Kamusi kubwa ya Kiswahili
(iv) Kivumishi na kishazi tegemezi, kwa mfano:
Mtoto mzuri aliyepewa zawadi
(v) Kivumishi na Kielezi kimoja au zaidi, kwa mfano:
Kiti ni kizuri mno
Amenunua mpira mweusi mzuri sana
Dhima ya Kirai kivumishi
Kirai kivumishi kinadhima ya kuvumisha.
Kirai Kielezi
Kirai kielezi ni kirai ambacho neno lake kuu ni kielezi. Kirai
kielezi kimejengwa na miundo mbalimbali kam ifuatavyo:
Miundo ya Kirai kielezi
(i) Kielezi kimoja au zaidi, kwa mfano:
Anatembea polepole.
(ii) Anaongea haraka sana.
(iii) Kielezi na kivumishi, kwa mfano:
Amekwenda shuleni kwetu.
(iv) Kielezi na kihusishi kimoja au zaidi, kwa mfano:
Amekaa ofisini kwa mwalimu.
Amenunua gari zuri kwa fedha za mkopo.
Dhima ya Kirai kielezi
Kirai kielezi kinafanya kazi ya kueleza.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
34
Kirai Kihusishi
Kirai kihusishi ni kikundi ambacho neno lake kuu ni kihusishi.
Kirai kihusishi kimekitwa kwenye miundo ifuatayo:
Miundo ya Kirai Kihusishi
(i) Kihusishi kimoja au zaidi na nomino
Ameweka fedha juu ya kabati
Nyimbo zitaimbwa wakati wa ibada ya mchana
(ii) Kihushi na nomino cha kitenzi jina, kwa mfano:
Amehukumiwa kwa kusaini mkataba wa kilaghai
Amepewa zawadi kwa kucheza kimasai
Dhima ya Kirai kihusishi
Kirai kihusishi hufanya kazi ya huhusisha na kueleza nomino,
kivumishi, kitenzi na kielezi
Ndugu wanafunzi baada ya kubainisha kategoria za virai
Kiswahili kwa kuzingatia vigezo vya aina, muundo na dhima
yake katika lugha, kwa sasa hatunabudi kufanya zoezi lifuatalo
ili kukazia maarifa kwa yale tuliyojifunza. Hebu sasa chukua
kalamu na daftari la mazoezi ili tuweze kufanya zoezi hili.
Zoezi
1) Tunga sentensi 10 kisha bainisha :
(a) Kirai nomino (b) Kirai kivumishi
(b) Kirai kitenzi (d) Kirai kielezi
(e) Kirai kihusishi
2) Eleza kwa mifano dhima ya Kirai Nomino katika Kiswahili.
3) Pigia mstari virai katika sentensi zifuatazo:
(i) Uwajibikaji wake ulinusuru kipato cha familia yake.
(ii) Askari wa jeshi la anga Kibaha atafanya ziara yake kesho.
35
(iii) Mamba wengi hukaa kwenye ukingo wa mto.
(iv) Hawa wametumia madaraka ya kiofisi kwa manufaa yao.
(v) Furushi hilo lilipatikana katikati ya taka nyingi.
4) Bainisha dhima ya kisarufi ya kihusishi.
5) Fafanua miundo mbalimbali ya virai vya Kiswahili.
Kubainisha Vishazi vya Kiswahili
Katika kubainisha vishazi vya Kiswahili tutachunguza aina na
muundo wa vishazi tegemezi na dhima za vishazi hivyo katika
tungo za lugha ya Kiswahili. Ndugu mwanafunzi, jiandaye
kupitia mada yetu hii ndogo kwa ufasaha ili uweze kuelewa
kwa undani kuhusiana na aina ya vishazi:
Aina za Vishazi
Katika lugh lugha ya Kiswahili kuna aina kuu mbili za vishazi
ambavyo ni:
i. Kishazi Huru ( K/H)
ii. Kishazi Tegemezi ( K/Tg)
Kishazi Huru
Kishazi huru ni kishazi ambacho kinaweza kusimama peke yake na
kuleta maana kamili. Kwa mfano:
(a) Baba anakula.
(b) Tunda limedondoka.
Kishazi Tegemezi
Ni kishazi ambacho hakiwezi kusimama peke yake na kukamilisha
maana kamili. Kwa mfano:
(a) Mtoto aliyekuja jana ..............................................................
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
36
(b) Mwalimu aingiapo darasani ...................................................
Muundo wa Vishazi Tegemezi
i. Vishazi tegemezi vyenye muundo “o” rejeshi. Hivi ni vile
vishazi tegemezi ambavyo huundwa na “o” rejeshi na -
amba-. Vishazi hivi hurejelea nyuma jambo
linalozungumzwa na Kirai Nomino Kwa mfano:
Ukuta uliojengwa umebomoka
Mbuzi aliyekata kamba amekatwa tena
ii. Muundo wa Vishazi tegemezi vyenye viambishi vya
masharti. Hivi ni vile viambaishi rejeshi ambavyo
huundwa na viambishi vya masharti kama vile : ki, nge,
ngali nk) Kwa mfano:
Wananchi wakinichagua hawatajuta.
Miundo mbinu ingeimarishwa maendeleo makubwa
yangepatikana.
Maneno yalokozwa wino hapo juu ni vishazi tegemezi
ambavyo vinadokeza masharti fulani katika tungo hizo.
iii. Vishazi tegemezi vyenye muundo wa viunganishi tegemezi.
Hivi ni vishazi ambavyo hujengwa na maneno ambayo
hudokeza utegemezi. Viambishi tegemezi huweza
kujitokeza mwanzoni mwa tungo vile: kama, ikiwa, kwa
kuwa, kwamba, japo, iwapo nk. Kwa mfano:
(a) Kama utakubali tutasafiri sote
(b) Ikiwa katiba mpya itakubaliwa wananchi
watanufaika sana.
(c) Kwa sababu zisizozuilika mkutano umeahirishwa
Maneno kuwa, kama, na ikiwa ni vishazi rejeshi vyenye
viunganishi vya masharti
iv. Vishazi tegemezi vyenye muundo wa viambishi vya wakati.
Hivi ni vishazi tegemezi ambavyo hudokezwa na matumizi
ya vihusishi vya wakati. Mara nyingi vishazi rejeshi hivi
huwa kama vijalizo katika sentensi Kama vile: hadi, kwa
37
sababu, baada ya, kabla ya nk. Vilevle vishazi rejeshi
nyenye muundo huu kiambishi “ko” cha mahali na “po” cha
hali. Tazama mifano ifuatayo:
(a) Nitafurahi mno kazi hii itakapomalizika.
(b) Mgeni rasmi amekwenda wanakofuga mbuzi
(c) Sipendi namna vijana wanavyovaa.
Dhima za Vishazi Tegemezi
Katika muundo wa Kiswahili kishazi tegemezi huwa na dhima
zifuatazo:
i. Vishazi tegemezi huwa na dhima ya kivumishi cha Nomino
kwa maana hutoa taarifa juu ya Nomino/ KN. Aghalabu
vishazi hivyo huwa vimeshushwa hadhi na kushika nafasi
ya KN
(a) Mchezaji aliyetia fora amepata zawadi.
(b) Wanafunzi waliokaa wasimame.
ii. Pia kishazi tegemezi hufanya kazi ya kielezi. Hivi ni vishazi
ambavyo huwa vimeshushwa hadhi na kushika nafasi ya
kiezi au KE. Kwa mfano:
(a) Mtoto amekwenda wanakovua samaki.
(b)Mwanafunzi amechaguliwa anapopapenda.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia mada ndogo in inayohusu
uanishaji na uchambuzi wa vishazi, hebu sasa chukua kalamu yako
na daftari la mazoezi ufanye zoezi lifuatalo ili kujimairisha zaidi na
kuakazia maarifa katika mada hii.
Zoezi
Jibu maswali yafuatayo:
(1) Tunga sentensi 10 zenye vishazi huru na vishazi tegemezi.
(2) Tunga Vishazi tegemezi 5 vyenye viambishi vya masharti.
(3) Tunga vishazi tegemezi 10 vyenye viunganishi tegemezi.
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
38
(4) Kwa kutumia mifano dhahiri bainisha kazi za kisarufi za
kishazi tegemezi.
Ndugu mwanafunzi, mada yetu ndogo inayofuata inahusu
kubainisha sentensi za Kiswahili kwa kuangalia muundo wake.
Karibu ili tuweze kuipitia mada hii kwa ufasaha:
Kubainisha Sentensi za Kiswahili
Katika mada hii ndogo, tutabainisha aina za sentensi kwa kigezo
cha kimaana na kimuundo (sintaksia) ila hatutajikita sana
kuzungumzia sentensi kwa mujibu wa kimaana kwani kozi yetu
inahusika na muundo pekee.Vilevile tutashughulikia sifa na
miundo ya sentensi mbalimbali. Hivyo sentensi za Kiswahili
zinaainishwa kama ifuatavyo:
Aina za Sentensi kwa Kigezo cha Maana/ amilifu (kisemantiki)
Katika kigezo hiki sentensi huainishwa kwa kuzingatia uamilifu
wake hususani ujumbe uliobebwa na kuwasilishwa na sentensi
hiyo. Hivyo kwa kigezo hiki tunapata sentensi zifuatazo:
(i) Sentensi swali/ ulizi. Sentensi hizi uamilifu wake ni kuuliza.
Kwa kawaida sentensi hizi huwa na pengo la taarifa
linalohitaji kujazwa na taarifa fulani na hutambulishwa kwa
uwepo wa alama ya kuuliza. Rejea mifano ifuatayo:
(a) Wanafunzi wanasoma kweli?
(b) Juma amekwenda wapi?
(ii) Sentensi maelezo/ taarifa/ arifu. Ni sentensi ambazo hulenga
kutoa taarifa fulani. Sentensi hizi huishia na nukta/ kituo
kikuu. Mifano ya sentensi za aina hii ni kama ifuatavyo:
(a) Walimu wetu wanafundisha kwa bidii.
(b) Asha ameondoka.
iii) Sentensi amri/ agizi. Sentensi hizi kwa kawaida huwa
hazina kiima na huwa na lengo la kuamuru tendo fulani
39
lifanywe. Huundwa na kitenzi cha kuamuru. Sentensi hizi
huishia na alama ya mshangao. Zingatia mifano ifuatayo:
(a) Njoo hapa!
(b) Kaa chini haraka!
iv) Sentensi mshangao:
Hizi ni sentensi zinazooyesha kushangazwa kwa msemaji
na tukio fulani. Ni sentensi za kitashititi ambazo huweza
kuuliza swali ambalo jibu lake linafahamika. Rejea mifano
ifuatayo:
(a) Baba kafariki kweli?
(b)Timu yetu imefungwa kweli?
(c) Hata wewe umefeli?
Aina za Sentensi kwa Kigezo cha Kimuundo (kisintaksia)
Uainishaji wa sentensi kimuundo huzingatia muundo wa sentensi
hususani muundo wa vipashio vilivyounda sentensi na mahusiano
ya vipashio hivyo. Kimuundo sentensi huweza kuainishwa katika
makundi yafuatyo:
(i) Sentensi sahili
(ii) Sentensi changamani
(iii) Sentensi ambatano.
Labda tuanze kuzichambua mojamoja ili kuelewa miundo yake.
Sentensi Sahili
Hizi ni sentensi zinazoundwa kimsingi na kishazi kikuu/huru
kimoja ambacho maana yake ni kamilifu. Mara nyingi sentensi
sahili huwa na muundo wa kiima na kiarifu. Vile vile sentensi
sahili huwa na wazo moja.
Muundo wa Sentensi Sahili
Sentensi sahili huweza kuundwa na vijenzi vifuatavyo:
i. Kitenzi kikuu au kishazi huru kimoja, kwa mfano:
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
40
- Mkulima analima.
- Rais anahutubia taifa
ii. Kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi, kwa
mfano:
- Mama alikuwa anapika chakula.
- Mama alikuwa anataka kupika chakula.
iii. Kitenzi kishirikishiki, kwa mfano:
- Ndizi zi mbovu.
- Mimi ni kiongozi.
- Kapu halina kitu.
Sentensi Changamani
Hizi ni sentensi zinazoundwa na kishazi kikuu/ huru kimoja na
kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Hivyo, sentensi changamani
inatokana na kuwapo kwa vipashio yenye hadhi tofauti katika
tungo moja yaani kishazi tegemezi na kishazi huru. Sasa tutazame
miundo mbalimbali ya sentensi changamani kama ifuatavyo:
i. Muundo wa vishazi tegemezi vyenye urejeshi na kishazi huru
kwa mfano:
- Chuo kilichofungwa kimefunguliwa
- Mtoto alipozawadiwa zawadi alikimbia
ii. Muundo wa vishazi tegemezi vyenye viunganishi tegemezi na
kishazi huru kwa mfano:
- Wakati mvua inanyesha wageni walikuja.
- Ikiwa katiba mpya itakubaliwa wananchi watanufaika
sana
iii. Muundo wa vishazi tegemezi vyenye viambishi vya masharti na
kishazi huru, kwa mfano:
- Wananchi wakinichagua hawatajuta
- Angekuja kuniomba ningemsaidia
41
Sentensi Ambatani/Ambatano
Hizi ni sentensi ambazo huundwa na vishazi huru viwi au zaidi.
Vishazi huru hivi huweza kunganishwa na viunganishi ambatani
kama: na, lakini, tena, wala nk. Tutazame miundo ya sentensi hii:
i.Vishazi huru viwili au zaidi, kwa mfano:
- Siogopi wala kutishika.
- Mama analima na kupanda lakini watoto wanacheza.
ii. Vishazi tegemezi na vishazi huru, kwa mfano:
- Mtoto uliyemuona jana ameondoka na mama yake
amesafiri.
- Mahindi yaliyokobolewa ni ya Juma lakini yale
ambayo hayajasagwa ni ya Asha.
iii.Vishazi huru visivyounganishwa na viunganishi ambatani, kwa
mfano:
- Mwambie aondoke
- Ametibiwa hajapona
Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia mada yetu ndogo ya
kubainisha sentensi za Kiswahili, hebu sasa tufanye zoezi fupi
lifuatalo ili kupima uelewa wetu na kukazia maarifa:
Zoezi
Jibu maswali yote kwa ukamilifu:
1. Tunga sentensi tano kwa kila aina ya sentensi zifuatazo yaani;
sahili, ambatani, amri, ulizi, changamani, arifu.
2. Jadili miundo ya sentensi mbalimbali (sahili, changamani,
ambatani).
Uchanganuzi wa Tungo
Ni mchakato wa kubainisha vipashio mbalimbali vinavyounda
tungo. Vipashio hivyo hubainishwa kwa kuanzia vipashio vikubwa
hadi vidogo. Vipashio hivyo huainishwa kwa njia mbalimbali
kama vile:
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
42
i) Maelezo,
ii) Mshale
iii) Jedwali/ visanduku
iv) Matawi/ ngoe/ mchoroti
Aidha, uchanganuzi wa tungo hujiegemeza katika mkabala fulani
yaani hutumia mtazamo/ mkondo fulani wa mawazo. Hivyo, katika
uchanganuzi wetu tutatumia mikabala yote miwili yaani; mkabala
wa sarufi mapokeo na mkabala wa sarufi muundo virai.
Uchanganuzi wa Tungo kwa Mkabala wa Kimapokeo
Kutokana na mjadala uliopita, tukumbuke ya kwamba, sarufi
mapokeo ilijikita katika kuchanganua sentensi sahili pekee.
Vilevile katika sarufi hiyo sentensi zilichanganuliwa kwa
kuzingatia uamilifu yaani kazi za vipashio hivyo katika tungo. Hata
hivyo, uchanganuzi wa tungo katika mkabala ulipitia awamu
mbalimbali, kilichojitokeza katika awamu hizo ni mabadiliko ya
istlahi za kiuchambuzi. Mkabala wa kimapokeo ulitumia vigezo
vifuatavyo:
(i) Kubainisha sehemu kuu mbili za sentensi yaani kiima na kiarifu
(ii) Kubainisha aina za maneno
Ndugu mwanafunzi baada ya kupitia vigezo vitumikavyo
katika uchanganuzi wa tungo kimapokeo sasa tutachanganua
tungo kwa kutumia vigezo hivyo:
a) Njia ya maelezo, kwa mfano,
Mtoto anakula chakula kizuri.
Sentensi imeundwa na kiima na Kiarifu. Kiima kimeundwa na
nomino, nomino ni mtoto. Kiarifu kimeundwa na kitenzi,
shamirisho na chagizo. Kitenzi ni anakula, shamirisho ni nomino
na chagizo ni kielezi. Nomino ni chakula na kielezi ni kizuri.
43
b) Njia ya matawi
Mwanafunzi ameleta machungwa mengi.
S
K A
T SH CH
N T N E
Mwanafunzi ameleta machungwa mengi
c) Njia ya jedwali
Walimu wanne wamekuja leo
S
K A
N V T CH
E
Walimu Wane Wamekuja Leo
d) Njia ya mshale
Kijana mtanashati amenunua gari zuri.
S K + A
K N + V
N Kijana
V mtanashati
A T + SH + CH
T amenunua
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
44
SH N
N gari
CH E
E zuri
Ndugu wanafunzi katika uchanganuzi wa tungo kimapokeo
tumeona kuwa kuna istlahi mbili zimejitokeza yaani kiarifu
shamirisho na chagizo. Ni vema tukazieleza kwa kifupi kabla ya
kuendelea zaidi
Kiarifu
Kiarifu ni kategoria maalum katika sentensi inayotaja kiambajengo
kikubwa kimojawapo katika muundo wa sentensi ambacho ni kirai
kitezi. Kiarifu hubeba viambajengo vingine muhimu vya sentensi
vikitanguliwa na kitenzi abavyo hujadiliwa pamoja. Ni kategoria
ambayo kwa ujumbe wake hutupa habari kuhusu kiima cha
sentensi. Mfano:
(i) Mtoto amekula chakula
ii) Mama amenunua kikombe kizuri sana
Shamirisho (yambwa, yambiwa)
Ni kipashio cha kikazi (kiuamilifu) ambacho hutokea katika
sehemu ya kiarifu hudokeza mtendewa au kitendewa na mtendwa
au kitendewa na jambo. Kwa maneno mengine shamirisho ni
nomino inayojitokeza upande wa kiarifu. Rejea mifano ifuatayo:
(i) Mama anapika ugali
ii) Mwalimu amempa mwanafunzi zawadi
Chagizo
Ni kipashio cha kikazi ambacho hutokea upande wa kiarifu hutoa
taarifa juu ya tendo namna, wapi saa ngapi limefanyika. Hivyo,
chagizo ni sehemu ya tungo inayokaliwa na kielezi. Zingatia
mifano hapa chini:
(i) Ondoka upesi
(ii) Mwanafunzi anatembea harakaharaka
45
Uchanganuzi wa Tungo kwa Mkabala wa Kimuundo
Katika uchanganuzi wa tungo kwa mkabala wa sarufi miundo virai
vigezo vifuatavyo huzingatiwa. Rejea hapa chini:
i. Kubainisha aina ya tungo
ii. Kubainisha sehemu kuu mbili ya kikundi nomino na
kikundi kitenzi (KN na KT)
iii. Kubainisha virai vinavyounda sehemu kuu za sentensi
iv. Kubainisha aina za maneno katika virai vilivyobainisha
v. Andika sentensi tena mwishoni
Ndugu mwanafunzi, baada ya kutizama vigezo vya kuzingatia
katika kuchambua tungo kimuundo sasa tuingie katika uchanganuzi
wa tungo kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo:
a) Njia ya Mshale
Mwanafunzi hodari amefaulu mitihani yake
S Sahili
S KN + KT
KN1 N1 +KV1
N1 Mwanafunzi
KV1 V1
V1 Hodari
KT T +KN2
T Amefaulu
KN2 N2 +KV2
N2 Mitihani
KV2 V2
V2 Yake
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
46
b) Njia ya Matawi
Kuku mgeni atakaa na kamba mguuni
S. Sahili
KN KT
N1 KV T KH KE
V H KN2 E
N2
Kuku mgeni atakaa na kamba mguuni
c) Njia ya Maelezo
Mwanafunzi aliyeleta vitabu ameondoka leo.
Sentensi mwanafunzi aliyeleta vitabu ameondoka leo ni sentensi
changamano ambayo imeundwa na Kirai Nomino na Kirai Kitenzi.
Kirai nomino kimeundwa Nomino na Kirai Kivumishi, Nomino ni
mwanafunzi na Kirai kivumishi kimeundwa na kivumishi na
Nomino. Kivumishi ni aliyeleta na nomino ni vitabu. Kirai kitenzi
kimeundwa na kitenzi na Kirai kielezi, kitenzi ni ameondoka na
Kirai kielezi kimeundwa na kielezi. Kielezi ni leo.
Angalizo: Katika uchanganuzi wa sentensi changamano kishazi
tegemezi huweza kuchanganuliwa kama kirai kivumishi, kirai
kielezi na sentensi. Rejea zaidi kwenye kipengele cha dhima za
kishazi tegemezi hapo juu (2.5)
d) Njia ya Visanduku
Baba mkubwa analima shambani na watoto wa jirani wanacheza
mpira.
47
S. Ambatani
S1 U S2
KN KT KN KT
N1 KV T KE N2 KH T KN
V E H N N
Baba Mkubwa analima shambani na Watoto wa jirani wanacheza mpira
Somo la Pili Error! No text of specified style in document.
48
Muhtasari wa Somo
Katika somo hili ya pili, tumejifunza sehemu uchambuzi wa
sintaksia ya Kiswahili. Somo hili imejikita kuchambua kategoria za
kisintaksia ambapo imeanza kwa kufafanua dhana za msingi kama
vile: kategoria, tungo, neno, kirai, kishazi na sentensi. Vilevile,
somo hili limemakinikia kwa kubainisha kategoria za maneno,
virai, vishazi na sentensi ambapo katika ubainishaji huo aina,
miundo na dhima za kategoria hizo vimeelezwa kwa kina ili
kujenga msingi thabiti katika uchanganuzi wa tungo mbalimbali.
Mwisho, katika somo hili la pili sentensi zimechanganuliwa kwa
njia mbalimbali na kwa kutumia mikabala ya sarufi mapokeo na
miundo virai. Katika somo hili pia, tumejifunza sehemu kuu mbili
za sentensi katika muundo wa Kirai Nomino (KN) na Kirai Kitenzi
(KT). Pia tumejifunza sifa mbalimbali za lugha pamoja na uhusiano
uliopo kati ya tanzu mbalimbali za fasihi.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia vipengele hivyo hapo
juu, hebu tufanye zoezi fupi la kujipima uelewa wako
kuhusiana na mada yetu tuliyojifunza. Hebu chukua kalamu
yako na daftari la mazoezi ufanye zoezi hili.
Zoezi la Somo
Jibu maswali yafuatayo:
1. Changanua tungo zifuatazo kwa kutumia mkabala wa sarufi
miundo virai:
(i) Kitabu kilichopotea jana kimeokotwa shimoni (matawi)
(ii) Mwalimu hodari anafundisha kwa bidii na wanafunzi
makini wanasikiliza kwa makini lakini wanafunzi watundu
wanacheza bila woga (mshale)
(iii) Baba analima na mama anachota maji bombani kwa John
(Jedwali)
(iv) Askari kanzu wa Mwanalumango aliyeongoza magari
amepewa zawadi (maelezo)
2. Tunga sentensi tano kisha changanua kwa kutumia mkabala
wa sarufi mapokeo (tumia njia zote)
49
3. Kwa kutumia mifano dhahiri fafanua vipengele vifuatavyo:
(i) Kiima
(ii) Kiarifu
(iii) Shamirisho
(iv) Chagizo
4. Tofautisha uchanganuzi kwa kutumia mkabala wa sarufi
mapokeo na ule wa sarufi miundo virai.
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
50
Somo la Tatu
Kufafanua Semantiki ya Kiswahili
Utangulizi
Katika sura hii ya tatu tutashughulikia semantiki ya Kiswahili
katika muktadha wa maana kwa kuzingatia misingi ya kinadharia
ya kiisimu. Semantiki ya Kiswahili itafafanuliwa kwa kuzingatia
mambo yafuatayo: Kwanza, sura hii itafafanua dhana ya maana na
utata wake katika kufasiliwa.Vilevile katika sura hii
tutashughulikia mikabakla ya semantiki, aina mbalimbali za maana
na uhusiano wa kifahiwa. Sura hii pia itafafanua nadharia ya maana
kimuktadha ambapo misingi ya nadharia hii itaelezwa. Mwisho
sura itafafanua ubora na udhaifu wa nadharia kimuktadha.
Matokeo
Baada ya kukamilisha somo hili utaweza:
Kufanunua dhana ya semantiki na maana
Kuchambua mikabala ya semantki
Kufafanua aina za maana
Kufafanua Nadharia y
Kufafanua Dhana ya Semantiki na Maana
Dhana ya semantiki imejadiliwa na wataalamu wengi kwa
mitazamo tofautitofauti kama inavofafanuliwa hapa chini:
Richards et al (1985) wanaeleza kuwa, semantiki ni stadi ya maana.
Awali neno semantiki lilitumika kumaanisha sayansi ya “maana”
kwa ujumla na ambayo ilishughulikiwa na wanasaikolojia,
wanamantiki, wanaanthropolojia na wengine. Baadaye stadi hii
ilijishughulisha zaidi na maana katika muktadha wa lugha ya
mwanadamu.
Semantiki ni utanzu wa isimu unaochunguza maana za maneno
katika lugha ya mwanadamu (Habwe na Karanja, 2004).
51
Matinde (2012) anafasiri dhana ya semantiki kama utanzu wa isimu
unaochunguza maana katika lugha.
Ndugu mwanafunzi, kwa kuzingatia mitazamo ya wataalam
mbalimbali kuhusiana na dhana ya semantiki tuaweza kusema
kuwa, semantiki ni tawi la isimu linaloshughulikia maana za
maneno katika tungo za lugha ya Kiswahili katika viwango
mbalimbali. Vilevile, tunaweza kusema kuwa, semantiki ni utanzu
wa isimu unaochunguza maana katika lugha ya mwanadamu kwani
hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo. Maana
hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha kama vile sauti,
maneno na sentensi.
Kuchambua Mikabala ya Semantiki
Maana ndicho kiepengele muhimu zaidi katika uchunguzi wa lugha
ya mwanadamu. Hii ni kwa sababu kazi kuu ya lugha ni
mawasiliano na mawasiliano huhusisha upashaji wa ujumbe ambao
hueleweka katika maana ya tamko. Pasipo kupasha ujumbe
hapatakuwa na mawasiliano na kwa hivyo lugha haitakuwa
imetekeleza wajibu wake. Ujumbe hudhihiriki katika maana na
ufafanuzi wa maana zilizobebwa na vipashio vya lugha
vinavyohusika kama vile fonimu, neno na sentensi. Lengo la
kisheria za kifonolojia na kisintaksia ni kuunda tungo zenye maana
katika muktadha wa sentensi.
Kwa sababu hii ni sawa kusema kuwa maana hushughulikiwa
katika tanzu za isimu kama fonolojia, mofolojia na sintaksia.
Semantiki inakuwa ndio makutanio ya taaluma hizi kama
ilivyowakilishwa katika mchoro ufuatao:
Fonolojia Mofolojia
SEMANTIKI
Sintaksia
Aidha semantiki huonyesha uhusiano baina ya vipashio na dhana
au vitu ambavyo vipashio hivi huwakilisha katika mazingira.
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
52
Ndugu mwanafunzi, kwa ujumla semantiki hujishughulisha na
masuala sita (6) ya msingi. Sasa hebu zingatia madondoo
yafauatayo ili uweze kuelewa kwa undani dhana hii ya
semantiki na maeneo ambayo taaluma hii imejikita:
1. Maana na uanishaji wa maana za maneno
2. Maana za tungo
3. Taratibu za kuchambua maana
4. Etimolojia za maana ya maneno
5. Uhusiano wa kimaana katika sentensi
6. Nadharia za uchambuzi wa maana
Ndugu mwanafunzi, zipo sababu mbalimbali ambazo zilifanya
tawi hili la semantiki kutokuendelea kama matawi mengine ya
isimu. Hii inaonekana kwamba, katika uchunguzi wa kiisimu,
inaonyesha kuwa semantiki ndilo tawi ambalo
halikushughulikiwa kwa undani na upana kama matawi yale
mengine. Hebu sasa tupitie mjadala huu mfupi ili tuweze
kuelewa sababu hasa zilizofanya tawi hiili kuwa nyuma.
Sababu za Tawi la Semantiki Kutoendelea kama Matawi
mengine ya Isimu
Tawi la semantiki ni tawi ambalo halikutiliwa mkazo na wanaisimu
wengi kinadharia na pia katika maandishi. Hii ni kwa sababu ya
utata uliokuwa umezuka miongoni mwa wanaisimu kuhusiana na
tawi hili. Utata huo umetokana na sababu zifuatazo:
1. Taswira miongoni mwa baadhi ya wanaisimu kuwa semantiki ni
taaluma ngumu. Ugumu huu unatokana na kuwa taaluma hii
haijajulikana katika kiwango cha nadharia, kama tutakavyoona
baadaye, misingi ya kinadharia ya semantiki si thabiti kama ilivyo
katika tanzu nyingine za kiisimu kama fonolojia, mofolojia na
sintaksia.
2. Baadhi ya wanaisimu hushughulika na muundo wa lugha na
kuupuuzia misingi ya kisarufi ktegemea maana kwa imani kuwa ni
rahisi kuchunguza muundo kwani una ruwaza inayotambulika ilhali
maana ni ya kinadharia. Kwa mfano, ni rahisi kuchambua muundo
wa neno “mwalimu” kama {mu + alimu} kuliko kueleza maana
yake. Hii ni kwa sababu, katika kuchambua maana, licha ya kujua
muktadha wa matumizi ni sharti ufahamu fikra za mzungumzaji
53
jambo ambalo si rahisi. Hii ndiyo sababu iliyofanya maana
kushughulikiwa zaidi katika filosofia hapo awali.
3. Maana wakati mwingine hurejelea vitu ambavyo havipatikani
katika mfumo wa lugha na hivyo huhitaji ujuzi mwingi wa
mazingira yaliyo ne ya lugha. Hapana mtu aliye mjuzi wa mabo
yote yaliyo katika mazingira.
4. Hakuna misingi mahususi ya kinadharia misingi mahususi ya
kinadharia ambayo imezuliwa kuhusu semantiki. Kuna mitazamo
mingi inayotofautiana kuhusu taaluma hii ya semantiki ambayi
imeletezea kuwepo na utata na matawi mengine. Utata huu
unatokana na ukweli kuwa semantiki ni tawi la isimu lenye
usambamba na matawi mengine ya isimu. Kwa mfano, uhusiano
wa mofu na mofimu katika mofolojia na ule wa muundo wa ndani
na wan je wa sentensi katika sintaksia ni uhsiano wa kimaana. Hata
hivyo si rahisi kuonyesha wazi kwa kutumia nadharia muafaka na
kuweka mipaka kati ya mofolojia na semantiki au kati ya sintaksia
na semantiki au kati ya sintaksia na semantiki katika mifano hii.
Hivyo basi, semantiki haishughulikiwi kikamilifu kwa sababu
haijulikani ni wapi iambatishwe.
5. Hata hivyo taaluma hii imeanza kushughulikiwa na wataalamu
wengi wa isimu katika miaka ya hivi karibuni kwamba hata misingi
yake ya kinadharia imeanza kuaimarika. Ingawa bado taaluma hii
haijakua kiasi cha tanzu nyingine lakini imeaendelea kwa kiasi
fulani kuliko kipindi cha hapo awali.
Viwango vya Maana
Kama tulivyoeleza hapo awali, jukumu la kimsingi la semantiki ni
kueleza maana ya maneno na dhana katika viwango mbalimbali
kama ifuatavyo:
Kwanza, ni kiwango cha vipashio huru ambapo wanasemantiki
hushughulikia maana katika viwango vya kipashio huru na maana
ya vipashio hivi katika tungo. Hii ina maana kuwa maana
huchunguzwa katika kiwango cha maana cha maneno huru na
maana katika tungo kama vile sentensi ambacho huitwa maana ya
kileksika.
Pili, ni kiwango cha maneno ya kisarufi ambacho huitwa maana ya
maneno ya kisarufi katika sentensi.
Tatu ni kiwango cha matini ambapo baadhi ya wanaisimu
wameshughulikia maana kwa kaiwango cha matini. Uchunguzi wa
maana kwa kiwango cha matini huitwa pragmatiki. Ni vigumu sana
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
54
kuweka mipaka katika vitengo hivi vya uchunguzi. Hata hivyo ni
muhimu kutambua kwamba ili mtaalamu yeyote wa semantiki
kufaulu, ni sharti awe na ujuzi wa kutosha wa muundo na
utamaduni wa lugha.
Ndugu mwanafunzi, baada kujadili kwa kina historia ya
semantiki na ufafanuzi wa dhana hii kwa mujibu wa wataalam
mbalimbali, hebu sasa tupate ufafanuzi wa dhana ya maana
kama ifuatavyo:
Dhana ya Maana
Dhana ya maana imeshughulikiwa na wataalamu wengi kama vile:
Habwe na Karanja (2004), Massamba (2004), Matinde (2012) na
wengineo. Hata hivyo, wataalamu hawa wanakiri kwa dhati kuwa
dhana ya maana ina utata katika kufasiliwa kwake. Kuna mogororo
mkubwa kati ya wataala wa isimu kuhusiana na dhana ya maana.
Utata huo unatokana na ukweli kwamba:
- Maana ni dhana dhahania ijengekayo kichwani mwa msemaji
na msikilizaji
- Hakuna mlandano wa moja kwa moja baina ya maana na
taswira, jambo au kitu
kinachozungumziwa/kinachowakilishwa
- Aidha utata wa kufasiri maana unatokana na ukweli kwamba
baadhi ya maana hazibainishwi na neno, au ishara yoyote bali
hujidhihirisha katika kinyume cha kitu kizungumzwacho.
Hivyo, kutokana na madai hayo ndiyo maana tunaona kuwa dhana
ya maana ni telezi yaani haiwezi kuelezwa kiuraisi na kijuujuu.
Hali hali hii ilipelekea kuzuka nadharia mbalimbali zinazotanzua
dhana ya maana.
Kwa mujibu wa Ogden na Richards (1923) kama alivynukuliwa na
Wanjala (2002), wametoa orodha ndefu sana ya maana ya dhana ya
maana kama ifuatavyo: Maana kama:
- Sifa halisi ya kitu
- Maneno yanayofafanua neno
- Athari ya kitu Fulani katika mustakabali wetu
- Unasibishaji wa neno
55
- Nafasi ya kitu katika mfumo kama vile chai ni kiamsha
kinywa.
- Uwezekano wa kiuaminifu wa kitu
- Kinachorejelewa na mtumiaji ishara fulani
- Kinachoaminika kuwa kinarejelewa na mtumiaji ishara Fulani.
- Kinachoaminika kurejelewa na mpokeaji kuwa kinarejelewa na
mtumiaji ishara Fulani.
Wataalamu hawa mametoa orodha hii kuonesha mkanganyiko
utokeao kutokana na jamii kutokukubaliana juu ya maana ya
istilahi za kimsingi katika lugha. Hata hivyo, wanakubali kuwa
fikra na lugha haviwezi kutenganishwa.
Bloomfield (1933) kama alivyonukulia na Wanjala (2002),
anajaribu kutanzua mgogoro huu kwa kupendekeza kuwa mtindo
wa kisayansi utumike katika utafutaji wa maana yaani kueleza
maana ya dhana kwa kutaja viambato vyake.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2004:204) neno maana lina
fahiwa nyingi. Watu wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu
mbalimbali. Kwa mfano baadhi ya fahiwa zake ni kama
zinavyoelezwa katika matumizi yafuatayo ya sentensi za Kiswahili:
1. Una maana gani kwa kufika umechelewa?
2. Yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa hivi
3. Hiyo nguo nyekundu inamaanisha hatari.
4. Neno “vilua” lina maana gani?
5. Mradi huu una maana kubwa.
Tungependa kuangalia maana inayozingatiwa wakati neno
linapotumiwa katika masuala kama vile katika sentensi ya (4) hapo
juu. Katika kujaribu kueleza maana ya maana, wanaisimu
wameieleza dhana hii katika vitengo viwili vikuu; maana ya msingi
na maana ya ziada
Maana ya ziada pia huweza kuwa na vitengo vyake kama maana
husishi, maana elekezi na maana ya umaanisho.
Dhana ya maana ni ya kidhahania kwa sababu maana haina
muundo thabiti kama vile viamabjengo vingine vya lugha vya
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
56
kifonolojia, kimofoloji au kisintaksia. Maana hutegemea pia
dhamira ya mtoa ujumbe na fasiri ya mpokeaji. Maana kwa hiyo ni
dhana tata ambayo si rahisi kueleweka kwa uwazi.
Hata hivyo, wanaisimu wamejaribu kuieleza dhana hii ya maana
kitendaji. Kama tulivyoona hapo awali, maana inaweza
kubainishwa kiisimu katika kiwango cha neno na katika kiwango
cha tungo kama vile sentensi na zaidi ya sentensi yaani kiwango
cha matini.
Kufafanua Aina za Maana
Aina za Maana
Wanaisimu mbalimbali wameeleza dhana ya aina za maana katika
vitengo viwili vikuu; maana ya msingi na maana ya ziada. Hata
hivyo Leech (1981) amebainisha aina za maana zifuatazo:
1. Maana ya msingi (conceptual meaning)
Hii ni aina ya maana ambayo haibadiliki mfano; mwanamke,
mwanaume. Maana hii hutaja sifa zake kuu pamoja na zile sifa
bainifu ambazo hupelekea kupata maana kuhusu mtu au kitu.
Maana ya msingi huweza kuwekwa katika viwango mbalimbali
kwa mfano, katika kiwango cha neno huru huitwa maana ya
kileksika. Hii hurejelelea maana ya msamiati wa lugha ambayo ni
ile inayowakilishwa na vidahizo kama kamusi. Vidahizo hivi ni
kwa mfano maneno kama vile “gari”, “mtu”, “barabara”, na
mengine yenye kujisimamia kama maneno huru.
Maana ya kileksika pia huitwa maana ya msingi ambayo ndiyo
maana kuu ya neno. Maana hii huwa haibadiliki kutegemea athari
za kimazingira au muktadha. Fahiwati nyingine zote za maana
zinazoibuka, huibuka kutokana na msingi na maana hii. Maneno
katika muktadha wa maana kimsingi yanaweza kuwa na maana
nyingi za ziada lakini zote zikiibuka hutokana na maana hii ya
msingi.
2. Maana ya Kisarufi
Hii ni aina nyingine ambayo hurejelea maana katika muktadha wa
matumizi. Hapa maana ya neno huangaliwa kulingana na mazingira
ambamo limetumiwa. Hii ndiyo maana inayorejelwa wakati mtu
57
anapoulizwa swali kuwa: una maana gani? Katika kujibu tukio
fulani la mawasiliano.
3. Maana ya Ziada
Maana hii hurejelea ile maana ya kimuktadha au kimazingira,
lakini yenye kuwa na msingi, kuzalishwa na kuhusiana na maana
ya msingi Hapa tunaweza kusema kuwa kile mtu anachokisema si
lazima kiwe ndicho anachokimanisha. Kile anachokisema ndicho
maana ya msing na kila anachokimaanisha ndicho maama ya
muktadha. Kwa mfano, tuangalie maana katika sentensi zifuatazo:
4. Maana dokezi (Connotative meaning)
Ni aina ya maana ambayo hutokana na umbo la kitu, kisaikolojia,
kimatamshi mf. Kiumbo kushika mimba, kisaikolojia umama.
5. Maana ya kijamii / kimtindo (social meaning)
Ni aina ya maana ambayo hupatikana kutokana na mazingira ya
kijamii, wakati, utamaduni, kijiografia, kiuwasilishaji, hadhi,
ubinafsi n.k
6. Maana ya kihisi (emotive meaning)
Ni maana za kihisia ambazo hutokana na upotoshaji wa aina fulani
wa maana ya msingi. Ni maana itokanayo na utumizi usio wa moja
kwa moja ili kutoa maana. Maana ya kitu huwa ni ya mzunguko,
fiche, kwa mfano maana za hisia hutegemea sana Kiimbo
kiwekwacho katika neno au Kiimbo kiwekwacho katika sentensi.
7. Maana ambatani (collocative meaning)
Maana ambatani au tangamano, ni aina ya maana itokanayo na
utangamano au uambatani wa baadhi ya maneno. Kwa maneno
mengine ukitaja neno fulani linaukilia maana fulani. kwa mfano:
- Mrembo – Msichana
- Ujamali – Mvulana
- Jitu hili ni la miraba mine – Mwanaume
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
58
Katika lugha maneno pia hujengwa kwa mtindo huo mifano zaidi
Samaki – Kiumbe wa majini/baharini au Swala - Kiumbe wa
msituni. Ukitaja kimoja tu mfano samaki unakuwa umekiondoa
kingine swala.
8. Maana ya kidhima/kidhamira (thematic meaning)
Hizi ni aiana za maana ambazo ujumbe wake unapangwa kufuatana
na msisitizo wa kitu. Maana hutokana na dhamira ambayo msemaji
alikusudia ili imfikie msikilizaji, kwa mfano sentensi zifuatazo:
(a) Mwalimu amempiga mtoto (Mwl. Mtenda)
(b) Mtoto amepigwa na mwalimu (Mtoto Mtendwa)
(c) Msichana yupo darasani (Jibu la swali lililoulizwa) – Msichana
yuko wapi?
(d) Darasani kuna msichana (Swali)
9. Maana akisi/Kimwangwi (reflected meaning)
Ni maana ambazo ukitaja kitu fulani au maana fulani unakonyeza
maana nyingine. Maana akisi haziachani kwa mfano: Jamii –
Mkusanyiko wa watu pamoja.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kujadili kwa kina aina
mbalimbali za maana kuna haja ya kuangalia uhusiano wa
maneno mbalimbali katika semantiki. Uhusiano huu huitwa
uhusiano wa kifahiwa. Karibu sasa katika mada yetu hii ili
tuweze kuipitia kwa undani.
Uhusiano wa Kifahiwa katika Semantiki
Uhusiano wa kifahiwa ni kipengele kimojawapo katika semantiki
leksia. Maneno katika lugha yoyote huingia katika mahusiano
mbalimbali. Licha ya mahusiano ya vikoa vya maana, maneno
huweza kuhusiana hivi kwamba maana ya neno moja inaweza
kuwa kinyume cha maana nyingine. Katika uhusiano huu maana ya
neno moja kueleweka na pengine hata kuwepo kwa neno lingine
katika mfumo mzima wa ishara za lugha ( Saussure 1916).
Mahusiano ya maneno haya husaidia kutoa maana ya maneno
mengine. Kuna aina nyingi za uhusiano wa kifahiwa katika lugha
za binadamu kama ifuatavyo:
59
Sinonimia
Usinonimia ni uhusiano wa kileksia ambapo huwa kuna maumbo
kati ya lugha amabyo maana zake zake ni sawa. Maumbo haya
huitwa sinonimu ambavyo ni visawe vya dhana moja. Maneno haya
yanaingia katika uhusiano mwimo. Usinonimia huweza kuletwa na
sababu mbalimbali kama ifatavyo:
(i) Ukopaji wa msamiati: Kwa mfano, teknolojia –technology
(ii) Jinsia: Kwa mfano, hali ya kuwa na sura nzuri hurejelewa kwa
kisaawe cha urembo kwa wanawake na ujamali kwa wanaume.
(iii) Dini: Kwa mfano neno kwaresma kwa wakristo na saumu kwa
waisilamu au neno mjahidina kwa waisilamu na muumini wa
wakristo, neno msikiti wa kwa waisilamu na kanisa kwa wakristo.
(iv) Tofauti za kimaeneo: Kwa mfano neno ugali linaweza likawa
sima Tanzania, sembe Congo, Rwanda na Burundi.
(v) Tofauti za kilahaja: Kwa mafo neno chumvi na munyu, kwa
hiyo maneno haya yana maana moja lakini hutumika katika
maeneo tofautitofauti.
(vi) Taaluma: Kwa mfano neno aya katika riwaya na neno ubeti
katika shairi, zote zina maana inayofanana.
(vii) Wakati, kwa mfano:
Kwa kuhitimisha kipengele cha usinonimia, kwa mfano kuwepo
kwa neno “mahaba” katika Kiswahili kunasaidia kueleza neno
“mapenzi”. Tunaweza kusema kuwa, maneno haya huweza kuingia
katika uhusiano wa aina hii unaitwa usinonimia. Maana ya maneno
haya hayapatikani kwa misingi wa vijenzi vya lugha lakini kwa
jinsi ambavyo yanahusiana na maneno mengine.
Hebu tuangalie aina nyingine za mahusiano ya kifahiwa kama
ifuatavyo:
Hiponimia
Ni maneno ambayo maana yake hujumuishwa katika maana ya
neno jingine, yaani uhusiano uliopo kati ya neno maalum na lile la
kijumla. Kwa maneno mengine haiponimia ni uhusiano wa lugha
ambapo maana Fulani ya neno ni sehemu ya maana kubwa ya neno.
Neno hilo lenye maana kubwa huitwa neno jumuishi ilihali maneno
yenye maana ndogo huitwa haiponimu. Katika lugha ya Kiswahili,
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
60
neno mnyama, ambalo ni neno kuu, lina uhusiano wa kihaponimia
na maneno ng’ombe, mbuzi, duma, nguchiro, nguruwe n.k. Kwa
hiyo neno mnyama limejumuisha maneno yote yaliyotajwa hapo
juu.
Homonimia
Huu ni uhusiano mwingine wa kileksika ambapo kuna mafano wa
maneno katika maumbo yake lakini yana maana tofauti. Hata hivyo
kufanana huku ni kwa kisadfa tu kwani maeneo haya hayan usuli
mmoja wa kihistoria. Maana za maneno haya huwa ni tofauti.
Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya homonimia katika lugha ya
Kiswahili:
(a) Panda –kuweka mbegu ardhini
Panda – kukwea mti au mlima
Panda – kugawaika kwa njia
Panda – chombo cha mgambo
(b) Ota – kuona picha usingizini
Ota – kuonyesha kwa kidole
Ota – kukaa juani ili kujipasha joto
Tunasema kuwa maneno haya ni homonimu kwa sababu
yamefafana katika maubo ya kifonetiki. Katika kamusi maneno
haya huingizwa kwa vidahizo tofauti (Taz Kamuisi ya Lugha
Sanifu, 1981). Hii ina maana kuwa kila homonimu huwa na leksia
na huwa na mnyambuliko wake tofauti. Kwa kuhitimisha tunawe
za kusema kuwa, homonimia huwa ni maneno yenye maana tofauti
na yaya historia tofauti katika lugha lakini kufanana kwake katika
maubo ni kwa kisadfa tu.
Polisemia
Hii ni hali ambapo maneno huwa na maana zaidi ya moja na
maneno hayo yanakuwa na uhusiano wa kihistoria. Tofauti na
homonimia ambapo maneno hayana uhusiano wakati katika
polisemia, maneno huwa na uhusiano. Polisemi ni uhusiano
ambapo kuna umbo moja la neno lenye maana mbalimbali. Mifano
ya polisemi ni kama ifauatavyo:
(i) Mdomo- neno mdomo hapa inaweza kumaanisha mdomo wa
binadamu au Mdomo wa chupa
61
(ii) Mguu - neno hili linaweza kumaanisha – mguu wa binadamu
au mguu wa meza au kiti.
(iii) Jicho – neno hili linaweza kumaanisha jicho la mti, jicho la
sindano n.k
Aghalabu, polisemia ni uhusiano ambapo maana moja hutokana na
maana ya neno jingine. Hali hii huwepo kwa sababu kuna sifa
Fulani za kufanana katika vitajwa viwili. Kwa mfano, kuna
uhusiano baina ya “mdomo wa chupa” na “mdomo wa binadamu”.
Antonimia
Ni uhusiano wa kimuundo ambapo kuna maneno katika lugha
anbayo maana za ke ni kinyume, yaani many ya maneno
hupingana. Kwa mfano:
Cheka --- lia
Nenda --rudi
Pata – poteza
Penda --- chukia
Moto -- baridi
Mara nyingi katika lugha huwa kuna vinyume vya utoano.
Vinyume vya viwango ni kama vile moto/ baridi. Hii ina maana
kuwa ni maana ambazo ziko kwenye mkondo mmoja. Kitum
kinapokuwa baridi huwa kina moto mdogo ilhali kitu kinapokuwa
moto sana huwa na baridi kidogo. Antonimu zingine huwa ni za
kimtoano kwa maana kuwa anaposema huwa unatoa ile nyingine.
Kwa mfano, neno “mke” na “mume” ni antonimu za kiutoano.
Ndugu mwanafunzi, baada ya kujadili kwa kina uhusiano wa
maneno mbalimbali katika semantiki yaani mahusiano ya
kifahiwa. Karibu sasa katika mada yetu hii ndogo ya mwisho ili
tuweze kufikia tamati ya moduli yetu.
Kufafanua Nadharia ya Maana Kimuktadha ya Ludwig Wittgenstain
Ndugu mwanafunzi kabla ya kuzama kiundani katika kufafanua
nadharia ya Ludwig ni vema tukadurusu kwa kifupi dhana nzima
ya nadharia ili kujenga mwega wa mhadhara wetu kama ifuatavyo:
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
62
Kufafanua dhana ya nadharia
Massamba (2004) anafasili dhana ya nadharia kuwa ni taratibu,
kanuni na misingi ambayo imejengwa katika muundo wa mawazo
kwa madhumuni ya kutumiwa kama kiolezo cha kuelezea jambo.
Kwa mantiki hiyo, nadharia inaweza kufasiliwa kuwa ni maelezo
yanayojengwa katika misingi ya kanuni na taratibu ambazo
huongoza katika kutekeleza jambo na hatimaye kupata hitimisho
fulani.
Nadharia ya Maana Kimukutadha
Nadharia hii iliasisiwa na mwanafalsafa Ludwig Wittgenstein
katika miaka ya 1930. Katika nadharia yake anadai “maana ya neno
ni matumizi yake katika lugha” (Philosophical Investigations,
1963:43). Hii ina maana kuwa ili kupata maana ya neno ni sharti
lihusishwe na muktadha wa matumizi wa neno hilo.Hivyo,
nadharia hii inachukulia kuwa muktadha ndiyo mwafaka na
muhimu katika kufasiri na kufafanua maana ya maneno mbalimbali
nadharia hii imejengwa katika misingi ifuatayo:
- Nadharia hii inasisitiza kuwa katika muktadha wa kijamii
ndipo maana hupatikana. Hii ina maana kuwa kuna maneno
ambayo huwa, na maana katika jamii fulani na yasiwe na
maana katika jamii zingine. Kwa mfano jamii ya wafugaji
huwa na majina fulani yanayorejelea mifugo yao lakini hali
itakuwa kinyume kwa jamii isiyofuga. Katika matumizi ya
neno ndipo unaweza kupata maana. Kwa manzili hiyo neno
haliwezi kupata maana bila kupelekwa katika uwanja wake wa
kimatumizi
- Vilevile nadharia inaona kuwa ili maana ipatikane ni sharti
ihusishwe na muktadha wa usemaji. Kwa manzili hiyo ni
dhahiri kuwa muktadha wa usemaji ndio huongoza uteuzi wa
maneno fulani. Kwa mfano, neno “chai mbili” litapata maana
ikiwa litatumiwa mgahawani, hotelini na sehemu yoyote
inayotoa huduma ya chakula kinyume na hapo neno hilo halina
maana.
- Aidha nadharia inasisitiza kuwa maana hupatikana kwa
kutumia muktadha wa kiisimu. Hii ina maana kuwa maana ya
neno hutegemea nafasi ya utokeaji katika sentensi. Kwa mfano
neno “kifaru” litapata maana yake kutokana na mazingira ya
kiisimu ambamo neno hilo limetumika.
63
Nadharia hii haina matatizo ya nadharia zilizotangulia kwa vile
inawezekana kabisa kuzungumzia matumizi ya neno lolote lile, na
kwa hakika, ni matumizi yaukiliayo maana za maneno. Watoto
wajifunzapo lugha hujifunza maana za viyambo vya lugha
kutokana na jinsi viyambo hivyo vitumiwavyo na wanalugha, na
jinsi wao wenyewe wavitumiavyo viyambo hivyo katika
kuwasiliana na wanalugha hao.
Kufafanua Ubora na Udhaifu wa Nadharia ya Maana Kimuktadha
Ubora wa nadharia ya maana kimuktadha unaweza kuelezwa kama
ifuatavyo:
a) Ni kweli maana za maneno hupatikana pale maneno hayo
yanapotumika
b) Wajifunzaji lugha hujifunza jinsi mneno yanavyotumiwa na
wanalugha husika
Aidha nadharia hii ina mapungufu yafuatayo:
a) Si kweli kuwa maana hupatikana katika matumizi yake
kwani kuna maneno mengi katika lugha huweza kupewa
maana yake kabla ya kutumiwa. Kwa mfano ‘istilahi’ au
maneno yaelezayo dhana mpya huundwa kabla maneno
hayo hayajatumiwa kama vile: neno “tehama”.
b) Kwa kutumia nadharia hii maana za mneno zinaweza
zikapunguzwa Kwa mfano neno “moshi” tunaweza
kutambua kuwa fahiwa yake katika muktadha huo ni “kileo
kikali”, hatuwezi kusema kuwa maana ya moshi ni
matumizi yake yarejeleayo “kileo kikali”. Badala yake
tutasema kuwa mojawapo ya maana ya ‘moshi’ ni kileo
kikali.
Ndugu wanafunzi tufanye zoezi lifuatalo:
Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.
64
Muhtasari wa Somo
Katika moduli hii mwanafunzi amepitia mada mbalimbali
zimepangwa katika masomo mbalimbali; Somo la kwanza imejadili
dhana ya mkabala, aina na misingi ya sarufi mapokeo na miundo
virai. Pia, sehemu hii imegawanyika katika sehemu mbili, yaani ya
sehemu ya kwanza na sehemu ya pili. Misingi ya Mkabala wa
Sarufi Mapokeo, Misingi ya Mkabala wa Sarufi Mapokeo na
Misingi ya Mkabala wa Sarufi Miundo Virai, Misingi ya Mkabala
wa Sarufi Miundo Virai. Katika mada hizi vipengele vifutavyo
vilipitiwa: kategoria ya neno au virai vinavyounda kirai nomino
(KN), au virai vinavyounda kirai kitenzi (KT) na maneno
yanayounda virai vilivyoainishwa na kufafanua dhana za
kisintaksia lugha na sarufi na kuonyesha uhusiano uliopo katika
tanzu za sarufi.
Somo hili ya tatu imeshughulikia ufafanuzi wa semantiki ya
Kiswahili. Katika ufafanuzi huo mambo yafuatayo
yameshughulikiwa. Kwanza, sura hii imefasiri dhana za semantiki
na dhana ya maana kwa undani. Pili, somo hii imefafanua mikabala
ya semantiki.
Somo hili imefafanua aina mbalimbali za maana. Mwisho somo
limefafanua nadharia ya maana kimuktadha ya Ludwig
Wittgeinstein ambapo nadharia imejadiliwa kwa ufasaha
sambamba na kufafanua ubora na upungufu wa nadharia hii. Baada
ya kupitia moduli yetu hii, mwanafunzi atakuwa amepata maarifa
ya kutosha huhusiana na moduli hii.
65
Zoezi la Somo
Jibu maswali yote kwa kuandika ili kujipima uelewa wako, katika
mada hii ya utumizi wa lu
1. Fafanua aina mbalimbali za maana.
2. Elezea chanzo cha mgogoro kuhusiana na dhana ya maana.
3. Elezea mtazamo wa Bloomfield kuhusiana na dhana ya maana.
4. Kuna aina nyingi za uhusiano wa kifahiwa katika lugha za
binadamu. Jadili mahusiano ya kifahiwa katika semantiki kwa
kutoa mifano.
5. Jadili misingi mbalimbali ya nadharia ya maana kimuktadha.
6. Fafanua ubora na udhaifu wa nadharia ya maana kimuktadha.
7. Bainisha viwango vya maana kwa kutoa mifano.
Marejeleo Error! No text of specified style in document.
66
Marejeleo Besha, R. M. (1994). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es
Salaam: Dar es Salaam University Press.
Habwe, J. na Peter, K. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phonix.
Khamis, A. M na John. K. G. (2002). Uchanganuzi wa Sarufi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Massamba, D. P. B. na wenzie (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. (SAMIKISA), Dar es Salaam: TUKI.
Massamba, D. P. B (2004), Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha, Dar es Salaam: TUKI.
Matei, A. K. (2008). Darubini ya Sarufi ya Kiswahili: Ufafanuzi Kamili wa Sarufi. Nairobi: Phonix.
Matinde, R.S (2012). Dafina ya Lugha: Isimu na Nadharia,Kwa sekondari, Vyuo vya kati na Vikuu, Mwanza, Tanzania: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.
Wahiga G. (2003). Sarufi Fafanuzi. Nairobi Longhorn Publishers Ltd.
Wesana-Chomi, E. (2003). Kitangulizi cha Mofolojia ya Kiswahili. Sebha: Chuo Kikuu cha Sebha.
Ogden, C. K & Richards, I. A. (1923). The meaning of meaning. London: Routledge & Kegan Paul.
Kimeandaliwa na:Taasisi ya Elimu ya Watu WazimaS.L.P 20679, Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2150836 Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.iae.ac.tz