mwalimuwakiswahili.co.tz · web viewkatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano...

281
KENYATTA UNIVERSITY INSTITUTE OF OPEN LEARNING AKS 400 SOCIOLINGUISTICS NA PAMELA M. Y. NGUGI NA LEONARD M. CHACHA IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA © KUIOL 2004

Upload: others

Post on 08-Feb-2020

39 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

KENYATTA UNIVERSITY

INSTITUTE OF OPEN LEARNING

AKS 400SOCIOLINGUISTICS

NA

PAMELA M. Y. NGUGI NA LEONARD M. CHACHA

IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA

© KUIOL 2004

Page 2: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

YALIYOMOLengo la Kozi ....................................................................(i)

SOMO LA KWANZA ............................................................1ISIMUJAMII ...................................................................11.0 Utangulizi ...............................................................11.1 Madhumuni .............................................................11.2 Isimu-jamii ni nini? ..................................................11.3 Mikabala ya Isimujamiii ........................................31.4 Historia fupi ya Isimujamii........................................ 41.5 Lugha na Jamii ........................................................101.6 Isimujamii na Taaluma nyingine ................................121.7 Mitazamo ya lugha ...................................................14

SOMO LA PILI ...................................................................18NADHARIA ZA KIJAMII .................................................182.0 Utangulizi ................................................................182.1 Madhumuni .............................................................182.2 Nadharia a Kiisimu................................................... 182.2.1   Uamilifu .................................................................182.2.2 Umaksi---------------------------------------------------------- 21

SOMO LA TATU .................................................................26DHANA ZA KIMSINGI KATIKA ISIMUJAMII .................263.0 Utangulizi ................................................................263.1 Madhumuni .............................................................263.2 Lugha .....................................................................263.2.1  Matumizi ya Lugha   .................................................283.2.1 Mitazamo Elezi na Elekezi ya Lugha--------------------- 293.3 Lahaja------------------------------------------------ ---------- 323.3.1 Maana ya Lahajai ....................................................323.3.2 Kuzuka kwa Lahaja ----------------------------------------- 333.3.3 Nadharia ya Mawimbi---------------------------------------- 343.3.4 Istilahi Zinazotumika katika Lahaja----------------------- 353.5 Aina za Lugha------------------------------------------------- 363.6 Lugha au Lahaja--------------------------------------------- 383.7 Mtindo Pekee......................................................... 403.8 Mtindo--------------------------------------------------------- 403.9 Sajili------------------------------------------------------------ 463.10 Jumuia Lugha------------------------------------------------- 51SOMO LA NNE ...................................................................57LUGHA ZA MAWASILIANO PANA ...................................574.0 Utangulizi ................................................................57

2

Page 3: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

4.1 Madhumuni .............................................................574.2 Lingua franka ..........................................................574.3 Pijini na Kirioli ..........................................................584.4 Nadharia za Asili ya Pijini ..........................................63

SOMO LA TANO .................................................................67UWILI  LUGHA ...............................................................675.0 Utangulizi ................................................................675.1 Madhumuni .............................................................675.2 Uwili lugha ..............................................................675.3 Sababu za kuwepo na uwili lugha .............................685.4 Uchaguzi wa lugha katika jamii zenye uwili-lugha ......695.5 Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uwili-lugha .....705.6 Lugha Rasmi na Lugha ya Taifa ...............................735.7 Diglosia na Triglosia ...............................................745.8 Triglosia ................................................................825.9 Kubadili msimbo ....................................................825.10 Utowekaji wa lugha ...............................................84

SOMO LA SITA .................................................................91UPANGAJI LUGHA .........................................................916.0 Utangulizi ...............................................................916.1 Madhumuni ............................................................916.2 Upangaji lugha .......................................................916.3 Mawanda ya Upangaji lugha ....................................946.4 Mchakato wa upangaji lugha ....................................976.5 Lugha ya Taifa na Lugha Rasmi ................................1026.6 Sera ya lugha nchini Kenya .......................................102

SOMO LA SABA ...................................................................112ISIMU JAMII NA ELIMU ..................................................1127.0 Utangulizi .................................................................1127.1 Madhumuni ...............................................................1127.2 Ufunzaji, ujifunzaji na usomaji ....................................1127.3 Lugha katika Elimu .....................................................114

SOMO LA NANE ...................................................................124LUGHA NA JINSIA ............................................................1248.0 Utangulizi ..................................................................1248.1 Madhumuni ...............................................................1248.2 Jinsia na Isimu Jamii------------------------------------------ 1248.3 Lugha ya Wanawake na Wanaume ..............................125

3

Page 4: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Muhtasari   wa   Kozi Lengo la kozi hii ni kudadisi na kueleza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.Somo  hili  linalenga  kuchunguza  hali  mbalimbali  za  kijamii  na  jinsi  zinavyoathirimatumizi  ya  lugha  katika  miktadha  mbalimbali. Aidha,  kozi  hii  itawawezeshawanafunzi  kudhibiti  mbinu  na  ujuzi  wa  mawasiliano  miongoni  mwao  na  watuwengine kwa kuzingatia kaida za lugha husika.

4

Page 5: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA KWANZAISIMUJAMII

1.0 UtanguliziKatika  somo  hili tutatoa  maana ya  isimujamii pamoja  na kueleza historia yake.Tutaeleza mikabala mbalimbali ya isimujamii.   Vile vile tutaeleza uhusiano uliopokati ya lugha na jamii.   Aidha, tutaonyesha uhusiano wa isimujamii na taalumanyingine. Na  mwisho  tutajadili  mitazamo  mbalimbali  kuhusiana  na  swala  lalugha.

1.1 Madhumuni

Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:i.   Kutoa maana kamili ya isimujamii pamoja na kueleza historia yake.ii.  Kueleza kikamilifu mikabala ya isimujamii.iii.  Kuonyesha uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.iv.  Kueleza uhusiano wa isimujamii na taaluma nyingine.

1.2   Isimujamii ni nini?Wataalamu  wametoa  fasiri  mbalimbali  za  neno   isimujamii . Labov  (1992:183)anaeleza   kuwa, isimujamii   ni   mtazamo   wa   kiutafiti   wa   isimu   unaolengamatumizi   ya   lugha   katika   jumuia  lugha .   Pride   (1972:287)   anasema  kuwaisimujamii ni uchunguzi wa lugha kama sehemu ya utamaduni na jamii .  Lyons(1981) anaiainisha isimujamii kama tawi moja muhimu la isimumakro(microlinguistics),   matawi   mengine   yakiwa   isimunafsia,   isimuethnolojia,   n.k.Hudson   (1980:1)   anaieleza   isimujamii   kuwa   ni, uchunguzi   wa   jinsi   lughainavyohusiana na jamii .

Kwa  hivyo  tunaweza  kusema  kuwa  isimujamii  ni  taaluma  inayochunguza lughakama  inavyotumiwa  na  jamii  katika  fani  na  mazingira  mbalimbali  ya  kila  siku.

5

Page 6: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Mkazo  katika  isimujamii  umewekwa  kwa  watumiaji  wa  lugha  wenyewe. Basiisimujamii ni taaluma ambayo inapanua mawanda ya kimuktadha ya isimu kupitayale mazungumzo.KUMBUKA

Isimu jamii imejumuisha maneno mawili: Isimu na jamii.Isimu ni sayansi ya lugha.Jamii ni mkusanyiko wa vitu vinavyofana.

1.2.1 Isimu jamii inahusu nini?Wardhaugh (1986} anasema kuwa isimujamii inahusika na uchunguzi wa kuwekawazi uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii ikiwa na lengo la kuelewa muundowa lugha na jinsi lugha inavyofanya kazi katika mawasiliano.   Katika isimujamiitunaichunguza jamii ili kufahamu mengi zaidi kuhusu lugha.

Labov  (1980)  aneleza  kuwa  eneo  jingine  la  utafiti  ambalo  limeongezwa  katikaisimujamii  ni  sosholojia  ya  lugha.Hii  hushughulika  na  maswala  mengi  yakijamii na jinsi yanavyoingiliana na lugha na lahaja.  Haya ni pamoja na matatizoyanayohusishwa na kudhoofika na hata kufa kwa lugha na kumezwa kwa lughazenye  watu  wachache,  maendeleo  ya  uwili-lugha,  usanifishaji  wa  lugha,  naupangaji wa lugha hasa katika mataifa yanayoendelea.

Eneo  lingine  ambalo  linajumuishwa  katika  isimujamii  na  linahusika  na  lughakatika matumizi yake ni ethnografia ya mawsiliano.   Ethnografia ni maelezoya kisayansi kuhusu mbari, mila, utamaduni wa binadamu.  Mambo yanayohusikahapa ni kueleza na kuchanganua ruwaza za matumizi ya lugha na lahaja katikautamaduni   fulani:   matukio   yanayozusha   mazungumzo,   uhusiano   kati   yamzungumzaji,   hadhira,  mada,   njia  ya   kuwasilisha   na  muktadha.   Pia  katikaisimujamii kuna sajili au  rejista ambayo  hurejelea  matumizi tofauti tofauti yalugha.

6

Page 7: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Pamoja na hayo kuna kuchanganya lugha tofauti hivi kwamba tunapata kubadilimsimbo  (code  switching)  na  kukopa,  na  jinsi  lugha  tofauti  zinavyoingilianahata kusababisha pijini na krioli.

Hudson   (1984:4-5)   anasema  kuwa, isimujamii   hushughulikia  wazungumzajibinafsi kama wanachama wa makundi ya kijamii na huuliza maswali kama vile,kwa nini kuna tofauti nyingi kati ya makundi haya, na tofauti hizo ni zipi   .

1.3 Historia Fupi ya IsimujamiiKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lughana  jamii  umepelekea  kukua  kwa  taaluma  mpya  inayoitwa  isimujamii. Ingawakulikuwa   na   haja   ya   kuichanganua   lugha   kulingana   na   miktadha   yake   yamatumizi  katikati  mwa  karne  iliyopita,  jina  la isimujamii halikutumika  hadimwaka   wa   1952   katika   kazi   ya   Haver   C.   Currie,   aliyekuwa   Mshairi   naMwanafalsafa(Tazama Mesthrie (2001). Miaka kumi baadaye istilahisociolinguistika ilitumika Urusi, na katika mwaka wa 1964 utafiti wa isimujamiiukasambaa Marekani.

Isimujamii kama  taaluma imekua  na kupata  maendeleo makubwa katika miakaya mwishoni mwa sitini (1960 s) na mwanzoni mwa sabini (1970 s).   Hata hivyouchunguzi ulioihusisha lugha na jamii umekuwepo tangu zamani hasa wataalamuwalipochunguza lahaja na uhusiano kati ya maana ya maneno na utamaduni.

Kongamano  la  kwanza  la  isimujamii  lilifanyika  katika  Chuo  cha  University  ofCalifornia-  Los  Angeles  mwaka  wa  1964. Huu  ndio  mwaka  ambao  isimujamiiimejitokeza kikamilifu kama taaluma.   Tangu hapo utafiti mwingi umefanywa nawaandishi mashuhuri wa taaluma hii miongoni mwao wakiwa, Grimshaw, Hymes,Fishman,  Gumperz,  Labov,  na  Lieberson. Taaluma  hii  imejulikana  pia  kamasosholojia ya lugha.

7

Page 8: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1.4  Mikabala ya Isimu JamiiKama  tulivyosema  hapo  mwanzoni,  wanaisimujamii  hawafasiri  isimujamii  kwanamna moja.  Zipo sababu nyingi za kutofanya hivyo, lakini tutatoa tatu tu:(a) Sababu   ya   kwanza   inatokana   na   fasiri  ya  lugha. Wapo  wanaisimu

wachache kama vile Labov 1972, Trudgill 1974, Halliday and Martin 1981n.k  ambao  bado  wanaichambua  lugha  ya  jamii  kwa  kufuata  misingi  yakiisimu.

(b) Wataalamu  waliofafanua  isimujamii,  walilielewa  neno   jamii   kwa  namnatofauti. Baadhi walishikilia maana pana ya kuhusisha watu wote waishiokatika   taifa   moja   (lenye   makabila   na   mataifa   mbalimbali   pamoja).Wengine  wamechukua  maana  finyu  ya  kuhusisha  wale  watu  waishiokatika sehemu moja walio na lugha moja na kuchangia utamaduni mmoja.

(c) Pia  kumekuwepo  na  misisitizo mbalimbali katika ufafanuzi wa isimujamii.Wapo wanaisimu wanaoelezea lugha ya jamii kwa kufuata mwelekeo wakisaikolojia, kisosiolojia, kianthropolojia, kihistoria, kiethnolojia, nk.

Kwa sababu hii kumetokea mikabala mitatu ya isimujamii:(a) Mkabala wa kimaikro(b) Mkabala wa kimakro(c) Mkabala kati

1.4.1 Mkabala wa KimaikroMkabala wa kimaikro unajumuisha mitazamo yote ambayo inafafanua isimujamiikwa  kufuata  mbinu  na  nadharia  za kiisimu.   Mkabala huu  hutazama isimujamiikama mwendelezo wa taaluma ya isimu.

Je,  ni  nini  mawanda  ya  isimujamii  kwa  mujibu  wa  mkabala  huu? Si  rahisikusema kwa mkato kuwa mawanda ya isimujamii yanaanza hapa na kuishia pale.

8

Page 9: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Tunachoweza  kusema  ni  kuwa  wakati  uchambuzi  wa  kiisimu  unatilia  mkazomaana  itokanayo  na  kuchunguza  uhusiano  wa  maneno  kiwima  na  kiusilisila(syntagmatic uhusiano  wa  kiulalo  wa  vipashio  vya  tungo)  katika  sentensi,uchambuzi  wa  kupata  maana  kiisimujamii unaongezea juu  yake sifa za kijamii.Kwa mfano:(i) Amekwenda ntoni kuchota maji(ii) Mtoto ayupo apaKatika mifano hii, mtaalamu wa isimu atakuwa na haya ya kusema.1.  Atagundua kwamba mwandishi ametumia maneno  ntoni ,  ayupo ,  apa

badala ya  mtoni ,  hayupo  na  hapa  . Katika ufafanuzi wake atasema kuwahayo si maneno sanifu ya Kiswahili ni maneno yatokanayo na lughambalimbali.  Ataeleza ni kina nani wanazungumza lugha ya Kiswahili hivyo.

2.  Licha ya kasoro za matumizi ya maneno hayo, sentensi zote mbili zinatoamaana zilizokusudiwa.   Katika sentensi ya kwanza tunafahamu kuwa mtajwahakwenda mahali pengine isipokuwa mtoni kwa madhumuni ya kuchota maji.Sentensi ya pili ina maana kuwa mtu ambaye hayupo ni mtoto wala si mtu warika  jingine.   Tunazipata  maana kwa  kuzingatia  uhusiano  wa maneno kamayalivyotumika katika sentensi.Mwanaisimu jamii atazichambuaje sentensi hizo hapo juu?Kwanza, atakubaliana na uchambuzi uliofanywa hapo juu pamoja na maanazake.Pili, atataka kujua watu gani (wa sehemu gani [kabila], umri gani, kisomogani, kipato kipi, wake au waume) wanaotamka  ntoni ,  ayupo  na  apabadala ya mtoni, hayupo na hapa.Tatu,  atataka kujua sababu zinazowafanya watamke hivyo.Nne, atataka pia kujua ni wakati gani na katika mazingira gani mtu hutamkahivyo.  Inawezekana wanatamka hivyo wanapoongea na watu wa makabilayao lakini wanayatamka vizuri wanapoongea na watu wa makabila tofauti.

Uchambuzi wa Kiisimujamii unatuonyesha mambo kadha wa kadha ya

9

Page 10: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

kimsingi: Baadhi ya maneno (ntoni, ayupo na apa) yaliyotumika katika sentensi zetu

yanahusishwa  na  aina  mbalimbali  za  watu  katika  jamii.Hii  ina  maanakuwa lugha si tu kuelewa maana ya maneno bali pia hutumika kuielewajamii ilivyo.

Pili,  hatuwezi  kudai  kuwa  mtu  anayetumia  maneno  ya   vilugha   katikamazungumzo  yake  hajui  kutamka  maneno  ya  Kiswahili  sanifu. Mtuanaweza  kutumia  vilugha  kwa  sababu  zake  mbalimbali  ikiwemo  ile  yakutaka  kuonyesha  mshikamano  wake  na  watu  wa  kabila  lake  au  watuwatokao sehemu moja kihistoria na kijiografia.

Miongoni mwa wafuasi wa mkabala huu ni pamoja na Labov (1972) na Trudgill(1974).  Labov (1972) amejitokeza kuwa mwanaisimu mashuhuri katika miaka yasabini  (1970)  kutokana  na  utafiti  wake  ulioonyesha  uwezekano  wa  kuoanishaalama za kiisimu (linguisitic forms) na zile za kijamii na kufanikiwa kupata habarizaidi juu ya jamii hiyo.

Labov aliufanya utafiti mjini New York ulioonyesha kuwa watu wa tabaka la chinihutamka sauti (r) inayosikika katika kuyatamka maneno yenye fonimu /r/ kulikowatu  wa  matabaka  mengine. Labov  anatumia  nadharia  na  mbinu  zile  zile  zaisimu  kuelezea  isimu  jamii. Pia  anachunguza  ni mazingira yapi  na  sababu  zipi(kiisimu/kijamii) zinazoleta ubainifu miongoni mwa watumiaji wa lugha.

1.4.2 Mkabala wa KimakroHuu  ni  mkabala  unaoangalia  isimujamii  kinyume  na  mkabala  wa  kimaikro. Nimkabala  wa  kimakro  kwa  sababu  unahusisha  watu  wengi  kijiografia.   Mkabalahuu unaeleza na kufafanua lugha kwa kutumia mwingiliano wa mbinu na dhanambalimbali kutoka taaluma nyingine za kijamii.   Mkabala huu huangalia mamboyote  yanayohusu  utumiaji  wa  lugha  kwa  ujumla  katika  jamii. Kujua  lugha

10

Page 11: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

zilizopo katika jamii na uhusiano wake na lugha nyingine ni moja tu ya mamboya kimsingi ya mkabala huu.

Kwa  mfano,  mwanaisimu  jamii  wa  mkabala  huu,  hupenda  kujua  sababu  zamsingi  zinazofanya  lugha  moja  iteuliwe  kuwa  lugha  ya  taifa,  lugha  rasmi,  aulugha  ya  kufundishia  katika  elimu. Sababu  kama  hizo  aghalabu  huwa  hazinabudi  zitokane  na  misingi  ya pamoja  ya  kiisimu  na  kijamii.   Pia,  hata  zile lughaambazo  hazikuteuliwa  kuchukua   dhima  fulani  kitaifa,  bado  kwa  mujibu  wamkabala   huu   lugha   hizo   ni   muhimu   kukuzwa   na   jamii   zinazohusika   ilikuziimarisha.   Nani anazungumza lugha ipi, wapi, kwa nini, na kwa madhumunigani, ni miongoni mwa maswala muhimu yanayoshughulikiwa na mkabala huu.

Mwanaisimujamii haangalii maana ya tamko peke yake bali huangalia maana kwakuzingatia   taratibu   na   kanuni   za   mawasiliano   zinazotumika   katika   jamiiinayohusika.   Hii ina maana kwamba, uchambuzi wa kupata maana katika lughahaufanywi  nje  ya  taratibu  za  kijamii  na  mazingira  ya  tamko  lenyewe. Nenomazingira   hapa  lina  maana  ya  kuhusisha  mahali  tamko  liliposemwa,  kujuahabari za mzungumzaji na msikilizaji pamoja na uhusiano wao na kujua taratibuna kanuni zinazotawala mawasiliano ya lugha inayohusika.Mkabala huu hauchambuisentensi   zisizotumiwa   katika mazungumzo   yamajibizano.  Ni katika msingi huu ndipo sentensi:

(i) Amekwenda ntoni kuchota maji.(ii) Mtoto ayupo apa.

haziwezi   kutupatia   uchambuzi   unaoridhisha   kwa   mujibu   wa   mkabala   huu.Tunahitaji  kuchambua  sentensi  au  matamko  yatokanayo  na  mazungumzo  namajibizano kama mfano wetu hapa chini unavyoonyesha:

(iii) Baba Mkwe:  Mwanangu, umefika salama?(iv) Mkwe:  Ndiyo baba, tumefika salama.(v) Mkwe:  Haya baba, mfike salama.

11

Page 12: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(vi) Baba Mkwe:  Asante Mwanangu.

Katika   kuchambua   maana   za   sentensi   hizi   uhusiano   wa   mzungumzaji   namsikilizaji  ni  muhimu  sana  kuzingatiwa.  Uchambuzi  unatuonyesha  kuwa  katikasentensi (iv) mkwe ametumia kiambishi cha wingi  tu   badala ya umoja. Vile vilekatika  sentensi  (v). Je,  tunaweza  kusema  kuwa  huyu  mkwe  hajui  matumizisahihi ya viambishi nafsi?

Hapa, maswala kama ya utamaduni, kaida na kanuni za mawasiliano katika jamiin.k.   yanafaa   kuzingatiwa   katika   uchambuzi. Kwa   mujibu   wa   kanuni   zamawasiliano  ya  jamii  hiyo,  mtu  aliye  mdogo  katika  umri  hutakiwa  kutumiakiambishi cha  nafsi ya  kwanza wingi  badala ya  umoja  anapozungumza  na  mtuwa umri mkubwa kama dalili ya kuonyesha heshima.  Tumefikia maana hii baadaya   kuzingatia   taratibu   na   kaida   zinazotumiwa  katika  mawasiliano  ya  lughainayohusika.

Fishman(1972)  amesema  kuwa  ni  muhimu  kwa  wataalamu  wa  lugha  kutumiambinu za pamoja (kiisimu na kijamii) katika kufikia uteuzi wa lugha ili zichukuedhima mbalimbali katika jamii.

Zoezi

Je, unaweza kuonyesha tofauti kati ya isimu kimaikro na isimu kimakro kwakutumia mifano kutoka kwa jamii yako?

1.4.3 Mkabala KatiKimsingi,  mkabala  huu  unazingatia  yale  mambo  ya  kimsingi  tu  kutokana  namikabala  yote  miwili. Kudai  kuwa  lugha  ielezwe  na  kufafanuliwa  kwa  kufuatakanuni  za  kiisimu  peke  yake,  ni  dai  la  kiwango  cha  juu. Lakini  mkabala  wa

12

Page 13: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

kimaikro bado una mambo yake ya kimsingi ambayo yanaweza kuchukuliwa nakutumiwa  katika  kueleza  lugha  kiisimujamii.   Kwa  mfano,  baadhi  ya  kanuni  zafonolojia na mofolojia zinaweza kutumiwa sambamba na sifa nyingine za kijamiiili   kueleza   kaida   zinazofuatwa   na   watumiaji   wa   lugha   katika   mazingirambalimbali.

Mwanaisimujamii   anao   uhuru   wa   kushughulikia   uchambuzi   wa   lugha   kwaviwango na idadi ya watu (watumiaji wa lugha) apendao mwenyewe kulinganana lengo la kazi yake.

Ervin  Tripp  (1971)  ni  miongoni  mwa  wanaisimujamii  wachache  wanaofuatamkabala   wa   kati. Anasisitiza   umuhimu   wa  kuchunguza   kanuni   za   kijamiizinazotawala  mazungumzo  mbalimbali ya  kila siku.   Anadai  kuwa mazungumzoyanayofanywa  na watu  hayafanywi  kiholela bali  hufuata kanuni za mawasilianokatika  jamii  zinazohusika. Kwa  mujibu  wa  mtazamo  huu,  isimujamii  inapaswakushughulikia   uchunguzi   wa   kanuni   na   kawaida   za   kijamii   zinazotawalamawasiliano kwa jumla.

Tumeona  kuwa  isimujamii  ni  taaluma  pana  na  inayovuka  mipaka  ya  isimu  nakuhusisha taaluma nyingine za kijamii.   Si rahisi kuweza kueleza mipaka kati yaisimu na isimujamii.  Hii ni kwa sababu taaluma hizi zinaingiliana sana.

Mwanaisimujamii hashughuliki na utoaji wa maamuzi yahusiyo lugha kwa niabaya jamii.   Kazi ya mwanaisimujamii ni kueleza na kufafanua lugha kwa misingi yaisimujamii.   Utoaji wa maamuzi yahusuyo lugha yameachiwa watumiaji wa lughawenyewe.

Swali

Ukizingatia kila mkabala, onyesha jinsi lugha inavyotumiwa katika jamii yako.

13

Page 14: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1.5 Lugha na JamiiIsimujamii  ni  dhana  ambayo  imetokana  na  isimu  na  inaingtia  lugha  kamainavyotumiwa  katika  jamii. Lugha  si  kifaa  tu  cha  kuwasilisha  habari  bali  ninamna muhimu ya kuanzisha na kudumisha uhusiano  miongoni mwa watu.

Kila  tunapozungumza,  wasikilizaji  wetu  hupata  habari  fulani  kuhusu  sehemutunazotoka na sisi ni watu wa aina gani.   Hata mielekeo yetu na mawazo yetuvinaweza kutumiwa na wengine kutuelewa zaidi.  Mambo mawili haya ni muhimusana kutokana na mtazamo wa kijamii.

(a) Dhima ya lugha ya kuanzisha mahusiano ya kijamii.(b) Dhima ya lugha ya kuwasilisha habari fulani kuhusu mzungumzaji.

Kiisimu, lugha sanifu haichukuliwi kuwa bora kuliko lahaja au lugha nyinginezo.Lugha  zote zina mifumo tata yenye kanuni za kipekee.  Kule kusema kuwa lughamoja  ni  bora  kuliko  nyingine  ni  jambo  la  kijamii,  si  la  kiisimu. Ikiwa  watu  nimaskini  au  wa  ngazi  ya  chini,  basi  hata  lugha  zao  zitadharauliwa.   Kwa  hivyomielekeo yetu kuhusu  vilugha  hivi huonyesha muundo wa kijamii wa watu.

Katika  kuonyesha  uhusiano  uliopo  baina  ya  lugha  na  jamii,  wataalamu  wengiwamezungumzia nadharia tete ya Sapir-Whorf (Edward Sapir na Benjamin LeeWhorf).   Nadharia   hii   inaeleza   kuwa   lugha   asilia   ya   mtu   hutawala   jinsianavyouelewa  ulimwengu.  Hii  ina  maana  kwamba  tofauti  za  kiisimu  huwezakuzusha  utambuzi  unaotofautiana.   Ina   maana kwamba  hatuwezi kuwaza bilalugha.   Basi ikiwa mtu anaweza kudhibiti lugha wanayojifunza watu, atakuwa nauwezo wa kudhibiti mawazo yao.

Kulingana  na  Sapir-Whorf  (1956),  binadamu  huelewa  mazingira  kupitia  kwalugha  wanayoitumia. Wanatoa  mfano  wa  Waeskimo  ambao  wana  maneno

14

Page 15: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

mengi  yanayoelezea hali mbalimbali za theluji,  huku  Kiingereza  kikiwa na nenomoja tu snow.  Pia katika jamii ya Hopi, lugha yao inataja vitu kama  mawinguna  mawe  kama vitu vilivyo hai.   Hali hii inawafanya waufikirie ulimwengu kwanjia tofauti na watu wengine.

Eneo   analoishi   mtu   hujitokeza  katika   lugha   yake  hasa   katika   muundo   wamsamiati.  Kwa mfano, mfumo wa aila katika jamii hujitokeza katika msamiati waaila kama vile mtoto, binti, babu, nyanya, shangazi, n.k.

Pia maadili ya jamii yanaweza kuwa na athari katika lugha ya jamii hiyo.   Hayahutokea kupitia kwa miiko.   Miiko huhusika na tabia ambazo zimekatazwa katikajamii fulani.  Katika lugha, miiko inahusishwa na vitu au maneno yasiyotumika aukutajwa.   Maneno ambayo ni mwiko katika lugha fulani hutuonyesha (kwa kiasifulani) mfumo wa maadili na imani za jamii hiyo.

Kwa hivyo mwiko ni swala la kiisimu kama lilivyo la kijamii.   Miiko husababishamaneno fulani kupotea kutoka kwenye lugha na mengine kuzuka.

Kwa hivyo, isimujamii ni sehemu ya isimu inayoiangalia lugha kama sehemu yakijamii na utamaduni wa watu.   Inachunguza nyanja za lugha na jamii, na inauhusiano   wa   karibu   na   taaluma   nyingine   kama   anthropolojia,   sosholojia,saikolojia na hata jiografia.

1.6 Isimujamii na Taaluma NyingineSi  watafiti  wa  isimu  na  isimujamii  pekee  wanaohusika  na  uchunguzi  wa  lughakatika jamii. Wataalamu kutoka kwa taaluma nyingine kama vilewanaanthropolojia, wanasaikolojia, n.k huhusika pia.

15

Page 16: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1.61 Isimujamii na SaikolojiaTaaluma hizi mbili hushughulikia swala la mielekeo (attitudes) kuhusu aina fulaniza  lugha. Ingawa  wanaisimujamii  wanachunguza  kwa  kina  swala  la  mielekeokuhusu  lugha,  hili  ni  jambo  la  kisaikolojia  kwa  kuwa  lipo  katika  akili  ya  mtu.Uchunguzi  huu  ni  muhimu  katika  kueleza  mabadiliko  ya kiisimu  yanayojitokezakatika   lugha. Mara   nyingi   sababu   hii   hutumiwa   kueleza   kwa   nini   lahajainabadilika,   lini   na   jinsi   inavyobadilika. Kwa   mfano,   nchini   Kenya   vijanawanatamka neno  best  kama  beshte  ili kuafikiana na mielekeo ya vijana kuhusumatamshi ya maneno fulani hasa mijini.

Wanasaikolojia  hutueleza  jinsi  mtoto  anavyojifunza  lugha  kupitia  kwa  uwezomaalum anaozaliwa nao (innate capacity), lakini pia lazima tufahamu jinsi tofautiza  kimazungumzo  (mf  kijinsia)  zinavyokuzwa  katika  mchakato  wa  kuingilianakijamii.

1.6.2 Isimujamii na AnthropolojiaAnthropolojia  ni  taaluma  inayohusika  na  elimu  ya  binadamu,  hususan  elimuinayohusu habari za asili na maendeleo yake ya awali.   Inachukuliwa kuwa jinsibinadamu huyu alivyokua katika kikundi, alikuwa anazungumza lugha fulani.

Wanaanthropolojia kadha wamefanya utafiti ambao una misingi ya kiisimujamii,kwa mfano, kwa kuchunguza mfumo wa aila wa jamii.  Tunajua kuwa mfumo waaila hujitokeza katika msamiati.  Kwa mfano, utaona kuwa jamii nyingi za Kiafrikazina  msamiati  mpana  unaoelezea uhusiano  wa kiaila kuliko  lugha  za Wazungu.Jambo hili linatueleza mengi kuhusu jamii hizo.   Kwa mfano, lugha ya Kiingerezahuzungumzia  aina  moja  tu  ya  shangazi  (aunt)  lakini  katika  lugha  nyingi  zaKiafrika kuna maneno ya uhusiano huu kwa upande wa baba na wa mama.Zoezi

Taja majina ya kiaila katika jamii yako na ulinganishe na ya Kiingereza.

16

Page 17: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1.6.3 Isimujamii na ElimuWanaelimu   wanatakiwa  kutoa  maamuzi  kuhusu   maswala  yanayohusu   lughakama  vile  ufundishaji  wa  lugha  sanifu. Wanaisimujamii  wamekuwa  wakijaribukushawishi wanaelimu wabadili mielekeo yao kuhusu lugha fulanizinazozungumzwa  na  watoto  fulani  shuleni  kama  vile  lugha  zao  za  kwanza.Wapangaji lugha huhitajika kuwa na ufahamu fulani wa kiisimu ili waweze kutoauamuzi unaofaa kuhusu aina ya lugha inayotakiwa kukuzwa na kuhimizwa katikamiktadha fulani, daraja na shule nk.

1.6.4Isimujamii na UtamaduniWanaanthropolojia hushughulikia utamaduni ili kuweza kueleza tabia za watu zakiisimu;  wanaisimujamii  huoanisha  lugha  na  utamaduni  kwa  kuzingatia  sarufi.Uhusiano kati ya taaluma hizi mbili unatokana na ile haja ya kuyaelewa makundimbalimbali ya watu.   Hivi ni kusema kwamba ni vigumu kwa wanaanthropolojiakuchunguza  jamii  za  kale bila kuzingatia  lugha  za  watu  hao;  na  pia ni  vigumukuchunguza lugha bila kuzingatia uamilifu wa mazungumzo fulani katika jamii.

Kwa   kuzingatia   lugha,   maana   ya   ujumbe   fulani   ni   kile   kitu   ambachokimewasilishwa  kila  wakati  mwanajamii  anapoongea. Na  tukizingatia  tabia  zakijamii,  maana  ni  kile  kitu  ambacho  kimewasilishwa  wakati  mwanajamii  fulaniametenda (kitu fulani) kitendo cha kitamaduni.   Kwa hivyo lugha na utamadunini tabia za binadamu.   Mtazamo wa kipragmatiki hutupa zaidi ya ile maana yamaneno.Unaangalia  pia  vikwazo  vya  kijamii  anavyokabiliana  navyo  mtumiajilugha,  na  athari  nyinginezo  za  kijamii  katika  matumizi  ya  lugha. Lazima  piatuzingatie muktadha wa maongezi ili tuielewe kauli fulani.

17

Page 18: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1.6.5 Isimu na Sosholojia (Elimujamii)Wanaisimujamii  hutalii  miundo  ya  kijamii  na  namna  miundo  hiyo  inavyoathirilugha.  Kuna  nguvu  fulani  za  kijamii  ambazo  husababisha  wanajamii  kutakakuongea  au  kutamka  maneno  kwa  njia  fulani.Mkondo  unaochukuliwa  nakibadala  (variant)  fulani cha  kiisimu  katika jamii si jambo  linalojitokeza kiholelatu, bali ni kitu kinachotokana na tathmini za kijamii.  Uchaguzi wa kipashio fulanicha  kiisimu  unatokana  na  jinsi  jamii  inavyochukulia  kipashio  hicho.Lughahutueleza mengi kuhusu mtu katika jamii.

Kumbuka

Kwa sababu isimu-jamii ni taaluma inayohusika na jamii moja kwa moja,Ina uwezo wa kuhusiana na taaluma nyingi sana.

1.7 Mitazamo ya LughaWanazuoni mbalimbali wakiwemo Greenberg (1957), Hymes (1974), Dik (1978)nk  wanaiangalia  lugha  kwa  mitazamo  miwili:  mtazamo  wa  kiisimu  na  ule  wakiisimujamii.

Katika mtazamo wa kwanza (wa kiisimu), lugha inaelezwa kuwa ni mfumo wasauti nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofananaili   kuwasiliana.   Mtazamo   huu   unachukulia   lugha   kuwa   kitu   halisi  ambachokinaweza  kuainishwa  katika  vipande sauti vidogo  vidogo  ambavyo  kwa pamojahuunda mfumo wa lugha wa mawasiliano.

Chomsky   (1957)   aliunga   mkono   mtazamo   huu.   Katika   kuifafanua   lugha,alitofautisha hali ya umilisi na utendaji.  Umilisi ni kile ambacho mzungumzajianafahamu  kuhusu  lugha  yake. Uwezo  huu  humwezesha  kuelewa  na  kutoasentensi   nyingi   jinsi   anavyotaka   kuwasiliana. Huku   ni   kufahamu   kanuni

18

Page 19: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

zinazoitawala lugha husika na uwezo huu umo akilini mwake.   Utendaji ni jinsimzungumzaji anavyoitumia lugha.

Kutokana na maelezo haya ni kama Chomsky anatueleza kwamba tusiichunguzelugha  katika  matumizi  yake,  au  hata  jinsi  tunavyojifunza  lugha,  bila  kwanzakufahamu  lugha  ni  nini. Anaona  kuwa  kazi  ya  mwanaisimu  ni  kuandika  aukutunga sarufi na kukuza uelewa wetu wa lugha.

Kuna wataalamu ambao wamepinga msimamo huu.   Kwa mfano, Labov anaionasarufi kama mali ya kikundi/jamii au jumuia lugha na wala si mali ya kisaikolojiaya mtu binafsi.   Hudson (1980:19) anaona kuwa mtazamo wa lugha usiohusishajamii  una  upungufu. Nadharia fika  ya  lugha  lazima  itaje  matumizi  ya  lughahiyo. Anasema  kuwa  unweza  kuitenga  lugha  na  jinsi  ya  kwa  nini  inatumiwa.Kwa hivyo lugha ni sehemu ya jamii.

Umilisi wa kimawasiliano hauhusu tu kufahamu mfumo wa lugha, bali pia ni niniunachosema  na  kwa  nani,  na  namna  utakavyokisema  katika  muktadha  fulani.Unashughulikia   ujuzi   wa   kijamii   na   kitamaduni   ambao   hudhaniwa   kuwawazungumzaji  wanao  unaowawezesha  kufasiri  mifumo  ya  kiisimu. Fonolojia,sintaksia   na   msamiati   ni   sehemu   tu   ya   vipashio   vinavyotumiwa   katikamawasiliano. Pamoja  na  hivyo  lazima  kuwepo  semantiki,  muktadha  na  kwajumla mtazamo wa kijamii wa lugha.

Hivyo  basi  ufafanuzi  wa  Chomsky  wa  lugha  una  upungufu  kwani  unaichukulialugha  kama  kitu  kinachojitosheleza. Unaiondoa  lugha  kutoka  kwenye  jamii.Hapa ndipo isimujamii inapoingilia ili ilete kipengele cha jamii katika lugha.

Mtazamo wa pili wa lugha ni wa kiisimujamii.   Mtazamo huu unaangalia lughakama  sehemu  ya  utamaduni  wa  jamii  ulio  na  ruwaza  ambazo  hurithishwa  nawatu  wenyewe  kutoka  kizazi  kimoja  hadi  kingine. Mtazamo  huu  unaichukulia

19

Page 20: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

lugha kama mali ya jamii.   Wanaisimujamii wanakubaliana na fasiri   hii ya pili yalugha.

Zoezi

Isimu jamii ni nini? Taja mikabala mitatu ya isimujamii na uonyeshe kwa kutoa mifano jinsi

inavyoingiliana na kutofautiana. Eleza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii. Isimujamii ni taaluma inayoingiliana na taaluma nyingi katika jamii.

Fafanua kauli hii.

Muhtasari

Katika   somo   hili,   tumeeleza   maana   ya   isimu   jamii   na   mambo   hayayamezingatiwa; Tumeonyesha mikabala mitatu ya isimujamii. Tumeonyesha uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii. Tumeonyesha jinsi isimujamii inavyoingiliana na taaluma nyingine. Tumeeleza mitazamo miwili ya lugha kwa kuzingatia maoni ya wataalamu

mbalimbali.

20

Page 21: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Marejeleo TeuleChomsky, N.(1957),Syntactic structures.The Hague. MoutonDik, S.C.(1978)   Functional      Grammar   .  North-Holland Linguistics Series.  North-Holland Publishing Company.  New York.Fishman, J.A. (1967)  Sociolinguistics and the Language Problems of DevelopingCountries   katika   Fishman, J.A. et.al. (eds.)   Language      Problems      of      Developing   

Nations.  John Wiley and Sons. Inc. London.(1972) Domains and the Relationship between Micro and MacroSociolinguistics katika Gumperz,   John   &   Dell   Hymes   (eds.)         Directions      in      Sociolinguistic:The Ethnography of communication.Basil Blackwell.oxfordGreenberg, J.H. (1957)   Essays      in      Linguistics   , Chicago: Phoenix Books.Hudson, R. (1980)   Sociolinguistics   : Cambrdige, University Press, Cambridge.Hymes, D. (1974)   Foundations      in      Sociolinguistics   : University of PennyslavaniaPress,  Philadelpia.Labov  (1980)  (Mhr.)  Locating      Language      in      Time      and      Space   .  Academic  Press.New York.Mesthrie, R. et.al. (2000)   Introducing      Sociolinguistics   .  Edinburgh UniversityPress, Edinburgh.Msanjila, Y.P. (1995)  Mawanda ya Isimu Jamii   katika Mbogo, E. na McOnyango,O. (wahariri)   Baragumu    Juzuu la 2 Nam. 1 & 2 Uk. 65-71,  Chuo Kikuu Maseno.Pride, J. G. &  Holmers J. (eds.) (1972)   Sociolinguistics    Harmondsworth:Penguin.Wardhaugh, R. (1992)   An      Introduction      to      Sociolinguistics   .  Blackwell.Whorf,  B.L.  (1956),      Language,      Thought      and      Reality   :  Selected  Writings,  J.B.Carroll (ed). Cambridge, MA:MIT press

21

Page 22: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA PILI

NADHARIA ZA KIJAMII

2.0 UtanguliziSehemu hii inashughulika na kueleza nadharia za kijamii ambazo hutumika katikakuelewa uhusiano mbalimbali katika jamii. Nadharia hizi zinasaidia kuelewa waziswala la lugha na jamii.

2.1  MadhumuniMnamo mwisho wa somo hili utaweza kutimiza yafuatayo:1.  Kueleza nadharia za kijamii.2.  Kuonyesha jinsi  nadharia hizo zinavyoingiliana na swala

la lugha.

2.2  Nadharia za KiisimuIli  kuzingatia  sehemu  ya  kijamii  iliyo  katika taaluma  ya  isimujamii, ni muhimukuelewa  mitazamo  mbalimbali  inayotumiwa  kuchunguza  jamii  za  wanadamu.Katika   sosholojia kunazo nadharia tatu kuu zinazoielezea jamii.   Kuelewa lughakatika jamii kunahitaji pia kuzielewa nadharia hizi  za kijamii.  Katika

mada hiitutazijadili nadharia mbili  za mwnzo kati ya hizi tatu.  Nadharia hizo tatu ni:(a) Uamilifu (functionalism)(b) Umaksi (marxism)(c) Muingiliano (interaction)

2.2.1  UamilifuHii ni nadharia iliyoibuka kati ya miaka ya arobaini na sitini (1940 s and 1960 s).Inaeleza  kuwa  jamii  inaweza  kuchukuliwa  kama  mfumo  ulio  na  sehemu  zenyeuamilifu.   Ili  kuelewa sehemu  yo  yote  ya  jamii (kama  familia au shule), lazimasehemu hiyo ichunguzwe kwa kuangalia uhusiano wake na jamii nzima.   Kamavile   mwanabiolojia   anavyochunguza   mchango   wa   moyo   katika   kuendeleza

22

Page 23: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

maisha  ya  binadamu  ndivyo  sehemu  ya  jamii  inavyochunguzwa  kulingana  namchango wake katika kuendeleza mfumo wa kijamii.

Mfumo  wa  kijamii unayo  mahitaji fulani ambayo  yanahitaji kutekelezwa ili jamiiidumu.  Mahitaji haya  ni  pamoja  na  chakula,  mavazi  na  malazi. Uamilifu  wasehemu yo yote ya jamii ni ule mchango wake katika kuendeleza na kuimarishajamii   hiyo   kwa   jumla. Hii   ina   maana   kwamba   kuna   kiwango   fulani   chamuingiliano kati ya sehemu zote ambazo huunda jamii.

Wanauamilifu  wanadai  kuwa  utaratibu  na  uimarikaji  ambavyo  huwa  ni  vitumuhimu vya kuendeleza jamii hutokana na kuwepo kwa amali (za pamoja) sawa,yaani  makubaliano  kuhusu  mambo  fulani  katika  jamii. Kutokana  na  mtazamohuu   wanajamii   hushughulikia   mifumo   midogo   ya   kijamii   na   amali   sawazinazowaunganisha wanajamii.

Dhana  zinazosisitizwa  katika  nadharia  hii  ya  elimujamii  na  ambazo  ni  muhimukwa  mwanaisimu  jamii ni  pamoja na: utamaduni, ujamiishaji (socialisation),kaida, amali, hadhi na majukumu/dhama.

(i) UTAMADUNIUtmduni hurejelea jinsi jamii inavyoishi; yaani mkusanyiko wa mawazo na tabia

wanazojifunza  na  kupokeza  kutoka  kizazi  kimoja  hadi  kingine. Katika  hali  hiiutamaduni  ni  mpangilio  wa  jinsi  watu  wanavyoishi.  Utamaduni unafafanuamambo yanayokubalika na mfumo wa tabia katika jamii fulani.

(ii) UJAMIISHAJIDhana hii inarejelea njia ambazo kwazo watu hujifunza utamaduni wa jamii zao.Ujamiishaji  wa   kimsingi   au   awali  hutokea  utotoni,  aghalabu   katika  familia.Mahirimu au marika (peer group) ni kukundi muhimu cha kuendeleza ujamiishaji.Marika humsaidia kumkuza mtu kijamii na kiisimu.

23

Page 24: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(iii) KAIDA NA AMALI(a) KAIDAKaida ni mwongozo maalumu wa jinsi ya kutenda mambo na kaida hueleza tabiazinazokubalika na zile zinazofaa katika miktadha maalumu.   Mifano ya kaida hiziinaonekana   katika   mavazi   ya   shuleni,   ya  vijana,ya  nyumbani,  au  ya  dhifambalimbali.  Katika hali ya ujamiishaji, kaida hufunzwa kwa kutuza (kumpa mtotoperemende, maneno ya kusifia) au kuadhibu.   Baadhi ya kaida hufanywa kuwasheria  za  kutumikia  umma  wote. Kwa  mfano,  kukataza  kuoga  hadharani  auwanawake kuhitajika kufunika nyuso zao hadharani.

AMALIAmali  hutoa  miongozo  ya  kijumla  ya  mambo  ambayo  yanachukuliwa  kuwamazuri  na  yenye  thamani.Kwa  mfano,  katika  jamii  nyingi  za  kisasa,  watuhuthamini  maisha  ya  binadamu  sana.  Baadhi  ya  amali  zinazopendekezwa  niumoja,uaminifu, upendo, n.k..

Wanauamilifu   wanaamini   kuwa   ikiwa   kaida   hazitakubaliwa   na   kushirikishwamiongoni  mwa  wanajamii,  jamii  haziwezi  kushirikiana  na  kufanya  kazi  pamoja.Hivyo basi jamii inahitaji kaida na amali za pamoja.   Jambo hili limekuwa msingiwa tafiti nyingi za isimujamii.

(iv)HADHI NA MAJUKUMUHadhi  hurejelea cheo cha mtu katika jamii  (si lazima iwe kazi).  Hadhi kama hizihuenda  zimerithiwa,  yaani  mtu  anapozaliwa  anajipata  ana  hadhi  fulani  kwamfano malkia au mfalme. Anapoendelea kukua anajipata kuwa yeye ni mke aumume  .  Hadhi  pia  huenda  ikapatikana  kutokana  na  juhudi  za kibinafsi za mtu,kwa mfano, kujiendeleza kitaaluma na kuwa mwalimu, daktari, mwanamichezo,n.k.

24

Page 25: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kila  hadhi  katika  jamii  huwa  na  idadi  fulani  ya  kaida  ambazo  zinaeleza namnamtu aliye katika hadhi  hiyo anatakiwa kuendesha maisha yake.  Kikundi  hiki chakaida  huitwa  dhima  au  majukumu.  Majukumu ya  kijamii  ndiyo  huongozatabia.   Kufikia mwisho mwa siku, mtu huwa ametekeleza majukumu mbalimbali:mwalimu (kazini), mama au mke (nyumbani), mteja (benki), manju (kilabu chastarehe), n.k.   Kila jukumu huhitaji tabia fulani zizingatiwe, zikiwa ni pamoja natabia za kiisimu.  Kila jukumu la kijamii humfanya mtu achague elementi fulani zakiisimu. Huku  akitekeleza  majukumu  yake  atatumia  lugha  kwa  njia  tofautitofauti.

Zoezi

Je, kwa maoni yako, unafikiri nadharia  ya uamilif  inajitokeza vipi katika jamiizetu na lugha tunazozitumia?

2.2.2 UMAKSIUmaksi  unahusiana  na  nadharia  kadhaa.   Tunapoongea  kuhusu  uhakiki  wa  ki-maksi, huwa tunairejelea mikabala mbalimbali ambayo misingi yake   ni mawazoyanayohusishwa na Karl Marx na Friedrich Engels.

Nadharia hii imepitia mabadiliko makubwa tangu kuweko kwa wataalamu hawa.Umaksi  unahusu  nyanja  mbalimbali kama  uchumi,  historia, jamii na mapinduzi.Umaksi una sifa ya kijumla inayojitokeza katika mwelekeo wake wa kuligusia kilaeneo, na kuwa na la kusema kuhusu takriban kila kitu ikiwemo lugha.

Mawazo  ya  Karl  Marx  kuhusu  historia na  miundo  ya  kijamii yana nafasi kubwakatika  nadharia  hii. Umaksi  ni  falsafa  yakinifu  hasa  kwa  kuwa  pana  msisitizomkubwa kwenye msingi wa hali za kiyakinifu za maisha kama mazingira ya kuishikuliko mawazo katika maisha ya binadamu. Umaksi hauegemezi mfumo wake wa

25

Page 26: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

kifalsafa   kwenye   dhana   dhahania   kama   urembo,   ukweli   au   ndoto   baliunayaegemeza kwenye uhalisi unaoonekana.

Hebu basi tuchunguze mawazo ya kimsingi ya nadharia hii:(1) Historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu

ya  kiuchumi. Misingi  hii  itachunguza  njia  za  uzalishaji  mali  pamoja  namiundo   ya   kiuchumi   inayoathiri   sio   uzalishaji   mali   hiyo   tu   bali   nausambazaji wake.   Swala hili la uzalishaji mali na usambazaji wa mali hiyolinaunda kile ambacho hujulikana kama msingi au muundo msingi (base =infrastructure).   Kwenye msingi huo ndiko kunakoegemezwa muundo wajuu au kikorombwezo (superstructure).   Muundo wa juu ndio unaohusishamaadili, itikadi, dini, utamaduni ,n.k.

Sifa  za  muundo  juu  zinaathiriwa  kwa  kiasi  kikubwa  na  muundo  msingi.Hata hivyo mabadiliko yanayotokea katika muundo wa juu kama mageuzikatika muundo wa kiutawala huweza kuathiri muundo msingi.

(2) Daima historia ya binadamu itadhihirisha au kuakisi harakatizinazoendelea  katika  matabaka  ya  kiuchumi-jamii. Karl  Maksi  aliwahikusema kuwa historia ya maisha ya binadamu ni ya harakati za kitabaka.Je, harakati hizi zinasababishwa na nini?   Tunajua kuwa kitu cha msingikatika maisha ya binadamu ni kula na kunywa, kupata malazi na mavazina mambo mengine.

Tendo  la  kwanza  la  kihistoria  kwa  hiyo,  ni  kutafuta  njia  ya  kuyakidhimahitaji  haya  ya  kimsingi. Ili  kufanikiwa  katika  lengo  hilo,  binadamuhulazimika  kujiunga  pamoja  au  kuunda  umoja  ili  kuimarisha  ubora  nawepesi wa kuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo.  Muungano huo huwana ugawaji wa majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwa kwamatabaka  katika  jamii. Hatua  ya  juu  ya  mwendeleo  huu  ni  ukuzaji  wamfumo wa ubepari.   Katika mfumo huu, mali inamilikiwa na idadi ndogo

26

Page 27: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

ya watu.   Watu hao wanaipata mali yao kutokana na unyonyaji wa ummana hasa wafanya kazi.

Kumbuka

Zingatia maoni haya katika muktadha wa lugha.  Kwa mfano lugha-wenyeji na lugha za kigeni zilizopo hapa nchini.

Kadiri   mfumo   wa   ubepari   unavyoendelea   ndivyo   ubora   wa   uzalishaji   majiunavyoongezeka  na  tofauti  kati  ya  matabaka  kuimarika  kwa  kuwa  kuna  watuwanaofaidika  kwa  njia  zisizo  za  haki. Kufaidika  huko  kwa  njia  zisizo  za  haki,pamoja   na   mbegu   za   kujiangamiza   zilizomo   kwenye   mfumo   wa   ubeparivinachangia   kuuangusho   mfumo   wenyewe. Marx   anaamini   kuwa   hayayanatokana na mfanyiko wa kiasilia wa kihistoria.  Mfanyiko huo ni wa kipembuzi(dialectics). Kwa  mujibu  wa  mawazo  haya,  historia  huendelea  kutokana  namfululizosafu  wa mkinzano wa mawazo.   Matokeo ya mkinzano huo ni kuzukakwa  hatua  nyingine  mpya  ya  kihistoria. Huu  ndio  msingi  wa  kile  kinachoitwaupembuzi wa kiyakinifu  (dialectical materialism).

(3) Matamanio na matakwa yaliyopo katika jamii na hasa tabaka lenye nguvuyanaakisiwa  katika  itikadi  iliyopo  katika  jamii,  jinsi  na  miundo  ya  mawazoambayo aghalabu huwa imeshika kwa nguvu na huwapo kila mahala kiasi chakuwa huenda wanajamii wasiitambue kwa haraka.(4) Njia ya kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa mfumo wakibepari ni kudadisi, kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua batili iliyopokatika itikadi ya kibwanyenye inayooimarisha ubepari.

Dhana za kimsingi zimeibuka katika nadharia hii:   ukengeushi; ubidhaaishaji naitikadi.

27

Page 28: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(i) Ukengeushi (alienation):  Ugawaji wa kazi unaishia kusababisha utenganofulani   kati   ya   wanaohusika   au   binadamu. Hii   ni   hatua   ya   kimsingi   yaukengeushi . Mfumo  wa  kibepari  unapoendelea  kuboreka  unasababisha  haliambapo uhusiano uliopo kati ya mfanya-kazi na tokeo la nguvu zake ni wa kitukigeni (alien object).   Watu wanaishia kukengeushwa na jamii yao kutokana namfumo wa kiainisho (specialization) unaosisitizwa na kukuzwa na ubepari.

(ii) Ubidhaaishaji:   Maksi anaitumia dhana ya bidhaa kukieleza au kukirejeleakitu kinachozalishwa sio kwa nia ya kutumiwa bali kubadilishwa katika mfumo wakibepari  wa  soko. Bidhaa  hizo  hazitathaminiwi  kutokana  na  kazi  yake  bali  nikutokana na bei zinazoweza kuvuta.   Yaani msingi wa kuzitathmini sio thamanikimatumizi bali ni thamani kimabadilishano.   Katika msingi huu, bidhaa zinaishiakuhusisha  nguvu  au  kanuni  fulani  fiche  ambazo huwavuta  watu na kuwafanyawawe na mvuto mkubwa wa kukimiliki kitu fulani ambacho kinawasisimua.   Huundio msingi wa  kuabudu bidhaa  (fetishism of commodities).

Hii  ni  sifa  kuu  katika  mfumo  wa kibepari  na ni  msingi  wa uchumi  wa  kibidhaaambapo  watu  husukumwa  na  kani  za kununua  na  kumiliki  vitu  ambavyo labdahawavihitaji au wanavikinai haraka na kutamani vingine.  Sifa hii ya ubidhaaishajiinaishia kuwahusu binadamu ambao hawathaminiwi kama binadamu ila kutokanana uwezo wao wa kuzalisha mali.

(iii) Itikadi: Ni dhana telezi, lakini kimsingi ni uwasilishi wa pamoja wa mawazo,fikira na tajriba hasa ikiwa vitalinganuliwa na uhalisia wa kiyakinifuvinakoegemezwa. Dhanahii inaweza kufafanuliwa katika  muktadha  wa lughapale  ambapo  watu  wanaamini  kuwa  kuzungumza  lugha  ya  mama  ni  dalili  yaushamba au kinyume chake kwamba kuzungumza lugha ya Kiingereza ni dalili

ya kuwa mtu wa tabaka la juu.

28

Page 29: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Zoezi

Kwa kuzingatia hali ya lugha nchini Kenya, ni kwa njia gani nadharia yaUmaksi inaeleza hali hii (zingatia mvutano kati ya lugha ya Kiingerezana lugha nyinginezo za Kiafrika).

Swali

Huku ukitumia nadharia moja ya Elimujamii, onyesha namna lughainavyoingiliana na jamii

2.4 HITIMISHOKatika  somo  hili  tumejadili  nadharia mbili  za  kijamii  ambazo  zitatusaidiakuelewa jamii.   Nadharia hizi zitachangia katika kuelewa swala la lugha katikajamii.

Marejeleo Teule

Eagleton, T. (1983)   Literary      Theory:      An      Introduction   .  Oxford: Blackwell.Mesthrie,   R.   et   al   (2001)         Introducing      Sociolinguistics   ,   Edinberg,EdinbergUniverstity Press.Wamitila, K.W. (2002)   Uhakiki      wa      fasihi:      Misingi      na      Vipengele      vyake   .  Nairobi.

Phoenix Publishers Ltd.

29

Page 30: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA TATULUGHA NA JAMIIDHANA ZA KIMSINGI KATIKA ISIMU-JAMII

3.0   UtanguliziKatika somo hili, tutashughulikia  dhana za kimsingi katika isimujamii.  Dhana hizini  pamoja  na  lugha,  lahaja,  mtindo-pekee,  sajili  au  mtindo  na  jumuiya  lugha.Tutazingatia dhana hizi kwa kuonyesha maana yazo pamoja na kuonyesha jinsizinavyohusiana na uwanda mzima wa isimujamii.

3.1   Madhumuni

Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1.  Kueleza maana ya lugha na matumizi yake.2.  Kueleza maana ya lahaja na jinsi lahaja zinavyoibuka.3.  Kueleza maana ya mtindo-pekee.4.  Kueleza maana ya mtindo na sajili pamoja na kueleza sajili mbalimbali.5.  Kueleza ni nini maana ya jumuiya lugha.

3.2   LughaLugha  ni  chombo  kilichoundwa  na  wanadamu  kwa  ajili  ya  matumizi  yao;  kwahivyo kama wanadamu wasingekuwapo, hapana shaka kusingekuwapo na lughapia.  Kutokana na huu uhusiano kati ya lugha na binadamu, ni dhahiri kuwa tabiana mabadiliko ya wanadamu yataiathiri lugha vilevile (Mdee, 1986).  Wanaisimu,katika   kuichunguza   lugha,   wanaichukua   kama   kitu   na   kuanza   kuifafanua,wakiangalia  miundo  ya  vipengele  mbalimbali  vinavyoijenga  na  kuikamilisha  najinsi   inavyoathiriwa   na   mabadiliko   ya   kisiasa,   kiuchumi,   kiutamaduni   nakisaikolojia ya wazungumzaji.

30

Page 31: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Swali

Je, lugha ni nini?

Kujibu  swali  hili  ni  rahisi  kwa  sababu  wanaisimu  mbalimbali  wamejaribu  kutoamawazo yao juu ya swali hili.  Hebu tuangalie wanachokisema wanaisimu.

Kwa mujibu wa Otto Josepersen, Encyclopedia Britannica, lugha ni njia yoyote yamawasiliano kati ya viumbe vyenye uhai.  Kwa maana hii lugha ina maana kubwasana. Tunaona  kwamba  fasili  hii  inaeleza  kimantiki  kuwa  kila  kiumbe  chenyeuhai kina lugha.   Kwa hivyo, tunapata lugha kwa wanadamu, wanyama, waduduna mimea.

Kwa maana yake maalum lugha ni njia yoyote wanayoitumia wanadamu   katikakuwasiliana. Maana  hii  ni  sawa  kidogo  na  hiyo  ya  mwanzo  lakini  mkazoumetiliwa  kwa  wanadamu  tu. Maana  hii  inalingana  na  Trudgil  (1974)  katikaSociolinguistics anayesema kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwakwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.

Kwa  maana  ya  kiisimu,  lugha  ni  utaratibu  wa  sauti  za kusemwa, za nasibu, zajamii  yenye  utamaduni  fulani  ambazo  huzitumia  kwa  kuwasiliana. Hapa,basi,tunaona  kwamba  maana  hii  inabagua  kabisa  maana  zake  tulizotaja  mwanzoni.Kwa kutumia maana hii,hebu tuchambue kila kipengele:

Lugha:(a) ni   sauti   ya   kusemwa. Mtu   hutoa   sauti   fulani   ambayo   ina   maana.

Tunatumia midomo, taya, ulimi, meno, koo, nyuzi, ufizi na kadhalika.(b) ni  sauti  za  nasibu.Sauti  hizi  zimetokea  tu  kwa  bahati  katika  ile  lugha

isemwayo. Hakuna  kitu  kilichofanyika  kupatana  juu  ya  maneno. Kwa

31

Page 32: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

mfano,  maneno  haya  haya  ya  lugha  mbalimbali  huwakilisha  neno   kitiendeve   (kimaragoli),   chair   (Kiingereza) na kadhalika.

(c) ni sauti zenye utaratibu kamili.   Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwakwa  kufuata  utaratibu  fulani  unaokubaliwa  na  jumuia  hiyo  ya  watu.Utaratibu huo huitwa sarufi.   Kwa mfano, hatusemi  Maria tunda ana  balijumuia imepatana kusema  Maria ana tunda .

(d) ni sauti ya watu  wa utamaduni fulani.   Utamaduni ni mila na desturi zamaisha ya watu zilizojengwa tangu awali.   Lugha inatawaliwa na manenoya utamaduni wa watu hao.   Kwa mfano, wazungu wana maneno mengiya sayansi wakati Waafrika hawana maneno ya kuelezea, k.m. motokaa,santuri na kadhalika ni vitu ambavyo havikuwapo katika utamaduni wao.

(e) ni sauti za kueleza wazo. Yaani ni sauti zinazowawezesha watu kupashanaau kujulishana habari.

3.2.1  Matumizi ya LughaKwa jumla matumizi ya lugha yoyote hutegemea:(a) Mahali,  kwa mfano  nazi  kwa watu wa pwani.(b) Wakati, kwa mfano, maneno ya kisiasa ya miaka hii kama vile, uwazi, haki

za binadamu na kahdalika.(c) Umri, kwa mfano, maneno ya  sheng  ambayo hutumiwa zaidi na vijana.(d) Hali ya kike au ya kiume,   Kwa mfano,  Aka  kwa mwanamke,  Ebo  kwa

wanaume,  Bee  kwa wanawake na  Naam  kwa wanaume.(e) Kisomo, kwa mfano,  ziara  badala ya safari,  stashahada  badala ya cheti

na kadhalika.(f) Pia matumizi na mabadiliko ya lugha yanaweza kutegemea jadi, ada, kazi

au daraja ya mtu.

32

Page 33: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Swali

Jadili   kauli   kwamba   Lugha   na   jamii   hukamilishana   na   kuathirian a

3.2.2.  MITAZAMO ELEZI NA ELEKEZI YA LUGHA(i)  Mtazamo  elezi  wa  lugha  ni  ule  ambao  unafafanua  vipengele  vya  lughajinsi vilivyo.   Ni mtazamo unaochunguza na kuweka wazi jinsi makundi tofauti yawatu  yanavyoitumia  lugha  katika  miktadha  mbalimbali.Uchunguzi  kama  huuhaupendelei lugha ya kikundi kimoja kuwa ni bora kuliko ile ya vikundi vingine.Kwa mfano, mtu anaweza kuelezea lugha inayotumiwa darasani, ya wafanyakaziwa viwanda, ya wachuuzi mjini Nairobi, n.k, bila ubaguzi wo wote.

(ii)  Mtazamo  elekezi wa lugha  huhusika  na  kanuni  au  adabu  katika  lugha.Huu ni mtazamo ambao unajaribu kuweka sheria za matumizi sahihi ya lugha iliwatumiaji wa lugha walazimike kuzifuata sheria hizo.

Mtazamo elekezi hujitokeza vizuri zaidi katika sarufi mapokeo, ambapo dhima yamwalimu   wa   lugha   inaonekana   ni   kuhakikisha   kuwa   lugha   safi   au   nzuriinahifadhiwa na kutumiwa.   Hapa kanuni zinatolewa kuhusu vipashio mbalimbalivya matumizi ya lugha kwa mfano:

Sarufi: Sentensi huanza kwa herufi kubwa.Msamiati: Msamiati unaofaa umetumika.Maana: Kwamba mtu amemaanisha kile alichonuia.Matamshi:  Mtu ametamka sauti ipasavyo.

Wanaoshikilia mtazamo huu wamejitetea kwa hoja zifuatazo:1. Kuna matumizi ya lugha yaliyo bora na yenye mantiki kuliko mengine.2. Wanarejelea  mifumo  iliyothibitika  kuwa  mizuri  (classical  form). Wakati

mwingine  wanasarufi  hutilia  mkazo  uamuzi  wao  kwa  kurejelea  lugha

33

Page 34: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

zilizodhaniwa  kuwa  bora  hapo  zamani. Lugha  kama  Kilatini,  Sanskrit,Tamil  na  Kiarabu  zilichukuliwa  kuwa  vielelezo  vya  kuigwa. Mara  nyingiKiingereza kililazimishwa kufuata mfumo wa Kilatini ili kionekane pia kuwasahihi.

3. Hupendelea mifumo ya zamani ya lugha hiyo.Wanaoshikilia mtazomo elekezi katika lugha huwa hawataki kuiona lughayao ikipitia mabadiliko yo yote.   Hawataki visawe viongezeke, au maana,au mabadiliko ya kimuundo, yajitokeza katika lugha.

4. Wanakataza matumizi ya maneno ya kigeni.Huwa hawataki kukopa maneno ya kigeni na kuyatumia katika lugha zao.Kwa mfano, huko Ufaransa kuna taasisi inayoitwa   The French Academy(Chuo   cha   Ufaransa)   ambayo   ina   kazi   ya   kukitakasa   Kifaransa  kwakuondoa maneno yote ya lugha nyingine, hasa Kiingereza,yanayojipenyeza kwenye lugha hiyo.

Wanaopinga mtazamo elekezi wa lugha wanasisitiza kwamba lugha zote ni sawa,hakuna lugha au lahaja iliyo bora kuliko nyingine.   Wanaisimu wanasema kuwamisingi  ya lugha  elekezi imejikita katika  matumizi ya  lugha  au kiisimu ya watuwa  tabaka  la  juu  katika  jamii,  na  si  katika  dhana  ya  usawa. Wamesemayafuatayo katika kuupinga mtazamo huo:

1. Mtazamo  wa  kimantiki  wa  lugha  kama  vile  ilivyo  katika  hisabati  unamatatizo. Kama   utafiti   wa   sarufi   uliofanywa   na   Chomsky   (1965)ulivyoonyesha,  kutatokea  utata  mwingi kwani sheria za lugha  ni chungunzima.

2. Wanasema kuwa kila lugha ina upekee wa aina fulani.  Kwa hivyo, hakunahaja  ya  kulazimisha  lugha  fulani  kufuata  mfumo  wa  lugha  kielelezo  auiliyochukuliwa kuwa bora hapo zamani.

3. Kuhusu  matumizi  ya  mifumo  ya  zamani  ya  lugha,  wanaisimu  wanasemakuwa   daima   lugha,   hubadilika   kwa   njia   mbalimbali.   Sheria   mpya

34

Page 35: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

zinapoibuka zinaingiliana na zile za zamani.   Hili haliathiri ubora wa lughahiyo.

4. Wanaisimu elezi wanasema kuwa lugha zote hukopa maneno.  Ukopaji wamaneno ni sehemu muhimu ya ukuaji wa lugha.   Mara nyingi mabadilikoyanayotokea  katika  lugha  huakisi  mabadiliko  yanayotokea  katika  jamiikama vile  vitu vipya, mitindo mipya, nk.

3.2.3 MJADALA ZAIDIKwa  muda  mrefu  wanaisimu  wamepuuza  mtazamo  elekezi  katika  kuifafanualugha.   Hata  hivyo,  inafikiriwa kwamba  ikiwa kusudi ni kuzungumzia matumiziyote ya lugha na mielekeo kuhusu lugha basi, wanaisimu jamii sharti watambuemtazamo  elekezi.Matumizi  mabaya  na  mazuri  ya  lugha  yapo  katika  jamii.Kama vile usafi ulivyo muhimu kwa afya bora, ndivyo lugha sahihi inavyohitajikakatika matumizi ya kila siku ya lugha.

Pili,  hata  wale  ambao  wanaupinga  mtazamo  elekezi  huwa  wanatumia  lughasahihi katika  maandishi  na matamshi  yao.   Wakati  mwingine wahakiki hukosoawanaisimujamii  kwa  kuhimiza  au  kukubali  lahaja  zote  huku  wao  wanatumialahaja  au  lugha  sanifu. Hata  darasani  watawaadhibu  wanafunzi  wao  kwakutotumia  lugha  sanifu.   Kwa hivyo,  hatuwezi kuepuka  kuwepo  kwa kanuni  zalugha.

Inaonekana basi kwamba mtazamo wa kati unahitajika; ule unaozingatia pandezote mbili.   Katika matumizi yasiyo rasmi tunaweza kuitumia lugha tunavyotakalakini katika miktadha rasmi, kama ufundishaji wa lugha darasani, tutumie lughasanifu.

Hata  wanaisimujamii  hualikwa  kama  wataaalamu  kushiriki  katika  upangaji  walugha.   Katika hali kama hizo, wao huulizwa kufanya uchaguzi kuhusu vibadalafulani  vya  lugha  vinavyofaa,  maneno  na  misemo.Hivyo  basi  wanaisimujamii

35

Page 36: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

hawawezi  kupuuza  wazo  kwamba  ubora  wa  lugha  ni  sehemu  ya  mazingira  yalugha katika jamii nyingi.

ZoeziHuku ukitumia mtazamo elekezi, toa mifano kumi ya makosa yanayofanywana watu katika lugha kisha urekebishe makosa hayo.

3.3   LAHAJAImethibitika kuwa  lugha  haitulii,  huenda  ikibadilika  kila  wakati.  Hata katikalugha ya kundi moja, tofauti nyingi hudhihirika.  Crystal (1995:3) amezungumziavibadala vifuatavyo vya lugha.

Vibadala kijamii/kitabakaVibadala vya muda

Vibadala kibinafsi Vibadala kimaeneo

Jinsi lugha inavyotofautiana kimfumo ni jambo linalowashughulishawanaisimujamii.   Lugha  pia  inaweza kubadilika  kulingana  na muktadha, wakatina mzungumzaji au mhusika.   Katika somo la isimujamii msisitizo huwa ni kwakikundi   cha   jamii   na   wala   sio   kwa   mtu   binafsi. Taaluma   ya   lughainayoshughulikia lahaja kwa ujumla huitwa elimulahaja (Dialectology).

3.3.1  MAANA YA LAHAJA

36

Page 37: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Lahaja  ni  mojawapo  ya  migao  ya  lugha  ambayo  hutokana  na  mabadiliko  yalugha.   Chambers  &  Trudgill (1980:3)  wanaeleza  kuwa  katika matumizi ya kilasiku, ambayo yana upotoshi fulani, lahaja ni lugha ya kiwango cha chini ambayohaijakua vizuri, isiyo fahari, na inayohusishwa na makabwela.   Katika matumizikama haya, inachukuliwa kwamba lahaja huzungumzwa katika sehemu za duniazilizojitenga  na  ni  aina  ya  uzungumzi  ulio  na  mushkili  na  usiofuata  kanuni  zalugha  sanifu. Lakini  tunajua  kwamba  mawazo  haya  hayana  msingi  wo  wote.Katika   lugha   tunaamini   kwamba   hakuna   lugha   au   lahaja   iliyo  bora  kulikonyingine duniani   lugha au lahja zote ni sawa.

Tunaweza kusema kuwa lahaja ni aina ya uzungumzaji unaotumiwa na kikundicha  watu  aghalabu  katika  eneo  maalum,  na  hutofautiana  na  uzungumzaji  wavikundi  vingine  vya  lugha  hiyo  moja katika  matamshi, msamiati  na  kwa nadrasana sarufi.

Inaonekana kuwa lahaja ni kama matagaa ya lugha moja.  Mkusanyiko wa lahajahuunda  lugha.   Aina hizi za uzungumzaji hazitatizi mawasiliano kati  ya vikundimbalimbali vya jamii vinavyozungumza lugha moja.   Inaonekana kuwa kila mtuhuzungumza lahaja.

Lahaja  sanifu  huwa  na  hadhi  ya  juu  kuliko  zile  lahaja  zingine  kwani  huwaimeendelezwa kimsamiati na kimuundo.

3.3.2 KUZUK KWA LAHAJAKuzuka   kwa   lahaja   mbalimbali   duniani   ni   dhihirisho   kuwa   daima   lughainabadilika. Wakati  mwingine  haya  mabadiliko  hukithiri  kiasi  kwamba  hakunauelewano. Inapotokea  hivyo,  basi  zile  lahaja  hujitosheleza  zenyewe  na  kuwalugha   kamili. Hivi   ndivyo   ilivyokuwa   kwa   Kilatini   ambapo   lahaja   kadhaa

37

Page 38: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

zilibadilika   na   kuwa   lugha   za   Kifaransa,   Kihispania,   Kiitaliano,   Kireno,   naKiromenia (Wardhaugh 1987).Kuna mambo matatu muhimu katika uzukaji wa lahaja.  Mambo hayo ni:(a) vizuizi(b) umbali(c) muda

(i) Vizuizi (Barriers)Lahaja  huzuka  kutokana  na  vizuizi  vinavyoibuka  kati  ya  makundi  ya  watuwanaozungumza  lugha  moja. Vizuizi  hivi  vinaweza  kuwa  vya  kijiografia  kamavile  bahari,  mito,  milima, misitu mikubwa, n.k.   Vizuizi vinaweza pia  kuwa vyakisiasa kama vile mipaka, uongozi, n.k.  Vinaweza pia kuwa vya kijamii kama vilerangi ya mtu, kabila, tabaka, dini, n.k; au vinaweza kuwa vya kiuchumi.

(ii) Umbali (Distance) na Muda (Time)Watu  wanaozungumza  lugha  moja  wakihamia  maeneo  tofauti  na  kutengwa nawenzao  kwa  umbali  fulani,  baada  ya  muda  lugha  yao  itaanza  kuwa  tofautihasa ikiwa hakuna uhusiano mkubwa wa kimawasiliano kati ya makundi hayo.

Pia  tunajua  kwamba  lugha  hupokezwa  kutoka  kizazi  kimoja  hadi  kingine,  nabaada  ya  muda  mabadiliko  ya  kimatamshi  na  kisarufi  yanayoletwa  na  kizazikipya hukita.   Mabadiliko haya yakikosa kusambaa katika eneo lote basi tofautizinajitokeza na tofauti hizi ndizo zinazoitwa lahaja.

3.3.3 NADHARIA YA MAWIMBI (WAVE THEORY)Nadharia   ya   mawimbi   inaweza   kutumiwa   kuonyesha   jinsi   lahaja   huibuka.Mwasisi  wa  nadharia  hii  ni  Johanness  Schmidt  (1872). Inasemekana  kuwamabadiliko ya kiisimu husambaa nje kuanzia kwenye kitovu fulani vile ambavyomawimbi   yanafanya   unapotupa   jiwe   kwenye   kidimbwi. Mawimbi   haya

38

Page 39: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

yanatofautiana  kwa  ukubwa  na  yatakuwa  na  vitovu  tofauti.  Jinsi  mawimbiyanavyosafiri kwenda mbali yanazidi kufifia.

Mawimbi  haya  ya  mabadiliko  husafiri  kupitia  kwa  maeneo  ya  kijiografia  au  yakijamii au yote mawili.   Yanaweza kuzuiwa au kupunguziwa kasi na vizuizi kamatabaka,  jinsia,  umri,  kijiografia,  n.k. Mabadiliko  haya  huwasilishwa  na  watubinafsi,  na  wakati  fulani  badiliko  litakuwa  limefikia  watu  fulani  na  kutowafikiawengine.

3.3.4 ISTILAHI ZINAZOTUMIKA KATIKA LAHAJA(i) Kizingasifa (Isogloss)Katika  utafiti  wa  lahaja  tunaweza  kuchora  ramani  kuonyesha  mahali  ambapomatamshi, msamiati au muundo fulani hutumiwa.   Kuna njia mbili za kuonyeshamambo haya:(a) Kwa kutumia ishara(b) Kwa kuunganisha sehemu hizo kwa laini inayoitwa kizingasifa.

Kizingasifa ni mpaka unaochorwa kulizungushia eneo ambalo lina sifa maalum zamatamshi, sarufi au msamiati katika ramani ya kiisimu.Kizingasifa hutumika ili kutenganisha sehemu zilizo na sifa fulani na zile ambazohazina sifa hizo.  Tazama  mchoro huu.

Kizingasifa

39

Kiidakho KimaragoliMukhwasi

KhMukwasi

k

Page 40: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Ruwaza  ya  vizingasifa  huelezwa  kwa  kuzingatia  vizuizi  vya  kijiografia  ambavyovinatenganisha jamii mbili au zaidi zilizopakana.   Vizuizi hivi ni kama mto wenyekina  kirefu,  msururu  wa  milima,  n.k. Vizuizi  vinaweza  kuwa  ni  vya  kijamii aukisiasa.   Watu wa eneo fulani wanaweza kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa nakijamii na hivyo wakawa na utamaduni tofauti na maeneo waliyopakana nayo.

(ii) Eneo la Fahari (Centre of Prestige)Vizingasifa  vingine  huwa  na  ruwaza  inayoonyesha  kusambaa  kwa  kipashio  chakiisimu kutoka kwa eneo la fahari au kitovu, ambalo aghalabu huwa mji.   Hapa,vizingasifa  hivi  hufanana  na  viwimbi  vinavyotokana  na  jiwe  lililotupwa  majini.Ndivyo  tulivyopata  nadharia  ya  mawimbi. Wanaoshikilia  nadharia  hii  huaminikwamba mabadiliko ya kiisimu husambaa kama mawimbi.

(iii) Sehemu masalio (Relic Areas)Wakati  mwingine  ruwaza  hujitokeza  ikionyesha  sehemu  ndogo  ndogo  ambazozimeachana lakini zenye sehemu zinazofanana kiisimu.  Sehemu hizi hazina eneola fahari kama miji.   Hizi ni zile sehemu ambazo hazijafikiwa na miundo mipya.Mara   nyingi   sehemu   hizi   huwa   katika   maeneo   yaliyojitenga   kama   milima,mabonde au mipaka ya lugha fulani.(iii) Sehemu za Mpito (Transitional Areas)Hii ni sehemu ambayo mawimbi ya eneo la fahari moja hukutana na mawimbi yaeneo  la  fahari  jingine. Katika  hali  kama  hii  eneo  hilo  halina  sifa  maalumutambulishi  bali  linashiriki  sifa  za  maeneo  mawili  ya  fahari  yaliyo  jirani. Kwamfano, Luanda, iliyo kati ya mkoa wa Nyanza na Magharibi.

3.5 AINA ZA LAHAJAKuna aina mbili za lahaja:3.5.1.  Lahaja za KijiografiaHizi  ni  lahaja  zinazozungumzwa  katika  maeneo  fulani,  nazo  hutokea  watu  walugha  moja  wakihamia  maeneo  tofauti  halafu  wakatengwa  kimawasiliano  kwa

40

Page 41: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

umbali, milima, bahari, mipaka, n.k (Fromkin & Rodman 1974:254).   Mifano yalahaja  za  kijiografia  ni  zile  za  Kiswahili:  Kiunguja,  Kimvita,  Kiamu,  Kimrima,Kimgao, Kitumbatu, n.k.

Watu wanaofanyiwa utafiti ili kuthibitisha kuwepo kwa lahaja hizi ni wazee waliona umri mkubwa ambao wameishi mahali hapo kwa muda mrefu, wana kisomokidogo au hawana, na ambao hawajapata athari ya lugha au lahaja nyingine.

ZoeziTaja lugha nyinginezo mbili unazozifahamu na uonyeshe lahaja zake.

3.5.2.  Lahaja za Kijamii/KitabakaHizi ni lahaja zinazotumiwa na makundi ya watu kulingana na hadhi yao, tabaka,elimu,  kazi  wanayofanya,  pato,  umri,  uana,  na  vipengele  vingine  vya  kijamii.Watu  wanaokuwa  katika  lahaja  moja  ya kijamii si lazima wawe wanaishi katikaeneo moja.

William Labov,  mwanaisimu  wa Kimarekani, aliona kuwa  lugha  inao mfumo wavibadala ambao unaweza kuelezwa kuzingatia tofauti za kimatabaka katika jamiifulani.

Utafiti   uliofanywa   na   watafiti   wengi   wakiwemo   Labov   na   John   Fischerunaonyesha  kuwa  watu  hutumia  vipashio  fulani  vya  kiisimu  si  kwa  sababu  nirahisi kuvitamka bali kwa sababu ya jinsi wanavyohisi kuhusu hadhi yao na walewanaowazungumzia.  Kwa mfano kusema:

Maalim badala ya mwalimu

Nchini Kenya, kumekuwepo na lahaja za kijamii kama Kisetla na Kihindi.

41

Page 42: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Zoezi

Je, kuna lahaja zingine zipi za kimatabaka nchini Kenya?

3.6 LUGHA AU LAHAJA?Vipengele  vifuatavyo  hutuwezesha kuamua  kama  tofauti za kiisimu zinazotokeazinaashiria   tofauti   za   lahaja   au   za   lugha.Unajuaje   kuwa   jinsi   mbili   zakuzungumza ni lahaja za lugha moja au ni lugha mbili tofauti?

3.6.1.  Kusikilizana (Mutual Intelligibility)Ingawa   lahaja   hutofautiana,   watu   wanapozungumza   huelewana. Ikiwa

wazungumzaji  wawili  walio  na   tofauti   fulani  katika   lugha   zao  wataelewanawanapozungumza, basi itachukuliwa kwamba wanatumia lahaja tofauti za lughamoja. Lakini  ikiwa  hawataelewana  basi  wanazungumza  lugha  tofauti. Hatahivyo,   kuna   viwango   mbalimbali  vya   kuelewana  kati   ya   lahaja  mbalimbali.Wazungumzaji  wa  Kinyala  na  Kibukusu   kwa  mfano  ,wataelewana kwa  sababuhizi  ni  lahaja  za  lugha  moja,  lakini  wazungumzaji  wa  Kiingereza  na  Kikambahawataelewana.Watu wengi husema kuwa kipengele muhimu cha kuamua kamani lugha au lahaja ni hiki.

3.6.2. Mwendeleo lahaja (dialect continuum)Dhana hii hurejelea mfuatano wa jinsi lugha zinavyopakana kijiografia, yaani AB C D E F G ...    Katika mkururo huo, huwa kuna kusikilizana katikalahaja zilizopakana, lakini zile zilizotengana kwa mbali huwa hakuna masikilizano.Kwa mfano, kuna uwezekanao kuwa wazungumzaji wa A na G hawataelewana.Hapa ndipo tatizo linazuka.  Je, bado tunaweza kusema kuwa A na G ni lahaja zalugha moja?

3.6.3.  Lugha sanifu

42

Page 43: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kuwepo   kwa   lugha   sanifu   au   maandishi   yanayotumiwa   na   kundi   la   watuhutusaidia kujua kama zinazohusika ni lahaja au lugha.  Ikiwa makundi mawili auzaidi  yanayotofautiana  katika  maongezi  hukubaliana  kuwa  yana  mfumo  mmojaulio  sanifu  au  yanatumia  aina  moja  ya  maandishi,  basi  inachukuliwa  kuwayanazungumza lahaja tofauti na wala si lugha tofauti.

Kwa  mfano,  nchini  Uchina  wazungumzaji  katika  sehemu  mbalimbali  za  nchihutumia   Mandarin,   Cantonese,   Wu,   Hakka   au   Fukien. Wazungumzaji   wavibadala  hivi  hawaelewani  lakini  kwa  sababu  wanatumia  mfumo  mmoja  wakuandika   (wa   Kichina)   na   kusoma   basi   inachukuliwa   kuwa   hizo   ni   lahajambalimbali za Kichina.

3.6.4.  Vipashio visivyo vya KiisimuSifa fulani zisizo za kiisimu hutumiwa pia kuamua kama kinachohusika ni lahajaau  lugha. Sifa  hizi  ni  kama  utamaduni  mmoja,  utii  wa  kisiasa  au  dhamiri  zawazungumzaji (conscious of the speakers).

Kwa  mfano,  wazungumzaji  wa  Cantonese  (China  kusini  )  na  Mandarin  (  ChinaKaskazini)  hawaelewani  wanapozungumza  lakini  inachukuliwa  kuwa  wanatumialahaja tofauti za Kichina kwa sababu wote wanaishi Uchina (siasa) na wanashirikiutamaduni mmoja wa Kichina.  Pia wanatumia mfumo mmoja wa maandishi.

Aidha, wazungumzajiwa Swedish, Danish na Norwegian wanasikilizanawanapozungumza   lakini  kwa   sababu   wanaishi  katika   nchi   tofauti   na   wanatamaduni tofauti inachukuliwa kwamba wanazungumza lugha tofauti.

Hata pale ambapo sifa za kisiasa hazijitokezi sana, utamaduni pekee hupelekeawazungumzaji kufikiriwa kuwa wanazungumza lugha tofauti, kwa mfano, Wazuluna   Waxhosa   huelewana   wanapozungumza,   lakini   wanahisi  kwamba  wao  nitofauti  na  hata  wana  lugha  tofauti  kwa  sababu  wana  tamaduni  tofauti.  Mfano

43

Page 44: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

mwingine ni wa Wasuba na Waluo ambao wanaona kuwa wanazungumza lughatofauti.

Swali

1. Je, lugha yako ina lahaja ngapi?  Andika maneno yanayotofautishalahaja moja na nyingi.

2.   Kwa  kurejelea  nchiya   Kenya ,onyesha  zile lahaja ambazo  zinaonekanakuwaLugha tofauti ilhali  wazungmaji wanaelewana.

3.7 MTINDO-PEKEEWazungumzaji wote wa lugha fulani huelewana wanapozungumza, lakini hakunawatu wawili wanaozungumzakwa namna moja. Tofauti zinazotokeahusababishwa  na  umri,  uana,  afya  ya  mtu,  ukubwa,  hulka,  hali  ya  kimawazo,tajriba na ubinafsi wa mtu.   Tofauti hizi hujitokeza katika msamiati, matamshi nakwa kiasi kidogo katika sarufi.   Sifa ya namna ya uzungumzi unaohusishwa namtu binafsi huitwa   mtindo      pekee   .

Mtindo pekee ni matamshi ya kipekee ya msemaji au mzungumzaji yanayotokanana  athari  za mazingira.   Hii ina  maana kwamba  kuna  mfumo  fulani wa kiisimuunaohusishwa  na  kila mzungumzaji.   Jambo hili linadhihirika wazi pale ambapotunamtambua  mtu  kupitia  kwa  matamshi  au  sauti  yake  bila  kumwona. Kilamzunguzaji wa lugha ana mtindo wa kipekee wa lugha.   Mtindo pekee wa mtuhuweza kubadilika katika vipindi mbalimbali vya maisha yake.Zoezi

Pambanua tofauti za kiisimu zinazojitokeza miongoni mwa marafiki zako.

44

Page 45: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

3.8   MTINDODhana ya mtindo ni tatanishi kwa sababu kuna misimamo na mitazamo chungunzima inayotokana nayo.   Kwa mfano, dhana ya lafudhi inayomaanisha ubinafsikatika matumizi ya lugha, inayomtambulisha mtu kama   mtu,

yaelekeakupendekeza kuwa labda kuna mitindo mingi ya matumizi ya lugha kama kulivyona  watumizi  wengi  wa  lugha  husika. Kwa  hivyo  yaonekana  kwamba  kila  mtuulimwenguni ana mtindo wake.

3.8.1 Maana ya mtindo.Ili  kutoa maana ya dhana ya mtindo hebu tuangalie yale wanayosema Crystal naDavy   (1969)   katika         Investigating      English      Style      .Wamefafanua   mtindo   kwakutumia mitazamo ifuatayo.(i) Mtindo kama tabia za mtu katika matumizi ya lugha.(ii) Mtindo kama tabia za kimakundi katika matumizi ya lugha.(iii) Mtindo kama tabia za kitathmini yaani kiupimaji.(iv) Mtindo kulingana na lugha ya fasihi.Hebu basi tutoe maelezo ya kila moja.

(i) Mtindo kama tabia ya mtu.Kwa mujibu wa mtazamo huu, uchambuzi humulika na kuangalia tabia za kiisimuzinazoambatana  na  lugha  ya  mtu  katika  uyakinifu  wake. Neno   tabia   katikamuktadha huu linatumiwa kumaanisha kanuni za kiisimu zinazotambulisha lughaya mtu anayehusika.

Mtindo hutumiwa hapa kurejelea namna mtu anavyotumia lugha.  Jambo ambalolina upekee  fulani wa  kiisimu.   Huu  upekee ndio  unaotambulisha na kumsawiriyeye kama yeye.

Mtazamo huu ndio unaowaruhusu wachambuzi kuzungumza kuhusu mtindo wawaandishi au wasemaji mbalimbali (tazama Kitsao 1975).   Kwa mfano, unaweza

45

Page 46: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

kuzungumza kuhusu mtindo wa uandishi wa Shaaban Robert, Ebrahim Husseinau Said Ahmed Mohamed.

Buffun katika hotuba aliyoitoa mnamo Agosti 27, 1753, alisema kuwa   mtindo nimtu  mwenyewe ,  na  huu  umekuwa  msingi  wa  mtazamo  huu. Maoni  hayayanajadili kuwa kila mwandishi au msemaji ana lugha yake ambayo hudhihirikakatika  kazi  zake  zote  na  ambayo  humtofautisha  na  waandishi  au  wasemajiwengine.   Hivi ni kusema kwamba hulka ya mwandishi inatarajiwa kuonekana aukudhihirika kutokana na matumizi yake ya lugha.

Uchunguzi unaonyesha kuwa katika kujifunza lugha, kwa kawaida, watu hukuzana  kupalilia  tabia  fulani  za  kipekee  katika  matumizi yao ya  lugha.   Matokeo nitabia  za  kibinafsi  ambazo  hubainika  kwenye  mawasiliano  yake. Hivyo  basi,mtindo   unakuwa   matokeo   ya   moja   kwa   moja   ya   jinsi   mtu   anavyojielezakulingana na tajriba yake katika kujifunza lugha.

Zoezi

Pambanua tabia za kiisimu ambazo zinaibuka katika usemi wa rafikiyako.  Taja elementi tano za kiisimu kwa kila moja ambazo humtofautishana mtu  mwingine.

Kwa vile imetambuliwa kwamba kuna mitindo mingi kama kulivyo na waandishina  wasemaji,  uchambuzi  wa  mtindo  hauna  budi  kumshughulikia  kila  mtunzikivyake. Kwa  mfano,  tunaweza  kusema  kuwa  mwandishi  Shabaan  Robertanajulikana kwa matumizi ya sentensi ndefu hata zinazofikia maneno thelathini.Aidha anatumia uhuishi na jazanda katika kazi zake.

46

Page 47: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(ii) Mtindo kama tabia za kimakundi.Katika  upana  wake  dhana ya  mtindo  inaweza kurejelea tabia  za kundi la watukatika matumizi yao ya lugha. Mtazamo huu ndio mhimili wa misingi ya sajilikatika   matumizi   ya   lugha. Kwa   hivyo,   mtindo   wa   matumizi   ya   lughaunapokubalika  kimakundi  unakuwa  utaratibu  unaofaa  kuzingatiwa  katika  sajiliinayohusika.

Kwa  mfano,  kuna  kanuni  za  kuanzisha  na  kuhitimisha  ngano  katika  jamii  zaKiafrika:Msimulizi: PaukwaHadhira: PakawaMsimulizi: Kaondokea chanjagaa

Kajenga nyumba kakaaMwanangu mwana SitiKijino kama ChikichiCha Kujenga kikuta navilango vya kupitia.

Au:Msimulizi: Hadithi!  Hadithi!Hadhira: Hadithi njooMsimulizi: Hapo zamani za kale paliondokea ...

Pia  kuna  mtindo  wa  kuandika  mashairi  ya  kimapokeo. Mwandishi  anazingatiaidadi  ya  mizani  katika  mshororo,  vina,  idadi  ya  mishororo  katika  ubeti  nautoshelezi.  Katika uandishi wa tenzi mwandishi huanza kwa ombi na kadhalika.

47

Page 48: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Zoezi

Eleza mtindo unaodhihirika katika bara rasmi na fomu za serikali.

(iii) Mtindo Kiutathmini.Madhumuni  ya  kuwasiliana  huwekewa  vikwazo  au  mipaka  na  mtazamo  huuhupima   na   kutoa   masharti   kuhusu   namna   ya   kuwasilisha   wasilisho   fulani.Mtazamo huu unaongozwa na maoni kwamba kila mtindo unao maneno yafaayona mahali pafaapo kwenye muundo wa sentensi.   La muhimu hapa ni kwamba,ujumbe  utolewe kwa  njia ifaayo kabisa  kisarufi  na kimaana:  Hebu  tueleze kwakutoa mifano ya sentensi hizi:

1 (a)   Kwa sababu ya kuchelea kuwa huenda ng ombe wake akapotea tena,mchungaji  alimkamata  na kumfunga miguu  ya mbele na ya nyuma  kwakamba.

1 (b)   Kwa sababu ya kuchelea kuwa huenda ng ombe wake akapotea tena,mchungaji alimkamata na kumfunga kwa kamba miguu yake ya mbele naya nyuma.

Katika sentensi hizi mbili tunaona kuwa mpangilio wa maneno ni tofauti.

Zoezi

Eleza tofauti za kimaana zinazotokea katika mifano ya sentensi hapo juu

48

Page 49: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Wakati  mwingine,  tatizo  huwa  kubwa  zaidi  kiasi  cha  kuhitaji  sio  tu  manenokupangwa upya bali pia kurekebishwa au kubadilishwa kwa viwakifishi.

Wataalamu wamefafanua mtazamo huu kwa kutilia mkazo kwamba mtindo mzurihutokana na kuchagua taashira zifaazo kwa wasilisho linalonuiwa kuwasilishwa.

Kwa  ufupi,  uchambuzi  wa  mtindo  kulingana  na  mtazamo  unaohusika  hapa  nikukadiria namna mwasilishi alivyofaulu katika wasilisho lake, kulingana na uteuzikimsamiati na kisarufi.

(iv) Mtindo kulingan na lugha ya Fasihi.Kwa mujibu wa mtazamo huu mtindo ni utunzi wa fasihi ya hali ya juu kabisa.Hata   hivyo   tunaona   kuwa   maelezo   haya   yanatatiza   kimaana   kwa   sababuhayazingatii kikamilifu mahusiko ya dhana ya mtindo yenyewe.   Vile vile, maonihaya yanalifinya swala hili la mtindo.   Inaonekana kuwa maoni haya yanalengaumbuji  au  ubunifu  wa  kurejelea  mbinu  za  kujieleza  kama  vile  matumizi  yatamathali za usemi.   Lakini mtindo, tunajua ni zaidi ya mbinu hizi.  Mtindo sio tujinsi waandishi wanavyoandika lakini pia ni njia mbalimbali zinazotumiwa na watukuongea au kuandika katika hali za kawaida za kila siku.   Kwa hivyo, mtindo nijumla ya namna lugha inavyotumiwa na wanajamii.

Swali

Onyesha tofauti zilizopo kati ya:1.  Mtindo kama tabia za mtu na mtindo kama tabia za kimakundi.

49

Page 50: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

3.9  SAJILIKulingana  na      Kamusi      Sanifu      ya      Isimu      na      Lugha     (1990)  sajili,  ambayo  piainajulikana kama rejista ni lugha inayotumika katika muktadha maalumu.   Sajilihuelekea   katika   kupambanua   lugha   ifaayo   katika   miktadha   fulani. Sajilihutofautiana kutegemea mambo kama vile, miundo ya lugha, msamiati, uundajiwa sentensi, kupanda na kushuka kwa sauti na unyambuaji.

Sajili ni sehemu ya umilisi wa mawasiliano ambao kila mzungumzaji huwa nao.Umilisi huu humwezesha kubadili matumizi ya lugha, kuteua vipengele fulani vyamatamshi, msamiati na kadhalika katika miktadha mbalimbali.

Akishughulikia  swala  la  sajili,  Halliday  (1964)  alisema  kuwa  sajili  hutofautianakutokana na :(a) Mada inayozungumzwa.(b) Uhusiano  kati  ya  watu  wanaowasiliana. Kwa  mfano, nani  anashiriki

katika mazungumzo?   Ni mtu na mkubwa wake, au ni mtoto na mzazi auni rafiki tu?

(c) Njia ya  mawasiliano ambayo  inatumiwa  ikiwa ni andishi  au zungumzi auishara?

3.9.1 CHANZO CHA SAJILI.Inawezekana  kwamba  matumizi  ya  sajili  mbalimbali  yameibuka  kutokana  namikatale ya kijamii.   Watu wana miiko mbalimbali inayohusu matumizi ya lugha,kwa mfano, ukitumia lugha inayoambatana na mazingira kama vile inayoonyeshafuraha  mazikoni  basi  huenda  ukaathiriwa.   Kwa  hivyo,  lugha  imegawika  katikasajili mbalimbali kutokana na imani za watu na pia kukidhi mahitaji ya muktadha.Mfano  mwingine  ni  kwamba  baadhi  ya  jamii  huamini  kwamba  lazima  nganozihadithiwe mahali maalumu, wakati maalum na sharti ziambatane na matumizimaalumu ya lugha.

50

Page 51: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Pili,  tunaweza  kutuhumu  kuwa  sajili  inatokana  na  kugawika  kwa  jamii  katikamakundi   ya   kazi   mbalimbali   ili   kujikimu. Kila   kundi   likiwa   na   msamiatiunaoelezea hali, mazingira na zana zake za kazi.

Msamiati  huu,  na  upekee  wa  uzungumzaji  ulizua  sajili  mbalimbali. Tunawezakuhusisha  jambo  hili  na  ukuaji  wa  binadamu  kimaendeleo. Jinsi  binadamualivyoendelea  ndivyo  kazi  mbalimbali  zilivyojitokeza  na  hivyo  kukawa  na  lughamaalum  ya  kuelezea hali hizo.   Kwa mfano,  maendeleo upande  wa sayansi nateknolojia yamezua sajili ya kisayansi na kiteknolojia.

3.9.2  MIFANO YA SAJILI NA SIFA ZAKE ZA KIISIMU1. Matangazo ya biashara:

Sifa zake1. Lugha ya mvuto.2. Lugha ya kimajazi.3. Lugha shawishi au msukumo (kutaka mtu awe mteja wao).4. Misemo maalumu inayonasa.5. Wingi wa porojo.6. Kuchanganya lugha.7. Uradidi wa sauti au maneno.

2.  Matangazo ya mpira1. Lugha changamfu 7. Matumizi ya kidato cha juu2. Lugha ya kutia chumvi. 8. Maswali ya balagha.3. Lugha batebate. 9. Mbinu rejeshi.4. Lugha hugeuka kuwa kelele. 10. Msisitizo.5. Kuchanganya lugha. 11. Kutokamilika kwa sentensi.6. Uundaji wa msamiati.

51

Page 52: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(Kwa ufafanuzi zaidi wa aina a sajili,rejelea mtaala wa AKS 101)Zoezi

Taja sifa za sajili zifuatazo:i.  Sajili ya kidini.ii.  Sajili ya sheria-(andishi).

3.9.4MASHARTI YA MATUMIZICrystal  na  Davy  (1969) pamoja  na  Kitsao  (1988) wameshughulikia masharti yamatumizi   ya   lugha. Haya   ni   mambo   yanayomwongoza   mzungumzaji   aumwandishi  ili  kuteua  sajili  inayofaa  katika  mawasiliano  yake. Crystal  na  Davy(ibid)  wameyaita   mawanda  ya  matumizi  kimuktadha   na  wamejadili vipengelevinane.1. Ubinafsi2. Lahaja.3. Wakati.4. Kazi.5. Hadhi.6. Namna ya kuwasilisha.7. Upekee.8. Aina ya mazungumzo

Kitsao (1988) kwa upande wake amejadili masharti kama:1. Mazingira.2. Uhusiano.3. Cheo.4. Hali.5. Madhumuni.6. Kichwa cha mazungumzo.

52

Page 53: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

7. Lugha azijuazo mtu.8. Tabaka na malezi.9. Umri.

Hebu tutoe maelezo kwa masharti anayotoa Kitsao(ibid)

(i) MazingiraKulingana  na  lugha katika  mazingira, itaonekana, kwa  mfano, kuwa  matanganikutakuwa   na   matumizi   ya   lugha   ya   huzuni,   kupeana   mkono   wa   pole   nakuliwazana. Pia mtu  akiwa  ofisini  analazimika  kutumia  lugha  rasmi  lakiniakiingia mitaani miongoni mwa watani atazungumza lugha isiyo rasmi.

(ii) UhusianoUhusiano wa watu  katika jamii husababisha lugha kutumiwa kwa mtindo fulaniufaao.  Kati ya mzazi na mwanawe kuna miiko inayowataka wawasiliane kwa njiaya  heshima. Mathalani,  si  kawaida  mzazi  na  mwanawe  kutaniana  au  mwanakumwita  babake  kwa  jina  lake katika  jamii za   Kiafrika.   Lakini  watani wa mtuhuwa na uhuru mkubwa katika matumizi ya lugha miongoni mwao.

(iii) CheoCheo ni muhimu katika matumizi ya lugha kwani kuna lugha anayostahili kutumiaProfesa, kuna lugha ya wazee, lugha ya vijana na kadhalika.   Ndiposa tunawezakusikia lawama kuwa ijapokuwa fulani ana cheo hazungumzi kulingana na cheochake.

(iv) HaliNi kweli kwamba lugha ya mtu hubadilika au kuathirika kulingana na hali ya mtuhuyo.   Mtu  anapokuwa mgonjwa hutumia lugha ya kuvuta huruma.   Lugha yamlevi  huwa  legevu  na  ovyo. Mtu  anapokasirishwa  hutumia  lugha  kali  na  yakutisha.

53

Page 54: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(v)MadhumuniLugha inaweza kutumiwa kulingana na madhumuni au msimamo wa mtu katikajambo fulani.   Inawezekana kuwa madhumuni ni kuvutia au kuteka watu kiakiliambapo mwongezi atatumia lugha nyenyekevu na ya ushawishi mkubwa.  Lughayaweza   kutumiwa   kwa   lengo   la   kuchukiza,   kuchekesha,   kuamrisha   kupigavijembe na kadhalika.

(vi) Kichwa cha MazungumzoSajili mbalimbali zitafaa kwa vichwa tofauti vya mijadala.  Kwa mfano, ikiwa watuwanazungumza juu ya mambo ya kisheria itabidi warejelee sajili ya kisheria kwakutumia  istilahi  zifaazo  kama  hakimu,  mshtakiwa,  wakili  na  kadhalika. Katikamazungumzo  kama  haya  haitakuwa  muhali  kuingiza  sajili  ya  matangazo  yampira.  Maoni yetu ni kwamba vichwa mbalimbali vya mada ndio msingi wa sajili.

(vii)Lugha azijuazo MtuSharti hili ndilo msingi wa kubadili msimbo.   Mtu   asiyejua Kiingereza hataingizalugha  hiyo  kwenye  matumizi  yake  ya  lugha. Lakini  yule  anayefahamu  lughanyingine anaweza kuzitumia lugha hizo zote kwa pamoja.

(viii) Tabaka na MaleziTabaka na malezi tofautitofauti hukuza viwango mbalimbali vya ujuzi wa lugha.Jinsi mtu anavyowezeshakutalii na kumudu lugha kikamilifu ndivyoatakavyoweza  kuitumia  kwa  ukwasi  na  ufasaha  zaidi. Mtu  mwenye  malezimazuri huchuja lugha yake lakini mwenye malezi mabaya hutumia lugha yenyematusi.

(iX) UmriInaonekana  kuwa  lugha  miongoni  mwa  jamii  hukua  na  kukomaa  kulingana  najinsi mtu anavyokua kutoka utotoni hadi uzeeni.   Kwa hivyo, mtoto anapotumia

54

Page 55: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

lugha  isiyokuwa  na  ustaarabu  kama Naenda  kukojoa ,  kijana  wa  makamoatatumia  lugha  yenye  heshima kidogo  kwa kusema   Naenda haja ndogo   ilhalimzee atatumia lugha fiche kama vile  Naenda kutema mate .

Bila shaka kunayo masharti mengi sana yanayosimamia matumizi ya lugha lakinihayo machache yanatosha.

Zoezi

Eleza kwa kutoa mifano, jinsi kila moja ya masharti hayoyanavyoweza kuathiri lugha  anayotumia mtu.

3.10   JUMUIA LUGHAKimsingi, wana-elimujamii huchunguza jamii kwa kuzingatia kategoria kama vilematabaka, ukoo, usehemu na uchumi.

Dhana ya  Jumuia  ni neno linalorejelea ile hali ya kundi la watu kufahamu jambofulani  kwa  pamoja,  au  wana  umiliki  sawa  wa  tabia  zinazofanana. Wanaisimuhuhusisha  dhana  hii  ya   Jumuia   na  swala  la  lugha,  ndipo  tunapata  dhana  yaJumuiya lugha.

Kulingana na TUKI (1990) jumuia lugha ni kundi la watu wanaokaa katika eneomoja na kutumia namna moja ya lugha.

Kimsingi dhana hii inasisitiza kwamba tabia au matendo ya lugha yanaweza kuwakitu ambacho kinaunganisha kundi fulani la watu.   Hata hivyo, kumekuwepo nautata  mwingi  juu  ya  maana  halisi  ya  dhana  hii. Jambo  hili  linadhihirika  wazikutokana na jinsi wataalamu mbalimbali walivyoifasiri.

55

Page 56: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Yule (1996) anasema kuwa jumuia lugha ni kikundi cha watu ambao wana kaida,sheria na matarajio ya pamoja kuhusiana na matumizi ya lugha.

Lyons (1970) anasema kuwa, jumuia lugha ni jumuia ya watu wanaotumia lughamoja (au lahaja moja).

Kutokana na maelezo haya, jumuia lugha zinaweza kuingiliana (kwa mfano, palekuna  watu  ambao  wanaongea  lugha  zaidi  ya  moja)  na  watu  hawa  hawahitajikuwa  na umoja wowote wa kijamii au kitamaduni.   Ukweli ni kwamba ni rahisikutenga jumuia lugha kwa njia hii, kwa sababu tunaweza kuzitenganisha lughana lahaja.

Hocket  (1968), Bloomfield  (1933) na Gumperz  (1962) wanakubaliana kuwa kilalugha   huifasiri   jumuia   lugha   na   kwamba   jumuia   lugha   ni   kundi   la   watuwanowasiliana ama moja kwa moja au kwa njia nyingine kupitia kwa lugha moja.

Katika  fasiri  hii,  tunaona  kuwa  kigezo  cha  muingiliano  wa  mara  kwa  marakinajitokeza. Hii  inaweza  kuchukuliwa  kuwa,  ikiwa  jamii  mbili  zinazozungumzalugha moja lakini hazina utagusano basi zitachukuliwa kuwa jumuia lugha tofauti.Fasiri hii imeondoa msisitizo wa lugha ya pamoja na kuzingatia mawasiliano.

Nao   Hymes   (1972)   na   Halliday   (1978)   wanasema   kuwa,   tunapozungumziajumuia lugha ni muhimu kuzingatia sheria za pamoja za uzungumzaji na ufasiriwa matendo ya uzungumzaji.  Katika fasiri hii, tunaona kuwa msisitizo unawekwakwa  jumuia  lugha  kama  ni  kikundi  cha  watu  ambao  wanahisi  kuwa  wao  nijumuia.

Naye Labov (1972) anatilia mkazo mielekeo ya watu kwa lugha na thamani zaokuhusu miundo ya lugha na matumizi.

56

Page 57: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Fasiri hizi zote ni sahihi kwa sababu zinaeleza jumuia lugha ni nini.  Kutokana nafasiri hizi basi tunapata sifa zifuatazo za jumuia lugha:1) Ni kundi la watu.2) Watu wanaowasiliana kwa lugha moja.3) Wanaweza kuwa wanaishi eneo moja au maeneo tofauti.4) Kuna mtagusano au kuingiliana kwa watu hawa mara kwa mara.5) Ni watu walio na mielekeo sawa kuhusu lugha.6) Ni watu walio na utamaduni sawa.

SwaliJe, unaweza kusema kuwa Kenya ni Jumuia-lugha moja?  Toa sababuza kukubali au kupinga taarifa hii.

HITIMISHO

Maswala kadha wa kadha ya lugha yameshughulikiwa katika somo hili.Tulianza kwa kueleza maana ya lugha pamoja na matumizi yake.  Kishatuliona  kuwa  lugha  huweza  kujitenga  katika  makundi  mbalimbali  ambayoyanajulikana  kama  lahaja.Tuliona  jinsi  lahaja  inavyozuka,  na  tukarejeleanadharia  ya   mawimbi  kutilia   msingi   hoja   hii. Vile  vile  tuliona   jinsi  mtuanavyoweza kutambua lahaja na lugha.  Swala la mtindo pekee kamaishara ya tabia za kiisimu za mtu fulani limejadiliwa.  Isitoshe, swala lamtindo na sajili vimeshughulikiwa kwa kuchunguza jinsi lugha inavyotumiwana vikwazo vinavyosimamia matumizi ya lugha. Na mwisho, dhana yajumuiya-lugha imeelezwa.

57

Page 58: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Marejeleo Teule1.   Chacha, L.M. na wengine (2003)  AKS 100:   Introduction      to      the      Study      of      

Language:   Kiswahili   Module .   Nairobi.   Institute of Open Learning,Kenyatta University.

2. Chambers, J.k. & Trudgill P. (1980)   Dialectology   .  Cambridge.  CambridgeUniversity Press.

3.  Crystal, D. and Davy, D. (1969)   Investigating      English      Style   .  New York:Longman.

4.   Fromkin, V. &  Rodman, R. (1988)   An      Introduction      to      Language   ,   New YorkHarvourt Brace.  Jovanivich College Publishers.5.  Halliday, M.A.K. et.al. (1964)   The      Linguistic      Science      and      Language      Teaching   .

London.  Longman.6.  Kitsao, J. (1975)  A Stylistic Approach Adopted for the Study of Kiswahili

Prose Texts .  M.A. Thesis: Nairobi University.  (haijachapishwa).7.  Lyons, J.L. (ed.) (1970)   New      Horizons      in      Linguistics   .  Penguin Book.8.  Mdee, J.S. (1986)   Kiswahili:      Muundo      na      Matumizi      Yake   . Nairobi,

Intercontinental Publishers Ltd.9. Musau, P.M. (1990)   Swahili      Part      Three:      Kiswahili      in      the      Twentieth      Century   .

Nairobi: University of Nairobi.10. Onyango, J.O. (2002)   AKS      102:      Historical      Development      of      Kiswahili:      Kiswahili   

Module.  Nairobi.  Institute of Open Learning, Kenyatta University.11.  Ryanga, S. na Mukobwa, M. (2003) AKS 101:         Language      Skills      in      Kiswahili1      :  

Kiswahili   Module :  Nairobi  Institute  of  Open  Learning,  KenyattaUniversity.

12.  TUKI (1990)   Kamusi      Sanifu      ya      Lugha      na      Isimu   .  Dar es Salaam, Universityof  Dar es Salaam.

13.  Wardhaugh, R. (1987)   Languages      in      Competition   , Oxford, Basil BlackwellCo.

58

Page 59: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA NNE

LUGHA ZA MAWASILIANO PANA

4.0 UTANGULIZIKatika  somo  hili,  tutashughulikia  lugha  za  mawasiliano  pana.Hizi  ni  lughaambazo  zinavuka  mipaka  ya  jamii  moja.  Tutajadili  hizo  pamoja  na  dhana  zalingua franka, Pijini na Kirioli.

4.1 Madhumuni

Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1.  Kueleza maana ya lingua franka.2.  Kueleza maana ya Pijini na Kirioli na kuonyesha kuibuka kwa lugha hizi.

4. 2  Lingua FrankaLingua franka ni lugha inayotumiwa kama chombo cha mawasiliano kati ya watuambao hawana lugha moja asilia wanayofahamu wote.  Hii ni lugha inayotumiwana  watu  wote  katika  eneo  kubwa  hata  kama  wana  lugha  zao  nyingine. Kwamfano, Kiingereza ni   lingua      franka    ya ulimwengu wote.   Wakati fulani Kifaransakilikuwa lingua franka ya itifaki (diplomacy) na kilatini kilikuwa pia lingua frankaya dini ya Ukristo.

Baadhi   ya   lugha   zinazotumiwa   kwa  maana   hii,   kwa   mfano,   Kiingereza   naKifaransa  si  za  kiasili  bali  huwa  zimefahamika  kupitia  kwa  elimu  ya  shuleni  auelimu  rasmi. Hata  hivyo,  lingua  franka  nyingine  barani  huwa  za  kiasilia  nahupata  jukumu  hilo  kutokana  na  kabila  linalohusika  kuwa  na  nguvu  za  kisiasakama vile Luganda; au kwa kuwa wafanyibiashara mashuhuri kama vile Kiswahili.

59

Page 60: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kihausa ni lingua franka ya Afrika Magharibi kwa sababu ya nafasi yake katikabiashara.Kiyunani  kilikuwa  lingua  franka  hapo  zamani  hasa  kwa  sababu  ya  vita  vyaAlexander the Great .

Kilatini  vile  vile  kilikuwa  lingua  franka  katika nchi  za magharibi kwa  sababu  yaupanuzi wa utawala wa Roma.

Lugha  ya  Kiswahili  inaweza  kudai  kuwa  lingua  franka  ya  sehemu  za  AfrikaMashariki na kati.   Jambo hili ni wazi hasa tukizingatia lugha mbalimbali ambazozinatumika katika sehemu hii.   Kando na hayo, Kiswahili bado kimebakia imarahata  katika  hali  ya  ushindani  kutoka  kwa  lugha  mbili  zilizo  na  nguvu  yaaniKiingereza   na   Kifaransa. Kiswahili   kimeweza   kuendelea   sana   hata   katikamazingira  hatari,  hasa  kuanzia  kipindi  cha  kwanza  cha  karne  ya  18  na  karneiliyopita. Ni  lugha  ambayo  inatumiwa  sana  katika  sehemu  nyingi  za  AfrikaMashariki na Kati.

Baadhi  ya  lingua  franka  nyingine  katika  bara  la  Afrika  ni  Bambara  na  Wolof,ambazo zote zinapatikana Afrika Magharibi, (Chimera 2000).

Swali

Kiswahili sio lugha ya Afrika Mashariki tu, bali ni lugha ya Kimataifa.Fafanua kauli hii.

4.3  PIJINI NA KIRIOLIUtafiti katika lugha za kipijini na kikirioli unakisiwa ulianza mnamo mwishoni mwakarne ya 19 na mwansaisimu-jamii, Hugo Schuchardt, Swale

(1997).

60

Page 61: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Yasemekana kuwa alichapisha mfululizo wa vitabu vilivyojulikanakamaKroelische   Studien  katika miaka ya 1880.Hata hivyo,  somo  hili  lilipuuzwa. Lakini  baada  ya  kupuuzwa,  utafiti  katikanyanja  ya  pijini  na  kirioli ulianz  hasa  mwanzo  mwanzoni  mwa  karne  ya  20.Kufikia mwaka 1945 ndipo wanaisimu walipojitosa tena katika utafiti wake.  Tafitichache zilifanywa katika kipindi cha vita vikuu vya kwanza na vya pili.  Baadhi yawanaisimu wa mwanzo kutafitia pijini na kirioli ni pamoja na Jacobs (1932), Boas(1933), Reinecke na Tokimasa (1934), Hall (1948, 1953) na Turner (1949).

4.3.1 SIFA BAINIFU ZA PIJINIWanaisimu-jamii  wengi  wameafikiana  kuwa,  lugha  za  kipijini  na  krioli  ziliibukakatika miktadha ya kibiashara na katika zama za biashara ya utumwa.  Lugha hiziziliibuka ili kuwawezesha watu walioongea lugha tofauti tofauti kuwasiliana kwadhamira fulani fulani.  Kama asemavyo David Decamp (1975:15),

Pijini ni lugha ya mawasiliano na ambayo kwa hali za kawaida,si lugha asilia ya watumizi wake.

Pijini   nayo,   huwa   krioli   pale   inapopata   waongeaji   wazaliwa,   yaani   pijiniinapokuwa  ni  lugha  ya  kwanza  ya  mtu. Muhlhauster  (1986:1)  anasema  yakwamba, dhana ya pijini huenda ilitokana na hali au miktadha ifuatayo:(i) Kutokana   na   matamshi   ya   jamii  ya   Wachina   ya   neno   la   Kiingereza

business .(ii) Kutokana na neno la Kiyahudi   pidjom .(iii) Kutokana na neno  Pidian  la Wahindi wekundu  wa Amerika Kusini; na(iv) Kutokana  na  matamshi  ya  jamii  ya  watu wa  Bahari  za  Kusini  ya  neno

beach .

Tunaporejelea  asili  na  miktadha  mbalimbali  hapo  juu,  inatubainikia  wazi  kuwalugha   za   kipijini   ziliibuka   miongoni   mwa   jamii   za   watu   walioongea   lugha

61

Page 62: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

tofautitofauti kwa minajili ya kufaulisha mawasiliano baina yao (Tazama Chachana wengine katika AKS 100: Introduction to the Study of Language).

Mwanaisimu-jamii Loreto Todd (1990) anapambanua na kutofautisha pijini-finyuna pijini-pana.

(i) Pijini-finyuPijini-finyu  huibuka  katika  muktadha wa  dharura  sana  kati  ya  jamii  za  watuwanaoongea lugha tofauti.   Pijini zinazoibuka katika miktadha ya aina hii, huwana sifa bainifu zifuatazo:(a) Huwa na miundo sahili hasa ya kisintaksia na aghalabu, huhusisha kauli

za  kuamrisha  na  huambatisha  ishara  za kimwili kama za mikono, machona  viungo  vingine  vya  mwili. Kwa  mfano,  pijini  za  Afrika  Magharibizilizoibuka  kipindi  cha  vita  vikuu  kati  ya  askari  jeshi  Waingereza nawenyeji wa eneo hilo.

(b) Idadi kubwa ya msamiati hutokana na lugha ya tabaka la juu au tawala,na  kutiwa  kwenye  mfumo  wa  matamshi  ya  lugha  ya  wenyeji. Toddanadai kuwa  Kisetla  kilichotumika nchini Kenya kati ya masetla wazunguna   Waafrika   ni   mfano   mwafaka.Hili   ni   jambo   ambalo   wanaisimuwanaweza kulitafitia ili kulithibitisha.

(c) Aghalabu  pijini  finyu  huhusisha  lugha  mbili  tu na  uhusiano  kati  yazounapokatishwa  basi  pijini  ile  hufa.   Miktadha yake aghalabu  huwa ni yadharura za kimawasiliano kama vile katika shughuli za biashara, shughuliza kijeshi na hii leo, katika shughuli za sekta ya utalii.

(ii) Pijini – PanaSifa za pijini-pana ni  kamai zifuatazo:(a) Huibuka kutokana na kudumishwa kwa mazingira ya pijini finyu.

62

Page 63: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(b) Maneno   ya   pijini   finyu   yanapopanuka   huwa   ni   lugha   ambayo   badohaijakuwa  thabiti  kimuundo,  kimsamiati  na  kadhalika  bali  ni  matumizi  yakeyanayopanuka.(c) Inapoimarika  na  kupata  waongeaji  wazaliwa,  basi  huwa  ni  kirioli  na

hatimaye  inaweza  ikawa  lingua  franka  (lugha  sambazi) ya eneo fulani lakijiografia.

4.3.2   Dhana ya KirioliBickerton (1971) anasema kuwa, lugha za kikirioli zinaweza kuibuka kutokana namiktadha au mazingira yafuatayo:(a) Pijini zilizopata wazungumzaji wazaliwa.(b) Katika  jamii  ambamo  asilimia  ishirini  (20%)  ya  waongeaji  ni  wenyeji  na

asilimia themanini (80%) ni  ya matumizi ya lugha zingine za kigeni.(c) Krioli   huwa   na   miundo   iliyoimarika   ya   kisarufi   msamiati   mpana   na

kadhalika na hazitumii ishara (kwa wingi) wala uigizaji ili kufafanua maanakama ilivyo  pijini.

Sifa  hizi  zinazifanya  krioli  kuwa  na  hadhi  ya  lugha  kama  lugha  zingine  asilia(zisizoibuka   katika   mazingira   tuliyotaja)   na   hutumika   rasmi   katika   elimu,biashara,  kuandika  fasihi  na  hata huweza kuwa  lingua  franka.   Mfano  wa nchizinazotumia kirioli ni Sierra Leone, Liberia, Gambia, Hawii, na Mauritius.

Wanaisimu-jamii  wengi  wanasema  kuwa  dhana  za  kipijini   na  kikrioli  ni  mfanobora  wa  jinsi  binadamu  wote,  wanavyoweza  kuutumia  uwezo  wao  jumuishikatika mazingira tofautitofauti.

Majedwali haya yanaeleza kwa muhtasari jinsi kirioli inavyoibuka.

63

Page 64: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

1. Lugha za wazazi (Pijini)

Uwezo jumuishi

Lugha ya watoto (Kirioli)

2.Pijini ya mama Pijini ya babaLugha finyu Lugha finyu

Mazingira

Kirioli (lugha ya watoto)

3. Pijini finyu 4 Pijini finyu

Kirioli Pijini Thabiti(krioli ya Hawaii)

Kirioli(Krioli ya Kiingereza ya

Torress Straits)

5 Pijini   finyu

Pijini   Thabiti

Pijini  Pana Thabiti

64

Page 65: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kirioli (Tok Pisini ya Papua New Guinea)

Kutokana  na  majedwali  haya,  inatudhihirikia  kwamba,  ili  lugha  yoyote  ya  pili(kama  Pijini)  iwe  lugha  asili  (ya  mama)  au  kirioli,  itabidi  ifanyiwe  marekebishofulani   fulani   na   watumizi  wake.Marekebisho   yenyewe  yatahusu   kuondoaupungufu wowote   uliomo   katika   viwango   vyote   vya   kiisimufonolojia,mofolojia,  sintaksia  na  msamiati. Hapo  ndipo  lugha  hiyo  (kirioli)  itakapowezakuwa  chombo  kiaminifu  na  kinachosadifu  mawasiliano  ya  jamii  husika  katikangazi mbalimbali.

4.4   NADHARIA ZA ASILI YA PIJININadharia kadhaa zimependekezwa kuelezea asili ya pijini:1. Nadharia mahsusi za lugha.

(a) Nadharia ya lugha ya kibaharia (nautical jargon)(b)   Nadharia ya lugha ya kitoto (baby talk)

2. Nadharia za kijumla.(c) Nadharia ya uundaji upya leksimu (relexification)(d)   Nadharia jumlishi (universalist)

3. Nadharia zinazozingatia tofauti.(e) Nadharia zenye kiini kimoja (common-core)(f) Nadharia zenye safu msingi (substratum)

Hebu tuzifafanue nadharia hizi.4.4.1  Lugha ya Kitoto.Hii   ni   nadharia   inayoshikilia   kwamba   pijini   zilizuka   kutokana   na   kuiga   nakurahisisha lugha aliyoisikia mtu.   Hii   ina maana kwamba, mtu anajifunza lughalakini hajifunzi lugha hiyo vyema.  Kuna hata wataalamu, kama Hesseling (1933),wanaodai kuwa pijini zilizuka kutokana na ujifunzaji makosa wa lugha uliofanywana watumwa.

65

Page 66: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Bloomfield   (1933)   anaeleza   kuwa   pijini  ilizuka  pale ambapo watu  walijaribukuiga  jinsi  wenzao  wasioifahamu  lugha  vizuri  wanvyozungumza. Kwa  mfano,mwajiri  (Bwana)  anapozungumza  na  mtwana  anairahisisha  ile  lugha  yake  nakuiga  lugha  mbovu  ya  mtwana  yule  ili  waelewane. Vivyo  hivyo,  mtu  mzimaanapozungumza  na  mtoto  ambaye  bado  hajaimudu  lugha  vizuri  anairahisishalugha  yake  ili  ilingane  na  ile  ya  mtoto. Basi  mtwana  anaposikia  jinsi  mwajiriwake anavyozungumza anakosa kielelezo cha kuiga na anaiga lugha mbovu.

Nadharia   hii basi inazo harakati mbili.   Moja huanzishwa na wazungumzaji walugha yenye hadhi ya juu ambao hurahisisha lugha yao.   Ya pili, huanzishwa nawazungumzaji wa lugha ya hadhi ya chini ambao hurahisisha lugha wanayoisikiapale wanapojaribu kujifunza lugha hiyo.  Katika hali ya kwanza, kikundi cha hadhiya chini kinaiga kinachosikia kutoka kwa kundi lenye hadhi ya juu.  Katika hali yapili, kundi lenye hadhi ya chini ndilo huongoza katika kufanya makosa, na lile lahadhi ya juu linaimarisha tu makosa hayo.

4.4.2. Lugha ya Kibaharia (Nautical jrgon theory)Kwa   mujibu   wa   nadharia   hii   meli   zilizoabiri   bahari   zilikuwa   na   mabahariawaliozungumza lugha na lahaja tofauti.   Kwa hivyo ilibidi kuwepo na lugha mojailiyoeleweka   na   mabaharia   wote. Lugha   hii   iliyotumiwa   na   mabahariaikafahamika  na  Waafrika,  Wazungu  na  Wahindi  waliofanya  kazi  ya  ubaharia.Yamkini msamiati wa kibaharia ulikuwa kiini cha lugha hii, na lugha hii ilipanuliwakwa nyongeza kutoka kwa lugha za asili za mabaharia.  Hii ndiyo sababu pijini nakrioli katika maeneo fulani ulimwenguni zitafanana, lakini zitofautiane na zile zamaeneo mengine.

Nadharia   hii   inapata   msukumo   kutokana   na   utafiti   wa   Todd   (1990:33)anayesema   kuwa   kuanzia  karne   ya   17  mabaharia   walikuwa   na  lugha  yaomahsusi. Pia  kuna  msamiati  wa  kibaharia  katika  pijini  nyingi  duniani. KatikaCameroon pidgin tunapata maneno kama:

66

Page 67: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Hib < heave sukumaKapsal < capsize pindukaManawa < man of war   mtu wa vita

Reinecke  (1937) alifanya  utafiti na  akakuta  kwamba  mabaharia waliozungumzalugha tofauti katika meli moja waliunda msamiati mpya wanaoufahamu wote wamaneno 300 katika kipindi cha miezi michache.

Ingawa tunakiri kwamba mabaharia walisambaza msamiati   wa kibaharia katikapijini mbalimbali ulimwenguni, nadharia hii haielezi kwa nini pijini zenye misingiya Kiingereza, Kifaransa, Kireno, na Kihispaniola zinafanana.

4.4.3.Asili moja (Monogenesis Theory)Usuli wa nadharia hii ya asili moja ni kwamba pijini zote zinahusiana kinasaba nazimetoka kwa proto-pijini au pijini-mame moja.   Kwa hivyo, kule kufanana kwapijini  kunaelezwa  kuwa  kunatokana  na  jadi  moja  (common  ancestor)  hapozamani.

Inafikiriwa kwamba hii proto-pijini inayozungumziwa katika nadharia hii ni pijiniya Kireno ambayo labda ilikuwa ni mabaki ya lugha ya Sabir.  Sabir ilikuwa linguafranka ya zamani iliyotumiwa na wapiganaji wa Kikristo (crusaders) na pia kamalugha ya kibiashara ya eneo la Mediterranean.

Nadharia hii inafafanua kwamba tofauti zinazopatikana katika pijini mbalimbali nimatokeo   ya   kubadilisha   msamiati  kunakoendelea.Kulingana   na  nadharia  hii,kipijini  cha  Kireno  ndicho  kilikuwa  msingi  wa  pijini  nyingine  ambazo  ziliundwabaadaye,  lakini  pijini  hizi  zilibadilisha  msamiati  wa  pijini  msingi  na  kutumiamsamiati   kutoka   kwa   lugha   nyingine   huku   zikihifadhi   msingi   wa   kisarufiunaofanana.

67

Page 68: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Njia  hii  ya  kubadilisha  msamiati  wa  lugha  fulani  huku  ukihifadhi  muundo  wakisintaksia inajulikana kama uundaji upya wa leksimu (relexification).

Kwa hivyo nadharia hii inadai kuwa pijini na kirioli za Ulaya ni vibadala vya pijiniya  Kireno  ya  Karne  ya  15  vilivyoundiwa  msamiati  mpya. Pijini  hii  mwanzoilitumiwa katika upwa   wa Afrika na baadaye ikafika India na nchi nyinginezo zaMashariki  ya  Mbali  (Far  East). Kwa  njia  hii,  pijini  zote  za  Ulaya  zinahusianakupitia  kwa mchakato wa kudumisha sarufi na kubadili msamiati.

4.4.4 Maendeleo Sambamba (Independent Parallel).Msingi  wa  nadharia  hii  ni kwamba pijini na  krioli zilizuka  kila moja  kivyake  na

zikaendelea   kukua   sambamba   kwa   sababu   zilitumia   malighafi   ya   kiisimuiliyofanana na zilikulia katika mazingira yaliyofanana.

Kwanza,  lugha  kuu  za  wazungu  hazikuwa  tofauti  kimuundo. Vile  vile  lughanyingi za waafrika (watumwa) zilitokana na kikundi kimoja cha familia ya lughaambazo wanaisimu huzibainisha kama  Lugha za Afrika Magharibi.

Hall (1961) alieleza kuwa ingawa lugha hizi zilizuka kila moja kivyake kulikuwepona maeneo machache ya mwingiliano kama inavyoonyeshwa hapa chini.

English Melanesian(French n.k) (Chinese,

African n.k.)

4.4.5 Lugha ya hadhi ya chini (Substratum theory)Mahlhausler  (1986:119)  anatoa  wazo  kwamba pijini huunganisha msamiati   walugha  yenye  hadhi  ya  juu  (superstratum)  na  sarufi ya lugha  ya hadhi  ya chini(substratum).  Hii ina maana kwamba pijini  ni lugha ya mseto.

68

Page 69: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Naye Romaine (1988:102) anadai kuwa sura mbalimbali za kifonolojia, kisintaksiana   kileksia,   zinazopatikana   katika   pijini   zimetokana   na   lugha   za   Kiafrika.Wanazuoni  wengi  wanasema  kuwa  pijini  na  kirioli  zina  msingi  wa  Kiafrika.Goodman (1964) ametoa hoja  kwamba  ni baada tu ya kukubali kuwa kirioli zotezenye msingi wa Kifaransa zina asili yake Afrika Magharibi ndipo tutaelewa kwanini zinafanana.

Pijini   na   kirioli   huzungumzwa   hasa   katika   nchi   za   ulimwengu   wa   tatu.Zinahusishwasana  na  maswala  ya  kisiasa  na  kijamii.   Kuna  takriban  pijini nakirioli  mia  moja  duniani.   Pijini  nyingi  zina  misingi  yake  katika  lugha  za  Ulaya,hususan  Kihispania,  Kireno,  Kifaransa,  Kiingereza  na  Kidachi. Kikundi  kinginekinachofuata kwa ukubwa kina misingi yake katika lugha za Kiafrika.

Zoezi

Kwa kuzingatia nadharia hizi, unafikiria Sheng ni pijini au kirioli.  Toa sababuzako.

4.6  HITIMISHO

Katika somo hili, tumeanza kwa kujadili swala la lingua franka natumeonyesha majukumu yake katika jamii.  Vilevile tumeeleza nakuonyesha jinsi zinavyotumika kama lingua franka. Pili, tumefafanuadhana za pijini na kirioli  na vilevile  kuonyesha nadharia mbalimbaliambazo zimetolewa na wanaisimu kuhusiana na swala la kuzukakwa  lugha hizi..

69

Page 70: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Marejeleo   Teule Bickerton, D. (1971) Inherent Variability and Variable Rules.      Foundations      of      

Language   7 .Bloomfield,L. (1933)   Language   .  New York.  Holt. Rinehart and Winston.Chimera, R. (2000)   Kiswahili:      Past,      present      and      Future      Horizons   .  Nairobi.

Nairobi  University Press.Guthrie, M. (1967)   The      Classification      of      the      Bantu      Languages   .  London Dawsons

of Pall.Mbaabu,I.  (1978)   Kiswahili      Lugha      ya      Taifa   .  Nairobi: Kenya Literature Bureau.Onyango, J.O. (2002)   AKS      102:      Historical      Development      of      Kiswahili:Kiswahili   

Module.  Nairobi:  Institute of Open Learning, Kenyatta University.Polome,  E.C. (1967)   Swahili      Language      Handbook   .  Washington D.C. Centre for

Applied Linguistics.Swaleh A. (1997)  Lugha ya Kiswahili (ni) pijini au krioli? Makala

yaliyowasilishwa katika Idara ya Kiswahili.  Chuo Kikuu cha Nairobi.Todd, L. (1990)   Pidgins      and      Creoles   .  Routledge.London.

70

Page 71: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA  TANOUWILI LUGHA

5.0   UtanguliziKatika somo hili tunanuia kuelezea maana ya uwili-lugha na ulumbi.   Pamoja nahayo, tutaonyesha athari ambazo hutokana na lugha mbili au zaidi kuwa pamoja.Vile vile tutajadili swala la lugha rasmi, lugha ya taifa , diglosia na triglosia.   Namwisho tutaangalia swala la utowekaji wa lugha katika jamii.

5.1   Madhumuni

Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1.  Kueleza maana ya uwili-lugha na kuonyesha athari zake.2.  Kueleza maana ya lugha rasmi na lugha ya taifa.3.  Kueleza kwa fasili dhana za diglosia na triglosia.4.Kuonyesha sababu za utowekaji wa lugha na jinsi ya kuzilinda lugha hizi.

5.2   UWILI-LUGHAMtagusano  wa wanajamii huzua hali ya uwili lugha katika jamii mbalimbali.  Kwamujibu wa  Bloomfiled  (1933)  uwili-lugha  ni  umilisi  wa  lugha  mbili  kama  ulealionao mzawa wa lugha moja katika lugha yake.

Haugen  (1956)  naye  anaona  kuwa  uwili-lugha  ni  kitu  ambacho  huanza  wakatimzungumzaji  wa  lugha  moja  anapoweza  kutoa  kauli  kamili  na  zenye  maanakatika lugha nyingine.

Katika   hali   ya   wingi   lugha  tunaweza   kuzungumzia  kuhusu   mtu   mmoja  auwanajamii wote au wengi kuwa wana wingi-lugha.

71

Page 72: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Mtaalamu Grosjean  (1982:vii)  anakadiria  kuwa  karibu nusu  ya idadi  ya  watuulimwenguni huzungumza zaidi ya lugha moja.   Naye Romaine (1989:6) anadaikuwa  hata  zile  nchi  ambazo  zinafikiriwa  kuwa  na  lugha  moja  tu  kama  vileUfaransa,  Ujerumani  na  Uingereza  zina  wazungumzaji   ambao ni   wana  uwililugha.   Kwa mfano, utapata kuwa maeneo ya kimipaka, kwa mfano, Ufaransa,kuna  lugha  hizi:-Breton,  Flemishi,  Occitan,  na  kadhalika. Mara  nyingi watuwanaopakana hujipata wakizungumza lugha ya jirani zao.ZingatiaKatika  somo  hili  tutatumia  istilahi  ya  uwili-  lugha  kurejelea pia wingilugha

5.3 Sababu za kuwepo na Uwili lugha .Kunazo sababu  nyingi  ambazo  zinawafanya  watu  kuzungumza  zaidi  ya  lughamoja.  Sababu hizi ni pamoja na:

1. Ndoa   mseto Hali  ya  ndoa  mseto  ni  jambo  la  kawaida  katika  ulimwengu  wa  sasa. Hali  hiiinapotokea mke au mume hulazimika kujifunza lugha ya pili.

2.      Elimu      Aghalabu watu  wanapoenda  shuleni  wanafunzwa  lugha  ya  pili. Kwa  mfano,mtoto   anapokuwa   mdogo   hujikuta   katika   mazingira   ambayo   wazazi   wakewanatumia lugha wenyeji.   Anapotimia umri wa miaka sita, mtoto huyu hujiungana  shule. Shuleni,  hufunzwa  Kiingereza  na  Kiswahili. Ripoti  ya  hivi  karibuniinaonyesha  kuwa zaidi ya  wanafunzi elfu  mia  nne wako  katika nchi  mbalimbalikwa masomo ya juu.   Wale walio katika nchi zinazotumia lugha nyinginezo kamavile  Kijerumani  au  Kifaransa  hulazimika  kujifunza  lugha  hizi hata  kabla  yakujiunga na vyuo hivyo.

72

Page 73: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

3.      Dini      Dini anayofuata mtu inaweza kuwa katika lugha fulani, kwa mfano, ikiwa dini niya Kiislamu, utapata kwamba Waislamu wengi wanafahamu Kiarabu kwa sababuhii ndiyo lugha ambayo hutumiwa sana katika mahubiri hasa kukariri korani.

Swali

Je, waweza kufikiria sababu zingine zinazomfanya mtu kutaka kujua zaidiya lugha moja?

5.4   Uchaguzi   wa   lugha   katika   jamii   zenye   uwili-lugha-   Dhana  yahimaya

Tunapoangalia  Afrika kwa  mfano,  tunaona  kuwa  mtu  yeyote  anayesafiri  kwasababu  za  kiuchumi  au  kuhamia  sehemu  fulani  kwa  sababu  mbalimbali  huwamwana uwili lugha.   Hata   kama kuna wazungumzaji wa lugha moja tu, wengiwa watu ni wana uwili-lugha, (Myers- Scotton 1993).

Tafiti nyingi ambazo zimefanywa katika jamii zenye uwili-lugha zimejihusisha natabia ya uchaguzi wa lugha wanaofanya wazungumzaji.   Istilahi hii ya   tabia yauchaguzi ni  muhimu. Katika  hali  nyingi,  wazungumzaji  wanaweza  kutumialugha   zao   wanapozungumza   na   wenzao.   Ukweli   ni   kwamba,   lugha   fulanihuhusishwa  na  miktadha  fulani. Kwa  mfano,  mandhari,  mada  na  wahusikakatika mazungumzo hayo, Mesthrie (2000).

Mtaalamu   Fishman   (1967)   katika   kulishughulikia   swala   hili,   alijihusisha   nakuonyesha   ruwaza   ya   matumizi   ya   lugha. Aliibuka   na   dhana   ya   himaya(domains)  kama  namna  ya  kuonyesha  ruwaza  hizi. Alidai  kuwa  katika  jamiiyenye uwili-lugha, lugha mbalimbali huhusishwa na himaya tofauti za matumizi.

73

Page 74: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Mifano ya himaya hizi ni pamoja na familia, elimu, kazi au ajira, urafiki, utawalawa kiserikali, n.k.

Hivyo basi katika himaya hizi, mtu atachagua mojawapo ya lugha anazozifahamuili kuzitumia.  Kwa mfano, Myers  Scotton (1992) amegundua kuwa katika bara laAfrika,   ruwaza   ambayo   inajitokeza   kwa   wingi   ni   lugha   ya   kwanza   yamzungumzaji, pamoja na lingua franka ya wenyeji, kwa mfano, Kiswahili, kishalugha ya kigeni kama vile Kiingereza au Kifaransa.

Ruwaza ya matumizi ya lugha katika sehemu nyingi za Afrika zinategemea hali yakijamii  ya  mtu  na aina ya  muingiliano ambayo  mtu  hujihusisha  nayo (Mesthrie2002).

Zoezi

Kwa kuzingatia dhana ya himaya, onyesha namna marafiki zakowanavyotumia lugha wanazozifahamu.

5.5 Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uwili-lugha

Mtaalam Makey (1962) anapendekeza mambo manne ambapo fasiri yo yote yauwili  lugha   inahitaji  kuzingatia:   kiwango,   dhana,   ubadilishaji  na   athari  (auuingiliaji).

(a) KiwangoTumeona kuwa mwana uwili-lugha ni mtu ambaye anazungumza lugha mbili kwaustadi.Kwa mfano, Bloomfied anadai kuwa mwana uwili-lugha anahitaji kuwa naustadi, katika lugha ya pili kama alionao katika lugha yake ya kwanza.

74

Page 75: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Tunapowasikia   watu   wakiongea,   tunatanbua   kuwa  watu   hawa  hutofautianakatika  jinsi  wanavyodhibiti  lugha  yao  ya  kwanza,  na  hali  hii  inawakumba  walewanaojifunza   lugha   ya   pili. Ni   lini   tunaweza   kuamua   kuwa   sasa   mtuanazungumza lugha ya pili  kama anavyozungumza lugha yake ya kwanza ?.

Hivyo basi swali tunalohitaji kujiuliza ni je, kwa kiasi gani mzungumzajianafahamu lugha hizo mbili au tatu?

Mtazamo  tofauti  na  huu  ni  ule  ambao  unachukuliwa  na  wanaisimu  ambaohawatazami  uwili-lugha  kwa  kuzingatia  kiwango  bali  kwa  kuzingatia  dhima  yalugha hiyo.

2.  DhimaWana  uwili-lugha  huchagua  lugha  kulingana  na  kile  watakachofanya  na  lughahiyo. Kwa mfano, uhusiano wao na watu wanaoongea nao na kilewanachozungumzia. Ruwaza  ya  uwili-lugha  hubadilika  kila  mara  kulingana  nakazi itakayotendwa na lugha iliyochaguliwa kutumika.

Tuchukue mfano wa Mkenya ambaye ameishi Ujerumani kwa miaka mingi.   Mtuhuyo   anakifahamu   Kijerumani,   Kiingereza   na   Kiswahili. Sasa   anaporudinyumbani na kwenda benki anafikiria kutumia Kiswahili.  Lakini anatambua kuwahawezi  kujieleza  vilivyo  kwa  lugha  ya  Kiswahili  kwa  sababu  hajawai  kuwa  namajadiliano ya aina hii kwa Kiswahili.   Itambidi achague lugha nyingine ambayoni Kiingereza ili kuwasiliana na meneja.

Hii  inamaanisha  kuwa  kuna  hali  nyingi  ambazo  wana  uwili-lugha  wanawezakujieleza vizuri kwa lugha moja kuliko katika lugha nyingine.

3.  Uingiliaji

75

Page 76: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kuna  tajriba  fulani  katika  maisha  ambazo  humfanya  mtu aweze kujieleza vizurikwa lugha moja kuliko nyingine.   Hii haimaanishi kuwa hawaielewi lugha hiyo,La. Tatizo  ni  kwamba  wao  hujikuta  kuwa  hawalipati  neno  mwafaka  ambalowanaweza  kulitumia  wanapozungumzia  mada  fulani. Weinreich  (1953)  anadaikuwa uingiliaji ni ile hali ambayo ukiukaji wa kaida katika lugha hutokea katikamazungumzo ya wana uwili-lugha kutokana na wao kujua zaidi ya lugha moja.Uingiliaji  unaweza  kutokea  katika  viwango  vyote. Kwa  mfano,  unaweza  kuwakatika  kiwango  cha  fonetiki  ambapo  matamshi  ya  mtu  yanakuwa  kama  yaleyanayopatikana  katika  lugha  nyingine. Katika  kiwango  cha  semantiki,  mtuhuweza kushindwa kuchagua neno linalofaa.   Ni rahisi kuona kuwa hata katikakiwango cha kisantaksia uingiliaji huu hutokea hasa katika mpangilio wa manenokatika sentensi.

4.  UbadilishajiKatika  hali  hii  tunaangalia  kiasi  ambacho  mzungumzaji  hubadili  mazungumzokutoka kwa lugha moja hadi nyingine.

Zoezi

Ukirejelea Chacha L.M. na wengine (2002) AKS100:      Introduction      to      the      Study   of   Language , onyesha athari mbali  mbali za kiisimu zinazojitokezakatika jamii yenye wingi lugha.

Kumbuka

Uwili lugha ni hali ambapo mtu anaweza kuzungumza lugha mbili.  Wingi-lughani hali ya mtu kuzungumza zaidi ya lugha moja.

76

Page 77: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Swali1.   Uwili lugha ni nini?2.   Fafanua dhana ya himaya katika swala la uwili lugha3.   Ni  mambo  gani  tunahitaji  kurejelea  ili  kujua   viwango  vya  ufahamu  vya

mzungumzaji fulani  katika hali ya uwili lugha.

5.6   LUGHA   RASMI   NA   LUGHA   YA   TAIFA

5.6.1 Lugha Rasmi

Hii ni lugha ambayo imeteuliwa katika nchi fulani ili itumiwe katika mawasilianoyote rasmi katika nchi hiyo.   Lugha hii huchaguliwa ili kutumiwa katika shughuliza serikali, kwa mfano,   afisini, kuzungumza na wageni, katika taasisi mbalimbalina ndiyo hutumiwa kwenye vyeti na shahada.

Nchi  nyingi  zilizotawaliwa  zinatumia  lugha  za  waliokuwa  watawala  wao  kamalugha  zao  rasmi. Wakati  mwingine  baada  ya  nchi  kupata  uhuru,  huamuakutumia lugha ya humo nchini kama lugha rasmi.  Kwa mfano, Kenya na Ugandahutumia  lugha  ya  Kiingereza  kama  lugha  rasmi ilhali nchi ya Tanzania hutumiaKiswahili   kama   lugha   rasmi. Tunasubiri  kuona  jinsi  lugha   ya  Kiswahli  naKiingereza zitatumika iwapo katiba mpya itakubali kuwa Kiswahili kiwe pia lugharasmi nchini.5.6.2 Lugha  ya TaifaHii  ni  lugha  ambayo  kisiasa,  kijamii  na  kiutamaduni  inawakilisha  watu  fulani.Viongozi  wa  nchi  huchagua  lugha  ya  taifa  hasa  wanapogundua  kuwa  lugha  nikipengele muhimu katika utamaduni wa taifa (Chimera 2002).   Hivyo basi lugha

77

Page 78: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

ya taifa huwa ni lugha inayotambulisha na kutumiwa na taifa fulani.   Lugha hiihuweza vile vile kuwaunganisha wananchi wa matabaka mbalimbali. Tukitazamakwa mfano, viongozi wanaoshika hatamu, tunaona kuwa wanaweza kuchukuliwatu kama viongozi wa taifa zima bali sio wa makabila mbalimbali iwapo watatumialugha moja ya taifa.

Lugha ya taifa inaweza   kulinganishwa   na bendera ya taifa ya nchi.Vivyo hivyolugha   huitambulisha taifa.   Lugha ya taifa huwa na kusudi la kuibusha uzalendomiongoni mwa watu, (Chimerah 2002).

Katika  baadhi, ya nchi utapata kuwa lugha rasmi ndiyo pia lugha ya taifa ingawasio lazima mambo yawe hivyo.  Kwa mfano, katika nchi ya Tanzania, Kiswahili  nilugha rasmi na pia lugha ya taifa.

Kumbuka

Si lazima kila nchi iwe na lugha ya taifa ingawa ni lazima kila nchi iwena lugha rasmi.

Swali

Huku ukitoa mifano  eleza maana ya lugha Rasmi na lugha ya Taifa.

5.7 DIGLOSIA NA TRIGLOSIADiglosia  ni  hali  ya  kuwepo  kwa  lahaja  mbili  za  lugha  moja,  kila  moja  ikikidhimahitaji tofauti ya kijamii.

Kuna  wataalamu  wawili wa  isimujamii walioifafanua dhana  hii ya  diglosia lakinikwa misisitizo mbalimbali.  Hawa ni Ferguson (1959)   na Fishman (1967).

78

Page 79: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

5.7.1 MAELEZO YA DIGLOSIA KAMA YANAVYOTOLEWA NA FERGUSONFerguson  alitambua  kwamba wazungumzaji hutumia vibadala tofauti  vya lughakatika   miktadha   tofauti.Alieleza   kuwa  kulikuwa   na   hali  maalum  ambapovibadala  viwili  vya lugha  vinakuwepo  ubavu  kwa ubavu  katika  jamii fulani, kilamoja ya vibadala hivyo ikiwa na dhima mahsusi.  Hali hii ndiyo aliyoiita diglosia.

Ferguson aliona kuwa hali hii ni tofauti na pale ambapo lugha sanifu na lahajanyingine ya lugha hiyo zilitumika, au pale ambapo lugha mbili tofauti zilitumiwakatika jumuia lugha, kila moja ikiwa na dhima yake.

Ferguson aliifafanua dhana ya diglosia kupitia kwa vigezo tisa:dhima (function)fahari(prestige)urithi wa fasihi (literary heritage)upataji au ujifunzaji lugha (acquisition)usanifishaji (standardization)uthabiti/utangamano (stability)sarufi (grammar)leksimu (lexicon) msamiatifonolojia (phonology)

(i)DHIMADhima ndicho kigezo muhimu sana katika diglosia.   Ferguson asema kuwa huwakuna vibadala viwili vya lugha hiyo moja, ambapo moja huwa ni lahaja ya Juu (J)na nyingine ni lahaja ya Chini (CH).   Katika Kiarabu, J ni lugha kielelezo ya kale(Classical  Arabic)  ambayo  ndiyo  iliyotumiwa  katika  Korani,  na  CH  hutumiwakatika miktadha isiyo rasmi na ya kujiburudisha.  Hapa kuna mifano:

79

Page 80: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Hali/Miktadha na uteuzi wa (J) au (CH) katika diglosia

Hali J CH-Mahubiri kanisani au msikitini + _-Maagizo kwa watumishi, wahudumuhotelini, wafanyakazi, makarani _ +-Barua (ya kirafiki) - +-Hotuba bungeni + _-Mhadhara katika Chuo Kikuu + _-Mazungumzo kati ya marafiki x-Matangazo ya habari x _Lugha ya magazeti x _

(ii) FAHARIMielekeo  ya  wazungumzaji  katika  jamii  zenye  diglosia  ni  kwamba  J  ni  bora,yenye madaha, sanifu, na yenye mantiki zaidi.  Inaaminiwa kwamba CH ni duni.

(iii) URITHI WA FASIHIKuna fasihi au maandishi mengi katika J ambayo yanafurahiwa   na kuvutiwa najumuia lugha hiyo.   Aghalabu utamaduni wa fasihi ya J huwa hauna msingi wakekatika  jamii ya  kisasa.   Misingi  yake  ipo  katika  wakati uliopita au jumuia lughanyingine (Kifaransa, Kijerumani nk).

(iv) UPATAJI AU UJIFUNZAJI LUGHAKatika diglosia, ujifunzaji wa lugha huwa tofauti kati ya kibadala J na CH.   CHitatumiwa kuzungumza na watoto, na pia kati ya watoto wenyewe; hivi kwambawatu watafahamu CH bila juhudi za kimakusudi.

80

Page 81: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

J huwa ni lugha ya ziada au ya pili ambayo watu hujifunza baada ya kuifahamuCH. J  hufahamika  kupitia  mafunzo  ya  shuleni. Hii  ina  maana  kwamba  walewanaojifunza J kamwe hawawezi kupata ufasaha kama ule wanaofikia katika CH.Hii ni kwa sababu CH hutumiwa mara kwa mara katika mawasiliano ya kila sikuilhali J hujifunzwa kwa kukariri (memorise) sheria za kisarufi.

(v) USANIFISHAJIJ  ndiyo  husanifishwa  kwa  kuwekewa  mpangilio  kamili. Makamusi,  vitabu  vyasarufi, miongozo ya matamshi bora, na kwa ujumla vitabu vya matumizi sahihi yaJ huandikwa.  Alfabeti na sheria za maendelezo katika J huwekwa.

Huwa  hakuna  uchunguzi  wa  kiusomi  wa  lahaja  CH. Hata  kuandika  katika  CHhuwa  vigumu  kwa  sababu  hakuna  sheria  za  hijai  zilizoimarika,  na  pia  hakunaanayetaka kuandika katika CH.

(vi) UTHABITIDiglosia huwa ni hali iliyo thabiti na inaweza kudumu karne kadhaa.  Ili lugha iwena  zaidi  ya  lahaja  au  kibadala  kimoja,  sharti  pawepo  na  diglosia  katika  lughahiyo.   Mvutano kati ya J na CH katika diglosia hupungua kwa kiasi pale ambapokunatokezea mfumo wa lugha wa kati, unaochukua baadhi ya sifa za J na Ch.  Nikawaida kwa CH kukopa maneno kutoka kwa J; lakini matumizi ya msamiati waCH  katika J si jambo la kawaida.

(Viii) SARUFIIngawa J na CH ni maumbo ya lugha hiyo moja, huwa kuna tofauti nyingi kati yasarufi ya J na CH.  Sarufi ya CH huwa sahili kuliko sarufi ya J.

(ix) MSAMIATIMsamiati wa J na CH hutumiwa katika lugha zote mbili.   Istilahi na msamiati wakiusomi hupatikana tu  katika J.   Katika CH kuna msamiati unaorejelea vyombo

81

Page 82: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

vya nyumbani kama vifaa vya shambani, vyombo vya kupikia/jikoni nk ambavyohavina vingine vinavyolingana navyo katika J.

Sifa  ya  kuvutia  sana  katika  diglosia  ni  kuwepo  kwa  visawe  (msamiati  pacha)ambapo CH na J kila moja zinachangia neno kwa dhana hiyo moja.  Kwa mfano:

children - rasmikids - simo

baba - rasmibuda - simo

Katika jamii zilizo na diglosia, mfumo  wa J ndio unaowekwa katika maandishi nawa CH ndio unaotarajiwa kuwa katika mazungumzo ya kila siku.

Swali

Toa mifano ya sifa hizi tulizozitaja za diglosia kulingana na haliya lugha nchini Kenya.

Ferguson alichukulia Diglosia kuwa ni hali thabiti ya lugha ambayo, pamoja nalahaja za kimsingi za lugha hiyo, huwa na kibadala kilicho tofauti, cha hali ya juu,na  chenye  mpangilio  kamili.Kibadala  hiki  huwa  na  kusanyiko  kubwa  la  fasihiandishi lililotoka kwa jumuia lugha nyingine au kipindi cha awali cha lugha hiyo.Huwa inafunzwa shuleni na kutumiwa katika maandishi mengi na mazungumzorasmi.Lakini hakitumiwi na kitengo cho chote cha jamii hiyo kwa shughuli za kilasiku.

82

Page 83: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

HATIMA YA DIGLOSIAFerguson  (1972:248)  anaeleza  kuwa  diglosia  huweza  kuwa  na  hatima  tatutofauti:(a) itabakia thabiti kwa muda mrefu.(b) katika hali fulani, shinikizo fulani zinaweza kusababisha kumalizika kwake.

Kwa  mfano;  ongezeko  la  watu  waliosoma,  kutanda  kwa  mawasilianokatika nchi.

Watu  wengi  wanapoifahamu  J  na  kutumia  lugha  ya  kimaandishi  kwa  wingi,matokeo yake yanakuwa ni kupungua kwa tofauti za kiisimu kati ya J na CH.  Piakukua  kwa  utaifa  kunakoambatana  na  tamaa ya  kuwa na  lugha  ya  taifa kamaishara inayowaunganisha watu huchangia kumalizika kwa diglosia.(c) J itakua na kuwa lugha au lahaja sanifu.

J inaweza kuwa sanifu ikiwa:(i) tayari J ni lugha sanifu katika jumuia nyingine.(ii) ikiwa jamii hiyo yenye diglosia itaungana na jamii hiyo nyingine.

5.7.2 DIGLOSIA KWA MUJIBU WA FISHMANFishman (1967) anaamini kwamba tunahitaji kutofautisha kwa makini dhana zadiglosia na uwili lugha.  Anasema kuwa uwili lugha ni swala linaloshughulikiwa nawanasaikolojia  na  wanaisimunafsia;  inarejelea  uwezo  wa  mtu  binafsi  kutumiazaidi  ya  vibadala  au  launi  moja  ya  lugha  (language  variety launi  za  lughanamna  tofauti  za  matumizi  ya  lugha  kutegemea  mazingira,  wakati,  muktadha,nk,  k.v.  lahaja,  rejesta,  nk). Diglosia  hushughulikiwa  na  wanaelimujamii  nawanaisimujamii kulingana na dhima zake.

Fishman alibadilisha mapendekezo ya Ferguson kwa namna mbili:1. Fishman  hasisitizi  sana  umuhimu  wa  hali  zilizo  na  vibadala  viwili  tu  vya

lugha. Anaruhusu   kuwepo   kwa   misimbo   mingi   tofauti   inayowezakugawika katika makundi mawili:  Juu na Chini.

83

Page 84: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

2. Huku Ferguson (1972) akiona kuwa diglosia inachukua mstari wa kati wakiisimu  (anasisitiza  kwamba  diglosia  huwa  na  tofauti  nyingi  kuliko  ilivyokati ya mitindo, na chache kuliko ilivyo baina ya lugha tofauti), Fishmananalegeza  mipaka  hiyo. Anaona  kuwa  diglosia  haipo  tu  katika  jamuiazenye  ulumbi  ambazo  kirasmi  zinatambua  lugha  mbalimbali,  na  pia  sikatika  jumuia  zinazotumia  lugha  wenyeji  (vernacular)  na  lugha  vielelezo(classical varieties), lakini pia katika jamii zinazotumia lahaja tofauti, sajili,au vibadala vya lugha vyenye dhima tofauti.

Fishman   anatumia istilahi  diglosia  kurejelea kiwango cho chote cha tofauti zakiisimu kuanzia kwenye tofauti ndogo za kimtindo katika lugha moja hadi kwenyematumizi  ya  lugha  mbili  tofauti.Jambo  muhimu  ni  kwamba  tofauti  hizo  zakiisimu ziwe zimetambuliwa na kupewa dhima tofauti katika jamii.

Uwili lugha humaanisha kuwa udhibiti wa J na CH unapatikana katika jamii yote.Diglosia hurejelea mgawanyo wa dhima kati ya J na CH.

UHUSIANO KATI YA UWILI LUGHA NA DIGLOSIA

Diglosia________________________________________

+ -

1.  Diglosia na 2. Uwili lugha bilauwili lugha diglosia.

Uwili lugha 3.  Diglosia bila 4.  Hakuna uwili lughauwili lugha wala ulumbi.

1.   Diglosia   na   uwili   lugha

84

Page 85: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Katika jumuia lugha kama hiyo karibu kila mtu atafahamu J na CH.   Kwa mfano,kule Paraguay, Guarani ni CH na Kihispania ni J.  Kihispania ni lugha ya Kihindi-Kizungu na Guarani ni lugha ya wenyeji wa Marekani.

2.   Diglosia   bila   uwili   lugha Ili  kuwa  na  hali  kama  hii,  kunahitajika  makundi  mawili  tofauti  katika  kitengokimoja  cha  kisiasa,  kidini  na  kiuchumi. Kundi  moja  linakuwa  la  watawala  nalinazungumza  J  pekee.   Kundi  la  pili,  ambalo ndilo kubwa, halina uwezo katikajamii na huzungumza tu CH.   Kwa mfano, barani Afrika, wakoloni walizungumzaKiingereza huku wenyeji wakizungumza lugha zao.

Jumuia  za kidiglosia  zisizo  na  uwili  lugha  si jumuia lugha  kwa sababu  makundihayo  mawili  hayaingiliani  kwa  mawasiliano  isipokuwa  kwa  kiasi  kidogo  sanakupitia kwa wakalimani au kwa kutumia pijini.

3.   Uwili   lugha   bila   diglosia Fishman  anasema  kuwa  hali  hii  inarejelea  jumuia  ambazo  zina  wazungumzajiwengi  wenye  uwili  lugha,  lakini  hawatengi  lugha  hizo  kwa  miktadha  au  dhimamaalum. Lugha  yo  yote  kati  ya  hizo  inaweza  kutumiwa  kwa  dhima  yo  yote.Jumuia kama hizo huwa chache.

Uwili  lugha  bila  diglosia  hutokana  na  kuvuja  kwa  diglosia. Diglosia  inayovujainarejelea hali ambazo,   kibadala kimoja cha lugha kinavuja na kuchukua dhimazilizokuwa zimetengewa kibadala kingine.   Matokeo ya uwili lugha bila diglosia niama kuzuka kwa kibadala kipya ambacho ni mchanganyiko wa J na CH, au mojakuchukua   mahali   pa   nyingine. Kwa   mfano,   huko   Ubelgiji   katika   eneokunakozungumzwaKijerumani, kuna mabadiliko ambapo watu wengiwanazungumza Kifaransa (J) ingawa mwanzoni walizungumza Kijerumani (CH).

85

Page 86: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

4.   Hakuna      Uwili      lugha      wala      diglosia   

Hali hii inahitaji kundi ndogo lililojitenga linalozingatia usawa.  Lazima pawepo nalugha  moja  tu  na  hakuna  tofauti  za  majukumu  zitakazopelekea  kuwepo  hatatofauti za kimtindo katika maongezi.

5.8 TRIGLOSIARuwaza  ya  matumizi  ya  lugha  nchini  Tanzania  ni  ile  iitwayo  triglosia  Mekacha(1993).   Hii ni hali ambapo watu wengi wanatumia lugha tatu tofauti kutegemeamuktadha. Kiingereza  kinatumiwa  katika  shughuli  za  Kimataifa,  kisayansi  nakiteknolojia.   Kiswahili kinatumiwa katika shughuli za kiserikali, mahakamani, nakatika  utawala.Hii  ndiyo  lugha  inayozungumzwa  na  watu  wote. Tatu,  kunalugha  wenyeji. Hizi  hutumiwa  ili  kuendeleza  mahitaji  ya  makundi  madogomadogo.Zoezi

Onyesha jinsi diglosia inavyodhihirika katika matumizi yako ya lughakatika miktadha mbalimbali

Swali

Diglosia inahusiana na uwili-lugha .  Jadili kauli hii.

5.9 KUBADILI MSIMBOTunaweza kueleza kuwa kubadili msimbo ni kutumia lugha mbili au zaidi kwenyematini moja wakati wa mawasiliano.   Hata hivyo fasiri hii ni pana mno.   Kachru(1977:107) anaeleza kubadili msimbo kuwa ni kuchagua kutumia msimbo fulaniau  ule  mwingine  kutegemea  hali  ilivyo. Yeye  anatofautisha

dhana  hii  nakuchanganya  msimbo  (code  mixing),  anayoeleza  kuwa  ni  kuhamisha  vipashiovikubwa  vya  lugha  kutoka  kwa  msimbo  mmoja hadi  mwingine.   Katika kozi  hiihatujaribu kutofautisha kati ya kubadili msimbo na kuchanganya msimbo.

86

Page 87: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Haugen  (1956)  anasema  kuwa  kubadili  msimbo  ni  hali  ambapo  mwana  uwililugha  anaingiza  neno  ambalo  halijatoholewa  katika  lugha  yake  kutoka  kwanyingine.

Myers-Scotton (1998) anaeleza kuwa kubadili msimbo ni matumizi ya lugha mbiliau zaidi katika mazungumzo, bila kutohoa kifonolojia lugha moja ili iingiliane nanyingine.

Kamusi   Sanifu   ya   Isimu   na   Lugha   (1991)  inaaeleza  kuwa  kubadili  msimbo  nikutumia   aina   mbili   tofauti   za   misimbo   kwenye   matini   moja   wakati   wamawasiliano.

Katika  hali ya  kawaida  wazungumzaji  wa  lugha  hutumia sarufi na msamiati walugha moja wanapozungumza. Dhana ya kubadili msimbo ni dhanainayochunguzwa  na  wanaisimu  jamii  na  wanaisimu  nafsia.   Kuna  uhusiano  wamoja  kwa  moja  kati  ya  uteuzi  wa  lugha  na  muktadha  wa  kijamii. Katikaisimujamii  wachunguzi  wanaangalia  ni kwa  nini mtu  anabadilisha  msimbo;  mtuhuyo yuko katika hali gani?   Katika kiwango cha isimunafsia kunachunguzwa uleuwezo unaomfanya mtu kubadili msimbo.

Baadhi  ya  watu  wanachukulia  kubadili  msimbo  kama  ishara  ya  kuoza  kwa  uleuwezo  wa  kiisimu.   Wanaona  kwamba  kubadili msimbo  ni matokeo  ya kutojualugha  moja  vilivyo.   Kiisimu,  hatuwezi kusema  hivyo,  kwa sababu  kule kubadilimsimbo ni sifa muhimu katika usemi wo wote unaohusu uwili lugha.Kwa mfano1.Nilitaka kwenda kaw ofisi ya Foreign Affairs.

Kubadili msimbo ni mbinu ya kimazungumzo inayotumiwa (a) kuipa nguvu amri(b) kuchochea hisia (c) kuifanya kauli iwe na ukali (d) kusisitiza.

87

Page 88: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Uchunguzi wa kubadili msimbo uliofanywa ulionyesha kuwa: Kubadili  msimbo  katika  jamii  zenye  uwili  lugha  kuna  maana.   Kunatekeleza

jukumu fulani katika mazungumzo. Uteuzi wa lugha wa mzungumzaji huhusu kujaribu kujitambulisha na wenzake

kijamii.Zoezi

Andika sentensi kumi zinazoonyesha namna watu wanavyobadili msimbo nazingine kumi zinazoonyesha kuchanganya msimbo.

Swali

Wazungumzaji hubadili misimbo na kuchanganya misimbo kwa sababufulani bali siyo ishara ya kutomilisi kikamilifu mojawapo ya lughazinazohusika.Tathmini kauli hii.

5.10  UTOWEKAJI WA LUGHASifa  muhimu  inayopatikana  katika  jamii  zilizo  na  uwili  lugha  ni  mabadiliko.  Ninadra  kupata  hali  ambapo  lugha  hizo  mbili  zinadumu  zikiwa  katika  hali  yakulingana.  Ikiwa  lugha  ya  hadhi  ya  chini  inaweza  kuendelea  kuwepo  licha  yashinikizo  na  athari  kutoka  kwa  lugha  zenye  nguvu,  basi  tunaiita  hali  hiyoudumishaji   lugha  (language maintenance).   Kinyume na hali hiyo utakuta lughaduni zinasalimu amri na wazungumzaji wake wanamezwa na utamaduni wenyenguvu. Hali hii huitwa   ugeuzaji      lugha    (language shift).   Ugeuzaji lugha ni dhanainayotumiwa  kurejelea  hali  ambapo  lugha  moja  inachukua  nafasi  ya  nyinginekama chombo muhimu cha mawasiliano na ujamiishaji katika jumuia.

Mambo mengine yanayoweza kutokea lugha zinapoingiliana ni kama ukopaji wamsamiati  kati  ya  lugha  hizo.Pia  kunaweza  kutokea  lugha  ya  kati  ambayo

88

Page 89: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

aghalabu   huwa   pijini   au   krioli.   Mwisho   kunaweza   kutokea   kifo   cha   lugha(language death).

5.10.1 KUFA KWA LUGHALugha  inaweza  kufa  polepole.  Hii  ina  maana  kwamba  lugha  moja  itachukuanafasi ya nyingine polepole.

Lugha  inaweza  kufa  ghafla. Inapofanyika  hivi  huwa  hakuna  kipindi  cha  uwililugha hapo katikati.   Mzungumzaji wa mwisho wa lugha hiyo huwa anajua lughamoja tu.  Kwa mfano, Tasmanian.

Pia   wazungumzaji   wanaweza   kuamua   kutotumia   lugha   yao   kwa   sababuwanaogopa   kudhuriwa   kisiasa. Katika   hali   hii   lugha   inakufa   ikiwa   nawazungumzaji fasaha. Vile vile   wazazi wanaweza kukataa kuwafundisha watotowao  lugha  hiyo.  Kwa  mfano,  mauaji  ya  maelfu  ya  Wahindi  huko  El  Salvadormwaka 1932 yaliwafanya walionusurika kutoongea lugha za Cacaopera na Lencaili  wasitambuliwe  kuwa  Wahindi.  Hali  kama  ile  ilyowakumba  Wahutu kuleRwanda ni mfano wa njia ambazo zinaweza kuua lugha.

Kloss  katika Mesthrie (2000) anazungumzia aina tatu za vifo vya lugha.(a) Lugha itakufa ikiwa wazungumzaji wake wote wamekufa.(b) Lugha hufa kwa sababu ya ugeuzaji lugha.(c) Lugha  hufa  baada  ya juhudi  nyingi za kuidunisha.   Lugha  huteremshwa

hadhi kuwa lahaja wakati jumuia lugha itaacha kuitumia katika maandishina watumie nyingine.

5.10.2 LUGHA HAI AU ILIYOKUFA?Ili tuseme kwamba lugha fulani i hai, lazima pawepo na wazungumzaji asilia walugha  hiyo  walio  hai  na  wanaoitumia.   Katika  sehemu  nyingi  za  ulimwengu,  si

89

Page 90: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

rahisi kuthibitisha kwamba kuna wazungumzaji asilia wa lugha hizo walio hai nawanaozitumia.

Ingawa   lugha   kama   Kilatini,   Kiyunani   cha   kale,   na   Sanskrit   huitwa   lughazilizokufa, hali hii si ya kawaida katika isimujamii.   Lugha hizi zilibadilika kutokakizazi  kimoja  hadi  kingine,  zikawa  lahaja  na  baadaye  lugha  sanifu.Siku  hiziKilatini  kipo  kama Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiitaliano na Kiromenia.   Lughaza Ulaya zilizokufa kabisa ni Gothic, Pictish na Etruscan.

Kiebrania (Hebrew) kilikufa kwa muda lakini kikafufuliwa mwishoni mwa karne ya19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

5.10.3  HALI ILIVYOInakisiwa   kwamba   kuna   lugha   6,000   zinazozungumzwa   ulimwenguni   leo.Thuluthi ya  lugha hizi zimo katika hatari ya kufa (Mesthrie 2000).   Pia thuluthimoja  ya  lugha  zote  ulimwenguni  huzungumzwa  na  watu  wasiozidi  1,000.Nilugha kama 600 tu hivi ambazo hazijatishwa na kifo.

Unajuaje kuwa lugha karibu ife?   Ukiona wazazi hawawafunzi watoto wao lughayao asilia, na watoto hawataki kuifahamu, basi unajua kuwa lugha hiyo inaelekeakufa.

Katika ripoti ya hivi punde ya Umoja wa Mataifa (UN), 16 kati ya lugha za Kenyaziko  katika  hatari  ya  kuangamia.   Tayari zingine zimeshakufa Suba, El Molo,Oropom, Lonioti, Yaaku, Sogoo, Kore, Segeju, Omotik na Kinare.   Lugha zinginekama  Dahalo  (pwani),  Bongom  na  Terik,  lugha  inayofanana  na  Kiluhya  nainayopatikana katikati ya Wamaragoli na Wakalenjin i karibu kufa, (Opala, 2002,Ladefoged (1992) (Tazama ramani inayoonyesha lugha ambazo zinaelekea kufanchini Kenya na Tanzania).

90

Page 91: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Nchini Ethiopia, Ongota ina wazungumzaji 19, na Gafat haina .

5.10.4  KWA NINI HATUTAKI LUGHA IFE?Wanaisimu husema kwamba kila lugha ina upekee wa aina fulani.  Lugha hubebautamaduni wa watu, inapokufa na utamaduni huo unapotea.

Pia wamesema kuwa lugha ni hifadhi ya mawazo ya muda mrefu na tajriba zawatu.Humo tunapata methali, misemo, jazanda; na haya yote ni elimu iliyokuzwakwa kipindi kirefu.

Katika miaka ya 1930, Edward Sapir na mwanafunzi wake Benjamin Lee Whorfwalidai   kuwa   lugha   huelekeza   fikra   zetu. Lugha   ndiyo   huamua   jinsitunavyofikiria. Kwa  hivyo  tukipoteza  lugha  tutapoteza  namna  ya  kuiangaliadunia.   Kila jamii ina tabia zake za kiakili, na kila jamii ina namna ya kuiangaliadunia.

5.10.5  MAMBO YANAYOSABABISHA KUFA KWA LUGHALugha hufa kutokana na mabadiliko ya kitamaduni na kugeuza lugha kwa sababuya kumezwa na utamaduni na lugha yenye nguvu zaidi. Inasemekana kwambakati ya 1490 1900,  nusu ya lugha zote ulimwenguni zilikufa baada ya wazungukuanzisha makoloni katika sehemu nyingi duniani ambako lugha zaozilizungumzwa.  Utandaradhi umeleta  ubeberu  lugha  (language  imperialism)unaofifisha lugha ndogo.

Maswala  ya  kiuchumi  pia  huchangia  kufa  kwa  lugha. Vijana  hutoka  vijijini  nakwenda mijini kutafuta ajira.   Huko hawazungumzi lugha zao asilia.  Watoto waohawatafahamu lugha hizo asilia.  Baada ya kizazi kimoja, kina babu wanapofariki,

91

Page 92: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

lugha inakufa.   Biashara, kama ile ya utumwa, husababisha kufa kwa lugha asiliana kutokea kwa pijini.

Magonjwa  yanaweza  kuua  watu  wote  wanaozungumza lugha  moja na  kufanyalugha hiyo ipotee.  Kwa mfano, mwaka 1962, Trumai, iliyozungumzwa katika kijijikimoja  kandoni  mwa  Mto  Culuene  kule  Venezuela,  ilipunguziwa  wazungumzajihadi 10 kutokana na ugonjwa  wa  homa kali (influenza).

Sera  ya  lugha  katika  nchi   inaweza kuathiri baadhi ya  lugha.   Kule Marekani  ,Kijerumani kilikuwa lugha iliyosambaa zaidi kikifuatwa na Kiingereza, wakati wauhuru. Hivi   sasa   Kiingereza   kimechukua   nafasi  ya   kwanza   na   Kijerumanikinafahamika kama simo.

Mwelekeo   hasi   katika   sera   za   serikali   na   jamii   kunakotumika   lugha   hiyohusababisha kufa kwake. (Tazama, Ngugi, P. na Osore,M . 2003).

5.10.5  NAMNA YA KUZUIA LUGHA ZA KIAFRIKA ZISIFE1. Wakati huu wa demokrasia, lugha ichukuliwe kama haki ya kidemokrasia.2. Sera ya lugha ilenge lugha zote nchini.3. Mafunzo katika lugha wenyeji yahimizwe.4. Kifungu cha 9 cha Haki za Kiisimu Duniani kinasema   Jumuia lugha zote

zina haki ya kusanifishwa, kuhifadhi, kukuza na kuendeleza lugha zao bilakuingiliwa.

Zeozi

Pendekeza njia zingine zinazoweza kuzuia kufa kwa lugha

92

Page 93: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Swali

Swala         la       utandarithi       limesabisha       utowekaji      wa       lugha      nyingi ulimwenguni.   Jadili kauli   hii.

Hitimisho

Katika somo hili, swala la uwili-lugha na ulumbi limejadiliwa.  Tumeonyeshaathari za kiisimu zinazotokana na wanajamii kuongea zaidi ya lugha moja.Tumelijadili pia swala la Diglosia na Triglosia.  Mwisho tumeona utowekaji walugha, sababu za kutoweka kwa lugha na jinsi ya kuzuia lugha zisife.

Marejeleo TeuleBloomfied,  L. (1933)      Language   .  New York. Holt Rinehart and Winston.Chimera, R. (1999)  Kiswahili through The Ages: The Question of Lexicon

Makala   Yaliyowasilishwa  katika  Idara  ya  Kiswahili,  8 Agosti, Chuo Kikuucha Egerton, Njoro.

Denison, N. (1977)   Language death or Language Suicide .  International Journalof the Sociology of Language.

Fasold, R.W. (1997)   Motivations and Attitudes influencing Vernacular Literacy:four  African  Assessments katika      Vernacular      Literacy   :  A  Re-Evaluation.Oxford.  Clarendon Press.

Fergerson,  C. (1959)  Diglossia. Word   15 .Haney, D. (1995)  Linguistic Crisis looms as native tongues die   in   Daily      Nation   

93

Page 94: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

28, 1995.Haugen, E.. (1956)      Bilingualism      in      the      Americas   .  TUSCOLOOSG.  University of

Alabama Press.Kachru, B.B. (1977)   Code Switching as a Communicative Strategy in India

Saville-Troike,  Murie  (wah) Linguistics   and   Anthropol ogy. Washington.

Georgetown University.Ladefoged,  P. (1992)   Another View of Endangered Language Language   68 .Mbaabu, I. (1995)   Linguistic and Cultural Dependency in Africa   in   Baragumu   ,

Vol. 2 No. 1.Mekacha, R.D.K. (1993) The Sociolinguistic Impact of Kiswahili on Ethnic

Community   on   Languages   in   Tanzania. A   Case   Study   of   Ekinata.Bayreuth African Studies.

Mesthrie, R. et. al. (2000)   Introduction      to      Sociolinguistics   .  Edinburg UniversityPress, Edinburgh.

Myers-Scotton,   C.   (1992)   Language   in   East   Africa:   Linguistic  patterns  andPolitical  ideologies ,  in  J.A.  Fishman(ed)      Advances      in      the      Study      of      Societal      Multilingualism.Moton.The Hague .

Ngugi, P. na Osore M. (2003)  Linguistic Genocide of the African Languages:Protecting   and Empowering .   Makala iliyowasilishwa katika Kongamanola LASU Dar es Salaam Tanzania, Agosti 21 24.

Weinreich , U.  (1974)      Languages      in      Contact   .  The Hague.  Mouton.

94

Page 95: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA SITA

UPANGAJI LUGHA

6.0 UtanguliziKatika  somo  hili  tutazungumzia  swala  la  upangaji  lugha  kwa kuonyesha  jinsililivyoshughulikiwa   na   wataalamu   mbalimbali.   Pia   tutashughulikia   mawandambalimbali  ya  upangaji  lugha, na  kuangalia  majukumu  mbalimbali  ya  lughakatika  uwanda  mpana  wa  upangaji  lugha  pamoja  na  mchakato  wa  upangajilugha.   Vile  vile  tutazingatia  swala  la  lugha Taifa na  lugha  Rasmi.   Pamoja  nahayo, tutachunguza sera ya lugha nchini Kenya.

6.1  Madhumuni

Baada ya kulipitia somo hili tunatarajia kwamba utaweza:(i) Kueleza maana ya upangaji lugha.(ii) Kueleza mawanda ya upangaji lugha na majukumu yanayopewa lugha.(iii) Kueleza mchakato wa upangaji lugha, lugha ya Taifa na lugha Rasmi.(iv) Kueleza sera ya lugha nchini.

6.2 UPANGAJI LUGHAKupanga ni tendo la kibinadamu  linalotokana na haja ya kupata suluhisho kwashida  fulani.   Tendo  hili linaweza kuwa  (limepangwa  na) la kimakusudi au liwelimetokea  tu  bila  mpango  kamili. Linaweza  kutekelezwa  na  watu  binafsi  aulinaweza   kuwa   rasmi. Mpango   wa   kijamii   ni   tendo   lililo   na   mawandayaliyofafanuliwa vyema katika jamii.   Ikiwa upangaji umefanywa vema utahusuhatua kama ukusanyaji wa habari ili ukweli ufahamike, kuwa na njia badalia zakutekeleza   jambo   hilo,   kufanya   maamuzi,   na   utekelezaji   wake   katika   njiamahsusi.

95

Page 96: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Utaratibu  uliotajwa  hapo  juu  unatumika  pia  katika  Upangaji  Lugha  (UL). ULhuhitajika pale ambapo kuna matatizo ya lugha.   Ikiwa watu wanahisi kwambahali fulani ya kiisimu haifai, basi kuna nafasi ya UL kutekelezwa hapo.  Istilahi yaupangaji  lugha   ilianzishwa  na  mwanaisimu  wa  Kimarekani  aliyeitwa  EinarHaugen   katika   miaka   ya   mwisho   ya  1950,  na  inarejelea  juhudi  zote  zakimakusudi  zenye  lengo  la  kubadilisha  tabia  za  kiisimu  za  jumuialugha. Inajumlisha  mambo  yote  kuanzia  kupendekezwa  kwa  nenojipya hadi kupendekezwa kwa lugha mpya.

Wakati   mwingine   istilahi   ya   sera   ya  lugha   imetumiwa   kama   kisawe   chaupangaji  lugha. Hata  hivyo,  sera  ya  lugha  hurejelea  malengo  ya  kijumla  yakiisimu, kisiasa na kijamii ambayo ndiyo msingi wa mchakato wa upangaji lugha.

Upangaji   lugha   ni   tukio   ambalo   limesambaa   na   limetekelezwa   kwa   mudamrefu.Hata hivyo ni katika miaka ya sitini (1960 s), ambapo nchi nyingi za Afrikana  Asia  zilizokuwa  zimejinyakulia  uhuru  zilikumbana  na  swala  la  uchaguzi  nautekelezaji  wa  lugha  ya  taifa.Hapa  ndipo swala  la  sera na  upangaji wa lughalimejitokeza kama eneo la uchunguzi katika isimujamii.

6.2.1.  UPANGAJI LUGHA NI NINI?Hapa kuna maelezo ya istilahi hii kutoka kwa wataalamu mbalimbali.

Rubin (1972), katika  Can Language be Planned?,  anaeleza kuwa hii ni mbinu yakuchunguza mabadiliko na matumizi ya lugha ili kuweza kufanya ubashiri kuhusujinsi   ya   kutekeleza   mabadiliko   hayo. Upangaji   wa   lugha   unamaanishamaendeleo,  utekelezaji  na  utathmini  wa  mbinu  maalumu  za  kutatua  matatizomahsusi ya lugha.

96

Page 97: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Haugen (1972), anasema , upangaji lugha ni shughuli ya kutayarisha othografia,sarufi,  na  makamusi  ili  kuwaongoza  wazungumzaji  na  waandishi  katika  jamiiyenye  lugha  nyingi. Kwa  kweli  haya  ni  matokeo  ya  UL.Kwa  hivyo  UL  niutathmini wa mabadiliko ya lugha.

Das Gupta (1971) alieleza kuwa UL huchukulia lugha kama amali na nyenzo yakijamii inayoweza kufanyiwa mabadiliko na inayohitaji hatua zilizopangwa kupitiakwa juhudi za pamoja za mamlaka za kisiasa, kielimu, kiuchumi na kiisimu.

Moshe Nahir (1977) anapendekeza kwamba upangaji lugha uangaliwe kama uliona   majukumu   matano   bainifu   ambayo   yamejikita   katika   shughuli   ambazowapanga lugha hujihusisha nayo.  Majukumu hayo ni:(a) Uchujaji au utakasaji au usahihishaji lugha (Language purification)

Kuelekeza matumizi sahihi na kuhifadhi usafi wa lugha.(b) Ufufuaji Lugha

Huu ni ufufuaji wa lugha ya kale katika hadhi yake ya zamani au ufufuajiwa lugha iliyokufa, kwa mfano, ufufuaji wa Kiebrania.

(c) Ugeuzaji au Urekebishaji Lugha (Language Reform)Kuwezesha   matumizi   ya   lugha   kupitia   kwa   usahihishaji   au   urahisishaji   wamsamiati na tahajia.(d) Usanifishaji wa Lugha (Standardization)

Kuhakikisha  kwamba  lugha  moja  au  lahaja  moja  katika  eneo  au  taifafulani imekubaliwa kama lugha kuu ya eneo au taifa hilo katika matumiziya jumla.  Kwa mfano:Tanzania - KiswahiliEthiopia - Kiamharic

(e) Uingizaji usasa katika msamiati (Lexicomodernization)Kuziba pengo kati ya msamiati wa lugha na istilahi mpya zinazotokana nateknolojia ya kisasa.

97

Page 98: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kamusi   Sanifu   ya   Isimu   na   Lugha   (1991)   inasema  kuwa  upangaji  lugha  nijitihada  za kuweka  sera mbalimbali za  lugha  ambazo husaidia  kutatua  tatizo lamawasiliano  katika  jamii,  kwa  kuchunguza  lugha  na  lahaja  zilizopo  ili  kuteuazinazofaa kutumika.

Upangaji  lugha  ni  sehemu  ya  sera ya  lugha.   Hii inamaanisha kwamba  serikalifulani  huchukua  sera  fulani  kuhusiana  na  lugha  zinazozungumzwa  katika  jamiifulani  na  ikatekeleza  sera  hiyo  kwa  njia  ya  upangaji  lugha. Hali  yo  yote  yaupangaji   lugha   itafanywa   kwa   kuzingatia   sera   ya   lugha,   na   jambo   hililitadhihirisha wazi sera za kijumla za serikali.

Zoezi

Kwa kuzingatia mtazamo wa Nihir, onyesha jinsi ambavyo lugha ya Kiswahiliimeshughulikiwa.

6.3 MAWANDA YA UPANGAJI LUGHAKloss (1969) alibainisha aina mbili za kimsingi za upangaji lugha:(a)  Upangaji lugha kiukongoo (corpus planning)(b)  Upangaji lugha kihadhi (status planning)

(a) Upangaji lugha kiukongooKongoo  ni  kusanyikoo  la  data  za  semi  zilizoandikwa  au  kunukuliwa  ambazohutumiwa kama kianzio cha ufafanuzi wa kiisimu.

Upangaji  lugha  kiukongoo  unahusika  na  muundo  wa ndani  wa lugha.   Mamboyanayozingatiwa hapa ni pamoja na kuunda othografia kwa lugha ambazo badohazijaandikwa,  kuanzisha  mabadiliko  katika  tahajia,  kubuni  maneno  mapya  nakuchapisha vitabu vya sarufi.  Jambo la kimsingi katika upangaji lugha kiukongoo

98

Page 99: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(na  pia  upangaji  lugha)  ni  usanifishaji  wa  lugha. Huu  hueleweka  kuwa  niuanzishaji na uendelezaji wa kaida za kiisimu zilizo sare.

(b) Upangaji lugha kihadhiUpangaji  huu  hurejelea  utoaji  wa  dhima  mpya  kwa  lugha  (kama  vile  kuitumialugha hiyo kufunzia shuleni au kama lugha rasmi).   Jambo hili huathiri dhima yalugha  katika  jamii. Kwa  mfano,  uamuzi  wa  kutumia  Kiebrania  kama  lugha  yamafunzo katika shule za Wayahudi huko Palestine kuanzia mwishoni mwa karneya 19, ni mfano wa upangaji lugha kihadhi.   Kabla ya hapo, Kiebrania hakikuwakinatumiwa  katika  mawasiliano  ya  kila  siku  ila  katika  maombi na  maandishi  yakidini  na  kiusomi.Uanzishaji  wa  shule  zinazotumia  Kiebrania  ulijenga  hali  yakufufua Kiebrania kama lugha ya mawasiliano ya kila siku.   Hadhi   ya Kiswahilinchini Kenya pia imeinuliwa katika ngazi mbalimbali.

Wapangaji lugha hutofautisha majukumu mengi ambayo lugha huwezakutekeleza katika jamii.  Haya ni:1. Lugha rasmi  - hutumiwa katika miktadha ya kitaifa  na inaunganisha watu

kisiasa  na  kitamaduni.  Aghalabu hadhi  hii  huwa  imetangazwa  kwenyekatiba.

2. Lugha rasmi ya mkoa au jimbo matumizi ya lugha kama lugha rasmi yaeneo au jimbo  fulani.   Kazi ya lugha hii hutengewa mkoa si nchi nzima.Kwa  mfano,  katika  mkoa  wa  Canada  unaoitwa  Quebec,  Kifaransa  ndiyolugha  rasmi  tangu  mwaka  1974,  ilhali  Kiingereza  na  Kifaransa  hutumikakama lugha rasmi katika mikoa mingine yote.

3. Mawasiliano mapanamatumizi ya lugha kama chombo cha mawasilianokinachovuka  mipaka  ya lugha  mbalimbali katika  nchi moja.   Hii ni  kamalingua franka.   Kwa mfano, Kiswahili nchini Kenya na Tanzania, Kihindi naKiingereza nchini India.

99

Page 100: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

4. Lugha  ya  kimataifa -  matumizi  ya  lugha kama  chombo  kikuu  chamawasiliano katika uwanja wa kimataifa; kama vile katika itifaki, utalii nabiashara.  Kwa mfano, lugha ya Kiingereza ina dhima hiyo  leo.

5. Lugha ya kikundi  - matumizi ya lugha kama chombo cha mawasiliano kwawatu wa kundi moja au kabila moja.

6. Elimu  - matumizi ya lugha kama chombo cha kufunzia shuleni.7. Dini   - kuitumia lugha fulani katika matambiko ya dini fulani.  Kwa mfano:Kiislamu  - Kiarabu

Judaism   - Kiebrania8. Vyombo  vya  habari-  lugha  inayotumiwa  kwenye  televisheni,  redio  na

magazeti.9. Kazini  - matumizi ya lugha  kama chombo cha mawasiliano kazini.10. Fasihi  - lugha ya kiusomi.

Hata  ingawa  wapangaji  lugha  hutenga  upangaji  lugha  kikongoo  na  upangajilugha kihadhi, ni muhimu kuelewa kuwa zote mbili zinahusiana sana.   Kutolewakwa dhima mpya kwa lugha fulani huhitaji mabadiliko katika mfumo wa kiisimuwa lugha hiyo.

Hivi majuzi aina nyingine mbili za upangaji lugha zimejitokeza, nazo ni:

(a) Upangaji lugha kifahari (prestige planning)Upangaji  lugha  kifahari  hulenga  katika  kutoa  mielekeo  chanya  ya  kisaikolojiaambayo ni muhimu ikiwa kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangajilugha. (Fahari  kuu  ambayo  Kiebrania  kilikuwa  nayo kama  lugha  ya  kidiniilisababisha   kutokuwepo   na   haja   ya   kuwa   na   upangaji   kifahari).   Upangajikifahari huwa muhimu pale ambapo lugha ambayo imeteuliwa ilikuwa ya hadhiya  chini  (kama  ilivyo  katika  diglosia).  Ili  watu  wakubali  hadhi  ya  lugha  hiyoiliyotwazwa,  kuna  haja  ya  kuboresha  na  kuendeleza  ufahari wa  lugha  hiyo.Hivyo basi, upangaji kifahari aghalabu hutangulia upangaji kihadhi.

100

Page 101: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(b) Upangaji lugha Kiurithi (acquisition planning)Hizi ni juhudi za kusambaza na kuendeleza ujifunzaji wa lugha.   Hapa tunaonataasisi  za  kitamaduni  zinazosambaza  na  kuendeleza  lugha  mbalimbali. Kwamfano, British Council na Taasisi ya Goethe ziliundwa na kufadhiliwa na serikalizao ili kusaidia ujifunzaji wa Kiingereza na Kijerumani kama lugha ya pili katikanchi nyingine.   Pamoja na taasisi kuna zingine kama vile French Cultural Centre,Japanese Cultural Centre n.k. Taasisi hizi hutoa mafunzo ya mara kwa mara kwawalimu wanaofundisha lugha hizi.Swali

Kwa kurejelea lugha mbalimbali za Kenya, onyesha jinsi ambavyomawanda ya  Upangaji  lugha  yameshughulikiwa.

6.4 MCHAKATO WA UPANGAJI LUGHAHaugen  (1966,  1972,  1987)  alisema  kuwa  mchakato  wa  upangaji  lugha  unazohatua nne ambazo zinaweza (ingawa si lazima) kufuatana.  Hatua hizo ni:

1. Uteuzi  (selection)2. Ukuzaji msimbo (codification)3. Utekelezaji (implementation)4. Upanuzi (elaboration)

(i) UteuziUpangaji  lugha  huanza  kukiwepo  na  uwezekano  wa  kuchagua  moja  kati  yavibadala  vingi  vya  kiisimu.Uteuzi  huu  utatokea  baada  ya  watu  kutambuakwamba  kuna  shida  fulani  ya  kiisimu.Basi  lahaja  au  lugha  moja  kati  ya  zilezinazotumika  huchaguliwa kuwa  msingi  wa usanifishaji.   Uteuzi ni ule uchaguziwa lugha au lahaja ili ipewe dhima fulani katika jamii, kwa mfano, iwe rasmi, yakufunzia,  ya  dini,  n.k.  Hii  ina   maana  kwamba  lugha  au  lahaja  ya  fahari  zaidi

101

Page 102: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

ndiyo  inayochaguliwa. Uchaguzi  unazingatia  umuhimu  wa  lahaja  hiyo  kijamii,kisiasa, kibiashara, kielimu nk.  Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili:

Kiunguja - kibiasharaKiamu - kiusomiKimvita - kiusomi na kijamii

Kiunguja  kilichaguliwa.  Pia  katika  mwaka 1974 (Julai 4), Kenyatta  alipotangazaKiswahili  kiwe  lugha  ya  taifa,  hii  inamaanisha  kwamba  Kiswahili  kilichaguliwakutoka kwa lugha nyingi zinazozungumzwa humu nchini..

Uteuzi  huu  unaweza  kutanguliwa  na  mijadala  mikali  kati  ya  watu  hadi  palewanapokubaliana,  au  unaweza ukaamuliwa na  viongozi  siku  moja tu  kama vileAtaturk alivyobadilisha hijai ya Kituruki kutoka kwa ile ya Kiarabu hadi kwa ile yaKiroma.   Uteuzi hutekelezwa na jamii, kupitia kwa viongozi wake.   Wanaohusikakatika  uteuzi  huu  si  tu  taasisi  za  serikali  bali  pia  watu  binafsi,  vikundi  kamamakanisa, vyama vya kisiasa, mikoa na nchi yote.

Lahaja au lugha fulani inapochaguliwa inapendelea watu wanaoizungumza kwaniinawapa   fahari   na   hawapotezi   muda   kujifunza. Uteuzi   mbaya   unawezakusababisha mgawanyiko katika nchi.

Wakati mwingine wapangaji lugha huunganisha lahaja mbalimbali.   Kwa mfano,usanifishaji wa Basque, lugha inayozungumzwa kusini   magharibi mwa Ufaransana kaskazini magharibi mwa Uhispania.   Basque sanifu iliundwa miaka ya 1960kwa kuweka pamoja lahaja zake zote nne.

(ii) Ukuzaji MsimboSehemu   hii   hutekelezwa   na   wanaisimu   au   wataalamu   wa   lugha. Lahajailiyoteuliwa huwekewa kanuni au taratibu za matumizi.   Huku ni kukuza mfumowa  lugha  hiyo  k.v.  fonolojia  (othografia  na  matamshi),  sarufi,  msamiati  namaana.

102

Page 103: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Ukuzaji msimbo ni uundaji wa kiwangogezi (norm or standard) cha kiisimu kwamsimbo fulani wa kiisimu.  Shughuli hii hufanywa kupitia  kwa hatua tatu:

(a) Kukuza mfumo wa maandishi (graphisation)(b) usarufishaji (grammatication)(c) uleksikishaji (lexicalisation)Kukuza   mfumo   wa   maandishi Ikiwa lugha inayohusika ilikuwa ya kimazungumzo tu basi inatayarishiwa mfumowa   maandishi. Wakati   mwingine   kinachofanyika   ni   kwamba   wataalamuwanakopa  mfumo  wa  kimaandishi  wa  lugha  nyingine. Wataalamu  wanaamuamfumo  wa  maandishi  utakaoifaa  lugha  hiyo. Ni  ule  wenye  msingi  wa  sauti(vokali na konsonanti), silabi au maneno? Kwa mfano lugha ya Kiswahili kwanzailiandikwa kwa herufi za kiarabu kabla ya kutumia zile za Kirumi.

Usarufishaji Hii ni sehemu nyingine ya mchakato wa upangaji lugha.  Inahusu  kuunda kanuniza  kisarufi. Wanaamua  maumbo  na  miundo  ambayo  itakuwa  sanifu. Hali  hiihupunguza vibadala  au  tofauti  katika  matumizi  ya  kisarufi.Vitabu  vya  sarufihutayarishwa.

Uleksikishaji Hurejelea  uchaguzi  na  utayarishaji  wa  msamiati  unaofaa. Kimsingi,  hatua  hiiinahusu  kuamua  maneno  fulani  yatumiwe  katika  mitindo  ipi. Mara  nyingiuleksikishaji hushughulikia uondoaji wa maneno yenye asili ya kigeni kutoka kwalugha.   Hivi ndivyo  ilivyokuwa  wakati  Kihindi  kilisanifishwa  huko India, ambapomaneno   mengi   ya   mkopo   kutoka   Uajemi,   Uingereza   na   nchi   nyinginezoyaliondolewa  na  maneno  ya  Sanskrit  yakatumiwa. Makamusi  ya  lugha  hiyohutayarishwa.

103

Page 104: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Matokeo ya ukuzaji mfumo huwa othografia mpya, sarufi na makamusi ambayoni elekezi.

Kuhusu  lugha  ya  Kiswahili,  ukuzaji  mfumo  ulitekelezwa  na  kamati  ya  Lugha(Kiswahili) ya Afrika Mashariki kwa niaba ya serikali za Afrika Mashariki.

(iii)Utekelezaji.Utekelezaji unahusisha shughuli za waandishi, taasisi, na serikali katika kuitumiana kuisambaza lugha ambayo imeteuliwa na kukuziwa msimbo.   Hili linafanyikakwa  kutoa  au  kuchapisha  vitabu,  majarida,  magazeti,  na  makala  katika  lughahiyo   iliyokuziwa   msimbo. Wenye   mamlaka   huhakikisha   kwamba   lugha   hiiinatumiwa  pia  kwenye  vyombo  vya  habari  kama  kwenye  redio,  televisheni  namagazeti.

Huku wanaisimu wakihusika sana na sehemu ya ukuzaji msimbo, sehemu hii yautekelezaji hushughulikiwa na dola.

Inabidi  kuwepo  na  mbinu  za  kibiashara  za  kusambaza  lugha  hii. Waandishiwanaochapisha  vitabu  kwa  lahaja  hii  sanifu  wanatuzwa,  wafanyakazi  serikaliniwanaoifahamu lahaja hii sanifu wanapandishwa vyeo kazini, na lugha au lahajahii  inatangazwa  sana.   Wakati  mwingine  kunawekwa  sheria ambazo  zinahimizamatumizi yake.

Lugha hii inahitaji kupata ukubalifu katika jamii. Ikiwa itakubalika itawaunganishawatu wanaozungumza lugha tofauti.

Kuhusu   Kiswahili,   Kamati   ya   Lugha   (Kiswahili)   ya   Afrika   Mashariki   iliandaamashindano  ya  kuandika  insha  na  vitabu  katika  Kiswahili  sanifu  na  washindiwalituzwa. Pia kumekuwepo na tume mbalimbali za elimu ambazozimependekeza   sera   mbalimbali   za   lugha.Mfano   ni   tume   ya   Mackey(1981)

104

Page 105: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

iliyopendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa 8-4-4.   Katika mfumo huu wa elimu,Kiwahili ni somo la lazima katika shule za msingi na sekondari na linatahiniwa.

(iv)UpanuziHii  inarejelea  ukuzaji  wa  istilahi  na  mitindo  ili lugha iliyokuziwa msimbo  itimizemahitaji ya kisasa ya mawasiliano katika ulimwengu unaoendelea kasi kisayansina kiteknolojia.   Huku ni kuendelea tu na utekelezaji wa kiwangogezi ili kutimizadhima za lugha katika ulimwengu wa kisasa.  Sehemu muhimu ya upanuzi lughani hiyo ya kuunda na kusambaza istilahi mpya, na kuhakikisha kuwa kuna mbinumbalimbali za kuundia msamiati.   Hali kama hii inatokea katika lugha ya Kihausakule   Afrika   Magharibi   chenye   takriban   wazungumzaji   milioni   50.Kihausakinatumia mbinu tatu za kuufanya msamiati wake kuwa wa kisasa:(a) Ukopaji (kutoka kwa Kiarabu na Kiingereza)(b) Kupanua maana ya istilahi(c) Kubuni maneno mapya

Upanuzi  wa  lugha  huendelea  kila  wakati. Hii  ni  kwa  sababu  lugha  inahitajikujengwa upya kila siku kwani kuna dhana na vyombo vipya vinavyojitokeza kilasiku. Kuna  haja  ya  kuwa  na  taasisi  za  kushughulikia  upanuzi  wa  msamiati.Kuanzishwa kwa taasisi ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Kenyatta mwaka wa2003 ni hatua nzuri katika kuliendeleza jambo hili.

Kwa  mujibu  wa  Haugen  (1987),  ukuzaji  msimbo  na  upanuzi  ni  sehemu  yaupangaji  lugha  kiukongoo,  ilhali  uteuzi  na  utekelezaji  ni  sehemu  ya  upangajilugha  kihadhi  (pia  kifahari  na  kiurithi). Kielelezo  hiki  cha  upangaji  lugha  chaHaugen  ni  cha  kiduara  kwani  upangaji  lugha  kihadhi  unaweza  kutokana  naupangaji   lugha   kiukongoo.   Upangaji   kiukongoo   ukifaulu   au   ufeli,   utaathiriupangaji lugha kihadhi.

105

Page 106: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Zoezi

Kwa kurejelea mapendekezo ya Haugen (1972) ya mchakato wa upangajilugha, fafanua hatua nne za kufuata katika kupanga lugha.

6.5  Lugha ya Taifa na lugha Rasmi(Rejelea somo la 5.5 kuhusu mada hizi mbili).

6.6  SERA YA LUGHA NCHINI KENYA

Katika AKS   102:   Historical   Development   of   Kiswahili ,   Onyango   (2002)amefafanua swala la sera ya lugha nchini Kenya hasa baada ya Uhuru.   (Rejeleakazi hiyo)

Baada  ya  Uhuru,  sera  ya  lugha  nchini  Kenya  iliongozwa  na  mapendekezo  yatume  zilizoteuliwa  kuchunguza  maswala  yanayohusu  Kiswahili. Pia  sera  hiyoilitokana na maagizo ya watu mashuhuri.   Onyango ameshughulikia matumizi yaKiswahili katika elimu, shughuli za serikali na vyombo vya habari.

6.6.1  ELIMUTume  mbalimbali  ziliundwa  ili  kutoa  mapendekezo  kuhusu  matumizi  ya  lughashuleni na vyuoni.  Tume hizo ni kama zifuatazo:

(a) Tume ya Ominde (1964)The Kenya Education Commission Report

Tume hii ilitoa mapendekezo yafuatayo:(i) Lugha ya kufundishia shuleni iendelee kuwa Kiingereza.(ii) Kiswahili kiwe somo la kufundishwa shuleni bila kutahiniwa.(iii) Idara ya Kiswahili ianzishwe katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

106

Page 107: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(iv) Mafunzo ya Kiswahili kwa walimu wa shule za msingi yaendeshwe wakatiwa likizo.(Ominde 1964,  Chimera 2000).

Mambo yafuatayo yalitekelezwa:(i) Kozi za kuwapandisha walimu vyeo zilianzishwa katika Chuo Kikuu Kishiriki

cha Kenyatta kuanzia mwaka wa 1978.(ii) Idara  ya  Isimu  na  lugha  za  Kiafrika  ilianzishwa  katika  Chuo  Kikuu  cha

Nairobi mwaka wa 1969 ambapo Kiswahili kilianza kufundishwa.

(b) Tume ya Wamalwa (1972)“The Training Review Committee”

Tume hii ilitoa mapendekezo yafuatayo:(i) Lugha za Kimataifa kama vile Kifaransa na Kijerumani zifundishwe.(ii) Kozi  za  Kiswahili  zianzishwe  katika  Taasisi  ya  utwala  ya  Kenya  (Kenya

Institute  of  Administration)  na  Taasisi  ya  kutoa mafunzo  kwa watumishiwa serikali (Government Training Institute).   Hii ni kwa sababu kulikuwana  watumishi  wengi  wa  umma,  wakiwemo  wakuu  wa  wilaya  ambaohawakuweza kuwasiliana kwa lugha ya taifa.

Mambo yafuatayo yalitekelezwa:(i) Kozi za lugha za kigeni zilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi na ChuoKikuu cha Kenyatta.(ii) Vyuo vingi vya kutoa shahada za diploma nchini vilianza kufundisha lughaza kigeni.

(c)  Tume ya Gachathi (1976)The National Committee on EducationObjectives and Policies”

107

Page 108: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Tume   hii   ilitoa   mapendekezo   yafuatayo: (i) Kiswahili kiwe somo la lazima na la kutahiniwa katika shule za msingi, za

upili na vyuo vikuu.(ii) Kiingereza  kifundishwe kama  somo kuanzia  darasa  la kwanza kisha kiwe

lugha ya kufundishia kuanzia darasa la nne.(iii) Lugha za kienyeji zitumiwe kufundishia kuanzia darasa la kwanza hadi la

tatu.(iv) Walimu wengi  wa Kiswahili wapewe mafunzo.

(v) Elimu ya ngumbaro iendeshwe  kwa lugha za kienyeji.Yaliyotekelezwa:

Pendekezo  la  (i)  na la (iv)  yalianza kutekelezwa  tu  baada  ya  Tume ya  Mackaykuanzisha   mfumo   wa   elimu   wa   8-4-4.   Pendekezo   la   (iii),   na   la   (iv),hayakutekelezwa kikamilifu kwa sababu haikuwezekana kuchapisha vitabu katikalugha  zote  za  kienyeji  ambazo  ni  zaidi  ya 40, wala watu  wa kuviandika vitabuhivyo   hawakuwepo. Pia   haikuwezekana   kutoa   mafunzo   kwa   walimu   wakufundisha lugha hizo zote.

(d) Tume ya Mackay (1981)Report  of  the  Presidential  Working  Party  on  the  Establishment  of  the

Second University in KenyaTume hii ilipendekeza yafuatayo:

(i) Mfumo wa elimu wa 7-4-2-3 ubadilishwe na kuwa 8-4-4.(ii) Chuo  Kikuu  cha  pili  kianzishwe na  Kiswahili  kifunzwe  chuoni  humo

kama somo la lazima.  Hii  ni kwa sababu kulikuwa na wanafunzi wengiwaliofuzu  kutoka  chuoni  lakini  hawakuweza  kujieleza  kwa  ufasahakatika lugha ya taifa.

108

Page 109: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Mambo   yafuatayo   yalitekelezwa: (i) Mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulianzishwa mwaka wa 1982  ambapo Kiswahilikilianza kuwa somo la lazima na la kutahiniwa katika mtihani wa darasa la nane(K.C.P.E 1985) na kidato cha nne (K.C.S.E 1989).(ii) Chuo  Kikuu  cha  Moi  kilianzishwa  pamoja  na  Idara  ya  Kiswahili  mwaka

1987.(iii) Wanafunzi  wa mwaka  wa kwanza  katika  vyuo  vikuu vya kitaifa walianza

kufunzwa  vipengele  vya  Kiswahili  kama  sehemu  ya  kozi  ya  lazima  yamawasiliano.

Hii  ndiyo  tume  pekee  yake  ambayo  inaonyesha  kuwa  na  ajenda  bora  kuhusulugha  ya  Kiswahili  kama  lugha  katika  elimu. Kutokana  na  Tume  hii  tumeonaufanifu   katika   utekelezaji   wa   mapendekezo   yake.Kule   kukifanya   Kiswahilikutahiniwa  katika  darasa  la  nane  na  vile  vile  kukifanya  kuwa  somo  la  lazimakatika  shule  za  Sekondari  imetoa  mwelekeo  mpya  kwa  wakenya,  hasa  vijanaambao ni washiriki maalumu katika lugha hii, Chimerah (2000).

(e)  Tume ya Kamunge (1988)Report of the Presidential Working Party on Education and ManpowerTraining for the next decade and beyond

Uchunguzi uliofanywa na tume hiyo ulionyesha kwamba usajilishaji wa wanafunziwa  gumbaro  ulianza  kupungua  baada  ya  kufikia  kilele  mwaka  wa 1978.   Hii nikwa  sababu  vitabu  mwafaka  vya  kusomwa  katika  baadhi  ya  lugha  za  kienyejihavikuwepo.   Kwa   hivyo  ilipendekezwa  kwamba  vitabu  hivyo  viandikwe katikalugha  mbalimbali.Lakini kama  Mbaabu  (1991b)  anavyosema,  ingefaa  zaidikama vitabu hivyo vingeandikwa kwa Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa.

109

Page 110: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(f)  Tume ya Koech (1999)Yafuatayo   ni   baadhi   ya   mambo   yaliyopendekezwa :

(i) Mfumo   wa   elimu   wa   8-4-4   ubadilishwe   na   kuitwa   TIQET   (TotallyIntegrated  Quality  Education  and  Training)  ambapo  mtihani  wa  C.P.E.utafanywa katika darasa la saba na mtihani wa G.C.S.E. utafanywa katikakidato cha nne.

(ii) Lugha ya Kiswahili, Kiingereza na hesabu yawe masomo ya lazima katikashule za msingi na za upili.

(iii) Lugha  ya  Kiswahili  na  somo  la  fasihi  yafundishwe  kama  masomo  mawilitofauti.  Kadhalika lugha ya Kiingereza na fasihi ya Kiingereza yafundishwekama masomo mawili tofauti.

(iv) Wanafunzi  wa  darasa  la  kwanza  hadi  la  tatu  waruhusiwe  kujifunza  kwalugha zao za kwanza (lugha ya mama) kwa sababu wengi wao hawawezikuwasiliana  kwa  Kiingereza. Lakini  wale  wanaosomea  mjini  watumieKiswahili.

(v) Masomo  ya  kitendaji  (practical  subjects)  yafundishwe  katika  shule  zamsingi   lakini   yasitahiniwe   kwa   sababu   yanapoteza   wakati   na   tenayanawavunja moyo wanafunzi, wazazi na walimu.

(vi) Katika mtihani   wa C.P.E.,  masomo matano  pekee  yatahiniwe badala  yamasomo saba yanayotahiniwa katika K.C.P.E.(vii) Katika mtihani wa G.C.S.E., kiwango cha chini cha masomo

yatakayotahiniwa  ni  masomo  saba  lakini  alama  zitolewe  katika  masomosita ambayo mwanafunzi atafanya vyema zaidi.

(viii) Mtihani  wa  kidato  cha  nne  (G.C.S.E)  ufanywe  mara  mbili  kwa  mwakaambapo  wanafunzi  wanaofeli  mara  ya  kwanza  wanaweza  kuruhusiwakuufanya tena mara ya pili.

Baadhi   ya   mapendekezo   hayo   tayari   yameanza   kutekelezwa. Hata   hivyo,msimamo wa serikali ni kwamba utekelezaji kamili wa ripoti ya Koech utagharimu

110

Page 111: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

pesa nyingi sana, hivyo basi, baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa yatafanyiwamarekebisho kabla ya kutekelezwa.

Swali

Kati ya Tume hizi zote, ni ipi ambayo unaona imechangia sana ukuaji walugha ya Kiswahili?  Toa maelezo.

6.6.2.  SHUGHULI ZA SERIKALIMatumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa katika shughuli za serikali kwa ujumlayanajitokeza kwa njia zifuatazo:(i) Mawasiliano  ya  kila  siku  baina  ya  wananchi,  wanasiasa  na  maafisa  wa

serikali.   Kwa mujibu  wa  King ei (2001:02) moja  katika  ya sifa za usemiwa  kisiasa  nchini  Kenya  ni  kubadili  na  kuchanganya  msimbo,  na hali hiihutatiza maendeleo ya Kiswahili.

(ii) Bungeni: Ni  wabunge  wachache  sana  ambao  hutumia  Kiswahili  katikamijadala,hasai   wale   wanaotoka   Pwani   na   labda   wale   wasiokimuduKiingereza   vizuri.Kiingereza   ndicho   hutumiwa   kuendesha   shughuli   zaBungeni.

(iii) Magereza: Kiswahili  hutumiwa  katika  kuendesha  shughuli  za  magerezaingawa stakabadhi nyingi huandikwa kwa Kiingereza.

(iv) Katiba:   Hivi sasa katiba ya Kenya yapatikana tu kwa lugha ya Kiingereza.Katiba  Rasmi  mpya  ambayo  inajadiliwa  sasa  imetafsiriwa  kutokana  namapendekezo ya watu wengi kwamba katiba itafsiriwe ili wananchi wengiwaisome na kuzielewa sheria za nchi hii vilivyo.   Pamoja na kuzijua hakizao  ili  kutimiza  lengo  hilo  la kuwaelimisha wananchi kikatiba, msomi waKiswahili, Prof. Kimani Njogu, amekuwa akichapisha mfululizo wa makalayanayoitwa Zijue   Haki   zako  ,  katika  gazeti  la  Taifa  Leo.Katiba  mpyaimependekeza Kiswahili kuwa lugha rsmi pamoja na Kiingereza.

111

Page 112: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(v) Sherehe   za   Kitaifa :   Sherehe  muhimu  za  kitaifa  na  hotuba  zinazosomwakatika  sherehe  hizo  huwa  kwa  Kiingereza  lakini  Kiswahili  hupewa  nafasikatika mazungumzo ya ziada.

(vi) Mikutano:   Mikutano ya hadhara ya wanasiasa huendeshwa kwa Kiswahilikatika  sehemu  nyingi  nchini  isipokuwa  mikutano  ya  sehemu  fulani  zavijijini.

(vii) Vituo vya Polisi na kambi za wanajeshi pia hutumia Kiswahili.(viii) Viapo  vya  watumishi  wa  serikali  huendeshwa  kwa  Kiswahili.   Watumishi

hao ni pamoja na Rais, mawaziri na wasaidizi wao na pia mahakimu.(ix) Baadhi ya vyeti kama vile vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na vya kifo,hati

za  kusafiri,  fomu  mbalimbal  za  serikali  huandikwa  kwa  Kiingereza  naKiswahili pia.

Kwa  jumla  bado  kuna  mengi  ambayo  yanatarajiwa  kufanywa  kuhusu  lugha  yaKiswahili.   Serikali ya Kenya haijabuni sera dhahiri ya kuendeleza Kiswahili kamalugha ya taifa.   Mara nyingi lugha rasmi ya Kiingereza na hata lugha za kikabilahutumiwa   katika   miktadha   ambamo   lugha   ya   taifa   (Kiswahili)   ingepaswakutumiwa na jambo hili linatatiza maendeleo ya Kiswahili.

6.6.3  VYOMBO VYA HABARIVyombo  vya  habari  vinajumlisha  redio,  runinga,  magazeti,  majarida,  filamu  natarakilishi, yaani  kompyuta .   Idhaa zinazotangaza kwa Kiswahili nchini Kenya nipamoja  na  Kenya  Broadcasting  Corporation  (K.B.C), Nation F.M.,  Radio Citizen,Baraka  F.M.,  Pwani  F.M.,  Iqra  F.M.,  Kameme  F.M.,  Rehema  F.M.,  East  F.M.,Redio Sayari ,Eldoret, Radio Waumini, Kenya Television Network (K.T.N.), HopeF.M  na Family T.V.

Kwa mfano, katika redio ya KBC vipindi vinavyoendeleza Kiswahili ni pamoja naLugha Yetu Ongea Lugha Sanifu ya Kiswahili ,   Ukwasi wa Lugha ChemshaBongo   na   Ushikwapo Shikamana. Katika runinga ya K.B.C. kuna vipindi kama

112

Page 113: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Sanaa ya Kiswahili ,   Vituko   na   Burudani la Taarabu .   Katika redio ya NationF.M.,  kuna  kipindi  cha   Kamusi  ya  Changamka   na  katika  runinga  ya  Nation,kuna   Lulu  ya Nation .  Vipindi  vya kanisa vinavyoonyeshwa  kwenye televisheniau kupitia redio vimechangia pakubwa ustawi wa Kiswahili.

Kulingana  na  Musau  (2001:39)  tatizo  kubwa  ni  kwamba  nchini  Kenya  hakunasera  dhahiri  katika  vyombo  vya  habari  inayoendeleza  Kiswahili  na  kuhifadhiutamaduni  wa  kitaifa. Inaonekana  kwamba  vituo  vingi  vya  redio  na  runingahutangaza kwa Kiingereza na kuonyesha vipindi vya Kigeni.

Zoezi

Tathmini  matumizi ya lugha katika vyombo vya habari nchini Kenya.Zingatia sarufi na matumizi ya sheng; pamoja na mielekeo ya watu.

Kwa  upande  mwingine  uchapishaji  wa  magazeti  ya  Kiswahili  nchini  Kenya  nijambo la kusikitisha sana.   Hivi sasa kuna magazeti mawili tu, gazeti la   Taifa      Leo   

ambalo  huchapishwa  kila  siku  na  toleo  la  Jumapili,  na  pia  gazeti  la      Jamhuri   

ambalo hutulewa mara chache.         Taifa      Leo      ndio gazeti kongwe zaidi la Kiswahilihapa nchini.   Gazeti la Jamhuri ni jipya na halijakita mizizi kikamilifu.   Ni gazetiambalo  lina  mwelekeo  unaofaa  wa  kukuza  Kiswahili  na  linashughulikia  madangumu zinazohusu lugha na maisha ya Kijamii.   Gazeti hili lina uwezo wa kuletasura mpya katika ramani ya vyombo vya habari nchini Kenya.   Kinyume na haliilivyo  nchini  Tanzania,  nchini  Kenya  magazeti  mengi  na  majarida  huchapishwakwa Kiingereza na lugha za kikabila kama vile Kikuyu na Dholuo.

Kuna   pia   vijarida   (newsletters)   vya   Kiswahili   ambavyo   huchapishwa   namakampuni  ya  kibinafsi  na  mashirika  ya  kidini  lakini  havisambazwi  sehemunyingi. Kwa   ujumla   magazeti   ya   Kiswahili  yanayochapishwa   nchini   Kenyayamechangia  ukuzaji  wa lugha  ya  Kiswahili kwa  njia  nyingi ikiwa ni pamoja na

113

Page 114: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

kuandika   habari,   makala,   mashairi,   mafumbo   ya   kujaza   maneno,   methali,vitendawili, tahakiki za vitabu vipya, hadithi, matangazo, majaribio ya mitihani yaKiswahili,  maoni  na  hata  kuchora  vibonzo. Onyango  (2000:8)  ameeleza  kwautondoti mchango wa magazeti katika ukuzaji wa Kiswahili; amesisitiza kwambamagazeti  yanapotumiwa  vilivyo,  yanaweza  kustawisha  lugha  hii  na  wakati  huohuo kuwafahamisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha kikamilifu wananchi.

Zoezi

Tathmini ubora wa magazeti ya Kiswahili yanayopatikana humu nchini

Swali

Huwezi kutenganisha lugha na siasa.Jadili kauli hii kwa kurejelea haliya lugha nchini Kenya.

HitimishoKatika somo hili, tumezungumzia swala la upangaji lugha na hatua zote ambazohurejelewa  katika  upangaji  lugha.  Tumeangalia  sera  ya  lugha  nchini  na  jinsiambavyo  tume  mbalimbali zimechangia katika  kuendeleza Kiswahili.Tumeona  piajinsi  shughuli  za  serikali  zinavyochangia,  na  mwisho  tumeangalia  mchango  wavyombo vya habari.

Marejeleo TeuleChimera, R. (2000)   Kiswahili:      Past,      Present      and      Future      Horizons   .  Nairobi.

Nairobi  University Press.

114

Page 115: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Haugen, E.  (1956)      Bilingualism      in      the      Americas   .  University of Alabama Press.Tuscaloosa.

_______ (1983)   The Implementation of Corpus Planning: Theory and Practice .Katika      Progress      in      Language   ,  eds.  J.  Cobarrubias  and  J.A.  Fishman.Mouton.  Berlin.

King ei, G. (2001)   Matatizo ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari:Mifano  kutoka  Kenya, katika      Swahili      Forum      VII     German.   University ofKoln Uk. 45-56.

Mbaabu, I. (1996)   Language      Policy      in      East      Africa   , Educational Research andPublication; Nairobi.

Mesthrie R. et.al. (2000)   Introduction      to      Sociolinguistics   .  Edinburgh.  EdinburgUniversity Press.

Mukhwana, A. (1995)   Kiswahili Sanifu:  Je, kipo   katika   Baragumu   , Juzuu 2 Nam1 & 2, Maseno, Chuo Kikuu cha Maseno.

Musau, P. (2001)   Freeing the Airwaves or Cultural Enslavement:  The case ofmedia   in   Kenya katika   Kiswahili:   A   tool   for   Development Themultidisplinary Approach Eldoret: Moi University Press.

Onyango, J.O. (2000)   Magazeti ndio uti wa mgongo katika ustawishaji waKiswahili  katika Gazeti la Jamhuri, Desemba 17-30, 2000 uk. 8.

____________ (2002) AKS 102: Historical     Development   of       Kiswahili :Nairobi.  Institute of Open Learning.  Kenyatta University.

Rubin, J.R. na Jernudd, B. (1972)   Can      Language      Be      Planned   ? University Press.Hawaii.  Honolulu.

115

Page 116: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

SOMO LA SABAISIMUJAMII NA ELIMU

7.0   UTANGULIZIIsimujamii-Elimu  ni  kitengo  cha  Isimu-jamii  ambacho  hujihusisha  na  uhusianouliopo baina ya lugha na elimu. Tafiti nyiingi zilizofanywa  zimezingatia mazingiraya darasani.   Hata hivyo, bado kuna maswali mengi kuhusu lugha katika elimu-iso rasmi kama vile elimu ya gumbaro na hata elimu-huria.

Katika  somo hili tutatoa  maana  ya  elimu  na ujifunzaji.   Kisha tutaonyesha jinsilugha  katika  fasiri yake  pana  ni  muhimu  katika  ufunzaji  na tajriba za ujifunzajiambazo  hutokea  shuleni. Tutaangalia  lugha  katika  elimu  pamoja  na  sera  yalugha katika elimu na mwisho tutaangalia lugha ya darasani.

7.1   Madhumuni

Kufikia mwisho wa somo hili, tunatarajia kuwa utaweza: Kueleza maana ya elimu, ujifunzaji na ufunzaji. Sera ya lugha katika elimu nchini. Matumizi ya lugha darasani.

7.2 UFUNZAJI, UJIFUNZAJI NA USOMAJIKatika kila  jamii   huwa  kuna  arifa ambazo  kila mwanajamii anahitaji kupata.Vile  vile  anahitaji  kupata  maarifa fulani  ili  aweze  kutekeleza  majukumu  yakekama mwanajamii.

Elimu hapa inarejelea ile hali ya kufunza na kujifunza (teaching and learning)ambapo wanajamii huweza kupata arifa hizi pamoja na maarifa, Mesthrie (2000).Aghalabu ufunzaji husimamiwa na watu waliopewa mamlaka katika jamii na wao

116

Page 117: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

hufanya  hivyo  kwa  niaba  ya  jamii  kwa  minajili  ya  watoto  wao. Harakati  hiihujulikana kama ujamiishaji wa mtoto (child sociolization).

Hata hivyo ufunzaji pia huibuka miongoni mwa vizazi (generations),kwa   mfano   ,   mtu   anapojifunza   jinsi   teknolojia   mpya   kama   vile   tarakilishiinvyofanya kazi. Hapa hivi tunaona  kuwa watu wazima pia huwa wanafunzi.

Katika jamii za Kijadi, dhana ya elimu inajumuisha kule kuwatayarisha vijana kwakuwatia jandoni au sherehe nyingine ambazo zinaonyesha mpito kutoka hali yautoto hadi utu uzima.

Elimu   pia   inahusisha   uchunguzi   na   uigaji   wa   wasanii   na   watu   wenginewaliomakinika katika kazi za kisanii.  Mambo yote yanayohusiana na utambaji wahadithi au malumbano ya hadharani ni sehemu ya ufunzaji na ujifunzaji.

Katika jamii za kisasa, utoaji wa arifa na maarifa hutokea kote katika jamii.  Hatahivyo  jukumu  rasmi  kuhusu  elimu  linapewa  taasisi  maalumu hasa  shule  nahuwa  haiachiwi  watu  binafsi. Mambo  wanayosoma  watu  katika  mazingira  yashule  huenda  yakawa  tofauti  sana  na  yale  wanayojifunza  nyumbani  au  mahalipopote pale katika jamii.   Tofauti kati ya matumizi ya lugha ya nyumbani na yashule ndio huzua matatizo katika elimu.   Hivyo basi lugha na elimu ni mada iliyona shauku kubwa katika tafiti za kiisimu-jamii.

Zoezi

Mfumo wa jadi wa elimu ulikuwa tofauti kwa njia gani na mfumowa sasa?

117

Page 118: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

7.3 LUGHA KATIKA ELIMUMifumo  ya  elimu  kote  ulimwenguni  imetambua  umuhimu  na  nafasi  ya  lughakatika  harakati  ya  kujifunza  na  kufunza.  Lopez  (2000)  anachukulia  harakati  zakujifunza na kufunza kuwa ni ubadilishanaji mawazo na mawasiliano katika uasiliwake. Anaona  kuwa, mawasiliano  kwa  upande  mmoja  ni  sharti  muhimu  iliujifunzaji   na   ufunzaji   uweze   kutekelezwa.   Kwa   upande   mwingine,   anaonamawasiliano kama njia na namna walimu na wanafunzi wanavyowasiliana katikashughuli zao za darasani.  Na hii ndio sababu kuwa kote ulimwenguni mfumo waelimu  unasisitiza  mawasiliano  na  lugha  na  huzichukulia  kama  vitengo  muhimuvya  mtalaa shuleni. Sio  tu  katika  lugha  na mawasiliano  ndio tunaona uhusianowa karibu, bali pia kati ya lugha na fikra (Crystal 1994; Lopez 2000).

Ingawa  swala  la  lugha  ni  muhimu  na  ni  jambo  la  uhalisia  katika  harakati  yaujifunzaji  na  ufunzaji  katika  jamii  zote,  kuna  matatizo  ambayo  huibuka  katikajamii  zenye  wingi  lugha  (Tazama  Sura  ya  4  kwa  maelezo  kuhusu  uwili-lugha),ambapo wanafunzi hujiunga na mfumo wa shule wakiwa wanafahamu lugha zanyumbani  (au  lugha  ya  mama)  ambazo  mara  nyingi  huwa  tofauti  na lugha  zaelimu.  Katika hali hii, wanafunzi hawapati tu lugha zao za nyumbani ili kuzitumiakatika  kupata  maana  ya  ulimwengu  unaowazingira  bali  pia  umilisi katika  lughazao za kwanza huwa kitangulizi cha kuweza kujifunza lugha nyingine.   Hizi lughanyingine  ambazo  mtoto  anakumbana  nazo  huwa  ni lugha za mawasiliano panakatika jamii (Tazama Somo la 4 kuhusu lingua franka).

Watoto katika jamii kama hizi wanazo haki na wanatarajiwa kujifunza lugha hiziili waweze kuwa  waamilifu  katika  serikali yao  na ulimwengu  mzima kwa jumla.Matumizi ya lugha ya mama kama lugha ya ufundishaji inachukuliwa kuwa ndiohumsaidia  mtoto  kukuza  dhana  ambazo  humsaidia  kupata  ujuzi  kwa  urahisikatika lugha ya pili au hata ya tatu; na vivyo hivyo kumpa mtoto tajriba kuhusuutamaduni wa jamii zao (Muthwii, 2002; Sifuna, 1980; Parry, 2000; Milon, 1992).Isitoshe, lugha ya ufunzaji ni njia ambayo wanafunzi wachanga huweza kueleza

118

Page 119: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

tajriba zao katika harakati za kusoma.   Hivyo basi, swala la lugha katika elimu niswala  muhimu  katika  harakati  ya  ujifunzaji  na  ufunzaji.Ni  kwa  sababu  yaumuhimu  huu  wa  lugha  ndio  tunapata  kuwa  sera  za  lugha  katika  jamii  zenyewingi  lugha  zinahitaji kuwa  wazi  ili kuonyesha uhusiano unaohitaji kuwepo  katiya lugha zinazotumika katika jamii na zile za elimu.

Umuhimu wa nafasi ya lugha katika elimu unaweza kupanuliwa zaidi.  Tunawezakudai  kuwa  katika  kumfundisha  mtu  binafsi,  njia  ya  mafunzo  (medium  ofinstruction) ni njia ambayo mwanafunzi kama huyu anaweza kupata na kuelewaarifa ambazo  zitamsaidia aweze kupata  maarifa  maishani mwake  na kuyatumiamaarifa  hayo  na  vilevile  kuweza  kuelewa  harakati  ya  jinsi  anavyokua,  ikiwemokuelewa  ukomavu  wa  kiuana. Utumiaji  wa  maarifa  aliyoyapata  hujumlishamielekeo  kuhusu  kazi  na  uwezo  wa  kufanya  kazi  hiyo.Maarifa  ya  maisha  nipamoja na kuelezwa kuhusu mielekeo, amali na uwajibikaji katika jamii.

Zoezi

Je, wewe ulifahamu lugha ngapi kabla ya kujiunga na shule ya msingi?Ni matatizo gani uliyokumbana nayo shuleni katika kujifunza lugha mpya?

7.3.1 SERA YA LUGHA NA MATUMIZI NCHINI KENYASera  ya  lugha  nchini  Kenya  imefasiriwa  na  kufanywa  upya  mara  nyingi  katikamiongo   iliyopita   (Tazama   Somo   la   Sita). Hata   hivyo   mabadiliko   hayayameathiriwa  na nadharia  zinazobishana, mielekeo tofauti, mitazamo tofauti yakisiasa  na  shauku,  na  kutokuwa  na  uamuzi.Mambo  haya  yote  yameathiripakubwa  harakati  ya  ufunzaji  na  ujifunzaji.   Hata ingawa sera ya hivi karibuniimefaidika na tajriba za awali bado zinatoa changamoto kwa washikadau katikaelimu,( Muthwii,2002).

119

Page 120: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

(Katika  Somo  la  6,  tumeangalia  sera  ya  lugha  kulingana  na  mapendekezombalimbali ya Tume zilizoundwa.  Ipitie sehemu hiyo tena).

Katika  sehemu  iifuatayo  tutaangalia  sera  ya  lugha  kwa  kuzingatia  elimu  nchiniKenya.

7.3.2 HALI ILIVYOKUWA NCHINI KENYAKabla   ya   ripoti   kuhusu   Elimu   ya  Waafrika  nchini  Kenya  mwaka   wa  1949,wanafunzi  wa  shule  za  msingi  walifunzwa  kupitia  lugha  zao  za  mama  katikamiaka  mitatu  ya  mwanzo  ya  shule,  (Colony  and  Protectorate  of  Kenya  1949).Hata hivyo, ripoti hii ilipendekeza kwamba lugha ya Kiswahili ifanywe kuwa lughaya  kufunzia  katika  viwango  vya  chini  vya  elimu. Ripoti  ya  mwaka  wa  1951,kuhusu   sera   ya   Elimu   na   utekelezi  Afrika   Mashariki   na   kati,  kwa   upandemwingine,   ilipendekeza   kuwa   lugha   ya   Kiswhaili   iondolewe   kabisa   katikamadarasa ya awali ya shule za msingi.

Ripoti  iliyofuata  hii  katika  mwaka  wa  1953  ilipendekeza  kwamba  katika  miakaminne ya mwanzo, lugha wenyeji iwe lugha ya kufunzia (The Nuffield Foundationand  the  colonial  Office  1953). Mapendekezo  ya  ripoti  hii  kuhusu  lugha  yakufunzia yalitekelezwa mara moja na serikali ya kikoloni.  Hivyo basi katika miakaya hamsini, wanafunzi wote wa shule za msingi nchini walifunzwa kupitia lughazao mbalimbali katika miaka minne ya mwanzo ilhali Kiingereza kilifunzwa kamasomo  kwa  miaka  miwili  au  mitatu  na  baadaye  ikawa  lugha  ya  kufunzia  katikadarasa la 5 8 (Sifuna, 1980).

Kufikia  katikati  ya  miaka  ya  hamsini,  kulikuwa  na  kutoridhika  miongoni  mwawatu kuhusu matokeo ya mitihani ya kitaifa miongoni mwa watoto wa Kiafrika naKieshia  (Kihindi)  hasa  katika  uandishi  ikilinganishwa  na  watoto  wa  Kizungu,(Sifuna,1980).   Walidai kuwa matokeo haya mabaya yalitokana na matumizi yalugha  ya  mama  kama  lugha  ya  kufunzia  kwa  muda  mrefu  katika  masomo  ya

120

Page 121: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

msingi. Hivyo  basi  wizara  ya  elimu  ilianzisha  kituo  maalumu  katika  idara  yaukaguzi wa shule mwaka wa 1957.   Kituo hiki maalumu kilikuwa na jukumu lakutayarisha  vifaa  vya  ufunzaji  na  kuwatayarisha  walimu  kwa  jaribio  la  kuanzakutumia  Kiingereza kama  lugha  ya kufunzia kuanzia  darasa la kwanza.   Jaribiohilo  ambalo  lilianzishwa  katika  shule  za  watoto  wa  Kieshia,  lilipanuka  kwa  kasikupitia mvuto wake kama lugha ya kufunzia na kwamba kulikuwa na vifaa vyakufunzia.   Basi, kile kilichoanza kama jaribio la lugha ya Kiingereza kama lughaya kufunzia, ndio ulikuwa mwanzo wa mapinduzi katika elimu katika shule zoteza   msingi   nchini  Kenya. Mapinduzi   haya   yalijulikana   kama New   PrimaryApproach (NPA), (Mbaabu 1996: sura ya 6).   Kulingana na Sifuna (1980) katikamwaka wa 1961, kulikuwa na shule moja tu iliyotumia vifaa vya kufunzia lakinikufikia mwaka wa 1965, takribani madarasa 2,871 yalikuwa yanatumia vifaa hivi.Mfumo wa NPA ulisisitiza mtazamo wa kumweka mtoto kuwa katikati au kitovucha masomo kupitia lugha ya Kiingereza kama lugha ya kufunzia katika mtaalamzima wa shule ya msingi.   Lugha ya Kiswahili ilifunzwa kama somo la lazima,(Muthwii, 2002).

Mabadiliko  hayo  ya  ghafla  katika  elimu,  falsafa  na  mbinu  yaliandamana  namatatizo chungu nzima kulingana na Hutasoit na Prator (1965) kwa mfano, idadiya  wanafunzi  ilizidi  walimu  na  vifaa  vilivyokuwepo  ili  kutekeleza  kazi  hii  nzuri.Tulikuwa na walimu wengi ambao hawakuwa wamepata mafunzo ya ualimu nawalimu hawa walipewa majukumu ya kufunza NPA  baada ya kupatia kozi fupi.Vile vile ukaguzi wa shule haukutekelezwa vilivyo na majengo ya shule na vifaavya kufunzia havikutosha.  Matokeo yalikuwa, hapakuwa na usare wowote katikaviwango  vya  mpango  wa   NPA . Sehemu  ambazo  zilifaidika  na  mpango  huuzilikuwa  ni  sehemu  za  mjini.   Matatizo  haya,  pamoja  na  maoni  kwamba  lughamama ndio lugha ambayo mwanafunzi anaweza kusoma na kuandika nayo vizurikatika darasa la kwanza, yalizua mabadiliko mengine katika mjadala wa lugha yakufunzia.

121

Page 122: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Katika  kuendelea  kuunga  mkono  lugha  mzazi,  Anderson  (1970  :70)  alisemaTajriba   ya   muda   mrefu   imeonyesha   kuwa   lugha   wenyeji  kama   lugha   ya

kufunzia,  kielimu  ni  bora  kwa  sababu  ili  pawe  na  ufunzaji  wa  maana,  lazimapawe  na  asilimia  fulani  ya  mtagusano  kati  ya  maisha  ya  mtoto  nyumbani,  nalazima  ufundishaji  uhusishe dhana  zilizojengwa  na  mtoto  katika  tajriba zake zaawali kabla hajajiunga na shule.Kufikia   miaka 1976, lugha mzazi ilichukuliwakuwa  ndiyo  lugha  bora  kutumiwa  katika  shule  nyingi  za  msingi. Katika  shuleambazo hapakuwa na lugha ya mama moja, kwa mfano  sehemu za mjini, lughaya Kiswahili ilitumika( Mbaabu 1996).   Kufikia sasa, sera ya lugha imependekezakuwa katika shule za msingi, lugha ya mama itumike   kama lugha ya kufunzia(hadi  darasa  la  tatu). Kiingereza  na  Kiswahili  zinafunzwa  kama  masomo  yalazima,  lakini Kiingereza  kinatumika  kama lugha  ya kufunzia masomo mengine,Mbaabu (ibid).

Zoezi

Ni matatizo gani yanayokumba wizara ya elimu kuhusu kuwa na lughaza   mama   kama   lugha   za   kufunzia   nchini?   Ni   vipi   tunaweza   kuyasuluhisha?

Kwa  kuzingatia  nafasi  ya  lugha  katika  uwanda  wa  kujifunza  na  kufunza  kamatulivyoeleza,  inaweza  kuchukuliwa  kuwa  sera  za  lugha  ambazo  zimechukuliwakwa  sababu  mbalimbali  zinazua  mtanziko  kwa  wazazi,  wanafunzi  na  walimukatika nchi hii yenye wingi-lugha.  Kwa mfano, wazungumzaji wengi ni wanauwiliuwili au wana-wingi lugha, hivyo basi wao huchagua Kiingereza kama lugha yakufunzia katika shule za msingi.  Kwa sababu Kiingereza ni lugha ya elimu ya juu,wale  ambao  huchagua  Kiingereza  kama  lugha  ya  kufunzia  kuanzia  darasa  lakwanza  huwa  hatua  moja  mbele  ya  wale  wanaotumia  lugha  ya  mama  auKiswahili.  Na hii ndio hali ambayo husababisha kutokuwa na usawa kielimu.  Vilevile hali hii inakanusha sera inayohimiza lugha ya mama kama lugha ya kufunziana ukweli uliopo kuwa mtoto anapoendelea kukua katika mfumo wa elimu, lugha

122

Page 123: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

ya Kiingereza hutawala lugha nyingine.   Lugha ya mama hupewa nafasi ya chinisana baada ya masomo ya shule ya msingi na inaondolewa kabisa katika mitihaniya Kitaifa katika elimu ya msingi.   Hata hivyo, watoto wenyewe hawaoni lughazao zikipewa majukumu katika sekta nyingine yoyote isipokuwa nyumbani.   Kwasababu hiyo, jukumu la kukamilishana ambalo linahitajika kuwepo baina ya lughaya elimu na ile ambayo inatumika katika mazingira mapana ya uchumi-jamii yamtoto  hayapo. Hata  katika  hali  zile  ambazo  tunaona  majaribio  yakifanyika  ilikutekeleza  sera  ya lugha,  walimu  katika  jamii nyingi hawawezi kutekeleza serahiyo  kwa  sababu  ya  matatizo  ya  kutokuwa na  vifaa vya  kutosha na  pia wengiwao hawazifahamu barabara lugha zao za kwanza.

Zoezi

Umeombwa kutoa mhadhara kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili katikaMaisha ya mwanafunzi, kwa  wanafunzi ambao hawafanyi vizuri katikasomo   hili.  Je, ni mambo gani utakayowaelezea?

7.3.4   LUGHA YA DARASANITafiti  nyingi  zimefanywa  katika  nchi   za magharibi  na hata  humu  nchini katikakuangalia uhusiano uliopo kati ya lugha na elimu, (Meshrie ,2000).

Watfiti hawa wamekubaliana kuwa ufunzaji na ujifunzaji unaoendeshwa darasaniunategemea  matumizi  ya  lugha  kwa  kiwango  kikubwa.   Tafiti  hizi  zimegunduakuwa hata ingawa walimu watatumia vifaa-saidizi vya ufunzaji kama vile picha ilikuwasilisha  arifa  mpya,  mazungumzo  ya  mwalimu  ni  njia  ya  msingi  katikaufunzaji  darasani  (taz  Muthwii,  2002).Kwa  upande  mwingine,  mwanafunzianatarajiwa  asikilize,  ajibu  maswali  na  aulize  maswali. Muhimu  pia  ni  lugha-andishi  ambayo  inapatikana  darasani.Lugha  hii  andishi  inahusu  kuandikaubaoni, kusoma vitabu maktabani na vifaa vingine.

123

Page 124: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kutokana  na  umuhimu  wake  katika  swala  la  ufunzaji  na  ufundishaji,  lugha  yadarasani  inadhibitiwa  na  mwalimu. Walimu  ndio  huwa  waongezi  darasani  nalugha   ya   mwalimu   ndio   huwa   sajili   ya   msingi   wa   matumizi. Wanafunzihawachukui  nafasi kubwa katika mazungumzo ya darasani.

Bali  na  kuwa  wazungumzaji  wakuu  katika  maongezi  ya  darasani,  walimu  piahuwa  wasimamizi  wa  mazungumzo  hata  kama  wao hawazungumzi.   Wao ndiohuamua mada zitakazoshughulikiwa darasani na hutawala haki ya kila mtoto yakuongea  kuhusu  mada  hizo.Pia  wanasimamia  muda  au  wakati  ambao  kilamwanafunzi atatumia katika mjadala.

Mwalimu  pia  huwaongoza  wanafunzi  katika  mbinu  za  uandishi.   Huwaonyeshatofauti kati ya uandishi na mazungumzo ya ana kwa ana.

Tofauti kati ya lugha ya darasani na lugha ya nyumbani pamoja na tamaduni zawatu, ni baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kusababisha matatizo ya lughaanayokumbana nayo mwanafunzi.   Kwa mfano, Mesthrie (2000) ananukuu utafitiuliofanywa  na  Susan  Phillips  (1972  na  1983)  kuhusu  tofauti  baina  ya  mamboyanayotawala   mazungumzo   na   ukimya   unaopatikana   katika   mazingira   yakinyumbani nchini India na yale yanayopatikana katika shule za umma.   Katikajamii  hizi  watoto  hufunzwa  katika  maisha  yao  ya  awali  kuwa  mazungumzo  nimambo yaliyotengewa watu wazima; watoto wapo kusikiliza tu mazungumzo yawatu  wazima,  na  wanatakiwa  wajifunze  tu  kile  wanachosikia. Inachukuliwakuwa watoto hawa wakiwa watu wazima, watakuwa wamepata arifa za kutoshakuzungumzia au kuwaambia watoto wao na hata vizazi vijavyo.

Katika mandhari ya darasani, maana za kijamii ambazo zinahusishwa na ukimyazinatafsiriwa  tofauti  na  walimu  na  watawala  wengine. Katika  mazingira  yashuleni, ukimya   wa mwanafunzi unaashiria mwanafunzi kutomaliza kazi ya ziada

124

Page 125: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

ya nyumbani, kutokuwa mzingativu darasani hasa kwa mijadala ya darasani aukukataa kushiriki darasani.

Hivyo basi, tofauti za utamaduni kati ya mazingira ya nyumbani na shule huzuamatatizo ya mawasiliano  katika elimu.

Swali

1.  Sera ya lugha ni kipengele muhimu katika elimu.  Tathmini ukweli wakauli hii ukirejelea hali ya lugha nchini Kenya kwa ujumla.

2. Lugha na utamaduni huingiliana sana. Fafanua kauli hii kwa kurejelea seraya lugha ktika elimu.

7.4 HITIMISHO

Katika somo hili, tumeshughulikia swala na lugha na elimu.  Tumeangaliadhana ya elimu, ufunzaji na ujifunzaji na usomaji.  Tumeangalia sera yalugha kuhusu elimu nchini, na mwisho tumeangalia swala la lugha ya darasanina lugha ya nyumbani na jinsi utamaduni ambao amekulia mtoto unaathirimatumizi ya lugha darasani.

125

Page 126: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Marejeleo TeuleColony and protectorate of Kenya (1949):  African Education in Kenya.      Report      of      

the Committee  appointed  to  inquire  into  the  Scope,  Content,  Methodsand   Administrtion   of   the   African   Education   (Beecher  Report)  Nairobi:Government Printer.

Crystal, D. (1994)   The      University      of      Cambridge      Language      Encyclopaedia   .Madrid. Taurus.

Hutasoit, M. and Prator C. (1965)   A      Study      of      the      New      Primary      Approach      in      the   

Schools   of   Kenya .  Ministry of Education & Ford Foundation.Lopez, L.E. (2000)   Cognition, Culture, Language and Learning:  An introduction

to  Education  Planners  in  Multilingual  and  Multicultural  Contexts   KatikaDistance   Learning   Course   in   the   language   of   Instruction   in   Basic   Education (Nov. 27, 28, 29, December 2000).

Mbaabu, I. (1996)   Language      Policy      in      East      Africa   , Nairobi Educational Researchand Publication.

Mesthrie, R. et.al. (2000)   Introducing      Sociolinguistics   , Edinburg, EdinburgUniversity Press.

Milon, J.P. (1992)   Discourse in the Primary English syllabus of Botswana  katikaUdo  Bude  (ed.)      Culture      and      Environment      in      Primary      Education   . Thedemands   of   the   Curriculum   and   the   Practice   in   Schools   in   Sub-Saharan Africa. Bon.  Education  Science  and  Documentation  Centre. GermanFoundation for International Development.

Muthwii, M. (Mha.) (2002)   Language,      Policy      and      Practices      in      Education      in      Kenya   

and   Uganda .  Nairobi, Phoenix Publishers.Mwaura, P. (2003)  Children learn Better in Mother Tongue Katika   Daily      Nation   ,June

19, 2003.Parry, K. (Mha.) (2002)   Language      and      Literacy      in      Uganda   :   Towards      a      Sustainable   

Reading   Culture .  Kampala.  Fountain Publishers.

126

Page 127: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Sifuna, D.N.  (1980)      Short      essays      in      Education      in      Kenya   . Nairobi  KenyaLiterature

Bureau.

SOMO LA NANELUGHA NA JINSIA

127

Page 128: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

8.0 UTANGULIZIMatumizi  ya  baadhi  ya  maneno  katika  jamii  huwekewa  vizuizi  mbalimbali. Hiihaimanishi kwamba maneno hayo ni mabaya au mazuri.   Lakini inamaanisha tukuwa hali hii inaakisi mitazamo ya jamii au mtu binafsi kuhusu maneno hayo.

Katika  somo  hili  tutazungumzia  swala  la  lugha  na  jinsia.   Tunataka  kuonyeshajinsi  matumizi  ya  maneno  huakisi  mielekeo  ya  jamii  kuhusu  kikundi  fulani  chawanajamii.   Kwa mfano, ni kwa nini wanawake watarajiwa kuongea kwa namnafulani wala si nyingine.

8.1  Madhumuni

Tunatarajia kuwa kufikia mwisho utaweza:Kuonyesha jinsi lugha inavyoakisi mielekeo ya jinsia katika jamii.

8.2 Jinsia na isimu jamiiHoja  kwamba  wanawake  na  wanaume  hutumia  lugha  tofauti  lina  misingi  yakekatika  isimu-mila  (folk  linguistics). Dhana  hii  hurejelea  seti  fulani  za  imanikuhusu lugha.

Utafiti kuhusu lugha ya wanaume na wanawake umeanza katika miaka ya 1920,1930 na 1940.  Hata hivyo tafiti kuhusu jinsia na lugha kama eneo pana la utafitizimeanza mwanzo wa miaka 1970.   Hivyo basi lugha na jinsia ni mada ambayoina  shauku  kubwa  sana  na  ni  muhimu  kwa  sababu  ya  ule  mchango  wake  wakusaidia  kuelewa  lugha  na  jinsi  inavyofanya  kazi  na  hasa  katika  uwanda  waisimu-jamii.

Kama mada ya utafiti, swala la lugha na jinsia limepata mchango kutoka maeneombalimbali  kama   vile   anthropolojia,   uchanganuzi   lugha,  elimu,  nadharia  zaKifasihi, Saikolojia ya jamii na elimu-jamii.

128

Page 129: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

8.2   LUGHA  YA WANAWAKE NA WANAUMECoates   (1986)   anadai   kuwa   lugha   haina   jinsia   lakini   inaweza   kutumiwakuonyesha uana katika jamii. Jinsia ni neno linalotumiwa kuelezea mambo yoteyanayohusiana na hali ya kuwa mke au mume.

Sifa  inayobainika  kati  ya  lugha  na  jinsia  ni  mielekeo  ya  watu  kuhusu  manenofulani  katika  lugha  husika.  Mielekeo  kama dhana  ni mitazamo ya  watu  kuhusumaisha.   Mitazamo  hii  inaweza  kuwa   inayofaa  au  isiyofaa kutegemea na jamiihusika. Mielekeo ya Kijinsia inachukuliwa kama mitazamo ya jamii kuhusu hali yaKijinsia na mambo yote au majukumu wanayotekeleza kulingana na tofauti zaokijinsia.

Lugha kama chombo cha jamii kinafungamanishwa na miundo ya kijamii.   Hivyobasi tofauti za matumizi ya lugha zinatokana na mielekeo hii.   Katika muktadhawa kijamii, wanawake na wanaume wanatofautiana na hivyo basi jamii huwapamajukumu  tofauti  na  kwa  sababu  hii,  jamii  inatarajia  tabia  tofauti  kutoka  kwawanajamii kulingana na jinsia yao.  Hivyo basi, lugha inayotumika inaakisi tofautiza kifikra, kitabia na mahusiano yao.   Kwa kutegemea mielekeo hii makundi yakijinsia   yanaweza   kusawiriwa   kwa   njia   tofauti,   na   matumizi   ya   lugha   nimojawapo.

Miiko ni jambo linaloathiri matumizi ya lugha kijinsia.   Miiko ni lile jambo au kituambacho  mtu  haruhusiwi kutenda  kwa sababu  ya  imani  fulani.   Kwa   kawaidamiiko  huwa  haina  maelezo  ya  kimantiki. Hata  hivyo  kila  jamii  huwa  na  miikotofauti  kulingana  na  utamaduni  na  imani  za  wanajamii. Baadhi ya  miiko  hiihuathiri  matumizi  ya  lugha  katika  jamii  kijinsia. Kwa  mfano,  katika jamii yakikhoxa ya Afrika kusini ni mwiko mwanamke kutaja jina la babamkwe ambapohuenda akapata sauti [z] ambayo ni mwiko kuitamka.  Neno kama amanzi (maji)litaeupukwa na wataibuka na neno amandabi ili wasitamke sauti {z}.  Hivyo basi

129

Page 130: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

tunaona  kuwa  wanawake  hawa  wana  uwezo wa  kuzitamka  sauti  hizi  lakinihawaruhusiwi na mila kuzitamka.

Katika   utafiti   alioufanya   Rochefort   mwaka   wa   1965   (Taz.   Mesthrie   2000)miongoni   mwa   Wahindi   wa   Carib,   aligundua   kuwa   wanaume   walikuwa   namatumizi tofauti ya lugha na wanawake, na hakuna aliyetaka kuongea lugha yajinsia nyingine katika kuchelea kuchekelewa au kudharauliwa.

Tofauti   za   kiisimu   katika   lugha   mbalimbali  zinaonyesha  ithibati  kuwa  kunamiundo maalum ya kijinsia.   Na katika miundo hii tofauti za kisarufi zinajitokezabaina ya wazungumzaji wa kike na wa kiume.   Ushahidi wa awali kuhusu dai hilila kiisimu unadhihirika katika utafiti alioufanya Mary Haas (1944) katika jamii yaWakoasati  ya  Wamerika  Asili  (Native  Americans). Kwa  mfano,  alipata  tofautikatika miundo ya vitenzi.

Miundo   ya   wazungumaji   wakike Miundo ya Kiume Maana Lakaw în laka î*s usikiinuelakawwil lakawwis ninaiinua

láwwili niliinualakawwilit

Tofauti za kimuundo zilizorekodiwa na Haas zilijitokeza sana katika wazungumzajiwazee, na zilionyesha kupungua miongoni mwa vijana.Wahakiki  walioshughulikia  tofauti  za  miundo  hii  waliona  tofauti  hizi  kuwa  niishara ya mazoea ya kijamii na imani zao.   Na lugha ilifanya kazi kama kioo chajamii, kikimulika tofauti za kijamii, (Mesthrie 2000).   Mesthrie (ibid) anamnukuuFurlery (1944) anayedai kuwa tofauti kati ya miundo ya wanawake na wanaumeinamaanisha  wazungumzaji  walitambua  kuwa  wanawake  na  wanaume  wamokatika kategoria mbili tofauti.

130

Page 131: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Lugha  ambayo  imezua  mijadala  kuhusu  miundo  wanayotumia  wanawake  nawanaume ni lugha ya kijapani.  Inasemekana kuwa tofauti za kijinsia zinajitokezawazi katika fonolojia, mofolojia na leksia ya lugha hii (Tazama mifano wanayotoaMesthrie (2000)  katika jedwali lifuatalo).

Pronomino   katika   lugha   ya   Kijapani Nafsi   ya   (1) Usemi   wa   wanaume Usemi wa wanawakeRasmi watakusi watakusi

Watasi atakusiSio rasmi boku watasi

AtasiSio ruhusiwa ore Ø

Nafsi   ya   2 Rasmi anata anataSio rasmi kimi anata

anta* anta*sio huhusiwa ome Ø

kisama alama hizi zinadhihirisha tofauti za kilahaja kijamii.

Katika  jedwali  hili,  tofauti  mbili  zinajitokeza  hapa.Kwanza  ni  toauti  katikakiwango  cha  urasmi. Kiwango  cha  urasmi  cha  watasi  ni  cha  kirasmi  kwawanaume  lakini  sio  rasmi  kwa  wanawake. Lakini  ile  ya  anata  ni  rasmi  kwawanaume na huenda ikawa rasmi au isiwe-rasmi kwa wanawake.  Hii  ina maanakwamba   wanawake   watarajiwa   kutumia   miundo   mingi   iliyo   rasmi. Piatunatambua  kuwa  pronomino  ambazo  hazikubaliki  kama  vile  ore,  omae  nakisama zinajitokeza  katika  miundo  ya  wanaume  lakini sio miongoni mwa usemiwa  wanawake. Hakuna  neno  lisilokubalika  ambalo  linatumika  katika  uneni  wawanawake.

131

Page 132: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Matumizi haya ya miundo tofauti ni ishara ya mielekeo tofauti.  Kukwepa kutumiamaneno   yasiyokubalika   ni   ishara   ya   adabu   nzuri. Hivyo   basi   tofauti   zakikategoria   katika   mkusanyiko   huu   wa   pronomino   unadhihirisha   ishara   yaheshima  na  adabu  miongoni  mwa  wanawake. Jambo  hili  linafanya  uneni  wawanawake  uonekane  kuwa  wenye  adabu  zaidi  (Ide  1989/1990  katika  Mesthrie2000).

Reynolds  (1980/90)  ametambua  kuwa,  matumizi  ya  boku  mimi  (mwanamume)miongoni mwa wasichana wa sekondari yamekuwa kitu cha kawaida mjini Tokyo.Kwa   sababu   wasichana   wanajua   kuwa lugha   ya   boku haikubaliki   katikamazingira nje ya shule, wao hutumia lugha-watasi (wanawake)wanapozungumza   na   wanajamii   wengine. Inaweza   kuchukuliwa   kwamba,wasichana hawa wa shule ni wana uwili-lugha ambao wanatumia misimbo miwilitofauti a  boku   na   ya  watasi  . Na  wao  huchagua  msimbo  kulingana  namazingira.

Picha inayodhihirika katika miundo hii pia inaonyesha wanawake wakiwa wapole,wenye  heshima,  taratibu  na  wangwana  wasioteta  na  wana  uwezo  wa  kuhisimaono ya wengine (Okomoto, 1995).

Finalyson (1995)  anajadili matokeo ya utafiti alioufanya Afrika Kusini katika jamiiya Wakhoxa.   Alichunguza   matumizi ya hnolipha (au isihnolipho saba jazi, lughaya kiheshima ya wanawake). Aligundua kuwa wanawake katika jamii hii hukwepakutamka  silabi  ambazo  zinajitokeza  kwenye  majina  ya  wakwe  zao  hasa  babamkwe,  mama-mkwe  na  ndugu  za  babamkwe  na  wake  zao  na  dada  zakebabamkwe.

Hivyo  basi  wanawake  wameibuka  na  harakati  fulani  za  kiisimu  ambazo  waohutumia  ili  kukwepa  kutamka  silabi  hizo. Wanaweza  kudondoa  konsonanti,

132

Page 133: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

wabadilishe  konsonanti  moja  na  nyingine,  wabadilishe  neno  moja  na  lingineambalo linakaribiana kisemantiki au   waunde upya sentensi au ikiwa wamesoma,watatumia maneno ya Kiingereza au Kiafrikaans.   Kwa mfano, ikiwa mwanamkeatapata baba mkwe ambaye jina lake ni Bheki au Bhengu atahitaji kukwepa silabibhe  katika  maneno  kama  vile  i-bhekile  (mkebe). Anaweza  kuchagua  kutokamojawapo wa miundo hii:

l-ekile (undondoaji wa konsonanti)l-wekile (kubadilisha konsonanti)I konkxa (sinonimu)lsikhelelo (uundaji upya-kitu ambacho kinatumiwa kuchotea)

Mazoea   na   matumizi   ya   hlonipha   yanaendelezwa   na   familia   pana   ambayomsichana ameolewa. Hlonipha pia inahusishwa na miundo mingineinayoonyesha heshima kwa watu wazima hasa wanaume.  Kando na matumizi yalugha,   mwanamke   anahitaji   pia   kujitenga   na   asitembelee   sehemu   ambazowanaume wanazoea kutembelea.  Hali hii ya kuepukana iwe ya kiisimu au la niishara ya heshima na pia inahakikisha kuwa mtu mgeni na ambaye anachukuliwakuwa wa hadhi ya chini katika boma hilo hatawafanya watu kufikiria juu yake.

Hata hivyo hlonipha haitumiki sana katika sehemu za mjini kwa sababu hakunauhusiano wa moja kwa moja na wakwe wa msichana.

Hlonipha   inaonyesha   wazi   tofauti   kati   ya   wanawake   na   wanaume,   naimehusishwa  na  kutokuwa  na  uwezo  wa  wanawake  hasa  katika  jamii  jadi.Hlonipha  inadhihirisha  hadhi  ya  chini ya  kijamii ya  wanawake na kama kitendocha kila siku inaendeleza tofauti ya kijinsia katika jamii.

Zoezi

133

Page 134: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Je,  lugha  yako  inadhihirisha  tofauti  zozote  za  matumizi  kati ya wanawake nawanaume?  Onyesha  tofauti hizo.

Mara  nyingi  katika  maneno  ambayo  ni  horomo,  maneno  yasiyodhihirisha  wazijinsia   huweza   kufanya   jamii   kupendelea   jinsia   moja. Kwa   mfano,   watuwanaposikia   sentensi   kama   hii, Binamu   wangu   ni   profesa,   au   daktari   auChansla   watachukulia kuwa huyu ni mwanamume.  Wazo hili halitokani na lughahii  tu  bali  linatokana  na  sababu  za  kihistoria,  kwamba  wanawake  hawakuwawakishikilia nyadhifa  kama hizi (Fromkin  na  Rodman,  1988).   Vivyo  hivyo, mtuakisikia  mwenzake  akisema  kuwa  binamu  wake  ni  nesi,  mwalimu  wa  shule  yamsingi au mhazili, mtu kuchukulia kwamba binamu huyu ni mwanamke.

Kutokana  na  hali  hii  tuliyoeleza  hapo  juu,  maneno  horomo  hufanywa  kuwamaneno ambatani ambapo ule muundo wake wa kimsingi unaweza kutumika najinsia yoyote.   Kwa hivyo tunapata maneno ya Kiingereza kama vile malenurse,lady  doctor,  madam  President.   Haya  hutumika  kwa  lengo  la kudhihirisha wazimaana ya maneno hayo.

Tafiti zinazohakiki lugha inayotumika na wanaume katika kurejelea wanawake naambayo   yana   maana   ya   kushusha   heshima   au   yanadokeza   kujamiana,zinaonyesha  kuwa  matumizi  ya  maneno  kama  haya  yalianza  zamani. Wakatifulani, maneno hayakuwa ya kukashifu lakini hupata   sifa za kikashifa baadayeFromkin na Rodman (1986) wanatoa mifano ya maneno haya katika Kiingereza.Wanasema kuwa baada ya muda maneno haya yamekuja kupata maana tofauti

hussy, laundress, a needleman, a spinister maneno haya baadaye yalitumikakama tasfida ya hawara.

Maneno yanayorejelea wanawake na hasa yale ambayo yanatumika kama matusini  mengi. Maneno  haya  ni  kama  vile  malaya,  ambapo  inachukuliwa  kuwa

134

Page 135: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

mwanamke  tu  ndiye  malaya.   Mifano  mingine  inajitokeza  wazi  katika  lugha  yaKiingereza bitch, piece of ass na kadhalika.

Jambo lingine linalodhihirika hasa katika lugha ya Kiingereza ni kwamba majinaya   kiume   huwa   hayana   utambulisho   lakini   ya   wanawake   yanaundwa   kwakuongezea mofimu nyingine za kiutambulisho.  Kwa mfano:

Prince PrincessAuthor authoressCount CountessPoet Poetess

Nomino zisizo na utambulisho zinazorejelea wanaume hutumika kurejelea dhanaza  kijumla. Kwa  mfano,  maneno  kama  brotherhood  na  mankind  hujumlishawanawake pia lakini sisterhood haijumlishi wanaume.

Maneno mengine ya kijozi ya kijinsia huwa na maana tofauti ingawa neno ni lilelile. Kwa   mfano,   governor   ni   mtu   anayetawala   nchi,   lakini  governess  nimwanamke  anayetunza  watoto.   Neno  mistress  halina  maana  sawa  na  masterkatika  Kiingereza. Mara  nyingi  tunazungumzia  kuhusu  unwed  mothers wala siunwed  fathers  au  career women  wala  si career  men.   Kwa nini?   Kwa sababukihistoria  mwanamume asiyeoa  hatiliwi  waa au stigma  yoyote na pia wanaumewanatakiwa  wawe  wafanyikazi. Hata  hivyo,  hivi  karibuni  tumeanza  kusikiamaneno   kama   vile   househusband,   hali   ambayo   inaakisi   mabadiliko   katikamienendo ya jamii hasa uchumi ambapo mwanamke ndiye mfanyikazi na mumehana kazi.

Vilevile  tunaona  kuwa  ni  jambo  la  dharau  mwanamke  kuitwa  spinister,  kwamaana  ya  mwanamke  asiyeolewa  lakini  jamii  inaruhusu  mwanamume  kuitwabachelor.   Hakuna chochote cha matusi katika neno spinister ila kwamba maanakimatilaba   inatokana   na   mielekeo   ya   wanajamii   kuhusu   wanawake   ambao

135

Page 136: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

hawajaolewa.   Wanawake kama hawa wanachukuliwa kama vimada, dai ambalosi   kweli. Hivyo   basi   sio   lugha   ambayo   imejaa   dhanagande   bali  ni   jamiiinapotaasisha mielekeo hii, basi lugha inaanza kudhihirisha upendeleo.

Mabadiliko mengi yamejitokeza ambayo yanaakisi utetezi wa haki na usawa wawanawake.   Wanajamii nao wametambua kuwa lugha huakisi mielekeo ya jamiina  kuendeleza  dhanagande  na  upendeleo. Hivyo  basi  kuna  maneno  ambayoyameanza   kutumika   badala   ya   yale   ya   upendeleo. Wanafanya   hivi   kwakuchukulia kwamba hata wanawake wanaweza kutekeleza majukumuyaliyotengewa  wanaume  katika  jamii. Haya ni mabadiliko ambayo  yanatokanana  mabadiliko  ya  kiuchumi  katika  jamii. Kwa  mfano  neno  people  linachukuamahali  pa  mankind,  personnel badala  ya  manpower,  nurturing  badala  yamothering,  to  operate  badala  ya  to  man,  chair  badala  ya  chairman. Manenomengine ni kama vile, postworker, fire fighter na public safety officer yanatumikabadala ya mailman, fireman, na policeman.

Swali

Lugha huakisi tofauti za kijinsia katika jamii .  Fafanua kauli hii.

136

Page 137: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

8.3 Hitimisho

Katika somo hili tumeonyesha jinsi lugha inavyoakisi tofauti za kijinsi.Tumetoa mifano katika jamii ambazo hali hii inadhihirika wazi.Mwisho tumeonyesha jinsi watetezi wa haki za wanawake wamejaribukuondoa au kubadilisha maneno yanayodhihirisha jinsia na kupendekezayale ambayo hayataonyesha tofauti hizi.

Marejeleo Teule

Coates, D. (1986)   Women,Men      and      Language   , Longman

Fromkin V. na Rodmn R.(1988)   An      Introduction      to      Language   . New York,HarcourtBrace Jovanich College Publishers.

Mesthrie R. et. al. (2000) Introducing Sociolinguistics. Edinburg. EdinbergUniversity Press.

137

Page 138: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Marejeleo ya Jumla

Bickerton, D. (1971)   Inherent Variability and Variable Rules , katika   Foundations      of   Language   7. Bloomfield, L.  (1933)         Language   .  New York. Holt.  Rinehart and Winston.Chacha, L.M. et l (2003)   AKS      100:      Introdution      to      the      Study      of      Language   :Kiswahili Module.  Nairobi. Institute of Open Learning. Kenyatta University.Chambers,  J.K. & Trudgil, P. (1980)         Dialectology   .  Cambridge.  CambridgeUniversity Press.Chimera, R. (1999)  Kiswahili through the Ages: The Question of Lexicon .Makala  Yaliyowasilishwa  katika  Idara  ya  Kiswahili,  Agosti  8,  Njoro.  EgertonUniversity.(2000)   Kiswahili:      Past,      Present      and      Future      Horizons   .  Nairobi, NairobiUniversity Press.Coates, D. (1986)         Women,      men      and      language   .  Longman.Crystal, D.  and Davy, D. (1969)      Investigating      English      Style   .  New YorkLongman.Crystal, D. (1994)   The      Unviersity      of      Cambridge      Language      Encyclopaedia   .  MadridTaurus.Dik, S.C. (1978)      Functional      Grammar   .  New York. North-Holland LingusticSeries. North Holland Publishing Company.Denison, N. (1977)   Language death or Language Suicide?   International Journalof the   Sociology      of      Language   .Fasold, R.W. (199&)   Motivations and Attitudes.  Influencing Vernacular Literacy:Four  African Assessments   Katika   Vernacular      Literacy   : A Re-Evaluation. Oxford.Clarendon Press.Ferguson, C. (1959)  Diglossia .  Word, 15.

Fishman, J.A. (1967)  Sociolinguistics and the Language problems of Devleoping

138

Page 139: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Countries   katika Fishman J.A. et.al. (Wah.)   Language      Problems      of      Developing   

Nations. London. John wiley and Sons Inc.(1972)   Domains and the Relationshipbetween micro- and macro- Sociolinguistics .  In John and Dell Hymes (eds).Greenberg, S.H. (1957   Essays      in      Linguistics   , Chicago Phoenix Books.Gumperz, J.J. (1962)   Social Network and Language Shift   katika J.J. Gumperz(Mhr.)   Discourse      Strategies   .  Cambridge.  Cambridge University Press.Guthrie,   M.   (1967)         The      Classification      of      the      Bantu      Languages   . London.Dawsons of Pall.Halliday,  M.A.K.  et.al.  (1964)      The      Linguistic      Science      and      Language      Teaching   .London.Longman.(1978)      Language      as      Social      Semiotic   :   The   Social  Interpretation   ofLanguage and Meaning.  London. Edward Arnold.Haney D. (1995)  Linguistic Crisis looms as Native Tongues Die   Katika   Daily      Nation, 28.Haugen E. (1956)   Bilingualism      in      the      Americas   .  Tuscoloosa. University ofAlabama Press.(1983)   The Implementation of Corpus Planning: Theory andPractice   Katika   Progress      in      Language    (Wah.) J. Cobarrubias and J.A. Fishman.Berlin. Mouton.Hocket, C. (1958)   A      Course      in      Modern      Linguistics   .  Macmillan.Hudson, R. (1980)   Sociolinguistics   .  Cambridge.  Cambridge University Press.Hutasoit, M. and Prator, C. (1965)   A      Study      of      the      New      Primary      Approach      in      the   

Schools   of   Kenya .  Ministry of Education & ford Foundation.Hymes, D. (1974)   Foundations      in      Sociolinguistics   .  Philadelpia.  University ofPennyslavania.Kachru, B.B. (1977)  Code-Switching as a Communicative Strategy in Indiakatika  Saville-Troike,  Murie  (Wah.)      Linguistics      and      Anthropology   . Washington.Georgetown University.King ei, G. (2001)   Matatizo ya Matumizi ya Lugha katika Vyombo vya Habari.Mifano kutoka Kenya   katika         Swahili      Forum      VII   , German. University of Koln 45-56.

139

Page 140: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Kitso, J. (1975) A stylistic Approach Adopted for the Study of Kiswahili ProseTexts   M.A Thesis. University Of Nairobi (Haijachapishwa)Labov, N. (1980) (Mhr.)         Locating      Language      in      Time      and      Space   .  New York.Academic  Press.  (1972)Sociolinguistic   Patterns . University  of  pennyslavaniaPress.Lopez, L.E. (2000)   Cognition, Culture, Language and Learning: An Introductionto Education Planners in Multilingual and Multicultural Contexts   Katika   Distance   

Learning   Course   in   the   Language   of   Instruction   in   Basic   Education .Mackey, W.F. (1962)   The Description of Bilingualism   Canadian Journal ofLinguistics.Mbaabu, I. (1996)      Language      Policy      in      East      Africa   , Nairobi.  Educational Researchand   Publication.(1978)         Kiswahili      Lugha      ya      Taifa   ,   Nairobi.   Kenya   LiteratureBureau.Mdee, J.S. (1986)   Kiswahili:      Muundo      na      Matumizi      Yake   .  Nairobi.Intercontinental Publishers Ltd.Mesthrie, R.  et. al. (2001)   Introducing      Sociolinguistics   , Edinberg. EdinbergUniversity Press.Milon, J.P. (1992)   Discourse in the Primary English Syllabus of Botswana   katikaUdo Bude (Wah.)   Culture      and      Environment      in      the      Curriculum      and      the      Practice      in   Schools     in      Sub-Saharan   Africa . German Foundation for InternationalDevelopment.Msanjila, Y.P. (1995)  Mawanda ya Isimu Jamii   katika Mbogo, E. na McOnyango, O. (Wah.)   Baragumu   . Juzuu la 2 Nam. 1 & 2. Maseno.   Chuo KikuuMaseno.

Mukhwana, A. (1995)   Kiswahili Sanifu: Je, Kipo   katika   Baragumu   , Juzuu, 2Nam. 1 & 2, Maseno, Chuo Kikuu cha Maseno.Musau, P.M. (2001)  Freeing the Airwaves or Cultural Enslavement: The Case ofMedia  in  Kenya   katika      Kiswahili:      A      tool      for      Devleopment:      The      Multidisplinary      Approach.  Eldoret. Moi University Press.

140

Page 141: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Muthwii, M. (Mh.) (2002)   Language      Policy      and      Practices      in      Education      in      Kenya   

and   Uganda .  Nairobi.  Phoenix Publishers.Myers-Scotton, C. (1992)   Code-Switching as a Mechanism of Deep Borrowing ,Language   Shift   and   Language   Death .  Brenzinger Mathias (Mhr.)Mwaura, P. (2003)  Children Learn Better in Mother Tongue   in   Daily      Nation   ,June 19.Ngugi, P. na Osore, M. (2003)   Linguistic Genocide of the African Languages:Protecting and Empowering   Makala iliyowasilishwa katika Kongamano la LASUDar-es-Salaam Tanzania.Onyango, J.O. (2002)   Magazeti ndio Uti wa Mgongo katika Ustawishaji waKiswahili katika Jamhuri, Desemba 17-30.(2002)   AKS      102:      Historical      Devleopment      of      Kiswahili   . Nairobi.   Institute of Open

Learning. Kenyatta University.Parry, K. (Mha.) (2002)   Language      and      Literacy      in      Uganda:      Towards      a      Sustainable   

Reading   Culture .  Kampala Fountain Publishers.Pride, J.B. & Holmes, H. (Wah.) (1972)   Sociolinguistics   .  Harmondsworth.Penguin.Rubin, J.R. na Jernudd, B. (1972)   Can      Language      Be      Planned   ? Honolulu.University Press.  Hawaii.Ryanga,  S.  na  Mukobwa,  M.  (2003)      AKS      101:Language      Skills      in      Kiswahili      1   :Kiswahili Module, Nairobi.  Institute of Open Learning, Kenyatta University.Swaleh, A. (1997)  Lugha ya Kiswahili (ni) Pijini au Krioli? Makala Yaliwasilishwakatika Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi.

Sifuna, D.N. (1980)   Short      Essays      in      Education      in      Kenya   .  Nairobi.  KenyaLiterature Bureau.Trugdill, P. (1974)   Sociolinguistics:      An      Introduction   .  Penguin.(1986)   Dialects      in      Contact.      Basil   .  Blackwell.  Oxford.TUKI  (1990)   Kamusi      Sanifu      ya      Isimu      na      Lugha    .   Dar es Salaam, University ofDar es Salaam.

141

Page 142: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

Todd, L. (1990)   Pidgins      and      Creoles   .  Routledge.Wardhaugh, R. (1992)   An      Introduction      to      Sociolinguistics   .  Blackwell.(1994)      Investigating      Language   .  Central Problems in Linguistics.Oxford Blackwell.Weinreich, U.  (1974)   Languages      in      Contact   .  Mouton: The Hague.Whitely, W. (1969)      Swahili.      The      Rise      of      a      National      Language   .  New Feter Lare.Methuen and Co. Ltd.

Page 143: mwalimuwakiswahili.co.tz · Web viewKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lugha. na jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii

142