mpango wa huduma ya afya na usa˜ shuleni - tawasanet.or.tz wa kamati ya shule.pdf · iwajibike...

22
Mpango wa Huduma ya Afya na Usafi Shuleni Mwongozo kwa Kamati ya Shule Utunzaji na Uendelezaji wa Miundombinu ya Vyoo na Usafi Shuleni

Upload: others

Post on 29-Aug-2019

12 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

Mpango wa Huduma ya Afya na Usa� Shuleni

Mwongozo kwa Kamati ya Shule

Utunzaji na Uendelezaji wa Miundombinu ya Vyoo na Usafi Shuleni

Page 2: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

1

Mwongozo huu umeandaliwa na:

Kwa Ufadhili wa: Msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa Poland

Mradi huu umefadhiliwa na Programu ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Poland chini ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Poland

Chapisho hili linaakisi mawazo ya mwandishi na haliwakilishi msimamo rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Poland.

Mchoraji Katuni: Rashid Mbago (MG Graphics)

Kimepigwa Chapa na: Goldprints ISBN 978-9976-9953-3-6

Mwongozo wa Kamati.pdf 1 23/07/2018 09:53

Page 3: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

2

YALIYOMOUtangulizi.....................................................................3

Wajibu wa Kamati ya Shule katika masuala ya usa� na kulinda afya...........................................4

Kupanga na kukazia wajibu wa Wazazi na majukumu ya kuboresha usa� na afya shuleni............................................................................6

Njia za kusimamia na kukusanya fedha kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya usa�........................................9

Changamoto zinazoweza kuikabili Kamati....15

Majumuisho na Hitimisho.....................................16

Page 4: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

3

UtanguliziMwongozo huu umeandaliwa maalum kwa ajili ya kusaidia kukuza uelewa wa Kamati za Shule ili ziweze kutimiza wajibu wake, hususani kwenye masuala yanayohusu afya na usa� Shuleni.

Kamati za Shule zimelengwa kutokana na ukweli kwamba ndizo zenye dhamana ya kuendesha na kusimamia maendeleo mbalimbali katika Shule. Ni chombo kinachopanga mikakati na kusimamia utekelezaji wake kwa ajili ya mafanikio ya kiujumla ya Shule.

Ikumbukwe kuwa Kamati ya Shule ndiyo inayosimamia rasilimali zote katika ngazi ya Shule. Rasiliali ni pamoja na vitu kama madarasa, mabweni, kumbi za mikutano, maabara, nyumba za walimu, o�si za walimu, maktaba, viwanja vya michezo n.k. hivyo vyote vinatazamwa na kusimamiwa kwa ukaribu zaidi na Kamati ya Shule husika.

Page 5: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

4

Kwa minajili hii, Kamati ya Shule ndiyo chombo mahususi kabisa katika kuhakikisha mipango inapangwa, inatekelezwa, inafanyiwa tathmini, na kusimamiwa katika kila hatua ili kuhakikisha mazingira ya Shule yanakuwa katika hali bora zaidi.

Serikali katika ngazi ya Kijiji, Mtaa au Kata huitegemea Kamati ya Shule kupata taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa kushirikisha jamii ya eneo husika.

Wajibu wa Kamati ya Shule katika masuala ya usa� na kulinda afyaKama ilivyobainishwa hapo juu, Kamati za Shule zina majukumu makubwa, na mengi ikiwemo kuhakikisha rasilimali zinalindwa na kuongezwa kutoka katika vyanzo mbalimbali kwenye maeneo yao.

Page 6: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

5

Kutokana na umuhimu wa masuala ya usa� na afya Shuleni, hasa katika kukuza ufaulu na kuhamasisha tabia na mwenendo mwema wa wanafunzi, kwa masuala yanayohusu usa� na kulinda afya zao, Kamati za Shule zina wajibu ufuatao: Kuhamasisha uboreshaji wa usa� na afya shuleni kwa kutoa maelekezo kwa uongozi wa Shule (likiwa ni jukumu la kushughulikia masuala ya kila siku Shuleni).

Page 7: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

6

Kuhamasisha ujenzi wa miundombinu ya kutunza taka, pamoja na utunzaji wa vifaa husika Shuleni.

Kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo, kubainisha mahitaji ya rasilimali na kiwango fedha kinachotakiwa kwa ajili ya kuyakamilisha. Waraka wa elimu namba 3 wa Mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa elimu msingi bila malipo unaelekeza Kamati/Bodi za Shule za Serikali, pamoja na ya mambo mengine, “ kuishirikisha jamii katika maazimio ya masuala mbalimbali yanayohusu maslahi na maendeleo ya Shule kwa ujumla.

Maazimio yanayohusu uchangiaji wa hiari, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kwa lengo la kupata kibali”. Hivyo Kamati ya Shule inapopanga kuhama sisha michango kutoka kwa wanajamii na wazazi, isisite kuwasiliana na Mkurugenzi wa

Page 8: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

7

Halmashauri husika mapema kwa kadiri inavyowezekana kwa ajili ya kujadiliana na kupewa kibali cha kuendelea na zoezi la uchangiaji. Kuweka vipaumbele vya ukarabati, pamoja na kusimamia ukarabati husika. Mwongozo wa Matumizi ya fedha za ruzuku ya uendeshaji kwa shule za msingi za serikali kufuatia uamuzi wa serikali kutekeleza elimu msingi bila malipo – unaelekeza kwamba:- “Ukarabati wa miundombinu ya shule utahusu majengo, mifumo ya maji, umeme na samani. Utaratibu wa ukarabati utasimamiwa na Kamati za Shule, na utaz ingatia sheria, Kanuni na taratibu za manunuzi ya umma. Aidha, ukarabati wa miundombinu ya Shule utazingatia vipaumbele vya shule vilivyoidhinishwa na Kamati ya Shule husika”. Hivyo Kamati ya Shule haipaswi kujisahau katika kupanga na kusimamia. Jukumu hili likitimizwa vizuri,

Page 9: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

8

masuala ya matengenezo yatafanyika kwa wakati bila kuchelewa, hivyo kutoathiri huduma kwa wanafunzi walio katika Shule husika.

Kupanga na kukazia wajibu wa Wazazi na majukumu ya kuboresha usa� na afya shuleniKamati ya Shule hata ikiwa na muundo jumuishi na wenye sifa mbalimbali za viongozi na wawakilishi, haitaweza ku�kia malengo yake bila kuwa na juhudi za wananchi.

Muunganiko na ushirikiano huu ni nguzo kuu ya mafanikio katika Shule yoyote. Hivyo Kamati ya Shule isitegemee tu uwezo wa kimaamuzi wajumbe wake, bali idhamirie kuunganisha nguvu na wazazi pamoja na wanajamii.

Ifahamike kwamba mafanikio katika ngazi ya Shule yanategemea sana mwamko na utayari wa wananchi. Hivyo ni muhimu sana kwa Kamati ya Shule kuweza kukazia wajibu wa wananchi, ikiju-muisha wazazi na walezi.

Page 10: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

9

Katika kuhakikisha Kamati ya Shule inapanga na kukazia wajibu wa wazazi na majukumu ya kuboresha hali ya usa� na afya shuleni, Kamati inategemewa kutimiza yafuatayo:-i. Kuweka vipaumbele na kuandaa bajeti kwa kushirikiana na wazazi na wanajamii. Ushirikishwaji huu utatengeneza hisia za umiliki wa program husika katika Shule, pia itashawishi juhudi kutoka kwa wahusika hasa wakati wa utekelezaji wake.

ii. Kufanya uhamasishaji kwa wazazi. Ikumbukwe kwamba Mtoto akiwa na siha mbaya, mzazi atakabiliwa na gharama kubwa ili kuhakikisha matibabu sahihi yanapatikana na afya ya Mtoto irejee katika hali ya kawaida ili aendelee na masomo. Wazazi wahamasishwe kuthamini taratibu za kukinga na maradhi. Kamati ya Shule iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”.

iii. Kushirikiana na Wazazi katika kuhakiki sha Watoto wanaelimishwa juu ya utunzaji wa miundombinu tangu wakiwa

Page 11: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

10

nyumbani. Uharibifu wa miundombinu katika ngazi ya Shule mara nyingi hufanywa na watoto ambao hata nyumbani hua na tabia hiyo. Hivyo, wakati wa vikao na katika mazingira mengine yatakayowakutanisha Kamati na Wazazi, hakuna budi kupewa msisitizo wa umuhimu wa kuboresha malezi bora kwa Watoto ili wathamini utunzaji wa miundombinu iliyopo. Watoto wafundishwe kuwa “Kitunze kikutunze”, na waelekezwe kinagaubaga kuhusiana na umuhimu wa utunzaji wa vifaa vyote vya afya na usa� Shuleni pamoja na nyumbani.

Njia za kusimamia na kukusanya fedha kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya usa�Miongoni mwa majukumu muhimu ya Kamati ya Shule ni kubainisha vyanzo vya mapato na kusimamia ukusanyaji fedha pamoja na matumizi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Shule kamvile:- kuboresha uendeshaji wa miundombinu pamoja na matengenezo ya vifaa

Page 12: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

11

vya usa� kila inapohitajika.Kamati ya Shule inaweza kuwa na njia nyingi za kusimamia uendeshaji na matengenezo. Mwongozo huu unapendekeza baadhi ya njia zinazoweza kutumiwa na Kamati ya Shule katika usimamizi wa uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya usa�. Miongoni mwa hizo ni kama zifuatazo:-i. Kuitisha mikutano ya mara kwa mara, kulingana na kalenda ya mikutano ya Kamati ikijumuisha mikutano ya dharura, na kuweka ajenda ya usimamizi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya maji na usa�. Hii iwe miongoni mwa ajenda muhimu za mkutano huo. Ajenda hii ipewe muda wa kutosha na kila anayehitaji kuchangia apewe fursa ili maamuzi yanapo�kiwa, asiwepo atakaye�kiri kuwa mawazo yake yamepuuzwa kwa sababu mawazo yake yamepuuzwa.

Page 13: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

12

ii. Kuandaa mpango kazi wa namna ya kuendesha na kufanya matengenezo ya miundombinu ya Usa�, kulingana na mazingira ya eneo husika.iii. Kuweka mpango wa kujifunza kutoka kwenye Kamati za Shule hususani Shule zingine zinazofanya vizuri katika maeneo mbalimbali, ikiwemo afya na usa�. Hii itachangia kubadili shana uzoefu na mbinu za utendaji kazi. Angalizo ni kuwa, baada ya kujifunza mbinu kutoka eneo jingine, Kamati ya Shule ni muhimu ikazingatia muktadha wa eneo lao ikijumuisha haiba ya wanajamii, pamoja na vigezo vingine kwa ajili ya ufanisi. Sio kila mbinu ya eneo moja, inaweza kufanya kazi vizuri katika eneo jingine.

iv. Kuhamasisha jamii nzima ya Shule katika kufa nya shu ghulizinazohusiana na usa� na afya. Bila uhamasishaji, hakuna jambo litakalozingatiwa. Hivyo ni muhimu baada ya maazimio, pia juhudi iongezwe kuhamasisha utekelezaji wa shughuli zinazohusiana na afya na usa� katika Shule husika.

Page 14: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

13

v. Kutoa taarifa usahihi na kwa wakati. Ushirikiano hutoweka pale ambapo Kamati ya Shule haitoi taarifa kwa usahihi na kwa wakati uliokusudiwa Ili kufanikiwa katika utendaji kazi wa kila siku, Kamati ya Shule izingatie kutoa taarifa za maendeleo ya maazimio, taarifa hizo ziwe sahihi na zitolewe kwa wakati bila kisingizio chochote. Juhudi za makusudi zifanyike ili upatikanaji wa taarifa uwe wa uhakika ndani na nje ya Kamati.

Pamoja na kutumia mbinu zilizoorodheshwa hapo juu, rasilimali fedha ni muhimu kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya miundombinu shuleni. Kwa kawaida zipo njia nyingi zinazotumika kutunisha fedha. Inashauriwa kuwa njia hizo ziwe rahisi, halali na zisiwe za gharama kubwa. Baadhi ya njia halali zinazopendekezwa kutumiwa na Kamati ya Shule katika kukusanya fedha kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya usa� shuleni kama zifuatazo:-

Page 15: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

14

i. Kubainisha mahitaji yote ya miundombinu katika ngazi ya Shule (vifaa, na rasilimali fedha vinayohitajika kwa usahihi). Bila kuwa na mchanganuo mzuri, upatikanaji wa fedha kutoka kwenye chanzo chochote utakuwa ni mgumu.

ii. Kubainisha idadi ya Wadau mbalimbali wan aoweza kushirikiana na Kamati ya Shule katika kusaidia juhudi zilizopo ili kuondoa changamoto zinazoikabili Shule husika. Wadau wana oweza kubainishwa, wanaweza kuwa ni pamoja na; Serikali ya Kijiji, Jamii, Halmashauri, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Watu Mashuhuli, Makampuni, Wafanyabiashara n.k. Kamati ifanye tathmini kulingana na mazingira husika.

Ni ukweli kuwa fedha inayotengwa na Serikali kwa ajili ya miundombinu ya Shule haitoshelezi, hivyo kamati za Shule zinapaswa kubuni vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule, ikijumuisha ya afya na usa� shuleni.

Page 16: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

15

iii. Kubainisha mbinu shirikishi kwa wadau tofauti tofauti, mfano:- a. Kuandika maandiko ya miradi na kuyawasilisha kwa wadau wanaohusika, mfano makampuni na wahisani katika maeneo yao. b. Kuandaa makongamano ya kuchangia miundombinu ya afya na usa� ya Shule. Hapa Kamati inaweza kumwalika Kiongozi mashuhuri katika ngazi ya Wilaya, au Mkoa, au ngazi nyingine za juu kwa ajili ya kuchagiza uhamasishaji. c. Kuandaa mashindano ambayo wadhamini na kila mshiriki atakuwa na mchango fulani wa kuchangia kuboresha miundombinu ya afya na usa� Shuleni. d. Kuandaa chakula cha hisani na kualika wadau ili washiriki katika kuchangia Kuchangia uboreshaji wa miundombinu ya afya na usa� Shuleni.

Page 17: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

16

SHULE YETU IMEBAHATIKA KUPATA MRADI HUU WA UJENZI WA VYOO BORA NI JUKUMU LETU SASA KUTUNZA VYOOVYETU

MKUU ITABIDI ZOEZI LA KUWAPIKIA CHAKULA WANAFUNZI LIANZE KESHO MAANA KILA KITU KIPO TAYALI

SAWA MWALIMU HAUNA TATIZO

iv. Kuanzisha na kusimamia utaratibu wa wazi wa kuchangia fedha na michango mbalimbali kutoka kwa wananchi kulingana na nafasi na uwezo wao. Hii inashauriwa itanguliwe na uhamasishaji wa jamii kikamilifu kutambua kuwa miundombinu hii ni yao na ni kwa faida ya Watoto wao na vizazi vijavyo. Jamii iguswe na matatizo ya shule wanayosoma Watoto wao. Baadhi ya michango inayoweza kutole wa na wanajamii

Page 18: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

17

ni pamoja na:- Mchanga, mbao, mawe, mifugo kama vile kuku, bata, kanga, mbuzi, kondoo, ng’ombe, na vinginevyo vilivyo ndani ya uwezo wa jamii. Kimsingi vitu hivyo viweze kubadilishwa kwa njia ya mnada ili kupata thamani halisi ya fedha kwa kile kilichochangiwa.

Pia mchango wa nguvu kazi ni muhimu uthaminiwe kwani utafanikisha kuokoa sehemu kubwa ya fedha kama ingetumika kulipa nguvu kazi.

v. Miradi ya uzalishaji mali katika ngazi ya shule, mfano bustani ya shule, shamba la shule, kuwa na mifugo ya shule n.k. Miradi kama hiyo inaweza kutumika kama chanzo cha fedha katika mfuko wa shule, ambapo sehemu ya mapato hayo itatumika kufanikisha uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya afya na usa� Shuleni.

Page 19: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

18

Changamoto zinazoweza kuikabili KamatiKatika kuhamasisha na kusimamia uendeshaji wa miundombinu ya afya na usa� Shuleni, Kamati inaweza kukutana na changamoto mbalimbali. Baadhi ya changamoto hizo zinaweza kuwa :- Kupinga uchangiaji kwa maelezo kuwa hauendani na Sera ya Elimumsingi bila malipo. Suluhisho: Wananchi waelimishwe utofauti wa gharama ambazo Serikali inazi�dia, pamoja na na wajibu wao. Kama ilivyoelekezwa, Mkurugenzi wa Halmashauri aonwe kwa ajili ya kutoa kibali iwapo kuna uchangiaji wa hiari unaokusudiwa. Baadhi ya wanajamii kutokuwa tayari kuchangia kwa sababu hawana watoto wanaosoma katika shule husika. Suluhisho: Wananchi waelimishwe kuwa ni jukumu la kila mmoja kuweza kuandaa mazingira bora kwa Watoto. Wao ni viongozi wa baadae, ambapo uwekezaji mkubwa unahitajika kwa faida ya jamii na taifa zima.

Page 20: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

19

Baadhi ya wanajamii kutoa�kiana na mapendekezo yanayotolewa na Kamati. Suluhisho: Mikutano ya Kijamii itumike kurasimisha maamuzi na kutumia sheria ndogondogo zilizopo.

Kamati itathmini kwa kina changamoto hizi na nyinginezo zitakazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi mapema kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya Shule na Watoto.

Majumuisho na Hitimisho Kamati ya Shule haipaswi kusubiri maamuzi yote kutoka ngazi za juu. Wajumbe wake wanapaswa kuwa wabunifu zaidi na kutumia mazingira yaliyopo kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Page 21: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

20

Kamati isisahau kuwa inawajibika kwa wadau wake ambao ni (wanafunzi, walimu, wazazi, na jamii inayozunguka shule} Maamuzi ya Kamati yasipokuwa wazi kwa wadau husika, mara nyingi ni vigumu sana ku�kia malengo yanayotarajiwa.

Kamati za Shule zikiwajibika ipasavyo, zikiwa na ubunifu na weledi katika kutatua changamotozinazokabili shule, matatizo mengi yatabaki kuwa historia katika Shule zote.

Page 22: Mpango wa Huduma ya Afya na Usa˜ Shuleni - tawasanet.or.tz wa Kamati ya Shule.pdf · iwajibike kuwakumbusha kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba”. iii. Kushirikiana na Wazazi katika

-

-

-

:

: