msirudi nyuma - mwalimu wa kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao....

80
1

Upload: others

Post on 26-Apr-2020

57 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

1

Page 2: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

2

MSIRUDI NYUMA

Mwl. John Magoda jr.

Page 3: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

3

Kitabu hiki kimeandaliwa na

John Magoda jr

S.L.P.30407 KIBAHA ,PWANI

+255 718821168

[email protected]

Page 4: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

4

YALIYOMO

1.TABARUKU.............................

2.SHUKURANI...............................

3.UTANGULIZI.....................................

4.MAHAKAMANI .................................

5.UKWELI WANGU...............................

6.MSIRUDI NYUMA................................

Page 5: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

5

TABARUKU

Napenda kukitabaruku kitabu hiki kwa walimu

wote wa shule za msingi ndani na nje Tanzania kwa

mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu

chao.

Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki

yangu Salumu Mustafa kwa kunipa changamoto

chanya mpaka kukimaliza kuandika kitabu hiki

hakika hiki ni kitabu chako.

Page 6: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

6

SHUKURANI .

Kwanza nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu

muumba wa mbingu na ardhi kwa kutujalia uhai na

heri zote za dunia hii lakini pia ni kwa mapenzi yake

yeye pekee ndio yamefanikisha kukamilika kwa

kitabu hiki.

Lakini katika kukiandaa kitabu hiki wako wengi

walioshiriki kwa hali na mali hasa ushauri na

kunitimia moyo wako wengi lakini nitawataja

wachache kwa niaba ya wengine marafiki zangu

Patrick Alex Shampundu , Antony Chavala , Adeltus

Mutajwah , Jackson Msigwa ,Dickson Turuka,

Page 7: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

7

Benjamini Mwakitalu,Costantine Peter

Masele,Brother Chriss, Jacob Joel , Yustina

Joseph ,Salum Mustapha.

Lakini pia katika eneo la ushauri wa kiuandishi

Shukurani ziende kwa Elenzian Komba ,Rasi

Mbwana, Mwanagenzi Michael the

Great ,Dk.Raymond Nusura Mgeni , kwa ushauri

wao katika kazi zangu.

Lakini shukurani zangu za dhati ziende kwa walimu

wangu na wahadhiri wangu wote kwani maarifa yao

yamekuwa na msaada mkubwa sana katika kusaidia

kuandaa kitabu hakika Mungu awabariki sana .

Page 8: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

8

Pia shukurani zangu ziende kwa wasomaji wangu

wote wa kazi zangu hakika nawashukuru sana

maana naandika kwa ajili yenu na wamekuwa kila

wakisoma huwa wanarudisha mrejesho juu ya kazi

zangu hakika mwenyezi Mungu awabariki sana .

Pia mwisho kwa mkururo napenda kutoa shukurani

zangu za dhati kwa mpenzi wangu na rafiki yangu,

mshauri wangu Kandi kwa upendo wake kwangu

hakika amekuwa mtu ambaye akinifariji sana na

amekuwa nami katika vipindi vyote vya raha na

shida hakika nakupenda sana.

Page 9: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

9

UTANGULIZI

MSIRUDI NYUMA ni kitabu kilicho katika muundo wa

barua ambacho kinaangalia suala la taaluma ya ualimu na

walimu kwa ujumla lakini pia lengo kubwa la kitabu hiki

ni kuwatia moyo na kuwapa hamasa na walimu ambao

ndio kiungo muhimu sana katika suala la elimu mahali

popote duniani .

Lakini pia lengo ni kutaka kukumbusha na kuelekeza

baadhi ya mambo kuhusiana na walimu na taaluma ya

ualimu na kuleta mwanga kwa ajili ya wanajamii ili

waweze kutambua masuala muhimu kuhusu taaluma ya

ualimu na maisha ya walimu kimawanda mapema .

Page 10: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

10

Licha ya kuwa kitabu kinazungumzia masuala ya

kitaaluma na kijamii kuhusu taaluma ya ualimu na

walimu wenyewe lakini pia kimetumia lugha ya kifasihi

lengo likiwa ni kuwafanya wasomaji kuchota maarifa kwa

kutumia lugha yenye ujazo mwingi wa vionjo vya kisanii

katika suala la lugha .

Lakini kitabu kiwe taa ya kuwamulika waandishi wengine

waanze kuibuka na kuaandika kuhusu taaluma hii ya

ualimu na walimu kwa ujumla katika nyanja zote za

kielimu lakini pia kitabu hiki kimekuja wakati ambao kwa

sasa taaluma ya ualimu iko katika mtikisiko mkubwa sana

na changamoto mbalimbali mbali na zile ambazo

zimezoeleka lakini hili la sasa ni tabaka la baadhi ya

viongozi wa kiserikali kuingilia taaluma ya ualimu pasipo

Page 11: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

11

kufuata taratibu na kuwa vikwazo na sehemu ya

kuwashusha morali walimu wengi sana nchini Tanzania .

Hivyo nikutakie usomaji mwema na wenye tafakuri ya

kina .

John Magoda jr.

©2019

Page 12: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

12

MAHAKAMANI.

Ni majira ya asubuhi kabisa huku siku ikiwa imeanza kwa

ubaridi mororo na jua likiwa limechelewa kuchomoza ,

na sauti za kunguru na ndege ndio zilikuwa zikisikika tu

kwa wingi hii ni kutokana eneo la mahakama kulikuwa

kuna miti iliyokuwa mikubwa ambayo ndo ilikuwa ni

makazi pendwa kabisa kwa ndege kupumzika baada ya

siku ndefu ya kutafuta chochote kitu kwa ajili ya kujilisha

wao pamoja na makinda yao .

Nikitizama naona kundi kubwa la watu ambao

wamefurika kwa wingi katika eneo la mahakama ili kuja

kushuhudia hukumu ya kesi yangu ambayo imegubikwa

na utata wa hali ya juu labda niseme kuwa ni kwa mara

ya kwanza kushuhudia idadi kubwa ile ya watu katika

Page 13: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

13

eneo la mahakama kwani ni wazee ,vijana hadi watoto

labda niseme unaweza kufananisha idadi ya watu ile

idadi ya kumpokea mgombea wa urais kwa tiketi ya

ukawa Ndugu Edward Lowasa katika uchaguzi wa

mwaka 2015 pale jijini mbeya lakini kumbe ni eneo la

mahakama wengi wakisubiria hukumu yangu .

Muda wa kuingia mahakamani ulifika watu walisimama

pale hakimu alipokuwa ameingia ndani ya mahakama ile

ambayo ilijaa watu ndani na nje ya mahakama na mpaka

ikapelekea askari wa jeshi la polisi kuongezeka eneo la

mahakama na huku wakiwa wamejidhatiti kabisa kama

vile kuna kesi ya ugaidi inaendelea katika eneo la

mahakama kumbe ni kesi ya kijana mzalendo wa

Page 14: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

14

kitanzania mzalendo wa moyo ambaye ameponzwa na

ukaribu wake na ukarimu kwa wanafunzi wake .

Lakini ninachokiamini ni mimi na Mungu pekee ndiyo

tunaojua ukweli wa tukio hilo kwani kwa walimwengu

licha ya kujieleza kadri ya uwezo wangu kuwaambia

kuwa kamwe sikuhusika na tukio hilo na sitambui lolote

lile kwao ilikuwa ni ngumu sana maana mshikwa na

ngozi ndio mla nyama na kweli ngozi ilishikwa kwangu

lakini kamwe kwa dhati ya moyo hiyo nyama sikuila

lakini kwa vile hali imeshatokea hakuna nmna zaidi ya

kusubiria kile ambacho Mheshimiwa hakimu atakiamuru

lakini ndani ya akili yangu nilijua kuwa tayari

nimeshapoteza dira na uelekeo wa maisha yangu mapema

kabisa .

Page 15: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

15

Ndani ya mahakama ile nilipokua nikitazama watu

machoni mwao hasa walimu wenzangu wengi macho

yalikuwa ni mekundu sana wengi wakijizuia kulia

kutokana na uchungu lakini kwa vile ni eneo la

mahakama ilibidi wajikaze kisawasawa hili kusubiria

hukumu ya muheshimiwa hakimu kuitoa juu yangu dhidi

ya tukio la mauaji ambalo lilitokea ambalo liligubikwa na

utata mkubwa sana .

Na ikumbukwe kuwa zilikuwa zimepita wiki kama mbili

nyuma kuna mwalimu alihukumiwa kwa kunyongwa

mpaka kufa kwa kosa la kumuadhibu mwanafunzi hali

iliyoacha simanzi kubwa sana katika taaluma ya ualimu

lakini pia kuna walimu ambao waliandamana kwa ajili ya

madai ya malipo yao na kutopandishwa madaraja kwa

Page 16: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

16

muda mrefu lakini waliishia mikononi kwa polisi ambapo

walipigwa na kupelekea wengine kupata ulemavu wa

viungo hiyo yote ni kwajili ya kudai haki yao stahiki

yao ,lakini pia ni katika mfuatano huo wa matukio ndo

ambapo kuna mwalimu alifuatwa na kiongozi wa kata

ofisni na kutolewa lugha ya matusi na kebehi ya hali ya

juu kabisa kwa hakika taaluma ya ualimu ilikuwa katika

miezi migumu sana lakini hapo sijaelezea wale walimu

ambao walikuwa wanasumbuliwa na imani za kishirikina

kutoka kwa wanajamii yani usiku wanalala ndani na

asubuhi wanajikuta wamelala mchangani na wengine

wakijikuta wako juu ya miembe .

Page 17: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

17

Kwa muda huo mahakama ilikuwa imetulia watu

wote wakiwa wametulia ili kujua nini hatima ya kesi

yangu huku wakimsubiria hakimu Patrick

Shampundu kutoa hukumu hiyo na baada ya taratibu

za kimahakama kumalizika sasa ilifika kipindi cha

kusikiliza hukumu juu ya kesi yangu iliyokuwa

inanikabiri hakika nafsi na moyo vilisimama kwa

muda mpaka nikahisi labda nimepooza mara baada

ya hakimu Patrick Shampundu alipoanza kuisoma

hukumu yangu ndipo alipotamka hukumu ambayo

kwangu ilikuwa kama mkuki wa moto uliopenya

ndani ya moyo wangu .

Page 18: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

18

Hakika nilibubujikwa na machozi ambayo sijawahi

kububujikwa na machozi kiasi kile hasa niliposikia

kuwa nahukumiwa kunyongwa mpaka kufa hakika

sio ndani ya mahakama tu bali hadi nje ya

mahakama vilisikika vilio kama vile kuna msiba

mkubwa sana kama ule wa mwaka 1999 wa hayati

baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

hakika watu hawakuamini kuwa naweza kusitisha

maisha yangu ndani ya muda mfupi kabisa hakika

hili lilikuwa pigo kubwa sana sio kwa familia yangu

tu bali kwa taifa kwa ujumla kusubiria hukumu

yangu hiyo hakika ilikuwa ni siku mbaya zaidi

kwangu .

Page 19: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

19

Basi ikawa hivyo hukumu ikatoka natakiwa

kunyongwa na sio kunyongwa tu mpaka nife hakika

niliumia sana na watu wote waliumia sana hasa

walimu wenzangu wote waliumia zaidi sana maana

ni muda mfupi tu tangu nihamie katika shule hiyo

ambayo ilikuwa nyuma kielimu lakini mabadiliko

makubwa sana yalianza kuonekana lakini hakuna

nmna lazima nitumikie hukumu yangu hiyo hakika

niliondoka eneo la mahakama huku nyuma vilio

vikiongezeka sana nikawa sina budi kuwapungia

mikono na kuwaambia kamwe wasirudi nyuma .

Mbaya zaidi hukumu yangu ilivyopita ilikuwa katika

orodha na majina ya hukumu yangu yalisainiwa na

Page 20: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

20

rais wa nchi tukiwa na wengine hivyo ikawa

inabakia siku ya kunyongwa kwangu

Hakika majonzi na huzuni viliendelea kutawala

mtaani na maeneo ya Tanzania kwa ujumla

walihuzunika sana tena sana huku mimi moyoni

nikiwa nalia sio tu kwa ajili ya kunyongwa bali

ndoto zangu na mipango yangu mikubwa katika

elimu ya nchi yangu ya Tanzania na ambavyo

sijaitumia kabisa maarifa yangu na ujuzi wangu

kikamilifu hicho ndo kinachoniuma zaidi.

Siku ya kunyongwa ilikuwa ni tarehe 30/4/1990 na

nilikuwa na siku mbili tu za kuendelea kuwa hai

Page 21: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

21

lakini nilikuwa na nafasi moja tu ya kuwaelezea

umma wa Tanzania kuhusu yale yaliyonisibu na

kuhusu taaluma ya ualimu na elimu kwa ujumla

licha ya kuwa na changamoto mbalimbali kamwe

msirudi nyuma . Ndipo nilipewa peni na karatasi ili

niweze kuaga kabla tamati ya maisha yangu kufika .

Page 22: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

22

UKWELI WANGU.

Kwenu Wanajamii .

Nashika kalamu ndogo kabisa lakini naiona nzito

mithili ya chuma chenye uzito wa kilo mia tano

sabini na huku moyo wangu ukivuja damu kutokana

na uchungu mkubwa wa maisha yangu kuishia

njiani kwa namna hii lakini natambua kuwa kila

nafsi itaonja umauti ila katika njia ambayo

mwenyezi Mungu pekee ndio anafahamu hivyo

nikiendelea kuhuzunika kwa hakika nitakuwa na

mkufuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na

ardhi inanibidi nimuachie yeye pekee kwa yote

Page 23: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

23

yaliyotokea mimi mwenzenu lakini kamwe msirudi

nyuma .

Kutoka ndani ya moyo wangu licha ya kuwa na

kinyongo kizito lakini haina budi nikiri kupitia

waraka huu kuja kwenu walimu wenzangu

nimewasamehe wale wote katika kipindi cha maisha

yangu walinikiwaza na kuniudhi lakini pia hata

katika kesi iliyokuwa ikinikabiri pia nawasamehe

sitaki kuondoka katika dunia hii pana kabisa nikiwa

na kinyongo cha namna yoyoye ile hivyo moyo

wangu kwa sasa ni mweupe mithili ya theluji ya

mlima Kilimanjaro unaoangaza Afrika nzima

Page 24: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

24

kutokea kaskazini mwa nchi yangu ninayoipenda

tokea utoto wangu hadi hatua hii .

Lakini pia kwa wale ambao nilishawahi kuwakwaza

au kuwa kero katika kipindi chote cha maisha yangu

nichukue nafasi hii kuwaomba radhi najua kabisa

ombi langu litawafikia huko popote mlipo wale wote

kuanzia chekechea hadi elimu yangu ya juu hadi

kule finland msamaha wangu ufike huko hadi kusini

mwa nchi yangu msamaha ufike na uvuke mipaka

yote ya nchi kutoka ndani ya moyo wangu nasema

kuwa nahitaji msamaha wenu ndugu zangu

nafahamu fika sina nafasi nyingine ya kuwaomba

msamaha isipokuwa katika waraka wangu huu kwa

Page 25: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

25

hakika naomba Mungu uwajalie roho nyepesi ya

kuweza kunipatia msamaha ndugu yenu .

Nikifikiri siku yangu ya kuwekwa ndani ya kitanzi

na kunyongwa hakika moyo wangu unakuwa mzito

na mwili unashikwa na ganzi kabisa lakini sina tena

nafasi ya kuwa nanyi kimwili isipokuwa kimawazo

naweza ishi nanyi milele na milele hasa nikiangalia

kwa jicho la kumbukizi safari ya maisha yangu ya

kitaaluma tokea elimu ya awali hadi kufikia katika

shahada ya pili na huku nikiwa katika kumalizia

kuandika tasnifu yangu ya shahada ya tatu kuhusu

ubora wa darasa la awali na mafanikio ya kitaaluma

ambapo naamini ingeenda kuwa msaada mkubwa

Page 26: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

26

sana kwa elimu ya awali ambayo ndo msingi

mkubwa sana katika maendeleo ya kielimu katika

taifa lolote lile ulimwengu .

Nafahamu fika imetolewa hukumu ndani ya muda

mfupi tu na pia nikahukumiwa adhabu ya

kunyongwa mpaka kufa hakika mpaka sasa sifahamu

ni nani aliyeamua hayo yote kunifika mimi kabisa

hakika ndo nashikwa na uchungu kutoka ndani ya

moyo wangu lakini lakini kamwe siwezi mlaumu

mtu yeyote yule kuhusu suala la hukumu yangu

sababu kwa hali halisi ilivyokuwa hakika sio hakimu

wala polisi na hata wapelelezi wa kesi yangu lakini

kwa uchungu kabisa naingalia safari yangu ya

Page 27: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

27

kitaaluma na malengo yangu na mipango yangu yote

inaelekea kupotea hewani hakika nafsi inaniuma

sana lakini hakuna namna naamini kupitia waraka

huu kuna vitu mfajifunza na tutakwenda kupiga

hatua lakini mwili na nafsi vyote vinauma na masaa

nayo yanakimbia kwa mithili ya moto wa nyika

uliowekewa mafuta ya petroli ukisindikizwa na

upepo mkali kama wa kanda ya kati Dodoma hasa

katika maeneo ya kongwa ndo nilivyoyaona masaa

hayo yalivyokuwa yakikimbia.

Hakika naomba waraka huu ufike pande zote za nchi

kuanzia kusini kule kwa ndugu zangu na upande

hadi kanda ya kati kote lakini pia ufike hadi kule

Page 28: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

28

nyanda za juu kusini mikoa yenye uzalishaji

mkubwa kabisa wa chakula katika taifa langu lakini

waraka usikomee huko bali upande hadi kaskazini

mwa nchi yangu ikibidi ufike hadi katika kilele cha

mlima Kilimanjaro lakini ushuke na kufika

magharibi mwa taifa langu hadi mashariki huko na

pia uvuke mipaka ya nchi kwa majirani zetu wote

wenye mapenzi ya dhati na sisi .

Hakika uwafikie wanafunzi wote ,wakulima na hata

wale waajiriwa wa serikali na hata wafanyakazi

waliojiajiri wenyewe lakini pia uwafikie wakina

mama wote walioko mahospitalini wanaojiandaa

kutuletea watoto wapya katika uso huu wa dunia hii

Page 29: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

29

iliyojaa walimwengu wa kila aina lakini waraka

uwafikie hata kule katika vijiji vya ndani kabisa ya

taifa hili kwa watu wa jinsia zote ,rangi zote hakika

naamini kuwa siku zangu za kuendelea kuishi ni

chache kabisa kuendelea kuishi nilikuwa na malengo

na maono makubwa sana ya kuja kutumia taaluma

yangu ya ualimu na utaalamu katika elimu kuja

kuinua suala la elimu ya awali na kwa wanafunzi

wenye mahitaji maalum hasa matatizo mahususi ya

ujifunzaji kwa lugha ya kiingereza wanaita specific

learning difficulties .

Natambua kuwa hukumu yangu ilitoka na wengi

walikuwa na maswali mengi na asilimia kubwa

Page 30: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

30

walipata habari juu kuwa nimeua mwanafunzi wa

kike na kumuweka ndani ya kabati baada ya

kumuingilia kimwili mbaya zaidi hadi kinyume cha

maumbile ili niweze kupata utajiri na kupata vyeo

katika taaluma ya ualimu na kupata nafasi ya

kualikwa zaidi na zaidi katika makongamano

makubwa duniani kama muelimishaji ndo maana

nikaamua kufanya mauaji hayo ya kinyama tena kwa

mwanafunzi ambaye nilikuwa naye bega kwa bega

tena wa jinsia tofauti na mimi jina lake Asha hakika

nafsi yangu inaumia sana nilivyokuwa nikisikia

shutuma zangu dhidi ya suala hilo lakini kwa vile

nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuelezea lakini

Page 31: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

31

sikueleweka zaidi niliambulia kupigwa zaidi na

kupelekea mwili wangu kuwa na vidonda na mambo

mengi niliyofanyiwa hakika siwezi sema nitakufa

nayo .

Kwa dhati ya moyo kabisa sikuweza fanya tukio hilo

wengi wakihusisha tukio hilo na maendeleo yangu

ya kitaaluma na safari nyingi za nje ya nchi kwenye

mataifa makubwa na bora kielimu nilipokuwa napata

nafasi ya kwenda kushiriki katika maboresho ya

masuala yao ya kielimu na kupelekea kupata kipato

kikubwa sana na mara thelathini zaidi ya mshahara

wangu wa ualimu wa shule ya msingi tena nikiwa

nimechagua kufundisha kama mwalimu wa elimu

Page 32: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

32

ya awali na huku nikiwa nimekataa ofa za kazi zaidi

ya arobaini kutoka katika vyuo vya ndani ya nchi na

nchi jirani kuwa mhadhiri kwenye vyuo vikuu na

vya kati lakini kutokana na tangu nikiwa mtoto

mdogo nilisema nitakuwa mwalimu wa awali

nilifanya hivyo

Labda niwaeleze jinsi jumba bovu hilo la kesi ya

mauaji liluvuonitokea mimi mwenzenu nilikuwa

mwalimu wa awali katika shule moja huko nyanda

za juu kusini ambako ndo chimbuko la asili yetu na

kweli nilipendwa sana na wanafunzi wangu

waliokuwa idadi ya wanafunzi hamsini na katika

Page 33: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

33

shule hiyo kutokana na mfumo wa ufundishaji

ambao niliokuwa nau

tumia katika kuwafundisha wanafunzi hao yani

mwalimu nilikuwa kama sehemu ya muwezeshaji

lakini wao ndio walikuwa wagunduzi wakubwa

kutokana na kuwa mbobezi katika eneo hili na huku

nikiwa na ongozwa na kauli mbiu ya "don't teach

them everything but let them discover "ambayo

ilikuwa inaendana kabisa na elimu ya awali kwa

hakika darasa langu lilikuwa ni darasa ambalo

lilikuwa linavutia sana sio kwa wanafunzi wangu tu

bali hata kwa wanajamii husika wa eneo lenyewe na

hata wanafunzi wa madarasa mengine walikuwa

Page 34: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

34

wanatamani waanze chekechea kwa ajili tu ya

mambo yalivyokuwa yanakwenda katika darasa

langu hilo .

Kwa hakika darasa langu hilo lilikuwa na sifa za

kimataifa kwa ajili ya darasa la awali kwani

nilitumia vyema maarifa na ujuzi wangu wote

niliopata katika vyuo vikuu mbalimbali duniani

kutoka katika nchi zenye maendeleo makubwa

katika sekta ya elimu ndio lilifanya darasa langu

kupendeza na kuvutia na kwa kuwa kazi ya ualimu

ilikuwa ni moja ya taaluma ambayo tangu nikiwa

mdogo nilitamani sana nije kuwa mwalimu maana

nilikuwa na utamaduni wa kucheza michezo ya

Page 35: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

35

kitoto na nikiwa kama mwalimu katika kundi la

watoto wenzangu huku wengine wakitaka kuwa

makomando na wengine polisi hivyo kutokana na

sinema za kivita walizokuwa wanaziangalia.

Kwa kuwa shule ambayo niliyokuwa nafundisha

ilikuwa haina umeme lakini haikuwa mbali sana na

nguzo za shirika la umeme Tanzania (Tanesco)

hivyo kwa kutumia urafiki wangu na wanafunzi

wenzangu niliyosoma nao shahada ya pili katika

masuala ya elimu ya awali nchini Finland hakika

nilipata ufadhilii wa kuweka umeme katika darasa

hili na vile tukaweza kujenga madarasa mawili

mapya kabisa yenye viwango vya kimataifa lakini

Page 36: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

36

pia nikiomba ruhusa kwa mkuu wa shule ili

nikabidhiwe jukumu la kuchukua wanafunzi wa

awali walionekana wameshindikana kabisa kuelewa

katika shule za jirani na nilipewa ruhusu hiyo na

darasa langu likaanza .

Mshahara wangu wa ualimu niliamua kuutumia

katika uboreshaji wa mfumo wa ujifunzaji na

ufundishaji hapo shuleni hasa katika elimu ya awali

kwani nilikuwa nafundisha kwa kuwa nilikuwa

naipenda taaluma ya ualimu lakini sio kwa ajili ya

kupata kipato kwani kwa muda huo nilikuwa

namiliki biashara mbalimbali na mashamba

makubwa sana ya mpunga huko kyela na kilimo cha

Page 37: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

37

umwagiliaji katika bonde la mto Rufiji katika mkoa

wa Pwani mbali na hayo bado nilikuwa nimeweza

kumiliki idadi kubwa ya ng'ombe huko kaskazini

katika mkoa wa Manyara katika wilaya ya Simanjiro

hivyo nilifundisha kama kulipa fadhila kwa jamii na

vilevile ni kitu ambacho nakipenda sana.

Kwa hakika ilikuwa mtu yeyote akifika katika

darasa langu la awali lazima aulize ni darasa

linalomilikiwa na mtu binafsi au serikali maana

wengi huwa wanaamini kuwa vitu vizuri vipo katika

shule za binafsi hivyo hii ilifanya suala la utoro

kutokuwepo kwa wanafunzi wangu maana ulikuwa

ukiingia darasani lazima ukumbuke enzi za utoto

Page 38: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

38

maana darasa lilikuwa linaongea maana picha za

herufi na wanyama mbalimbali zilikuwa ukutani

lakini pia meza pana na zenye viti vyake vya kitoto

lakini pia hapo ilikuwa ni sehemu ya darasa la

kujifunzia ambao mbele kulikuwa na ubao mweupe

ambao unatumia maka peni na sio chaki kama

ilivyozoeleka na walimu wengi hapa nchini kwetu .

Lakini pia kulikuwa kuna screen kubwa sana ya inchi

zaidi ya thelathini na sita aina ya sony ambayo

ilikuwepo ukutani huku pembeni kukiwa kuna redio

kubwa kiasi aina ya sabufa pembeni ya meza lakini

pia kulikuwa kuna projekta ndogo yenye uwezo wa

Page 39: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

39

kuonyesha picha kwa kiwango cha HD hapo

nikimaanisha high definition hivyo wanafunzi

walikuwa na nafasi ya kuwaona wanafunzi wenzao

kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa maana

niliandika barua ya maombi ya udhamini wa kupata

intaneti ya bure na ikakubaliwa na mtandao mmoja

wa simu nchini.

Kwa hakika nikifikiria hali ya darasa langu na

wanafunzi wangu hakika napata uchungu sana

kutoka moyoni nikiwa sijui kama wanafunzi wangu

wataendelea kupata huduma ambazo mwalimu wao

nilikuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu ili waweze

Page 40: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

40

kuzipata maana wengi sana waliokuwa

wakinishangaa kwa nini nisianzishe shule binafsi ya

awali kwa ajili ya kujipatia fedha lakini lengo langu

lilikuwa ni kujenga msingi imara kwa elimu ya

watoto wa awali maana hicho ni kipindi cha

muhimu sana katika kujitambua vyema .

Yale yalikuwa mazingira katika darasa la kujifunzia

kwenye kile chumba cha kwanza lakini pia katika

chumba cha pili ambacho kilikuwa kipana zaidi

humo ndani kulikuwa na vifaa mbalimbali vya

kujifunzia na kuchezea kwa watoto na katika

chumba hicho cha pili nilikipa jina chumba cha

Page 41: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

41

ubunifu (creativity room )ambapo niliamini kuwa

watoto wanahitaji kucheza zaidi na kushiriki katika

shughuli nyingi zaidi za kitoto katika kukuza hali ya

ubunifu na afya ya akili hivyo kuanzia

midoli ,magari ,mikasi na kila aina ya zana na vifaa

vya kitoto vilipatikana ndani ya darasa langu hilo .

Lakini kwa nje pia kulikuwa na uwepo wa bembea

mbali mbali na kuburudika na hata za kuzungusha

ambazo zilikuwa zinawatamanisha na hata watu wa

wazima wa eneo husika maana watoto walikuwa

wanajifunza kwa raha zao hakika walikuwa

wanajifunza kwa furaha na nilikuwa naamini kuwa

kujifunza kwa burudani ni bora zaidi kuliko kwa

Page 42: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

42

vitisho na hasira na hiyo inanikumbusha

nilipohudhuria semina ya wiki tatu ya mafunzo ya

elimu ya awali nchini Finaland mkurugenzi wa Bodi

ya elimu nchini Finaland alisema kua (an educated

country can not created by force "akiwa na maana

kuwa taifa lililoelimika haliwezi kuandaliwa kwa

kutumia nguvu akiwa na maana mfumo wa elimu

uwe wa kushirikiana na sio kushindana .

Kwa hakika wanafunzi wangu walikuwa na utofauti

kabisa na wanafunzi wengine na nilikuwa na

ushirikiano wa kutosha wazazi wa wanafunzi hao

huku nilikuwa nawapa darasa elekezi kwa ajili ya

malezi ya watoto wao kwani niliwahi kuhudhuria

Page 43: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

43

mafunzo ya Family and school Partnership nchini

Singapore hivyo nilikuwa na ujuzi wa kutosha

kabisa ambao leo hii unaambulia adhabu ya

kunyongwa mpaka kufa .

Inaniuma sana zaidi ya sana pale nilipoambiwa

kuwa nimehusika kumuua na kumuingilia kinyume

na maumbile mwanafunzi wangu wa kike na tukio

hilo lilihisishwa na imani za kishirikina ili niweze

kuendelea kupata mafanikio zaidi na kukubalika kwa

wanajamii maana walisema haiwezekani mtu

kutumia mali zake kwa ajili ya watoto wasio wake

hakika walijua tu kuwa nilikuwa natumia imani za

kishirikina na kutokana na imani hiyo ilipelekea

Page 44: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

44

kumuua mwanafunzi wangu kitu ambacho sio cha

kweli na ndo kinanipa uchungu kabisa kutoka ndani

ya moyo wangu huku nikijiuliza kuwa iweje leo hii

mimi ambaye nilikuwa natumia muda mwingi kwa

ajili ya wanafunzi wangu na niliyekuwa natumia

taaluma yangu yote kwa ajili ya wanafunzi na

kuinua eneo la elimu ya awali leo nifanye mauaji

kwa binti mdogo kabisa asiyekuwa na hatia yeyote

ile kabisa tena wengi wanamini kuwa inawezekana

kuwa nilikuwa nafanya mapenzi na katoto hako

maana nilikuwa nakapa sana zawadi na nilikuwa

nako karibu sana tena kwa michezo mbalimbali

hivyo katika hilo hapakuwa na shaka na muda

Page 45: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

45

mwingine walikuwa wananiita mwalimu rafiki

wakiwa hivyo kutokana na kushindwa hivyo

wakawa wananiita rafiki hakika jamii ilifikiria

tofauti kabisa na hali halisi na ikapelekea kukosa wa

kunitetea hakika siwalaumu hata kidogo sababu

kutokana na mwili wa binti huyo mdogo ulivuokuwa

umeharibiwa vibaya kweli halafu wanapata taarifa ni

mimi ndiyo nilikuwa nahusika kwa kuwa walifika

katika hatua ya juu kabisa ya hasira hivyo adhabu ya

kunyongwa waliona ilikuwa halali yangu kabisa .

Nakumbuka Asha ni mwanafunzi ambaye alikuwa

chini ya uangalizi wangu wa kitaaluma na

kisaikolojia na kifizikia licha ya kutokuwa katika

Page 46: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

46

elimu ya awali lakini nilipewa jukumu la kujua

tatizo lake ni nini hasa na alikuwa ni kabinti kadogo

kazuri na kacheshi lakini mwenye tabia ya udadisi

sana muda mwingi alikuwa ni mtu wa maswali na

aina ya uulizaji wake ulikuwa ni kwa nini na vipi ,

kiumri Asha alikuwa na miaka sita kama sio saba

lakini anayepata tabu katika kusoma na kuandika

kwa kiwango kikubwa sana lakini alikuwa ni

muongeaji sana na mwimbaji mzuri wa nyimbo

hicho ni kiliwafanya wengi waamini kuwa Asha

alikuwa na kiburi na hakupenda kusoma kabisa

sababu vitu vingine alikuwa anafanya kwa nini suala

la kusoma na kuandika limshinde .

Page 47: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

47

Walimu waliamua kuwa wanamchapa sana na

wengine wakimuona ni mjinga na kisirani sana

mpaka wakamkatia tamaa jambo lilifanya familia

yake wamsuse baada ya kupata taarifa hizo

nikiomba awe katika uangalizi wangu wa kitaaluma

na kisaikolojia sababu suala alilokuwa akisumbuliwa

nalo Asha ni gumu kwa walimu wengi

hawakufundishwa namna ya kuwasaidia wanafunzi

wa nmna ile lakini kwa vile nilikuwa nimebobea

katika eneo ambalo kitaalamu linaitwa specific

learning difficulties yaani matatizo mahususi ya

ujifunzaji nilitambua fika neema alikuwa na shida .

Page 48: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

48

Nakumbuka baada ya kukaa kwa karibu na kwa

muda wa miezi miwili na kumpa majaribio ambayo

niliyopata nilipokuwa nachukua shahada yangu ya

pili nchini Finland katika chuo kikuu cha Henlisiki

kwenye ubobezi wa matatizo mahususi ya ujifunzaji

ambapo Asha alikuwa anasumbuliwa na matatizo

mawili moja ni dyslexia ambalo ni matatizo katika

suala la usomaji na dysgraphia ambalo ni matatizo

katika suala la uandishi ambao mtoto anakuwa na

uwezo wa kufanya mambo mengine vizuri lakini

linapokuja katika maeneo hayo mawili anakuwa

anapata ugumu sana hivyo ilibidi niwe naye karibu

Page 49: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

49

sana na kumuanzishia programu maalum kwa ajili

yake.

Kwanza kwenye suala la ujifunzaji ilikuwa lazima

nitumie mbinu mbadala ambazo ikiwa na mazoezi

ya awali yani pre reading exercise lakini pia katika

suala la kuandika ilibidi nimpe mazoezi ya mikono

na shughuli mbalimbali za kuongeza nguvu katika

vidole vyake ikiwa pamoja na kutumia sana mikasi

katika ukataji wa maboksi kwa muda wa wiki zaidi

ya tatu mabadiliko makubwa sana nakumbuka

yalianza kutokea kwa Asha mpaka walimu na watu

wa karibu na Asha hawakuweza kuamini kama Asha

sasa alianza kusoma na kuanza kuumba herufi

Page 50: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

50

hakika kwangu lilikuwa ni jambo la furaha sana

kwani niliweza kumsaidia Asha mpaka

akawa anaweza kusoma na kuandika vizuri kabisa

baada ya matumizi ya mbinu mbalimbali hakika

ukaribu wangu na Asha alikuwa mkubwa sana

sababu kisaikolojia wanafunzi wenye matatizo ya

namna hiyo inashauriwa tuwe nao karibu sana

ilifikia kipindi Asha alikuwa akigoma kufanya kitu

hasikilizi mpaka niende mimi.

lakini nakumbuka nilipata kazi ya kuandaa programu

ya kufundishia walimu wa shule za msingi katika

wilaya fulani hivyo nilihitajika kuindaa hivyo

Page 51: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

51

nilikuwa nashinda shule kwa muda mfupi sana lakini

wanafunzi wangu walikuwa tayari nilishawapa

mapumziko ya kitaaluma hivyo walikuwa wanakuja

kucheza tu kumbe nilikuwa sijapata taarifa kuwa

Asha naye hakuwepo nyumbani kwao walimtafuta

sana hawakumpata mpaka inafika usiku

hawakumuona mpaka inafika saa tatu usiku

nakumbuka hawakumuona lakini usiku ambao

kwangu ulikuwa ni mchungu sana maana nilikuwa

katika chumba changu ambacho kilikuwa kama ofisi

yangu ndogo maana kazi zangu nyingi nilikuwa

nafanya humo na siku hiyo nilichelewa sana kulala

na mlango sikuwa nimefunga.

Page 52: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

52

Ghafla nikasikia mlango ukifunguliwa kwa ghafla na

mtu akaingia huku nikiwa nashangaa kumba alikuwa

Asha muda huo alikuwa akivuja damu na

zikuchuruzika katika mapaja yake huku nikiwa

katika hali ya mshangao ghafla Asha alidondoka

chini kabisa kama gunia lilikuwa limesimamishwa

ukutani huku akiwa anakoroma kwa kweli

nilishikwa na butwaa kubwa huku nikiwa

nimeduwaa na kushikwa na mshangao kama dakika

tano nikiwa sitambui nini cha kufanya yani nilikuwa

kama sanamu ambalo limechongwa na

kusimamishwa ama kweli kumbe siku ya kufa nyani

miti huteleza mara nilisikia sauti za hodi kutoka nje

Page 53: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

53

hivyo kwa hali hiyo niliamua kumsukumia Asha

katika kabati lililokuwa tupu pembeni ya chumba

kile .

Kumbe walikuwa ni mapolisi na wazazi wa Asha na

walimu wengine ambao waliamua kuja kwangu

kunipa taarifa na kunilizia mimi sababu mimi ndo

nilikuwa moja kati ya walimu ambao tulikuwa

karibu sana na Asha waliingia mapolisi watatu na

wazazi na walimu wengine kuniulizia hata kabla

hawajaongea chochote ghafla mlango wa kabati

ambapo nilimuweka Asha kwa muda ili kutathimini

hatua za kuchukua katika tukio lile mlango wa

kabati ukafunguka na mwili wa Asha ukaanguka

Page 54: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

54

chini hakika watu wote walibaki na mshangao

mkubwa sana ghafla bila kutarajia nilipokea kofi

zito kutoka kwa afande aliyekuwa upande wa

kushoto kwangu na ilipigwa simu ya ghafla wakaja

askari wengine na taarifa zilisambaa kwa kasi ya

ajabu sana juu ya tukio hilo na ikaenea kuwa mimi

nimemuua Asha na kufanya naye mapenzi kwa

nguvu yaani nilimbaka.

Hakika nilikuwa nimebaki na butwaa sikuamini kile

kilichotokea nikiendelea kulia kwa uchungu sana

kutokana na hali ile sababu moja ya wanafunzi

wangu ambao nilijitolea kumfundisha kwa hali na

mali kabisa leo anakufa lakini nashutumiwa mimi

Page 55: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

55

mbaya zaidi nahusishwa na imani za kichawi

kutokana na mafanikio yangu makubwa katika eneo

la elimu kwa kweli taarifa zilisambaa Tanzania

nzima hadi nje ya mipaka ya Tanzania lakini ilikuwa

ni vigumu sana watu wasiamini kuwa mimi sihusiki

lakini kwa hali halisi watu wengi waliamini kuwa

nahusika kwa kiwango kikubwa sana kwa kweli

lilikuwa ni pigo kubwa sana.

Taratibu zote nakumbuka zilifuatwa za kipelelezi na

kisheria mpaka naingia kwenye hukumu juu ya

kunyongwa hadi kufa kwa kweli hadi leo sifahamu

ni nani aliyemtendea unyama ule mwanafunzi

wangu mpendwa hivyo hawakuumiza sana vichwa

Page 56: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

56

bali nilihusishwa moja kwa moja na kutokana na

hilo nikahukumiwa kunyongwa .

Lakini kutoka ndani ya moyo wangu sikuhusika na

tukio hilo kabisa mpaka sasa zimebakia siku mbili tu

niweze kunyongwa lakini naumia sana zaidi ya sana

moyo wangu unamaumivu kama kidonda kibichi

kilichomwagiwa maji ya betri nikililia nafsi lakini

mbaya zaidi taifa langu kwenye masuala kielimu

kwa kweli nilikonda ndani ya siku mbili tu lakini pia

niliumia kuwa mipango yangu katika suala la elimu

yatakuwa yamepotea hivyo lakini pia taaluma ya

ualimu itakuwa kama imeingiliwa jini baya sana la

mikosi maana matukio mengi sana yalitokea na hili

Page 57: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

57

la kuhukumiwa kunyongwa likiwa pigo jingine

kubwa sana katika taaluma ambayo naimani

itasababisha walimu wengi kuamua kuacha taaluma

ya ualimu lakini kamwe msirudi nyuma hivyo

niwaombe sana walimu wenzangu msirudi nyuma

taifa linatutegemea sana.

Mpaka hapa nilipo naumia sana zaidi ya sana lakini

namuomba mungu licha ya kuwa nitanyongwa na

kufa lakini naamini siku moja ukweli utakuja

kubainika ni nani aliyesababisha mauaji ya

mwanafunzi Asha angali mdogo kiasi kile lakini

alikuwa na ndoto ya kuja kuwa mwanasheria

mbobezi ili aje kuwatetea wanyonge wote

Page 58: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

58

wanaonewa na wenye fedha lakini ndoto zake

zimekatizwa pasipo kutimia barua hii naimani

itakuwa imetoa dukuduku langu la kuzungumza hali

halisi ya tukio husika kuhusu utata wa kifo cha Asha

huko mliko msichoke kumwombea Mungu

amuweke mahali pepa peponi amina.

Ni mimi

Mwalimu J.M

Page 59: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

59

MSIRUDI NYUMA.

Habari za huko mliko walimu tarajiwa natuma

salamu zangu za dhati kabisa kutokea huku niliko

mbali na uso wa dunia ambayo nyie mpo ,salamu

zangu zifike kwenye vitivo vyote vya elimu katika

vyuo vikuu kuanzia kule chuo kikuu cha Dar es

salaam hadi kule katika kitivo cha elimu pale chuo

kikuu cha Dodoma lakini salamu zangu ziwafikie

hadi wale wa DUCE lakini zipande hadi kaskazini

mwa nchi yangu kule Makumira na zipandishe hadi

kanda ya ziwa zifike SAUT pale maeneo ya

malimbe lakini upepo uvumishe salamu zangu

mpaka nyanda za juu kusini kule Muce na Rucu

Page 60: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

60

lakini zisogee juu kidogo kule Teku na kipindi

zinarudi ziwafikie pale Mzumbe na pale Jordani

Hakika kwa dhati ya moyo pia natuma salamu zifike

kwa walimu wa ngazi za vyeti hadi diploma

vilivyopo pande zote za taifa langu la Tanzania

lakini salamu zivuke mawimbi ya bahari mpaka

Zanzibar nako huko zifike lakini ikiwezekana zivuke

na mipaka ya nchi zifike hadi kwa majirani zetu

tunaopakana nao ni salamu ambazo nazituma huku

ikiwa ni nafasi ya pekee ya kutuma salamu zangu na

kuwasalimu na hatua kuwakumbusha yale machache

lakini ya umuhimu naandika haya huku nikiwa na

maumivu makali lakini napata faraja kubwa nikiona

Page 61: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

61

kundi kubwa la vijana makini ambao wameamua

kuingia katika taaluma hii nzito kabisa hapa chini ya

jua baada ya kuandika waraka huu kwenu naimani

kabisa kuwa moyo wangu utakuwa mweupe kama

theluji ya Mlima Kilimanjaro sababu kuchanika kwa

jamvi sio mwisho wa maongezi hakika naamini .

Labda niseme kwa dhati ya moyo wangu popote pale

mlipo hakika nyie ni majemedari makini kabisa

ambao mmeamua kumuunga mkono hayati

Mwalimu J.K.Nyerere kupigana vita kati ya moja ya

maadui wale wa tatu yaani adui ujinga kwa hakika

hilo ni jambo la kupendeza sana na kutia moyo

maana adui huyu akishambuliwa na akiwa katika

Page 62: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

62

hali mbaya hakika inakuwa rahisi sana

kuwashambulia kwa urahisi kabisa hao maadui

wengine yani maradhi na umaskini sababu nia ya

kuwapiga tunayo na nguvu ya kuwapiga tunayo

hakika niwapongeze sana kutoka ndani ya moyo

wangu natamani mngeweza kuona ndani ya moyo

wangu licha ya kuwa na maumivu lakini naliona

tumaini jipya na lenye matumaini mazuri kabisa

hakika hata siku ya hukumu yangu ikitekelezwa

nafahamu kuwa kuna watu imara wako na nia ya

dhati kabisa katika taifa letu.

Walimu tarajiwa natambua fika kuwa wengi wenu

mmeacha taaluma mbalimbali na kuamua kuja

Page 63: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

63

katika taaluma hii ya ualimu iwe kwa kupenda au

mfumo umekufanya kuchagua kuja huku hiyo

haitakufanya usihesabike kama mwalimu napenda

utambue kuwa mbali na changamoto mbalimbali

lakini umechagua fungu lililo jema kabisa maana sisi

ndo ambao bila sisi maana halisi ya elimu rasmi

haiwezi kutokea lakini pia tambua kuwa walimu

tunamsaidia Mungu katika uumbaji na ni watumishi

ambao Mungu anatuamini kwa kiwango kikubwa

sana .

Napenda nikwambie yale baadhi ya mambo ambayo

yanapatikana katika taaluma hii ya ualimu yapo ya

kufurahisha na hata kuzunisha na kukatisha tamaa

Page 64: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

64

kabisa lakini kamwe msirudi nyuma maana hatma ya

taifa hili limo mikononi mwenu walimu tarajiwa

kwanza ni vijana lakini pia mmetokea katika zama

za sayansi na teknolojia hivyo mna nafasi kubwa

sana ya kuleta mabadiliko katika mfumo wa elimu

hasa ya awali maana huko ndiko mahali ambako

wamepasahu lakini naamini kuwa mtakuja na mbinu

na njia mbalimbali za kusaidia katika eneo hilo

hakika nyie ni watu muhimu sana na Mungu

analitambua hilo fika licha kuwa kwa sasa thamani

yetu imeshuka kwa kasi kubwa .

Naongea haya kuhusu nyie walimu tarajiwa ambao

ndio mmeamua kuingia katika mfumo huu wa

Page 65: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

65

taaluma maana kuna kipindi mnaweza kata tamaa

lakini kamwe msirudi nyuma sababu watoto wa taifa

hili wapo mikononi mwenu na nyie ndo wenye

uwezo wa kujenga taifa imara au taifa lisilo imara

maana wanafunzi wanawasakiliza kwa umakini sana.

Naandika haya nikiwa naingalia jamii yangu kuhusu

mitazamo yao kuhusu taaluma ya ualimu na asilimia

kubwa wengi wanaichukulia taaluma yetu kama

sehemu ambayo watu ambao wamefeli au wamepata

alama ambazo zinawafanya wakose sifa ya

kuchaguliwa katika taaluma nyingine na ndo maana

mkaamua kuja katika taaluma hii huenda ikawa

kweli lakini sio kwa wote kuna waalimu wenye

Page 66: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

66

ufaulu mkubwa kabisa lakini wamekuja katika

taaluma hivyo licha ya maneno hayo kamwe msirudi

nyuma maana endapo mkiamua kurudi hakika

mtakuwa imerirudisha nyuma sana taifa lenu tena

kwa kiwango kikubwa kabisa hivyo kamwe msirudi

nyuma .

Lakini pia natambua kabisa kuna kipindi kitafika

viongozi wengi watakuja kwenu na kutoa matamko

ya kudhalilisha na kejeli sana dhidi yenu tena baadhi

ya viongozi hao wengi wenu mmewazidi elimu

lakini mbali na kuwazidi elimu na wengine hata

umri lakini watawasema sana kuhusu kufeli kwa

wanafunzi kama vile kuna mwalimu anayependa

Page 67: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

67

kuona mwanafunzi wake anafeli bila kusahau kuwa

katika suala la ufundishaji na ufaulu sio suala la

mwalimu tu bali inabidi kuwe na timu shirikishi

ambayo itajumuisha serikali ,shule na ambayo

inajumuisha walimu na wafanyakazi wengine wa

shuleni lakini pia inajumuisha na wanajamii pia

lakini hao wote hawataonekana utaonekana wewe

pekee ndio mhusika mkuu kamwe usije ukarudi

nyuma katika hilo maana litakuwa kosa kubwa sana

cha msingi ni kupiga moyo konde na kusonga mbele

kwa niaba ya taifa lako.

Natambua fika kutokana na makato kutoka bodi ya

mikopo ya elimu ya juu mshahara wako utabaki

Page 68: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

68

kidogo licha ya ahadi kubwa ambazo mtaendelea

kupokea kutoka kwa viongozi na siku zitakwenda

bila kupatiwa lakini kamwe usirudi nyuma tambua

fika furaha na baraka ya mwalimu ni kuona

wanafunzi wake wanafaulu vizuri sana najua

maumivu yatazidi sana pale ambapo wenzenu

walioenda katika sekta nyingine watakavyokuwa

wakiongezewa mishahara yao kimya kimya na

posho juu lakini hali kwako itakuwa tofauti kabisa

usirudi nyuma bali ongeza juhudi katika kufundisha

wanafunzi wako huenda siku moja watakuja

kukusaidieni katika maboresho ya sera nzuri kuhusu

walimu hivyo kipato kuwa kidogo najua itakuwa

Page 69: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

69

changamoto lakini unaweza jiongeza kuwa kuanza

kufanya shughuli nyingine za kuongeza kipato

kutokana na mshahara wako unaweza ukalima na

hata ukafuga au ukaingia kwenye shughuli za

ununuzi wa hisa au suala la usafirishaji lengo kuu

likiwa kuongeza kipato chako lakini usijisahau sana

mpaka ikapelekea kusahau majukumu yako ya

kiutumishi hakika utakuwa ujautendea haki ualimu

wako kamwe mbali na hayo usirudi nyuma .

Mwalimu tarajiwa najua unasikia mengi sana lakini

pia unajua kuwa kuna chama cha walimu ndio

chama kipo na tena ndio wawakilishi wetu lakini

tambua kuna mengi ambayo yapo nyuma yao hasa

Page 70: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

70

kuhusu katika taaluma yetu ya ualimu wengi wao

kabla ya kupata nafasi za kuiongoza chama hicho

harakati zao zote za utetezi wa walimu huwa

unapotea maana labda kwa vile madaraka yanalevya

na wengine wanasema kuwa viongozi wengi ni

wanachama hai wa wenye dola yetu hivyo ni ngumu

sana kwenda kuwapigania walimu sababu

watakuwa wanakwenda kinyume na chama tawala

lakini bado mwalimu una nafasi ya kuchagua

viongozi wenye uzalendo na taaluma lakini wenye

uzalendo wa kutosha na taaluma lakini pia wana

elimu na uelewa wa kutosha juu ya taaluma husika

na masuala ya wafanyakazi hiyo itawasaidia sana

Page 71: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

71

katika kutetea maslahi yenu kupitia chama chenu

cha taaluma najua kabisa mambo yatakuwa mengi

kabisa na mtawalalamikia sana na huenda ikapelekea

kupunguza morali ya kazi kwenu kamwe hasira

dhidi yao usiirudishe katika darasa lako na

kupelekea kuathiri suala zima la ujifunzaji na

ufundishaji nakuomba sana kamwe usirudi nyuma .

Wewe ni mwalimu na sifa ya mwalimu sio tu

kufundisha lazima utambue hili kuwa mwalimu

huwa anakuwa zaidi ya mwalimu anatekeleza

majukumu zaidi na ufundishaji kwa mwanafunzi

wake kuna muda utakuwa kama

daktari ,mshauri ,mlezi ,kocha ,na mengine mengi

Page 72: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

72

lazima ujitahidi kadri ya uwezo wako kumjenga

mwanafunzi katika maeneo yote muhimu

kimwili ,kiakili na kiroho pia hii itamfanya

mwanafunzi awe na uwezo mkubwa sana wa

kutumia akili yake ipasavyo nafahamu kuwa kuna

wanafunzi ambao huwa wanatabia ambazo kwa

kweli huwa hazipendenzi kabisa lakini kwa kuwa

wewe ni mwalimu kero hizo za mwanafunzi huyo

zisikutishe tamaa na ikapelekea kumsusa kabisa

kamwe usifanye kosa hilo tambua taifa

linakutegemea sana .

Nilipenda niandike mengi sana kuwahusu walimu

tarajiwa na taaluma husika lakini muda wangu ni

Page 73: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

73

mdogo sana na hata karatasi niliyopewa kwa ajili ya

kuandikia barua yangu hii imeshajaa naamini kuwa

mtakwenda kufanya mabadiliko makubwa sana

katika mfumo wa elimu katika nchi ya Tanzania na

mabadiliko makubwa sana yatakwenda kutokea

katika mfumo wetu wa elimu .

Natuma salamu hizi ziwafikie huko mliko kuwa

nawapenda sana ndugu walimu wenzangu hakika

Mungu atakuwa nanyi siku zote kwa maisha yenu na

yatakuwa na baraka kubwa sana .

Lakini walimu tarajiwa tambueni kuwa wanajamii

ambao wanawazunguka wanauelewa mdogo sana

Page 74: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

74

kuhusu masuala ya elimu na wengi wanatambua na

kuamini kuwa mwalimu na shule pekee ndio

wanajukumu la kufuatilia suala la elimu kitu

ambacho siyo cha kweli basi msichoke kuwapa

semina elekezi kuhusu umuhimu wa ushiriki wao

katika kuinua elimu hapo lazima kuwepo umoja

baina ya jamii ,wanafunzi na walimu mkilifanikisha

hili mtakuwa mmelisaidia sana taifa katika eneo la

elimu .

Natambua kuwa wengi wenu baada ya kuhitimu

masomo yenu ya ualimu mtaingia shuleni na kuanza

kufundisha na kuna kipindi mtakuwa mnapata

semina elekezi kuhusiana na taaluma husika

Page 75: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

75

kitaalamu ni induction program lakini kwa kiwango

kikubwa wanaochaguliwa kujiunga na programu

hizo ni wachache na tena ni kwa upendeleo hivyo

isikukatishe tamaa ya kutafuta maarifa sehemu

nyingine kuhusu taaluma yako ili uendane na

mabadiliko ya ulimwengu wa elimu huu itakusaidia

kuwa mwalimu makini kabisa .

.

Lakini walimu tarajiwa lazima tufahamu kuwa

mwalimu sio Mungu mtu bali ni daraja bora la

ujifunzaji na ufundishaji shuleni hivyo pale ambapo

wanafunzi watakuwa wanaleta mawazo na maoni

Page 76: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

76

yao kamwe usiyakatae na ushirikiane nao na uwe

tayari kujifunza kutoka kwao maana na wewe ni

binadamu huwezi kuwa unatambua kila kitu hii

itaongezea wigo mpana wa kuyatambua mengi zaidi

sana mwalimu tarajiwa .

Ubunifu katika ufundishaji na ujifunzaji ni suala

muhimu sana kulitambua walimu tarajiwa lazima

ukae na ufikirie jinsi ya kuja na mbinu na njia

ambazo ni rafiki katika ujifunzaji na ufundishaji

kuliko kutumia mbinu zilizozoeleka miaka yote

lazima mbinu za ufundishaji ziwe na ubunifu mzuri

kabisa yaendane sambamba na matumizi ya zana na

ufundishaji mwalimu hata kama serikali haitaleta

Page 77: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

77

lakini lazima utambue kutumia mbinu mbalimbali za

kiualimu katika kuandaa zana zako za ufundishaji

wako yaani improvisation in education media and

technology Sababu tunaishi katika jamii ambazo

kuna malighafi ambazo tunaweza kuzitumia katika

ujifunzaji na ufundishaji.

Mwisho kabisa naandika haya nikiwa natambua

kuwa walimu tarajiwa mtakuja kuleta mabadiliko

makubwa na tambueni kuwa heshima na thamani ya

taaluma ya ualimu iko mikononi mwenu kamwe

msikubali wachache waishushe heshima ya taaluma

hii adhimu kabisa hivyo ilindeni kwa jasho na damu

ilindeni taaluma yenu kamwe narudia tena

Page 78: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

78

msiruhusu kikundi cha watu wachache washushe

heshima ya taaluma ya ualimu maana hapo ndio

chemchem ya maarifa ya taifa ilipo hivyo inabidi

patunzwe kwa hali ya juu na hekima na busara

kubwa sana.

"The best teacher teach from the heart not from the

book"

Our main focus is children not the subject matter"

Teaching is mother of all other Profession

Page 79: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

79

Hakika Mungu awajalie hekima na busara nyingi

sana kwenu ili muweze kushirikisha maarifa bora

kwa manufaa ya taifa .

Ni mimi mwalimu mwenzenu.

J.M.

Page 80: MSIRUDI NYUMA - Mwalimu Wa Kiswahili · mioyo yao ya upendo juu yetu hakika hiki ni kitabu chao. Lakini pia nakitabaruku kitabu hiki kwa rafiki ... ambapo kuna mwalimu alifuatwa na

80

ASANTENI SANA.

S