mwanzo gazeti tando la kikristo la kila wiki mwanzo ......wa zimbabwe, uebert angel ambaye alikuwa...

12
PATA HABARI ZA KIKRISTO KIGANJANI MWAKO Toleo Na. 002 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo Kwa habari mlipuko ingia www.mwanzonews.com Kwa habari kutoka maeneo mbalimbali jisajili kusoma gazeti tando la Kikristo la kila wiki la Mwanzo. Kwa habari na makala za uchambuzi wa kina jisajili kusoma jarida la mtandaoni la Pastor’s Life Magazine Ukiwa na habari ya Kikristo tupigie 0754 649 941 Tunakufunulia Ukweli Askofu Kakobe: Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering Church (ECG), Nabii Shepherd Bushiri, anadaiwa kununua nyumba yenye thamani ya dola milioni 12 (sawa na shilingi bilioni 27). Bushiri, ambaye hufahamika pia kwa jina la utani la Major 1, ni raia wa Malawi. Ana makanisa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania ambapo kanisa lake lipo eneo la Survey, Mwenge, jijini Dar es Salaam. (chanzo:ukurasa wa facebook wa Zimbabwe Today). NABII MWENYE KANISA DAR ANUNUA MJENGO WA SH. BILIONI 27 ZAMBIA YAPIGA MARUFUKU MAKANISA KUUZA MAFUTA YA UPAKO UK. 2 ASKOFU ALIONYA KANISA, ATAKA LISEME UKWELI, LIACHE USHABIKI HABARI Miujiza inayotendeka sio ya kudumu Na Morning Star, Zanzibar Mahakama ya Zanzibar hivi karibuni (Alhamis Julai 20,mwaka huu) imetoa hukumu kwamba kanisa haliwezi kuendelea na ujenzi wa jengo la kuabudia ambalo kwa miaka minane kanisa hilo limejaribu kupambana kumaliza ujenzi wake, imefahamika. Mahakama Zanzibar yaungana na Waislamu kuzuia ujenzi wa kanisa Inaendelea Uk. 4 n Asema ndio maana Lazaro kipofu licha ya kuponywa lakini alikufa

Upload: others

Post on 22-Jan-2021

49 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 1Mwanzo PATA HABARI ZA KIKRISTO KIGANJANI MWAKO

Toleo Na. 002 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017

Gazeti Tando la Kikristo la kila wikiMwanzo Kwa habari mlipuko ingia www.mwanzonews.com

Kwa habari kutoka maeneo mbalimbali jisajili kusoma gazeti tando la Kikristo la kila wiki la Mwanzo. Kwa habari na makala za uchambuzi wa kina jisajili

kusoma jarida la mtandaoni la Pastor’s Life Magazine

Ukiwa na habari ya Kikristo tupigie 0754 649 941

Tunakufunulia Ukweli

Askofu Kakobe:

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering Church (ECG), Nabii Shepherd Bushiri, anadaiwa kununua nyumba yenye thamani ya dola milioni 12 (sawa na shilingi bilioni 27). Bushiri, ambaye hufahamika pia kwa jina la utani la Major 1, ni raia wa Malawi. Ana makanisa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania ambapo kanisa lake lipo eneo la Survey, Mwenge, jijini Dar es Salaam. (chanzo:ukurasa wa facebook wa Zimbabwe Today).

NABII MWENYE KANISA DAR ANUNUA

MJENGO WA SH. BILIONI 27

ZAMBIA YAPIGA MARUFUKU MAKANISA KUUZA MAFUTA YA UPAKO UK. 2

ASKOFU ALIONYA KANISA, ATAKA LISEME UKWELI, LIACHE USHABIKI

HABARI

Miujiza inayotendekasio ya kudumu

Na Morning Star, Zanzibar

Mahakama ya Zanzibar hivi karibuni (Alhamis Julai 20,mwaka huu) imetoa hukumu kwamba kanisa haliwezi kuendelea na ujenzi wa jengo la kuabudia ambalo kwa miaka minane kanisa hilo limejaribu kupambana kumaliza ujenzi wake, imefahamika.

Mahakama Zanzibar yaungana na Waislamu kuzuia ujenzi wa kanisa

Inaendelea Uk. 4

nAsema ndio maana Lazaro kipofu licha ya kuponywa lakini alikufa

Page 2: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

2 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo Habari

Askofu Kakobe: Miujiza inayotendeka sio ya kudumuNa Mwandishi Wetu

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, amesema ingawa watu wengi wanapokea baraka kwa kutendewa miujiza mbalimbali katika maisha yao, lakini miujiza na baraka hizo hazina maana sana, kwa kuwa ni za muda tu, badala yake kilicho muhimu ni baraka kuu ambayo ni uhakika wa mwanadamu kuondolewa dhambi zake.

“ T u m e s i k i a unapozungumzia baraka, wengi wanafikiria ni pesa, nyumba, magari, au mali mali hivi..Ndio, hizi baadhi yake ni baraka, lakini ipo baraka kuu na ambayo ndio muhimu zaidi. Na hiyo baraka kuu ni ule uhakika wa wewe kuondolewa dhambi zako,” alisema Askofu Kakobe katika mahubiri yake nchini Sweden, hivi karibuni, ambayo kanda yake ya video gazeti hili linayo.

Askofu huyo ambaye alifundisha somo lenye kichwa kisema ‘Baraka Kuu’ na kujikita zaidi kuzungumzia juu ya Toba ya kweli na Msamaha wa Dhambi, alisema ni kweli kwamba Mungu aliyetenda miujiza zamani hata leo anaendelea kutenda miujiza

kwa kuwa Yeye ni Mungu wa miujiza, lakini toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi ni jambo muhimu zaidi kwa kila Mkristo.

“Kila neno halisi la Mungu likihubiriwa ishara na miujiza hufuatana nalo. Leo ni siku ambayo kila mmoja atapokea baraka kutoka kwa Mungu. Unahitaji baraka utapata baraka. Lakini hapa hatuzungumzii baraka au miujiza inayohubiriwa na wahubiri wengi sehemu mbalimbali duniani. Hatuzungumzii miujiza hii ya mwilini, tunazungumza baraka kuu na maisha ya milele yanayotokana na kuondolewa kwa dhambi zako,” alisema.

Askofu huyo alinukuu maandiko kutoka Marko 2: 1-12 na kueleza kuwa Yesu alipopelekewa mgonjwa aliyepooza kule Kapernaumu kila mmoja alitarajia kuwa angemponya, lakini tofauti na matarajio yao Yesu alizungumzia kuhusu kusamehewa dhambi. “Watu wale walikaa wakitarajia kuona Yesu akimfanyia uponyaji yule mtu, lakini Yeye akamwambia dhambi zako zimesamehewa,” alisema Kakobe.

Andiko hilo linasema: “Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha

wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa anasema nao neno lake. Wakaja watu wenye kumletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.

Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwepo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza , Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwishe godoro lako, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo

amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwishe godoro lako uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwisha godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema Namna hii hatujapata kuiona kamwe.”

Askofu Kaobe alisema: “Hapo Yesu alikuwa akizungumzia baraka iliyo kuu. Alikuwa hazungumzii hii miujiza na baraka za ajabu ajabu. Yule mtu aliponywa, lakini alikufa. Hata Lazaro upofu ulitoweka lakini alikufa tena. Hii miujiza ni ya muda tu sio ya kudumu. Watu watafanyiwa miujiza lakini watakufa tu, lakini kama tuna msamaha wa dhambi na wokovu haya ni ya milele.”

Aliongeza kusema Askofu: “Yesu alisema kwa kuwa tunaishi katika dunia hii tutapita katika magumu mengi, lakini tukifika mbinguni hatutakuwa na maumivu, hatutaomboleza..itakuwa ni furaha juu ya furaha ya milele, na mambo yote yaliyopita yatakuwa historia.”

Kwa kusikiliza mahubiri hayo ya Askofu Kakobe nchini Sweden kwa ukamilifu ingia katika tovuti ya habari za Kikristo ya mwanzonews.com

Zambia yapiga marufuku makanisa kuuza mafuta ya upakoNa Zambia Daily Mail

Serikali ya Zambia imeyataka makanisa nchini humo kuacha kuuza mafuta na maji ya upako, matendo ambayo yameenea katika baadhi ya makanisa.Waziri wa Mwongozo wa Kitaifa na Mambo ya Dini nchini humo, Godfridah Sumaili ameelezea uuzaji wa mafuta na maji ya upako kuwa ni sawa na kuchezea akili za watu na ni kuwadhulumu.“Kuuza mafuta ya upako na maji matakatifu ni wizi, ni jinai, acheni kuwauzia watu wasio na uelewa. Uweza unatoka kwa Mungu; Mungu anawatumia nyie [wachungaji] kama chombo, mmepokea bure kutoka kwa Mungu ni lazima mtoe bure,” alisema Sumaili, ambaye naye ni mchungaji.Akizungumza na wachungaji wanachama wa ushirika wa Livingstone Pastors Fellowship, hivi karibuni, Mchungaji Sumaili alisema

manabii wanaouza mafuta na maji ya upako wanajinufaisha kupitia baadhi ya watu waliokata tamaa.Alisema ni bahati mbaya Wazambia wamekuwa wakichezewa akili na kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa manabii kwa kubadilishana na miujiza, mafuta ya upako na maji matakatifu.Miezi michache iliyopita Serikali ya Zambia ilitangaza kuwa haitaruhusu manabii na wamisionari kuingia nchini humo kwa lengo la kujipatia fedha kupitia huduma za kiroho, kutoka kwa Wazambia maskini waliokata tamaa.Mchungaji Sumaili alisema nchi hiyo ni taifa la Kikristo lenye sheria zinazoliongoza na Serikali inatarajia kuona manabii wote na watumishi wa Mungu wengine wakizingatia sheria.“Ni watu wa Mungu pekee, iwe wachungaji, wamisionari na manabii wanaohubiri injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo ndio watakaoruhusiwa

hapa nchini. Wizara yangu inapenda kuona hekima katika mwili wa Kristo”, alisema Mchungaji Sumaili.Alisema watumishi wa Mungu wanaotaka kutoza fedha kwenye mikutano yao hawataruhusiwa nchini humo.Alikuwa akizungumzia hatua ya Serikali ya kumzuia kuingia nchini humo Nabii wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia kwa kulipa Kwacha 20,000 (sawa na Shilingi za Tanzania zaidi ya milioni 10). Kongamano hilo lilidaiwa kuwa lililenga kuwapa washiriki mbinu za ‘kiroho’ za kuwa mamilionea na lilijulikana kama Milionare Academy.“Ni kuwafanya watu waone kuwa jambo hili ni kweli, hasa wale ambao wamekata tamaa na wameweka matumaini yao kiroho kupitia mikutano kama hiyo. Je, injili ni kwa watu

matajiri peke yao? Vipi kuhusu Wazambia maskini? Manabii wengine wanataka waje wajipatie fedha na waondoke zao, jambo ambalo wizara yangu haitaliruhusu”, alisema.Wakati huo Idara ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda ilimzuia kuingia nchini Zambia Nabii Uebert AngelNabii Uebert, ambaye ni mwanzilishi wa huduma ya Kipentekoste ya Spirit Embassy nchini Zimbabwe alikuwa akitokea nchini Uingereza akiwa na mkewe pamoja na watu wengine wawili, walipanda ndege ya shirika la Emirates.Aliwasili katika uwanja huo majira ya saa tisa alasiri ambapo Uebert na kundi lake walikataliwa kuingia Zambia na hivyo kulazimika kurejea Uingereza kwa kutumia ndege hiyo hiyo. Vyanzo: Zambia Daily Mail/Lusakatimes.com/Mwanzonews.com

Na Peter Mkwavila, Dodoma

Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania, Donald Manase amewataka viongozi wenzake wa Kanisa kutojiingiza katika migogoro, ikiwemo ya kisiasa kwa kuingiza ushabiki katika mambo ya msingi, na badala yake wasimamie haki na kusema ukweli.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 41 wa Maaskofu na Wachungaji wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania, uliofanyika mjini Dodoma, wiki hii, Askofu Manase alisema:

“Nyinyi viongozi wenzangu msikubali kabisa kujiingiza kwenye migogoro ya aina yoyote, iwe makanisani, kwenye makundi makundi ya kisiasa, badala yake mkasimamie haki na kusema ukweli bila kuingiza ushabiki katika mambo ya msingi.”

“Kanisa haliko tayari kuona nchi inaingia katika machafuko kwa kuwaruhusu watu wachache wakitumiwa kufanya vurugu,na huku Katiba yetu ya nchi inavunjwa.”

“Lazima tujue kuwa viongozi wote waliopo serikalini wanatokea katika nyumba zetu za ibada, kama kweli tunataka kutunza amani ya nchi ni lazima tushirikiane na kukemea na kuonya pale ambapo inaonekana wazi kuwepo kwa uvunjifu wa amani.”

Mgeni rasmi katika mkutano huo alitarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. Hata hivyo, hakuhudhuria na hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu kutokuwepo kwake.

Askofu Manase alisema kuwa mojawapo ya kazi kubwa ya Kanisa ni kuhakikisha linasimamia taifa katika kutenda haki, huku demokrasia ikiwa inalindwa na kusimamiwa na katiba yake.

Alisema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kufanya kazi na serikali huku wakitimiza wajibu wao pia kwa kukemea vitendo visivyo vya haki, wizi,rushwa pamoja na ufisadi.

Katika hatua nyingine askofu huyo alisema kwa sasa Kanisa la Baptist Tanzania linafanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya elimu, afya pamoja na kuiombea serikali ili amani iweze kudumu nchini.

Aliwataka maaskofu na wachungaji kujiepusha wa kanisa hilo kujiepusha na migogoro kwani hukwamisha maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla. Alisema kama kanisa likiwa na migogoro haliwezi kutimiza kwa ufanisi wajibu wake mkuu wa kuhubiri injili, na wala haliwezi kutekeleza miradi ya maendeleo kwa jamii kama vile elimu na afya.

Askofu alionya Kanisa, ataka liseme ukweli, liache ushabiki

Page 3: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 3Mwanzo

Mtume asema kanisa lazima lijifunze kufikiri tofauti

Habari

Na Suzy Butondo, Shinyanga

Mwangalizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Sehemu ya Kaskazini, Jimbo la Shinyanga, Mchungaji Emmanuel Herman amewataka Wakristo kuwa na utaratibu wa kumkumbusha Mungu juu ya mahitaji mbalimbali waliyoyaomba ili aweze kuwajibu.

Alitoa wito huo kwenye Semina ya Wanawake waumini wa Kanisa hilo Sehemu ya Kaskazini, iliyofanyika katika kijiji cha Mwamagunguli, kilichoko katika Manispaa ya Shinyanga, hivi karibuni.

Alisema kuna wakati Mungu anahitaji akumbushwe ili afanye ambacho Mkristo amekiomba kwani wanaoomba ni wengi, na anayeomba hatakiwi kukaa tu na kusubiri kujibiwa, bali anatakiwa kuendelea kuomba maombi ya kumkumbusha Mungu.

Mchungaji Herman alisema kuna watu wengi wamekuwa wakimuomba Mungu mara moja tu, na hawaendelei tena kumkumbusha. Alisema kwa kufanya hivyo mtu anaweza kukaa akisubiri bila kujibiwa, hivyo ni vizuri kumkumbusha Mungu ili aweze kumpa haki yake mwombaji.

Hata hivyo, mchungaji huyo alisema ili kujibiwa maombi kwa wakati mtu anatakiwa asitende dhambi kwani kutenda dhambi humfanya Mungu akate mawasiliano na mhusika. Alisema Adamu alivyokula tunda mawasiliano baina yake na Mungu yalikosekana. Mchungaji huyo alirejea maandiko katika Isaya 59:1-2.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Sehemu hiyo ya Kaskazini, Ernel Kitoki aliwataka wanawake kuiona dhambi kuwa ni sawa na sumu, na hivyo wadumishe utakatifu na maombi ya kumaanisha ili Mungu awajibu mahitaji yao.

“Sisi kama wanawake tufikie mahali tuione dhambi kama sumu jamani, tuwe na tahadhali katika kutenda dhambi. Ukiiona dhambi inakuijia tafuta kila namna kuiondoa ili mahusiano yetu na Mungu yasivunjike,”alisema Kitoki.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake wa Kristo (WWK), Jimbo la Shinyanga, Leokadia Masele alisema mafanikio yanapatikana kwa Mungu peke yake, kinachotakiwa ni kumwamini kuwa anaweza. Alihimiza maombi ili Mungu afungue njia na baraka zitokee.

Mchungaji ahimiza maombi ya kumkumbusha Mungu Na Suzy Butondo, Shinyanga

Mwangalizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Sehemu ya Kaskazini, Jimbo la Shinyanga, Mchungaji Emmanuel Herman amewataka Wakristo kuwa na utaratibu wa kumkumbusha Mungu juu ya mahitaji mbalimbali waliyoyaomba ili aweze kuwajibu.

Alitoa wito huo kwenye Semina ya Wanawake waumini wa Kanisa hilo Sehemu ya Kaskazini, iliyofanyika katika kijiji cha Mwamagunguli, kilichoko katika Manispaa ya Shinyanga, hivi karibuni.

Alisema kuna wakati Mungu anahitaji akumbushwe ili afanye ambacho Mkristo amekiomba kwani wanaoomba ni wengi, na anayeomba hatakiwi kukaa tu na kusubiri kujibiwa, bali anatakiwa kuendelea kuomba maombi ya kumkumbusha Mungu.

Mchungaji Herman alisema kuna watu wengi wamekuwa wakimuomba Mungu mara moja tu, na hawaendelei tena kumkumbusha. Alisema kwa kufanya hivyo mtu anaweza kukaa akisubiri bila kujibiwa, hivyo ni vizuri kumkumbusha Mungu ili aweze kumpa haki yake mwombaji.

Hata hivyo, mchungaji huyo alisema ili kujibiwa maombi kwa wakati mtu anatakiwa asitende dhambi kwani kutenda dhambi humfanya Mungu akate mawasiliano na mhusika. Alisema Adamu alivyokula tunda mawasiliano baina yake na Mungu yalikosekana. Mchungaji huyo alirejea maandiko katika Isaya 59:1-2.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Sehemu hiyo ya Kaskazini, Ernel Kitoki aliwataka wanawake kuiona dhambi kuwa ni sawa na sumu, na hivyo wadumishe utakatifu na maombi ya kumaanisha ili Mungu awajibu mahitaji yao.

“Sisi kama wanawake tufikie mahali tuione dhambi kama sumu jamani, tuwe na tahadhali katika kutenda dhambi. Ukiiona dhambi inakuijia tafuta kila namna kuiondoa ili mahusiano yetu na Mungu yasivunjike,”alisema Kitoki.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake wa Kristo (WWK), Jimbo la Shinyanga, Leokadia Masele alisema mafanikio yanapatikana kwa Mungu peke yake, kinachotakiwa ni kumwamini kuwa anaweza. Alihimiza maombi ili Mungu afungue njia na baraka zitokee.

Kampala, Uganda

Kanisa mara nyingi linataka kubadilisha maisha ya watu, lakini kile ambacho linapaswa kukifanya kwanza ni kubadili namna yake ya kufikiri, mwinjilisti maarufu anayehubiri kupitia televisheni nchini Uganda, Mtume Alex Mitala, amesema.

Akizungumza na mamia ya Wakristo wakati wa Kongamano la Kuzaliwa Upya-2017 Renewal Summit lililofanyika katika Kanisa la Community lililopo Gaba, jijini Kampala, nchini Uganda, Jumanne wiki hii, Mtume Mitala, (pichani) alieleza kuwa suala la mabadiliko na namna ya kuyafikia, haihitaji tu kubadilika kimatendo, bali pia

kubadilika namna ya kufikiri.

Katika hili, Mitala alinukuu maandiko kutoka kitabu cha Hesabu 14:24: “Lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.”

“Kanisa lazima lijifunze kufikiri tofauti, lakini huwezi kufikiri tofauti mpaka uwe umebeba roho tofauti-roho nyingine,” alisema na kuongeza,” Fanya kitu

k i t a k a c h o d u m u . Angalia ng’ambo, acha kuogopa, angalia mbele….watu wanaobadilisha mambo hufikiri tofauti.”

Aliwapa changamoto wanaopanda makanisa na Wachungaji k u t o h u b i r i madhabahuni kile ambacho watu

wanataka kukisikia ibadani. “Wanaobadilisha mambo

hawahubiri ujumbe laini laini, wanahubiri ujumbe utakaowapa uhai watu. Unatarajia Mungu atende miujiza na maajabu wakati unachokifanya ni kupiga kelele tu,” alisema.

Mchungaji ahimiza maombi ya kumkumbusha Mungu

Na Rebeca Duwe, Tanga

Licha ya kumpongeza Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo kwa kuonyesha msimamo wa kupinga ndoa za jinsia moja, Daktari mstaafu aliyehudumu katika hospitali ya kanisa hilo, Dk John Naema Mbilu, amemwomba askofu huyo kukaa na maaskofu wote wa KKKT ili kujadili namna ya kuwasaidia Wakristo walioko nchini Ujeruman kimasomo na kihuduma, wasishawishiwe kuingia katika ndoa za namna hiyo.

Daktari huyo bingwa mshauri wa magonjwa ya uzazi na wanawake, ambaye aliwahi kuhudumu katika

hospitali ya KKKT Bumbuli, mkoani Tanga, alikuwa akizungumzia msimamo uliotolewa na Mkuu wa KKKT wa kupinga ushoga, kufuatia Ujeruman, nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa Kilutheri, kuhalalisha ndoa za jinsia moja,hivi karibuni.

Dk Mbilu ambaye alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa anapongeza msimamo huo wa Askofu Mkuu, alisema Kanisa lihakikishe watumishi wake walioko katika nchi hiyo ya Ujeruman wanayasimamia vizuri maamuzi ya Kanisa kama yalivyotolewa na Askofu Dk. Shoo.

Alisema ni vyema Kanisa litoe tamko moja lenye kuonyesha kauli ya pamoja ya kupinga ndoa hizo bila

kuangalia urafiki wa karibu na maslahi ya aina yeyote, ambayo yanaweza kugeuza kusudi la Mungu.

Akizungumzia msimamo wa Mkuu wa KKKT, daktari huyo alisema kuwa ni hatua nzuri na ya ujasiri kwa kuwa inaliokoa kanisa, kwani msimamo wake kama kiongozi kupinga ndoa za jinsia moja unaliamsha KKKT kuwa kinyume na uchafuzi huo.

Ujerumani, ambayo ni nchi chimbuko la dhehebu la Kilutheri, mwezi Juni mwaka huu imehalalisha ndoa za jinsia moja licha ya Kansela wa nchi hiyo, Angel Markel kupiga kura ya hapana. Markel anatoka chama cha Christian Democratic Union.

Askofu Mkuu KKKT aombwa kulihami Kanisa dhidi ya ushoga

Katibu wa Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK) wa Kanisa la TAG, Sehemu ya Kaskazini, Jimbo la Shinyanga, Mwinjilisti Petronia Lazaro akihubiri Neno la Mungu kwenye mkutano wa injili uliofanyika katika kijiji cha Mwamagunguli, Manispaa ya Shinyanga, hivi karibuni. Mkutano huo uliandaliwa na uongozi wa WWK. (Picha na Suzy Butondo.

Mtume Mitala alizungumzia tabia za mtu anayebadilisha mambo kuwa ni mtu au kanisa linalofikiri tofauti, linaloona mbele zaidi kuliko sasa, lenye picha ya huko linakoelekea, kunuia mafanikio bila kujali mazingira yaliyolizunguka, lenye roho nyingine inayohudumu kwa kuangalia matokeo, kwa utukufu wa Mungu.

Mitala alianzisha Timu ya Uinjilisti ya Back to the Bible Truth [BBT] mwaka 1979, na kwa kipindi cha miaka 9 iliyopita amehudumu kama Mwenyekiti wa New Birth Fellowship, inayowakilisha makanisa zaidi ya 20,000 nchini Uganda. Kanisa la Gaba Community linasema chini ya uongozi wake, maelfu ya makanisa yamepandwa.

Chanzo: Uganda Christian News

Page 4: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

4 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo Habari

Uvumilivu humsaidia mtu kupata baraka-MchungajiNa Agnes Mayagila, Arusha

Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembilies of God (TAG) Sayuni, lililoko katika kijiji cha Oldadai, nje kidogo ya jiji la Arusha, Meshack Miock, amesema uvumilivu ni jambo ambalo linaweza kumsaidia mwanadamu kupata baraka za Kimungu pamoja na matunda mengine yatokanayo na kuvumilia.

Alisema hayo alipokuwa akihubiri katika ibada iliyofanyika Jumapili iliyopita

kanisani hapo. Mchungaji huyo ambaye alifundisha somo lisemalo ‘Uvumulivu’, alisema kuwa mwanadamu anapokuwa na uvumilivu katika kila jambo, ni lazima azipate baraka za Mungu kwakuwa Mungu anapendezwa na watu wavumilivu.

Aliwataka Wakristo kuvumilia katika hali zote wanazopitia ili waweze kuvuna matunda ya uvumilivu.

Akinukuu maandiko matakatifu katika kitabu cha Mwanzo 29:16-29, Mchungaji Miock alisema kuwa Yakobo ilimlazimu

kutumika kwa miaka kumi na nne ili ampate Rahel aliyekuwa anampenda, na aliliweza hilo kwa kuwa alikuwa na moyo wa uvumilivu.

Kutokana na mfano huu, Mtumishi huyo wa Mungu aliwataka Wakristo kuvumilia katika hatua zote mbaya wanazopitia kwa kuwa hakuna namna wanaweza kufanikiwa, bila kupitia hatua hizo.

Awali katika ibada hiyo, familia ya Joseph Mayagila, ambao ni waumini

katika kanisa hilo, walipata fursa ya kumshukuru Mungu kufuatia msiba walioupata wa kufiwa na mtoto wao wa kiume, Humphrey Mayagila, hivi karibuni.

Mayagila alisema kuwa, kufiwa kunaumiza moyo lakini Mungu aliwapigania na kuwatia nguvu katika hali zote. Alilishukuru kanisa, ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza katika kipindi hicho kigumu ambacho familia yake ilikipitia.

Na Suzy Butondo, Shinyanga

Mchungaji wa Kanisa la Filadefia Miracle Temple, lililopo Ndembezi, mjini Shinyanga, Laiser Baraka, amesema ni jambo la lazima kwa Wakristo kuwatii na kuwaheshimu viongozi wao wa makanisa kwa kuwa wao wanasimama badala ya Mungu na ni sauti yake hapa duniani. Amerejea maandiko kutoka Luka 10:16.

Akihubiri katika ibada iliyofanyika Jumapili iliyopita kanisani hapo, Mchungaji Baraka aliwasihi Wakristo kuwa na utii kwa viongozi wao wa makanisa kwa sababu wanaoongozwa na Mungu.

Alisema viongozi au wachungaji wana kazi kubwa ya kuwaombea waumini wao, wanakesha kwa ajili ya roho zao na Mungu anawatumia kuwaonya ili wasifanye dhambi au kufanya kitu kibaya cha kumchukiza.

“Mkristo anatakiwa kumtii kiongozi wake kwa sababu anafanya kazi kubwa ya kumuombea ili aendelee kubarikiwa, na kuweza kuishi ndani ya neno la Mungu, kwani asipofanya maombi atadaiwa na Mungu,”alisema Baraka.

Alisema ili kuonyesha heshima na utii ni lazima muumini awe mtii kwa kile anachoagizwa na mchungaji wake au kiongozi wake mkubwa wa kanisa anayemwongoza. Alirejea maandiko kutoka Warumi 13:7, kisha akasema,” ili utimize malengo yaliyowekwa ndani ya kanisa ni vizuri uonyeshe utii na unyenyekevu na kuwasikiliza”. Alirejea Nehemia 2: 11 -18.

Baadhi ya washirika waliokuwa wamehudhuria ibada hiyo; Neema Fedrick na Rebeka Kulwa, walisema kweli siku hizi kwenye makanisa mengi kuna matatizo kwani Wakristo wengi wamekosa utii kwa viongozi wao, na badala yake wamejawa na dharau kwa sababu hawajui kuwa viongozi wanaowaongoza wanatumiwa na Mungu.

Walisema Wakristo wengi wamekuwa wakiagizwa na wachungaji wao, au viongozi wao mbalimbali, lakini wanapuuzia na kutotekeleza maagizo hali ambayo inamchukiza Mungu kwa sababu ya kutomtii mtumishi wake.

“Mimi naona ni kwa sababu ya kujisahau na kuleta mazoea kwa kiongozi, kujisahau kama huyo kiongozi anatumiwa ma Mungu, hivyo ili tusimkosee Mungu na hatimaye atupe kisogo na kuacha kutujibu mahitaji yetu. Ni vizuri tujichunguze, tuwatii viongozi wetu kwa sababu maneno wanayotuambia wanatumiwa na Mungu”, alisema Fedrick.

Wakristo kuwatii viongozi wao ni agizo la Mungu, Mchungaji asema

Na Peter Mkwavila, Dodoma

Wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu nchini wameshauriwa kutotegemea

ajira kutoka serikalini na badala yake watumie elimu wanayoipata vyuoni kujiajiri

na kuajiri wengine, huku wakifanya kazi kwa ubunifu mkubwa ili huduma au bidhaa watakazozalisha ziweze kupenya kwenye soko ambalo lina ushindani mkubwa.

Ushauri huo umetolewa na Mhasibu katika Idara ya Elimu Kanisa la TAG, Thadei Mbuta, kwenye mahafali ya wanafunzi waliohitimu katika vyuo vikuu ambao walikuwa wakifadhiliwa na huduma ya mtoto ya Compassion, yaliyofanyika mjini Dodoma, wiki hii.

Mbuta alisema vijana wengi wanasoma huku mawazo yao wakiyaelekeza katika kupata ajira za kuajiriwa, jambo ambalo alisema kwa sasa ni gumu. Alisema vijana wengi wanalazimika kutembea na vyeti mikononi wakisaka ajira, na inapotokea

wanakosa ajira wanainyoshea vidole serikali.

Alisema ni vyema sasa vijana wakabadili mtazamo huo na kuanza kuwekeza mawazo na mtazamo wao katika kujiajiri wao wenyewe.

“Ni lazima sasa kubadilika na kuitumia elimu mnayoipata kwa kujiajiri

wenyewe na baadaye kuajiri wenzenu badala ya kusubiri ajira toka serikalini,’’

alisema.Aidha aliwataka vijana

wanaobahatika kuajiriwa serikali au kwa watu binafsi, kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.

Alisema vijana wengi hutaka kupata maendeleo kwa muda mfupi, na hivyo wengine

kujiingiza katika mambo ambayo yanapoteza uaminifu wao.

“ Uadilifu ni jambo kubwa kwa sisi vijana, mara tunapoajiriwa lakini

jambo kubwa jingine ni uzalendo katika nchi yetu. Ni lazima muwe wazalendo kwa nchi,’’ alisistiza.

Wahitimu elimu ya juu washauriwa kuhusu ajira

Wanafunzi waliohitimu elimu ya juu katika vyuo mbalimbali mkoani Dodoma, ambao walikuwa wakifadhiliwa na Shirika la kidini la Compassion wakiwa katika picha ya pamoja na watenda kazi wa shirika hilo, baada ya hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika mjini Dodoma, hivi karibuni. (Picha na Peter Mkwavila).

Na Morning Star, Zanzibar

Mahakama ya Zanzibar hivi karibuni (Alhamis Julai 20,mwaka huu) imetoa hukumu kwamba kanisa haliwezi kuendelea na ujenzi wa jengo la kuabudia ambalo kwa miaka minane kanisa hilo limejaribu kupambana kumaliza ujenzi wake, imefahamika.

Waislamu wenye msimamo mkali wamekuwa wakipinga ujenzi wa jengo hilo la Kanisa la Pentecostal Assemblies of God tangu mwaka 2009, ambapo kabla ya uamuzi huo wa mahakama waliwahi kulivunja jengo hilo mara mbili. Wanadai kuwa aliyeuza eneo kwa kanisa hakuwa mmiliki.

Wakristo wanaamini kuwa mahakama katika visiwa hivyo vyenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu kuliko watu wa dini nyingine ilifikia uamuzi wake kwa upendeleo wa misingi ya kidini. Awali, mahakama iliruhusu ujenzi wa jengo hilo la kuabudia kuendelea.

Mchungaji Amos Lukanula wa kanisa la Pentecostal Assemblies of God alisema hivi karibuni kuwa uamuzi huo wa mahakama una maana kubwa kwa mwelekeo wa kanisa hilo visiwani humo, na kwamba kanisa linapanga kukataa rufaa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

“Waumini wetu wamekuwa wakifanya kazi sambamba na mimi na wamechanganyikiwa na wanaonekana kuchoka, lakini mara zote tuna matumaini kuwa Mungu bado ataingilia kati,” mchungaji Lukanula alisema na kuongeza,”Hatutaruhusu Waislamu waweke msikiti kwenye eneo la kanisa.”

Kesi hiyo imekuwa mahakamani kwa kipindi cha miaka minane huku Waislamu wa eneo hilo wakilifanya kanisa hilo lililoko eneo la Chukwani kuingia gharama za kisheria kiasi cha karibu Sh 250,000/= kwa mwezi katika jitihada za kulibakiza mkononi mwake eneo hilo, vyanzo vimesema.

Mchungaji Lukanula alisema kuwa mahakama ilikuwa ikisubiri kanisa lishindwe kuhudhuria mahakamani katika utaratibu lililokuwa limeuweka wa kesi kusikilizwa kila mwezi, ili litoe hukumu kwa kuzingatia makosa ya kifundi.

Kanisa lilinunua eneo hilo mwaka 2004 na kuanza kujenga jengo la muda, lakini Waislamu katika eneo hilo walilivunja. Kanisa baadaye lilitumia miaka mitatu kujenga jengo jingine imara kidogo, ambalo Waislamu hao pia waliliharibu, vyanzo vinasema.

Baada ya jengo la tatu ambalo lilijengwa kwa matofali kukaribia kukamilika mwaka 2009, Waislamu walisimamisha ujenzi huo kwa zuio la

mahakama hadi mgogoro wa kisheria utatuliwe. Kitendo hicho kililazimisha kanisa kuchangisha shilingi milioni 5.7 kwa ajili ya gharama za kesi ikiwemo kumsafirisha wakili kila mwezi kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar, gharama ambayo ni kama shilingi 250,000/= kila safari moja.

“Tulinunua kipande cha ardhi kutoka kwa Haruni Gikaro Wanzo, ambaye alifariki dunia mwaka 2009, na sasa mjane wake ndiye aliyebaki hapo,” Mchungaji Lukanula alisema na kuongeza,” kanisa lilimruhusu

mjane wa Wanzo, Anna Philipo Barihuta, kubaki aishi katika eneo hilo. Sasa naye atapoteza ardhi hiyo, na ana watoto wengi anawatunza. Tunaomba msaada na maombi wakati tukikata rufaa ili haki itendeke.”

Februari 21, 2011, mahakama ya mwanzo ililipa ushindi kanisa, ambalo liliendelea na ujenzi. Lakini baada ya kufariki Amina Binti Saleh, ambaye alimuuzia eneo hilo Wanzo, Waislamu katika eneo hilo

Mahakama Zanzibar yaungana na Waislamu kuzuia ujenzi wa kanisa

Inaendelea Uk. 11

Page 5: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 5MwanzoMakala

Jinsi ya kuepuka udanganyifuna mafundisho ya Uongo

Na Mwandishi Maalum

Imeandikwa juu ya watu wa Beroya kwamba, “Watu hawa … walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” (Matendo 17:11). Tunapaswa kufanya vilevile ili mafundisho mapya ya siku hizi yasitufanye mateka, ili “tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Waefeso 4:14).

Na nikushirikishe kitu fulani chepesi ambacho kilinisaidia mimi kwa kiwango kikubwa kwa miaka mingi. Kama mtu yoyote akifundisha kitu kipya ama tofauti ama hukitambui toka kwenye Biblia, jiulize, ‘Hii imeandikwa wapi kwenye Biblia?’ Kwa mfano, mhubiri mmoja aliwaambia wasikilizaji, ’Kama huna ndoto, huna chochote cha kupigania.’ Haya ni mawazo yaliyo finyu kwa uhakika. Kama ni kweli, ni muhimu kwetu kuelewa hili. Kwa hiyo ni wapi nitayapata kwenye Biblia, zaidi hasa, haya yanapatikana wapi kwenye Agano Jipya? Jibu, haliko popote! Hakuna kitu kama hiki kinachofundishwa na Biblia. Ni ubunifu tu wa msemaji. Basi, ni vema nisiyajali.

Wengine wanafundisha kwamba kama ukiwa na shida katika maisha yako (ya kiroho au nyingine) inawezekana ya kuwa ‘laana’ imeingia kwenye maisha yako! Wanasema kwamba kama mojawapo wa babu yako (hata kama aliishi miaka 500 iliyopita!) alifanya dhambi bila kutubu mbele ya Mungu, ndipo babu huyo hakusamehewa, na dhambi zake zinaipeleka hukumu ya Mungu hata kufikia mpaka maisha yako, na zinampa Shetani haki kukutesa na kuzuia maendeleo ya maisha ya kiroho yako! Wapi Bwana Yesu au Mitume wanafundisha mambo haya? Hawataji hata neno moja juu ya hayo! Ni ubinifu tu wa watu wanaotafsiri Agano la Kale vibaya kabisa. Basi, ni vema nisiyajali.

Wengine wanafundisha juu ya ‘siri ya mafanikio’ au ‘ujasiriamali’. Wapi Yesu au Mitume wanafundisha juu ya ‘siri ya mafanikio’. Hamna! Neno ‘mafanikio’ halipo katika mafundisho ya Yesu wala ya mitume! Urahisi na nguvu ya neno la Mungu ni, “Utafuteni KWANZA ufalme wa Mungu…” Bwana asifiwe kwa neno lake la kirahisi (ni rahisi kuelewa kwa wote!) na lenye nguvu!

Mafundisho yale ni ubunifu wa watu, na maelfu maelfu ulimwenguni wanawapenda na wanawafuata wahubiri wafundishao juu ya ‘Mafanikio’ na ‘Ujasiriamali’ kwa sababu ya hamu yao kupita kiasi ya kupata pesa, yaani, kwa msingi, kwa sababu ya uchoyo wa mioyo yao! Wanayo hamu kufanikiwa katika biashara yao kuliko kufuata neno la Mungu. Vivyo hivyo Paulo anavyofundisha: “Lakini hao watakaokuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.” (1 Tim.6:9,10).

Wengine waliofikiri wao ni matajiri walijidanganya kabisa, sawasawa na maneno ya Yesu: “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye

mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” (Ufunuo 3:17). Kwa hiyo Paulo aliwaandikia washirika wa Korintho: “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.” Kumbe, hata wengine waliookoka na huduma ya Paulo walidanganywa na wale ambao walijitukuza huduma zao!

Udanganyifu ulikuwa matokeo ya namna ifuatayo: “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho NYINGINE msiyoipokea, au Injili NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!” Kwa hiyo, na tusishangae kama siku hizi vilevile inatokea – watu wanaojidai wao ni nabii au mitume wanahubiri Yesu mwigine na injili nyingine! (2 Wakor.11:4,13,20)

W e n g i n e wananukuu mistari kama Luka 6:38 na Malaki 3:10, nao wanaahidi kama nitoe pesa (kwa ajili ya huduma yao!) ndipo Mungu atanirudishia mara mia moja! Wanasema utoaji wangu ni kama mbegu nami nitavuna mengi baadaye! Hiyo ndiyo dhambi kubwa sana! Sababu kutoa pesa siyo kwamba ili nipate pesa zaidi! Hiyo ni biashara! Je, unataka kufanya biashara na Mungu! ‘Kumbe, nilipe shilling elfu moja tu, nitapata baadaye laki moja!’ Huo ni uchoyo, siyo sadaka! Hutoi ili upate! Yesu alisema, “Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume…’. (Mat.6:3).

Ndiyo, Mungu atatubariki, lakini sababu ya kutoa pesa kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa maskini, siyo nitapata pesa zaidi! Sababu ya kutoa ni upendo wangu kwake Bwana na kwao watu wake! Bwana Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu, si kitu kikubwa tutoe sadaka kwa hiari na kwa furaha kwa ajili ya watu wake bila kutafuta faida kwa ajili yangu! Kwamba Mungu atanibariki ni jambo la wema wake na huruma yake – na Yesu alithibitisha ukweli huo – lakini siyo sababu kutoa pesa.

Mamilioni ulimwenguni wanaanguka katika dhambi hiyo, na wanafanya hiyo kwa furaha! “Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha. Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.” (2 Wakor.11:19,20). Kama iliyokuwa siku za Paulo vivyo hivyo ni siku hizi.

Wapo watu leo wanaotumia huduma kujenga majengo makubwa ya makanisa kwa ajili yao. Wanavaa mavazi mazuri yenye thamani kubwa sana kwa sababu wanadhani kimakosa kwamba hiyo inaonyesha baraka za Mungu na hiyo ndiyo

alama ya maisha ya kiroho yenye mafanikio! Na wanajaribu kushawishi na wengine kufikiri hivyo. Na wengi sana wanawafuata bila kuelewa mafudisho ya Biblia!

Kwakweli, tunaweza kuomba kwa ajili ya ndugu zetu kama Yohana alivyofanya, “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.” Tunaona ‘kufanikiwa’ hapa lina maana kama ‘bariki’ lakini muhimu zaidi ni kwamba Yohana hachochei uchoyo katika moyo wa msomaji! Hatoi wala hafundishi mbinu ili tuwe tajiri! Sisemi lazima kubaki katika umaskini. Hapana. Lakini njia ni ‘Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu…’ na siyo kuchochea uchoyo!

Lakini Mungu apewe sifa kwa ajili ya neno lake! Kwa msingi sihitaji kwenda shule ya Biblia au Chuo Kikuu kuelewa neno la Mungu kwa maisha yangu. Kwa kweli inawezekana yapo

mambo yasiyo rahisi kuelewa katika Biblia, LAKINI mambo yale ambayo ni lazima nielewe kwa maisha yangu ya kila siku kama mkristo naweza kusoma na kuelewa kama moyo wangu ni sawa mbele ya Bwana!

“Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.” (Mat.11:25,26)

“…huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…” (Yoh.16:13)

“Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote…” (1 Yoh.2:27)

Mistari hii haimaanishi kwamba tunaweza kujitenga na watu au tusiwasikilize wengine wafundishao neno la Mungu, lakini mistari hii ina maana yake kwa ajili ya faida yetu na kwa ajili ya USALAMA wetu wakati wengine wanapohubiri udanganyifu! Mungu apewe sifa sana kwa wema wake na huruma yake kwetu!

Page 6: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

6 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo

Wiki hii Rais Dk John Pombe Magufuli amemwapisha Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Katika haf la ya kumwapisha naibu mkurugenzi huyo iliyofanyika Ikulu, Rais Magufuli aliendelea kukumbusha kuimarishwa kwa upelelezi pamoja na uandaaji wa mashtaka, ili kuhakikisha watu wanaojihusisha na rushwa hawatumii udhaifu wa mashtaka na ushahidi, kuepuka kufungwa. Rais alisisitiza kuwa anataka kuona watu wengi zaidi wakifungwa kutokana na kujihusisha na rushwa.

Tunamuunga mkono mheshimiwa Rais, kwamba vyombo vyote vya dola vinavyohusika katika vita dhidi ya rushwa lazima vitimize wajibu wake kwa weledi ili kukabiliana na watu wanaojihusisha na rushwa. Athari ya rushwa ni kubwa mno katika maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, wakati tunampongeza mheshimiwa Rais, tutumie fursa hii kulikumbusha kanisa kwamba, katika vita hivi dhidi ya rushwa lenyewe ndilo hasa linapaswa kuwa mstari wa mbele. Tunalikumbusha kanisa kwa kuwa tunafahamu kwamba sheria peke yake bado sio mwarobaini dhidi ya adui tunayekabiliana naye.

Hatusemi kuwa tunabeza matumizi ya sheria, bali tunajaribu kuonyesha ukweli ambao kanisa lenyewe linaufahamu, na hivyo kuliamsha lisiachie wanasiasa vita hivi na badala yake nalo liingie kwa dhati katika mapambano. Ukweli tunaojaribu kuuonyesha hapa ni ule ambao umeifanya nchi kama China, ambayo imeweka sheria ya kuua mtu ambaye anapatikana na hatia ya kushiriki vitendo vya rushwa, lakini leo bado iko katika nafasi ya 79 miongoni mwa nchi 176 kwenye orodha ya kiwango cha rushwa katika nchi iliyotolewa na taasisi inayofuatatilia vitendo vya rushwa ya Transparency Internatioanal.

Katika Agano Jipya Mtume Paulo anaweka wazi kwamba sio Sheria zitakazotuokoa ingawa tutazitumia katika maisha (Warumi 7:21-25).

Paulo aliandika hivi katika hili:“Basi nimeona sheria hii, ya kuwa

kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

Hamasa ya kuchukia ufisadi inapaswa ifanywe zaidi na kanisa. Sisi wakati fulani tumekuwa tukishangazwa kidogo kwa mfano na kauli za viongozi wa kanisa wakitoa wito kwa wanasiasa kukomesha ufisadi! Wanasiasa hawawezi kukomesha ufisadi kwa kuwa siasa zenyewe sasa zimefungamana na matendo ya ufisadi, baadhi ya wanasiasa wanajiingiza kwenye ufisadi ili wawe na nguvu ya fedha, kwa kuwa wanaamini wakiwa na fedha watanunua wapigakura. Wanasiasa wengi wanapinga rushwa majukwaani na mbele ya vyombovya habari, lakini gizani wanashiriki matendo hayo hayo.

Sisi tunaamini Kanisa ndilo tumaini na ndilo lenye wajibu wa kiroho wa kubadili mioyo ya watu katika kumaliza tatizo la rushwa na ufisadi. Tunaamini kwamba Kanisa linaweza kumaliza rushwa na ufisadi iwapo litaungana na kuipeleka Injili kwa mataifa yote, huku likiwaona waumini wake wanaohusishwa na ufisadi na ambao maisha yao ya kila siku yanathibitisha ufisadi wao kuwa ni wenye dhambi, na wao wenyewe watambue hivyo, ili waombewe, badala ya kuwaona kuwa ni wafadhili wa makanisa na kuwatengea viti vya mbele.

Tunasema hivyo kwa kuwa, imani yetu kubwa ni kwamba Injili halisi humbadilisha mtu, kwa kuwa injili hiyo huzungumza ukweli na huweka wazi uovu kabla ya

Kanisa lisiwaachie wanasiasa vita dhidi ya ufisadi

TAHARIRI

Simu: +255 (0) 784 942443 +255 (0) 754 649 941

Idara Matangazo: +255 (0)754 649941Email: [email protected]

Dar es Salaam, Tanzania

Gazeti hili hutolewa na FUNGUKA SASA MEDIA

Tahariri/Katuni/Uchambuzi

Uchambuzi

Na Mwandishi Maalum, Mwanza

Mungu hana upendeleo kati ya watu wake, hata hivyo, Biblia inatuambia kwamba Mungu amewachagua Wayahudi kuwa watu wake kwa sababu wao ndiyo pekee waliomtii Mungu badala ya miungu mingine.

Kumbukumbu 7:6 inasema, “Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” Hii haimanishi kwamba Wayahudi ndio moja kwa moja ‘wameokoka’ na wataenda Mbinguni. Ili kuwa na uhakika wa uzima wa milele mbinguni, inampasa kila mtu amwamini Yesu mwana wa Mungu. Kwa maana ni mpango wa Mungu kuwaokoa Wayahudi katika nyakati za mwisho, hivyo Israeli watamgeukia Masihi wake na kuokolewa. Hivyo basi, wakati huo huo waumini wa Yesu wanakuwa “wamepandikizwa ndani” na wanaweza kula toka Mti wa uzima.

Ni kwa nini Mungu aliwateua Israeli kuwa taifa lake (taifa maalumu)?

•Maagizo yake kwa waadamu kwa ujumla yalipata upinzani toka kwa wanadamu pale penye mnara wa Babeli (Mwanzo 11:1-9), na Mungu akalazimika kuwachanganya lugha na kuwatawanya kuwa mataifa mbalimbali.

•Ahadi ya Mungu ya Mkombozi kuupatanisha ulimwengu uliopotea na Yeye mwenyewe ilimlazimu Mungu afanyike mwanadamu siku moja ili azaliwe katika taifa na watu wa aina ya kipekee.

•Taifa la jinsi hiyo ingebidi liandaliwe, kwa ufunuo wa kiroho

na uzoefu wa kitaifa ili waweze kuwa taifa lile ambalo Mwokozi angekuja.

• Kwa hiyo, Mungu alimchagua mtu mmoja, Abraham ili kuanzisha taifa jipya ambalo kupitia kwao, “mataifa yote ya Ulimwengu watabarikiwa.”

Siyo tu kwamba watu wa Israeli ni watu maalumu waliochaguliwa na Mungu, bali nchi yao pia ni maalumu. Katika Kumbukumbu 11:12, tunasoma, “Nayo ni nchi itunzwayo na BWANA Mungu wako, macho ya BWANA Mungu wako ya juu yako tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.” Mungu amekuwa akishughulikia ukombozi wa Israeli tangu wakati wa Agano la Kale. Mungu alitaka Masihi azaliwe humo na Kanisa lianzishwe humo.

Mungu amekuwa na mpango wake madhubuti kwa ajili ya watu wake na nchi yake Israeli. Katika miaka michache ijayo, idadi kubwa ya Wayahudi watakuwa wanaishi katika nchi ya Israeli, na katika siku za hivi karibuni tumejionea Wayahudi wengi wakirudi kuishi Israeli. Wayahudi zaidi ya milioni moja wamerudi nyumbani, wakiwa wametokea kaskazini (Urusi ya zamani - USSR) na kusini (Ethiopia) kama nabii Isaya alivyotabiri. Hivi sasa Mungu amekuwa akileta mabadiliko makubwa ya kiroho ndani ya watu wake hivi mpango wa Mungu wa milele kwa watu wake, Kanisa na Ulimwengu wote utatimia. Mpango huo utatimia katika nchi au ardhi halisi ya Israeli na Watu wake ambao ni Wayahudi waliorejea toka nchi mbalimbali za ulimwengu. Matokeo ya mwisho yatakua umilele wa amani na baraka kwa wanadamu wote.

Kwanini Waisraeli ni watu waliochaguliwa na Mungu?

Inaendelea Uk. 9

Page 7: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 7MwanzoMakala/Tangazo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Aprili mwaka 2008 jijini Dar es Salaam lilitokea tukio ambalo lilishtua watu wengi. Watoto wawili walidaiwa kudondoshwa na wachawi katika eneo la Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, mchana saa nane siku ya Jumapili wakati ibada ikiendelea kanisani hapo.

Vijana hao ambao walijitambulisha kwa majina ya Ramadhani na Yusuf, baada ya kuhojiwa na kuombewa walieleza kuwa wametokea mkoani Mtwara, na shughuli ambayo wamekuwa wakiifanya katika maisha yao ni kufukua makaburi mapya ya watu waliokufa na kuchukua baadhi ya viungo vya marehemu kwa matumizi ya chakula.

Sina kumbukumbu ni kwa muda gani watoto hao walikaa katika kanisa hilo, lakini ukweli ni kwamba siku chache baadaye Ramadhan ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 12, alikamatwa na walinzi katika

lango la kuingilia katika chuo kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) akiwa na kichwa cha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu.

Kabla ya kukamatwa, Ramadhan alikuwa amefanikiwa kuwapita walinzi kwa kuwadanganya kuwa alikuwa anaenda kumwona shangazi yake lakini baadaye walinzi wale walishtuka baada ya kuona midomo yake imetapakaa damu, na walipokagua kifurushi alichokuwa amekibeba mtoto huyo walikuta kichwa cha mtoto aliyekuwa amesukwa nywele kwa mtindo wa ‘twende kilioni’ huku kikichuruzika damu.

Jambo la kushangaza baada ya kukamatwa, Ramadhani alikichukua kichwa hicho mbele ya walinzi na kuanza kufyonza damu na kujilamba, huku akiwauliza kwa ujasiri wale walinzi walikuwa wanashangaa nini kwani kwao (Ramadhani) ni kitu cha kawaida kula nyama za watu.

Ingawa baadaye Ramadhani alifikishwa mahakamani,

Matukio ya watoto kupotea kichawi, na mbinu za manabii kuwarejesha

RATIBA YA IBADAJumatatu: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Mazoezi ya KwayaJumanne: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Chama cha Wanawake (WWI)Jumatano: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Mafundisho ya Biblia (Bible Study)Alhamis: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Chama cha Vijana (CGM)Ijumaa: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Ibada ya Maombi na MaombeziJumamosi: Saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni Mazoezi ya KwayaJumapili: Saa 3.00 mpaka saa 7.00 mchana Ibada ya asubuhi

lakini zipo dhana nyingi zimekuwa zikiibua mijadala kuhusiana na ushiriki wa watoto katika vitendo vya uchawi, ama watoto kupagawa na mapepo. Katika baadhi ya makanisa ya jijini Dar es Salaam, kwa mfano, kumekuwepo na ongezeko kubwa la watoto kuombewa na ama kuripotiwa kupotea katika matukio yanayohusishwa na uchawi.

Tovuti ya Agenzia Fides imefichua kwamba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), maelfu ya watoto wamekataliwa na familia zao, na kulazimika kuishi mitaani, kwa kuwa wanatuhumiwa kuwa wachawi.

Tovuti hiyo inasema, maelfu ya watoto nchini humo wanatuhumiwa kuwa wachawi, wanaleta mikosi au wamepagawa na mapepo hivyo kujikuta wanajiondoa wenyewe kwenye jamii. Kiasi cha watoto 30,000 wanaishi mitaani Kinshasa, jiji kubwa zaidi nchini DRC.

Watoto hao wanaohusishwa na uchawi hupaswa kufanyiwa utakaso au ibada za kuwaondolea mapepo, hasa katika jamii za Kipentekoste. Taratibu hizi kwa mujibu wa tovuti hiyo zinawafanya wachungaji wasaka fedha kujitajirisha. Hata watoto wanaposemekana kuwa wamefanyiwa maombi na kupokea uponyaji, familia nyingi zinaripotiwa kukataa kuwachukua, na wengi wao wanalazimika kuingia katika maisha ya kuombaomba au kuiba mitaani. Wasichana waliotengwa na kukataliwa na wazazi wao wanajiingiza kwenye ukahaba.

Katika kanisa moja jijini Dar es Salaam, kiongozi wa kanisa hilo ambaye hujulikana kama nabii alikuwa akiwaambia wazazi wa watoto waliokuwa wamepotea kuwa alikuwa na uwezo wa kuwarejesha baada ya muda fulani. Waumini na wazazi hao walikuwa wakipiga makofi kushangilia utukufu wa Bwana.

Hakuna ushahidi kwamba nabii huyo alikuwa akiwatoza fedha wazazi ili aweze kuwarudisha watoto hao, lakini lililo wazi ni kwamba wazazi hao walikuwa wanamtolea Bwana sadaka iliyonona. Maswali ambayo yamekuwa yakiibuka ni pamoja na: ni kwanini kumekuwa na kasi ya watoto kupotea katika mazingira ya kichawi, na inakuwaje nabii huyo anaweka muda maalum wa kupatikana kwa watoto wanaokuwa wamepotea?

Mchungaji Msaidizi wa kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, jijini Dar es Salaam, Noah Lukumay (kulia) akiwa na watumishi wenzake wakiwaombea watoto baada ya kudaiwa kudondoshwa na watu waliodaiwa kuwa ni wachawi katika eneo la kanisa hilo, mwaka 2008. (Picha ya maktaba).

Page 8: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

8 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo Habari katika picha

Mmoja wa Maaskofu akisoma Neno la Mungu kwenye mkutano huo.

Wanakwaya kutoka Kanisa la Baptist Mbeya ambao walihudumu katika mkutano huo.

PICHA 2,3 na 4 ni Maaskofu na Wachungaji wa kanisa hilo wakimsikiliza Askofu Mkuu wa kanisa hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania, Dolnad Manase akifungua Mkutano Mkuu wa 41 wa kanisa hilo kanisa hilo uliofanyika Chuo kikuu cha UDOM, Dodoma hivi karibuni. Picha zote na Peter Mkwavila

MKUTANO MKUU WA 41 WA KANISA LA BAPTIST TANZANIA UDOM, DODOMA

2

3

4

Page 9: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 9MwanzoMakala

Baltimore, Marekani

Mchungaji baba wa watoto wawili ambaye alidai Mungu amemtuma atoke Afrika na kuja Marekani kwa ajili ya kuponya wagonjwa wa kansa iliyotokana na kulogwa, amegongwa na gari na kisha kuuawa kwa kuchomwa kisu na mwanaume mmoja ambaye kabla ya kutekeleza tukio hilo alimshusha mkewe kwenye kanisa la mchungaji huyo lililoko Windsor Mill, Maryland, Jumamosi wiki iliyopita.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na polisi wa jiji la Baltimore inasema kuwa, Mchungaji Raphael Happy-Ikenwilo, 53, wa Kanisa la Rahamis Ministry International Church alichomwa kisu na mtuhumiwa mara kadhaa huku mkewe akiangalia bila msaada.

Lakini gazeti maarufu la mtandaoni la Daily Mail Online la Uingereza limeeleza kuwa mtu aliyemuua mchungaji huyo alifikia uamuzi huo baada ya kubaini mkewe alikuwa amebadilika baada ya kuanza kuhudhuria katika Kanisa la Rahamis Ministry Internatioanl Church.

“Askari wa upelelezi walibaini kuwa mtuhumiwa alimshusha mkewe kwenye eneo la maegesho ya magari la kanisa na kumwona marehemu akishuka kwenye gari lake, huku mkewe akibakia ndani ya gari. Mtuhumiwa aliendesha gari lake na kwenda kumgonga marehemu na baadaye kuligonga gari la marehemu. Mke wa marehemu hakujeruhiwa. Baadaye mtuhumiwa alimchoma kisu mara kadhaa mchungaji huyo kabla ya kuendesha gari lake kutoka kwenye eneo hilo. Baadaye alienda kujisalimisha kwenye mahabusu ya Howard,” taarifa ya polisi ilisema.

Mtuhumiwa, ambaye alijitambulisha kwa jina la Daniel Patrick Degoto, 41, alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi. Baadaye alifunguliwa mashtaka ya kuua kwa kukusudia kufuatia mchungaji huyo aliyekuja Marekani akitokea Afrika mwaka 2012, kufariki dunia akiwa hospitalini. Mke wa Ikenwilo, Jennifer, hakuumizwa katika tukio hilo.

“Lilikuwa tukio baya na la kuogofya,” Frank House, mchungaji mwingine anayeishi jirani na mahali lilipotokea tukio hilo, aliliambia gazeti la Fox Baltimore. “Tunaishi kipindi kisicho cha furaha. Thamani ya maisha haionekani kama

Mchungaji aliyedai kuwa na tiba ya Kansa inayotokana na kulogwa auawa kanisani

ni muhimu. Tunapaswa kuona na kutambua maisha yetu ni muhimu.” Aliongeza.

Polisi waliliambia gazeti la Kikristo la Christian Today Jumatatu iliyopita kuwa hawajaelewa sababu zilizo nyuma ya mauaji hayo kwa kuwa upepelezi bado unaendelea.

Katika kampeni yake iliyojulikana kama “2014 Indiegogo”, Mchungaji Happy-Ikenwilo alieleza kuwa maisha yake na familia yake yalikuwa hatarini kutokana na wachawi ambao hawakutaka afichue shughuli zao za kutengeneza kansa kichawi.

“Huko Afrika tunawafahamu, lakini huku Marekani wana taratibu

zao, wamejipanga zaidi, ni werevu, ni mapepo waovu na hatari, wanafuata ajenda iliyopangiliwa, hukutana kila baada ya kipindi fulani kwenye jimbo la North Carolina na kuwekea mitego watu wasio na hatia kila sehemu katika Marekani. Kwa kuwa wanatekeleza mambo yao katika eneo la kiroho, kansa nyingi hazina sababu za kitaalamu au hazina maelezo,” aliandika katika mabango yake ya kampeni ambayo ilifanikisha kukusanya dola za Marekani 25 (sawa na Shilingi za Kitanzania 58,000 hivi) tofauti na lengo lake la kukusanya dola milioni 6 (sawa na Shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 13.

“Pale ambapo watu hawa wenye matendo ya giza wanapoona kuwa nimegundua shughuli zao, walinionya nisiziweke wazi kwa mtu yeyote na tangia hapo maisha yangu na jamaa zangu yamekuwa ukingoni. Ukiangalia maelekezo, niliambiwa kupigana na huyu shetani, kuandika kitabu ambacho kitaonyesha matokeo ya uchunguzi wangu kuhusu matendo haya maovu, kutoa mwongozo kwa wale walioathirka na kansa, kumulika zaidi matendo hayo ya giza. Nimeamua kukiita kitabu hicho: Kansa Bandia nchini Marekani, Kesi ya Hamlet NC,” alieleza.

Alidai kuwa kabla Mungu hajamtuma Marekani alifundishwa na malaika hadi kiwango cha udaktari katika sayansi ya kiroho.

“Nilikuwa nimeandaliwa kuchukua kiti cha baba yangu katika shughuli za matendo ya gizani (uchawi) ambapo ningekuwa kiongozi wa wachawi kijijini kwetu, lakini nilikataa na kumfuata Mungu nikipinga kumfuata baba yangu. Nilihitimu mambo ya kiroho kama daktari wa sayansi ya kiroho mwaka 2005. Kama mtumishi, nimeshughulika na ‘Kansa Feki’ na magonjwa mengine ya kulogwa kwa miaka 22 iliyopita. Nina uelewa wa kutosha juu ya matendo ya giza na mikakati yake na nimekuja Marekani kufanya uchunguzi kuhusu kansa kwa mamlaka ya muumba mbingu na nchi,” aliandika.

Katika kampeni yake ya hivi karibuni ya kuchangisha dola 20,000 kwa ajili ya huduma yake iliyofanyika Julai, mwaka huu, Ikenwilo alionekana akiwa na mkewe na kuzungumzia misheni ya kuiponya Afrika na dunia.

•Yadaiwa muuaji alikasirika mkewe kuvurugwa kiakili na mchungaji huyo

Mchungaji aliyeuawa

Mchungaji aliyeuawa akiwa na mkewe

Muuaji

hukumu... ya Mungu. Hapa tunazungumzia

suala la haki. Kwa mfano, wakati ishara na miujiza ni mambo yanayotarajiwa na muumini wa kweli, mambo hayo lazima yawe katika mzania wa haki. Kuhubiri kwamba mtu anaweza kupata utajiri hata kama hana kazi sio tu udanganyifu; ni ufisadi. Ni mahubiri ya uongo na ni dhambi. Ni mahubiri yanayotupeleka kwenye kushibikia ufisadi.

Vita dhidi ya ufisadi nchini Tanzania

ni vita dhidi ya roho na mwelekeo wa Taifa. Kama ilivyo kwa kansa, ufisadi unaiua nchi hatua kwa hatua. Ni wakati wetu sote; waliopewa mamlaka ya kidola pamoja na sisi kanisa, kupambana kwa kushiriki moja kwa moja katika vita hivi. Matatizo yetu makubwa ni: kukosa unyofu wa mioyo, anguko la kimaadili na fikra, pamoja na kuchanganyikiwa. Kanisa ndicho chombo au taasisi inayoweka na kusimamia viwango vya unyofu na maadili yetu waumini, ambao ndio tunashiriki rushwa. Bwana Yesu asifiwe!

Inatoka Uk. 6

Kanisani liwasaidie wanasiasa vita dhidhi ya ufisadi

Page 10: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

10 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo Makala

Mavazi yanayofaa kuvaliwa na wanawake makanisani

Na Norah Lema

Wakati huu ambapo suala la mavazi linachukua nafasi katika mijadala mbalimbali inayohusisha mwelekeo wa kanisa katika siku za leo, wanawake wengi wanachanganyikiwa juu ya aina ya mavazi yanayowafaa wanapoenda kanisani. Kiukweli, mwanamke Mkristo sio tu anapaswa kuvaa nguo za heshima

wakati anapokwenda kanisani, bali wakati wote anatakiwa kuvaa

nguo zinazosetiri mwili.Hata hivyo, umakini

mkubwa zaidi unatakiwa kuchukuliwa wakati

u n a p o c h a g u a nguo za

k u v a a

kwa ajili ya

kwenda kanisani. Mara zote ni muhimu unapoenda kanisani kuvaa nguo simple lakini zaidi ni muhimu kuvaa nguo ambazo zitakufanya ujisikie vizuri, yaani comfortable muda wote wa ibada. Sio unavaa nguo ibadani halafu unakuwa unahangaikahangaika, hili sio jambo jema na linaharibu ibada yako.

Kwa wanawake na wadada wanaopenda magauni na sketi, nguo hizo zisiwe zinazobana sana na zisiwe fupi sana, na unaweza kuchagua sketi za mshono wa A kwa sababu zinakubali miili (shape) ya aina zote ya wadada au wanawake kwa ujumla. Ivae na blauzi nzuri inayopendeza pamoja na viatu vya pumps au flats.

Kama ni mwanamke unayependa kuvaa suruali (nafahamu kuna maoni tofauti kuhusu mwanamke kuvaa suruali, lakini nafahamu pia suruali za kike hazina tatizo lolote Kibiblia kwa mwanamke kuvaa. Tunaweza kuwa na mjadala katika hili), kwanini usivae suruali yako unayoipenda ya jeans au suruali yako ya kitambaa, ukatupia na kikoti chako au blauzi?

Ukurasa huu utakuwa unakuletea aina mbalimbali za mavazi yafaayo ibadani kwa wote-wanawake na wanaume, na utatumika kujadili eneo hili la mavazi na mitindo. Hii ni mifano ya mavazi yanayofaa kuvaliwa na wanawake ibadani: Kudhamini ukurasa huu wasiliana na 0754 649941 au email: [email protected]

Page 11: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 11Mwanzo

Na Agnes Mayagila, Arusha

Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho ya ushuhuda wa mwimbaji wa nyimbo za injili Daniel Safari ambaye sasa ameingia katika huduma ya uchungaji akichunga kanisa mkoani Arusha. Endelea..

Anasema kuwa kipindi chote hicho cha mateso alikuwa na mchumba wake ambaye alichangia kwa sehemu ya mateso hayo kwa kuwa huyo mchawi hakupenda awe naye kwani alitaka amwoe yeye.

Anasema mapema mwaka 2000 akiwa Sumbawanga Mungu alimpatia mke mzuri ambaye alikuwa ameokoka na kumjua Mungu huku yeye akiwa hajaokoka.

Anasema siku moja mke wake alimshawishi waende kanisani akakubali, ambapo alikutana na Mungu wakati wa mahubiri ya Mchungaji Yohana Mwandunga katika Kanisa la TAG Sumbawanga. Anasema siku hiyo muda wa maombezi ulipowadia aliombewa na kutokwa mapepo lakini akajazwa roho mtakatifu hapo hapo na kuanza kunena kwa lugha. Anasema tangu wakati huo alishikamana na Mungu na kuanza vita rasmi na wachawi.

Safari, anasema kwamba mnamo mwaka 2004 alitembelewa na wazazi wake huko Sumbawanga ambapo aliamua kuwapeleka kwa kaka yake kwakuwa tayari alikuwa anaishi mwenyewe baada ya kuoa. Anasema muda mfupi baadaye waliletewa chakula ambapo moyo wake ghaf la ulikosa amani kwa kile chakula.

“Nilimwambia baba chakula hiki kina hatari. Muda mfupi baada ya kula kile chakula nilianza kuumwa tumbo kiasi cha kuhisi utumbo unanitoka. Nilikimbizwa katika hospitali inayojulikana kama ‘Kwa Mzava’ ambapo nilipimwa lakini ugonjwa haukuonekana. Wakati ule sikujua kama ni yule mchawi wa kwanza alihusika au la,” anasema Safari.

Anasema baada ya hapo alipona na kuendelea na kazi zake za biashara ambapo alisema kwamba aliendelea kukumbwa na misukosuko kama ya kupata ajali mara kwa mara katika kipindi hicho cha kuingia katika maisha ya wokovu, lakini anasema hakuogopa kwa kuwa tayari alikuwa ameishatangaza vita na wachawi kuwa hawatamuua.

Safari anasema mwaka 2006 alikuja jijini Dar es Salaam ili aweze kurekodi albamu yake ya kwanza ya nyimbo za injili ambayo aliita ‘Safari’. Anasema akiwa jijini aliishiwa fedha na chakula alichokibeba akiwa na vijana watatu waliokuja kumsaidia kuingiza sauti. Anasema alikuwa amemaliza kurekodi na alikuwa anaishi katika nyumba ya mtumishi mmoja wa Mungu ambaye alikubaliana naye kuwa afanye mauzo ya cd na tamasha ili apate nauli ya kurudi

Daniel Safari: Nilikataa kufa kwa kulogwa, sasa ni mchungaji-2

Makala

nyumbani. Hata hivyo, anasema muda

mfupi baada ya makubaliano hayo, Mchungaji wake wa Sumbawanga alipiga simu kwa mtumishi huyo akimweleza kuwa asimruhusu kufanya tamasha Dar es Salaam, bali arudi nyumbani haraka kwa madai kuwa ametelekeza familia na wanaishi maisha ya tabu ambapo alimtaka mtumishi huyo amfukuze Safari nyumbani kwake.

Anasema kwamba walifukuzwa hapo na kuanza kuishi maisha ya mtaani wakiombaomba ili wapate chakula na nauli ya kurudi Sumbawanga. “Nilifanikiwa kupata hela kidogo nikawasafirisha wale vijana mimi nikabaki napambana ili nipate chochote cha kuipelekea familia yangu, maana naipenda sana wala sikuwa nimeitelekeza kama yule mchungaji alivyodai,” alisema.

Safari anasema kwamba

aliendelea kuishi maisha ya uchokoraa akiombaomba mitaani na jioni kulala popote, mara nyingine kwa mtu au barabarani, anasema siku moja ya ajabu kuna mtu alikuja Dar es Salaam akitokea Sumbawanga na akawa anamtafuta. Mtu huyo alitaka wakutane Kariakaoo na wakati huo yeye alikuwa anaishi Gongo la Mboto.

Anasema siku hiyo hakuwa hata na nauli ya kumpeleka Kariakoo,hivyo aliamua kutembea kwa mguu mpaka Kariakoo akaonana na mtu huyo ambaye baada ya mazungumzo alimpatia shilingi elfu tano. “Yaani kwangu ulikuwa muujiza kupokea hiyo shilingi elfu tano,” anasema.

Siku mbili baadaye anasema alisikia mkutano wa injili ukitangazwa kufanyika katika kanisa la EAGT Riverside (wakati huo sasa lilishabadili jina) kwa Mchungaji Efraimu Mwansasu ambapo alienda na kuomba kuhudumu kwa njia

ya uimbaji. Anasema baada ya kuhudumu mchungaji Mwansasu alimwambia ameipenda huduma yake na kumwomba wafanye kazi pamoja.

Anasema kwa mara ya kwanza akiwa kanisani hapo kwa mbali alianza kujiona ni mtu miongoni mwa watu,lakini muda mfupi baadaye yule mchungaji wake wa Sumbawanga alimfuatilia na kutaka afukuzwe, lakini hakufukuzwa kwa kuwa alikuwa ameshamueleza mchungaji Mwansasu juu ya maisha yake.

Baada ya hapo anasema alitangaza nia ya kutorudi Sumbawanga na kuamua kukaa Dar es Salaam mpaka amwone Mungu. Mnamo mwaka 2006 mwishoni aliihamisha familia kutoka Sumbawanga na kuileta Dar es Salaam japokuwa maisha yake yalikuwa hayajawa mazuri na watu walikuwa ‘wakimchora’ kwa maisha aliyokuwa. Anasema aliendelea kumtumaini Mungu kuwa siku moja atambariki.

Safari anasema kuwa kwa kipindi chote hicho hakuacha kumtumaini Mungu ambapo anasema mwaka 2008 alianza kuona maisha yakimnyookea alipokuwa katika kanisa la TAG Ubungo ambapo alidumu hapo kwa miaka mitatu baadaye akawa amehamia katika kanisa la TAG Tandika Maghorofani kwa mchungaji Samson Kameta ambapo alihudumu kama mwinjilisti na kiongozi wa kikundi cha Kusifu na Kuabudu

Anasema kwamba anamshukuru Mungu kwakuwa amekuwa mwaminifu sana kwake ambapo anasema pamoja na mapito yake kuwa na changamoto nyingi, lakini hakuwahi kujuta. Alitoa wito kwa wanadamu kutambua kuwa kuwa kila jambo linalotokea katika maisha ya mtu lina kusudi. Aliwataka wa wavumilivu na kumngoja Bwana kwa kuwa wakati unapofika hakuna anayeweza kupinga.

Kama unahitaji sehemu ya kwanza ya ushuhuda huu wasiliana nasi kwa simu namba 0754 649941 au barua pepe [email protected] ili tukutumie nakala ya gazeti toleo lililopita.

na binti wa Saleh, Jilubai Binti Saleh, wakafungua kesi nyingine ya rufaa kuzuia ujenzi wa kanisa mwaka 2011. Waislamu hao walidai kuwa kijana wa Saleh, Sadik, hakuwa mtoto wa kuzaliwa wa marehemu mumewe, Abdul Shakar, hivyo hakuwa na haki ya kumiliki ardhi iliyouzwa kwa

Wakristo. Walishikilia msimamo kuwa binti wa Saleh, Jilubai Binti Saleh, ndiye alikuwa mrithi halali.

Katika jitihada za kuonyesha kuwa marehemu mume wa Barihuta, Wanzo, alikuwa na haki ya kuuza ardhi hiyo kwa kanisa, mjane huyo masikini pamoja na familia yake wameingia gharama kubwa za kesi hiyo. Barihuta ni muumini wa kanisa

hilo.Waislamu walidai mahakamani

kuwa Barihuta alivamia ardhi ya Saleh mwaka 2004 na kung’oa minazi 20, kisha akajenga nyumba kinyume cha sheria, na mwaka 2007, Mchungaji Lukanula akajenga kanisa katika eneo la makazi kinyume cha sheria na kuharibu miti yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Inatoka Uk. 4

Mahakama Zanzibar yaungana na Waislamu kuzuia ujenzi...

Page 12: Mwanzo Gazeti Tando la Kikristo la kila wiki Mwanzo ......wa Zimbabwe, Uebert Angel ambaye alikuwa ahubiri kwenye kongamano la ‘kiroho’ jijini Lusaka, ambalo watu walitakiwa kuingia

12 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017 Mwanzo

Na Agness Mayagila, Arusha

Mwimbaji wa nyimbo za injili wa hapa nchini, Goodluck Gozbert, amewataka Wakristo na wadau wa muziki wa injili kuacha kile ambacho amesema ni tabia ya kuwasema vibaya waimbaji wa nyimbo za injili, na badala yake wawaombee ili kuwaokoa wasipate madhara yanayotokana na maneno mabaya.

Alitoa wito huo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Ujumbe na Muziki’ cha redio ya Kikristo ya Safina ya Arusha, kilichorushwa wiki hii. Aliwataka Wakristo na Watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kuwatamkia baraka watumishi wa Mungu, ikiwemo waimbaji wa nyimbo za injili.

Goodluck alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu kuwasema vibaya waimbaji wa nyimbo za injili kutokana na tabia zinazoonekana kwa baadhi ya waimbaji, alisema badala ya kuwasema vibaya watumie muda huo kuwaombea.

“Waimbaji tunasemwa sana, ila niwaombe wapendwa wetu, Wakristo wenzetu pamoja na wadau wa huduma yetu, badala ya kutusema watuombee maana watatuokoa na madhara ya maneno mabaya,”alisema Goodluck.

Alisema kuwa duniani kuna matatizo na uovu mwingi, na waimbaji nao ni wanadamu kama wengine hivyo wanajaribiwa kama wanadamu wengine. Alisema magumu ambayo watu au watumishi wengine wanayapitia wao waimbaji

nao wanayapitia.Akizungumzia huduma yake,

Goodluck alisema kuwa alianza huduma ya uimbaji mwaka 2008 kama mwimbaji binafsi baada ya kumwimbia Mungu kupitia kwaya. Anasema huo huo alifanikiwa kutoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Nimelipiwa deni’ , na mwaka 2012 alitoa albamu ya ‘Nimeuona’, kabla ya mwaka 2015 kutoa albamu ya ‘Ipo Siku’ ambayo mwenyewe anakiri kuwa ndio imemtambulisha.

Alisema kwamba uimbaji kwake ni huduma kamili kama ilivyo huduma nyingine katika kazi ya Mungu, hivyo matarajio yake makubwa ni kuona vijana wengi wanaokoka kupitia huduma yake, na wengine wakijiunga katika huduma ya uimbaji.

Akizungumzia mafanikio katika huduma alisema kwamba amepata mafanikio makubwa hasa kuona kile Mungu alichokiweka ndani yake kinawafikia wengi. Aliongeza kusema kuwa maisha aliyokuwa akiyaishi zamani sio yale anayoishi sasa kwani Mungu amembadilisha kimwili na kiroho.

Aliongeza kuwa maisha yake ndani ya huduma ya uimbaji yamemfanya kuwa karibu zaidi na Mungu, kumfahamu zaidi Mungu kwani anadumu katika neno ili Mungu aseme naye juu ya kile anachopaswa kuimba ili kiiguse jamii.

Goodluck alisema kwamba kiwango chake cha utumishi na kumjua Mungu kimeongezeka akijilinganisha na alipoanza kumtumikia Mungu, hivyo anaendelea kunyenyekea mbele

zake yeye aliyemtuma ili viwango vyake vya utumishi vizidi kuimarika.

Alibainisha kuwa waimbaji wanapitia mapito magumu hivyo kuwataka wajipe moyo na kuzidi sana kumwomba Mungu ili awatie nguvu waweze kuvuka salama. Aliwatia moyo kuwa mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana yupo kwa ajili ya kuwaokoa hivyo wasonge mbele.

Akinukuu maandiko matakatifu katika Mithali 19:21, alisema kwamba wanadamu wanasema mengi lakini aliwataka waimbaji kutokatishwa tamaa na watu bali waangalie kusudi la Mungu katika huduma na maisha yao kwa ujumla.

Mwanzo

Goodluck Gozbert: Mkituombea mtatuokoa

Mavazi yanayofaa

kuvaliwa na wanawake

makanisaniUK. 10Toleo Na. 002 Jumapili Agosti 27 - Septemba 3, 2017