mwongozo kwa lugha rahisi wa sera ya maendeleo ya · pdf fileya shughuli za uchumi wa...

28
Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006 Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Upload: dinhtu

Post on 31-Jan-2018

346 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera yaMaendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama

vya Ushirika Tanzania BaraUmetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na

Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIALINGEPENDA KUPATA MAONI YAKO KUHUSU KIJITABU HIKI. TAFADHALI ANDIKA KWA:

Katibu Mtendaji,Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,

Ghorofa ya 9, Jengo la UshirikaMtaa wa Lumumba

S.L.P. 2567Dar es Salaam

Simu: 255 (0) 22 218 4081–5Nukushi: 255 (0) 22 2184081

Barua pepe: [email protected]: www.ushirika.coop

TAARIFA ZAIDI

Kwa taarifa zaidi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika kuna nyaraka kuu tatu za kusoma:

• Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003• Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004• Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002

Inawezekana kupata nyaraka hizi kutoka kwa:Ofisa Ushirika wa Wilaya wako;

- Mrajis Msaidizi wa Mkoa wako;- Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (anwani ya hapo juu);

au

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika,Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,

S.L.P. 201, Dodoma.

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIALINGEPENDA KUPATA MAONI YAKO KUHUSU KIJITABU HIKI. TAFADHALI ANDIKA KWA:

Katibu Mtendaji,Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,

Ghorofa ya 9, Jengo la UshirikaMtaa wa Lumumba

S.L.P. 2567Dar es Salaam

Simu: 255 (0) 22 218 4081–5Nukushi: 255 (0) 22 2184081

Barua pepe: [email protected]: www.ushirika.coop

TAARIFA ZAIDI

Kwa taarifa zaidi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika kuna nyaraka kuu tatu za kusoma:

• Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003• Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004• Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002

Inawezekana kupata nyaraka hizi kutoka kwa:Ofisa Ushirika wa Wilaya wako;

- Mrajis Msaidizi wa Mkoa wako;- Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (anwani ya hapo juu);

au

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika,Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,

S.L.P. 201, Dodoma. Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya

Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyamavya Ushirika Tanzania Bara

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera yaMaendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama

vya Ushirika Tanzania Bara

Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera yaMaendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama

vya Ushirika Tanzania Bara

Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA i

YALIYOMO

Dibaji ………………………………………………………………...…….…..…... ii

Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002………………………………....….…..... 1

Ushirika ni nini?……………………………………………………....…................ 1 Kwa nini tunahitaji sera ya ushirika?…………………….…..……........................ 1 Serikali imedhamiria kukuza aina gani ya ushirika?………....................................2 Ushirika na Maendeleo…………………………………….………....................... 3 Muundo wa ushirika…………………………………….…………........................ 3 Nani watakaoongoza vyama vya Ushirika ?…………….………………............... 4 Elimu na Mafunzo ya Ushirika………………………….…………….................... 5 Asasi za kiushirika za Fedha…………………………….…………....................... 6 Wajibu wa Serikali………………………………….………………........................ 7

Sheria ya Vyama vya Ushirika 2003 na Kanuni za Vyamavya Ushirika 2004….................................................................................... 8

Ni aina gani ya vyama vitakavyosajiliwa?……………………………….................8

Chama cha msingi kitaanzishwaje?…….........................………………….......... 9 Vyama vya Ushirika vya Msingi...………......................................………............. 10 Haki na Wajibu wa Mwanachama..........……………............................…............ 14 Dhima za Wanachama……………………………...............……………….......... 15 Usimamiaji wa Vyama vya Ushirika………………….............…………................ 16 Kazi za Vyama Vilivyosajiliwa……………………….....................………............. 18 Shirikisho la Vyama vya UshirikaTanzania……..................................................... 18

Taarifa zaidi na anwani muhimu...........................………………………...... 20

ii USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

DIBAJI

Vyama vya Ushirika vimekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya Tanzania kwa miaka 75. Ni kweli kwamba vimepata mafanikio mengi na matatizo, katika kipindi chote hicho hakuna taasisi nyingine yoyote zaidi ya Ushirika iliyowaunganisha pamoja watu wengi katika azma na lengo linalofanana. .

Baada ya Azimio la Arusha, vyama vya ushirika vilipewa kipaumbele katika kujenga moyo wa kujitegemea. Hata hivyo, kufuatia kuanzishwa kwa mfumo wa soko huru, vyama vya ushirika vimejitahidi kushindana na sekta binafsi na vingi havikuweza kuwapa wanachama wake huduma wanazozihitaji. Serikali imelishughulikia tatizo hili kwa kutunga Sera ya Maendeleo ya Ushirika (2002) ili kuvisaidia vyama vya ushirika kurudisha tena umuhimu wake katika maisha ya watu kiuchumi na kijamii. Sera inaeleza jinsi serikali inavyopanga kuwezesha maendeleo ya eneo maalum la uchumi kama vile kilimo, elimu au ushirika. Wakati ambapo sera zinatueleza mipango ya serikali ilivyo, sheria zinahitajika kuwezesha mipango hiyo kutekelezeka. Sheria zinaeleza jinsi ambavyo vyama kama vile vya ushirika vinavyopaswa kutenda katika njia ya kidemokrasia na ya kibiashara.

Sheria:• Zinataja haki na wajibu wa taasisi na watu binafsi. • Zinaeleza mfumo wa utekelezaji wa maagizo.• Zinaongoza mahakama katika kutekelezaji wake.

Kwa hiyo, sheria zinawapa wadau haki na majukumu. Sera zinatoa tu mwongozo wa jinsi gani wadau wanavyoweza kuhusishwa.

Kijitabu hiki kinaeleza hoja kuu za Sera ya Maendeleo ya Ushirika1 na Sheria2 na Kanuni3

ambazo zimetungwa ili kuifanya sera hiyo itumike. Kimebuniwa kuzisaidia jumuiya kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya ushirika wao wenyewe. Aidha, kitawezesha jamii kuzungumza na wawakilishi wao waliowachagua kuhusu jinsi ambavyo serikali inapaswa kuzifanya sheria katika siku zijazo zitakazowasaidia kuwa na ushirika unaofanya kazi vizuri kwa wale wanaoamua kuwa wanachama.

Wadau ni kina nani?

Ni wale wote wenye nafasi katika sera, ikiwa ni pamoja na wale ambao:• wanaathiriwa na sera• wanatekeleza sera• wanatoa fedha ili kusaidia sera

1Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya 2002

http://www.tzonline.org/pdf/cooperativedevelopmentpolicy.pdf 2Sheria ya Vyama vya Ushirika 2003

http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/20-2003.pdf3Kanuni za Chama cha Ushirika 2004

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 1

SERA YA MAENDELEO YA USHIRIKA

Ushirika ni nini?Ushirika ni muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia mwenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano. Wanachama wa ushirika wanaamini katika uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine.

Kwa nini tunahitaji sera ya ushirika?Serikali na wadau wameamua kuunda sera na sheria mpya kwa ajili ya maendeleo ya ushirika kwa sababu:

• Vyama vingi vya ushirika havijafanikiwa katika uchumi wa soko huru. Matokeo yake vimeshindwa kutoa huduma za pembejeo, mikopo na masoko ya mazao kwa wanachama.

• Serikali inauona ushirika kuwa ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo. Watu wanaofanya kazi pamoja wanaweza kutatua matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa na mtu mmoja mmoja.

• Sera na Sheria za awali hazikushughulikia ipasavyo baadhi ya masuala ambayo ni muhimu kwa ushirika unaofanya kazi katika soko huru kama vile nafasi ya mwanawake katika Ushirika, kutunza mazingira na wajibu walionao wadau mbalimbali katika maendeleo ya ushirika.

Wachuuzi binafsi hawajaziba pengo

lililoachwa na kuanguka kwa ushirika. Kwa hiyo,

watu wanapaswa kuungana ili kutoa huduma kwa ajili

ya jumuiya zao.

2 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Serikali imedhamiria kukuza aina gani ya ushirika?Serikali inataka ushirika nchini Tanzania ufanye kazi kwa mujibu wa maadili yanayotumika katika nchi nyingi. Maadili hayo yanaitwa Kanuni za Kimataifa za Vyama vya Ushirika:

Kanuni Maana

Uanachama wa Hiari na ulio wazi

Ushirika uko wazi kwa watu wote walio tayari kukubali majukumu ya uanachama bila ya aina yoyote ya ubaguzi.

Wanachama na Udhibiti wa kidemokrasia

Wanachama wote wana haki sawa ya kupiga kura (mwanachama mmoja, kura moja).

Ushiriki wa wanachama katika shughuli za kiuchumi

Wanachama wanachangia kwa usawa na kwa kidemokrasia wanadhibiti mtaji wa ushirika wao. Wanachama wanaweza kugawa ziada kwa moja au yote ya madhumuni yafuatayo: kuwekeza katika ushirika wao au kuwanufaisha wanachama kwa uwiano wa hisa zao katika ushirika.

Uhuru na kujitegemea

Vyama vya Ushirika ni vyombo huru na vinavyojitegemea chini ya uongozi na usimamizi wa wanachama. Endapo ushirika utafanya makubaliano na asasi nyingine, ikiwa ni pamoja na serikali, au kutafuta fedha nje ya ushirika, unafanya hivyo endapo tu wanachama wote wameamua kidemokrasia kuwa hivyo ndivyo wanavyotaka. Pia makubaliano yoyote lazima yahakikishe kuwa ushirika unabakia kuwa huru.

Elimu, mafunzo na taarifa

Ushirika unatoa elimu na mafunzo kwa wanachama wake na wafanyakazi ili waweze kusaidia maendeleo ya ushirika wao.naujulisha umma mzima kuhusu faida za ushirika.

Sheria na sheria ndogo za vyama vyote vya ushirika zifuate Kanuni za Kimataifa.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 3

Ushirika miongoni mwa Vyama vya Ushirika

Ushirika unaimarisha vyama vyote vya ushirika kwa kushirikiana kupitia mitandao ya wananchi, taifa, kanda na ya kimataifa.

Ushirika kuijali Jamii

Ushirika unafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, jamii na utamaduni wa wanachama wake na jumuiya nzima. Pia unajali kutunza mazingira na vizazi vijavyo.

Ushirika na MaendeleoKwa miaka michache serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Mchakato huu unatambua umuhimu wa asasi zinazowaunganisha pamoja watu maskini, kama ushirika. Kama sehemu ya programu ya kupunguza umaskini, serikali inataka kuwahamasisha watu kuunda ushirika ili kuboresha matarajio yao ya kiuchumi.

Serikali ingependa kuona ushirika unapanuka katika sekta mbalimbali, kama vile fedha, nyumba, viwanda, madini, mifugo, uvuvi, ufugaji nyuki na usafirishaji. Ili watu wengi iwezekanavyo waweze kuhusishwa katika chama cha ushirika, serikali:

• Itahakikisha kwamba wanawake wanahamasishwa kuwa wanachama kamili wa ushirika.

• Itasaidia vikundi vyenye biashara ndogo ndogo vinavyohusisha vijana, wanawake, wahitimu wa vyuo wasio na ajira na walemavu kujiunga kwenye ushirika.

Muundo wa UshirikaKatika kipindi kilichopita zimekuwepo na ngazi nyingi za ushirika nchini ikiwa ni pamoja na vyama vya msingi, vyama vikuu, vyama vikuu kilele na Shirikisho la Vyama vya Ushirika. Kwa nyakati tofauti vyama vikuu vimepoteza mawasiliano na vyama vyao vya msingi na vikaanza biashara ambazo hazikuhusiani na zile zilizokuwa zikifanywa na vyama vya msingi. Mpango uliopo sasa ni kukifanya chama cha msingi kuwa ngazi muhimu na ya msingi ya ushirika na kuhakikisha kuwa vyote vinajitegemea na vinadumu. Ushirika wa ngazi ya juu unawajibika kutoa ushauri na kujenga uwezo wa vyama vya msingi kibiashara.

Kuwahimiza watu kuunda aina tofauti za vyama vya ushirika, Serikali inaweza kutoa ushauri kwa watu ni namna gani kila chama cha

ushirika kinavyoweza kuleta manufaa.

4 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Aidha ushirika wa juu una jukumu la kuwa mwakilishi makini wa vyama vya msingi ngazi ya Taifa na Kimataifa katika kutetea haki, kutafuta masoko n.t.

Kwa sasa Serikali ina mipango ifuatayo4:• Kuhamasisha sekta mbalimbali za kiuchumi

kuunda ushirika.• Kusaidia vikundi vya biashara ndogo ndogo

kusajiliwa katika ushirika.• Kuhamasisha uanzishaji wa asasi za kifedha

katika vyama vya Ushirika vya msingi.• Kuwezesha vyama vya ushirika kujijengea uwezo wake wa fedha.• Kusaidia vyama vya ushirika kupata mikopo kutoka benki.• Kutoa udhamini kwa baadhi ya mikopo kutoka

kwenye mabenki kwenda vyama vya ushirika.• Kuhamasisha vyama vya msingi kuwa na

biashara ya pamoja na vyama vingine vya msingi ili kuongeza ufanisi.

Pia serikali kuendelea kutoa ushauri kuhusu baadhi ya vyama vya ushirika kuungana kila itakapoona inafaa.

Nani watakaoongoza vyama vya Ushirika?Siku zilizopita vyama vingi vya msingi vilikuwa vikiongozwa vibaya kwa sababu:

• Baadhi ya viongozi walikuwa wakishika madaraka kwa muda mrefu sana.• Hapakuwa na sheria za kuwabana viongozi kuwa watendaji wazuri na kufanya

kazi kwa maslahi ya wanachama.• Wanasiasa wameingilia mara kwa mara katika masuala ya vyama vya Ushirika.• Kumbukumbu sahihi na taarifa za utendaji havikuwekwa na hesabu

zilizokaguliwa hazikuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka.• Viongozi wamekuwa wakitoa maamuzi bila ya kuwahusisha wanachama katika

Mkutano Mkuu wa Mwaka.

Ili kuboresha hali hii serikali inataka kuhakikisha kuwa viongozi wa vyama vya Ushirika:

• Wanazo sifa za kufanya kazi za uongozi• Watiifu kwa wanachama wa chama cha Ushirika• Wanawajibika kwa wanachama wao kupitia uwasilishaji kwa bodi na mikutano

mikuu ya mwaka wa taarifa za ukaguzi wa hesabu, makisio, mipango ya shughuli na taarifa za utendaji

Ushirika unapaswa kuendeshwa kama biashara endapo utataka kudumu

katika soko huria

Serikali inatambua kuwaushawishi mkubwa wa

kisiasa katika kuendesha ushirika hapo zamani

mara nyingi ulisababisha uendeshaji mbaya wa

ushirika

4Kupitia mabadiliko ya ushirika na mpango wa kufanya ushirika uwe wa kisasa (CRMP), mpango wa miaka

kumi, ambao ulianza Januari 2005.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 5

• Wanachaguliwa kidemokrasia na wanachama• Hawana maslahi ya nje ambayo yatakiathiri

chama cha Ushirika.

Ili kufanya hivyo, sera iliyopo inaainisha kwamba serikali ina mpango wa:

• Kuunda kamati imara za usimamizi katika vyama vya Ushirika.• Kuweka ukomo wa muda wa uongozi katika Vyama vya Ushirika• Kuanzisha kanuni za maadili ili kuwafanya viongozi wawajibike kwa

wanachama na kwa kamati.

Pia serikali itahakikisha kuwa wafanyakazi ambao wanaajiriwa wanafanyakazi kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji kwa wanachama. Kwa sababu hii, serikali itahamasisha ushirika kuwavutia wafanyakazi wenye sifa kwa kuweka mazingira mazuri ya kazi.

Elimu na Mafunzo ya UshirikaSerikali inaamini kuwa ni muhimu kuwaelimisha watu katika maadili ya ushirika. Wakati soko huru lilipoanzishwa, mafunzo yasiyotosheleza yalitolewa kwa ushirika kuhusu namna ya kujiendesha katika mazingira mapya.

Matokeo yake biashara ya Ushirika imeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 Ushirika unashughulikia kiasi kidogo cha biashara ya wananchi ikilinganisha na hapo awali.

Wafanyakazi lazima wawe na ujuzi unaofaa ili kuhakikisha ushirika una faida kwa wanachama.

6 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Sera inasisitiza kusisitiza umuhimu wa ukuzaji wa elimu ya ushirika, ambayo italenga:• Kuwa na viongozi wa ushirika walioelimika na wanaowajibika ambao wanaweza

kudumisha maadili ya ushirika na kuendesha shughuli za biashara kwa ufanisi.• Kuboresha usimamizi, biashara na ujuzi wa ujasiriamali wa wafanyakazi wa

ushirika na wajumbe wa kamati.• Kuhakikisha kuwa wanaushirika wanaarifiwa na kufahamu hali halisi

ya shughuli za uchumi wa ushirika, kazi na majukumu yao na manufaa yanayotokana na uanachama wao katika ushirika.

• Kuuarifu umma kwa ujumla kuhusu hali halisi ya ushirika.• Kuingizwa kwa Elimu ya Ushirika kwenye Mitaala na mfumo wa Elimu.• Kuhakikisha kuwa ngazi zote za uongozi wa kiutawala wana hamasishwa

kuhusu maadili na umuhimu wa ushirika.

Asasi za Fedha za UshirikaBaada ya kuanzishwa kwa soko huru, Serikali ilipunguza kusaidia Vyama vya Ushirika moja kwa moja. Kwa kuwa ushirika haukuweza tena kupata fedha kutoka benki, ina maana ilikuwa vigumu kutoa huduma zinazofaa kwa wanachama. Wachuuzi binafsi waliweza kuchukua nafasi na kujinufaisha na hali hiyo, lakini matokeo yake yamekuwa ni huduma duni kwa wazalishaji wadogo.

Serikali inazichukulia asasi za fedha za ushirika kama mbadala muhimu kwa mfumo wa uendeshaji benki kibiashara. Sababu ni kwamba ushirika unaweza kuhamasisha kuweka akiba na uangalifu katika kutumia fedha. Pia mikopo inaweza kutolewa kwa

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 7

wanachama kwa masharti nafuu kuliko ile itolewayo na benki za biashara. Asasi za kiushirika za fedha ni muhimu kwa sababu benki za biashara zinavichukulia vyama vya Ushirika kuwa havikopesheki.

Hivyo, Serikali inataka kuhamasisha uundaji wa asasi za fedha za ushirika kama vile:

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS)Serikali inatambua kuwa kasi ya ukuaji wa SACCOS imekuwa ndogo, hususan katika maeneo ya vijijini. SACCOS nyingi zimeanzishwa mijini na maeneo ya kazi. Matokeo yake wanachama wa vyama vya msingi vijijini wameshindwa kupata mikopo.

Ili kuboresha hali hiyo, serikali inahamasisha uanzishaji wa SACCOS katika maeneo ya vijijini. Ushauri utatolewa katika ngazi ya chini kuhusu kuanzisha SACCOS na msaada wa kitaalamu pia utapatikana kwa SACCOS zote zilizopo ili ziweze kuboresha huduma zao na kuwa endelevu.

Benki za UshirikaUanzishaji wa benki za ushirika utakuwa ni sehemu muhimu ya uanzishaji wa asasi za fedha za ushirika zilizo imara.

Serikali imeazimia kuhamasisha na kusaidia uanzishaji wa benki za Ushirika ili baadaye kuwa na benki ya Ushirika ya kitaifa iliyo imara.

Jukumu la SerikaliSiku za nyuma serikali ilikuwa na jukumu kubwa katika ushirika. Ilijihusisha kwa kiasi kikubwa katika kutoa pembejeo, fedha na mafunzo.

Kwa siku zijazo Serikali itawajibika katika uandaaji tu wa mazingira mazuri ya ushirika kustawi. Mihimili mikuu ya kukua itakuwa wanachama na menejimenti ya ushirika wenyewe. Lengo ni kuwezesha vyama vya ushirika kujenga uwezo wa kujitegemea kidemokrasia na kujimudu kiuchumi.

Mfumo wa zamani wa Serikali kujihusisha katika

mambo yote ya uhai wa ushirika ulikuwa na

gharama kubwa kwa nchi.

Katika ngazi ya Wilaya Ofisa Ushirika wa Wilaya atamuwakilisha Mrajis.

Mikopo inapaswa kupatikana kwa urahisi

kwa wanachama wa SACCOs katika vipindi muhimu vya mwaka.

8 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA Na. 20 YA 2003 NA KANUNI ZA VYAMA VYA USHIRIKA ZA 2004

Sheria na kanuni hizi zinaelezea jinsi ushirika unavyopaswa kuanzishwa na kuendeshwa nchini Tanzania. Zinakusudia kutekeleza kwa vitendo sera ambayo tumekuwa tunaizungumzia hapo juu..

Sheria ya Vyama vya Ushirika inaeleza kwamba ushirika unapaswa kuanzishwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Kimataifa za vyama vya Ushirika zilizotajwa mwanzoni mwa kijitabu hiki.( Ukurasa wa 2 - 3)

Serikali na Waziri mwenye dhamana ya Ushirika wana wajibu wa kuunda sheria ambazo zinahamasisha uanzishwaji wa ushirika nchini. Aidha Rais kumteua Mrajis wa Vyama Vya Ushirika ambaye ndiye Afisa msimamizi wa utekelezaji wa Sheria na Kanuni zake.

Kazi za Mrajis ni pamoja na:

• Kusajili, kuendeleza, kukagua na kuvishauri vyama vya ushirika.

• Kumshauri Waziri wakati vyama vya ushirika vinapohitaji msaada.

• Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya ushirika mbali mbali katika maeneo yote ya uchumi.

Kadri ushirika utakavyokua na kukomaa ndivyo ambavyo Mrajis wa Vyama Vya Ushirika atakamilisha majukumu yake (ya mafunzo, ushauri n.k.) kwa vyama vyenyewe, na kubakia na majukumu ya lazima ya usajili za usimamizi wa Sheria.

Ni aina gani ya vyama vinavyoweza kusajiliwa?Kwa sababu serikali imepania kuhamasisha uanzishwaji wa ushirika katika sekta zote za uchumi, Mrajis anaweza kusajili ushirika katika maeneo kama vile:

• Kilimo, mifugo, uvuvi au ufugaji nyuki• Uchimbaji madini• Akiba na kukopa,• Biashara ya jumla au rejareja miongoni mwa wanachama• Viwanda• Ushirika wa Nyumba unaojishughulisha na ujenzi, majengo na programu za

nyumba kwa wanachama wao• Ushirika wa ujuzi maalum n.k.

Kwa sasa sera ya Serikali ni kuhamasisha ukuaji wa kujitegemea wa ushirika kwa kuwapa watu taarifa

na ushauri ambao ni rahisi kuufuata na ambao unapatikana kwa urahisi.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 9

Chama cha msingi kitaanzishwaje?

Chama cha msingi kinaweza kuanzishwa na:• Watu 50 au zaidi kama ni chama cha kilimo• Watu 20 au zaidi kama ni ushirika wa kuweka na kukopa• Watu 10 au zaidi kama kinahusisha watu wenye ujuzi maalumu• Watu 10 au zaidi kwa aina nyingine za Vyama vya ushirika

Nani anaweza kuwa mwanachama?• Umri wake haupungui miaka kumi na

nane na mwenye akili timamu• Yuko katika shughuli inayohusu

chama cha msingi• Ana mahitaji yanayofanana na ya

wanachama wengine• Anaweza kulipa ada na kununua hisa• Hata hivyo Kijana mwenye umri

usiopungua miaka 15 anaweza kuwa mwanachama na haki zote za kuwa kiongozi katika chama cha Ushirika cha shule.

Chama cha Ushirika cha Mwanzo ni asasi ya uchumi au kijamii

inayoanzishwa kwa hiari na watu binafsi wenye maslahi sawa na

kufanya kazi pamoja kama chama.

10 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Vyama vya Ushirika vya awali, na jinsi ya kuanzisha Chama cha Ushirika kama huna wanachama wa kutoshaSerikali itavitambua na kuvilea vikundi vya watu wenye muelekeo wa Ushirika hatimaye viwe vyama vya Ushirika kamili.

Ili kuanzisha Ushirika lazima pawe na angalau watu watano. Ili kuweza kutambuliwa, kikundi kinatakiwa kwanza kuandika barua kwa Ofisa Ushirika wa Wilaya kuelezea nia yake na hivyo kuomba kutambuliwa.

Uandikishwaji wa chama utakuwaje?

Wanachama wa Ushirika wa awali wapange kukutana chini ya uenyekiti wa afisa Ushirika wa wilaya ili kuchagua Bodi ya uundaji yenye Mwenyekiti na Katibu. Bodi ya uundaji itabidi ikamilishe majukumu yafuatayo:

• Kuamua ni aina gani ya chama kitakachoundwa

• Kutayarisha sheria ndogo za chama; • Kutathmini kiwango cha shughuli cha

wanachama waanzilishi• Kutabiri chama kitakuwa na

wanachama wangapi wa siku zijazo na viwango vya shughuli ambazo chama kitafanya

Upembuzi yakinifu utajumuisha taarifa kuhusu idadi ya wanachama muhimu

ambao chama kinaweza kuwa nao na viwango vyao vya biashara. Pia utazungumzia uwezo wa uongozi wa chama ili kuhakikisha chama

kinapata faida na kuendeshwa kwa maslahi ya wanachama wote.

Mwombe msaada Ofisa Ushirika wa Wilaya

wakati wa kukamilisha kazi hizo.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 11

• Kuandaa taarifa ya upembuzi yakinifu• Kuandaa orodha ya wanachama waanzilishi na kurekodi mtaji wa hisa zao na

michango• Kuandaa orodha ya wanachama wanaotarajiwa na kurekodi mtaji wa hisa na

michango wanayoweza kutoa• Kuandaa mfumo mzuri wa utunzaji wa hesabu na nyaraka mbalimbali.• Kuteua mwakilishi mfawidhi wa kuwakilisha kikundi katika mambo yote ya

kiraia

12 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Sheria ndogo?

Kila kikundi chenye mwelekeo wa Ushirika na chama cha Ushirika kinapaswa kuwa na masharti ili kuhakikisha kuwa vinaongozwa katika njia ambayo inawanufaisha wanachama wote kwa usawa. Masharti haya yanajulikana kama sheria ndogo. Aina mbalimbali za vyama zinaweza kutunga sheria ndogo ndogo za aina mbalimbali. Kwa mfano, chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kitakuwa na sheria ndogo tofauti na za chama cha ushirika wa kilimo.

Inaweza kuwa muhimu kupata msaada kutoka kwa Afisa Ushirika wa Wilaya au mtu mwingine mwenye sifa husika wakati wa kutengeneza sheria hizo ndogo. Kuna idadi ya sheria ndogo ambazo zinapaswa kutungwa na aina zote za vyama. Sheria hizo ndogondogo zitafafanua:

• Jina la chama na mahali pa kufanyia shughuli zake.• Lengo la chama.• Madhumuni ya kuomba fedha kwa ajili ya chama na jinsi fedha

zitakavyotunzwa, kutumiwa au kuwekezwa.• Kanuni za uanachama ikiwa ni pamoja na masharti ya kuingia,

hisa na ada ya kuingilia.• Kanuni kuhusu malipo, kama yapo, iwapo mwanachama

atafukuzwa au kuacha.• Hisa zitahamishiwa kwa nani endapo mwanachama atafariki.• Kiwango cha madeni ya mwanachama katika kikundi na jinsi

kitakavyoamuliwa.• Jinsi mikutano mikuu itakavyoendeshwa na nini

kitakachoamuliwa katika mikutano hiyo.• Kanuni kuhusu kazi za wajumbe wa Bodi, jinsi

watakavyochaguliwa, watakaa madarakani kwa muda gani na wataondolewaje kama itabidi kufanya hivyo.

• Kanuni kuhusu kazi za wajumbe wa Bodi, jinsi watakavyochaguliwa, watakaa katika nafasi hizo kwa muda gani na wataondolewaje kama itabidi kufanya hivyo.

• Kumwidhinisha ofisa kutia saini nyaraka kwa niaba ya chama.

Vyama vya aina tofauti vitakuwa na masharti mengine tofauti. Kwa mfano, chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo kitahitaji masharti ya ziada kuhusu viwango vya riba, masharti ya mikopo, dhamana ya mikopo na kanuni za kushindwa kulipa deni. Chama cha ushirika wa biashara kitahitaji sera ya kupanga bei kuongezea katika kanuni zilizopo.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 13

Faini: Ni muhimu kutambua kwamba vyama vinaweza kuunda masharti ambayo yanaweza kumtoza faini mwanachama endapo atakiuka kanuni za chama. Faini hizo zitakuwa kama faini za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika na zinaweza kulipwa mahakamani kama ni lazima.

Pindi wanachama wa kikundi chenye muelekeo wanapotaka kuwa chama cha ushirika cha awali watakamilisha taratibu zote za uanzishwaji wa chama, wanapaswa kutuma maombi kwa Mrajis au mwakilishi wake. Wawakilishi wa Mrajis ngazi ya mkoa (Mrajis Msaidizi) na ngazi ya Wilaya (Afisa Ushirika wa Wilaya).

Ni kitu gani kinachohitajika kwa ajili ya Maombi ya usajili?

• Nakala iliyothibitishwa ya azimio lililopitishwa katika mkutano wa kwanza wa kikundi na Afisa Ushirika wa Wilaya

• Nakala nne za masharti za chama zilizopendekezwa

• Nakala nne za taarifa ya upembuzi yakinifu

• Hati nyingine zozote zitakazoombwa na Mrajis• Ada ya Usajili

Kama maombi yatakubaliwa Mrajis atatoa barua ya utambuzi. Barua hiyo inakiruhusu kikundi kufanya shughuli kwa miaka miwili kama chama kilichopo katika majaribio mpaka kitakapotimiza masharti yanayotakiwa ili kuwa chama kamili cha ushirika. Kama chama hakikutimiza masharti baada ya miaka miwili, kwa mfano hakikupata wanachama wa kutosha, basi barua hiyo itabatilishwa.

Endapo Mrajis atakataa kusajili chama, wanachama wana haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo kwa Waziri wa Ushirika na Masoko ndani ya siku 60. Uamuzi wa Waziri ni wa mwisho.

Mrajis au Afisa Ushirika wa Wilaya pia wanaweza

kuomba barua kutoka kwa watu wanaokusudia kujiunga, taarifa zaidi kuhusu kuwepo kwa mtaji au taarifa zaidi kuhusu uwezo wa chama

kinachotarajiwa kusimamia biashara yake vizuri.

14 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Haki na Wajibu wa Wanachama

Wanachama wote wa vyama vya ushirika mara wanapolipa kiingilio, hisa, na malipo mengine wanakuwa na haki zifuatazo:

• Majina na saini zao kuingizwa katika Daftari la Wanachama• Kupiga kura na kupigiwa kura. • Kila mwanachama ana kura moja bila ya kujali idadi ya hisa anazomiliki• Kupewa hati za hisa mara tu wanapolipia hisa zao• Kushiriki katika nafasi za uongozi• Kuitisha mikutano kwa mujibu wa sheria ndogo• Kuteua mrithi-kufuatana na masharti ya chama.• Kupata taarifa kuhusu masuala yote ya chama na kuweza kukagua nyaraka za

chama• Kuarifiwa kuhusu masuala yote ya chama na kuweza kukagua nyaraka za

chama• Kupata kipato kutokana na shughuli za biashara ya chama• Kushiriki katika kuandaa sheria ndogo za chama• Kujitoa katika uanachama• Kufanya uchunguzi katika masuala ya chama• Kushiriki katika kuandaa na kurekebisha masharti ya chama• Kukata rufaa• Kwa vyama vya Akiba na Mikopo,mwanachama ana haki ya kulipa kwa kuzingatia

mwanachama ana Akiba na amana za kutosha

Tahadhari

Ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanachama hata mmoja anayekuwa na udhibiti mkubwa katika chama, ni kinyume cha sheria kwa mwanachama mmoja kumiliki zaidi ya moja ya tano ya hisa za chama. Kwa sababu kama hizo, ni kinyume cha sheria kwa kampuni iliyosajiliwa kuwa mwanachama wa chama cha ushirika mpaka Mrajis aandike barua inayoidhimisha kuwa kampuni hiyo itakuwa na manufaa kwa chama. Pia ni kinyume cha sheria kwa mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili vinavyojihusisha na aina moja ya shughuli (katika eneo moja) kwa kuwa hali hiyo italeta mgongano wa kimaslahi.

Wanachama wana Wajibu ufuatao:

• Kufuata masharti na taratibu za chama.• Kulipia hisa zao, stahili na madeni mengine yoyote wanayodaiwa na chama• Kushiriki katika shughuli za chama• Kuhudhuria mikutano ya chama na kufuata maamuzi yaliyotolewa

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 15

• Kuteua warithi wao• Kulinda na kutetea mali ya chama

Ukomo wa uanachama

Mtu anaweza kukoma kuwa mwanachama wa chama endapo:

• Ataacha kumiliki hisa au kutoa michango iliyowekwa katika masharti ya chama.

• Atahama na kwenda mbali na eneo la chama• Atafukuzwa au kusimamishwa baada ya

kufanya kosa• Kutunza na kulinda sifa na heshima ya chama• Kifo• Kushindwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi za chama kufuatana na

masharti ya chama• Kurukwa akili• Kuacha uanachama kwa hiari.• Atakuwa hashiriki katika shughuli za chama.

Dhima za wanachamaWanachama wanaweza kubeba dhamana ya madeni ya chama katika moja ya njia mbili:Dhima kwa hisa – Hiki ni kiwango cha kawaida cha dhima na kinamaanisha kuwa mwanachama anawajibika kulingana na uwiano wa hisa zake za chama.

Wanachama wote lazima wafahamu kuhusu biashara ya chama.

16 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Dhima kwa dhamana – Kama masharti ya chama yanaruhusu, mwanachama anaweza kukubali kuwajibika kwa kiasi kikubwa kuliko hisa yake. Hii inajulikana kama dhima kwa dhamana.

Usimamizi wa Vyama vya Ushirika

Mikutano MikuuUdhibiti wa jumla wa chama cha ushirika unafanywa na wanachama katika mikutano mikuu. Mikutano Mikuu inapaswa kufanywa angalau mara moja kwa mwaka. Masuala yote ya chama yanaweza kujadiliwa, yakiwemo;

• Uchaguzi, kusimamishwa au kuondolewa kwa Bodi• Kuteua Mkaguzi wa Hesabu• Kuzingatia na kuridhia hesabu zilizokaguliwa• Kuamua kuhusu mgao wa ziada• Kuamua kiasi cha posho itakayotolewa kwa

wa wajumbe wa Bodi na maofisa wasiolipwa mishahara

• Kuzingatia bajeti na mipango ya kazi• Kuzingatia marekebisho ya masharti ya chama• Kuamua kuhusu ununuzi au uuzaji wa mali za

chama

Angalizo

Ili kutoa maamuzi katika mkutano lazima pawepo na angalau nusu ya wanachama, au wanachama 100, wowote walio wachache. Wanachama wote lazima wapewe notisi ya wiki tatu ya tarehe, mahali na muda wa mkutano.

Bodi• Kila chama cha ushirika ni lazima kichague

Bodi ya wajumbe wasiopungua watano na wasiozidi tisa

• Ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanachama au kikundi cha wanachama wanaojaribu kuwa na sauti zaidi katika kuendesha chama, hakuna mjumbe wa Bodi atakayeshika nafasi ya ujumbe kwa zaidi ya miaka tisa mfululizo

• Katika miaka ya kwanza ya chama, theluthi moja ya Wajumbe wa Bodi wanapaswa kubadilishwa kila baada ya miaka mitatu ili kuendana na sheria

Kubadili wajumbe wa Bodi mara kwa mara kunahakikisha kuwa

hakuna mtu au kikundi kinachoweza kuwa na mamlaka zaidi katika

chama.

Kwa kuongeza, Mrajis au mwakilishi wake, Ofisa Ushirika wa Wilaya, anapaswa kwanza

kuwapima Viongozi na watendaji wote kabla

ya kuwaajiri.

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 17

• Hakuna mwanachama atakayechaguliwa kwenye Bodi kama anamiliki, anasimamia au ana ushawishi katika biashara inayofanana na shughuli za chama

• Kila mwaka, kila mjumbe wa Bodi lazima ajaze fomu akitaja mali na biashara alizonazo, anazosimamia na lazima wakabidhi fomu hizo kwa Mrajis.

Bodi inawajibika kuhakikisha kuwepo kwa uongozi mzuri wa chama kwa mujibu wa masharti ya chama. Ili kusaidia katika kazi hiyo Bodi inaweza kuajiri watu wanaofaa kusimamia uendeshaji wa kila siku wa chama. Kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu atakayeajiriwa na ushirika kama hana elimu na ujuzi wa kufanya kazi iliyotangazwa. Kwa mfano, ni kinyume cha sheria kuwaajiri wafanyakazi kwa misingi ya uhusiano wao na mjumbe wa Bodi, rangi yao, kabila au utajiri wao. Pia ni kinyume cha sheria kwa mtu kutoa malipo ili kushawishi uamuzi wa kuajiriwa.

Aidha, kila mfanyakazi wa chama cha msingi anapaswa kudhaminiwa na mdhamini. Mdhamini atawajibika endapo mfanyakazi atahusika na upoteaji au kushindwa kulipa deni.

Mikutano Mikuu MaalumuKama theluthi moja au zaidi ya wanachama wanataka kujadili jambo maalumu wanaweza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum. Ili kufanya hivyo, wanachama husika wanapaswa kuandika barua inayoelezea dhamira yao na ni lazima watume nakala ya barua hiyo kwa Mrajis. Inatakiwa watoe notisi ya siku saba.

Mrajis (au Afisa aliyemteua), ana mamlaka ya kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu wa chama kama anaona ni lazima. Hii inaweza kutokea kufuatilia ukaguzi wa mambo ya chama. Katika mkutano huo Mrajis au Afisa aliyemteua ana mamlaka ya kuisimamisha Bodi iliyopo na kuweka Bodi ya muda kama itaonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo. Anaweza pia kutoa amri ya kukivunja chama.

18 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Kazi za Vyama Vilivyosajiliwa

Kuweka Kumbukumbu Vyama vyote vya ushirika vinapaswa kuweka kumbukumbu ambazo zinaweza kukaguliwa na wanachama na Mrajis au mwakilishi wake. Kumbukumbu hizo ni pamoja na:

• Orodha ya wanachama na hisa zao• Maelezo ya hesabu za biashara zinazohitajika kwa wanachama zinazoonyeshwa

kwa umma.• Hesabu zilizoidhinishwa na Mkaguzi wa Hesabu aliyechaguliwa na Mkutano

Mkuu na kuidhinishwa na Mrajis• Nakala ya Sheria ya Ushirika 2003, Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004 na

masharti ya chama chenyewe

Marekibisho ya Masharti ya ChamaMarekebissho ya masharti ya chama ambayo yameidhinishwa na mkutano mkuu yanapaswa kupelekwa kwa Mrajis kwa ajili ya kuidhinishwa. Hilo linafanyika ili Msajili aweze kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa sheria.

Taarifa ya HesabuKila chama cha ushirika kinapaswa kutunza taarifa sahihi za hesabu. Mkaguzi wa Hesabu aliyesajiliwa anapaswa kukagua hesabu hizo angalau mara moja kwa mwaka. Hesabu hizo zinapaswa kuidhinishwa na Mrajis na wanachama katika Mkutano Mkuu wao na baadaye kutumwa kwa Mrajis. Kama chama kitashindwa kutayarisha hesabu katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wake wa fedha, Mrajis atakuwa na uhuru wa kuondoa Bodi ya Uongozi iliyopo madarakani na kuweka nyingine. Wajumbe wa Bodi wanaoondolewa kwa jinsi hiyo, hawawezi kuchaguliwa tena kwenye Bodi kwa miaka sita. .

Endapo Mrajis anaona ni muhimu, anaweza kukagua akaunti za chama zilizopo benki au mahali popote na anaweza kutoa amri ya kukielekeza chama kuchukua hatua ya kurekebisha kasoro zozote zitakazoonekana.

Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC)

TFC ni nini?Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) ni asasi mama ya ushirika kitaifa ambayo inakuza, kuhudumia na kuratibu maendeleo na ustawi wa vyama vyote vya ushirika Tanzania bara. TFC ni asasi isiyo ya Kiserikali inayojitegemea na isiyo ya kisiasa inayomilikiwa na wanachama na kusimamiwa kwa mtazamo wa kanuni na maadili ya ushirika yanayotambuliwa kimataifa. Ni mwanachama wa Muungano wa

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 19

Vyama vya Ushirika Duniani (ICA) na linashirikiana na mashirika mengine kadhaa ya kitaifa na kimataifa yenye muelekeo unaofanana.

TFC lilisajiliwa tarehe 8 Desemba 1994 (Namba ya usajili 5503).

Wanachama wa TFC ni nani?Wanachama wake wa sasa ni: Vyama vikuu vilele vya ushirika vinavyosimamia mazao ya pamba na tumbaku; Vyama vikuu maalum vinavosimamia Ushirika wa viwanda na Akiba na Mikopo nchini – TICU na SCCULT5; na Vyama vikuu vya Ushirika wa mazao vitano ambavyo ni Karagwe District Cooperative Union (KDCU), Kagera Cooperative Union (KCU), Tandahimba-Newala Cooperative Union (TANECU), Mtwara-Masasi Cooperative Union (MAMCU) na Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU).

Uanachama wa Shirikisho ni wazi kwa Vyama vyote vya Ushirika kuanzia ngazi ya Msingi mpaka Ngazi ya Vyama vikuu vilele ili mradi chama hicho si mwana chama wa chama kingine ngazi ya kati. Mfumo mzima wa TFC unafanyiwa rejea ili kubaini maeneo muafaka ya kufanyia maboresho kwa manufaa na maendeleo ya wanachama.

Uanachama wa jumla wa TFC unajumuisha Vyama vya msingi 5,700 vyenye wanachama binafsi zaidi ya 700,000.

Maarubu ya TFCShirikisho litajitahidi kuwa asasi mama ya ushirika ya taifa yenye uhai ambapo aina zote za ushirika zitaunganishwa katika kuvutia na kuhamisha maadili ya ujasiriamali na utawala bora. Madhumuni yake ni kuimarisha uendelevu wa ushirika ili wanachama wafaidike moja kwa moja kutokana na kupambana kwao dhidi ya umaskini kupitia ushirikishwaji kiuchumi katika ujenzi wa uchumi.

5TICU – Tanzania Industrial Cooperative Union Ltd; and SCCULT – Savings and Credit Cooperative Union

League of Tanzania.

20 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Malengo ya TFC

Malengo yake ni kujenga msingi imara wa ushirika kwa:

• Kuwezesha na kuratibu uanzishwaji, maendeleo na ukuaji wa ushirika endelevu na wa kidemokrasia;

• Kufanya utafiti na kutoa huduma za ushauri kwa vyama vya ushirika wanachama katika maeneo ya masoko, biashara, fedha, bidhaa na huduma mpya;

• Kukusanya takwimu na taarifa kuhusu hali ya ushirika, masoko na bei na kuvisambaza kwa wanachama;

• Kuanzisha elimu shirikishi ya ushirika na programu za mafunzo miongoni mwa wanachama wake; na

• Kutangaza na kuhamasisha kuhusu aina zote za shughuli za ushirika nchini.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi:

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA Ghorofa ya 9, Ushirika Building,

Barabara ya Lumumba,S.L.P 2567,

Dar es Salaam.

Simu: 255 (0) 22 218 4081 – 5Faksi: 255 (0) 22 2184081

Baruapepe: [email protected]• • • • • • • • • • • • •

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera yaMaendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama

vya Ushirika Tanzania BaraUmetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na

Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIALINGEPENDA KUPATA MAONI YAKO KUHUSU KIJITABU HIKI. TAFADHALI ANDIKA KWA:

Katibu Mtendaji,Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,

Ghorofa ya 9, Jengo la UshirikaMtaa wa Lumumba

S.L.P. 2567Dar es Salaam

Simu: 255 (0) 22 218 4081–5Nukushi: 255 (0) 22 2184081

Barua pepe: [email protected]: www.ushirika.coop

TAARIFA ZAIDI

Kwa taarifa zaidi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika kuna nyaraka kuu tatu za kusoma:

• Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003• Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004• Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002

Inawezekana kupata nyaraka hizi kutoka kwa:Ofisa Ushirika wa Wilaya wako;

- Mrajis Msaidizi wa Mkoa wako;- Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (anwani ya hapo juu);

au

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika,Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,

S.L.P. 201, Dodoma.

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIALINGEPENDA KUPATA MAONI YAKO KUHUSU KIJITABU HIKI. TAFADHALI ANDIKA KWA:

Katibu Mtendaji,Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,

Ghorofa ya 9, Jengo la UshirikaMtaa wa Lumumba

S.L.P. 2567Dar es Salaam

Simu: 255 (0) 22 218 4081–5Nukushi: 255 (0) 22 2184081

Barua pepe: [email protected]: www.ushirika.coop

TAARIFA ZAIDI

Kwa taarifa zaidi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika kuna nyaraka kuu tatu za kusoma:

• Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003• Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004• Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002

Inawezekana kupata nyaraka hizi kutoka kwa:Ofisa Ushirika wa Wilaya wako;

- Mrajis Msaidizi wa Mkoa wako;- Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (anwani ya hapo juu);

au

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika,Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,

S.L.P. 201, Dodoma. Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya

Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyamavya Ushirika Tanzania Bara