mwongozomwongozo wa maderevawa madereva … · uvumilivu. iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva...

68
Mwongozo Mwongozo Mwongozo Mwongozo wa Madereva wa Madereva wa Madereva wa Madereva Wanafunzi Wanafunzi Wanafunzi Wanafunzi Kwa wale wanaojifunza magari madogo na magari mengine ya kawaida

Upload: phamthuy

Post on 02-Mar-2019

467 views

Category:

Documents


35 download

TRANSCRIPT

Page 1: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

MwongozoMwongozoMwongozoMwongozo wa Maderevawa Maderevawa Maderevawa Madereva WanafunziWanafunziWanafunziWanafunzi

Kwa wale wanaojifunza magari madogo na magari mengine ya kawaida

Page 2: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

ii

©Wizara ya Miundombinu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Julai 2009

ISBN 978 9987 9171 2 9

Page 3: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

iii

Yaliyomo

Dibaji.................................................................................1 Utanguluzi .........................................................................3 Mambo gani yanayomfanya dereva kuwa mzuri?...............5 Jukumu lako ktika mfumo wa barabara .............................6 Sheria na madereva wanafunzi..........................................6 Kujua kuhusu gari lako na jinsi kulidumisha......................7

Vijenzi vya msingi........................................................................8

Kulikagua gari ...........................................................................12

Ushauri kwa madereva wa magari yenye nguvu ya magurudumu ya

mbele na ya nyuma ...................................................................14

Kuwa katika hali nzuri ya kuendesha...............................14 Uwezo wa kuona .......................................................................14

Uchovu.....................................................................................15

Kunywa pombe .........................................................................16

Kutumia dawa na kuendesha.......................................................17

Hali na ugonjwa.........................................................................17

Jinsi ya kuanza, kunyonga, kusimama na kurudi nyuma..18 Utangulizi .................................................................................18

Kuwasha injini...........................................................................20

Kunyonga .................................................................................21

Kuondoka .................................................................................22

Kubadili gia...............................................................................22

Kuendelea kulidhibiti gari............................................................23

Kufunga breki ...........................................................................24

Kurudi nyuma ...........................................................................25

Kuliacha gari .............................................................................26

Uendeshaji salama barabarani.........................................27 Kuendesha barabarani................................................................27

Mwendo....................................................................................31

Kulipita gari jingine....................................................................32

Makutano .................................................................................36

Ushauri maalumu kwa madereva kwenye sehemu zenye mzunguko.41

Uendeshaji wa usiku au kwenye hali mbaya ya hewa .....................42

Kurudi nyuma ...........................................................................43

Kuwajali watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara

wanaoweza kuathirika ................................................................44

Kurudi ulikotoka ........................................................................46

Reli Inayokatisha .......................................................................47

Page 4: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

iv

Kuegesha.........................................................................48 Uegeshaji wa 900.......................................................................49

Uegeshaji sambamba .................................................................50

Uegeshaji wa mshazari...............................................................50

Kuegesha kilimani......................................................................51

Alama za barabarani........................................................52 Jaribio la udereva ............................................................53

Maombi ya kufanya jaribio la udereva ..........................................53

Kujiandaa kwa jaribio.................................................................53

Yaliyomo kwenye jaribio .............................................................54

Jaribio ......................................................................................54

Baada ya jaribio ........................................................................56

Kuharibika .......................................................................57 Iwapo kuna ajali..............................................................58 Muhtasari wa mafunzo ya madereva wa magari madogo (Leseni za Daraja B & D) .................................................59

Page 5: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

1

Dibaji

Mwongozo wa Madereva Wanafunzi unajumuisha taarifa na maelekezo

kwa wale wanaojifunza kuendesha magari madogo na magari mengine

ya kawaida. Umeweka viwango kwa ajili ya programu za mafunzo ya

udereva, na wafundishaji wote wa udereva lazima wawafundishe

wanafunzi wao ujuzi na maarifa yaliyoelezwa humu. Watu wengi sana

wamekuwa wakiuawa na kujeruhiwa bila sababu kwenye barabara zetu,

na sababu kuu ni makosa ya dereva. Kila siku tunaona mifano ya tabia

za hatari za madereva, ambao ama hawajui sheria au wasiojali kuhusu

usalama wa wengine.

Ni matumaini yetu kuwa Mwongozo huu utasaidia uzalishaji kizazi kipya

cha madereva bora, salama. Iwapo utausoma Mwongozo vizuri, utapata

maelekezo mazuri – bora, na daima jaribu kujiendeleza, uwe na malengo

marefu na salama ya udereva mbele yako.

Page 6: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

2

Page 7: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

3

Utanguluzi Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi ni mwongozo rasmi kwa

wanaojifunza kuendesha magari madogo na magari mengine ya kawaida.

Uendeshaji gari mzuri na salama kwenye barabara zetu huhitaji ujuzi

unaofaa, uzoefu, na tahadhari. Lazima ujue:

• Namna ya kuvitumia vidhibiti vya gari lako

• Namna ya kuliweka gari lako katika hali nzuri barabarani

• Wakati unapokuwa katika hali isiyo nzuri kwa kuendesha gari

• Namna ya kuliendesha gari lako kwa usalama

• Sheria za barabarani na maana ya alama na michoro ya barabarani

• Nini cha kufanya katika tukio la gari kuharibika au ajali.

Seti hii yenye stadi mbalimbali ngumu si kitu unachoweza kujifunza kwa

urahisi kutoka kwa marafiki na ndugu – lazima upate maelezo ya

kitaalamu kutoka kwenye shule ya udereva yenye kibali.

Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi umeandikwa ili kuzipatia shule

za udereva miongozo ya maudhui ya programu zao za ufundishaji

madereva. Wana wajibu wa kuwafundisha wanafunzi kwenye nyanja zote

za udereva si jinsi ya kulidhibiti gari tu. Mwongozo unaonyesha kile

ambacho mwanafunzi anapaswa kufundishwa. Baadhi ya ushauri

umechukuliwa kutoka kwenye Kanuni za Barabara, lakini wanafunzi

wanatakiwa kuzipata nakala zao za Kanuni za Barabarani, kwani zina

taarifa za alama zote za barabarani, na taarifa nyingine muhimu.

Utakapoona maneno LAZIMA au SI LAZIMA maana yake ni kuwa

unatakiwa kisheria kufuata maelekezo haya. Iwapo hutafuata moja kati

ya maelekezo haya umevunja sheria, na iwapo utakamatwa na

kuthibitika, unaweza kutozwa faini na kuondolewa kutoka kwenye

udereva. Pia unaweza kupelekwa jela mpaka miaka mitano. Sheria za

Barabarani zitabadilika katika miaka ijayo na uwasiliane na polisi wa

eneo lako iwapo una shaka yoyote kuhusu sheria za sasa.

Mwongozo wa Madereva Wanafunzi unajaribu kuelezea mambo kwa

lugha rahisi, lakini baadhi ya istilahi zilizotumika zinaweza kuwa ngeni

kwako au zenye maana tofauti kidogo na ile unayoifahamu. Mwongozo

mfupi umetolewa hapo chini:

Page 8: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

4

“Dereva” maana yake ni mtu yeyote anayeendesha gari au vitu vingine

(pamoja na baiskeli) au anayechunga wanyama barabarani

“Njia mbili” maana yake ni barabara ambazo zinapishana na

kutenganishwa kati au na kizuizi

“Achia njia” maana yake ni kuwa dereva asiendelee, iwapo kufanya

hivyo kutawalazimisha madereva wa magari mengine kubadili mwendo

au mwelekeo kwa haraka

“Njia” maana yake sehemu ya barabara ambayo imeonyeshwa kwa ajili

ya mstari mmoja wa magari yanayokwenda

“Mtumiaji wa barabara” maana yake mtu yeyote anayesafiri, au

aliyemo barabarani, au ndani ya gari barabarani

“Magari barabarani” maana yake magari yanayotembea

“Gari” maana yake mashine yoyote inayoendeshwa barabarani kwa

nishati yoyote, na ikijumuisha uzungukaji pedeli, mikokoteni ya

kusukumwa kwa mikono na mikokoteni ya kuvutwa na wanyama

“Alama za pundamilia” maana yake alama za kivuko cha watembea

kwa miguu inayoonyeshwa na mistari myeupe sambamba na mwelekeo

wa barabara.

Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi umetolewa na Kitengo cha

Usalama Barabarani cha Wizara ya Miundombinu kwa kushirikiana na

Jeshi la Polisi Tanzania. Kazi hii ilisaidiwa na Shirika la Kimataifa la

Misaada ya Maendeleo la Denmark. Waandishi wanashukuru kwa

matumizi ya maelezo kutoka Mwongozo wa madereva Wanafunzi wa

SATCC, na Kanuni za Barabarani za nchi nyingine ikiwa ni pamoja na

Uganda. Vielelezo vingi vimetolewa kwa hisani ya Wizara ya Ujenzi,

Nyumba na Mawasiliano, Jamhuri ya Uganda. Maelezo mengi

yamechukuliwa kutoka kwenye toleo la mwanzo la Mwongozo

lililoandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa msaada wa fedha

kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway.

Page 9: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

5

Mambo gani yanayomfanya dereva kuwa mzuri?

Dereva mzuri anahitaji ustadi na uzoefu, na mtazamo sahihi. Mwalimu

wako wa udereva atakufundisha ustadi na utauendeleza kwa kutenda.

Uzoefu utakuja kadiri unavyoendesha mara nyingi na kukabiliana na

mazingira mengi. Ubora unaochangia kuwa na mtazamo sahihi wa

udereva ni kama ufuatao:

Uwajibikaji –kuwafikiria wengine. Gari ni mashine ambayo inaweza

kuuwa kwa urahisi, kwa hiyo lazima uzingatie usalama wako, usalama

wa abiria wako, na usalama wa kila mtumiaji mwingine, hususan

watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na watumiaji wengine wa

barabara wanaoweza kudhurika. Daima lazima uzingatie usalama na

kamwe usifanye jambo ambalo linaweza kuwaingiza wengine hatarini.

Wakati wote kumbuka kuchukua tahadhari zaidi, kwa sababu kosa dogo

linaweza kusababisha ajali inayoweza kuua mtu.

Umakini. Pamoja na uwajibikaji kuna umakini katika kazi ya udereva.

Lazima uwe makini wakati wote iwapo unataka kuendana na hali

inayojitokeza barabarani. Usiendeshe ukiwa umechoka,

umechanganyikiwa au kuumwa. Usiwaruhusu abiria wakusumbue na

maongezi yao, na usitumie simu yako ya mkononi.

Matarajio. Umakini husaidia kutarajia kitakachotokea. Unatakiwa daima

kuangalia kile ambacho watumiaji wengine wa barabara wanafanya, na

tumia busara yako kupima kile ambacho kitatokea baadaye. Kwa njia hii

utakuwa tayari na kuweza kuendana na kuitikia kwa usalama katika hali

yoyote ambayo itatokea.

Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine

anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari,

utakuwa unaelekea kupata ajali. Endelea kuwa mtulivu na idhibiti hasira

yako. Fuata sheria za barabarani.

Kujiamini. Unahitaji kujiamini ili kuendesha vizuri katika mazingira ya

kisasa ya barabara. Madereva wapya bila shaka hawatajiamini, lakini

kujiamini kutakuja kutokana na kukua kwa ujuzi na uzoefu. Hata hivyo,

usijiamini kupita kiasi, kwani hili linaweza kukusababishia uendeshaji wa

hatari. Daima dhibiti uendeshaji wako na jaribu kurekebisha makosa

yoyote yatakayojitokeza.

Page 10: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

6

Jukumu lako ktika mfumo wa barabara

Wakati unatumia barabara unaweza kujifikiria kama unafuata mfumo

unaojumuisha vitu vinne:

Magari – Magari madogo (la kwako na mengine), malori, mabasi,

baiskeli, n.k.

Watumiaji barabara – madereva wa magari (wewe na wengine) na

watumiaji barabara wanaoweza kudhurika (watembea kwa miguu,

waendesha baiskeli na pikipiki)

Mazingira ya barabarani – barabara na sehemu zake, pamoja na

alama na michoro ya barabarani

Sheria za barabarani (Katika Sheria za Barabarani na Kanuni za

Barabarani) – zinazodhibiti mwingiliano kati ya watumiaji wa barabara

(pamoja na wewe) magari na mazingira ya barabara.

Kwa pamoja, mambo haya manne yanaunda mfumo wa barabara. Ili

mfumo ufanye kazi vizuri mambo haya manne lazima yafuatwe vizuri

kwa kila moja na kila moja litumike bila ya makosa. Mazingira ya

barabarani yamekuwa yakiboreshwa taratibu, na sheria za barabarani

zimetungwa (ingawa si kila mmoja anazifahamu). Wajibu wako ni kuona

kuwa wewe na gari lako mnaenda bila makosa.

Sheria na madereva wanafunzi

Leseni za madereva wanafunzi. Madereva Wanafunzi lazima wawe na

leseni za madereva wanafunzi kabla ya kuendesha gari kwenye barabara

za umma. Leseni hizi huombwa kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato

Tanzania (TRA). Leseni hii hudumu kwa miezi mitatu, lakini inaweza

kuombwa upya kwa kipindi cha miezi mitatu mingine kwa wakati mmoja.

Leseni haiwezi kuombwa upya zaidi ya miezi 15 isipokuwa kama

umefanya na kushindwa jaribio la udereva katika kipindi hicho.

Unaweza kuomba leseni ya kuendesha baiskeli moto mara tu ufikishapo

umri wa miaka kumi na sita. Unatakiwa kuwa na angalau miaka 18 kabla

hujaruhusiwa kuendesha gari dogo, pikipiki au magari mengine ya

kawaida. Unaweza kutakiwa kuthibitisha umri wako.

Unapoomba leseni ya madereva wanafunzi unaweza kutakiwa kuonyesha

kuwa umefanya mipango ya kupata mafunzo kutoka kwenye shule yenye

Page 11: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

7

kibali cha mafunzo ya udereva. Lazima uonyeshe kasoro zozote au

ulemavu mwilini wakati unaomba leseni ya dereva mwanafunzi.

Wanafunzi lazima waendeshe chini ya usimamizi wa Mwalimu wa

udereva aliyesajiliwa. Usiendeshe bila ya mwalimu wako kwenye kiti

cha mbele cha abiria. Hata hivyo madereva wa pikipiki wanafunzi

wanaweza kuendesha peke yao.

Kiwekwe “kibao cha L” Gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi

lazima liwekwe “Vibao vya L” mbele na nyuma.

Jaribio la udereva. Dereva mwanafunzi anaweza kuomba polisi afanye

jaribio la udereva pindi atakapokuwa ameendesha kwa angalau mwezi

mmoja baada ya kutolewa kwa leseni ya dereva mwanafunzi. Iwapo

atafaulu jaribio, atapatiwa cheti cha kufuzu, na hiki kitamuwezesha

kuomba leseni kamili ya udereva. Angalia vifungu vingine mbele kwa

taarifa zaidi kuhusu jaribio la udereva.

Gari. Gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi lazima liwe na nyaraka

halisi za usajili, leseni ya barabara, na sera ya bima ya gari. Pia lazima

liwe na hali nzuri kutembea barabarani.

Kujua kuhusu gari lako na jinsi kulidumisha

Ni vizuri kuwa na maarifa ya msingi ya jinsi gari lako linavyofanya kazi.

Lazima ujue kazi za vyombo mbalimbali vya gari na sehemu vilipo.

Maarifa haya yatakusaidia kuliweka gari katika hali nzuri ya kutembea

barabarani.

Hali ya kiufundi ya gari lako lazima iendane na kanuni za gari. Fundi

mchundo mwenye ujuzi anaweza kuchunguza iwapo gari lako linakidhi

viwango vinavyotakiwa. Iwapo gari lako litahitaji matengenezo

inashauriwa kutumia karakana zenye uzoefu na zinazoaminika. Epuka

kutumia vipuri vyenye ubora mdogo au vya kughushi, ukidhani unaokoa

fedha unaponunua vipuri vya bei rahisi. Daima huweza kuwa hatari kwa

kuvunjika ghafla au kuchakaa haraka.

“Kitabu cha Mwongozo” kwa ajili ya gari lako ni chanzo kizuri sana cha

ushauri wa namna ya kulitumia gari na kulifanya lidumu katika hali nzuri.

Fuata maelekezo haya kwa makini. Kumbuka kuwa gari linalotunzwa

Page 12: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

8

vizuri halitakugharimu sana kulitumia, halitaharibika mara kwa mara na

litakuwa salama.

Vijenzi vya msingi

Injini. Injini ni mashine inayolifanya gari kutembea. Nishati huhamishwa

kupitia kwenye klachi kwenda kwenye giaboksi na hatimaye kwenye

magurudumu. Injini za petroli ni nyingi lakini baadhi ya magari madogo

na magari mengi ya magurudumu manne na magari madogo ya mizigo

yamewekwa injini za dizeli.

Ulainishaji. Injini lazima ilainishwe kwa mafuta/vilainishi ili iweze

kufanya kazi vizuri na bila kuharibika. Vilainishi vya Injini huchafuka na

huhitaji kubadilsihwa, kwa kawaida kila baada ya km 5,000 au kila baada

ya miezi sita (yoyote itakayotangulia). Pima kiasi cha oili kila wiki. Iwapo

taa ya tahadhari ya oili itawaka kwenye chombo cha kuonyeshea wakati

unaendesha simama na kupima kiasi cha oili. Ni jambo zuri kuwa na

dumu la oili ya injini kwenye gari lako.

Uwashaji. Mfumo wa uwashaji hupatia injini ya petroli kichocheo

ambacho huifanya petroli kulipuka na kuzalisha nishati kwenye silinda.

Plagi lazima ziwe safi na kufungwa vizuri, ili zitoe kichocheo kikubwa.

Injini za dizeli hazina mfumo huu wa uwashaji.

Mfumo wa upozaji. Injini hupata moto sana kwa hiyo lazima kuwe na

mfumo wa kuipoza. Mfumo huu kwa kawaida hufanya kazi kwa kupeleka

maji (kipozeo) kuzunguka injini kupitia mipira na mirija. Angalia kiasi cha

maji kwenye tangi kila wiki na angalia uvujaji kwenye mirija ya maji.

Iwapo mshale kwenye kipimo unaonyesha kuwa joto la injini ni la juu

sana lazima uzime injini kuepuka uharibifu. Maji yatakuwa moto sana na

yanaweza kukuunguza – hivyo, kama unahitaji kujaza tena, subiri hadi

injini ipoe.

Mfumo wa mafuta. Mafuta hunyonywa kutoka kwenye tangi la

mafuta/vilainishi na pampu na kisha huchanganywa na hewa na

kusukumwa kwenye injini. Injini inaweza kuharakishwa kufanya kazi kwa

kubonyeza kwenye pedeli ya kichapuzi ambayo hurekebisha

mchanganyiko wa mafuta/hewa.

Giaboksi. Giaboksi husafirisha nishati kutoka kwenye injini kwenda

kwenye magurudumu hivyo nishati ya kutosha kuendesha gari

Page 13: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

9

inakuwepo kwenye mwendo tofauti. Magari mengine yana giaboksi za

mikono. Magari haya yana gia 4 au 5 za kwenda mbele zinazoitwa ya

kwanza, ya pili, ya tatu ya nne na ya tano, na gia moja ya kurudi nyuma.

Wakati mwingine mpangilio huonyeshwa kwenye sehemu ya gia yenye

muundo wa “H” – angalia kielelezo.

Kwa kawaida unatumia gia ya kwanza kulifanya gari lianze kutembea na

kisha polepole endelea na gia zinazofuata kadiri mwendo

unavyoongezeka. Kanyaga pedeli ya klachi kutenganisha injini na

giaboksi wakati unabadili gia na wenzo wa gia.

Magari mengine yamewekwa mfumo wa otomatiki ambao hubadili gia

kwa ajili yako – unachotakiwa kufanya kabla ya kuondoka ni kukanyaga

pedeli ya breki, kuondoa kichaguzi cha gia kutoka kwenye “kuegesha”

kupeleka mbele au “kurudi nyuma”, kisha kuachia pedeli za breki.

Mfumo wa otomatiki:

Mpango wa pedeli

BrekiKlachi Kichapuzi

Wenzo wa kichaguzi

K

K

N

K

2

uegeshaurudi nyumayutrouendesha

L

Breki

Mpango wa pedeli

Kichapuzi

1 3 5

2 4 R

1 3

2 4 R

1 3

2 4

R

R maana yake gia ya kurudi nyuma

Mpangilio halisi wa giaboksi

Nyutro Nyutro

Page 14: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

10

Breki. Gari lina mfumo wa breki ambao unatumia mafuta ya haidroliki

(kilainishi/mafuta ya breki) kuendesha pedi ambazo hubana

magurudumu na kuyapunguza mwendo. Pedi hizi huweza kuchakaa na

huhitaji kubadilishwa kila baada ya wakati fulani. Breki hufanya kazi kwa

kukanyaga pedeli za breki. Ni muhimu kuangalia kiasi cha

kilainishi/mafuta ya breki kwenye akiba kila wiki. Daima tumia

kilainishi/mafuta halisi ya breki, si mengine ya bei rahisi yasiyo halisi. Ni

muhimu sana kwa usalama wako na kwa usalama wa watumiaji wengine

wa barabara breki kuwa katika hali nzuri, iwapo hazifanyi kazi vizuri na

kwa ubora (gari huenda upande, breki hupiga kelele, au pedeli za breki

kuwa laini na kubonyea) lazima ziangaliwe haraka. Matengenezo ya

mfumo wa breki yafanywe na karakana yenye ujuzi.

Magari yote madogo yana breki ya mkono, ambazo lazima zitumiwe

wakati wa kuegesha. Lazima iwe na uwezo wa kulifanya gari liendelee

kusimama hata kwenye kilima kikali.

Usukani na Viangiko. Magari mengi sasa yamewekwa nishati ya

usukani ambayo huufanya usukani kunyongwa kirahisi. Unyongaji wa

usukani lazima uhamishe mzunguko wa usukani kwenye magurudumu

taratibu na kwa ufanisi. Kusiwe na nguvu nyingi kwenye unyongaji.

Chunguza jambo hili kwa kuzungusha usukani mpaka upate kizuizi halisi

– Iwapo unaweza kunyonga usukani zaidi ya sm 2-3 kuna kudorora

kwingi. Uchunguze usukani kwa kukata kona kali katika mwendo mdogo

– iwapo kuna kelele zisizo za kawaida au usukani haufanyi kazi vizuri,

lipeleke gari kwenye karakana yenye ujuzi kwa kukaguliwa kwa makini

na matengenezo.

Mfumo wa viangiko (springi na shokomzoba) hudhibiti uendaji juu na

chini wa magurudumu ili uendeshaji uendelee kuwa mzuri. Mfumo huu ni

muhimu zaidi kwa usalama; unayaweka magurudumu katika

kukandamiza vizuri barabara, hususan wakati wa kufunga breki.

Shokomzoba zina kazi ngumu na huhitaji kubadilishwa mara kwa mara.

Wakati wa kubadili shokomzoba badili pande zote, kuepuka kutokuwepo

uwiano.

Matairi na magurudumu. Matairi ni sehemu ambayo hulifanya gari

lako likae barabarani, na eneo la kukanyaga kwa kila tairi kwa wastani ni

kubwa kama mkono wako. Iwapo utahitaji kufunga breki au kupinda

ghafla utendaji wa eneo hili dogo la tairi unaweza kuwa mkubwa kwa

usalama wako, hivyo, ni muhimu sana kuwa na matairi mazuri. Matairi:

Page 15: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

11

• Yaenee vizuri kwenye magurudumu

• Yawe na sehemu ya kukanyagia yenye kina cha kutosha – mm3 ni

kina cha chini kinachopendekezwa

• Yawe na upepo sahihi

• Yakae vizuri ndani, kuepuka kukatika, kuvimba au maeneo ambayo

umbo la ndani linaonekana

• Yote yawe ya aina na utengenezaji mmoja.

Fuata ushauri wa mtengenezaji juu ya wakati gani wa kubadili matairi.

Usijaribu kutengeneza matairi yaliyoharibika vibaya. Matairi

yaliyotengenezwa yanaweza kukupa matatizo na yanaweza yasiwe

salama. Iwapo utafunga matairi yenye ubora na kuyatunza utapunguza

hatari ya tairi kupasuka wakati unaendesha. Upasukaji wa matairi

husababisha ajali za mara kwa mara.

Pancha inaweza kutokea wakati wowote. Daima uwe na tairi la akiba

kwenye gari, pamoja na jeki ya kulinyanyua gari, na spana ya kufungulia

nati za gurudumu. Hakikisha kuwa tairi la akiba liko katika hali nzuri na

kujaza upepo sahihi. Fanya mazoezi ya namna ya kubadilisha matairi.

Betri na mfumo wa umeme. Betri inatoa nishati kwenye stata na

huhifadhi nishati ya ziada inayotoka kwenye altaneta. Hakikisha altaneta

ina chaji betri wakati injini inafanya kazi (magari mengine yana taa ya

kuashiria kwenye dashibodi). Iweke betri katika hali nzuri – aina nyingine

huhitaji kujazwa tena maji ya betri mara kwa mara. Hakikisha kuwa kebo

zimefungwa vizuri kwenye betri, kwani mara nyingi zikilegea zinafanya

umeme usipite.

Taa, indiketa na viakisi. Lazima uhakikishe kuwa na:

• Taa mbili nyeupe za mbele ambazo zinaweza kuteremshwa (yaani

kumulika chini)

• Taa mbili nyeupe mbele na taa mbili nyekundu nyuma

• Indiketa za njano mbili mbele na mbili nyuma

• Taa mbili nyekundu nyuma za kusimamia ambazo huwaka wakati

breki ikifungwa.

• Angalau kiashiria kimoja nyuma.

Hakikisha kuwa taa za mbele zimerekebishwa ili wakati zikiteremshwa

mwanga uende chini na kushoto. Ziangalie taa zako mara kwa mara – ni

kinyume cha sheria kuendesha wakati moja au zaidi ya taa hizi haifanyi

kazi.

Page 16: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

12

Mfumo wa ekzosi. Huu huitoa gesi iliyoungua kutoka kwenye injini na

kuisukuma kupitia kwenye sailensa kabla ya kuitoa nje kupitia kwenye

bomba la ekzosi. Usiuache mfumo wa ekzosi kuwa katika hali mbaya kwa

sababu hili litasababisha kelele, na gesi ya ekzosi inaweza kuambaa

kwenye gari.

Dashibodi. Mpango wa dashibodi hutofautiana kulingana na

mtengenezaji na aina ya gari, lakini kielelezo kinaonyesha mpango halisi.

Angalia “Kitabu cha Mwongozo” iwapo kuna taa zozote au vipimia

ambavyo huna uhakika navyo.

Kulikagua gari

Ni muhimu gari lako kufanyiwa matengenezo ya kawaida ya mara kwa

mara na karakana yenye ujuzi, lakini vitu vinaweza kuharibika baada na

kabla ya matengenezo mengine, hivyo ni lazima uendelee kulikagua

mwenyewe.

Kabla ya kila safari angalia kuwa:

• Hakuna tairi lisilo na upepo

• Chungulia uvunguni mwa gari kuona iwapo kuna kuvuja kokote,

wanyama, watoto n.k.

• Kioo chako cha mbele na madirisha ni safi

• Vioo vyako vya pembeni viko mahali sahihi ili uone vizuri.

• Hakuna taa yoyote ya tahadhari inayowaka kwenye dashibodi

HF

E C

FUEL TEMP

P

R

ND2

L

40

20

0

60

80 100120

140

160

180km/h

Kipimia mwendo

Kipimiamafuta

Kuendesha

Indiketa ya kuliaIndiketa ya kushoto

Taa za mbele

Mahali pa

taa ya tahadhariMahali pa

taa ya tahadhari

Kipimia joto

Page 17: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

13

Vitu ambavyo unapaswa kuvichukua kwenye gari:

• Leseni ya biashara, waraka wa usajili wa gari, stika ya leseni ya

barabara, na stika ya bima (vibandikwe ndani kwenye kioo cha

mbele)

• Kisanduku cha huduma ya kwanza

• Tairi la akiba- lijazwe upepo sahihi

• Spana ya gurudumu

• Vibao viwili vya tahadhari vya Pembetatu vyekundu (hivi huhitajika

kisheria)

• Tochi.

Vingine muhimu ni:

• Mfuko wa Spana na bisisbisi

• Utepe

• Pampu ya mguu

• Mkanda wa feni wa akiba

• Oili ya injini

• Mafuta ya breki

• Kipozeo cha akiba

• Kamba ya kuvutia

• Fyuzi za akiba kwa ajili ya mfumo wa umeme

• Kebo kwa ajili ya kuchajia betri

• Poda kavu ya kuzimia moto isiyo pungufu kg 1.

Kila wiki lazima uangalie:

• Uchakaaji wa matairi na upepo

• Nati za magurudumu

• Kiasi cha oili

• Kiasi cha mafuta ya breki

• Kiwango cha upozaji

• Indiketa na taa ni safi na zinafanya kazi

• Honi inafanya kazi

• Kiasi cha betri na kukaza kwa vifungo vya betri

• Weipa za kioo cha mbele zinafanya kazi na chupa ya kuzioshea imejaa

maji

• Kioo chote ni safi ndani na nje, na kuwa vioo na viashiria ni safi

• Funua boneti kuona kama kuna kitu chochote chenye matatizo

• Chunguza kelele zisizo za kawaida wakati injini inaunguruma.

Page 18: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

14

Iwapo unaendesha umbali mrefu kila siku, au gari lako limechakaa,

fanya uchunguzi wa yaliyoandikwa hapo juu mara kwa mara badala ya

mara moja kwa wiki.

Kila mwezi chunguza:

• Kukaza kwa mkanda wa feni

• Kuvuja kwa mipira ya maji.

Ushauri kwa madereva wa magari yenye nguvu ya magurudumu ya mbele na ya nyuma

Magari yenye nguvu ya magurudumu ya mbele na nyuma yana faida

kubwa kuliko magari madogo kwani yanaweza kupita kwa urahisi kwenye

barabara mbaya na vilima vikali. Hata hivyo utendaji wake wa usalama

umechanganywa. Mahali pa uendeshaji ni pazuri na panaonekana

kumlinda vizuri dereva na abiria ajalini, kwa sababu ya ukubwa wake.

Lakini yana kitovu cha mvutano mkubwa ambao huyafanya kuelekea

kupinduka. Uwe mwangalifu kunyonga na kufunga breki taratibu,

hususan wakati unaendesha kwa mwendo wa kasi, au iwapo tairi la

mbele litapasuka. Pia ukumbuke kuwa ukimgonga mtembea kwa miguu,

mwendesha baiskeli au pikipiki kwa magari ya namna hii yana

uwezekano mkubwa wa kupata ajali mbaya, hivyo uwe makini zaidi

viwapo karibu. Kuendesha gari kubwa hakukupi haki ya kuwasukuma

wengine walio karibu na wewe – unatakiwa kujali wakati wote.

Kuwa katika hali nzuri ya kuendesha

Kuendesha gari ni kazi ngumu inayoendelea kwa hali ambayo si ya

kawaida kwa binadamu. Matukio yasiyotarajiwa hutokea ambayo

yanakuhitaji kutenda haraka. Hivyo, unahitaji kuwa na uwezo mzuri wa

kuona, kutenda upesi, na kuwa na tahadhari na kuwa makini. Iwapo

utakuwa umechoka au kunywa pombe au kutumia dawa fulani unaweza

usiwe katika hali nzuri ya kuendesha.

Uwezo wa kuona

Taarifa nyingi anazohitaji dereva humfikia kupitia macho yake. Kwa hiyo

uwezo wa kuona vizuri ni muhimu kwa uendeshaji salama. Lazima uweze

kusoma kibao cha namba za gari kutoka umbali wa kiasi cha mita 20

katika mwanga mzuri wa mchana. Iwapo unahitaji kuvaa miwani (au

lenzi zilizobandikwa kwenye mboni) kuona, lazima uvivae wakati wote

Page 19: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

15

unapoendesha. Wakati unaomba leseni ya udereva utatakiwa kuonyesha

cheti kinachoonyesha kuwa uwezo wako wa kuona uko katika viwango

vinavyotakiwa.

Kadiri watu wanavyozeeka na uwezo wao wa kuona hupungua. Wakati

mwingine mabadiliko huwa ya polepole kiasi cha kutoyagundua. Upimaji

wa mara kwa mara wa macho ni muhimu.

Uonaji wa kawaida

Vitu ambavyo moja kwa moja viko mbele yako vinaweza kuonekana kwa

uwazi zaidi, lakini uonaji wako wa pembeni kwa kawaida ni mzuri

kugundua mienendo ya eneo pana kuelekea kwako. Uonaji huu wa

pembeni ni muhimu, kwa sababu unahitaji kuona kitu chochote haraka

(magari, watembea kwa miguu) vinavyokuja kwako kutoka pembeni.

Wakati unaendesha kwa kasi hutaweza kutumia vioo vyako vya pembeni

kikamilifu. Hii inamaanisha kuwa utaikaribia hatari kubwa kabla

hujaweza kuigundua. Kitu kama hicho hutokea pindi ukinywa pombe –

vioo vyako vya pembeni hutiwa ukungu na kuwa vidogo.

Uchovu

Kuendesha kunaweza kukufanya ujisikie usingizi, na hili kwa kiasi

kikubwa hukuongezea hatari ya kupata ajali. Unaweza kuepuka usingizi

kwa kuhakikisha kuwa kuna hewa nzuri ndani ya gari, na umekaa

sehemu nzuri ya kuendeshea. Kitu chochote kinachosababisha ugumu

katika uendeshaji, mfano uchafu kwenye kioo cha mbele, vitakuchosha

kwenye safari ndefu.

Upunguaji wa uwezo wa kuona pembeni baada ya kunywa pombe au kwenda kwa mwendo wa kasi

Page 20: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

16

Inashauriwa kuwa upumzike kwa dakika 30 kila baada ya saa 3 za

kuendesha. Epuka kuanza safari ndefu usiku sana au baada ya saa za

kazi. Usiendeshe kwa zaidi ya saa 9 kwa siku. Madereva wa magari ya

biashara lazima wafuate kanuni za saa za madereva.

Iwapo unajisikia kuchoka tafuta sehemu salama usimame na kupumzika.

Toka ndani ya gari na utembee kidogo. Unywaji wa vikombe viwili vya

kahawa unaweza kukusaidia. Usitumie dawa ili usilale.

Kunywa pombe

Kamwe usinywe pombe kabla ya kuendesha. Pombe hupunguza uwezo

wa mfumo wa akili yako, kupunguza utendaji wako, kuathiri uamuzi

wako wa mwendo unaofaa, umbali sahihi na hatari itakayotokea, na

kukupa hisia zisizo sahihi za kujiamini.

USIENDESHE gari iwapo umekunwya pombe nyingi kiasi cha kushindwa

kuimudu. Hairuhusiwi kuendesha ukiwa na kiasi cha pombe kwenye

damu cha juu zaidi ya mg 80/ml 100, lakini uendeshaji wako unaweza

kuathiriwa kabla hata ya kufikia kikomo hiki. Kwa hiyo, ni vizuri

kutokunywa kabisa kilevi chochote kabla ya kuendesha.

Kumbuka kuwa inachukua muda kwa kwa kilevi kuondoka mwilini

mwako, hivyo unaweza kutokuwa katika hali nzuri ya kuendesha jioni

baada ya kunywa pombe wakati wa chakula cha mchana.

Pombe ni sababu ya ajali nyingi za barabarani, hususan zile zinazotokea

usiku. Hivyo, kuendesha ukiwa na pombe kwenye damu ni kosa kubwa,

na iwapo utakamatwa, adhabu inaweza kuwa kali sana, ikiwa ni pamoja

na faini, kufukuzwa udereva, na kufungwa. Iwapo polisi

watakusimamisha kwa kukuhisi kunywa pombe wanaweza kupima

haraka kiwango cha pombe kwenye damu yako kwa kukutaka kupumua

kwenye kifaa kiitwacho kipimaulevi (alcometer).

Page 21: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

17

Pombe na hatari ya ajali

Chanzo: kulingana na matokeo ya tafiti Marekani na Canada.

Kutumia dawa na kuendesha

Kutumia dawa kunaweza kuathiri uwezo wako wa kuendesha katika

namna nyingi. USIENDESHE gari kama umekunywa dawa

zitakazokufanya kushindwa kulidhibiti gari vizuri. Dawa nyingi zina athari

mbaya, mfano kukufanya kulala kuliko kawaida, hivyo kuwa makini na

hili na ikibidi acha kuendesha. Daktari au mfamasia wako akushauri

iwapo ni salama kuendesha. Utumiaji wa vichocheo, dawa za kubadili

akili, na vitu vingine haramu inaweza kuwa hatari, hasa vikienda pamoja

na pombe.

Hali na ugonjwa

Usiendeshe wakati una hasira, ukiwa na furaha zaidi au kuchanganyikiwa

sana kuhusu jambo fulani. Usiendeshe kama hujisikii vizuri. Iwapo una

tatizo la kiafya litakalokufanya kuelekea kuzimia au kifafa, au kupata

ulemavu wa mwilini lazima umuulize daktari wako iwapo ni salama

kwako kuendelea kuendesha. Iwapo daktari wako atakuambia uache

kuendesha, ipeleke leseni yako Polisi. Fanya hivyo hivyo iwapo uwezo

wako wa kuona utaathirika na kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa.

0 10 50 100 150 200

MARA 5

MARA 15

KIKOMOKISHERIA

80

Mchanganyiko wa damu na pombe(mg za pombe kwa 100 ml za damu)

Hatari ya ajalibila pombe

Hatari kubwa yaajali baada yakunywa pombe

Watu wanaoathiriwazaidi na pombe

Wanaoathirika zaidi

Wanaoathirika kidogo

Page 22: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

18

Jinsi ya kuanza, kunyonga, kusimama na kurudi nyuma

Utangulizi

Kabla hujaliendea gari lako ili uendeshe ni muhimu kuwa na tabia ya

kupanga safari yako. Unajua kwa uhakika unakokwenda na namna ya

kufika kule? – Kama hujui, angalia kwenye ramani au pata ushauri

kutoka kwa mtu anayelijua eneo hilo. Unapopanga safari yako fikiria

kuhusu msongamano wa magari, matengenezo ya barabara, hali mbaya

ya barabara, au matatizo mengine.

Unapolielekea gari lako anza kufanya uchunguzi wa awali kabla ya safari:

• Hakuna tairi lolote linaloonekana kutojaa (au kujaa sana)

• Hakuna uvujaji wowote chini ya gari

• Kioo chako cha mbele na madirisha ni safi

• Hakuna vizuizi vinavyokuzuia kuondoka

• Kama una mafuta ya kutosha kwa safari

• Kiti chako kimerekebishwa vizuri – angalia chini kwa taarifa zaidi

• Mkanda wa kiti umeshikizwa vizuri – na abiria wako wote wamefunga

mikanda yao (sheria inaagiza wewe na abiria wako wa kiti cha mbele

LAZIMA mjifunge mikanda)

• Kizuizi chako cha kichwa kimerekebishwa ili sehemu yake ya juu iwe

sawa na sehemu ya juu ya kichwa chako na kuna pengo dogo au

hakuna pengo kwenye sehemu hiyo na sehemu ya nyuma ya kichwa

chako-pia angalia vizuizi vya vichwa vya abiria wako

• Milango imebanwa na kufungwa vizuri

• Kuwa hakuna vitu vilivyozagaa vinavyoweza kukuchanganya wakati

unaendesha au vitu vinavyoweza kuruka ajali ikitokea

• Kuwa vifurushi vyovyote au vitu vingine vilivyobebwa vimefungwa

kiusalama

• Hakuna taa yoyote ya tahadhari inayowaka kwenye dashibodi

• Una leseni yako ya udereva, waraka wa usajili wa gari, stika ya leseni

ya barabara, na stika ya bima (stika zibandikwe ndani ya kioo cha

mbele).

Urekebishaji kiti ili kupata sehemu nzuri ya kuendeshea. Shika

usukani kwa mkono mmoja wakati unatumia mkono mwingine kulegeza

kizuizi cha mahali pa kiti. Sukuma kiti mbele au nyuma hadi pale

ambapo mguu wako wa kulia utakapokanyaga vizuri pedeli ya breki huku

ukiwa umepinda kidogo, si kunyooka. Ni muhimu kuweza kudhibiti pedeli

Page 23: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

19

vizuri lakini kwa msukumo mzuri inapohitajika. Mikono yako iwe

imepinda kidogo kwenye kiwiko, ili uweze kuufikia usukani vizuri – usiwe

mbali sana kiasi cha kukufanya ujinyooshe ili kuufikia, wala mikono yako

isiwe karibu sana kiasi cha kupinda sana ili kuukamata usukani. Nyuma

ya kiti kuwe katika hali ya wima na si kunyooka. Lazima uweze kuona

vizuri juu ya usukani. Iwapo wewe ni mfupi unaweza kuinua kiti – la

sivyo, tumia mto thabiti.

Kurekebisha vioo vyako. Unahitaji kutumia vioo vyako sana wakati wa

kuendesha. Ni muhimu virekebishwe ili uweze kuviona kirahisi, na

vionyeshe vizuri eneo la nyuma.

Kioo cha ndani kionyeshacho nyuma - bila ya kuondoa kichwa chako

kutoka mahali pa kuendeshea, kishike kioo hicho na kukirekebisha ili

uweze kuliona dirisha la nyuma kwa ukingo wa kulia wa kioo ulioungana

na ukingo wa kulia wa dirisha la nyuma – lazima uone vizuri nyuma na

nyuma kulia kwa gari.

Kioo cha nje cha upande wa kulia – Geuza kichwa chako kidogo kutoka

mahali pa kuendeshea na kirekebishe kioo hiki ili uweze kuona pembeni

kidogo ya gari – kioo kitaonyesha upande wa nyuma kulia kwa gari.

Kioo cha nje upande wa kushoto - geuza kichwa chako kidogo upande wa

kushoto na rekebisha kioo kionyeshe upande wa nyuma wa kushoto wa

gari.

Kumbuka kuangalia ukaaji wa vioo vyako wakati wote wa kuondoka.

Kumbuka pia kuwa vioo vingine ni vya mbinuko na kuwa vitu

vinavyoonekana kuwa karibu kuliko ilivyo katika hali ya kawaida.

Maeneo yaliyofichika. Pamoja na ukweli kuwa umevirekebisha vioo

vyako kiusahihi kuna

maeneo mengi karibu na

gari lako ambayo huwezi

kuyaona – haya huitwa

“maeneo fiche”. Maeneo

haya yako upande wa

nyuma kushoto na kulia

kwa gari nje ya eneo

linaloonekana kwa vioo

vyako. Wakati wowote

unapohitaji kubadili

uelekeo wa gari lako,

kwanza angalia vioo vyako na kisha haraka geuza kichwa chako

Page 24: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

20

kuangalia eneo fiche kwenye upande unaohitaji kwenda. Jizoeshe

kufanya hivi ili uweze kufanya haraka na bila taabu. Epuka kuendesha

kwenye maeneo fiche ya wengine – rudi nyuma polepole au endesha

mahali ambapo dereva mwingine anaweza kukuona kwa urahisi zaidi.

Kuwasha injini

Kabla ya kuwasha injini, hakikisha kuwa breki ya mkono imewekwa na

kuwa gari haliko kwenye gia – Angali kuwa wenzo uko kwenye

“KUEGESHA” (kwa otomatiki) au NYUTRO ( kwa manyu gia boksi). Pia

angalia kuwa hakuna aliyesimama mbele au nyuma ya gari. Weka

ufunguo kwenye swichi ya kuwashia na iwashe (mahali penye ON) –

dashibodi itaanza kufanya kazi. Zungusha ufunguo wa kuwashia mahali

pa kuwashia na sikiliza sauti ya injini – mara ukishasikia injini imeanza

kuunguruma achia swichi (angalia Kitabu cha Mwongozo kwa ushauri

wowote maalumu wa kutumia pedeli ya kichapuzi wakati wa kuwasha).

Iwapo una gari lenye injini ya dizeli lazima usubiri taa ya indiketa ya

PLAGI INAYONG’AA (kwa kawaida ni ya rangi ya chungwa) lazima kabla

ya kunyonga ufunguo kutoka ON, hadi START.

Kamwe usiendelee na stata kwa zaidi ya sekunde 10 – iwapo injini

haitawaka, achia swichi na subiri kwa dakika 5 hadi, 10, kisha jaribu

tena.

Wakati injini inafanya kazi angalia taa za indiketa na vipimia. Vionyeshe

kuwa kila kitu kiko sawa.

Iwapo umekuwa ukijaribu kuwasha injini ya petroli kwa muda fulani,

huenda labda ukawa umeijaza injini petroli. Iwapo hili litatokea kanyaga

pedeli ya kichapuzi hadi chini na acha hapohapo wakati unazungusha

swichi ya kuwashia ili kuwasha (START). Jaribu tena kama haifanyikazi

kama mwanzo. Mara injini itakapowaka, achia pedeli ya kichapuzi

haraka.

Angalia Kitabu cha Mwongozo kwa maelezo zaidi ya namna ya kutatua

tatizo la ugumu wakati wa kuwasha.

Page 25: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

21

Kunyonga

Mwazoni ni changamoto kufanya vitendo vichache mfano kupinda, na hili

litahitaji umakini wako mkubwa. Kwa kufanya mazoezi na baada ya

muda, utakuwa na uwezo wa kuliongoza gari kirahisi na kwa kujiamini.

Kuzungusha usukani kulia hulifanya gari lako lipinde kulia na kuzungusha

usukani kushoto hulifanya gari lako kupinda kushoto.

Usijaribu kupinda usukani wakati gari limesimama, kwani hii husababisha

kuharibika mapema kwa matairi na mfumo wa usukani. Daima gari liwe

kwenye mwendo, hata kama ni polepole, wakati

unanyonga usukani shika usukani kama

inavyoonyeshwa

kwenye kielelezo –

Iwapo utauchukulia

usukani kama saa,

mikono yako itakuwa

kwenye saa 3.15 au

4.10.

Iwapo utaanza kwenye sehemu ya kawaida ya

kuendeshea na unataka kukata kona kali

kushoto, anza kwa kushika juu ya usukani kwa

mkono wako wa kushoto na kuvuta chini. Kisha

shika chini ya usukani kwa mkono wako wa kulia

na kupeleka juu. Shika juu ya usukani kwa

mkono wa kushoto tena na kusukuma chini.

Iwapo kona ni kali sana unaweza kurudia

kusukuma huku kwa mkono wako wa kulia na

kusukuma kwa mkono wako wa kushoto mara nyingi.

Unapotaka kwenda moja kwa moja tena unaweza kunyonga usukani

nyuma kwa mikono kwa kutumia njia ileile kwa kurudisha tofauti na

mwanzo (kuvuta kwa mkono wa kulia na kuvuta kwa kushoto). Hata

hivyo, wakati unaendesha kwa kasi ya kawaida ni rahisi kuuacha usukani

kuzunguka kurudi upande ulikotoka kwenye mikono yako wakati

unaendesha polepole. Uwe tayari kuushika usukani tena kurekebisha

mwelekeo wa mwisho wa gari.

Kamwe usipinde usukani sana wakati unaendesha kwa mwendo mkali –

gari linaweza kuteleza au kupinduka.

Page 26: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

22

Kuondoka

Baada ya kuwa umewasha injini kwenye gari kwa kutumia gia boksi ya

manyu, kanyaga klachi, na ingiza gia ya kwanza. Kisha achia breki ya

mkono. Taratibu achia pedeli ya klachi mpaka sauti ya injini

itakapobadilika wakati gari linajaribu kuondoka – tumia nguvu kidogo

kwenye kichapuzi, na kisha polepole achia pedeli ya Klachi wakati huo

huo ukianza kukanyaga kwa nguvu kichapuzi. Gari litaanza kwenda, na

kadiri nishati zaidi inapopelekwa kwenye magurudumu mwendo

utaongezeka taratibu. Baadaye itakulazimu kubadili kuwa gia ya pili.

Kuondoka wakati gari lako limesimama juu ya kilima, tumia breki

ya mkono. Kanyaga pedeli ya klachi, ingiza gia ya kwanza, na kanyaga

kidogo kwenye kichapuzi. Kisha polepole achia klachi hadi utakaposikia

sauti ya injini inabadilika – ukiachia breki ya mkono gari litasimama na

kutulia – na, iwapo utakanyaga kichapuzi kidogo zaidi na polepole

ukaachia klachi moja kwa moja, gari litaanza kupanda kwenda mbele juu

ya kilima.

Kwa gari la mfumo wa otomatiki, kanyaga pedeli ya breki na hamisha

mahali pa kichaguzi kutoka kuegesha kwenda kuendesha. Kisha kanyaga

kichapuzi kidogo, achia breki ya mkono na kisha pedeli ya breki – gari

litaanza kupanda kwenda mbele. Taratibu za kuanza kilimani ni sawa na

giaboksi ya mkono, isipokuwa unaachia pedeli ya breki badala ya klachi.

Kubadili gia

Maelekezo haya yametumika tu unapokuwa unatumia giaboksi ya

manyu. Kubadili gia bila shida inaweza ikakuchukua muda mrefu

kujifunza.

Kubadili gia (juu). Ili kuongeza mwendo wa gari bila ya kuongeza zaidi

mzunguko wa injini unahitaji kubadili gia. Isikilize injini na usikie wakati

inaanza kuzunguka zaidi; huu ni wakati wa kubadili gia. Hatua ni:

• Kanyaga pedeli ya klachi chini wakati unaachia kichapuzi - klachi

ikanyagwe kwa kiasi cha sekunde kabla ya kuachia kichapuzi (siri ya

kwanza ya kubadilisha gia vizuri).

• Sogeza sehemu ya gia kutoka ilipo hadi kwenye gia mpya (mwanzoni

wakati wa mafunzo hili hasa litahusisha kutoka gia ya kwanza kwenda

ya pili – kupitia nyutro)- usilazimishe mahali pa gia – uweze

kuhamisha taratibu kwenda mahali papya kwa nguvu za wastani.

Page 27: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

23

• Iache pedeli ya klachi ipande polepole, na wakati huohuo (au muda

mfupi baadaye) polepole kanyaga pedeli ya kichapuzi kwenda chini

(siri ya pili ya ubadilishaji gia vizuri).

Kubadili gia (chini)

• Achia kichapuzi na funga breki, hadi gari liende kwa mwendo

unaotakiwa

• Kanyaga klachi

• Peleka wenzo wa gia panapotakiwa gea ya chini

• Achia klachi polepole na ongeza moto kwenye kichapuzi.

Unaweza kurekebisha mwendo wako vizuri kwa kutumia moto wa

wastani kwenye kichapuzi na kusukuma klachi kiasi cha kutosha

kuachanisha kidogo injini. Njia hii ni nzuri wakati unataka kwenda

mwendo mdogo, mfano wakati unaegesha au kuendesha kwenye foleni.

Usiitumie mara kwa mara kwani utaharibu haraka klachi.

Kumbuka kuwa gari lazima lisimame kabisa kabla ya kuweka gia ya

kurudi nyuma.

Kuendelea kulidhibiti gari

Lazima daima ulidhibiti vilivyo gari. Kuwa makini na mwendo wako na

urekebishe kuendana na barabara na hali ya magari ilivyo mbele yako.

Uwe na tahadhari na tabiri kila ambacho wengine watafanya, ili

usilazimike kufunga breki ghafla au kukwepa ili kuepuka kugongana.

Iwapo utaona hatari mbele yako, mfano kona kali, punguza mwendo

kabla ya kupinda, na kisha endesha polepole kupita hapo – hili

litakuwezesha kulidhibiti gari vizuri kadiri ya mwelekeo wa gari.

Kamwe usiendeshe gari kwa gia ya nyutro au klachi ikiwa imekanyagwa.

Kwa hakika hupunguza udhibiti ulionao wa gari – iwapo unashuka

kilimani, gari litaongeza mwendo haraka na utatumia breki mara nyingi

kuendelea kulidhibiti gari. Kabla ya kushuka kilima kikali, chagua gia ya

chini, ili injini iweze kukusaidia kulizuia gari kwenda mwendo wa kasi

zaidi.

Kuwa makini zaidi kwenye barabara zisizo na lami, kwani matairi yako

yatakuwa yakikamata barabara kidogo, na kukufanya uwe na uwezekano

mkubwa wa kuteleza ikiwa utajaribu kwenda kwa kasi. Mwendo wako

uwe chini ya km 80kwa saa na nyonga usukani taratibu.

Page 28: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

24

Kufunga breki

Iwapo unataka kupunguza mwendo wako fanya taratibu, ondoa mguu

wako kwenye kichapuzi. Hii itakufanya upunguze kasi yako. Wakati

unataka kupunguza mwendo haraka funga breki. Wakati mwendo

unapungua unatakiwa urudi kwenye gia za chini.

Umbali unaohitajika kusimamisha gari hutegemea hasa mwendo gani

unaokwenda – angalia kielelezo. Tambua kuwa kadiri unavyoongeza kasi

yako mara dufu umbali wako wa kusimama huongezeka mara tatu.

Iwapo unaendesha kwenye majimaji au barabara isiyo na lami matairi

yako yatakuwa na mgandamizo mdogo, hivyo umbali wako wa kusimama

unaweza kuwa mara mbili ya umbali ulioonyeshwa hapa. Iwapo gari lako

limejaza litakwenda pia mbali kabla ya kusimama. Kumbuka pia kuwa

magari makubwa na pikipiki daima huchukua muda kusimama kuliko

magari madogo.

Wakati unajua kuwa utasimama, punguza mwendo polepole.

Usisubiri hadi mwisho kufunga breki. Kanyaga pedeli ya breki polepole

kwanza na kisha kwa nguvu zaidi wakati umeanza kusimama. Achia

moto kabla ya gari kusimama, ili usimame bila taabu na vizuri. Kanyaga

pedeli ya klachi kabla ya kwenda kusimama, ili injini isishindwe

kuendelea. Iwapo utafunga breki kwa nguvu matairi yatajibana

(yataacha kuzunguka) na kuteleza kwenye ardhi – utashindwa kuudhibiti

usukani na umbali wako wa kusimama utaongezeka. Iwapo utateleza,

nyonga kwenye mwelekeo ambao sehemu ya nyuma ya gari inaelekea

na ondoa mguu wako kwenye pedeli ya breki hadi utakapolidhibiti tena

gari.

Iwapo utasimama ghafla (usimamaji wa dharura) Kanyaga pedeli

za breki kwa nguvu (lakini si nguvu sana kiasi cha kuyazuia matairi) na

wakati huohuo kanyaga klachi. Kitendo hiki hufanya injini izizuie breki,

na husaidia kuyazuia matairi kutokwenda. Pia hujirahisisha kwenye injini.

Page 29: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

25

Kurudi nyuma

Kurudi nyuma ni hatari zaidi ya kwenda mbele, hivyo usirudi nyuma zaidi

ya inavyotakiwa. Wakati unataka kurudi nyuma kwanza ingiza gia ya

kurudi nyuma – kamwe usifanye hivi mpaka gari lisimame kabisa. Kisha

weka mkono wako wa kulia kwenye usukani mahali ambapo ni sawa na

saa 6 kamili kwenye saa na geuza kichwa chako na sehemu ya juu ya

mwili wako kushoto. Hili litakuwezesha kuangalia kupitia begani kwako

na kupitia kwenye dirisha la mwisho-angalia kielelezo. Endesha polepole

wakati unarudi nyuma. Ikibidi dhibiti mwendo wako kwa kukanyaga

vizuri pedeli ya klachi.

Kabla ya kuanza kurudi nyuma lazima

uhakikishe kuwa hakuna mtu – labda

Umbali Halisi wa Kusimama

km 30 kwa saa

mita 12 au urefu wa magari 3

km 50 kwa saa

km 80 kwa saa

km 100 kwa saa

mita 23au urefu wa magari 6

mita 53au urefa wa magari 13

mita 73au urefu wa magari 18

Umbali wa kufikiria

Wastani wa urefu wa gari = mita 4

Umbali wa kufunga breki

Page 30: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

26

mtoto - aliyejificha kwenye eneo fiche. Angalia kwenye mwelekeo wako

lakini angalia pia pande nyingine. Ni vizuri kumpata mtu kusimama

nyuma ya gari kukuongoza. Hili ni muhimu hasa kama unaendesha gari

la mizigo au gari lolote ambalo kuna ugumu dereva kuona eneo la nyuma

ya gari.

Kumbuka kuwa, kama unapinda wakati unarudi nyuma, sehemu ya

mbele ya gari itakwenda upande tofauti wa mwelekeo. Kuwa makini

kuona kuwa sehemu ya mbele haigongi kitu chochote wakati wa kupinda.

Kuliacha gari

Pindi gari lako likisimama weka breki ya mkono. Kwa gari lenye mfumo

wa otomatiki sogeza wenzo wa kichaguzi kwenye kuegesha. Kwa gari la

giaboksi ya manyu peleka wenzo wa gia kwenye nyutro (madereva

wengine hupenda kuyaacha magari yao kwenye gia ya kwanza au ya

kurudi nyuma). Kisha zima injini yako.

Zima taa zote, vifuasi, kiyoyozi n.k. na funga madirisha. Zungusha

funguo za kuwashia kwenye sehemu ya kuzimia na kutoa funguo.

Angalia kupitia bega lako la kulia na iwapo hakuna gari linalokuja, fungua

mlango na kutoka nje. Hakikisha unalifunga gari. Tembea kupitia upande

wa nyuma wa gari unaoangalia barabara na kisha vuka barabara.

Waeleze abiria wako kushuka kwenye gari kwa upande wa kushoto

ambako kuna uwezekano mdogo wa wao kugongwa na magari

yanayopita.

Page 31: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

27

Uendeshaji salama barabarani Kuendesha barabarani

Endesha kwa usalama. Sheria inasema USIENDESHE kwa hatari au

kwa uzembe. Hii huelezwa kama tabia ambayo dereva mwenye ujuzi

ataichukulia kama hatari – mfano kulipita gari jingine mahali ambapo

pana kona kali kiasi kuwa huwezi kuona vizuri mbele.

Endesha kwa makini. Sheria inasema USIENDESHE bila kujali. Lazima

uwe macho na uchukue tahadhari wakati wote. Ni kutokuwa makini

kuruhusu kusumbuliwa wakati unaendesha au kutoangalia vizuri kuona

kama barabara haina kikwazo kabla ya kuiingia.

Wathamini wengine. Usiendeshe kama vile uko kwenye mashindano

na madereva wengine. Endesha kwa utulivu na kuwa mvumilivu iwapo

wengine watafanya makosa. Usiyaruhusu magari madogo kutoka kwenye

njia yako.

Kuwa mwangalifu – usisumbuliwe. Epuka kuzungumza au kubishana

na abiria. Usile, usinywe, usisome au kuvuta sigara wakati unaendesha –

hata kama una kifaa cha kuifanya mikono isiwe na kazi. Tafuta sehemu

nzuri usimame, na kisha tumia simu yako.

Endelea kutazama

sehemu zote. Usiangalie

sehemu moja kwa zaidi ya

sekunde 2 – endelea

kuhamisha macho yako

sehemu zote kuhakikisha

kuwa hukosi kuona kitu

chochote – angalia mbele

zaidi na kushoto na kulia –

na kila sekunde 5 angalia

kwenye vioo vyako, hata

kama unadhani hakuna magari karibu.

Jifunze Uendeshaji wa Kujihami. Angalia nje kwa uwezekano wa

matatizo mbele, mfano mtoto anayecheza mpira, au gari linakuja kwa

kasi pembeni mwa barabara. Iwapo kuna gari pembeni mwa barabara

lenye dereva ndani, tegemea litaingia mbele yako ghafla. Iwapo basi

Page 32: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

28

limesimama mbele yako, jitayarishe kwa abiria kuvuka barabara kutoka

nyuma yake. Iwapo utaona uwezekano wa tatizo kama hili punguza

mwendo na jiandae kuchukua hatua kuepuka kugongana.

Tumia ishara kuwaonya na kuwaarifu watumiaji wengine wa

barabara. TUMIA viashiria vya

mwelekeo au ishara ya mkono kabla

ya kubadili mwendo au mwelekeo,

kusimama au kuondoka. Toa ishara

inayoeleweka kwa muda wa kutosha

(sekunde 5-10 kabla ya kitendo), na

kumbuka kuacha baada ya kutenda

kitendo.

Tumia honi tu iwapo ni lazima

uwaonye watumiaji wengine wa

barabara kuwa uko pale. Iwapo

madereva watatumia honi kupita

kiasi, watumiaji wa barabara

hawatasikiliza. Usitumie honi

“kusalimia” au kuonyesha

umekasirishwa na mtu, au kumueleza

dereva aliye mbele kuharakisha na

kuongeza mwendo. Usitumie honi nje

ya hospitali, mahakamani na shuleni,

au kati ya saa 5 usiku na saa 12

asubuhi mjini. Epuka kutumia honi

kwenye Hifadhi za Taifa na Mbuga za

Wanyama.

Washa taa zako tu pale utakapotaka

kuwajulisha watumiaji wengine wa

barabara kuwepo kwako, katika

mazingira ambayo honi inaweza kutosikika au mjini wakati wa usiku.

Usiwashe taa zako ghafla kuonyesha kuwa umekasirika au kujaribu au

kuomba haki ya njia. Iwapo dereva mwingine atakuwashia taa ghafla,

usiichukulie kuwa ni ishara ya kukuruhusu kupita.

Fuata alama za barabarani. LAZIMA ufuate alama zote za barabarani,

na ishara na michoro ya barabarani. Hakikisha kuwa unajua na kutenda

kulingana na alama na michoro yote mingine ya barabarani. (Angalia

Ishara kwa watumiaji wengine wa barabara

Kupinda kulia

Kupinda kushoto

Kupunguza mwendo

Page 33: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

29

Kanuni za Barabara kwa ufahamu zaidi wa alama za barabarani) LAZIMA

pia ufuate ishara zinazotolewa na maofisa wenye sare za polisi na watu

wengine wenye mamlaka. Ishara zao zinazidi alama na michoro yote

mingine.

SIMAMA Askari wa barabarani

anayeashiria mbele na nyuma

Alama za maofisi wa Polisi au watu wengine wenye mamlaka

SIMAMA Askari wa barabarani

anayeashiria kwa mbele

SIMAMA Askari wa barabarani

anayeashiria kwa upande mmoja

PITA PITA

SIMAMA Askari wa barabarani

anayeashiria kwa nyuma

Page 34: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

30

Kuondoka. Kabla ya kuondoka, daima tumia vioo vyako, toa ishara na

tazama nyuma ya mabega yako kuona kuwa barabara haina kikwazo.

Ondoka iwapo umejiridhisha kuwa ni salama kufanya hivyo.

Pita kushoto. LAZIMA uendeshe upande wa kushoto wa barabara.

Vyombo vinavyokwenda polepole (baiskeli, mikokoteni inayokokotwa na

ng’ombe kwa mikono na matrekta, n.k.) lazima vipite upande wa

kushoto na kuruhusu magari yaendayo kasi kuvipita.

USIENDESHE kwenye njia ya watembea kwa miguu au maeneo ya

watembea kwa miguu.

Vioo – alama – kitendo. Tumia vioo vyako daima ili wakati wote ujue

kilichoko nyuma na pembeni yako. Tumia vioo vyako vizuri kabla ya

kupinda au kubadili njia, na kisha toa ishara ifaayo.

Waendesha pikipiki wanashauriwa kuangalia nyuma yao kabla ya kubadili

njia na kupinda kulia.

Chunguza katika kioo,

pima, amua

Toa ishara sahihi

Fanya tendo

Page 35: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

31

Usiweke msururu wa magari nyuma yako. USIENDESHE taratibu bila

sababu. Iwapo unaendesha gari kubwa au linalokwenda polepole na kuna

foleni ya magari nyuma yako, LAZIMA utafute sehemu ya kuingilia kwa

usalama na ruhusu magari mengine yakupite.

Foleni ya magari. Iwapo kuna msururu wa magari mbele, ingia nyuma

yake. Usiuruke msururu huo. Kuwa mvumilivu. Daima simamisha gari

lako ili uweze kuyaona matairi ya nyuma ya gari la mbele – linaweza

kurudi nyuma kidogo wakati linaanza kuondoka. Iwapo utafika kwenye

alama za pundamilia wakati uko kwenye foleni, usisimame juu ya alama

hizo za kuvukia– ziache wazi ili watembea kwa miguu wazitumie.

Endesha kwenye njia. Pale penye njia zaidi ya moja zenye mwelekeo

mmoja, tumia njia ya kushoto kwenda mbele na nyingine kwa ajili ya

kuvipita vyombo vingine, kupinda kulia, au kuyapita magari

yaliyosimama. Usibaki kwenye njia ya kulia muda mrefu zaidi ya

unaohitajika. Wakati wa kubadili njia kumbuka vioo – ishara - kitendo.

Mwendo

Endesha kwa mwendo salama. USIENDESHE kwa mwendo ambao

unaweza kuwa wa hatari kwa wengine. Daima rekebisha mwendo wako

kulingana na mazingira. Kwa mfano, punguza mwendo kama unakaribia

kona, daraja jembamba, au makutano, au eneo lenye watembea kwa

miguu wengi. Chagua gia itakayokuwezesha kulidhibiti gari zaidi.

Endesha polepole zaidi iwapo barabara ina majimaji, au huwezi kuona

vizuri. Endesha polepole zaidi usiku, kwa kuwa ni vigumu kuwaona

watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wanyama, na magari

yaliyoegeshwa au kuharibika.

Kuendesha kwenye barabara zisizo na lami. Daima endesha

polepole zaidi kwenye barabara zisizo na lami, nyonga usukani polepole,

na epuka kufunga breki kwa nguvu. Barabara zisizo na lami zina ardhi

inayoteleza zaidi ya zenye lami, na matairi yako yana pungufu ya

asilimia 50 ya kiwango cha ubanaji.

Endesha katika namna ya kusimama wakati wote kuepuka

kugonga kitu chochote. Endesha katika mwendo utakaokuruhusu

kusimama vizuri katika umbali unaouona kukufaa. Usiendeshe kwa kasi

kwenye kona au juu ya kilele cha mlima – itakuwaje iwapo gari

litaharibika mahali ambapo huoni vizuri?

Page 36: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

32

Kumbuka kuwa, ukiongeza maradufu mwendo wako, umbali wako wa

kusimama unaongezeka mara tatu – angalia mchoro. Umbali wa

kusimama utakuwa mrefu zaidi ya huu kwenye barabara zenye majimaji

zisizo na lami. Magari makubwa na pikipiki daima huchukua muda mrefu

kusimama kuliko magari madogo.

Kama sheria/kanuni ya jumla daima acha pengo la sekunde – 2 kati ya

gari lako na lililo mbele yako. Moja ya njia inayotumika kupima pengo hili

wakati wa kuendesha ni kuhesabu “elfu moja na moja, elifu moja na

mbili” wakati gari lililo mbele yako litakapopita sehemu iliyowekwa.

Iwapo utapita mahali palipowekwa kabla ya kumaliza hesabu yako, uko

karibu mno.

Fuata ukomo wa mwendo. USIPITISHE mwendo wa kiwango cha juu

kilichoruhusiwa cha gari lako. Kwa sasa ukomo wa kisheria ni:

Km 50 kwa saa kwa magari yote kwenye maeneo ya makazi (hata

kama hakuna alama ya barabarani)

Km 80 kwa saa kwa magari makubwa ya mizigo (> uzito halisi wa gari

wa kg 3500) na magari ya huduma za umma (mabasi, mabasi ya safari

ndefu, lakini si teksi) nje ya maeneo ya makazi

Km 100 kwa saa ni mwendo unaoshauriwa wa juu kwa magari madogo

na magari mengine ya wastani nje ya eneo la makazi.

Ukomo huu wa mwendo unaweza kutofautiana kwa mwendo wa vijijini

unaoonyeshwa na alama za udhibiti za barabarani. USIZIDISHE mwendo

wa mwisho wa juu zaidi unaoonyeshwa kwenye alama. Kumbuka kuwa

ukomo wa mwendo haumaanishi kuwa daima itakuwa salama

kuendesha katika mwendo huo. Lazima uendeshe katika mwendo

ambao ni salama kwa barabara hiyo, vyombo vingine vya usafiri na hali

ya hewa.

Kulipita gari jingine

Kabla ya kulipita gari jingine LAZIMA uhakikishe kuwa:

• barabara haina vikwazo vyovyote

• gari lililo nyuma halijaanza kulipita gari lako

• gari la mbele halijaanza kulipita gari jingine

• kuna upenyo mkubwa wa kutosha mbele ya gari unalotaka kulipita

Page 37: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

33

Usilipite gari jingine isipokuwa kama una uhakika unaweza kufanya hivyo

bila ya kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa barabara au kwako

mwenyewe. Iwapo una mashaka usilipite gari jingine.

Usilipite gari linalotembea au lililoegeshwa:

• iwapo gari linakaribia kutoka upande mwingine – isipokuwa kama una

uhakika unaweza kufanya hivyo bila ya kulilazimisha gari hilo

kupunguza mwendo au kupinda ghafla ili kukuepuka

• pale gari linalohitajika kupitwa linaashiria kupinda kulia

• pale ambapo huwezi kuona umbali wa kutosha mbele, mfano kwenye

kona au karibu ya kilele cha kilima

• kwenye makutano

• kwenye alama za pundamilia au karibu na alama hizo au mahali

pengine wanapovuka watembea kwa miguu

• kwenye reli au karibu na reli

• ambapo unatakiwa kuingia kwenye njia iliyo maalum kwa mabasi au

waendesha baiskeli

• ambapo unatakiwa kupita kwenye eneo lenye mistari ya mshazari au

ya umbo la V

• ambapo kulipita gari jingine hakuruhusiwi kwa alama ya “Hakuna

kulipita gari jingine” au michoro ya barabarani.

Michoro ya barabarani ambayo inakuonyesha mahali ambapo

unaweza kulipita gari jingine. Iwapo mstari mweupe wa katikati ya

barabara unachorwa kwa kukatikakatika (----) unaweza kuvuka ili

kulipita gari jingine, kama ni salama kufanya hivyo. Iwapo mstari

mweupe wa katikati ya barabara haujakatikakatika ( ____ ), USIVUKE

mstari huo, isipokuwa kama ni muhimu kulipita gari lililosimama au

kupinda kwenye barabara ya upande mwingine. Pale ambapo pana

mistari miwili mstari ulio karibu na wewe ndio utakaoutumia.

USIVUKE mstari

wa katikati

USIVUKE mstari

wa katikati

Unaweza kuvuka

mstari wa katikati

kama ni salama

kufanya hivyo

Page 38: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

34

Sehemu zisizo salama kulipita gari jingine

Alama za pundamilia

Karibu na kilele cha

kilima

Kwenye kona isiyo na michiro

ya kuruhusu kulipita gari

jingine

Mahali reli inapokatisha

barabara

Kwenya kona kali

Karibu na

makutano

Page 39: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

35

Utaratibu wa msingi wa kulipita gari jingine. Kabla hujaanza kulipita

gari hakikisha kuwa barabara haina vikwazo mbele kukuwezesha kulipita

gari na kurudi kushoto bila ya

kulilazimisha gari jingine

kupunguza mwendo au kupinda

haraka ili kukukwepa.

Kama una shaka – usilipite gari

jingine. Tumia vioo vyako

kuona kuwa hakuna gari

linalokupita. Toa ishara kabla

ya kuanza kutoka [1]. Kuwa

mwangalifu zaidi usiku na

kwenye ukungu au mvua kubwa

wakati inapokuwa vigumu

kuamua kuhusu mwendo na

umbali. Kumbuka: vioo -

ishara - kitendo

Iwapo huna hakika na kile

ambacho dereva wa gari la

mbele atafanya, piga honi.

Unapokuwa umeanza kulipita

gari jingine, [2] nenda haraka

kulipita gari hilo na liache kwa

umbali fulani. Unapozipita

baiskeli au pikipiki vipatie

angalau umbali zaidi kuliko ule wa gari. Rudi upande wa kushoto wa

barabara haraka iwezekanavyo, [3] lakini usirudi haraka kiasi kuwa gari

unalolipita kulazimika kufunga breki au kupinda haraka ili kukukwepa.

Fanya hivi kwa kuliangalia gari kwenye kioo chako.

Iwapo gari lingine litakuwa linakupita. Usiongeze mwendo wako

unapokuwa unapitwa. Sogea kushoto kama unaweza kufanya hivyo kwa

usalama. Punguza mwendo ikibidi kuliacha gari linalokupita lipite haraka

na kwa usalama.

Lipite gari lingine upande wa kulia. Daima lipite gari jingine upande

wa kulia, isipokuwa kama:

Page 40: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

36

• gari la mbele yako linaonyesha ishara ya kupinda kulia, na kuna nafasi

ya kulipita kwa usalama kushoto (usiendeshe kwenye njia ya waendao

kwa miguu)

• magari yanakwenda polepole kwenye njia, na magari kwenye njia ya

kulia yanakwenda polepole zaidi yako.

Pale wengine watakapokuashiria upite. Wakati mwingine dereva wa

gari la mbele yako anaweza kukuashiria kuwa barabara haina vikwazo

kwako kupita. Usidhani kuwa dereva yuko sahihi. Lipite gari hilo tu pale

utakapoona kuwa barabara haina kikwazo chochote.

Iwapo gari unalolipita litaongeza mwendo au kuonyesha kukataa

kwa namna yoyote, acha kujaribu kulipita. Usishindane kamwe na dereva

mwingine.

Makutano

Kukaribia makutano ya barabara. Kugongana kwingi hutokea kwenye

makutano, hivyo chukua tahadhari zaidi. Angalia makutano yaliyo mbele

yako, na fikiria hatua ipi ya kuchukua, iwapo utatakiwa kufanya hivyo.

Hakikisha kuwa gari lako liko mahali sahihi kwa hatua unayotaka

kuichukua na kuwa unaendesha kwa mwendo unaofaa.

Kaa kwenye njia au mahali

sahihi. Iwapo barabara itakuwa na

alama za njia, ingia kwenye njia sahihi

kwa wakati mzuri. Fuata mishale

inayoonyesha njia ipi ni ya mwelekeo

upi. Usibadili njia bila sababu ya msingi.

Iwapo kuna foleni ya magari mbele yako,

usijaribu kuivuka foleni hiyo – kuwa

mvumilivu.

Fuata kanuni za kipaumbele. Kwenye

makutano yenye alama ya “SIMAMA” (pia itakuwa na mstari mweupe

usiokatikakatika wa “SIMAMA” kukata barabara) LAZIMA usimame kabisa

kwenye mstari huo. Angalia kwa makini kuona kama kuna gari lolote

linalokuja. Subiri upate upenyo salama kabla ya kupita.

Kwenye makutano yenye alama au mchoro wa “KURUHUSU” (mstari

mweupe uliokatikatika kukata barabara) LAZIMA uyaruhusu magari ya

Usiivuke

foleni

Page 41: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

37

kwenye barabara nyingine. Subiri upate upenyo salama, kabla ya kupita

– usiyalazimishe magari mengine kupunguza mwendo haraka au

kukukwepa ghafla.

Pale ambapo hakuna alama na mchoro wowote, daima kumbuka

kuyaruhusu magari yanayotoka kulia.

Haki za msingi za njia

Angalia vizuri. Usitupe macho tu kuona kama kuna kitu kinakuja –

angalia vizuri – angalia waendesha pikipiki na baiskeli. Iwapo utatumia

zaidi ya sekunde 2 kuangalia mwelekeo mmoja, kisha lazima uangalie

tena mwelekeo mwingine kuona kama bado hakuna vikwazo.

Pale ambapo una haki ya kupita, nenda mbele kwa tahadhari na uwe

tayari ikibidi kupunguza mwendo na kusimama kuepuka kugongana.

Usiingie kwenye makutano mpaka njia iwe salama. Usisababishe

msongamano bila sababu. Subiri na ruhusu magari mengine yapite

SIMAMA

RUHUSU GARI LIPITE

Simamana subiri

Simamana subiri

Page 42: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

38

mbele yako. Kama madereva watakuwa wavumilivu na kutumia maarifa

yao ya kawaida, kila mmoja atafika anakokwenda kwa haraka zaidi.

Kupinda kulia

1. Hakikisha usalama kabla ya kupinda kulia, tumia vioo vyako kuona

kuwa magari yaliyo nyuma yako yapo umbali salama

2. Onyesha ishara ya kupinda kulia na anza kwenda polepole

3. Nenda kwenye sehemu ya kushoto ya katikati ya barabara

4. Mara tu panapokuwa na upenyo salama wa magari yanayokuja

mbele yako pinda kulia-usipite njia ya mkato.

Angalia waendesha baiskeli, pikipiki watembea kwa miguu – iwapo kuna

watembea kwa miguu wanaovuka barabara kwenye sehemu unayoelekea

kupinda, lazima usimame na kuwaacha wapite.

Waangalie watumiaji wengine wa barabara, hususan waendesha

pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu, na wajulishe kile unachotaka

kufanya kwa kuonyesha ishara vizuri.

Yaruhusu magari marefu kupinda. Yanaweza kutumia upana wote wa

barabara ili kupinda.

Page 43: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

39

Kupinda kushoto

1. Hakikisha usalama kabla ya kupinda kushoto, tumia vioo vyako

kuona kuwa hakuna gari linalokuja nyuma yako upande wa kushoto

2. Onyesha ishara ya kupinda kushoto na anza kwenda polepole

3. Kama barabara haina vikwazo pinda huku ukiwa karibu na ukingo wa

upande wa kushoto wa barabara (madereva wa magari marefu

wanaweza kuhitaji kwenda katikati ya barabara ili kuweza kupinda).

Kuwa makini na waendesha baiskeli na pikipiki ambao wanaweza

kutokea kwa upande wako wa kushoto - waache wakupite na angalia

usalama kabla ya kupinda. Kuwa makini na watembea kwa miguu -

iwapo kuna watembea kwa miguu wanaovuka barabara upande

unaopindia, lazima usimame na kuwaacha wavuke.

KAMWE usilipite gari lingine na kisha kupinda kushoto mbele ya gari hilo.

Kupinda kwenye barabara mbili zinazokwenda upande mmoja.

Wakati unapita au unapinda kulia kwenye barabara mbili za upande

mmoja, angalia ili uone iwapo nafasi kati ya barabara hizo mbili (kati)

ina upana wa kutosha kumudu urefu wote wa gari lako. Iwapo hivyo

ndivyo, pita kwa usalama kwenda katikati na kisha subiri pale hadi

upatikane upenyo salama wa magari kwenye barabara ya pili. Iwapo

Angalia kwenye

kioo chako kuona kama pikipiki au

baiskeli zinakuja

upande wako wa

kushoto

Page 44: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

40

eneo la katikati halina upana wa kutosha, lazima usubiri hadi pale

utakapoweza kuvuka njia zote mbili kwa pamoja.

Kupinda kulia kwenye makutano ya barabara mbili wakati gari

linalokuja pia linapinda

kulia. Utaratibu wa

kawaida ni kupinda kulia

mbele ya gari jingine

(angalia kielelezo hapo

chini). Gari jingine

linaweza kukuziba kuona

magari yanayokuja, hivyo

endelea kwa tahadhari na

usipinde mpaka uwe na

uhakika kuwa njia iko

salama.

Fuata ishara ya taa za barabarani. LAZIMA usimame nyuma ya

mstari mweupe wa “SIMAMA” isipokuwa kama ishara ni ya kijani. Kama

taa za njano zitawaka unaweza kupita iwapo tu umeupita mstari wa

simama au uko karibu nao sana kiasi kuwa kusimama kunaweza

kusababisha kugongana. Elekea kwenye taa kwa mwendo ambao

utakuwezesha kusimama haraka iwapo taa zitabadilika kuwa njano.

Nenda mbele tu wakati taa za kijani zitakapowaka, iwapo njia yako haina

vikwazo, au unajiandaa kupinda kulia.

Iwapo taa za barabarani hazifanyi kazi, na hakuna ofisa wa polisi

anayeongoza magari, nenda mbele kwa makini, na toa kipaumbele kwa

magari yanayotoka kulia kwako.

Kuendesha kwa kujihami. Kwa mfano, wakati unasubiri kupinda

kwenda barabara kuu kutoka kwenye barabara za pembeni hakikisha

kuwa gari linalotoka kulia na kuashiria kwenda kushoto linaanza kupinda

kabla hujaendelea - ikiwa dereva mwingine hana lengo la kupinda

kushoto, lakini amesahau kuondoa ishara baada ya kupinda kwa

mwanzo.

Page 45: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

41

Ushauri maalumu kwa madereva kwenye sehemu zenye mzunguko

Kabla hujafika kwenye kiplefti hakikisha unapunguza mwendo wako,

amua ni njia ipi unahitaji kupitia, angalia kioo chako, na ingia kwenye

njia sahihi (angalia ushauri hapo chini) ukifika kwenye kiplefti yaruhusu

magari ambayo tayari yako kwenye mzunguko yapite. Angalia kwa

makini waendesha baiskeli na pikipiki, ambao inaweza kuwa vigumu

kuwaona iwapo kuna magari mengi. Kumbuka kuwa pia kunaweza kuwa

na watembea kwa miguu wanaovuka barabara - kutoka kushoto na pia

kulia.

Wakati unapinda kushoto:

1. Ashiria kupinda kushoto

2. Pita kwenye njia ya kushoto

3. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko

4. Pita kushoto kwenye mzunguko

5. Endelea sehemu ya kutokea, ukiwa bado unaendelea kuashiria

kushoto.

Wakati unakwenda mbele moja kwa moja:

1. Pita kwenye njia ya kushoto (isipokuwa kam njia ya kushoto

imeonyeshwa kwa ajili ya magari yanayopinda kushoto tu) –

usionyeshe ishara

2. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko yapite

3. Ungana na magari, yaliyo kwenye njia ya kushoto

Njia sahihi ya kuitumia kwenye mzunguko

Page 46: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

42

4. Onyesha ishara ya kwenda kushoto baada ya kupita njia ya kutokea

kabla ya ile unayohitaji

5. Endelea kwenye njia yako ya kutokea, ukiwa bado unaonyesha ishara

ya kwenda kushoto.

Wakati wa kupinda kulia au kuzunguka:

1. Onyesha ishara ya kwenda kulia

2. Pita kwenye njia ya kulia

3. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko

4. Jiunge na msururu, pita kulia

5. Endelea kuashiria kwenda kulia hadi upite barabara ya kwanza ya

kutokea kabla ya ile unayohitaji, kisha onyesha ishara ya kwenda

kushoto

6. Endelea sehemu ya kutokea.

KAMWE usisimame au kuegesha gari kwenye mzunguko. Wakati uko

kwenye mzunguko usilipite gari refu – linaweza kukugonga.

Uendeshaji wa usiku au kwenye hali mbaya ya hewa

Endesha kwa mwendo ambao utakuruhusu kusimama katika

umbali unaouona unafaa. Iwapo utashusha taa zako (yaani kuzifanya

zimulike chini), au kumulikwa na taa za magari yanayokuja lazima

upunguze mwendo – mbele gizani kunaweza kuwa na gari bovu au

mwendesha baiskeli.

LAZIMA utumie taa usiku (adhuhuri hadi alasiri) au mchana ambapo

ni vigumu kuona kwa sababu ya moshi, ukungu, mavunde au mvua

kubwa. Kwa mwongozo wa jumla washa taa zako unapokuwa huwezi

kuona vizuri kwa zaidi ya mita 100. Usichelewe kuziwasha-zinakufanya

uonekane zaidi kwa wengine.

Angalia taa zako za mbele kuwa ni safi, zinafanya kazi na

zimerekebishwa vizuri. Taa lazima ziwekwe kiusahihi ili zitoe mwanga

wa kawaida bila ya kuwaathiri madereva wengine - fundi wa magari

mwenye ujuzi anaweza kukusaidia kuangalia.

Tumia taa zinazomulika chini:

• Wakati magari yanakuja mbele yako

• Wakati unaendesha nyuma ya gari, au unalipita gari jingine

• Wakati unaendesha mijini ambako kuna mwanga wa kutosha mtaani.

Page 47: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

43

Usiwafanye watumiaji wengine wa barabaraa kutoona vizuri. Usiwashe

taa za mavunde au taa nyingine isipokuwa kama kuna mavunde sana au

ukungu.

Kurudi nyuma

USIRUDI nyuma zaidi ya inavyotakiwa.

Kabla ya kurudi nyuma hakikisha kuwa hakuna watembea kwa miguu au

vitu kwenye barabara nyuma yako-kumbuka kuwa watoto wadogo

wanaweza kuzibwa na sehemu ya nyuma ya gari. Rudi nyuma kwa

makini na kamwe isiwe zaidi ya inavyotakiwa. Kama hutaweza kuona

vizuri, mtafute mtu akuongoze. Mtu huyu pia anaweza kuwatahadharisha

watumiaji wengine wa barabara kupisha. Tumia taa za kurudia nyuma

kuwafanya wengine wajue wakati wa mchana, na kuona vizuri wakati wa

usiku. Usihangaike barabarani – liweke gari lako mbali kidogo na ukingo

wa barabara.

Kuwa makini hasa wakati unarudi nyuma ili utoke kwenye jengo, uzio,

kiwanja cha nyumba – ukuta au uzio unaweza kuwaziba watembea kwa

miguu ambao wanakaribia kupita sehemu ya kutokea gari. Ikiwezekana,

geuzia ndani, ili uweze kutoka nje kwa mbele.

Mulika taa zako chini kwa ajili ya gari linalokuja

Mulika taa zako chini wakati unalifuata gari jingine

Page 48: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

44

Usirudi nyuma

kamwe kwenye

barabara ndogo

pembeni mwa

barabara kuu. Usirudi

nyuma kamwe

kwenye makutano

makuu. Usirudi

nyuma kamwe

mahali wavukapo

watembea kwa

miguu, au mahali reli

inapokatisha

barabara.

Kuwajali watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara wanaoweza kuathirika

Kuwa makini na watembea kwa miguu. Watembea kwa miguu wako

katika hatari kubwa pindi wanapogongwa na magari. Na watembea kwa

miguu wengi, hususan wale wa maeneo ya vijijini, hawajazoea barabara

zenye magari na hawajui jinsi barabara ilivyo hatari. Endesha kwa makini

sana na punguza mwendo hadi km 50 kwa saa au chini ya hapo iwapo

kuna watembea kwa miguu mahali hapo, hususan katikati ya miji yenye

watu wengi, kwenye masoko na karibu na vituo vya mabasi. Kuwa

makini na watembea kwa miguu wanaovuka barabara ghafla kutoka

nyuma ya gari lililoegesha au kusimama (labda basi).

Page 49: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

45

Kuwa makini sana kama watoto wako karibu, na wakati unaendesha

karibu na shule. Usiwategemee watoto kutenda kama watu wazima.

Uwezo wao wa kuona na kusikia una ukomo na hawawezi kutambua

mwendo vizuri. Hawako makini, na wanapokuwa hatarini wanaweza

kusimama tuli kwa hofu, badala ya kuondoka mahali hapo. Mahali

ambapo pana watoto punguza mwendo na kuwa makini sana.

Wasaidie wazee na walemavu

pindi inapokuwa vigumu kwao

kuvuka barabara. Waache

wavuke kama ni salama

kufanya hivyo. Daima punguza

mwendo unapokuwa karibu na

shule na hospitali.

Iwapo kuna watembea kwa

miguu wanaovuka barabara

mahali ambapo unapinda

kuelekea huko, simama na kuwaacha wavuke mbele yako.

Alama za Pundamilia. Unapofika kwenye mahali pa kuvukia waenda

kwa miguu penye alama za mistari myeupe (“alama za pundamilia”) uwe

tayari kupunguza mwendo na kusimama kuwaacha watu wawavuke.

LAZIMA usimame kama mtu yeyote anavuka au anakaribia kuvuka.

USILIPITE gari lolote ambalo limesimama kuruhusu watembea kwa

miguu kuvuka. Na USIEGESHE gari lako kwenye kivuko cha waendao

kwa miguu – au ndani ya eneo la umbali wa mita 5 kutoka alama hizo.

Page 50: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

46

Ishara zinazoongoza kuvuka kwa watembea kwa miguu. Sehemu

nyingine za kuvukia zinaongozwa na taa za barabarani. Fuata ishara za

taa za barabarani. Watembea kwa miguu wanaweza kuvuka barabara

mbele yako, taa NYEKUNDU ikiwa inawaka.

Kuwa makini na wandesha pikipiki na baiskeli. Vyombo vyenye

magurudumu mawili ni vigumu zaidi kusimama ukilinganisha na magari

makubwa. Daima viangalie vyombo hivyo unapoingia na kutoka kwenye

makutano. Waachie nafasi ya kutosha waendesha pikipiki na baiskeli

wakati unawapita, hususan iwapo unaendesha gari refu au gari linalovuta

tela. Kamwe usiwapite na kupinda karibu mbele yao. Kadhalika wapite

kwa uangalifu waendesha mikokoteni.

Kurudi ulikotoka

Wakati mwingine utahitaji kurudi kwenye mwelekeo uliotokea. Mjini

fanya hivi kwa kupinda kushoto (au kulia) na kuzunguka mitaa hadi

urudi kwenye barabara uliyotoka – hili hukuepusha kurudi nyuma

ulikotoka. Pia unaweza kutumia mzunguko kwa usalama kubadili

mwelekeo. Pia unaweza kurudi ulikotoka kwa kutumia sehemu ya

kuegeshea au eneo la wazi ambapo unaweza kuzunguka kwa usalama

nje ya barabara yenye magari yanayopita.

Iwapo huwezi kufanya moja ya haya utatakiwa kupinda katika umbo la U

au kugeuza kwa kurudi nyuma. Iwapo barabara ni pana vya kutosha

unaweza kugeuza gari katika umbo la U, lakini zingatia kuwa kugeuza

kwa U aghalabu hukatazwa kwenye barabara pana na barabara mbili

(angalia alama za kudhibiti za barabarani) kwani huvuruga kasi ya

magari na si salama. Katika mazingira haya toka nje ya barabara kuu

kwenye upande wa barabara usio na magari mengi na geuza gari lako

kwenye barabara hiyo.

Iwapo utatakiwa kugeuza kwa

kurudi nyuma chagua mahali

ambapo unaweza kuona mbali

mbele na nyuma. Ikiwezekana

tumia upande wa kushoto

pembeni ya barabara, kisha

pinda kulia kubadili mwelekeo –

angalia kielelezo. Usifanye hivi

iwapo kuna magari mengi

Page 51: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

47

upande huo wa barabara – tafuta barabara isiyo na magari mengi.

Katika barabara isiyo na magari mengi unaweza kugeuza katika hatua

tatu. Anza kwa kuendesha upande wa kushoto sana. Kisha nyonga

usukani kulia kabisa na kuvuka barabara. Halafu, nyonga usukani

kushoto na kurudi nyuma upande mwingine wa barabara. Kumbuka

usinyonge usukani wakati gari limesimama. Kisha vuka na endesha

kwenye mwelekeo sahihi.

Ama utageuza kwa U au

kugeuza kwa kurudi nyuma,

kumbuka kuwa hiki ni

kitendo cha ujanja ambacho

kinapaswa kufanywa kwa

uangalifu mkubwa. Chagua

sehemu yako ya kugeuzia

kwa makini, tumia viashiria

vyako, na angalia magari

mengine.

Reli Inayokatisha

Kwenye reli inayokatisha bila vizuizi, ishara au mtu yeyote anayeongoza

magari, punguza mwendo kabla ya kuingia kwenye reli ili kuchunguza

kama magarimoshi yanakuja. Madereva wa mabasi, na magari

yanayobeba vitu vinavyoweza kuwaka moto, LAZIMA wasimame na

kuangalia kabla ya kuendelea. Sikiliza king’ora cha garimoshi. Kamwe

usishindane na magarimoshi – mara zote yana haki ya kupita. Hakikisha

ni salama kabla ya kuvuka, na uwe makini zaidi pale penye njia za reli

zaidi ya moja.

Pale ambapo reli inayokatisha inaongozwa na vizuizi, ishara au mtu

mwenye mamlaka hayo, LAZIMA uvifuate. Kamwe usijaribu kuongeza

mwendo ili upite haraka wakati vizuizi vinashushwa chini. Kamwe

usiondoke hadi alama za taa zinapozima na vizuizi vimefunguliwa kabisa.

Waache watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wapite kwanza.

Kamwe usiendeshe kwenye reli inayokatisha hadi pale barabara

itakapokuwa wazi upande mwingine, na usilikaribie sana gari la mbele

yako. Kamwe usisimame au kuegesha kwenye reli au karibu na reli.

Iwapo gari lako litaharibika kwenye reli, watu watoke ndani ya gari

Page 52: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

48

haraka na kukaa mbali na hatari. Mwarifu msimamizi wa reli, kama yupo,

na fuata maelekezo yake. Vinginevyo, piga simu polisi. Iwapo hakuna

garimoshi linalokuja omba msaada wa kulisukuma gari kutoka kwenye

reli. Iwapo utalisikia au kuliona garimoshi likija ondoka kwenye reli

haraka, jaribu kumuonya dereva wa garimoshi bila ya kujiweka hatarini.

Kuegesha

Wakati unataka kusimama au kuegesha, kumbuka vioo-ishara-

kitendo. Toka nje ya barabara ikiwezekana kwenda kwenye eneo

linalofaa kuegesha. Iwapo itakubidi usimame barabarani, simama karibu

kadiri iwezekanavyo na upande wa kushoto. Daima angalia iwapo ni

salama kuegesha gari na iwapo inaruhusiwa kuegesha mahali hapo.

Kabla ya wewe au abiria wako kufungua mlango, hakikisha hautamgonga

mtu yeyote anayepita barabarani au kwenye njia ya waendao kwa miguu

– angalia kwa makini waendesha baiskeli na pikipiki. Kumbuka kuwa ni

salama kushuka kwenye gari upande wa kushoto karibu na ukingo wa

barabara.

USIEGESHE gari:

• bila ya kujali na kuwafikiria wengine

• kwenye alama za pundamilia au mita 5 karibu na alama hizo

• mita 5 ndani ya makutano au mahali reli inapokatisha barabara

• kwenye kituo cha basi au mita 15 toka pande zote za alama ya “kituo

cha basi”

• kwenye njia ya waendao kwa miguu

• mbele ya sehemu ya kuingilia magari

• kwenye barabara yenye mistari myeupe miwili ya katikati, hata kama

moja ya mistari hiyo umekatikakatika

• ambapo haparuhusiwi kuegesha gari kwenye alama ya USIEGESHE

na/au mistari ya njano kwenye ukingo wa barabara.

Usiegeshe mahali popote ambapo itakuwa hatari au kusababisha

matatizo kwa watumiaji wengine wa barabara, kwa mfano:

• Karibu na geti la shule

• Karibu na kilele cha kilima

• Kwenye kona kali

• Upande mwingine wa gari lililoegeshwa (uegeshaji wa magari mawili)

• Mkabala na kizingwa

• Pale ambapo gari lako litakiziba kituo cha teksi

Page 53: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

49

• Pale ambapo gari lako litaziba alama au ishara ya barabarani.

Usiegeshe usiku kwenye barabara zenye magari mengi au mahali

ambapo magari yanakwenda kwa kasi. Iwapo huwezi kuepuka kufanya

hivi, washa taa za kuegeshea. Wakati wa usiku egesha upande wa

kushoto wa barabara tu.

Egesha gari lako kwa unadhifu, kwa uzuri na usalama. Unahitaji udhibtii

mzuri wa mwendo wako na usukani na pia uamuzi sahihi wa nafasi.

Chagua sehemu yako ya kuegesha kwa makini –

• kuna sehemu ya kutosha?

• ardhi inafaa – kuna vikwazo vyovyote?

• gari lako litakuwa salama?

Kumbuka daima kuendesha gari polepole wakati unanyoosha usukani –

usinyonge usukani wakati gari limesimama. Kunyonga usukani ili gari

lirudi nyuma huhitaji umakini, lakini usisahau kuangalia magari na

watembea kwa miguu nje. Kumbuka kuwa kadiri upande wa nyuma ya

gari lako unapopinda upande wa mbele utakwenda kwenye mwelekeo

mwingine. Tumia viashiria vyako kuwaeleza madereva wengine

unachokifanya.

Uegeshaji wa 900

Jaribu na egesha pale ambapo

unaweza kuendesha mbele na

kutoka kwenye maegesho.

Hata hivyo, katika maegesho

mengi utatakiwa kurudi nyuma

- ama mahali pa maegesho au

nje ya hapo. Kwa kawaida ni

vizuri kurudi nyuma kwenye

maegesho, kwa sababu hili

litakuwezesha kwenda mbele wakati unatoka – hali itakayokuwezesha

kuona vizuri magari na watembea kwa miguu. Usiliweke gari lako karibu

sana na gari la jirani kwani dereva wake au abiria atapata taabu kuingia

kwenye gari hilo. Usiegeshe kwenye maeneo yaliyoachwa kwa ajili ya

walemavu isipokuwa kama una uhalali wa kuyatumia.

Page 54: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

50

Uegeshaji sambamba

Lazima uwe na uwezo wa kuegesha gari lako kwenye mstari wa wengine

sambamba na ukingo wa barabara – huu huitwa uegeshaji sambamba,

na ni wa kawaida mijini. Angalia nafasi ya kiasi cha mara moja na nusu

ya urefu wa gari lako. Ni vizuri kuingia kwa kurudi nyuma, isipokuwa

kama eneo lenyewe ni refu vya kutosha. Endesha ukipita sehemu tupu

na simama upande wa gari la kwanza baada ya eneo hilo – kiasi cha mita

moja (1) kutoka kwenye gari hilo.

Kisha rudi nyuma polepole

hadi sehemu ya nyuma ya

gari lako itakapoipita

sehemu ile ya gari la mbele

yako, kisha pinda kushoto

kabisa na endelea kusogea

nyuma. Pale tairi lako la

upande wa kushoto

litakapokuwa karibu na

ukingo wa barabara na

katika pembe ya 45º kutoka

hapo, nyonga usukani kulia kabisa, na endelea kwenda polepole nyuma

hadi gari lako litakapokuwa sambamba na ukingo kisha unaweza kuhitaji

kwenda mbele kidogo kuliweka gari katikati ya mahali hapo.

Usiyaguse kamwe magari mengine kwa gari lako. Wakati unarudi nyuma

kwenye maegesho upande wa kulia wa barabara fuata taratibu zilezile za

msingi.

Uegeshaji wa mshazari

Ziko sehemu ambazo utatakiwa kuegesha mshazari kwenye kingo za

barabara. Kuendesha kwenda kwenye maegesho hayo ni rahisi: angalia

vioo vyako na maeneo fiche, ashiria kwenda kushoto, punguza mwendo

taratibu, na kisha nyonga kwa nguvu kuingia eneo hilo. Yanyooshe

matairi na simama pamoja na gari la mbele kwenye ukingo wa barabara.

Kuacha sehemu si kitu rahisi, kwa sababu utatakiwa kurudi nyuma, na

magari mengine yaliyoegesha yanaweza kukukinga kuona magari

yanayokuja. Jaribu kumtafuta mtu wa kusimama nyuma ya gari na

kukuongoza utoke. Rudi nyuma taratibu sana na angalia wakati wote

magari – pindi sehemu ya mbele ya gari lako itakapokuwa sawa na

sehemu ya nyuma ya gari lililoegeshwa kando yako, anza kupinda kwa

Page 55: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

51

nguvu – angalia kuwa sehemu ya mbele ya gari lako iwe inapita kwenye

sehemu ya nyuma ya gari la jirani upande mwingine – kisha nyoosha na

simama – kisha utakuwa tayari kuondoka.

Kuegesha kilimani

Unapoegesha kilimani liache gari likiwa matairi ya mbele yamegeuzwa

kwenye upande wa barabara. Iwapo breki za mkono zitashindwa kufanya

kazi gari litakwenda nje ya barabara. Iwapo gari lako linatumia giaboksi

ya manyu liache gari kwenye gia ya kwanza au gia ya kurudi nyuma. Hii

itasaidia kulizuia gari lisitembee iwapo breki za mkono zitashindwa

kufanya kazi.

Page 56: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

52

Alama za barabarani

Alama za barabarani zinasaidia kutoa tahadhari, kudhibiti, kuongoza na

kuwapa taarifa watumiaji wa barabara. Zinajumuisha ishara za

barabarani za nguzo za wima, taa za barabarani, na michoro ya

barabarani.

Kuna makundi manne ya alama za barabarani:

Alama za udhibiti kuwaambia madereva kipi lazima wafanye na kipi

wasifanye

Alama za tahadhari kuwatahadharisha madereva juu ya hatari au

ugumu wa barabara mbele

Alama za taarifa kuwasaidia madereva kuangalia huduma na

maeneo wanayoyataka

Alama za mwongozo kuwasaidia madereva kuona njia

wanakokwenda.

Alama za makundi mengine

zina umbo maalum na rangi

kuwasaidia madereva

kuzitambua haraka. Alama

mbili muhimu sana ni alama

za “Simama” na “Ruhusu,”

zina maumbo yake maalum.

Ambapo pana haja ya

kupambanua au kupanua

taarifa ya kwenye alama kuu

taarifa ya ziada

imejumuishwa kwenye kibao

chini ya alama kuu.

Ishara za barabarani zinatumika kudhibiti magari na watembea kwa

miguu kwenye makutano na kwenye alama za pundamilia.

Michoro ya barabarani inagawanywa kwenye michoro ya udhibiti,

tahadhari na mwongozo.

Rejea kwenye Kanuni za Barabarani kwa maelezo ya kina ya alama

zote za barabarani.

Alama za mviringo zinatoa maelekezo

Alama za pembetatu zinatoa tahadhari

Alama za mraba

au mstatili - alama ya kijani inatoa taarifa;

alama ya bluu inatoa maelekezo

Page 57: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

53

Jaribio la udereva

Maombi ya kufanya jaribio la udereva

Kama unafikiri kuwa uko tayari kufanya jaribio la udereva lazima:

• Upate cheti kutoka kwenye shule ya udereva yenye leseni kuonyesha

kuwa umemaliza kozi ya maelekezo

• Uwe na leseni halali ya dereva mwanafunzi

• Upate fomu ya maombi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania na

kulipa ada ya jaribio

• Andika barua ya maombi kwa polisi wa usalama barabarani

ukionyesha siku ambayo unataka kujaribiwa; ambatisha nakala za

cheti kutoka kwenye shule yako ya udereva, leseni yako ya dereva

mwanafunzi, na cheti cha kipimo cha macho/kuona kutoka kwenye

kituo cha vipimo vya macho kinachotambulika

• Kuwe na barabara inayofaa, gari lililothibitishwa la aina sahihi la leseni

unayoiomba.

Kujiandaa kwa jaribio

Kama dereva mpya unahitaji maelekezo sahihi kabla ya kwenda kwenye

jaribio. Kama umejiandaa kikamilifu unaweza kufaulu jaribio baada ya

kujaribu kwa mara ya kwanza.

Iwapo unajifunza kuendesha LAZIMA upate mafunzo kutoka kwa

mwalimu wa udereva aliyesajiliwa anayefanya kazi kwenye shule ya

udereva yenye kibali. Wakati unachagua shule ya udereva, jaribu kupata

mapendekezo kutoka kwa wanafunzi waliopita, angalia hali ya gari la

mafunzo, na angalia wanafunzi wangapi wengine watakuwa wanachangia

gari na wewe. Baadhi ya shule zinatoa kozi ambazo zimethibtiishwa na

serikali. Shule lazima ikufundishe nyanja zote za uendeshaji salama, na

si tu jinsi ya kufaulu jaribio la udereva.

Gari ambalo utalitumia kufanyia majaribio lazima liwe safi na linalofaa,

na liwe limesajiliwa vizuri, lenye leseni na kuthibitishwa. Pia lazima liwe

na giaboksi ya manyu - hutaruhusiwa kufanya jaribio kwenye gari lenye

mfumo wa otomatiki. Viti vya mbele lazima viwe na mikanda ambayo

inafanya kazi.

Page 58: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

54

Yaliyomo kwenye jaribio

Lengo la jaribio hili ni kuona kama unaweza kuendesha vizuri. Ni lazima

umridhishe mtahini wa udereva kuwa unaweza kulidhibiti gari lako kwa

usalama, onyesha uungwana na kuwajali watumiaji wengine wa

barabara, na fuata Kanuni za Barabarani. Pia lazima uwe na ufahamu wa

Sheria ya Barabarani [Ibara ya 168 R.E ya 2002) na alama zote za

barabarani na michoro iliyoelezwa kwenye Kanuni za Barabarani.

Sheria ya Barabarani inaeleza kuwa jaribio ni kwa ajili ya kuangalia

uwezo wako wa:

• Kulidhibiti gari barabarani

• Kulisimamisha gari kutoka kwenye mwendo wa kawaida

• Kukata kona kwenye barabara kuu, kukatisha barabara, na kupinda

kutoka kwenye barabara ndogo kuingia barabara kuu

• Kuyapita magari mengine barabarani

• Kurudisha gari nyuma kwenye barabara iliyonyooka na yenye kona

• Kupinda barabarani

• Kuelewa na kufuata Sheria na ushauri wa Kanuni za Barabarani.

Jaribio

Jaribio limeandaliwa ili kuona kama una uwezo mkubwa wa kuendesha

na iwapo unajua Sheria za Barabarani na alama za barabarani. Liko

kwenye sehemu mbili: nadharia, na jaribio la vitendo.

Jaribio la nadharia linaweza kuwa la mdomo au kuandika. Maswali

yatachukua nyanja zote za udereva, pamoja na mbinu za msingi za

udereva, alama za barabarani, michoro, Kanuni za Barabarani, na Sheria

za Barabarani. Mtahini atasahihisha majibu yako, na iwapo 70% au zaidi

ni sahihi, utakuwa umefaulu jaribio.

Iwapo utafaulu jaribio utaruhusiwa kufanya jaribio la vitendo. Hili

hufanywa barabarani., huku mtahini akiwa amekaa mbele kwenye kiti

cha abiria. Mtahini atakuwa anaangalia kuona kuwa:

• Unatumia vizuri vioo

• Unaonyesha ishara za lazima kwa usahihi na kwa wakati unaofaa

• Unachukua hatua inayofaa papo hapo kwa alama zote za barabarani,

ishara, na michoro

• Unadhibiti mwendo wako ili daima uwe wa salama na unaofaa katika

mazingira uliyopo na namna unavyoendesha

Page 59: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

55

• Unakuwa mwangalifu nakuangalia vizuri kabla ya kuingia, au

kukatisha makutano yoyote

• Unaonyesha ufahamu na matarajio kwa vitendo vya watembea kwa

miguu, waendesha baiskeli, na madereva wengine

• Liweke gari lako kwenye njia sahihi barabarani – wakati unaendesha

moja kwa moja na wakati unapinda kwenye makutano.

Jaribio la vitendo husahihishwa kwa njia ya kupunguza alama. Unaanza

na alama 100 na mtahini atakuwa anapunguza alama kwa kila kosa

unalofanya. Idadi ya alama zinazopunguzwa hutegemea na ukubwa wa

kosa – alama 10 kwa kila kosa kubwa na alama 5 kwa kila kosa dogo.

Kama bado utakuwa na alama 70 au zaidi mwishoni mwa jaribio utakuwa

umefaulu.

Ni kawaida kuwa na wasiwasi wakati wa kufanya jaribio, lakini kadiri

unavyofanya mazoezi zaidi ndivyo utakavyojiamini zaidi. Kwa kawaida

jaribu kuendesha kwa jinsi ulivyofundishwa.

Ukijiona umefanya kosa, usiogope kuhusu kosa hilo. Mtahini hatasema

bila sababu wakati unaendesha kwa sababu hili linaweza

kukuchanganya. Hakikisha kuwa umejifunga vizuri mkanda wako wakati

unaendesha.

Iwapo una ulemavu wa viungo mtahini ataelewa matatizo yako na

kukusaidia kadiri awezavyo. Unaweza kuchagua mtahini wako

azungumze Kiswahili au Kiingereza. Haishauriwi kutumia wakalimani.

Ni muhimu kuonyesha kwa mtahini kuwa unajiamini (lakini si kujiamini

kupita kiasi) katika kuendesha barabarani. Endesha vizuri na si kwa

kusitasita sana, au kutoweza kutumia upenyo salama barabarani wakati

wa kupinda. Usiwe mpole sana kiasi cha kuyaruhusu magari yapite bila

sababu – hili linaweza kusababisha kujichanganya na unaweza kuyazuia

magari ya nyuma yako bila sababu. Kamwe usiwaashirie watembea kwa

miguu kuvuka barabara mbele yako – unaweza kuwasababishia hatari

kutoka kwenye magari mengine.

Mtu yeyote anayetoa zawadi au fedha au kishawishi kingine kwa mtahini

kwa lengo la kuathiri uamuzi wake anaweza kushitakiwa kwa kosa kubwa

la ‘kujaribu kutoa rushwa.'

Page 60: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

56

Baada ya jaribio

Iwapo umefaulu. Kwa kufaulu mtihani utakuwa umeonyesha kuwa

wewe kimsingi ni dereva mzuri. Hata hivyo, bado huna uzoefu, na una

mengi ya kujifunza. Jaribu kuendelea kuboresha ujuzi wote wa udereva

kwa uzoefu zaidi na umakini zaidi wa mbinu zako za udereva. Hili

liendelee wakati wote wa maisha yako ya udereva- daima kuna

mawanda kuendelea zaidi.

Iwapo utashindwa. Utashindwa tu iwapo utafanya makosa mengi ya

udereva au kuwa na maarifa madogo ya udereva. Mtahini atakupa taarifa

ya kushindwa ambapo ataonyesha vipengele vya udereva wako

vinavyohitaji umakini zaidi. Makosa yatakayoonyeshwa yatakuwa ni yale

yaliyokusababisha kushindwa jaribio, lakini yanaweza kuwako mengine,

ambayo ni madogo. Hivyo, wakati taarifa ya kushindwa ikusaidie wewe

na mwalimu wako kurekebisha makosa haya makubwa, jaribu kuboresha

nyanja zote za udereva wako.

Iwapo utashindwa lazima usubiri kwa kiasi cha wiki nne kabla ya

kujaribiwa tena. Mtahini anaweza kuongeza kipindi hiki hadi wiki tisa (9)

kama ataona kuwa unahitaji muda zaidi wa kuboresha udereva wako.

Page 61: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

57

Kuharibika

Iwapo gari lako litaharibika, au kupata pancha, jaribu kulisogeza gari

lako nje ya barabara. Kama hili haliwezekani liweke gari karibu na ukingo

wa kushoto wa barabara na mbali ya makutano, madaraja, kona na

sehemu nyingine za hatari.

Iwapo huwezi kuepuka

kusimama barabarani

LAZIMA utoe tahadhari kwa

magari mengine kwa

kuweka kiashiria chekundu

cha pembetatu karibu na

ukingo wa barabara si chini

ya mita thelathini (30)

nyuma ya gari-pamoja na

kiashiria kingine cha

pembetatu katika umbali

uleule mbele ya gari. Pia lazima utumie taa zako za tahadhari ya hatari

(indiketa mbili-zote zikiwaka kwa pamoja). Iwapo umesimama kwenye

kona au karibu ya kilele cha kilima tafuta mtu mmoja arudi nyuma

barabarani kuyatahadharisha magari yanayokuja.

LAZIMA ujaribu na kuliondoa gari haraka iwezekanavyo. Ofisa wa polisi

ana mamlaka ya kupanga namna ya kuliondoa gari lolote iwapo ataona

linahatarisha usalama. Utapaswa kulipa gharama za kuliondoa.

Jaribu kutosimama au kutoshughulika na gari mahali ambapo utakuwa

katika hatari ya kugongwa na magari yanayopita. Unapolitengeneza gari

usimwage dizeli au kilainishi kingine barabarani, kwani inaathiri

barabara.

Fanya kila jitihada kulitengeneza gari au kuliondoa barabarani, kabla ya

giza kuingia. Iwapo utalazimika kuliacha gari bovu barabarani usiku,

washa taa za kuegeshea na hakikisha kuwa kuna vibao vya tahadhari

vya pembetatu barabarani mbele na nyuma ya gari kuwatahadharisha

madereva wengine. Waarifu polisi.

Hakikisha kuwa mawe uliyotumia kuzuia matairi ya gari yameondolewa

barabarani wakati unapoondoa gari.

Page 62: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

58

Iwapo kuna ajali

Iwapo umehusika kwenye ajali au umesimama kusaidia:

• wape tahadhari madereva wa magari mengine kwa kuwasha taa zako

za tahadhari ya hatari (indiketa mbili) na, ikibidi, waashirie madereva

wengine wapunguze mwendo. Dhibiti magari ili kuepuka ajali nyingine.

Waombe madereva wengine na wanakijiji wakusaidie.

• waombe madereva kuzima injini zao na kutokuwa na sigara zozote

• wasiliana na polisi mara moja – waeleze eneo hasa la ajali na idadi ya

magari na watu waliojeruhiwa – waombe watu wengine kufanya hivi ili

kuhakikisha kuwa ujumbe umefika

• jiandae kutoa huduma ya kwanza

• iwapo majeruhi wameumia sana, na kuna matumaini madogo ya

kupata msaada haraka, fanya utaratibu wa kuwapeleka majeruhi

kwenye hospitali ya karibu

• wahudumie walioathirika na tunza mali zao – na mshawishi kila mmoja

kufanya hivyo.

Ukiyaona magari yamesimama mbele, punguza mwendo na uwe tayari

kusimama. Iwapo ukiona tayari kuna watu wa kutosha wanaotoa msaada

usisimame na kusababisha kizuizi. Wakati unapita mahali penye ajali

usibabaike – kuwa makini na barabara mbele yako. Fuata amri za

maofisa wa polisi walio kwenye tukio, na kuwa mvumilivu iwapo

kutakuwa na kukaa kwa muda mrefu.

Iwapo umehusika kwenye ajali ambapo mtu amejeruhiwa LAZIMA utoe

jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa gari, kama ni

tofauti) kwa mtu yeyote aliyehusika na ajali na LAZIMA utoe taarifa ya

ajali kwenye kituo cha polisi cha karibu au kwa ofisa wa polisi haraka

iwezekanavyo.

LAZIMA usimame na kuwasaidia watu waliojeruhiwa kwenye ajali,

isipokuwa kama unahofia usalama wako. Iwapo umehusika kwenye ajali

ya barabarani ambapo hakuna aliyejeruhiwa huhitaji kutoa taarifa polisi,

lakini LAZIMA utoe jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa

gari, kama ni tofauti) na namba ya usajili ya gari lako kwa mtu mwingine

yeyote aliyehusika.

Page 63: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

59

Muhtasari wa mafunzo ya madereva wa magari

madogo (Leseni za Daraja B & D)

1. Gari

Mwanafunzi lazima:

a) Awe na uelewa wa msingi wa jinsi gari inavyofanya kazi

b) Ajue matumizi na kazi za vidhibiti vya gari (mf. Usukani, breki na

gia) injini, mwako na sehemu nyingine za kiufundi

c) Aweze kusoma na kuelewa vifaa vya gari (mf. Spindometa) na

umuhimu wake

d) Kutambua hatari zinazotokana na kushindwa kufanya kazi kwa

sehemu mbalimbali za gari na jinsi ya kugundua hitilafu,

e) Ajue jinsi ya kufanya safari za awali, ukaguzi wa kila wiki na kila

mwezi,

f) Awe na uelewa wa jinsi aina mbalimbali za magari madogo (mf.

Magari madogo ya kawaida, pikapu, magari yenye kutumia

magurudumu yote manne) yanavyokuwa yakiendeshwa na jinsi ya

kuyaendesha kwa usalama.

2. Kufaa kuendesha

Mwanafunzi lazima:

a) Awe na mtazamo sahihi wa uendeshaji:- kuwajibika, kuwa makini,

matarajio, uvumilivu na kujiamini

b) Aelewe jinsi pombe inavyoathiri uwezo wa kuendesha gari, ajue

sheria inasemaje kuhusu kunywa pombe na kuendesha gari na jinsi

sheria inavyotekelezwa

c) Aelewe umuhimu wa kutoendesha gari wakati amechoka na ajue

miongozo kuhusu ni mara ngapi anatakiwa kupumzika

anapoendesha gari

d) Aelewe kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuathiri uwezo wa

kuendesha gari na ajue jinsi ya kuzitambua

e) Aelewe jinsi ya kubadilikabadilika na ugonjwa kunavyoathiri uwezo

wa kuendesha gari

f) Aelewe umuhimu wa kuona vizuri na jinsi ya kutambua hali ya

macho.

3. Dereva na Gari

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue nafasi inayotaiwa kuendeshea na jinsi ya kuingia sehemu hiyo

Page 64: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

60

b) Ajue jinsi ya kurekebisha vioo, kujua ukomo wake na kujua kuhusu

maeneo yasiyo mazuri (“blind zone”)

c) Ajue jinsi ya kurekebisha udhibiti wa kichwa vizuri

d) Aelewe umuhimu wa kufunga mikanda, jinsi ya kuifunga vizuri na

sheria inayohusika

e) Ajue namna nzuri ya kubeba watoto kwa usalama

f) Ajue jinsi ya kubeba mizigo na wanyama kwa usalama.

4. Dereva na Sheria

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue sheria muhimu, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu kusababisha

ajali kutokana na kuendesha gari vibaya na kwa uzembe, kuendesha

wakati mtu amekunywa pombe na dawa za kulevya, kuendesha kwa

kasi n.ik..

b) Awe na uelewa wa msingi wa masharti ya gari kuwa zima

c) Ajue masharti ya leseni ya udereva, ikiwa ni pamoja na yale

yanayowahusu madereva wanafunzi

d) Ajue majukumu ya kisheria ya kuhusu kugongana

e) Ajue masharti ya bima ya gari na umuhimu wa kukata bima inayofaa

f) Awe na uelewa wa msingi wa jinsi sheria za usalama barabarani

zinavyotekelezwa (ikiwa ni pamoja na faini za papo hapo) na adhabu

za makosa ya uendeshaji gari.

5. Udhibiti na uratibu

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kuwasha injini, kuondoka na gari, kuongeza mwendo,

kubadilisha gia, kurudi nyuma, kuendesha kwenye kupanda mlima

na kushuka na kukata kona, na kufunga breki kusimama kwa

usalama bila taratibu na kiumahiri

b) Aweze kusimama na kuondoka kwenye mlima bila tatizo na bila ya

kurudi nyuma

c) Ajue jinsi mtindo wa uendeshaji unavyoathiri matumizi ya mafuta,

starehe na usalama wa abiria.

6. Uendeshaji salama katika foleni

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kuednesha katika hali inayoonyesha kujali kuzingatia na

uvumulivu

b) Ajue umuhimu wa kuwa makini katika kazi ya kuendesha na

kuepuka kuwa sehemu nyingine kimawazo na kujua ni vitu gain

vinaweza kumchanganya dereva

Page 65: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

61

c) Aweze kuendelea kuchunguza barabara kwa mbele na pembeni (kwa

kutumia vizuri vioo) na kutazamia hali fulani itakavyojitokeza na

kuchukua hatua sahihi waendeshaji magari wengine na mazingira ya

hatari

d) Atumie mchakato wa hatua katika ishara ya kioo

e) Aweze kupita magari yaliyosimama na vizuizi kwa usalama

f) Ajue ni jinsi gain na wakati gain wa kutoa ishara kwa kutumia

indiketa na ishara za mkono

g) Ajue nani mwenye kipaumbele wakati magari yanapokutana kwenye

mzunguko au hali ya kupitana

h) Aliweke gari vizuri barabarani na akae kwenye mkondo wake

i) Ajue jinsi ya kuamua umbali gain ni salama kutoka kwenye gari iliyo

mbele na aweze kukaa katika umbali huo kwenye foleni

j) Ajue jinsi ya kutumia njia mbili kwenye barabara yenye njia nyingine

k) Aelewe kwa nini tabia zinazoonekana kuwa ni mbaya, kama vile

kuondoka kwenye foleni, na kuendesha pembeni mwa barabara

kwenye eneo la watembea kwa miguu, ni hatari na haifai.

7. Mwendo kasi

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue kuwa hatari ya kugongana inaongezeka kadri mwendo

unavyoongezeka

b) Aweze kuendesha kwa mwendo salama katika mazingira

c) Ajue vizuri jinsi ya kuepuka kuteleza na afanye nini utelezi

unapotokea

d) Awe na uelewa wa jumla wa umbali wa kusimama na jinsi

unavyotofautiana kulingana na mazingira ya barabara na mambo

mengine

e) Ajue mipaka ya mwendo kasi wan chi wa eneo, umuhimu wake na

jinsi inavyotekelezwa

f) Ajue kwamba kikomo cha mwendo kasi hakina maana na kwamba

wakati wote itakuwa ni salama kuendesha katika mwendo huo.

8. Kupita gari

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue wakati gain ni salama kulipita gari

b) Ajue maeneo ambayo si salama kulipita gari – na wapi alama za

barabara zinaonyesha ni kosa kulipita gari

c) Aweze kulipita gari jingine katika hali ya usalama na umahiri, bila

kusababisha gari linalotoka katika mwelekeo tofauti kupunguza

mwendo au kubadili uelekeo ili kuepuka kugongana.

Page 66: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

62

9. Makutano (tofauti na mzunguko)

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kuendesha gari kwa kupita katika aina zote za makutano

katika hali ya usalama na umakini, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo

katika barabara iliyogawanywa sehemu mbili, mitaa ya njia moja na

zile zinazoongozwa na alama za barabarani

b) Ajue umuhimu wa kukaribia makutano kwa mwendo unaofaa,

kuingia katika njia na nafasi sahihi, kutii sheria muhimu kuangalia

vizuri na kutozuia misururu mingine ya magari kutembea

c) Atumie vizuri ishara.

10. Mizunguko

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kupita kwenye mizunguko katika hali ya usalama na umahiri

b) Ajue ni njia gani ya kutumia anapoingia na kukata kona na

kuondoka kwenye mzunguko

c) Atumie vizuri ishara

d) Ajue nani mwenye kipaumbele.

11. Vivuko vya watembea kwa miguu

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue aina mbalimbali za vivuko vya watembea kwa miguu – sehemu

ya katikati ya kuvukia kwa waendao kwa miguu, vivuko vya

pundamilia, taa za barabarani na jinsi alama zinavyofanya kazi

b) Ajue sheria kwa matumizi ya kila aina ya kivuko cha watembea kwa

miguu

c) Aelewe umuhimu wa kutolipita gari au kuegesha karibu na alama za

pundamilia za kuvuka barabara

d) Ajue muda wenye hatari zaidi na sehemu zenye hatari kubwa.

12. Kuendesha gari usiku na katika hali mbaya ya hewa

Mwanafunzi lazima:

a) Aelewe umuhimu wa kuendesha katika mwendo ambao utamruhusu

kusimama katika umbali ambao anaweza kuona vizuri

b) Ajue ni wakati gani wa kuwasha taa za mbele zenye mwanga mkali

c) Ajue ni wakati gani wa kutumia taa za mbele zenye mwanga hafifu

d) Aelewe jinsi hali ya unyevunyevu itakavyoathiri umbali wa kusimama

e) Ajue jinsi ya kukabiliana na mvua kubwa, mafuriko, ukungu, barafu

na upepo mkali.

Page 67: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

63

13. Kuharibika na dharura

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kutumia breki na gia ili kuweza kusimamisha gari haraka bila

ya kuteleza na bila ya kuzima injini

b) Ajue atafanya nini kama atahusika katika kugongana au kusimama

kutoa msaada

c) Ajue atafanya nini kama ataharibikiwa gari barabarani na hususan

jinsi ya kuepuka kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa

barabara.

14. Kutambua hatari

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue muda, mahali na hali ya hewa ambapo hatari ya kugongana ni

kubwa kuliko kawaida

b) Ajue aina za kugongana zinazotokea sana na kwa nini zinatokea

c) Ajue hatari mahsusi zinazomkabili dereva wakati analipita basi

lililosimama; anapoingia kwenye mzunguko ambapo kuna magari

mawili, anakata kushoto ambako kuna magari mawili; anaingia

barabara kuu wakati upeo wa kuona pembeni ni mdogo anakata

kulia kwenye barabara yenye njia mbili zinazotumiwa na watu;

analipita gari kubwa/refu kwenye mzunguko; anageuza gari kutoka

kwenye jengo au kwenye geti katika ukuta anakaribia njia ya reli

inayokatisha; kuna watoto wadodo pembeni mwa barabara.

15. Kugeuza gari kwa kuzunguka barabarani

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kujua kama ni salama ni sheria na ni busara kugeuza gari

kwa kuzunguka barabarani

b) Ajue wakati gani wa kugeuka kwa mzunguko wa U, kugeuzia kwenye

njia ya pembeni na kutumia ugeukaji wa point i– 3

c) Aweze kugeuka alikotoka kwa hali ya usalama na umakini, kwa

usimamizi mzuri, kutumia usukani kwa usahihi na kuwaangalia vizuri

watumiaji wengine wa barabara.

16. Maegesho

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kuamua kama ni salama ni sheria na ni busara kuegesha

sehemu yoyote

b) Aweze kuegesha sambamba, maegesho ya 90º, na maegesho

mshazari katika hali ya usalama na umahili kwa usimamizi mzuri,

uelekeo sahihi na uzuiaji mdogo wa magari mengine

Page 68: MwongozoMwongozo wa Maderevawa Madereva … · Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari, utakuwa

64

c) Kuweza kuegesha kwa usalama kwenye mteremko (mwinuko na

mteremko).

17. Kurudi nyuma

Mwanafunzi lazima:

a) Aweze kujua kama ni salama ni sheria na busara kurudi nyuma

b) Aweze kurudi nyuma katika hali ya usalama na umakini katika

mstari ulionyooka, katika kona ya kushoro na kulia na katika

barabara zilizo tambarare na katika miteremko.

18. Alama ishara na michoro ya barabara

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue makundi makuu manne ya alama za barabarani na sifa za

maumbo yake na rangi

b) Ajue alama zote za udhibiti, ishara na alama za usalama barabarani

na jinsi ya kuzifuata

c) Aweze kutambua vizuri 80% ya alama na ishara nyingine

d) Ajue ishara zinazotolewa na maofisa wa polisi na watu wengine

walioidhinishwa na jinsi ya kuzifuata.

19. Mfumo wa barabara

Mwanafunzi lazima:

a) Awe na uelewa wa jumla wa barabara zipi ziko chini ya Mamlaka ya

Taifa ya Barabara Tanzania (TANROADS), ambazo ni mali ya

Halmashauri za wilaya na ambazo ni binafsi

b) Ajue umuhimu wa kutozuia trafiki kwenye barabara au kuharibu

barabara zetu au kuiba au kuuza au kuharibu alama au vifaa vingine

vya barabarani.

20. Huduma ya Kwanza

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue utaratibu hatari–mwitikio–njia ya hewa–kupumua-mzunguko

b) Ajue jinsi ya kuzuia upotevu mkubwa wa damu (bila kujiweka

mwenyewe hatarini)

c) Ajue jinsi ya kuwashughulikia waathirika wa mshtuko

d) Ajue jinsi ya kupata msaada

e) Ajue jinsi ya kumweka majeruhi katika sehemu atakapopata nafuu.

21. Kujitayarisha kwa jaribio la udereva

Mwanafunzi lazima:

a) Ajue jinsi ya kuomba kufanyiwa jaribio la udereva na mahitaji yake

b) Ajue muundo wa upimaji wa udereva na jinsi atakavyopewa alama.