sheria ya taasisi za kazi, 2004

Upload: jeremia-mtobesya

Post on 14-Apr-2018

435 views

Category:

Documents


13 download

TRANSCRIPT

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    1/39

    1

    _______

    SURA YA 300

    ____

    SHERIA YA TAASISI ZA KAZI

    SHERIA KUU

    MPANGILIO WA VIFUNGU

    SEHEMU YA I

    VIFUNGU VYA AWALI

    Kifungu Jina

    1. Jina fupi na kuanza kutumika kwake.

    2. Tafsiri

    SEHEMU YA II

    BARAZA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA KAZI,

    UCHUMI NA JAMII

    3. Kuanzishwa kwa Baraza

    4. Muundo wa Baraza

    5. Kazi na Mamlaka ya Baraza

    6. Muda wa kushika cheo na masharti ya uanachama

    7. Kuondolewa kwa mjumbe na kujaza nafasi

    8. Kamati za Baraza

    9. Mikutano ya Baraza

    10. Usimamizi wa Baraza

    11. Taarifa ya mwaka ya Baraza

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    2/39

    2

    SEHEMU YA III

    TUME YA UPATANISHI NA USULUHISHI

    12. Kuanzishwa kwa Tume

    13. Uhuru na hadhi ya Tume

    14. Kazi za Tume

    15. Mamlaka ya Tume

    16. Muundo wa Tume

    17. Muda na Masharti ya Utumishi wa Makamishna

    18. Mkurugenzi wa Tume

    19. Wapatanishi na wasuluhishi

    20. Mamlaka ya wapatanishi na wasuluhishi.

    21. Viapo.

    22. Wafanyakazi wa Tume.

    23. Usimamizi wa fedha za Tume.

    24. Mahesabu na Ukaguzi.

    25. Mamlaka ya Kuingia Mikataba.

    26. Kukasimisha madaraka ya Makamishna.

    27. Ukomo wa uwajibikaji na ukomo wa ufichuzi.

    28. Taarifa ya Mwaka ya Tume

    SEHEMU IVKAMATI YA HUDUMA ZA MSINGI

    29. Uanzishwaji wa Kamati ya Huduma za Msingi.

    30. Kazi za Kamati ya Huduma za Msingi.

    31. Uteuzi wa Kamati ya Huduma za Msingi.

    32. Taarifa ya Mwaka ya Tume

    33. Usimamizi wa Kamati ya Huduma za Msingi.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    3/39

    3

    SEHEMU YA V

    BODI YA UJIRA

    34. Tafsiri.

    35. Uteuzi wa Bodi ya Ujira.

    36. Kazi na Mamlaka ya Bodi ya Ujira.

    37. Uchunguzi.

    38. Taarifa ya Bodi ya Ujira.

    39. Kuweka amri ya ujira.

    40. Kipindi cha Utendaji Kazi wa amri ya ujira

    41. Matokeo ya Kisheria ya amri ya ujira.

    42. Usimamizi wa Bodi ya Ujira.

    SEHEMU VIUSIMAMIZI WA KAZI NA UKAGUZI

    43. Uteuzi wa Kamishna wa Kazi na Maafisa wengine.44. Kukasimisha Madaraka.45. Mamlaka ya Afisa wa Kazi46. Amri tekelezi.47. Pingamizi dhidi ya amri tekelezi48. Rufaa dhidi ya amri ya Kamishna wa Kazi49. Makosa dhidi ya Maafisa wa Kazi.

    SEHEMU YA VIIMAHAKAMA YA KAZI

    50. Uanzishwaji na muundo wa Mahakama ya Kazi.51. Mamlaka ya Mahakama ya Kazi.52. Madaraka ya Mahakama ya Kazi.53. Washauri wa Mahakama.54. Msajili na Kaimu Msajili wa Mahakama ya Kazi55. Kanuni na Mahakama ya Kazi56. Uwakilishi kwenye Mahakama ya Kazi57. Rufaa dhidi ya Uamuzi wa Mahakama ya Kazi.58. Marejeo ya suala la kisheria kwenye Mahakama ya Rufaa.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    4/39

    4

    SEHEMU YA VIII

    MASWALA YA JUMLA

    59. Usiri.60. Uzito wa kuthibitisha kosa.61. Dhanifu ya nani ni mwajiriwa.62. Miongozo63. Makosa.64. Adhabu65. Kanuni.66. Vifungu vya akiba na mpito.

    _______JEDWALI

    _______

    Sheria kwa ajili ya kuanzishwa kwa Taasisi za Kazi kuainisha kazi,

    mamlaka na wajibu, na kuainisha mambo mengine yanayofanana

    na hayo.

    [1/02/2005]

    [TS Na. 14 La

    2005]

    Sheria No. 8 ya 2006.

    SEHEMU YA I

    VIFUNGU VYA AWALI

    Jina fupi 1. Sheria hii Itaitwa Sheria ya Taasisi za Kazi, ya Mwaka 2004 na itaanza

    kutumika katika tarehe itakayoainishwa na Waziri kwenye notisiitakayochapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

    Tafsiri Isipokuwa pale muktadha unavyokusudia vinginevyo, Sheria hii-

    Tume| maana yake Tume ya Upatanishi na Usuluhishi iliyoanzishwa

    kwa mujibu wa Kifungu cha 12;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    5/39

    5

    Baraza maana yake Baraza la Jamii, Kazi na Uchumi lililoanzishwa

    kwa mujibu wa kifungu cha 3;

    Sura ya 366 ELRA maana yake Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini;

    Kamishna wa Kazi maana yake Kamishna wa Kazi aliyeteuliwa kwa

    mujibu wa masharti ya kifungu cha 43(1) na endapo Kamishna wa

    Kazi hayupo, basi Naibu Kamishna wa Kazi;

    Mahakama ya Kazi Maana yake Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi

    kama kilivyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 50;

    Sheria za Kazi zinajumuisha Sheria hii na sheria zingine zozote ambazo

    Waziri anawajibika nazo;

    Afisa Kazi maana yake ni afisa wa kazi kama ilivyoainishwa na

    kifungu cha 43(3) na inajumuisha Kamishna wa Kazi au Naibu

    Kamishna wa Kazi;

    Waziri kwa mujibu wa kifungu cha 34(a), maana yake ni Waziri

    mwenye dhamana ya mambo ya kazi;

    Katibu Mkuu isipokuwa pale itakavyoelezwa vinginevyo ndani ya

    sheria hii, Katibu wa Wizara yenye dhamana ya mambo ya kazi;

    Msajili wa Mahakama ya Kazi maana yake ni Msajiri aliyeteuliwa kwa

    mujibu wa kifungu cha 54;

    Msajili wa Vyama maana yake ni Msajiri aliyeteuliwa kwa mujibu wa

    masharti ya kifungu cha 43(3) na endapo Msajiri hayupo, basi

    Naibu Msajiri aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha

    (2);

    Sekta maana yake ni shughuli au huduma au sehemu ya shughuli au

    huduma.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    6/39

    6

    SEHEMU YA II

    BARAZA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA KAZI, UCHUMI NA JAMII

    Kuanzishwa

    kwa Baraza3. Kutakuwa na Baraza linaloshughulikia masuala ya Kazi, Uchumi na

    Jamii;

    Muundo waBaraza na kazi

    zake

    4-(1) Baraza litakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Waziri

    kwa mujibu wa kifungu hiki.

    (a) Mwenyekiti ambaye hatakuwa-

    (i) mjumbe,afisa au mwajiriwa wa chama cha

    wafanyakazi, chama cha waajiri au shirikisho; au

    (ii) mwajiriwa wa utumishi wa umma ndani ya serikali ya

    Jamhuri ya Muungano;

    (b) Wajumbe wengine kumi na sita ni-

    (i) Katibu Mkuu na wajumbe wengine watatu

    watakaowakilisha maslahi ya serikali;

    (ii) wajumbe wanne watakaowakilisha maslahi ya

    waajiri;

    (iii) wajumbe wanne watakaowakilisha maslahi ya

    waajiriwa;

    (iv) wajumbe wanne watakaoteuliwa kwa kuzingatia

    utaalamu wao katika masuala ya kazi, uchumi na

    uuandaaji wa sera za kijamii;

    (2) Kabla ya uteuzi wa wajumbe wa Baraza, Waziri atatoa notisi kwa

    maandishi ya kualika mapendekezo kutoka-

    (a) Vyama vya wafanyakazi na mashirikisho ya vyamavya wafanyakazi, yaliyosajiliwa endapo mjumbe atatakiwa

    kuwawakilisha wafanyakazi au

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    7/39

    7

    (b) Vyama vya waajiri na mashirikisho ya vyama

    vya waajiri, endapo mjumbe atatakiwakuwawakilisha waajiri;

    (c ) Wale wajumbe wa wa Baraza wanaowakilisha maslahi

    ya waajiri na wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu

    kidogo cha (1) (b)(iv);

    (3) Kwa idhini ya Waziri, Baraza linaweza kuwashirikisha

    wajumbe wengine ili kulisaidia katika utendaji kazi, ingawa wajumbe hao

    hawatapiga kura kwenye mikutano ya Baraza.

    Kazi na

    Mamlaka ya

    Baraza

    5-(1) Kazi za Baraza zitakuwa ni-

    (a)Kuishauri serikali kupitia Wizara katika mambo yafuatayo-

    (i) hatua za kuhamasisha ukuaji wa uchumi na usawa

    katika jamii;

    (ii) sera za kijamii na uchumi;

    (iii) mabadiliko yoyote ya msingi katika sera za Kijamii na

    kiuchumi kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri;

    (iv) kuhamasisha uratibu sera kwenye masuala ya kikazi,

    kiuchumi na kijamii;

    (b) Kumshauri Waziri kuhusu-

    (i) sera ya taifa ya soko la ajira;(ii) mapendekezo yoyote ya sheria ya kazi kabla

    hayajawasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri;

    (iii) kuzuia na kupunguza upungufu wa ajira;(iv) suala lolote lililoainishwa na Shirika la Kazi la Dunia;(v) suala lolote lililoainishwa na vyama vya kitaifa au

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    8/39

    8

    kimataifa ambavyo Tanzania ni mwanachama;

    (vi) kanuni za utendaji bora wa kazi;(vii)kukusanya na kujumuisha habari na takwimu kuhusu

    usimamizi wa sheria za kazi;

    (viii)suala lolote la ajira lililopelekwa kwenye Baraza naWaziri au Baraza linadhani kuwa linafaa ili kufikia

    malengo ya sheria za kazi;

    (c)kuhakikisha waajiri na wafanyakazi kila upande unapendekeza;

    (i) Washauri kwa ajili ya uteuzi wa baraza la washauri wa

    mahakama kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 53;

    (ii)watu kwa ajili ya uteuzi wa wajumbe wa chomo cha

    utawala cha Tume kwa mujibu wa kifungu cha 16;

    (iii) watu kwa ajili ya uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya

    Huduma za Msingi kwa mujibu wa kifungu cha 29;(d)kupitia na kuchanganua masuala ya kijamii na kiuchumi;(e)kwenda sambamba na maendeleo ya kimataifa katika sera za

    kijamii na kiuchumi;

    (f) kutathimini ufanisi wa sheria na sera zinazoathiri sera yakijamii na kiuchumi;

    (g)Kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara mbalimbali, vyombovilivyoanzishwa kisheria mikakati na vyombo vingine au

    Taasisi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na uundaji na

    utekelezaji wa sera za kazi, kijamii na kiuchumi;

    (2) Katika utekelezaji wa kazi zake, Baraza linaweza-

    (a) kufanya uchunguzi kadri itakavyolazimu;(b) Kufanya utafiti wa sera za kazi, kijamii na kiuchumi;

    (3) Baraza linaweza kuamua kuandaa kanuni zake ili kutekeleza

    utendaji wa kazi.

    Uteuzi namasharti yauanachama

    6.-(1) Mjumbe wa Baraza-

    (a)atateuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu; na(b)anaweza kuteuliwa tena baada ya kumaliza muda wake.

    (2) Mjumbe wa Baraza atalipwa posho kwa ajili ya mikutano, usafiri

    na kujikimu kwa kiwango kitakachopangwa na Waziri kwa mapendekezo

    ya Katibu Mkuu baada ya kushauriana na Katibu Mkuu Menejimenti ya

    Utumishi wa Umma.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    9/39

    9

    Kuondolewa

    kwa wajumbena kujaza

    nafasi

    7.-(1) Waziri atamuondoa mjumbe kutoka kwenye wadhifa huo endapo

    mjumbe-

    (a) amejiuzulu kwa maandishi na amewasilisha barua yakujiuzulu kwa Katibu Mkuu;

    (b) hawakilishi tena maslahi kama alivyoteuliwa kwa mujibuwa kifungu cha 5(1)(b)(i),(ii) au(iii);

    Ikizingatiwa kuwa, kuondolewa kwa mjumbe kwa sababu hii

    kutafanyika endapo ameombwa na wawakilishwaji ambao yeye

    anawakilisha maslahi yao;

    (c) amefanya kosa kubwa la utopvu wa nidhamu kuhusiana nautendaji kazi kama mjumbe;

    (d) hawezi kutekeleza majukumu yake kama mjumbe (kwasababu ya ugonjwa au sababu nyinginezo);

    (e) hajahudhuria vikao vitatu vya Baraza bila ya kuwa naruhusa au sababu maalum;

    (f) ametangazwa kuwa amefilisika; au(g) ametiwa hatiani kwa kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo

    bila ya kuwa na mbadala wa kulipa faini.

    (2) Inapotokea nafasi iliyowazi kwenye Baraza, Waziri atamteua

    mjumbe ili kujaza nafasi kwa muda uliobaki na anapofanya uteuzi huo

    atalazimika kufuata masharti yaliyoainishwa katika kifungu cha 4.

    Kamati za

    Baraza8.-(1) Katika kutekeleza majukumu yake, Baraza laweza-

    (a) kuunda kamati kwa ajili ya kufanya kazi maalumu zaBaraza; na

    (b) Kwa mujibu wa idhini ya Waziri, kugawa majukumuyoyote ya kazi zake kwenye kamati kwa masharti kama

    litakayoona yanafaa;

    (2) Kamati iliyoteuliwa na Baraza-

    (a) itakuwa na watu watatu;(b) itakuwa na angalau wajumbe wake watatu; na(c) inaweza kuhusisha idadi yoyote ya wajumbe wa kamati

    zingine, ingawa wajumbe hao hawatapiga kura kwenye

    vikao vya kamati ikiwa kamati hiyo imegawiwa

    majukumu ya kutekeleza kwa mujibu wa kifungu kidogo

    cha (1)(b)

    (3)Kazi yoyote itakayofanywa na kamati kwa mujibu wa kifunguitatambuliwa kama kazi iliyofanywa na Baraza.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    10/39

    10

    Mikutano ya

    Baraza9.-(1) Mwenyekiti ataitisha-

    (a) angalau mikutano mitatu ya Baraza ndani ya mwaka wakalenda;

    (b) mikutano ya Baraza kwa mujibu wa kanuni zake; na(c) mkutano maalumu cha Baraza-

    (i) kwa ombi la ushawishi la maandishi la wajumbewanne; au

    (ii) Kwa ombi la Waziri.(2) Mwenyekiti akiwepo ataongoza mikutano yote ya Baraza.

    (3)Ikitokea mwenyekiti hayupo, wajumbe wanaweza kumchagua

    mwenyekiti miongoni mwao ili kuongoza kikao.

    (4)Wingi wa wajumbe wa Baraza wataunda akidi pale tu

    kutakapokuwepo na angalau mjumbe mmoja anayewakilisha maslahi yawafuatao-

    (a) serikali;(b) waajiri; na(c) wafanyakazi

    (5) Maamuzi ya wajumbe wengi wa Baraza waliopo kwenye kikao

    utakuwa ndio uamuzi wa Baraza.

    (6) ikitokea kura zimelingana, mjumbe anayeongoza mkutano atakuwa

    na kura ya turufu itakayongezwa kwa upande wa wajumbe ili kukata

    shauri.

    (7) Baraza litalazimika kutunza kumbukumbu za vikao vyake.

    Usimamizi wa

    Baraza10.-(1) Katibu Mkuu-

    (a) atawateua watumishi waliopo wa Wizara kuwa wajumbewa sekretarieti ya Baraza ili kutekeleza utendaji kazi; na

    (b) anaweza kumteua afisa kutoka Wizarani kuwa Katibu waBaraza.

    (2) Baraza linaweza kuingia katika mkataba na watu wengine ili

    kusaidia utendaji kazi wake-

    (a) baada ya kushauriana na Katibu Mkuu; na(b) kupata kibali cha Katibu Mkuu kuhusiana na masharti ya

    mkataba.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    11/39

    11

    Taarifa ya

    mwaka yaBaraza

    11. Baraza litawasilisha Taarifa ya mwaka ya shughuli zake kila mwaka

    wa kalenda kwa Waziri kabla ya tarehe thelathini ya Juni ya mwaka

    unaofuata.

    SEHEMU YA III

    TUME YA UPATANISHI NA UAMUZI

    kuanzishwakwa Tume

    12. Kutakuwa na Tume ya Upatanishi na Uamuzi.

    Uhuru naHadhi ya Tume

    13.-(1) Tume itakuwa-

    (a) idara huru ya Serikali;(b) haitadhibitiwa au kuwajibika kwa mtu yeyote au mamlaka

    yoyote katika utendaji wake wa kazi; na(c) haitajihusisha na chama chochote cha siasa, wafanyakazi,

    waajiri, shirikisho la vyama vya wafanyakazi au waajiri.

    (2) Serikali, mamlaka za umma na vyama vingine vilivyosajiriwa na

    mashirikisho vitatoa ushirikiano ili kusaidia utekelezaji wa vipengele vya

    kifungu kidogo cha (1).

    (3) Kwa kuzingatia masharti ya sheria hii, sheria yoyote inayohusiana

    na idara ya umma itatumiwa na Tume na ofisi yoyote iliyoanzishwa chini

    ya Tume itakuwa ni ofisi ya umma.

    Kazi za Tume 14.-(1) Kazi za Tume zitakuwa-

    (a) kupatanisha mgogoro wowote ulioletwa mbele yake kwamujibu wa sheria yeyote ya kazi;(b) kuamua mgogoro wo wote ulioletwa kwa uamuzi kama-

    (i) sheria ya kazi inahitaji mgogoro utatuliwe kwauamuzi;

    (ii) wahusika wa mgogoro wamekubaliana mgogoroutatuliwe kwa uamuzi;

    Sura ya 366 (iii) Mahakama ya Kazi imepeleka mgogoro kwenye Tumeili utatuliwe kwa usuluishi kwa mujibu wa kifungu cha

    94(3)(a)(ii) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini;Sura ya 366 (c)kuwezesha uanzishwaji wa jukwaa la ushiriki wa wafanyakazi,

    kama ikibidi kufanya hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 72 cha

    Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini;(2) Tume inaweza-

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    12/39

    12

    (a) kwa maombi, kushauri na kutoa mafunzo kuhusiana nakuzuia na au kutatua migogoro kwa waajiriwa, waajiri,

    vyama vilivyosajiliwa na mashirikisho;(b) kujitolea kupatanisha migogoro ambayo haijaletwa mbele

    yake;

    (c) kuendesha na kusimamia uchaguzi au kura za chama chawafanyakazi au waajiri kama-

    (i) imetakiwa kufanya hivyo na Mahakama ya Kazi; au(ii) kwa maombi ya chama husika.

    Mamlaka ya

    Tume15.-(1) Katika utendaji kazi wake, Tume inaweza-

    (a) kuteua mkurugenzi, wapatanishi na wasuluishi;(b)kuwaagiza wapatanishi au wasuluishi kupatanisha na kuamuamgogoro kwa mujibu wa sheria za kazi yoyote;(c)kuanzisha ofisi katika maeneo na ngazi za kiutawala kadiri

    itakavyoamua;(d)kuanzisha vitengo vya Tume na kuvipa majukumu

    maalumu;

    (e)kuandaa kanuni ili kusimamia-(i) utawala wa ndani ya Tume;(ii) taratibu na mwenendo wa kuendesha upatanishi

    wa migogoro;

    (iii) taratibu na mwenendo wa kuendesha usuluishi wamigogoro;

    (iv) taratibu na mwenendo wa Kamati ya Hudumaza muhimu;(f) kuchapisha miongozo;(g) kuchapisha kanuni za maadili kwa ajili ya wapatanishi na

    wasuluhishi.

    (2) Tume, kwa notisi kwenye Gazeti la Serikali, itachapisha kanuni au

    miongozo kama ilivyoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) (e) na (f).

    Muundo waTume

    16.-(1) Tume itakuwa na-

    (a)Mwenyekiti, ambaye hatatakiwi kuwa-(i) mjumbe, afisa au mwajiriwa wa chama cha

    wafanyakazi, chama cha waajiri au shirikisho; au

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    13/39

    13

    (ii) mfanyakazi katika sekta ya umma;(b)makamishna wengine sita.

    (2) Mwenyekiti atateuliwa kutoka miongoni mwa watu wenye elimu nauzoefu na aliyejihusisha sana na masuala ya kikazi.

    (3) Rais atamteua-

    (a)Mwenyekiti, kutoka katika orodha ya watu watatuwaliopendekezwa na Baraza;

    (b)makamishna wawili waliopendekezwa na wajumbe wa Barazakuwakilisha maslahi ya wafanyakazi;

    (c)makamishna wawili waliopendekezwa na wajumbe wa Barazakuwakilisha maslahi ya waajiri;

    (d)makamishna wawili kuiwakilisha Serikali;(4) Uteuzi ulioainishwa kwenye kifungu kidogo cha (3) utafanywa kwa

    mapendekezo ya Waziri baada ya kushauriana na Baraza.

    Muda na

    Masharti yautumishi wa

    Makamishna

    17.-(1) Kamishna atashika madaraka hayo kwa muda wa kipindi cha

    miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena baada ya kipindi cha kwanza

    kuisha.

    (2) Ofisi ya Kamishna itakuwa si ya kudumu na kamishna hatalipwa

    mshahara bali atalipwa posho kwa jiri ya kuhudhuria mikutano, kusafiri

    na kujikimu kwa kiasi ambacho kitapangwa na Waziri kwa mapendekezo

    ya Katibu Mkuu baada ya kushauriana na Katibu Mkuu, Menejimenti ya

    Utumishi wa Umma.

    (3)Ofisi ya Kamishna itakuwa wazi endapo Kamishna

    (a)atajiuzulu;(b)ataondolewa ofisini kwa mujibu wa kifungu kidogo cha

    (4).

    (4) Rais, kwa mapendekezo ya Waziri atamwondoa Kamishna kwenye

    ofisi ikiwa Kamishna-

    (a) hawakilishi maslahi yaliyopelekea yeye kuteuliwa kwamujibu wa kifungu cha 16(3);

    Ikizingatiwa kuwa, kuondolewa kwa Kamishna kwa sababu hii

    kutafanyika endapo ameombwa na wawakilishwaji ambao

    Kamishna anawakilisha maslahi yao;

    (b) amefanya kosa kubwa la utovu wa nidhamu linalohusianana utendaji kazi wa kamishna;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    14/39

    14

    (c) hawezi kutekeleza majukumu ya kamishna (kwa sababu yaugonjwa au sababu nyinginezo);

    (d) hajahudhuria mfululizo vikao mitatu vya Tume bila ruhusaau sababu ya msingi;

    (e) ametangazwa kuwa amefilisika; au(f) amekutwa na hatia ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo

    bila ya kuwa na mbadala wa kulipa faini.

    (5)Waziri atashauriana na Baraza kabla ya kupendekeza kwa Rais

    kuondolewa kwa kamishna ofisini.

    (6) Wakati wo wote ofisi ya Kamishna inapokuwa wazi, Rais,

    atalazimika kuteua kamishna kujaza nafasi kwa kipindi kilichobaki na

    wakati akifanya uteuzi huo atazingatia masharti yaliyoainishwa chini ya

    kifungu cha 16(3).

    Mkurugenzi wa

    Tume18.-(1)Atateuliwa Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi wa Tume.

    (2)Tume baada ya kushauriana na Waziri, itamteua Mkurugenzi naNaibu Mkurugenzi miongoni mwa watu wenye elimu, ujuzi na uzoefu

    katika masuala ya uhusiano kazini na kuzuia na au kutatua migogoro.

    (3) Mkurugenzi atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa Tume na

    atawajibika kwa mujibu wa maelekezo na usimamizi wa Tume.

    (a) atawajibika kufanya maamuzi yanayohusiana na sera za Tumena shughuli za kila siku za kiutawala na usimamizi wa

    mambo ya Tume;

    (b) atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria zozote zakazi au majukumu yaliyokasimishwa kwa mkurugenzi naTume;

    Sura ya 366 (c)anaweza kupatanisha au kusuluisha mgogoro uliopo mbele yaTume kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

    (4) Isipokuwa kwa jambo lolote maalumu ambalo Tume itakielekeza

    vinginevyo kwa maandishi, Mkurugenzi atahudhuria mikutano ya Tume

    ila hatapiga kura.

    (5) Mkurugenzi kwa kushauriana na Tume anaweza kukasimisha

    majukumu yake yoyote au ya Tume kwa mpatanishi, msuluishi au

    mfanyakazi.

    (6) Bila kuathiri masharti ya Sheria hii, Mkurugenzi anaweza

    kupeleka Mahakama ya Kazi mgogoro wo wote uliopo mbele ya Tume

    kwa ajiri ya uamuzi kama inafaa kufanya hivyo kwa maslahi ya umma.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    15/39

    15

    Wapatanishi na

    Waamuzi19. (1) Tume itawateua wapatanishi na wasuluishi wengi kadiri

    itakavyoona inafaa kufanya kazi za Tume.

    (2) Tume inaweza kuteua wapatanishi na wasuluishi aidha wa mudawote au wa muda mfupi na kwa masharti itakayopanga, kwa kushauriana

    na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

    (3) Wakati wa kuteua mpatanishi, Tume itazingatia uundwaji wa

    Tume huru na ya kitaaluma.

    (4) Tume itaandaa kanuni za maadili kwa wapatanishi na wasuluishi

    na kuhakikisha wanazifuata katika utendaji kazi wao.

    (5) Tume itawajibika kusimamia na kuadabisha wapatanishi na

    wasuluishi ili mradi usimamizi na uadibishaji hautaingilia uhuru wa

    mpatanishi au msuluishi dhidi ya mgogoro wo wote.

    (6) Tume inaweza kumuondoa mpatanishi au msuluishi ofisini

    endapo-

    (a)amefanya utovu mkubwa wa nidhamu kuhusiana na kazi zampatanishi au muamuzi;

    (b)amekosa uwezo wa kutekeleza majukumu kama mpatanishiau muamuzi;

    (c)amevunja kanuni za maadili kwa mujibu wa kifungu kidogocha (4).

    Sura ya 366(7) Sheria hii au Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini haitazuia-

    (a)mtu kuteuliwa kuwa mpatanishi na msuluishi chini ya kifunguhiki;

    (b)mtu huyo kupewa jukumu la kufanya kazi zote kamampatanishi au msuluishi katika mgogoro.

    (8)Majukumu kwa mujibu wa kifungu kidogo cha 7(b) yatafanyika pale

    tu kutakapokuwepo na kanuni na miongozo imetolewa ili kusimamia

    utekelezaji wa majukumu hayo kwa mtu huyo.

    Mamlaka ya

    wapatanishi na

    wasuluishiSheria na. 8 ya

    2006

    20.- (1) Wapatanishi na waamuzi walioteuliwa kwa mujibu wa sheria hii

    wanaweza-

    (a)Kumuita mtu yeyote kumhoji au kuhudhuria siku yakusikilizwa kwa upatanishi au uamuzi kama mpatanishi au

    msuluishi anadhani uwepo wa mtu huyo utasaidia utatuzi wa

    mgogoro;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    16/39

    16

    (b)Kumuita mbele ya mpatanishi au msuluishi mtu yeyoteambaye anasadikiwa kuwa anamiliki au anashikilia kitabu cho

    chochote, nyaraka au kitu husika kwa utatuzi wa mgogorokwa ajili ya kuhojiwa na kutoa kitabu, nyaraka au kitu hicho

    halisia;

    (c)kulisha kiapo au kumthibitisha kusema ukweli kutoka kwamtu yeyote aliyeitwa kutoa ushahidi; na

    (d)kumhoji mtu yeyote kuhusu suala lolote muhimu kuhusiana namgogoro.

    (2) Ada ya ushahidi kwa mtu anayeitwa kutoa ushahidi mbele ya

    mpatanishi au msuluishi kwa mujibu wa kifungu hiki italipwa na upande

    unaomwita shahidi.

    (3) Ikiwa shahidi ameitwa na Tume yenyewe, gharama za shahidi

    zitalipwa na Mkurugenzi wa Tume.

    (4) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo (2), kwenye baadhi ya kesi,Kamishna anaweza kuamuru gharama za shahidi zilipwe na Mkurugenzi

    wa Tume.

    (5) Mtu yeyote, ambaye anafanya au anaacha kufanya jambo lolote

    liloainishwa kwenye aya (a) mpaka (i) za kifungu hiki kidogo, anafanya

    kosa la kuidharau Tume:

    (a) ikiwa mtu ameitwa mbele ya mpatanishi au msuluishiakashindwa kufika mahali, tarehe na muda uliopangwa

    kwenye samansi bila sababu ya msingi;

    (b)ikiwa baada ya kufika kwa mujibu wa samansi mtu huyoakashindwa kusubiri mpaka aruhusiwe na mpatanishi au

    msuluishi;

    (c)endapo atakataa kula kiapo au kuthibitisha kuwa atasemaukweli kama shahidi anapotakiwa kufanya hivyo na

    mpatanishi au msuluishi;

    (d)kwa kukataa kujibu swali lolote kikamilifu au kufikia kiwangocha uelewa au imani ya mtu huyo, isipokuwa pale ambapo

    sheria haimruhusu kufanya hivyo;

    (e)endapo mtu, bila kuwa na sababu ya msingi, anakataa kutoakitabu, nyaraka au kitu kilichoainishwa kwenye samansi;

    (f) endapo mtu huyo anamzuia mpatanishi au msuluishi kufanyakazi yoyote aliyopewa na au kwa mujibu wa sheria yoyote ya

    kazi;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    17/39

    17

    (g)ikiwa mtu huyo anatukana, anabeza au anamdharaumpatanishi au msuluishi, au anamdhulumu au anashinikiza

    mwenendo wa shauri vinginevyo au anahisia vibaya uamuziwa mpatanishi au msuluishi;

    (h)kwa makusudi anaingilia mwenendo wa upatanishi au uamuziau utovu wa nidhamu wa namna ye yote wakati wa mienendo

    hiyo;

    (i) kwa kufanya jambo lolote mbele ya Tume, ambalo endapojambo kama hilo likifanywa mbele ya mahakama ya sheria

    lingekuwa ni dharau kwa mahakama.

    Viapo 21. Kamishna, Mkurgenzi, Mpatanishi na Msuluishi atakula kiapo cha

    kutekeleza ipasavyo majukumu kama ilivyoainishwa kwenye jedwali

    ndani ya Sheria hii kabla ya kuanza kutekeleza majukumu ya ofisi.

    Wafanyakazi

    wa Tume22.(1) Mkurugenzi anaweza kuteua wafanyakazi baada ya kushauriana

    na Tume.

    (2) Tume baada ya kushauriana na ofisi ya Menejimenti ya Utumishi

    wa Umma itaamua malipo ya wafanyakazi.

    (3) Mkurugenzi atawajibika kwa kusimamia na kuadabisha

    wafanyakazi.

    Usimamizi wafedha za Tume

    23.-(1) Pesa na rasilimali za Tume zitahusisha-

    (a) pesa zilizotengwa na Bunge;(b) michango, misaada na urithi kadiri Tume itakavyopokea

    bila kuathiri uhuru wake;(c) pesa nyingine au mali zinazotokana na Tume-

    (i) chini ya sheria ye yote; au(ii) kwa namna nyingine yoyote katika utendaji wake

    wa kazi.

    (2)Tume itawajibika kwa Bunge katika mapato na matumizi yake.

    (3) Mwaka wa fedha wa Tume unaanza tarehe 1 Julai kila mwaka na

    kuisha tarehe 30 Juni ya mwaka unafuata.

    (4) Katika kila mwaka, kwa muda utakaopangwa na Waziri, Tume

    itawasilisha bajeti yake ya mwaka unaofuata pamoja na makadirio ya

    mapato na matumizi ya Tume na kiasi cha pesa kilichopendekezwa

    bungeni.

    (5) Uandaaji wa makadirio kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4)

    Tume itazingatia ushauri wa Waziri na Waziri wa Fedha.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    18/39

    18

    (6) Waziri atalazimika, baada ya kupokea bajeti ya mwaka

    kuiwasilisha bungeni.

    Hesabu na

    ukaguzi24.-(1) Tume-

    (a) itatunza vitabu vya mahesaabu ya fedha na kumbukumbuza mapato, matumizi, mali na madeni;

    (b) itachukua tahadhari kuhakikisha kuwa rasilimali za Tumezinatunzwa na kutumiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa;

    Sura ya 348 (c) itaandaa makadirio ya pesa kwa mujibu wa Sheria yaUsimamizi wa Fedha za Umma ya 2001.

    (d) itaandaa mahesabu ya mwaka katika shughuli zake zotekwa mujibu wa taratibu za kihasabu zilizokubalika.

    (2) Taarifa ya mahesabu ya Tume yatakaguliwa na Mdhibiti na

    Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa kila mwaka wa fedha.

    (3) Baada ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za

    serikali atathibitisha taarifa ya mahesabu ya Tume na kuiwasilishakwenye Tume.

    Mamlaka ya

    kuingiakwenye

    Mkataba

    25.-(1) Tume inaweza kuingia kwenye mkataba na mtu yeyote ili-

    (a)kufanya kazi kwa ajili ya Tume; na(b)kufanya kazi ye yote kwa niaba ya Tume.

    (2) Mtu yeyote ambaye ameingia mkataba na Tume atawajibika kwa

    matakwa yanayoitaka Tume kuwa huru chini ya kifungu cha 13.

    Kukasimisha

    Mamlaka yaTume

    26.-(1) Tume kwa maandishi inaweza kukasimisha madaraka, isipokuwa

    madaraka au kazi zilizoainishwa hapa chini, kwa mjumbe ye yote wa

    Tume, mkurugenzi, kamati ya Tume, mpatanishi au msuluishi

    aliyeteuliwa kwa masharti ya kifungu cha 19.

    (2) Madaraka ambayo Tume haitayakasimisha ni-

    (a) kumteua mkurugenzi;(b) kuteua mpatanishi na msuluishi kwa mujibu wa kifungu cha

    19;

    (c) kupitisha bajeti ya mwaka au bajeti ya ziada kwa ajili yakuiwasilisha kwa Waziri kwa mujibu wa kifungu cha 23;

    (3) Tume inaweza kuweka masharti kwenye kukasimu na kubadili aukufuta kukasimu kwa muda wowote.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    19/39

    19

    (4) Tume inaweza kubadili au kuondoa uamuzi wowote uliofanywa na

    mtu aliyekasimishwa madaraka kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1).

    Ukomo wa

    Uwajibikaji na

    Utoaji waTaarifa

    27.-(1) Tume itawajibika kwa hasara yoyote aliyoipata mtu yeyote kwa

    kufanya au kutofanya kitu Fulani kwa nia njema ili kutekeleza majukumu

    ya Tume.

    (2)Tume haiwezi kutoa kwa mtu ye yote au kwa mahakama ye yote

    taarifa au nyaraka iliyopatikana kwa misingi ya usiri au bila kuathirika

    wakati wa upatanishi.

    (3) Katika sehemu hii, Tume ni pamoja na Tume, Kamishna na mtu

    yeyote aliyeajiriwa, aliyeteuliwa au mwenye mkataba na Tume.

    Taarifa ya

    Mwaka ya

    Tume

    28.-(1) Ndani ya miezi sita baada ya mwisho wa mwaka wa fedha, Tume

    itaandaa na kuwasilisha Bungeni kupitia kwa Waziri Taarifa ya Mwaka

    kwa mujibu wa mwaka huo itakayokuwa na-(a) nakala ya taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya Tume;(b) taarifa ya mkaguzi ya mahesabu hayo;(c) taarifa ya utendaji wa Tume; na(d) taarifa nyinginezo ambazo Waziri anaweza kuhitaji.

    (2) Waziri atawasilisha taarifa Bungeni mapema iwezekanavyo.

    SEHEMU YA IV

    KAMATI YA HUDUMA MUHIMU

    Uanzishwaji

    wa Kamati yaHuduma

    muhimu

    29. Kutakuwa na Kamati ya Huduma muhimu ndani ya Tume

    Kazi za Kamati

    ya Hudumamuhimu.

    Sura ya 366

    30. Kazi za Kamati ya Huduma muhimu zitakuwa ni-

    (a) kuanisha huduma za msingi kwa mujibu wa kifungcha 76(3) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini; na

    (b) kuamua mgogoro wenye kutambua na au kutotambuakama mfanyakazi au mwajiri anahusika na huduma za

    muhimu zilizoainishwa.

    Uteuzi wakamati ya

    huduma zamsingi

    31.-(1) Waziri baada ya kushauriana na Baraza-

    (a)atateua wajumbe watano walio na ufahamu na uzoefu washeria za kazi na mahusiano ya kazi kama wajumbe wa

    Kamati ya Huduma muhimu.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    20/39

    20

    (b)atateua mjumbe mmoja kuwa mwenyekiti wa kamati.(2) Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati za Huduma muhimu

    (a)watateuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu; na(b)Wanaweza kuteuliwa tena baada ya kumaliza kipindi cha

    kwanza.

    (3) Waziri baada ya kupata mapendekezo kutoka kwa Katibu Mkuu

    anaweza akaamua posho za wajumbe wa Kamati ya Huduma za Msingi

    pale wanapoudhuria vikao, safari na mahitaji ya kujikimu.

    (4)Katibu Mkuu atashauriana na Katibu Mkuu Menejimenti ya

    Utumishi wa Umma kabla ya kutoa mapendekezo, kama ilivyoainishwa

    kwenye kifungu kidogo cha tatu (3)

    (5)Waziri atamuondoa mjumbe madaraka hayo ikiwa;

    (a)amejiuzulu kwa maandishi na kuwasilisha barua yake kwaKatibu Mkuu;

    (b)ana kosa kubwa la utovu wa nidhamu linaloendana na utendajiwa majukumu kama mjumbe.

    (c)hawezi kutenda kazi kama mjumbe (labda kwa sababu yaugonjwa au sababu nyingine yoyote ile); au

    (d)hakuudhuria kwa mfulilizo vikao vitatu vya Kamati yaHuduma muhimu bila ya kuwa na ruhusa au sababu ya msingi;

    (e)ametangazwa kuwa amefilisika;(f) ametiwa hatiani kwa kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo

    bila ya kuwa na mbadala wa kulipa faini.

    (6)Nafasi yoyote itakayoachwa wazi kwenye baraza la huduma muhimu,

    Waziri atateua mjumbe kujaza nafasi hiyo ili kumalizia muda uliobaki na

    uteuzi huu utazingatia vigezo vyote vilivyoainishwa kwenye kifungu

    kidogo (1).

    Mamlaka

    kamati yahuduma muhimu

    32.-(1) Kamati ya Huduma muhimu inaweza-

    (a)kumuita mtu yeyote kwenye shauri na kumhoji iwapo kamatiitaona ni vyema kuwa uwepo wa mtu huyo utasaidia utendaji

    kazi wake;

    (b)kumuita mtu yeyote ambaye anaaminiwa kuwa anamiliki auanamamlaka na kitabu chochote, nyaraka au kitu chochote

    husika kwa ajiri ya utendaji kazi, kufka mbele ya kamati ili

    kuulizwa na kutoa kitabu,nyaraka au kitu chochote.

    (c)kusimamia kiapo au kukiri, kutoka kwa mtu yeyote aliyeitwakutoa ushahidi; na

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    21/39

    21

    (d)Kumhoji mtu yeyote kwa suala lolote lile linalohusu utendajikazi.

    (2)Bila kujali matakwa ya kifungu cha kwanza (1) mtu yeyotehatatakiwa kujibu swali lolote au kutoa maelezo, kitabu, nyaraka au kitu

    chochote ikiwa kama kuna sababu za kisheria za yeye kutofanya hivyo.

    (3)Tume italazimika kulipia gharama za mashahidi watakaoitwa na

    kufika mbele ya mpatanishi au msuluhishi kwa mujibu wa jambo husika

    kulingana na kifungu hiki.

    Usimamizi wa

    kamati za

    hudumamuhimu

    33-(1) Kamati ya Huduma muhimu inaweza ikaweka kanuni kwa ajili ya

    uendeshaji vikao.

    (2) Tume itatumia wafanyakazi waliopo kuunda sekretarieti yaKamati ya Huduma muhimu ili kusaidia utendaji kazi.

    SEHEMU YA V

    BODI YA UJIRA

    Tafsiri 34.Kwa mujibu wa kifungu hiki, Waziri maana yake ni-

    (a) Waziri anayehusika na maswala ya utumishi wa umma iwapokwa mujibu wa vifungu hivi vitatumika kwenye sekta kwa

    ujumla au sehemu ya utumishi wa umma;au

    (b)Waziri anayehusika na masuala ya ajira bila kujali sektayoyote.

    Uteuzi wa Bodiya Ujira

    35.-(1) Waziri anaweza kuteua Bodi ya Ujira juu ya sekta ili kuchunguza

    malipo na mapatano na masharti ya ajira kwa kila sekta na eneo na

    italazimika kutoa taarifa za utafiti na mapendekezo kwa Waziri.

    (2)Waziri atalazimika kuchapisha notisi kwenye Gazeti la Serikali

    kuainisha-

    (a) majina ya watu walioteuliwa kama wajumbe wa Bodi yaUjira;

    (b)mambo ya kuzingatia kwenye uchunguzi , kama-(i) sekta na eneo linalotakiwa kuchunguzwa;(ii)

    aina na matabaka ya wajiriwawatakaochunguzwa

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    22/39

    22

    (iii) mambo ya kuchunguzwa;na(c) Mwaliko kwa umma ili kuleta maandishi yao ndani

    ya kipindi kitachokuwakimeainishwa kwenye notisi.Sheria Na. 8 ya

    2006(3) Bodi ya ujira itakua na wajumbe wafuatao ambao watateuliwa na

    Waziri-

    (a) mwenyekiti;(b)wajumbe wawili watakaoteuliwa na wajumbe wa Baraza

    ambao watawakilisha maslahi ya waajiriwa;

    (c)wajumbe wawili watakaoteuliwa na wajumbe wa Barazaambao watawakilisha maslahi ya waajiri;

    (d)wajumbe wawili watakaopendekezwa na Baraza kuwakilishamaslai ya serikali;

    (e)Mjumbe mmoja atakaeteuliwa na Waziri kwa mujibu wataaluma yake;

    (4) Mjumbe wa Bodi ya Ujira atashikilia madaraka hayo mpaka pale-

    (a)Waziri atakapoifuta Bodi ya Ujira;(b)Waziri atakapomuondoa kwamujibu wa kifungu kidogo cha

    (5)

    (5)Waziri-

    (a)anaweza kumuondoa mjumbe kwenye nafasi hii kwa mudawowote;

    (b)atalazimika kumuondoa mjumbe kwenye nafasi hii ikiwa-(i) amejiuzulu kwa maandishi na amewasilisha barua ya

    kujiuzulu kwa Katibu Mkuu;(ii) ana kosa kubwa la utovu wa nidhamu linalohusu na

    utendaji kazi kama mjumbe.

    (iii) hawezi kutekeleza majukumu yake kama mjumbe (labdakwa sababu za ugonjwa au sababu nyingine yoyote);

    (iv) hakuhudhuria kwa mfulilizo vikao vitatu vya Bodi yaUjira bila ya kuwa na ruhusa au sababu ya msingi;

    (v) ametangazwa kuwa amefilisika;(vi) ametiwa hatiani kwa kosa la jinai na kuhukumiwa

    kifungo bila ya kuwa na mbadala wa kulipa faini.

    (6) Kwa nafasi yoyote itakayoachwa wazi kwenye Bodi ya Ujira,

    Waziri atateua mjumbe ili kujaza nafasi hiyo kwa mujibu wa kufungu

    kidogo cha (2) na (3).

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    23/39

    23

    (7) Waziri baada ya kupata mapendekezo kutoka kwa Katibu Mkuu

    anaweza akaamua posho ya mjumbe wa Bodi ya Ujira anayopaswa

    kulipwa ahudhuriapo mkutano.(8) Katibu Mkuu atalazimika kushauriana na Katibu Mkuu

    Menejiment ya Utumishi wa Umma kabla ya kufanya mapendekezo

    yaliyoainishwa katika kifungu kidogo cha (7).

    Kazi na

    mamlaka ya

    Bodi ya Ujira

    36.-(1) Kazi za Bodi ya Ujira zitakuwa kwa mujibu wa hadidu za rejea

    kama vile-

    (a)kufanya uchunguzi dhidi ya malipo duni na masharti mengineya ajira;

    (b)kuhamasisha makubaliano ya pamoja kati ya vyama vyawafanyakazi vilivyosajiliwa, waajiri na vyama vya waajiri

    vilivyosajiliwa;

    (c)Kuandaa na kupeleka mapendekezo kwa Waziri dhidi yamalipo ya kima cha chini na masharti ya ajira.

    (2) Wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kulingana na hadidu za

    rejea, Bodi ya Ujira, inaweza-

    (a)kumhoji mtu yeyote ili kupata taarifa zilizo sawia nauchunguzi wowote husika;

    (b)kuhitaji kwa maandishi mtu yeyote kutoa taarifa,kitabu,nyaraka au kitu chochote halisia dhidi ya uchunguzi;

    (c)kuandaa mikutano ya hadhara;(d)

    kusaidia majadiliano dhidi ya malipo ya kima cha chini namasharti ya ajira kati ya vyama vya wafanyakazi

    vlivyosajiriwa, waajiri na vyama vya waajiri vilivyosajiriwa

    kwenye sekta;

    (3)Itakuwa ni kosa kukataa kutoa majibu ya swali lolote au taarifa

    yoyote,kitabu, nyaraka au kitu chochote bila ya kuwa na sababu zozote za

    kisheria;

    (4) Kwa maombi ya Bodi ya Ujira, Tume italazimika kutoa msuluhishi

    ili kusaidia majadiliano kwa mujibu wa kifungu kidogo (2)(d)

    Uchunguzi 37. Katika uchunguzi, Bodi ya Ujira italazimika kuzingatia yafuatayo-

    (a) Ibara ya 22 na 23 ya Katiba ya Jamuhuriya Muungano waTanzania;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    24/39

    24

    (b)mkataba wowote ulioridhiwa au mapendekezo ya Shirika laWafanyakazi Duniani, hata kama Tanzania siyo mdau wa

    mkataba huo;(c)mawasilisho yote na taarifa zingine zote zitawasilishwa kwenye

    Bodi;

    (d)na mambo mengine sawia yote ikiwemo-(i) uwezo wa waajiri kuendesha biashara zao vizuri(ii) utekelezaji kazi wa shughuli za kibiashara za kati, ndogo

    na ndogo sana;

    (iii) biashara mpya;(iv) gharama za kuishi;(v) kupunguza umaskini;(vi) kiwango cha chini cha kujikimu;(vii)malipo na makubaliano na masharti ya ajira kwa waajiriwa

    wa sekta ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

    (viii)makubaliano yoyote ya pamoja ya malipo na mapatano namasharti ya ajira kwenye sekta.

    (ix) tukio la sharti lolote la ajira lililopendekezwa kwa ajira yawakati huo au uuandaaji wa ajira;

    (x) jambo lolote husika;Taarifa ya Bodiya Ujira

    38.-(1) Baada ya uchunguzi kukamilika na baada ya kupitia mawasilisho

    yote, Bodi ya Ujira italazimika kuaandaa taarifa na kuiwasilisha kwa

    Waziri, taarifa ambayo itakuwa na-

    (a)utafiti wa Bodi;(b)mapendekezo yake kwenye-

    (i) ujira wa kima cha chini katika sekta na eneo;(ii) makubaliano na masharti yoyote ya ajira kwa mujibu wa

    eneo au sekta, ikiwemo utofauti wowote wa masharti ya

    msingi ya ajira kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha

    9 cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini.Sura ya 366 (2) Ikiwa katika matokeo yoyote ya usaidizi wa Bodi ya Ujira,

    vyama vya wafanyakazi, vyama vya wajiri vilivyosajiliwa na waajiri

    kwenye sekta wataadhimia makubaliano ya pamoja kwenye mambo

    yaliyoainishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) (b), Bodi-

    (a) italazimika kupendekeza ongezeko la muda wa mkataba kwawajiri na wajiriwa wote kwenye sekta na eneo ikiwa wahusikawa mkataba ni wawakilishi toshelevu wa wajiri na wajiriwa

    kwenye sekta na eneo; au

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    25/39

    25

    (b)inaweza kupendekeza ongezeko la muda wa mkataba auvifungu vya mkataba kwa wajiri wote kwenye sekta na eneo

    ikiwa wahusika wa mkataba si wawakilishi toshelevu wawajiri na wajiriwa kwenye sekta na eneo.

    (3) Kama mjumbe wa Bodi ya Ujira hatakubaliana na taarifa ya Bodi

    au sehemu yake yoyote ile, atalazimika kuwasilisha taarifa ndogo ambayo

    itaambatana na taarifa ya Bodi.

    Utoaji wa amriya ujira

    39.-(1) Baada ya kukubaliana na mapendekezo ya taarifa ya Bodi ya Ujira

    iliyoteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 35, waziri anaweza kutoa amri ya

    ujira inayobainisha kima cha chini cha ujira na masharti mengine ya kazi

    kwa waajiriwa kwa sekta yoyote na eneo la uchumi-

    (a)kwa mujibu wa mapendekezo;(b)kwa notisi kwenye Gazeti la Serikali; na(c)kutumika kuanzia tarehe iliyoanishwa kenye Gazeti la Serikali.

    (2 ) Amri ya ujira inaweza, kuhusu sekta na eneo-

    (a) ikaweka malipo ya kima cha chini;(b)ikatoa marekebisho ya kima cha chini cha malipo;(c) ikaweka makubaliano na masharti ya chini ya ajira ikiwemo

    utofauti wowote wa masharti ya msingi ya ajira kama

    ilivyoainishwa kwenye kwenye kifungu cha 13 cha Sheria ya

    Ajira na Mahusiano Kazini.Cap. 366Sura ya 366

    (d)ikarekibisha kadiri zitakavyojitokeza, kazi ndogo, kazi zanyumbani na kazi za mikataba;

    (e) ikaweka viwango vya chini vya afya kwenye makazi kwawajiriwa watakaokaa kwenye maeneo ya mwajiri;

    (f) ikaainisha masharti ya chini kwa wanafunzi;(g)ikarekebisha maeneo ya mafunzo na elimu;(h)ikarekebisha jambo lolote lile linlohusiana na malipo au

    makubaliano na masharti ya ajira.

    (3) Kifungu chochote cha amri ya ujira kinaweza kutumika kwa wote au

    baadhi ya waajiri na wafanyakazi kwenye sekta na eneo husika.

    (4) Ikiwa Waziri hatakubaliana na mapendekezo ya Bodi ya Ujira

    anaweza kuyarudisha mapendekezo hayo kwenye Bodi ili kupitiwa tena

    hali akiwa ametanabaisha mambo asiyokubaliana nayo.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    26/39

    26

    (5) Ikiwa Waziri hatatoa amri ya ujira ndani ya siku sitini baada ya

    kupokea taarifa ya Bodi au aamue kutotoa amri ya ujira kulingana na

    mapendekezo ya Bodi ya Ujira , Waziri atalazimika ndani ya siku kumina nne kuwasilisha taarifa na mapendekezo Bungeni, na kama

    itawezekana analazimika kuambatanisha sababu zilizopelekea kutotoa

    amri hiyo-

    (a)baada ya uamuzi, ikiwa Bunge linaendelea na kikao;(b)kama Bunge haliendelei na kikao, baada ya kuanza kikao

    kinachofuata cha Bunge;

    (6) Kila mwajiri analazimika kuwajulisha wafanyakazi kima cha

    chini cha ujira kilichopitishwa kwa kuweka notisi sehemu za kazi au kwa

    njia yoyote ile ambayo ni thabiti.

    Muda wa amri

    ya ujira

    40.-(1) Vifungu vya amri ya ujira vitatumika mpaka-

    (a)vitakaposimamishwa au kubatilishwa na Waziri kwa mujibu wakifungu kidogo cha (2)

    (b)vitakaporekebishwa au kutanguliwa na amri mpya ya ujira; au(c)Kutanguliwa na makubaliano ya pamoja

    (2) Waziri, baada ya kushauriana na Bodi ya Ujira na wahusika wa amri

    ya ujira, anaweza akasimamisha au akabatilisha mambo yote au sehemu

    tu ya amri kwa kuchapisha notisi kwenye Gazeti la Serikali.

    Matokeo yakisheria ya

    amri ya ujira

    41.-(1) Amri ya ujira itatumika kwa wote waajiri na wafanyakazi kama

    ilivyobainishwa kwenye notisi.

    Sura ya 366 (2) ikiwa kuna jambo linadhibitiwa na sehemu ya III ya Sheria yaAjira na Mhusiano Kazini,pia linadhibitiwa na amri ya ujira, vifungu

    vilivyoko kwenye amri ya ujira vitatumika.

    (3) Mfanyakazi yeyote atakayelipwa ujira chini ya kima kilichowekwa

    anaweza akafanya maombi kwenye mahakama ya Wilaya au ya Hakimu

    Mkazi ili kurudishiwa kiasi chote ambacho alikuwa hajalipwa.

    Usimamizi waBodi ya Ujira

    42.-(1) Kamishna wa kazi-

    (a) atalazimika kuwatumia wafanyakazi wa Wizara waliopo ilikusaidia utendaji kazi wa Bodi ya Ujira.

    (b)anaweza kumteua afisa kwenye Wizara kuwa Katibu wa Bodiya Ujira.(2) Bodi ya Ujira inaweza kuingia mkataba na mtu ili kusaidia

    utendaji kazi;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    27/39

    27

    (a)baada ya kushauriana na Kamishna wa kazi;na(b)kwa uthibitisho wa Katibu Mkuu kuhusu masharti ya

    kimkataba ya ajira;

    SEHEMU YA VI

    USIMAMIZI WA KAZI NA UKAGUZI

    Uteuzi waKamishna wa

    kazi na

    maaofisawengine.

    43.-(1) Rais atalazimika kumteua Kamishna wa Kazi na Naibu Kamishna

    wa Kazi, ambao watakuwa na wajibu wa kusimamia sheria za kazi.

    (2) Waziri atalazimika kumteua Msajili wa Vyama na Naibu Msajiri

    ambao watakuwa na wajibu wa kusimamia kanuni za vyama vya

    wafanyakazi, vyama vya waajiri na mashirikisho kwa mujibu wa sehemuya VI ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

    Sura ya 366 (3) Waziri atalazimika kumteua Kamishna wa Kazi Msaidizi ili

    kuongoza kitengo cha mahusiano kazini, ukaguzi kazini na mfuko wa

    jamii.

    (4) Kutakuwa na maafisa wa kazi wengi ilazimikavyo ili kusimamia

    utekelezaji wa sheria za kazi.

    Kakasimu 44.-(1) Kamishna wa Kazi, kwa maandishi anaweza kukasimisha kwa

    Naibu Kamishna wa Kazi, Kamishna wa Kazi Msaidizi au Afisa Kazi,

    majukumu au wajibu wowote wa kikamishna.

    (2) Msajili wa Vyama, kwa maandishi, anaweza kukasimisha kwa

    Naibu Msajiri mamlaka, majukumu au wajibu wowote wa usajili.(3) Kamishna wa Kazi au Msajili wa Vyama kama itakavyonekana

    inafaa, anaweza-

    (a)kuambatanisha masharti kwenye kukasimu na anawezakuyarekebisha au kuyatengua muda wowote;

    (b)Kubadilisha au kufuta maamuzi yaliyopitishwa na mtualiyekasimishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo (1) au (2)

    Mamlaka ya

    afisa kazi45.-(1) Kwa madhumuni ya usimamizi wa sheria za kazi, afisa kazi

    anaweza-

    (a)kwa muda wowote unaofaa akaingia eneo lolote akiwa na chetihusika chenye kumhalalisha na-

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    28/39

    28

    (i) kuhitaji eneo au sehemu yake isifanyiwe usumbufu wakatiwa ukaguzi itakapolazimu kufanya upekuzi;

    (ii) akafanya upekuzi na kutathimini taarifa yoyote,kitabu,nyaraka au kitu chochote halisia;

    (iii) kamata, kutoa nakala ya taarifa yoyote,kitabu,nyaraka aukitu chochote halisia;

    (iv) kuchukua sampuli ya kitu chochote alichokikuta;(v) kuchukua vipimo, masomo,rekodi au picha; na(vi) kumuhoji mtu yeyeote aliye kwenye eneo hilo;

    (b)amrisha, kwenye fomu teuzi kwa mtu yeyote kuja mbele yakekwa tarehe elekezi, muda na sehemu na kumhoji;

    (c)kuhitaji mtu yeyote ambaye ana mamlaka juu ya taarifayoyote,kitabu,nyaraka au kitu chochote halisia kutoa na

    kuelezea uingizwaji wa taarifa,kitabu,nyaraka au wa hicho kituhalisia;

    (d)kutathmini,kutoa nakala au kukamata kitabu chochote,nyarakaau kitu chochote kilichotolewa kwa mujibu wa aya (c);

    (e)kuchukua sampuli ya kitu chochote kilichotolewa kwa mujibuwa aya (c);

    (f) kutoa maelekezo kuhusu notisi zitakavyotakiwa kuwekwa kwamujibu wa sheria hii;

    (g)kumuomba askari wa jeshi la polisi kumsaidia kutekelezamadaraka yake kama ilivyoainishwa na hiki kifungu kidogo;

    (h)kumuomba mtu yeyote kumsaidia kama mtafsiri au vinginevyokwa utekelezaji wa madaraka yake kama ilivyoainishwa na hiki

    kifungu kidogo; na

    (i) Kufungua mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi au yaWilaya na kushtaki kwa niaba ya Kamishna wa Kazi pale tu

    kunapokuwa na uvunjifu wa sheria za kazi.

    Amri tekelezi 46-(1) Afisa wa kazi akiamini kuwa na sababu za msingi kwamba mwajiri

    hakutekeleza matakwa ya vifungu vya sheria ya kazi anaweza kutoa amri

    tekelezi kwenye fomu ya agizo-

    (2) Afisa kazi atalazimika kuwasilisha amri tekelezi kwa-

    (a)mwajiri;(b)kwa wajumbe wa chama chochote cha wafanyakazi

    kilichosajiliwa ambao wajumbe wake ni kati ya wafanyakaziwataaoathiriwa na amri hii;

    (c)kila mwajiriwa atakayeathiriwa na amri hiyo.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    29/39

    29

    (3) Kitendo cha Kutowalisha amri hii kwa watu kama ilivyoainishwa

    kwenye kifungu kidogo cha (2) (b) hakitaibatilisha amri.

    (4) Mwajiri atalazimika kubandika nakala ya amri kwa kila eneo lakazi lillotajwa kwenye amri hiyo ili wafanyakazi wanaoathiriwa na amri

    hiyo waweze kuipata.

    (5) Mwajiri atalazimika kutimiza matakwa ya amri tekelezi iliyotolewa

    kwa mujibu wa kifungu kidogo (1) kulingana na muda ulioainishwa

    kwenye amri hiyo.

    (6) Kamishna wa kazi atapeleka maombi kwenye Mahakama ya Kazi

    ili kutekeleza amri tekelezi ikiwa kama mwajiri hajaitekeleza na hajatoa

    pingamizi lolote dhidi ya amri hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 47(1).

    Pingamizi dhidi

    ya amritekelezi

    47-(1) Mwajiri anaweza akapinga kwa maandishi amri tekelezi

    iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha 46 ndani ya siku 30 tangukupokelewa kwa amri hiyo.

    (2) Mwajiri atalazimika-

    (a)kuwasilisha pingamizi kwa Kamishna wa kazi;(b)kuwasilisha nakala ya pingamizi kwa chama chochote cha

    wafanyakazi kilichosajiliwa kwa wajumbe husika kati ya

    waajiriwa.

    (c)Kubandika nakala ya pingamizi kwa kila sehemu ambayo nirahisi kwa wafanyakazi wanaoathiriwa na amri hiyo kuipata.

    (3) Kamishna wa kazi, kwa sababu za msingi, anaweza akapuuza

    pingamizi lililocheleweshwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1)

    (4) Baada ya kuzingatia mawasilisho yoyote ya mwajiri,wafanyakazi

    au chama chochote cha wafanyakazi kilichosajiliwa, kamishna wa kazi-

    (a) anaweza kuthibitisha, kubadilisha au kufuta amri;(b)atalazimika kubainisha kipindi ambacho mwajiri anapaswa

    kufuata dhidi ya uthibitisho wowote au mabadiliko ya amri;

    (5) Kamishna wa kazi atagawa nakala ya amri iliyotolewa kwa mujibu

    wa kifungu kidogo cha (4) kwa-

    (a) mwajiri(b)chama chochote cha wafanyakazi kilichosajiliwa ambao

    wajumbe wake ni kati ya wafanyakzi wanaoathiriwa na amri

    hiyo;na

    (c)Wafanyakazi wanaoathiriwa na amri hiyo;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    30/39

    30

    (6) Kitendo cha kutowasilisha nakala za amri hiyo kwa watu husika

    kama ilivyoainishwa kwenye kifungu kidogo cha (5)(b)na(c)

    hakitabatilisha amri hiyo.(7) Kama Kamishna wa kazi atathibitisha au atabadilisha amri

    iliyopitishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4) mwajiri atalazimika

    kuitekeleza amri hiyo kwa kipindi kitakachokuwa kimebainishwa na amri

    hiyo.

    (8) Kamishna wa kazi atapeleka maombi kwenye Mahakama ya Kazi ili

    kutekeleza amri tekelezi ikiwa kama mwajiri hajaitekeleza na hajakata

    rufaa kwa mujibu wa kifungu cha 48.

    Rufaa dhidi ya

    amri ya

    Kamishna wakazi

    48.-(1) Mwajiri anaweza kukataa rufaa kwenye Mahakama ya Kazi dhidi

    ya uamuzi wa Kamishna wa kazi ndani ya siku 30 tangu kupokelewa kwa

    amri hiyo.

    (2) Kwa maombi ya mwajiri Mahakama ya Kazi kulingana namakubaliano na masharti inaweza ikasimamsisha amri ya Kamishna wa

    Kazi mpaka pale amri ya mwisho ya Mahakama ya Kazi au rufaa yoyote

    dhidi ya maamuzi ya Mahakama ya Kazi.

    (3) Mahakama ya Kazi kwa sababu za msingi, inaweza ikapuuza rufaa

    yoyote iliyoletwa baada ya siku 30 kuisha.

    (4) Mahakama ya Kazi inaweza ikathibitisha, ikabadilisha au ikafuta

    amri, na amri liliyothibitishwa, iliyobadilishwa au kufutwa italazimu

    kuainisha kipindi ambacho mwajiri anapaswa kufuata amri

    iliyothibitishwa au iliyobadilishwa.

    Makosa dhidiya maafisa wa

    kazi

    49-(1) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) mtu yeyote atakayetenda

    lolote kati ya haya yafuatayo atakuwa na hatia ya kutenda kosa-

    (a) kukinza au kumzuia afisa kazi kutekeleza utendaji kazi auanapotumia mamlaka ya kiafisa;

    (b) kukataa au kushindwa kujibu, bila ya sababu za msingi swalilolote alilohoji afisa wa kazi kwa mujibu wa kifungu cha

    45(1)(a)(vi) au (1)(c);

    (c)kukataa au kushindwa kuitikia wito kwa mujibu wa kifungucha 45(1)(b)

    (d)kukataa au kushindwa kutoa taarifa yoyote, kitabu, nyaraka aukitu halisia baada ya kuhitajika kufanya hivyo kwa mujibu wa

    kifungu cha 45(1)(c)(e)kwa utashi kutoa taarifa za uongo au kumdanganya afisa kazi;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    31/39

    31

    (f) kukataa au kushindwa kutii ombi lolote halali la kisheria auamri halali ya afisa wa kazi au mtu yeyeote yule anayatekeleza

    majukumu kwa mujibu wa sheria hii, au sheria yoyote ile yakazi.

    (g)kwa uongo kudai kuwa yeye ni Afisa Kazi.(2) Haitakuwa kosa kukataa kujibu swali au kutoa taarifa yoyote,

    kitabu, nyaraka au kitu halisia ikiwa kuna sababu za kisheria za kutofanya

    hivyo.

    SEHEMU YA VII

    MAHAKAMA YA KAZI

    Uanzishwaji na

    muundo waMahakama yaKazi

    50.-(1) Kitaanzishwa kitengo cha Kazi cha Mahakama Kuu.

    (2)Kitengo cha Kazi cha Mahakama Kuu kitakuwa na-Sheria na. 8 ya2006

    (a) idadi ya majaji kama Jaji Mkuu atakavyoona inalazimu,ambapo Jaji Mkuu atamteua mmoja wao kuwa Jaji

    Mfawidhi

    (b)majopo mawili ya washauri wa mahakama walioteuliwa kwamujibu wa kifungu cha 53

    (3) Kitengo cha Kazi cha Mahakama Kuu kitakaa na Jaji pamoja na

    angalau washauri wawili wa mahakama walioteuliwa na Jaji anaeendesha

    shauri hilo kutoka kwenye jopo lililoteuliwa kwa mujibu wa kifungu

    kidogo cha (2)(b) cha kifungu hiki, ingawa sio lazima kwa Jaji kukaa na

    wazee wa mahakama-

    (a)kwenye mashauri ya maombi;(b)kama wahusika wa shauri watakubaliana;au(c)kama kuna ulazima wa kuamua shauri kwa uharaka zaidi.

    . (4) Uamuzi wa Mahakama ya Kazi utafikiwa pale tu baada ya

    kuzingatia mawazo ya washauri wa Mahakama kama yapo. Iwapo kama

    Jaji hatakubaliana na mawazo yao, atalazimiaka kutoa sababu za msingi.

    (5) Hakuna Mwenendo wa shauri katika Kitengo cha Kazi

    Mahakama Kuu hautakuwa batili kwasababu-

    (a)uteuzi wa washauri wa mahakama ulikuwa na dosari;(b)mwanzoni mahakama ilianza kusikiliza shauri bila ya kuwa na

    washauri wa mahakama;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    32/39

    32

    (i) mshauri wa mahakama hawezi kuendelea na shauri

    (ii) Jaji amemwondoa mshauri wa mahakama kwenye shaurikwa maslahi ya utendaji haki.

    (6) Jaji Mkuu anaweza akaondoa malipo ya ufunguzi wa shauri,

    malipo ya gharama na riba kwenye Mahakama ya kazi ya aina yoyote ile

    kwa kila mgogoro wa kikazi ulioletwa mbele yake.

    Mamlaka ya

    mahakama ya

    kaziSheria na. 8 ya

    2008

    51. Kwa mujibu wa katiba na sheria za kazi, Mahakama ya Kazi ina

    mamlaka ya pekee katika kutoa uamuzi kwa shauri lolote linalaotokana na

    sheria ya kazi na ajira za aina yoyote zinazotokana na sheria za kawaida

    zilizoandikwa ya sheria madhara, dhima ya mwakilishi au uvunjifu wa

    mkataba ndani ya mamlaka ya Mahakama Kuu.

    uwezo wa

    makakama ya

    kaziSheria na.8 ya

    2006

    52.-(1) katika utekelezaji wa utendaji kazi zake Mahakama ya Kazi

    itakuwa na mamlaka yote ya Mahakama Kuu katika kutoa hukumu, amri

    na uamuzi ambao ni sawia na mahakama inaweza kuzingatia-

    (a)kuendeleza makusanyo ya juu ya mitaji ya ndani ili kuongezana kukuza kiwango cha uchumi na kutoa nafasi nyingi za ajira;

    (b)kuendeleza na kupanua kiwango cha ajira;(c)kuendeleza malipo ambayo ni matokeo ya mipango, au malipo

    mengine ya motisha, ambayo yatawashawishi wafanyakazi

    kuongeza bidii ili kuongeza kiwango cha uzalishaji;

    (d)kuzuia ongezeko la ujira kwa wafanyakazi ili wasiathiriwekinyume na ongezeko la bei lisilokuwa na msingi au ulazima;

    (e)kutunza na kuhamasisha hali ya ushindani wa bidhaa za ndanikwenye soko la ndani pia na masoko ya nje;

    (f) kuanzisha na kuendeleza utofauti thabiti wa tuzo kati yavitengo tofauti ya ujuzi na viwango vya uwajibikaji;

    (g)ndani ya Jamhuri ya Muungano kuleta ulinganifu wa biasharana ulinganifu wa malipo;

    (h)kuhakikisha serikali inakuwa na uwezo endelevu wa kufadhilimipango ya maendeleo na matumizi ya mara kwa mara

    kwenye sekta ya umma;

    (i) kudumisha uhusiano usio na upendeleo baina ya sektambalimbali za jamii; au

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    33/39

    33

    (j)jambo lolote la kisayansi au kijamii lenye umuhimu mkubwaambalo mahakama inaona kuna ulazima wa kulizingatia;

    (2) Kwa mujibu wa maelezo ya kifungu kidogo cha (1) kwa maombiya upande wowote na baada ya kusikilizwa pande hizo au kwa maamuzi

    yake yenyewe bila ya notisi hiyo, Mahakama ya Kazi inaweza kwa hatua

    yoyote kuhamisha shauri lilioletwa mbele yake na yote yanayongojea

    uamuzi, kusikilizwa au kuondolewa;

    Ikizingatiwa kwamba mwafaka haujafikiwa na Mahakama ya Kazi

    yenye mamlaka ya peke yake kwenye migogoro inayotokana na sheria za

    kazi kwenda kwenye mahakama nyingine yenye mamlaka zaidi.

    (3) Shauri lolote litakalohamishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha

    (2), mahakama yenye mamlaka ya zaidi italazimika kulisikiza upya au

    kuanzia pale lilipoishia kabla ya kuhamishwa.

    washauri waMahakama

    Sheria Na. 8 ya

    2006

    53.-(1) Jopo la washauri wa mahakama kama ilivyoainishwa kwenyekifungu cha 50 (2)(b) litakaa kama ifuatavyo-

    (a) jopo la waajiri lililotokakana na orodha ya majina yawajumbe walioteuliwa na Baraza ili kuwakilisha maslahi ya

    waajiri;na

    (b)jopo la wafanyakazi lililotoakana na orodha ya majina yawajumbe walioteuliwa na Baraza ili kuwakilisha maslahi ya

    wafanyakazi.

    (2) Jaji Mkazi anaweza kumuondoa mtu kutoka kwenye jopo la

    washauri wa mahakama;

    (a) ikiwa mtu huyo amejiuzulu kwa maandishi na amewasilishabarua yake ya kujiuzulu kwa Msajiri wa Mahakama ya Kazi.

    (b)kwa kosa la utovu wa nidhamu kinyume na maadili yawashauri wa mahakama;

    (c) kwa kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu kamawashauri wa mahakama (kwasababu za ugonjwa au sababu

    zingine)

    (d)ikiwa mtu huyo hatahudhuria mashauri bila ya kuwa na ruhusaya Jaji.

    (e)kama mtu huyo ametangazwa kuwa amefilisika(f) ikiwa mtu huyo ametiwa hatiani kwa kosa la jinai na

    kuhukumiwa kifungo.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    34/39

    34

    Msajiri wa

    Mahakama yakazi

    Sheria Na. 8 ya2006

    54.-(1) Kutakuwa na Msajili wa Mahakama ya Kazi ambaye atateuliwa na

    Jaji Mkuu na atakuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Kazi

    ambaye kwa mujibu wa sheria hii atawajibika kwa Jaji Mfawidhi.

    (2) Kutakuwa na Manaibu Wasajili kwa idadi itakayotathiminiwa na

    kuteuliwa na Jaji Mkuu.

    Kanuni za

    Mahakama ya

    Kazi

    55.-(1) Jaji Mkuu, baada ya kushauriana na Waziri, ataandaa kanuni ili

    kusimamia utendaji na mwenendo wa mashauri ya Mahakama ya Kazi.

    (2) kanuni zitatolewa kwenye notisi na kuchapishwa kwenye Gazeti

    la Serikali.

    Uwakilishi

    kwenyemahakama yakazi

    56.Kwa kila mwenendo wa shauri mbele ya Mahakama ya Kazi mhusika

    katika shauri atasimama mwenyewe au atawakilishwa na-

    (a)afisa wa chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa au chama chawaajiri;

    (b)mwakilishi binafsi wa mhusika kulingana na uchaguzi wake;au

    (c)wakiliRufaa dhidi ya

    maamuzi ya

    mahakama yakazi

    57. Mhusika yeyote kwenye mwenendo wa mashauri ya Mahakama ya

    Kazi anaweza kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama kwenye

    Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa suala la kisheria tu.

    Hadidu za rejea

    za kamishna wa

    Kazi kwenyeMahakama ya

    Kazi naMahakama ya

    Rufaa ya

    Tanzania.

    58. Kamishna wa kazi anaweza-

    (1)kupeleka suala lolote la kisheria mbali ya suala la kisherialililorejewa kwenye kifungu kidogo cha (2) kwenye

    Mahakama ya Kazi;

    (2)kupeleka suala la kisheria kwenye Mahakama ya Rufaa ikiwa-(a)kama kuna utofauti wa maamuzi kwenye Mahakama

    ya Kazi juu ya suala lile lile la kisheria;na

    (b)wahusika wa shauri katika maamuzi hayo hawajakatarufaa.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    35/39

    35

    (3)Kamishna wa Kazi atalazimika kuwasilisha rejeo lolote kwamujibu wa kifungu kidogo cha (1) na (2) kwenye Baraza.

    (4)Shirikisho au Chama chochote kilichosajiliwa ambacho kinamaslahi kwenye rejeo lolote kwa mujibu wa kifungu kidogo

    cha (1) au cha (2) kinaweza kuiomba mahakama ambapo rejeo

    zimeelekezwa ili kujumuishwa kama mhusika kwenye

    mwenendo wa shauri.

    SEHEMU YA VIII

    MASUALA YA UMLA

    Usiri 59.-(1) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) itakuwa ni kosa kwa mtu

    yeyote kutoa taarifa yoyote inayohusiana na usimamizi wa fedha aumambo ya kibiashara ya mtu mwingine ikiwa taarifa hiyo ilipatikana

    kutokana na utendaji kazi au utekelezaji wa mamlaka yoyote

    yaliyoainishwa na sheria hii.

    (2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika ikiwa taarifa iliyotolewa

    ilizingatia matakwa ya sheria hii-

    (a) ili kumuwezesha mtu kutenda kazi zake au kutumia mamlakayaliyoainishwana sheria hii;

    (b) kwa mujibu wa sheria yoyote;(c)kwa lengo la uongozi yakinifu kwa mujibu wa sheria hii;(d)kwaajili ya usimamizi wa haki

    Uzito wauthibitishaji

    kosa

    60.-(1) Kwa kila shitaka lolote linalohusiana na uvunjifu wa sheria yoyote

    ile ya ajira itamlazimu mwajiri-

    (a)athibitishe kumbukumbu alizonazo ni halali na sahihi;(b)aliyeshindwa kutunza kumbukumbu zinazotakiwa kwa mujibu

    wa sheria yoyote ya ajira athibitishe dhidi ya kifungu

    chochote cha sheria hizo.

    (2) Katika mwenendo wowote wa madai yanayohusiana na uvunjifu washeria ya ajira-

    (a)mtu anayedai kuwa haki au ulinzi ulioainishwa na sheriayoyote ya ajira kuwa umevunjwa atalazimika kuthibisha

    ukweli huo ili kudhihirisha uvunjifu, isipokuwa tu palevifungu vya kifungu kidogo cha (1) (b) vitakapotumika; na

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    36/39

    36

    (b) mhusika anayeshutumiwa dhidi ya uvunjifu huo atalazimikakuthibitisha kuwa mwenendo mzima haukusababisha uvunjifu.

    Udhanifu kwa

    nani ni

    mfanyakazi.

    61. Kwa mujibu wa sheria ya ajira, mtu ambaye anafanya kazi au anatoa

    huduma kwa mtu yeyote anadhaniwa, mpaka itakapothibitishwa

    vinginevyo, kuwa ni mfanyakazi, bila kujali aina ya mkataba, ikiwa moja

    ya au zaidi ya vigezo vifuatavyo vitakuwepo;

    (a)namna ya mtu anavyofanya kazi iko chini ya uangalizi aumaelekezo ya mtu mwingine;

    (b)saa ya kazi ya mtu yako chini ya uangalizi au maelekezo yamtu mwingine;

    (c) labda ikiwa kuna mtu anafanya kazi kwenye chama mtu huyoni sehemu ya chama hicho;

    (d)mtu anayefanya kazi kwa mwingine kwa wastani wa saaangalau 45 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita;

    (e)mtu ni tegemezi kiuchumi kwa mtu mwingine ambayeanafanya kazi au anatoa huduma;

    (f) mtu amepewa vifaa vya biashara au dhana za kazi na mtumwingine; au

    (g)mtu anafanya kazi au anatoa huduma kwa mtu moja tu.Miongozo 62.-(1) Waziri baada ya kushauriana na Baraza, anaweza-

    (a)kutoa miongozo kwa usimamizi yakinifu wa sheria hii;(b)kubadilisha au kurejesha mwongozo mwingine;

    (2)Mwongozo wowote au mabadiliko yoyote dhidi ya , au marejesho

    ya, sheria au mwongozo italazimu kuchapishwa kwenye Gazeti la

    Serikali;

    (3) Mtu yeyote anayetafsiri au anayetumia sheria hii atalazimika

    kuzingatia mwongozo wowote uliochapishwa kwa mujibu wa kifungu

    hiki.

    (4) Mtu asipozingatia mwongozo, huyo lazima atoe sababu za

    kuthibitisha uhalali wa kutozingatia.

    Makosa

    Sheria Na.8 ya

    2006

    63.-(1) Itakuwa ni kosa kuvunja masharti yaliyoainishwa kwenye vifungu

    vya 36, 49, 59, au kifungu chochote au kanuni zilizoandaliwa kwa mujibu

    wa sheria hii.

    (2)Itakuwa ni kosa-

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    37/39

    37

    (a)kujaribu kumshawishi isivyopaswa mtu anayetekelezautendaji kazi kwa mujibu wa sheria hii au sheria nyingine

    yoyote ya ajira.(b)kupata au jaribu kupata nyaraka yoyote kwa njia ya

    udanganyifu, ulaghai, au kwa kuwasilisha au kutoa uongo au

    nyaraka za kughushi.

    (c)kujidai kuwa ni mtu yeyote aliyeteuliwa kwa mujibu wa sheriahii au sheria nyingine yoyote ya ajira;

    (d)kutoa taarifa za uongo huku akijua taarifa hizo ni za uongo;(e)kuficha au kumzuia mtu yeyote kutekeleza majukumu kwa

    mujibu wa sheria hii au sheria yeyote ya ajira;

    (f) kushindwa kutii au kwa makusudi akaenenda kinyume na amriyoyote ya kisheria au maelekezo yaliyotolewa au yaliyotokana

    na Mahakama ya Kazi au kwa mujibu wa sheria hii.

    Adhabu 64.-(1) Mahakama ya Wilaya inayojumuisha Mahakama ya Hakimu

    Mkazi itakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu kwa kosa lolote liloainishwa

    na sheria hii.

    (2) Mtu yeyote aliyekutwa na hatia dhidi ya makosa yaliyoainishwa

    chini ya kifungu cha 63(1) atawajibika-

    (a)kulipa fidia isiyozidi shilingi milioni tano;(b)kufungwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu;(c)kulipia fidia na kifungo;

    (3)Mtu yeyote aliyekutwa na hatia dhidi ya makosa yaliyoainishwa

    chini ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 63 atawajibika-

    (a)kulipia fidia isiyozidi shilingi milioni kumi;(b)kufungwa kwa kipindi cha miezi sita;(c)kulipia fidia na kifungo;

    Kanuni 65.-(1) Waziri baada ya kushauriana na Baraza, anaweza kuandaa kanuni

    na fomu za maagizo kwa lengo la uangalifu au kutekeleza kanuni na

    vifungu vya sheria hii.

    (2) Bila kuathiri sheria kwa ujumla wa mamlaka yaliyotolewa kwa

    mujibu wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, Waziri anaweza

    kuandaa kanuni za au kwa ajili ya yote au lolote kati ya haya-

    (a)maagizo ya mambo yote yaliobainishwa na sheria hii;(b)uchunguzi wa Baraza;(c)

    taratibu za kumteua mjumbe wa Baraza ili kuwakilishamaslahi ya mwajiri na wafanyakazi.

    (d)kusimamia uanzishwaji na mwenendo wa Kamati za Baraza;

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    38/39

    38

    (e)kuteua na kufuta Bodi za Ujira;(f) kusimamia uchunguzi, mikutano ya hadhara na kusaidia

    majadiliano ya Bodi ya Ujira;(g)taratibu za kusimamisha, kufuta, kurekebisha au kusimamisha

    Amri ya ujira;

    (h)kusimamia mamlaka ya afisa kazi dhidi ya utekelezaji wauchunguzi na mashtaka;

    (i) kusimamia utoaji wa amri tekelezi na mapingamizi dhidi yaamri hizo;

    (j) kusimamia uondoshwaji wa wajumbe, Makamishna,Wapatanishi na Wasuluhishi kutoka kwenye nyadhifa zao;

    (k)kusimamia ripoti za mwaka za Baraza na za Tume.Vifungu vya

    akiba na mpitoSura ya 366

    66.-(1) Kwa mujibu wa kifungu hiki sheria zilizofutwa maana yake ni

    sheria zilizofutwa kwa mujibu wa kifungu cha 103 cha Sheria ya Ajira naMahusiano Kazini.

    (2) Kamishna wa Kazi, Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi, Kaimu

    Msajili wa Vyama vya wafanyakazi na Maafisa wa Kazi walioteuliwa chini

    ya sheria zilizofutwa watahesabika kuwa wameteuliwa chini ya Sheria hii

    kama Msajili wa vyama, Kaimu Msajili wa vyama na maafisa wa kazi.

  • 7/27/2019 SHERIA YA TAASISI ZA KAZI, 2004

    39/39

    ______

    JEDWALI

    _________

    KIAPO CHA OFISI

    (Kwa mujibu wa kifungu cha 21)

    KIAPO CHA MAKAMISHNAMimi,..baada ya kuteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya

    Upatanishi na usuluishi , naapa/nathibitisha kuwa nitatekeleza majukumu yangu bila ya

    upendeleo na kwa aina yoyote ile, sitafichua taarifa zitakazokuja kwangu bila ya idhini ya

    Tume au Mahakama ya Kazi.

    MUNGU NISAIDIE

    Ameapa/amethibitisha mbele yangu leo.siku ya 20

    ..

    Rais

    KIAPO KWA MKURUGENZI, MPATANISHI NA MUAMUZI

    Mimi,..baada ya kuteuliwa kuwa

    Mkurugenzi/Mpatanishi/Msuluishi wa Tume ya Upatanishi na Usuluishi, naapa/nathibitisha

    kuwa nitatekeleza majukumu yangu bila ya upendeleo na kwa aina yoyote ile, sitafichua taarifa

    zitakazokuja kwangu bila ya idhini ya Tume au Mahakama ya Kazi.

    MUNGU NISAIDIE

    Ameapa/amethibitisha mbele yangu leo.siku ya 20

    ..

    Jaji wa Mahakama Kuu

    ___________________