timu ya rasilimali ya jamii ya ujamaa · ukijaribu kuratibu sheria mbalimbali za ardhi tanzania –...

11
Tanzania TIMU YA RASILIMALI YA JAMII YA UJAMAA Empowered lives. Resilient nations. Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

Upload: others

Post on 04-Feb-2020

28 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Tanzania

TIMU YA RASILIMALI YA JAMII YA UJAMAA

Empowered lives. Resilient nations.

Miradi ya EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Timu ya Rasilimali ya Jamii ya Ujamaa na haswa mwongozo na mchango wa Edward Loure Parmelo na Paul Senyael. Picha ni za Timu ya Rasilimali ya Jamii ya Ujamaa, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia.

Nukuu ZiadaUnited Nations Development Programme. 2012. Timu ya Rasilimali ya Jamii ya Ujamaa, Tanzania. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

MUHTASARI WA MRADITimu ya Rasilimali ya Jamii ya Ujamaa inafanya kazi kaskazini mwa Tanzania, kutetea haki za jamii za wafugaji, wakulima-wafugaji na wawindaji ambao wengi wao wameathiriwa vibaya na kuwepo kwa maeneo tengefu makubwa nchini. Kikundi hiki kinatumia mbinu inayojikita katika sheria za ardhi za vijiji ambazo huziwezesha jamii husika kutunga sheria ndogo na kuweka mipango ya matumizi ya ardhi yao na pia kimejikita katika kuboresha uwezo wa jamii hizi kusimamia mfumo wa bayoanuwai.Kwa kuyasaidia makundi yaliyowekwa pembezoni katika mchakato mgumu wa kupata haki ya ardhi, asasi hii isiyo ya kiserikali imefanikiwa kufanya mikataba mikubwa ikiwemo uwekaji wa mipaka ya kisheria ya kijiji cha kwanza cha wakusanya matunda Tanzania. Kukuza uwezo, usuluhishaji wa migogoro, na ustawi endelevu wa maisha ndiyo msingi wa mpango huu na vinasaidia kuongeza ufanisi wa jamii hizi kama wasimamizi wa ardhi na rasilimali.

MUHTASARIMSHINDI WA TUZO YA EQUATOR: 2008

ULIANZISHWA: 1998

ENEO: Northern Tanzania

WANAOFAIDI: Pastoralist & agro-pastoralist communities

MAZINGIRA: Community-conserved areas

3

TIMU YA RASILIMALI YA JAMII YA UJAMAATanzania

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 5

Matokeo ya Kimazingira 7

Matokeo ya Kijamii 7

Matokeo ya Kisera 9

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 10

Maono 10

Wahisani 10

4

Timu ya Ujamaa ya Rasilimali za Kijamii (UCRT) ni asasi isiyo ya kibiashara ya mazingira na haki za kijamii inayofanya kazi na makundi ya kijadi yenye tamaduni mbalimbali kaskazini mwa Tanzania. Jamii lengwa ni zile zinazotegemea mifumo ya usimamizi wa rasilimali za kijamii katika kuendesha maisha yao.

Hatari zinazozikabili jamii za pembezoni

Kazi ya UCRT ilianza mwaka 1998 chini ya asasi iliyokuwa ikiitwa TAZAMA Trust kabla ya kusajiliwa rasmi. Asasi hii inalenga kukuza uwezo wa jamii za wachache kaskazini mwa Tanzania hususani jamii jamii za wafugaji, wawindaji na wakusanya matunda kama vile Wamasai, Wabarabeigi, Waaki, Wasonjo na Wahadzabe. Maisha ya jamii hizi yanakabiliana na hatari ya matumizi makubwa ya rasilimali za asili, kutengwa kisiasa, kupungua kwa rasilimali na elimu duni. Kutengwa kwa jamii hizi kumeongezeka zaidi kwa sababu za kijiografia hasa kuwa mbali na miji. Kwa mfano, kijiji kilichopo karibu kabisa na Arusha kipo umbali wa kilometa 85, wakati vijiji vingine vipo umbali wa kilometa 370 kutoka mji wa karibu.

Kuandaa sheria na sera kwa ajili ya jamii za pembezoni

Lengo la UCRT ni kuboresha ustawi wa vijiji katika jamii za maeneo ya pembezoni kupitia usimamaizi wa kijamii wa maliasili. Usimamizi jumuishi wa maliasili ni msingi mkuu wa kazi ya asasi hii ambao umejengwa juu ya taasisi za kimila, njia za kijamii za usimamizi wa ardhi na mifumo ya kijadi ya usimamamizi wa rasilimali. UCRT inaziangalia sheria na sera kama vyombo vya kuzijengea uwezo jamii zinazotegemea rasilimali na huku wakitambua vizuizi wanavyoweza kukutana navyo (na mara nyingi hukutana navyo). Kwa kusaidia usimamizi wa rasilimali wa kijamii, taasisi za kijadi, na haki za ardhi za kijamii, asasi inalenga siyo tu kuihifadhi bayoanuwai ya Serengeti na Tarangire lakini pia kuzilinda jamii hizi kutokana na vitendo visivyo halali na vya kinyonyaji vya unyang’anyaji wa ardhi.

Asasi hii inafanya kazi na vijiji 40 katika wilaya sita za mikoa ya Arusha, Manyara na Shinyanga. Mafunzo ya kujenga uwezo yanatolewa katika kila kijiji kuhusu namna ya kushawishi na kubadili michakato iliyopo ya sera na sheria. Uboreshaji wa serikali za mitaa umetoa fursa kwa jamii zinazotegemea rasilimali kupata haki za pamoja za kumiliki mali na rasilimali. Hata hivyo, ili kunufaika inatakiwa kufahamu ni wapi na ni jinsi gani ya kuzipata haki hizo. Kwa sababu hiyo, UCRT wamejikita kwenye elimu na mafunzo kwa viongozi wa jamii ili kuwajengea uwezo wa kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa sera na mifumo ya sheria inayotawala upatikinaji wa ardhi na rasilimali.

Historia na Mandhari

55

Majukumu Makuu na Ubunifu

UCRT inafanya kazi na wafugaji, wakulima wanaofuga na wawindaji na wakusanya matunda. Lengo ni kuzisaidia jamii hizi za pembezoni kupata haki ya ardhi na rasilimali, kuboresha uwezo wao wa usimamizi wa maliasili, kukuza maarifa na vitendea kazi katika usimamizi wa rasilimali zao kwa ufanisi zaidi, kuanzisha maeneo tengefu ya kijamii kwa kuzingatia njia za kijadi za usimamizi wa ardhi na kudumisha manufaa ya kiuchumi yanayotokana na ardhi yao na mifumo ya kimazingira (hususani kupitia ecotourism). Eneo husika katika mpango huu ni kaskazini mwa Tanzania ikiwemo maeneo yenye utajiri wa bayonuwai ya Serengeti na Tarangire. Kazi ya UCRT ipo katika maeneo manne muhimu: matumizi ya ardhi, usimamizi wa maliasili, uwezeshaji wa jamii na utetezi.

Mifumo ya matumizi na upatikanaji wa ardhi

Kipengele kimoja muhimu cha kazi ya UCRT ni kuandaa mipango ya maendeleo inayozihakikishia jamii zinapata haki ya kumiliki mali na rasilimali. Tangu kuwepo kwa Sheria ya Ardhi ya 1999, inatakiwa kuwe na rekodi rasmi ya kusaidia madai ya ardhi. Kupata hati ya kijiji au ya kimila ya umiliki wa ardhi jamii ni lazima ziandae mipango ya matumizi ya ardhi zikibainisha kusudi la matumizi kwa kila eneo. UCRT imekuwa ikijihusisha na upimaji wa maeneo, uchoraji wa ramani na uwekaji mipaka wa ardhi ya jamii ili kupunguza migogor ya kijamii katika urasmishaji wa umiliki. Mbali na kusaidia katika kuandaa rasimu za mipango ya matumizi ya ardhi, UCRT imesaidia pia kurahisisha utekelezaji wa mipango katika vijiji.

Usimamizi wa kijamii wa maliasili na maisha

Eneo lingine muhimu katika kazi ya Ujamaa ni usimamizi wa maliasili. Nia ni kuhakikisha kwamba vijiji vina uwezo wa kubainisha na kurekodi maliasili walizonazo na kuweza kuzitumia kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi na kijamii. Ili kuwasaidia katika mchakato huu, UCRT huunda tume katika mabaraza ya vijiji kusimamia mipango ya rasilimali na matumizi yake. Zoezi la uchoraji ramani za rasilimali limesababisha kuwepo kwa ushirikiano kati ya jamii, waendeshaji wa

shughuli za utalii wa kiutamaduni, kuanzisha makampuni ya utalii ambayo yanaziongezea jamii kipato cha ziada. Katika kufanya hivyo, UCRT imehakikisha kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya biashara ya utalii na jamii, hasaa katika maeneo ambayo watu wana ardhi na rasilimali.

Uwezeshaji wa jamii na ujenzi wa taasisi za kijadi

Kazi nyingine ya UCRT ni uwezeshaji wa jamii. Kazi kubwa katika Nyanja hii inahusisha kufanya kazi na mabaraza ya vijiji ambavyo ni vyombo vya kiutawala vilivyowekwa na serikali kuu ingawa watendaji wake wamepewa mafunzo rasmi kidogo sana kuhusu viwango vya utawala bora, mipango ya usimamizi wa fedha (ikiwemo mgawanyo wa mapato ya kijiji), na majukumu ya usimamizi wa ardhi. ECRT imeliziba pendo hili kwa kutoa warsha kwa wajumbe wa mabaraza ya kijiji kuhusu baadhi ya masuala haya na kwa kuweka taarifa za msingi kuhusu kazi yao. Kila baraza la kijiji limeundwa kamati tatu: usalama, usimamizi wa fedha na mipango, na masuala ya maendeleo kwa ujumla. UCRT hutoa mafunzo muafaka katika maeneo haya yote kwa wanakijiji wanaoshiriki katika kamati maalum. Mafunzo yanahusisha pia taarifa kuhusu sheria za ardhi na rasilimali kama zile zilizomo mipango ya uboreshaji wa serikali za mitaa. Kupitia mafunzo haya, jamii zinasaidiwa kuelewa vizuri zaidi haki zao za ardhi chini ya sheria za Tanzania. Zaidi ya hayo, habari hutolewa kuhusu kazi na majukumu ya mabaraza ya ardhi ya vijiji na mikutano mikuu ya vijiji ambayo ndiyo inayohusika na utungaji wa sheria ndogo.

Ushawishi na utetezi

Suala jingine muhimu katika kazi ya UCRT ni kuelimisha jamii kuhusu sera za serikali zilizopo na zile zinazoundwa ili kuwapa taarifa zinazohitajika kuweza kupigania haki zao na kushawishi mabadiliko ya sera.mojawapo ya sera ambazo zimeingizwa katika mafunzo haya ni Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA), ambao unatoa mwelekeo wa kitafifa katika utekelezaji wa Dira 2025. Malengo ya mkakati huu yamejikita katika ukuzaji wa

66

uchumi na kupunguza umasikini, kuboresha maisha na ustawi wa jamii na kuboresha utawala na uwajibikaji. Mwongozo unatolewa pia kuhusu mipango mingine muhimu kama vile Programu ya Urasimishaji wa Mali na Biashara (MKURABITA) ambao umelenga kurahisisha ubadilishaji wa mali na biashara zisizo rasmi ili ziweze kuwa rasmi na kuendeshwa na vikundi; Programu ya Mabadiliko ya Serikali za Mitaa, ambayo inalenga kuzipa nguvu mamlaka za serikali za mitaa katika utowaji wa huduma sawa za jamii, na Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Sheria za Ardhi ambao umekuwa ukijaribu kuratibu sheria mbalimbali za ardhi Tanzania – Sheria ya Ardhi (1999), Sheria ya Ardhi za Vijiji (1999), na Sheria ya Mahakama ya Migogoro ya Ardhi (2002).

Kupitia mafunzo yanayotolewa maeneo ya kazi, UCRT imeweza kukuza elimu kuhusu sera hizi na jinsi zinavyohusiana na usimamizi wa kijamii wa maliasili. Jamii zinashauriwa jinsi ya kukabiliana na sheria mpya na namna ya kutoa hoja kwa ajili ya kurekebisha vipengele vyenye mashaka. Kwa mfano, kujenga uwezo wa jamii limekuwa ni suala muhimu sana sehemu ambazo jamii zimenyang’anywa ardhi yao kwa ajili ya uhifadhi wa kibiashara. Ingawa UCRT hufanya kazi kama chombo cha kutoa angalizo la mapema kwa jamii kuhusu sheria za ardhi zisizo za haki, wameweza pia kuzipa jamii za wenyeji sauti ya moja kwa moja kuhusu michakato ya kisheria. Jamii zimewezeshwa kuwasiliana na kuwashawishi wanasiasa wa ngazi za chini, na walipewa nafasi ya kusikilizwa bungeni kwa ajili ya Sheria ya Wanyama pori (2010) na Sheria ya Mifugo Tanzania (2010).

“Waandaaji wa sera lazima wazingatie mahitaji ya jamii za wenyeji kabla ya kuweka sera. Kwa namna hiyo hiyo, njia za jadi za uhifadhi wa wanyamapori zimekuwa na mafanikio kwa miaka mingi na ni lazima zitambuliwe. Uhifadhi na ustawi wa maisha ya jamii za wenyeji siyo malengo

yanayokinzana na yanaweza kutekelezwa kwa pamoja.” Edward Loure Parmelo, Timu ya Rasilimali ya Jamii ya Ujamaa

7

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRAMradi wa Ujamaa umekuwa na manufaa makubwa katika bayoanuwai ya kaskazini mwa Tanzania hasa kutokana na uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi ya jamii katika maeneo ya wanyamapori ya mazingira ya Serengeti. Mifano ya maeneo ya hifadhi ni Loliondo na Simanjiro ambayo yana idadi kubwa ya pofu, mbwa mwitu, duma na choroa.

Eneo muhimu katika kazi ya UCRT limekuwa ni kuweka uwiano wa vipaumbele vya uhifadhi, mahitaji ya jamii ya rasilimali na utalii wa mazingira. Asasi hii imesaidia kuwepo kwa shughuli za utalii wa kimazingira n maslahi mengine ya kibiashara kutambua faida za kuhifadhi uoto kwa ajili ya mifugo na wanayamapori na siyo kuigeuza ardhi kwa ajili ya matumizi ya kilimo. Kupitia programu yake ya ‘easement’, makampuni ya utalii hulipa dola za kimarekani 5,000 kila mwaka kwa vijiji vinavyomiliki ardhi karibu na mbuga ya Tarangire (ambako pofu huja kwa ajili ya malisho), kwa ajili ya jamii kujitolea kuhifadhi ardhi. Kuna mikataba baina ya vijiji na wenye makampuni ya utalii ambayo inahakikisha kwamba uhifadhi wa bayoanuwai na ustawi wa kijamii na kiuchumi wa jamii husika vinazingatiwa.

Kadhalika, UCRT imefanya kazi ya kupunguza migogoro kati ya wafugaji na wahifadhi wa wanyamapori ambayo imekuwa ikisababisha kutokuelewana kati ya jamii za weneyeji na wahifadhi. Kwa mfano, pofu kutoka Hifadhi ya Taifa ya Tarangire huhamia Simanjiro wakati wa masika na kusambaza magonjwa kwa mifugo. Hii inamaanisha kwamba jamii haziwezi kulisha mifugo katika maeneo haya. UCRT imefanya kazi na jamii zilizoathiriwa kuanzisha jitihada mbadala za kuahakikisha afya ya mifugo na kuyalinda makundi ya pofu.

Upatikanaji wa haki za ardhi na rasilimali kwa jamii za wenyeji umeleta manufaa ya kibayoanuwai kwa usimamizi wenye ufanisi wa ardhi na kwa kutoa uhakika wa uwekezaji wa muda mrefu. Mfano unaojulikana wa jamii kupigania ardhi yake ni wa Hanang. Mnamo miaka ya 1970, shirika la kiserikali la NAFCO lilimiliki ekari 100,000 za

ardhi kwa ajili ya kilimo cha ngano na kuwaacha maelfu ya wakazi wakiwa hawana ardhi. Baadhi ya usimamizi mbovu wa mashamba na kushindwa kwa mradi wa ngano, serikali iliamua kurejesha kiasi fulani cha ardhi kwa wafugaji wa Hanang. Mchakato huo ulitekwa na wanasiasa wenyeji walioamua kuwapa ardhi wakulima wa Mlima Hanang badala ya wafugaji. Kwa msaada wa Oxfam Ireland, UCRT iliweza kushinikiza serikali kurejesha ardhi kwa wafugaji.

Hatimaye, ekari 28,000 za ardhi zilirejeshwa kwa vijiji vya Ming’enyi, Mulbadaw, Gidika, Basatu na Gawidu, ikizifaidisha zaidi ya familia 8,000. Mfano mwingine wa ushawishi wa UCRT kwa ajili ya kurejesha ardhi kwa jamii ni ule wa Emboreet ambako wafugaji wanaoishi upande wa mashariki ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire walinyang’anywa na serikali hekta 29,00 za ardhi. Ardhi hiyo ilichuliwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa kilimo cha biashara cha maharage. Mradi uliposhindwa, serikali ilidai kuwa na haki ya kuendelea kuimiliki ardhi badala ya kuirejesha kwa wafugaji. UCRT ilishirikiana na Chama cha Hifadhi ya Wanyamapori kusaidia kuwarejeshea ardhi kwa wamiliki halali. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, hekta zote 29,000 za ardhi zilirejeshwa kwa jamii.

MATOKEO YA KIJAMIIMoja ya athari kuu za kuchumi za kazi ya UCRT imekuwa ni kuongeza ushirikiano na sekta binafsi ambao umewezesha vijiji kupata kipato kutokana na uhifadhi wa wanyamapori kwa njia ya shughuli za kijamii za utalii wa mazingira. Katika Wilaya ya Ngorondoro, vijiji saba vya Wamasai vimetumia utalli wa mazingira kuongeza vipato vyao kutoka dola za kimarekani 30,000 mwaka 1998 hadi dola 300,000 mwaka 2007. Vijiji vinavyoshiriki vimejenga boma za kiutamaduni ambako wanawake wanazalisha bidhaa za kibunifu ambazo zinauzwa kwa watalii. UCRT iliendesha mafunzo katika kila kijiji kuhusu usimamizi wa jamii wa maliasili na uendelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.

Ili utalii wa mazingira usijitenge na shughuli za kiuchumi na kiutamaduni, UCRT ilisisitiza kuwepo kwa uwiano wa vipaumbele vya mazingira na masuala mengine ya kimazingira na kiuchumi. Vijiji shiriki vilipatiwa pia msaada wa kisheria wakati wa majadiliano na waendeshaji wa makampuni ya utalii, ili kuhakikisha kuwa mikataba isiwapendelee wadau wa sekta binafsi. Kwa mfano, katika kijiji cha Engaresero, UCRT ilisaidia kuandaa mkataba shirikishi na wa wazi kati ya jamii na kampuni ya utalii ambayo, pamoja na mambo mengine, ulitambua haki ya jamii ya maliasili. Biashara ya utalii wa mazingira ilizalisha ajira kwa ajili ya vijiji tisa na pia pato la mwaka 2009 lilifikia dola 30,000. Mapato yamekuwa yakiwekezwa kwenye miundombinu ya shule, ada za shule, mipango ya kuweka na kukopa kwa ajili ya wanawake na vijana, utoaji wa huduma na ujenzi wa kituo cha afya.

UCRT hufanya kazi kupitia Mpango wa Maendeleo wa Wafugaji Olalaa, Kikundi cha Wanawake cha Kujiongezea Kipato Simanjiro na makundi ya wanawake wa Hanang kuwezesha na kusaidia miradi ya shughuli mbadala za kimaisha kwa wanawake wa jamii za wenyeji. Hadi sasa, zaidi ya vyama vya ushirika vya wanawake 20 vimeundwa. Kila kikundi kinajihusisha na kilimo cha kujikimu katika mashamba madogo ya ekari mbili. Kila kikundi kimepewa jembe la kukokotwa na ng’ombe ambalo limepunguza ugumu wa kazi za mkono na kuongeza uzalishaji. Vyama vya ushirika vya wanawake vimepia mbuzi (zaidi ya 600 hadi sasa), ili kuwasaidia kuongeza shughuli za kujiendeshea maisha kupitia ufugaji. UCRT pia imevitumia vikundi hivi kuzalisha aina mbalimbali za mazao ya kilimo na kusambaza zaidi ya kilo 300 za mbegu za maharage na zaidi ya kilo 100 za mbegu za mahindi.

Programu za kuwawezesha wanawake zinaendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la Wanawake Wafugaji la Tanzania: Asasi Isiyo ya Kiserikali (NGO) inayofanya kazi na vikundi vya wafugaji kaskazini mwa Tanzania kutetea haki za wanawake na elimu kwa wasichana wa kimasai. Tangu kuanzishwa kwake, UCRT imetambua kuwa uwezeshaji wa wanawake ni kipengele muhimu katika kazi yake ya kutafuta haki za jamii kumiliki mali na ardhi. Wanatambua pia kuwa jamii iliyogawanyika haiwezi kuzitetea haki za pamoja

kwa mafanikio kama jamii ambayo inazingatia kwa usawa haki za wanajamii wote. Kwa jinsi hiyo, UCRT iliwaunganisha wanawake ili wajihusishe na waonekana katika uandaaji na utekelezaji wa miradi ya kijamii. Kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali na asasi zisizo za kiserikali, UCRT hutoa mafunzo kwa wanawake kuhsu masuala ya haki ya ardhi, kujitegemea kiuchumi na kuwa na shughuli mbalimbali za kuendesha maisha (ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa shanga, utengenezaji wa sabuni na utalii wa mazingira). Mbali na kuwa washiriki katika kutetea haki za ardhi, wanawake wa jamii za wenyeji wamekuwa viongozi na vinara wa haki za jamii za umiliki wa mali.

Pia asasi hii imejishughulisha na kuendeleza elimu ya kusoma na kuandika kwa vijana waliotengwa kijiografia, kiuchumi na kijamii. UCRT ina programu inayosaidia kulipa ada za masomo ya sekondari kwa watoto wanaotoka katika familia masikini ambao wamefaulu mitihani yao shule za msingi lakini hawawezi kusoma kwa sababu za kifedha. Wakati ripoti hii inaandikwa, zaidi ya wanafunzi 150 walikuwa wakisaidiwa kupata elimu kupitia mpango huu. Udhamini wa elimu unatolewa pia kwa familia za wafugaji jamii za wawindaji za Wahadzabe na Waaki kwa ajili ya kugharamia ada, mavazi na usafiri. Kwa kupitia mpango unaofanana na huu, UCRT iligaramia ujenzi wa kituo cha yatima na kwa inasaidia watoto yatima 33 kupata elimu ya sekondari. Sharti muhimu la udhamini wa UCRT kwa ajili ya ada za shule ni kwa wahitimu kurejea kijijini kwa angalau miaka mitatu na kufanya kazi kama waelimisha rika. Wanafunzi wanapata msaada kupitia UCRT hukutanishwa katika mkutano wa mwaka ambapo hupeana uzoefu na mipango ushirikiano baadaye. Pia UCRT imeijumuisha elimu ya UKIMWI/VVU katika programu zake kwa kuzingatia zaidi vijiji vya pembezoni na vilivyoachwa nyuma kimaendeleo. Asasi hii imewafundisha waelimisha rika wake kutoa elimu kuhusu ugonjwa huu na jinsi unavyoenezwa baina ya jamii za zilizotengwa za wachache kama vile makabila ya Wamasai na Barabaig.

8

MATOKEO YA KISERAUCRT ni moja ya asasi pekee nchini Tanzania iliyoweza kuondoa tofauti iliyopo baina sera za kitaifa za ardhi na mifumo ya haki za umiliki wa kijamii wa umiliki wa mali. Mwaka 2008, UCRT iliwaunganisha wawakilishi wa jamii kwenda Dodoma kwa ajili ya kushinikiza Bunge la Tanzania kukataa muswada wa wanyamapori. Endapo muswada huu usingekataliwa, ungezilazimisha jamii za wafugaji kuondoka katika maeneo yanayodhibitiwa na hifadhi ambayo yalitangazwa kuwa maeneo tengefu bila kuwahusisha wanajamii, kuziondoa jamii hizi katika maisha ya kijadi. Hivi karibuni, asasi hii imesaidia kuhakikisha sauti za jamii zinazingatiwa katika uundwaji wa Sheria ya Wanyamapori (2009) na Sheria ya Ardhi ya Mifugo (2010). Asasi hii ina dhima kuu ya mawasiliano na utetezi, ikiziunganisha jamii za wafugaji kufanya mazungumzo na wawakilishi wa serikali na wadau wengine.

Kupambana na urasimu wa serikali na siasa za serikali za mitaa ni sehemu ya programu ya UCRT. Hata wakati mipango ya matumizi ya ardhi na umiliki ikiwa imekubalika ndani na baina ya jamii, kunakuwa na ucheleweshaji mkubwa kwenye ngazi ya serikali za mitaa ambako

michakato ya kuidhinishwa kwa sheria ndogo za vijiji hufanyika. Kuna mfano mmoja ambapo maafisa wa wilayani huhitaji malipo ya kushiriki katika mikutano ya kuidhinisha sheria. Mara nyingi maafisa hao hudai dola za kimarekani 32 kwa siku kwa mchakato unaoweza kuendelea kwa wiki tatu au nne. Katika hatua mojawapo ya uidhinishaji, huhitajika maafisa tisa wa wilaya.

Mwezi Julai 2009, serikali kuu iliisaidia kampuni ya uwindaji ya kigeni kuwaondoa Wamasai kutoka katika vijiji tisa vilivyopo katika maeneo ya karibu na Mbuga ya Taifa ya Serengeti – miundombinu ya vijiji na maboma ya kitamaduni ya Wamasai yalichomwa moto. Hili lilikuwa ni tukio la karibuni kabisa katika historia ndefu ya migogoro kuhusu eneo la ardhi ambayo imekuwa ikisimamiwa kiuendelevu na Wamasai kwa vizazi vingi. Tukio hili liliwaathiri wafugaji zaidi ya 10,000 na kuhamisha zaidi ya ng’ombe 50,000 ambao wengi wao walikufa miezi iliyofuata kutokana na uhaba wa malisho na maji. Ingawa watu hawa waliendelea kukaa bila ardhi, UCRT imejitahidi kuvihusisha vyombo vya habari na vikundi vya kupigania haki katika ngazi za mitaa, kitaifa na kimataifa katika kuweka kumbukumbu za jamii hizi. Ufahamu kuhusu kunyang’anywa huku kwa ardhi umepanuka na kumekuwa na shinikizo kwa serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hili.

9

10

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUUCRT inategemea misaada ya fedha kutoka kwa wahisani. Asasi hii imeweza kuendeleza kazi yake kupitia programu mbalimbali za ush-irikiano zikiwemo za misaada ya mara moja na ile ya kuendelea. Kwa mfano, Mfuko wa Dorobo na Oxfam Ireland ni wahisani wanaotoa fedha kwa mwaka. Pia UCRT ilipata msaada wa Dola za Kimarekani 27,000 kutoka Programu ya Misaada Midogo kwa kipindi cha 2009-2010. Wakati jamii zikijihusisha na utalii wa mazingira, UCRT yenyewe haijihusishi na shughuli za kuzalisha faida. Kwa sasa, Asasi hii inatafuta mhisani wa muda mrefu ili kusaidia katika kazi yake ili kuhakikisha uendelevu wa shughuli zake kifedha.

Ili kuhakikisha uendelevu wa uongozi wa Asasi, wafanyakazi wa-naajiriwa kutoka katika jamii ambamo UCRT inafanya kazi. Wengi wa wafanyakazi wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na programu za ngazi ya chini na wengi wao huugawanya muda wao kati ya shughuli za maeneo husika na ofisi ya UCRT ya Arusha. Mabwana misitu hufanya kazi wakati wote katika vijiji husika ili kurahisisha ma-wasiliano kati ya maeneo ya kazi na makao makuu. Pia wafanyakazi wanasaidiwa kupata elimu ya ngazi ya shahada na vyeti kwa mfano, katika Kituo cha Mafunzo ya Ushirikiano wa Maendeleo cha Arusha au Chuo Kikuu cha Kenyata, Kenya.

MAONOMradi wa UCRT umekuwa mfano wa kuigwa kwa ajili ya miradi min-gine kama huu. Asasi hii imeweza kusaidia upatikanaji wa ardhi na rasilimali katika jamii za vijiji zaidi ya 40. Mbali na kusaidiwa kupata uhakika wa umiliki wa ardhi lakini pia kuboresha maisha na kuwa na shughuli mbalimbali za kuendesha maisha. Sababu kuu ya ma-fanikio ya UCRT imekuwa ni kuweka mipango jumuishi ya matumizi ya ardhi na kutengeneza sheria ndogo za vijiji. Mfumo wa asasi hii wa kuziwezesha jamii kupigania uhakika wa ardhi na haki za kumiliki mali umetumiwa sehemu nyingine kulingana na uhitaji; jamii nyingi zimekwenda UCRT na kuomba kusaidiwa katika kuutumia mfumo huu wa matumizi ya ardhi na matumizi ya rasilimali katika vijiji vyao.

Kubadilishana uzoefu kupitia elimu rika kumekuwa muhimu sana kwa UCRT katika mabadiliko ya sera na mfumo wa umiliki wa ardhi. Pia ushirikiano na makundi kama vila Asasi Zisizo za Kiserikali za Wafugaji wa Jadi na Baraza la Wanawake wa Jamii za Wafugaji umesaidia kujenga mfumo thabiti wa ushawishi. Ni kwa njia hii ya ushirikiano ndipo tunaweza kukabiliana na majukumu na hatari zinazohusiana na kazi ya utetezi.

WAHISANI• African Initiatives (Asasi Isiyo ya Kiserikali iliyoko Uingereza) am-

bayo awali ilikuwa mhisani lakini ikajitoa mwaka 2007. Shirika la OXFAM Ireland hutoa michango ya kila mwaka.Norwegian People’s Aid (NPA) makes annual financial contributions

• Shirika la Misaada la Watu wa Norway (NPA) hutoa michango ya fedha ya kila mwaka.

• Programu ya Misaada Midogo (GEF) ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hutoa michango ya fedha ya kila mwaka.

• Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori hutoa mchango wa fedha wa kila mwaka.

• Asasi ya Cordaid (ya Uholanzi) hutoa mchango wa fedha kila mwaka.

• Asasi Isiyo ya Kiserikali ya Wafugaji wa Jadi (PINGO’s Forum) Hufanya utetezi wa haki za jamii za kijadi katika ngazi ya kitaifa.

• Baraza la Wanawake wa Jamii za Wafugaji Tanzania (PWC) hufanya kazi za uwezeshaji wa kijinsia katika jamii za wafugaji kaskazini mwa Tanzania.

• Dorobo Fund hutoa mchango wa fedha kila mwaka.• Mfuko wa Doroboo hutoa mchango wa fedha kila mwaka. • Mfuko wa Msaada wa Ubelgiji (BSF) hutoa mchango wa fedha

kila mwaka. • Mfuko wa Bole and Klingenstein Foundation (BKF) hutoa mi-

chango ya kifedha ya kila mwaka.• Mfuko wa Flora Family Foundation ulitoa mchngo wa kifedha

mwaka 2010/2011.

MAREJELEO YA ZIADA

• Ujamaa Community Resource Team (UCRT). 2010. Participatory Land Use Planning as a Tool for Community Empowerment in Northern Tanzania. IIED, Gatekeeper 147, December (with Fred Nelson, Malisaili Initiatives). http://pubs.iied.org/pdfs/14608IIED.pdf

• ResourceAfrica UK, A Plain Plan, (YouTube) http://www.youtube.com/watch?v=wuy8h1F7GvE• Ujamaa Community Resource Team PhotoStory (Vimeo) (English) https://vimeo.com/15783140 (Swahili) https://vimeo.com/15783208

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa: