siku hiyo p kalvaridownload.branham.org/pdf/swa/swa60-0925 that day on...2 lilenenolililonenwa...

25
SIKU HIYO P ALE KALVARI Mungu akubariki Ndugu Neville na asante sana. Habari za asubuhi marafiki. Ni majaliwa kuwa hapa Maskanini tena asubuhi ya leo kumtumikia Bwana kwa kulihubiri Neno na kuwaombea wagonjwa. Nami ninashukuru sana kwa ajili ya siku hii. Nilishangaa mara tu nilipoingia. Ndugu alikuja akasema, “Sitaki kuwa kama yule mwenye ukoma asiyestahili aliyeponywa.” Ilikuwa Ndugu Wright. Nilimwombea, naye Bwana amemponya kabisa. Ndipo akaja akilia kunipa mkono na kusema ya kwamba alitaka kumshukuru Bwana kwa kuponywa. Alitaka kurudi na kutoa shukurani. Wote umekwisha. Yeye ni mzima kabisa sasa. Tunashukuru kwa ajili ya shuhuda hizo. Na lo, Charlie, wewe pamoja na Ndugu Jefferies, mkitaka kuja, njooni mketi kwenye viti hivi hapa, nanyi mnakaribishwa sana hivyo haitawabidi kusimama. Yule Ndugu mwingine pale, Ndugu Wood njoo hapa, kuna nafasi kadhaa hapa kwenye ubao wa kukalia, hivyo haitakubidi kusimama. Naamini kuna nafasi kadhaa hapa, naam, ndiyo, mmekaribishwa kabisa mje mketi mahali hapa. Tunafurahi…Naamini ilisemwa wakati mmoja, “Nalifurahi waliponiambia, (Mungu akubariki Ndugu. Asante. Asante. Asante.) “Nalifurahi waliponiambia, ‘Na twende nyumbani kwa Bwana.’” Hiyo ndiyo majaliwa ya Mkristo na furaha yake—kwenda katika nyumba ya Bwana. Nikitazama kila mahali na kuwaona marafiki wangu wengi sana humu asubuhi ya leo, ninafurahi sana juu ya jambo hili. Nina furaha kumwona Ndugu na Dada Dauch hapa kutoka Ohio. Nawaona Ndugu na Dada Armstrong kule nyuma waliotoka Ohio. Mungu awabariki nyote pia. Na…Lo, ukitazama kila mahali unaona wengi sana, ingekuwa vigumu kutaja majina yao yote. Dada Hoover tunafurahi kukuona humu asubuhi ya leo kutoka kule Kentucky, na Charlie pamoja na Nellie, Ndugu Jefferies pamoja na jamaa yake na wengi sana humu kutoka nje ya mji huu. Kwa hivyo tunatarajia wakati mzuri sana katika Bwana asubuhi ya leo. Tukimtarajia Mungu kukutana nasi kwa namna fulani apate kubariki nafsi zetu na kutuhudumia mambo tunayohitaji. Nami ninapoangalia kila mahali, kama nikianza kuwaita marafiki zangu walio humu, ningechukua karibu asubuhi mzima nikiwataja watu mbalimbali. Inanifanya nijisikie vizuri kurudi kanisani kuwaona watu wote humu na kukutana…

Upload: nguyentuyen

Post on 05-Jul-2019

299 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI

Mungu akubariki Ndugu Neville na asante sana. Habariza asubuhi marafiki. Ni majaliwa kuwa hapa Maskanini

tena asubuhi ya leo kumtumikia Bwana kwa kulihubiri Nenona kuwaombea wagonjwa. Nami ninashukuru sana kwa ajili yasiku hii.

Nilishangaa mara tu nilipoingia. Ndugu alikuja akasema,“Sitaki kuwa kama yule mwenye ukoma asiyestahilialiyeponywa.” Ilikuwa Ndugu Wright. Nilimwombea, nayeBwana amemponya kabisa. Ndipo akaja akilia kunipa mkono nakusema ya kwamba alitaka kumshukuru Bwana kwa kuponywa.Alitaka kurudi na kutoa shukurani. Wote umekwisha. Yeye nimzima kabisa sasa. Tunashukuru kwa ajili ya shuhuda hizo.

Na lo, Charlie, wewe pamoja na Ndugu Jefferies, mkitakakuja, njooni mketi kwenye viti hivi hapa, nanyi mnakaribishwasana hivyo haitawabidi kusimama. Yule Ndugu mwingine pale,Ndugu Wood njoo hapa, kuna nafasi kadhaa hapa kwenye ubaowa kukalia, hivyo haitakubidi kusimama. Naamini kuna nafasikadhaa hapa, naam, ndiyo, mmekaribishwa kabisa mje mketimahali hapa.

Tunafurahi…Naamini ilisemwa wakati mmoja,“Nalifurahi waliponiambia, (Mungu akubariki Ndugu. Asante.Asante. Asante.) “Nalifurahi waliponiambia, ‘Na twendenyumbani kwa Bwana.’” Hiyo ndiyo majaliwa ya Mkristo nafuraha yake—kwenda katika nyumba ya Bwana.

Nikitazama kila mahali na kuwaona marafiki wangu wengisana humu asubuhi ya leo, ninafurahi sana juu ya jambo hili.Nina furaha kumwonaNdugu naDadaDauch hapa kutokaOhio.Nawaona Ndugu na Dada Armstrong kule nyuma waliotokaOhio. Mungu awabariki nyote pia. Na…Lo, ukitazama kilamahali unaona wengi sana, ingekuwa vigumu kutaja majinayao yote. Dada Hoover tunafurahi kukuona humu asubuhi yaleo kutoka kule Kentucky, na Charlie pamoja na Nellie, NduguJefferies pamoja na jamaa yake na wengi sana humu kutoka njeya mji huu.

Kwa hivyo tunatarajia wakati mzuri sana katika Bwanaasubuhi ya leo. Tukimtarajia Mungu kukutana nasi kwanamna fulani apate kubariki nafsi zetu na kutuhudumiamambo tunayohitaji. Nami ninapoangalia kila mahali, kamanikianza kuwaita marafiki zangu walio humu, ningechukuakaribu asubuhi mzima nikiwataja watu mbalimbali. Inanifanyanijisikie vizuri kurudi kanisani kuwaona watu wote humu nakukutana…

Page 2: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

2 LILE NENO LILILONENWA

Itakuwaje tutakapofika Mbinguni, na tukutane huko katikawakati huo mkuu wa ushirika wa milele na usio na mwishotukiwa pamoja kukizunguka kiti cha enzi chaMungu—na barakazile ambazo sote tumezithamini. Huko sisi tutafanywa katikasura Yake, katika mfano Wake, na Roho Wake akiwa juu yetutukimwabudu na kumtumikia Yeye milele yote, hatutachokakamwe.

Waza tu, hakuna cho chote unachoweza kuwazia,ambacho ungetaka kufanya, ila kile ambacho mara kwa marakinakuchosha kukifanya. Charlie, nakisia mimi na wewetumewinda kindi kuliko cho chote ambacho tunapenda kufanyakatika njia hiyo, bali unajua wewe huchoka kufanya hivyo.Napenda kutembea kwa miguu, kupanda milima na kutembeatu, bali wakati mwingine mimi huchoka na kutaka kufanyajambo jingine. Nami napenda kuendeshamotokaa.

Wakati mwingine mimi huanza kusikia uchovu, kuchokakabisa na kushikwa na wasiwasi mwingi. Ningeingia katikamotokaa yangu, niiendeshe, na kushikilia usukani nikiendeshabarabarani huku ninaimba, “Nina furaha sana kwamba nawezakusema mimi ni mmoja wao” ama cho chote kile. Nikishikasana huo usukani na kuimba na kufanya vishindo kwa mguuwangu na kupaza sauti. Naam, baada ya kitambo kidogoninachoka, kisha, ninarudi nyumbani na kuanza jambo jingine.Bali tutakapoanza kumwabudu Mungu katika huo ufalmempya, hakutakuwepo na muda wa uchovu…Itakuwa daimani baraka tu na kuendelea daima. Lakini bila shaka tutakuwatumebadilishwa wakati huo; hatutakuwa kama tulivyo sasa.Tutakuwa watu tofauti, viumbe tofauti na vile tulivyo wakatihuu. Kwa hiyo tuna furaha.

Nilikuwa nikiwaza. Sijui kama nimewahi kutaja hili ama la,Ndugu Charlie. Wakati mmoja nilikuwa kule Kentucky pamojanaye, naye alisema, “Ndugu Branham, je, wadhani katika uleUtawalawaMiaka Elfumimi nawewe tutawinda kindi?”

Nikasema, “Sifikiri hivyo Charlie.”Akasema, “Vema, tunapenda sana kufanya hivyo, unafikiri

tutafanya hivyo tutakapoingia katika ule Utawala wa MiakaElfu?”

Nikasema, “Sivyo, hamna kitakachouawa katika uleUtawala wa Miaka Elfu.”

Naye akasema, “Naam, tunapenda sana jambo hili.”Nikasema, “Charlie, vipi kama ningalikushawishi ya

kwamba wakati mmoja ulikuwa nguruwe mwitu, kishaukainuliwa kuwa kiumbe cha hali ya juu, ukawa mwanadamu.Je, ungelitaka kamwe kurudi nyuma ukafurahie anasa zanguruwe mwitu?”

Akasema, “La.”

Page 3: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 3

Nikasema, “Waona, ungelikuwa juu sana kuliko nguruwemwitu sasa kwa kuwa wewe ni mwanadamu, haungalitakakuwa nguruwe mwitu tena.” Nikasema, “Sasa zidisha hilo maraelfu kumi, na hivyo ndivyo utakavyokuwa utakapobadilishwakutoka hapa kuingia vile utakavyokuwa. Hautataka kamwekuwa binadamu tena.” Hiyo ni kweli. Itakuwa jambo tofauti.Nina furaha sana hata kuyawazia. Nikijua tu ya kwamba sikumoja tutapanda juu zaidi.

Vema, sasa kama Bwana anapenda, Jumapili ijayo ambayoitakuwa kama…Basi nitaondoka kwenda Wyoming pamoja narafiki mpendwa, ama kule Idaho na rafiki mpendwa, NduguMinor Arganbright na Ndugu Clayt Sonmore, wa WafanyiBiashara Wakristo.

Juma lifuatalo baada ya hili lijalo—sasa ni tarehe saba—napaswa kuwa Dallas, Texas, katika Mkutano wa Sauti yaUponyaji, na nitahubiri katika usiku wa tarehe saba. Kishanitarudi kwenda Idaho pamoja na Ndugu Arganbright pamojana Wafanyi Biashara Wakristo, na huenda nikawa na usikummoja kule Minneapolis kabla hatujaondoka. Kisha mara mojakatika kifungua kinywa chaWafanyi BiasharaWakristo.

Bwana akipenda, Jumapili ijayo asubuhi, nataka kurudihumu Maskanini tena; na kama hiyo inaruhusiwa na iwe nimapenzi ya Bwana, nataka kunena juu ya somo la Upepo waKisulisuli katika Upepo; Bwana akipenda.

Ilionekana kuwa moyoni mwangu juma nzima; na hivimajuzi asubuhi, asubuhi na mapema yapata saa 10 usiku,niliamka nikapata wazo hili Siku Hiyo Pale Kalvari. Natakakuzungumzia hilo asubuhi ya leo.SikuHiyo PaleKalvari.

Na sasa kwa somo hili hebu na tuzifungue Biblia zetu, katikamaandiko, katika Injili ya Mathayo Mt. kwenye sura ya 27, nasitutaanzia katika aya ya 27 na kusoma sehemu ya andiko hilikupata msingi wetu. Ndipo tutaanza mara moja, kisha baada yaibada ya mahubiri tutawaombea wagonjwa.

Tangu mara ya mwisho hapa, nikikumbuka kwakulinganisha huduma yangu mpya, nilipata shuhuda nyingizaidi kutoka katika mkutano huo kuliko nilizopata katikamkutano wo wote kwa muda mrefu. Kuna jambo ambalokwamba huna budi kuwasiliana na mtu mwenyewe haidhuruni mambo mangapi ya kimbinguni yanayoonyeshwa. Lakinimnaona, uponyaji hauna budi kutegemea imani yamtu binafsi.

Sasa iwapo mtu ana imani, nao waone endapo RohoMtakatifu anaenda juu ya wasikilizaji na kusema, mambo fulanina fulani yatatendeka: “Jina lako ni fulani,” “Umetoka mahalifulani,” na “…jambo fulani ulilotenda,” na “Itakuwa hivi,” nauone yote yakitendeka hivyo, hata hivyo mtu huyo anayeketihapo anapaswa kutazama juu na kusema, “Hapana shaka huyo

Page 4: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

4 LILE NENO LILILONENWA

ni Mungu. Nakubali nimeponywa.” Bali badala ya hayo mtuhuyo anasema, “Niwekemikono na uniombee ili nipate kupona.”

Lakini hivyo ndivyo tulivyofundishwa hapa Amerikatuamini hivyo, na bila shaka hayo ni maandiko. Bali sasatunaona kule Afrika na mahali mbalimbali, hebu tu jambokama hilo litendeke, wasikizi wote wanainuka mara mojana kuukubali uponyaji wao—kwa sababu hawajafundishwakitu, mwaona. Hata hawajafundishwa uponyaji. Halafu ndipowanapoona hilo, wao wanajua ya kwamba kuna Mungu aliyehai; na iwapo yu hai, Yeye yu mwenyezi. Naye huponya, nahilo latosha. Kwa sababu msingi tayari umewekwa—msingi—ya kwamba Yeye ni Mponyaji na huwaponya watu. Ndipowanapouona uwepo huu ukitenda kupitia kwa kanisa Lake,ndipo wao husema, “Hilo latosha. Hilo tu ndilo tunalohitaji.” Ilasisi tumefundishwa kuwawekelea wagonjwa mikono na mambokama hayo. Hiyo ndiyo sababu haitendi kazi vizuri sana katikaAmerika.

Sasa, kumbukeni, Jumapili ijayo asubuhi, Bwana akipenda,(Ndugu Neville atalitangaza, bila shaka) Upepo wa KisulisuliKatika Upepo.

Sasa, nimewapa wakati mdogo kuyafungua maandiko yenukatika Mathayo 27. Hebu tuanze kusoma katika aya ya 27ya Injili ya Mathayo Mt. Sasa hebu tusikize kwa makinitunaposoma.

“Nao askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani yaPraitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima.

Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.

Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwachake, na mwanzi katika mkono wake: wakapigamagoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu,Mfalme wa Wayahudi!

Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi,wakampiga-piga kichwani.

Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi,wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha,

Hata walipokuwa wakitoka, wakamwona mtuMkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutishaauchukue msalaba wake.

Na walipokwisha kupanda kwenda…walipokwendamahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa,

Wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo,lakini yeye alipoionja hakutaka kuinywa.

Walipokwisha kumsulubisha, waligawa mavazi yake,wakapiga kura; Lili litimie neno lililonenwa na nabii,

Page 5: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 5

Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi languwalipiga kura.]Wakaketi, wakamlinda huko.Wakaweka juu ya kichwa chake mashtaka yake,

yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WAWAYAHUDI.Wakati uo huo wanyang’anyi wawili wakasulubiwa

pamoja naye, mmoja mkono wake wa kuume, na mmojamkono wake wa kushoto.Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana,

wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema,Ewe uliyelivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,

jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu,shuka msalabani.Kadhalika na wale wakuu wa makuhani

wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee,wakasema,Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Kama

yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani,nasi tutamwamini.Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama

atamwokoa; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana waMungu.Pia wale wanyang’anyi waliosulubiwa pamoja naye,

walimshutumu vile vile.Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote

hata saa tisa.Kama saa tisa, Yesu akapasa sauti yake kwa nguvu

akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Munguwangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Na baadhi ya waliohudhuria, waliposikia, walisema,

Huyu anamwita Eliya.Marammoja akaendambio, akatwaa sifongo, akaijaza

siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha.Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya

atakuja amwokoe.Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu,

akaitoa roho yake.Tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili

toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; na miambaikapasuka;Makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya

Watakatifu waliolala;

Page 6: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

6 LILE NENO LILILONENWA

Nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baadaya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu,wakawatokea wengi.Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye

wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi namambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema,Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”Mathayo Mt. 27:27-54

Na tuviinamishe vichwa vyetu kwa muda mfupi wamaombi. Bwana, tunajua ya kwamba Wewe ni Mungu, nabaada ya kulisoma hili Neno Takatifu lililowekwa wakfu,tungali tunaweza kuona ya kwamba tabia Yako haijabadilika.Wewe daima ni Mungu. Na ilionekana kana kwamba Yesuasingalipata msaada wo wote, ya kwamba Yeye alichukuliwana mikono miovu na kukatakatwa vipande, akatemewa mate,akadhihakiwa na huku amesulubishwa msalabani, akitokwana damu, akifa; na ilionekana kana kwamba hapakuwepona msaada mahali po pote, hata Yeye Mwenyewe akalia,“MunguWangu, MunguWangu, mbona Umeniacha?” Bali Weweunatenda katika wakati ambapo hakuna kitu kingine chochotekinaweza kutenda kazi.

Tumejulishwa, Bwana, ya kwamba kama tuna mito ambayohatuwezi kuvuka, kama tuna milima tusiyoweza kupanda,Mungu ni stadi wa kutenda mambo ambayo wengine hawawezikufanya. Wewe ni stadi wa kazi hiyo. Kwa kuwa Wewe unajuasababu ya siku hiyo pale Kalvari. Wewe, ukiwa Mungu, Asiye naMwisho, ulijua wakati huu hauna budi kuja. Bali ulipotimizwa,basi ukaonyesha ya kwamba Wewe ni Mungu. Ulionyesha niNani alikuwa Bosi.

Uliitikisa nchi, na watakatifu waliolala ardhini wakafufuka.Ulilitia giza jua usiku—kama giza la usiku—ikionyesha yakwambaWewe ulikuwaMungu, lakini ilionekana kama kwambaumenyamaza kwamudamrefu. Hebu nasi kwa hilo tutoe uamuzihuu, ya kwambamradi tu tunatembea katika Roho, tukiongozwana mkono wa Mungu, haidhuru nini kinaonekana kimekwendakombo, hata hivyo sisi tunaelekea Kalvari, Mungu atanenakatika saa ifaayo, wakati unaofaa.

Sasa Baba Mungu, tungeomba msamaha wa dhambi zetu namakosa yetu. Nasi tungeomba kwamba Roho Wako atuongoze.Tuongoze kama Hua alivyomwongoza yule Mwana-Kondoo.Hebu na tuwe watiifu kwa lo lote litakalotupata, tukijua hili,ya kwamba Mungu hutenda mambo yote vizuri, na kujua yakwamba itakuwa sawa.

Uwe nasi leo katika ibada hii. Twaomba ya kwambautawaokoa wale walio tayari kuokolewa nao wanautafutawokovu. Wajaze hao na uzima wa milele wanaoutafuta.Twaomba ya kwamba utawaponya hao walio wagonjwa na

Page 7: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 7

wanaoteseka ambao wamekuja wakiutafuta uponyaji. Nasitutakutukuza kwa ajili ya jambo hilo. Tunaomba katika jina laMwanaWako,Mwokozi wetu, YesuKristo. Amina.

Sasa katika mazungumzo ya asubuhi ya leo, tunatakakuwakumbusheni fungu la maneno niliyochagua kuzungumzia,Siku Hiyo Pale Kalvari. Inaonekana kama itakuwa nje kidogoya wakati unaofaa. Hili linapaswa kuwa katika Ijumaa Kuu.Kalvari inapaswa kukumbukwa kila siku. Tumesikiamengi sanakuihusu. Tumesomamengi sana juu yake.Wahubiri wameihubiritangu mwanzo wa wakati. Waimbaji wameimba juu yakekatika nyakati zote. Manabii walitabiri miaka elfu nne kablahaijatukia, na manabii wa siku hizi wanatuonyesha kule nyumailipotendeka. Ni siku muhimu sana.

Ni moja ya siku zilizo muhimu sana ambazoMungu amepatakuzishusha duniani. Na kama ni muhimu sana kwa jamii yakibinadamu, Kalvari, nafikiri ni vizuri kwetu kurudi nyumatukachunguze tuone kwamba ina maana gani kwetu. Kwa kuwanina hakika katika saa hii iliyochelewa tunayoishi, tunatafutakila umuhimu wa Mungu tunaoweza kujua; na yote tunayowezakujua, tuko hapa kujifunza hayo. Kuona ni yapi yaliyo yetu,na yale Mungu aliyotutendea, na kuona yale Yeye aliyoahidikututendea. Na hilo ndilo linalotuleta kanisani.

Hiyo ndiyo sababu mhubiri huubiri. Hiyo ndiyo sababuyeye husoma na kuyatafakari Maandiko na kutafuta uvuvio—ni kwa sababu yeye ni mtumishi wa umma kwa watuwa Mungu, naye anajaribu kupata kitu ambacho…ambachoMungu angewaambia watu Wake, kitu ambacho kingewasaidia.Labda huenda ikawa ni kuwahukumu katika dhambi zao, balikingekuwa chenyemanufaa kuwainua; wapate kuziacha dhambizao kisha wainuke wakamtumikie Bwana. Nao wahudumuhawana budi kuyatafuta mambo haya.

Iwapo siku hii ni muhimu sana, moja ya siku zilizo kuu sana,hebu na tuangalie mambo matatu ambayo siku hiyo ilimaanishakwetu. Tungechukua mamia. Bali asubuhi ya leo nimechagua tumambo matatu tofauti yaliyo muhimu sana ambayo tunatakakuyachunguza katika muda mfupi ujao; ambayo Kalvariilimaanisha kwetu. Nami naomba ya kwamba itamhukumu kilamwenye dhambi aliyeko, ya kwamba itamfanya kila mtakatifukupiga magoti yake, ya kwamba itamfanya kila mgonjwa ainueimani yake kwa Mungu na aondoke ameponywa, kila mwenyedhambi aokolewe, kila aliyerudi nyuma arudi na ajionee aibu, nakila mtakatifu afurahi na apate tumaini jipya na tumaini jipya.Jambomoja kuumuhimu ambalo Kalvari inamaanisha kwetu naulimwengu ni, ilimaliza swali la dhambimaramoja tu.

Mwanadamu alikuwa na hatia ya dhambi, na dhambiilikuwa adhabu ambayo hamna mwanadamu aliyeweza kulipa.Adhabu ilikuwa kubwa sana hata hamnamtu angaliweza kulipa

Page 8: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

8 LILE NENO LILILONENWA

adhabu hiyo. Naamini kabisa ya kwamba Mungu aliikusudiahivyo—ya kwamba adhabu ingekuwa kubwa sana hata hamnamtu angaliweza kuilipia—kusudi afanye hivyoYeyeMwenyewe.

Sasa, adhabu ya dhambi ilikuwa mauti. Nasi sotetulizaliwa katika dhambi, tukaumbika katika maovu, tukajaulimwenguni tukinena uongo. Kwa hivyo, hamna hata mmojawetu aliyestahili, ama wao hawangempata mtu ye yote dunianialiyestahili.

Nayo dhambi haikuanza duniani. Dhambi ilianza Mbinguni.Lusifa, ibilisi, alikuwa kiumbe kilicholaaniwa kwa ajili ya kuasikwake kabla hata hajaingia duniani. Dhambi ilianza Mbinguni,ambako Mungu aliwaweka malaika na wengineo kwenye msingiule ule ambao Yeye aliwaweka binadamu. Maarifa…mti wamaarifa. Mti wa uzima, namti wamaarifa, ambapomwanadamuangejichagulia. Na Lusifa alipopewa mamlaka ya kuchagua,yeye alitaka kitu bora kuliko kile alichokuwa nacho Mungu.Hiyo ikasababisha matata.

Na kulikuweko na deni la dhambi. Madai yake yalikuwamauti. Adhabu ilikuwa mauti, na hiyo ni…Tungewezakuzungumzia hili kinaganaga, kwa maana siamini kuna mautiila moja. Kuna uhai mmoja. Nami naamini ya kwamba mtualiye na Uzima wa Milele hawezi kufa, pia naamini kunakuangamizwa kabisa kwa hiyo nafsi itendayo dhambi, kwa kuwaBiblia ilisema, “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa”—simtu, nafsi itendayo dhambi. Kwa hivyo Shetani hana budi kufaapate kuangamizwa kabisa. Sikubaliani na watu wa Kijumlaambao husema Shetani ataokolewa! Alitenda dhambi, nayendiye mwanzilishi wa dhambi. Na nafsi yake ilitenda dhambi,naye alikuwa roho. Roho huyo ataangamizwa kabisa asisaliekitu.

Nayo dhambi ilipoingia duniani kule nyuma mwanzonikama shuka nyeusi ikishuka kutoka mbinguni, ilipoozeshadunia. Ilikitupilia kila kiumbe duniani, na viumbe vyote vyaMungu, utumwani. Mwanadamu alikuwa katika utumwa wamauti, ugonjwa, taabu, huzuni. Viumbe vyote vikaangukapamoja naye. Dhambi ndiyo nusukaputi ambayo kweliiliipoozesha dunia. Na ndipo tukawekwa humu, tumekatatamaa, kwa sababu kila kiumbe duniani kilitiishwa chiniyake, na kila mmoja iliyezaliwa duniani alitiishwa chini yake.Kwa hiyo ilipaswa kuja kutoka mahali fulani ambako hakunadhambi. Isingalitoka duniani.

Mmoja wetu asingeliweza kumkomboa mwingine. Ilipaswakutoka kwa mwingine. Kwa hivyo, mwanadamu alipotambuaya kwamba alikuwa ametenganishwa na Mungu wake, akawamzururaji. Walilia, walipasa sauti, walitaabika, wakazunguka-zunguka milimani, na katika jangwa, wakiutafuta mji ambaoMwenye Kuujenga na Mwenye Kuubuni ni Mungu. Kwa kuwa

Page 9: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 9

alijua ya kwamba kama akirudi kwenye uwepo wa Mungu,angeliweza kusemezana hayo pamoja Naye. Bali hapakuwepona njia ya kurudia. Akawa amepotea. Hakujua aende wapi,kwa hivyo akaanza tu kutangatanga, akijaribu kupata mahaliambapo angepata njia ya kurudi mahali hapo. Kitu fulanindani yake kilimwambia ya kwamba alitoka mahali palipokuwapakamilifu.

Hakuna mtu hapa katika wasikizi hawa waliopo hapaasubuhi ya leo, ama katika wasikizi wa kanda za sumakuambako zitasambazwa duniani kote, hakuna hata mmoja hapaama po pote pale, ila yule anayeutafuta ule ukamilifu. Unapolipamadeni yako, unafikiri hilo linatosha. Unapolipa madeni yako,ndipo kuna mtu mgonjwa katika jamaa yako. Magonjwayanapokwisha, ndipo una madeni mengi zaidi ya kulipa. Pundesi punde nywele zako zinapata mvi, ndipo unataka kurudiaujana. Na kuna jambo fulani kila wakati, daima, kwa sababuya hilo wimbi la dhambi. Lakini moyoni mwako, kwa kuwaunatafuta hilo, inaonyesha ya kwamba kuna ukamilifu mahalifulani. Kuna kitu mahali fulani.

Hiyo ndiyo sababu mara nyingi siku hizi mwenye dhambiangali anatanga-tanga. Msichana mrembo atakata vishungi vyanywele zake apate kupendwa na watu wengi, atajipaka rangiusoni mwake apate kuonekana mrembo, atavaa nguo kuonyeshamaumbile ya utu wake— kwa sababu ndilo jambo pekeeunaloweza kupata…Kupata mahali fulani…kujaribu kupatakitu fulani kimrudie; anapoweza kumfanya mwanamumeampigie mluzi, ampungie mkono, afanye ubembe naye. Kijanamwanamume atamfanyia mwanamke jambo lile lile. Kujaribukuwamtuwa kuvutia kwa huyomwanamke. Majirani watajenganyumba na kuifanyiza namna fulani kwa sababu itaonekanabora kuliko kwa jirani yake. Ndivyo ilivyo kila wakati.Tunatafuta-tafuta kitu fulani, na kitu fulani daima kinaendeleakupanda juu yake kidogo.

Huyo kijana mwanamke atapata kumwona kijanamwanamke anayependwa sana na watu kuliko yeye. Jiraniatagundua kuwa kuna nyumba iliyo bora kuliko yake.Mwanamke atamwona mwanamke mwingine aliyevalia kwanjia fulani ambayo inaonekana bora kuliko yeye alivyo. Ni kitundani yetu kinachotafuta kitu fulani, na inaonyesha ya kwambatumepotea. Tunataka kupata kile kitu kitakachotutosheleza,kitakachoijaza hiyo sehemu ya njaa mle ndani; lakiniinaonekana kana kwamba hatuwezi kukipata.

Wanadamu walikijaribu katika zile nyakati zote.Wakakililia. Wakalia machozi. Wakafanya kila kitu walichojuakufanya, bali hata hivyo hawakukipata walipotangatangaulimwenguni.

Page 10: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

10 LILE NENO LILILONENWA

Hatimaye siku moja—hiyo ni ile siku pale Kalvari—Mtu mmoja akashuka akaja kutoka Utukufuni— Mtu mmojaaliyeitwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu Yeye aliyetokaUtukufuni, kisha Kalvari ikatengenezwa. Hiyo ndiyo sikuambayo ile gharama ililipwa, na swali la dhambi likatatuliwamilele, naye akafungua njia ya kitu hiki tunachokionea njaa nakukionea kiu. Ilileta mahali pa utoshelevu.

Hakuna mtu aliyepata kutembelea Kalvari na kuona jinsiilivyokuwa, anayeweza kubaki alivyokuwa. Kila alichooneashauku au kutamani sana kinapatikana anapofika mahali hapo.Ilikuwa siku muhimu sana na jambo muhimu sana, hataikaitikisa dunia. Iliitikisa dunia jinsi ambavyo haijatikiswa hapoawali, Yesu alipokufa pale Kalvari naye akalilipia swali ladhambi.

Dunia hii yenye dhambi ilitiwa giza kabisa. Jua lilituamchana nalo likazimia roho kwa wasiwasi. Miamba ikatikisika.Milima ikapasuka. Miili ya waliokufa ikafufuka ghafla kutokakaburini. Ilifanyaje? Mungu akalenga shabaha pale Kalvari.Akamjeruhi mnyama huyo aitwaye Shetani milele.

Sasa amekuwa mkali zaidi tangu wakati huo, kwa sababuiliwaletea nuru jamii ya binadamu; na kila mtu anajua yakwambamnyama aliyejeruhiwa ndiye mkali sana…akijikokotahuku mgongo wake umevunjika.

Sasa, Shetani aliangushwa chini pale Kalvari. Nchiilithibitisha ya kwamba ndivyo ilivyokuwa. Gharama kuu sanailiyopata kulipwa, na Mtu pekee ambaye angeilipia, alikuja naakafanya hivyo pale Kalvari. Hapo ndipo ile gharama iliyo kuuilipolipiwa. Jambo hilo ndilo moja yamambo hayo.

Mungu alihitaji hilo. Hakuna mtu aliyestahili. Hakuna mtualiyeweza. Hakuna mtu angaliweza kufanya hivyo. Naye Munguakafa Mwenyewe akafanyika mwanadamu, akaishi maisha yakibinadamu chini ya tamaa za kibinadamu, kisha akasulubiwakule Kalvari. Na pale, wakati Shetani alipodhani kwambaYeye asingelifanya hivyo— kwamba Yeye asingelistahimili—Yeyealiistahimili Gethsemane; na kila jaribu lililowahi kumkabilimwanadamu, Yeye alipitia huko kama watu wote; lakini Yeyeakalipa ile gharama na hiyo ndiyo iliyoitia giza kabisa dunianzima—kama ile nusukaputi ya kumtia ganzi mtu anapofanyiwaupasuaji.

Daktari anapompa mtu hiyo nusukaputi, kwanza humfanyaapoteze fahamu kabla hajafanya upasuaji. Naye Mungualipolifanyia kanisa upasuaji, dunia ilipata nusukaputi.Maumbile yakapata mshtukomkubwa sana.

Si ajabu, Mungu katika mwili wa kibinadamu, alikuwaakifa. Ilikuwa saa ambayo ulimwengu uliitazamia, hata hivyowengi wao hawakuijua. Kama ilivyo siku hizi, watu wengiwanayatazamia mambo haya, hata hivyo hawayatambui. Wao

Page 11: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 11

hawajui njia ya kuepukia. Wao wangali wanajaribu kutafutaanasa na mambo ya ulimwengu, wakijaribu kupata njia yakuepukia.

Kumekuwa na vibao vingi vilivyoelekeza kwenye siku hiyo.Dalili nyingi kuu zilizoonyeshwa awali kwa njia ya mwana-kondoo, na ng’ombe mume, na hua na mambo haya yote; hatahivyo yasingeweza kuivunja. Yasingaliweza kuvunja hiyo ngomeya mauti. Kwa kuwa Shetani aliitawala dunia—miamba ileile ambayo wakati mmoja alitembea juu yake huku na hukoduniani, kiberiti kilichowaka moto. Lusifa alikuwa mwana waasubuhi, naye alitembea duniani ilipokuwa volkano inayowakamoto.) Miamba hiyo hiyo iliyokuwa imepata baridi, wakati Yesualipokufa Kalvari, ilibubujika toka ardhini. Gharama iliyopwa,na utumwawa Shetani ukavunjiliwambali.

Mungu akairudisha mkononi mwa mwanadamu, njia yakurudia kile alichokuwa akitafuta. Haikumpasa kulia tena.Wakati Yeye alipouvunja uti wa mgongo wa Shetani KuleKalvari—uti wa mgongo wa dhambi, wa magonjwa—na hiyoikamrudisha kila mwanadamu duniani katika uwepo wa Munguhuku dhambi zimesamehewa.

Haleluya! Dhambi zetu zimesamehewa! Shetani hawezitena kututia giza akatuondoa kwa Mungu. Kuna njia kuuiliyotengenezwa. Kuna simu pale. Kuna simu inayoelekeaUtukufuni. Inamleta kila mtu karibu na simu hiyo.

Kama mtu amejaa dhambi, inamuunganisha na “makaomakuu ya kale.” Anaweza kusamehewa hiyo dhambi. Si hivyo tu,bali dhambi hiyo imekwisha lipiwa tayari. Utukufu! Haikupasikusema, “Mimi sistahili.” Hakika hustahili. Haungaliwezakamwe kustahili. Bali Mtu aliyestahili alipachukua mahalipako. Uko huru. Haikupasi kutangatanga tena. Haikupasi kuwamtafuta anasa tena huku nje duniani. Kwa kuwa:

“Damu imebubujika,Ni ya Imanweli;Wakioga wenye taka,Husafiwa kweli.”

Haikupasi kupotea; kuna njia kuu na njia. Nayo inaitwa,“Njia ya utakatifu.” Mwenye taka haipitii, kwa kuwa yeye hujakwenye chemchemi kwanza; kisha anaingia katika njia kuu.

Yeye alizivunja nguvu za Shetani. Aliifungua milango yagereza ya Kuzimu. Kwa kila mtu aliyefungiwa katika dunia—hii—katika magereza—akiogopa wakati wa kufa, kile mautiyangefanya kwake; pale Kalvari Yeye aliifungua hiyo milangoya gereza na kumwachilia huru kila mfungwa. Haikupasitena kunyanyaswa na dhambi. Haikupasi tena kuvitoa viungovyako kufanya dhambi, kunywa pombe, kuvuta sigara, kuchezakamari, kusema uongo.

Page 12: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

12 LILE NENO LILILONENWA

Unaweza kuwa mwaminifu, mwenye haki, mtu mwenyeadili; naye Shetani hawezi kufanya lo lote kuhusu hilo, kwakuwa umeshikilia kamba, kamba ya kuokolea. Imetiwa nangakatikaMwambaWenye Imara. Hakuna kinachoweza kukuondoahapo. Hakuna upepo unaoweza kukuondoa kwake. Hakuna kitu,hata mauti yenyewe haiwezi kututenganisha na upendo waMungu ulio katika Kristo Yesu.

Hivyo ndivyo Kalvari ilimaanisha. Watu waliokuwakifungoni waliwekwa huru. Watu walioogopa mauti hawawezikuogopa mauti tena. Mtu anayeuonea shauku mji ambaoMwenye Kuujenga na Mwenye Kuubuni ni Mungu, anawezakutembea katika njia iliyo kuu na kuuelekeza uso wake,kuelekea Mbinguni, kwa sababu yuko huru. Haleluya!Amekombolewa. Haimpasi kutangatanga tena, kwa kuwa kunanjia ya kujua kama uko sahihi ama sivyo. Mungu hutupa uzima.Dhambi zetu zimeondolewa. Siku hiyo pale Kalvari gharamaililipwa.

Tunapoona hayo yote, si ajabu yulemshairi aliandika:“Huku miamba ikipasuka na mbingu zikiwagiza,

Mwokozi wangu alikiinamisha kichwa Chakeakafa.

Pazia iliyofunguliwa ilifunua njia,Ya shangwe za mbinguni na siku isiyo namwisho.”

Haikumbidi Ibrahimu kuendelea kutangatanga zaidi kotenchini akiutafuta mji. Mwenye dhambi hapaswi kuwa nawasiwasi tena iwapo ataokolewa au la. Mgonjwa hapaswikuwa na wasiwasi kama anaweza kuponywa ama hawezi. Paziailiyofunguliwa siku hiyo pale Kalvari alifunua njia ya ushindikamili. Mungu alitupa nguvu za RohoWake tupate kuishi tukiwawashindi wa mambo haya yote; tunatakiwa tu kuamini hilo—hilo lilitendeka siku hiyo pale Kalvari.

Hapajakuwepo na siku kama hiyo. Hakutakuwepo nanyingine kama hiyo. Haihitajiki tena. Gharama ililipwa,nasi tumekwisha kukombolewa. Mungu ashukuriwe,tumekombolewa!

Haikupasi tena kuwa na wasiwasi, hamna tena kukisia.Zote zimeondolewa. Ile pazia ilifunguliwa—pazia—nasi tukokwenye barabara kuu, tusiwe na wasiwasi tena, bali kuamini nakupiga hatua mbele. Tutatembea hata katika uwepo wa Munguulio mkuu.

Ibrahimu alijua, na wengine walijua ya kwamba wakatiwalipokuwa wakiutafuta ule mji, wao walijua walitoka mahalifulani. Jambo fulani lilikuwa limetendeka. Wao walikuwawakiishi katika dunia iliyopooza. Matetemeko ya nchi yakaja,tufani zikaja, vita na mauaji. Mbwa mwitu na mwana-kondoo

Page 13: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 13

wanakulana, ama mbwa mwitu akamla mwana-kondoo, nayesimba anamla ng’ombe. Haionekani sawa. Kuna kasoro. Waowalijua kulikuweko na kasoro. Mwanadamu, ndugu alimuuandugu. Baba akamuua mwana; mwana anamuua baba. Kunakasoro. Yeye anazeeka. Yuafa. Anatoweka. Anashikwa naugonjwa. Yuko utumwani. Miti hukua bali si ya kudumu, hufa.Milima hubadilika. Bahari hukauka. Maji huisha. Kuna kasoro,naye akatafuta mahali, mji ambamo hayo hayakutendeka tena.Alijua ya kwamba kama angaliweza kurudi katika uwepo wayuleMtu aliyeubuni, angezungumza hayo pamojaNaye.

Lo, ni majaliwa jinsi gani, mwenye dhambi, asubuhi ya leokujua ya kwamba umepata njia sasa. Siku hiyo pale Kalvariilifungua njia; kwa kuwa hao wazee wetu wote walimtafuta sanaYeye, wakautafuta. Kalvari ilikupa hiyo bure.

Unawezaje kuikataa? Unawezaje kuikataa kisha ujiungena dhehebu? Unawezaje kuikataa halafu uibadilishe na kitukingine, anasa za ulimwengu. Mbona usiikubali?

Pazia iliyofunguliwa humleta mtu moja kwa mojaikamrudisha katika uwepo wa Mungu bila dhambi ya namnayo yote juu yake, na inaitayarisha njia mbele yake ya kuelekeakwenye kitu anachokitafuta— Mbinguni, utukufu, amani, uzimawa milele—kila kitu mbele yake.

Siku hiyo ilikuwa pigo la mauti kwa nguvu za Shetani.Ilimaliza kila kitu, nami naweza kumwona Yeye pale. Alikuwayule Mwana-kondoo wa Edeni tangu kivuli cha kwanzakilichotokea, wakati Habili kwa imani alimtolea Mungudhabihu iliyo bora kuliko Kaini.

Hapana shaka alikuwa amefunga mzabibu shingoni mwahuyo mwana-kondoo, akamvuta hata mwambani, akatwaa jiwemkononi mwake kama kisu, akakivuta kichwa chake nyumakisha akamkatakata na kumchonga kwa nguvu hata akafa, namanyoya yakalowa damu yake. Yeye alilowa kwa damu yake.

Ilikuwa kivuli, bali siku hiyo pale Kalvari, hapakuwepoMwana-kondoo wa dunia hii, bali ni Mwana-Kondoo wa Mungualiyekuwa anakufa—akagaagaa katika damu Yake Mwenyewe.Alikatakatwa kwa nguvu, akakatakatwa, akapigwa, akatemewamate, akatupwa chini, akapigwa makofi, na kufanyiwa kila kituna walimwengu, huku damu inatiririka chini ya vishungi Vyake.Mwana-kondoo wa Habili alipokufa, alikufa akinena katikalugha ambayoHabili hakuifahamu. Alikuwa akilia. Na

Mwana-Kondoo wa Mungu alipokufa siku ile pale Kalvari,Huyo alinena katika lugha ambayo hakuna mtu alimwelewaYeye, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha.”Alikuwa ni Mwana-Kondoo wa Mungu, aliyekatwa vipande-vipande, akakatakatwa.

Alikuwa Mwana-Kondoo yule yule ambaye Habilialikuwa akiwazia. Wakati alipomwona mzao wa mwanamke

Page 14: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

14 LILE NENO LILILONENWA

aliyeahidiwa. Yeye alikuwa Mwana-Kondoo ambaye Danielialimwona “aliyechongwa mlimani bila kazi ya mikono.”Alikuwa “gurudumu ndani ya gurudumu” kwa manabii. Nayote waliyotangulia kuona yalitimizwa siku hiyo—siku hiyo paleKalvari. Hilo liliingiza kile kitu kikuu. Hiyo ilimvunja Shetanimgongo.

Kwanza, inatupasa kutafuta kujua maana ya siku hiyo.Pili, inatupasa kuona yale hiyo siku iliyotufanyia, sasa vileilivyotufanyia. Sasa ya tatu, hebu na tuone yanayotupasakuifanyia siku hiyo, yatupasa kufanya nini.

Kwanza, inatupasa kuichunguza, kwa kuwa ni siku kuu—siku kubwa ya zote. Gharama ya dhambi ilimalizika. Nguvu zaShetani zilivunjwa. Na sasa tunataka kuona yatupasayo kutendakwa shukrani.

Sasa mahali pake, Yesu alipokufa msalabani, pale Kalvarisiku hiyo, Yeye hakulipa tu gharama ya dhambi zetu, balialilipa gharama hiyo na pia akatufanyia njia tupate kumfuataYeye. Kwa maana sisi, kama Adamu aliyeanguka ambayeamekombolewa, kama Roho alivyomwongoza Adamu—Adamuwa kwanza—kwa Roho ambaye alikuwa na mamlaka juu yamaumbile yote. Ndipo sisi—Adamu wa pili—ama watu waduniani, tumekombolewa naKristo tangu siku hiyo paleKalvari,tunaweza kumfuata Yeye.

Basi, alipokufa pale Kalvari, alitengeneza njia. Alitoa Roho,Roho Mtakatifu ambaye alimtuma arudi duniani kwa ajili yakona mimi tupate kuishi kwake. Hiyo ndiyo maana ya Kalvarikwetu kumfuata Yeye.

Kwanza, ichunguze. Uone iliyotutendea, na sasa inatulazimusisi kufanya nini kuhusu hiyo siku. Mimi na wewe yatupasatufanyeje? Sasa, tunasema, “Naam, nayathamini hayo. Hayo nimema sana.” Lakini hatuna budi kuyakubali. Na kuyakubali nikuikubali nafsi Yake, Kristo, mioyoni mwetu. Ndipo tunakuwahuru na dhambi. Kwa hivyo, hakuna kabisa pingu za dhambizinazoning’inia kwetu. Mungu…kama tu kwamba hatukuwahikutenda dhambi.

Ile sadaka iliyo kamilifu ilitufanya wakamilifu. Kwa kuwaYesu alisema, “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Babayenu wa Mbinguni alivyo mkamilifu.” Ndipo hamna jingine lakufanya, bali sisi tunafanywawakamilifumbele zaMungu.

Sasa hapo ndipo tunapopotezamahali petu. Kama hatukuwawaangalifu, tunajaribu kuangalia kule nyuma jinsi tulivyokuwa;na maadamu tunaangalia nyuma kuona tulichokuwa, iledhabihu haina maana kwetu. Lo, kanisa, hamwezi kuona?Nisingeijaribu hiyo kazi, siwezi, wala wewe pia. Hakuna hajaya kujaribu. Jambo la kwanza wewe umepotea mradi tuunategemea yale uliyotenda. Lakini usitazame yale umefanya,tazama yale siku hiyo pale Kalvari iliyokufanyia.

Page 15: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 15

Ililipa gharama yako. Ilimaliza lile swali. Dhambi zako ziwenyekundu sana, zinakuwa nyeupe kama theluji. Nyekundu kamabendera, nyeupe kama sufu. Basi huna dhambi. Huna dhambikabisa. Haidhuru ulifanya nini ama ufanye nini, ungali hunadhambi. Mradi tu umemkubali Yesu Kristo kama Mwokoziwako, dhambi zako zimesamehewa. Cho chote kilichosamehewakimeondolewa na kusahauliwa.

Ndipo inafanya nini? Inakupa wewe baada ya hali hiyo RohoWake kumfuata, na kufanya kama ilivyofanya, kwa wenginewanaofuata.

Yeye alikuwa Mtu mmoja tu, Mtu aliye mkamilifu. Alitoauhai Wake, naye alitoa mfano kwako.

Sasa, inatupasa kufanya nini. Sasa, jambo la kwanzaninalotaka kusema ni: Yesu hakujiishiaMwenyewe.Maisha Yakeyalitumika kwa ajili ya wengine. Huo ni uzima wa milele hasa.Unaposema unaenda kanisani na unatenda mambo mazuri, hiloni sawa. Bali unapojiishia maisha yako binafsi, hauna uzima wamilele. Uzimawamilele ni kuishi kwa ajili yawengine.

Ilithibitika alipokuja Mwana-Kondoo wa Mungu. Aliishina alikuwa na uzima wa milele kwa sababu, Yeye hakujiishiaYeye Mwenyewe. Aliishi kwa ajili ya wengine. Nawe unaupokeauzima wa milele kwa kuipokea hiyo siku, nawe hujiishii binafsitena. Unawaishia wengine.

Mtu mmoja alisema, “Wawezaje kusimama na kumwachamtu ye yote akuite majina mabaya kama hayo?” Haujiishiimwenyewe. Unawaishia wengine upate kumkomboa mtu huyo.Mnafanyika wana; na shida yake ni kwamba kanisa limesahauya kwamba wao walikuwa wana. Ninyi ni wana. Mnapachukuamahali pa Kristo. Ninyi ni wana; kwa hivyo msijiishie wenyewe,waishieni wengine.

“Vema, Ndugu Branham, naweza kumwishia ndugu huyukwa sababu yeye ni mtu mzuri sana.” Hivyo sivyo. Mwishie mtuhuyo anayekuchukia. Mwishie mtu huyo ambaye angalikuuakama angaliweza. Hivyo ndivyo walivyomtendea. WalimuuaYeye, naye alikufa apate kuwaokoa wao. Huo ndio uzima wamilele. Unapoupata huo ndani yako, unaelekeaMbinguni wakatihuo. Lakini toa dhabihu vitu vyako. Vitoe kama mwana-kondooanavyotoamanyoya yake. Unaangalia Kalvari.

Natumaini hili linakusaidia kufikia mahali…Hivyo ndivyoMaskani haya, hivyo ndivyo watu wote wanapaswa kufanya—nikujua ulivyo, na kusudi lake ni nini.

Kanisa si kuenda kanisani kupiga tu muziki, kuimbanyimbo. Kanisa ni mahali pa masahihisho. Hukumu huanziakatika nyumba ya Mungu. Sharti tujihesabu sisi wenyewe kuwawafu na tulio hai kwa Kristo. Kisha akatengeneza njia tuwezekujitoa dhabihu kwa ajili ya hudumaYake kumfuata Yeye. Kamatukimfuata, tunaishimaisha aliyoishi Yeye. Hilo ni la ajabu sana.

Page 16: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

16 LILE NENO LILILONENWA

Yesu alisema na akanena juu yake…Hebu ninukuu machachekuhusu jambo hili. Sikilizeni kwamakini. Msilikose.

Yesu alisema katika siku hiyo atawabagua watu kamakondoo na mbuzi, kisha atawaambia hao mbuzi, “Simameniupandewa kushoto,” na kondoo, “Simameni upandewa kuume.”Naye akawaambia mbuzi, “Ondokeni Kwangu, kwa sababunilikuwa na njaa nanyi hamkunilisha. Nilikuwa kifungoni,msije kunitazama. Nilikuwa uchi, msinivike nguo. Nilikuwana kiu, msininyweshe. Nilikuwa mgonjwa, msije kunitazama.Kwa hivyo ondokeni kwangu.” Na upande wa kondoo, alisema,“Nilikuwa na njaa mkanilisha. Nilikuwa uchi mkanivika.Nilikuwa mgonjwa mkanihudumia.” Tena angalia, msikosekulipata hili, kanisa! Liwekeni hili mioyoni mwenu milele!Yalitendwa bila kujua kabisa. Watu hawafanyi hivyo kamajukumu lao. Mtu anayekupa kitu fulani kwa sababu anapaswakufanya hivyo, mtu anayekulisha kwa sababu inampasa kufanyahivyo, ana wazo la kichoyo. Inapaswa kuwa maisha yako halisi,matendo yako halisi.

Iliwashangaza sana hawa kondoo hata wakasema, “Bwana,ni lini ulipokuwa na njaa tusikulishe? Ni lini ulipokuwana njaa, tukakulisha? Ni lini ulipokuwa uchi, tukakupanguo? Ulikuwa na kiu lini, tukakunywesha? Ni lini ulikuwamgonjwa, tukakuhudumia?” Yalifanywa bila kufikiria kabisa—kwa upendo. Ni maisha yao waliyoishi.

Mungu jalia watu waone kile Kalvari ilichotufanyia. Tukiotu, “Ni lini ulikuwa…,Bwana. Sisi hatukujua hilo.”

Tazama yale Yesu aligeuka akasema, “Kadirimlivyowatendea hawa, mlinitendea Mimi.” Maisha yasiyo yakichoyo. Si wazo la pili, si kuliwazia; bali umekufa kabisakwa mambo ya ulimwengu huu, uko hai kabisa katika Kristo,na unatembea imara kwenye ile njia kuu, hata mambo hayayanatukia yenyewe tu. Unatenda tu.

Unasema, vema “Sasa Bwana angenitaka kufanya hivyo.” Sihivyo. Wewe ni sehemu Yake tu. Roho Wake yumo ndani yako,nawe unatenda jinsi Yeye alivyotenda. Unafahamu? “Iko njiaionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ninjia za mauti.” “Si wote wasemao Bwana, Bwana, watakaoingia,bali ni wao wafanyao mapenzi ya Baba Yangu”—kutoka tumioyoni mwao, kwa unyofu tu.

Sasa, siku hiyo pale Kalvari ililipa gharama tuweze kuwahivyo. Si kusema, “Unajua, mjane Jones wakati mmoja hakuwana makaa, nami nikaondoka nikaenda nikamnunulia makaakidogo.” “Nakwambia nalimwona ndugu aliyehitaji suti, naminikaondoka nikaenda nikamnunulia suti. Mungu abarikiwemimi ni Mkristo.” Lo, jamani, ewe mtu mchoyo, maskini,mwenye mashaka! Ninyi ni wanafiki. Usiache mkono wa kulia

Page 17: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 17

ujue yale wa kushoto unalofanya, wala wa kushoto usijue wakulia unalofanya.

Umekufa kabisa katika Kristo hata utalitenda kwavyovyote. Ni asili yako, ndivyo ulivyoumbwa. Utafanya hivyokwa vyovyote. Ni uhai tu unaoishi ndani yako. Umejitoa kabisakwa Roho huyo, naye Mwenyewe anaishi maisha Yake ndaniyako.

Lo, unamsikia huyu Roho aliyebarikiwa? Huo uhai. “Si miminiliye hai,” kasema Paulo, “bali Kristo yu hai ndani yangu.”Inatukia hivyo tu.

“Naam, nakwambia, NduguBranham. Sisi niWakristo hapa.Tunawasaidia watu hawa. Tunawasaidia hao watu.” Lo, jamani,huna aibu! Huo si Ukristo. Ukristo ni tukio linalotendeka tu.Unasahau kuhusu hayo, kuhusu yote…Nenda utende hayo.

Kristo aliyakabidhi kikamilifu maisha Yake kwa Mungu.Alijitoa Binafsi kama mtumishi wa umma kwa watu. Aliutoauhai Wake bure. Haikumbidi kutenda hilo. Hakulitenda kwauchoyo. Hakusema, “Sasa ndugu, nyote yawapasa kunifikiriasana Mimi kwa sababu nilikuja kuwafia ninyi.” Hakusema nenokuhusu hilo. Alikufa kwa vyo vyote. Kwa sababu ilikuwaMungundani Yake. Ni Mungu ndani yako. Ni Mungu ndani yanguanayetufanya tuwaangalie wengine.

Kondoo upande mmoja. Mmoja wao atasema, “Naam,Bwana, nalifanya hili, na Bwana, nalifanya hilo.”

Alisema, “Ondokeni Kwangu enyi mtendao maovu.Sikuwajua ninyi kamwe.”

Laiti kanisa lingefikia kweli hizo za kimsingi! Hilo si jambounalojaribu kufanya. Wewe unajitahidi kufanya hivyo. Ni kituulichozaliwa nacho.

Samahani, marafiki zangu Wapentekoste. Mimi niMpentekoste, lakini marafiki zangu Wapentekoste wamefikiamahali ambapo inabidi kuwe na muziki moto moto, bendi fulaniikiimba, kupiga makofi, ama matari kusababisha vifijo. Huo nimsisimuko tu! Watu hucheza bendi kabla hawajaenda vitanikuwaingiza watu katika msisimuko wa vita. Nakubalianana muziki. Nakubaliana na kupiga makofi, bali nakubalianana mambo haya. Hiyo ni kweli kabisa. Inatupasa kuwa nahayo, lakini mmeacha mambo makuu bila kuyafanya. Ni hayomaisha ya kujitoa mwenyewe, ambayo Mungu anaishi ndaniyako, ukitenda bila kufikiria tu yaliyo haki, kwa sababu nihaki—ukiendelea tu, hata hauliwazii, unaishi hivyo tu. Halafuangalia—unaona yanayoendelea, wewe—uko katika njia kuu.Hivyo ndivyo Kalvari ilimaanisha kwako kwenye njia kuu—iliyofunguliwa kwa ajili yako siku hiyo.

Sasa kumbuka, hauwezi ukawa nusu mbuzi na nusukondoo. Hawawezi kuchanganyika. Sasa, kuna watu wengi sana

Page 18: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

18 LILE NENO LILILONENWA

wanaosema, “Naamunajua? Tunamadhehebu katika kundi letu.Tunawasaidia maskini. Tunafanya hivi.” Hiyo ni sawa, lakiniunajigamba. Usifanye hivyo. Toa sadaka zako katika siri, Yesualisema. Kwako ni jambo tu unalotenda bila kufikiria.

Si tofauti na kwenda ukachukuamaji ukanywa.Unakuwa nakiu. Kamamtu aliye karibu nawe ana kiu, mfikirie, pia. Mahitajiya mtu aliye karibu na wewe, mfikirie jinsi tu ungelifikiriamahitaji yako, na usijali, endelea kuishi tu.

Sasa hauwezi kuwa nusu kondoo na nusu mbuzi.Kwa hiyo kama ukisema, “Kanisa letu lina madhehebu.Tunawatolea maskini. Tunafanya hivi, tunafanya vile, nakufanya vinginevyo.” Kama ulikuwa na hilo bila lile jingine—maisha yaKristo ndani yako—unayofanya ni ubatili mtupu.

Paulo alisema katika I Wakorintho 13, “Nijapotoa malizangu zote kuwalisha maskini, na kuutoa mwili wangu niunguemoto kama dhabihu, si kitu mimi.” Sasa hili ni gumu bali nikweli. Huna budi kuifikia hiyo kweli. Tambua yale Kalvariiliyokutendea.

Tunaitazama na kusema, “Lo, ndiyo, hilo ni sawa.” Sivyoilivyo. Kama ilimpasa huyo Mwana wa Mungu kwenda Kalvariakasulubishwe, kila mwana ajaye hana budi kwenda Kalvari.Lazima awe na Kalvari pia. Lazima uwe na siku hiyo ya Kalvari.Sina budi kuwa na hiyo siku ya Kalvari. Hiyo inalimaliza swalila dhambi. Si kupeana mikono na mhubiri, si kupewa mkonouingizwe kanisani, si kuingia kwa barua, si kuingia kwa kukiri,bali kuingia kwa kuzaliwa.

Yeye hakutoa barua. Yeye hakutoa kukiri, Yeye alitoakuzaliwa. Hivyo ndivyo tunavyoingia. Ndipo kutokea hapo,tunaishi maisha ya Kikristo moja kwamoja.

Sasa tamshi lingine. Nusu mbuzi, nusu kondoo: hawana kitukama hicho.Wewe si nusumbuzi na nusu kondoo, wewe nimbuziau ni kondoo. Sasa kama unafanya mambo mazuri, na unafikiriunaweza kuingia kwa hayo, basi hapakuweko haja ya kuwa nasiku ya Kalvari. Torati ilikuwa na hayo. Lakini sababu ya sikuya Kalvari kuhitajika ni kuingiza hilo ndani—kusudi tusiwe tuwashiriki wa kanisa, bali tuwe wana wa kiume na wa kike waMungu.

Hivyo ndivyo ile siku ya Kalvari ilivyokuwa. Hivyo ndivyoilivyomaanisha kwako. Kusudi ufanye, umfuate na utende kamaYesu…

Sasa mto hautiririki kuelekea juu na kuelekea chini wakatiule ule. Mto hutiririka kuelekea upande mmoja tu, na Rohowa Mungu huelekea upande mmoja. Hajichanganyi na mambo.Huelekea upande ule ule.

Mtazameni Yesu, tunapofunga. Yesu alisema, “Kazinizifanyazo Mimi, ninyi nanyi mtazifanya, na kubwa kuliko

Page 19: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 19

hizo mtazifanya, kwa kuwa Mimi naenda kwa Baba.” Sisemihili hasa kwa kanisa hapa, mnafahamu, bali jumbe hizizinanaswa kwenye kanda. Watu makumi elfu huzisikiliza koteulimwenguni. Nitalijibu swali hilo kwa ajili ya mtoa lawamasasa hivi. Mara nyingi nimeambiwa, wao husema, “Ni vileunavyoamini Biblia?” Yesu alisema, “Kazi hizi nizifanyazoMimininyi nanyi mtazifanya; naam, na kubwa kuliko hizi mtazifanyakwa kuwaMimi naenda kwa Baba.”

Unaweza kuwa mbaya jinsi gani bwana? Unawezakutangatanga mbali na upambanuzi jinsi gani kwa hekimaya theologia yako, kwa mawazo ya akili yako juu ya jambo lolote? Rafiki yangu mwema uliyepotea, je hauwezi kufahamuya kwamba Biblia hii inafasiriwa kiroho? Yesu alimshukuruBaba kwamba Yeye alikuwa ameyaficha hayo kwa wenye elimu,watu werevu, wenye hekima, na akili, naye atawafunulia watotowachanga ambao wangekuja Kalvari.

Sasa tazama, Yesu alisema…Tazama jinsi alivyolielezea!“Kazi nizifanyazo Mimi…” (Anazifanya hizo sasa hivi.) “Kazininazofanya sasa—kuwaponya wagonjwa, kuwafufua wafu,kuyafungua macho ya vipofu—kazi hizi mtazifanya nyinyipia. Mtazifanya hizi kama mnaniamini Mimi. Mtazifanyahizi kazi, halafu kubwa kuliko hizi mtazifanya. Kwa kuwanaenda kwa Baba Yangu. Bado kitambo kidogo na ulimwenguhautaniona tena. Bali ninyi mtaniona. Nitakuwa pamoja nanyi,hata ndani yenu hata ukamilifu wa dahari. Sitawaacha ninyibila faraja. Nitamwomba Baba. Naye atawapelekea Msaidizimwingine, ambaye ni Roho Mtakatifu, ambaye ulimwenguhauwezi kumpokea, bali ninyimnaweza kumpokeaHuyo.”

Sasa tazama zile kazi kubwa zaidi zilikuwa kupata nguvukanisani, si kuwaponya tu wagonjwa kwa maombi, kuwatoapepo kwa maombi, bali kuwapa waamini uzima wa milele. RohoMtakatifu alikuwa yuaja na aliwekwa mikononi mwa kanisaapate kuwapa uzima. Lo! hiyo ndiyomaana yaKalvari.

Alichukua wanaume na wanawake waliodhiliwa nawalioshushwa vyeo naye akawainua mpaka mahali ambapowamekuwa wana na binti za Mungu, kuwaponya wagonjwana kuwapa uzima wa milele. Kwa kuwapa Roho Mtakatifuwaaminio watiifu. Watu ambao siku moja walikuwa wasioaminikuwafanya waamini na kuwapa uzimawamilele.

Ni kuu zaidi kiasi gani kumwambia mwanamke huyumgonjwa anayelala hapa, “Naweza kuomba ombi la imani”,naye ataponywa. Hilo ni jambo kuu. Hilo ndilo alilokuwaakifanya wakati huo; bali akasema, “Kubwa kuliko hizimtazifanya. Nitawapa nguvu, si kumwinua juu tu kwa mudakidogo, bali kumpa UzimawaMilele—ambao utakuwawamilelena milele.”

Page 20: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

20 LILE NENO LILILONENWA

Watu maskini, vipofu, wanyonge, mnakosaje hilo? Je,hamuoni hilo jambo kuu ni nini? Hilo ndilo jambo kuu sanaambalo lingaliweza kutendeka, lilikuwa kuwapa watu Uzimawa Milele.

Je, uzima wa milele ni nini? Maisha aliyoishi Yeye. Uhaiuliokuwa ndani Yake, kuwapa huo wengine. Je, mwanadamuanaweza kufanya hivyo? Mwana wa Mungu anaweza. Yesualisema, “Wo wote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa.Wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.” Sasa, hapandipo Kanisa Katoliki na mengine mengi yalitenda kosa laokubwa. Wao wanaondoka na kusema, “Nakusamehe dhambizako.” Haikuwa hivyo.

Je, hao walisamehewa dhambi zao vipi katika Biblia? Petroalilijibu swali hilo kwenye siku ya Pentekoste. Wao walisema,“Tufanyeje tupate kuokolewa? Tupateje hiki mlicho nacho ninyinyote?”

Yeye alitoa maelezo. Akawaambia la kufanya. Alisema,“Tubuni, kila mmoja wenu kwaMungu, mkabatizwe katika Jinala YesuKristo.” Kwa nini? “KwaOndoleo la dhambi zenu.” Ndizohizo zile kazi kubwa.

Ni wangapi wenu wahubiri asubuhi ya leo, ni wangapi wenumnaosikiliza asubuhi ya leo, ni wangapi wenumnaosikiliza nenolangu kwenye kanda ya sumaku, je, mko tayari kwenda Kalvariasubuhi ya leo? Kutazama yale Mungu aliyowafanyia kule, namuachane na kanuni zenu za imani ya kimadhehebu mkaihubiriInjili. Haleluya! Ni juu yenu sasa. Mtafanyaje nayo? Kwa nini?Habari ya toba na ondoleo la dhambi lazima kuhubiriwa katikajina Lake ulimwenguni kote kuanzia Yerusalemu. Haleluya!Ndivyo hivyo.

Je, Kalvari ina maana gani kwako? Siku hiyo ilikufanyianini? Je, ilikujaza theolojia chungu nzima? Je, ilikufanyamwenyekiburi, ama ilikufanya Mkristo? Aliyejitoa kabisa! Haleluya!Dhambi ikaondolewa. Kazi kubwa kuliko hizi ninyi mtazifanya.Mnaona mahali ninyi walipo, sivyo? Kazi kubwa kuliko hizi,kuondoa dhambi katika jina la Yesu Kristo. Lakini kupitiakanuni za imani, na madhehebu, na kadhalika ulifungwa sanahata kufikia mahali ambapo ungali unautumikia ulimwengu.Niambieni, mwanaume ye yote, niambieni, mwanamke ye yote,anayeweza kuja Kalvari, na kujaribu kuwa mtu mashuhuri kwasababu mtu fulani alisema jambo fulani…Niambie ni wapiunakoweza kutazama uso wa Kalvari katika nuru yake iliyosahihi siku hiyo katika Kalvari.

Unawezaje kuwa na siku yako pale Kalvari kisha utokemtu mwenye majivuno? Wawezaje kutoka huko ukiwa kibarakawa madhehebu fulani kuhubiri mafundisho yaliyobuniwa namwanadamu? Mbona isikufanye mnyenyekevu kwa Neno laMungu? Ukienda pale, utatoka ukiwa mnyenyekevu. Wawezaje

Page 21: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 21

kutamani kuwa mtu fulani mkuu katika dhehebu lako ukiwana majivuno, huku Kristo, Mwana wa Mungu alijinyenyekezahata akakatakatwa mwili na “kutemewa mate usoni” hataaibu na fedheha, walipomvua nguo Zake na kumsulubishambele ya ulimwengu, akidharau aibu? Wawezaje kwenda katikaKalvari na utoke ukiwa kitu tofauti na vile Yeye alivyokuwa?Fedheha, aibu.

“Naam,” unasema, “watanifukuza.” Hebu na wakufukuze.Pata siku yako kule Kalvari. Mungu atajua la kukutendea. Hebuninukuu hilo tena. Pata siku yako pale Kalvari, Mungu atajua lakukutendea. Hebu tuombe.

Bwana, EeMungu, tupeleke sote hadiKalvari sasa hivi. Hebuna tutoke katika ubinafsi, Bwana—kumwogopa mwanadamu,kuogopa yale mtu fulani atakayosema. Kwani, ulimwengumzima ulimcheka Yeye, ukamfedhehi. Lakini alikuwa mtii hatamauti. Alikuwa mtii hata fedheha. Alikuwa mtii hata kwaserikali kuu, nasi tunatambua ya kwamba Shetani alipoipigadunia hii, alifanyika mtawala na mwenye mamlaka katika duniahii. Alishuhudia jambo hilo mbele ya Bwana wetu akasema,“Milki hizi ni zangu. Nitazifanyia kama nipendavyo.” Nasitunatambua ya kwamba tangu siku hiyo hadi wa leo, ulimwenguhuu, chini ya laana, umetawaliwa na yule aliyeulaani. BaliMungu, EeMungu, sisi tunautumikia ufalme usiolaaniwa.

Baba Mungu, ni ajabu vipi kwamba umefanya mambomakuu katika ulimwengu wa sinema siku hizi. Ukiruhususinema hizi za mambo makuu kama Amri Kumi, na kadhalika,zitokee, ukawaruhusu wanaume na wanawake kuziona,ambao hata hawangalithubutu kuingia katika mlangowa kanisa, bali ukawaruhusu waone vile zilivyo. Njia yaMungu ni Njia iliyokataliwa na walimwengu, kwa sababutuko hasa…tunaingia Urusi chini ya Ukomunisti…Tumokatika ulimwengu huu, bali sisi si wa ulimwengu huu.Tumekwisha kwenda Kalvari. Tumejisulubisha, pamoja naufalme wa Mungu, kuwa mmoja wa hao walio Wake. Haidhuruulimwengu utasemaje, tunaungana nawale wachachewaMunguwaliodharauliwa. Tunapiga hatua kuelekea ule ufufuo, nasitunaamini umekaribia sana Bwana wakati tutafufuliwa katikaufalme utakaoutwaa ulimwengu huu kama Danieli alivyouonaawali; na Yeye akauvunjilia mbali ulimwengu vipande-vipandekama makapi ya sakafu za kupepetea wakati wa hari na upepoukavipeperusha. Bali ule mlima, lile jiwe, likakua likawa mlimamkubwa ulioijaza dunia. Jiwe hilo litakuja. Ee Mungu, sisitunataka kuwa sehemu yake. Hebu na tujikane wenyewe,tuutwae msalaba wetu kila siku. Tumwishie Kristo, tuwaishiewengine, tujalie Bwana.

Kama kuna baadhi ya watu hapa asubuhi ya leo wasiomjuaYeye kama Mwokozi nao wangetaka kukumbukwa katikamaombi ya kumalizia na wangetaka hii iwe siku yao pale

Page 22: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

22 LILE NENO LILILONENWA

Kalvari, waweza kuinua mkono wako useme, “Niombee, NduguBranham. Nataka kumjua Yeye kama Mwokozi wangu.” Munguakubariki, kijana. Mwingine? Mungu akubariki, ndugu yanguhuko nyuma. Kuna mwingine atakayesema, “Nataka kumjua.Nataka hii iwe siku ya pale Kalvari kwa ajili yangu. Miminaugua na nimechoka. Kuna faida gani kwangu kufanyamchezo hapa na kitu halisi nilichozaliwa kufanya? Nilipozaliwa,nilizaliwa kuwa mwana wa Mungu, na mimi niko hapanikiyashikilia mambo ya ulimwengu.Mungu, hebu nisulubishweleo. Hebu nijisulubishe leo pamoja na mawazo yangu, nipatekuishi pamoja naKristo na nipate kuwaishia wengine. Haidhuruwatanifanyaje, hata wakinidhihaki, wakinitesa, na kusemamaovu yote dhidi yangu na kadhalika, hebu nitembee kwaunyenyekevu, mnyenyekevu kama mwana-kondoo, kama Yeyealivyofanya. Na siku moja ameahidi kunifufua tena katika sikuya mwisho. Ninaitazamia siku hiyo.”

Je, kuna mikono mingine itakayoinuliwa? Mungu akubarikihuko nyuma, nawewe. Vema,wengine.Mungu akubariki,Munguakubariki. Wengine kabla hatujaomba.

Baba yetu wa Mbinguni, ilisemwa Petro alipohubiri kwenyesiku ya Pentekoste, “Wote walioamini wakazidi kuongezekakatika kanisa.” Wao wameamini kabisa kwa mioyo yao yote,hawa watu ambao sasa wameinua mikono yao. Naaminiya kwamba wameamini kwa mioyo yao yote. Na iwapowamefanya hivyo, tayari kuna kidimbwi chamaji kinachongojeahapa. Wanataka msamaha wa dhambi hizo, na kuna mtuhapa anayeweza kuwabatiza katika Jina hilo, na Jina pekeelililopo chini ya Mbingu walilopewa wanadamu, ambalo kwalotunapaswa kuokolewa. Kwa kuwa nilinukuu Maandiko mudamfupi uliopita, ya kwamba “habari ya toba na ondoleo ladhambi lazima vihubiriwe katika Jina Lake ulimwenguni kote,kuanzia tangu Yerusalemu.” Na kule Yerusalemu, wakati habariza toba na ondoleo la dhambi zilihubiriwa, wale mitumewaliwaambia habari za maandiko na kusema lazima watubukwanza, kisha wakabatizwe katika jina Lake Yesu Kristo. Hiyoilikuwa kazi ya muhubiri kufanya. Wao watubu, naye awabatizekwa ondoleo la dhambi zao. “Wo wote mtakaowaondoleadhambi, wameondolewa. Wo wote mtakaowafungia dhambi,wamefungiwa.”

Baba, walimwengu walipatwaje na hamaki waliyo nayo?Mbona wasiamini injili iliyo rahisi? Nao hata huingiza kwaajili ya hiyo kutia majina ya uongo badala yake, mabatizo yauongo, ubatizo wa uongo wa Roho Mtakatifu, kupeana mikonona wahudumu, wakitumia vyeo vya Baba, Mwana, na RohoMtakatifu ambao haupo katika Maandiko—mpango uliewekwana watu wa Kirumi, si mafundisho ya Kikristo. Hakuna mahalipo pote katika Biblia. Ondoleo la dhambi haiwezi kuondolewakwa vyeo, bali kwa Jina Lake Yesu Kristo.

Page 23: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI 23

Sasa Baba, tunajua haipendwi sana na watu. Njia Zakozimekuwa hivyo daima; bali hebu wanaume na wanawakeasubuhi ya leo waje kwenye siku hiyo, siku hiyo pale Kalvari.Ambapo Yesu akiidharau siku hiyo, aibu hiyo ya kuvuliwa nguo,kukatwa vipande-vipande, kutemewa mate na kudhihakiwa naulimwengu mzima, na kanisa, na watu waliostahili kumpenda;hata hivyo katika hayo yote, Hakukifungua kinywa Chakena akaenda akawafia watu hao waliokuwa wakimfanyia Yeyedhihaka.

Mungu, tupeleke Kalvari asubuhi ya leo, na kama wakisemasisi tumerukwa na akili, wakisema hatukuyaelewa maandiko,cho chote wapendacho kusema, Mungu, wao hawawezikusimamambele zaMungu waseme ni kosa.

Hawawezi kuzifunika dhambi zao kwa Biblia. Bibliahuzifunua dhambi zao, kutokuamini kwao, kutaka kupendwana watu, kutenda kama watu wengine. Hebu wao waje Kalvariasubuhi ya leo na waanzie Yerusalemu, ili kwamba tobana ondoleo la dhambi lazima vihubiriwe katika Jina Lakekwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu. Hebu na wazichukuehatua zile zile za kusulubishwa, wakatwe-katwe na kutemewamate, wadhihakiwe na kuitwa cho chote wanachoweza kuitwakama wanaobadili dini zao—wanaoyavunja makanisa, yotewanayotaka kuwaita.

Tujalie nasi, Bwana, asubuhi ya leo tuungane nawachache wa Bwana wanaodharauliwa. Tujalie tutembee kamawalivyofanya mitume, tusigeukie upande wa kulia ama kushoto,na kwa unyofu wa mioyo yetu tumtumikie Mungu. Tujalie hayo,Baba.

Sasawaponyewagonjwa nawanaotesekawanaokuja kwenyemstari wa maombi. Wajalie hawa walioiinua mikono yao,watubu mioyoni mwao sasa hivi. Wajalie hao waliosimamanyuma kwa muda mrefu waingie majini upesi wapate ondoleola dhambi zao katika Jina la ile dhabihu, Yesu Kristo Mwana waMungu. Amina.

Page 24: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

SIKU HIYO PALE KALVARI SWA60-0925(That Day On Calvary)

Ujumbe huu uliohubiriwa na Ndugu William Marrion Branham, uliotolewahapo awali katika Kiingereza mnamo Jumapili asubuhi, Septemba 25, 1960,katika Maskani ya Branham huko Jeffersonville, Indiana, Marekani, umetolewakwenye kanda ya sumaku iliyorekodiwa na kuchapishwa bila kufupishwa katikaKiingereza. Tafsiri hii ya Kiswahili ilichapishwa na kusambazwa na Voice OfGod Recordings.

SWAHILI

©1989 VGR, ALL RIGHTS RESERVED

VOICE OF GOD RECORDINGS

P.O. BOX 950, JEFFERSONVILLE, INDIANA 47131 U.S.A.www.branham.org

Page 25: SIKU HIYO P KALVARIdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA60-0925 That Day On...2 LILENENOLILILONENWA ItakuwajetutakapofikaMbinguni,natukutanehukokatika wakatihuomkuuwaushirikawamilelenausionamwisho

Ilani ya haki ya kunakili

Haki zote zimehifadhiwa. Kitabu hiki kinaweza kuchapishwa kwa matbaa ya nyumbani kwa matumizi ya kibinafsi ama kusambaza, bila malipo, kama chombo cha kuitangazia Injili ya Yesu Kristo. Kitabu hiki hakiwezi kikauzwa, kunakiliwa kwa wingi, kuwekwa kwenye mtandao, kuhifadhiwa kikatolewe tena, kufasiriwa katika lugha zingine ama kutumiwa kuomba fedha bila idhini halisi iliyoandikwa moja kwa moja kutoka Voice Of God Recordings®.

Kwa habari zaidi ama kwa vifaa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Voice of God RecoRdinGsP.o. Box 950, JeffeRsonVille, indiana 47131 U.s.a.

www.branham.org