somo la 6 kwa ajili ya agasti 8, 2020 › descargar.php?id=sw_2020t306.pdf“kwa kusudi la...

10
Somo la 6 kwa ajili ya Agasti 8, 2020

Upload: others

Post on 02-Feb-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Somo la 6 kwa ajili ya Agasti 8, 2020

  • Yesu hakutuamuru kuihubiri tu injili kwa ulimwengu, lakini pia alitupatia karama zinazotuwezesha kutimizautume huo.

    Karama za roho zina ubora wa kiungu na zimetolewa naRoho Mtakatifu ili kuujenga mwili wa Kristo nakuwawezesha waaumini kuwa mashahidi bora kwaulimwengu.

  • “Lakini sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja.” (1 Wakorintho 12:20)

    Paulo aliwalinganisha washiriki wa Kanisa na mwili wamwanadamu. Katika mlinganisho huu, Kanisa ndilo mwili waKristo (1Kor. 12:12-27).

    Kama hivi, kila mshiriki wa Kanisa ni wa pekee na ana karama zake za pekee. Kila kiungo cha mwili kina jukumu, na hakuna mshiriki wa Kanisa asiye nakarama.

    Mikono, macho, na mapafu vina utofauti sana. Kila mshiriki ana tabiana kazi za pekee.

    Wote wamepewa angalau karama moja ya roho. Inatupasa kufanya kazi pamoja kuzitumiakarama hizo kuushiriki upendo na ukweli waKristo kwa ulimwengu wote.

    Hakuna washiriki wa kutolewa au wasio na kazi. Wale wanaohubiri kwenye mikutano wanathamani sawa na wale wanaoomba kimyakimya.

  • “Ni kwa maagizo ya Bwana kwamba

    watumishi wake wawe na karama

    tofauti. Ni kwa uteuzi wake kuwa

    wanadamu wenye akili tofauti

    wameletwa kanisani, ili kuwa

    watendakazi pamoja Naye. Tuna mawazo

    mengi sana na yaliyo tofauti ya kukutana

    nayo, na karama nyingi zinahitajiwa.

    Watendakazi wa Mungu wanapaswa

    kufanya kazi kwa maelewano thabiti.”

    E.G.W. (This Day With God, September 10)

  • “Lakini kazi hizo zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”(1Wakorintho 12:11)

    Biblia inaeleza kuwa kila karama iliyobora hutoka kwa Mungu. Roho Mtakatifuhuwapatia kama apendavyo Yeye(Yakobo 1:17).

    Kwanini tusijichagulie karama zetu?

    Kwasababu tuna ufahamu kidogo sanajuu ya jinsi ya kuutimiza utumetuliopewa.

    Pale tunaposalimisha mioyo yetu kwaYesu, Mungu hutupatia karama zilizobora Zaidi, ili zitumiwe vyema kulifanyaKanisa likue.

    Kwa nyongeza katika karama maalumu, Mungu pia ametupatia kazi maalumutuzifanye kwa kushirikiana na wengine.

  • “Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya hudumaitendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” (Waefeso 4:12)

    Zipo orodha za karama zilizotolewa kwa wauminiwa kwanza katika Warumi 12:6-8, 1 Wakorintho12:8-10, 28-30 na Waefeso 4:11.

    Zipo karama nyingi Zaidi ukilinganisha na za haowa kwanza, kama kuhariri picha na video, kuendesha ndege, kusimamia mitandao yakijamii… Lengo lao ni kumwezesha kila

    muumini kutimiza kazi yaokatika ukuaji na kulilisha Kanisa, ili tuhubiri na kuuhudumiaulimwengu.

    Karama za roho siyo talanta za asili. Japokuwa, Roho Mtakatifuanaweza kutakasa talanta za asili na kuziweka katika hudumaya Kristo (zinakuwa karama za roho).

  • “Wanadamu wote hawapokei karama

    zilizo sawa, lakini kwa kila mtumishi

    wa Bwana karama fulani ya Roho

    imeahidiwa. […] Ikiwa

    wameunganishwa na Kristo, ikiwa

    karama za roho ni zao, walio

    masikini na wasiojua kabisa kati ya

    wanafunzi Wake watakuwa na nguvu

    itakayoongea na mioyo. Mungu

    huwafanya kuwa mfereji wa

    kutekeleza jukumu la juu kabisa

    katika ulimwengu.”E.G.W. (The Faith I Live By, October 13)

  • “Hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu

    Yesu Kristo […]” (1 Wakorintho 1:7)

    Wote tumepokea karama… ni ipi uliyonayo?

    Namna nzuri ya kuzipata ni “kuzifanyia kazi”. Anza kufanyakazi ya huduma katika kanisa lako mahalia. Kwa njia hiyoutajua ikiwa una karama sahihi kwa kazi hiyo au la. Hebu tujaribu kueleza baadhi ya dhana:

    Karama

    HudumaKazi

    Karama: Ujuzimaalumu (k.m. kufundisha kwaurahisi)

    Huduma: Maeneomakuu ya huduma(k.m. ShuleSabato)

    Shughuli: Matukiomalumu (k.m. kuongoza darasa la Shule Sabato)

    Ikiwa unaijua karama yako tayari, utapata huduma au kazisahihi kwa urahisi.

    Ukijihisi vizuri katika huduma maalumu, utaweza kugunduakarama zako katika eneo hilo na kazi zilizo nzuri kwa ajili yakrama zako.

    Ukiifanya kazi Fulani vizuri, utazijua karama zako na hudumasahihi kwa ajili yako unapokuwa katika kazi hiyo.

  • “Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, nakuongezewa tele; lakini asiye na kitu hatakile alichonacho atanyang’anywa.” (Mathayo

    25:29)

    Katika kisa cha talanta, Yesu anaeleza kuwa kilammoja anapokea karama, lakini baadhi yawatu wanapokea zaidi ya wengine(Mathayo 25:14-30).

    Japokuwa, huo ni mwanzo tu. Tunaweza“kushauriana” na karama zetu za awali.

    Zitakuwa kadri tunavyozitumia, na tutapokeakarama mpya. Tuwe makini, kwa kuwatunaweza kuzipoteza karama zetu kamahatutazitumia.

    Mwombe Mungu akuonyeshe ni karama ganiAlizokupatia na namna ya kuzitumia. Haijalishini karama kiasi gani ulizopewa, lakini ni namnagani unazitumia.

  • “Kwa watumishi Wake Kristo ametoa

    ‘wema Wake’— jambo ililowekwa ili

    walitumie kwa ajili Yake. Anampatia

    ‘kila mtu kazi yake.’ Kila mmoja ana

    nafasi yake mbinguni katika mpango

    wa uzima. Kila mmoja anapaswa

    kufanya kazi kwa kushirikiana na

    Kristo kwa ajili ya wokovu wa roho.

    Kwa hakika hakuna sehemu Zaidi

    zilizoandaliwa kwa ajili yetu katika

    makazi ya mbinguni Zaidi ya sehemu

    maalumu zilizojengwa duniani

    mahali tunapofanya kazi ya Mungu.”E.G.W. (Christ’s Object Lessons, cp. 25, p. 326)