ufafanuzi wa agano jipya marko - african pastors fellowship · 2017-01-03 · mtu wa kawaida tu,...

163
Ufafanuzi Wa Agano Jipya Marko www.africanpastors.org Na Dorothy Almond mwisho na Askofu Francis Ntiruka

Upload: others

Post on 09-Feb-2020

131 views

Category:

Documents


52 download

TRANSCRIPT

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Marko

www.africanpastors.org

Na Dorothy Almondmwisho na Askofu Francis Ntiruka

Ufafanuzi WaAgano Jipya

MarkoDorothy Almond

© African Pastors Fellowship 2010

Kimetolewa na:AFRICAN PASTORS FELLOWSHIP

Station House, Station Approach, AdishamCanterbury, Kent CT3 3JE

United Kingdom

www.africanpastors.org

DIBAJI

Aliyeandika kitabu hiki cha ufafanuzi ni Sista Dorothy Almond aliyeishiTanzania kwa miaka 31, na sasa yu Uingereza hali amestaafu. Alikuwamwalimu katika Chuo cha Theologia, Kongwa kwa miaka 16 na katikaShule ya Biblia, Morogoro kwa miaka 6 na katika Shule ya Biblia, Msalatokwa miaka 4.

Mchoraji ni Peter Kasamba. Yeye ni Mwuganda anayeishi huko Kampala.Kwa muda mrefu amechora picha zote kwa vitabu vya APF. Anaongozapia Kwaya ya AYF.

Kitabu hiki chatolewa kwa msaada wa African Pastors Fellowship. Lengo nikuwasaidia watumishi wa Kanisa wanaosoma katika Shule za Biblia naMasomo ya Nyumbani

RAMANI YA PALASTINA WAKATI WA KRISTO

MARKO 131

U T A N G U L I Z I(a) MwandishiMarko amefikiriwa kuwa mwandishi. Injili yenyewe hakuna neno linalosema niMarko wala hamna maelezo zaidi ya kutusaidia kuelewa alikuwa nani. Hatahivyo yafikiriwa na wataalamu wengi kwamba huyo Marko alikuwa YohanaMarko, mwana wa mwanamke tajiri, Mariamu, ambaye nyumba yake paleYerusalemu ilitumika na Wakristo wa kwanza kwa mikutano yao, hatayawezekana ni katika nyumba hiyo Yesu alikula chakula cha mwisho nawanafunzi wake (Mk.14:15; Mdo.12:25; 15:39). Hivyo, Marko alikuwa kati yamambo ya Kikristo tangu mwanzo na kujulikana na Mitume na wenzao.

Papia, mwandishi mmoja wa Kikristo, aliyeishi miaka mia baada ya kuandikakwa Injili hiyo alisema kwamba Marko aliandika Injili yake kutoka mahubiri namafundisho ya Mtume Petro. Katika 1 Pet.5:13 Marko aliitwa ‘mwanangu’.Mjomba wake alikuwa Barnaba na katika safari kubwa ya kwanza ya Injili,Paulo, Barnaba na Yohana Marko walitoka Antiokia ya Shamu kwenda Kipro nasehemu za Pamfilia na Pisidia. Ila Yohana Marko aliwaacha pale Perge nakurudi Yerusalemu (Mdo.13:13). Kwa jinsi habari hizo zilivyoandikwainaonekana Paulo hakupendezwa na tendo hilo la Marko, hata hakuwa tayarikumchukua kwa safari ya pili. Jambo hilo lilisababisha Paulo na Barnabakutengana, Barnaba alimchukua Yohana Marko mpaka Kipro na Pauloalimchukua Sila badala ya Yohana Marko, nao wakafanya safari ndefu(Mdo.15:36-41). Kisha, baadaye sana, Yohana Marko na Paulo waliafikianatena, na Paulo alitaka amfikie pale Rumi mahali alipofungwa (Kol.4:10; Fil.24; 2Tim.4:11).

(b) WalioandikiwaYafikiriwa kwamba Marko aliandika Injili hiyo kwa ajili ya WaMataifa walioishiRumi. Sababu ya kufikiri hivyo ni kwa jinsi Marko alivyotoa maelezo ya mila nalugha ya Kiyahudi. Yesu alitumia lugha ya Kiaramu (5:41; 7:3; 12:42). Wakristowalikuwa wakiteswa kwa ajili ya imani yao na Marko alitaka kuwaelimisha watujuu ya imani ya Kikristo na kuwasaidia kuelewa mambo ambayo Wakristowanaamini na kueleza msingi wa matendo yao. Wakristo walionewa mashakakwa sababu ya madai yao ya kumfuata Yesu kama Mfalme wao na kumpaYeye utiifu zaidi ya Kaisari, Mfalme Mkuu wa Dola. Pengine Marko aliandikakaribu na wakati wa Petro na Paulo kuuawa pale Rumi mnamo B.K.64.

(c) Mahali ilipoandikwaYafikiriwa Marko alikuwa Rumi, maana upo ushuhuda wa kupatana na wazohilo. Petro alikuwa Rumi wakati fulani na tumeona ya kuwa Markoamemtegemea Petro kwa habari zake. Kama si Rumi, mapokeo fulani husemakwamba Marko aliishi Misri wakati fulani.

MARKO132

(d) Tarehe ya kuandikwaPengine Marko aliandika kama miaka 35 baada ya Yesu Kufufuka, kamaB.K.65. Wakristo walikuwa wakisimulia habari za Yesu katika mikutano naibada zao. Labda baadhi ya habari hizo zilikuwa zimeandikwa, ila Markoaonekana kuwa wa kwanza kuzitumia katika kuitunga Injili yake. Alichaguakatika habari nyingi na misemo mingi vilivyokuwepo, ndipo akazipanga kwautaratibu. Karibu mambo yote yaliyomo katika Injili hiyo yaonekana pia katikaInjili za Mathayo na Luka. Tukumbuke kwamba nyakati zile kila nakalailiandikwa kwa mkono juu ya mafunjo, hivyo nakala zahitilafiana.

(e) Shabaha ya kuandikaMarko alitaka kusisitiza uwezo wa Yesu pamoja na neno la Yesu kuwa siMasihi wa Kiyahudi tu bali pia alikuwa Mwana pekee wa Mungu (1:1; 9:7)ambaye hakujifanya kuwa mwanadamu bali alikuwa mwanadamu kweli,alifanya kazi ya mikono, alisikia hisia za kibinadamu n.k. (1:9; 13:32). Markoalitaka kuonyesha jinsi Yesu alivyoshangaza watu kwa mafundisho na matendoyake. Yesu alikuwa shujaa katika vita iliyoko kati ya mema na mabaya, na katiya Mungu na Shetani, akiwa mshindi kwa kutoa mapepo mabaya nakuwaponya wagonjwa n.k.

(f) Mtindo wa InjiliKufuatana na shabaha yake ya kumwonyesha Yesu kuwa mjasiri mambokatika Injili hiyo yaenda mbio. Marko alipenda kutumia neno ‘mara’ na mamboyameandikwa kwa uchangamfu. Yesu alishinda majaribu yake (1:12,13) alitoapepo wachafu na kupona magonjwa (1:23ku). Alishinda adui zake katikamajadiliano (12:13ku) halafu aliuawa ndipo akafufuka akiwa mshindi wa mauti.Hasa Yesu alishinda, si kwa sababu ya mafundisho yake, bali kwa matesoyake. Karibu nusu ya Injili yahusu mateso na Kifo chake, kuanzia 8:31. Kwasababu hiyo maisha ya Kanisa hayana budi yafanane na maisha ya Yesu,Wakristo wasishtuke wanapoteswa kwa sababu Mkuu wao aliteswa, na kamaYeye alivyofufuka, wao nao watafufuka na kuwa pamoja naye mwishowe.Marko alionyesha kwamba kweli hizo ni vigumu kuzipokea, na hata wafuasiwake wa kwanza walikosa kuzielewa (8:33; 9:34). Imani inatakiwa, imani yakumtegemea Yesu kabisa, na kumruhusu Yeye awaongoze kufahamu mambohayo vizuri zaidi.

Marko alitaka wasomaji wake wasikie furaha kubwa kama yeye alivyosikiaalipomwamini Kristo na kujikabidhi kwake.

MARKO 133

U F A F A N U Z I

Marko aliandika kwa wazi na kwa ufupi. Kwake kiini cha Injili ni YesuMwenyewe, Yeye ni asili yake na ya mambo yaliyomo pamoja na kuwa mhubiriwake (k.14). Marko hakutoa habari ya ukoo na kuzaliwa kwake wala hakutajamaisha yake ya ujana. Alitaka kusisitiza kazi alizozifanya ambazo zilisababishakifo chake. Pia alitaka kusisitiza umuhimu wa kifo chake kwa wanadamu wote(nusu ya Injili yahusu jambo hilo) na ajabu la kufufuliwa kwake. Kwa hiyo,alianza na habari za yule aliyemtangulia na kutangaza habari zake kabla yaYesu kutokea na kuanza huduma yake. Habari za huyo Yohana Mbatizajizaonekana katika 1:1-13 ndipo habari za Yesu kuanza huduma yake ni katika1:14.

Wakati huo nchi ya Palestina ilikuwa na shida nyingi. Watu wa kaskaziniwalioishi Galilaya walitofautiana na wale wa kusini walioishi Yudea na kati yaowaliishi Wasamaria ambao walidharauliwa na kutengwa hasa na wale wakusini. Walitawaliwa na Warumi na kutozwa kodi kubwa. Mara kwa marawaliinuka wana mapinduzi waliojitahidi kupata kundi la watu kuwasaidiakupindua serikali. Kwa hiyo ilikuwepo siasa ya motomoto na Yesu alifanyahuduma yake katika hewa ya moto huo. Wengi walitamani sana shujaa atokeeatakayefaulu kuwafukuza Warumi. Katika Maandiko yao Mungu alikuwaamewaahidi kutuma Masihi, nao walitamani sana atokee bila kukawia. YohanaMbatizaji alipotokea wengi walidhani kwamba yeye ndiye huyo Masihiwaliyeahidiwa. Lakini alikana kwa nguvu na kusema wazi kwamba yeye siye.

Yohana alinyosha njia ya Yesu kwa kuhubiri toba kwa watu wote na kwakuwabatiza wale waliotubu dhambi zao. Alifanana na Eliya katika mavazi yakena katika kusema kwake kwa mamlaka kama walivyofanya manabii wa zamani.

1.1-8 Yohana Mbatizaji na ujumbe wake‘Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu’. Neno ‘mwanzo’ niukumbusho wa Mwa.1:1 Mungu alipofanya uumbaji wa vitu vyote. Ni kamaMarko amedokeza habari ya ‘uumbaji mpya’ wa watu wapya wa Mungu. KatikaKristo Mungu hufanya jambo jipya la kuwapatia wanadamu uwezekano wakuzaliwa mara ya pili, kuokolewa na dhambi zao, na kupewa uzima wa Mungu,uzima wa milele. ‘Injili’ maana yake ni habari njema. Habari hiyo njema nihabari ya matendo makuu ya Mungu kwa njia ya Yesu Kristo katika kuishi, kufa,kufufuka na kupaa kwake. Ni habari njema kwa sababu kwa matendo hayomakuu wanadamu hutolewa katika utumwa wa dhambi, na hii ni habari njemakabisa. Ni habari ya mambo yaliyotendeka kweli kihistoria, si mawazo yahewani. Habari hiyo huthibitisha kwamba Mungu amejitoa kabisa kwawanadamu na mambo yao. ‘Yesu Kristo’ Yesu lilikuwa jina la kawaida laWayahudi wengi. Maana yake ni ‘Yehova ni Wokovu’ (Mt.1:21) na Yesu alipewajina hilo kwa agizo la malaika (Lk.1:31; 2:21). Kristo ni Kigriki kwa jina laKiebrania, Masihi, maana yake ‘aliyetiwa mafuta’ neno la kuonyesha cheo

MARKO134

chake. Wafalme na makuhani wakuu walitiwa mafuta. Wakristo waliwekamajina hayo mawili, Yesu na Kristo, pamoja kuonyesha kwamba Yesu ni yuleMasihi aliyetazamiwa kwa muda mrefu (Mdo.2:38). Ila mawazo ya Mungukumhusu Masihi na mawazo ya wengi yalihitalifiana sana. Wayahudi walitamanimtu atakayewaokoa na watawala wao, kwa kutumia nguvu za kimwili, yaanikwa vita. Ila Yesu si Mwokozi wa aina hiyo. Yeye si Masihi wa Wayahudi tu, balikwa watu wa Mataifa wote, tena Yeye atawaokoa na nguvu ya dhambi. Wokovuhuo hautapatikana kwa vita ya kimwili, bali kwa njia ya kujitoa mpaka kufa kuwafidia ya dhambi. ‘Mwana wa Mungu’ Marko alikuwa akiandika Injili yake baadaya kufa na kufufuka kwa Yesu, mambo ambayo yalimdhihirisha Yesu kuwaMwana wa Mungu, ila wakati Yesu alipokuwa hai, wengi hawakumtambua.Katika Injili yake Marko anaonyesha kwamba Yesu hakutambulikana kwaurahisi, hata wanafunzi wake, akina Petro na wenzake walichukua muda wakumtambua. Petro alimkiri kuwa Masihi (8:27ku) na polepole walifikia hatua yakumwona kuwa Mwana pekee wa Mungu. Marko alisisitiza umuhimu wa Yesukuwa Mwana wa Mungu (3:11; 5:7; 15:39). Kwa hiyo, habari njema, si habari yamtu wa kawaida tu, bali ni ya yule aliyekuwa Mungu na kufanyika mwanadamukwa kusudi la kuwaokoa wanadamu.

Marko hakusema mahali alipotoka Yesu, ni kama alitokea tu, kama ghafula.Jambo muhimu kwake ni shughuli za Yesu, kuhubiri na kufundisha kwake namatendo yake ya ajabu na wito aliotoa kwa watu kumfuata. Ni wakati mpya wautendaji wa Mungu unaolingana na wakati wa uumbaji wa kwanza. Yesu aundajamii mpya wa wanadamu.

k.2-3 Katika Injili yake ni hapo tu Marko mwenyewe ametaja Maandiko. Yesu niyule aliyetokea kwa mapenzi ya Mungu. Mungu alikuwa akitenda na kusemakwa upya na kwa mara ya mwisho kwa njia ya Yesu (Ebr.1:1-3). Mjumbealitangaza kutimia kwa unabii wa Isaya. Ila maneno hayo ni mwungano wamaneno ya Kutoka 23:20 na ya unabii wa Isaya (Isa.40:3) na ya nabii Malakialiyeishi wakati ambapo makuhani walikosa kutimiza wajibu zao, nayo yalikuwatishio na kuonyesha haja ya utakaso wa ibada na maisha ya watu wa Mungu.Jambo hilo lilipatana na kazi ya Yohana Mbatizaji na ubatizo wa toba, ‘mjumbe’ni Yohana Mbatizaji, ‘uso wako’ ni Yesu. Ndipo katika k.3 twapata maneno yanabii Isaya. ‘sauti ya mtu’ ni sauti ya Yohana Mbatizaji na maneno yanayofuatani habari za kazi zake. Kwa vifungu hivi twahakikishiwa kwamba Yohanaalitokea wakati ulioamriwa na Mungu na kwa kusudi maalum la kuwaweka watutayari kwa kutokea kwa Masihi ambako kulikuwa karibu. Ni vigumu kufikirikwamba Isaya alielewa kabisa kwamba alikuwa akitabiri habari za Yohana naYesu ila kwa sababu alijua Mungu anao mzigo juu ya watu wake alikuwa nauhakika kwamba Mungu atamtuma mtu kuyatatua matatizo ya watu wake. Bilamatayarisho ingalikuwa vigumu kwa Yesu kufika na kufanya kazi yake. Ilihitajimaandalio, wala si ya Yohana tu, hata historia yote ya Wayahudi iliyotanguliailikuwa maandalio. Hivyo, habari njema ina uhusiano wa karibu kabisa naufunuo mzima wa Mungu uliotangulia, na kwa sababu hiyo, ni matimizo ya

MARKO 135

Agano la Kale. Marko hakusema lolote juu ya Yesu kabla ya kutokea kwaYohana Mbatizaji.

k.4 Kutokea kwa Yohana Mbatizaji. Moja kwa moja na kwa maneno machacheMarko alisema kwa ufupi habari za kazi ya Mbatizaji. Hakutaja jinsi alivyozaliwakwa wazazi wazee n.k. Marko aliyaandika yale tu yaliyohusika na Yesu.Mbatizaji alifanya mawili yaliyokwenda pamoja. Alihuburi ujumbe wa lazima yatoba, ndipo aliwabatiza wale waliotubu katika mto Yordani. Hakubatiza kwa jinala Yesu, wala hakusema ni ubatizo wa Roho. Toba ilihitajika ili watu wampokeeYesu na kuishi maisha ya kumpendeza. Yesu ni yule wa kuleta uhai mpya iliwatu waishi maisha mapya. Jambo la kigeni lilikuwa kubatiza Wayahudiwenzake. Walikuwa na maosho mbalimbali, ila hawakubatizwa. WaliwabatizaWaMataifa walioigeukia dini yao, lakini ubatizo wao kwa wao haukuwepo nawatu walishtuka kabisa. Ubatizo wa Yohana ulikuwa ishara ya watu kusafishwana dhambi zao tayari kwa Masihi.

Yohana alifanya kazi zake nyikani, karibu na mpaka wa mashariki namagharibi. Hapo Warumi walikuwa macho kwa adui. Sehemu zile zilikuwa nakumbukumbu nyingi za historia yao, hapo zamani Lutu alikwenda kuishi(Mw.13) na Yakobo aliuvuka mto kwenda kukutana na Esau (Mwa.33) naYoshua aliingia nchi ya ahadi (Yos.3). Hapo nabii Eliya na Elisha walifanyahuduma zao. Mungu aliwalisha watu wake miaka arobaini pale nyikaniwalipotoka Misri. Ni mahali ambapo Mungu alisema atakutana na watu wake(Hos.2:14). Kwa hiyo kule kutokea kwa Yohana Mbatizaji pale jangwanikuliamsha mawazo mengi kwa Wayahudi. Kuwabatiza Wayahudi wenzake nikama kuwadokezea kwamba kuwa Wayahudi siyo kusema kwamba wanachokibali cha Mungu, wanahitaji kuanza upya. Hata yawezekana kuwa watu wa dinini kizuizi cha kuwafanya waridhike na hali yao hata wasiwe tayari kumpokeaMasihi wao.

k.5-6 Yohana alifanya kazi ya mpiga mbiu akihubiri na kuwaita watu wajiweketayari kwa Mfalme wao, kama watu walivyozoea zamani. Mpiga mbiu alitangazakuja kwa Mfalme, na kazi zake nyingine zilikuwa kuwaitisha watu kwa mkutanowa kuamua mambo ya eneo lao; na wakati wa michezo mikubwa kuwatangaziawachezaji sheria za michezo yao.

Tukumbuke kwamba hakuna nabii aliyetokea kati yao kwa muda wa miaka mianne hivi, wa mwisho alikuwa Malaki. Kwa hiyo, watu walishtuka mno naowalikuwa tayari kumjali Yohana. Kwa kungoja kwa muda mrefu kuliwafanyawazidi kuwa na hamu ya kutaka Mungu kutuma kwao nabii hata Masihimwenyewe. Waliumizwa na kunyenyekezwa sana na utawala wa Kirumi.Yohana naye, kwa upande wake, aliwavuta akisema kwa nguvu, bila wasiwasi,tena kwa wazi na kwa mamlaka, kama mtu aliyetumwa na Mungu.Walipomwona walikumbushwa manabii wa zamani, kama Eliya na Elisha, kwakuvaa kwake (2 Waf.1:8) na kwa kuishi kwake maisha magumu na kwa

MARKO136

kutangaza ujumbe wa hukumu ya Mungu kwa wale wasiotubu na kumrudiaMungu. Alifaulu kuvuta watu na wengi walimwendea na kubatizwa,wakiziungama dhambi zao.

k.7 Hapo Marko ametoa mafupisho ya ujumbe wake. Mbatizaji alikuwamnyenyekevu sana, alikuwa tayari kuwa mtumwa wa Kristo. Alisisitiza nguvu zayule ajaye nyuma yake ambaye kwa kujilinganisha naye alijiona kuwa mdogokabisa. Ilikuwa kazi duni kabisa kulegeza gidamu ya viatu. Kwa kusema hiviama Yohana alikuwa akijinyenyekeza kuliko kawaida ya wanadamu au alikuwaakimkuza Yesu kuliko kawaida ya wanadamu. Ni dhahiri kwamba alikuwaakimkuza Yesu kwa haki na kwa kweli. Kila wakati Yohana alinyosha kidolechake kwa Yesu na kutaja ubora na ustahili wake. Ilihitaji neema nyingi kufanyakazi kwa nguvu bila kujijali kwa ajili ya yule atakayemfuata. Alikuwamnyenyekevu kwelikweli. Bila hali hizo angaliweza kuharibu mambo. Yohanahakudhani kwamba ni yeye atakayeweza kurudisha Israeli kwa Mungu, yeyealikuwa ‘sauti’ tu. Alionyesha tofauti kubwa kati yake na Yesu. Yesu si nabiimwingine katika mfuatano wa manabii, yeye ni zaidi ya nabii, hata kuliko yeyealiye nabii wa mwisho, aliyepewa heshima ya kutayarisha njia ya Masihi. TenaYesu si Masihi mwenye asili katika wanadamu. Manabii walitabiri kwambaMungu atakuja kuhukumu na kuwaokoa watu wake. Katika kuja kwa Yesu,Mungu alikuwa amekuja, na kwa jinsi alivyosema Mbatizaji alikuwaakiyaelekeza mawazo ya watu ili wafahamu kwamba huyo Yesu ndiye Mwanawa Mungu (1:1).

k.8 Ndipo Mbatizaji alitofautisha ubatizo wake wa kutumia maji na ubatizo waYesu wa Roho Mtakatifu. Yesu hakuleta habari tu za Roho Mtakatifu balialikuwa na uwezo na mamlaka ya kutoa kipawa hicho kwa wotewatakaomwamini ili watiwe nguvu na uwezo wa kumfuata sawa. YohanaMbatizaji alitahadharisha watu kwamba Yesu atatoa kipawa kikubwa cha Rohona itawapasa wamfuate Kristo si yeye. Yohana aliishi chini ya Agano la Kale,Yesu alianzisha Agano Jipya la msamaha wa dhambi na uzima wa milele(Mt.11:11). Hatujui kama ni Yohana tu aliyebatiza watu au yawezekanawanafunzi wake walifanya chini ya uongozi wake. Hatuna habari ya Yesukuwabatiza watu ila twajua wanafunzi wake walifanya (3:22; 4:2). Yohanaalitangaza habari za Kuja kwa Ufalme wa Mungu (Mt.3:2) Yesu ni kiini chake,Ufalme umejengwa juu yake. Msingi wa Ufalme ni katika huduma ya Yesu.Uenezi wa Ufalme wa Mungu ulifuata kushuka kwa Roho wakati waPentekoste, kwanza juu ya Wayahudi (Mdo.2) halafu juu ya WaMataifa(Mdo.10). Hivyo ujumbe wa Yohana ulikuwa na mpaka, pia ubatizo wake, hatahivyo, huduma yake ilikuwa ya maana sana katika mpango wa Mungu.

1:9-11 Yesu alibatizwa (Mt.3:13ku; Lk.3:21-22; Yn.1:32-34)Kama ilivyokuwa desturi yake Marko ameandika habari hizo kwa ufupi. Yesu

alitoka Nazareti, mji usiokuwa na sifa yoyote katika historia ya nchi (Yn.1:46)alikuja kama mtu wa shambani, alishiriki na kundi la watu waliokusanyika kando

MARKO 137

ya mto Yordani, wakiziungama dhambi zao na kubatizwa na Yohana. Katikakumjia Yohana alionyesha ule uhusiano mkubwa uliopo kati yao. AlimjiaYohana na kubatizwa naye ubatizo wa toba sawa na wale watu. Ila Yesuhakuungama dhambi kwa sababu hakuwa na dhambi, ila katika kuupokea huoubatizo wa toba Yesu alionyesha utayari wake wa kujihusisha na wenyedhambi.

Yesu amekuja ulimwenguni ili awe Mwokozi wa wenye dhambi, na kwa ajili hiyoalifanyika kuwa mwanadamu. Katika kubatizwa Yesu alijihusisha na wanadamuwalio wenye dhambi huko amekataa kwamba dhambi ina haki ya kuwepo katikamaisha ya wanadamu, kwa sababu ubatizo ulikuwa wa toba, yaani wa kukataadhambi. Ilikuwa njia ya Yohana kutambua kwamba wakati wake umeelekeakwisha na wakati umefika kumwachia Yesu nafasi kufanya huduma yake iliYesu azidi na yeye apungue (Yn.3:30). Kwa Yesu ulikuwa wakati wa pekee wakujiweka wakfu kwa Mungu, Baba yake, kukubali mapenzi ya Baba yakuwaokoa wanadamu kwa njia yake, hivyo katika ubatizo alijitwika wajibu wakuwa Masihi, Mtumishi ateswaye.

Marko ameandika kama mambo hayo yalimhusu Yesu hasa. Ni Yesu aliyeonambingu zikipasuka, na Roho, mfano wa hua, akishuka juu yake, ndipo akasikiasauti kutoka mbinguni. Zamani zile Wafalme na Makuhani wakuu walitiwamafuta, na hapo Yesu, kama Mfalme na Kuhani Mkuu alitiwa mafuta ya RohoMtakatifu na kusimikwa rasmi kwa kazi yake. Hayo yalitokea mwanzoni mwaHuduma yake, kusudi awe na uwezo wa kutimiza yote yaliyokusudiwa naMungu. Luka ametaja kwamba Yesu alikuwa akiomba wakati huo. ZamaniRoho alikuja juu ya watu kwa kazi maalumu. Roho aliendelea kukaa juu yaYesu (Yn.1:32). Ni wakati wa dahari mpya na uumbaji mpya, wa watukuhuishwa na Roho. Wakati wa umbaji wa kwanza, Mungu alinena na Rohoalitulia juu ya uso wa maji (Mwa.1:2). Sasa Mungu alinena na Roho alishuka.Kwa jinsi Marko alivyoziandika habari hizo inaonekana ni Yesu tu aliyeyaonamambo hayo. Katika Mathayo na Luka inaonekana Yohana na wenginewaliyaona. Yohana Mbatizaji alisema kwamba jambo hilo lilitokea ili apatekumtambua Yesu kuwa ni Masihi (Yn.1:33). Nabii Isaya alisema kwambakumwagwa kwa Roho ni ishara ya kufika kwa Masihi (Isa.61:1). Luka alisemakwamba Roho alishuka kwa mfano wa kiwiliwili kama hua. Maana yake nikwamba Roho alishuka katika umbo la mfano wa hua, haina maana kwambaRoho ni hua. Mbingu kufunuka ni ishara ya kufika kwa wakati wa Mungukujifunua kwa upya katika Yesu Kristo. Ni wakati wa utendaji wa Roho na kwamatimizo ya ahadi za manabii.

Sauti iliyosema na Yesu ilikuwa ya Baba yake aliyeushuhudia uana wake, nakumhakikishia kwamba Yeye Baba yu radhi naye, kwa sababu, kwa njia yake,mapenzi yake yatafanyika. Kwa Yesu maneno ya Baba yalimthibitishia wito wakuwa Masihi atakayetimiza unabii wa Isaya 53 juu ya Mtumishi ateswaye.Maneno aliyoyasema Mungu Baba yalitoka katika Zaburi moja iliyofikiriwa kuwa

MARKO138

inamhusu Masihi (Zab.2:7) pamoja na maneno ya Nabii Isaya juu ya mtumishiatakayefanya mapenzi ya Mungu (Isa.42:1). Baba alimtia moyo nakumhakikishia na kumshuhudia kuwa Mwana wake, mpenzi wake, na Masihialiyeahidiwa. Yesu atatafsiri kwa upya na kuonyesha maana ya kweli yaUmasihi wake ili watu warekebishe mawazo yao na matazamio yao. Katikaubatizo wa Yesu Utatu wa Mungu ulidhihirika vizuri sana. Twaona Babaalisema, Mwana alikuwepo katika mwili, na Roho alishuka, mfano wa hua.Katika ubatizo wa Yesu uhusiano wao na umoja wao ulionekana.

Tusifikiri kwamba Yesu alifanywa kuwa Mwana wa Mungu na Masihi katikaubatizo wake. Alikuwa hivyo tangu mwanzo (1:1). Katika kubatizwa Yesuyalifunuliwa yaliyomo ndani yake na maana yake na gharamaatakayogharimiwa katika kuwa fidia ya dhambi. Ilimpasa awe Mtumishiatakayeteswa na kuuawa kama mwana kondoo wa Mungu. Pia gharama kwaBaba yake katika kumtoa na kumruhusu Mwana Mpenzi awe Mtumishi huyo.Twakumbushwa habari za Ibrahimu na Isaka wakati Ibrahimu alipompelekaIsaka, mwana wake pekee, mpenzi wake, akiwa tayari kumtoa kama sadaka(Mwa.22). Yesu kwa utii wake atawapatia wenye dhambi uwezekano wa kutubuna kupata msamaha wa dhambi zao na maisha mapya yenye uwezo wakushinda dhambi.

1:12-13 Yesu alijaribiwa (Mt.4:1-11; Lk.4:1-13)Marko ameandika habari hizo kwa ufupi sana. Baada ya kubatizwa Yesu

alienda mahali pa upweke, nyikani, kusudi huko azingatie huduma iliyo mbeleyake na njia za kuitimiza. Marko alitumia neno la nguvu akisema ‘Rohoakamtoa aende jangwani’ kwa hiyo alikwenda nyikani kwa uongozi wa Mungukama mtu aliyekuwa na haraka ya kupambana na adui wake. Nchi kati yaYeriko na Yerusalemu ilikuwa na milima milima na miamba miamba, hapakuwana mimea na miti ila vichaka tu. Hapa hatakutana na mtu, atakuwa peke yakepamoja na wanyama wa mwitu.

Alikuwako huko siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani muda huo wote. (siku40 ni ukumbusho wa muda wa Musa kuandika maneno ya Agano (Kut.34:28)na Eliya kukaa bila kula (1 Waf.19:8) na siku arobaini za Yesu kuwatokeawanafunzi wake baada ya Kufufuka Kwake na kabla ya Kupaa Kwake(Mdo.1:3). Marko ametuambia hali ya mahali alipokuwapo, alikuwa pamoja nawanyama wa mwitu. Watu walidhani kwamba mapepo wabaya na mashetaniwalikuwa na makao yao nyikani.

Tofauti na Mathayo na Luka, Marko hakutaja majaribu yake. Wao wametajaaina tatu za majaribu ambayo yalihusu namna za kuwavuta watu kumrudiaMungu na kumpenda. i) njia moja ya kufaulu ni kutosheleza haja za kimwili zakibinadamu ii) njia nyingine ni kuutumia uwezo wake wa kipekee na kuundajeshi la wapigania uhuru, maana watu walitamani sana shujaa wa kuwafukuzaWarumi, ama jambo la namna hii la kutumia mabavu na nguvu za kimwili. iii)

MARKO 139

njia nyingine ilikuwa kuwastaajabisha watu ndipo bila kukawia wengi watavutwakumfuata. Ila Yesu alifahamu njia kamili ya kuwavuta watu ni kuwapenda, sikwa kutoa rushwa ya chakula, wala si kwa ahadi za uhuru wa nchi, wala si kwamaajabu. Njia ni ya kuwapenda kiasi cha kuutoa uhai wake katika kuzifidiadhambi zao. Kwa kuwapenda kiasi hicho itamlazimu afe kwa ajili yao. Hivyo,alichagua njia ngumu na kuzikataa njia nyepesi za kuepa shida. Iliyomsaidiakukata shauri ni Neno la Mungu. Kila mara alimjibu Shetani kwa ufupiakiyatumia maneno ya Maandiko.

Je! alijaribiwa kweli? kama mwanadamu kweli? au alijifanya kuwa amejaribiwa?Alijaribiwa kweli, angaliweza kuchagua kutokufuata njia ya Msalaba (Ebr.4:15).Alisikia uvutano wa njia zilizopandwa katika mawazo yake, zilizotoka kwaShetani. Wala hakujaribiwa mara moja, alijaribiwa kwa muda wa siku arobaini,wala si kwa wakati huo tu (Ebr.4:15; 5:7ku).

Shetani ni nani? Je! ni roho mbaya mwenye nafsi? Wayahudi walimwona hivyo,wakimwita kwa majina mbalimbali - Ibilisi, Yule Mwovu, Mpinzani, majinayanayoashiria kazi zake. Kama ni mwenye nafsi au kama ni ‘nguvu’ ya uovu,wote huunga mkono kwamba kuna nguvu ya uovu inayofanya kaziulimwenguni.

Marko ametaja kwamba malaika walikuwa wakimhudumia Yesu. Je! malaika niakina nani? Je! ni wenye nafsi? waonekana kuwa wajumbe wa Munguwanaotumwa kuwaongoza wanadamu. Wao humwabudu Mungu mchana nausiku (Ufu.7:11). Je! walimhudumia Yesu wakati alipojaribiwa au mara baadaya kujaribiwa, alipoishiwa nguvu. Hatujui. Kama Yesu aliwaona malaika ausiyo, si kitu, jambo kubwa ni kwamba alitiwa nguvu na Mungu ili avumilie shidazake. Hata na sisi tutatiwa nguvu na Mungu ili tuyashinde majaribu yetu.

Bila shaka, wakati fulani, Yesu aliwaambia wanafunzi habari hizo kwa sababualikuwa peke yake muda wote wa kujaribiwa. Twajifunza kwamba Yesu alikuwamwanadamu kweli pamoja na kuwa Mungu kweli. Maovu ni jambo halisi katikaulimwengu huo, hatuna budi kupambana nayo na kuyashinda. Markoameandika kwa kumdhihirisha Yesu kuwa Yule mwenye nguvu aliyekwendakwa ushujaa nyikani na kupambana na adui wake mkuu na kumshinda. Baadaya habari hizo za Yohana Mbatizaji, ubatizo na majaribu ya Yesu, moja kwamoja Marko aliendelea na habari za Yesu na huduma yake.

1:14-15 Yesu alianza huduma yake (Mt.4:12ku; Lk.4:14ku;Yn.4:1-3)Marko alisema kwamba Yesu alikwenda Galilaya baada ya Yohana kutiwagerezani. Hakutaja habari za Yesu kufanya kazi kusini na jinsi yeye na Mbatizajiwalivyokuwepo kusini, kila mmoja akifanya kazi (Yn.3:22ku). Katika 6:17-29Marko alieleza habari za kufungwa na kuuawa kwa Mbatizaji. Injili ya Yohanaina habari nyingi za huduma ya Yesu pale kusini na Injili tatu zinazowiana zinahabari nyingi za Huduma yake katika Galilaya. Alipokwenda Galilaya Yesu

MARKO140

alikwenda mahali pa hatari kwa sababu mtawala wa eneo hilo alikuwa MfalmeHerode yule aliyemkamata na kumwua Yohana Mbatizaji. Galilaya ilikuwamahali hai kwa upande wa uchumi na siasa. Penye njia panda wanajeshi,wafanyabiashara, mabalozi n.k. walipitapita. Masokoni lugha za Kishamu,Kiebrania, Kiaramu zilitumiwa na watu wa mataifa mbalimbali. Kwa hiyo Yesuhakuanza huduma mahali pa utulivu bali katika hewa ya uvutano,mchanganyiko wa ukabila, na shughuli nyingi.

Marko amesema kwamba Yesu alitangaza Habari Njema ya Mungu. Hivyohakuleta mpango wa mashauri mema na maadili hasa bali alitangaza kwambaMungu kwa njia yake afanya jambo jipya, kwa sababu katika Yeye Munguamekuja kutawala mioyo ya wanadamu na kuwa Mfalme wao. Katika kufikakwake huo utawala umeanza. Yesu alisema ‘wakati umetimia, na ufalme waMungu umekaribia’. Kwa miaka mingi Mungu alikuwa amekusudia na kupangajambo hilo, ili mpaka wanadamu wajaliwe uwezekano wa kutoka chini yautawala wa dhambi mambo yalishindikana. Utawala wa dhambi katika maishayao ulikuwa mbaya hata kuliko utawala wa siasa wa kutawaliwa na Warumi.Kwa hiyo Ufalme wa Mungu hauhusu mahali, kama eneo la nchi kama wakatiwa Daudi, hautahitaji majeshi wala silaha kuulinda, wala hakitawekwa kiti chaenzi pale Yerusalemu. Ufalme wa Mungu ni utendaji wa Mungu katikamioyo ya wanadamu.

‘Wakati umetumia’ ni kuonyesha kwamba ni Mungu aliye mtawala juu yamambo yote. Yeye ni mwanzilishi wa kuuingiza Ufalme wake kati yawanadamu. Wakati wa Yesu kutokea ulikuwa wakati muhimu sana katikahistoria ya ulimwengu. Wakati huo unabii wote na matayarisho yoteyaliyotangulia yalitimizwa. Kwa nini ni wakati muhimu na wa maana kubwasana? Ni kwa sababu Ufalme wa Mungu umekaribia. Hii ndiyo sababu. Mfalmeamekuja kutawala, mkazo ni juu ya Mfalme si juu ya ufalme kama eneo. Je!hapo nyuma Mungu hakuwa Mfalme? Alikuwa Mfalme wa Israeli (Isa.41:21;43:15) na Mfalme juu ya Mataifa (Yer.10:7; Mal.1:l4) ila tangu kuja kwa Yesujambo hilo litajulikana, halitafichwa kwa watu. Katika Yesu itadhihirika ni kwanjia gani Mungu ni Mtawala, na atatawala kwa misingi gani. Ufalme wakeulikuja katika Yesu na unazidi kuja, si kitu kilichokaa tu, ni kitu kilicho hai,kinachokua.

Kama wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia, ni nini wajibu wawanadamu? Wanadamu wanawajibika kwa mambo mawili. Kwanza ni kutubu,maana yake ni kubadili mawazo na kuyaacha matendo yao mabaya, nikugeuza mwenendo ili upatane na mapenzi ya Mungu kama Yesuatakavyoyafunulia. Halafu, jambo la pili, ni kuiamini Injili, yaani kuamini kwambaUfalme wa Mungu umekuja katika Yesu na ya kwamba Mungu ataka kutawalamioyo na nia za watu. Kwa hiyo, raia wa ufalme wake ni wale watakaotubu nakujikabidhi kwa Yesu. Ni katika Yesu tu watu hupata uwezo wa kushindadhambi zao na maovu yaliyomo ulimwenguni.

MARKO 141

Watajuaje Ufalme huo umekaribia? watajua watakapomwona Yesu akiwatoamapepo wabaya na kuwaponya wagonjwa na kutenda matendo makubwa(Lk.11:20).Je! Mungu hakuwa Mfalme kabla ya hapo? Wakati wote Mungu amekuwaMfalme ila katika Yesu amekuja kutawala kwa hali mpya. katika mioyo yawanadamu. Amemtuma Yesu auokoe ulimwengu na uovu uliomo ndani yake.Ufalme wake utatimizwa Yesu atakaporudi tena katika utukufu (Mk.13:26).Yesu aliwaongoza wafuasi wake kuomba ‘ufalme wako uje’ yaani uzidi kuja.Utazidi kuja kwa njia ya hiyo Habari Njema kutangazwa ulimwenguni mwote nakatika watu wote kujulishwa habari za ushindi wa Yesu katika kutatua tatizokubwa la wanadamu wote, yaani dhambi na kupambana na yule mwovu nakumshinda (Kol.2:15). Hivyo, Injili huleta matumaini mazuri kwa watu. Vita juuya uovu ni vita ndefu na kali ila ni vita ambayo mwisho wake umeishajulikana,ni vita ya ushindi. Ufalme ni kipawa, ni utendaji wa Mungu ila twawezakujiweka tayari na kuukaribisha tukimruhusu Yesu ayatawale maisha yetu.

1:16-20 Yesu aliwaita wanafunzi wanne wa kwanza (Mt.4:18ku; Lk.5:1ku;Yn.1:35ku)

Marko alisema kidogo sana juu ya huduma ya Yesu ndipo alitoa habari ya Yesukuwaita wengine ili washirikiane naye katika huduma yake. Kwa hiyo Injili yakeina habari ya huduma ya Yesu na wanafunzi wake, wakifanya kazi kama timu.Ijapokuwa walikuwa na shida nyingi na mara kwa mara badala ya kumsaidiawalimsumbua, hata hivyo, alikuwa amejitoa kwao na wao walikuwa wamejitoaKwake na atakapoondoka duniani wao wataendeleza habari zake.Yesu alikuwa akielekea mji wa Kapernaumu na alipopita kando ya bahari yaGalilaya aliwakuta wavuvi katika shughuli zao. Yesu aliwaita wawili wao Simonina Andrea kumfuata akiwaahidi kwamba atawafanya kuwa wavuvi wa watu.Mara wakaitika na kuziacha nyavu zao na kumfuata. Ndipo mbele kidogoakawakuta wawili wengine na kuwaita, Yakobo na Yohana, nao wakaitika mara,wakamwacha baba yao Zebedayo na watumishi wake, wakamfuata Yesu. Witowa hao wanne huonekana kuwa ghafula bila nafasi ya kuujadili, ilatukilinganisha na Injili ya Yohana twajifunza kwamba haikuwa mara ya kwanzakwa baadhi yao kukutana na Yesu na kujihusisha naye (Yn.1:25-32).Inaonekana walikuwa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji na kuandamana nayemara kwa mara Yohana alipokuwa akifanya kazi kusini ya nchi. Wakati fulaniYohana aliwaonyesha Yesu na kusema ‘Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu’ndipo waliondoka kwenda kuzungumza na Yesu na pengine walifuatana nayekwa muda. Kwa hiyo, hapo ni wakati wa Yesu kutoa wito maalumu kwao wakuziacha shughuli zao za kupata riziki na kupunguza uhusiano wao na familiazao kwa kutokubaki nyumbani muda wote ili waandamane naye. Katika jambohilo twaona mamlaka ya Yesu, Yeye aliwachagua na kuwaita (Yn.15:16) sisitwampenda kwa sababu Yeye ametupenda kwanza (Yn.10:4). Aliwaita wajitoeKwake na kuambatana naye; hakuwaita wayashike mafundisho na itikadi fulanikwanza.

MARKO142

Hao wanafunzi walitoka tabaka ya kawaida, walikuwa na kazi ya kawaida yawengi wa sehemu ile. Walikuwa wameifaulu hiyo kazi kiasi cha uwezo wakuwaajiri watumishi na kuwa na vyombo vyao n.k. Hawakusoma katika mashuleya marabi ila katika ‘shule ya maisha’ nao walikuwa na ujuzi wa kutosha. Yesualiwakuta kazini, mahali walipozoea, na kusema nao kwa lugha waliyoifahamu,ndipo, hatua kwa hatua, wangejifunza ni nini yaliyomo katika wito wao(Amo.7:14-15).

‘Njoni, nifuate’ Budi tujihakikishe tunamfuata Yesu. Yesu aliwaahidi‘nitawafanya kuwa wavuvi wa watu’ Watajifunza kwa Yesu mbinu za kuwatoawatu katika mazoea yao na kuwaingiza katika maisha mapya katika Yesu. Kaziya uvuvi ilihitaji subira na busara na hali hizo wangezihitaji katika kazi yauinjilisti (Mt.10:16). Yesu aliwaita na kuwapa kazi ya kufanya ili wamtumikie.Mpaka leo hii ndiyo shabaha ya Kanisa, budi tujiweke muda wa kazi ya uinjilistina uinjilisti utangulie katika mipango ya shughuli za Kanisa.

Si wote wanaoitwa kuacha kazi zao na familia zao, ila sote twaita kuacha tabiambaya zinazotuzuia tusimfuate Yesu sawasawa. Bila shaka ilikuwa vigumukuachana na nyavu zao na baba n.k. hata kwetu si rahisi. Kwa Waislamumpaka leo ni jambo gumu sana kukata shauri la kumfuata Kristo kwa sababumara nyingi uhusiano wao na familia huguswa sana hata kiasi cha kukataliwana jamaa. Kuna wakati ambapo ni wajibu wa mtu kukaa nyumbani na kutunzajamaa, inategemea ni nini ambacho Yesu anamwitia mtu kufanya kwa ajili yake.Zebedayo alibaki na watumishi walioajiriwa, hakuachwa peke yake. Yesualiwachagua wengine kwa kazi fulani na wengine kwa kazi aina nyingine. Hanaupendeleo, kwa sababu Yeye hujua kila mtu na hali yake na uwezo wake nakumwita kulingana na hali yake.

Bila shaka tutachekwa na wengine watakapoona kwamba tumeacha kazi fulanikwa ajili ya kumtumikia Mungu. Kwa dhihaka watatuuliza, ‘mtaishije?’ ‘mtapatawapi pesa katika kazi za Kanisa?’ n.k. Ikiwa Yesu anatuita tusiyajali hayo.Yesu huita watu akina yahe, wala hangojei mpaka watu wamehitimu. Yeyehutazama mbele na kuona jinsi watakavyokuwa watakapoendelea kushirikiananaye.

Watu hupaswa kuitika wito wa Yesu anapowaita. Ni kwa neema ya Mungu watuhuitwa. Marabi walingoja mpaka watu walikuja kwao, Yesu, tofauti na wao,alitoka nje na kuwaita. Wito wake hauna hoja wala majadiliano. Awaita waleanaowataka, haidhuru wanafanya kazi gani. Simon na Andrea, Yakobo naYohana, walibadilisha kazi ya uvuvi wa samaki kwa uvuvi wa watu, nakumwacha baba yao kwa familia mpya wa watu wa Mungu.

Hao wanne, Simoni (Petro), Yohana na Yakobo, na Andrea hutangulia katikaorodha ya majina ya Mitume walioitwa baadaye. Tena hao wote, isipokuwa

MARKO 143

Andrea, walishirikiana kipekee na Yesu wakati fulani (1:29; 5:37; 9:2; 13:3;14:33) wakiwa wajoli wa karibu sana.

Katika jambo hilo la Yesu kuwaita hao watu twaona mamlaka na utawala wake.Yeye ndiye Mkuu, watu humfuata.

1:21-28 Yesu alionyesha mamlaka yake kwa Neno na kwa Tendo katikaKufundisha na katika Kutoa pepo (Lk.4:33-37)Yesu alifika Kapernaumu, pwani ya Ziwa la Galilaya. Kapernaumu kamaNazareti ni mji usiotajwa katika Agano la Kale, lakini ni hapo ambapo Masihialionyesha uwezo wake. Ilikuwa Sabato na kama desturi yake Yesu alihudhuriaibada sinagogini. Sinagogi ilijengwa mahali popote walipokuwapo kama familiakumi. Hekalu lilikuwa moja, pale Yerusalemu. Ibada ya sinagogi ilikuwa namambo matatu, maombi, masomo kutoka Agano la Kale, na maelezo ya somo.Hawakuwa na mhubiri au rabi wa palepale, walitegemea marabiwaliozungukazunguka kuwasaidia. Mkuu wa sinagogi alifanya mipango yasomo, mhubiri, n.k. Yesu alikuwa ameanza kujulikana kama rabi (mwalimu).Katika Injili hiyo Marko amesisitiza huduma ya kufundisha ya Yesu, ameitajamara 16 na kumwita Yesu rabi mara 11. Ila Marko hakufafanua yaliyomo katikamafundisho yake, tofauti na Injili zingine zinazoeleza mafundisho yenyewe.Sabato hiyo Yesu alipewa nafasi kuhubiri na mpaka baadaye, upinzaniulipozidi, alitumia nafasi hizo.

k.22 Hapo Marko amesema makubwa kuhusu mafundisho ya Yesu. Kwanzaametaja jinsi watu walivyoshangazwa sana na mafundisho yake, na pili, Yesualifundisha kwa mamlaka, si kama waandishi. Kwa hiyo, tofauti kubwa kati yakena waandishi, ilikuwa hiyo mamlaka yake ya kibinafsi. Waandishi walihesabiwakuwa wamestahili kuwafundisha watu. Walikuwa wamejitoa kuyachunguzaMaandiko, hasa vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale, yaani Torati, nakuifafanua kwa watu. Walipofundisha walitegemea na kuyatumia madondoo yawaalimu mashuhuri, wakisema ‘Mwalimu maarufu fulani amesema hivi....’n.k.Lakini Yesu alisema kwa nafsi yake, ‘mmesikia watu wa kale walivyoambiwa,Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni....’(Mt.5:21,27,33,38,43). Tofauti hiyo inaonekana kwa mfano wa waalimu wawiliwa jiografia. Mmoja aeleza habari za mahali fulani, mito na milima yake, sura yanchi, hali ya hewa n.k. kwa ujuzi alioupata kwa vitabu. Mwingine kwa sababualikuwa ameishi pale afundisha kwa ujuzi wa kibinafsi si wa vitabu. Yesualielewa nafsini mwake ule ukweli alioufundisha, alikuwa na uhakika juu yake.Alimjua Mungu Baba kwa sababu ametoka Kwake, yu Mwana wake pekee,tena alimtii. Wengine walifundisha juu ya Mungu bila kumjua wala kumtii. Siajabu watu walishangaa mno.

k.23-24 Marko aliendelea kwa kutoa habari ya tendo kuu la Yesu lililofanyikamle sinagogini kwa mtu aliyeshikwa na pepo mchafu. Ni mwujiza wa kwanzauliotajwa na Marko. Alitaka kuonyesha kwamba Yesu ni yule mwenye nguvu

MARKO144

aliyekuja kumshambulia yule mwovu na kutoa pepo wake wachafu. Mapepowalikuwa chini ya Shetani, na katika Yesu walikutana na mshindi wao, naowakashindwa. Kwa Marko ilikuwa dalili nyingine ya kufika kwa Ufalme waMungu katika kuja kwa Yesu na kuanza kwa utawala wa Mungu maishani mwawatu. Ilimbidi Yesu amshambulie Shetani katika ngome yake.

Kuwepo kwa Yesu kulimfanya yule mwenye pepo mchafu apaze sauti nakusema ‘tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! umekuja kutuangamiza?’. Pepoalimtambua Yesu sawasawa, alifahamu kwamba shabaha ya kuja kwa Yesuulimwenguni ni kufanya vita na uovu wa aina zote. Alijua kwamba pepo wabayawataangamizwa Utalme wa Mungu utakapowadia. Alimwita Yesu ‘Mtakatifu waMungu’. Ni kukiri mizizi yake ya kibinadamu na asili yake ya kutoka mbinguni.Aliogopa utakatifu wa Yesu. Iwapo alishikwa na pepo Je! alitaka pepo amtoke?pengine alihofu maumivu ambayo pengine angeyasikia pepo atakapomtoka(k.26) au alihofu mabadiliko yatakayotokea maishani mwake. Hatujui.

k.25-26 Yesu aliitika kilio chake kwa amri fupi ‘Fumba kinywa, umtoke’.Hakutaka Umasihi wake kutangazwa na enzi za uovu. Pia alitofautisha pepo nayule mtu aliyepagawa. Ndipo pepo akamtii Yesu na kumtoka yule mtu. Ilikuwadalili ya kuja kwa Ufalme wa Mungu (3:27). Yesu alifanya kwa mamlaka yanafsi yake, kwa kusema neno tu, hakutegemea kitu kingine chochote, hatahakumtaja Mungu wala kumwomba. Hakutumia virai vya mganga kamampunga pepo alivyofanya. Ajabu ni kwamba huyo mtu alikuwa amehudhuriasinagogi na kumwabudu Mungu, huko anaye pepo mchafu, bila kuwa na nia yakutolewa pepo, ila mara Yesu alipofika ndipo vita ilianza. Yesu alikuwa amekujaashindane na maovu ya kila aina, pepo, magonjwa, na mauti. Katika Injili tofautiimewekwa kati ya kuwa na pepo, na kuwa mgonjwa.

k.27-28 Hapo tena Marko ametaja jinsi watu walivyoushangaa uwezo wa Yesukatika kutoa pepo na jinsi pepo alivyomtii. Watu walishindwa kuelewa maanayake ila walitambua kwamba jambo jipya linatokea. Ijapokuwa walishangaahawakuwa tayari kutubu na kumwamini Yesu (Mt.11:23-24). Pepo alimtambua,wao walikuwa bado, wala wengi wao hawatamtambua, hilo ndilo sikitiko kubwa.Habari za Yesu zilienea kotekote katika eneo la Galilaya

1:29-34 Yesu alimponya mkwewe Simoni na wengine wengi (Mt.8:14-17;Lk.4:38-41)k.29-31 Marko aliendelea kwa kusisitiza Ufalme wa Mungu na nguvu yake najinsi ulivyokuwa ukienea kati ya watu. Baada ya habari ya kwanza kuhusukutolewa pepo twapewa habari ya kwanza ya uponyaji wa mtu. Ilitokeahadharani katika sinagogi, ya pili ilitokea sirini katika nyumba ya mtu binafsi.Alipotoka sinagogini Yesu alikwenda pamoja na Yakobo na Yohana mpakanyumbani ya Simoni na Andrea. Hao walikuwa watu wa Bethsaida (Yn.1:44)

MARKO 145

waliokuja kuishi Kapernaumu na kuendesha shughuli zao za uvuvi wa samaki.Walipoacha nyavu zao hawakuacha kuishi nyumbani, na ni hapo kwaoinaonekana Yesu aliweka kituo chake, akitoka na kurudi hapo. Ilikuwa alasiriwaliporudi nyumbani kutoka sinagogini nao wakamkuta mkwewe Simoniamelala kitandani hali ameshikwa na homa kali na kushindwa kazi, penginewalikuta chakula hakijapikwa bado. Walimwambia Yesu habari zake nayeakamwendea, akasogea karibu naye na kumwinua kwa kumshika mkono, ndipohoma ikamwacha, akawatumikia. Mara huyo mama alikuwa mzima, hakusikiaudhaifu, hakuhitaji kupumzika, akaanza kuwahudumia. Yesu alimponya marana yeye mama alitoa shukrani zake kwa kutumika mara. Marko anataka tupatepicha ya Yesu anayemtii Mungu na kujitoa kutumika bila kujali gharama, nayeanatumaini kwamba wafuasi wake watakifuata kielelezo chake.

Yesu aliwahudumia watu hadharani, pia nyumbani, na mahali popotealipowakuta. Hakujali kama waliopo walikuwa wengi, ama walikuwa wachache,Yeye alikuwa tayari kuwasaidia.Kwa habari hiyo twajifunza kwamba Petro alikuwa na mke ambaye baadayealikwenda pamoja naye katika safari za kuhubiri (1 Kor.9:5). Ijapo wanafunziwalikuwa wameandamana na Yesu kwa muda mfupi walikuwa wamejifunzakuleta shida zao kwake.

k.32-34 Hapo tumefika wakati wa jioni, na mwisho wa sabato. Watu walikuwana uhuru wa kuwabeba wagonjwa wao. Yesu ameishaponya wawili katikasabato hiyo. Kwa desturi Wayahudi hawakuwashughulikia wagonjwa siku yasabato isipokuwa walikuwa katika hatari ya kufa. Hatusikii kwamba wakuuwalisema lolote, kwa sababu, katika sinagogi Yesu alitoa pepo baada ya pepokulia, na baadaye alimponya mkwewe Simoni nyumbani, na bila shaka niwachache waliofahamu habari hizo. Tena Mafarisayo hawatajwi mpaka 2.16,hao ndio walioshikilia sheria sana. Mtu aliweza kuuawa kwa kuvunja mashartiya Torati (Hes.15:35). Ilipofika jioni wengi walikusanyika nje ya nyumbaalimokaa Yesu. Habari zake zilikuwa zimeenea, na wagonjwa wengi waliletwapamoja na wale wenye pepo. Ijapokuwa Yesu alikuwa ameshughulika sanamchana kutwa, hakujihurumia, alijitoa kuwahudumia watu tena. Yesu hakujalimahali walipo, barabarani au nyumbani, aliwahudumia popote alipowakuta.Walimtafuta ili wapate kitu kwake, hasa uponyaji. Yesu hakuruhusu pepowanene habari zake, hakutaka waseme kwa sababu hawakufanya kwa hiariyao. Katika Injili ya Marko neno la Yesu kuwa Masihi ni ‘siri’ na kila mara Markoameonyesha kwamba hata wanafunzi wake walishindwa kumwelewa, hadimpaka mwisho. Tena Marko ameandika habari za miujiza ya Yesu kanakwamba Yesu hakufanya kwa kusudi la kuuthibitisha Umasihi wake. Alifanyakwa sababu ya kuwapenda na kuwahurumia wale waliosumbuliwa miilini mwao,alitoa pepo kwa sababu aliona pepo hawana haki ya kukaa ndani ya mtu nakuharibu maisha yake. Pamoja na hayo hakutaka kuvuta uadui na chuki zawakuu. Ilikuwa muhimu aendelee kutangaza habari za Ufalme wake. Shidaitatokea ikiwa watu watamwona na kumtangaza kuwa mfanya miujiza, maana

MARKO146

Yeye ni zaidi ya mfanya miujiza, amekuja kuwaokoa ulimwenguni na dhambi nakatika kufanya hivyo ni lazima afe. Neno hilo wanafunzi wake na watu kwajumla hawakulifahamu, wala hawatalifahamu sawasawa mpaka ameisha Kufana Kufufuka. Jambo la kuzingatia ni kwamba wakati sinagogi zilipofungwa nashughuli rasmi za ibada zimekwisha, ndipo kazi muhimu na ya kweli kuhusuUfalme wa Mungu ilifanyika nje barabarani. Sisi wana Kanisa twapaswatuzingatie neno hilo.

1:35-39 Yesu alijitenga faraghani na kumwomba MunguTumeishaona kwamba Yesu alikuwa ameshughulika sana mchana kutwa hadijioni na bila shaka alisikia uchovu. Hata hivyo alisikia haja ya kushirikiana naBabaye katika maombi, kwa hiyo akaamka mapema sana, akaenda mahalipasipokuwa na watu, na katika utulivu mzuri alizungumza na Babaye. Ni daliliya ukweli wa ubinadamu wake, alikuwa na haja ya kupata uongozi na kutiwanguvu. Alimtegemea Mungu Baba amfunulie njia ya kufuata katika kuendeleana huduma, aijenge juu ya misingi iliyopatana na mapenzi ya Mungu. Simoni(Petro) na wenzake walipoona Yesu hakuwemo nyumbani, wakaendakumfuata. Walishangaa walipomkuta hayupo nyumbani huku watu wengiwalikuwa wakimtafuta. Hata walipomkuta walimwambia ‘watu wotewanakutafuta’. Yesu akawajibu tofauti na matazamio yao. Aliwaita waondokepamoja naye kwenda mpaka vijiji vingine na kuhubiri huko na kutoa pepo.Hivyo, aliyarekebisha mawazo yao na kuwaonyesha kwamba huduma yakehasa, si uponyaji, bali ni kuhubiri habari za Ufalme wa Mungu. Hii ndiyo kaziyake muhimu, na kazi aliyotumwa kufanya. Tena kazi hiyo ilikuwa na haraka,hawatakaa mahali pamoja tu, bali watazungukazunguka. Pengine Yesualijaribiwa kukaa pale Kapernaumu na kuwahudumia umati wa watuwaliomtafuta. Katika maombi alipata nuru ya Baba juu ya huduma yake nanamna ya kuifanya. Kuhubiri hutangulia, na uponyaji n.k. hufuata nyuma.

Kanisa wakati wote hutatizwa na namna ya kuwahudumia watu, na jinsi yakujihusisha nao. Halina budi kuhusika na hali na mahitji ya watu, ila ujumbewake, yaani Injili ya kweli, ni uongozi kwa mambo yote mengine. Katikakujihusisha na watu lazima tuwaambie kweli za Mungu, au tunapotafuta njia zakujenga uhusiano nao tutakuwa tunasafiri bila ramani au dira. na mwisho nikufika jangwani. Mengine yote yatakuwa hewa tupu, maana mwisho wa kila mtuni kufa na kuhukumiwa na Mungu kwa dhambi zake, asipoelewa habari zamsamaha wa dhambi atapotea.

1:40-45 Yesu alimponya mwenye ukoma (Mt.8:1-4; Lk.5:12-16)Huenda muda ulikuwa umepita tangu habari za hapo juu na habari ya huyomwenye ukoma. Wenye ukoma walitawaliwa na sheria kali, waliposikia kishindocha mtu au watu kuwa karibu iliwabidi watangaze wazi ‘Mimi mchafu, mimimchafu’. Hawakuruhusiwa kuingia nyumba za watu n.k. (Law.13 na 14). Kwa

MARKO 147

hiyo ni ajabu kuona huyo mwenye ukoma akimjia Yesu na ni ajabu zaidi kuonaYesu alimponya na ni ajabu zaidi sana kumwona Yesu alimgusa alipomponya.Mwenye ukoma alisema maneno yaliyofunua mawazo yake juu ya Yesu.Aliamini kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kumponya ila hakujua kwambaYesu yu tayari kumponya. Au twaweza kusema alijua Yesu ni mwenye uwezoila bado hajaelewa kwamba Yesu ni mwenye upendo. Ndipo twasoma kwambaYesu alimhurumia, alinyosha mkono wake na kumgusa, kisha akasemamaneno ya kutibu mashaka yake ‘nataka, takasika’. Kwa kumgusa huyomwenye ukoma Yesu alivunja mapokeo ya miaka mingi na kumwonyesha jinsialivyompenda sana. Maneno na matendo yalilingana. Katika Yesu uwezo naupendo umeungana. Yesu alivunja sheria juu ya kumgusa kwa sababualitawaliwa na sheria nyingine iliyozidi ile iliyoandikwa, sheria ya upendo. Maraukoma ukamtoka, akatakasika. Kila mara twasoma kwamba wenye ukomawalitakaswa, si waliponywa, kwa sababu walihesabiwa kuwa wamenajisika nayeyote aliyemgusa mkoma aliambukizwa unajisi.

k.41 Katika nakala zingine za zamani maneno ni tofauti na ‘naye akamhurumia’zina maneno ‘naye akasikia hasira’. Yawezekana maneno hayo ndiyo ya asili,ila baadaye, watu waliona vigumu kuyapokea hayo, kwa hiyo, wakayabadili.Ikiwa ni kweli Yesu alisikia hasira, swali lililopo ni ‘kwa nini asikie hasira?’. Nikwa sababu ya kuona jinsi maisha na miili ya wanadamu inavyoharibika kwaajili ya maradhi n.k. ambayo asili yake kabisa ni katika Anguko la Wanadamu(Mwa.3).

Yesu hakuwa mtu baridi, alisikia hisia kubwa ndani yake. Twaona tena Yesualifanya jambo lililokuwa tofauti na kawaida za watu. Bila shaka mtu huyoalitaka kusema kwa kila mtu jinsi alivyoponywa lakini Yesu alimkataza kwanguvu asiseme kwa mtu yeyote habari hizo. Hapo tena twaona lile jamboambalo tuliliona katika k.34, hali ya siri na ya kujificha kumhusu Yeye naUmasihi wake. Mtu huyo hakumtii Yesu, kwa maneno mengi alitangaza jinsiYesu alivyomfanyia. Jambo hilo lilileta shida kwa Yesu, hakutaka kupatawafuasi kwa njia ya uponyaji. Yesu hakuponya watu kwa hila kama peremendeyake ya kuvuta watu kwake. Ni sehemu katika mashindano yake na uovu nakatika kuwaweka watu huru, ila kama tulivyoona hapo nyuma kazi yake muhimuna ya kwanza ni kuutangaza Ufalme wa Mungu. Kwa sababu hiyo Yesualijificha na iliwabidi watu waende kwake mahali pasipokuwa na watu na ni waletu wenye nia waliomwendea. Yesu aliona kwamba umati wa watu wanaotakauponyaji tu bila kuyajali na kuyapokea mafundisho yake ni kizuizi kwake.

Ijapokuwa Yesu alivunja sheria juu ya kumgusa mwenye ukoma, hata hivyo,alimwagiza huyo aliyetakaswa atimize sheria iliyowekwa kwa walewaliotakaswa ukoma. Aende kwa kuhani na kujionyesha kwake ili kuhaniauhakikishie ukweli wa utakaso wake ndipo yeye atoe shukrani kwa ajili yake(Law.13:3; 14:2ku. Kum.24:8). Ni dhahiri kwamba Yesu hakudharau sheria yanamna hiyo iliyofundisha watu kumshukuru Mungu kwa mibaraka waliyopata.

MARKO148

Pamoja na kuushuhudia ukweli wa uponyaji wa huyo mtu, kuhani alipata kujuahabari za Yesu na kushuhudiwa ukweli wa uwezo wake. Kwa kutimiza kanunihiyo huyo mtu alirudishwa rasmi katika jamii, ila alipomgusa Yesu ameishakumkaribisha kibinafsi.

2:1-12 Yesu alimponya mwenye kupooza na kumsamehe dhambi zake(Mt.9:1-8; Lk.5:17-26)Hapo nyuma tuliona kwamba Yesu aliondoka Kapernaumu kwenda kwa vijijivya Galilaya na kuhubiri huko. Ndipo akarudi Kapernaumu na watu walipopatahabari hiyo walikusanyika kwenye nyumba alimokaa na Yeye aliwafundishaneno lake. Huenda ilikuwa nyumba ya Simoni na Andrea. Ndipo wakaja watuwanne waliombeba mgonjwa wa kupooza, wakajaribu kumfikisha kwa Yesu ilahawakuweza kwa sababu ya umati wa watu waliosongamana mlangoni.Waliposhindwa kumfikisha kwa Yesu waliamua kupanda ngazi na kutoboa darina kumpitisha huyo mgonjwa. Twaweza kujifunza mambo kuhusu imani.Walikuwa na imani kwamba Yesu aweza kumponya rafiki yao, hata walithubutua) kumbeba kutoka nyumbani kwake b) hawakujali jinsi watuwatakavyowawazia, na aibu watakayosikia ikiwa Yesu hatamponya c)hawakujua mwenye nyumba ataonaje dari ya nyumba yake kutobolewa, kamaatawakasirikia au vipi d) wala hawakujua Yesu ataonaje vijiti na udongovitakapoanguka karibu naye. Twajifunza kwamba imani ya kweli ni ileinayotenda kitu, tena inakazana, haikati tamaa, njia fulani ikishindikana, basi,mtu wa imani ya kweli yu tayari kujaribu njia nyingine.

k.5 ‘Yesu alipoiona imani yao’ hatujui kama ni imani ya rafiki zake na mgonjwaau ni imani ya rafiki zake tu. Bila shaka maneno ya kwanza aliyoyasema Yesukwa mgonjwa yalimshtua ‘Mwanangu, umesamehewa dhambi zako’ Kwaniaseme maneno hayo na huyo mtu amemjia kwa shabaha ya kuponywa kimwili?Wayahudi waliamini kwamba mtu huugua kwa sababu ametenda dhambi, nikama adhabu. Hii ndiyo hoja kubwa ya rafiki za Ayubu waliosema kwamba nilazima Ayubu alitenda dhambi, au asingaliugua (Ayu.4:7). Yesu hakukubalikwamba kila mgonjwa ameugua kwa sababu ametenda dhambi fulani (Yn.9:2;Lk.13:1-5). Ila katika kuunganisha uponyaji wa mwili na wa roho pamojainaonekana Yesu alikubali upo uhusiano mkubwa kati ya hayo mawili. Kwajumla wanadamu wote wamerithi laana iliyotolewa wakati wa Anguko laWanadamu (Mwa.3:1ku) maana yake upo uhusiano kati ya Anguko na taabu nashida za kimwili zipatazo wanadamu. Watu wengine hushikwa na hatia yadhambi hata wamekuwa kama wamepoozwa.

Je! ilikuwaje kwa huyo mtu? Yawezekana alikuwa amefanya dhambiiliyosababisha ugonjwa wake, na Yesu alifahamu hivyo; kama sivyo Yesu alijuaametawaliwa na mawazo ya Kiyahudi na alihitaji apewe neno la msamahalitakalomwezesha kupokea uponyaji wake. Pengine Yesu alikuwaamezungumza naye na kupata habari zake au alijua kwa sababu ya uwezowake wa kusoma mioyo ya wanadamu. Yesu aligusa kiini cha shida yake na

MARKO 149

kumtibu kimwili na kiroho. Neno ‘mwanangu’ linaonyesha kwamba Yesu alitakakujenga uhusiano mzuri naye, dalili ya kumkaribisha kwa moyo. Yesualiyatamka maneno ‘umesamehewa dhambi zako’ kwa mamlaka yakemwenyewe, hakusema ‘Mungu akusamehe’ alisema kwa nafsi yake kwa kuwaYeye Mwenyewe alikuwa na mamlaka hiyo.k.6ku Hapo twakuta kundi la waandishi, wale waliowekwa kuuhakikisha usahihiwa mafundisho yaliyotolewa katika Israeli, huenda walikuwa wamefika pale iliwampeleleze Yesu. Yesu hakuwahofu, katika kusema kama alivyosemaalikuwa amewapa changamoto, maana alifahamu jinsi watakavyoyawazamaneno yake. Kwao ni maneno ya kufuru. Tena, walisema kweli kabisawalipouliza ‘Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiyeMungu?’ wala hakuna ambaye angalibisha, hata Yesu Mwenyewe. Dhambi nikosa juu ya Mungu hasa na mwishowe ni Mungu peke yake ambaye awezakusamehe dhambi. Lakini jambo ambalo hawakuwa tayari kukubali ni Yesukuwa Mungu Mwana mwenye mamlaka sawa na Mungu kusamehe dhambi.Yeye amekuja kwa kusudi la kutoa nafsi yake kuwa fidia ya dhambi, ili watuwapate msamaha wa dhambi na uzima wa milele (10:45). Yesu alifahamumawazo yao kwa njia gani? Isingalikuwa vigumu kuhisi kwamba hao waandishiwaliwaza hivyo. Pia Yeye sawa na Mungu alijua siri za wanadamu(Zab.139:1ku; Mdo.15:8). Ni mara ya kwanza ya Marko kutaja habari ya Yesukushtakiwa.

k.9 Ndipo Yesu akawapa changamoto nyingine, waamue kati ya mambo mawiliyaliyo magumu ya kufanya; ‘amsamehe huyo mtu’ au amponye kwakumwambia ‘aondoke, ajitwike godoro lake, aende’. Yote mawili ni mepesi yakusema ila magumu kutenda. Ila la kwanza halina thibitisho la wazi, ni naniatakayejua ikiwa dhambi imesamehewa? ila la pili lina thibitisho la wazi,likitendeka itakuwa wazi kwa wote. Ndipo Yesu akiunganisha msamaha wadhambi zake na uponyaji wa mwili wake alimgeukia mwenye kupooza nakumwambia ajitwike godoro lake na kurudi nyumbani, na mbele ya wote ndivyoalivyofanya. Msamaha wa dhambi ni mgumu sana kwa sababu uwezekano wakusamehe dhambi hauji kwa kutamka neno tu; kutapatikana katika Yesu kutoanafsi yake kuwa fidia ya dhambi atakapokufa Msalabani. Kwa hiyo Yesu alidaikuwa na haki na mwenye mamlaka nafsini mwake kusamehe dhambi, na kwasababu hiyo Ufalme wa Mungu umekuja karibu na watu. Katika habari hiyotwajifunza kwamba Yesu hakutaka ajulikane kuwa mtenda miujiza na mponyajiwa watu tu, bali alitaka kuwaelekeza watu wazingatie kazi yake muhimu yakutibu shida kubwa ya wanadamu, yaani dhambi. Walipomwona yule mgonjwaanatembea walijua kwamba Yesu ameweza yote mawili, kusamehe nakuponya, kutibu roho na kutibu mwili. Kwa kusudi Yesu aliyaunganisha yotemawili ili wafahamu jambo hilo (k.10).

Ni mara ya kwanza kwa Marko kutaja Yesu akijiita ‘Mwana wa Adamu’ jinaambalo alipenda kutumia mbele za watu. Baadaye alilitumia alipodai mambomakubwa. Maana ya Jina hilo haikuwa wazi sana, kwa hiyo, Yesu aliweza

MARKO150

kulitumia kwa kuuficha Umasihi wake. Limetoka katika Danieli 7:13, sehemuinayosema juu ya mmoja kama mwana wa adamu ambaye ameteuliwakuushiriki Ufalme wa Mungu milele na milele. Ni wenye imani tu ambaowatamtambua (ling.Mk.8:28,31; 10:45). Yesu hakusita kudai mambo makubwayaliyo halisi.Dhambi na magonjwa huleta masumbufu mengi kwa wanadamu na kuharibumaisha ya watu. Katika jina la Ufalme wa Mungu, Wakristo wapaswawashambulie mambo yote yanayoleta shida kwa wanadamu. Kwa jinsi Markoalivyoandika habari hiyo alilenga kusisitiza madai ya Yesu ya kusamehedhambi akitumia habari za huyo mtu kama kielelezo cha kufundishia jambo hilo.Kwa jinsi alivyofanya Yesu alikuwa akizishambulia taratibu za dini ya Kiyahudi.Kumwamini Mungu ni kumtegemea Yeye na kujikabidhi Kwake.

k.12 Itikio la watu lilikuwa kustaajabu, kama ambavyo tumeona hapo nyuma.Walimtukuza Mungu, huku waandishi wakisikia wivu na kukasirika. Hawakusikiahaja ya msamaha na kwa sababu hiyo waliondoka bila baraka (k.17). Watuhawakufikiri kwamba Yesu amekufuru kama waandishi walivyoona. Walitambuamambo hayo ni mapya, ni ishara nyingine ya kuja kwa Ufalme wa Mungu nakwamba nguvu zake zinafanya kazi kwa siri mioyoni mwa watu.

Kwa nini viongozi walishindwa kumpokea Yesu? Sababu moja ni kwambawalikuwa wameganda katika mawazo na mafundisho yao. Matazamio yaokumhusu Masihi yalikuwa membamba sana, walikuwa wamepanga mawazofulani juu yake, na Yesu alipofanya tofauti na matazamio yao, walisikia shida.Walimdharau na kumwona kama mtu tu, Mnazareti, asiyeelimishwa katikamashule ya marabi (k.7 ‘huyu’). Pamoja na hayo walishikwa na wivu kwa jinsialivyokuwa na uwezo wa kuwavuta watu. Ni vema watumishi wa Kanisawajitahadharishe na hali hizo za dharau na wivu.Je! Makasisi wa leo wanao uwezo wa kusamehe dhambi? La! Ni Mungu tumwenye uwezo huo, ila Kanisa limekabidhi baadhi ya watumishi wake mamlakaya kuwatangazia watu msamaha wa Mungu kwa wale watubuo kwa kweli. (Taz.ghofira katika Kitabu cha Sala cha Kianglikana - ‘Yeye huwasamehe’). Tangazohilo limejengwa juu ya Injili ambayo wao ni watumishi wake (2 Sam.12:13b;Yn.20:22-23). Ni tangazo la msamaha, msamaha wenyewe hutoka kwa Mungu.Katika habari hiyo twaona chanzo cha upinzani, upinzani ambao utazidi kwakadiri Yesu anavyoendelea na huduma yake. Hata Kanisa likifanya vizuri nakuwahudumia watu vema, hata hivyo, watakuwapo wale wa kulipinga.

2:13-17 Mwito wa Lawi/Mathayo (Mt.9:9ku. Lk.5:27ku)k.13ku Yesu aliondoka nyumbani kwenda mpaka baharini, yaani Ziwa laGalilaya, na watu wengi walimwendea, naye aliwafundisha. Twaona jinsi Markoalivyopenda kusisitiza hiyo kazi ya Yesu ya kufundisha. Katika kupita kwakealimwona Lawi wa Alfayo kwenye kazi yake ya kutoza ushuru wa bidhaa.Huenda haikuwa mara ya kwanza Yesu kumwona pale, pengine Lawi alikuwa

MARKO 151

amemsikiliza Yesu alipokuwa akihubiri hata yawezekana wamezungumzanawakati fulani. Hatujui. Siku hiyo ilikuwa kubwa katika maisha ya Lawi kwasababu Yesu alimwambia ‘nifuate’ na mara akaacha meza yake na vitabu vyakazi yake, akamfuata. Ni siku kubwa, kwa sababu tofauti na Simoni nawenzake, alipoondoka kazini hakuweza kuirudia tena. Hao akina Simoni kamawavuvi waliweza kurudi kwenye uvuvi wa samaki wakati wowote. Hivyo alikatashauri kubwa la maana sana. Lawi alikuwa katika utumishi wa Mfalme Herodena kwa sababu hiyo hakupendwa kwa vile alimsaidia Herode kukusanya kodikutoka wananchi. Jambo la kutoa kodi kwa Warumi liliwachukiza watu. Alitozaushuru kwa bidhaa iliyopitishwa kwenye pwani hiyo. Pamoja na hayo sababunyingine ilikuwa kwamba kima halisi hakikuwekwa, kwa hiyo, mradi walete kilekima alichotaka Herode watoza ushuru waliweza kutoza zaidi na kuwekamfukoni mwao sehemu iliyozidi. Wengi waliweza kuishi maisha mazuri kwamapato yao. Pamoja na hayo walikutana na WaMataifa katika kazi yao, naWayahudi walifikiri wamenajisika ikiwa wataguswa na MMataifa. Hivyo,kutokana na mambo hayo ni watu wasiopendwa katika jamii. Kwa kawaida sisiwanadamu hatupendi kulipa kodi.

Je! Lawi huyo alikuwa nani? maana katika Injili ya Mathayo, yupo mtu aliyeitwana Yesu jina lake Mathayo. Katika orodha za Mitume, jina la Mathayolimeonekana. Yadhaniwa kwamba Mathayo na Lawi ni mtu mmoja.Twaona nguvu na mamlaka ya Yesu katika mwito wa Lawi. Yesu alichaguawatu tofauti tofauti; watu waliopendwa na jamii na watu wasiopendwa na jamii;watu wa elimu na watu wasio na elimu; watu wa kutumia wavu na watu wakutumia kalamu. Baadaye Lawi/Mathayo alitumia vizuri kalamu yake katikakuandika Injili yenye jina lake.

k.15ku. Kwa furaha nyingi Lawi aliandaa karamu kubwa na kuwaita rafiki zakena wenzake wa kazi ili wapate kukutana na rafiki yake mpya ambaye amekubalikumfuata. Kwa kukubali kukaa na watu wa aina hiyo hata kula nao, Yesu alitoachangamoto kali kwa ‘watoza ushuru na wenye dhambi’ na kuwalazamishawatafakari kwa upya shabaha ya dini ya kweli. Tusiwaze kwamba hao wotewaliokuwepo walikuwa wenye maisha mabovu bali baadhi tu. Hasa watozaushuru walihesabiwa kuwa watu wasio na kibali cha Mungu nao waliwekwakando na viongozi wa dini ya Kiyahudi kwa sababu katika kazi yao walikutanana WaMataifa na hivyo walinajisika machoni mwa Wayahudi ‘safi’. Tena, watuwaliitwa ‘wenye dhambi’ ikiwa hawakushika mapokeo ya waandishi, yaani ikiwahawakujali zile sheria ndogondogo nyingi zilizowekwa na waandishi. Hainamaana kwamba walikuwa wakivunja Amri Kumi. Kwa hiyo, kufanya uasheratina kula nyama ya nguruwe, kuiba na kutokunawa mikono, kulihesabiwapamoja, ni kuvunja sheria. Kwani iwe hivyo? ni kwa sababu waandishi waliwekavisheria vyao kuhusu kutokula nyama ya nguruwe na kutokunawa mikono kuwasawa na Amri Kumi. Kwa furaha kubwa Lawi aliandaa karamu na kuwaitawenzake waje kula pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Kula pamoja kulikuwaalama kuu ya ushirikiano na kibali. Alitaka wakutane na huyo rafiki yake mpya

MARKO152

aliyemwita kumfuata. Lakini machoni mwa wakuu hao walikuwa kundi la watuwa sifa na tabia mbaya.

Waandishi na Mafarisayo walipowaona hao wote wakila pamoja kwa furaha nabila wasiwasi hawakupendezwa, hawakuweza kuelewa kwa nini Yesu, ikiwa niMasihi, ameshindwa kuwatambua hao watu kuwa watu wasiofuata sawasawamambo ya sheria. Ni kama Yesu ameunga mkono hali za hao watu bila kujaliupungufu wao. Hawakumkabili Yesu moja kwa moja bali walipitia kwawanafunzi wake na kuwauliza ‘Mbona anakula...?’ ‘Mbona’ yao inaonyeshakwamba kuna ufa mkubwa kati yao na Yesu. Walikuwa na swala kubwa kuhusujinsi Yesu alivyojihusisha na watu hao. Ijapokuwa walikuwa wamewaulizawanafunzi, Yesu alikuwa ameyasikia waliyoyasema, akawajibu. Katika kuwajibualisema jambo ambalo ni dhahiri kwa wote, wanaohitaji tabibu ni wagonjwa,wasio wagonjwa hawamhitaji. Daktari hana budi kuhusika na wagonjwa; vivyohivyo, Mwokozi wa wenye dhambi budi ahusike na wenye dhambi wanaohitajiwokovu. Hivyo alikuwa akidai kuwa tabibu wa wagonjwa na mwokozi wa wenyedhambi. Hao walioketi naye walijitambua kwamba ni wagonjwa. ‘sikuja kuwaitawenye haki’ Je! ina maana kwamba hakuna wagonjwa wa roho, yaani, hakunawasio na dhambi, ambayo haki yao inatosha? La! Maandiko yasema wazikwamba hakuna mwenye haki hata mmoja, wote ni wenye dhambi nakupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum.3:10,20,23). Ila wako wanaojidhaniakuwa wenye haki, haki yao yenyewe. Yesu alisisitiza shabaha ya Kuja kwake,amekuja kwa ajili ya wenye dhambi ili awaokoe na dhambi zao. Wenye shidawaende wapi kwa msaada? Kutokusikia upungufu na haja ya msaada nikujenga ukuta kati ya mtu na Mungu. Haja yetu ya msaada ni kama pasipotikwa rehema za Mungu. Ni hatari kubwa kwa mgonjwa ikiwa hatambui kwambani mgonjwa!!

Kwa tendo lake la kushirikiana kwa ukaribu na hao watu Yesu alidhihirisha tabiaya Mungu, Yeye hupokea watu kabla hawajatimiza matakwa ya Sheria. Yeyehuhesabu kwamba wamehitimu na kupata maksi mia iwapo bado hawajafikiamaksi hizo. Eti! si itambidi angoje mpaka milele kwa mtu yeyote kufaulu? Hainamaana kwamba Yesu hapendi watu wema, la, awapenda sana, ila hawezikumsaidia mtu anayedhania ni mwema. Wako wagonjwa wasiojua ni wagonjwa,wadhanio kwamba ni wazima, hao hawamwendei daktari, hawasikii kuwa nahaja ya matibabu. Lakini Yesu alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali mwenyedhambi, naye husogea karibu nasi katika udhaifu wetu (Rum.5:6,8). Yesualikuwa akijali kwamba hao watu walikuwa ‘wagonjwa’ ila hakukubali kwambanjia ya kuwasaidia ni kukaa mbali nao na kuwahukumu na kungoja mpakawamerekebisha maisha yao. Aliishi kati ya watu na kushirikiana nao bilakuzishiriki dhambi zao. Alitoka nje kwenda kuwatafuta (Lk.19:1ku). Alikuwamwenye uwezo wa kuwasamehe na kuwaokoa, tofauti sana na Mafarisayo naWaandishi waliojitenga na watu na kuwahukumu, huku hawakuwa na mawazowala uwezo wa kusaidia, dawa yao ilikuwa kuwapiga na fimbo la Torati tu.Hakuna daktari wa kweli anayeogopa kusogea karibu na wagonjwa wake.

MARKO 153

Tumaini la wanadamu halipo katika uwezo wa kushika sheria bali katikakumtegemea Kristo na kumgeukia kwa msaada, yaani ni kuishi kwa neema sikwa sheria. Hivyo, Yesu aliwashtua sana na matendo yake na maelezoaliyoyatoa alipojitetea. Katika kujibu ‘mbona yao’ alitoboa wazi kiini cha hudumayake na kufunua shabaha ya Kuja Kwake.

Kwa hiyo, huduma ya Yesu ilichukua hatua nyingine iliyowashtua wafuasi wakena kuwachukiza wale waliokataa kumfuata. Je! hao wanafunzi wenginewalionaje Mathayo alipoitwa na Yesu na kujiunga nao na kushirikiana pamojanao katika kundi la pekee? Huenda walisikia shida.

2:18-22 Habari ya Kufunga na Njia ya kale na Njia mpya(Mt.9:14ku.Lk.5:33ku)Waandishi na Mafarisayo walizidi kutafuta sababu za kumlaumu Yesu. Walionakwamba wanafunzi wao pamoja na wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walifunga,ila wanafunzi wa Yesu hawakufunga. Watu walifunga kwa mambo mawili,kuonyesha toba la kweli na wakati wa maombelezo. Bila shaka wanafunzi waMbatizaji walifunga Yohana alipouawa. Kwa sheria ya Musa (Law.16:29)Wayahudi walifunga mara moja kwa mwaka Sikukuu ya Upatanisho, ila wakatiwa Yesu kwa uongozi wa Mafarisayo walifunga mara mbili kwa juma (Lk.18:12).Mara nyingi walifanya katika hali ya kujionyesha kwa watu kulikokujinyenyekeza kwa Mungu. Yesu alikubali jambo la kufunga ila kuwe kwalengo la kujinyenyekeza kwa Mungu na kufanywa kwa siri, bila kujionyesha kwawatu (Mt.6:16ku).

Yesu aliwaambia wazi kwamba wanafunzi wake hawakuweza kufunga wakatihuo, kwa sababu ni wakati wa arusi na Yeye yu pamoja nao kama bwana-arusi.Wayahudi walitumia mfano wa arusi kueleza furaha ya kuja kwa Ufalme waMungu (Isa.54:1ku).

Katika kusema hivi Yesu alidokezea ‘kuondolewa kwake’. Neno la ‘kuondolewa’lilionyesha kwamba ataondolewa kwa nguvu kwa njia isiyo kawaida ya mtukuondoka. Neno hilo wanafunzi wake hawakulielewa (8:31-32). Hapo twaonakwamba Yesu alifahamu mapema mwisho wake na ya kwamba hatakaa naokwa muda mrefu. Wanafunzi wake wataomboleza atakapoondolewa, lakinibaada ya muda mfupi huzuni yao itageuzwa kuwa furaha (Yn.16:6,20). Watuwa Yesu ni watu wa furaha, na furaha ni tunda la Roho Mtakatifu (Gal.5:22).Furaha yao, kama furaha ya Yesu, si dalili ya kutokujali au kutokutia maananimambo mazito, la, hata kidogo. Watu walimwona Yesu kuwa mlegevu katikamambo ya dini yao. Hiyo karamu iliyoandaliwa na Lawi ilifaa sana kwakuonyesha hali mpya na ilifunua tofauti na ufa uliozidi kutokea kati ya Yesu naviongozi wa dini.

MARKO154

k.21-22 Halafu Yesu alitoa mithali mbili za kuonyesha kwamba kuja kwaUfalme wa Mungu kwahitaji mambo mapya ‘nguo mpya’ na ‘viriba vipya’,hayawezi kupokelewa na kuhifadhiwa katika mipango ya kale ya dini yaKiyahudi. Upo uhai mpya wa Roho Mtakatifu na watu kuzaliwa upya. Waandishina wenzao wameishatambua kwamba Yesu alitofautiana nao, na ndivyoilivyokuwa. Yesu aliposema kwamba haiwezekani kushona kiraka cha nguompya katika vazi kuukuu na kutia divai mpya katika viriba vikuukuu ameungamkono jinsi walivyomwona. Mipango mipya ilihitajika ili watu waishi kwa neemasi kwa sheria, yaani waishi katika uhusiano mwema na Mungu badala yakujitahidi kujistahilisha mbele zake. Haiwezekani watu waishi kwa njia mbili,mguu mmoja katika imani ya Kiyahudi na mguu mwingine katika imani ya Injili.Wao walitimiza masharti mengi ya dini kwa shabaha ya kumvuta Munguawapokee na kuwapenda. Kumbe! katika Yesu wameisha kupendwa upeo nakupokelewa bila masharti. Kwa tendo kuu na la ajabu Yesu atatoa uhai wakekwa ajili ya dhambi zao. Inayotakiwa ni kujikabidhi kwake, kumwamini kwa dhatina kumtii badala ya kushika sheria baridi isiyo na nafsi. Kumtii Yesu(Mungu/Mwanadamu) mwenye nafsi ni bora kuliko kutii sheria ambayo hainanafsi. Kusema ‘vazi kuukuu’ na ‘viriba vikuukuu’ Yesu alitoboa wazi kwambahali ya dini yao imekuwa ngumu, haina unyumbufu, imekauka. Kuna nguvu nauwezo katika nguo mpya na divai mpya kuzidi kabisa uwezo na nguvu ya vazikuukuu na viriba vikuukuu.

Jambo hilo liko mbele ya Kanisa pia, kwa njia gani Kanisa laweza kutoa nafasikwa ‘uhai mpya’ bila kukata uhusiano na mambo yaliyopita? Mara kwa marakatika historia yake Kanisa limepata ‘uamsho’ na Roho Mtakatifu amefanya kazikwa nguvu mioyoni mwa watu. Mara kwa mara imekuwa vigumu kujua ni kwanjia gani na mipango ipi ambayo hiyo divai mpya ihifadhiwe? Hekima ya Munguinahitajika.

2:23-28 Kutunza Sabato vizuri (Mt.12:1-8; Lk.6:1-5)Hapo tunayo habari ya shtaka la nne kutoka kwa viongozi wa dini juu ya Yesu,nalo lilihusu Sabato. Lilifuata jambo la kusamehe dhambi; kula pamoja wawatoza ushuru; na jambo la kufunga. Ni ajabu kuona kwamba hao Mafarisayowalikuwako shambani siku ya Sabato, Je! walikuwapo kwa bahati? au kwakusudi la kumvizia? Kila mara walitokea Yesu alipokuwa pamoja na wanafunziwake na wale walioandamana naye.

Yesu na wanafunzi walikuwa wakipita mashambani na inaonekana walikuwahawajala bado (Mt.12:1) kwa hiyo, walipokuwa wakipita, wakavunja masuke nakula na Yesu hakuwakemea. Haikuhesabiwa ni wizi, mgeni aliruhusiwa kufanyahivi (Kum.23:25). Ndipo Mafarisayo waliwashtaki kwa Yesu kwamba walikuwawamevunja Sabato? Hapo ni vema tuzingatie shtaka hilo. Walikuwa wakiivunjaAmri ya Mungu? au walikuwa wakiyavunja mapokeo yao? Kwa jinsi Yesualivyowajibu ni wazi kwamba Yeye hakuwaza kwamba wamevunja Amri yaMungu. Katika jitahada zao za kulinda Sabato iliyosema ‘usifanye kazi...’

MARKO 155

waandishi walikuwa wameandika orodha yenye aina 39 za kazi, na aina hizozilikuwa na vitawi vilivyoongeza hesabu hiyo. Kwa hiyo, machoni mwawaandishi na wazee haikuwa halali kubeba kitu siku hiyo, ndiyo sababuwagonjwa walipaswa kungoja mpaka jioni baada ya sabato kupita ndipowabebe wagonjwa wao. Waliweza kutembea kiasi fulani ‘mwendo wa sabato’wakienda hata kiasi kidogo zaidi ilihesabiwa mapokeo yao yamevunjwa,haidhuru sababu ilikuwa nini. Haikuwa halali ya kuvuna siku ya Sabato nailihesabiwa kwamba wanafunzi wamevuna, walipovunja masuke. Kwa mapokeoyao watu walisikia kulemewa mno nao waliishi kwa hofu ya kuvunja visheriahivi. Mkulima akienda kuvuna mashambani siku ya Sabato alivunja sabato.Lakini Je! kuvunja masuke ni sawa na kuvuna ikiwa ni kwa ajili ya kusikia njaa?

k.25 Yesu aliwajibu kwa kuwarudisha kwenye Maandiko, ambayo walidaikuyajua sana na kuona fahari juu yake. Aliwaonyesha kwamba hata Daudi,wakati yeye na wenzake waliposikia njaa alithubutu kufanya jambo lililokataliwakabisa na sheria. Aliingia nyumba ya Mungu na kuchukua mikate ya kipekee,ya onyesho, na kula yeye na wenzake (1 Sam.21:1ku). Kila sabato mikate kumina miwili iliwekwa mezani na mwisho wa juma makuhani waliila ile iliyowekwasabato iliyotangulia na kuiweka mipya. Ni makuhani tu walioruhusiwa kuila hiyomikate (Law.24:5) lakini kwa sababu ya njaa Daudi, ambaye hakuwa kuhani,alivunja sheria hiyo. Yesu aliona kwamba wanafunzi wamefanya jambolililolingana na lile la Daudi kwa sababu walifanya kwa sababu ya njaa.

(Marko ameandika kwamba habari ya Daudi ilitokea wakati wa Abiathari, lakinikatika 1 Sam.21 kuhani mkuu ameitwa Ahimeleki. Walikuwepo kundi lamakuhani pale Nobu wakati huo (1 Sam.22:20 Abiathari alikuwa mwana waAhimeleki (2 Sam.8:17; 1 Mam.ya Nya.18:16).

k.27 Baada ya kusema juu ya jambo la wanafunzi Yesu aliendelea na kusemajuu ya maana na shabaha ya Sabato katika mpango wa Mungu tangu kuumbwakwa vitu vyote. Katika kusema juu ya mambo hayo alionyesha kwamba alikuwana mamlaka juu ya kuamua mambo ya sabato na kueleza shabaha yake.Katika utaratibu wa uumbaji wanadamu waliumbwa kwanza ndipo sabatoilifuata mara kwa ajili yao. Shabaha ya sabato ni kuleta manufaa kwawanadamu, ni kumpatia mtu pumziko kwa mwili wake na burudiko kwa rohoyake katika utulivu na ibada. Mungu hakukusudia Sabato iwe mzigo mzito wakumlemea mtu jinsi wazee walivyoifanya kwa mapokeo yao, bali iwe baraka.Huenda nia yao ilikuwa njema, walitaka kuilinda sabato, lakini katika kuilindawamefunika shabaha yake. Sabato ilikuwapo kabla ya Amri Kumi, iliingizwakatika utaratibu wa Uumbaji, siku sita Mungu aliziumba mbingu na nchi na vituvingine, kisha, siku ya sabato alistarehe. Kwa kutaja ‘mwanadamu’ Yesualionyesha kwamba Sabato inahusu wanadamu wote si Wayahudi tu. Hivyo,Sabato ni mtumishi si bwana wa wanadamu, mtu akiwa na hitaji la lazima, hilolatungulia sabato. Hivyo Yesu ametufundisha kushika lengo la sabato si andikojuu yake tu.

MARKO156

Hata hivyo, Yesu hakufundisha kwamba Sabato ivunjwe pasipo sababumaalum. Yeye alikubali kabisa kwamba Sabato iliwekwa na Mungu, mwanzoni,wakati wa Uumbaji, ndipo ilisisitizwa ilipowekwa kuwa amri mojawapo katikaAmri Kumi. Yesu alifundisha kwamba mtu anao uhuru wa kuitumia kwakulingana na mahitaji yake ya lazima. Kwa mfano, mtu aweza kumbebamgonjwa kwenye baiskeli na kumpeleka hospitalini, hana haja ya kungojampaka sabato imepita, wala si lazima aende kusali kama likitokea jambo kubwalinalohitaji msaada wake. Hata makasisi hufanya kazi maradufu siku hiyo,wengi hujichosha siku ya Jumapili (Mt.12:5).

Alipojiita ‘Mwana wa Adamu’ Yesu alidai kuwa na mamlaka ya kuamua mamboya Sabato, kwa sababu Yeye ni Bwana wake, mkuu wake, mwenye mamlakaya kufanya hivyo. Je! alikuwa akidai kuwa Masihi? au yule aliyetajwa katikaDan.7:13-14, hatujui. Hatusikii kwamba wakuu walizidi kumpinga aliposemahayo, ila tutaona katika sura ya tatu waliendelea kumvizia kuhusu Sabato.

3:1-6 Yesu alimponya mwenye kupoozwa mkono siku ya Sabato(Mt.12:9ku. Lk.6:6ku)Kama ilikuwa bahati au siyo Mafarisayo walikuwapo shambani, hakuna bahatikatika habari ya kukutana sinagogini siku ya Sabato. Hapo twamwona Yesusinagogini siku ya Sabato akiwafundisha watu. Si wazi kama habari hii ilifuatamara ile tuliyosoma hapo juu. Pengine muda umepita na Marko aliiweka hapokwa shabaha ya kuonyesha jinsi uadui ulivyozidi kati ya Yesu na viongozi wadini. Huenda huyo mtu hakuzaliwa na mkono uliopooza ila ulisababishwa naajali au ugonjwa. Luka alitaja ni mkono wa kulia. Bila shaka alishindwa kufanyakazi.

k.2 Hatuambiwi ni akina nani waliomvizia, ila yaonekana ni Mafarisayo nawaandishi. Hawakumvizia kwa udadisi bali kwa nia mbaya ya kupata ushuhudautakaowasaidia kumshtaki. Wameishaelewa tabia ya huruma ya Yesu, piawalijua uwezo wake wa uponyaji, nao walitazamia kwamba Yesuatakapomwona huyo mtu atamponya hata ikiwa ni sabato. Akifanya hivyowamepata neno la kumshtaki kwa sababu siku ya Sabato haikuruhusiwakumtibu mtu isipokuwa alikuwa katika hatari ya kufa, na ni wazi kwamba huyomtu hakuwa katika hatari hiyo. Inaonekana walitaka Yesu amponye huyo mtu iliwapate kumshtaki na pengine walimweka mahali pa mbele ili Yesu amwone. Niajabu walivyotumia mtu mwenye shida ili wamnase Yesu, lakini hicho ndichokiasi cha chuki zao. Ila Yesu hakusita kuwakabili, alitaka watu watambue kosana hitilafu katika mafundisho ya Mafarisayo. Kwa jinsi alivyofanya walisaidiwakutambua hayo. Hivyo Yesu alikuwa akipambana na mawili: ugonjwa wa yulemtu, na kosa katika mafundisho ya Mafarisayo.

k.3 Kwa wazi na kwa kusudi Yesu alimwita yule mgonjwa aje mbele nakusimama katikati ili watu wote waone vizuri na kujua aliyosema na aliyofanya.

MARKO 157

Alitaka Mafarisayo wakabili na kupima nia zao na kuelimishwa kusudi waeleweshabaha na maana halisi ya Sabato.

k.4. Moja kwa moja aliwauliza swali ‘Ni halali kutenda mema? (kuponya) aukutenda mabaya (kutokuponya)? kuponya roho au kuiua?’. Kwa njia hiyo Yesualibadili hoja, isiwe juu ya sheria bali iwe juu ya mema na mabaya. Kwamaneno mengine swala kubwa ni ‘sheria ni kwa kuwaokoa wanadamu aukuwaangamiza?’ Watu walioulizwa walidai kujua yaliyo halali kuhusu sheria.Yesu alitumia Sabato kwa kufanya mema na kwa kumponya mtu. Wao katikakutokumhurumia huyo mtu na kutokutaka aponywe waliitumia Sabato kwakufanya mabaya na kuua. Labda katika kutaja kuua Yesu alidokezea jambo lakumvizia ili wapate kumshtaki. Yesu aliwafikirisha juu ya visheria vyao vyakutunza sabato ambavyo vilihusu ‘kutokufanya....’ Badala yake Yesualifundisha kwamba shabaha ya Sabato ni kufanya mema. Lipi lampendezaMungu? Mungu hupendezwa na hali ya kutafuta njia halisi za kutunza sabatokwa kutenda mema. Yawezekana mtu aache kufanya kazi zake za kawaida,lakini, Je! ametenda jema lolote, kama kumtembelea mgonjwa au mwenyekukaa peke yake au mwenye shida? Mungu hupendezwa na mema kutendekakama Isaya alivyosema (Isa.56:6; 58:6-14). Katika kuponywa watu Yesuhakufanya kazi hasa, mara nyingi alisema neno tu nao wakaponywa. Kwa swalilake Yesu aliwabana wafanye, ama mema au mabaya. Watakuwa wamefanyamabaya ikiwa wamemzuia huyo mtu asiponywe siku ya Sabato potelea mbalisheria yao isemavyo.

Wapinzani waliitikia changamoto waliyopewa na Yesu kwa kunyamaza.Walishindwa kujibu hoja yake. Yesu alishinda nguvu za uovu zilizotawalamawazo yao na kuutikisa msimamo wao, nao hawakupendezwa.

k.5 Ndipo Yesu akawakazia macho pande zote (ilikuwa desturi yake 3:34;5:32; 9:8) alisikia huzuni pamoja na hasira. Hasira kwa jinsi hao wakuuwalivyoharibu shabaha ya Sabato iliyowekwa na Mungu kwa manufaa yawanadamu. Huzuni kwa jinsi walivyokosa kumwonea huruma huyo mtualiyehitaji msaada, hata walikuwa tayari angoje mpaka kesho au siku nyinginekwa kuponywa. Angaliweza kuponywa kesho yake, lakini, kwa nini angojempaka siku nyingine? Yesu aliona wakuu walikuwa wagumu sana, walikuwawamesahau neema na rehema za Mungu. Hapo twaona Yesu alikuwamwanadamu kweli, mwenye kusikia hisia kubwa kama sisi. Twapaswa kusikiahasira tunapomwona mwingine ametendewa isiyo haki, pia tunapomwonaMungu amenyimwa heshima yake. Mara nyingi Marko ametaja Yesu kuwa nahisia mbalimbali (1:43; 3:5,7,34; 8:12; 10:14,21).

Kisha Yesu akamwambia yule mtu aunyoshe mkono wake na bila kumgusa,mkono ulipona, akaunyosha. Aliamini neno la Yesu na kwa njia hiyo Yesualiwafundisha watu wote waliokuwepo maana ya kutenda mema siku ya

MARKO158

Sabato. Hao wakuu walikuwa vipofu, hawakutambua kwamba wakati mpyaumefika na Ufalme wa Mungu umekuja kati yao.

k.6 Hapo twakuta jambo la ajabu. Mafarisayo walitoka nje kwenda kushaurianana Maherode jinsi ya kumwangamiza Yesu. Kwa kawaida Mafarisayo naMaherode walichukiana. Maherode walikuwa watu wa siasa, marafiki waHerode Antipa aliyetawala eneo la Galilaya. Kwa upande wa siasa MaHerodewaliunga mkono utawala wa Warumi, kwa hiyo, walikuwa kinyume cha nia yaWayahudi wengi na Mafarisayo waliotaka uhuru. Jambo hilo lilionyesha upanawa upinzani juu ya Yesu, waliochukiana walishauriana pamoja kwa sababuwalimchukia Yesu zaidi!! na asili ya chuki yao ni katika Yesu kumponya mtusiku ya Sabato. Herode na wenzake hawakutaka kuwa na mtu kama Yesukatika eneo lake kwa kuwa walihofu kwamba ataongoza mapinduzi ya serikali.Walihofu kwamba ikitokea ghasia za mapinduzi Warumi wangekuja na kuwekawatu wasio wana-nchi katika utawala nao wangenyimwa vyeo vyao.

Yesu aliondoka sinagogini, wala hakurudi tena, isipokuwa mara moja nyingine,pale Nazareti (6:1ku). Twapata habari za Mafarisayo na Maherode kuwapamoja tena katika jitihada za kumnasa Yesu katika maneno yake (12:13).

3:7-12 Yesu aliwaponya watu wengi (Mt.4:24-25; Lk.6:17-19)Inayofuata ni majumlisho ya shughuli za muda zilizofanywa na Yesu. Ijapokuwaviongozi wamemchukia umati wa watu walimpenda sana. Twasoma kwambaYesu alijitenga, aliacha kufundisha katika masinagogi na badala yakealifundisha hadharani karibu na Ziwa la Galilaya. Alifanya hivyo ili asigonganena wakuu kusudi apate kuendelea kuitimiza huduma yake kabla ya kuuawa.Alitaka nafasi ya kuwafundisha watu ambao walimwaza kuwa Mponyaji tu nakumtafuta kwa ajili hiyo. Alitaka kuwaelimisha juu ya Umasihi wake iliwasimwaze kuwa yule wa kuipindua serikali ya Kirumi na kuwaweka huru.

Kwa maneno yake Marko amechora picha dhahiri jinsi ambavyo watu wengisana walimjia tena walitoka maeneo mbalimbali; kutoka kusini, na mashariki, nakaskazini; Wayahudi pamoja na watu waliokaa mpakani na WaMataifa, nahuenda WaMataifa pia. Alisisitiza jinsi Yesu alivyowavuta watu wa aina zote.Kwa hiyo, katika kujitenga, huduma yake ilipanuka na kuwagusa watu kutokambali. Ni dalili ya watu kumpokea Yesu dhidi ya viongozi waliomkataa. Alipokeaumati wa watu tofauti na viongozi wa dini walioelekea kudharau watu. Walimjiakwa sababu walikuwa wamesikia habari zake.

k.9 Hapo twapata picha ya jinsi mambo yalivyokuwa, wengi walimsonga, nawenye misiba walimrukia katika jitihada zao za kumgusa. Yesu aliwaombawanafunzi wampatie chombo kidogo na kukiweka karibu ili asisongwe na umatiwa watu kusudi awafundishe, chombo kilikuwa mimbari nzuri.

MARKO 159

k.11 Pepo wachafu walimwangukia na kulia na kumkiri kuwa Mwana waMungu. Walitambua nguvu za Mungu ndani yake na mamlaka yake. Yesualiwatoa na kuwakataza wasiseme habari zake. Walilazimika kumtii nakuwatoka wale waliopagawa. Hakupenda kuupokea ukiri wao wa kweli kwasababu pepo walifanya bila hiari, hali wamesukumwa kufanya hivyo baada yakukutana na uwezo mkuu wa Mungu katika kuwatoa. Yesu hakutaka watuwafahamu kwamba Yeye ni Masihi mpaka wameelewa zaidi juu ya Umasihiwake kuwa wa namna gani. Namna yake itadhirika pale Msalabani katika Kufakwake.

3:13-19Yesu aliwachagua Mitume kumi na wawili (Mt.10:1ku; Lk.6:12ku)Tumeishaona kwamba viongozi wa dini wamezidi kumkataa na Yesu alitambuakwamba haitawezekana kujenga uhusiano mzuri nao kwa sababuhawakumtaka. Alitambua kwamba zipo nafasi tele za kuvuta watu waliokuwa nahaja ya mchungaji (Mt.9: 35). Pamoja na hayo alijua kwamba mbeleni atauawakwa sababu ya chuki za wakuu. Hivyo, kwa busara aliweka kundi maalumu lawale watakaoshika huduma baada ya kuondolewa kwake. Ilimpasa apatenafasi ya kutosha ya kuwafundisha na kuwatayarisha kwa kuondoka kwake, iliwaiendeleze huduma yake kwa njia za kumpendeza. Baadhi ya waliochaguliwawalikuwa wameandamana naye kwa muda baada ya kuitwa (1:16ku.Yn.1:35ku) nao walikuwa Simoni, Andrea, Yohana, Yakobo, Bartholomayo, naMathayo. Bila shaka walikuwapo wengine pia. Twajua kwamba wakati fulanialiwatuma watu sabini (Lk.10:1ku).

Aliwaita wawe kundi maalumu, na kuwaweka kuwa msingi wa watu wapya waMungu, badala ya Israeli ya zamani, Mitume 12, msingi wa Israeli mpya,kulingana na Israeli ya zamani yenye msingi katika makabila 12. Ndiyo sababualiwaita watu kumi na wawili. Marko ametumia neno Thenashara. Lukaamesema Yesu aliwaweka kuwa Mitume.

Yesu alipanda mlimani na kukesha usiku kucha katika maombi, (Lk.6:12) daliliya jambo hilo kuwa hatua kubwa na ya maana sana. Mbeleni yote yatategemeahali zao na uaminifu wao.

k.13 ‘akawaita aliowataka mwenyewe, wakamwendea’ Hapo ni wazi kwambaYesu aliwachagua kati ya wengine, huenda wengi, hawakumchagua Yeyekwanza (Yn.15:16). ‘akaweka watu kumi na wawili’ aliwafanya kuwa kundirasmi. ‘wapate kuwa pamoja naye’ ili wajifunze kwake kwa njia ya kuishipamoja naye kwa ukaribu sana, waone mwenendo wake, matendo yake,mwitikio wake kwa mambo mbalimbali, mbinu zake za kuwaunganisha kamandugu wa Baba mmoja, wayasikie maneno yake wakati wa furaha na wakati wahuzuni, wakati wa kuchoka na wakati wa kuchangamka. Hasa waone jinsialivyowahudumia watu kwa upendo na kwa kuwahurumia badala yakuwahukumu. ‘na kwamba awatume kuhubiri’ kazi yao itakuwa kama Yake,alipowaita wavuvi aliwaambia ‘nitawafanya kuwa wavuvi wa watu’ kusudi utume

MARKO160

wake uendelezwe na hao (6:7-13). Ndivyo ilivyotokea Siku ya Pentekoste nasiku za baadaye (Mdo.2-14). ‘tena wawe na amri ya kutoa pepo’ aliwashirikishaamri yake juu ya nguvu za yule mwovu. Kazi zao ni kupambana na maovuyaliyomo ulimwenguni kama Yeye alivyopambana nayo. Watashiriki uwezowake na ushindi wake.

Hivyo kwa neno na kwa tendo, kwa kutangaza Injili na kwa matendo yakuwahudumia watu, watafanya sawa na Yesu alivyofanya na Ufalme wa Munguutaendelea kusimamishwa kati ya watu. Yesu alipambana na maovu na yulemwovu na yawapasa watumishi wake wafanye vivyo hivyo. Uovu wa binafsi nauovu unaofanywa na mashirika na madaraka mbalimbali, na taasisi zinazooneawatu na kwa ajili ya faida hufanya udhalimu mkubwa unaoleta shida kwawanadamu. Shetani hujificha ndani ya vitu vya namna hiyo. Kanisa laitwakusimama imara na kupambana na maovu popote yanapoonekana. Yesualikuja kwa shabaha ya kuwaokoa wenye dhambi na kuukomboa ulimwengukusudi afanye uumbaji mpya wa watu wa Mungu, taifa jipya la wanadamumahali pa taifa la kwanza la Adamu.

k.16-19 Hapo Marko ameorodhesha majina ya wale walioitwa.Tukilinganisha na orodha za Mathayo na Luka na Matendo 1:13ku. Simoniamewekwa mwanzoni kila wakati. Marko amewataja mmoja mmoja. YudaIskariote ametaja mwishoni na ya kuwa alikuwa msaliti. Yesu aliwapa watatujina lingine, Simoni alimpa jina la Petro, kwa sababu atakuwa yule wa kusemakwa niaba ya wote. Atatokea kama mwamba. Haina maana kwamba awe nacheo kikuu kupita wenzake. Yakobo na Yohana aliwaita Boanerge, maanayake, wana wa ngurumo, inaonekana kwamba mara kwa mara walisema kwanguvu kupita kiasi (Mk.9:38; Lk.9:54). Simoni Mkananayo pengine yeye alikuwakatika kundi la Wazelote waliokuwa na wivu juu ya taifa nao walitaka kuipinduaserikali. Iskariote pengine aliitwa hivyo kwa sababu alitoka kijiji cha jina hilo,kilichokuwa kusini. Yawezekana ni yeye tu aliyetoka kusini na wengine wotewalitoka Galilaya. Katika orodha nyingine wawili wawili wametajwa pamoja.Wengi wametatanishwa na habari ya Yesu kumchagua Yuda Iskariote, ni vematukumbuke kwamba alimwita kwa sababu zile tatu ambazo tumeziona hapo juu- kuwa pamoja naye, kwenda kuhubiri, na awe na amri ya kutoa pepo. Ni fumbokujua kwa nini Yuda hakuhitimu, huku wengine, ambao waliteleza mara kwamara walihitimu. Yesu hakumwita, eti!. amsaliti. La! Walipoitwa hawakuwawakamilifu, wa kwanza katika orodha ni Petro aliyemkana, na wa mwisho niYuda aliyemsaliti!!!.

Kila mara katika sura zifuatazo Marko amesisitiza jinsi hao wanafunziwalivyokuwa pamoja na Yesu, alilihesabu kuwa jambo muhimu na hasa kwashabaha ya utekelezaji wa Utume wake baada ya Kufufuka Kwake (14:28;16:7).

MARKO 161

3:20-30 Yesu alirudi Kapernaumu na vikundi mbalimbali wameshindwakumwelewa na kumwaminiIjapokuwa Marko hakutaja Kapernaumu inafikiriwa kuwa ‘akaingia nyumbani’ ninyumba ya Simoni na Andrea pale Kapernaumu mahali ambapo Yesu alikuwaameweka kituo chake. Kama hapo nyuma (2:2) watu wengi walikusanyika naYesu na wanafunzi hawakuwa na nafasi ya kula.k.21 ‘jamaa zake’ walionyesha hali ya kutokushirikiana na Yesu katika hudumayake. Ndugu zake ambao hawakumwamini (Yn.7:5) wametajwa tena pamoja namama yake (k.31). Walipopata habari za wingi wa watu kumsonga na jinsialivyojitoa kuwahudumia bila kujihurumia walidhani kwamba amerukwa na akili,amesukumwa na nia ya kutumika kuliko ilivyompasa. Wakaja ili wamtoe kwanguvu pale na kumrudisha nyumbani. Hivyo, twajifunza jinsi ambavyo walewaliokuwa karibu naye kimwili waliguswa na mafanikio ya huduma ambayoyalionekana katika umati wa watu kumtafuta na kumpenda. Hawakuangaliaumuhimu wa kazi zake bali jinsi zilivyozidi na kumfanya atumike kwa saa nyingibila kuwa na nafasi ya kula na starehe. Hawakuelewa kwamba ilimpasa atendekazi za Babaye maadamu ni mchana. Bila shaka Yesu alisikia shida alipoonahali yao na nia yao ya kumwondoa pale asiwahudumie watu. Walifanya kwa nianzuri ya kumpenda na kumhurumia. Ilikuwa vigumu kuelewa hayo yoteyaliyokuwa yakitokea kwa sababu walikumbuka jinsi alivyozaliwa na kukuamiongoni mwao na kuonekana kama mmoja wao.

k.22ku. Ndipo Marko aliendelea kusema juu ya kundi lingine la watu,Mafarisayo na waandishi waliotoka Yerusalemu kwa shabaha ya kumchunguzana kumkagua. Hao walikuwa wataalamu katika mambo ya dini, waliotegemewakuamua mafundisho na mambo ya dini. Hao pia walivutwa kuja kwa sababuwalisikia jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakimwendea Yesu pamoja nahabari za uponyaji wake na uwezo wake wa kutoa pepo. Ni dalili ya mafanikioya huduma ya Yesu na jinsi walivyomwona kuwa hatari kwa yale yotewaliyokuwa wakiyategemea.

(Katika Mathayo na Luke ipo habari ambayo Marko hakuisema. Katika Mathayo9:32-34 na 12:22ku. na Luka 11:14ku. ipo habari ya Yesu kutoa pepo katikamtu aliyekuwa kipofu, bubu, na mwenye pepo. Yesu alimtoa pepo na mtu alionana kusema. Ndipo Mafarisayo wakaanza kumshtaki).

Walisemaje hao waandishi waliotoka Yerusalemu? walimshtaki mambo mawili(a) Yeye ‘ana Beelzebuli’ ‘ana pepo mchafu’ (k.30) (b) ‘Kwa mkuu wa pepohuwatoa pepo’. Hakumwambia hayo ana kwa ana. Lakini Yesu aliwaita kwakena kuwajibu bila wasiwasi wowote. Kwanza alijibu shtaka la kuwa anatoa pepokwa mkuu wa pepo, maana yake, atoa ama kwa Shetani au Beelzebuli, aulabda hao wote ni wamoja k.24-27. Jibu kwa shtaki la kwanza la kuwa naBeelzebuli au pepo mchafu lapatikana katika k.28-29. Jibu kwa shtaka la pilihutangulia k.24-27. Si mara hii tu ambayo alisemwa kuwa na pepo (Yn.7:20;8:48,52; 10:20). Yalikuwa mashtaka mazito yakielekea kufuru, ni kusema

MARKO162

kwamba kazi zake si halali na ya kwamba ameungana na enzi za uovu.(Beelzebuli - lilikuwa jina la mungu wa Ekroni. Katika 2 Wafalme 1:2 ni jina kwa‘bwana wa mainzi’ na kwa dharau Wayahudi waligeuza kuwa ‘bwana wa mavi’).Kwa kumwita Yesu hivyo walionyesha dharau kubwa sana, na hasa,tukikumbuka kwamba asili ya habari hiyo ni katika kumwezesha mtu bubu nakipofu kusema na kuona tena na pepo kumtoka. Ni dalili ya upofu wao kwasababu walijua kwamba wakisema amefanya kwa nguvu za Mungu iliwapasawampokee, na hilo hawakutaka. Hawakuweza kukana miujiza yake ilawalifanya juu chini kuieleza kwa kuonyesha kwamba Yesu alifanya kwa niambaya.

k.23ku Yesu alitumia mithali ili awatobolee ujinga wa msimamo wao,akawauliza ‘Awezeje Shetani kumtoa Shetani’ hakusema Beelzebuli baliShetani. Walisema kwamba alikuwa anatumia nguvu ile ya Shetani na kutendakazi katika eneo na chini ya madaraka ya Shetani kama ni mjumbe wa uovu.Lakini haiwezekani Shetani aupindue ufalme wake! ni sawa ya kufikiri mwiziatajiibia!! au Shetani atajiua!! Shetani ni mwerevu kiasi cha kutokufanya hivyo.Ilikuwa dhahiri kwamba Shetani alikuwa angaliko na nguvu zake, bado zilikuwazikifanya kazi (k.26). Swala kubwa ni, ikiwa jambo hilo limefanyika kweli, napepo ametolewa; ni kwa uwezo gani? na zaidi, ni kwa mamlaka gani? Kwahiyo, swali lililopo ni ‘uwezo huo na mamlaka hiyo, ni ya nani?’.

k.27 Kuna ‘mwenye nguvu kuliko Shetani’ ambaye amemfunga Shetanikwanza ndipo ameteka nyumba yake, yaani kutoa pepo zake. Nguvu ni yaRoho Mtakatifu, Yesu alipewa Roho Mtakatifu kwa ukarimu, naye atatoa RohoMtakatifu kwa wafuasi wake baada ya Kutukuzwa Kwake (Yn.7:39;Mdo,.2:1ku). Badala ya kuwa na mkuu wa pepo Yesu alikuwa na RohoMtakatifu, badala ya kuwa ameungana na Beelzebuli, bwana wa mainzi, munguwa mavi, Yeye alikuwa na roho safi. Badala ya Yeye kuwa ameungana naShetani, Yeye ni Mwana mpendwa wa Baba ambaye alitumwa kwa kusudimaalum la kufanya vita na Shetani na enzi zake. Katika Yesu Shetaniamekutana na Mwenye kumshinda ambaye atakapokufa msalabaniatamnyang’anya enzi yake (2:31; 16:11; Kol.2:15).

Hao Mafarisayo na waandishi walitofautiana na jamaa za Yesu. Hao jamaawalisikia shida katika kumwelewa Yesu na kumwamini, ila hao waliotokaYerusalemu, walikusudia kutokumwelewa vizuri, Wivu uliwapofusha macho, namambo ambayo watu walitambua bila shida, hao walishindwa kuyakubali.

Kutolewa pepo wabaya hakuwa jambo geni katika Wayahudi ila jambo geni nikatika Yesu kufaulu kila wakati. Sivyo ilivyokuwa kwa wengine (9:38;Mdo.19:14). Swali lililokuwapo kwa wale waliofaulu kutoa pepo lilikuwa Je! haowalitumia uwezo wa Shetani au vipi? hakuna ambaye angalikubali kwambawaliutumia uwezo wa Shetani, bali uwezo wa Mungu (Mt.12:27).

MARKO 163

k.28-30 Katika k.23-27 Yesu ameeleza mambo kwa maarifa ya kawaidaalipotumia mithali. Lakini jambo lililotokea la yule mtu mwenye pepo, kipofu, nabubu (Mt.12:22) lilipaswa kuelezwa zaidi ya kutumia maarifa ya kawaida. Kwajinsi alivyoshtakiwa na waandishi kwamba amemponya kwa uwezo waBeelzebuli jambo lilihusu mambo ya kiroho na lilipaswa litafsiriwe kiroho. Kwahiyo Yesu aliendelea kusema juu yake. Kwanza alitanguliza kwa kutumia neno‘Amin’ akisisitiza ukweli na uzito wa maneno yaliyofuata. Tamko lenyewelilihusu kila dhambi na kila kufuru kusamehewa, ahadi pana sana na katikaahadi hiyo ukarimu wa Mungu umeonekana na neema ya Kristo umedhihirika.Ila ahadi hiyo ilifuatwa na onyo kali sana, ni onyo mojawapo katika Maandikolinalotisha sana. Ipo dhambi moja isiyo na msamaha, na dhambi hiyo haowaandishi walikuwa katika hatari ya kuifanya, yawezekana walikuwawameishafanya. Kwa nini wamekuwa katika hatari ya kufanya dhambi hiyo?Wamefanyaje ili wafikie hatua hiyo ya hatari sana kiroho? Yesu alionyeshasababu yake katika k.30 ‘kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu’. Hii ndiyosababu, na twapaswa kukumbuka mazingira ya maneno hayo, kwa sababuwengi wameshikwa na wasiwasi wakihofu kwamba wamefanya dhambi hiyo.

Walimkufuru Roho Mtakatifu waliposema kwamba ile kazi njema sana ya yulemtu kuponywa ilikuwa kazi ya Shetani, kazi ambayo ilikuwa wazi kwa wengikuwa kazi ya Mungu. Walimshtaki Yesu kuwa na uhusiano na mkuu wa pepo.Kumbe ni wao si Yesu walio na uhusiano na Shetani, kiasi cha kumnyima Yesusifa na pongezi kwa jambo hilo jema. Ni kuupotosha ukweli, ni kusema wema niubaya na nuru ni giza. Si kama ilikuwa kosa la kuuliza maswali na kuhoji, walasi kosa la kutokufahamu au kutokuelewa vizuri, bali kwa kusudi na kwa chuki nakwa sababu hawakumtaka walikataa kumpa Yesu sifa na kukiri kwambaamefanya kwa uwezo wa Mungu. Walirudisha mlango usoni mwake na kwakufanya hivyo walirudisha mlango kwa yule mwenye msamaha. Ikiwa nuru nigiza na wema ni ubaya waliwezaje kutubu, kwa kuwa walishindwa kutambuawema na kweli? Roho atawezaje kuwaleta kwenye nuru na kweli na tobawanapokataa kumkiri Roho kuwa asili ya nguvu ya Yesu. Wasipotubu hakunamsamaha. Ni yule tu mwenye kuukataa msamaha ambaye atakosakusamehewa. Walikataa neema ya Mungu ilipodhihirika wazi kabisa katikautendaji wa kumponya yule kipofu na bubu mwenye pepo na zaidi ya kuikataawalisema ni ya Shetani. Shida kubwa ni kwamba ilikuwa msimamo wao daima.

3:31-35 Ujamaa wa kweliKisha Yesu alipambanua kati ya walio jamaa yake na wasiokuwa jamaa yake,wale walio ndani na wale walio nje (nje - k.31,32;4:11). Mama yake na nduguzake walikuja, pengine kutoka Nazareti, hali wamevutwa na yote waliyoyasikiajuu ya Yesu. Walipofika walikuta wengi wameketi, wakimzunguka. Hawakuwezakufika karibu na Yesu na pengine Yeye hakuweza kuwaona kwa sababu yaumati wa watu waliomzunguka. Ndipo aliambiwa kwamba mamaye na nduguzewalikuwa wakimtafuta. Bila shaka hao watu walifikiri kwamba jamaa zake

MARKO164

wamestahili kupata nafasi ya kusema naye na bila shaka wao wenyewewalifikiri wana haki ya kusema naye.

Yesu alifanya nini alipoambiwa habari zao? Alisema na hao watu waliokuwanaye ndani, akawauliza swali ‘mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?’Halafu aliwatazama wale waliokuwa wakimsikiliza akasema ‘Tazama, mamayangu na ndugu zangu!’ Kwa njia gani mtu aweza kuhesabiwa ni mama aundugu yake? Ni kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Familia yake hawakuwezakutatua tatizo la kumfikiria kuwa mwanadamu tu, walikuwa wamemzoea,amelelewa miongoni mwao, walishindwa kutambua jinsi Alivyo hasa, Mwanawa Mungu. Bila shaka maneno ya Yesu yalishtua wale watu pamoja na kushtuajamaa zake. Ni kama hakuwajali mama na ndugu zake. Haikuwa rahisi kwaYesu, aliyejaa upendo, kusema maneno kama hayo. Ila shabaha ya Yesu kujaduniani ilikuwa kuunda jamii mpya wa wanadamu, shirika jipya; badala ya Jamiiya Wanadamu chini ya kichwa cha Adamu itatokea Jamii Mpya chini ya kichwacha Kristo (Rum.5:12ku) na badala ya Taifa la Israeli, Kanisa litakuwa IsraeliMpya. Hayo yote yalitegemea itikio la kibinafsi la kila mtu kwa Yesu Mwenyewe.Yesu alisema dhidi ya mawazo ya wanadamu, mambo ya ukoo hayana nguvukatika Ufalme wake. Jinsi alivyosema juu ya ndugu zake, ndivyo YohanaMbatizaji alivyosema juu ya Waisraeli (Mt.3:9; Yn.8:39). Injili inamdai kila mtuamweke Mungu na mapenzi yake kuwa juu ya mambo yote mengine (10:29).Baadaye mama na ndugu zake walimwamini, walikuwa katika kundi la walewaliosubiri Kushuka kwa Roho Mtakatifu (Mdo.1:14).

Katika sehemu hiyo Marko ametaja wale waliompinga Yesu sana, na walewaliotatizwa naye, na wale waliomsikiliza kwa makini na kujitoa kumfuata.

Sura ya nne ina mifano mitatu kuhusu Ufalme wa Mungu (4:1-34) Hapo Markoamekusanya mafundisho ya Yesu katika mifano mitatu iliyokuwa na shabaha yakufunulia pamoja na kuficha siri ya Ufalme wa Mungu. Katika sura ya pili na yatatu tumeona kwamba huduma ya Yesu imefanyika hasa katika vijiji na miji yaGalilaya, haikufanyika katika wale walioongoza maoni ya umma, hivyo ilikuwana mpaka. Katika sura hizo tumewakuta wenye kushuku na wenye kupinga, nawenye sauti na uongozi walizidi kumkataa Yesu. Hata katika umati wa watuwaliomfuata shaka ilikuwapo kwamba baadhi yao walivutwa na miujiza yakekuliko kuja kwa Ufalme wa Mungu. Hivyo shaka ni kwamba shauku yao itadumuau siyo? Mambo hayo yote yalitatiza. Inawezekanaje makusudi ya Munguyapingwe? Kwa nini ujumbe wa nguvu wa kuleta mabadiliko ulikosa kuvutakibali cha wengi? Je! ni kweli ‘Wakati umetimia’? (1:15). Sura ya nne inahusikana maswala hayo makubwa kuhusu Huduma ya Yesu na jinsi mamboyalivyokuwa yakitokea. Hata dhana zetu juu ya Mungu kutimiza makusudi yakehupimwa na kufunua kiasi cha kuelewa kwetu.

MARKO 165

4:1-9 na 13-20 Mfano wa Mpanzi na maelezo yake (Mkt.13:1-9; Lk.8:4-8)Yesu alikuwapo tena karibu na Ziwa la Galilaya (2:13;3:7) na kama ilivyokuwadesturi yake aliwafundisha watu tena. Neno ‘tena’ (3:7) linadokeza kwambaamewaacha wale waliokosa kumfahamu na kushika kwa upya utume wake.Njia yake ni ya upweke (Ebr.13:11-13) alikataliwa na jamii, hata hivyo, wakowale waliokuwa tayari kumfuata dhidi ya masumbufu ya viongozi wa dini.Kawaida ya waalimu ni kufurahi wapatapo wafuasi wengi ila Yesu sivyo. Yeyealifahamu kwamba watu walikuwa na nia mbalimbali (Yn.2:25) naalipowafundisha kwa njia ya kuitumia mifano alikuwa akichunguza mioyo yaona kupambanua kati yao akitafuta itikio la kiroho la kujitoa kwake, hakulengakupima akili zao. Alitaka kuwatia moyo ili watie maanani mafundisho yake.Wakati ule lilikuwa kama jambo la kufanya kwenda kumsikiliza ila Yesuhakudanganya na umati wa watu. Alitaka wamwamini na kujitoa kwake, nakudumu katika mafundisho yake. Walikuwapo marabi wengiwaliozungukazunguka, hata walikuwapo wafanya miujiza pia. Yesu hakutakawatu ambao watamfuata kwa muda tu, bila kutia maanani yaliyomo katikaufuasi wake. Pia alitaka watu wawe na utambuzi wa maana ya ndani ya mifanoyake. Juujuu, mifano yake ilieleweka bila shida, ilihusu maarifa ya kawaida nabila watu kuizingatia na kutia maanani watashindwa kugundua fundisho lake.

Mifano hiyo mitatu ilitoka katika kilimo, jambo ambalo kila mtu alielewa. Kwasababu ya mkusanyiko mkubwa wa watu Yesu alipanda chomboni na kukitumiakama mimbari. Yesu alikuwa mwepesi wa kutumia njia yoyote ili afundishewatu, wala hakujali mahali wala hesabu ya watu. Alifundisha ziwani, sinagogini,hekaluni, barabarani, katika arusi na katika mazishi; kwa mtu mmoja, kwa kundidogo, na kwa umati wa watu, popote penye watu Yeye alikuwa tayari kuhubiri.

4:3ku Mfano wa Mpanzi (Mt.13:1-9; Lk.8:4-8)k.3-k.8 Na maelezo ya Yesu k14-k20. Yesu alianza jambo jipya alipotumiamifano na bila shaka sababu yake ni katika mazingira ya huduma yake na jinsiilivyokuwa ikiendelea. Tumeona ya kuwa watu wengi walimfuata wakivutwa namiujiza yake kuliko maneno yake. Wakuu walizidi kumpinga na Yeye alihitajikujihusisha zaidi na wanafunzi wake na kuwatayarisha kwa wakatiatakapoondolewa. Kwa hiyo, kwa njia ya mifano, alieleza mambo yahusuyoUfalme wa Mungu bila kudai kuwa Masihi kwa wazi. Mifano ilikuwa njia yakuwabainisha wale waliokuja kwa mafundisho na wale waliokuja kwa kuonamiujiza tu. Hao waliokuja kuona miujiza walisikia mifano bila kutambua maanayake ya ndani. Ndiyo sababu Yesu alisema ‘Sikilizeni’; ‘Tazama’ na k.9 ‘aliye namasikio ya kusikilia, na asikie’. Ndani ya mifano yalikuwepo mafundishomakubwa (siri) ambayo hayakuwa dhahiri pasipo mtu kutega masikio nakuzingatia yaliyosemwa. Kwa njia hiyo Yesu aliwaita watu wajihusishe nayaliyosemwa na kuamua la kufanya. Watu hawakuhitaji kisomo au elimu yadini; yeyote aliyetega masikio alifunuliwa siri ya Ufalme wa Mungu. Matumainiya mavuno yalikuwepo kwa njia ya mpanzi kuendelea na kazi yake.

MARKO166

Fundisho kubwa ni kwamba Ufalme wa Mungu umeingia katika ulimwengu huumfano wa mbegu inapopandwa kuingia ardhini. Mungu yu katikati ya jambohilo. Hivyo Ufalme wa Mungu hauji katika jambo kubwa la ajabu la kuwashtuawatu na kuuvuta usikivu wao, la, siyo, bali hutambulikana na wale walisikiaoNeno la Mungu na kulizingatia. Mafanikio hutegemea maitikio ya watu, namaitikio yao hutegemea hali ya ‘udongo’ yaani hali ya mioyo yao.

k.4 na k.14 Mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, mahali ambapo watuhukanyaga na kwa sababu hiyo udongo huwa mgumu na mbegu hushindwakupenya ndani. Tukumbuke kwamba katika nchi ya Palestina wakati wa Yesu,watu walipanda mbegu kwanza na kulima kwa plau baada ya kupanda. Yesualieleza maana yake katika k.14. Kwa sababu udongo ulikuwa mgumu mbeguilikaa juu ya ardhi ikishindwa kupenya ndani yake, ndipo ndege, yaani Shetani,adui wa Neno alikuja akainyakua. Hivyo wengine hawajali Neno la Ufalme. Hatahivyo mpanzi huendelea na kazi yake. Yesu aliamini kwamba ijapokuwawengine walimpinga ni baadhi tu. Shida haikuwa katika mbegu, wala katika haliya hewa, bali katika hali ya udongo.

k.5-6 na k.16,17 Halafu mbegu nyingine ilipandwa na kuanguka mwambani,penye mdongo mchache, ikaota, kisha ikaungua na kunyauka, ilishindwakupata nafasi ya kutia mizizi chini kwa sababu ya uchache wa udongo. Udongoulikuwa mzuri ila ulikosa kina. Ni mfano wa watu wengine ambao hulipokeaneno kwa furaha ila hawawi tayari kukabili shida, au majaribu, au dhihaka kwaajili ya Kristo. Wampokea Kristo bila kuhesabu gharama kwanza. Shida nikatika hali ya udongo. Baadhi ya watu huwa na maisha mepesi na hukosa kinakatika maisha yao.

k.7 na k.18,19 Ndipo mbegu nyingine ilipandwa na kuanguka penye miibandipo ikaota na kumea pamoja na miiba na magugu na kwa sababu hiyohaikupata nafasi njema ya kukua. Ilisongwa na kukosa kuzaa matunda. Nimfano wa watu walio na mambo mengi katika maisha yao, hawalengi jambomoja, wavutwa na vitu mbalimbali kama kutaka pesa, cheo, michezo,maburudiko n.k. Ndivyo ilivyo kwa wengi siku hizi. Hasa katika miji yetu, na kwasababu hiyo wameshindwa kumtanguliza Yesu katika maisha yao. Hata hivyo,mpanzi hakukata tamaa, kwa sababu alijua mbegu zake zingine zitaangukapenye udongo mzuri na kuzaa.k.8 na k.20 Hapo mbegu zingine (hapo juu nyingine imetajwa mara tatu) ilahapo ni zaidi ya moja. Zingine zilipandwa na kuanguka penye udongo mzuri nakuzaa, zote zilizaa, ila kwa tofauti. Ni mfano wa watu walisikiao neno la Munguna kulipokea, na kuliwekea nafasi katika maisha yao na kuzaa. Mbegu zilikuwanzuri na udongo ulikuwa mzuri na hata katika udongo, uzuri ulionekana kwakiasi mbalimbali.

MARKO 167

(Tukifanya hesabu, mbegu sita zilipandwa, kati yao tatu hazikuzaa, na katikatatu zingine, zote zilizaa, ila kwa tofauti ya thelathini, sitini, na mia)

Hivyo Yesu alisisitiza jinsi mavuno yatakavyokuwa mengi, ijapokuwa upinzaniupo na wengine hawaitiki vema. Mwishowe mavuno yatapatikana kwa wingi.Kwa hiyo, Mungu atashinda. Yesu atateswa na kuuawa, atafufuka siku ya tatuna wafuasi wake watafurahi na kwa msaada wa Roho watauendeleza Utumewake, Neno la Ufalme litazidi kuhubiriwa kotekote ulimwenguni, na watu wa kilahali na kila mahali watapewa nafasi. Katika umati wa hao, wengine hawatalijali,wengine watakuwa watu wasio na kina ambao Neno litaota ndipo litakauka bilakuzaa, wengine watajaa mambo mengi maishani mwao wakikosa kutoa nafasiya kutosha kwa Neno kuzaa. Wengine watalikaribisha Neno kwa furaha nakulitia maanani. Potelea mbali wateswe na kupata shida, wachukiwe na watun.k. wataendelea kumfuata Kristo kwa uaminifu (Mt.9:37; Yn.4:35; 1 Kor.15:58)

Kwa hiyo katika mfano huo Yesu ameeleza jinsi ambavyo mambo yalikuwawakati wake na jinsi ambavyo mambo yatakuwa mbeleni hadi mpaka mwishowa dahari, wakati Ufalme wa Mungu utakapokamilishwa na mavuno yaletwaghalani.

k.9 Ijapokuwa Yesu alionyesha kwamba matumaini ya mavuno yapo, hatahivyo, alitoa onyo kwamba inayohitajika ni mtu kulizingatia lile Nenoanapolisikia, kulitia maanani, na kukata shauri la kulipokea na kulitii katikamaisha yake.

4:10-12 Matumizi ya mifanok.10 Pengine Yesu alitoka chomboni na kuachana na umati wa watu na kubakina wanafunzi wake pamoja na wengine. Ila twaona mifano mingine hufuatahabari hiyo pamoja na tafsiri ya Yesu kwa mfano wa mpanzi.

Katika Mathayo 13:10 wanafunzi walimwuliza ‘kwa nini wasema nao kwamifano?’ na Luka 8:9 ‘maana yake nini mfano huo?’. Kwa hiyo wanafunziwalitaka kujua mambo hayo mawili ila Marko hakueleza wazi maswali yao.

k.11-12 Jibu la Yesu kama alivyoliandika Marko limewatatanisha watu wengisana. Kwa sababu inaonekana Yesu alitoa sababu ya kuitumia mifano kuwa ‘iliwatu wasione......wasije wakongoka...’ kana kwamba alitumia mifano kwashabaha ya kufanya watu wawe wameshindwa kuelewa yaliyosemwa. Kama nihivyo ni kinyume cha Maandiko yasemayo kwamba Mungu hupenda watu wotewaokolewe - tena ni kinyume cha shabaha ya Yesu kuja ulimwenguni ambayoilikuwa kuwaokoa wenye dhambi. Tukifikiri mfano kama wa Mwana Mpotevu,Kondoo aliyepotea, n.k. ni vigumu kufikiri kwamba kusudi la mifano ilikuwakuwapofusha watu. Ni vigumu kusema kwamba Marko amekosa katikakuandika kwake, kwa hiyo ni vema tuchunguze zaidi jambo hilo katikamazingira yake na kwa kulinganisha na Mathayo na Luka. Luka ameandika kwa

MARKO168

ufupi sana na Mathayo ameandika kwa urefu. Yawezekana shida imetokea kwasababu Marko amefupisha habari hiyo. Mfano wa taa (k.21-25) unaofuatahabari hii unatoa mwanga juu ya habari hiyo na unasisitiza habari ya taakuwekwa juu na kuyafunua yaliyofichwa (k.21-23).

Wengine hawaoni wala hawasikii kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Hatahivyo wamewajibika kwa itikio lao. Mungu hataki kuwalazimisha watu kuamini.Imani inahitajika, na kuficha siri ya Ufalme wa Mungu kunalinda uhuru wa mtuwa kuamini au kutokuamini. Tofauti imetokea katika wale waliomwamini nakujihusisha naye (wanafunzi) ambao walifundishika na wale ambao mpakawakati huo hawajajiaminisha Kwake. Hao washindwa kumfahamu, na kwasababu hiyo, Yesu aliona vema aitumie mifano. Kwa mifano hakukusudiakuwapofusha, maana wameisha kuwa vipofu, kwa hali na tabia ilidhihirikakwamba walikuwa nje ya Ufalme wake na kwa kuitumia mifano jambo hilolilithibitishwa na utengano kati ya watu ulionyeshwa, ilibainika ni akina naniwaliokuwa ndani ya Ufalme na ni akina nani walio nje. Swali lililopo ni ‘ni kwanjia gani wale waliokuwa nje walipata kufika ndani’? maana wote walikuwa njemwanzoni. Neno hilo litajibiwa baadaye, ila ni vema kuona kwamba ni walewaliokuwa ndani waliouliza maswali juu ya matumizi ya mifano. Kwa mifanowatu walivutwa tena wamsikilize Yesu na kulizingatia Neno lake. Kwa hiyokatika kuitumia njia hiyo Yesu alikuwa akilingana na hali yao na jinsi walivyozidikufanya migumu mioyo yao. Aliwaonyesha kiasi kile ambacho waliwezakukiona. Walikuwa na mpaka katika uwezo wao wa kuona. Wakisikiliza kwamoyo wa kweli watakuja kutambua kwamba Ufalme wa Mungu umekuja katikaYeye. Katika jambo hilo kuna ukweli kimsingi nao ni huu: Ufalme wa Munguhauonekani kwa macho ya kibinadamu, ni siri ambayo hutambulikana kwaimani. Kwanza mtu ajikabidhi kwa Kristo ndipo atajua, imani hutangulia kujua(Yn.7:17). Hali ya kusikia, na kusikiliza, hutawala matokeo. (Mit.25:2) Munguhuificha siri ya Ufalme kwa sababu wanadamu hawana hali ya utambuzi wakujua Yesu ameuleta huo Ufalme wa Mungu nao wamepaswa kujihusisha naye.Yesu ni ‘mfano’ ambao Mungu alitumia ili ajifunue kwetu ‘Neno alifanyika mwili,akakaa nasi, nasi tukauona utukufu wake’ (Yn.1:14).Alipotaja unabii wa Isaya Yesu alifananisha wakati wake na wakati wa NabiiIsaya, watu walipokuwa wakimwasi Mungu na kuukataa ujumbe wake.Ijapokuwa watu waliitwa wauamini ujumbe wake wa kutubu, kumbe! ujumbehaukutokeza ile imani iliyotakiwa. Imani si kitu rahisi.

Mtumishi wa Mungu hawezi kuyatawala matokeo ya Injili anayohubiri, sawa namkulima ambaye hana madaraka juu ya vitu vingine vinavyogusa matokeo yamavuno.

4:21-25 Mithali ya Taa na ya Pishi (Mt.5:14-16; 13:12; Lk.8:16-18)Katika mithali hiyo Yesu alieleza jambo la kufunua na wajibu wa kupokeaufunuo. Marko ameweka pamoja mithali kadha ya Yesu ambayo alitumia marakwa mara. Alirudia kusema juu ya kusikia na umuhimu wa kuzingatia

MARKO 169

alivyosema ‘Mwaonaje?’ ni wito wa kutafakari. Alikuwa akisema na akina nani?wale wa k.10 au umati wa watu? hatujui. k.21-22 Tabia ya Mungu na Yesu nikufunua na katika Yesu Mungu amejifunua na kujificha kwa wanadamu. KamaUfalme na Umasihi wa Yesu umefichwa, umefichwa kwa muda tu, na katikaYesu siri hii inazidi kufunuliwa kwa wale wenye kusikiliza kwa makini na kuwatayari kumwamini na kujitoa kwake. ‘Taa huja’ si kawaida kwa taa kuja, kawaidani taa kuletwa. Je! alikuwa akijisemea na kutaja Kuja Kwake kwa usemi huo? Niujinga kabisa kuwasha taa na kuiweka mahali ambapo mwanga wakeumefichwa. Yesu alikuja kumfunua Mungu kusudi watu wamfahamu Mungu najinsi Alivyo na makusudi yake kwa wanadamu. Haina maana kwamba ‘siri’ yaUfalme iendelee kufichwa. Ijapokuwa katika kuitumia mifano Yesu alikuwaameuficha Ufalme wa Mungu na mambo yake, sivyo ilivyo hasa, tabia yaMungu ni kuudhihirisha huo Ufalme, na kama umefichwa, umefichwa kwa mudatu kwa sababu ni wale tu watakaoifungua mioyo yao kwa Neno lakewatakaougundua. Shabaha ya mafundisho yake na miujiza yake ilikuwa kutoamwanga na katika kutoa mwanga watu waliwajibika kuitika vema. Ila nenomuhimu ni kwamba wala mafundisho yenyewe, wala miujiza yenyewe, pekeyake, haitoshi kutokeza itikio jema, bila kuwa na imani ya kuzingatia nakutambua, hayo yamebaki mafundisho na miujiza tu. Yesu alikuwaameishawapa wanafunzi wake siri ya Ufalme nao wameipokea naowataitangaza. Imefichwa ili ijulikane mbeleni, tazama maneno ‘ila makusudi’yametaja mara mbili. Kuficha hutangulia kudhihirisha. Yahusu uwezo wa mtukusikia ‘mtu akiwa na masikio’. Hata wanafunzi ambao ufahamu wao ulikuwabado haujakamilika watafunuliwa zaidi na zaidi yale ambayo kwa wakati ulewalikuwa wameshindwa kuelewa.

k.24-25 Yesu aliendelea kwa kusema ‘angalieni msikialo’ kwa sababuwaliyoambiwa yalikuwa muhimu sana na wasikilizaji walipaswa watege masikioili wasikie sawasawa. Mara nyingi watu husikia yale tu wanayotaka kuyasikia,wala si yale yanayosemwa hasa. Kipimo ni kipimo gani? ni kipimo cha kusikiavema. Mtu atakayetega masikio na kusikia vizuri na kuyatia maanani yaleanayosikia, basi huyo mtu atazidi kuelewa na kukua katika ufahamu wake.Ataweza kupokea zaidi na zaidi. Itikio jema kwa kweli ni msingi katika kujuazaidi. Kipimo cha utambuzi kinalingana na kipimo cha usikilizaji mwema. Mtuhupata kulingana na nia yake. Wale waliokuja kumsikiliza Yesu bila shabaha yakujitoa Kwake waliondoka mikono mitupu, na wale waliokuja wenye nia yakujifunza Kwake walibarikiwa na ufahamu wao wa kiroho ulipanuka. Ni jambolinalohusu wakati wa kusikia ‘mwenye kitu’. Twakumbushwa mfano wa mpanzi,ujumbe ulikuwa mmoja kwa wote, ila udongo uliopokea ujumbe ulikuwa tofautitofauti. Yesu alisema ‘ombeni nanyi mtapata; tafuteni nanyi mtaona, bisheninanyi mtafunguliwa’ (Mt.7:7).

Zaidi ya kusikia vema liko jambo la kuhusu wale ambao hawakusikia vizuri,ambao hawakujali yaliyosemwa na kuyaona si kitu kwao. Kwa hali yaowalikosa kupokea zaidi. Hata yale waliyodhani kuwa nayo waliyapoteza. Ni

MARKO170

mfano wa mtu asiyetumia viungo vya mwili wake. Asipoutumia mkono, mkonoutadhoofika. Dhamiri za wengine zimekufa ganzi kwa sababu wamezoeakutokujali sauti yake. Hivyo Yesu alisisitiza umuhimu wa itikio la mtu.Wanadamu hupewa nafasi ya kuchagua. Injili inapohubiriwa ni wakati na nafasiya kuokolewa au kupotea. Mwishoni hali ya yule mtu asiyejali ni mbaya kulikohali yake ya kwanza. Yesu aliwawaza watu kuwa wasikilizaji. Wakimpa masikioYeye atawajalia kujua siri za Ufalme wa Mungu. Wasiompa masikiowatanyimwa ujuzi huo. Kwa hiyo, mbele za wanadamu ipo nafasi ya faida auhasara. Wanafunzi ingawa walikuwa na udhaifu mbalimbali walikuwawamempokea Yesu na kuendelea naye, wote isipokuwa Yuda.

4:26-29 Mfano wa mbeguMfano huu hupatikana katika Injili ya Marko tu. Yesu alitafuta jambo la kawaidakatika maisha ya watu ili awafundishe ukweli uliohusu Ufalme wa Mungu.

k.26ku. ‘Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama..’ Ni sawa na kusema hii ndiyonjia ambayo kwayo Mungu hutekeleza makusudi yake kwa ulimwengu. Munguni Mfalme, naye anashika utawala, na hii ndiyo njia mojawapo ya kutawalaKwake. Hivyo, alifananisha njia kuwa ile ya mbegu iliyo na uhai ndani yake.Mbegu inao uwezo wa kuota na kumea na kukua na kupevuka, kisha kuzaa. Nikama inajiendea kwa sababu Mungu ameweka kanuni hiyo na uwezo huo ndaniyake. Ndivyo ilivyo kwa Ufalme wa Mungu. Kazi ya mwanadamu ni kupandambegu, yaani Neno la Mungu, na hilo Neno la Mungu linao uwezo wa kuzaamatunda.

k.27 Ukuaji wake ni fumbo kwa wanadamu, inaonekana kwamba mtu hana lakufanya. Mfano hausemi juu ya kulima, kupalalia, kutia mbolea, wala hausemijuu ya vidudu na ndege na wanyama waharibifu, wala habari za ukosefu auwingi wa mvua. Haina maana kwamba hakuna kupalia na kutia mbolea n.k.neno linalosisitizwa ni uwezo uliomo katika mbegu si uwezo alio nao mtu. ‘Mtuhulala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua,asivyojua yeye’. Uwezo umekaa katika mbegu si katika mkulima. Wanadamuwatalima na kupalalia na kutoa magugu n.k. ila liko jambo moja ambalohawawezi kulifanya nalo ni hili la kuipa mbegu uhai. Uwezo huo ni katikambegu si katika mwanadamu ‘asivyojua yeye’.

k.28 ‘maana nchi huzaa yenyewe’ Mfano huo ulitolewa baada ya ule wampanzi uliosisitiza hali ya udongo. Pengine wanafunzi walikata tamaawalipofikiri juu ya hali tatu za udongo zipokeazo mbegu na mfano huo wambegu na uwezo wake uliwatumainisha kwamba, kwa siri, pasipo kutambulika,mbegu ilikuwa ikiota na kumea nayo itatokeza mavuno. Hivyo, wasipimemambo kwa yale yanayoonekana tu. Wapaswa kusubiri katika tumaini la kupatamavuno.Hasa ni Mungu anayetawala mambo hayo, Mungu hakomi kufanya kazi. Uzimawote wa mimea na wa wanadamu hutoka kwa Mungu. Mwenendo wa mbegu

MARKO 171

hauonekani wazi, twakuta mbegu imeota, hatukuona ikiota; twakuta mmea bilakuona ukimea; twakuta mmea umekua bila kuona ukikua. Mwujiza hufanyikakwa siri na kwa kimya na bila msaada wa wanadamu. Kwa hiyo Ufalme waMungu umekuja katika Yesu, nao hukua sirini, kwa sababu ni Munguanayefanya kazi mioyoni mwa wanadamu. Jambo hilo lahitaji imani ililitambulike. Wanafunzi, wala sisi wafuasi wa Kristo wakati huo, hatuwezikuuleta huo Ufalme. Wajibu wetu ni kulisikiliza Neno lake na kuwahubiriwengine habari zake na Mungu ataangalia mengineyo (Lk.17:20; Isa,55:11).Hatuwezi kutawala kazi ya Mungu, twapaswa kuwa wanyenyekevu na kuifanyahali tukijua yote hutegemea kwamba Yeye atatutumia kwa jinsi apendavyoYeye.Habari hiyo ilikuwa kinyume cha mawazo ya Wayahudi waliodhani kwambaMungu atatenda makuu na kuleta Ufalme wake kwa nguvu na kwa wazi.Kumbe Yesu alikuja kwa kuzaliwa kibinadamu na wazazi waliokuwa na hali yachini, aliishi katika kijiji kisichokuwa na sifa yoyote, wala hakuelimishwa katikamashule ya Marabi. Aliwaita wavuvi wa samaki, mtoza ushuru, n.k. wawewanafunzi wake. Alitembea huko na huko, alisikia uchovu, alisikia njaa, aliishibila makuu, hakutaka kutumikiwa bali kutumika. Ila siri kubwa ilikuwa kwambakatika Yeye Ufalme wa Mungu ulikuwa umeletwa karibu na wanadamu (Mt.3:2;4:17).

k.29 Jambo la mwisho kuhusu mbegu iliyopandwa ni kuiva kwake na mavunokupatikana. Ufalme wa Mungu utashinda, uovu wote utaangamizwa na siku yamwisho, siku ya hukumu, ngano italetwa ghalani. Haidhuru inavyoonekana kwamacho ya kibinadamu upo uhakika wa ushindi (Yoe.3:13; Yak.5:7-8). Mbeguilipandwa kwa lengo moja tu, la kupata mavuno, na uhakika wa mavunokupatikana ni katika uwezo wa mbegu iliyopandwa, uwezo ambao ulitoka kwaMungu Mwenyewe. Kutangazwa kwa Neno la Mungu kwasababisha mavuno(Ebr.4:12; Isa.55:10-11).

4:30-32 Mfano wa punje ya haradali (Mt.13:31-31; Lk.13:18-19)k.30 Yesu alitaka kuwafundisha jambo jingine kuhusu Ufalme wa Mungu naalianza kwa kuuliza swali ‘tuulinganishe na nini Ufalme wa Mungu?’. Alitafutanjia ya kujihusisha na watu akitumia jambo walilofahamu na kuwafundishajambo ambalo hawakulifahamu. Alitumia tena jambo la mbegu, punje yaharadali.

k.31 Punje ya haradali ilikuwa mbegu ndogo sana hasa ilipolinganishwa nammea mkubwa uliotokea kama mti wenye matawi imara ya kubeba ndege.Wayahudi walizoea kusema ‘kama punje ya haradali’ walipotaka kusisitizaudogo wa kitu fulani.

k.32 Jambo kubwa ni tofauti kati ya udogo wa punje hiyo na ukubwa wa mtiunaotokea wa kama futi 8-12. Fundisho lake ni kwamba ijapokuwa chanzo chaUfalme wa Mungu chaonekana kuwa kidogo, mfano wa punje ya haradali,

MARKO172

mwisho wake utakuwa mkubwa. Utatoa kivuli kwa ndege; pengine Yesualikuwa akidokezea kwamba hata WaMataifa watakaribishwa katika Ufalme waMungu. Mti uliopandwa na Mungu umetajwa katika Agano la Kale (Zab.104:12;Dan.4:12,21; Eze.17:23; 31:6). Chanzo cha Ufalme ni katika Kuja kwa Yesuambaye hakuonekana kama Mfalme, hakuwa na fahari ya Kifalme, hakuwa namakuu, watu walisikia uhuru wa kumwendea na kutoa maoni yao na Yeyehakuona shida katika kuishi kati ya watu na kujihusisha na watu wa kila aina.Hakutumia umati wa malaika kumsaidia bali aliwaita na kuwawezesha watukama Simoni na Andrea, Mathayo na Yakobo. Hakutegemea silaha za upangana mikuki bali silaha zake zilikuwa upendo na Neno lake. Lakini mwishoutakuwa nini? Mwisho ni mti mkubwa, yaani Ufalme wake utakuwa na watuwengi kutoka pande zote za dunia; wadogo kwa wakubwa, maskini kwamatajiri, wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa watu wazima. Wote watapatahifadhi katika huo Ufalme, watakaribishwa kwenye makao ya milele.

Bila shaka wanafunzi walikata tamaa walipoona jinsi ambavyo wakuuhawakumjali Yesu, huku wao wenyewe hawakuwa na sauti na uwezo katikauongozi wa nchi. Watawezaje kubadili taratibu zilizopo na kusimamisha utawalampya. Wao pamoja na watu walitazamia kwamba Ufalme wa Mungu utakujakwa nguvu na kwa kuonekana wazi kabisa, watu wakitiishwa na nguvu yake, sikama punje ya haradali. Ila walipaswa wawe na subira na ufahamu, wajuekwamba ijapokuwa chanzo chake ni kidogo, hata hivyo, mwisho wake nimkubwa. Katika punje ya haradali umo uwezo wa kutosha kuleta mabadiliko,ila imani huhitajika ili watu watambue kwamba Ufalme wa Mungu umeishafikakatika Yesu. Hata leo watu hutazama Kanisa na kuliona kama kitu hafifu, hatahivyo, mpaka leo watu wangali wanaendelea kumwamini na kumfuata Kristokwa uaminifu.

4:33-34 Kutumia mifanoMarko amesema mambo mawili kuhusu mifano. Moja ni kwamba Yesu alisemamifano mingi, na ya pili ni kwamba yeye alichagua baadhi yake tu na kutoahabari zake katika Injili hiyo. Mifano ilikuwa kwa wote, ila maelezo yalikuwa kwawanafunzi wake walipokuwa faraghani. Kwa njia hiyo ya kuihifadhi ‘siri’ yaUfalme wake akiwanyima umati wa watu kweli zenyewe ilionekana kwambaYesu hakutaka waelewe. Lakini sivyo ilivyokuwa maana Marko amesemakwamba Yesu alitumia mifano kulingana na uwezo wa wasikilizaji. Ni kama njiaambayo kwayo huenda baadhi ya watu watakuja kumwamini. Yesu aliona njiahii ilifaa kwa wakati ule na kupatana na hali yao. Iliwapa watu nafasi yakuzingatia alivyosema, badala ya kuwavamia na kuwatisha, hasa, kwa sababumawazo yao kuhusu Ufalme wa Mungu yalihitilafiana sana na jinsi Ufalmeulivyo hasa. Ilikuwa njia ya kutikisa mawazo yao ili waanze kuwaza kwa upyajuu ya Ufalme wa Mungu. Pamoja na hayo ilidhihirisha upungufu wa uwezowao wa kupokea kweli moja kwa moja bila mfano.

MARKO 173

k.34 Haina maana kwamba wakati wote Yesu alifundisha kwa njia hiyo tu ilailikuwa kawaida yake kuitumia mifano. Ndipo wanafunzi walipokuwa peke yaopamoja naye aliwafafanulia maana ya mambo hayo na kusema zaidi juu yaUtume wake, kwa sababu, hata hao nao hawakuelewa yote aliyoyasema ilawalikuwa wamejitoa kumfuata. Yawezekana hata wanafunzi walikuwa zaidi yaMitume, pengine wale waliotajwa katika k.10 ambao pia walitaka kujua zaidi.Twajifunza kwamba ufahamu wa Ujumbe wa Mungu na Utume wa Yesu unazidikwa wale wanaojihusisha na Yesu na kushirikiana naye kibinafsi.

4:35-41 Yesu alituliza dhoruba (Mt.8:24-27; Lk.8:22-25)k.35-37 Yesu alikuwa ametumika sana mchana wote, akifundisha watu kwamifano, ndipo baadaye aliifafanua kwa wanafunzi wake. Kufika jioni alikuwaamechoka sana, hivyo, aliwashauri wanafunzi waende naye mpaka ng’ambo yaZiwa, mbali na watu. Pengine wanafunzi waliwaaga watu, na bila kukawia,walimtii Yesu na kuondoka jinsi walivyo. Hawakuwa na haja ya kutafutachombo kwa sababu alikuwa amehubiri kutoka chomboni. Hatujui ni akina naniwaliokuwa katika vyombo vingine. Twaona kwamba Marko ametaja kwa usahihiwakati Yesu alipowaambia wavuke ng’ambo, kwa sababu alitaka kuunganishamambo mawili, Yesu kufundisha, na Yesu kufanya miujiza. Amefuata habari zamifano yake na habari za miujiza yake. Matendo makuu ya Yesu yalithibitishamaneno yake na kuwa ishara ya Uungu wake, na changamoto kwa watukumwamini. Miujiza ilimshuhudia Yesu kuwa Mwana wa Mungu. (Markoametaja miujiza 20 pamoja na kujumlisha kutoa pepo na kuponya wagonjwawengi 1:32-34; 3:7-12; 6:53-55).

k.37 Bahari ya Galilaya ilijulikana sana kwa jinsi dhoruba ilivyoweza kutokeaghafula. Milima imezunguka Ziwa ambalo limekaa chini kama bakuli. Pepozivumapo zapita kati ya milima kwa kasi na kushuka juu ya maji kwa nguvu nakukosa njia ya kupitia. Inaonekana dhoruba hiyo ilitokea ghafula na ilikuwa kalikiasi cha maji kuanza kujaa chombo. Tukumbuke baadhi ya wanafunziwalikuwa wavuvi waliozoea bahari hiyo na kujua hatari yake.k.38 Ajabu ni kwamba Yesu alikuwa amelala kwenye sehemu ya shetri, nakuweka kichwa chake kwenye mto (kiti cha ngozi au mbao) na hata dhorubahaikumwamsha. Alikuwa amechoka sana, dalili ya ubinadamu wake wa kweli.Alihitaji kulala, alihitaji kula, kama wanadamu wengine. Katika hofu yao yakuangamia walimwendea na kumwamsha na kwa jinsi walivyosema ni kamawalimkemea. Waliona kwamba hakujali kwamba wanaangamia, labdawalishangaa kwamba hata Yeye hakujali hiyo hatari ya kuangamia. Kamawakizama si wote wataangamizwa? Walikuwa hatarini maana walisematunaangamia, si tutaangamia. Ni kama Yesu amekosa kuwapenda. Penginewaliwaza kwamba ni Yesu aliyewaingiza katika hatari hiyo kwa sababuwaliondoka kwa shauri lake. Huenda walitazamia kwamba watakuwa salamakwa sababu wamemtii Yesu. (zamani Yona alikuwa katika hatari ila ilikuwa kwasababu alikuwa amemwasi Mungu na shauri lake).

MARKO174

k.39 Itikio la Yesu lilikuwa kuukemea upepo na kuinyamazisha bahari. Alisemanavyo kama ni vitu hai na neno lililotumika kwa kukemea ni lile alilotumiaalipomkemea pepo (1:25). Mara upepo ulikoma na mawimbi ya bahari yalitulia,kukawa shwari kuu. Mara na kwa ghafula mabadiliko makubwa yalitokeakufuatana na agizo la Yesu. Katika Agano la Kale neno la utawala wa MunguMwumbaji juu ya uumbaji wake limesisitizwa (Ayu.38:8-11; Zab.107:23-32).

k.40 Kama kwa hali ya kuwakemea Yesu aliwauliza wanafunzi sababu ya hofuyao. Kwani aliwauliza hivyo? maana walikuwa hatarini kweli na si ajabu wasikiehofu. Yesu aliona kwamba hofu yao haikupatana na kumwamini Yeye, ni kamabado hawajamwamini sawasawa. Imani na hofu si vitu vinavyokwenda pamoja.Ilitosha Yeye awe nao chomboni, maana Yeye ndiye mwenye uwezo naupendo wa kutosha kuwaokoa. Ijapokuwa wamekuwa pamoja na Yesu kwamuda na kusikia na kuona mengi wangali na imani haba. Haina maana kwambahawakuwa na imani yoyote. Kwa upande wake ilikuwa haki alale. Ajabu nikwamba Yesu aliweza kulala huku chombo kilikuwa kikiyumbayumba majini.Wao walitaka Yesu afanye neno; Yesu alitaka wao wamtegemee. Kutegemeani kiini cha ufuasi, ilitosha Yeye awepo tu.

k.41 Walikuwa na hofu kwa ajili ya dhoruba, sasa walikuwa na hofu kuu kwasababu ya maneno ya Yesu kwao. Yesu alikuwa amefanya yale ambayoMungu peke yake Aweza kufanya. Walishangaa kwa ufunuo mpya wamadaraka na uwezo wa Yesu juu ya viumbe vya asili, upepo na bahari. Muhuriulitiwa kwenye mamlaka yake na katika kuendelea kushirikiana nayehawakuweza kusahau hilo jambo lililowapata jioni ile.

Neno ‘msiogope’ limesisitizwa zaidi ya neno lingine lolote katika Biblia, katikaAgano la Kale na katika Agano Jipya. Mara kwa mara Wakristo wameelekezwamatazamio, mafanikio, msisimuko, maendeleo n.k. katika maisha ya Kikristo, ilahayo si malengo ya kweli. Yatosha Kristo awe nasi katika safari yetu ya kwendambinguni, ambayo ndani yake hutokea mema na mabaya, shida na mafanikio,mambo magumu na mambo mepesi.

5:1-20 Yesu alitoa pepo kwa Mgerasi (Mt.8:28-34; Lk.8:26-39)k.1 Katika 4:35 tumeambiwa kwamba Yesu na wanafunzi waliondoka nakuvuka Ziwa la Galilaya na baada ya kupigwa na dhoruba wakashuka ng’amboya pili, huenda kusini mashariki, kwenye nchi ya Wagerasi. Walitokewa na mtumwenye pepo (Mathayo wametajwa wawili Mt.8:28) inaonekana aliwajia kwaharaka (k.6). Je! alikuwa ameangalia kwa mbali ilivyotokea wakati wa dhoruba?

k.2-5 Marko ameeleza kwa kirefu habari za huyo mtu na jinsi alivyoteseka.Aliishi katika mapango ya makaburi na milimani mbali na watu, kwa sababuwatu walikuwa wamejaribu kumshika na kumfunga ila haikuwezekana. Kwasababu ya kuonewa na pepo hakutulia; sikuzote, usiku na mchana, alikuwa

MARKO 175

akipiga kelele na kujikatakata. Alijitesa kwa kujikatakata. Hakuvaa nguo (Lk.8.27) na watu waliogopa sana hata hawakupitia njia ile (Mt.8:28). Kwa hiyo,alikuwa mtu wa kuhurumiwa sana. Kwa vyovyote wanadamu walishindwakumsaidia, wamejaribu kumfunga, ikashindikana, hivyo, wakamfukuza mbali iliaishi peke yake.

k.6 Hapo twakuta jambo la ajabu sana, alipomwona Yesu kwa mbali, alivutwakuja Kwake, akaja kwa mbio, akamsujudia. Ni vigumu kujua maana ya‘kumsujudia’ Je! alimwabudu kama Mwana wa Mungu, au alimwinamia kwakumheshimu tu? ni vigumu kujua. Hakuja kwa Yesu katika tumaini bali kwahofu. Je! alikuja mbio ili amdhuru Yesu? hilo nalo hatujui. Hapo Yesuamekabiliwa na nguvu kubwa ya kiroho ya uovu, itakuwaje? Ijapokuwa watuwalikuwa wazito wa kumtambua Yesu, pepo walimtambua mara (Yak.2:9).k.7-8 Je! maneno hayo ni ya pepo au ya yule mwenye pepo au ya wote wawilihali pepo amemtawala? Alimwita Yesu ‘Mwana wa Mungu aliye Juu’. Alitakakujua upo uhusiano gani kati yake na Yesu kwa sababu Yesu alikuwaamemwagiza pepo amtoke. Je! alitaka Yesu amfanyie kama ambavyo Munguanawafanyia, yaani, kutokuwaangamiza kabla ya siku ya mwisho ili waendeleekuishi kwa sasa (Mt.8:29 Je! umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?). Ni wazikwamba pepo alifahamu kwamba kwa vyovyote atatolewa, lakini swali ni‘atakwenda wapi?’

k.9 Je! Yesu alimwuliza jina lake, yule mtu au pepo? Ikiwa ni yule mtu Je!alilenga nini? Je! Yesu alikuwa na shabaha ya kumsaidia yule mtu autambueubinafsi wake na kutambua hali yake mbaya ya kutawaliwa na pepo ili atamanikuwekwa uhuru. Ila aliyemjibu Yesu ni pepo akitamka jina lake kuwaLegioni/Jeshi kwa sababu walikuwa wengi. Hapo twajifunza jinsi sura ya Mungukatika huyo mtu na hali ya ubinadamu wake zilivyopotoshwa kiasi cha pepokusema kwa njia yake.

k.10-13 Mbele ya Yesu yule pepo mwenye jina la Jeshi alijua kwa hakikakwamba itamlazimu amtoke yule mtu kwa sababu ya madaraka aliyo nayoYesu juu yake. Hivyo alifanya patano na Yesu juu ya mahali pa kwenda,akamsihi sana asiwapeleke mbali na nje ya nchi ile na eneo walilozoea. Nikama mmoja alisema kwa niaba ya wote. Inaonekana pepo wapenda kujisitirindani ya mtu au mnyama au mti, hawataki kuwa bila ‘sitara’. Pepo wako tayarikuachana na yule mtu na kwenda penginepo nao wote wakamwombaawaruhusu kuingia kundi la nguruwe waliokuwa wakilisha mlimani, wakitakakujisitiri ndani yao. Walikuwa ng’ambo ya Ziwa, eneo lililoitwa Dekapoli, maanayake, Miji 10, tisa ilikuwa ng’ambo ile na mmoja tu ng’ambo ya magharibi. Hapowaliishi WaMataifa wengi. Ilikuwa mwiko kwa Wayahudi kufuga nguruwe nakula nyama yake, kwa hiyo, ama wenye nguruwe walikuwa WaMataifa, auwalikuwa Wayahudi wasiojali masharti ya dini yao. Pepo walipoingia kwenyenguruwe, kundi lote walitelemka kwa kasi na kufa baharini, hesabu yao kama

MARKO176

elfu mbili, wengi sana. Hasara kubwa sana. Labda pepo waliwaingia kwa nguvuna kelele na kuwashtua na kwa sababu walikuwa kwenye mtelemkowalipokimbia hawakuweza kujizuia wasiingie majini.

Ni vigumu kufikiri kwamba Yesu alikusudia kuleta hasara ya nguruwe kwa haowatu? Ni vigumu kufikiri kwamba ikiwa hao nguruwe walikuwa mali yaWayahudi ilikuwa njia yake ya kuwaadhibu kwa uasi wao. Hasara hiyo ilitokeakwa bahati mbaya katika kumletea mwanadamu mmoja baraka kubwa yakuwekwa uhuru mbali na pepo, watesi wake. Mambo mengine hayana haki yakuuzuia ukombozi wa mtu. Kwa kuona yaliyowapata nguruwe yule mtualihakikishiwa kabisa kwamba pepo wamemtoka na kupotea, vilevile wenyejinao walijua hakuna sababu ya kumhofu tena.

k.14ku. Wachungaji wa nguruwe walikimbia na kuwaambia watu habari hiyo nawatu walikwenda pale ili wao wenyewe waone jinsi mambo yalivyokuwa.Walimkuta Yesu angalipo pale pamoja na yule mtu. Kumbe! hali yake yule mtuimebadilika kabisa; ametulia kabisa, ameketi, wala halii, walahazungukizunguki, wala hajikatikati. Tena amevaa nguo, badala ya kuwa uchi.Pia ana akili timamu. Hali zake zote zilitofautiana sana na wakati alipokuwa napepo. Walijua hakika kwamba pepo amemtoka na wao wako salama, wawezakupitia njia ile bila wasiwasi, wala hawana haja ya kujaribu kumfunga tena.Aweza kurudi nyumbani na kuishi kati yao bila shida.

k.16ku. Lakini kwa upande wao shida ilikuwa kupotea kwa mali yao. Waliifikiriahasara ya nguruwe kuliko faida ya mwenzao ambaye sasa yu mzima. Nivigumu kujua kwa nini walimsihi Yesu aondoke mipakani mwao? Je! walikuwana wasiwasi na kufikiri kwamba Yesu atafanya nini zaidi akikaa nao? Ila, Je!ataleta baraka nyingi kama alivyofanya kwa yule mtu? Wanadamu sikuzotehusikia shida wakipata hasara ya mali kwa ajili ya usalama wa mwanadamumwenzao. Katika ulimwengu wa sasa yapo maswala makubwa kuhusumakampuni yanayochafua hali ya hewa katika kuendeleza biashara yao; auwale wakatao misitu ya wenyeji kwa faida yao bila kuwaza wenyeji na maishayao. Mara nyingine wafanyakazi hupatwa na afya mbaya kwa sababu waajiriwao hawajali hali nzuri kuhusu kazi wanazofanya.

k.18ku. Yesu hakukaa pale, hakuona vema akae mahali asipotakiwa. Ilahasara ni kwa wale wanaoachwa, si kwake. Yeye ataendelea mahali penginena kuhubiri habari njema na kuwaponya watu na kutoa pepo. Yule aliyetolewapepo alionyesha nia tofauti na wenyeji wenzake, yeye aliomba awe pamoja naYesu. Ila Yesu hakumruhusu, alitaka arudi nyumbani na kuwaambia watuhabari za rehema za Bwana na jinsi alivyotendewa na Bwana. Alimtii Yesu, nakatika eneo lote la Dekapoli aliwaambia watu habari hizo. Kwa hiyo Yesualiwaachia wale waliomkataa shahidi wa kuwakumbusha habari zake. Yule mtualirudi kwa jamaa yake na kujihusisha nao tena. Kwa nini Yesu ambaye kwadesturi aliagiza watu wasitangaze habari zake lakini kwa huyo alimwagiza

MARKO 177

azitangaze? Huenda sababu yake ni kwamba angetoa ushuhuda mahali paWaMataifa wengi ambao hawakuwa na mawazo yaliyopotofu juu ya Masihi nautume wake. WaMataifa wangesikia habari kutoka mmoja wao ambayeameonja nguvu za Yesu maishani mwake, mtu ambaye amemtambua Yesuvizuri.

Tumeona kwamba hata uponyaji wa ajabu wa huyo mtu haikutokeza imanikatika watu, wala miujiza peke yake haikusababisha imani. Budi watuwatazame nyuma ya tendo lenyewe kwa yule mtendaji wake. (Mara kwa maraMarko alitaja habari za pepo 1:23ku.32,34; 3:11-12,15,22-30).

5:21-43 Kuponywa kwa mwanamke mgonjwa na kufufuliwa kwa bintiYairo (Mt.9:18-26; Lk.8:40-56)

Mambo hayo mawili yameingiliana, habari inaanza na Yairo kuja kwa BwanaYesu, halafu, njiani wakati wa kwenda mwanamke mgonjwa alipitapita kati yaumati wa watu na kuyagusa mavazi ya Yesu, akaponywa. Ndipo baada yakuzungumza naye Yesu aliendelea na safari mpaka nyumba ya Yairo nakumrudishia uhai wake binti yake ambaye alikuwa amekufa.

k.21-24 Yesu na wanafunzi walivuka bahari na kurudi ng’ambo ya magharibi,huenda karibu na Kapernaumu. Walipopata habari kwamba ameisharudi watuwengi walimjia. Ndipo akaja mkuu mmoja wa sinagogi aliyewajibika kuangaliataratibu za ibada na maadili ya dini. Alikuwa mheshimiwa kati ya jamii na mtualiyejulikana sana. Kwa kawaida hao hawakumpenda Bwana Yesu kwa vilealivyoonekana anakwenda kinyume cha mapokeo yao juu ya Sabato n.k. Bilashaka amewahi kumwona Yesu na kumsikiliza, pengine alikuwapoalipowaponya watu. Alikuwa na binti mmoja tu (Lk.8:42) wa miaka kumi namiwili ambaye alimpenda sana. Huyo binti aliugua na hali yake ilizidi kuwambaya. Yairo aliamini kwamba Yesu ataweza kumponya, hivyo, akamwendeana kwa heshima sana akaanguka miguuni pake na kumsihi sana aende pamojanaye mpaka nyumbani. Yesu akakubali, alikuwa tayari kuacha mipango yakena shughuli zake kati ya umati wa watu ili amhudumie huyo ambaye alikuwakatika kundi la watu waliokuwa kinyume chake. Hapo habari ya Yairo imeachwampaka k.35.

25-34 Katika umati wa watu waliomfuata Yesu, na wanafunzi, na Yairo,alikuwemo mwanamke mmoja mwenye shida ambayo imemsumbua kwa miakakumi na miwili. Alikuwa amejaribu matibabu mbalimbali mpaka amemaliza maliyake, na hata hivyo, hali yake badala ya kupata nafuu, ilizidi kuwa mbaya.Ugonjwa wa kutoka damu ulimfanya awe najisi machoni pa sheria(Law.15:19ku). Ilimbidi ajitenge na watu, kwa hiyo, kwa muda mwingi hakuwana uhuru wa kushirikiana vizuri na watu. Aliposikia kwamba Yesu alikuwaakipita akajiunga na umati wa watu waliomsonga, akaja kwa nyuma akamfikiaYesu na kuyagusa mavazi yake. Alikuwa na imani kwamba akiyagusa mavazi

MARKO178

yake tu itatosha, atapona. Imani yake haikuwa katika mavazi ya Yesu balikatika Yesu Mwenyewe, hakufanya jaribio, maana alisema moyoni mwakekwamba ‘nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona’. Kwa nini aje nyuma ya Yesu?hatujui. Pengine alisikia haya kwa ajili ya hali yake; labda hakutaka kuuvutausikivu wa watu, huenda hakutaka kumchelewesha Yesu katika safari yake.

k.29 Akapona mara, tena kabisa, hata mwilini alisikia afya nzuri, damu yakeimekauka, na hakusikia kama alivyokuwa amejisikia kwa miaka kumi na miwiliya hapo nyuma.

k.30 Yesu alisikiaje? na alifanyaje? Alifahamu kwamba nguvu zilikuwazimemtoka. Yesu alikuwa ameitikia imani yake na kutoa nguvu mpaka mwili wahuyo mama na kumponya. Ijapokuwa alisongwa na umati wa watu waliompashida ya kwenda alijua miongoni mwao yumo mmoja ambaye amemgusa kwakusudi maalumu. Hivyo, akauliza swali ‘Ni nani aliyeyagusa mavazi yangu?’akageuka na kutupia macho kwenye umati wa watu ili amwone huyoaliyemgusa. Alitaka kumwona, si kwa shabaha ya kumkemea, bali kwashabaha njema ya kumkaribisha Kwake na kujenga uhusiano naye nakumrudisha kwenye jamii ya watu, ili azidi kupata baraka za amani na uzima.Wanafunzi waliona swali la Yesu kuwa upuzi, kwa sababu ya watu wengiwaliomsonga na kumgusa, shida yao ilikuwa kuchukua maneno yake yalivyo.Yesu alitaka kujua ni nani ambaye alimgusa kwa kusudi na kwa kutakamsaada. Wengi humgusa Yesu kwa juujuu, ila Yesu ajua wale wanaomgusakwa kusudi la kutaka baraka. Alitaka kukutana naye ili azungumze naye.

k.33 Yule mwanamke aliogopa na kutetemeka, akijua hakika ni yeyealiyemgusa naye alikuwa najisi. Haikuwa rahisi ajitokeze wazi mbele za umatiwa watu, ila Yesu alitaka kumpa baraka nyingine. Kisha akaja na kumwangukiana kumwelezea mambo yake yote. Yesu akafanyaje? Akamwita ‘binti’akijihusisha naye kwa upendo na kwa kumrudisha kwenye jamii ya watu. Tanguhapo alisikia uhuru wa kushirikiana na wenzake bila shida, unajisi wakeumeondoka mara ugonjwa wake ulipoponywa. Yesu aliendelea kusemakwamba ‘imani yako imekuponya’. Ni nguvu za Yesu zilizomponya lakini mferejiwa kuzileta mwilini mwake ulikuwa imani yake. Yesu alijua kwamba aligusa kwaimani ya kweli, hata akawa tayari kuondoka bila kusema naye. ‘enenda zakokwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena’ ndipo Yesuakamwongezea baraka za amani na uzima na kumhakikishia kwambahataugua tena ugonjwa ule. Twajifunza kwamba katika umati wa watu Yesu yutayari kumshughulikia mmoja tu mwenye shida amtazamaye kwa imani. Ilikuwawajibu wa huyo mama kumtukuza Yesu na kumshukuru (Zab.50:15;Lk.17:17,18). Bila shaka wakati huo wote Yairo alizidi kuwa na wasiwasi juu yabinti yake, ila kwa kumwona huyo mama na jinsi Yesu alivyomtendea, bilashaka imani yake ilijengwa. Pengine hii ndiyo sababu mojawapo ya Yesukusimama na kufanya huyo mama ajitokeze wazi ili Yairo asikie habari zake.Yesu hakusema lolote juu ya nguvu zake na upendo wake.

MARKO 179

k.35ku Hapo twarudia habari za Yairo. Imani ya Yairo ilijaribiwa sana kwa jinsiwalivyochelewa kufika nyumbani. Ndipo habari mbaya ilimfikia kusema kwambabinti yake ameishafariki dunia. Kwa hiyo, wamechelewa kabisa. Hakuna lakufanya. Kama Yesu hakusikia, au kama alichagua kutokujali, hatujui, ilaalimwambia Yairo asiogope, aendelee kuamini. Jambo gumu sana kwa kuwabinti ameishakufa.

k.37 Walipofika nyumbani Yesu hakuwaruhusu watu wamfuate ila wanafunziwatatu, Petro, Yakobo, na Yohana (9:2; 14:33). Walikuta maombolezo yalikuwayameanza, na kama ilivyokuwa desturi yao wapiga filimbi walikuwepo pamojana wale waliofika kushirikiana nao hali wakilia. Kwa hiyo, ilikuwa wazi kwambawote waliamini kabisa kwamba binti amefariki, maana hakuna anayeanzamatayarisho ya mazishi mpaka mtu amekata roho. Yesu akajaribu kuleta hali yautulivu pale akawauliza ‘Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, baliamelala tu’. Katika kusema hakufa Yesu alikuwa akimaanisha kifo kama Munguanavyokiona na kama Wakristo baadaye walivyokiwaza, ni kulala tu, kwasababu ya uhakika wa kuamka tena katika uzima wa milele (1 The.4:13-14).Lakini watu walijua uhakika wa kufa kwake yule binti, hata wakamcheka Yesusana. (Ni vigumu kucheka wakati wa mazishi!!).

Hata katika ghasia zile Yesu alionyesha madaraka yake, akawatoa wote nje,akawachukua Yairo na mkewe na wale wanafunzi watatu na kuingia mle ndaniya chumba alimolala yule binti. Ni wale wa karibu kabisa ambao wangeonajambo hilo kubwa la kumfufua binti Yairo. Akamshika mkono na kumwambia‘Msichana Inuka’ kumbe! mara moja akasimama na kwenda. Huzuni zao zoteziligeuza kuwa furaha kubwa. Waliocheka, walionaje? twasoma wakashangaamshangao mkuu. Yesu alionyesha uwezo wake juu ya mauti na kutokuaminikwa watu. Mamlaka yake hufika hata ng’ambo ya pili ya mauti.

Kisha akawaonya watu wasitangaze habari hizo. Ndipo akakumbuka yulemsichana, katika furaha zao huenda walikuwa wamesahau kumpa chakula,akawaamuru apewe chakula. Kumpa chakula waliweza ila kumrudishia uhaihawakuweza. Mungu hafanyi yale tuwezayo wenyewe kuyafanya.

6:1-6 Yesu alikataliwa Nazareti (Mt.13:53-59; Lk.4:16:30)

Habari iliyoandikwa katika Luka ina mambo tofauti na ile iliyo katika Mathayo naMarko. Yafikiriwa kwamba habari katika Luka ilitokea kabla ya ile ya Marko naMathayo, na ikiwa hivyo, Yesu alikataliwa pale Nazareti mara mbili.

k.1 Wakati huo wanafunzi walikuwa pamoja naye. Ilikuwa desturi ya Yesukusali katika sinagogi siku ya Sabato. Alijulikana kama rabi na kupewa nafasiya kufundisha, jambo ambalo Marko alipenda kusisitiza.

MARKO180

k.2 Watu walikuwa wengi nao waliposikia mafundisho yake na kujua habari zamiujiza yake, walishangaa sana. Mambo hayo mawili, mafundisho na miujiza,yaliashiria kufika kwa Ufalme wa Mungu. Walikuwa na maswali mawili: (a) Asiliya hekima yake na uwezo wake ‘Huyu ameyapata wapi haya’? na (b) ‘maana’yake ‘Ni nini miujiza hii mikubwa’?. Kila wakati ukweli wa miujiza yakeulikubalika; adui zake hawakuikana wala jamaa na rafiki zake ambaohawakumwamini mpaka baadaye.

Swali lao, kwa upande mmoja, lilikuwa jema; Waandishi na Mafarisayo waliulizahilo swali katika 11:28. Ila upungufu ulikuwa katika shabaha yao, walitaka kujuaasili ya hekima na uwezo wake kuliko kujua kwa nini awe na hekima na uwezohuo. Kuhusu asili, ama amepata kwa Mungu, ama kwa wanadamu, ama kwaShetani/pepo. Jibu ambalo lilikuwa dhahiri ni kwamba amepata kwa Mungu, ilahawakuwa tayari kukiri hivyo. Kwa nini?

k.3 Shida yao ilikuwa walimdharau kwa sababu alikuwa mmoja wao. Alilelewakati yao, jamaa zake waliishi pale, alijulikana na wengi. Alipokuwa kijanaalifanya kazi za mikono. pengine ya seremala ila neno lililotumika ni lile kwa‘fundi’ (babake alikuwa seremala). Waliposema ‘mwana wa Mariamu’ Je!walikuwa wakidokezea kwamba alizaliwa katika zinaa (Yn.8:41) kwa sababundivyo ilivyodhaniwa na wengi. Au, pengine, Yusufu ameishafariki dunia.Yafikiriwa ilikuwa kwa dharau walimwita ‘mwana wa Mariamu’ kwa sababuilikuwa desturi kutumia jina la baba hata ikiwa baba alikuwa amekufa. (bilakukusudia walikuwa wakilinda imani ya Yesu kuzaliwa na bikira). Lakini kwavyovyote hawakuweza kumpokea kama yule rabi ambaye huku nyuma alifanyakazi za mikono kati yao. Pamoja na hayo mama na ndugu zake waliishi palepale, watu walizoea kuwaona na kuzungumza nao n.k. Hivyo, walishindwakumwaza tofauti na hayo waliyoyafahamu kimwili juu yake. Hao nduguwaliotajwa Je! walizaliwa na Mariamu na Yusufu baada ya Yesu kuzaliwa?wengi hufikiri hivyo. La, sivyo, neno ‘ndugu’ limetumika kwa jamaa wa karibu.Ndugu zake hawakumwamini mwanzoni (Yn.7:5) ila baadaye walitajwa kuwepokatika kundi la waumini waliomngojea Roho Mtakatifu (Mdo.1:14) kwa hiyokutokuamini kwao kuligeuzwa kuwa kuamini. Yakobo amejulikana katikahistoria ya Kanisa kuwa kiongozi maarufu wa Kanisa la pale Yerusalemu(Mdo.12:17; 15:13-29; 21:18; 1 Kor.15:7; Gal.1:19; 2:9,12; Yak.1:1)

Amedhaniwa kuwa mwandishi wa Waraka wenye jina hilo. Yuda amedhaniwakuwa mwandishi wa Waraka wa Yuda. Maumbu zake hawakutajwa kwa majina.Kwa kutaja ndugu zake, kila mmoja kwa jina lake, kuliongeza mkanganyikowao. Marko ameishataja wazi jinsi mama na jamaa zake walivyoshindwakumwamini, ila hawakumpinga kama viongozi (3:20-21; 31-35). Swali lao‘ameyapata wapi haya?’ Je! walitaka kuunga mkono wale waliodhani kwambaalifanya kazi kwa uwezo wa enzi za uovu? ila hawakuwa tayari kutamka wazijambo hilo. Yawezekana, ila si lazima tufikiri hivyo, ila wasipokubali amefanyakwa Mungu swali limebaki ‘amefanya kwa nani?’ kwa wanadamu, au vipi?

MARKO 181

Walishindwa kukubali hekima na uwezo wake vilitoka kwa Mungu, na kwasababu hiyo, zaidi ya kutokumwamini na kumkataa, walikwazwa (1 Pet.2:6-8).

k.4 Yesu aliona kwamba hali yao ilikuwa kawaida ya watu, haikuwa hali ngeni(Yn.4:44). Ijapokuwa alikuwa zaidi ya nabii, hata hivyo, walishindwa kumpokeakama nabii, licha ya kuwa Mwana wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu. Yesualikuwa amefikia hatua ya chini sana katika kukataliwa pale Nazareti, na hatawanafunzi wake walishiriki kudhiliwa kwake.

k.5 Yesu hakuwa tayari kufanya uponyaji na miujuza katika hali na hewa yakutokuamini, aliheshimu uhuru wao wa kuchagua kati ya kumwamini nakutokumwamini. Yesu hakuwa mtenda miujiza tu, aliyetumia uwezo wake bilashabaha. Uwezo wake haukuwa na mipaka ila alijiwekea mpaka iliasiwalazimishe kuamini kinyume cha nia yao. Shabaha ya Utume wake ilikuwakuleta watu kwenye uhusiano mwema na Yeye, watu waje Kwake nakujikabidhi kwake. Walikuwa wamekwazwa na ubinadamu wake kwa hiyowalishindwa kujikabidhi kwake kwa hiyo walishindwa kujua ni kwa jinsi ganiMungu anavyosema na kutenda kwa njia yake. Ila kwa wale wachachewaliokuwa tayari kujikabidhi kwake aliwaponya. Ni jambo la ajabu kuonaMwenye uwezo wote kama amepuuzwa kwa sababu Yeye mwenyewe hawitayari kuivunja ile heshima aliyowapa wanadamu ya kuchagua kati yakumwamini au kutokumwamini. Hatawafanya kama mashini, ambayo swichiyake ikibonyezwa mashini hufanya kazi jinsi ilivyotengenezewa kufanya. Sisihatuwi mashini, tu wenye nafsi.

k.6a Itikio la Yesu lilikuwa kustaajabia hali yao ya kutokuamini. Ni katikaMathayo 8:10 na hapo twaambiwa kwamba Yesu alistaajabiwa. Pale katikaMathayo ilikuwa kwa sababu ya kumwamini kulikofanywa na mtu asiyekuwaMyahudi; hapo ni kwa ajili ya kutokuamini kwa watu wa mji wake. Alikuwa nahaki ya kupokelewa kwa ajili ya yote aliyoyafanya katika kufundisha na kuponyakwake. Haikueleweka kwa nini wawe na hali hiyo, maana ilikuwa ujinga mtupukumkataa Yeye mwenye kuleta nuru na uzima.k.6b Hata hivyo, wasingeuzuia Utume wake, ataendelea kuzungukazungukavijijini kwa sababu ilimpasa afanye huduma yake katika mazingara yakutokuamini kwa wengi. Bila shaka wanafunzi wake walipata mafunzomakubwa kwa huduma ya baadaye ambayo Yesu angewakabidhi.

6:7-13 Mitume walitumwa kuhubiri n.k. (Mt.9.35-10:15;Lk.9:1-6)k.7 Neno ‘kuanza’ linaonyesha kwamba hii ni mara ya kwanza mitumewalipotumwa peke yao. Ni wakati wa kuwaingiza katika Utume wake. Ni kamamazoezi, hatua katika kuwaandaa kwa kazi za baadaye. Yesu alitambuakwamba Yeye hawezi kufika kila mahali na kutangaza habari za Kuja kwaUfalme, hivyo, aliwashirikisha hao ambao walikuwa wameshirikiana naye kwamuda, wameyaona matendo yake na kuyasikia mafundisho yake, na faraghaniwameelezwa yale waliyoshindwa kufahamu (4:10,34). Kwa hiyo ilikuwa hatua

MARKO182

ya maana sana Kwa njia hiyo watashirikishwa uwezo wa Kristo na kufanya kazibila Yesu Mwenyewe kuwa pamoja nao kimwili, tayari kwa wakatiatakapowaachia na kurudi kwa Baba. Pamoja na kuwa nafasi ya mazoezi kwaMitume ilikuwa pia nafasi kwa watu wa Galilaya kutangaziwa habari za Kujakwa Ufalme wa Mungu katika Yesu.

Hapo nyuma alipowaita wanafunzi wanne wa kwanza aliwaambia kwambawatakuwa wavuvi wa watu (1:17) na alipowachagua Thenashara alisemaatawatuma kuhubiri na kutoa pepo (3:14). Sasa wakati umefika kwa kutimizaahadi hizo na kuwapa nafasi ya kufanya kazi hizo. Kwa hiyo, hawatafanyamambo mapya, ile yale yale ambayo Yeye aliyafanya, ni kuendeleza hudumayake.

k.7 Aliwatuma wawili wawili, ili wasaidiane na kushirikiana, pia ushuhuda waouwe halali, kwa sababu, katika Israeli kanuni kuhusu ushuhuda ulihitajimapatano ya watu wawili (Kum.17:6, 19:15; Hes.35:30; 2 Kor.13:1). Ndipoakawashirikisha uwezo na mamlaka yake kutoa pepo wachafu na kuwaponyawatu na kuhubiri. Wao wafanye kama Yeye kwa uwezo wake, si kwa uwezowao. Kanisa lilizoea kutuma watu wawili wawili (Mdo.3:1ku. 8:14ku. 11:30;12:25; 14:28; 15:40; 1 Kor.9:6). Ajabu ni kwamba aliwashirikisha uwezo namamlaka yake ingawa walikuwa bado wangali wanafunzi, Yesu alikuwa tayarikuwaamini.

k.8-9 Ndipo aliwapa mwongozo kwa safari yao. Kwa sababu ilikuwa ya mudatu, hawakuhitaji kwenda na vitu vingi. Hali yao yote ionyeshe kwambahawakujitegemea bali walikuwa wakimtegemea Yule aliyewatuma, na yakwamba ujumbe waliouleta ulikuwa muhimu kuliko hali zao binafsi. Wasipotezewakati kwa sababu muda wao ni mfupi, mambo ni muhimu na yenye haraka,kwa hiyo, wasitafute maisha ya raha, mahali pazuri pa kukaa n.k. Waridhike namahali watakapokaribishwa, hata wakikaribishwa mahali pazuri zaidi baadaye,wakae tu. Ni kama kudokezea kwamba watatunzwa. Hawakuwa na haja yakuchukua pesa, au chakula, wala wasiombeombe (mkoba ulitumiwa nawaombaji). Ila ikiwa ujumbe wao unakataliwa budi waondoke, hawana mudakukaa mahali pa upinzani. Iwe dhahiri kwamba wamekuja na ujumbe maalumuwa maana sana.

k.10 Yesu alitazamia kwamba watakaribishwa na kutunzwa na watu. Jambokubwa ni kukaribishwa kama wajumbe si kama wageni. Wasipoteze mudakatika mambo madogo yasiyolenga shabaha yao.

k.11 Yesu alifahamu kwamba watapatwa na yale yaliyompata Yeye,kupokelewa na wengine na kukataliwa na wengine. Wafanye nini watuwatakapowakataa? Aliwaambia kukung’uta mavumbi ya miguu kuwa ushuhudakwao. Nini hii? Kufanya hivyo hakumaanishi kwamba wao wenyewewameudhika. La, ni tendo la ishara la kuonyesha kwamba katika kuwakataa na

MARKO 183

hasa katika kuukataa ujumbe wao watu waliofanya hivyo wamefanya jambo zitona la hatari sana. Wayahudi walizoea kufanya hivyo waliporudi nchi yao baadaya kutoka nchi ya WaMataifa, ni kama kuuondoa unajisi. Huenda kwa njia hiyowatu watachokozwa na kushurutisha kutafakari sana walivyofanya, ili wabadilimawazo yao. Kwa ishara hiyo mgawanyiko ulidhihirika kati ya wale walioaminina wale ambao hawakuamini na kuhesabu wale waliowakataa kuwa sawa nawapagani. Kufanya ishara hiyo kwa Wayahudi wenyewe lilikuwa tendo zitogeni. Tendo hilo lilionyesha kwamba kila mtu aliwajibika kwa itikio lake.

k.12-13 Mitume walikwenda na kufanya kama Yesu alivyowaagiza. Hudumayao ilikuwa na mambo matatu, kuhubiri; kutoa pepo (Jambo ambalo Markoamesisitiza katika Injili yake) na kuwaponya wagonjwa. Kazi kubwa ilikuwakuhubiri. Marko ametaja kwamba wagonjwa walipakwa mafuta (Lk.10:34;Yak.5:14) hatusomi kwamba Yesu aliwapaka watu mafuta, watu hawakuhitajikuhakikishiwa baraka za Mungu wakati wa Yesu kuwepo. Baadaye Kanisalilifuata desturi hiyo. Mafuta yalikuwa dalili ya Roho Mtakatifu. Bila shakakufanya hivyo kulivuta usikivu wa wagonjwa na kuamsha imani ndani yao nakuwahakikishia baraka za Mungu. Waliwaita watu kutubu, kama YohanaMbatizaji alivyofanya (1:4) na kama Yesu alivyofanya (1:15) maana yakewalihubiri kwa shabaha ya kuleta watu kwenye toba, si kwamba kila mahaliwalisema ‘tubuni, tubuni’.

Tusifikiri kwamba watu wa siku hizi wanapokwenda kuhubiri Injili hupaswakufuata kanuni za kwenda bila mahitaji kama pesa na nguo za kubadili n.k. la,sivyo. Kuishi kwa umaskini na kwa kujinyima si kanuni kwa wote ila ni kwawachache wanaofanya kazi zinazohitaji waishi kwa ugumu, pengine wapelekwakatika nchi kadha n.k. Ila wakati wote watumishi wa Injili hupaswa kuonyeshamzigo juu ya kazi zao kwa kutokutanguliza matakwa yao. Wasitafute raha naanasa, wawe radhi na mambo rahisi, wasitake makuu. Thenashara walitakiwakutoa ripoti ya kazi zao kwa Bwana Yesu na inaonekana walifanikiwa katikahuduma yao (6:30).

6:14-29 Mfalme Herode na Kifo cha Yohana Mbatizaji (Mt.14:1ku.Lk.9:7-9)k.14-16 Kwa nini Marko ameingiza habari za kifo cha Mbatizaji iwapo ilikuwaimetokea hapo nyuma. Pengine hakutaka wanafunzi wafikiri kwamba upinzanikwa ujumbe wao wa Ufalme wa Mungu unapoa. Inaonekana kwamba walikuwawamepokelewa vizuri walipokwenda kuhubiri, lakini sivyo itakavyokuwabaadaye. Pia huenda ni njia ya Marko ya kuandaa mawazo tayari kwa kuuawakwa Yesu ambako kungetokea mbeleni. Wakati wote ufuasi wa kweliutapingwa. Kwa hiyo Marko aliingiza habari za kuuawa kwa Yohana na Herode.Habari za huduma ya Yesu na wanafunzi wake zilimfikia Mfalme Herode.Herode alikuwa mwana wa Herode Mkuu, naye alitawala eneo la Galilaya naPerea tangu K.K.4 hadi B.K.39. Ameitwa Mfalme ila alikuwa liwali si Mfalme,Warumi hawakupenda aitwe Mfalme.

MARKO184

Hatuambiwi alikuwa amesikia nini hasa, ila bila shaka alikuwa amesikia habariza matendo makuu ya Yesu na ya wanafunzi wake na jinsi alivyowavuta wengialipozungukazunguka mijini na vijijini Galilaya na kutangaza habari za Ufalmewa Mungu.

k.15 Hapo tumepewa kuona jinsi watu walivyochanganyikiwa katika kumwazaYesu kuwa nani. Wengine walimwona kuwa Eliya. Nabii Malaki alisemakwamba Eliya, mjumbe wa Agano, atakuja kabla ya kuja kwa siku kuu yakuogofya ya Mungu na hukumu yake (Mal.3:1ku. 4:5ku). Wengine walimdhanikuwa nabii mojawapo mfano wa wale waliotokea mara kwa mara katika historiayao. Pengine baadhi walimwaza kuwa yule nabii aliyetabiriwa na Musa(Kum.18:15). Hata baadhi walifikiri kwamba Yohana Mbatizaji ametoka kwawafu na kupewa nguvu mpya. Hayo yote huushuhudia uwezo wa Yesu. Herodealiunga mkono wazo la Yesu kuwa Yohana Mbatizaji kwa sababu dhamiri yakeilimshtaki sana juu ya kumwua. Alikuwa mtu wa ushirikina na kwa sababu hiyo,alidhani kwamba Mbatizaji amerudi kumsumbua. Alijisikia nafsini mwake hatiakwa kifo cha Yohana. Kama hakudhani kwamba Yesu ni Mbatizaji aliyerudikutoka wafu yawezekana alikuwa akimaanisha kwamba katika Yesuamekabiliwa na mtu wa matata anayemsumbua kama Yohana alivyofanya.Yohana Mbatizaji hakufanya miujiza (Yn.10:41). Wale waliojua uhusiano kati yaMbatizaji na Yesu na jinsi Yesu alivyobatizwa na Yohana hawakuweza kufikirihao wawili ni mtu mmoja. Mambo hayo huonyesha jinsi watu walivyoshindwakumwelewa Yesu vizuri, ila kwa jumla, wengi walimwaza kuwa rabi na nabii.

k.17-29 Kwa sababu Marko ametaja habari ya tendo la Herode la kumkatakichwa Mbatizaji aliona vema aingize hapo habari hiyo ambayo tendo lenyewelimeishatendeka muda uliopita. Herode alikuwa amemwacha mke wakealiyekuwa binti wa Mfalme Aretas wa Nabatia na kumchukua Herodia, binti waAristobulus mwana wa Herode Mkuu. Herodia alikuwa mke wa Filipo mwanawa Aristobulus. Jambo hilo lilikatazwa katika Torati (Law.18:16; 20:21). YohanaMbatizaji hakuogopa, kila mara alimwonya Herode juu ya dhambi hiyo na kwasababu hiyo Herode alimfunga gerezani. Yohana alikuwa mnyofu kabisa,hakusita kuwaita wa nyumba ya Mfalme kutubu sawa na wenyeji. Kwa upandemmoja Herode alimstahi Yohana, alimwona kuwa mtu wa haki, mtakatifu, naalijaribu kumlinda. Katika k.19 twasoma Herodia alimvizia ila alikuwa badohajafanikiwa.

Pamoja na hayo Herode alikuwa na hofu ya vita kati yake na WaNabateawaliochukizwa na tendo lake la kumfukuza mke wake. Pengine Herodealimfunga Yohana ili amlinde na hasira ya Herodia aliyejaa chuki ya ndani, ilaHerodia hataridhika mpaka Yohana ameondolewa kabisa. Alijua kwambamaadamu yu hai ipo nafasi kwa Herode kubadili mawazo yake na kumjaliYohana na kumwondoa yeye. Pamoja na hayo Herode alifahamu kwambawenyeji hawakupendezwa na jambo hilo maana walimwona Yohana kuwa nabii(Mt.14:5). Hivyo Herode alivutwa kila upande na katika udhaifu wake alishindwa

MARKO 185

kufanya yale ambayo aliyafahamu kuwa sawa, alivutwa na kumheshimuYohana akitaka kufanya iliyo haki huku alivutwa na mapenzi kwa Herodia nakufanya isiyo haki.

k.21ku Ndipo nafasi kwa Herodia ilitokea. Wakati wa kuadhimisha sikukuu yakuzaliwa kwake, Herode aliandaa karamu kubwa na kuwaita wakubwa nawenye cheo akijivunia fahari yake mbele zao. Katika sherehe hiyo binti waHerodia aliingia na kucheza mbele zao. Je! mama yake alikuwa amemshauriHerode ampe nafasi hiyo? Watu walilewa na kama ilivyo katika karamu zanamna hiyo walivutwa sana na msichana huyo na kufurahiwa na mchezo wake.Herode naye alifurahi sana na kutoa ahadi ya kumpa kitu chochote alichotakahata nusu ya Ufalme (haukuwa wake). Maana yake alimwahidi atatoa kitu kwaukarimu bila kujali gharama yake.

k.24ku Binti alitoka na kumwuliza mama aombe nini? Mara moja mama alijibu‘kichwa cha Yohana Mbatizaji’ ishara ya chuki yake kubwa sana. Yule bintiakaingia kwa haraka na kuomba apewe sasa hivi kichwa cha Yohana katikakombe. Ni ajabu sana, kuona hao wanawake wawili wapatane kabisa nakuomba kitu cha namna hiyo, tena wakione kichwa katika kombe. WalitakaHerode afanye haraka kabla hajapata nafasi ya kutafakari na kubadili uamuziwake na kukataa. Hakuwa na la kufanya kwa sababu alikuwa ametoa ahadimbele za wale wakuu wote, tena kwa kiapo. Itakuwa aibu kubwa wakionaameshindwa kutimiza ahadi yake. Bila shaka alitambua kwamba Herodiaamemdanganya na kwa hila na chuki amembana. Angeweza kutoka katikashida kama angesema kwamba kitu alichoahidi kilikuwa kipawa si tendo ladhambi. Kwa hiyo ahadi yake ya haraka ilimaanishwa kuwa ukarimu na kibalichake kwa ombi la udhalimu lilimaanishwa kuwa uaminifu kwa neno lake. Bintialimtii mama hata katika kufanya dhambi.k.29 Wanafunzi wa Yohana waliozoea kumtembelea gerezani (Mt.11:2) wakajana kuuchukua mwili wake na kuuzika kaburini . Pia walimwarifu Yesu habarihizo (Mt.14:12). Hivyo, twaona gharama ya kuwa mwaminifu na hatari yakuogopa kupatwa na aibu mbele za watu.Ijapokuwa Herode alimwondoa Yohana Mbatizaji hakuweza kumsahau, sautiyake iliendelea kumshtaki katika dhamiri yake, na aliposikia habari za Yesualidhani kwamba Yohana amefufuka. Si rahisi ulimwengu kupata huru mbali nasauti za manabii wake.

6:30-34 Mitume walirudi na kutoa ripoti na Yesu aliwachukua faraghaniHabari ya kurudi kwa mitume imeandikwa kwa ufupi. Walimpa Yesu ripoti kamiliya matendo yao na mafundisho yao. Inaonekana walipewa muda wa kurudi,walitoka sehemu mbalimbali na kufika kwake ‘wakakusanyika mbele ya Yesu’.Ni hapo tu ambapo Marko ametumia neno ‘mitume’ si neno la cheo bali ni nenola kuashiria jambo la kutumwa na Yesu. Ni Yesu aliyewatuma na waliporudiKwake waliwajibika kutoa ripoti. Hivyo Marko amesisitiza umuhimu wa uhusiano

MARKO186

wao na Yesu kuliko yale waliyoyafanya. Baada ya hapo waliendelea kuitwawanafunzi na uwiano kati ya kujifunza na kutumwa ni siri ya mafanikio yao. Nineno bora kwa Wakristo kumrudia Yesu kila wakati na kumwambia habari zayale waliyoyafanya.

k.31 Yesu aliona kwamba wao pamoja na Yeye mwenyewe walihitaji nafasi yautulivu na mapumziko. Hasa kwa sababu kila siku watu wengi waliwajia hatawakashindwa kupata nafasi ya kula n.k. Bila shaka habari za Yesu zilieneasana kutokana na safari za wanafunzi vijijini. Wengine walimfuata Yesu kilaalipokwenda na wengine walikuja na kuondoka mara kwa mara. Ni Mitume tuambao Yesu aliwaita kwenda pamoja naye mpaka mahali pasipokuwa na watu‘njoni ninyi peke yenu’.

k.32 Ndipo wakaondoka kwa mashaua kuelekea kaskazini mashariki ya Ziwa.Luka ametaja Bethsaida (Lk.9:10) ila ni vigumu kupatanisha jambo hilo naMk.6:45.

k.33-34 Kazi za wanafunzi vijijini zilisababisha watu wengi kujulishwa habari zaYesu. Watu waliwaona pamoja na Yesu wakiondoka mashuani,wakawatambua, wakamua kwenda kwa miguu ili wafike pale watakaposhukaYesu na wanafunzi. Hivyo ulikuwapo uhusiano kati ya watu na wanafunzi. Nidhahiri kwamba Yesu alipendwa sana na wengi.

Kwa jinsi Marko alivyoandika Yesu na wanafunzi walitangulia kufika, maanawalipofika walikuta mkutano wa watu, ndipo Yesu akawatokea. Huenda watuwaliwatangulia wale katika mashua kwa muda ndipo mwishowe ni Yesu nawanafunzi waliofika kwanza maana mwendo wa bahari ulikuwa maili 4, kwamiguu maili 10.

Kwa hiyo, iwapo Yesu na wanafunzi walitafuta utulivu na mapumziko mbali nawatu, kinyume chake, walikuta umati wa watu, sawa na hali waliyoacha. Yesualionaje? Je! aliwakasirikia? Je! aliamua kuondoka kwenda mahali pengine? Je!aliamua kutokuwahudumia? La, Sivyo. Aliwahurumia, alijiweka mahali pao,aliwaona kuwa kama kondoo wasio na mchungaji. Kiroho walihitaji malisho,uongozi, na ulinzi, mambo ambayo iliwapasa viongozi wao kuwapatia ilawaliopo walikuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao. Musa alipokaribia kufaalimwomba Mungu awapatie Israeli ‘mchungaji’ na Mungu alimwinua Yoshua(maana ya jina lake Mwokozi sawa na Yesu) (Hes.27:17) Taz. 1 Waf.22:17kuhusu hali ya Israeli walipokosa viongozi waaminifu (Ling. na Eze. 34:1-5; 23).

Yesu alijitoa kuwa Mchungaji kwa umati huo wa watu, aliwahurumia, alijiwekakatika hali rahisi ya kuweza kupatikana. Haja yao kubwa ilikuwa kufundishwakweli za Mungu. Wengi waliomfuata walikuja kwa ajili ya miujiza (Yn.6:2) ilahasa walihitaji kufundishwa habari za Ufalme wa Mungu (Lk.9:11).

MARKO 187

Walipoondoka kwa mashua, bila shaka, waliwaza kwamba kwa hakikawatapata huo utulivu waliotamani, kumbe, siyo.

6:35-44 Kulisha watu zaidi ya elfu tano (Mt.15:15-21; Lk.9:12-17; Yn.6:1-15)Mwujiza huu ni ule mmoja tu ambao habari zake zimeandikwa katika Injili zotenne. Kwa hiyo, inaonekana wanafunzi waliona huo mwujiza kuwa wa maanasana kwa upande wao.

k.35 Yesu alikuwa ameshinda mchana kutwa katika kuwahudumia watu.Wanafunzi walianza kuwa na wasiwasi juu ya hao watu na haja yao ya chakula.Yesu alikuwa akiendelea kuwafundisha kama hakujali saa, na watu waliendeleakumsikiliza bila kuangalia saa na umbali wa kupata chakula. HuendaWanafunzi walitaka kukwepa wajibu wa kutatua tatizo la chakula, maanawalijua kwamba wao wenyewe hawakuwa na akiba ya kutosha, na pili, watuwaliweza kwenda mashambani na vijijini ikiwa watawahi kuondoka kabla ya juakuchwa. Pengine walisikia kama deni kwa watu hao walipokumbuka jinsiwalivyokaribishwa na watu wakati wa kufanya uinjilisti. Huenda wanafunzihawakutaka kunyimwa nafasi ya kuwa na Yesu peke yao na walichukizwawalipomwona Yesu akizidi kufundisha watu huku ameshinda nao mchanakutwa.

k.36 Hivyo walimwendea Yesu na kujiingiza kati ya mafundisho yake nakumshauri awaage watu ili waende kutafuta chakula.

k.37 Ila Yesu aliwajibu kwa ufupi kwa kuwapa changamoto na wajibu walio naokuwapatia chakula ‘wapeni ninyi chakula’. Aliwalazimisha wawe na mzigo juuya hao watu na watazame uwezekano wao wa kuwapatia chakula. Tukumbukekwamba hao wanafunzi walikuwapo Yesu alipogeuza maji kuwa divai pamojana kumwona mara kwa mara akifanya miujiza. Pia walipotumwa nayewaliwaponya wagonjwa na kutoa pepo n.k. Je! watakumbuka hayo nakumwamini kufanya mwujiza tena. Hatusikii kwamba walikuwa na mawazokama haya. Kinyume chake walifikiria mambo kwa hali ya kibinadamuwakiwaza gharama ya kununua mikate na kuona ya kwamba ilipita uwezo wao(dinari ilikuwa malipo ya mshahara wa kutwa kwa mfanya kazi).

Kisha Yesu aliwashauri waende kutazama walicho nacho, yaani akibailiyoachwa mashuani au pale walipotua. Wakarudi na kumpa hesabu ya mikatemitano, na samaki wawili. Yesu hakuwaruhusu kujiondoa katika jambo hilo,alijitahidi kuwaingiza. Hawawezi kukwepa wajibu wa kuwalisha hao watu, iwapoYeye Mwenyewe alijua tangu mwanzo atakalofanya (Yn.6:6). Mpaka hapomawazo yao yamebanwa katika uwezo wa kibinadamu.

k.39-40 Walipomletea hiyo mikate na samaki Yesu alitaka mambo yoteyatendeke kwa taratibu na kwa wazi. Watu walikuwa wengi, wenye njaa, naYesu hakutaka fujo itokee. Hivyo aliwaagiza wanafunzi waongoze watu kukaa

MARKO188

safu kwa safu, ili mikate igawanywe kwa urahisi, pia hesabu ya watu ipatikane.Ilihitaji imani wafanye kama Yesu alivyowaagiza maana mbele yao ni umati wawatu, na hamna chochote kilichoonekana isipokuwa mikate mitano na samakiwawili. Wasije wakaaibika sana kama Yesu hatafanya neno la ajabu.

k.41 Ndipo Yesu alipokea kile kidogo walicho nacho walichomletea, na kamaMyahudi mwanaume alivyozoea kufanya kila wakati wa kula, alimshukuruMungu kwa ajili yake. Alitazama mbinguni, ishara ya kumtukuza Mungu nakuonyesha jinsi alivyomtegemea Babaye katika jambo hilo. (Yesu hakuibariki ilemikate au kusema maneno kama mganga juu yake). Ndipo akamega ile mikatena samaki na kuwapa wanafunzi ili wawape watu. Mwujiza ulitokea lini na kwanjia gani? Hatuambiwi, kama mikate iliongezeka mikononi mwa Yesu aumikononi mwa wanafunzi hatujui. Lililokuwa dhahiri ni kwamba kilawalipomwendea Yesu kwa chakula walipewa. Huenda mikate mingi na samakinyingi haikuonekana, ila ilipotakiwa ilikuwepo. ‘Neema yake yatosha’ ndivyoalivyojifunza Paulo (2 Kor.12:9).

k.42-43 ‘wakala wote wakashiba’ Maneno hayo yaonyesha ukarimu wa Mungu,walikula na kushiba, hata chakula kilibaki, dalili ya kuonyesha kwamba kamakingine kingalihitajika kingalipatikana. Mwishoni walikuwa na kiasi zaidi ya kilewalichokuwa nacho mwanzoni!! Waliokota vipande si makombo tu ambavyoviliwatosha wanafunzi baadaye navyo viliwakumbusha habari ya mwujiza huobaada ya siku yenyewe kuwa imepita. Iwapo vyakula vilitosha na kuzidi Yesuhakuruhusu wavitupe. Mungu hupenda tuwe mawakili waaminifu wa vipawavyake.

k.44 Mwishowe twapewa habari ya idadi ya watu wa kiume waliokula, walikuwaelfu tano. Katika idadi hiyo hamna wanawake na watoto. Ni vigumu kufikiri haohawakuwepo. Kwa desturi ya siku zile wanaume walikula peke yao nawanawake na watoto peke yao. Bila shaka watu walikumbuka jinsi baba zaowalivyolishwa na Mungu jangwani kwa miaka kama arobaini. Pia jinsi Eliya naElisha walivyolishwa kipekee na Mungu wakati wa shida (1 Waf.17: 8ku. 2Waf.4:1-7; 42-44). Je! Marko alitaka kuonyesha tofauti kati ya Karamu yaMasihi na ukarimu wa Mungu na ile karamu ya ulafi na ulevi iliyoandiliwa naHerode kwa wakuu wake. (Mwujiza huo hauwi sawa na sakramenti, kwasababu katika sakramenti ni kidogo tu kinachotolewa nacho kinaashiria Kifo chaBwana Yesu). Yawezekana Marko alidokezea Chakula cha Bwana kwa sababumaneno katika k.41 ‘kutwaa, kushukuru/bariki, kumega, kuwapa’ ni yaleambayo Yesu aliyatumia wakati wa kufanya Chakula cha Bwana (Mk.14:22). Ilatujue kwamba katika mwujiza huo watu walikula chakula cha kawaida kutulizanjaa ya kimwili.

Hasa mwujiza huo uliwafundisha wanafunzi mambo makuu kuhusu hudumayao ya mbeleni. Kwanza, wawe na mzigo na huruma kwa watu, wasiwe na haliya kutokutaka kuwahudumia watu hata ikiwa ni wakati usiofaa. Pili, wao

MARKO 189

wenyewe wajue kwa hakika kwamba walicho nacho ni kidogo tu, walahakitaenea watu. Yesu aliwalazimisha watazame kile walichokuwa nacho. Tatu,ni kile kidogo walicho nacho ambacho Yesu hutaka kiletwe Kwake. Hatumii kitukingine. Ila mpaka kimeletwa kwake kitabaki kama kidogo tu. Yesu alimshukuruMungu kwa kile kidogo walichokuwa nacho, hakukidharau, wala hakukiwekakando. Kwa hiyo, angewabariki watakapojitoa kwake, ndipo watakuta kwambaneema yake itawatosha. Kumega mkate kuliashiria Kifo chake Msalabani, mwiliwake utakapovunjwa kwa uhai wa ulimwengu.

Kanisa laonekana kuwa dhaifu sana, lisilo na uwezo wa kukabili mahitaji yawatu, ila waumini wakimruhusu Bwana Yesu kuwaongoza katika matumizi yavipawa vyao, basi, Kanisa lita’shibisha’ roho za watu pamoja na mahitaji yao yakimwili. Katika utumishi wa Kikristo kuwa na nia ya kuwahurumia watu ni niasafi na jambo jema.

6:45-52 Yesu alitembea juu ya bahari (Mt.14:22ku; Yn.6:15ku)k.45-46 Baada ya kuwalisha watu Yesu aliwalazimisha wanafunzi wakewapande mashuani na kuvuka mpaka ng’ambo ya magharibi. Yeye alibaki palena kuwaaga watu, katika jambo hilo twaona mamlaka ya Yesu kwa sababuwatu walikuwa katika hali ya msisimko kwa vile alivyowalisha nao walitakakumshika na kumfanya awe Mfalme wao. Walimwona kama Musa wa pili, wakwanza aliwalisha watu jangwani, na huyo Yesu amefanya vivyo hivyo iwapokwa mara moja tu (Yn.6:15ku). Yawezekana wanafunzi pia walishiriki nia yahao watu, na kama wangalikuwepo wangalijiunga na hao watu, maana mpakabaadaye sana waliwaza kwamba Yesu atausimimisha Ufalme wake hapoduniani.

Kwa Yesu jambo kubwa la kwanza ni maombi si mapumziko iwapoamewashughulikia watu mchana kutwa hadi jioni (1:35) na alipomaliza kuombaaliwaendea wanafunzi ili awaokoe na taabu za bahari. Yesu alisikia kujaribiwavikali sana. Jangwani alijaribiwa na Shetani kuujenga ufalme wake juu yamiujiza kwa kugeuza mawe yawe mikate kwa ajili ya njaa yake. Pale jangwaniyalikuwa mawazo tu, hapo ni tofauti, kiutendaji iliwezekana asimikwe kuwaMfalme. Tukumbuke watu walikuwa wengi, wa kutosha kuwa jeshi la kupigana.Ila tangu mwanzo Yesu alijua mwito wake na utume wake ni kuwa Mtumishi wakuteswa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu kama Isaya alivyotabiri (Isa.53).Wakati wote alibanwa kati ya haja ya kuwavuta watu ili wamtambue nakumpokea kama Masihi na kuwaelimisha juu ya aina ya Umasihi wake. Hivyo,mara moja aliachana na watu na kwenda mlimani ili ashirikiane na Babaye nakuhakikishiwa mapenzi yake na kupewa nguvu ya kukwepa njia zote zilizokinyume cha mapenzi ya Babaye.

k.47 Walipoondoka bila Yesu wanafunzi walipatikana na taabu, upepo wambisho uliwapa shida sana katika kuvuta makasia, ilikuwa usiku, na hali hiyoiliendelea kwa muda mpaka walipokuwa mbali sana na pwani. Bila shaka

MARKO190

waliwaza kwamba Yesu atafika katika mashua nyingine wala hatakuja mpakaasubuhi. Katika mawazo na katika hali za kimwili walikuwa na masumbufumengi. Walikuwa wameondoka kwa amri ya Yesu kama wakati mwinginewalipopata shida (4:35ku). Kumbe! kwa kutii kwao wamejikuta wako hatarini.

k.48b Ilipopata kama zamu ya nne ya usiku, mnamo saa tisa hivi Yesualiwaendea hali akitembea juu ya maji yaliyochafuka na mawimbi makali naupepo wa mbisho. Bila shaka walishangaa sana kuona ‘kivuli’ kama cha mtuakitembea juu ya maji na ‘kivuli’ hicho kiliwakaribia na kufanya kama kinawapitana kwenda mbele yao. Je! Yesu alikuwa akiipima imani yao?

k.49-50 Wote walimwona na kufadhaika sana na kupiga yowe. Haikuwa ndoto,wala hawakupotewa na akili, wala hayakuwa maono ya uwongo. Alikuja iliwamwone. Alikusudia kuwadhihirishia utukufu wake wa Mwana wa Adamu(Kut.33:18ku. 1 Waf.19:11ku). Alijitambulisha kwao na kuwaambiawachangamke kwa kuwa Ni Yeye Mwenyewe. Maneno aliyotumia niukumbusho wa Kut.3:14; Isa.41:4, 43:10, 52:6. Jina ambalo Musa alipewa.Hawana haja ya hofu. Aliwapa nafasi ya kumkaribisha chomboni, wakakubali,wakamkaribisha chomboni na mambo yakawa shwari. Walibaki na mshangaomkubwa mioyoni mwao, na Marko ametoa maoni yake ‘hawakufahamu habariza ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito’. Maana yake ijapokuwawalimsaidia Yesu katika kugawa mikate na kujua hakika kwamba mwujizamkubwa ulifanyika, bado hawajamtambua Yesu sawasawa kuwa Mwana waMungu mwenye uwezo sawa na Mungu Mwenyewe. Waliona mwujizahawakutambua Mwana wa Mungu. Tukumbuke kwamba hapa nyuma Yesualinyamazisha bahari na upepo (Mt.4:35ku) na hivi karibuni wamerudi baada yakufanya huduma ya kutoa pepo na kuwaponya wagonjwa.

Yesu alitaka kuwafundisha nini? Huenda wajifunze kutambua haja yao ya kuwana Yeye, kabla ya Yeye kuwajia na kuwasaidia. Ujuzi wa maisha ya nyumaunaweza kutufariji au kutuogofya kutokana na kadiri tunavyojifunza na maishayaliyopita. Iliwapasa wanafunzi wawe wamejifunza kwamba Yesu huwajalipotelea mbali amelala usingizi wakati wa chombo kuyumbishwa na maji auwakati yupo mlimani akiomba huku wao wametaabika katika safari ya kuvukabahari. Yeye huwaangalia na kuwajali hata ikiwa hali zilizopo hazionyeshikwamba ndivyo ilivyo.

Watu kadha wamejaribu kusema kwamba Yesu hakutembea juu ya maji kweliila tukumbuke kwamba wanafunzi walikuwa mbali sana na pwani walipomwonaYesu akitembea juu ya maji. Wao wenyewe walifahamu bahari hiyo sana,ingalikuwa vigumu waogope bila sababu kubwa.

6:53-56 Kuponya wengi katika nchi ya GenersaretiHapo tena Marko amejumlisha habari za uponyaji wa watu wengi (1:32ku;3:7ku; 6:33). Genesareti ilikuwa kusini ya Kapernaumu nchi iliyojaa watu wengi,

MARKO 191

nchi yenye rutuba. Yesu amefikia upeo wa Huduma yake katika Galilaya. Watuwalimtambua kwa sababu alikuwa amefanya shughuli nyingi pale Kapernaumuna kandokando yake. Walitoka vijijini, mijini, na shambani, na kuleta wagonjwawao kwake kila mahali waliposikia Yeye yupo. Aliwaruhusu kugusa pindo lavazi lake (Num.15:38ku. Kum.22:12) yawezekana watu walifikiri hii ndiyo njianzuri wakikumbuka yule mwanamke mwenye kutoka damu (5:24ku) na kwaimani ya namna hiyo Yesu aliwaponya. Hawakusikia haja ya kujihusisha naYesu zaidi na hatusomi kwamba Yesu aliwafundisha au alitoa pepo kamailivyokuwa desturi yake. Imani ni kitu muhimu njia ya kuionyesha si kitu. Yesualichukuliana nao kwa kuwa alitaka kuwasaidia wengi. Hali yao ilikuwa tofautisana na watu wa Nazareti, mji wake (k.5).

7:1-23 Yesu alipambanua kati ya Amri ya Mungu na mapokeo ya wazeek.1 Wakati mwingine (3:22) waandishi walitoka Yerusalemu na walimshtakiYesu vibaya. Hapo tena wamekuja kutoka Yerusalemu pamoja na Mafarisayo(baadhi ya Mafarisayo walikuwa waandishi) ili wazidi kumshtaki. Yesu,aliyekubalika kuwa rabi mwenye wanafunzi alionekana kama mtu asiyefaakuwa kiongozi katika dini kwa sababu alikuwa mlegevu sana juu ya kushikamapokeo yao. Yeye na wanafunzi wake hawakuwa na mzigo wa kuyashikamafundisho yote yaliyolenga kuifafanua Torati iliyotoka kwa Mungu. Yesuhakufuata sheria juu ya kuuondoa unajisi alipomgusa mwenye ukoma naalipoguswa na mwanamke aliyetoka damu, mambo ambayo machoni mwamapokeo yao yalimtia unajisi. Pia alishirikiana na watu bila kujali hali zao kamamtu asiyehofu kunajisika. Hivyo, walikuwa wakimvizia Yeye na wanafunzi wakeili wamshtaki (2:28,24). Walitaka kujua sababu zake za kuwa na msimamotofauti na msimamo wao. Waandishi walitumia nafasi zao zote katika kufafanuaTorati ili watu waelewe njia za kuitimiza Torati kwa ukamilifu. Ila Yesualionyesha kwamba lile boma la mapokeo waliloizungushia Torati kwa shabahaya kuilinda Torati, badala ya kuilinda, liliipotosha.

k.2 Katika kumvizia Yesu waliwaona kwamba baadhi ya wanafunzi wakehawakufuata mapokeo yao juu ya kunawa mikono kabla ya kula. Sheria hiyoilihusu kuuondoa unajisi si jambo la afya.

k.3-4 Hapo Marko ametoa maelezo kuhusu visheria vyao kuhusu unajisi kwasababu wasomaji wake walio WaMataifa hawakujua mambo hayo. Wayahudiwalifikiri wamenajisika wakigusa au kuguswa na MMataifa hata ikiwahawakukusudia kufanya hivi, kama wakiwa sokoni n.k. Vitu kadhaa vilipigwamarufuku kama maiti, mwanamke wakati wa kutoka damu, n.k. Iliwabidi wawena tahadhari juu ya kukutana na mtu au watu fulani; juu ya vyakula kadha; juuya kugusa vitu kadha; na juu ya hali ya mwili. Kwa hiyo walikuwa na desturi yamaosho mbalimbali ya kuuondoa unajisi waliopata, pengine bila kujua na bilakukusudia. Ndipo walihesabiwa ‘safi’ wakiweza kusali na kushirikiana nawengine. Lakini ‘usafi’ wao ulikuwa tofauti sana na ule uliosisitizwa na Yesukatika mafundisho yake. Yesu aliona kwamba usafi wao ni wa juujuu, ule

MARKO192

aliosema Yeye ulikuwa wa kweli, wa ndani, uliodaiwa na Mungu nakumpendeza.

k.5 Mazungumzo kati ya Mafarisayo na waandishi na Yesu hayakuwa mjadalatu wa kila mmoja kujitetea upande wake. Hasa kwa upande wao walileta shtakajuu ya Yesu. Yesu kwa upande wake alitikisa msingi wa hayo mapokeo nakuonyesha kwamba asili yake ilikuwa katika wanadamu tofauti na Torati, hasaAmri 10, yenye asili katika Mungu. Walimwuliza, si juu ya habari ile ya baadhiya wanafunzi kutokunawa mikono tu, bali juu ya mwenendo wao wa kila wakatiulioelekea kutokufuata mapokeo ya wazee.

k.6-7 Katika kuwajibu Yesu aliwakumbusha maneno ya Nabii Isaya ambayoYesu alisema kwamba yaliwahusu si wale wa nyakati za Isaya tu, bali wao pia‘alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki’. Tena Yesu aliwaita ‘wanafiki’ neno zito,kwa sababu waliridhika hata kuifurahia hali yao ya kuvishika visheria vingivilivyo vidogo, huku wakiacha sheria kuu za Mungu juu ya kumpenda Mungu nakumpenda jirani. Walipendelea kufuata desturi zao na kutimiza mambo kwa njehuku hawakujali hali yao ya moyo na ya kiroho. Waliweka juu andiko lenyewebadala ya kuchunguza maana yake. Kama Isaya alivyosema juu ya watu wasiku zake ‘huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami; naowaniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu’.Waliweza kutimiza maneno na matendo kwa nje bila kujitoa kwa moyo kutimizashabaha yake. Hasa walikuwa wamefanya dini yao kuwa bure, wakiwatwishawatu mzigo wa kushika visheria vingi walivyotunga wenyewe. Siyo kwambakuwa na mapokeo ni vibaya, wala Yesu hakufundisha kwamba tusiwe namapokeo, ila mapokeo yasiwe badala ya kumpenda Mungu kwa moyo. Munguhupenda tumheshimu kwa midomo yetu (Efe.5:19) pamoja na kumheshimukatika matendo yetu.

k.8-13 Yesu aliendelea kwa kusisitiza ile tofauti kubwa kati yake na dini yao.Shida yao kubwa ilikuwa kuacha amri ya Mungu na kuweka mapokeo yawanadamu badala yake. Ya Mungu wameacha, ya wanadamu wameshika!!! Ilimapokeo yao yasimame wamekuwa tayari kutangua amri ya Mungu. Jambo laajabu. Huenda mwanzoni, walipotia bidii kuyaandika mapokeo yaohawakukusudia kufanya hivyo ila ndivyo ilivyotokea.

Ndipo Yesu akatoa mfano wa jambo hilo. Ulihusu amri ya 5 juu ya utunzaji wawazazi. Mungu alisema kwamba ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ naYesu aliwakumbusha kwamba ni Musa, yule ambaye walidai kumpenda sana,aliyepewa amri hiyo kutoka kwa Mungu. Mtu alipaswa kuwatunza wazazi wake,na kutia maanani neno hilo na kuutimiza wajibu wake kwa wazazi wake, hataalilaaniwa kama hakuwafanyia vema wazazi (21:16; Law.20:9; Kum.27:16).Kwa hiyo, utunzaji wa wazazi ulifikiriwa kuwa jambo zito na la maana sana.Lakini kwa mapokeo yao mtu aliweza kuukwepa wajibu huo kwa kuweka wakfumali yake au sehemu yake kwa kusema ni kipawa kwa hekalu, hata bila kutoa

MARKO 193

mali hiyo. Ni kama kuweka kando mali fulani ili mwingine asiweze kuipata. Tenamtu aliweza kutoa kiapo hata kabla hali mbaya haijawapata wazazi, ili ikitokeashida ya wazazi kuuhitaji msaada, hataweza kuwapa msaada. Jambo lilizidikuwa baya kwa sababu hakuweza kukitangua kiapo chake hata ikiwa alitakakufanya hivyo (k.12). Hivyo Amri ya Mungu iliwekwa kando ili yasimamemafundisho ya wanadamu ambayo yalidhaniwa kuwa yamejengwa juu yake.Yesu alionyesha kwamba hatuwezi kuukwepa wajibu wetu kwa kulisaidiaKanisa kwa fedha au kitu kingine. Waandishi walikuwa wamesahau kwambaTorati iliwekwa kwa faida ya wanadamu na katika kuipa maana kwa njia yakufuata barabara kila neno lililoandikwa walikuwa wamepotosha shabaha yake,yaani wameshika andiko, na kupoteza lengo la lile andiko. Ipo hatari kwaWakristo kufanya walivyofanya Wayahudi.

k.13 Yesu alitoa mfano mmoja tu katika mingi iliyopo ili aonyeshe upuuzi naubaya wa msimamo wao juu ya mapokeo. Ni dhahiri kwamba kwa njia yakuyasimamisha mapokeo yao wameacha kutimiza mapenzi ya Mungu nabadala ya kutimiza Torati walikuwa wamekwenda kinyume chake.

k.14-17 Baada ya kujadili na Mafarisayo na waandishi Yesu alirudiakuzungumza na mkutano. Aliona jambo hilo juu ya ‘usafi’ na kunajisika nimuhimu sana na kiini cha shabaha ya dini. Hivyo, aliona vema awaite watu nakusema zaidi habari hizo. Kwa ufupi alisema juu ya chakula kiingiacho mtukutoka nje. Haiwezekani roho au nafsi ya mtu kuguswa na kunajisika kwa kitukutoka nje, na kwa kusema hivyo aliondoa ule utaratibu wa Kiyahudi uliowekatofauti kati ya chakula kilichomtia mtu unajisi (kama nyama ya nguruwe) nachakula kisichomtia mtu unajisi. Mpango huo uliandikwa katika Lawi 11 naKumbukumbu 14. Shabaha yake ilikuwa kuweka tofauti kati ya taifa teule laIsraeli na Mataifa mengine, kusudi wasiambukizwe na desturi na imani zakipagani na kuvutwa kuabudu miungu mbalimbali n.k. Hasa shabaha yampango huo ilikuwa kuulinda ufunuo wa Mungu wa kipekee waliojaliwaWaisraeli kwa kusudi maalumu la kuweka tayari watu watakapompokea Masihiatakapokuja. Ndipo, baada ya huyo kufika haitakuwapo haja wala sababu yasheria hizi kuendelea, wala tofauti kati ya Israeli na WaMataifa, kwa sababuwote ni wenye dhambi na Yeye Masihi ataukomboa walimwengu wote nadhambi. Kwa hiyo hakuna haja tena ya kitu cha kuwatofautisha na wengine.Wala kugusa vitu au kuguswa na vitu fulani hakutanajisi mtu. Kwa hiyo Yesualibomoa mipango ya aina yoyote inayogawa vitu kuwa safi au vichafu. Hasaumuhimu wa alivyosema ni katika kusisitiza usafi wa maisha, si usafi wa vitu.

k.17-23 Baada ya kuzungumza na Mafarisayo na wenzao na mkutano wawatu, alirudi nyumbani, na wanafunzi walitaka kuelezwa maana ya hayoaliyosema. Mpaka hapo, ijapokuwa wameshirikiana naye kwa ukaribu, nakuelezwa mengine kwa faragha, hata hivyo, wamekosa ufahamu, hata wamambo ambayo Yesu alitazamia kwamba wangekuwa nao. Ndipo aliendeleakuwafafanulia mfano wa chakula n.k.

MARKO194

Alionyesha kwamba chakula hakihusiki hata kidogo na jambo la kutiwa unajisi.Chakula na moyo ni vitu viwili tofauti sana. Yesu alitaja mwenendo wa chakula,kwanza chatoka nje, ndipo chaingia ndani kwa njia ya midomo, chapita mpakatumboni, kisha chatoka kwenda chooni. Katika mwenendo huo wote, hakigusimoyo, wala roho, wala akili za mtu. Katika kupitia mwilini kinachujwa na uzuriwake huingia misuli na mifupa n.k. na kutia mwili nguvu na afya na ‘takataka’yake hutoka nje katika choo. Kutokudhuru kwa chakula kwadhihirishwa katikamwisho wake. Chakula ni kama mgeni wa muda mfupi katika mwili, ni ugeniusiokaa. Neno hilo lahusu chakula cha aina zote, mwisho wa kila chakula nichooni. Petro alipewa fundisho hilo katika maono kabla ya kwenda kwaWaMataifa (Mdo. 10:9ku). Kwa muda mrefu Kanisa lilipambana na swala hilokwa ajili ya ushirikiano kati ya Wakristo wa Kiyahudi walioshika mapokeo hayona Wakristo wa KiMataifa ambao hawakuwa na mambo hayo (Mdo.11:2-18;15:7-29; Gal.2:11ku).

k.21 Baada ya kusema juu ya vitu vitokavyo nje ya mtu Yesu alifikia kiini chamambo hayo yote, unajisi wa ndani, dhambi ndani ya wanadamu wote, ambayohumtia kila mtu unajisi mbele za Mungu. Jambo kubwa si chakula bali ni moyo,kwa sababu kutoka moyo hutoka mambo yote mabaya. Moyo (si wa kimwili) nikiini cha nafsi ya mtu, ni katikati ya utu wake. Alipowakemea Mafarisayoalitumia dondoo kutoka Isaya 29:13 lililotaja moyo. Ndipo Yesu alitaja mambombalimbali yatokayo na moyo wa wanadamu, alitaja mambo sita kwa ‘wingi’(kama ni matendo yanayofanywa mara kwa mara) na sita kwa ‘umoja’ (kama niaina za uovu). Ni vema tuyazingatie hayo yanayoorodheshwa. Chakula chatokanje ila dhambi tayari imo katika utu wa mtu. Kwa maelezo hayo Yesu alifafanua‘mtu’ kuwa zaidi ya mwili, mtu huwa na nafsi, dhamiri, akili n.k.

Twaona ‘urahisi’ wa mpango wa Mafarisayo na waandishi, kwa kunawa mikonowatu walidhani kwamba unajisi wa nje unaondolewa. Je! walisemaje juu yaunajisi wa ndani, yaani dhambi? Hawakusema lolote. Lakini kuuondoa unajisiwa ndani, yaani dhambi katika utu wa mtu, ni jambo gumu sana. Ni Yesu tu,peke yake, kwa kifo chake cha kufidia dhambi, aliye na uwezo wa kusafishamoyo wa mtu. Mafarisayo na wenzao walisisitiza usafi wa nje Yesu alikazausafi wa ndani. Wanadamu wenye dhambi hawawezi kuufikia ule usafi wamoyo unaotakiwa na Mungu kwa kushika visheria vidogovidogo vya njevilivyotungwa na wanadamu, kama ingewezekana isingekuwapo haja ya YesuKuja kuwa Mwokozi.

Twajifunza wema wa Mungu katika uumbaji, chakula ni kitu chema ambachotumepewa ili tuwe na afya na mwili mzuri. Pia twajifunza kwamba tusilaumumambo ya nje kama mazingira yetu, vielelezo vya watu wabaya, matusi nalaana ya watu n.k. Ijapokuwa mambo kama hayo hayatusaidii kuishi maishamema, hata hivyo, hayakubaliki kuwa udhuru kwa dhambi zetu. Dhambi niugonjwa wa moyo usio na matibabu nje ya Kristo.

MARKO 195

Kwa mafundisho ya Yesu Kanisa liliwekwa uhuru na hali ya kushikilia andikobila kutafakari maana yake na kulitafsiri kwa mazingara ya wakati wake.Hakuna haja kuyashika yote ya Agano la Kale, yale yaliyohusu maandalio yaKuja kwa Kristo yaliisha wakati Alipofika. Ila mambo yahusuyo adili hudumu nakuhusu wakati wote, maana Yesu alisema kwamba haki yetu hupaswa kupitaile ya Mafarisayo (ling.Mt.5:17ku).

7:24-30 Yesu alimponya binti wa Mwanamke MMataifa (Mt.15:21-28)k.24 Yesu aliondoka katika nchi ya Wayahudi na kuingia nchi ya WaMataifawalipoishi Wasirofoinike, walioabudu miungi yao, na kutumia lugha ya Kiyunani.Walitoka katika WaKanaani na nchi yao ilikuwa katika jimbo la Shamu.

Hatujui sababu za Yesu kwenda huko, kwa maneno ‘akataka asijulikane namtu’ inaonekana hakuja kufanya uinjilisti bali alitaka kupumzika na kuwa nautulivu na wanafunzi wake. Huenda alitaka kuepukana na Mafarisayo na aduizake waliotaka kumwua pamoja na wale waliotaka kumshika awe Mfalme.Lakini haikuwezekana akae pale bila kujulikana. Hakuwa mfanyamazingaombwe mwenye uwezo wa kutoweka, alikuwa mtu kweli. Hapo nyumaMarko ametuambia kwamba wenyeji wa nchi ile walikuwemo katika umati wawatu waliomfuata (3:8). Kwa hiyo, habari zake zilikuwa zimeenea mpaka huko.Twaona uwezo wa Yesu kuwavuta watu Kwake.

k.25 Ndipo akaja mwanamke, mwenyeji wa nchi ile, aliyekuwa amehuzunikasana kwa hali ya binti yake aliyepagawa na pepo (ling.9:17-18,22). Aliangukamiguuni pake, dalili ya unyenyekevu na heshima kwa Yesu. Hakuwa nawasiwasi yoyote kwamba yeye ni mwanamke, tena MMtaifa. Akamwombaamtoe pepo binti yake, ambaye alikuwa amemwacha nyumbani. Ni ombi la‘mchafu’ machoni mwa Wayahudi, na Yesu kama rabi asingalitazamiwakujihusisha na mwanamke, aliye MMtaifa, aliye na binti aliyepagawa na pepomchafu. Lakini Yesu hakujali hayo.

k.27 Ijapokuwa inaonekana Yesu hakumjibu vizuri, huenda alitumia mithaliiliyojulikana, ila maneno yake yalikuwa kama katazo, hata hivyo, ndani yaketumaini lipo, maana alisema ‘waache watoto washibe kwanza’ neno ‘kwanza’ nikuonyesha kwamba wengine waweza kuhudumiwa baadaye. Pia ‘mbwa’ (walewa nyumbani) huzoea kulishwa na makombo yaangukayo mezani, wakati uleule wa watoto kula, kwa hiyo, kama ni hivyo, liko tumaini la kupata makombobila kukawia. Yesu aliacha mlango wazi kidogo na huyo mwanamke akachukuanafasi yake kwa kukubali aliyosema Yesu. Akajinyenyekeza na kukubali kuwa‘mbwa’ wa kupewa ‘makombo’. Kwa ajili ya binti yake hakubisha wala kuudhika.Mambo hayo mengine yalikuwa madogo machoni pake, jambo kubwa lilikuwahali ya binti yake. Alijua kwamba machoni mwa Wayahudi WaMataifa waliitwa‘mbwa’. Alijua kwamba hakustahili kushiriki karamu ya Masihi. Neno ‘kwanza’liliashiria utangulizi wa Wayahudi katika mpango wa wokovu. Walichaguliwa

MARKO196

kuwa ‘watoto wa Mungu’ kipekee ambao Masihi atatoka kwao, na Injiliitahubiriwa kwao kwanza (Kum.14:1; Kut.4:22; Mdo.3:26; 13:46; Rum.1:16;2:9ku). Kwa hiyo, katazo la Yesu lilikuwa la muda mfupi tu. Yesu alivuta imaniyake, nayo ilitiwa nguvu kwa kadiri alivyokazana atimiziwe ombi lake la bintiyake kuponywa. Kamwe Yesu hakuwa na ubaguzi wa jinsia wala wa rangi walawa tabaka. Kwa maneno ya yule mama hakuna haja ya kusema ni amaWayahudi ama WaMataifa, inawezekana iwe Wayahudi na WaMataifa, na Yesuhana haja ya kuacha mpango wake wa kuhudumia Wayahudi hasa.

k.29-30 Kisha Yesu akamwambia arudi nyumbani kwa sababu pepo ameishakumtoka binti yake, huyo mama akaondoka, na alipofika nyumbani akamkutabinti alikuwa amelala kitandani bila kusumbuliwa na pepo. Kwa maneno hayotwaona kwamba Yesu alikuwa amemtoa pepo akiwa mbali, bila kumwona nabila kusema naye. Yesu alipendezwa na imani ya WaMataifa waliomjia naalisema wazi kwamba WaMataifa wenye imani wataingia katika Utalme wakena Wayahudi (wana wa Ufalme) wasiomwamini watatupwa nje (Mt.8:10ku).Ukuta kati ya Wayahudi na WaMataifa huzidi kubomolewa. Imani ya huyomama ilitofautiana sana na kutokuamini kwa Mafarisayo.

7:31-37 Yesu alimponya mtu bubu na kiziwiHabari hii haikuandikwa katika Injili zingine. Yesu aliondoka mipaka ya Tirokwenda kaskazini ya Sidoni na kutoka pale akaelekea mashariki kusini kwakupitia Galilaya mpaka Dekapoli, eneo lenye miji 9 upande wa pili wa Bahari nammoja upande wa magharibi. Kwa hiyo, Yesu alifanya mzunguko mkubwa, nahatuambiwi sababu yake. Twaweza kukisia kwamba alitaka nafasi yakuwafundisha wanafunzi wake, mara mbili alikuwa amejaribu kupata nafasi yautulivu pamoja nao, ilishindikana (6:31; 7:24). Katika Dekapoli walikuwepoWayahudi walioishi kati ya WaMataifa. Katika eneo hilo Yesu alitoa pepo wengikatika mtu (5:1ku).

k.32 Watu walimletea kiziwi ambaye pia alikuwa na shida ya kusema, huendakwa sababu hakuweza kusikia vizuri. Hakuwa bubu kabisa, maana ya neno ni‘alisema kwa shida sana’. Hatujui kama walikuwa Wayahudi au WaMataifawaliomleta; wala hatujui kama mtu mwenyewe alikuwa Myahudi au siyo.Yawezekana alikuwa Myahudi kwa sababu Yesu alitamka neno la KiAramu, ilahatujui. Je! walimleta ili Yesu amponye? au ambariki? Walimsihi amwekeemikono, kwa hiyo, hatujui walilenga nini.

k.33 Yesu alimtenga na mkutano na kumhudumia faraghani ili ajenge uhusianowa kibinafsi naye, maana yule mtu hakuweza kusikia vizuri Yesu aliposemanaye. Yawezekana hakufahamu vizuri sababu za kuletwa pale. Yesuhakupenda kujionyesha katika matendo yake. Ndipo Yesu alifanya vitendo vyakipekee ili avute usikivu wa yule mtu na kuchochea imani yake ili amwaminiYeye Mwenyewe. Alitia vidole vyake katika masikio yake ili amsaidie kuelewakwamba anatibu uziwi wake, ndipo akatema mate, na kuugusa ulimi wake,

MARKO 197

ishara ya kuutibu ulimi wake, kisha Yesu akatazama juu mbinguni ishara yakumwonyesha yule mtu kwamba uwezo wa kumtibu unatoka kwa Mungu,haupo katika mate n.k. Halafu twasoma kwamba Yesu aliugua. Alikuwa nahamu sana ya kuona mtu huyo awe mzima tena, awe na uwezo wa kusikia nakusema vizuri. Pengine ndani ya kuugua kwake alionyesha jinsi alivyochukizwana dhiki za wanadamu. Kisha kwa yule mtu alitamka neno moja kwa mamlakakatika lugha ya KiAramu (lugha ya Yesu Mwenyewe) Efatha. Marko alielezamaana ya neno hilo ‘funguka’. Ni ishara ya kuonyesha kwamba Yesu alitakayule mtu awe huru katika maisha yake yote, si katika masikio na ulimi wake tu.

k.35 Mara moja yule mtu alisikia na kusema vizuri. Hapo nyuma aliwezakusema kwa shida, sasa aliweza kusema kwa wazi.

k.36 Yesu aliwaonya watu wanyamaze, wasiseme habari hizo.Hatujui sababu ya katazo hilo, kwa sababu hawakuwa katika nchi ya Wayahudi.Hata hapo nyuma alimruhusu yule mtu aliyetolewa pepo wengi arudi nyumbanina kutangaza habari zake, na tulisoma kwamba alifanya hivyo katika Dekapoli(5:19-20).

k.36 Marko aliona shida sana katika kupata neno la kueleza kiasi kikubwa chamshangao wa watu uliopita kiasi. Walishuhudia kwamba Yesu amefanyamambo yote vema, pengine walikumbuka na mengine aliyoyafanya. Niukumbusho wa Mwanzo 1:31 mwisho wa umbaji. Yawezekana Marko alitakawatu waone jambo hilo lilihusika na unabii wa Isaya 35:5-6 utabiri juu ya Masihina jinsi atakavyofanya atakapokuja.

8:1-10 Kulishwa kwa watu elfu nne (Mt.15:32ku)Tumeona ya kwamba Marko alichagua kuandika habari za baadhi tu ya miujizaya Yesu aina tofauti tofauti, kwa hiyo, ni vigumu kujua kwa nini ameandikahabari ya mwujiza huo ambao unafanana na mmoja ambao habari zakezimeandikwa katika 6:35ku. Hata baadhi ya watalaamu hufikiri kwamba nihabari za mwujiza mmoja tu, ule uliotokea hapo nyuma. Lakini ni vigumu kufikirikwamba ni hivyo, kwa sababu, ijapokuwa baadhi ya mambo yamefanana,mambo mengine ni tofauti. Tofauti ni hizi: (a) mahali ulipofanyika mwujiza huo,pameitwa ‘nyikani’ na Yesu aliwaagiza waketi chini (si katika majani mabichi).Pamoja na hayo inaonekana walikuwa wangali ng’ambo ya pili ya Bahari, katikanchi ya Dekapoli iliyokuwa na WaMataifa wengi. (b) Alipolisha watu elfu tanowatu walikuwa wameshinda pamoja naye kutwa nzima. Hapa Yesu atajakwamba wamekaa naye siku tatu (Wayahudi walizoea kuhesabu ni siku hatakama ilibaki sehemu tu ya siku) kwa hiyo wameshinda naye sehemu ya siku,kutwa kuchwa, mpaka kesho yake. (c) chanzo cha mambo ni tofauti. Yesualipowalisha watu elfu tano ni wanafunzi waliojiingiza wakati Yesu alipokuwaakifundisha na kumshauri awaage watu. Hapo ni Yesu Mwenyewe aliyeanzakuwahoji juu ya watu kupata chakula. (d) Halafu iko tofauti katika idadi ya watuwaliokula (e) Iko tofauti katika hesabu ya mabaki (f) iko tofauti katika neno

MARKO198

lililotumika kwa vikapu, kwa watu elfu tano ni neno ‘vikapu’ ni vile vilivyotumiwana watu. Hapa kwa watu elfu nne ni neno ‘makanda’ vikapu vikubwa, nenolililotumika Paulo aliposhushwa ukutani (Mdo.9:25). Vikapu hivi vilitumiwa naWaMataifa na wafanya biashara. Ni tofauti na neno lililotumika kwa mabaki.Yesu aliwakumbusha wanafunzi juu ya miujiza hiyo miwili, hata alipambanuakati ya hesabu ya watu, hesabu ya mabaki, na vikapu na makanda (8:19ku).

k.1 Yesu amekuwa katika eneo la WaMataifa tangu 7:24. Katika 7:27-28alionyesha kwamba upo ‘mkate’ kwa watoto na kwa mbwa, yaani kwaWayahudi na pia kwa WaMataifa. Marko hakutaja mahali walipokuwapo ilayadhaniwa kwamba Yesu na wanafunzi walikuwa wangali katika eneo laDekapoli, mahali alipomponya mtu aliyekuwa kiziwi na bubu. Eneo lamchanganyiko wa Wayahudi na WaMataifa. Si wazi kama hao watu walikuwaWayahudi au WaMataifa, pengine walikuwa mchanganyiko, maana wenginewalitoka kwa karibu na wengine kwa mbali (k.3). Watu walizidi kumtafuta nakumsikiliza Yesu na kwa jinsi walivyokaa kwa muda mrefu ni dhahiri kwambahawakupenda kuachana naye kwa sababu ya mafundisho yake na ubingwa wakufundisha. Ni wazi kwamba hawakuja kwa ajili ya chakula tu. Tumeishaonakwamba Yesu alipenda sana kuwaelimisha watu juu ya Ufalme wake.

k.2-3 Twaona kwamba ni Yesu aliyetangulia kutaja mahitaji ya kula ya haowatu, tofauti na ilivyokuwa kwa wale elfu tano. Alisikia huruma sana kwa haliyao, alijua kwamba wakiondoka bila kula watazimia njiani. Alitaka wanafunziwake wajifunze kutoka Kwake tabia ya huruma, ili baadaye katika huduma yaowawahurumie watu kama Yeye alivyowahurumia.k.4 Wanafunzi waliitikia mawazo yake ya kuwahurumia watu kwa kuonyeshakwamba bado wangali wakipima mambo kwa hali ya kidunia na kwa kutazamahali zilizopo. Twaonaje jibu lao tukikumbuka kwamba walishirikiana kabisa naYesu katika kuwalisha wale elfu tano? Pengine waliogopa kumwambia arudiekufanya jinsi alivyofanya wakati ule. Pengine walikuwa na maana ya kuuliza‘unakusudia kufanya nini?’ Hawakutaja ule mwujiza uliopita, si kana kwambawameusahau, ila pengine hawakutazamia Yesu aufanye tena. Markoamesisitiza upofu wa wanafunzi, yawezekana alitaka kuonyesha kwamba upofuwao uliendelea na kuonekana tena katika jambo hilo. Yesu alichukua jukumumoja kwa moja tofauti na wakati ule mwingine.

k.5-8 Ndipo Yesu aliwauliza juu ya hesabu ya mikate waliyo nayo naowakamjibu ‘saba’. Samaki hawakutajwa mpaka k.7. Yesu aliwaagiza watuwakae chini, kisha akachukua ile mikate na kumshukuru Mungu na kuimegandipo akawapa wanafunzi ili waigawe kwa watu. Vivyo hivyo, na samaki.Vyakula vilienea, watu walishiba, hata vilibaki. Walikusanya mabaki yaliyojaamakanda saba. Kubaki kwa chakula kuliashiria kwamba hata kinginekingalipatikana ikiwa kingalihitajika.

MARKO 199

k.9 Ndipo Yesu aliwaaga watu; walikuwa wamefundishwa, walikuwawamelishwa, kwa hiyo, waliondoka kwa amri yake. Yesu alikuwa amewalishawatu, mchanganyiko wa Wayahudi na WaMataifa, dalili ya wote kukaribishwakatika Ufalme wake na wote ni ‘sawa’ machoni mwake. Alidhihirisha hurumayake kwa WaMataifa na ya kwamba mwujiza aliofanya mara moja awezakurudia kuufanya tena, mahali pengine, na kwa watu tofauti.

k.10 Baada ya kuwaaga mkutano Yesu na wanafunzi walipanda chomboni nakwenda upande wa magharibi wa Bahari. Watalaamu hawajui kwa hakikaDalmanutha ni mahali gani hasa, Mathayo alitaja jina la mahali kuwa Magadani.Yesu alionyesha madaraka juu ya kuwaongoza watu; alipowaaga, wakaondoka.Vilevile aliwaongoza wanafunzi watoke pale walipo na kwenda pamoja nayempaka mahali pengine. Zamani WaIsraeli walilishwa jangwani na Isaya alitabirikwamba katika dahari ya Masihi jangwa litashangilia na kuchanua maua n.k.(Isa.35:1-10).

8:11-13 Yesu alikataa ombi la Mafarisayo kuonyesha ishara (Mt.16:lku)k.11 Mafarisayo walitokea, hatujui walitoka wapi, wakaanza kuhojiana na Yesu.Tumeishaona hali yao ya kumpinga Yesu na walipohojiana naye hawakuwa nania safi. Hawakutaka kujua iliyo kweli, ila walitafuta sababu za kumshtaki nakumwua. Hapo twaona waliomba ishara ya kipekee. Zamani za kale Musaalipewa uwezo wa kufanya ishara zilizomthibitisha kuwa yule aliyetumwa naMungu kuwaokoa Israeli; na Nabii Isaya alimshauri Mfalme Ahazi kuombaapewe ishara (Isa.7:10-11) kwa hiyo, huenda walikuwa na haki ya kumwombaYesu athibitishe dai lake la kuwa Masihi kwa kufanya ishara. Ila, nia yaohaikuwa safi. Hakuna kipofu zaidi ya yule asiyetaka kuona! Wamepewa isharanyingi za watu kuponywa na kulishwa kipekee, za watu kutolewa pepo, n.k.Hizo zote ziliudhihirisha uwezo wa Yesu na mamlaka yake juu ya vitumbalimbali. Zilimshuhudia kuwa na kibali cha Mungu, Baba yake, na jinsialivyokuwa na uhusiano wa kipekee naye. Hayo yote Mafarisayo na wenzaowalisema asili yake ilikuwa Shetani. Ishara waliyotaka wakati huu ni ‘isharaitokayo mbinguni’ yaani jambo la ajabu kutoka juu la kuthibitisha kabisakwamba Mungu yu pamoja naye na aweza kuaminika. Lakini Yesu hakutakawamwamini na kumfuata kwa ajili ya kuona mambo ya kipekee. Alitakawamwamini kwa sababu ni Yule wa Kuaminika, wamfuate kwa sababu za hakina kweli si kwa faida ya kimwili tu.

k.12 Aliugua rohoni mwake, ndani kabisa alisikia huzuni na uchungu na hasira.Hakupendezwa na ukosefu wa imani (9:19) na hapo alishangazwa na hali yaoya kutokumwamini. Ndipo akakataa kabisa kuwapa hiyo ishara waliyotaka.Katika Mathayo 16:4 alisema watapewa ishara ya ‘Yona’ ya Kufufuka Kwake.Shida yao kubwa ilikuwa kutokuamini, walitegemea ujuzi wao wa kibinafsi, ujuziuliowafanya wajione na kujivuna na kujaa kiburi (1 Kor.8:1). Ishara alizozifanyaYesu zilikuwa za kuwahurumia watu na kuwasaidia wenye shida (6:34; 8:2).Yesu hakulenga kuwashurutisha watu waliokuwa kama watazamaji

MARKO200

wamwamini. Kuamini kwa sababu ya ishara si imani ya kweli, ni kinyume chahali ya imani inayotajwa katika Maandiko. Ishara huwasaidia waliowanyenyekevu, walio na mioyo iliyofunguka tayari kuongozwa katika kweli.Kuamini ni kuona (Ebr.13:1ku).

k.13 Kisha aliwaacha, kimwili aliondoka pale alipo, pia kiroho aliwaacha katikaupofu na ugumu wa mioyo yao, aliona kwamba kwa hali yao hawasaidiki, kwasababu hawakutaka kusaidiwa. Akavuka bahari pamoja na wanafunzi wake.

8:14-21 Yesu aliwakemea wanafunzi wake kwa upofu wa mioyo yaok.14-15 Walipoondoka, pengine kwa haraka, wanafunzi walikuwa wamesahaukuchukua mikate, chomboni walibaki na mmoja tu. Walisikia kushtakiwa katikadhamiri zao kwa ulegevu huo wa kusahau mkate, walibishana wao kwa wao.Ndipo Yesu alianza kuwaonya juu ya ‘chachu’ ya Mafarisayo na ya Herode.

k.15ku Hatujui kwa nini Yesu alitumia mfano wa ‘chachu’ katika kuwaonya, ilamara moja wanafunzi waliunganisha neno chachu na habari ya kusahaumikate. Waliwaza kwamba Yesu anawaza ‘chachu’ iwekwayo katika mkate.Kumbe Yesu alikuwa na maana tofauti, alikuwa akisemea mafundisho na tabiaya Mafarisayo na Herode, yaani unafiki wa Mafarisayo na hali na tabia yakidunia ya Herode.

Yesu aliwauliza maswali mazito na makali. Ni dhahiri kwamba hakupendezwana kutokuamini kwao na kutokuelewa kwao kwa jinsi walivyokuwa na wasiwasijuu ya kusahau mkate. Wamekosa kujifunza kwamba Yesu aweza kutimizamahitaji yao ya kula. Hapo nyuma alipowatuma aliwaambia wasichukue vitukwa sababu watu watawatunza, na ndivyo ilivyotokea (6:8). Walishirikiana nayealipowalisha umati wa watu mara mbili. Kwa hiyo, Je! atashindwa kuwalishawao walio wachache kwa mkate mmoja tu? Walikuwa wameandamana nayekila siku, wamejaliwa kuona mambo ya ajabu na kuelezwa kwa faraghamafundisho yake, hata hivyo, wamefanana na watu wa nje, wamekuwa vipofukama wale wengine. Mara kwa mara Marko ametaja hali hiyo ya wanafunzi(4:13,40; 6:52; 7:18). Kwa nini Yesu alifananisha mafundisho yao na chachu.Chachu ina hali tatu 1) hufanya kazi kwa siri, haitambulikani mpaka dongelimevimba 2) ina nguvu ya kuvimbisha 3) ina hali ya kuenea na kugusa dongezima. Aliwaonya juu ya unafiki wa Mafarisayo (Lk.12:1) na hali ya kidunia yaHerode; hali ya kushuku; na hali ya kushikilia mapokeo. Kwa nini Yesualiwaonya kwa ukali wakati huo? Ni kwa sababu amefikia hatua kubwa katikahuduma yake, upinzani wa adui zake umezidi, ameishafanya uinjilisti katika mijina vijijini na watu wamepewa nafasi ya kuamua juu yake, hivyo alitamani sanawanafunzi wake wamwelewe vema. Siyo kusema hawakumwamini kuwaMasihi, ila bado hawajaelewa siri za Ufalme wake na jinsi impasavyo afe iliausimamishe huo Ufalme. Hasa alifikiri kwamba kwa sababu aliwalisha umatiwa watu mara mbili wangalifahamu kwamba ikiwa hawana mkate wa kutoshaYeye angaliweza kukabili na kutatua tatizo hilo. Walikuwa katika hatari ya

MARKO 201

kuwaza mambo kama ulimwengu unavyoyawaza, Yeye ni zaidi ya mtendamiujiza, Yeye ni Mwana wa Mungu mwenye uwezo wote, na utume wake nizaidi ya kuwapatia watu mahitaji ya mwili, ni kutibu roho zao, kuwaleta kwenyetoba na ufuasi wake. Mawazo ya Mungu ni juu sana kama Isaya alivyosema(Isa.55:8). Aliwakemea si kwa sababu walisahau mkate bali kwa sababuwalikosa imani.

8:22-26 Yesu alimponya kipofu huko BethsaidaMarko ameandika habari ya miujiza miwili ambayo haionekani katika Injilizingine. Mmoja ni ya kiziwi na bubu (7:31ku) na mwingine ni huo wa hapo.Katika miujiza hiyo miwili mengine yafanana: Yesu aliwatenga na watu;aliwatemea mate na kuwawekea mikono; aliwakataza wasitangaze habari zake.Pia tofauti zipo. k.22 Yesu na wanafunzi walifika Bethsaida (mahali alipotokaPetro Yn.1:44) kaskazini mashariki ya Bahari karibu na mahali pa kulishwawatu elfu tano. Ijapokuwa pameitwa kijiji, hasa wakati huo, kutokana na HerodeFilipo, liwali wa eneo hilo, kijiji kilipata hadhi ya kuwa mji. Huyo kipofu aliletwana wengine, hatujui kama walikuwa jamaa au rafiki zake. Alihitaji watu wakumwongoza. Kwa kumleta walionyesha mzigo juu yake na upendo wakimsihiYesu amguse.

k.23 Yesu alimshika mkono, kama kusema ‘Mimi nitakuongoza’ akampelekanje ya kijiji, hatujui sababu yake, pengine kwa kuuvuta usikivu wake, aupengine kwa sababu hakutaka kufanya hadharani mwa watu. Alitaka kujengauhusiano wa kibinafsi naye, kumtia moyo, na kuamsha tumaini ndani yake ilihuyo mtu apate ujasiri wa kuamini kwamba aweza kuponywa. Ndipo Yesuakatema mate na kumpaka machoni na kumwekea mikono, ili azidi kujengauhusiano naye ili aweke tumaini lake kwa Yesu hasa. Halafu Yesu alimwuliza‘Waona kitu’ akipima kiasi cha kuona kwake. Mtu alijaribu kutumia macho yake,alitazama juu yaani mbele yake, na kumbe aliona watu, ila si kwa wazi,walikuwa wakitembea, na walionekana kwake kama miti, hakutambua maumboyao sawasawa (tukumbuke kwamba hajapata kuona watu wala vitu kabla yawakati huo). Yesu alimhusisha katika kila hatua ya uponyaji wake. Kisha Yesualiweka mikono yake tena kwenye macho yake na kwa mara ya pili yule mtuakatazama sana, yaani alikazana kuangalia mbele yake. Aliweza kuona vizuri,watu walionekana kama watu, vile vile aliviona vitu vingine sawasawa. Akawamzima. Hivyo Yesu alimponya kwa hatua mbili, mara mbili alimwekea mikono,ila tusifikiri kwamba hatua hizo zilichukua muda mrefu, ya pili ilifuata ya kwanzamara. Hatujui kwa nini Yesu alitumia njia hiyo, ni vigumu kufikiri kwamba Yesualishindwa kumponya mara moja maana tumeishaona kwamba Yesu aliponyawatu wengi mara moja, wengine kwa mbali, bila kuwagusa, hata bila kusemaneno. Huenda huyo mtu alikuwa na imani haba na Yesu hakukata tamaa juuyake, alimvuta kuamini zaidi. Kugusa ni jambo la maana sana kwa kipofu naYesu alijua hivyo, alimshika mkono na kumwongoza, aligusa macho yake nakuyapaka n.k. Twajifunza kwamba Yesu alimfanyia kila mtu kibinafsi, hakufuatataratibu moja tu. Alimwaza kila mtu na kufanya kulingana na jinsi alivyofikiri

MARKO202

kutamfaa na kumjenga. Hasa kila mara alitafuta kujihusisha na mtu na kujengauhusiano wa kibinafsi naye ili mtu amwamini na kujikabidhi Kwake. Kazi zote zaYesu zilikuwa kamili, hakuzifanya kwa nusu nusu au kwa mradi tu.

k.26 Kisha Yesu hakumruhusu kupitia vijijini na kuwaambia rafiki zake jinsialivyotendewa ila alimwagiza arudi nyumbani moja kwa moja. Hatuambiwi itikiola huyo mtu, wala la wale waliomleta, wala la wale waliojua habari hizo.

Yawezekana Marko ameandika habari hizo mara bado ya kuutaja upofu wawanafunzi akitaka kuonyesha jinsi upofu wa kimwili na upofu wa kiroho ulivyomgumu kutibiwa. Kama yule mtu aliyeponywa na upofu wake wa kimwili, vivyohivyo, wanafunzi wataponywa na upofu wao wa kiroho hatua kwa hatua. Hasahawataelewa mambo sawasawa mpaka Siku ya Pentekoste, wakati RohoMtakatifu atakapowashukia.

8:27-30 Petro alimkiri Yesu kuwa Ndiye Kristo (Mt.16:13-23; Lk.9:18-21)Yesu amefika njia panda katika Huduma yake. Twaweza kugawa Injili ya Markohapo. Tangu hapo huduma yake huelekea Yerusalemu na kwa Kifo chakekitakachotokea pale. Kwa sababu hiyo aliona jambo muhimu ni kuwatayarishawanafunzi kwa tukio hilo. Kwa upande wa wanafunzi jambo la Yesu kuuawahalikuwamo mawazoni mwao, lilikuwa jambo geni kabisa kwao. Hivyo Yesualiwachukua kaskazini, maili 25 hivi kutoka Bethsaida, mahali pasipokuwa naWayahudi, chini ya milima ya Hermoni, penye chanzo cha Mto Yordani.

Hakwenda huko ili afanye huduma hadharani bali kwa kupata nafasi yakuchunguza na kuwaelimisha wanafunzi. Alitaka kujua wamefika hatua ganikatika kumtambua.

Walipofika sehemu ile Yesu alianza kuwahoji akianzisha mazungumzoyaliyomhusu Yeye Mwenyewe. Luka amesema kwamba alikuwa akiomba ndipoalianza kuwauliza (Lk.9:18). Alianzia kwa mbali akitafuta kujua mawazo yaumma juu yake. Walimfikiri kuwa nani? Wanafunzi walimjibu kwa kutajamanabii kadhaa wa zamani; Eliya, Yeremia (Mt.16:14), Yohana Mbatizaji. Haponyuma tumeona kwamba Mfalme Herode alidhani kwamba Yesu alikuwaYohana Mbatizaji ambaye alidhani kwamba yu hai tena; au Eliya (6:15; Yn.1:21;Mal.4:5). Hata mmojawapo wa manabii. Kwa upande mmoja maoni hayo yaumma yalikuwa sawa, maana Yesu alikuwa nabii. Ila Je! alikuwa nabii tu? auzaidi ya nabii? Wote waliotajwa walikuwa watangulizi wa Masihi, Yesu ni Nenola mwisho kutoka kwa Mungu (Ebr.1:1ku). Kwa hiyo Yesu hakuridhika na maonihayo. Kisha akawageukia wanafunzi na kutoa changamoto kwao ili waowaseme jinsi walivyomfikiria. Neno ‘ninyi’ linatawala swali lake. Bila shakawanafunzi wamewahi kuzungumza wao kwa wao neno hilo na Petro aliyekuwamsemaji wao alitamka maoni yao niaba ya wenzake. Ndipo akamjibu Yesu nakukiri wazi na kwa maneno mafupi ‘Wewe ndiwe Kristo’ (Ling. Mt.16:16). Ukirihuo ulikuwa wa maana kubwa sana na bila shaka ulimtia moyo Bwana Yesu.

MARKO 203

Yesu alijua kwamba Petro hakufikia hatua hiyo ya utambuzi bila msaada waRoho Mtakatifu, alimtia moyo na kutaja uheri wake (Mt.16:17). Walimkiri kuwaYule aliyeahidiwa na Mungu tangu zamani, ambaye habari zake ziliandikwakatika Agano la Kale (2 Sam.7:12ku. Isa.55:3-5; Yer.23:5). Yesu hakukanakuwa Masihi, maana jibu la Petro lilikuwa sahihi ila kasoro moja ni kwambamawazo yao kumhusu huyo Masihi, namna yake na kazi yake, hayakuwasahihi. Jambo hilo lilidhihirika katika mazungumzo yaliyofuata. Maana ya neno‘Masihi’ (Kiebrania na ‘Kristo’ Kiyunani) ni ‘mtiwa mafuta’ na katika Israeli watukadhaa walitiwa mafuta waliposimikwa rasmi katika kazi, waliwekwa wakfu kwanjia hiyo kuonyesha kwamba wameitwa na Mungu na kuwezeshwa na Mungu;waliotiwa mafuta walikuwa wafalme, manabii, makuhani (Kut.29: 7,21; 1Sam.10:1,6; 16:13; 1 Waf.19:16; Zab.105:15; Isa.61:1ku).

k.30 Bila shaka Petro alikuwa na hali ya kusisimua na kutaka kuwatangaziawengine, lakini Yesu aliwaonya wanafunzi wote wasiseme habari hizo kwa mtuyeyote. Neno ‘Masihi’ liliamsha mawazo mbalimbali. Wengi waliwaza ‘Masihi’ niyule wa kuwaokoa na Warumi; ni wachache tu walioelewa kwamba Masihi niyule wa kutengeneza mambo ya kiroho. Yesu alijitahidi kunyosha mawazo yawatu ili wamwelewe Masihi kwa kulingana na mapenzi ya Mungu, si mapenzi yawanadamu. Hata Petro na wanafunzi walihitaji kurekebishwa mawazo yao.Ilikuwa hatari kumtaja Yesu kuwa Masihi, lazima washike ‘siri’ hiyo.

8:31-33Yesu alitangaza kifo na kufufuka kwake kwa mara ya kwanza(Mt.16:21-23; Lk.9:22)Baada ya Petro kumkiri Yesu kuwa Masihi na Yesu hakukana kuwa Masihi,Yesu alianza kuwafunulia wanafunzi wake namna ya Umasihi wake na nimambo gani yaliyomo ndani yake kwa Yeye Mwenyewe.

k.31 ‘akaanza’ neno hilo laonyesha kwamba ni mara ya kwanza kwa Yesukusema kwa wazi habari hizo. Kwa njia ya matendo na mafundisho yakeUmasihi wake umedhihirika, ila kwa hali ya kuficha. Kama ambavyotumeishasema Marko aliona jambo hilo kuwa hatua kubwa ya pili katikaHuduma ya Yesu (Ling.4:17 Yesu alipoanza kuhubiri). Ni jambo gani lililo jipyahasa? Ni jambo la Masihi kupatikana na mateso, kukataliwa, kuuawa, ndipokufufuka. Yesu alisema ‘imempasa Mwana wa Adamu (Dan.7:13-14) kupatwana hayo yote. Katika Agano la Kale manabii walitoa mawazo makubwa mawilijuu ya Masihi. Wazo moja lilikuwa atakuwa Mshindi (Isa.11) na wazo linginelilikuwa kwamba atakuwa Mtumishi Ateswaye (Isa.53). Wayahudi walishikiliawazo la Masihi kuwa Mshindi na kuweka kando wazo la Yesu kuwa MtumishiAteswaye. Haswa walifanya hivyo kwa sababu walitawaliwa na Mataifamengine, nao walitamani sana kupata uhuru, na kuwa na Mfalme waowenyewe kama zamani za Mfalme Daudi.

MARKO204

Neno ‘imempasa’ laonyesha kwamba nyuma ya mambo hayo ni mapenzi yaMungu. Hata zamani manabii waaminifu, walioleta ujumbe wa kweliusiopendwa na watu, waliteswa. Ina maana kwamba hakuna njia nyingine kwaYesu kukanyaga akitaka kutimiza mapenzi ya Baba yake. Ndipo Yesu alitamkawazi hatua zilizopo katika kudhiliwa kwake mpaka hatua ya kuadhimishwa.Mambo hayo yaliwashtua na kuwashangaza wanafunzi, yalitofautiana

sana na mawazo yao. Walishika jambo la mateso na jambo la kufufuka ni kamahawakulisikia.

k.32 Yesu alitamka wazi matukio kadhaa ambayo wanafunzi hawakuelewa,matukio ambayo hawakupenda kuyasikia. Petro aliyekuwa wa kwanza kumkirikwa niaba ya wenzake alikuwa wa kwanza kuonyesha jinsi habari hiyoilivyomchukiza yeye na wenzake. Hata twasoma kwamba akamchukua BwanaYesu na kuanza kumkemea. Ni ajabu kuona kwamba wanafunzi walisikia uhuruwa kutoa maoni yao bila shida. Katika kumkemea Yesu Petro alijiinua juu yaYesu kana kwamba alijua vizuri zaidi yake. Mara Yesu akageuka, nakuwatazama wanafunzi, na mbele yao akamkemea Petro kwa ukali. Bila shakaalisikia kujaribiwa vikali sana. Kwa hila, Shetani alikuwa amejificha katikamawazo ya Petro, rafiki yake mpendwa sana, akijaribu kumvuta Yesu amwasiBaba yake, asifanye mapenzi yake. Ni sawa na alivyofanya Shetani mwanzonimwa huduma ya Yesu alipomshauri juu ya njia za kufanikiwa katika hudumayake. Petro hakuwa adui wa Yesu Mwenyewe, ila alikuwa kinyume cha njiailiyompasa Yesu aifuate. Tena Shetani hakumshauri afanye maovu au kufuru,bali ajihurumie na kukwepa mateso yaliyo mbele yake; hii ndiyo sababu shaurilake lilikuwa la hatari sana. Bila shaka Yesu alisikia uzito alipomkabili Petro, ilailimbidi afanye hivi, kwa usalama wake Mwenyewe, na kwa usalama wa Petrona wenzake. Yesu alikuwa mwanadamu kweli na alijaribiwa kama wanadamuwanavyojaribiwa (Ebr.2:17).

‘nenda nyuma yangu, Shetani’ maneno hayo yanafanana na manenoaliyosema Yesu wakati wa kujaribiwa jangwani (Mt.4:10; Lk.4:8) nayoyaonyesha kwamba Yesu alijua ni Shetani aliye nyuma ya shauri la Petro. Petroalikuwa amekosa kufahamu haja na lazima ya Yesu kusulibiwa. Ni dhahirikwamba alifahamu maneno ya Yesu. Yesu alifahamu mapema yoteyatakayompata, na alirudia kutamka habari hizo mara mbili tena (9:31; 10:33).Haikuwa rahisi afahamu mapema mambo hayo. Sidhani kwamba mtu apendakujua mapema atakufa lini na kwa njia gani!!

MARKO 205

8:34-9.1 Yesu aliwaita wanafunzi wajitoe kabisa katika kumfuata(Ling. Mt.16:24-28; Lk.9:23-27)

k.34 Baada ya kuzungumza na wanafunzi aliwaita makutano wamsikilize. Kwahiyo, ina maana kwamba alitaka watu wote wawe wanafunzi wake, pia wajitoekabisa katika kumfuata. Kujitoa Kwake kabisa si neno kwa wachache tu, kamaalitaka baadhi tu ya waumini wawe ‘watakatifu’. Twajifunza kwamba hataalipokuwa akizungumza na wanafunzi wake faraghani, watu walikuwa karibu.‘Mtu yeyote’ maneno hayo yaonyesha kwamba neno la kujikana ni kwaWakristo wote si kwa wanafunzi tu.

Yesu aliendelea kwa kusema juu ya kupata faida na kupata hasara. Alitoamwito mgumu ‘mtu ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate’;maana yake mtu aache kujitegemea na amtegemee Mungu kabisa. Mwito wakujikana ni zaidi ya kutokuishi kwa anasa na raha. Ni mwito wa kumweka Yesukatikati ya maisha na kujinyenyekeza kwake na kumtii katika mambo yote. Nimwito mgumu kwa wanadamu wapendao kujiongoza na kutawala maisha yaona kufanya wanavyotaka wenyewe. Halafu Yesu alisema ‘ajitwike na msalaba’bila shaka neno ‘msalaba’ liliwashtua kabisa, maana walizoea kuona watuwakipelekwa kusulibiwa, hali wakibeba miti ya msalaba ambao juu yakewatafungwa. Hao walipelekwa kinyume cha mapenzi yao, ila wafuasi wa Yesukwa hiari watajitoa kwa Yesu, pengine kwa kupata mateso au dhiki au kifo kwaajili yake. ‘anifuate’ yaani ajiunge na Yesu na kukanyaga nyayo zake na kuwamtiifu Kwake. Ni dhahiri kwamba mwanadamu awaye yote hawezi kufanyahivyo kwa nguvu zake mwenyewe bila kukirimiwa neema ya Kristo na uwezowa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, tangu mwanzo, ilitazamiwa kwamba Wakristowatapata shida, dhiki, mateso, hata kufa, kwa ajili ya uaminifu wao kwa Yesuna Injili yake.

k.35 Halafu Yesu alionyesha umuhimu wa jambo hilo. Ingawa inaonekanakuwa hasara tupu mtu ajitoe na kukana nafsi yake, haswa, ni faida kubwa, sihasara, kwa sababu, kwa njia ya kukana nafsi yake na kujitoa kwa Yesu, mtuhujisalimisha, ‘ataona’ maisha. Wala hakuna njia nyingine ya kuyasalimisha.Kwa sababu mtu anayeishi kwa kujipendeza akiepa shida na dhiki, na kuishikwa raha, atajikuta kwamba amepoteza maisha yake. Mwishoni atakuwa ‘tupu’atapoteza yale aliyotaka kuyasalimisha. Mtu aliyejitoa kwa Yesu hana chochotecha kupoteza na vyote alivyo navyo ni faida. Tukishikilia maisha yetu wakatihuu twapoteza maisha ya baadaye; tukiishi katika mwanga wa maisha yabaadaye twahifadhi maisha ya kweli, ya kiroho. Yatupasa tuzingatie ni mambogani yaliyostahili kupotezwa na ni mambo gani yaliyostahili kusalimishwa.

k.36-37 Hapo Yesu aliuliza maswali mawili makali ‘itamfaidia mtu nini kuupataulimwengu wote akipata hasara ya nafsi yake?’ kwa sababu hata ikiwa mtuatajaliwa mafanikio mengi, vitu vyake vyote vitaishia hapa duniani wakati wakufa, hata maisha aliyoyazoea hayataendelea baada ya kufa. Ni vema mtu

MARKO206

akumbuke kwamba tukimfuata Yesu kwa kukanyaga nyayo zake, mwisho nikufika mbinguni, Aliko Yeye. ‘ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?’ Hamnakitu kingine ambacho mtu aweza kutoa badala ya nafsi yake. Nafsi yake ni yathamani sana, ni yeye mwenyewe. Hamna kitu kiwezacho kukomboa maishayaliyojengwa juu ya kanuni mbovu na malengo yasiyofaa. Mtu hupata hasaraisiyorekebishwa. Mambo aliyoyategemea hayatadumu, yataisha ndipo atabakihana kitu cha kutegemea.

k.38 Kisha Yesu alimwonya mtu juu ya kumwonea haya Yeye na maneno yakewakati wa kuishi hapa kati ya uasi na madhambi ya dunia hii. Mtu huhitaji ujasirina moyo thabiti akitaka kumkiri Yesu dhidi ya hali zilizopo. Akimkiri Yesu sasa,baadaye ataheshimiwa na Yesu kwa sababu Yesu atamtambulisha wazi mbeleya watu wote na kumkiri kuwa Wake. Wakati huo Yesu aonekana kuwa hanautukufu, ila wakati ule, atatokea katika utukufu wa Baba yake, akija juu yamawingi pamoja na malaika watakatifu (Mt.10:32-33; Lk.12:8-9). Yesu alitumwaili audhihirishe utukufu wa Baba ila watu hawakuweza kuutambua huo utukufuwa tabia njema, kwa sababu wamelewa na utukufu wao wenyewe (8:36)wakitafuta heshima na vyeo na maendeleo na fahari ya ulimwengu huo ambaoni wa muda tu. Hivyo mambo mawili yaliyotajwa katika Agano la Kale kuhusuMasihi yatatimizwa; Kudhiliwa kwake, Kuteswa na kuuawa Kwake; na Ushindiwake. Lakini la pili lafuata la kwanza (Flp.2:8ku) na watu walitazamia na kutakala pili tu. Ni juu yetu kuchagua, ama, kulaumiwa na kushtumiwa wakati huo nakutukuzwa baadaye, ama, kuheshimiwa sasa na kukataliwa baadaye. Ni hasara(ya kukosa mali, sifa, raha n.k.) tukimfuata Yesu sasa ila ni hasara zaidi kukosa(msamaha, uzima wa milele, furaha, amani, n.k.) tukishindwa kumfuata. Nivema kukumbuka na kuzingatia wakati wa baadaye wala si wakati huu tu.Kuaibika kwa ajili ya Kristo sasa au kuaibishwa na Yesu baadaye.

9:1 Maneno ‘mwana wa Adamu’ yatoka Dan.7:13-14 na Yesu alipenda sanakutumia maneno hayo kuhusu Yeye Mwenyewe. Yesu alikuwa akisemea wakatigani? kwa sababu alisema kwamba baadhi ya wale waliomsikia hawatakufakabla ya ‘kuuona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu’. Swali la kuuliza niwatauona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu wakati gani? Ni vigumu kufikiriwakati ni mwisho wa mambo yote, kwa sababu hao watu watakuwawameishafariki dunia kabla ya tukio hilo. Wengi hufikiri ni wakati wa kushukakwa Roho Mtakatifu na chanzo cha Injili kuhubiriwa na wengi kuitikia mwito wakumwamini Kristo, jinsi tusomavyo katika Matendo ya Mitume. Ile punje yaharadali ilianza kukua kuwa mti. Yesu alithibitishwa kuwa mshindi katikaKufufuka na Kupaa Kwake na katika Kushuka kwa Roho. Pengine ni vemakukubali kwamba katika mambo hayo yote Ufalme wake ulikuja kwa nguvu, nautazidi kuja hadi Kurudi Kwake. Matukio hayo yote yamefungamana na kuwakama jambo moja la kuja kwa Ufalme wake kwa nguvu. Neno muhimu nikwamba utukufu ni kwa Yesu, na aibu ni kwa wale wote wasiokubali kumfuatawakati huu.

MARKO 207

9:2-8 Yesu aligeuka sura mbele ya wanafunzi watatu (Mt.17:1ku; Lk.9:28ku)Huenda kuna uhusiano kati ya tukio hili na kifungu kilichotangulia kuhusu watukuuona ufalme wa Mungu kuja kwa nguvu. Watatu wa wanafunzi walijaliwakuona mabadiliko katika hali ya kuonekana kwa Yesu, walimwona amevikwautukufu wa ajabu.

k.2 Kwa desturi Marko hataji wakati kwa usahihi ila hapa ametuambia kwambajambo hilo lilitokea juma moja baada ya mazungumzo ya Yesu na wanafunzipale Kaisaria Filipi na baada ya kuwaambia watu juu ya kujikana nafsi.Tumeishaona kwamba ule ufunuo aliowapa wanafunzi juu ya Kuuawa Kwakeuliwafadhaisha, ulikuwa kinyume cha mawazo yao. Kwa hiyo, jambo hilo lakugeuka sura mbele za wanafunzi wake watatu lahusika kabisa na hayoyaliyotangulia. Wale watatu walikuwa pamoja naye alipomfufua binti Yairo naowatakuwa karibu naye zaidi ya wenzao katika Bustani ya Gethsemane (14:33).Yadhaniwa mlima mrefu ulikuwa Mlima Hermoni maili 12 kaskazini mashariki yaKaisaria Filipi. Katika Agano la Kale mlima ni mahali pa Mungu kujifunua(Mwa.22; Kut.19; 1 Waf.19). Luka amesema kwamba jambo hilo lilitokea wakatiYesu alipokuwa akiomba pengine usiku, kwa sababu wanafunzi walikuwawamelala, ndipo wakaamka (Lk.9:29,32).

k.3 Marko ametaja habari ya mavazi yake kumeta-meta na kuwa meupe sana(weupe ni rangi inayoashiria utakatifu). Mathayo ametaja uso wake kung’aakama jua (Mt.17:2). Hizo ni dalili za usafi usio wa ulimwengu huu. Hayo yoteyalidhihirisha utukufu wake wa asili, aliouweka kando alipofanyika mwili nakuishi maisha ya mwanadamu, maana angalivaa huo utukufu wakati wote bilashaka watu wangalimhofu na kukimbia. Je! ule utukufu ulikuwa wa KiMungu?au ulikuwa utukufu wa mwanadamu asiye na dhambi, mwanadamu mkamilifubila mawaa na kasoro?

k.4 Eliya na Musa waliwatokea (Eliya ametajwa kabla ya Musa ijapo Musaaliishi kabla yake). Hao waliwakilisha Torati na Manabii, ni kama kusemakwamba Yesu anatimiza ahadi zote na unabii wote wa Maandiko.Hawakuzungumza na wanafunzi ila waliongea na Yesu, na Luka ametuambiakwamba neno lililozungumziwa lilihusu Kufariki Kwake (Lk.9:31). InaonekanaMusa na Eliya walikuwapo kweli kwa kuwa walisema na Yesu. Wote wawiliwalitumwa na Mungu na kukataliwa na watu; wote walikutana na Mungumlimani; wote wawili walitoweka isiyo kawaida; Eliya alikwenda moja kwa mojambinguni bila kufa (2 Waf.2:11) na katika Kum.34:6 twasoma ‘Bwana alimzikaMusa’ na Waisraeli hawakujua mahali pa kaburi lake.

k.5-6 Petro kama ilivyokuwa hali yake aliona vema atoe maoni yake.Alimwambia Bwana Yesu kwamba ilikuwa vizuri kuwapo pale, na ni vemawaendelee kukaa pale, na kwa sababu hiyo aliomba wafanye vibanda vitatukwa ajili ya Eliya, Musa, na Yesu. Marko ameandika kwamba Petro alishindwakujua aseme nini, alikosa kutambua maana ya tukio hilo na yeye na wenzake

MARKO208

walishikwa na hofu nyingi. Kosa la Petro lilikuwa kumweka Yesu sawa na Musana Eliya. Yesu awapita hao wawili, hao walikuwa wanadamu, wenye asili katikawanadamu, na Yesu ni Mungu aliyefanyika Mwanadamu, Mwana wa Mungu,mwenye asili katika Mungu si katika wanadamu. Pengine Petro alifikiri kwambawakikaa huko mlimani kwenye utukufu haitakuwepo haja ya Yesu kwenda chinina kuelekea Yerusalemu na kuuawa, jinsi alivyowaambia. Kwa kutokewa naMusa na Eliya Yesu alitiwa moyo wa kuendelea mbele, kukabili magumu yoteyaliyo mbele yake, hali akijua, kwa kufanya hivyo anatimiza yote yaliyoandikwajuu yake katika Agano la Kale. Wanafunzi waliguswa sana na tukio hilo nahalikutoweka mawazoni mwao (2 Pet.1:16-18).

k.7 Wingu lilikuwa dalili ya Kuwapo kwa Mungu (Kut.13:21; 19:9: 33:9; 24:15-18; Hes.9:15; Eze.1:4) (Yesu ni Emanueli, Mungu pamoja nasi) nalo liliwatiauvuli, ndipo sauti ilisema na wanafunzi kutoka lile wingu, sauti ya Mungu Baba.Mungu alisema nini? alimtambulisha Yesu kuwa Mwana wake, mpendwawake, na ya kuwa ni wajibu wao kujiweka chini ya mamlaka yake na kumtii.Hapo nyuma Petro alikuwa amemkemea Yesu alipowaambia juu ya kuteswa nakuuawa kwake (8:32). Ina maana kwamba Yesu anatimiza mapenzi ya Babayake katika kwenda Yerusalemu na kukubali kushikwa na kuuawa. Ni muhimukabisa wajali yote Yesu anayowaambia. Baada ya tukio hilo ni kama hawananjia isipokuwa kumfuata hata ikiwa watagharimiwa maisha yao yote. Musaalipozungumza na Mungu uso wake uling’aa (Kut.34:29) na Yesualipozungumza na Baba yake sura yake iling’aa na kubadilika.

k.8 Kisha walipotazama huku na huku hawakuwaona Musa wala Eliya tena, ilaYesu tu. Yesu aliendelea kuonekana na kuwa pamoja nao (kwa muda). Yeye nimkuu zaidi ya manabii wote, na ni Mkuu kuliko Torati na Musa aliyewapaWaisraeli hiyo Torati.

9:9-13 Kushuka mlimani (Mt.17:9-13)k.9-10 Yesu na wanafunzi watatu walishuka mlimani na Yesu aliwaamuruwasimwambie mtu yeyote habari za mambo waliyoyaona mpaka atakapofufukakutoka wafu. ‘waliyoyaona’ pale mlimani ni mambo yaliyotokea kweli hayakuwandoto wala maoni wala mambo waliyobuni au kutunga. Yesu aliwawekeampaka wa muda wa kushika agizo lake nao walilishika mpaka Yesu alipofufukana muda umepita wa watu kumwaza kuwa Masihi wa kupindua serikali aukumfikiria kuwa mleta mafanikio ya kimwili. Mara kwa mara Yesu alikuwaameagiza watu wanyamaze ila ni hapo tu Yesu aliweka mpaka. Umuhimuulikuwa katika maana ya tukio hilo na baadaye wangefahamu vizuri maanayake na kuwaambia watu.

Wanafunzi hao watatu walitatizwa waliposikia Yesu akitaja Kufufuka Kwake.Tukumbuke kwamba sisi twaweza kuelewa jambo hilo bila shida kwa sababutunajua yote yaliyotokea, ila hao hawakujua uhalisi wake kwa sababu yalikuwabado hayajatokea, ila Yesu ameyataja. Wayahudi waliamini kwamba kuna

MARKO 209

ufufuo wa watu wote mwisho wa mambo yote, ila kwa jinsi Yesu alivyoutajaulionekana ni tofauti na ule ufufuo wa mwisho.

k.11 Kwa jinsi walivyofahamu, na kwa jinsi waandishi wao walivyofundisha,ilikubalika kwamba Eliya atamtangulia Masihi (Mal.4:5-6). Walimwona Eliyapale mlimani, lakini wameisha kumkiri Yesu kuwa Masihi. Imekuwaje Eliyaalitokea mlimani na Yesu ameishakubali ukiri wao wa kuwa Masihi? Tenailitabiriwa kwamba Eliya atatayarisha njia ya Masihi kwa kuwaweka watu tayarikumpokea. Imekuwaje watu wanazidi kumkataa? Tena kutaja Kufufuka inamaana kwamba Yesu atakufa? Eliya hakufa (2 Waf.2:8ku). Hivyo, wanafunziwalichanganyikiwa.

k.12 Ndipo Yesu alisema kwa wazi juu ya unabii kuhusu Eliya kuja kwanza nakazi yake ya kurejeza watu kwa Mungu. Yesu alikubali unabii huo ulikuwasawa. Ndipo Yesu aliendelea kwa kuunganisha unabii juu ya Eliya na unabii juuya Mwana wa Adamu ambaye ni Yeye. Kama unabii wa kwanza ni sawa, unabiijuu ya Masihi kuteswa na kudharauliwa ni sawa pia.

k.13 Kisha Yesu aliwaeleza kwamba Eliya amekwisha kuja, kwa sababu ‘Eliya’(wa unabii wa Malaki) si yule wa zamani bali ni Yohana Mbatizaji (Mt.17:13:Lk.1:16-17). Si kana kwamba ‘roho’ ya Eliya iliingia ndani ya Yohana Mbatizajibali alifanana na Eliya kuhusu kazi yake na kuteswa kwake (1 Waf.19:1-10).Eliya wa kwanza aliteswa na Mfalme Ahabu na mkewe Yezebeli, YohanaMbatizaji aliteswa na Mfalme Herode na Herodia ambaye Mfalme alimchukuakuwa mkewe. Wote wawili, Masihi na Mtangulizi wake Yohana, walipatwa na‘mwisho’ mmoja. Hivyo yaliyoandikwa ni mapenzi ya Mungu. Kwa sababuMbatizaji aliuawa vivyo hivyo na Mwana wa Adamu atauawa, na kama YohanaMbatizaji amestahili kuitwa ‘Eliya’ vivyo hivyo na Yesu amestahili kuitwa Masihi.Kama watu walivyomkataa mtangulizi wa Masihi vivyo hivyo watamkataa Masihimwenyewe (Lk.7:30). Kwa hiyo katika mazungumzo ya Yesu na walewanafunzi watatu walipokuwa wakishuka mlimani ule utukufu ulitoweka na nenola Msalaba limeweka kivuli chake. Mbatizaji alitayarisha njia ya Masihi katikakutoa mfano wa ‘mwisho’ wa Masihi katika ‘mwisho’ uliompata yeye.

Kwa hiyo ‘Eliya’ ameishafika na kuondoka, na Yesu ameishafika na yu tayarikuondoka. Katika maelezo hayo Yesu alipindua kabisa mawazo ya Wayahudi,‘Eliya’ waliyemtazamia wamekwisha kumwua, vivyo hivyo, na ‘Masihi’wanayemtazamia yumo miongoni mwao, nao wako tayari kumwua. Kwa hiyo,wanafunzi wasidanganywe na ule ‘utukufu’ wa mlimani. Yesu ni Mwana waUtukufu atakayefufuliwa na kutukuzwa baada ya kuteswa na kukataliwa.Wanafunzi wapaswa kupokea neno la mateso ‘msikieni Yeye’ sawa na sauti yaBaba iliyosema nao mlimani na kama Yesu alivyosema kwa wanafunzi wotepale Kaisaria Filipi.

MARKO210

9:14-29Yesu alimponya mvulana bubu na kiziwi, mwenye pepo aliyemtiakifafa (Mt.17:14-20; Lk.9:37-43a)k.14-15 Yesu na wale wanafunzi watatu walishuka mlimani na kufika kwawanafunzi tisa waliobaki bondeni. Walikuta mambo tofauti sana na utukufu nautulivu wa mlimani. Waandishi walipokuwa wakijadiliana na wanafunzi;alikuwepo baba aliyehangaika akitafuta msaada kwa kijana wake; na yupokijana mwenyewe aliyeonewa sana na pepo; na kati ya hayo yote walikuwepowanafunzi walioshindwa kutoa msaada huku wamezungukwa na umati wa watuambao walikuwa tayari kuifurahia miujiza bila kuitia maanani na kujikabidhi kwaYesu.

Watu walishangaa walipomwona Yesu nao wakamwendea mbio nakumkaribisha. Hatujui hasa kwa nini walishangaa. Labda kwa sababu ametokeawakati usiotazamiwa, au pengine ni kwa sababu Kuwapo Kwake kulitoshakuleta mshangao. Kwa nini waandishi walikuwa wakijadiliana na haowanafunzi? Pengine ni kwa sababu wanafunzi wamejaribu kutoa pepo katikamvulana na walitaka kujua mamlaka ya kutoa pepo imetoka wapi na ni nanialiyewapa amri hiyo? Huenda waandishi walikuwa wakifurahi walipoonawanafunzi wameshindwa kutoa pepo. Kama walitaka wanafunzi waonyesheuhalali wao wa kutoa pepo, kwa nini, wao wenyewe hawakutoa pepo iliwaonyeshe uhalali wao wa kuwa viongozi.

k.16-18 Mara Yesu aliwakabili waandishi na kuwauliza sababu ya majadiliano.Ndipo mtu mmoja alijitokeza na kumjibu, si kwa kusema juu ya majadiliano, balikwa kutaja habari ya mwana wake (wa pekee Lk.9:38) aliyesumbuliwa sana napepo. Inaonekana alikusudia kumleta kwa Yesu na alipomkuta hayupoaliwaomba wanafunzi wake wamsaidie, nao wakashindwa. Hapo nyumawalipotumwa kufanya uinjilisti walipewa mamlaka ya kutoa pepo, na huenda,walidhani kwamba wataweza kutoa pepo wakati huo (6:7,30). Halafu yule mtualimwelezea Yesu hali mbaya ya mvulana wake. Alikuwa na pepo aliyemtiaububu na uziwi na pamoja na hayo, pepo alimtia kifafa kiasi cha kuhatarishamaisha yake, akimbwaga chini kama anataka kumwangamiza.

k.19 Yesu aliitika kwa kuwalaumu ‘kizazi kisichoamini’ dalili ya kuonyesha jinsialivyosikia uchungu ndani yake kwa hali yao. Katika ‘kizazi hicho’ wamowaandishi waliopenda kujadili mambo kuliko kutoa msaada; pia wamowanafunzi walioshindwa kumsaidia kijana kwa sababu ya upungufu wa imaniyao; tena, kuna baba mwenye imani ndogo. Pamoja na hayo yote ipo ‘hewa’ yakutokuamini. Ndipo Yesu aliwauliza ‘nikae nanyi hata lini? nichukuliane nanyihata lini?’ ni kama Yesu anajiuliza Mwenyewe swali Je! aweka mpaka kwawakati wa kuwahudumia watu? akidokezea kwamba muda wa kukaa naohautaendelea. Kisha Yesu alimhurumia yule baba na kuwaambia wamletekijana. Iwapo Yesu alikuwa amesema maneno ya kukatisha tamaa, hata hivyo,tumaini lipo katika kuomba walete kijana Kwake.

MARKO 211

k.20-22a Alipofika kwa Yesu, pepo alionyesha dharau kwa Yesu, mara alimtiakijana kifafa, na kijana alianguka chini na kugaa-gaa, na kutokwa na povu.Ndipo, kabla ya kumponya Yesu alitaka kujenga uhusiano wa kibinafsi na babayake, na kumpa nafasi ya kumwamini kabla ya kumponya kijana. Hivyo,alimwuliza baba juu ya muda wa kijana kuwa mgonjwa, na baba alimjulishakwamba amekuwa na hali hiyo kwa muda mrefu. Hivyo baba alipewa nafasi yakuwaza juu ya ukubwa wa shida ya kijana wake na ule muda mrefu wakusumbuliwa kwake, ili atakapoponywa awe na shukrani ya kweli.

k.22b-27 Katika kumwelezea Yesu shida za kijana wake baba alijua tumainilake ni katika Yesu tu, alimwambia Yesu ‘lakini ukiweza neno lolote,utuhurumie, na kutusaidia’ bila shaka alikumbuka kushindwa kwa wanafunzi.Yule mtu alimpenda sana kijana wake. Alitambua kwamba Yesu alitakakuwasaidia, ila hakujua kama Yesu anao uwezo wa kuwasaidia. Lakini Yesualimtupia mpira yule mtu na kumpa changamoto ya kuamini. Shida si katikaYesu kuwa na uwezo ila ni katika yule mtu kuwa na imani. Hamna mpaka katikauwezo wa Mungu kwa wale wenye ujasiri wa kutumaini watasaidiwa. Yule mtuhakukawia kumwitikia Yesu, alipaza sauti na kukiri kwamba aliamini ila kwaunyenyekevu alikiri upungufu wake pia na kumwomba Yesu amsaidie ili awe naimani timilifu. Yesu aliridhika na jinsi yule baba alivyosema na alipoona watuwanakusanyika mbio, alisema moja kwa moja na pepo mchafu, alimkemea nakumwamuru amtoke kijana, akimtambulisha ‘Ewe pepo bubu na kiziwi’ ndipoakamwamuru asimrudie tena. Pepo akatoka kwa kumdhuru tena na kumwachahali ameishiwa nguvu, hata wengine walidhani kwamba amekufa, ila Yesualimshika mkono akamwinua, na huyo kijana akawa mzima, akasimama. Yesualitoa neno la amri tu na pepo akamtii.

k.28-29 Baada ya jambo hilo, walipoingia ndani ya nyumba, wanafunzi walitakakujua kwa nini walishindwa kumtoa pepo. Bila shaka walitatizwa kwa sababuhapo nyuma walikuwa wametoa pepo Yesu alipowatuma kufanya uinjilisti. Yesualionyesha shida ilitokana na upungufu wa kuomba. Yawezekana walifikirikwamba wamepewa kipawa hicho, nao waweza kukitumia wakati wo wote,kumbe Yesu alitaka wafahamu kwamba hakuna uhakika wa kuendelea nauwezo huo pasipo kumtegemea Mungu kila wakati badala ya kujitegemea.Imani inayotakiwa ni imani inayoomba na kumtegemea Mungu. Kwa hiyo jambomuhimu kuliko yote ni maombi. Imani inapokutana na enzi za Shetani ni uwezowa Mungu ulio tegemeo la uhakika na utawala wa Mungu ni mpaka wake.Katika Mathayo upungufu wa imani umetajwa (Mt.17:14,20) na kufunga, yaanikujitawala. Hata imani si kitu ambacho kinaweza kuwekwa akiba bali ni kipawacha Mungu anachoendelea kutoa kwa kadiri tunavyojihusisha naye katikamaombi.

MARKO212

9:30-32 Tangazo la pili la Kuuawa Kwake (Mt.17:22-23; Lk.9. 43b-45)

k.30-31a Yesu na wanafunzi waliondoka sehemu za Kaisaria Filipi na Mlimaalipogeuka sura, wakapita katikati ya Galilaya, Yesu akianza safari yake yakwenda Yerusalemu, hali akisikia msukumo wa kuelekea kusini. Wakati ulikuwakama miezi sita kabla ya Kuuawa Kwake. Hakutaka kufanya uinjilisti tenakatika eneo lile ambapo watu walikuwa wamemzoea, hasa alitaka watu wasijuekwamba Yeye yupo kati yao. Shabaha yake ilikuwa kupata nafasi nzuri yakuwafundisha wanafunzi wake na kuwatayarisha kwa kuondoka kwake, maanailikuwa dhahiri kwamba walikuwa hawajaelewa kwamba atauawa paleYerusalemu, hasa hawakuelewa kwa nini imepaswa kuwa hivyo.

k.31b-32 Ndipo twapata tangazo au onyo la pili juu ya Kuuawa Kwake. Lakwanza limetajwa katika 8:31. Bila shaka Yesu alikuwa akisemea jambo hilomara kwa mara, ila katika Injili tatu zinazowiana, zote zimetaja matangazomatatu maalum.

Tangazo hilo lilikuwa fupi, na jambo moja jipya lilikuwa lile la ‘yuaenda kutiwakatika mikono ya watu’. Maneno hayo yana maana mbili. Maana moja yahusuYuda kumsaliti, ila maana muhimu ni katika Mungu kuwa nyuma ya mamboyote yatakayompata pale Yerusalemu (Mdo.2:23; Rum.4:25; 8:32). Katikatangazo la kwanza lazima ya kifo chake ilikazwa, hapa mkazo ni juu ya uhakikawake.

Ijapokuwa maneno ya Yesu yalikuwa wazi, wanafunzi hawakuyafahamu kwasababu walikuwa wakiwaza kwa hali ya kibinadamu, nao walisikitika (Mt.17:23).Waliogopa kumwuliza, huenda walihofu kwamba wataambiwa mambowasiyotaka kuyasikia, au yawezekana walikumbuka jinsi Yesu alivyomkemeaPetro alipothubutu kutoa mawazo yake yaliyopinga yale aliyosema Yesu.Twajifunza ‘upweke’ wa Yesu katika safari hiyo ya kuelekea Yeresalemu.Hakuna aliyeshirikiana naye kiroho na kuelewa afanyayo.

9:33-37 Unyenyekevu wa wafuasi wa kweli (Mt.18:1-5; Lk.9:46-48)

k.33 Baada ya kupitia Galilaya Yesu na wanafunzi wakafika Kapernaumu,mahali pa kituo chake na nyumba ya Petro na Andrea. Pengine nyumbailiyotajwa ni ya Petro au pengine Yesu alikuwa amepanga nyumba pale. Njianiwanafunzi walikuwa wamebishana wao kwa wao juu ya yupi atakayekuwamkubwa. Labda walioneana wivu na kupata shida Yesu alipowachagua watatukwenda naye mlimani. Mara kwa mara ilionekana Petro alikuwa kiongozi namsemaji wao, lakini Je! atakuwa mkubwa? huenda walikumbuka jinsi Yesualivyomkemea na kuwa na mashaka kwamba yeye atakuwa mkubwa. Bilashaka walizoea kuzungumza wao kwa wao juu ya mambo mbalimbali na kutoamawazo yao kwa uhuru wakati Yesu hakuwa pamoja nao.

MARKO 213

k.34-35 Hawakumjibu Yesu alipowauliza ‘mlishindania nini njiani?’ penginewalisikia aibu, wakijua hali yao ni dhidi ya hali yake. Ndipo Yesu aliwasaidiakwa njia mbili. Kwanza aliketi chini ili awafundishe neno la unyenyekevu nautumishi, ndipo aliwafundisha kiutendaji. Aliwaambia wazi kwamba katikakumfuata Yeye jambo kubwa ni kutumika kwa unyenyekevu, kwa sababukanuni za Ufalme wake huwa tofauti sana na falme na tawala za dunia hii. Kiinicha Ufalme wake ni utumishi, kila mmoja awe msaada kwa wenzake ‘mpendejirani yako kama nafsi yako’. Hivyo hakuna nafasi kwa ‘ukubwa’ na ‘vyeo’. Vyeovitakuwapo katika Kanisa, lakini si vyeo vya kutawala wengine, wenye vyeowatatumika. Kiburi ni dhambi kubwa ambayo hata katika mambo ya kirohohuonekana, ni dhambi ambayo Mungu peke yake aweza kutibu.

k.36-37 Ndipo baada ya kuwafundisha kwa maneno aliwafundisha kiutendajialipomchukua mtoto na kumweka katikati yao na kumkumbatia. Huyo mdogoalikuwa kati ya ‘wakubwa’ kwa umbo ambao pia wamekuwa na vichwa vikubwana kuwaza makuu na kutaka ukubwa. Katika kumfuata Yesu mtu apaswakujiwaza kuwa mtoto, hata Wakristo na hata Mitume, watakaowaongozawenzao baada ya Yesu kuondoka. Hali ya ufuasi wao na hali ya utumishi waoifanane na huyo mtoto, aliye mdogo, asiye na mawazo marefu, wala nguvu.Hata Mitume wawe kama watoto na kila muumini pia. Tena wampokee mtuyeyote kama mtoto (haina maana kwamba wafanye mambo ya kitoto).Wakifanya hivyo watakuwa wamempokea Yesu, na wakimpokea Yesuwatakuwa wamempokea Mungu Baba aliyemtuma. Njia ya utukufu ni njia yakujinyenyekeza, maana Bwana wao yuaenda Yerusalemu na kujinyenyekezahata Kufa Msalabani (Flp.2:5ku). Kwa njia hiyo watu watatambua kwamba tuwafuasi wa Kristo. Haina maana kwamba tusiwe na vyeo katika Kanisa, walahaina maana kwamba tukae hali tumejificha na kutokuonekana. La! hatakidogo, ila ina maana kwamba kila mtu awe ameuvika unyenyekevu kama vazilake analovaa katika kila wakati na kwa kila jambo. Ni utumishi kwanza, ‘mimi’mwisho (ling.10:41ku).

Ni ajabu kuona jinsi wanafunzi walivyokuwa mbali na Bwana wao ingawawameishi naye kwa muda mrefu na kuona hali yake ya upole na unyenyekevu.Aliwapenda watoto sana, pia watu wasiopendwa na wenzao, watu waliowekwakando ya jamii. Anataka waumini wake wafuate kielelezo chake, wawe tayarikujiunga na watu wa chini na kuwashughulikia na kuwakaribisha katika shirikazao. Ni rahisi kutaka kushirikiana na ‘wakuu’, si vibaya kutaka kuwavutaKanisani, ila wakati wote wasiwekwe mbele ya wengine kama ni watu bora.Wanafunzi walishikwa na mawazo ya ukubwa huku hawakumjali Yesu nakutambua jinsi Yeye alivyojisikia.

9:38-41 Wafanye nini na wale wasiofuatana nao (Lk.9:49-50)k.38 Marko hakumtaja Yohana peke yake ila hapo tu. Hatuambiwi ni liniambapo wanafunzi walimkuta mtu akitoa pepo kwa jina la Yesu, pengineulikuwa wakati walipotumwa kufanya uinjilisti. Hatujui ni nini iliyomsukuma

MARKO214

Yohana kumwuliza Yesu juu ya jambo hilo. Pengine aliguswa na mafundisho yaYesu juu ya kumkaribisha mtoto, pengine alisikia wivu, au labda hakupendayule mtu atumie jina la Bwana wake bila kujiunga naye. Iwapo ni Yohanaaliyeuliza swali wanafunzi wenzake walikuwa wamemwona yule mtu na kuwazakama yeye alivyowaza. Walikuwa wamemkataza yule mtu kwa sababu moja tu,ya kutokufuatana nao. Inaonekana yule mtu alikuwa mtu wa kweli, aliyetumiajina la Yesu kwa kweli si kama maneno ya uchawi. Hakufanana na walewaliotajwa jina lake katika Matendo 19:13-16. Pia alifanikiwa kutoa pepo.(wanafunzi walishindwa hivi karibuni 9:28).

k.39 Yesu alisemaje? Je! alikasirika kwa sababu eti mtu anatoa pepo kwa Jinalake bila kujiunga naye? La! Yesu hakusumbuliwa na habari hiyo. Kamaalikuwa akitegemea uwezo wa Jina lake itakuwa vigumu yule mtu awe dhidiyake na kumsemea vibaya. Yawezekana alikuwa mfuasi wa kweli ila hakuwakatika kundi la wale waliojitoa kufuatana naye kila wakati. Kwa kulitumia jinalake alikuwa ametambua mamlaka ya Yesu juu ya mapepo. Tusimaanishekwamba Yesu alifundisha kwamba ni vema kufanya kazi ya Kikristo halitumejitenga na wengine.

k.40 Ikiwa mtu hawi kinyume cha Yesu na wafuasi wake ni kama amekuwaupande wake. Kama watu wamebarikiwa na kutolewa katika utumwa wadhambi na maovu kwa msaada wa wengine walio wa dhehebu jingine aushirika lingine, tusiwazuie au kuwapoza. Maneno hayo ya Yesu ni kemeo kwauadui na wivu na uvutano uliopo kati ya madhehebu, na ni kemeo kwa hali yakujiona shirika letu kuwa safi kuliko jingine.

k.41 Neno hilo lahusika na watumishi wa Kanisa na ukaribishaji wao.Watumishi wawe radhi na jambo lolote, hata likiwa dogo, wanalotendewa kwasababu ni watumishi wa Kristo. Jambo linalofanya ‘kikombe cha maji’ kuwa chamaana ni kwa sababu kinatolewa kwa ‘watu wa Kristo’ na ikiwa kimetolewa kwawatu wake kimetolewa Kwake, ni kipawa Kwake (Mt.25:37-40). Kila afanyalomfuasi wa Kristo afanye kwa nia safi. Ni rahisi sana kumpa mtu kikombe chamaji, hakumgharimia mtu kitu, ila kwa njia yake mtu hushirikiana katika utumewa Yesu na wa Kanisa. Yesu hakufundisha kwamba tufanye mambo kamahayo ili tupate thawabu, hatuwezi kujistahilisha mbele zake, ila alitaka tujuekwamba machoni mwake hadharau mambo madogomadogo yanayofanyikakwa ajili yake, tusifikiri ataka mambo makubwa kama kutoa pepo tu.Inayotakiwa ni kumwamini na kumtii na kumpenda.

Twajifunza kwamba Yesu hapendi tabia ya kutokuchukuliana na wengine, walahapendi tuwachukie wale walio nje. Tusifikiri kwamba tumekosa katika utiifuwetu Kwake tunapowakaribisha wengine, yote hutegemea ‘Jina lake’ jambokubwa ni kwa watu kukiri Jina lake kwa kweli.

MARKO 215

9:42-48 Kuwakosesha wengine na kujikoseshaHapo Yesu aweke mbele za wafuasi wake matakwa yake makali ya kujitawala.

k.42 ‘wadogo’ waweza kuwa watoto au waumini dhaifu na waliodharauliwa.Yesu alifundisha kwamba ni dhambi kubwa kufanya neno la kumwangusha aukumfanya mtu akate tamaa na kuacha kumfuata Kristo. Labda yule aliyetajwakatika k.38 aliyekatazwa na wanafunzi asitoe pepo, alikatishwa tamaaasiendelee kutoa pepo tena. Yesu alisema hukumu itakuwa kali kwa mtuatakayemkosesha mwingine. Jiwe la kusagia lililotajwa lilikuwa lile kubwalililoendeshwa na punda, si lile dogo lililoendeshwa na mwanamke. Ni tahadharikubwa kwa wafuasi wa Kristo. Imetupasa kuwakaribisha kwa moyo wauminiwenzetu walio dhaifu, wasio na uvutiko, wasio na marafiki, walio na hali yachini, na wale walio tofauti na sisi wenyewe.

k.43ku Baada ya kusema juu ya kuwakosesha wengine Yesu alisema juu yakujikosesha wenyewe. Yaani kuwa na mambo katika maisha yetu yaliyokinyume cha mapenzi ya Mungu. Shauri la Yesu ni kwamba tuwe kali kwadhambi zetu, tusijihurumie, tusibembeleze dhambi, na tusitengeneze maishayetu juu juu na nusu nusu. Mikono, miguu, macho ni viungo vya maana sana,navyo vyawakilisha mwili wetu mzima. Kwa viungo hivi twafanya matendombalimbali, na tunawajibika kwa yale yanayotendeka. Yesu hakuwa na maanakwamba tukate mkono hasa ila ni lugha ya kuonyesha ukali unaotakiwa katikakujizuia ili tusifanye dhambi. Na kwa nini tuwe wakali namna hiyo? ni kwasababu maisha yanayopatana na mapenzi ya Mungu ni ya maana sana kupitamaisha ya kimwili tu. Kuingia katika uzima na kuingia katika Ufalme wa Mungu,ni maneno ya kuonyesha ubora wa maisha ya kiroho dhidhi ya maisha yakimwili.

Jehanum limepata jina lake kutoka Bonde la wana wa Hinomu, mahali ambapowatoto walitolewa dhabihu kwa Moleki ambaye amedhaniwa kuwa mungu waWaamoni (2 Waf.23:10; 2 Nya.33:6; Yer.7:31). Baadaye Yosia, Mfalmemwema, alibadili matumizi ya bonde hilo na kupaweka kuwa mahali pa kutupiatakataka za Yerusalemu na kuzichoma moto ulioendelea kuwaka daima. Markoalirudia kutaja kiungo fulani na hukumu ya jehanum ili asisitize uzito na hatariya kuruhusu dhambi katika maisha. Mtu achague kati ya ‘kufuga’ dhambi nakupotea, au kuwa mkali kwa dhambi na kuifukuza mara ili awe mzima nakuendelea hadi afike kwenye uzima wa milele. Maneno ya k.48 ni ukumbushowa maneno ya Isa.66:24 yanayosisitiza hukumu ya Mungu isiyobadilika, iliyo namatokeo katika umilele.

9:49-50 Habari ya chumvik.49 Ni vigumu kuelewa habari hiyo. Kazi ya chumvi ni kuzuia maozo nakutunza afya na uzima wa vitu. Sadaka za Waisraeli zilitiwa chumvi (Law.2:13;Eze.43:24) ‘kila mtu atatiwa chumvi kwa moto’ huenda maana yake mtuhutakaswa kwa mateso anayopata kwa ajili ya Kristo (1 Pet.1:7; 4:12). Mkristo

MARKO216

huitwa kujitoa kama dhabihu iliyo hai (Rum.12:1). Moto huharibu vituvinavyopotea na kusafisha vitu vinavyodumu.

k.50 Ila chumvi huhitaji kushika hali yake ya chumvi, ikipoteza hali hiyo hakunanjia ya kuirudishia. Haina kazi tena. Inaonekana neno la mwisho ‘mkakae kwaamani ninyi kwa ninyi’ yahusu mashindano waliyokuwa nayo wanafunzi haponyuma.

10:1-12 Swala la Talaka (Mt.19:1ku)Yesu aliondoka Kapernaumu na kuanza safari ya kwenda Yerusalemu,akielekea kusini mashariki ya Mto Yordani, eneo la Perea katika utawala waMfalme Herode Antipa. Pengine alivuka Mto Yordani mara kwa mara na kuingiaYudea na kurudi tena eneo la Perea. Ni katika sehemu hizo ambapo YohanaMbatizaji alifanya huduma yake.

‘Makutano mengine wakakutanika tena’ pengine maneno hayo yajumlisha jinsiumati wa watu walivyokutanika mara kwa mara. Tuliona ya kuwa kwa miezikadha Yesu hakufanya huduma ya hadharani huko Galilaya, lakini alipotelemkachini alirudia kufanya huduma ya namna hiyo. Marko alipenda kusisitizamazoea yake ya kuwafundisha watu. Alishika kila nafasi iliyopatikana yakuwaelimisha watu juu ya Ufalme wa Mungu.

k.2 Mafarisayo walimwendea wakitaka kujua maoni yake juu ya swala mojalililozungumziwa sana. Ila hawakuwa na nia safi, walitaka kumtega kwakumwulia swali ambalo akijibu hivi watamshtaki na akijibu tofauti watamshtaki.Daima walikuwa na uadui juu yake (2:16,24; 3:6,22; 7:1ku. 8:11). Kwa swali laowalitafuta kupunguza sifa zake mbele za watu na kuonyesha jinsi asivyofaakuwa Masihi wao. Huenda hila yao ilikuwa kumvuta Herode apate neno juuyake. Yohana Mbatizaji aliuawa kwa sababu alimshtaki Herode kuwa amekosakatika kumchukua Herodia awe mkewe. Ikiwa watamvuta Yesu atoe maoni yakulingana na yale ya Mbatizaji, yawezekana Herode atamchukulia hatua.Pamoja na hayo walitaka kuona kama atakwenda kinyume cha alivyoamuruMusa.

k.3-4 Yesu aliwakabili moja kwa moja na kuwauliza ‘Musa aliwaamuru nini?’Katika Amri 10 moja ilisema ‘usizini’ ila walipojibu hawakutaja amri hiyo bali ileruhusa ya Musa kuhusu talaka (Kum.24:1). Musa alitoa ruhusa kwa mtukumwandikia mkewe talaka ikiwa ameona ‘neno ovu kwake’. Lakini ‘neno ovu’ni neno gani? Wakati wa Yesu walikuwapo marabi wawili mashuhuri, Hilleli naShammai, kila mmoja alikuwa na wafuasi. Shammai alikuwa na maoni makalina alisema kwamba neno ovu ni moja tu, la mke kuzini. Ila Hilleli alikuwamlegevu alisema kwamba neno ovu laweza kuwa kama mke ameharibuchakula, au amesema sana kwa sauti kubwa nyumbani kiasi cha jirani zakekumsikia, na mambo madogo kama hayo. Wayahudi kwa jumla walikubalitalaka iwepo.

MARKO 217

k.5 Lakini Yesu alieleza sababu za Musa kuruhusu talaka. Shabaha yakeilikuwa kuleta nafuu ili lisiwe jambo la kawaida kwa mtu kuachana na mkeweisipokuwa kwa kuzini tu. Tena Musa alifanya jambo jema katika kuamurukwamba mtu anayemwacha mkewe sharti amwandikie hati kusudi haki za mkezihifadhiwe, asiachwe ovyo tu. Katika ugumu wa mioyo yao walikosakuonyesha huruma na msamaha kwa wake zao. Kwa njia hiyo Musa alitambuaudhaifu wa wanadamu akichukuliana na dhambi yao ya kutokukaa katikamapenzi ya Mungu.

k.6-9 Lakini Yesu aliona ‘kwa nini wazungumze juu ya talaka, afadhaliwazungumze juu ya ndoa na asili yake katika uumbaji na mapenzi ya Mungu’.Hivyo aliwarudisha nyuma ya wakati wa Musa kwa wakati wa Uumbaji. Ndoailitoka kwa Mungu kwa sababu aliwaumba wanadamu kuwa jinsia mbili, uke naume. Ndipo aliamuru mume mmoja aache uhusiano wake na wazazi iliamchukue mwanamke mmoja na kukaa naye katika uhusiano wa karibu kabisa(Mwa.1:27; 2:24). Wanadamu wa kwanza walikuwa mume mmoja na mkemmoja (si wake). Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu na mpango wake safi. Kwajinsi walivyoumbwa, kila mmoja umeumbwa kwa ajili ya mwenzake, kwa kuishinaye kwa karibu kabisa hata wahesabiwe ‘mwili mmoja’. Katika ndoa Munguanawaunganisha, kwa sababu ni mapenzi yake waishi hivyo. Kwa hiyo mapenziya Mungu ni kwamba ndoa iwe kwa maisha yote, wala haitanguki. Ni amri yaMungu kwa wanadamu wote, si kwa Wakristo tu. Tuwe na tahadharitunaposema ‘ndoa ya Kikristo’ ipo ndoa ya Wakristo na inatazamiwa kwamba,kwa neema ya Mungu, watatimiza mapenzi ya Mungu. Ila mapenzi ya Mungu sikwa Wakristo tu bali ni kwa watu wote, ndoa iliingia mara wanadamuwalipoumbwa kuwa jinsia mbili. Hivyo Yesu aliinua ndoa ili iwe na heshimakubwa kama Mungu alivyokusudia, ni kipawa chake chema kwa wanadamuwote. Yesu alionyesha kwamba Mungu hapendezwi na talaka, talaka ni isharaya ugumu wa wanadamu wasiokaa katika mapenzi yake. Hata tukisema niniamri ya Mungu ingali imesimama kwa Uumbaji wote.

Kwa hiyo Yesu alisisitiza mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi wakati wauumbaji wa wanadamu (Mwa.1:22; 2:24). Ni vigumu kusema kwamba Musaaliamuru au aliunga mkono kuwepo kwa talaka (k.4 hata Mafarisayohawakusema Musa aliamuru talaka) ila kwa hali iliyokuwepo ya ndoa nyingikuvunjika yeye alileta nafasi hiyo kwa shabaha ya kuleta nafuu. Musa alijuakwamba shida si katika mapenzi ya Mungu bali katika udhaifu na ugumu wawatu wasiotaka kukaa katika mapenzi ya Mungu. Musa aliingiza jambo la talakabaada ya kuonekana kwa shida hiyo.

Tuseme nini juu ya wakati wetu wa sasa, wakati ambapo jambo la ndoalinashambuliwa sana na wengi sana wameshindwa kufuata mapenzi ya Mungu.Lazima Kanisa lisimame imara katika kushikilia mapenzi ya Munguyasiyobadilika na kushuhudia kwamba kupeana talaka si njia bora wala nenojema. Hata hivyo Kanisa linawajibika kuwasaidia wale ambao wameshindwa na

MARKO218

kukubali talaka iwepo, hata likiwa si jambo jema, ni afadhali kuliko watu kuishiovyo bila kanuni yoyote. Talaka husaidia watu kujipatia haki zao kisheria ilakamwe isihesabiwe kuwa neno bora. Hii ni tofauti na kukubaliana na jamii yawatu wasemao kwamba talaka ni sawa.

Ni vema kufundisha watu juu ya Ndoa, asili yake na makusudi yake, na yakuwa ni mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.Ndoa si patano la kibinadamutu. Kuvunja ndoa si kuvunja patano tu, bali ni kuvunja makusudi ya Mungu kwawanadamu walioumbwa kwa jinsia mbili tofauti.

k.10-12 Waliporudi nyumbani wanafunzi wakamwuliza Yesu juu ya neno hilo.Inaonekana walitaka kujua kuhusu wale wanaowaacha wenzao. Ikiwa mtuameacha au ameachwa, Je! aweza kuoa au kuolewa tena? Yesu aliweka jinsiambili kuwa sawa, tofauti na Wayahudi ambao walimruhusu mtu atoe talaka kwamkewe lakini hakumruhusu mke atoe talaka kwa mumewe, ila Warumi kwasheria yao waliwaruhusu wake kumpa talaka mume zao. Yesu alisema kwambakuoa au kuolewa tena ni kuzini, tena ni kuzini juu ya (si kwa) mkewe aumumewe. Kuoa/olewa tena ni kama sawa na kuharibu ‘mwili mmoja’, ikiwatalaka hairuhusiwi, kuoa/olewa hakuruhusiwi. Hakuna maana ya kuruhusutalaka bila kuruhusu kuoa/olewa tena. Mathayo katika Injili yake (19:9) aliwekanafasi kwa talaka kwa sababu ya ‘uasherati’ ila Marko na Luka hakuweka nafasihiyo. Fundisho la Yesu lilikuwa gumu na lilikuwa jipya katika kuwaweka mumena mke sawa katika wajibu wa kila mmoja kuwa mwaminifu kwa mwenzake.

10:13-16 Yesu aliwabarikia watoto (Mt.10:13-15; Lk.18:15-17)k.13 Hatuambiwi watoto hao waliletwa na akina nani, baba na mama zao, auwatoto wenzao; wala hatuambiwi walikuwa nje au karibu na nyumba alimokaaYesu. Pengine wanafunzi walikuwa mlangoni na walipoona hao watotowakiletwa na jamaa zao waliamua kwamba ni vema Yesu asisumbuliwe nao.Waliwakemea wale waliowaleta. Pengine walitaka kumlinda Yesu apatemapumziko; pengine wao wenyewe hawakutaka kuwashughulikia hao watoto;au huenda waliwaza kwamba hao watoto hawahusiki na huo Ufalme hasa.Katika mawazo yao kushughulikia watoto hakukulingana na shabaha ya Yesuna Ufalme wake, si ataipindua serikali atakapofika Yerusalemu!

k.14 Ila Yesu alichukizwa, ni hapo tu katika Injili twasoma habari za Yesukuchukizwa, ni kama aliona huzuni kubwa na hasira. Pengine aliwaza kwambawanafunzi walijichukulia madaraka ya kuamua ni akina nani wa kukaribishwa.Tukumbuke kwamba hapo nyuma walikuwa wamemkataza mtu aliyekuwaakitoa pepo kwa sababu hakuwa mmoja wao na Yesu aliwakemea. Tenawalipogombana wao kwa wao juu ya nani atakayekuwa mkubwa (9:33-37)Yesu alichukua mtoto na kumweka katikati yao. Bado hawajajifunza kutokanana habari hizo. Haidhuru walikuwa na sababu zipi, ilikuwa dhahiri kwamba Yesuhakukubaliana nao. Hivyo aliwarekebisha kwa kuwaambia ‘waacheni watoto

MARKO 219

wadogo waje kwangu msiwazuie kwa maana watoto kama hawa ufalme waMungu ni wao’. Wanafunzi walikosa kuelewa mambo kadhaa:

a) watoto ni wa thamani sana na inawapasa wapokelewe vizuri;b) yeyote atakaye kuuingia Ufalme wa Mungu apaswa afanane na mtoto;c) hali na tabia ya Ufalme wa Mungu zafanana na hali na tabia ya mtoto.

k.15 Yesu aliendelea kwa kutilia mkazo wa uzito wa maneno yake kwa kutumianeno ‘Amin, nawaambieni’ ni tamko kubwa kuhusu njia ya kuupokea Ufalme waMungu. Mtu ataingia Ufalme wake akifanana na mtoto ambaye kawaida yake nikupokea kitu kwa urahisi. Mtu apaswa aupokee Ufalme kama mtoto apokeavyokipawa fulani. Mtoto ni mdogo na hajitegemei; huwategemea wazazi nawengine kwa msaada wa kuishi kwake. Vivyo hivyo, Ufalme wa Mungu ni kwawale wasiojiona kuwa na uwezo, wasiotaka kujistahilisha mbele za Mungu. Nikwa wanyonge na waliowekwa nje na jamaa; kwa maskini na wasiotakakuonekana. Ufalme ni kipawa cha kupokelewa tu. Tena, Yesu kwa mafundishoyake ameonyesha kwamba watoto waweza kuushiriki Ufalme kabla hawajawawatu wazima; na ni watu wazima wanaopaswa wajigeuze kuwa watoto iliwaushiriki. Siyo kusema kwamba watoto hawana dhambi ila wanazo tabiakadha zinazotakiwa, utayari wao wa kupokea kitu bila shida, wepesi wakuwaamini na kuwategemea wengine. Watu hupenda kuleta ajenda zao, nivigumu waje mikono mitupu na kupokea neema ya Mungu bure, na kuifurahia.

k.16 Kisha Yesu alithibitisha mafundisho yake kwa tendo la ajabu sana.Aliwapokea hao watoto walioletwa, mmoja mmoja, alimkumbatia kila moja nakumwekea mikono, na kumbariki. Tendo hilo lilikuwa fundisho kubwa sana lakutilia mkazo mafundisho yake. Kwake, watoto ni wa thamani sana, na Ufalmewake hufanana nao katika urahisi wake wa kupatikana, mtu apaswa ampokeeKristo kama wanavyompokea mtoto, wasitafute makubwa. Hivyo Yesualionyesha kwamba kuishi chini ya utawala wa Mungu katika Ufalme wake nitofauti na kuishi kwa desturi na kawaida za umma.

Katika sehemu ifuatayo twaona Yesu akisema mengi kuhusu mali nakuonyesha jinsi ambavyo madai yake ya kujitoa kabisa Kwake na hali ya kuwana mali vinavyopishana na kuleta shida kwa mtu mwenye mali anayetakakujitoa Kwake.

10:17-22 Habari ya kijana, tajiri, aliyemjia Yesu (Mt.19:16-30; Lk.18:18-30)k.17 Yesu na wanafunzi walisafiri tena na walipokuwa njiani mtu mmoja akajambio. Mathayo ametaja kwamba huyu alikuwa kijana (Mt.19:22) na Lukaamemtaja kuwa mkubwa (Lk.18:18) na wote walisema alikuwa tajiri.

Alikuja kwa mbio, kama mtu mwenye bidii akitaka kujua jinsi ya kupata uzimawa milele. Alimjia Yesu kwa adabu na kwa heshimu alimpigia magoti. Ndipoakasema ‘Mwalimu mwema’, tena neno ‘mwema’ liliongeza heshima kwa Yesukwa sababu haikuwa kawaida kuwaita Marabi namna hiyo. Bila shaka alikuwa

MARKO220

akifanya hayo yote kwa ukweli wa moyo. Swali lake lilikuwa la maana sana,tena kubwa sana, la kiroho ‘nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?’(pamoja na k.30 ni hapo tu ambapo Marko ametumia neno ‘uzima wa milele’ ilakatika Injili ya Yohana ni neno lililotumika sana). Kwa hiyo, ni dhahiri kwambahuyo mtu, ijapokuwa alikuwa na mali nyingi na amejitahidi kushika amri zaMungu, bado angali akisikia upungufu maishani mwake.k.18 Yesu alishika neno ‘mwema’ na kumfanya alizingatie zaidi. ‘Kwa ninikuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu’. Tusifikirikwamba Yesu alikana kuwa mwema, wala hakuwa Mungu, ila alitaka huyokijana anapowaza ‘wema’ hasa amwaze Mungu ili apate kujua ‘wema’ halisi.Mungu ni Mwema kabisa, Yesu ni mwema kwa kadiri anavyohitimu maisha yakibinadamu kwa kuyashinda majaribu yake. Yesu alijifunza utii kwa yaleyaliyompata (Ebr.5:8). Mapenzi ya Mungu yamefunuliwa katika Amri kumi,mapenzi ya Mungu ndiyo ‘wema’ hasa. Ni wazi kwamba Yesu hakuja kuondoaTorati katika shabaha yake ya kuwa mwongozo na ufunuo wa mapenzi yaMungu. Alikuja kuiondoa kuwa njia ya Wokovu kwa sababu hakuna mtuawezaye kuitimiza, hata hivyo, daima inadumu kuwa kanuni na msingi wawema na utakatifu. Yesu alifunua viini vyake katika Mathayo 5 na 6.k.19 Yesu aliendelea kwa kuzitaja amri kadhaa, zote alizozitaja zilitoka katikasehemu ya pili ya Amri 10, zilizohusu ‘kupenda jirani’.

k.20 Kijana akaitika kwa kusema kwamba alikuwa amezishika hizo zote tanguutoto wake. Si vema tuwaze kwamba alikuwa akijivuna, au alikuwa akidai hakiyake kibinafsi, maana amemjia Yesu kwa unyenyekevu akikiri upungufu kwanjia ya swali lake. Kama angalitosheka asingalimjia, wala asingalimwuliza swalikama lile alilomwuliza. Ila alidhani kwamba amezishika, ila machoni mwa Yesusivyo, amezishika juujuu tu. Kwa nini hana amani ikiwa amewapenda jirani zakekama nafsi yake? Alikuwa akingojea kuambiwa afanye jambo moja kubwa na laustahili litakalompatia hali njema kuliko aliyokuwa nayo kwa mali na maishasafi. Alihisi kwamba kuna jambo lipitalo lile la kushika amri.

k.21 Kisha Yesu akamgusa penye shida yake, shida ya kufikiri kwamba awezakufanya jambo litakalomstahilisha machoni mwa Mungu na kumleta katikaushirikiano mwema naye. Hii ndiyo shida na kosa la wanadamu kutokana nakiburi chake cha kujitegemea (Rum.7:18). Yesu akamkazia macho,akampenda. Mbele yake ni kijana mzuri sana, mwadilifu, aliye na kila kitu chadunia hii, kijana alitafuta kwa bidii kitu bora kuliko vyote alivyo navyo, yaani,uzima wa milele. Kwa hiari yake amemjia Yesu. Yesu alitaka sana kumsaidia,alimhurumia katika hali yake. Alimpenda, si kwa sababu yoyote ila ile yakumhurumia tu. Na katika upendo huo alimfunulia jinsi msingi wa maisha yakeusivyokuwa imara. Alikuwa na ‘mungu’ mwingine, mali, ambayo aliiabudu kama‘sanamu’ na kwa sababu hiyo, potelea mbali amedai kushika Amri, ameivunjaile ya kwanza kabisa iliyo msingi wa amri zote ‘usiwe na miungu mingine ilaMimi’. Mali ilikuwa imemshika, mali ambayo si kitu imara cha kujenga maishajuu yake. Yesu akampa changamoto ya kuachana na mali yake na kumfuata

MARKO 221

Yeye kila siku. Ajifunze kwamba uzuri wa maisha ni katika kuishi kwa neema narehema za Mungu si kuishi kwa mali. Akifanya hivyo atakuwa amemwaminiKristo kweli na kuacha utumishi wa mali na dunia hii. Kwa jinsi Yesualivyomwambia ‘enenda, ukauze ulivyo navyo..’ Yesu alimfunulia kipaumbelechake, na itambidi abadili kipaumbele hicho kwa sababu mali itamzuiaasimfuate Yesu kwa moyo na kwa kweli. Abadili hazina ya duniani kwa ile yambinguni.

Yesu hakuwa na maana kwamba mtu ataokolewa kwa matendo mema au kwakutenda tendo moja kubwa kama kuachana na mali La! mtu huokolewa kwakujihusisha na Yesu Mwenyewe. Hapo Yesu amejiweka juu sana kuwa yule wakufuatwa, aliyestahili kupata utiifu wote wa mtu, sawa na Mungu Mwenyewe.Hivyo kwa maneno yake alikuwa amedai kuwa Mungu bila kutamka kwa wazi.

k.22 Yule kijana alionaje? Akashindwa kuyapokea mashauri ya Yesu. Yulealiyemjia kwa moyo mkuu akaondoka hali uso wake umekunjamana, kamawingu jeusi limemfunika, furaha yake ilibadilika kuwa huzuni, kwa nini? kwasababu alikuwa na mali nyingi. Aliomba dawa kwa upungufu aliosikia, ila dawaaliyopewa hakuipenda, akakataa kuimeza, na upungufu wake ulibaki. Alitakakuchagua la kufanya na kutokufanya, alitaka kuwa ‘bwana’ wa maisha yake, naalipenda kuendelea na mali yake kuliko kupata maisha ya uzima; mali ilikuwa‘bwana’ wake na yeye alikuwa ‘mtumishi’ wake. Hatujui ikiwa baadaye alijihojina kuubadili uamuzi wake.

Neno la Yesu lilikuwa kwake, si neno kwa kila mtu kila wakati. Yesu alijua shidayake na kusema naye kulingana na haja yake na ndivyo atakavyofanya kwa kilaatakaye kumfuata.

Habari hiyo ina fundisho kubwa. Twajifunza kwamba iwapo kuwa na mali sidhambi, ikiwa imepatikana kwa halali, hata hivyo, ni hatari. Agano Jipya lotelasema juu ya hatari yake. Mali huleta wajibu mkubwa kwa mtu. Bila shaka kwamawazo ya kibinadamu huyu kijana alikuwa mtu wa kupewa pongezi. Uzima wamilele ni kipawa cha Mungu, mtu haupati kwa kuhitimu mtihani na kupata maksiza juu. Mtu hupata kwa kujihusisha vema na Yesu ambaye msingi wa maishayake ulikuwa ‘ni bora kutoa kuliko kupata’. Huyo kijana aliwezaje kujihusishavema na Yesu asipokuwa tayari kubadili msingi wa maisha wa kufikiri ‘ni borakupata kuliko kutoa’, si watapishana! Kuwa na mali na cheo na sifa na usalamasi msingi imara, huyo kijana kwa jinsi alivyokataa mwito wa Yesu hakuwa tayarikuishi kwa kanuni za Ufalme wa Mungu. Yesu alimwita aende kinyume chamaisha yake ya hapo nyuma, naye hakuwa tayari kubadili mwenendo wake.

Yesu hakufanya lolote la kumshawishi kijana aubadili uamuzi wake, alimwachaaondoke, na hatujui kama alifanyaje baadaye. Yeye hapunguzi madai yakewala hamsumbui mtu.

MARKO222

10:23-31 Shida za kuwa na malik.23 Kijana alipoondoka Yesu alibaki na wanafunzi wake. Bila shaka wanafunziwalikuwa na maswali mengi na Yesu alijua hayo. Aliendelea kuongea nao juuya shida za kuwa na mali kwa mtu atakaye kuingia katika Ufalme wake au kwalugha nyingine kwa mtu atakaye kuupata uzima wa milele. Yesu alisisitiza tenayale aliyosema kwa kijana ila kwa kutia chumvi juu ya shida za mali. Hakusemamali nyingi, bali mali, (neno ni vitu) kama hata vitu ni shida, pengine si fedha tu,bali mali aina yoyote na alitaja kutegemea mali (k.24).

k.24 Wanafunzi walishangaa sana, kwa sababu alivyosema Yesu ilikwendakinyume cha mawazo ya Wayahudi. Wao walidhani kwamba kuwa na mali nidalili ya baraka za Mungu (Kum.28:1-14; 1 Nya. 29:12) na dhidi yake, kuwamaskini ilikuwa ishara ya Mungu kutokupendezwa na mtu. Ndiyo hoja ya rafikiza Ayubu, wakati wa Ayubu kupatwa na hasara kubwa. Walimlaumu Ayubualipojitetea kuwa bila hatia, kwa sababu, wao vilevile walishika mawazo hayo(Ayu.15:29; 4:7,8; 5:2) ila watu wangalielewa Agano la Kale vizuri wangalionakwamba yalikuwemo mafundisho yaliyokanusha mawazo ya mafanikio kuwadalili ya baraka za Mungu (Zab.73:12,18; Yer.9:23,24). Ili awavute kujali mambohayo Yesu aliwaita wanafunzi ‘watoto’ akionyesha upendo wake kwao na jinsialivyokuwa na mzigo juu yao ili waelewe vizuri mafundisho yake. Ijapokuwawalikuwa dhaifu na kuwa watu waliokosa kuelewa vizuri, hata hivyo,alichukuliana nao kwa upendo. Alitaka watambue hatari ya kutegemea kituchochote nje ya kumtegemea Yeye Mwenyewe. Hata maskini waweza kutakautajiri.

k.25 Ndipo Yesu alitumia methali ya kuchekesha, kwa kutaja ‘ngamia’ mnyamamkubwa kuliko wengine wote katika Palestina, na tundu la sindano, litoalonafasi ndogo sana kwa kitu kulipitia. Kusudi lake lilikuwa kuonyesha jinsiisivyowezekana kwa mtu yeyote, licha ya matajiri, kujiokoa wenyewe. Kwa jinsiisivyowezekana kamwe ngamia apenye tundu la sindano, vivyo hivyo, mtukamwe hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa nguvu au akili au jitihadaau mali zake mwenyewe. Watu walidhani kwamba ni rahisi zaidi kwa matajiri,lakini Yesu alizidi kutia makali mafundisho yake.k.26 Kutokana na Yesu kutia makali mafundisho yake wanafunzi wakazidikushangaa hata wakamwambia ‘Ni nani, basi, awezaye kuokoka?’ Penginendilo lengo lake katika mazungumzo hayo yote, alitaka wajifunze kwambahakuna mtu yeyote awezaye kustahili wokovu, ni kipawa cha Mungu, kamaalivyokuwa akionyesha alipowapokea wanyonge, watoto wadogo, nakukaribisha wale watu ambao hawakuhesabiwa kuwa kitu na jamii. Ni vigumukwa mtu yeyote kwa sababu kila mtu anacho ‘kitu’ kinachowakilisha utajiriwake, ambacho apaswa kuwa tayari kuachana nacho ili auingie Ufalme waMungu. Yesu alitaka kubomoa mawazo ya wale waliofikiri kwamba kufanyamatendo mema ni msingi wa Mungu kupokea au kutokupokea watu (Efe.2:8)(matajiri walifikiri kwamba kwa misaada mbalimbali waliyofanya kwa watuwatapokelewa na Mungu). Wote huanzia kwa usawa, usawa wa ‘utupu’,

MARKO 223

asiyekubali kuwa ‘mtupu’ hawezi kupokelewa. Hivyo, Yesu aliyapindua mawazoya watu kuhusu Ufalme wa Mungu, ni kinyume cha kawaida za ulimwengu huu.

k.27 Yesu alizidi kuwavuta, akawakazia macho ili audake usikivu wao.Akawaambia kwamba lisilowezekana kwa wanadamu, lawezekana kwa Mungu.Ni neno la kuwatumainisha na neno la kuonyesha kwamba Mungu hufanya kazikatika maisha ya wanadamu, hata katika maisha yao.

k.28 Petro, aliyekuwa msemaji wa wenzake, alisema kwa niaba yao, haliwamejifikiria wenyewe jinsi ambavyo walikuwa wameacha jamaa zao na kazizao za kila siku, ili wamfuate. Huenda walitambua jinsi walivyofanya walipoonayule kijana akiondoka, hali ameshindwa kuacha mambo yake mwenyewe.‘Tumeacha vyote tukakufuata wewe’ Katika Mathayo kuna nyongeza ‘tutapatanini?’. Mambo yenyewe yaliyoachwa si kitu, jambo kubwa ni kwamba mtuameyaacha, kama ni madogo au kama ni makubwa.

k.29-30 Yesu aliwahakikishia kwamba mtu hapati hasara katika kuacha vitukwa ajili yake na kwa ajili ya Injili. Atafanyiwa kwa ukarimu sana, Mungu hawezikuwa mdeni kwa mtu. Sijui kwa nini alitaja ‘mama’ asitaje ‘baba’ huenda kwasababu ya kumwaza Mungu kuwa ndiye ‘baba’ yetu hasa. Alitaja mahusiano yaukaribu sana. Kwa sababu katika Injili watu huishi kwa kanuni tofauti na zaulimwengu; waumini wenzao watakuwa kama ‘mama’ na ‘ndugu’ kwao, hivyo,hawatapata shida. Jambo hilo limethibitishwa na watumishi wengi na waliojitoakwa kazi ya Mungu. Hata wanafunzi watakapoachwa na Yesu na kuendelea nakazi za kuhubiri Injili hawana haja ya kuogopa. Ila pia wasisahau kwambawatateswa kwa ajili yake na kwa ajili ya Injili. Kwa hiyo yale watakayoyakosakwa ‘jamii ya ulimwengu huu’ watayapata katika ‘jamii mpya, familia ya Mungu’ambayo Kristo amekuja kuiunda. Jamii hiyo mpya huendeshwa na nguvu yaInjili inayomwokoa mtu na dhambi za kujipenda na kujiona na kujiendeleza(3:31-35). Pamoja na baraka za hapa duniani muumini atajaliwa uzima wamilele.

k.31 Kisha Yesu aliwaonya wanafunzi. Wao ni wa kwanza kumfuata, naowatakuwa wa kwanza kupeleka habari zake ulimwenguni, ila siyo kusemakwamba watakuwa ‘wa kwanza’ katika uzima wa milele, kwa sababu katikauzima wa milele, wa kwanza watakuwa wa mwisho na wa mwisho wa kwanza.Maana yake mambo hayawi kama yalivyo katika ulimwengu huu. Katika Ufalmewa Mungu jambo kubwa si vyeo na heshima bali ni kutumika. Yesu hatakiwafuasi wake wapate roho ya kufanya mapatano (Mt.20:1-16) wakumbuke yakuwa katika Ufalme wake, wajane, na maskini, na waliowekwa kando na jamii,na watoto hukaribishwa kwa moyo. Ufuasi ni utumishi si vyeo. Wasiishi kwamawazo ya kujistahilisha hata katika utumishi, ni hatari baada ya kuokolewakwa neema, kutokuendelea kutumika kwa neema.

MARKO224

10:32-34 Onyo la tatu kuhusu Kifo chake (Mt.20:17-19; Lk.18: 31-34)k.32 Yesu na wanafunzi walikuwa wakienda Yerusalemu na kwa kadiriwalivyoukaribia Mji Mkuu ndivyo Yesu alivyozidi kushikwa na mawazo yamateso atakayopata pale. Ni mara ya kwanza Marko kutaja Yerusalemu, paleYerusalemu ni mahali pa kutimizia mapenzi ya Mungu juu ya Masihi wake.Katika kwenda walifanana na maandamano, Yesu alitangulia, na Thenasharawalifuata wakishangaa, ndipo baada yao watu waliogopa, hao ni walewaliofuatana nao mara kwa mara. Kwa jinsi ambavyo Marko ameandika habarihizo Yesu alishikwa na nia ya kukazana kwenda mbele kwa yale yaliyokuwambele yake (Lk.9:51) pengine alitembea kwa haraka na kwa uzito wa hali ilapamoja na uzito alisikia furaha nyingi alipoelekea kufikia upeo wa Utume wakekatika Kufa Kwake. Wanafunzi walisikia shida sana walipomtazama na kuonahali yake, na huenda uzito wa hali uliwafanya watembee kwa upole. Bila shakawalikuwa wakitafakari onyo lake juu ya mateso yake.

k.32b Akatwaa wale Thenashara na kurudia kuwaambia juu ya mambo yaliyombele yake na mbele yao. Mambo hayo yalikuwa kwao si kwa walewaliofuatana nao.

k.33 ‘Angalieni’ neno la kuuvuta usikivu wao likiwa na tahadhari ndani yake.Yesu alisema mambo wasiyotaka kuyasikia, ila lazima waambiwe, ni sehemukatika matayarisho yao, kwa sababu, yatakayotokea yatakuwa dhidi ya mawazoyao yote. Kisha akawafafanulia yale mambo. Mara mbili ameishawambiamambo kadha (8:31; 9:31) ila hapo aliongeza kwa kutaja mambo yenyewe;kudhihakiwa, kutemewa mate, n.k. Yote yalifanyika (15:15ku). Alitaja piaKufufuka Kwake, ila kwa sababu ya hali yao inaonekana walishindwa kusikiahabari hiyo vizuri. Kama wangalidaka neno hilo mambo yote yangalionekanatofauti. Yesu alionyesha kwamba atauawa baada ya kuhukumiwa na BarazaKuu la Sanhedrini lenye viongozi wa dini, viongozi wa kiroho. Na baada ya haokutoa hukumu ya kufa ndipo atapelekwa kwa WaMataifa, yaani Warumi, iliauawe kwa kusulibiwa (Mt.20:19). Hakusema mambo hayo kama mtoa taarifabali kwa kuwathibitishia kwamba ni nia yake afe. Kwa hiyo Wayahudiwatamhukumu afe, na WaMataifa watajiunga nao na kumsulibisha. Neno lakuongeza shida yake ni katika watu wake wenyewe, wateule wa Mungu,kumtia mikononi mwa watu wa WaMataifa, watu wa nje. Ni upeo wa chuki nakukataliwa. Kwa kadiri alivyosogea Yerusalemu, ndivyo mawazo ya Kifo chakeyalivyozidi kumshika mpaka katika Bustani ya Gethsemane yalimtia wasiwasina masononeka mengi. Matendo ya ukatili yalizidi kuwa ung’avu rohoni mwake.

Yesu alipotoa onyo hilo alilitangulia kwa kujiita ‘Mwana wa Adamu’ yulealiyetajwa katika Danieli 7:13-14 ambaye atapokea heshima kutoka kwa watuwote na kutawala ulimwengu mzima. Ni kweli kuona kwamba Yesu alitumiaJina hilo huku ametaja mateso yake makali na maudhi na aibu vitakavyompataakiwa huyo Mwana wa Adamu.

MARKO 225

10:35-40 Ombi la Yakobo na Yohana kupewa vyeo (Mt.20:20-23)k.35 Mathayo amesema kwamba mama yao alikuja pamoja nao na kuleta ombikwa Yesu (Mt.20:20). Mama yao aliitwa Salome anayefikiriwa kuwa dada waMariamu, mama wa Yesu, kwa hiyo hao ndugu walikuwa binamu wa Yesu(15:20; Mt.27:56; Yn.19:25). ‘Mwalimu, twataka utufanyie lolotetutakalokuomba’ ombi pana sana.

k.36 Yesu aliwaomba waseme wazi ni nini hasa walichotaka. Hakutaka kujitoakuwafanyia mpaka amepata kujua kutoka kwao ni nini walichotaka.

k.37 Wakatamka wazi kwamba walitaka kuketi mahali pa heshima kubwakatika Ufalme wake. Wametambua kwamba jambo kubwa litatokea paleYerusalemu kuhusu Ufalme wa Mungu na walikuwa na imani kwamba Yesuatafaulu, ila kama ambavyo tumeona wakati wote, wameshindwa kutambua haliya Ufalme huo na njia ambayo kwayo utasimamishwa. Pengine waliwazaKaramu ya Masihi ambayo Wayahudi walifikiri kwamba itafanyika. Ni ombi laajabu tukikumbuka hivi karibuni Yesu amewaambia wazi habari za KudhiliwaKwake, Kuteswa Kwake, na Kuuawa Kwake. Jambo hilo linatuonyesha kwambawalikuwa mbali sana na Yesu katika kuelewa Utume wake. Wameshikwa natamaa ya ukuu, wakiwaza ya kibinafsi, badala ya kujiweka upande wa Yesu nakujiunga naye katika uzito wa matazamio yake ya kuteswa. Huenda walitakakuwahi matukio ambayo walidhani kwamba yatatokea Yerusalemu, yaani Yesukuipindua serikali. Wamekuwa katika kundi la Mitume, tena wamekuwa katikakundi la wale watu ambao Yesu aliwateua kuwa naye mara nyingine (5:37; 9:2).Je! walikuwa na wivu juu ya Petro? Hatujui hasa walisukumwa na nini, huendasi utiifu kwa Yesu bali tamaa ya ukuu. Kwa upande mmoja walikuwa na imanikwamba makubwa yatatokea pale Yerusalemu na Bwana wao atatawazwa, naowalitaka kuwa karibu naye kabisa.

k.38 Kama wangalijua wanaomba nini pengine wasingaliomba. Yesualiwarekebisha ‘Hamjui mnaloliomba’ wamekuwa vipofu, katika kuombaheshima wanaomba mateso! Halafu Yesu alitaja yale yatakayompata ‘kunyweakikombe’ na ‘kubatizwa’. Katika Agano la Kale ‘kikombe’ kiliashiria mambomawili tofauti. Kikombe cha furaha na wokovu (Zab.16:5; 23:5; 116:13) na‘kikombe’ cha hukumu na ghadhabu ya Mungu juu ya dhambi (Zab.11:6;Isa.51:17,22; Yer.25;15,17; Zab.42:7; 69:1,15; 124:4,5; Isa. 43:2). Kikombe chamateso na huzuni kubwa; ubatizo wa kuzama katika hatari na msiba. Hayondiyo yaliyokuwepo kati yake na utukufu wake, ataingia ufalme wake kwa njiaya mateso na kifo. Na kama ilivyo Kwake, ndivyo itakavyokuwa kwa wanafunziwake; wao nao watateswa na kupata dhiki kwa ajili yake, ndipo wataingiakwenye utukufu, si ule wa hapa duniani, bali ule wa mbinguni. Hamna shartilingine kwa uanafunzi wala hamna daraja katika uanafunzi.

k.39 Walipoulizwa kama wataweza kufuata njia hiyo walijibu ‘twaweza’. Hatawalipojibu hivyo ni kama bado hawajaelewa. Ila kwa hao wawili ndivyo

MARKO226

ilivyotokea. Yakobo aliuawa (Mdo.12:2 na Yohana alifukuzwa mpaka PatmoUfu.1:9). Kisha Yesu alisisitiza tena uhusiano uliopo kati yake na wao nauwiano uliopo kati ya mateso na utukufu wake na wao. Ila tusiwaze kwambamateso yao huwa sawa na yale yaliyompata Yesu. Mateso yake na Kifo chakehasa kilikuwa kwa ajili ya kutoa fidia ya dhambi. Yeye atakufa kwa dhambi zaulimwengu, wao watateswa kwa sababu ya kumfuata.

k.40 Halafu Yesu alijibu ombi lao kuhusu vile viti, watapewa wale ambao Babaamewatayarisha kuketi juu yake. Yesu alimnyenyekea Baba na kuona ni hakiya Baba, si haki yake. Si kwa sababu hakuwa sawa na Baba, wala si kwasababu hakuwa Mungu Mwana, la, ila wakati wote hakusikia kwamba ana hajaya kunyang’anya mambo kama hayo (Flp.2:5ku). Hakutaka kutwaa mamlakaholela. Yesu aliposulibiwa wawili walikuwepo, mmoja upande wa kulia, nammoja upande wa kushoto, wote wawili, wahalifu! Na mmoja wao aliahidiwa naYesu kwamba atakuwa pamoja naye peponi kwa sababu alijihusisha vemanaye dakika zake za mwisho za kuishi hapa duniani, wakati ambapo hakuwa nanafasi yoyote ya kujistahilisha mbele zake, ila ile ya kujikabidhi kwake Kristo tuna kutegemea rehema zake.

10:41-45 Ukuu wa kwelik.41 Wanafunzi wengi waliposikia habari za Yakobo na Yohana kuomba vitivya heshima waliwakasirikia. Huenda walidhani kwamba wamefanya hila auwaliwaonea wivu kwa sababu wao vile vile walitamani ukubwa, hawakuwatayari kuwa wa mwisho. Hawakutofautiana nao.

k.42 Yesu kama ilivyokuwa desturi yake na kama Marko alivyopenda kutaja,aliwaita wanafunzi wote Kwake na kuwafundisha tena juu ya ukubwa katikaUfalme wake, kama alivyowaambia hapo nyuma (9:33ku). Aliwakumbushailivyo katika dunia hii, wakuu hupenda kutumia nguvu zao na kuwafanya waliochini yao waonje uzito wa mamlaka yao; hufurahia ukubwa wao na kuutumiakwa faida yao binafsi.

k.43-44 Halafu Yesu aliwaambia wazi kabisa ‘haitakuwa hivyo kwenu’. Ipotofaui kubwa kati ya jinsi wakuu wa dunia wafanyavyo na jinsi iwapasavyo waokufanya. Atakaye kuwa mkubwa atakuwa mtumishi na atakayekuwa wa kwanzaatakuwa mtumwa wa wote. Mtumishi na mtumwa walio nyumbani wapo kwashabaha ya kuwatumikia wenye nyumba. Si vibaya kutaka ukubwa sharti mtuamekubali amewiwa kutumika (kuhusu askofu 1 Tim.3:1 ‘atamani ‘kazi njema’ sicheo). Kuwa mkubwa katika Ufalme wa Mungu ni kupenda na kujitoa. Jamiinzima ya Kikristo waitwa kuwa jamii ya utumishi.

k.45 Ndipo Yesu alijisemea mwenyewe, Yeye alikuwa Mtumishi wa Kujitoa.Katika maisha yake yote alikuwa akizunguka miji na vijiji akihubiri na kuponyawatu na kutoa pepo na kusamehe dhambi na kuwatumainisha wale waliowekwakando ya jamii na kuwainua wale waliokata tamaa. Hakujihurumia, hakujali kula

MARKO 227

na kupumzika, maadamu watu walihitaji msaada alikuwa tayari kujitoa nakuwasaidia. Sasa yu njiani kwenda Yerusalemu ili aufanye ule utumishimkubwa wa kutoa nafsi yake kuwa fidia ya wengi, yaani afe kwa dhambi zaulimwengu. Alisema kwamba alikuja kwa ajili hiyo, ndiyo shabaha hasa ya kujakwake.Alikuja kufanya kazi ile ambaye hakuna aliyeweza wala kustahili kuifanya, kwaajili ya wengi, ili wao wasiwe na haja ya kuifanya. Neno fidia ni neno muhimukabisa, ni neno la kuonyesha kwamba Yesu alitoa gharama ya kuwaokoawanadamu na dhambi zao, kuwakomboa, kuwatoa chini ya utawala wa dhambina Shetani (Kut.21:30; Hes.35:31-32; Law.18:15; 25:51-52) (ling. na 1 Yn.2:2' 1Pet.2:24; 3:18; Rum.3:25). Katika kujitaja kuwa Mtumishi Ateswaye bila shakaYesu alikuwa akidokezea unabii wa Isaya 53. Kwa hiyo, wanafunziwasingalihesabu ni jambo gumu kwa sababu Yesu amekuwa kielelezo chao namsukumo wao (1 Yn.3:16). ‘fidia ya wengi’ haina maana kwamba kuna mpakakatika idadi ya wale watakaokombolewa, ila ina maana kwamba wengiwatapata baraka kutokana na Kifo chake, wote walio tayari kumpokea watajuabaraka hiyo. Yesu alifika upeo wa utumishi wake alipokufa Msalabani. Iwapowanafunzi waliandamana na Yesu kwenda Yerusalemu ni Yeye tu ambayealisikia nafsini mwake upweke wa Utume wake, hata katika wale walioishi nayekila siku kwa miaka mitatu, hakuna mmoja aliyeshiriki hali yake na kumwelewakwa ndani.

Neno la faraja na tumaini ni kuona kwamba Yesu alifaulu kuunda jamii mpya yawanadamu na viongozi wa kwanza wa Kanisa walitoka katika hao watu waliojaa‘umimi’ na kutaka ukubwa, waliogombana wao kwa wao, na kuoneana wivu n.k.Imetupasa kuomba kwamba watumishi katika Kanisa la leo na hasa viongozi,wawe wamejivika tabia za Bwana Yesu, wala si hao tu, hata kila muumini.

10:46-52 Yesu alimponya Bartimayo, kipofu (Mt.20:29-34; Lk.18:35-43)Mathayo ametaja vipofu wawili na Luka amesema kwamba jambo hilo lilitokeawalipoingia Yeriko.

k.46 Yesu na wanafunzi walivuka Mto Yordani na kufika Yeriko, maili kama 18kaskazini mashariki ya Yerusalemu na mji wa mwisho kabla ya kufikaYerusalemu. Mkutano mkubwa ulimfuata Yesu, wakiwa wakiiendea Sikukuu yaPasaka. Kando ya njia kipofu mwombaji alikuwa amekaa, jina lake Bartimayo(Bar maana yake ‘mwana’ baba aliitwa Timayo). Yesu na wanafunzi na umatiwa watu walikuwa wakiondoka Yeriko na huyo kipofu aliposikia kishindo chawatu wengi alitaka kujua ni nani aliyekuwa akipita. Iwapo hakuweza kuonamasikio yake yalikuwa mepesi.

k.47 Aliambiwa ni ‘Yesu wa Nazareti’ (alizoea kuitwa hivyo) ijapokuwa wengiwalitumia kwa dharau, kwa sababu Nazareti haukujulikana katika historia yaWayahudi kwa jambo lolote la maana. Mara alipofahamu ni Yesu anayepita,akapaza sauti yake na kusema ‘Mwana wa Daudi, unirehemu’. Katika Agano la

MARKO228

Kale ilitabiriwa kwamba Masihi atawapa vipofu uwezo wa kuona (Isa.35:5;61:1). Alimwomba Yesu amhurumie na kujali unyonge na umaskini wake,maana ilimbidi sikuzote akae njiani na kuomba. Alifahamika kwa wengi.

k.48 Lakini watu walimkemea wakitaka anyamaze. Huenda sababu yaohaikuwa mbaya, pengine waliona si vema amsumbue huyo Yesu, au huendakwa sababu ya hamu yao ya kufika Yerusalemu kwa Sikukuu hawakutakakucheleweshwa katika safari yao. Lakini kwa sababu ya haja yake kubwa yakuona hakuwa tayari kunyamaza, akazidi kupaza sauti yake.

k 49-50 Yesu Mwenyewe ijapokuwa yeye naye alikuwa amekaza mwendo iliafike Yerusalemu. hata hivyo, akakubali kucheleweshwa, na kati ya kishindocha watu wengi alisikia kilio cha huyo kipofu, akawa tayari kumhudumia.Akawaambia watu ‘Mwiteni’; nao wakamwita na kumpa maneno ya kumtiamoyo ‘Jipe moyo, inuka, anakuita’ (Isa.35:4-5). Mara Bartimayo akatupa vazilake, akaja mbio kwa Yesu akifurahi sana kwamba Yesu amekisikia kilio chake.Alionyesha nia na bidii akitaka sana aponywe upofu wake. Kwa kumwita‘Mwana wa Daudi’ alimkiri Yesu kuwa Masihi, yule mwenye uwezo wakumponya kama nabii Isaya alivyotabiri (Isa.35:1ku).

k.51-52 Yesu alijihusisha naye kibinafsi na kumwomba ataje ni nini hasaalilotaka. Aseme wazi hitaji lake (pesa? maana alizoea kupata pesa (kitu asichonacho) au ‘uwezo wa kuona’ (kitu asichoweza mtu yeyote kumpatia). AkamjibuYesu kwa wazi ‘Mwalimu wangu, nataka nipate kuona’. Neno kwa ‘mwalimu’ nilile alilotumia Mariamu Magdalene alipomwona Yesu bustanini siku ya Ufufuo(Yn.20:16) na ni hapa na pale tu ambapo neno hilo limetumika, lina nguvukuliko rabi/mwalimu. Yesu akaitika kwa kumwambia aweza kuondoka kwasababu kutokana na imani yake amepona. Ajabu ni kwamba, dakika mojaalishindwa kuona kitu chochote, ndipo dakika iliyofuata aliweza kuonasawasawa. Akamfuata Yesu njiani. Hatujui shabaha ya Bartimayo katikakumfuata, kama alikuwa amekubali kujiunga na Yesu na kuwa mfuasi wake, aukama alijiunga naye katika safari ya kwenda Yerusalemu ili pale hekaluni atoeshukrani zake kwa Mungu. Alimtukuza Mungu na watu walijiunga naye katikakumsifu Mungu (Lk.18:43).

Ijapokuwa Yesu Mwenyewe alikuwa na uzito wa hali katika safari hiyo, hatahivyo, hakukosa kuwa na moyo na mzigo juu ya wengine, akawa mwepesi wakusikia kilio cha mtu aliyemwomba amhurumie.

Sura hizi zote zinazofuata zahusu muda mfupi wa siku nane katika maisha nahuduma ya Yesu, dalili ya kuonyesha kwamba waandishi wa Injili walionakwamba upeo wa utume wake ulifikiwa katika Kufa na Kufufuka Kwake, ndiyosababu waandishi wa Injili nne walitumia sehemu kubwa kwa kuandika habariza matukio hayo.

MARKO 229

11:1-11 Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangwe (Mt.21:1-9; Lk.19:28-38;Yn.12:12-19)k.1-2 Yesu na wanafunzi waliondoka Yeriko kuelekea Yerusalemu mwendo wakama maili 18. Walifika Bethania, maili 2 kutoka Yerusalemu (Bethfage ulikuwakati ya Bethania na Yerusalemu). Kutoka pale walivuka Bonde la Kidroni nakuingia mjini kwa mlango wa kaskazini. Yesu aliwatuma wanafunzi wawilikwenda kijijini kwa shabaha ya kumletea mwana-punda. Huyo mwana-pundaalikuwa hajapandwa bado. Kwa nini Marko ataja jambo hilo. Pengine alitakawasomaji wake waone kwamba huyo punda alilingana na wanyama waliotajwakatika Agano la Kale. Waliotumika kwa kazi takatifu walikuwa wa pekee(Hes.19:2; Kum.21:3; 1 Sam.6:7). Mathayo ametaja punda wawili, mama namwana punda. Inaonekana ama Yesu alikuwa amepanga tayari na mtu kablaya wakati huo, au kwa ujuzi wa pekee alifahamu mahali watakapomkuta punda.Yesu hakuwa na mali, aliazima huyo punda kwa muda mfupi kusudi autimizeunabii juu ya Masihi kuja Yerusalemu kama Mfalme wa Amani, mnyenyekevu,mpole, mwenye haki na wokovu (Zek.9:9ku). Ijapokuwa Marko hakutaja jambohilo kwa kusisitiza Umasihi wa Yesu, hata hivyo, mawazo hayo yamefichwakatika yale aliyoyaandika. Yohana alitaja kwamba hata wanafunzihawakufahamu yaliyomo ndani ya tendo hilo mpaka baadaye (Yn.12:16).Mambo hayo yote yaliashiria Umasihi wake. Pengine Marko katika kutajamahali halisi pa punda kufungwa alitaka kuwakumbusha wasomaji wake juu yaunabii kuhusu kabila ya Yuda ambayo Masihi atatoka kwake (Mwa.49:8-12hasa k.11).

k.3 Yesu aliwaambia jinsi ya kujibu ikiwa wataulizwa juu ya kumchukua punda.Waseme ‘Bwana ana haja naye, na ya kwamba atamrudisha mara’. Neno‘bwana’ lina maana gani? Wengi huwaza kwamba ni ‘Bwana Yesu’ ilawachache wanaona kwamba si desturi ya Marko kumwita Yesu ‘Bwana’ naKanisa halikuanza kutumia neno hilo kwa Yesu mpaka baada ya KufufukaKwake. Katika mawazo yao neno ‘bwana’ lahusu yule mwenye punda, ambayepengine hakuwepo. Ila ni vigumu kupokea wazo hilo kwa sababu Luka alisemani wenye punda waliouliza swali (Lk.19:33). Bwana Yesu alihitaji punda, iliautimize unabii wa Zekaria.

k.4-6 Wale wanafunzi wawili waliotumwa walikuta mambo sawasawa na jinsiYesu alivyowaambia na kujibu sawasawa na jinsi Yesu alivyowaagiza. Katikahayo yote Yesu anaonekana kuwa mwenye ujuzi na utawala juu ya matukiohayo.

k.7-8 Yesu alipanda mwana-punda ambaye hajapandwa bado na mtu nawanafunzi walitandaza mavazi yao juu yake ndipo Yesu akaketi juu yake. Watuwengi walijiunga nao na kufanya maadamano ya kuelekea Yerusalemu; baadhiwalitandaza mavazi yao njiani na baadhi walikata matawi na kuyaweka njiani.

MARKO230

k.9-10 Walikuwepo wale waliokuwa pamoja na Yesu pamoja na wenginewaliokwenda Bethania kumwona Lazaro baada ya kufufuliwa kwake, hao piawalijiunga na maandamano (Yn.12:1,12). Walikuwa na moyo mkuu na katikahali ya kusisimua, wakiziimba nyimbo walizotumia wakati wa Sikukuu (Zaburi113-118). Hapo waliimba maneno ya Zab.118:25-26. Neno ‘Hosana’ maanayake ni ‘Bwana aokoe sasa’ au ‘Bwana aokoe, twaomba’. ‘Ndiye mbarikiwaajaye kwa jina la Bwana’ neno ‘ajaye’ lilikuwa na maana kubwa, Yesualijulikana kama ‘Yule Ajaye’. Kwa tendo lake maalum la kuja Yerusalemu Yesualikuwa akidai kutawazwa Mfalme wao; ikiwa watamkataa, atakataliwa kamaMfalme, Masihi wao, aliyeahidiwa na manabii akina Zekaria, Isaya, na wengine.

Bila shaka ni wachache tu waliomtambua kuwa Mwana Kondoo wa Pasaka, natimizo la unabii wa Isaya 53 juu ya Mtumishi Ateswaye. Wengi walimdhaniakuwa mpinduzi wa serikali atakayewaokoa na adui zao Warumi na kuwawekahuru mbali na utawala wa Kirumi. Wakati wa Pasaka mawazo yao yalijaa habariya jinsi Mungu alivyowaokoa wenzao wa zamani kutoka utumwa wa Misri chiniya mkono hodari wa Musa. Huenda baadhi ya wasafiri waliotoka Galilayawalikuwa wale ambao hapo nyuma walitaka kumshika na kumweka kuwaMfalme, wakati alipowalisha watu wengi na mikate na samaki (Yn.6:15). Zaburi118:22-23 ilisema juu ya Jiwe lililokataliwa. Yesu alipokea mashangilio yao kwasababu ilikuwa haki yake ashangiliwe, kwa sababu Yeye ndiye yule wa kuletahaki na wokovu, ila si kwa hali na njia waliyodhani.

k.11 Ilikuwa jioni walipofika Yerusalemu, na Yesu alikwenda mpaka hekaluni.Bila shaka wale walioandamana naye walikwenda zao kutafuta mahali pakukaa. Yesu aliangalia pande zote za hekalu, si kwa shabaha ya kujua mamboyaliyopo, ila katika hali ya kuonyesha madaraka juu yake, ni nyumba ya Babaaliyemtuma, ndipo kesho alikusudia kurudi pale na kufanya tendo kuu lakulitakasa. Kisha akaondoka pamoja na wanafunzi wake na kwenda Bethania,pengine kwa nyumba ya Martha na Mariamu au pengine walilala nje kwenyeMlima wa Mzeituni.

11:12-14 na 20-26 Mtini usiozaa matunda na mafundisho ya Yesu baada yamtini kukauka (Mt.21:18-22)

Marko ameandika habari hiyo kwa sehemu mbili na kuweka habari ya Yesukulitakasa hekalu katikati. Kwa hiyo twaangalia sehemu hizo mbili halafu habariya hekalu kutakaswa.

k.12 Yesu na wanafunzi waliondoka Bethania asubuhi kuelekea Yerusalemu.Twasoma kwamba ‘Yesu aliona njaa’ hatujui kama alikuwa ameamka mapemasana kwa kuomba au vipi, au alikuwa amelala nje kwenye Mlima wa Mzeituni;wala hatujui kama na wanafunzi wake pia waliona njaa. Twajifunza Yesualikuwa mwanadamu kweli mwenye kusikia njaa kama sisi.

MARKO 231

k.13 Kifungu hicho chatatanisha wengi. Yesu kwa mbali aliona mtini ulio namajani, akadhani kwamba atakuta matunda, kumbe, hakuna kitu ila majani tu.Watu hutoa mawazo mbalimbali juu ya mtini; wengine husema kwamba, kwakawaida mtini huwa na majani na matunda kama kwa wakati mmoja, kwa hiyokuwa na majani ni kuwa na matunda pia. Wengine husema kwamba mtinikutokeza matunda mabichi kwanza (Hos.9:10) pengine matunda yaliyoliwa namaskini na watu wa mashambani, ndipo baadaye hutokeza majani na matundamazuri. Maneno yanayoleta shida ni ‘maana si wakati wa tini’. Huenda ni vemakuwaza kwamba kama mtini ulikuwa na majani basi ulitazamiwa utakuwa namatunda, haidhuri ni matunda aina gani au wakati ni wakati gani, jambo kubwani yakiwapo majani matunda yangalikuwepo pia. Kwa hiyo, kuwa na majani bilamatunda ni bure, ni kama kutoa ahadi bure isiyo na matimizo au kujionyeshabila kuwa na kitu. Yesu alitazamia kwamba atayakuta matunda kwa sababualiyaona majani.

k.14 Itikio la Yesu alipoukuta mtini wenye majani bila matunda ilikuwa kutamkaneno la ajabu ‘tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako’; yaani, hali yakeiendelee kama ilivyo. Maneno hayo si ya laana (ni Petro aliyetumia neno ‘laana’v.21). Ni vigumu kuwaza kwamba Yesu alichukizwa au kukasirika eti! ana njaa,na mtini hauna matunda kwa sababu si wakati wa kuzaa matunda. Kwa hiyo,vema tutafute maana yake katika mazingira ya habari hiyo. Mtini ulikuwa isharaya Taifa la Israeli (Yer.8:13, 29:17; Eze.17:24; Yoe.1:7; Hos.9:10, 16ku;Mic.7:1ku). Taifa lilijaa mambo ya dini, mfano wa mtini kuwa na majani, ilahalikuwa na matunda ya haki. Taifa lilijifanya kuwa na matunda kama mtiniulivyojifanya. Mtini ulikuwa nakali yake. Wakuu walikuwa wakifanya mipango yakumwua Masihi wao, huku taratibu zote za dini ziliendelea na kufanikiwa. Lakiniiweje kwa mtini usiokuwa na matunda? tangu sasa hautakuwa na matunda, haliya kutokuzaa itaendelea. Hukumu yake ililingana na hali yake. Ndivyoitakavyokuwa kwa Taifa la Israeli. Yesu alifuliza mafundisho hayo juu ya kuzaakwa Taifa la Israeli (Mt.21:43). Wanafunzi walisikia maneno hayo ya Yesu juuya mtini ila hatuambiwi walionaje. Hapo nyuma Yesu alikuwa ameishatoamfano juu ya mtini uliokosa kuzaa uliopewa muda wa kujirekebisha (Lk.13:6-9).

Hapa tunaruka mpaka k.20-26:k.20 Katika 15-19 tunapata habari ya kutakasa helaku, tendo ambalo Yesualifanya mchana ule baada ya kufika Yerusalemu, ndipo jioni akaenda kulalanje ya mji. Asubuhi Yesu na wanafunzi wakaja tena kwa njia ile waliyoitumiasiku iliyotangulia. Walikuta ule mtini umenyauka toka shinani. Petro alishangaakwa sababu ya wepesi wa kunyauka kwake na kwa nguvu ya maneno ya Yesu.Akamwambia Yesu ‘Rabi, yaani Mwalimu, tazama, mtini ulioulaani umenyauka’.Katika mawazo ya Petro Yesu alikuwa ameulaani mtini. Haikuwa tabia ya Yesukuutumia uwezo wake mkuu katika kuharibu kitu, bali daima aliutumia katikakuleta afya na uzima na kuokoa maisha ya wanadamu. Kwa hiyo, ni vemakuona umuhimu wake si katika mtini kukauka bali katika neno linaloashiriwa natendo hilo. Ishara ilihusu Israeli na Hekalu. Marko ameweka habari ya

MARKO232

kulitakasa hekalu katikati ya Yesu kuuambia mtini na mtini kukauka. Kama mtiniulivyokauka ndivyo itakavyokuwa kwa taifa la Israeli na kwa Hekalu ambalolitabomolewa baadaye (13:1ku).

k.22-23 Yesu alichukua nafasi hiyo kufundisha wanafunzi juu ya imani namaombi na msamaha. Yesu alipata nguvu yake kwa kumtegemea Baba kabisa,kamwe hakujitegemea. Alijua Baba ni Mwaminifu kabisa. Alisema nao kamawale watakaokabidhiwa kazi baada ya Yeye kuondoka hivi karibuni. Itawapasanini hasa? Watawezaje mambo makubwa na magumu yaliyo mbele yao?Jambo kubwa ni kumwamini Mungu; kumtegemea kabisa kama Yeyealivyofanya; wajue kwa hakika kwamba Mungu ni Mwaminifu, hawezikuwaachia bila msaada na uwezo wa kufanya yote yaliyowapasa. Wakiwa naimani ya kweli wataweza kukabili mambo makubwa mfano wa ‘mlima huu’ nakuyashinda kwa mfano wa ‘mlima kutupwa baharini’. Lolote lile lililo mapenzi yaMungu wataliweza. Imani ni muhimu kwa jambo lolote litegemealo uwezo waMungu. Hakuna kazi yoyote ipatanayo na mapenzi ya Mungu ambayoitawashinda wenye imani. Imani ndiyo msingi kabisa, na kwa imani uhusianowao na Mungu unajengwa (Ebr.11:6).

k.24 Wenye imani watamwomba Mungu na kwa kushirikiana naye watajuauwezo wake katika ujuzi wa maisha yao ili wafanye mapenzi yake. Watajifunzamapenzi yake katika kushirikiana naye katika maombi. Ni hao wenye nia yakufanya mapenzi ya Mungu ambao wanayo haki ya kuomba. Hawataweza nenololote bila kuomba. Yesu aliwapa kielelezo (1:35; 6:46; 14:32-40).

k.25 Pamoja na kuomba imempasa kila anayeomba awe amemsamehemwenzake. Ni tabia ya kusamehe inayotakiwa, hali mtu anajua kwa hakikakwamba yeye mwenyewe daima huhitaji kusamehewa na Mungu. Kwa hiyo,wawe na uhusiano mwema na Mungu pamoja na uhusiano mwema na wenzao.

k.26 Kifungu hicho hakimo katika nakala nyingi za kwanza. Ni manenoyanayofanana na Sala ya Bwana. Haina maana kwamba msamaha wa Munguhutegemea msamaha wetu, la! ila msamaha ni msingi wa maisha ya kiroho namaisha ya kuomba. Kutokuwa tayari kusamehe kunamfanya mtu akose hali yakuupokea msamaha wa Mungu, ni kama hajaonja uzuri wa kusamehewa naMungu.

11:15-19 Yesu alitakasa Hekaluk.15 Walipofika Yerusalemu tena Yesu alikwenda moja kwa moja mpakahekaluni. Alikuwa ameishatazama pande zote za hekalu jioni iliyotangulia. Nidhahiri kwamba alikuwa ameyaona mengi yaliyomkasirisha, hivyo, alikuja kwakusudi maalumu la kufanya marekebisho, yaani kuondoa biashara iliyofanyikahumo. Hekalu lilifanana na ule mtini uliokuwa na majani mengi. Hekalu lilikuwajengo zuri sana, kubwa, lenye nafasi mbalimbali, lilikuwapo ua la WaMataifayaani kwa watu wasio Wayahudi waliovutwa na dini ya Kiyahudi, kuja na kusali

MARKO 233

kwa Mungu wa Israeli. Lilikuwapo ua la wanawake ambao hawakuruhusiwakuingia katika sehemu nyingine. Ndipo ua kwa wanaume wa Israeli, ndipo jengolililoitwa ‘Patakatifu’ ambapo makuhani walifanya huduma zao kama kutoleadhabihu za wanyama n.k. Ndipo ndani kabisa palikuwapo ‘Patakatifu paPatakatifu’ mahali ambapo Kuhani Mkuu peke yake, mara moja kwa mwaka,aliruhusiwa kuingia mle ndani akienda na damu ya dhabihu.

Kwa jinsi Yesu alivyosema inafikiriwa kwamba hiyo biashara ilifanyika katikaUa la WaMataifa, mahali pamoja tu walioruhusiwa kuabudu. Kwani iwepo hajaya biashara? Asili ya biashara ni katika mahitaji ya watu kupata wanyama wasadaka, hasa wale waliotoka mbali. Ilikuwa msaada kwao kupata mnyama kwakaribu badala ya kusafiri naye kutoka mbali. Tena, kwa sababu, kila mnyamaalikaguliwa na kuhani, mara kwa mara ilitokea kwamba mnyama aliyeletwahakukubalika, kwa sababu ya doa au waa fulani au kwa kujeruhiwa njiani.Pamoja na hayo pesa iliyoruhusiwa kutolewa ilikuwa ya pekee na watu walihitajimahali pa kubadilisha pesa, hivyo nafasi ilitolewa pale hekaluni. Tena kilaMyahudi alitakiwa kutoa nusu shekeli kwa hekalu mara moja kwa mwaka(Kut.30:13ku). Lakini Je! ilikuwa jambo zuri kwa shughuli hizo kufanyika mahaliambapo paliwekwa kwa ajili ya kusali kwa WaMataifa? Yasemekana kwambamasoko manne yalikuwepo karibu penye Mlima wa Mzeituni na soko hilo lahekalu liliwekwa na Kuhani Mkuu na wenzake kwa faida yao. Nafasi ilikuwawazi kwa watu kudhulumiwa, kwa kutozwa bei kubwa kwa wanyama, na kulipagharama zaidi ya haki kwa kubadilishana fedha. Waliofaidiwa walikuwawahusika wa hekalu, makuhani na wenzao.

k.15-16 Yesu alifanyaje baada ya kuwa amepima hayo yote alipofika jioni ileiliyotangulia? Alitumia nguvu zake za kimwili na kuwafukuza wenye biashara nakupindua meza zao na viti vyao na kuwaondoa. Pamoja na hayo inaonekanawatu walizoea kupita pale na kupatumia kama njia ya mkato, jambolililokatazwa ila watu hakujali, waliendelea kupita pale. Yesu alishikwa na wivujuu ya heshima ya nyumba ya Baba yake.

Katika habari hiyo twaona tofauti kubwa kati ya Yesu na viongozi wa dini yaKiyahudi. Wote walikuwa na wivu juu ya hekalu kwa sababu lilikuwa kitovu chadini ya taifa na alama ya taifa lenyewe. Wakuu walichukizwa na kelele zawatoto waliosema ‘Hosana’ (Mt.21:15) huku wameruhusu kelele za wafanyabiashara. Walikuwa na mzigo juu ya kuendeleza shughuli za dini zilizoonekana,maana hizo ndizo zilikuwa za maana kwao. Ila kwa Yesu, hekalu ni mahali pasala kwa watu wote, si Wayahudi tu. Tena si mahali pa biashara, licha yabiashara ya kudhulumu watu chini ya kivuli cha dini. Yesu alitamani sanaWaMataifa wawe na nafasi kumwabudu Mungu katika utulivu. Bila shakaviongozi walihofu sana walipotambua kwamba Yesu amesisitiza haki yaWaMataifa kumwabudu Mungu wa Israeli bila shida. Malaki alitabiri kwambaMasihi atakuja kwa hekalu na kulitakasa (Mal.3:1-4).

MARKO234

k.17-18 Ndipo Yesu aliendelea kwa kutoa mafundisho na kwa maneno alielezatendo lake la nguvu na hasira. Aliwakumbusha juu ya maneno ya Nabii Isayakuhusu hekalu kuwa nyumba ya Sala. Sababu kubwa ya kuwepo kwa hekaluilikuwa ibada si biashara ambayo fujo zake na kelele zake zilikuwa kinyumekabisa cha utulivu uliotakiwa kwa sala. Tena Hekalu si kwa Wayahudi tu, bali nikwa WaMataifa pia. Lengo la Mungu lilikuwa kwamba kwa njia ya Wayahudiawalete watu wasio Wayahudi katika kumtambua Mungu wa Israeli kuwaMungu wa kweli. Lengo hilo lilifunuliwa zamani za kale, wakati wa chanzo chaTaifa la Israeli, wakati wa Ibrahimu kuitwa (Mwa.12:3). Ila Wayahudiwalipotosha shabaha ya Wito na Uteule wao. Wamekuwa watu wa kuwekawengine nje. Mungu hataendelea kuwavumilia kama ambavyo mtinihaukuvumiliwa. Majani bila matunda ni bure.

Pamoja na kutaja unabii wa Isaya Yesu alitaja maneno ya Nabii Yeremia 7:11juu ya nyumba ya sala kuwa pango la wanyang’anyi. Wamekuwa wanyang’anyikwa njia mbili. Kwa kufanya biashara ya udhalimu na kwa kuwanyang’anyaWaMataifa mahali pa sala.

Tendo hilo lilikuwa neno lake la mwisho katika kuihukumu hali yao ya kujipendawenyewe na kuwaweka wengine nje. Katika Kifo chake atapasua njia wazi iliyeyote aweze kumjia Baba kwa kutegemea ule upatanisho atakaoufanya katikaKifo chake. Ndipo kwa neema kila mtu atakaribishwa katika Ufalme wake bilaubaguzi wa aina yoyote.

Katika mambo hayo yote Yesu alikuwa akidai kuwa Masihi bila kutamka wazi(Isa.4:4; Mal.3:1ku; 4:1). Ni fundisho kuu kwa Kanisa ili lifahamu kazi yakemaalumu ni kuweka nafasi kwa watu kumkaribia Mungu kwa njia ya Kristo bilakizuizi chochote na bila ubaguzi wowote. Kanisa lahitaji fedha za kuendelezashughuli zake ila kamwe fedha isiwe jambo la kutawala mipango yake.

k.18 Tendo hilo la Yesu liliwachukiza sana viongozi wa dini ya Kiyahudi, hatawale ambao kwa kawaida hawakupendana walijiunga pamoja na kuamuakwamba kwa vyovyote lazima Yesu aondolewe. Walitambua kwamba Yeye nihatari kabisa kwao kwa jinsi asivyoweza kuvumilia hali yao ya kuitumia dini kwafaida yao. Ila, kwani wasimshike mara na kumwondoa? Haikuwezekana.Walijua kwamba umati wa watu wamemsindikiza kwa shangwe mpakaYerusalemu. Wengi wao walikuwa WaGalilaya waliojulikana kuwa watu wakuwaka moto wa siasa ya mapinduzi. Tena walishindwa kugeuza mawazo yawatu juu yake kwa sababu wengi walifurahia kazi yake ya kulitakasa hekalu.Hasa silaha kali ya Yesu ilikuwa mafundisho yake, wakati wote watuwalishangazwa na mamlaka na ujuzi wa pekee wa mafundisho yake.

k.19 Jioni ile Yesu na wanafunzi walitoka kwenda kulala nje ya mji, penginekwa usalama wao, au pengine kwa kumpa Yesu nafasi ya kuomba na kutuliabaada ya shughuli za kila siku (Lk.21:37). Kwa hiyo katika kuwiana kwa habari

MARKO 235

ya mtini na kutakaswa kwa hekalu tunayo mambo mawili yanayotiana nuru nakutoa ujumbe mmoja juu ya hukumu iliyokaribia kufika juu ya taifa na ibada yaIsraeli. Ni mifano miwili kiutendaji juu ya kutokuzaa kwa Israeli na unabii wakimfano juu ya hukumu yake.

(Katika Injili ya Yohana kuna habari ya Yesu kutakasa hekalu mwanzo waHuduma yake, na Yohana hataji habari ya Yesu kutakasa hekalu mwisho waHuduma yake, kama waandishi wa Injili tatu zinazowiana walivyofanya. Je!Yesu alitenda tendo hilo mara mbili au vipi? Baadhi ya wataalamu hudhanikwamba alilitenda mara moja tu, mwisho wa huduma, na Yohana aliliwekakama lilitokea mwanzoni. Lakini hakuna haja ya kufikiri hivyo. Yesu alifanyamara ya kwanza, alipokuwa bado angali sehemu za Yerusalemu, kabla yakwenda Galilaya na kufanya huduma ya muda mrefu huko. Alirudia kufanyaaliporudi Yerusalemu, baada ya kumaliza huduma yake ya miaka mitatu hukoGalilaya. Si ajabu kwamba watu walirudisha biashara yao, kwa sababu ya faidayake, hasa kwa sababu wahusika walikuwa viongozi wenyewe. Tena, kamaambavyo tumeishaona, lilikuwa tendo la kuonyesha Umasihi wake, kamamanabii walivyotabiri kwamba, Masihi atakuja Yerusalemu na kwenye hekalulake. Ilimbidi kwa mara ya mwisho aweke dai lake kuwa Masihi mbele ya Taifakwa tendo hilo la nguvu na mamlaka lililoashiria Umasihi wake).

Mawazo kuhusu hasira na wivu na Yesu kutumia nguvu: Watu wametatizwa nahabari hii ya Yesu kuwa na hasira na wivu na kutumia nguvu za kimwili. Lakinihasira na wivu vyaweza kuwa, ama vya dhambi, ama vya haki. Je! ni wivumbaya kwa mtu kukasirika akiona mke wake akianza kuonana na mtumwingine? La, ni wivu mzuri na ingekuwa jambo la kustaajabia kamaasingalisikia wivu. Mara kwa mara sisi wanadamu huwa tunakasirika autunasikia wivu kwa sababu sisi wenyewe tumetendewa yasiyopendeza.Twasikia wivu eti! kwa sababu fulani amekuwa na kitu fulani ambachotunapenda kuwa nacho. Hasira na wivu hizo ni dhambi. Ni sawa, tena inatakiwatukasirike tunapoona watu wameonewa, wamekosa kupata haki zao za kweli,wamedhulumiwa n.k. Twapaswa kuwa na wivu juu ya heshima ya Mungutunapoona mambo yake yanachezewa na jina lake latumiwa kama tusi n.k.(Efe.4:26).

11:27-33 Swala juu ya mamlaka ya Yesu (Mt.21:23-27; Lk.20:1-8)

Yesu na wanafunzi walirudi tena mjini baada ya kulala nje kwa usiku. Yesualitembea hekaluni penye ukumbi mbalimbali zilizotumiwa na marabi kwakuwafundisha watu. Bila shaka tendo la kulitakasa hekalu lilikuwalimewashtusha na kuwasumbua viongozi. Yesu hakuomba ruksa kwao walahakupata idhini yao, huku watu wengi walimdhani kuwa Masihi. Walikuwawalinzi wa hekalu na mambo ya dini katika Israeli kwa hiyo waliwajibikakuchukua hatua ama kuliunga mkono tendo hilo au kulipinga. Walifanyaje?Basi, kundi rasmi wa wajumbe wa vikundi vitatu walioshika nafasi katika Baraza

MARKO236

la Sanhedrin walimwendea Yesu. Mara kwa mara hao wenyewehawakuafikiana ila katika jambo la kumwondoa Yesu wote walimwona kuwahatari kwao. Walimjia ili wamhoji kuhusu madaraka yake hasa kwa sababu yatendo lake la kutakasa hekalu pia kwa kufundisha pale kila wakati. Pamoja natendo la kulitakasa hekalu alikuwa ameingia Yerusalemu akizipokea shangweza watu na kutendewa kama Mfalme. Hata nyuma katika huduma yakeamefanya mengi makubwa yaliyowapa wasiwasi walipoona mamlaka yake.Shida ilikuwa hawakuwa tayari kumpokea kama Masihi, mwenye madaraka yaMungu, kwa sababu alifanya kinyume cha matakwa yao. Yesu kwa upandewake alikuwa hajatamka wazi kuwa Masihi, ila kwa matendo yake alikuwaamedai hivyo.

k.28 Walipenda kutunga swali gumu ili wamnase Yesu na kufanya watu waonemashaka juu yake. Swali lao lilikuwa wazi, ila halikuulizwa eti! wapate jibusahihi, bali wamnase!. Akidai kuwa ametumwa na Mungu, na mamlaka yakeimetoka kwa Mungu, watasema kwamba ‘amekufuru’. Akidai kuwa ‘Mwana waDaudi’ watamshtaki kwa Kaisari kuwa msaliti wa Dola. Akisema kwamba hanamamlaka ila ya kwake mwenyewe tu, basi, watamshtaki kuwa ayari, mwenyekudanganya watu.

k.29 Yesu hakuwajibu moja kwa moja, ila tusidhani kwamba kwa kuwaulizaswali alikuwa akikwepa kulijibu swali lao. Katika kujibu swali lake watakuwawamepata jibu sahihi kwa swali lao. Hasa alikuwa akiwafanya warudi nyuma nakuzingatia huduma na ushuhuda wa Yohana Mbatizaji.

k.30 Swali lake lilimhusu Yohana Mbatizaji. Yohana alipata wapi mamlakayake?. Yeye kama Yesu hakupitia kwa wakuu na kupata idhini au ruksa yao.Alitokea tu jangwani, akisema kwa mamlaka kama mtu aliyetumwa na Mungu.Tena alishuhudia kwamba hakuwa Masihi ila mtangulizi wake. Pamoja na hayoalikuwa amenyosha kidole chake kwa Yesu na kusema ‘Tazama, MwanaKondoo wa Mungu....’. Kwa hiyo, wasemaje juu ya Yohana na mamlaka yake?Je! alitumwa na Mungu au alijituma mwenyewe? Hivyo Yesu aliweka pamojamamlaka ya Yohana na mamlaka yake, zote zilikuwa na asili moja, wote wawiliwalitumwa na Mungu. Yesu alikuwa na uhusiano wa ukaribu sana na Yohana,mamlaka yao ilitoka kwa Mungu, ila Yohana alikuwa mwanadamu na Yesualikuwa Mungu.

k.31 Kwa swali lake Yesu alikuwa amewabana kabisa na kuwatahayarisha namsimamo wake. Iliwabidi wasemezana wao kwa wao na kupima jibu lao kwauangalifu sana kwa kufuata siasa yao bila kujali msingi halisi wa mambo hayo.Wakikiri kwamba ubatizo (ubatizo ni jumlisho la huduma yake) wa Yohanaulitoka kwa Mungu kwa nini hawakuupokea ushuhuda wake juu ya Yesu?

k.32 Kwa upande wa pili, wakisema ulitoka kwa wanadamu walihofu sanawatu, kwa sababu watu walimtambua Yohana kuwa nabii halisi aliyetumwa na

MARKO 237

Mungu. Walimwendea na kubatizwa naye wakitubu dhambi zao na kujiwekatayari kumpokea Masihi anayemfuata. Hawakuwa tayari kuwakabili watu.

k.33 Hivyo wakatoa jibu la ajabu kwa Yesu ‘Hatujui’ jibu la uwongo, afadhaliwangalisema ‘hatuko tayari kukujibu’. Kwa jibu lao waliondoa haki yao ya kuwawaalimu na viongozi katika Israeli. Walikuwa na uwezo gani kuwafundisha watumapenzi ya Mungu ikiwa walishindwa kutambua asili ya mamlaka ya YohanaMbatizaji? Pia hawakuwa na haki ya kuendelea kumhoji Yesu. Yesu akaitikakwa kuwaambia wazi kwamba hatawaambia ni kwa mamlaka gani anayatendamambo yake. Ni kama Yesu alisema ‘mkikataa kunijibu sawasawa sina haja yakuwasaidia kunielewa’. Kiini cha shida yao ilikuwa kukataa mapenzi ya Mungu,sawa na baba zao walivyofanya walipowakataa manabii waliotumwa kwao.Katika mfano na mafundisho yanayofuata Yesu aliendelea kupanua jambo hilo.

12:1-12 Mfano wa Shamba la Mizabibu (Mt.21:33-46; Lk.20:9-19)Katika sura iliyopita Yesu alikuwa amedokezea kuwa Masihi bila kutamka wazi.Hapo, tena kwa njia ya kubuni hadithi, aliendelea kutoa changamoto kwaviongozi kuhusu mamlaka yake ya KiMasihi, bila kutamka wazi kuwa Masihi.Katika kusimulia hadihi hiyo alitaka kuonyesha kwamba hata historia yao yanyuma imefikia upeo katika hayo yanayotokea na kumpata Yeye wakati huo.

k.1 Shamba la Mizabibu ni Israeli (Isa.5:1-7; Zab.80:8ku; Yer.2:21). Maelezokuhusu kuzungusha ugo, kuchimba shimo, na kujenga mnara. n.k.yanaonyesha jinsi shamba hilo lilivyotayarishwa na kutunzwa vizuri sana.Mwenye shamba, Mungu Mwenyewe, alifanya yote yaliyowezekana ili shambalizae vizuri. Ni habari za jinsi Mungu alivyolishughulikia Taifa teule la Israelikusudi Masihi wake aje, kwa wakati wake, na kuwakuta watu walio tayarikumpokea na kuelewa shabaha ya Kuja Kwake. Mambo yote waliyofanyakuhusu maadili yalimwashiria, yalikuwa ‘vivuli’ vya mambo yajayo kama Warakakwa WaEbrania unavyoonyesha.

k.2 Mizabibu ilipandwa ili izae matunda. Kwa hiyo kila wakati mtu alitumwa naMwenye shamba (yaani Mungu) ili apokee matunda kwa wakulimawaliopangwa. Wakulima hawa walikuwa akina nani? ni viongozi wa Israeliwaliowekwa kutunza taifa la Israeli. Mtumwa ni mfano wa akina nani? ni mfanowa manabii waliotumwa mara kwa mara kuliita taifa litengeneze mambo yakekusudi lizae matunda, yaani lifanye mapenzi ya Mungu.

k.3-5 Lakini ilitokeaje? Watumwa waliotumwa mara kwa mara walifanyiwavibaya sana, walipigwa na kufanyiwa jeuri, hata baadhi waliuawa. Tangumwanzo hadi mwisho (aliyekuwa Yohana Mbatizaji) hawakupokelewa vizuri,kwa sababu wakulima walikuwa wamekosa kutimiza wajibu wao juu ya utunzajiwa shamba (Mt.23:34ku). Huu ndio mwenendo wao kihistoria. Hawakutambuamamlaka ya manabii waliotumwa na Mwenye shamba wala wajibu wao wakumzalia Mungu matunda, bali walijilisha wenyewe (Eze.34:1ku).

MARKO238

k.6 Hata hivyo, mwenye shamba alikuwa na subira nyingi, hakukata tamaa,akajaribu mara moja tena. Ila wakati huo, badala ya kumtuma mtumishi, nabii,alimtuma Mwana wake mpendwa, akidhani kwamba watamstahi kwa sababu niMwana wake. Mpaka hapo Mungu alikuwa na matazamio makubwa juu ya‘mwana wake Israeli’. Alijitoa kabisa kwa ajili yake. Hakuwa na neno lingine lakufanya ila kumtoa Mpenzi wake, Mwana wake wa pekee, hali akidhanikwamba watu watamtambua na kumthamini na kumstahi na kuzingatia upendomkuu wa Mungu kwao. Ni kama nafasi yao ya mwisho kabla ya kupatwa nahukumu yake. Mungu hupenda kuokoa si kuhukumu, kuhukumu ni neno lake lamwisho.

k.7-8 Itikio lao kwa upendo wa Mungu lilikuwa kuamua kwamba auawe huyoMwana ila wautwae urithi. Walikuwa wajinga kabisa, kwa sababu, hatawakimwua Mwana, shamba si lao, bado Mwenye shamba yupo, Yulealiyepanda shamba na kuwapangisha. Yesu alikuwa akisema kama nabiiakitabiri Kifo chake kitakachotokea baada ya siku chache. Kitafanyika paleYerusalemu na wenye kukipanga ni wale wale waliomwuliza swala juu yamamlaka yake. Mamlaka yake ni ya Mwana aliyetumwa na Baba, mwenyeshamba. Maneno ‘wakamtupa nje ya shamba’ yanaashiria jinsiatakavyokataliwa kabisa hata bila kujali maziko yake. Nao watafanya, si kwasababu walikosa kumtambua, bali kwa sababu walimtambua na ndiyo sababuwalimwua. Kama wasingalitambua wangaliweza kusamehewa.

k.9 Lakini Je! mambo yaishia hapo? La, hata kidogo? Yesu aliweza kuonambeleni baada ya Kuuawa Kwake. Kwanza wakulima waliopangwawataondolewa: pili, wengine watapewa shamba. Jambo la kwanza litawaumizasana, ila la pili litawaudhi sana, watakapoona WaMataifa wanaingia urithi wao(Mt.8:11,12; 21:43). Watakaopewa shamba ni wale watakalolitunza yaani walewatakaoeneza Injili ya Kristo na kuendeleza Ufalme wa Mungu hapo duniani.Kanisa limerithi shamba hilo. Taifa la Israeli liliangamizwa mwaka B.K.70 wakatiWarumi walipofanya vita juu yake na kulibomoa jengo la Hekalu na Mji wao nawengi walikufa na wengine walisambaa katika nchi zingine. Mpaka hapowalikuwa na nafasi ya kujihoji na kubadili uamuzi wao juu ya Yesu.

k.10-11 Halafu Yesu aliwakumbusha juu ya maneno ya Zaburi 118 waliojuasana na kuimba wakati huo wa Pasaka. Ni kutoka Zaburi hiyo watu waliimbamaneno ‘Hosana’ walipomkaribisha Yesu mjini. Yeye Yesu ni jiwe ambalowaashi watalikataa (waashi ni viongozi wa Israeli) lakini ijapokuwa atakataliwanao Mungu atamchukua, atamfufua kutoka wafu na kumweka kuwa jiwe kuu lapembeni, jiwe la kuunganisha jengo ambalo ndani yake Wayahudi naWaMataifa watashirikiana. Waashi walipaswa wajue vizuri ‘jiwe’ la kufaa, ilahawakulitambua, na hata ikiwa walilitambua, hawakulitaka. Hapo Yesu alitabiriKufufuka Kwake na Kutukuzwa Kwake (Flp.2:5ku; Mdo.4:11; 1 Pet.2:6-8;Rum.9:33; Efe.2:20).

MARKO 239

k.12 Wakuu walitaka sana kumkamata Yesu kwa sababu walitambua kwambahuo mfano uliwasema. Lakini katika ujinga wao na uovu wao, badala yakuuzingatia na kujihoji, wakaendelea kufuliza mipango ya kumwua. Hakunakipofu kuliko yule asiyetaka kuona! Wakashindwa kumpata wakati huo kwasababu mpaka hapo umati wa watu walikuwa wakipenda kumsikiliza Yesu, nawakuu hawajafaulu bado kuyageuza mawazo yao.

Mungu hawezi kuzuiliwa asitimize mapenzi yake ya kuleta ukombozi waulimwengu, hata hivyo, itakuwa kwa gharama kubwa ya Kufa kwa Mwanawempendwa. Mungu atatengeneza Agano Jipya na kuunda jamii mpya, IsraeliMpya, yaani Kanisa. Ila swali limebaki Je! Kanisa litatimiza wajibu wake nakufanya mapenzi ya Mungu? Mara kwa mara ni vema Wakristo wajihoji naKanisa liangalie mwenendo wake ili lisikataliwe kama Israeli ya zamani.

12:13-17 Swali juu ya kumlipa Kaisari kodi (Mt.22:15-22; Lk.20:20-26)k.13 Inaonekana kwamba viongozi walikuwa wameshauriana wao kwa wao nakwa pamoja kutunga maswali waliyodhani kwamba yatamnasa Yesu. Hivyowajumbe wa Mafarisayo na Maherodi walimjia, watu waliotofautiana sana,Mafarisayo walikuwa na mzigo juu ya dini na Maherode walihusika na siasa. Ilakwa sababu walikuwa na shabaha moja ya kumwondoa Yesu walijiungapamoja. Kwa kila kundi Yesu alikuwa hatari. Hapo nyuma Marko alitaja habariya hao kujiunga pamoja wakati mwingine (3:6). Luka amesema kwambawalikuwa wapelelezi (Lk.20:20) na Mathayo amesema kwamba waliokujawalikuwa wanafunzi si viongozi wenyewe (Mt.22:16).

k.14 Waliuliza swali hilo lililo tofauti sana na lile la kuhusu mamlaka yake(11:28). Wakati ule walitoa changamoto kwa kumwuliza moja kwa moja. Wakatihuo walianza kwa kumsifu sana, ila hasa zilikuwa sifa za kumpaka mafuta nakuondosha fikra dhanifu ili asiwe na tahadhari. Sifa zenyewe zilikuwa kwelikabisa; ‘mtu wa kweli’ ‘hujali cheo cha mtu’ haina maana kwamba Yesu hakujaliwatu ila alikuwa na msimamo wake mwenyewe bila kujali cheo cha mtu aukundi lake. ‘hutazami sura ya mtu’ yaani asema kwa kadiri anavyoonamwenyewe potelea mbali ni nani amwulizaye. ‘katika kweli waifundisha njia yaMungu’ ni kukiri kwamba Yesu alikuwa na mzigo wa kuwafundisha watu njia yakweli ya Mungu. Sifa za ajabu! Ila ni hila yao. Baada ya kumpaka mafutawakamwuliza swali la kumtega, swali ambalo walitaka jibu la ‘ndiyo’ au ‘siyo’maana walidhani kwamba kwa kumbana akisema ‘ndiyo’ au ‘siyo’ watakuwawamempata kwa sababu walidhani kwamba hakuna jibu lingine ila ‘ndiyo’ au‘siyo’. Ni mtego usiofyatuliwa kwa urahisi.

k.15a Wakazidi kutilia mkazo namna ya swali lao kujibiwa kwa kusema kamajibu liwe ‘tumpe’ au ‘tusimpe’ kana kwamba hamna jibu la kupitia kati nakukwepa kusema ama ‘tumpe’ au ‘tusimpe’. Lakini Yesu amekwishaelewa hilayao na kuutambua unafiki wao. Wako tayari kufanya lolote lile litakaloifanikishashabaha yao ya kumnasa, hata kwa kujiunga pamoja na kuuliza swali ambalo

MARKO240

jibu ‘tumpe’ litawafurahisha wengine na jibu ‘tusimpe’ litawafurahisha wengine.Akisema ‘tumpe’ Maherode watafurahi ila watu hawatafurahi kwa sababuwalichukizwa sana na jambo la kulipa kodi kwa Kaisari, nao watamwona Yesukuwa hafai kuwa Masihi wao. Mafarisayo ijapokuwa kwa ndani watakubaliananaye akisema ‘tusimpe’ kwa nje watafurahi kwa sababu watakuwa wamepataneno la kumshtaki kuwa msaliti wa nchi.k.15b Alipitaje? alijibuje? Kwanza aliwajulisha kwamba alitambua unafiki wao.Hawakumwuliza kwa shabaha ya kusaidiwa kuelewa mapenzi ya Mungu katikahabari hiyo ila kwa sababu walitaka kumnasa. Ndipo akawaomba wamleteedinari ili aione, pesa iliyotumika katika maisha ya kila siku. Si kana kwambahakujua jinsi dinari ilivyo, ila alitaka kuuvuta usikivu wao na kuwatafakarisha juuyake.

k.16 Alipopewa dinari, akawauliza ‘Ni ya nani sanamu na anwani hii?’ Ndipowakamjibu ‘Ni ya Kaisari’ kichwa chake kilikuwa upande mmoja na anwani‘mwana wa mungu’ upande wa pili, ishara ya kuwa yeye ndiye mtawala wa nchiile. Katika kuitumia Wayahudi walikuwa wakikiri kwamba wako chini ya utalawawa Kirumi na wakipenda, wasipende, waliwajibika kulipa kodi.

k.17 Kisha Yesu akawapa jibu ‘Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo yaMungu mpeni Mungu’. Kulipa kodi ni kulipa deni kwa uhifadhi na mibaraka yoteiletwayo na serikali. Usalama, usafiri, na huduma za elimu, matibabu, n.k. Ni juuya kila mwananchi kutambua kwamba analo deni kwa misaada inayoletwa naserikali, na njia ya kulipa deni ni kulipa kodi. Ila Yesu aliendelea kwakuwakumbusha juu ya deni lingine walilo nalo, deni lao kwa Mungu.Wameumbwa katika mfano na sura ya Mungu, na kwa sababu hiyowamewajibika kumpa heshima alizostahili pamoja na utiifu wao. Kwa hiyokatika yote ya halali na haki yanayodaiwa na serikali waliwajibika kutoa, ilaserikali haina haki kupita mipaka ya eneo lake na kuingilia eneo la Mungu, watuhupaswa kumtii Mungu kwanza. Utiifu wao kwa serikali ni sehemu mojawapokatika utiifu wao wa Mungu, ila ni sehemu tu. Yesu alikataa kwamba madai yaKaisari ni sawa na madai ya Mungu ila alikubali kwamba ni mtawala wa nchi.Tangu wakati huo jibu la Yesu limeongoza mawazo ya watu kuhusu uhusianowa serikali na Mkristo, aliye raia wa Ufalme wa Mungu pamoja na kuwa raia wanchi yake (Rum.13: 1-7; 1Tim.2:1-6; Tit.3:1ku; 1Pet.2:13-17). Uraia mmojahauweki nje nafasi kwa uraia mwingine. Nafasi zipo kwa zote; ni haki kulipakodi kwa ajili ya huduma tunazozipata kwa serikali, ila ni Mungu peke yake aliyena haki ya kuudai utiifu wetu wote. Madai mengine yote yatimizwe katikamwanga wa utiifu wetu kwa Mungu. Yesu katika hekima yake kamili alitoa jibula ajabu sana. Wale waliokuja kumtega wakaondoka hali ya kumstaajabia sana.

12:18-27 Swali la kuhusu Ufufuo (Mt.22:23-33; Lk.20:27-40)Mathayo amesema kwamba hao Masadukayo walikuja siku ile walipoondokawale wengine (Mt.22:23).

MARKO 241

k.18 Ni hapo tu ambapo Marko ametaja kundi la Masadukayo, na kwa sababuhiyo alitoa maelezo machache juu yao. Walikuwa wakuu na matajiri katika nchi.Hasa tofauti yao na Mafarisayo ilikuwa kwamba hawakuamini kwamba kunakiyama. Walikuwa makabaila wenye sauti katika Sanhedrin na viongozi washughuli za Hekalu, Kuhani Mkuu pamoja na makuhani wengi walikuwaMasadukayo, ila walikuwa wachache, si wengi, kama Mafarisayo. Walikubalivitabu vitano vya kwanza vya Maandiko ila walikataa mapokeo ya waandishi,walipenda vyeo, heshima, na raha za dunia, hawakuwa watu wa kiroho.

k.19a Walileta swali lililotofautiana sana na lile la Mafarisayo na Maherode.Swali la kitheologia si swali la siasa. Pengine hawakutaka kumnasa Yesu ilashabaha yao ilikuwa kumwaibisha mbele za watu kwa kuonyesha jinsi ilivyoupuzi mtupu kuamini neno la ufufuo. Kama wakiweza kuonyesha kwamba Yesusi mtheologia, pia ni mjinga kwa kuamini jambo la ufufuo ndipo watafaulukumwaibisha mbele za watu na kumshinda, jambo ambalo Mafarisayo naMaherode hawakuliweza.

k.19b-22 Swali lao lilihusu desturi iliyowekwa na Musa kuhusu wakati wa kifocha mtu aliyemwacha mkewe bila watoto (Kum.25:5ku). Jambo la kupatawatoto lilikuwa muhimu kwa sababu lilihusu kuendelezwa kwa ukoo wa mtu.Kwa hiyo, si swali la hatari wala la siasa, ila la mafundisho. Ndipo wakaendeleakwa kutoa mfano wa mwanamke aliyechukuliwa mara saba na mfuatano wandugu wa mumewe. Ajabu ni kwamba hakumzalia hata mmoja wao mtoto,ndipo yeye mwenyewe akafa. Kama ilikuwa imetokea hivyo au kama ni mfanotu, si neno.

k.23 Masadukayo walitaka kujua, ukiwapo ufufuo wa wafu na hao wotewatafufuka, huyo mama atakuwa mke wa yupi? Ni vigumu sana kufikiri itatokeahivyo, ila walitia chumvi ili upuzi wa jambo la ufufuo udhihirike.

k.24 Yesu hakusema lolote juu ya desturi ya ndugu wa yule mtu aliyekufakumchukua mkewe, ila moja kwa moja, alisema wazi kwamba wamekosakuelewa jambo la ufufuo kwa sababu mbili. Kwanza ijapokuwa wametajaMaandiko hawakujua Maandiko sawasawa. Sababu ya pili ni kukosa kulitafakarijambo hilo bila kutambua uweza wa Mungu. Kwa hiyo wamekosa kuelewamafundisho ya Maandiko pamoja na uwezo wa Mungu. Kwa sababuhawakuamini neno la ufufuo ilibaki njia hiyo ya kuendeleza uzazi kwakudumisha jina la mtu.

k.25 Walikosa walipolinganisha maisha ya sasa na maisha ya baadaye.Maisha ya baadaye si maendeleo ya maisha hayo. Katika maisha ya baadayehakuna kifo na kwa sababu hiyo hakuna haja ya kuzaa ili wanadamuwaendelee, na ikiwa hakuna haja ya kuzaa hakuna haja ya kuoana kwa sababuni katika uhusiano wa ndoa uzazi unatokea kwa halali ya kufuata mpango waMungu. Maisha ya baadaye ni kipawa cha Mungu cha maisha mapya. Ndoa ni

MARKO242

uhusiano wa pekee uliopangwa na Mungu kwa watu wawili tu, ila katika maishamapya hakuna nafasi kwa uhusiano wa namna hiyo wa watu wawili tu wakupendana na kuoneana wivu, hali zilizo nzuri katika ndoa. Katika maisha yabaadaye hamna jinsia ila upendo utaendelea, upendo wa hali ya juu, upendokama aliokuwa nao Yesu alipojitoa Kufa kwa ajili yetu. Kama Pauloalivyofundisha (1 Kor.15:35-50) ufufuo sio kuendelea kuishi bali ni kubadilishwakutoka hali ya sasa hadi hali mpya. Hivyo Yesu aliwakumbusha juu ya viumbevingine vya mbinguni, malaika ‘kama malaika walio mbinguni’. Bila shaka watuwengi hudhani kwamba bila kuoana furaha zao zitapungua

lakini Mungu anao uwezo wa kuleta furaha za ajabu, za kiroho, kwa sababumabadiliko yatatokea ndani yetu, nasi tutayaonja mambo mapya.

k.26 Halafu Yesu aliendelea kusisitiza ukweli wa ufufuo kutoka Maandikoakichagua dondoo kutoka Kitabu kimojawapo cha Musa walichokubali. Alitumiahabari za Musa jangwani wakati alipoitwa na kutumwa na Mungu kwa kazimaalumu ya kuwatoa Waisraeli utumwani, Misri. Mungu alijitambulisha kwakekwa kusema ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu waYakobo’ (taz. neno ‘Mungu’ limerudiwa kwa kila mmoja). Mungu hakusema‘nalikuwa Mungu wa...’ bali Mimi ni Mungu wa....’ kana kwamba hao walioishimiaka mingi kabla ya Musa walikuwa wangali hai. Walikuwa na uhusiano naMungu hai ambao uliendelea kuwepo hata baada ya kufa. Neno muhimu lahusutabia za Mungu, Mungu aliye hai, Mungu Mwaminifu, Mungu aliyefanya Aganona watu wake. Haiwaziki kwamba, uhusiano wa mtu na Mungu wa namna hiyoutakatika mara mtu wake aondokapo duniani. Ni vigumu kufikiri kwamba Munguatawaacha watu wake mwisho wa maisha yao na kuwatupa kama takataka.Bila shaka uhusiano wake na watu wake utaendelea kwa vile Yeye Yu hai, tenaYeye huwa mwaminifu kabisa. Tumaini la ufufuo limejengwa juu ya ujuzi wabinafsi wa kushirikiana na Mungu Aliye Hai (Yn.17:3). Agano lake halivunjikikwa urahisi, wala upendo wake hauwi wa muda.

k.27 Mwisho kabisa Yesu akatoa tangazo wazi ‘Yeye, si Mungu wa wafu, baliwa walio hai’ hakuridhiana wala kuhojiana nao. Aliwaambia wazi kabisawamepotea sana katika ufahamu wao wa Mungu na katika kuelewa Maandikona katika kuwaza kwamba maisha ya baadaye yatalingana na maisha ya sasa.

Mara kwa mara tumepewa mwitikio wa watu, ila hapo, hatuambiwi jinsi walewalioleta swali walivyoona wala hatujui wasikilizaji walivyofikiri. Bila shakaMafarisayo walifurahia jibu la Yesu kwa sababu lilithibitisha msimamo wao.Hata hivyo hawakuwa tayari kubadili mashauri yao ya kumwondoa nawalijiunga na wengine ili walete swali lingine.

12:28-34 Swali juu ya amri iliyo kuu (Mt.22:34-40)Tumeona kwamba Yesu ameisha kuwajibu kwa busara Mafarisayo naMaHerode waliomjia na swali la kuhusu kodi. Ndipo aliwajibu kwa hekima

MARKO 243

Masadukayo waliomwuliza juu ya Ufufuo. Halafu akaja mtu mmoja mwandishi,hao waandishi walijishughulisha na mambo ya sheria na mapokeo, naowalijadiliana wao kwa wao juu ya amri ipi iliyo kuu. Pengine walikuwa wakitafutamsingi ufaao ambao juu yake watajenga mipango yao ya sheria.

k.28 Mathayo amesema kwamba huyo aliyekuja alikuwa Farisayo nainaonekana alitumwa na Mafarisayo baada ya kuona jinsi Yesu alivyowashindaMasadukayo. Pia Mathayo amesema kwamba alikuja ili amjaribu Yesu ilaMarko hakuonyesha kwamba alikuja kwa nia mbaya. Alitambua kwamba Yesuamewajibu vizuri wale waliotangulia kuleta maswali, hivyo, alitaka kujuamawazo ya Yesu kuhusu amri na kujua ni zipi ambazo Yesu aliziona kuwamuhimu. Kwa hiyo, huyo mtu alionekana kuwa tofauti na wale waliomtangulia,mtu wa kweli, mwenye akili ya kupima mambo bila kuanza na msimamo fulaniwa kutetea. Alimheshimu Yesu. Swali si la siasa wala mafundisho bali ni lamaadili.

k.29-31 Yesu hakuleta mbele yake amri ngeni bali ile iliyosemwa mara mbilikwa siku na kila Myahudi tangu zamani za Musa. Walipenda kuyaweka manenohayo katika visanduku walivyovaa kichwani, pia waliyaweka sandukuni nakuweka mlangoni pa nyumba zao. Iliitwa ‘Shemai’ maneno yaliyojumlisha nakuwa mafupisho ya imani yao na msingi wa maombi yao. Maneno yenyeweyalitoka Kumbukumbu 6:4-5,8-9. Yesu aliunganisha maneno hayo na mengineyaliyotoka Lawi 19:18 yaliyohusu kupenda jirani kama nafsi yako. Yawezekanani Yesu aliyekuwa wa kwanza kuziweka amri hizo mbili pamoja kuwa kamaamri moja iliyo na sehemu mbili. Mungu ni wa pekee, ni Mmoja tu, nayeawapenda wanadamu upeo, kwa hiyo anayo haki ya kuwaita wanadamuwampende Yeye kabisa. Vivyo hivyo, wanadamu hupaswa kuwakaribisha nakuwapenda wanadamu wenzao kabisa, kwa kiasi kile ambacho mtu hujipendamwenyewe. Kwa kawaida mtu hujipenda mwenyewe, kwa hiyo, awe na halihiyo katika kumpenda jirani kama nafsi yake. Mungu ameonyesha upendokatika matendo yake, ni zaidi ya kujisikia upendo kwa ndani. Kwa vyovyoteupendo wa kweli, wa moyo, hutokeza upendo kiutendaji. Upendo wa namnahiyo hauwezi kuelezwa kwa sheria wala kuwekwa au kubanwa katika amri tu, nikiini cha sheria kwa sababu unagusa sababu na nia za kutenda kwetu. Amrizote mbili zinatawaliwa na neno la upendo.

Tena katika upendo jambo linalosisitizwa ni kufanya kuliko kutokufanya.Tukipenda mtu mwingine ni hakika kwamba hatutamdhuru, kama kumwibia, aukumwua, au kumchukia, n.k. ila kwa upande mwingine twaitwa kumpenda kwakutoa msaada, kumhurumia, kusema vizuri juu yake n.k. (1 Kor.13:1ku.Rum.13:8-10). Upendo wa kujitoa kwa Mungu na watu hutokana na sababu yakuwa ‘wana, watoto wa Mungu’ kwa kuzaliwa naye. Mara nyingi watuhutanguliza kuwapenda wanadamu na kuona waweza kufanya hivyo bilakumwabudu Mungu. Hii si sawa. Pamoja na hayo wako wengine wanaodaikumpenda Mungu, ila hawajali wanadamu wenzao. Hilo nalo si sawa. Amri

MARKO244

inayotangulia ni kumpenda Mungu ndipo kutokana na upendo huo mtuhumpenda jirani kama nafsi yake. Amri hizo mbili zisitengwe. Katika maishayake yote Yesu aliishi kwa kuzitii amri hizo mbili.

k.32-33 Mwandishi alitambua kwamba Yesu amemjibu kwa busara nayeameridhika. Alitambua kwamba jibu la Yesu lilichimba chini kabisa ya manenoya amri na kuvifunua viini vyake. Alitambua kwamba kumpenda Mungu kabisana kumpenda jirani kama nafsi yake ni bora zaidi ya dhabihu na sadakawalizozitoa daima. Kwa wakati huo Yesu hakuwa na maana kwamba sadakaziondolewe, ila bila upendo hazina manufaa. Yesu hakuweza kushtakiwakwamba amedharau Torati au amri fulani kwa sababu alionyesha kwamba kwanjia ya kumpenda Mungu na jirani Torati hutimizwa kwa ukamilifu.

k.34 Yesu alimtia moyo huyo mwandishi kwa unyofu wa kuwaza kwake, alionakwamba alihitaji kuchukua hatua nyingine ya kujikabidhi Kwake, yaanikumwamini, ndipo atakuwa ameingia Ufalme wa Mungu badala ya kuwa karibuyake tu. Halafu Marko alimaliza habari hiyo kwa kusema kwamba hakunaaliyethubutu kumwuliza Yesu swali tena. Amethibitishwa kuwa Mwalimu stadi,mwenye hekima ya kipekee, mwenye uwezo wa kutoa majibu yaliyochimbachini kabisa na kugusa misingi ya mambo. (Ling.Rum.13:8-9; Gal.5:14; Yak.2:8)Ilitabiriwa katika Zaburi 2:2 kwamba Masihi atahojiwa sana na wakuu, na unabiihuo ulitimizwa wakati huo.

12:35-37 Swali la Yesu juu ya Kristo kuwa nani (Mt.22:44-45; Lk.20:41-44)

Yesu aliendelea na huduma yake ya kuwafundisha watu katika kumbi la Hekalukama marabi wengine. Tumeishaona kwamba Marko amependa kusisitiza kazihiyo ya Yesu. Kwa Yesu ilikuwa nafasi yake ya mwisho kuwaelimisha watu juuya Utume wake na Nafsi yake. Bado hajatamka wazi kuwa Masihi ila ndani yausemi na utendaji wake yamefichwa madai ya kuwa Masihi, kwa hiyo, walewatakaouzingatia usemi na utendaji wake watatambua Cheo chake na Nafsiyake. Yule kipofu wa Yeriko alimwita ‘Mwana wa Daudi’ na umati wa watuwaliomsindikiza alipoingia Yerusalemu walimwita vivyo hivyo, kwa hiyo, Yesualiona vema awafanye watu watafakari sana juu ya maana ya maneno ‘Mwanawa Daudi’.

k.35 Baada ya kushambuliwa na maswali yao aliona vema awaulize swali lamaana sana kuhusu Kristo (Masihi) kuwa Mwana wa Daudi. Kwa neno‘husemaje waandishi ya kwamba..’ inaonekana alikuwa akiwaza waandishi namafundisho yao naye alitaka kuwavuta watu wazingatie kwa upya Jina la‘Mwana wa Daudi’ kwa kutazama kwa makini maneno ya Zaburi 110. Wotewalikubaliana kwamba Zaburi hiyo ilitungwa na Daudi na ilimhusu Masihi. Yesuhakutaka kuwatega kama wao walivyomtega wala hakutafuta jibu la nadharia,hasa shabaha yake ilikuwa wamwaze Masihi na jinsi itakavyompasa, Utumewake ni wa namna gani? yaani amekuja kufanya nini hasa? Hivyo, aliuliza swali

MARKO 245

na kulijibu kwa njia ya kuuliza swali lingine ambalo liliachwa hewani ili waowenyewe walizingatie na kuona jinsi linavyogusa Utume wake.

k.36 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu, uketi mkono wangu wa kuume.....’Maneno hayo yalisemwa na Daudi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, kamaunabii juu ya Masihi. ‘Bwana, yaani Mungu, alimwambia Bwana wangu, yaaniMasihi/Mfalme - yaani Mungu alimwambia Masihi aketi mkono wake...... ‘HivyoDaudi alikuwa akitaja’ mwingine ambaye alimwita ‘Bwana’. Huyo si Mungu kwasababu Zaburi inasema kwa Mungu na ni huyo Mungu anayesema kwa huyo‘Bwana’. Hivyo Daudi alimwita Masihi ‘Bwana wangu’. Kwa hiyo, awezajeMasihi awe ‘mwana’ wa Daudi na ‘Bwana’ wa Daudi? Maandiko yalisema wazikwamba Masihi atatoka viunoni vya Daudi (2 Sam.7:11-16). Yesu hakukanakuzaliwa kwake Bethlehemu kama Mwana wa Daudi katika ukoo wa Daudi iliaitwe kwa halali mwana wake; hiyo si hoja yake. Hoja yake ni kwamba yeyealiyezaliwa ni zaidi ya ‘Mwana’ wa Daudi, ni ‘Bwana’ wake, mwenye asilinyingine, ametoka kwa Mungu, ni Mwana pekee wa Mungu, na ndivyo Daudialivyomtaja katika Zaburi 110, alipoukuza ukuu wa Masihi. Kwa hiyo, katikakutumia Jina hilo, ‘Mwana wa Daudi’ watu walidai madogo badala ya makubwa.Wayahudi walitazamia huyo Masihi ataurudisha Ufalme katika hali yake yazamani za Daudi. Daudi alikuwa mtu wa vita, hodari sana, aliyeshinda Wafilistina kuliweka huru taifa la Israeli. Kwa hiyo, maneno ‘Mwana wa Daudi’ yalijaavidokezo vya mawazo ya siasa na uzalendo. Hivyo, katika mawazo ya watu,Jina hilo lilihitaji mtu wa vita, vita vya kuwafukuza Warumi. Kumbe huyo Masihini tofauti na mwimba Zaburi alivyotabiri, Masihi wa kweli atokaye kwa Mungu,na kuzaliwa katika ukoo wa Daudi, atatawala kutoka mbinguni, atauleta Ufalmewa tofauti sana na falme za dunia. Yeye ni shina na mzao wa Daudi(Ufu.22:16). ni Mfalme wa haki na wa amani, silaha yake ni Neno lake. Manenohayo yametabiri Kufufuka na Kutukuzwa kwa Yesu. (Rum.1:3-4; Mdo.2:34-35;13:23; 1 Kor.15:15; Ebr.1:13; 10:12). Hivyo, Yesu, bila kusema wazi, amedaikuwa Masihi wa kweli, na matimizo ya unabii wa Zaburi 110. Ni tofauti sana najinsi walivyozoea kumwaza Masihi. Yeye si kama yule walivyomdhani nakumtazamia.

k.37 Inaonekana watu waliomsikiliza walifurahi, pengine kwa kuona kwambaameyashambulia mafundisho ya waandishi.

12:38-40 Onyo la Yesu juu ya waandishi (Mt.23:1ku; Lk.20:45-47; 11:39-52)k.38 Waandishi walikuwa wajuzi wa Maandiko na waliyashughulikia nakuyafafanua kwa watu, kama kundi la wataalamu. Wengine walikuwaMafarisayo. Baadhi yao walikuwa wazuri (12:28) hata hivyo, wengi walitumianafasi zao kwa kujipenda, kujionyesha, na kujitajirisha. Kwa kawaida,wanadamu hupenda kuonekana na kuheshimiwa na wenzao, ila hao waandishiwalipita kiasi. Yesu alitaja jinsi walivyopenda kuvaa mavazi marefu kila wakati,walivaa nguo ndefu, nyeupe, ya kitani. Kwa njia hiyo walijitangaza kuwa watuwa dini. Walipenda kusalimiwa sokoni wakijifanya kuwa bora kuliko wengine.

MARKO246

Vilevile walipenda viti vya mbele sinagogini na katika karamu za wakuu. Sineno jema wajionyeshe kwa watu, na kujionyesha kwa watu huku wamejaachoyo na hila mioyoni mwao ni vibaya. Walikuwa wanafiki, na walijifanya kuwawatauwa. Walipotembelea wajane na wanyonge walisali sala ndefu hukuwakitazamia wapewe pesa nyingi na hao wajane. Wakati ule walifanya kazi yawanasheria iliyowapa nafasi ya kutoza gharama kubwa kuliko ilivyokuwa haki.Walijipendekeza kwa watu, hasa wakuu, kinyume cha Torati iliyohitaji watuwampe Mungu sifa zote. Kosa lao halikuhusu kazi yao ya kuyafafanuaMaandiko, waliyafafanua vizuri na kuyaheshimu kwa nje ila hawakuyatimizakatika maisha yao. Ufahamu wao wa nje ulihitilafiana na hali ya moyoni iliyojaakiburi na choyo. Walikuwa

wametumia vibaya cheo chao na mapendeleo yao. Hivyo walitumia dini kuwanjia ya kupata faida na kama ‘nguo’ ya kuficha choyo chao na kujipenda kwao.

k.40b Yesu alisema kwamba hukumu kwa waandishi wa namna hiyo itakuwakubwa. Walipewa heshima kubwa nao walidaiwa uaminifu mkubwa katikakutimiza wito wao. Kuwa wa kweli na mnyofu ni muhimu kuliko nguo safi nasalaam za watu. Neno hilo lahusu viongozi na watumishi wa Kanisa, maanawakati wote wenye vyeo na uongozi hujaribiwa sana kwa upande wa ‘heshima’na ‘sifa’. Katika habari hiyo Yesu amebainisha thamani halisi za Ufalme wakena thamani zinazosifiwa katika ulimwengu huu.

12:41-44 Yesu alimsifu mjane na toleo lake (Lk.21:1-4)k.41 Baada ya kuwasema waandishi kwa ukali Yesu alisema kwa uzuri juu yamjane mmoja ambaye hakutaka kuonekana tofauti na hao waandishiwaliotembeza uzuri wao mbele za watu. Hakuwa na cheo wala kuhesabiwakuwa wa maana machoni mwa watu. Hata hivyo alimpenda Mungu sana nakumpa vyote alivyokuwa navyo. Katika habari hiyo Yesu alibainisha utoaji wakweli. Alikuwa ameketi karibu na ua la wanawake, pengine alikuwa amechokabaada ya shughuli za kufundisha. Katika ukuta wa ua la wanawake yalikuwapomasanduku 13 yenye sura ya tarumbeta, yaliyowekwa kwa watu kutoa sadakazao kwa hekalu. Hivyo Yesu alikuwa akiangalia jinsi watu walivyoweka vipawavyao masandukuni na aliweza kuona kiasi walichotoa kwa sababu wenginewalipenda watu waone kiasi walichotoa. Yesu aliona kwamba matajiri wenginewalitoa pesa nyingi kutoka utajiri wao ila alijua kwamba wamebaki na pesanyingi zaidi.

k.42 Ndipo akaja mwanamke, mjane, maskini; yeye naye aliweka kipawachake sandukuni, kilikuwa senti mbili, pesa ndogo kabisa, hata Marko aliielezakwa wasomaji wake kuwa ‘nusu pesa’ yaani ndogo kabisa, ila tofauti yake nawale matajiri ilikuwa kwamba hakubaki na nyingine nyumbani.

k.43 Yesu aliona tendo hilo la huyo mjane kuwa tendo la maana sana, na kwasababu hiyo, aliwaita wanafunzi ili watafakari hilo alilolitenda huyo mjane. Ndipo

MARKO 247

aliendelea kuwaonya juu ya kupima mambo kwa kufanya ulinganifu wa kiasicha pesa, kiasi si kitu, bali cha maana zaidi ni kiasi ambacho mtu amebakinacho baada ya kutoa, pamoja na hali ya moyo katika kutoa. Mtu atoe kwamoyo mkunjufu na kwa kulingana na alicho nacho. Wale wengine walitoa fedhanyingi, ila walibaki na nyingi, hawakuumizwa. Ila huyo mjane alitoa fedha yotealiyokuwa nayo, angaliweza kubakiza senti moja, ila alitoa zote mbili, haliakimwamini Mungu kwa riziki zake. Alijitoa kabisa kiasi cha kuumia, kwasababu alimpenda Mungu. Kila alipopata nafasi Yesu aliwafundisha wanafunzi,ili katika huduma yao ya baadaye wakumbuke sana kielelezo chema cha huyomama. Watajaribiwa kuwaheshimu wale wenye uwezo mkubwa wa kusaidiakazi za Kanisa na kutokujali wenye uwezo mdogo wa kutoa, ila wasipofushwemacho. Mungu hutaka watu wajitoe kabisa Kwake, na kumtegemea kwamahitaji yao ya kila siku. Jambo hilo lilifuata onyo lake juu ya waandishi na halizao za kufanya wajane kuwa mawindo yao.

13:1-37 (Mt.24:1-51; Lk.21:5-38)Sura hii nzima ni hotuba ndefu ya Bwana Yesu kuhusu Anguko la Hekalu lapale Yerusalemu pamoja na mambo yatakayotokea hadi Atakaporudi tenakatika Utukufu. Katika Injili hiyo ni hapo ambapo Yesu amesema kwa kirefu. Nivema tuone mahali pa habari hiyo katika utaratibu wa Injili hiyo, ni baada yaHuduma yake na kabla ya Kufa Kwake. Hivyo, uhusiano mkubwa upo kati yahukumu ya Mungu juu ya Yerusalemu na Taifa la Israeli na Kifo chake. Mamboyanayotajwa katika sura hii yanawiana na mambo yaliyotangulia. Kuangukakwa Yerusalemu ni zaidi ya itikio la Warumi kwa ukaidi wa Wayahudi. Ni itikio laMungu la hukumu kwa uasi wao wa siku nyingi uliofikia upeo katika kumkataaMasihi wao wa kweli, Yesu Mwenyewe.

Hekalu lilikuwa mboni ya jicho kwa Wayahudi, muhimu kabisa katika maisha yaTaifa teule. Kila Myahudi aliliwaza kwa kusikia fahari ya kitaifa. Kusemakinyume chake kulihesabiwa kusema juu ya Mungu na Taifa lake teule. Ilakatika mawazo ya Yesu lilikuwa jengo lililotengenezwa kwa mikono nawanadamu na Mungu. Kwa njia ya Kufa na Kufufuka Kwake Munguatatengeneza jengo jipya, jengo lisilofanyika kwa mikono, jengo ambalo ni jamiiya watu wanaomwamini na kumtegemea Kristo katika maisha yao (14:58;15:29).

Habari hiyo haikutolewa kwa shabaha ya kutoa taarifa kwa wafuasi wake jinsimambo yatakavyotokea katika historia itakayofuata Kufa na Kufufuka Kwake.La! hasa Yesu alitaka kuwapa wafuasi wake tahadhari ili wawe wameandaamawazo yao tayari kuzikabili shida zitakazotokea, wasidanganywe na walewatakaosoma shida hizo kuwa ishara ya mwisho. Kila mara katika hotuba yakeYesu aliwasihi wasikilizaji wake wajihadhari wasije wakadanganyika.

MARKO248

13:1-2 Utangulizi wa habari ya maangimizo ya hekaluYesu na wanafunzi walikuwa wakiondoka hekaluni, mahali ambapo tanguwalipofika Yerusalemu wamehudhuria kila siku na Yesu amewafundisha watu.Inaonekana wakati huo ni mara ya mwisho (ling.Mt.23:38 ‘nyumba yenummeachiwa ukiwa) na kwa Yesu ni kama nafasi ya kuliaga. Wanafunziwalimwonyesha hekalu na uzuri wake wa ajabu, mawe yake makubwa n.k.Kweli lilikuwa jengo la ajabu sana, lilipakwa dhahabu juu, iliyometameta katikajua; mawe yake yalikuwa meupe, kama marimari, makubwa, kila jiwe kama futi30 kwa urefu. Lilijengwa kwa miaka 46 na bado halijamalizika (Yn.2:20).Lilikuwa jengo imara sana. Wanafunzi waliona fahari juu yake na kulishangaakabisa.

k.2 Ndipo Yesu akajibu kwa kuwaambia kwamba litabomolewa kabisa, hatajiwe moja halitabaki juu ya jingine. Bila shaka walishtuka sana kwa habari hiyo.Ni wazo lisilowazika! Onyo la kwanza kwa wanafunzi ni kwambawasiyategemee majengo wala vitu vya nje vya dini.

13:3-13 Habari za dhiki mbalimbaliWalipokwisha kuvuka bonde la kijito cha Kedroni, wakaketi katika mlima waMizeituni wakitazama hekalu, hali likimetameta juani. Ndipo wanafunzi wanne,wale waliokuwa wa kwanza kuitwa (1:16-20) walitaka kujua zaidi juu ya neno lahekalu kubomolewa. Pengine wanafunzi wengine walikuwepo ila ni haowalioongoza maulizo hayo. Walitaka kujua ni lini tukio hilo litakapotokea nadalili yake, yaani ni jambo au mambo gani yatakayoashiria kufika kwa wakatihuo. Je! walitaka kujua habari za kubomolewa kwa Hekalu na Anguko laYerusalemu tu, au ndani ya swali lao kuhusu ‘mambo hayo’ wamewaza mwishowa mambo yote (Mt.24:3). Kwa wengi kubombolewa kwa hekalu kutakuwamwisho wa ulimwengu wao kwa sababu hawakuweza kuwaza moja bila la pili.Kuanguka kwa Yerusalemu na mwisho wa ulimwengu ni mambo mawili tofauti,hata hivyo, yanawiana, na katika sura hiyo ni vigumu kujua kwa hakika ni habariipi inayohusu mwisho wa Hekalu na Kuanguka kwa Yerusalemu na ipiinayohusu mwisho wa mambo yote.

k.5 Kabla ya kutaja shida mbalimbali zitakazotokea Yesu alitoa tahadhari kwawanafunzi wake juu ya kudanganywa. Hakutaka watu wawaze kwamba mwishou karibu kuliko ulivyokuwa na ya kwamba mambo kadhaa ndiyo ishara halisiambayo hasa siyo ishara yake na kwa sababu hiyo zisitumiwe katika kusisitizakuhusu kuja kwa huo mwisho. Katika vizazi vyote tangu Yesu aliposema hayoWakristo kadha wamekosa kujali onyo hilo, wengine wamewadanganya watuna kupotosha imani zao na wengine wamedanganyika na mpaka leo ndivyoilivyo.

MARKO 249

k.6 Tahadhari moja ilihusu kutokea kwa Masihi wa uongo, watu waliojichukuliajina na mamlaka ya kuwa wametumwa na Mungu kuleta ujumbe wa kipekee.Wakati wa Agano la Kale walitokea manabii wa uongo, nao walipokelewa, kwasababu walileta ujumbe mwepesi, huku manabii waliotumwa na Mungu wenyeujumbe mgumu wa kuita watu watengeneze mwenendo wao waliteswa. Alitoaonyo hilo tena k.21-22.

k.7-8 Tahadhari nyingine ilihusu habari za vita, matetemeko ya nchi, na njaa.Hayo yote hayana budi kutokea, nayo yatazidi kutokea, ila siyo kusema vitafulani, au njaa kubwa fulani, au tetemeko kubwa fulani, ndiyo lile linalofikishahuo mwisho. Hayo yote yanaashiria kuja kwa ule mwisho, lakini siyo kusemakwamba jambo fulani ndilo lile la kuufikisha huo mwisho. Utakuwepomwenendo mrefu wa dhiki mbalimbali, nazo zitazidi kwa ukali, hata hivyo, nihatua tu, sio mwisho wenyewe. Hazina budi kutokea kabla Mungu hajatimizamapenzi yake ulimwenguni. Wafuasi wa Yesu wapaswa wajiandae kwa dhiki namateso, kuliko kukunja mikono na kuungojea mwisho (1 The.4:11; 2The.2:1-3).

k.9-13 Halafu Yesu aliendelea kwa kutoa tahadhari nyingine kabla ya kutajashida nyingine. Yeye, kama mchungaji mwema wa kutunza kondoo zakehakuwa mtangazaji wa habari tu, kwa hiyo, alitoa onyo kuhusu dhikiwatakazopata baada ya Yeye kuondoka. Wafuasi wake watateswa,watashtakiwa barazani, na kupigwa sinagogini na Wayahudi wenzao(Kum.25:2-3; 2 Kor:11:24) wala si hivyo tu, watashtakiwa mbele ya watawala naviongozi wa maeneo na nchi (Mdo.12:1-3; 23:24; 24:27). Jambo hilo ijapokuwani baya lina uzuri wake, linatoa nafasi kwa Mkristo kumshuhudia Bwana wake.Ushuhuda huo utawajulisha washtaki wao kwamba wamemkataa Kristo nawokovu wake. Hawatateswa kwa ajili yao bali kwa ajili ya Kristo. Hawana kosaila lile la kumtetea Kristo na kuweka mbele ya watu madai na haki ya Kristokupewa utiifu wao. Kwa hiyo Yesu aliwafundisha kwamba wito wa Kanisa nikuhubiri Injili (Mdo.1:8) na kuteswa kwa ajili yake. Kanisa halina sababunyingine ya kuwepo. Katika historia yake Kanisa limekuwa na nguvu namafanikio wakati wa mateso, na dhidi yake, limekuwa dhaifu wakati wakujipendekeza kwa watu wa dunia hii. Neno muhimu ni kuhusu Injili kuhubiriwakwa mataifa yote, maana yake, huo mwisho hauji mpaka dunia imepatakujulishwa wokovu wa Yesu Kristo.

k.10 Makusudi yanayotawala mipango ya Mungu tangu awali ni kuhubiriwakwa Injili kwa watu wote, na waumini wameingizwa na kupewa wajibu wakutekeleza mapenzi hayo ya Mungu. Hayo mapenzi yake hayazuiliki namateso. Upo uwiano, mateso yatokana na Injili kuhubiriwa na Injili kuhubiriwakunasababisha mateso.

k.11 Wanafunzi waliambiwa kwamba hakuna haja ya wasiwasi wakati wakuletwa barazani. Huenda watakamatwa ghafula, bila nafasi ya kuandaa majibuyao. Tukumbuke wafuasi wengi wa kwanza hawakuwa na elimu,

MARKO250

wangalishindwa kutunga utetezi stadi, hata hivyo, Yesu aliwatia moyo wakuahidi kwamba Roho Mtakatifu atawasaidia kuelewa namna ya kujibumashtaka. Mungu hushirikiana nao wanapokabili mamlaka za ulimwengu huu.Ila wasidhani kwamba Roho atawaokoa, ila atawasaidia kutoa jibu sahihi. Nenohilo halihusu wahubiri na maandalizi ya hotuba zao. Ni juu yao kuandaa vizurikwa msaada wa Roho ndipo kumwachia Roho awasaidie wakati wa kuhubiri.

k.12 Mateso yataleta mafarakano katika jamii za waumini. Mahusianoyatakatika, wengine watashawishiwa kusaliti ndugu zao, lakini Mkristo apaswaawe mtiifu kwa Kristo zaidi ya (si badala ya) kuwa mtiifu kwa familia. Yesualiwatahadharisha kwamba waweza kupata shida kutoka pande zote, kutokaadui na kutoka rafiki.

k.13 Halafu Yesu aliwaambia kwamba watachukiwa na watu wote, yaani kwakila aina ya watu, potelea mbali ni wa tabaka gani, rangi gani, jinsia gani naumri gani. Mateso yatatoka kwa aina zote za watu; ila haina maana kwambakila mtu atawachukia, wengine watawadharau na kutokuwajali tu. Tenawalikumbushwa kwamba hayo yote yatatokea kwa sababu ya ‘Jina lake’ yaaniwanapokuwa waaminifu Kwake na kuhubiri Injili. Watahitaji subira, maanamambo hayo si ya wakati mmoja tu, yahusu wakati wowote na mahali popote.Wawe waaminifu wakati wa mateso na uasi. Ila mwishowe ushindi utapatikana.Wataokolewa kabisa kutoka mazingira yote ya uovu, watafika salama kwaUfalme wa Mungu (Ebr.9:28). Bila shaka, mbeleni, wanafunzi walipopatwa namambo hayo walitiwa moyo kwa kukumbuka jinsi Yesu alivyowaelezea hayoyote ni katika mpango wa Mungu wa kuuleta Ufalme wake kwa utimilifu,mwisho wa mambo yote, atakaporudi Yesu katika Utukufu.

13:14-23 Yerusalemu kushambuliwa na WarumiKama ambavyo tumeishafikiri kwamba sura hii inahusu matukio mawili ambayohabari zake zinaingiliana, tukio kubwa la Kuanguka kwa Yerusalemu (B.K.70)na tukio kuu la mwisho wa ulimwengu. Baadhi ya wataalamu hufikiri kwambavifungu hivi vinahusu mambo hayo mawili. Ila baadhi hufikiri sehemu hiyo yoteinahusu Kuanguka kwa Yerusalemu. Hilo ndilo wazo linalofuatwa katikamaelezo yafuatayo, ila si kosa kusema kwamba habari za mambo hayo mawilizimeingiliana, maana hatujui kwa hakika.

k.14 ‘chukizo la uharibifu’ limetajwa katika Dan.9:27; 11:31; 12:11 ni kuhusuneno la kufuru ambalo linapotendeka katika mahali patakatifu linachukiza.Pengine ni jambo fulani au tendo la mtu fulani (1 Waf.21:26; 2 Waf.16:3). Katikahistoria ya nyuma jambo la namna hiyo lilitokea wakati wa Mfalme AntiokusEpifania alipoweka sanamu ya kipagani hekaluni na kutoa dhabihu ya nyamaya nguruwe madhabahuni. Jambo hilo lilitokea K.K.168 ndipo YudaMakabadayo na wenzake waliinuka na kupigana vita na kuwashinda haowageni. Mwaka B.K.44 Kaisari Kaligula alijaribu kuweka sanamu yake hekaluni,akashindwa. Ni nini iliyotokea wakati wa Yerusalemu kushambuliwa na Warumi

MARKO 251

kuanzia B.K.66 hadi B.K.70?. Tukifuata Injili ya Luka 21:20 inaonekana nijambo linalohusu majeshi ya Kirumi kuuzunguka Mji Mtakatifu halafu baadayekuingia mle ndani wakibeba bendera zao zenye alama ya tai na sanamu yaKaisari ndipo wakazisimamisha hekaluni baada ya kuuteka Mji. Yesu aliwaonyawanafunzi juu ya jambo la namna hiyo kutokea. Ni wazi kwamba, kwa jinsimwandishi mmoja wa historia ya Kiyahudi (Josephus) alivyoandika juu ya sikuhizo, dhiki kubwa ilitokea. Warumi walizunguka mji kwa miaka miwili na watuwalishindwa kutoka na kuingia, chakula kiliadimika, hata watu walithubutu kulawatoto wao n.k. Inasemekana kwamba hata wengine walijiingiza masadukanikungojea kufa hali wakielekeza nyuso zao hekaluni katika tumaini la kutokeakwa Masihi wa kuwaokoa.

k.14b-18 Neno la Yesu kwa wanafunzi na waumini wake watakapoona tukiohilo lilikuwa ‘kimbieni kwa haraka’ waende nje ya Yerusalemu kwa harakakabisa. Wasiingie chumbani kuchukua kitu, wala wakulima wasirudi nyumbanikuchukua nguo nyingine. Ndiyo hali ya haraka iliyotakiwa, kwa sababu maishayao ni ya thamani kuliko vitu vyao. Yesu alitaja wenye mimba na watotowadogo akiwahurumia kwa shida watakazozipata. Aliwashauri waombekwamba jambo hilo litokee wakati wa hewa nzuri, si wakati wa baridi ambapomito itajaa maji n.k.

k.19-20 Hali ya siku zile itakuwa mbaya kupita uwezo wa mtu kuwaza(Eze.7:14-23). Maneno ya 19b ‘wala haitakuwa kamwe’ yameongoza wenginekufikiri kwamba maneno hayo yanahusu mwisho wa ulimwengu si Anguko laYerusalemu. Ila kama ambavyo tumeishaona katika unabii jambo fulani huwana timizo la hivi karibuni pamoja na timizo kamili baadaye. Ni vigumu kuondoasehemu hii inayohusu Kuanguka kwa Yerusalemu na kuifanya kuwa inahusumambo ya mwisho. Maneno yanaashiria ukubwa wa dhiki za siku zile. Hatahivyo, matumaini yapo, Mungu hawi mbali kama hahusiki na tukio hilo, katikamapenzi yake alikuwa amekuja kuwahukumu watu wake kwa uasi wao na Yeyeatafupisha siku za dhiki na uzito wa taabu hizo. Wateule wake wapya, wauminiwa Kristo watajisalimisha watakapolikumbuka onyo hilo la Yesu na kukimbiaYerusalemu kwa haraka.

k.21-23 Lakini dhiki hiyo siyo ishara ya kufika kwa ‘mwisho’. Wenginewatatokea ambao watashauri kwamba hakuna haja ya kukimbia. Ila wauminiwasiwajali wale waletao ujumbe unaosema kwamba Kristo yupo. Wakati huoKristo huja kwa siri kuhukumu uasi wa watu wake, Israeli ya kale, haji wazi.Hata wengine wakifanya miujiza, ni wadanganyaji, waumini wasiwaamini.Kufanya miujiza si dalili ya kweli inayouhalalisha ujumbe wa mtu, zamani zakale walikuwapo manabii wa uongo waliofanya miujiza (Kut.7:11) naowataendelea kutokea mara kwa mara. Kusema Kristo yu karibu ni dhana yenyekosa na hoja ya uwongo. Neno la Yesu ni wazi kabisa, watakapoliona chukizola uharibifu, wakati Warumi wakija kuuteka Mji, wakimbie kwa haraka mno.Ndipo Yesu alirudia kuwaambia wanafunzi ‘jihadharini, nimekwisha kuwaonya

MARKO252

yote mbele’. Wakristo wengi waliondoka Yerusalemu na kwenda mpaka Pellakatika eneo la Perea, ng’ambo ya Yordani. Kati ya Kuja kwake mara ya kwanzana Kuja kwake mara ya pili, hakuna ishara ambayo itaondoa haja ya kuwa naimani.

13:24-32 Ushindi wa Yesu, Mwana wa AdamuHapo inaonekana Yesu alisema juu ya tukio kubwa la ‘mwisho’ wa mambo yoteambayo ishara yake ni Kurudi kwa Yesu Mwenyewe katika utukufu nakuwakusanya Kwake wafuasi wake.

k.24-25 Jambo la kwanza kuhusu tukio hilo ni mabadiliko katika maumbile, juakutiwa giza, mwezi kutokutoa mwanga wake, na nyota kuanguka chini, nanguzo za mbinguni kutikisika. Maneno hayo yaweza kuwa lugha ya kuelezamachafuko na misukosuko kati ya mataifa, uchumi, taratibu za kawaida zamaisha ya wanadamu n.k. Isaya alitumia lugha hiyo aliposema juu ya kuangukakwa tawala za kipagani na machafuko katika siasa. Tangu kutokea kwa elimuya ‘atomu’ na uwezo wa ‘bomu la atomu’ yafikiriwa kwamba hata manenoyaweza kuhusu maumbile yenyewe (Yoe.2:10, 3:15; Isa.13:10, 34:4; Eze.32:7-8; Amo.8:9).

k.26 Ndipo Mwana wa Adamu, Jina ambalo Yesu alipenda kujiita (2:10)ataonekana wazi akija juu ya mawingu, kwa nguvu nyingi na utukufu. Jambokubwa si mabadiliko katika maumbile bali Utukufu na Ushindi wa Kristo. KatikaAgano la Kale ‘mawingu’ yalikuwa dalili ya Kuwepo kwa Mungu. YesuMwenyewe ndiye ishara ya mwisho, hamna haja ya nyingine. Ndipo atawatumamalaika, watumishi wa waumini (Ebr.1:14) ili watu wake wakusanyike Kwakekutoka mahali pote. Hamna mahali palipo mbali au nje ya tukio hilo, kilamuumini atamwona. Zamani Waisraeli walizoea kukusanyika pale Hekalunilakini tangu Kuja kwa Kristo mara ya kwanza watu wake hukusanyika Kwake,kwa kiroho sasa, ndipo baadaye watakuwa pamoja naye milele na milele.Kuondolewa kwa hekalu kutaweka nafasi wazi kwa Yeye kuwa badala yahekalu, ‘Mwili’ wake ndio ‘hekalu’ na Kanisa ni ‘Mwili’ wake. Zamani zilemakusudi ya Mungu yalihusu taifa teule la Israeli lenye Mji wake mkuu paleYerusalemu, ila siku zijazo makusudi ya Mungu yatahusu jamii ya waumini waYesu ambao hawana mji mmoja maalumu, bali waishi sehemu zote zaulimwengu na Yerusalemu utapoteza ukuu wake baada ya muda mfupi. Wakatiule maneno hayo yaliwashtusha watu kwa sababu Yesu alionekana dhaifu, bilanguvu, bila utukufu, ambaye hivi karibuni atatundikwa msalabani. Mapinduzimakubwa yatatokea mbeleni na hasa Atakaporudi. Hapo kati mabadilikomadogo madogo yatatokea kwa kadiri watu wanavyoutambua na kuupokeaUfalme wake.

k.28-37 Ndipo Yesu alitoa maonyo ya upole juu ya kukesha. Yalihusika namatukio hayo makubwa mawili yaliyozungumzwa katika k.3-k.27 kuanguka kwaYerusalemu na mwisho wa mambo yote.

MARKO 253

k.27-29 Kwa kuutumia mfano wa mtini Yesu aliwatahadharisha wanafunziwawe na utambuzi wa kiroho juu ya mwenendo wa historia ambayo ndani yakeMungu hutekeleza makusudi yake. Lengo la Yesu katika kuutoa unabii lilikuwakuwaandaa wanafunzi na wanafunzi kuwaandaa waumini wa baadaye, ili kilaMkristo wa kila wakati awe tayari kwa matukio hayo makubwa. ‘myaonapomambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu mlangoni’. Ni mambogani? ni Kuanguka kwa Yerusalemu na kubomolewa kwa hekalu ambakokumeelezwa katika k.14-23.

k.30 Yesu alisisitiza umuhimu wa maneno yafuatayo kwa kusema ‘Amin,nawaambieni’ ‘kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie’ yaani Kuangukakwa Yerusalemu na Hekalu kutatokea katika maisha ya baadhi ya waliomsikia(9:1; 14:62). Ni kama kusema kwamba Yeye Mwenyewe hatakuja wakati huo.Maneno hayo yaweza kuwa yanahusu ‘mwisho’, pia, kwa sababu kamaambavyo tumeona, unabii unaweza kuhusu tukio fulani la hivi karibuni, pamojana kuwa na timizo lake kamili baadaye. Ni rahisi zaidi kufikiri kwamba ‘kizazihiki’ ni wale wa wakati ule, na ya kuwa neno linalozungumziwa ni Kuangukakwa Yerusalemu.

k.31 Ni neno la Yesu kuhusu uthabiti na kudumu kwa maneno yake. KatikaAgano la Kale ni Mungu aliyesema kwamba Neno lake ni la kudumu, na Yesualisema vivyo hivyo, akijiweka sawa na Mungu (Isa.40:8; 1 Pet.1:24-25;Yn.6:63,68; 14:10). Watu hufikiri kwamba ulimwengu ni imara na wa kudumu,lakini, hautadumu, ni wa muda tu, mabadiliko makubwa yatatokea katikauumbaji kutokana na Kuja kwa Kristo tena (Rum.8:18-22). Ila Neno la Munguna maneno ya Yesu yatadumu, na kwa sababu hiyo, ni neno linalohusu watuwa vizazi vyote, na wa hali zote, na wa mahali pote. Katika unabii wa matukiomakubwa ya historia Yesu amesisitiza kwamba watu wapaswa kuujali unabiiwake zaidi hata pengine kuliko Yeye Mwenyewe, ndio umuhimu wake.

k.32 Inaonekana maneno hayo yahusu mwisho wa mambo yote kwa sababuya maneno ‘walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye....’ Alipotajamfano wa mtini Yesu aliwaelekeza wanafunzi kufikiri kwamba ‘mavuno nikaribu’ ‘tambueni ya kuwa yu karibu milangoni’ (k.28,29). Pia waliambiwawajifunze kwa mtini, yaani wasome dalili zilizoonyesha kwamba tukio laKuanguka kwa Yerusalemu limekaribia. Lakini hapo Yesu amesema kwambahakuna ajuaye, na mfano unaofuata ni wa mwenye nyumba kuondoka na watukutokujua ni lini atakaporudi. Hivyo, ni tofauti na mfano wa mtini. Kwa hiyo,maneno hayo yahusu Kurudi kwa Yesu baadaye. Hakuna shaka kwambaAtarudi, ila kuhusu lini hakuna ajuaye. ‘hata malaika’ hao wanao uhusiano waukaribu sana na Mungu, tena wahusika katika jambo la Yesu kurudi (Isa.6:1-3;Mt.18:10; l3:41; 24:31; Ufu.14:19). ‘wala Mwana’ (ni hapo tu katika Injili yaMarko ambapo neno ‘Mwana’ limetumika). Neno la Mwana kutokujualimetatanisha watu (10:40) kwa sababu, ni kama kusema kwamba Yesu anaoupungufu wa ujuzi, tena yu chini ya Baba, hayuko sawa naye. Ila Yesu

MARKO254

alipofanyika mwanadamu, kwa hiari, aliweka kando uwezo wake wa Uungu,akikubali kuishi kama wanadamu wengine ambao hawajui yote. Kama angalijuayote angalijifanya kuwa mwanadamu. Ila katika ujuzi wa kiroho alijua kabisa.Alikuwa Mungu mkamilifu na mwanadamu mkamilifu (Kol.1:19; Ebr.2:17, 4:15).Ni fumbo kwa sisi kufahamu jinsi alivyoweza kuwa ‘wa milele’ na wa ‘muda’kuwa na ‘bila mipaka ya uwezo’ na kuwa ‘na mipaka ya uwezo’ ilatunavyoamini hali hizo zote ziliwiana kwa usawa katika huyo Yesu Kristo, si kwanusunusu, bali kila hali kwa ukamilifu. Ni kwa ajili yetu na ukombozi wetu Yesualikubali kuwekewa mipaka katika ufahamu na mamlaka yake wakati wa kuishihapo duniani; aliishi kwa imani na kwa kumtii Baba, ilimbidi aombe na kushindamajaribu kama inavyotupasa sisi. Watu wanaotumia muda wao katikakuchunguza wakati wa Kurudi kwa Yesu wanapoteza muda wao bure, ni nenolisilojulikana wala haliwezi kamwe kujulikana na wanadamu.

13:33-36 Haja ya kukeshaJambo muhimu ni kwamba ‘Baba ajua’ ni neno dhamini na siri yake. Kwa hiyoni juu yetu, si kuchunguza siku bali kukesha, kwa sababu hatujui ni lini Kristoatakaporudi (k.32, 33, 35) Sisi wanadamu hatupendi kukiri udhaifu wetu wakutokujua mambo kadhaa na kutokuwa na uwezo juu yake. Ijapokuwa hatujui nilini, hata hivyo, kwa imani tuna hakika kwamba litatokea, na kila mmojaamewajibika kujiandaa. Ila ajiweke tayari kwa njia gani? kwa kuketi chini nakukunja mikono, na kusubiri tu? La! hata kidogo, kila mmoja apaswa aendeleena shughuli zake kwa uaminifu na kwa bidii.

k.34 Katika kutaja ‘mwenye nyumba kusafiri’ Yesu alidokezea kuondoka kwakekwa muda, pengine kwa muda mrefu, na kuwaachia watumishi wake kazi yakufanya, hata bawabu apaswa akeshe. Wanafunzi waliachiwa kazi ya kuhubiriInjili (k.10) na mpaka leo kila muumini ameitwa kumshuhudia na kumtumikiaKristo kwa njia mbalimbali. Hakuna haja ya wasiwasi kwa sababu jambo hilolitatokea haraka na kwa ghafula. Tuone kwamba kusema ghafula siyo sawa nakusema mara. Yesu hakusema atarudi mara, ila alisema atarudi ghafula, yaanikwa wakati usiotazamiwa.

k.35-36 Wakati wa Kurudi Kwake ni wakati wowote. Wajibu wetu ni kuomba nakukesha, ndiyo sababu Yesu alitoa tahadhari za sura hiyo (k.5,9,23,33).Waumini waangalie matumizi ya wakati walio nao, wakitambua kwamba zikohatari mbalimbali za kudanganywa, kupoa, na kumezwa na shughuli zisizohusuUfalme wa Mungu. Kwa hiyo, kama ambavyo Yesu alisisitiza kila wakati, imaniinatakiwa, ni kuwa na matumaini na ujasiri wa kujua kwamba hakika Atarudi.

k.37 Maneno hayo ya Yesu yanahusu watu wa vizazi vyote. Ni wajibu wa kilamuumini kuwa macho, Kanisa lapaswa kuishi katika mwanga wa kujua Kristoatarudi. Ili tuwe tayari kwa siku ile vema tuwe tayari leo, na kesho, na keshokutwa.

MARKO 255

14:1 - 15:47 Sura hizi mbili zinazo habari za Mateso na Kifo cha Yesu14:1-2 na k.10-11 Shauri la kumwua Yesu na Yuda kujitoa kwa wakuukumtia mikononi mwao (Mt.26:1-5; Lk.22:1-2; Yn.11:45-53)

k.1 Marko ameeleza wakati na kuonyesha jinsi ilivyokaribia sana Sikukuu yaPasaka (14 Nisan) na Siku za Mikate isiyochachwa zilizofuata mara (tangu 15hadi 21 Nisan). Halafu tumeambiwa jinsi wakuu walivyotatizwa kwa kuwawalitaka kumwondoa Yesu mapema, kwa sababu, kwa kadiri alivyoendeleakuwafundisha na kuwavuta watu, idadi ya wale waliokuwa upande wake ilizidi.Wakimshika kwa wazi waliogopa ghasia itatokea, na ghasia ikitokea, walihofukwamba Warumi watawaondoa katika vyeo vyao na kuweka utawala wa kijeshi.Kwa siku nyingi waliwaza kumwondoa (Mk.3:6; 11:18; 12:12). Neno si kamawamwondoe au siyo, wameisha kuamua kumwondoa, ila tatizo ni lini.

k.2 Waliposhauriana waliona vema kungoja mpaka Siku za Pasaka, zimepita,wakati watu watakapofunga safari za kurudi makwao, ndipo wamshike kwa siri,na kumwua. Afadhali wasubiri na kungojea wakati wa kufaa. Yasemekanakwamba watu kama mia mbili na hamsini elfu walifika Yerusalemu kwaSikukuu, kwa hiyo, sababu ya kuhofu ilikuwa na msingi. Iliwabidi wapange kwauangalifu sana. Kwa hiyo, uamuzi wao ni ‘isiwe kwa wakati wa sikukuu’ ilampango wa Mungu uliokusudiwa tangu awali ulikuwa ‘iwe wakati wa sikukuu’kwa sababu Yesu alikuwa ‘Mwana Kondoo’ wa Mungu.

k.10-11 Hapo tumepewa habari ya jambo lililowasaidia sana wakuu nakuwafanya waubadili mpango wao wa kungojea mpaka Sikukuu zimepita.(Tumesema sikukuu zimepita kwa sababu wakati huo Sikukuu ya Pasaka naSiku za mikate isiyochachwa zilihesabiwa pamoja kuwa Sikukuu (Lk.22:1).(Kut.12:6-20,48; Hes.9:2-14; Kum.16:1-8). Mwana kondoo wa Pasakaalichinjwa 14 Nisan ndipo usiku ule kuamkia 15 Nisan Siku za mikateisiyochachwa zilifuata.

Yuda Iskariote aliitwa na Yesu kumfuata, na Yesu alimchagua kuwa katika wale12 (Mitume) walioandamana naye daima na kutumwa naye walipokwendakuhubiri na kuponya watu na kutoa pepo. Yohana ametuambia kwamba niyeye aliyetunza mfuko wao na ya kuwa alikuwa mwizi (Yn.12:6) kwa hiyo,hakuwa mwaminifu kwa muda mrefu, hali amejificha. Wakuu walitafuta njia yakumkamata Yesu; Yuda alitafuta njia ya kumsaliti. Yuda aliwasaidia sana kwasababu haikuwa rahisi wamkamate Yesu hali mji ulijaa maelfu ya wageni napasipo mtu kuwajulisha mahali pa kumpata wasingalipajua mahali pakumtafuta. Walihitaji habari kamili juu yake. Hivyo kwa msaada wa Yudawalifanikiwa katika mpango wa kumshika Yesu, ila wakati utakuwa uleuliowekwa na Mungu (Lk.22:22; Mdo.2:23; Efe.1:11). Hivyo, Yuda hakubadilimpango wao wa kumwua ila alirahisisha njia ya kumkamata. Yuda alikuwa nanafasi ya kuwasaidia, maana alijua kwa usahihi mahali alipo Yesu na aliwezakumtambulisha kwao bila kosa. Hivyo, twaona jinsi mpango wa Mungu na hiari

MARKO256

ya mapenzi ya mwanadamu vilivyowiana. Tendo la Yuda halipunguziwi uzito wadhambi yake kwa sababu lilitimiza mapenzi ya Mungu. Yuda alifanya kwa hiariyake mwenyewe, tena alifanya kwa fedha na baada ya Yesu kumhoji asifanyena kumwonya juu ya matokeo yake. Hakufanya katika ujuzi wa mapenzi yaMungu wala katika nia ya kufanya mapenzi ya Mungu. Wengine hudhanikwamba Yuda alikata tamaa kwa sababu Yesu hakuonyesha nia ya kupinduaserikali ya Kirumi na kuweka uhuru taifa la Israeli. Badala ya kutaja mambokama hayo alishambulia biashara iliyofanyika mle hekaluni na kutabiri juu yakuanguka kwake. Ikiwa Yuda alishikwa na hali ya uzalendo ni wazi Yesuhakumtumainisha juu ya mambo hayo. Kwa hiyo, kama alikuwa ameshindwakumfuata Yesu kwa sababu hiyo, au kama hakuwa tayari kujitoa kabisa Kwake,kwa nini hakumwacha bila kumsaliti? Na kama aliona ni vema amsaliti, mbonaafanye kwa fedha? Ilikuwa lazima Yesu afe, ila si lazima Yuda amsaliti.Alimruhusu Shetani amwingie (Yn.13:27). Yeye ni onyo kwa wote ambaowamepewa mapendeleo mengi na Mungu bila kuitika vema (Ebr.6: 4-8).

14:3-9 Yesu alipakwa mafuta Bethania (Mt.16:6-13; Yn.12:1-8)Yawezekana jambo hilo lilitokea siku chache kabla ya siku zile mbili za k.1.Yohana amesema ilikuwa siku sita kabla (Yn.12). Inafikiriwa kwamba Markoaliweka habari hiyo hapo ili abainishe choyo na uovu wa Yuda na ukarimu nawema wa huyo mama - tendo la kumsaliti dhidi ya tendo la kumpaka marhamu.Wengine walikuwa wakipanga kumfanyia Yesu mabaya na hapo tunayo habariya tendo moja jema la mwanamke mmoja.

k.3 Kama ambavyo tumeishaona Yesu alipenda kukaa Bethania (11:11)alipoondoka Yerusalemu kila jioni. Tukilinganisha na Injili ya Yohana, huyomama alikuwa Mariamu, dada wa Lazaro ambaye hivi karibuni Yesu alikuwaamemfufua kutoka katika wafu. Lazaro naye alikuwemo pamoja na Marthaaliyehusika na maandalizi ya chakula. Pengine ilikuwa karamu ya kumshukuruYesu kwa kumfufua ndugu yao. Hatujui Simoni mkoma alikuwa katika jamaahiyo au ni yupi hasa, pengine alikuwa baba ya hao watatu aliyeishi nao (2Nya.26:21) au pengine ni mkoma aliyeponywa na Yesu, ila kwa jinsi alivyotajwainaonekana alijulikana na wengi. Ni vigumu kufikiri alikuwa angali mwenyeukoma, kwa sababu asingaliweza kushirikiana na watu akiwa bado ana ukoma.Walipokuwa chakulani akaja huyo mwanamke akileta kibweta cha nardo safi,ghali sana, akakivunja kibweta na kummiminia kichwani nardo iliyokuwamo(Yohana ametaja miguu kupakwa). Nardo ilitengenezwa kutoka mizizi ya mmeauliopatikana Bara Hindi. Kwa kuvunja kibweta Mariamu alikusudia kuitumianardo yote iliyomo ndani, isibaki yoyote kwa nafasi nyingine. Kiasi chakekilikuwa ratli mia (Yn.12:3) nyingi sana; pia ilikuwa ya bei ghali zaidi ya dinarimia tatu (dinari ilikuwa mshahara wa kutwa kwa kibarua, hivyo ilikuwa kamamshahara wa karibu mwaka).

MARKO 257

k.4-5 Ndipo watu walianza kumnung’unikia huyo mama na kumlaumu, si kwasababu ya kumpaka Yesu, ila kwa sababu ya kutumia pesa nyingi kwakununulia nardo safi nyingi. Inaonekana Yuda alianza manung’uniko ndipowanafunzi walimwunga mkono (Mt.26:8; Yn.12:4). Hawakujiweka mahali paYesu na kufikiri jinsi tendo hilo lilivyomgusa. Katika siku hizo chache alitendewamengi mabaya, ila tendo hilo jema lilimfariji sana. Ijapokuwa Yuda alitajamaskini hakuwa na mzigo juu yao, ila alipenda kupata pesa hizo mwenyewe.

k.6-7 Kwa kweli ilionekana pesa nyingi zimepotezwa ambazo zingalifaa jambojingine ila Yesu hakuwaruhusu waendelee kumsumbua huyo mama. Akamteteana hilo jambo jema alilomtendea. Yesu alionyesha kwamba jambo hilo si lakuchagua kati yake na maskini, bali ni muhimu sana kwa sababu ya wakati.Wakati huo Yeye angalipo pamoja nao, baada ya siku chache hatakuwapamoja nao, kwa hiyo, ni wakati wa kumfanyia mema. Maskini wapo wakatiwote, na nafasi za kuwasaidia zipo wakati wote. Walizoea kuwasaidia maskini(Yn.13:29). Yesu alimshauri yule tajiri atoe fedha zake zote kwa maskini, kwahiyo, ni wazi alikuwa na mzigo juu ya maskini, lakini wakati huo ni wa pekee,kwa hiyo, ‘kupoteza’ fedha nyingi kwa ajili yake wakati huo ni vema.

k.8 Kisha Yesu alilitafsiri hilo tendo kuwa tendo la kuupaka mwili wake kwa ajiliya maziko. Hatapakwa baadaye, maana atazikwa kwa haraka, bila manukato(16:1) ndipo baada ya Sabato, wanawake walipoondoka mapema kuupakamwili, walikuta mwili haumo kaburini kwa sababu Yesu amefufuka. KamaMariamu alitambua kwa hakika kwamba amempaka tayari kwa maziko nivigumu kujua, ila iliyo wazi ni kwamba alikuwa na utambuzi kuliko wengine woteya kuwa wakati wa Kifo chake umekaribia, na kwa sababu hiyo, alishika nafasiya kumwonyesha upendo wa kibinafsi. Kwa kiasi cha fedha zilizotumika katikakununua kibweta cha nardo nyingi safi inaonekana alikusudia kwa mudakutenda tendo hilo na kwa siku nyingi aliweka kando fedha kwa ajili yake. Kwahiyo, kifo cha Yesu kililetwa mbele za waliopo, alikuja ulimwenguni ili afe na nibudi wanafunzi wakumbuke jambo hilo. Kifo chake kiliashiriwa kwa harufu nzuriya nardo safi si kwa tisho baridi la kukata tamaa.

k.9 Yesu alitamka maneno ya kutilia uzito usemi wake. Aliona ya kwambahabari hiyo isisahaulike mbeleni. Katika habari za kutangaza Kristo na matendoyake yote, wasisahau habari ya tendo hilo la huyo mama. Ni ajabu kwambajambo la maziko latajwa pamoja na kutangazwa kwa habari njema. Katikashangwe za kumshangilia wasimsahau. Hata kabla ya kuuawa, alikuwa nauhakika wa ushindi, alitaja kuhubiriwa kwa Injili katika ulimwengu wote.Hateseki bure, hafi bure, atafufuka, na wanafunzi watahitimu na kuutekelezautume wa kupeleka habari zake mbali. Ni njia nzuri sana ya huyo mamakukumbukwa! Hakutumia busara za kimwili na kufanya hesabu ya fedha balikwa upendo mwingi alijitoa na kutumia fedha nyingi ili amwonyeshe Yesuupendo wake.

MARKO258

14:12-21Maandalizi ya Pasaka na Tangazo la kusalitiwa (Mt. 26:17-25;Lk.22:7-14, 21-23; Yn.13:21-30)Pasaka iliadhimisha tendo kuu lililofanyika zamani katika historia ya Taifa laIsraeli, wakati Mungu alipowaokoa watu wake kutoka utumwani huko Misri. Kwatendo hilo la Mungu, chini ya uongozi wa Musa, Israeli ilikombolewa nakufanyika kuwa taifa. Kila mwaka Taifa zima lilifanya kumbukumbu lake. Kwahiyo Marko aliandaa habari hii akiona kwamba wakati wa Pasaka mpya umefikana ukombozi wa kutoka utumwa wa dhambi unafanyika ambao utasababishakuundwa kwa Taifa jipya, jamii mpya ya wanadamu wanaotoka mataifa yote,chini ya kiongozi na mkombozi, Yesu Kristo, atakayefanya Agano Jipya kwanjia ya kumwaga damu yake.

k.12 Siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa ilifuata 14 Nisan Siku ya kuchinjaPasaka, ila watu hawakuwa waangalifu katika kutofautisha kati ya siku hizo.Kwa hiyo, jambo ambalo Marko ameeleza lilitokea jioni iliyotangulia. Pasakaililiwa tarehe 14 Nisan, hivyo wataalamu wametatanishwa kujua ni Pasaka aukaramu badala yake ambayo Yesu na wanafunzi waliila, ila Marko ameiitaPasaka. Yohana katika Injili yake amesema kwamba Pasaka ililiwa jioni baadaya Yesu kusulubiwa (Yn.18:28; 19:14,31,42). Pengine Marko amefuata desturiya Warumi kuhesabu siku kuanza tofauti na Wayahudi. Kwa Warumi sikuilianza asubuhi mapema mpaka asubuhi iliyofuata. Kwa Wayahudi walihesabusiku kuanza baada ya jua kuchwa mpaka kesho yake au pengine walitumiakalendari tofauti. Haidhuru ilikuwa Pasaka au karamu badala yake, kwavyovyote mambo yalitokea katika mazingira na mwanga wa Pasaka.

Kwa sababu Yesu alitamani sana kushirikiana na wanafunzi wake katikachakula kabla ya Kufa kwake (Lk.22:15-16) alikuwa ametayarisha mambo kwauangalifu sana. Tukumbuke Yerusalemu ulijaa wageni wengi na kwa sheriailiwapasa waile Pasaka ndani ya kuta zake, hivyo Yesu alikuwa amepanga namtu fulani amwekee chumba tayari kwa ajili hiyo. Wanafunzi walipomwulizakuhusu mahali pa kuandalia Pasaka aliweza kuwaelekeza vizuri. Pamoja namatayarisho ya kupanga chumba aliweza kuwaongoza mahali pa chumba hichokwa ujuzi wa kipekee aliokuwa nao uliolingana na habari ya punda wakati wakuingia Yerusalem. Pasaka ya Kwanza (Kut.12:11) ililiwa hali watuwamesimama, tayari kuondoka Misri. Wakati huo waliila hali wameegama kwasababu wamestarehe katika nchi yao yenyewe.

k.13-14 Yesu aliwatuma wanafunzi wawili (Petro na Yohana Lk.22:8) nakuwapa maelezo yaliyoeleweka kuhusu mahali pa kuandaa tayari. Ijapokuwamaelezo yalikuwa wazi, hata hivyo, Yesu hakutaja mahali penyewe, wala jina lamwenye nyumba, kusudi Yuda asielewe, wala adui zake ambao walikuwawakimtafuta na walikuwa wameishatoa amri kwamba mtu yeyote akijua alipobasi wataarifiwe ili waje na kumkamata (Yn.11:57). Yesu aliwapa haowanafunzi wawili ishara ya kumtambua mtu ambaye itawabidi kumfuata mpakanyumba fulani. Ishara yenyewe haikuwapa shida, kwa kawaida wanawake

MARKO 259

waliteka maji, na huyo mwanaume angekuwa mtumishi wa nyumba, si mwenyenyumba. Halafu Yesu aliwapa maneno ya kumwambia mwenye nyumba.‘Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile.....?’ Ilitoshawaseme ‘mwalimu’ maana alijulikana sana. Maneno yana hali ya kumtofautishana wageni wengine waliokuja Yerusalemu kwenye Pasaka. ‘chumba changu’ nimaneno ya mtu mwenye mamlaka ya KiMasihi. Yadhaniwa huyo mwenyenyumba alikuwa mfuasi wa Yesu. Yesu alikuwa na rafiki na wafuasi wengiambao majina yao hayajulikani. Watu wamefikiri kwamba alikuwa baba waMarko, mwandishi wa Injili. Tunajua kwamba nyumba ya mamaye ilitumiwa naWakristo wa kwanza, na huenda ndiyo hiyo iliyotajwa hapo (Yn.20:19; Mdo.2:1;12:12). Yesu alitamani sana kushirikiana na wanafunzi wake kwa utulivu usikuhuo wa maana sana kabla ya kukamatwa, na kwa sababu hiyo, alikuwaamepanga na huyo mtu apewe chumba na alitunza siri hii kwa usalama wao, iliatimize shabaha ya kuongea nao kabla ya Kuuawa Kwake.

k.15-16 Wale wanafunzi walikuta mambo yote sawa na jinsi Yesualivyowaambia; walimkuta yule mtu mwenye mtungi; wakamfuata, wakasemana mwenye nyumba; wakakuta chumba kilichowekwa tayari, chenye meza,magadoro ya kuegemea, bakuli, maji, kitambaa n.k. Ndipo wanafunzi walifanyamaandalizi ya chakula cha Pasaka.

k.17 Jioni ile Yesu na wanafunzi wakaja Yerusalemu na kuingia chumbani.Tukilinganisha na Injili ya Yohana jambo la kwanza lililotokea ni Yesukuwatawadha miguu wanafunzi wake (Yn.13:3ku) kwa sababu kati yao hakunaaliyejitoa kufanya kazi hiyo ndogo, iliyokuwa desturi ya watu baada ya kusafiri.Luka amesema kwamba walikuwa wamegombana wao kwa wao juu ya yupialiye mkuu (Lk.22:24-30). Habari ya kutawadha miguu haipo katika Marko.

Katika maandalizi ya chakula na katika kula hatuambiwi kama walichinjamwana kondoo au sivyo. Ikiwa haikuwa karamu halisi ya Pasaka labda ndiyosababu mwana kondoo hatajwi, ila Marko ameiita Pasaka. Au, kwa sababu,Yesu Mwana Kondoo halisi yu pamoja nao, tayari kwenda kuchinjwa, basi,hamna haja ya kuchinja mnyama aliyekuwa ishara yake. Hatujui kwa uhakikakama walikula mwana kondoo au siyo. Ila iliyo wazi ni kwamba walikula pamojakaramu iliyohesabiwa kuwa Pasaka. Kwa desturi waliegama kwenye magodorokwenye mezi ndefu na fupi ya kwenda juu, kila mmoja uso wake ukielekeamezani na miguu nyuma. Waliketi kwa mfano wa herufi ya U, Yesu kichwani, nammoja upande wa kushoto na mmoja upande wa kulia, na wengine wotekwenye pande mbili ndefu za meza. Ilikuwa vigumu wote wasikie vizuriyaliyosemwa. Wote walihisi mambo makuu yatatokea, bila kuelewa hasayatakayotokea, huenda, mapinduzi ya nchi, au tukio la namna hiyo.

k.18 Watu walijaa furaha katika kuiadhimisha Pasaka, walikumbuka kwashukrani jinsi baba zao walivyotolewa utumwani mwa Misri kwa mkono hodariwa Mungu baada ya wao kuchinja kondoo na kuila nyama yake, hali wamevaa

MARKO260

tayari kuondoka kwa haraka (Kut.12:11). Ila sivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi.Mmoja wao angefanya jambo baya mno ambalo lingaliweza kuvunja ushirikawao. Yesu alifahamu habari hiyo ambayo wao hawana habari nayo na ilimbidiYesu awatahadharishe ili litakapofanyika wawe tayari kulikabili. Baada ya kuketichini na kuanza kula Yesu alitamka wazi kwamba mmoja wao, tena mmojaanayekula pamoja naye, atamsaliti. Alisema habari hiyo kwa kutangulizamaneno ya kutia uzito ‘Amini, nawaambieni’. Kumbe, Yesu alijua habari zaYuda, ila hakutaja wazi jina lake. Marko amesisitiza neno Thenasharak.10,17,43 kama kuonyesha ubaya wa huyo msaliti, ni mmoja aliyethubutu kulapamoja na Yesu, huko amepanga kumsaliti, na yu tayari kuondoka kufanyahivyo (Zab.41:9). Maneno ya Yesu yalikuwa wazi kabisa.k.19 Wanafunzi walishtuka kabisa na kuhuzunika, ni jambo ambalohalikuwemo mawazoni mwao. Kila mmoja akaanza kuuliza kwa hali ya kutetea,Si mimi? (ndiyo maana ya Kiyunani). Yesu katika upendo wake kwa Yudaalikuwa amemlinda. Bila shaka wangalijua mapema wangalimzuia asiondokechumbani na pengine wangalimpiga. Yuda alikuwa amejificha sana, hakunaaliyenyosha kidole chake na kusema ‘ni huyu’, hakuna aliyedhani ni mwenzake.Kwa kumwachia Yuda aondoke na kuwazuia wenzake wasimdhuru Yesuhakuchukua nafasi ya kuzuia mpango wa kumsaliti na kuponyoka mikononimwa adui zake. Ila alijua hakika njia ya Msalaba ndiyo njia ya kuwaokoa wenyedhambi.

k.20 Halafu Yesu alirudia kusisitiza kwamba ni mmoja wao, anayeshirikiananaye mezani na kuchovya katika bakuli. Ama walikuwa na bakuli mmoja nawote walichovya katika bakuli hiyo, au walikuwa wakishiriki bakuli kadha, naikiwa Yuda aliketi karibu na Yesu, yeye na Yesu walichovya katika bakuli moja.Hivyo, licha ya kula pamoja naye, alichovya pamoja naye katika bakuli. Yohanaametuambia kwamba Yesu alimtolea tonge, dalili ya upendo wa kumheshimukama rafiki mpendwa (Yn.13:26). Mpaka mwisho, Yesu alijitahidi kumwondoakatika mpango wake mbaya. Ilihesabiwa kuwa tendo la chuki kabisa kwa mtukumtendea vibaya yule aliyeshirikiana naye katika chakula (Zab.41:9)haikuwazika kwamba mtu atamfanyia mwenzake hivyo. Kula pamoja kuliwazwakuwa tendo takatifu, tendo la thamani sana.k.21 Kisha Yesu akamwonya Yuda akitamka neno ole kwake. Kwanzaalionyesha kwamba Yeye yuaenda zake, yaani kusulibiwa, kamaalivyoandikiwa. Aende kwa sababu ni mapenzi ya Mungu na mpango waMungu kwa wokovu wa wanadamu, tangu awali. Mpango huo ulidhihirishwakatika Maandiko ya Agano la Kale. Kwa hiyo, Yesu hakuwa na wasiwasi juu yamwenendo wake, alijua, baada ya Kufa atafufuka kutoka wafu na Kurudi kwaBabaye. Lakini, Je, habari za yule atakayemtia mikononi mwa adui zake?Itakuwaje kwake? aweza kuwa na udhuru, eti amesaidia kutimiza mapenzi yaMungu? La, hata kidogo. Mwenye kumsaliti amefanya kwa hiari yakemwenyewe na dhidi ya mapenzi makuu ya Yesu aliyemsihi sana asiendelee nampango wake mbaya. Haikuwa lazima amsaliti. Tumeishaona kwamba wakuuwalikuwa na mpango wa kumwua baada ya Sikukuu kupita. Yuda angaliweza

MARKO 261

kubadili mpango wake, ila kwa kuwa ametelezateleza siku nyingi ilikuwavigumu abadilishe hali yake. Yesu Mwenyewe alimwona kuwa na hatia, tenahatia kubwa sana. Alikuwa amepewa mapendeleo sana na Yesu, kuwekwakatika kundi la Thenashara, kushirikiana naye kwa ukaribu sana n.k. hivyokwenda kinyume cha hayo yote kulihesabiwa dhambi nzito. Mpaka dakika yamwisho Yesu alimwachia nafasi ya toba, lakini Yuda akaikataa, akatoka nje,akaenda kwa wakuu.

14:22-26Yesu alianzisha Chakula cha Bwana (Mt.26:26-29; Lk.22:19-26; 1Kor.11:23-25)k.22 Wakati wa kula, huenda walikuwa wamemaliza kula ‘Pasaka’ ndipo Yesualitwaa mkate, na kutoa shukrani, kama ilivyokuwa desturi ya Kiyahudi.Aliumega na kuwapa wanafunzi na kusema ‘Twaeni, huu ndio mwili wangu’.Hapo Pasaka imekwisha na Chakula cha Bwana kimeanza. Maneno namatendo yake yalikuwa rahisi. Neno ‘kutwaa’ linaonyesha kwambaanachowapa ni kipawa Chake, kipawa cha wao kujitwalia na kujilisha ili waonjebaraka zake maishani mwao, sawa na jinsi ambavyo mtu anakila chakula ilikiwe ndani yake na kuleta afya ya mwilini. Ni dhahiri kwamba alikuwa akitoakielelezo cha Kifo chake kwa njia ya mwili wake kuvunjwa na damu yakekumwagwa pale Msalabani. Yeye atakuwa chakula na kinywaji cha watu wake.Si maneno ya kupokelewa yalivyo, Wakristo siyo watu wa kula nyama yakibinadamu! Kama kula na kunywa huwa msingi wa maisha yetu vivyo hivyoYesu huwa msingi wa maisha ya mfuasi wake, Kifo chake ni asili ya uzima waMkristo ili awe hai na mwenye afya rohoni mwake. Katika lugha ya Kiaramualiyotumia Yesu hakuna neno kwa ‘ndio’. Yesu alipotamka maneno hayoalikuwa angali na mwili wake, na damu yake haijamwagika bado. Kwa hiyo,maneno hayo yana maana gani? Ni vigumu kufikiri kwamba maana yake nimwili wake na damu yake ya kimwili. Mkate ni ishara ya Yeye Mwenyeweambaye alijiita Mkate wa Uzima. Alizoea kusema ‘Mimi ni Mlango....Mzabibu waKweli...Chakula cha Uzima...n.k. Hakuwa na maana alikuwa Mlango, ilakwamba kama mlango ni kiingilio, Yeye naye ni kiingilio kwa uzima...n.k. Kuulamkate na kuinywa divai ni ishara ya kushirikiana na Yeye, Bwana Aliye hai, nakuzishiriki baraka za Kifo chake. Ni ahadi ya Yeye kuwa pamoja nao daima.Wote walikula katika mkate mmoja na kikombe kimoja (1 Kor.10:16-17). Nisikitiko kubwa kwamba Chakula cha Bwana, ambacho kingewaunganishawaumini wa madhehebu yote, imekuwa sababu ya kutengana.

k.23 Kama alivyofanya na mkate, vivyo hivyo na kikombe. Yesu alitwaakikombe na kumshukuru Mungu, na kuwapa, na wote wakakinywea. Kwamaneno yake alionyesha uhusiano wa damu yake na Agano ambalo, kwa njiaya Kufa Kwake, analitengeneza. Ni Agano Jipya linalofanyika ndipo lile lakwanza kati ya Mungu na Taifa teule la Israeli liondolewe. Kama Yeremiaalivyotabiri, Agano Jipya liletalo msamaha wa dhambi na ushirika wa moyoni naMungu. Agano la kwanza lilitiwa muhuri na damu ya wanyama (Kut.24:8) hiloJipya nalo linatiwa muhuri na damu, ila ni damu ya tofauti sana, ya thamani

MARKO262

mno, damu ya mwanadamu, si mnyama; tena ya Yesu Kristo, Mungualiyefanyika Mwanadamu aliye Mwana Kondoo na Mwana pekee wa Mungu. NiAgano la neema, si la sheria, ni agano la kuwakaribisha wote wamwekeaoYesu tumaini lao, wanaokubali Kifo chake kuwa wokovu wao. Yesu kufa wakatiwa Pasaka ilikuwa ishara iliyomthibitisha kuwa huyo Mwana Kondoo halisi,aondoaye dhambi za ulimwengu wote. Yesu alikuwa na uhakika wa yale yoteyaliyokuwa yakitokea na ya kuwa yanatimiza mapenzi ya Mungu katikakuwapatia wanadamu wokovu wa dhambi zao. Hivyo alianzisha hicho Chakulacha Bwana, kabla ya Kufa Kwake, katika imani na ujasiri na uthabiti wamwenendo wake kwenda kuuawa. ‘kwa ajili ya wengi’ ni ukumbusho waIsa.53:11,12 na Mk.10:45 ‘fidia ya wengi’. Wengi watakuja kumwamini nakufanyika ‘jamii mpya ya watu wa Mungu, Israeli Mpya, wateule wake wapya’ (1Pet.2:9,10). Luka na Paulo katika 1 Kor.11:24 walitaja jambo la kufanyakumbukumbu la karamu hiyo, ila Marko hakutaja neno hilo. Ni wazi kwambaKifo chake hakikuwa kosa wala msiba wala bahati mbaya, bali kilikuwa Kifo chaukombozi wa wanadamu.

k.25 Hapo inaonekana Yesu alifanya kiapo cha kutokunywa divai tena mpaka‘siku ile nitakapoinywa mpya katika Ufalme wa Mungu’. Ni kama aliagana nawanafunzi wake kwa njia ya kushirikiana pamoja nao katika karamu hiyo yaPasaka na Chakula cha Bwana. Amekazana kuendelea na azimio lake lakufanya mapenzi ya Mungu na kufa kwa ajili yao. Maneno yake yanaashiriamwisho wa Pasaka ya Kiyahudi, na kipindi cha Agano la Kale, na mwanzo waChakula cha Bwana na kipindi cha Agano Jipya. Ni wakati wa mgawanyo katikahistoria ya wanadamu. Hivyo, aliwatazamisha mbele kwa ushindi wake, wakatiwatakaposhirikiana naye katika ushirikiano usiokatika wala kukoma. Ni kuanzakwa wakati mpya na dahari mpya. Wayahudi walizoea kuwaza mambo ya heriya baadaye kwa mfano wa Karamu ya Masihi itakayoleta furaha ya ajabu.

k.26 Walipomaliza hayo yote waliimba, kama ilivyokuwa desturi ya Kiyahudi,kutoka Zaburi 112-118, hivyo, walipotoka kwenda Gethsemane, maneno yaZaburi hizo yalikuwa mawazoni mwa Yesu. Alikwenda kwa moyo mkuukuwakabili adui zake.

14:27-31 Yesu abashiri kukimbia kwa wanafunzi wote na Petro kumkana(Mt.26:30-35; Lk.22:31-34; Yn.13:36-38)Bila shaka hali ya wasiwasi ilizidi, wanafunzi wakihisi kwamba msiba mkubwautatokea hivi karibuni, maana Yesu amewajulisha habari za Yuda kumsaliti, nawakati wa kula ametaja mwili wake kuvunjwa na damu yake kumwagika. LakiniJe! wanafunzi wenyewe watafanya nini hayo yatakapotokea? Je! watawezakuyastahimili na kuwa imara? Yesu alifahamu yatakayotokea kwa upande wao.k.27 Si wazi kama Yesu alisema maneno hayo njiani kwenda Mlima waMzeituni au wakati walipokuwa wangalimo chumbani (Luka na Yohanawamesema kwamba walikuwa wangalimo chumbani).

MARKO 263

Yesu ameishatoa habari za Yuda na usaliti wake, ila si Yuda tuatakayemwacha. Yesu aliwaambia wazi kwamba hata wao wote watakimbia naPetro atamkana. Kwa nini iwe hivi? Ni kwa sababu ya Kuuawa Kwake. Jambohilo ni chukizo kwao, nao watajikwaa, na Mchungaji wao, kiongozi wao,atakapouawa watafanana na kondoo wasio na mchungaji, nao watakimbia. IlaYesu alijua habari hiyo kabla haijatokea, ilikuwa dhiki mojawapo katika dhikizake zote, ataachwa peke yake bila hata mmoja wao kubaki naye kwa ukaribuna kumfariji. Habari hiyo iliandikwa katika Agano la Kale, Nabii Zekaria alisemahabari za mmoja atakayepigwa, ila hapo Marko ameonyesha kwamba ni Munguatakayempiga Mchungaji ‘Nitampiga....’ kwa sababu nyuma ya Kifo cha Yesu niMungu atakayeweka juu yake dhambi za watu wote na kuzihukumu katika Yeye(Isa.53:6; Rum.8:32). Usiku ule, wanafunzi watakapomwona Bwana waoanakamatwa na kupelekwa mahakamani, watachukizwa, hawatataka kuwapamoja naye, nao watamwacha. Imani yao itajaribiwa, nayo itaadimika.

k.28 Lakini hilo si neno la mwisho. Baada ya kuuawa, Yesu atafufuka kutokawafu na kuonana nao tena huko Galilaya. Kama mchungaji mwemaatawatangulia (Jn.10:27). Kila alipotaja Kufa Kwake Yesu alitaja KufufukaKwake (8:31ku. 9:31ku. 10:32). Kila mara wanafunzi walikosa raha, ni kamahawakulisikia neno la ufufuo kwa sababu mawazo yao yalivurugika marawalipolisikia neno la kufa. Galilaya ni mahali pa kukutana naye tena (16:7;Mt.28:16; Yn.21:1-23; 1 Kor.15:6). Ni mahali pa kurudishwa, ni mahali pakuanza upya, ni mahali pa wote kumrudia Bwana na kurudiana wao kwa wao,tayari kwa kutumwa naye kwenda kuihubiri Habari Yake Njema.

k.29 Petro aliposikia habari hiyo ya wanafunzi kujikwaa na kumwacha Yesukutawanyika, hakuweza kuipokea. Kimawazo akajitenga na wenzake na kudaikwamba hata ikiwa wao watafanya hivyo, yeye kamwe hatakwazwa. Alijiinuajuu ya wenzake na kujifanya kuwa bora, ila hakujijua mwenyewe walahakuutambua udhaifu wake ambao utakaonekana hivi karibuni. Alijivuna badalaya kunyenyekea na kujitegemea badala ya kumtegemea Bwana.

k.30 Ila Yesu akaendelea na kusema na Petro, akitumia maneno ya kutia uzito,‘Amin, nakuambia wewe’ halafu alimwambia wazi kabisa kwamba ‘Leo, usikuhuu....’ atamkana mara tatu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili. Licha yakukimbia, atamkana, atajiondoa Kwake kabisa, kama hamtaki, wala hatakikujulikana kama mmoja wa washiriki wake. Tena atafanya mara tatu. Itatokeausiku ule, katika kesha la tatu, huenda kati ya usiku wa saa nane au saa tisahivi. Warumi waligawa usiku katika kesha nne.

k.31 Hata baada ya kuonywa Petro akaendelea kusisitiza kwambahaitawezekana yeye amkane; kwa sababu yeye yu tayari kufa kwa ajili yake,Alirudia kusema neno hilo, hata na wenzake wote walijiunga naye na kusemavilevile. Hakuwa mwongo, wakati wa kumfuata katika hali ya kujitoa kabisahaujafika bado (Yn.13:36). Baada ya Yesu Kufa na Kufufuka, yeye na wenzake

MARKO264

watawezeshwa na Roho Mtakatifu na kwa neema ya Mungu watamfuata kwauaminifu na kwa ushujaa. Kwa sasa, katika nguvu na ujasiri wa kimwili,wameshindwa.

Bila shaka, kwa sababu Yesu aliwaambia mambo hayo mapema kablahayajatokea, yalipotokea walisikia faraja na kuwa na tumaini la kutazama mbelekwa wakati watakapomwona Yesu kwa jinsi alivyosema. Hawakuwezakulaumiana kwa sababu wote walianguka na wote walihitaji kurudishwa. YesuMwenyewe alikuwa tayari kwa magumu yote yatakayompata usiku ule, aliyajuayote yatakayompata, ila haikuwa rahisi ajue mapema hayo yote. Ni nani katiyetu ambaye apenda kujua mambo mabaya yatakayompata maishani mwakekabla hayajatokea? Bila shaka ni wachache sana. Yesu alifahamu yaleyatakayotokea hivi karibuni na yale yatakayotokea mbeleni, alikuwa na uhakikajuu ya hayo yote. Ni ajabu kuona amani yake na uthabiti yake wakatialipokaribia Kufa Kwake.

14:32-42Yesu aliomba katika bustani ya Gethsemane (Mt.26:36-46;Lk.22:40-46; Yn.18:1)

k.32 Baada ya kuila Pasaka na kuondoka chumbani Yesu akaja pamoja nawanafunzi wake, bila Yuda, mpaka bustani yaGethsemane penye Mlima waMzeituni. Maana ya neno ‘Gethsemane’ ni shinikizo la mzeituni. Waliingia mlendani ya bustani hiyo ya mizeituni, inaonekana ilizungukwa na ukuta; pengineilikuwa mali ya mtu fulani. Walikuwa wamezoea kufika pale mara kwa mara (Lk.22:39; Yn.18:2). Wakati huo Yesu alikuja kwa kusudi maalum la kuomba ili kwakushirikiana na Baba yake asaidiwe kukaza nia yake kwa mara ya mwishokusudi apambane na dhiki zote zilizo mbele yake kabla ya kukamatwa nakuhukumiwa na kuuawa. Ilikuwa kipindi kigumu sana Kwake. Marko ametoahabari za mara mbili zingine Yesu alipojitenga na kwenda kuomba wakatimuhimu katika huduma yake (1:35; 6:46).

k.33 Yesu aliendelea mle ndani pamoja na Petro, Yohana naYakobo, wananewaliachwa karibu na mahali walipoingia. Yesu alipenda hao watatu wawe karibunaye na kumfariji, wasiwe watazamaji tu. Hapo nyuma Yesu amekuwa naamani hata wakati alipotaja kukamatwa na kuuawa kwake, lakini hali yakewakati huo ilibadilika sana alipokaribia kabisa na kutazamia kutendeka kwamambo hayo. Yesu alijaa fadhaa na wasiwasi na kutishwa sana. Aliwajulishahao watatu jinsi alivyojisikia rohoni mwake. Hao watatu walikuwa pamoja nayeMlimani alipogeuka sura na kumwona hali amevaa utukufu wa ajabu. Kwa niniawachague hao watatu tena? Ni rahisi kuwaza kwamba alitaka kuwa na rafikizake karibu wakati huo wa dhiki yake ili wamfariji. Ila zaidi aliwachagua haokwa sababu walikuwa wamethubutu kujitetea na kusema walikuwa na uwezowa kushinda majaribu ya kumkana na kumwacha; wana wa Zebedayowalisema kwamba waliweza kukikinywea ‘kikombe’ cha mateso; Petro alisemakwamba haidhuru wote watamwacha yeye hatamwacha kamwe. Sasa

MARKO 265

wameingia mahali pafinyu, na kubanwa na mambo yatakayoupima ukweli wamajivuno yao. Maneno ya Kiyunani ya kueleza shida za Yesu ni mazito sana, nikama alishtuka, na kutishwa, na kuogopa, alishikwa na huzuni nyingi na kujaamajonzi. Kwa nini awe hivyo? Ni nini iliyomwogofya na kumdhikisha? Mawazoya maumivu ya kimwili na aibu za kutundikwa msalabani? Pengine, kwasehemu, ndiyo. Kifo cha kusulibiwa kilikuwa kibaya sana sana; hata hivyo,wengine wamevivumilia vifo vya shida sana. Zaidi sana alisononekaalipozingatia hali ya kubeba dhambi za ulimwengu na kupatwa na hukumu yaMungu kwa ajili yake. Jambo hilo lilimtisha sana kwa sababu, kamwe Yeyehajajua hali ya kutokusikia Kuwepo kwa ukaribu kwa Baba yake, ilaatakapohesabiwa mwenye dhambi atasikia hali hiyo, kwa kuwa hukumu yadhambi ni kutengwa na Mungu (15:34). Ni vigumu kwa mwanadamu awayeyote kupenya ndani ya jambo hilo na kujua jinsi ilivyokuwa kwa Yesu. Iliyodhahiri ni kwamba hata kuyawaza haya kulitosha kumtisha sana. Ilimbidiamwendee Baba na kuhakikishiwa kwamba hii ndiyo njia hasa (2 Kor.5:21; 1Pet.2:24;3:18)

k.34 Halafu aliwaambia wale watatu wakae pale walipo na kukesha, si kwa ajiliyake, bali kwa ajili yao wenyewe, maana wataingizwa katika mambo nakujaribiwa sana kujiondoa Kwake.

k.35-36 Ndipo Yeye aliendelea mbele kidogo, kama kiasi cha kutupa jiwe(Lk.22:41) alikuwa peke yake ila si mbali nao, kwa kuwa waliweza kusikiaaliyoyasema. Kwa desturi, Wayahudi waliomba kwa sauti. Akaanguka kifudifudina kuomba na kiini cha maombi yake kilikuwa kwamba Baba amwepushie njiahiyo, ni kama kusema kwamba, ikiwa iko njia nyingine amwonyeshe, nayeataikubali. Ila hakukataa kufanya mapenzi ya Babaye, hata ikiwa njia ni hii iliyombele yake. Alimwita ‘Baba’ ushuhuda wa uhusiano wa kipekee, wa ukaribukabisa. ‘kikombe hiki’ ni mateso na zaidi ya mateso ni hasira ya Mungu juu yadhambi (Zab.60:3; 75:8; Isa.51:17,22). Iwe dhahiri kwamba amepatwa nahukumu ya Mungu juu ya dhambi (2 Kor.5:21). ‘Walakini, si kama nitakavyomimi, bali utakavyo Wewe’. Alikuwa amezoea kumtii Baba, alizoezwa kufanyamapenzi yake (Ebr.5:7-8). Yeye alikuwa na hiari yake ya mapenzi tofauti na yaBaba, ila wakati wote yalinyenyekezwa kwa Baba. Dhambi iliingia ulimwenguniwanadamu walipomwasi Mungu na kutokumtii. Msamaha utapatikana kwa njiaya Mwanadamu mmoja, Yesu Kristo, kumtii Mungu, Baba yake kwa ukamilifu.Katika mashindano hayo kati ya mapenzi yake na mapenzi ya Mungu twaonaukweli wa ubinadamu wake. Ilimwia vigumu atii mapenzi ya Babaye kwasababu ya gharama yake, si gharama ya kufa tu, bali gharama ya kuhesabiwamwenye dhambi na kuadhibiwa kama mwenye dhambi hali amewekewadhambi na hatia za wanadamu, huku Yeye ameishi bila kufanya dhambi. Kwaupande mmoja ni kweli kwamba mambo yote yawezekana kwa Mungu, ila kwaupande mwingine haikuwezekana Yesu awe Masihi wa kweli huku akikwepakutoa fidia ya dhambi ambayo ni mauti. Ni mikingano, kusema Masihi bilakutaja Kifo cha upatanisho, ni maelezo yanayopingana yenyewe. Adui zake

MARKO266

walidhani kwamba Masihi si yule wa kufa (15:32). Katika kusema ‘si kamanitakavyo mimi’ alishuhudia ubinadamu wake pamoja na ushindi wake, kwasababu bila Yeye kukubali kabisa kufanya hayo mapenzi ya Baba asingaliwezakuyastahimili yote yaliyo mbele yake.

k.37 Baada ya kipindi cha kwanza cha kuomba akawarudia wanafunzi iliawaangalie. Kama mchungaji mwema, kati ya dhiki zake, alikuwa na mzigo juuyao, wasije wakashindwa. Akawakuta wamelala, huenda walisinzia kwa sababuilikuwa usiku nao walikuwa wamechoka sana, pamoja na kulemewa na huzunina wasiwasi wakishindwa kuelewa maana ya hayo yote. Petro alikuwaamesema hatamkana, kumbe, ameshindwa hata kukesha, hivyo Yesuakamwuliza Je! Simoni, umelala? (Yesu alimwita Simoni, jina lake la asili, si lileambalo amempa, yaani, Petro, maana yake mwamba, hajawa mwamba bado).Ni kama alimkemea kwa sababu alikosa kukesha.

k.38 Yesu alirudia kuwaonya wote wakeshe ili wasiingie majaribuni. Siwakeshe kwa ajili yake, bali kwa ajili yao wenyewe. Roho i radhi bali mwili nidhaifu. Aliwakumbusha udhaifu wa mwili uliotaka kulala badala ya kukesha.Iliwapasa waitawale miili yao, wasiipe nafasi ipumzike kama ilivyotaka.

k.39 Yesu akaenda mara nyingine na kuomba, kama alivyoomba mara yakwanza. Kiini cha maombi ni Yeye afanye mapenzi ya Baba ya kuwa fidia yadhambi (10:45).

k.40 Alipowajia tena kwa mara ya pili aliwakuta hali wamelala kwa sababumacho yao yalikuwa mazito. Wakashindwa kujua namna ya kumjibu. Ndipoakajitenga nao tena kwenda kuomba tena. Ilimbidi akazane mpaka amepataushindi na kuleta mapenzi yake yalingane na mapenzi ya Baba, ayakubalikabisa kwa moyo wa kutaka. Habari hiyo inatuhakikishia kwamba alikuwa naubinadamu kweli si wa juujuu tu.

k.41 Kisha akawajia kwa mara ya tatu na kuwaruhusu waendelee kupumzika.Yeye amemaliza maombi yake, amepata ushindi, amesikia uthabiti wa nia yakufanya mapenzi ya Baba, hivyo, akawa tayari kwenda kumkabili msaliti wake.‘Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi’ maneno hayo yanamaana mbili. Kwa upande wa kibinadamu, kiutendaji atatiwa na Yuda, msalitiwake ambaye amekaribia kufika pale walipo. Kwa upande wa kiroho, Munguataruhusu hayo yote yatokee ili kwa Kufa Kwake, dhambi ishindwe, Shetaniashindwe, na ukombozi wa wenye dhambi upatikane. Mashindano yalianzapale bustanini na kuendelea hadi aliposulibishwa. Vita ilikuwa kali, Yesu alitoajasho kama damu, na alitiwa nguvu na malaika ili asife mapema kabla yakusulibiwa (Lk.22:43,44).

k.42 Walipoziona taa za Yuda na wale waliokuja pamoja naye Yesuakawaambia ‘Ondokeni, twendeni zetu’ ‘zetu’ ijapokuwa wamekosa kukesha,

MARKO 267

wameshindwa kushirikiana naye, hata hivyo, bado ni kondoo zake. Atawalindampaka mwisho. Amekata shauri, Yeye yu tayari kukaribisha hiyo saa nakukitwaa hicho kikombe. Wanadamu walimwasi Mungu, mara ya kwanza,katika Bustani ya Adeni, na kifo kiliingizwa kuwa adhabu yake (Mwa.3:1ku).Katika Bustani nyingine ya Gethsemane uasi huo ulipinduliwa kwa utii waKristo, na dhambi ilipata tiba (Ebr.5:7-10). Fundisho kubwa kwetu ni kwambaushindi unapatikana kwa njia ya maombi, yale tunayokata shauri kabisa juuyake katika maombi twaweza kuyatekeleza katika maisha.

14:43-50 Yesu alikamatwa (Mt.26:47-56; Lk.22:47-53; Yn.18:3-11)k.43 Yuda alikuja pamoja na kundi kubwa la watu wenye silaha, upanga narungu. Walitoka kwa Kuhani Mkuu na waandishi na wazee. Pengine walikuja nakikosi cha askari wa Kirumi (Yn.18:3). Walikuwa na mamlaka ya viongozi waTaifa na kwa sababu hiyo Yesu alipelekwa kwao ili hukumu ianze kwao. Yudaalijua vizuri mahali atakapomkuta Yesu, maana Yesu na wanafunzi walizoeakwenda pale. Pamoja na kujua mahali Yuda alimjua Yesu pia, hivyo alikuwa nauwezo wa kumtambulisha kwao pamoja na kuwaleta mahali alipo. Ameitwa‘mmoja wa Thenashara’ kusisitiza ubaya wa tendo lake. Yohana ametajakwamba kabla ya kuwaruhusu wamshike, Yesu alionyesha nguvu ya pekee juuya wale waliokuja kumkamata (Yn.18:6).

k.44 Yuda alikuwa amewapa ishara ya kumtambulisha, ‘busu’. Wanafunziwalionyesha heshimu kwa waalimu wao kwa tendo la kubusu na kwakuwasalimia ‘Rabi’. Yuda alitumia tendo hilo, si kwa kumheshimu bali kwakumwaibisha. Busu ni ishara ya upendo kati ya rafiki, ila Yuda aliitumia kwakuonyesha chuki. ‘mkamateni, mkamchukue salama’. Hakutaka wakosekumshika, kwa sababu ameishapewa fedha na itampasa azirudishe ikiwawatakosa kumpeleka. Huenda alidhani kwamba fujo itatokea na wanafunziwatampigania Bwana wao (Lk.22:38 walikuwa na panga mbili) ndipo Yesuataponyoka, maana ilikuwa usiku na wakati wa giza na katika miti ya bustaniangaliweza kujificha.

k.45-46 Hivyo, Yuda akamjia Yesu na kumwita Rabi, ndipo akambusu.Akamwita ‘mwalimu’ kama alivyofanya wakati wa kula Pasaka. Katika Kigrikineno kwa kumbusu lina nguvu, kama alifanya kwa bidii. Yesu alijaribukumfanya Yuda ajihoji juu ya tendo hilo na kulitubu (Lk.22:48; Mt.26:50).

k.47 Mmoja akajaribu kuonyesha ujasiri, akaufuta upanga na kumpiga mtumwawa Kuhani Mkuu na kukata sikio lake. Yohana amesema kwamba huyo alikuwaPetro ambaye hata mpaka wakati huo hakukubali kwamba Masihi afe. Yohanaamesema huyo aliyekatwa sikio aliitwa Malko (Yn.18:10). Luka ametuambiakwamba Yesu alimrudishia sikio la kuume (Lk.22:51). Yesu hakutaka mtuyeyote apate hasara kwa kukamatwa kwake (Yn.18;8,9).

MARKO268

k.48-49 Itikio la Yesu kwa hayo yote lilikuwa kuwakemea waliokuja na silahakumkamata, ni kama jambo lililomwudhi. Hakuna haja ya kutumia nguvu.Alionekana kama ni mnyang’anyi na mtu wa kutumia mabavu. Walikuwa nanafasi nyingi za kumkamata mchana, na kwa wazi, pale hekaluni, alipokuwaakifundisha. Ilikuwa usiku wa maana sana wa watu kujiandaa kwa Pasaka,kumbe Makuhani na viongozi wa Israeli walimchukia kiasi cha kutokujali huousiku wa Pasaka wakishughulikia kumkamata badala ya kuzingatia jinsiwalivyotolewa utumwani mwa Misri zamani zilizopita. Katika kusema hivi Yesualiwafunulia hatia yao. Lakini masumbufu hayo yote yaliingizwa katika mpangowa Mungu (Isa.53:12).

k.50 Kisha wakamshika Yesu na wanafunzi wote wakakimbia, hata mmojahakubaki kama Yesu alivyotabiri (k.27). Baadaye Petro na Yohana walimfuatakwa mbali. Yesu alikuwa amekwenda pale kwa hiari yake mwenyewe,alikwenda hali akijua mipango ya Yuda. Kama isingalikuwa mapenzi ya Munguasingalikwenda mahali palipofahamika na Yuda. Kila mmoja alifanya kamaalivyotaka mwenyewe na kila mmoja alikuwa na hatia ya tendo lake. Katikahayo yote Yesu alisaidiwa kwa kuona jinsi unabii wa Agano la Kaleulivyotimizwa. Hivyo, alihakikishiwa kwamba alikuwa akitimiza mapenzi yaMungu yaliyokusudiwa tangu awali. Hakuna neno lililomshtua.

14:51-52 Kijana aliyekimbiaNi vigumu kujua shabaha ya habari hiyo kuingizwa hapo isipokuwa ni habari yammoja aliyeshuhudia yaliyotokea bustanini. Marko, mwandishi wa Injili hiyo,amedhaniwa kuwa huyo kijana. Kama waliila Pasaka katika nyumba yamamaye na ni nyumba hiyo iliyotumiwa na Wakristo (Mdo.12:12) inaonekanakwamba alipopata kufahamu kwamba Yesu na wanafunzi wametoka njekuelekea Mlima wa Mzeituni, akakata shauri kwa haraka kuwafuata, haliamejifunika nguo moja tu. Pengine alifahamu kwamba watu wamekwendakumkamata Yesu, kwa hiyo, alitaka kuona jinsi mambo yatakavyotokea, yeyeakiwa upande wa Yesu. Ila katika kishindo kilichotokea alikamatwa na kuponeachupuchupu kwa kuiacha nguo na kukimbia yu uchi. Jambo hilo linaonyeshahatari iliyokuwepo kwa wanafunzi, si ajabu walikimbia.

MARKO 269

14:53-65 Yesu mbele ya Kuhani Mkuu (Mt.26:59-68; Lk.22:63-71; Yn.18:12-14; 19:24)Tukilinganisha na Injili tatu zingine Yesu alihojiwa mara nyingi:a) Na Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu hapo nyuma, bado

alikuwa na sauti katika mambo. Inaonekana walimpeleka pale iliwaandae mashtaka yatakayofaulu (Yn.18:12ku)

b) Na Kayafa na wajumbe kadha wa Barazac) Na Baraza zima la Sanhedrin, wakati huo waliandaa mashtakad) Na Pilato (15:1ku)e) Na Mfalme Herode, Mfalme wa Wayahudi (Lk.23:8-12)f) Na Pilato tena (Lk.23:13-16)

k.53 Yesu aliletwa mbele ya Kuhani Mkuu Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuutangu B.K.18-36. Pamoja naye walikuwa wajumbe wa Baraza lao, wakuu wamakuhani, wazee, na waandishi. Marko amependa kuorodhesha wahusika.Yesu alikuwa mbele ya Baraza la dini, na iliwabidi waandae mashtakayatakayosimama mbele ya Pilato, liwali ya Kirumi, kwa sababu walitaka Yesuauawe kwa kusulibiwa, nao hawakuwa na mamlaka hiyo kwa sababuwalitawaliwa na Warumi. Walimchukia Yesu sana kwa sababu alikuwaamehukumu matendo yao ya kufanya biashara hekaluni. Waliogopa kwambaghasia ikitokea wao wataulizwa sababu yake na ingewezekana waondolewevyeo vyao. Walidhani kwamba ni wao waliojua mapenzi ya Mungu, walahawakupenda huyo aliyedai kusema kweli kwamba alikuwa na uhusiano waasili na ‘Baba’ Mungu wao. Hayo yote yaliwachukiza, nao walitaka aondolewe.

k.54 Hapo Marko ametaja habari ya Petro kumfuata kwa mbali. Yesu yu ndanimbele za wakuu huku Petro yu chini behewani mbele ya watumishi.Yawezekana Petro alikumbuka jinsi alivyosema kwamba hatamwacha, kwahiyo, alifanya juhudi kufika karibu. Yohana alikuwa pamoja naye, yeyealijulikana na mtu fulani, na kwa sababu hiyo yeye na Petro waliruhusiwakuingia ndani ya behewa karibu na mahali alipopelekwa Yesu (Yn.18:15ku).Kwa sababu ya baridi Petro alisogea karibu na watumishi na kukota moto.Marko ametaja jambo hilo hapo, tayari kueleza habari ya jinsi atakavyomkana,kwa sababu, wakati Yesu alipokuwa akihojiwa na Kayafa Petro alikuwaakihojiwa na mjakazi juu ya kumjua Yesu.k.55-56 Marko ameonyesha jinsi ambavyo Yesu alikosa kupata hukumu yahaki. Lengo lao lilikuwa ahukumiwe kufa, kwa sababu wameishakata shaurihilo. Walijitahidi kwamba ionekane kuwa wamejaribu kufanya kwa halali. Katikasheria ya Kiyahudi, mshtakiwa alikuwa na haki ya kujitetea. Mtu hakuwezakushtakiwa mpaka wamepatikana mashahidi wawili wenye ushuhudauliopatana kabisa (Kum.17:6; 19:15ku. Hes.35:30). Kwa hiyo wakuu walitafutamashahidi na wengi walipatikana ila hawakutoa ushuhuda wa kweli walaushuhuda uliopatana.

MARKO270

k.57-59 Kisha wawili walitokea waliotaja kwamba Yesu alisema mambo kadhajuu ya hekalu, ila hawakutoa maneno yake halisi (13:2; Yn.2:57-58). Yesuhakusema ‘Mimi nitalivunja....’ wala hakuwa na maana ya ‘jengo’ la hekalu balihekalu la ‘mwili’ wake utakaovunjwa Msalabani na kufufuliwa siku ya tatu. Hatakama alisema juu ya kulivunja jengo la hekalu alitaja kwamba atalijenga kwasiku tatu!! Ushuhuda wao wa uongo ulikuwa karibu na kweli, wa kutoshakumponza. (Neno la hekalu lilikaa mawazoni mwa watu mpaka mwisho (15:29).Kitheologia hawakuwa mbali na kweli maana Yesu ata’jenga’ jamii ya watuambao hawatahitaji jengo la mawe. Wakiwa na jengo maalumu nguvu yaoitapungua wakati Injili itakapopelekwa kwa WaMataifa, kwa sababu WaMataifawatawaza kwamba Ukristo ni dhehebu ya Kiyahudi.k.60 Yesu hakusikia wajibu wa kuyajibu mashtaka kwa sababu yalikuwa yauongo. Kuhani Mkuu alikasirika kwa vile walivyoshindwa kumponza.

k.61 Yesu akanyamaza, hakusema lolote, kwa sababu haikuwa juu yakekujishuhudia. Kwa hiyo Kuhani Mkuu alikuwa ameshindwa kupata mashtaka yakumpeleka mbele kwa Pilato. Mashahidi hawakupatana, na Yesu alinyamaza.Jambo muhimu kwao ni Yesu ni nani hasa? Kisha Kuhani Mkuu akafanyajambo ambalo halikuwa halali kufanya, pia alitumia kiapo (Mt.26:63) alimwulizaYesu kukiri kwa wazi kuwa Kristo, Mwana Mtukufu wa Mungu. Hapo nyumaYesu alikuwa hajasema wazi kwamba alikuwa Masihi, ila kwa matendo namadai yake alionyesha kuwa Ndiye. Ni vigumu kujua kama Kayafa aliulizamaswali mawili au kwa kusema Mwana wake Mtukufu alisisitiza Umasihi waYesu kwa sababu Wayahudi walifikiri hayo mawili ni mamoja (Zab.2:7). Hivyo,Yesu alipewa changamoto ya kukiri wazi kuwa Masihi. Alijua kwamba akisema‘Ndiyo’ amejiandikia cheti cha kufa, kwa kuwa watakuwa wamepata mashtakaya kutosha ya kumpeleka kwa Pilato. Yesu aliona kwamba ikiwa itambidi afe,na afe kwa sababu ya kweli ya kuwa Masihi, Mwana wa Mungu, wala si kwasababu nyingine.

k.62 Ndipo, kwa wazi kabisa, Yesu alijibu ‘Mimi ndiye’ Jina la Mungu (Kut.3:14)halafu, akatumia Jina la ‘Mwana wa Adamu’ (Dan.7:13) Jina alililozoeakulitumia (8:31; 9:31; 10:33-34; 13:26) aliendelea kwa kusema kwambawatamwona ameketi mahali pa heshima kuu, mkono wa kuume wa nguvu, nayeatakuja na mawingu ya mbinguni. Aliwaonyesha kwamba ni Yeye atakayerudikufanya hukumu ya mwisho na kutawazwa juu ya WaMataifa. Kwa hiyo, ndaniya jibu lake liko onyo zito na ilimpasa Kuhani Mkuu ajihoji juu ya ukweli wa ukirihuo wa Yesu. Yesu aliyaunganisha maneno ya Zab.110:1 na Dan.7:13,maneno ambayo Wayahudi waliamini kuwa yalimhusu Masihi. Iliwapasa kamaviongozi katika Israeli, wawe na utambuzi kuhusu Masihi, ila kwa sababu yaupofu wao wa kiroho na kwa kupenda vyeo vyao na heshima za wanadamukuliko heshima ya Mungu walishindwa kumtambua. Mathayo amesema alijibu‘Wewe umesema’ kama kusema kwamba kama asingaliulizwa swali hiloasingalitoa jibu hilo (Mt.26:64). Yawezekana Yuda alikuwa amewajulishamambo kadha ambayo Yesu alikuwa amesema kwa siri kwa wanafunzi wake.

MARKO 271

k.63 Kisha Kuhani Mkuu akararua nguo yake kuonyesha jinsi alivyochukizwana jibu la Yesu. Machoni pake Yesu amekufuru, ila Yesu alikuwa hakusemaneno lolote juu ya Mungu na Jina lake. Kuhani Mkuu alifikiri kwamba Yesuamemnyima Mungu utukufu wake na kupunguza heshima yake, kwa sababu niMungu peke yake atakayemketisha Masihi wake. Kwa sheria Kuhani Mkuuhakuruhusiwa kurarua nguo zake ila kwa jambo zito (Law.21:10).

k.64 Halafu Kuhani Mkuu aliwauliza wenzake katika baraza ‘mwaonaje ninyi?’ndipo wote walimwunga mkono kwamba imempasa Yesu auawe. Hivyo, ilibakikazi ya kunyosha mashtaka ili yawe katika hali ambayo liwali Pilato atayajali.Yasiwe mashtaka ya dini, na ‘kufuru’ ni la dini; budi wayageuze kuwa ya siasa.

k.65 Mara baada ya kufaulu katika kupata mashtaka yaliyokubalika, yakupeleka kwa Pilato, watu walisikia uhuru wa kumshambulia Yesu nakumtendea kwa jeuri, kumtemea mate, kumfunika uso na kumpiga n.k. Ni kamawalikuwa wakimjaribu ajionyeshe Umasihi wake kwa kutabiri ni nani aliyempigan.k. Hivyo walimdharau sana.

14:66-72Petro alimkana Bwana Yesu (Mt.26:69-75; L.22:55-62; Yn.18:15-18,25-27)k.66 Yesu alikuwa amepelekwa kwa chumba cha kuhojiwa na Petro alikuwabehewani chini kwa sababu Yohana alipata ruhusa kwa kuwa alijulikana naKuhani Mkuu. Kutokana na mambo yaliyofuata ni rahisi kufikiri kwamba Petroalikuwa mwoga, ila kwa upande mwingine alikuwa na ujasiri wa kumfuata Yesu,ingalau kwa mbali, hata akathubutu kuingia behewani, akiwa peke yake bilawenzake. Kwa hiyo ni Petro tu aliyejaribiwa kumkana Yesu kwa sababu ni yeyealiyejiweka mahali pa kujaribiwa. Tukumbuke kwamba alikuwa amemkata sikioMalko (Yn.18:10).

k.67 Akaja mjakazi mmoja wa Kuhani Mkuu (mgoja mlango Yn.18:17)akamwangalia Petro ndipo akamwambia ‘Wewe ulikuwapo pamoja na yuleMnazareti, Yesu’. Kwa kawaida, maneno ‘yule Mnazareti’ yalitumika kwadharau na pengine ndivyo alivyowaza mjakazi. Hivyo, Petro alijulikana kwauhusiano wake na Yesu.

k.68 Ghafula Petro alishikwa na hofu, akakana kwamba alimjua Yesu hatakuelewa yaliyosemwa na huyo mjakazi. Mara akatoka nje, pengine alidhanikwamba watu hawataweza kumtambua kwa urahisi katika giza kuliko akikaakatika mwanga wa moto. Ndipo jogoo akawika, ukumbusho wa maneno yaYesu (14:27-31).

k.69 Halafu yule mjakazi akawaambia wengine kwamba ‘Huyu ni mmoja wao’.Si ajabu kwamba habari hii ilipoanza kusemwa wengine walivutwakuizungumzia (Ling. Mt.26:71 mwanamke mwingine; Lk.22:58 mwanaume;Yn.18,26-26 jamaa wa Malko).

MARKO272

k.70 Petro akakana tena. Ndipo, baada ya muda, wengine waliosimama palewakamwambia ‘Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe’.Alitambulikana kwa usemi wake.

k.71-72 Petro alianza kulaani na kuapiza kwamba hakumjua huyuwaliyemnena. Hakutaja jina la Yesu (8:38). Hakumlaani Yesu bali alisema kamahivi ‘Mungu alete uovu juu yangu ikiwa mimi sisemi iliyo kweli (yaani ikiwa mimininamjua Yesu). Kisha jogoo akawika tena, akimkumbusha Petro maneno yaYesu na jinsi ambavyo hapo nyuma alionywa na Yesu juu ya jambo hilo.Alipotafakari habari hiyo akalia. Bila shaka alisikia aibu kubwa na huzuni nyingi.Alijitegemea mwenyewe akifikiri kwamba ataweza kuwa imara na mwaminifu,ila Yesu alijua kwamba alikuwa dhaifu na ya kwamba atakapobanwa atamkana.Maneno ya Yesu yalikuwa thabiti. Luka alisema kwamba Yesu alimkazia macho(Lk.22:61). Hivyo, Yesu alihojiwa mbele za Kuhani Mkuu, akawa mwaminifu,huku Petro alihojiwa na mjakazi na wengine akashindwa kuwa mwaminifu. Kwahiyo, pamoja na kupatwa na chuki nyingi kutoka kwa adui zake, Yesu alionjamaumivu ya kukanwa na rafiki yake mpendwa.

Kwa nini Petro hakuwa tayari kuushuhudia uhusiano wake na Yesu? Kwasababu aliogopa kukamatwa; hakujiandaa kwa kuomba pale Gethsemane(14:38). Alikuwa kati ya wageni, watu wa Yudea ambao kwa jumlahawakumpenda Yesu. Hata pengine alikuwa amekata tamaa juu ya Yesualipokubali kukamatwa bila kutumia nguvu. Tukijumlisha sababu za Petrokuanguka twaona kwamba alikuwa na majivuno juu ya uwezo wake wa kuwamwaminifu (k.29) ndipo alitoroka hatari ilipotokea (k.50) ndipo alimfuata Yesukwa mbali (k.54) kisha alijiweka pamoja na adui wa Yesu (k.54). Ila kila hatuaya kuteleza ilikuwa pia nafasi ya kuwa imara na kusimama bega kwa bega naYesu. Wakati wa kushindana na majaribu ni kabla hayajatokea na kwa maombiya kukaza nia kama Yesu alivyofanya.

Yesu alikutana na Petro peke yake siku ile Alipofufuka (Lk.24:34). BaadayeYesu akamrudisha hadharani mwa wenzake na kumkabidhi kazi ya kuchungakondoo zake (Yn.21:15).

15:1-15Yesu mbele ya Pilato, liwali Mrumi (Mt.27:1-16; Lk.23: 1-25;Yn.18:28-19:16)

k.1 Baada ya mazungumzo katika Baraza la Sanhedrin, Kuhani Mkuu nawenzake, asubuhi na mapema, walimpeleka Yesu kwa liwali ya Kirumi, haliwamenyosha mashtaka tayari kwa Pilato kuyapokea na kutoa hukumu ya kufa.Kwa sababu walikuwa chini ya utawala wa Kirumi hawakuruhusiwa kutoahukumu ya kufa. Kwa hiyo, wakamfunga Yesu na kumleta kwa Pilato, ambayemwanzoni hakuwa tayari kuwapokea, maana hawakutaja wazi mashtaka, nayeye hakuwa tayari kuendelea mpaka wameyataja (Yn.18:28-32). Ila walikuwana tatizo moja; katika Baraza lao kosa la Yesu lilikuwa kufuru, ila walijua

MARKO 273

kwamba Pilato hatajali mambo ya dini, hivyo, wakayageuza ili yawe katika haliya siasa. Kuwa Masihi na kuwa Mfalme wa Wayahudi ni mamoja ila nenoMasihi lilikuwa neno la Kiyahudi kwa yule waliyemtazamia atakuja nakuwaweka huru. Kwa kutumia neno ‘Mfalme’ waliingiza siasa na kudokezeakwamba Yesu amekuja kuipindua serikali. Ajabu ni kwamba, kwa sababu Yesuamekataa kuwa Masihi wa kuipindua serikali wamemkataa. Kwa hiyo, baada yakuhukumiwa na Wayahudi Yesu alihukumiwa na serikali ya Kirumi. Pilatoalikuwa liwali B.K.26-36 akitawala Jimbo la Shamu. Alikuwa mkatili walahakuwajali Wayahudi na mila zao, hapo nyuma alikuwa amewachukiza marakwa mara (Lk.23:2). Hivyo, hakuwa tayari kufanya neno la kuwapendeza.

k.2 Pilato akamwuliza Yesu ‘Wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?’ Neno ‘wewe’lina nguvu na linatawala sentensi hiyo, kana kwamba Pilato alishangaakumwona huyo aliyekuwa mbele yake aweza kufikiriwa kuwa mfalme. Yesuakamjibu kama kukubali bila kusema ndiyo. Kwa sababu jinsi Pilato alivyowaza‘ufalme’ na maana yake kwa Yesu ilikuwa tofauti sana. Kwa hiyo Yesu alikubalikuwa mfalme ila si kwa kulingana na mawazo ya Pilato. Tukilinganisha naYohana 18:29-31;34-37 Yesu alijaribu kufafanua maana halisi ya ‘ufalme’ wake.Ufalme wake si wa hapa duniani, wala hali yake si kama zilivyo falme za dunia.

k.3 Wakuu wa makuhani waliona kwamba mambo hayaendi kama walivyotaka,kwa hiyo, walizidi kumshtaki mengi (Lk.23:5-12) mambo yenye harufu ya siasa,mambo yaliyompasa Pilato ayajali, kwa kuwa, ikiwa Yesu ni mwana mapinduziwa serikali kama walivyosema hawezi kumwachilia bila kuyahakikishiamashtaka hayo.

k.4-5 Lakini Yesu akakaa kimya, kadiri waliyozidi kumshtaki Yeye alizidikunyamaza, hata Pilato alishangaa. Yesu hakujibu kwa sababu mashtakayalikuwa uongo, yasiyostahili kujibiwa. Pilato alimwona kuwa tofauti sana nawengine ambao waliposhtakiwa walizidi kupaza sauti na kujitetea, piaalitofautiana sana na washtaki wake. Pilato alitaka kumsaidia ila aliona kwa jinsiYesu hakusema neno alishindwa kupata nafasi. Awezaje kumwachilia hukumashtaka juu yake ni mengi? Manabii walitabiri kwamba Masihi atanyamaza(Isa.42:1-4; 53:7; 57:15; Zek.9:9).

Pilato aliposikia kwamba ametaharakisha watu kutoka Galilaya mpaka Uyahudi,alifurahi (Lk.23:2-5). Aliona amepata njia ya kukwepa kutoa uamuzi juu yaYesu, akampeleka kwa Mfalme Herode ili yeye atoe uamuzi (Lk.23:6-12).

k.6 Herode alipomrudisha Yesu kwa Pilato ilimbidi Pilato apate njia nyingine zakumwokoa Yesu. Kama ni Pilato aliyekumbuka, au ni watu waliomkumbusha,ilikuwepo desturi moja kwa liwali kumwachilia mfungwa mmoja wakati waPasaka, kama kutuliza watu, maana wakati wa Pasaka waliwaka moto wakutaka uhuru wakikumbuka jinsi baba zao walivyotolewa utumwani.k.7-8 Alikuwepo mfungwa mmoja mashuhuri aliyeitwa Baraba (maana ya jina

MARKO274

‘mwana wa baba’) mtu aliyefanya fitina na uuaji, yawezekana alikuwa katikajamii ya Wazeloti. Alikuwa mhalifu aliyeishahukumiwa adhabu akingojeakusulibiwa. Yesu hakuwa mhalifu na alikuwa bado hajahukumiwa adhabu. Kwahiyo uchaguzi haukuwa sawa; ulikuwa kati ya mtu aliyehukumiwa kosa na Yesuambaye hakuhukumiwa kosa. Hata kama Pilato angalimfungulia Baraba,hakuna sababu ya Yesu kuwa badala yake kwa sababu hakuwa na kosa.

k.8ku Ndipo watu walikuja na kumwomba Pilato afuate desturi hiyo yakumfungulia mtu. Yawezekana baadhi yao walikuwa rafiki wa Baraba.Inaonekana walikuwepo makundi mawili ya watu; wale waliotoka Galilayaambao walikuwa upande wa Yesu, na wale wa Yerusalemu, Kuhani Mkuu nawenzake waliokuwa kinyume chake (Mt.21:10-12). Pilato hakutambua kwambakuna hatari yoyote kwa Yesu wala hakutambua hila ya viongozi katikakuwashawishi watu, wala hakuona kwamba nia za watu zitageuzwa kwaharaka. Akawauliza ‘Je! mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?’akitazamia jibu litakuwa ‘ndiyo’. Ameishatambua kwamba Yesu hakuwa hatarikwa serikali ya Kirumi na ya kwamba Wayahudi walikuwa wamemleta kwakufuata agenda yao. Alifahamu Yesu alipendwa sana na watu wengi (12:37) naya kwamba viongozi walimwonea wivu. Bila shaka alitatizwa kufikiri kwa niniwanamtaka Yesu auawe, maana hawakusifiwa kwa uaminifu wao kwa Dola yaKirumi, walikuwa watu wa matata sana walioleta masumbufu mengi. Kwa niniwalipiga kelele Yesu asulibiwe ikiwa walilotaka ni Baraba afunguliwe? Ilikuwavigumu Pilato afahamu sababu ya Wayahudi kutaka Myahudi mwenzao auawekifo cha ukatili sana. Pilato hakuwa na nia ya kujikomba kwao.

k.11 Lakini wakuu wa makuhani walifanya juhudi ya kuwashawishi watukumwomba Baraba badala ya Yesu. Huenda wakati huo Pilato aliupokeaujumbe kutoka mkewe wa kumwambia kwamba asihusike na shauri la Yesu(Mt.27:19). Jambo hilo lilimtia moyo wa kukazana kupata njia ya kumwachiliaYesu, ila kwa sababu aliogopa kwamba Wayahudi wangepeleka ripoti kwaKaisari, ndipo angeondolewa cheo, hakuwa tayari kumfungulia moja kwa moja,kama ilivyokuwa haki. Kila mara alisema hakuona hatia juu yake, kwa hiyo,ilimpasa amfungulie mara.

k.12 Katika kutangatanga kwake na hofu yake ya kupoteza cheo chake Pilatoaliwaulizia watu afanye nini na Yesu, Mfalme wao. Amekosa kuwa na nguvu yakutawala hiyo kesi maana haikuwa haki hakimu aulize swali hilo, maana mpakahapo hayakupatikana mashtaka ya halali juu yake. Huenda alidhani kwambawataridhika na adhabu ndogo (Ling. Yn.19:1ku).

k.13 Watu walikuwa wamemwelewa vizuri Pilato, walijua ya kuwa alikuwamwoga akiogopa kupoteza cheo chake (Yn.19:12). Kusulibisha kulikuwaadhabu ya Kirumi. Wayahudi wangaliweza kumpiga kwa mawe au kumkatakichwa, ila kwa sababu atachukua mahali pa Baraba atasulibishwa, kwa

MARKO 275

sababu ndiyo adhabu kwa mwana mapinduzi kama Baraba. Yesu alibanwa katiya siasa ya Kiyahudi na ya Kirumi na hizo zilikutana na kusababisha hukumu yakufa kwa njia ya kusulibishwa. Hayo yote yalikuwemo katika mpango wa Munguwa kuokoa ulimwengu.

k.14 Hata hivyo, Pilato hakuona vema amtoe Yesu kwa kusulibiwa kwa kuwabado hajapata neno halisi la kutoa hukumu hiyo. Akawauliza tena ‘Kwani, niubaya gani alioutenda?’. Hakuna msingi wowote wa haki atolewe kuuawa. Ilawatu walikazana kuomba asulibishwe kinyume cha hakimu na nia yake, hakimumpagani!! Hicho ndicho kiasi cha chuki yao kwa Yesu. waliitikia kwa kuzidishakelele za kuomba asulibishwe (Mdo.3:13-15). Bila shaka Yesu aliudhika sanana hali ya watu wake.

k.15 Kisha Pilato, hali akiogopa ghasia itatokea (Mt.27:24) aliwaridhishamkutano, akamfungulia Baraba, na kumtoa Yesu ili asulibiwe. Ila kabla yakumtoa Yesu alipigwa mijeledi. Ilikuwa desturi kufanya hivyo, maana kwakupigwa mijeledi wahalifu walidhoofishwa hata na wengine waliwahi kufa, nawengine hawakukawia kufa walipowekwa mtini. Haikuwa halali ampige Yesukama ni mhalifu huku amemtangaza mara kwa mara kuwa hana hatia.Walipopigwa mijeledi watu waliumizwa sana, nyama yake ilikatwakatwavipande vipande na ngozi ilichubuka. Mjeledi ulikuwa wa ngozi na katika nchazake vipande vya mifupa au chuma viliwekwa. Tukilinganisha na Injili yaYohana twaona kwamba mwishowe Wayahudi waligeuza mashtaka na kutajawazi neno la kufuru ambalo hasa lilikuwa shtaka lao (Yn.19:17). Markoamefupisha habari za hukumu ya Yesu.

Pilato alifikiri kwamba usalama wa cheo chake ni muhimu kuliko kufanyahukumu ya haki na adili. Alikuwa na shingo gumu, hakuwa tayari kubadiliuamuzi wake hali alifahamu kabisa kwamba Yesu hakuwa na kosa. Neno laYesu kuwa bila hatia limesisitizwa sana katika habari hizo. Marko alielekeakuwalaumu Wayahudi kuliko Pilato katika habari hizo. Baadaye Pilatoaliondolewa cheo chake kwa mambo mengine ambayo Wayahudi walipelekahabari zake huko Rumi.

Uovu ni fumbo kubwa kwa wanadamu ila fumbo lililo kubwa zaidi ni jinsi Munguawezavyo kufanya kazi njema hata wakati wanadamu huchagua kufanyamaovu, maovu ambayo wanayo hatia juu yake, na maovu hayo Munguhuyafuma katika makusudi yake mema, ya wokovu, kwa ulimwengu. Mungualigeuza kifo kisicho halali cha Bwana Yesu kuwa njia ya kuwaokoa wanadamu(Mdo.2:23).

15:16:20 Yesu alidhihakiwa na askari (Mt.27:27-31; Yn.19:2,3)Makuhani na wenzao wameisha kumdhihaki Yesu (14:65) ndipo ilikuwa zamuya WaMataifa kumdhihaki. k.16 Pilato alikuja Yerusalemu kutoka Kaisariawakati wa Pasaka, kwa kusudi la kuhifadhi usalama iwapo Wayahudi

MARKO276

watawasha moto wa siasa ya kutaka uhuru. Alikuja na kikosi cha askari.Alimkabidhi Yesu kwao ili wamtayarishe kwenda kusulibiwa. Hao askariwalikuwa wakatili wenye moyo mgumu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ngumumara kwa mara. Walikuwa wamesikia mashtaka juu ya Yesu kuwa Mfalme waWayahudi. Hao hawakuwa Wayahudi, nao waliwadharau Wayahudi. Hivyowalipomchukua Yesu walimdhihaki kulingana na mashtaka yake. Bila shakawalimwona kama mjinga kabisa katika kudhani hata kuthubutu kushindana nanguvu za utawala wa Kirumi katika jaribio la kuipindua serikali. Kwa hiyo, hanabudi, apate matokeo ya ujinga wake. Ila walikuwa wamekosa kuelewa kwambasivyo ilivyo kwa upande wa Yesu; wengine walimtaka kuwa mwana mapinduzi,Yeye mwenyewe amekataa kabisa kuwa mwana mapinduzi, na ndiyo sababuhasa ya watu wa taifa lake kumkataa. Yeye amehukumiwa adhabu kama ndiyemwana mapinduzi, huku Baraba, aliyetamani sana kuipindua serikaliameachiliwa!!! Hata hivyo, Yeye ndiye Mfalme ambaye atasimikwa rasmi naMungu kutawala mataifa yote, hata ni Mfalme wa hao askari bila waokumtambua.k.17 Walimvika vazi la rangi ya zambarau (Mt.27:28 jekundu) huenda lilikuwavazi kuukuu la askari ambalo rangi yake imechujuka. Ndipo wakasokota taji yamiiba, wakaitia kichwani mwake na Mathayo amesema kwamba walimpamwanzi ashike mkononi. Kisha wakamsalimu na kumpigia magoti nakumsujudu kama mfalme. Hayo yote yalilingana na madai yake ya kuwamfalme. Ulikuwa upeo wa dharau na dhihaka kubwa, maana Yesu alikuwaMfalme kweli, Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana, ila si kwa aina yawafalme wa dunia hiyo. Dhihaka hizo ziliwakumbusha Wayahudi kwambawalikuwa chini ya utawala wa Kirumi, bila kuwa na mfalme wao wenyeweisipokuwa yule Herode ambaye hakuwa Myahudi kamili, tena aliwekwa naWarumi. Wayahudi hawakumpenda Herode. Hivyo walionyesha dharau kubwakwa Yesu na kwa taifa la Kiyahudi.

k.19 Pamoja na kufanya vichekesho hivyo walitumia nguvu za kimwili nakumpiga Yesu na mwanzi kichwani na kumtemea mate. Manabii walitabirimambo hayo (Isa.53:3ku) na Yesu pia alikuwa ametabiri habari hiyo (10:33-34).Bila shaka aliumia sana rohoni mwake pamoja na kuzidi kusikia maumivumwilini mwake, maana ameishapigwa mijeledi, na hapo tena amepigwa namwanzi.

k.20 Baada ya kufanya hayo yote, wakamvua vazi la rangi ya zambarau nakumvika mavazi yake mwenyewe, ndipo wakamkabidhi kwa askari wanne naakida wao, nao wakampeleka nje kwenda mpaka mahali pa kusulibiwa(Yn.19:23).

15:21-32Kusulibishwa kwa Bwana Yesu (Mt.27:32-56; Lk.23:26-49;Yn.19:17-37)Kifo cha kusulibishwa kilikuwa cha ukatili sana na aibu kubwa. Waandishi waInjili nne wameziandika habari hizo bila kusisitiza maumivu ya kimwili, kwa

MARKO 277

sababu walitaka wasomaji wazingatie maumivu yake ya kiroho na sababu namaana ya kifo hicho kwa wokovu wa wanadamu.

k.21 Yesu alidhoofika sana kwa kupigwa mijeledi na mwanzi. Njiani askariwalimkuta mtu na kumshurutisha aubebe msalaba. Kwa sababu walitawala nchiwalikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo. Yawezekana Simoni Mkirene alikuwamtu wa Afrika Kaskazini aliyeishi Yerusalemu, au pengine alikuja Yerusalemukwa Pasaka. Iskanda na Rufo wana wake walijulikana na Marko, penginewalikuwa waumini katika Kanisa la Rumi (Rum.16:13) ila hakuna uhakika kwasababu wengi walikuwa na majina hayo.

k.22 Mahali aliposulibiwa paliitwa Golgotha kwa Kiebrania na Kalvari kwaKilatini. Pengine paliitwa hivyo kwa sababu ya sura yake au huenda fuvu lakichwa lilipatikana pale.

k.23 Kabla ya kumweka Yesu kwenye miti ya msalaba walimpa mvinyo uliotiwamanemane ili aunywe, Yesu akaukataa. Lilikuwa tendo la huruma kupunguzamaumivu wakati wa kupigiliwa misumari miguuni na mikononi na kusimamishwajuu. Yesu alikataa kuinywa kwa sababu alitaka kuwa na fahamu timamu nakuelewa kabisa alichokuwa akifanya pale katika kuzibeba dhambi za ulimwenguna kuwa sadaka wa ajili ya kuwapatia wanadamu msamaha na uzima wamilele. Aliweza kutamka maneno saba ya maana sana. Alikuwa akijitoa kwahiari ya mapenzi katika kumtii Mungu mpaka kufa. Wanyama wa sadakawaliletwa madhabahuni bila kuelewa kwamba wamekuwa sadaka za dhambi(Heb.9:13ku. 10:5-10). Yesu hakufa tu, bali katika kufa alifanya upatanisho katiya Mungu na wanadamu.

k.24 Askari waligawa mavazi yake. Ilikuwa desturi kufanya hivyo, ni kamakuzawadiwa kwa kazi hiyo ngumu, nao walilipigia kura vazi moja badala yakulipasua (Yn.19:20; Zab.22:18) Warumi walisulibisha watumwa na waasiwasio Warumi kwa shabaha ya kutisha watu na kulinda amani katika nchiwalizotawala wasije wakafanya fujo za mapinduzi.

k.25 Marko ametaja saa ya Yesu kuwekwa msalabani. Ni saa tofauti na ileiliyotajwa katika Injili ya Yohana. Ni vigumu kuelewa kwa nini ni tofauti,yadhaniwa Yohana alifuata hesabu iliyotumiwa na Warumi au amechanganyana kutaja saa ya hukumu siyo saa ya kusulibiwa (Yn.19:14).

k.26 Ilikuwa desturi ya Warumi kuwatembeza wahalifu katika njia za mji ili watuwawaone na kuogopa. Walilazimisha wahalifu kuvaa shingoni ubao uliotangazakosa lao ndipo waliposulibiwa hiyo anwani iliwekwa juu ya msalaba ili kila mtuasome kosa la mhalifu. Anwani ya Yesu iliyosema ‘Mfalme wa Wayahudi’iliandikwa katika lugha tatu (Lk.23:38) na kuwekwa juu (Mt.27:37). Wayahudiwalichukizwa, ni kama dharau kwao na walimwomba Pilato aibadili, akakataa(Yn.19:21,22). Ilionekana upuzi mtupu kusema kwamba huyo mtu dhaifu

MARKO278

anayekufa katika aibu kubwa aweza kuwa Mfalme wao. Ilikuwa dhahiri kwambaYesu alisulibiwa kama mwasi na mwana mapinduzi wa serikali ya Kirumi.

k.27-28 Wahalifu wawili walisulibiwa na kuwekwa upande wa kushoto na wakulia na Yesu alikuwa kati. Kama Baraba hakuachiliwa yeye angalikuwa juu yamsalaba badala ya Yesu. Yawezekana wale wawili walikuwa rafiki zake. Nenohilo lilitimiza unabii wa Isa.53:12 na shabaha ya Yesu kuwa rafiki wa wenyedhambi. Alikufa kati yao huku akifa kwa ajili yao.

k.29-30 Wengi walipitia pale, na bila shaka wengi walikuja pale ili wauonemwisho wa huyo Yesu waliomtumaini kuwa Masihi wao. Watu walifanyadhihaka wakitikisa-tikisa vichwa. Walikumbuka maneno yake juu ya kuvunjahekalu, wakamsuta na kumpa changamoto ya kushuka msalabani kwa kuwaalisema kwamba atalivunja jengo la hekalu na kulijenga tena. Je! mbonahashuki msalabani kama anao huo uwezo?. Ni ajabu jinsi neno hilo lilivyokaamawazoni mwa watu na mwa wakuu. Ila ni mwili wa Yesu ambao ni hekalu, naoulivunjwa pale Msalabani na katika siku ya tatu akauchukua tena. Ndiyo maanaya maneno yenyewe tangu mwanzo (Yn.2:19ku).

k.31-32 Marko ametaja watu mbalimbali waliokuwepo na kuangalia mambohayo (wanafunzi hawakuwepo). Pamoja na watu hata wakuu wa makuhani nawaandishi walimdhihaki wakizungumza wao kwa wao hali wakijua Yesualiyasikia hayo waliyosema. Kwa kejeli walisema ‘Aliponya wengine, hawezikujiponya mwenyewe’ ushuhuda wa kweli na wa ajabu sana. Kama angalishukana kujiponya mwenyewe sisi wanadamu tungalikosa wokovu. Alikuwaakiwaokoa watu kwa Kifo chake. Wokovu huo hauna gharama kwetu, ilaulimgharimia Yeye maisha yake yote mpaka Kufa, Kufa msalabani (Flp.2:5ku).Walitaka athibitishe madai yake kuwa Masihi, ila kama angalishuka angalikuwaMasihi wa uongo. Wale wahalifu pia walimsuta ila Luka ametuambia kwambabaadaye mmoja alibadili hali yake na kumgeukia Yesu na kumwombaamkumbuke atakapoingia katika Ufalme wake (Lk.23:39-43). Mpaka mwishowatu walitaka ishara, kitu kilichoonekana wazi, kilichoweza kuguswa, iliwamwamini. Mpaka leo Kristo hutaka tumwamini kibinafsi. Ukuu wa kazi yakeya kuokoa unaonekana katika udhaifu wake mkubwa. Waliosulibiwa walikufapolepole kwa kuishiwa maji na nguvu mwilini na kwa uchovu kabisa.

(Hivyo Yesu alitoa ile fidia ya dhambi (10:45) na kukinywea kikombe chaghadhabu ya Mungu juu ya dhambi (14:36) na kutoa mkate na divai vya AganoJipya (14:22-24). Taz.Rum.3:21ku.2 Kor.5:18-19; 1 Pet.1:18-20; 3:18). Markohakutoa maelezo ya Kifo cha Yesu ila kwa kutaja maneno ya Yesu naMaandiko mengi yaliyotimizwa, maana yake imeeleweka vizuri. Baadayewaandishi wa Agano Jipya walikitafsiri kuwa fidia ya dhambi na ya kwambaYesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi na badala yao).

MARKO 279

15:33-37 Kifo cha Bwana Yesu (Mt.27:45-56; Lk.23:44-49; Yn.19; 25,28-30)k.33 Yesu aliwekwa msalabani kama saa tatu asubuhi, na katika muda huoalitamka maneno matatu yaliyotajwa na Luka 23:34,43,36. Ndipo giza kuulilikuja juu ya nchi yote, wakati wa adhuhuri, na liliendelea mpaka saa tisa.Lilifunika nchi yote, si palepale tu. Lilisababishwa na nini? ni vigumu kutoamaelezo isipokuwa kusema kwamba lililetwa na Mungu. Ni vigumu kufikirikwamba jua lilipatwa, maana wakati wa Pasaka ulikuwa mwezi mpevu. Tenaijapokuwa upepo mkali ulivuma mara kwa mara ni vigumu kufikiri uligusa nchiyote kwa muda wa saa tatu, na hasa katika saa zilezile Yesu alipokuwa akifakwa ajili ya dhambi. Ni wazi kwamba jambo hilo halikusahaulika, waandishiwote walilitaja kama lilikuwa jambo la kipekee la uwezo mkubwa. Liliashirianini? tukikumbuka mafundisho ya Agano la Kale twaona kwamba gizalilifungamana na hukumu ya Mungu juu ya dhambi, ishara ya ghadhabu yakejuu ya uasi wa watu wake (Isa.5:30; 60:2; Yoe.2:30,31; Amo.5:18,20;Zef.1:14ku. Mt.24:29,30; Mdo.2:20; 2 Pet.2:17; Ufu.6:12ku). Tena giza hilo niishara ya kueleza maneno mazito ya Yesu (k.34) maneno yaliyoashiria gizarohoni mwake alipojitwisha dhambi zetu zote. Giza liliuvuta usikivu wa watu iliwalizingatie hilo jambo kuu lililotendeka pale, jambo pekee katika historia yaulimwengu. Ni kama umbaji ulishirikiana na Mwumba wake (Yesu Yn.1:1-3)kana kwamba ulishindwa kumtazama alipotundikwa Msalabani.

k.34 Katika kifungu hicho tunalo tamko la nne la Yesu nalo limeandikwa naMathayo na Marko tu. Luka na Yohana wameandika matamko sita mengine(Lk.23:34,43,46; Yn.19:26,28,30). Hilo la nne lilikuwa la kati katika manenosaba aliyoyatamka Yesu. Inaonekana Yesu alikuwa akizingatia Zaburi 22inayoanza na maneno hayo. Ni Zaburi inayosema juu ya mtu wa hakialiyeonewa ndipo mwishowe alipata amani na ushindi. Ni vigumu kwetuwanadamu kupima na kuelewa kina na upeo wa uzito wa maneno hayoyaliyosemwa na Yesu juu ya kuachwa na Babaye.

Ni vema kumaanisha kwamba Yesu hakusema hayo kwa jinsi alivyojisikiamwenyewe tu, bali kama jambo lililotokea kweli, ya kuwa aliachwa na Babaye.Mungu hushindwa kutazama dhambi na aliuficha uso wake kwa Mwanawedhambi ilipowekwa juu yake. Ni Mwana wake mpendwa asiyekuwa na dhambiwala hakufanya dhambi (Hab.1:13) Aliachwa ili sisi tusiachwe kamwe(Ebr.13:5). Ndiyo sababu huzuni yake ilizidi, alisononeka sana paleGethsemane alipoyawaza hayo. Yeye ambaye zaidi ya mtu yeyote alisikianafsini mwake ukaribu wa Baba alionja taabu ya kutengwa naye kwa ajili yetu,alilipa gharama yote ya dhambi. Hata hivyo hakumkana Mungu, alilia ‘Munguwangu’. Upendo mkamilifu na utakatifu mkamilifu wa Mungu ulikutana katikaKifo cha Yesu. Alifanywa kuwa dhambi (2 Kor.5:21) na laana (Gal.3.13) dhambiza ulimwengu ziliwekwa juu yake (Isa.53). Hivyo twajua hakika kwamba dhambizetu zimepata msamaha na deni letu limelipiwa. Kwa maneno hayo Yesualieleza taabu za rohoni mwake.

MARKO280

k.35-36 Wengine waliposikia neno hilo walifikiri kwamba Yesu alikuwaakimwita Eliya. Pengine walijifanya kama hawakuelewa, wakitumia nafasi hiyokwa kumdhihaki tena. Ila mmoja, pengine askari, alimhurumia akaenda kwaharaka na kujaza sifongo siki, huenda ilikuwa divai chungu, iliyotumiwa naaskari, ambayo ilikuwa na sifa ya kukata kiu. Yohana ametaja kwamba Yesualilia ‘naona kiu’ na pengine hii ndiyo sababu ya mmoja kumletea hiyo divai.Ilikuwa tofauti na ile waliyotaka kumpa mwanzoni (k.23) ambayo alikataakuipokea kwa sababu ilikuwa na dawa ya kupunguza akili na maumivu.

k.37 Ndipo Yesu akatoa sauti kuu; Yohana ametaja tamko la sita ‘Imekwisha’Yesu alitangaza ushindi wake kwa nguvu, ndipo Luka ametuambua tamko lamwisho, la saba ‘Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu’. Maneno hayo niishara ya Yeye kukata roho kwa kuamua mwenyewe mara alipoona kazimaalumu ya kufidia dhambi imetendeka, hakuna sababu aendelee kusumbuka.Pilato alishangaa aliposikia kwamba ameisha kufa (k.44).

15:38-41Pazia la hekalu lilipasuka, akida aliamini, wanawake walitazamakwa mbalik.38 Pazia la hekalu lilipasuka kutoka juu kuashiria mwisho wa mpango wakale, taratibu za ibada na kutoa dhabihu za wanyama kuwa sadaka, na kanunizilizohusu kumkaribia Mungu. Tangu zamani za Musa, kwanza kwa Hema yaKukutania na baadaye kwa Hekalu, palikuwapo mahali palipoitwa Patakatifu paPatakatifu palipotengwa na Patakatifu kwa njia ya pazia ndefu ya futi 60.Hakuna aliyeruhusiwa kuingia Patakatifu pa Patakatifu isipokuwa Kuhani Mkuu,mara moja kwa mwaka, Siku ya Upatanisho.

Patakatifu pa patakatifu paliashiria ‘Kuwepo kwa Mungu’. Bila shaka pazialilipopasuka kutoka juu na pote palikuwa wazi makuhani waliotumika mlewalitishwa sana. Jambo hilo lilitendwa na Mungu Mwenyewe kuonyeshakwamba kwa Kifo cha Yesu njia imepasuliwa na ni wazi kwa mtu yeyote, wakatiwowote, na mahali popote, kumkaribia Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kwaimani katika Kifo chake (Ebr.10:19-22; Kut.21:33; 26:31ku. 36:35; 40:21;Ebr.6:19; 9:3). Baadaye makuhani wengi waliamini (Mdo.6:7). B.K.70 Jengo lahekalu lilibomolewa. Mpaka wakati huo taifa lilipewa nafasi ya kumwaminiYesu kutokana na ushuhuda wa Mitume na Wayahudi waumini ila taifa kwajumla halikubadili uamuzi wake wa kumkataa Yesu kuwa Masihi wao.

k.39 Akida wa wale askari waliomsulibisha Yesu alikuwa amekaa pale nakuona yote yaliyotendeka. Hasa alipata nafasi ya kumwona Yesu katika mudawote wa kukaa msalabani. Kwa kawaida, waliosulibiwa walilaani na kutukanakwa sababu ya maumivu makali, ila tangu mwanzo Yesu alisema manenomachache, tena ya kuwahurumia wengine, hata aliwaombea msamaha kwawale waliomsulibisha. Ndipo alikufa bado angali akiwa na nguvu. Mambo hayoyote yalimvuta akida kumkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu. Kwa jinsi alivyokufapamoja na yote yaliyotangulia alikuwa na hakika kwamba Yesu hakuwa na

MARKO 281

hatia wala kosa (Lk.23:47 ‘mwenye haki’). Kufuatana na mashtaka ya kuwaMfalme na kutajwa ‘Mwana wa Mungu’ pamoja na dhihaka za viongozialielekezwa kumwaza Yesu kuwa Mwana wa Mungu. Hivyo, huyo mpagani,alikuwa wa kwanza katika WaMataifa kumshuhudia. Katika unyonge naunyenyekevu wa msalaba alivutwa kumtumaini Yesu, hakuhitaji ishara kubwaya Yesu kushuka msalabani au kutenda tendo la ajabu, la, aliweza kutambuakwamba alikuwa Mfalme kweli, kama mmoja wa wahalifu alivyomtambua(Lk.23:42). Tumeambiwa jinsi watu walivyoitika wakijipigapiga vifua (Lk.23:48).Hivyo watu wake wenyewe walimkataa huku wapagani wakimwamini! Walewaliojua machache walikuwa na imani kubwa.

k.40 Wanawake wengi walimhudumia Yesu alipokuwa Galilaya na wenginewalikuja pamoja naye mpaka Yerusalemu. Hao walikaa mbali na msalaba nakutazama mambo yote yaliyotendeka. Mama wa Yesu ambaye alikuwa amekaakaribu na msalaba pamoja na Mtume Yohana aliondolewa kabla ya mwisho(Yn.19:27). Hao wanawake walikuwa waaminifu mpaka mwisho,walimwonyesha Yesu upendo mpaka mwisho. Marko ametaja baadhi yao,Mariamu Magdalene, na Mariamu mwingine ambaye alikuwa mama wa Yakobomdogo na Yose; na Salome mkewe Zebedayo, mama wa Yohana na Yakobo.Hao walishuhudia yote. Walishuhudia Kifo Chake, ndipo Kuzikwa Kwake (k.47)baadaye Kufufuka Kwake (16:1-8). Hivyo, wale wasiofikiriwa kuwa wa maana,tena wasioruhusiwa kuwa mashahidi, walikuwa mashahidi wa mambo hayomakubwa.

15:42-47 Yesu alizikwa (Mt.27:57-61; Lk.23:50-56; Yn.19:38-42)k.42 ‘ikiisha kuwa jioni’ jioni iligawiwa katika sehemu mbili; kuanzia saa 9 jualilipoanza kupoa; ndipo saa 12 hadi saa 1. Wayahudi walihesabu siku kuanzasaa 1 (jioni) mpaka saa 12 kesho yake. Kwa hiyo ilikuwa Ijumaa Yesualipozikwa na Sabato ilianza usiku ule. Sabato ilikuwa Sabato kuu ya Pasaka.Haidhuru hakuna kukubaliana juu ya saa ya Yesu kusulibiwa ni hakika kwambaalizikwa jioni iliyotangulia Sabato. Ijumaa iliitwa Siku ya Maandalio, kwa sababuwatu waliandaa kwa ajili ya Sabato hiyo kuu. Kwa hiyo, muda uliotajwa hapo nibaada ya saa tisa na kabla ya saa 1, na katika muda huo shughuli za kumzikaYesu zilihitaji kufanyika. Lakini ni nani atakayemzika Yesu? Wanafunzi hawapo,wamekimbia kwa hofu ya Wayahudi wala hawakutokea tena mpaka baada yaYesu kuwa amekufa; Mtume Yohana alikuwa amemchukua Mariamu mamayeYesu mpaka nyumbani kwake, kwa hiyo, inaonekana kwamba hakuna mtu wakuangalia shughuli hizo. Pamoja na jambo hilo, kwa desturi ya Kiyahudi ilikuwalazima maiti ya wahalifu izikwe kabla ya Pasaka ili isiitie nchi unajisi(Kum.21:22-23). Lakini kwa Warumi, kufa hakuwa mwisho wa kumwaibishamtu, wahaini walipoteza haki zao zote, hata haki ya kuzikwa. Kwa kawaidawalitupwa ovyo na ikiwa jamaa walitaka kuzika wafu wao walihitaji hati yaruhusa kutoka hakimu. Pengine maiti iliachwa mtini ili ioze au iliwe na ndege auwanyama. Ila katika habari ya maziko ya Yesu tunaona kwamba siku zakudhiliwa kwake zilikuwa zimeisha, ametoa fidia ya dhambi katika kuyatimiza

MARKO282

mapenzi ya Baba yake, hakuna haja tena aibishwe zaidi. Kama Isayaalivyotabiri alikufa kati ya wahalifu na kuzikwa kati ya matajiri (Isa.53:9).Ilitokeaje iwe hivyo? kwanza, kwa sababu aliwahi kufa, kwa kawaida,waliosulibiwa walikufa polepole, ila Yesu alikufa haraka (kama angalikufawakati wa wenzake yawezekana wote wangalitupwa shimoni tu); pili, Yusufualitokea na kujitoa kwa kazi hiyo.

k.43 Huyu Yusufu aliyekuwa mtu wa Arimathaya hakutajwa hapo nyuma.Ameitwa mstahiki, mtu aliyejulikana kuwa mtu mwema. Alikuwa mjumbe waBaraza la Sanhedrin, lile lililomhukumu Yesu afe; hakukubaliana na shauri lao(Lk.23;51). Pia alikuwa mtu aliyetazamia kuja kwa Masihi, akishika tumaini lataifa lake. ‘akafanya ujasiri’ (k.43) jambo la kumwendea Pilato na kumwombaapewe maiti ya Yesu kwa maziko halikuwa jambo jepesi. Pilato hakupendaWayahudi wala hakutaka kuwaridhisha, alikuwa amekataa kubadili anwaniiliyoandikwa juu ya msalaba wa Yesu. Kwa hiyo kumwomba Pilato afanyeupendeleo wa namna hiyo ni kumwomba afanye jambo la pekee. Tena Yusufualitenda dhidi ya wenzake wa baraza ambao walitaka Yesu aibike upeo.

k.44-45 Pilato alistaajabu aliposikia kwamba Yesu ameisha kufa. Alitakakupata uhakika wake, hivyo, akamwita akida aliyekabili msalaba ili amhakikishiejambo hilo. Akida alijua kazi hiyo, alifahamu kama mtu amekufa au siyo.Tunajua kwamba askari walipomjia Yesu walimkuta ameishafariki dunia nabadala ya kuvunja mifupa na kuharakisha kufa, walimchoma mkuki (Yn.19:

Kaburi la mwamba

MARKO 283

31ku). Hayo yote yalitimiza mapenzi ya Mungu. Kanisa lilitilia mkazo jambo lakumzika Yesu kwa sababu wapinzani waliopinga habari ya Kufufuka Kwakewalisema kwamba hakufa kweli, ila katika baridi ya kaburi alivuvia; wenginewalisema kwamba wanawake walikosa mahali na kufika kwa kaburi lisilotumikabado. Akida na askari walijua kwa hakika kwamba Yesu alikuwa amekufa kweli(1 Kor.13:3ku).

k.46 Yusufu alikwenda msalabani na kuushusha mwili wa Yesu na kumfungiasanda ya kitani, na kumweka katika kaburi lake mwenyewe, jipya, lisilotumikabado, lililochongwa mwambani katika bustani karibu na Golgotha (Mt.27:60;Lk.23:53; Yn.19:41). Alikuwa na muda wa kama masaa mawili tu ya kufanyahayo yote. Pengine alisaidiwa na watumishi wake na Nikodemo alikujakumsaidia (Yn.19:39). Alizikwa kwa mila za Kiyahudi kwa heshima kubwa. Jiwelilivingirishwa kuzuia waibaji na wanyama. Mwili wake ulihifadhiwa na kuwekwavizuri na kulindwa, tayari kwa siku ya Kufufuka Kwake. Katika hayo yote twaonamapenzi ya Mungu kutendeka, aliruhusu watu wafanye walivyotaka, kama nimema au kama ni mabaya. Yusufu na Nikodemo waliokuwa wafuasi wa siriwalijitokeza wazi na kuandaa mambo yawe tayari kwa siku ya tatu, mamboambayo hata wao hawakuwa na habari juu ya tukio kuu litakalotendeka sikuhiyo. Mungu peke yake Ndiye aliyejua yatakayotokea katika siku hiyo kwasababu ni Yeye Mwenyewe peke yake atakayelitenda. Ni hakika kwambawahusika hawakutazamia kwamba Yesu atafufuka katika siku tatu, maanaYesu amevikwa sanda, jiwe limewekwa kaburini, na wanawake wamekwendakuandaa manukato. Kwa watu ni ‘mwisho’.

k.47 Wanawake wawili wametajwa ambao walitajwa katika k.40 nao walikuwamashahidi wa mahali alipowekwa. Wapinzani wamesema kwamba walikosa nakwenda kaburi lingine lililokuwa tupu (wakuu na matajiri walizoea kuchongamakuburi yao mapema) lakini sivyo ilivyokuwa! walikuwa wamepatazama nakuhakikisha mahali alipowekwa. Ni vigumu kufikiri kwamba wangalikosa katikajambo hilo la maana sana kwao, kwa sababu walikusudia baada ya Sabato kujapale na kumhudumia kwa mara ya mwisho.

16:1-8Yesu alifufuka kutoka wafu (Mt.28:1-8; Lk.24:1-12; Yn.20:1-10 (1Kor.15:1-8))k.1-2 Baada ya saa 12 Sabato ilikwisha na Jumapili ilianza ambayo ni siku yatatu baada ya Yesu kusulibiwa. Huenda wanawake walikuwa wameishakununua manukato tayari. Luka amesema walipumzika siku ya Pasaka(Lk.23:56) au pengine walinunua mara baada ya Sabato kwisha. Walikuwawale waliotajwa 15:40 pamoja na Yoana na wengine (Lk.24:10). Siku yakwanza ya juma kwa Wayahudi ni sawa na Jumapili yetu. Siku ya sabatoilikuwa siku ya saba. Yesu alifufuka siku iliyofuata Sabato, yaani siku yakwanza ya juma ambayo kwa hesabu zetu ni Jumapili. Ni jambo mojalinaloushuhudia ukweli wa Ufufuo wa Yesu, waumini wote wa kwanza walikuwaWayahudi waliozoea kumwabudu Mungu siku ya saba ya juma, Jumamosi,

MARKO284

yaani Sabato. Wasingalibadili siku yao ya kumwabudu Mungu bila sababu kuuya tukio la Yesu kufufuka, tena walifanya bila kuagizwa na Yesu. Kila Jumapiliwalifanya kumbukumbu lake.

k.3-4 Njiani walikumbuka lile jiwe lililowekwa na kufikiri ni nani atakayewasaidiakulivingirisha, maana ilikuwa mapema sana na watu hawakuwepo. (Wanafunziwa kiume wako wapi?). Tena kuondoa jiwe kwenye mfuo wake kulikuwavigumu kuliko kuliweka. Tena Mathayo ametaja habari ya jiwe kutiwa muhuri nawalinzi kuwekwa (Mt.27:62ku). Pengine hawakujua habari hizo zilizotajwa naMathayo, maana Ijumaa jioni walitazama mahali Yesu alipowekwa nakuondoka. Walipokuwa wakizungumza shida hiyo walitazama mbele na kuonakwamba jiwe limeisha kuvingirishwa, kama ni neno lililowashtua, maana Markoametaja jiwe lilikuwa kubwa mno. Jiwe liliondolewa ili wanawake, na baadaye,Petro na Yohana, waingie mle ndani na kuhakikisha kwamba Yesu hakuwemo.Halikuondolewa kwa kumsaidia Yesu atoke (Mt.28;2ku). Twaona uaminifu wahao wanawake, walikuwa wa mwisho karibu na msalaba, na kwa mbaliwalipatazama mahali pa kaburi ndipo walikuwa wa kwanza kufika kaburini,mapema ilivyowezekana, ili wamhudumie Yesu kwa mara ya mwisho. Ni dhahirikwamba walitazamia wataikuta maiti ya Yesu mle ndani. Kuondolewa kwa jiwekulikuwa ishara ya kwanza ya tukio la ufufuo.

k.5 Wanawake waliingia mle ndani ya kaburi na kumkuta kijana ameketiupande wa kuume, hali amevaa vazi jeupe. Mathayo ametaja malaika na Lukaametaja malaika wawili. Kwa jinsi alivyowapa ujumbe maalumu huyo kijanaalifikiriwa kuwa malaika. Wanawake walistaajabu, hawakutazamia kwambawatamkuta yeyote aliye hai ndani.

k.6 Kijana/malaika akawaambia wasistaajabu. Alimtaja Yesu kuwa YesuMnazareti, aliyesulibiwa. Ukumbusho wa ubinadamu wake na ukweli waKuuawa Kwake. Ni yule waliyemfahamu na kufuatana naye kutoka Galilayaambaye siku mbili zilizotangulia walimwona ametundikwa msalabani. Ndipoaliwaambia kwamba ‘amefufuka’ hakusema lini wala kwa jinsi gani ila alitajatukio lenyewe tu. Ijapokuwa Yesu alikuwa ametaja Kufa na Kufufuka Kwakehaikuwa wazi kwao ni nini ambayo imetokea mpaka malaika alipowaelezea.Kwa mawazo yao mwili ungaliweza kuondolewa tu na kuwekwa mahalipengine, ila habari njema ni kwamba ‘amefufuka’. Halafu malaika akawaitawapatazame mahali alipolazwa. Yawezekana vitambaa vilikuwapo (Yn.20:5ku)pengine ilikuwa kazi ya malaika kuvilinda, ushuhuda kwa ajili ya Petro naYohana waliokuja mbio baada ya kuambiwa na Mariamu Magdalene yakwamba mwili wake haumo. Kumbe walikuja wakitafuta mfu, wakaambiwa mfuyu hai!!! Katika Injili yake Marko amesisitiza uzito wa wanafunzi wake na hapotena twaona kwamba ameonyesha uzito wa hao wanawake wasiotambua kwaupesi kwamba Yesu amefufuka walipoona kaburi lilikuwa wazi mpaka malaikaalipotamka wazi ‘amefufuka’.

MARKO 285

k.7 Kisha malaika akawaambia wanawake waende na kuwaambia wanafunzi,akimtaja Petro hasa, ya kwamba Yesu amekwenda mbele yao mpaka Galilaya,na huko ndiko watakakokutana naye, sawa na jinsi alivyowaambia, wakatialipotabiri kwamba Petro atamkana na wote watamwacha (14:28). Ni chanzocha mambo mapya, ya kale yamepita, kumkana na kumwachakumesamehewa, kwa hiyo, malaika aliwaelekeza mawazo yao, si kwa kaburitupu tu, wala kwa mwili kutokuwepo, bali kwa tazamio la kuonana na Yesu aliyehai baada ya kufa. Kaburi tupu lilikuwa ishara ya Yesu kukutana nao tena.Wanawake walipewa wajibu wa kutoa ushuhuda; kwa sheria ya Kiyahudiwanawake hawakukubalika kuwa mashahidi, hata wanafunzi waliona shidakatika kuupokea ushuhuda wao (Lk.24:11, 22-24, Mk.16:11). ‘huku mtamwona’Kwa Marko neno la Yesu lilikuwa muhimu kuliko mambo yote, Yesu alikuwaamesema atakutana nao tena huko Galilaya, na ndivyo itakavyokuwa.

k.8 Wanawake wakatoka nje na kukimbia. Walitetemeka na kushangaa nanjiani hawakumwambia mtu yeyote habari hizo kwa ajili ya kuogopa. Hatujui nihofu gani na ya nini? twasoma wanafunzi watatu waliogopa walipomwona Yesuamegeuka sura pale mlimani (9:6). Huenda hofu yao ni itikio lao kwa tendo kuula Mungu katika kumfufua Yesu kutoka wafu wakiona jambo hilo ni kubwakupita uwezo wao wa kushika maana yake mara moja. Kama ambavyotumeona mara nyingi katika Injili hiyo Marko amesisitiza umuhimu wa imani.Wakati wote Mungu hutenda mambo katika hali ya kuwaachia watu haja nanafasi ya kuamini. Tendo la Ufufuo lilikuwa la kweli kabisa, hata hivyo, mpakahapo Marko hajataja bado habari ya mtu yeyote kumwona Yesu Mwenyewe.Wakienda Galilaya watamwona huko (Ebr.11:1).

Maelezo kuhusu 16:9-20: Wataalamu wengi huafikiana katika kusema kwambasehemu hiyo haikuandikwa na Marko. Sababu kubwa ya kwanza ni kwambasehemu hiyo haionekani katika nakala kubwa za zamani zinazotegemewa. Ilaipo katika nakala nyingine zisizotegemewa. Sababu nyingine ni kwamba lughana mtindo wa sehemu hiyo hutofautiana na hali ya Injili yenyewe. Sehemu hiyoni kama ‘baridi’ haikolei, haisisimui kama sehemu yote iliyotangulia. Kuna haliya kukatika kwa mawazo kati ya kifungu cha nane na cha tisa. MariamuMagdalene aliyetajwa katika k.1 ametajwa kama anatajwa kwa mara yakwanza.

Kwa jinsi Marko alivyotaja ujumbe wa malaika kuwa Yesu atakutana nawanafunzi huko Galilaya, katika k.9-20 hamna habari hiyo. Mara mbili ametajaYerusalemu; Yesu alimtokea Mariamu Magdalene (Yn.20:14-18) na wawiliwaliotoka Yerusalemu kwenda Emau (Lk.24:13-35). Aliwatokea wanafunzi bilakutaja wapi (Lk.24:36-38). Wakati huo aliwapa utume wa kwenda ulimwengunina kuihubiri Injili (Mt.28:16ku). Ni kama Marko amejumlisha habari hizo bilakuziandika jinsi zilivyotokea. Pale kaburini malaika aliwatazamisha kukutana naYesu huko Galilaya, lakini habari hiyo haisumiliwi katika sehemu hiyo.

MARKO286

Kwa hiyo, tukijiuliza: Je! Marko aliandika au hakuandika 16:9-20 jibu la wengi nihakuiandika.

Basi, ikiwa Marko hakuiandika Je! alikusudia au hakukusudia kufunga Injili yakekatika k.8? Wako wanaofikiri kwamba alikusudia kuifunga hapo akiwaachiawatu kama hewani, kwa shabaha ya kuwaachia nafasi ya kupima mambo hayona ushuhuda wa hao wanawake ndipo waamue wenyewe kuamini aukutokuamini. Hivyo alifunga na habari ya wanawake kutetemeka na kushangaana kunyamaza kimya kwa hofu. Mwisho wa ajabu.

Wako wasemao kwamba Marko hakumaliza Injili yake hapo penye k.8 ilamwisho wake umepotea, kipande cha mafunjo kiliondoka au kuharibika na kwasababu hiyo Kanisa liliona vema liandike nyongezo ya kuifunga Injili vizuri kwakutumia habari kutoka Injili zingine na kufanya hitimisho ya habari za Yesukutokea watu mbalimbali.

Ikiwa kipande cha karatasi hakikupotea yawezekana Marko alishindwakumaliza ama kwa kuugua au kupatwa na madhara.

Kama Marko alimaliza Injili katika k.8 inaonekana alifikiri kwamba maneno yakijana kwa wanawake yalitosha. Aliondoa mawazo yao wasifikiri zaidi habari yakaburi kuwa wazi na tupu bali wawe na hamu ya kukutana na Yesu Hai hukoGalilaya, kwa sababu pale watamwona. Katika Injili nzima tabia ya Markoilikuwa kujizuia asielekeze watu kufikiri kwamba Mungu hujifunua kwa nguvukwa ulimwengu kama kuulazimisha ulimwengu umtambue kwa njia ya nguvuzake. Mungu alikuwa amejificha katika huduma ya Yesu, na mwenye imanindiye anayemtambua. Kwa Marko neno la Yesu ni imara na thabiti na lakuaminika; mara tatu Yesu alitamka wazi atakufa ndipo kufufuka (8:31; 9:31;10:34). Neno lake latosha (13:23). Hivyo, Marko katika k.1-8 amesema yotealiyotaka kusema.

Kwa hiyo, kwa mawazo hayo msomaji aweza kutafakari neno hilo na kuchaguamaelezo anayopenda, ila wote hukubaliana kwamba ni vigumu kujua kwahakika ni nini iliyo kweli hasa.

16:9-11Kumtokea Mariamu Magdalene (Mt.28:9,10; Yn.20:1-18 na hasa 11-18)Habari hii imetajwa ijapokuwa imeisha kudokezewa (k.1,6). Habari ni fupi sikama ilivyoandikwa kwa kirefu katika Yn.20:14-18. Marko ametaja jambolililomsababisha Mariamu Magdalene ampende Yesu sana, alitolewa pepo saba(Lk.8:2). Kama ambavyo ameonyesha katika Injili yake nzima Markoamesisitiza kutokuamini kwa wanafunzi wake na ndivyo ilivyokuwa Mariamualipowaambia wanafunzi kwamba amemwona Yesu. Walikuwa wangali wakiliana kuomboleza.

MARKO 287

16:12-13 Kuwatokea wawili waliosafiri (Lk.24:13-35)Hapo tena habari imetajwa kwa ufupi tofauti na Luka (Lk.24:13-35). Yesualiwatokea hao wawili kama msafiri mwenzao; kwa Mariamu alionekana kamamtunza bustani. "sura nyingine" Yesu alikuwa na uwezo mpya baada yaKufufuka Kwake. Tofauti moja na Luka, Marko ametaja jinsi ambavyo haowawili waliporudi kwa wanafunzi, wanafunzi hawakuamini kwambawamemwona Yesu (Lk.24:33). Huenda baadhi waliamini na baadhihawakuamini (Mt.28:17; Lk.24:34-41). Hapo tena, Marko amesisitizakutokuamini kwa wanafunzi walipoambiwa kwamba Yesu yu hai.

16:14-18 Kuwatokea wanafunzi (Lk.24:36-43)k.14 Yesu alipowatokea wale kumi na mmoja (wamejumlisha kwa lugha hiyo,ila tusifikiri kwamba kila mara wote walikuwepo pamoja) aliwakemea kwakutokuamini kwao na kwa jinsi walivyokataa kuamini. Kwa nini Yesualiwakemea? Kwa sababu walikuwa wamejulishwa na wanawake, ndipo nawale wasafiri wawili, hata hivyo walikuwa wazito wa kuamini. Jambo hilolinatuonyesha jinsi ambavyo hawakuwa tayari kwa tukio hilo ingawa Yesualikuwa amewaambia habari zake mara kwa mara na kila mara alipotaja KufaKwake alitaja Kufufuka Kwake pia. Kwa hiyo, iwapo tumezoea kumlaumuTomaso kwa kutokuamini kwake, yeye hakuwa tofauti na wenzake.

k.15 (Ling.Mt.28:16-20) Hata hivyo, Yesu alikuwa na tumaini kubwa juu yaokwamba watajipa moyo na kutimiza lengo la kuwachagua kuwa mashahidiwake, watangazaji wa habari njema ya msamaha wa dhambi na uzima wamilele. Ujumbe wao ni kwa ulimwengu mzima, waende kotekote na kuihubiriInjili. Kama Baba alivyomtuma Yeye, Yeye naye anawatuma (Yn.20:21).

k.16 Mkazo ni juu ya kuamini, mtu akiamini ataokoka na kwa kawaidaatashuhudia kuamini kwake katika ubatizo. Mtu asiyeamini, haidhuruatabatizwa au sivyo, atahukumiwa. Jambo kubwa ni imani si ubatizo.

k.17-18 Marko hakutaja habari za wao kupewa kipawa cha Roho Mtakatifu ilaalitaja mambo watakayofanya kwa jina lake. Pamoja na kuhubiri watajaliwauwezo wa kufanya ishara mbalimbali. Hapo nyuma alipowatuma walitoa pepona kuwaponya wagonjwa. Ishara nyingine ni kusema kwa lugha mpya, najambo hilo lilitokea Siku ya Pentekoste (Mdo.2:4). Nyingine ni kushika nyokabila madhara (Mdo.28:3-5). Juu ya kunywa kitu cha kufisha kama sumu bilakudhuriwa, hakuna mfano wake katika Agano Jipya; wapelekwa hushuhudiakutokea kwa jambo hilo. Ni kama jumlisho ya mambo yaliyofanyika na Kanisaambayo habari zake zimeandikwa katika Matendo ya Mitume.

Je! uwezo wa kufanya ishara ulikuwa hasa kwa ajili yao na kwa wakati waowalipokwenda ulimwenguni kwa mara ya kwanza na kuhubiri Injili? Baadhi yawatu hufikiri kwamba walijaliwa nguvu za kipekee wakati ule ili wasaidiwekusimamisha Kanisa katika ulimwengu na kwa shabaha ya kuwathibitishia watu

MARKO288

ukweli wa ujumbe wao. Baadaye kilipatikana kitu ambacho wa kwanzahawakuwa nacho, yaani Andiko la Agano Jipya ambalo huwasaidia watu nakuwahakikishia ukweli wa ujumbe wa Injili. Hata hivyo, wako wengine ambaohufikiri kwamba uwezo wa ishara upo mpaka leo na ni kwa sababu ya upungufuwa imani Kanisa linakosa kuamini kwamba ni mapenzi ya Mungu isharazifanyike.

Kwa hiyo, katika sehemu hiyo ya k.9-18 neno linalosisitizwa ni lile la Injili nzima,la kuamini na kutokuamini. Wanafunzi hawakuamini ripoti ya Mariamu (k.11);wanafunzi hawakuamini ripoti ya wawili waliokwenda Emau (k.13); Yesualiwakemea wanafunzi kwa kutokuamini kwao (k.14). Watakapohubiri Injili niwenye kuamini na kubatizwa ambao wataokolewa; na wasioamini Injili,watahukumiwa. Wenye kuamini watapewa uwezo wa Mungu kufanya ishara.Ndipo mwishowe wanafunzi wanaamini na kumtii Bwana wao na kwendakuhubiri na kupata thibitisho waliloahidiwa na Mungu kufanya ishara kwa njiayao.

16:19-20 Yesu kupaa mbinguni (Lk.24:50ku; Mdo.1:6-8)k.19 Marko, kama Luka, amemaliza Injili kwa kutaja Kupaa kwa Yesu na KuketiKwake mkono wa kuume wa Mungu, mahali pa heshima ya kushiriki uwezo namamlaka ya Baba yake. Kwa upande mmoja Yesu alikuwa amemaliza kazizake. Ila kwa upande mwingine bado angali anaendelea kufanya kazi kwa njiaya Kanisa lake. Yesu hufanya kazi katika wale wanaolitii agizo lake nayehuithibitisha huduma yao. Kwa Kupaa Kwake Yesu aliachia nafasi kwa hudumaya watumishi wake kuanza. Badala ya kuwa mbali nao alikuwa karibu nao nakuwawezesha. Sehemu hiyo inaelekeza mawazo kwa ushindi wa Eliyaaliyepanda juu (2 Waf.2:11) na kwa maneno ya Zaburi 110:1, Zaburi iliyotumiwana Yesu kabla ya Kufa Kwake alipomjibu Kuhani Mkuu, Zaburi iliyomhusuMasihi. Yesu alipata ushindi, na kuadhimishwa mno huko juu.

Machache kuhusu Ufufuo wa Yesu:Upo ushuhuda wa nguvu wa kuuthibitisha Ufufuo wa Yesu:

1. Kaburi lilikuwa tupu

2. Hakuna aliyeuleta mwili/maiti yake

3. Rafiki zake wasingeuiba (wangefanya nini nao?) walikwenda kaburiniwakitaka kuupaka mafuta.

4. Adui zake wasingeuiba (walitamani sana kuupata ili wakanushe kabisauvumi wa Kufufuka Kwake)

5. Kutokea kwa Kanisa na jamii ya Wakristo waliovumilia mateso na kifokwa ajili ya Neno hilo la Ufufuo. Iliwezekanaje waupate umoja nanguvu na wote kujitia katika kutangaza habari kama zilikuwa zauongo? Wateswe na kuuawa kwa neno ambalo walijua ni uongo?

MARKO 289

6. Kutokea kwa Jumapili, Wanafunzi wa kwanza walikuwa Wayahudiwalioshikilia sana Sabato kwa ibada zao. Ni nini iliyowafanya waibadilisiku yao ya ibada? Kwa sababu walikumbuka Kufufuka kwa Bwanawao.

7. Kutokea kwa Andiko la Agano Jipya ambalo jambo kuu linalosisitizwani Ufufuo wa Yesu, kama Paulo alivyosema kumwamini Kristo ni burenao wamekuwa mashahidi wa uongo wa Mungu, kama Kristohakufufuka (1 Kor.15:14ku). Paulo alidai kwamba alikuwa amekutanana Yesu Hai miaka kadhaa baada ya Yesu Kupaa, alipokwendaDameski (Mdo.9:1ku) na alijenga maisha yake yote juu ya jambo hilo.