trade facility reference on the context

16
https://www.dullonet.com/?p=16676 IMEELEZWA kuwa asilimia 65 ya mfumko wa bei katika nchi za Afrika Mashariki unasababishwa na kupanda kwa bei za vyakula.Mfumko huo pia unachangiwa na vizuizi vilivyopo mipakani vinavyojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwatoza fedha nyingi wafanyabiashara ambao hulipiza kwa walaji na watumiaji wa mwisho. Hayo yalielezwa na Balozi Dk Diodorus Kamala alipokuwa akifungua mkutano wa Bodi ya Taasisi ya Sera ya Afrika Mashariki (EPF), uliofanyika mkoani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita. Lengo la mkutano huo ni kujadili mpango mkakati wa miaka mitano na kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa ipasavyo hasa mipango ambayo inaonekana kutekelezwa kwa urahisi itekelezwe hasa kiuchumi. Alisema kuwa kwa sasa upande wa uzalishaji wa vyakula katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mdogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya walaji. Alisema kuwa suala lingine linalosababisha kupanda kwa bei za vyakula ni kutokana na vizuizi vilivyopo mipakani ambavyo vinajihusisha na vitendo vya rushwa hali ambayo inawafanya wafanyabiashara kupandisha bei kwa kutaka kurudisha fedha wanazotoa katika vizuizi hivyo. “Katika mkutano huu nimeshauri kwamba hakuna sababu za kuwa na vizuizi kila mahali na hatuhitaji fedha za kigeni kumaliza tatizo hili maana mwisho wa siku wanaoumia ni walaji wa mwisho ambao ni wananchi wa hali ya chini,” alisema Balozi Kamala. Alisema kuwa kwa sasa kinachotakiwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumaliza suala la kuwa na kituo kimoja cha ushuru wa forodha na kuondoa vikwazo vya kiuchumi katika nchi hizo. Balozi Kamala alisema kuwa baadhi ya viongozi wanakiuka makubaliano ya kodi ambazo zimekubaliwa kwa pamoja na viongozi wa nchi zote lakini matokeo yake wanaamua wao wenyewe na kutoza kodi tofauti na makubaliano hali inayosababisha mfumko wa bei.

Upload: jackson-loceryan

Post on 08-Nov-2015

277 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

reference on trade facility.

TRANSCRIPT

https://www.dullonet.com/?p=16676

IMEELEZWA kuwa asilimia 65 ya mfumko wa bei katika nchi za Afrika Mashariki unasababishwa na kupanda kwa bei za vyakula.Mfumko huo pia unachangiwa na vizuizi vilivyopo mipakani vinavyojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwatoza fedha nyingi wafanyabiashara ambao hulipiza kwa walaji na watumiaji wa mwisho.

Hayo yalielezwa na Balozi Dk Diodorus Kamala alipokuwa akifungua mkutano wa Bodi ya Taasisi ya Sera ya Afrika Mashariki (EPF), uliofanyika mkoani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita.

Lengo la mkutano huo ni kujadili mpango mkakati wa miaka mitano na kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa ipasavyo hasa mipango ambayo inaonekana kutekelezwa kwa urahisi itekelezwe hasa kiuchumi.

Alisema kuwa kwa sasa upande wa uzalishaji wa vyakula katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mdogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya walaji.

Alisema kuwa suala lingine linalosababisha kupanda kwa bei za vyakula ni kutokana na vizuizi vilivyopo mipakani ambavyo vinajihusisha na vitendo vya rushwa hali ambayo inawafanya wafanyabiashara kupandisha bei kwa kutaka kurudisha fedha wanazotoa katika vizuizi hivyo.

Katika mkutano huu nimeshauri kwamba hakuna sababu za kuwa na vizuizi kila mahali na hatuhitaji fedha za kigeni kumaliza tatizo hili maana mwisho wa siku wanaoumia ni walaji wa mwisho ambao ni wananchi wa hali ya chini, alisema Balozi Kamala.

Alisema kuwa kwa sasa kinachotakiwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumaliza suala la kuwa na kituo kimoja cha ushuru wa forodha na kuondoa vikwazo vya kiuchumi katika nchi hizo.

Balozi Kamala alisema kuwa baadhi ya viongozi wanakiuka makubaliano ya kodi ambazo zimekubaliwa kwa pamoja na viongozi wa nchi zote lakini matokeo yake wanaamua wao wenyewe na kutoza kodi tofauti na makubaliano hali inayosababisha mfumko wa bei.

Alizitaka nchi hizo kuanza mikakati ya kujitegemea katika bajeti yao ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea wafadhili na kwamba siku wafadhili hao wakiamua kujiondoa mipango yote ya Jumuiya hiyo itakufa.

Kwa kweli changamoto ni nyingi lakini pamoja na mfumko wa bei za vyakula kuna suala lingine ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa makini ambalo ni kuanzisha mchakato wa kujitegemea katika bajeti vinginevyo wafadhili wakiamua kuondoka hakuna mipango itakayoendelea, alisema Balozi Kamala

http://www.majira.co.tz/index.php?page=read_more&name=news&id=617

Kigoda: Rushwa mipakani chanzo uchumi kushuka

Monday, December 16 2013, 11 : 2

Waziri wa Viwanda na Biashara,Dkt.Abdallah Kigoda amesema kuna tatizo kubwa la rushwa mipakani hivyo kuwa kikwazo cha biashara hali ambayo inachangia kushuka kwa uchumi nchini.

Dkt.Kigoda aliyasema hayo jana jijini DaresSalaam wakati wa mkutano wa kujadili kero na vikwazo vya biashara katika kukuza uchumi.

Alisema kuwa uchumi wa nchi unategemea zaidi uzalishaji wa viwanda na biashara hivyo wakati wa kuwa taifa la kushangaa maendeleo ya nchi jirani umekwisha ni muhimu kuondoa vikwazo ili kupiga hatua katika maendeleo.

"Tuacheni kuwa taifa la kushangaa maendeleo ya wenzetu hawafanikiwi kwa miujiza ni kwa kujipanga na kutekeleza sera na mikakati ya maendeleo, tuondoe vikwazo hasa vya rushwa mipakani tufanye kazi kwa timu moja kuondoa vizuizi ili tupige hatua," alisema.

Aliwataka wadau hao wa biashara kuelewa kuwa ndiyo chachu ya uzalishaji hivyo jukumu la kukuza uchumi walilonalo ni kubwa ni wajibu kutoa elimu ya kutosha kwa wawekezaji na wajasiriamali ili kuondoa changamoto.

Aidha pia alihimiza sekta binafsi kuelewa kuwa ndiyo nguzo ya maendeleo katika kuongeza kiwango cha kukuza uchumi wa nchi hivyo ni muhimu kuacha fikra za kukumbatia wawekezaji wakubwa pekee na kuacha wajasiriamali wadogo wadogo kwani hao ndio wazalishaji wanaofahamu sehemu za vitega uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa (TAN TRADE) Jacqueline Maleko alisema mkutano huo pamoja na kujadili changamoto wamewezesha maazimio ya kuhakikisha sekta muhimu katika usafirishaji biashara zinakaa pamoja na wadau wengine ili kuondoa vikwazo wanavyokabiliana navyo ili kuwezesha biashara wezeshi kwa jamii.

http://www.mwananchi.co.tz/Makala/TRA-haina-takwimu-za-mapato-yanayopotea/-/1597592/2054754/-/ehr439/-/index.html

Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 12:10 PM

Wiki iliyopita Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitiliya alizungumzia kodi ya ardhi, vyanzo vya kodi na changamoto katika mahojiano na mwandishi wa jarida la biashara na uchumi, John Stephen.

Leo tutaangalia utaratibu wa kutoza kodi, kwa nini wafanyabiashara wadogo halipi kodi na pamoja na mambo mengine.Utaratibu upi unatumika kutoza kodi kutokana na pato la mtu kwa siku, mwezi hadi mwaka?

Utaratibu unaotumika umegawanyika katika malipo ya kodi umegawanyika sehemu mbili. Kwanza wafanyabiashara wasiotunza kumbukumbu (mahesabu) kabisa za gharama na mauzo ya biashara zao, na pili, wafanyabiashara wenye kumbukumbu kwa kiasi fulani za gharama za mauzo yao.

Wafanyabiashara wasiokuwa na kumbukumbu wanatozwa kodi kwa kutumia mauzo yao ambayo yanawekewa viwango maalum (fixed rates), na wenye kumbukumbu kwa kiasi fulani hutozwa kodi kwa kutumia asilimia ya mauzo yao.

Kwa nini hamuwatozi kodi wafanyabiashara wadogo?

Tafiti zilizopo zinabainisha kwamba wafanyabiashara wadogo hawatunzi kumbukumbu za biashara na hivyo wanashindwa kulipa kodi.

Kutokana na hali hiyo Serikali inafanya tafiti mbalimbali za kubaini viwango vya mauzo ya wafanyabiashara wadogo wadogo wasiotunza kumbukumbu na kukokotoa mapato yao ili walipe kodi.

Je ni kiasi gani cha fedha kinapotea kutokana na wafanyabiashara kukwepa kodi wakati wa kuingiza bidhaa zao nchini kutoka nje ya nchi?

Kuhusu suala la maeneo ya mipakani, mamlaka haina takwimu au kumbukumbu za kiasi cha fedha kinachopotea kwa kuwa wafanyabiashara wanaokwepa kodi wanafanya kwa usiri mkubwa.

Suala la kukwepa kodi ni kosa la jinai kisheria, hivyo hakuna takwimu ndani ya mamlaka ya vitendo vya kukwepa kodi.

TRA imekuwa ikilaumiwa kwa muda mrefu kwa kushindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato. Je, nini msimamo wako kuhusu hili?

Mamlaka imekuwa ikitoa mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato kila mwaka kama sheria iliyoanzisha TRA inavyotamka. Sehemu kubwa ya mapendekezo yamekuwa yakikubalika na kujumuishwa kwenye maboresho ya mfumo wa kodi na hivyo kuchangia katika uboreshaji wa mapato ya serikali.

http://www.raiamwema.co.tz/wafanyabiashara-tunduma-wakimbilia-zambia

Felix Mwakyembe Mbeya Toleo la 245 27 Jun 2012SERIKALI inakabiliwa na uhaba wa fedha, bungeni kunawaka moto bajeti kutegemea zaidi wanywaji, lakini wakati huo huo wakubwa wengine serikalini wanagawa baadhi ya vyanzo vya mapato nchi jirani.

Ukosefu wa ubunifu katika kuibua vyanzo vipya vya mapato vinaifanya Serikali kila mwaka kukamua wanywaji pombe, soda na wavuta sigara kutokana na utamaduni wake wa kila mwaka kuongeza kodi kwenye mahitaji hayo pamoja na kuwakamua wafanyakazi kwa kuwaongezea kodi kwenye mapato yao ya mwezi.

Lakini hali ikiwa hivyo kwa wanywaji na wafanyakazi, kwa upande wa wafanyabiashara ni tofauti, wao wanayo nafasi ya kukwepa na wakati mwingine husaidiwa na maofisa wa Serikali kukwepa kodi.

Biashara za ndani ikiwemo zile za maduka makubwa na madogo, biashara ndogo ndogo kwa ajili ya bidhaa za viwandani, na biashara za mazao ya kilimo, ni sehemu muhimu katika kuipatia mapato Serikali iwapo kutakuwa na umakini, uadilifu na nidhamu miongoni mwa watumishi waliokabidhiwa dhamana ya ukusanyaji mapato nchini.

Hata hivyo, ushahidi unaonyesha kuwapo udhaifu mkubwa katika kusimamia biashara hizo ili ziweze kuchangia katika pato la Taifa badala ya kutegemea zaidi kodi katika vinywaji, sigara na wafanyakazi.

Miongoni mwa maeneo yenye udhaifu huo ni pamoja na yale ya mipakani ambapo kutokana na jiografia ya nchi, Tanzania ina nafasi kubwa zaidi kunufaika na biashara za mipakani, kwani kwa namna moja ama nyingine inaungana na nchi zote za Afrika Mashariki na Kati pamoja na zile za Kusini.

Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya ni miongoni mwa mipaka yenye biashara kubwa kutokana na eneo lake kuwa ndilo lango kuu la nchi kuelekea nchi za Afrika Kati na Kusini, hivyo ingetegemewa mamlaka zinazohusika kujenga mazingira mazuri ya kuvutia wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya mapato zaidi.

Katika hali ya kushangaza, mamlaka hizo, hususani ile ya Halmashauri ya Mji huo wa Tunduma, inaona fahali wafanyabiashara hao kuhamia nchi jirani ya Zambia kuendelea na biashara zao kule badala ya upande wa Tanzania ambako ndiko kwenye bidhaa zinazohitajika kwenye nchi hizo jirani, nayo kujikusanyia mapato ya moja kwa moja toka kwa wafanyabiashara hao.

Wafanyabiashara wahamishiwa Zambia

Uchunguzi wa Raia Mwema wa takribani majuma mawili sasa umebaini kuwapo kwa wimbi kubwa la wafanyabiashara wa Kitanzania mpakani hapo kuhamia upande wa pili wa mpaka huo, nchini Zambia, wakikimbia mazingira magumu ya kibiashara nchini.

Hadi tunaenda mitamboni kulikuwa na taarifa za wafanyabiashara zaidi ya 3,500 kutoka upande wa Tanzania waliokimbilia upande wa Zambia kuendelea na biashara baada ya kuchoshwa na mazingira kandamizi ya kibiashara nchini.

Hawa ni wafanyabiashara wakubwa na wa kati, lakini hivi karibuni hata wafanyabiashara wadogo, maarufu kwa machinga, wametakiwa na Halmashauri ya Mji Tunduma waondoke eneo la mpakani zilipo ofisi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na zile za Uhamiaji, na badala yake kuelekezwa waende upande wa Zambia eneo la Kituo cha TAZARA nchini humo.

Wamachinga wote mnatakiwa kufanya biashara eneo mlilotengewa na Halmashauri ya Nakonde ambalo ni TAZARA Station upande wa Zambia. Hamruhusiwi kupita mitaani. Kwa maulizo fika Ofisi za Halmashauri ya Mji Tunduma, linasomeka tangazo hilo lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma.

Wakati uongozi wa Halmashauri hiyo ya Mji Tunduma ikiwaelekeza wamachinga kuhamia eneo la Kituo cha TAZARA nchini Zambia, kwa upande wa huku nchini imewazuia wafanyabiashara hao wadogo kuendelea na biashara zao kwenye eneo kama hilo la Kituo cha TAZARA, upande wa Tanzania kwa madai kuwa ni eneo la mpaka (buffer zone).

Eneo hilo la Kituo cha TAZARA upande wa Tanzania linapendelewa zaidi na wafanyabiashara wadogo kutokana na mahali lilipo, kwani linazikutanisha nchi tatu, Tanzania, Malawi na Zambia, hivyo ni rahisi kwa wanunuzi kutoka nchi hizo mbili kuingia nchini kwa shughuli zao za kibiashara kwa urahisi zaidi.

Hivi sasa eneo hilo la TAZARA upande wa Tanzania liko kwenye mgogoro kati ya wananchi waliokuwa wakiendesha shughuli zao pale na Halmashauri ya Mji Tunduma, na tayari kesi ipo mahakama ya ardhi jijini Mbeya.

Ni eneo la mpaka buffer zone kila kitu lazima kipangwe kwa utaratibu, wapo wanaojenga kesi zipo mahakama ya ardhi, kila mji unakuwa na plan, anasema Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduma, Idan Mwashiga, katika mahojiano yake kwa simu na mwandishi wa makala haya.

Hata hivyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi inakuwaje eneo lililopangwa kwa makazi kama alivyodai likajengwa majengo ya kudumu ya biashara, Kaimu Mkurugenzi huyo alikwepa na kudai anaingia kwenye kikao akisema: Samahani bwana ngoja niingine kwenye kikao.

Pamoja na kudai kesi ipo mahakamani kwa wale waliojenga, ushahidi kutoka eneo hilo unabainisha kuwa iliyoko mahakamani ni kesi dhidi ya wafanyabiashara wadogo, kwani wenye nguvu ya fedha wanaendelea na ujenzi wa majengo ya biashara kwenye eneo hilo hilo walilondolewa wananchi wenye asili nalo.

Kwa upande wao, nchi jirani ya Zambia inawavutia wafanyabiashara hao kutoka nchini kwa kuwatoza viwango vidogo vya kodi ikilinganishwa na hapa nchini pamoja na kuwahakikishia kodi ndogo vile vile kwenye vyumba vya biashara, lengo likiwa kukusanya mapato zaidi yatokanayo na kodi za wafanyabiashara hao.

Watu wanapenda kufanyia biashara zao upande wa Zambia kutokana na mazingira mazuri ya biashara kule, huku kwetu kodi za vyumba ziko juu sana, ushuru nao juu, kule hatusumbuliwi na kodi zao ziko chini, ukienda soko la Komesa pale Lusaka, Kamwala au hapa Nakonde asilimia kubwa ya wafanyabiashara ni Watanzania, anasema mfanyabiashara wa Tunduma aliyeomba kutotajwa jina.

Mfanyabiashara huyo pamoja na wenzake wanaishangaa Halmashauri ya Mji huo kuwaelekeza wafanyabiashara wadogo kwenda kwenye soko walilotengewa nchini Zambia badala ya kuwatengenezea huku huku nchini kwao, kwani kwa kufanya hivyo inajikosesha mapato ambayo ingepata kutokana na kodi mbalimbali.

Mtu na elimu yake hawezi andika yale, wenzetu wajanja, bidhaa zinatoka huku kwetu, kwa hiyo wanatuvutia kuhamia kwao kwa ajili ya kupata kodi, anasema mfanyabiashara huyo.

Katika mahojiano yake na Raia Mwema, Kaimu Mkurugenzi Mwashiga alipingana na tangazo lake mwenyewe kwamba hawajawaelekeza wamachinga kwenda upande wa Zambia.

Hatuwaelekezi kwenda Zambia, nasi tuna maeneo yetu, baada ya kuona wanasongamana, tulikaa na wenzetu, tukakubaliana kuwatengea maeneo kuondoa msongamano pale Customs, anasema Kaimu Kurugenzi huyo ikiwa ni tofauti na tangazo lake alilolininginiza kwenye uzio wa mpakani.

Maofisa TRA wasema haina tatizoWakati wafanyabiashara katika mji huo wa Tunduma wakishangaa Serikali kwa kuwasababishia wakimbilie nchi jirani hivyo kukosa mapato yatokanayo na kodi za biashara zao, baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) nchini wamesema hakuna tatizo katika hilo.

Raia Mwema ilitaka kufahamu faida na hasara ya wafanyabiashara hao kukimbilia nchi jirani badala ya kuendelea na shughuli zao hizo hapa nchini, na mmoja wa maofisa wa TRA anasema.

Mtu anaruhusiwa kufanya biashara popote duniani. Wakiwa huko watatozwa kodi kulingana na sheria za huko, huku nako tunatoza kodi, wakipata faida huko watarudisha nyumbani kwa kuwekeza katika shughuli mbalimbali, ni jambo la kawaida.

Kauli ya afisa huyo inalingana na Meneja TRA Mkoa wa Mbeya, Arnold Maimu ambaye anasema mwananchi ana haki kwenda kokote atakako mradi havunji sheria.

Pamoja na kufanya biashara na kulipa kodi Zambia, ataleta mapato yake nchini, kwa mfano, atajenga nyumba, atakuja na fedha za kigeni, na sisi wapo wawekezaji toka nje kwa hiyo sioni ajabu Mtanzania akienda nje kwani ataleta mapato, anasema Meneja huyo.

Hata hivyo, kitendo cha Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma kuwaelekeza wafanyabiashara ndogo ndogo hao upande wa Tanzania waende kufanya biashara zao Nakonde Zambia kinaelezwa kukiuka sheria za kimataifa.

Ni kinyume cha sheria za kimataifa, kwamba mtu wa nchi moja kuwahamishia watu wake nchi nyingine, anasema Afisa Uhamiaji mmoja.

Anasema iwapo Zambia imewakaribisha, Tanzania haiwezikuingilia, lakini akitahadharisha kuwa Serikali haijatoa tamko lolote kuwahamishia wafanyabiashara wake nchini humo.http://www.parliament.go.tz/polis/index.php?r=session/default/viewAns&id=6177 Answer to Question number 354-4-2011 Wananchi wa Manyovu hufanya biashara na nchi jirani za Burundi na Rwanda, lakini kumekuwa hakuna masoko ya mipakani yanayotambuliwa na hivyo kufanya Wananchi kuonekana kana kwamba biashara hizo ni za magendo:-

(a) Je, ni lini Serilai itaweza kutambua umuhimu wa masoko ya mipakani na kwa upande wa Tanzania ni lini masoko hayo yataanzishwa na kutambuliwa?

(b) Kwa nini Wananchi wanasumbuliwa mipakani kwa kukamatwa na mizigo yao huku tukijua kwamba hatujaweka utaratibu wa njia za kupita na Serikali itawasaidiaje Wananchi hao ili wafanye biashara zao kwa amani?

WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Albert Obama Ntibaliba, Mbunge wa Manyovu, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuanzisha masoko ya mipakani ili kukuza na kuendeleza biashara iliyo rasmi kati ya Tanzania na nchi jirani, hususan katika kipindi hiki ambacho tumeingia katika Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kufanikisha azma hii, Wizara ilitembelea maeneo ya mipakani kufanya tathmini ya biashara kati yetu na nchi jirani. Tathmini hiyo ambayo ilihusisha pia mpaka kati ya Tanzania na Burundi, eneo la Mnanila (Manyovu) katika Wilaya ya Kasulu, ilionesha umuhimu wa kujenga soko la mpakani katika eneo hilo. Soko hilo ni moja kati ya masoko saba yanayojengwa katika maeneo ya mipakani katika kipindi hiki. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa soko la mpakani kati ya Tanzania na Burundi na eneo la Manyovu, utatekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji wa Sekta ya Kilimo (District Agricultural Sector Investment Project ? DASIP), unaoratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Taratibu za kuanza kwa ujenzi huo zinaendelea na ujenzi unatarajiwa kuanza katika kipindi cha mwaka 2011/2012.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na TAMISEMI, kuhakikisha soko hilo linajengwa mpakani kutokana na kutambua umuhimu wa kuwepo soko katika mpaka wa Manyovu. Hii itasaidia kuwarahisishia wafanyabiashara walioko mpakani, kufanya biashara rasmi, kuongeza mapato kwa Serikali na kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara wanapovuka na mizigo mpakani.

Mheshimiwa Spika, Wizara hutoa elimu kuhusu Sheria na taratibu za biashara kati ya nchi na nchi kwa wafanyabiashara wadogo mipakani ili waweze kuzizingatia na kuondokana na bughudha za kukamatwa. Aidha, jitihada zinafanyika ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za mipakani mahali pamoja ili kupunguza bughudha ya huduma za wakaguzi mipakani pamoja na kupunguza gharama na muda wa kupitisha mizigo na magari.

http://startvtz.com/wafanyabiashara-mutukula-walalamikia-viwango-vya-ushuru/

Wafanyabiashara Mutukula walalamikia viwango vya ushuru

Jan 26th, 2015

Na Mariam Emily,Bukoba.Wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo mkoani Kagera wameiomba Mamlaka ya Mapato nchini TRA kuweka kiwango cha ushuru kinachoeleweka ili kuwaondolea adha wanayoipata katika mpaka wa Mutukula pindi wanapotoa bidhaa zao nchi jirani ya Uganda.

Malalamiko hayo yametolewa na wafanyabiashara hao katika kikao cha pamoja baina yao na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika mjini Bukoba.

Kikao cha pamoja baina ya wadau wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kinachojumuisha wafanyabiashara na wajasirimali wadogo, changamoto kadhaa zinawekwa hadharani kuhusiana na suala zima la ushuru wa forodha hususani katika mpaka wa Mutukula kuingia nchi jirani ya Uganda.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wanaitupia lawama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokuwa na viwango vinavyoeleweka vya ushuru katika mpaka huo hali inayosababisha sintofahamu kubwa miongoni mwao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Amantius Msole anasema kinachojitokeza ni kila nchi kuwa na mfumo wake katika kodi za ndani.

Kikao hicho kililenga kujua changamoto walizonazo wafanyabiashara wa Kitanzania katika ushindani wa soko la jumuiya ya Afrika ya mashariki ambapo Wizara husika imeahidi kuyafanyia kazi baadhi ya malalamiko.

http://www.parliament.go.tz/polis/index.php?r=session/default/viewProc&id=40537

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi ya kuchangia Kamati hizi za Nishati na Madini na ya Miundombinu. Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo natakiwa ni-declare, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, lakini nitachangia zaidi upande wa miundombinu hususan maeneo ya mipakani. Mheshimiwa Naibu Spika, mipaka yetu nchini, Mpaka wa Tunduma, Namanga, Sirali, Holili na mingine ni sehemu ambayo ndiyo inaweza kupelekea mapato mengi katika hili Taifa. Nasema haya kwa sababu kila siku ndani ya Bunge tunasema na bado Serikali haisikii ni namna gani wanawezaa kutumia mipaka kama sehemu ya mapato. Tunayasema haya kwa mfano pale Tunduma, Jimboni kwangu, leo ukienda msongamano unaokutana nao wa Dar es Salaam haufikii, wa Dar es Salaam unatembea lakini wa Tunduma ni mgumu sana kutembea. Haya yote yanatokana na mfumo wa Serikali kushindwa kushirikiana. Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia Wizara ya Uchukuzi, kupitia Mheshimiwa Waziri Mwakyembe, walikubaliana kufanya kazi saa 24. Mamlaka ya Bandari (TPA), wanafanya kazi saa 24 wanapakuwa magari. Magari haya yote kwa mfano ni magari ya mizigo yanakwenda katika mipaka ambapo ndiyo kwenye ushuru wa forodha (Custom); kwa mfano,Tunduma wapo watu wa TRA pale wanafanya kazi saa nane. Ukienda kwa utaratibu huu mmoja yupo Dar es Salaam anafanya kazi saa 24, mwingine yupo mpakani anafanya kazi saa nane. Hapa hakuna ratio, sasa unashangaa Serikali inafanya kazi namna gani! Matokeo yake ni nini? Badala ya msongamano wa magari sasa kuwa Bandarini msongamano wa magari ya mizigo unabaki kuwa mipakani ambapo ni hatari zaidi kwa usalama wa nchi tofauti na ilivyokuwa bandarini. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili tutataka kuliangalia upya. Mimi ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kwa sababu TRA ndiyo wanaohusika sana katika maeneo ya mipaka na wao sasa wafanye kazi saa 24 kama tulivyokuwa tunapendekeza kila siku. Hapa maana yake Dar es Salaam watatoa magari saa 24 na mipakani TRA watafanya kazi saa 24, maana yake nchi muda wote itakuwa inafanya kazi. Huu mgongano hutokana na Mamlaka ya Mapato ipo chini ya Wizara ya Fedha na TPA ipo chini ya Mamlaka ya Bandari. Matokeo yake, Wizara ya Fedha ina misingi yao ya kazi na Mamlaka ya Bandari chini ya Wizara ya Uchukuzi wana misingi yao ya kazi. Sasa hatuwezi kuendelea na huu mfumo, kwa hiyo, lazima tukubaliane kuwa na mfumo mmoja wa kulisaidia hili Taifa hususan kuondoa hii misongamano. Kwa hiyo, nashauri lazima kuwe na ushirikiano. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ukienda hapo hapo Bandarini kuna wizi wa ajabu sana. Ningependa Serikali itolee majibu. Wizi wenyewe ni nini? Kuna watu wanaita ICD hawa wanahusika na masuala ya kuhifadhi magari wanafanya kazi saa nane, siku za Jumamosi na Jumapili hawafanyi kazi. Jumamosi na Jumapili hawafanyi kazi, lakini mtu akinunua gari anachajiwa siku saba. Gari likikaa mwezi mmoja maana yake na zile siku nane za weekend analipa mtu ambazo wao hawafanyi kazi analipia huu si wizi. Sasa Jumamosi na Jumapili ICD hawafanyi kazi, lakini hizo hizo siku mtu anapokwenda kulipa storage ya gari hizo siku mbili analipishwa; huu si wizi wa ndani na ulio wazi kabisa? Mheshimiwa Naibu Spika, haya yote yapo chini ya Wizara ya Uchukuzi pamoja na kwamba, ICD ipo privately owned. Tungependa sasa Serikali nalo hili mjaribu kulizingatia. Kwa hiyo, kama wao hawafanyi kazi Jumapili na Jumamosi na kama wao vilevile wanafanya kazi saa nane, charging ya watu ya mizigo yao katika storage ilingane na muda wanaofanya kazi. Wasi-charge muda ambao hawafanyi kazi, ule ni wizi na tunawaibia sana Watanzania na Wafanyabiashara. Kwa hiyo, ningependa hili lizingatiwe. Hapa ni mfumo ubadilike kuanzia Wizara ya Fedha washirikiane na watu wa Uchukuzi angalau tukienda na huu mfumo hili Taifa tutasaidiana. Ninapenda sana kutolea mfano, eneo la Tunduma peke yake, huwa linaliingizia Taifa kila mwezi kuanzia shilingi bilioni 1.8 mpaka bilioni mbili. Maana ni karibu shilingi bilioni 24 kwa mwezi. Sasa tukiruhusu mfumo wa saa 24 tukapunguza msongomano wa magari kwa kutengeneza dual carriage way kama tulivyopendekeza. Unapotengeneza dual carriage way tafsiri yake ni kwamba, kunakuwa na njia ya magari ya mizigo kwenda nchi za nje. Ukiingia watu wanaendelea na kazi zao kama kawaida that's very simple hapatakuwa na msongamano, kazi zitaendelea, tutarahisisha mwenendo. Serikali itapata mapato mara tatu ya inavyopata wakati uliopo. Haya yote mnashindwa kuyazingatia na ni mambo rahisi na yanaweza kutekelezeka. Ningeomba hili suala lifanyike. Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine suala la One Border Post lisije likawa kitendawili kwa sababu mara nyingi kila siku tumekuwa tunaambiwa tutatengeneza. Tutakaporuhusu One Border Post kabla ya mwaka 2015 hata haya masuala ya kasungura kadogo yatatekelezeka. Sasa hivi itaendelea kubaki kuwa nadharia, One Border Post itajengwa itapita miaka mitano, sita, saba, lakini mwisho wa siku tutakuja kuwalaumu kwa kushindwa kutekeleza, jambo ambalo linawezekana kutekelezeka kwa sababu linarudisha. Hili ndilo tatizo kubwa la Serikali yetu kwamba, tumekuwa tukiweza katika Miradi isiyokuwa na manufaa tofauti na Miradi ambayo inaweza kuliingizia pato Taifa kama ambavyo sisi tumekuwa tunapendekeza. Kwa hiyo, hili ningeomba lifanyike. Kutokana na mikanganyiko ambayo inatokea Mipakani kama Tunduma, tulikuwa tunapendekeza kila siku, tunaomba manufaa ya Mipaka yetu, service levy ya 0.3 percent tulipwe na sisi. Mkiweza kuwa mnatupatia kama tuna uwezo wa kuwaingizia pato la bilioni mbili kwa nini msitupile service levy ya shilingi angalau milioni 60 mpaka 70 kwa mwezi. Nina uhakika hii tunaweza tukabadilisha maendeleo ya pale kwa sababu sisi ndiyo tunaokabiliwa na changamoto za pale mpakani. Tupo katika hatari ya moto, ujambazi, lakini vilevile pana maambukizi makubwa sana ya UKIMWI kutokana na msongamano mkubwa uliopo lile eneo. Nimelisemea sana, ningeomba sasa Serikali mli- consider na lifanyiwe kazi mara moja. Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni masuala ya barabara. Halmashauri nyingi nchini tumeomba kupandishiwa hadhi barabara zetu kwenda kupitia Wizara ya Ujenzi. Imekuwa ni muda mrefu, miaka miwili, watu wanasema unavyopeleka maombi watu wa Wizara kwenda kukagua barabara wanahitaji miaka miwili ili waipitie hiyo barabara waipandishe hadhi. Kibaya zaidi, barabara tunazoziombea zipandishwe hadhi kwa mfano sisi tumeomba barabara kutoka Kakozi - Kapele kwenda Namchinga mpaka Ilonga, kilomita 50.6. Tumeomba barabara kutoka Ntungwa - Chilulumo - Mkuluwe mpaka Namsamba, kilometa 51.1 zipandishwe hadhi, lakini miaka miwili sasa Serikali haijibu imekaa kimya inaingiza mapato. Kibaya zaidi, sisi tupo vijijini na ndiyo tunaoingiza sana Pato hili Taifa, lakini cha ajabu ni kwamba, asilimia 80 ya Watanzania maskini wanaolipa kodi na kuzalisha, kwa maana ya mazao ya mahindi na mazao ya biashara, hatuzingatiwi na Serikali. Kwa hiyo, Miradi yote kwa mfano hata mapato niliyotolea katika mipaka yanatoka maeneo ya vijijini Tunduma yanakwenda Serikali Kuu yananufaisha zaidi Dar es Salaam na Mijini yanaacha maeneo ya vijijini. Sasa hatuwezi, lazima haya tunayoyapeleka ni maombi yanayogusa Wananchi wengi na maskini, ningependa lizingatiwe. Jambo la tatu, mimi nilitaka nizungumzie suala la umeme vijijini. Wananchi wa vijijini wameteseka sana, tangu dunia ianze hawajawahi kuona mwanga. Sasa hawa ndiyo walipa kodi, wanaonewa na ndiyo wapiga kura wakuu wa Chama cha Mapinduzi. Tofauti na maeneo ambayo sisi Upinzani tunayaongoza, maana kule tunapoongoza sisi Upinzani ndiyo kuna umeme, maji na barabara. Wale ambao wanawapigia kura kwa nini mnawanyanyasa hivyo? Hatuwezi kuendelea kutumia umaskini wao na unyonge wao, wakati wanalipa kodi wanazalisha. Kwa hiyo, ningewaomba Serikali ndani ya kipindi hiki kifupi hususan Wilaya yangu ya Mombo tulete umeme haiwezekani sisi Wilaya ya Mombo ukiondoa Halmashauri ya Mji wa Tunduma peke yake, miaka yote hata Kata moja hakuna umeme, jamani hamtuonei huruma. Kila siku naongea hamnionei huruma! Sizungumzi kwa manufaa yangu, nazungumza kwa manufaa ya Wananchi wa Mbozi wanaowapigia kura. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi lessby Hon. David Ernest Silindehttp://www.wavuti.com/2015/04/jinsi-wanavyokwepa-kulipa-ushuru-halali.html

a video

Waziri wa fedha Saada Mkuya amejionea udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wa ukwepaji wa kodi ambapo katika tukio moja ameshuhudia bidhaa ikifanyiwa udanganyifu ambao ungeikosesha Serikali ushuru wa zaidi ya shilingi milioni 300/=

http://tanexa.blogspot.com/http://swahili.cri.cn/141/2013/05/20/1s118993.htmhttp://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/01/140107_eac_fedhahttp://www.trademarkea.com/projects/one-stop-border-post-at-taveta-kenya-holili-tanzania/http://www.newtimes.co.rw/section/article/2015-01-12/184873/http://www.zimborderguide.co.zw/index.php/61-chirundu-one-stop-border-post-inspires-osbp-for-tanzaniahttp://www.parliament.go.tz/index.php/sessions/contribution/1716/4/2http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Vizuizi--mizani-mzigo-mkubwa-/-/1597592/2330696/-/11jr07j/-/index.htmlhttp://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/Bandari-ya-D--Salaam-kuanza-kutoa-huduma-saa-24-kesho/-/1597568/2225030/-/o5dxd1z/-/index.html