ubadilishaji msimbo bungeni na athari zake kwa … · katika familia na jamii kwa ujumla. mungu...

118
i UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA WASIKILIZAJI Johanes Sylivester Tasinifu ya M.A. Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Septemba, 2011

Upload: others

Post on 10-Feb-2020

76 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

Page 1: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

i

UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA

WASIKILIZAJI

Johanes Sylivester

Tasinifu ya M.A. Kiswahili

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Septemba, 2011

Page 2: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

ii

UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA

WASIKILIZAJI

Na

Johanes Sylivester

Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha masharti ya Digirii ya M.A.

Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Septemba, 2011

Page 3: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

i

UTHIBITISHO

Aliyetia saini hapa chini anathibitisha kuwa amesoma tasinifu hii inayoitwa:

“Ubadilishaji Msimbo Bungeni na Athari Zake Kwa Wasikilizaji” na anapendekeza

ikubaliwe na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha Masharti ya

Digirii ya M.A. Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

………………………….………

Dkt E. K. F. CHIDUO

(Msimamizi)

Tarehe: ……………………

Page 4: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

ii

IKIRARI

NA

HAKIMILIKI

Mimi, Johanes Sylivester, nathibitisha kwamba tasinifu hii ni kazi yangu halisi na

haijawahi kuwasilishwa na haitawasilishwa katika Chuo Kikuu kingine kwa ajili ya

kutunukiwa Digirii nyingine yoyote.

Saini: …………………………………

Haki ya kunakili tasinifu hii inalindwa na Mkataba wa Berne, Sheria ya Haki ya

Kunakili ya mwaka 1999 na mikataba mingine ya Sheria za Kitaifa na Kimataifa

zinazolinda mali za Kitaaluma. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga au

kunakili kwa njia yoyote ile, iwe ama yote au sehemu ya tasinifu hii, isipokuwa kwa

shughuli halali, kwa ajili ya utafiti, kujisomea au kufanya marejeo ya kitaaluma bila ya

kibali cha maandishi cha Mkuu wa Kurugenzi ya Taaluma za Uzamili kwa niaba ya

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Page 5: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

iii

SHUKURANI

Kazi hii imekamilika kutokana na michango ya watu mbalimbali walioshirikiana nami

bega kwa bega kuhakikisha inafanyika kama ilivyopangwa. Sina budi kutoa shukurani

zangu za dhati na upendo kwa watu hao. Kwa kuwa ni wengi mno, ni vigumu kuwataja

wote ila itanilazimu kuwataja wachache tu kwa niaba ya wote kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, napenda kumshukuru msimamizi wangu Dkt E. K. F. Chiduo ambaye

amekuwa nami bega kwa bega ili kuhakikisha kazi hii inakuwa katika kiwango hiki.

Licha ya kazi zake nyingi hakusita kunipa miongozo ya kuboresha kazi hii.

Pili, niwashukuru Prof. Y. P. Msanjila na Dkt. P. S. Malangwa kwa kupitia kazi hii

kuanzia hatua za awali za uandishi wa pendekezo la utafiti hadi hatua za mwisho za

kazi hii na kunipa mchango na changamoto ambavyo vimesaidia katika kuiboresha na

kuifikisha katika kiwango hiki.

Bila shaka nisingeruhusiwa kufanya utafiti kama nisingekuwa nimekamilisha tamrini.

Hivyo, niwashukuru wahadhiri wangu ambao ni; Prof. D. P. B. Massamba, Prof. D. J.

Mkude, Prof. Y. M. Kihore, Prof. Y. P. Msanjila, Prof. Y. I. Rubanza, Prof. H. J. M.

Mwansoko, Prof. J. G. Kiango, Prof. M. M. Mulokozi, Prof. E. Kezilahabi, Prof. F. E.

M. K. Senkoro, Dkt. E. K. F. Chiduo, Dkt. S. S. Sewangi, Dkt P. S. Malangwa, Dkt A.

Mutembei, Dkt G. Mrikaria, Dkt S. E. Mrikaria na Dkt S. Omari kwa mchango wao

mkubwa darasani na wakati wa uwasilishaji wa mada ya tasnifu hii ambao

nimeuzingatia katika uandishi wa mwisho wa tasnifu hii.

Page 6: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

iv

Pia niwashukuru wanafunzi wenzangu wa M.A. Kiswahili kwa ushirikiano na upendo

walionionesha wakati wa kukamilisha tamrini na kwa kuhudhuria siku ya uwasilishaji

wa mada hii pamoja na mchango wao mkubwa ambao nimeuzingatia. Lakini nitakuwa

mchoyo wa fadhira iwapo sitowataja N. Mbiling’i, Ngowo Asnath, E. Mbogela, F.

Mwendamseke, na A. Gawasike ambao tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega

darasani na hata katika uandishi wa tasnifu hii.

Tatu, shukurani zangu za dhati ziwaendee dada yangu mpendwa Beatrice Balige na

mume wake Yesse Kanyuma kwa kunipatia kila lililohitajika katika harakati zangu za

masomo kuanzia sekondari hadi ninapomaliza tasnifu hii. Mchango wenu wa hali na

mali umekuwa msaada ambao kamwe sitausahau maishani mwangu.

Pia namshukuru mama yangu mpendwa Emelensiana Kokubanza kwa kunilea katika

hali iliyoniwezesha kupenda masomo na pia kwa kunitia moyo katika hatua zangu zote

za masomo. Nimshukuru pia baba yangu mpendwa Sylivester Mugyabuso Balige, japo

ulitangulia mbele ya haki nikiwa nasubiri kujiunga shahada ya awali lakini uliacha

changamoto kichwani mwangu ya nami siku moja kuwa mtu mwenye mchango chanya

katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi;

Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa Maria Masela kwa upendo

ulionionesha katika hatua zangu za awali za utoto. Bibi nitakuenzi kwa kuonesha

upendo kwa wengine.

Nne, niwashukuru wanafunzi na walimu walionisadia katika ukusanyaji wa data. Kwa

kuwa nafasi haitoshi niishie tu kutaja shule watokazo ambazo ni shule ya Sekondari

Page 7: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

v

Lubugu, Mkolani na Sekondari ya Mwanza. Nawashukuru sana, jitiada zenu

ziliniwezesha kupata data halisi. Pia, niwashukuru watafitiwa wote waliohusika katika

kutoa data, hakika mmekuwa mchango wa kunipa cha kuandika.

Pamoja na hayo, bila Mungu kuniwezesha michango ya hawa niliowataja isingezaa

matunda haya, hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha maana

“Nayaweza yote katika wewe unitiaye nguvu”.

Page 8: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

vi

TABARUKU

Kwa dada yangu mpendwa Beatrice Balige na mume wake Yesse Kanyuma ambao

jitihada zao zilinifanya kupata kila nyenzo ya kuniwezesha kusonga mbele katika hatua

zangu zote za masomo. Nawapenda sana na Mungu awabariki.

Page 9: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

vii

IKISIRI

Wakati takribani 5% ya watanzania ndio wanaofahamu Kiingereza (Msanjila 2004:45

akimnukuu Schmied 1989), hali halisi inaonesha kuwa mijadala ya Bunge inaendeshwa

kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kutokana na hali hii utafiti huu ulihusu

ubadilishaji msimbo Bungeni na athari zake kwa wasikilizaji na uliongozwa na modeli ya

Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” na mkabala wa Fishman (1971)

“Mkabala wa Mawanda”.

Kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na kwa usampulishaji

nasibu tabakishi tuliweza kuwatafiti wasikilizaji 775 kutoka Wilaya za Nyamagana na

Magu mkoani Mwanza. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, wastani wa 08.90% tu ya

wasikilizaji ndio wanaoelewa kwa kiwango kilichokusudiwa mijadala inayohusisha

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Pili, kwa wasioelewa takribani 59.23% hawatafuti

mbinu mbadala za kuelewa mijadala hiyo. Tatu, 81.68% ya watafitiwa hawafurahishwi na

uzungumzaji wa namna hii kwani hawapati ujumbe uliokusudiwa na kubadilisha Kiswahili

na Kiingereza ni kutokithamini Kiswahili na utamaduni wake. Ili kuondoa athari hasi

zinazosababishwa na ubadilishaji msimbo Bungeni, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza

kuwa Kiswahili kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa

wanatoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa; kinaeleweka kwa watanzania wengi na

hivyo kitawezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake; ni lugha ya taifa na

inafungamana na utamaduni wa watanzania; kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi;

kinaepusha utumwa wa kifikra; ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na itasaidia kukilinda na

kukikuza Kiswahili. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla ambayo kimsingi yanalenga

kukiimarisha Kiswahili kidhima.

Page 10: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

viii

YALIYOMO Ukurasa

Uthibitisho .............................................................................................

Ikirari na Hakimiliki …..........................................................................

Shukurani ..............................................................................................

Tabaruku ...............................................................................................

Ikisiri .....................................................................................................

Yaliyomo ……………………………………………………………...

Orodha ya Majedwali ………………………………………………...

Vifupisho ……………………………………………………………..

i

ii

iii

vi

vii

viii

xii

xiii

SURA YA KWANZA: UTANGULIZI 1

1.0

1.1

1.2

1.3

1.3.1

1.3.2

1.4

1.5

1.6

1.7

1.7.1

1.7.2

1.8

Utangulizi wa Jumla........................................................

Usuli wa Tatizo................................................................

Tatizo la Utafiti................................................................

Malengo ya Utafiti...........................................................

Lengo la Jumla.................................................................

Malengo Mahususi...........................................................

Maswali ya Utafiti............................................................

Umuhimu wa Utafiti........................................................

Mawanda ya Utafiti..........................................................

Kiunzi cha Kinadharia …………………………………

Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji …………………..

Mkabala wa Mawanda …………………………………

Vikwazo vya Utafiti ……………………………………

1

2

7

7

8

8

8

9

9

10

10

11

12

Page 11: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

ix

1.9 Hitimisho.......................................................................... 13

SURA YA PILI: MAPITIO YA MACHAPISHO 14

2.0

2.1

2.2

2.2.1

2.2.2

2.3

2.4

2.5

2.6

2.7

2.8

Utangulizi............................................................................

Maana ya Ubadilishaji Msimbo..........................................

Aina za Ubadilishaji Msimbo…………………………….

Ubadilishaji Msimbo Ndani ……………………………

Ubadilishaji Msimbo Kati ………………………………..

Tofauti Kati ya Ubadilishaji Msimbo na Ukopaji ………..

Sababu za Ubadilishaji Msimbo …………………………

Uelewekaji wa Maongezi Yanayohusisha Ubadilishaji

Msimbo…………………………………………………...

Mbinu za Kuelewa Matini zenye Ubadilishaji Msimbo …

Mtazamo wa Wasikilizaji Kuhusu Ubadilishaji Msimbo ..

Hitimisho …………………………………………………

14

14

18

18

23

25

29

32

36

36

39

SURA YA TATU: MBINU ZA UTAFITI 40

3.0

3.1

3.2

3.3

3.3.1

3.3.2

3.3.2.1

Utangulizi ............................................................................

Eneo la Utafiti .....................................................................

Populesheni Lengwa ya Utafiti ...........................................

Sampuli na Usampulishaji ..................................................

Sampuli...............................................................................

Usampulishaji......................................................................

Aina ya Usampulishaji........................................................

40

40

41

42

42

42

42

Page 12: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

x

3.4

3.4.1

3.4.2

3.4.3

3.5

3.6

Mbinu za Ukusanyaji wa Data............................................

Hojaji...................................................................................

Usaili...................................................................................

Mijadala ya Vikundi Lengani.............................................

Uchanganuzi wa Data.........................................................

Hitimisho …………………………………………………

45

46

46

47

48

49

SURA YA NNE: UWASILISHAJI, UCHANGANUZI NA

UFASIRI WA DATA

50

4.0

4.1

4.2

4.3

4.4

4.5

4.5.1

4.5.1.1

4.5.1.2

4.5.1.3

4.5.1.4

4.5.1.5

4.5.1.6

Utangulizi.............................................................................

Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge….................................

Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala…...………………..

Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni:

Mtazamo wa Wasikilizaji…………………………………

Ufuatiliaji wa Mijadala ya Bunge ……………………......

Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Maoni

ya Wasikilizaji …………………………………………...

Lugha ya Shughuli za Bunge na Kufaa kwa Kiswahili ….

Kiswahili Kinaeleweka kwa Watanzania Wengi ………...

Lugha ya Taifa na Utambulisho wa Watanzania …………

Lugha ya Umoja…………………………………..... …….

Kinawaepusha Watanzania na Utumwa wa Kifikra ………

Kukilinda na Kukikuza Kiswahili ………………………...

Kiswahili ni Lugha Rasmi ya Bunge la Afrika …………...

50

51

55

59

62

64

65

70

73

75

76

77

78

Page 13: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

xi

4.6

4.7

4.8

4.9

Mbinu za Kukifanya Kiswahili kuwa Lugha Pekee ya

Shughuli za Bunge………………………………………..

Kufaa kwa Kiingereza kuwa Lugha Rasmi ya Shughuli za

Bunge ……...……..............................................................

Kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza ……………………..

Hitimisho …………………………………………………

79

81

82

82

SURA YA TANO: MUHTASARI NA MAPENDEKEZO

85

5.1

5.2

5.3

5.4

Utangulizi............................................................................

Muhtasari............................................................................

Mapendekezo......................................................................

Hitimisho …………………………………………………

85

85

87

88

Marejeo.................................................................................................

Viambatanisho.....................................................................................

Kiambatanisho I: Hojaji ……………………………………………...

Kiambanisho II: Maswali ya Usaili …………………………………

Kiambanisho III: Maswali ya Vikundi Lengani …………………

Kiambatanisho IV: Mijadala ya Bunge ………………………………

Matini A: ……………………………………….

Matini B: ………………………………………....

Matini C: ………………………………………

Matini D: ………………………………………

89

97

97

100

101

102

102

102

102

103

Page 14: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

xii

ORODHA YA MAJEDWALI UKURASA

Jedwali la 1: Sampuli ya Utafiti Kutoka katika Wilaya za

Nyamagana na Magu ……………………………...

Jedwali la 2: Sampuli ya Utafiti Kutoka Kata tatu za Wilaya ya

Nyamagana ………………………………………..

Jedwali la 3: Sampuli kutoka Kata tatu za Wilaya ya Magu ……..

Jedwali la 4: Sampuli ya Utafiti …………………………………..

Jedwali la 5: Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge. ………………..

Jedwali la 6: Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala ……………

Jedwali la 7: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza: Mtazamo

wa Wasikilizaji……………………………………....

Jedwali la 8: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Unasababisha Wasikilizaji Wasifuatilie Mijadala ya

Bunge? ………………………………………………

Jedwali la 9: Mapendekezo ya Lugha ya Shughuli za Bunge …….

Jedwali la 10: Sababu za Kutetea Kiswahili Kuendeshea Shughuli

za Bunge….…………………………………………

Jedwali la 11: Ongezeko la Idadi ya Watumiaji wa Kiswahili

Tanzania……………………………………………

Jedwali la12: Sababu za Wasikilizaji Kutetea kuwa Kiingereza

Kinafaa kwa shughuli za Bunge …………………..

Jedwali la 13: Sababu za Wasikilizaji Kutetea Kiswahili na Kiingereza

Kufaa Kuendeshea Shughuli za Bunge………………….

43

44

44

45

52

56

60

62

67

69

71

81

82

Page 15: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

xiii

VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA

Kifupisho Maana

BAKITA Baraza la Kiswahili Tanzania

BAKIZA Baraza la Kiswahili Zanzibar

TATAKI Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Me Wanaume

Ke Wanawake

Nfs1u Nafsi ya kwanza umoja

Nsf1w Nafsi ya kwanza wingi

Nsf2u Nafsi ya pili umoja

Nsf2w Nafsi ya pili wingi

Nsf3u Nafsi ya tatu umoja

Nsf3w Nafsi ya tatu wingi

K/kiso Kitenzi kiso na ukomo

Ki/ng Kipatanishi ngeli

Lejico “Legico” legislative council (Baraza la Kutunga Sheria)

Nj Njeo

Rej Rejeshi

MOMWA Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji

MKAMA Mkabala wa Mawanda

Page 16: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

1

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

1.0 Utangulizi wa Jumla

Utafiti huu unahusu ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni na athari zake

kwa wasikilizaji. Utafiti unaongozwa na modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo

wa Wasikilizaji” na Mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda”. Katika

kufanya utafiti huu: kwanza, tumejikita kwa wasikilizaji tukitaka kubainisha uelewa wa

mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

miongoni mwa wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu. Uchanganuzi wa data

unaonesha kuwa 8.9% ya wasikilizaji ndio wanaoelewa, 14.58% wanaelewa baadhi ya

sentensi, 34.84% baadhi ya maneno na 41.68% hawaelewi mijadala yenye kuhusisha

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Uchanganuzi zaidi unaonesha kuwa kiwango

cha kuelewa au kutoelewa mijadala hii kinahusiana moja kwa moja na kiwango cha

elimu cha msikilizaji.

Pili, tulitaka kufafanua mbinu wazitumiazo wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya

elimu kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza. Data inaonesha kuwa, 85.04% ya wasikilizaji wasiojua kusoma na

kuandika na 70.86% wa kiwango cha elimu ya msingi hawatafuti mbinu mbadala za

kuwafanya waelewe mijadala hiyo. Kwa upande mwingine, asilimia kubwa ya

wasikilizaji wasomi (wa viwango vya sekondari na chuo) hupata maana ya mijadala ya

Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo kupitia vyombo vya habari na/au kuulizia

kwa wenzao. Pia, data inaonesha kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali

ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza katika mijadala ya Bungeni. Hata hivyo,

Page 17: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

2

pamoja na kutofurahishwa na namna hii ya uzungumzaji, katika sehemu ya nne tunaona

kuwa hali hii sio sababu pekee inayosababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya

Bunge.

Nne, kwa kuzingatia maoni ya wasikilizaji tumetoa mapendekezo ya kupunguza athari

hasi za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni. Katika sehemu ya tano

tumeona kuwa 85.55% ya watafitiwa wanapendekeza kuwa Kiswahili kiwe lugha rasmi

na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu wazitoazo ni kuwa; mosi,

kinaeleweka kwa watanzania wengi; pili, ni lugha ya taifa na inafungamana na

utamaduni wa watanzania; tatu, ni lugha ya umoja; nne, kinawaepusha na utumwa wa

kifikra; tano, ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na sita, ni lugha rasmi ya Bunge la

Afrika. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla kuhusu nini kifanyike kukifanya

Kiswahili kuwa lugha kidhi ya mijadala ya Bunge.

Katika utafiti huu, tumetumia istilahi ubadilishaji msimbo kama anavyoitumia Cromdal

(2000:2), anayetumia istilahi hii kumaanisha hali ya utumizi wa lugha mbili au zaidi

katika tamko moja, au mfuatano wa matamko kati ya wazungumzaji wawili au zaidi.

Hivyo, katika utafiti huu ubadilishaji msimbo unaainishwa kuwili: (i) ubadilishaji lugha

ndani ya sentensi moja ambao umerejelewa na baadhi ya wataalamu kama

uchanganyaji msimbo (Salimu-Sawe 2008) na (ii) ubadilishaji lugha baina ya sentensi

na sentensi.

1.1 Usuli wa Tatizo

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni chombo cha uwakilishi wa watu,

chenye misingi ya kikatiba kama inavyoainishwa katika sura ya tatu ya Katiba ya

Page 18: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

3

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Mathalani, katika ibara ya 62.-(1)

Katiba inaeleza kuwa;

kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na

sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.

Uwakilishi wa wananchi katika chombo maaalumu, chenye msingi wa kikatiba

uliasisiwa na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1926 (Nsekela 1965:166). Enzi hizo

kilijulikana kama “Baraza la Kutunga Sheria” au kwa kifupi Legico “lejiko”, jina

lililotokana na uhulutishaji wa “legislative council” (Mwansoko na Tumbo-Masabo

(1996:3).

Utumizi wa Kiswahili kwenye lejiko wakati huo ulichochewa na kuwapo kwa Waafrika

kwani wajumbe wa Kizungu wa lejiko walitosheka na mawasiliano kwa lugha ya

Kiingereza. Wawakilishi wa kwanza wa Kiafrika waliteuliwa mwaka 1945, ambao

walikuwa machifu A.S. Mkwawa, K. Makwaia na A.Shangali (Legere 1987:158).

Kipindi hiki Kiswahili kilitumika sana kama lugha ya ukombozi wa Waafrika na chama

kilichokuwa kikitetea maslahi ya wafanyakazi wa Kiafrika yaani Tanganyika African

Association (TAA), kilichoanzishwa mwaka 1929. Kudhibitisha hili, mwaka 1946

mkutano mkuu wa TAA uliazimia kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano

yake1.

Kutokana na mwamko huu wa kukithamini Kiswahili nchini, wawakilishi wa Afrika

kwenye lejiko walidai Kiswahili kitumike sambamba na Kiingereza katika mawasiliano

1 Legere 1987 uk. 153.

Page 19: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

4

ya lejiko muda mfupi baada ya wao kujiunga na Baraza la Kutunga Sheria, wazo

lililoungwa mkono na wakereketwa wa Kiswahili (Mwansoko na mwenzake 1996:3).

Tofauti na ilivyotarajiwa, hoja hii ilipingwa vikali na wajumbe wa Kiingereza wa lejiko

kwa visingizio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:-

I. Kwamba hali ilikuwa hairuhusu kwa lejiko kutumia lugha mbili

II. Kwamba Kiswahili kilikuwa hakijitoshelezi kisarufi na kimsamiati

III. Kwamba Kiswahili kingeshusha hadhi ya lejiko kwani hata Watanzania wa

tabaka la chini (yaani wasio machifu) ambao hawakusomeshwa kwa mfumo

wa elimu ya kikoloni wangeweza kuwa wajumbe wa lejiko.

Kutokana na pingamizi hili, iliwalazimu wana-lejiko wa Kiafrika kupunguza makali ya

madai yao. Sasa walidai hoja muhimu za lejiko zifasiliwe kwa Kiswahili na usambazwa

kwa maofisa wa Kiafrika wa serikali. Katika kikao cha 25 cha lejiko cha mwaka 1950

Chifu A. Shangali aliwasilisha rasmi hoja hii ya kutaka kufasiri hati zote za lejiko kwa

Kiswahili. Hoja hii pamoja na kuungwa mkono na wakuu wa majimbo (ma-PC),

wajumbe wa lejiko Waingereza pamoja na serikali yao walipinga.

Baada ya kuanzishwa chama cha TANU, mnamo tarehe 7/7/1954, pamoja na mambo

mengine kiliamua kwamba Kiswahili kitumike kama lugha ya pili kwenye lejiko.

Mwaka 1958 mkutano mkuu wa TANU uliazimia kukifanya Kiswahili lugha rasmi ya

taifa la Tanganyika pindi tu litakapojipatia uhuru wake. Baada ya kupata uhuru

(9/12/1961), wazalendo wakiongozwa na Rais wa TANU na serikali, Hayati Mwalimu

J. K. Nyerere walitambua vema dhima ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa

Page 20: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

5

nchi hii na hivyo hawakusita kukikuza na kukienzi ipasavyo. Kudhibitisha hili, mnamo

tarehe 10/12/1962 Hayati Rais J.K.Nyerere alihutubia Bunge kwa kutumia Kiswahili

kwa mara ya kwanza, hotuba ambayo ilipokelewa na Wabunge kwa shangwe kubwa2 .

Kutokana na hotuba hii iliyosisitiza kuwa na Kiswahili sanifu na kinachoeleweka, ilitoa

changamoto kwa wabunge hasa kuhusu lugha ya mawasiliano Bungeni. Ilidhihirika

kuwa Kiswahili kilikuwa na uwezo wa kukidhi mawasiliano ya Bungeni bila kuathiri

hadhi wala ufanisi wa Bunge. Kwa kuzingatia kuwa nchi ilikuwa imeishapata uhuru,

Wabunge wengi wazalendo walihamasika kukitumia na hivyo kuongeza shinikizo la

kutaka Kiswahili kiruhusiwe Bungeni.

Tarehe 12/2/1963 takribani miezi miwili tu baada ya hotuba ya kihistoria ya aliyekuwa

Rais, Hayati Julius Kambarage Nyerere, serikali ilikitangaza Kiswahili kuwa lugha ya

taifa. Kwa kuwa, kwa muda mrefu wabunge wazalendo walikuwa na shauku kubwa ya

kutumia Kiswahili Bungeni, kutangazwa kwake kuwa lugha ya taifa kulitoa fursa nzuri

ya kuingiza lugha hiyo Bungeni. Mara tu baada ya kutangazwa kuwa lugha ya taifa,

wabunge mashabiki wa Kiswahili walianza kukitumia rasmi kwenye mijadala ya

Bunge, yaani kuanzia kwenye mkutano wa 5, kikao cha 2, cha Februari 12, 19633.

Kwa kuzingatia hili, tunaweza kusema bila wasi wasi kuwa, matumizi ya Kiswahili

katika mijadala ya Bunge yalianza mapema mwaka 1963. Kwa kuwa Bunge lilikuwa na

wabunge wazalendo pamoja na wazungu (Waingereza), basi kulijitokeza matumizi ya

lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza. Wabunge wazalendo walitumia Kiswahili

2 Mwansoko na Tumbo-Masabo (wameshatajwa, ukurasa 5)

3 Mwansoko na Tumbo-Masabo, wakinukuu Hansard, 5

th session, 1963

Page 21: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

6

huku wabunge wazungu wakitumia Kiingereza. Hivyo basi, kutokana na sababu za

kihistoria, hadi leo Kiswahili na Kiingereza zinaendelea kuwa lugha rasmi za Bunge la

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2004

kanuni ya 118(1) inavyoelekeza;-

Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili

au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo kutolewa.

Kiswahili kilipotangazwa kuwa lugha ya taifa, ilidhaniwa kuwa kiuhalisia Bunge

lingekuwa miongoni mwa taasisi za umma ambazo wanasiasa wangezungumza

Kiswahili ili kuonesha utaifa wao au wangeelewa kuwa wasikilizaji walio wengi

hawawezi kuongea wala kuelewa Kiingereza. Hata hivyo, wanafanya hivyo lakini

katika namna ya kipekee, yaani ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza maarufu kama

Swaenglish4.

Katika jamiilugha ulumbi yoyote, ni jambo la kawaida mtu kuongea lugha fulani na

ghafla kubadilisha lugha au kuchanganya vipashio vya lugha mbili au zaidi ili kueleza

jambo (Rajabu 1991:24). Huu ndiyo huitwa ubadilishaji msimbo. Hata hivyo,

kinachofanya namna hii ya uzungumzaji kuonekana ya kipekee katika Bunge ni kuwa

taasisi hii ni rasmi na yenye hadhi kubwa. Urasmi wake unahitaji matumizi ya lugha

sanifu na fasaha, yenye kueleweka mara moja na isiyo na uvulivuli.

4 Kwa lugha ya mtaani lugha yenye mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza huitwa Swaenglish

Page 22: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

7

1.2 Tatizo la Utafiti

Bunge la Tanzania linatoa maamuzi ya mambo mabalimbali kwa njia ya vikao au

mikutano yake. Kwa hiyo, jambo lolote linalohitaji uamuzi wa Bunge, huamuliwa

katika mikutano rasmi ya Bunge. Ili kumudu jukumu hili, lazima kuwepo na lugha

inayofaa kuwezesha mawasiliano kati ya wabunge na serikali na kati ya wabunge na

wananchi na pia kati ya serikali na wananchi kupitia kwa wabunge. Kanuni za kudumu

za Bunge zinabainisha kuwa; “Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya

Kiswahili au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo kutolewa” (toleo la 2004 kanuni

ya 118(1)). Hata hivyo, mapitio ya taarifa rasmi za Bunge yanadhihirisha kuwa, wakati

wa mijadala wabunge wanatumia ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.

Tafiti zilizofanyika kuhusu ubadilishaji msimbo Bungeni ni pamoja na tafiti za

MacWilliam na Chuwa (1990) na Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996). Tafiti hizi

zimejikita katika kuainisha sababu za ubadilishaji msimbo Bungeni. Hakuna tafiti

zinazoonesha athari kwa wasikilizaji na watazamaji kwa kuzingatia matabaka yao

kielimu. Pia, maoni ya wasikilizaji juu ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

hayajabainishwa. Kwa kuzingatia hili, utafiti huu ulikuwa muhimu kufanyika ili

kufahamu athari kwa wasikilizaji zinazotokana na ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza Bungeni.

1.3 Malengo ya Utafiti

Sehemu hii inabainisha madhumuni ya utafiti huu ambayo yamegawanyika katika

sehemu mbili, yaani lengo la jumla na malengo mahususi.

Page 23: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

8

1.3.1 Lengo la Jumla

Utafiti huu unalenga kutathmini athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Bungeni kwa wasikilizaji na mtazamo wao kuhusu kaida hii ya utumizi wa lugha.

1.3.2 Malengo Mahususi

I. Kubainisha uelewa wa mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji

wa Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wasikilizaji wa viwango

mbalimbali vya elimu.

II. Kufafanua mbinu wazitumiazo wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya

elimu kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza.

III. Kubainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza Bungeni.

IV. Kutoa mapendekezo ya kuondoa athari hasi kwa wasikilizaji zinazotokana

na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni.

1.4 Maswali ya Utafiti

I. Uelewa wa mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili

na Kiingereza miongoni mwa wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya

elimu ukoje?

II. Wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wanatumia mbinu gani ili

kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza?

Page 24: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

9

III. Wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wana mtazamo gani kuhusu

tabia ya Wabunge ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni?

IV. Nini kifanyike ili kuondoa athari hasi kwa wasikilizaji zinazotokana na

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni?

1.5 Umuhimu wa Utafiti

Kwa kuwa utafiti huu unabainisha athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Bungeni kwa wasikilizaji, utawasaidia wabunge pamoja na wadau wa sera ya lugha

kuelewa athari za kiisimu za uzungumzaji wa namna hii. Hii itasaidia katika upangaji

lugha hasa kuhusu lugha inayofaa kutumika katika mijadala Bungeni.

Kutokana na kiwango cha ubadilishaji msimbo Bungeni kuongezeka mwaka hadi

mwaka, utafiti huu utaongezea katika uelewa kuhusu athari za kiisimu na kijamii

zinazosababishwa na ubadilishaji lugha Bungeni. Pia utawawezesha wadau (wabunge)

kuelewa mtazamo na kiwango cha wasikilizaji katika kuelewa mijadala

inayoendeshwa. Kwa wataalamu wa isimujamii, utafiti huu utakuwa chanzo kingine

cha habari na data kuhusu ubadilishaji msimbo na vipengele vingine vya jamiiilugha

ulumbi. Kwa kupata habari na data ya utafiti huu, tunapata data kuhusu ubadilishaji

msimbo na jamii lugha ulumbi. Mwisho utafiti huu unatarajiwa kutia chachu katika

tafiti zinazohusu ubadilishaji na ubadilishaji lugha hasa katika muktadha wa Bungeni.

1.6 Mawanda ya Utafiti

Kutokana na mapitio ya kumbukumbu za Bunge, imebainika kuwa wabunge mara

nyingi hubadilisha Kiswahili na Kingereza. Hata hivyo, kuna sehemu chache ambapo

Page 25: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

10

huchanganya na lugha za asili au Kiarabu lakini kwa kutoa maana zake katika

Kiswahili. Kwa kuzingatia hili, utafiti huu umejikita katika ubadilishaji wa Kiswahili

na Kingereza tu. Pili, utafiti haujashughulikia kubainisha sababu za ubadilishaji wa

Kiswahili na Kingereza kwa sababu tafiti zilizotangulia (rejea 2.4) zinaonesha sababu

mbalimbali za ubadilishaji msimbo. Kwa kuzingatia hili, tumejikita katika kubainisha

athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kingereza kwa wasikilizaji.

1.7 Kiunzi cha Kinadharia

Katika kutafuta nadharia za kutumika kama kiolezo cha utafiti huu, nadharia

mbalimbali zimepitiwa. Japokuwa zipo nadharia nyingine ambazo zingetumika kama

kiolezo katika utafiti huu, modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji”

na Mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda” zimeonekana kuwa mahususi

zaidi.

1.7.1 Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji (MOMWA)5

Hii ni modeli ya kiisimujamii iliyoasisiwa na Allan Bell mwaka 1984, inayozingatia

kuwa namna ya uzungumzaji inazingatia mtazamo wa wasikilizaji. Kwa modeli hii

wazungumzaji wanateua namna ya uzungumzaji kwa kutilia maanani wasikilizaji ili

kuleta umoja au ukaribu na wasikilizaji au kuzungumza tofauti na matakwa ya

wasikilizaji ili kuelezea kuwa kuna utofauti kati ya mzungumzaji na hadhira yake.

Modeli hii ilianzishwa kutokana na utafiti alioufanya Bell kuhusu utangazaji redioni

nchini Newsland. Utafiti wake ulijikita katika redio mbili ambazo zilitumia studio moja

5 Kwa Kiingereza inaitwa Audience-Design Model

Page 26: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

11

na baadhi ya watangazaji wale wale. Redio moja, redio ya taifa iliwavutia sana

wasikilizaji wa hali ya juu kiuchumi. Redio ya pili, redio ya jamii iliwavutia

wasikilizaji wengi ikiwa ni pamoja na wale wa tabaka la chini kiuchumi.

Katika kuchanganua data, Bell anabainisha kuwa watangazaji walizungumza kwa

namna tofauti tofauti kwa kuzingatia wasikilizaji wa redio husika. Kutokana na hali hii

anasema kuwa, kwa sababu mada, wazungumzaji na jambo la kuzungumzia vilikuwa

vile vile, jambo lililosababisha utofauti lilikuwa ni kwamba watangazaji walizungumza

kwa namna ya kutambua kuwa wasikilizaji walitarajia nini. Hivyo basi, mtazamo wa

wasikilizaji kuhusu namna ya uzungumzaji wa mzungumzaji ndio hutawala uteuzi wa

jinsi ya kuzungumza. Kwa mantiki hii, iwapo mzungumzaji atateua namna fulani ya

uzungumzaji ambayo wasikilizaji wake wana mtazamo hasi kwayo, basi

hawatamsikiliza na watakuwa na mtazamo hasi kwa huyo mzungumzaji. Hivyo basi,

modeli hii inasisitiza kuwa wasikilizaji ndio huongoza uteuzi wa namna au lugha ya

kuongea. Modeli hii ni muhimu katika utafiti huu hasa katika kipengele kinacholenga

kubainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu kaida ya ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza Bungeni.

1.7.2 Mkabala wa Mawanda (MKAMA)6

Mkabala huu unachukulia lugha au lahaja za lugha husika kuwa zimepewa dhima

maalumu katika jamii. Uliasisiwa na wanaisimujamii katika jitihada za kumaliza tatizo

la uteuzi wa lugha kwa kuzingatia muundojamii. Fishman (1971) ni miongoni mwa

watetezi wa mkabala huu. Anapendekeza kuwa kuna mazingira ya kitaasisi, yahusuyo

6 Kwa Kiingereza unaitwa The Domain Analytic Aproach

Page 27: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

12

mawanda ambapo kwayo lugha moja au lahaja ya lugha inafaa zaidi ya nyingine.

Mkabala huu unachukulia mawanda kujumuisha sehemu, mada na wahusika. Kwa

kuzingatia mtazamo huu wa kisosholojia, mkabala huu unachukulia kuwa muundojamii

ndio huongoza tabia ya watu kuhusu utumizi wa lugha. Hii inamaanisha kuwa, kwa kila

mazungumzo kuna kanuni maalumu ikiwa ni pamoja na kanuni zinazobainisha ni lugha

gani itumike.

Mkabala huu unachukulia kuwa, kwa kila taasisi kama vile Bunge iainishwe ni lugha

gani rasmi itatumika katika shughuli zake zote. Iwapo mkabala huu utazingatiwa katika

taasisi za serikali inategemewa kuwa Kiswahili na Kiingereza kila mojawapo itatumika

katika mawanda mahususi yanayozingatia sehemu/mahali, tukio, mada au wahusika.

Hivyo basi, utumizi wa lugha zote mbili Bungeni yaani Kiswahili na Kiingereza

unapingana na mkabala huu. Kwa ufupi mkabala huu unachukulia ubadilishaji msimbo

kama tabia ya uzungumzaji isiyokubalika katika jamii na hivyo wanajamii wana

mtazamo hasi kwa kaida hii ya uzungumzaji. Kwa kuwa mkabala huu unajihusisha na

mambo ya sera ya lugha na upangaji lugha, hivyo basi ni muhimu katika utafiti huu

hasa katika kipengele kinachohusu nini kifanyike kuondoa/kupunguza ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza (kama una athari hasi kwa wasikilizaji).

1.8 Vikwazo vya Utafiti

Kwa kuwa utafiti huu uligusia mambo ya Bunge watafitiwa wengine walitoa maoni

ambayo yalikuwa ya kisiasa zaidi kuliko kiisimu. Wengine walitoa kero zao kama

upungufu wa walimu, ukosefu wa huduma za jamii na kadhalika. Hii ilimpa kazi mtafiti

kuwarudisha katika mstari kuhusu nini kinahitajika katika utafiti huu. Ili kuweka

Page 28: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

13

mazingira ya kirafiki na watafitiwa, mara nyingine ilimpasa mtafiti kumwacha mtoa

data kuongea ananachohitaji huku mtafiti akichukua hoja zinazohusu mada ya utafiti.

Hii ilisaidia kuweka upamoja kati ya mtafiti na watafitiwa kwani kinyume na hapo

mtafiti angenasibishwa na walalamikiwa (serikali na Wabunge) na hivyo kuathiri

upatikanaji wa data. Hata hivyo, hali hii ilimlazimu mtafiti kuchukua muda zaidi ya

uliolengwa awali. Jambo jingine lililochangia hali hii ni kwamba mtafiti alikusanya

data kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu ambapo harakati za kisiasa zilikuwa katika

kiwango cha juu ambapo watu walikuwa tayari kuchangia katika mambo ya kisiasa

zaidi ya yale ya kiisimu.

1.9 Hitimisho

Sura hii imeanza kwa utangulizi wa jumla na kujadili usuli wa tatizo na baadaye

kubainisha tatizo la utafiti. Malengo na maswali ya utafiti yameainishwa kabla ya

kuelezea umuhimu na mawanda ya utafiti. Pia modeli na mkabala vitakavyoongoza

utafiti huu vimejadiliwa. Hivi ni modeli ya Bell (1984) “MOMWA” na mkabala wa

Fishman (1971) “MKAMA” vimejadiliwa. Mjadala huu unatupa mwanzo mzuri wa

kupitia machapisho na tafiti mbalimbali kuhusu ubadilishaji msimbo. Kwa mantiki hii,

sura inayofuata inajikita katika kupitia machapiosho mbalimbali kuhusu ubadilishaji

msimbo.

Page 29: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

14

SURA YA PILI

MAPITIO YA MACHAPISHO

2.0 Utangulizi

Sura hii inahusika na upitiaji wa machapisho mbalimbali yanayohusu ubadilishaji

msimbo. Katika sura hii tumeanza kwa kuelezea maana ya ubadilishaji msimbo na

baadaye kuainisha aina zake na kiwango cha utokeaji wake katika matini kabla ya

kutofautisha ubadilishaji msimbo na ukopaji. Baada ya hapo machapisho kuhusu

sababu za wabunge kubadilisha msimbo zimebainishwa na baadaye ni machapisho

kuhusu uelewekaji wa maongezi yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Pia,

machapisho kuhusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini zenye kuhusisha

ubadilishaji msimbo yamepitiwa. Mwisho ni mapitio ya machapisho kuhusu mtazamo

wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji msimbo.

2.1 Maana ya Ubadilishaji Msimbo

Istilahi hii imeelezwa na wataalamu wengi lakini wafuatao ndio watakaohusishwa

katika utafiti huu. Cromdal (2000:2) anasema kuwa, ubadilishaji msimbo ni utumizi wa

lugha mbili au zaidi katika sentensi moja au mfuatano wa sentensi nyingi kati ya watu

wawili au zaidi. Hii inamaanisha kwamba, ubadilishaji msimbo hutokea pale tu zaidi ya

lugha moja zinapotumiwa katika mazungumzo.

Wataalamu wengine wanasema kuwa, ubadilishaji msimbo ni utumizi wa mbadilishano

wa lugha mbili katika jamiilugha uwili ndani ya mada ile ile (Grosjean 1982:145,

Mirloy na Muysken 1995:7). Wataalamu hawa wanatumia istilahi ubadilishaji msimbo

kama istilahi jumuishi ambapo aina tofauti tofauti za jamiilugha uwili zimejuishwa.

Page 30: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

15

Wanatumia istilahi ubadilishaji msimbo ndani kumaanisha kubadilisha msimbo ndani

ya sentensi na ubadilishaji msimbo kati kumaanisha ubadilishaji msimbo kati ya

sentensi na sentensi.

Myers-Scotton (1993:1) pia anatumia istilahi ubadilishaji msimbo kama istilahi

jumuishi kwa kuielezea kama utumizi wa lahaja katika mada moja. Wataalamu

wengine kama vile Gardnne-Chloros (1991) pia wanasisitiza kuwa ubadilishaji msimbo

unaweza kutokea sio tu kati ya lugha na lugha bali kati ya lahaja moja na nyingine, na

pia kati ya namna ya uzungumzaji wa lugha moja.

Minloy na Muysken (1995:07) kama wanavyofasiliwa na Cromdal (2000:02), Grosjean

na (1982:145) nao wanasema kuwa ubadilishaji msimbo ni utumizi wa mbadilishano

wa lugha mbili au zaidi katika semo ile ile. Maana hii inahusu lugha moja au zaidi ya

moja zilizo tofauti. Kwa upande mwingine Muysken (1995:189) amepanua maana ya

ubadilishaji msimbo kwa kuhusisha vijenzi vya semo ambapo anasema kuwa ni utumizi

wa lugha mbili katika semo moja au kirai.

Badala ya kujikita katika kirai au semo, Eastman (1992) anatoa msingi mwingine

ambapo anasema kuwa ubadilishaji msimbo ni utumizi wa lugha mbili au zaidi au

lahaja za lugha moja kwa kuzingatia uchocheo unaotegemea hali na muktadha wa

mazungumzo. Maana hii ni nzuri (tukiachilia mbali dhana ya lahaja za lugha moja)

katika utafiti huu kwani modeli na mkabala vinavyoongoza utafiti huu vinachukulia

kuwa utumizi wa lugha lazima uzingatie muktadha na hali ya mazunguzo. Hii

inamaanisha kuwa, uwezo wa mzungumzaji kuwa na umilisi wa lugha mbili unamfanya

Page 31: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

16

kuwa na uteuzi wa lugha katika mazungumzo (Kadeghe 2000). Hata hivyo, uteuzi wa

lugha lazima uzingatie: (1) sifa na uhusiano wa msemaji na msikilizaji; (2) muktadha

wa mazungumzo (baa, kanisani, Bungeni n.k); (3) aina ya kilongo (majibizano,

mahojiano, usaili, hotuba n.k); na (4) mada. Jambo hili linabainishwa na Rubin (1968)

anayedai kuwa nchini Paragwai ambapo Kihispania na Kiguarani ni lugha rasmi, watu

hutumia lugha hizi kwa kuzingatia muktadha wa kijamii.

Dhana ya utumizi wa lahaja mbili au zaidi katika semo moja kama inavyojitokeza

katika maelezo ya Myers-Scotton (1993), Gardnne-Chloros (1991) na Eastman (1992)

kuhusu maana ya ubadilishaji msimbo na pia dhana ya ubadilishaji wa namna ya

uzungumzaji kama anavyobainisha Gardnne-Chloros (1991), zinaleta mkanganyiko

fulani zinapojumuishwa katika utafiti huu. Dhana hizi zinapanua wigo wa ubadilishaji

msimbo zaidi ya ilivyolengwa katika utafiti huu. Hii ni kwa sababu zinaingiza dhana

za; ubadilishaji wa namna ya uzungumzaji, ubadilishaji wa vipashio vya kiisimu (kama

vile lafudhi, toni, mkazo, kiimbo na kadhalika) vya lugha mbili tofauti, au hata

ubadilishaji msimbo unaohusisha lahaja za lugha moja. Kwa kuzingatia hili utafiti huu

unajikita tu katika ubadilishaji msimbo katika daraja la lugha.

Katika utafiti huu, tutatumia istilahi ubadilishaji msimbo kama anavyoitumia Cromdal

(2000:2). Anatumia istilahi hii kumaanisha hali ya utumizi wa lugha mbili au zaidi

katika tamko moja, au mfuatano wa matamko kati ya wazungumzaji wawili au zaidi.

Hii ni maana nzuri ya ubadilishaji msimbo kwa sababu inachukulia ubadilishaji

msimbo katika ngazi ya lugha, tofauti na maana nyingine ambazo kama ilivyodokezwa

awali zinaangalia ubadilishaji msimbo kati ya lahaja za lugha moja au namna ya

Page 32: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

17

uzungumzaji. Kwa kuzingatia maana hii ubadilishaji msimbo ni istilahi jumuishi

ambapo inaweza kutokea katika ngazi ya mofimu, neno, kirai, kishazi, sentensi na hata

katika ngazi ya kilongo. Jambo la kuzingatia ni kwamba, japo ubadilishaji msimbo

uhusisha lugha mbili au zaidi lakini lugha husika hazipotezi sifa zake za kiisimu

(Mochiwa 1979). Hii inamaanisha kuwa, mifumo ya lugha husika inaweza kuainishwa

kirahisi katika kilongo (Maggati 2004). Hili linaweza kudhihirishwa katika mfano

ufuatao:-

Mfano wa 2 (a)

.… zipo advantage za kutumia long term bonds na advantage ya kwanza ni

non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia internal source of finance

lakini rahisi ku-meet our development goals ….

(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge tarehe 12 Julai, 2007:32)

Tafsiri:

…… Zipo faida za kutumia mikataba ya mda mrefu na faida ya kwanza ni kuwa

haisababishi mfumko wa bei lakini faida ya pili tunatumia chanzo cha ndani cha

fedha lakini rahisi kufikia malengo yetu ya maendeleo…..

Katika matini hii mbunge alikuwa akibadilisha Kiingereza (maneno ya hati za italiki)

na Kiswahili. Mzungumzaji ameanza na neno la Kiswahili “zipo” na baadaye

akabadilisha kwenda Kiingereza “advantage” tena akarudi Kiswahili “za kutumia” na

tena Kiingereza “long term bonds” akaweka kiunganishi “na” (Kiswahili) na kufuatisha

neno la Kiingereza “advantages” . Mwendelezo wa maneno mengine katika matini hii

unaweza kuainishwa kama ifuatavyo “ya kwanza ni” (Kiswahili), “non inflationary”

(Kiingereza), “lakini” (Kiswahili) “advantage” (Kiingereza), “ya pili tunatumia”

Page 33: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

18

(Kiswahili), “internal source of finance” (Kiingereza), “lakini rahisi ku-” (Kiswahili),

“-meet our development goals” (Kiingereza). Pamoja na ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza, mfumo wa kileksika wa lugha ni rahisi kubainishwa kwa sababu kila

mfumo unajitegemea. Uzungumzaji wa namna hii ndio huitwa ubadilishaji msimbo.

Pamoja na kukumbwa na changamoto, maana zote za ubadilishaji msimbo kama

zilivyojadiliwa hapo juu zinatupa usuli kuwa, ubadilishaji msimbo huusisha walau

lugha mbili. Inahusisha ubadilishaji kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine wakati

wa mazungumzo. Sehemu ifuatayo inaainisha aina za ubadilishaji msimbo na kiwango

cha utokeaji wake katika matini kama zinavyobainishwa na wataalamu mbalimbali na

kama zinavyojitokeza katika mijadala ya Bunge.

2.2 Aina za Ubadilishaji Msimbo

Ubadilishaji msimbo hugawanywa katika aina kuu mbili ambazo ni ubadilshaji msimbo

ndani, ambao ni ubadilishaji lugha ndani ya sentensi na ubadilishaji msimbo kati,

ambao ni ubadilishaji kutoka lugha moja kwenda nyingine kati ya sentensi moja na

nyingine (Poplack 1981; 1982; Heller 1992; na Kamwangamalu 1992). Pamoja na

wataalamu mbalimbali kutofautiana katika kuelezea ubadilishaji msimbo jambo la

msingi katika mijadala kuhusu maana na aina zake ni kuwa, lazima lugha mbili au zaidi

au lahaja zihusike katika semo moja au tukio la kiusemaji.

2.2.1 Ubadilishaji Msimbo Ndani

Istilahi ubadilishaji msimbo ndani hutumika kumaanisha kubadilisha lugha ndani ya

sentensi moja (Stephens 2000). Hapa vipashio katika kiwango cha mofimu, maneno,

Page 34: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

19

virai, vishazi na ua sentensi kutoka lugha moja, mbili au zaidi vinapatikana ndani au

kati ya sentensi (Brice n.d, Muysken 2000 na Scotton 1990). Kwa mujibu wa Myers-

Scotton (1990), ubadilishaji msimbo ndani ni ubadilishaji wa lugha katika kiwango cha

mofimu, neno, kirai au kishazi. Muysken (2000:1) anabainisha vizuri zaidi kwa kudai

kuwa ubadilishaji msimbo ndani ni utumizi wa lugha ambapo vipashio vya kileksika na

kisarufi kutoka lugha mbili hujitokeza katika sentensi moja. Katika machapisho

mengine aina hii ya ubadilishaji msimbo huitwa uchanganyaji msimbo (Kalong

2008:11). Mfano ufuatao unaonesha aina hii ya ubadilishaji msimbo.

Mfano wa 2 (b)

Matini (a)

I. Mheshimiwa spika, India is one of the best country katika Railway network,

tukachukua ma-expert waje watusaidie lakini iwe chini yetu. ……….

Tutasafirisha abiria na mizigo na bidhaa at the end of the day hatuna kitu.

Halafu unampa contract ya 25 years is not a joke……

(Matini kutoka kumbukumbu rasmi za Bunge 12 Julai, 2007:83).

Tafsiri:

Mheshimiwa spika, India ni miongoni mwa nchi mashuhuri katika mtandao wa reli,

tukachukua wataalamu waje watusaidie lakini iwe chini yetu. ….. Tutasafirisha

abiria na mizigo na bidhaa mwisho wa siku hatuna kitu. Halafu unampa mkataba

wa miaka 25 sio utani ……

II. Je serikali haioni kwamba ni vyema tukajitahidi tukahakikisha kwamba the

only suppliers and the only producer wa zao hili kwa sababu tusipoingia

kwenye ku-monopolize hii product itafikia mahali suppliers wengine ndio

Page 35: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

20

watapata faida kuliko sisi ambao Mwenyezi Mungu ametujalia kuvipata vitu

hivi.

(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 30 Julai, 2007:14).

Tafsiri:

Je serikali haioni kwamba ni vyema tukajitahidi tukahakikisha kwamba

tunakuwa wazalishaji na wauzaji peke wa zao hili kwa sababu tusipoingia

kwenye kumiriki hii bidhaa itafikia mahali wauzaji wengine ndio watapata

faida kuliko sisi ambao Mwenyezi Mungu ametujalia kuvipata vitu hivi.

Matini (b)

1. …Possessive individualism ya ku-grab mali una-acquire au unazaliwa

nayo?

2. … hapa kila mtu anamwona na anaweza aji-reform zaidi kuliko hata

yule….. wengine wameji-reform wengine wanaendelea……

3. …..kwa mfano, katika nchi kama USA niliwaambia mwaka 1998 ambao

wame-import kitu kile halafu waka-export kitu kile kile……

4. …. huyu agent NDC anaji-commit kwa niaba ya serikali, inayoitwa

National Development Corporation sasa leo National Development inataka

kufanya biashara lakini inaingia in a wrong way inaji-commit kabisa………

(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge mkutano wa saba Aprili 2002:54)

Tafsiri:

1. ……. Umiriki binafsi wa kunyakua mali unauamili au unazaliwa nayo?

2. …….. hapa kila mtu anamwona na anaweza ajirekebishe zaidi kuliko hata

yule….. wengine wamejirekebisha wengine wanaendelea……

Page 36: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

21

3. …..kwa mfano, katika nchi kama USA niliwaambia mwaka 1998 ambao

waliingiza kitu kile kutoka nchi za nje halafu wakasafirisha nje kitu kile

kile……

4. …. huyu wakala NDC anajifunga kwa niaba ya serikali, inayoitwa National

Development Corporation sasa leo National Development inataka kufanya

biashara lakini inaingia in a wrong way inajifunga kabisa………

Mifano kutoka matini hizi inaonesha jinsi wazungumzaji wanavyobadilisha kutoka

lugha moja kwenda nyingine lakini ndani ya sentensi ile ile. Katika matini hizi kuna

ubadilishaji ulio ndani ya neno yaani kati ya mofimu na mofimu na ulio ndani ya kirai

na pia ndani ya kishazi ambapo viambajengo hivi kwa pamoja vianaunda sentensi.

Mathalani, ubadilishaji msimbo ulio ndani ya neno yaani kati ya mofimu na mofimu

upo katika maneno ma-expert, ku-monopolize, ku-grab, anaji-reform, wameji-reform,

wame-eport, waka-export, anaji-commit, na inaji-commit. Kimsigi maneno haya

yamekamilika na yanajitegemea kimaana na kimuundo japo yameundwa na mofimu za

lugha mbili tofauti ambapo mofimu zilizokolezwa ni za lugha ya Kiswahili na ambazo

zimeambikwa kwenye mzizi wa neno/maneno ya Kiingereza. Huu ndio huitwa

ubadilishaji msimbo ndani ya neno. Mchanganua wa mofimu katika maneno haya

unaweza kuwa kama ifuatavyo:-

Page 37: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

22

1. Ma - expert “wataalamu”

Nfs3w mz

2. A - na - ji - reform “anajirekebisha”

Nfs2u nj rej mz

3. Wa - me - ji - reform “wamejirekebisha”

Nfs3w nj rej mz

4. Ku - grab “kunyakua/chopoa”

K/kiso mz

5. I - na - ji - commit “inajifunga”

Ki/ng nj rej mz

Mnyambulisho wa maneno hapa juu unaonesha jinsi maneno hayo yalivyoundwa na

mofimu mbalimbali za lugha mbili ambapo mzizi ni wa lugha ya Kiingereza na wakati

viambishi awali vyake ni vya Kiswahili.

Page 38: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

23

Baada ya kupitia taarifa rasmi za Bunge imeonekana kuwa ubadilishaji msimbo ndani

ndio hujitokeza sana katika majadiliano ya Bunge. Hii inamaanisha kuwa wabunge

hawapendelei au hawawezi kuongea semo ndefu kwa lugha ya Kiingereza bila

kuchanganya na Kiswahili japo kinyume chake inawezekana.

Hoja ya ubadilishaji msimbo ndani kujitokeza zaidi inaungana na utafiti wa Kadeghe

(2000) na Kanyuma (2005), ambapo Kadeghe anaainisha kuwa walimu na wanafunzi

hupendelea ubadilishaji msimbo ndani ambapo ni takribani 65% ya ubadilishaji

msimbo unaojitokeza katika data za utafiti huo.

Naye Kanyuma (uk. 83) katika utafiti uliohusu ubadilishaji msimbo miongoni mwa

walimu na wanafunzi wa shule za msingi, data yake inabainisha kuwa 38% ni

ubadilishaji msimbo kati na wakati ubadilishaji msimbo ndani ni 62%.

2.2.2 Ubadilishaji Msimbo Kati

Ubadilishaji msimbo kati humaanisha kubadilisha lugha nje ya mipaka ya sentensi. Hii

inamaanisha kuwa matini nzima ya sentensi hutolewa katika lugha moja kabla ya

kubadilisha kwenda lugha nyingine katika semo ile ile (Myers-Scotton 1993).

Mfano 2 (c)

Matini (a)

Mheshimiwa Spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa

yeye, mtondogoo wao. I better warn you today comrades, you will not afford.

Hatutavumilia matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya watu

wachache. (Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 14 Julai, 2004:82).

Page 39: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

24

Tafsiri:

Mheshimiwa Spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa

yeye, mtondogoo wao. Ndugu zangu ni vizuri leo niwatahadharishe,

hamtaweza. Hatutavumilia matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya

watu wachache.

Matini (b)

Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu Minister ni nani, ni wale

wengine nisioongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe

hujui nani aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

nikamwambia uliteuliwa wewe. But you don’t seem to be. Why do you

understand me when we talk here together and when you go to your office you

are powerless, what is wrong?

(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 14 Julai, 2004:83).

Tafsiri:

Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu waziri ni nani ni wale wengine

nisiongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe hujui nani

aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikamwambia

uliteuliwa wewe. Lakini huonekani hivyo. Mbona tunapokuwa pamoja

tunaelewana lakini uendapo ofisini kwako unapoteza mamlaka, kuna tatizo

gani?

Katika matini hizi ((a) na (b)) sentensi “I better warn you today comrades, you will not

afford” kutoka matini (a) na “Why do you understand me when we talk here together

and when you go to your office you are powerless, what is wrong”?, kutoka matini (b)

Page 40: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

25

zinaonesha ubadilishaji msimbo kati. Hii ni kwa sababu tungo za Kiswahili zilizopo

awali na/au baada yake zinaonekana kuwa nje ya mipaka ya sentensi hizi na

zinajitegemea kimuundo na kimaana. Kwa mantiki hii tungo hizi sio sehemu ya

sentensi za Kiswahili zilizo karibu nazo. Hivyo basi, huu ndio ubadilishaji msimbo nje

ya mipaka ya sentensi uitwao ubadilishaji msimbo kati. Kinyume na utafiti wa Wu

(1985) na Grice (2000) wanaodai kuwa ubadilishaji msimbo kati ndio hutokea sana

katika maongezi, aina hii ya ubadilishaji msimbo inatokea mara chache katika

maongezi ya wabunge.

2.3 Tofauti Kati ya Ubadilishaji Msimbo na Ukopaji

Ubadilishaji msimbo ndani umeibua mjadala mkubwa katika tafiti za ubadilishaji

msimbo pamoja na makutano ya lugha kwa ujumla kwa sababu hakuna makubaliano

kati ya watafiti kuhusu jinsi ya kuutofautisha na ukopaji (Kibogoya 1998:03). Pamoja

na kuwa kumekuwepo na makubaliano kuwa dhana hizi inabidi zitofautishwe bado

hakuna makubaliano kuhusu ni vigezo gani vitumike kutofautisha dhana hizi. Kutokana

na hoja hii ndio maana sio rahisi kuelezea dhana mojawapo bila kudokeza tofauti zake

za msingi.

Miongoni mwa tofauti zilizopendekezwa na wataalamu mbalimbali ni pamoja na mosi,

urefu wa semo ambapo neno moja katika tungo lilichukuliwa kama ukopaji na sio

ubadilishaji msimbo (Clyne 1967; Grosjean 1982). Hoja ya msingi ni kuwa utumizi wa

neno moja au maneno ambatani yanayowakilisha neno moja yanamotishwa na uhitaji

wa kuziba mwanya wa kileksika ambayo hii ni motisha ya msingi ya ukopaji (Poplack,

Sankoff na Miller (1988), Bentahila na Davies (1983) na Bokamba (1988). Hii haiwezi

Page 41: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

26

kuwa tofauti ya msingi kwani mzungumzaji anaweza kubadilisha msimbo kwa

kuchanganya neno moja tu katika sentensi.

Mfano wa 2 (d)

1. Mimi nafikiri nalo hili tungeliangalia kwa sababu experience ndiyo inaweza

kutusaidia sana katika kujenga taasisi hii ya madini.

2. Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu Minister ni nani ni wale

wengine nisioongea nao au ni wewe tunayeongea wote…….

Katika matini hizi neno “experience” kama linavyojitokeza katika (1) na neno

“minister” kama linavyojitokeza katika (2) hayawezi kuchukuliwa kama maneno ya

mkopo kwani yana visawe vyake katika Kiswahili. Neno “experience” ni uzoefu na

“minister” ni waziri. Pia, maneno haya hayaendani na mofofonolojia ya Kiswahili.

Pili, ni kuwa iwapo neno au tungo imetoholewa katika lugha husika kimofolojia na

kifonolojia hivyo huo ni ukopaji. Hoja ya msingi ni kuwa usilimishaji wa kifonolojia na

kimofolojia wa neno husika ni kigezo cha kutofautisha ukopaji na ubadilishaji msimbo

ndani (Haugen 1973). Changamoto ya kutumia kigezo hiki ni kuwa utohoaji wa

kifonolojia ni vigumu kuubainishwa hasa pale utamkaji wa lugha fulani unapokuwa

umeathiriwa na lugha nyingine.

Kigezo kingine kinachopendekezwa na Shaffer (1975) ni cha kimtindo ambapo anadai

kuwa ubadilishaji msimbo hutokea katika mazungumzo yasiyo rasmi na wakati ukopaji

Page 42: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

27

hutokea katika mazungunzo rasmi. Katika utafiti huu hoja hii inakosa mashiko kwani

mazungumzo ya Bungeni ni rasmi lakini ubadilishaji msimbo hutokea.

Hoja nyingine inayopendekezwa kutofautisha dhana hizi na wataalamu kama Pfaff

(1979), Sridhar na Sridhar (1980), Kachru (1982), na Bentahila (1983) ni kuwa

ubadilishaji msimbo hutokea tu kwenye mazungumzo yenye kuhusisha lugha mbili

(jamiilugha uwili) ukopaji hutokea katika mazungumzo yenye kuhusisha lugha moja.

Kigezo hiki kinaibua changamoto kwani hata katika mazungumzo yenye kuhusisha

lugha mbili ukopaji unaweza kujitokeza. Mathalani, kulingana na kanuni za Bunge,

Mbunge anaruhusiwa kuchangia hoja kwa Kiswahili au Kiingereza. Lakini katika

mijadala Wabunge huweza kuhusisha maneno ya mkopo kama vile spika, kompyuta,

redio, data, ripoti na kadhalika.

Naye Berk-Seligson (1986) anaongezea tofauti nyingine kuwa maneno ya lugha moja

yanayotumiwa katika lugha nyingine lakini yakiwa na visawe katika lugha hiyo basi

ichukuliwa kuwa huu ni ubadilishaji msimbo. Changamoto katika hoja hii ni kuwa kuna

ukopaji unaosababisha uongezekaji wa visawe katika lugha husika. Kwa mfano,

maneno “shule” na “skuli” ni visawe na ni maneno ya mkopo.

Naye Myers-Scotton (1983:192) anatoa tofauti ya msingi kuwa msamiati unaotokana

na ukopaji huingia katika msamiati wa akilini mwa mzungumzaji na wakati ule

unaotokana na ubadilishaji msimbo hauwi katika mfumo wa kamusi ya akilini ya

mzungumzaji. Pia anaongezea kuwa msamiati wa ukopaji unatabirika na wakati ule wa

Page 43: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

28

ubadilishaji msimbo hautabiriki (uk. 207). Kimsingi japo hoja hii ni ya kinadharia kama

itakavyobainishwa baadaye inatupa usuli wa kutofautisha dhana hizi.

Katika utafiti huu dhana hizi ni muhimu zibainishwe utofauti wake pamoja na kuwa

wanaisimu wanaojihusisha na uchunguzi wa michakato ya uundaji wa maneno katika

lugha hasa wakijikita katika njia za ubadilishaji msimbo na ukopaji wameshindwa

kutoa tofauti za msingi za dhana hizi. Kinadharia tofauti kati yake iko wazi kwamba

ubadilishaji msimbo unajumuhisha utumizi wa vipashio kunjiano7 katika lugha lengwa.

Kiujumla inachukuliwa kuwa ubadilishaji msimbo ni ubadilishaji wa lugha wa

mzungumzaji katika muktadha fulani. Lakini ieleweke kuwa ubadilishaji kutoka lugha

moja kwenda lugha nyingine unahitaji umilisi wa lugha zote zinazohusika na hivyo

inamlazimu mzungumzaji kuelewa lugha husika. Tofauti na hili ukopaji hauhitaji

mhusika kuwa mmilisi wa lugha husika (lengwa na chanzi) bali ni matokeo ya

makutano ya lugha hizo. Kwa mantiki hii, ukopaji unaweza kutokea bila hata mzawa

wa lugha lengwa kujua au hata kuwahi kuongea lugha chanzi. Kwa mfano; Mswahili

ambaye hajui wala hajawai kusikia lugha ya Kiingereza anatumia maneno kama shati,

benki, data, baa, bia, kompyuta, redio na kadhalika ambayo kimsingi yamekopwa

kutoka lugha ya Kiingereza.

Kwa uelewa wetu ukopaji hutokea pale wazungumzaji wa lugha wanapoanza kutumia

maneno kutoka lugha mkopo bila kuwa na uelewa kuwa maneno hayo si msamiati

asilia wa lugha yao. Hata hivyo kwa vyovyote vile ukopaji na ubadilishaji msimbo ni

7 Imetafsiriwa kutoka dhana ya Kiingereza “Embedded elements”

Page 44: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

29

matokeo ya makutano ya lugha husika. Kwa mantiki hii hali ya kijamii ya dhana hizi

haiwezi kutupiliwa mbali.

Tofauti nyingine tunaungana na Scotton (keshatajwa) kuwa moja ya sababu nyingi

inayodokezwa katika machapisho mengi ni kuwa katika ubadilishaji msimbo maneno

yake hayawi msamiati wa akilini mwa mzungumzaji wakati ukopaji huongezea

msamiati katika kamusi ya akilini. Tofauti nyingine inabainishwa na Heller`s (1988:11)

kuwa ubadilishaji msimbo ni mbinu ya kimawasiliano ambayo wazungumzaji huitumia

katika hali ya utambuzi na wakati ukopaji kwa sababu umechukuliwa kama mfumo wa

lugha husika basi hutokea katika hali ya ung’amuzi bwete.

2.4 Sababu za Ubadilishaji Msimbo

Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusu ubadilishaji msimbo na sababu zake kwa ujumla.

Hizi ni pamoja na tafiti za Blommaert 1992; Myers-Scotton 1993; Romaine 1996,

Rajabu 1981 na Kanyuma 2005. Tafiti hizi kwa ujumla zimejikita katika ubadilishaji

msimbo katika mfumo wa elimu kwa mtazamo wa ufundishaji na mbinu za

kufundishia.

Katika muktadha wa matumizi ya lugha Bungeni na ubadilishaji msimbo kwa ujumla

wataalamu MacWilliam na Chuwa 1990; na Mwansoko na Tumbo-Masabo 1996

wameainisha sababu za ubadilishaji msimbo katika muktadha wa Tanzania. Kwa

kutumia data kutoka vipindi vya redio na taarifa za magazetini MacWilliam na Chuwa

(1990) pamoja na mambo mengine waliweza kuainisha sababu za ubadilishaji msimbo.

Hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la utafiti huu. Kwa kutumia sababu zilizopendekezwa

Page 45: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

30

na Grosjean (1982), waliweza kuainisha sababu zinazopelekea wabunge wachanganye

Kiingereza na Kiswahihili. Sababu hizo ni:-

a) Kujaza pengo lilipo katika msamiati ama wa mzungumzaji mwenyewe

ama wa lugha.

b) Kurejea usemi halisi wa mzungumzaji mwingine, au nahau ya lugha

nyingine.

c) Kusisitiza jambo au kutia chumvi/nguvu habari fulani.

d) Kujitambulisha na habari anazozitoa

e) Kujionyesha na kusisitiza umoja wa kundi fulani

f) Kumtenga mwingine

g) Kujishaua, kujiongezea wadhifa, kuonesha ujuzi

h) Kuwa na uvivu/kutojali

Nao utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) kwa kiasi kikubwa ulipata msingi

wake kutoka utafiti wa MacWilliam na Chuwa. Tofauti na utafiti wa awali, watafiti

hawa walifanya utafiti ambao uliwahusisha moja kwa moja wabunge na maofisa wa

Bunge.

Pamoja na mambo mengine watafiti waliwatafiti wabunge na maofisa wa Bunge

kuhusu sababu za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza wakati wa mjadala. Baada

ya kuchanganua hojaji sababu zifuatazo zilibainishwa.

a) Kutaka kueleweka/kufahamika

Page 46: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

31

b) Mazoea, ya kwamba Wabunge/wawakilishi wengi wamesoma kwa

kutumia Kiingereza na wamekuwa wakikitumia kazini kabla ya kuingia

Bungeni/Baraza la Wawakilishi

c) Kuwepo kwa neno moja la Kiingereza ambalo ni kuntu wakati hakuna

neno moja la Kiswahili na hivyo kulazimika kutumia maneno mengi ya

Kiswahili.

d) Upungufu na uchache wa neno/maneno ya Kiswahili kutotoa dhana

inayotakiwa

e) Kulemaa/ulemavu au kujionyesha

f) Kupata maana kamili ya fikra

g) Ufafanuzi wa haraka

h) Kufikiri kwa Kiingereza

i) Miswada na maandiko mengine Bungeni kutolewa katika Kiingereza

wakati majadiliano huweza kuwa katika lugha ya Kiingereza au

Kiswahili

j) Jazba (kwamba mzungumzaji anapokuwa na mori basi hajali lugha

anayotumia)

k) Kutoa mifano ambayo hueleweka vizuri zaidi kwa Kiingereza.

l) Kutojua Kiswahili barabara

m) Ugumu wa kupata maneno

n) Kanuni za Bunge hazimfungi mbunge asichanganye lugha, yaani

zinamruhusu mbunge kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

o) Kufupisha majadiliano (wabunge hupewa muda maalumu wa kutoa hoja

zao)

Page 47: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

32

Katika kipengele hiki, kama ilivyodokezwa katika utangulizi wao, wameweza

kupunguza kama si kumaliza mapungufu yaliyojitokeza katika utafiti wa MacWilliam

na Chuwa (1990) hasa katika kipengele cha sababu zinazomfanya mbunge kutumia

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni. Hii ni kwa sababu wamepata sababu

hizi kutoka kwa wabunge wenyewe. Kwa kuzingatia hili, inaonekana hakuna haja ya

kufanya utafiti tena kuhusu sababu za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Bungeni. Kwa kuwa kipengele hiki hakimo katika malengo ya utafiti huu, tuseme tu

kwamba inatosha kuzitaja sababu hizi bila kuzijadili kwa undani.

2.5 Uelewekaji wa Maongezi Yanayohusisha Ubadilishaji Msimbo.

Pamoja na kutofautiana katika kuelezea dhana ya lugha, wanaisimu wengi wakiwemo

Trudgil (1974), Sapir (1921) na Weber (1985) wanakubaliana katika dhana moja

muhimu kwamba dhima kuu ya lugha yoyote ni kuwezesha mawasiliano. Kwa

kuzingatia hoja hii, tafiti zimefanyika kubainisha kama ubadilishaji msimbo

unasababisha walengwa wa mazungumzo/maandishi kuelewa ujumbe uliolengwa na

mwandishi/mzungumzaji. Miongoni mwa watafiti hawa ni pamoja na Leung (2010),

Hammink (2000), Chung (2006), Adendorff (1996), MacWilliam na Chuwa (1990) na

Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996).

Adendorff (1996) alifanya utafiti wake nchini Afrika kusini. Utafiti huu unahusu

ubadilishaji msimbo kati ya Kiingereza na Kizulu katika muktadha wa darasani yaani

katika mijadala kati ya walimu na wanafunzi. Utafiti huu unabainisha kuwa,

ubadilishaji msimbo ni mbinu ya kimawasiliano inayowezesha walimu na wanafunzi

kuwasiliana vizuri.

Page 48: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

33

Utafiti wa Chung (2006) uliolenga kuangalia kama ubadilishaji msimbo unawezesha

mawasiliano miongoni mwa wanajamii wenye umahiri tofauti wa lugha husika. Ufafiti

uliwahusisha wanafamilia (baba, mama na watoto wao wawili) ambao walikuwa na

umahiri tofauti wa lugha za Kikorea na Kiingereza na ambao waliishi Marekani. Kwa

kuwa wanafamilia walikuwa na umahiri tofauti wa Kiingereza na Kikorea, mtafiti

anabainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unatumika kuwezesha mawasiliano miongoni

mwa wanafamilia. Utafiti huu unabainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unasaidia

kuepusha vikwazo vya kiisimu na tofauti za kiutamaduni miongoni mwa wanajamii.

Anaongeza kuwa ubadilishaji msimbo unawezesha utoaji wa maelezo ya ziada na

kusisitiza hoja. Hivyo basi, mtafiti anahitimisha kuwa, ubadilishaji msimbo ni mbinu

itumikayo kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wanajamiilugha uwili.

Tafiti hizi zinaungana na hoja ya Tay (1989) na Myers-Scotton (1995) kuwa,

ubadilishaji msimbo hutumika kama mbinu ya kimawasiliano miongoni mwa

wazungumzaji kwa kuzingatia lengo la mzungumzaji kubadili msimbo.

Utafiti mwingine ni utafiti wa MacWilliam na Chuwa (1990) ambao unajikita katika

ubadilishaji msimbo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Utafiti huu

unabainisha kuwa, maneno ya lugha ya kigeni yaliyotumiwa katika sentensi za

Kiswahili siyo maneno rahisi yanayoweza kubuniwa na mwenye kiwango kidogo cha

Kiingereza. Matokeo yake ni sentensi kutoeleweka kwa msikilizaji na hivyo kumnyima

fursa ya kufuata majadiliano ya wabunge.

Page 49: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

34

Athari nyingine iliyobainishwa katika utafiti wao ni ile ya upotoshaji wa ufasaha wa

lugha yenyewe. Ikiwa unatumia lugha mbili ambazo kimsingi ziko tofauti kabisa kuna

hatari ya kuathiri sarufi na maumbo mengine ya lugha. Hoja hii haitashughulikiwa

katika utafiti huu.

Utafiti huu kwa ujumla bado una mapengo yanayotakiwa kuzibwa. Kwanza, utafiti huu

haukuwashirikisha wazungumzaji ambao ni wabunge wala wasikilizaji yaani wananchi.

Hitimisho hili lilifikiwa kwa kusoma taarifa rasmi za Bunge, magazeti na kusikiliza

mijadala ya Wabunge redioni kama wanavyosema:-

….tulifuatilia kwa makini majadiliano ya Bunge la 1987 kwa kusikiliza

vipindi vya “LEO KATIKA BUNGE” vilivyotolewa redioni. Tulipata

pia fursa ya kuazima na kusoma nakala za majadiliano hayo kutoka

ofisi ya Bunge wakati wa kufanya utafiti huu….

Kwa kuzingatia hili, ni vigumu kubainisha kama wasikilizaji wanaelewa au hawaelewi

mijadala iendeshwayo Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza bila

kuwahusisha wasikilizaji wenyewe. Kwa mantiki hii, utafiti huu unalenga kubainisha

kama wasikilizaji wa matabaka mbalimbali wanaelewa mijadala ya Bunge inayohusisha

ubadilishaji msimbo ambapo wasikilizaji ndio chanzo cha data.

Utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) kwa kiasi kikubwa ulipata msingi

wake kutoka utafiti wa MacWilliam na Chuwa. Tofauti na utafiti wa awali, watafiti

hawa walifanya utafiti ambao uliwahusisha moja kwa moja wabunge na maofisa wa

Bunge. Nia hasa ya utafiti huu ilikuwa kusikia kutoka kwa wabunge, wawakilishi na

Page 50: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

35

maofisa walengwa wa majadiliano Bungeni kwa kuzingatia kuwa hadhira anayotarajia

mzungumzaji huathiri sana matumizi ya lugha.

Kuhusu walengwa wa mawasiliano ya wabunge na wawakilishi, utafiti unaonesha kuwa

90% ya wabunge walitambua kuwa hadhira yao ni wasikilizaji ambao ni wananchi na

umma unaowakilishwa na mbunge. Wakimnukuu mmoja wa wabunge wanasema:-

Mbunge kama mwakilishi wa wananchi na umma kwa ujumla hueleza ujumbe

wake kwa serikali kupitia spika ingawa umma wote unategemewa kumuelewa.

Katika kipengele hiki inaonesha watafiti walilenga kufahamu tu kama wabunge

wanafahamu hadhira yao ambayo ingekuwa na athari katika utumizi wao wa lugha

Bungeni. Kwa kuzingatia hili, bado kuna pengo linalotakiwa kuzibwa. Suala la msingi

si kufahamu tu hadhira yake bali ni kwenda mbali zaidi na kufahamu kama wasikilizaji

wanaelewa mijadala inayoendeshwa kwa ubadiloishaji wa Kiswahili na Kiingereza.

Ikumbukwe kuwa wabunge ndio hutumia ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Bungeni, hivyo kimantiki kuwauliza wao kuhusu athari za uzungumzaji na namna hii

kwa kiasi fulani inakosa mashiko, bali ni vizuri kuwahoji wasikilizaji ambao kwa kiasi

kikubwa ndio wanapata athari hizo. Kwa mantiki hii, utafiti huu unalenga kujaza pengo

lililoachwa katika utafiti huu.

2.6 Mbinu za Kuelewa Matini zenye Ubadilishaji Msimbo.

Dhima kuu ya lugha ni mawasiliano na ili mawasiliano yawepo ni lazima msikilizaji

aelewe nini msemaji amesema. Katika muktadha wa Bungeni, mbunge ni mtetezi

anayepaswa kuzungumzia matatizo ya wananchi Bungeni na wananchi wana shauku na

Page 51: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

36

haki ya kumsikia (na kumuelewa) mbunge wao akiwatetea (Msekwa 2000:58). Kwa

kuwa imedhihirika kuwa wabunge huchangia hoja kwa ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza na kwa kuwa Kiingereza hakieleweki vizuri kwa watanzania walio wengi,

baada ya kupitia tafiti mbalimbali imeonekana kuwa tafiti hizi hazioneshi ni kwa

namna gani wasikilizaji huelewa mijadala ya Bunge.

Utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) pamoja na mambo mengine ulijikita

katika kuelewa ni njia gani wazitumiazo wabunge na wawakilishi katika kutatua

matatizo yao ya lugha. Utafiti unabainisha kuwa, wabunge na wawakilishi hutumia njia

kadhaa ikiwa ni pamoja na kuangalia kwenye kamusi, marejeo katika maktaba ya

Bunge na hasa vitabu vya BAKITA, kuulizana, na kuunda neno linalohitajika.

Kutokana na majibu haya, bado kuna swali la msingi ambalo halijajibiwa. Kama

wabunge wanatumia njia hizi kutatua tatizo la lugha, je, wasikilizaji wanatumia njia

gani? Hivyo basi, utafiti huu unalenga kubaini mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa

mijadala ya wabunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.

2.7 Mtazamo wa Wasikilizaji Kuhusu Ubadilishaji Msimbo

Katika jamiilugha yoyote ile watu wanakuwa na mtazamo tofauti kuhusu tabia ya

ubadilishaji msimbo. Wapo wanaoichukulia kama mbinu ya kimawasiliano, huku

wengine wakiichukulia kama uzungumzaji usio na hadhi wala staha, mbaya au ukosefu

wa umahiri wa lugha husika (a). Pamoja na mitazamo hii tafiti zinaonesha kuwa

ubadilishaji msimbo ni sifa mojawapo ya jamiilugha uwili au ulumbi.

Page 52: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

37

Kutokana na hali hii tafiti kadhaa zimefanyika ili kubainisha mtazamo wa wasikilizaji

na au wazungumzaji kuhusu ubadilishaji msimbo. Miongoni mwa tafiti hizi ni pamoja

na Hammink (2000), Leung (2010), Rajabu (1991) na Kanyuma (2005).

Hammink (2000) amefanya utafiti wake nchini Meksiko kwenye jimbo la EI Paso

liliko mpakani mwa Marekani. Katika jimbo hili wanajamii wanatumia lugha za

Kiingereza na Kihispania japo katika viwango tofauti vya umilisi wa lugha husika. Kwa

mantiki hii, lugha zinazohusika katika ubadilishaji msimbo ni Kihispania na

Kiingereza. Katika utafiti huu, mtafiti amebainisha kuwa watafitiwa wanaonesha

mtazamo chanya kuhusu tabia ya ubadilishaji msimbo. Anaendelea kuelezea kuwa,

vijana (wanafunzi) ndio wanaopendelea zaidi namna hii ya uzungumzaji ambapo

69.23% ya wanafunzi wenye uwezo wa kuzungumza lugha mbili wana mtazamo

chanya kuhusu ubadilishaji msimbo. Hata hivyo, mtafiti anabainisha kuwa hali ni

tofauti kwa upande wa watu wazima ambapo wenye mtazamo chanya kuhusu

ubadilishaji msimbo ni takribani 50%.

Utafiti mwingine ni wa Leung (2010) uliofanyika nchini Hong Kong ambao pamoja na

mambo mengine amebainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji msimbo.

Utafiti huu ulijikita katika ubadilishaji msimbo kwenye matangazo ya kibiashara

unaohusisha Kichina na Kiingereza. Mtafiti anabainisha kuwa, watafitiwa wengi

walijibu kuwa wanajisikia vizuri na kawaida kusikia matangazo ya bidhaa yenye

kutumia mchanganyiko wa lugha hizi. Katika uchanganuzi wa data mtafiti

anahitimisha kwa kusema kuwa, ubadilishaji msimbo ni tabia ya utumizi wa lugha

iliyozoeleka nchini Hong Kong hivyo utokeaji wake katika matangazo ya biashara

Page 53: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

38

unaendana na hali ya maisha, utamaduni pamoja na utambulisho wa wanunuzi wa

bidhaa na hivyo ubadilishaji msimbo unakubalika miongoni mwa wanajamii hawa.

Katika utafiti huu watu wachache ndio waliokuwa na mtazamo hasi kuhusu ubadilishaji

msimbo. Hata hivyo, kuna bidhaa maalumu ambazo takribani 80% hawakupenda

zitangazwe kwa ubadilishaji wa lugha.

Kuhusu utafiti wa Rajabu (1991) alioufanya katika vyuo vikuu nchini Tanzania

alibainisha kuwa, watafitiwa walikuwa na mtazamo chanya kuhusu tabia ya ubadilishaji

msimbo. Anabainisha kuwa, 50% wanapendezwa na ubadilishaji msimbo na hujisikia

kawaida; 16% walidai kuwa hawafurahishwi na hali hii ya utumizi wa lugha. Kwa

upande mwingine 34% walidai kuwa mtu akibadilisha msimbo nao hubadilisha pia.

Kimsingi utafiti huu hauwezi kutoa jibu sahihi kuhusu mtazamo wa wasikiliaji kuhusu

ubadilishaji msimbo Bungeni katika muktadha wa Bunge la Tanzania. Hii ni kwa

sababu muktadha wa utumizi wa lugha vyuoni ni tofauti na ule wa Bungeni. Pili utafiti

huu unaonesha kuwa watafitiwa wanahusika katika uzungumzaji wa namna hii na

wanaelewa lugha zote husika yaani Kiswahili na Kiingereza. Hivyo basi kwa kuwa

walengwa wa mazungumzo na muktadha wa mazungumzo ni tofauti bado kuna

mwanya unaotakiwa kuzibwa.

Naye Kanyuma (2005) katika utafiti wake anabainisha kuwa, walimu na wanafunzi

wana mtazamo chanya kuhusu kaida ya ubadilishaji msimbo. Anabainisha kuwa 94%

ya walimu wanapendezwa na tabia ya ubadilishaji msimbo. Kwa upande wa wanafunzi

anadai kuwa 84% wanapendezwa na tabia hii ya uzungumzaji. Kimsingi kama ilivyo

Page 54: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

39

katika utafiti wa Rajabu (keshatajwa), muktadha na wahusika wa mazungumzo ni

tofauti na ya utafiti huu.

2.8 Hitimisho

Sura hii imejikita katika upitiaji wa machapisho mbalimbali yanayohusu ubadilishaji

msimbo. Katika sura hii tumeanza kwa kuelezea maana ya ubadilishaji msimbo na

baadaye kuainisha aina zake na kiwango cha utokeaji wake katika matini kabla ya

kutofautisha ubadilishaji msimbo na ukopaji. Baada ya hapo machapisho kuhusu

sababu za wabunge kubadilisha msimbo yamepitiwa na baadaye ni machapisho kuhusu

uelewekaji wa maongezi yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Pia, machapisho

kuhusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini zenye kuhusisha ubadilishaji

msimbo yamepitiwa. Mwisho, tumepitia machapisho kuhusu mtazamo wa wasikilizaji

kuhusu ubadilishaji msimbo. Upitiaji wa machapisho unatupa usuli wa kuelezea mbinu

zilizotumika katika utafiti huu. Hivyo basi, sura ifuatayo inaelezea mbinu za utafiti.

Page 55: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

40

SURA YA TATU

MBINU ZA UTAFITI

3.0 Utangulizi

Sehemu hii inahusu mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data na usampulishaji wa

populesheni. Mambo muhimu yaliyobainishwa ni eneo la utafiti, populesheni lengwa,

sampuli na usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data na uchanganuzi wa data.

Katika mjadala aina ya data iliyokusanywa imeainishwa ikiwa ni pamoja na mbinu

zilizotumika kukusanya data.

3.1 Eneo la Utafiti

Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mwanza. Mkoa huu umeteuliwa kuwa eneo la

utafiti kwa kuzingatia vigezo vingi ambavyo ni pamoja na, mosi; jamii ya wakazi wake

imeundwa na watu wa sifa mbalimbali kielimu, kiuchumi (Wakulima, Wafugaji,

Wavuvi, Wafanyabiashara na hata Wachimbaji wadogo na wakubwa). Kwa mantiki hii,

data iliyopatikana imetoka katika matabaka mbalimbali. Pili, mtafiti ameishi na

kufanya kazi mkoa huu, hii imerahisisha ukusanyaji wa data kwani mtafiti kwa kiasi

fulani anaelewa jiografia ya mkoa pamoja na mila na desturi za watafitiwa. Wilaya za

Nyamagana na Magu ndizo zilizohusika katika utafiti huu. Wilaya ya Nyamagana ni

moja kati ya wilaya mbili zinazounda jiji la Mwanza na wakati Magu ipo nje ya jiji na

hivyo inawakilisha maeneo ya vijijini.

Katika wilaya ya Nyamagana mtafiti aliteua kata za Mkolani, Pamba na Igoma. Kigezo

cha uteuzi wa kata hizi ni kwamba katika kata ya Mkolani ndipo kuna Chuo Kikuu cha

Mt. Augustini hivyo mtafiti aliweza kupata watu wa kiwango cha elimu ya chuo na

Page 56: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

41

chuo kikuu. Kata ya Pamba ni kata iliyo katikati ya jiji na hivyo inawakilisha maeneo

yenye msongamano wa watu wa aina na shughuli mbalimbali. Kata ya Igoma

inawakilisha maeneno ya pembezoni mwa jiji.

Kwa upande wa Wilaya ya Magu mtafiti aliteua kata tatu ambazo ni Lubugu, Ngasamo,

na Sukuma. Hata hivyo, mtafiti hakuwahoji watu katika eneo zima la kata husika bali

aliteua kinasibu baadhi ya vijiji. Vijiji vilivyoteuliwa ni Bubinza na Nsolla kutoka kata

ya Lubugu, Imalamate na Jiseka kutoka kata ya Ngasamo na Kitongo na Nyang’hanga

kutoka kata ya Sukuma. Hii ni kwa sababu kijiografia kata hizi zilionekana kuwa

kubwa na ingechukua muda mrefu na rasilimali kubwa kutafiti vijiji vyote vya kata

hizi.

3.2 Populesheni Lengwa ya Utafiti

Populesheni ni vitu au watu ambao kwao mtafiti anatarajia au amepata data ya utafiti

(Enon 199:13, Kanyuma 2005:63). Kwa mujibu wa Cooper (1989) na Vans (1990)

populesheni lengwa ya utafiti inahusisha jamii nzima, makundi ya watu, au vitu vingine

ambavyo kwavyo mtafiti amevihusisha kama chanzo cha data. Katika utafiti huu

populasheni imejumuisha watu kutoka matabaka mbalimbali, yaani wanaume,

wanawake, vijana, wazee, wasomi na wasio wasomi, wafanyakazi na wanafunzi, wa

vijijini na mjini, wakulima, wavuvi na wafanyabiashara.

Page 57: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

42

3.3 Sampuli na Usampulishaji

3.3.1 Sampuli

Sampuli ni kundi dogo la watafitiwa kutoka kundi kubwa ambalo humpa mtafiti data

zinazomsaidia kutoa hitimisho (Enon 1998:13). Sampuli hupatikana kwa mchakato wa

usampulishaji.

3.3.2 Usampulishaji

Usampulishaji ni mchakato wa uteuzi wa watafitiwa kutoka katika populesheni lengwa

ya utafiti ili wawe sampuli ya utafiti (Kothari 1990). Kutoka katika jamii ya watu wengi

watu wachache wanaweza kuteuliwa ili kuwa sampuli ya utafiti. Data inayopatikana

kutoka katika sampuli hiyo inatakiwa kutoa majibu ambayo yangepatikana iwapo

populasheni nzima ingehusika. Hii ni mbinu ya kupunguza gharama, muda na nguvu.

3.3.2.1 Aina ya Usampulishaji

Aina ya usampulishaji iliyotumika katika utafiti huu ni usampulishaji nasibu tabakishi.

Hii ni aina ya usampulishaji ambayo inahusisha usampulishaji tabakishi na nasibu

(Kothari 2004:16). Kwa kutumia njia hii mtafiti amepanga populasheni katika makundi

madogo madogo yaani matabaka. Matabaka yaliyopatikana ni ya makundi ya wakazi

wa mjini na wale wa vijijini, wakulima, wafanyakazi, wasomi (elimu ya msingi,

sekondari na chuo/chuo kikuu), wasiojua kusoma wala kuandika, wafanyabiashara na

pia wanaume na wanawake. Hata hivyo, kutokana na aina na malengo ya utafiti huu,

kigezo cha kiwango cha elimu ndicho kimetiliwa mkazo katika uchanganuzi na ufasiri

Page 58: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

43

wa data (itaainishwa katika sura ya nne)8. Baada ya kuainisha matabaka mtafiti

ametumia njia ya usampulishaji nasibu ili kupata idadi ya watafitiwa kutoka katika kila

tabaka. Hapa kila mtu katika tabaka husika alikuwa na nafasi sawa ya kujumuishwa.

Pia fursa na utayari wa mtafitiwa katika tabaka husika vilizingatiwa. Muainisho wa

sampuli ya utafiti huu umefupishwa katika majedwali yafuatayo:-

Jedwali la 1: Sampuli ya Utafiti kutoka katika Wilaya za Nyamagana na Magu

WILAYA

NYAMAGANA

MAGU

Jumla KIWANGO CHA

ELIMU

Me Ke Jumla Me Ke Jumla

Wasiojua Kusoma 13 16 29 41 57 98 127

Elimu ya Msingi 99 104 203 128 122 250 453

Elimu ya Sekondari 48 41 89 21 20 41 130

Chuo/Chuo Kikuu 31 25 56 06 03 09 65

Jumla 191 186 377 196 202 398 775

Jedwali hili linaonesha sampuli nzima ya utafiti kutoka katika wilaya za Nyamagana na

Magu ambayo ni watafitiwa 775 ambao ni; wanaume 387 (49.94%) na wanawake 388

(50.06%). Katika wilaya ya Nyamagana jumla ya watafitiwa ni 377 ambao ni wanaume

191 na wanawake 186. Kwa upande wa Magu jumla ya watafitiwa ni 398 ambao ni

wanaume 196 na wanawake 202.

8 Populesheni na sampuli ya utafiti inaoneshwa kwa kuzingatia kiwango cha elimu. Hata hivyo mtafiti

alihakikisha kuwa sampuli hiyo inajumuhisha watu wa tabaka mbalimbali yaani wakulima, wafugaji,

wafanyabiashara, wafanyakazi, wanafunzi/wanachuo, wakazi wa mjini na wakazi wa vijijini. Pia watu

wa rika na jinsia zote walijuishwa.

Page 59: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

44

Jedwali la 2: Sampuli ya Utafiti kutoka Kata Tatu za Wilaya ya Nyamagana

KATA MKOLANI PAMBA IGOMA

Jumla

KIWANGO

CHA ELIMU

Me Ke Jumla Me Ke Jumla Me Ke Jumla

Wasiojua Kusoma 4 6 10 3 4 7 6 6 12 29

Elimu ya Msingi 31 34 65 31 37 68 37 33 70 203

Elimu ya

Sekondari

18 15 33 16 13 29 14 13 27 89

Chuo/Chuo Kikuu 19 17 36 7 4 11 5 4 09 56

Jumla 72 72 144 57 58 115 62 56 118 377

Jedwali hili linaonesha sampuli ya utafiti katika kata tatu za wilaya ya Nyamagana

ambazo ni Mkolani, Pamba na Igoma. Katika kata ya Mkolani jumla ya watafitiwa ni

144 ambao ni wanaume 72 na wanawake 72; kata ya Pamba ni watafitiwa 155 ambao ni

wanaume 57 na wanawake 58 na kata ya Igoma ni watafitiwa 118 ambao ni wanaume

62 na wanawake 56.

Jedwali la 3: Sampuli kutoka katika Kata tatu za Wilaya ya Magu

KATA LUBUGU NGASAMO SUKUMA

KIWANGO CHA

ELIMU

Me Ke Jumla Me Ke Jumla Me Ke Jumla

Wasiojua kusoma 14 18 32 12 21 33 15 18 33

Elimu ya Msingi 42 42 84 43 39 82 43 41 84

Elimu ya

Sekondari

09 08 17 05 07 12 07 05 10

Chuo/Chuo kikuu 03 01 04 02 01 03 01 01 03

Jumla 68 69 137 62 68 130 66 65 131

Jedwali hili linaonesha sampuli ya utafiti kutoka kata tatu za Wilaya ya Magu.

Muanisho wa sampuli ni; kata ya Lubugu 137 (wanaume 68 na wanawake 69),

Ngasamo 130 (wanaume 62 na wanawake 68) na Sukuma 131 (wanaume 66 na

wanawake 65).

Page 60: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

45

Jedwali la 4: Sampuli ya Utafiti

KIWANGO CHA

ELIMU

IDADI YA WATAFITIWA

Me

%

Ke

%

Jum

la

%

Wasiojua kusoma na

kuandika

54

42.52

73

57.48

127

16.39

Elimu ya msingi 227 50.11 226 49.89 453 58.45

Sekondari 69 53.08 61 46.92 130 16.77

Chuo/Chuo kikuu 37 56.92 28 43.08 65 8.39

Jumla 387 49.94 388 50.06 775 100

Jedwali hili linaonesha sampuli nzima ya utafiti ambayo ni jumla ya watafitiwa 775.

Kwa kuzingatia kigezo cha elimu sampuli ya utafiti huu ina watafitiwa wasiojua

kusoma na kuandika 127 (16.39%) ambao ni wanaume 54 (42.52%) na wanawake 73

(57.48%); elimu ya msingi 453 (58.45%) ambao ni wanaume 227 (50.11%) na

wanawake 226 (49.89%); sekondari 130 (16.77%) ambao ni wanaume 69 (53.08%) na

wanawake 61 (46.92%); na chuo/chuo kikuu 65 (8.39%) ambao ni wanaume 37

(56.92%) na wanawake 28 (43.08%).

3.4 Mbinu za Ukusanyaji wa Data

Wataalamu mbalimbali akiwemo Cohen (2000) wanathibitisha kuwa, katika ukusanyaji

wa data za utafiti hakuna mbinu moja inayojitosheleza na hivyo kupendekeza

matumizi ya mbinu zaidi ya moja ili kupata taarifa sahihi katika sayansi ya jamii. Kwa

mantiki hii, utafiti huu umetumia mbinu kuu tatu za ukusanyaji data ambazo ni usaili,

hojaji na mijadala ya vikundi lengani. Sababu za uteuzi wa mbinu hizi zimeelezwa

katika 3.4.1, 3.4.2 na 3.4.3.

Page 61: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

46

3.4.1 Hojaji

Hii ni mbinu ya kutumia orodha ya maswali (yaliyoandikwa/kuchapwa) inayotakiwa

kujibiwa na kuelezewa na wanaotafitiwa. Mbinu hii ambayo inatumiwa sana na watafiti

wengi imetumika kwa sababu inaokoa muda na inawezesha kuwatafiti watu wengi kwa

wakati mmoja. Katika hojaji, maswali mengi yalikuwa funge ambapo watafitiwa

walitakiwa kuweka alama ya vema au kujaza sehemu zilizo wazi. Kwa kusaidiwa na

baadhi ya wanafunzi wa sekondari zilizomo katika maeneo husika watafitiwa kutoka

matabaka mbalimbali walipewa hojaji. Waliokuwa tayari walizijaza na kumrejeshea

mtafiti papo kwa papo. Kwa waliochelewa kukamilisha, mtafiti alizifuata baadae au

siku nyingine kulingana na makubaliano na mtafitiwa. Kwa zile zilizosambazwa na

wanafunzi zilirejeshwa kwa kiongozi wao aliyehakikisha zinamfikia mtafiti haraka

iwezekanavyo. Kwa kutumia njia hii hojaji 300 zilisambazwa na kila mtu aliyekuwa

tayari alipewa hojaji moja. Jumla ya hojaji 277 sawa na 92.33% zilirejeshwa na hivyo

kuwezesha kuwatafiti watu 277 ambao ni watu 194 wa elimu ya msingi, sekondari 55

na chuo/chuo kikuu 28. Katika utafiti huu mbinu hii imekuwa ya muhimu na msingi

kwa sababu imesaidia kuwahoji watafitiwa wengi kwa muda mfupi.

3.4.2 Usaili

Haya ni majibizano ya ana kwa ana (au simu, barua pepe n.k), kati ya watu wawili au

zaidi kwa lengo la kukusanya data au maoni kuhusu suala la kiutafiti (Kothari

2004:97). Katika utafiti huu watafitiwa waliulizwa maswali ya ana kwa ana ambayo

mtafiti aliyaandaa awali ili kuhakikisha kuwa mtu anatoa hoja na maoni yaliyo ndani ya

malengo ya utafiti. Mahojiano yalianza kwa mtafiti kwanza, kumsomea au kuwasomea

watafitiwa matini kutoka kumbukumbu za Bunge zinazoonesha jinsi Wabunge

Page 62: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

47

wanavyobadilisha Kiswahili na Kiingereza. Baadaye alielezea mada na malengo ya

utafiti na mwisho watafitiwa waliombwa kutoa hoja zao kwa kuzingatia maswali

yaliyoulizwa. Wakati wa mahojiano mtafiti alinakili majibu katika shajara na wakati

mwingine kinasa sauti kilitumika kurekodi (japo mara chache kwani watu wengi

hawakuwa tayari kurekodiwa) na baadaye majibu yaliwekwa katika maandishi.

Kutokana na utumizi wa mbinu hii mtafiti ameweza kuwahoji watu 227 ambao

muainisho wao ni wasiojua kusoma wala kuandika 57, elimu ya msingi 121, sekondari

33 na chuo/chuo kikuu 16. Mtafiti alihakikisha kuwa kila tabaka la watu linatoa maoni

na mchango wao kuhusu mada lengwa. Mbinu hii imesaidia sana hasa kwa watafitiwa

wasiojua kusoma na kuandika ambao hawangeweza kusoma na kujibu hojaji. Pia,

ilimpa nafasi mtafiti kufafanua maswali yaliyoonekana kuleta utata na wakati

mwingine kutoa maelekezo zaidi kwa watafitiwa. Mbinu hii pia imeepusha majibu ya

sijui au sina uhakika yaliyojitokeza katika hojaji.

3.4.3 Mijadala ya Vikundi Lengani

Vikundi lengani kwa kawaida hujumuisha kati ya watu watano na kumi na wawili

(Grbich 1999) kama alivyonukuliwa na Mutembei (2001). Jumla ya makundi 30 yenye

watu kati ya saba na kumi na mmoja yalitafitiwa ambapo makundi 16 yalitoka wilaya

ya Magu na 14 yalitoka wilaya ya Nyamagana. Mtafiti alihakikisha kuwa watu wa kila

tabaka wanahusika katika mjadala. Ilipojitokeza kuwa watu kutoka tabaka fulani

hawajapatikana katika eneo husika, mtafiti alihakikisha anatafuta watu hao katika kundi

linalofuata. Mathalani, ilikuwa kazi ngumu kuwapata watu wenye kiwango cha elimu

ya chuo au chuo kikuu katika maeneo ya vijini. Hawa mtafiti aliwapata maeneno ya

Page 63: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

48

mjini hasa mitaa ya karibu na chuo cha Mt. Augustini au walimu wa shule za sekondari.

Kwa kutumia mbinu hii mtafiti ameweza kuwatafiti watu 271 kutoka matabaka

mbalimbali ambao ni watu 70 wasiojua kusoma wala kuandika, 138 wa kiwango cha

elimu ya msingi, 42 sekondari na 21 chuo/chuo kikuu. Kabla ya kuanza kwa mjadala

mtafiti alijitambulisha na watafitiwa pia. Katika utangulizi mtafiti alielezea mada na

malengo ya utafiti. Pia mtafiti aliwasomea baadhi ya matini za kutoka kumbukumbu za

Bunge ili kuwajengea watafitiwa picha halisi ya utumizi wa lugha Bungeni. Kwa

upande wa watafitiwa walijitambulisha kwa kutaja jina (haikuwa lazima), umri,

kiwango cha elimu, kazi na mahali wanakoishi. Baada ya hapo mjadala uliodumu kwa

takribani kati ya dakika arobaini na tano na saa moja na nusu uliendeshwa ukijikita

katika maswali yaliyoulizwa na mtafiti ambayo yaliandaliwa awali. Ili kurahisisha

utunzaji wa kumbukumbu za majadiliano mbinu ya kurekodi (kutumia kinasa sauti)

ilitumika wakati wa mjadala japo si mara zote kwani watafitiwa wengine hawakuwa

tayari kurekodiwa.

3.5 Uchanganuzi wa Data

Utafiti huu umetumia mkabala wa utafiti usio wa kiidadi. Kwa mujibu wa Enon

(1998:24) huu ni mkabala wa utafiti ambao data zinazopatikana hazielezewi au

kuwakilishwa kitakwimu. Hii haimaanishi kuwa takwimu hazihusiki bali maelezo

ndiyo hutiliwa mkazo. Hata hivyo katika kuchanganua na kusasanyua data njia za

kitakwimu kama vile ujedwalishaji na utumizi wa asilimia zimetumika. Majedwali

yametumika hasa katika kuainisha majibu ya watafitiwa kiidadi na kwa kuzingatia

kiwango cha elimu. Utumizi wa asilimia umetumika kubainisha kiwango cha

kitakwimu cha waliotoa jibu husika ili kutoa ulinganifu wa data husika. Kwa kuzingatia

Page 64: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

49

jedwali husika na asilimia za data husika imewezesha kutoa uchanganuzi wa kimaelezo

unaothibitishwa na data katika idadi na asilimia ya data husika.

3.6 Hitimisho

Sura hii imebainisha na kujadili mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Mambo

muhimu yaliyobainishwa ni eneo la utafiti, populasheni lengwa, sampuli na

usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data na uchanganuzi wa data. Katika mjadala

aina ya data iliyokusanywa imeainishwa ikiwa ni pamoja na njia zilizotumika

kukusanya data. Sura inayofuata inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa matokeo ya

utafiti.

Page 65: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

50

SURA YA NNE

UWASILISHAJI, UCHANGANUZI NA UFASIRI WA DATA

4.0 Utangulizi

Sura hii inahusu uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data zilizokusanywa kutoka

uwandani. Kama tulivyoona katika sura ya tatu (kipengele cha 3.4) data zilikusanywa

kwa njia kuu tatu ambazo ni hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani. Uchanganuzi

wa data umefanywa kwa maelezo isipokuwa data zilizohitaji hesabu ndogondogo kama

vile kukokotoa asilimia, kikokotozi kilitumika. Majedwali na maelezo kuntu

vimetumika kuwasilisha matokeo ya utafiti.

Sura hii ina sehemu kuu tano. Sehemu ya kwanza ni mawasilisho kuhusu uelewekaji

wa mijadala ya wabunge kwa wasikilizaji yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo.

Sehemu ya pili inahusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa mijadala ya Bunge

yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Sehemu ya tatu ni mawasilisho ya mjadala

kuhusu mtazamo wa wasikilizaji kuhusu tabia ya wabunge ya ubadilishaji msimbo.

Sehemu ya nne, ni mjadala kuhusu kama ubadilishaji msimbo Bungeni unasababisha

wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge. Sehemu ya tano, ni mjadala wa maoni ya

wasikilizaji kuhusu mapendekezo ya kupunguza athari hasi za ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza Bungeni na lugha gani itumike kama lugha rasmi ya shughuli

za Bunge. Hii imegawanyika katika vijisehemu vidogo ambavyo ni lugha inayofaa

kuendesha shughuli za Bunge na mbinu za kuifanya lugha hiyo kutekeleza dhima hiyo.

Page 66: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

51

4.1 Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge

Sehemu hii inaonesha kiwango cha kueleweka kwa mijadala ya Bunge yenye kuhusisha

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kama tulivyoona katika sura ya pili

(kipengele 2.5), dhima kuu ya lugha yoyote ile ni kuwezesha mawasiliano miongoni

mwa wanajamii. Jambo muhimu la kuzingatia ni kuwa, wabunge wanapokuwa Bungeni

majadiliano yao yanavuka mipaka ya jengo kwa kutangazwa na vyombo vya habari na

hivyo kusikika kwa watu wengine wasiokuwepo Bungeni. Kwa mantiki hii, walengwa

wa majadiliano ya Bungeni sio tu wabunge bali pia ni wale wote wanaofuatilia

majadiliano hayo popote pale walipo. Hivyo basi, kwa kuongozwa na dhana hii tulitaka

kujua ni kwa kiwango gani wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wanaelewa

mijadala ya Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.

Kwa kutumia mbinu zilizoainishwa katika 3.4 tumeweza kupata data inayoonesha

viwango vya wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu kuelewa mijadala

inayoendeshwa Bungeni. Ili kujiridhisha na kuhakikisha kuwa majibu yanayopatikana

yanaaminika, tulijumuisha katika hojaji matini kutoka taarifa rasmi za Bunge zenye

mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza na kuwataka watafitiwa kueleza

wameelewa nini. Pia katika usaili na mijadala tuliwasomea matini hizo na kuwataka

kueleza walichokielewa kwa ufupi. Hili lilisaidia sana kwani iliepusha udanganyifu na

iligeuza zoezi zima kuwa la kivitendo. Matokeo kuhusu kiwango cha wasikilizaji

kuelewa mijadala ya Bungeni yameainishwa katika jedwali lifuatalo:-

Page 67: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

52

Jedwali la 5: Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge

KIWANGO

CHA ELIMU

Jum

la

%

Wan

aoel

ewa

%

Baa

dh

i y

a S

ente

nsi

%

Baa

dh

i y

a M

anen

o

%

Was

ioel

ewa

%

Wasiojua

Kusoma

127

16.39 00 00 15 11.81 35 27.56 77 60.63

Elimu ya Msingi 453

58.45 03 0.66 53 11.70 167 36.87 230 50.77

Sekondari 130 16.77 24 18.46 32 24.62 60 46.15 14 10.77

Chuo/Chuo

Kikuu

65 8.39 42 64.62 13 20

08

12.31

02 3.08

Jumla 775 100 69 8.9 113 14.58 270 34.84 323 41.68

Jedwali la 5 linaonesha viwango vya uelewekaji wa mijadala ya Bunge yenye

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Data inaonesha kuwa, wasikilizaji 77

(60.63%) wasiojua kusoma na kuandika, 230 (50.77%) wa kiwango cha elimu ya

msingi, 14 (10.77%) wa kiwango cha sekondari na 02 (3.08%) wa kiwango cha

chuo/chuo kikuu hawaelewi mijadala ya Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza. Kwa upande wa wasikilizaji wanaoelewa mijadala ni 00

(00%) wasiojua kusoma wala kuandika, 03 (0.66%) elimu ya msingi, 24 (18.46%)

sekondari na 42 (64.62%) chuo/chuo kikuu.

Wasikilizaji wengi wa kiwango cha elimu ya sekondari wakifuatiwa na wa elimu ya

msingi wanaonekana kuelewa baadhi ya maneno au baadhi ya sentensi. Mathalani,

wasikiliizaji 60 (46.15%) wa kiwango cha elimu ya sekondari wanaelewa baadhi ya

maneno, huku 32 (24.62%) wakielewa baadhi ya sentensi. Kwa upande wa wasikilizaji

wa kiwango cha elimu ya msingi data inaonesha kuwa 167 (36.87%) wanaelewa baadhi

ya maneno huku 53 (11.70%) wakielewa baadhi ya sentensi. Katika usaili na mijadala

Page 68: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

53

ya vikundi lengani pamoja na mambo mengine tulilenga kufahamu wanaoelewa baadhi

ya maneno au sentensi kama ni ya Kiswahili, Kiingereza au lugha zote mbili. Jumla ya

watafitiwa 89 waliulizwa swali hili na kati ya hao 14 (16.18%) walidai kuwa

wanaelewa maneno ya lugha zote mbili yaani Kiswahili na Kiingereza, huku 75

(84.27%) wakidai kuwa wanaelewa maneno ya Kiswahili tu. Kutokana na hali hii ni

idadi ndogo tu (16.18%) wanaoelewa sentensi au maneno ya Kiingereza. Kuelewa

baadhi ya maneno tu katika sentensi kunaweza kusababisha msikilizaji asifahamu

kinachozungumzwa. Hebu tuangalie mfano ufuatao:-

Mfano wa 4 (a)

….… nianze kwa kuelezea umuhimu wa infrastructure katika maendeleo ya

nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa sana, bahati yetu ni ambako

Mungu aliamua nchi hii iwe hapa iliko leo na maana yake ni geographical

position ya nchi yetu. Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie

advantage ya jiografia yetu kwa sababu engine ya maendeleo ni infrastructure,

mimi sijui nchi yoyote iliyoendelea duniani bila kuwa na infrastructure ……..

(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 12 Julai, 2007:30).

Tafsiri;

…….. nianze kwa kuelezea umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya

nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa sana, bahati yetu ni ambako

Mungu alimua iwe hapa ilipo na maana yake ni eneo la kijiografia la nchi yetu.

Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie faida ya jiografia yetu kwa

sababu injini ya maendeleo ni miundombinu, mimi sijui nchi yoyote

iliyoendelea duniani bila kuwa na miundombinu…………

Page 69: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

54

Iwapo msikilizaji hataelewa maana ya maneno infrastructure, geographical position,

advantage na engine itakuwa vigumu kuelewa matini nzima. Pamoja na hayo, hata

asipoelewa neno moja tu “infrastructure” bado itakuwa kazi ngumu kuelewa matini

nzima kwani hili ndilo neno la msingi katika matini hii na limerudiwarudiwa. Hii ndiyo

hali tuliyobaini kuwa inawakumba wasikilizaji. Mathalani, wapo waliotumia neno

“barabara” kama kibadala cha neno “infrastructure”. Kimsingi kibadala cha neno hili

ni “miundo mbinu” na japo barabara ni mojawapo ya miundombinu lakini ipo

miundombinu nyingine kama vile reli, viwanja vya ndege, bandari, minara ya simu na

kadhalika.

Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa wasikilizaji wa kiwango cha elimu ya

chuo au chuo kikuu 42 (64.62%) wanaelewa mijadala yenye kuhusisha ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza. Hii ni kwa sababu Kiingereza ndiyo lugha inayotumika

kufundishia kuanzia ngazi ya sekondari hadi chuo kikuu. Hata hivyo, pamoja na kuwa

wanachuo wanasoma kwa Kiingereza bado umahiri wao wa lugha hii si wa kiwango

cha kuridhisha. Hili lilijidihirisha tulipowataka kuelezea kwa ufupi wameelewa nini

kutoka matini zilizokuwa na mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza. Baadhi yao

walitoa maana zenye uvulivuli, utata na wengine kupotosha maana kabisa.

Kimsingi, data hii inaonesha kuwa wasikilizaji (hasa wa kiwango cha elimu ya chini)

hawaelewi mijadala ya Bungeni inayoendeshwa kwa kubadilisha Kiswahili na

Kiingereza. Kwa ujumla data inaonesha kuwa, 8.9% tu ya wasikilizaji wanaelewa

mijadala hii huku 41.68% wakiwa hawaelewi, 14.58% wakielewa baadhi ya sentensi

Page 70: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

55

wakati 34.84% wakielewa baadhi ya maneno. Majumuhisho ya data hii yanaonesha

kuwa, kiwango cha uelewaji wa mijadala ya Bungeni yenye kuhusisha ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza kinapanda kadri ya kiwango cha elimu kinavyopanda na

kinyume chake pia.

Matokeo ya utafiti huu yanapingana na tafiti za Adendorff (1996) na Chung (2000)

zinazobainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unawezesha mawasiliano miongoni mwa

watu wenye umahiri tofauti wa lugha. Pia, matokeo yanapingana na hoja ya Tay (1989)

na Myers-Scotton (1995) wanaodai kuwa, ubadilishaji msimbo hutumika kama mbinu

ya kimawasiliano miongoni mwa wazungumzaji kwa kuzingatia lengo la mzungumzaji.

Kwa upande mwingine matokeo ya utafiti huu yanaungana na hoja ya MacWilliam na

Chuwa (1990) inayodai kuwa, maneno ya lugha ya Kiingereza yanayotumiwa katika

sentensi za Kiswahili siyo maneno rahisi yanayoweza kubuniwa na mwenye kiwango

kidogo cha Kiingereza. Matokeo yake ni sentensi kutoeleweka kwa msikilizaji na hivyo

kumnyima fursa ya kufuatilia majadiliano ya wabunge. Hata hivyo, utafiti huu

umesogea mbele zaidi kwa kuainisha uelewekaji wa mijadala ya Bunge yenye

kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza kwa kuzingatia matabaka

mbalimbali ya viwango vya elimu.

4.2 Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala.

Kama ilivyoelezwa awali, dhima kuu ya lugha ni mawasiliano. Kwa kuwa ilibainika

kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji hawaelewi mijadala ya Bunge yenye kuhusisha

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza (rejea 4.1) na hivyo kuwa na vizuizi vya

Page 71: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

56

mawasiliano, tulitaka kujua mbinu wazitumiazo wasikilizaji hao kufahamu

yaliyojadiliwa katika vikao vya Bunge. Katika kipengele hiki tuliongozwa na dhana

kuwa, mbunge anachangia hoja ili aweze kueleweka si na wabunge wenzake tu bali pia

na wananchi na hivyo wasikilizaji huwa na haki na shauku ya kumsikia na kumuelewa.

Majibu ya swali hili yamefupishwa katika jedwali lifuatalo:-

Jedwali la 6: Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala.

KIWANGO

CHA ELEIMU

Jum

la

%

Kam

usi

%

Ku

uli

za

kw

a W

atu

%

Vy

om

bo

vy

a

Hab

ari

%

Was

iofu

atil

ia

%

Wasiojua

Kusoma

127

16.39

00

00 07 5.51 12 9.45 108 85.04

Elimu ya

Msingi

453 58.45 13 02.87 33 7.28 86 18.98 321 70.86

Sekondari 130 16.77 08 6.15 38 29.23 61 46.92 23 17.16

Chuo/Chuo

Kikuu

65

8.39 05

7.69

20

30.77

33

50.77

07

10.77

Jumla 775 100 26 0.03 98 12.65 192 24.77 459 59.23

Data inaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wasikilizaji wasiojua kusoma na kuandika na

wale wa kiwango cha elimu ya msingi hawatafuti mbinu mbadala za kuwafanya

waelewe mijadala ambayo hawakuielewa kutokana na kiwango cha juu cha ubadilishaji

wa Kiswahili na Kiingereza. Data inadokeza kuwa, wasikilizaji wasiofuatilia au

wasiotafuta mbinu mbadala za kuelewa mijadala ya Bunge ni; wasiojua kusoma na

kuandika 108 (85.04%), kiwango cha elimu ya msingi 321 (70.86%), sekondari 23

(17.69%) na chuo au chuo kikuu 07 (10.77%). Hii ni sawa na 59.23% ya watafitiwa

wote. Data hii inapingana na Mekacha (2000:36) anayesisitiza kuwa, katika

mawasiliano msikilizaji au msomaji huwa anafanya jitihada ya kuelewa

kinachokusudiwa.

Page 72: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

57

Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji wasomi

(wa viwango vya sekondari na vyuo) hupata maana ya mijadala ya Bunge yenye

kuhusisha ubadilishaji msimbo kupitia vyombo vya habari na au kuulizia kwa wenzao.

Mathalani, data inaonesha kuwa, 29.23% ya wasikilizaji wa viwanga vya sekondari

huulizia kwa wenzao huku 46.92% wakifuatilia kwenye vyombo vya habari. Kwa

upande wa wasikilizaji wa elimu ya vyuo na vyuo vikuu ni 30.77% wanaouliza kwa

wenzao na 50.77% wanaofuatilia kwenye vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu

kwanza, asilimia kubwa ya wasomi wanaishi mijini ambako vyombo vya habari kama

vile magazeti, runinga, redio na mitandao hupatikana kwa uhakika. Kadri ya kiwango

cha elimu kinavyopanda, uwezekano wa kutumia vyombo vya habari unaongezeka pia.

Sababu za msingi ni kuwa, wasomi wa ngazi ya juu ndio huishi mijini na pia wana

uwezo wa kununua magazeti, kutumia mtandao na hata kumiliki redio na runinga. Pia

sio rahisi kupata vyombo vya habari kama vile magazeti, runinga na mitandao katika

maeneo ya vijijini ambapo asilimia kubwa ya watanzania hasa wa viwango vya chini

vya elimu huishi. Redio ndizo hupatikana katika maeneo mengi ya vijijini lakini

kutokana na ukosefu wa umeme na umaskini, watu walio wengi hawazisikilizi mara

kwa mara na kwa wale wanaozisikiliza (hasa vijana) hutafuta vituo vinavyopiga

muziki.

Pili, wasomi wanaweza kuulizana wao kwa wao kwani kwa kiasi fulani wana uelewa

wa lugha ya Kiingereza. Hii inadhihirishwa na data kwani kadri kiwango cha elimu

kinavyoongezeka, asilimia ya wanaouliza kwa wenzao inazidi kupanda. Mathalani, data

inaonesha kuwa katika sampuli ya wasiojua kusoma na kuandika wanaotumia mbinu hii

Page 73: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

58

ni 07 (5.51%), elimu ya msingi ni 33 (7.28%), sekondari ni 38 (29.23%), na wasikilizaji

wa kiwango cha chuo/chuo kikuu ni 20 (30.77%). Jambo muhimu la kuzingatia katika

hoja hii ni kwamba, wasomi na wenye kujua Kiingereza ni takribani asilimia tano

(Msanjila 2004:45 akimnukuu Schmied 1989). Kwa mantiki hii Watanzania

wanaoelewa mijadala yenye kuhusiha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni

takribani asilimia tano9. Pia kama anavyodai Rubanza (2005:4) ndani ya lugha kuna

vionjo ambavyo havihamishiki kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Hata kama

tafsiri zitafanyika lazima maudhui ya yale yazungumzwayo katika lugha moja

hayajipambanui kikamilifu katika lugha nyingine. Kwa hoja hii, (kama tutakavyoona

katika 4.5.1) ili kuwezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake ni vema

lugha ya Kiswahili ikatumika wakati wote hasa pale ambapo hakuna hitaji la

kubadilisha lugha.

Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa watanzania hawana tabia na hulka ya

kurejea vitabu maalumu kama kamusi ili kutafuta kuelewa jambo fulani. Data

inaonesha kuwa, watafitiwa 13 (2.87%) wa kiwango cha elimu ya msingi, 8 (6.15%)

sekondari na 5 (7.69%) wa chuo/chuo kikuu ikiwa ni 0.03% ya watafitiwa ndio hutumia

kamusi kuelewa maneno ambayo hayakueleweka. Jambo hili linadhihirisha kuwa sio tu

kuwa watanzania walio wengi hawana kamusi bali pia na wale wenye nazo

hawazitumii kutatua matatizo ya kiisimu kama vile kutafuta maana za maneno. Pia,

katika ukusanyaji wa data neno “kamusi’ lilionekana kuwa geni kwa watafitiwa wa

kiwango cha elimu ya msingi na wale wasiojua kusoma na kuandika na baadhi ya

9 Kwa mujibu wa data ya utafiti huu (rejea 4.1) wanaoelewa mijadala yenye kuhusisha ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza ni 8.9% ya watafitiwa wote.

Page 74: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

59

watafitiwa wa sekondari. Hii inadhihirisha kuwa, shule nyingi hazina maktaba wala

vitabu muhimu vya rejea kwa wanafunzi ikiwemo kamusi.

Kimsingi katika kipengele hiki tulilenga kubainisha kama kuna mbinu mbadala

zitumiwazo na wasikilizaji kupunguza vikwazo vya kimawasiliano vinavyosababishwa

na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Data inabainisha wazi kuwa, asilimia

kubwa ya watanzania wa viwango vya chini vya elimu hawana mbinu mbadala na

hivyo hawapati ujumbe kama ulivyokusudiwa na mzungumzaji yaani mbunge.

Mathalani, data inaonesha kuwa wasikilizaji 108 (85.04%) wasiojua kusoma wala

kuandika, na 321 (70.86%) wa kiwango cha elimu ya msingi hawana mbinu mbadala za

kuelewa mijadala inayohusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Ikumbukwe

kuwa, kitakwimu watanzania wenye kiwango cha elimu ya msingi/kati na wale

wasiojua kusoma na kuandika ni zaidi ya 85% ya populesheni nzima ya watanzania.

Kwa mantiki hii, zaidi ya 85% ya watanzania hawaelewi mijadala ya Bungeni yenye

kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza na mbaya zaidi hawana mbinu

mbadala za kuwafanya waelewe mijadala hii. Kiisimu hii ni kinyume cha dhima kuu ya

lugha kwani maongezi yoyote lazima yafikishe ujumbe kwa mlengwa wa mawasiliano.

4.3 Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Mtazamo wa Wasikilizaji

Kama ilivyoelezwa katika 2.7 katika jamiilugha yoyote watu wanakuwa na mitazamo

tofauti kuhusu tabia ya ubadilishaji msimbo pamoja na kuwa ni sifa mojawapo ya

jamiilugha ulumbi. Wapo wanaoichukulia kama mbinu ya kimawasiliano huku wengine

wakiichukulia kama uzungumzaji usio na hadhi wala staha au ukosefu wa umahiri wa

lugha husika. Kwa mantiki hii, kuna kambi mbili kuhusu hili. Kambi ya kwanza

Page 75: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

60

inayochukulia ubadilishaji msimbo kama mbinu ya kuwezesha mawasiliano ina

mtazamo chanya huku kambi ya pili inayochukulia ubadilishaji msimbo kama ukosefu

wa umahiri wa lugha husika ina mtazamo hasi.

Kutokana na mjadala huu tumeonelea ni vema kubainisha mtazamo wa wasikilizaji

kuhusu tabia ya wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Hivyo basi, watafitiwa

waliulizwa kama hawafurahishwi, hawajali, wanajisikia kawaida au wanapendezwa na

namna hii ya uzungumzaji wa wabunge. Majibu ya maswali hayo yamefupishwa katika

jedwali lifuatalo ambapo muainisho wake umezingatia viwango vya elimu.

Jedwali la 7: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza: Mtazamo wa Wasikilizaji

KIWANGO

CHA ELIMU

JUM

LA

%

Was

iofu

rah

i-

shw

a

%

Was

ioja

li

%

Kaw

aid

a

%

Wan

aop

end

e-

zwa

%

Wasiojua

Kusoma

127 16.39 112 88.19 09 07.09 02 1.57 4 3.15

Elimu ya Msingi 453 58.45 394 86.98 19 4.19 18 3.97 22 4.86

Sekondari 130 16.77 90 69.23 4 3.08 25 19.23 11 8.46

Chuo/Chuo

Kikuu

65

8.39 37

56.92

01

1.54

20

30.77

07

10.77

Jumla 775 100 633 81.68 33 4.26 65 8.39 44 5.68

Jedwali la 7 hapo juu linaonesha kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali

ya wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Kwa maneno mengine tunaweza

kusema kuwa, wana mtazamo hasi kuhusu namna hii ya ubadilishaji msimbo. Data

inaonesha kuwa, wasikilizaji 112 (88.19%) wasiojua kusoma na kuandika, 394

(86.98%) wenye elimu ya msingi, 90 (69.23%) sekondari na 37 (56.92%) wa kiwango

Page 76: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

61

cha chuo/chuo kikuu hawafurahishwi na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza

Bungeni.

Hata hivyo, tofauti na wanaisimu kama vile Bloomfield 1927; Weinreich 1953;1968 na

Becker 1997 ambao wanauchukulia ubadilishaji msimbo kama ukosefu wa umahiri wa

mzungumzaji wa lugha husika na hivyo wana mtazamo hasi, watafitiwa wana mtazamo

hasi kwa sababu zilizoainishwa katika 2.5. Miongoni mwa sababu hizi ni pamoja na:-

a) Wasikilizaji hawaelewi mijadala na hivyo kutopata ujumbe uliokusudiwa

b) Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni kutoithamini lugha ya taifa yaani

Kiswahili na utamaduni wake

c) Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni kuwatenga wasikilizaji wasioelewa

mojawapo ya lugha hizo.

Data inaonesha kuwa, idadi ya wasikilizaji wasiofurahishwa na ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza inapungua kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka na

kinyume chake kwa wale wanaopendezwa. Pia idadi na kiwango cha wasiojali

kinapungua kadri ya kiwango cha elimu kinavyoongezeka huku wanaojisikia kawaida

idadi yao ikiongezeka kadri ya kiwango cha elimu kinavyoongezeka. Data hii

inadokeza jambo muhimu kuwa, kuna sababu tofauti tofauti zinazofanya watu wawe na

mtazamo hasi. Tunaweza kusema kuwa, idadi inakuwa kubwa kwa wale wa viwango

vya chini vya elimu kwa sababu pamoja na sababu walizonazo wale wa viwango vya

juu vya elimu, inaongezeka sababu ya kutoelewa Kiingereza, huku wale wa viwango

vya juu vya elimu wakiwa na sababu za kukithamini Kiswahili na utamaduni wake,

kuiheshimu hadhi ya Bunge na kadhalika.

Page 77: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

62

4.4 Ufuatiliaji wa Mijadala ya Bunge.

Kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji wana mtazamo hasi

kuhusu wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza, tulitaka kujua kama hali hii

inaweza kusababisha wasikilizaji waamue kutofuatilia mijadala ya Bunge inayorushwa

kupitia vyombo vya habari kama vile redio na runinga. Kwa mujibu wa Bell (1984)

mtazamo wa wasikilizaji kuhusu namna ya uzungumzaji wa mzungumzaji ndio

hutawala uteuzi wa jinsi ya kuzungumza. Kwa mantiki hii, iwapo mzungumzaji atateua

namna fulani ya uzungumzaji ambayo kwayo wasikilizaji wake wana mtazamo hasi,

basi hawatamsikiliza na watakuwa na mtazamo hasi kwa huyo mzungumzaji. Kwa

kuongozwa na hoja hii, tuliwahoji wasikilizaji ili kujua kama ubadilishaji msimbo

unasababisha wasifuatilie mijadala ya Bunge. Majibu ya swali hili yamefupishwa

katika jedwali lifuatalo:-

Jedwali la 8: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Unasababisha Wasikilizaji

Wasifuatilie Mijadala ya Bunge?

KIWANGO

CHA ELIMU

Jum

la

% Nd

iyo

%

Kw

a K

iasi

Fu

lan

i

%

Hap

ana

%

Wasiojua Kusoma 127 16.39 28 22.05 35 27.56

64

50.39

Elimu ya Msingi 453 58.45 91 20.09 104 22.96 258 56.95

Sekondari 130 16.77 07 5.38 31 23.85 92 70.77

Chuo/Chuo Kikuu 65 8.39 01 1.54 08 12.31 56 86.15

Jumla 775 100 127 16.39 178 22.97 470 60.65

Data inaonesha kuwa, ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza una asilimia ndogo

(16.39%) ya kusababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge. Mathalani,

wasikilizaji 28 (22.05%) wasiojua kusoma na kuandika, 91 (20.09%) elimu ya msingi,

Page 78: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

63

07 (5.38%) sekondari na 01 (1.54%) chuo/chuo kikuu, wote walidai kuwa ubadilishaji

wa Kiswahili na Kiingereza hausababishi washindwe kufuatilia mijadala ya Bunge.

Wakati huo, watafitiwa 178 (22.97%) walidai kuwa kwa kiasi fulani unasababisha

wasifuatilie mijadala ya Bunge. Kwa upande mwingine, wasikilizaji 470 (60.65%)

walidai kuwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza hauwasababishii waamue

kutofuatilia mijadala ya Bunge. Mathalani, wasikilizaji 64 (50.59%) wasiojua kusoma

na kuandika, 258 (56.95%) elimu ya msingi, 92 (70.77%) sekondari na 56 (86.15)

chuo/chuo kikuu walisema kuwa ubadilishaji msimbo hausababishi waache kufuatilia

mijadala ya Bunge.

Pia data inaonesha kuwa, kiwango cha kufuatilia mijadala ya Bunge kinapanda kadri

kiwango cha elimu cha wasikilizaji kinavyopanda. Kama ilivyoainishwa katika 4.2 hii

ni kwa sababu wasomi ndio wako mijini na wana uwezo wa kupata vyombo vya habari

kama vile redio, rununga, magazeti na mtandao.

Kimsingi, data hii kwa ujumla inapingana na mawazo ya Bell (keshatajwa) kwani kama

tulivyoona katika kipengele 4.3 wasikilizaji wana mtazamo hasi kuhusu hali ya

wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza lakini bado wanaweza kufuatilia

mijadala yenye kuhusisha uzungumzaji wa namna hii. Jambo hili linadhihirisha

umuhimu wa Bunge kwa wasikilizaji kwani japokuwa hawapati ujumbe kama

ilivyokusudiwa (rejea 4.1) na japokuwa wana mtazamo hasi kuhusu tabia ya wabunge

kubadilisha Kiswahili na Kiingereza (rejea 4.3) bado wanaweza kufuatilia mijadala ya

Bunge.

Page 79: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

64

Hata hivyo, katika mijadala na mahojiano ilibainika kuwa wasikilizaji walio wengi hasa

wa vijijini hawafuatilii mijadala ya Bungeni mara kwa mara. Walipodadisiwa kama

kuna sababu nyingine zinazowafanya wafuatilie mijadala mara chache, miongoni mwa

sababu zilizotajwa ni: (1) kukosa muda wa kuangalia au kusikiliza kutokana na kuwa

na shughuli nyingi, (2) umaskini unaosababisha wakose redio au runinga, (3) ukosefu

wa umeme, (4) wabunge kutochangia hoja muhimu zenye kutia hamasa ya kusikiliza na

(5) kutokuwa na hobi ya kusikiliza mijadala ya Bunge.

4.5 Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Maoni ya Wasikilizaji

Kutokana na uchanganuzi wa data, imebainika kuna makundi makuu mawili ya maoni

yaliyotolewa na wasikilizaji. Haya yote yanalenga kuondoa athari za ubadilishaji

msimbo Bungeni kwa kupendekeza mbinu zitakazowafanya wabunge wasichangie hoja

kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Sehemu ya kwanza inahusisha maoni

kuhusu ni lugha gani inayofaa kuendeshea shughuli za Bunge ambapo tumepata

makundi madogo matatu ya wasikilizaji, yaani wanaopendekeza Kiswahili tu,

wanaopendekeza Kiingereza tu na wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza. Bila

shaka, kila kundi limetoa sababu zake kuhusu sababu za kupendekeza lugha mojawapo.

Kama tutakavyoona data inaonesha kuwa, asilimia 85.55% ya watafitiwa

wanapendekeza Kiswahili tu. Hawa wanaongozwa na dhana kuwa, iwapo Kiswahili tu

kitateuliwa kuwa lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge, pamoja na mambo

mengine kutakuwa na uwezekano wa wabunge kutochanganya Kiswahili na Kiingereza

na hivyo wasikilizaji kupata ujumbe kama ulivyokusudiwa. Kundi la pili la maoni ni

maoni ya jumla yanayolenga kuhakikisha kuwa ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza unakomeshwa au kupunguza athari zake kwa wasikilizaji. Kimsingi

Page 80: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

65

tukichanganua kwa undani maoni ya kundi hili yanalenga kukifanya Kiswahili kuwa

lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge.

4.5.1 Lugha ya Shughuli za Bunge

Bunge ni chombo cha uwakilishi wa watu. Chombo hiki kimeundwa kwa mujibu wa

Katiba ya nchi, na muundo wake, pamoja na baadhi ya majukumu yake, vile vile

yameelezwa katika katiba hiyo. Majukumu ya Bunge yametamkwa katika ibara ya

63(2) ya katiba ya nchi kwamba:

Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho

kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, ya kusimamia na kuishauri

Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji

wa majukumu yake.

Bunge linatekeleza majukumu yake yote kwa njia ya vikao vyake. Kwa hiyo jambo

lolote linalohitaji uamuzi wa Bunge, huamuliwa katika mikutano rasmi ya Bunge. Bila

shaka, ili kumudu jukumu hili lazima kuwepo na lugha inayofaa kuwezesha

mawasiliano kati ya wabunge na serikali na kati ya wabunge na wasikilizaji yaani

wananchi na pia kati ya serikali na wananchi kupitia kwa wabunge. Lugha inayofaa

kwa mujibu wa Sewangi (2004:87-88) kama anavyowanukuu wanaisimu Rubagumya

(1986) na Massamba (1993), ni ile inayofikisha ujumbe au inayoeleweka kwa watu

wanaohusika. Kanuni za kudumu za Bunge zinadai kuwa; “Shughuli za Bunge

zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo

kutolewa” (toleo la 2004 kanuni ya 118(1)).

Page 81: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

66

Kimsingi tuseme tu kwamba, suala la ni lugha gani inafaa kuendeshea shughuli za

Bunge linahusiana moja kwa moja na dhana ya upangaji lugha. Huu ni mchakato

unaohusu uamuzi wa makusudi kabisa wa kuchagua lugha mojawapo, kati ya lugha

zilizopo, na kuiendeleza na kuikuza kwa ajili ya matumizi maalumu (Msanjila

2009:76). Ikumbukwe kuwa, uamuzi wa lugha gani itumike, wapi, kwa matumizi gani

na kwa kiwango gani ni uamuzi wa kisera; na kama tujuavyo utungaji wa sera ni wajibu

wa serikali baada ya kuidhinishwa na Bunge.

Pamoja na hayo, ili serikali ifikie uamuzi huo ni lazima iwahusishe wataalamu wa

masuala hayo ili kujiridhisha kuwa maamuzi hayo yanaendana na hali halisi ya jamii

husika na makusudi ya uteuzi wa lugha hiyo. Bila shaka, wataalamu hukamilisha kazi

hii kwa kufanya tafiti zenye kuihusisha jamii. Kwa kuongozwa na dhana hii, tuliwataka

wasikilizaji kutoa maoni yao kuhusu nini kifanyike kwa upande wa lugha ya kutumia

Bungeni au kwa maneno mengine ni lugha gani inayofaa/zinazofaa kuwa lugha rasmi

ya/za kuendeshea shughuli za Bunge.

Maoni ya wasikilizaji kuhusu swali hili yalijitokeza katika makundi makuu matatu

yaani wanaopendekeza Kiswahili tu, wanaopendekeza Kiingereza tu na

wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza. Bila shaka, kila kundi lilitoa sababu za

kupendekeza lugha hiyo au hizo ambazo zitabainishwa baadaye. Baada ya kuchanganua

data matokeo yake yamewasilishwa katika jedwali lifuatalo:-

Page 82: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

67

Jedwali la 9: Mapendekezo ya Lugha ya Shughuli za Bunge

KIWANGO

CHA ELIMU Jum

la

%

Kis

wah

ili

tu

%

Kii

ng

erez

a tu

%

Kis

wah

ili

na

Kii

ng

erza

%

Wasiojua Kusoma 127 16.39 118 92.91 00 00 09 7.09

Elimu ya Msingi 453 58.45 403 88.96 05 1.10 45 9.93

Sekondari 130 16.77 101 77.69 04 3.08 25 19.23

Chuo/Chuo Kikuu 65 8.39 41 63.08 4 6.15 20 30.77

Jumla 775 100 663 85.55 13 1.68 99 12.77

Mchanganuo wa data unaonesha kuwa, wasikilizaji 663 (85.55%) wanapendekeza

kuwa Kiswahili kinafaa zaidi, 99 (12.77%) wanapendekeza Kiingereza na 13 (1.68%)

wanapendekeza Kiswahili na Kiingereza kuendelea kutumika kwa pamoja.

Muainisho zaidi kwa kuzingatia matabaka mbalimbali ya kielimu unaonesha

wanaopendekeza Kiswahili tu ni: wasiojua kusoma na kuandika 118 (92.91%), elimu

ya msingi 403 (88.96%), sekondari 101 (77.69%), na elimu ya chuo/chuo kikuu 41

(63.08%). Wanaopendekeza Kiingereza tu ni: wasiojua kusoma na kuandika 00 (00%),

elimu ya msingi 05 (1.10%), sekondari 04 (3.08%), na elimu ya chuo/chuo kikuu 04

(6.15%). Kwa upande wa wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza ni: wasiojua

kusoma na kuandika 09 (7.09%), elimu ya msingi 45 (9.93%), sekondari 25 (19.23%),

na elimu ya chuo/chuo kikuu 20 (30.77%).

Kwa ujumla data inaonesha kuwa, idadi kubwa ya wasikilizaji wanapendekeza

Kiswahili tu. Mathalani, data inaonesha kuwa watafitiwa 663 ambao ni sawa na 85.55%

ya sampuli nzima ya utafiti wanapendekeza kuwa Kiswahili kinafaa kuwa lugha rasmi

na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hii inaungana na mkabala unaoongoza

Page 83: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

68

utafiti huu “MKAMA” kama ulivyoasisiwa na Fishman (1971) unaodai kuwa, lugha au

lahaja za lugha husika zipewe dhima maalumu katika jamii. Kama matokeo ya utafiti

yanavyobainisha, mkabala huu unatetea kuwa kuna mazingira ya kitaasisi yahusuyo

mawanda (mada, sehemu na wahusika) ambapo kwayo lugha moja inafaa zaidi ya

nyingine. Hivyo basi, kadri ya mkabala huu inatakiwa ianishwe ni lugha gani rasmi ya

kutumika katika shughuli zake zote. Kwa mantiki hii, data inaungana na mkabala huu

kwamba lazima lugha moja yaani Kiswahili katika muktadha wa Bunge la Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania iwe lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge kwani

kinaendana na muktadha (mahali, matukio, mada na wahusika) wa sehemu hii.

Ikumbukwe kuwa, muundojamii ndio huongoza uteuzi wa lugha husika kwa kuzingatia

sababu maalumu. Kwa kuzingatia hili watafitiwa, walitoa sababu kadhaa kutetea kuwa

Kiswahili kinafaa zaidi ya lugha nyingine ambapo sababu hizo zimewasilishwa katika

jedwali lifuatalo:-

Page 84: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

69

Jedwali la 10: Sababu za Kutetea Kiswahili Kuendeshea Shughuli za Bunge

Sababu za kufaa kwa Kiswahili tu

Idadiya wasikilizaji

%

Kinaeleweka kwa Watanzania wengi 643 96.98

Ni lugha ya taifa 617 93.06

Kinatambulisha utaifa wa Watanzania 570 85.97

Kimefungamana na utamaduni na jadi ya Watanzania 557 84.01

Kinawaunganisha Watanzania kama kilivyowaunganisha katika

kudai uhuru kutoka kwa mkoloni

555 83.71

Kinaendana na jamii ya Watanzania 530 79.94

Hakijinasibishi na tabaka au kabila lolote hivyo kuondoa ubaguzi 477 71.95

Sio Wabunge wote wanaofahamu Kiingereza 470 70.89

Kinawaepusha Watanzania na utumwa wa kifikra 456 68.78

Ni rahisi kueleweka kwani kinaendana na lugha za kibantu 444 66.97

Ili kukilinda na kukikuza Kiswahili 411 61.99

Ili kuondokana na kero ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza 332 50.08

Kimeruhusiwa kutumika katika Bunge la Afrika 192 28.96

Jedwali la 10 hapa juu linaonesha sababu za kutetea kufaa kwa Kiswahili kuendeshea

shughuli za Bunge kama zilizotolewa na watafitiwa. Baadhi ya sababu zilitolewa na

watafitiwa walio wengi10

wakati baadhi zikitajwa na wachache. Hata hivyo, hoja hizi

zinaonesha kuingiliana na hivyo tunaweza kuzichanganua zaidi na kupata sababu

zifuatazo:-

I. Kiswahili kinaeleweka kwa Watanzania wengi

II. Ni lugha ya taifa na inafungamana na utamaduni wa Watanzania

10

Watafitiwa walikuwa huru kutaja sababu nyingi kadri wawezavyo, hivyo kuna sababu ambazo pamoja

na kutaja sababu nyingine zilikuwa zikitajwa mara kwa mara

Page 85: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

70

III. Ni lugha ya umoja

IV. Kinawaepusha na utumwa wa kifikra

V. Ili kukilinda na kukikuza Kiswahili

VI. Ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika

4.5.1.1 Kiswahili Kinaeleweka kwa Watanzania Wengi

Hoja hii inaunganisha sababu tatu kama zinavyojitokeza katika jedwali la 10 ambazo

ni: mosi, kwamba Kiswahili kinafahamika kwa watanzania wengi; pili, kwamba sio

wabunge wote wanafahamu Kiingereza; na tatu ni kwamba ni rahisi kueleweka kwani

kinaendana na lugha za kibantu. Katika muktadha huu watafitiwa wanatetea kuwa sifa

hizi zinatosha kukifanya Kiswahili kufaa kuwa lugha rasmi na pekee ya kuendeshea

shughuli za Bunge. Kama tulivyoona katika 4.5.1 lugha inayofaa ni ile inayofikisha

ujumbe au inayoeleweka na kufahamika kwa watu wanaohusika. Kwa mujibu wa

Mekacha (2000:85) wanaisimu na watu wengine wote wanakubaliana kuwa, hadi

mwaka 2001 watanzania takribani wote (100%) wanafahamu na kutumia Kiswahili

kwa namna moja au nyingine. Ongezeko la idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini

Tanzania kuanzia mwaka 1870 hadi 2000 linaainishwa katika jedwali lifuatalo:-

Page 86: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

71

Jedwali la 11: Ongezeko la Idadi ya Watumiaji wa Kiswahili Tanzania

Mwaka Idadi ya watu wote

(milioni)

Watumiaji wa Kiswahili

(milioni)

Asilimia

(%)

1870 4 0.08 2

1900 6 1 17

1940 9 3 33

1960 12 6 50

1978 15 11 74

1985 22 20 90

2000 30 30 100

Chanzo: Mekacha (2000:86)

Jedwali hili linaonesha jinsi kunavyokuwepo na ongezeko la watumiaji wa Kiswahili

kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya lugha hii katika kipindi chote cha historia ya

kuenea kwake. Kwa mantiki hii, kama kigezo cha kueleweka na kufahamika kwa

wasikilizaji kikizingatiwa, tunategemea Kiswahili kupewa hadhi ya kuwa lugha rasmi

na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.

Pia, izingatiwe kuwa Kiswahili kinaendana na lugha za kibantu ambazo kimsingi

zinaunda idadi kubwa ya lugha zinazopatikana Tanzania. Ni kutokana na hoja hii

watafitiwa walipendekeza kuwa kiruhusiwe kutumika kama lugha rasmi ya kuendeshea

shughuli za Bunge kwani itakuwa rahisi kwa mtanzania anayefahamu lugha mojawapo

ya kibantu kuelewa kinachozungumzwa Bungeni. Wakati wa kukusanya data mtafiti

alilishuhudia hili kivitendo kwani kuna watafitiwa waliokuwa hawawezi kuongea

Kiswahili kabisa (waliongea Kisukuma) lakini kwa kuwa mtafiti aliongozana na mtu

aliyefahamu Kiswahili na Kisukuma, ilimlazimu mtu huyo awe mkalimani. Hata hivyo,

Page 87: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

72

mkalimani alikuwa na kazi ya kutafsiri katika Kiswahili kinachosemwa na mtafitiwa

(aliyetumia Kisukuma) huku maswali yaliyoulizwa na mtafiti kutohitaji kutafsiriwa

kwani watafitiwa walielewa Kiswahili japo wanashindwa kukiongea. Pia kuna maneno

mengine ya Kisukuma ambayo mtafiti aliyaelewa bila kutafsiriwa na mkalimani (japo

mtafiti hafahamu Kisukuma) kwani yaliendana na Kiswahili. Kwa ushahidi huu,

inatosha tu kusema kwamba, kwa kuwa Kiswahili kinaendana na lugha za Kibantu

(Chachage 2004:12) na jamii ya watanzania walio wengi ni wabantu ni vema kikawa

lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.

Hoja nyingine iliyodokezwa ni kwamba, si wabunge wote wanafahamu na kukielewa

Kiingereza. Katika mijadala ya vikundi lengani mtafitiwa mmoja alikuwa na haya ya

kusema:-

Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (akiinukuu ibara

ya 67 (a) japo hakuitaja katika mjadala) mojawapo ya sifa ya mtu kuwa mbunge

ni kuwa awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza. Kwa

mantiki hii mtu anayeelewa kusoma na kuandika Kiswahili tu ana sifa ya kuwa

Mbunge. Hivyo basi, Kiswahili kiwe lugha pekee ya Bunge ili kuwafanya

wabunge wenye sifa hii kuelewa na kuwa katika nafasi nzuri ya kujenga hoja.

Pointi ya msingi inayopatikana katika hoja hii ni kuwa, suala la kutoelewa Kiingereza

haliwakumbi wasikilizaji tu bali pia na wabunge wenyewe. Hatusemi kuwa wabunge

wote hawaelewi Kiingereza vizuri, la hasha; wapo wataalamu na mahiri wa lugha hii ila

uzuri ni kuwa wanaelewa na Kiswahili pia kwani ndiyo lugha wanayoitumia katika

harakati za kuomba ridhaa kwa wananchi. Hivyo basi, Kiswahili kinafaa kutumika

Page 88: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

73

kwani kitaondoa tatizo la kiisimu kwa wasikilizaji na wabunge pia kwa sababu umahiri

katika lugha ni msingi wa ufikishaji ujumbe kwa usahihi zaidi bila ya upotoshaji (Shoo

2004:80). Kama tutakavyoona baadaye mojawapo ya njia ya kuwezesha hili ni

kuhakikisha kuwa miswada na nyaraka muhimu za Bunge zinakuwa katika lugha ya

Kiswahili.

4.5.1.2 Lugha ya Taifa na Utambulisho wa Watanzania

Hoja hii inaunganisha sababu nne kama zinavyoainishwa katika jedwali la 4.6, ambazo

ni: mosi, Kiswahili ni lugha ya taifa; pili, kinautambulisha utaifa wa watanzania; tatu,

kimefungamana na utamaduni na jadi ya watanzania; na nne, kinaendana na jamii ya

watanzania.

Tukianza na hoja kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa, lugha hii ilipewa hadhi hii mwaka

1963. Kutokana na hadhi hii watafitiwa wanadai kuwa, kwa kuwa Bunge ni taasisi na

mhimili mmojawapo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vema

Kiswahili kikawa lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Wanadai kuwa

kukifanya Kiswahili kuwa na hadhi hii kunaashiria uzalendo wa kukithamini kilicho

chao yaani lugha ya taifa na kuachana na lugha ya kigeni (Kiingereza).

Hoja hii inafungamana na sababu ya pili kuwa Kiswahili kinautambulisha utaifa wa

watanzania. Utambulisho kwa mujibu wa Msanjila (2009:46) ni jumla ya vigezo

maalumu vinavyotumiwa kumtambulisha mtu, kundi la watu, jamii au taifa fulani ili

kuonesha kuwa liko tofauti na taifa jingine, jamii fulani iko tofauti na jamii nyingine,

kundi fulani liko tofauti na kundi jingine au mtu fulani yuko tofauti na kundi jingine au

Page 89: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

74

mtu fulani yuko tofauti na mtu wa kundi jingine, jamii nyingine au taifa jingine. Kwa

mujibu wa Tabouret-Keller (1989) kama anavyonukuliwa na Msanjila (Keshatajwa)

utambulisho wa mtu umefungamana na mambo mengi ya kijamii kama vile lugha,

utamaduni, mila na desturi, mavazi, chakula, dini (imani mbalimbali), historia ya jamii,

siasa na uchumi. Hoja za wataalamu hawa zinaungana na maoni ya wasikilizaji kuhusu

ni lugha gani inayofaa kuwa lugha rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Ili kubaini

utambulisho wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, watafitiwa wanasema

kuwa ni vema kutumia Kiswahili sanifu na kisichohusisha ubadilishaji wake na lugha

nyingine kama vile Kiingereza. Huu utakuwa utambulisho wa Watanzania kwani

matamshi ya mzungumzaji yeyote ni matamshi ya utambulisho wake.

Sababu nyingine ni kuwa Kiswahili kimefungamana na utamaduni na jadi ya

watanzania. Jambo la kuzingatia ni kuwa lugha ni mojawapo ya nguzo muhimu za

utamaduni. Bila shaka hii ndiyo ilikuwa sababu ya msingi ya wasikilizaji

kukipendekeza Kiswahili kuwa lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za

Bunge. Watafitiwa wanadai kuwa Kiswahili kupewa hadhi hii ni kuuinua na kuuenzi

utamaduni wa nchi yetu kwani nchi yeyote huru lazima ijivunie utamaduni wake na iwe

na itikadi na vitu vya kuitambulisha kama vile lugha, bendera ya taifa, wimbo wa taifa,

vazi la taifa na kadhalika. Katika hoja hii tunahitimsha kuwa, ni vema kuyaenzi maneno

ya Hayati mwalimu Julius K. Nyerere (1974:91) kuwa nchi isiyo na utamaduni wake

haina tofauti na mkusanyiko wa watu ambao hawana roho iwawezeshayo kuwa taifa.

Katika muktadha huu, Bunge lisilouenzi utamaduni wa nchi yake yaani kwa kutumia

lugha yenye kutambulisha taifa lake halina tofauti na mkusanyiko wa watu ambao

hawana roho iwawezeshayo kuwa Bunge la taifa.

Page 90: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

75

Sababu ya nne ni kuwa Kiswahili kinaendana na jamii ya watanzania. Kimsingi sababu

hii ni jumuishi kwani inaunganisha sababu tatu zilizojadiliwa awali katika kipengele

hiki. Kiswahili kuendana na jamii ya watanzania kunanasibishwa na kuwa lugha ya

taifa, kuwa lugha ya utambulisho na kufungamana na utamaduni na jadi ya watanzania.

Katika hoja hii inatosha tu kusema kwamba, maoni ya watafitiwa yanaungana na hoja

ya Kiango (2004:70) kama anavyowanukuu Sapir (1958) na Worf (1958) kuwa lugha

ina dhima kubwa katika utamaduni wa jamii. Ni mfumo wa mawasiliano na ni njia ya

kuongoza fikra za wazungumzaji. Kwa vile lugha hutofautiana, tunatarajia kuwepo kwa

mikwamo katika mawasiliano ya watu wa tamaduni tofauti. Hivyo basi, kwa kuwa

Kiswahili kimefungamana na kinaendana na utamaduni wa watanzania ni vema kikawa

lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.

4.5.1.3 Lugha ya Umoja

Hoja hii inajumuisha sababu mbili ambazo ni kwamba; mosi, Kiswahili

kinawaunganisha watanzania kama kilivyowaunganisha katika harakati za kudai uhuru

kutoka kwa mkoloni; pili, ni kwamba hakijinasibishi na tabaka au kabila lolote hivyo

kuondoa ubaguzi. Jambo lililoonekana kusisitizwa na watafitiwa ni kuwa hakuna jamii

au tabaka linaloweza kudai kuwa Kiswahili ni lugha yake binafsi. Kwa mantiki hii

wanadai kuwa, kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya watanzania wote na hakijinasibishi na

jamii au tabaka lolote ni vema kikapewa hadhi ya kuwa lugha pekee ya kuendeshea

shughuli za Bunge. Tofauti na hili watafitiwa wanadai kuwa kuruhusu Kiingereza kuwa

lugha mojawapo au lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge ni kuleta ubaguzi

miongoni mwa watanzania kwani lugha hii ni ya matabaka maalumu hasa wasomi.

Page 91: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

76

Wakirejea historia watafitiwa wanadai kuwa Kiswahili ni lugha iliyotumika

kuwaunganisha watanzania wa kabila na itikadi tofauti katika harakati za kudai uhuru.

Kwa mfano, katika mahojiano mtafitiwa mmoja alisema:-

...…. Hakuna lugha yoyote iliyotetea maslahi ya taifa letu kama Kiswahili.

Ni Kiswahili kilichotumika katika harakati za kudai uhuru na hatimaye

kutuletea uhuru na umoja wa kitaifa ambao matokeo yake ni utulivu. Utulivu na

amani ndivyo vilivyowawezesha wasomi kusoma, na kupata madigrii

yanayowapa kiburi na kukidharau Kiswahili hivi leo. Napenda kukiri kuwa si

wote, lakini wapo watu wa namna hiyo na wengine ni viongozi tena wenye

dhamana kubwa waliyopewa ama na Rais au wananchi. ………

Hapa mtafitiwa anazinadi sifa zinazokipa sifa Kiswahili kufaa kuwa lugha pekee ya

Bunge. Pia mtafitiwa anaonekana kuwalaumu wasomi kuwa ndio wanaotumia fursa ya

kufahamu Kiingereza kukidharau Kiswahili. Hivyo basi, watafitiwa wanadai kuwa

Kiswahili ni lugha inayotetea maslahi ya kitaifa kwani inaleta umoja wa kitaifa na

kuwezesha harakati za kimaendeleo. Kwa kuwa Bunge ni taasisi ya watanzania wote, ni

vema lugha inayopewa hadhi ya kuwa lugha pekee ya Bunge iwe lugha

inayowaunganisha watanzania wote na isijinasibishe na tabaka au jamii yoyote.

4.5.1.4 Kinawaepusha Watanzania na Utumwa wa Kifikra.

Katika hoja hii watafitiwa wanadai kuwa kukikumbatia Kiingereza ni kujiingiza au

kuendeleza utumwa wa kifikra. Hawa wanaongozwa na dhana kuwa Kiingereza ni

lugha ya mkoloni na kwa kuwa Tanzania ilishajipatia uhuru wake ni vema ikawa na

uhuru wa kutumia lugha yake katika shughuli zote za kiserikali. Wanachotetea ni kuwa,

Page 92: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

77

uhuru haupaswi kuwa wa bendera tu bali uwe wa nyanja zote ikiwa ni pamoja na

utamaduni ambapo nguzo mojawapo ya utamaduni ni lugha. Hivyo basi, kwa hoja hii

watetezi wa Kiingereza kuwa mojawapo ya lugha za Bunge wananekana watumwa wa

kifikra.

4.5.1.5 Kukilinda na Kukikuza Kiswahili.

Hii ni hoja iliyotolewa na watafitiwa katika kutetea kuwa Kiswahili kinafaa kuwa lugha

pekee ya kuendesha shughuli za Bunge. Hii inabeba sababu mbili kuu ambazo ni; mosi,

ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na pili, ili kuondokana na ubadilishaji wa

Kiswahili na Kiingereza. Kimsingi watafitiwa walionesha kutambua kuwa lugha

yoyote ile inafaa kukuzwa na kulindwa. Watafitiwa wanadai kuwa ili Kiswahili kiwe na

msamiati wa kutosha kuelezea mambo muhimu yanayoendana na maendeleo ya sayansi

na teknolojia na pia kuweza kuendana na kasi ya utandawazi ni vema kikapewa hadhi

ya kuendeshea shughuli za Bunge kama lugha pekee ya mawasiliano. Wanaendelea

kudai kuwa si kwamba Kiswahili hakina istilahi na msamiati wa kutosha kuwezesha

mawasiliano ya Bunge, ila tatizo ni kuwa, kwa kuwa kunakuwepo na mbadala wake

(Kiingereza) wabunge hawajishughulishi kutafuta msamiati wa kuelezea dhana fulani.

Kutokana na hili ndio maana mbunge akikwama kupata msamiati wa Kiswahili

huchanganya Kiingereza na kinyume chake pia. Kutokana na hali hii ndio maana

kunajitokeza uzungumzaji wa kubadilisha Kiswahili na Kiingereza.

Kimsingi hoja hii ililenga kujibu hoja zinazotolewa na watetezi wa Kiingereza kuwa ni

lugha ya utandawazi, kilaalamu na kitaaluma na ina istilahi zinazokidhi haja za

kuelezea dhana mbalimbali (rejea 4.7). Hizi haziwezi kuwa sababu muafaka na kuntu

Page 93: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

78

za kutushawishi kukubali kuwa Kiingereza kiwe mojawapo au lugha pekee ya

kuendeshea shughuli za Bunge. Tukubaliane kuwa Kiswahili kinakidhi dhima yake

yaani kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wanajamii (rejea 4.5.1) na hivyo hakuna

haja ya kuendelea kukikumbatia na kukitetea Kiingereza.

Tuseme tu kwamba, serikali haina budi kuunga mkono kikamilifu juhudi za kukuza

Kiswahili ikitilia maanani kuwa, kama asemavyo Broomfield (1931) hata lugha ya

Kiingereza ambayo kwa sasa hivi ina uwezo mkubwa sana ilipokuwa katika hatua zake

za mwanzo za maendeleo, ilidharauliwa na kutazamwa kama lugha ambayo haikuwa na

uwezo wa kufafanua dhana za sayansi na teknolojia. Hivyo basi kama asemavyo

Mulokozi (2009:82) jukumu letu sisi wakuzaji wa Kiswahili ni kuufanya utandawazi

utandawaze Kiswahili.

4.5.1.6 Kiswahili ni Lugha Rasmi ya Bunge la Afrika

Hii ni hoja iliyotolewa na watafitiwa katika kutetea kuwa Kiingereza kisipewe hadhi ya

kuwa lugha ya kuendeshea shughuli za Bunge kwa kigezo kuwa ni lugha ya kimataifa.

Katika kujenga hoja mtafitiwa mmoja alikuwa na haya ya kusema:

….. ni lazima tutambue kuwa Kiswahili tayari ni lugha ya kimataifa kwani

tangu mwaka 2004 kimekubaliwa kutumika rasmi katika vikao vya umoja wa

Afrika…. Bunge la Afrika Mashariki tayari lipo, na shughuli za kisiasa ndani ya

Afrika Mashariki zinatumia sana Kiswahili na dalili zinaonesha kuwa Kiswahli

kitakuwa ndiyo lugha kuu ya umoja wa Afrika Mashariki……

Page 94: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

79

Nukuu hii inaonesha ni jinsi gani watafitiwa wanavyokithamini na kukitetea Kiswahili.

Pamoja na hayo inaonekana Kiswahili kinaweza kuongezwa katika lugha za umoja wa

mataifa na hivyo kuwa lugha ya kimataifa (Gikambi 2010). Katika hoja hii tuhitimishe

kwa kusema kuwa, Kiswahili katu hakitastawi na kuchanua katika ukanda huu kama

kitabakia kuwa lugha ya sokoni tu bila kupewa hadhi ya kuendesha shughuli zote za

serikali na taasisi zake na bila kuingizwa na kutumiwa katika ngazi za juu za elimu na

teknolojia.

4.6 Mbinu za Kukifanya Kiswahili kuwa Lugha Pekee ya Shughuli za Bunge.

Kama tulivyoona katika kipengele 4.5.1 wasikilizaji wanapendekeza kuwa Kiswahili

kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hata hivyo, hawakuishia

hili tu bali walikwenda mbali zaidi kwa kutoe mbinu mbadala za kuwezesha lengo hili.

Yafuatayo ni maoni yao:-

1. Kanuni za kudumu za Bunge zifanyiwe marekebisho na kuweka vipengele

vifuatavyo:-

(a) Kwamba wakati wa mijadala mbunge yoyote asichanganye Kiswahili na

Kiingereza au lugha iwayo yote bali atumie Kiswahili fasaha.

(b) Kama itakuwa ni lazima kuchanganya lugha kwa sababu maalumu,

mbunge alazimike kuelezea au kufasiri alichomaanisha kwa Kiswahili

fasaha.

2. Miswada yote inayowasilishwa Bungeni iandaliwe katika lugha ya Kiswahili ili iwe

rahisi kwa wabunge wote na pia isiwalazimu wabunge kutumia Kiingereza

wanaporejelea au kunukuu kwenye kifungu fulani katika muswada husika. Pia

Page 95: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

80

sheria zote ziandikwe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri zilizoandikwa

kwa lugha za kigeni.

3. Sera na miongozo yote ya serikali itolewe kwa Kiswahili ili kukipa hadhi yake. Pia,

taarifa za mikutano, semina na warsha nchini zitolewe kwa Kiswahili kwa manufaa

ya wananchi.

4. Bunge liwe na kitengo maalumu cha tafsiri ambacho kitahusika na ufasiri wa

kumbukumbu na nyaraka mbalimbali, sheria na miswada ya Bunge viliyoandikwa

kwa lugha ya Kiingereza. Pia, wabunge wakitumie kitengo hiki kupata fasiri sahihi

za nyaraka wazipatazo kutoka vyanzo mbalimbali zilizoandikwa kwa lugha

nyingine.

5. Lugha ya kufundishia iwe Kiswahili kwa ngazi zote za elimu ili kuwafanya

watanzania kuwa na istilahi na msamiati wa kutosha wa lugha hii. Hii itasaidia

wahitimu na wabunge wa baadaye kuwa mahiri wa Kiswahili kwa kuwa na istilahi

za taaluma mbalimbali.

6. Serikali ihakikishe kwamba kunakuwepo machapisho ya kutosha yanayoorodhesha

istilahi muhimu zinazoendana na mazingira ya Bungeni. Haya yaandaliwe kwa

ushirikiano na taasisi maalumu zenye jukumu la kulinda na kukuza Kiswahili kama

vile BAKITA, TATAKI na BAKIZA.

Page 96: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

81

4.7 Kufaa kwa Kiingereza kuwa Lugha Rasmi ya Shughuli za Bunge.

Kama tulivyodekeza awali, kulijitokeza watafitiwa wanaotetea kuwa Kiingereza tu

kinafaa kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa walikuwa watafitiwa 13 (1.68%) kati ya

sampuli nzima ya utafiti. Sababu za kukitetea Kiingereza zimeainishwa katika jedwali

lifuatalo:-

Jedwali la 12: Sababu za Wasikilizaji Kutetea Kuwa Kiingereza Kinafaa kwa

Shughuli za Bunge

Sababu za kufaa kwa Kiingereza tu

Idadi ya wasikilizaji

%

Ni lugha ya utandawazi 13 100

Inaeleweka kwa wanajuiya ya Afrika Mashariki 11 84.62

Wabunge ni wasomi na wanakielewa Kiingereza vizuri 10 76.92

Ni lugha ya kitaalamu na kitaaluma 9 69.23

Ina istilahi muhimu zisizopatikana katika Kiswahili 9 69.23

Miswada huandikwa kwa Kiingereza 8 61.54

Nyaraka nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza 6 46.15

Tuseme tu kwamba baadhi ya watafitiwa wa viwango vya juu vya elimu (ngazi ya chuo

kikuu na baadhi sekondari) ndio walionekana kupendekeza lugha hii (rejea jedwali la

4.5). Sababu ya msingi inaweza kuwa ni kwa sababu wanaelewa Kiingereza na hivyo

maamuzi haya hayana athari hasi kwao. Hata hivyo, sababu za uteuzi wa Kiingereza tu

zinaonekana kukosa mashiko kwani sababu zinazotolewa na watetezi wa Kiswahili tu

(rejea 4.5) zinaonekana kutoa majibu yake.

Page 97: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

82

4.8 Kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza.

Kundi hili lilikuwa na watetezi wachache ambao ni watafitiwa 99 (12.77%) katika

sampuli nzima ya utafiti. Kundi hili pia lilihusisha watafitiwa wenye kuelewa

Kiingereza na Kiswahili kwa namna moja au nyingine. Hoja zao zimewasilishwa katika

jedwali lifuatalo:-

Jedwali la 13: Sababu za Kutetea Kuwa Kiswahili na Kiingereza Zinafaa.

Sababu za kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza

Idadi ya

wasikilizaji

%

Kumpa Mbunge uhuru wa kujieleza kwa lugha anayoimudu zaidi

ili mjadala unoge

90

90.91

Wabunge ni wasomi wanaoweza kujieleza kwa lugha hizi 85 85.86

Zote zinatumika katika ngazi zote za elimu kama somo au lugha ya

mawasiliano

81

81.82

Ili kuwamotisha watoto kujifunza lugha hizi 76 76.77

Bunge hupata wageni wasiojua Kiswahili, hivyo wakiwepo

Kiingereza kitumike zaidi.

62

62.63

Nchi imekuwa na wasomi wengi wanaofahamu Kiswahili na

Kiingereza

49

49.49

Itoshe kusema tu kwamba mjadala wa 4.5 unatoa majibu ya hoja hizi. Kwa mantiki hii

hoja hizi hazitajengewa mjadala.

4.9 Hitimisho

Sura hii ilihusu uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data zilizokusanywa kutoka

uwandani. Mjadala umewasilishwa katika sehemu kuu tano. Sehemu ya kwanza ilihusu

uelewekaji wa mijadala ya wabunge yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Katika

Page 98: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

83

sehemu hii tumeona kuwa, 8.9% ya wasikilizaji ndio wanaoelewa mijadala yenye

kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza huku 41.68% wakiwa hawaelewi,

14.58% wakielewa baadhi ya sentensi, na 34.84% wakielewa baadhi ya maneno.

Uchanganuzi zaidi unaonesha kuwa kiwango cha kuelewa au kutoelewa mijadala hii

kinahusiana moja kwa moja na kiwango cha elimu.

Sehemu ya pili ilihusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa mijadala ya Bunge

yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Tumeona kuwa 59.23% ya wasikilizaji

hawatafuti mbinu mbadala za kuwafanya waelewe mijadala ya Bunge yenye kuhusisha

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo, imeonekana kuwa kwa kiasi

fulani wasomi wanatumia mbinu mbadala kama vile kuuliza kwa wenzao, vyombo vya

habari na hata kusoma kamusi.

Katika sehemu ya tatu tumeona kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali ya

wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo, pamoja na kutofurahishwa

na namna hii ya uzungumzaji, katika sehemu ya nne tumeona kuwa hali hii sio sababu

pekee inayosababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge.

Katika sehemu ya tano tumeona kuwa 85.55% ya watafitiwa wanapendekeza kuwa

Kiswahili kiwe lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu

wazitoazo ni kuwa; mosi, kinaeleweka kwa Watanzania wengi; pili, ni lugha ya taifa na

inafungamana na utamaduni wa Watanzania; tatu, kinawaunganisha Watanzania kama

kilivyowaunganisha kudai uhuru na hivyo kuondoa ubaguzi; nne, Kinawaepusha na

utumwa wa kifikra; tano, ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na sita, ni lugha rasmi ya

Page 99: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

84

Bunge la Afrika. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla kuhusu nini kifanyike

kukifanya Kiswahili kuwa lugha kidhi ya mijadala ya Bunge na shughuli nyingine za

kiserikali.

Kimsingi mawasilisho ya mjadala ya matokeo ya utafiti yanatupa mwanzo mzuri wa

sura inayofuata. Sura hii inahusu hitimisho na mapendekezo kuhusu tafiti nyingine.

Page 100: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

85

SURA YA TANO

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

5.1 Utangulizi

Sura hii inahitimisha sura za awali za tasnifu hii kwa kudokeza vipengele muhimu

katika kila sura. Kuna sehemu ambayo inatoa muhtasari wa mambo muhimu katika sura

za awali ambayo yanaendana na malengo ya utafiti huu. Baada ya hapo ni sehemu

inayotoa mapendekezo ya utafiti mwingine na mwisho hitimisho.

5.2 Muhtasari

Kama ilivyoelezwa awali utafiti huu ulihusu ubadilishaji msimbo Bungeni na athari

zake kwa wasikilizaji. Sura ya kwanza inajumuisha utangulizi, usuli wa tatizo, tatizo la

utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mawanda ya utafiti,

kiunzi cha kinadharia na vikwazo vya utafiti.

Sura ya pili ilihusika na mapitio ya machapisho yanayohusiana na maana na aina za

ubadilishaji msimbo, tofauti kati ya ubadilishaji msimbo na ukopaji, sababu za

ubadilishaji msimbo, kueleweka kwa maongezi yenye ubadilishaji msimbo, mbinu

wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini za mchanganyiko wa lugha, na mtazamo wa

wasikilizaji kuhusu hali ya ubadilishaji msimbo. Katika sura hii tumeona kuwa hakuna

tafiti zilizojadili athari za ubadilishaji msimbo Bungeni kwa wasikilizaji. Kutokana na

hili utafiti huu umelenga kuziba pengo hili la kiutafiti.

Sura ya tatu inajadili mbinu zilizotumika katika utafiti huu. Vipengele vilivyojadiliwa

ni eneo la utafiti, populesheni lengwa ya utafiti, sampuli na usampulishaji

Page 101: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

86

kinachojumuisha sampuli, usamulishaji na aina ya usampulishaji, mbinu za ukusanyaji

wa data ambazo ni hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na mwisho ni kipengele

cha uchanganuzi wa data.

Sura ya nne ilijikita katika uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data ya utafiti.

Matokeo yanaonesha kuwa, kwanza; 8.9% tu ya wasikilizaji ndio wanaoelewa mijadala

ya Bunge inayoendeshwa kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza, 41.68%

hawaelewi, 14.58% wanaelewa baadhi ya sentensi na 34.84% wanaelewa baadhi ya

maneno. Majumuisho yanaonesha kuwa, kiwango cha uelewekaji wa mijadala ya

Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza kinapanda kadri ya

kiwango cha elimu kinavyopanda na kinyume chake pia. Pili; matokeo yanaonesha

kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na ubadilishaji wa Kiswahili na

Kiingereza Bungeni. Hata hivyo idadi ya wasiofurahishwa inapungua kadri ya kiwango

cha elimu kinavyoongezeka. Pia, tumeona kuwa pamoja na kutofurahishwa na namna

hii ya uzungumzaji Bungeni siyo sababu pekee inayosababisha wananchi kutofuatilia

mijadala ya Bungeni inayorushwa kupitia vyombo vya habari. Sababu nyingine ni

pamoja na; (1) kukosa muda wa kuangalia au kusikiliza kutokana na kuwa na shughuli

nyingi, (2) umaskini unaosababisha kukosa redio au runinga, (3) ukosefu wa umeme,

(4) Wabunge kutochangia hoja muhimu zenye kutia hamasa ya kusikiliza na (5)

kutokuwa na mazoea ya kusikiliza mijadala ya Bunge.

Tatu, matokeo yanaonesha kuwa, ili kuondoa athari za ubadilishaji msimbo kwa

wasikilizaji, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza Kiswahili kuwa lugha pekee ya

kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu zinazotolewa kutetea hoja hii ni pamoja na

Page 102: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

87

kuwa; (1) Kiswahili kinaeleweka kwa watanzania wengi, (2) ni lugha ya taifa na

inafungamana na utamaduni wa watanzania, (3) kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi,

(4) kinaepusha utumwa wa kifikra, (5) ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na (6)

itasaidia kukilinda na kukikuza Kiswahili.

Sura ya tano inahusu hitimisho na mapendekezo. Sura hii imejikita katika kuelezea kwa

mhitasari mambo yaliyojadiliwa katika sura za awali. Pia katika kipengele cha

mapendekezo pendekezo la utafiti mwingine linatolewa.

5.3 Mapendekezo

Kwa kawaida matokeo ya utafiti huanzisha tatizo la utafiti mwingine. Utafiti huu

ulijikita katika ubadilishaji msimbo na athari zake kwa wasikilizaji. Wasikilizaji katika

utafiti huu walimaanisha wananchi walio nje ya Bunge wanaofuatilia Bunge kupitia

vyombo vya habari hasa redio na runinga. Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya

Muungano ya Tanzania ibara ya 67 (a) mojawapo ya sifa ya mtu kuwa mbunge ni kuwa

awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza. Kwa kuzingatia hili

upo uwezekano wa kuwepo wabunge wanaofahamu kusoma na kuandika Kiswahili tu

na wasiofahamu Kiingereza.

Pamoja na hayo kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2004 kanuni ya 118(1) inaeleza

kuwa Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili au ya Kiingereza, bila

tafsiri ya lugha hizo kutolewa. Kutokana na hali hii wabunge wenye kuelewa

Kiingereza kwa namna moja au nyingine huchangia hoja kwa kubadilisha Kiswahili na

Kiingereza na wakati mwingine Kiingereza pekee. Pia miswada mingi ya Bunge

Page 103: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

88

huandikwa katika Kiingereza tu. Kwa mantiki hii kuna haja ya kufanya utafiti

unaoendana na huu utakaojikita katika kubainisha matumizi ya Kiingereza Bungeni na

athari zake kwa wabunge. Katika utafiti huu kwa kuzingatia viwango mbalimbali vya

elimu vya wabunge, ulenge:-

I. kubainisha kama wabunge wanaelewa mijadala inayoendeshwa kwa

Kiingereza au kubadilisha Kiswahili na Kiingereza na pia kama wanaelewa

miswada inayoandikwa kwa Kiingereza.

II. ubainishe mtazamo wa wabunge kuhusu namna ya uzungumzaji ya

ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni.

III. ubainishe maoni ya wabunge kuhusu lugha inayofaa kuendeshea shughuli za

Bunge na kuandikia miswada na sheria za nchi na kwa namna gani lugha hiyo

iwezeshwe kukidhi dhima hiyo.

5.4 Hitimisho

Sura hii ilihusu hitimisho na mapendekezo ambapo kwanza inaanza kwa utangulizi

unaodokeza vipengele muhimu katika sura nzima. Sehemu iliyofuatia ni muhitasari

unaodokeza kwa ufupi lakini kwa undani mambo muhimu yaliyojadilwa katika sura za

awali za tasnifu hii. Baada ya hapo ni sehemu inayotoa mapendekezo ya utafiti

mwingine na kisha hitimisho.

Page 104: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

89

MAREJEO

Becker, K.R. (1997) “Spanish/English Bilingual Code-Switching Asyncretic

Model”, in Bilingual Review, Volume 22 pp 1, 3 – 28

Bell, A. (1984) “Language Style as Audience Design”, in Coupland, N. and Jaworski

(1997, eds.) Sociolinguistics, a Reader and Coursebook, pp. 240-50

Bentahila, A. and Davies E. (1983) “The Syntax of Arabic-French Code-switching” in

Lingua 59, pp 301-330

Berk-Seligson, S. (1986) “Linguistic Contraints on Intra-sentential Code-switching:

A Study of Spanish/Hebrew Bilingualism” in Language in Society Volume

15 (3), pp 313-348

Bloomfield, J. (1927) “Literate and Illiterate Speech”, in American Speech, Volume 2,

pp 432 – 439

Bokamba, E. G (1988) “Code Switching, Language Variation and Linguistic Theory”

Evidence from Bantu Languages” in Lingua Volume 76

Brice, A (2000) “Code Switching and Code Mixing in the ESL Classroom, A Study of

Pragmatic and Syntactic Features, Advances in Speech Language

Pathology”, in Journal of the Speech Pathology Association of Australia,

Volume 1, No. 20, pp. 19-28

Broomfield, G.W. (1931) Sarufi ya Kiswahili, London, The Sheldon Press

Chachage, S.L.C. (2004) “Kiswahili Katika Muktadha wa Utandawazi” katika

Kiswahili na Utandawazi, Dar es Salaam, Baraza la Kiswahili la Taifa, Uk.

1-17

Page 105: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

90

Chung, H.H. (2006) “Code Switching as a Communicative Stratey: A Case Study of

Korean-English Bilingual”, in Bilingual Research Journal, Defence

Language Institute, pp 293-307

Clyne, M. (1967) Transference and Triggering Martinus Nijhof, The Hague.

Cooper, H.M (1989) Personal Management and Practise, Eastlagh

Hampshire, DP Publishing House

Cohen, L (2000) Research Methodology in Education, 5th

ed, London, Ruttedge Farmer

Cromdal, J. (2000) Code Switching for All Practical Purposes, Bilingual

Organization of Children’s Play, Linkoping Universilet, New York. St

Mattin’s Press Inc.

Enon, J. C. (1998) Education Research, Statistics and Measurements, Kampala,

Makerere University

Fishman, J. (1971) “The sociology of Language: An Interdisciplianary Approach to

Language and Society”, in J. Fishman (ed) Advances in the Sociology of

Language, The Hague, Mouton, pp 217-404

Gardnne-Chloros, P. (1991) Social Development of Linguistic Change in Bilingual

Austria, New York, Academic Press

Gikambi H. (2010) Kiswahili: a UN Working Language?

http://www.azaniansea.com/2010/06/kiswahili-un-working-language.html

retrieved on Monday, 27th

June, 2011

Grosjean, F (1982) Life With Two Languages, An Introduction to Bilingualism,

Cambridge Mass and London, Harvard University Press

Habwe, J. na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili, Nairobi, Phoenix

Publishers Ltd

Page 106: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

91

Hammink, J.E (2000) A Comparison of the Code Switching Behavior an Knowledge of

Adults and Children, http://hamminkj.tripod.com/hamminkCS.pdf retrieved

on Wednesday, 15th

December, 2010

Haugen, E. (1973) “Bilingualism, Language Contact and Immigrant Languages in the

United States”, A Research Report 1956-1970 in Sebeok, T.A. (Ed) Current

Trends in Linguistics, The Hague, Mouton de Gruyter

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (2005) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania ya Mwaka 1977, Dar es Salaam, Mpigachapa Mkuu wa Serikali

Kachru, B.B (1982) “The Bilingual’s Linguistic Reportoire” in Valdman, A et al (Eds)

Issues in International Bilingual Education, New York, Plenum Press

Kadeghe, M. (2000), The Implication of Bilingualism in Learning and Teaching: The

Case of Tanzania Sekondary Schools, Dar es Salaam, University of Dar es

Salaam, Unpublished Doctorial Thesis

Kalong, R.I.A.S. (2008) Code Switching in Informal Among a Group of 4th

Year TESL

Students of UTM, Univesiti Teknoloji Malaysia, Unpublished Bachelor

Degree Project

Kanyuma, Y. (2005) Social Motivations for Code-Switching Among Members of

Primary School Communities: A Case Study of Rubour Ward, Tarime

District, University of Dar es Salaam, Unpublished M.A Dissertation

Kiango, J.G. (2004) “Ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na

Moja” katika Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na Moja, Dar es Salaam,

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Kibogoya, M. A (1998) “Single Word Switches in Kiswahili/English Codeswitching”

in Journal of Linguistics and Language in Education Volume 4, pp 1-23

Page 107: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

92

Kothari, C. J. (2004) Research Methodology, Methods and Technique, New Delhi

India: International (P)

Legele, K. (1987) “Kiswahili na Lugha Nyingine katika Harakati za Kudai Uhuru

Tanganyika (1945-1961)”, katika Kiswahili, Juzuu la 54/1 na 54/2, Dar es

Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, uk.152-166

Leung, C.H. (2010) An Empirical Study on Code Mixing in Print Advertisements in

Hong Kong, http://www.scialert.net/fulltext/?doi=ajm.2010.49.61&org=10,

retrieved on Friday, 10th

December, 2010

MacWilliam, A. na Chuwa, A. (1990) “Kubadili Msimbo Bungeni” katika Kiswahili

Juzuu 57, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Uk. 33-45

Maggati, C. (2004) The Influence of Kiswahili on Non-Bantu Languages: The Case of

Dholuo in Tarime, University of Dar es Salaam, Unpublished M.A

Dissertation

Massamba, D.D.P. (1993) “The Role of Language in Education and Research” in

Preceedings African/Japanese Scholars Conference for Cooperation in

Educational, Cultural and Environmenatal Spheres in Africa, Tokyo

Meeuwis, M. na Blommaert, J.(1998) “A Monolectal View of Code-Switching,

Layered codeswitching among Zairians in Belgium”, in Peter Auer (ed.),

Code-switching in Conversation, New York, Routledge, pp 76-98

Mekacha, R.D.K. (2000) Isimujamii: Nadharia na Muktadha wa Kiswahili, Minoo city,

Osaka, Japan Osaka, University of Foreign Studies

Mirloy, L. na Muysken, P. (1995) One Speaker, Two Languages, Cross Disciplinary

Perspective on Code Switching, Cambridge University Press, Cambridge

Page 108: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

93

Mochiwa, Z.S.M (1979) The Impact of Kiswahili Language on Ethnic Languages: A

Case Study From Handeni Disrict. Unpublished M.A Dissertation,

University of Dar es Salaam

Msanjila Y.P (2004) “Kiswahili Kitumike Kufundishia Shule za Sekondari na Elimu

ya Juu Tanzania” katika Kiswahili katika Karne ya Ishirini na Moja, Dar

es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Msekwa, P. (2000) Bunge la Kwanza Katika Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa

Tanzania: 1995-2000, Dar es Salaaam Tanzania, DUP {1996} LTD

Mulokozi M.M.(2009) “Mustakabali wa Kiswahili Katika Ukanda wa Maziwa Makuu”

katika Mulika Na. 28, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Mutembei, A (2001) Poetry and Aids in Tanzania: Changing Metaphor and

Metonymies in Haya Oral Tradition, Research School of Asian, African

and Amerindian Studies, Netherlands, Laiden University, Unpublished

Doctorial Thesis

Muysken, P (2000) Bilingual Speech, A Typology of Code-mixing, Cambridge,

Cambridge University Press

Mwansoko, H.J.M. na Tumbo-Masabo, Z.N.Z (1996), Matumizi ya Kiswahili Bungeni,

Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Myers-Scotton, C (1983) “The Negation of Identities in Conversation: A Theory of

Markedness and Code Choice”, in International Journal of the Sociology of

Language, Volume 44

__________, (1993) Duelling Languages: Grammatical Structure in Code Switching,

Oxford, Clarendan Press

Page 109: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

94

Nsekela, A.J. (1965) Minara ya Historia ya Tanganyika: Tanganyika Hadi Tanzania,

Dar es Salaam, Longman Tanzania

Nyerere, J.K. (1974) Binadamu na Maendeleo, Naorobi, Oxford University Press

Pandit, Ira (1986) Hindi English Code Switching: Mixed Hindi English, Dheli:

detta Book Center

Pfaff, C. (1979) “Contraints on Language-mixing: Intrasentential Code-switching and

Borrowing in Spanish/English Language” in Journal of the Linguistic

Society of America 55(2), pp 291-318

Poplack, S. Sankoff, D. and Miller C. (1988) “The social Correlates and Linguistic

Processes of Lexical Borrowing and Assimilation”, in Linguistics 26, pp 47-

104

Rubagumya, C.M. (1986) “Planning in the Tanzania Education System: The Problems

and Prospects”, Journal of Multilingual and Multicultural Development,

Volume 7, No. 4, pp 289-300

Rubanza, Y.I. (2006) “Utandawazi bila Lugha Miliki? Nafasi ya Kiswahili” katika

Makala ya Kongamano la Kimataifa la Jubilee ya TUKI-2005 (2), Dar es

Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Salimu-Sawe, K (2008) “Ubadilishaji Msimbo wa Wanautatu-lugha: Uchunguzi wa

Kisarufi” katika Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za

Kiafrika, Nairobi, Moi University Press

Sapir, E. (1958) Selected Writings in Language Culture and Personality, Berkely,

University of Califonia Press

_________, (1921) Language, New York, Harcourt Brace

Page 110: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

95

Shaffer, D. (1975) “The Place of Code-switching in Linguistic Contact” Second Annual

Forum, Linguistic Association of Canada

Sewangi, S.S. (2004) “Nafasi ya Lugha katika Maendeleo ya Uchum: Mfano wa

Kiswahili katika Tanzania” katika Kiswahili katika Karne ya Ishirini na

Moja, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Uk. 87-93

Shoo, G (2004) “Nafasi ya Kiswahili Katika Vyombo vya Habari Wakati huu wa

Utandawazi” katika Kiswahili na Utandawazi, Dar es Salaam, Baraza la

Kiswahili la Taifa, Uk. 79-87

Sridhar, S. and Shridhar K. (1980) “The Syntax and Psycholinguistics of Bilingual

Code-mixing” in Studies in the Linguistic Sciences, Volume 10, No. 1

Swigart, L. (1992) “ Two Codes or One? The insiders’ View and the Description of

Codeswitching in Dakar”, Journal of Multilingual and Multicultural

Development, pp 13:83-102

Tabouret-Keller, A. (1989) “Seminar danthropologie du langage”, MSH Informations,

Bulletin de la Fondation des Sciences de I’Homme NO. 59, pp 15-17

Tabouret-Keller, A. and Le Page R.B. (1986) “The Mother-Tongue Metaphor”, Grazer

Linguistische Studien, Volume 27, pp 249-259

Tay, W.W. (1989) “Code Switching and Code-mixing as a Communicative

Strategy in Multilingual Discourse”, Journal of World Englishes, Volume 8,

pp 407-417

Vans, V. (1990) Introduction to Social Research, mcgraw-Hill, Unwin Hyman

Weber, H. (1985) A Dictionary of Phonetics and Linguistics, Longman, Harlow

Weinreich, U. (1953) Languages in Contact, The Hague, Mouton

Page 111: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

96

Whorf, B.L. (1958) Language, Thought and Reality, New York, MIT & John Wiley &

Sons Ltd

Wu, Y. (1985) “Code-Mixing by English-Chinese Bilingual Teachers of the People’s

Republic of China”, Journal of World Englishes, Volume 4(3), pp.303-317

Page 112: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

97

VIAMBATANISHO

KIAMBATANISHO I: HOJAJI KWA WASIKILIZAJI

MAELEKEZO: Weka tiki katika kisanduku unachoona kina jibu sawa kwa swali la 2

hadi 5 na 7 hadi 11 (a) na 12 hadi 15. Kwa swali la 6, 11 (b) na 15 hadi 18 andika

maelezo mafupi katika sehemu zilizo wazi. Unaombwa kutomuuliza mtu wala kusoma

kokote bali toa maoni yako kwa kuzingatia uelewa wako tu.

1. Jina …………………………………………………(si lazima)

2. Mahali unapoishi:- vijijini [ ] mjini [ ]

3. Jinsia: mme [ ] mke [ ]

4. Umri: 18-27 [ ] 58-67 [ ]

28-37 [ ] 68-77 [ ]

38- 47 [ ] 78…. [ ]

48-57 [ ]

5. Kiwango cha elimu:-

Shule ya msingi/kati [ ]

Shule ya sekondari [ ]

Chuo/chuo kikuu [ ]

6. Kazi…………………………………………………..

7. Unaweza kuzungumza na au kuelewa lugha gani?

a) Kiswahili [ ]

b) Kiingereza [ ]

c) Nyinginezo [ ]

d) (itaje/zitataje)…………………………………

8. Wabunge wamekuwa na kawaida ya kuchangia hoja bungeni kwa kuchanganya

Kiswahili na Kiingereza. Unalifahamu hili?

a) Ndiyo [ ]

b) Sijui [ ]

c) Sina uhakika [ ]

9. Je, wabunge wanapochanganya Kiswahili na Kiingereza huwa unaelewa

kinachozunguzwa?

a) Ndiyo [ ]

b) Kwa baadhi ya sentensi [ ]

c) Naelewa neno moja moja [ ]

d) Sielewi kabisa [ ]

Page 113: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

98

10. Pale ambapo Mbunge anachangia hoja kwa kuchanganya Kiswahili na

Kiingereza na hivyo kusababisha usimuelewe. Huwa unatimia mbinu gani

kuwamuelewa?

a) Nafuatilia kwenye kamusi [ ]

b) Nauliza kwa watu wengine [ ]

c) Nafuatilia magazetini na kwenye taarifa za habari (redio/TV) [ ]

d) Sifuatilii na hivyo kutoelewa chochote kuhusu kilichosemwa [ ]

11. Soma sentensi ifuatayo; -

“zipo advantage za kutumia long term bonds na advantage ya kwanza ni

non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia internal source of

finance lakini rahisi ku-meet our development goals….” (12 Julai, 2007)

a) Je umeelewa kinachozungumzwa?

I. Ndiyo [ ]

II. Nimeelewa baadhi ya sentensi [ ]

III. Nimeelewa baadhi ya maneno [ ]

IV. Sijaelewa kabisa [ ]

b) Kama umeelewa kwa maneno yako eleza kwa ufupi umeelewa

nini………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………

…………………………………………………………

12. Je, huwa unafuatilia majadiliano ya Bunge kupitia redio, luninga/TV na ua

magazeti?

a) Ndiyo [ ]

b) Mara chache [ ]

c) Sifuatilii kabisa [ ]

d) Sina uhakika [ ]

13. Je, uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza unakusababisha ushindwe

kufuatilia mijadala ya bungeni?

a) Ndiyo [ ]

b) Kwa kiasi fulani [ ]

c) Hapana [ ]

14. Inasemekana ni jambo la kawaida kusikia watu wakichanganya lugha kama vile

Kiswahili, Kiingereza na hata lugha za asili katika mazingira yasiyo rasmi (

kama vile vijiweni, kwenye daladala, virabu vya pombe, sokoni n.k). Je,

unajisikiaje namna hiyo hiyo ya uzungumzaji inapojitokeza bungeni?

a) Sifurahishwi [ ]

b) Sijali [ ]

c) Ninajisikia kawaida [ ]

d) Napendezwa [ ]

Page 114: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

99

15. Unashauri ni lugha gani itumike kuendeshea shughuli za Bunge.

a) Kiswahili na Kiingereza [ ]

b) Kiswahili tu [ ]

c) Kiingereza tu [ ]

d) Nyingine [ ] Itaje/zitaje…………………….

16. Kwa nini umechagua hiyo/hizo lugha hapo juu? (eleza kwa ufupi)

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

17. Unaishauri nini Serikali kuhusu lugha rasmi ya/za kutumia katika shughuli za

Bunge.

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………

18. Ukikutana na Mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali yake au ya wenzake ya

kuchanganya Kiswahili na Kiingereza

Bungeni………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………

………………………………………………………..

Ahsante sana kwa ushirikiano wako!

Page 115: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

100

KIAMBATANISHO II: MASWALI YA MWONGOZO WAKATI WA USAILI11

1. Baadhi ya wabunge wamekuwa na tabia ya kuchanganya Kiswahili na

Kiingereza wakati wa mijadala Bungeni. Je, una habari kuwa aina hii ya

uzungumzaji inatokea katika vikao rasmi vya Bunge?

2. wabunge wanazungumza Bungeni kwa niaba ya wananchi (wasikilizaji) na

wasikilizaji wanapaswa kufahamu wanachozungumza. Je, wabunge

wanapozungumza kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza huwa unaelewa

kinachozungumzwa? (Baada ya hapo mtafiti alisoma sentensi kwenye matini

kutoka kumbukumbu za Bunge na kumtaka mtafitiwa kutoa maana yake kwa

Kiswahili).

3. Pale ambapo mbunge anachangia hoja kwa kuchanganya Kiswahili na

Kiingereza na hivyo kusababisha usielewe. Je, huwa unatumia mbinu gani

kuelewa au kupata ujumbe uliokusudiwa?

4. Ni jambo la kawaida kusikia watu wakichanganya Kiswahili, Kiingereza na

wakati mwingine lugha za asili (k.v. Kisukuma, Kikerewe, Kihaya n.k) katika

mazungumzo yasiyo rasmi (k.v. baa, kwenye daladala n.k ). Je, unadhani inafaa

aina hiyo ya uzungumzaji ijitokeze katika mijadala rasmi ya Bunge?

5. Huwa unafuatilia mijadala ya Bunge kupitia vyombo vya habari?

6. Je, uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza huwa unakufanya kutopendelea

kufuatilia mijadala ya Bunge? Kama kuna sababu nyingine zitaje.

7. Wewe kama mdau na mlengwa wa mijadala iendeshwayo Bungeni, ni athari

gani unazozipata kutokana na wabunge kuchanganya Kiswahili na Kiingereza?

8. Kanuni za kudumu za Bunge zinamruhusu mbunge kuchangia mjadala kwa

Kiswahili au Kiingereza bila tafsiri kutolewa. Je, hii inafaa? Kama haifai kama

mdau unaishauri nini serikali kuhusu ni lugha gani inayofaa/zinazofaa

kuendeshea shughuli za Bunge?

9. Kwa nini umechagua lugha hiyo/hizo kuwa lugha rasmi ya/za kuendeshea

mijadala Bungeni?

10. Ukikutana na mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali ya wabunge

kuchanganya Kiswahili na Kiingereza Bungeni?

11

Kabla ya kuanza kwa maojiano mtafiti alimsomea mtafitiwa matini kutoka kumbukumbu rasmi za

Bunge zinazoonesha ni jinsi gani wabunge wanavyochanganya Kiswahili na Kiingereza. Hii ilisaidia

kumjengea uelewa mtafitiwa.

Page 116: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

101

KIAMBATANISHO III: MASWALI YA KUONGOZA MIJADALA KATIKA

VIKUNDI LENGANI12

1. Je, huwa unafuatilia mijadala ya Bunge kupitia vyombo vya habari?

Vitaje/kitaje?

2. Kwa nini unapendelea/haupendelei kufuatilia majadiliano ya Bunge?

3. Wakati wa mijadala baadhi ya wabunge wamekuwa na kasumba ya

kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Je, una mtazamo gani kuhusu namna

hiyo ya uzungumzaji Bungeni?

4. Je, wabunge wanapozungumza Bungeni kwa kuchanganya Kiswahili na

Kiingereza huwa unaelewa wanachozungumza?

5. Sikiliza kwa makini sentensi hizi kutoka kumbukumbu za Bunge na kisha

uelezee ulichoelewa kwa Kiswahili (rejea kiambatanisho III).

6. Je, namna hii ya uzungumzaji Bungeni inakusababishia usipendelee kufuatilia

mijadala ya Bunge?

7. Ikitokea kwamba hujaelewa huwa unatumia njia na mbinu gani kuelewa

alichomaaanisha mbunge?

8. Kikanuni Kiswahili na Kiingereza zote zinaruhusiwa kutumika kuendeshea

mijadala ya Bunge. Je, hii ni sawa? Unatoa ushauri gani kwa serikali kuhusu

lugha ya kutumika Bungeni?

9. Ukikutana na mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali ya wabunge

kuchanganya Kiswahili na Kiingereza Bungeni?

12

Kama ilivyokuwa katika usaili watafitiwa walisomewa matini kutoka kumbukumbu za bunge zenye

mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza.

Page 117: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

102

KIAMBATANISHO IV: MATINI KUTOKA KUMBUKUMBU ZA BUNGE

MATINI: A

12 JULAI, 2007 Uk. 30

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nilitaka nianze na kuelezea umuhimu wa wa

infrastructure katika maendeleo ya nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa

sana, bahati yetu ni ambako Mungu aliamua nchi hii iwe hapa iliko leo na maana yake

ni ni geography position ya nchi yetu. Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie

advantage ya jeografia yetu kwa sababu engine ya maendeleo ni infrastructure, mimi

sijui nchi yoyote iliyoendelea Duniani bila kuwa na infrastructure. Kwa hiyo

tunapokuwa tunapanga barabara zetu, tunapanga resources zetu lazima tujenge

barabara hizi kule ambako tunaamini tukipeleka pesa zetu zitarudi, kuna barabara

ambazo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu barabara ya kwanza ni Manyoni,

Itigi, Tabora na Kigoma. Siyasemi haya kwa sababu labda natoka Kigoma lakini

niwaambie advantage tukijenga barabara hii Kongo ya Mashariki kuna mzigo wa tani

miliono nne, tunao mzigo Burundi, tunao mzigo Rwanda ukijenga ile transit business

peke yake itatuingizia pesa nyingi sana kwenye nchi yetu kwa hiyo lazima maamuzi

yetu yaende haraka tuweze kufanya vizuri kwenye area hiyo. Tunayo barabara ya

Tunduma, Sumbawanga, Mpanda mpaka Kanyani tunayo barabara Kigoma Nyakanazi,

Mwandiga, Manyovu, Mpanda, Tabora, Sumbawanga mpaka Kasanga Port. (Makofi)

MATINI B.

12 JULAI, 2007 Uk. 32-33

Mheshimiwa Spika, lakini nilitaka niongezea pia jambo lingine, jana rafiki yangu

Kaboyonga aliliongea hapa, ujenzi wa barabara unahitaji pesa nyingi sana na mimi

nakubali lakini liko suala la kutumia long term bonds, long term bonds ni sources of

finance ni govern papers hizi tunaziuza, ziko advantage za kutumia hizi long term

bonds na advantage ya kwanza ni non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia

internal source of finance lakini rahisi ku-meet our development goals tumepanga

kufanya jambo hili hatuna pesa government inauza zile government bonds kwa hivi

financial institutions miaka 15 inapofika miaka 10 hujaweza kulipa zile pesa ni rahisi

una-issue nyingine ili pesa imlipe huyu unaenda mbele. Halafu tutumie load fund board

yetu iwe inatenga fedha kidogo kwa ajili ya kulipia hizo interest kwenye hizo long term

bonds zetu, nawaambieni tukifanya jambo hili nchi hii tutawashangaza Mataifa,

tutajenga nchi hii na tutaenda kwa kasi kubwa kweli kweli.

MATINI C.

12 JULAI, 2007:83

Mheshimiwa Spika, India is one of the best country katika Railway netwok,

tukachukue ma-expert waje watusaidie lakini liwe chini yetu. Tutakuja kupakiwa rangi

haya mabehewa tushindwe kuleta pamba Dar es Salaam kusafirishwa. Tutasafirisha

abiria na mizigo na bidhaa at the end of the day hatuna kitu. Halafu unampa contract ya

25 years is not a joke. (Makofi)

Page 118: UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA … · katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi; Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa

103

MATINI D.

14 JULAI, 2004 Uk. 82-83

Mimi kama mwanataaluma nawaachieni sina tatizo kama nchi hii inaingia kwenye

southern grid. Bora mradi iingie ikiwa na umeme wa kutosha siku nyingine tukiwa na

matatizo watuuzie na siku nyingine tuwauzie wao. Lakini Wizaara ya Nishati na

Madini inaendeshwa na watu utadhani ni mamluki kumbe ni Watanzania. Mimi

nashindwa hata kuwaelewa. (Makofi)

Ninajua ni wasomi najua kila ninaloelewa wanalielewa, najua yako mengine

wanaelewa kuliko mimi, sasa ni nguvu ipi inayowasukuma waihujumu Tanzania. Mimi

najua arrogance ya Wizara hii niwaambie tu inawezekana wana-rub shoulders na press

and bosses tutawaadhibu baadaye. You wili answer there is no way nchi hii itaendelea

kuteseka sababu mtu mmoja analeta maamuzi yanayoua wananchi.

Mheshimiwa spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa yeye,

mtondogoo wao. I better worn you today comrades, you will not afford. Hatutavumilia

matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya watu wachache. (Makofi)

Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu minister ni nani ni wale wengine

nisiongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe hujui nani

aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikamwambia uliteuliwa

wewe. But you don’t seem to be. Why don’t you understand me when we talk here

together and when you to your office you are powerless. What is wrong? (Makofi)