ufunuo 1 · mifano mengine yanapishana, simba wa yuda anageuka kua mwana kondoo (5:5-6) mwanamke wa...

15
UFUNUO 1 Picha za Hukumu na Tumaini Mtu akigeukia kitabu cha Ufunuo kando ya vitabu vingine vyote vya Agano Jipya, ataona kama anaingia kwenye nchi ya kigeni. Badala ya masimulizi na nyaraka zenye maelezo ya wazi ya mambo halisi na maagizo, anaona kitabu kilichojaa malaika, baragumu, matetemeko ya nchi, wanyama, majoka, na mashimo ya kuzimu Yapo yanayoeleweka kwa urahisi, mf Yohana anapotambulisha kitabu 1:9 Maelezo mengine yanaweza yakawa rahisi, 6:12-17 na mengine magumu 11:1-10, kuelewa. Ni kitabu kunachogawa wakristo katika makundi ya ”ufafanuzi” Vipo vitabu vingi vya ufafanuzi wa siri za Ufunuo, Katika somo hii tutazingatia Exegeses, Tunataka kufahamu yanayofahamika Tutatoa ashauri ya jinsi ya kusoma kitabu hiki bila kupotea….

Upload: others

Post on 16-Feb-2021

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • UFUNUO 1• Picha za Hukumu na Tumaini

    • Mtu akigeukia kitabu cha Ufunuo kando ya vitabu vingine vyote vya Agano Jipya, ataona kama anaingia kwenye nchi ya kigeni. Badala ya masimulizi na nyaraka zenye maelezo ya wazi ya mambo halisi na maagizo, anaona kitabu kilichojaa malaika, baragumu, matetemeko ya nchi, wanyama, majoka, na mashimo ya kuzimu

    • Yapo yanayoeleweka kwa urahisi, mf Yohana anapotambulisha kitabu 1:9

    • Maelezo mengine yanaweza yakawa rahisi, 6:12-17 na mengine magumu 11:1-10, kuelewa.

    • Ni kitabu kunachogawa wakristo katika makundi ya ”ufafanuzi” • Vipo vitabu vingi vya ufafanuzi wa siri za Ufunuo, • Katika somo hii tutazingatia Exegeses, • Tunataka kufahamu yanayofahamika • Tutatoa ashauri ya jinsi ya kusoma kitabu hiki bila kupotea….

  • UFUNUO 2

    • Muundo wa kitabu cha Ufunuo • Waraka, barua = Yohana anawaandikia makanisa • Unabii = Inasema juu ya mambo yatakayokuja, na pia

    yaliyokuwepo kwa wakati wake. Rejea zinazotumika ni za wakati ule.

    • Ufunuo [apokalypsis] = kufunua siri, lakini pia kutokana na yanayoeezwa imepata maana ya ”mambo ya mwisho pia”

    • Ni muhimu sna kutambua na kufahamu aina hii ya maandiko kama tutaweza kufaidi kitabu cha Ufunuo.

  • UFUNUO 3• Ufunuo kama andiko ya mambo yajayo [apocalypsis] 1

    • Ni moja kati ya maandiko ya ”ki-apocalyptic” inayofahamika na iliyoandikwa kati ya mwaka 200kK hadi 200 bK. Ingawa yalikuwa ya namna nyingi pia yapo kadhaa yanayofanana nayo ni;

    • 1. Misingi yake tunaipata katika AK na hasa kwenye vitabu kama vya; Ezekieli, Danieli Zekaria na sehemu ya Isaya. Yanahusu mambo ya mwisho na jinsi Mungu atakavyotenda katika ushindi kwa kukomesha uovu.

    • 2. Mwandishi ameambiwa aandike (1:9) si kama vitabu vya kiunabii ambavyo hasa ni rejea ya utabiri ya nabii fulani.

    • 3. Lugha ni ya maono, ndoto, siri mafumbo a mifano. waandishi mara nyingi walitumia jina la bandia ya mtu maarufu wa zamani, na kitabu kilidai kuwa sasa muda wa kufunuliwa imeingia ndiy o maana linaandikwa. Hao wazee waliyaona hayo zamani lakini hawakuruhusiwa kuyafunua hadi wakati wake, wakati ambayo ulikuwa umeingia.

  • UFUNUO 4• Ufunuo kama andiko ya mambo yajayo [apocalypsis] 2

    • 4. Lugha ya mifano tumezoea sana tunaposoma Biblia na Yesu mwenyewe alitumia mifano sana, lakin mifano yake yalihusu yanayoeleweka. Mt 5:13, Lk 17:37, Hos 7:11, Hos 7:8. Lakini picha na mifano ya Ufunuo ni tofauti. Ingawa tunatambua kwa mfano simba, akini hapa anaunganika na kiumbe kingine na matokeo yake ni mambo ya ajabu.Uf 13:1, Uf 12:1, Uf 9:10.

    • 5. Kwa vile viliandikwa moja kwa moja, viliandikwa kwa muundo wa makusudi. Walipanga maandiko yao katika vikundi . Walikuwa na ”michezo ya mahesabu”. Utakuta kazi ilipendeza sana. Mara kwa mara makundi haya yanapowekwa pamoja, huonyesha kitu (k.m., hukumu) bila kulazimika kupendekeza kuwa kila picha iliyojitenga huifuata ya awali.

    • Ufunuo wa Yohana unafuata taratibu hizo isipokua kwa sehemu moja. Anayeandika anatajwa nahatumii jina la bandia. Anajitambulisha kwa wasomji. (Sura ya 2-3), halafu aliambiwa kuandika na aliambiwa asifiche maandishi haya sababu mda unakaribia (22:10)

  • UFUNUO 5• Ufunuo kama unabii

    • Sababu moja yake ya kuacha kutumia jina la mtu mwingine inaweza kua kwamba aliishi katika ”tayari ila bado”. Anafahamu kwamba siku za mwisho zimeanza kupitia kazi ya Yesu. Kitu ambayo ilithibitisha kuwa aliishi katika karne mpya ilikua kwamba Roho wa Bwana alikua amemiminwa juu ya watu. Wengine waliokuwa wameandika vitabu kama vyake walikuwa wakiishi katik enzi ya ‘‘Roho aliyezimishwa’’ . Yeye alikuwa ”katika Roho” wakati alipopewa ufunuo huo (1:10-11)

    • Anazungumzia kitabu chake kama unabii huo (1:3; 22:18-19) anasema kuwa yeye na kanisa linaloteswa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu (1:9; 20:4) ambao ushuhuda huo ni ”Roho wa unabii” (19:10) Bila shaka hiyo ilithibitisha kua Roho wa unabii alikua ameshawasili.

    • Ufunuo inatumia lugha isiyoeleweka kwa urahisi, lakini pia lugha ambayo inaeleweka bila matatizo, lugha ambayo tumezoea kuiona katika maandiko ya manabi katika Agano la Kale. (Na pia katika siku zetu)

  • UFUNUO 6

    • Ufunuo kama Waraka / Barua • Kitabu kimeandikwa kwa sababu ya hali fulani, imeandikwa kwa

    makanisa waliyo na mahitaji ya kusikia ujumbe huo na wanaishi katika mazingira fulani. Anawasalimu kama vile tulivyozoea katika barua zingine ya Biblia. (1:4-7; 22:21)

    • Kwa hiyo ni muhimu kujua mazingira na historia ya wakati ule, kusudi tufahamu hali iliyokuwepo na kwa jinsi hii tuelewe ujumbe wa maandishi.

  • UFUNUO 7• Umuhimu wa exegeses 1 • Tunarudia mafundisho ambayo tumeshayapitia lakini tunalenga

    katika kitabu chetu cha sasa. Kanuni chache cha *exegeses. • 1. Kazi ya kwanza ni kujaribu kugundua kusudi ya mwandishi,

    pamoja na Roho Mtakatifu. Kusudi la kuandika kitabu cha ufunuo. Kuna ujumbe gani ambao anapenda kuwapatia makanisa ya Asia ndogo ? Lazima tutegemee kwamba wao waliweza kufahamu barua waliyoipata ! Inawezekana kwao haikuwa kazi sana maana waliishi wakati ule na pia walikua wamezoea lugha ya namna ile.

    • 2. Ufunuo nikitabu kinacho tabiri, kwa hiyo inaweza ikawa na maana ”ya pili” ambayo imepewa na Roho Mtakatifu, ambayo siyo rahisi sana kuuelewa, hata Yohana na yalemakanisa inawezekan yalipata shida na machache ya kitabu hiki. Lakini *exegeses haihusiki na ujumbe uliyofichika, inahusika na yale yanayoeleweka kabisa. Hermeneutics inahusika na yale ya mafumbo.

  • UFUNUO 8• Umuhimu wa exegeses 2

    • 3. Kuweka Ufunuo katika *analojia na vitabu vingine vya agano jipya siyo vizuri kwa sababu hatuelewi kama Yohana alikuanavyo wakati alipoandika Ufunuo. Tunaweza kutambua lugha inayotumika katika Ufunuo tukisoma baadhi ya maandiko ya Agano la Kale, lakini haitusaidii katika utafsiri inatufanya tu tutambue aina ya lugha inayotumika. Lazima tutafute ndani ya kitabu chenyewe kama tunataka kupata ”ufunguo wa ufumbuzi” wa kitabu cha Ufunuo.

    • 4. Mifano au picha zinazotolewa ni tatizo nyingine pia. Inawezekana mawazo mengine ameyapata katika Agano la Kale, lakini pia katika vitabu vigine ambavyo vilipatikana wakati ule. (Kumbuka tunaongelea lugha tu siyo ujumbe) Kwa mfano: Ukimwandikia mchumba, au ukiandika barua ya kiofisi utakuta lugha inayotumika ni tofauti sana) Hata kama ametoa picha zingine katika maandiko mengine haileti uhakika kwamba anakusudia kuipatia maana ile ile. Inawezekana kwamba yeye na Roho Mtakatifu wameweza kubadili maana kidogo.

  • UFUNUO 9• Umuhimu wa exegeses 3.

    • Picha / mifano mengine ni kama tunayatambua kutoka AK, na pia inaonekana kwamba tafsiri yake ni sawa sawa na AK. Kwa mfano ; ”Mnyama anayetoka baharini” maana yake ni kwamba utakuja utawala fulani, siyo mtu ni nchi. Lakini mifano mengine yanapishana, Simba wa Yuda anageuka kua mwana kondoo (5:5-6) Mwanamke wa sura ya 12 anasimamia kitu kizuri lakini wa 17 ni mbaya. 

Baadhi ya mifano tunapewa tafsiri yake katika maandishi yenyewe. ”Vinara vya taa saba” (1:12- 20) ni kanisa, Joka wa sura ya 12 ni Ibilisi. Yohana anapotupatia tafsiri ya picha fulani hiyo inakua msingi wetu katika kuelewa analolisema. (1:17-18; 1:20: 12:9; 17:9; 17:18) 

Ni muhimu koelewa hizo picha kama ujumla fulani, siyo kuchambua picha moja moja kwa njia ya *kialegoria. Kidogo ni kama mifano ya kwenye Injili, ni muhimukuelewa point iko wapi. Mifano na picha zinatumika kwa kuongeza ujumbe tuweze kuipata sawa sawa

    • 5. Ufunuo siyo kitabu ambayo inaeleza jinsi itakavyokua siku za mwisho kwa mpango wa ”A mpaka Z”. Inayokusudi nyingine. Ujumbe wake hasa ni kutufahamisha kwamba Mungu anaye ”control” katika historia na katika yatakayokuja na wakati tuliyonao. Ataokoa waliyowake na atahukumu dunia.

  • UFUNUO 10

    • Mazingira ya kihistoria • Tuko pale tena...tufanyeje ???? • Anza kwa kusoma kitabu chote mpaka unapoanza kukipatapata. • Rudia tena chukua notes na referenses ambayo yanaweza kuwa ya

    maana (Kazi hii tutaipitia zaidi wakati wa kusoma ufunuo wa Yohana)


    • Mazingira ya maandishi • Lazima kuangalia maandiko yote katika ujumla,ni hatari kuchambua

    fungo fulani halafu kuipatia tafsiri ya peke yake.. • Kila fungo ni ”block” katika jengo nzima. Kuondosha ”block” moja

    hapa na nyingine pale na kuamini ndipo tafsiri kamili itapatikana. Lazima kuangali lote.

    • Kumbuka Ufunuo ni barua pia yenye mtiririko wa habari. Tofauti na vitabu vya manabii wa AK

  • UFUNUO 11• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 1 • Kazi ya kwanza haina tofauti na vitabu vingine vya Biblia, ni lazima tuelewe ujumbe wa wapokeaji

    wa barua wakati ule. Kitabu cha Ufunuo ni kitabu cha kiunabii kwa hiyo pia tunaelewa kwamba ili husu siku zao za mbele.

    • Mara nyingi inahusu ”siku za mbeke za karibu” hiyo kwetu itakua ni historia. (Kama vile Yeremia alivyotabiri kweli Yuda wakawa mateka, na pia kama vile Yohana alivyonena pia Warumi walipewa hukumu ya mda)

    • Tunapoona matokeo ya maneno waliyonena, na yanapothibitishwa katika maandiko ya kihistoria inakua ni rahisi kuelewa alichokitabiri. Tunaweza kuangalia sababu za hukumu na kujihadhali tusije tukahukumiwa kwa sababu hizo. Yanatufundisha kwamba Mungu anahukumu dhambi, na kwamba atahukumu kila nchi inayowafanyia wakristo ,watu wake, mabaya.

    • Pia tunajifunza kwamba ufuasi siyo kitu rahisi lazima tukubali msalaba wakati tunapomfuata Yesu wetu. Hatujaahidiwa ushindi juu ya kifo na mateso baali tumeahidiwa ushindi kupitia kifo na mateso.

    • Hiyo inafanya Ufunuo kua kitabu ambacho inawapa moyo wakristo wanaoishi katika mateso mbali mbali kwa ajili ya imnai yao. Inawapa ahadi kwamba Mungu anayo ”control” juu ya mambo yote. Ameyaona anajua la kufanya.

    • Mafundisho hayo ni muhimu kurudia mara kwa mara mana ni lazima kanisa liwe linaishi ndani ya ukweli wa namna hii, ukishindwa kugundua ujumbe huo katika Ufunuo, hakika umeshindwa kupata ujumbe wowote.

    • Lakini pia kuna mengine......na hiyo bila shaka ni tatizo pia. Mengi yanayohusu wakati ule pia inahusu wakati wa mwisho. Lakini kuyachambu vizuri siyo rahisi mana yanasukwa pamoja katika mchanganyiko usiyo chambuliwa. Msaada kidogo tunaweza kupata tukitumia taratibu zifuatazo:

  • UFUNUO 12• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 2

    • 1. Lazima tuelewe kwamba mifano na picha ni mifano na picha siyo hali halisi. Zinapenda kutuonyesha hali fulani lakini siyo hali hii katika ukamilifu. Pia inawezekana kua baadhi ya mambo hayatakiwi kuchukuliwa katika utafsiri zipo tu kama chumwi kidogo. Kwa hiyo parapanda zile nne zinapolia na kuwakilisha taabu zitakazokuja. Inawakiloisha taabu ila inaweza ikawa tofauti na jinsi inavyoelezwa katika kitabu.

    • 2. Pia kuna picha zinazo eleza juu au hukumu ambayo itakuja, na ulazima wakuja kwa hukumu hiyo, lakini haina maana kwamba itatokea sasa hivi au katika mda wa karibu. Wakati shetani alipotupwa chini kutoka mbinguni (sura 12), kwa sababu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, alianza vita yake na kanisa. Alifahamu kwamba mda wake ni mfupi na kwamba una mipaka, lakin haisemi urefu wa mda wake wala hata yeye hawezi kujua. Sisi tunaelewa kwamba ipo siku yake ya kufungwa na haachiwi tena, ila hatujui siku wala saa..

  • UFUNUO 13• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 3

    • 3. Mifano ambayo inakua na hali ya sasa lakini pia yanakaribia mambo ya baadaye ni lazima tuweze kuvichambua katika miwili, hata kama waliyoisoma mara ya kwanza walitegemea kwamba yote yatatokea kwa wakati wao. Picha hizo zinasimulia hukumu na wokovu utakaokuja na pia zinakua na hali ya ”sasa ila baado” ndani yake. Lakini hakuna kanuni zakufuata katika kuelewa vizuri ipi ni ipi, hatuwezi kusema kwa uhakika hiyo ni siku ya mwisho au hiyo itatokea wakati tungali hapa.

    • Kitu muhimu ni kujaribu kujihadhali sana tusije tukakwama katika kujaribu kuelewa nini itatokea sasa na nini ni la baadaye. Kitabu hiki haikuhusika na vita vya Ruanda, Burundi na Zaire. Wala haikutaja ukommunisti, uislamu na sijui nini ambayo sisi tunaweza kuliiingiza katika kufafanua kwetu. Wala haituletei ratiba ya siku za mwisho....

  • UFUNUO 14• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 4

    • 4. Ingawa kuna sehemu katika Ufunuo ambayo mpaka leo haijatokea wala kufafanuliwa kihakika, hatuja pewa vifaa vya kutumia tunaposoma juu ya mambo haya. Hapo AJ inaonyesha wasi wasi kidogo au kuyumba. Mpinga Kristo ni mfano mmoja ambao inatupa shida. Paulo anapomsema anaonekana ni mtu binafsi (2Thess 2:3-4) na katika Ufunuo 13-14 anajitokeza kama kaisari wa Roma. Katika mifano yote hio miwilini kama atajitokeza kwa siku za mbele. Lakini katika 1Yoh ni kama inaletwa tafsiri nyingine, inaweza kua mtu yeyote yule ambaye anaharibu kazi ya kanisa kwa ndani. Sasa tumweleweje huyo Mpinga Kristo.

    • Katika historia yetu watawala wengi wametajwa kama wao ndio mpinga kristo; Hitler, Idi Amin na wengi wengine. Na kwa kweli wote hao wanaweza wakawa tafsiri mojawapo ya Mpinga Kristo, na inaweza kua tafsiri juu ya neno kwamba wapinga kristo wengi watajitokeza (1Yoh 2:18).

    • Lakini je! atakua mtawala wa ulimwengu wote ambaye ataongoza mambo yote ya dunia katika siku za mwisho, je, ni hivyo tutakavyoelewa Ufunuo 13-14? Siyo lazima ! Lakini pia inawezekana. Kwa vile A.J. halina msimamo kamili itabaki makisio to hakuna uhakika...

  • UFUNUO 15

    • Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 5 • 5. Mifano na picha ambazo ni za siku za mwisho kabisa, lazima

    tuziruhusu kubaki pale pale kwa mfano: 11:15-19, na 19:1-22:21, zinahusika na wakati wa mwisho kabisa. Sehemu hizo ni lazima ziangaliwe kama kipindi ambacho baado halijatufikia katika hali yoyote.

    • Kama vile sura za kwanza katika Biblia zinahusu Mungu na uumbaji kitabu cha mwisho inahusika na mwisho wa kila kitu hapa duniani. Tunaona kwamba Mungu atayamaliza yote kama vile alivyokusudia kila kitu kwa mda wake na mpango wake. Kuelewa hiivyo inatupa moyo wa kuvumilia katika yote tunayoyapata, kama vile ilivyowafariji waliyosoma Ufunuo wakati ule.

    • Mpaka hapo tutaishi katika ”sasa ila baado” ambapo ”sasa yetu” ni kwamba tunasoma maneno yake Mungu na kuyafuata, pamoja nakupokea yale yote anayotupatia. Lakini tunategemea kwamba kutakuja siku moja ambayo mambo mengi yatakua tofauti ”Hawatakua na haja ya kufundishana....maana watanijua” (Jeremia 31:33)