uhakiki wa mtindo katika diwani ya mashairi ya...
TRANSCRIPT
UHAKIKI WA FANI NA MAUDHUI KATIKA MASHAIRI YA SAUTI YA DHIKI YA
ABDILATIF’ ABDALLA
SAMWEL IKIARA KULU
Tasnifu inayowasilishwa kwa Shule ya Mafuzu ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya
Shahada ya Uzamili katika Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Egerton.
CHUO KIKUU CHA EGERTON
SEPTEMBA, 2016
ii
UNGAMO NA IDHINI
Tasnifu hii ni kazi yangu binafsi na haijawahi kuwasilishwa na yeyote kwa mahitaji ya shahada
katika Chuo Kikuu chochote kile.
_________________________ ________________________
Sahihi Tarehe
Samwel Ikiara Kulu
(AM12/2621/10)
IDHINI
Tasnifu hii ya uzamili imewasilishwa kwa ushauri na idhini yetu kama wasimamizi
walioteuliwa rasmi na Chuo Kikuu cha Egerton.
_________________________ _______________________
Sahihi Tarehe
Prof. James Onyango, Ogola
Idara ya Mawasiliano na Mtalaa wa Fasihi, Chuo Kikuu cha Laikipia.
_________________________ ________________________
Sahihi Tarehe
Prof. Wendo, Nabea
Idara ya Mawasiliano na Mtalaa wa Fasihi, Chuo Kikuu cha Laikipia
iii
HAKILINZI
©2016, Samwel Ikiara Kulu
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupigisha chapa, kutafsiri au kuitoa
tasnifu hii kwa jinsi yoyote bila idhini ya mwandishi au Chuo Kikuu cha Egerton.
iv
TABARUKU
Naitabaruku ripoti hii kwa wapendwa wafuatao: Dkt Wendo Nabea, Kelly Gakii na Abib
Ufanisi.
v
SHUKURANI
Namshukuru Mwenyezi Mungu kisha Chuo Kikuu cha Egerton kwa kuniruhusu kusomea
huko hadi kuhitimu. Nachukua fursa zaidi kwa heshima na taadhima kuu kuwashukuru
wasimamizi wangu katika utafiti huu. Hawa ni Profesa James Onyango Ogola na Dkt. Wendo
Nabea ambao walirekebisha kazi yangu kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa kuwajibika bila
kuchoka. Bila ya mchango wao kazi hii ingebaki ndoto ya mchana.
Nashukuru waalimu wawili Bw. Humphreys Omwaka na Bwana Peter Owino wote wa
Moi Forces Academy – Lanet kwa mchango wao mkuu katika kazi hii. Bwana Omwaka
akanipa vitabu tele adimu huku Bw. Owino akinifaa kwa huduma za maktaba ya kifaransa
anayoongoza shuleni.
Namshukuru pia mke wangu Bi. Kelly Gakii na wanangu Kinya, Wesley na Abib kwa
kunipa nguvu hata wakati wa changamoto kuu. Baba yangu japo marehemu Bw. Daniel M.
Ikiara aliyenizaa na kunilea na hata kunielimisha hadi nilipo anakumbukwa kikamilifu kwa
heshima. Pia Bi. Kebaso na Bw. Eric Odhiambo walinifaa kwa kupiga chapa kazi nzima. Wote
walionisaidia kwa njia moja au nyingine wanakumbukwa. Ahsanteni sana. Zaidi ya wote,
Mwenyezi Mungu apokee shukrani na sifa kwa kunipa nguvu kufanya kazi ngumu na kufaulu.
vi
IKISIRI
Kwa kipindi kirefu mashairi yametambulika kama sehemu ya usomi wa Kiswahili.
Mashairi ya arudhi yamekuwepo kwa karne kadha zilizopita. Haya yalilazimisha uzingativu wa
sheria za utunzi. Wataalamu wa baadaye kama Euphrase Kezilahabi,M.M Mulokozi na C.Kahigi
nao wakazua mashairi huru ambayo hulenga zaidi ujumbe na maudhui badala ya arudhi za
utunzi. Mashairi mapokeo yakapigwa vita kwa kupuuza maudhui yakizingatia fani. Kufuatia
kukubalika kwa mashairi huru,utafiti zaidi ulihitajika ili kuendelea kudumisha nafasi yake katika
fasihi ya Kiswahili. Aidha tasnifu za uhakiki hasa wa diwani ya Sauti ya Dhiki zilizopo hadi sasa
zinalenga swala mojamoja badala ya vipengele kadha vya ushairi. Utafiti huu ulilenga kuhakiki
fani na maudhui ya mashairi teule katika diwani ya Sauti ya dhiki ya Abdilatif’ Abdalla. Haya ni
mashairi mapokeo. Uteuzi huo ni kutokana na kufanana miundo kwa mashairi mengi katika
diwani husika. Ilitafitiwa jinsi malenga alivyotumia kipengele cha uhusika, kuhakiki ufundi wa
lugha na muundo pamoja na maudhui. Mashairi yaliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia idadi ya
beti, aina ya wahusika, tamathali za usemi na aina ya maudhui. Nadharia za
umuundo,umuundoleo na uamilifu zilitegemewa. Mbinu ya utafiti ilihusu uchambuzi wa
yaliyomo katika matini (mashairi husika). Maktaba na tovuti mbalimbali zilitegemewa kupata
taarifa kulenga mashairi mapokeo. Mchango wa utafiti huu ni kutoa mwanga muhimu wa
kuhakiki mashairi kwa wanafunzi na wasomi wa vyuo na vyuo vikuu pamoja na wapenzi binafsi
wa ushairi wa Kiswahili na uhakiki wake.
vii
ABSTRACT
For long time poetry has remained a very important part in the study of Kiswahili literature.
Prosodic poems have existed for several centuries now. These poems required the poet to follow
a specific structure while composing them. Later Kiswahili scholars like Euphrase Kezilahabi,
M.M Mulokozi and C. Kahigi came up with free verse poems which focused most on themes and
message. Prosodic poems were therefore criticized for preferring form and style to themes.
Following the widespread acceptance of free verse poems, further research in prosodic poems is
required so as to continue preserving their place in Kiswahili literature .On the other hand, up to
now available research reports about analysis of Sauti ya Dhiki poems touch on single aspects of
poems instead of several. This research aimed at analyzing style and themes in selected poems
in Abdilatif’ Abdalla’s Sauti ya Dhiki. Such selection is due to similarity of the structure of many
poems in the anthology. It was researched on how the poet has used characters, poetic devices
and structure and how these components generate certain themes. The poems were purposively
sampled based on the type of characters, poetic devices, number of stanzas and themes generated
by these aspects. The research relied on structuralism, poststructuralism and functionalism
theories. The method of research used was content analysis of the relevant selected poems. It
involved visiting various libraries and websites to get information relevant to prosodic poems.
The results of the research are expected to give important insight on poetic analysis to students
and scholars in colleges and universities as well as individuals interested in Kiswahili research
and poetry.
viii
YALIYOMO
UNGAMO NA IDHINI.............................................................................................ii
HAKILINZI...............................................................................................................iii
TABARUKU………………………………………………………………………..iv
SHUKURANI……………………………………………………………………….v
IKISIRI……………………………………………………………………………..vi
ABSTRACT ..............................................................................................................vii
YALIYOMO………………………………………………………………………viii
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI ..................................................................1
1.1 Usuli wa Mada .....................................................................................................1
1.2 Suala la Utafiti ....................................................................................................4
1.3 Madhumuni ya Utafiti ..........................................................................................5
1.4 Maswali ya Utafiti................................................................................................5
1.5 Umuhimu wa Utafiti ............................................................................................6
1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti ...................................................................................7
1.7 Maelezo ya Istilahi ...............................................................................................8
SURA YA PILI :MAPITIO YA MAANDISHI NA MISINGI YA NADHARIA
2.1 Utangulizi .............................................................................................................10
2.2 Wahusika wa Mashairi .........................................................................................10
2.3 Mbinu za Lugha au Tamathali za Usemi .............................................................13
2.4 Muundo wa Mashairi ...........................................................................................19
2.5 Maudhui ya Mashairi……………………………………………………………25
2.6 Tafiti zinazohusiana na Utafiti huu ......................................................................29
2.7 Misingi ya Nadharia .............................................................................................33
SURA YA TATU : MBINU ZA UTAFITI ............................................................39
3.1 Utangulizi .............................................................................................................39
3.2 Muundo wa Utafiti ...............................................................................................39
3.3 Mahali pa Utafiti ..................................................................................................40
3.4 Uteuzi wa Sampuli ...............................................................................................40
ix
3.5 Ukusanyaji wa Data………………………………………………………. 41
3.6 Uchanganuzi wa Data ..........................................................................................42
SURA YA NNE: UWASLISHAJI, UCHANGANUZI NA UFASIRI WA DATA
4.1 Utangulizi ...............................................................................................................43
4.2 Jinsi mshairi alivyotumia wahusika……………………………………………43
4.2.1 Sifa mbaya za wahusika………………………………………………………..44
4.2.2 Wahusika wapekuzi na werevu ...........................................................................47
4.3 Tamathali za usemi au mbinu za lugha .................................................................54
4.4 Muundo katika mashairi ......................................................................................74
4.5 Maudhui katika mashairi yaliyoteuliwa ..................................................................84
SURA YA TANO ........................................................................................................95
MUKHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ..........................................95
5.1 Utangulizi.…………………………………………………..…………………….95
5.2 Jinsi mshairi alivyotumia wahusika .....................................................................…95
5.2.2 Tamathali za usemi au mbinu za lugha ............................................................…97
5.2.3 Muundo .............................................................................................................…99
5.2.4 Maudhui ............................................................................................................…101
5.3 Hitimisho…………………………………………………………………………..102
5.4 Mapendekezo ...................................................................................................….107
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1 Usuli wa Mada
Dhana ya ushairi katika jamii ya Waswahili imekuwepo katika fasihi simulizi kwa muda mrefu.
Mashairi ya tenzi yakawa kazi za kwanza wakati mashairi yalianza kuandikwa ikiwemo Utenzi
wa Mwalemba kuandikwa katika karne ya kumi na sita. Mwaka 1728 Mwego bin Athumani
akatunga Utenzi wa Tambuka naye Muhamadi Kijumwa akaandika Utendi wa Fumo Liyongo
mwaka 1913. Baada ya tenzi, Muyaka bin Hajji (1876) akatunga mashairi ya arudhi kama
tathlitha na tarbia kisha washairi wa baadaye kama Shaaban Robert (1933), Mathias Mnyampala
(1965) na pia Abdilatif’ Abdalla (1969) wakamuiga Muyaka kwa kiwango kikubwa katika utunzi
wao. Mashairi ya kabla ya uhuru nchini Kenya kwa mfano yaani miaka ya 1963 na kurudi
nyuma yalilenga maswala ya kidini na kijamii na pia kuanzia mwaka 1968 yakakumbwa na
upinzani kutokana na kuzuka kwa mashairi huru. Aina hizi mbili za mashairi kila wakati huwa
na fani na maudhui. Katika mantiki hii, swala la mashairi mapokeo kutungwa na hata
kuhakikiwa laonekana kuwa la lazima. Pia kuhifadhi nafasi yake katika usomi wa fasihi andishi
ya Kiswahili kusingewezekana kikamilifu bila tasnifu inayolenga vipengele kadha vya mashairi
ikiwa si vyote.
Utafiti huu ulichagua na kuhakiki mashairi teule katika diwani ya Sauti ya Dhiki ya Abdilatif’
Abdalla. Lengo lilikuwa kuweka wazi fani na maudhui ya mashairi haya. Diwani ya Sauti ya
Dhiki ni mojawapo ya diwani za mashairi yaliyojipambanua kwa kutoa mchango unaoaminika na
wasomi wengi kuwa mfano bora wa ufundi wa mashairi ya arudhi. Diwani hii ni muhimu sana
katika ushairi wa Kiswahili kwani takribani muundo wa tarbiya ambao aghalabu hutumika katika
ushairi wa Kiswahili wabainika katika diwani hii.
Abdilatif’ Abdalla ni mmojawapo wa washairi wa kusifika sana katika ulimwengu wa Kiswahili.
Alitunga diwani hii akiwa jela Shimo la Tewa na Kamiti (1969 – 1972), nchini Kenya. Yeye ni
mmojawapo wa washairi wa Kiswahili wasifika sana walio hai. Kazi yake imetafitiwa kama njia
mojawapo ya kuendeleza ushairi asilia wa Kiswahili wenye dhima nzito hata kwa ushairi wa leo
hii. Kuchanganya ushairi na siasa imekuwa sifa ya jamii ya Waswahili kwa muda na hata
2
kihistoria Uswahilini, washairi kama Liyongo Fumo na Muyaka bin Haji walishiriki siasa za
maeneo yao pamoja na kutunga mashairi. Kama wakwasi hawa wa kabla yake, Abdalla ameishi
miongoni mwa Waswahili wenzake na hata kuwahi kutengwa nao akitumikia miaka mingi ya
kifungo na uhamisho. Alitumikia zaidi ya miaka mitano ya uhamisho kule Tanzania (Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam) na zaidi ya mingine kumi na tano kule London. Alishirikiana na
watetezi wengine wa kisiasa kama Ngugi wa Thiong’o kupinga utawala dhalimu wakati wa Rais
wa pili wa Kenya.
Baada ya kusoma mashairi ya mjombake wakati Abdilatif’ akiwa na umri wa miaka kumi na
miwili, pia alipata fursa ya kuzuru maeneo mengi ya Uswahilini ambapo Kiswahili
huzungumzwa. Mifano ni Mombasa,Iringa kule Tanganyika,Faza katika kisiwa cha Pate, kule
Lamu na Archipelago na Takaungu.Yeye hutumia lahaja ya Kimvita katika mashairi yake na pia
anaelewa lahaja nyinginezo nyingi. Mchango wake kustahili kutafitiwa una mashiko zaidi kwa
kuwa amechipuka kwa familia thabiti ya Waswahili katika makabila kumi na mawili ya
Mombasa jamaa zake wakiwa wasomi wa Kiislamu,washairi na matabibu wa kimila. Ndugu
zake ni kama Sheikh Adilahi Nassir, msomi maarufu wa Kiislamu na mchapishaji wa awali na
mwanasiasa wa Uswahilini pamoja na Ustadh Ahmad Nassir Juma Bhalo ambaye pia ni mshairi
maarufu na tabibu. Washairi kama hawa Uswahilini huthaminiwa sana kama wenye maarifa na
jukumu la kuzungumza kwa niaba ya wanajamii wenzao.
Abdilatif’ anatambulika zaidi kwa kazi zake nyinginezo kama ‘Kenya Twendapi.’Akapata tuzo
yake ya kwanza katika uandishi wa fasihi katika shairi lake toka kwa Kurani la Utenzi wa Adamu
na Hawaa. Kazi zake zaidi pia ni mihadhara kuhusu nafasi ya mashairi katika jamii na uhariri wa
mashairi. Zaidi ya hayo, Abdilatif’ ameandika tafsiri za Kiswahili ikiwemo riwaya ya Ayi Kwei
Arma ya Wema Hawajazaliwa pamoja na ile ya Mahmood Mamdam ya Waislamu wazuri,
Waislamu wabaya. Haya yote yanamuonyesha kama msomi maarufu wa kutoka Uswahilini na
pia aliyesifika nje ya Uswahilini. Ushairi wake ni kiwakilishi cha muoano wa ufundi wa
kizamani na wa kisasa kitaifa na kimataifa. Ushairi wake unawapa nafasi wasomi wengi wa
Afrika mashariki na kwingineko duniani kupata mguso wa ushairi wa Kiswahili uliotungwa na
Mswahili asilia.
3
Kumekuwako na imani ya kimapokeo kuwa mashairi yoyote yale ni lazima yajifunge katika
kanuni za utunzi (arudhi maalum) kama inavyodhaniwa amefanya mtunzi huyu. Mifano ya
arudhi au sheria za utunzi ni uwiano wa mizani, vina, vipande na mishororo, muwala (mpangilio
mzuri wa mawazo) kwenye maneno, vipande, mishororo na beti na matumizi ya lugha Kteule
inayovutia. Mtunzi angekiuka kanuni hizi, mashairi yake yangeonekana chapwa na
yasiyokubalika kamwe. Kitula King’ei, mmoja wa watetezi wa mashairi mapokeo kwa mfano
katika utangulizi wa mashairi yake ya Miale ya Uzalendo anapinga mavue kwa kusema kuwa
dhana ya mashairi vue ni geni kabisa na isiyoambatana kamwe na kaida za ushairi wa Kiswahili.
Anasema mavue yaliletwa kwa pupa kwa kupapia ugeni toka utamaduni wa Kiingereza wala
hayana mashiko katika utamaduni wa ushairi wa kiafrika.
Lengo la utafiti huu ni kuangaza maswala kuhusu mashairi ya arudhi. Katika mashairi mapokeo
kama haya na mengineyo, ufundi wa utunzi wa mashairi ndio hutumika kukadiria kiwango cha
ubingwa wa mshairi. Kuna tafiti kadha zilizofanywa kuhusu mada tofautitofauti kulenga
mashairi ya Abdilatif’ Abdalla na Sauti ya Dhiki. Hata hivyo, vipengele vya fani na maudhui
nilivyohakiki havikulengwa katika tafiti hizo. Hili lathibitisha kuwa hakuna uhakiki kamili wa
kitaalamu uliofanywa hapo awali kulenga fani na maudhui ya mashairi haya yaliyohakikiwa.
Kipengele cha uhusika hasa kimetajwa tu katika tasnifu nyingi. Ikagundulika kuwa chahitaji
kuangaziwa zaidi. Ni kutokana na msukumo huu ulipopatikana mshawasha wa kuhakiki
vipengele hivi. Mifano ni muundo, lugha, wahusika na maudhui. Kwa kifupi, hili ndilo pengo
lililolengwa kuzibwa kuhusiana na uhakiki wa mashairi haya.
1.2 Suala la Utafiti
Malenga Addilatif’ Abdalla ni maarufu sana katika ulimwengu wa ushairi wa Kiswahili. Kuna
wataalamu kadha waliowahi kutilia guu kutafitia utunzi wake katika mashairi tofautitofauti.
Tafiti kama hizo zililenga mada fulani maalumu au kutoa mashairi yake kama mifano ya
kufafanua mada za wataalamu hao. Katika tafiti hizo, ni bayana kuwa hakuna utafiti hata mmoja
uliojitokeza kuhakiki vipengele vyote vya fani na maudhui katika tasnifu moja. Isitoshe, fani na
maudhui anayotumia ni za kipekee ingawa hazijaeleweka kikamilifu kwa wasomi wengi. Hii ni
kwa sababu mojawapo ya vipengele vya fani anavyotumia ni uhusika katika ushairi wake jambo
ambalo halijadhihirika kwa wengi. Ufundi wake wa lugha pia pamoja na muundo ni vipengele
4
vinavyofaa kuchunguzwa kwa jicho la ndani zaidi kuliko vilivyobainishwa na wataalamu wa
hapo mbele. Wengi wametafitia ushairi wa Abdilatif’ lakini kwa fani na maudhui bado kuna
pengo. Kipengele cha uhusika na vile vingine vya fani na maudhui vimetafitiwa na wataalamu
wengine lakini havibainiki kutiliwa uzito unaostahili huku baadhi ya watafiti kama Marani(2014)
wakisisitiza shairi halina wahusika isipokuwa kwa tenzi na ngonjera. Kauli hii ni upotoshi kwa
wanafunzi wa ushairi. Hili lahalalisha utafiti wa kina kuhusu kipengele hiki na maudhui
yanayozuliwa nacho.
1.3 Madhumuni ya Utafiti
(i) Kutathmini jinsi mtunzi/malenga anavyotumia kipengele cha uhusika katika mashairi
yake.
(ii) Kuchambua ufundi wa lugha au tamathali za usemi katika mashairi teule ya Sauti ya
Dhiki.
(iii) Kuhakiki muundo wa mashairi teule katika diwani.
(iv) Kufafanua maudhui yanayozuliwa na fani katika mashairi yaliyoteuliwa.
1.4 Maswali ya Utafiti
(i) Kipengele cha uhusika kimetumika vipi katika mashairi teule ya Sauti ya Dhiki?
(ii) Mtunzi ametumia mbinu zipi za lugha au tamathali za usemi katika mashairi yake?
(iii) Ni vipengele vipi vya muundo alivyozingatia mtunzi katika mashairi yaliyoteuliwa?
(iv) Vipengele vya fani vinazua maudhui ya aina gani katika mashairi husika?
1.5 Umuhimu wa Utafiti
Uhakiki wa ushairi ni mada muhimu sana katika fasihi yoyote ile iwe simulizi au andishi. Usomi
wa fasihi nao ni kipengele kisichoweza kupuuzwa katika somo la Kiswahili.Utafiti huu
ulichagua sampuli za mashairi kumi na mawili katika diwani ya Sauti ya Dhiki kisha kuhakiki
fani na maudhui yaliyotumiwa na malenga. Wahusika, muundo, mbinu za lugha na tamathali za
usemi na namna vipengele hivi vinavyozua maudhui maalumu ni mambo yaliyotathminiwa.
Inaelekea kwamba wanafunzi wa viwango mbalimbali vya usomi ikiwemo wa vyuo vya juu
hupata changamoto kadha kuhusiana na uchambuzi wa mashairi. Wengi wao hata hawana
5
fununu kuhusu fani ya ushairi. Marani(2006) anapotafitia hali ya Kiswahili katika vyuo vikuu
kwa mfano anaeleza kwamba vyuo vingi vya umma na vya kibinafsi vina idara za Kiswahili.
Katika idara hizo, lugha ya Kiswahili hutegemewa kufunza kozi za Kiswahili. Pia anasema
vitabu vya fasihi ya Kiswahili vyuoni ni vichache mno. Tasnifu hii inalengwa kuwa nyenzo ya
ziada kwa vitabu kama hivyo. Zaidi ni kuwa mada ya ushairi hutajwa kwa ufinyu katika vyuo
vingi vikuu kwani msisitizo huwekwa kwa semantiki, mofolojia na kazi nyinginezo za fasihi
lakini ushairi ukitajwa kwa kiwango fulani tu.
Inatarajiwa matokeo ya utafiti huu ni nyenzo ya kuimarisha usomi wa ushairi wa Kiswahili
pamoja na waratibu wa mitaala ya fasihi kupata mwanga mpya katika juhudi zao. Pamoja na
hayo, maarifa yaliyopo kwa sasa kuhusiana na pia yanayokaribiana na ya Abdilatif’
yataongezwa. Wanaojifunza ushairi wa Kiswahili kwa mara ya kwanza watafaidika zaidi. Lugha
ya Kiswahili ikiimarika sasa hivi ni afueni kubwa kwa taifa la Kenya hasa kwani tangu mwaka
wa 2010 lugha hii ni ya taifa na pia rasmi kulingana na sehemu ya 7(1), (2) na (3) sheria za
Kenya. Mwisho, uchambuzi wa ushairi ni njia mojawapo wa kueleza msamiati wa utunzi kwa
kuweka maana yake wazi hivyo basi kuimarisha mawasiliano. Pia msamiati huu ni njia
mojawapo ya kukejeli hali fulani mbaya katika jamii na hivyo kuimarisha maadili ya jamii yetu.
1.6 Upeo na Mipaka ya Utafiti
Mashairi yote yaliyohakikiwa yalitoka kwa diwani ya Sauti ya Dhiki. Kwa kuzingatia vipengele
vinne vya mada vilivyohakikiwa fani na maudhui zilihakikiwa. Sampuli kumi na mbili za
mashairi ziliteuliwa na kuchunguzwa baada ya kupangwa ifuatavyo:-
a) Mashairi yenye wahusika binadamu:- Katika kikundi hiki nilihakiki mashairi kama vile:
‘Kutendana’, ‘Ukamilifu wa mja’ na ‘Mja si mwema’.
b) Mashairi yaliyo na lugha teule na ya kitamathali. Hapa kulikuwa na mashairi kama vile
‘N’shishielo ni lilo’, ‘Wasiwasi enda zako’ na ‘Telezi’.
c) Kwa mashairi yenye muundo wa tarbia na yaliyobuniwa kwa chini ya beti kumi kulikuwa
na mashairi kama ‘Siwati’, ‘Leo nisingekuwako’ na ‘N’sharudi’.
d) Mashairi yaliyolenga maudhui ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yalikuwa na ‘Wasafiri
Tuamkeni’, ‘Kichu Hakiwi na uchu’ na ‘Mamaetu Afrika’.
6
Jumla ya mashairi katika diwani ni arubaini ila haya kumi na mawili yakateuliwa kimakusudi
kwani hayakulengwa na watafiti waliotangulia hasa wakilenga mada au nadharia ya utafiti huu.
Kuzingatia kigezo hiki kuteua sampuli hizi ndicho faafu zaidi kwa kuwa kililenga vipengele
vyote vya fani na maudhui vilivyohakikiwa. Baadaye mada lengwa ilihakikiwa kwa undani
katika kila kikundi cha mashairi kulingana na madhumuni ya utafiti. Kwa kila kikundi cha
sampuli fani zilielezwa kama zilivyobainika hivyo kuchukuliwa kama kiwakilishi mwafaka cha
ufundi wa mtunzi katika mashairi husika.
1.7 Maelezo ya Istilahi
Dhamira:- Lengo, kusudi au nia ya mshairi
Diwani :- Kitabu cha mashairi
Falsafa ya mwandishi :-Huu ni msimamo wa malenga kuhusu suala linalorejelewa katika shairi.
Maoni yake kuhusu jambo fulani ni yapi ?
Fani :- Ni jinsi au ufundi wa kuwasilisha maudhui ya shairi.
Kunga za kishairi :- Hizi ni mbinu za kishairi kama vile urefusho, ukopaji wa maneno ya
kigeni, matumizi ya maneno ya kizamani, uborongaji, lugha fiche na kadhalika.
Maudhui:- Ni mukhtasari wa mambo muhimu au hoja muhimu anazojishughulisha nazo mtunzi
wa kazi ya fasihi.
Mbinu za lugha :- Ni tamathali za usemi pamoja na fani mbalimbali zilizotumika na mshairi
kutosheleza maudhui yake. Mifano ni methali, takriri, istiara na kadhalika.
Mtindo:- ni namna ya kupanga fani au maudhui ili kujenga shairi kwa njia ambayo hubainisha
upekee wa shairi. Hujumuisha vipengele vyote vya ushairi kama vile muundo,
matumizi ya lugha, wahusika na maudhui.
Muktadha :- Sifa zinazijitokeza katika shairi kisiasa, kiuchumi, kijamii, kikazi na kadhalika.
Muktadha hutuelekeza kwenye maudhui na dhamira.
Muundo :- Ni mpango na mtiririko wa kazi ya fasihi. Katika ushairi hurejelea namna shairi
lilivyoumbwa.
Tamathali za usemi :- Ni maneno, nahau au sentensi ambazo hutumiwa na msanii wa fasihi ili
kutia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika maandishi ama kusema.
Toni :- Huu ni ule mtiririko au msuko wa lugha unaodhihirisha au unaoashiria hisia ya furaha,
msiba, huzuni na kadhalika katika shairi.
7
Uguni :- Ni dosari au kasoro fulani katika shairi.
Uhakiki :- Haya ni maelezo yanayoeleza undani wa kazi fulani ya fasihi (kama vile shairi] kwa
kumulika uzuri na udhaifu wake. Uhakiki wa mashairi hulenga dhamira na maudhui,
umbo, kunga za kishairi na matumizi ya lugha.
Uhuru wa kishairi :- Ni uhuru mshairi wa Kiswahili anao wa kutunga pasi na kuzingatia kanuni
za sarufi.
Umbo :- Ni sura ya nje ya shairi inayotokana na bahari, mpangilio wa mizani, vina, vipande,
mistari, vituo na idadi ya beti.
Utoshelezi :- Shairi kuwa na wazo linaloendelezwa na kukamilishwa kimantiki.
Nafsineni - ni mhusika anayesema ujumbe fulani katika shairi. Ni jina jingine la mshairi katika
shairi husika.
8
SURA YA PILI
MAPITIO YA MAANDISHI NA MISINGI YA NADHARIA
2.1 Utangulizi
Sura hii ililenga kuangazia maandishi ya wataalamu mbalimbali kuhusu ushairi wa Kiswahili.
Kwa kuongozwa na madhumuni ya utafiti huu, sura hii ililenga wahusika katika mashairi,
kuchambua ufundi wa lugha au tamathali za usemi, kuhakiki muundo wa mashairi hayo kisha
maudhui. Tafiti zilizofanywa kuhusiana na diwani ya Sauti ya Dhiki na namna zilifaidi au
kutofautiana na utafiti huu ziliangaziwa. Hatimaye mtafiti akaelezea nadharia zilizokuwa msingi
wa utafiti.
2.2 Wahusika wa Mashairi
Kuhakiki shairi kwahitaji kuelewa kuhusu wahusika. Kisia na Mwarandani (2007) wanasema
kuwa katika ushairi wapo wahusika. Mhusika wa kwanza ni mtunzi mwenyewe. Yeye huwa ana
kisababisho cha utunzi huo kilichompata yeye au kukisikia kuhusu mtu ambaye ataka aseme
katika utungo wake. Pia kuna wale ambao anawasiliana nao, wale anaowakusudia ujumbe; kuna
msomaji na msikilizaji.
Kwa vile mhusika ni mtendaji, hata mtunzi hukifanya kitu kisicho na uhai ambacho huwa
amekifanya huyo mhusika wake. Ama mtunzi huweza kutumia mbinu ya litifati – mbinu ambayo
ni kama ile ya msemo halisi, ambapo mtunzi anasemewa maneno yake na mhusika mwingine
lakini maneno yenyewe yakawa kama kwamba yanasemwa na mhusika wa kwanza.
Ansani (2011) anasisitiza kwamba wahusika katika ushairi si muhimu kama walivyo kwa
nathari. Anasisitiza kuwa twaweza pata mashairi mengi yasiyo na wahusika. Mara nyingine
hakuna kiumbe yeyote hai katika ushairi. Hata hivyo, ni vigumu kupata tamthilia au riwaya bila
wahusika. Anasema pia kuna mashairi yenye wahusika ingawa wamebanwa kutokana na ufupi
wa kazi yenyewe ya sanaa. Wahusika katika shairi hutumika tu kudokeza jambo. Kulingana na
Makala yake kuhusu ‘Kujenga wahusika katika shairi’ Mei 4, 2011, shairi hutaja tu jambo
kuhusu maisha ya mhusika halafu msomaji akaachwa kulitafakari.
9
Uhakiki wa mashairi ya Robert Frost uliofanywa na Sparknote (2012) nao unaonyesha kuwa
mashairi mengine huandikwa katika nafsi ya kwanza yakiwa na mhusika maalumu. Ingawa
mshairi aweza kuwa si yuleyule, kuna mambo yanayohusu sauti ya Frost mwenyewe. Haya
yanaonyesha uhusika wa Frost mwenyewe k.m anavyopambana na hali za maisha kama vile
upweke, msongo wa mawazo na mengine anapofuata njia ambayo haifuatwi na watu wengine
katika jamii. Mara nyingine mshairi mwenyewe (Frost) anajitenga na uhusika ili kuzua kinaya
kuhusu maana nzima ya shairi. Utafiti huu ulifaidi wangu kwa kuwa nilihakiki nafsineni kama
alivyosawiriwa. Pia nilihakiki sifa za wahusika waliotumiwa na mshairi huyu aidha kama
binadamu au wa aina tofauti kuwakilisha binadamu. Msisitizo wa wataalamu waliotangulia ni
kwa mashairi tofauti wangu ukiwa kwa diwani ya Sauti ya dhiki.
Kulingana na Njogu na Nganje (2006), mashairi mengi hayana wahusika lakini mashairi ya
masimulizi huwa nao. Tungo kama hizo huwa ni za kimajibizano na wahusika huongea kishairi.
Tungo nyingi hutumia wahusika katika ujengaji na upelekaji mbele wa maudhui.Wanasisitiza
kuwa katika kuhakiki wahusika twafaa kuangalia wahusika hao wana sifa za aina gani, yaani
tabia zao, wanaingiliana vipi na ni taswira gani tunayopata tukizingatia matendo yao au maneno
yao.
Waititu na Ipara (2005) wakizungumzia fani katika mashairi ya arudhi wanasema kuwa uhusika
ni kipengele mojawapo cha fani.Wanasema kuwa mengi ya mashairi ya jadi hayana wahusika
bayana. Hatahivyo, yapo machache yenye wahusika wa dhati. Watafiti hao wanatoa mfano wa
shairi la ‘N’sharudi’ wakisisitiza kuwa mhusika wa shairi hilo ni mshairi mwenyewe. Mchango
wa watafiti hao umekuwa kichocheo kwa huu hadi kuishia kuhakiki uhusika hata katika mashairi
mengine ya diwani hiyohiyo. Msisitizo ni kuwa hata katika shairi hilohilo la ‘N’sharudi’ kuna
wahusika zaidi ya nafsineni tu. Mifano ni wale wapinzani wake, jamaa na marafiki. Hata
hivyo,katika kuhakiki wahusika shairi hilo halikulengwa. Pamoja na hayo, katika madhumuni ya
kuhakiki muundo, shairi hilo limelengwa na hata wahusika zaidi ya waliotajwa na watafiti hao
kubainishwa.
Utafiti huu, unakubaliana na watafiti hawa japo shingo upande. Kwa mtazamo wa utafiti huu,
maoni yao haya ni ya kijumla na kijuujuu kwa kiwango fulani. Isipokuwa katika uhakiki wa
10
mashairi ya Frost, hakuna mashairi yoyote maalumu yaliyolengwa na wataalumu hawa.
Ninaweza pia kuchukua kauli kuwa hata hayo mashairi ya Frost ni ya Kiingereza wala si ya
Kiswahili ikieleweka utafiti wangu huu ni wa ushairi wa Kiswahili hasa wa Abdilatif’ Abdalla.
Zaidi ya hayo, katika utafiti huu Ansani alipingwa kikamilifu kwa kusema kuwa haiwezekani
ushairi kutokuwa na wahusika. Katika diwani ya Sauti ya Dhiki, hakuna shairi hata moja
lisilopata wahusika wake kubainika na kuhakikiwa. Sidhani ningepotoka au kuenda nje ya mada
nikisema kuwa wataalamu hawa hawajalenga kazi yoyote ya Abdilatif’ Abdalla au hata ushairi
wa Uswahilini.
2.3 Mbinu za Lugha au Tamathali za Usemi
Uhakiki wa shairi kila wakati unalazimu mhakiki kufahamu mbinu za lugha zilivyotumika.
Ngure (2014) anapozungumzia fasihi bora anasema kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha ili
kueleza maisha na tajriba ya binadamu hasa kwa namna anavyotangamana na binadamu wenzake
pamoja na mazingira yake. Anasema kuwa fasihi ni sanaa inayotuchorea taswira ya uhalisia wa
maisha ya binadamu. Hivyo inawasilisha hali, maingiliano, mivutano na mikinzano miongoni
mwa binadamu na mazingira yake.
Msomaji au msikilizaji wa kazi ya fasihi hupata na tajriba za hali inayowasilishwa na wahusika
wa kazi hiyo kama walivyosawiriwa. Kutosheka tunakopata katika kazi ya fasihi hakutokani tu
na habari tunazozipokea katika kazi hiyo bali pia kutokana na ufinyanzi wa lugha teule yaani
umbuji. Kwa maoni ya Ngure (2014) njia mojawapo ya kuelimisha, kufaulisha, kufundisha na
kuzindua kupitia fasihi ni kuteua maudhui yenye mguso kwa jamii na kuyasimulia kwa kiwango
cha juu cha umbuji.
Senkoro (1982) kwa upande wake ana maoni kuwa lugha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi na bila
hiyo, hakuwezi kuwa na fasihi. Ndiyo hutumiwa na msanii kuyaibusha mawazo yake katika kazi
hiyo. Kulingana naye kuna matumizi ya lugha ya aina aina. Humu tunagundua tamathali za
usemi, misemo, nahau, methali, lugha za wahusika hasa lahaja zao, uchaguzi wa msamiati,
miundo ya sentensi, ufundi wa kutoa maelezo hasa ya wahusika na utamu wa lugha yenyewe
itumiwayo. Mtaalamu huyu anachukulia tamathali za usemi kuwa maneno, nahau au sentensi
ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika
11
maandishi ama kusema. Hizi wakati mwingine hutumiwa kwa njia ya lugha kuipamba kazi ya
fasihi na kuongeza utamu wa lugha. Diwani ya Sauti ya Dhiki ina matumizi ya lugha
niliyohakiki.
Ingawa maoni haya ya Ngure yanalandana na utafiti huu kwa upande mmoja, mtaalamu huyu
ameegemea upande wa kazi ya riwaya hasa ile ya Kidagaa kimemwozea ya Ken Walibora.
Hajagusia chochote kuhusu uhakiki wa ushairi ikiwa si kuhakiki mashairi ya Sauti ya Dhiki.
Senkoro pia amehakiki mseto wa kazi mbalimbali za fasihi ikiwemo riwaya, hadithi, mashairi na
hata tamthilia. Naweza kuchukua mwelekeo na hata msimamo kuwa hata yeye japo ametoa
mchango tambulika katika uhakiki, bado hajalenga au kuhakiki haya mashairi niliyohakiki.
Mmoja wa wataalamu waliohakiki diwani ya Sauti ya Dhiki ni Chacha (1992). Anasisitiza
utamthlia wa baadhi ya mashairi ambao wasomi waliotangulia pia walikuwa wameutaja.
Mashairi anayoyataja ni ‘Vuta N’kuvute’ na ‘Kutendana’. Japo mashairi anayohakiki ni kutoka
diwani ya Sauti ya Dhiki, tofauti na utafiti wangu ni kuwa anazingatia mashairi manne tu na pia
mada anayotafitia ni utamthlia wa mashairi hayo tu wala si vipengele vyote vya fani na maudhui
kama nilivyohakiki.
Matteru (1975) vilevile ni mmoja wa wasomi waliohakiki diwani ya Sauti ya Dhiki. Anadokeza
juu ya fani na mada mbalimbali ambazo mwandishi anaziibua. Katika Matteru (1975:28)
anaonyesha jinsi Sauti ya Dhiki ilivyo utetezi, maombolezo, ujumbe, kiu ya heri, sauti ya shime,
mjadala wa nafsi na kitulizo. Ieleweke kwamba Matteru anaashiria ujumbe huku nikilenga fani
na maudhui kwa ujumla. Faida yake kwa utafiti huu ni kuwa kazi yake ilitokea kuwa chanzo cha
kuhakiki diwani tena.
Ingawa Chacha anajishughulisha na swala la fani au mtindo, mwegemeo wa utafiti wake si fani
na maudhui ya mashairi haya bali tu utamthilia wake. Hata hivyo, utafiti huo unafaidi wangu
kwani kwa kiwango fulani umezingatia mawili ya mashairi niliyochunguza katika diwani hii ya
Sauti ya Dhiki. Hapa kwa hivyo nikapata upenyo muhimu wa kuhakiki kilichobaki kwa kulenga
fani na maudhui.
12
Mohammed (1977) anaiona fani ya Sauti ya Dhiki kama zao la kariha, ghamidha na ghadhabu za
mtunzi. Anapoijadili fani anataja mtindo wa utunzi, lahaja anayotumia kiutunzi na uteuzi wa
maneno kama njia yenye mguso hasa katika kuelezea maudhui. Ingawa anadokeza fani na
maudhui, yeye haingilii vipengele hivi kwa kina. Nililenga kuhakiki vipengele vyote vya fani na
maudhui vinavyotambulika katika mashairi haya teule.
Zaidi ya watafiti hao, Mwamzandi (1996) amehakiki matumizi ya mbinu za kimaigizo katika
tungo za Abdilatif Abdalla. Tungo zilizoshughulikiwa ni pamoja na Utenzi wa maisha ya Adamu
Hawaa (1991), ‘Mnazi, Vuta N’kuvute’, ‘Kutendana’ na ‘Usiniuwe’. Yeye hazingatii mashairi
mengi bali haya manne tu kutoka kwa diwani ya Sauti ya Dhiki. Pia halengi sehemu kadha za
fani na maudhui kama nifanyavyo ila mbinu za kimaigizo peke yake. Hii ndiyo tofauti kati ya
tafiti zetu.
Mekacha (1996) anauona ushairi kama mojawapo ya tanzu za sanaa itumiayo lugha ili kusawiri
na kuakisi uyakini wa maisha. Pia ni utanzu wa fasihi ambao kama tanzu nyingine za fasihi
huwa na maudhui. Lyndon Harries na marehemu W. Hichens (1962) wana maoni kuwa mshairi
huweza kuwa na ufundi wa kutumia maneno ya kigeni kwa mfano lugha ya Kiarabu au Kituruki
katika shairi la Kiswahili. Hii huonyesha athari kutokana na mazingira au dini ya mshairi. Pia
kuna ufundi wa kupangua maneno katika mshororo. Lengo hapa huwa kuzua mubalagha au
kusisitiza jambo. Utafiti huu ulilenga kupinga hali kama hiyo kwa kusisitiza kuwa hufanyika
katika utunzi maalumu au hata kipindi maalumu cha wakati pamoja na mazingira ya utunzi
wenyewe. Katika hali ambayo mshairi hakuathiriwa au hataki athari yoyote ya kigeni, ushairi
wake utakuwa katika lugha ya Kiswahili pekee.
Kuhusiana na dhana ya uradidi katika Kiswahili, Ashton (1944:316) ameonyesha matumizi ya
aina nne za dhana hii: Kutilia mkazo jambo, kuonyesha uendelezo wa jambo na kuonyesha
mueneo wa jambo. Polome (1967:82, 84, 94, 104-105) pamoja na Kapinga (1983:180)
wamegusia uradidi kwa kusema kuwa huhusu kutaja kitu kilekile mara mbili. Maelezo ya
wataalamu hawa yameonyesha kwa mifano kuwa tendo la kukariri au urudiaji wa sauti ndio
msingi wa dhana hii ya uradidi kama aelezavyo Winter (1970:190) kuwa “uradidi unaweza
13
kusemwa kuwa ni urudiaji wa sauti nzima au sehemu yake au mfuatano wa sauti katika neno.
Ufundi huu ukatajwa hapa na ukaenea hadi kutafitiwa katika tasnifu hii. Hii ni faida si haba.
Ingawa Ilihakikiwa takriri kama mojawapo ya matumizi ya lugha, imeonyeshwa aina zaidi ya
takriri kuliko zinazotajwa na wataalumu hawa. Mifano ni takriri ya vina vya kati na vya mwisho,
ya kibwagizo na hata ya umbo la shairi kama vile la tarbia katika shairi moja au hata mashairi
kadha. Hata hivyo, sababu ya kutumika hivyo ilibainika kuwa ileile ya kusisitisa ujumbe au
kudumisha ufundi wa mashairi.
Mtaalamu zaidi aliyeshughulikia fani ya mashairi ni Alembi (1999). Anasema fani ya ushairi
hutathmini mkondo ambao kupitia kwake ujumbe wa shairi hupitishwa kwetu. Hurahisisha
uelewa wetu wa shairi. Kulingana na Alembi, fani huhusisha shada, mkazo/ msisitizo, mizani/
mapigo, takriri, vina, tashihisi, taswira, ishara (kuwakilisha dhana), uteuzi na matumizi ya
maneno, onomatopia / tanakali sauti, takriri ya silabi za mwanzo, mshabaha wa irabu za shada
katika maneno mawili au zaidi na mubalagha/ kutia chumvi.
Utafiti wa mtaalamu huyu unahusiana na huu kwani ililazimu kuhakikiwe vipengele hivi vya
fani kama vinavyotumika katika diwani ya Sauti ya Dhiki. Pia yafaa kueleweka kwamba Alembi
pamoja na wataalamu waliotangulia hawakujishughulisha na diwani hii. Hii ndiyo tofauti ya
utafiti huu na wao. Kwa upande mwingine, Ramadhani (Mulika na.3) anazieleza sifa za msingi
zinazohusu ushairi wa Kiswahili. Anasema hizi huwasilishwa kwa msomaji kwa njia ya lugha
teule ya kitamathali. Pia shairi ni muungano wa yaliyomo (maudhui) na fani.
Ilihakikiwa ni kwa nini Abdilatif alilenga kuwasilisha hisi zake kwa lugha teule na ikiwa hii ni
ya kitamathali. Pia ikahakikiwa namna aina ya maudhui aliyozungumzia mshairi
yanavyosababisha au kuchangia lugha ya kitamathali. Euphrase Kezilahabi naye anasema ushairi
ni hali, tukio au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno
fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha. Kulingana na J.
Ramadhani, katika ushairi vitu hupewa nafsi na utu; picha ni sifa muhimu za ushairi na huweza
kuwa na mpangilio wa maneno usio wa kawaida. Pia una ridhimu[mizani],mlingano wa sauti na
mapigo na shairi ni lazima lionyeshe sifa ya kiuimbaji lisiwe nakala ya shairi jingine. Kuhusiana
14
na diwani hii nililenga kuhakiki iwapo Abdilatif alizingatia kigezo hiki au la kwani Ramadhani
hakumrejelea kamwe.
Kwa upande wa lugha katika Utenzi wa Mwanakupona, Mulokozi (2000) anahakiki ni lahaja ipi
imetumiwa na ikiwa mshairi anaimudu vizuri, ikiwa ni lugha nyepesi au inayolenga kuonyesha
ubingwa wa mshairi kwa kutumia maneno mazito na msamiati mgumu. Pia anaangalia lugha ya
picha hususan tashbiha, istiara na taswira. Nilipofanya uhakiki wa Sauti ya Dhiki nilizingatia
kilahaja (Kimvita) wala si Kiamu kama katika Utenzi wa mwanakupona na pia uzito au wepesi
wa lugha na msamiati, yote haya yakizingatiwa na washairi husika kwa azma tofauti.
David na Wamuhu (1989) nao wanasema kuwa ni muhimu kupata hisia na maoni ya mshairi
kwani hueleza tajriba yake. Ufundi waweza kuhusu lugha rahisi kueleweweka kama lugha ya
Wimbo wa Lawino. Ni muhimu kuelewa maana ya ushairi kwanza. Taswira ndiyo tamathali
muhimu zaidi kwa shairi. La sivyo, ushairi utakuwa sawa na nathari. Taswira hupatikana kwa
mshairi kuzingatia mifano ya maisha halisi. Wanasisitiza kuwa kuna aina mbili za taswira. Ya
kwanza ni istiara au jazanda. Mfano ni kusema mtu fulani ni ‘simba’ ikiwa na maana ya ndani.
Pia kuna taswira kwa tashbihi. Baada ya hapa ni muhimu kuelewa hali au toni ya shairi. Hii
yamaanisha hisia au mwelekeo wa sauti katika shairi. Mshairi aweza kutoa hasira, upendo,
furaha, huruma, msongo, kuchanganyikiwa au kejeli. Washairi hushirikiana nasi kero au silika
kuu waliyonayo. Hii ni sawa na hatibu ambaye huzungumza hotuba wala si kuipa hadhira nakala
ya hotuba iliyoandikwa . Kuna ridhimu ya sauti pamoja na takriri. Baadhi ya mashairi hutegemea
sauti za maneno kuliko mashairi mengine. Pia kuna kuanza mshororo kwa konsonanti moja.
2.4 Muundo wa Mashairi
Katika kuhakiki mashairi, muundo hutiliwa maanani. Kuhusu muundo wa kazi ya fasihi Senkoro
(1982) anasema muundo ni mpango na mtiririko wa kazi hiyo kwa upande wa visa na matukio.
Hapa basi tunachunguza vile ambavyo msanii au mtunzi alivyofuma, alivyounda na
alivyounganisha tukio moja na lingine, kitendo kimoja na kingine, wazo na wazo, sura moja na
nyingine, ubeti na ubeti na hata mstari wa ubeti na mwingine. Licha ya maelezo kuhusu muundo,
Senkoro hakulenga chochote kuhusu muundo wa mashairi haya ya Sauti ya Dhiki niliyohakiki.
15
Topan (1971) akizungumzia muundo wa mashairi anasema ingawa tenzi zimetukuka sana toka
mwaka 1728 mpaka miaka hii ya leo, watunzi wengi wamependa kutumia zaidi mashairi kuliko
tenzi. Mashairi ya tathlitha, yenye mistari mitatu kila ubeti na ya takhmisa, yenye mistari mitano
kila ubeti yametumiwa na washairi wachache sana lakini mashairi ya tarbia yenye mistari minne
kila ubeti na hasa ya uzani wa mizani kumi na sita iliyogawanyika kwa mizani nane nane
yamestawishwa vikubwa. Imekuwa kama mtu akiamua kuandika mashairi kwa kawaida
ataandika shairi la muundo huo. Litakuwa na mizani kumi na sita zilizogawanyika katikati, vina
vya ndani na vya mwisho na pia kituo.
Kulingana na Mekacha (1996), uwezo wa kuathiri linaokuwa nao shairi unatokana na lile umbo
lake maalumu. Baadhi ya vipengele vinavyolipa umbo la shairi upekee ni mpangilio wa sauti
wenye mapigo ya kimuziki na wizani, maelezo mafupi na yenye kunata, matumizi bora ya picha,
ishara na tamathali za semi na ukiukaji wa mfuatano wa kawaida wa maneno katika tungo
(Kahigi 1975, Mulokozi 1975 na Finnegan 1970 na 1977).
Mekacha anasema washairi huweza kuwianisha sauti za lugha na ujumbe unaodhamiriwa.
Muafaka huu wa sauti na maana husababisha baadhi ya sauti kubebeshwa maana za zaidi licha
ya maana za msingi. Jambo hili laweza kufanywa kwa mfano kwa kurudiarudia. Shairi vilevile
laweza kuwa na wizani fulani utokanao na mapangilio wa sauti fulani katika lugha, kwa mfano:
‘Titi la mama li tamu hata likiwa la mbwa’. Mashairi mengine ya kimapokeo huwa na urari wa
vina na mizani. Urari huu hutokea kuwa na mguso wa kipekee unaotekenya ngoma za masikio.
Mpangilio wa sauti za lugha huleta mguso wa kiusikivu na wa kisanaa.
Abdulaziz (1979) anadai kuwa kuhusiana na mashairi mapokeo kuna marefu ya beti nyingi na
hata mafupi ya ubeti mmoja tu. Pia anasema kubadilika kwa idadi ya silabi (mizani) katika
kipande husababisha shairi la mapokeo kuwa guni. Utafiti wangu ulifaidika sana na maoni haya
ya Kahigi (1975), Mulokozi (1975), Finnegan (1977) na Abdulaziz (1979). Hii ni kwa sababu
nilihakiki mashairi marefu na pia ya beti nyingi. Kuhusiana na muundo, beti, mishororo, vina na
mizani zilikuwa baadhi ya arudhi za utunzi nilizohakiki.
16
Quinn (1992) anapozungumzia namna ambavyo fasihi hufanya kazi anasema kuwa shairi fupi ni
muundo changamano; muundo wa maneno na sintaksia. Kuelewa linavyofanya kazi huhusisha
kuchunguza namna lilivyounganishwa, yaani ule ujenzi au muundo wake. Shairi pia laweza
ashiria jinsi ulimwengu unavyofanya kazi. Anasema tusome riwaya au shairi kwa kutegemea
kazi hiyo ilivyo na kwa kuridhika tunakopata kutokana na maneno ya shairi hilo yalivyopangwa
na yanavyofanya kazi. Anasema mashairi huwasilisha uhalisia au ukweli ambao ni lazima
tuuelewe na hatuwezi kuupuuza. Twafaa kuelewa mtunzi anamaanisha nini au anajaribu
kumaanisha nini. Kulingana na Quinn (1992:211), ili kazi ya sanaa ifanye kazi kama riwaya au
shairi kwa vyovyote vile, ni lazima iwe na dhima ya kimaadili kwa jamii. Anasisitiza kuwa wazo
fulani laweza ingizwa na mtunzi kwa kazi ya sanaa likihitaji kuchunguzwa kwa undani. Zaidi ya
hayo, anasema kuwa mhakiki akitenga muundo na maudhui kwa azima ya uhakiki, riwaya au
shairi hilo hutawanyika kwa mawazo yetu mpaka tutakapoliunganisha tena upya. Anamalizia
kwa kusema shairi ambalo huadilisha kwa njia ya moja kwa moja kama mahubiri ni shairi bovu.
Kazi ya sanaa kwa hivyo haifai kutuelekeza kwa njia ya moja kwa moja kwa ambacho twafaa au
tusichofaa kufanya.
Quinn (1992) anaelezea pia kuwa muundo huhusu mipangilio ambayo hutawala kazi ya sanaa.
Anasema umbo huweza kuchunguzwa katika matini fulani maalumu. Umbo ndilo kazi fulani ya
sanaa huweza au inaweza kuzishirikisha kazi zingine kiutoshelevu bila kuonekana kama familia
au tamaduni. Muundo huo ndio huleta upekee wa kazi fulani ya sanaa.
Massamba (1983:5) anarejelea Shaaban Robert, mmoja wa wanamapokeo kuhusiana na maana
ya ushairi. Shaaban anasema, “Ushairi ni sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno
machache au muhtasari”. Kuhusu wimbo, ushairi na tenzi anasema kuwa wimbo ni shairi dogo,
ushairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi. Kina nacho ni mlingano wa sauti za
herufi. Kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti na ufasaha ni uzuri wa lugha. Mawazo,
maoni na fikra za ndani zinapoelezwa kwa muhtasari ujumbe wa shairi huvuta moyo kwa namna
ya ajabu.
Maelezo ya Mulokozi (1999) kuhusu Utenzi wa Mwanakupona yanasisitiza kuwa fani ya ushairi
huzingatia mambo yafuatayo: Mpangilio wa mawazo, ikiwa kuna kujirudiarudia, mpangilio wa
17
beti (zipi zafaa kuwa mwanzoni au mwishoni), na ni sehemu ipi inatawala, kama vile dua. Pia
tunaangalia mpangilio wa mizani na vina.
Zaidi ya hao,Williams anahakiki Diwani ya Mnyampala. Kuhusu muundo anatambua kuwa
mengi yana wa aina moja tu – yaani mistari minne kila ubeti (mstari wa nne ukiwa ndio kituo na
silabi zikiwa kumi na sita, nane nane kila kipande na vina vyenye utaratibu wa :
a b
a b
a b
b a
Mshairi mwenyewe asema kuwa afuata muundo huu kwa sababu ndio muundo ambao umezoewa
na wasomaji na wasikilizaji mashairi toka jadi. Mshairi anapojaribu kubadili muundo huu
anamletea taabu mwimbaji aliyezoea muundo wa tarbia na wasomaji wengi wanaonekana kuwa
hawapendi mabadiliko. Hivyo, Mnyampala kajaribu kuyaunda mashairi yake katika muundo
mpya anaouita ‘msisitizo’. Muundo hapa ni wa mishororo sita kila mshororo mmoja ukiwa
mfupi kuliko mingine ili kutoa msisitizo. Shaaban Robert pia alitumia muundo kama huu kwa
kuandika ukwapi kwa Kiswahili na utao kwa Kiingereza. Kinyume na washairi wengi,
Mnyampala alitunga mashairi yenye ubeti mmoja tu kwa mfano shairi aliloandika juu ya taifa.
Indende (2008:73 – 94), anapozungumzia taswira ya umbo awali na umbo la kisasa anasema
kuwa wanakipindi cha urasmi mkongwe na urasmi mpya walienzi sana umbo la shairi
lililoasisiwa na Muyaka bin Hajji, Shaaban Robert, Mathias Mnyampala, na mwalimu Hassan
Mbega na kadhalika. Walidumisha na kuendeleza umbo hili kiasi cha kwamba yeyote ambaye
angeulizwa juu ya ufafanuzi wa ushairi wa Kiswahili angeeleza kuwa ushairi wa Kiswahili ni
tarbia na huwa na umbo lifuatalo;
___________ 8a ________8b
____________8a __________8b
____________8a __________8b
____________8b__________8a
18
yaani mishororo minne kila ubeti, mizani nane kila kipande na urari wa kina cha kati na cha
mwisho. Kina cha mshororo wa nne hubadilishana nafasi ambapo kile cha mwisho huja kati na
cha kati huja mwisho au mshairi aamue kuzua kina kingine ilivyoonyeshwa katika muundo huo.
Utawala na uzoefu wa umbo hili uliwafanya wahakiki, watafiti, wanafalsafa wa kifasihi na
wasomi wengineo kufikiria kwamba ushairi wa Kiswahili haubadiliki.
Kulingana na utafiti wa Massamba (1983:57), Abdilatif Abdalla naye akasema kwamba utungo
ufaao kupewa jina la shairi si utungo wowote bali ni utungo ambao katika kila ubeti wake kuna
ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenziye; wenye vipande vilivyo na
ulinganifu wa mizani zisizo zaidi. Vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato
maalum na yenye lugha nyoofu, tamu na laini, lugha ambayo ina uzito wa fikra tamu kwa
mdomo wa kusema, tumbuizi kwa masikio ya kusikia na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na
kama ilivyokusudiwa.
Wataalamu wa uhakiki wa ushairi wakiwemo King’ei na Kemoli (2001:19) na Mwai (1988:44),
wameelezea kwamba utungo wa unne au tarbia ulizuka karne ya 18 hasa katika utunzi wa
mashairi ya Muyaka. Njogu na Chimerah (1999:100) nao wameeleza kuwa utungo ukiwa na
mishororo minne huitwa tarbia na ukiwa na mishororo mitano huitwa takhmisa. Pia King’ei na
Kemoli (2001:18) wanafasili tarbia kuwa shairi lililo na mishororo minne katika beti zake
(unne).
Mayoka (1984:3) ana maoni kuwa ushairi ni mtungo wa kisanaa ulio na mpangilio maalumu na
lugha ya mkato ambayo ndani yake ina vina, urari wa mizani na muwala maalumu ambavyo kwa
pamoja huwa na fani na maudhui yahusuyo hisi fulani au tukio juu ya maisha ya mtu au watu wa
mazingira na wakati maalum. Kufafanua haya Indende anatoa mfano wa shairi la ‘Mcheza kwao
hutuzwa’ la Wallah (1988:154).
Kitula na Kemoli(2001) nao wanatambua kuna tathlitha yenye vipande viwili vya mizani 6a – 6b
na pia ya vitatu vyenye 8 – 8 – 8. King’ei (2008) anatumia vichwa vya mashairi, umbo na
mtindo, msamiati na maudhui kuonyesha mashairi ya Muyaka Bin Hajji yalivyowaathiri
washairi wa karne ya ishirini kama Ahmad Nassir. Katika utafiti huu King’ei anadokeza kuwa
19
washairi wa hivi karibuni walibuni upya kimaudhui shairi la Abdalla liitwalo “Usiniuwe” likawa
“Nimekuua”, “Nishakuua” na kadhalika. King’ei anataja shairi hili tu wala hajahakiki fani na
maudhui yake kamwe. Utafiti wangu unaingilia hapa ili kuliziba pengo hili. Kuhusiana na umbo
na mtindo, King’ei anazungumzia mtindo wa “Nudhuma” yaani mshairi kutumia neno lilelile
kuanzia kila mshororo katika shairi zima. Anaonyesha namna Nassir alivyoiga mtindo huo kwa
Muyaka kama inavyobainika katika shairi la Nassir linaloitwa ‘Owa’. Pia anazungumzia utarbia
wa Mashairi ya Nassir, mizani nane nane na pia kina cha mwisho. Nassir pia anatia mkarara
katika mshororo wa mwisho kila ubeti kama alivyofanya Muyaka.
2.5 Maudhui ya Mashairi
Kuelewa maudhui ya shairi ni kulielewa shairi. Ongang’o (2002) anachambua mambo ambayo
mshairi anazingatia katika shairi lake. Haya ndiyo anaita maudhui. Anasema kila ubeti unaweza
kuwa na maudhui yake maalum. Jina lingine la maudhui ni ujumbe. Maudhui yanaweza
yakagawanywa mara mbili :-
(a) Maudhui kuu, yaani wazo kuu linalojitokeza (linalotawala) katika beti zote au shairi lote.
(b) Maudhui madogo, yaani mawazo madogo yanayosaidia kukuza au kujenga maudhui kuu.
Kulingana naye, umuhimu wa maudhui ni kuwa hutuambia mshairi anazungumzia juu ya nini.
Pia hutuambia mshairi anatungia mtu au watu gani, anasifu au anatetea mtu au watu gani, na pia
anaponda au kukosoa mtu au watu gani na kwa nini anafanya hivyo. Msimamo wa mshairi juu
ya hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kuyatatua maswala anayoshughulikia katika shairi lake pia
ni umuhimu wa maudhui. Mshairi huyu anahakiki mashairi yake mwenyewe bali hataji chochote
kuhusu kazi za Abdilatif Abdalla.
Mtaalamu mwingine aliyehakiki ushairi wa Kiswahili ni Msokile (1993 :55). Anayaona maudhui
kama jumla ya mambo yanayoeleza kazi ya kifasihi. Maudhui hujumuisha dhamira, mtazamo
ama msimamo, ujumbe, maadili na falsafa. Mtaalamu huyu anahakiki shairi la ‘Ua la Moyoni
Ua’ na kuonyesha kuwa linazungumzia mapenzi. Pia anahakiki shairi la ‘Siafu wamekazana’
akidokeza kuwa shairi hili linahusu swala la kisiasa ambapo umma unafanya mambo mengi kwa
kujitoa mhanga ili kupata ukombozi. Huu ni mgogoro wa juhudi za ukombozi dhidi ya
Wajerumani kule Tanzania. Hata kama Msokile amehakiki mashairi kadha ya Kiswahili, ni
20
muhimu kuelewa kuwa pia naye hajahakiki kazi yoyoyote ya Abdilatif Abdalla ambayo uhakiki
huu ulilenga.
Wamitila (2003 :225) kwa upande wake anaona huwa maudhui ya shairi kuwa neno
linalotumiwa kujumlisha yaliyomo katika kazi ya kifasihi. Msomaji anapaswa kuangalia
dhamira, ujumbe na falsafa ya mshairi. Anasema dhamira ya mtunzi ni lengo lake katika utungo
huo. Dhamira hutokeza kwa wazo kuu ambalo hukuzwa katika utungo unaohusika kuanzia
mwanzo mpaka mwisho. Katika kuliendeleza wazo hili kuu masuala mengine huibuka.
Mtaalamu huyu anaambatanisha maelezo haya na kuhakiki shairi la ‘Mamba’ katika diwani ya
Sauti ya Dhiki. Anaeleza kuwa shairi hilo lina dhamira ya kumtahadharisha kiongozi wa
kimabavu kuwa dhuluma ina mwisho. Mshairi ametumia fumbo akimlinganisha kiongozi huyo
na mamba majini. Maji hapa ni sitiari nyingine inayosimamia nchi, taifa au hata nguzo ya watu.
Mamba huyo amedanganywa na hadaa za ulimwengu ; ametawaliwa na kileo cha cheo na
kudhani ataishi milele. Mshairi anamtanabahisha mamba (kiongozi) huyu kuwa siku yake ya
‘kufa’ au kuondoka madarakani itafika. Katika ubeti wa mwisho tunatambua kuwa
anayezungumziwa ni binadamu. Kwa upande mmoja shairi hili ni onyo kwa viongozi wa kiimla
ilhali kwa upande mwingine linawatia moyo wanaoteswa wajue hakuna refu lisilokuwa na
mwisho.
Kuhusu ujumbe wa shairi kama sehemu ya maudhui, Wamitila anasema ni neno ambalo
humaanisha taarifa aipatayo msomaji asomapo shairi au kazi ya kifasihi. Anasema ujumbe
unaweza kuwa mbaya au mzuri. Mfano ni katika shairi hilo ambapo tunaelezwa kuwa dhuluma
ina mwisho na kuwa hakuna refu lisilokuwa na mwisho. Huu ni ujumbe wa kuwashajiisha na
kuwatia moyo wanaodhulumiwa kisiasa.
Mwisho, Wamitila anasema falsafa ya mwandishi ni fikra kuu za mtunzi au mwandishi wa kazi
ya kisanaa. Fikra hizo hutokana na imani na misimamo ya mwandishi anayehusika na huathiri
kwa kiasi kikubwa jinsi anavyoyatazama mazingira yake. Mazingira hayo yanaweza kuwa ya
kisiasa, kitamaduni, kiuchumi au kijamii. Shairi hili linaonyesha falsafa ya mwandishi ya
kupinga udhalimu, mateso na uongozi wa ki-imla.
21
Ingawa Wamitila amelihakiki shairi la ‘Mamba’ kutoka diwani ya Sauti ya Dhiki, alichozamia ni
maudhui pekee wala hajagusia chochote kuhusu vipengele vingine vya fani ya shairi lenyewe
wala mashairi mengine ya diwani husika. Vipengele hivi vilipohakikiwa katika utafiti huu, bila
shaka ni mkondo tofauti wa uhakiki.
Kwa upande wake, mtaalamu Indende (2001) alizingatia diwani ya Sauti ya Dhiki alipochunguza
uchanganuzi wa kipragmatiki wa kazi za sanaa za Kiswahili zinazohusu maswala ya kisiasa.
Inabainika mifano aliyozingatia ni Sauti ya Dhiki ya Abdilatif Abdalla (1973), Cheche cha Moyo
ya Alamin Mazrui (1988) na Ficho la Ndani ya S. A. Mohammed (2002). Shairi analorejelea
Indende katika Sauti ya Dhiki ni ‘Wasiwasi enda zako’ (uk. 32). Hili linahusu wakati mgumu
aliopitia mshairi katika maisha ya jela. Hapa anapinga matakwa ya moyo wake kwa kuzungumza
nao kana kwamba ni binadamu. Hii ni mbinu ya tashihisi. Hii inazua upweke wake kuhusiana na
maisha ya jela.
Indende vilevile anadokeza shairi ‘Nshishielo ni Lilo’ (uk. 21) anapotaja kuwa mshairi alifungwa
jela kwa kusema ukweli na kuapa kuwa hataacha kamwe. Pia anarejelea shairi la ‘Mamba’ (uk.
10) kuzua ileile tashihisi ya kijamii na kisiasa. Mtaalamu yuyu huyu katika Swahili Forum 15
(2008 :73-94) anaandika mada kuhusu, ‘Mabadiliko katika umbo la ushairi na athari zake katika
ushairi wa Kiswahili’. Hapa anataja mashairi mawili katika diwani ya Sauti ya Dhiki. Anasema
kuwa shairi la ‘Mnazi vuta N’kuvute’ la Abdilatif Abdalla (1973 : 17-22) ni ngonjera
inayoonyesha taswira ya watu wawili ambapo Badi amekwea mnazi na kuukatalia na Ali
amenyimwa nafasi ya kuukwea huo mnazi. Hata hivyo, Indende hataji kingine chochote kuhusu
shairi hili.
Shairi lingine analotaja katika diwani hii ni lile la ‘Sikate tamaa’. Anasema kuwa Abdilatif
anajitokeza katika kundi la wanamapokeo lakini anapomwandikia Said Ahmed Mohammed
utangulizi wa ‘Sikate tamaa’ anampongeza kwa ujasiri aliofanya katika kubadilisha miundo ya
ushairi zoelevu. Inaelekea Indende analitaja shairi hili tu na kinachozungumziwa wala sio fani
yake kamwe. Baada ya utafiti wa wataalamu hawa nami nikapate mwanya wa kutoa mchango
22
wangu kuhakiki fani na maudhui katika baadhi ya mashairi hata waliyohakiki kwani walilenga
mada na hata nadharia tofauti.
2.6 Tafiti zinazohusiana na Utafiti huu.
Senkoro (1982 :28) anapotafitia fani ya kazi ya fasihi anabainisha kwamba kuhusiana na aina
mabalimbali za fani, aina hizi huweza kutolewa kauli tu pale ambapo mhakiki au hadhira huwa
amekwisha zipitia kazi mabalimbali za msanii ahusikaye ili kuweza kuzitolea kauli moja.
Senkoro anachunguza mtindo wa kishairi ujitokezao katika kazi zisizo za kishairi kama vile
riwaya, hadithi fupi, tamthilia na uandishi wa habari. Anachunguza fani ya kazi ya kiimbila ya
Ubeberu utashindwa na pia kazi za Kezilahabi kama riwaya ya Rosa mistika pamoja na Diwani
ya Kichomi. Zaidi ya kazi hizo anachunguza riwaya na mashairi ya Shaaban Robert na pia ya
Mnyampala.
Hali kadhalika anatoa mifano ya mashairi kama ‘Al-Inkishafi’ na ‘Utenzi wa Mwanakupona’
katika diwani ya Tenzi tatu za kale. Pia anazungumzia taswira ya maisha ya jela aliyopitia
Abdilatif’ Abdalla kwa kutoa mifano ya mashairi ya ‘Usiniuwe’ na ‘Mnazi’ toka diwani ya Sauti
ya Dhiki. Ingawa mtaalamu huyu ametoa mifano ya mashairi ya Abdilatif’ hajahakiki fani na
maudhui yake na hapo ndipo utafiti huu ulipata pengo. Abdilatif’ ni miongoni mwa washairi
wachache wa kijadi ambao wamejitahidi katika uandishi wao wa mashairi. Ustadi anaodhihirisha
katika utunzi wake unastahili kutafitiwa kwa undani. Kulingana na Chacha (1992), kufikia sasa
ni kazi chache sana zilizojishughulisha na ushairi wa mtunzi huyu. Kutokana na sababu hiyo,
utafiti huu ulilenga kuhakiki fani na maudhui aliyotumia mshairi.
Knappert (1967) alichunguza mtindo wa drama katika kazi za Abdilatif’ Abdalla. Alilenga
Utenzi wa maisha ya Adamu na Hawaa katika utafiti wake. Utafiti wake unahusiana na huu kwa
sababu sote twalenga kuhakiki tungo za Abdilatif’ Abdalla japo ni tungo tofauti. Tofauti ni kuwa
twalenga vipengele tofauti vya sanaa, yeye akilenga drama, nami fani na maudhui kwa ujumla.
Pia twalenga kazi tofauti.
Zaidi ya hayo, Topan naye (1971 :67-79) anahakiki kazi kadha za tamthilia kama vile
‘Nakupenda lakini’ ya Henry Kuria pamoja na ule mchezo wa Gerishon Ngugi wa ‘Nimelogwa!
Nisiwe na Mpenzi ?’ Lengo la Topan ni kuonyesha umbo la mchezo wa kuigiza katika kazi hizo.
23
Katika uhakiki wake Topan anarejelea tenzi kama vile Utenzi wa maisha ya Adamu na Hawaa
uliotungwa na Abdilatif’ Abdalla Muhammad wa Mombasa. Anaeleza kuwa utenzi huu (wenye
beti, 630) unahadithia kisa cha Adamu na mke wake jinsi walivyoonja tunda marufuku wakaja
wakatolewa peponi wakaletwa duniani. Kuhusiana na tenzi hizi pia analenga kuonyesha sifa za
mchezo wa kuigiza. Anatafakari drama inayotendeka. Ieleweke kwamba utenzi huu pamoja na
diwani ya Sauti ya Dhiki ni kazi za mwandishi mmoja ; Abdilatif’ Abdalla. Tofauti ya kazi
yangu na ya Topan ni kuwa nalenga fani na maudhui katika Sauti ya Dhiki. Tunafanana tu kwa
kuhakiki kazi za Abdilatif’ ingawa mbili tofauti.
Chacha (1992) anasisitiza utamthilia wa baadhi ya mashairi ya Abdilatif’ ambao wasomi
waliotangulia pia walikuwa wameutaja. Mashairi anayotaja ni ‘Vuta N’Kuvute’ na ‘Kutendana’
katika diwani ya Sauti yaDhiki. Japo anayoyalenga ni kutoka diwani ya Sauti ya Dhiki, tofauti na
utafiti huu ni kuwa anazingatia mashairi manne tu wala si fani na maudhui kwa ujumla.
Mshairi huyu anaanza kwa kueleza historia fupi ya maisha ya mwandishi katika tasnifu yake
ukurasa wa tatu hadi tisa. Msingi wa nadharia anaozingatia ni ule wa umaksi (uk. 9 – 11) katika
utenzi aliohakiki na pia mashairi ya Sauti ya Dhiki. Pia anazungumzia ujuzi wa Abdalla kama
mshairi. Mwelekeo wake ni kueleza ujumbe wa mashairi haya kwa kuzingatia muktadha
yalimotungwa na pia maadili kuhusu maisha ya binadamu na pia uozo wake. Zaidi ya hayo,
anaeleza jinsi Muyaka na Abdalla walivyoathiriwa na usuli sawa.
Utafiti mwingine wa hivi karibuni zaidi kulenga diwani hii ya Sauti ya Dhiki ulifanywa na
Maitaria (2008). Mtafiti huyu alitathmini matumizi ya methali kama fomula katika utunzi na
uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili akisisitiza kuwa utanzu huu una historia ndefu na kuwa
matumizi ya methali bado yanaendelea kutegemewa hata wakati wa sasa. Alizungumzia ushairi
unaotumia methali nyingi na unaotumia chache. Alizingatia mashairi yaliyotumia methali mbili
au zaidi. Mifano ni ‘Mnazi vuta N’kuvute’, ‘Kutendana’ na ‘Zindukana’.Mtafiti huyu ana maoni
kuwa methali huweza kutumiwa katika shairi kama mbinu ya kuibua taharuki kwa hadhira.
Mtafiti huyo aliufaa utafiti huu kwa kutafitia fani ya methali katika Sauti ya Dhiki. Utafiti huo
unatofautiana na huu kwa kuhakiki mada tofauti kwani hata katika shairi la ‘Kutendana’
haikuhakikiwa methali kwani Maitaria ashafanya hivyo tayari.
24
Walibora(2009) pia ni mmoja wa watafiti waliotafitia mashairi ya Sauti ya Dhiki. Mada yake ni
kuhusiana na mashairi yalitotungwa katika mazingira ya jela. Walibora anaelezea kuwa
Abdilatif’ alitumikia kifungo jela kwa uhaini wakati wa utawala wa Jomo Kenyatta baada ya
uhuru. Mtafiti huyu anaelezea kuwa kuandikia jela kulikuwa na athari kuu kwa umbo na
maudhui ya ushairi wa Abdalla.
Walibora aendelea kusema kuwa kwa kiwango kikubwa mazingira mabaya ya jela aliyokumbwa
nayo mshairi yalisababisha na kuimarisha athari ya kisaikolojia na kifalsafa hivyo kusababisha
toni ya aina mbalimbali katika mashairi husika. Lengo la Walibora hasa lilikuwa kusoma diwani
ya Sauti ya Dhiki huku akitathmini hisia za Abdalla kwa mateso aliyopata jela.
Utafiti wake uliufaa huu katika kuhakiki maudhui tu ilipoonyeshwa mateso aliyopata Abdalla
lakini katika mada tofauti na ya Walibora ikilengwa fani na maudhui jambo ambalo hasa
halikulengwa naye. Utafiti huu umeonyesha wahusika na sifa zao, ufundi wa lugha na maudhui
kwa kila shairi lililohakikiwa jambo ambalo Walibora hakufanya.
Utafiti wa hivi majuzi zaidi unaohusiana na huu ni uliofanywa na Karanja (2014). Alichunguza
matumizi ya taashira,istiari na tashbihi katika diwani ya Sauti ya Dhiki. Mojawapo ya
madhumuni yake ilikuwa ni kuwapa watafiti wengine shauku za kuchunguza mbinu nyingine za
tamathali alizotumia mshairi. Mtafiti huyu alilenga tamathali hizi tatu pekee katika mashairi
ishirini kati ya arubaini. Alitumia nadharia ya mtindo. Utafiti wake uliufaa huu kwani ametoa
mifano michache kwa mashairi yaliyohakikiwa hapa. Tofauti yake kuu ni pale kazi yake
inaonyesha mfano wa kiuchanganuzi wa mishororo ya mashairi husika tu na kutawaliwa na
mbinu hizo tatu pekee anazolenga. Kwa mantiki kama hiyo ikalazimu kufanywa uhakiki
kamilifu wa tamathali kadhaa pamoja na wahusika,muundo wa mashairi na hata maudhui
,mambo ambayo mtafiti huyo hakulenga hata kidogo. Bila shaka hata anapozingatia nadharia ya
mtindo na utafiti huu ukihusisha umuundo, umuundoleo na uamilifu ni tofauti tosha.
Mgeni(2014) anapozungumzia fani na maudhui, anasema kuwa ni vipengele vinavyojenga shairi.
Anasema kuna uhusiano mkubwa kati ya fani na maudhui kwa mtunzi yeyote wa kazi ya sanaa.
25
Kuhusiana na wahusika, mtafiti huyu anasema kuwa mashairi ya kawaida hayategemei sana
wahusika ili kuwasilisha ujumbe. Hata hivyo, kuna baadhi ya bahari za ushairi ambazo hutumia
sana wahusika ambao aghalabu hutumiwa kama kinywa cha kuwasilishia hadhira jumla ya fikra
za mtunzi. Anasema pamoja na bahari hizo, ni ngonjera au tenzi ambazo mara nyingi hubainisha
kuwepo kwa nafsineni na nafsinenewa, sifa ambayo aghalabu huandamwa na mashairi ya
Kiingereza.
Utafiti huo uliufaa huu kwa kuwa kitangulizi cha kipengele cha uhusika katika ushairi. Hata
hivyo, hakuna lolote lililotajwa kuhusu ushairi wa Abdilatif’ Abdalla. Utafiti ulikita mizizi
katika uhusika kama maudhumuni mojawapo. Imebainishwa kuwa mashairi yana wahusika
tofauti na alivyosema Mgeni kuwa hawako.
2.7 Misingi ya Nadharia
Utafiti ulitegemea nadharia za umuundo na umuundoleo kuonyesha jinsi vipengele vya fani
vinashiririkiana kujenga mashairi yaliyohakikiwa pamoja na uamilifu kuonyesha jukumu
linalotekelezwa na kila kipashio.Nadharia zilichangishana kwa kila shairi lililohakikiwa.
2.7.1 Umuundo
Utafiti ulijikita katika nadharia ya umuundo,umuundoleo na ile ya uamilifu. Nadharia ya
umuundo iliasisiwa na wataalamu wawili:- Ferdinard de Saussure na Claude Levi Strauss. De
Saussure alikuwa mwanaisimu wa Kiswisi aliyegawa lugha katika matapo mawili:- Langue na
Parole. Langue ni zile sheria zilizo kwenye ubongo wa mtumiaji lugha. Parole ni utendaji kwa
kutumia sheria hizo katika muktadha mahsusi. Hali hizi mbili zikaendelezwa na Noam Chomsky
kama umahiri na utendaji. Mambo hayohayo yakaendelezwa na William Labov. Alipendekeza
kwamba lugha imegawanywa katika umahiri wa kiisimu na umahiri wa kimawasiliano.Claude
Levi Strauss alisema kwamba jamii imeundwa na vipengele kama uchumi, siasa na kadhalika.
Nadharia imeshikilia kuwa kila kitu ni zao la ushirikiano wa vipande mbalimbali. Ushairi kwa
mfano umeundwa na maudhui, dhamira, ujumbe, wahusika, lugha na kadhalika. Lengo la
kuchunguza lugha au ushairi ni kutambua au kupata miundo na ruwaza zake. Kulingana na
26
umuundo, kuna madaraja tofautitofauti ya vipashio tofauti, kategoria, ruwaza na mahusiano.
Vipashio tofauti huhusiana kati yao katika kufanya kazi.
Kulingana na Grimes (1975) na Stubbs (1983), umaumbo hutafuta vipashio vidogo au vijenzi
ambavyo vina uhusiano kati yao na ambavyo hutokea katika mpangilio mahsusi unaotawaliwa na
sheria au mikabala.Wanamiundo huchunguza muundo ulio zaidi ya Sentensi au Kishazi (Stubbs,
1983) na Van Djik (1985:4). Huchunguza viwango au madaraja tofauti kwa misingi ya vipashio
tofauti, kategoria, ruwaza na mahusiano. Msingi wa umaumbo ni jinsi vipashio tofauti huhusiana
kati yao katika kufanya kazi. Kila neno ni lazima kuonyeshwa maana yake kimatumizi.
Umuundo wa baadaye ulitokea miaka ya 1950-1960. Mwelekeo huu ulianzishwa na wahakiki wa
fasihi kama Roland Barthes ambao hawatafuti kueleza matini maalumu. Badala yake wanalenga
mtindo wa ujenzi wa matini fulani. Umuundo unahusu kuhakiki matini bila kushughulika na
athari za nje ya matini husika. Hupuuza maswala ya kitamaduni au ya kijamii na kulenga namna
ujumbe husika umejengwa.
Umuundo wa miaka ya sabini na themanini ulihusika na uhuru wa parole au utendaji. Unaitwa
umuundoleo. Kulingana na Katoto (2015), hatuwezi kuzungumzia nadharia ya umuundoleo bila
ya kuhusisha umuundo. Kwa maana hiyo, nadharia hizi huzungumziwa kwa pamoja. Matokeo ya
umuundoleo yaliingia katika fasihi ya Kiingereza na Kimarekani miaka ya themanini. Mwanzo
wa karne ya ishirini, umuundo huu pamoja na uhakiki mpya wa fasihi ulikita mizizi. Nadharia hii
huchukulia fasihi kuwa huru na hivyo kutofautisha kazi iliyo ya kisanaa na isiyo ya kisanaa.
Husisitiza kuwa kila kitu ni ubunifu na kupinga uwezekano wa kuwa na ukweli wa kilimwengu
unaowakilishwa na ubunifu husika.
Msingi wa kijamii, watu au kihistoria ulioathiri kazi husika hupuuzwa. Hulenga beti na ufundi
mzima wa ushairi. Sababu ya kuchagua nadharia hii ni kuwa mshairi wa Sauti ya Dhiki
anazungumzia vipengele tofautitofauti vya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kuhusiana na fani na
maudhui kuna vipengele ambavyo huijenga. Hivi ni maudhui, muundo, lugha na wahusika.
Nguzo za Umuundo
1. Ujumbe wa matini sio wala hauwezi kuwa nyenzo kamili inayowakilisha uhalisia wa
kilimwengu.
27
2. Hatuwezi kutoka nje ya ujumbe wa matini na kufaulu kupata chochote zaidi ya hapo.
3. Nadharia inakisia kwamba uzungumzi au ujumbe wa matini ndio wa pekee tunaoweza
kujua au kujadili.
4. Kufafanua au kuhakiki vijenzi vya kazi fulani ya sanaa,yaani kilichomo kwa matini
husika ni toshelevu kuelezea mada inayohusika.
Umuundo umetegemewa sana katika uhakiki wa riwaya lakini kila uchao nadharia hii inazidi
kutegemewa kwa wingi katika uhakiki wa mashairi. Ingawa kimsingi ilikuwa nadharia ya
Kiingereza na hasa Kifaransa iliyonawiri miaka ya sitini, wakati huo ilipendelewa sana na
wahakiki wa Kimarekani. Hulenga kuhakiki matini kwa mbinu fulani ingawa nadharia yenyewe
imelaumiwa kuwa inakinzana na historia ya fasihi. Hii ni kwa sababu mwanamiundo huamini
kuwa kazi husika ni muhimu kuliko mtunzi, hadhira na ulimwengu ilimochotwa. Pia
wanamiundo hawashughuliki na hisia za mshairi, majibu ya hadhira kwa shairi au ukweli na
uhalisia wa kilimwengu unaowakilishwa na kazi hiyo.
2.7.2 Uamilifu/ Ujukumu
Nadharia hii ilipendekezwa na wataalamu Branslaw Malinowski, Radicliffe Brown, Emile
Durkheim, Isadore OKpeihwo, Edward Leech na Raymond Firth. Mwanzo wa nadharia hii ni
kazi za Emile Durkhein ambaye alihusika hasa na namna jamii yaweza kuwa imara au thabiti.
Nadharia hutafsiri kila kipengele cha jamii kwa misingi ya namna kila kimoja huchangia uthabiti
wa jamii nzima. Aliamini kuwa jamii ni muhimu kuliko kipengele kimoja kwa hivyo kila kimoja
chafaa kutenda kazi ili kuleta uthabiti wa jamii hiyo nzima. Durkheim alisisitiza kuwa vipengele
tofauti kimsingi ni taasisi za jamii na kila kimoja pia huwa na matokeo kwa jamii nzima.
Vipengele hivyo tofauti hutegemeana. Nadharia hii imejikita katika misingi ya nadharia mfumo.
Inashikilia yafuatayo:-
Kila kitu kinajengwa na vipengele ambavyo kila kimoja hushirikiana na wenziwe katika
kudumisha kuendelea kuwepo kwa kitu hicho. Kila mojawapo ya vitu hivyo kina kazi mahsusi
katika mfumo wa kitu kizima. Mhakiki akitumia nadharia hii anafaa:
a) Kueleza kitu hicho na jinsi kinavyofanya kazi kwa pamoja
b) Unatenganisha vipande na kuchukua kipande kimoja na kukitafutia utendakazi wake.
28
c) Unachunguza kile kipande ulichoamua katika mazingira yake ya kutenda kazi.
Nadharia ya uamilifu huchukulia lugha kama chombo cha kuwasilisha maana ya kiutenda kazi.
Hutilia mkazo mwelekeo wa kisemantiki na ule wa mawasiliano badala ya sifa za kisarufi pekee.
Uamilifu hujihusisha na majukumu ya kijamii yanayotekelezwa na matumizi fulani ya lugha.
Swala muhimu pia ni kuchunguza muktadha ambao hulazimu aina fulani ya matumizi ya lugha
kama vile wa kitamaduni. Lugha hutekeleza majukumu tofautitofauti na kuonyesha utofauti wa
wanajamii. Kulingana na Leech (1983), lugha ni kioja cha kijamii.
Uamilifu au ujukumu huhusisha vipengele vya lugha vinavyohusu maana na utendakazi badala
ya vipashio vya muundo na sarufi. Lugha ina majukumu ambayo yako nje ya mfumo wenyewe
wa lugha. Majukumu haya huathiri mpangilio wa ndani wa mfumo wa lugha. Sababu ya
kuchagua nadharia hizi ni kuwa mshairi wa Sauti ya dhiki anazungumzia vipengele tofautitofauti
vya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kuhusiana na fani na maudhui, kuna vipengele ambavyo
huijenga. Hivi ni maudhui, muundo, lugha na wahusika. Pia ni majukumu fulani
yanayotekelezwa na aina fulani ya fani na maudhui.
Namna nadharia ziliongoza Utafiti
Nadharia ya umuundo iliongoza utafiti kwa kufafanua au kuhakiki vijenzi vya mashairi yote
yaliyolengwa kutegemea madhumuni yaani wahusika, mbinu za lugha, muundo na vipengele
vyake pamoja na maudhui. Ushirikiano wa vijenzi hivi vya fani na maudhui uliwekwa bayana
kupitia nadharia hii. Umuundo nao ukatumika kwa kuwa kila kipengele cha muundo
kinaathiriwa na mazingira ya kutumiwa kwa mfano muktadha wa wakati.
Kwa upande mwingine ikalazimu kutegemea nadharia ya pili, yaani ile ya uamilifu. Sababu ni
kuwa kufafanua maudhui ya kisiasa ni swala halisi la kihistoria katika muktadha maalumu wa
wakati nchini Kenya. Maudhui kama vile tamaa, dini, migongano ya kitabaka na mapinduzi ya
kijamii ni mambo yanayolandana na uhalisia wa kilimwengu ulioathiri utunzi wa mashairi
husika. Mambo kama haya hayawezi kulengwa na nadharia ya umuundo na umuundoleo pekee.
Pia, kuonyesha namna vijenzi vya sanaa kama wahusika, lugha na muundo vinavyozua maudhui
maalumu ni swala la kiuamilifu. Kwa mantiki hii, kutegemea nadharia za umuundo na
umuundoleo pamoja na uamilifu zikifidiana likawa jambo lisiloepukika.
29
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Katika sura hii kuna muundo wa utafiti, mahali pa utafiti huo, uteuzi wa sampuli na ukusanyaji
wa data. Mwishowe kumeonyeshwa namna uchanganuzi wa data nzima ulivyofanywa. Sura hii
inaangazia jinsi utafiti wenyewe ulivyofanywa. Inaangazia mahali halisi data ya utafiti
ilikusanywa, uteuzi wa sampuli, mbinu za kukusanya data hiyo na jinsi data
ilivyochanganuliwa.
3.2 Muundo wa Utafiti
Utafiti huu uliongozwa na muundo wa kimaelezo. Huu ni muundo wa kisayansi unaohusu
utazamaji na uelezaji wa hali ya kitu pasipo kukishughulisha au kukirekebisha kwa vyovyote vile
(Mugenda, O. na Mugenda, A. (1999). Utafiti huu ulilenga kuchunguza kwa uhakiki mashairi
halisi katika diwani ya Sauti ya Dhiki. Muundo wa utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo. Lengo la
muundo wa aina hii ni kueleza data na sifa ya vipengele vya fani na maudhui vilivyochunguzwa,
yaani wahusika, lugha, muundo na maudhui. Muundo huu ulihusu umaratokezi, ujumla na sifa za
kihesabu. Ingawa muundo huu ni sahihi kwa kiwango cha juu hauelezi visababisho vya hali
fulani. Muundo huu wa utafiti ulitegemewa zaidi kwa kuwa utafiti ulilenga kupata kuelewa zaidi
kuhusu ufundi wa mashairi husika. Muundo wenyewe hutegemewa kuchunguza kazi
zilizoandikwa kwa mfano vitabu mtafiti akilenga kilichoandikwa tayari. Hali ilielezwa ilivyo
katika mashairi hayo bila kuyaathiri au kuyarekebisha kwa vyovyote vile. Lengo lilikuwa kupata
taswria ya jumla ya utunzi husika.
Muundo wenyewe ulitegemewa pia kwa kuwa haiwezekani kupima sampuli nyingi
zinazohusika. Matokeo yalitegemewa kukadiria ubora au udhaifu wa mashairi au diwani husika.
Muundo huu wa utafiti huweza kuelekeza ni wapi kwa kuchunguzwa kiuwingi idadi. Udhaifu wa
muundo huu ni kuwa vibadiliki vinavyochunguzwa haviwezi kuhesabika hivyo kuchunguzwa
kisayansi.
3.3 Mahali pa Utafiti
Huu ni utafiti wa fasihi andishi ya kiswahili. Kazi iliyohakikiwa ni ya kishairi. Mashairi yote
yalitolewa kutoka kwa diwani ya Sauti ya Dhiki ya Abdilatif’ Abdalla wa Mombasa. Kazi
30
tofautitofauti za kishairi na zinginezo kuhusu maudhui, muundo, lugha na wahusika zilipekuliwa
kwa uangalifu kulenga mada ya utafiti huu. Pia tasnifu za tafiti za wataalamu waliolenga mada
hii na ushairi kwa ujumla zilichunguzwa kwa uangalifu. Kwa njia hii, kisicholengwa na watafiti
husika kuhusu fani na maudhui katika mashairi hayo kilitambulika. Hilo likawa pengo
lililozibwa na utafiti huu. Kwa kifupi, huu ni utafiti wa maktabani.
3.4 Uteuzi wa Sampuli
Sampuli za mashairi ziliteuliwa toka diwani ya Sauti ya Dhiki ya Abdilatif’ Abdalla. Madhumuni
ya utafiti wenyewe yalitiliwa maanani zaidi katika kuteua sampuli hizo ili zijumuishe
madhumuni yote. Kulikuwa na mashairi matatu kwa kila sampuli na ambayo hayakuwa
yamehakikiwa na wataalamu waliotangulia wakilenga mada hii. Mashairi yaliyo na wahusika
bainifu yaliteuliwa yakifuatwa na yenye lugha teule (isiyo ya kawaida) na tamathali za usemi
pamoja na muundo maalumu na maudhui ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kisha baadaye, upekee
wa mshairi kwa kila kikundi cha sampuli ulihakikiwa na kuripotiwa ifaavyo.
3.5 Ukusanyaji wa Data
Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa uchambuzi wa yaliyomo katika sampuli za mashairi
yaliyoteuliwa kuegemea maudhui, muundo, lugha na wahusika katika mashairi hayo. Mbinu hii
huhusu uchambuzi wa matini zenye ujumbe. Mifano ni vitabu, majarida, magazeti au matini
zungumzwa au andishi. Kabla ya 1940, mbinu hii ilihusu kazi zenye data ambayo yaweza kuwa
na sifa za kuchanganuliwa kiuwingi idadi. Hizi ni sifa zilizoweza kutambuliwa. Baada ya 1950,
mbinu hii ilijihusisha na uchambuzi wa ujumbe husika kiuthamano. Mbinu hii ya utafiti
inahusiana na Bernard Berelson. Ililenga kuchambua kilichomo katika kazi husika au kazi
lengwa. Uchambuzi wa kilichomo katika matini husika ulizingatia kuangalia na kupima vipimo
vya kila kipengele husika.
Uchambuzi wa kilichomo katika matini huwa muhimu sana mtafiti anapotafitia matini
zilizozungumzwa. Utafiti huu unahusu kuhakiki matini iliyochapishwa. Uchanganuzi waweza
kuwa katika kiwango sahili au changamano. Huwa changamano mtafiti anapochunguza mielekeo
ya mchapishaji kuhusiana na kazi fulani. Utafiti huu ulikuwa kwa uchanganuzi sahili. Hii ni kwa
sababu vipengele vyote vya maudhui, muundo, lugha na wahusika viliweza kutambulika
31
waziwazi kwa diwani hii na hata kuhesabika. Kwa kifupi diwani yenye mashairi husika
ilipekuliwapekuliwa kwa uangalifu kwa kuzingatia madhumuni husika ili kupata data
iliyotarajiwa. Data husika ilipatikana kwa kuyasoma mashairi husika kwa kina. Utafiti wa
Maktabani ulitegemewa ili kupata yale ambayo yamekwisha fanywa kuhusu mashairi mapokeo
na hata yale ya Sauti ya Dhiki. Kudurusu katika mitandao na tovuti mbalimbali pia kulitegemewa
sana.
3.6 Uchanganuzi wa Data
Mwanzo ilikuwa ni kusoma mashairi kwa uangalifu, wahusika, muundo lugha na maudhui
vikitiliwa maanani. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuhakiki na kufafanua vipengele
vyote vya fani na maudhui katika sampuli za mashairi yaliyolengwa. Kuhusu wahusika nilihakiki
sifa za nafsineni zinazobainika katika mashairi yote lengwa na vitu vinavyowakilisha watu au
wanyama. Pia ni nani au vitu gani anazungumza navyo na kilichomsababisha kuzungumza
hivyo. Nililenga jinsi mtunzi mwenyewe anavyoonekana kwa kila shairi husika yaani zile sifa
zake chanya au hasi. Pia nilihakiki wanyama na sifa zao kisha hatimaye kueleza sifa za wahusika
wa aina hiyo.
Kwa upande wa tamathali za usemi au matumizi ya lugha ililengwa misemo na nahau, sitiari na
tashbihi, lahaja, toni, taswira, tashihisi na aina zote za takriri zinazobainika. Pia ni lugha ya
kigeni na ufundi kwa jumla na namna haya yanaafiki muktadha husika. Kuhusu muundo,
yaliyolengwa ni mishororo, vipande, beti, vina na mpangilio mzima wa mashairi pamoja na
bahari zinazobainika. Pia mandhari ya mashairi yalilengwa.
Mwisho ilikuwa maudhui ambapo mambo kama tamaa, dini, utabaka na migongano ya hadhira
yalilengwa. Maelezo sahihi ya maudhui, muundo, lugha na wahusika katika sampuli hizo za
mashairi yalitolewa. Maelezo haya yalitumiwa kama ithibati ya fani bora au duni aliyotumia
mshairi huyu.Utafiti huu ulifanywa kwa kipindi cha miezi saba kati ya Machi 2014 na
Septemba 2014. Umuhimu wake unatarajiwa kuboresha uhakiki na hatimaye ubora wa usomi wa
mashairi kwa wanafunzi na wasomi wengineo wanaopendelea ushairi.
32
SURA YA NNE
UWASILISHAJI,UCHANGANUZI NA UFASIRI WA DATA
4.1 Utangulizi
Sura hii inalenga kuonyesha matokeo ya data iliyobainika katika mashairi yote yaliyohakikiwa
kwa kila kikundi. Maelezo yametolewa kwa kufungamana na madhumuni ya kwanza hadi ya
nne. Hali kamili kama ilivyo kwa kila shairi imetolewa maelezo bila kubadilisha chochote.
Mifano ya mashairi yenye sifa husika kwa kila madhumuni imeonyeshwa. Mihimili ya nadharia
nayo imeonyeshwa ilivyobainika kwa kila madhumuni. Nadharia hizi zinabainika katika
matokeo ya kila madhumuni.
4.2 Jinsi mshairi alivyotumia Wahusika
Katika mashairi yaliyohakiwa hapa, wahusika ni binadamu wa jinsia ya kike na kiume na walio
na sifa tofautitofauti. Pia, sifa za Mwenyezi Mungu zimeangaziwa hapa na pale. Sifa za
binadamu zimeelezwa kwanza. Shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ kwa mfano linazungumzia
binadamu kwa kutaja sifa zake za ndani kwa kulinganisha na sehemu zake za mwili. Lile la ‘Mja
si mwema’ nalo linaonyesha mshairi akitumia ufundi wa tashihisi kuzungumza na mkono wake
kana kwamba ni binadamu. Anautaka uandike shairi kwa hati nzuri ili wenye kusoma
waifahamu. Huyu ndiye mhusika wa kwanza wa shairi hili. Wahusika wengine ni wale wasomaji
wa shairi ambao watakiwa kuwa na sifa ya kufahamu na kuyapima yaliyomo. Katika ubeti wa
pili mkono watakiwa usikawie. Kuna walimwengu nao ambao watakiwa kujitunza. Zaidi ya hao
kuna mhusika ambaye ni mja.
Shairi la ‘Kutendana’ kwa upande wake limezungumzia sifa za mwanaume na pia zile za
mwanamke. Ikiwa tutajiuliza ni kwa nini mshairi akatumia wahusika kama hawa, twafaa
kuelewa kuwa maisha ya binadamu yana pande mbili; kuukeni na kuumeni. Katika shairi hili pia
kumetajwa sifa za kimada wa mume ambaye ataangaziwa sifa zake baadaye.
4.2.1 Sifa mbaya za Wahusika
Katika mashairi matatu yaliyohakikiwa hapa, kunaonekana sifa ya wahusika kuwa wabaya au
waovu. Mshairi katika ubeti wa saba wa shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ anasema kuwa kuna watu
wema na waovu, wenye heshima na wengine adabu mbovu. Anasema pia kuwa kuna wahalifu
sugu ingawa pia kuna watiifu wa vitendo na misemo. Ubeti huo ni ufuatao:
33
Ubeti wa 7
Kuna waja walo wema, kadhalika na waovu,
Wako wenye na hishima, na wenye adabu mbovu
Na wako wenye huruma, piya na watenzi nguvu
Mtu kuwa na kidevu, si kwamba mekamilika
Katika ubeti wa kumi wa shairi lili hili, mshairi anaendelea kuzungumzia waja wakorofi na
wachochezi wa kutia mambo chuku. Kuna wenye moyo mweupe na wengine mbaya. Anataja
kuwa sifa ya kuwa na ulimi haimkamilishi mja yeyote. Zaidi ya sifa hizi zote, kuna waja
wengine wakarimu na wengine bahili. Kuna pia madhalimu na wadhulumiwa. Mshairi akasema
mtu aweza kuwa na pua na asikamilike.
Ubeti wa 10
Kuna watu wakorofi, abadani hawatumi
Na wako wataswarufi, moja huzalisha kumi
Kuna wenye roho swafi, Wingine zao sisemi
Mtu kuwa na ulimi, si kwamba mekamilika (uk. 13)
Zaidi ya hayo katika shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ mshairi anazungumzia sifa mbaya za mhusika
anayeitwa Mwafulani. Mshairi alimwamini naye mja huyo asiaminike ingawa ni baada ya
mshairi kufikwa na jambo baya tayari. Huyo mwafulani haaminiki, amemtenda mshairi vibaya
na ni katili asiye na imani, watu humwambaa ili asiwahasiri na pia hana haya usoni mwake.
Aidha ni mbaya kwani huchimba shimo ili wenzake waanguke mle. Pia hufurahia maumivu ya
wenzake hivyo basi mshairi anaifahamisha hadhira kuwa ni mja mmoja tu kwa mia ambaye
huwa mzuri. Beti mbili zifuatazo, yaani ule wa tano na wa sita zafafanua sifa hizo.
5
Meniuwa mja, mja ni nduli, tahadharini
Mjaye daraja, nda kikatili, hana imani
Muonapo mja, kaani mbali, mujitengeni
Asije akaja, kwa habari, kuhasirini
6
34
Mja hana haya, haya hazimo, mwake usoni
Mja ni mbaya, hutimba shimo, ungiye ndani
Na ukishangiya, azome zomo, furaha gani!
Mmoja kwa miya, ndiye hayumo, baya kundini
(Sauti ya Dhiki, uk. 34)
Shairi la ‘kutendana’ pia lina sifa mbaya za wahusika. Shairi linachora mume kuwa na sifa
mbaya kwani akipata pesa nyingi, yeye hugura nyumbani asijulikane aliko. Yeye ni mbadhirifu
na akimaliza na kubaki bila peni hurudi hadi kwa mke mlangoni akijiliza ili aonewe imani. Sifa
nyingine mbaya ya mume huyu ni kuwa hana shukrani. Alimpa mke mashaka pamoja na taabu
zisizoelezeka. Pia hakumbuki alivyopewa pesa kwa furaha. Mke ajidhikisha kwa kumpa mume
pesa na pia furaha. Ufidhuli wa mume huyu umetiwa kikomo. Beti zifuatazo zina sifa mbaya ya
mume.
MWANAMKE
Kila mambo naelewa, yaliyo ndiyo na siyo
Si mwana wa kuhadawa, Khaswa kwa unambiyayo
Japo wasema ni dawa, sikupi ngakuwa nayo
Na kama yatakuwa, kuja kwa maradhi hayo
N’lishakupeleleza, hata n’kakubaini
Muda pesa ukijaza, humo mwako mfukoni
Huanza kujikimbiza, na kunigura nyumbani
Ngapita kukuuliza, uliko hujulikani
Ukisha kuzimaliza, kutolibakisha peni
Ndipo ndiyo huongoza, hadi kwangu mlangoni
Na kuanza kujiliza, n’kuonee imani
Leo sitakusikiza, hata unganambiyani
(Sauti ya Dhiki, uk. 90)
Mume yuyu huyu anamdharau mkewe licha ya kuwa mke alimtunza hapo awali wakati mume
hakuwa na kazi. Mume anatafuta kimada. Tunaona mume akimwonyesha mkewe uhuni. Aidha
35
twaweza sema hana jamala kwa mazuri aliyotendewa na mkewe. Kimada naye ana sifa mbaya
ya kuwa mzinzi kwani anakubali mahusiano ya kuwa mpenzi wa mume ambaye ana mke na
familia. Aidha ni nduma kuwili kwani hatimaye anamfukuza mume kutoka kwake. Anamkataa
ghafla na kukataa fadhila zote alizokuwa akimtendea hapo awali. Hii ni licha ya kula vya mume
huyo.
4.2.2 Wahusika wapekuzi na werevu
Sifa zaidi ya wahusika katika mashairi yaliyohakikiwa ni kuwa ni wapekuzi na werevu
wanaofahamu barabara kinachoendelea katika jamii zao au miongoni mwa wanajamii wenzao.
Katika shairi la ukamilifu wa mja kwa mfano ubeti wa tatu, mshairi anasisitiza kuwa kuna watu
werevu na kuna pia wapumbavu wasiojua hata jambo moja. Pia kuna wenye nguvu na wengine
dhaifu ambao huonewa. Kwa hivyo mtu kuwa na kifua hakumkamilishi. Mshairi anazidi
kusisitiza kuwa kukamilika kwa mja ni kuielewa dunia kwa marefu na mapana, kupitia njia
zenye miiba michungu na kuvuka bahari zenye vina virefu.
Mshairi au nafsineni katika shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ naye anabainika kuwa mshauri
anayeiasa hadhira / wasomaji wa shairi kuhusu matarajio kulenga mja aliyekamilika. Mshairi
huyu ni mdadisi anayeelewa wanajamii anaoishi nao. Hii inathibitishwa na kule kufahamu sifa
zao. Yeye ni mfumbaji kwani anaitaka hadhira kujipelelezea hulka za mja aliyekamilika.
Anasema hivi:
Ubeti wa 3
Kuna waliyo werevu, ambao ni waelewa
Na kuna na wapumbavu, Moja jambo wasojuwa
Piya kuna wenye nguvu, na dhaifu huonewa
Mtu kuwa na kifuwa, si kwamba mekamililka.
(Sauti ya Dhiki, uk. 12)
Ubeti wa 18
Aiyelewe duniya, kwa marefu na mapana
Azipite zile ndiya, za miba mitungu sana
Avuke bahari piya, zilo na virefu vina
36
Hiyo ni yangu maana, ya mja kukamilika.
(Sauti ya Dhiki, uk. 14)
Tukiendelea na sifa ya mshairi katika shairi la ‘Mja si mwema’ mshairi / nafsineni anaonekana
kuwa tayari amefunzwa na ulimwengu kuchuja watu wa kuamini na wasio wa kuamini. Sasa
amebaki kuamini mtu mmoja tu kwa mia. Nafsineni anawataka wanajamii wenzake wajue
alichotendewa na mja mwenzake ili wabaki salama bila kuhasirika kama yeye. Hata hivyo hapo
mbeleni aliamini watu bila kuwadadisi hulka zao kamili hadi hatimaye akahasirika. Baya
likamfika kwa kukosa uangalifu. Amebaki kujutia makosa yake na kujilaumu kwa kumuamini
mja mwenzake. Anasema hakupasa kumthamini hata sehemu. Msisitizo hapa ni kuwa mshairi
mwenyewe sasa amezinduka na kuwa mpekuzi na mwerevu baada ya kuteswa na wanajamii
wenzake.
Kwa upande mwingine, katika shairi la ‘Kutendana’ mwanamke ameerevuka hasa kwa kurejelea
ubeti wa nne. Mume anapofika nyumbani akiwa na mwako unaomsababisha hata kunyiwa na
mvua akitaka kusaidiwa na mkewe, mke anakataa kwani mume huyo hamsaidii kwa chochote
wakati wote. Mwanamke anashangazwa na hata kutamaushwa na huo ukosefu wa kila wakati.
Mke huyu amezinduka kwani anamtaka mume arudi atokako na kutafutia mwako wake njia ya
kuutolea. Hataki kusikia lolote kwani yeye sio jaa la kutupiwa takataka za mume. Ubeti
wenyewe ni huu ufuatao.
MWANAMKE
Rudi kuko utokako, siniletee udhiya
Tafutia mwako wako, ndiya ya kuutoleya
Mimi ndiye jaa lako, takazo kunitupiya?
Mwanamume nenda zako, sina n’takalosikia
(Sauti ya Dhiki, uk. 89)
Katika beti zinazofuata mwanamke anasawiriwa kuwa mwenye kuelewa mambo yaliyo na
yasiyo. Hapa hawezi kuhadawa na maneno ya mume. Yeye ni mwenye msimamo thabiti. Mke
anasisitiza kuwa penzi lake kwa mume limekwisha. Anasema amefumbuka macho hivyo
kumtaka mume aache kujisumbua kwani tayari wametengana.
37
4.2.3 Wahusika Maskini
Kuna baadhi ya wahusika wenye sifa ya umaskini. Nafsineni katika shairi la ‘Ukamilifu wa mja’
anasema pale ubeti wa nne kuwa kuna watu matajiri kupindukia ingawa wengine ni maskini
zaidi.
Ubeti wa 4
Kuna wasemao kweli, na wasemaji urongo
Kuna waliyo na mali, zilizopita kiwango
Na wingine zao hali, nda kuinamisha shingo
Mtu kuwa na maungo, si kwamba mekamilika(Sauti ya Dhiki, uk. 89).
Lile shairi la ‘Kutendana’ nalo linaonyesha mwanaume akiwa na sifa hii ya umaskini katika
ubeti wa kwanza. Anaomba kupewa kitu na mwanamke na asipompa atakopa kisha alipe
baadaye. Hata hivyo, yeye hana cha kumpa huyo mwanamke.
MWANAUME
Kama bure utanipa, nipa sinisimbuliye
Kama hutaki ‘takopa, nikulipe baadaye
Hivi sasa cha kukupa sina; kweli nikwambiye
Mtu huwa hakutupa, amfaapo mwenziye.
(Sauti ya Dhiki, uk.89).
Sifa ya umaskini inaandamana na ya utajiri kwa mke. Mke anasisitiza ameamuacha mume
kikamilifu. Anasema, “Kama waweza kuumba, umba mimi mwinginewe’’ (uk.101). Pia, yeye ni
tajiri kwani anakataa hata pesa za mume. Mke huyu ameweza kujinunulia mafuta aliyofukiza
vyema. Pia ana nyudi za Arabuni, ambari na kujivika leso mbili mpya kutoka dukani siku hiyo
hiyo. Kichwani napo ana nywele nzuri, pini na shada la asumini. Utajiri huo wa mke
unamwezesha kujipamba kwa kidani shingoni. Pia amejipamba kwa liwa (pambo la Kiswahili)
usoni ungadhani si mja bali malaika (uk.103).
Mke amepaka wanja wa manga machoni na kupaka mdaa midomoni. Ana vyombo vya dhahabu
viungoni, kipini puani, vipuli masikioni, pete vidoleni na bangili mikononi. Pamoja na urembo
wake asilia, mapambo hayo yanamzidisha urembo kiwango mpita njia angemwona moyo
38
ungemwenda mbio na bila shaka ashiki zikazidi kumpanda. Mke huyu hamtegemei mume tena
kwa kuwa amejitegemea kiuchumi.
4.2.4 Wahusika Waaminifu
Zaidi ya sifa hizo, wahusika katika mashairi haya ni wenye imani kwa Mungu. Mshairi katika
shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ ni mfano. Anasema kuwa hakuna mja kamilifu ila Mola tu.
Anasisitiza kuwa kukamilika kwa mtu ni tofauti na kwa Mola. Mtu hukamilika tu akifika daraja
aliloumbiwa. Kuna binadamu wenye sifa nzuri na wengine mbaya. Mhusika mwingine
anayebainika ni Mwenyezi Mungu. Sifa zake naye ni kuwa yeye ni kamilifu na tofauti na
binadamu. Ukamilifu wake ni tofauti na ule wa mja na pia ndiye Muumba. Imani kwa Mungu
inasababisha mja kuwa mwadilifu. Mja kuwa kamilifu ni kufikia daraja aliloumbiwa na Mungu,
kuielewa dunia kwa marefu na mapana na pia kuwa na ujasiri wa kuvumilia miiba michungu na
kuvuka bahari zenye vina virefu. Pia ni kwa kusubiri yote yatakayomfika hata kwa maisha ya
baadaye. Mshairi naye ni mwadilifu kwa kuwa kuna maadili aliyothamini na ambayo anashikilia
kama falsafa yake. Mifano ni huruma, Subira, utiifu, wema na kadhalika. Ithibati ni beti mbili
zifuatazo:
Ubeti wa 16
Hakuna mja kamili, ndivyo twalivyoambiwa,
Kadhalika mimi hili, nasema li sawasawa
Mkamilifu wa kweli, nakubali ni Moliwa
Maana yangu’ tatowa, ya mja kukamilika.
Ubei wa 17
Kukamilika kwa mja, ni mbali na kwa Moliwa
Kwa mja nitakutaja, ili upate kwelewa
Ni kufikiya daraja, ile aliyoumbiwa
Hapo ndipo huambiwa, mja amekamilika
(Sauti ya Dhiki, uk.14)
Kwa upande wa shairi la ‘Kutendana’ mke amechorwa kuwa mcha Mungu/ mwenye imani kwa
Mungu. Anasema Mungu amzidishie mume uhodari wa kumsaidia kwa maisha ya mbeleni
39
ingawa kwa mke huyu mume hathaminiwi. Licha ya imani hiyo kwa Mungu, mke huyu vilevile
ni mshirikina. Katika beti za kumi na mbili hadi kumi na tano, mke anamtaka mume akatolewe
pepo kilingeni. Pia amejua mume ana macho ya nje kwa kuwa mume huyo ana pesa zake.
Madhumuni haya ya kwanza yanapohusishwa na nadharia ya umuundo, ni bayana kuwa kila
shairi hapa limeundwa na wahusika mbalimbali. Wahusika hawa ni kama vile mshairi,
wanajamii wenzake (wazuri na wabaya) pamoja na mwenyezi Mungu katika shairi la ‘Ukamilifu
wa mja’. Bila hawa, mshairi asingefaulu kupitisha ujumbe wake kulenga sifa zao kikamilifu.
Ametumia wahusika hawa kwa kutaja sehemu zao za mwili kama vile miguu, macho, meno,
mikono na zinginezo akisisitiza kuwa si muhimu sana maishani ikiwa mja hana hulka nzuri
ndani yake. Vipashio hivi vya muundo vimetajwa na mshairi katika kila ubeti. Kila hulka
imetajwa pamoja na kuonyesha upungufu unatokea mja anapokosa hulka fulani ingawa ana
sehemu husika ya mwili. Sehemu hizi za mwili pamoja na hulka hizo japo zina uhalis kijamii.
Kwa muktadha wa nadharia ya umuundo, ni sahihi kusema kuwa huu ni ubunifu wa kisanaa tu
lakini unaopitisha ujumbe kwa njia isiyokanganya. Kazi hii inabaki kuwa muhimu sana kuikosoa
na hata kuwaelimisha wanajamii kwa mujibu wa nadharia ya ‘uamilifu’.
Katika shairi la ‘mja si mwema’ pia nadharia ya umuundo na hata ya uamilifu zinabainika.
Umuundo unashikilia kuwa kila kitu ni zao la ushirikiano wa vipande mbalimbali. Shairi hili
kwa upande wa wahusika limeundwa na mshairi / nafsineni, mkono wake (tashihisi),
walimwengu wanaotakiwa kujitunza na hata mja (Mwafulani). Kila kipashio kulingana na
nadharia ya uamilifu kinatarajiwa kutekeleza jukumu lake katika ule ushirikiano. Mkono katika
ubeti wa kwanza `watakikana kuandika shairi kwa hati njema inayosomeka ili isomwe na
watakaosoma na hata kuifahamu. Pale ubeti wa pili hadi wa sita pametajwa mja ambaye
anatenda mabaya kwa mshairi baada ya kumuamini, kumuua mshairi kikatili, kuhasiri wenzake
na kufurahia mshairi na wanajamii wenzake wakiingia kwa matatizo au shimoni. Sifa kama hizi
za kutajwa mja au binadamu wa aina hii bila kutaja jina la mwanajamii maalumu ni kwamba
kuna uwezekano kuwa na watu wengi wa aina hii katika utangamano wetu.
Kwa nadharia ya ujukumu / uamilifu, ujumbe kutokana na sifa za mhusika huyu unaimarisha
maisha ya mtu anapoendelea kutangamana na wenzake katika maisha ya kila siku. Kuna maadili
40
wanayofunzwa watu katika shairi hili. Mifano yake ni kuelewa pande mbili za hulka na
kuchagua wema kila wakati hasa kwa kumuiga mwenyezi Mungu. Kila sifa ya wahusika
iliyotajwa kwa kila ubeti wa shairi ingawa kwa daraja tofauti inahusiana na sifa katika hizo beti
zingine ili kujenga ujumbe mzima anaolenga kupitisha mshairi kwa mshikamano wenye mnato.
Masuala au muktadha katika mashairi ya ‘ukamilifu wa mja’, ‘mja si mwema ‘ na hata
‘kutendana’ ni wa kijamii.
Nadharia hizi vilevile zimefungamana na uhakiki wa shairi la ‘kutendana’. Shairi hili lina
wahusika watatu. Hawa ni mume, mke na kimanda wa mume. Wote wanashirikiana kulijenga
shairi hili. Umoja wa wahusika hawa Ukitengwa, shairi halitapitisha ujumbe kwa njia ifaayo.
Ujumbe katika shairi hili ni ubunifu wa kisanaa na umewekwa wazi katika shairi. Baada ya
kuhakiki sifa za wahusika hawa, dhamira ya mshairi ya kuwazindua wanawake wanaoteswa na
waume inapitishwa kwa njia ya waziwazi. Haya ni kwa kutegemea nadharia ya umuundo.
Kuhusiana na uamilifu mume ametumika kuwakilisha hulka mbaya na hata adhabu kwa
wahusika wa aina yake hasa kutokana na kimanda aliyemwacha baada ya kupata pesa za mume.
Mke wa mume anatumika kuonyesha wanawake wanaonyanyaswa, kuchukua hatua na hatimaye
kukatalia mbali urafiki na waume waliowatesa. Muktadha hapa ni wa maisha ya ndoa na
changamoto zake, yaani wa kijamii.
4.3 Tamathali za Usemi au Mbinu za Lugha katika Mashairi teule
4.3.1 Kisengerenyuma na Kiona mbele
Katika kuhakiki ufundi huu, kila mbinu ya lugha au tamathali imeangaziwa pamoja na mifano
yake katika mashairi yote yaliyohakikiwa. Mashairi yaliyohakikiwa ni ‘N’shishiyelo ni lilo’,
‘Wasiwasi enda zako’ na ‘Telezi’. Katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ kuna mbinu ya
kisengerenyuma hasa katika ubeti wa pili ikionyesha urejeshi wa uneni wa walimwengu wa
zama zilizopita kwamba kweli ni chungu kwa aambiwaye. Ubeti huo ni huu:
2
Walinena walimwengu, wa zama zilopisiye
Kwamba kweli i utungu, kwa yule aambiwaye.
Nami haya ndugu yangu, sasa niyaaminiye
Asojuwa nasikiye, apeleleze ajuwe. (uk.1)
41
Katika shairi la ‘wasiwasi enda zako; kuna mbinu ya utabiri au kiona mbele. Hapa ni pale
mhusika ambaye ni ‘wasiwasi’ anamwambia mshairi kuhusu yatakayotokea baadaye. Wasiwasi
unamwambia nafsineni kuwa atakapotoka mle gerezani, kule nje angojewa na maisha magumu.
Hili ni jambo ambalo bado halijatokea lakini langojewa siku za usoni. Mbinu ya urejeshi
inatumika ili nafsineni kuonyesha kuwa jambo analozungumzia kuhusu ‘kweli’ ni la tangu jadi
kwa hivyo si geni. Utabiri huu nao ni kiwakilishi cha hisia inayopita kwa maisha ya mshairi
kuhusiana na kusekwa jela.
Shairi la ‘Telezi’ pia lina mbinu inayokaribiana na kisengerenyuma. Hii ni ile ya usimulizi. Hii
yahusiana na matukio ya shairi kusimuliwa katika wakati uliopita. ‘Mvua’ inaelezwa kuwa
ilinyesha, mimea ilitekuka, wakulima wakafikwa na hasara, walioogopa mvua wakakimbia
majumbani, mvua ilibwaga shindo kubwa, tope zilitapakaa kote na telezi zikambwaga nafsineni.
Haya yote ni masimulizi katika wakati uliopita. Hata shairi hili lina mbinu ya kionambele au
utabiri. Mbinu hii inabainika katika ubeti wa sita mshairi anapotaja mambo ya siku za usoni.
Kuanzia ubeti wa kwanza hadi wa tano, ujumbe umetajwa katika wakati uliopita lakini unapofika
hapa unatajwa katika wakati ujao. Mfano wa ubeti ni ufuatao:
6
Japo hivyo zilikuwa, ndiya hazipitiki
Bali mimi haamuwa, kwenenda japo kwa dhiki
Kumbe vile nitakuwa, ni mfano wa samaki
Ni mfano wa samaki, kuiendeya ndowana.
(Sauti ya Dhiki, uk. 24)
Mbinu hii imerudiwa katika ubeti wa nane hadi wa kumi na moja. Nafsineni anangojea siku
ambayo idhilali itaisha na jibu kumwondokea. Pia anangoja kwa matarajio makuu siku ambayo
jasho jembamba litamtoka njia mbili kisha atetemeke kwa uchungu utakaozidi sana kisha moyo
wake ufurahie. Mwishowe anatarajia kuliuguza jeraha kwa kulitia dawa hadi lipoe na afya yake
irudi halafu aruke na kucheza kwa kuingiwa na furaha tele.
42
4.3.2 Tashihisi
Kando na mbinu hizo zinazokaribiana, kuna mbinu ya tashihisi inayoonekana kutanda katika
madhumuni haya ya pili. Katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ tunaelezwa kuwa kweli
imemfunga nafsineni ndani ya chumba asitoke nje. Kweli hiyohiyo inasemekana kumlaza
nafsineni chini kwenye baridi kali. Katika ubeti wa 12 nao kweli inamnyima haki zilizo ngomeni
kama vile jamaa kuja kumtazama, kuandika wala kuletewa barua. Hapa chini kuna ubeti wa
kumi na mbili.
12
Kweli pia meninyima, haki zilizo ngomeni
Wangu kuja nitizama, hilo haliwezekani
Haya nnayoyasema, ndivyo yalivyo yakini
Baruwa sitakikani, Kwandika wala kwetewa
(Sauti ya Dhiki , uk.2)
Mshairi anatumia mbinu hii ili kuepuka shutuma kutoka kwa aliopinga kisiasa. Hapa anailaumu
kweli aliyosema badala ya kulaumu watawala aliokosoa kisha kuishia kufungwa jela. Pia
kutumia ufundi huu ni njia mwafaka ya kuzua mguso katika shairi na hadhira iishie kutekwa na
ujumbe zaidi.
Shairi la ‘Wasiwasi enda zako’ laonekana kutawaliwa hata zaidi na ufundi huu wa tashihisi.
Nafsineni anazungumza na hisia ya wasiwasi kana kwamba ni kiumbe hai kama vile binadamu.
Kuanzia ubeti wa kwanza anauambia wasiwasi huo umwondokee uende zake, uondoke uandame
njia na kumwondoshea uso wake. Pia anauuliza ikiwa unasikia na kuutaka uwache jeuri zake na
kujishughulisha na mambo yake badala ya yale ya mshairi.
Katika ubeti wa pili anaujuza wasiwasi huo kwamba haitaki suhuba yake kwani si nzuri na
haistahimiliki kwani uovu umekithiri. Suhuba ya wasiwasi hata ikinyoshwa hainyoki hivyo
mshairi hataki shari. Anautaka wasiwasi huo uende zake. Ubeti wa tatu unasisitiza ileile tashihisi
kwa kusisitiza kuwa hauna kazi uifanyayo ila kuwafitinisha na kuwagonganisha viumbe. Hii
ndiyo kazi yenye kufurahisha, isiyochosha na ambayo wasiwasi umeizoea.
43
Kwa upande mwingine, wasiwasi huo wamvunja mshairi moyo kwa sababu wakaapo
humwambia hayawi ayatakayo na kuwa hata akitia tamaa asumbua moyo wake tu. Pia ni
kwamba hata akingojea hayo ayangojeayo hatayapata bali ni kujisumbua bure. Zaidi ya hayo, ni
tashihisi kuwa wasiwasi unamletea habari kuhusu mambo yalivyo nyumbani kuwa si mazuri na
yote ni mabaya. Wamtaka afikiri kuwa yasemwayo ni kweli lakini wasiwasi huo ukitaka apate
kusononeka tu.
Wasiwasi utapata kufurahika kwa kurejelea ubeti wa sita. Tashihisi inazidi kuonekana wakati
wasiwasi unamwambia kuhusu afya za wenzake walio nyumbani. Kila mara unamwambia kuwa
hali zao zi taabani. Unazidi kumkata moyo kwani hata atakapotoka gerezani maisha magumu
yamngojea nje. Mshairi anashangaa ikiwa ulilokusudia ni kumtia wazimu. Naye anauambia
kuwa ikiwa hiyo ndiyo hamu ya wasiwasi wenyewe utaaibika. Hatimaye, nafsineni anakataa
urafiki na wasiwasi na kuutaka utokomee.
Sababu za nafsineni kutumia ufundi kama huu ni kuwa anazungumza na hisia ya wasiwasi iliyo
ndani yake kwa sababu hana mwingine wa kuzungumza naye. Katika mandhari ya jela,
Abdilatif’ hakuruhusiwa kutangamana na jamaa au rafiki. Ni kawaida kwa kila binadamu akiwa
katika hali kama hii kujaribu au kujitahidi kujituliza mwenyewe kwa vyovyote vile. Inatarajiwa
pia kuna sababu ya kutosha kumsababisha mfungwa kama huyu kuwa na mawazo ya kujali
jamaa na marafiki aliowaacha nyumbani na hivyo kuwa na mawazo mengi kuwahusu kwani
hawaonani. Mifano ni kule kuhangaika kuhusu afya ya jamaa zake hao kule nyumbani. Pia,
maisha magumu anayotarajia nafsineni baada ya jela / kifungo ni lazima kumtisha mfungwa
kama huyu. Hii ndiyo sababu tunamuona akihangaishwa na maisha hayo ya baadaye.
4.3.3 Sitiari/ Jazanda
Uhakiki wa mashairi haya umegundua yametumia ufundi wa sitiari au jazanda. Katika shairi la
‘N’shishiyelo ni lilo’ pale ubeti wa tatu kuna istiara ya kutaja kweli kuwa kama sumu. Mfano
mwingine ni mshairi kuwa ‘firauni’ kwa kusema kweli. Pia mshairi analindwa chumbani bila
kuruhusiwa kutoka. Analindwa kama simba marara. Ubeti wa tatu ni ufuatao:
Kweli nnaifahamu, haipendwi aswilani
Kwa mja hiyo ni sumu, mbaya iso kifani
Mwenye kuitakalamu, hapendezi katwaani
44
Sasa nshayaamini, ni kweli haya ni kweli
(uk.1)
Sitiari katika shairi la ‘wasiwasi enda zako’ inapatikana kwa mshororo mmoja tu. Mfano huo ni
ubeti wa pili nafsineni anaposema kuwa hataki suhuba ya wasiwasi kwani si nzuri. Hii ina maana
ya ndani kuwa hataki wasiwasi huo umwingie kwa vyovyote sawa na suhuba iingiavyo mtu
moyoni.
Kuna jazanda zaidi katika shairi la ‘telezi’. Ufundi huu unahusu kutaja vitu vilivyozoeleka katika
mazingira yetu ingawa katika shairi maana yake ni ya ndani. Baadhi ya jazanda hapa zina utata
yaani kufasirika kwa maana zaidi ya moja. Mfano wa kwanza ni mvuwa (mvua). Nafsineni
anasema kuwa mvua kubwa ya maradi na ngurumo ilinyesha bila kipimo kutwa kucha. Hata
hivyo haikuwanufaisha wakulima bali iliwaletea hasara. Hii ni kwa sababu mvua hiyo ilitekua
mimea yao na kazi yao ngumu ikaharibika hadi wakakosa kuvuna matunda waliyokuwa
wakitaka. Iliwalazimu walioiogopa mvua hiyo kukimbilia upenuni na wengine majumbani mwao
na kuikomea milango. Maji hayo yakajaa barabarani na matope kutapakaa kote hadi
kukakosekana njia ya kupitia.
Ingawa njia hazikupitika, nafsineni aliamua kwenda lakini ikawa kama samaki kuiendea ndoana.
Alishindwa kutembea kwa telezi hadi zikambwaga chini. Licha ya hayo, anaahidi kutowacha
lakini kubadili mwendo. Mbali na maana ya kijuujuu kuhusu faida ya mvua na hasara yake kwa
mimea na wakulima, neno mvua laweza kuwa na maana tofauti. Yamaanisha jumuiya ya shairi
hili la ‘telezi’ haikunufaika kikamilifu kwa juhudi za kumtimua mkoloni na hatimaye kujitwalia
utawala wa kisiasa. Wanajamii kujikomboa na kupata uhuru kuliingia kwa kishindo ikitarajiwa
faida kuu kwa kila mwanajamii jambo ambalo lilitokea kuwa kinyume cha matarajio hayo.
Katika shairi, inasemekana mvua ilinyesha kwa radi na ngurumo kutwa kucha lakini wakulima
wakafikwa na hasara. Mbinu hii ya jazanda imetumiwa na nafsineni kama njia ya kukosoa
utawala wa jumuiya kwa njia fiche isiyoonekana na watawala kama dharau kwao kwa kuwa
mshairi hakuusema kwa njia ya moja kwa moja.
4.3.4 Ufundi wa Kinaya
Mbinu mojawapo iliyobainika katika uhakiki huu ni ile ya kinaya. Katika ubeti wa tano wa shairi
la ‘N’shishiyelo ni lilo’ kuna mbinu hiyo. Baada ya kusema kweli mshairi analipwa kwa
45
kuwekwa taabuni. Hii ni kinyume cha matarajio ya hali halisi ya maisha. Kwa kupinga utawala
wa serikali anashikwa himahima na kuadhibiwa ndani ya ngome ili ajute. Kuna kinaya pia kwa
sababu nafsineni anapewa adhabu kali za kila aina ili aache kunena lakini anasema bado atainena
kweli na mateso hayatakuwa dawa ya kumzuia kusema. Pia ni kinaya kusema kuwa ukijaliwa
mateso ya duniani umshukuru mwenyezi Mungu na kujikaza kuyachukua (ubeti wa 17). Kuna
wanaharakati wengi ambao tayari wanasumbuliwa na kuuliwa kwa kusema ukweli na hata hivyo
kutobadili nyoyo. Mshairi anasisitiza kuwa naye vilevile ataandama njia hiyohiyo na kufuata
nyayo zao. Hii ni kinaya.
Ubeti wa 17
Ama hakika mwendani, kwa mwenye moyo wa sawa
Mateso ya duniani, wakati kijaaliwa
Hushukuru Rahamani, Kajikaza kutukuwa
Nami yangawa yakuwa, Hikaza moyo si ila.
(Sauti ya Dhiki uk. 3)
Mbinu hii imetumika kama njia ya kusisitiza bidii aliyo nayo mshairi katika kuendeleza maadili
hayo ya kusema kweli kwa jumuiya yake ambayo haiko tayari kuipokea kweli yenyewe.
Hata shairi la ‘Telezi’ limetungwa kwa ufundi huu wa kinaya. Ni kinaya kuwa mvua tele
ilinyesha nabadala ya kuwaletea wakulima faida kwa mimea kunawiri ikaiharibu mimea
yenyewe. Ufuatao ni ubeti wa pili ambao una ujumbe huo:
Mimeya waliopanda, ilitekukatekuka
Kazi ngumu walotenda, yote ikaharibika
Hawakuvuna matunda, waliyo wakiyataka
Waliyo wakiyataka, yakawa ya mbali nao
(Sauti ya Dhiki, uk.24)
Mfano mwingine ni kuwa nafsineni mwenyewe baada ya wanajamii wenzake kuiogopa mvua
kisha kujificha majumbani mwao, yeye aliamua kwenenda japo kwa dhiki. Inashangaza yeye
kuchagua dhiki wenzake wakichagua usalama. Kinaya ni kuwa hali hiyo ilibadilika kuwa mfano
wa samaki kuiendea ndoana. Hatimaye, telezi zilimbwaga kwa kutojua kuziendea. Licha ya
matatizo hayo anaahidi kutoacha kutembea ila kubadili mwendo.
46
4.3.5 Tamathali ya Takriri
Mashairi yote matatu yametumia mbinu ya takriri ya mishororo minne katika kila ubeti. Shairi la
‘Wasiwasi enda zako’ nalo limetumia aina nyingine ya takriri. Katika ubeti mmojammoja kuna
mbinu hii katika vina vya kati na vile vya mwisho. Vina vya kati vinafanana katika mishororo ya
kwanza mitatu. Mfano ni ubeti wa kwanza hapa ulio na ya, wa pili ki, wa tatu yo, ule wa nne ya,
wa tano ri, wa sita ya, ule wa saba ni ya, na wa nane ko. Vina vya mwisho navyo kuanzia ubeti
wa kwanza ni ko, ri, sha, yo, ni, mu na sha.
Katika shairi la ‘Telezi’ mbinu hii ya takriri pia imetumika katika vina vya kati kufanana katika
ubeti mmojammoja yaani katika ubeti ingawa tofauti toka ubeti hadi ubeti. Vile vya mwisho
navyo pia vyafanana katika ubeti. Mfano ni ubeti wa kwanza ambapo vina ni sha, mo katika
mishororo ya kwanza mitatu. Ubeti wa pili ni nda, ka na wa tatu ni wa, ni. Ule wa nne nao ni
ndo, ni na wa tano ya, pe. Ubeti wa sita ni wa, ki na wa saba ya, pe. Ubeti ni tofauti kikamilifu.
Mapigo haya ya vina vinavyofanana katika ubeti hulipa shairi mdundo unaopendeza hadhira na
pia kusababisha shairi liimbike.
4.3.6 Chuku
Halikadhalika, kuna mbinu ambazo zimetumika katika mashairi fulani tu lakini hazikutumika
kwa mashairi yote. Katika shairi la ‘N’ shishiyelo ni lilo’ kwa mfano kumetumika mbinu ya
chuku katika ubeti wa tisa. Mlinzi kuwa mlangoni pasi na kuondoka wakati wowote ni chuku.
Hii yatumika kusisitiza namna nafsineni alivyozuiliwa gerezani kwa lengo la kumzuia
kuendeleza harakati zake za kusema kweli.
Katika shairi la ‘Telezi’ nalo, ni chuku kuwa mvua iliponyesha mimea yote ilitekuka, wakulima
kukimbilia majumbani mwao lakini nafsineni akaamua kuenenda japo kwa dhiki. Kiwango
chake cha ujasiri kimepigiwa chuku kama vile ‘Kumbe nitakuwa mfano wa samaki kuiendea
ndoana.’ (uk. 24).
4.3.7 Utohozi,Taswira na Taharuki
Mbinu myingine iliyotumika katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ ni ile ya utohozi. Mshairi
kulala ‘simitini’ ni mfano wake. Katika ubeti wa kumi na moja nao kuna taswira ya mandhari ya
jela. Mshairi yumo ngomeni mwenye kuta ndefu bila kutangamana na mahabusu wengine lengo
47
likiwa asinene alilo nalo akawaambukiza wenzake. Shairi la ‘Telezi’ pia limejaa tamathali hii ya
taswira takribani katika beti zote. Tunapata picha ya mawazoni kuhusu hali ilivyokuwa wakati
mambo fulani fulani yanapotajwa. Mifano ni mvua kutajwa ikiwa na radi na ngurumo usiku na
mchana, mimea iliyopandwa kutekuka, wenye kuicha mvua isiwatose mwilini kukimbilia penuni
na kuikomea milango, mikondo ya maji kujaa barabarani, kutapakaa tope kote na njia kutopitika.
Aidha, kuna taharuki katika ubeti wa mwisho nafsineni anaposema kuwa hatawacha kutembea
ila kubadili mwendo. Baada ya kushindwa kuziendea telezi kisha kubwagwa chini, hatujui
kilichojiri baadaye au hata matokeo ya kubadili mwendo kwake. Mbinu hii ya taswira
imetumiwa ili kuisababisha hadhira kupata ujumbe wa shairi kikamilifu kwa kutumia mifano
halisi iliyozoeleka katika mazingira ya jamii hasa msimu wa mvua.
4.3.8 Balagha na Uzungumzi nafsia
Mbinu ya balagha imetumika katika shairi la ‘Wasiwasi enda zako’ peke yake. Mifano ni katika
ubeti wa kwanza, wa sita na saba. Ubeti wa kwanza kwa mfano ndio huu hapa chini:
Wasiwasi n’ondokeya, ondoka enenda zako
Ondoka andama ndiya, n’ondosheya uso wako
Ondoka! Wanisikiya? Ziwate jeuri zako
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?
(Sauti ya Dhiki, uk. 32).
Mbinu hii inatumika kuonyesha msimamo wa nafsineni wa kupinga au kukataa matakwa ya
mwenzake (wasiwasi). Haikosi hata huku kuzungumza na wasiwasi ni tamathali ya uzungumzi
nafsia kwani wasiwasi wenyewe umo ndani ya mshairi huyu ingawa ufundi wa shairi
wauonyesha kana kwamba ni mhusika mwingine kando. Ni bayana kuwa kitovu cha ushairi
mzima huu ni uzungumzinafsia. Swali ni je, ingawa tashihisi inabainika, inawezekanaje mshairi
huyu akazungumza na wasiwasi wenyewe kana kwamba ni binadamu mwenzake? Ieleweke
kwamba ana mdahalo na nafsi yake mwenyewe. Lile swala zima la kusekwa jela akiwa pweke
linazua hali kama hii katika hisia zake. Sababu ni mradi kujituliza kwa namna yoyote awezayo.
Wasiwasi wenyewe unamkaba hadi kuzungumza kwa upweke. Nafsineni amekumbwa na
48
matatizo kama vile kusumbua moyo, kutengwa na jamaa (ubeti wa tano) kuteseka kwa afya za
jamaa hao, uwezekano wa maisha magumu baada ya jela, masikitiko na mateso.
4.3.9 Tamathali ya Mvutano
Katika shairi la ‘wasiwasi enda zako’ peke yake kuna ufundi wa lugha unaojulikana kama
mvutano. Hapa ni pale ambapo wahusika wawili au taswira mbili huvutana katika kazi ya fasihi
hasa ushairi. Katika shairi hili tunaona nafsineni akiendelea kuvutana na kuzungumza na
wasiwasi hadi hatimaye akaushinda kwa kukatalia matakwa yake yote. Twaweza kukubali kuwa
hili ni funzo maalumu kwa hadhira ya shairi kama hili kuwa yafaa kuyashinda mawazo au silika
zote hasi kama vile wasiwasi. Kuushinda wasiwasi ni mfano bora pia wa tamathali ya uadilifu
wa kifasihi. Kwa kuwa wasiwasi ni mfano wa mhusika mkuu kuanzia mwanzo wa shairi hili hadi
mwisho, yeye ni mhusika mkinzani.
4.3.10 Uhuru wa Kishairi: Kilahaja na Inkisari
Kibali cha kishairi katika mashairi haya kwa upande mwingine ni jambo lililotumika na
nafsineni kuimarisha ufundi wake. Maneno ya kikale ni mfano kama huo. Hii ni lugha ya
Kiswahili cha kizamani; maneno ambayo leo hii hutumika kwa mashairi mapokeo pekee bali si
kwa lugha sahihi.
Mifano ni nipulikiza (uk.1) ikimaanisha nisikilize na idhilali ikimaanisha dhaifu. Mtima nao ina
maana ya moyo na katiti ni kidogo. Haya ni katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’. Uhakiki
umebainisha kuwa mifano yenyewe imetumika kuhifadhi historia ya maendeleo ya lugha ya
Kiswahili. Ni bayana kuwa maneno kama haya huenda yakasahaulika na kubaki kutumika kwa
uchache.
Katika shairi lili hili kumetumika uhuru wa inkisari. Hii inahusu kufupisha maneno katika
mshororo ili kupata idadi ifaayo ya mizani katika kila mshororo wa ubeti. Mifano ni kadha katika
shairi hili. Ndu yangu imetumika badala ya ndugu yangu, nasikiye ikimaanisha na asikie na pia
iso kwa maana ya isiyo. Tabuni yafaa kuwa taabuni na menibaidisha ni imenibaidisha. Zaidi ya
49
hayo kuna menitenganisha ikifaa kuwa imenitenganisha na walo kwa walio. Mifano mingine ni
mesema badala ya nimesema, ilo na baridi ikifaa kuwa iliyo na baridi na ‘tasonga’ kwa maana ya
nitasonga.
Shairi la ‘Telezi’ pia limebuniwa kwa uhuru huu wa inkisari. Mfano ni kazi ngumu walotenda
badala ya waliyotenda, waliyo kwa waliyotaka na haamua ilkifaa kuwa nikaamua. Zaidi pia kuna
kuzendeya telezi badala ya kuziendea talezi. Mshairi ametumia uhuru huu katika mashairi husika
ili kupata mizani zinazotosha katika kila mshororo yaani nane katika ukwapi na nane katika utao.
4.3.11 Tabdila
Uhuru wa tabdila nao unahusu kubadilisha umbo la neno bila kuongeza au kupunguza idadi ya
mizani. Lengo lake huwa kuzua mapigo ya aina moja hasa kwa vina vya ndani au nje katika
ubeti wa shairi. Mapigo kama haya hupelekea shairi husika kuimbika. Mifano katika shairi la
‘N’shishiyelo ni lilo’ ni siwati kwa maana ya siiwachi, lilo ikiwa hilo na ajuwe badala ya ajue.
Mifano zaidi ni ingawaje ikiwa ingawaye na wamenitiya ikifaa kuwa wamenitia. Halikadhalika
kuna wangi badala ya wengi na dasturi ikiwa desturi. Mahabusu wingine iwe mahabusu wengine
na mambo mingine iwe mambo mengine. Hoja ya kimsingi kuhusiana na uhuru huu wa tabdila ni
kuwa idadi ya mizani katika neno haifai kuongezeka wala kupunguka. Usahihi wa neno tu ndio
uliovurugika. Hali kama hii huchangiwa na lafudhi au eneo la kijiografia atokalo mshairi husika.
Yeye huthamini kuhifadhi matamshi ya kikwao na anapofanya hivi hatarajii kukosolewa na
wanaisimu au wataalamu wa sarufi.
Shairi la ‘wasiwasi enda zako pia lina tabdila. Baadhi ya maneno yamevurugwa kiumbo kwa
hivyo yakawa sio sahihi. Mifano ni uwovu badala ya uovu. Pia kuna ela kuwafitinisha badala ya
ila kuwafitisha. Zaidi ya hayo kuna najisumbuwa badala ya najisumbua na ningojeyayo badala
ya niyangojeayo. Kuna pia hunijiya kwa nafasi ya hunijia. Mifano zaidi ni kukhusu badala ya
kuhusu, waliyo iwe walio, yaningojeya kwa yaningojea na kutiya wazimu ikifaa kuwa kutia
wazimu.
Zaidi ya mifano iliyotolewa katika mashairi hapo juu, lile la ‘telezi’ nalo lina tabdila. Mifano
anayotumia nafsineni ni kama vile mvuwa, mimeya, wakakimbiliya, hawakutuwa, kukomeya
50
milango, isibakiye udhiya, kuiendeya ndowana sikujua na pia kutembeya. Kisahihi maneno haya
yanafaa kuwa mvua, mimea, wakakimbilia, hawakutua kukomea milango, isibakie udhia,
kuiendea ndoana, sikujua na kutembea. Tunasema ni tabdila kwa sababu idadi ya mizani
haipungui wala kuongezeka katika neno husika. Mshairi ametumia uhuru huu ili shairi liwe na
mdundo unaoweza kukaririka au kuimbika vizuri.
4.3.12 Kuboronga Sarufi
Katika mashairi yaliyohakikiwa kulibainika uhuru wa kuboronga sarufi. Hii inahusu kupangua
maneno katika baadhi ya mishororo ya shairi. Mifano katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ ni
‘ninenayo usikiye badala ya usikie ninenayo. Zaidi kuna ‘yaliyo moyoni mwangu ningependa
nikwambiye’ badala ya ‘,ningependa nikwambie yaliyo moyoni mwangu’. Pia kuna ‘ndani
waniweke badala ya waniweke ndani’. Nyingi mno adhabu nayo yafaa kuwa adhabu nyingi mno
na juwa kuota ni dhiki’ nayo ‘iwe ‘kuota jua ni dhiki.’ Daima ni yangu hali yafaa kuwa hali
yangu daima.’
Katika ubeti wa kumi na mbili kuna sitakikani kuandika wala kuetewa barua ambayo yafaa kuwa
sitakikani kuandika wala kuletewa barua. Kainama wangu mdomo nayo iwe mdomo wangu
kainama. Mno wanganiadhibu, kweli siati kusema katika uhai wangu yafaa kuwa ‘Siachi kusema
kweli katika uhai wangu. Tunaweza kukubali kuwa uhuru huu wa kishairi ni mpangilio wa
wamaneno usiokuwa katika lugha ya kawaida kama vile ya nathari.
Hata katika shairi la ‘wasiwasi enda zako’ mshairi ameboronga sarufi. Kuna kwa mfano ‘sitaki
yako shari, enda zako wasiwasi badala ya siitaki shari yako, wasiwasi enda zako. Kuna pia vitwa
kuwagotanisha badala ya kuwagotanisha vichwa pamoja na mno umeizowea badala ya umeizoea
mno. Kwa upande mwingine kuna ‘Kwamba tamaa ngatiya nasumbua wangu moyo ambayo
yafaa kuwa ‘ningatia tamaa, nasumbua moyo wangu. Bure najisumbua, na kingine kisahani,
kuhusu zao afiya na kama hiyo ndiyo hamu nayo yawe najisumbua bure, na kisahani kingine,
kuhusu afya zao na kama hiyo ndiyo hamu yako.
Mwisho, shairi la ‘telezi’ pia limeborongwa sarufi. Mifano ni ‘ilibwaga kubwa shindo’ badala
ya ‘ilibwaga shindo kubwa. Pia kuna kunyesha iliposiya badala ya iliposiya kunyesha. Mfano
51
mwingine ni ukawa mwingi udhiya badala ya udhiya ukawa mwingi. Mifano zaidi ni: Pa kupita
zisitupe, japo hivyo zilikuwa, zikanibwaga telezi na lakini tena siwezi. Yafaa kuwa zisitupe pa
kupita, japo zilikuwa hivyo telezi zikanibwaga na lakini siwezi tena. Sababu ya mshairi
kuboronga sarufi / kubananga sarufi katika mishororo hii ni ili kufaulu kujenga urari wa vina vya
kati au vile vya mwisho, yaani kumalizia na neno lenye silabi itakayofanana na za mishororo
iliyotangulia. Hapa kwa mfano ni ubeti wa tano katika shairi hili la ‘telezi’.:
Kunyesha iliposiya, kukatapakaa tope
Zilijaa kila ndiya, isibakie nyeupe
Ukawa mwingi udhiya, pa kupita zisitupe
Pa kupita zisitupe, kwa ndiya kukosekana
(Sauti ya Dhiki, uk.24).
Katika ubeti huu mshairi ameweza kupangua maneno katika mishororo fulani ili kuhakikisha
vina vya kati ni ya na vya mwisho pe.
4.3.13 Kilahaja
Mbinu ya kilahaja nayo inaonekana kutamalaki katika mashairi yaliyohakikiwa. Katika shairi la
‘N’shishiyelo ni lilo,’ lahaja iliyotumika na mshairi ni ile ya Kimvita. Kulingana na Chiragdin na
Mnyampala (1977:40), Kimvita ni lahaja ambayo asili yake ni kisiwa cha Mombasa. Hapo
zamani kuliitwa Mvita kutokana neno vita. Wenyeji wa kisiwa hiki walikuwa mara kwa mara
wakipigana vita na watawala wa kigeni; Wareno, Waarabu na hata Waingereza. Pia walipigana
na miji mbalimbali ya mwambao iliyokuwa ikishirikiana na wageni hao. Wataalamu hawa wa
historia ya Kiswahili wanafafanua kwamba katika Kimvita sauti /h/ huwa /ch/ katika lugha
sahihi, /nd/ huwa /nj/ na /v/ huwa /z/. Wanasisitiza kuwa Kimvita ni mojawapo ya lugha za
Kiswahili zenye historia ndefu ya fasihi. Mmoja wa washairi wa Kiswahili cha Kimvita ni
Muyaka wa Muhaji wa Mombasa.
Mtunzi wa mashairi haya Addilatif’ Abdalla naye pia ni mzawa wa mji huohuo. Ni bayana kuna
athari kuu ya Muyaka kwa washairi wa baadaye kama Abdilatif Abdalla. Mulokozi (2002: 16)
anadokeza kwamba kipengele kimoja cha uhakiki wa fani ya mashairi ni lahaja iliyotumika na
mshairi na hufaa kuchunguzwa ikiwa anaimudu vizuri, ikiwa ni lugha nyepesi au inayolenga
52
kuonyesha ubingwa wa mshairi kwa kutumia maneno mazito na msamiati mgumu. Musa na
Hijazy (1977:1) nao wanaeleza kwamba mtunzi wa mashairi huathiriwa sana na lahaja ya mahali
alipozaliwa na hii hudhihirika kwa mashairi yake. Kuna ushahidi wa lahaja ya Kimvita katika
shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’. Mifano ni maneno kama ‘siwati’ badala ya Siiwachi imani, ndu
kuwakilisha ndugu, utungu kuwakilisha uchungu, nti hini badala ya nchi hii, moya ikifaa kuwa
moja ilipowatoma kumaanisha ilipowachoma, nde kumaanisha nje, wanati badala ya wananchi,
mtana kusema mchana, kutukuwa ikiwa kuchukua na awate kumaanisha awache, Pia kuna sil’ati
kumaanisha siliachi. (Sauti ya dhiki, uk. 1-3)
Katika shairi hili, mshairi anaonekana kutumia lugha ya Kiswahili kwani ujumbe wake
unaeleweka kwa kiwango fulani. Twaweza kusema kuwa lugha hii ni rahisi. Hata hivyo, yale
matumizi ya tamathali au ufundi wa lugha pamoja na vipengele kadhaa vya idhini ya kishairi
yamesababisha utata japo kwa upeo mdogo. Kuna maneno yasiyokuwa Kiswahili sahihi
kutokana na ukweli kuwa yamefupishwa, kurefushwa au umbo lake kuvurugwa. Mifano ni
usikiye, ndu, zilopisiye, ujuwe, niishishiye, ilipowatoma na mengineyo. Baadhi ya maneno pia
yameegemea kwa lahaja ya Kimvita na pia lugha ya kikale. Nafsineni ametumia kilahaja kwa
lengo la kujinasibisha na lugha na jamii yake anayothamini sana na pia kwa lengo la kutia shairi
mguso wa kisanaa.
Ingawa shairi la ‘Wasiwasi enda zako’ halijatumia uhuru wa kilahaja, lile la ‘telezi’
limeuzingatia uhuru huu hapa na pale. Lahaja yenyewe ni ileile ya Kimvita iliyotumika katika
‘N’shishiyelo’ ni lilo’. Mifano yake ni ndiya ikifaa kuwa njia. Pia kuna haamua kwa maana ya
nikaamua na henezi ikiwa polepole au taratibu. Mwisho kuna sitawata kwa maana ya sitawacha.
Mifano hii ni michache kwa kuwa shairi hili linalenga jumuiya nzima ya Wakenya baada ya
uhuru. Kamwe swala hili si la pwani au Mvita peke yake. Pia kutumia kilahaja yaonekana kuwa
ufundi mwafaka wa kupitisha ujumbe kwa hadhira kwa jinsi yenye mguso na mnato na pia
kuepuka lugha kavu isiyovutia au isiyo na ladha kisanaa. Katika shairi hili, licha ya mshairi
kutumia uhuru wa kishairi wenye miundo, msamiati au mpangilio wa lugha usiokuwa sanifu
hapa na pale, bado hajatoka nje ya misingi ya lugha inayohusika. Shairi hili linaendelea
kueleweka na mtu anayefahamu lugha ya Kiswahili.
4.3.14 Idhini ya Mazida
53
Zaidi ya idhini hiyo, kuna uhuru wa mazida, yaani kurefusha maneno. Lengo lake huwa kupata
idadi ya mizani zinazolingana kwa kila mshororo. Katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ kuna
niishishiyo badala ya niishiyo na kuniadhibisha ngomeni badala ya kuniadhibu ngomeni.
Inabainisha kwamba baada ya mshairi kutumia tabdila na inkisari, hakupata matatizo mengi ya
kumhitaji kutumia mazida ili kusawazisha mizani ndipo akatumia mifano hii miwili tu.
Katika shairi ‘Wasiwasi enda zako’ pia kuna mazida. Mifano ni ‘ondoka enenda zako’ ikifaa
kuwa ‘ondoka enda zako’. Hapa mizani zimeongezwa zikawa tatu badala ya mbili. Pia kuna
‘hiino ndiyo kaziyo’ kwa maana ya ‘hii ndiyo kazi yako’. Neno hiino limerefushwa na kupata
mizani tatu badala ya mbili. Katika ‘telezi’ kuna mifano kama maradi badala ya radi (ubeti wa
kwanza), ilitekukatekuka ambayo silabi zimerudiwa katika ubeti wa pili na pia mijaji badala ya
maji katika ubeti wa nne. Hata mazida imetumika na mshairi kusawazisha idadi ya mizani katika
mishororo. Njia hii imetumika hasa pale mshairi amegundua asipolirefusha neno moja katika
mshororo kwa njia yoyote ile, mizani hapo zitapungua.
4.3.15 Maneno ya Kigeni/ Kukopwa
Uhakiki wa shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ ulibainisha kwamba mshairi ametumia maneno ya
kigeni kama njia ya kuonyesha kibali chake cha kishairi. Maneno kama haya hukopwa kutoka
kwa lugha ngeni na kutumika yakiwa vilevile bila kubadilishwa na mshairi kwa vyovyote vile.
Mfano ni neno Rasuli katika ubeti wa ishirini ambalo chanzo chake ni lugha ya Kiarabu na
hutumika katika dini ya Kiislamu yenye asili Arabuni. Zaidi ya hilo, kuna neno Rahamani katika
ubeti wa kumi na saba. Msamiati kama huu una chimbuko lake katika dini ya mshairi. Ingawa
ameteswa ngomeni (jela), anaendelea kuamini Mungu aliyempa maadili ya kusema kweli.
Katika shairi lili hili kumetumika maneno yaliyokopwa na kutoholewa (kuswahilishwa) na neno
‘Firauni’ ni mfano wake. Latokana na jina la cheo cha wafalme wa zamani wa Misri. Pia
lamaanisha mtu yeyote mwenye vitendo vichafu. Mshairi amelitumia katika ubeti wa nne,
mshororo wa tatu anaposema, ‘Wameniona mbaya kumshinda Firauni?’ Kuna pia maneno
‘burangetini’ kutokana na neno la Kiingereza ‘blanket’. Pia kuna neno ‘simitini’ kutokana na
cement’. Matumizi ya utohozi yanachangiwa na ukweli kuwa nomino hizi zimeingia Uswahilini
kutoka maeneo au mataifa ya nje ya Afrika au Afrika mashariki. Toni katika shairi hili nayo ni
ile ya msongo na hasira. Ingawa hii si uhuru wa kishairi, mshairi anaeleza kuhusu jinsi kujitoa
54
mhanga kusema kweli kulivyomletea uchungu na adhabu ya kufungwa gerezani (ngomeni).
Baada ya kuwaambia wakuu (viongozi) pamoja na wananchi kuhusu kweli hiyo, mshairi
anateseka sana. Kweli yenyewe iliwachoma kwelikweli. Licha ya machungu anayopata
nafsineni, msisitizo wake ni kuwa haachi kusema kweli ile hata kama itaishia kwa kifo.
Umuhimu wa kutumia ufundi kama huu katika shairi husika ni kuwasilisha ujumbe kwa jamii,
watu waielewe hali halisi ilivyo katika uongozi wa jumuiya kwa kurejelea usuli wa wakati huo.
Ufundi aliotumia ni wa wastani isipokuwa maneno ya kilahaja ya Kimvita ambayo huweza
kutatiza mtu wa kawaida kuelewa ujumbe wa shairi.
Ieleweke kwamba nadharia zilizoongoza utafiti huu zimebainika katika mashairi yaliyohakikiwa
hapa. Kwa msingi wa nadharia ya umuundo, mshairi ameonyesha umahiri wa kimawasiliano
kama alivyotaja Noam Chomsky. Umahiri huo umedhihirika kwa kutumia ufundi wa lugha
aliotumia mshairi. Ujumbe wa mshairi umefika kwa hadhira ya mashairi kwa kutumia mbinu
kama chuku, kinaya, tashihisi, takriri, mvutano, balagha na hata jazanda na taswira pamoja na
mbinu zinginezo.
Nafsineni vilevile ametegemea uhuru kemkem wa kishairi ikiwemo inkisari, mazida, kilahaja,
kubananga sarufi na uhuru mwingineo kama ulivyotajwa kwa maelezo yaliyotangulia.
Tunalazimika kukubali kuwa mashairi yote matatu, yaani ‘N’shishiyelo ni lilo’, ‘wasiwasi enda
zako’ pamoja na ‘telezi’ ni zao la ushirikiano wa mbinu hizi mbalimbali za lugha pamoja na ule
uhuru wa kishairi. Vyote vyafanya kazi kwa pamoja ili kupitisha dhamira na ujumbe wa kila
shairi kwa njia yenye mguso na ya kutamanika. Ni bayana kuwa mbinu zote zilizotumika
zingaliondolewa kwa mashairi husika, lengo la mshairi lisingetimia ifaavyo.
Hata kwa kuoanisha mashairi haya na umuundo wa baadaye, mshairi huyu amefaulu kuzingatia
mtindo wa matini kwa njia ifaayo na hata uhakiki wake si lazima kushughulishwa na athari za
nje ya shairi husika. Japo maswala ya kitamaduni na kijamii yaliyolengwa na mshairi ni swala
halisi la kihistoria nchini Kenya, kamwe haijawa lazima kuyahakiki mashairi haya kwa misingi
hiyo. Uhakiki kama huu kwa hivyo haujajikita kwa athari za nje ya mashairi husika. Haimhitaji
mtu kujishughulisha na athari hizo ili kuyaelewa mashairi haya. Katika ufafanunuzi wa mbinu
55
zilizotumika, imebainika kuwa mashairi yanaeleweka kwa kutegemea yaliyomo katika mashairi
husika kama mifano toshelevu ya mbinu hizo za sanaa. Kwa hivyo mada husika hapa inaeleweka
barabara bila kutegemea mashairi zaidi.
Kuhusiana na nadharia ya uamilifu, kila mbinu ya lugha iliyotumiwa na mshairi ina nafasi yake
katika kudumisha kuwepo kwa kila shairi husika. Umuhimu au nafasi hiyo imeelezwa kwa
maelezo yaliyotolewa kuhusu kila mbinu husika ya lugha. Ni bayana kuwa kila mbinu
haijatumika na mshairi hivihivi tu kwani inatekeleza jukumu lake katika kila shairi. Jukumu hilo
ni kuzua taswira mwafaka kwa hadhira, kuhifadhi siri ya kishairi na hata kuleta mvuto.
4.4 Kuhakiki Muundo katika Mashairi
4.4.1 Beti, Mishororo na Vipande
Katika madhumuni haya, mashairi yaliyolengwa ni ‘siwati’, ‘Leo N’singekuwako’ na
‘N’sharudi’. Uhakiki wa mashairi haya ulithibitisha kuwa yote yana muundo unaokaribia
kufanana. Hata hivyo kulibainika tofauti za hapa na pale. Shairi la ‘Siwati’ kwa upande wake
lina umbo la beti nne, mishororo minne kila ubeti na kiishio. Kiishio hapa ni ule mshororo wa
mwisho katika kila ubeti ambao unatofautiana kutoka ubeti hadi ubeti. Kila mshororo hapa
umegawanywa katika ukwapi na utao isipokuwa ubeti wa kwanza mshororo wa kwanza na ubeti
wa nne mshororo wa tatu. Mishororo hii miwili imegawanywa katika ukwapi, utao na
mwandamizi, yaani sehemu tatu. Katika ubeti wa kwanza sababu ya kipande cha pili ni kutoa
msisitizo kuwa nafsineni hawachi aliloshikilia kwani hana sababu maalumu ya kufanya hivyo.
Mshororo wenyewe ni: ‘Siwati n’shishiyelo, siwati, Kwani niwate? (Sauti ya Dhiki uk.9).
Katika ule ubeti wa mwisho mshororo wa tatu, nafsineni ametumia sehemu ya pili kulinganisha
kuacha aliloshika na nzi hasa kwa kuwa nzi hawi na maono ya mbali. Mshororo huo nao ni:
‘Siwati kisha nikawa, kama nzi; hivyo siwi. (uk.9).
Kuhusiana na shairi la ‘Leo N’singekuwako,’ hili vilevile ni shairi la arudhi ambalo lakaribiana
kimuundo na lile la ‘Siwati.’ Hata hivyo, kuna tofauti za kimuundo hapa na pale. Katika shairi
hili, kuna jumla ya beti tano katika shairi zima. Ingawa beti hizi zahusu kukumbuka madhila,
machungu na mateso aliyopitia mshairi akiwa jela, kila ubeti una wazo lake au ujumbe wake kwa
hivyo tunaweza kukubali kuwa hapa napo pana utoshelezi wa beti. Ubeti wa kwanza kwa mfano
56
unaeleza kwamba taabu ingekuwa mauti mshairi asingekuwako kwani angekuwa maiti
aliyebakiza sikitiko tu. Angekuwa mfu na kufunikwa kwa mchanga.
Katika ubeti wa pili, nafsineni anasema kuwa leo hii angekuwa amesahaulika na ikaachwa
kusemekana tu kwamba aliwahi kuishi. Ule ubeti wa tatu unaeleza kuwa angekuwa marehemu
aliyekwishaoza na kusahau masumbufu, taabu na masumbuko yake. Anauliza ikiwa taabu hizo
zingeweza kufika aliko. Ule ubeti wa nne nao unarejelea mshairi kuombolezwa na jamaa
kuomba dua ili aende salama baada ya kifo. Baadaye ingekuwa kusahauliwa kwa moyo na
matamko. Ubeti wa tano unadokeza kuwa licha ya mateso aliyopata, bado leo hii yu hai kwa
kuwa moyo wake wahimili masumbuko na kwa hivyo angetamaushwa na yaliyompata, hakika
asingekuwa hai sasa hadi kuandika shairi hili. Msisitizo hapa ni kuwa katika beti zote hizi, kila
ubeti umejitosheleza kutoa ujumbe wake bila kutegemea ubeti mwingine. Umuhimu wa hali
kama hii ni kuwa mshairi ameonyesha umahiri wake katika kumudu stadi hii muhimu katika
utunzi wa mashairi mapokeo stadi ambayo inawezesha beti chache tu kama hizi tano kupitisha
ujumbe wenye maadili kemkem.
Sawa na shairi la ‘siwati’, la ‘leo N’singekuwako’ pia lina mishororo minne katika ubeti likiwa
pia ni tarbia. Kila mshororo nao una ukwapi na utao ikiwa bahari ya mathnawi. Katika shairi hili
kumetumika kibwagizo /kipokeo au mkarara ambao ni ‘leo N’singekuwako kama tabu ni mauti.’
Mkarara huo umerudiwa katika kila ubeti kwa lengo la kusisitiza ujumbe mkuu wa nafsineni.
Anasisitiza kuwa asingekuwa hai ingekuwa kupata taabu ni sawa na mauti. Kipokeo hicho pia
kinasababisha taswira ya kudumu kwa hadhira na pia hakikisho kuwa mshairi sasa yu hai licha
ya dhuluma zote alizopitia.
Halikadhalika, shairi la ‘N’sharudi nalo limezingatia muundo wa beti tano. Kila ubeti una
mishororo minne na hata hilo likiwa muundo wa tarbia. Kila mshororo nao una ukwapi na utao
hiyo ikiwa bahari ya mathnawi. Zaidi ya arudhi hizo, sawia na mashairi yaliyotangulia, katika
madhumuni haya, mawazo yanaonyesha muumano ufaao kuanzia pale ubeti wa kwanza hadi wa
tano. Katika ule wa kwanza kwa mfano, mshairi anatoa utangulizi wa kuwa anayezungumza sio
mwingine bali ni yule yule kijana wa kutoka Mvita, mtaaa wa Kuze. Anaeleza hapo ndipo shina
lake na kusisitiza kuwa amerudi kwao nyumbani tena hivyo aliye na la kusema aseme. Katika
57
ubeti wa pili anasisitiza kuwa amekuja na ingawa amenyamaza kwa muda mrefu, leo ndio
anazungumza tena. Ubeti wa tatu unaeleza kuwa hajachoka wala kuogopa kuzungumza kuhusu
jambo liendalo kombo atakaloliona katika jumuiya yake. Anasema katika ubeti wa nne kuwa
macho yake bado yanaona na masikio vilevile yanasikia ili yamwingie hata yaliyompita siku
zilizotangulia. Anamalizia kwa kusisitiza kuwa hata hivyo ahitaji kwanza kupata muda wa kuona
mambo ya kutosha ili ayazungumzie na hivyo hataki kuzungumza moja kwa moja ingawa
amerudi kwao.
Inabainika kuwa ujumbe mkuu katika shairi ni mmoja unaojengwa kwa jinsi inayokaribiana sana
katika beti hizi tano. Yabainika hakuna tofauti kubwa sana ya ujumbe toka ubeti mmoja hadi
mwingine. Kauli ya jumla yaweza tolewa kuwa shairi hili tofauti na yaliyohakikiwa hapa halina
utoshelezi kamilifu wa beti kwani kila ubeti haujitegemei kikamilifu kupitisha wazo lake. Hii ni
kwa sababu ujumbe wa ubeti umejengwa sana kwa kutegemea ubeti uliotangulia.
4.4.2 Mizani
Kipengele zaidi cha muundo kilichotambulika katika uhakiki wa mashairi haya ni kile cha
mizani. Katika shairi la ‘Siwati’, kuna mizani kumi na sita yaani nane nane kwa kila mshororo
isipokuwa mishororo miwili iliyo na sehemu tatu. Vina vya kati navyo vinafanana katika
mishororo ya kwanza mitatu katika ubeti mmojammoja. Vile vya mwisho navyo vinafanana
katika mishororo hiyohiyo mitatu. Kina cha mwisho katika mshororo wa tatu kila ubeti nacho
chatokea kuwa cha kati katika mshororo wa nne kwa kila ubeti. Mfano bora ni ubeti wa kwanza
hapa;
Siwati nshishiyelo, siwati; kwani niwate?
Siwati ni lilo hilo ‘talishika kwa vyovyote.
Siwati ni mimi nalo, hapano au popote
Hadi kaburini sote, mimi nalo tufukiwe.
(Sauti ya Dhiki, uk. 9)
Inaweza kukubalika mshairi akitumia mpangilio kama huu wa vina vya kati na vya nje ili shairi
lake liweze kuzua mahadhi ya mapigo ya kimuziki yanayoweza kuimbika. Mbali na kuonyesha
ufundi wake wa kutumia takriri, mpangilio kama huu pia unasaidia kusisitiza msimamo wake
katika shairi zima. Umbo zima la shairi hasa kule kutunga ushairi mfupi wa beti nne tu
58
kunaelekea kutufahamisha kuwa tayari hadhira yake imepokea ujumbe wake kuhusu
anachoshikilia kama falsafa na maadili yake. Hapa haina haja kutunga utungo mrefu tena ila
kusisitiza kuwa hawachi aliloshikilia na kuamini. Katika muktadha huu basi, shairi lenyewe ni
fupi.
Shairi la ‘Leo N’singekuwako’ nalo sawia na lile la ‘Siwati’ limebuniwa kwa mizani kumi na
sita kwa kila mshororo isipokuwa ubeti wa tatu mshororo wa tatu na ule wa nne mshororo wa
kwanza. Kila mshororo kati ya hii miwili ni mizani kumi na tano. Mlingano wa mizani kila
mshororo ni muhimu sana ili kusababisha mapigo ya kimuziki na ufundi unaopelekea shairi
kukaririka au kuimbika kwa mahadhi ya kuvutia. Hata mahali pasipofaa mizani kumi na sita,
mshairi amedumisha uhuru wa mazida na hata inkisari ili aidha kupunguza au kuzidisha mizani
hadi zitoshe. Hata hivyo, nafsineni amedumisha mizani hizo kumi na tano kwa kuwa mishororo
hiyo yazungumzia matokeo ya kifo chake kama vile kuondokewa na taabu na kuliliwa na jamaa
jambo ambalo halikutendeka kwani bado yu hai. Upungufu kama huo hapa wafaa. Kibwagizo
cha shairi kina mizani kumi na sita hata katika beti zenye mshororo mmoja wenye mizani kumi
na tano.
Ufafanuzi wa mizani unapoendelea ni bayana kuwa shairi la ‘N’sharudi’ lina mizani nane katika
ukwapi na nane katika utao kwa kila mshororo. Katika shairi hivyo basi, kumezingatiwa takriri
kwa kiwango cha juu. Umbo la tarbia limerudiwa katika beti zote tano. Mkarara kila ubeti ni
‘basi’ n’sharudi aliye na lake nanene.’ Katika ukwapi na utao, kuna mizani kumi na sita na vina
vinavyotiririka. Maelezo haya yanaonyesha muoano katika ufundi na umbo au muundo. Ni
bayana kuwa shairi hili, kutokana na mpangilio unaovutia wa mizani na vina linaweza kuimbika
na hata kukaririka kwa urahisi.
4.4.3 Bahari za Mashairi
Zaidi ya vipengele vilivyotajwa kuhusiana na muundo, mshairi amezingatia bahari za mashairi
kama vile mathnawi, ukaraguni, kikwamba na sakarani. Mathnawi ni bahari yenye sehemu ya
ukwapi na utao kwa mishororo kama ilivyo katika shairi la ‘siwati.’ Mishororo kama ile ya
kwanza mitatu kuanza kwa neno moja kama ilivyo hapa nayo ni bahari ya kikwamba yaani neno
‘siwati’ kutumiwa mwanzo wa kila mshororo. Ufuatao ni ubeti wa pili katika shairi hilo:
59
Siwati ngaadhibiwa, adhabu kila mfano
Siwati ningaambiwa, tapawa kila kinono
Siwati lililo sawa, silibanduwi mkono
Hata ningaumwa meno, mkono siubanduwi
(Sauti ya Dhiki, uk.9)
Vina vya kati vinatofautiana na pia vya mwisho ni tofauti kila ubeti. Bahari kama hii nayo ni
ukaraguni. Kuchanganya bahari hizi mbalimbali katika shairi moja nako kunazua bahari ya
sakarani. Kwa maoni hayo, haikosi ushairi huu ni tarbiya, mathnawi, kikwamba, ukaraguni na
pia sakarani.
Katika shairi la ‘leo N’singekuwako’ vina vyote vya mwisho vinafanana. Vyote ni ko. Vile vya
kati navyo vinafanana katika beti zote isipokuwa ubeti wa kwanza. Vina hivi ni ti katika ubeti
huo wa kwanza lakini wa katika beti hizo zingine. Vya kibwagizo ni ko, ti. Ni ubeti wa kwanza
tu au utangulizi wa shairi ulio tofauti na beti zingine kuhusiana na mpangilio mzima wa vina.
Mpangilio wa vina ambapo vyote vya mwisho vinafanana na vya kati kutofautiana ni bahari ya
ukara. Shairi hili ni bahari ya mathnawi pia kwa sababu kuna ukwapi na utao katika kila
mshororo. Kwa muktadha wa ujumbe anaopitisha mshairi, ujumbe kuhusu maisha yake unatajwa
katika sehemu ya utao. Huu ndio anaosisitizwa kwa kutumia neno lenye silabi ya mwisho ko ili
kusababisha mapigo yanayotekenya ngoma za masikio ya hadhira kisha ujumbe kunata zaidi.
Maneno yote yenye ko kama vile kuweko, sikitiko, funiko, alikuwako na mengine yametumiwa
mwishoni mwa kila mshororo ili kusisitiza ujumbe wa mshairi. Katika shairi la ‘N’sharudi’ nalo,
vina vyote vya kati ni le na vya mwisho na. Kule kufanana kwa vina vyote vya kati na pia vyote
vya mwisho kunasababisha bahari ya mtiririko. Vina vya kibwagizo ni na, ne navyo pia
vikifanana kila ubeti. Aidha, kina cha mwisho mshororo wa tatu kinatokea kuwa cha kati katika
mshororo wa mwisho kila ubeti. Kina hicho ni na. Kuna urari wa vina vya mwisho na hata vya
kati. Kupanga vina kwa njia hii kunamwezesha mshairi kudumisha mwendo wa ujumbe
aliodhamiria kufikia hadhira kiustadi na hata ukanata kwao. Inabainika swala kama hili la
mvutano baina ya nafsineni na waliomfunga jela ni swala nyeti linalohitaji wapinzani wa mshairi
kupata na kuelewa msimamo wake kwa njia barabara. Jambo hilihili limesisitizwa kwa kutumia
bahari ya pindu pale ambapo kina cha mwisho wa mshororo wa tatu kinatumika kama kina cha
60
kati katika ukwapi wa kabwagizo. Hapa chini kumetolewa ithibati toka ubeti wa kwanza na wa
pili katika shairi hili.
Si mwingine ni yuyule, wa Ki-mvita kijana
Mzawa mji wa kale, mtaa Kuze kwa jina
Huwo ndiwo mzi mle, tipuzi ya langu shina
Basi n’sharundi tena, alo na lake nanene
Nijile tena nijile, mneni nijile tena
Zangu tomi zinyemele, Zinyemele kwa maana
Tangu siku n’toshile, hi’leo ndiyo nanena
Basi n’sharudi tena, alo na lake nanene
(Sauti ya Dhiki, uk, 111).
4.4.4 Utoshelezi wa Arudhi za Utunzi
Katika shairi la N’sharudi, mshairi anaonyesha kujifunga katika arudhi zote zinazotarajiwa
kuzingatiwa katika mashairi mapokeo. Isipokuwa kwa lugha iliyosukwa kwa njia maalumu kama
kilahaja, idhini ya kishairi na tamathali za usemi, kusingekuwa na changamoto kwa hadhira
kuhusiana na muundo. Kuna utoshelezi wa arudhi katika kila ubeti.
Katika shairi la ‘Siwati’, kutumia neno ‘siwati’ kila ubeti kunasababisha utoshelezi wa beti.
Inaibuka kwamba kila ubeti unawasilisha ujumbe wake kikamilifu bila kutegemea ubeti
mwingine. Pia kila ubeti umezingatia arudhi za utunzi kama vile ubeti, mshororo, vipande na
mizani kama ilivyo katika beti zote. Kuna mfano wa bahari ya mandhuma pale ambapo ukwapi
unatoa wazo na utao kutoa jibu la wazo hili. Inaonekana mawazo kwa kila mshororo na pia beti
yamefululiza kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa muungano unaofaa ili mshairi afaulu
kupatanisha mawazo ya ujumbe wake mzima. Muundo mzima wa shairi hili pamoja na mapigo
ya kimuziki katika vina vya kati na vya nje yanaathiri hadhira barabara kwa kufikisha ujumbe
mzima kwa njia yenye mnato ufao.
Shairi hilo japo fupi la beti nne tu linawasilisha ujumbe wa mshairi kwa ukamilifu hasa kutokana
na kurudiarudia neno kuu la ujumbe wake mzima. Kwa muktadha huohuo kunaonekana muundo
61
wa kinyumbizi au mnyambuliko katika ubeti wa tatu mshororo wa kwanza. Hii yamaanisha
urudiaji ambapo neno fulani linanyambuliwa na kuunda maneno mengine yanayofanana nalo.
Kimsingi, hii ni sifa inayoingiliana sana na muundo wenyewe wa lugha ya Kiswahili na lugha
zetu mbalimbali. Huwa muhimu sana katika ukuzaji na uimarishaji wa wizani au ridhimu.
Mshororo wenyewe ni ufuatao:
‘Siwati si ushindani, mukasema nashindana?
(Sauti ya dhiki, uk.9)
Hapa, neno ‘nashindana ni mnyambuliko kutoka kwa ‘ushindani’. Mshairi amezingatia ukamilifu
wa arudhi zote za utunzi wa mashairi mapokeo hasa yale ya tarbia. Arudhi hizi zinasababisha
ujumbe wake kueleweka barabara licha ya kutumia uhuru wa kishairi kwa njia kadha. Licha ya
kuwa beti ni nne tu, adili lililolengwa limegonga ndipo na hata ameepuka kutumia mkarara ili
asipoteze nafasi yote ya kutoa msimamo zaidi. Kwa hivyo hataki marekebisho ya mwanajamii
yeyote katika msimamo wake au imani maishani. Hata akisema kwa kifupi namna hii au hata
kwa kirefu, hilo halibadili msimamo wake huo. Maelezo haya yanalandana na nadharia ya
uamilifu kwa kuonyesha utendakazi wa muundo wa aina hii. Kuunganisha vipengele vyote vya
muundo kama ailivyofanya mshairi ni njia bora ya vijenzi hivi kuunda shairi kwa pamoja nayo
ikioana na nadharia ya umuundo.
Kuhusiana na shairi la ‘Leo n’singekuwako’ inaonekana usambamba mwingine pamoja na
kinyumbizi au mnyambuliko. Katika ubeti wa kwanza maneno ‘ningekuwa yameendelea
kurudiwa katika kila ukwapi nayo maneno ‘kungebaki’ katika ubeti wa pili. Maneno
yananyambulika na kuishia kutofautiana hapa na pale kwa mfano ‘n’singekuwako, ningekuwa,
ningekuwako na ‘n’ngekuwa. Vilevile kuna mabadiliko katika maneno haya kwa kuangalia
mizani kwa kuwa zinazidi kutofautiana idadi kutoka neno hadi neno licha ya kuwa maneno hayo
yametokana na neno moja. Huku kubadilika kunafanya swala hili hili kuchukuliwa kuwa la
muundo badala ya la ufundi wa lugha. Ubeti wa kwanza na wa pili ndizo hizi:-
Kama tabu ni mauti, Leo n’singekuwako
Ningekuwa ni maiti, Mebakiza sikitiko
Ningekuwako tiyati, mtanga ndilo funiko
Leo n’singekuwako, kama tabu ni mauti
62
Hivi leo n’ngekuwa, kana kwamba sikuwako
Kitambo n’shafukiwa, nimo kaburini huko
Kungebaki kuambiwa; Atifu alikuwako;
Leo n’singekuwako, kama tabu ni mauti.
(Sauti ya Dhiki, uk. 63)
Katika mashairi haya inakubalika mshairi amefaulu kuunganisha arudhi zote za utunzi wa
mashairi mapokeo hadi kuzua shairi la beti nne katika shairi la ‘siwati’, tano katka ‘Leo
N’singekuweko’ na tano katika ‘N’sharudi’ Mawazo ya kila ubeti pia yameunganishwa kwa njia
bora kuanzia mwanzo hadi mwisho. Haya ni kwa kulinganisha na nadharia ya umuundo ambapo,
mishororo, vina, vipande na vipengele vyote vya muundo vinaonekana kushirikiana kwa
mshikamano murua ili kujenga kila shairi kiwango kwamba kila mojawapo imetawala nafasi
yake kisahihi. Kwa maneno machache, mshairi huyu ameweza kupitisha maadili ya kutowacha
mambo yafaayo hadi kaburini, kuvumilia mateso na taabu pamoja na msimamo wake wa
kuikosoa jumuiya iliyopotoka. Vipengele vyote vya kimuundo vemeshirikiana kikamilifu
kupitisha maadili yote haya na hivyo utunzi wenyewe unatimiza majukumu fulani maalumu
kulingana na nadharia ya uamilifu. Kila kipashio kina jukumu lake.
4.5 Maudhui katika Mashairi yaliyoteuliwa.
4.5.1 Pingamizi na Unyanyasaji
Mashairi yaliyohakikiwa katika madhumuni haya ni ‘Wasafiri tuamkeni; ‘kichu hakiwi ni uchu’
na ‘Mamaetu Afrika’. Katika mashairi haya kulionekana maudhui ya pingamizi na unyanyasaji.
Katika shairi la ‘wasafiri tuamkeni’ mshairi anawahimiza wanajamii wenzake ambao ni wasafiri
wasichoke wala kuwa dhaifu ingawa safari yao ni ndefu. Juhudi nzima inayozungumziwa katika
shairi, kama kawaida ya shughuli yoyote ya kisiasa ina wapinzani. Katika ubeti wa kumi na
mbili mshairi anazungumzia adui ambaye hataki safari ifanyike. Huyo anasemekana kuwa adui
wa wasafiri hawa na hata kwake mwenyewe. Mshairi anamkumbusha kuwa asifikiri atafaulu
kwa lengo hilo la kuwapinga. Juhudi nzima yahitaji mshikaji bendera kuishika vizuri na daima
kuwa imara bila kulegea. Pia afaa kuiongoza barabar hadi wafike huko waendako.
Shairi la ‘Kichu hakiwi ni uchui’ nalo lina maudhui sawa au yaliyokaribiana na haya. Kuna
maudhui ya ubinafsi na unyanyasaji. Mshairi anazungumzia mtu aliye na vitu kwa milima (tajiri)
63
mkubwa lakini wa kujifaa yeye binafsi bali sio binadamu wenzake. Yeye huvikusanya
(kujilimbikia mali) na kuendelea kuitazama tu. Mtu huyo analinganishwa na ndovu. Hapa kuna
pia maudhui ya kupuuza na kunyanyasa maskini. Katika ubeti wa thelathini mshairi anataja mtu
aliye na mali iliyokiuka mipaka lakini anatupilia mbali wenye shida na mashaka. Ubeti wa
thelathini na moja unataja mhusika anayezungumziwa katika shairi kuwa na nguvu za kimabavu
na kutumia magumi na mateke hadi kuwanyima wenzake utulivu. Akitokea hao hutetemeka kwa
kumuogopa. Mtu huyo huishia kuzitumia nguvu hizo mitaani akidhulumu wenzake ambao ni
wanyonge mfano wa ‘mnyonge msonge’ bila wa kumzuia. Mshairi hapa anarejelea matumizi
mabaya ya cheo /madaraka. Anazumgumzia mhusika huyo kuwa na cheo juu ya wenzake wote
lakini wawapo na shida, yeye kamwe hawasaidii kwa chochote au hata kutaka kuwasikia. Kuna
mfano wa ubeti wa thelathini na moja hapa chini:
Au awe yuna nguvu, Kikubwa kifuwa chake
Ziwe nguvu za mabavu, na magumi na mateke
Iwe sasa utulivu, hawaupati wenzake
Iwe ni watetemeke, muda’ye akitokeya
(Sauti ya Dhiki, uk. 86)
Badala ya kuchukua fursa hiyo na kuitumia vizuri, yeye huanzisha takaburi, kuwatesa
anaowaongoza na hata kuwatendea jeuri. Mshairi anasisitiza kuwa mtu kama huyo hafai kuitwa
mtu bali mnyama wa porini.
Katika lile shairi la ‘Mamaetu Afrika’ mshairi ameonyesha nyanyaso kwa bara la Afrika.
Anarejelea Afrika kama ‘mama yetu.’ Mbinu ya tashihisi kwa hivyo imetegemewa sana.
Anaangazia swala la utengano wa Waafrika pale mwanzo wa shairi. Waafrika wamekumbwa na
msiba kwani ndugu hawasikizani. Kila mmoja wao ataka kuwa kiongozi wa wenzake. Kwa
jambo hili ambalo nafsineni anasema haliwezekani, anaitaka Afrika iwaamue. Anazungumzia pia
fitina inayochochewa na wale maadui (wakoloni) ambao hawataki kuiona Afrika ikipata amani.
Unyanyasaji zaidi ni kuwa kuna dhuluma ya wakoloni toka Ulaya ambao walitawala maeneo
mengi ya Afrika kabla ya uhuru. Mshairi anataja kuwa bado wamo duniani wakiwa na fikra
zilezile za kikoloni. Wanatamani kuidhulumu Afrika tena. Waliishikia Afrika shokoa na kupora
mali yake yote. Wakaijaza mali hiyo vyomboni kama shehena wakaipeleka mataifa yao. Kwa
64
hivyo ni wezi. Hawakuona huruma yoyote kwani waliiacha Afrika maskini bila kujali vizazi
vijavyo vingetegemea nini. Utumwa nao unatajwa ambapo watu weusi ambao ni ndugu za
nafsineni walitiwa utumwani bila utu. Kutokana na rangi yao nyeusi walionekana kama nyani .
Hao watumwa walitegemewa kufanya kazi kule Ulaya bila malipo yoyote. Mshairi anasisitiza
kuwa mali toka Afrika ilitajirisha Ulaya na kuipa sifa kemkem. Sifa hizo zisingalikuwapo leo hii
isingalikuwa kutokana na mali na kazi ya watumwa toka Afrika. Mali hiyo iliwalisha wakoloni,
kujenga miji yao na hata kuwatajirisha sana. Mshairi anaeleza kuwa kabla ya ukoloni hata hiyo
Ulaya ilikuwa maskini. Hapa kunanakiliwa mifano ya ubeti wa tisa na kumi kufafanua maudhui
hayo.
9
Mama lau si wanayo, kupelekwa ugenini
Lau kwamba si maliyo, kubwakurwa mikononi
Hivi leo bara hiyo, iitwayo Ulayani
Ingekuwa haifani, na kupawa sifa mama
Ndiyo yaliyowalisha, na kutengenezeya huko
Miji wakasimamisha, kwa nguvu za mali yako
Lililowatajirisha, ni jasho la mwili wako
Na damu ya wana wako, ndiyo kuwa hayo mama
(Sauti ya Dhiki, uk. 37)
4.5.2 Kiburi na Utawala Mbaya
Kuna maudhui ya kiburi pamoja na utawala mbaya katika mashairi haya. Japo hivyo, swala hili
labainika zaidi katika shairi la ‘Kichu hakiwi ni uchu’ na lile la ‘Mamaetu Afrika. Katika shairi
la ‘Kichu hakiwi ni uchu’ mshairi anauliza ni nani aliyeambiwa yu mtu kwa kuwa na kitu.
Mshairi huyu anataja huo kuwa uongo kwani utu wa mtu kwa wenzake ndio kitambulisho cha
umuhimu wake. Hata kama kuna watu wengi walio na pato la juu, utu wao haupimwi kwa
kiwango chao cha pato bali kwa utu kwa wanajamii wenzao. Mshairi anatumia jazanda ya ndovu
akigawanywa vipande vitatu ili kuweza kufahamishana kuhusu utu. Mwili wa ndovu ni mkuu na
mwituni hana mfano wake. Kwa sehemu zote za mwili, umbo lake ni nono na la kipekee. Hata
65
kuna wanajamii ambao kwa ukuu wao huwaona wenzao kama ndovu aonavyo wenzake mwituni.
Yule ndovu huwahangaisha viumbe wengine pamoja na miti kutokana na uwezo wake mkubwa.
Huwahangaisha hadi kuwatia mbioni wakihofia kuumizwa.
Kuhusu kiburi, nafsineni anazungumzia watu ambao hujisifia nguvu zao kwamba wao huweza
kuvutana hata na watu mia. Hujidai kuwa hata watu hao wakiungana kumvuto kwa pamoja
hawamwezi kutokana na uwezo wake mkubwa. Ndovu (mtu) kama huyo hung’oa miti na pia
kuangamiza wenzake kwa teke na pia kwa pumzi zake. Mtu kama huyo vilevile hujivunia
thamani au sifa zake zinazojulikana pembe zote za dunia mjini na vijijini na kumfanya
kutambulika. Yule ndovu pia ana pembe ambazo huuzwa mnadani kwa bei ghali hivyo uwezo
wake huwa ni si haba.
Mshairi anazidi kusisitiza ule mfano aliotoa wa ndovu ambaye ana uwezo kama vile ukubwa na
thamani kuu. Kila mtu kwa hivyo hutafuta uwezo kama huo na akiupata huringa na hata
kufurahi hadi magego kuonekana. Mshairi anatamaushwa na kuwa hata mtu ambaye
anamrejelea kama ‘mnyama mwitu’ akipata uwezo kama huo unaosifiwa huchukuliwa kuwa mtu
mzuri. Hata hivyo, anasema kuwa hata mtu mjinga seuze mwenye akili hafai kukubali kuwa
uwezo wa mtu mbaya waweza mfanya mzuri. Rafiki mwenyewe akiambiwa mambo kama hayo
atayapuuzilia mbali na kuyaona yasiyo na mashiko.
Mshairi ameonyesha maudhui ya utawala mbaya katika shairi la ‘kichu hakiwi ni uchu’ na pia
‘Mamaetu Afrika.’ Mtu mwenye nguvu anatawala kwa makonde na mabavu (ubeti wa 40).
Wanaoongozwa hulazimika kwenda mbio kwa kumuogopa kiongozi kama huyo. Kuna pia
matumizi mabaya ya nafasi au uwezo. ‘Ndovu’ huyo apandwapo na ghadhabu huviharibu hadi
kuviangamiza vitu vyote. Huviharibu hadi kuviangamiza vitu vyote vilivyo karibu naye kama
vile kulaza mwitu, manyasi na miti yake. Jazanda hizi ni mifano ya watawala wenye nguvu
kuwaangamiza na kuwanyanyasa walio wengi katika jamii na ambao wako kwa madaraja tofauti
ingawa huangamizwa na ndovu mmoja tu. Hapa napo pameonyeshwa ubeti huo wa arobaini:
Na kwa wa nguvu upande, ‘tawaleza pasi shaka
Iwapo ni wa makonde, na mabavu kutumika
Watu iwe mbiyo wende, kwa kucha kuzidirika
66
Vifenene kadhalika, viumbe viwili hivi
(Sauti ya Dhiki, uk. 87)
Utawala mbaya katika shairi la ‘Mamaeta Afrika’ unahusiana na ukoloni mamboleo. Wakoloni,
licha ya mapambano dhidi yao yaliyofanywa na Waafrika hadi kufaulu hawakukata tamaa ya
kupata walichotamani Afrika. Walianza kuwatawanya Waafrika ili waendelee kuwatumikia.
Wakawatumia baadhi yao kama vibaraka waliorudi Afrika kuiba kilichobaki na kukipeleka
ulaya. Hao vibaraka ndio huleta michafuko ya kisiasa kwani adui amewanunua. Hata hivyo,
mshairi anasema kuwa watapata masumbuko kwa haya wayatendeayo bara lao. Nafsineni na
Waafrika wenzake wanaendelea kuungana walinde bara lao ingawa vibaraka hawana nia moja na
wao. Hao wanachukua rasilimali za kiafrika na kuziuza kirahisi hadi kuivunjia Afrika hadhi. Huu
ni ubinafsi unaoishia kuporomosha chumi zetu.
4.5.3 Maudhui ya Ukombozi
Maudhui ya ukombozi vilevile yanabainika katika mashairi haya. Haya yanachochewa zaidi na
ukoloni pamoja na utawala mbaya ambao tayari umetolewa maelezo. Katika shairi la ‘Wasafiri
tuamkeni’ nafsineni anawahimiza wanajamii wenzake ambao anawataja kuwa wasafiri
wasichoke wala kuwa dhaifu ingawa safari yao ni ndefu. Anawataka pia waondoe hofu kwa
kuwa huu ni mwanzo tu wa safari yenyewe. Kinachosababisha maudhui ya ukombozi kuonekana
ni taashira ya bendera katika ubeti wa pili. Kwa kawaida bendera huashiria uhuru. Wanajamii
hawa wanausaka uhuru wao. Nafsineni kwa hivyo anawataka wasonge mbele na wasianguke
hadi wafikie mlima mbele yao na pale kileleni waitundike bendera.
Mshairi anazungumzia ugumu wa safari hivyo kuwataka kuwa na stahamala. Anataja jazanda ya
miiba yenye sumu akiwataka wenzake watahadhari wasianguke. Kuna pia misitu yenye miti
mirefu njiani iliyojaa wanyama mwitu. Kila mmoja kwa nafasi yake wakikiona kitu ni lazima
wakishike. Changamoto nyingine inayokumba mapambano yao ni bahari pana yenye kina kirefu
na mawimbi makubwa yenye nguvu ila anawahimiza wenzake wapambane hadi waivuke. Safari
pia ni ngumu na hatari lakini anawataka wasitishike kwani ni lazima waimalize licha ya urefu
wake.
67
Zaidi ya hayo, anawasisitizia ileile haja yao ya kuitundika bendera na hivyo hawafai kukata
tama, nia kutetereka au nyoyo kuvunjika. Zaidi kuna maudhui ya ushirikiano wa wanajamii wote
katika juhudi hizi za kupata uhuru au kujitawala. Waume kwa wake watakiwa kujifunga
vibwebwe kikamilifu na kuingia safarini bila kubabaika. Kujikomboa hakuhitaji kujilegeza wala
kutetemeka kwa kuwa haja ni kuimaliza safari yenyewe kikamilifu. Wanajamii wahimizwa
kutegemea mbinu fulani maalumu kama vile mwenye chake kujitwika, kupanga mistari na safu
na kushirikiana wana na wazee kwa mchanganyiko. Aidha kwahitajika wakitaka wasitake, walio
na afya wanyoshe miguu na vilema wabebwe na wanajamii wenzao.
Dhamira ya mshairi katika shairi hili kuanzia kwa kichwa cha shairi ni kuwazindua na
kuwahamasisha wanajamii wenzake kujitayarisha kwa safari yao ambayo ndio tu mwanzo wake.
Pia analenga kuwatanabahisha kuwa safari yenyewe ina changamoto tele kabla wafikie lengo lao
la kujikomboa. Mifano ya changamoto ni ugumu wa safari, njia yenye miiba, misitu na
wanyama mwitu na bahari pana yenye mawimbi makali. Pia analenga kuwakumbusha kuwa
wanafaa kutia bidii na makundi yote kuungana ili kumshinda adui yao anayepinga kufaulu kwa
juhudi zao.
Ujumbe tunaopata katika shairi ni chanya. Ni kuwa juhudi za kujikomboa hasa kisiasa (kwa
kutaja bendera) sio rahisi kwani ni safari ngumu na ndefu yenye changamoto tele na hata
upinzani mkali. Juhudi hizo huhitaji watu kujitoa, kuwa na lengo maalumu la kujua wanakoenda
(mlima ule) na hata kutia bidii. Aidha kwahitajika ushirikiano wa makundi yote ya wanajamii
kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Falsafa ya mshairi hapa ni kuwahimiza wanajamii kuwa kupata ukombozi au uhuru sio mchezo.
Ni safari ndefu yenye changamoto, matatizo na upinzani mkali. Kwa sababu hiyo, swala zima
haliwezi kufaulu bila bidii, ushirikiano na hata azma yenyewe ya kufaulu hatimaye. Kwa mantiki
ya nadharia ya uamilifu, Abdilatif anasifika sana kama mshairi mwenye maono yaliyokuwa
mwafaka kwa taifa la Kenya katika muktadha wake wa kiwakati kwani ilikuwa miaka michache
sana baada ya uhuru. Kwa maoni yake, aliona uhuru wa pili ambao ulikumbwa na dhuluma na
upinzani anaozungumzia katika shairi lake. Kwa sababu hiyo kulihitajika juhudi kabambe za
wanajamii wote ili kufaulu. Twaweza kukubali kuwa changamoto zilizokumba nchi ya Kenya
68
baada ya uhuru kama vile kisiasa, kiuchumi na hata kijamii hazikuwa rahisi kutatua na hata
hazingetandarukiwa na watu wachache kwani mkono mmoja haulei mwana.
Maudhui ya ukombozi yanazidi kuzungumziwa katika shairi la ‘Mamaeta Afrika’. Nafsineni
anasema kuwa baada ya bara Afrika kunyang’anywa mali na kukosa mtu wa kulitetea, Waafrika
walijitokeza kulilia bara lao. Wakati huo, ingawa walikuwa dhaifu na kuanguka chini
waliposukumwa, walisimama na kuwatia wakoloni mbaroni hadi kuwashinda. Ubeti wa kumi na
tatu unathibitisha hayo kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
Kwani siku hizo mama, twali dhaifu yakini
Mtu akitusukuma, twali kianguka tini
Sisi nao kusimama, na kuwatiya mbaroni
Ikawa haimkini, sisi kuwashinda mama
(Sauti ya Dhiki, uk. 37)
Wakoloni walipogundua mambo yaliwaendea vibaya walianza kutumia mbinu mpya ya kuvunja
juhudi za mapambano. Wakaanza kuwatenganisha Waafrika ili umoja wao ukiondoka waendelee
kuwanyanyasa. Hapo ndipo kuliwekwa mipaka ya maeneo na hata kutenganisha koo.
Kulitokea vita vya kumfukuza mkoloni. Taabu ilipozidi, Waafrika waliamua kuwaondoa kwa
njia ya silaha. Ingawa walikuwa mbalimbali na kila ukoo kivyake, wote kutoka pembe zote
walikaribiana, watoto kwa wazee wakaingia vitani. Kufa kupona walipambana hadi kukata
minyororo ya utumwa na Afrika ikawa huru. Hata hivyo damu nyingi ya Waafrika ilimwagika na
wengi kuaga dunia. Rasilimali nyingi pia zilitumika. Uhuru ulipatikana hatimaye. Walimshinda
adui hadi akalazimika kutoka. Kwa kuwa na tamaa ya kuendelea kuidhuru Afrika mkoloni
nusura adinde kuondoka. Licha ya uhuru kupatikana, mshairi anadokeza kuwa kuna maeneo au
mataifa ambayo wakati huo yalibaki utumwani. Mifano ni maeneo ya Afrika Kusini. Msumbiji,
Zimbabwe, Angola na Guinea- Bisau. Nafsineni anasema kuna matumaini yao pia kuwa huru
kutokana na mapigano kuendelea na kuungana kujitoa mhanga kwa lengo moja la kuwashinda
wakoloni hao.
69
Baada ya hapo, ukombozi ukafuatwa na majuto. Adui alipoona chakula kitamu kishamtoka
kinywani, alichanganyikiwa akakosa la kufanya ndipo akafikiri jinsi ya kukirudisha kwake. Hata
hufikiria kurudi ingawa huogopa mapambano. Ikiwa ni kuja mwenyewe au kutuma wanawe, ajua
kuwa hilo haliwezekani kamwe. Waafrika sasa hivi wanalinda bara lao usiku na mchana lisije
tawaliwa tena na wakoloni.
Mwisho kuhusiana na maudhui ni kuwa katika shairi la ‘kichu hakiwi ni uchu’ kunaonekana
maudhui ya fahari. Nafsineni anajivunia uwezo wake wa utunzi `wa mashairi kwa lahaja ya
Kimvita. Anageuza Kiswahili cha kigunya alichobambanya alivyoweza kuanzia ubeti. Kutokana
na ubahili, matajiri huibana mali yenyewe zaidi. Ile jazanda ya ndovu inafaa sana hapa. Nadharia
nazo zimezingatiwa ifaavyo. Kuhusiana na umuundo ni kuwa ujumbe katika mashairi haya
umehakikiwa kama ulivyo na likiwa swala la kifasihi. Chochote nje ya mashairi husika
hakikutiliwa maanani. Katika utafiti, ujumbe wa matini ndio uliozingatiwa katika uhakiki
wenyewe. Kuhakiki vijenzi vya Wahusika, ufundi wa lugha, muundo na maudhui kumeonekana
kuwa toshelevu katika kueleza mada inayohusika. Hii ni kwa sababu vipengele vyote vinavyofaa
kuchunguzwa kulenga uhakiki wa mashairi vinaeleweka. Mada nzima ilizingatia mashairi hayo
zaidi kuliko mtunzi au ulimwengu yalimochotwa.
Kwa misingi ya uamilifu ni kuwa kila shairi hapa limejengwa kwa vipengele hivi vinne ambavyo
ni muhimu sana na hata kimoja kikiondolewa hakutakuwa na shairi. Kazi ya wahusika kwa
mfano ni kupitisha maudhui pamoja na dhamira ya mashairi husika. Muundo wa mashairi
unawezesha kila wazo kupitishwa katika ubeti wake na vina na vibwagizo kudumisha mapigo
yafaayo ili kuivutia hadhira. Ufundi wa lugha katika mashairi nao ni njia ya kupitisha baadhi ya
maudhui kwa njia fiche na ufundi mwingine ukionyesha uwezo wa mshairi katika utunzi. Lugha
kama hiyo pia inaleta mvuto kwa hadhira kiwango kwamba kuelewa anacholenga mshairi
kunafaulu kirahisi. Kupitia maudhui aliyobuni mshairi ndipo tunaelewa msimamo wake na hata
falsafa yake kwa maswala hayo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
70
SURA YA TANO
MUHTASARI,HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Katika sura hii, mtafiti amejishughulisha na muhtasari wa matokeo ya utafiti kama yalivyoibuka
katika mashairi yaliyoteuliwa toka kwa diwani ya Sauti ya Dhiki. Vilevile, mtafiti ameangazia
manufaa ya utafiti huu na hali kadhalika matatizo yaliyokumba uhakiki pamoja na mapendekezo
ya utafiti zaidi. Kumetolewa mukhtasari wa kazi nzima kuanzia madhumuni, njia ya utafiti na
matokeo. Lengo ni kuonyesha uwiano au utofauti na maoni ya wataalamu mbalimbali
inapolazimu. Mfuatano wa vipengele vyote vilivyolengwa katika madhumuni umezingatiwa.
Mapendekezo pamoja na hitimisho ya mada husika yametolewa. Pengo la utafiti zaidi kulenga
mada husika au hata mahali pa utafiti limeonyeshwa hapa na pale inapolazimu.
5.2 Muhtasari wa Matokeo
Sehemu hii inatoa matokeo ya utafiti huu kwa kifupi kwa kuegemea madhumuni manne ya
uhakiki wa fani na maudhui katika mashairi ya diwani ya Sauti ya Dhiki. Madhumuni ya kwanza
ilihusu kutathmini jinsi malenga alivyotumia wahusika katika mashairi hayo, ya pili ikihusu
kuchambua ufundi wa lugha. Ya tatu ilihusu kuhakiki muundo na ya mwisho kufafanua
maudhui yaliyozuliwa na fani katika mashairi hayo teule.
5.2.1 Kutathmini Malenga alivyotumia Wahusika
Katika kuangazia madhumuni ya kwanza kuhusu malenga alivyotumia wahusika katika mashairi
teule ya Sauti ya Dhiki, ilibainika kuwa katika mashairi hayo kuna wahusika. Mifano ni nafsineni
na nafsinenewa. Kukabainika sifa za wahusika hao kuwa hasi na nyingine chanya. Pia
kukabainika mhusika zaidi ambaye ni Mwenyezi Mungu lakini sifa zake zikiwa chanya pekee.
Hata hivyo,hakukuonekana kitu chochote kisicho uhai ambacho kimetumiwa na malenga kama
mhusika wa shairi lolote. Pia mshairi hakuonekana kusemewa maneno aliyofaa kusema na mtu
mwingine. Ni bayana kuwa kila shairi lilionekana kuwa na wahusika. Shairi la ‘Ukamilifu wa
mja’ kwa mfano lina wahusika kama nafsineni, binadamu(waja) na Mwenyezi Mungu. Wahusika
hawa wametajwa kwa njia waziwazi katika shairi husika. Lile la ‘Mja si mwema’ pia lina
nafsineni, mja na walimwengu wanaozungumziwa. Katika mashairi haya mawili, wahusika hawa
71
ni muhimu sana na ni lazima wawepo ili ujumbe wa mshairi ufikie na kunata hadhira ifaavyo.
Ikiwa tunaweza kukubali maoni ya Ansani, hali ingekuwa hata potovu zaidi katika shairi la
‘Kutendana’. Wahusika wa shairi hili ni mwanamke na mwanaume ambao wanazungumza kwa
njia ya waziwazi na ambao sifa zao ni bayana. Ikiwa wahusika kama hawa si muhimu, basi
haitakuwa tofauti na kulitupilia mbali shairi zima. Hapa pia, hakuna kitu chochote kisicho hai
ambacho kimetumika kuwakilisha wahusika. Utafiti huu kwa hivyo umefaulu kuchukua
mwelekeo unaokinzana na yale maoni ya Kisia na Mwarandani pamoja na ya Ansani.
Kwa kulinganisha na mashairi ya Robert Frost, kuna mfanano na baadhi ya mashairi ya Abdilatif
Abdalla ingawa sio katika kikundi hiki cha mashairi yanayolenga wahusika. Mfano wa shairi
linaloonyesha mshairi mwenyewe akizungumza ni lile la ‘N’sharudi’. Hata hivyo, huyu ni
mshairi mwenyewe anayezungumza katika nafsi ya kwanza bali si watu wengine waliopewa
nafasi hiyo.
Zaidi ya hoja hizi, katika shairi la ‘Mja si mwema’ nafsineni anaonekana kutumia au
kuzungumza na sehemu ya mwili, yaani mkono wake akiutaka kuandika yaliyomsababishia
majuto. Kutumia sehemu ya mwili kama mhusika kwa kunena nayo kama binadamu ni jambo
ambalo halionekani mara nyingi katika mashairi na hata wataalamu waliotafitia wahusika wa
ushairi hawakutaja aina hiyo ya uhusika. Sababu ya nafsineni kuzungumza na mkono wake ni
kuwa amebaki kujiamini yeye tu baada ya waja wenzake kumponza na hata kutoaminika. Hali
kama hii inaoana na mashairi ya Robert Frost ambaye anaonekana kupambana na hali
tofautitofauti katika hisia zake. Hata Abdilatif hapa si tofauti kwani kuzungumza na mkono wake
ni sawa na kuzungumza na hisia zake mwenyewe (uzungumzi nafsia) kwani hapati mja
mwaminifu wa kuzungumza naye wakafaana.
Katika madhumuni haya ya kutathmini jinsi mtunzi alivyotumia wahusika katika mashairi yake,
kumebainika wahusika wa aina mbalimbali ikiwemo wa kike na kiume pamoja na Mwenyezi
Mungu. Wahusika wote wamefafanuliwa sifa zao barabara hivyo basi kueleweka kukawa rahisi
kwa hadhira. Wamepitisha ujumbe unaokaribiana na hali halisi ya maisha katika jumuiya jambo
linalofanya mashairi haya kuwa faafu katika kuiadilisha jamii inavyofaa.
72
5.2.2 Kuchambua Ufundi wa Lugha au Tamathali za Usemi katika Mashairi teule ya Sauti
ya Dhiki
Kuhusiana na mukhtasari kulenga tamathali za usemi na mbinu za lugha ni kuwa mashairi
yaliyohakikiwa yametumia mbinu mbalimbali za lugha ambazo zilibainika katika uhakiki huo.
Maoni ya Ngure (2014), kuwa fasihi bora yafaa kuwa sanaa inayotumia lugha ili kueleza maisha
na tajriba ya binadamu katika mazingira na utangamano na wenzake na hata kutuchorea taswira
ya uhalisia wa maisha ni jambo linalobainika baada ya kuhakiki mashairi katika sehemu hii.
Katika shairi la ‘N’shishiyelo ni lilo’ kwa mfano lugha imesukwa kwa kutumia tamathali kadha
za usemi hali inayosababisha hata hadhira kumhurumia nafsineni kwa yaliyompata. Akasema
ukweli ndipo akatiwa jela ili asirudi kusema ukweli huo tena. Nafsineni akapata yasiyoridhisha
kamwe swala zima likilenga ukweli wa maisha ya kila siku.
Mtaalamu huyo (Ngure) anaposema kuwa kutosheka tunakopata tusomapo kazi ya fasihi
kunatokana na ufinyanzi wa lugha teule au umbuji ni mawazo yanayokubalika na kudhihirika
waziwazi katika matokeo ya utafiti huu. Mtunzi wa ‘N’shishiyelo ni lilo’ amethibitisha mawazo
haya ya Ngure kwa kutumia ufundi wa urejeshi, istiara, kinaya , balagha, tashihisi na utohozi.
Mawazo haya pamoja na ya Senkoro yanapata mashiko katika uhakiki wa shairi hili. Ufundi na
tamathali hizi zote za usemi umeweza kulipamba shairi hili kikamilifu na hata kulipa nguvu ya
kufundisha na kuzindua jumuiya inayolengwa.
Swala moja ambalo ni bayana na mbalo watafiti waliotangulia kuhakiki diwani ya ‘Sauti ya
Dhiki’ hawakusisitiza ni lile la kibali cha kishairi. Hili limetiliwa maanani sana katika utafiti huu.
Uhakiki huu umebainisha waziwazi kuwa Abdilatif’ ametumia uhuru wa maneno ya kikale,
inkisari, tabdila, maneno ya kigeni, utohozi, kilahaja, mazida na hata kuboronga sarufi kwa
kiwango cha kupigiwa mfano. Matumizi ya uhuru wa kishairi ni mtindo ulio na mueneo kwa
wingi katika mashairi haya matatu. Inaonekana kana kwamba malenga ameegemea zaidi katika
uhuru kama huu au anaupenda sana. Matokeo yake ni kuwa ushairi wenyewe unaelekea kuwa na
mguso kwa mfano wa lahaja ya mshairi yaani Kimvita. Pia unasaidia kudumisha siri ya kishairi.
Mashairi yote yaliyohakikiwa katika madhumuni haya ya pili yananuia kuonyesha mgogoro wa
swala nyeti la kisiasa ambalo kama mshairi asingelitunga fumbo la jazanda na hata kutumia
uhuru kama huu wa kishairi, swala hilo lingemponza hata zaidi. Kwa njia isiyo ya moja kwa
73
moja kwa hivyo, akaamua kutoa ujumbe kwa hadhira iliyojumuisha hata wale watawala
waliomhangaisha.
5.2.3 Kuhakiki Muundo wa Mashairi teule katika diwani
Kuhusu uhakiki wa muundo, mashairi yaliyohakikiwa yameonyesha ukaribiano wa muundo japo
yana tofauti za hapa na pale. Uhakiki wa shairi la ‘Siwati’ umeonyesha limebuniwa kwa beti nne
zenye mpangilio wa mishororo unaolingana. Licha ya kuwa kila ubeti una ujumbe wake,
kibwagizo kimetumiwa kila mwisho wa ubeti jambo ambalo linasababisha muumano ufaao wa
beti hizo nne. Kuna muungano wa ubeti hadi ubeti.
Abdilatif’ kwa kutunga shairi hili la tarbia amethibitisha kuwa mashairi ya tarbia na mizani kumi
na sita kila mshororo yamestawishwa sana. Hata hivyo shairi hili limethibisha kuwa mashairi
mapokeo hayawi na urari wa vina na mizani pekee lakini ule wa vina waweza kuwa katika ubeti
mmojammoja kivyake kama ilivyo kwa shairi hili la ‘Siwati; kuna mguso wa kiusikivu japo kwa
kiwango fulani tu.
Uhakiki wa muundo tu katika shairi vilevile umeweza kupinga mawazo ya Quinn (1992:11)
kuwa mhakiki akitenga muundo na maudhui kwa azma ya uhakiki, ushairi huo hutawanyika kwa
mawazo yetu mpaka tutakapouunganisha tena upya. Imegundulika kauli hii ni potovu kwa kuwa
uhakiki wa shairi lolote lile utategemea lengo la mhakiki husika. Ikiwa lengo hilo ni kuhakiki
muundo peke yake basi jambo hilo litafanyika bila tashwishi. Haya ndiyo yalifanyika katika
shairi hili. Mawazo ya William pia yamepingana na uhakiki wa shairi hili. Alisema kuwa
muundo uliozoewa na wasomaji na wasikilizaji wa mashairi toka jadi ni ule wa mistari minne
kila ubeti na silabi zikiwa kumi na sita au nane nane kila kipande na vina vyenye utaratibu wa:
a b
a b
a b
b a
Yapingwa maoni haya baada ya kuhakiki shairi hilo la ‘Siwati’ kwa kusema kuwa mashairi
mengi kama hili lilivyo huweza kuwa na ukwapi wenye mizani nane, utao mizani tatu na
mwandamizi tano, yaani 8, 3, 5. Hali hii ni bayana katika ubeti wa kwanza mshororo wa tatu.
74
Zaidi ya hayo, wanamapokeo kama Muyaka Bin Hajji, shaaban Robert, Mathias Mnyampala na
Mwalimu Hassan Mbega waliposema kuwa ushairi wa Kiswahili ni tarbia yenye umbo la mizani
nane katika ukwapi na nane katika utao ni jambo ambalo utafiti huu umeonyesha kuwa si la
lazima. Massamba anashikilia msimamo huohuo kuwa utungo ufaao kuitwa shairi ni lazima uwe
na ulinganifu wa vina na mizani katika beti.
Katika uhakiki wa muundo uliofanywa hapa, Abdilatif’, licha ya kuathiriwa na washairi hao
waliotajwa ameonyesha kwamba vina vya kati vyaweza fanana katika ubeti mmoja lakini
kutofautiana na beti zinginezo za shairi lilo hilo. Hali hii ni kweli katika shairi la ‘Siwati’ kwani
ni tofauti kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kuhusiana na mizaniyasisitizwa kuwa arudhi ya
mizani sawa katika ukwapi na utao (8a, 8b) nayo ni sheria isiyokuwa ya lazima hasa katika kila
ubeti. Katika muktadha wa uhakiki huu wa muundo, Abdilatif amezingatia mizani chache katika
baadhi ya mishororo hasa anapozungumzia swala nyeti katika ujumbe mzima wa shairi lake
husika. Mfano ni katika shairi la ‘Siwati’ ubeti wa mwisho mshororo wa mwisho mshairi
anapotamatisha shairi kwa dua kwa Mwenyezi Mungu. Hapa anatumia mizani kumi na saba
kutofautisha na mishororo mingine ya shairi iliyozingatia mizani kumi na nane kila mmoja.
Mifano mingine ni katika shairi la ‘Leo ‘N’singekuwako’ mshairi alipotunga kwa mizani kumi
na sita kila mshororo lakini kumi na tano katika ubeti wa tatu mshororo wa tatu anaposema, ‘Na
taabu haondokewa, ‘ngenijiya niliko?’ Licha ya kuwa mshairi bado yu hai, anataja kifo chake
ambacho ni swala nyeti hivyo kutofautisha ujumbe huo na ule wa mishororo mingine katika beti
zote. Kuna mfano pia wa ubeti wa nne mshororo wa kwanza anaporejelea namna ambavyo
angeliliwa na jamaa zake ikiwa angeaga dunia. Sababu ya kutaja haya yote ni kuwa inapingwa
maoni ya wataalamu wa kimapokeo waliotajwa katika utafiti huu kwa kusisitiza kuwa ufundi wa
muundo wa shairi utategemea jambo analorejelea mshairi fulani maalumu.
5.2.4 Kufafanua Maudhui katika Mashairi Yaliyoteuliwa
Mukhtasari wa mwisho ni kuhusiana na maudhui ya mashairi ‘Wasafiri tuamkeni’, ‘Kichu
hakiwi na uchu’ na ‘Mamaetu Afrika’, katika uhakiki wa maudhui ya kisiasa, ya kijamii na
kiuchumi katika mashairi husika. Mifano ya maudhui ni dhuluma za wakoloni kwa Waafrika,
uporaji wa mali ya umma, kiburi na mengineyo mengi.
75
Katika shairi la ‘Wasafiri tuamkeni’ kwa mfano, nafsineni ana falsafa kuwa mapambano yoyote
ya kisiasa si lelemama. Anayalinganisha na safari kwa kuwa huenda yasichukue muda mfupi.
Mapambano yao yalihitaji kujitahidi na hata kuondoa hofu. Aidha, mshairi anaamini kuwa licha
ya jumuiya yake kupata uhuru wa bendera (wa kisiasa) bado wanahitaji kujikomboa kutoka kwa
madhalimu wa leo hii. Hadhira wasipotahadhari huenda wakadungwa na miiba yenye sumu au
hata kuumizwa na wanyama wa mwitu. Changamoto zote alizotaja mshairi ikiwemo kuikabili
bahari, urefu wa safari na zinginezo zingekabiliwa kwa ushirikiano wa wanajamii wote, watoto
kwa wazee. Katika ‘kichu hakiwi ni uchu’ nalo, nafsineni anasisitiza kuwa kamwe haiwezekani
utu wa mtu katika jamii ukipimwa kwa uwezo wake wa kiuchumi bali kwa utu wake wa kuwafaa
na kuwasaidia wenzake anaoishi nao. Hii ndiyo maana kamili ya utu. Katika shairi la ‘Mamaetu
Afrika,’ anaendelea kukumbusha hadhira kuwa bara lilikuwa na uwezo wa rasilimali kabla ya
kuporwa na wakoloni na hivyo kuwahimiza Waafrika wasikubali kudhulumiwa tena hata kama
uozo huo utafanywa na Waafrika wenzao walio na nia mbaya kwa bara.
Katika mashairi haya, mtunzi amefaulu kujumuisha mseto wa vipengele vya muundo kama vile
beti, mishororo minne kila ubeti, ukwapi, utao, mkarara pamoja na vina vya mwisho
vinavyotiririka kuzungumzia maudhui yenye mchomo, mnato na hata ushawishi mzito kwa
hadhira. Wanajamii wasiojua hali ilivyokuwa kwa mfano au hata nafasi yao katika juhudi nzima
za ukombozi wa kisiasa wanapata fursa nzuri kupitia mashairi haya.
5.2 Hitimisho
Hitimisho katika sehemu hii limefanywa kwa kufungamana na madhumuni ya utafiti. Kwa
kulenga wahusika, inakaziwa kuwa uhakiki kama huu una nafasi ya kutegemewa kuhakiki
uhusika katika mashairi mengine ya Abdilatif’ Abdalla na hata washairi tofauti ikiwa ni pamoja
na kupinga kikamilifu maoni ya wataalamu wanaoshikilia kuwa wahusika katika ushairi hawana
umuhimu mkubwa. Kwa maoni haya, yasisitizwa kuwa uhusika ni uti wa mgongo wa shairi
kama ilivyo kwa tamthilia, riwaya na hadithi fupi na hata kwa tungo za fasihi simulizi.
Katika muundo, mshairi amezingatia zaidi umbo la tarbia, ukwapi na utao na pia mpangilio wa
vina vya kati na nje uliokaribia kufanana katika mashairi yote yaliyohakikiwa na hata idadi ya
76
mizani kumi na sita kila mshororo. Hata hivyo, katika shairi la ‘Mja si mwema’, ametumia
ukwapi, utao na mwandamizi. Ieleweke kwamba muundo huu wa tarbia kutamalaki si hoja
kwani ufundi wake wa lugha unadumisha ujumi wa kutamanika katika mashairi yote husika. Pia
maudhui anayolenga ni tofautitofauti jambo ambalo linazidisha mvuto wa hadhira kwa mashairi
yote. Mafunzo au maadili nayo ni kemkem kutoka shairi moja hadi jingine.
Mshairi huyu vilevile anaonekana kufuata nyayo za washairi wenzake wa jadi ambao kwa
kiwango kikubwa walibuni mashairi yenye umbo kama lake. Kwa tathmini ya jumla ya washairi
kama mwalimu Sikujua, Suud bin Said al-Mamiry, Muyaka bin Hajji, Shaaban Robert na
Mathias Mnyampala, washairi hawa isipokuwa Shaaban Robert wamezingatia tarbia kikamilifu
katika mashairi yao. Mfano ni yale mashairi ya Muyaka ambayo umbo lake ni lile moja tu la
tarbia katika mashairi yote. Mnyampala vilevile katika Diwani ya Mnyampala amezingatia umbo
lilo hilo katika mashairi yake yote.
Zaidi ya hayo, ufundi wa kilahaja waonekana kudumishwa sana katika mashairi yote jambo
ambalo laweka ukweli bayana kuwa mshairi huyu athamini lugha ya kwao sana. Pia anaonekana
kuzingatia na hata kuutawala uhuru wake wa kishairi kwani kwa mashairi yake yote
yaliyohakikiwa na hata yaliyobaki, ni nadra kukosa mazida, inkisari, tabdila, kubananga sarufi na
hata maneno ya kale. Mshairi ametumia kibali chake hicho barabara katika mashairi hayo
yaliyolengwa kuhakiki matumizi ya lugha. Abdilatif’ ametumia maneno ya kigeni kwa uchache
sana katika mashairi hayo. Hata yale aliyotumia ni yenye chimbuko katika dini yake ya
Kiislamu. Hata mafunzo / maadili mengi anayotoa Abdilatif yamefungamana na mafunzo ya
Kiislamu. Hata hivyo, kule kurudia neon ‘Mungu’ kila wakati katika mashairi haya
hakukuchangiwa tu na imani ya dini pekee bali pia na msongo na matatizo aliyopata jela
ikiwemo kunyimwa vitabu vyote akaruhusiwa kurani na shashi tu.
Lugha inayotumiwa katika mashairi yote yaliyohakikiwa ni Kiswahili na inaeleweka kwa
wasomi wa lugha hii katika viwango mbalimbali. Uasilia wake ni wa kupigiwa mfano hasa kwa
Abdilatif’ kutumia lahaja ya kwao nyumbani. Ujumbe huu unaifikia na hata kuinata hadhira
barabara hasa kuhusiana na ujumbe unaofaa kupokelewa kwa njia ya moja kwa moja.
Panapoonekana kuwa na utata tu ni katika shairi la ‘kutendana’ kwa sababu kuwa swala zima
pale ni mvutano wa kijamii (wa mume na mke) pamoja na tabia mbovu za mume. Kwa kawaida
77
swala hili halisemwi kwa njia ya hadharani kikamilifu. Hata njia kama hii ya kutunga shairi
inadumisha adabu na heshima kwani mambo yote hayasemekani waziwazi. Ingawa kwa tathmini
ya ubora wa shairi, shairi lenyewe ladumisha siri ya kishairi, mshairi/ nafsineni kusema ‘nyege ni
kunyegezana’ inaonekana kama ukosefu wa adabu au maadili hasa kwa wanajamii wenye umri
mdogo kama vile watoto.
Yasisitizwa zaidi kuwa mashairi haya ya Abdilatif’ ni ya kiwango cha kutajika kwani amefaulu
kuepuka lugha ya Kiingereza katika mashairi yake yote au hata kuonyesha uchanganyaji wa
lugha kwa kiwango cha kukinaisha. Mchango wake kwa hivyo katika fasihi ya Kiswahili ni wa
kutajika na wa kustahili wasomi kuhamasishwa kumuiga inapowezekana. Mshairi huyu, sawa na
Muyaka, Ali koti, Seyyid Omar bin Amir Zaid, Mngumi na Mwego Athumani waliohamisha
ushairi kutoka msikitini hadi sokoni, naye amezingatia au kutungia maswala kadha ya kijamii,
kiuchumi na kisiasa badala ya kidini peke yake.
Kuhusiana na maudhui, Abdilatif kwa upande mwingine ameangazia matatizo ya bara la Afrika
hasa kuhusiana na mapambano na wabeberu wa kikoloni waliotawala maeneo mbalimbali ya
bara hili. Anazungumzia tatizo la ukoloni mamboleo pamoja na juhudi zinazolazimu kufanywa
ili kupambana na tatizo hili. Haya yamezingatiwa katika shairi la ‘Mamaetu Afrika’ huku akitaja
kinachofaa kufanywa na wazalendo wa kiafrika ili kuzuia wakoloni kurudisha dhuluma hata
baada ya wao kuondoka.
Hapa imedokezwa kuwa mshairi ametoa mchango muhimu sana katika mashairi yake haya.
Amefaulu kuwakilisha ukweli wa maisha ya watu ambao amewazungumzia katika mashairi
haya. Ujumbe katika mashairi kama vile ‘Ukamilifu wa mja’ ‘Mamaetu Afrika’ ‘Mja si mwema’
na hata ‘Kichu hakiwi ni uchu’ una nguvu na uwezo wa kuleta mapinduzi katika maisha na fikra
za watu kwa faida yao wote.
Kwa upande wa nadharia zilizoongoza utafiti huu, ni bayana kuwa kuhusiana na umuundo,
vipashio vyote vya muundo wa mashairi haya vimeunganishwa kwa njia yenye mvuto wa
kutosha na hata muwala unaokubalika katika ushairi wa kimapokeo. Utendaji kazi wa kila
78
kipashio nao kwa kuhusisha na nadharia ya uamilifu ni mwafaka kwani kila mojawapo
chaonekana kutekeleza jukumu lake barabara.
Kwa upande wa pili, inasisitizwa kuwa hakuna kizuri kisicho na ila kwani si kila alichofanya
Abdilatif katika mashairi haya kinachoweza kusemekana kuwa cha kiwango tambulika. Ni
bayana kwa mfano kuwa shairi lake la ‘Kutendana’ ni refu na lenye beti nyingi zaidi kiwango
kwamba urefu huo unaathiri kueleweka kwa shairi lenyewe na hata ufaafu wake katika kupitisha
maadili kwa njia ya waziwazi.
Hata kama shairi lenyewe linaangazia kuzinduka kwa mwanamke hadi kutetea haki zake, shairi
kama hili lingeandikwa kwa beti chache kuliko hali ilivyo hapa ili ujumbe kama huo hata uifae
jamii / hadhira lengwa kwa mguso zaidi. Mshairi pia ameruhusu mhusika mmoja kutawala beti
nyingi zaidi hata kabla ya mwenzake kutoa ujumbe wake. Hali kama hii inamzuia msomaji
kufuata muwala wa kadhia nzima kutoka kwa beti zilizotangulia.
Katika shairi la ‘Mja si mwema’ nalo, mshairi ametilia chuku sifa za mja kwa kusema kuwa ni
mja mmoja tu kwa mia asiye mbaya kundini. Jambo hili linakosolewa kwa kuwa ni mshairi
mwenyewe aliyejiponza kwa kuamini ‘mja’ bila uangalifu. Afaa kujilaumu badala ya
kuwalaumu waja wote na pia asisahau kuwa baniani mbaya kiatu chake dawa. Waja wote
hawawezi kuwa wabaya kiwango anachozungumzia mshairi huyu. Hata hivyo, shairi hili ni
muhimu sana katika kutoa elimu kwa vijana au watoto ambao watarajiwa kuwachuja watu wa
kutangamana nao kwani baadhi waweza kuwachafua tabia. Hawafai kungojea hadi wahasirike
kisha wajute kama alivyofanya mshairi.
Katika shairi la ‘Ukamilifu wa mja’ nalo sifa za mja zimewekwa bayana kikamilifu yaani upande
wake mzuri na mbaya. Jambo hili nalo latuwezesha kufahamu tunachofaa kutarajia katika
uhalisia wa maisha yaani kutarajia mazuri na hata mabaya kwa mja. Kule kulinganisha sifa hizi
na za Mungu nako kunampa mja matumaini kuwa inawezekana kuiga sifa nzuri kwa Muumba.
Hata kwa muundo, mshairi ameonyesha udhaifu wa kutegemea tarbia katika mashairi yote ikiwa
kwaweza kuwa na miundo zaidi. Hata hivyo, uhakiki wa mashairi umebaini kuwa yana mseto wa
79
mawaidha, maswala ya dini, siasa, historia, uvumilivu na hata utamaduni. Kwa upande wa
ufundi hasa bahari za mashairi haya ni chache sana. Imekuwa nadra kuonekana pindu, msuko na
hata mtiririko. Pia katika baadhi ya mashairi, isipokuwa kwa kutumia kilahaja, ujumbe
unaeleweka kwa njia rahisi zaidi kuliko katika mashairi ya watunzi kama Muyaka au hata
Shaaban Robert. Sehemu hii yahitimishwa kwa kusema kwamba mtafiti yeyote wa ushairi ako
huru kuzamia mada kama vile matumizi ya fasihi simulizi katika fasihi andishi hata akilenga
sampuli zizi hizi za mashairi zilizohakikiwa hapa.
5.3 Mapendekezo
Baada ya matokeo na mukhtasari wa utafiti huu, kwanza inapendekezwa watafiti kulenga
kipengele cha uhusika katika mashairi. Pengo linalobaki baada ya kuhakiki uhusika katika
tasnifu hii ni kuwa kuna mashairi yaliyobaki katika diwani ya ‘Sauti ya Dhiki’ bila kuhakikiwa
kipengele hiki. Hata yale yaliyolenga vipengele tofauti kama lugha, muundo na maudhui
yanaweza hakikiwa baadaye yakilenga kipengele hiki hiki cha uhusika.
Zaidi ya mapendekezo hayo, kuhusiana na madhumuni ya kuhakiki tamathali za usemi au mbinu
za lugha, kwatolewa mwanya wa utafiti na hata uhakiki zaidi katika mashairi yayo hayo
yaliyohakikiwa mradi utafiti kama huo unuie kuhakiki maudhui, muundo au swala jingine lolote
bora lisiwe lililohakikiwa katika tasnifu hii. Watafiti zaidi wanaweza pia kuhakiki mashairi ya
diwani husika wakilenga ufundi wa lugha na hata uhuru wa kishairi. Hayo nayo yawe ni mashairi
yaliyobaki bila kuhakikiwa katika utafiti huu.
Hata kulenga maudhui, mashairi yaliyolengwa katika sehemu hiyo au mengineyo katika diwani
husika yanaweza hakikiwa ingawa kwa sharti moja kwamba uhakiki kama huo utachukua
mkabala tofauti na umuundo au uamilifu na hata ikiwezekana mada tofauti.
80
MAREJELEO
Abdalla, A. (1973). Sauti ya Dhiki. Nairobi : Oxford University Press.
Abdulaziz, M. H. (1979). Muyaka, 19th Century Swahili Popular Poetry. Nairobi: Kenya
Literature Bureau.
Ahmed, N. (1997). Mwangaza Wa Kiswahili. Nairobi-Kampala: East African Educational
Publishers.
Alembi, E. B. (1999). Understanding Poetry.Nairobi: Acacia Stantex Publishers.
Amana, B. (1971). Malenga wa Vumba. New York: Oxford University Press.
Davin ,D. and Wamuhu ,P. (1989). Enjoying Poetry. London: Macmillan Press Limited.
Emenyonu, E.N (edt). (2006). New directions in African literature. Nigeria PLC Ibadan:
Heinemann educational books.
Farouk, M. T (Mh). (1971). Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili. New York: Oxford
University Press.
_____(1977). Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili. London: Oxford University Press.
Freadman & Miller. (1992). Re-thinking theory. Cambridge University Press.
Glazer,M.(1996).’’Functionalism’’www.utpa.edu/faculty/mglazer/Theory/fuctionalism.htm-
06.02.2012-9.10am
Glencoe. (1976) . Literrature: The readers choice. U.S.A: MC Graw Hill.
81
Gromov, M. D. (2006). “The question of Kiswahili Style Again?’’ The Poetry of Kithaka Wa
Mberia in Kiswahili: Jarida La Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Juz 69: 109 – 126.
Holman, H, Harmon, W. (5th Edition). (1986). Ahandbook to literature. U.S.A: Macmillan
Publishing Company.
HURIA, (2007). Journal of the Open University of Tanzania, Volume II, No.2, Dar es Salaam.
Indende F. (2008b), Mabadiliko Katika umbo la shairi na athari zake katika ushairi wa
Kiswahili Swahili Forum Journal, 15: 73 – 94.
Jim,R.(1965).Understanding poetry. London: Heinemann.
Kenneth, Q. (1992). How literature works. The Macmillan press ltd.
Kothari, C. R. (2011), Reseach Methodology, Methods and Techniques. New Age International
Publishers.
Kuhenga, C. (1977). Tamathali za usemi. Nairobi: East African Literature Bureau.
Lauri R, Breman, P (eds). (2008). The heritage series of black poetry,1962-1975. U.S.A: Ashgate
publishing ltd.
Lawrence, A. & Brenda ,T. (2009). The literature review.U.S.A: Corwin Press.
Leitch, Vincent, B. (ed)(2010). The Norton Anthology of Theory and criticism 2nd edition. New
York: W.W. Norton and Company.
Maina, K. (2013). ‘‘Uchanganuzi wa lugha na itikadi za mamlaka ya kijinsia katika nyimbo za
harusi kutoka jamii ya Wakikuyu wilaya ya Kirinyaga.’’ Tasnifu ya M.A ya Chuo Kikuu cha
Egerton.
82
Mathooko, J. M, Mathooko, F. M, Mathooko, P. M. (2007). Academic Proposal Writing: A
guide to preparing proposals for academic research, UMU Press.
Msokile, M. (1993). Misingi ya uhakiki wa fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.
Mugenda, O.M. na Mugenda, A.G (1999). Research methods: Quantitative and Qualitative
Approaches. Nairobi. Act Press.
Mulokozi, M. M (Mh). (1999). Tenzi tatu za kale. TUKI: Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam.
Musa, M. & Omari, S. H. (1977). Tujifunze Mashairi. Nairobi: Macmillan Educational
Publishers Ltd.
Mwamzandi I. Y. (1996), Mbinu za kimaigizo katika tungo za Abdilatif Abdalla, M. A thesis,
Egerton University.
Mwihaki A. N. (1998), Phonetics and the stylistic appreciation of Kiswahili verses in Kiswahili:
Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Juz 61:74 – 78.
Njogu K. na Nganje D. K. (2006), Kiswahili kwa vyuo vya ualimu, J. K. F.
Ong’ang’o G. O. (2002), Nyota elekezi ya ushairi, Frajopa printers mall, Nairobi.
Podis A. L & Podis M. J. (1984), Writing: Invention, form and style, Scott Foreman and
Company, Glenview, Illinois.
Richards, J. C & Rodgers T. S (1986), Approaches and methods in language teaching: A
desription and analysis, Cambridge University Press.
Senkoro, F. E. M. K. (1982). Fasihi. Dar es Salaam: Press and publicity centre.
83
_ (2007). Lugha na fasihi ya Kiswahili Afrika mashariki. Dar es Salaam: CHAKAMA.
Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha fasihi simulizi na andishi. Nairobi: Focus Publishers
Limited.
Wamitila, K. W. (2003), Kamusi ya Fasihi, Istilahi na nadharia. Nairobi: Focus Publication Ltd.
Wanyonyi M. M. (2010), “Style and meaning in funeral oratory : The Case of Babukusu
Khuswala Kumuse”. Unpublished M. Phil Thesis, School of Arts and Social Sciences, Moi
University.
The Journal of Pan African Studies, Vol. 2, no.8, March 2009.
Rubanza, Y. I. (1997), “Dhana ya Uradidi katika Kiswahili” in Kiswahili: Jarida la Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili. Juz 59: 53 – 56.
Wisker, G. (2005). The good supervisor : Supervising postgraduate and undergraduate research
for Doctoral Theses and Dissertations,Palgrave Macmillan.
84
VIAMBATISHO
KIMBATISHO A
Kutendana
MWANAMUME
Kama bure utanipa, nipa sinisimbuliye
Kama hutaki “takopa, nikulipe baadaye
Hivi sasa cha kukupa sina; kweli nikwambiye
Mtu huwa hakutupa, amfaaapo mwenziye
MWANAMKE
‘Sina’ Kila siku ‘sina’, ‘Sina’ kwako i maisha
Huna siku utanena :ninacho ‘kanirambisha?
Hiyo ‘Sina’ yako Bwana, sasa ishanichokesha
Nyege ni kunyegezana, kwangu huba zinkwisha
MWANAMUME
Nnatoka nitokako ,mwendo kiguu na ndiya
Sikujali masumbuko, ya mvua kuninyiya
Mwenzi wako nina mwako, tafadhali niridhiya
Nipa kwa hisani yako, wata kunisimbuliya
MWANAMUME
Rudi kuko utokako,siniletee udhiya
Tafutia mwako wako,ndiya ya kutoleya
Mimi ndiye jaa lako,takazo kunitupia?
Mwanamume nenda zako,sina n’takalosikia
MWANAMKE
85
Laiti kwamba wajua,uhisivyo wangu moyo
Laiti ungetambua, niumiavyo mwenziyo
Kattu hungenisumbua,na kunifanyia choyo
Ndiwe wa kuiyondoa,hii dhiki niliyo nayo
Mwenziyo n’nalemewa, si dhihaka n’semayo
Sina pa kwenda itowa, hii hamu nilonayo
Na hata wewe wajuwa, kwamba sina badaliyo
Ni mgonjwa nauguwa, na dawa yangu ni hiyo
MWANAMKE
Kila mambo naelewa, yaliyo ndiyo na siyo
Si mwana wa kuhadawa, khaswa kwa unambiyayo
Japo wasema ni dawa, sikupi ngakuwa nayo
Na kama yatakuuwa, kufa kwa maradhi hayo
N’ilishakupeleleza, hata n’kakubaini
Muda pesa ukijaza, humo mwako mfukoni
Huanza kujikikimbiza,na kunigura nyumbani
Ngapita kukuuliza,uliko hujulikani
Ukisha kuzimaliza, kutolibakisha peni
Ndipo ndiya huongoza, hadi kwangu mlangoni
Na kuanza kujiliza, n’kuonee imani
Leo sitakusikiza, hata unganambiyani
MWANAMUME
Amma um’badilika , hu tena kama zamani
Waniona nadhikika hutaki kuniauni
Mwenziyo naatabika, hunionei imani
86
Hufanyi hafarijika, hatowa pepo kitwani?
Waniwata nateseka, hali ni wako mwendani
Huwati hafarijika, haondosha tabu hini?
Jambo la chache dakika, bure nyonda wanikhini
Nipa nipate ondoka,nikuondokee matoni
MWANAMKE
E mtu mume ondoka, sin’etee kisirani
Hilo ambalo wataka, kwangu halipatikani
Ni bure utasumbuka, sikupi ungasemani
Usidhani ni dhihaka, nisemayo ni yakini
Usemayo ni hakika,si urongo aswilani
Ni kwa kuwa nnachoka,kukufanya mhisani
Ndipo n’kabadilika, hakutowa maanani
Mjinga ‘meerevuka,mwerevu u mashakani
Pepo aliyekushika,mimi anikhusiyani?
Kumtowa ukitaka, nenda naye kilingeni
Mimi sitashughulika, kumpunga pepo duni
Tafuta pa kumpeka, pepo wako masikini
Kwa huyo unakopeka, pesa zako mwafulani
Na leo kuko geuka, nenda akakuauni
Apate kukutunuka, akuondowe tabuni
Sikubali kusumbuka, na faida siioni
MWANAMUME
Zako sijaziafiki, jawabu za ukaidi
87
Ungazijibu sichoki, na wala nyuma sirudi
Kwa sababu n’na dhiki, nami kwako sina budi
Ni kweli kwamba hutaki, au ni yako inadi?
MWANAMKE
Hata usipoafiki, huo si wangu muradi
Lako halitimiziki, leo bwana hufanidi
Mzito hutukuliki, mno n’najitahidi
Kikwelikweli sitaki, ni heri kuko urudi
MWANAMUME
Tushakaa wewe nami,kwa siku tumbi nzima
Sijainuwa ulimi,kukueneza lawama
Baya kwako silisemi, la kukuudhi mtima
Leo unani na mimi, haja yangu kuninyima?
Mwenzangu huyatizami,twalotoka nayo nyuma?
Nyuma ungeangalia, toka twalipoanzana
‘Ngekumbuka mazoweya , na wema tulotendana
Ungejua ni vibaya, kunifanyia khiyana
Mwenzako nihururumiya,si vizuri kutesana
Siku zote twalokuwa, pamoja tukiwekana
Nili sijakutunguwa, kukwelewa ewe nana
Leo n’nafunukiwa,mahaba na mimi huna
Tamaa itakuuwa, iwa na hadhari sana.
MWANAWAKE
Wajuwa yake maani,ya la wama kutendana
88
Naapa n’na yakini,huyajuwi, hungenena
Lau ungeyabaini ,vilivyo haya maaana
Wallahi hungetamani, uso wako kwonekana
Fadhila ungekumbuka,hayano usingenena
Kwako mno’mesumbukoa, hayano, tena
kwa kila namna
Nikawa nakueleka, kana kwakwamba
mbwangu mwana
Hayo usingetamka, lau wajua maana
Hii kaa ukijua, kwako huba sina tena
Mizizi n’shaingowa ,hayawezi shikamana
Uwate kujisumbua, mi nawe tushatokana
Nilikuwa sina niya, nawe kukashifiyana
Kwani si yangu tabiya, maneno kutupiyana
Ni jambo nalitukiya, sipendi kuliona
Hishima kumuwekeya, kiumbe napenda
sana
Lau hungenianziya, singesubutu kunena
Kwakuwa ‘metanguliya, kunipaka baya jina
N’nakuwa sina ndiya, ela ni kujibizana
Siwezi kuvumiliya, kutukanwa nikiona
Na ambayo ‘takwambiya, sidhani waweza
kana
Kwani ni mambo sawiya, urongo ndani
hamuna
Urongo sitatumiya, kweli tupu tainena
Mwanamume huna haya, hunayo; kabisa
huna
MWANAMUME
Sikuja kukuandamiya, kwamba tuje
kuzozana
Na wala sikukujiya, tuje kuhutubiyana
Nililolifuwatiya, kitambo n’shalinena
Au unkusudiya, mwenzangu kunitukana?
MWANAMKE
Ungapandwa na hamaki, sitakuwata kuesma
Lile ambalo ni haki, kulisema ni lazima
Endaye tokoza nyuki, pana budi kumuuma?
Mwenzangu huswarifiki, si leo n’nakupima
Urongo sita tumiya,kweli tupu ‘tainena
Sikutaka kujinaki,kulipiga langu goma
Na wala sifurahiki, kukusimbuliya njema
Na kunyamaa ni dhiki, bure ’tajipa nakama
Unamtokoza nyuki, ndipo sasa akuuma
Unnitafuta baa, pasi kukuanza shari
Kwakuwa n’nakataa, haja yako kuikiri
Wasema n’natamaa, na kwamba nitahadhari
Wajuwa wajihadaa, hiliwajuwa vizuri
89
Hakika linniwasha, tamshi ulotamka
Sitaweza kuipisha, ila ulonibandika
Ndipo name najibisha, japo hili sikutaka
Na unnilazimisha, ya zamani kukumbuka
Naanza kukukumbusha, kama ushaghafilika
Ni habari ’takupasha, ambazo zintendeka
Nawe ’kiweza jibisha, unalo lajibika
Au iwa kukanusha, ambalo lakanushika
Nali hijikalifisha, kwamba nipate kuweka
Hifunguwa langu kasha, kila likihitajika
Nikawa nikikulisha, pamoja na kukuvika
Vipi wanambiya kasha, tama inishika?
Nikikusitarehesha, kwa kila unachotaka
Hikupa mema maisha, upate kufurahika
Hikupa cha kukutosha, chakula na cha
kukuweka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Ulikuja unkwisha, muwili untukuja
Ulikuwa untusha, uso unsawidika
Umbo likawa latisha, kwa
kukombokakomboka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Mno ukisikitisha, kwangu miye hakuweka
Hawa hikutononesha, nawe ukatononeka
Ndipo hakunenepesha, ukawa wanang’anika
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishik
Hawa ‘kijibidiisha, dakika kila dakika
Kila la kutangamsha, na furaha kukuweka
N’kawa hakusemesha, usipate ungulika
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
Mtu wewe hutanisha, zingapita nyingi nyaka
Un’jisahaulisha,ulivyonipa mashaka?
Mno unnikutisha, tabu zisoelezeka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Pesa ‘kinitumilisha,idadi isosemeka
Matumizi yasokwisha, ungiyapo na kutoka
Nazo kila zikikwisha, hikupa huku nateka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Raha ‘kikuonesha, kikupa unachotaka
Japo kwa kujidhikisha, upate kusitirika
N’lilo ‘kiliepusha, upate azirika
Vipi wanambiya kasha, tamaa innisha?
Hilo halikunichosha, siku moja sikuchoka
Wala sikukimwa; hasha! Na wala
kununu’unika
Bali ‘ kinifurisha,hiona wafurahika
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
90
MWANAMUME
Ewe wangu mliwaza, yote hayo yajihani?
Badili ya kunutuza, na kunitowa tabuni
Wazidi kuniumia, na kunitoma moyoni
Yaliyokwwisha jilaza, wayaamshiya nini?
MWANAMKE
Ndiwe uloyaamsha, mimi Siye niletaka
Siku tumbi zinkwisha, ‘mepata kuyatamka?
Kidonda‘menitonesha, ndipo name n’karuka
Kwamba menikokomosha,panabudi
kutapika?
Ilipoanza kunisha, akiba nilokiweka
Haanza kuviswafisha, vyangu vya
kudhamika
Mpaka mwisho langu kasha, likawa
linkauka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika
Vyombo vya dhamani tosha, rahani
nikaviweka
Kimoja sikubakisha, dhahabu na kadhalika
Vyote n’kavisozesha, upate kusitirika
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Rahani ikiviwekesha, bila kuwa na hakika
Itakayoniwezesha, kuvikomboa hitaka
Piya nikajasirika, haidhuru hitamka
Vipi wanambiya kasha, tamaa innishika?
Na hiyo vilipokwisha, vikawa vishasozeka
Hayo hayakunitosha, vingine nkajitweka
Hangiliya kukopesha, kwa n’naoaminika
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
Hapo hajirafikisha, kwa walio na maduka
Kwao hajiaminisha, wasinitilie shaka
Wakawa wanikopesha, kwa n’naoaminika
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
Kwa kucha kuwajulisha, deni hazitolipika
Nikawa nabadilisha, duka baada ya duka
Kote n’kajizungusha, hadi yakaamalizika
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
Deni zikanikondesha, kwa zilivyonizunguka
Afiya yangu ikesha, na muwili kunyauka
Zikawa zinikosesha, usingizi ngautaka
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
Wakawa wakinitisha, pesa zao wazitaka
Sizidi kuchelewesha, wazitaka kwa haraka
Au watanigikisha, mbele kwenye mashitaka
Vipi wanambiya kasha, tmaa innishika?
Kwa kutaka kuy’ondosha, japo nusu ya
mashaka
Nguo zangu hafungasha, niuze za kuuzika
Nipate kujiepusha, na deni zilonifika
Vipi wanambiya kisha, tamaa innishika?
91
Nguo sikuzibakisha, ela zisotamanika
N’kawa n’kijivisha, nguo zilizotatuka
Haya zikinionyesha, nde hishindwa kutoka
Kisha baada ya kwisha, tamaa in’kushika!’
Amma yanitekesha, hayo uloyatamka
Kwisha kunikorofisha, n’kawa ndaa nanuka
Leo wajisimamisha, na kuanza kupayuka
Ati wanihadharisha, tama innishika
Maelezo
Tangu hapo mwanamke, akisema kwa ukali
Na rangi ya uso wake, ikawa imbadili
Mwili umtetemeke, mkali ja pilipili
Kwa sababu ya mwenzake, alivyo
kumfidhuli
Ukali ulimzidi, palipotajwa tama
Na khaswa nyuma ‘kirudi, kwa maisha
walokaa
Hapo akaona hadi, mwanamume hajifaa
Ndipo akakosa budi, maudhiko kumjaa
Na kwa hakika laudhi, tamko la huyo bwana
Lavundiya mtu hadhi, kwa ajuwaye maana
Ni yupi mwenye kuridhi, mtu aje mtukana
Kisha hayo ayaridhi, bila yakujibizana
Mwanamume alituli, bibi alichokinena
Ameitunza akili, asikiza vyema sana
Huku nyuso zao mbili, zali zinlekeyana
Bwana asikiza kweli, ambayo asema nana
Mwamume alidhani, ni maneno ya dhihaka
Mwanzo hakuyaamini, bibi alokitamka
Hakujuwa mwa fulani, kamba mambo
‘megeuka
‘kionekana zamani, ‘tapata anachotaka
Hakuiona sababu, ya bibiye kumnyima
Itakwendaje muhibu, leo awe atagoma?
Hajapata kujaribu, maisha yetu mazima
Akawa taratibu, na kwenye moyo kusema
Hakuweza kukumbuka, japo kuwa siku moja
Ambayo ‘mehangaika, kuipata yake haja
Muda alipokipata, hakuwa ‘kipawa hoja
‘kitimiziwa haraka, bila ya kwambiwa ngoja
Alipokufunukiwa, dafule halifuniki
Katakata ‘mekatwa, hataki bibi hataki
‘kazidi mnyonge kuwa, maguu hayamshiki
Yu mgojwaauguwa, na mwenye twiba
hataki
Akija akiyapima, aloambiwa na mwana
Vyema akayatizama, kwa marefu na mapana
Bibi kweli maisema, urongo ndani hamuna
92
Toka mwanzo hadi tamma, kweli
inaandamana
Mate yakamkauka, akakosa la kunena
Angaa la kujibika, akatafuta hakuna
Hasira zikamushika, akakasirika sana
Moyoni akatamka : leo n’napatikana
Kwenenda pasi kujibu, maneno aloambiwa
Akaona kuba tabu, japo yote ni ya sawa
Kuondoka ni aibu, bila jawabu kutowa
Kwamba limpe jawabu, bongo akalisumbua
Bongo likamfunziya, maneno ya kujibisha
Ukavu akajitiya, na mato kuyakausha
Akajikosesha haya, tembe hakuzibakisha
Bibi akamlekeya, hayano akampasha
MWANAMUME
Vyema n’nayasikiya, yote uliyoyanena
Orodha ‘menipangiya, ya mambo kila
namna
Yote ‘menihisabiya, ulobakisha hakuna
Ni kweli ‘menifanyiya, moja siwezi likana
Basi kwa kutenda wema, ndiyo sasa
wauimba?
Hayo usingeyasema, ela kwamba wajigamba
Sikuja n’kasimama, mlango ya wako
nyumba
Kama ‘masikini mama’, na kuanza
kukuomba
Bure silete utesi, kwa hayo uyanenayo
Sikukushika kikosi, unitimiziye hayo
Ni yako mwenye nafusi, na pendo la wako
moyo
Mayowe nda nini basi, hayo unipigiayo?
MWANAMKE
Katika uhai wangu, sijapata kumuona
Mwinginewe mlimwengu,ambaye fadhila
hana
Wewe ndiye mosi kwangu, wala sitaona
tena
Naapa haki ya Mn’ngu ! kamawe sitamuona
Nikweli hukunijiya, ukaomba n’kufaye
Ni kweli hikufanyiya, kwa hiyari yangu mie
Na wewe ukipoyeka, kusudi tumbo lijae
Nilipo hikwegesheya, kwanini usikatae?
Maelezo
Dume hiyo kusikiya, bibiye aloyatamka
Kuona sasa vibaya, kooni yalimfika
Uso ukangiya haya, tunu akauinika
Akatamani kiliya, kwa aibu kumfika
Akangiwa na kidaka, mdomo kutofunguwa
Moyo ukampasuka, vipandepande ukawa
Akadangana hakika, kwa jawabu alopawa
93
Amma aliaibika, mpenda kuegeshewa
Vyema mpate elewa, dume lilivyohizika
Ni kama alovuliwa, nguo zikamuanguka
Yu tuputupu akawa, na hali anainuka
Huotama twaambiwa, bali ye aliinuka
Ikamjia akili, ya kubadili msemo
Akaona afadhali, ni kuipiga horomo
Kwani wake ufidhuli, anshatiwa kikomo
Ili kusudi anali, akatengeza mdomo
Kumrai akaanza, na huku akumsifu
Mno akamtukuza, kwa kila la utukufu
Ulingoni kamkweza, juu palipo parefu
Kusudi apate weza, kupawa kwa ukundufu
Si kwamba ‘kumdanganya, la! Sivyo! Hata
nusu
Maradhi yalimpenya, akawa yu mahabusu
Alobakisha kufanya, ni maguu kumbusu
Moyo asingeukanya, ‘ngejitiya hata kisu
Halafu akaingilia, mno kujisikitisha
Lau ungemsikiya, alivyo kujisemesha
Ungemsikitiya, sikitiko lisokwisha
Naye akiyatiliya, mahanjamu ya kutosha
Hakubakisha kusema, kila la kumtamkika
Na hapo akalalama, mwisho wa kulalamika
Kumweleza mwana-mama,tabu iliyomfika
Amuonee huruma, ampe analotaka
Akasema ‘mejaribu, kutafuta usingizi
Kusudi hii adhabu,ngaa inipe pumzi
Bali ikawa ni tabu, kufumbika langu ozi
Nipoza wangu tabibu, ni mgojwa sijiwezi
MWANAMUME
‘Mejaribu kila ndiya, halikutaka fumbika
Kila nikiliambiya, yangu halikuyataka
Mwenzangu nisaidiya, siniwate hateseka
Tabu yangu yakweleya, sivyo n’livyoshikika
N’nangaangaa mno, kitanda changu shahidi
Lau chasema maneno, ningefanya jitihadi
N’kakileta hapano, kikueleze zaidi
N’ondosheya tabu hino, nana usinikaidi
N’nahisabu boriti, moja baada ya moja
Kwamba nivute wakati, usingizi kuungoja
Sikuona tafauti, wala ishara ya kuja
Yomi n’siye bahati, n’saidiya mbeja
La kutenda n’kakosa, ‘ngetendani? Nambiya
Aseme kwa kugigisa, na sauti ya kuliya
Na mato kuyapepesa, yakawa kutotuliya
Shingo utadhani sasa, tini itaangukiya
Ela akazidi sema, wewe kukufikiriya
Hainuka hasimama, na kuiandama ndiya
N’liona ni lazima, mwenzangu
kukuandamiya
94
Basi huoni huruma, langu ukakubaliya
Itizame inyeshavyo, hebu itizame mvuwa
Hisi kitetemeshavyo, kibaridi cha kuuwa
Piya haja vivyo hivyo, kwa kuwa
nimelemewa
Basi nana hivi ndivyo, nenende bila
kupawa?
Maelezo
Una mambo ukosefu, ukitokusubiriwa
Hupa mtu kuwa pofu, kadhalika zuzu kuwa
Akajiona yu dufu, hafai kudhaminiwa
Akawa mtu dhaifu, hajiwezi ‘ngaonewa
Na hapa mtu kusema, yasiyofaa kusemwa
Za upuuzi kalmia, zake na za kuazimwa
Akaziona ni njema, kwanza zafaa ungamwa
Na kutojali hishima, yu radhi awe mtumwa
Bibi kusikiya haya, akalianguwa teko
Teko akamtekeya, lile lile la kimeko
Lililojaa kinaya, na sitihizai fuko
Ni mfano kumwambiya: kwangu mimi huna
lako
95
MWANAMKE
Mn’ngu akuzidishiye, uhodari wa uneni
Ili kusaidiye, kwa maisha ya mbeleni
Elakini kwangu miye, hauna tena dhamani
Hata lipi unambiye, kweli yeke siioni
Licha maneno matamu, ambayo waniambiya
Hata matozi ya damu, lau hayo utaliya
Hayawezi n’lazima, wewe kukuhurumiya
Uombe wako ugumu, upate kusaidiya
N’nani aliyeanza, kufanya mwende mjinga
Si wewe? Hebu nambiza, au urongo natunga?
‘ Mepata ulichoweza, nacho ushakibananga
Basi sikae ‘ kiwaza, kwamba kwangu utaunga
Maelezo
Ni kama jiwe moyowe, mgumu kulainika
Hata lipi uambiwe, hauwi kubadilika
Afadhali hilo jiwe, lipondwa hupondeka
Mwanamume ki mwenyewe, moyoni akatamka
Tamaa hakuikata, akazidi bembeleze
Akasema yalopita, ni bora kuyanyamaza
Kuliok kuyafuwata, na kisasi kulipiza
Yalopita yashapita, si vyema kuyaregeza
MWANAUME
Nayakubali makosa, niswamehe wangu nyonda
Nayatubu hivi sasa, uaminifu kuvunda
96
Nadhani hutaniwasa, mswamaha kuuonda
Mwenziyo radhi niwiya, nipa nafasi nyingine
Nitakudhihirisha, wewe mwenyewe uwone
Kwamba sitaendeleya, kutenda baya jingine
Kamwe sitakutendeya, tuketi tusikizane
Ni radha kukufanyayi, lolote ilisemalo
Piya kukutimiziya, kila lile utukalo
Haya na mfano haya, sitakataa liwalo
Na wewe niangaliya, sendi kinyume na hilo
Kumbuka tulivyokuwa, tukipendana zamani
Piya sasa kwangu iwa, ulivyokuwa mwanzoni
Natusiyatiye dowa, mahaba yetu mwendani
Ni mgonjwa niaguwa, nioneleya imani
MWANAMKE
Moyoni mwako nitowa, unifute n”siwemo
Mahaba n”shayatuwa,moyoni mwangu hayamo
Siwi wala sitakuwa, kama zamani; horomo:
Niwapo hivyo ‘takuwa, najitiya kwenye shimo
Sasa nihisabu kwamba, n’shakufa kwako wewe
Na kaburi ukatimba, nimo ndani nifukiwe
Siwe na haja kuomba, kurudiyana mi nawe
Kama waweza kuumba, umba mimi mwinginewe
Mimi nawe tuagane, wenende huko wendako
Wende kwa huyo mwingine, abebe mahaba yako
Asaa musikizane, ukapata farijiko
Sitakubeba vyengine, n’shafunguwa mbeleko
97
Labda si mimi tena, hili fahamu ujuwe
Sinite kwa langu jina, hirudiyana mi nawe
Na lau utaniona,mauti yanitukuwe
Kurudi huna namna, bure usijizuzuwe
Maelezo
Kila ye akiambiwa, wimbo huo siuwimbe
Yeye hujibu ya kuwa, n’taubakiza tembe
Hana la kumtopowa, ela huba za mpambe
Ndwee hii kuuguwa, binadamu ‘siombe
Juu ya jawabu hizo, si kwamba kuyarudiya
Hakutoshelezwa nazo, hakuona ‘mejibika
Ile ile yakwe nguzo, akazidi kuishika
Mfano wa hamnazo, akarudi kuropoka
Maneno yayo kwa yayo, akawa kuyarudiya
Tokeya maneno hayo, mtu ‘kiona nda ndiya
Hata mwisho masikiyo, yakachoswa kusikiya
Mwanamume ana payo, hawezi kujizuwiya
Akamtajiya pesa, mwanamume kazitaja
Kwamba ati toka sasa, na siku ambaazo zaja
Hatakuwa akikosa, kumtimiziya haja
Tena kilala anasa, atampa bila hoja
MWANAMUME
Zozote uzitakazo, ‘takuwa radhi kutowa
Zote ‘tazokuwanazo, kibindoni’ tafunguwa
Kila muda hipatazo, peni sitalinyotowa
98
Kwako nitakuja nazo, sitangoja kuambiwa
MWANAMKE
Ituze yako akili, ituze kama unayo
Si mali Bwana si mali, niliyo na haja nayo
Mahaba yangu ni ghali, na bei yake si hiyo
Kwangu tena huyanali, hata kwa bei iwayo
Hata lau yangekuwa, kwa pesa yanunulika
Na kwamba wewe ukawa, kuyanunuwa wataka
Yasingelinunuliwa, na mtu wewe hakika
Kwani’ngeliradhiwa, kaburini kuyazika
Maelezo
Zilikuwa zishapita, saa tano za usiku
Ni hapo alipokata, shauri la kuja huku
Dirisha akaligota, Ku! Ku! Ku! Ku! Ku! Ku!
Ili Bibiye kumwita, kwa kubwa mno shauku
Bibi ali mejinyosha, kitanda cha ukumbini
Taa aliirudisha, utambi ukawa tini
Kusudi kuliepusha, joto lisizidi ndani
Na piya halikutosha, kipepeo mkononi
Manukato muwilini, leso mbili ‘mejivika
Mpya ambazo dukani, leo zintoka
Nazo piya chetezoni, alikuwa ‘meziweka
Zafurahisha puani, harafu njema zanuka
‘Kimtizama kitwani, nyele zilivyotanika
Uzitizame na pini, jinsi alivyotomeka
99
Na shada la asumini, alivyo kulipatika
Lazima utatamani, ngaa upate zishika
Basi uje na shingoni, shingo mfano ya ninga
Ni mjuzi kwa yakini, huyo aliyeitonga
Ukitizame kidani, shingoni alojifunga
Sijuwi ni fundi gani, ambaye alikitunga
Liwa jembamba usoni, alikuwa ampaka
Akatinda na sikini, vizuri ikatindika
Nacho kijembe nyushini, hakikusahaulika
Umwonapo utadhani, si mja ni malaika
Na humo mwake matoni, ni wanda ameupaka
Ule wamda wa Mangani, mno unaosifika
Namo mwake midomoni, wekundu unzunguka
Si wa rangi Ulayani, ni mdaa kutumika
Vya dhahabu viungoni, vyombo amvipambiza
Kipini kimo puwani, kilipo kimpendeza
Vipuli masikiyoni, vyandani pete ongeza
Na bangili mikononi, kiyasi hakuzijaza
Kwa ufupi hakubaki, kwa mapambo kujiunda
Mpita hiyo twariki, angataka kujipinda
Moyo utataharaki, uwe ni mbiyo kumwenda
Na bila shaka ashiki, zitzzidi kumpanda
Ndipo hapo kusikiya, dirishale la chumbani
Hakuwa yakimeleya, aligotaye ni nani
Papale akabakiye, hakutukutika sini
Wala kusema ngojeya, au hivyo mathalani
100
Alipoona kwazidi, kugogotwa dirishani
Ikawa itambidi, kumuuliza n’nani
Agotaye kwa juhudi, huyuno ni mtu gani?
Jawabu haikurudi, ya kusema ni furahi
Basi alipoinuka, kwenenda kujioneya
Jito likamdirika, aliyemfahamiya
Baada ya shaka shaka, na vyema kutunguliya
Akaipata hakika, ndiye alemdhaniya
Kabla kumuuliza, asema aliojiya
Naye kabla kuweza, kunena alofwatiya
Kila mtu akaganza, mwenziwe kumngojeya
Na kila mato kuanza, yenze kuyakodoleya
Lilompa kungojeya, Bibi ‘kawa kutonena
Alistaajabuya, Bwana kujizusha tena
Nyezi nyingi zimesiya, tangu walipokutana
Aligura hata ndiya, hakuwa ‘kionekana
Akatafuta ni lipi, leo lilomrundisha?
Au yuwatoka wapi, hapo akajipitisha?
Na siku zote yu kupi, mbona alijihamisha?
Leo yankwenda vipi, kuja kwake akabisha
Bibi alivyo ‘mepanga, ndani mwa akili yake
Alitaka kulifunga, hilino dirisha lake
Kusudi mwenye kugonga, hapo pake aondoke
Ende pasi na kuzingza, atokomee na zake
101
Naye mume saa hiyo, akaona ni lazima
Haja yake alonayo, asifite kuisema
Aukaze wake moyo, amweleze mwana-mama
Na tumbi visingiziyo, vilivyompa kuhama
Ndipo hapo mvutano, ulipoanza mwanzowe
Utadhani mashindano, ya malenga mfanowe
Kila atowaye neno,’kijibiwa na mwenziwe
Ukawa ule mfano, wa ‘twaa’ na ‘twaa wewe’
Hebu msomaji wangu, ulipofika simama
Kaa tupige mafungu, haya mambo kuyapima
Tujuwe tama an tungu, la kumiza na kutema
Ukiyakubali yangu, kidogo turudi nyuma
Pili twangaliye saa, yalipotukiya hayo
Giza lali mesambaa, kwa mvuwa kuu inyayo
Hata zile nyingi taa, mbingu ziing’arishayo
Hata mojapo angaa, haikujitokezayo
Katika huu ubeti, nataka kukwelezeya
Giza ndiye afiriti, wa kukuza maasiya
Lingiyapo huzatiti, nyoyo zikayaendeya
Lenyewe halijifiti, kila mtu yamweleya
Ongeza na kibadiri, kilicho cha kuviviya
Hicho kinaposhitadi, na mfupani kungiya
Rafiki hukosi budi, pa joto kukimbiliya
Basi hapo si zaidi, kwa mwenye huu udhiya
Tatu hebu kumbukiya, manukato nilotaja
Bibi aliyojitiya, kuikusudiya haja
102
Naku yanavyonukiya, nuka tena mara moja
Halafuye niambiya, baadaye sasa ngoja
Nne timiza mapambo, bibi alojipambiwa
Fikiri vipi mrembo, ambavyonalitokeya
Lau angekuwa chombo, samaki angeshikiya
Yaswawiri haya mambo, n’nayodondoleya
Fikiri wewe mwenyewe, zi vipi ashiki zake
Sasa hayoyatukuwe, kwa la kwanza uyapeke
Yawake pamoja yawe, pamoja yakutanike
Ili kwamba uijuwe, mwanamume hali yake
Bila shaka taabani, haliye ilivyokuwa
Mbaya isiyo kifani, vigumu kuhadithiwa
Pima mwako akilini, huna haja kuambiwa
Kwani sitaweza sini, ‘ngataka fafanuwa
Sasa naturudi nyuma, pale twalipowatiya
Mke alipo kinena, ya pesa kuyajibuya
Tumsikize na Bwana, vipi aliendelea
Msikize vyema sana, ‘endeleyavyo kuliya
MWANAMUME
Un’tendavyo si vyema wala si haki mwendani
Na kweli n’kiisema, haya sikutumaini
‘Mejikosesha huruma, chache hunayo moyoni
Toba Yaa Rabbi salama, kiumbe n’nakoshani?
Natoseka kwa mvuma, ni chapachapa mwilini
Aua hivi ni muruwa, kusema kwa dirishani?
103
Mlango hebu funguwa, uwate ningine ndani
Ngaa nipate pumuwa, japo hutaniauni
MWANAMKE
Bwana jishikiya ndiya, rudi kuko utokako
Siwezi kufunguliya, siijali tabu yako
Wakatiwo ushasiya, kwangu hupati mashiko
Sina ‘talokutendeya, rudi ulikokuwako
Na hili n’kueleza, lipate kukueleya
Hapa sijicheleweze, hivi sasa n’ondokeya
Nina mtu n’kwambize, na miyadi ‘metimiya
Bwana usinivundize, usoweza nijengeya
Maelezo
N’na mtu ni tamko, Bibi alilotumiya
Lali kama mripuko, wa kombora nakwambiya
Tena kuripuka huko, liliporikiya
Liliripuka ambako, kwa asolitarajiya
Sivyo ambavyo aruke! Kwa kombora kuripuka
Mwaname moyo wake,jinsi ulivyo gutuka
Lau si bahati, kwenye kiguzo kiguzo kushika
Angeona kazi yake, lazima angeanguka
Mke kwisha kuyasema ,hayano maneno yake
Zaidi hakusimama,kutupa wakati wake
Ela alilisukuma, ‘kafunga dirisha lake
Akakomelea hima, na tumbuu yake
Kitendo hicho baada, kilipokwisha tukiya
Akasimama kwa muda, akizidi kungojea
104
Akifikiri labuda, Mwana ‘tabadili niya
Hakuiona shahada,ya alotumainiya
Kisha ‘kakata kauli, hapo kujiondokea
Mchofu kama hamali, mbebaji magunia
Enda huku kwenye mwili, mvuwa yamnyeshea
Guu mosi guu pili, huyo akasshika ndiya
Ndiya aliyoshika, nikueleza mwendani
Nindiya ya kumpeka, hadi kwa mishi nyumbani
Kwa huyo ndiyo kumbuka Bwana kipeka mapeni
Ndipo sasa akataka, enda akalipwa ndani
Akambwa nasitikika, nafasi sinayo Bwana
Na ambalo nakutaka, ni kutenda kiungwana
Anza sasa kugeuka, ndiya I swafi na pana
Mi nawe tulipofika, mbele hatwendi tena
Bwana hata hakuiweza, kusema neon liwalo
Akabaki kunyamaza, kama hakusikiyalo
Jambo alilofanyiza, ni kulitimiza hilo
Uso’we akageuza, lipa tena jinginelo?
Fulifuli mijitozi, enda huku yamtoka
Ndiya mbili mitilizi, ‘kawa yamminika
Sababu vyake vipenzi, vyote visha mgeuka
Yawaliya kwa simanzi, aliya adsikitika
Akazurura na ndiya, badala kwenda nyumbani
Ovyo akajilanginya, kote mabalabalani
Ni kama alopoteya, bado yu kuzururani
105
Mnong’ono kwa msomaji
Ndoo n’kunongo’neze, au tunoong’onezane
Nilonayo n’kweleze, ya maana tupanane
Ndoo kwangu jijongeze, sitaki kusilikane
Jifite sijitokeze, kwamba tusionekane
Hebu kweli niambiya, mi nawe tusifitane
Hivi ukiy’angaliya, haya waja watendene
Yupi alotenda baya, kumtendea mwingine?
Ni yupi mwenye hatiya? Usinifite mnene
Ni mwanamke wa kwanza, alejitweka ulezi?
Mwanamume ‘kamtunza, wakati hanayo kazi
Hilino alilofanya, lali ni la upuuzi?
Sidhani litakutanza, lenyewe li waziwazi
Ingawa sote twajuwa, mambo haya hutokeya
Lakini tukiyunguwa, kwaza kiutu tabiya
Alifanya sawasawa, dume kuliangaliya
Na hali huyo hakuwa, mwenzi wake wa shariya?
Na hilino neon zima , pia nalo n’julisha
Tushamwona mwana-mama, a’vyomsarhesha
Je alifanya vyema, mwendo kudadirisha
Mwenziwe kuja mnyima, alipomzoesha?
Kisha tizama na hili, mwanamke alotenda
Ni sawa huyu fahali, kwa bibi huyo kwenenda?
Akapewa maakul, nguo pamwe na kitanda?
Na yeye akakubali, moja basi kulikinda?
106
Je hivi ndivyo kiume, bwana alivyofanyiza?
Ni sawa kwa mwanaume, hivino kukilegeza?
Badalaye ajitume, japo kunazi kuuza
Kwa maguuye akwime, asipate kulombeza
Na hili liangaliye, unipe hukumu yake
Kati yao afaaye, kumweka mwenzi wake
Ni mke awekwe yeye, aula yeye awekw?
Angaliaunambiye, lifunuwe lifunuke
Lifuwatalo lipime, tena vizuri kabisa
Waone ni wanaume, amaye ana makosa
Kwa kurudi amuume, aliye akijiasa
Ajili amtizame, tabu ‘siwe kumgusa?
Wakati alipokuwa, hana mbele hana nyuma
Sote piya tushajua, alionewa huruma
Vyema akapokelewa, na huyuno mwana-mama
Kwa kila kitu kupewa, na vyema kumtazama
Aliponafasikiwa, kuanza kuwa na chake
Alivyafanya ni sawa, kumpiga mwende teke?
Na kusahau ya kuwa, ndiye mfadhili wake?
Afaa kuhukumiwa, kumuhuni mwanamke?
Na mwisho ni huyu mishi, alotenda tushaona
Kwa kumuiza bilashi, alipomwendeya Bwana
Uweke kando ubishi, alitenda kiungwana?
Usiwe mlalamishi, sitaki lalamishi
Alitenda kiungwana, kumkataa ghafla?
107
Na hali vya huyu bwana, ni yaye alo ‘kivila?
Halafu vili tena, kuzisahau fadhila?
Tafuta yakwe maana, uyajibu masuala
Mwisho wa hayano yote, nitowe yangu maoni
Singetaka n’kufite, yaliyo mwangu moyoni
Kwa hivyo sasa niwate, n’kupe wangu undani
Kwangu mimi hao wote, nawatiya makosani
Si huyu Mishi baini, mkukutaji mwenzake
Wala si la samahani, hilo jenginewe jike
Na wala dume, ‘sidhani, tamuwata aondoke
Wote wamo makosani, kila mtu kosa lake
Na ambavyo nawaona, watendaji hivi visa
Wantafauiyana, kwa kadiri ya makosa
Yuko aliyekazana, kidogo akayagusa
Wako walozidiyana, na alozidi kabisa
Sasa palipobakiya, ni pako si pangu tena
Kazi n’takuwatiya, tuwe kusaidiyana
Hili ukiliridhiya, anza bongo kulikuna
Upate kunifanyiya, hii kazi ‘tayonena
Hawano watu watatu, walopatwa na hatiya
Muhukumu kila mtu, kulingana na shariya
Siwe kuogopa kitu, na wala kupendeleya
Wala ‘sidhulumu mtu, wala kumhurumiya
Sisemi kadiri gani, ya makosa walonayo
Sitakwambiya Fulani, afaa hukumu hiyo
Sikwambii aswilani, haya ya makadiriyo
108
Tafuta yako mizani, ya kuyapimiya hayo
Patoosha n’lipofika, hapa ndipo ‘tapokoma
Kalamu tini naweka, kusema kwingi si kwema
Kitu n’nachokutaka, shairi wishapo soma
Jaribu kuyaepuka, haya ulosoma nyuma
KIAMBATISHO B
N’sharudi
Si mwingine ni yuyule, wa ki-Mvita kijana
Mzawa mji wa kale, mtaa Kuze kwa jina
Huwo ndiwo mzi mle, tipuzi ya langu shina
Basi n’sharudi tena, alo na lake nanene
Nijile tena nijile, mneni nijile tena
Zangu tomi zinyemele, zinyemele kwa maana
Tangu siku n’toshile, hi’ leyo ndiyo nanena
Basi n’sharudi tena, alo na lake nanene
Maozi yangu mbonile, yatizama na kuona
Na masikizi vivile, nayasikiziya sana
Ili kwamba yaningile, yaliyonipita jana
Basi n’sharudi tena, alo na lake nanene
Sitatongowa tongole, leo niya hiyo sina
Leo sikukusudile, kungali mapema sana
Mwanzo n’atani niole, mambo nipate yaona
Basi n’sharudi tena, alo na lake nanene
109
KIAMBATISHO C
Ukamilifu wa Mja
1
Twaa nakupa pokeya, pokeya usidharau
Yaliyomo ni ya ndiya, katika waadhi huu
Twaa kwa kuzingatiya, mazingatiyo makuu
Mtu kuwa na maguu, si kwamba mekamilika
2
Ameumbwa mwanadamu, kwa lililo zuri umbo
Basi si wote fahamu, waliyo na sawa mambo
Wako waliyo timamu, na wingineyo wa kombo
Na mtu kuwa na kifuwa, si kwamba mekamilika
3
Kuna waliyo werevu, ambao ni waelewa
Na kuna na wapumbavu, moja jambo wasojuwa
Piya kuna wenye nguvu, na dhaifu huonewa
Mtu kuwa na kifuwa, si kwamba mekamilika
4
Kuna wasemao kweli, na wasemaji urongo
Kuna waliyo na mali, zilizopita kiwango
Na wingine zao hali, nda kuinamisha shingo
Mtu kuwa na maungo, si kwamba mekamilika
5
Kuna waliwo wembamba, na walo wanene mno
Na wako ambao kwamba, wako kati ya hawano
Mwenyezi ametuumba, kwa mbali mbali mifano
Mtu kuwa na mikono, si kwamba mekamilika
110
6
Kuna walo mafidhuli, lugha yao ni matango
Na kuna wenye kauli, zisokuwa na ushingo
Kuna wake kwa wavuli, vipofu na wenye tongo
Na mtu kuwa na shingo, si kwamba mekamilika
7
Kuna waja walo wema, kadhalika na waovu
Wako wenye na hishima, na wenye adabu mbovu
Na wako wenye huruma, piya na watenzi nguvu
Mtu kuwa na kidevu, si kwamba mekamilika
8
Kuna walio warefu, na wenye vifupi vimo
Wako walo wahalifu, wa kupitisha kipimo
Piya kuna watiifu, kwa vitendo na misemo
Mtu kuwa na mdomo, si kwamba mekamilika
9
Kuna walo kimya sana, na wenye mingi maneno
Kuna watu wa maana, wahishimiwao mno
Wingine hilo hawana, wapuuzi hawano
Na mtu kuwa na meno, si kwamba mekamilika
10
Kuna watu wakorofi, abadani hawatumi
Na wako wataswarufi, moja huzalisha kumi
Kuna wenye roho swafi, wingine zao sisemi
Mtu kuwa na ulimi, si kwamba mekamilika
11
111
Kuna walo makarimu,na mabakhili elewa
Na wakubwa kwa hirimu,wazazi kwa wazaliwa
Kadhalika madhalimu,na wanaodhulumiwa
Na mtu kuwa na puwa,si kwamba mekamilika
12
Kuna walo makhawafu, ‘kitishwa hwenenda mbiyo
Na kuna wasiyokhofu, ni shujaa zao nyoyo
Kuna walo wapotofu, na waongofu waliyo
Na kuwa na masikiyo, huko si kukamilika
13
Kuna walio na haya, zilowajaa na mato
Kuna watenda mabaya, wazi pasi na ufito
Kuna wenye swafi niya, na kuna wenye vijito
Na mtu kuwa na mato, si kwamba mekamilika
14
Kuna walo na fikira, na wenye vibovu vitwa
Kuna walo na subira, husubiri; kucha kutwa
Wengine tabiya bora,hino hawanayo katwa
Na mtu kuwa na kitwa, si kwamba mekamilika
15
Nilivyotaja si vyote, viungo vya muilini
Vinginevyo tuviwate, tuifupishe lisani
Ili kwamba tutafute, haya ‘mesema kwa nini
Nikupe yangu maani, ya mja kukamilika
112
16
Hakuna mja kamili, ndivyo twalivyoambiwa
Kadhalika mimi hili, nasema li sawa sawa
Mkamilifu wa kweli, nakubali ni Moliwa
Maana yangu ‘tatowa ya mja kukamilika
17
Kukamilika kwa mja, ni mbali na kwa Moliwa
Kwa mja nitakutaja, ili upate kwelewa
Ni kufikiya daraja, ile aliyoumbiwa
Hapo ndipo huambiwa, mja amekamilika
18
Aiyelewe duniya, kwa marefu na mapana
Azipite zile ndiya,za miba mitungu sana
Avuke bahari piya, zilo na virefu vina
Hiyo ni yangu maana, ya mja kukamilika
19
Akishafika na hayo, si kwamba ndiyo akhiri
Lazima awe na moyo, wa kuweza kusubiri
Kuyasubiri ambayo, yote yatayomjiri
Kama huyo ‘tamkiri, ni mja mekamilika
13 Mei 1970
KIAMBATISHO D
Wasiwasi Enda Zako
1
Wasiwasi n’ondokeya, ondoka enenda zako
Ondoka andama ndiya,n’ondosheya uso wako
113
Ondoka! Wanisikiya? Ziwate jeuri zako
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani
2
Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri
Haisitahamiliki, uwovu umekithiri
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri
Siitaki yako shari, enda zako wasiwasi
3
Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha
Viumbe na zao nyoyo, vitwa kuwagotanisha
Hiino ndiyo kaziyo, yenye kukufurahisha
Ni kazi isokuchosha, mno umeizoweya
4
Tukaapo wanambiya, hayawi niyatakayo
Kwamba tama ngatiya, nasumbuwa wangu moyo
Kwamba hata hingojeya, hayo niyangojeyayo
Ng’o Siyapati hayo, ni bure najisumbuwa
5
Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani
Ati mambo si mazuri, mambo yote tafashani
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini
Nisononeke moyoni, upate kufurahika
6
Au mara hunijiya, na kingine kisahani
Kukhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani
Huwa hwishi kunambiya, hali zao taabani
Zingawa; watakiyani? Ni zako au ni zao
114
7
Na mara huja nambiya, nitakapotoka humu
Ya kwamba yaningojeya, nde maisha magumu
Ulilonikusudiya,ni kunitiya wazimu
Kama ndiyo yako hamu,basi unshatahayari
8
Huo urafiki wako, wa kuja niungulisha
Kunipa masikitiko, na mateso yasokwisha
Kutoka leo ni mwiko, sitautaka maisha
Kamwe hutanikondesha,tokomeya mwana kwenda
KIAMBATISHO E
Mja si Mwema
1
Mkono inuka inuka hima twaa kalamu
Upate ya’ndika kwa khati njema hino nudhumu
Ipate someka wenye kusoma waifahamu
Wapate yashika na kuyapima yaliyo humu
2
Kuandika anza anza ‘sikawe mkono wangu
Na mimi naanza kisa chenyewe cha mlimwengu
Alivyonifanza nao wajuwe waja wenzangu
Wapate jitunza salama wawe hawa ndu zangu
3
Mja sikudhani sikudhania tanizunguka
Nikamuamini hafikiria hatageuka
Kumbe mwafulani hakuzoweya kuaminika
115
N’shambani ingawa baya lishanifika
4
Menitenda kisa kisa adhimu mja mcheni
‘Mezinduka sasa n’shafahamu najuwa kwani
Ni yangu makosa najilaumu kumuamini
Sikuwa napasa hata sehemu kumthamini
5
Meniuwa mja mja ni nduli tahadharini
Mjaye daraja nda kikatili hana imani
Muonapo mja kaani mbali mujitengeni
Asije akaja (kwani habali) kuhasirini
6
Mja hana haya haya hazimo mwake usoni
Mja ni mbaya hutimba shimo ungiye ndani
Na ukishangiya azome zomo furaha gani!
Mmoja kwa miya ndiye hayumo baya kundini
10 Januari 1971
KIAMBATISHO F
Mamaetu Afrika
1
Mamaetu Afrika, wanayo tu msibani
Msiba ametufika, ndugu hatusikizani
Kila mmoja ataka, awe mshika sukani
Litawezekana lini? Hebu tuamuwe mama
2
Wale maadui zetu, haweshi kutufitini
116
Si watu hawa si watu, ni wanyama wa mwituni
Hawapendi mamaetu, kukwona u furahani
Bali uwe simanzini, ndivyo watakavyo mama
3
Hawa ndiwo wale wale, madhalimu wa zamani
Usidhaniye wafile, wakalimo duniyani
Na fikira zile zile, zikali mwao vitwani
Wakali wakitamani, kukudhulumu wewe mama
4
Mama madhalimu hawa, walikujiya zamani
Wakakushika shokowa, nyayo hadi utosini
Vyako vikatukuliwa, hata vilivyo mwilini
Mali nyingi ya thamani, wakakupokonya mama
5
Mali ulokuwanayo, ndiyo waloyatamani
Wakajaza mali hayo, shehena mwao vyomboni
Wakenenda nayo mbiyo, hadi mwao majumbani
Ni wevi waso kifani, walokuibaya mama
6
Mno waliyapapiya, pasi kuona imani
Ilikuwa yao niya, kukuwata masikini
Hawakukufikiriya, kisha’ye utafanyani
Au utakula nini, na sisi wanayo mama
117
7
Si mali tu mamaetu, hawakutosheka kwani
Vile vile ndugu zetu, wakatiwa utumwani
Hawakuthamini utu, wa walo na ngozi hini
Wakituona manyani, kwamba tu weusi mama
8
Wakenda nao makwao, huko bara Ulayani
Ndugu zetu nguvu zao, zikatiwa makazini
Pasi na kulipwa nao, ingawa malipo duni
Wanali wakoloni, kwa bwerere hiyo mama
9
Mama lau si wanayo, kupelekwa ugenini
Lau kwamba si maliyo, kubwakurwa mikononi
Hivi leo bara hiyo, iitwayo Ulayani
Ingekuwa haifani, nakupawa sifa mama
10
Ndiyo waliyowalisha, na kutengezeya huko
Miji wakasimamisha, kwa nguvu za mali yako
Lililowatajirisha, ni jasho la mwili wako
Na damu ya mwana wako, ndiyo kuwa hayo mama
11
Juu ya zao akili, zisifikazo kabisa
Walipungukiwa mali, mali ndicho walokosa
Wakaona afadhali, waje kwako kupukusa
Maliyo pasi ruhusa, wakakutwalia mama
118
12
Wakakunyang’anya vyako, hivi mtana mtana
Mmoja hakukuwako, wakusubutu kunena
Mama uli peke yako, hata muombezi huna
Ila sisi wako wana, tukakuliliya mama
13
Kwani siku hizo mama, twali dhaifu yakini
Mtu akitusukuma, twali kianguka tini
Sisi nao kusimama, na kuwatiya mbaroni
Ikawa haimkini, sisi kuwashinda mama
14
Tulipopata fahamu, kuweza kukuteteya
Wakaona madhalimu, yatawendeya vibaya
Ndipo walipoazimu, kutumiya mpya ndiya
Kuzivunda zetu niya, wazidi kukula mama
15
Hapo wakakatikiwa, kwamba watutenganishe
Kwani wa moja tukiwa, tutawakanyaga weshe
Waona kubwa dawa, wano watutenganishe
Ili wakukorofishe, na kukunyonya wewe mama
16
Tukawekewa mipaka, kila ukoo na pao
Walifanya kwa kutaka umoja tusiwe nao
Walijuwa pasi shaka, u karibu mwisho wao
Wa kushungiwa makwao, wakuhame wetu mama
119
17
Wakawa waendelea, kutukuwa yako mali
Na sisi wanayo pia, wakitupa idhilali
Tukawa twalingjeya, mwisho wake jambo hili
Sikuye ikiwasili, tutende kitendo mama
18
Tulipoona ya mno, yashatukoma kooni
Tukasema tabu hino, sasa natuyondosheni
Tukakunduwa mikono, tukaingiya vitani
Kuwapiga wakoloni, wakwambaye wetu mama
19
Japo twali mbali mbali, kila ukoo pekee
Tukaona afadhali, kila tapo lisongee
Kila pembe na mahali, adui tumlemee
Wana walo wazee, tukawa vitani mama
20
Mama tukaanza vita, kukupiganiya wewe
Maguu tukayakita, tukasema tufe nawe
Minyoo tukayakata, ili kwamba huru uwe
Twalolitaka mwishowe,tukawa tunalo mama
21
Nyingi mno damu yetu, ikabidi kumwaika
Baadhi ya ndugu zetu, roho zao zikatoka
Na kila kilicho chetu, kwa wingi kikatumika
Kwa kutaka kuiweka, hadhi yetu nawe mama
22
Adui tukamshinda, ikawa sasa atoke
Tukamwamba toka nenda, na kumpiga mateke
120
Alikuwa yuwadinda, hakutaka kwenda zake
Kwa nyingi tama yake, ya kukudhulumu mama
23
Baadhi ya wana wako, bado wangali tabuni
Wangali na masumbuko, kwa wateswavyo wendani
Wakoloni wangaliko, kwa wanao wa kusini
Bado wangali na kani, kutesa wanayo mama
24
Msumbiji vile vile, bado hawajakondoka
Nako Zimbabwe wa tele, hawajataka kutoka
Na Angola wabakile, wangali wakikushika
Guinea-Bissau kadha’ka, wamekugandama mama
25
Watoto wako hawano, ni midume sawa sawa
Wamo kwenye mapigano, kutaka kukukombowa
Na kwa lao ungamano, na moyo wa kujitowa
Adui watamtowa, hilo litakuwa mama
26
Adui hivyo kuona, kishamtoka kanwani
Chakula kitamu sana, tena hakipatikani
Akawa amendangana, hajui afanye nini
Ili kwamba mkononi, akirudishecho mama
27
Ikawa anapokaa, huwa roho yampapa
Hurudiwa na tamaa, ya kuja tena kujepa
Bali aogopa baa, lau atarudi hapa
Ni mbwa kuona fupa, akacha kuliguguna
121
28
Kurudi yeye mwenyewe, kuja kuyatwaa mali
Au kutuma mwanawe, aitimize shughuli
Haya mama utambuwe, yote kwake ni muhali
Ajuwa kwamba si kweli, hawezi faulu mama
29
Kwani wingi wa wanayo, mato yao yako wazi
Kutokeya siku hiyo, hawanao usingizi
Hata yao masikiyo, daima ni masikizi
Angaja kwa unyenyezi, watamsikiya mama
30
Tamaa hakuikata, ya kupata atakalo
Kufikiri hakusita, lipi liwezekanalo?
Litalonipa kupata, lile nihitajilo
Kwani sina buni nalo, ndivyo kiwaza’ye mama
31
Tahamaki akazua, jambo atakalofanya
Akaona kubwa dawa, ambayo itamponya
Ni wanayo hawa hawa, aanze kuwatawanya
Mapande kuwagawanya, wamtumikiye mama
32
Baadhi awatumiye, wawe vibaraka vyake
Baadaye wakujiye, watimize kazi yake
Wanayo wakuibiye, chako kipelekwe kwake
Hiyo ndiyo haja yake, aliyoitaka mama
122
33
Wanayo hao ni hawa, waletao machafuko
Adui ‘mewanunuwa, wamo ndani kwa mfuko
Ndu zetu wameradhiwa, kuikosa radhi yako
Watapata masumbuko, kwa wayatendayo mama
34
Badala ya kuungana, tuwe ni kitu kimoja
Tupate shirikiyana, sisi na wao pamoja
Tukulinde sana sana, kwa kila litakalokuja
Bali wao yao haja, si sawa na yetu mama
35
Ndiyo mwanzo ndugu zetu, wenda kinyume na sisi
Wakishika kila chetu, na kukiuza rahisi
Waivunda hadhi yetu, sote tuliyo weusi
Wapenda zao nafusi, na maaduizo mama
36
Sisi hatutakubali, kurudishwa utumwani
Kurudiya idhilali, tuliyo pawa zamani
Mama wala yako mali, kupelekwa Ulayani
Hatarudi mkoloni, tuamini wetu mama
37
Tukakulinda vilivyo, pasipo kurudi nyuma
Na vyote ulivyonavyo, vitabakia salama
Vitabaki vivyo hivyo, kimoja hakitahama
Tutamtafuna nyama, atakaye kugusa mama
123
38
Tu tayari damu zetu, kwa mikondo imwaike
Tu tayari roho zetu, kwa maelfu zitoke
Tukuhami Mamaetu, kila baya likuepuke
Hishimayo tuiweke, Afrika wetu mama
29 Januari 1971
KIAMBATISHO G
Wasiwasi Enda Zako
1
Wasiwasi n’ondokeya, ondoka enenda zako
Ondoka andama ndiya,n’ondosheya uso wako
Ondoka! Wanisikiya?Ziwate jeuri zako
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani
2
Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri
Haisitahamiliki, uwovu umekithiri
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri
Siitaki yako shari, enda zako wasiwasi
3
Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha
Viumbe na zao nyoyo, vitwa kuwagotanisha
Hiino ndiyo kaziyo, yenye kukufurahisha
124
Ni kazi isokuchosha, mno umeizoweya
4
Tukaapo wanambiya, hayawi niyatakayo
Kwamba tama ngatiya, nasumbuwa wangu moyo
Kwamba hata hingojeya, hayo niyangojeyayo
NG’O’ Siyapati hayo, ni bure najisumbuwa
5
Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani
Ati mambo si mazuri, mambo yote tafashani
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini
Nisononeke moyoni, upate kufurahika
6
Au mara hunijiya, na kingine kisahani
Kukhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani
Huwa hwishi kunambiya, hali zao taabani
Zingawa; watakiyani? Ni zako au ni zao
7
Na mara huja mambiya, nitakapotoka humu
Ya kwamba yaningojeya, nde maisha magumu
Ulilonikusudiya, nde maishani magumu
Ulilonikusudiya, ni kunitiya wazimu?
8
Huo urafiki wako, wa kuja niungulisha
Kunipa masikitiko, na mateso yasokwisha
Kutoak leo ni mwiko, sitautaka maisha
Kamwe hutanikondesha mwana kwenda
125
1
KIAMBATISHO H
N’shishiyelo ni Lilo
1
Nipulikiza ndu yangu, ninenayo usikiye
Yaliyo moyoni mwangu, ningependa nikwambiye
Ujue imani yangu, ambayo niishishiye
Siiwati ingawaye, n’shishiyelo ni lilo
2
Walinena walimwengu, wa zama zilopisiye
Kwamba kweli i utungu, kwa yule aambiwaye
Nami haya ndugu yangu, sasa niyaaminiye
Asojuwa nasikiye, apeleleze ajuwe
3
Kweli nnaifahamu, haipendwi aswilani
Kwa mja hiyo ni sumu, mbaya iso kifani
Mwenye kuitakalamu, hapendezi katwaani
Sasa nshayaamini, ni kweli haya ni kweli
4
Kweli imenitongeya, kwa kuinena mwendani
Wale nalowaambiya, wamenitiya dhikini
Wameniona mbaya, kumshinda Firauni
Kweli, sasa naamini, si wangi waipendao
5
Kweli naliwambiya, wakuu wa nti hini
Haelaza moya moya, kwa wanati wa ntini
Kuhusu walofanyiya, upande wa Upinzani
126
Sasa kuwamo tabuni, nalipwa kwa hiyo kweli
6
Kweli ilipowatoma, kama desturi yake
Wao wakaona vyema, afadhali wanishike
Wanishike hima hima, hima ndani waniweke
Ngomeni n’adhibike, nijute kusema kweli
7
Kweli yanipasha tabu, ndugu yangu niamini
Na ninyi mno adhabu, za moyoni na mwilini
Yote haya ni sababu, ya kunena kweli hini
Ndipo sasa hamini, kweli i utungu kweli
8
Kweli menibaidisha, na huko kwetu mjini
Pia menitenganisha, na walo wangu nyumbani
Kuja kuniadhibisha, kwa kunileta ngomeni
Yote sababu nini? Ni kwamba mesema kweli
9
Kweli menifunga ndani, ya chumba nde sitoki
Kutwa kucha ni chumbani, juwa kuota ni dhiki
Na mlinzi mlangoni, yu papo kattu ha’ndoki
Nilindwavyo bilhaki, ni kama simba marara
10
Kweli yanilaza tini,ilo baridi kali
Ningawa burangetini,natetema kweli kweli
Na maumivu mwilini,daima ni yangu hali
Shauri ya idhilali,ya kulazwa simitini
127
11
Kweli japo ni ngomeni,kwenye kuta ndefu nene
Kabisa sitangamani ,na mahabusu wingine
Na lengo kubwa nadhani,ni :nilonalo ‘sinene
Hazuwa mambo mingine,kwa kuambukiza watu
12
Kweli pia meninyima ,haki zilizo ngomeni
Wangu kuja nitimizama ,hilo haliwezekani
Haya nnayoyasema,ndivyo yalivyo yakini
Baruwa sitakikani,kwandika wala kwetewa
13
Sendi mbele ‘tasimama ,sikupi kwa tafswili
Kusudi nirudi nyuma ,kwa ubeti wa awali
Ili nipate kusema,imani yangu kamili
Ujuwe kwa jambo hili,mtima wangu ulivyo
14
Nilipoenua kimo,kutaka niseme kweli
Nilidhani yaliyomo,hinena sina aili
Kanama wangu mdomo,waja fungika kauli
Nisiseme bilkuli,kuwaeleza wanati
15
Mno wanganiadhibu ,adhabu kila namna
Na mengi yanganiswibu ,ya usiku na mtana
Hayatakuwa sababu ,ya kuniasa kunena
Kweli nitakapoiyona ,tanena siinyamai
16
128
Mateso yao yangawa,nda kuumiza mtima
Hayatakuwa ni dawa,ya kutonipa kusema
Ni bure wajisumbuwa , nilipo nnasimama
Si ‘mi wa kurudi nyuma ,kweli ilipo ‘tasonga.
17
Ama hakika mwendani ,kwa mwenye moyo wa sawa
Mateso ya duniani ,wakati kijaaliwa
Hushukuru Rahamani ,kajikaza kutukuwa
Nami yangawa yakuwa,hikaza moyo si ila
18
Mateso humbadili,aso na moyo thabiti
Apawapo idhilali ,Japo ingawa katiti
Huona ni afadhali ,awate yakwe ya dhati
Ela langu siliwati ,n’shishiyelo ni lilo
19
Wangi washasumbuliwa,waneni wa kweli hiyo
Na wangi washauliwa ,kwa kutobadili nyoyo
Na mimi nimeradhiwa,ku’yandama sera hiyo
‘Tafuwata zao nyayo , n’shishiyelo ni lilo
20
Atwambizile Rasuli ,kipenzi cha bwana Mn’gu
Ya kwamba tuseme kweli,japokuwa i utungu
Na mimi siibadili ,ni yiyo imani yangu
Nililoamini tangu ,ni lilo hilo sil’ati.
129
21
Kweli naitiya tamma ,nikuage ndugu yangu
Kweli si mwenye kukoma,kuwambiya walimwengu
Kweli si’yati kusema,katika uhai wangu
Nami kwa upande wangu,hi’yambiwa ‘takubali
KIAMBATISHO I Septemba 1969
Telezi
Mvua iliyonyesha ,ya maradi na ngurumo
Kutwa na kucha kukesha ,kunyesha pasi kipimo
Haikunufaisha wakulima ,wenye kazi na vilimo
Wenye kazi za vilimo,walifikwa na hasara
2
Mimeya waloipanda ,ilitekukatekuka
Kazi ngumu walotenda,yote ikaharibika
Hawakuvuna matunda ,waliyo wakiyataka
Waliyo wakiyataka ,yakawa ya mbali nao
3
Wenye kuicha mvuwa,isiwatose mwilini
Baadhi yao wakawa ,wakimbiliya penuni
Wengine hawakutuwa ,hadi mwao majumbani
Hadi mwao majumbani ,na kukomeya milango
4
Wenzangu dhihaka kando,nisemayo ni yakini
Ilibwaga kubwa shindo ,mvuwa hiyo jamani
Na mijaji kwa mikondo ,yakawa barabarani
Yakawa barabrani,mvua kwisha kunyesha
130
5
Kunyesha iliposiya ,kukatapakaa tope
Zilijaa kila ndiya,isibakiye nyeupe
Ukawa mwingi udhiya ,pa kupita zisitupe
Pa kupita zisitupe,kwa ndiya kukosekana.
6
Japo hivyo zilikuwa, ndiya hazipitiki
Bali mimi haamuwa ,kwenenda japo kwa dhiki
Kumbe vile nitakuwa,ni mfano wa samaki
Ni mfano wa samaki, kuiendeya ndowana.
7
Zikanibwaga telezi,sikujua kuzendeya
Ningekwenda kwa henezi,yasingenifika haya
Lakini tena siewezi,mwendo huo kutumiya
Sitawata kutembeya,ila tabadili mwendo.
3 Agosti 1973
7
Jambo nilingojeyalo ,ni kutimu yake siku
Ningojeyalo ni hilo,tena kwa kubwa shauku
Itimupo ndimi nalo,ja mwewe na mwana huku
Ni furaha hiyo siku,kwangu na wenzangu piya.
8
Siku ya kuiva kwake ,hiyo ndiyo siku kweli
Huo ndiwo mwisho wake ,na mwisho wa idhilali
Idhilali in’ondoke ,mimi nayo tuwe mbali
Siku hiyo ni wawili,kuteka au kuliya
131
9
‘Taliminya litumbuke ,lisinisumbue tena
Usaha wote utoke ,utoke nikiuona
Midamu itiririke ,kama ng’ombe alonona
Jipu hili mwana lana,Mn’ngu mbwalipa hizaya.
10
Jasho jembamba litoke,ndiya mbili likitona
Na hapo nitetemeke,si kwa baridi kuona
Bali kwa utungu wake,utakaozidi sana
Hapo ndipo nitasona ,na moyo kufurahiya
11
Baada ya yote haya,jaraha niliuguze
Kwa madawa kulitiya ,ili kwamba yalipoze
Irudi yangu afiya ,na zaidi niongoze
Nirukeruke niteze,kwa furaha kiningiya
KIAMBATISHO J
Siwati
Siwati nshishiyelo ,siwati ;kwani niwate?
Siwati ni lilo hilo ,’talishika kwa vyovyote
Siwati ni mimi nalo,hapano au popote
Hadi kaburini sote,mimi nalo tufukiwe
Siwati ngaambiwa ,adhabu kila mifano
Siwati ningaambiwa,’tapawa kila kinono
Siwati lililo sawa, silibanduwi mkono
Hata ningaumwa meno,mkono siubanduwi
132
Siwati si ushindani,mukasema nashindana
Siwati ifahamuni ,sababuye waungwana
Siwati ndangu imani ,niithaminiyo sana
Na kuiwata naona,itakuwa ni muhali
Siwati nimeradhiwa,kufikwa na kila mawi
Siwati ningaambiwa ,niaminiyo hayawi
Siwati kisha nikawa ,kama nzi; hivyo siwi
Thamma nakariri siwi ,na Mn’gu nisaidiya
-15 machi 1970
KIAMBATISHO K
Leo N’singekuwako
Kama tabu ni mauti, leo n’singekuwako
Ningekuwa ni maiti ,’mebakiza sikitiko
Ningekuwako tiyati, mtanga ndilo funiko
Leo n’singekuwa ,kama tabu ni mauti
Hivi leo n’ngekuwa ,kana kwamba sikuwako
Kitambo n’shafukiwa ,nimo kaburini huko
Kungebaki kuambiwa :’Atifu alikuwako
Leo n’singekuwako,kama tabu ni mauti
Marehemu ningekuwa,n’shaoza ni mnuko
Hawata kusumbuliwa ,ni tabu na masumbuko
Na tabu haondokewa ,’ngenijiya niliko?
Leo n’singekuwako , kama tabu ni mauti
Kwa siku ngeliliwa ,na jamaa waliyoko
Na maduwa kuombewa ,nende salama nendako
Kisha hasahauliwa ,kwa moyo na matamko
Leo n’singekuwako ,kama tabu ni mauti
133
Na kwamba hata yakawa,hadi leo hawa niko
Ni kuwa huu moyowa, wahimili masumbuko
Ngeliya kwa yalokuwa ,hakika singekuwako
Leo n’singekuwako,kama tabu ni mauti
-14 juni 1971
KIAMBATISHO L
Wasafiri Tuamkeni
1
Bado safari ni ndefu,wasafiri tusichoke
Natusiwe madhaifu ,twendeni hadi tufike
Tusafiri bila hofu,wenye nazo ziwatoke
Huu ndiwo mwanzo wake, siwo mwisho wa safari
2
Twendeni tusonge mbele,twendeni tusianguke
Mwauona mlima ule? Pale ndipo mwisho wake
Tupande chake kilele,bendera tuitundike
Huu ndiwo mwanzo wake ,siwo mwisho wa safari
3
Twendeni tukifahamu ,kila mtu akumbuke
Safari yetu ni ngumu,si rahisi ndiya yake
Kuna miba yenye sumu, tunzani tusidungike
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
4
134
Ni ndiya yenye misitu, na mirefu miti yake
Imejaa nyama mwitu ,kila mmoja na pake
Na wakionapo kitu,ni lazima wakishike
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
5
Na kuna bahari pana , na kirefu kina chake
Mawimbi makubwa sana, ni ajabu nguvu zake
Hiyo hatuna namna ,ni lazima tuivuke
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
6
Japo ni ngumu safari ,wendaji tusigutuke
Ingawa ina hatari ,twendeni tusitishike
Ingawa ndefu safari,lazima imalizike
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
7
Tamaa tusiikate,niya zisiteteleke
Ndiya natuifuate, nyoyo zisituvundike
Haja yetu tuipate,bendera yetu tutweke
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
8
Vibwebwe tujifungeni,tuvifungeni vifungike
Tuvikaze viunoni ,waume kwa wanawake
Tungiyapo safarini,twende tusibabaike
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
9
Wenzangu nawahimiza ,haya shime muinuke
135
Tuwate kujilegeza ,wala tusitetemeke
Haja ni kuimaliza ,isiwatwe nusu yake
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
10
Tuenukeni twendeni,mwenye chake najitweke
Ngiyani misitarini,safu safu mupangike
Wana na wazee ndani,pamoja tutanganyike
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
11
Kusafiri ni lazima ,tukitaka tusikate
Wale waliyo wazima ,maguu nayanyosheke
Na aliye na kilema ,naabebwe na wenzake
Huu ndiwo mwanzo wake,siwo mwisho wa safari
12
Mwenye kutaka safari,ya kwamba isifanyike
Huyo aduwi dhahiri ,kwetu pamoja na kwake
Na wala asifikiri ,atafaulu kwa lake
Huu ndiwo mwanzo wake, siwo mwisho wa safari
13
Na mshikaji bendera, kwa vizuri naishike
Daima nawe imara , wala asilainike
Ayongoze barabara, huko twendako tufike
Huu ndiwo mwanzo wake, siwo mwisho wa safari
4 Septemba 1971
KIAMBATISHO M
Kichu Hakiwi ni Uchu
136
1
Ni nyani ambidhiweo , yu nchu kwa chake kichu?
Ni nyani nnena hao, ntaka hadaa vachu
Nadhengee vangineo, jura hatopacha kwechu
Nchu kwambiwa yu nchu, ni uchu kwa wendiwe
2
Na kama ni chwambiwavo,kichu na uchu ni chicho
Dhiko na dhingi dhilidho,dhenye dhichu kochokocho
Chwambe dhina uchu nadho,thibabu ni lavo pacho?
Nchu si kwa lake pacho,ni uchuwe kwa wendiwe
3
Hela ndovu chunchude ,awe ni mfano wechu
Chumuawanye dhipande ,awe dhipande dhichachu
Ili kasidi chwenende ,chufahamishe uchu
Chuyive nchu ni kichu ,au uchu kwa wendiwe?
4
Kwanda ni mwili wake,uliyo nkuru nno
Kwa namna mwichu wendake ,hauna wakwe mfano
Apeche umbo la pweke ,kuru tena lilo nono
Si chanda si lakwe ino,si madodi ila mato
5
Ndhengee avoneo,mwene kuwavona vachu
Vachu ndovu wavoneo,awapo kachika mwichu
Umvudhe :vachu hao,wavonao hicho kichu
Achi huwaye wendechu,sura wataajabuvo
6
Pili nguvu alonadho,dhiyani dhalomweneya
Ni nguvu dhiwachishadho,dhiumbe na michi piya
137
Dhidirikano nadho,hadhina budi kuliya
Au mbiyoni kungiya,kwa kucha kudhidirika
7
Vako ambao hunena,nguvudhe kudhisifiya
Kwamba huwedha vuchana ,na hata na vachu miya
Na hata vangaungana ,kumvucha kwa pamoja
Hawawi kuwedha piya,kwa nguvu alidhonadho
8
Ata dhiumbe vanche, kwa nguvu alidhopowa
‘kichumiya kifuwache ,awapo andoudhiwa
Mishi isiyo michache ,hungiliya kuang’owa
Nyuteni yivani kuwa ,hawi mbwa kudhivilika
9
Kando ni lakwe iteke,libikapo hwangaamidha
Pumudhidhe pweke yake,chwaambiwa huumidha
Dhivudhiyapo chendake ,mbali hukichokomedha
Humbiriya dhikapadha,na tiyati kuchangusha
10
Chachu ni yakwe thamani ,asoiyiva hakuna
Ichengee duniani ,kupi kaiyulikana
Dhiungani na miyini,nno huchambulikana
N’nyani mwene kunena,haiyisi thamaniye
11
Pacha kwenda utukuni,pembedhe dhidhanyiwapo
Au nenda nnadani,kwahali dhinadiwapo
138
Uyivwonee matoni,n-da dhinunuliwapo
Ndipo utayiwa hapo,thamani ya nama thamaniye
12
Thamani yakwe si chocho,thamani ya nana huu
Chakwe iye kidhanuwacho,hoko kwene utukuu
Mwene kukinunuwacho ,hulipiya bei kuu
Beiye kwamba i yuu,ndipo kudhanywa hiyau
13
Kiswahili cha kigunya ,kwacho ‘kiwazungumza
‘Mejaribu kubambanya ,kiyasi n’livyoweza
Sasa n’takalofanya ,nataka kukigeuza
Kwamba n’pate maliza,n’lilolikusudiya
14
N’likijuwa zamani,tangu utotoni mwangu
Wakati ni magunyani,pamoja na babu yangu
Na tangu huko nihuni,si leo miyaka tungu
Kwa hivyo fahamu yangu ,kwacho ‘menipungikiya
15
Changu ni cha kimvita ,tangu mwa mama tumboni
Sikwenda kukitafuta ,n’likikuta nyumbani
Mi nacho ni kama pata,twendapo hatuwatani
Na tangu kwinukiyani,hicho ndicho hutumiya
16
Kwangu ndicho mahasumu,mno nakipendeleya
Ndicho kinishacho hamu,mashairi hitungiya
139
Huwa siyaoni tamu,hiwata kuchadikiya
Huyaona ni mabaya ,ha ya tamu ha ya nyamu
17
Hicho ndicho kiswahili,ambacho chanipendeza
Kwake sioni badali,ndipo nikakitukuza
Kwangu ki kama asali,tamu isokinaiza
Ndicho hunitosheleza ,wakati wa kutungiya
18
Kwanza nataka fasiri ,maana ya neno ‘kitu’
Tueleze vizuri ,afahamu kila mtu
Maanaye idhihiri ,kwa kila mmoja wetu
Mtu kiambiwa ‘kitu’,lipate kumueleya
19
Ni mengi maana yake,nikianza yadondowa
Lau yote niandike ,iwe kuyafafanuwa
Ndugu zangu mukumbuke ,kazi kubwa itakuwa
Basi yote sitatowa ,ingawa yanieleya.
20
Katika lugha iweyo,hata iwe nda Kichina
Kuna maneno ambayo ,kwa mato ukiyaona
Utayadhaniya hayo,hayana maana pana
Yaani yao maana, moja hayakuzidiya
21
Lakini sivyo yalivyo ,si ambavyo huwa
Vilivyo ambavyo ndivyo ,ambavyo vilivyo sawa
140
Hutegemeya ambavyo,neno linavyotumiwa
Ndipo utapamabanua ,maanaye mbalimbali
22
Na Kiswahili ni vivyo,vyenginewe usidhani
Neno ulitumiyavyo,liwapo li kifunguni
Nalo ndivyo likupavyo ,tafauti ya maani
Ukaweza kubaini ,maana yatakiwayo
23
Kwa maana ya jumla,ya neno ‘kitu’ wenzangu
Ni ambacho au kila ,kilo kwenye ulimwengu
Mfano nguo ,chakula ,neno,roho au rungu
Jiwe,mtu au tungu,kila kimoja ni kitu
24
Ndipo mfano hatowa,wa ndovu alivyonavyo
Ukubwa aliopawa,ni kama hivyo ulivyo
Na nguvuze twazijuwa,zistaajabishavyo
Na thamaniye ilivyo,si ndogo meelezeya
25
Vyote hivino ni vitu,tena si vitu vidogo
Ndivyo vitu kila mtu,huviwekeya mitego
Kimojapo mwenzi wetu, ‘kipata hutupa shingo
Hufurahi hadi jego,likawa laonekana
26
Iwapo ni hicho kitu,mno kinachosifiwa
Ndicho kimpacho mtu,naye yu mtu kwambiwa
141
Basi huyu nyama mwitu,ambaye meelezewa
Kitu chamfanya kuwa,kwambiwa naye yu mtu?
27
Licha mtu akili ,ambayo iko razini
Hata mjinga wa kweli,mtopeya ujingani
Hataweza kukubali,kabisa hataamani
Ati nyama wa mwituni,awe yu sawa na mtu
28
Lau hayo watamka,na kumwambiya mwendani
Hakika atakuteka,akutiye uzuzuni
Maana kufikiria ,hayangii akilini
Hilo haliwezekani ,ni bure ungamwambiya
29
Basi na mtu ambaye ,yuna vitu kwa milima
Maadamu vyake yeye,hafalii binadama
Bali huvikusanyaye,na kupenda vitizama
Huwa sawa na mnyama,tuliyemuelezeya
30
Mfano awe na mali ,yalokiuka mipaka
Akatupiliya mbali ,wenye shida na mashaka
Akawa hata hajali ,tabu zinazowafika
Huyo si mtu hakika ,kwani mtu mbwake utu
31
Au awe yuna nguvu,kikubwa kifuwa chake
Ziwe nguvu za mabavu,na magumi na mateke
142
Iwe sasa utulivu,hawaupati wenzake
Iwe ni watetemeke,muda’ye akitokeya
32
Nguvu hizo sasa ziwe,hatumii ajikinge
Bali ndiyo mwanzo awe ,kwenye mitaa arange
Akidhulumu wenziwe,ambao kwamba wanyonge
Yawe ‘mnyonge msonge, hana wa kumzuwiya
33
Au awe yuna cheo ,juu ya wenziwe wote
Na kisha wemziwe hao,alonao saa zote
Wawapo na shida zao,hawafai kwa chochote
Iwe ‘poteleya pote,hataki kuwasikiya
34
Badili hiyo furusa ,kuitumiya vizuri
Kwake sivyo ;bali sasa ,huanzisha takaburi
Wende awe kuwatesa,awatende jeuri
Huyo ni mnyama wa pori,hafai kuitwa mtu
35
Walio na sifa hizo,viumbe niwanenao
Mali wangakuwa nazo,ukubwa wangawa nao
Wangawa na nguvu hizo,wadhiliyazo wenzao
Siweki viumbe hao,kwenye daraja ya watu
36
Uliyo wangu muradi,wa kuyanena hayo
Viumbe hao idadi ,pamoja na ndovu huyo
143
Sikioni cha zaidi ,kati ya waliyonayo
Naona wa sawa kwayo,kipi walopitaniya
37
Iwapo ni hayo mali,watu yasosaidiya
Sababu ya ubakhili,wakawa wayabaniya
Wasijali wasibali,dhiki za wapita ndiya
Na ndovu anayo piya, kama nalivyoeleza
38
Ndovu na bakhili sawa,ha wa mbali kwa masafa
Ya bakhili hurithiwa ,baada ya kwake kufa
Mara nyingi hutumiwa ,ovyo pasi maarifa
Na ya ndovu ni kufa ,ndipo yake yatwaliwe
39
Kwa hivyo hapa twaona ,viumbe hivi viwili
Ambavyo wamfanana ,kwa hayano yao mali
Hayawi kupatikana ,ela watwawe na nduli
Kuna gani afadhali,baina wawili hawa?
40
Na kwa wa nguvu upande, ‘taweleza pasi shaka
Iwapo ni wa makonde,na mabavu kutumika
Watu iwe mbiyo wende,kwa kucha kuzidirika
Vifenene kadhalika,viumbe viwili hivi
41
Apandwapo na ghadhabu ,huyu ndovu ‘mewambiya
Vilivyo naye karibu ,na alivyovilekeya
144
Huanza kuviharibu ,vikawa kuangamiya
Huulaza mwitu piya,manyasi na miti yake
42
Kwani muda hifikiri ,hizo nguvu walonazo
Ni nguvu za kuhasiri,na kudhili wasonazo
Hazitumiwi kwa kheri,bali kwa maangamizo
Basi wafenene kwazo,ipi tafauti yao
43
Na iwapo ni ukuu,huyo mtu alonao
Ukuu wa kudharau,wasiwo na hicho cheo
Basi ndovu nao huu,na yeye piya anao
Ipi tafauti yao,walotafautiyana
44
Basi tusidanganyike ,tusiwe mbwa kuhadawa
Mtu si kwa kitu chake,japo kwacho asifiwa
Utu wake kwa wenzake,ndiwo wa kuhisabiwa
Vyengine sitaambiwa,nami nikaviamini
145