ujitoe kabisa · wake, nguvu zake, au akili yakemimi sitafuti kitu kwako. . sitafuti kufaidika...

88
- 1 - UJITOE KABISA Mafundisho Yanayohusu Utoaji wa Mkristo kwa Mungu Wake. Kimeandikwa na Steven Sherman 1011 Aldon Street, Grand Rapids, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

Upload: others

Post on 04-Nov-2020

15 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 1 -

UJITOE KABISA

Mafundisho Yanayohusu Utoaji wa Mkristo kwa Mungu Wake.

Kimeandikwa na

Steven Sherman

1011 Aldon Street, Grand Rapids, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

Page 2: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 2 -

UJITOE KABISA Copyright © 1998 GMI Publications

GMI Publications ina haki zote za kitabu hiki. Hairuhusiwi kuchapa na kuuza sehemu yo yote ya kitabu hiki bila ruhusa ya GMI Publications. Vilevile hairuhusiwi kuuza nakala za kikompyuta (digital copies) bila ruhusa ya GMI Publications.

Wahariri – Mch. Albert Juliano Simwanza, Martin Haule, Steven Sherman

Kama Biblia nyingine hazijatajwa, dondoo zote za kunukuu Biblia zinatumia Swahili Union Ver-sion (SUV): Haki miliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

GMI Publications ni idara ya Grace Ministries International; misheni ifanyayo kazi na makanisa ya Neema duniani, pamoja na Wakristo wote wanaomwamini Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao.

Yaliyomo

Sababu za Watu Kutojitoa Ipasavyo ........................................................ 4

Uhusiano wa Mkristo na Mali Zake ......................................................... 7

Raha ya Kweli ................................................................................................ 16

Mahitaji ya Mkristo ..................................................................................... 27

Utoaji Huongeza Baraka za Mungu ....................................................... 33

Mungu Huwapa Watu Wake Kulingana na Asili Zake ................... 42

Mungu Anamiliki Vitu Vyote ................................................................... 45

Uwakili ............................................................................................................. 48

Taratibu za Utoaji ........................................................................................ 56

Kutomtolea Mungu ni Wizi ...................................................................... 79

Faida ya Utoaji Ulio Bora .......................................................................... 80

Kupanga Utoaji Wetu ................................................................................. 83

Mwisho ............................................................................................................. 88

Page 3: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 3 -

KUSUDI LA KITABU HIKI Kuandika kitabu ni kazi kubwa. Hakuna anayeweza kuanza kazi hii bila kusudi. Ninalo

kusudi la kuandika kitabu hiki lakini nafikiri wengi wangekisia vibaya kama ningewaomba waniambie kusudi langu la kukiandika. Labda wengine wangesema kusudi langu ni kuongeza mapato ya Kanisa wakati wengine wangesema lengo langu ni kuona majengo mazuri zaidi, au ofisi zenye uwezo zaidi, au wachungaji wakitunzwa vizuri zaidi. Mambo hayo yote ni mambo mazuri, tena yanahitajika, lakini siyo kusudi langu kuu.

Kusudi langu kuu ni kukufaidisha wewe unayejitoa. Yaani, nataka ufaidike kutokana na kitabu hiki. Hakika Mungu anambariki yule anayejitoa kwake, kama ni kwa mali yake, muda wake, nguvu zake, au akili yake. Mimi sitafuti kitu kwako. Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka-na na utoaji wako. Ninachotaka ni wewe uweze kuwa katikati ya mpango wa Mungu na kusudi lake kwa ajili ya maisha yako. Ukiwa kwenye mpango wa Mungu utaona maisha yako yanaboreka kuliko unavyoweza kuamini. Ni kama Paulo alivyosema katika Wafilipi 4:17, “Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.”

Ninayo furaha kuweza kukuelimisha juu ya utoaji kwa jinsi Neno la Mungu linavyofundisha. Kwa kawaida, wakati mchungaji au mwalimu anaposimama kufundisha kuhusu utoaji, washiri-ka wote wanakuwa na wasiwasi au hofu. Huanza kufikiria juu ya pesa na mali zao, pia huwaza jinsi watakavyoitetea hali yao ya kutojitoa. Mchungaji naye anahofu kwamba washirika wake hawatamsikiliza na pia hufikiri watamsema vibaya kwamba anajitafutia mahitaji. Mara nyingine ni kweli. Baadhi ya wachungaji wanafundisha kuhusu utoaji kwa sababu ya mahitaji yao wenyewe au mahitaji mengine ya Kanisa.

Hofu hizi zote hazitakiwi kulitawala suala hilo la utoaji. Kitu ambacho kinapaswa kutawala ni Neno la Mungu. Mungu amelitoa Neno lake kwa ajili ya watu wake ili waweze kujua kuhusu Mungu mwenyewe na namna anavyotaka waishi. Sisi sote tulio Wakristo tunataka kumpendeza Mungu. Lakini, hatuwezi kumpendeza Mungu tusiposoma Neno lake na kulitii. Mimi sihofu kuongea kuhusu utoaji kwa sababu Neno la Mungu lenyewe linazo sehemu nyingi zinazofun-disha kuhusu utoaji. Kama unataka kumpendeza Mungu, na unataka kubarikiwa na Mungu, ina-bidi uyaelewe yale yote ambayo Biblia inasema kuhusu utoaji.

Hivyo naomba ujisikie amani tutakapoanza kuangalia Neno la Mungu kuhusu somo hili la utoaji. Hakika atakayefaidika zaidi ni wewe kama utayaelewa mafundisho ya Neno la Mungu kuhusu utoaji na kuyatii.

Page 4: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 4 -

- 1 - Sababu za Watu Kutojitoa Ipasavyo

• Unajisikiaje wakati inatangazwa utafundishwa kuhusu somo la utoaji?

• Je wewe unafikiri sababu za Wakristo kutojitoa ipasavyo ni nini?

Katika kulifundisha somo hili nilipata nafasi ya kuwauliza watu wengi sababu za kutojitoa ipasavyo. Nilipata mawazo mengi yaliyo tofauti. Yafuatayo ni baadhi ya mawazo yaliyotolewa:

Washirika hawafundishwi juu ya utoaji

Jibu moja lililotolewa kuwa sababu ya watu kutojitoa ni ukosefu wa ufahamu. Wengine walidai somo lenyewe halifundishwi. Mara nyingi wachungaji wanaogopa kuhubiri au kufun-disha juu ya somo la utoaji kwa sababu wanaogopa washirika watafikiri wachungaji wanataka mali zao. Vilevile washirika wengine hawataki kulisikia somo hili kwa sababu hiyo hiyo. Lakini, wachungaji na viongozi wengine wa Kanisa hawapaswi kuogopa kulifundisha somo hilo. Utoaji ni somo muhimu katika Kanisa. Ingekuwa somo hili ni wazo la wachungaji tu, ningekubali wasi-fundishe. Lakini wazo hilo ni la Mungu mwenyewe na kwa sababu hiyo viongozi wanatakiwa kulifundisha.

• Je, Utoaji unafundishwa katika tawi lako? Viongozi hawajatimiza wajibu wao

Viongozi wanakula mali ya Kanisa - Ni vigumu kuamini lakini wengine wanadai kwamba viongozi wa Kanisa wamekula pesa za Kanisa. Hivyo washirika wanakataa kutoa cho chote kwa sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya faida yao wenyewe. Hii siyo shida ya utoaji, lakini ni shida ya uongozi. Hii ndiyo sababu sadaka zote za Kanisa zinapaswa kuwekwa wazi katika kitabu cha uhasibu ili wote waweze kuona matoleo yote yanatumika kwa kazi zilizolengwa.

Viongozi hawaitumii mali ya Kanisa inavyostahili - Wengine hawadai kwamba viongozi wamekula, isipokuwa hawajazitumia sadaka zao kwa uwakili mzuri. Labda wametangaza kani-sani kwamba wanataka watu kujitoa kwa ajili ya jambo maalum kama vile ujenzi wa kanisa. Watu wanajipa moyo na wanajitahidi kujitoa kwa ujenzi huo. Lakini, baadaye wanaona kwamba kanisa halijengwi na wanataka kujua sababu. Pengine viongozi watajieleza kwamba kulitokea shida ya dharula na ikabidi wazitumie pesa hizo kwa ajili ya shida hiyo. Kwa kawaida mambo kama hayo huivunja mioyo ya washirika. Hasa wanapofikiria sadaka zao ambazo hazikufanya kazi iliyokusudiwa. Washirika wanaweza kufika mahali ambapo wanakata tamaa katika kujitoa tena kanisani.

Mipango mibaya ya viongozi - Pengine viongozi wenyewe ni waaminifu lakini wanakosa uwezo wa kupanga vizuri matumizi ya sadaka za kanisa. Hali hii nayo hukatisha tamaa ya washirika kujitoa. Viongozi wa kanisa wanatakiwa kuwa waaminifu na wenye mipango mizuri inayotimilika. Wakijulikana hivyo watu watakuwa tayari kujitoa. Tena wazo linaloweza kusaidia ni kutengeneza njia ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa mipango hiyo.

Wachungaji hawawajibiki ipasavyo - Biblia inafundisha kwamba ni wajibu wa kanisa ku-wasaidia wachungaji katika mahitaji yao ya kimwili. Washirika wengi wanafahamu hivyo lakini wengine wanakataa kutoa sadaka kwa ajili ya mchungaji wao kwa sababu wanaona mwenyewe hatimizi wajibu wake kama mchungaji. Siyo rahisi kwa mchungaji kuendelea kudai msaada wa kanisa lake wakati hafanyi kazi zake za kichungaji. Hapo ninaweza kukubaliana na washirika kwamba mchungaji hastahili mshahara wakati hafanyi kazi. Lakini kwa wachungaji wanaotimi-za wajibu wao, kanuni ya Biblia inasema yule anayelisha washirika kiroho anastahili kusaidiwa kimwili akichangiwa na washirika wake. Mawasiliano ni muhimu kati ya kanisa na mchungaji ili kila mmoja aweze kuelewa wajibu wake. Ni muhimu vilevile wahudumu wa kanisa watimize wajibu wao au sivyo wasifikiri kanisa linawajibika kuwasaidia.

Page 5: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 5 -

• Kuna mifano ya namna hii katika tawi lako? • Tunaweza kufanya nini ili kurekebisha mambo hayo?

Mungu atunze watumishi wake!

Nimewahi kusikia washirika wengine wakisema juu ya mchungaji wao kwamba yeye ni mtumishi wa Mungu hivyo amtegemee Mungu. Yaani, wanakwepa wajibu wa kumsaidia mchungaji wao wakiinua wazo la kusema ni wajibu wa Mungu. Hawa wamekosa ufahamu kwamba chombo ambacho Mungu anakitumia kuwatunzia watumishi wake ni Kanisa lenyewe na washirika wake.

• Tuwajibuje watu wanaohoji hivyo? Washirika hawajakua kiroho na hawaelewi umuhimu wa utoaji

Washirika wengine wamekuwa ndani ya Kanisa miaka mingi lakini pamoja na hayo wame-baki kama watoto katika Kristo. Labda ni kosa la viongozi kutowalea vizuri, au ni kosa la mshirika mwenyewe ambaye hataki kupiga hatua za kukua kiroho. Kwa vyo vyote vile wako wengine kanisani wanaohitaji kukua ili wawe watu wazima katika Kristo. Biblia inaeleza kwamba mtu mzima katika Kristo ni mtu ambaye ana uhusiano mzuri na Mungu, tena anaelewa Neno la Mungu na mafundisho yake. Mtu huyo anasimama imara ndani ya Kristo na anaujua wajibu wake kama Mkristo. Mtu huyo haoni wajibu huo kuwa mzigo bali kwa sababu anamfa-hamu Mungu wake, anafurahi kuyatimiza yote anayoyataka Mungu.

Wajibu mmojawapo wa kila Mkristo ni kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Washirika wengi hawajauelewa wajibu huo. Maagizo ya kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu ni fundisho lililo wazi ndani ya Biblia. Shida moja iliyopo ni kwamba mara nyingine washirika hawafundishwi kuto-kana na sababu zilizotajwa hapo juu. Hakuna mtu atakayeutimiza wajibu huo bila kuuelewa kuwa ni wajibu wake. Zaidi ya hayo, mtu anaweza akauelewa wajibu wake wa kujitoa na akashindwa kwa sababu ya kutojua namna ya kufanya. Hivyo ni wajibu wa viongozi wa kanisa kuwafahamisha washirika juu ya utoaji ili wasiwe gizani juu ya jambo hilo.

Shida nyingine iliyo kubwa ni wakati watu wanakosa imani. Kama ni kufundishwa, wengine wamekwisha fundishwa. Wajibu wao wa kutoa mali zao kwa ajili ya kazi ya Mungu wanaujua. Kila kitu wanakielewa lakini hawaamini kwamba Mungu anaweza kuwatunza wakijitoa. Wanapofikiria mahitaji yao wanashindwa kumtolea Mungu kwa sababu wanafikiri kwamba hawatabakiwa na vya kutosha kwa ajili ya mahitaji yao. Kama wamebaki na 1000 |=, na Juma-tatu wanahitaji kusaga mahindi mashineni, hawawezi kutoa pesa hizo Jumapili kwa sababu ya kukosa kumwamini Mungu. Hili ni suala la kukua kiroho. Aliye mtu mzima katika Kristo anawe-za akaishi kwa kuziamini ahadi za Mungu.

• Je watu katika tawi lako wamekua kiroho? • Je wewe unamwamini Mungu kiasi gani kuhusu mahitaji yako? • Tuwasaidieje watu wetu ili wakue kiroho?

Hali ya uchumi

Sababu nyingine ya kutojitoa ninayoisikia mara nyingi ni hali ya uchumi. Wakristo wengi wanadai kwamba wangetoa zaidi lakini hawana uwezo. Hasa kama ni mkulima ambaye hana mshahara.

Kwanza ni lazima niseme wazi kwamba uwezo wa kutosha upo ndani ya uchumi wa watu wa Mungu kanisani. Mfano mzuri ni vikundi vya vijana katika makanisa. Tunapoona vijana wanataka kupata chombo cha muziki tunakuta wanafaulu; tena ndani ya muda mfupi. Mwaka 1996 kwaya moja iliniletea shilingi 80,000 ili niwatafutie kinanda. Kwa kuwa nilikuwa kwenye bodi ya Kanisa niliona ripoti za mapato ya tawi lile katika kipindi kile ambacho vijana walitoa pesa hizo. Ripoti ya miezi mitatu ilisema malipo ya mchungaji ilikuwa shilingi 3,000 kwa miezi yote mitatu. Kanisa lilidai hawakuwa na uwezo wa kumlimpa mchungaji wao. Lakini, je, wali-wezaje kupata pesa zote hizo kwa ajili ya chomba cha muziki ikiwa kanisa halikuwa na uwezo?

Mara nyingi vijana wameonesha uwezo wa kuzikusanya pesa nyingi kwa muda mfupi. Sababu ni hamu yao kupata vyombo hivi. Tena kumbuka hawa ni vijana na mapato yao ni ma-

Page 6: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 6 -

dogo ukiwalinganisha na watu wazima ndani ya kanisa. Hakika uwezo upo wa kutosha ndani ya makanisa.

Kumbuka kwamba Mungu haombi watu kujitoa zaidi kuliko uwezo walio nao. Biblia inasema wazi kwamba Mkristo atoe kulingana na uwezo wake. Shida ni kwamba wengi hawatoi kulingana na uwezo wao na badala yake wanajidai hawana uwezo.

Wivu

Hakuna anayetaka kuitwa mwenye wivu. Lakini hii ni sababu moja iliyotolewa kuhusu wale wasiojitoa ipasavyo. Wengine hawajitoi kwa sababu hawataki kuwaona wengine, kama vile wa-chungaji, wakipata kitu kilicho bora kuliko walivyo navyo wenyewe. Bila maelezo nafikiri wote wanaweza kukubaliana nami kwamba hali hii haitakiwi kuwemo kanisani. Wazo la kwamba mtumishi wa Mungu anatakiwa kuishi maisha duni kuliko watu wa kawaida ni wazo lisilo la kweli; tena ni wazo baya. Angalia katika moyo wako na uhakikishe kwamba huna mawazo ya namna hii.

• Je maisha ya mchungaji yanapaswa kuwa duni kuliko washirika wake, sawa na washirika wake, au bora kuliko washirika wake?

• Je tunapojitoa, tunajitoa kwa Mungu au kwa watu watakaopokea mali hizo? • Je umewahi kuwa na wivu juu ya watumishi waliobarikiwa na Mungu?

Lazima utoaji uwe pesa tu

Sababu nyingine inayotolewa ni kwamba watu wanafikiri kujitoa ni suala la pesa. Kwa sababu hii wanapoamka asubuhi ya Jumapili wakikuta hawana pesa wanaona hawawezi kujitoa. Tutajifunza kwamba utoaji na uwakili havihusiani na pesa peke yake. Vinahusu mali, mazao, nguvu, muda, ujuzi, na kila kitu ambacho Mungu amekupa.

Haitanisaidia

Wengine hawajitoi kwa sababu wanafikiri hawatafaidika wenyewe. Wazo hilo limemsahau Mungu, tena ni wazo hafifu la mtu ambaye haoni mbali. Hakika Mungu atamnufaisha yule anayejitoa. Isitoshe, wakati mshirika anajitoa kwa Kanisa lake, ni kwa faida yake kwa kuwa yeye ni mshirika atakayezishiriki huduma hizo bora.

Pamoja na hayo, lazima tuseme, lengo la Mkristo katika kujitoa kwa Mungu wake halipaswi kuwa kufaidika mwenyewe. Mtu mzima katika Kristo ambaye amekua kiroho hujitoa kama shukrani na kwa kuutimiza wajibu wake bila kuitafuta faida yake mwenyewe.

• Je ni lazima anayejitoa afaidike mwenyewe na utoaji wake?

Ndivyo tufanyavyo miaka yote

Wengine wanaiangalia historia wakisema hatujitoi kwa sababu ndivyo tulivyo; au ndiyo desturi yetu. Hilo silo wazo zuri. Kama tufanyavyo miaka yote ni kinyume na Neno la Mungu, wakati umefika wa kubadilika. Ni kitu gani kitakachotawala? Neno la Mungu au desturi zetu?

Page 7: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 7 -

- 2 - Uhusiano wa Mkristo na Mali Zake

Wakristo wana wajibu kujitoa kwa ajili ya Mungu na kazi zake. Tumeshaona baadhi ya vi-

zuizi na udhuru unaotolewa na Wakristo wenyewe walipoulizwa kwenye semina zangu. Sasa tuziangalie baadhi ya sababu nyingine zinazozuia Wakristo wasijitoe ipasavyo. Katika sura hii tunataka kuchambua mawazo mbalimbali kuhusu mali na pesa kwa sababu mara nyingine mawazo yetu kuhusu vitu hivyo hayajanyoka. Mawazo mabaya kuhusu mali na pesa zetu yana-weza kutufanya tusijitoe ipasavyo.

Kwa ujumla tutajifunza kwamba Mungu hajali kiasi cha pesa au mali Mkristo aliyo nayo. Jambo muhimu kwake Mungu ni jinsi gani Mkristo anavyoifikiria na anavyoitumia mali aliyo nayo. Mungu hataki watu waifikirie mali kuliko wanavyomfikiria Mungu mwenyewe. Mungu hataki watu waitafute mali kuliko wanavyomtafuta Mungu. Yaani, haitakiwi mali kupewa kipaumbele katika maisha ya mtu kwa kuwa hali hiyo itaingilia uhusiano wake na Mungu kwa njia mbaya.

Tukishaanza kuwaza vibaya kuhusu mali ndipo tutatetelesha uhusiano wetu na Mungu na zaidi kuipunguza nia yetu ya kujitoa kwake. Tutaanza kutamani mali za wengine na kujaa wivu, pia kumfikiria Mungu kwamba hajali maisha yetu ya pesa na biashara. Mawazo kama hayo yote huharibu saikolojia ya mtu. Ukweli ni kwamba mali ni chombo tu cha kutimiza mahitaji yetu na mahitaji ya kazi za Mungu duniani. Ni kweli tunahitaji mali, lakini zaidi tunamhitaji Mungu. Kuipenda mali mno na kuitumikia, tutaishia katika hasara na masikitiko. Bora tuione mali jinsi Mungu anavyoiona ili tuishi kwa kuzifuata kanuni zake na kwa namna itakavyompendeza yeye. JE, PESA INA UBAYA?

Mawazo yasiyo ya kibiblia

1. Pesa ni chombo cha Shetani. 2. Pesa inasababisha dhambi. 3. Pesa ni nje ya mambo ya kiroho.

Wakristo wengine wanafikiri pesa ni mbaya. Wengine wanasema ni chombo cha Shetani. Wengine wanafikiri ni mbaya kwa sababu inasababisha dhambi katika maisha ya watu wengi. Labda wengine hawasemi pesa ni mbaya lakini wanaiona pesa yao ni kitu kilicho nje ya mambo ya kikanisa. Yaani wanadai pesa siyo kitu cha kiroho. Tena wangesema pesa haiwezi kuwa ta-katifu.

Mawazo kama hayo hutokana na kutoielewa baadhi ya mistari ya Biblia. Tuiangalie mistari hii ili tuweze kuielewa Biblia inafundisha nini. Maana ya kujiwekea hazina mbinguni

Mathayo 6:19-21 - “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi ha-wavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

Wengine wanasema mistari hii inathibitisha kwamba hatupaswi kuwa na pesa wala mali. Kwa haraka inaonekana agizo la Mungu ni kuwa tusijikusanyie mali hapa duniani. Lakini, tunahitaji kuyaelewa mafundisho ya Yesu kwa ndani zaidi. Katika mistari hii hazina ina maana ya kitu kile unachokijali zaidi. Fundisho kuu la mistari hii lahusu hali ya moyo wa mtu, siyo mali aliyo nayo. Kuwa na pesa au mali siyo shida, lakini ukiiangalia mali kuwa hazina ya kuitunza na kuitegemea kwa moyo wako wote, hiyo ndiyo shida. Hazina ya mtu ni kitu anachokipenda kuli-ko vitu vingine. Siyo vizuri kwa mtu kuijali na kuipenda pesa na mali kuliko anavyomjali Mungu na mambo yake. Kama hazina yako ni mambo ya kidunia nina hakika utatoa maisha yako na nguvu zako kuyapata na kuyatunza mambo ya kidunia. Mwisho utakuta lengo lako halijawa na maana kwa sababu vitu hivi vyaweza kuibiwa na utakapokufa huwezi kwenda navyo.

Page 8: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 8 -

Kujiwekea hazina mbinguni haina maana kwamba tunaweka pesa na mali katika mahali fu-lani ili tutakapofika mbinguni tutaweza kuitumia. Kujiwekea hazina mbinguni ni kuyapenda na kuyajali mambo ya Mungu zaidi kuliko mambo yote mengine tukiwepo hapa duniani. Tukifanya hivyo tunajua, pamoja na baraka tutakazopewa hapa duniani, kuna thawabu tutakazopewa tutakapofika mbinguni. Kama katika akili zetu tunafahamu kuwa hazina yetu ni mambo ya mbinguni, ina maana mioyo yetu inayajali na kuyapenda mambo ya Mungu kuliko mambo ya kidunia.

Hivyo mistari hii haijaagiza mtu asiwe na pesa hapa duniani, bali ameagizwa auweke moyo wake katika kuyajali mambo ya Mungu kuliko mambo ya duniani. Kuwa na mali au kutokuwa na mali siyo hoja, bali tunavyofikiri juu ya mali hiyo na juu ya Mungu, ndilo jambo lenye maana.

Maana ya kutotumikia mabwana wawili

Mathayo 6:24 -“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; au atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Mstari huu unalandana na ule wa kuweka hazina mbinguni. Tena mstari huu unatusaidia kuielewa maana ya mistari ile. Tunaambiwa na wengine, kutokana na mstari huu, kwamba mali ni mbaya tena ni dhambi. Wameshindwa kulielewa fundisho la Yesu. Neno kuu katika mstari huu ni “kutumikia”. Msingi wa neno hilo ni utumishi au hata utumwa.

Yesu anaitumia kanuni inayoeleweka duniani. Katika utumishi wo wote duniani hakuna anayeweza kuwa na mabwana wawili. Mtumishi kama mtumishi lazima ayafuate maagizo yote ya bwana wake. Itakuwaje kama bwana moja atamtuma mjini kununua mahitaji yake na bwana mwingine atamtuma shambani kuvuna mahindi kwa wakati mmoja. Itamlazimu, kama mtumishi, amchague mmoja kati ya mabwana hawa ili amtii. Ndiyo maana ya Yesu juu ya mali na Mungu. Kuwa na mali siyo shida usipotawaliwa nayo. Pale ambapo mali inaanza kuyaongoza maisha ya mtu badala ya kuongozwa na Mungu, ndipo kumwacha Mungu na uongozi wake huanza katika maisha ya mtu.

Katika mistari inayofuata Yesu anaongea juu ya watu wanaosumbukia maisha yao, waki-hangaika juu ya mahitaji yao. Yesu anataka kuonesha kwamba wanaweza kumtumikia Mungu na Mungu atawatimizia mahitaji yao yote. Wanaweza kumtegemea Mungu. Lakini pale ambapo wanahangaikia mali, hiyo ndiyo ishara kwamba hawajamtegemea Mungu kama watumishi wake, bali wameanza kuwa watumishi wa mali yao; hali isiyotakiwa.

Tena mstari huu haujasema Wakristo wasiwe na mali, bali ni suala la mali itakuwa na nafasi gani katika maisha yao. Hata wale ambao wanafundisha pesa ni mbaya wanaitumia pesa katika maisha yao. Kama tungesema pesa ni mbaya, ingetubidi tuache kuitumia po pote pale. Lakini, tulishaona, pesa haina ubaya wala uzuri. Ubaya na uzuri upo katika matumizi ya pesa tu. Pesa kama vitu vingine haina ubaya wala uzuri

Pesa yenyewe ni kitu cha kidunia na Mungu ameviumba vitu vyote. Mchungaji Elias Kashambagani anaeleza vizuri juu ya vitu vya dunia hii katika kitabu chake, “Nimefika Mwisho”. Tazama anavyosema:

“Ni muhimu kwetu sisi kutambua ukweli wa Biblia. Mungu aliumba dunia ikiwa nzuri ili pawe nyumbani pa mwanadamu akijipatia mahitaji yake. Neno la Mungu katika Mwanzo mlango wa kwanza hutuambia kuwa baada ya tendo la kuumba kitu au vitu Mungu alisema kazi yake “ni njema.” (Soma Mwanzo 1:4a 12b, 18b, 21b, 25b na 31). Mungu alitegemea vitu alivyoviumba vingetumiwa kwa kusudi jema. Matokeo yake hai-kuwa hivyo. Lakini hayo si makosa ya vitu vyenyewe au yule aliyeviumba bali ni mwa-nadamu ambaye alivuruga mpango mzuri wa Mungu.”

Mchungaji Elias Kashambagani anatoa mawazo matatu juu ya pesa yaliyo ya kibiblia. (1) Vitu havina wema ndani yake. Viko katikati, si vyema wala viovu, mwanadamu

anapaswa kuwa ndiye mwadilifu. Vitu ni njia yake kumwezesha awe tajiri au apate ma-tumizi kama pesa na vitu vinginevyo.

Page 9: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 9 -

(2) Vitu ni vyombo na vifaa. Vinafaa na ni muhimu lakini si vya milele. Vitu vinaisha au kuachwa, vinapofanywa kuwa vya milele huwa sanamu ya kuabudiwa, hasa vinap-omtawala mwanadamu na kuichukua nafasi ya Mungu.

(3) Vitu vinapaswa kutumiwa badala ya kuleta uchoyo na ubahili. Watu wengine leo hufanana na tajiri yule mjinga katika Luka 12:13-21. Akalimbikiza pesa kwa ajili ya mai-sha yake yote. Mungu anatutazamia kuzitumia pesa alizotupa kwa ajili ya mahitaji ya ja-maa zetu, sisi wenyewe, neema kwa wengine na kwa ajili ya ufalme wa Mungu hapa du-niani.

Kufuatana na mawazo hayo tunaweza kusema Mungu aliumba vitu vyote, pamoja na mali zote akisema vyote ni vyema. Hivyo, mali haina ubaya lakini inaweza kutumika kwa mambo mazuri au mabaya. Hata Yesu alitumia pesa na mali alipoishi duniani.

• Katika maisha yako unawekaje hazina mbinguni? • Kwa nini haiwezekani kumtumikia Mungu na mali wakati mmoja? • Je, pesa ni nzuri au ni mbaya? Kwa nini?

MKRISTO ASIZIDI SHILINGI NGAPI ILI ASIYAHARIBU MAISHA YAKE YA KIROHO? Wazo moja linalosikika mara nyingine ni kwamba walio maskini zaidi ndiyo wenye maisha

bora zaidi ya kiroho. Wazo hilo siyo kweli lakini wanaofikiri hivyo wanaweza kujiuliza swali kama hili, “Mkristo anaweza kuwa na kiasi gani cha pesa bila kuyaharibu maisha yake ya kiroho?” Wazo ni kwamba kuna kiwango fulani cha pesa, na kama Mkristo atazidisha kiwango hicho, atauona upungufu katika maisha yake ya kiroho. Isitoshe, wengine wangesema anayezid-isha kiwango hicho hawezi kuwa Mkristo.

Mawazo hayo hutokana na wazo la kwamba pesa na mambo ya kiroho haviendani. Lakini kama tulivyoona tayari, pesa yenyewe haina ubaya. Cha muhimu ni jinsi gani tunavyozitumia pesa zetu. Maana ya “Heri walio maskini wa roho”

Mathayo 5:3 - “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.”

Wapo wengine wanaosema mstari huu unafundisha kwamba umaskini ni kitu kizuri kwa sababu walio maskini wataingia mbinguni. Kosa lao ni kufikiri kwamba neno “maskini” katika mstari huu linazungumzia umaskini wa pesa. Wanadai mtu ambaye ni maskini hana uwezo wa kujisaidia na hivyo yuko tayari kumtegemea Mungu, yaani, hana budi kumtegemea Mungu na matokeo yake maskini anakuwa mtu wa kiroho. Pili wanadai kwamba walio maskini hawazijali pesa (ndiyo maana wenyewe ni maskini) na hawapotezi nguvu zao katika kuyafuata mambo ya kidunia bali wanaweka nguvu zao katika kumjua Mungu na kumtumikia.

Tuanze na neno hilo “maskini” katika mstari huu. Ni kweli maana ya kawaida ya neno “maskini” ni ufukara, umaskini wa mali, pesa, au mahitaji, yaani vitu vya kidunia. Lakini wakati wo wote unapotaka kujua maana ya neno kwa jinsi mtu alivyomaanisha, ni lazima uangalie mazingira ya neno lile ndani ya sentensi yake. Yesu alisema, “Heri walio maskini wa roho.” “Wa roho” ni mazingira yanayoeleza maana ya neno “maskini” katika sentensi hii. Yesu hajasema “Heri walio maskini wa pesa au mali.” Hivyo ni lazima tujiulize maana ya “maskini wa roho”. Mtu ambaye ni maskini wa roho ni mtu ambaye amejinyenyekeza. Ni mtu ambaye anajua hawezi bila Mungu. Anajua anauhitaji msamaha wa Mungu. Tabia yake ni tabia ya kauli nzuri mbele ya Mungu akijua bila msaada wa Mungu hajiwezi. Ndilo fundisho la mstari huu. Yule ambaye ana-jinyenyekeza mbele ya Mungu na anamtegemea Mungu kwa vitu vyote ndani ya maisha yake, pamoja na msamaha na wokovu, atapewa ruhusa kuingia mbinguni.

Sasa tujibu dai lao la kwanza. Wanadai mtu aliye maskini yuko tayari kumtegemea Mungu. Nakuuliza, wote walio maskini wanamtegemea Mungu? Hapana. Kuwa maskini siyo kusema moja kwa moja mtu atamtegemea Mungu. Hakika kuna wengi sana walio maskini ambao wanaendelea kujitegemea katika mambo yote yakiwa mahitaji ya kimwili au hata ya kiroho. Kwa hiyo haifuati kusema yule aliye maskini wa pesa ataingia mbinguni. Siyo suala la utajiri wala umaskini wa mali. Tukiangalia matajiri tunakuta kuna wengine wanaomtegemea Mungu na wengine ambao hawamtegemei.

Page 10: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 10 -

Suala lenyewe linahusu hali ya moyo wa mtu na jinsi anavyojiwasilisha mbele ya Mungu bila kuhesabu huyu ni tajiri au maskini wa mali. Kwa mfano tuangalie mfano mmoja Yesu aliuo-toa juu ya mtoza ushuru na Farisayo katika Luka 18:10-14. Wote wawili walienda hekaluni kuomba kwa Mungu. Farisayo yule alikuwa mfano wa mtu asiye maskini wa roho. Alipoomba alitaka kumwonesha Mungu mambo yote mazuri aliyoyafanya. Akashukuru kwa sababu hakuwa kama wengine - wadhalimu na wazinzi. Akaonesha jinsi alivyoweza kuifuata Sheria ya Musa katika kufunga na kutoa zaka. Farisayo huyu hakumtegemea Mungu po pote pale bali alifika mbele ya Mungu akiwa na kiburi na hali ya kutangaza uzuri wake mbele za Mungu. Maneno yake yalijaribu kuthibitisha anastahili vyote vinavyotoka kwa Mungu kwa sababu ya matendo yake mema katika kujitegemea. Tofauti kati ya Farisayo huyu na mtoza ushuru huyu ni kwamba mtoza ushuru hakudai cho chote, bali alijinyenyekeza mbele ya Mungu akiomba msamaha na rehema ya Mungu kwa sababu alijua hajiwezi. Alijua mbele ya Mungu yeye ni mwenye dhambi na hakuna anachoweza kukifanya ili astahili neema ya Mungu. Hivyo alikuwa maskini wa roho mbele ya Mungu. Yesu alisema kwa sababu hiyo alihesabiwa haki na kwa maana hiyo anayo nafasi mbinguni. Yesu hakuongelea cho chote juu ya utajiri wala umaskini wa mali katika mis-tari hii kwa sababu kiasi cha pesa mtu alicho nacho hakina uhusiano na jinsi mtu anavyompendeza Mungu.

Sasa tuangalie dai lao la pili. Wanasema walio maskini hawajali pesa na hawapotezi nguvu zao katika kutafuta utajiri wa dunia hii. Tunapowatazama maskini tunaowafahamu tunajua mo-ja kwa moja wazo hilo si kweli. Kutokuwa na mali haina maana mtu haitafuti au haitaki mali. Wapo wengi sana, walio maskini, ambao wanaweka nguvu zao zote katika kupata mali. Ni kweli kuna matajiri ambao wana nia moja katika maisha yao, kupata mali zaidi. Lakini hatuwezi kumyoshea kidole mtu mwenye pesa na kumdharau tukisema yeye hayajali mambo ya Mungu bali mambo ya pesa tu. Wala hatuwezi kumtazama maskini na kusema kwa sababu hana pesa ina maana anayajali mambo ya Mungu tu, na siyo mambo ya pesa. Tukumbuke kwamba kuwa na mali au kutokuwa na mali siyo hoja mbele ya Mungu. Mungu anachojali ni hali ya moyo wa mtu mbele yake. Jinsi anavyozitumia mali zake ni ishara ya hali ya moyo wake, siyo kiasi cha pesa alizo nazo. Maana ya Yesu kutamka maskini watakuwepo siku zote

Yohana 12:8 - “Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi...”

Wengine wanasema mstari huu unafundisha kwamba Mungu anaukubali umaskini wa mali. Yaani, wanasema, Mungu anataka wengine wawe maskini kila wakati. Wazo hilo si kweli. Mstari huu haufundishi hivyo. Hakuna mistari ndani ya Biblia inayosema umaskini wa mali ni baraka wala hali inayotakiwa. Yesu alikuwa anasema ukweli ambao upo duniani alipotamka sentensi hii. Ni kweli wakati wote kutakuwa maskini. Lakini Yesu hakusema Mungu anataka iwe hivyo. Hakika, tunaweza kusema Mungu hataki iwe hivyo.

Tunapoangalia mazingira ya mstari huu tunaelewa maana ya Yesu. Yesu alikuwa kwenye nyumba ya Mariamu, Martha na Lazaro. Ilikuwa yapata wiki moja kabla hajafa msalabani na Yesu alijua alikuwa amebakiwa na muda mfupi duniani. Mariamu aliitwaa ratli ya marhamu ya nardo safi, yenye thamani nyingi, akaipaka juu ya miguu ya Yesu. Yuda alinun’gunika akisema wangeweza kuzitoa pesa hizo kwa ajili ya walio maskini. Yohana alieleza hali ya moyo wa Yuda. Alisema Yuda hakujali maskini kweli, bali hakupenda jinsi Mariamu alivyotenda kwa sababu mwenyewe alikuwa mwizi akinufaika na pesa za mfuko wa kumi na wawili wale. Mwishowe Yesu akajibu kwamba maskini watakuwepo muda wote lakini yeye mwenyewe atakuwepo kwa muda mfupi tu. Maana yake ilikuwa kwamba yeye mwenyewe ana umuhimu kama mwana wa Mungu anayekaribia kifo msalabani. Mariamu alikuwa anaonesha jinsi alivyoyaelewa mambo yale ambayo Mungu alikuwa anayafanya ndani ya Yesu. Yuda hakuyajali mambo ya Mungu wala walio maskini, yeye alijali pesa tu. Yesu alitaka kuonesha kwamba ilikuwa halali kwa Mariamu kufanya tendo hilo la kumwabudu Yesu kabla hajafa kwa kuwa thamani ya Yesu ni kubwa kuliko thamani ya vitu vile hata kuliko mahitaji ya walio maskini. Yaani, kwa kawaida ingekuwa vema zaidi kuwasaidia maskini lakini kipindi hiki kilikuwa maalum ambacho hakitarudiwa tena kwa kuwa Yesu alikuja kufa duniani mara moja tu.

Page 11: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 11 -

Hivyo tunasema Mungu haukubali umaskini wa pesa ingawa utaendelea kuwepo kwa sababu dunia hii imeharibiwa na dhambi. Mungu anapowaagiza watu wake, tena na tena, ku-wasaidia walio maskini, inathibitisha Mungu anaijali hali ya maskini. Lakini Yesu alikubali tendo la Mariamu kwa sababu ilikuwa tukio maalum siku chache kabla ya kifo chake.

Maana ya kupenda fedha kuwa shina la mabaya

1 Timotheo 6:10 – “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

Mstari huu haujasema fedha au mali ni mbaya. Bali unadai ubaya unapatikana katika moyo wa mtu ambaye anapenda fedha kuliko mambo mengine yaliyo muhimu zaidi.

Maana ya Yesu kumwambia tajiri auze vyote

Luka 18:18-27 (22) -”Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.”

Tajiri huyu alitimiza sheria nyingi za Musa lakini alikosea sheria kuu ya kumpenda Mungu kuliko mambo yote mengine – yaani ampende Mungu kwa moyo wake wote. Sheria ya Musa haisemi ni lazima kila mtu atoe mali yake yote kwa maskini kama Yesu alivyomwomba afanye. Lakini tajiri huyu aliupenda utajiri wake kuliko alivyompenda Mungu na Yesu aliujua moyo wake. Ndiyo sababu alimpima na kuibainisha bayana hali yake kwa kumwagiza kuuza vyote alivyokuwa navyo na kuwapa walio maskini. Kwa sababu tajiri huyu alipenda utajiri wake kuli-ko Mungu alishindwa kumtii Yesu.

Maana ya ngamia kupita katika tundu la sindano

Luka 18:24-25 - “Yesu alipoona vile alisema, kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu! Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajri kuingia katika ufalme wa Mungu.”

Ngamia hawezi kupita kwenye tundu la sindano. Yesu anatumia mfano huu, akitia chumvi, kuonesha jinsi ilivyo rahisi kwa mtu tajiri kujitegemea na kutomtegemea Mungu. Hakika mataji-ri waliookoka ni wengi ambao wataenda mbinguni kwa sababu wameamua kumtegemea Mun-gu. Lakini, Yesu anazidisha mfano wake kuonesha jinsi ilivyo vigumu kwa mtu kumtegemea Mungu wakati anaweza kujitegemea katika dunia hii kutokana na utajiri wake.

Maana ya matajiri kutotumainia utajiri wao

1 Timotheo 6:17-19 – “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wa-siutumainie utajiri usiyo yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvi-tumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.”

Fundisho hilo la Paulo linafanana na lile Yesu alilofundisha katika Luka 18; yaani ni rahisi kwa matajiri kutomtegemea Mungu na badala yake kuutegemea utajiri wao. Paulo hajaagiza matajiri waachane na mali zao. Paulo hajasema matajiri hawawezi kuwa Wakristo. Bali, Paulo amesema wasiutumainie utajiri wao, bali wamtumainie Mungu. Mwisho

Tuliianza sehemu hii tukiuliza swali, “Mkristo asizidi shilingi ngapi ili asiyaharibu maisha yake ya kiroho?” Jibu letu ni: Hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kumharibu Mkristo. Kinachowaharibu Wakristo ni kutomtegemea Mungu.

• Kama pesa haina ubaya, ni kitu gani kinachofanya pesa kuwa mbaya katika maisha yetu? • Kwa nini Yesu alimwambia tajiri auze yote wakati kufanya hivyo siyo sharti la kupata

uzima wa milele?

Page 12: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 12 -

• Yesu aliposema, “heri walio maskini wa roho”, alikuwa na maana gani? • Kwa nini ni vigumu zaidi kwa matajiri kumtegemea Mungu?

PESA INA NAFASI GANI KATIKA MAISHA YAKO? Pesa ni kitu kilicho cha lazima katika kuishi hapa duniani. Bila kutumia pesa huwezi kuishi.

Kwa sababu pesa ni lazima inatakiwa tujiulize uhusiano wetu na pesa ukoje.

Je pesa ina nafasi ya ibada ya sanamu katika maisha yako?

Ni vigumu kufikiri Mkristo anaweza kuabudu sanamu. Biblia inasema wazi kwamba kuna Mungu mmoja na watu hawapaswi kukiabudu kingine cho chote kama sanamu. Zamani mababu zetu waliabudu sanamu nyingi. Hata leo wengine wanaendelea kuviabudu vitu kama milima, maziwa, au miungu mingine isiyo Mungu wa kweli. Sanamu ni nini? Kawaida, tunapofikiri juu ya sanamu tunawaza kitu kilichochongwa na mwanadamu, kama vile jiwe au mti. Lakini ukweli ni kwamba sanamu inaweza kuwa kitu cho chote tunachokiweka juu kuliko Mungu. Yaani cho chote tunachokiamini au kukitegemea kuliko tunavyomtegemea Mungu wa kweli. Hivyo pesa au utajiri unaweza kuwa sanamu.

Wakolosai 3:5-6 - “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu: Kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Ujiulize kama unazitegemea pesa kuliko Mungu. Ujiulize kama unapenda pesa kuliko Mun-gu. Nafikiri Wakristo wote wangesema wanampenda Mungu kuliko pesa. Lakini mara nyingine ukiangalia maisha yao unaweza kupata picha nyingine. Unaweza kufikiri kwa matendo yao kwamba wanajali pesa kuliko Mungu. Maswali haya yafuatayo yanaweza kukuonesha unachokipenda zaidi, pesa au Mungu.

• Unatumia muda gani kufikiria pesa zako kila siku? • Unatumia muda gani kufikiri jinsi utakavyoweza kupata pesa zaidi? • Unatumia muda gani kutafakari jinsi biashara yako inavyoendelea?. • Unatumia muda gani katika kazi za kutimiza mahitaji yako? • Sasa unatumia muda gani katika maombi na kusoma Neno la Mungu kila siku? • Unapokutana na familia yako na marafiki zako, je, unaongea mambo gani zaidi? Unaon-

gea mambo kama bei ya mahindi au shida uliyo nayo ya pesa, au zaidi unaongelea jambo jipya ulilojifunza juu ya Mungu au mambo mengine ya kiroho?

• Unatumia muda gani kuhesabu pesa zako na kutunza kumbukumbu?

Ukijibu maswali haya kiukweli utaona Wakristo wengi tunatumia muda mwingi katika mambo yanayohusiana na pesa, na muda mchache katika mambo ya kiroho. Tunahitaji kuhakikisha kuwa Mungu ni namba moja katika maisha yetu. Hatutaki pesa na utajiri vichukue nafasi ya kwanza katika maisha yetu na kuwa kama sanamu tunayoiabudu.

Sisi sote tunachezea mali kila siku. Tunanunua vitu kwa ajili ya mahitaji yetu. Tunaingiza pesa zetu katika biashara zilizo mpya kwa tumaini la kutajirika zaidi. Lakini mara nyingi wakati mambo haya yanaendelea kutokea tunasahau kumwomba Mungu ili tupate kuyajua mapenzi na hekima yake. Hii ni ishara kwamba tumeona mambo ya pesa na bishara hayahusiki katika mambo ya kiroho. Pia ni ishara kwamba tumetegemea pesa na kujitegemea kuliko kumtegemea Mungu. Tunapomwacha Mungu nje ya mambo yetu ya pesa na biashara tuko katika hatari ya kuzikosa baraka za Mungu katika maisha yetu.

Je, pesa ina nafasi ya wivu na tamaa katika maisha yako?

Nimewahi kuwasikia watu wakisema wangependa kuwa na pesa kama zile za mtu fulani waliyemtaja. Kwa kawaida, anayeongea ni mtu maskini, lakini angependa kuwa na pesa kama zile za mtu fulani aliye tajiri. Huwa katika maongezi haya maskini yule anaanza kutaja mambo yale ambayo angeyafanya angekuwa na pesa zile.

Page 13: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 13 -

Mara nyingi mtu mwenye wivu wa mali ya mwingine anajisikia kama yeye amedhulumiwa. Pengine anafikiri Mungu hajamtendea haki. Au anafikiri matajiri wamechukua kilicho chake. Huwa watu hawa wanafikiri matajiri wote wamepata utajiri wao kwa njia ya wizi au ni walanguzi. Ni kweli inatokea hivyo lakini tukubali kwamba wapo matajiri wengi waliotajirika kwa kutoa jasho na kutumia pesa zao kwa busara tu.

Kwa kawaida watu wenye wivu hawana raha. Kila siku wanailalamikia hali yao. Huwa ni wazembe ambao hawataki kujisaidia, wanataka kila kitu bure. Biblia inasema wazi juu ya watu wa namna hiyo.

Mithali 21:25-26 - “Matakwa yake mtu mvivu humfisha, kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi. Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa; bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.”

Kutoka 20:17 - “Usitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”

Kutokuwa na wivu ni agizo la Mungu. Wivu unaweza kuyatawala maisha ya mtu akitamani vitu vya wengine. Hali hii ni mbaya kwa sababu inasababisha mtu alalamike na kutomtumikia Mungu ipasavyo. Tena inamfanya mtu akose raha na amani vilivyokusudiwa na Mungu.

Je, pesa ina nafasi ya tamaa ya kutajirika katika maisha yako?

Siyo lazima tamaa iangalie vile wengine walivyo navyo. Tamaa ya wengine ni juu ya utajiri kwa ujumla bila kuangalia watu wengine. Watu kama hawa wana shabaha moja katika maisha yao; kutajirika. Kawaida watu wa namna hii siyo wazembe. Wanaweka bidii yao yote na akili zao zote katika mbinu za kutajirika. Wako tayari kujikana ili waweze kutajirika. Wengine wanaacha wajibu wao kama baba au mama tena kama mume au mke ili waweke nguvu zote katika kutaji-rika. Hivyo familia zao zinaweza kuvunjika kwa sababu ya kutafuta pesa. Ikitokea wachague kati ya rafiki na pesa, pesa zinashinda kila mara. Kusema uongo au kuwadanganya hata marafiki zao si kitu kama matokeo ni utajiri zaidi:

Mithali 15:27 - “Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe.”

Waebrenia 13:5-6 - “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubu-tu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

1 Timotheo 3:3 - “...Wala asiwe mwenye kupenda fedha;”

1 Timotheo 6:10 - “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

Je, pesa ina nafasi ya chombo ukitumiacho kisicho na uzuri wala ubaya katika maisha yako?

Kama tulivyoona tayari pesa haina ubaya. Tunaweza kuongeza wazo jingine; pesa haina uzuri. Pesa yenyewe ni chombo tu. Ni chombo ambacho mtu anaweza kukitumia kwa mambo mazuri au mambo mabaya. Ukichukua 8000 tsh. na kununua pombe, unazitumia pesa kwa njia mbaya. Pesa hizo zitaleta ubaya na uharibifu ndani ya maisha yako. Lakini ukitumia 8000 tsh. kununua Biblia kwa ajili ya mtu fulani, pesa zile zitaleta uzuri na uzima. Siyo suala la pesa yenyewe bali ni suala la jinsi unavyoitumia.

Mungu haoni pesa kuwa mbaya wala nzuri. Anachojali Mungu, ni mawazo yetu juu ya pesa na matumizi yetu ya pesa. Tunaweza kuwa na pesa kiasi kidogo au kiasi kikubwa; cha muhimu ni jinsi tunavyofikiri juu ya pesa hiyo. Biblia inasema:

Mithali 23:7 - “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.”

Yaani tunavyofikiri ndivyo tulivyo. Kama katika mawazo yetu tunategemea pesa kuliko Mungu sisi ni waabudu sanamu ya pesa. Tukitamani utajiri wa wengine katika mawazo yetu ina maana tuna uhusiano mbaya na pesa. Matendo yetu ni muhimu kwa sababu yanaonesha jinsi tulivyo. Tunaweza kuongea kwa namna moja lakini kama matendo yetu hayaendani na tuna-vyosema, tunajulikana kwa jinsi tulivyo si kwa jinsi tunavyosema.

Page 14: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 14 -

Mada ya sura hii inahusu uhusiano kati ya Mkristo na mali. Tumeonesha Biblia haijali kiasi cha mali Mkristo alicho nacho. Tena Biblia hufundisha mali si kitu kibaya wala kizuri machoni pa Mungu. Mungu anajali tu jinsi Wakristo wanavyowaza kuhusu pesa na wanavyozitumia. Mkristo hapaswi kuwa na wivu au tamaa kuhusu pesa. Mkristo hapaswi kutafuta pesa kuliko anavyomtafuta Mungu. Mkristo hapaswi kuona pesa ni muhimu kuliko Mungu. Bali Mkristo aone pesa kuwa chombo cha kukitumia kwa ajili ya mahitaji yake na kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kuendeleza kazi zake hapa duniani.

Wakati Wakristo wanawaza vibaya kuhusu pesa na mali, uhusiano wao na Mungu huharibika na pia kazi ya Mungu inaathirika. Mawazo mabaya kuhusu mali (kama vile kui-tegemea, wivu, tamaa, n.k.) huwafanya Wakristo wasijitoe ipasavyo. Maana, ni vigumu mtu anayezitamani pesa azitoe pesa zake kwa ajili ya kazi ya Mungu.

• Eleza jinsi kujitoa maisha yote kwa ajili ya kutajirika ni kama kuabudu sanamu? • Je, una wivu juu ya vitu vya watu wengine katika maisha yako? Kuna haja ya kutubu na

kubadilisha mawazo yako kuhusu mali? • Je, kuna tamaa katika maisha yako? Ufanye nini kuachana na hali za tamaa?

MUNGU ANAJALI KILA SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO 1 Wakorintho 10:31 – “Basi mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa

utukufu wa Mungu.”

Wakristo wengi wanayagawa maisha yao katika sehemu kadhaa. Sehemu moja ni sehemu ya Kanisa au ukristo. Sehemu hii ina nyakati zake na kanuni zake. Kwa mfano Jumapili ni siku ya kwenda kanisani. Tena wanapoenda kanisani ziko njia za kujifanya kulingana na mahali walipo. Kwa mfano katika nyakati zile za ukristo wanaangalia usemi wao ili wasiseme mambo ya-siyotakiwa. Wanazibeba Biblia zao, na kila kitu wanachokifanya kinaendana na mambo ya kiroho.

Sehemu nyingine inaweza kuwa biashara yao. Kwa wengine, sehemu hiyo ya biashara haina uhusiano na sehemu ile ya ukristo. Hivyo unaweza ukayakuta mambo yasiyoendana na mambo ya kikristo katika biashara zao. Wamezitenganisha sehemu hizo katika maisha yao, na hawaru-husu kanuni za kiroho kuingilia kanuni za biashara.

Lakini Wakristo hawapaswi kuishi hivyo. Kwa mfano, Wakristo hawapaswi kusema uongo au hata kuvunja sheria za nchi katika sehemu yo yote ya maisha yao, iwe ni ndani ya familia yao, biashara yao, starehe zao n.k. Inasikitisha, lakini, mara nyingi katika biashara tunaona Wakristo wakiachana na mambo ya kiroho ili waendeshe biashara zao kwa kanuni za kidunia. Kwa mfano Wakristo wengine wanakwepa kulipa ushuru wa mazao yao. Pengine wanapoulizwa juu ya kiasi cha mazao waliyo nayo wanaweza kusema uongo ili kiasi cha ushuru kipungue. Wengine wakienda mjini kuuza mazao wanapita njia za panya kusudi wasipite sehemu ile wanapotoza ushuru.

Wengi wanahesabu sehemu ya ukristo kuwa tofauti na sehemu ya biashara. Wanazigawa kwa namna ambayo inaonesha hakuna uhusiano wo wote ule. Wanafikiri Mungu anayajali mai-sha yao ya kiroho, lakini hayajali maisha yao ya kibiashara. Zaidi ya kutojali sehemu ya biashara wanafikiri Mungu haitazami sehemu hiyo. Ndiyo sababu hawauoni umuhimu wa kuziendesha biashara zao kwa namna inayoweza kumpendeza Mungu.

Lakini Mungu hayagawanyi maisha ya Wakristo katika sehemu kadha wa kadha ambazo zinatofautiana. Mungu anaona Mkristo ana maisha ya aina moja tu. Kila sehemu ya maisha haya ina uhusiano na sehemu nyingine zote. Hakuna maisha ya ukristo yaliyo na sehemu nyingi zilizo tofauti. Maisha ya kiroho yanahusika katika kila sehemu ya maisha ya Wakristo. Kama ni mam-bo ya familia, biashara, urafiki, kazi, mahitaji, au michezo, vyote vinahusika na ukristo wa Mkristo.

Page 15: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 15 -

- 3 -

Page 16: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 16 -

-3- Raha ya Kweli

Tumeona ni muhimu kuielewa nafasi ya mali katika maisha yetu kufuatana na ukweli wa Neno la Mungu. Tukiwa na mawazo mabaya kuhusu mali tutakula hasara katika maisha yetu ya kiroho na vilevile kazi ya Mungu itadumaa kwa sababu ni vigumu kutoa mali zetu kwa Mungu wakati mawazo yetu hayajanyoka kuhusu mali.

Katika sura hii tunataka kuangalia kizuizi kingine kinachozuia watu wasimtolee Mungu ipasavyo. Mada ya sura hii inahusu mawazo yaliyo katika mioyo ya watu. Yaani, wanadamu wote wanatafuta kitu kimoja kwa bidii katika maisha yao yote. Kitu wanachokitafuta ni raha ya kweli, yaani raha inayoridhisha ili waweze kutulia katika hali ya amani wakilala vizuri na kuamka kila siku na hamu ya kuishi maisha waliyo nayo.

Kutafuta kuwa na raha ya kweli ni jambo zuri. Hata Mungu anataka kila mwanadamu awe na raha ya kweli. Lakini hatari ya kuitafuta raha ya kweli imo katika njia ambayo mtu atatumia kuitafuta. Ziko njia nyingi za kuitafuta raha ya kweli lakini kuna njia moja tu inayoweza kuileta raha hiyo katika maisha ya mtu. Njia zote nyingine ni za uongo. Zinaahadi kuleta raha lakini daima hazifanikishi lengo lenyewe. Badala yake njia hizo za uongo zinawaharibu watu pia zi-naiharibu kazi ya Mungu duniani.

Pamoja na uharibifu wa njia hizo mbaya utashangaa kujua njia hizo zinafuatwa sana na wanadamu, hata Wakristo. Wakristo wakishaziamini njia hizo za uongo wanajikuta wanashindwa kujitoa kwa Mungu wao ipasavyo. Hivyo wanakula hasara mara mbili. Kwanza hawafanikishi lengo lao la kuwa na raha ya kweli na pili wanakosa baraka za Mungu kwa kuwa wanaishi kwa njia isiyompendeza Mungu. Isitoshe huduma za Mungu zinaumia kwa kuwa Wa-kristo ambao wangejitoa kuzisukuma huduma hizo hawafanyi kwa kuwa wamevutwa na mawazo ya kidunia wakitafuta raha kwa njia zake.

Katika sura hii tutajifunza njia peke ya kupata raha ya kweli ni njia ya Mungu, tena ni zawa-di kutoka kwa Mungu. Tukizifuata kanuni za Mungu katika maisha yetu tutapata faida ya kuwa na raha ya kweli na pia kazi ya Mungu duniani itafaidika kwa kuwa hatutaogopa kujitoa ipasavyo. Yaani, hatutafikiri tunahitaji kuchagua kati ya kumfuata Mungu na kuwa na raha ya kweli. Tutajua vitu hivi viwili vinaendana na tutajua katika kutomtii Mungu ndipo tutakosa raha ile tunayoitafuta.

WATU WANATAKA NINI KATIKA MAISHA YAO?

Katika kuuliza swali hilo nimewahi kupewa majibu mengi. Tunachokitafuta ni kuyajua

mambo gani yanayotamaniwa zaidi. Pata muda wa kufikiri juu ya yale unayoyataka katika mai-sha yako. Majibu mbalimbali ni kama yafuatayo:

Pesa Nyumba kubwa Chakula Umaarufu Utajiri Gari Mavazi Kupendwa Amani Usalama Akiba Mamlaka Raha Elimu Uzima Watoto wengi

Ukiiangalia orodha hii utakuta kwamba kuna vikundi viwili. Kimoja ni vitu ambavyo tuna-weza kuwa navyo na cha pili ni jinsi tunavyojisikia. Mimi nafikiri kitu kinachotafutwa hasa ni “Raha”. Vyote vingine vinakiangalia kitu hiki kimoja. Kama ni pesa au vitu, vinatafutwa kusudi vimpe mtu raha. Pesa yenyewe ni kitu ambacho hakina maana bila kukitumia. Yaani chenyewe hakiliwi wala chenyewe hakileti raha. Lakini watu wanaitaka pesa kwa sababu wanafikiri wanaweza kuinunua raha. Hawataki gari ili wawe nalo gari, bali wanalitaka gari kusudi liwape raha. Hata elimu au mamlaka havifai vyenyewe. Mtu anaitaka elimu au mamlaka kwa sababu anafikiri itampa raha. Ukiwa na usalama ina maana unayo raha. Bila usalama hakuna raha. Ni-najaribu kuonesha lengo kuu la kila mtu ni kupata raha na vitu vyote vingine vinavyotamaniwa vinatafutwa kwa lengo hilo moja la kuwa na raha.

Page 17: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 17 -

NJIA ZA KIDUNIA HAZILETI RAHA YA KWELI Wote wanaitafuta raha ya kweli, tena raha inayodumu ambayo inautuliza moyo wa mtu

aweze kupumzika na kujisikia vizuri. Hii ni kweli kwa Wakristo na Wapagani pia. Kufanikiwa kunategemea jinsi wanavyoitafuta raha hiyo.

Mfano wa utajiri wa mali

Dunia hii inaamini kwamba raha ya kweli iko ndani ya mambo ya kidunia. Ndiyo sababu watu wanalenga kutajirika. Ni shabaha ya kila mtu kutafuta namna gani atakavyoweza kuyaon-geza mapato yake. Inasababisha wengine kuingia katika wizi kwa sababu wanataka utajiri wa haraka. Ingawa wanalenga utajiri, shabaha ya kweli ni kwamba wanaitafuta raha. Kwa ujumla mawazo yao ni kufikiri utajiri utawaletea raha.

Lakini tunaona kwamba matajiri wakuu katika dunia hii bado hawajatosheka. Kila mmoja anasema, “Nikishapata kiasi hiki nitatosheka.” Lakini kila mara wanapofikia kiasi kile wali-chokitaja, wanaweka malengo mapya. Hii ni kwa sababu kiasi walicholenga hakikuwaridhisha kama walivyofikiri kitafanya. Lakini badala ya kukubali kwamba utajiri hauleti raha ya kweli, wanaendelea na wazo lile lile wakidai kwamba itapatikana katika kiasi kikubwa zaidi. Wapo watu katika dunia hii walio na utajiri sawa na baadhi ya nchi. Hata kama wangetumia shilingi bilioni moja kila siku wasingezimaliza pesa zao zote kabla hawajafa. Lakini utakuta hawa hawa ni wa kwanza kufika kazini kila asubuhi. Hawa hawa wanachemsha bongo kila siku ili wapate pesa zaidi. Amini, usiamini, hakuna raha ya kweli katika utajiri.

Mfano wa ulevi

Angalia mtu anayetafuta raha katika pombe. Kila siku analewa ili awe na raha. Ni kweli ku-na raha kiasi ndani ya pombe (ingawa ni raha ya kudanganya). Shida yake ni kwamba raha yake haidumu. Kesho yake ni lazima alewe tena kwa sababu raha imekwisha. Zaidi ya kuleta raha pombe inaleta hasara. Familia za walevi zinavunjika. Mahitaji yao ya kila siku hayatimizwi kwa sababu pesa na mali zimeliwa na gharama za pombe.

Mfano wa Sulemani

Tuuangalie mfano wa Mfalme Sulemani katika Biblia. Sulemani aliitafuta raha kwa njia za kidunia. Mwisho aliweza kusema njia hizi hazifai katika kuleta raha ya kweli. Lengo lake kuu lilikuwa kuona maana katika maisha yake. Maana inayodumu. Laiti angeliyaona maisha yenye maana, angeliweza kutulia na kuiona raha. Tuone jinsi alivyoitafuta na jinsi alivyoamua juu ya njia hizo. Mwisho tujifunze kutokana na majaribio yake.

Mhubiri 2:1 - “Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha; basi uji-furahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.”

Sulemani alizijaribu anasa. Akatafuta vitu katika dunia hii vinavyoleta raha kwa njia ya kuuburudisha mwili na mawazo. Kwa mfano alioa wake wengi akifikiri inaweza kumletea raha akijifurahisha na hawa wote. Biblia inasema alikuwa na wake 700 na masuria 300. Lakini ndani ya mambo ya namna hii akaona hakuna maana, hakupata raha ya kweli.

Mhubiri 2:2 - “Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini?”

Hata mambo ya kuchekesha hayakufaa. Wengi wanapenda kukaa na wenzao na kusikia hadithi zinazochekesha. Lakini hata hii haidumu. Wakishatawanyika shida ile ya kutokuwa na raha moyoni inarudi na inabidi mtu aendelee kuitafuta kwa njia nyingine.

Mhubiri 2:3 - “Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo.”

Kama tulivyoongea hapo juu wengine wanaitafuta raha ya kweli ndani ya pombe. Sulemani naye akaiona kuwa njia ambayo dunia inafuata, na hivyo akaijaribu. Nayo akaona kuwa bure.

Mhubiri 1:17 - “Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima . . . nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo.”

Page 18: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 18 -

Hekima na elimu ni lengo la wengi la kujipatia raha ya kweli. Yote mawili ni mambo mazuri lakini hayaleti raha ya kweli. Wengi katika dunia hii wanaitaka elimu ili waweze kutajirika zaidi na waijue namna bora ya kuishi. Lakini mambo haya, yakiwa nje ya Mungu, ni bure na hayata-fanikisha malengo yao.

Mhubiri 2:4 - “Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa.”

Sulemani aliona labda ujenzi ungeweza kuuburudisha moyo wake akiweza kuyaona yale aliyoyajenga na akisifiwa na wengine kama mjenzi mzuri. Akajenga nyumba kubwa kuliko hekalu alilomjengea Mungu. Akapanda mashamba makubwa na hata misitu yenye kila aina ya matunda. Mwisho akaona havijauburudisha moyo wake.

Ni kweli wengi wanataka kuvijenga vitu vikubwa wakitegemea kukumbukwa wataka-pokufa. Ndiyo maana katika majengo mengine wanaliweka jina la mtu kwenye jiwe la msingi ili mtu huyu akumbukwe.

Mhubiri 2:7 - “Nami nikanunua.”

Kisha Sulemani akaanza kuitafuta raha na maana ya maisha katika vitu. Akanunua wa-tumwa, ng’ombe na kondoo. Akakusanya fedha na dhahabu na tunu za kifalme. Akaajiri waimbaji wa kumwimbia kila wakati. Vitu, vitu, vitu... Kama ilivyo kwa wengi leo, alifikiri vitu hivi vingemfurahisha lakini havikuweza kumridhisha.

Mhubiri 2:9-11 - “Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Ye-rusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo. Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yali-chokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote...Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.”

Tunapaswa kujifunza kutokana na uwezo ambao Sulemani alikuwa nao. Alikuwa mfalme mwenye mali nyingi na mamlaka yote. Anapodai kwamba hakujizuia ina maana alikuwa na uwezo wa kupata cho chote kile alichokitaka. Sasa ujiulize. Kama Sulemani, ambaye alikuwa na uwezo kuliko wewe na mimi, alijaribu kila njia ya kidunia ili apate raha ya kweli, na ikashindi-kana, kwa nini sisi tunaendelea kujaribu njia hizo hizo tukiwa na tumaini la kujipatia raha ya kweli?

Mwisho - Njia za kidunia zinatuzuia tusimtolee Mungu ipasavyo.

Tukirudi katika somo letu tunakuta suala la kutafuta raha ya kweli ni sababu moja ambayo inasababisha watu wasijitoe ipasavyo. Sababu hiyo ni kwamba wametegwa na mawazo ya dunia hii. Wanatafuta kitu kizuri, raha ya kweli, lakini wanaitafuta kwa njia za kidunia. Njia za kidunia zinazuia mtu asitoe sadaka na pia haziwafanikishi katika lengo lao la kupata raha ya kweli.

Kwa mfano wengine hawatoi kanisani kwa sababu kwa kipindi hiki watoto wao wako sek-ondari. Kinachotafutwa ni elimu. Elimu ni kitu kizuri lakini hatuwezi kuibadilisha elimu, isiyo na uwezo wa kuleta raha ya kweli, kwa utiifu kwake Mungu, ambao unaleta raha ya kweli.

Kama Wakristo, tunapaswa kuacha kuitafuta raha ya kweli kwa njia za dunia hii. Tunataki-wa kuanza kumtii Mungu katika maagizo yake yote na kumtumikia yeye. Agizo mojawapo la Mungu ni kutoa sadaka na zaidi kujitoa kwa ujumla kwake Mungu (yaani hali na mali). Hatu-taiona raha ya kweli kamili mpaka tuanze kumtumikia Mungu ipasavyo. Tena makanisa yetu hayataona maendeleo mpaka tutakapokubali kwamba njia za kidunia hazifai kutupatia raha ya kweli.

• Wewe unatafuta kupata raha ya kweli kwa njia gani? Mali? Vitu? Elimu? Anasa? Kicheko? Usalama?

• Unaweza kufanya nini ili utafute raha ya kweli kwa njia ya Mungu? MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU RAHA YA KWELI

Tofauti ya raha ya kweli na utajiri wa mali

Badala ya kusema raha ya kweli tunaweza kusema utajiri wa kweli tukiwa na maana moja. Kwa kawaida tunapolisikia neno “utajiri” tunawaza juu ya pesa au mali. Tunapoona mtu ana

Page 19: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 19 -

gari, nyumba kubwa, amesomesha watoto wake wote, na amenenepa, tunasema yule ni tajiri. Hii ni njia moja ya kulifafanua neno “utajiri”. Ni kweli kuna watu wengi walio matajiri wa namna hiyo. Tungeona pesa walizo nazo benki tungeshangaa. Tungesema bila wasiwasi, “Huyu ni taji-ri”.

Utajiri huo ni mzuri lakini kuna utajiri mwingine ulio bora. Kuwa na mali nyingi siyo ahadi kwamba mtu ana raha katika maisha yake. Wengine wanazo pesa nyingi lakini hawayapendi maisha yao. Wanafikiri kwamba zingeongezeka kidogo zaidi ndipo wangekuwa na furaha. Lakini tena na tena wanapoongeza mali yao wanakuta bado kuna kasoro fulani. Hali hii ni kwa sababu hawana utajiri wa kweli ingawa wana utajiri wa mali.

Utajiri wa kweli unagusa sehemu zote za maisha yetu. Utajiri wa mali unahusu mali tu. Wa-tu wanaweza kuwa na mali nyingi bila utajiri wa kweli.

Luka 12:15 - “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.”

Yesu alisema hivi, kuonesha tofauti za utajiri. Wingi wa vitu ni utajiri wa mali tu. Yesu amesema uzima, au utajiri wa kweli, haupo katika wingi wa vitu. Utajiri wa kweli unahusu mai-sha yako ya kiroho, ya hisia, ya kimwili, ya kiakili, na ya mahusiano yako na watu wengine. Mtu mwenye utajiri wa kweli ni yule ambaye ana utajiri katika sehemu hizi zote.

Bila wokovu na msaada wa Mungu hakuna raha ya kweli

Raha ya kweli inaanzishwa na Mungu mwenyewe. Mungu anao mpango kwa ajili ya maisha ya kila mtu. Tunapokuwa katikati ya mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yetu ndipo tuna-pokuwa na raha ya kweli.

Raha hiyo inaanza na wokovu. Mungu amemtuma mwana wake afe msalabani kwa ajili ya kuulipa mshahara wa dhambi zetu. Yaani aliteswa badala yetu. Mungu amesema tukiiweka ima-ni yetu ndani ya Yesu, ambayo ina maana ya kuitegemea kazi aliyoifanya msalabani, tutapata msamaha wa dhambi na tutakuwa na uhusiano mzuri na Mungu ili tuweze kuona baraka zake zote. Ni lazima kila mtu apige hatua hii kwanza ya kuokolewa kwa kuiweka imani ndani ya Yesu. Hakuna mtu atakayeiona raha ya kweli bila Yesu kuwa ndani ya maisha yake. Ni Wakristo tu wanaoweza kutajirika katika dunia hii na utajiri huo ulio bora uitwao raha ya kweli. Raha ya kweli iko ndani ya kusudi la Mungu kwa maisha ya mtu

Mpango au mapenzi ya Mungu ndiyo yanayomfaa kila Mkristo. Mungu amemwumba kila mtu. Katika jinsi alivyoumba kila mmoja amemwumba kulingana na makusudi yake. Yaani Mungu ameweka ndani ya kila moja, ujuzi, karama, uwezo, saikolojia, hisia n.k. zinazoendana na kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yake. Ili kila mmoja awe na raha ya kweli inambidi alitimize kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yake. Kwa kuwa ameumbwa kwa kusudi maalum, ha-taridhishwa na malengo au makusudi mengine ya kimaisha kwa sababu makusudi haya men-gine hayataendana na jinsi alivyo kutokana na kusudi la Mungu katika kumwumba.

Kusudi kuu la Mungu kutuumba sisi sote lilikuwa tuwe viumbe wanaomtukuza Mungu. Kama ni usemi wetu, kazi yetu, michezo yetu, au cho chote kingine, tuna sababu hii kubwa kuwepo duniani, ambayo ni ile ya kumtukuza Mungu. Tusipoishi kwa namna inavyomtukuza Mungu hatutaiona raha ya kweli kwa sababu tutakuwa tunaishi kwa njia iliyo kinyume na jinsi tulivyoumbwa na Mungu.

Kuna mambo mbalimbali yaliyo makusudi ya Mungu kwa ajili ya kila mwanadamu. Kwa mfano kumtukuza Mungu, kumtii Mungu, kupendana, kutotenda dhambi, n.k. Kwa kadiri watu wanavyoyatimiza makusudi haya ndivyo watakavyoiona raha ya kweli katika maisha yao.

Lakini pia, Mungu ana kusudi maalum kwa kila Mkristo lililo tofauti na makusudi aliyo nayo kwa Wakristo wengine. Ili mtu aweze kuiona raha ya kweli ni lazima amtumikie Mungu kama alivyokusudia katika kumwumba. Kwa mfano, kama mtu ameumbwa na Mungu kuwa na uwezo, karama, na tabia za uongozi, kisha amesomea uongozi, mtu huyu hawezi kuridhika na maisha yasiyo ya nafasi za uongozi. Hii ni kwa sababu maisha yo yote mengine hayataendana na jinsi alivyoumbwa, Yaani, hayataendana na kusudi la Mungu kwake.

Katika mambo ya kawaida ya dunia hii sisi sote tunaielewa kanuni hiyo. Kanuni yenyewe inasema watu huridhika zaidi wanapopata maisha yanayoendana na karama, elimu, tabia, na

Page 20: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 20 -

uwezo wao. Kwa mfano mtu ambaye amesomea useremala na ana ujuzi kwa kazi za useremala, hafai katika kazi ya umakanika. Ukimlazimisha afanye kazi ya umakanika hawezi kuona raha kwa sababu atakuwa anafanya kazi asiyoifahamu. Hatalitengeneza gari hata siku moja na mwi-sho atajisikia kuwa mjinga. Lakini akiifanya kazi yake aliyoisomea na anayoijua, ataona raha kwa kuwa ana uwezo nayo.

• Kwa nini mtu hawezi kuwa na raha ya kweli bila wokovu wa Yesu? • Eleza jinsi raha ya kweli inavyopatikana katika kutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya

maisha ya mtu. • Je, wewe unayo raha ya kweli katika maisha yako? Kama hapana, je, unafikiri unayatimiza

mapenzi ya Mungu katika maisha yako?

MANENO YA BIBLIA YANAYOHUSU RAHA YA KWELI Tuone maneno ambayo Biblia inatumia kuelezea raha ya kweli. Utayaona maneno hayo ni

mambo ambayo kila mtu anayataka katika maisha yake. Ni maneno yanayoelezea sifa na hali zilizo nzuri, tena za kutamani. Maneno hayo huelezea hali mbalimbali zinazochangia raha ya kweli katika maisha ya mtu. Tumeyataja baadhi ya maneno ambayo Biblia huyatumia kuuelezea ujumla wa raha ya kweli. Lakini kuna maneno mengine katika Biblia ambayo nayo yanaeleza au kuchangia wazo hilo la raha ya kweli.

Kusimama - Mkamilifu - Mapenzi ya Mungu

Wakolosai 4:12 - “...akifanya bidii sikuzote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.”

Kutokana na maombi ya Epafra tunajifunza yafuatayo katika mstari huu. Alikuwa akiomba Mungu awafanyie mambo matatu. Kwanza waweze kusimama vizuri. Mtu ambaye anasimama vizuri ni mtu mzima, au mtu hodari. Inaelezea hali nzuri ambayo kila Mkristo anatakiwa kuwa nayo ndani ya Kristo. Kusimama imara ni hali moja inayochangia raha ya kweli.

Pili anatumia neno “wakamilifu”. Hakuna ambaye anapenda kuwa na makasoro au mapun-gufu. Sisi sote tunataka kuwa wakamilifu. Lakini kuwa mkamilifu inawezekana tu ndani ya Kristo. Hakuna kitu kilicho kamili nje ya Kristo. Ukamilifu huo unahusu kila sehemu ya maisha yetu. Unahusu mioyo yetu, akili zetu, matendo yetu, saikolojia yetu, hisia zetu, n.k. Mungu anatutaka tuwe wakamilifu kwa jinsi yeye anavyoufafanua ukamilifu. Mungu hushughulika nasi kila siku akiendelea kutukamilisha (Fil 1:6). Kwa kadiri tunavyokamilika, vivyo hivyo na raha ya kweli itakavyoongezeka katika maisha yetu.

Mwisho anaomba wawe katika mapenzi ya Mungu. Raha ya kweli inatokana na kuwa katikati ya mapenzi ya Mungu. Ye yote aliye nje ya mapenzi ya Mungu hawezi kuiona raha ya kweli. Wakati tutakapotimiza kusudi la kuumbwa kwetu, ndipo tutaiona raha.

Kusitawi

Mithali 11:28 - “Azitegemeaye mali zake ataanguka, mwenye haki atasitawi kama jani.”

Neno lingine ambalo Biblia inalitumia kuielezea raha ya kweli ni neno “kusitawi”. Kitu kili-chositawi ni kitu chenye afya nzuri. Ni kitu kilicho hai au kamili ambacho kimekomaa. Mstari huu unaeleza wazi kwamba kuitegemea mali siyo njia ya kusitawi wala kuiona raha ya kweli. Njia yenyewe ya kuona raha ya kweli ni kumtegemea Mungu na kuhesabiwa haki naye. Mema - Heri

Mithali 16:20 - “Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye Bwana ana heri.”

Biblia huielezea raha ya kweli kwa kutumia neno “mema”. Mema ni yote yaliyo bora. Ni nani ambaye hayataki yaliyo bora katika maisha yake? Tena mstari huu unatumia neno “heri”. Heri, vilevile, ni hali nzuri inayotafutwa katika maisha ya kila mtu. Mema na heri, yaani raha ya kweli, vinapatikana katika kumwamini Mungu na Neno lake. Mtu akitaka kujiongezea raha ya

Page 21: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 21 -

kweli katika maisha yake anatakiwa kulitafakari Neno la Mungu kila siku na kumwamini Mungu katika kila sehemu ya maisha yake. Usalama - Amani

Isaya 26:3-4 - “Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumaini Bwana siku zote, Maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele.”

“Usalama” ni neno lingine. Anayelindwa na Mungu yuko mahali palipo na usalama wa hali ya juu. Humo ndimo ilimo raha ya kweli. Hakuna usalama katika dunia hii nje ya Mungu. Kuna vita, wezi, majambazi, na hata maadui wanaojifanya kuwa marafiki. Lakini mtu ambaye anal-indwa na Mungu ana usalama hata kama yu katikati ya vita. Anajua hakuna kinachoweza kumtokea bila ruhusa ya Mungu.

“Amani” kamilifu ni njia nyingine ya kuielezea raha ya kweli katika Biblia. Amani ni jambo muhimu. Haifai kuwa tajiri asiye na amani. Haifai kuwa na mamlaka kuliko wote bila amani.

Mfano wa mti

Yeremia 17:5-8 - “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.”

Kupata raha kwa njia ya kidunia

Kupata raha kwa njia ya Mungu

Mistari hii ni mizuri sana kwa kuwa inaonesha hali zote mbili. Kuna njia mbili za kuishi. Ni

juu ya kila mtu kuchagua kama ataishi kwa kumtegemea Mungu au kwa kuwategemea wana-damu (au kujitegemea kama mwanadamu). Njia ya wanadamu ni kuzifuata akili, hekima, na mawazo yao. Njia ya Mungu ni kuweka tumaini lote ndani ya Mungu.

Kuwategemea wanadamu ni kuzifuata njia za kidunia. Matokeo yake yanaelezwa kuwa hali mbaya; ni kama kuishi jangwani ambapo hakuna kilicho hai, hakuna mema, tena ni mahali pabaya.

Kumtegemea Mungu kunaleta raha ya kweli. Mistari hii inatupa maneno mengine yanayo-ielezea hali hiyo. Kwanza ni hali ya mti ulio karibu na mto. Sisi sote tunapata picha mara moja ya mti mkubwa wenye afya nzuri. Matawi yake ni makubwa, majani yake ni kijani. Hii ndiyo raha

Page 22: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 22 -

ya kweli. Zaidi, Yeremia anaeleza kwamba hakuna hofu wakati wa hari wala hali ya kuhangaika. Maana hii ni afya ya kweli.

Tungepewa uwezo wa kuchagua kati ya hali hizi mbili, hakuna ambaye angechagua hali ya jangwani. Lakini utashangaa unaposikia kwamba Wakristo wengi wanaichagua hali hiyo. Wamemjua Mungu, lakini hawajapata kumtegemea. Bado wanazifikiria njia za kidunia kuwa bora. Bado wanatafuta raha ya kweli kwa njia za kidunia bila mafanikio. Katika mioyo yao wamebaki kama fukara nyikani. Kweli inasikitisha kuwaona watu wengi wakikosa raha ya kweli kwa sababu hawajaiamini njia yake Mungu.

Najua wewe unachotaka katika maisha yako ni picha ile nzuri ya mti uliopandwa kando ya mto. Lakini ujiulize, unaitafuta hali ile kwa njia gani? Hakikisha unamtegemea Mungu na utakuwa kama mti huo ulio karibu na maji.

Sasa tuangalie maneno tuliyoyakusanya katika mistari hii. Kumbuka maneno haya ni ufafanuzi mbalimbali wa mada yetu “Raha ya Kweli”.

Kusimama Mapenzi ya Mungu Mema Mkamilifu Mti karibu na maji Heri Usalama Hakuna kuhangaika Kusitawi Baraka Hakuna hofu Amani Jani bichi Kuzaa matunda

Dunia hutafuta hali ya maneno haya kwa njia mbalimbali zilizo tofauti na njia ya Mungu.

Lengo ni lile lile lakini watu wamedanganywa kufikiri kwamba raha ya kweli inapatikana kupitia nyumba kubwa, mamlaka, utajiri wa mali, n.k. Biblia hufundisha njia ya kuipata raha ya kweli ni kumtegemea Mungu na kuyatimiza makusudi yake kwa ajili ya maisha yako. Biblia in-amwangalia zaidi mtu alivyo na jinsi anavyojisikia kuliko vitu alivyo navyo. Raha ya kweli ya Biblia ni kitu kinachodumu na ni kitu chenye ubora.

• Wewe umechagua njia gani katika maisha yako? • Je, kuna haja ya kuibadilisha njia unayofuata ? • Eleza jinsi maneno yote hayo yanavyochangia wazo hilo moja la raha ya kweli.

RAHA YA KWELI NI KARAMA YA MUNGU Mhubiri 2:24-26 - “Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho

yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu. Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi? Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia.”

Katika mistari hii Sulemani alikuja kuelewa jinsi mtu anavyopata raha ya kweli. An-apoongea maneno kama, “Kula, kunywa, na kazi” anamaanisha maisha ya mtu kwa ujumla. Ni mifano tu ya mambo tunayoyafanya katika maisha yetu na hivyo ipo kwa niaba ya maisha kwa ujumla.

Mtu ambaye analiona jema na akaburudishwa katika jambo hilo (maisha yake) ni mtu mwenye raha ya kweli. Shughuli zake hazibadiliki bali hali ya moyo wake na fikira zake hu-badilika. Watu wawili wanaweza kufanya kazi moja na mmoja anaweza akawa anaifurahia kazi hiyo na mwingine hapana. Siri ni kwamba raha ya kweli inapatikana kwa Mungu tu. Sulemani anadai inatoka “mkononi mwa Mungu”.

Mhubiri 3:9-14 - “Je! mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.......Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi. Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche yeye.”

Page 23: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 23 -

Katika sehemu hii Sulemani anaonesha jinsi uwezo wa kuwa na raha katika dunia hii ni karama ya Mungu. Tena ni karama inayodumu milele. Ukitaka kuwa na raha ya kweli ujue utai-pata kwa njia ya Mungu tu. Ni lazima umwamini Mungu, umtegemee na umtii katika maisha yako, hatimaye atakubariki akiongeza raha ya kweli inayodumu katika maisha yako.

Naamini jambo mojawapo linalowazuia watu wasijitoe ipasavyo ni kule kuziamini ahadi za kidunia kwamba njia zake zitawaletea raha ya kweli.

• Kama raha ya kweli ni karama ya Mungu unaweza kufanya nini ili ujipatie raha ya kweli? MUNGU ANATAKA KILA MKRISTO AWE NA RAHA YA KWELI

Kwa kuwa raha ya kweli ni karama kutoka kwa Mungu, je, Mungu anataka tuwe na raha hiyo? Yaani, kama hatuwezi kujipatia raha ya kweli, na badala yake, tunapaswa kumtegemea Mungu, itakuwaje kama Mungu hataki kutupa raha hiyo? Unamwelewaje Mungu wetu? Mungu ana kauli gani kwetu? Je, anataka wengine kuwa na raha na wengine hapana? Je, hataki ye yote awe na raha? Au, je, anataka wote wawe na raha? Mawazo mbalimbali kuhusu Mungu

Kutokana na jinsi watu walivyofundishwa katika maisha yao, watu wanayo mawazo tofauti tofuati juu ya Mungu. Wengine wanamwona Mungu kuwa mzee aliye na tabia mbaya. Kila wa-kati hukasirishwa na wanadamu. Ametunga sheria nyingi zinazotakiwa zifuatwe na wanadamu, na wanapozikosea Mungu hupenda kuwaadhibu. Mungu huyu anapenda kuweka mitego ili aweze kuwanasa wakosaji.

Wengine wanamwona Mungu kama mtu aliye na shughuli nyingi mpaka hana muda wa kushughulika na wanadamu. Mungu huyu ameiumba dunia kisha anaendelea na shughuli nyingine na hajali kinachoendelea katika dunia hii.

Ukipata kuongea na watu utashangaa jinsi kila mtu anavyomwona Mungu kwa namna tofauti. Mambo yako hivi kwa sababu nyingi. Wengine walikuwa na baba mzazi aliye na tabia mbaya na hivyo wanafikiri Mungu yuko hivyo pia. Wengine wamesoma baadhi ya mistari ya Biblia juu ya Mungu, inayoelezea upande mmoja wa tabia za Mungu, na hivyo wameona hii ni picha kamili ya Mungu. Tutajuaje hali halisi ya Mungu? Ni muhimu tumwelewe katika ukweli wa Neno la Mungu badala ya kujitengenezea mawazo yetu wenyewe.

Biblia nzima inaelezea jinsi Mungu alivyo

Mungu wetu ni wa ajabu na mwenye asili na tabia nyingi ambazo zote huchangia katika Mungu huyu mmoja. Ni lazima tumwelewe kwa jinsi Biblia nzima inavyoelezea ili tupate picha kamili. Tukiiangalia haki ya Mungu tu, tunaweza kufikiri tuko mahakamani kila wakati. Tukiuangalia upendo wa Mungu tu, tunaweza kufikiri Mungu hajali tunapotenda mabaya. Ni lazima tumjue Mungu wetu katika asili na tabia zake zote kwa ujumla.

Nasema haya yote kama utangulizi. Kichwa cha sehemu hii chasema Mungu anamtakia raha ya kweli kila Mkristo. Ni kweli. Mungu anatupenda na anatujali. Anajali tunavyoishi na anataka kutubariki. Anataka tuwe na raha katika maisha yetu na tuwe na uzima. Vilevile anataka tuka-milike, yaani tuwe na utajiri wa kweli unaogusa kila sehemu ya maisha yetu.

Kusudi la kuja kwake Yesu

Wengine hawaamini Mungu ana nia njema kwa wanadamu. Wanafikiri Mungu anajali utiifu wao katika amri zake lakini ni vigumu kukubali kwamba Mungu anawajali kila mmoja katika moyo wake. Mawazo haya si kweli. Jamani, Mungu wetu anataka kuyaona maisha yetu yanaku-wa yenye raha na yenye hali iliyo bora. Tazama jinsi Yesu anavyoeleza sababu yake ya kuja hapa duniani:

Yohana 10:10 - “...Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

Yesu alikuja duniani kwa sababu ya upendo wake. Aliwajali sana wanadamu kiasi cha kuyatoa maisha yake mwenyewe. Sababu ya kuyatoa maisha yake ilikuwa kuwaandalia wana-damu njia ya kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Uhusiano huo ndiyo chanzo cha uzima. Yesu

Page 24: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 24 -

alitaka tuwe na uzima. Tazama mstari huu hausemi, “Uzima wa milele” bali unasema, “Uzima tele”. Hizo ni hali mbili tofauti zinazoendana. Ni kweli wote wanaomwamini Yesu na kuokoka wanapewa uzima wa milele. Yaani, aliyeokoka anao uzima wote wa milele tayari. Lakini kuna uzima mwingine unaopatikana katika maisha ya Mkristo ambao ni uzima tele.

Yesu alisema alikuja pia ili wawe na uzima tele. Uzima huo unapatikana kwa wale wanaomwamini Yesu lakini una taratibu zake. Maana ya uzima huo ni hali bora ya maisha, au kwa maneno yetu katika kitabu hicho - raha ya kweli. Uzima huo unapatikana katika viwango. Yaani Wakristo wengine wana kiasi kidogo cha raha ya kweli na Wakristo wengine wana kiasi kikubwa. Lakini nia ya Yesu ni kwa wote kuwa na raha ya kweli ya kutosha, yaani uzima tele. Maana ya “tele” hapa ni kuonesha ni uzima unaotosheleza; linaeleza kiasi cha uzima tunachoweza kuwa nacho tukimfuata Yesu na kuishi kwa mpango wa Mungu. Tafsiri ya Biblia ya kisasa inasema, “Uhai kamili”. Yaani ni uzima wote bila kasoro. Uzima huo, ambao ni kama mai-sha bora au raha ya kweli, unapatikana leo kwa wote watakaozifuata kanuni za Mungu katika maisha yao. Ni zawadi au karama itokayo kwa Mungu. Lakini watu wanakuwa nayo kulingana na jinsi wanavyomtii na wanavyomtegemea Mungu wakizifuata njia zake.

Kwa kweli Mungu anatujali na anataka tuwe na uzima tele. Hatuwezi kutia mashaka yo yote juu ya wazo hilo kwa sababu Biblia yenyewe inasema hiyo ndiyo sababu ya Yesu kuja duniani. Raha ya kweli ni tunda la Roho Mtakatifu

Wagalatia 5:22-23 - “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”

Sababu moja tunajua Mungu anataka tuwe na raha ya kweli ni kwamba kupitia kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu Mungu anazalisha furaha. Yaani Roho Mtakatifu anakaa nda-ni ya Mkristo akizalisha matunda mbalimbali ndani yake. Ni wazi furaha inayozalishwa na Roho Mtakatifu ni raha ya kweli, siyo raha ya muda wala raha inayotegemea mazingira mazuri tu katika maisha ya mtu mwenye furaha hiyo. Lakini matunda hayo mengine, yanayozaliswha na Roho Mtakatifu, nayo yanachangia raha ya kweli. Jaribu kufikiri ni watu wenye tabia zipi ambao wana raha zaidi katika maisha yao? Huwa tunasema mtu mwenye amani ni mtu mwenye raha. Hata upendo huwa ni ishara ya mtu mwenye raha ya kweli. Tena kila tunda la Roho Mtakatifu linachangia jumla ya raha ya kweli ya Mkristo. Yaani, tunasema, mtu mwenye matunda haya yote katika maisha yake kwa wingi (upendo, furaha, uvumilimu, utu wema, fadhili, uaminifu upole, kiasi) ni mtu mwenye raha ya kweli.

Hakika Mungu anataka tuwe na raha ya kweli. Ili Mkristo awe na matunda haya kwa wingi zaidi katika maisha yake anapaswa kutembea na Roho Mtakatifu; yaani, akubali kazi hizo ziten-deke ndani yake akiutegemea uwezo wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yake na asiizimishe kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake (Rum 8:1-17, Efe 4:29-31). Raha ya kweli hutokana na ushirikiano na Mungu

1 Yohana 1:3-4 – “Hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. Na haya tunayaandika, ili furaha yetu itimizwe.”

Yohana anonesha tena lengo la Wakristo kuwa na raha ya kweli. Katika mstari huu kuna ushirikiano mbalimbali unaowezeshwa na kazi ya Yesu Kristo msalabani (soma mistari 1-2). Yohana anamshuhudia Yesu na kazi zake akiwahubiria watu ili wapate kuwa na ushirika wa Wakristo kwa Wakristo, Mungu Baba, na Yesu Kristo. Katika mahusiano hayo raha ya kweli in-apatikana na kutimia.

• Katika maisha yako umemwelewaje Mungu? • Je, unavyomwelewa ni sahihi kulingana na ushuhuda wa Neno la Mungu? • Kila siku unaposoma Neno la Mungu utafute jibu la swali, “Mungu yukoje?” • Je unaamini Mungu anataka wewe kuwa na raha ya kweli? • Ingawa huwezi kujipatia raha ya kweli, unaweza kufanya nini kuongeza nafasi ya Mungu

kukupa raha ya kweli kama zawadi kutoka kwake?

Page 25: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 25 -

JE, KUWA NA RAHA YA KWELI INA MAANA MKRISTO HATAONA UGUMU WO WOTE MAISHANI MWAKE?

Ni lazima tulijibu swali hili ili tusiwadanganye wengine. Kwa jinsi tunavyoendelea kufun-

disha kuhusu raha ya kweli, mwingine anaweza akaelewa maana yake kuwa hakuna ugumu katika maisha ya Mkristo mwenye raha ya kweli. Lakini, raha ya kweli haimaanishi kutokuwepo kwa mateso, wala haina maana Mkristo atapata kila anachokitaka.

Raha ya kweli ina maana katika mazingira yo yote aliyo nayo mtu, yakiwa mazingira safi au magumu, atakuwa na raha na amani moyoni mwake. Hata kama yuko katikati ya mateso, kwa ujumla, atakuwa na raha ya kweli moyoni mwake. Paulo aliliongea hili katika kitabu cha Wafilipi akionesha kwamba ana raha ya kweli katika hali zote.

Wafilipi 4:11-12 - “...maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye ani-tiaye nguvu.”

Kuona radhi kwake iliwezekana tu kwa sababu ya nguvu ya Mungu. Ni Mungu anayetoa uwezo kwa mtu kutoshelezwa au kuridhika katika hali yo yote. Hali yake ya radhi ni kama alivyoongea katika mstari wa saba:

Wafilipi 4:7 - “Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

Amani hii inatafutwa na wanadamu wote. Kila mtu anaitaka amani ya namna hii katika maisha yake. Inapatikana kwake Mungu tu. Amani hiyo ni raha ya kweli isiyotegemea maisha bila upungufu (kwa jinsi dunia inavyoelewa upungufu) au maisha bila mateso. Yaani amani hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu na inapatikana hata wakati magumu yanaendelea katika maisha yetu.

1 Wathesalonike 1:6 - “Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.”

Tazama tena jinsi furaha ni tunda la Roho Mtakatifu. Lakini pia uone jinsi Paulo anavyo-sema walikuwa na dhiki nyingi na furaha wakati mmoja. Yaani furaha hiyo ya kweli haitegemei kutokuwepo kwa dhiki.

Mfano wa Ayubu

Ayubu 1:8-12 - “Kisha Bwana akamwuliza shetani, Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe.”

Mungu anamtetea Ayubu kuwa mtu mzuri anayempendeza kuliko wanadamu wote. Hivyo tungefikiri Ayubu angebarikiwa na Mungu kufuatana na somo tuliloliona tayari. Na kweli Ayubu alikuwa amebarikiwa. Lakini hapo tunamwona Shetani jinsi alivyopata ruhusa kutoka kwa Mungu kumtesa Ayubu. Ayubu alijaribiwa ili ijulikane kama ataendelea kumcha Mungu au la. Cha kujifunza ni kwamba hata tukimtii Mungu katika hali zote Mungu anaweza kuwa na kusudi lingine katika maisha yetu hatimaye tukajikuta tuko katikati ya shida. Mungu ni mtawala na hatuwezi kumlalamikia. Lakini hata kwa Ayubu tunaona kwamba Mungu alikuja kumbariki kwa namna ya ajabu zaidi baada ya kukamilisha kusudi lake jingine. Isitoshe tunajua hata wakati wa mateso ya Ayubu Mungu alikuwa akimbariki kwa namna zilizo nyingine.

Page 26: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 26 -

Mti uliopandwa kando ya mto

Yeremiah 17:8 - “Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.”

Hata Yeremia anapoeleza kuhusu mtu anayemtegemea Mungu anaonesha wazi kwamba katika maisha yake lazima kutakuwa vipindi vya hari na uchache wa mvua ambazo ni mifano ya mateso na magumu. Yaani kila kitu hakitakuwa safi kila wakati kwa sababu Mungu ana ma-kusudi yake mengine katika maisha yetu. Makusudi kama vile kutukuzwa kwake, ukuaji wetu wa kiroho, mipango yake ya kuhudumia wengine, n.k. Lakini tazama jinsi mtu wa Mungu atakavyokuwa atakapokutana na mazingira mabaya. Yeye bado atakuwa na raha ya kweli na ataweza kuvumilia vipindi hivyo na hata kutoa matunda wakati wa vipindi hivyo. Ni ishara ya afya na hali iliyo bora. Katika moyo wake ana raha ya kweli kwa kuwa hahangaiki. Tena haoni hofu anapoingiliwa na mateso. Kwa hiyo tukubali kwamba Wakristo watakutana na mateso katika maisha yao lakini mateso hayatauondoa msingi wao wa raha ya kweli (au uzima tele). Ahadi ya mateso

Yakobo 1:2-3 - “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”

Mara nyingine tunaweza kufikiri mateso katika maisha yetu kuwa upungufu. Lakini mstari huu unatuonesha kwamba mateso yenyewe ni sehemu ya kutukamilisha ili tusiwe na upungufu wo wote. Maana unaweza kupungukiwa kitu cha kidunia ili nafsini mwako upate kukamilika zaidi.

Hii ndiyo sababu Yakobo aliweza kusema tunapaswa kuyafurahia mateso. Katika akili zetu tamko hilo halieleweki. Tunaona mateso kuwa jambo baya. Lakini Mungu katika hekima zake anajua mateso yana faida zake. Ili tusipungukiwe, mara nyingine Mungu anatuletea mateso na magumu. Kufanya hivyo ni sehemu ya kuitimiza ahadi yake ya kutukamilisha ili tusipungukiwe.

Tena na tena tunaona katika Neno la Mungu kwamba watu wa Mungu wanaitiwa mateso. Yesu alisema kama tutamfuata tutateswa kama vile alivyoteswa yeye, zaidi alituita kumfuata kwa kujikana na kubeba misalaba yetu.

Tofauti kati ya Mkristo na mtu asiye na Kristo ni jinsi Wakristo wanavyoweza kujisikia wa-kati kuna mambo magumu katika maisha yao. Wakristo wenye kiasi kikubwa cha raha ya kweli watajiskia raha, amani, na kufurahia mateso wanayokutana nayo.

Kusema hivyo haimaanishi Wakristo wenye raha ya kweli hawaoni maumivu na masikitiko. Mambo mengi katika dunia hii husababisha hisia mbaya na hisia hizo ni halali. Wakristo ni wanadamu wa kawaida wanaolia machozi na kujisikia hisia mbaya wakati wa magumu maishani mwao. Hakika hawacheki wakati wa vilio na mateso mengine mbalimbali. Lakini kati-ka msingi wa hisia zao wana uwezo wa kuwa na amani na raha ya ndani kulingana na jinsi wanavyomtegemea Mungu katika mpango wake. Yaani hawawezi kuyumba katika imani yao wakijua Mungu yu pamoja nao na ana mpango mwema na kila jambo watakalolikuta. Kwa nje, wanalia machozi, wakati ndani kuna uwezo wa kuvumilia, wakijua mateso ya dunia hii ni ya muda mfupi. Hawafurahii mateso lakini wanafurahi jinsi Mungu anavyowakamilisha kupitia mateso. Hawafurahii ugumu lakini wanafurahi Mungu anawapa raha na amani katika mioyo yao.

• Unajisikiaje unapojifunza Mungu ameahidi utateswa? • Inawezekanaje mtu ateswe na aone raha ya kweli wakati mmoja? • Je, kuogopa mateso na magumu yanakuzuia kumtumikia Mungu ipasavyo? Kama ndiyo,

ufanye nini kubadilisha mawazo hayo?

MWISHO Kwa nini tumejifunza kuhusu “raha ya kweli” au “utajiri wa kweli” kwa urefu hivi? Nime-

tumia nafasi kubwa kuifafanua raha ya kweli kwa sababu ninataka kuwasaidia watu waweze kuipata kwa njia ya Mungu ambayo ni njia peke ya kulifanikisha lengo la kuwa na raha. Hakika wote wanaitaka raha ya kweli katika maisha yao. Isivyo bahati, wengi wameisikiliza dunia na

Page 27: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 27 -

wanazifuata njia zake kuipata, lakini wanashindwa kulifanikisha lengo lao la kuwa na raha ya kweli kwa sababu njia za kidunia haziwezi kuileta.

Tunapouangalia utoaji wa Wakristo kwa Mungu wao, tunakuta kuna udhaifu mkubwa mara nyingi. Sababu mojawapo ya hali hii kuwepo ni kwamba watu wanatafuta raha ya kweli kwa njia za kidunia. Siyo rahisi watu watoe mali, muda, au nguvu zao kwa kazi ya Mungu wakati wanaamini raha ya kweli imo ndani ya vitu hivyo. Watataka kubaki navyo ili wawe na raha ya kweli. Lakini, kumbe, wamedanganywa na mawazo ya kidunia na kwa njia hiyo watakosa raha ile wanayoitafuta. Wenyewe wanakula hasara (maana hawapati raha wanayoitafuta) na pia kazi ya Mungu inakula hasara kwa kuwa imekosa nguvu kutokana na watu kutojitoa ipasavyo.

Wewe kama mshirika wa kanisa lako, usiamini kwamba huna uwezo wa kujitoa. Usiogope kujitoa kwa kufikiri kwamba utashindwa kupata raha ya kweli katika maisha yako. Usiamini mambo ya dunia hii kwa sababu ndani ya njia zake wote wanaumizwa. Badala yake uamini kwamba raha ya kweli inapatikana katika Mungu tu. Ni karama ya Mungu inayotokana na nee-ma yake. Zaidi inaendana na baraka za Mungu kwa wale wanaomtii na kuishi kulingana na taratibu zake.

• Je, unataka raha ya kweli katika maisha yako? • Je unaitafuta raha ya kweli kwa njia ya kidunia itakayokuzuia usijitoe ipasavyo? • Au je, unakubali kutafuta raha ya kweli kwa njia ya Mungu? • Unakubali Mungu anataka kukubariki na raha ya kweli?

- 4 - Mahitaji ya Mkristo

Jambo moja linalofikiriwa sana na watu wote ni mahitaji yao. Hakika ni lazima kila mtu afi-

kirie mahitaji ya familia yake kwa sababu hakuna mwingine hapa duniani ambaye atamfanyia. Nyumba, chakula, usafiri, elimu, mavazi na mambo mengine mengi ni ya lazima katika maisha ya watu. Lakini mara nyingi Wakristo wanashindwa kujitoa kwa Mungu wao ipasavyo kwa kuwaza vibaya kuhusu mahitaji yao. Wenyewe huogopa kumpa Mungu cho chote mpaka wametimiza mahitaji yao kwanza. Wazo hilo huleta shida kwa sababu hakuna siku ambayo mwanadamu ataona ameyakamilisha mahitaji yake yote. Kwa sababu hiyo, hakuna siku ambayo mwanadamu ataweza kumtolea Mungu wake ipasavyo.

Ni kosa kwa mtu kufikiri anajitegemea katika kuyakamilisha mahitaji ya familia yake. Mungu yupo na ameahidi kuwasaidia wote katika mahitaji yao kulingana na makusudi yake kwa ajili ya maisha yao. Mkristo anapaswa kumtii Mungu katika maagizo yake yote, hata agizo la ku-jitoa kwake Mungu. Kumtii Mungu katika suala la utoaji kunawezekana kwa sababu Mungu ameahidi kuwatunza watu wake na kuwapatia mahitaji yao. Hivyo hakuna hatari ya kushindwa kuyapata mahitaji yetu kwa sababu tumemtolea Mungu mali yetu.

Lakini Wakristo wengi humpa Mungu cho chote kidogo kilichobaki baada ya kujaribu kuyakamilisha mahitaji yao wenyewe kwanza. Kama ni muda, nguvu, akili, au hata mali zao, wenyewe humpa Mungu nafasi ya mwisho. Kwa njia hii mahitaji ya mtu ni kizuizi kinachomzuia asijitoe kwa Mungu wake ipasavyo. Tusome Biblia ili tuweze kuyanyosha mawazo yetu kuhusu mahitaji yetu kusudi yasiwe kizuizi cha kujitoa kwetu kwa Mungu wetu.

MAHITAJI NI NINI?

Mahitaji ya kimwili

Kwa kawaida tukimwuliza mtu juu ya mahitaji yake ataorodhesha mambo ya kimwili. Nda-ni ya orodha hii anaweza kuweka mambo mengi kama chakula, mavazi, nyumba, n.k. Tena kwa kawaida katika kuyaorodhesha mahitaji yake mtu huchanganya pamoja yale yaliyo mahitaji kweli na mambo mengine anayoyataka tu, ambayo siyo mahitaji kweli.

Page 28: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 28 -

Katika Biblia neno mahitaji humaanisha mambo yale ambayo ni ya lazima ili mtu aweze kuendelea kuishi katika dunia hii. Ina maana bila vitu hivi atakufa. Yaani ni mambo yaliyo ya msingi kwa uhai wa mtu.

• Orodhesha baadhi ya mahitaji uliyo nayo ya kimwili. Mahitaji mengine

Ndani ya mambo haya yaliyo ya lazima kuna mambo mengine ambayo watu husahau kuyaorodhesha. Naamini Mungu anayaangalia mambo haya kuwa ni sehemu ya mahitaji yaliyo ya lazima. Kwa mfano kila mtu anahitaji kupendwa. Pia tunahitaji kuheshimiwa. Kuwa na uhusiano na wengine pia ni jambo lililo la lazima kwa sababu sote tumeumbwa na Mungu katika mfano wake.

Mahitaji yetu yanaangalia kila sehemu ya maisha yetu. Mwili ni sehemu mojawapo tu. Se-hemu nyingine ni akili zetu, saikolojia zetu, hisia zetu, na hata maisha yetu ya kiroho. Sehemu hizi zote zina mahitaji yake yaliyo ya lazima.

Mahitaji yanayotokana na mapenzi ya Mungu

Sehemu nyingine ya mahitaji yetu ni yale tunayoyahitaji ili tuweze kuutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yetu. Mungu anao mpango kwa kila mtu. Katika mpango wake ana-wataka watu waishi kwa namna fulani wakifanya kazi (huduma) fulani. Mungu katika ku-wapangia kazi anahakikisha wanayo mambo yale ambayo ni ya lazima ili waweze kuyatimiza mapenzi yake.

Kwa jinsi hii mahitaji ya watu hutofautiana kwa sababu mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha ya mmoja ni tofauti na mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha ya mwingine. Hapo in-aeleweka tutakuwa na mahitaji yanayotofautiana ili wote tuweze kuyatimiza mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu.

Kwa kawaida tungesema hakuna mtu ambaye atakufa kwa kukosa kuwa na baiskeli/pikipiki na kwa jinsi hii, baiskeli/pikipiki, kwa kawaida, siyo hitaji la lazima. Lakini kama katika mpango wa Mungu kwa maisha ya mtu anahitaji kuwa na baiskeli/pikipiki ili ayatimize mapenzi yake, basi hilo sasa ni jambo la lazima au hitaji katika maisha yake.

Kwa mfano mwingine, ni Mpango wa Mungu kuwachagua wengine kuwa matajiri ili wa-saidie kazi zake kwa uwezo mkubwa zaidi.

Wote wanapewa karama zilizo tofauti kulingana na mapenzi ya Mungu. Kwa mfano, mwingine anapewa karama ya kufundisha na mwingine karama ya uongozi. Mungu huwapa watu karama kulingana na mahitaji yao ili waweze kuutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yao.

Ni kama wafanyakazi walioajiriwa kuzifanya kazi zilizo tofauti. Ukiajiri mtu mmoja kukata nyasi hitaji lake ni fyekeo. Ukiajiri mwingine kufanya kazi ya useremala, basi, mahitaji yake ni msumeno, randa, na nyundo. Wafanyakazi hawa hawataweza kuzifanikisha kazi zao bila kutimiziwa mahitaji yao kwanza. Hii ndiyo sababu tunasema mahitaji ya kila mtu yanatofautia-na kulingana na kazi ambayo Mungu amempa.

2 Wakorintho 9:8 - “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.”

Ahadi ya mstari huu inaonesha jinsi Mungu atakavyoyawezesha mahitaji yetu. Lakini ndani yake tunapata fundisho letu la kwamba anatupatia mahitaji yetu ili tuweze kuutekeleza mpango wake kwa maisha yetu. Ndiyo sababu Paulo anasema, “Mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.” Matendo hayo ndiyo matendo ambayo Mungu ametupangia. Katika kutupangia matendo haya mema (Waefeso 2:10) anatupa kila tutakachokihitaji ili tuvitumie kukamilisha mapenzi yake.

Mahitaji kama kikwazo

Mahitaji ya mwili ni sababu mojawapo kubwa ya watu kutojitoa kanisani na katika maisha yao kwa ajili ya Mungu. Ukimpa mtu uchaguzi kati ya kuwa na chakula kwa leo au kutoa chakula hiki katika kanisa lake, kwa kawaida angechagua kula mwenyewe. Njaa ina nguvu sana. Hakuna anayeipenda njaa na hivyo kila mmoja anatafuta namna ya kuikwepa.

Page 29: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 29 -

Jinsi watu wanavyoyafikiria mahitaji yao huwazuia wasijitoe kwa Mungu katika maisha yao. Kawaida watu wanajitahidi kuyatimiza mahitaji yao ya kimwili kwanza ndipo zilizobaki wamtolee Mungu. Shida ni kwamba, kwa kawaida, hakuna zilizobaki. Ni jambo la kawaida ku-waza mahitaji yetu yanazidi mapato yetu.

Mawazo ya watu kuhusu jinsi Mungu anavyotimiza mahitaji yetu hugawanyika katika ma-kundi mawili. Kundi la kwanza ni wale ambao hawaamini kwamba Mungu atawatimizia mahitaji yao. Wamemwelewa Mungu kwa mawazo ya kidunia. Katika dunia hii kila mmoja anatakiwa kujiangalia. Hawawezi kumtegemea mwingine ayatimize mahitaji yao. Kwa hiyo ili wawe na uhakika wa kuishi wanayaangalia mahitaji yao kwanza na kama kuna mabaki wanamtolea Mungu. Mwisho mazoea haya ya kidunia yanaletwa katika uhusiano wao na Mungu. Badala ya kumtegemea Mungu wanaamini wanapaswa kujitegemea au sivyo hawatayafanikisha mahitaji yao.

Wamekosa imani. Mungu anaahidi kwamba atayatimiza mahitaji yao lakini wanaogopa kujaribu. Kwa mfano kama mtu anazo shilingi 1000 Jumapili, na anajua ni lazima asage mahindi Jumatatu, hatazitoa kwa sababu ataiangalia shida ya kusaga. Hayuko tayari kumwamini Mungu kuhusu kesho. Ana uhakika na kile alicho nacho mkononi. Anaogopa kumtolea Mungu leo kwa kuwa atalazimika kumtegemea kesho. Anafuata usemi wetu wa Merikani unaosema, “Bora ndege mmoja mkononi kuliko ndege wawili kichakani.” Hakika ndege wawili ni bora, lakini kuwepo kwao kichakani hakumaanishi mtu ataweza kuwapata. Anaweza akatoa yule mmoja wa mkononi kwa tumaini la kupata wawili na mwisho akose wote. Hivyo, kwa kukosa kumwamini Mungu, watu hawajitoi ipasavyo wakidhani ni lazima wajitegemee na Mungu hategemeki.

Kundi la pili ni watu wale ambao wanaamini Mungu atawatimizia mahitaji yao lakini wanafikiri nia ya Mungu ni kutoa riziki tu. Yaani wanamwelewa Mungu kuwa mnyimivu ambaye atatimiza mahataji yao ya lazima tu na hawaitaki hali hiyo. Kwa mfano kama mtu anaweza kuishi chini ya kipande cha plastiki porini wanafikiri Mungu hajaahidi zaidi. Au kwa upande wa chakula, kama mtu anaweza kuishi kwa maharage 20 kila siku, basi, Mungu hawezi kumpa 21. Katika kumwelewa Mungu hivyo wanakataa kumtegemea kwa kuwa wanaelewa mahitaji yao tofauti na jinsi wanafikiri Mungu anavyoyaelewa. Wanaona ni bora kujitegemea kwa sababu kwa njia hiyo watapata angalau maisha mazuri zaidi.

Watu wanaojitegemea hawawezi kujitoa ipasavyo kwa Mungu. Ni lazima kila wakati waone mahitaji yao yanazidi mapato yao. Mwisho hawatamtolea Mungu kwa kuwa bado wanatafuta kutumiza mahitaji yao kwanza. Hiki ni kizuizi kikubwa kinachowazuia watu wasimtolee Mungu.

• Eleza jinsi unavyoelewa ufafanuzi wa neno “mahitaji”. • Eleza jinsi mahitaji ya watu yanavyotofautiana kulingana na mpango wa Mungu kwa ajili

ya maisha yao.

MUNGU HUTIMIZA MAHITAJI YA WATU WAKE Mathayo 6:25-34 - “Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au

mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghala-ni; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? au Tunywe nini? au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Mistari hii ni rahisi kuielewa. Tena ni wazi kwamba kinachoongelewa ni mahitaji ya kim-wili. Yesu mwenyewe ametamka mifano ya chakula, kinywaji, na mavazi, mambo yanayohusika katika mahitaji ya kimwili hasa. Tunapaswa kuyaelewa na kuyaamini mafundisho ya Yesu ku-husu mahitaji yetu.

Page 30: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 30 -

Mungu huwajali wanadamu kuliko viumbe wengine

Hoja moja ya Yesu ni kwamba Mungu anawajali wanadamu kuliko viumbe wengine. Hakika Mungu anawatunza viumbe wengine katika hali nzuri. Kama ni ndege, maua, au mengine, ni Mungu anayewapatia mahitaji yao. Wanyama hawalimi. Wanakula tu yale ambayo Mungu ame-waandalia. Hata miti na mimea mingine haijishughulishi na cho chote. Miti ipo tu ikiendelezwa na Mungu.

Katika kuumba ni kiumbe mmoja tu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Yaani, kiumbe huyu anafanana na Mungu katika namna ambayo viumbe wengine hawafanani naye. Kiumbe huyu ni mwanadamu. Mungu aliwaumba wanadamu wawe viumbe maalum. Alitaka kuwa na uhusiano nao. Hata walipoanguka akamtuma mwanawe afe msalabani kwa ajili yao. Yesu hakufa kwa ajili ya ndege au viumbe wengine. Alikufa kwa ajili ya kiumbe yule ambaye Mungu anamthamini zaidi, yaani, mwanadamu.

Hivyo, Mungu anaiona thamani kubwa katika wanadamu kuliko anavyoiona thamani ya viumbe wengine. Lakini, Mungu anayatimiza mahitaji ya viumbe hivyo visivyo na thamani kubwa. Kama Mungu atatimiza mahitaji ya viumbe visivyo na thamani, si ni lazima Mungu atayatimiza mahitaji ya wanadamu anaowathamanisha kuliko viumbe wale wengine?

Kujisumbukia ni bure

Hata kama unafikiri kwamba Mungu hatakutimizia mahitaji yako ujue huwezi kuyatimiza wewe mwenyewe. Yesu anauliza ni nani ambaye, akijibidisha, anaweza kuiongeza hata siku moja kwa maisha yake. Hakuna! Hakika wengi wanafikiri wanao uwezo wa kuyakamilisha mahitaji yao lakini wamejidanganya. Nguvu, akili, uwezo, na uhai walio nao, unatoka kwa Mun-gu. Hakuna ambaye angelima bila kupewa nguvu na Mungu.

Hivyo tukubali kwamba msingi wa kutimizwa kwa mahitaji yetu unatoka kwa Mungu. Kujisumbua haina maana. Ujisumbue, usijisumbue, bado ni Mungu atakayeyatimiza mahitaji yako.

Maana ya kujisumbua hapa ni katika moyo wako. Jinsi mtu anavyohangaika akifikiri kwamba anaweza kushindwa kuyatimiza mahitaji yake. Jinsi anavyokosa amani moyoni. Anashindwa kulala usiku kwa sababu anawaza juu ya kesho na mahitaji yake.

Hatuna sababu ya kuishi hivyo. Mungu ndiye anayetutawala na atayatimiza mahitaji yetu. Ndiyo sababu Yesu anasema tuwaze juu ya mambo ya Mungu (ufalme wa Mungu). Mawazo ya-nayoitawala mioyo yetu yahusu mambo ya Mungu, na siyo mambo ya dunia hii, kwa sababu kuhangaikia mahitaji yetu ni kujisumbua bure kwa kuwa hatuwezi kuyapata mahitaji yetu bila msaada wa Mungu.

Mungu anataka tuishi kama watoto wadogo. Watoto hulala vizuri sana kuliko watu wazima. Watoto hawahangaiki kuhusu mahitaji ya maisha yao na kwa sababu hiyo wanalala fofofo wakiwa na amani moyoni. Watoto wanaweza kuishi hivyo kwa sababu wanaamini wazazi wao watawatimizia mahitaji yao. Wakati baba anakuwa macho akisumbuka na ukosefu wa mvua kwenye shamba lake, mtoto analala vizuri tu akijua kwa namna moja au nyingine baba atamli-sha. Tuseme watoto huishi kwa imani. Na sisi tunapaswa kuishi kwa imani vilevile, kwa kuwa Baba yetu wa mbinguni ana uwezo mkubwa sana kuliko baba zetu wa duniani, na ameahidi atatutunza.

Mungu ayajua mahitaji yako

Vilevile katika mistari hii tunajifunza kwamba Mungu anayaelewa mahitaji yetu. Hii ina maana mahitaji yetu yote. Mungu hawezi kushindwa kuyatimiza mahitaji yetu kwa kukosa kujua tunahitaji nini.

Wafilipi 4:19 - “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”

“Kila”. Angalia jinsi ahadi hiyo inasema “kila”. Mungu anaahidi kwamba kila hitaji lako atalitimiza. Habari ya kila hitaji anayo, uwezo wa kutimiza anao, na nia anayo. Uamini. Angalia mistari ifuatayo inayoongelea jinsi Mungu anavyotimiza mahitaji yetu.

Page 31: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 31 -

Zaburi 72:12-13 - “Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.”

Zaburi 40:17 - “Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu Ee Mungu wangu, usikawie.”

Waebrania 13:5 - “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.”

2 Wakorintho 9:8 - “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.”

1 Petro 5:6-7 - “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari; ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”

Isaya 46:4 - “Na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.”

Watu wanaona ni vigumu kuamini, lakini Biblia inasema wazi kwamba Mungu anayatimiza mahitaji ya watu wake. Hatutakiwi kuhangaika wala kukosa amani moyoni kwa sababu ya mahitaji yetu. Hatutakiwi kutojitoa kanisani na katika maisha yetu kwa sababu ya kufikiri kwamba tukifanya hivyo tutakosa mahitaji yetu. Huwezi kukosa mahitaji yako unapomtolea Mungu. Mungu huyatimiza mahitaji yetu kupitia kazi zetu

Mungu ana njia nyingi za kuyatimiza mahitaji yetu. Mara nyingine anazitumia njia za ajabu kama mwujiza lakini mara nyingi zaidi anayatumia mambo ya kawaida katika dunia hii. Ana-weza kutusaidia kupata kazi yenye malipo mazuri au anaweza kutusaidia kupata mahitaji yetu kwa bei nafuu. Mara anafanya mashamba yetu kusitawi au anafanya mifugo yetu kutougua. Siku nyingine anazuia wizi nyumbani mwetu au anaweza kutusaidia tusiugue na kupata gharama za ziada za matibabu. Kwa kweli njia za Mungu ni nyingi kuliko hizi chache tulizozitaja. Ahadi yake kwa sisi tunaomfuata ni kwamba atayatimiza mahitaji yetu; ni juu yake kuamua jinsi atakavyotufanyia. Lakini, tunajua njia mojawapo, tena njia kuu, ni kupitia mikono yetu sisi wenyewe.

1 Wathesalonike 4:11-12 – “Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya ka-zi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.”

2 Wathesalonike 3:10 -12 – “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughul-isha na mambo ya wengine. Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

Hakika mpango wa Mungu katika kutupatia mahitaji yetu huanza na sisi wenyewe. Mungu anataka kila mtu afanye kazi akitegemea kula ndani ya kazi zake. Mungu anatuwezesha akitupa nguvu, akili, na mambo mengine ili tuweze kufaulu katika kazi tulizo nazo (Tazama pia 1 Tim 5:8).

Mahitaji yetu yanatimizwa kupitia wengine

2 Wakorintho 8:14 – “Bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.”

Mungu anajua tu wadhaifu na hatuwezi kila wakati kutimiza mahitaji yetu sisi wenyewe. Ndiyo maana Mungu anataka watu wake kusaidiana ili tuweze kuvuka vipindi vingine vilivyo vigumu. Mungu aliumba Mwili wa Kristo akiwa na kusudi la viungo vya mwili huo kusaidiana wakati wa shida. (tazama vilevile 2 Kor 11:9, Efe 4:28, Rum 12:13, Tit 3:14)

• Taja njia mbalimbali ambazo Mungu anaweza kuzitumia kukutimizia mahitaji yako.

Page 32: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 32 -

• Ikiwa Mungu ameahidi kutimiza mahitaji yako, ni kitu gani kinachokuzuia usijitoe ipasavyo?

• Je, unaamini Mungu atatimiza mahitaji yako? • Je, unahangaika kuhusu mahitaji mengine katika maisha yako? Ufanye nini ili upate

kuyatuliza mawazo hayo? TOFAUTI YA MAHITAJI NA MATAKWA

Wengine wanachanganya mahitaji yao na yale wanayotaka. Mungu hajaahidi kwamba ata-

tupa kila tunachokitaka bali atatimiza mahitaji yetu yote. Mahitaji ni mambo yale ya lazima ili tuweze kuishi na kuyatimiza makusudi ya Mungu kwa

ajili ya maisha yetu. Mambo tunayoyataka ni ya ziada nje ya yale tunayohitaji. Mambo haya huleta ubora wa

maisha. Kawaida ni mambo yanayorahisisha kazi zetu au yanayotupendeza. Kwa mfano bati ni kitu cha kutaka. Kuezesha nyumba kwa nyasi inatimiza hitaji letu lakini bati inaboresha.

Mambo ya kutaka yasiuzuie mpango wa Mungu

Mambo tunayoyataka ni tofauti na mambo tunayoyahitaji. Yale ya kutaka ni mambo am-bayo siyo ya lazima katika maisha yetu, lakini tungependa kuwa nayo.

Wengi wanafikiri kwamba Mungu hataki tuwe na vitu tunavyovitaka sisi. Kwa maana nyingine, wanafikiri kwamba Mungu anatunyima mambo yale ambayo yanatufurahisha. Wanaf-ikiri Mungu atatutimizia tu mahitaji yetu basi. Hakuna zaidi, wala hana mpango wa kutupatia zaidi. Mawazo haya hayalingani na Neno la Mungu.

Neno la Mungu linaeleza kwamba sisi ni watoto wa Mungu na kwamba Mungu anatujali kama watoto wake. Ni baba gani ambaye hapendi kuwapatia watoto wake yote yaliyo bora? Vilevile Mungu kama baba yetu anataka tuwe na yote yaliyo bora.

Zaburi 84:11b - “Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu.”

Tena na tena Neno la Mungu linasema kwamba Mungu ni mwenye neema, rehema, na up-endo kwa ajili yetu. Hata akamtoa mwanawe asulubiwe msalabani. Haikuwa kitu cha lazima bali ilikuwa neema kusudi tuwe ni kitu kilicho bora ingawa hatukustahili.

Usiogope kumwomba Mungu mambo ambayo unafikiri labda siyo ya lazima katika maisha yako lakini ungeyapenda. Kwa hekima yake, Mungu ataamua akupe au la.

Sharti kuu ambalo linaweza kumzuia Mungu asitupe sawa na maombi yetu ni kama kitu tunachokiomba kinaweza kutuzuia tusiutimize mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Vitu vin-gine tunavyoomba vinaweza kutuharibu. Vitu vya namna hii Mungu hawezi kutupatia. Pengine vinaweza kuwa kikwazo ili tusiutimize mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yetu. Hata kama sisi hatuoni jinsi kitu hicho kitakavyozuia mpango wa Mungu, tukumbuke Mungu ni mwenye kujua yote na anafahamu mioyo yetu kuliko tunavyoifahamu wenyewe.

Hata Paulo aliomba mwiba uondolewe katika maisha yake. Lakini Mungu alijibu kwamba mwiba utabaki kwa manufaa ya Paulo mwenyewe. Hatujui Paulo alisumbuliwa na nini lakini tunaona Paulo alifikiri ingemfaa kama Mungu angeuondoa mwiba ule. Paulo aliwaza tofauti, lakini Mungu alimwonesha sababu ya kutouondoa.

2 Wakorintho 12:7-9 - “Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha...” Mwisho

Tunamtumikia Mungu wa ajabu. Mungu wetu anafahamu mahitaji yetu kuliko tuna-vyoyafahamu wenyewe. Mungu wetu ana uwezo kututimizia mahitaji yetu yote. Cha ajabu Zaidi ni moyo wa Mungu wetu. Mungu si mnyimivu bali ni baba yetu anayetujali watoto wake akitaka tuwe na yote yaliyo bora katika maisha yetu. Mungu hataki tutimiziwe mahitaji ya msingi tu, bali afurahi tunapoyapata na mengine tunayoyataka ingawa si mahitaji. Tuweke imani yetu kwake

Page 33: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 33 -

kuhusu shida za mahitaji yetu. Tufanye hivyo ili tuachane na hali ya mahangaiko; tutulie ndani yake tukifahamu atatutimizia haja zetu zote.

Fundisho hilo tulilojifunza linapaswa kuhusishwa katika utoaji wetu. Mungu anataka kutu-tumia kwa ajili ya kufanikisha huduma zake hapa duniani. Kwa mfano, anataka uinjilisti ufanyi-ke, wenye njaa walishwe, wanyonge watetewe haki zao, n.k. Mungu anataka sisi kushiriki kazi zake kwa hali na mali. Anataka tujitoe ili kazi zake zitendeke. Anataka tutoe nguvu zetu, akili zetu, muda wetu, na hata mali zetu kusaidia mambo yake. Lakini tunapowaza kwamba ni lazima tujitegemee, au sivyo mahitaji yetu hayatatimizwa, inatuharibu. Inazuia kujitoa kwetu kwa Mungu kwa kuwa hatujaamini Mungu atatimiza mahitaji yetu. Biblia inatusihi kumwamini Mungu, tutulie ndani ya matunzo yake, na tumtii katika kushiriki huduma zake hapa duniani.

• Taja vitu unavyohitaji na vitu unavyotaka. • Kuna tofauti gani kati ya vitu hivyo? • Kwa nini mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yetu humfanya kutotupa mambo men-

gine?

- 5 - Utoaji Huongeza Baraka za Mungu

Tumeangalia ubora wa raha ya kweli na pia tumeangalia jinsi Mungu anavyotutimizia

mahitaji yetu. Mambo haya yote ni baraka za Mungu kwa ajili ya watoto wake. Tumehoji kwamba hatuwezi kuwa na raha ya kweli bila Mungu kutupa na pia mahitaji yetu hayawezi kutimizwa kikamilifu bila Mungu kutusaidia.

Katika sura hii tunaongea kuhusu baraka za Mungu kwetu tulio watoto wake. Mungu ana sababu nyingi za kutubariki. Zote zatoka moyoni mwake zikitegemea asili zake kama Mungu. Baraka nyingi zaidi za Mungu hazina masharti yo yote kwetu. Bali Mungu huamua kutubariki na kututunza ili tuweze kumtolea na kuyatimiza mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu. Kwa nam-na hii baraka za Mungu zinatangulia utoaji wetu, tena zinawezesha utoaji wetu. Baraka hizi siyo hamasa ya kuishi Mungu anavyotaka ili tufaidike nazo. Maana utoaji wetu haufanyiki ili tupewe baraka hizo. Badala yake, baraka zenyewe zinatangulia ili tuwe na uwezo wa kumtolea Mungu.

Lakini, baraka nyingine za Mungu zategemea tunavyoishi mbele zake. Bado baraka hizo zatoka moyoni mwa Mungu na zinategemea neema yake kwetu. Lakini kwa ujumla Mungu ana-taka tuyatimize mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu na hivyo anatupa motisha ya nyongeza ya baraka. Ndani ya mapenzi haya kuna mambo mengi kama vile kuwa watiifu, watakatifu, kufanya matendo mema, kumtegemea, kumwamini, kumtumaini, n.k. Tukitembea na Mungu wetu na kutimiza mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu, matembezi haya huongeza baraka za Mungu kutokana na ahadi zake ambazo nazo zilikuja kwa njia ya neema (yaani hatukustahili).

Sehemu mojawapo ya mapenzi ya Mungu inahusu kujitoa kwetu mbele za Mungu. Mungu anataka tujitoe kwa hali na mali kwake. Tunaposema kwa hali na mali tunamaanisha matendo ya kutoa pesa, vitu, na mali kwa ujumla pamoja na mambo mengine kama vile kutoa nguvu, akili, mamlaka, hekima, muda, n.k. Hakika Mungu anataka tujitoe kwa ujumla kwake na siyo nusu nusu tu. Ndiyo maana ya Paulo akisema, “itoeni miili yenu” na siyo mali tu.

Warumi 12:1 – “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”

Kwa sababu ya baraka za Mungu tunao uwezo wa kujitoa kikamilifu mbele za Mungu. Pia, kwa sababu ya neema yake, Mungu huahidi kuongeza baraka zetu tunapojitoa kwake. Baraka hizo ni motisha ya Mungu akilenga kutushawishi kutimiza mapenzi yake ndani ya maisha yetu. Katika sura hii tunataka kuendelea kukuhimiza kuwa tayari kujitoa kwa Mungu bila hofu kwamba utapungukiwa kwa sababu umejitoa kwake. Hatupaswi kuhofu kupungukiwa kwa sababu Mungu alishaahidi kututunza na kutubariki kama watoto wake bila hata kuhesabu jiti-

Page 34: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 34 -

hada zetu. Tumewekwa huru ili tuweze kujitoa kwake kwa furaha bila kuhangaika kuhusu mahitaji yetu. Pia hatupaswi kuhofu kupungukiwa tukijua kujitoa kwetu kutaleta baraka za zi-ada kuliko tunavyoweza kujitimizia wenyewe.

Onyo - hatuwezi kustahili baraka

Kabla hatujaanza kuongea kuhusu yale ambayo Mkristo anatakiwa kuyafanya ili awe katika mahali pa baraka za ziada za Mungu, ni lazima tuzielewe baraka hizo. Kuna hatari kwa sababu mtu anaweza kuelewa vibaya akifikiri kwamba anaweza kustahili baraka za Mungu. Anaweza kufikiri kwamba Mungu ameyaweka masharti na akiyatimiza masharti haya ndipo ataweza kumdai Mungu kwa vile anastahili baraka zake sasa.

Lakini, baraka kama baraka ni kitu ambacho hatuwezi kustahili. Kama tunastahili kile tunachokipokea kutoka kwa Mungu tujue siyo baraka tena. Kama tulivyosoma katika kitabu cha Mhubiri, uwezo wa kuyaona mema na raha ya kweli katika maisha yetu ni karama ya Mungu. Kwa maneno mengine tungesema ni neema ya Mungu. Wanadamu hawawezi kudai kitu cho chote kwa Mungu. Kwa sababu hiyo, cho chote anachotupatia ni baraka au neema na hatujaki-stahili.

Kubariki, kutobariki, na namna ya kubariki ni uamuzi wa Mungu

Mungu ana mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu. Kwa mfano anataka tuwe na uhusiano naye, anataka tukamilike ndani ya Kristo, anataka tuwatendee watu wengine kwa upendo, na mambo mengine mengi sana. Ili tuyatimize mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu Mungu hutupatia maagizo ya kuyatii, mafundisho ya kuelewa, uongozi wa dhamiri na Roho Mtakatifu ndani yetu, na motisha ili tuvutwe kuingia katika mapenzi yake.

Biblia hufundisha kwamba tunapoyatimiza mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu Mungu hupenda kutubariki kwa njia mbalimbali. Baraka hizi ni baraka za ziada zilizo tofauti na baraka zile nyingi anazotupa tayari kwa sababu ya upendo wake kwa ajili yetu kama watoto wake na kwa sababu ya mpango wake kwa ajili ya maisha yetu. Lakini hatuwezi kumdai Mungu baraka hizo za ziada kwa kujitahidi katika kuyatimiza mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu. Kutubariki au kutotubariki ni uamuzi wake kulingana na hekima na mipango yake. Ni kweli mara nyingi Mungu hupenda kutubariki kulingana na jinsi tunavyofaulu katika kuyatii maagizo yake, katika kumwiga Yesu, katika kuishi kwa kuzifuata kanuni za Biblia n.k. Lakini kwa kuwa kila baraka tunayopewa ni kwa njia ya neema ya Mungu, ina maana kufuatana na makusudi mengine ya Mungu anaweza kuamua asitubariki mara nyingine kwa ajili ya tendo letu fulani linalotimiza mapenzi yake.

Pengine baada ya tukio fulani, ambalo ndani yake tumeyatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu, Mungu ana kusudi lingine ambalo halitafanikishwa akitubariki wakati huo huo. Lakini tujue hata kusudi hilo lingine la Mungu ni baraka. Yaani wakati wo wote Mungu anafanya kazi ndani ya maisha yetu, kazi hiyo italeta jambo zuri kwetu, yaani baraka.

Kwa sababu hiyo labda ni bora kusema daima Mungu ataongeza baraka wakati tunaishi kufuatana na mapenzi yake lakini yeye mwenyewe ataamua ni wakati gani na namna gani atakavyotubariki. Yaani anaweza kutubariki baadaye katika maisha yetu au hata wakati tutaka-pofika mbinguni. Sina hakika kama kuna vipindi vingine ambavyo Mungu anaamua kutotubariki kwa ajili ya matendo yetu mema lakini ninajua kawaida yake ni kutubariki kwa sababu kufanya hivyo kunampa Mungu raha. Lakini Mungu ni Mungu na anaweza kuamua anavyotaka yeye na ndiyo sababu nasema ni uamuzi wake kutubariki au kutotubariki.

Pale ambapo Mungu anaamua kutubariki kwa sababu tunayatimiza mapenzi yake, yeye ni mwenye uamuzi wa namna ya kutubariki. Bila shaka tungependa kuwa na uwezo wa kumshauri Mungu namna ya kutubariki. Yaani, huwa tunapendelea baraka moja kuliko baraka nyingine. Hakika siyo kosa kumwomba Mungu atubariki katika namna tunayoipendelea. Lakini Mungu ni mwenye hekima sana kuliko sisi na kwa sababu hiyo ni bora yeye achague namna ya kutubariki. Tuamini Mungu atazichagua baraka zitakazotusaidia vizuri zaidi katika maisha yetu kuliko am-bavyo tungechagua sisi. Maana Mungu husuka mambo mengi kwa pamoja. Yaani Mungu ana-weza kuyalenga mahitaji yetu, raha yetu, makusudi na mipango yake, na hata mahitaji ya watu wengine wakati mmoja katika baraka moja anayotubariki nayo. Mungu wetu ni wa ajabu!

Page 35: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 35 -

Ziko baraka za aina mbalimbali

Mara nyingine mioyo yetu hutaka baraka za aina moja tu. Yaani, tunapendelea baraka za kimwili na zinazoleta raha katika maisha yetu. Tunapenda mali zetu ziongezeke, mahusiano yetu kuwa rahisi, mateso yasiwepo maishani mwetu n.k. Lakini baraka ambazo Mungu anaweza kutupa ni za namna nyingi sana. Kuna baraka za kimwili, kiroho, kisaikolojia, kihisia, kiakili n.k. Hapo chini nimezitaja baraka mbalimbali ili kukukumbusha wingi wa Baraka ambazo Mungu anaweza kukubariki.

• Wokovu • Kusamehewa dhambi zetu • Kuwa wana wa Mungu • Yesu kutuombea kwa Mungu • Urithi wa watakatifu • Uzima wa milele • Kutimizwa kwa mahitaji yetu • Faraja ya Roho Mtakatifu • Amani ya Mungu mioyoni mwetu hata wakati wa shida • Upendo wa Mungu • Msaada wa mtu mwingine aliyetumwa na Mungu • Ushauri wa mtu mwingine aliyetumwa na Mungu • Thawabu za mbinguni • Uhusiano ulio karibu na Mungu • Mahusiano mazuri na watu wengine • Kuona raha katika kazi zetu • Usalama • Kuwa na watoto • Kuwa na mke au mume mzuri • Msaada wa kuboresha tabia zetu • Mateso yanayotujenga • Kupewa huduma za kufanya • Kupewa uwezo wa kufanya huduma • Maisha yenye sifa • Hekima ya kuishi nayo • Akili ya kufaulu katika mambo mengi • Msaada wa kupatanisha ndugu waliofarakana

Tungeweza kuendela kutaja hata baraka maelfu ambazo Mungu anaweza kuzitumia ku-tubariki. Bila shaka wewe mwenyewe ungeweza kuongeza baraka nyingi katika orodha hii.

Mara nyingine tunajisikia Mungu hajatubariki kwa kuwa tumezoea kutambua aina chache za baraka. Tunastahili kujifunza baraka zote za Mungu ili tuweze kuzitambua katika maisha yetu na kumshukuru Mungu. Hakika Mungu ana njia nyingi za kutubariki na kwa hekima yake anachagua baraka zinazotufaa.

Mungu huahidi baraka ili atupe motisha kutimiza mapenzi yake

Mungu anafahamu tulivyo na anajua mwanadamu huvutwa na mambo yanayomfaidisha. Kwa sababu hiyo Mungu hutumia faida zetu kama motisha ya kutimiza mapenzi yake katika maisha yetu. Baraka hizo hulenga kutuingiza kwenye mapenzi ya Mungu. Tujue, tusijue, kuishi kwa kuzifuata kanuni za Mungu ni bora kwa ajili yetu. Kuishi kwa kuzifuata kanuni za kidunia huleta hasara, maumivu, na mwishowe maangamizi. Mungu anataka tuzifuate kanuni zake kwa kuwa anatupenda na anatujali. Shida ni jinsi tunavyouamini uongo wa dunia hii. Dunia huahidi raha ya kweli kupitia taratibu zake na sisi huamini na kuzifuata tukitia mashaka juu ya taratibu za Mungu. Kwa sababu Mungu anajua njia za kidunia zitatuletea hasara yeye hujaribu kutuvuta kwenye njia zake kwa kutumia motisha ya baraka.

Page 36: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 36 -

Ndiyo maana Mungu hueleza jinsi atakavyotubariki kufuatana na jinsi tutakavyotimiza mapenzi yake. Mungu huonesha kuna thawabu mbinguni zinazotegemea tunavyoishi hapa du-niani. Tena Mungu huahidi kuyatimiza mahitaji yetu yote wakati bado tuko duniani kulingana na jinsi tunavyomfuata. Isitoshe Mungu ameahidi zaidi ya mahitaji yetu akitubariki kutokana na mwenendo wetu tunavyotembea naye.

Sababu muhimu zaidi za kututaka tuyatimize mapenzi ya Mungu katika maisha yetu

Ingawa Mungu huongeza baraka kama motisha ili tuvutwe kuyatimiza mapenzi yake, Neno la Mungu huonesha sababu nyingine za kuyatimiza mapenzi ya Mungu tofauti na hiyo inayof-ikiria faida yetu. Sababu hizo nyingine zina kipaumbele katika hamu yetu ya kumfuata Mungu, yaani ni muhimu zaidi.

Sababu moja tunajitahidi tuyatimize mapenzi ya Mungu katika maisha yetu ni kuzionesha shukrani zetu kwake. Mungu ametutendea kwa neema, upendo, na mema. Ametuokoa, anatupa uhai, anaendeleza uhai wetu, na zaidi ametubariki tusivyostahili. Itikio letu linapaswa kuwa shukrani. Kuliko kuitafuta faida katika kumtumikia Mungu tunapaswa kujitoa ili tuoneshe shukrani zetu kwake.

Zaburi 107:8-9 – “Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wana-damu. Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema.

Wakolosai 3:16-17 – “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.”

Sababu nyingine ya kuishi kwa Mungu ni kumtukuza Mungu. Mungu alituumba kwa ajili ya utukufu wake. Anataka atukuzwe yeye kwa jinsi tunavyoishi hapa duniani. Kujitoa kwetu hupaswa kulenga faida hii ya Mungu na siyo faida yetu kwanza.

2 Wathesalonike 1:11-12 – “Kwa hiyo tunawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesa-bu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu; jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.”

Sababu ya mwisho tutakayotaja hapa (ingawa ziko sababu nyingine nyingi) ni kusema tun-apaswa tuyatimize mapenzi ya Mungu kwa sababu anastahili. Thamani yake Mungu kutokana na asili zake na matendo yake hudai tuishi kulingana na mapenzi yake.

1 Wathesalonike 2:12 – “ili mwende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.”

Ufunuo 4:11 – “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako viliku-wako, navyo vikaumbwa.”

Kitabu cha Ufunuo unatangaza wazi Yesu Kristo na Mungu wanastahili kutukuzwa katika maisha yetu; yaani wanastahili sisi kujitoa kwao. Tafsiri ya Kiswahili imeficha kidogo maana ya Paulo katika kitabu cha Wathesalonike kikisema, “wajibu wenu kwa Mungu”. Katika Kiyunani neno “kustahili” katika kitabu cha Ufunuo ni neno lile lile linalotumika katika Wathesalonike 2:12. Yaani Paulo anasema, “ili mwende kama anavyostahili Mungu.” Mwenendo wetu una-paswa uyatimize mapenzi ya Mungu kwa sababu Mungu anastahili. Yaani, hata kama sisi hatu-pati faida, na hata kama sisi hatumpi shukrani mioyoni mwetu, bado Mungu anastahili tutimizie mapenzi yake kwa kuwa yeye ni Mungu.

Katika sura hii tunawahamasisha Wakristo wajitoe kwa Mungu kwa kuwa Mungu ameahidi kuiongeza baraka kulingana na kujitoa kwao. Tunalisisitiza wazo hilo kwa kuwa Neno la Mungu linafundisha wazo hilo. Lakini Neno la Mungu linafundisha sababu nyingine pia za kuyafanya mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Ndiyo sababu tumejaribu kuzitaja baadhi ya sababu hizo hapa ili tuishi kwa uwiano kulingana na mafundisho ya Neno la Mungu. Hatutaki kuwa Wakristo wanaojitafutia faida tu ingawa Mungu hutumia baraka kama motisha. Bali Neno la Mungu lina-

Page 37: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 37 -

fundisha kuna sababu zilizo nzito zaidi za kufanya mapenzi ya Mungu. Tukumbuke wazo hilo tunapoendelea kufundisha juu ya mada hiyo.

Mungu hubariki kwa sababu ya upendo wake

Ukisoma katika Waefeso sura ya kwanza kuhusu baraka zote za kiroho tulizo nazo ndani ya Kristo, utakuta maneno yanayoelezea kwa nini Mungu anatoa baraka kwa ajili ya watoto wake. Katika mstari wa nne tunasoma, “Katika pendo”. Hata kwa baraka yake kuu ya kumtuma mwanawe afe msalabani tunasoma, “Mungu aliupenda ulimwengu”. Hakika Mungu hubariki wa-toto wake kutokana na upendo wake, wala siyo kwa sababu wanastahili cho chote. Tukirudi katika Waefeso tunayaona maneno mengine haya yakielezea sababu za baraka za Mungu: Nee-ma yake, mapenzi yake, uradhi wake, na kusudi lake. Yote yanamwangalia Mungu na uamuzi wake. Hakuna hata neno moja linalowaangalia wanadamu, tabia na matendo yao, kana kwamba wanaweza kustahili baraka hizo. Sababu ni kwamba hatuwezi kustahili baraka za Mungu.

Hata maagizo na ahadi za Mungu ni kwa neema

Ni kweli Mungu ameyatoa maagizo yake na ahadi zake. Pia ni kweli Mungu ameahidi kwamba tukiishi kwa taratibu zake tutabarikiwa zaidi. Lakini tuelewe kwamba hata maagizo na ahadi hizo zinatokana na neema na upendo wake. Yaani, kwa kuwa kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu huleta baraka, ni neema kupewa maagizo hayo ili tujue namna ya kumpendeza yeye. Mungu kama Mungu anaweza kudai tumtii bila hata kutubariki lakini kwa neema yake ameongeza baraka. Hata ahadi za Mungu hazikuwa lazima. Lakini alikusudia ku-tubariki ingawa hatukustahili. Hivyo, ahadi zenyewe ni baraka.

Baraka za Mungu zina makusudi mbalimbali

• Mungu hutubariki ili tuwabariki wengine. • Mungu hutubariki ili tuwe na mioyo ya shukrani kwake. • Mungu hutubariki ili tumtegemee yeye. • Mungu hutubariki ili atukuzwe yeye. • Mungu hutubariki ili afurahi awaonapo watoto wake wana raha. • Mungu hutubariki ili aijenge imani yetu. • Mungu huweka motisha ya baraka ili tuyatimize mapenzi yake.

Haya ni makusudi machache ya Mungu katika kutubariki. Ana makusudi mengine mengi lakini nayataja haya kwa kifupi ili uanze kuyapanua mawazo yako.

Katika sura hii tunalikazia kusudi la Mungu kutumia baraka kama motisha kutushawishi tuyatimize mapenzi yake katika maisha yetu. Lengo ni atubadilishe tunavyoishi. Mungu anataka tumwamini, tumtii, tumtegemee, na tuishi kwa kanuni zake. Tukifanya hivyo, matokeo yake ni maisha bora (k.m. sifa njema, mahusiano bora, amani, mema, n.k.) bila hata kuhesabu baraka ambazo Mungu atatuongezea.

Mungu huwabariki wenye imani

Mpaka sasa tumefundisha kuhusu baraka za Mungu kwa upana ili tuwe na msingi wa kuelewa kwa usahihi hoja kuu ya sura hii kwamba Mungu huongeza baraka kwa wanaojitoa kwake. Sasa tumefika kwenye jambo lenyewe.

Kuliko mambo yote Mungu anatutaka tumwamini yeye. Anatutaka tumtegemee na kumtu-maini Yeye. Ni bora tusikitumaini cho chote kingine ili kuyafanikisha maisha yetu. Yaani, tuna-paswa kumtegemea Mungu kwa kuwa anategemeka – yaani Mungu anastahili imani na utegemezi wetu. Kuliweka tumaini letu katika cho chote kingine ni sawa na kukubali kushindwa. Hakuna kingine cha kukitegemea. Mungu anafahamu hivyo na ndiyo sababu anatuagiza kum-wamini.

Kwa neema yake hajaagiza tu, lakini ametuahidi kwamba itakuwa bora kwa ajili yetu wenyewe tukimwamini.

Waebrania 11:6 - “Lakini bila imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtamfutao.”

Page 38: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 38 -

Kumwamini Mungu ni kukubali anaweza na zaidi ni kukubali atafanya alivyosema. Hata ndani ya mstari huu kuna ahadi kwamba Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao. Hakika kumpendeza Mungu kwa njia ya imani yetu huleta baraka katika maisha yetu.

2 Mambo ya Nyakati 20:20 - “....Mwamini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waamini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.”

Katika mstari huu Yehoshafati mfalme wa Yuda anawaambia watu wake kwamba watafaulu katika vita dhidi ya adui yao. Hakika jeshi lao lilikuwa dogo likilinganishwa na lile la adui yao. Lakini kwa sababu Mungu aliwaahidi kwamba watashinda, walipaswa kumwamini. Kuwa na imani kwao kulileta baraka ya kufanikiwa kwenye vita.

Sisi sote tunataka kufanikiwa katika maisha yetu kulingana na mpango wa Mungu. Ahadi za Mungu ni nyingi. Kinachotakiwa ni kuamini tu.

Zaburi 34:8 - “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.”

Mithali 16:20 – “Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye Bwana ana heri.”

Mungu anaaminika kwa sababu mwenyewe ni mwema. Wema wake unamsababishia ku-wabariki wale wanaomtumaini. Atakayemtumaini au kumwamini Mungu atatajwa kwa neno “heri”. Heri ni jambo zuri, ni raha ya kweli.

Isaya 26:3-4 - “Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumaini Bwana siku zote, Maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele.”

Yeremiah 17:5-8 - “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake.”

Mistari ni mingi, kuliko tulivyoitaja hapa, inayoelezea kwamba yule anayemtegemea Mun-gu, anayemtumaini Mungu, na anayemwamini Mungu atabarikiwa na Mungu katika sehemu zote za maisha yake.

Ni lazima tueleze maana isiyo maana yetu. Wengine wanasema mtu akitaka kitu fulani, lazima awe na imani tu na atapewa. Pengine mtu anataka pesa kiasi fulani au chombo fulani. Wanadai mtu akishalenga kitu, ni juu yake kukiomba kwa Mungu na kuwa na imani. Akiwa na imani atapata. Kama ameomba kitu fulani kwa Mungu na hajapata, ni kwa sababu hajawa na imani ya kutosha.

Hii siyo maana yetu. Ni kweli tunapaswa kuyapeleka maombi yetu kwake Mungu, lakini ni juu yake kuitumia hekima na maarifa yake, kuamua kama atupatie kile tunachokiomba. Siyo su-ala la imani tu. Pengine tunaweza kuomba kitu ambacho Mungu anajua kitatuharibu. Kama ni hivi Mungu hawezi kutupatia hata tukiwa na imani ya ajabu. Wakati Paulo aliomba mwiba wake uondolewe, Mungu hakumwambia hapana kwa sababu imani yake haikutosha. Alimwambia hapana kwa sababu ya uamuzi wake Mungu, akidai kwamba neema yake inamtosha Paulo. Maana yake ni kwamba, Paulo angeendelea kuomba na kuongeza imani yake, bado jibu lin-gekuwa hapana.

Imani ni njia ya kumpendeza Mungu na Mungu huongeza baraka kwa wale ambao wanampendeza. Imani siyo njia ya kumlazimisha Mungu kutenda tunavyotaka sisi.

Tunaihitaji imani katika kujitoa kwetu kwake Mungu. Hakuna atakayejitoa kwa Mungu asipomwamini Mungu kwamba atamtunza na kumpatia mahitaji yake. Kujitoa ni kupunguza uwezo wetu wa kuyakamilisha mahitaji yetu. Tukitoa mali yetu, ina maana tunatoa mali ambayo tungeweza kuitumia kutimiza mahitaji yetu na hata kufanya mambo mengine ambayo yangeleta raha na starehe katika maisha yetu. Tukiutoa muda wetu kwa ajili ya Mungu ina maana tunau-punguza muda ambao tungeutumia kwa mambo mengine tunayopendezwa nayo. Yaani mwa-nadamu hupenda kutumia mali, nguvu, muda, na akili zake ili atafute maisha bora yenye raha ya kweli. Mungu anaahidi hayo yote tukimwamini yeye na kumtegemea katika maisha yetu. Kwa hiyo tuna uamuzi, aidha tuamue kujitafutia raha ya kweli (ambayo tulishaona itashindikana) au tuishi kwa Mungu na kuamini yeye atatutimizia mahitaji na raha ya kweli.

Ni suala la imani, na bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Tunapojitoa kwa Mungu tunaonesha kwa matendo yetu imani tuliyo nayo kwamba Mungu ndiye anayetutunza na bila

Page 39: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 39 -

yeye hatujiwezi. Hivyo tujitoe kwa Mungu kwa imani tukijua tutavuna baraka zake na hatuta-pungukiwa.

Mungu hubariki watiifu

Mungu ametupa Neno lake kwa sababu ndani yake tunapata kumwelewa Mungu na jinsi anavyotaka tuishi. Neno la Mungu ni mwongozo wetu katika kuyajua maagizo ya Mungu. Ni lazima tulisome na kulitendea kazi. Tunapomtii Mungu huwa baraka zinafuata. Nyingine za-tokana na kanuni zilizoundwa na Mungu zinazosema kwamba tukiishi kwa kuzifuata kanuni fulani, itakuwa bora kwetu. Hii ni kweli kwa Mkristo pamoja na Mpagani. Na baraka nyingine ni jambo analolifanya Mungu katika maisha yetu wakati huu au wakati ujao.

Zaburi 34:9-10 - “Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.”

Kumcha Bwana ni sawa na kutii kila asemacho. Ni kulisoma Neno lake na kulifuata. Ahadi iko wazi kwamba mtu ambaye atafanya hivyo hatahitaji kitu na zaidi atapewa yote yaliyo mema. Tena mstari huu unaangalia kila sehemu ya maisha ya Mkristo na siyo mali yake tu. Tuna mahitaji mengi. Mengine yanahusu hisia zetu, akili zetu, mahusiano yetu, pamoja na mahitaji yetu ya kimwili. Yote yanachangia katika raha yetu ya kweli. Tukipungukiwa hata sehemu moja tutaikosa raha ya kweli. Mungu anahidi kututimizia mahitaji yetu yote tukiwa tunamtii yeye.

Kumbukumbu la Torati 6:24 - “Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema sikuzote, ili atuhifadhi hai kama hivi leo.”

Musa anaongelea sheria aliyopewa na Mungu katika mstari huu, lakini hata leo kanuni ni ile ile. Tunaelewa kwamba Mungu ameanzisha daraka lingine liitwalo Daraka la Neema. Tunaelewa kwamba hatupaswi kuitii Sheria ya Musa katika Kanisa la leo. Lakini bado kuna maagizo, amri, na kanuni nyingi za Mungu zinazotulenga katika Kanisa. Kufuatana na kanuni hii, kumtii Mungu ni njia ya kuyaona mema zaidi na uhifadhi wa Mungu katika maisha yetu.

Mathayo 6:33 - “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishi-wa.”

Mstari huu unahusu mazungumzo ya Yesu kuhusu kusumbuka katika maisha yetu. Anaonesha kwamba wapagani wanayatafuta mahitaji ya maisha yao wakiwa wameyaweka ku-wa jambo la kwanza. Yaani wanatafuta kujiwekea hazina hapa duniani. Yesu anafundisha kwamba ni kweli tuna mahitaji ya lazima katika maisha yetu, lakini ni lazima tuutafute ufalme wa Mungu kwanza. Kipindi kile Yesu alikuwa akihubiria Waisraeli watubu kwa kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa unakaribia. Kwa ujumla Waisraeli hawakutubu na hivyo Mungu hakuwaletea ufalme wake wa miaka elfu. Badala yake alianzisha daraka jipya liitwalo Daraka la Neema lenye Kanisa lililo Mwili wa Kristo. Leo Yesu hasemi kwa Kanisa lake kutafuta ufalme wa Mungu lakini kanuni bado ni ile ile. Yaani leo Yesu angesema, “tafuteni kwanza mambo ya Mungu”. Maana yake, leo Yesu anataka tumfuate Mungu katika kila njia inayompendeza. Ina maana ni lazima tumtii Mungu na kufanya kazi naye. Tayari Mungu anajali maisha yetu na anatimiza mahitaji yetu. Tukiamua kumweka Mungu awe wa kwanza katika maisha yetu kuna baraka za ziada. Humo humo ndimo ilimo raha ya kweli. Raha ya kweli ni kitu kinachotoka kwa Mungu, hatuwezi kujipatia. Hivyo tuache kujaribu kujipatia, tumtii Mungu katika mapenzi yake, na tujue yeye at-atupa raha ya kweli pamoja na kuyatimiza mahitaji yetu yote.

Yakobo 1:25 - “Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.” (au tafsiri ya habari njema) “Atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.”

Kuna hali mbili zinazoangaliwa hapa. Kuna yule anayesoma Neno la Mungu (sheria katika mstari huu) halafu halitii katika maisha yake. Mtu kama huyu hawezi kutegemea baraka za zi-ada kutoka kwa Mungu. Lakini yule ambaye atasoma Neno la Mungu na kuanza kulitenda na ku-litii huongezewa baraka za Mungu.

Page 40: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 40 -

Zaburi 1:23 - “Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”

Tumeshaona jinsi Biblia inavyoyatumia maneno kama matunda na mti uliopandwa karibu na maji kuwa mfano wa mtu mwenye raha ya kweli. Hapo tunaona baraka za namna hii zinaen-dana na jinsi mtu atakavyojizamisha katika Neno la Mungu. Siyo mara kwa mara lakini ni mchana na usiku. Mtu anayefanya hivyo humpendeza Mungu. Kumpendeza Mungu huleta baraka. Baraka kutoka kwa Mungu huleta raha ya kweli.

Mungu anatuagiza kujitoa kwake. Anatutaka tuitoe mali yetu na anatutaka tuzifanye huduma zake – yaani kwa hali na mali. Biblia inafundisha tukijitoa kwake ataziongeza baraka zetu. Ni juu yetu kuwa watiifu.

Mungu huwabariki wanaowasaidia wahitaji

Hakika Mungu anawajali wahitaji wote duniani. Kwa sababu hiyo ameahidi baraka kwa kila mmoja ambaye atamsaidia mhitaji ye yote.

Mithali 19:17 - “Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.”

Katika mstari huu tunajifunza kwamba tunapomsaidia maskini tunachofanya ni kumsaidia Mungu. Kwa sababu tendo la namna hii linamfurahisha Mungu, naye ameahidi kwamba atamli-pa mtu yule kwa ajili ya tendo lake jema. Mstari wenyewe hausemi jinsi Mungu atakavyomlipa lakini tunaweza kujua Mungu ataichagua njia iliyo bora. Naona ni bora Mungu achague jinsi ya kunilipa kuliko mimi kujichagulia kwa kuwa maarifa yake yanazidi maarifa yangu.

Mithali 28:27 - “Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.”

Kanuni inasema kwamba ukimsaidia maskini wewe mwenyewe hutakuwa na hitaji. Katika maisha yetu tunahitaji mambo mengi. Huwa mtu akisoma mstari huu anafikiri maneno “hata-hitaji kitu” yanaongelea mahitaji ya kimwili peke yake. Lakini hakika mahitaji yetu ni makubwa kuliko mahitaji yetu ya kimwili tu. Naamini kwamba mahitaji yanayoongelewa hapa ni mahitaji ya kimwili pamoja na mahitaji yote mengine tuliyo nayo. Naamini kwamba Mungu anaweza ku-tutimizia yote ili tusikose kitu, tuwe na raha ya kweli, na tumtukuze yeye.

Ni muhimu tuone pia kwamba yule ambaye hatawasaidia wahitaji haachwi hivi hivi. Kuna hatua inayochukuliwa dhidi yake ambayo ni hatua ya laana.

1 Timotheo 6:17-19 - “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wa-siutumainie utajiri usiyo yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvi-tumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.”

Hata wenye mali wanatakiwa kuliweka tumaini lao kwa Mungu. Wanaagizwa kuwasaidia wengine kwa mali waliyo nayo. Kwa jinsi hii watakuwa wanajiwekea akiba mbinguni. Zaidi wa-tapata uzima ulio wa kweli kweli hapa duniani, yaani raha ya kweli. Kufuata njia za kidunia ni kupata uzima usio wa kweli. Kufuata njia za Mungu (ambayo mojawapo ni kuwasaidia wahitaji) ni kupata uzima ulio wa kweli ambao ndiyo maisha yaliyobarikiwa na Mungu.

Luka 6:38 - “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”

Tena tunaona kwamba ukiwasaidia wengine nawe utasaidiwa. Hii inaweza kutokea kwa njia mbili. Kwanza yule ambaye anamsaidia mwingine, akijikuta ni mhitaji, yule aliyesaidiwa atakuwa na moyo wa kumsaidia kwa sababu mwenyewe aliwahi kusaidiwa naye.

Pia mstari huu unaangalia jinsi Mungu atakavyotufanyia tukiwa tunawasaidia wahitaji. An-galia maneno anayoyatumia. Siyo kurudishiwa ile uliyotoa tu, lakini kiasi cha kuzidisha, kujaa, kushindiliwa, na kusukwa-sukwa.

Page 41: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 41 -

Mungu humbariki mtiifu katika kujitoa kwake

Mithali 3:9-10 - “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.”

Mithali 11:24 - “Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.”

Malaki 3:10 - “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkani-jaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbingu-ni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

Hakika matoleo ni sehemu ya maagizo ya Mungu na sehemu ya kumpendeza Mungu. Kanuni na ahadi zaonekana katika mistari hii kwamba anayemtolea Mungu atabarikiwa katika maisha yake. Si kwamba kwa matendo yetu ya kutoa tunastahili baraka. Tendo lenyewe lina maana kwa kuwa linatangaza jinsi tunavyomtumaini Mungu kuliko mali yetu. Tena “utiifu” ni neno kuu. Katika kulitii Neno la Mungu ndipo tunaonesha tunavyokubali Mungu anajua kilicho bora kwa ajili ya maisha yetu. Kuwasaidia wengine kunaonesha jinsi tunavyoamini kwamba Mungu atayatimiza mahitaji yetu. Kujitoa kwa ajili ya mambo ya Mungu ni ushahidi unaosema, ingawa tunaihitaji mali hiyo (au muda au nguvu n.k.), tunamtegemea Mungu kwa mahitaji yetu na tutamtii katika maagizo yake.

Wafilipi 4:15-19 – “Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sa-daka yenye kibali, impendezayo Mungu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”

Katika mistari hii Paulo anaonesha kanuni kwamba Mungu huwatunza na kuwabariki wale ambao wanajitoa kwa ajili ya kazi zake. Wakristo wa Filipi walikuwa wamejitoa kwa Mungu wakimsaidia Paulo katika huduma na mahitaji yake. Paulo alitambua kwamba watavuna mengi mazuri katika maisha yao kwa sababu Mungu atawajazia akiitikia utayari wao wa kujitoa. Anaonesha kwamba Mungu hutunza “hesabu” ya matoleo yao akikusudia kuwarudishia na zaidi. Si kwamba wanastahili baraka ya Mungu bali Mungu anawabariki kwa neema yake kwa kuwa aliahidi kuwabariki wale wanaojitoa kwake.

Mwisho

Tusihofu kujitoa kwa ajili ya Mungu wetu. Mungu wetu ni wa neema na mwenye kutubariki ili atuwezeshe kujitoa kwake na kutimiza mapenzi yake katika maisha yetu. Isitoshe, tukimwa-mini na kumtii katika kujitoa kwake, kwa neema yake, Mungu ameahidi kutuongezea baraka nyingine.

• Je, unaziona baraka za Mungu katika maisha yako? • Kuna haja ya kuuongeza ufahamu wako kuhusu njia ambazo Mungu huzitumia kukubariki

ili uzitambue baraka ambazo hujawahi kuzitambua? • Katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu, eleza jinsi mara nyingine unavyojaribu kustahili

baraka za Mungu? • Kwa nini hatuwezi kustahili baraka za Mungu? • Je, unaamini Mungu anayatimiza mahitaji yako yote ili uweze kujitoa kwake? • Je, unaamini Mungu atakubariki kuliko hata mahitaji yako ukijitoa kwake? • Kwa nini Mungu anapendezwa na imani yetu? • Kwa nini hali ya kutaka kufaidika na Mungu kutokana na utoaji wetu ni mawazo ya

uchanga katika maisha ya Mkristo? • Eleza sababu nyingine, zilizo muhimu zaidi, za kujitoa kwa Mungu. • Je, ni lazima Mungu atubariki kila tunapomtolea? Kwa nini?

Page 42: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 42 -

- 6 - Mungu Huwapa Watu Wake Kulingana na Asili

Zake Mara nyingi tu dhaifu katika utoaji wetu kwa kuwa hatujamfahamu Mungu kiasi cha

kutosha. Mungu ametupa Neno lake ili tuweze kumjua. Biblia huonesha Mungu akihusiana na wanadamu. Kupitia matukio kwenye mahusiano hayo tunajifunza mengi kuhusu Mungu. Vilevile Biblia inafundisha kwa kutamka ukweli ulivyo kuhusu Mungu. Isitoshe tunajifunza kuhusu Mungu wakati tunapiga zoezi la kutembea naye katika maisha yetu.

Mungu wetu ni wa ajabu kiasi kwamba hatuwezi kuelewa yote. Njia zake zipo juu kuliko njia zetu na mawazo yake yapo juu kuliko mawazo yetu. Lakini bado Mungu anataka tupate kumfahamu kiasi tunachoweza ili tuweze kuhusiana naye kwa njia bora na kumwamini zaidi na zaidi katika maisha yetu. Kazi ya kumjua Mungu ni kazi endelevu tutakayopambana nayo mai-sha yetu yote. Siku hadi siku tutamwelewa kidogo zaidi tukiwa na lengo la kumjua Mungu.

Daima utoaji wetu utaongezeka kulingana na jinsi tunavyomjua Mungu. Tunapouelewa wema wake, uwezo wake, upendo wake n.k. tunatiwa moyo kujitoa kwake tukijua anastahili utoaji wetu na tukijua pia tunaweza kumtegemea atutimizie mahitaji yetu yote. Hatutahofu ku-jitoa tukifikiri tutapungukiwa kwa kuwa kumjua Mungu kutaondoa hofu yote.

Basi tuangalie asili chache za Mungu tukijifunza jinsi zinavyohusika katika utoaji wetu.

Mungu ni mwenye maarifa yote

Biblia inatufundisha kwamba Mungu anayajua mambo yote. Ina maana akili yake iko juu sana na sisi hatuwezi kuzifahamu njia zake.

Isaya 55:8-9 - “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sa-na kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”

Katika kuyajua yote, mawazo yake yote ni kamili tena mema. Hakuna kasoro katika fahamu zake. Hii ndiyo sababu tunaweza kumtegemea katika maamuzi yake juu ya maisha yetu.

1 Yohana 3:20 - “...kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.”

Sasa tunapofikiri jinsi Mungu anavyotutimizia mahitaji yetu, na jinsi anavyotupatia hata mambo mengine ambayo si mahitaji, tunaweza kuamini anafanya kwa njia iliyo bora kulingana na hekima na maarifa yake. Hawezi kukosa kutupa kile tunachokihitaji, eti, kwa sababu hakujua. Anajua! Anayajua mahitaji yetu yote. Anaujua mpango wake kwa ajili ya maisha yetu na mambo yepi ambayo yangetusaidia kuutimiza mpango huo. Wakati tunapoomba kitu anajua kama kitatufaa au hakitufai.

Mathayo 6:32 - “...kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

• Je, unaamini Mungu anayafahamu mahitaji yako yote? • Je, unaamini Mungu anafahamu namna bora ya kukutimizia mahitaji yako? • Kama umejibu hapana katika maswali hayo ufanye nini ili uamini hivyo?

Mungu ni mwenye nguvu zote

Mathayo 19:26 - “Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.”

Hakika Biblia inasema Mungu ni mwenye nguvu zote, mwenye uwezo wote, na mwenye en-zi yote. Mambo yote yawezekana kwake. Hakuna anayeweza kumshinda wala hakuna shida inayoweza kumzidi. Ni kwa sababu ya uwezo wake tunaweza kutegemea atayatimiza mahitaji yetu yote na zaidi.

Page 43: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 43 -

Wafilipi 4:19 - “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya KristoYesu.”

Hatuwezi kukosa mahitaji yetu kwa sababu kile kinachoyatimiza hakina mwisho. Mungu anatumia nguvu yake na utajiri wake kututimizia mahitaji yetu. Utajiri wake hauna mwisho. Haiwezekani ikatokea siku moja Mungu akadai kwamba urudi siku nyingine kwa sababu ameishiwa mpaka labda mwisho wa mwezi.

Tunapounganisha fahamu zake na uwezo wake tuna uhakika kwamba tunaweza kumtegemea na kwamba bila yeye hatujiwezi.

• Ungependa kuutegemea uwezo wako, ulio na mipaka katika kuyatimiza mahitaji yako, au ungependa kumtegemea Mungu aliye na uwezo wote? Kwa nini?

• Ni shida gani katika maisha yako ambayo Mungu haiwezi? Mungu yuko mahali pote

Asili nyingine ya Mungu ni kwamba yuko mahali pote. Ina maana po pote utakapoenda Mungu yupo. Kama ni mlimani au chini ya bahari yupo. Hii ni habari njema kwa sababu ina maana kila wakati Mungu yupo nawe akiyachunguza mahitaji na hali yako na kuyashughulikia.

Mithali 15:3 - “Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.”

Mungu habadiliki

Biblia inasema Mungu habadiliki. Jinsi alivyokuwa jana tunaweza kutegemea ndivyo atakavykuwa leo na kesho.

Yakobo 1:17 - “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.”

Tena hii ni habari njema. Ikiwa Mungu ameahidi leo kwamba atatutimizia mahitaji yetu, basi, tunaweza kuitegemea ahadi hiyo hiyo kesho kwa sababu Mungu habadiliki. Ikiwa leo Mungu ni mwenye uwezo wote, na ndiye anayeweza kututimizia mahitaji yetu, vilevile hata kesho Mungu atakuwa na uwezo wote. Mungu ni mwema na mwenye ukarimu

Mwanzo 1:28-30 - “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkai-jaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.”

Katika mwanzo wa mambo yote, mara tu baada ya kuwaumba wanadamu, Mungu akaanza kuwabariki na kuwapa mamlaka na mahitaji yao ili waweze kuishi na kuutimiza mpango wake kwa ajili ya maisha yao.

Yohana 14:2-3 - “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaam-bia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”

Hata katika maisha ya baadaye mbinguni Yesu anajiandaa kutupokea, tena kwa njia nzuri huku akiwa anatubariki kuliko tunavyostahili.

Yohana 3:16 - “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Tatizo letu kuu lilikuwa dhambi. Mungu alitupenda kwa kiasi kikubwa mpaka aliweza kumtoa mwanawe kwa ajili yetu. Kwa kweli Mungu anajitoa kwetu kwa ukarimu. Hakuna mfano ulio bora wa ukarimu wa Mungu kuliko kutoa uhai wa mwanawe. Haikuwa lazima. Ilikuwa gha-

Page 44: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 44 -

rama kuliko gharama zote. Lakini Mungu, kwa sababu ya upendo na ukarimu wake, alitusaidia katika shida hiyo.

Yakobo 1:17 - “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.”

Vitu ambavyo Mungu anatoa kwetu ni vyema na kamili. Hii ndiyo ishara ya ukarimu. Mungu anatujali na hivyo hutaka tupewe vitu vinavyofaa, visivyo na kasoro.

Mungu ni mwenye ukarimu unaozidi mahitaji ya lazima

Zaburi 34:8-10 - “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamfuatao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.”

Mungu ni mwema hivyo anawafanyia watu wake wema. Si kwamba atayatimiza mahitaji yao tu, lakini hawatakosa cho chote kilicho chema. Watu wa Mungu watakuwa na vitu vyema ndani ya maisha yao kutokana na asili ya Mungu mwenyewe kuwa mkarimu.

Mathayo 6:33 - “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishi-wa.”

Malaki 3:10 - “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkani-jaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbingu-ni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

Luka 6:38 - “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”

Lugha inayotumiwa katika mistari hii siyo lugha ya kusema Mungu atatoa kile kilicho cha lazima tu. Haioneshi kwamba yeye ni Mungu ambaye hataki kuvitoa vitu vyake.

Hapana! Mistari hii inaonesha kwamba yeye ni Mungu ambaye yuko tayari kuwabariki wa-tu wake, tena elezo la moyo wake ni kwamba anatamani kuwabariki. Maneno kama “kuzidishi-wa” na “kumwaga baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha” ni maneno ya kuonesha kiasi kikubwa kuliko mahitaji tu.

Yule ambaye ni mjanja katika biashara ya mahindi hupenda kulijaza gunia huku akiwa mwangalifu kutotikisa mfuko sana. Wanataka faida zaidi kwa hiyo hawataki kujaza gunia sana. Lakini kama mnunuzi yupo ni lazima mwenyewe atalisukasuka gunia lile ili lijazwe kikamilifu. Uone jinsi Mungu anavyofanya kwa watu wake wanaomfuata, “kushindiliwa”, “kusukwa-sukwa hata kumwagika”. Mungu hawezi kutunyima bali anatafuta kutuongezea zaidi.

Mwisho

Asili (tabia au sifa) za Mungu zatuongoza kujitoa ipasavyo. Hatutakiwi kuogopa kwamba tutakufa kwa njaa au tutakosa muda kwa mambo mengine yaliyo muhimu tukijitoa kwake Mungu. Asili zake zinamsaidia kujua mahitaji yetu na zinamsaidia kuweza kuyatimiza mahitaji yetu. Tena asili zake zinahakikisha hatabadilisha ahadi na mipango yake kwa ajili ya maisha yetu.

Pia inatufaa kuondoa mawazo mabaya tuliyo nayo kuhusu Mungu. Mungu siyo mnyimivu. Tuanze kuuona wema wake na ukarimu wake kwetu ili tuweze kumkubali kulingana na jinsi anavyotufanyia.

• Taja njia ambazo Mungu amekutendea kwa ukarimu. • Kama Mungu mwenye uwezo wote anatutendea kwa ukarimu, kwa nini mara nyingine

tunajisikia tumenyimwa au kupungukiwa? • Eleza jinsi mawazo yako kuhusu Mungu alivyo yamepungukiwa mara nyingine. Ulikuwa

unawaza mawazo gani yasiyo sahihi?

Page 45: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 45 -

- 7 - Mungu Anamiliki Vitu Vyote

Kuna maneno ambayo tunayatumia kila siku. Maneno haya ni kikwazo katika uwezo wetu

wa kujitoa ipasavyo. Maneno yenyewe ni, “changu”, “chetu”, “yangu”, “yetu”, “wangu”, “wetu”n.k. Maneno haya humtambulisha yule anayemiliki kitu au vitu. Kila siku tunayatumia tukisema, “Haya ni mahindi yangu, hii ni basikeli yangu, hii ni nyumba yangu” n.k.

Kumiliki kitu humpa mtu mamlaka juu ya kitu kile. Mwenyewe anaamua jinsi kitakavyo-tumika na wakati gani kitakapotumika. Atavilinda vitu vyake kwa nguvu zake zote. Akiamua kuvitoa vitu vile kwa wengine ni uamuzi wake. Lakini siyo rahisi avitoe kwa wengine wakati yeye mwenyewe anavihitaji. Labda kama vitakuwa vitu vya ziada ambavyo havihitaji, ataweza kumsaidia mwingine.

Lakini kwa kawaida, mtu akiombwa na mtu mwingine kuvitoa vitu vya mtu huyu, ataona kuna urahisi kuvitoa kwa jinsi alivyoagizwa. Hataona ugumu kwa sababu haumii kuvitoa kwa vile siyo vitu vyake.

Sababu nyingine ya watu wa Mungu kutojitoa ipasavyo ni mawazo yao ya kufikiri ni wamiliki wa vile walivyo navyo. Wakija kuelewa kwamba siyo vitu vyao bali ni vitu vya mwingine, ndipo wataona ni rahisi zaidi kuvitoa kulingana na agizo la mmiliki.

Anayeumba ndiye mwenye kumiliki

Mwanzo 1:1 - “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.”

Biblia inatuambia kwamba Mungu aliumba vitu vyote. Katika Wakolosai Paulo anasema, “vitu vinavyoonekana, na visivyoonekana”. Hakuna kitu ambacho hakijaumbwa na Mungu. Mwenye kuumba anamiliki vyote alivyoviumba.

Ayubu 41:11 - “Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.”

Ayubu anaonesha jinsi Mungu alivyokuwa wa kwanza. Hakukuwa kitu kabla ya Mungu. Mungu hategemei mtu, kitu, wala mamlaka yo yote ile. Vyote vilivyopo vyatokana na yeye mwenyewe. Ndiyo sababu Ayubu anasema hakuna anayeweza kumdai Mungu. Ambaye ni mmiliki wa vyote hawezi kudaiwa na mwingine kwa sababu hakuna mmiliki mwingine. Tazama jinsi Mungu mwenyewe anavyosema, “Kila kitu ni changu.”

Mathayo 6:13 - “Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.”

Wakati Yesu alipowafundisha wanafunzi wake namna ya kuomba alitaka watamke ndani ya ombi hilo kwamba Mungu ndiye mmiliki wa vyote. Ni muhimu tuwe na wazo hilo kila wakati kwa sababu tunapoanza kufikiri kuwa sisi ni wamiliki inatuchanganya kiasi kwamba hatuwezi kutenda jinsi Mungu anavyotutaka.

Kumtolea Mungu ni kumpa vilivyo vyake

1 Mambo ya Nyakati 29:14 - “Kwa hiyo Daudi akamwahidi Bwana mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele. Ee Bwana, Ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na ku-wawezesha wote. Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu. Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako, na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.”

Daudi aliielewa hali halisi ilivyo. Alionesha kwamba Mungu amemiliki vitu vyote na wazo hilo lilimsumbua wakati alipokuja kumtolea Mungu. Huwa tunapomtolea Mungu tunafikiri tunamsaidia. Tunafikiri tunampa vitu vyetu. Daudi aliuona ukweli ni kwamba mawazo haya

Page 46: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 46 -

mawili hayaendani. Kama hujamiliki kitu haiwezekani utoe kitu. Aliona tunajifanya kama tunamtolea Mungu kwa hiari yetu wakati ukweli ni kwamba vilikuwa vitu vyake tayari.

Jasho hutudanganya

Katika kuishi tunafanya kazi kila siku. Kama wewe ni mkulima, unalima, unapanda, unapal-ilia, na unavuna. Kazi zote unazifanya kwa mikono yako mwenyewe tena kwa kutoa jasho. Mwishowe ni rahisi kufikiri ni mazao “yako” sasa.

Wengine wanajenga nyumba kwa mikono yao wenyewe. Wanafyatua matofali, wanayabeba, na wanajenga. Hakuna anayewasaidia. Kama ni muda, ni muda wao. Kama ni nguvu, ni nguvu zao. Kama ni akili, ni akili zao. Mwishowe wanaona wameimiliki nyumba ile.

Matendo 17:24-25 – “Mungu aliyefanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.”

Pumzi ni muhimu katika maisha ya mtu. Bila hewa ya kuvuta wote watakufa. Biblia inadai kwamba kila ulicho nacho kimetoka kwa Mungu. Kama ni akili yako, nguvu yako, hata muda wako. Hakuna anayeweza kulima wala kujenga bila Mungu. Tusijidanganye kufikiri kwamba tumevimiliki vitu kwa sababu ya jasho tulilotoa. Maana hata pumzi tuliyopumua wakati wa ku-jenga tulipata kutoka kwa Mungu.

Vitu vyote vipo kwa ajili yake

Wakolosai 1:16 - “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mam-laka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.”

Hata ukikubali kwamba Mungu amemiliki vitu vyote, wengine wanadai kwamba vitu hivi vipo kwa ajili yao. Tukiangalia katika kitabu cha Mwanzo wakati Mungu alipoumba tunaona kwamba akawaweka wanadamu juu ya vitu vyote na akawaambia watajipatia mahitaji yao kutokana na vitu vile. Maelezo haya huwadanganya wengine mpaka wanafikiri shabaha ya Mungu ya kuviumba vitu vingi ilikuwa kwa ajili ya faida yetu tu.

Lakini Mungu alikuwa nayo shabaha iliyo kubwa kuliko sisi. Sababu ya Mungu kutuumba, pamoja na vitu vingine vyote, ilikuwa yeye atukuzwe. Kama Wakolosai inavyosema, vyote vipo kwa ajili ya Kristo mwenyewe aliyeviumba. Mungu ana mpango kwa ajili ya maisha ya kila Mwanadamu na amewapa uwakili wa vitu vyake ili mpango wake utimizwe.

Vitu vingine vipo kwa ajili ya kuendeleza uhai wetu na kazi zetu. Lakini shabaha ya kuen-

deleza uhai wetu ni kutuwezesha kumtumikia Mungu katika mpango wake kwa ajili ya maisha yetu. Kwa jinsi hii vitu vyote vipo kwa ajili yake na kwa ajili ya mipango yake.

Hata sisi tupo kwa ajili yake

1 Wakorintho 6:19-20 - “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la roho Mtakatifu aliye ndani yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Warumi 12:1 - “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”

Biblia inasema wazi kwamba hata mwili tulio nao hatujaumiliki. Katika kutuumba Mungu ametumiliki na zaidi katika msalaba ametununua kwa damu yake. Yesu alitukomboa. Tulikuwa

Page 47: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 47 -

watumwa wa dhambi tukiitumikia dunia hii na kiongozi wake. Lakini Yesu aligharimia uhai wake ili aweze kutukomboa na kutuokoa. Kwa sababu hii sisi ni mali yake.

Wazo hili ni gumu kuliko mawazo mengine. Tungeenda mahakamani tusingeweza kusikia mawakili wakihojiana juu ya mwili wa mtu aliye hai, wakidaiana kwamba mwili huu umem-ilikiwa na mwingine. Kama mwanadamu, kuna kitu kimoja ambacho tuna hakika nacho, kwam-ba angalau tumemiliki miili yetu.

Neno la Mungu linadai tofauti lakini. Linasema kwamba miili yetu ni nyumba ya mwingine aliyeimiliki. Katika Warumi 12 Paulo anatusihi kuitoa miili yetu kwa ajili ya Mungu. Si kwamba Mungu hajaimiliki tayari lakini anataka tukubali miili yetu ni mali yake. Tukifanya hivyo tutampendeza Mungu.

Mwisho

Ni vita vya mawazo. Hakika wengi hawajitoi ipasavyo kwa sababu wanaamini kujitoa ni kuvitoa vitu vyao wanavyovimiliki. Kwa mawazo yao, mahitaji yao na matakwa yao, wakilin-ganisha na walivyonavyo tayari, wanaona havitoshi. Mwisho wake wanashindwa kumpa Mungu kwa kuona ni haki yao kubaki navyo vile walivyomiliki.

Lakini tukishaelewa kwamba mali tuliyo nayo siyo yetu, tutaona ni rahisi zaidi kumtolea Mungu vitu vilivyo vyake wakati anapotuagiza kufanya hivyo.

• Je katika maombi yako wewe hutamka utambuzi wako wa jinsi Mungu amilikivyo vitu vyako vyote?

• Je unakubali Mungu amemiliki vitu vyote? Kama jibu lako ni hapana, ni vitu gani ambavyo Mungu hajavimiliki?

• Kwa nini ni muhimu kutambua hata miili yetu siyo mali yetu? • Kujua Mungu amemiliki vitu vyote kunabadilisha mawazo na matendo yako kivipi? • Eleza jinsi kumtolea Mungu ni kumpa vitu vilivyo vyake tayari. • Eleza jinsi jasho letu linavyotudanganya.

Page 48: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 48 -

- 8 - Uwakili

Tumejifunza kwamba Mungu amemiliki vitu vyote. Wengine wanaweza kuuliza kwa nini

tunavyo vitu kama vyote ni vya Mungu. Au zaidi wanaweza kuuliza kwa nini Mungu anaomba tutoe vitu vyetu kama hatunavyo. Jibu liko katika neno uwakili. Hatujavimiliki vitu tulivyo navyo bali tumekabidhiwa ili tuwe mawakili.

UFAFANUZI WA WAKILI

Katika Biblia wakili ni mtu ambaye amepewa mamlaka katika nyumba ya mtu aiendeshe na aitunze badala ya mwenye nyumba mwenyewe au wakati mwenye nyumba hayupo. Ina maana yule wakili anafanya kazi zote za nyumba ile. Kama ni biashara ataiendesha, kama ni wageni atawapokea, kama ni chakula atakisimamia. Kwa kweli wakili alikuwa mtu mwenye wajibu mkubwa. Mwenye nyumba alimtaka wakili wake amletee faida, siyo kutunza tu akiwa anajaribu kuizuia hasara.

NANI NI WAKILI?

Mwanzo 1:28-30 - “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkai-jaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.”

Hapo mwanzo, wakati Mungu alipoiumba dunia hii na vyote vilivyomo, Mungu aliwaweka wanadamu juu ya yote ili watawale na kutunza mali ya Mungu. Mungu hakuwapa ili wavimiliki. Mungu bado anamiliki vyote, lakini wanadamu ndiyo wanaoitunza na kuisimamia. Kwa maana hii wanadamu wote wamepewa uwakili juu ya uumbaji wa Mungu. Wapagani na Wakristo, wote wamepewa uwakili huo. Shida ni kwamba wengi hawautimizi wajibu wao.

1 Wakorintho 4:1 - “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.”

Mstari huu unaongea juu ya viongozi katika Kanisa kipindi cha Paulo. Unatuonesha jinsi Paulo alivyoelewa uwakili na kwamba siyo vema kumfuata kiongozi mmoja badala ya mwingine kwa kuwa wote ni watumishi wa Mungu anayemiliki vitu vyote akimgawia kila mtu uwakili wake. Kama Wakristo, kuna uwakili maalum ambao tunapewa. Tunapewa uwakili wa mambo ya Mungu (siri zake). Huu ni uwakili ulio tofauti na uwakili ule ambao wanadamu wote wanao juu ya uumbaji wa Mungu.

Kwa hiyo nani ni wakili? Kila mwanadamu na kila Mkristo. Upende, usipende, wewe ni wakili na inakubidi kujifunza juu ya uwakili wako kwa sababu siku moja utahitaji kumjibu Mungu kuhusu namna ulivyoutekeleza uwakili uliopewa na Mungu.

• Je, wewe ni wakili wa Mungu? • Kuwa wakili ina maana gani?

WAKRISTO NI MAWAKILI WA NINI?

Tu mawakili juu ya miili yetu

1 Wakorintho 6:19-20 - “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Page 49: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 49 -

Uwakili wetu wa kwanza ni juu ya miili yetu. Miili yenyewe siyo mali yetu. Tunaitawala miili yetu na hivyo Mungu anataka tuitumie kwa utukufu wake. Mungu amekupa mwili ulio nao ili uutumie kwa ajili ya kazi zake na mipango yake.

Kila siku unafanya maamuzi mengi katika mawazo, maongezi na matendo yako. Usisahau kwamba Mungu anakuchunguza ili aone uwakili wako juu ya mwili huu aliokupa. Ndiyo sababu Paulo anatuagiza, “itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.”

Tu mawakili juu ya watoto wetu

Waefeso 6:4 - “Nanyi, akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”

Biblia inasema wazi kwamba sisi wazazi tumepewa watoto na Mungu. Kama mawakili tun-apaswa kuwalea, kuwatunza, na kuwafundisha ili wakue wawe watu wazima ndani ya Kristo. Ni uwakili kweli kweli na kila mmoja anawajibishwa ndani ya uwakili huo.

Inasikitisha kuwaona wengi hawawatunzi watoto wao vizuri. Hata wachungaji wengine wanajishughulisha sana na kazi ya Mungu wakiwa wamewasahau watoto wao. Wanawafun-disha wengine kuhusu Mungu wakiwa kanisani lakini nyumbani hawawafundishi watoto wao juu ya Mungu. Hawa ni mawakili wabaya.

Tu mawakili juu ya maskini na wahitaji

1 Timotheo 5:16 - “Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.”

Mathayo 25:37-40 - “Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukari-bisha, au u uchi tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”

Kama ni maskini, wajane, au watoto yatima, Mungu ametupa wajibu na uwakili wa ku-watunza na kuwasaidia katika maisha yao. Tunapomwona mhitaji, maana yake, Mungu anataka tuvitumie vitu vyake alivyotukabidhi katika uwakili wetu ili tuwasaidie. Tu mawakili juu ya Kanisa

I Timotheo 3:5 - “Yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Ka-nisa la Mungu.”

Tito 1:7 - “Maana imempasa askofu (mwangalizi) awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu.”

Watu wa Mungu wamepewa uwakili wa Kanisa lake Mungu. Hivyo Mungu amelipatia Kani-sa viongozi ambao wanapaswa kuhakikisha kwamba Kanisa lenyewe linatunzwa na kuendeshwa kwa njia inayompendeza Mungu.

Ni wajibu wa kila Mkristo kulijali na kulichangia kanisa lake ili kanisa liweze kulitimiza kusudi lake katika dunia hii.

Tu mawakili juu ya muda wetu

Zaburi 90:12 - “Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.”

Waefeso 5:15-16 - “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasiyo na hekima, bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”

Muda wote tulio nao hapa duniani tulipewa na Mungu. Hivyo tu mawakili juu ya muda wetu. Mungu anataka tuutumie muda wote tulio nao kwa namna iliyo bora tena inayompendeza yeye.

Page 50: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 50 -

Tu mawakili juu ya karama zetu

1 Petro 4:10 - “Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; ka-ma mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.”

Mungu ametupa karama mbalimbali. Tuna karama za Roho ambazo ni taaluma mbalimbali za huduma ndani ya Kanisa. Hata uwezo wo wote mwingine tulio nao tulipewa na Mungu. Juu ya karama hizo sisi ni mawakili. Maana, Mungu anataka tuzitumie kwa ajili ya mambo yake.

1 Wakorintho 12:7 - “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo (karama) wa Roho kwa kufaidiana.”

Katika Maelezo ya Paulo tunapata kuelewa kwamba karama tunazopewa na Mungu siyo kwa ajili ya faida yetu bali ni kwa ajili ya wengine ndani ya Mwili wa Kristo. Mungu ana mpango ndani ya Kanisa lake na ndiyo sababu anazitoa karama hizo ili zitumike katika kuutekeleza mpango wake.

Tu mawakili juu ya mali

Luka 16:11 - “Basi kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani ataka-yewapa amana mali ya kweli?”

Mungu anapompa mwanadamu mali, tukumbuke bado ni mali ya Mungu. Hivyo anamweka mwanadamu yule kuwa wakili wa mali hiyo. Mungu anaweza kumpa mmoja mali kuliko mwingine. Yule anayepewa mali zaidi, anapewa wajibu zaidi vilevile katika uwakili wake. Mun-gu anataka wote waitumie mali yao kwa ajili ya kazi zake.

Tunaposema mtu ni wakili wa mali ya Mungu hatumaanishi kwamba anatakiwa kumtolea Mungu kiasi fulani kutoka ndani yake. Ina maana mtu ni wakili wa mali yake yote. Ni kweli ana-paswa kumtolea Mungu sehemu yake. Lakini hata sehemu ile aliyobaki nayo anapaswa kuitumia kama wakili mwema. Mungu anayachunguza matumizi yake ya sehemu ile iliyobaki pia.

Tu mawakili juu ya Injili ya Yesu

1 Wakorintho 9:17-18 - “Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili. Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.”

1 Wathesalonika 2:4 - “Bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mi-oyo yetu.”

2 Wakorintho 5:19-20 - “Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimuwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.”

Wakristo wamepewa kazi ya kuieneza Injili ya Yesu. Mungu analiangalia jambo hili kama uwakili. Anasema tumewekewa amana Injili. Yaani, Mungu ametuamini sisi tuichukue Injili hiyo na kuieneza duniani. Hivyo ni juu yetu kuzitumia nguvu zetu, mali yetu, miili yetu, na kila tulicho nacho kuhakikisha tumeipeleka Injili ya Yesu mahali pote.

Uwakili huu ni mkubwa sana. Injili yenyewe ni yenye thamani kubwa kuliko vitu vyote kwa mpotevu. Tu mawakili juu ya Neno la Mungu na mafundisho yake

2 Timotheo 2:2 - “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.”

Neno la Mungu lenyewe na mafudisho yake ni kitu kingine ambacho Mungu ametukabidhi. Hataki tulitunze tu lakini zaidi ni kulipeleka kwa wengine ili walijue linasemaje. Sisi tu mawakili wa Neno la Mungu.

Vilevile, maana yake ni kwamba tunapaswa kulifundisha Neno la Mungu kwa usahihi bila kuongeza wala kupunguza kitu.

Page 51: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 51 -

• Taja mambo katika maisha yako ambayo Mungu amekupa kama wakili wake. • Habari ya uwakili wako? Unafikiri Mungu amefurahia uwakili wako? • Unafikiri ni sehemu gani ya uwakili wako inapaswa kuboreshwa?

WAKILI AWEJE?

Wakili wa Mungu anapaswa kujali

Yohana 10:12-13 - “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na ku-watawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake.”

Katika mistari hii Yesu anajieleza kwa jinsi anavyotenda kazi yake. Hata mawakili wa Mun-gu wanatakiwa kuwa hivi. Mungu ametuita tujali. Hatupaswi kuwa kama mchungaji huyu wa mshahara ambaye hajali yanayowapata kondoo. Wakili wa Mungu huwa ni tofauti na mawakili wa kidunia. Kwa kawaida, mawakili wa kidunia hawako tayari kujitoa nafsi zao ili wayatunze vizuri zaidi yale ambayo wamepewa kuwa mawakili juu yake. Ndiyo kusema, kwa sababu siyo mali yao, hawaijali.

Lakini sisi tulio mawakili wa Mungu tunatakiwa kuwa na moyo tofauti. Tunatakiwa kujali na kujitahidi kwa nguvu zetu zote kuwa mawakili wazuri juu ya mali ya Mungu.

Wakili wa Mungu anapaswa kukesha

Luka 12:37 - “Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha.”

Kukesha inamaanisha kuwa tayari, kuwa macho. Katika mfano huu Yesu anaongelea juu ya kurudi kwake. Siku moja Yesu atarudi na atawakuta wengine waliopewa uwakili ambao ha-washughuliki nao. Watakuwa wamepumzika kwa muda au kuuacha wajibu wao moja kwa moja. Haitakuwa vizuri kwao kwa sababu Mungu anatutaka tuwe mawakili wema kila wakati ili siku atakaporudi atukute katika uwakili wetu. Wakili wa Mungu anapaswa kuwa mwaminifu

Luka 12:42-43 - “Bwana akasema, ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.”

1 Wakorintho 4:2 - “Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili; ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.”

Uaminifu ni tabia muhimu. Kwa kawaida tukimkabidhi mtu mali yetu ili aitunze, kwanza tunataka tuujue uaminifu wake. Kama mtu huyu siyo mwaminifu haiwezekani kumkabidhi mali yetu.

Mungu anataka tuwe waaminifu. Ana mipango yake ambayo inatakiwa itekelezwe na sisi. Tusipokuwa waaminifu mambo mengi yatalala na kuharibika.

Wakili wa Mungu anapaswa kuwa asiyeshitakiwa

Tito 1:7 - “Maana imempasa mwangalizi awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu.”

Mawakili wa Mungu wanatakiwa kuishi kwa namna fulani ambayo haitaleta sifa mbaya kwake Mungu. Katika mstari huu mambo ambayo yanaweza kusababisha mtu ashitakiwe ya-natajwa. Tabia hizi zinaeleza kuhusu wakili asiyefaa.

Page 52: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 52 -

Wakili wa Mungu anapaswa kumwiga Bwana wake

Waefeso 5:1-2 - “Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika up-endo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi; tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.”

Wakili ni mtu anayesimama badala ya yule anayestahili. Jinsi wakili atakavyowatendea wengine ndivyo watakavyomwelewa bwana wake. Kwa mfano katika nyakati za Biblia wakili alikuwa na wajibu kuwapokea wageni wa bwana wake wakati bwana hakuwepo. Wakili huyu angewatendea vibaya wangejua ndivyo bwana wake anavyowaona. Hivyo inambidi wakili kuzi-iga kauli na tabia za bwana wake.

Katika mstari huu tunaona upendo wa Mungu. Hii ni sehemu moja tu. Mungu ana tabia na asili zilizo nyingi ambazo tunapaswa kuziiga kama mawakili wake tukiwa hapa duniani kwa ni-aba yake.

• Unaoneshaje kwamba wewe ni wakili anayejali? • Eleza jinsi unavyoweza kuwa mwaminifu katika uwakili wako. • Unawezaje kumwiga Mungu katika uwakili wako?

MSAADA WA MUNGU KATIKA UWAKILI WETU

Wafilipi 4:12 - “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”

2 Wakorintho 3:5-6 - “Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya”

1 Timotheo 1:12 - “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake.”

Isaya 41:10 - “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”

Uwakili ni wajibu mkubwa. Pengine unaweza kuhofu kwamba hutauweza uwakili uliopewa na Mungu. Usihangaike kwa sababu wakati wo wote Mungu anatuita kusudi tufanye kazi kwa ajili yake, anatutia nguvu na kutuwezesha kuitimiza kazi aliyotuitia.

Mungu hawezi kukupa kazi ambayo huiwezi. Amekuumba na katika kukuumba amekupa ujuzi, akili, na tabia ulizo nazo. Zaidi ulipookoka, Roho Mtakatifu alikupa karama inayokuweze-sha kufanya huduma katika Kanisa. Mungu anakufahamu ulivyo na hivyo anapokupa uwakili lazima ulingane na jinsi ulivyo.

Pia pamoja na uwezo wetu ni uwezo wake. Anaendelea kutenda ndani yetu ili tuweze kuutimiza mpango wake katika maisha yetu.

Tunatakiwa kuwa na imani tu. Tusome Biblia zetu ili tuone ahadi ambazo Mungu amezitoa na tumtegemee tukiwa tunaamini atatuwezesha.

• Je, kuwa wakili wa Mungu unakutia hofu au wasiwasi? • Kujua Mungu ameahidi kukusaidia kunakufanya ujisikiaje?

WOTE WATATOA HABARI JUU YA UWAKILI WAO Warumi 14:12 - “Basi na hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe

mbele za Mungu.”

1 Wakorintho 3:12-15 - “Lakini mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile it-adhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikite-ketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.”

Page 53: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 53 -

Biblia inatufundisha kwamba kila mtu atahukumiwa siku moja. Katika mistari hii Paulo anaongea kuhusu Wakristo. Hukumu ya Wakristo haihusu kuingia mbinguni au la. Jambo kama hili halihusiki kwa sababu wokovu wa Mkristo hautegemei matendo ya Mkristo mwenyewe. Mwenyewe hajaweza kufanya kazi yo yote ili astahili wokovu wake. Kwa sababu hiyo, matendo yake hayawezi kupimwa kuona kama ameokoka au la. Ni tendo la Yesu msalabani tu, linaloweza kuokoa. Biblia inasema juu ya waliookoka kwamba walichaguliwa na Mungu, waliitwa na Mun-gu, na walihesabiwa haki na Mungu (Rum 8:29-30). Wajibu wao ni kuliamini tendo la Yesu Kristo basi.

Hukumu ya watu ambao hawajamwamini Yesu ni kutupwa katika ziwa la moto. Hukumu ya wale waliookoka inaangalia kama watapewa thawabu au la.

Katika 1 Wakorintho 3:12-15 Paulo anaonesha jinsi Mkristo atakavyohukumiwa. Kinacho-angaliwa ni kazi zake. Kwa nini Mungu atapima kazi zetu? Kwa sababu mwenyewe alipanga tuwe tunafanya kazi mbalimbali kama mawakili wake. Anataka kujua kama tulifanya yale ali-yoyataka au la.

Kwa sababu Mungu amekupa mali, uwezo, ujuzi, akili, nguvu, na karama, anategemea kwamba utazitumia zote kwa ajili ya kazi na mapenzi yake. Ujue siku moja Mungu atakuuliza jinsi ulivyoitumia mali yako. Atataka kujua kama uliwasaidia maskini. Atataka kujua kama ulilisaidia Kanisa lake. Kuhusu ujuzi na akili zako, ulizopewa na Mungu, atataka kujua kama ulizitumia kuendeleza kazi zake. Kama umepewa karama ya kufundisha, atataka kujua kama umewafundisha wengine kuhusu yeye mwenyewe n.k.

Hakuna hatari kwamba unaweza kupoteza wokovu wako. Paulo anasema, “Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa.” Wokovu wetu ni wa milele tena ni salama.

Cha kukosa ni thawabu. Paulo anasema, “Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.” Ina maana kama Mungu atafurahishwa na kazi yako utapewa thawabu huko mbingu-ni. Kama umekuwa mwaminifu katika uwakili wako utapata thawabu. Haieleweki thawabu hizi zitakuwa za namna gani. Lakini Mungu anatueleza juu ya thawabu hizi ili ziwe mvuto kwa ajili yetu kutenda mema tukifanya mapenzi yake. Kwa sababu hiyo najua kwamba zitakuwa thawabu kweli zenye kutamanika. Kwa namna fulani ukikosa thawabu hizo utajisikia vibaya. Mfano wa talanta

Mathayo 25:14-30 - “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja ta-lanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. 17 Vilevile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. 18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa wa-tumwa wale, akafanya hesabu nao. 20 Akaja yule aliyepokea talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwa-minifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna ni-sipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang=anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang=anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”

Page 54: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 54 -

Talanta ni uwakili uliotoka kwa Mungu

Katika mfano huu Yesu anataka kuonesha uwakili ambao watu wa dunia hii wanao. Kama mfano, hadithi hii ina mafundisho mazuri yanayoigusa kila sehemu ya maisha yetu.

Bwana yule ni mfano wa Mungu. Mungu ni mwenye kumiliki vitu vyote na amewakabidhi wanadamu mambo mbalimbali, akiwapa uwakili juu yake.

Watumishi katika mfano huu ni wanadamu wote. Kila mwanadamu anao uwakili mbele ya Mungu. Kama ni Wakristo au Wapagani wote wamepewa ujuzi, akili, nguvu, na mali na Mungu. Mungu atawachunguza wote aone kama wamevitumia vile alivyowapa kwa ajili ya mambo yake.

Talanta yenyewe ni yale tunayopewa na Mungu. Katika mfano huu pesa ndiyo talanta lakini katika maisha yetu talanta ni cho chote tulichopewa na Mungu. Kila mmoja anapewa uwakili ulio tofauti

Mfano huu unatuonesha jinsi Mungu anavyowagawia wanadamu uwakili kwa njia mbalim-bali. Bwana yule alipoondoka akawatolea watumishi wake idadi tofauti za talanta. Ndivyo ilivyo katika maisha yetu. Moja ana mali kuliko mwingine. Mwingine ana akili kuliko mwenzake. Wen-gine wanazaliwa na ujuzi wa hali ya juu na wengine hapana. Hata karama za Roho zinatofautia-na.

Kilicho muhimu ni kwa kila mtu awajibike kwa yale aliyopewa. Bwana huyu hakuzidai ta-lanta tano kwa yule aliyepewa mbili. Kwa sababu mwenye mbili aliongeza mbili, akaonekana kuwa mwaminifu. Alipongezwa sawa na yule aliyeongeza tano.

Mungu hawezi kukudai zaidi ya uwezo aliokupa. Lakini ni lazima tuwe tunatumia kiasi kile tulichopewa kwa manufaa ya mambo ya Mungu. Kiasi siyo muhimu, bali jinsi tunavyokitumia kiasi tulichopewa ndiyo muhimu. Kuna thawabu au hasara kutegemeana na uaminifu

Bwana yule aliporudi alitoa hukumu. Kila mtumishi alichunguzwa na ikabidi aweze kuone-sha kama alikuwa mwaminifu. Fundisho kuu ni kwamba thawabu na hasara zinatokana na uaminifu. Yesu hajaeleza kila aina ya mfano. Kwa mfano ingekuwaje kama mtu angepewa mbili na akaongeza moja. Bila shaka kwake kungekuwa thawabu kwa upande aliofanya na hasara kwa upande alioshindwa.

Kwenye mfano huu bwana anaitoa hukumu kali kwa mtumishi yule ambaye hakuleta faida yo yote. Kama kutupwa kwenye giza ambako kuna kilio na kusaga meno inamaananisha ziwa la moto, basi, lazima tuelewe kwamba mtumishi huyu alikuwa hajaokoka. Sijui kama Yesu ali-maanisha hukumu ya ziwa la moto katika mfano huu au kama alitaka kusema tu wakili mbaya atakula hasara. Kwa vyo vyote vile tunajua kutokana na maelezo mengine ya Biblia haiwezekani mtu aliyeokoka atupwe katika ziwa la moto milele.

Mtumishi huyu wa mwisho ni mfano mzuri wa mtu ambaye hajaokoka. Sababu nasema hivi ni kwamba haiwezekani mtu aliyeokoka kutokuwa na matunda angalau kiasi. Biblia inafundisha imani ya kweli lazima izae matunda. Ni kweli kuna utofauti katika uzaaji wa matunda kwa Wa-kristo, wengine hawazai ipasavyo, lakini naamini kama mtu ni Mkristo kweli, ni lazima atazaa matunda angalau kiasi fulani.

Kwa jinsi tulivyosoma katika Wakorintho tumejifunza kwamba kuna hasara ya kweli kwa yule ambaye hatautendea kazi uwakili wake. Inawezekana baadhi ya kazi zake zitasalia na nyingine zitateketezwa. Kwa zile zinazosalia kuna thawabu. Kwa zile ambazo hakuwa mwa-minifu na zikateketea, kuna hasara.

Kufaulu siyo lengo

Wengine wanaweza kuelewa kutokana na mfano huu kwamba ni lazima kila mmoja alete faida sawa na yale aliyopewa. Katika mfano huu, aliyepewa tano aliongeza tano na aliyepewa mbili aliongeza mbili.

Lakini lengo la Mungu katika mfano huu ni kwa watumishi wake kutenda kwa uaminifu. Faida au matunda ni kitu ambacho Mungu atakileta ndani ya kazi zetu. Tunatenda kwa kusaidi-wa na Mungu mwenyewe. Ubaya wa mtumishi yule aliyepewa talanta moja ni kwamba hakufanya kitu, yaani hakuwa mwaminifu. Bwana wake mwenyewe alisema kwamba ilimpasa

Page 55: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 55 -

aiweke benki ili apate angalau riba. Yesu hajasema kuna idadi wala kiasi kinachopaswa ku-zalishwa, bali anadai uaminifu. Mtumishi huyu hakuhukumiwa kwa sababu ya kutofaulu kiasi fulani bali kwa sababu hakujaribu, yaani, hakuwa mwaminifu.

Hofu ni adui

Katika mfano huu mtumishi mbaya alionesha hofu yake. Alihofu ukali wa bwana wake na hivyo aliogopa angeweza kuipoteza talanta ile moja kama angeifanyia kazi. Alihofu kuwa atashindwa. Hatupaswi kuhofu kwa sababu tofauti na mfano huu Bwana wetu hajasafiri kwenda kwingine. Wakati Mungu anatupa yaliyo yake anabaki nasi akitusaidia kuyatimiza mapenzi yake yaliyo uwakili wetu.

• Kwa nini uaminifu ndiyo kufaulu katika kuwa wakili mwema badala ya hesabu nyingine? • Kwa nini Mungu anawapa watu wakili mbalimbali zilizo tofauti? • Je, umewahi kuwa na wivu kuhusu uwakili wa mtu mwingine? Eleza.

NA WEWE JE? Chukua muda kujichunguza. Tafuta kwanza ujue ni mambo gani ambayo Mungu amekupa

wewe?

• Unao ujuzi gani uliopewa na Mungu? • Unao uwezo gani uliopewa na Mungu? • Unayo mali gani uliyopewa na Mungu? • Unayo akili gani uliyopewa na Mungu? • Unayo nguvu gani uliyopewa na Mungu? • Unayo karama ya Roho gani uliyopewa na Mungu?

Jibu halisi ni kwamba kila kitu ulicho nacho umepewa na Mungu. Katika kuyajibu maswali haya usitofautishe mambo ndani ya maisha yako, ukisema hili nimepewa na Mungu na hili hap-ana. Unapaswa kufanya utafiti ndani ya maisha yako ili upate kujua una uwakili juu ya nini. Utofauti ni kati ya wewe na wengine. Wengine wamepewa uwakili tofauti.

Sasa kuhusu yale Mungu aliyokupa kama uwakili wako, habari ya maendeleo yako?

• Unaitumiaje mali uliyopewa na Mungu? • Unautumiaje ujuzi uliopewa na Mungu? • Unautumiaje uwezo uliopewa na Mungu? • Unaitumiaje akili uliyopewa na Mungu? • Unaitumiaje nguvu uliyopewa na Mungu? • Unazitumiaje karama za Roho ulizopewa na Mungu?

Ni bora uyajibu maswali haya leo hii na kuanza kuparekebisha pale ambapo pana kasoro. Utakapoulizwa na Yesu mwenyewe ujue hutapata nafasi tena ya marekebisho. Mambo yatasalia jinsi yalivyo.

• Habari ya uwakili wako? • Je, unayatumia yale Mungu aliyokupa kwa ajili ya mambo yako binafsi? • Au unayatumia kwa mambo ambayo yanampendeza Mungu?

MWISHO Uwakili ni somo muhimu. Utoaji kanisani ni sehemu moja tu ya suala la uwakili. Uwakili ni

mpana zaidi kwa sababu unaihusu kila sehemu ya maisha yako. Sababu mojawapo ya watu kutojitoa ipasavyo ni kwamba wanafikiri vitu walivyo navyo

wamemiliki wenyewe. Lakini Neno la Mungu lasema kwamba kila ulicho nacho ni mali ya Mun-gu akiwa amekukabidhi kama wakili. Katika uwakili huo hajakuacha uitumie mali yake una-vyotaka wewe mwenyewe. Ameyaweka masharti ya kuyafuata. Wakili mwema na mwaminifu ni yule anayeyafuata masharti haya.

Hakika wakili mwema ni yule ambaye anatoa mali, nguvu, ujuzi, na akili zake kwa ajili ya kazi ya Mungu. Usikose thawabu zako kwa sababu ya kutokuwa wakili mwaminifu.

Page 56: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 56 -

- 9 - Taratibu za Utoaji

WAKRISTO WANAPASWA KUTOA NAMNA GANI?

Kwake Mungu swali, “Namna gani?” ni muhimu sana. Namna gani inahusu hali ya moyo wa

mtu anavyoyatimiza maagizo ya Mungu. Kuliko sadaka zenyewe tunazomtolea, Mungu anajali zaidi jinsi tunavyofikiri na kujisikia wakati tunapojitoa. Sababu yenyewe ya kutuagiza kuitoa sadaka si kwamba Mungu anahitaji vitu vyetu. Bali ni kwa faida yetu katika mawazo yetu na maisha yetu ya kiroho. Hii ndiyo sababu Mungu anajali sana hali ya mioyo yetu wakati tunapoi-toa sadaka kwake.

Mungu alimwambia nabiii Hosea juu ya mambo kama haya wakati watu wake walipokuwa wakizitoa sadaka zao za kuteketezwa. Walikuwa wanaitii sheria ya Mungu. Lakini Mungu hakufurahishwa na sadaka zao. Sadaka zenyewe zilikuwa nzuri kulingana na sheria, lakini shida ilikuwa hali ya mioyo yao.

Hosea 6:6 - “Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za ku-teketezwa.”

Walikuwa wakitoa sadaka wakati katika maisha yao kulikuwako dhambi nyingi bila kuzi-jali. Sadaka zenyewe zilikuwa za kutimiza sheria badala ya matoleo ya kumheshimu Mungu. Hata Mika anaielezea hali hii na mawazo ya Mungu juu yake.

Mika 6:6 - “Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nim-karibie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”

Si kwamba Mungu aliziondoa sadaka kama agizo lake. Walipaswa kuendelea kuzitoa sadaka zao lakini Mungu alitaka ziendane na mabadiliko katika hali ya mioyo yao. Kwa Mungu, tuna-vyofikiri na kujisikia ni muhimu, hasa wakati tunatimiza maagizo yake. Hivyo tuangalie jinsi Mungu anavyotutaka tujitoe kwake. Mungu anatutaka tuzitoe nafsi zetu kwanza

2 Wakorintho 8:5 -“Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.”

Katika sura ya 8 na 9 za kitabu cha 2 Wakorintho, Paulo anayatoa mafundisho mengi ku-husu utoaji. Wakristo katika kanisa la Korintho walikuwa hawajitoi ipasavyo. Hivyo Paulo alitaka awafundishe kuhusu utoaji ili waweze kuutimiza uwakili wao ingawa hakuwapa amri. Njia ya kwanza aliyoitumia kuwafundishia ilikuwa kuwapa mfano wa wengine ambao wanatoa kwa njia iliyo bora. Mfano huu ulikuwa wa makanisa ya Makedonia.

Jambo la kwanza tunalojifunza juu yao ni kwamba walijitoa nafsi zao kwanza. Ina maana wakatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu. Walimpenda Mungu, walimshukuru Mungu, na walitaka kuyatimiza mapenzi yote ya Mungu. Kama ni muda wao, akili zao, au nguvu zao, walikuwa tayari kukifanya cho chote Mungu alichokitaka.

Kwa sababu walikuwa na mioyo ya namna hii, walikuwa tayari hata kutoa mali zao. Mtu ambaye anampenda Mungu, na anataka kumpendeza katika kila sehemu ya maisha yake, atatoa hata mali yake kama sehemu mojawapo ya njia za kumpendeza Mungu.

Basi, tumejifunza kwamba kile ambacho kinamfurahisha Mungu zaidi, ni watu wakijitoa nafsi zao kama Paulo alivyoagiza katika Warumi 12:1, “Itoeni miili yenu”. Mungu anatutaka sisi. Anataka tumfuate, tumtegemee, tumtumaini, na tumtumikie. Utoaji wa mali yetu ni tunda tu la maisha yaliyotolewa kwanza kwa Mungu.

Page 57: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 57 -

Kuna hatari mbili hapo. Kwanza kuna wengine ambao wanadai kwa sababu wanayatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu hawatakiwi kuitoa mali yao. Labda ni mchungaji ambaye kazi yake kwa ujumla ni kwa ajili ya kazi za Mungu. Kwa sababu hiyo anaweza kufikiri kwamba siyo lazima kwa ajili yake kuitoa mali yake pia. Wazo hilo si kweli. Kama tulivyoona, kuitoa mali yetu ni tunda linalotokana na kuyatoa maisha yetu kwanza. Kama moyo wa mchungaji huyu upo katika hali inayotakiwa, hatajizuia kuitoa mali yake. Mungu anataka yote - maisha pamoja na mali. Sababu ni kwamba yule asiyetoa mali yake anaonesha tabia mbaya ya kutomtegemea Mungu. Hiki ni kitu ambacho Mungu anataka akione katika maisha ya kila Mkristo. Zaidi anataka kila Mkristo aweze kutambua jinsi anavyomtegemea Mungu katika maisha yake.

Hatari ya pili ni yule ambaye anataka kuitoa mali yake tu. Wamakedonia waliitoa mali yao lakini Paulo anafurahi jinsi walivyozitoa nafsi zao kwanza. Wengine wana shughuli zao nyingi na hivyo hawautoi muda, akili, wala nguvu zao kwa ajili ya kazi ya Mungu. Maana yake hawazitoi nafsi zao. Lakini wengine wanajisikia vibaya na wanaona ili wasiwe na hatia inafaa waitoe mali yao kwa kufikiri kwamba italeta uwiano zote. Kama tulivyoona katika sadaka za kuteketezwa kwa Israeli, sadaka zenyewe zilikuwa lazima lakini Mungu alijali zaidi hali ya mioyo yao wakitembea naye. Mungu anataka tujitoe nafsi zetu kwanza na mali yetu iwe ya pili. Mungu anatutaka tujitoe kwa hiari si kwa lazima

Suala moja gumu katika makanisa mengi ni suala la kuzitofautisha amri na hiari. Hakika wote wanakubali kwamba katika Agano la Kale Waisraeli walipaswa kutoa mali yao kufuatana na Sheria ya Musa. Kama ni fungu la kumi, au sadaka nyingine zilizokuwa nyingi, lilikuwa suala la amri, tena kiasi chake kilikuwa cha lazima.

Lakini hata katika Agano la Kale Mungu hakufurahishwa na watu waliotoa sadaka zao kwa sababu ilikuwa lazima tu. Yaani, wengine hawakutaka kutoa katika mioyo yao lakini walifanya tu kwa sababu ilikuwa sheria. Kama mkuu wa chuo ninafurahi wakati watumishi wa chuo wanafanya kazi zao kwa hiari, yaani, wanapoonesha kwamba wanazifurahia kazi zao kwa sababu wanajitoa kwa Mungu. Ni kweli wanapewa mshahara. Ni kweli kama mkuu naweza ku-waamuru watende ninavyotaka. Lakini, kwa kawaida sijisikii vizuri ninapotakiwa kuwalazi-misha wafanyakazi kufanya kile ambacho ni wajibu wao. Ni suala la mioyo yao. Ninapata wasi-wasi juu ya mtumishi ambaye ni lazima nimsukume ili autimize wajibu wake. Ninaanza kujiuliza ikiwa huyu yuko upande wa shule au la. Inazalisha swali kama katika yote anayoyafanya anata-futa ubora na manufaa ya shule au sivyo. Anayejituma hutafuta kuiboresha shule. Hivyo, kama mkuu, nafurahi zaidi na watumishi wenye moyo huo. Ndivyo ilivyo hata kwake Mungu. Mara nyingi alisikitishwa na watu wake Israeli kwa sababu waliitimiza sheria lakini kwa kulazimish-wa badala ya kujitoa wakivutwa na moyo wa shukrani kwa Mungu.

Katika Kanisa lililo Mwili wa Kristo hakuna sheria ihusuyo utoaji kama amri inayotaja kiasi fulani cha kutoa kwa Wakristo leo. Lakini tusifikiri maana yake ni kwamba utoaji siyo lazima leo. Bado Mungu ameyatoa maagizo kwa ajili yetu kujitoa kwake.

Tofauti ni kwamba hakuna sheria leo kama Waisreali walivyokuwa nayo katika Agano la Musa kati yao na Mungu. Katika agano lile kulikuwa ahadi za baraka na maonyo ya laana kutegemea na jinsi walivyotii. Upungufu wa utoaji wa sheria ni jinsi ambavyo sheria huleta hisia zilizo mbaya. Zinamshurutisha mtu akifanye kitu hata kama hataki kukifanya. Zinamsukuma mtu kwa njia ya kumfanya aogope adhabu. Kwa sababu hii, watu walitii ili wakwepe adhabu hiyo. Lakini utiifu unaotokana na hofu haumpendezi Mungu kwa kuwa Mungu anajali zaidi wanadamu waweze kujitoa kwa hiari; kwa mioyo safi mbele yake.

Ni kama mzazi na mtoto wake. Kama wazazi tunaweza kuwalazimisha watoto wetu watutii kwa njia ya adhabu. Tunaweza kuwalazimisha kufanya vile tunavyotaka, lakini mara nyingine utiifu wao utafanyika pamoja na kulalamika. Hata tukiwanyamazisha wasilalamike, tujue kwamba mioyoni bado wataendela kulalamika. Hali hii haifurahishi kwa sababu inaonesha wa-toto wetu hawataki kutupendeza na uhusiano wao nasi haujawa sawa. Kama wazazi hatutaki watoto wetu kututii kutokana na kuhofu mamlaka tuliyo nayo kama wazazi. Tunafurahi sana zaidi wanapotutii wakiwa na mioyo ya kutaka kutupendeza, yaani, wanapotii kwa heshima na upendo bila kunun’gunika.

Sababu au motisha ya utoaji katika Mwili wa Kristo inatokana na mambo yaliyo tofauti na msukumo wa sheria. Badala ya kulazimishwa na sheria, maagizo katika Mwili wa Kristo huun-

Page 58: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 58 -

ganishwa na sababu nyingine za kujitoa katika Agano Jipya. Sababu hizo husababisha hali ya raha na amani badala ya hisia mbaya mioyoni mwa watu. Mambo yenyewe yanayotuvuta katika Mwili wa Kristo ni kama vile shukrani tukimshukuru Mungu, upendo wetu kwa Mungu, nia yetu kuona Mungu atukuzwe, n.k. Mambo hayo tutayaangalia baadaye lakini kwa sasa turudi kwenye suala la kujitoa kwa hiari na siyo kwa sheria.

2 Wakorintho 8:4 - “Wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shi-rika hili la kuwahudumia watakatifu.”

Hapo tunaona hiari ya Wamakedonia. Wenyewe, katika mioyo yao, walitaka nafasi hii ya kusaidia Wakristo wenzao. Paulo hakuwalazimisha kuitoa mali yao ili wawasaidie Wakristo wengine wenye shida, bali walikuja kwake wakimsihi wapewe nafasi hii ya kusaidia. Huu ndiyo mfano bora ambao Paulo anataka kuuinua au kuusifu ili tuufuate leo.

2 Wakorintho 9:5 -“Basi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu.”

Shida inayoongelewa katika mstari huu ni kwamba Wakorintho waliahidi watatoa mali yao kusaidia. Waliweka ahadi hii ya kusaidia kwa hiari yao, yaani walikuwa hiari pia kuamua kutosaidia. Lakini mwaka mzima ulikuwa umepita tangu walipotoa ahadi ya msaada bila kuufanikisha. Ndiyo sababu Paulo anawaarifu kwamba anakuja kuipokea ahadi yao waliyotoa kwa hiari. Hivyo, iliwabidi kujitayarisha. Bado Paulo alitaka waweze kutoa msaada huo kwa hia-ri. Lakini Paulo alikuwa tayari kuwalazimisha kulingana na ahadi yao, kama angekuta hawajati-miza ahadi hiyo kwa hiari. Si kwamba angewalazimisha kujitoa, bali angewalazimisha kuitimiza ahadi yao. Mungu hakutaka wajitoe kwa shuruti bali kwa mioyo ya hiari. Ndiyo sababu Paulo aliwaarifu ili wawe na muda wa kutafakari na kuamua kufanya kwa hiari.

2 Wakorintho 9:7 - “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”

Hapo Paulo anayatoa mafundisho hasa. Katika kufundisha anatamka wazi kwamba Mungu anampenda mtu anayejitoa kwa hiari siyo kwa kushurutishwa au kulazimishwa. Kufuatana na maagizo ya Mungu kwa ajili ya Mwili wa Kristo, ni lazima Wakristo wajitoe, lakini Mungu anajali sana waweze kujitoa bila kulazimishwa. Badala yake, Mungu anataka Wakristo wajitoe kwa fu-raha, wakimshukuru Mungu wao na kuonesha wanajali kazi za Mungu hapa duniani.

Mungu anataka tujitoe kwa raha

Wakati Daudi aliandaa kulijenga hekalu la Mungu alitoa mali yake nyingi. Pia aliwaomba Waisraeli wajitoe. 1 Mambo ya Nyakati 29:6 inasema, “Wakajitoa kwa hiari yao.” Hekalu ilikuwa jengo la ajabu lililompa Mungu sifa. Lilikuwa alama kwamba Waisraeli walimheshimu Mungu kuliko vitu vyote. Katika kumtolea Mungu walimfurahisha kwa sababu katika mioyo yao walio-na raha kuweza kutenda hivyo.

1 Mambo ya Nyakati 29:9 - “Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo , kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu.”

Mungu anataka tuwe na raha mioyoni tunapojitoa. Ukiwa na raha moyoni ina maana umetoa kwa hiari. Anayelazimishwa hana raha moyoni, wala hatamjali yule anayemtolea. Ni kama wakati bibi anatoa kitu kwa mjukuu wake. Mjukuu anafurahi lakini bibi anafurahi zaidi. Hajalazimishwa kutoa, ameamua kutoa. Kwa sababu anamjali huyu mjukuu wake, anafurahi sa-na kuona amemletea furaha katika maisha yake.

2 Wakorintho 9:7 - “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” (Tafsiri Haba-ri Njema “maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha”)

Paulo anasema, “Si kwa huzuni”. Huzuni ni kinyume cha furaha. Huwa tunafurahi tukiweza kutenda sawa na jinsi tunavyokusudia moyoni. Ndivyo Paulo anavyosema. Anasema kila mmoja

Page 59: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 59 -

atoe kwa jinsi alivyokusudia, si kwa jinsi alivyoagizwa. Hivyo kila mmoja ataweza kuwa na raha katika matoleo yake.

Mungu anataka tujitoe kwa nia na kusudi

2 Wakorintho 8:10-12 - “Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, licha ya kutenda hata na kutaka pia. Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo. Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.”

Tuendelee na wazo letu la kwamba hali ya mioyo yetu ni muhimu wakati tunapojitoa kwake Mungu. Mungu anaichunguza mioyo yetu na kufuatana na mioyo yetu anapima matoleo yetu.

Wakorintho walitoa ahadi iliyoeleza nia au kusudi lao. Lakini nia bila matendo ni uongo. Mungu anataka tuweze kujichunguza na kuamua kiasi kile tutakachotoa. Pili anataka tutende sawa na nia yetu.

Kwa mfano mtu akikusudia katika moyo wake kutoa 1000 na kweli anakuja kutoa sawa na nia yake, Mungu atapendezwa naye katika kutoa hizo 1000. Lakini kama mtu atakusudia kutoa 1000 na labda kwa sababu viongozi wanamsukuma kutoa zaidi, anakuja kutoa 1500, Mungu atapendezwa zaidi na zile 1000 alizokusudia kutoa. Mungu hatafurahishwa jinsi alivyozitoa zile 500 kwa sababu hakutaka kuzitoa na mwisho alizitoa kama mtu anayelazimishwa. Aliona huzuni katika kuzitoa lakini akafanya kwa sababu wengine walimbana. Hajatoa kwa hiari wala kwa moyo wa ukunjufu.

Mungu anataka tupange matoleo yetu. Matoleo yetu ni jambo muhimu na tunapaswa kuyafikiria tukimwomba atuongoze na atupe imani ya kutoa kulingana na mapenzi yake. Mwi-sho tunavyokusudia chini ya uongozi wake, Mungu anataka tutende. Tusipunguze, wala tu-siongeze kwa kulazimishwa. Kama ni kuongeza iwe kwa sababu tumekusudia kuongeza kwa moyo wa furaha tukijisikia Mungu anataka tuongeze.

Mungu anataka tujitoe kwa ukarimu

Ukarimu ni namna nyingine ambayo Mungu anataka tutoe. Ukarimu ni neno linaloelezea hali ya kuwakaribisha watu wengine au kuwasaidia katika matatizo yao. Pia msingi wa neno hili katika kiyunani lina maana ya wingi au hali ya kuzidisha.

Wakati Paulo aliongea kuhusu Wamakedonia alionesha jinsi walivyotoa kwa ukarimu. Si kwamba walitoa nyingi kwa sababu wenyewe walikuwa maskini. Lakini kulingana na yale waliyokuwa nayo walitoa nyingi.

2 Wakorintho 8:2 - “Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.”

2 Wakorintho 9:6 - “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.”

Kinyume cha haba ni nyingi. Inawezekana neno “ukarimu” katika Kiswahili halina maana ya wingi lakini mstari huu unaonesha maana hiyo.

2 Wakorintho 9:11 - “Mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpa-tiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.”

Paulo anataka tuwe na “ukarimu wote”. Ni ushauri kwa Wakristo wote kwa sababu kutoa hivyo kunampendeza Mungu. Nidyo kusema lengo la Mungu ni kwa ajili yetu kujitoa kwa wingi tuwezavyo bila yeye kutaja kiasi fulani kamini cha kisheria.

Mungu anataka tujitoe kwa kutafuta ufalme wa Mungu

Mathayo 6:33 - “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishi-wa.”

Page 60: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 60 -

Yesu alifundisha Waisraeli kuutafuta ufalme wa Mungu katika maisha yao kama kipaum-bele. Mpango wa kuanzisha ufalme wa Yesu Kristo wa miaka 1000 hapa duniani ulihusu Waisraeli. Katika huduma zake, Yesu aliwahubiria Waisraeli kutubu na kumfuata Mungu kwa kuwa ufalme ulikuwa umekaribia. Kuliko kuyafikiria mahitaji yao ya kimwili, Yesu alitaka waji-funze kumweka Mungu na mambo yake nafasi ya kwanza katika maisha yao. Katika fundisho lingine, Yesu alisema waweke hazina yao mbinguni. Maana yake ni kwamba wayajali mambo ya Mungu kuliko mambo ya dunia.

Leo katika Mwili wa Kristo sisi Wakristo tunapaswa kuendelea kuifuata kanuni hiyo. Hatu-tafuti ufalme wa Yesu uliohusu Waisraeli lakini tunamtafuta Mungu na mambo yake katika maisha yetu. Yaani, tunapaswa kuyajali mambo ya Mungu kuliko mahitaji yetu binafsi. Kuitoa mali yetu kwa Mungu ni sawa na kusema mambo ya Mungu ni muhimu kuliko mambo mengine yote. Mungu anataka kuona tumeelewa umuhimu wake na umuhimu wa kazi zake. Njia moja ya kuonesha uelewa huo ni katika utoaji wetu.

Mungu anatutaka tujitoe kwa upendo

1 Wakorintho 13:3 - “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo hainifaidii kitu.”

Katika 1 Wakorintho 13 Paulo anafundisha kuhusu upendo. Mungu anasema upendo ni jambo muhimu katika maisha ya Mkristo. Mstari huu unaongelea hali ya moyo wa mtu wakati anaitoa mali yake. Paulo anasema kujitoa ni bure kama amejitoa bila kuwa na upendo moyoni.

Upendo huu ni upendo unaomlenga Mungu na mwanadamu mwenzetu. Biblia inasema tunampenda Mungu kwa sababu alitupenda kwanza. Tunapojitoa kwake tunafanya kwa sababu tunampenda. Kama hatumpendi Mungu, Mungu hataki mali zetu. Maana Mungu hahitaji mali zetu lakini anataka tuzitoe kwake ile tuuoneshe upendo wetu kwake (pamoja na mambo men-gine kama vile shukrani zetu, utegemezi wetu n.k.)

Mungu anatutaka tujitoe kwa haki

2 Wakorintho 8:20-21 - “Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.”

Wapo watu wanaostahili kusaidiwa na matoleo yetu na wengine ambao hawastahili. Kuna mambo mengine yanayostahili matoleo yetu na mengine ambayo hayastahili. Mungu anataka tutoe kwa njia iliyo bora. Anataka tukichambue kile tunachokitolea. Anataka tuwe na hakika kwamba matoleo yetu yanahitajika au yanastahili kwa kitu au mtu fulani. Yaani, kwa ujumla, Mungu anataka tutoe kwa haki.

Kwa mfano ni vigumu kuzitolea idara au taasisi za Kanisa ambazo hazitoi ripoti kuhusu matumizi yake ya pesa. Hatuwezi kutegemea watu wote (au taasisi, shirika, makamati, vikundi n.k.) kuwa waaminifu. Wengine wanajitangaza kama watu wenye mahitaji wakati siyo. Wengine wanaomba pesa kwa ajili ya huduma wakati pesa nyingi wanazozikusanya hazifanyi huduma walizozitaja. Yaani, wamewadanganya watoaji.

Hakika tunapaswa kuwa waangalifu katika kutoa mali zetu ili tuhakikishe pesa hizo zi-natumiwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Tunaangaliwa na Mungu na hata wanadamu. Kama mawakili tunapaswa kujali na kuzitoa mali zetu kwa watu na huduma zinazozihitaji kweli na pia kwa wale watakaozitumia jinsi walivyoahidi. Yaani tunatakiwa kuhakikisha zinatumiwa kwa haki.

Mungu anataka tujitoe kwa mpango

1 Wakorintho 16:2 - “Siku ya kwanza ya juma kila mtu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja.”

Wakati Paulo alikuwa akiwashauri Wakorintho kuhusu namna ya kujitoa tunajifunza kitu kingine. Alitaka watoe kwa mpango. Alisema wanatakiwa kuangalia mapato ya kila wiki halafu waweke kiasi wanachokusudia kutoa pembeni ili wakati wa matoleo yatakapofika wawe nazo za kutoa.

Page 61: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 61 -

Wengine wanatoa bila mpango au utaratibu. Mara nyingi matokeo yake ni kwamba hawana cha kutoa wakati kuna hitaji. Wanasubiri hitaji liwepo kwanza ndipo wanajichunguza kama wanacho cha kutoa.

Matokeo mengine ya kutokuwa na mpango katika matoleo ni kwamba watu hawatoi kwa kadiri ya uwezo wao. Kadiri ni kipimo kinachohitaji mahesabu. Lakini mtu asiyepanga utoaji wake, hapigi hesabu, na hivyo atakuwa hatoi kwa kadiri ya uwezo wake.

Katika kutoa kwa mpango kuna mambo mawili. Kwanza kuna mpango wa kukata kiasi katika mapato yote tunayopata na kukiweka kama akiba mpaka tutakapoweza kukitoa. Kwa namna hii tutakuwa na cha kutoa kila wakati kulingana na kadiri ya mapato yetu. Tukiwa na mpango hatutamwibia Mungu. Bila mpango mtu anasahau alitoa kiasi gani na kawaida ata-jidanganya akifikiri ametoa vya kutosha wakati hajafanya.

Jambo la pili ni kuamua juu ya mambo yanayostahili matoleo yetu na kutoa kwa mpango. Kama ni kanisa, au idara, au huduma, inafaa tupange kile tunachokusudia kukitolea kila wakati katika mfululizo, halafu tukitekeleze. Hata kuwatolea maskini au wahitaji tungepanga na kuwe-ka akiba fulani kila wakati ili wakati hitaji litakapoonekana tuwe tayari kusaidia.

Lakini kutoa kwa mpango hakuna maana kwamba tusiwasaidie watu ambao hatujapanga kuwasaidia. Yaani tunapaswa kuwa na mipango kwa ajili ya matoleo yetu ya kawaida. Lakini mara kwa mara Mungu anaweka mtu au huduma maalum katika maisha yetu ghafula bila sisi kupanga. Hapo tunahitaji kutegemea jinsi Mungu anavyogusa mioyo yetu. Mara nyingine tu-meshatoa matoleo yetu tuliyopanga na Mungu anatuonesha hitaji la dharura. Hapo tukijisikia Mungu anataka tusaidie inatubidi kumwamini Mungu na kutoa hata zaidi ya matoleo yetu ya kawaida tuliyoyapanga.

• Kwa nini namna tunavyojitoa ni muhimu kwake Mungu kuliko kiasi tunachokitoa? • Kwa nini ni muhimu tujitoe nafsi zetu kwanza kabla ya matoleo mengine? • Je, mtu anaweza kutoa nafsi yake kwa Mungu na asitoe mali yake? Kwa nini? • Eleza sehemu ya utoaji wetu ambayo tuna hiari ndani yake na sehemu ambayo siyo hiari. • Umewahi kuona raha ulipomtolea Mungu? Taja mifano ya matoleo yako yenye raha. Je,

kwa nini matoleo hayo yamekupa raha? • Katika kujipima, unafikiri unajitoa kwa ukarimu (yaani wingi)? • Katika maisha yako unamwekaje Mungu nafasi ya kwanza na mambo yake? • Kuna haja ya kurekebisha unavyomheshimu Mungu katika utoaji wako? • Mambo gani ni motisha yako katika kumtolea Mungu? Au huna motisha kumtolea Mungu? • Je, ni bora kutolea watu na huduma mbalimbali bila kuchunguza mahitaji na matumizi

yao au ni bora kutafiti wale unaowatolea? Kwa nini? • Je, kuna mifano gani ya hitaji la kumtolea Mungu katika mazingira ambayo huwezi

kuhakikisha ni haki kutoa? WAKRISTO WANA SABABU GANI ZA KUTOA?

Wakristo hawajitoi kwa kulazimishwa na sheria

Swali kuu hapa ni kujua kwa nini tunajitoa. Ni kitu gani kinachotusababisha tujitoe kwa ajili ya kazi za Mungu. Wengine wanapenda kuwapa Wakristo sheria. Wanaamini kwamba watu ha-watatoa kama hakuna sheria. Wanataka kuwalazimisha washirika wajitoe. Ubaya ni kwamba njia hii huleta hali mbaya katika mioyo ya wale wanaojitoa kutokana na kulazimishwa. Hali hii mbaya haimfurahishi Mungu. Yaani, ni kweli kupitia sheria, mara nyingine, viongozi wa kanisa wanaweza kutoza washirika wao kiasi kikubwa zaidi, lakini hapo watajitoa kwa kulazimishwa na si kwa hiari wakati Mungu hufurahishwa na wanaojitoa kwa hiari.

Tujue kwamba katika Uwakili wa Neema, ulio Mwili wa Kristo, hatuna sheria kuhusu kiasi gani cha kutoa. Baada ya Mwili wa Kristo kuanza katika kitabu cha Matendo, na kipindi cha She-ria ya Musa kuisha, hakuna agizo tena linaloagiza kiwango au asilimia fulani kama vile Sheria ya Musa ilivyowaagiza Waisraeli. Kwa sababu hii, kama viongozi wa Kanisa, hatuwezi kuwalazi-misha washirika wetu wajitoe kufuatana na mipango yetu. Hatuwezi kutamka kiwango fulani ambacho kila mshirika anapaswa kukitoa. Hatuwezi kusema wasipotoa kiasi fulani watalaaniwa au hawatakuwa washirika wa tawi (au adhabu nyingine tutakayobuni).

Page 62: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 62 -

Kwa sababu Mungu hajaamuru kiasi fulani cha kutoa, je, ina maana Mungu hajali tukijitoa au la? Hapana! Kutoa inampendeza Mungu, na kutotoa inamsikitisha. Kutoa huleta baraka za Mungu, na kutotoa huleta hasara katika maisha yetu. Isitoshe Mungu ameagiza watu katika Ka-nisa lililo Mwili wa Kristo kujitoa. Hivyo kujitoa ni muhimu tena ni lazima.

Ingawa tumeagizwa na Mungu kutjitoa katika Mwili wa Kristo, agizo hilo halipaswi kuwa sababu yetu kuu ya kujitoa kwake. Kuna sababu nyingine zilizo muhimu zaidi zinazomvuta Mkristo kujitoa badala ya kumsukuma na kumlazimisha. Sheria inashurutisha na kumlazimisha Mkristo ajitoe hata kama moyoni mwake hataki. Lakini, neema inamvuta Mkristo kufanya uamuzi katika moyo wake atake kujitoa. Zote mbili zinafanikisha matoleo lakini neema inafanya kwa njia inayompendeza Mungu. Kupitia neema mtu hutoa kwa hiari akiwa na moyo safi mbele za Mungu.

Shida nyingine ya sheria ni kwamba inaweka mipaka. Kawaida watu hawawezi kuzidi ki-wango ambacho sheria inadai. Neema haina mipaka lakini inafuatana na jinsi mtu anavyokusudia.

Mungu anafurahi kuona watu wake wakijitoa kwa hiari yao. Inamwonesha kwamba wanampenda na kumheshimu, na wanajali mambo yake. Hii ndiyo sababu Mungu anataka tu-jitoe kwa neema si kwa sheria.

Hofu ya wachungaji na wajumbe wa baraza la tawi ni kwamba bila sheria watu hawatajitoa. Lakini mtazamo wa Mungu ni kwamba watu walio chini ya neema watatoa kuliko watu walio chini ya sheria.

Neema ni njia iliyo bora lakini ni lazima watu wafundishwe kuhusu sababu walizo nazo za kujitoa. Wanahitaji kuyajua mambo yale ambayo yatawavuta wajitoe ipasavyo. Wanahitaji kuyajua mambo kama yafuatayo:

Upendo wa Mkristo kwa Mungu humfanya ajitoe

2 Wakorintho 8:8 - “Sineni ili kuwaamuru bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu.”

2 Wakorintho 8:24 - “Basi waonesheni mbele ya makanisa hakika ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.”

Paulo anadai kwamba hawapi sheria ya kujitoa, bali anataka waelewe sababu bora ya ku-jitoa. Upendo ni sababu mojawapo iliyo bora ya kujitoa. Mungu anatupenda. Ametuumba na anatutimizia mahitaji yetu kwa sababu ya upendo wake kwa ajili yetu. Hata akamtoa mwanawe peke afe msalabani kwa sababu ya upendo wake kwa ajili yetu.

Tunapaswa kuukubali na kuuiga upendo huo. Biblia inasema, “Sisi tunapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza” ( 1 Yoh 4:19). Tena Biblia inatuagiza kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote. Tunapompenda Mungu, upendo huo utatuvuta kujitoa kwa ajili yake. Jinsi tuna-vyojitoa kwa Mungu ni ishara ya kiasi cha upendo tulio nao kwa ajili yake Mungu. Sheria haitulazimishi, bali upendo wetu unatulazimisha kwa njia nzuri ili tujitoe. Siyo kwa msukumo utokao nje yetu, bali ni mvuto unaoanzia ndani yetu. Matunda ya upendo wetu kwa Mungu yataonekana namna tunavyojitoa kwake. Kumbuka tunaiga upendo wake kwetu na jinsi alivyojitoa kwetu kutokana na upendo ule.

Pia upendo unaotuvuta kujitoa ni upendo wetu kwa ajili wanadamu wenzetu wenye mahitaji. Biblia inasema tunapaswa kuwapenda wengine kwa sababu Mungu anatupenda sisi. Ni upendo wa Mungu unaotupitia sisi wenyewe. Hatuhitaji kumlazimisha mtu amsaidie mwingine ambaye tayari anampenda. Kama wazazi wanaowapenda watoto wao, hatuhitaji kuwatungia sheria inayosema ni lazima wawasaidie watoto wao. Watawasaidia kwa sababu ya upendo walio nao bila kulazimishwa.

Ndivyo ilivyo katika utoaji. Mungu anataka tujitoe kwake kwa sababu ya upendo tulio nao katika mioyo yetu kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wengine.

Kuitikia neema ya Kristo humfanya Mkristo ajitoe

2 Wakorintho 8:9 - “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”

Page 63: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 63 -

Sababu nyingine ambayo Paulo anaitoa ili kutuvuta tujitoe kwake Mungu ni kwa sababu ya neema yake kwetu. Kama wanadamu tulipotea katika dhambi zetu na tulikuwa tunaelekea ziwa la moto. Ingawa hatukustahili, Mungu akamtuma mwanawe kuwa mwokozi wetu kwa neema yake. Ndani ya wokovu huu tumekuwa matajiri wa baraka nyingi kutoka kwa Mungu.

Tunapaswa kuiitikia neema hii. Mungu ametufanyia sisi mambo makubwa na anataka sisi tumfanyie yeye mambo madogo (ni madogo tukiyalinganisha na yale aliyotufanyia). Kumtii Mungu humfanya Mkristo ajitoe

Biblia nzima hufundisha watu wa Mungu kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu, wenye mahitaji, na mambo mengine ambayo Mungu anayajali. Katika Agano la Kale, chini ya Sheria ya Musa, utoaji kwa ajili ya ujenzi wa hekalu, utunzaji wa watumishi wa hekalu, gharama za ibada na sherehe, pamoja na msaada kwa ajili ya wenye mahitaji, ni wazi. Katika vitabu vya Injili She-ria ya Musa inaendelea na hivyo taratibu zake zinaonekana katika mafundisho ya Yesu.

Baada ya Mwili wa Kristo kuanza tunaona mabadiliko katika taratibu nyingine lakini kanuni za kujitoa kama watu wa Mungu zinaendelea kufundishwa. Kwa mfano Paulo, mtume aliyeifunua habari ya Kanisa linaloitwa Mwili wa Kristo, anaongea sana mambo ya pesa na uto-aji.

1 Wakorintho 16:2 – “Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja”

Kwanza Paulo anatoa agizo akisema utoaji wa mali uwe unafanyika katika mpango wa ku-jitoa kila wiki. Alikuwa akiongea kuhusu mchango maalum kwa ajili ya Wakristo wa Yerusalemu ambao walikuwa katika shida ya njaa.

2 Wakorintho 9:13 - “Kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.” Biblia habari njema inasema, “Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa hudu-ma hii yetu wanamtukuza Mungu”

Katika mstari huu Paulo anaendelea kuongea utoaji wa Wakorintho kwa ajili ya Wakristo wa Yerusalemu. Hapa anasema kujitoa kwao pesa hizo ni sehemu ya utiifu wao wa Injili. Yaani, kwa kuwa wameamini Injili na kuokoka kuwa Wakristo, uthibitisho wa imani yao katika Injili ni jinsi wanavyojitoa hali na mali kwa mambo ya Mungu.

Kuhusu utoaji Paulo anatoa maagizo mengi. Kwa mfano anaagiza Wakristo wajitoe kwa ajili ya kuwasaidia wajane kweli kweli (1 Tim 5:3-16), kutunza watumishi wa Kanisa (1 Tim 5:17-18), kuwasaidia watu wenye mahitaji (Rum 12:13, 2 Kor 8:14), na kwa ujumla kusaidiana kwa hali na mali katika Kanisa (Gal 6:2).

Anaagiza matajiri kuwa wakarimu wakishirikiana na wengine.

1 Timotheo 6:17-18 – “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wa-siutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine.”

Agizo hilo si kwa ajii ya matajiri tu lakini anakaza matajiri akijua Mungu amewawezesha zaidi ili watoe zaidi. Lakini Paulo anataka Wakristo wote kujitoa hata walio maskini. Sababu moja tunajua hivyo ni kutokana na jinsi alivyouinua mfano wa Wamakedonia, kama watu walio maskini, akiwataka Wakristo wengine kuwaiga katika utoaji wao.

Warumi 12:1 ni agizo tosha linalowaagiza Wakristo kuitoa miili yao. Yaani maisha ya Mkristo ni maisha ya kujitoa kwa Mungu kwa hali na mali kwa ujumla.

Warumi 12:1 – “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu”

Mwanzo hadi mwisho wa Biblia kupitia madaraka yote Mungu anaagiza watu wake kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya kuiendeleza mipango yake katika dunia hii. Bila sababu nyingine, kuyatii maagizo ya Mungu kunaweza kuwa sababu tosha kwa ajili yetu kujitoa. Lakini kama tunavyoendelea kuona ziko sababu nyingi na utiifu ni mojawapo tu. Isitoshe Mungu hupendelea tujitoe kwa sababu hizo nyingine kuliko sababu hiyo ya kutii.

Page 64: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 64 -

Kumheshimu Mungu humfanya Mkristo ajitoe

Mithali 3:9 - “Mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote.”

Heshima inatusukuma kufanya mambo mengi. Kama tuko na mzee ni lazima tumwoneshe heshima. Si kwa sababu ni sheria, bali kwa sababu anastahili.

Mungu anastahili heshima yetu. Ametuumba, anauendeleza uhai wetu, ametuokoa, na zaidi. Yeye ni mwenye nguvu zote na akili zote. Mambo hayo yote yanatulazimisha kumheshimu kwa sababu anastahili.

Njia moja ya kumheshimu Mungu ni katika kuitoa mali, muda, miili yetu n.k. Hitaji hilo la kumheshimu linatuvuta kumtolea; linatufanya tutake, kutoka kwenye mioyo yetu, kumtolea Mungu. Shukrani ya Mkristo kwa Mungu humfanya ajitoe

2 Wakorintho 9:12 - “Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.”

Waefeso 5:20 - “Na kumshukuru Mungu baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.”

1 Wathesalonike 5:18 - “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.”

Shukrani inatakiwa. Nimehesabu mistari 135 katika Biblia inayoelezea jinsi wanadamu wanavyotakiwa kumshukuru Mungu na bila shaka sijaitambua mistari mingine yenye agizo hilo. Katika dunia hii ni vigumu mtu atendewe vizuri sana bila kumshukuru yule aliyemtendea. Ni ajabu wengi wanasahau kumshukuru Mungu ambaye amewatendea mema kuliko mwanadamu ye yote yule.

Matoleo yenyewe ni njia ya kumshukuru Mungu. Kwanza yule anayejitoa anashukuru kwa njia ya matoleo yake na pili wanaosaidiwa wanatoa shukrani kwa Mungu kwa jinsi walivyosaidiwa. Kumpendeza Mungu humfanya Mkristo ajitoe

Wafilipi 4:18 - “Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.”

Sadaka zetu zinampendeza Mungu. Ni nani ambaye hataki kumpendeza Mungu? Mungu ni mwumbaji wa yote na mtunzaji wa yote. Mungu ni Baba yetu aliye mbinguni na Mwokozi wetu. Hakika kuna sababu za kutaka kumpendeza Yeye.

Kama mwalimu ninaona mara nyingi wanafunzi hufanya mambo mengi kwa sababu ya kumpendeza mwalimu tu. Kwa sehemu ni heshima na kwa sehemu ni kwa sababu wanajua mwalimu akipendezwa nao itakuwa faida kwao. Kuna sababu kubwa zaidi za kumpendeza Mungu kuliko walio walimu wetu hapa duniani. Maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu. Inatupasa kumpendeza kwa matoleo yetu.

Mkristo hajitoi ili asifiwe na wanadamu

Mathayo 6:2-4 - “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwi-sha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume.”

Baadhi ya watu wanavutwa kutoa sadaka ili watukuzwe na wengine. Wanataka ijulikane wametoa kiasi fulani tena kwa ajili ya nani. Kusifiwa na wengine siyo sababu kutuvuta kujitoa kama Wakristo. Kama Yesu alivyosema, Mungu hafurahishwi na sababu hiyo, hivyo hawezi kumpa mtu huyu thawabu kwa tendo hilo jema. Bali, ameshapata thawabu yake katika sifa alizopewa na wanadamu.

Page 65: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 65 -

Mkristo hajitoi kwa sababu nyingine zilizo mbaya

Hakika mara nyingi tunajitoa kwa sababu zilizo mbaya. Sababu hizi hazimpendezi Mungu. Wengine wanajitoa kwa sababu katika kutoa wanajisikia vizuri. Yaani kinachowasukuma ni hisia ile ya kuweza kujisikia vizuri.

Wengine wanaona hatia mbele ya Mungu au mbele ya wanadamu. Kwa sababu hii wana-jitahidi kujitoa ili waweze kutuliza hisia zile za kujisikia hatia. Huu siyo mvuto mzuri. Mvuto mzuri ni upendo, shukrani, heshima n.k.

Wengine wanajitoa ili waweze kutawala kile wanachokitolea. Kama ni kanisa, mara nyingine kuna watu wenye mali ambao wanajitoa zaidi kuliko wengine ili waweze kuhakikisha kanisa linaendeshwa kufuatana na mapenzi yao. Nia yao siyo kujitoa, bali ni kutaka kutawala.

Wengine wanajitoa kwa sababu wanawekewa shinikizo na wengine. Kama ni viongozi wao, au marafiki zao, wanabanwa wajitoe mpaka wanakuja kufanya. Lakini hii siyo sababu nzuri kwa sababu katika moyo wa mtu huyu hajajitoa kwa hiari.

Mwisho

Yapo mambo mengi yanayoweza kutuvuta tujitoe ipasavyo. Mambo haya yanailenga mioyo yetu. Yule ambaye atakuja kuelewa jinsi Mungu alivyomtendea, akiwa na moyo mzuri, hataona ugumu kujitoa kwake Mungu. Zaidi itakuwa vigumu kumzuia asitoe. Moyo wake utakuwa umejaa upendo, heshima, neema, na shukrani. Mambo haya yote yatamsababishia kumtii Mungu katika matoleo.

Zaidi Mungu atapendezwa kwa sababu, tofauti na sheria, sababu hizi zinatoka kwenye moyo ulio mweupe unaompendeza Mungu.

• Je, utoaji wa kulazimishwa na sheria unaweza kuwa na mafanikio? • Utoaji wa kulazimishwa na sheria una matatizo gani? • Je, kujitoa kwa Mkristo ni lazima katika kipindi hiki cha Uwakili wa Neema? • Wewe unajitoa kivipi? Kwa lazima au sheria? • Unampenda Mungu kiasi gani? Utoaji wako unaonesha unampenda Mungu kiasi gani? • Je, Paulo anaagiza nini kuhusu utoaji kwa ajili ya Wakristo wa leo? • Je, kipaumbele cha Mungu ni kwa Wakristo kujitoa kwa sababu ya kutii? Kwa nini? • Kwa nini Mungu anastahili kuheshimiwa kwa utoaji wako? • Una sababu gani za kumshukuru Mungu katika maisha yako? Je, utoaji wako unamwone-

sha Mungu shukrani? • Je, umewahi kujitoa kwa sababu zilizo mbaya? Sababu zipi? Ufanye nini ili ujitoe kwa

sababu zilizo bora?

WAKRISTO WANAPASWA KUTOA KIASI GANI? Hili ni swali linaloulizwa na wengi. Kuna sababu mbili kuu za kuuliza swali hilo. Sababu

mojawapo hutokana na moyo usio safi. Wengine wanauliza swali hilo kwa sababu wanataka kutoa vya kutosha, vilivyo vya lazima, lakini wanataka kuhakikisha wasizidishe. Wanataka ku-wajibika tu bila kuongeza. Wanatafuta baraka za Mungu wakitafuta kima cha chini kinachoweza kuwafanikisha. Kauli hii ni mbaya na haiwezi kumpendeza Mungu anayejua mioyo ya watu wote.

Wengine wana moyo mweupe mbele za Mungu na sababu inayowafanya kuuliza swali hilo ni kutaka kumtii Mungu. Kama kuna kiwango kilicho cha lazima wanataka wakijue ili wasim-kosee Mungu kwa kuwa nia ya mioyo yao ni kumpendeza Mungu.

Jibu halisi ni kwamba hakuna kiwango au kiasi kamili tunachoweza kutaja ambacho Wa-kristo katika Mwili wa Kristo wameagizwa kutoa. Maana ya neno “hiari” ni kwamba tunapaswa kutoa kiasi ambacho mioyo yetu inatuongoza kutoa kulingana na upendo, heshima, na shukrani zetu kwake Mungu. Mungu hataki kuweka mipaka kwa sababu anajua watu wakiifikiria mipaka, hawatatoa zaidi. Isitoshe, Mungu hapendi wakati watu wanatoa kwa ulazima wa sheria, hali isiyoonesha uhusiano mzuri. Bali, Mungu anaona ni bora zaidi kwa watu kujitoa kwa hiari kulingana na upendo na shukrani yao. Kwa njia hii hakuna mipaka na kiasi kikubwa zaidi kinaweza kikatolewa, tena katika hali inayofaa mioyoni mwa watu.

Page 66: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 66 -

Je, Wakristo wanapaswa kutoa fungu la kumi?

Wakristo wengi wanaamini tunapaswa kutoa fungu la kumi. Wanaangalia katika Sheria ya Musa, jinsi Waisraeli walivyopaswa kutoa fungu la kumi na wanadai hata Wakristo wa leo wanapaswa kutoa kufuatana na sheria au kanuni hiyo. Isitoshe wanasema fungu la kumi limo katika Agano Jipya wakionesha jinsi Yesu alivyoendeleza agizo lake katika Mathayo 23:23 na Luka 11:42. Lakini kipindi Yesu alipofundisha agizo hilo alikuwa akiishi bado chini ya Sheria ya Musa. Hivyo hakuna tofauti kati ya kipindi cha Yesu na kipindi cha Agano la Kale.

Tunapofika katika barua za Paulo na hata barua za Petro, Yohana na Yuda, hatuoni tena agizo la kutoa fungu la kumi. Yaani, baada ya Yesu kufundisha fungu la kumi katika vitabu vya Injili, wakati Sheria ya Musa bado ilikuwa inatumika, hatuoni fundisho wala maneno hayo tena katika Agano Jipya. Sababu agizo hilo halionekani baada ya kuanza kwa Mwili wa Kristo ni kwamba walio katika Mwili wa Kristo hawako chini ya Sheria ya Musa. Tena na tena Paulo anasema Wakristo wa leo hatuko chini ya sheria hiyo (k.m. Rum 6:14). Kuna baadhi ya mambo katika Sheria ya Musa yaliyoendelezwa katika Uwakili wa Neema, lakini huwa tunategemea maandiko ya Neno la Mungu yaliyoandikwa kwa ajili ya Mwili wa Kristo kuzirudia sehemu zile za sheria tunazopaswa kuendelea kuzifuata ili tujue zinatulenga. Hakika, kama Kanisa lilipaswa kuendelea kutoa fungu la kumi, Paulo angetoa agizo hilo tena. Lakini Paulo hajasema tutoe fun-gu la kumi katika Kanisa na badala yake ametoa mafundisho yaliyo tofauti.

Wengine wanaotaka fungu la kumi katika Kanisa la leo huhoji kwamba Abramu (Mwa 14:20) na Yakobo (Mwa 28:22) walimtolea Mungu fungu la kumi kabla Sheria ya Musa hai-jatolewa kwa Waisraeli. Lakini kuna mambo mengi yaliyofanyika kabla ya Sheria ya Musa am-bayo hatupaswi kuyafuata leo. Kwa mfano watu wa Mungu walipaswa kutunza sabato kabla ya Sheria ya Musa na pia walipaswa kutahiriwa. Lakini leo katika Kanisa tumefundishwa kutofuata mambo haya. Hivyo hoja ya kusema fungu la kumi lilifanyika kabla ya Sheria ya Musa haitoshi kuonesha fungu la kumi ni kwa ajili ya leo pia. Badala yake tunatafuta mafundisho yenyewe ya-nayolenga Kanisa ili kuona ni maagizo gani tunayopaswa kuyafuata. Tutaonesha baadaye kwamba Kanisa limepewa taratibu nyingine mpya badala ya fungu la kumi.

Isitoshe hatuwaoni Abramu na Yakobo wakiagizwa na Mugu kutoa fungu la kumi. Tuna mfano moja katika maisha ya Abramu akitoa fungu la kumi kutoka vitu vile alivyoteka katika vita. Lakini Biblia haisemi kwamba Abramu aliagizwa kufanya hivyo na zaidi hatujui kama kufanya hivyo kulikuwa kawaida yake kama alivyofanya mara hii. Hata mfano wa Yakobo una matatizo yake. Kwa hiari (bila kuagizwa) aliamua kumtolea Mungu fungu la kumi lakini alimpa Mungu masharti akisema atafanya hivyo ikiwa Mungu atamlinda, atamlisha, na atamvalisha. Si-dhani kama Wakristo leo tunataka kuwafundisha watu kumpa Mungu masharti katika matoleo yao kama vile Yakobo alivyofanya.

Shida nyingine ya fundisho linalosema fungu la kumi ni agizo kwa ajili ya Kanisa la leo, ni jinsi fundisho hilo linavyoshika sehemu moja ya Sheria ya Musa kuhusu matoleo na kuacha se-hemu zingine. Aidha wamekosa kuielewa Sheria ya Musa au wameamua tu kutii sehemu wanazotaka wenyewe, na kutotii sehemu zingine. Maana, fungu la kumi ni sehemu ndogo ya matoleo yaliyoagizwa katika Sheria ya Musa. Hatuna nafasi kujifunza juu ya sheria zote zinazo-husu utoaji katika Agano la Kale, lakini inatufaa kuelewa kwamba kulikuwapo na matoleo mengi, ambayo yalikuwa ya lazima, tena yalizidi asilimia 10 ya fungu la kumi. Wanateolojia wengine wameonesha, kutegemeana na aina za mapato, kwamba Waisraeli walipaswa (kwa sheria) kutoa kati ya 22% - 35% ya mapato yao yote kila mwaka. Lakini leo, wanaofundisha tutoe fungu la kumi katika Kanisa, hawasemi tutoe asilimia zote hizo ili tuwe tunazifuata sheria kikamili. Lakini kama tutafuata sheria, tunapataje ruhusa kuchagua sheria moja na ruhusa ya kutotii zingine?

Hakika chini ya Neema hakuna sheria inayohusu kiasi gani cha kutoa. Mawazo ya Mungu ni kwamba bila sheria watu wake watatoa zaidi kuliko vile ambavyo wangefanya chini ya sheria. Kama mtu atayaelewa yote Mungu aliyomtendea atawezaje kujizuia asitoe kwa wingi?

Wakristo wanafundishwa kutoa kwa kadiri

Matendo 11:29 - “Na wale wanafunzi , kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Uyahudi.”

Page 67: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 67 -

2 Wakorintho 8:11-12 - “Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo. Maana kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.”

1 Wakorintho 16:2 - “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake.”

Tena na tena Biblia inasema Wakristo wanapaswa kutoa kwa kadiri ya uwezo wao. Hali hii inaeleweka kwa sababu Mungu hawezi kumwomba mtu atoe 10,000 wakati anazo 2,000 tu.

Kusema kwamba tunatakiwa kutoa kulingana na uwezo wetu siyo kusema tutoe fungu la kumi. Ndani ya neno kadiri hakuna kiwango kamili wakati fungu la kumi ni kiwango kamili cha asilimia kumi. Paulo angekusudia Wakristo watoe fungu la kumi angekuwa amesema, “kwa kadiri ya asilimia kumi ya kufanikiwa kwake.” Lakini hajasema hivyo. Ni kweli kutoa fungu la kumi ni njia moja ya kupima kadiri ya uwezo wa mtu. Lakini kama tulivyosema Mungu hajaagiza kiasi kamili na ukweli ni kwamba kwa wengine kutoa asilimia kumi isingekuwa kutoa kwa kadiri ya uwezo wao.

Kadiri ina maana gani sasa? Kwanza tunaweza kusema kwamba mwenye zaidi anastahili kutoa zaidi (yaani asilimia kubwa zaidi), na mwenye kiasi kidogo anapaswa kutoa kiasi kidogo zaidi (yaani asilimia ndogo zaidi). Lakini unaona hatujatamka kiasi gani kamili. Kiasi gani ni uamuzi wa kila Mkristo kuamua chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu akijaribu kutoa kulingana na kadiri ya uwezo wake.

Kama mtu anataka kutoa asilimia fulani basi, afanye hivyo. Lakini isiwe kwa sababu ame-lazimishwa na mtu wala Mungu. Iwe kwa sababu amekusudia katika moyo wake kufanya hivyo. Kama ni 10%, 20%, 30%, au zaidi. Asilimia ya kiasi kimoja haiwezi kufaa Wakristo wote, hivyo ukitaka kupanga utoaji wako kufuatana na asilimia, basi uchague mwenyewe asilimia yako ukimwomba Mungu akuongoze na akupe imani ya kujitoa.

Kutoa kwa kadiri kunategemea jumla ya mapato mtu aliyo nayo pamoja na jumla ya mahitaji yake. Mtu akitimiza mahitaji yake na bado anabaki na hela nyingi, mtu huyu angetoa asilimia kubwa zaidi ya mapato yake ili aoneshe anatoa kwa kadiri ya uwezo wake. Lakini mtu maskini ambaye mapato yake yanashindwa kutimiza mahitaji yake, mtu huyu angetoa asilimia ndogo zaidi ambayo kwake itakuwa kujitoa kwa kadiri ya uwezo wake. Kwa mfano, tuseme wastani wa mahitaji ya mtu ni 100,000 tsh kwa mwezi. Ikiwa mtu anahitaji 100,000 tsh kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine ya kimsingi, na ana mapato ya 105,000, itakuwa vigumu mtu huyu atoe 20,500 tsh (ambazo ni 10%) Yuko hiari kutoa 20,500 katika kumtegemea Mungu lakini kufanya hivyo kwake ni uamuzi wa kukosa mahitaji mengine (huu ndiyo moyo ambao hakika ungempendeza Mungu). Kwa namna nyingine tunaweza kusema akitoa kiasi hicho atakuwa ametoa kuliko kadiri ya uwezo wake. Lakini mtu mwingine mwenye mahataji hayo ya 100,000 tsh kwa mwezi akiwa na mapato ya milioni moja ina maana baada ya kugarimia mahitaji yote atasalia 900,000 tsh kama akiba. Kwake huyo kutoa 20,500 tsh kusingekuwa ku-toa kwa kadiri ya uwezo wake. Hata angetoa 100,000 tsh (ambazo ni fungu la kumi, au asilimia 10 ya mapato yake) bado atakuwa hajatoa kwa kadiri ya uwezo wake. Yaani, mtu huyu baada ya kutimiza mahitaji yake bado amebaki na 900,000 tsh na hivyo kadiri ya uwezo wake ni kubwa sana zaidi na hivyo anapaswa kutoa asilimia kubwa zaidi kulingana na uwezo wake. Ndiyo maana tunasema kutoa kwa kadiri ya uwezo ni tofauti na kutoa fungu la kumi. Mtu mwenye uwezo huo mkubwa kutoa fungu la kumi ingekuwa kutoa chini ya kadiri ya uwezo wake. Yaani kadiri haiwezi kuwa asilimia moja kwa watu wote kwa sababu kadiri ya uwezo wa mtu mmoja inaweza kuwa 10% wakati kadiri ya uwezo wa mwingine ni 75%.

Ni vizuri kila mtu aangalie uwezo wake na kuufanya uamuzi katika moyo wake mwenyewe akiwa anaomba kwa Mungu uongozi kuhusu uamuzi huo. Ni vizuri apange jambo kamili ambalo atalifuata kila wakati. Kutofanya hivyo husababisha mtu asijitoe ipasavyo. Ni suala la uwakili. Kama tulivyojifunza, mwenye kupewa zaidi hupewa wajibu zaidi vilevile.

Kwa sababu hiyo ni muhimu kufikiria upya utoaji wetu wakati mapato yetu yanabadilika. Tukizoea kutoa asilimia fulani tuliyokusudia na Mungu anatubariki akiongeza mapato yetu, ni bora tufanye mpango mpya wa utoaji wetu unaoendana (kwa kadiri) na hali mpya ya mapato yetu.

Page 68: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 68 -

Wakristo wanafundishwa kutoa kutoka katika umaskini wao

Marko 12:41-42 - “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano wa-tiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaam-bia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.”

Yesu anafundisha somo moja muhimu katika mistari hii. Ingawa Yesu alifundisha watu walio chini ya Sheria ya Musa, alitaka kuwafundisha watoe kwa kumtegema Mungu kuliko kutoa kwa kutimiza sheria tu. Tunaona kanuni hiyo katika Biblia nzima wakati wa sheria na hata wa-kati sheria imetanguliwa. Ingawa Yesu alifundisha fungu la kumi kwa ajili ya Waisraeli, hapa anaonesha kuna kanuni muhimu zaidi ya kutoa kwa kadiri na pia kutoa kwa namna inayoone-sha mtu anamtegemea Mungu. Tunapoongelea kiasi cha kutoa, Mungu hatafuti kiwango kamili bali anaangalia moyo wa mtu katika kiasi anachoamua kutoa. Mwingine anaweza kutoa milioni bila kumtegemea Mungu wala kutoa kwa kadiri ya uwezo wake na mwingine anaweza kutoa shilingi hamsini na katika kiasi hicho amemtangazia Mungu kwamba anamtegemea.

Mungu hupendezwa na Wakristo wanaojitoa kutoka katika umaskini wao. Ni sawa na kusema tutoe mpaka inatuumiza au mpaka iwe na maana kwamba tutakosa mahitaji mengine na kulazimika kumtegemea Mungu. Mwingine anayetoa milioni moja hajaumizwa kwa sababu anazo milioni kumi. Mwenyewe anaweza kuona hahitaji kumtegemea Mungu kwa sababu at-ategemea milioni tisa zile zilizobaki. Hivyo ametoa kutoka katika utajiri wake, yaani, ametoa pesa za ziada ambazo hakuzihitaji.

Lakini Mungu anapendezwa wakati tunapomtolea pesa ambazo tunazihitaji kwa sababu inamwonesha kwamba tunamtegemea na tunategemea kutekelezewa mahitaji yetu kupitia uwezo wake.

Ili tuelewe kanuni hiyo tuangalie mfano wa kuku, ng’ombe, na nguruwe. Siku moja wote wakakubaliana kukusanyika ili wale chakula pamoja. Kila mmoja alipaswa kuleta kiasi cha chakula alichoweza kukitengeneza yeye mwenyewe. Kuku alitaga mayai ambayo alikusudia kuyaleta. Ng’ombe akatoa maziwa ambayo alikusudia kuyaleta. Kwa sababu nguruwe anafaa tu kwa nyama ya kitimoto, ikabidi ajiumize kupata kipande cha nyama ili aweze kuchangia mlo huu. Katika mfano huu ni nguruwe aliyejitoa kweli kweli. Kuku na ng’ombe hawakuumizwa. Wakatoa yale ya ziada.

• Katika maisha yako unafanana na nani? Kuku au nguruwe? • Uko tayari kujitoa mpaka ifikie lazima ya kumtegemea Mungu?

Mjane huyu katika mfano wa Yesu alitoa yote aliyokuwa nayo. Yesu anasema alitoa riziki yake. Tunaweza kusema alitoa kuzidi kadiri ya uwezo wake, yaani alitoa kutoka katika umaskini wake. Hii siyo kawaida, lakini ni jambo lililompendeza Mungu. Kwa kawaida, sisi Wakristo, tun-apenda kutimiza riziki yetu kwanza ndipo tumtolee Mungu kutoka yale yanayobaki. Bora tuji-funze kutoa kutoka umaskini wetu na siyo utajiri wetu. Kwa njia hii tutakuwa tunaonesha moyo wetu wa kumtegemea Mungu anayetutimizia mahitaji yetu.

Wakristo wanafundishwa kutoa kwa ukarimu

Tumeshaliongelea neno hili lakini niliona inafaa tulirudie wakati tunaongelea kiasi gani. Hata neno hili halileti kiwango kamili lakini linatuongoza kuelewa kwamba ni kiasi kikubwa tu, kulingana na uwezo wetu. Ukarimu humaanisha wingi au kuzidisha. Kila mmoja anatakiwa kujiuliza kama matoleo yake yanaelekea kwenye ukarimu. Bila maelezo marefu nafikiri kila mmoja anaweza kujibu swali hilo juu yake mwenyewe hata kama ufafanuzi wetu kuhusu ukarimu utatofautiana.

• Kwa nini Wakristo hupenda kujua kiasi gani Mungu anachoagiza katika utoaji wao? • Biblia ingetaja kiasi cha kutoa, je, utoaji ungekuwa kwa hiari tena? • Agizo la Neno la Mungu kutoa fungu la kumi lililenga watu gani? Kwa nini halitulengi sisi

Wakristo wa leo?

Page 69: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 69 -

• Kwa kuwa Wakristo wa leo hawako chini ya Sheria ya Musa, wanapaswa kukitumia kipi-mo gani katika utoaji wao?

• Kwa nini wazo la Wakristo wote kutoa asilimia 10 ya mapato yao lingefanya wengine kutotoa kwa kadiri ya uwezo wao?

• Kwa nini kutoa kwa kadiri ni bora kuliko kusema wote watoe asilimia moja? • Wewe umeamua kutoa asilimia ngapi katika maisha yako? • Eleza jinsi utoaji wako unavyoweza kuonesha jinsi unavyomtegemea Mungu.

WAKRISTO WANAPASWA KUTOA WAKATI GANI? Biblia haijaeleza sana kuhusu wakati gani. Tunao mstari mmoja tu wa Paulo akisema siku

ya kwanza ya kila wiki. Sidhani kwamba alitaka kutunga sheria mpaka tuulizane siku ya kwanza ni siku gani ili tusikose kutoa katika siku hiyo yenyewe.

Maana yake zaidi ilikuwa kusema tujitoe kwa mpangilio. Maana Biblia inaeleza kwamba tunapaswa kuangalia mapato yetu yote. Bora tufanye njiani badala ya kufika mwishoni mwa mwaka na kujaribu kukumbuka mapato yetu yote. Kila tunapopata mapato ndiyo wakati unaofaa kutoa yale tunayokusudia kwa kadiri ya uwezo wetu.

Biblia inafundisha kwamba tunatakiwa kuwasaidia wahitaji. Tukiuliza swali, “Wakati gani?” ingebidi tujibu wakati inapohitajika. Hatuwezi kumwambia mwenye hitaji kwamba siwezi ku-kusaidia kwa sababu siyo siku ya kwanza ya wiki. Bali tunapaswa kumsaidia wakati ana hitaji kwa kadiri ya uwezo wetu.

WAKRISTO WANAPASWA KUTOA VITU GANI?

Mara nyingine pesa ni kikwazo kinachomzuia mtu asijitoe. Watu wengi hawachezi sana na

pesa. Wanaweza kujitimizia mahitaji mengi katika shamba, bustani, na nguvu zao. Hata mara nyingine wanabadilisha mahindi au mazao mengine ili wapate vitu vingine. Tunaona hali hii hasa kijijini. Mjini huwa ni tofauti kwa kuwa watu wamezoea kuishi kwa pesa.

Kwa sababu wengi wanaishi kwa njia zisizo za pesa, kwa kawaida hawana pesa za kutoa kanisani. Jumapili inapokuja wanajiuliza kama wanazo pesa, na kama hawana, basi hawatoi. Hali hii imejengwa juu ya wazo baya. Wazo lenyewe linasema kwamba lazima utoaji uwe pesa.

Kwa wengine ni ujanja tu wa kukwepa matoleo. Wanajua hawatakuwa na pesa kwa hiyo wanaona ni hoja nzuri katika kujitetea kwamba hawawezi kujitoa. Lakini watu hawa hu-jidanganya kwa kuwa Mungu anajua mioyo yao.

Biblia inaleta picha tofauti. Biblia inaangalia mali yote ya mwanadamu anayopewa na Mungu. Kila alicho nacho amepewa na Mungu, na kutoka vitu vile, Mungu anategemea matoleo kwake.

Mambo ya Walawi 27:30,32 - “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. ...Tena zaka yote ya ng,ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana.”

Wakati Waisraeli walijenga hema ya kukutania, kwa maagizo ya Mungu, walitoa vitu vingi. Soma mistari hii ukiwa unatafuta aina mbalimbali za vitu walivyotoa.

Kutoka 35:21- 35 - “Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apende, nao wakaleta sadaka za kumpa Bwana, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja, waume kwa wake wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa Bwana. Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi, na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, akavileta. Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya Bwana; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yo yote ya huo utumishi akauleta. Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri. Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima

Page 70: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 70 -

wakasokota hizo singa za mbuzi. Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani, na viungo vya manukato na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri.

Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; naye amemjaza roho ya Mungu, katika heki-ma, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti atumike katika kazi za werevu kila aina. Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Ohaloiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani. Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufu-ma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.”

• Taja vitu vilivyotolewa na Waisraeli: • Taja vitu wewe unavyoweza kutoa:

Tukisoma jinsi walivyotoa tunakuta kwamba walitoa yapata vitu 19 vilivyo tofauti. Ha-wakutoa pesa tu. Walitoa kile walichokuwa nacho. Cho chote ambacho kingesaidia kazi ina-yotendeka na Mungu.

Zaidi tunaona walitoa ujuzi na uwezo waliopewa na Mungu pia. Sisi sote tumepewa karama na ujuzi na Mungu. Sehemu ya uwakili wetu ni kujitoa katika kazi mbalimbali za Mungu ambazo tuna uwezo nazo. Kwa mfano wengine ni mafundi seremala na njia moja wanayoweza kujitoa ni kwa kujenga vitu kama mabenchi kwa ajili ya kanisa. Mwingine ni mwalimu wa serikali ambaye anaweza kujitoa kwa kufundisha washirika namna ya kusoma na kuandika n.k.

Tusiamini kwamba kuna njia moja ya kipekee ya kumtolea Mungu, yaani, ni pesa tu. Vipo vitu vingi tunavyoweza kuvitoa. Nikiwaza naweza kuorodhesha vitu kama kalamu, daftari, nguo, gunia, mazao, mbao, mkeka, kuni, ndoo, vyombo vya kupikia, shoka, basikeli, spea za basikeli, mayai, kuku, mbuzi, chumvi, saa, bati, chokaa, n.k. Yaani, vinaweza kuwa vitu vyo vyote. Kama kanisa haliwezi kukitumia ulichotoa, angalau linaweza kukiuza na kuzitumia pesa watakazopata katika mauzo. Pia tusisahau muda wetu na ujuzi wetu. Kutokana na hayo tuna utajiri mwingi. WAKRISTO WANAPASWA KUJITOA KWA AJILI YA NINI?

Mungu ametoa mawazo mengi kuhusu yale ambayo anataka yasaidiwe kutokana na

matoleo yetu. Ni vizuri kila Mkristo aweze kujitoa kwa mambo mbalimbali kulingana na maa-gizo ya Neno la Mungu. Mara nyingine tunapendelea kutolea jambo moja ambalo Mungu ana-taka na tunasahau mambo mengine ambayo Mungu anakusudia tuyatolee vilevile.

Kuna mambo mengi yanayohitaji matoleo yetu. Tuko huru kujitoa pale tunapoona Mungu anatuongoza kutoa. Lakini kati ya mambo mengi haya, mojawapo huchukua kipaumbele. Mungu ana chombo kimoja tu katika dunia hii. Chombo kile kinaitwa Kanisa lililo Mwili wa Kristo. Nda-ni ya chombo hicho na kupitia chombo hicho huduma zote zahusika kwa namna moja au nyingine. Hivyo matoleo yetu ya msingi hulenga kanisa letu kwanza ambamo huduma za Mungu zinafanyika zikilenga Wakristo na watu wa dunia hii wasiomjua Kristo. Yesu ni kichwa cha Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa. Yesu siyo kichwa cha chombo cho chote kingine.

Waefeso 1:22 - “Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa ambalo ndilo mwili wake.”

Wahudumu wote katika Biblia wanakuwa ndani ya Kanisa. Kazi zao hazitendeki nje ya mamlaka ya Kanisa. Mungu ameweka viongozi katika Kanisa lake ili waweze kuyaongoza mam-bo yote yanayotendeka.

1 Wakorintho 12:28 - “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu...”

Kwa maana hii Kanisa ndilo linaloangaliwa zaidi katika matoleo. Kanisa ndilo linaloendesha huduma mbalimbali za Mungu. Kanisa linatawala na kuhakikisha yote yanatendeka kwa njia inayompendeza Mungu.

Page 71: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 71 -

Wakristo wanapaswa kumtolea Mungu

Kutoka 25:2 - “Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.”

1 Mambo ya Nyakati 29:9 - “Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana.”

Mithali 3:9 - “Mheshimu Bwana kwa mali yako.”

Po pote ambapo tunajitoa tujue kimsingi tunamtolea Mungu. Tukisaidia kulijenga kanisa, tunamtolea Mungu. Tukiwasaidia maskini, tunamtolea Mungu. Ni muhimu tuweze kukumbuka kanuni hiyo. Mara nyingine watu hawatoi kwa sababu hawampendi mchungaji wao au ha-waupendi uongozi wa kanisa lao. Hawaelewi kwamba kutotoa kwao ni kutomtolea Mungu. Wajue hawa wengine si kitu isipokuwa ni Mungu tu ambaye tunamtolea kweli kweli.

Ni kama maneno ya Yesu katika Mathayo 25. Wakati watu watakapohukumiwa na Yesu atawaambia wengine:

Mathayo 25:34 - 40 - “Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa.... Na mfalme atajibu akiwaambia, Amin nawaam-bia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”

Vivyo hivyo kwa matoleo yetu. Anayehusika hasa ni Mungu. Ni kweli matoleo yetu yana-saidia mambo katika dunia hii kama majengo, watu, na huduma, lakini tunayemtolea ni Mungu mwenyewe.

Wakristo wanapaswa kujitoa kwa watumishi

Tukisema watumishi, tunamaanisha watumishi wa Mungu. Watumishi wa Mungu wana-weza kuwa wachungaji, wainjilisti, waalimu au viongozi wengine. Zaidi, ni ye yote anayemtumikia Mungu kama kazi kuu katika maisha yake au anamtumikia Mungu kiasi kikubwa kinachozuia asiweze kujitafutia mahitaji yake yote mwenyewe.

Kanuni ya Biblia inasema kwamba watumishi wa Mungu wanatakiwa kulishwa ndani ya kazi wanayoifanya.

1 Wakoritho 9:14 - “Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.”

Huduma za Kanisa ni kazi. Ni sawa na kuajiriwa. Aliyeajiriwa anapaswa kulipwa kwa kazi yake na muda wake. Neno riziki linaeleza mahitaji ya msingi. Sisi sote tunafanya kazi fulani katika maisha yetu inayotuwezesha kupata mahitaji yetu yaliyo riziki.

1 Timotheo 5:17-18 - “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.”

Ni wazi kwamba Paulo anaongelea wahudumu ndani ya Kanisa katika mistari hii. Jina analolitumia ni “wazee”. Hii siyo kusema mzee wa kanisa anastahili mshahara. Bali inategemea na kazi ambayo mzee anaifanya. Wazee wengi wanafanya kazi ya vikao na kutatua shida katika kanisa. Pia mara kwa mara wanaweza kufundisha shule ya jumapili au hata kuhubiri. Lakini wazee wa namna hii hufanya kwa muda tu wakati kazi yao ya kudumu ni kazi nyingine.

Katika mistari hii Paulo anaongelea wazee wenye hadhi tofauti. Kipindi cha Paulo wazee wengine walifanya kazi ya kudumu katika Kanisa. Kama anavyosema katika mistari hii, “Waji-taabishao kwa kuhutubu na kufundisha.” Kujitaabisha inaonesha si kazi ya ziada. Ni kazi ina-yokula masaa mengi hasa katika vitu hivi viwili vya kuhubiri na kufundisha. Leo hii tunaita viongozi wa namna hii “wachungaji”, “walimu”, au “wainjilisti”.

Hoja ya Paulo ni kwamba kiongozi ye yote ambaye anatoa muda wake kwa Kanisa anasta-hili kutunzwa na Kanisa. Muda huo ni zaidi ya huduma za kawaida kwa sababu Biblia inafun-disha kwamba kila Mkristo anapaswa kujitoa katika kufanya huduma mbalimbali katika Kanisa

Page 72: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 72 -

bila malipo. Tofauti ni kwamba wazee wa namna hii wanajitoa muda mrefu kiasi kwamba wanashindwa kutimiza baadhi ya mahitaji ya maisha yao. Hivyo wanastahili kusaidiwa na Ka-nisa kwa sababu wanalisaidia Kanisa kwa muda wao mwingi.

1 Wakorintho 9:4 - 11 - “Je! hatuna uwezo wa kula na kunywa? 5 Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine na ndugu wa Bwana, na Kefa? 6 Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusiyo na uwezo wa kutokufanya kazi. Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? 7 Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? 8 Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au Torati nayo haisemi yayo hayo? 9 Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Je! hapo Mungu aangalia mambo ya ng’ombe? 10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini; naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. 11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?”

Kuna kanuni inayoeleweka po pote duniani. Kanuni hiyo inasema kwamba kila mtenda kazi anastahili mshahara wake. Ndiyo hoja ya Paulo hapa. Anatoa mifano ya askari, mkulima, na mchungaji, kuonesha jinsi wote wanavyopata mahitaji yao ndani ya kazi zao.

Ni ajabu, lakini, wengine wanaiamini kanuni hiyo moja kwa moja, isipokuwa inapomhusu mtumishi wa Kanisa. Wanataka wachungaji wao au viogonzi wengine kutoa muda na nguvu zao, lakini wanaamini kwamba pamoja na hayo ni juu ya mchungaji kujitegemea au kumtegemea Mungu.

Haya siyo mawazo ya Paulo, hata kidogo. Mistari hii inasema wazi mno. Hakuna anayeweza kuchanganya maana yake hapa. Kwanza katika mstari wa 4 anaonesha kwamba tunaongelea mahitaji ya kimwili. Anasema, “Hatuna uwezo wa kula na kunywa?”. Kula na kunywa ni misingi ya mahitaji yetu. Kwa utangulizi huo Paulo anaanzisha mafundisho yake kuhusu kutunza wa-tumishi wa Kanisa.

Katika mstari wa kumi anakuja kuuliza swali lingine. Anasema mambo haya yahusu ng’ombe au ni kwa ajili yetu? Hakika anasema ni kwa ajili yetu. Neno “yetu” linahusu nani? Katika mazingira ya mistari hii Paulo anawaongelea watumishi wote wa Kanisa wanaodumu kwa muda mwingi katika kazi ya Mungu. Ndiyo sababu anakuja kusema katika mstari wa 14, “Bwana...ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.” Tazama jinsi hii ni amri ya Mungu. Siyo suala la hiari kwa upande wa washirika wa Kanisa. Mungu ametuamuru tuwatunze watumishi wa Kanisa. Sasa ni muhimu tujue kwamba tusipozitii amri za Mungu kuna adhabu na kukosa baraka.

Tujiulize kwa nini makanisa mengi hayaendi vizuri. Sababu mojawapo ni kwamba sisi washirika hatujamtii Mungu. Hivyo tunazikosa baraka nyingi za Mungu ambazo zingezigusa se-hemu nyingi za maisha ya Kanisa. Mungu ameiweka amri hii kwa sababu anajua kazi hii ni ngumu. Wakristo wakilitii agizo hilo la Mungu, watumishi wa Kanisa wataweza kuweka bidii zao zote ndani ya kazi yenyewe. Lakini wakati mchungaji au kiongozi mwingine hatunzwi, ina maa-na anajitegemea na hivyo hawezi kulitumikia kanisa ipasavyo. Mwisho wake kanisa halipigi hatua za maendeleo.

Mstari wa 11 unafafanua kwa undani zaidi. Paulo anasema, “Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?” Hakuna mashaka juu ya maana ya Paulo. Kupanda vitu vya rohoni ni kufanya kazi za kiroho. Kufundisha, kuhubiri, kuo-nya, kufanya uinjilisti, kuongoza, n.k. Kazi hizi zote ni kwa manufaa ya washirika wote. Kutoka-na na kazi za watumishi wa Kanisa, watu wa Mungu wanapata faida kubwa ya kumjua Mungu wao zaidi na kuweza kumtumikia kwa ubora zaidi. Kwa sababu kila mshirika anafaidika kuto-kana na kazi za watumishi wa Kanisa, inawapasa kuwatunza watumishi hawa. Hiyo ndiyo maa-na ya Paulo asemapo kuvuna vitu vya mwilini. Vitu vya mwilini ni vitu vile vinavyompatia mtumishi mahataji ili aweze kuendelea na huduma zake.

Mwingine anaweza kuuliza juu ya watumishi wengine kama wainjilisti, wamishonari, au viongozi katika ofisi kuu ya Kanisa. Ni wajibu wa nani kuwalisha hawa kimwili?

Kwanza tuangalie wainjilisti na wamishonari. Kanuni ya Paulo hapo juu inasema wale wanaolishwa kiroho wanapaswa kuwarudishia msaada wa kimwili. Lakini huduma za wainjilisti

Page 73: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 73 -

na wamishonari zinalenga wapagani; watu walio nje ya Kanisa. Haiwezekani walipwe na wapa-gani hawa ingawa huduma ya kiroho yenyewe imewalenga. Basi ni wajibu wa nani? Kumbuka kwa nini wanafanya kazi hiyo ya uinjilisti. Ni wajibu wa nani kueneza injili katika dunia hii? Mungu anakifahamu chombo kimoja tu. Chombo kiitwacho Kanisa. Ni wajibu wa Kanisa kuhakikisha Injili imeenezwa duniani pote. Basi, tumepata jibu letu. Kama ni wajibu wa Kanisa kuieneza Injili, ni wajibu wake kuwatuma wainjilisiti na wamishonari na kuwatunza ili wafaulu katika kazi hiyo. Wakishindwa katika kazi hiyo, kwa sababu ya kutotunzwa, hukumu siyo juu yao, bali hukumu ni juu ya Kanisa.

Vipi watu kama mwangalizi mkuu, katibu mkuu na watumishi wa idara mbalimbali za Ka-nisa ambao hawana kanisa (tawi) la kuwalisha. Je, mahitaji yao yatoke wapi? Tutumie kanuni ya Paulo kujibu. Paulo anasema wale wanaohudumiwa kiroho wanapaswa kuwasaidia kimwili wahudumu wao wa kiroho. Je, Mwenyekiti na Katibu wanawahudumia nani? Si wanayahudumia makanisa yote? Kama ni mambo ya serikali wanatumika kwa niaba ya Kanisa zima. Kama ni ku-leta maendeleo au kuyatatua matatizo, ni maendeleo ya nani na shida za nani? Si ni kwa maendeleo na shida za Kanisa kwa ujumla. Hivyo tunaweza kusema wanalihudumia Kanisa zima na Kanisa zima linawajibika kuwatunza kimwili.

Je, wachungaji walio kijijini ambao ni wakulima, wanastahili kusaidiwa nao? Hapa Tanzania tunao wachungaji wengi ambao wanajitegemea, hasa vijijini. Sababu ni kwamba washirika wanaona kwamba wachungaji wao wanaweza kulima sawa na wengine na hivyo hawastahili msaada. Ni kweli, wachungaji wengine wana muda sawa na washirika katika kujitafutia mahitaji yao. Lakini ni bora tusiwaite wachungaji kwa sababu kama wana hali hiyo basi hawafanyi kazi ya uchungaji ipasavyo. Kazi ya uchungaji ni kazi inayohitaji masaa mengi. Kuna maandalizi ya masomo na hotuba, kuna kuwatembelea wagonjwa na washirika, kuna vikao vya tawi na vya senta, na vya mkoa. Kuna kutatua shida mbalimbali, kuna kulea viongozi wengine. Kazi ni nyingi, na kama mchungaji ana muda wa kulima na kuyatafuta mahitaji mengine sawa na mku-lima wa kawaida, basi, hakika hawezi kufanya kazi ya uchungaji ipasavyo.

Maendeleo ya kanisa yanafuatana na masaa ya kutumika kwa viongozi wake. Kijijini jambo la kwanza ambalo kanisa linaweza kufanya ni kuwalimia viongozi wao. Sisemi mtindo huu wa siku moja katika kupanda na siku moja katika kuvuna. Hii ni msaada lakini siyo kuwalimia. Afadhali wamlimie kwa uhakika ili aweze kuzifanya huduma zake. Hata kama mchungaji atali-ma, hii ni sehemu tu ya mahitaji yake. Kila mtu ana shughuli nyingine anazozifanya kila wakati ili apate mahitaji mengine ambayo kilimo chake hakitayatimiza. Kwa mfano kupasua mbao, ku-tunza bustani, kununua na kuuza samaki, n.k. Tena kuna muda wa kukusanya kuni, au kufyatua matofali na kuong’oa nyasi za kuezekea. Sasa kama mchungaji analima na kwa muda mwingine anafanya huduma za kanisa, ni wakati gani atafanya shughuli hizo nyingine zitakazompatia mahitaji mengine kama watu wa kawaida wafanyavyo? Kweli wachungaji na viongozi wetu wanastahili msaada wa kimwili hata kama wanayo mashamba na wanatumia kiasi cha muda wao katika kilimo.

Nimewahi kusikia washirika wengine wakisema mchungaji anapaswa kumtegemea Mungu. Katika kutamka hivyo washirika hujiondoa kutoka nafasi yao ya kuwa chombo ambacho Mungu anaweza kukitumia kuwatunza watumishi wake. Sielewi mawazo haya. Sijui kama wanafikiri Mungu atadondosha pesa kutoka mbinguni au itakuwaje. Najua tu, wakisema mchungaji amtegemee Mungu, maana yao ya msingi ni kusema asitutegemee sisi.

Wengine wanadai kwamba Paulo alifanya kazi yake bila malipo ili asiwe mzigo kwa Kanisa. Wanatumia mistari kama:

2 Wathesalonike 3:8 - “Wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na ma-sumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.”

2 Wakorintho 11:9 - “Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena nitajilinda.”

Kutokana na mistari ya namna hii wanataka watumishi wote kutokuwa mzigo kwa Kanisa kwa sababu Paulo hakuwa mzigo kwa Kanisa. Kwanza ni lazima tuseme, ingawa Paulo hakuwa mzigo kwa Kanisa la Korintho au Thesalonike, tunaona ndani ya maelezo yake kwamba aliweza

Page 74: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 74 -

kuishi katika Korintho kwa sababu alisaidiwa na Kanisa la Makedonia. Hapo tunaona mara nyingine Paulo alikuwa mzigo kwa kuwa ndiyo waliojitoa kwa ajili ya mahitaji yake ya kimwili.

Muhimu zaidi ni mafundisho ya Paulo kuhusu jambo hili. Mwenyewe analiambia Kanisa la Korintho kwamba ana haki kuwadai katika mahitaji yake ya kimwili. Tuliona madai yake tulip-osoma maelezo yake katika 2 Wakorintho 9:4-11. Hata kwa Wathesalonike anasema hakuwa mzigo kwao lakini ilikuwa haki yake kusaidiwa kama mtumishi aliyewahudumia kiroho.

1 Wathesalonike 2:6 - “Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wen-gine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo.”

Tunachojifunza ni kwamba Paulo alikuwa na haki kutunzwa kimwili na wale aliowa-hudumia kiroho (ndiyo kusema mara nyingine alisaidiwa kutokana na haki yake). Lakini mara nyingine mtume Paulo hakulazimishwa aikatae haki yake bali kwa hiari yake aliiacha. Makanisa mengine yanataka kuwalazimisha wachungaji na watumishi wao kutopata haki yao kwa sababu Paulo aliisamehe haki yake mara nyingine. Tatizo ni kwamba jambo hili ni uamuzi wa mtumishi mwenyewe kama Paulo, wala siyo uamuzi wa Kanisa. Hatuwezi kuwalazimisha watumishi wetu wasidai haki zao, ni hiari yao wakiamua wenyewe. Lakini wakiamua kwamba wanataka kupata haki zao ni wajibu wetu kama Kanisa kuwatimizia mahitaji yao kufuatana na maagizo ya Mungu.

Tunaweza kuwasaidia wachungaji kwa njia mbalimbali. Kama Kanisa, kanuni inasema washirika wanatakiwa kuwasaidia watumishi. Njia moja ni kutoa msaada pale pale katika tawi la mchungaji mwenyewe. Lakini kwa mawazo ya watu wengine wangependa kila mchungaji asaidiwe kutoka ofisi kuu ya Kanisa. Hata njia hii ni sawa wakielewa kwamba ofisi kuu haina mali au pesa nje ya washirika wake. Kama washirika wanataka kuyatoa matoleo kwa ajili ya mchungaji wao yaende ofisi kuu halafu yarudi kwa wachungaji, naona ni sawa. Ni sawa kwa sababu bado wanaohudumiwa kiroho ndiyo wanaowalisha watumishi wao kimwili.

Lakini washirika wasiukwepe wajibu wakidhani ofisi kuu inapaswa kuwatunza wachungaji wa Kanisa wakitumia njia nyingine za mapato. Kwanza ofisi kuu haina mapato kutoka sehemu nyingine. Ofisi kuu ya Kanisa ni kichwa tu cha mwili na mwili ni matawi yote ndani ya Kanisa lile. Ni kama maua. Maua yana mizizi mingi chini ya ardhi. Mizizi ndiyo inayolisha mmea mzima. Hata maua yanalishwa na mizizi yake. Mizizi haiwezi kudai ilishwe na maua kwa sababu maua hayana uwezo bila mizizi. Ndivyo ilivyo kwa Kanisa. Kinacholisha kichwa ni mizizi au mwili wake ulio matawi yote.

Pili ni kwa sababu kutenda hivyo inavunja kanuni ya mafundisho ya Paulo. Anasema wanaohudumiwa kiroho wawalishe wale wanaowahudumia. Viongozi wale hawatakiwi kulish-wa kutokana na chombo kilicho nje. Wakilishwa kutoka nje inaleta hali isiyo nzuri. Kwanza chombo kile cha nje kitawatawala kwa sababu ndicho kinachowalisha. Pili kichwa chenyewe hakitaona sababu ya kulisha makanisa kiroho kwa sababu hakilishwi na makanisa yale. Kuna sababu nyingi zinazosema wazo hilo ni baya. Kanuni ya Paulo ndiyo inayofaa, tena ni agizo la Mungu.

• Je, mchungaji katika tawi lako anasaidiwa kiasi gani? Anaweza kuishi kwa msaada anaopewa?

• Je, tawi linafaidika na jinsi mchungaji wako anavyotunzwa au linaathirika? Linafaidikaje? Linaathirikaje?

• Je, tawi lako linawasaidia na kuwawezesha watumishi wengine kama wamishonari au wainjilisti?

Wakristo wanapaswa kujitoa kwa wahitaji

Mistari ni mingi sana inayoeleza kwamba Mungu anataka watu wake kumsaidia mhitaji ye yote.

Mithali 25:21 - “Adui yako akiwa ana njaa mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa.”

Wagalatia 2:10 - “Ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.”

Waebrenia 13:16 - “Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.”

Page 75: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 75 -

Mungu ana moyo kwa ajili ya wahitaji wote. Kama ni umaskini, ugonjwa, au shida nyingine Mungu anawataka watu wake wawasaidie. Mungu anaweza kuifanya miujiza na kumsaidia ye yote wakati wo wote, lakini katika hekima yake ameamua kuyashughulikia mambo kama haya kupitia watu wake hasa.

Mfano wa Msamaria mwema unatufundisha juu ya moyo wa Mungu. Sheria ya Musa ilisema watu wa Mungu wanapaswa kumpenda Mungu na kuwapenda majirani zao. Swali lilikuja nani ni jirani yangu? Maana, wengine waliwapenda wale ambao waliwakubali kuwa majirani zao, lakini hawakutaka kuwasaidia wengine ambao walifikiri siyo majirani zao. Labda walikuwa wa kabila lingine au dini nyingine na hivyo waliona hakuna haja ya kuwapenda. Katika mfano huu Yesu aliwafundisha kwamba jirani ni ye yote aliye mhitaji. Maana ni kwamba Mungu anatutaka tuwasaidie wahitaji bila kujali ni akina nani. Suala kuu ni hitaji, na wajibu wa Mkristo ni kuliti-miza.

Lakini kuna kanuni nyingine pia ya Biblia inayosema katika mambo kama haya Mungu an-ataka tuziangalie familia za kikristo kwanza. Sisi kama familia ni lazima tutunzane. Tena ni ushuhuda mzuri mbele ya wapagani tukionesha jinsi tunavyosaidiana katika umoja.

Wagalatia 6:10 - “Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; hasa jamaa ya waaminio.”

Warumi 12:13 - “Kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.”

Ni sawa na familia za kawaida ambazo huweza kutegemeana na kusaidiana. Kama ndugu yako ana shida atakuja kwako kama familia kwanza kabla hajaomba msaada mahali pengine. Hakika Mwili wa Kristo ni familia yenye umoja na tunatakiwa kusaidiana katika hali zote.

Lakini tuelewe vilevile kwamba tunapaswa kuwasaidia wengine ambao hawamo ndani ya familia yetu. Mistari mingi haitofautishi Wakristo na wengine. Inasema tuwasaidie wahitaji, basi. Kumbuka sisi ni chumvi na taa katika ulimwengu huu na katika kumsaidia mhitaji ye yote tunaitangaza Injili ya Mungu na yeye anapewa sifa.

Mathayo 5:16 - “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

Swali linakuja, msaada wa namna hii unapaswa kutolewa kivipi? Kwanza kutokana na mfano wa Msamaria mwema tunaelewa kwamba pale ambapo unaikuta shida unatakiwa ku-saidia kama una uwezo. Mambo kama haya, tukisema lazima yaingie katika vikao kwanza na yapitishwe, tutakuta hatumsaidii mtu ye yote. Shida na mahitaji ni mambo yanayojitokeza gha-fula mara nyingine na msaada huhitajika mara moja. Tusipozitatua shida nyingine kipindi am-bacho shida ipo tutakuwa tumepoteza nafasi ya kusaidia. Mtu akija nyumbani kwako akiwa na shida na una uwezo wa kumsaidia, inabidi umsaidie wakati ule ule kama shida yenyewe ni yenye hatari isipotatuliwa mara moja. Kufanya hivyo inampendeza Mungu kwa sababu Mungu ni mkarimu na anataka sisi tuwe wakarimu.

Ni lazima niseme pia kwamba kuna haja kuwasaidia wahitaji kikanisa kama shirika. Kanisa lina sadaka zake na ndani ya sadaka hizo (au mara nyingine waweza kufanya matoleo maalum) ni lazima kanisa lijiulize kama kuna wengine ambao ni wahitaji wanaostahili msaada aidha nda-ni au nje ya kanisa. Watu binafsi huwasaidia wahitaji na kanisa kwa ujumla linawajibika vilevile. Kama tulivyosema, lazima kanisa liangalie washirika wake kwanza katika kuwasaidia wahitaji. Pia linapaswa kuwangalia hata Wakristo wa matawi mengine. Lakini Biblia inafundisha pia wa-wasaidie hata wahitaji wasio Wakristo. Hakuna uinjilisti ulio bora kama kuonesha kwamba ka-nisa letu linamjali mtu kama binadamu na linampenda. Upendo wetu hauonekani bila matendo yanayouthibitisha.

• Kuna wahitaji gani katika tawi lako? • Kuna wahitaji gani katika kijiji au mji wako? • Eleza jinsi ulivyomsaidia mtu mwenye hitaji katika maisha yako.

Page 76: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 76 -

Wakristo wanapaswa kujitoa kwa ajili ya majengo ya Kanisa

Ni wazi kwamba majengo ya Mungu yanatakiwa kujengwa na watu wake, kama ni shule au kanisa au majengo mengine. Katika Agano la Kale tunaona jinsi Waisraeli walivyolijenga hekalu la Mungu. Hata lilipobomolewa, wenyewe wakalijenga tena. Mungu hafanyi miujiza ya kudon-dosha majengo kutoka mbinguni. Amewapa watu wake wajibu wa kuyajenga. Kama ni kuitoa mali yao au nguvu zao, yote ni juu yao kuyatekeleza.

• Je, jengo lako la kuabudia linaonesha kwamba washirika wake wanajitoa kwa kazi ya Mungu?

• Kuna mambo gani madogo yanayoweza kuboreshwa ili kuonesha washirika wanaijali nyumba ya Mungu iliyo kanisa lao?

• Kuna mambo gani makubwa yanayoweza kufanyika ili Mungu asifiwe zaidi katika jengo lako la kuabudia?

Wakristo wanapaswa kujitoa kwa ajili ya huduma za Mungu

Huduma za Mungu ni pana. Kuna mambo mengi ambayo yanahesabika katika huduma za Mungu. Huduma hizi tumepewa na Mungu. Kwa mfano tumepewa huduma ya upatanisho yaani wajibu wa kuieneza Injili.

2 Wakorintho 5:19-20 - “Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajum-be kwa ajili ya kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu.”

Ni uwakili wetu na tunatakiwa kuitekeleza kazi hii kwa uwezo wetu wote kama ni kuitoa mali yetu au kuitenda huduma sisi wenyewe. Kuna huduma za kufundisha na kuhubiri, kufanya semina na kuwasaidia wahitaji. Kuna huduma za kuwasimamia watu wa Mungu. Ni wajibu wa Kanisa kuhakikisha mambo haya yanatendeka ili watu waweze kuokoka halafu wakue katika mahusiano yao na Mungu. Huduma hizi zote zina gharama. Huduma zingine zinahitaji usafiri. Usafiri siyo juu ya mhudumu mwenyewe. Yeye anaenda kwa niaba ya kanisa. Kupitia yeye, ka-nisa linautimiza wajibu wake, hivyo wanatakiwa kushiriki katika kumwezesha. Kanisa linahitaji vifaa mbalimbali kama chaki, kalamu, daftari na bahasha. Bila vifaa hivyo kazi nyingine hazitendeki. Katika uwakili wa kanisa ni lazima kazi itendeke na hivyo ni juu ya kanisa kuhakikisha vifaa vipo vya kuzifanikisha huduma zote. Vifaa vingine ni vya muziki, au vya ku-wafundishia watoto kama vile picha. Hata kipaza sauti ni kifaa muhimu katika kuitangaza Injili.

Hatuwezi kukwepa wala kutegemea vitu hivi vitoke sehemu nyingine. Hatuwezi kukaa na kusubiri kwa sababu kila dakika tunayosubiri ni dakika nyingine ambayo hatujautimiza uwakili wetu tuliopewa na Mungu.

• Huduma zipi zinaathirika katika tawi lako kwa kukosa udhamini? • Wewe utachangia huduma gani zaidi katika utoaji wako kutokana na kujifunza kanuni za

utoaji?

MUNGU ASTAHILI VILIVYO BORA Tukumbuke jinsi tulivyoanza tukisema kwamba matoleo yote ni kwa ajili ya Mungu hasa.

Kuna hali ambayo siifurahii kuiona. Wengine wanakubali kazi ya Mungu iwe katika hali ya kuai-bika. Kama ni nyumba ya Mungu ambayo ni jengo la kanisa, hawajali ikipendeza au la. Ha-waelewi ni ushuhuda mojawapo wa jinsi tunavyomjali Mungu wetu. Sisemi ni lazima Wakristo wajenge majengo ya ajabu. Hapana, ni lazima waishi ndani ya uwezo walio nao. Lakini kuna hali nyingine ambayo haitakiwi. Mara nyingine unazikuta nyumba za washirika zipo safi; kuna bati, madirisha mazuri, sakafu ya sementi n.k. Wakati huo huo wanadai hawawezi kuyafanya mambo haya kwa ajili ya nyumba ya Mungu ambayo haina madirisha, mabenchi ni ovyoovyo, nata usafi wa mazingira unaleta ushuhuda mbaya.

Si majengo ya makanisa tu. Wakristo wengine wanajaribu kuendesha kazi ya Mungu bila vifaa vinavyotakiwa kwa sababu wamekubali kwamba siyo lazima kazi ya Mungu iwe na vifaa vilivyo bora. Wanachukia kama kazi hazitendeki lakini hawataki kujitoa ili kanisa liwe na vifaa vinavyohitajika.

Page 77: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 77 -

Kumbuka Mungu ni nani. Anastahili heshima zote na kutukuzwa. Lakini mara nyingine kwa jinsi sisi Wakristo tunavyoziendesha kazi zake naona aibu tupu.

Wakristo wengine wanasema watumishi wa Mungu wawe maskini kuliko washirika wa kawaida. Wanasema watumishi wasivae kwa jinsi iliyo bora kuliko wengine. Mawazo haya ya-metoka wapi? Si mchungaji ni mtumishi wa Mungu aliye juu ya mambo yote. Si anayo nafasi muhimu ndani ya Kanisa na amepewa wajibu mzito na Mungu. Ni sifa gani mbele ya dunia hii wakati watumishi wa Mungu hawatunzwi vizuri? Watu wanasema nini juu ya kanisa kama hilo? Na tusisahau Mungu mwenyewe anasemaje? Je, Mungu anapendezwa anapoona watumishi wake hawatunzwi wakati yeye mwenyewe ameamuru walishwe kupitia kazi hiyo. Mimi nadai kwamba watumishi wa Mungu wanapaswa kutunzwa vizuri sana kulingana na uzito wa kazi yao na wajibu wao. Wenyewe ni watumwa wa Mungu.

Kila sehemu ya kazi ya Mungu inatakiwa ionekane tumeifanya kwa ubora zaidi, tuna-vyoweza. Sisemi tujenge majengo ya ajabu. Sisemi wachungaji waishi kama matajiri. Bali nase-ma kazi za Mungu ziheshimike na tuoneshe kuzijali na kuwajali watumishi wake. Kumbuka ni jina la Mungu mwenyewe ndilo litakalosifiwa au kudharauliwa.

• Kwa nini Mungu anastahili umtolee vilivyo bora? • Eleza huduma ambayo umeiona inaendeshwa katika hali ya aibu? • Je, unaweza kufanya nini kuisaidia huduma hiyo isiendeshwe hivyo?

MUNGU APEWE KIPAUMBELE KATIKA MALI ZETU Kutoka 23:19 - “Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyum-

ba ya Bwana, Mungu wako.”

Hesabu 18:12 - “Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa Bwana...”

Mithali 3:9 - “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.”

Mistari hii inaelezea agizo la Mungu kwa watu wake Waisraeli. Kwa sababu walikuwa wakulima na wafugaji, agizo linalenga mapato ya kazi za namna hii. Mungu alitaka watoe katika yale ya kwanza. Yaani siku waliyovuna walitakiwa kumtolea Mungu kwanza. Pia tunaona walipaswa kutoa “yaliyo mazuri”. Yaani kati ya mazao yao au mifugo yao walitakiwa kumtolea Mungu sehemu iliyo bora. Hii inafuatana na kanuni tuliyoiangalia, inayosema, Mungu anastahili vilivyo bora.

Ingawa hatuko chini ya Sheria ya Musa, kanuni bado ni kweli kwetu. Kulikuwa na sababu iliyomfanya Mungu awape maagizo haya na sababu hii ni ya kweli mpaka leo. Sababu yenyewe ni kwamba tunapompa Mungu mapato yetu ya kwanza, na tena yaliyo bora katika mapato yetu, inaonesha jinsi tunavyomtegemea na kumheshimu Mungu.

Kwa kawaida watu wanamtolea Mungu baada ya kuangalia mahitaji yao kwanza. Kufanya hivyo humaanisha kwamba hawatatoa ipasavyo na hawatoi kwa kumheshimu Mungu. Mahitaji hayana mwisho. Kuna nyumba, nguo, vifaa vya kilimo, biashara, kusomesha watoto, kusaga, chakula n.k. Mahitaji hayo yote humaliza mapato yote na hakuna kinachobaki kwa ajili ya Mun-gu. Kuna ukweli kwamba watu wenye mapato ya kawaida hushindwa kutimiza mahitaji yao yote.

Lakini, kanuni ni kumtolea Mungu kabla hatujafikiria mahitaji yetu kwa kuwa tunamtegemea Mungu mwenyewe na hatutegemei mapato yetu. Kuangalia mahitaji kwanza kunaonesha kwamba mtu hamtegemei Mungu. Kunaonesha jinsi anavyofikiri anahitaji kuyakamilisha mahataji yake yeye mwenyewe. Kunaonesha anaogopa Mungu hatatimiza mahitaji yake yote, au atatimiza kwa njia asiyoipenda Mkristo huyu mwenyewe. Mwisho, ina maana mahitaji yake yamemtawala na anafikiria namna ya kuyakamilisha mahitaji yake kuliko kumheshimu Mungu (au kumshukuru na kuuonesha upendo wake kwa Mungu). Hivyo Mungu anawekwa mwisho kwa sababu mahitaji mengine ni muhimu kuliko Mungu machoni pa yule anayemtolea Mungu.

Lakini Mungu anataka tumtolee yeye kwanza, kwa sababu kufanya hivyo ni ishara kwamba tunamtegemea yeye. Ikiwa tunamtolea Mungu bila kujali wala kuyahesabu mahitaji yetu kwan-

Page 78: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 78 -

za, inaonesha kwamba tunaamini Mungu atayatimiza mahitaji yetu na anastahili matoleo yetu. Hakika, mara nyingine tutakapomtolea Mungu, tutahitaji kumpa mapato mengine ambayo tutayahitaji. Lakini kwa sababu tunamtegemea Mungu yeye ni tumaini letu tunapomtolea na ahadi ni kwamba hatutakuwa na hitaji kwa kuwa Mungu ni tegemeo letu.

Ukweli, hata kama hatujatambua, ni kwamba maisha yetu yamo mkononi mwa Mungu. Tu-pende, tusipende, tunamtegemea Mungu tayari hata tusipompa cho chote katika matoleo yetu. Ni hali halisi ya kila mwanadamu. Mungu hutupatia hewa ya kupumua, nguvu za kutenda kazi, afya, mvua kwa kilimo chetu, n.k. Yaani Mungu huwatunza wanadamu wote na bila utunzaji wake wote wangekufa, tena mapema. Mungu anataka tukubali kwamba hali hii ni kweli. Tumtolee, tusimtolee, bado tunamtegemea Mungu. Hivyo ni bora kumtolee katika hali ya utii, shukrani, upendo, na heshima, kwa kuwa tunamtegemea kwa vyo vyote vile.

Ndiyo sababu ni muhimu kumtolea Mungu mara baada ya kupata mapato kabla hatujaanza kufikiria mahitaji yetu. Hii ni kanuni ya kuifuata kama ni pesa, mavuno, au faida yo yote nyingine. Tutoe kwa Mungu kiasi tunachokusudia moyoni kabla hatujaanza kuyafikiria mengine. Kufanya hivyo kunampendeza Mungu sana.

Faida ya kufanya mara moja ni kwamba kunahakikisha matoleo yetu. Tukikaa na mapato yetu, shida nyingine hutujia, na mwisho matoleo yetu yanatumika katika mambo mengine hata kama hatujakusudia iwe hivyo. Watu wengine wanasema pesa haikai. Maana yake, pesa hutafu-ta pa kutumika. Tusipompa Mungu, zitatumika mahali pengine. Katika nchi yangu tuna usemi unaosema pesa hutoboa mashimo mfukoni. Yaani tukikusudia kutunza pesa kama akiba kwenye mfuko wa suruali zetu, tutashindwa. Si kwamba kutakuwa shimo kweli, lakini pesa zile zita-tumika na kutoweka haraka, sawa na kuziweka kwenye mfuko wenye shimo.

• Je, wewe unamtolea Mungu kwanza kabla hujafikiria mahitaji yako? • Je, wewe unamtegemea Mungu kuyatimiza mahitaji ya maisha yako? • Eleza wakati ambao hukumweka Mungu kwanza katika matoleo yako.

Page 79: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 79 -

- 10 - Kutomtolea Mungu ni Wizi

Nimeamua kutoa sura nzima kwa jambo hili ingawa halina maelezo marefu. Ni muhimu kila

Mkristo aelewe kwamba utoaji siyo mchezo. Siyo suala la hiari. Mtu hawezi kutoa au kutotoa na kufikiri yote ni sawa. Chini ya neema, Mungu amesema tutoe kwa hiari lakini Mungu mwenyewe anategemea tutatoa kwa sababu ni agizo lake. Sehemu iliyo hiari ni kiasi gani tunayopaswa ku-toa kufuatana na kadiri ya uwezo wetu. Tunapopewa uwakili inaeleweka kwamba ndani ya uwakili huo kuna wajibu. Sehemu ya uwakili wetu ni kuiendesha huduma ya Mungu kwa muda, nguvu, na mali zetu.

Paulo mwenyewe hajatoa amri ya kutoa sadaka lakini maongezi yake yote yanaonesha kwamba utoaji unapaswa kuwa jambo la kawaida katika Kanisa. Yapo maagizo ya kuwasaidia wengine, kutunza watumishi, kufundisha Neno la Mungu, kuieneza Injili, n.k. Ndani ya maagizo hayo yote inaeleweka tutahitaji kutoa muda, nguvu, akili na mali zetu ili kazi hizi za Mungu zitendeke.

Mali, muda, na nguvu tuliyo nayo vimemilikiwa na Mungu tayari. Mungu anataka tuzitumie mali zake (zetu) kwa uwakili mzuri tukiyaendesha mambo yake katika dunia hii. Kwa sababu ni mali yake tayari, tukiitumia kwa mambo yetu tu, ni wizi.

Malaki 3:8-12 - “Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na Mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.”

Katika mistari hii Mungu anaongea na taifa lake Israeli. Alikuwa amelifanya agano maalum nao kwamba atawabariki wakiitii Sheria ya Musa na atawalaani wasipoitii. Ndani ya sheria kulikuwa sadaka nyingi za lazima. Mungu alitegemea kuiendesha nyumba yake na huduma zake kwa njia ya sadaka hizo. Anasema, “Ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.” Kuwa na chakula ni alama ya hali nzuri. Chakula ni msingi wa uhai na kukua kwa vitu. Mungu alitaka sadaka zao kwa sababu zilikuwa zinaleta uhai ndani ya kazi zake.

Leo Mungu anaendesha kazi zake kwa kanuni hiyo hiyo ingawa si kwa njia ya sheria. Anategemea watu wake kutoa sadaka na kujitoa kwa ujumla. Mungu anataka tumrudishie kiasi cha mali yake (na baraka ya nguvu, muda, ujuzi n.k. alizotupa kama mawakili) kwa ajili ya huduma zake. Tusipofanya hivyo, huo ni wizi kwa kuwa Mungu ametupatia mali yake ili tujipa-tie mahitaji yetu lakini pia ili tuiendeshe huduma zake duniani.

Hakika wizi hauwezi kumpendeza Mungu. Kama wewe hutoi ipasavyo wewe ni mwizi. Wengine watauliza, basi tutoe kiasi gani? Hakuna kiasi kamili. Ni tofauti kwa kila mtu. Inategemea jinsi unavyokusudia mwenyewe kwa kadiri ya uwezo wako kufuatana na uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yako. Naomba ujiulize kama unajitoa ipasavyo. Usiwaze kuhusu kiwango fulani. Angalia tu katika moyo wako na uone kama unavyojitoa sasa hivi in-ampendeza Mungu au la. Uamue mwenyewe. Unaweza. Wengi wetu katika mioyo yetu tunajua hatujajitoa vya kutosha ingawa Mungu hajataja kiwango kamili cha kutoa. Tunaweza kujishitaki na tunapofanya hivyo ni bora tuubadilishe utoaji wetu.

Mungu ametamka wazi kwamba tusipoitumia mali aliyotupatia kwa ajili ya kazi zake, basi, sisi ni wezi. Unaweza kutojali sasa lakini siku moja utakuwa mbele ya Mungu mwenyewe na pale utatoa hesabu ya matumizi ya mali ambayo Mungu alikupa. Mungu ataamua kama wewe ulikuwa mwizi au la, yaani ataamua kama ulikuwa wakili mwema au la. Ukionekana kuwa mwizi ujue kuna baraka na thawabu nyingi ambazo utakosa. Ni mjinga tu anayefikiri anaweza kumwi-

Page 80: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 80 -

bia Mungu bila kukamatwa. Kumbuka hukumu haihusu kipindi cha kufika mbinguni tu. Sasa hivi katika maisha yako Mungu anazuia baraka au hata kutoa adhabu wakati unaiba kwake.

Ujilinde. Usije ukaonekana kuwa mwizi. Fuata moyo wako katika utoaji ukiwa unamshukuru Mungu kwa yote aliyokupa.

• Je, unayo haja ya kutubu kwa kuwa hujajitoa ipasavyo kwa Mungu?

- 11 - Faida ya Utoaji Ulio Bora

Mungu wetu ni wa ajabu. Sisi kama watu wa dunia hii hatustahili kitu cho chote kwake.

Yote tunayopewa naye ni kwa neema yake. Mungu angeweza kutuagiza kutoa sadaka bila faida yo yote kwetu. Angeweza kusema ni amri tu. Lakini kwa sababu Mungu ni mwenye neema na ukarimu ameamua kutubariki wakati tunatoa. Kuna faida nyingi zinazotokana na utoaji wetu. Baraka hizi zinaweza kuwa mvuto wa kutuvuta kujitoa ipasavyo.

Kujitoa kwetu kunawatia moyo wengine kujitoa

2 Wakorintho 9:2 - “Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa ajili yenu kwa Wamake-donia, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi wao.”

Wakorintho walikuwa tayari kujitoa na hivyo walijitangaza juu ya kusudi lao la kusaidia. Ilipojulikana hivi wengi wao waliamua kujitoa. Inawezekana wale wengine wasingejitoa lakini kwa sababu ya mfano wa wengine walipata wazo na moyo wa kufanya hivyo.

Tujue faida moja tutakayopata tukijitoa ni kwamba tutawafanya wengine wajitoe kwa hiari yao pia. Tujitahidi kuwa wa kwanza. Mara nyingi watu wako tayari kujitoa lakini hawataki kufanya peke yao. Hawataki kulibeba Kanisa peke yao na hivyo wanasubiri waone kama wen-gine watatoa kwanza. Shida ni kwamba ni lazima mmoja awe wa kwanza. Kila mmoja wetu aamue kuwa wa kwanza tukijua kwamba tutaleta faida kuwafanya wengine waanze kujitoa.

• Je, unaweza kuwa wa kwanza kujitoa au wewe husubiri wengine kuanza kutoa kabla hu-jatoa?

• Eleza jinsi utoaji wa wengine umekutia moyo wa kujitoa katika maisha yako.

Kujitoa kwetu kunaleta shukrani kwa Mungu

2 Wakorintho 9:11-12 - “Mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii wa-takatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.”

Ni kweli sadaka zetu zinawasaidia watu wengine kama vile watumishi wa Mungu au wa-hitaji. Pale ambapo watu wanasaidiwa ndipo Mungu anaposhukuriwa. Hata sisi tunaotoa msaada hushukuriwa lakini inaeleweka kwamba matendo yetu mema yanaleta sifa kwa Mungu hata tusiposhukuriwa sisi. Ni Mungu anayetenda ndani ya mioyo ya watu ili waweze kujitoa, na wanapojitoa, watu humshukuru Mungu.

Kujitoa kwetu kunasababisha wengine kutuombea

2 Wakorintho 9:14 - “Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu.”

Faida nyingine ni kwamba watu watatuombea. Katika kuwasaidia, tutapendeza machoni pao na zaidi majina yetu yatabaki katika fikra zao. Kwa hali hii ni lazima watatukumbuka wakati wanapoomba. Kwa sababu tumewasaidia watamwomba Mungu atusaidie vilevile.

Page 81: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 81 -

Kujitoa kwetu kunaleta sifa kwa Mungu

2 Wakorintho 9:13 - “Kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.”

Kusudi letu kuu katika dunia hii ni kumtukuza Mungu. Kila siku maisha yetu yanatakiwa yalete sifa kwa Mungu. Biblia inasema utoaji wetu ni njia mojawapo ya kumtukuza Mungu. Kwanza kutenda kwetu kunamtukuza Mungu kwa sababu kunakubali kwamba Mungu anastahi-li sadaka zetu na pia kunatangaza kwamba tunamtegemea Mungu. Pili wengine wanaouona uto-aji wetu, au wanaosaidiwa na utoaji wetu, watamtukuza Mungu.

Kujitoa kwetu huleta baraka katika maisha yetu leo hii

Wagalatia 6:7-10 - “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tu-patavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”

Kuna kanuni iliyowekwa na Mungu ambayo tunaweza kuitegemea. Kanuni yenyewe inasema tutavuna tulichopanda. Shida ya kanuni hii ni kwamba tukipanda yaliyo mabaya tutavuna yaliyo mabaya. Inategemea tunavyopanda. Kanuni hii inaangalia hata utoaji wetu mbele ya Mungu.

Mithali 11:24-25 - “Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.”

Mithali 21:13 - “Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.”

Mithali 28:27 - “Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.”

Mithali 3:9-10 - “Mheshimu Bwana kwa mali yako, na Kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.”

Luka 6:38 - “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”

2 Wakorintho 9:6 -11 - “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote...”

Tazama ahadi zote katika mistari hii. Kuna faida katika kujitoa kwa uaminifu. Katika Wako-rintho Paulo anaongelea utoaji. Anasema kanuni ya kupanda na kuvuna inahusu pia utoaji. Anaonesha ahadi kwamba tukipanda kwa ukarimu tutavuna kwa ukarimu. Ni Mungu anayetupatia mavuno haya. Paulo anasema Mungu anaweza kutujaza kila neema kwa wingi. Haya ndiyo mavuno yenyewe. Tazama jinsi ni mavuno ya leo hii, siyo tusubiri mpaka tufike mbinguni. Baraka ya kwanza ni kupata riziki zetu. Lakini ni zaidi ya riziki. Anasema Mungu ni mwenye kuzizidisha kiasi kwamba tutakuwa tumetajirishwa katika vitu vyote.

Swali linakuja, baraka hizi zinakuwaje? Je, ina maana tukitoa pesa tutavuna pesa? Jibu ni kwamba ni juu ya hekima ya Mungu kuamua. Kwa vyovote vile baraka za Mungu ni za kweli. Baraka zenyewe zinaweza kuwa mambo mengi. Kwanza ni mahitaji yetu au riziki. Pili kuna njia

Page 82: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 82 -

nyingine nyingi ambazo Mungu anaweza kuzitumia katika kutubariki. Mara nyingine ni mali. Ndiyo sababu anasema, “Mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote.” Mungu anaweza kuongeza mali yetu akiwa na kusudi tuwakirimu na wengine. Pengine badala ya kutupatia mali Mungu atatulinda tusipate kuugua. Magonjwa yanakula mali nyingi. Anaweza kuziondoa shida mbalimbali katika maisha yetu. Anaweza kutubariki kwa kutupatia amani nda-ni ya familia yetu. Anaweza kutufanikisha katika kazi zote tunazozitenda. Tusimbane Mungu katika baraka moja, yeye anazo baraka za kila namna na anajua ni baraka gani ambayo itatufaa zaidi.

Malaki 3:10 - “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkani-jaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbingu-ni, na kuwamwagieni baraka, isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

Mungu ana tabia ya kupenda kutubariki katika maisha yetu. Tena anapenda kutubariki kwa wingi. Ndiyo faida mojawapo tuliyo nayo katika kujitoa kwake.

• Je, unaamini kweli kweli Mungu ana nia ya kukubariki? • Taja njia mbalimbali ambazo Mungu amezitumia kukubariki.

Kujitoa kwetu kunafanikisha kazi ya Mungu

Huwa tunalalamika wakati tunapoona kazi za Mungu zimelala. Kwa mfano mara nyingine tunaona hakuna makanisa yanayojengwa, hakuna watu wanaookoka, au hakuna watumishi wanaotumika. Sababu moja inayosababisha hali hii ni kutojitoa kwa watu wa Mungu. Pamoja na watu wenye moyo wa kufanya kazi ya Mungu, pia mali inahitajika. Bila mali ni vigumu kwenda mbali. Kama sisi tunataka kuiona kazi ya Mungu ikiwa inaendelea, tuwe tayari kujitoa pia kwa mali zetu.

• Je, umewahi kulalamika kwamba kazi ya Mungu haiendi? • Je, ulijitoa ipasavyo kwa ajili ya huduma hizo?

Kujitoa kwetu kunatuwekea hazina mbinguni

Kama tulivyoona, kuna baraka za Mungu katika maisha yetu ikiwa tutajitoa. Lakini ziko baraka kwa ajili ya baadaye pia. Tena na tena Mungu anaongelea jinsi atakavyowapa thawabu wale waliokuwa waaminifu. Yote inategemea jinsi tunavyotenda wakati tunaishi katika dunia hii. Tunaweza kujiwekea hazina katika dunia hii au mbinguni.

Luka 12:33 - “Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.”

1 Timotheo 6:18-19 - “Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; Huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri wa wa-kati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.” Kujitoa kwetu kunampendeza Mungu

Waebrenia 13:16 - “Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.”

Tunapotenda mema na kusaidiana kwa hali na mali, Mungu anafurahi. Hakuna faida iliyo bora kuliko kumpendeza Mungu.

Kujitoa kwetu kunaleta ushirika unaofaa

Kanisa lenye uwakili mzuri ni kanisa lililo hai. Ni kanisa lenye afya nzuri inayopendeza. Katika kanisa lenye uwakili mzuri kuna furaha na kuna utekelezaji wa kazi ya Mungu. Watu hu-penda kujiunga na kanisa kama hilo. Kuna ushirikiano katika mambo yote. Hiyo ni faida ya ku-jitoa kwetu.

Kila mtu anataka kusali katika kanisa linalofurahisha. Wanataka kushiriki katika kazi am-bayo inasifiwa kuwa ni kazi iliyo bora. Wanapenda kushirikiana na watu wanaopendana, walio tayari kusaidiana.

Page 83: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 83 -

Je, unataka kanisa lako kuwa katika hali hii. Pamoja na mambo mengine utoaji mzuri una-weza kuleta hali hii.

• Faida za utoaji ni nyingi. Kati ya hizo tulizotaja ni ipi inayovuta moyo wako zaidi kujitoa? • Je, unaweza kutaja faida nyingine za utoaji ambazo hatukutaja hapo juu?

- 12 -

Kupanga Utoaji Wetu Kawaida ya watu ni kutumia pesa au mapato yao bila mpango kamili. Siku ambayo tunapata

mapato tunaanza kuwaza namna ya kuyatumia mapato yale mara moja. Kwa njia hii matumizi yake yanaweza kuwa mazuri au mabaya kwa kubahatisha. Kwa kawaida kitu kinachotuvutia zaidi kitagharimiwa kwanza ingawa inawezekana kuna mambo mengine yaliyo muhimu zaidi. Ukweli ni kwamba pesa hazikai. Hivyo, ukosefu wa mpango husababisha pesa zitumike ovyo.

Watu hujikuta katika shida ndani ya maisha yao kwa sababu hawana mpango mzuri. Ha-wajaangalia jinsi wanavyoitumia mali yao na hivyo wakati shida ya dharula inajitokeza wanashindwa kuitatua.

Hii ni kweli kwa watu wenye mapato makubwa na wenye mapato madogo. Wenye mapato makubwa wanaweza kuyamaliza mapato yao kwa haraka wasipokuwa na mpango sawa na wengine.

Sura hii ina kusudi la kutusaidia kujua namna ya kuyapangia matumizi mapato yetu kwa njia ambayo itampendeza Mungu.

Tutunze kumbukumbu ya mapato yetu

Ili tuweze kupanga vizuri ni lazima tuyaelewe mapato yetu. Wengi wetu hatujui tunapata kiasi gani. Kwa kawaida tunafikiri mapato yetu ni madogo kuliko yalivyo. Hii ni kwa sababu hakuna wakati ambao tuna pesa nyingi mfukoni. Lakini mapato yanaingia na kutoka kila wakati. Cha kufahamu ni kiasi gani kinachoingia.

Tunaposema mapato tunamaanisha cho chote kinachoingia kwetu chenye thamani. Inawe-za kuwa pesa, mazao, au mali nyingine. Yote hayo ni mapato yetu.

Ni muhimu kuyafahamu mapato yetu kwa sababu ndiyo msingi wa uwakili wetu katika mali ambayo Mungu ametukabidhi. Tunajitoa kwa kadiri ya uwezo wetu, lakini kama hatujui uwezo wetu, tutashindwa kujitoa ipasavyo.

Nimewahi kufundisha wanafunzi katika shule ya Biblia kuhusu kutunza vitabu vya mahe-sabu. Nilipowauliza kuhusu mapato yao wakadai ni madogo sana. Wakasema hakuna wakati ambao wanaweza kuwa na zaidi ya 500 tsh mfukoni. Tulianza kuorodhesha matumizi yao. Nili-walazimisha kuandika kila kitu wanachogharimia kwa mwezi. Wakaanza kuandika mambo ka-ma: kusaga, viberiti, mafuta ya taa, sabuni, mboga, chumvi, mafuta ya kupikia, chai, sukari, kal-amu, mavazi, ada, sadaka, madaftari, n.k. Tulikuta kwa wastani kila mwanafunzi alikuwa anagharimia angalau 10,000 kwa mwezi (ilikuwa mwaka 1995). Wenyewe walishangaa na wa-lishindwa kuelewa pesa hizi zilitoka wapi kwa kuwa walikuwa wanafunzi. Lakini walikuwa na ushahidi na ikabidi wakubali kwamba pesa hizo zilikuwa zinaingia mifukoni mwao kila mwezi.

Kama tunataka kuwa waaminifu mbele ya Mungu inatupasa kutunza kumbukumbu za mapato yetu. Inaweza kuchukua mwaka mzima kabla hatujapata picha kamili ya mapato yetu yalivyo, hasa kwa wasio na mshahara wa wiki au mwezi.

Ni vizuri kuandika thamani ya vitu katika pesa ili tuweze kuhesabu. Kwa mfano tunapovuna mahindi kama tulipata gunia 6, tuandike kwenye kumbukumbu zetu thamani ya mahindi katika kipindi kile cha mavuno. Kama gunia moja katika kipindi kile ni shilingi 30,000, tungeandika mapato yetu kuwa ni shilingi 180,000. Tukila mahindi hayo njiani, thamani yake katika kum-bukumbu zetu inabaki katika mapato ya kiasi kile. Lakini baadaye tukiuza gunia moja kwa shilingi 60,000 ina maana mapato yetu yameongezeka kiasi cha shilingi 30,000. Ni lazima sasa

Page 84: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 84 -

tuingize shilingi 30,000 hizo katika kumbukumbu zetu kwa kuwa tumefaidika jumla ya shilingi 60,000 sasa.

Hata vitu vingine tunapaswa kuingiza kwenye kumbukumbu zetu. Labda tunayo bustani na tunayatumia mazao yake kwa chakula chetu. Kama ni vitunguu au nyanya, yote ni mapato. Tus-ingelima ingebidi tununue mboga hizo kwa pesa. Hivyo ni muhimu kuandika thamani za vitu hivyo ndani ya madaftari yetu. Pengine tumepewa kitu na mtu mwingine. Labda ndugu yetu ametupa baiskeli ya zamani. Tukio kama hilo ni baraka kutoka mikononi mwa Mungu na ni se-hemu ya mapato yetu. Tutunze thamani yake katika kumbukumbu zetu. Baada ya kutunza kumbukumbu kwa muda tutaweza kupanga vizuri zaidi utoaji wetu na hata maisha yetu ya baadaye.

• Chukua karatasi na utaje aina za mapato uliyo nayo katika maisha yako ndani ya mwaka mmoja.

Tutunze kumbukumbu ya matumizi yetu

Tunapata pesa na mali kwa njia nyingi. Mara nyingi tungeshangaa kiasi gani tunachokitu-mia kugharimia mambo mengine. Tunafikiri hatuna matumizi mengi lakini tunapoanza kutunza kumbukumbu tutashangaa jinsi vitu vingine vidogo vidogo vinavyokula pesa.

Matumizi ni ya namna mbalimbali. Mengine ni ya lazima na mengine ni ya kujifurahisha tu. Ni muhimu tujue jinsi tunavyozitumia pesa zetu. Ni muhimu tupange kuzitumia kwa ajili ya mambo yaliyo ya lazima kwanza, au sivyo tutakuta pesa zimekwisha katika mambo yasiyo ya lazima na tumebaki katika shida kubwa.

Chukua daftari na anza kutunza kumbukumbu za matumizi yako. Kila kitu unachotoa kama pesa, au mali nyingine kama mazao, lazima uandike ili uone jinsi unavyoyaendesha maisha yako.

Ukifanya hivyo utaweza kujua yale yaliyo ya lazima yanachukua kiasi gani. Pia utaweza kujizuia na mambo mengine yasiyo ya lazima kwa kujua mahitaji mengine yapo na mapato yanakomea wapi.

Bila kujua mapato na mahitaji na kupanga kufuatana na hali halisi, tutaanza kuingia katika madeni kwa sababu ya ulazima wa vitu vingine. Hata madeni yenyewe tutashindwa kuyalipa na tutaonekana kuwa watu wasio waaminifu. Tuishi kulingana na uwezo wetu

Wivu na tamaa ni adui wa kanuni hii. Mungu anataka tutosheke na hali tuliyo nayo. Shida ni kwamba wengi wanatamani walivyo navyo wengine na wanataka kuvipata, ingawa uwezo ha-wana. Tunatofautiana katika uwezo na bidii yetu. Mwingine anaweza kuwa na nyumba ya bati na mwingine hapana. Mwingine anavaa vizuri kila wakati, mwingine hawezi.

Wafilipi 4:11-13 - “Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi, na kupun-gukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”

Pale ambapo mtu hajaridhika na hali yake na uwezo wake, hupata matatizo. Ataanza kununua vitu anavyotaka wakati hana uwezo. Ataingia katika madeni asiyoyaweza. Mwisho ataanguka na zaidi ataipeleka familia yake kwenye shida. Watakosa mahitaji yao waliyozoea kuyapata na hivyo hawatakuwa na amani nyumbani kwao.

Labda wengine wanaweza kujizuia wasigharimie vitu vingine, lakini bado wataishi bila amani mioyoni kwa sababu hawajatosheka na yale waliyo nayo.

Mungu anataka tuweze kuishi ndani ya uwezo wetu na kumtegemea yeye ambaye anatuwezesha.

Tusijiingize kwenye madeni

Warumi 13:8 - “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana.”

Neno la Mungu husema kwamba madeni ni mabaya. Mungu hapendezwi na madeni kwa sababu ya uharibifu wake. Binafsi, naamini kwamba Neno la Mungu halijatoa amri ya kusema

Page 85: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 85 -

haiwezekani kukopa madeni, bali linatoa onyo kali linayoonesha kanuni inayofaa. Yaani, kanuni ni kwamba tusiingie katika madeni kwa sababu kwa kawaida matokeo yake ni mambo mabaya.

Kwanza, sababu yenyewe ya kuingia katika madeni inamsikitisha Mungu. Kwa kawaida inamaanisha mtu hajatosheka na maisha yake aliyo nayo. Anataka kuishi kwa namna ambayo inazidi uwezo wake. Mungu hawezi kuifurahia hali hii.

Pili, hata kama mtu ameingia katika deni kwa nia nzuri mara nyingi inamwangusha katika maisha yake na wajibu wake mbele ya Mungu. Ndivyo madeni yalivyo.

Hata kumdhamini mwingine aingie katika deni ni mbaya kama huna uwezo.

Mithali 22:26-27 - “Usiwe mmoja wao wapanao mikono; au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; kwani akuondolee kitanda chako chini yako.”

Ndiyo kusema tuishi ndani ya uwezo wetu. Kama tutaingia katika deni kwa sababu hatuna uwezo sasa hivi, tujue baadaye tusipokuwa na uwezo hata kitanda chetu kinaweza kuchukuliwa.

Sababu za ubaya wa madeni ni nyingi. Tuangalie sababu nyingine ili tuweze kupata hofu ya kutosha kutoingia katika madeni.

1. Madeni yanasababisha utumwa.

Mithali 22:7 - “Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.”

Unapoingia katika madeni ni lazima uyalipe. Kama hukuwa na uwezo wakati wa kukopa kwa sababu ya mahitaji mengine, ujue mahitaji mengine yatakuwepo baadaye pia na unaweza kushindwa kulipa madeni hayo. Kwa sababu hii utakuwa mtumwa wa deni lile. Itabidi uanze kutafuta mbinu za kulimaliza. Deni lenyewe litaanza kukutawala mpaka ulimalize. Utakapoenda kanisani hutaweza kutoa sadaka kwa sababu hata deni hujalimaliza bado.

Mungu alisema huwezi kutumikia mali na Mungu. Kuingia katika madeni ni kuitumikia ma-li. Ndiyo sababu ni mbaya. Tunapaswa kuwa watumwa wa Mungu na siyo wa madeni.

Nehemia 5:3-5 - “Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa. Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme, kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu. Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Tunawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu.”

Wakati wa Nehemia wengine walivuna walichopanda. Waliingia katika madeni, tena kwa sababu zilizo nzuri kama njaa, na mwishowe wakawa watumwa. Mpaka hata binti zao wali-chukuliwa katika hali ya utumwa kama malipo ya madeni. Wala hawakuweza kuwakomboa kwa sababu hata mashamba yao yalichukuliwa kwa sababu ya madeni hayo.

Hali hii ilitokana na kutopanga vizuri juu ya mahitaji yao. Wakati wa njaa walikuwa hawaja-jiandaa. Mwisho walivuna ubaya wa madeni.

2. Madeni unamwambia Mungu hutaki kumtegemea kukupa unachohitaji katika wakati wake.

Kama tulivyoangalia hapo juu, tunapaswa kutosheka na hali tuliyo nayo. Tunapaswa kumtegemea Mungu na kumsubiri atupatie kulingana na mawazo yake. Tunapomwahi Mungu yeye hafurahi na sisi tunaingia katika shida.

3. Madeni ni mabaya kwa sababu hujui kinachokuja kesho.

Yakobo 4:14 - “Walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.”

Watu wengi wanaingia katika madeni wakiwa na mpango mzuri wa jinsi watakavyoyalipa. Kitu ambacho wamesahau ni kwamba hawajui kitakachotokea kesho. Labda kutakuwa ma-gonjwa au msiba. Labda hali ya hewa itakuwa mbaya na hawatapata mavuno kwa kiasi wali-chokitegemea. Labda wataibiwa. Huwezi kujua, na ndiyo sababu madeni ni mabaya. Wakati mi-pango yako inaanguka bado unadaiwa. Bado ni lazima utafute njia ya kulipa.

Page 86: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 86 -

2 Wafalme 4:1 - “Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.”

4. Madeni yanazuia mtu asiyafuate mambo ya Mungu.

Bila madeni mtu yuko huru kumtumikia Mungu na muda wake pia na mali yake. Mtu huyu anajitawala na anaweza kufanya uamuzi wo wote ule. Lakini akishaingia katika deni anatawali-wa na mwingine mpaka wakati atakapomaliza deni hilo. Kwa mfano unaweza kupata deni la 5,000 tsh na kukubali kulimaliza deni hilo tarehe 30. Katika kujitahidi labda umeweza kufanya biashara na tarehe 29 umezipata shilingi 5,000 hizo za kulipia deni lako. Sasa kwa sababu ya deni inabidi umpe zote 5,000 tarehe 30. Mapato mazima yalikuwa 5,000 tu. Ndani ya mapato haya ni wajibu wako kumtolea Mungu lakini huwezi kwa sababu ya deni hilo. Hata ukikutana na mhitaji wakati unaenda kulipa deni huwezi kumsaidia kwa sababu huitawali mali yako, bali inatawaliwa na mwingine.

5. Madeni yanaondoa amani nyumbani.

Hakika madeni yanaweza kuleta ugomvi nyumbani. Kuwa na madeni humaanisha unataka kupata kitu ambacho huna uwezo nacho. Pengine ni shida ya kipindi tu, na kwa sababu hii unaamua kuingia katika deni kwa kujua utakuwa na uwezo baadaye. Shida inatokea wakati mahitaji yanapokosekana nyumbani. Ndipo ugomvi huanza. Hasa kama ukosefu wa mahitaji umesababishwa na deni ulilo nalo. Wakati unadaiwa na mwingine, na ni lazima umlipe, na kati-ka kumlipa unakosa mahitaji, ugomvi utakuwepo. Mke anaweza kumlaumu mume kwa ku-waingiza katika deni hata kama kipindi kile alilikubali deni hilo.

6. Madeni huvunja urafiki.

Wengi wanaingia katika deni halafu wanaposhindwa kulilipa deni hilo wanaanza kumkwepa yule aliyewakopesha. Mara nyingi ni marafiki ambao wanakopeshana. Mara nyingine, wakati rafiki anashindwa kulipia mkopo wake shida inaanza kati yeye na rafiki yake. Aliyekopesha anaanza kuona mashaka juu ya uaminifu wa rafiki yake. Na mwenye deni anaona aibu anaposhindwa kutimiza ahadi yake hivyo anaanza kumkwepa rafiki aliyemkopesha. Mwi-sho urafiki unavunjika. Hasara moja kubwa ya madeni ni jinsi yanavyotutenganisha na marafiki yetu.

7. Madeni yanampa Mkristo na Mungu wake sifa mbaya.

Kutomaliza madeni yetu kwa wakati wake hujulikana kwa wengi. Ni kwa sababu aliyetu-kopesha huanza kusambaza habari juu yetu tunaposhindwa kulimaliza deni letu. Kwa njia hii jina la Kanisa na jina la Mungu huchafuka. Tupende, tusipende, sisi ni wajumbe wa Mungu na matendo yetu yote yanaleta sifa kwa ajili ya Mungu, ikiwa sifa nzuri au mbaya.

Tupange utoaji wetu pamoja na familia yetu

Utoaji na uwakili ni mambo ya kifamilia. Ni juu ya baba kama kichwa cha familia kuongoza, lakini ni vema wote wachangie mawazo kuhusu utoaji wa familia ile. Wote wanaguswa na jinsi bajeti itakavyopangwa. Kama uamuzi ni kutoa zaidi kwa Mungu na kupungukiwa mahitaji men-gine inafaa wote wajue na kukubali. Maana ni wote watakaouona ugumu wa kukosa mahitaji. Kama wote wamekubali hali hii, Mungu atawashukuru na amani itatawala nyumba ile.

Kuna faida nyingine pia. Ukipanga matoleo yako pamoja na watoto wako, wenyewe wataji-funza mapema maisha ya kumtolea Mungu. Wataona jinsi ninyi, kama wazazi, mnavyomhesh-imu Mungu kwa mali yenu. Ni vema hata watoto kufundishwa kumtolea Mungu mapato yo yote wanayoyapata hata katika utoto wao. Tuamue kumtolea Mungu tunavyokusudia

Tukishaingiza mapato, ndiyo wakati wa kuamua jinsi tutakavyomtolea Mungu. Kumbuka hakuna kiasi kilicho cha lazima bali ni jinsi tunavyokusudia chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu. Pale pale mapato yanapoingia ni vema kutoa shukrani kwa Mungu na kuamua jinsi tutakavyomtolea ndani ya mapato yale.

Page 87: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 87 -

Wengine wataamua asilimia fulani ya kila pato watakalopata. Hivyo, matoleo yao ni tofauti kila wiki kutegemea na mapato yao ndani ya wiki ile. Wengine wataamua kutoa kiasi fulani kila wiki kulingana na jinsi wanavyoelewa mapato yao kwa mwaka. Kwa jinsi hii hawaangalii mapato ya wiki ile, bali wanatoa kiasi kile kwa imani. Hawajui jinsi watakavyopata kiasi hicho kila wiki lakini wamekusudia moyoni kufanya hivyo, na wanamtegemea Mungu kuwasaidia kui-timiza ahadi yao.

Tuwe na akiba ndani ya mpango wetu

Wengi wanaishi bila kuweka akiba yo yote pembeni. Ndiyo sababu wakati kuna jambo la dharura wanashindwa. Kama ni ugonjwa au jambo jingine wanakosa uwezo wa kuimaliza shida hiyo peke yao. Kanuni nzuri ni kuweka akiba angalau kila wakati tunapopata mapato. Najua mahitaji yanazidi, lakini hata tukiweka kiasi kidogo pembeni kila wakati, baadaye itakuwa kiasi cha kutosha kwa ajili ya mambo mengine ya dharura.

Ni vizuri vilevile kuweka kiasi pembeni kila wakati kwa ajili ya uzee wetu. Siku moja hatutaweza kufanya kazi na ni vizuri tuweze kuzifikiria siku hizo.

Ugumu ni uwezo wa kujitawala. Wengine wakianza kuweka pesa pembeni wanaona ugumu kutozigusa pesa zile kwa ajili ya mambo mengine. Wakati mfuko unapoongezeka watu huanza kuyafikiria mambo mengine ambayo siyo ya lazima. Wakizitumia, watapata shida wakati wa dharura.

Tuamue yaliyo ya lazima

Ni muhimu katika maisha kwa familia nzima iweze kuamua ni mambo gani yaliyo ya lazi-ma. Kwanza kuna mahitaji ya msingi. Ni lazima haya yakamilishwe kwanza. Ni mbaya kuanza kugharimia vitu visivyo vya lazima wakati hatujamaliza yaliyo ya lazima kwanza. Kufanya hivyo ina maana tutashinda kuyakamilisha mahitaji yaliyo ya lazima.

Baada ya kupanga yaliyo ya lazima ni vizuri ndani ya familia tukubaliane kuhusu yale tunayoyataka. Hakika hatuwezi kuyatimiza yote tunayotaka, kwa hiyo ni lazima tuyachague yale tutakayoyalenga kwanza. Pengine tunataka kununua baisikeli, lakini pia tunataka kupata simu mpya. Kama hatuna uwezo kuvipata vyote viwili tutalazimika kukichagua kimoja na kukiacha kile cha pili mpaka baadaye. Tukikubaliana kama familia itafaa kwa sababu wote tutakuwa na lengo moja tukijitahidi kulitimiza.

Page 88: UJITOE KABISA · wake, nguvu zake, au akili yakeMimi sitafuti kitu kwako. . Sitafuti kufaidika mwenyewe kutoka- ... sababu wanafikiri viongozi watazitumia sadaka zao kwa ajili ya

- 88 -

- 13 - Mwisho

Mwisho ningependa kukukumbusha kwamba suala la utoaji na uwakili linakulenga wewe.

Katika kitabu hiki nimejaribu kuonesha jinsi gani utafaidika mwenyewe ukiwa wakili mwema mbele ya Mungu. Ni kweli kuna faida kwa wengine pia, kama vile watumishi na Kanisa lenyewe, lakini nataka ukumbuke jinsi jambo hili ni kati ya wewe na Mungu.

Kumbuka kwamba Mungu anataka wewe kuwa na raha ya kweli katika maisha yako kama vile na wewe mwenyewe unavyoitaka raha ya kweli. Lakini ili uipate raha ya kweli inakupasa kuyafuata maagizo ya Mungu. Yeye anao mpango unaohusu maisha yako na ni lazima uishi nda-ni ya mpango huo ili uipate raha ya kweli katika maisha yako.

Kuna vitu vitatu hasa ambavyo vinaweza kukuzuia usiwe wakili mwema anayejitoa ipasavyo. Kwanza ni hali ya kutaka kuyaendesha na kuyatawala maisha yako wewe mwenyewe. Ukiukataa utawala wa Mungu na mapenzi ya Mungu ujue utaikosa raha ya kweli.

Pili ni kukosa imani. Tumejifunza mambo mengi kuhusu Mungu. Tumeona jinsi yeye atakavyokutunza katika maisha yako na kukubariki. Tumeona jinsi raha ya kweli ni karama kutoka kwake. Tumeona atakayemtegemea Mungu hatakuwa mhitaji. Lakini mambo haya ya-nategemea imani yako na jinsi utakavyoweza kumtegemea Mungu.

Tatu ni kutokuwa na shukrani. Tumejifunza kwamba Mungu amekuumba na amekumiliki. Tumeziona baraka nyingi ambazo anakufanyia. Bila yeye usingeweza hata kuishi. Moyo wa shukrani unatakiwa. Bila shukrani huwezi kuwa wakili mwema, wala huwezi kujitoa ipasavyo, tena hutaona raha ya kweli katika maisha yako.

Usilichukue wazo la kwamba Mungu anataka pesa zako tu. Mungu anataka zaidi ya pesa zako (ambazo tulijifunza ni mali ya Mungu tayari). Mungu anakutaka wewe. Anaitaka kila se-hemu ya maisha yako: muda wako, mali yako, mwili wako, akili yako, nguvu zako, n.k. Wewe ni mjumbe wa Mungu katika dunia hii na anataka umtumikie yeye katika huduma zake, familia yako, kijiji chako na zaidi. Mungu anataka ujitoe kikamilifu. Mungu anataka usimnyime hata se-hemu ndogo.

Wakati Mungu anaomba ujitoe hivyo anatoa ahadi zake. Unaweza kuyafuata maagizo na ushauri wake kwa sababu tayari ameahidi kukubariki. Mungu anakusudia mambo mengi ya-nayokufaa katika maisha yako. Mungu hataki kukunyima hata kitu kimoja kilicho chema am-bacho amekiandaa kwa ajili yako. Mungu ni mwaminifu na atakupa mahitaji yako na zaidi. Baraka na ahadi hizo hukuweka huru kujitoa kwake bila hofu ya kukosa yaliyo bora katika mai-sha yako. Kuna faida kubwa katika kumfuata Mungu na kuyatenda mapenzi yake kwa ajili ya maisha yako.

Lakini neno la mwisho ni kukukumbusha Mungu anastahili utoaji wako. Sababu kuu ya utoaji wako kwa Mungu siyo kufaidika wewe mwenyewe. Faida unazopata zinakuweka huru kumtolea Mungu ipasavyo. Ndiyo kusema jinsi Mungu anavyotanguliza kukutunza na ku-kubariki inakuwezesha kumtolea. Si kwamba unamtolea ili akutunze na akubariki. Ndiyo saba-bu Mungu astahili utoaji wako.

Ni ombi langu kwamba Mungu atakubariki zaidi na zaidi wakati unazitekeleza kanuni za Biblia ulizojifunza katika kitabu hiki!