upande 1.0 bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. kama kufanya kazi nje ja mji...
TRANSCRIPT
Upande 1.0
Bajeti yako
Bajeti (Budget) ni muhustari wa njisi wewe (na familia yako) mnavyopata na kutumia pesa. Inaunganisha pesa zinazoingia nyumbani kwako (Kipato/
income) na zile unazotumia (matumizi/expenses). Siyo lazima Bajeti iwe sawa na pesa unazozipata na kuzitumia kutokana na hizi nambari kubadilika. Bajeti
yako inapaswa kuwa lengo unalojiwekea ambalo unajitahidi kwenda sambamba nalo.
Kwa nini ni muhimu kuwa na bajeti?
Inakusaidia kutambua ni wapi utumie pesa zako Inakusaidia kuamua unavyotumia pesa zako katika siku za mbeleni
Inakusaidia kutunza pesa zako
Inakuweka katika nafasi ya kuzuia pesa zako
KIPATO
Orodhesha sehemu zote kiapato chako kitatokea kwa mwezi ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango vya pesa baado):
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
_________________________
2
MATUMIZI Matumizi (Expenses) ni vitu vyote vinavyokulazimu kutumia pesa zako. Zipo
aina mbili za matumizi: Fixed Expenses (Matumizi yasiyobadilika) na Flexible Expenses (Matumizi yanayobadilika). Matumizi yasiyobadilika ni yale
yasiyoweza kubadilika mwezi hadi mwezi. Matumizi yanayobadilika ni matumizi yale unayoweza kuyabadilisha ikibidi kufanya hivyo. Viwango vya pesa
unavyotumia katika matumizi yanayobadilika vinaweza kuwa tofauti kila mwezi.
Matumizi yasiyobadilika Tengeneza orodha ya matumizi yasiyobadilika utakayokuwa nayo mwezi
ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango baado). Kumbuka kwamba matumizi yasiyobadilika ni yale yasiyotofautiana mwezi hadi mwezi.
KODI______
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
3
Matumizi yanayobadilika Tengeneza orodha ya matumizi yanayobadilika unayoweza kuwa nayo
mwezi ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango baado). Kumbuka matumizi
yanayobadilika ni yale unayoweza kuyazuia aidha kwa kutotoa pesa au kwa kutumia pesa kiasi.
MAHITAJI vs. MATAKWA
Ni muhimu kuweza kuelezea tofauti kati ya mahitaji (Needs) na matakwa (Wants). Mahitaji ni kitu ambacho ni LAZIMA uwe nacho. Mifano ya
mahitaji ni umeme, kodi ya nyumba na chakula. Matakwa ni vile vitu ambavyo ungependa kuwa navyo ili kuboresha au kurahisisha maisha. Mifano yake ni kama
kufunga cable au ungo vya TV, soda, na pipi au peremende. Unapokuwa unataka kununua kitu unapaswa kufikiria kama kweli unakihitaji. Hii inaweza kuwa ngumu
lakini utashitushwa na wingi wa vitu ambavyo ungeweza kununua visivyo mahitaji
ya kweli. Kama kitu haukihitaji kweli ni bora ukatunza pesa kwa ajili ya siku za mbeleni. Unapaswa kutumia pesa kwenye mahitaji kabla ya matakwa.
_____CHAKULA______
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
___________________
Need ni kitu
ambacho ni lazima uwe
nacho
Want ni kitu ambacho
ungependa kwa ajili ya kuboresha au kurahisisha maisha..
4
Kazi: Mahitaji na Matakwa yako
Orodha ya Mahitaji:
Mahitaji Ni muhimu kiasi gani
kuwa nacho?
Orodha ya Matakwa:
Matakwa Ni kiasi gani unakitaka?
5
‘Matakwa’ ambayo sitanunua:
Kutoka kwenye ‘Orodha ya juu’, tambua ambavyo hautanunua mwezi huu.
‘Matakwa’ Nitakayonunua:
6
Kutoka kwenye ‘Ordha ya juu’tambua baadhi
ya vile utakavyonunua mwezi huu
JILIPE MWENYEWE – AKIBA
Umeweka akiba kama matumizi? Umeiweka wapi,
katika matumiziyasiyobadilika au yanayobadilika? Unapopangilia bajeti yako unatakiwa kuweka baadhi ya akiba
zako kama, atumizi yasiyobadilika. Hizi ni pesa unazojitolea
ahadi mwenyewe ya kuziweka kama akiba kila mwezi. Kujilipa mwenyewe yamanisha kwamba kuweka akiba ndiyo jambo la kwanza kutekeleza
kila mwezi na siyo la mwisho. Bajeti nzuri yapaswa kuwa na kiasi cha kutosha kukidhi matumizi yako ya
kwaida, pesa taslimu kwa ajili ya matumizi ambayo hayakutalajiwa na akiba ya kutosha kwa ajili ya wakati ujao. Miezi Fulani utaweza kuwa na akiba zaidi. Miezi
kadha hutaweza kuweka akiba kabisa. Lakini kila mwezi unapaswa kujaribu kuweka akiba angalau kiasi.
UTUMAJI PESA – KUTUMA PESA NYUMBANI Sasa baada ya kufika Marekani, unaweza kutaka kutuma pesa nyumbani kwa wanafamilia. Hilo ni jambo la kawaida na linaloeleweka. Hata hivyo ni
muhimu usitume pesa zaidi ya uwezo wako. Hii ina maana kwamba baada ya kutambua matumizi yako kwa ujumla na kipato chako, kama kuna pesa
inayosalia, unaweza kuweka katika bajeti unaweza kuongezea pesa ya kutuma nyumbani. Uwe makini usitume pesa zaidi ya uwezo wako. Ukifanya hivyo
unaweza kulipia bili zako au ukose pesa ya kulipia mambo muhimu.
7
Wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu sana kutuma pesa ukiwa ndo
umefika Marekani kwa sababu unaweza ukawa baado hauna kazi, na unaweza kutakiwa kutumia pesa kuanza maisha (mfano kununua nguo, vitu vya ndani ya
nyumba yako…). Katika hali kama hii, wakati mwingine ni bora zaidi usubiri hadi utakapojua kipato na matumizi yako ni kiasi gaini kwa mwezi kabla ya kutuma
pesa nyumbani.
8
MONTHLY BUDGET WORKSHEET KARATASI YA BAJETI YA MWEZI
INCOME/KIPATO
Monthly Income KIPATO KWA MWEZI
Amount KIASI
Mshahara wako $
Mshahara wa mke
$
Msaada wa pesa wa serikali $
Msaada wa pesa kutoka LFS $
Food Stamps/Msaada wa kulipa chakula
$
Usitawi wa jamii(SSI)
Matunzo ya watoto
Kipato kingine ____________ $
Kipato kingine $
Kipato kwa ujumla $
One Time Income KIPATO CHA WAKATI MMOJA
Amount Kiasi
Msaada wa dharula (Unatolewa na LFS)
$
Pesa ya mapokezi (Inatolewa na LFS)
$
Kipato kwa ujumla $
9
EXPENSES/MATUMIZI (Inaunganisha kila kitu kutoka kwenye orodha ya
‘Mahitaji’ na ‘Matakwa’ yakununua hapo juu)
Fixed/Yasiyobadilika Matumizi kwa mwezi Kiasi
Kodi ya nyumba
$
Maji/majitaka/mengineyo (Kadilia)
$
Simu(Hudumaza kawaida/siyo masafa marefu)
$
Pesa za usafiri(basi) $
Matunzo ya watoto $
Akiba $
Mengine _______________
$
Mengine _______________
$
Jumla ya matumizi
yasiyobadilika
$
10
Flexible/Yanayobadilika
Matumizi kwa mwezi
Chakula $
Simu (Masafa marefu) $
Umeme
$
Mavazi
$
Elimu $
Vifaa vya Shule $
Usafi wa mwili (Sabuni, shampoo, dawa ya mswaki..)
$
Huduma za afya (Dawa)
$
Kadi za simu
$
Kutuma pesa nyumbani
$
Kufua
$
Mkopo wa usafiri
$
Mengine ____________
Mengine ____________
Jumla ya matumizi $
11
Bajeti yako vs. Ukweli wako
KUFUATILIA MATUMIZI YAKO
Mwisho wa kila wiki, utaweza kujumlisha kila ulichokitumia kwenye
chakula, mavazi, burudani, na matumizi ya kila aina. Mwisho wa mwezi utapata jumla ya kiasi ulichokitumia katika kila kitengo na kujaza kwenye
karatasi ya muhtasari wa matumizi kama ifuatavyo hapa chini. Ukiisha rekodi kila unachokitumia kwa wastani wa mwezi, unatakiwa
kuipitia bajeti yako sasa ili uhakikishe kwamba inakubalika. Kama bajeti na matumizi yako haviendi sambamba, utahitaji kubadilisha kimoja wapo au
vyote.
Kodi
Umeme
Utunzaji
Watoto
Akiba
Chakula
Mavazi
Burudani
Wiki1
$
$
$
$
$
$
$
Wiki 2
$
$
$
$
$
$
$
Wiki 3
$
$
$
$
$
$
$
Wiki 4
$
$
$
$
$
$
$
Jumla
$
$
$
$
$
$
$
12
MAPITIO YA BAJETI vs MATUMIZI Je mpango wa matumizi uko sawa na matumizi halisi? Kama sivyo,
ulitumia kidogo au zaidi ya vile ulivyotarajia? Sababu ni zipi? Ni vipi utaweza kuboresha mipango yako mwezi ujao? Andika baadhi ya majibu ya swali hili
hapo chini:
____________________________________________________ ____
____________________________________________________ ____
KUIMARISHA BAJETI YAKO
Kipato Ni maoni gani kwa ajili ya kuongezea kipato?
____________________________________________________ ____
Utumiaji Ni maoni gani kwa ajili ya kupunguza matumizi?
_______________________________________________________ _
13
ONGEZA KIPATO CHAKO Njia moja ya kuimarisha bajeti yako na kupata pesa zaidi za akiba au za
kutumia ni kuongeza kipato. Mara huwa ni vigumu kupata kazi inayolipa zaidi.
Pamoja na hayo, huwa kuna vitu tunavyoweza kufanya kuongeza kipato chetu kiana. Zaidi ya njia tulizojifunza darasani, njia za kupunguza matumizi
zinajumlisha:
Tumika masaa zaidi: Ukitumika zaidi ya masaa 40 kwenye kazi
moja unatakiwa kulipwa pesa zaidi ya kiwango chako cha kawaida
kwa saa moja. Hii inaitwa “working overtime-kutumika muda wa
ziada” na boss wako anapaswa kukulipa and your boss 1.5 X ya pesa unazotumikia kawaida. Kawaida kama unapata $8.00 kwa saa
unaweza kulipwa $12.00 kwa saa kwa muda wowote uliotumika juu ya masaa 40.
Mke kufanya kazi: Kipato cha familia yako kitaongezeka sana
kama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu,
nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi nyumbani au ya ziada itarahisisha kulipa bili zako au kuweka akiba ya familia kwa
ajili ya wakati ujao.
ELimu: Kurudi shuleni kukamilisha sekondari ya juu, chuo kikuu au
masomo mengine ni moja ya njia nzuri za kuongeza kipato cha
familia yako.
Misaada ya Serikali: Kama kipato chako kiko chini au unayo familia kubwa kuna uwezekano wa kukubaliwa misaada ya serikali.
Kutokana na kipato chako na ukubwa wa familia yako unaweza kustahili kupewa:
Cash Assistance(Msaada wa pesa taslimu): Kusaidia katika
matumizi ya kila siku Food Stamps Kusaidia kulipia chakula
Rental Assistance kusaidia kulipa kodi ya nyumba Medical Assistance kusaidia kupata bima ya afya ya bure.
Zana za kujaribu:
211 (taarifa kuhusu msaada uwezekanao) Mengine?
14
KUPUNGUZA MATUMIZI
Inaweza kuwa ngumu kwa watu wengi kuongeza
kipato chao sana. Kwa walio wengi, ni rahisi zaidi kudhibiti kiasi cha pesa wanachotumia kuliko kupata kazi inayolipa
zaidi au kutumika masaa mengi. Zaidi ya njia tulizojifunza darasani, njia za kupunguza matumizi ni:
Tembea na pesa taslimu kidogo tu ili usishikwe
na majaribu ya kutumia. Kula nyumbani au uende na chakula chako badala ya kula nje.
Lipa bili zako kwa wakati ili usilazimike kulipishwa pesa za kuchelewa.
Jihadhari matumizi madogo madogo kama soda, pipi na chipsi.
Tumia kuponi. Nunua vitu vya mnada, lakini uendelee kuhemea.
Hemea kwenye maduka yanye punguzo (Maduka yanayouza vitu dollar moja).
Hemea kulingana na mahitaji yako, siyo na matakwa. Usikubaki kushaurishwa na mtu kununua kitu ambacho hauhitaji.
Kama umenunua au umekubali kitu ambacho hauhitaji kirudishe au usimamishe hiyo huduma.
Uwe makini na bajeti yako iliyoandikwa. Hemea wakati wa bei nzuri kama unafikiria kununua kitu chenye
gharama. Tunza risiti za vitu ulivyonunua ili uweze kuvirudisha ukiwa na
tatizo. Epuka mitego ya matumizi!
Kumbuka kwamba
wakati unapojaribu kuweka akiba ya
pesa hata $1 au $5 kwa siku itageuka
kuwa pesa nyingi
Kumbuka Kutunza
risiti zako!
15
SPENDING TRAPS/MITEGO YA MATUMIZI
Mitego ya matumizi ni bidhaa au huduma ziishiyazo kukugharimu zaidi ya thamani yake au ambavyo haukutegemea.
Mara nyingi hizi huduma huonekana ni za bei nafuu lakini kabla hujakubaliana na moja wapo unapaswa kuelewa gharama zake
kikweli.
Check-Cashing and Money Orders
Kupewa pesa taslimu za cheki na Hawala za pesa
Maduka yanayotoa pesa taslimu za cheki uliyopewa hutoza pesa nyingi ili
upewe pesa taslimu. Ada inakuwa mara nyingi sawa na asilimia 8% za pesa wanazokupa. Kwa mfano, kama ulikuwa na cheki ya $100 na
ukaipeleka kwenye duka linalotoa pesa taslimu kwa ajili ya cheki utatakiwa kulipa $8 ili kupata pesa zako taslimu.
Credit Card Interest and Fees/Riba na Ada za kadi ya mkopo
Kama tutakavyoyazungumzia baadae, kutumia kadi za mkopo kwa
busara yaweza kuwa muhimu wakati ujao kifedha. Ni rahisi sana kujikuta
kwenye matatizo makubwa kutokana na kadi za mkopo. IKama ni lazima ulipe riba ya kadi yako ya mkopo unaweza kujiingiza kwemye madeni
makubwa ambayo ni vigumu kuyaepuka. Wakati huo huo ni vyema kulipa deni la kadi yako ya mkopo kila mwezi (ili usilazimike kulipa riba).
Na unapaswa kulipa kiwango cha chini. Kama hukufanya hivyo, utalipishwa riba na ada, mara nyingi $15 or $20 kila wakati.
Over Drawing Accounts/Kuchukua pesa zaidi kwenye akaunti
Hii hutokea unapo andika cheki au kujaribu kuchukua pesa kwenye
mashine ya ATM ukiwa hauna pesa zilizosalia kwenye akaunti yako. Ukifanya hivyo, benki itakutoza ada ya juu sana. Mara nyingi ada
inaweza kuwa kubwa zaidi ya cheki uliyoandika.
Payday Loans/Mikopo ya kulipa kwa siku
Mikopo ya kulipa kwa siku ni miongoni mwa mitego ya matumizi mibaya
zaidi. Kama unahitaji pesa angalau siku mbili kabla ya kulipwa, wakopeshaji wa kulipwa kwa siku watakutaka uandike cheki ambayo
hawatachukulia pesa taslimu hadi utakapopokea cheki yako ya malipo. Hata hivyo, kama unahitaji $100 kabla ya siku yako nyingine ya malipo,
16
watakutaka uandike cheki ya $125. Kwa hiyo kukopa $100 kwa wiki
itakugharimu $25 za ziada! Ni karibu riba ya asilimia 1,300%!
Rent-to-Own/Kodi hadi Umuliki
Maduka ya Kodi hadi umiliki ni mtego mwingine mbaya wa matumizi.
Haya maduka yanakuuzia vifaa vya ndani ambavyo hauna uwezo wa kuvilipia bei yake kwa ujumla. Kila mwezi unatoa sehemu ya malipo.Hata
hivyo, haya maduka yanatoza faida au riba kubwa. Hadi kufikia muda wa
kumiliki kifaa ulichouziwa, utakuwa umelipa kati ya mara 3 hadi 10 zaidi ya thamani yake!
Interest Free Purchases/Mauzo bila riba
Baadhi ya maduka yanatangaza kwamba unaweza kununua kitu, ukalipa
baadae na usilipe riba kwa muda wa miaka miwili. Unapaswa kuwa makini na hizi ahadi kwa sababu utakapotakiwa kulipa riba itakuwa ya
juu sana. Kama utanunua kitu bila riba kwa mwaka mmoja au miwili, unatakiwa kukilipia kwa ujumla katika ule muda ambao hautakiwi kulipa
riba.
17
Upande 2.0
Shopping/ Grocery Ununuzi/Biashara ya vyakula
THE SUPERMARKET – NI NINI?
NI DUKA KUBWA LINALOUZA VIFAA NA
VYAKULA Maduka mengi yanayouza vyakula Marekani
yanakuwa na sehemu ya vyakula, bucha, sehemu ya kutengeneza mikate, matunda na mbogamboga, na
vyote katika ndani ya duka moja. Unaweza kwenda
kwenye soko kubwa kila unapohitaji – yaliyo mengi yanafungua masaa 24. Katika maeneo mengi,
utakuwa na chaguo la maduka makubwa mawili. Kila moja wapo litakuwa na vyakula vyako vya msingi na vitu kadha wa kadha, vinavyoongezea baadhi ya
vitu maalum na vya asili.
Maduka mengine:
Specialty Stores/Maduka maalum: Zaidi ya maduka makubwa, yapo maduka madogo madogo maalum yanayohusika na aina
chache za vitu mfano kama bucha na masoko ya vitu vya asili.
Small neighborhood markets/Masoko madogo ya mitaani:
Mitaa mingi inakuwa na maduka madogo yanayouza vitu vya
msingi (mikate, maziwa, jibini au chizi). Haya maduka yanafaa lakini yanakuwa na gharama kuliko maduka makubwa.
Specialty Stores/Maduka maalum: Wakati yapo maduka maalum au ya asili yanayouza vitu visivyopatikana katika maduka
makubwa ya kawaida (Masoko ya vitu kutoka asia, maduka ya kiafrika…). Watu wanaojitolea wanaweza kusaidia familia kujua
haya maduka yalipo.
UNDERSTANDING PRICING/KUELEWA BEI
Store brands/Matoleo ya duka: Mara nyingi yanakuwepo
matoleo mengi ya kila bidhaa moja maalum. Maduka makubwa
18
yaliyo mengi yanakuwa na matoleo yake (mfano Kroger), ambayo
yanakuwa ya bei nafuu kuliko mengine. Matoleo mengine mengi yanafanana katika maduka mengi na yote ya na ubora
unaokubalika na ni salama kwa matumizi.
Buying in bulk/Kununua vitu kwa wingi: Njia nyingine nzuri ya kuweza kuweka akiba ya hela ni kununua vitu kwa wingi. Hii ni
njia bora ya kuweka akiba ya hela kwa sababu unaweza kufaidika na punguzo litokanalo na kununua vitu kwa wingi. Na utahifadhi
vile utakavyovihitaji kwa baadae, hasa hasa unavyovitumia sana, au vitu visivyoharibika haraka.
Maduka makubwa yanauza bidhaa zake kwa njia nyingi. Hata kama alama inasema “Mnada”, unapaswa kuelewa utakachikipata kwa
hela yako. Kwa mfano, maduka makubwa yanakuvuta kwa kutumia
vitu kama “2 for $5”. Ukisoma alama kwa undani inaweza ikawa kwamba unaweza kununua kitu kimoja kwa bei ya mnada. Kingine,
kunaweza kuwa “Nunua moja, pata moja bure”. Hii ina maana kwamba unalipa bei kamili kwa ajili ya kitu cha kwanza halafu
unaongezewa kingine bila malipo.
<Mifano ya vitambulisho>
19
Coupons/Kuponi: Kuponi ni vipande vidogo vya karatasi vinavyotangaza bidhaa za maduka makubwa. Unazipeleka kwenye
maduka na unazitumia kupata punguzo kwenye bidhaa fulani. Kuponi ni sawa na pesa taslimu. Kwa mfano, kama unayo kuponi
ya dola $1.00 kwenye boxi ya nafaka, muuzaji ataipokea kuponi kama ambavyo ingelikuwa ni pesa taslimu. Ufikapo kaunta, kabidhi
kuponi zako kwa muuzaji, atazikagua na mashine na kasha kukutoza pesa inayobaki kwa ajili ya kitu kile ulichonunua.
Kuponi zinapatikana kwa njia nyingi tofauti.
Tovuti za maduka na eKuponi
Mitandao ya tovuti inayouza kuponi
Gazeti la sunday Vipeperushi vy maduka makubwa vya katikati ya wiki
Tovuti za viwanda au watengenezaji Eneo la kuponi kwenye maduka
Kuponi za risiti (nyuma ya risiti yako) Njia ya posta
Store discount cards/Kadi za punguzo za duka: Kadi ya uaminifu, kadi za zawadi, kadi za pointi, kadi za
heri, kadi ya klabu ni kadi ya karatasi au plastiki, ambayo inafanana na kadi ya mkopo
au kadi ya benki, inamtambulisha mwenyenayo kama mwanachama katika mpango wa
uaminifu. Ni njia ambayo maduka makubwa
yanatumia kukuhamasisheni kuendelea kuhemea kwao. Kwa kutumia hiyo kadi unapata
bei nzuri na punguzo kwa baadhi ya bidhaa. Kujua kama bidhaa zimepunguzwa bei, tazama katika vipeperushi
vya duka au chunguza bei kwenye rafu (note to volunteer: explain how items have a price for use with, and without loyalty card. And
you only get discount when card it presented at each purchase). Kupata kadi ni rahisi na ni bure. Jaza tu fomu ya kujiunga kwenye
meza ya huduma kwa wateja, na utakuwa tayari kuanza kuitumia kadi. Uje na kadi yako kila mara unapokuja kuhemea na
uimuonyeshe muuzaji; lakini usiwe na hofu, unaweza kupewa
20
nyingine ukiipoteza. Pitisha kadi yako kwenye mashine au
uimukabidhi muuzaji. Punguzo lako litakatwa kwenye malipo yako.
Comparison shopping/kufananisha mahemezi: Ukubwa wa furushi haumanishi bei bora zaidi. Wakati mwingine kununulia pamoja vinatoa
bei nafuu, wakati mwingine vinakuwa na bei ya juu. Njia moja tu ya uhakika ni kufananisha bei za kila kipimo. Kawaida vipimo vinakuwa
katika aunsi au paundi. Maduka mengi yanabandika bei kwenye rafu, hali ambayo inarahisisha ufananishaji. Kitambulisho cha bei kitakuonyesha ni
kiasi gain kila kipimo cha hiyo bidhaa kinauzwa.
Mahemezi na bajeti Hakikisha kwamba mahemezi yanakwenda sambamba ba bajeti yako, (Mahitaji vs Matakwa)
Unayo maelfu ya vyakula ya kuchagua katika duka, kwa hiyo ni rahisi
kujisahau na kununua vingi, kununua vitu unavyovitaka lakini ambavyo huvihitaji, au kusahau kitu ambacho unakihitaji
kweli. Andaa orodha ya vitu utakavyonunua kabla ya kwenda dukani. Kuandaa orodha
inaokoa muda nakusaidiakuhakikisha unanua kile unachokihitaji.
Amua ni pesa kiasi gain unazoweza kutumia
katika bajeti yako KABLA ya kwenda dukani. Kwa mfano kama unanunua
chakula kila wiki, jua ni kiasi gain unaweza kutumia kwa wiki, na utumie hicho
kiasi tu. Kama hauna pesa kwa ajili ya kila kitu kilichoko kwenye orodha yako,
amua vilivyomuhimu na uvinunue hivyo (vitu kama mkate, maziwa,
mbogamboga, mchele…) na usinunue vitu ambavyo havina umuhimu na
visivyo kwenye ‘orodha yako ya mahitaji’ (Vitu kama soda, pipi).
Jumlisha mahemezi yako kadiri unavyokwenda Mashine ndogo ya mahesabu inaweza kukusaidia kufuatilia ni kiasi gani
cha pesa umetumia kadiri unavyohemea. Jumlisha bei ya kila kitu unapokiweka
kwenye torori au kikapo chako. Utaweza kujua kiurahisi ulizojumlisha kabla kufika kwenye eneo la malipo au mbele ya muuzaji.
Ni MUHIMU SANA kufuatilia mahemezi yote
uliyoyafanya na kadi yako ya chalula (Food Stamp Card) ili uweze kujua ni pesa kiasi gani ulizobaki nazo kwenye
21
kadi yako!!!!! Hivi unaweza kuvifanya kwa kutunza na kujumlisha risiti zote
za mahemezi ya kadi. Kujua salio kwenye kadi, tazama upande unaofuata hapo chini juu ya kadi ya chakula (Food Stamps).
Kupangilia kabla na kuchukua maamuzi mazuri
Kingine, pangilia mapishi unayotaka yako katika siku chache zijazo na
uorodheshe viuongo utakavyohitaji. Nunua vyakula vya kutosha
vitakavyokufikisha siku ya mahemezi mengine na huku ukihakikisha
kwamba hautumii pesa zaidi ya zile ulizopanga kwenye bajeti yako.
Unaweza kutumia mashine ya mahesabu kujumlisha vitu kadiri
unavyoviweka kwenye torori yako.
Hata kama unayo orodha, unahitaji kuchukua maamuzi kadhaa sokoni.
Inasaidia unapofikiria kama mpishi. Mpishi mzuri anatengeneza orodha ya
viungo, lakini anaangalia nyama na mazao kujua vilivyo vibichi na vinavyouzwa
vizuri zaidi. Kama mapishi fulani yanahitaji kitunguu lakini kikawa siyo kizuri
au hakipo dukani, mpishi atachagua aina nyingine ya kitungu kilicho bora zaidi.
Au kama kuna samaki iliyo mbichi zaidi, mpishi anaweza kuipendelea kuliko ile
iliyoko kwenye orodha ya mahemezi.
FOOD STAMPS/KADI YA CHAKULA Unavyoweza au Usivyoweza kununua na kadi ya Chakula (Food Stamps).
Kwa kutumia kadi yako ya chakula (Food Stamp) unaweza kununua vyakula unatumia kama:
Maziwa na vitu vyote vitokanavyo na maziwa; nyama, samaki, kuku, mayayi na maharage; nafaka,
mchele, tambi na vitu vingine vya mbegu; viungo vyote vinavyotumika kuchoma au kupika;
matundana mbogamboga; vyakula vya baridi kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani; barafu na maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu; maziwa ya watoto,
baadhi ya vyakula maalum vya lishe au vya watu wenye kisukari na vyakula asilia au vyakula hai, mbegu za bustani na mazao
ya vyakula vya kupanda nyumbani. Kwa kutumia kadi yako ya chakula (Food Stamp) huwezi kununua
vifuatavyo: Aina yoyote ya vileo, pombe au mvinyu; aina yoyote ya tumbaku; bidhaa zote
zisizo za vyakula kama vitu vya kusafishia, sabuni na bidhaa za karatasi, nepi; madawa kama aspirin, dawa za kikohozi na vitamini, vifaa vya kutunzia
22
vyakula kama majagi na mitungi ya kupozea, vyakula vya moto vilivyo tayari
kuliwa, na vyakula ambavyo siyo vyakutumiwa na binadamu kama vyakula vya wanyama.
…
Kwa vitu ambavyo huwezi kununua na kadi yako ya chakula, utapaswa
kulipa pesa taslimu.
Checking balance on Food Stamps/Kuangalia salio kwenye kadi yako
ya chakula: Njia nzuri ya kufuatilia salio la kadi yako ni kufuatilia kwa makini
matumizi yako yote. Unaweza pia kuita namba 1-800 iliyoko upande wa pili wa
kadi kujua salio (japo unaweza kufanya hivyo kama mara 3 tu kwa mwezi).
Inawezekana pia kufuatilia salio lako kwenye mtandao lakini utahitaji kujisajili
na kuwa na jina na ufunguo wa siri. Jina la kadi hapa Colorado ni Quest card.
TAXES ON NON-FOOD ITEMS/USHURU WA BIDHAA ZISIZO
ZA VYAKULA (Vipi vilipavyo ushuru na visivyolipa ushuru) Vitu ambavyo havilipi ushuru ni pamoja na vyakula kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani. Mifano, lakini siyo hiyo tu, nyama, kuku, samaki, mikate, nafaka, mbogamboga, matunda, juisi ya matunda au mbogamboga,
maziwa na vitu vitokanavyo na maziwa, kahawa, chai, nazi, pipi, jojo,
viungo, vinywaji baridi, keki, chipsi, vyakula maalum, vyakula vilivyorutubishwa, maziwa ya watoto, vitu vilivyotengenezwa kuwa
vyakula (kwa mfano mafuta ya nguruwe, mafuta yatokanayo na mbogamboga).
Vitu vinavyolipa ushuru hadi asilimia 3.62% ni pamoja na uuzaji na ununuzi wa bidhaa za matibabu kama vitamini na madini vinavyouzwa
kama mbadala vyakula mbadala, vitu vinavyosaidia afya kama aspirin, dawa za kikohozi, dawa za mafua vitu vinavyozuia asidi. Vyakula
mbadala, visaidizi vya afya, na dawa za kunua madukani vinalipa ushuru kwa viwango vya asilimia 3.62%.
Bidhaa za vyakula zisizouzwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu zinalipiwa ushuru katika
viwango vya asilimia 3.62%. Mifano inaweza kuwa vyakula vya wanyama, mbegu kwa ajili ya ndege, na vyakula vingine vya wanyama.
23
Vitu vinavyochukuliwa kama vyakula chini ya mpango wa serikali kuu wa
Food Stamp lakini ambavyo havikubaliki kama vyakula vinavyoweza kuuzwa na kusamehewa ushuru isipokuwa vikinunuliwa kwa kadi ya
vyakula au vocha au cheki za WIC ni: Maji yenye dioksidi ya kaboni yanayouzwa kwenye mitungi (Kwa mfano
maji yenye viputo vidogo vidogo au maji ya seltzer). Pipi/jojo.
Mbegu na mazao ya kukuza vyakula. Saladi/kachumbari iliyotengenezwa inayohitaji kutiwa baridi, iwe
imetengenezwa na duakani au kwenye ghala, au watengenezaji wanaouza au kuwalanguzia wauzaji.
Salad bars. Sandwichi za baridi
Trei za deli Chakula kilichopikwa au chakula kinachouzwa kwa ajili ya matumizi ya
papo hapo.
24
Upande 3.0
Banking/Kutumia Benki
UTARATIBU WA KUTUMIA BENKI
Ili kuishi kulingana na bajeti yako na usimamie pesa zako kwa njia iliyo mwafaka kwako, utahitaji kufungua
akaunti katika benki au umoja wa mikopo.
Disadvantages of Using Cash/Kasoro za kutumia pesa taslimu
Kutembea na pesa nyingi na kulipia kila kitu na pesa taslimu yaweza kuwa hatari, usumbufu na ghali sana. Ubaya wa kutumia pesa taslimu ni:
Siyo salama (unsafe) kwa sababu pesa taslimu zikipotea au zikaibiwa, huwezi kuzipata tena.
Ni usumbufu (inconvenient) kwa sababu unalazimika kutembea na pesa nyingi kama una mpango wa kununua kitu cha gharama
na kila unapohitaji pesa zaidi lazima wende nyumbani kuzichukua. Ni gharama (expensive) kwa sababu utapaswa kulipa ili upewe
pesa taslimu badala ya cheki zako na hawala za fedha.
Advantages of Banks and Credit Unions/Faida za Benki na Vyama vya Mikopo
Benki na Vyama vya mikopo ni biashara zinazotoa sehemu zilizo salama na rahisi kutunza pesa. Zinatoa huduma nyingi tofauti zinazofanya usimamizi
wa pesa zako salama na rahisi zaidi kuliko kutumia pesa taslimu. . Benki na vyama vya mikopo viko salama (safe) kwa sababu serikali
ya Marekani inavipa bima karibu vyote. Kwa njia hiyo, kama benki itashindwa
kukurudishia pesa zako, serikali ya Marekani itakulipa.Hii inaitwa bima ya FDIC. Unatakiwa kuhakikisha kwamba kila unayemupa pesa zako anayo hii
aina ya bima. . Benki na vyama vya mikopo ni rahisi (easy) kwa sababu vilivyo
vingi vinayo maeneo mengi unapoweza kuchukulia pesa zako. Cheki zinarahisisha pia kulipia au kununua vitu vya gharama.
Benki na vyama vya mikopo vyaweza kutokuwa na gharama ( cheap) kwa sababu,
ikuchagua iliyo sahihi, hawatakulipisha ukifungua akaunti au ukichukua pesa zako.
Hata kukiwa na ada itakuwa ndogo kuliko kutumia biashara zinazotoa pesa taslimu
kwa ajili ya cheki au kununua hawala za fedha.
Tofauti kati ya Benki na vyama vya mikopo Tofauti kubwa kati ya benki na chama cha kukopa ni vile ambavyo benki
zinajaribu kuzalisha pesa lakini vyama vya kukopa havifanyi hivyo. Hiyo ina
25
maana kwamba vyama vya kukopa vinatoa huduma kwa gharama nafuu kuliko
benki.
AINA ZA AKAUNTI
Zipo aina tatu za akaunti za benki au za vyama vya mikopo tutakazozungumzia, Checking Accounts/Akaunti matumizi ya kila siku,
Savings Accounts/Akaunti ya Akiba na Mutual Funds/Hazina ya ubia. Kila moja ya hizi akaunti ni tofauti na inapaswa kutumiwa kwa sababu
zilizotofauti. Unaweza hata kutaka zaidi ya akaunti moja. Tutazungumzia hizi akaunti kwa kirefu zaidi.
Akaunti ya matumizi ya kila siku Akaunti ya checking inapaswa kutumiwa kwa ajili ya pesa unazohitaji
kuzifikia kila siku. Pesa utakazotumia kulipa kodi ya nyumba, pesa unazodaiwa, chakula na matumizi mengine zinatakiwa kuwa kwenye akaunti
ya Checking. Akaunti za checking ni bora zaidi kwa matumizi ya kila siku kwa
sababu zinakupa urahisi wa kufikia fedha zako. Unaweza ukapata pesa taslimu kwenye benki au mashine ya ATM au andika cheki kulipa bili.
Kabla ya kuchagua akaunti ya matumizi ya kila siku (checking) unatakiwa kulinganisha:
Minimum Balance/Baki ya chini: Baadhi ya benki na vyama vya mikopo vinalazimisha kuacha kiasi Fulani cha pesa katika akaunti
yako. Ukiwa na pesa kidogo katika akaunti yako wanakutoza ada. Kadiri baki inavyokuwa ndogo inakuwa bora zaidi.
Unatakiwa kuweka pesa za
matumizi ya kila siku katika
akaunti ya checking
account.
Unatakiwa
kuweka pesa usizohitaji katika
akaunti ya akiba. Savings
account.
Kama huwezi kutumia akaunti ya akiba kwa
sababu za kidini au hautahitaji pesa kwa
muda unaweza kufungua akaunti ya
Mutual Fund.
26
Fees/Ada:
o Annual Fees/Ada za mwaka: Benki tofauti zinatoza viwango tofauti vya pesa kwa ajili ya kufungua akaunti.
Baadhi ya zinatoa huduma hiyo bure wakati zingine zinatoza ada ya mwezi au ya mwaka.
o ATM Fees/Ada za mashine ya ATM: Baadhi ya benki zinatoza ada kwa kutumia mashine zake za ATM. Kama
utajaribu kutumia ATM ya benki nyingine, ada itakuwa kubwa.
o Overdraft Fee/Ovadrafti (Sawa na deni katika akaunti): Kama utajaribu kuchukua pesa nyingi kwenye
akaunti yako zaidi ya zile ulizonazo, benki itakutoza ada ya ovadrafti.
Number of Transaction/Idadi ya shughuli za biashara: Baadhi ya benki
zinaruhusu kuandika cheki au kuchukua pesa mara kadhaa kwa mwezi. Ukiandika
cheki zaidi ya zile unazoruhusiwa basi benki inaweza kukutoza ada ya ziada.
Akaunti ya akiba Akaunti ya akiba ni sehemu ya kuhifadhi pesa kwa ajili ya wakati ujao.
Ukiweka pesa kwenye akaunti ya akiba, benki zinakulipa pesa ambazo
zinajulikana kama riba kwa kipindi chote utakachoacha pesa kwney akaunti.
Hivyo pesa zako zinaongezeka! Zipo aina tofauti za akaunti za akiba. Yapo mambo machache
yakuzingatia unapo amua ni akaunti gaini ya akiba inayokufa zaidi.
The interest rate/Kiwango cha riba: Kumbuka toka somo la 1, unapoweka pesa benki, benki inazitumia zile pesa kwa kipindi
chote zitakuwa kwenye akaunti yako. Benki itakulipa kwa kuiruhusu kutumia pesa zako. Kiwango cha pesa wanazokulipa
kinaitwa riba. Baadhi ya akaunti za akiba zinalipa riba zaidi ya zingine. Unatakiwa kuchagua akaunti inayotoa riba ya juu
unayoweza kupata. Minimum Balance/Baki ya chini: baadhi ya benki au vyama
vya mikopo vinalazimisha kuacha angalau kiasi Fulani cha pesa kwenye akaunti. Ukiwa na pesa kidogo ya zile kwenye akaunti
yako, wanakutoza ada.
27
o Fees/Ada:
o Annual Fees/Ada za mwaka: Benki tofauti zinatoza viwango tofauti vya pesa kwa ajili ya kufungua akaunti.
Baadhi ya zinatoa huduma hiyo bure wakati zingine zinatoza ada ya mwezi au ya mwaka.
o ATM Fees/Ada ya mashine za ATM: Baadhi ya benki
zinatoza ada kwa kutumia mashine zake za ATM. Kama utajaribu kutumia ATM ya benki nyingine, ada itakuwa
kubwa.
o Overdraft Fee/Ada ya ovadrafti (Sawa na deni katika akaunti): Kama utajaribu kuchukua pesa nyingi kwenye
akaunti yako zaidi ya zile ulizonazo, benki itakutoza ada ya
ovadrafti.
Terms/Mihula: Zipo akaunti ambazo ukiweka hela kwenye akaunti unapaswa kuziacha zikae kwa muda Fulani. Wakati
mwingine inaweza kuwa mwezi mmoja, wakati mwingine mwaka mmoja, wakati mwingine miaka mingi. Ukijaribu kuchukua pesa
zako kabla ya muhula kuisha, wanakutoza ada kubwa sana.
28
KARATASI YA TAARIFA ZA AKAUNTI ZA BENKI
Hapo chini ni orodha ya akaunti za akiba na matumizi ya kila siku katika benki muhimu San Diego. Kwa kuzingatia kwamba benki inalo tawi katika maeneo unayoishi, ada, viwango vya riba na baki ya chini unatakiwa
uchague akaunti inayokufaa zaidi. Zipo aina nyingi za akaunti zinazopatika San Diego na The International Rescue Committee haiwezi kupendekeza akaunti fulani juu ya zingine, kwa hiyo unatakiwa kuangalia uwezekano
mwingine.
Checking Accounts/Akaunti ya matumizi ya kila siku
Bank Benki
Minimum
Balance Baki ya
chini
Interest
Rate Kiwango
cha riba
Free
Checks per
Month Cheki za
bure kwa
mwezi
Annual Fee
Ada ya mwaka
ATM Fees
Ada ya
ATM
Overdraft
Fee Ada ya
ovadrafti
Number of
Locations Idadi ya
matawi
29
30
Savings Accounts/Akaunti ya Akiba
Bank
Benki
Minimum
Balance
Baki ya chini
Interest Rate
Kiwango cha riba
Annual Fee
Ada ya mwaka
ATM Fees
Ada
ya ATM
Overdraft Fee
Ada ya ovadrafti
Number of
Locations
Idadi ya matawi
31
Mutual Funds/Hazina ya ubia Akaunti za akiba ndiyo njia rahisi ya kuweka akiba ya pesa na kuzifanya pesa zako ziongezeke
kwa ajili ya mahitaji yako ya muda mrefu. Hata kama dini yako haitakuruhusu kukubari riba
itokayo katika akaunti yako ya akiba, pesa zako zitaendelea kuongezeka katika hazina ya ubia.
Kama unazo pesa nyingi katika akaunti yako
akiba unaweza kuamua kuweka kiasi katika hazina ya ubia kwa kuwa zinaweza kuongezeka haraka kuliko katika akaunti ya
akiba. Lakini hili halitokei kila wakati.
Unapowekeza pesa zako katika hazina ya ubia unakuwa umenunua sehemu ndogo ya biashara kubwa sana. Biashara inavyokuwa ndivyo na pesa
zako zinavyoongezeka. Zipo hazina nyingi za ubia unapoweza kuweka pesa zako.s the businesses grow, so does your money. Hazina za ubia zina utata
kuliko akaunti za akiba kwa sababu biashara unayonunua ukifanya vibaya unaweza kupoteza pesa zako.
Kwa sababu zina utata zaidi unatakiwa kupata taarifa zaidi kabla ya
kuweka pesa zako katika hazina za ubia. Kama unahitaji taarifa zaidi uliza case manager wako IRC.
32
UJUZI WA KUTUMIA BENKI
Opening an Account/Kufungua Akaunti
Kabla ya kufungua aina yoyote ya akaunti katika benki au chama cha mkopo unatika kuhakikisha kwamba hiyo akaunti inakufaa. Unatakiwa
kufahamu yafuatayo: The interest rate/Kiwango cha riba: Kumbuka toka somo la 1,
unapoweka pesa benki, benki inazitumia zile pesa kwa kipindi
chote zitakuwa kwenye akaunti yako. Benki itakulipa kwa kuiruhusu kutumia pesa zako. Kiwango cha pesa wanazokulipa
kinaitwa riba. Baadhi ya akaunti za akiba zinalipa riba zaidi ya zingine. Unatakiwa kuchagua akaunti inayotoa riba ya juu
unayoweza kupata. Minimum balance/Baki ya chini: Kumbuka, baki ya chini ni kiasi
kidogo kabisa cha pesa unachoruhusiwa kuwa nacho benki. Ukienda chini ya kile kiasi, benki itakutoza ada. Kama baki ya chini
ni zaidi ya pesa unazoweza kuacha benki, unatakiwa kutafuta benki au akaunti nyingine.
Fees/Ada: Baadhi ya benki zinatoza ada kufungua akaunti. Zingine zinatoza ada kila mwezi. Kama benki ina ada ya juu
unaweza kuacha kufungua akaunti nao. Number of Transactions/Idadi ya shughuli za biashara:
Baadhi ya benki zinaruhusu kuandika idadi Fulani ya cheki au
kuchukua pesa mara kadhaa kwa mwezi.
Kufungua akaunti unatakiwa kwenda benki na kuzungumza na mfanya kazi
wa benki. Ukienda unavyotakiwa kuwa navyo ni: Namba yako ya Social Security
Vitambulisho vya aina mbili (Angalau kimoja chenye picha yako, baadhi ya benki zinaomba vitambulisho viwili vyenye picha)
Kielelezo cha anwani yako (Hati ya madai ya karibu inatosha)
33
Kuandika cheki
Unapomwandikia cheki mtu ni sawa na kumpa pesa taslimu. Wanapopeleka cheki yako kwenye benki zao pesa zitachukuliwa moja kwa
moja kutoka kwenye akaunti yako.
The IRC
4535 30th Street #5
San Diego, CA 92116
PAY TO THE
ORDER OF:
Date:
101
$
Dollars
Memo:
[:1234567]: 123456789012 1234
San Diego National Bank
3526 University Ave, San Diego, CA 92117
Benki itaweka
jina na anwani
yako hapa
Unaandika
jina la
unayemlipa
hapa
Benki itaweka
namba ya cheki
hapa. Kila cheki
ina namba
tofauti inayoanza
na 1.
Unaandika tarehe
ya siku ya siku
unapoandika cheki
hapa
Unaweza kuandika
maelezo madogo
kuhusu sababu ya
cheki. Kama unalipa
bili andika namba ya
akaunti ya hiyo bili.
Andika kiasi cha cheki kwa
tarakimu hapa
Unasai
cheki
hapa
Andika kiasi cha cheki
kwa maneno hapa.
Unaweza kuandika senti
kwa kifupi. Kwa mfano
unaweza kuandika 40/100.
Baada ya kuandika kiasi,
chora msitari mwishoni ili
mtu yeyote asibadilishe
ulivyoandika.
34
Activity/Zoezi: Writing a Check/Kuandika cheki Jaribu kujaza cheki ifuatayo hapo chini kama vile ungelikuwa unahemea
katika duka la Ralph’s na umenutumia $51.50 kwenye chakula.
Your name
123 40th Street
San Diego, CA 92116
PAY TO THE
ORDER OF:
Date:
101
$
Dollars
Memo:
[:1234567]: 123456789012 1234
San Diego National Bank
3526 University Ave, San Diego, CA 92117
35
Withdrawing Cash/Kuchukua pesa taslimu Unapoandika cheki, unachukua pesa kwenye akaunti
yako kumlipa mtu mwingine. Zipo njia zingine mbili za kuchukua pesa kwenye akaunti yako.Unaweza kwenda
kwenye tawi la benki na kumuomba (teller) mfanyakazi wa benki kuchukua pesa toka kwenye akaunti yako.
Kama hautaki kusubiri kwenye mustari au kama hauwezi kwenda benki unaweza kutumia (Automatic Teller Machine) mashine maalum ya benki.
Zinaitwa pia ATMs. ATMs ni mashine zitakazochukua pesa kutoka kwenye akaunti yako kwa niaba yako. Zipo ATMs katika kila eneo la mji ili ziweze
kufikiwa kiurahisi na haraka kuliko kwenda benki. Matatizo ya ATMs ni kama: Kuwa na urahisi wa kuzifikia pesa zako huweza kupelekea kununua
vitu ambavyo kwa kweli hauhitaji.
Kila ATM inamilikiwa na benki. Kama utatumia ATM ambayo haimilikiwi na benki yako, watakutoza dola $2 au $3 kutumia
mashine. Kama utatumia hizi ATMs sana inaweza kukugharimu pesa nyingi. Unatakiwa kutafuta ATMs zenye maandishi ya jina la
benki yako.
The teller ni
mfanyakazi wa benki na yupo
kujibu maswali yako uliyonayo.
36
Depositing Money in Your Account/Kuweka pesa kwenye
akaunti yako
Deposit Slips/Stakabadhi za amana Kuweka pesa kwenye akaunti yako unatakiwa kujaza stakabadhi ya amana. Unakabidhi stakabadhi ya
amana kwa mfanyakazi wa benki au ATM pamoja na pesa taslimu au cheki unazoweka. Utakuta stakabadhi nyuma
ya kitabu chako cha cheki pamoja na taarifa zako zikiwa
zimechapwa hapo. Kama hauna zenye taarifa zako, benki itakuwa nazo stakabadhi ambazo hazijajazwa. Kama
unatumia stakabadhi ya amana ambayo haijajazwa, hakikisha unaweka taarifa zako zote ili benki ielewe kamba ni pesa zako!
Subtotal
Less Cash
Back
Checking or Savings Account Number
Date
Deposit (check one): Checking Saving
Name:
Address:
Signature:
X
Checks
Total $
Cash
Andaka namba ya
akaunti yako hapa.
Kama haujui namba
yako, muulize
mfanyakazi wa
benki
Unaweka alama
pembeni ya aina
ya akaunti
unapotaka kuweka
pesa
Unaweka
tarehe ya
siku
unayoweka
pesa
Andika jina
lako, anwani
na usaini hapa.
Andika kiasi cha
kila cheki
unayoweka katika
kila moja ya hizi
boxi
Andika kiasi
cha pesa
taslimu
unazoweka
Weka jumla ya
cheki zote na pesa
taslimu unazoweka
hapa.
Weka
senti
hapa.
Kumbuka, kama hauna uhakika jinsi ya
kujaza fomu, mfanyakazi wa benki
(teller) yupo kujibu maswali yako.
Jumlisha
pesa zote
ulizoweka
Kama unataka
mfanyakzi wa benki
akurudishie pesa,
andika ni kiasi gani
unataka hapa.
37
Activity/Zoezi: Depositing Money/Kuweka pesa Jaribu kujaza stakabadhi ya amana hapo chini kama vile ungelikuwa unaweka cheki mbili, moja ya dola $158.22 na nyingine ya $40.00 katika
akaunti yako ya matumizi ya kila siku. Unataka pia mfanyakazi wa benki akurudishie dola $40 taslimu. Namba yako ya akaunti ni 123456789.
Subtotal
Less Cash
Back
Checking or Savings Account Number
Date
Deposit (check one): Checking Saving
Name:
Address:
Signature:
X
Checks
Total $
Cash
38
Endorsing Checks/Wekea mkono au sahihi cheki Unapoweka cheki uliyoandikiwa benki, unapaswa kusaini nyuma ili itambue kwamba ilikuwa ni wewe. Hii inaitwa kuwekea kuwekea mkono au
sahihi cheki.
KUWA MAKINI! Cheki ikiisha wekewa sahihi mtu yeyote anaweza
kuibadilisha na pesa taslimu. Kwa hiyo, subiri hadi utakapo kuwa benki
ili uweke sahihi yako!
Tumia kila wakati karamu yenye rangi nyeusi au blu.
Weka sahihi yako pale palipo andikwa “Endorse here”tu.
Weka jina lako vile vile linavyoonekana kwenye ule mustari usemao
“Pay to the Order Of” upande wa mbele wa cheki. Andika namba ya
akaunti chini ya sahihi yako.
Kama unataka kuweka cheki, andika “For Deposit Only” juu ya sahihi
yako na uweke namba ya akaunti yako chini ya sahihi yako.
Kama unataka kuweka sahihi lakini cheki iende kwa mtu mwingine,
andika“Pay to the Order Of” ufuatishe jina la mtu unayetaka ile cheki
iende kwake. Halafu weka jina lako chini yake.
ENDORSE HERE
WEKA SAHIHI YAKO HAPA
________________________________
________________________________
________________________________ Do not write, stamp, or sign below this line. Reserved for
Financial Institution Use.
39
Balancing Your Checkbook/Kusawazisha kitabu chako cha
hundi
Kama unayo akaunti ya matumizi ya kila siku, kiasi cha pesa katika hiyo
akaunti yako kitabadilika sana kwa kipindi cha mwezi. Unapaswa kufahamu vizuri ni kiasi gani cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako ili uhakikishe
haundiki cheki inayozidi pesa ulizonazo. Kufanya hivyo, unapaswa kufuatilia kwa makini kila
unapochukua pesa kwenye akaunti yako, unapoandika cheki au kuongeza pesa kwenye
akaunti yako. Kufuatilia kiasi cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako inaitwa kusawazisha kitabu
chako cha hundi/cheki.
Kama utaandika cheki/hundi yenye thamani
ya pesa zaidi ya ulizonazo benki, inaitwa kurudishiwa cheki. Ukirudishiwa cheki, benki inakutoza ada ya ziada, inaweza kufunga akaunti yako na
kukuweka kwenye orodha ya ChexSystems. Hii itaathiri kiwango cha kuaminiwa kwenye mikopo na inaweza kusababisha kuwa vigumu kwako
kufungua akaunti na benki nyingine kwa kipindi cha miaka mitano.
Kama kuna tatizo unaposawazisha kitabu
chako cha hundi unaweza kupiga simu benki. Namba
ya simu itakuwa kwenye kadi yako ya ATM au taarifa
yako ya benki.
40
How To Balance Your Check Book/Jinsi unavyosawazisha
kitabu chako cha hundi Kufuatilia cheki zako, pesa unazoweka na kutoa benki, tumia rejesta ya
cheki inayokuja na cheki zako. Kutumia rejesta ya cheki, fuata hatua zifuatazo:
1) Kama unaandika cheki andika namba za cheki kwanza.
2) Andika tarehe 3) Andika maelezo kwa kifupi ya kile unachokifanyar. Kama ni pesa
unachukua kwenye akaunti yako andika uliyemlipa au ulichozichukulia (kodi, mavazi, chakula). Kama unaongeza pesa
kwenye akaunti yako andika pesa zimetoka wapi (malipo ya kazini, zawadi).
4) Kama umetoa pesa kwenye akaunti yako au kuandika cheki weak kiasi katika mnara wa “malipo/mtoe” (“Payment/Debit”).
5) Kama unaongeza pesa kwenye akaunti yako weka kiasi katika mnara
wa Kuweka/Mkopo (Deposit/Credit). 6) Andika kiasi cha nyongeza au pungufu katika mnara wa wa mwisho.
Toa au ongeza kiasi kwenye baki halafu weka baki mpya kwenye mustari unaofuata.
Number Date Transaction Description Payment/Debit Deposit/Credit Balance
Kama
unarekodi
cheki weka
namba hapa.
Andika neno moja au
mawili ya maelezo ya nani
uliyemwandikia cheki, kwa
nini umechukua au kuweka
pesa kwenye akaunti yako.
Andika kiasi cha pesa
zozote unazoweka kwenye
akaunti yako hapa. Pesa
zinazoingia tu ndizo
zinazowekwa katika huu
mnara.
Andika
tarehe
hapa
Andika kiasi cha pesa
unachotoa kwenye akaunti
yako hapa. Kumbuka kuweka
cheki na pesa taslimu
ulizochukua kwenye ATM au
kupewa na mfanyakazi wa
benki. Pesa zinazotoka tu
ndizo zinazowekwa katika
huu mnara
Andika kiasi cha pesa
ulizonazo kwa sasa kwenye
akaunti yako katika mnara
huu wa rangi ya kijivu.
Halafu andika kiasi cha pesa
unazoongeza au kutoa
kwenye eneo la rangi
nyeupe. Ongeza au toa
hicho kiasi kujua baki yako.
41
Activity/Zoezi: Balancing Your Checkbook/Kusawazisha
kitabu cha hundi Jaribu kurekodi shughuli za pesa zifuatazo na usawazishe kitabu cha
hundi kifuatacho hapo chini. Tutafanya huu mfano kwa pamoja kama darasa. Chukulia kwamba unaanza na baki ya dola $700.
Novemba 3 uliandika cheki ya mwenye nyumba ya dola $650.00 Novemba 7 ulilipwa cheki ya $530.00
Novemba 10 uliandika cheki (namba 125) ya $48.87 ya Ralph’s.
Number
Date
Transaction Description
Payment/Debit
Deposit/Credit
Balance
Sasa jaribu kufanya mfano huu pekee yako. Unaanza na baki ya $531.13
Desemba 1 ulilipwa $800.00 Desemba 4 unachukua $75 taslimu kutoka benki
Desemba 6 unaandika cheki namba 126 kulipa deni la kadi yako ya mkopo ya dola $122.08
Number Date Transaction Description Payment/Debit Deposit/Credit Balance
$700.00
42
Upande 4.0
Credit/Mkopo
Katika upande huu tutazungumzia mkopo ni nini, umuhimu wake, kwa nini unauhitaji na jinsi unavyoweza kutumiwa.
BASIC DEFINITION/UFAFANUZI WA MSINGI Mkopo ni mapatano juu ya malipo ya taratibu ambayo kawaida hufanyika
kati ya taasisi za fedha kama benki au kampuni za kadi za mikopo. Hizi kampuni mara nyingi huitwa wakopeshaji kwa sababu zinakopesha pesa. Kwa
kifupi, ni sehemu ambayo mkopeshaji anakupa pesa kwa sasa na kubadilishana pesa kwa baadae. Benki zinafanya hivyo kwa masharti mawili:
1. Wakopeshaji wanaamini kwamba wewe
ni mwaminifu na kwamba utazirudisha pesa;
2. Wakopeshaji watatoza ada kwa kufanya
hivi.
Ili uwe mwaminifu kwa mtazamo wa wakopeshaji unapaswa au
kuendeleza historia ya kukopesha pesa na kuzirudisha baada ya muda. Kadiri unavyozidi kufanya hivi, ndivyo mkopeshaji atakuamini. Wakopeshaji hupanga
ada kwa misingi ya jinsi wanavyoamini wewe ni mwaminifu. Kawaida, wakikuamini zaidi ada inakuwa ndogo.
CREDIT BASICS/MISINGI YA MIKOPO Marekani, mkopo ni muhimu sana. Unatumika kama msingi wa kununua
bidhaa zilizo nyingi na huduma. Mara nyingi watu wanakuwa hawana pesa za kutosha kununua bidhaa Fulani na huduma, kama meza, mashine za kufulia na
kukaushia nguo, magari, nyumba, simu, au matengenezo. Mtu anapaswa kutumia mkopo kununua hizi bidhaa na huduma, ambavyo ni sawa na
kukopesha pesa za kununua bidhaa au huduma kwa wakati huu na kulipa zile pesa kwa baadae.
Kwa mfano, kujenga mkopo ni sawa na
kujenga nyumba—inachukua muda, vinapaswa kufanyika kwa uangalifu, na
vinapaswa kuwa na msingi imara. Unapojengwa vizuri unakuwa imara Sana.
Credit/Mkopo ni
wakati benki au kampuni nyingine
inakukopesha pesa
na kukuamini kwamba
utazirudisha.
43
HOW IS CREDIT USED/MKOPO UNAVYOTUMIWA Tutazame mfano kama wakunua gari. Mohamed anaamua ni gari gain
anayotaka kununua moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine au kutoka kwa mfanyabiashara. Anafahamu kuwa inauzwa $15,000, lakini hana kiasi hicho
cha pesa. Ili ainunue, Mohamed anapaswa kuzungumza na mkopeshaji ambaye atapaswa kutoa kulipia gari. Hizi pesa anapewa mmiliki wa gari au
muuza magari. Lazima sasa Mohamed arudishe zile pesa kwa mkopeshaji.
Swali ni kama mkopeshaji atazimpa pesa Mohamed? Mkopeshaji ataweza kuamini kwamba Mohamed atarudisha pesa? Swali la kwanza atakalouliza
mkopeshaji ni kama Mohamed aliwahi kuazima pesa kabla. Kama ndiyo, sasa watauliza ni wapi ili wachunguze. Watabaini kama Mohamed alizingatia muda
katika malipo yake au hapana.
Kama Mohamed aliazima pesa mara nyingi na kuzilipa kwa muda sasa
atakuwa ana kitu kinachoitwa “historia nzuri ya mkopo”. Kama hakufanya hivyo, basi atakuwa ana “historia mbaya ya mkopo”. Inaweza kuwa kwamba
Mohamed hajawahi kuazima pesa na hana “historia ya mkopo”. Tutazame yote matatu:
1. Historia nzuri ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopeshaji ataelekea
kumpa pesa Mohamed.
2. Historia mbaya ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopesahji hatampa pesa Mohamed.
3. Hakuna historia ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopeshaji
anaweza kumpa pesa kidogo tu Mohamed ili aweze kujenga historia ya mkopo. Mohamed anaweza kuhitaji kununua gari ndogo.
Hii ndiyo maana mkopo ni muhimu sana. Unaonyesha historia ya kulipa mikopo. Inaweza kuwa nzuri au mbaya. Kama wewe ni mzuri wa kulipa
mikopo yako, mkopo unaweza kuwa mzuri kwa sababu unakuwezesha kuazima pesa. Kama una mkopo mbaya, inaweza kusababisha kuwa ngumu au
kushindikana kuazima pesa.
Different uses of the word Credit
Matumizi mbali mbali ya neo mkopo
Credit Card/Kadi ya mkopo: Kadi ndogo ya plastiki yenye namba
maalum inayotolewa na mkopeshaji ambayo inakuwezesha kuazima
pesa. Zilizozoeleka ni kutoka VISA, Mastercard or Discover.
44
Credit Agency/Wakala wa mkopo: ni kampuni inayofuatilia historia
ya mkopo. Zinatoa pointi kwa wakopeshaji kuonyesha kwamba una historia nzuri, mbaya au hauna kabisa historia ya mkopo.
Credit Score/Pointi za mkopo: nambari zinazoonyesha jinsi mkopo
ulivyo mzuri au mbaya
Credit Report/Ripoti ya mkopo: Wakala wa mikopo anatoa ripoti na
pointi za mkopo kwa wakopeshaji, ambayo inaunganisha historia ya mkopo.
Kadi za mkopo Ripoti/pointi za mkopo Wakala mikopo
CREDIT SCORE/POINTI ZA MKOPO
Sehemu muhimu ya ripoti ya mkopo itakuwa pointi za mkopo. Pointi
zako za mkopo ni namba inayoonyesha jinsi ulivyo katika kulipa pesa ulizoazima kwa mkopeshaji. Kampuni za kadi za mikopo, benki au vyama vya
mikopo vvote vitatumia namba hii kuamua kama vinaweza kukukopesha pesa.
Inakuwa mahali Fulani kati ya 100 na 900. Pointi zikiwa nyingi, mkopo unakuwa mzuri. Hii hapa ni maana ya pointi za mkopo:
700 to 800: Mkopo ulio bora sana
600 to 700: Mkopo mzuri 550 to 599: Mkopo mbaya
100 to 549: Mkopo mbaya sana
45
Ukiwa na pointi nzuri za mkopo, benki na biashara zingine zitakukopesha
pesa na kukutoza riba na ada ndogo. Kupata mkopo itakuwa rahisi na bei nafuu.
Kwa hiyo ni vipi wakala wa mikopo anatoa pointi zako za mkopo?
46
Credit Diagram
Mchoro wa mkopo
Kama mchoro unavyoonyasha, mikopo na kadi za mikopo ripoti mikopo
mizuri. Kwa mara nyingine, njia pekee ya kujenga mkopo wako ni kuazima pesa na kuzilipa!
*Note: Benki yako inaweza kukupa “Kadi” yenye nembo ya Visa. Kutumia hii kadi ni sawa na
kuandika cheki, na pesa inatoka kwenye akaunti yako ya benki. Hii siyo kadi ya mkopo, huwezi
kuazima pesa, na haikusaidii kujenga mkopo.
What Are the Different Kinds of Credit? Ni zipi aina tofauti za mkopo? Unaweza kupata mkopo katika njia tofauti. Aina zilizozoeleka ni:
Credit Cards/Kadi za mikopo
Buying a home/kununua nyumba: Wakopeshaji watakupa rehani ili uweze kununua nyumba. Kawaida unailipa benki kwa
muda wa miaka 30.
Collection
Agencies/Wakala wa
ukusanyaji
Credit
Agencies/Wakala wa mikopo:
TransUnion
Experian Equifax
Utilities/Hudum
a za umma
Gas Electric
Phone Landlord/Rent
Mwenyenyumba/Kodi
Checks credit
Reports only
negative credit
Loans/Miko
po
IOM Loan Car Loan
School Loan Home Loan
Bank Loan
Checks credit
Reports
positive and negative
credit
Credit Cards
Kdai za mikopo
VISA*
Mastercard
Discover Store Cards
(gas, department
store, etc.) Bank Cards
Checks credit
Reports
positive and negative
credit
Other
Mengineyo
Medical Bills
Parking Tickets
Subscriptions
Sometimes
checks credit
Reports only negative credit
47
Buying a car/Kununua gari: Wakopeshaji watakupa mikopo ya
kununua gari. Buying major appliances/Kununua vifaa muhimu vya ndani:
Wakopeshaji watakupa mikopo ya kununua mashine za kufulia na kukaushia nguo, kipozeo, mashine ya kuosha vyombo na jiko.
College/Shule: Serikali na wakopeshaji watakupa mikopo ya kwenda shule.
48
Bankruptcy/Taflisi ina
maana kwamba huwezi kulipa deni lako.
Kutangaza kufilisika yamaanisha kwamba
hulazimiki kulipa hili
deni. Pamoja na hayo,
kutangaza kufilisika vitaathiri viwango vyako
vya mkopo kwa muda wa miaka saba. Itakuwa
vigumu sana kuazima pesa yoyote kwa wakati
huu. Pili, maamuzi yote kuhusu hali ya kifedha
yatatoka mikononi mwako na kuwekwa
katika mikono ya hakimu. Tatu, hakimu
atatoa amri ya
kutokuruhusu kusimamia nyingi kati ya mali zako.
THE IMPORTANCE OF CREDIT
UMUHIMU WA MKOPO
Kuwa na mkopo na kujua kuusimamia ni moja
ya ujuzi wa kifedha muhimu zaidi unaoweza kuwa nao. Kama unatumia mkopo kwa hekima inaweza
kukusaidia kuyafikia malengo yako kifedha. Kama utatumia mkopo visivyo unaweza kukuathiri vibaya
wewe na familia yako. Hizi hapa takwimu mbili kukuonyesha jinsi mkopo unavyoweza kuwa mzuri au
mbaya: 68% ya Marekani wanamiliki nyumba zao
(US Census Bureau). Walio wengi kati yao walikopesha pesa kununua nyumba zao.
Miaka 30 ijayo, 38% ya familia za
kimarekani watatangaza kufirisika (zaidi ya mmoja kwa kila watu watatu).
The Benefits of Credit/Faida za mkopo Tayari tumezungumzia faida muhimu za mkopo:
Nyumba, gari, elimu: mkopo unakusaidia
kununua vitu kama nyumba, gari
ambavyo usingeweza kuvilipia kama ungelitakiwa kulipia vyote kwa pamoja.
Kufaa kwake: Badala ya kutembea na pesa taslimu unaweza kununua vitu kwa
kutumia kadi yako. Dharura: Kuwa na mkopo inakupa uwezekano wa kutumia zaidi
kwa wiki au mwezi kuliko uwezo wako wa kawaida. Kama una dharura ya muda mfupi, mkopo unaweza kukusaidia kununua
unachokihitaji, hata kama ulikuwa hauna uwezo wa kukinunua kwa wakati huu. Kwa mfano, kama kipozeo chako kikiharibika au mtu
mmoja katika familia yako akaumwa na akatikiwa kwenda hospitali.
49
The Dangers of Credit/Hatari za mkopo Tayari tumezungumzia pia hatari kubwa za kutumia mkopo. Moja kati ya wa Marekani watatu watafilisika katika miaka 30 ijayo. Matumizi mabaya ya
mkopo ndiyo chanzo kikubwa cha kufilisika. Hii ni kwa sababu: Watu wengi hawatumii kwa hekima kwa sababu hawatakiwi kulipia
wanavyovitaka papo hapo. Ukiwa na kadi ya mkopo ni rahisi kutumia zaidi ya ulivyotakiwa.
Kununua vitu kwa mkopo leo yamaanisha kwa utatakiwa kulipia
hivyo vitu na kipato chako cha siku zijazo. Kama unanua chakula cha usiku kwa kutumia kadi yako ya mkopo leo unaweza kukilipia
kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, hata mwaka kesho. kama unalipa ada na riba inaweza kuwa gharama kubwa. Kama
unanua kitu kwa dola $100 kutumia mkopo na kurudisha pesa kwa muda mrefu unaweza
kuishia kulipa dola $150, $200 au zaidi kwa kitu
ambacho kingekugharimu dolar $100 tu.
How Much Can Buying on Credit Cost? Ni kiasi gani unaweza kununua kwa gharama ya mkopo?
Kama unazo dola $500 kwenye kadi yako ya mkopo na malipo ya chini
ya dola $10 kwa mwezi na riba ya asilimia 18% kwenye kadi yako ya mkopo
itakuchukua miaka 8 kumaliza kulipa unavyoidaiwa. Kwa muda huo utakuwa umelipa dola $440 za riba. Kwa hiyo ulichokinunua kwa dola $500
kilikugharimu $940!
CREDIT REPORTS/RIPOTI ZA MIKOPO
Benki na kampuni zingine hazitakuacha uazime moja
kwa moja pesa kwao. Watawapa mkopo watu wanaofikiria
Familia nyingi za kimarekani zinatumia mkopo kununua wanavyovitaka lakini hawana uwezo navyo. Ni rahisi
kuendelea kununua vitu ambavyo hauna uwezo navyo kwa mkopo hadi utakaposhindwa kulipa mikopo yako.
Hapa ndipo mkopo unapoweza kugeuka jinamizi. Utaratibu mzuri ni kutonunua kamwe kitu ambacho
haukihitaji kweli kwa mkopo labda kama ungekilipia mwezi huo.
Ripoti ya mkopo
inaonyesha ulivyolipia deni la
kadi yako ya mkopo na mikopo mingine.
50
watarudisha pesa zao tu. Kuamua kama utawalipa hizi kampuni zinaangalia
ulivyoshughulikia mikopo ipindi kilichopita. Hapa ndipo inapotumiwa ripoti yako ya mkopo.
Kama unataka kununua nyumba, kununua gari, kukodi nyumba,
kununua mpango wa simu ya mkononi… kwanza muuzaji atapiga simu kuulizia ripoti yako ya mkopo kutoka kwa wakala wa mikopo. Ripoti ya mkopo ni
muhtasari wa nyakati zote ulizojikopesha pesa katika maisha yako (ukiwa Marekani). Itaorodhesha kiasi ulichojikopesha, kama ulilipa kwa muda na kiasi
unachodaiwa kwa muda huu. Itaonyesha ni mara ngapi ulichelewesha malipo na kama ulichelewa siku 30, 60, 90 au zaidi. Ripoti ya mkopo haitoi rekodi ya
taarifa kuhusu rangi yako, dini yako, historia ya afya yako, utaratibu wa maisha yako, rekodi ya makosa ya jinai, au siasa. Ripoti za mikopo
zinaandaliwa na kampuni tatu za mikopo: Equifax, Experian, and TransUnion. Kampuni zilizokukopesha pesa zinawapa taarifa hizi. Taarifa ya mkopo
inaorodhesha taarifa zitakazomsaidia mtu kuamua kama atakupa mkopo au la.
Taarifa zinazoorodheshwa zinaunganisha:
Identifying information/Taarifa za utambulisho: jina lako, anwani ya sasa na ya zamani, namba ya simu, namba ya Social Security, tarehe ya
kuzaliwa, mwajili wako wa sasa na wa zamani.
Credit information/Taarifa za mkopo: Taarifa kuhusu kadi za mkopo, mikopo ya shule, na mikopo mingine. Kwa mfano, mkopo wa IOM
utaorodheshwa kwenye ripoti yako ya mikopo. Taarifa maalum zinahusu: Malipo yanafanyika kwa muda unaotakiwa? Kama hapana,
yanacheleweshwa siku 30, 60, 90+ au zaidi? Ukikamilisha malipo ya mkopo wa IOM, hili litaonekana katika ripoti yako mikopo pia.
Tarehe uliofunguliwa Tarehe ulipofungwa
Kiasi unachodaiwa
Baki Malipo kwa mwezi
Ukusanyaji (wakati kampuni inayokudai inapoita mawakala wa ukusanyaji kwa sababu haulipi)
Kunyanganywa (kampuni inapokunyanganya kitu ilichokuuzia kwa sababu umeshindwa kulipa)
Ukusanyaji, kunyanganywa na ucheleweshwaji wa malipo unaojirudia ni vitu vibaya sana katika ripoti yako ya mkopo. Vikiwa vingi vitakusababishia ugumu
wa kupata mkopo.
Public record information/Rekodi ya taarifa za serikali: rekodi za kufilisika, nyumba kufungwa, ushuru unaodaiwa au ambao haukulipiwa,
uamuzi wakifedha wa mahakama, na pesa za malezi ya watoto ambazo baado zinadaiwa.
51
Inquiries/Maulizo: majina ya wale walioomba nakala ya ripoti yako ya mikopo na tarehe walipoyiomba. Kampuni haiwezi kuomba ripoti yako ya
mikopo bila ridhaa yako (kwa maandishi au kwa mdomo). Kwa mfano, kama unafanya maombi ya ripoti yako ya mikopo au ripoti yako ya mikopo
inapovutwa ili upate taarifa kuhusu kununua gari. Maulizo mengi yanweza kuathiri mkopo wako kwa sababu inaonekana unahangaika kupata mkopo.
Credit score/Pointi za mkopo: namba inayotumiwa kutabiri jinsi mtu
anavyoelekea katika kulipa kwake mkopo mpya. Pointi za mkopo zitazungumziwa kwa upana wakati ujao.
How to order your credit report/Namna ya kuomba ripoti ya mkopo:
Checking for mistakes/kuchunguza makosa: Chunguza kwa makini
makosa katika ripoti yako ya mkopo na uhakikishe yanasahihishwa. Kwaida ripoti ya mkopo inaunganishwa na taarifa juu ya namna ya kusahihisha
makosa. Anzia kupiga simu kwa wakala wa mikopo (namba zimeorodheshwa hapo juu). Kwaida inafuata barua inayoelezea/fafanua kosa. Unaweza kuhitaji
kuambatanisha cheki zilizobatilishwa au vielelezo vingine vya malipo. Mfano
Getting Your Report/Kupata ripoti yako
Kwa mjibu wa sheria, wanunuzi wote Marekani wanahaki yakupewa ripoti ya mkopo (1) bure kwa mwaka kutoka kila moja ya ofisi kubwa za mikopo: Trans
Union, Equifax and Experian. Ni rahisi sana kuziomba:
Phone: 1(877)-322-8228
Address: P.O. Box 105281, Atlanta, GA 30348-5281 Web Site: www.Annualcreditreport.com
Au omba ripoti yako ya mkopo kutoka kwa mmoja kati ya mawakala watatu wa
mikopo:
Experian 1-888-EXPERIAN (1-888-397-3742) www.experian.com
Equifax 1-800-685-1111 www.equifax.com Trans Union Corporation 1-800-916-8800 www.transunion.com
Utahitaji kutoa jina lako, namba yako ya social security, tarehe ya kuzaliwa, na
anwani. Unaweza kuomba ripoti zote tatu kwa wakati mmoja, au moja kila miezi nne.
52
wa barua ya kuwatumia wakala wa mikopo kwa ajili ya kusahihisha makosa
inapatikana katika kiambatanisho. Kama wakala wa mikopo hatasahihisha kosa na baado wewe unaamini lipo kosa, wapigie simu wakopeshaji moja kwa
moja na uwaombe wawatumie mawakala wakuripoti mikopo taarifa sahihi. Tuangalie mfano wa ripoti ya mikopo katika kiambatanisho tuone
inavyofanana.
The Cost of Buying a Home/Gharama ya kununua nyumba:
MALIPO KWA MWEZI KWA REHANI YA MIAKA 30 ISIYOBADILIKA
Mortgage/ Rehani ni mkopo mkubwa unaotumika kununua nyumba. Unatunza pesa
kwa ajili ya malipo ya kwanza, benki inakununulia nyumba, halafu unailipa benki
taratibu, kawaida kwa miaka 30.
Tutazame jinsi viwango vya riba ulivyonavyo kwenye rehani yako
vinavyoweza kuathiri malipo yako kwa mwezi…
Kumbuka: Hii chati haiunganishi ada ya umiliki wa nyumba inayoweza kuombwa kwenye
nyumba za condos
Loan
Amounts Kiasi cha
mkopo
Interest Rates/Viwango vya riba
5.5% 6% 6.5% 7% 7.5% 8% 8.5% 9% 9.5%
$20,000 $114 $120 $126 $133 $140 $147 $154 $161 $168
$40,000 $227 $240 $253 $266 $280 $294 $308 $322 $336
$60,000 $341 $360 $380 $399 $420 $440 $461 $483 $505
$80,000 $454 $480 $506 $532 $559 $587 $615 $644 $673
$100,000 $568 $600 $632 $665 $699 $734 $769 $805 $841
$150,000 $852 $1049 $1261
$200,000 $1136 $1398 $1682
$250,000 $1419 $1748 $2102
$300,000 $1703 $2098 $2523
$350,000 $1987 $2447 $2943
$400,000 $2271 $2797 $3363
$450,000 $2555 $3147 $3784
$500,000 $2839 $3496 $4204
$800,000 $4542 $5594 $6727
$2,000,000 (2 MILLION!)
$11,356 $13,984 $16817
53
Kama unavyoona, kiwango cha riba kinavyokuwa kidogo, malipo kwa mwezi kwa ajili ya rehani yako ndivyo yanavyokuwa madogo. Pointi za mkopo
wako zikiwa nzuri, kiwango chako cha riba kitakuwa kidogo!
54
Zaidi ya kuangalia pointi zako za mkopo, uanpokwenda
kununua nyumba,
mkopeshaji/dalali atakuuliza maswali ili atambue kama
unakubalika kupewa mkopo: Kipato chako ni kiasi
gani? Historia yako ya kazi iko je?
Una historia ya mkopo? Unalipa madeni yako kwa
muda? Una akiba ya pesa
kwenye akaunti yako ya benki kwa ajili ya malipo
ya kwanza na gharama za kufunga? (kawaida
malipo ya kwanza ni kati
ya asilimia 5-20% ya bei ya kununua)
Una madeni gani kwa wakati huu?
Utayaweza malipo ya mwezi? Malipo
yanategemeana na kiasi cha mkopo, riba, na
muda wa malipo (kawaida miaka 30).
Wanaweza pia kuongeza ada ya umiliki wa
nyumba.
Tutazame mfano wa tofauti katika kupata mkopo wa nyumba kwa watu
watatu.
Azra anakwenda benki. Anataka kununua nyumba.
Mfanyakazi wa benki anavuta ripoti yake ya mkopo kutoka
kwa wakala wa mkopo na anakuta kwamba pointi zake
zinakaribia 800. Pointi zake za mkopo zinaonyesha kwamba anaweza
kuwa kivutio kwa mkopeshaji na anaweza kupata mkopo kwa riba ndogo ya asilimia
(5.5%). Kwa sababu anazo pointi nyingi za mkopo, itakuwa rahisi
sana kuweka pamoja fomu
za mkopo na dalali hatozi ada kubwa. Bila kuchukua
muda mrefu, Azra anaweza kuhamia nyumba yake mpya!
Pili Kalel anakwenda benki ile.
Anataka kununua nyumba. Pointi zake za mkopo siyo nzuri kama za Azra lakini siyo
mbaya sana. Ziko kati ya 600-700. Anaweza kupata mkopo lakini riba itakuwa
kubwa na mkopo hautakuwa rahisi. Labda atalazimika kutoa nakala za karatasi
anazopokelea mshahara na taarifa za benki. Labda wadhamini watahitaji kuitwa.
Inaomba mambo ya ziada kuhakikisha
kwamba ataulipa mkopo. Kwa sababu ni kazi nyingi, pamoja na riba ya juu sana,
benki itatoza ada kubwa na itachukua muda mrefu kabla hajahamia kwenye
nyumba yake mpya.
Tatu, Ibrahim anakwenda benki ile ile. Anataka kununua nyumba. Mfanyakazi wa benki anavuta ripoti yake ya mkopo na anagundua
kwamba pointi zake ni 300 na ana taarifa ya kulisika kwenye ripoti yake. Ni mara chache amefanya malipo yake kwa muda, na malipo
mengi yalicheleweshwa kwa zaidi ya siku 90. Mfanyakazi wa benki hawezi kumpa mkopo kwa sababu mkopo wake ni mbaya sana!
Atatakiwa kumaliza miaka mingi akiboresha mkopo wake kabla ya kununua nyumba. Tutazama njia za kujenga na kuboresha mkopo.
55
HOW TO GET A GOOD (OR BETTER) CREDIT SCORE
NAMNA YA KUPATA POINTI NZURI ZA MKOPO
Kama unavyoweza kuelezea, kuwa na ripoti nzuri ya mkopo yaweza kuwa muhimu sana kwa
ajili ya malengo yako ya muda mrefu. Utatakiwa kujifunza namna ya kusimamia mkopo wako ili,
wakati ukiwa mwafaka, unaweza kuazima pesa za shule, gari au hata nyumba. Hizi hapa hatua
muhimu zaidi unazoweza kuchukua kujenga au kuimarisha pointi zako za mkopo.
Lipa madeni yako kwa wakati kila mara. Hata kama unalipa
kiwango cha chini ni muhimu sana ulipe angalau hicho kiasi kwa
wakati. Hii ni pamoja na deni la kadi yako ya mkopo, malipo ya mkopo, malipo kwa ajili ya huduma za umma, na kodi ya nyumba.
Deni la International Organization of Migration (IOM) mkopo wa nauli ya ndege iliyokuleta Amerika.
Ideas for paying your bills on time/Mawazo ya kulipa deni kwa wakati
: Weka alama kwenye kalenda ni lini unapaswa kulipa deni kila
mwezi Lipa madeni moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya
matumizi ya kila siku kila mwezi (lakini kumbuka kuhakikisha kuna pesa za kutosha kulipa deni kwenye akaunti yako).
Mafuta ya gari, umeme, simu, bima na makampuni mengine mara nyingi yanaruhusu wateja wake kulipa kwa njia hii.
Ukienda nje ya mji, fanya mpango wa kulipa madeni kwa
wakati (lipa kabla ya muda, nk.) Ukipata taarifa juu ya malipo yaliyochelewa, ni muhimu sana
kulipa deni papo!
Make More Than Your Minimum Payments/Lipa zaidi ya kima cha chini cha malipo. Ukilipa kima cha chini tu
itakuchukuwa miaka mingi kulipia ulivyonunua.
Spend wisely/Tumia kwa makini. Nunua ulivyo na uwezo navyo tu. Ni rahisi sana kuweka kitu kwenye mkopo kama hauna uwezo
nacho kwa sasa. Lakini kumbuka, kadiri vitu vinavyokaa muda mrefu kwenye kadi yako ya mkopo ndivyo unavyolipa riba kubwa
na ndivyo vitu ulivyonunua vinavyopanda bei. Kama leo hauna
Kumbuka, pointi za mkopo
zinavyokuwa nyingi, ndivyo inavyokuwa rahisi
kupata mkopo mbeleni. Unapokopesha pesa utalipa riba ndogo.
56
uwezo wa dola $50 kwa ajili ya kitu, huenda kesho usipate dola
$75 kwa ajili ya kitu kile kile!
Use Credit/Tumia mkopo. Kutokopesha pesa haikusaidii kupata pointi nzuri za mkopo kwa sababu makampuni hayatajua cha
kutegemea. Hii haina maana kwamba utatakiwa kutumia pesa usizokuwa nazo.
Increasing
Your Credit Score
Kuongeza pointi zako za
mkopo
Decreasing
Your Credit Score
Kupunguza pointi zako za
mkopo Kulipa madeni kwa muda kila mwezi Kudai kiasi kikubwa kinachowezekana
Kutumia pesa kwenye mahitaji na
mikopo kabla ya kutumia kwenye matakwa.
Kutokulipa madeni
Kutumia mkopo kwa uangalifu Kuchelewa kulipa madeni Kulipa baki yote kwenye kadi za mkopo kila mwezi
Kutangaza kufilisika
Kutumia kadi za mkopo kwenye mahemezi pale unapokuwa na pesa
taslimu zinazotosha mahemezi hayo
Kupunguza deni
Caution/Tahadhari: Kaa mbali na makampuni yanayorekebisha
mokpo “Credit Repair”!
57
CREDIT CARDS/KADI ZA
MKOPO Kuwa na kadi ya mkopo ndiyo aina ya
mkopo ya kawaida watu wanayotumia. Zipo taarifa za msingi kuhusu kadi za mkopo
unazohitaji kujua kabla ya kufikiria kujisajiri kupata moja.
CHOOSING A CREDIT CARD
KUCHAGUA KADI YA MKOPO Unapofikiria kuhusu kujisajiri kupata kadi
ya mkopo unatakiwa kuhakikisha unajua unachokubali. Baadhi ya kadi za mkopo zinatoza ada na riba za juu
zaidi ya zingine. Kwa hiyo unatakiwa kulinganisha angalau mbili kabla ya
kuweka sahihi.
Nyumba ya kila kadi ya mkopo inayouzwa ipo boxi yenye taarifa
muhimu kuhusu kadi ya mkopo. Unatakiwa kuzisoma hizi taarifa kwa
makini ili upate moja yenye riba
ndogo, isiyolipisha ada na inayotoa kipindi kirefu cha uvumilivu.
Ukielewa sheria na taratibu za kadi ya mkopo unaweza kuepuka kulipa ada na gharama zingine.
Credit Limit/Mpaka wa mkopo
Kuwa na kadi ya mkopo yamaanisha kukubaliwa kuazima kiasi Fulani cha
pesa wakati wowote. Hii inaitwa mpaka wa mkopo wako. Wakati wowote unapolipa unachodaiwa unaruhusiwa kukopesha kadi ule mpaka wa mkopo
wako tena. Kwa hiyo, mpaka wa mkopo wako ulikuwa ni dola $1,000
na ulikuwa unadaiwa dola $500 unaweza kuazima zingine dola $500.
Ukilipa dola $500 ulizokuwa
unadaiwa unaweza sasa kuazima dola $1000 kamili. Lakini ukitumia
zaidi ya mpaka wa mkopo wako unavyokuruhusu, unapaswa kulipa
ada kuvuka ule mpaka wako.
Islam and Credit
Cards/Uislamu na kadi za mkopo “Kwa waislamu,
inawezekana kuwa na kadi ya mkopo, lakini hatua kali
zinapaswa kuchukuliwa kuepuka
kuchelewa kulipa baki yote kwa ujumla,” ili kutokusababisha
riba. “ (Kutoka Muslim-investor.com)
Remember/Kumbuka: Jaribu kulipa baki yako kwa ujumla kila mwezi. Lakini,
bila kujali lolote, lipia kadi yako ya mkopo kima chako cha chini. Ukisahau kulipa
kima chako cha chini, kampuni ya kadi za mikopo itakutoza ada ya kuchelewa na
riba ya ziada. Hii inaongeza gharama zaidi. Kama una matatizo ya kulipa
madeni yako, wapigie simu wakopeshaji
wako kabla ya kushindwa malipo.
58
Kwa mfano: Mpaka wa mkopo wako ni dola $1,000. Ukinunua gari
lilotumika kwa gharama ya dola $1,200 na kadi yako ya mkopo. Taarifa yako ya benki inayofuata itaonyesha ada ya kuvuka mpaka. Hii inaweza kuwa
dolahis $30, $40, au $50! Utatakiwa kulipa hii ada kila mwezi utakaokuwa umevuka mpaka wa mkopo wako.
Interest Rate/Kiwango cha riba Usipolipa kiasi chote cha pesa unazodaiwa mwezi wa kwanza utatozwa
riba juu ya kile unachodaiwa kila mwezi baada ya hapo. Kama utalipa kima cha chini baado utatozwa riba juu kile unachodaiwa ambacho hukulipia. Hii ada
(ambayo inaitwa pia finance fee) inakuwa mara nyingi karibu asilimia 1% au 2% ya kile unachodaiwa kila mwezi. Hii ina maana kwamba riba kwa mwaka
inakuwa kati ya asilimia 12% na 24%. KIwango cha riba kinaitwa pia Annual Percent Rate (APR).
Hata riba za chini zinaweza kugeuka kuwa malipo ya riba za juu (finance
fees)! Kwa mfano: kadi nyingi za mkopo zinatangaza 0% ya riba ya APR. Lakini ukisoma mandishi madogo yaliyochapishwa, mara nyingi utagunduwa
kwamba viwango vya riba vinaweza kubadilika haraka sana. Ukichelewesha malipo mara moja tu kwa ajili ya moja ya kadi/mkopo wako, kiwango cha riba
kinaweza uongezeka hadi asilimia 12%, 18%, hata 24% au zaidi! Kwa hiyo, kwa dola $200 za nguo, ni rahisi kujikuta unatumia dola $36 za ziada kwenye
riba!
Annual Fee/Ada ya mwaka Baadhi ya kadi za mkopo zinakutoza ada kwa kuwa nayo kila mwaka. Kampuni nyingi hazifanyi hivyo. Unapokuwa unatafuta kununua kadi unatakiwa
kuangalia isiyokuwa na ada ya mwaka.
Grace Period/Kipindi cha kuvumiliwa
Hii ni idadi ya siku baada ya kupokea taarifa kwamba kampuni ya kadi ya mkopo itaanza kukutoza riba. Ukilipa kabla ya muda kuisha hautatozwa riba.
59
Minimum Payments/Malipo ya chini kabisa
Kila mwezi unapaswa kulipa kiasi Fulani kama sehemu ya kile
unachodaiwa. Hichi kinaitwa malipo yako ya chini kabisa na huwa mara nyingi kama dola $20 kila mwezi. Usipolipa hata hicho kiasi kidogo, kampuni
ya kadi za mkopo itakutoza ada ya kuchelewa. Hii ada inaweza kuwa kati ya dola $15 na $30 kila mwezi usipolipa.
Example/Mfano: Baki ya kadi yako ya mkopo ni dola $1,000, kwa riba APR ya asilimia 18%. Malipo yako ya chini kabisa ni dola $30. Ukitoa malipo ya
chini kabisa tu kila mwezi, utalipa kwa ujumla dola $698 za riba kwa muda takribani wa miaka minane! Kama Usipotoa hata malipo ya chini kabisa,
utaishia kuharibu pesa nyingi zaidi katika ada za ucheleweshwaji.
Balance/Baki Baki yako ni kiasi unachodaiwa kwenye kadi yako ya mkopo. Ukilipa kiasi
chote kwa ujumla baki yako itakuwa dola $0. Usipolipa kwa ujumla kiasi chote unachodaiwa baki yako inaweza kuendelea kuongezeka.
CREDIT CARD STATEMENTS/TAARIFA ZA KADI ZA
MKOPO
Kila mwezi utapokea taarifa ya kadi ya mkopo ambayo ni muhtasari wa kila kitu kilichotokea katika akaunti yako. Unatakiwa kuutazama huu
mhutasari na kuhakikisha kwamba unakubaliana na kila kitu kinachojionyesha katika taarifa.
Kama ilivyo benki, makampuni ya kadi za mikopo wakati zinafanya
makosa. Kama utakuta kitu katika taarifa yako na ni kitu ambacho hauna
ku
mb
uku
Kumbuka
kutunza rekodi
zako!
60
mbu ya kukinunua na kadi yako ya mkopo unatakiwa kuipigia simu kampuni
yako ya kadi ya mkopo papo hapo.
Tutazame mfano wa taarifa ya kadi ya mkopo kwenye kiambatanisho ili tuone inavyofanana taarifa.
Record Keeping/Kutunza rekodi Baada ya kuchunguza taarifa ya kadi yako ya mkopo unatakiwa kuitunza
taarifa yako kwa kufuata ule mtindo wa kutunza nyaraka tuliokufundisha. Kila mwezi weka taarifa yako kwa kufuata mtindo wa kutunza vitu tuliokufundisha.
Hii itakuwasaidia wakati unapokwenda kufuatilia taxes, kuomba mkopo, au ukitaka kuanzisha biashara yako. Ukilazimika kumpa mtu nakala ya taarifa
yako, hakikisha unabaki na karatasi halisi au nakala.
61
IDENTITY THEFT/WIZI WA UTAMBULISHO Wizi wa utambulisho ni swala zito kabisa. Wizi wa utambulisho ni pale
mtu mwingine anapotumia jina lako, anwani yako, tarehe yako ya kuzaliwa, namba ya social security na/au jina la ubatizo la mama yako katika mambo
yasiyo halali kama kutumia akaunti yako ya benki au kadi ya mkopo kwa jina lako, kupata mikopo, kununua gari, kupata misaada ya kijamii kwa jina lako.
Hili linaweza kuharibu mkopo wako na kuwa ngumu kurekebisha. Haya ni mambo unayotakiwa kufanya kuepuka wizi wa utambulisho:
Chana chana karatasi za maombi ya mkopo, risiti za kadi ya mkopo,
nyaraka zenye taarifa za madeni au za kifedha usizozitaka kabla ya kuviweka kwenye kopo la takataka.
Toa barua zako kwenye sanduku la barua siku ile ile zinapoletwa.
Leta barua zinazokwenda nje kwenye masunduku ya posta ya kukusanyia barua au kwenye ofisi ya posta iliyokaribu. Usiziache katika
masanduku ya barua yasiyo salama.
Kamwe usitoe taarifa zako binafsi kwa njia ya simu labda uwe umpiga simu hiyo mwenyewe.
Kamwe usiache risiti kwenye mashine za benki, etc. Zichanechane wakati
hauzihitaji tena.
Weka kichwani namba yako ya social security na namba zote za siri. Usiziandike popote halafu ukaweka kwenye mkoba wako au pochi.
Saini kwenye kadi kadi zote za mkopo unapozipata au uandike tazama
kitambulisho (“see ID”) badala ya sahihi.
Pitia taarifa za benki za mwezi na utunze risiti zote za kadi za mkopo
Toa kadi za mkopo za ziada na vitambulisho kwenye pochi yako.
Futa kadi zote za mkopo usizozitumia.
Tunza orodha ya kadi zote za mkopo unazozitumia pamoja na namba za
simu za kuita zikipotea
Kadi yako mkopo ikiisha muda wake na usipopokea nyingine mpya kwa njia ya posta, pigia simu kampuni ya kadi za mkopo papo.
Omba ripoti ya mkopo na uyipitie walau mara moja kwa mwaka.
Sahihisha makosa yoyote.
62
Toa taarifa kwenye kampuni yako ya kadi ya mkopo na benki unapobaadilisha anwani na namba za simu
Ripoti kwenye kampuni kadi za mkopo zilizopotea au kuibiwa papo hapo
Zijue barua na simu zinazoahidi zawadi kupata taarifa zako binafsi.
Zikisikika kuwa nzuri sana kuelekea ukweli, mara nyingi zinakuwa kweli!
Unapopokea ripoti yako ya mkopo unatakiwa kuhakikisha umeichunguza
kwamba haina makosa. Kama kuna kitu chochote usichokubaliana nacho
kwenye ripoti yako ya mkopo, unaweza kujaribu kuomba
kiondolewe. Taarifa zaidi zimetolewa
katika kiambatanisho kuhusu kusahihisha makosa ya mkopo au
zungumza na mkufunzi wako. Kitu bora zaidi ni kujaribu
kuzuia wizi wa utambulisho katika nafasi ya kwanza.
Ukihisi kwamba utambulisho wako umeibiwa, unaweza kuwasiliana na
namba zifuatazo:
Ofisi ya Sheriff iliyoko karibu
Equifax: 1-800-525-6285 Experian: 1-800-397-3742
TransUnion: 1-800-680-7289
63
IF YOU CANNOT GET CREDIT/KAMA HUWEZI KUPATA
MKOPO Start Building Your Credit/Anza Kujenga mkopo Unatakiwa kujenga mkopo kwa muda. Kama wageni wapya huenda hamkuwa au baado hamjakuwa na historia ya mkopo. Kwa sababu hiyo,
Makampuni ya Kimarekani yajajua mengi juu yenu au jinsi mtakavyowalipa. Kwa hiyo, katika kujiweka salama, yanaweza kuamua kutowakopesha pesa
kabisa. Hili linaweza kusababisha matatizo makubwa unapokuwa unataka kununua gari au nyumba lakini huwezi kupata mkopo.
Kuanza kujenga mkopo unaweza:
Fungua akaunti ya akiba nay a matumizi ya kila siku na uyisimamie
kwa uangalifu.
Jisajili kwa ajili ya kadi ya mkopo ya mafuta ya gari au kitengo cha
duka. Ni rahisi kupata kuliko kadi ya mkopo ya kawaida.
Chukua mkopo mdogo wa gari au vifaa vya ndani na uulipe kwa wakati.
Jisajili kwa ajili ya kadi ya mkopo yenye dhamana.
SECURED CREDIT CARDS/KADI ZA MKOPO ZENYE
DHAMANA Kadi za mkopo zenye dhamana ni nzuri zaidi kwa watu wasio na historia
ya mkopo au wenye historia mbaya ya mkopo. Kadi ya mkopo yenye dhamana
inaomba kutunza pesa kwenye akaunti ya akiba ili kampuni ya kadi za mkopo ijue kwamba italipwa. Kawaida, benki italipa kiasi kidogo cha riba kwenye pesa
uliyoweka benki. Riba utakayotozwa kwenye pesa unayodaiwa kwenye kadi ya mkopo itakuwa kubwa zaidi. Kiwango kidogo unachoweka benki ni kiasi
cha pesa unachotakiwa kukiacha kwenye akaunti ili uweze kuitumia kadi ya mkopo.
Kama ilivyo kadi ya mkopo ya kawaida, unatakiwa kutafuta kadi yenye
ada na riba ndogo. Zifuatazo hapo chini ni orodha ya kadi za mkopo zenye dhamana zipatikanazo California. The International Rescue Committee
haipendekezi kadi yoyote kati ya hizi kuliko nyingine. Huenda zipo kampuni zingine zenye kadi zenye kadi dhamana na unatakiwa kutafuta inayokidhi
vizuri zaidi mahitaji yako.
64
Bank Benki
Phone Number
Namba ya simu
Annual Fee Ada ya
mwaka
Interest Rate on
Credit Card Riba
kwenye kadi ya
mkopo
Minimum
Deposit Kiasi cha
chini kuweka
benki
Bank of America (800) 732-9194 $29 15%
$250
Washington Mutual (800) 884-1789 $50 14%
$300
US Bank (800) 285-8585 $35 19%
$300
Wells Fargo (800) 642-4720 $18 17.24%
$300
CREDIT CARD STATEMENTS/TAARIFA ZA KADI ZA
MKOPO Kila mwezi utapokea taarifa za kadi ya mkopo ambayo ni mhutasari
wa mambo yaliyofanyika kwenye akaunti yako. Unatakiwa kuutazama huu mhutasari na kuhakikisha kwamba unakubaliana na kila kilichoko katika
taarifa.
Kama ilivyo kwa mabenki, kampuni za kadi za mkopo na zenyewe wakati mwingine hufanya makosa. Kama kuna kitu katika taarifa ambacho
haukununua na kadi yako unatakiwa kuipigia simu kampuni ya mkopo papo hapo.
Record Keeping/Kutunza Rekodi Baada ya kuipitia taarifa ya kadi yako ya mkopo
unatakiwa kuitunza taarifa yako katika jalada lile la nyaraka tulilokupatia. Kila mwezi uweke taarifa yako
katika jalada lile la kutunza nyaraka tuliokupatia. Hili litakusaidia wakati wa kufaili ushuru wako, kufanya
maombi ya mkopo, au kuanzisha biashara yako.
Ukitaka kumpa mtu nakala ya taarifa yako, hakikisha unabaki na karatasi ya asili au nakala.
Kumbuka kutunza rekodi zako!
65
66