wananchi wa chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · wananchi wa chwaka...

5
WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji chao na kuondosha tatizo lililokuwa likiwakabili la ukosefu wa huduma hiyo kwa kipindi kisichopungua miaka saba. Wakisoma risala yao mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuuzindua mradi wa maji safi na salama kijijini hapo akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Katika maelezo yao kwenye risala yao waliyoisoma, wananchi wa Chwaka walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa msaaada mkubwa wa fedha zilizotumika kuunulia mambomba yaliotumika katika kumalizia mradi huo.Wananchi hao wa Chwaka walieleza kuwa walijitolea kwa hali na mali katika kufanikisa mradi huo na kuweza kuchangia Tsh. Milioni 37 pamoja na nguvu kazi na kuchimba mtaro pamoja na kufukia mabomba kutoka kisimani hadi Chwaka eneo lenye kilomita 7. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua maji ya Mfereji kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji cha Chwaka,Wilaya ya Kati Unguja,alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja. Wananchi hao wa Chwaka walitoa shukurani kwa wale wote waliochangia katika mradi huo akiwemo Mwakilishi wa Jimbo hilo Issa Haji Gavu aliyechangia Tsh. Milioni 41 zilizotumika kununulia mabomba na pambu ya kusukumia maji.Aidha, katika risala yao hiyo wananchi wa Chwaka walitumia fursa hiyo kutoa shukurani kutoka kwa wavuvi wa kijiji hicho kwa kuthamini kilio chao cha muda mrefu. Katika kuufanya mradi huo uwe endelevu wananchi hao wa Chwaka waliahidi kuwa wako tayari kushirikiana na Mamlaka ya Maji (ZAWA) katika kutoa day a matumizi ya maji kama

Upload: others

Post on 29-Dec-2019

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji

WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji chao na kuondosha tatizo lililokuwa likiwakabili la ukosefu wa huduma hiyo kwa kipindi kisichopungua miaka saba. Wakisoma risala yao mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuuzindua mradi wa maji safi na salama kijijini hapo akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Katika maelezo yao kwenye risala yao waliyoisoma, wananchi wa Chwaka walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa msaaada mkubwa wa fedha zilizotumika kuunulia mambomba yaliotumika katika kumalizia mradi huo.Wananchi hao wa Chwaka walieleza kuwa walijitolea kwa hali na mali katika kufanikisa mradi huo na kuweza kuchangia Tsh. Milioni 37 pamoja na nguvu kazi na kuchimba mtaro pamoja na kufukia mabomba kutoka kisimani hadi Chwaka eneo lenye kilomita 7.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua maji ya Mfereji kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji cha Chwaka,Wilaya ya Kati Unguja,alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo

katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Wananchi hao wa Chwaka walitoa shukurani kwa wale wote waliochangia katika mradi huo akiwemo Mwakilishi wa Jimbo hilo Issa Haji Gavu aliyechangia Tsh. Milioni 41 zilizotumika kununulia mabomba na pambu ya kusukumia maji.Aidha, katika risala yao hiyo wananchi wa Chwaka walitumia fursa hiyo kutoa shukurani kutoka kwa wavuvi wa kijiji hicho kwa kuthamini kilio chao cha muda mrefu. Katika kuufanya mradi huo uwe endelevu wananchi hao wa Chwaka waliahidi kuwa wako tayari kushirikiana na Mamlaka ya Maji (ZAWA) katika kutoa day a matumizi ya maji kama

Page 2: WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimtwisha ndoo ya maji Asha Mohamed Abdulla,wa Kijiji cha Chwaka,mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama, Sherehe ya ufunguzi wa Mradi huo umefanyika Kijijini

hapo,alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.

ilivyopangwa na Serikali.Sambamba na hayo, wananchi hao wa Chwaka walimuomba Rais kuwa mlezi wa mradi huo ambapo ombi lao hilo lilikubaliwa na Rais pamoja na maombi yao yote waliyoomba ikiwa ni pamoja na ukarabati wa nyumba ya madaktari pamoja na kupatiwa madaktari. “ Sisi wananchi wa Chwaka tunaahidi kuwa tuko tayari kushirikiana na wewe mwenyewe binafsi pamoja na Serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa”,alieleza wananchi hao katika risala yao. Katika hotuba yake Rais wa Zanzibar na Mwwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwapongeza wananchi wa Chwaka kwa uvumilivu wao pamoja na kuipongeza Jumuiya ya Maendeleo ya wananchi wa Chwaka na viongozi wao wa Jimbo pamoja na Mamlaka ya Maji Zanzibar kwa juhudi zao katika kuendeleza mradi huo. Dk. Shein pia, aliipongeza Wizara yake ya Fedha katka jitihada zake za kuhakikisha mradi huo unafanikiwa huku akieleza kuwa miundombinu ya kupata maji ni mingi na inahitaji fedha nyingi na ndio maana Serikali yake ikaamua kuikopa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), kiasi cha Bilioni 67 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji nchini. Aidha, Dk. Shein aliwasisitiza wananchi hao kuyatumia maji kwa umakini zaidi hasa ikizingatiwa kuwa kiwango cha maji kimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya Tabia nchi.Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imo katika kufanya jitihada ya kuhakikisha tatizo la maji linapungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwani tatizo la maji si dogo kama linavyofikiriwa. “Serikali ina jukumu la kuhakikisha wananchi wake wanapata maji safi na salama na ndio maana imedhamiria kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya maji Unguja na Pemba kwa kuanzisha miradi mbali mbali”,alisema Dk. Shein.

Page 3: WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban,(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Vuai Mwinyi,na Viongozi wengine wakielekea katika

viwanja vya mpira Chwaka katika mkutano na Wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa maji safi na Salama,Kijijini hapo, ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Nae Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban alieelza kuwa utekelezaji wa mradi wa maji safi na salama wa Chwaka ni miongoni mwa jitihada za Serikal ya Mapinduzi Zazibar ambao umegharimu Tsh. Milioni 330 zimetumika katika ujenzi. Alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa unaoitwa Mradi wa maji salama (Safe Water Project) uliogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzbar kwa kushirikiana an wananchi wa Chwaka.

Akitoa taarifa ya kiufundi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mirza alieleza kuwa harakati za ujenzi wa mradi huo zilianza Maci 29 mwaka jana kwa kuchimba kisima huko Hanyegwamchana na Mei 17 kazi zote za uchimbaji zilikamilikana tarehe 4, Novemba mradi wote ulimalizika ambapo wananchi wapatao 4600 wanafaidika.

Dk. Shein ataendelea na ziara yake kesho katika Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na kufanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa huo

Page 4: WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji

Wazee wa Kijiji cha Chwaka wakiwa na fuaraha kubwa na kumsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na salama Kijijini

hapo alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha

Page 5: WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya … · 2013-03-12 · WANANCHI wa Chwaka wameeleza kufarajika kwao baada ya kukamilika mradi wa maji safi na salama katika kijiji

Chwaka,Wilaya ya Kati Unguja,wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na salama katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamoja na Viongozi na Wananchi wakipongeza kitendo cha Rais, baada ya kuuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama, wa Kijiji chan Chwaka ,katika Sherehe ya ufunguzi wa Mradi huo uliofanyika kijijini hapo ,alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini

Unguja.