yaliyomo · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa mstari hausemi kuwa mungu ananafsi...

35

Upload: others

Post on 24-Jan-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa
Page 2: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

YALIYOMO

SOMO LA KWANZA ................................................................ 1

1 YOHANA 5:8. .................................................................... 1

SOMO LA PILI .......................................................................... 5

MUNGU NI NAFSI NGAPI? ................................................ 5

SOMO LA TATU ..................................................................... 11

UUNGU WA MWANA WA MUNGU ................................ 11

SOMO LA NNE ....................................................................... 23

ROHO MTAKATIFU NI NANI? ....................................... 23

Page 3: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

1

SOMO LA KWANZA

1 YOHANA 5:8.

Habari za muda huu mpendwa

katika Bwana. Binafsi huwa

sipendi kuingia katika mabishano

kwa maana naona kuwa hayaleti

umoja katika imani. Pia nimeona

kuwa Whatsapp au mitandao ya

kijamii sio njia nzuri sana ya

kuweza kuongea kwa kina kuhusu

kile ambacho nataka kusema. Kwa

kuona hivyo nimeona niandike

kwa ufupi yote ambayo nataka

kusema wenda unaweza

ukanielewa kwa kina na nikuache

ukitafakari.

Kama jinsi ilivyo mtu yoyote yule

ambaye anaamini katika fundisho

la utatu, unaamini kuwa kuna

Mungu mmoja Baba, mwana na

Roho mtakatifu. Unaamini kuwa

Baba ni nafsi ya kwanza, mwana ni

nafsi ya Pili, Roho mtakatifu ni

nafsi ya tatu. Ninajua kuwa wewe

ni mwanafunzi wa Biblia na

unapenda kufundisha kile

ambacho wewe unaona ni sahihi.

Na pia unapenda kujifunza Biblia.

Na Mungu akubariki kwa hilo.

Katika mazungumzo yetu tulikuwa

tunaongelea mambo mengi kwa

wakati mmoja na nimeona kwa

mtu wa wakaida ni vigumu sana

kunielewa kile ninachotaka

kusema. Kwanini inakuwa ni

ngumu kunielewa? Nikwasababu

kila hoja niliyokuwa naleta

hakukuwa na mtiririko mzuri ili

kwamba hata anayefatilia aweze

kuelewa vyema. Kwa kuona hivyo

nimeona sio jambo jema niliache

swala hili hewani na ukaondoka

hali hujanielewa. Kwa vile kila

kitu lazima kilinganishwe na jinsi

Biblia inavyosema, katika kitabu

hiki kidogo sitotumia kitabu

chochote kile ila Biblia.Kwa

kuanza naomba nianze na mstari

mkuu ambao tulikuwa tunaujadili,

mstari huu ni,

1 Yohana 5

8 Kwa maana wako watatu

washuhudiao [mbinguni, Baba, na

Neno, na Roho Mtakatifu, na

watatu hawa ni umoja

Huu ni moja kati ya mistari

ambayo inatumika kuthibitisha

kuwa Mungu ananafsi tatu. Katika

mstari huu kuna jambo ambalo

hata wewe unaweza kuligundua

kama ukisoma vizuri, utagundua

mambo haya,

1. Kuna Ushuhuda

2. Kuna Baba mwana na Roho

3. Kuna umoja kati ya Baba

mwana na Roho

Haya mambo matatu unaweza

kuyaona wazi kabisa. Katika

Page 4: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

2

mstari huu hata wewe unayesoma

unaona wazi kuwa Mstari hausemi

kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio

lengo langu nikuelewe vibaya

lakini nataka kukuonesha kuwa

mstari hausemi kuwa Baba mwana

na Roho ni nafsi tatu za Mungu.

Kwa vile sisi kama wakristo

tunatakiwa kutumia neno

“Imeandikwa” kama ndio msingi

katika kutafsiri maandiko na

kuelewa vyema maandiko,

tunaona wazi kuwa hakuna

ushahidi wa kile tunachotaka

kukizungumzia. Kwa macho

yangu na kwa macho yako wote

wawili tunaona kuwa mstari

haujasema kuwa Baba, mwana na

Roho mtakatifu ni nafsi za Mungu.

Sasa tutizame maana na neno

“umoja”. Nafikiri tumetumia hili

neno mara nyingi sana. Na pale

tunapolitumia tunawasilisha kile

ambacho tunataka wengine

wakielewe. Mara nyingi huwa tuna

tumia maneno kama vile “umoja ni

nguvu” hakuna hata mmoja

ambaye ataelewa vibaya kile

ambacho tunataka kumaanisha

katika kauli hiyo. Kila mmoja

ataelewa kuwa maana ya neno

“umoja” ni ushirikiano katika

chochote kile ambacho tutakuwa

tunafanya.

Napenda kukuuliza swali, je

nikisema Dani, Peter na David

wanaumoja, je maana itakayokuja

kichwani mwako ni kuwa Hawa

watatu wanaushirikiano, au hawa

watatu ni mtu mmoja katika nafsi

tatu?

Swali hili nimeuliza ili uweze

kutafakari kwa kina kuhusu maana

halisi ya umoja katika mstari huu.

Yesu alikuwa na mitume 12. Na

hawa mitume walikuwa na umoja.

Je umoja wao uliwafanya wawe

mtume mmoja katika nafsi 12?

Sidhani kama hata wewe unaweza

kuelewa hivyo. Umoja wa watu

hauwafanyi waungane na kuwa

mwili mmoja katika nafsi

mbalimbali. Bali kila mmoja ni

nafsi huru.

Sasa turudi katika mstari huo

ambao nimetoka kuuonesha.

Katika mstari huo imeonesha wazi

nini chanzo cha Baba, mwana na

Roho kuwa na umoja. Chanzo cha

Baba, mwana na Roho kuwa na

umoja ni ushuhuda wanaoutoa. Ni

wazi kuwa hata wewe ukiwa na

marafiki zako kama kile

unachosema ni sawa na kile

ambacho marafiki zako wanasema

ni wazi kuwa wewe unaumoja na

marafiki zako. Ushuhuda wa Baba

ni sawa na ushuhuda wa Mwana na

ushuhuda wa Mwana ni sawa na

ushuhuda wa Roho mtakatifu.

Kutokana na ushuhuda huu ndio

mana hawa watatu ni umoja.

Page 5: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

3

Tukumbuke kuwa Biblia imesema

kuwa hawa watatu ni “umoja” na

wala sio “Mungu mmoja” haya

maneno mawili hayapo sawa na

ndio maana watu wengi

wanashindwa kupata maana kamili

ya kile ambacho mstari unataka

kukisema. Kama ukisoma mstari

huu katika fikra kuwa hawa tatu ni

“Mungu mmoja” basi

utashawishika kuona Baba,

mwana na Roho ni nafsi tatu za

Mungu. Lakini ukweli ni kwamba

Mstari haujasema hivyo na wala

haujasema kuwa Baba, mwana na

Roho ni Mungu mmoja, bali

umesema kuwa Baba, mwana na

Roho ni umoja.

Nafikiri mpaka kufikia hapa

unaanza kuona utofauti na ule

mstari ambao umekuwa ukidhani

kuwa unaonesha kuwa Mungu ni

nafsi tatu sasa unaanza kuona

kuwa haoneshi hivyo. Kwa maana

kama kweli ni nafsi tatu basi Biblia

ingesema wazi kabisa kuwa Baba

mwana na Roho ni nafsi tatu za

Mungu mmoja. Hakuna mtu

yoyote ambaye angebishana na

Biblia. Lakini hata wewe

ukiangalia wazi mstari huo unaona

imesema,

1 Yohana 5:8

Kwa maana wako watatu

washuhudiao [mbinguni, Baba, na

Neno, na Roho Mtakatifu, na

watatu hawa ni umoja

Umoja wa Baba, Mwana na Roho

ni kutokana na ushuhuda

wanaoutoa. Hii inamaana kama

Baba anatoa ushuhuda tofauti na

Mwana basi ni wazi kuwa

hakutakuwa na umoja. Kile

ninachotaka kusema kimewekwa

wazi kabisa katika mstari unaofata,

1 Yohana 5:9

Kisha wako watatu washuhudiao

duniani], Roho, na maji, na damu;

na watatu hawa hupatana kwa

habari moja. Tukiupokea

ushuhuda wa wanadamu,

ushuhuda wa Mungu ni mkuu

zaidi; kwa maana ushuhuda wa

Mungu ndio huu, kwamba

amemshuhudia Mwanawe

Tunaona kuwa Roho, Maji na

damu hupatana katika habari moja.

Ni wazi kuwa ushuhuda wa Roho

ni sawa na ushuhuda wa Maji na

ushuhuda wa maji ni sawa na

ushuhuda wa damu. Hakuna mtu

yoyote ambaye anaweza kuelewa

kuwa umoja wa roho, maji na

damu yani washuhudiano duniani

unawafanya wawe mmoja katika

nafsi tatu. Hata wewe najua

hautaweza kukubali, bali utakubali

wazi kuwa watatu wanaoshuhudia

duniani hupatana katika habari

moja sawa na watatu wa mbinguni

Page 6: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

4

ambao pia wanapatana katika

habari moja.

Tukumbuke kuwa Yesu

alimwambia Petro kuwa

litakalofungwa duniani litakuwa

limefungwa mbinguni. Na pia

Yesu alitufundisha,

Mathayo 6

10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa

duniani kama huko mbinguni.

Inamaana kuwa Hata ushuhuda wa

watatu wa hapa duniani ni sawa na

ushuhuda wa watatu wa juu

mbinguni kwa maana Hapa

duniani ni kama huko mbinguni.

Hii inatosha kabisa kutufanya

tuelewe kuwa kama washuhudiao

Duniani wanapatana katika habari

mmoja, ni wazi kuwa hata

wanaoshuhudia mbinguni nao

wanapata katika habari moja.

Lakini mara nyingi tunaposoma

mstari huo tunashindwa kupata

maana kamili kile mstari unataka

kusema. Lakini naamini kuwa

maelezo kwa ufupi niliyoyatoa

kuhusu mstari huu yanatosha

kukupa mwangaza kuwa Biblia

haijasema kuwa Mungu ana nafsi

tatu. Na wala mstari haujasema

kuwa Baba, mwana na roho ni

nafsi za Mungu mmoja. Kama

umenielewa vyema hapa basi

nakukaribisha tena sehemu

nyingine. Kwa maana nataka kuwe

na matiririko mzuri wa hoja ili

uweze kunielewa. Kabla

sijazungumzia jambo lingine

napenda turudi tena kusoma ule

mstari kuhakikisha kuwa

tunauelewa vyema.

1 Yohana 5:8

Kwa maana wako watatu

washuhudiao [mbinguni, Baba, na

Neno, na Roho Mtakatifu, na

watatu hawa ni umoja

Ni wazi kabisa kuwa Biblia ipo

kimya kuhusu Baba, mwana na

Roho kuwa nafsi tatu za Mungu.

Kwa vile ipo kimya Baba, mwana

na Roho hizi sio nafsi za Mungu

mmoja. Katika mstari huu hata

wewe unaona wazi kabisa

Hausemi kuwa Baba, mwana, na

Roho ni nafsi za Mungu. Kama

Mstari hausemi kwanini sisi

tuseme kuwa Baba mwana na

Roho ni nafsi tatu za Mungu? Na

tunaenda mbali zaidi na kusema

Baba ni nafsi ya Kwanza, Mwana

ni nafsi ya Pili, na Roho ni nafsi ya

tatu wakati haya yote hayapo

katika mstari huu? Nafikiri muda

umefika inabidi tuisome Biblia na

tusiongezee mambo ambayo

hayapo katika Biblia.

Page 7: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

5

SOMO LA PILI

MUNGU NI NAFSI NGAPI?

Kwa vile nimesema kuwa Mungu

sio nafsi tatu, ni wazi kuwa swali

utakalotaka kuniuliza ni je Mungu

ananafsi ngapi? Kwa kuona hivyo

nimeona niwahi kutoa maelezo.

Mimi nataka kukupa mistari ya

Biblia kukuonesha kile ambacho

Biblia inasema kuhusu Mungu.

Naamini hata wewe unaamini

kuwa Mungu habadiliki. Kuwa

yeye sio kigeugeu kuwa

anabadilika. Kwa mantiki hiyo

najua utakuwa katika nafasi nzuri

ya kuelewa kile ninachotaka

kusema,

Kwanza nianze kwa kutoa mistari

hii.

Amosi 6:8

"Bwana MUNGU ameapa KWA

NAFSI YAKE asema BWANA

Mungu wa majeshi Naizira Fahari

ya yakobo, nachukizwa na

majumba yake kwasababu hiyo

nitautoa huo mji pamoja na wote

waliomo ndani yake"

Yeremia 51

14 BWANA wa majeshi ameapa

KWA NAFSI YAKE akisema

Hakika Nitakujaza watu kama

Nzige nao watapiga kelele juu

yako"

Isaya 42:1

"Tazama mtumishi wangu

nimtegemezaye mteule wangu,

ambaye NAFSI YANGU

imependezwa Naye nimetia roho

YANGU juu yake naye atawatolea

mataifa hukumu"

Isaya 42: 6

"MIMI BWANA nimekuita katika

haki nami nitakushika mkono na

kukulinda na kukutoa uwe agano

la watu na nuru ya mataifa

Isaya 45: 5

"MIMI NI BWANA wala Hapana

mwingine zaidi yangu MIMI

hapana Mungu, nitakufunga

mshipi ijapokuwa hukunijua

Hii ni mistari michache ambayo

najua inatosha kukuacha

ukitafakari. Mungu ni nafsi ngapi?

Jibu tunalolipata katika mistari hii

ya Biblia ni kwamba Mungu ni

nafsi moja tu. Ndio maana Mungu

anasema “Nafsi yangu” au

“Mimi”. Kwa maana Mungu

mwenyewe anayejifunua anasema

wazi kuwa yeye ni Nafsi moja.

Nafuta kokote katika Biblia kama

utaona sehemu ambayo Mungu

anasema yeye ni zaidi ya nafsi

moja kama jinsi alivyosema katika

mistari hii.

Page 8: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

6

Katika vitabu vinavyojulikana

kama vitabu vya agano jipya pia

havipo mbali kusema kuwa Kuna

Mungu mmoja. Na kama kuna

Mungu mmoja ni wazi kuwa

Mungu ni nafsi moja.

Wakolosai 1:3

TWAMSHUKURU MUNGU,

BABA YAKE BWANA WETU

YESU KRISTO siku zote

tukiwaombea"

Waefeso 1: 3

"ATUKUZWE MUNGU, BABA

WA BWANA WETU YESU

KRISTO aliyetubariki kwa baraka

zote za rohoni katika ulimwengu

wa roho ndani yake Kristo"

2wakoritho 1:3

"NA AHIMIDIWE MUNGU,

BABA WA BWANA WETU YESU

KRISTO, Baba wa Rehema,

Mungu wa faraja yote"

Katika Mistari hii michache

tunaona kuwa Paulo anasema wazi

kuwa MUNGU NI BABA YAKE

YESU KRISTO. Hakuna hata

mmoja ambaye anashindwa

kuelewa kuwa Baba wa Yesu

Kristo ni Baba mmoja. Na kama ni

Baba mmoja basi ni Mungu

mmoja. Paulo anaendelea kusema

kuwa,

1 Wakorintho 8:6

"Lakini kwetu sisi MUNGU NI

MMOJA TU, ALIYE BABA

ambaye vitu vyote vimetoka kwake

nasi tunaishi kwake, yuko na

Bwana mmoja Yesu Kristo ambaye

kwake vitu vyote vimekuwapo na

sisi kwa yeye huyo"

Paulo anaendelea kutuambia wazi

kuwa Kuna Mungu mmoja

ambaye ndiye Baba wa Bwana

wetu Yesu Kristo. Kuna Baba

mmoja, na Huyu ndiye Mungu

ambaye kama jinsi tulivyoona

alikuwa anaapa kwa nafsi yake.

Isaya 42:1

"Tazama mtumishi wangu

nimtegemezaye mteule wangu,

ambaye NAFSI YANGU

imependezwa Naye nimetia roho

YANGU juu yake naye atawatolea

mataifa hukumu

Huyu ndiye Mungu mmoja

ambaye ndiye Baba wa Bwana

wetu Yesu Kristo. Mpaka Mungu

aseme kuwa “NAFSI YANGU” ni

wazi kuwa Mungu ni nafsi moja tu.

Na Paulo akasema mara nyingi

kuwa Baba yake Yesu Kristo ndiye

Mungu. Yesu ana Baba mmoja

hivyo kuna Mungu mmoja. Na

Yesu anatusaidia kuelewa wazi

kuwa Baba yake ndiye Mungu wa

kweli,

Page 9: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

7

Yohana 17:3

"Na uzima wa Milele ndio huu

wakujue wewe MUNGU WA

PEKEE WA KWELI na Yesu

kristo uliyemtuma"

Yesu anaposema kuwa watu

wamjue Mungu wa kweli

haimaanishi kuwa yeye ni wa

uongo. Lakini anamaanisha wazi

Baba yake ndiye Mungu mkuu na

ambaye anatakiwa ajulikane

rasmi. Mwana siku zote anatafuta

kufanya mapenzi ya Baba. Hata

kiti cha enzi kile ambacho mwana

aliketi baada ya kushinda ni kiti

cha enzi cha Baba yake.

Ufunuo 3:21

Yeye ashindaye, nitampa kuketi

pamoja nami katika kiti changu

cha enzi, kama mimi nilivyoshinda

nikaketi pamoja na Baba yangu

katika kiti chake cha enzi.

Ni wazi kuwa Mwana

anamtegemea Baba. Na Baba

ndiye aliyempa mamlaka yote

mbinguni na duniani. Ni Baba

ndiye aliyeona vyema kumfanya

mwanae awe kama yeye.

Mpaka hapa tulipofikia naamini

umeweza kuona wazi kuwa

Mungu ni nafsi moja. Ni Mungu

ambaye akiapa huwa anaapa kwa

nafsi yake. Kama Mungu

angekuwa ni nafsi tatu basi ni wazi

kuwa isinge kuwa Mungu anaapa

kwa nafsi yake bali ingekuwa

anaapa kwa nafsi “zake”. Najua

kuna sehemu katika Mwanzo

Mungu alitumia neno “wetu”

lakini hayo yote utaelewa katika

somo lijalo lakini kwa sasa elewa

kuwa Kuna Baba mmoja basi kuna

Mungu mmoja.

Biblia imesema wazi kuwa Mungu

ni Mungu mwenye Nafsi moja. Na

Mungu huyo mmoja ana mwanae

ambaye Jina lake ni Yesu Kristo.

Yesu alisema wazi kuwa,

Yohana 14:28

Mlisikia ya kwamba mimi

naliwaambia, Naenda zangu, tena

naja kwenu. Kama mngalinipenda,

mngalifurahi kwa sababu naenda

kwa baba, KWA MAANA BABA NI

MKUU KULIKO MIMI

Na pia sehemu nyingine Yesu

anasema wazi kuwa Baba yake

ndiye Mungu mmoja, nani Mungu

wake pia

Yohana 20:17

"Yesu akamwambia usinishike kwa

maana sijapaa kwenda kwa Baba,

Lakini enenda kwa Ndugu zangu

ukawaambie Ninapaa Kwenda

kwa BABA YANGU NAYE NI

BABA YENU, KWA MUNGU

WANGU NAYE NI MUNGU

WENU"

Page 10: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

8

Yesu Kristo anasema kuwa Baba

yake ndiye Mungu mmoja ambaye

sisi tunatakiwa kumwabudu.

Anasema wazi kuwa Baba yake ni

ndiye Mungu wetu. Na pia Baba

yake ni Mungu wake pia. Hakuna

lugha nyepesi ambayo tunaweza

kujifunza kuliko hii. Ya kwamba

kuna Mungu mmoja ambaye ndiye

Baba yake Mwana wa Mungu

Yesu Kristo. Hii ndio injili

ambayo Paulo alikuwa

anafundisha. Kwamba Mungu ni

Baba yake Yesu Kristo. Katika

mantiki hii tunaelewa kuwa

Mungu ni nafsi moja tu. Na huyo

ndiye Baba yake Yesu Kristo.

Labda nikuulize swali na wewe, je

kokote uliposoma katika maandiko

matakatifu, kuna sehemu yoyote

ulipoona Yesu anasema yeye ni

nafsi ya Pili ya Mungu?

Hakuna sehemu yoyote katika

Biblia ambayo Yesu alisema kuna

zaidi ya Mungu mmoja. Bali

alisema, wazi kuwa kuna Mungu

mmoja,

Marko 12

29 Yesu akamjibu, Ya kwanza

ndiyo hii, Sikia, Israeli, BWANA

MUNGU WETU NI BWANA

MMOJA.

Yesu hakuwahi kusema kuwa

kuna Mungu zaidi ya mmoja.

Kama jinsi alivyosema kuwa Baba

ni nafsi moja, basi Mungu ni nafsi

moja. Kwa maana tuna Baba

mmoja tu. Paulo alisema pia,

Wafilipi 4

6 MUNGU MMOJA, NAYE NI

BABA WA WOTE, aliye juu ya yote

na katika yote na ndani ya yote

Kuna Baba mmoja tu na huyo ni

Baba wa Yesu Kristo. Baba wa

Yesu Kristo ndiye kama

tulivyoona pia ni Mungu wa Yesu

Kristo kama jinsi tulivyo sisi.

Paulo anaendelea kusema kuwa,

1 Timotheo 2

5 KWA SABABU MUNGU NI

MMOJA, na mpatanishi kati ya

Mungu na wanadamu ni mmoja,

Mwanadamu Kristo Yesu.

Kuna Mungu na Baba mmoja. Na

tuna mpatanishi mmoja. Hakuna

Mungu zaidi ya mmoja, ndio na

huyo ndiye Baba mmoja.

Yakobo 2

19 WEWE WAAMINI YA KUWA

MUNGU NI MMOJA; watenda

vema. Mashetani nao waamini na

kutetemeka

Tukumbuke kuwa Bila kumjua

Mungu wa kweli hatuwezi kupata

uzima wa milele, kwa maana Yesu

alisema hilo wazi kabisa, na Yesu

alisema wazi kuwa Baba yake

ndiye Mungu wa Kweli. Na kwa

Page 11: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

9

kusema hivyo alikuwa

anamuonesha Baba yake kama

ndiye Mungu rasmi ambaye sisi

tunapaswa kumwabudu.

Yohana 8

41 Ninyi mnazitenda kazi za baba

yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi

hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi

tunaye Baba mmoja, yaani,

Mungu. 42 Yesu akawaambia,

Kama Mungu angekuwa baba

yenu, mngenipenda mimi; kwa

maana nalitoka kwa Mungu, nami

nimekuja; wala sikuja kwa nafsi

yangu, bali yeye ndiye aliyenituma

Wayahudi walikuwa wanajua

kuwa kuna Baba mmoja ambaye

ndiye Mungu. Lakini walikuwa

hawataki kukubali kuwa Yesu

alikuwa ndiye Mwana wa Huyo

Baba mmoja ambaye walikuwa

wanasema wanamuamini.

Mistari hii mingi niliyotoa

nimejaribu kukuelewesha kuwa

kuna Baba mmoja hivyo Kuna

Mungu mmoja. Huyu ndiye

Mungu ambaye anaapa kwa nafsi

yake. Yeye ndiye Mungu wa

Kweli ambaye amempa mamlaka

yake Mwana wake Yesu Kristo

kwasababu anampenda sana

mwanae.

Yohana 3

35 Baba ampenda Mwana, naye

amempa vyote mkononi mwake.

Ukuu wa mwana unatokana na

Baba. Ni kweli kuwa Baba

amemnyanyua sana Mwana na

kwa Mwana kila goti litapigwa.

Lakini japokuwa na haya yote

Mwana anatuelekeza kwa Baba

kama huyo ndiye Mungu wetu

ambaye tunatakiwa kumwabudu

na kumuomba. Japokuwa na

uungu wake lakini Yesu hataki

tuelewe kuwa kuna Mungu zaidi

ya mmoja, bali anataka tuelewe

kuwa kuna Mungu mmoja na huyo

ni Baba yake.

Hata hapa duniani Mwana wa

mfalme anaweza kuwa na heshima

na mamlaka kama ya mfalme

lakini sikuzote atawaelekeza watu

kwa mfalme wa kweli ambaye ni

Baba yake.

Page 12: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

10

lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu,

aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka

kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na

Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye

kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa

yeye huyo (1wakorintho 8:6)

Page 13: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

11

SOMO LA TATU

UUNGU WA MWANA WA

MUNGU

Katika uumbaji

Kama jinsi tulivyo kwisha ona

katika somo lililopita kuwa Kuna

Mungu mmoja na huyo Mungu

anamwana wake ambaye ni

Mwana wa Mungu Yesu Kristo.

Tukumbuke kuwa Yesu alisema,

Yohana 17

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi

pamoja nawe, kwa utukufu ule

niliokuwa nao pamoja nawe kabla

ya ulimwengu kuwako

Kwamba mwana wa Mungu

alikuwepo hata kabla ya kuumbwa

kwa ulimwengu. Hakuna ambaye

atasoma huu mstari atashindwa

kuelewa kile ambacho mstari

unataka kusema, hata wewe

ukisoma najua kuwa hauwezi kosa

maana ile ambayo mstari

unazungumzia. Kwa mantiki hiyo,

tukisema kuwa Yesu Kristo

alianza kuwa mwana wa Mungu

alipobatizwa na yohana mbatizaji

kwasababu Mungu alisema

hadharani kuwa Yesu ni mwana

wake, tunashindwa kuelewa kuwa

kumbe wana wa Mungu alikuwepo

hata kabla ya ulimwengu kuwako.

Yesu anasema mara nyingi sana

kuwa yeye alikuwako hata kabla

Ibrahimu alikuwepo,

Yohana 8

58 Yesu akawaambia, Amin, amin,

nawaambia, Yeye Ibrahimu

asijakuwako, mimi niko

Wayahudi walitaka kumpiga

mawe kwa maana walijua kuwa

Yesu anajifanya ni Mungu hata

kusema kuwa yeye ni

“NIKO”ambaye wanajua kuwa

Mungu alipomtokea Musa alisema

yeye ni “NIKO.”

Kwa maana hiyo tunaendelea

kujifunza kuwa Yesu Kristo

mwana wa Mungu hakuanza kuwa

mwana wa Mungu alipobatizwa na

Yohana mbatizaji wala

alipozaliwa Bethlehemu kwa

maana alikuwa tayari mwana wa

Mungu hata kabla ya Ulimwengu

kuwako.

Waebrania 1

2 mwisho wa siku hizi amesema na

sisi katika Mwana, aliyemweka

kuwa mrithi wa yote, tena kwa

yeye aliufanya ulimwengu

Tunaona kuwa ni kwa kupitia

mwana Baba aliumba Ulimwengu

na Vyote ambavyo vipo. Yesu

anasema katika,

Page 14: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

12

Mithali 8

22 Bwana alikuwa nami katika

mwanzo wa njia yake, Kabla ya

matendo yake ya kale. 23

Nalitukuka tokea milele, tangu

awali, Kabla haijawako dunia. 24

Wakati visipokuwako vilindi

nalizaliwa, Wakati zisipokuwako

chemchemi zilizojaa maji. 25

Kabla milima haijawekwa imara,

Kabla ya vilima nalizaliwa. 26

Alipokuwa hajaiumba dunia, wala

makonde Wala chanzo cha

mavumbi ya dunia; 27

Alipozithibitisha mbingu

nalikuwako; Alipopiga duara

katika uso wa bahari; 28

Alipofanya imara mawingu yaliyo

juu; Chemchemi za bahari

zilipopata nguvu; 29 Alipoipa

bahari mpaka wake, Kwamba maji

yake yasiasi amri yake;

Alipoiagiza misingi ya nchi; 30

Ndipo nilipokuwa pamoja naye,

kama stadi wa kazi; Nikawa

furaha yake kila siku; Nikifurahi

daima mbele zake;

Katika mistari hii kuna jambo

ambalo utagundua kuwa Mwana

wa Mungu alikuwa pamoja na

Baba kabla kitu chochote

hakijaumbwa. Yesu anasema wazi

kuwa alizaliwa kipindi ambacho

kabla ya uumbaji. Hatujui ni muda

gani huo lakini tunachojua ni

kwamba alizaliwa kabla ya

uumbaji. Kabla ya dunia na kabla

ya malaika hawajaumbwa, kabla

ya vilindi vya maji, mwana wa

Mungu alizaliwa.

Na kwavile amezaliwa na Mungu,

tunaelewa kile ambacho Paulo

alisema kuwa,

Waebrania 1:3

Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa

utukufu wake na chapa ya nafsi

yake, akivichukua vyote kwa amri

ya uweza wake, akiisha kufanya

utakaso wa dhambi, aliketi mkono

wa kuume wa Ukuu huko juu;

Yeye ni m’ngao wa utukufu wake

na chapa ya “nafsi yake”. Katika

kauli hii tu inatosha kutuelewesha

kuwa kumbe Mungu ni nafsi moja.

Kwa maana Mwana wa Mungu ni

chapa ya “NAFSI” ya Mungu.

Hivyo Mungu hawezi kuwa ni

zaidi ya nafsi moja. Katika Mithali

tunagundua kuwa Baba na Mwana

ndio walioshirikiana kuumba

mbingu na dunia. Kwa maana

Yesu anasema wazi kuwa alikuwa

pamoja na Baba kama stadi wake

wa kazi.

Katika mantiki hiyo sasa turudi

katika kitabu cha mwanzo wakati

wa uumbaji,

Mwanzo 3:3

Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa

nuru

Page 15: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

13

Tukisoma sura yote ya kitabu cha

mwanzo tunaona kuwa ni Mungu

ndiye aliyekuwa naongea.

Tukumbuke kuwa Biblia imesema

wazi kuwa mwana wa Mungu

alikuwepo wakati Mungu

anaumba mbingu na nchi. Sasa

Mungu anasema, , Iwe nuru, Je

Mungu alikuwa anamwambia

nani? Bila shaka alikuwa

anamwambia yule ambaye yupo

pembeni yake kama stadi wake wa

kazi yani Mwana wa Mungu Yesu

Kristo.

Mithali 8

29 Alipoipa bahari mpaka wake,

Kwamba maji yake yasiasi amri

yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;

30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye,

kama stadi wa kazi; Nikawa

furaha yake kila siku; Nikifurahi

daima mbele zake;

Wenda umeanza kuelewa kile

ambacho anataka kukisema.

Kwamba Mungu alikuwa

anaongea na mwana wake ambaye

huyo ni chapa ya “nafsi yake”.

Aliyekuwa anasema “iwe nuru”

alikuwa ni Baba. Na alikuwa

anamwambia stadi wake wa Kazi

Mwana wake. Sasa tuje katika

mstari wa 26 wa kitabu cha

mwanzo,

Mwanzo 1

26 Mungu akasema, Na tumfanye

mtu kwa mfano wetu, kwa sura

yetu; wakatawale samaki wa

baharini, na ndege wa angani, na

wanyama, na nchi yote pia, na kila

chenye kutambaa kitambaacho juu

ya nchi

Tunaona kuwa Mungu anasema

tumfanye Mtu “kwa mfano wetu.”

Wengi wanapofika katika mstari

huu wanadhani kuwa Nafsi tatu za

Mungu ndizo zinafanya mjadala .

Lakini kama jinsi tulivyoona

katika somo lililopita kuwa Kuna

Baba mmoja na huyo ndiye

Mungu. Kama umeelewa vyema

katika somo lililopita itakuwa ni

rahisi kuelewa mstari huu. Kwanza

kabisa Mstari unaonesha wazi

kuwa Baba hakuwa mwenyewe

wakati anaumba Mbingu na nchi

alikuwa na mtu pembeni yake.

Kwa vile Baba anamwambia mtu

huyo tumfanye mtu “kwa mfano

wetu” ni wazi kuwa aliyepembeni

yake alikuwa anafanana na Baba.

Ni mmoja tu ambaye alikuwa na

Baba tangia siku ya kwanza ya

uumbaji ambaye ndiye alikuwa ni

chapa ya nafsi yake. Huyu ni

Mwana wake Yesu Kristo. Hivyo

tunaelewa kuwa Baba alikuwa

namwambia mwana wake kuwa

“tumfanye mtu kwa mfano wetu”

Page 16: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

14

Ni Baba ndiye aliyekuwa

anaongea na mwana kuhusu

kumfanya mtu kwa mfano wao.

“29 Alipoipa bahari mpaka wake,

Kwamba maji yake yasiasi amri yake;

Alipoiagiza misingi ya nchi; 30 Ndipo

nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa

kazi; Nikawa furaha yake kila siku;

Nikifurahi daima mbele zake”—Mithali

8:29-30

Je Yesu ni Melkizedeki?

Ili tujubu swali hili inabidi kusome

kitabu cha mwanzo tena,

Mwanzo 14: 17

7 Abramu aliporudi kutoka

kumpiga Kedorlaoma na wale

wafalme waliokuwa pamoja naye,

mfalme wa Sodoma akatoka

amlaki katika bonde la Shawe,

nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na

Melkizedeki mfalme wa Salemu

akaleta mkate na divai, naye

alikuwa kuhani wa Mungu Aliye

juu sana. 19 Akambariki,

akasema, Abramu na abarikiwe na

Mungu Aliye juu sana, Muumba

mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe

Mungu Aliye juu sana, aliyewatia

adui zako mikononi mwako.

Abramu akampa fungu la kumi la

vitu vyote.

Melkizedek alikuwa ni mfalme wa

Salemu napia alikuwa ni Kuhani

wa Mungu. Kuna jambo ambalo

kila mmoja atagundua kuwa

Kipindi ambacho Abram na

Melkizedek wanakutana, tayari

Melkizedeki alikuwa ni Kuhani na

pia alikuwa tayari ni Mfalme.

Paulo pia anasema,

Waebrania 7:1-3

Kwa maana Melkizedeki huyo,

mfalme wa Salemu, kuhani wa

Mungu aliye juu, aliyekutana na

Ibrahimu alipokuwa akirudi katika

kuwapiga hao wafalme,

akambariki; 2 ambaye Ibrahimu

alimgawia sehemu ya kumi ya vitu

vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza

ni mfalme wa haki, tena, mfalme

wa Salemu, maana yake, mfalme

wa amani; 3 hana baba, hana

mama, hana wazazi, hana mwanzo

wa siku zake, wala mwisho wa

uhai wake, bali amefananishwa na

Mwana wa Mungu); huyo adumu

kuhani milele.

Kitendo cha kwamba Melkizedek

anafananishwa na mwana wa

Page 17: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

15

Mungu Yesu Kristo inatosha

kutuambia kuwa Melkizedeki

hakuwa mwana wa Mungu. Bali

alifananishwa na mwana wa

Mungu, kwasababu mwana wa

Mungu ni Mfalme na pia ni

kuhani.

Lakini pia tunaona kuwa Mwana

wa Mungu Yesu Kristo hakuwa

Kuhani kabla ya msalaba bali

baada ya kufa msalabani.

Tukisoma vitabu vyote vya Agano

la kale tunaona kuwa kulikuwa na

makuhani na hao ndio waliokuwa

wanafanya kazi ya kupatanisha

watu wa Mungu kwa Mungu. Yesu

hakuwa Kuhani kabla ya kuja

kwake hapa duniani, bali baada ya

kufa msalabani. Paulo anasema,

Waebrania 9

11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye

kuhani mkuu wa mambo mema

yatakayokuwapo, kwa hema iliyo

kubwa na kamilifu zaidi,

isiyofanyika kwa mikono, maana

yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12

wala si kwa damu ya mbuzi na

ndama, bali kwa damu yake

mwenyewe aliingia mara moja tu

katika Patakatifu, akiisha kupata

ukombozi wa milele. 13 Kwa

maana, ikiwa damu ya mbuzi na

mafahali na majivu ya ndama ya

ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye

uchafu hutakasa hata kuusafisha

mwili; 14 basi si zaidi damu yake

Kristo, ambaye kwamba kwa Roho

wa milele alijitoa nafsi yake kwa

Mungu kuwa sadaka isiyo na

mawaa, itawasafisha dhamiri zenu

na matendo mafu, mpate

kumwabudu Mungu aliye hai?

Tunaona kuwa ukuhani wa Yesu

sio ukuhani wa hapa duniani bali

ni ukuhani katika hekalu la juu

mbinguni. Kristo alipokuja na

akafa msalabani anatumia damu

yake iliyomwagika pale msalabani

na kuingia nayo katika hekalu la

mbinguni kutoa upatanisho

kwaajili ya dhambi za ulimwengu.

Lakini Melkizedek alikuwa ni

kuhani wa hapa duniani. Ni wazi

kuwa Melkizedeki hakuwa Yesu

Kristo mwana wa Mungu.

Ukuhani wa Kristo haitumii damu

ya wanyama, bali unatumia damu

yake iliyobora kuliko damu za

wanyama, wakati ukuhani wa hapa

duniani ulikuwa unatumia damu

ya wanyama ukisubiri ujio wa

damu ya Kristo. Kwa vile

Melkizedeki alikuwa ni kuhani

tayari. Hii inamaana kuwa ukuhani

wa Melkizedeki ulitegemea damu

za wanyama.

Pia tunaona kuwa Melkizedeki

alikuwa ni mfalme wa Salem.

Lakini Ufalme wa Kristo ulikuwa

bado haujaja hivyo rasmi Kristo

alikuwa bado sio mfalme mpaka

wakati ambapo ufalme utakuja,

Page 18: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

16

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa

mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale

samaki wa baharini, na ndege wa angani,

na wanyama, na nchi yote pia, na kila

chenye kutambaa kitambaacho juu ya

nchi (Mwanzo 1:26)

Mathayo 6:9

Basi ninyi salini hivi; Baba yetu

uliye mbinguni, Jina lako

litukuzwe, Ufalme wako uje,

Katika Sala ambayo Kristo

aliwafundisha wanafunzi wake

inaonesha wazi kuwa ufalme wa

Mungu ulikuwa bado haujaja ndio

maana Kristo alitufundisha

kuomba kuwa ufalme wake uje.

Lakini Melkizedeki alikuwa tayari

ni mfalme wa Salem alikuwa

tayari anaufalme. Wakati ufalme

wa Kristo ulikuwa bado haujaja.

Hata sasa bado ufalme wa Kristo

haujaja kwa maana ufalme wa

Kristo utakuwa hapa duniani na

ambao watakaokuwa katika

Ufalme huo ni wale ambao

wamefua mavazi yao na

wamemfata Bwana wao kwa

kuikana nafsi zao. Kitabu cha

Ufunuo kinatupa uelewa kuwa

makao makuu ya ufalme wa

Mungu itakuwa ni Yerusalem

mpya na makao hayo makuu

yatashushwa hapa duniani yaani

Mungu na mwana wa Mungu

watakuwa hapa duniani.

Ufunuo 21:10-14

Akanichukua katika Roho mpaka

mlima mkubwa, mrefu,

akanionyesha ule mji mtakatifu,

Yerusalemu, ukishuka kutoka

mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

11 wenye utukufu wa Mungu, na

mwangaza wake ulikuwa mfano

wa kito chenye thamani nyingi

kama kito cha yaspi, safi kama

bilauri; 12 ulikuwa na ukuta

mkubwa, mrefu, wenye milango

kumi na miwili, na katika ile

milango malaika kumi na wawili;

na majina yameandikwa ambayo

ni majina ya kabila kumi na mbili

za Waisraeli. 13 Upande wa

mashariki milango mitatu; na

upande wa kaskazini milango

mitatu; na upande wa kusini

milango mitatu; na upande wa

magharibi milango mitatu. 14 Na

ukuta wa mji ulikuwa na misingi

kumi na miwili, na katika ile

Page 19: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

17

misingi majina kumi na mawili ya

wale mitume kumi na wawili wa

Mwana-Kondoo.

Wakati tayari Melkizedeki

alikuwa ni mfalme wa Salemu,

Kristo alikuwa anasubiri ufalme

utakaokuja katika wakati ujao kwa

maana wale watakao kuwa katika

ufalme huo ni wale ambao

wameamua kumuamini Yesu

Kristo. Ndio maana Paulo hasemi

kuwa Melkizedeki ni Yesu Kristo

bali anasema kuwa Ukuhani na

ufalme wa Yesu Kristo ni kama ule

wa Melkizedeki lakini

Melkizedeki na Yesu Kristo ni

wawili tofauti.

Je Yesu Kristo ndiye Baba?

Najua unaweza kuniuliza Mbona

Isaya 9:6 imesema kuwa Kristo ni

Baba wa milele inamaana kuwa

Baba sio mwingine ila Kristo. Kwa

kuanza naomba tusome tena kitabu

cha,

Isaya 9

6 Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto

mwanamume; Na uweza wa

kifalme utakuwa begani mwake;

Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,

Baba wa milele, Mfalme wa amani

Katika Mstari kuna mambo

ambayo napenda uelewe. Kuwa

katika mstari huu kuna mambo

ambayo yalitimia wakati Yesu

alipokuja na kuna mambo ambayo

yatatimia katika mbingu mpya na

nchi mpya. Ngoja nianze

kukuonesha

“Maana kwa ajili yetu mtoto

amezaliwa, Tumepewa mtoto

mwanamume; Na uweza wa

kifalme utakuwa begani mwake”

Maneno haya yalitimia wakati

Yesu amekuja hapa duniani. Yesu

alipokuja hapa duniani alikuja

kama mwanakondoo wa Mungu

achukuaye dhambi za ulimwengu.

Japokuwa uweza wa kifalme

ulikuwa katika mabega yake lakini

alikuwa rasmi bado sio mfalme

bali alikuja kama mwanakondoo

wa Mungu,

Yohana 1

29 Siku ya pili yake amwona Yesu

anakuja kwake, akasema, Tazama,

Mwana-kondoo wa Mungu,

aichukuaye dhambi ya ulimwengu

Yohana alimwona kuwa Yesu

alikuwa ni mwanakondoo ambaye

amekuja kuchukua dhambi za

ulimwengu. Japokuwa uweza wa

kifalme ulikuwa katika mabega

yake lakini Yesu alikuwa bado

hajawa mfalme na alipokuja

alikuja sio kama mfalme bali kama

ni mtumwa. Kristo mwenyewe

anasema kuwa hakuja hapa

Page 20: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

18

duniani kuwa mfalme wa

ulimwengu huu bali katika ufalme

ujao ambao hakutakuwa na

dhambi ndani yake. Yesu alisema,

Yohana 14

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna

makao mengi; kama sivyo,

ningaliwaambia; maana naenda

kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi

nikienda na kuwaandalia mahali,

nitakuja tena niwakaribishe

kwangu; ili nilipo mimi, nanyi

mwepo.

Hii inaonesha kuwa wakati yupo

hapa duniani bado makao ya watu

wake mbinguni yalikuwa bado

hayajaandaliwa. Na lengo kubwa

la Kristo kurudi kwa Baba ni ili

aandae ufalme ambao watu wake

watakuwa na makao ndani yake.

Hivyo tunaelewa kuwa wakati

Yesu amekuja hapa duniani

alikuwa na uweza wa kifalme

lakini bado hakuwa mfalme kwa

maana bado alikuwa hajaandaa

makao kwaajili ya watu wake.

“Naye ataitwa jina lake, Mshauri

wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,

Baba wa milele, Mfalme wa

amani”

Yesu kuwa mshauri wa ajabu

ilitimia wakati yupo hapa duniani

na hata baada ya kurudi mbinguni.

Kwa maana hata sasa Yesu ndiye

mshauri wetu kwa maana

anatupenda na kila siku anataka

tuwe katika hali nzuri kimwili na

kiroho.

“Mungu mwenye nguvu” Kama

jinsi tulivyoona katika somo

lililopita kuwa Yesu alikuwepo

wakati Mungu anaumba dunia.

Yeye naye aliumba dunia na vitu

vyote kwa maana yeye ndiye

alikuwa stadi wa kazi wa Mungu.

Hebu tazama viumbe wa Mungu,

miti, milima, bahari, mawingu ya

angani hivi vyote utaona ubunifu

wake Yesu Kristo. Ni kweli kuwa

yeye ni “Mungu mwenye nguvu”

kwa maana sio tu aliumba vyote,

bali pia alizaliwa na Mungu

mwenye nguvu. Na kwa kutumia

kanuni hii ya Biblia,

Yohana 3

6 Kilichozaliwa kwa mwili ni

mwili; na kilichozaliwa kwa Roho

ni roho.

Na kwa vile Kristo mwenyewe

alisema alizaliwa kabla ya

uumbaji,

Mithali 8

25 Kabla milima haijawekwa

imara, Kabla ya vilima nalizaliwa.

kwa kutumia kanuni hii ambayo

Kristo mwenyewe alisema, ni wazi

kuwa Aliyezaliwa na Mungu ni

Mungu. Na kwa vile Mungu ni

Mungu mwenye nguvu basi ni

Page 21: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

19

wazi kuwa aliyezaliwa na Mungu

mwenye nguvu ni Mungu mwenye

nguvu pia. Hivyo Kristo ni Mungu

kwasababu amezaliwa na Mungu.

Na amerithi uungu wa Baba yake

na hata jina lake,

Waebrania 1

4 amefanyika bora kupita malaika,

kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo

tukufu kuliko lao.

Kama jina alilorithi ni kuu kuliko

lile la malaika ni wazi kuwa

hakuna jina lingine ila jina la

Mungu. Kama jinsi mtoto

anavyorithi jina la Baba yake,

Kristo amerithi jina la Baba yake

lililokuu kuliko jina la Malaika.

“Baba wa milele” Sasa tuje katika

kiini cha swali na nafikiri ulikuwa

unasubiria kwa hamu kufika katika

sehemu hii, nisingeweza kuanza

mara moja katika sehemu hii bila

kuelezea sehemu zingine kwa

maana ni vyema tukapata uelewa

wa jumla.

Yesu Kristo katika isaya anaitwa

“Baba wa milele” wengi

waliposoma mstari huu walikuja

na hitimisho kuwa Baba ambaye

Yesu alikuwa anamzungumzia

alikuwa ni yeye mwenyewe.

Tukisema kuwa Yesu ndiye Baba

ambaye mara nyingi Yesu alikuwa

anamsemea, hii italeta maana

kuwa Yesu alikuwa anaomba

kwenda kwake mwenyewe, hata

ile sauti iliyosema “Huyu ni

mwanangu mpendwa” ilikuwa ni

sauti ya kwake mwenyewe. Lakini

ukweli ni kwamba Yesu ana Baba

na Baba yake ndiye tunasema

ndiye Mungu wetu.

Yohana 8

19 Basi wakamwambia, Yuko wapi

Baba yako? Yesu akajibu, Mimi

hamnijui, wala Baba yangu

hammjui; kama mngalinijua mimi,

mngalimjua na Baba yangu.

Katika mstari huu tunaelewa kuwa

Yesu na Baba yake ni watu wawili

tofauti. Na hakuna ambaye

atashindwa kuelewa kuwa Baba na

Yesu ni wawili tofauti, kwa maana

kila mmoja ambaye anaamini kuna

Baba, mwana na Roho mtakatifu

lazima aamini kuwa Baba na

mwana ni wawili tofauti.

Sasa kwanini Kristo anaitwa

“Baba wa milele”? tukumbuke

kuwa Yesu alisema,

Yohana 17

24 Baba, hao ulionipa nataka

wawe pamoja nami po pote nilipo,

wapate na kuutazama utukufu

wangu ulionipa; kwa maana

ulinipenda kabla ya kuwekwa

msingi ulimwengu.

Pia Yohana akasema,

Page 22: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

20

Yohana 1

12 Bali wote waliompokea

aliwapa uwezo wa kufanyika

watoto wa Mungu, ndio wale

waliaminio jina lake;

Paulo akasema,

Warumi 8

16 Roho mwenyewe hushuhudia

pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi

tu watoto wa Mungu;

Yohana pia akasema,

1 Yohana 5

2 Katika hili twajua kwamba

twawapenda watoto wa Mungu,

tumpendapo Mungu, na kuzishika

amri zake

Sasa tukumbuke kuwa Mungu

aliona vyema kumfanya mwanae

awe sawa na yeye,

Wafilipi 2

6 ambaye yeye mwanzo alikuwa

yuna namna ya Mungu, naye

hakuona kule kuwa sawa na

Mungu kuwa ni kitu cha

kushikamana nacho.

Sasa kwa vile Kristo aliomba

“Baba, hao ulionipa nataka wawe

pamoja nami po pote nilipo,

wapate na kuutazama utukufu

wangu ulionipa; kwa maana

ulinipenda kabla ya kuwekwa

msingi ulimwengu.”

Ni wazi kuwa Wale wote

waliokombolewa na Kristo, Yesu

anahaki ya kuwadai kama ni

watoto wake pia. Na kama kuna

mtoto basi ni lazima kuna Baba.

Kama waliokombolewa na Kristo

ni watoto wa Kristo, basi ni wazi

kuwa Yesu Kristo pia Baba yao.

Ndio maana anamuomba Baba

yake kuwa Watu aliowakomboa

wakae Pamoja nae. Lakini Ni

mpaka watoto wa Kristo

wajulikane ni nani na watoto wa

Shetani wajulikane ni nani ndipo

hapo ambapo Yesu atakaa pamoja

na watoto wake. Wakati tuliopo

bado Ngano na magugu

hayajatengwa. Ni ngumu kujua

nani ni mtoto wa Kristo na nani

siye. Kwa vile Ombi la Kristo ni

kukaa pamoja na watu wake, kama

vile Baba anavyokaa na watoto

wake, ni wazi kuwa ni kweli kuwa

watoto wa Mungu wapo hata sasa

na Yesu atakaa nao katika ufalme

wake,

Tukumbuke kuwa Yesu pia

alisema,

Yohana 17

6 Jina lako nimewadhihirishia

watu wale ulionipa katika

ulimwengu; walikuwa wako,

ukanipa mimi, na neno lako

wamelishika.

Akasema pia,

Page 23: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

21

Yohana 16

15 Na yote aliyo nayo Baba ni

yangu; kwa hiyo nalisema ya

kwamba atatwaa katika yaliyo

yangu, na kuwapasheni habari

Kwa vile Yesu anasema kuwa

“walikuwa wako, ukanipa mimi,”

Ni wazi kuwa watoto wa Mungu ni

watoto wa Kristo. Kama jinsi

Mungu ni Baba wa Yesu Kristo,

Yesu Kristo ni Baba wa wote

aliowakomboa. Hivyo ni kweli

kuwa Kristo ni Baba wa milele wa

wote aliowakomboa kwa damu

yake.

“Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani

mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo,

kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi,

isiyofanyika kwa mikono, maana yake,

isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu

ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake

mwenyewe aliingia mara moja tu katika

Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa

milele. (Waebrania 9:11-12)

Naye Neno ni Mungu

Kama jinsi tulivyoona hapo juu ya

kuwa Kristo alizaliwa na Mungu

hata kabla ulimwengu

haujaumbwa. Na kwa vile Kristo

amesema kuwa alizaliwa

inamaana kuwa kuna kipindi

ambacho hakuwepo ila Baba yake

alikuwepo. Mwana wa Mungu

alianza kuwa mwana pale

alipozaliwa na Mungu. Na Mungu

alianza kuwa Baba pale alipomzaa

mwana. Hatujui ni wakati gani

mwana alizaliwa na Baba lakini

tunachojua ni kwamba Alikuwa

mwana wa Mungu hata kabla ya

kuumbwa kwa chochote kile. Kwa

hiyo kwa vile alizaliwa na Mungu

ni lazima arithi uungu wa Baba

kwa maana ndio asili ya Baba

yake. Hivyo Yesu ni Mungu kwa

asili na mamlaka yale aliyorithi

kwa Baba yake.

Lakini unaweza kuuliza sasa

Mungu hasa ni nani? Katika

mantiki hii inabidi tutegemee

maneno ya Kristo na pia maneno

ya mitume kuwa Mungu mmoja

ambaye anafaa kutambuliwa kuwa

ni Mungu ni Baba yake Yesu

Kristo pekee. Lakini hii haizuii

mwana kuabudiwa kwa maana

kama tukimwabudu Mwana basi

tunamwabudu Baba. Kwa maana

Baba aliona vyema Mwana awe

kama yeye yani afanane naye.

Page 24: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

22

Lakini japokuwa Mwana na yeye

anauungu na ni Mungu, lakini

hakuwahi kusema kuwa yeye ni

nafsi ya Pili ya Mungu mmoja, au

kuna zaidi ya Mungu mmoja wala

hajawahi kusema kuwa yeye ni

Mungu wa Pili. Mwana wa Mungu

anamnyanyua Baba yake kuwa ni

Mungu ambaye sisi tunatakiwa

kumwabudu, Mungu aliyempa

yote mwana. Na hicho ndicho

alichofundisha kuwa,

Yohana 20

17 Yesu akamwambia. Usinishike;

kwa maana sijapaa kwenda kwa

Baba. Lakini enenda kwa ndugu

zangu ukawaambie, Ninapaa

kwenda kwa Baba yangu naye ni

Baba yenu, kwa Mungu wangu

naye ni Mungu wenu

Hatuwezi kukosa kuelewa kuwa

Kristo anamnyoshea kidole Baba

yake kama ndiye Mungu ambaye

tunatakiwa kumwabudu. Kwahiyo

tunaweza kusema kuwa Kuna

Mungu mmoja ambaye ni Baba wa

Yesu Kristo.

“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia,

Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama

mngalinipenda, mngalifurahi kwa

sababu naenda kwa Baba, kwa maana

Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana

14:28)

Page 25: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

23

SOMO LA NNE

ROHO MTAKATIFU NI

NANI?

Sio lengo langu nikuchoshe kwa

kusoma sana mambo mengi. Na

nimeona niishie sehemu hii kama

ndio sehemu ya mwisho ya hiki

kijarida kidogo. Kama unataka

kusoma kwa kina zaidi kuhusu

Fundisho la utatu unaweza

kudownload kitabu kidogo

kinachoitwa “UKWELI KUHUSU

FUNDISHO LA UTATU” katika

website

Ukweliwasasa.wordpress.com.

Utabarikiwa zaidi wakati unasoma

hicho kitabu. Sasa tuangalie

kuhusu Roho mtakatifu. Ili kujibu

swali letu je Roho mtakatifu ni

nani? Inabidi tuanze na mstari huu

kwa maana ndio mstari pekee

katika Biblia ambao unaoeleza

wazi zaidi.

2Wakorintho 3

17 Basi Bwana ndiye Roho;

walakini alipo Roho wa Bwana,

hapo ndipo penye uhuru

Katika kujua Roho mtakatifu ni

nani kila mtu ni lazima aanzie

katika mstari huu. Mstari unaeleza

wazi kuwa Bwana Yesu Kristo

ndiye Roho mtakatifu. Na kama

ndiye Roho inamaana yeye si mtu

mwingine tofauti. Tukumbuke

Yesu aliwahi kuwaambia

wanafunzi wake kuwa.

Mathayo 28

20 na kuwafundisha kuyashika

yote niliyowaamuru ninyi; na

tazama, mimi nipo pamoja nanyi

siku zote, hata ukamilifu wa dahari

Alisema wazi kuwa yupo pamoja

nasi siku zote mpaka ukamilifu wa

dahari. Tukumbuke kuwa maneno

haya Yesu aliyasema kuwa ni yeye

mwenyewe ndiye atakaye kuwa na

watu wake mpaka ukamilifu wa

dahari. Tukisema kuwa Roho

mtakatifu ni tofauti na Yesu

inamaana tunasema kuwa kwasasa

Yesu hayupo na sisi. Lakini Biblia

inasema kitu tofauti kuwa ni Yesu

mwenyewe ndiye atakayekuwa

pamoja na watu wake mpaka

mwisho.

Najua unaweza kuwa na wakati

mgumu kuelewa kile ninachotaka

kumaanisha. Na wenda

unamaswali mengi uniulize,

mojawapo ni Kama Bwana Yesu

ndiye Roho Mtakatifu, kwanini

aseme kuwa atakuja msaidizi

mwingine?

Hili ni swali wengi wameuliza

lakini ni swali ambalo linajibika.

Ili tuweze kujibu hili swali ambalo

wenda unaweza ukawanalo

kichwani, inabidi tuangalie,

Page 26: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

24

Yohana 14

16 Nami nitamwomba Baba, naye

atawapa Msaidizi mwingine, ili

akae nanyi hata milele; 17 ndiye

Roho wa kweli; ambaye

ulimwengu hauwezi kumpokea,

kwa kuwa haumwoni wala

haumtambui; bali ninyi

mnamtambua, maana anakaa

kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Tukumbuke ule mstari ambao

tulikwisha soma, wa Mathayo

28:20,

“na kuwafundisha kuyashika yote

niliyowaamuru ninyi; na tazama,

mimi nipo pamoja nanyi siku zote,

hata ukamilifu wa dahari”

Yesu anasema kuwa Huyo

msaidizi atakaa pamoja nao milele.

Kwa vile Yesu alisema kuwa ni

yeye mwenyewe ndiye atakaye

kaa na watu wake siku zote na

hakuna wakati ambao hatokaa na

watu wake inamaana kuwa huyo

msaidizi sio mwingine ile yeye

mwenyewe kwa maana ni yeye

ndiye aliyeahidi kuwa atakaa na

watu wake.

Pia Yesu aliwaambia wanafunzi

wake kuwa Huyo msaidizi

“watamtambua” lakini ulimwengu

hauwezi mtambua. Katika hali ya

kawaida hatuwezi mtambua mtu

tusiyemjua. Kwa kawaida kabisa

tunamtambua mtu tunayemjua au

tulishamuona tayari. Kitendo cha

kwamba Yesu anawaambia kuwa

Watamtambua Huyo msaidizi ni

wazi kuwa wanafunzi wake

walikuwa wanamjua huyo

msaidizi. Hata Daudi alikuwa

anamjua msaidizi. Alisema,

Zaburi 118

7 Bwana yuko upande wangu,

msaidizi wangu, Kwa hiyo

nitawaona wanaonichukia

wameshindwa.

Daudi alitambua kuwa Bwana

ndiye msaidizi wake siku zote.

Bwana sio msaidizi tu kwa Daudi

bali ni msaidizi wa wote ambao

wanaitwa kwa jina lake. Yesu

anaongezea na kusema kuwa huyo

msaidizi anakaa nao. Katika kauli

hii utagundua kuwa huyo msaidizi

sio mtu ambaye atakuja kukaa nao

kwa mara ya kwanza hapana bali

tayari huyo msaidizi anakaa nao.

Sidhani katika maelezo haya

utapata ugumu kuweza kuelewa

vyema. Yesu anasema kuwa huyo

msaidizi “anakaa kwenu” tunaona

kuwa sentensi iliyotumika hapa ni

ile ya wakati wa sasa “Anakaa

kwenu” wakati ile aliyosema kuwa

“atakuwa ndani yenu” ni ya wakati

ujao. Ni wazi kuwa Yesu Kristo

alikuwa anawaonesha kuwa yeye

ndiye msaidizi ambaye anakaa nao

lakini inabidi arudi kwa Baba ili

Page 27: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

25

aweze kukaa ndani yao. Yesu

alisema,

Yohana 14

18 Sitawaacha ninyi yatima; naja

kwenu. 19 Bado kitambo kidogo

na ulimwengu haunioni tena; bali

ninyi mnaniona. Na kwa sababu

mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa

hai.

Katika mstari huu aliyosema Yesu

kuna jambo ambalo hautapata

ugumu kulielewa. Yesu alisema

kuwa hatowaacha yatima.

Kwamba hatowaacha katika hali

ambayo hawana msaidizi. Hakuna

wakati ambao Bwana Yesu

hakuwa msaidizi wa wanadamu,

alikuwa msaidizi kwa Daudi

hawezi shindwa kuwa msaidizi wa

wanafunzi wake. Atakuwa nao

siku zote, na kwa kuongezea hapo

Yesu anasema kuwa Bado kitambo

kidogo na ulimwengu haumuoni

tena bali wao wanamuona. Hebu

tutumie sekunde kadhaa

kutafakari.

Anasema kuwa Hatowaacha

yatima bali anakuja kwao, Wakati

anakuja kwao ulimwengu

haumuoni bali wanafunzi wake

pekee ndiyo wanaomuona. Je

maneno haya Yesu alikuwa

anazungumzia ujio wake wa Pili

Mawinguni? Ukweli ni wazi kuwa

ni hapana, kwanini ni hapana? Ni

kwasababu Imeandikwa,

Ufunuo 1

7 Tazama, yuaja na mawingu; na

kila jicho litamwona, na hao

waliomchoma; na kabila zote za

dunia wataomboleza kwa ajili

yake. Naam. Amina.

Kila jicho litamuona wakati Yesu

Kristo anapokuja kwa mara ya pili.

Lakini kwanini atakapokuja

atajifunua kwa wanafunzi wake na

hatojifunua kwa ulimwengu?

Tukumbuke kuwa hili ndilo jambo

ambalo wanafunzi wake walielewa

na wakamuuliza kwanini anataka

kufanya hilo

Yohana 14

22 Yuda (siye Iskariote),

akamwambia, Bwana, imekuwaje

ya kwamba wataka kujidhihirisha

kwetu, wala si kwa ulimwengu?

Walielewa vyema kuwa Yesu

alikuwa na mpango

wakujidhihirisha kwao na wala sio

kwa ulimwengu. Hii inamaana

kuwa alipowaambia wanafunzi

wake kuwa,

Yohana 16

16 Bado kitambo kidogo nanyi

hamnioni; na tena bado kitambo

kidogo nanyi mtaniona.

Page 28: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

26

Japokuwa mstari huu unaweza

kutupa maana kuonyesha ujio

wake kwa mara ya pili, lakini pia

unatuonesha baada ya kufufuka

kwake. Kwa maana ni kweli kuwa

baada ya kufufuka kwake

wanafunzi wake walimuona. Na

hata leo hii tunamuona Yesu katika

maisha yetu. Si kwa sura, bali kwa

mambo anayotufanyia. Hivyo

kwavile Yesu aliahidi kuwa

hatotuacha yatima yeye

mwenyewe atakuja kukaa na sisi

na sio tu katika kipindi

atakapokuja kwa mara ya pili, bali

hata sasa yupo nasisi inamaan

kuwa, Yesu Kristo anakaa na sisi

sio kwa kuonekana kwa mwili bali

anakaa na sisi katika Roho yeye

ndiye msaidizi wetu.

Lakini kwanini Yesu

alimzungumzia msaidizi kama ni

mtu mwingine tofauti na yeye?

Kwa mfano,

Yohana 16

14 Yeye atanitukuza mimi, kwa

kuwa atatwaa katika yaliyo yangu

na kuwapasha habari

Yesu alipokuwa anamzungumzia

msaidizi mwingine kama ni mtu

tofauti na yeye, ni kwasababu ya

utenda kazi. Tukumbuke kuwa

wakati Yesu alipokuwa katika

ubinadamu alikuwa katika mipaka

ya ubinadamu. Katika mwili wa

kibinadamu ilikuwa haiwezekani

yeye kuwa ndani ya watu wake. Na

kuwa kila sehemu kwa wakati

mmoja. Lakini katika Roho

anaweza kuwa ndani yetu na

kuishi ndani yetu na kuwa kila

sehemu kwa wakati mmoja. Katika

roho alikuwa na uwezo wa

kuwakumbusha yale aliyoyasema

na hata pale ambapo walikuwa

hawajaelewa alikuwa

anawaelewesha kikamilifu.

Tukisema kuwa Roho mtakatifu ni

mtu tofauti kabisa na Yesu Kristo

itakuwa ni tofauti kabisa na ile

ahadi ambayo Yesu mwenyewe

alisema kuwa atakuwa pamoja nao

hata ukamilifu wa dahari.

Tukumbuke alisema kuwa ni yeye

mwenyewe ndiye atakaye kuwa

pamoja nao sio mtu mwingine.

Kutokana na hili ndio maana Paulo

anasema wazi kuwa Bwana Yesu

ndiye Roho mtakatifu.

Tukumbuke Pia Yesu alisema

kuwa huyo Msaidizi mwingine ni

roho wa Kweli. Lakini hatupati

ugumu kuelewa kuwa Yesu Kristo

mwenyewe ndiye kweli, kwa

maana alisema,

Yohana 15

6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi

njia, na kweli, na uzima; mtu haji

kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Page 29: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

27

Kwa vile huyo msaidizi ni roho wa

kweli, na kweli ni Yesu Kristo

mwenyewe, tunaelewa kuwa Yesu

Kristo ndiye Huyo msaidizi Roho

mtakatifu.

Mara nyingi tunaposikia neno

“Roho mtakatifu” huwa akili yetu

inaenda mbali sana. Kwa vile neno

hili limetolewa katika lugha ya

kiingereza yani “Holyspirit”

tunaelewa kuwa katika utafsiri,

neno halisi lingetakiwa liwe

“Roho takatifu” tutakapoweka

katika akili zetu uelewa kuwa

Kuna “Roho takatifu” ya Mungu

na ya Kristo, inatosha

kutuelewesha kuwa Roho takatifu

ya Yesu Kristo ni yeye mwenyewe

wala sio mtu mwingine. Kwa

maana hata wanadamu wanaitwa

“Roho”

Ezekieli 18

20 Roho itendayo dhambi, ndiyo

itakayokufa; mwana hatauchukua

uovu wa baba yake, wala baba

hatauchukua uovu wa mwanawe,

haki yake mwenye haki itakuwa

juu yake, na uovu wake mwenye

uovu utakuwa juu yake.

Kwa kusema “Roho itendayo

dhambi ndiyo itakayokufa”

Hakuna mtu ambaye atapata

ugumu kuelewa inamaanisha kuwa

“Mtu atendaye dhambi ndiye

atakayekufa” Kwa maana mtu ni

roho hata wewe unayesoma Roho

yako sio mtu mwingine tofauti na

wewe mwenyewe.

Hivyo pale ambapo Yesu

alimsemea Msaidizi mwingine

kama ni mtu tofauti, hakuwa na

maana kuwa yeye hatokaa pamoja

nao na kuwasaidia bali kwamba

utendaji kazi wake utakuwa tofauti

na utendaji kazi wake alipokuwa

katika mwili. Katika Roho

atafanya makubwa zaidi kuliko

alivyokuwa katika mwili. Hata

ukisoma kitabu cha Matendo

utaona kuwa baada ya msalaba

ukristo ulienea zaidi kuliko kabla

ya msalaba.

Ninachotaka uelewe ni kwamba

Biblia inaposema “Roho

mtakatifu” basi unatakiwa uelewe

kuwa ni uwepo wa Baba na mwana

wao wenyewe sio mwingine. Kwa

maana kama Mungu ni Roho na

Bwana Yesu ni Roho,

Yohana 4

24 Mungu ni Roho, nao

wamwabuduo yeye imewapasa

kumwabudu katika roho na kweli

Ina maana ni wazi kuwa kwa

ujumla tunapozungumzia Roho

mtakatifu sio mwingine ila uwepo

wa Baba na Mwana. Kama

tutasema kuwa Roho wa Mungu ni

tofauti na Mungu mwenyewe na

roho wa Kristo ni tofauti na Kristo

Page 30: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

28

mwenyewe, Inamaana hata

ukisema kuwa Mungu ni nafsi tatu

bado hautakuwa sahihi kwa maana

itakuwa kuna

1. Mungu Baba

2. Mungu Roho Wa Baba

3. Mungu Mwana

4. Mungu Roho Wa Mwana

5. Mungu Roho Mtakatifu

6. Mungu Roho Wa Roho

Mtakatifu.

Nafikiri hata wewe unaona hakuna

utatu tena bali kuna usita na bila

shaka hautakubali. Paulo alisema

wazi kuwa kuna Roho wa Mungu

na kuna roho wa Kristo,

Warumi 8

9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu

anakaa ndani yenu, ninyi

hamwufuati mwili; bali mwaifuata

roho. Lakini mtu awaye yote

asipokuwa na Roho wa Kristo,

huyo si wake.

Kama unaamini kuwa Roho wa

Mungu sio tofauti na Mungu

mwenyewe na Roho wa Kristo sio

tofauti na Kristo mwenyewe

kwanini inakuwa ngumu kuamini

ninaposema kuwa Roho mtakatifu

ndiye Yesu Kristo na ni Baba

mwenyewe? Kwa maana majina

“Roho wa Mungu” na “Roho wa

Kristo” na “Roho mtakatifu” ni

kitu kimoja na ni jambo hilo hilo.

Ni uwepo wa Baba na Mwana.

Kristo aliwahi kusema kuwa,

Ufunuo 3

20 Tazama, nasimama mlangoni,

nabisha; mtu akiisikia sauti yangu,

na kuufungua mlango, nitaingia

kwake, nami nitakula pamoja

naye, na yeye pamoja nami.

Naomba nikuulize swali, ni lini

ambapo Yesu Kristo alikuja kula

na wewe? Kwa vile Kristo hawezi

kusema uongo, ni wazi kuwa Pale

unaposali kwaajili ya chakula na

wakati unakula Kristo anakuwa

anakula na wewe japokuwa

haumuoni. Hata sasa Kristo

amekuwa anakula pamoja na

wewe muda wote na anatembea na

wewe kila siku na kile saa, najua

hili nililosema hauwezi kukataa,

hivyo ni kweli kuwa Yesu yupo

pamoja na wewe lakini sio katika

mwili kwamba utamuona bali

katika Roho. Kama ukisema kuwa

Roho na Kristo ni wawili tofauti

inamaana Yesu alisema uongo

kwa maana hakuna siku

uliyomuona amekuja kula na

wewe. Kwa maana aliposema

atakuja kukaa na kula pamoja na

wewe alisema ni yeye mwenyewe

sio mwingine.

Page 31: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

29

“Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku

zote, hata ukamilifu wa dahari”.

(Mathayo 28:20)

Ubatizo wa Yesu.

Nimeona pia nizungumzie Kuhusu

ubatizo wa Yesu Kristo kwa

maana kuwa wengi wanaotumia

tukio hilo la ubatizo wa Yesu kama

ni hoja ya kutofautisha Baba

Kristo na Roho mtakatifu.

Tusome,

Luka 3

22 Roho Mtakatifu akashuka juu

yake kwa mfano wa kiwiliwili,

kama hua; sauti ikatoka mbinguni,

Wewe ndiwe Mwanangu,

mpendwa wangu; nimependezwa

nawe.

Tuanze kuzungumzia ile sauti

iliyonena. “Wewe ndiwe

Mwanangu, mpendwa wangu;

nimependezwa nawe.” Ilikuwa ni

sauti ya Baba aliyembinguni. Na

alisema hadharani ili kila mmoja

aweze kumwamini Mwana kuwa

yeye ndiye aliyemtuma. Lakini

japokuwa Baba alinena wazi

wengi hawakumwamini.

Sasa Roho mtakatifu alishuka

kama Huwa, na watu walimwona

huyo Huwa akishuka, wengi leo

hii wamekuwa na uelewa kuwa

Roho mtakatifu ni njiwa. Na wengi

wamejaribu kumchora njiwa kama

ndiye Roho mtakatifu. Pia wengi

wanaposoma kisa cha kubatizwa

kwake Yesu wameishia kuwa na

mtazamo kuwa katika tukio hilo

Baba, mwana, na Roho wote

walikuwepo pale Mtoni. Lakini

tunasahau kuwa Yesu alisema,

Yohana 4

24 Mungu ni Roho, nao

wamwabuduo yeye imewapasa

kumwabudu katika roho na kweli.

Ukweli ni kwamba Ni Mungu

ndiye aliyeshuka kwa mfano wa

kiwiliwili kama hua na sio mtu

mwingine yoyote. Mungu ni roho,

na Roho ndiye aliyeshuka kama

njiwa, inamaana ni wazi kuwa ni

Mungu mwenyewe ndiye

aliyeshuka kama njiwa pale mtoni.

Page 32: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

30

Mungu asingeweza kushuka na

utukufu wake pale mto Yordani

kwa maana hakuna ambaye

angeishi. Na aliposhuka

akamtangaza mwanae wazi wazi

akisema kuwa huyu ni Mwanangu

Mpendwa.

Hivyo ni Baba na Mwana pekee

ndio waliokuwepo katika tukio la

ubatizo.

Kuzaliwa kwake Yesu.

Hili nalo ni jambo Muhimu

ambalo ni lazima tulielewe. Watu

wote ambao wanaamini kuwa na

imani ya Kikristo wanaamini kuwa

Mariam alipata Mimba kwa uweza

wa Roho mtakatifu.

Luka 1

35 Malaika akajibu akamwambia,

Roho Mtakatifu atakujilia juu

yako, na nguvu zake Aliye juu

zitakufunika kama kivuli; kwa

sababu hiyo hicho

kitakachozaliwa kitaitwa

kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Malaika Gabrieli alimwambia

Mariam kuwa atapata Mimba kwa

uweza wa Roho mtakatifu. Na yule

atakayezaliwa atakuwa ni mwana

wa Mungu. Kila mmoja anaamini

katika huu ukweli ya kwamba

Yesu Kristo hapa duniani alizaliwa

sio kama wengine wanavyozaliwa

yeye alizaliwa bila mwingiliano

wa Baba na Mama. Kipengele hiki

huwa mara nyingi

hatukizungumzii na mara nyingi

huwa tunakiruka lakini kina

umuhimu wake kwa maana

tukielewa hapa itakuwa ni rahisi

kuelewa yote niliyokuwa najaribu

kusema katika somo hili.

Sasa swali linakuja na ninapenda

kukuuliza wewe unayesoma, Nani

ndiye chanzo cha Mariam kuwa na

Mimba, je ni Mungu Baba au ni

Roho mtakatifu?

Kama ni Roho mtakatifu inamaana

kuwa Mungu hausiki kabisa na ile

Mimba ya Mariam, sasa kwa vile

Mariam alipata mimba kwa uweza

wa Roho mtakatifu, Baba wa Yesu

hapa duniani alikuwa ni nani?

Mungu Baba au ni Roho

mtakatifu?

Najua kuwa nimeuliza maswali

magumu, lakini lengo ni kukuleta

katika uhalisia wa mambo na

kuanza kutafakari vyema. Kama

unaamini kuwa Mungu Baba ni

tofauti na Roho mtakatifu, basi ni

Roho mtakatifu ndiye Baba wa

Yesu Kristo hapa duniani na sio

Mungu Baba.

Lakini najua mtu yoyote

akikuuliza Baba wa Yesu

alipozaliwa hapa duniani alikuwa

ni nani, hutosita kusema alikuwa

ni Mungu Baba sio Roho

Page 33: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

31

mtakatifu. Kwa nini hatusemi

alikuwa ni Roho mtakatifu? Ni

kwasababu Mungu Baba ndiye

huyo Roho mtakatifu. Ndio maana

tunaona mara nyingi Yesu Kristo

anamtaja Mungu Baba kuwa ndiye

Baba yake wala sio Roho

mtakatifu.

Hivyo hivyo kokote unapoona

Roho mtakatifu ametajwa basi jua

ni uwepo wa Mungu mwenyewe

na wa Yesu Kristo mwenyewe.

Kanisa la Thiatira

Tunaendelea katika kuchunguza

Maandiko, sasa tungalie Kanisa la

thiatira katika kitabu cha ufunuo.

Na ninaomba usome maneo

ambayo nitayakoleza .

Ufunuo 2

18 Na kwa malaika wa kanisa

lililoko Thiatira andika; Haya

ndiyo anenayo Mwana wa

Mungu, yeye aliye na macho yake

kama mwali wa moto, na miguu

yake mfano wa shaba

iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua

matendo yako na upendo na imani

na huduma na subira yako; tena

kwamba matendo yako ya mwisho

yamezidi yale ya kwanza. 20

Lakini nina neno juu yako, ya

kwamba wamridhia yule

mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye

nabii na kuwafundisha watumishi

wangu na kuwapoteza, ili wazini

na kula vitu vilivyotolewa sadaka

kwa sanamu. 21 Nami nimempa

muda ili atubu, wala hataki

kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama,

nitamtupa juu ya kitanda, na hao

wazinio pamoja naye, wapate

dhiki kubwa wasipotubia matendo

yake; 23 nami nitawaua watoto

wake kwa mauti. Na makanisa yote

watajua ya kuwa mimi ndiye

achunguzaye viuno na mioyo.

Nami nitampa kila mmoja wenu

kwa kadiri ya matendo yake.24

Lakini nawaambia ninyi wengine

mlioko Thiatira, wo wote wasio na

mafundisho hayo, wasiozijua

fumbo za Shetani, kama vile

wasemavyo, Sitaweka juu yenu

mzigo mwingine. 25 Ila mlicho

nacho kishikeni sana, hata

nitakapokuja. 26 Na yeye

ashindaye, na kuyatunza matendo

yangu hata mwisho, nitampa

mamlaka juu ya mataifa, 27 naye

atawachunga kwa fimbo ya

chuma, kama vyombo vya

mfinyanzi vipondwavyo, kama

mimi nami nilivyopokea kwa Baba

yangu. 28 Nami nitampa ile nyota

ya asubuhi. 29 Yeye aliye na sikio,

na alisikie neno hili ambalo Roho

ayaambia makanisa.

Hatutaangalia maana ya huu

unabii, lakini tunaangalia yule

aliyenena huu unabii. Mstari wa

mwanzo kabisa inanesha

anayenena hayo maneno ni mwana

Page 34: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

32

wa Mungu Yesu Kristo. Lakini

mstari wa Mwisho inaonesha

kuwa aliyekuwa anaongea hayo

maneno alikuwa ni Roho

mtakatifu. Ni wazi kabisa Mwana

wa Mungu ndiye roho mtakatifu na

tunarudi tena kwenye hitimisho

yetu kuwa Roho mtakatifu ni roho

ya Baba na Mwana na ni Baba

mwenyewe na Mwana

mwenyewe.

“Malaika akajibu akamwambia, Roho

Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu

zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;

kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa

kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”.

(Luka 1:35)

Nani aliyemtuma Yesu duniani?

Kristo alipoanza kazi yake ya

kuhubiri alianza kwa kusema,

Luka 4

18 Roho wa Bwana yu juu yangu,

Kwa maana amenitia mafuta

kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia

wafungwa kufunguliwa kwao, Na

vipofu kupata kuona tena,

Kuwaacha huru waliosetwa,

Yesu alisema kuwa ni Roho wa

Bwana ndiye aliyemtuma Duniani.

Kama jinsi nilivyokwisha kusema

hapo mwanzo, kama unaamini

kuwa Roho wa Bwana ni tofauti

kabisa na Mungu mwenyewe ni

wazi kuwa Yesu hajatumwa na

Mungu Baba bali na Roho wa

Bwana.

Lakini kama unaamini kuwa Yesu

alitumwa na Mungu Baba kuja

hapa duniani basi ni lazima uamini

kuwa Mungu Baba ndiye Roho wa

Bwana. Yesu alisema,

Yohana 5

36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi

ni mkubwa kuliko ule wa Yohana;

kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba

ili nizimalize, kazi hizo zenyewe

ninazozitenda, zanishuhudia ya

kwamba Baba amenituma.

Page 35: YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio lengo langu nikuelewe vibaya lakini nataka kukuonesha kuwa

33

Inamaana kuwa Roho wa Bwana

ambaye Yesu alisema amemtuma

kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao sio mwingine

ila Mungu Baba. Kama jinsi

nilivyosema hapo mwanzo kuwa

tunapozungumzia Roho mtakatifu

ni uwepo wa Baba na Mwana.

HITIMISHO.

Pole sana kwa kusoma maelezo

marefu sana ambayo nimeandika.

Lakini ilikuwa ni muhimu niweze

kueleza hili jambo kwa urefu

kidogo ili uweze kuelewa kile

ambacho Biblia inasema. Ni

mpango wa Mungu siku zote tujue

ukweli na ukweli huo utuweke

huru. Kama jinsi tulivyoona Biblia

haijasema kuwa Mungu ni nafsi

tatu, na ushahidi wa kimaandiko

unaonesha wazi kuwa hakuna

nafsi tatu. Kama unaona

yaliyonenwa katika kijarida hiki

kidogo ni maneno ya kweli, basi

unaweza kuamini. Lakini kama

unaona yaliyonenwa humu sio

sahihi basi usiamini. Mungu na

akubariki.