yaliyomo - in.tzembassy.go.tz

132

Upload: others

Post on 23-Oct-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz
Page 2: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz
Page 3: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

i

YALIYOMOYALIYOMO ................................................................................. iORODHA YA VIFUPISHO ......................................................... iii1.0 UTANGULIZI..................................................................... 12.0 MISINGI YA SERA YA TANZANIA KATIKA UHUSIANO

WA KIMATAIFA ................................................................ 73.0 TATHMINI YA HALI YA UCHUMI, SIASA, ULINZI NA

USALAMA DUNIANI KWA MWAKA WA FEDHA2020/2021 ......................................................................... 9

3.1 Hali ya Uchumi ............................................................... 93.2 Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ................................. 104.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA

WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 ............ 17Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 .......... 20Mapato............... ...................................................................... 20Fedha Zilizoidhinishwa............................................................. 21Fedha Zilizopokelewa na Kutumika ......................................... 214.1 Kusimamia na Kuratibu Masuala ya Uhusiano Baina ya

Tanzania na Nchi Nyingine .......................................... 224.1.1 Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ......................... 224.1.2 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Afrika.................. 234.1.3 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Asia na

Australasia ................................................................... 314.1.4 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Mashariki ya

Kati………………. ........................................................ 374.1.5 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Ulaya na

Amerika ..........................................................…………404.2 Kuratibu Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda na

Kimataifa ...................................................................... 504.3 Kufuatilia na Kusimamia Utekelezaji wa Mikataba ya

Kimataifa na Hati za Makubaliano ............................... 83

Page 4: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

ii

4.4 Kuratibu Masuala ya Itifaki, Uwakilishi na Huduma zaKikonseli....................................................................... 87

4.4.1 Ziara za Viongozi wa Kitaifa na Mashirika ya Kikanda naKimataifa Kutoka Nje ya Nchi ...................................... 87

4.4.2 Ziara za Viongozi wa Kitaifa Nje ya Nchi ..................... 954.4.3 Kuanzisha na Kusimamia Huduma za Kikonseli.......... 974.5 Uratibu wa Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi

(Diaspora) .................................................................... 994.6 Elimu kwa Umma ....................................................... 1004.7 Utawala na Maendeleo ya Watumishi........................ 1024.7.1 Uteuzi wa Viongozi .................................................... 1024.7.2 Mafunzo ..................................................................... 1034.7.3 Upandishaji Vyeo ....................................................... 1034.7.4 Kubadilisha Kada Watumishi ..................................... 1044.7.5 Uhamisho................................................................... 1044.8 Kuratibu na Kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya

Maendeleo ya Wizara na Taasisi Zilizo Chini yaWizara ........................................................................ 104

4.8.1 Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Wizara ........ 1044.8.2 Utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi Zilizo Chini ya

Wizara ........................................................................ 1055.0 CHANGAMOTO ZILIZOPO NA HATUA

ZILIZOCHUKULIWA ..................................................... 1126.0 SHUKRANI.................................................................... 1137.0 MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA

2021/2022 ..................................................................... 1178.0 MALENGO YA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA KWA

MWAKA WA FEDHA 2021/2022 .................................. 1199.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA

KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 ......................... 12210.0 HITIMISHO.................................................................... 124

Page 5: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

iii

ORODHA YA VIFUPISHO

AfCFTA - African Continental Free Trade Area

AfDB - African Development Bank

AICC - Arusha International Conference Centre

APRM - African Peer Review Mechanism

CFR - Centre for Foreign Relations

COMESA - Common Market for Eastern andSouthern Africa

DRC - Democratic Republic of Congo

EAC - East African Community

EPA - Economic Partnership Agreement

km - Kilometa

kV - Kilovolt

MINUSCA -United Nations MultidimensionalIntergrated Stabilization Mission in theCentral African Republic

MONUSCO -United Nations OrganizationStabilization Mission in the DemocraticRepublic of Congo.

Page 6: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

iv

MW - Megawatt

OACPS - Organisation of African, Carribean andPacific States

OSBP - One Stop Border Post

SADC - Southern African DevelopmentCommunity

TEHAMA - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

UNESCO - United Nations Educational, Scientificand Cultural Organisation

UNDP - United Nations DevelopmentProgramme

UNIDO - United Nations Industrial DevelopmentOrganisation

UNIFIL - United Nations Interim Force inLebanon

UVIKO-19 - Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafuunaosababishwa na Virusi vya Korona

Page 7: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

1

1.0 UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifailiyowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu naMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoahoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea nakujadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti yaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 na pialijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara yaMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwaMwaka wa Fedha 2021/2022.

2. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afyanjema na kuniwezesha kusimama mbele ya Bungelako Tukufu siku ya leo. Kwa kuwa Hotuba hii yaBajeti ni ya kwanza nikiwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napendakumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniaminina kuniteua kuongoza Wizara hii. Napendakumhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa nitafanya kazikwa uwezo wangu wote na kwa kudra za MwenyeziMungu nitatekeleza majukumu yangu ipasavyo katikakuleta maendeleo ya Taifa letu.

Page 8: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

2

3. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba,tarehe 17 Machi, 2021 Taifa lilipata msiba mzito wakuondokewa na Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano waJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, tarehe 24Julai, 2020 tulimpoteza Mheshimiwa Benjamin WilliamMkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania; na tarehe 17 Februari,2021 tuliwapoteza Mheshimiwa Maalim Seif SharifHamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais waZanzibar na Mheshimiwa Balozi Mhandisi JohnWilliam Hebert Kijazi, aliyekuwa Katibu MkuuKiongozi. Naomba kutumia nafasi hii kuungana naWaheshimiwa Mawaziri wenzangu waliotanguliakuwasilisha Hotuba zao kutoa pole kwa MheshimiwaRais, familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzaniawote kwa ujumla kwa misiba hii mizito. Wizara yanguinatambua na kuthamini mchango mkubwa waviongozi hawa katika kukuza taswira ya nchi yetukimataifa na mahusiano ya kidiplomasia baina yetu nanchi mbalimbali.

4. Mheshimiwa Spika, natumia nafasi hii piakutoa shukrani za dhati kwa nchi marafiki na jumuiyaya kimataifa kwa kuonesha mshikamano, kutufariji nakushiriki nasi katika kipindi cha majonzi makubwa kwaTaifa letu.

Page 9: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

3

5. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekeenaomba kutoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwauamuzi wake wa kuitisha kikao rasmi cha Baraza Kuula Umoja huo kwa ajili ya kumuenzi na kumkumbukaHayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waAwamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kilichofanyika tarehe 16 Aprili, 2021 MakaoMakuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York,Marekani. Kupitia kikao hicho, Nchi Wanachama waUmoja wa Mataifa zilielezea mafanikio makubwa yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniayaliyopatikana chini ya Uongozi wa Hayati Dkt.Magufuli katika kuboresha huduma za jamii kama vileelimu, maji, afya, nishati na miundombinu yausafirishaji. Tunawashukuru sana.

6. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kutoapole kwako na Bunge lako Tukufu kufuatia vifo vyaWaheshimiwa Khatibu Said Haji aliyekuwa Mbungewa Jimbo la Konde, Zanzibar aliyefariki tarehe 20 Mei,2021; Mhandisi Atashasta Justus Nditiye aliyekuwaMbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoa wa Kigoma,aliyefariki tarehe 12 Februari, 2021; na Martha JachiUmbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa waManyara, aliyefariki tarehe 21 Januari, 2021.Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemumahala pema peponi. Amina.

Page 10: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

4

7. Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa na kwamoyo mkunjufu napenda kutumia nafasi hiikumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Samia SuluhuHassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sitawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile,nawapongeza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango,kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania; na Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), kwa kuaminiwa na kuendeleakushika nafasi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania. Tuna imani na uongozi mpyaulioingia madarakani kuendelea kudumisha amani naMuungano wetu, kusukuma mbele gurudumu lamaendeleo na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasiana jumuiya ya kimataifa.

8. Mheshimiwa Spika, nampongeza piaMheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi; Mheshimiwa Othman Masoud OthmanSharif kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar; na Mheshimiwa Hemed SuleimanAbdulla kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar.

9. Mheshimiwa Spika, nchi yetu imewekahistoria ya kujivunia na kuigwa duniani kwa namna

Page 11: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

5

ilivyopata uongozi mpya wa juu wa Serikali kufuatiavifo vya Viongozi Wakuu waliokuwa madarakani.Mabadiliko hayo yalifanyika kulingana na misingi yaKatiba. Hatua hii ni kielelezo cha ukomavu, uimarawa demokrasia na misingi ya utawala wa sheria.

10. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikumpongeza tena Mheshimiwa Kassim MajaliwaMajaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa hotuba yake aliyowasilisha hapaBungeni ambayo imetoa dira na mwongozo wautekelezaji wa kazi za Serikali kwa Mwaka wa Fedha2021/2022. Nawapongeza pia Waheshimiwa Mawaziriwenzangu walionitangulia kuwasilisha hotuba zaokatika Bunge hili la Bajeti.

11. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongezawewe binafsi kwa uongozi wako madhubuti katikauendeshaji wa shughuli za Bunge. Aidha,nampongeza Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb),Naibu Spika; Wenyeviti wa Bunge; na Wenyeviti waKamati za Kudumu za Bunge kwa kazi nzuriwanazozifanya kukusaidia kusimamia na kuendeshashughuli za Bunge. Naomba Mwenyezi Mungu azidikuwajalia afya njema, busara na hekima katikakuongoza Mhimili huu muhimu kwa Taifa letu.

Page 12: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

6

12. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekeenapenda kuipongeza na kuishukuru Kamati yaKudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi naUsalama chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa MussaAzzan Zungu (Mb), pamoja na Makamu MwenyekitiMheshimiwa Vincent Paul Mbogo (Mb), kwa kazi nzurina ya kizalendo ya kuishauri Serikali hususan Wizarayangu. Naomba nikiri kuwa miongozo na ushauri waokatika masuala mbalimbali umekuwa na mchangomkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

13. Mheshimiwa Spika, naomba piakuwapongeza Waheshimiwa Eliadory Felix Kavejuruna Dkt. Florence George Samizi kwa kuchaguliwa hivikaribuni kuwa Wabunge wa Majimbo ya Buhigwe naMuhambwe, mtawalia. Aidha, nawapongezaWaheshimiwa Wabunge wenzangu wote kwakuaminiwa kuwawakilisha wananchi katika Bunge hiliTukufu. Vilevile, nitumie nafasi hii kuwapongezaviongozi wote walioteuliwa na Mheshimiwa Raiskushika nyadhifa mbalimbali Serikalini. Kuteuliwakwao ni kielelezo cha kuaminiwa na Mheshimiwa Raiskatika kuwaletea maendeleo wananchi.

Page 13: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

7

2.0 MISINGI YA SERA YA TANZANIA KATIKAUHUSIANO WA KIMATAIFA

14. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki ina jukumu lakusimamia uhusiano wa Kimataifa, Kikanda na bainaya Tanzania na nchi moja moja duniani. Aidha,Wizara ina jukumu la kuratibu ushiriki wa Tanzaniakatika Taasisi na Mashirika ya Kikanda na Kimataifa.Lengo kuu la uhusiano na ushirikiano huo ni kuteteana kulinda maslahi ya Tanzania ndani na nje ya nchi.Pamoja na masuala mengine, utekelezaji wamajukumu ya Wizara unaongozwa na Sera ya Mamboya Nje ya Mwaka 2001 inayoweka msisitizo katikadhana ya Diplomasia ya Uchumi. Msisitizo wa dhanahiyo umejikita katika kukuza biashara na kutafutafursa mpya za masoko ya bidhaa zinazozalishwanchini; kuvutia wawekezaji; kuvutia watalii; kutafutafursa za misaada na mikopo yenye masharti nafuu; nakutafuta fursa za ajira na ufadhili wa masomo nje yanchi.

15. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakujenga taswira nzuri ya nchi na kuhakikisha sauti yaTanzania inasikika katika medani za Kimataifa.Vilevile, imeendelea kuimarisha uhusiano baina yanchi yetu na nchi moja moja pamoja na Mashirika

Page 14: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

8

mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa. Lengo kuu nikuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kunufaika nafursa mbalimbali zinazopatikana kupitia uhusiano huosambamba na kuendelea kuwa mstari wa mbelekatika kusimamia na kutetea misingi ya Taifa letu.

16. Mheshimiwa Spika, historia ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania imesheheni misingi imarainayoiwezesha kuendelea kuwa miongoni mwa nchizilizo na ushawishi mkubwa kimataifa tangu Uhuru.Misingi ya nchi yetu kuheshimika kimataifa iliwekwana Waasisi wa Taifa letu kwa kupinga na kulaaniubabe, uonevu na ukandamizaji popote paleulipotokea duniani bila hofu. Hivyo, katika kusimamiamisingi hiyo, tumeendelea kulinda uhuru wetu;kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa;kulinda mipaka ya nchi yetu; kutetea haki; kuimarishaujirani mwema; na kutekeleza Sera yaKutofungamana na Upande Wowote kama dira namsimamo wetu kwenye uhusiano na nchi nyinginekatika jumuiya ya kimataifa.

Page 15: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

9

3.0 TATHMINI YA HALI YA UCHUMI, SIASA,ULINZI NA USALAMA DUNIANI KWAMWAKA WA FEDHA 2020/2021

17. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa fupikuhusu hali ya uchumi, siasa, ulinzi na usalamaduniani kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 kamaifuatavyo:

3.1 Hali ya Uchumi

18. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa yaBenki ya Dunia ya mwezi Januari 2021, ukuaji wauchumi wa dunia kwa mwaka 2020 ulipungua kwaasilimia 4.3 kutokana na athari za ugonjwa wa homakali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Korona(UVIKO-19) ambao uliathiri sekta nyingi za uchumihususan uwekezaji, uzalishaji, upatikanaji wa hudumana biashara ya kimataifa. Kasi ya kupungua kwaukuaji wa uchumi ilikuwa ndogo kwa asilimia 0.9ikilinganishwa na makadirio ya awali ya asilimia 5.2.Aidha, kwa mwaka 2021 uchumi wa duniaunakadiriwa kukua kwa asilimia 4 kutokana na kuanzakurejea kwa shughuli za kiuchumi katika nchimbalimbali. Ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wadunia, Benki hiyo inahimiza kuimarisha huduma zaafya, elimu, miundombinu ya TEHAMA, uwekezaji na

Page 16: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

10

biashara. Hatua hizi zina mchango mkubwa katikakujenga uchumi jumuishi na kupunguza umaskini.

19. Mheshimiwa Spika, pamoja na ukuaji wauchumi wa dunia kupungua kutokana na athari zaUVIKO - 19, mwezi Julai, 2020 Benki ya Duniailiitangaza Tanzania kukidhi vigezo vya kuwa nchiyenye uchumi wa kati. Hatua hiyo inatoa fursa kwanchi yetu kuaminiwa kimataifa katika juhudi zake zakuinua uchumi na kuvutia wawekezaji kwa maendeleoyetu.

3.2 Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama

A. Afrika

20. Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi nausalama imeendelea kuimarika katika maeneo mengibarani Afrika. Katika kipindi cha mwezi Julai, 2020hadi Aprili, 2021 nchi za Benin, Burkina Faso, Côted’Ivoire, Chad, Ghana, Jamhuri ya Afrika ya Kati,Niger, Shelisheli, Guinea, Uganda na Jamhuri yaKongo zilifanya chaguzi. TunawapongezaWaheshimiwa Marais wa nchi hizo kwa kuchaguliwana tunaahidi kuendelea kushirikiana na Serikali zaokwa lengo la kudumisha uhusiano baina ya nchi zetu.

Page 17: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

11

21. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kutumiafursa hii kutoa salamu za pole kwa Mheshimiwa Lt.Gen. Mahamat Idriss Déby, Rais wa Mpito wa Chadna wananchi wa nchi hiyo kwa ujumla kufuatia kifocha Mheshimiwa Idriss Déby Itno aliyekuwa Rais wanchi hiyo kilichotokea tarehe 20 Aprili 2021. Duniaitamkumbuka Hayati Idriss Déby Itno kwa kujitoa nakuwa mstari wa mbele katika juhudi za kuimarishausalama na utulivu katika eneo la ukanda wa Sahelna Afrika kwa ujumla. Tunatoa rai kuimarishwa kwaamani nchini humo na kurejeshwa utawala wa kiraiakama Katiba ya Umoja wa Afrika (AU) inavyoeleza.

22. Mheshimiwa Spika, pamoja na hali ya kisiasakuwa ya kuridhisha, uwepo wa tishio la ugaidi,uharamia, vikundi vya waasi, biashara haramu yausafirishaji wa binadamu, dawa za kulevya nautakasishaji wa fedha bado ni changamoto kwabaadhi ya nchi barani Afrika kama ifuatavyo:

Ethiopia

23. Mheshimiwa Spika, nchini Ethiopia hususankwenye jimbo la Tigray lililopo Kaskazini mwa nchihiyo kumekuwa na mvutano wa kisiasa tangu mwaka2019. Mvutano huo ulisababisha kuibuka mapiganokati ya Jeshi la Serikali ya Shirikisho na Jeshi la jimbo

Page 18: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

12

hilo. Mapigano hayo yalisitishwa mwezi Februari 2021na pande zote mbili zimeanza mazungumzo yaamani.

Jamhuri ya Afrika ya Kati

24. Mheshimiwa Spika, hali ya kiusalama katikaJamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kuwa yawasiwasi kutokana na mwendelezo wa mashambuliziya vikundi vya waasi dhidi ya majeshi ya Serikali naraia, licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani nakukamilika kwa zoezi la Uchaguzi Mkuu uliofanyikamwezi Desemba 2020. Tanzania inaendelea kuungamkono juhudi zinazofanywa na jumuiya ya kimataifakatika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ikiwemokuimarisha ulinzi na usalama wa nchi hiyo kwakuchangia vikosi vya kijeshi kwenye misheni yaUmoja wa Mataifa ya ulinzi wa amani (MINUSCA).

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

25. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliingiakwenye mgogoro wa kisiasa baada ya kuvunjika kwaSerikali ya Mseto iliyoundwa na muungano wa CapPour le Changement (CACH) unaoongozwa naMheshimiwa Felix Tshisekedi Tshilombo, Rais wa

Page 19: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

13

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na muungano waFront Commun Pour le Congo (FCC) unaoongozwana Rais Mstaafu, Mheshimiwa Joseph KabilaKabange. Kufuatia kuvunjika kwa Serikali ya mseto,Mheshimiwa Rais Tshisekedi aliunda Serikali mpyamwezi Aprili 2021.

26. Mheshimiwa Spika, Jamhuri ya Kidemokrasiaya Kongo pia inaendelea kukabiliwa na changamotoza kiusalama katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyoambapo vikundi vya waasi vyenye silaha vimeendeleakufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raiana majeshi ya nchi hiyo. Tanzania inaendelea kuungamkono juhudi zinazofanywa na jumuiya ya kimataifakatika kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi hiyokupitia misheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa(MONUSCO) inayojumuisha vikosi vya kijeshi kutokaTanzania.

Msumbiji

27. Mheshimiwa Spika, Msumbiji inaendeleakukabiliwa na changamoto za kiusalama katika eneola Kaskazini mwa nchi hiyo hususan jimbo la CaboDelgado kutokana na mashambulizi ya mara kwamara yanayodaiwa kufanywa na vikundi vya kigaididhidi ya Serikali na raia. Tanzania kama ndugu na

Page 20: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

14

jirani wa Msumbiji inaendelea kuwa sehemu ya juhudiza Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)katika kudhibiti na kuimarisha hali ya usalama kwenyeeneo hilo.

B. Mashariki ya Kati

28. Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi nausalama katika ukanda wa Mashariki ya Katiimeendelea kuimarika isipokuwa kwa baadhi yamaeneo kama ifuatavyo:

Yemen

29. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama nchiniYemen bado siyo ya kuridhisha kutokana namapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Serikali nakundi la wanamgambo wa Houthi. Mapigano hayoyamekuwa na athari kwa ustawi wa nchi hiyo.Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja waMataifa unaozitaka pande mbili zinazopiganakujadiliana na hatimaye kupata suluhu ya mgogorohuo.

Lebanon

30. Mheshimiwa Spika, Lebanon imeendeleakukabiliwa na changamoto ya uwepo wa makundi

Page 21: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

15

yenye itikadi kali zinazokinzana. Hali hii ikijumuishwana mdororo wa uchumi, mifumo dhaifu ya utawala nauhasama baina yake na Israel imechochea kuendeleakuwepo kwa machafuko ya mara kwa mara nchinihumo na kusababisha mgogoro wa kisiasa nakiusalama. Tanzania imeendelea kuunga mkonojuhudi za jumuiya ya kimataifa katika kuleta amani nausalama, ikiwemo kuchangia vikosi vya kijeshi katikamisheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchinihumo (UNIFIL).

Israel na Palestina

31. Mheshimiwa Spika, hivi karibuni mgogoro katiya Israel na Palestina umeongezeka na kusababishamadhara makubwa ikiwemo vifo na uharibifu wa malina miundombinu muhimu katika miji ya Gaza,Jerusalem, Tel Aviv na Ukingo wa Magharibi.Tanzania inaunga mkono maazimio ya Umoja waMataifa na Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro huoyanayozitaka pande husika kuheshimu makubalianoya kuwepo kwa nchi mbili ikiwa ni Palestina huru naIsrael salama.

Syria

32. Mheshimiwa Spika, Syria imeendeleakukabiliwa na mapigano ya ndani kati ya majeshi ya

Page 22: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

16

Serikali na vikundi vya uasi. Mgogoro huo uliodumukwa muda wa muongo mmoja sasa umekuwa naathari kubwa za kiuchumi na kijamii na kusababisharaia wengi kuikimbia nchi yao na kutafuta hifadhi yaukimbizi katika nchi mbalimbali duniani. Tanzaniainaunga mkono jitihada za kutafuta suluhu yamgogoro huo kwa njia ya majadiliano ili kurejeshaamani ya kudumu katika nchi hiyo.

C. Ulaya na Amerika

33. Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi nausalama katika nchi za Ulaya na Amerika imeendeleakuwa tulivu na Tanzania imeendelea kuimarishauhusiano wake na nchi hizo.

Uingereza

34. Mheshimiwa Spika, tarehe 9 Aprili, 2021Uingereza ilipata msiba mkubwa kwa kuondokewa naPrince Phillip, Duke of Edinburgh, mwenza waMtukufu Malkia Elizabeth II wa Uingereza na Mkuu waJumuiya ya Madola. Tanzania inatoa pole kufuatiamsiba huo na inaungana na Familia ya Kifalme,Serikali, Waingereza na Nchi Wanachama waJumuiya ya Madola kuomboleza kifo chake. MwenyeziMungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

Page 23: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

17

Marekani

35. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Marekani ilifanya Uchaguzi Mkuu ulioleta mabadilikoya utawala kutoka Chama cha Republican kwendaChama cha Democratic. Licha ya Rais aliyekuwepomadarakani kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madaiya kuwepo kwa udanganyifu katika baadhi yamajimbo, nchi hiyo iliweza kukamilisha zoezi lauchaguzi na kumuapisha Mheshimiwa JosephRobinette Biden Jr. wa Chama cha Democratic mweziJanuari 2021. Napenda kutumia fursa hiikuwapongeza Wamarekani kwa ukomavu wademokrasia na Rais Biden kwa kuchaguliwa kuwaRais wa 46 wa Marekani. Tanzania itaendeleakushirikiana na Serikali yake na kudumisha uhusianobaina ya nchi zetu.

4.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NABAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WAFEDHA 2020/2021

36. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuelezautekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwaMwaka wa Fedha 2020/2021, naomba nitajemajukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki kama yalivyoainishwa katika

Page 24: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

18

Muundo wa Wizara Toleo la tarehe 7 Julai, 2018kama ifuatavyo:

i. Kubuni na kusimamia utekelezaji wa Sera yaNchi ya Mambo ya Nje;

ii. Kusimamia na kuratibu masuala ya uhusianobaina ya Tanzania na nchi nyingine;

iii. Kusimamia na kuratibu masuala ya mikatabana makubaliano ya kimataifa;

iv. Kusimamia masuala yanayohusu kinga na hakiza wanadiplomasia waliopo nchini;

v. Kusimamia na kuratibu masuala ya itifaki nauwakilishi;

vi. Kuanzisha na kusimamia huduma za kikonseli;vii. Kuratibu masuala ya ushirikiano wa kikanda na

kimataifa;viii. Kuratibu na kusimamia masuala ya

Watanzania waishio ughaibuni;ix. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa masuala

ya Jumuiya ya Afrika Mashariki;x. Kuratibu na kusimamia miradi ya maendeleo ya

taasisi zilizo chini ya Wizara; naxi. Kusimamia utawala na maendeleo ya

watumishi Wizarani na katika Balozi zaTanzania.

Page 25: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

19

37. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wamajukumu ya Wizara uliongozwa na nyarakambalimbali ikiwemo Ilani ya Chama cha Mapinduzikwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015; Sera yaMambo ya Nje ya Mwaka 2001; Dira ya Taifa yaMaendeleo ya mwaka 2025; Mpango wa Pili waTaifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 -2020/21); Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika; Ajendaya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya Malengo yaMaendeleo Endelevu; Mkakati wa Maendeleo waJumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2017/2018 -2021/2022; Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya yaAfrika Mashariki wa mwaka 1999 kamaulivyorekebishwa na Itifaki zake; Mkataba waUanzishwaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika wa mwaka 1992 kama ulivyorekebishwa naItifaki zake pamoja na mikataba mingine ya Kikandana Kimataifa; maoni na ushauri wa WaheshimiwaWabunge wakati wa kujadili Mpango na Bajeti yaWizara kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2020/2021;Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti yaSerikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021; MpangoMkakati wa Wizara wa mwaka 2020/2021 –2024/2025; na maagizo yaliyotolewa kwa nyakatitofauti kwa Wizara na Viongozi wa Kitaifa, Kamati yaKudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na

Page 26: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

20

Usalama na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabuza Serikali.

Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha2020/2021

Mapato

38. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha2020/2021, Wizara ilipanga kukusanya shilingi2,550,879,000. Kati ya kiasi hicho shilingi 47,170,000ni makusanyo ya Makao Makuu ya Wizara na shilingi2,503,709,000 ni makusanyo kutoka Balozi zaTanzania. Vyanzo vya mapato hayo ni uhakiki wanyaraka, pango la majengo ya Serikali nje ya nchi namauzo ya nyaraka za zabuni.

39. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2020 hadi tarehe 30 Aprili 2021, Wizara ilikusanyajumla ya shilingi 756,182,081.71 sawa na asilimia29.6 ya lengo lililopangwa kwa Mwaka wa Fedha2020/2021. Kupungua kwa mapato hayo kumetokanana kukosekana kwa wapangaji katika baadhi yamajengo ya Serikali kwenye Balozi za Tanzaniakutokana na athari za uwepo wa janga la UVIKO-19.Nchi nyingi duniani zilichukua hatua za kudhibitimaambukizi ya ugonjwa huo kwa kufunga shughuli

Page 27: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

21

muhimu za kijamii na uzalishaji zilizosababishakampuni na ofisi nyingi kufungwa na kufanyia kazizake kutokea nyumbani.

40. Mheshimiwa Spika, mapato yaliyokusanywana Wizara katika kipindi cha mwezi Julai 2020 hadiAprili, 2021 yaliingizwa moja kwa moja kwenye MfukoMkuu wa Serikali kama taratibu zinavyoelekeza.

Fedha Zilizoidhinishwa

41. Mheshimiwa Spika, katika kutekelezamalengo ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021,kiasi cha shilingi 199,750,684,000 kiliidhinishwa. Katiya fedha hizo, shilingi 179,750,684,000 ni kwa ajili yaMatumizi ya Kawaida na shilingi 20,000,000,000 nikwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Katika fedhazilizoidhinishwa kwa Matumizi ya Kawaida, shilingi167,717,723,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyona shilingi 12,032,961,000 ni kwa ajili ya Mishahara.

Fedha Zilizopokelewa na Kutumika

42. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 30Aprili, 2021 Wizara ilipokea kutoka Hazina kiasi chashilingi 127,648,549,514.76. Kiasi hicho cha fedha nisawa na asilimia 63.9 ya fedha zote za bajeti

Page 28: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

22

zilizoidhinishwa katika Mwaka wa Fedha 2020/2021.Kati ya fedha hizo, shilingi 118,893,319,946.58 nikwa ajili ya Matumizi Mengineyo sawa na asilimia70.9 na shilingi 8,755,299,568.18 ni kwa ajili yaMishahara sawa na asilimia 72.8.

43. Mheshimiwa Spika, Wizara ilitumia kiasi chashilingi 106,601,250,300.11 sawa na asilimia 83.5 yafedha zilizopokelewa. Kati ya fedha hizo, shilingi97,846,020,731.93 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyona shilingi 8,755,229,568.18 ni mishahara.

44. Mheshimiwa Spika, baada ya kutajamajukumu ya Wizara, Miongozo mbalimbaliiliyozingatiwa na Wizara pamoja na taarifa ya mapatona matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha2020/2021, naomba sasa nitumie fursa hii kuelezakwa kifupi mapitio ya utekelezaji wa majukumu yaWizara katika kipindi husika kama ifuatavyo:

4.1 Kusimamia na Kuratibu Masuala yaUhusiano Baina ya Tanzania na NchiNyingine

4.1.1Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi

45. Mheshimiwa Spika, katika kutekelezaDiplomasia ya Uchumi kwa lengo la kuchangia

Page 29: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

23

maendeleo ya Taifa letu, Wizara kwa kushirikiana naWizara za kisekta imeendelea kutafuta masoko yabidhaa zinazozalishwa nchini; kuongeza idadi yawatalii na wawekezaji; kuongeza fursa za mafunzo njeya nchi; kutafuta misaada na mikopo ya mashartinafuu pamoja na kuimarisha ushirikiano katika nyanjanyingine za kiuchumi na kijamii. Matokeo mahsusikatika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumiyanatokana na kuendelea kuimarika kwa ushirikianobaina ya Tanzania na Jumuiya ya kimataifa.

4.1.2 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi zaAfrika

46. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda hapa nchini.Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Museveni namwenyeji wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniawalishuhudia uwekaji saini Mkataba wa Uenyeji katiya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naKampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki(EACOP) kuhusu Ujenzi wa Mradi wa Bomba lakusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Ugandampaka Chongoleani, Tanga.

Page 30: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

24

47. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu Ziara ya Kitaifa ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, nchini Kenya kufuatia mwaliko waMheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Jamhuriya Kenya. Ziara hiyo ya kwanza ya Kitaifa tangukuapishwa kwa Mheshimiwa Rais Samia SuluhuHassan, ililenga kuimarisha uhusiano wa kidugu naujirani mwema kati ya Tanzania na Kenya. Wakati waziara hiyo, nchi hizi mbili zilikubaliana kuharakishautekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lamiya Bagamoyo - Tanga – Horohoro – Lungalunga –Mombasa – Malindi (Km 454) na mradi wa kusafirishaumeme kV 400 kutoka Singida (Tanzania) hadi Isinya(Kenya).

48. Mheshimiwa Spika, aidha, Mheshimiwa RaisSamia Suluhu Hassan na mwenyeji wakeMheshimiwa Rais Uhuru Muigai Kenyattawalishuhudia uwekaji saini Hati ya Makubaliano yaKusafirisha Gesi Asilia kati ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri yaKenya na Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katikaMasuala ya Utamaduni, Sanaa, Mahusiano ya Jamiina Urithi wa Taifa. Vilevile, walishiriki jukwaa lawafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lililofanyikajijini Nairobi na kuwahakikishia kuwa Serikali za nchi

Page 31: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

25

zote mbili zitaendelea kuweka mazingira wezeshi yauwekezaji na biashara.

49. Mheshimwa Spika, kadhalika wakati wa ziarahiyo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassanalihutubia Kikao Maalum cha pamoja cha Bunge laTaifa na Bunge la Seneti la Kenya, ambapo pamojana masuala mengine alieleza nia ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kuendelea kudumishauhusiano wa kihistoria, kidugu na kirafiki kati ya nchihizi mbili.

50. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2021, Wizarailiratibu ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanianchini Uganda. Wakati wa ziara hiyo, MheshimiwaRais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wakeMheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais waJamhuri ya Uganda walishuhudia uwekaji sainimikataba mitatu ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba laKusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutokaHoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga. Mikatabailiyosainiwa ni:

i. Mkataba wa Uenyeji wa mradi kati ya Serikali yaUganda na kampuni za TOTAL Limited yaUfaransa na China National Offshore Oil

Page 32: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

26

Corporation (CNOOC) ya China zilizowekezakwenye mradi;

ii. Mkataba wa Wanahisa kati ya Serikali yaUganda, Serikali ya Tanzania na wawekezaji(TOTAL na CNOOC); na

iii. Mkataba wa Tozo ya Usafirishaji wa Mafuta katiya Serikali ya Uganda na wawekezaji.

51. Mheshimiwa Spika, mwezi Machi 2021,Wizara iliratibu Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamojaya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Jamhuri ya Burundiuliofanyika mjini Kigoma, Tanzania. Katika Mkutanohuo, Tanzania na Burundi zilikubaliana kuimarisha nakukuza ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemosiasa na diplomasia; ulinzi na usalama; uendelezajiwa miundombinu ya uchukuzi inayounganisha nchihizi mbili; na biashara na uwekezaji.

52. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huo, nchihizi pia zilikubaliana kushirikiana katika ufundishaji walugha za Kiswahili na Kifaransa na Burundi kutumiamasoko na mitambo ya kuchenjua madini hapa nchini.Vilevile, Chama cha Wafanyabiashara wenyeViwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chama cha

Page 33: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

27

Wafanyabiashara wa Burundi vilisaini Hati yaMakubaliano ya Ushirikiano ambayo inatoa fursa kwawafanyabiashara wa nchi hizi mbili kufanya biasharabila vikwazo.

53. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu ziara ya kikazi ya Mheshimiwa FilipeJacinto Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbijiiliyofanyika nchini kwa lengo la kufanya mazungumzomaalum na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. Katika ziara hiyo, viongozi haowalikubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya nchihizi mbili na kukuza kiwango cha biashara nauwekezaji pamoja na kuimarisha ujirani mwema.

54. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia yaShirikisho la Ethiopia iliyofanyika nchini. Tanzania naEthiopia zilikubaliana kuimarisha na kukuza uhusianowa kiuchumi hususan kuongeza kiwango chabiashara na uwekezaji; na kubadilishana utaalam nauzoefu katika uendeshaji wa viwanda vya kuongezathamani ya ngozi za mifugo. Nchi hizo piazilikubaliana kuwa Serikali ya Tanzania itatoamsamaha kwa wafungwa 1,789 raia wa Ethiopia ili

Page 34: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

28

warejeshwe kwao; na Tanzania kuisaidia Ethiopiakufundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu chaAddis Ababa na Chuo cha Diplomasia cha Ethiopia.

55. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ziara ya Mheshimiwa Dkt. NetumboNandi-Ndaitwah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri waUshirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Namibiailiyofanyika nchini. Katika ziara hiyo, nchi hizi mbilizilikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikianokwenye sekta za uvuvi hususan uvuvi wa bahari kuu,mifugo, biashara, uwekezaji na kilimo. Vilevile,Mheshimiwa Nandi-Ndaitwah alihudhuria Mahafali ya50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyikatarehe 8 Desemba, 2020 na kutunukiwa shahada yaheshima ya uzamivu ya falsafa kwa kutambuamchango wake katika kupigania uhuru, kutetea hakiza binadamu na ustawi wa watu wa Namibia na Afrikakwa ujumla.

56. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa ujumbe wa Tanzania katikamkutano wa ujirani mwema kati ya mikoa ya Kagerana Kigoma ya Tanzania na majimbo ya Makamba,Rutana, Cankuzo na Rumonge ya Burundi uliofanyikamjini Kigoma. Katika Mkutano huo, Tanzania naBurundi zilikubaliana kuimarisha ushirikiano katika

Page 35: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

29

masuala ya usalama, biashara, utamaduni namichezo katika maeneo ya mpakani. Mikutano ya ainahii ni muhimu katika kuimarisha ujirani mwema nakutatua changamoto za kiusalama na kibiasharakatika maeneo ya mipaka.

57. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara iliratibu ziara ya Mhe. Dkt. Mohamed HemedShaker Elmarkabi, Waziri wa Nishati wa Jamhuri yaKiarabu ya Misri na Mhe. Dkt. Asim Abdelhamid HafizElgazar, Waziri wa Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu yaMisri iliyofanyika nchini. Viongozi hao walijumuika naMheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakushuhudia uzinduzi wa uchepushaji wa maji katikamradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere.

58. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba 2020,Wizara iliratibu ziara rasmi ya Mheshimiwa Dkt.Lazarus McCarthy Chakwera, Rais wa Jamhuri yaMalawi iliyofanyika nchini. Katika ziara hiyo, pamojana mambo mengine, Tanzania na Malawi zilikubalianakukamilisha ujenzi wa Kituo cha Huduma kwa PamojaMpakani (OSBP) cha Songwe/Kasumulu; ujenzi wabarabara ya Mpemba - Isongole - Mbozi (km51)/Chitipa - Mbilima (km 32); na Mamlaka yaUsimamizi wa Bandari Tanzania kufungua ofisi nchini

Page 36: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

30

Malawi. Nchi hizi pia zilikubaliana kushirikiana katikautekelezaji wa miradi ya pamoja ya kufua umeme naumwagiliaji katika Bonde la Mto Songwe.

59. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba 2020,Wizara ilifanikisha uwekaji saini Hati ya Makubalianoya Ushirikiano Kuanzisha Ofisi ya Uhusiano yaMamlaka ya Bandari ya Tanzania nchini Burundi. Ofisihiyo ambayo imeanza kufanya kazi, inarahisishautoaji wa huduma za uagizaji na usafirishaji wa bidhaakwenda nchini Burundi kupitia Bandari ya Dar esSalaam kwa kuzingatia kuwa zaidi ya asilimia 95 yabidhaa zinazoingizwa nchini Burundi kutoka njezinapitia bandari hiyo. Hatua hii ni sehemu yautekelezaji wa maazimio ya mkutano wa viongoziwakuu wa nchi hizi mbili uliofanyika mwezi Septemba2020.

60. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara iliratibu ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa YoweriKaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Ugandailiyofanyika nchini. Katika ziara hiyo, Tanzania naUganda zilisaini Hati ya Makubaliano Kuanza Ujenziwa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima,Uganda hadi Chongoleani, Tanga.

Page 37: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

31

61. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara iliratibu ziara ya kikazi ya Mheshimiwa MejaJenerali Évariste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri yaBurundi iliyofanyika nchini. Katika ziara hiyo, Tanzaniana Burundi zilikubaliana kushirikiana kujenga reliyenye urefu wa kilomita 200 kutoka Uvinza, Tanzaniahadi Gitega, Burundi; kuanza ujenzi wa Kituo chaHuduma kwa Pamoja Mpakani Manyovu/Mugina; naBurundi kuuza madini yake katika masoko ya madininchini Tanzania. Nchi hizi zilikubaliana pia kuimarishaushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama;biashara na uwekezaji; na ujirani mwema.

4.1.3 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi zaAsia na Australasia

62. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara na Benki ya NMB ziliandaa mpango wakuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kuuzabidhaa zao katika soko la China. Kupitia mpango huo,Wizara itatafuta masoko na Benki ya NMB itatoamikopo kwa wafanyabiashara Watanzania kwa ajili yamitaji ya kuuza bidhaa nchini China. Benki ya NMBpia imekubali kufadhili ushiriki wa Tanzania katikamaonesho ya nne ya bidhaa za nje yatakayofanyikaChina mwezi Novemba 2021 kwa kutoa shilingi milioni

Page 38: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

32

100 kwa ajili ya kujenga banda la Tanzania kwenyemaonesho hayo.

63. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu ziara ya kikazi ya Mhe. Wang Yi,Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo yaNje wa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika hapanchini. Kufuatia ziara hiyo:

i. Serikali ya China ilitoa msaada wa shilingimilioni 350 kwa ajili ya kununua vifaa vyakarakana ya fani ya uvuvi katika Chuo chaMafunzo ya Ufundi Stadi VETA, Chato;

ii. Serikali ya China imeahidi kutoa misaada yafedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Taifa chaUsafirishaji; upanuzi wa Taasisi ya Moyo yaJakaya Kikwete; na ujenzi wa barabara kuu zaZanzibar zenye urefu wa kilometa 148;

iii. Serikali ya China imeahidi kutoa mikopo yamasharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa laUmeme la Ruhudji (MW 358) na njia yakusafirishia umeme kutoka Ruhudji hadi Kidasa(km 170, kV400); na ujenzi wa Bwawa laUmeme la Rumakali (MW 222) na njia ya

Page 39: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

33

kusafirishia umeme kutoka Rumakali hadiMbeya (Km 150, kV400);

iv. Serikali ya China ilitoa msaada wa Dola zaMarekani 20,000 kwa ajili ya kusaidia ununuziwa vifaa vya uvuvi kwa jumuiya ya wavuvi wamwalo wa Chato; na

v. Mwezi Mei, 2021 Serikali ya China imetoamsaada wa Shilingi Bilioni 35.37 kwa ajili yakutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleohapa nchini.

64. Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo, Mhe.Wang Yi pia alishuhudia uwekaji saini mkataba waujenzi wa awamu ya tano ya reli ya kisasa ya kiwangocha kimataifa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isakachenye urefu wa kilometa 341.

65. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutanowa wadau wa biashara wa Tanzania na China kuhususoko la mabondo ya samaki nchini China uliofanyikakwa njia ya mtandao. Mkutano huo ulizikutanishakampuni za Tanzania zinazojihusisha na biashara yasamaki pamoja na kampuni ya Alibaba ya China.Kampuni ya Alibaba imeonesha nia ya kutangaza

Page 40: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

34

mabondo ya samaki katika mtandao wake pamoja nakununua mabondo kutoka Tanzania.

66. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa mkatabautakaoiwezesha Tanzania kupata mkopo wa mashartinafuu wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Korea.Miradi itakayogharamiwa na fedha za mkopo huo niujenzi wa vituo vya kupoozea umeme katika njia yakusafirishia umeme ya Kigoma – Nyakanazi kwa kiasicha shilingi bilioni 102.9; uboreshaji wa huduma zamajitaka jijini Dodoma kwa kiasi cha shilingi bilioni160; na uimarishaji wa huduma za upimaji na ramanikwa kiasi cha shilingi bilioni 148.6. Fedha nyingine zamkopo huo kiasi cha shilingi bilioni 91.4 zitatumikakwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumizilizotokana na janga la UVIKO-19; na shilingi bilioni74.5 ni nyongeza katika mradi wa ujenzi wa Daraja laTanzanite linalojengwa jijini Dar es Salaam.

67. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara ilifungua Ofisi ya Mwakilishi wa Heshima waTanzania jijini Mumbai, India. Ofisi hiyo imerahisishautoaji huduma za kikonseli kwa watanzania wanaoishikatika jiji hilo. Ofisi hiyo pia itakuwa kiungo muhimu

Page 41: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

35

katika masuala ya biashara kati ya wafanyabiasharawa Tanzania na wafanyabiashara wa jiji la Mumbai.

68. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara ilifungua Ofisi ya Mwakilishi wa Heshima waTanzania katika jiji la Jakarta, Indonesia. Ofisi hiyoitaratibu masuala ya biashara, uwekezaji na utaliipamoja na kutoa huduma za kikonseli kwawatanzania wanaoishi Indonesia na wageniwanaotaka kutembelea Tanzania.

69. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa mkataba kati yaTanzania na China utakaowezesha Tanzania kuuzamaharage aina ya soya katika soko la China. Kupitiamkataba huo, Tanzania inakuwa nchi ya 12kuruhusiwa kuuza maharage hayo ambayo yana sokokubwa nchini humo. Kampuni 49 za Tanzaniazimepata vibali vya kuuza maharage hayo katika sokohilo na tayari mwezi Mei 2021, Tanzania imepelekashehena ya soya yenye uzani wa zaidi ya tani 120.

70. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba 2020,Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa Mkataba Maalumwa muda mfupi wa ushirikiano katika usafiri wa angakati ya Tanzania na India. Kupitia mkataba huo,ndege za ATCL zimefanya safari 36 ikiwemo

Page 42: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

36

kuwarejesha Watanzania wapatao 1,770 kutokanchini India katika kipindi cha UVIKO-19.

71. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu nakufanikisha upatikanaji wa kampuni ya PT Indesso yanchini Indonesia iliyojenga kiwanda cha kutengenezamafuta yatokanayo na majani ya mimea katika eneola Mgelema, Pemba kwa kushirikiana na Shirika laTaifa la Biashara la Zanzibar kwa gharama ya Dola zaMarekani milioni 1.4. Kiwanda hicho kilizinduliwamwezi Septemba 2020 na Mheshimiwa Dkt. AliMohamed Shein, aliyekuwa Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 1.2 za mafuta ghafi yamajani ya mkarafuu kwa mwaka.

72. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ubalozi waTanzania katika Jamhuri ya Korea imeendeleakutangaza utamaduni wa Tanzania kwa kufundishalugha ya Kiswahili nchini humo kwa hatua ya awali,kati na juu. Mpaka sasa wanafunzi 150 wamehitimumafunzo hayo. Vilevile, Ubalozi umekamilishamachapisho ya kufundisha lugha hiyo kwa ngazi yaawali, kati na juu yaliyoanza kutumika mwezi Oktoba2020.

Page 43: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

37

4.1.4 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi zaMashariki ya Kati

73. Mheshimiwa Spika, kufuatia utekelezaji waDiplomasia ya Uchumi, Wizara imefanikisha Tanzaniakuruhusiwa kuanza kuingiza nyama na bidhaa zanyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo katika masokoya nchi za Oman, Kuwait na Qatar. Vilevile, bidhaahizo zitaanza kuuzwa nchini Saudi Arabia baada yakukamilika kwa taratibu za kupata ithibati kutokakwenye mamlaka za nchi hiyo.

74. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ziara ya Mwana Mfalme Faisal bin Farhan AlSaud, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.Mwana Mfalme huyo alifanya mazungumzo naMheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania ambapo walikubalianakuendelea kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katiya Tanzania na Saudi Arabia hususan katika kuvutiauwekezaji na kuimarisha biashara ya mazao yamifugo, uvuvi na kilimo. Vilevile, Mheshimiwa Raisaliiomba Serikali ya Saudi Arabia kufungua ofisi yaUbalozi Mdogo Zanzibar.

75. Mheshimiwa Spika, vilevile, Mwana Mfalmehuyo alikutana nami pamoja na Mawaziri wenye

Page 44: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

38

dhamana za Viwanda na Biashara; Uwekezaji; Mifugona Uvuvi; Mawasiliano na Uchukuzi; na Fedha naMipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniapamoja na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano naUchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarambapo tulikubaliana kuendeleza ushirikiano baina yaTanzania na Saudi Arabia katika sekta hizo.

76. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara ilifanikisha upatikanaji wa vibali kwa kampuninane za Tanzania kuuza minofu ya samaki aina yasangara katika nchi ya Saudi Arabia. Vibali hivyovimetolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa yaSaudi Arabia baada ya kukidhi vigezo. Kampuni hizokwa sasa zipo kwenye maandalizi ya kuanzakupeleka minofu hiyo nchini humo. Aidha, SaudiArabia imeanza kununua maparachichi kutoka hapanchini.

77. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara ilifanikisha uwekaji saini Hati ya Makubalianokati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlakaya Uwekezaji ya Oman kwa ajili ya ujenzi wa Bandariya Mangapwani, Zanzibar. Mradi huo utajumuishaujenzi wa eneo la kuhudumia mizigo; gati la meli zauvuvi; gati la meli za mafuta na gesi; chelezo kwa ajiliya matengenezo ya meli; na mji wa kisasa katika

Page 45: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

39

eneo la Mangapwani. Mradi utakapokamilikautachochea ukuaji wa biashara na usafirishajiZanzibar.

78. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika Tamashala Kumi la Mashindano ya Majahazi lililofanyika nchiniQatar. Tamasha hilo lililohudhuriwa na nchi za Afrika,Mashariki ya Kati na Asia ni jukwaa muhimu katikakutangaza mila na tamaduni za nchi zenye historia yasafari za kale za majahazi. Tanzania ilitumia fursa yaushiriki kwenye tamasha hilo kutangaza bidhaazinazozalishwa nchini hususan korosho, asali,kahawa, pilipili, viungo na mafuta.

79. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza jitihadaza Serikali za kuleta mapinduzi ya kilimo nchini,Wizara inaendelea kuratibu mpango wa mafunzo yakilimo na mifugo kwa vitendo kwa vijana 100 waTanzania kwenda kusoma nchini Israel kila mwaka.Kwa mwaka wa masomo 2020/2021 vijana 36wanashiriki mafunzo hayo na vijana 64 waliobakiwanatarajiwa kwenda Israel pindi hali ya maambukiziya UVIKO-19 itakapodhibitiwa. Inatarajiwa kuwavijana hao watakaporejea wataweza kujiajiri na kuajiriwengine katika sekta za kilimo na mifugo.

Page 46: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

40

80. Mheshimiwa Spika, mwezi Agosti 2020,Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa mkataba wa mkopowa Dola za Marekani milioni 15.3 kutoka Mfuko waMaendeleo wa Kuwait kwa ajili ya mradi wa kilimo chaumwagiliaji kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta3,000 katika Bonde la Mto Luiche mkoani Kigoma.Mradi huo utaongeza uzalishaji wa mazao yampunga, mahindi na mbogamboga na hivyo kuinuakipato cha wakulima wa eneo hilo.

81. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara iliratibu na kufanikisha ziara ya ujumbemaalum kutoka kwa Sheikh Saud bin Saqr al Qasimi,Mtawala wa Ras Al Khaimah kutembelea Zanzibar.Ujumbe huo ulioongozwa na Mohammed AllyMusabbeh, Mshauri Mkuu wa Mtawala wa Ras AlKhaimah uliwasilisha taarifa kuhusu maendeleo yautafiti wa rasilimali ya gesi na mafuta katika visiwa vyaUnguja na Pemba kwa Mheshimiwa Dkt. Ali MohamedShein, Rais wa Awamu ya Saba wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

4.1.5 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi zaUlaya na Amerika

82. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ziara ya Kikazi ya Mhe. James Philip

Page 47: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

41

Duddridge, Waziri wa Uingereza anayesimamiamasuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje,Jumuiya ya Madola na Maendeleo. Wakati wa ziarahiyo Mhe. Duddridge alifanya mazungumzo naMheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na kukubalianakuimarisha ushirikiano katika masuala ya maendeleona kijamii. Aidha, Mheshimiwa Rais alieleza kuwaTanzania inaendelea kuboresha zaidi mazingira yabiashara na uwekezaji na kuiomba Serikali yaUingereza kuendelea kuiunga mkono Tanzania katikajuhudi za maendeleo na uimarishaji wa huduma zakijamii ikiwemo elimu, afya na masuala ya mazingira.

83. Mheshimiwa Spika, wakati wa ziara hiyo,Waziri huyo alifanya pia mazungumzo na MheshimiwaDkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambapowalikubaliana kuimarisha ushirikiano katika masualaya maendeleo na kijamii.

84. Mheshimiwa Spika, vilevile, ziara hiyoiliongeza msukumo wa kukamilika kwa majadilianokati ya Timu ya Tanzania na wawekezaji wa Kiwandacha Sukari cha Kilombero ambapo wawekezaji haowamepata idhini ya Serikali (kama mwekezajimwenza) kuongeza uwekezaji katika kuzalisha sukari

Page 48: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

42

hapa nchini utakaogharimu takriban kiasi cha Shilingibilioni 570. Serikali inamiliki hisa asilimia 25 namwekezaji anamiliki hisa asilimia 75. Ongezeko lauzalishaji wa sukari litakalotokana na uwekezaji huolitasaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo nje yanchi.

85. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ziara ya Kikazi ya Mhe. Mikhail Bogdanov,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na MjumbeMaalum wa Mheshimiwa Vladimir Putin, Rais waShirikisho la Urusi. Kiongozi huyo alikutana naMheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania ambapo pamoja namasuala mengine ya ushirikiano baina ya nchi zetumbili alimfahamisha kuhusu maandalizi ya Mkutanowa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika naUrusi unaotarajiwa kufanyika barani Afrika mwaka2022.

86. Mheshimiwa Spika, vilevile, Mjumbe huyoalikutana nami pamoja na Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango na Viongozi wa Vyombo vya Ulinziambapo tulikubaliana kuendelea kuimarishaushirikiano kwenye sekta za biashara, uwekezaji,ulinzi, utalii na fursa za mafunzo kwa Watanzanianchini Urusi.

Page 49: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

43

87. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu na kufanikisha kusainiwa kwamikataba sita ya msaada kati ya Tanzania na Umojawa Ulaya kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Umoja huokwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapanchini yenye thamani ya shilingi bilioni 307.9. Miradihiyo ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miakaminne ni: mradi wa maboresho ya sekta ya nishatiwenye thamani ya shilingi bilioni 96.7; mradi wamatumizi endelevu ya nishati mbadala ya kupikiawenye thamani ya shilingi bilioni 82.8; mradi wakuongeza mnyororo wa thamani katika ufugaji wanyuki wenye thamani ya shilingi bilioni 27.6; mradi wauboreshaji wa huduma za afya ya mimea na usalamawa chakula wenye thamani ya shilingi bilioni 27.6;mradi wa kusaidia uboreshaji wa mazingira ya ukuajiwa biashara na ubunifu wenye thamani ya shilingibilioni 63.5; na programu ya ushirikiano wa kitaalamyenye thamani ya shilingi bilioni 9.7.

88. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu na kufanikisha kusainiwa kwa Mkatabakati ya Tanzania na Ujerumani kuhusu msaada wenyethamani ya shilingi bilioni 18 kwa kipindi cha miakaminne kuanzia 2021 hadi 2024. Msaada huounahusisha ununuzi wa vifaa tiba na ujenzi wa

Page 50: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

44

hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania jijiniDodoma.

89. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Mhe. Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi (Mb.),aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki alifanya ziara ya kikazi nchiniUfaransa. Kufuatia ziara hiyo:

i. Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake laMaendeleo (AFD) ilikubali kuongeza kiasi chafedha za mkopo wa masharti nafuu Euro milioni178 na hivyo kufanya jumla ya mkopokuongezeka kutoka Euro milioni 600 hadi Euromilioni 778 kwa ajili ya kutekeleza miradimbalimbali ya maendeleo nchini;

ii. Tanzania na UNESCO kukubaliana kuanzataratibu za kuwa na siku rasmi ya kuadhimishalugha ya Kiswahili duniani kila mwaka. Tanzaniaimependekeza tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwasiku rasmi ya maadhimisho. Serikali kupitiaWizara inaendelea na majadiliano na UNESCOkufikia lengo hilo; na

iii. Kampuni 11 za Ufaransa zimeonesha utayari wakutekeleza miradi hapa nchini kwa kutumia fedha

Page 51: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

45

kutoka Serikali ya Ufaransa. Kampuni hizozinalenga kuwekeza kwenye sekta za viwanda,kilimo, maji, elimu, uvuvi, utalii na miundombinuya reli na barabara.

90. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu uwekaji saini Hati ya Makubaliano katiya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni yaTangen & Intertorco Group ya nchini Hispania kwa ajiliya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bandariya Mpigaduri, Unguja; Bandari ya Mkoani, Pemba; namradi wa kufua umeme kwa kutumia gesi. Hafla yauwekaji saini makubaliano hayo ilishuhudiwa naMheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

91. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu uwekaji saini Mkataba kati ya Serikaliya Tanzania na kampuni ya LZ Nicol ya nchiniUingereza kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya nickelyanayopatikana eneo la Kabanga wilayani Ngara,Kagera. Katika Mkataba huo pande zote mbilizilikubaliana kuunda kampuni ya ubia ambayoitapewa jina la Tembo Nickel Corporation ambapoSerikali ya Tanzania itamiliki asilimia 16 ya hisa zakampuni hiyo. Aidha, Serikali na kampuni ya LZ Nicolzilikubaliana kujenga kiwanda cha kuchenjua madini

Page 52: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

46

ya nickel, dhahabu na shaba katika wilaya yaKahama, Shinyanga. Utekelezaji wa mkataba huoutaongeza fursa za ajira kwa watanzania, uhaulishajiwa teknolojia ya uchimbaji madini na ongezeko lafedha za kigeni.

92. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziatarehe 31 Agosti, 2020 hadi tarehe 31 Januari, 2021,Tanzania ilipewa heshima ya kuwa Rais wa Baraza laMawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean naPacific (OACPS). Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwanchi yetu kushika nafasi hiyo tangu ilipojiunga naJumuiya hiyo mwaka 1975. Miongoni mwa sababu zakuchaguliwa kushika nafasi hiyo ni kuongezeka kwaushawishi wake kwenye Jumuiya ya OACPS, sera nahatua thabiti zinazochukuliwa na Tanzania katikakusimamia masuala ya kitaifa na kimataifa pamoja nautendaji madhubuti wa Wizara katika kusimamia Seraya Mambo ya Nje ikiwemo ushiriki mahiri katikamasuala yanayogusa maslahi ya Nchi Wanachamawa Jumuiya ya OACPS.

93. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha uongoziwetu kwenye Baraza hilo, Tanzania imesimamiaukamilishwaji wa majadiliano ya Ubia Mpya waUshirikiano kati ya Nchi za Jumuiya ya OACPS naUmoja wa Ulaya. Vilevile, imeimarisha ushirikiano

Page 53: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

47

miongoni mwa Nchi Wanachama; na ushirikiano bainaya Nchi Wanachama na wadau wa maendeleo katikamasuala ya biashara na uwekezaji. Aidha, katikakipindi hicho hali ya kifedha kwenye Sekretarieti yaOACPS imeimarika.

94. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 111 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachamawa Jumuiya ya OACPS uliofanyika kwa njia yamtandao chini ya uenyekiti wa Tanzania. KupitiaMkutano huo, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi10 za Jumuiya hiyo zitakazonufaika na utekelezaji wamradi wa kuongeza mnyororo wa thamani katikamazao ya samaki ujulikanao kama FISH4ACPunaogharimu shilingi bilioni 110. Katika mradi huoTanzania imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 8 kwaajili ya kuongeza thamani ya mazao ya samaki ainaya migebuka na dagaa kutoka mkoa wa Kigoma.Mradi huo utatekelezwa na Shirika la Umoja waMataifa la Chakula na Kilimo kwa kushirikiana naTaasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania.

95. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba 2020,Wizara iliratibu na kufanikisha kusainiwa kwa Mkatabakati ya Tanzania na Uswisi wa msaada wa shilingibilioni 39.15 kugharamia utekelezaji wa Awamu ya Pili

Page 54: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

48

ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini naMkataba wa shilingi bilioni 4.95 ikiwa ni msaada wakuchangia Mfuko wa Pamoja wa Afya. Pia, Wizarailiratibu kusainiwa kwa Mkataba kati ya Tanzania naUswisi wa shilingi bilioni 15.8 ikiwa ni msaada kwa ajiliya kutekeleza Programu ya Kitaifa ya KutokomezaMalaria Awamu ya Kwanza; na Mkataba wa shilingibilioni 24.76 ikiwa ni msaada kwa ajili ya kutekelezaProgramu ya Kuimarisha Mfumo wa Kutoa Hudumaza Afya Awamu ya Tatu. Misaada hiyo imeendeleakuchangia jitihada za Serikali katika kupunguzaumaskini na kuboresha huduma za afya nchini.

96. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumula kuvutia utalii, biashara na uwekezaji, Wizarailiratibu ziara zifuatazo za wafanyabiashara nawawekezaji hapa nchini:

i. Ziara za wawekezaji kutoka Austria na Uturukizilizofanyika nchini mwezi Desemba 2020 naFebruari 2021 mtawalia, ambao wamevutiwakuwekeza katika sekta za miundombinu, madini,elimu, sayansi na teknolojia na utalii;

ii. Ujio wa kampuni ya Green Iceland TradingCompany ya nchini Qatar ambayo imeoneshautayari wa kuanza kununua nyama ya ng’ombe

Page 55: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

49

na mbuzi; matunda na mbogamboga (maembe,maparachichi, mananasi na pilipili); na

iii. Ujio wa kampuni ya uandaaji wa matamasha namakongamano makubwa ya utalii na uwekezajiya nchini Qatar KON Group ambayo imekubalikuandaa makongamano ya biashara na utalii waTanzania nchini humo.

97. Mheshimiwa Spika, aidha, pamoja nachangamoto zilizosababishwa na UVIKO-19, Wizarailiendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwakutumia njia ya mtandao kuendesha makongamanona mikutano kama ifuatavyo:

i. Kongamano la 15 la biashara na uwekezaji katiya India na Afrika lililofanyika mwezi Septemba2020, ambapo Tanzania ilitangaza fursa zilizopokatika sekta za nishati, maji, kilimo,miundombinu, afya na TEHAMA;

ii. Kongamano la usalama wa chakula lililoandaliwana taasisi ya Improvate Teck Talk ya Israel mweziSeptemba na Novemba 2020, ambapo Tanzaniailitangaza mazao ya kilimo yanayozalishwa nchinikwa wingi kwa ajili ya kupata soko katika Ukandawa Mediterania;

Page 56: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

50

iii. Mkutano baina ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania,Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda naKilimo Tanzania, Jumuiya ya Wafanyabiasharana Wawekezaji wa Afrika Mashariki nchiniSweden na mataifa ya Nordic uliofanyika mweziNovemba 2020; na

iv. Mkutano kati ya wadau wa utalii wa hapa nchinina Chama cha Mawakala wa Usafiri wa Anga chaUturuki (TURSAB) uliofanyika mwezi Septemba2020, ambapo pande hizo mbili zilikubalianakuweka msingi wa ushirikiano katika kutangazavivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki nakuongeza ushiriki wa Tanzania katika maoneshoya utalii yanayoandaliwa nchini humo.

4.2 Kuratibu Masuala ya Ushirikiano waKikanda na Kimataifa

4.2.1 Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

98. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Wizaraimeendelea kuratibu ushiriki wa Tanzania katikaJumuiya ya Afrika Mashariki ili kunufaika na fursa zamtangamano kama ifuatavyo:

Page 57: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

51

Mkutano wa 21 wa Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

99. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiyaya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao.Katika Mkutano huo, Wakuu wa Nchi waliidhinishalugha za Kiswahili na Kifaransa kutumika rasmikwenye shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Hatua ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya Jumuiya nimuhimu kwa nchi yetu kwa sababu itachocheakuongezeka kwa matumizi ya lugha hiyo katika NchiWanachama na kutoa fursa za ajira kwa wataalamuwa Kiswahili hapa nchini kufundisha, kutoa hudumaya ukalimani na kutafsiri. Aidha, kurasimishwa kwalugha ya Kiswahili kutarahisisha mawasiliano yakibiashara miongoni mwa wananchi wa Jumuiya.

100. Mheshimiwa Spika, Mkutano huo pia uliazimiakwamba Nchi Wanachama zilizo tayari kuendelea naMkataba wa Ubia wa Uchumi (EPA) ziruhusiwekuanza mashauriano na Umoja wa Ulaya kwa kutumiakanuni ya Variable Geometry. Hii ni kutokana na kuwabaadhi ya Nchi Wanachama hazikubaliani na baadhiya vipengele vilivyopo katika Mkataba huo.

Page 58: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

52

101. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mkatabawa EPA kwa kutumia kanuni ya Variable Geometryunakabiliwa na changamoto. Kulingana na tafsiri yaMahakama ya Haki ya Afrika Mashariki katika ShauriNa. 1 la mwaka 2010, Kanuni hii ni nyenzo yautekelezaji wa makubaliano ya pamoja (consensus).Kwa mujibu wa Mkataba wa EPA Nchi zoteWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikizinatakiwa kusaini, kuridhia na kutekeleza Mkatabahuo kwa pamoja na endapo baadhi ya nchi zitasainina nyingine kutosaini, Mkataba hautakuwa waJumuiya na hivyo, kanuni ya Variable Geometryhaiwezi kutumika. Kwa muktadha huo, uamuziuliofikiwa wa kutumia kanuni hiyo kutekeleza Mkatabahautaathiri msimamo wa Tanzania wa kutakakufanyika kwa maboresho katika baadhi ya vipengelevya Mkataba kabla ya kusainiwa.

102. Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 21 waWakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya pia ulimteuaDkt. Peter Mathuki kutoka Kenya kuwa Katibu Mkuuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchukua nafasi yaBalozi Liberat Mfumukeko kutoka Burundi ambayeamemaliza muda wake. Vilevile, Mkutano huoulimchagua Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, Raiswa Jamhuri ya Kenya kuwa Mwenyekiti wa Jumuiyakwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Februari 2021

Page 59: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

53

na Jamhuri ya Burundi kushika nafasi ya Mnukuu waVikao vya Jumuiya.

103. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 40 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya AfrikaMashariki. Mkutano huo ulijadili na kupitisha Sera yaUwekezaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayolengakuboresha mazingira ya uwekezaji, kuvutia uwekezajipamoja na kuitangaza Jumuiya ya Afrika Masharikikama eneo moja la uwekezaji. Utekelezaji wa Sera hiiutawezesha kukuza uwekezaji, kurazinisha vivutio vyauwekezaji pamoja na kutangaza Jumuiya ya AfrikaMashariki kama eneo moja la uwekezaji.

104. Mheshimiwa Spika, vilevile, Mkutano wa 40wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masharikiulipitisha azimio la kuanzisha Taasisi ya Fedha yaJumuiya ya Afrika Mashariki ifikapo mwezi Julai,2021.

Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodhawa Afrika Mashariki

105. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa

Page 60: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

54

Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la AfrikaMashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao. Mkutanoulipokea na kuridhia Taarifa ya Biashara na Uwekezajiya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2019.

106. Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo imebainishakuwa thamani ya manunuzi baina ya NchiWanachama iliongezeka kutoka Dola za Marekanimilioni 2,835.9 mwaka 2018 hadi Dola za Marekanimilioni 3,175.8 mwaka 2019, sawa na ongezeko laasilimia 12. Thamani ya mauzo ya bidhaa baina yaNchi Wanachama iliongezeka kutoka Dola zaMarekani milioni 3,145.2 mwaka 2018 hadi Dola zaMarekani milioni 3,162.8 mwaka 2019, sawa naongezeko la asilimia 0.6.

107. Mheshimiwa Spika, kwa upande waTanzania, thamani ya bidhaa zilizouzwa kwenda NchiWanachama iliongezeka kutoka Dola za Marekanimilioni 444.3 mwaka 2018 hadi Dola za Marekanimilioni 674.4 mwaka 2019, sawa na ongezeko laasilimia 51.8. Thamani ya manunuzi ya bidhaa kutokaNchi Wanachama iliongezeka kutoka Dola zaMarekani milioni 302.7 mwaka 2018 hadi Dola zaMarekani milioni 329.2 mwaka 2019, sawa naongezeko la asilimia 8.7. Aidha, takwimu za awali zamwaka 2020 zinaonesha mauzo ya Tanzania kwenda

Page 61: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

55

Nchi Wanachama ni Dola za Marekani milioni 812.55wakati manunuzi kutoka Nchi Wanachama yalikuwaDola za Marekani milioni 324.31. Baadhi ya bidhaazilizouzwa kwa wingi ni mahindi, mchele, bidhaa zachuma, marumaru, karatasi na saruji.

108. Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendeleakuwawezesha wafanyabiashara wadogo kunufaika nafursa zilizopo katika Mtangamano wa Afrika Mashariki.Katika kipindi cha mwezi Julai 2020 hadi Aprili, 2021Tanzania ilitoa vyeti 37,111 vya uasili wa bidhaa kwawafanyabiashara wadogo wa Tanzania wanaofanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Vyeti hivyo, vimewasaidia wafanyabiashara kupataunafuu wa kodi kwa kutolipa ushuru wa forodha kwabidhaa zinazozalishwa nchini na zinazokidhi vigezovya uasili wa bidhaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Utekelezaji wa Miradi na Programu zaMiundombinu ya Kiuchumi na Huduma zaKijamii

109. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2021, Wizarailiratibu na kushiriki ziara ya ukaguzi wa mradi wa Majina Usafi wa Mazingira ya Ziwa Victoria Awamu ya Piliunaotekelezwa katika Wilaya za Geita na Sengerema;mradi wa Kimataifa wa Mawasiliano na Uchukuzi

Page 62: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

56

katika Ziwa Victoria; na mradi wa Kuhimili Mabadilikoya Tabianchi katika Bonde la Ziwa Victoriaunaotekelezwa wilayani Magu. Miradi hiyoinayotekelezwa kwa uratibu wa Kamisheni ya Bondela Ziwa Victoria itawezesha wananchi waishio katikaBonde la Ziwa Victoria kupata maji safi na salama,kuimarisha utunzaji wa mazingira na kunufaika namatumizi endelevu ya rasilimali za bonde hilo.

110. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2021, Wizarailiratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 20 waBaraza la Mawaziri la Kisekta la Afya la Jumuiya yaAfrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha. Katikamkutano huo, Nchi Wanachama zilikubaliana kuundaKamati ya Uratibu ya Kikanda ya UVIKO – 19 naKamati ya Ushauri ya Chanjo ya UVIKO – 19. Kamatihizo zitashauri namna ya kukabiliana na maambukiziya UVIKO - 19 na utaratibu wa chanjo ya ugonjwa huokatika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

111. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu na kushiriki katika ziara ya kikanda yaukaguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kufuaumeme cha Murongo/Kikagati (MW 14)unaotekelezwa kati ya Tanzania na Uganda katikabonde la Mto Kagera. Mradi unatekelezwa namwekezaji binafsi, kampuni ya Kikagati Power

Page 63: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

57

Company Limited (KPCL) iliyosajiliwa nchini Ugandana Tanzania.

112. Mheshimiwa Spika, mradi huo unahusisha piaujenzi wa njia za kusafirishia umeme wa msongo wakV 33 kutoka Murongo (Tanzania) hadi Kikagati(Uganda). Mradi utakapokamilika utahudumia maeneoya wilaya za Kyerwa na Karagwe ambayo kwa sasayanapata umeme kutoka Uganda kwa gharamakubwa.

113. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara iliratibu uwasilishaji wa miradi ya miundombinuya Tanzania katika awamu ya pili ya utekelezaji waProgramu ya Maendeleo ya Miundombinu ya Afrikakupitia Kamisheni ya Umoja wa Afrika. Hatua hii niutekelezaji wa programu ya miradi ya miundombinuya Bara la Afrika. Miradi mitano ya Tanzaniaimejumuishwa katika programu hiyo miongoni mwamiradi 71 ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrikaitakayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2021 –2030.

114. Mheshimiwa Spika, miradi ya Tanzaniailiyojumuishwa ni: ujenzi wa reli ya kiwango chakimataifa ya Dar es Salaam – Tabora - Isaka –Mwanza, Tabora – Uvinza - Kigoma kwenda Kigali

Page 64: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

58

(Rwanda) na Musongati/Gitega (Burundi); ujenzi wareli ya kiwango cha kimataifa ya Mtwara – MbambaBay yenye matawi kwenda Liganga na Mchuchuma;ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kutoka Masaka(Uganda) – Mwanza (kV 400); ujenzi wa Mkongo waTaifa wa Mawasiliano kwenda DRC kupitia ZiwaTanganyika; na ujenzi wa Mkongo wa Taifa waMawasiliano kwenda Msumbiji.

115. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara ilikagua utekelezaji wa miradi ya kikanda yamiundombinu katika mikoa ya Kigoma na Kagerainayotekelezwa na Serikali kupitia Programu yaKuendeleza Mtandao wa Barabara ya Jumuiya yaAfrika Mashariki. Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wabarabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260.6)unaohusisha pia ujenzi wa Kituo cha Huduma kwaPamoja Mpakani (OSBP) Manyovu/Mugina(Tanzania/Burundi); ujenzi wa barabara ya Bugene –Kasulo – Kumunazi (km 133); na ujenzi wa barabaraya Kyaka – Mutukula (km 30).

116. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilikagua hali yamiundombinu na uendeshaji wa Vituo vya OSBP vyaKabanga/Kobero(Tanzania/Burundi),Mutukula/Mutukula (Tanzania/Uganda) na Rusumo/Rusumo(Tanzania/Rwanda). Ukaguzi ulibaini changamoto

Page 65: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

59

zinazoathiri uendeshaji wa vituo vya OSBP nakupendekeza kuandaliwa mkakati wa Jumuiya yaAfrika Mashariki wa utatuzi wa changamotozilizobainika ili kuandaa modeli moja ya OSBP.Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwenyeSekretarieti ya Jumuiya kwa ajili ya hatua zaidi.

117. Mheshimiwa Spika, kufuatia ziara hiyo yaukaguzi, mwezi Novemba 2020, Wizara iliratibuuwekaji saini Hati ya Makubaliano baina ya Tanzania,Burundi, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Taasisi yaUwezeshaji Usafiri katika Ushoroba wa Kati. Hati hiyoinahusu kusimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wabarabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260.6)/Rumonge – Gitaza (km 45). Uwekaji saini ulifuatiwana makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Kituo chaHuduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP)Manyovu/Mugina (Tanzania/Burundi). Mradi huounatekelezwa kwa mkopo wa Dola za Marekanimilioni 256.2 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika.

118. Mheshimiwa Spika, barabara hiyo ni kiungomuhimu cha mtandao wa barabara kwa upande wamikoa ya magharibi mwa Tanzania inayounganishabandari ya Dar es Salaam na nchi za Burundi,Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Aidha, utekelezaji wake unahusisha uboreshaji wa

Page 66: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

60

miundombinu ya huduma za kijamii katika wilaya zaBuhigwe, Kasulu na Kibondo ikiwemo ujenzi wa stendimpya za mabasi; ukarabati wa masoko; ujenzi wamiundombinu ya kusambaza maji na usafi wamazingira; ujenzi wa vituo vya afya na ukarabati wahospitali za wilaya za Kasulu na Kibondo pamoja naununuzi wa magari manne (4) ya kubebea wagonjwakatika miji ya Makere na Busunzu.

119. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakuratibu Miradi ya Miundombinu ya Vipaumbele yaWakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwakufuatilia utekelezaji wake. Katika kipindi hiki mradiwa ujenzi wa Jengo la Abiria la Uwanja wa Ndege waKimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal III)umekamilika na ulizinduliwa mwezi Septemba 2020na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais waAwamu ya Saba wa Zanzibar.

120. Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara kupitiaJumuiya ya Afrika Mashariki iliratibu kupatikana kwafedha kiasi cha shilingi bilioni 371.36 kutoka Benki yaMaendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya ujenzi wabarabara kwa kiwango cha lami kipande cha Pangani– Mkange (km 124.5) na daraja la Pangani katikabarabara ya kikanda ya Bagamoyo – Tanga -Horohoro/Lungalunga - Malindi (km 425); Dola za

Page 67: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

61

Marekani milioni 256.2 kutoka AfDB kwa ajili ya ujenziwa barabara ya kiwango cha lami ya Kasulu –Kabingo - Manyovu (km 260.6)/ Rumonge – Gitaza(km 45); na Dola za Marekani milioni 12 kutoka AfDBkwa ajili ya ujenzi wa jengo la OSBPManyovu/Mugina. Aidha, Wizara iliratibu upatikanajiwa fedha kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukarabatiwa barabara ya Rusumo – Lusahunga kwa kiwangocha lami, ambapo taratibu za kumpata mkandarasizinaendelea.

121. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara iliratibu na kushiriki katika Maadhimisho yaSiku ya Mara yaliyofanyika Butiama mkoani Mara,kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingirakatika Bonde la Mto Mara. Maadhimisho hayoyalihusisha upandaji miti na majadiliano ya mikakatiya utunzaji wa mazingira ya bonde la mto huo.Kufanyika kwa maadhimisho hayo hapa nchinikumetoa fursa kwa wananchi wa maeneo ya wilaya yaButiama na maeneo mengine ya jirani kunufaika nafursa za biashara.

122. Mheshimiwa Spika, mwezi Agosti 2020,Wizara iliratibu na kushiriki kwenye uzinduzi wa Kitaifawa mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumiujulikanao kama “50 Million African Women Speak

Page 68: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

62

Networking Platform”. Uzinduzi huo ulifanywa naMawaziri wanaohusika na Maendeleo ya Jamii katikaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naSerikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mradi huuunatekelezwa katika nchi za Jumuiya ya AfrikaMashariki, Jumuiya ya Soko la Pamoja la Masharikina Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiyaya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).Kwa mwaka 2020, mradi uliwezesha wanawakewapatao 5000 kutoka pande zote mbili za Muunganokupata taarifa muhimu za ujasiriamali kwa njia yamtandao.

123. Mheshimiwa Spika, katika kufanikishautekelezaji wa mradi huo nchini, Wizara iliratibumafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumiyaliyofanyika mwezi Desemba 2020 jijini Dar esSalaam. Mafunzo hayo yalishirikisha takribaniwanawake 200 kutoka Taasisi za Serikali na Asasi zaKiraia zinazoratibu masuala ya maendeleo yawanawake kutoka pande zote mbili za Muungano.Mafunzo hayo yaliwajengea uwezo wa kutumiamtandao wa kuwaunganisha wanawake milioni 50Barani Afrika; kuwahamasisha kuwa mabalozi nawaelimishaji kwa wanawake wengine katika kutatuachangamoto zinazowakabili kibiashara; na kutoaelimu ya fursa za kibiashara.

Page 69: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

63

124. Mheshimiwa Spika, mwezi Julai 2020, Wizarailiratibu na kushiriki katika Mkutano wa Pamoja waMawaziri wa Mambo ya Nje, Afya na Miundombinu waNchi za Tanzania na Rwanda kujadili zuio la malori yamizigo kutoka Tanzania kuvuka mpaka wa Rusumokuingia Rwanda kwa lengo la kudhibiti kuenea kwaUVIKO-19. Mkutano huo uliwezesha kupatikana kwaufumbuzi wa mgogoro uliokuwepo kwa pande mbilikukubaliana kuendelea kutekeleza mwongozouliotolewa na Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya AfrikaMashariki katika Mkutano wa Dharura uliofanyikamwezi Machi 2020.

125. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikishakupatikana kwa wajumbe saba watakaoiwakilishaTanzania katika Bodi ya Wakurugenzi wa Kamisheniya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya ya AfrikaMashariki kwa kipindi cha miaka mitano kuanziamwaka 2020 hadi 2025. Kati ya hao, wajumbe wannewanatoka Tanzania Bara na watatu Zanzibar.

126. Mheshimiwa Spika, wajumbe hao ni Prof.James E. Mdoe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia; Dkt. Amos Nungu,Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Sayansi naTeknolojia; Dkt. Ali Ahmed Uki, Mkufunzi Mwandamizikutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU); Dkt. Rose Rita

Page 70: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

64

Kingamkono, Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi yaMaendeleo ya Wanawake kwenye Masuala ya Kilimo(CAWAT); Dkt. Asifu Petro Nanyaro, Katibu Mtendajiwa Tanzania Academy of Science - TAAS; Dkt. HajiMwevura Haji, Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha TaifaZanzibar (SUZA); na Dkt. Zidi Mussa Makame,Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Sayansi chaKarume (Zanzibar).

Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki

127. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakuratibu ushiriki wa Tanzania katika maandalizi yaRasimu ya Katiba ya Fungamano la Kisiasa la AfrikaMashariki kama hatua ya mpito kuelekea Shirikisho laKisiasa la Afrika Mashariki. Hadi kufikia mwezi Aprili2021, zoezi la kukusanya maoni na kutoa elimu kwaumma limefanyika katika nchi za Burundi na Uganda.Kulingana na ratiba ya zoezi hilo, timu ya wataalam yaJumuiya inayokusanya maoni kuhusiana na rasimu yakatiba hiyo itatembelea Tanzania mwezi Agosti 2021.

Demokrasia na Utawala Bora

128. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, nchimbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikiambazo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na

Page 71: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

65

Jamhuri ya Uganda zilifanya Uchaguzi Mkuu. Jumuiyaya Afrika Mashariki ilituma timu ya waangalizi wauchaguzi hapa nchini mwezi Oktoba 2020. Timu hiyoiliongozwa na Mheshimiwa Sylvester Ntibantunganya,Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Burundi. Katika uchaguzihuo Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufulialiyekuwa mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzialishinda nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania. Aidha, kwa upande wa Zanzibar,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi mgombeakutoka Chama Cha Mapinduzi alishinda nafasi yaRais wa Zanzibar.

129. Mheshimiwa Spika, taarifa ya timu yawaangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya AfrikaMashariki ilieleza kuwa uchaguzi huo ulifanyika katikamazingira ya amani na utulivu, na ulikidhi vigezo vyakuwa huru na haki kama ilivyoainishwa katikamwongozo wa uangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya yaAfrika Mashariki.

130. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika timu yawaangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya AfrikaMashariki kwenye Uchaguzi Mkuu nchini Uganda.Zoezi la uangalizi lililenga kuhakikisha kuwa misingiya demokrasia inatekelezwa kama ilivyoainishwa

Page 72: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

66

katika Kanuni za msingi za Jumuiya. Katika uchaguzihuo, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni mgombeakupitia Chama cha National Resistance Movementalishinda nafasi ya Rais. Taarifa ya awali yawaangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya AfrikaMashariki inaonesha uchaguzi huo ulifikia vigezo vyamsingi vilivyoainishwa katika mwongozo wa uangaliziwa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Masharikina Jumuiya Nyingine

a) Utatu wa COMESA-EAC-SADC

131. Mheshimiwa Spika, mwezi Machi 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wa Utatu waCOMESA – EAC – SADC wanaohusika na Biashara,Fedha, Uchumi, Mambo ya Ndani na Afya uliofanyikakwa njia ya mtandao. Mkutano huo uliridhia nakupitisha Mwongozo wa Kusimamia Uvukaji Salamawa Watu na Mizigo kwa kipindi cha mlipuko waUVIKO-19 kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewana Nchi Wanachama; na kuhimiza kuendeleakubadilishana uzoefu wa njia bora za kukabiliana nakudhibiti ugonjwa huo.

Page 73: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

67

132. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EneoHuru la Biashara la Utatu wa COMESA-EAC-SADCuliofanyika kwa njia ya mtandao. Mkutano ulipokeataarifa ya kusainiwa na kuridhiwa kwa Mkataba waEneo Huru la Biashara la Utatu wa COMESA-EAC-SADC.

133. Mheshimiwa Spika, nchi 10 kati ya 22zilizosaini Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Utatuwa COMESA-EAC-SADC zimeridhia na kuwasilishahati za kuridhia mkataba huo kwa Mwenyekiti waSekretarieti ya Utatu. Mkataba utapata nguvu yakisheria na kuanza kutekelezwa baada ya nchi 14kuridhia na kuwasilisha hati za kuridhia. Tanzaniainaendelea na taratibu za kuridhia Mkataba huo.

b) Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika

134. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 13 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali waUmoja wa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.Mkutano huo pamoja na maamuzi mengine,ulielekeza Nchi Wanachama kukamilisha majadilianoya Viambatisho vya Ufunguaji wa Biashara ya Bidhaa,

Page 74: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

68

Huduma na Vigezo vya Uasilia wa Bidhaa ili biasharakatika Eneo Huru la Biashara la Afrika iweze kuanzaifikapo tarehe 01 Januari, 2021. Hata hivyo, kutokanana kuendelea kuenea kwa UVIKO–19, NchiWanachama hazikufanikiwa kukamilisha majadilianoya Viambatisho husika na hivyo kuathiri mtiririko wabiashara baina ya Nchi Wanachama. Majadiliano yaViambatisho hivyo yanatarajiwa kukamilika Juni, 2021na biashara kuanza Julai, 2021.

c) Majadiliano ya Mkataba wa BiasharaBaina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki naUingereza

135. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutanowa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya AfrikaMashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao. Mkutanohuo ulijadili maombi ya Uingereza ya kufanyamajadiliano ya Mkataba rasmi wa Biashara naJumuiya ya Afrika Mashariki, kufuatia Uingerezakujitoa katika Umoja wa Ulaya.

136. Mheshimiwa Spika, Baraza la Mawaziri laKisekta, lilikubaliana na pendekezo la majadilianohayo na kuagiza Nchi Wanachama kushiriki

Page 75: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

69

majadiliano kwa pamoja kama Jumuiya. Aidha,ilipendekezwa Serikali ya Uingereza isogeze mbelemuda wa kukamilisha majadiliano kutoka tarehe 31Desemba, 2020 hadi tarehe 31 Desemba, 2021 ilikutoa muda kwa Nchi Wanachama kufanyamashauriano ya ndani.

137. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Uingerezahaikuafiki mapendekezo hayo ya Jumuiya ya AfrikaMashariki na kusisitiza azma yake ya kuendelea namajadiliano na nchi zitakazokuwa tayari. Kufuatiamsimamo huo, Kenya iliendelea na majadiliano nakusaini Mkataba huo mwezi Desemba, 2020. Hatahivyo, Ibara ya 37(4) ya Itifaki ya Umoja wa Forodhainazitaka Nchi Wanachama kutoa taarifa ya kusudio lakuingia Mkataba wa Biashara na Nchi nyingine nje yaUmoja wa Forodha, kwa lengo la kuwezesha nchinyingine kutoa maoni kama Mkataba huo una atharikwenye Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki.Hivyo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ameikumbushaJamhuri ya Kenya kuzingatia matakwa ya Ibara hiyo.

Bunge la Afrika Mashariki

138. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari hadiFebruari 2021, Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzaniakatika Mkutano wa Pili, Kikao cha Nne cha Bunge la

Page 76: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

70

Nne la Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia yamtandao. Mkutano huo ulijadili muswada binafsi washeria kuhusu mifugo. Lengo la muswada huo nikuweka mfumo wa kisheria wa kuratibu masuala yamifugo katika Jumuiya ikiwa ni pamoja na kudhibitimagonjwa yanayoathiri mifugo. Vilevile, Bunge lilijadilina kupitisha muswada binafsi wa sheria kuhusumasuala ya uadilifu na mapambano dhidi ya rushwa.Muswada huo unalenga kukuza uadilifu na kuimarishamfumo wa kisheria katika kuzuia na kupambana namasuala ya rushwa katika Asasi na Taasisi zaJumuiya.

4.2.2 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika (SADC)

139. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano waMawaziri wanaohusika na Masuala ya Kazi na Ajirakatika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.Kupitia Mkutano huo Nchi Wanachama wa SADCziliweka msimamo wa pamoja kuhusu maboresho yaKatiba ya Shirika la Kazi Duniani. Marekebisho hayoyanalenga kuongeza wigo wa demokrasia katikamaamuzi ndani ya Shirika hilo. Msimamo huo wa nchiza SADC unatarajiwa kuwasilishwa katika vikao vyaUmoja wa Afrika kwa majadiliano na kuweka

Page 77: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

71

msimamo wa pamoja wa nchi za Afrika kuhusumaboresho ya Katiba ya Shirika la Kazi Duniani.

140. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2021, Wizarailiratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutano waDharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TroikaMbili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrikauliofanyika jijini Maputo, Msumbiji. Troika Mbiliinajumuisha Jamhuri ya Msumbiji (Mwenyekiti wasasa wa SADC), Jamhuri ya Malawi (Mwenyekitiajaye), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mwenyekiti aliyemaliza muda wake), Jamhuri yaBotswana (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC yaUshirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama), Jamhuri yaAfrika Kusini (Mwenyekiti ajaye wa Asasi) na Jamhuriya Zimbabwe (Mwenyekiti wa Asasi aliyemaliza mudawake). Katika Mkutano huo Nchi Wanachamaziliazimia kuendelea kushirikiana kuimarisha hali yaulinzi na usalama kaskazini mwa nchi ya Msumbijihususan kwenye Jimbo la Cabo Delgado. Mkutanouliazimia kuiwezesha na kuitumia Standby Force yaSADC kutatua tatizo la ugaidi katika Jamhuri yaMsumbiji.

141. Mheshimiwa Spika, mwezi Machi 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo

Page 78: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

72

Kusini mwa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.Mkutano huo uliridhia kuongeza wigo wa matumizi yalugha ya Kiswahili katika mikutano ya kisekta yaSADC. Aidha, Mkutano uliielekeza Sekretarieti yaSADC kukamilisha ujenzi wa sanamu ya MwalimuNyerere inayojengwa katika Jengo la Amani naUsalama kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrikajijini Addis Ababa, Ethiopia ifikapo mwezi Aprili 2022.Vilevile, Mkutano huo uliridhia kufanyika kwamaadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 ya SADCna kuhimiza Nchi Wanachama kutangaza mafanikioya SADC na kuelimisha umma juu ya programuzinazofanywa na Jumuiya hiyo.

142. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Dharura wa Ngazi ya Juu wa Mashauriano waWakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Afrika Kusini,Botswana, Msumbiji, Tanzania na Zimbabweuliofanyika jijini Maputo, Msumbiji. Mkutano huouliweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha amanikatika Jumuiya ya SADC.

143. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Troika Mbili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusinimwa Afrika na Washirika wa Maendeleo uliofanyika

Page 79: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

73

kwa njia ya mtandao. Kupitia mkutano huo, NchiWanachama wa SADC na Washirika wa Maendeleozilikubaliana kujikita katika kujenga uwezo wakitaasisi na kitaalam, uhaulishaji wa teknolojia namisaada ya kifedha katika kutekeleza miradi yakuhifadhi mazingira.

144. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikaliwanaounda Utatu wa Asasi ya SADC ya Ushirikianokatika Siasa, Ulinzi na Usalama uliofanyika jijiniGaborone, Botswana. Mkutano huo pia ulishirikishanchi za Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) pamoja na nchi za Tanzania, Malawi na AfrikaKusini ambazo zinachangia vikosi vya kijeshi katikaKikosi Maalum cha Ulinzi wa Amani (ForceIntervention Brigade - FIB) kilichopo DRC. Mkutanohuo uliweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana naongezeko la matukio ya ugaidi na uvunjifu wa amanikatika nchi za Msumbiji na DRC. Aidha, Mkutano huouliridhia kuanzishwa kwa Kituo cha SADC chaKupambana na Ugaidi.

Page 80: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

74

4.2.3 Jumuiya ya Nchi za Ukanda waMwambao wa Bahari ya Hindi (IORA)

145. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchizilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA)uliofanyika kwa njia ya mtandao. Vilevile, mweziFebruari 2021, Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzaniakatika Mjadala wa Saba wa IORA uliofanyika kwa njiaya mtandao. Katika mikutano hiyo, Nchi Wanachamazilikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katikakukuza uchumi kupitia uchumi wa bluu; kuimarishaajira, biashara na uwekezaji; kuimarisha ulinzi nausalama wa bahari na kupunguza athari za maafa namajanga; kuimarisha usafiri na usafirishaji wabaharini; na kuendelea kuwawezesha wanawake navijana kiuchumi.

4.2.4 Umoja wa Afrika

146. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei 2021, Wizarailiratibu ushiriki wa Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwenye Mkutano wa Mtandao wa ViongoziWanawake Barani Afrika (AWLN) uliofanyika kwa njiaya mtandao. Wakati wa Mkutano huo, MheshimiwaRais alipongezwa kwa kuapishwa kuwa Rais wa

Page 81: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

75

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidiwakupewa ushirikiano katika masuala mbalimbaliyakiwemo maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii,haki za wanawake, amani na usalama wa kikanda nakukabiliana na janga la UVIKO–19.

147. Mheshimiwa Spika, pamoja na masualamengine, Mheshimiwa Rais ameahidi kuendeleakushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kimataifakatika kukuza maendeleo nchini na kuendeleakuwapa kipaumbele wanawake katika nafasimbalimbali za Uongozi Serikalini.

148. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa 34 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja waAfrika uliofanyika kwa njia ya mtandao. Baadhi yaagenda zilizojadiliwa katika Mkutano huo ni: programuya kutekeleza kaulimbiu ya mwaka 2021 inayosema“Sanaa, Tamaduni na Urithi katika kufikia Azma yaAfrika Tuitakayo”; mapambano dhidi ya UVIKO-19;uchaguzi wa uongozi mpya wa Kamisheni ya Umojawa Afrika kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024; nauchaguzi wa majaji wa Mahakama ya Afrika ya Hakiza Binadamu na Watu.

Page 82: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

76

149. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huo,Umoja wa Afrika pia uliridhia ombi la Tanzania lakujumuisha lugha ya Kiswahili na uanzishaji wa Kituocha Urithi wa Afrika jijini Dar es Salaam katikaprogramu ya kutekeleza kaulimbiu ya mwaka 2021inayosema “Sanaa, Tamaduni na Urithi katikakufikia Azma ya Afrika Tuitakayo”. Maamuzi hayoyamejumuishwa kwenye shughuli za programu hiyozinazotekelezwa na Umoja wa Afrika katika mwaka2021.

150. Mheshimiwa Spika, vilevile, katika Mkutanohuo Tanzania ilisisitiza umuhimu wa Afrikakuwajengea uwezo wataalam wake katika eneo latafiti kwenye sekta ya afya. Msisitizo uliwekwa katikakutengeneza dawa za kujikinga na kutibu maradhiikiwemo chanjo dhidi ya UVIKO-19 na magonjwamengine ili Afrika iweze kujitegemea katika sekta yaafya kwa kuongeza urahisi na unafuu wa upatikanajiwa dawa.

151. Mheshimiwa Spika, aidha, Nchi Wanachamazilimchagua Mhe. Moussa Faki Mahamat kutoka Chadkuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrikakwa muhula wa pili. Mkutano pia ulimchagua Mhe.Dkt. Monique Nsanzabaganwa kutoka Rwanda kuwaMakamu Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo. Viongozi hao

Page 83: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

77

watahudumu kwa kipindi cha miaka minne kuanziamwaka 2021 hadi 2024.

152. Mheshimiwa Spika, Mkutano huo pia ulifanyauchaguzi wa majaji wanne wa Mahakama ya Afrika yaHaki za Binadamu na Watu. Mhe. Jaji Imani Aboud,Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania alichaguliwa kwakura 51 kati ya kura 52 zilizopigwa kuhudumu katikaMahakama hiyo kwa muhula wa pili wa miaka sitakuanzia mwezi Februari 2021. Wingi wa kuraalizozipata Mhe. Jaji Imani Aboud ni ushahidi wakutosha wa ukomavu wa diplomasia yetu na kuungwamkono kwa nchi yetu na nchi nyingine za Afrika.

153. Mheshimiwa Spika, vilevile, Tanzania ilitumianafasi ya Mkutano huo kuzitaarifu nchi za Umoja waAfrika kuhusu hali ya kisiasa nchini na namnaambavyo nchi yetu inaendelea kuheshimu utawala washeria na haki za binadamu tofauti na habari potofuzilizokuwa zikisambazwa baada ya kukamilika kwaUchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Tanzaniailiuhakikishia Umoja huo kwamba uchaguzi ulikuwawa haki, huru na wazi, uliozingatia misingi yademokrasia na utawala bora, na ulifanyika katikamazingira ya amani na utulivu.

Page 84: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

78

154. Mheshimiwa Spika, mwezi Januari 2021,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika Mkutanowa Kamati Maalum ya Umoja wa Afrika ya Mawaziriwa Ulinzi uliofanyika kwa njia ya mtandao. Mkutanohuo ulipitisha mwongozo wa Umoja wa Afrika kuhusuupangaji, uendeshaji na usimamizi wa shughuli zaulinzi wa amani Barani Afrika.

155. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umojawa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao. Mkutanohuo ulijadili taarifa ya utekelezaji wa Mkakati waKumaliza Vita Barani Afrika ifikapo mwaka 2020.Mkutano uliongeza muda wa utekelezaji wa Mkakatihuo kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2021 hadi 2030ikiwa ni pamoja na kuendelea kuadhimisha mwezi wausalimishaji wa silaha haramu kwa hiari mweziSeptemba kila mwaka.

156. Mheshimiwa Spika, Mkutano huo pia uliamuakuwa ni vyema Nchi Mwanachama wa Umoja huokabla ya kuingia makubaliano ya kuwa wenyeji wakambi za kijeshi za mataifa ya nje kushauriana naBaraza la Amani na Usalama la Afrika, Jumuiya zakikanda pamoja na nchi jirani ili kuhakikisha zinakidhimalengo ya Umoja wa Afrika.

Page 85: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

79

157. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huo,Tanzania ilitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifakutoingilia mambo ya ndani ya Afrika. Tanzania piailisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendeleakuzungumza kwa kauli moja na kuhakikisha Afrikainapata nafasi mbili za kudumu na tano zisizo zakudumu za uwakilishi katika Baraza la Usalama laUmoja wa Mataifa.

4.2.5 Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa MaziwaMakuu (ICGLR)

158. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki waTanzania kwenye Misheni ya Jumuiya ya Nchi zaUkanda wa Maziwa Makuu ya uangalizi wa Uchaguziwa Rais wa Jamhuri ya Kongo uliofanyika tarehe 21Machi, 2021. Katika uchaguzi huo Mheshimiwa DenisSassou-Nguesso alishinda nafasi ya Rais kupitiaChama cha Congolese Labour Party kwa kupataasilimia 88 ya kura zilizopigwa.

159. Mheshimiwa Spika, mwezi Novemba 2020,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutanowa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiyaya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika kwanjia ya mtandao. Mkutano huo ulipokea na kujadilitaarifa ya hali ya amani na usalama katika Ukanda wa

Page 86: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

80

Maziwa Makuu. Taarifa hiyo, ilieleza kuimarika kwahali ya amani na usalama kwenye maeneo mengi yaukanda huo isipokuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati naeneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo ambayo yanaendelea kukabiliwa nachangamoto za kiusalama. Vilevile, Mkutano uliridhiawito uliotolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa Nchi Wanachama kuendelea kushirikiana katikakupambana na vikundi vyenye silaha ili kuimarishahali ya utulivu katika Ukanda huo.

4.2.6 Ushirikiano wa Kimataifa

160. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki waTanzania katika Kikao cha 46 cha Baraza la Haki zaBinadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika kuanziamwezi Februari hadi Machi 2021 Geneva, Uswisi.Katika Kikao hicho, Jamhuri ya Muungano waTanzania ilipata fursa ya kutoa taarifa kuhusuutekelezaji wa haki za binadamu nchini ikiwa nipamoja na hatua zilizofikiwa katika kutoa haki yaelimu, huduma za afya, maji safi na salama pamojana nishati.

161. Mheshimiwa Spika, Tanzania pia ilitumiaKikao hicho kuielezea jumuiya ya kimataifa kuhusuUchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba 2020

Page 87: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

81

ambao kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifaletu uligharamiwa kwa fedha za ndani; na kuwauchaguzi huo ulikuwa wa haki, huru na wazi,uliozingatia misingi ya demokrasia na utawala bora,na ulifanyika katika mazingira ya amani na utulivu.Hatua hizi, zimesaidia kujenga mtazamo chanya kwajumuiya ya kimataifa kuhusu Taifa letu ambao nimuhimu katika kuimarisha mahusiano na ushirikianokati ya nchi yetu na jumuiya ya kimataifa.

162. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki waTanzania katika Kikao cha 75 cha Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kilichofanyika kuanzia mweziSeptemba hadi Desemba 2020. Tanzania ilitumiafursa hiyo kuieleza jumuiya ya kimataifa kuhusu hatuazinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha hudumaza kijamii na kutengeneza fursa za kiuchumi kwakuimarisha miundombinu ya reli, barabara, maji,nishati, afya na elimu. Vilevile, Tanzania ilielezakuhusu hatua zinazochukuliwa katika kupambana narushwa na ubadhirifu wa mali za umma; kusimamianidhamu kwenye utumishi wa umma; na kuimarishaukusanyaji wa mapato ya Serikali.

163. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Umoja waMataifa, mashirika, taasisi na majukwaa ya kimataifa.

Page 88: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

82

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana naushiriki huo ni pamoja na:

i. Kujumuishwa kwa Tanzania katika ProgramuShirikishi baina ya Nchi na Washirika waMaendeleo kupitia Shirika la Umoja wa Mataifala Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) mweziNovemba 2020. Programu hii inalengakuzisaidia Nchi Wanachama kujileteamaendeleo jumuishi na endelevu ya viwanda.Majadiliano yanaendelea kati ya Serikali naUNIDO ya kuandaa andiko la utekelezaji waprogramu hiyo litakaloainisha vipaumbele vyanchi;

ii. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) umeridhia kutoa mkopo wa mashartinafuu wa Dola za Marekani milioni 58.8. Fedhahizo zitatumika kuendeleza sekta ya uvuvi kwakununua meli nane za uvuvi katika bahari kuuambapo meli nne zitatumika Tanzania Bara nanne Zanzibar. Vilevile, fedha hizozitatengeneza miundombinu ya ufugaji wasamaki na kuimarisha vikundi shirikishi vyausimamizi wa rasilimali za uvuvi katika maeneoya bahari kuu. Kadhalika, fedha hizo zitatumikakuimarisha uwezo wa Taasisi ya Utafiti wa

Page 89: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

83

Kilimo Tanzania na kuboresha uzalishaji wambegu bora katika mashamba ya Wakala waMbegu Tanzania; na

iii. Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti waKamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuula Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2020/2021.Kamati hiyo ina jukumu la kupitia hati zote zautambulisho zinazowasilishwa na Wakuu waNchi na Serikali au Mawaziri wa Mambo ya Njewa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa nakujiridhisha iwapo zimekidhi vigezo na mashartikwa mujibu wa sheria za kimataifa na Mkatabawa Umoja huo.

164. Mheshimiwa Spika, mafanikio haya ni isharaya kuaminika na kukubalika kwa misimamo na sera zanchi yetu kimataifa.

4.3 Kufuatilia na Kusimamia Utekelezaji waMikataba ya Kimataifa na Hati zaMakubaliano

165. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021, Wizara iliratibu na kushirikikatika majadiliano na kusimamia uwekaji saini

Page 90: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

84

Mikataba na Hati za Makubaliano ya Kimataifazifuatazo:

i. Mkataba wa Uenyeji kati ya Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Kampuni yaMafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP)kuhusu Ujenzi wa Mradi wa Bomba lakusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Ugandampaka Tanga, Tanzania mwezi Mei, 2021;

ii. Hati ya Makubaliano ya Kusafirisha Gesi Asiliakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kenyamwezi Mei 2021;

iii. Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katikaMasuala ya Utamaduni, Sanaa, Mahusiano yaJamii na Urithi wa Taifa kati ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenyamwezi Mei 2021;

iv. Hati ya Makubaliano kuhusu Mradi wa KufuaUmeme kwa Kutumia Nishati ya Gesi kati yaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar na kampuni yaMonitor Power System ya Norway mweziFebruari 2021;

Page 91: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

85

v. Hati ya Makubaliano Kuanzisha Ushirikiano waKijeshi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Falme zaKiarabu mwezi Februari 2021;

vi. Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katikaMapambano dhidi ya Rushwa kati ya Taasisi yaKuzuia na Kupambana na Rushwa ya Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naSerikali ya Taifa la Palestina mwezi Februari2021;

vii. Mkataba kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Wizara ya Ulinzi yaShirikisho la Ujerumani kuhusu Msaada waVifaa kwa kipindi cha tarehe 1 Januari 2021hadi tarehe 31 Desemba 2024;

viii. Hati ya Makubaliano Kuanzisha Tume yaPamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya Pakistanmwezi Desemba 2020;

ix. Hati ya Makubaliano kuhusu Mashauriano yaKisiasa kati ya Serikali ya Jamhuri ya

Page 92: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

86

Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuriya Kiislam ya Pakistan mwezi Desemba 2020;

x. Hati ya Makubaliano Kuanzisha Ushirikiano katiya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Wizara ya Mamboya Nje na Biashara ya Serikali ya Hungarykuhusu Mpango wa Mafunzo kwa mwaka 2021– 2023 mwezi Desemba 2020;

xi. Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana Bw. Jhody Prabawa, Mwakilishi wa Heshimawa Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania katika Jamhuri ya Indonesia mweziNovemba 2020; na

xii. Hati ya Makubaliano ya Kusimamia Utekelezajiwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kabingo –Kasulu – Manyovu (Kilometa 260)/ Rumonge -Gitaza (Kilometa 45) baina ya Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali yaJamhuri ya Burundi, Sekretarieti ya Jumuiya yaAfrika Mashariki na Taasisi ya Ushoroba wa Katimwezi Novemba 2020.

Page 93: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

87

166. Mheshimiwa Spika, Mikataba na Hati zaMakubaliano zilizosainiwa zinalenga kuimarishaushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi marafiki,Jumuiya za Kikanda na Kimataifa. Tanzania itanufaikana fursa zilizopo katika maeneo yaliyolengwa katikamikataba pamoja na makubaliano hayo.

4.4 Kuratibu Masuala ya Itifaki, Uwakilishi naHuduma za Kikonseli

167. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2020/2021 Wizara imeendelea kuratibu masuala yaitifaki na huduma za kikonseli kama ifuatavyo:

4.4.1 Ziara za Viongozi wa Kitaifa naMashirika ya Kikanda na KimataifaKutoka Nje ya Nchi

168. Mheshimiwa Spika, pamoja na changamotoza kusafiri kimataifa zinazosababishwa na janga laUVIKO-19, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha2020/2021 Wizara imeendelea kuratibu ziara zaviongozi wa kitaifa na mashirika ya kikanda nakimataifa waliotembelea nchini kama ifuatavyo:

i. Ziara ya Mheshimiwa Ezechiel Nibigira, Waziriwa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,

Page 94: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

88

Vijana, Michezo na Utamaduni na MjumbeMaalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi tarehe21 Mei, 2021;

ii. Ziara za Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni,Rais wa Jamhuri ya Uganda tarehe 20 Mei,2021 na 13 Septemba, 2020;

iii. Ziara ya Mheshimiwa Mikhail Bogdano, NaibuWaziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe Maalumwa Rais wa Shirikisho la Urusi tarehe 14 Mei,2021;

iv. Ziara ya Mheshimiwa James Duddrige, Waziriwa Uingereza anayeshughulikia masuala yaAfrika tarehe 11 Mei, 2021;

v. Ziara ya Mheshimiwa Balozi Dkt. AminaMohamed, Waziri wa Michezo, Utamaduni naUrithi wa Jamhuri ya Kenya, Mjumbe Maalumwa Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, Raiswa Jamhuri ya Kenya tarehe 10 Aprili, 2021;

vi. Ziara ya Mheshimiwa Sahle – Work Zewde, Raiswa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho laEthiopia tarehe 25 Januari 2021;

Page 95: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

89

vii. Ziara ya Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, Raiswa Jamhuri ya Msumbiji tarehe 11 Januari 2021;

viii. Ziara ya Mheshimiwa Wang Yi, Mjumbe waBaraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje waJamhuri ya Watu wa China tarehe 7 hadi 8Januari 2021;

ix. Ziara ya Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri waUshirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri yaNamibia tarehe 8 Desemba, 2020;

x. Ziara ya Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthyChakwera, Rais wa Jamhuri ya Malawi tarehe 7hadi 8 Oktoba, 2020; na

xi. Ziara ya Mheshimiwa Meja Jenerali ÉvaristeNdayishimiye, Rais wa Jamhuri ya Burunditarehe 19 Septemba, 2020.

169. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ziara zaviongozi mbalimbali waliokuja nchini kushiriki hafla yauapisho wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania iliyofanyika tarehe 5Novemba, 2020 jijini Dodoma. Viongozi hao ni:

Page 96: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

90

i. Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais waJamhuri ya Uganda;

ii. Mheshimiwa Emmerson Dambuzo Mnangagwa,Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe;

iii. Mheshimiwa Azali Assoumani, Rais waMuungano wa Visiwa vya Comoro;

iv. Mheshimiwa Slumber Tsogwane, Makamu waRais wa Jamhuri ya Botswana;

v. Mheshimiwa Alain Guillaume Bunyoni, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Burundi;

vi. Mheshimiwa Carlos Agostinho Do Rosário, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Msumbiji;

vii. Mheshimiwa Adan Mohamed, Waziri waUshirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo yaKikanda na Mjumbe Maalum wa MheshimiwaUhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Jamhuri yaKenya;

viii. Mheshimiwa Sultan Bin Saad Al – Muraikhi,Waziri wa Mambo ya Nje wa Taifa la Qatar naMjumbe Maalum wa Mtukufu Sheikh Tamim binHamad Al-Thani, Emir wa Taifa la Qatar; na

ix. Mheshimiwa Sylvestre Ntibantunganya, RaisMstaafu wa Jamhuri ya Burundi na aliyekuwa

Page 97: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

91

Mwenyekiti wa Timu ya Uangalizi wa UchaguziMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

170. Mheshimiwa Spika, hafla hiyo ilihudhuriwa piana Mawaziri kutoka nchi mbalimbali kama ifuatavyo:

i. Mheshimiwa Dkt. Naled Pandor, Waziri waMambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini;

ii. Mheshimiwa Andre Kabanda Kana, Waziri waNchi, Ofisi ya Rais Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo;

iii. Mheshimiwa Mohamed Sidik Mia, Waziri waUchukuzi na Ujenzi wa Jamhuri ya Malawi;

iv. Mheshimiwa Gospel Kazako, Waziri wa Habariwa Jamhuri ya Malawi;

v. Mheshimiwa Mhandisi Dkt. Asim Abdelhamid El-Gazar, Waziri wa Makazi wa Jamhuri ya Kiarabuya Misri; na

vi. Mheshimiwa Joseph Malanji, Waziri wa Mamboya Nje wa Jamhuri ya Zambia.

171. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ziara zaviongozi mbalimbali waliokuja nchini kushiriki katikamazishi ya kitaifa ya Hayati Dkt. John Pombe Joseph

Page 98: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

92

Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania yaliyofanyika tarehe 22Machi, 2021 jijini Dodoma. Viongozi hao ni kamaifuatavyo:

i. Mheshimiwa Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo,Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo naMwenyekiti wa Umoja wa Afrika;

ii. Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, Rais waJamhuri ya Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya yaAfrika Mashariki;

iii. Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, Rais waJamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Jumuiyaya Maendeleo Kusini mwa Afrika;

iv. Mheshimiwa Cyril Matamela Ramaphosa, Raiswa Jamhuri ya Afrika Kusini;

v. Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi,Rais wa Jamhuri ya Botswana;

vi. Mheshimiwa Azali Assoumani, Rais waMuungano wa Visiwa vya Comoro;

vii. Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera,Rais wa Jamhuri ya Malawi;

viii. Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu, Rais waJamhuri ya Zambia; na

Page 99: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

93

ix. Mheshimiwa Emmerson Dambuzo Mnangagwa,Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe.

172. Mheshimiwa Spika, viongozi wenginewalioshiriki ni:

i. Mheshimiwa Prosper Bazombana, Makamu waRais wa Jamhuri ya Burundi;

ii. Mheshimiwa Sylvestre Ntibantunganya, RaisMstaafu wa Jamhuri ya Burundi;

iii. Mheshimiwa Dkt. Nangolo Mbumba, Makamu waRais wa Jamhuri ya Namibia;

iv. Mheshimiwa Alain Guillaume Bunyoni, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Burundi;

v. Mheshimiwa Dkt. Edouard Ngirente, Waziri Mkuuwa Jamhuri ya Rwanda;

vi. Mheshimiwa Carlos Agostinho Do Rosário, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Msumbiji;

vii. Mheshimiwa Téte Antonio, Waziri wa Mambo yaNje wa Jamhuri ya Angola;

viii. Mheshimiwa Lamin Yahyaoui, Mjumbe Maalumwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabuya Saharawi;

Page 100: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

94

ix. Mheshimiwa Gotabaya Rajapaksa, MjumbeMaalum wa Mheshimiwa Dkt. Kana Kananathan,Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalistiya Sri Lanka; na

x. Mheshimiwa Richard Kabonero, Balozi waJamhuri ya Uganda nchini na Mjumbe Maalumwa Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Raiswa Jamhuri ya Uganda.

173. Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Mashirika naTaasisi za Kikanda na Kimataifa walioshiriki katikamsiba huo wa kitaifa ni pamoja na Wakuu wa Jumuiyaza Kikanda:

i. Balozi Libérat Mfumukeko, aliyekuwa KatibuMkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;

ii. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mtendaji waJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika;

iii. Mhe. Martin Ngonga, Spika wa Bunge la AfrikaMashariki;

iv. Mhe. Jaji Sylvain Oré, Rais wa Mahakama yaWatu na Haki ya Afrika;

v. Mhe. Jaji Nestor Kayobela, Rais wa Mahakamaya Haki ya Afrika Mashariki; na

Page 101: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

95

vi. Bw. Younouss Djibrine, Katibu Mkuu wa Umojawa Posta Afrika

174. Mheshimiwa Spika, Wizara pia inatoashukrani za dhati kwa Waheshimiwa Mabalozi naWakuu wa Mashirika na Taasisi za Kimataifawanaoziwakilisha nchi na Mashirika yao hapa nchinikwa kushiriki katika mazishi ya kitaifa ya Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Awamu yaTano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

4.4.2 Ziara za Viongozi wa Kitaifa Nje ya Nchi

175. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ziara zaViongozi wa Kitaifa waliokwenda katika nchimbalimbali kama ifuatavyo:

i. Ziara za Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi nchini Msumbiji kushiriki Mkutano waDharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TroikaMbili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika uliofanyika mwezi Aprili na Mei 2021,akimwakilisha Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania;

ii. Ziara Rasmi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Uganda kuhudhuria sherehe za

Page 102: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

96

uapisho wa Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mweziMei 2021;

iii. Ziara ya Kitaifa ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Kenya kufuatia mwaliko wa Mhe.Rais Uhuru Muigai Kenyatta mwezi Mei 2021;

iv. Ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Uganda kushuhudia uwekajisaini wa makubaliano ya kuanza ujenzi wa Mradiwa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la AfrikaMashariki kutoka Hoima, Uganda hadiChongoleani,Tanga mwezi Aprili 2021;

v. Ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania nchini Msumbiji kushirikiMkutano wa Dharura wa Utatu wa Asasi yaUshirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama yaWakuu wa Nchi na Serikali mwezi Desemba2020;

vi. Ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania nchini Botswanakushiriki Mkutano wa Utatu wa Wakuu wa Nchina Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama mwezi Novemba 2020;

Page 103: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

97

vii. Ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Samia SuluhuHassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania nchini Malawi kushirikikatika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 yaUhuru wa Jamhuri ya Malawi zilizofanyika mweziJulai 2020; na

viii. Ziara za Waheshimiwa Marais Wastaafu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenyemikutano mbalimbali nje ya nchi.

4.4.3 Kuanzisha na Kusimamia Huduma zaKikonseli

176. Mheshimiwa Spika, nchi yetu imeendeleakuongeza uwakilishi katika nchi mbalimbali ambapoSerikali imekamilisha taratibu za kufungua KonseliKuu mpya katika Jiji la Lubumbashi nchini DRC na Jijila Guangzhou nchini China. Ufunguzi wa Konseli Kuuhizo unafanya Tanzania kuwa na jumla ya Balozi 43na Konseli Kuu tano (5) na hivyo kuiwezesha nchiyetu kunufaika zaidi na fursa za kiuchumi nakibiashara.

177. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoahuduma za kikonseli kama ifuatavyo:

i. Kurahisisha upatikanaji wa viza kwa maafisana watendaji wa Serikali, viongozi wa vyama

Page 104: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

98

vya siasa, waheshimiwa wabunge na taasisinyingine zinazostahili huduma hiyo;

ii. Balozi zetu zimeendelea kuratibu utoaji wa vizakwa raia wa nje wanaoitembelea Tanzania;

iii. Kuratibu uwasilishaji wa Hati za Utambulishoza mabalozi wapya kutoka nchi za Ireland,Italia, Marekani, Msumbiji, Namibia, Pakistan,Uingereza, Uswisi, Uturuki na Viet Nam;

iv. Kushirikiana na mamlaka nyingine kutafutaufumbuzi wa changamoto mbalimbalizinazowakabili Watanzania wanaoishi nje yanchi;

v. Kutatua changamoto na kulinda maslahi yaWatanzania wanaofanya kazi kwenye Balozimbalimbali na Mashirika ya Kimataifa hapanchini; na

vi. Kutoa huduma za kikonseli kwa Balozi zote zanje na Mashirika ya Kikanda na Kimataifayaliyopo hapa nchini.

178. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee,napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Wizara

Page 105: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

99

iliratibu na kufanikisha kuwarejesha nyumbaniWatanzania wapatao 5,360 waliokuwa wamekwamakatika nchi mbalimbali duniani kutokana na vizuizi vyasafari vilivyowekwa na nchi hizo kama njia ya kudhibitikuenea kwa ugonjwa wa UVIKO-19. Hatua hiiimesaidia kuokoa maisha ya nguvu kazi ya Taifahususan wale waliokuwa katika nchi ambazo ugonjwahuo umeenea kwa kiasi kikubwa.

4.5 Uratibu wa Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi(Diaspora)

179. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuratibu masuala yanayohusu jamii za Diaspora ilikuongeza mchango wao katika maendeleo ya Taifa.Kupitia jukumu hili, Tanzania imeendelea kunufaikana Diaspora ambapo kwa mujibu wa Benki Kuu yaTanzania fedha zilizotumwa na Diaspora nchini kwamwaka 2020 zilikuwa ni Dola za Marekani milioni189.13. Vilevile, katika kipindi hiki Diasporawamenunua nyumba kupitia Shirika la Nyumba laTaifa (NHC) zenye thamani ya shilingi milioni 423.8.

180. Mheshimiwa Spika, mwezi Agosti 2020,Wizara iliratibu kufanyika kwa mkutano wa Diasporawanaoishi Uingereza na Jamhuri ya Ireland uliokuwana kaulimbiu isemayo “Mtu Kwao Umoja Wetu Ndiyo

Page 106: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

100

Ngao Yetu”, uliofanyika kwa njia ya mtandao.Mkutano uliwezesha Diaspora na wadau kutoka sektaya umma na binafsi nchini kubadilishana taarifa zabiashara za huduma na bidhaa zinazozalishwa nchinikwa ajili ya kutafuta masoko nje ya nchi nakuwahamasisha Diaspora kuwekeza nchini.

4.6 Elimu kwa Umma

181. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoaelimu kwa umma kuhusu fursa za ajira, elimu,biashara, uwekezaji na utalii zitokanazo nauanachama wa Tanzania katika Jumuiya za Kikandana Kimataifa pamoja na mahusiano na nchi nyingine.Fursa hizo hutangazwa kupitia makongamano,mikutano, maonesho ya biashara, maadhimisho yasherehe za kitaifa na vyombo vya habari kama vilevituo vya runinga na redio, magazeti, majarida,machapisho, tovuti na mitandao ya kijamii.

182. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katikamaonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar esSalaam (Sabasaba) yaliyofanyika mwezi Julai 2020;maadhimisho ya siku ya wakulima (Nanenane)yaliyofanyika kitaifa mwezi Agosti 2020 Pemba,Zanzibar; na maonesho ya biashara wakati waMaadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya

Page 107: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

101

Zanzibar yaliyofanyika mwezi Januari 2021. Wakatiwa maonesho hayo, Wizara ilitoa elimu kuhusumajukumu yake pamoja na kusambaza machapishokwa wananchi kuhusu Sera ya Mambo ya Nje, 2001na fursa zinazotokana na Mtangamano wa AfrikaMashariki.

183. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba 2020,Wizara iliendesha semina kuhusu masuala yaMtangamano wa Afrika Mashariki na fursa zake kwawanafunzi 200 wa Shule za Sekondari za Dodoma naViwandani zilizopo jijini Dodoma. Wanafunzi haowalielimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na nafasiya Tanzania katika Mtangamano wa Afrika Masharikina nafasi yao kama vijana na viongozi wa baadayewa Taifa. Vilevile, Wizara iliandaa makala ya videoyenye kuonesha namna ilivyotekeleza Diplomasia yaUchumi na kurushwa na Shirika la UtangazajiTanzania (TBC) mwezi Novemba 2020.

184. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,Wizara ilishiriki kwenye kongamano lawafanyabiashara wanawake wa Tanzanialililoandaliwa na Chama cha WafanyabiasharaWanawake lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kupitiakongamano hilo, Wizara ilitoa elimu kwa wanawake120 walioshiriki, kuhusu fursa zilizopo katika

Page 108: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

102

Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nataratibu zinazopaswa kufuatwa ili kunufaika na soko laAfrika Mashariki na Soko Huru la Biashara la Bara laAfrika.

4.7 Utawala na Maendeleo ya Watumishi

185. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakusimamia masuala ya utawala na maendeleo yawatumishi kwa lengo la kuboresha na kuimarishautendaji wa kazi. Wizara ina jumla ya watumishi 455wa kada mbalimbali. Kati yao watumishi 228 wapoMakao Makuu ya Wizara na watumishi 227 wapokwenye Balozi za Tanzania. Katika kuimarishautendaji kazi wa Wizara, masuala mbalimbaliyanayohusu utawala na maendeleo ya watumishiyameendelea kusimamiwa kama ifuatavyo:

4.7.1 Uteuzi wa Viongozi

186. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania aliniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki na viongozi wenginewalioteuliwa ni kama ifuatavyo: Mheshimiwa BaloziMbarouk Nassor Mbarouk (Mb) kuwa Naibu Waziri;Mheshimiwa Balozi Joseph Edward Sokoine kuwaKatibu Mkuu; Mheshimiwa Balozi Fatma Mohammed

Page 109: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

103

Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu; na MheshimiwaYusuph Tindi Mndolwa kuwa Balozi na Mkuu waItifaki. Aidha, Mheshimiwa Rais ameteua Mabalozi 23watakaoiwakilisha nchi yetu katika mataifa mbalimbalina wengine kupangiwa majukumu hapa nchini.Naomba kutumia fursa hii kuwapongeza viongoziwenzangu kwa uteuzi huo na kuwasihi tuendeleekuchapa kazi kwa bidii, uzalendo na weledi ili kuletamaendeleo kwa Taifa letu.

4.7.2 Mafunzo

187. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021, Wizara imeendeleakuwajengea uwezo watumishi wake ambapo jumla yawatumishi 219 walihudhuria mafunzo ya muda mrefuna mfupi katika fani mbalimbali ndani na nje ya nchi.Watumishi wanane walihudhuria mafunzo ya mudamrefu na watumishi 211 walihudhuria mafunzo yamuda mfupi.

4.7.3 Upandishaji Vyeo

188. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021, jumla ya watumishi 194 wakada mbalimbali wamepandishwa vyeo.

Page 110: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

104

4.7.4 Kubadilisha Kada Watumishi

189. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021, watumishi 12 walibadilishwakada ndani ya Wizara. Kati ya watumishi hao, mmojaalibadilishwa kuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi;sita kuwa Maafisa Mambo ya Nje Daraja la II; watatukuwa Maafisa Utumishi Daraja la II; na mtumishimmoja kuwa Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II.

4.7.5 Uhamisho

190. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha utendaji kazikatika Utumishi wa Umma, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021 watumishi 17 walihamishwakwenda Wizara na Taasisi nyingine za Serikali nawatumishi 37 walihamia Wizarani kutoka Wizara naTaasisi nyingine za Serikali.

4.8 Kuratibu na Kusimamia Utekelezaji wa Miradiya Maendeleo ya Wizara na Taasisi Zilizo Chiniya Wizara

4.8.1 Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yaWizara

191. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2020/2021, Wizara ilitengewa bajeti ya maendeleo ya

Page 111: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

105

shilingi 20,000,000,000 kwa ajili ya kutekeleza miradiya maendeleo iliyopo ndani na nje ya nchi.

192. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakufuatilia Wizara ya Fedha na Mipango fedha za bajetiya maendeleo zilizotengwa kwa Mwaka wa Fedha2020/2021 baada ya kukamilisha nyaraka za miradihiyo kama taratibu zinavyoelekeza.

4.8.2 Utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi ZilizoChini ya Wizara

193. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Wizaraimeendelea kuzisimamia taasisi zilizo chini yakeambazo ni: Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(AICC); Chuo cha Diplomasia (CFR); na Mpango waHiari wa Afrika wa Kujitathmini katika Masuala yaDemokrasia na Utawala Bora (APRM) katikakutekeleza majukumu yao kama ifuatavyo:

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)

194. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Kituocha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)kimeendelea kuendesha biashara ya mikutano;upangishaji wa nyumba na ofisi; na kutoa huduma yaafya kupitia hospitali inayomilikiwa na kituo hicho.

Page 112: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

106

195. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2020/2021 Kituo kilipanga kukusanyamapato ya shilingi 16,001,559,000. Hadi mwezi Aprili2021, Kituo kilikusanya mapato ya shilingi7,970,640,495 sawa na asilimia 48 ya malengo.Mapato hayo yalitokana na:

i. Huduma za kumbi za mikutano (AICC na JNICC)- shilingi 2,608,160,544 kati ya lengo la shilingi6,339,350,000;

ii. Upangishaji wa ofisi na nyumba za kuishi -shilingi 2,995,497,441 kati ya lengo la shilingi4,956,540,000; na

iii. Huduma za hospitali - shilingi 2,366,982,510kati ya lengo la shilingi 4,705,669,000.

Sababu za kushuka kwa mapato ya Kituo nikupungua kwa idadi ya mikutano hali iliyochangiwakwa kiasi kikubwa na changamoto ya UVIKO-19.

196. Mheshimiwa Spika, vilevile katika kipindihicho, Kituo kilifanikiwa kutekeleza yafuatayo:

i. Kuhudumia mikutano 143 ya kitaifa na minne yakimataifa ambayo ilileta washiriki 46,811 wakitaifa na 3,621 wa kimataifa;

Page 113: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

107

ii. Kufanya matangazo kwa njia ya kielektroniki,magazeti na “screen” kwenye makutano yabarabara za jiji la Arusha, pamoja na kwenyemitandao ya kimataifa kwa ajili ya kuvutia watejawa ofisi na nyumba za kupangisha pamoja nakumbi na huduma za mikutano;

iii. Kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wapatao55,452;

iv. Kuhuisha mifumo ya kielektroniki na usimamiziwa taarifa katika nyanja za uhasibu, miliki nauendeshaji wa hospitali;

v. Kukamilisha taratibu za umiliki wa kiwanjachenye ukubwa wa ekari 15 katika Mji waSerikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma kwa ajiliya ujenzi wa Kituo cha kisasa cha mikutano; na

vi. Kukarabati majengo ya Kituo yaliyopo Arusha naDar es Saalam.

197. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2020 hadi Machi 2021, Kituo kilitoa shilingi150,000,000 kama gawio la awali kwa Serikali.

Page 114: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

108

Chuo cha Diplomasia (CFR)

198. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Chuocha Diplomasia kimeendelea kutoa mafunzo nakufanya tafiti katika masuala ya diplomasia, uhusianowa kimataifa, stratejia, usuluhishi wa migogoro naujenzi wa amani.

199. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2020/2021, Chuo kilitengewa kiasi cha shilingi5,805,064,000. Kati ya fedha hizo, shilingi2,427,064,000 ni Mishahara, shilingi 1,000,000,000kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na shilingi2,378,000,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Aidha, Chuo kilipanga kukusanya shilingi2,988,195,000.

200. Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2021,Chuo kilipokea shilingi 2,662,052,633.30 kutokaHazina. Kati ya fedha hizo, shilingi 1,828,719,300 nikwa ajili ya mishahara na shilingi 833,333,333.30 nikwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Pia, Chuokilikusanya jumla ya shilingi 2,041,033,718 sawa naasilimia 68.3 ya lengo la mwaka.

Page 115: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

109

201. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mweziJulai 2020 hadi Mei 2021, Chuo kilitoa mafunzo yamuda mfupi na mrefu kwa Wizara/Taasisi naMashirika ya Serikali, mashirika na kampuni binafsi,balozi na watu binafsi; na kutoa mafunzo ya lughasaba za kigeni ambazo ni Kiarabu, Kifaransa,Kihispania, Kiingereza, Kichina, Kikorea na Kireno.Aidha, Chuo kimekamilisha mtaala wa mafunzo yalugha ya Kiswahili kwa wageni. Vilevile, katika mwakawa masomo 2020/2021 Chuo kimedahili wanafunzi1,514 kutoka wanafunzi 1,280 kwa mwaka wamasomo 2019/2020, sawa na ongezeko la asilimia18.3. Chuo pia kilitoa mchango serikalini kiasi chashilingi 32,000,000.

Mpango wa Hiari wa Afrika wa Kujitathmini katikaMasuala ya Demokrasia na Utawala Bora (APRM)

202. Mheshimiwa Spika, APRM Tanzania ilifanyatathmini kuhusu utawala bora nchini na kuandaataarifa ya utekelezaji wa mpango wa APRM nchiniTanzania. Taarifa hiyo imeangazia maeneo makuumanne ambayo ni: Demokrasia na Siasa; Usimamiziwa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; naMaendeleo ya Jamii. Taarifa imeainisha mafanikioyaliyopatikana katika kipindi cha 2015 hadi 2019kama ifuatavyo:

Page 116: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

110

i. Kuongezeka kwa ufanisi wa utendaji kazi katikasekta ya utumishi wa umma na hivyokuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi;

ii. Kuongezeka kwa makusanyo ya Serikalikutokana na hatua zilizochukuliwa kuzibamianya ya ukwepaji kodi na kuimarisha elimukwa walipa kodi;

iii. Kuimarika kwa Taasisi za Kuzuia naKupambana na Rushwa (TAKUKURU naZAECA) pamoja na mapambano dhidi yarushwa;

iv. Kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali zamadini na kuanzisha masoko ya madini ilikukuza ushiriki wa wachimbaji wadogo wadogokatika mnyororo wa thamani, kuzuiautoroshwaji na usafirishaji wa madini ghafi njeya nchi; na

v. Kuimarika kwa miundombinu ya uchumi kamareli, barabara na nishati; na huduma za jamiihususan elimu na afya.

Page 117: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

111

203. Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba 2020,APRM Tanzania iliendesha warsha ya kitaifa yauhakiki wa taarifa ya utekelezaji wa mpango waAPRM nchini kwa lengo la kupata maoni. Warsha hiyoilishirikisha wadau wa sekta ya umma na binafsikutoka pande zote mbili za Muungano.

204. Mheshimiwa Spika, kikao cha 30 cha Wakuuwa Nchi na Serikali zinazoshiriki Mpango wa APRM,kilichofanyika mwezi Machi 2021 kwa njia ya mtandaokilimteua Mheshimiwa Balozi Ombeni Yohana Sefue,Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti waJopo la Watu Mashuhuri wa APRM, Barani Afrika(The Panel of Eminent Persons). Napenda kutumiafursa hii kumpongeza kwa uteuzi huo. Tuna imanikuwa uzoefu wake wa muda mrefu na umahiri katikamasuala ya diplomasia, utaendelea kuwa hazina narasilimali ya kipekee kwa maslahi ya nchi yetu naBara zima la Afrika.

205. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2020/2021, APRM Tanzania ilitengewa shilingi800,000,000. Hadi kufikia mwezi Aprili 2021, APRMTanzania ilipokea na kutumia shilingi 666,666,666.70sawa na asilimia 83.3 ya bajeti yake.

Page 118: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

112

5.0 CHANGAMOTO ZILIZOPO NA HATUAZILIZOCHUKULIWA

206. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza bajetiya Mwaka wa Fedha 2020/2021, pamoja na kuwepomafanikio ya kiutendaji, Wizara ilikabiliwa nachangamoto mbalimbali ikiwemo:

i. Upungufu wa watumishi ukilinganisha na wingiwa majukumu; na

ii. Sekta binafsi kutotumia ipasavyo fursa zabiashara na uwekezaji zitokanazo namtangamano wa kikanda na masoko ya kikandana kimataifa.

207. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto hizo, Wizara imechukua hatua zifuatazo:

i. Kuendelea kuwasiliana na Mamlaka ya Ajirakwa ajili ya kupata vibali vya ajira mpya naajira mbadala vya kujaza nafasi zilizo wazi; na

ii. Kuendelea kushirikiana na sekta binafsi, asasiza kiraia na vyombo vya habari katika kutoaelimu kwa umma juu ya fursa mbalimbalizitokanazo na ushiriki wetu katika

Page 119: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

113

mtangamano wa kikanda na masoko yakikanda na kimataifa.

6.0 SHUKRANI

208. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hiikuwashukuru Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi zaUmoja wa Mataifa pamoja na Mashirika ya Kimataifahapa nchini kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoakufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleoinayotekelezwa na Serikali yetu chini ya uongozimahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

209. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleakupata mafanikio kutokana na ushirikiano kutoka kwawadau mbalimbali na Washirika wa Maendeleo kutokanchi na asasi za kikanda na kimataifa. Naombanitumie fursa hii kuzishukuru nchi za Algeria,Australia, Austria, Brazil, Canada, China, Cuba,Denmark, Ethiopia, Finland, Hispania, Hungary, Italia,Iran, Ireland, Indonesia, India, Israel, Jamhuri yaKorea, Japan, Kuwait, Malaysia, Malta, Marekani,Mexico, Misri, Morocco, New Zealand, Nigeria,Norway, Oman, Pakistan, Poland, Qatar, Romania,Saudi Arabia, Singapore, Sri Lanka, Sweden, Sudan,Thailand, Tunisia, Ubelgiji, Uganda, Ufaransa,

Page 120: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

114

Uingereza, Uholanzi, Ujerumani, Urusi, Uswisi,Uturuki, Ureno, Umoja wa Falme za Kiarabu,Venezuela na Viet Nam kwa kuchangia mafanikiohayo muhimu kwa Taifa.

210. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa shukranipia kwa African Capacity Building Foundation (ACBF);Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); Benki ya Dunia;Investment Climate Facility for Africa; Mfuko waKimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD); Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DfID); Mfukowa Maendeleo wa Abu Dhabi (ADFD); Shirika laFedha la Kimataifa (IMF); Mfuko wa Maendeleo waKuwait (Kuwait Fund); Shirika la Nguvu za AtomikiDuniani (IAEA); Shirika la Maendeleo ya Kimataifa laSweden (SIDA); Shirika la Kimataifa la KuzuiaMatumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW); Ofisi yaMwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN RCO);Mfuko wa Kukuza Mtaji wa Umoja wa Mataifa(UNCDF); Programu ya Maendeleo ya Umoja waMataifa (UNDP); Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadiya Watu (UNFPA); Shirika la Umoja wa Mataifa laKupambana na UKIMWI (UNAIDS); Shirika la Umojawa Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO); Shirika laUmoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO); Shirika la Umoja wa Mataifalinaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR); Shirika la Kazi

Page 121: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

115

Duniani (ILO); Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamaji(IOM); Shirika la Umoja wa Mataifa la KuhudumiaWatoto (UNICEF); Shirika la Maendeleo la Kimataifala Israel (MASHAV); Shirika la Kimataifa la Maendeleola Japan (JICA); Shirika la Misaada la Marekani(USAID); Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea(KOICA); Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umojawa Mataifa (UNIDO); Shirika la Umoja Mataifalinaloshughulikia Masuala ya Wanawake(UNWOMEN); Shirika la Mazingira la Umoja waMataifa (UNEP); Shirika la Umoja wa Mataifa laBiashara na Maendeleo (UNCTAD); Shirika la Umojawa Mataifa Kuhusu Madawa ya Kulevya na Uhalifu(UNODC); Umoja wa Ulaya (EU); Shirika la AfyaDuniani (WHO); na Shirika la Mpango wa ChakulaDuniani (WFP). Vilevile, napenda kuwashukuru Benkiya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika(BADEA); Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB); Shirikala Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GiZ); GlobalFund; International Committee of the Red Cross;International Federation of the Red Cross and RedCrescent Societies; Sekretarieti ya Jumuiya yaMadola; Khalifa Fund for Enterprise Development(Khalifa Fund); Medecins Sans Frontieres; Mfuko waDunia wa Wanyama Pori (WWF); The Association ofEuropean Parliamentarians with Africa; The Bill andMelinda Gates Foundation;TradeMark East Africa

Page 122: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

116

(TMEA); Umoja wa Posta Duniani (UPU); Umoja waPosta Afrika (PAPU) pamoja na Mifuko na Mashirikambalimbali ya Misaada. Ni dhahiri kuwa ushirikianowao umekuwa na mchango mkubwa katikakufanikisha malengo ya Serikali.

211. Mheshimiwa Spika, kwa moyo mkunjufu,napenda kuwashukuru watendaji na watumishi waWizara na Taasisi zake kwa kuniwezesha kutekelezamajukumu yangu ipasavyo. Kwa namna ya pekee,napenda kumshukuru Mheshimiwa Balozi MbaroukNassor Mbarouk (Mb), Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Balozi JosephEdward Sokoine, Katibu Mkuu; Balozi FatmaMohammed Rajab, Naibu Katibu Mkuu; WaheshimiwaMabalozi wa Tanzania; Wakuu wa Idara na Vitengo;Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara; na watumishiwote kwa kufanya kazi kwa umahiri, weledi na ufanisikatika kunisaidia kutekeleza majukumu yangu yakulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu ndani na njeya nchi.

212. Mheshimiwa Spika, kipekee napendakuwashukuru Mhe. Prof. Palamagamba John AidanMwaluko Kabudi (Mb), aliyekuwa Waziri; Mhe. Dkt.Damas Daniel Ndumbaro (Mb) na Mhe. William TateOle Nasha (Mb) waliokuwa Naibu Mawaziri; Mhe.

Page 123: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

117

Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge aliyekuwa KatibuMkuu na Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji aliyekuwa NaibuKatibu Mkuu kwa mchango wao mkubwa katikakutekeleza majukumu ya Wizara katika Mwaka waFedha 2020/2021.

213. Mheshimiwa Spika, kwa nafasi ya pekeekabisa, napenda kumshukuru mume wangu mpendwaMhandisi Dkt. George Steven Mulamula; watotowangu pamoja na familia yangu kwa ujumla kwauvumilivu wao na kuwa karibu nami wakati wote wakutekeleza majukumu yangu ambayo wakatimwingine yananilazimu kuwa mbali nao kwa mudamrefu.

7.0 MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WAFEDHA 2021/2022

214. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2021/2022, Wizara imeweka kipaumbele katikakutekeleza majukumu yafuatayo:

i. Kuendelea kutekeleza diplomasia ya uchumiikiwa ni pamoja na kuwezesha balozi zetukuwa kiungo muhimu cha kukuza uwekezaji,upatikanaji wa masoko ya bidhaa na hudumazinazozalishwa nchini na kuvutia watalii;

Page 124: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

118

ii. Kuendelea kuboresha na kuimarisha uhusianona nchi nyingine, jumuiya za kikanda namashirika ya kimataifa;

iii. Kuendelea kuweka mazingira wezeshi, kuratibuna kuhamasisha ushiriki wa Watanzaniawanaoishi nje ili kushiriki kikamilifu katikakuchangia maendeleo ya nchi;

iv. Kuendelea kulinda na kutetea misingi ya Taifaletu ndani na nje ya nchi;

v. Kuendelea kushawishi na kuhamasishamatumizi ya lugha ya Kiswahili kwa nchi mojamoja, jumuiya za kikanda na kimataifa;

vi. Kuendelea kushiriki katika juhudi za kulinda nakuimarisha amani duniani na maendeleokupitia Umoja wa Mataifa;

vii. Kuendelea kujenga na kukarabati majengo kwaajili ya balozi zetu ili kupunguza gharama nakuleta mapato kwa Serikali;

viii. Kuendelea kufungua ofisi za Balozi na KonseliKuu mpya katika nchi za kimkakati;

Page 125: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

119

ix. Kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarishautangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika (SADC);

x. Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusuutekelezaji wa majukumu ya Wizara, masualaya uhusiano wa kimataifa na utangamano wakikanda;

xi. Kuendelea kusimamia utekelezaji wamajukumu ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara;na

xii. Kuendelea kusimamia rasilimali watu na fedhaMakao Makuu ya Wizara na Balozini.

8.0 MALENGO YA TAASISI ZILIZO CHINI YAWIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(AICC)

215. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2021/2022, Kituo kimepanga kukusanyamapato ya shilingi 17,763,743,153. Kati ya mapato

Page 126: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

120

hayo, shilingi 16,202,606,216 ni kutoka vyanzo vyandani vya mapato na shilingi 1,561,136,937zitatokana na mkopo. Fedha za mkopo ni kwa ajili yakugharamia nyongeza ya mradi wa jengo la wagonjwawa nje la Hospitali ya AICC, ununuzi wa vifaa tibapamoja na gharama za awali za kujenga jengo labiashara jijini Arusha.

216. Mheshimiwa Spika, Kituo kinaendeleakufanya taratibu za kuanza ujenzi wa Kituo chamikutano kitakachoitwa Mount KilimanjaroInternational Convention Centre (MK-ICC) jijiniArusha. Kituo hicho kitaimarisha na kuongeza kasi yautekelezaji wa diplomasia ya mikutano na maoneshohapa nchini.

Chuo cha Diplomasia (CFR)

217. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2021/2022 Chuo kimepanga kukusanya shilingi3,511,965,000 kutoka katika vyanzo vya ndani. Aidha,Chuo kinatarajia kutekeleza majukumu yafuatayo:

i. Kuendelea kutoa mafunzo ya mahusiano yakimataifa; lugha ya Kiswahili kwa wageni; nambinu za kidiplomasia;

Page 127: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

121

ii. Kuendelea kufanya tafiti katika maeneo yamahusiano ya kimataifa na mbinu zakidiplomasia;

iii. Kutathmini matokeo ya mafunzo yaliyotolewana mipango ya mafunzo kwa ujumla;

iv. Kuendelea na ujenzi wa vyumba vyamihadhara kwa lengo la kuongeza udahili namapato ya Chuo; na

v. Kuendelea kutoa ushauri na huduma zakitaalamu kwa Serikali na Taasisi zake.

Mpango wa Hiari wa Afrika wa Kujitathmini katikaMasuala ya Demokrasia na Utawala Bora (APRM)

218. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2021/2022, APRM inatarajia kutekelezavipaumbele vifuatavyo:

i. Kuendelea kufanya tathmini za utawala bora zampango wa APRM ikiwa ni pamoja nakuhuisha mbinu za utafiti kwa kupitia upyahojaji ya APRM;

Page 128: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

122

ii. Kuboresha viashiria vya utafiti, kuzingatiamatumizi ya teknolojia katika utekelezaji waMpango na kupanua wigo wa zanazinazotumika katika utafiti;

iii. Kuratibu utekelezaji wa Mpango Kazi waAPRM kwa kushirikiana na Wizara, Idara naWakala za Serikali katika kuandaa taarifa yamwaka na kuweka mfumo madhubuti waufuatiliaji; na

iv. Kuimarisha mawasiliano na utoaji taarifakuhusu Mpango wa APRM kwa kuendeleakutekeleza Mpango wa Mawasiliano wa MiakaMitano 2021/2022–2025/2026.

9.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAWIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

219. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2021/2022, Wizara inatarajia kukusanya kiasi chashilingi 2,550,879,000 ikiwa ni mapato ya Serikaliyatakayopatikana kutokana na vyanzo vilivyopoMakao Makuu ya Wizara na Balozi za Tanzaniaambavyo ni pango la nyumba za Serikali zilizopo njeya nchi na kuthibitisha nyaraka.

Page 129: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

123

220. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha2021/2022, Wizara imetengewa bajeti ya kiasi chashilingi 192,265,438,000. Kati ya fedha hizo shilingi178,765,438,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaidazinazojumuisha shilingi 167,937,219,000 kwa ajili yaMatumizi Mengineyo; shilingi 10,828,219,000 kwaajili ya Mishahara; na shilingi 13,500,000,000 ni kwaajili ya Miradi ya Maendeleo.

221. Mheshimiwa Spika, kati ya fedha za bajeti yaMatumizi Mengineyo ya Wizara, shilingi 800,000,000ni kwa ajili ya Mpango wa Hiari wa Afrika waKujitathmini katika Masuala ya Demokrasia naUtawala Bora (APRM), shilingi 1,000,000,000 ni kwaajili ya Chuo cha Diplomasia (CFR), shilingi1,280,000,000 ni kwa ajili ya Mahakama ya Afrika yaHaki za Binadamu na Watu (ACHPR) na shilingi170,000,000 ni kwa ajili ya Bodi ya Ushauri waMasuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika (AUABC).Aidha, kati ya fedha zilizotengwa kwa ajili yaMishahara, shilingi 2,202,193,800 ni kwa ajili yamishahara ya Chuo cha Diplomasia.

222. Mheshimiwa Spika, kati ya shilingi13,500,000,000 zilizotengwa kwa ajili ya kutekelezamiradi ya maendeleo, shilingi 6,500,000,000 ni kwaajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa ofisi ya ubalozi

Page 130: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

124

na kitega uchumi ubalozi wa Tanzania Kinshasa,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; shilingi5,000,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makaziya Balozi, ubalozi wa Tanzania Muscat, Oman;shilingi 1,000,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi wamakazi ya Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia;na shilingi 1,000,000,000 ni kwa ajili ya kuendelezaujenzi wa vyumba vya mihadhara katika Chuo chaDiplomasia.

10.0 HITIMISHO

223. Mheshimiwa Spika, ili kuweza kutekelezakikamilifu majukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha2021/2022, naomba Bunge lako Tukufu liidhinishejumla ya shilingi 192,265,438,000. Kati ya fedha hizoshilingi 178,765,438,000 ni kwa ajili ya Matumizi yaKawaida na shilingi 13,500,000,000 ni kwa ajili yaBajeti ya Maendeleo.

224. Mheshimiwa Spika, naomba kutumia nafasi hiiadhimu kukushukuru tena wewe binafsi, MheshimiwaNaibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wote kwakunisikiliza.

225. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Page 131: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

125

Page 132: YALIYOMO - in.tzembassy.go.tz

126