somo 1 kwa ajili oktoba 6, 2018 - fustero.es · umoja na maelewano aliokuwa ameupanga mungu kwa...

9
Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018

Upload: buihanh

Post on 02-Mar-2019

302 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018

Page 2: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

“Akamleta nje, akasema, Tazamasasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwauzao wako. Akamwamini Bwana, nayeakamhesabia jambo hili kuwa haki” (Mwanzo 15:5-6)

FUNGU LA KUKARIRI

Page 3: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

1. Umoja wa Kwanza

Kuumbwa ili kupenda

2. Umoja wa wavujika

Tangu Adam hadi Gharika

Mnara wa Babeli

3. Kuurejesha Umoja

Mungu amuita Adamu

Israeli ya chaguliwa

Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajiliya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungualionesha upendo wake kwetu kwa kubuni mpango wakurejesha umoja huu. Urejeswaji wa mwisho ungekujakupitia kazi ya Kristo, lakini Mungu aliwachagua wanadamuwaoneshe upendo na neema yake kwa ulimwengu.

Page 4: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

Mungu aliumba kila kitu kikiwa “chemasana” (Mwanzo 1:31). Dunia, wanyama nawanadamu wakihusiana mmoja kwamwingine kwa amani.

Wanadamu, tofauti na wanyama, waliumbwa kwa sura ya Mungu. Walifanywa kuwa mawakili wa uumbaji.

Mungu ni upendo (1 Yohana 4:8), Hivyo sura yaMungu hujumuisha uwezo wa kupenda.

Sura ya Mungu ili tengenezwa na watu wawili, mwanaume na mwanamke. Kwa pamojawaliubwa kwa sura ya Mungu.

Huo ni umoja wenye upendo katika Msingi wake.

Page 5: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

“Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani] Ikawa walipokuwapouwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.” (Mwanzo 4:8)

Dhambi ya Adamu na Hawa iliharibu maelewano, umoja na upendo kati yamwanaume na mwanamke, Jamii ya wanadamu na uumbaji, Jamii ya wanadamu naMungu.

Mwanaumealimlaumumwanamke

(Mwanzo 3:12)

Asiliikaharibika

(Mwanzo3:17-18)

Kainiakamuua

Habili(Mwanzo 4:8)

Mwanadamuakaharibika

kabisa(Mwanzo 6:5)

Gharikalikaweka

ukoma wahistoria ya

mwanadamu(Mwanzo 6:7)

Hata hivyo, Mungu alichagua waliosalia (Nuhu na familia yake) na kuwapa wanadamu nafasi ya pili. Upinde wa mvua hutusaidiakukumbuka kuwa Mungu bado anataka kutimiza mpango wake wa awali kwa ajili yetu.

Page 6: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

MNARA WA BABELI“Kwa sababu hiyo jina lake likaitwaBabeli; maana hapo ndipo Bwana

alipoichafua lugha ya dunia yote; nakutoka huko Bwana akawatawanya

waende usoni pa nchi yote.”(Mwanzo 11:9)

Wanadamu walijaribu kutafuta umojabila Mungu. Hii ilipelekea ibada yasanamu na kujitukuza wenyewe.

Mungu alilazimika kuukomesha umojahuo wa uongo kwa kuumba lugha tofauti.

Dhambi ilileta ukosefu wa umojamiongoni mwa wanadamu na kuharibikakwa mpango wa mungu wa awali. Dhambi ilisababisha:

Machafuko kwenye ibada.

Kusambaa kwa kasi kwa uovu naukosefu wa maadili juu ya nchi.

Kugawanyika kwa wanadamukatika tamaduni, lugha na rangi.

Page 7: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

Alikuwa mtiifu.

Tumaini lake lilijengwa juu ya ahadiya Mungu.

Aliamini kuwa Mungu angetimizaahadi yake; Uzao kama nyota zaangani.

Aliuamini mpango wa Mungu wawokovu.

“Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwakwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.”

(Yakobo 2:23)

Mungu alijaribu kurejeshaumoja tena kupitia kwaIbrahimu.

Ibrahimu ni baba wawaamino wote. Tunawezakujifunza dhana za msingiza umoja miongoni mwawakristo katika kielelezochake:

Page 8: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

“Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kulikomataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu…”(Kumbukumbu la Torati 7:7-8)

Mungu aliwachagua Israeli kama watuwake kwa sababu aliwapenda. Hawakuwa wamefanya lolote la kuwafanya wafae kuchaguliwa.

Mungu alitaka kupeleka ujumbe wake kwa ulimwengu na kuwakomboawanadamu kupitia kwa Israeli.

Aliwapa nyenzo zote za kirohowalizohitaji ili kutimiza kusudi hilo.

Kanisa la kikristo ni Israeli mpya. Ni lazima tuelewe kuwa hatuna chakujivunambele yake(Mungu). Mungu alituchaguaili tuwe wamoja na yeye kwa sababu tuanatupenda (Wagalatia 3:28)

Page 9: Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018 - fustero.es · Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu

“Hoja yenye ushawishi zaidi tunayoweza kutoa kwa

ulimwengu kuhusu utume wa Kristo ni kuonekana

katika umoja mkamilifu. Umoja kama ulio kati ya Baba

na Mwana unapaswa kudhihirishwa miongoni mwa wote

wanao iamini kweli. Wale walio na umoja hivyo katika

utii dhati kwa neno la Mungu watajazwa nguvu.

Kama wote wangejiweka wakfu kwa Bwana, na kupitia

utakaso wa ile kweli wakiishi katika umoja mkamilifu,

Nguvu ya ushawishi ingeambatana na utangazaji wa hiyo

kweli! Ni huzuni iliyoje kwamba makanisa mengi

yanapotosha ule msukumo utakasao wa ile kweli, kwa

sababu hawaidhihirishi ile neema iokoayo ambayo

ingewafanya wawe wamoja pamoja na Kristo, kama

Kristo alivyo na umoja na Baba! Kama wote wangefunua

umoja na upendo unaopaswa kuwepo miongoni mwa

ndugu, Nguvu ya Roho mtakatifu ingejidhihirisha katika

msukumo wake uokao. Kwa uwiano na umoja wetu na

Kristo ndivyo itakavyokuwa nguvu yetu ya kuokoa

roho.” E.G.W. (Manuscript 88, 1905, “One, Even as We Are One”)