1.0 utangulizi unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. na sasa naendesha...

8
1 Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu 1.0 UTANGULIZI Kitabu hiki kinafafanua sehemu ya kazi za Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wanawake kupitia usuluhishi na mahakama. Kitabu hiki kina lengo la kuelimisha wanawake kupitia kesi za mfano zilizosimamiwa na kituo cha msaada wa Sheria kwa wanawake ili kuwatia moyo wanawake wawe wajasiri na wasikate tamaa katika kutafuta na kusimamia haki zao licha ya changamoto wanazokabiliana nazo. Licha ya kuelimisha, kitabu hiki kinalengo la kuainisha changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanakabiliana nazo katika kufuatilia haki zao ikiwemo kesi kuchukua muda mrefu, ugumu wa maisha unaosababisha wanawake walio wengi washindwe kuhudhuria kesi zao; pamoja na kutengwa, kukosa msaada au kukataliwa na ndugu na jamaa wa karibu.

Upload: others

Post on 06-Nov-2020

15 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

1

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

1.0 UTANGULIZI

Kitabu hiki kinafafanua sehemu ya kazi za Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wanawake kupitia usuluhishi na mahakama.

Kitabu hiki kina lengo la kuelimisha wanawake kupitia kesi za mfano zilizosimamiwa na kituo cha msaada wa Sheria kwa wanawake ili kuwatia moyo wanawake wawe wajasiri na wasikate tamaa katika kutafuta na kusimamia haki zao licha ya changamoto wanazokabiliana nazo.

Licha ya kuelimisha, kitabu hiki kinalengo la kuainisha changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanakabiliana nazo katika kufuatilia haki zao ikiwemo kesi kuchukua muda mrefu, ugumu wa maisha

unaosababisha wanawake walio wengi washindwe kuhudhuria kesi zao; pamoja na kutengwa, kukosa msaada au kukataliwa na ndugu na jamaa wa karibu.

Page 2: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

2

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

2.1 Kuanzisha Biashara baada ya kushinda kesi

Mimi ni mama wa watoto wawili; nilibarikiwa kufunga ndoa na mume wangu mnamo mwaka 2004 niliishi maisha ya raha na furaha. Lakini ndoto hiyo ilifikia ukomo mnamo mwaka 2011 ambapo mume wangu aliamua kuoa mke mwingine licha ya kwamba tulikuwa na ndoa ya kanisani.Nilipata wakati mugumu sana pale ambapo mume wangu alinifukuza kwenye nyumba ya ndoa tuliokua tunaishi. Sikuwa na pakukimbilia niliona maisha machungu na nilikuwa nikilia usiku na mchana. Kitu ambacho kilinikosesha usingizi ni kwamba niliona kama ni ndoto.

Nilipeleka tatizo langu kanisani na kwa ndugu ili kupata ufunbuzi ila mume wangu hakukubali ushauri wala kusuluhishwa.

Nilipata nafasi kusikia habari za Kituo cha Msaada wa Sheria (WLAC) kupitia mkutano wa kijiji na ndipo niliamua kwenda kupata ushauri.

WLAC walinisaidia kunifafanulia haki mbalimbali na kunielekeza jinsi gani ninaweza kupata haki zangu kupitia Sheria za nchi. Nilipata ujasiri baada ya kupata ushauri na pia kuona wanawake wenzangu ambao pia wanatafuta haki zao.

Nilifuatilia kesi Mahakama ya Mwanzo na mnamo tarehe 12 Agosti 2014 nilipata haki yangu na sasa naishi na watoto wangu. Nimeweza kuanzisha biashara ndogondogo zinazoniingizia kipato cha kujikimu.

Page 3: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

3

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

2.2 Kupata haki baada ya Ndoa kuvunjika

Jina langu ni ‘X’ tulifunga ndoa na mume wangu tarehe 19/6/2004 na ndoa ilidumu kwa miaka minne mpaka 2008 ambapo mume wangu alinitelekeza na kwenda kuishi na mwanamke mwingine. Baada ya hapo nilimuomba mume wangu tugawane mali ambazo tulichuma wote wakati tunaanza maisha.

Alikataa kufanya hivyo ndipo nikaamua kwenda WLAC kupata msaada wa kisheria.WLAC walinipa msaada na ushauri wa kisheria na kunielimisha zaidi kuhusu haki zangu kama mwanandoa, ambayo ilinisaidia kutoa ushahidi tosha kwa kesi yangu hadi kushinda na mwisho mahakama iliamuru nipewe kiwanja na nyumba iliyokuepo Mbezi Msuguli. Bila msaada wa Sheria nisingeweza kupata haki yangu.

Page 4: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

4

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

Rafiki yangu mmoja alinielekeza katika Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) ambako nilipeleka shauri langu.

Namshukuru Mungu nilipewa msaada wa Sheria na kuandaliwa nyaraka za Mahakama za kudai talaka na kugawana mali ambayo ni nyumba. Katika utetezi wake mume wangu alikuwa ameshabadilisha nyaraka za umiliki wa nyumba na kumwandika ndugu yake. Bahati nzuri nilikuwa nina nakala za zile nyaraka za mwanzo ambazi ziliniwezesha kuthibitisha madai yangu Mahakanani na kuweza kupata haki yangu Mahakani iliamru nyumba iuzwe na nikapewa asilimia hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema.

3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA

Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye ndoa kwa miaka 22. Sikubahatika kupata mtoto.

Awali maisha yangu hayakuwa mazuri kwa sababu mimi na mume wangu tulikuw na kipato cha chini sana. Licha ya ufinyu wa kipato chetu tuliishi kwa kuheshiminana furaha tele. Tuliendelea kufanya vibarua na biashara ndogo ndogo na hatimaye Mwenyezi mungu alitujalia mtaji ukakua na tukanunu kiwanja na kujenga nyumba.

Tulimshukuru Mungu kwa uwezo wake. Baada ya kujenga nyumba na kupata mali maisha yalianza kubadilika, mume wangu alianza kutoa maneno ya kashifa kwangu kuwa sizai watoto. Nilijitahidi kwenda hospitalin lakini sikufanikiwa. Hali ilizidi kuwa mbaya maana mausi na vipigo viliniandama na baaadae nilifukuzwa kwenye nyumba ya ndoa. Nilipeleka malalamiko kwa ndugu ambao pia hawakunisaidia. Wengine walidiriki kusema ni kweli mume anahitaji faraja ya watoto.

Page 5: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

5

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

Barua ya Ushuhuda wa Mteja

Page 6: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

6

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

Page 7: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

7

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

Msaada wa Sheria kwa njia ya simu ni mkakati madhubuti wa kuifikia jamii iliyo pembezoni.

“Uvumilivu na kutokata tamaa ni njia pekee ya kufikia mafanikio”

Page 8: 1.0 UTANGULIZI unaosababisha wanawake walio wengi ......hamisini (50%) ya mauzo. Na sasa naendesha maisha yangu vyema. 3.0 UMUHIMU WA KUHIFADHI NYARAKA Mimi ni mwanamke nilieishi kwenye

8

Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu

KWA MSAADA ZAIDI WA SHERIAONGEA MOJA KWA MOJA

NA WANASHERIA WA KITUO CHA MSAADA WA SHERIA KWA WANAWAKE BURE PIGA

SIMU BURE:-

0800780100

MUDA: Jumatatu mpaka Alhamisi: Saa 2:30 Asubuhi mpaka 11:00 jioni

Ijumaa: Saa 2:30 Asubuhi mpaka 9:30 Alasiri