12 aprili, 2013 mrema 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-hs-11-4-2013.pdf2 12...

136
1 12 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Nne - Tarehe 12 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 25 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) MHE. FAKHARIA KHAMIS SHOMAR (K.n.y. MHE. TAUHID C. GALLOS) aliuliza:- Mradi wa TASAF unasimamiwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Je, kwa upande wa Zanzibar, Mradi wa TASAF unasimamiwa na Wizara gani?

Upload: others

Post on 29-Oct-2019

0 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

1

12 APRILI, 2013

BUNGE LA TANZANIA________________

MAJADILIANO YA BUNGE___________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Nne - Tarehe 12 Aprili, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

MASWALI NA MAJIBU

Na. 25

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

MHE. FAKHARIA KHAMIS SHOMAR (K.n.y. MHE. TAUHID C.GALLOS) aliuliza:-

Mradi wa TASAF unasimamiwa kwa ushirikiano wapamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar.

Je, kwa upande wa Zanzibar, Mradi wa TASAFunasimamiwa na Wizara gani?

Page 2: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

2

12 APRILI, 2013

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU) alijibu:-

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,mradi wa TASAF unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa piliwa Rais wa Zanzibar. Mkurugenzi wa Uratibu katika ofisi hiyondiye anayehusika na uratibu wa shughuli zote za TASAF chiniya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar.

TASAF imeingia mkataba wa makubaliano (MoU) naKatibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa kujiridhishakuwa utekelezaji wake unazingatia malengo ya mradi. Vileviletuna Kamati za Uongozi Unguja na Pemba ambazo zinapitishamaombi ya miradi yote ya wananchi kutoka maeneo hayo.

MHE. FAKHARIA KHAMIS SHOMAR: Mheshimiwa Spika,kwa nini Wabunge walioko Zanzibar hawaingii katika vikaovya TASAF ina maana hayo ndiyo makubaliano ya Serikalizote mbili?

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Mheshimiwa Spika, kama ilivyo utaratibu TanzaniaBara Waheshimiwa Wabunge wanaotoka Visiwani niWajumbe wa Kamati hizo kama hawaudhurii basi ni matatizoyanatokana na utaratibu. Lakini tutawasiliana na Ofisi yaMakamu wa Pil i wa Rais i l i kuona kuwa Wabungewanahusishwa katika Kamati zinazohusika.

Na. 26

Huduma ya Maji Safi na Salama Vijijini

MHE. ENG. ATHUMAN R. MFUTAKAMBA aliuliza:-

Mradi wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria mpakaTabora linapitia Wilaya ya Uyui jirani na Jimbo la Igalula:-

Page 3: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

3

12 APRILI, 2013

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuunganisha hudumahiyo na Kata jirani za Kigwa na Igalula katika vijiji vyaKinamagi, Mbuyuni, Kigwa na katika kata ya Igalula vijiji vyaIgalula Barazani na Igalula Stesheni ambako kuna kero kubwaya maji.

(b) Je, ni lin i Serikali itavipatia huduma ya maji vijiji 48Jimboni Igalula kati ya vijiji 54 vilivyopo umbali wa zaidi yakm.12.5 kutoka bomba linalotoka Ziwa Victoria.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mhandisi AthumanRashid Mfutakamba, Mbubge wa Igalula lenye sehemu (a)na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo;-

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango wa kuvipatiamaji vijiji vyote vilivyopo umbali wa kilomita 12 kutoka bombakuu litakalopeleka maji mjini Tabora kutoka Ziwa Victoria.

Kwa sasa Serikali ipo kwenye utaratibu wa kumpatamtaalamu mshauri atakayefanya kazi ya usanifu wa mradihuo kwa aji l i ya ujenzi.Makampuni yaliyowasil ishamapendekezo yao ya kiufundi na kifedha tarehe 27Aprili,2013. Baada ya usanifu kukamilika na njia ya bombakuu kujulikana,vijiji vitakavyopatiwa maji kutoka bomba hilovitajulikana.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa mpango wa Serikalikulingana na uwezo uliopo ni kuvipatia maji vijiji vilivyo umbaliwa kilomita 12 kwa kila upande wa bomba kuu. Serikaliitafanya utafiti wa kujiridhisha kama maji yaliyopo yatawezakuhudumia vijiji vilivyopo umbali wa zaidi ya kilomita 12.

MHE. ENG. ATHUMAN R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaSpika, ninashukuru kwa majibu mazuri yanayotoa matumainikwa wananchi wa Jimbo la Igalula.

Page 4: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

4

12 APRILI, 2013

Pamoja na hayo nina maswali madogo mawili yanyongeza pamoja kupata maji kila mahala Jimboni Igalulalakini hakuna tone la maji ya kunywa.

Mheshimiwa Waziri anaweza kutuambia jeinawezekanaje Kata hizo 10 zipunguze adha hii ya upungufuwa maji?

Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui Isikizya wananchina Watumishi hawana maji kabisa sasa kuna mpango ganikwa wananchi na watumishi wa Isigizya Wilaya ya Uyuikuweza kupata huduma ya maji na kero hii iondokaneahsante?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naombakujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mfutakamba,swali lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Kuhusu suala la kuzipatia Kata zake miraji ya majikwa kutengeza mabwawa ni kwamba Wizara ya Majiinachofanya ni kutoa mwongozo, kutoa fedha na kutoaufundi kwa Halamsahuri zetu na mahali pengine.

Mipango inaanzia katika ngazi za vijiji, ngazi ya Katana ngazi ya Wilaya na katika ngazi ya Wilaya MheshimiwaMbunge ni Mjumbe wa Baraza la Madiwani, ambaowanaweza kupitisha mipango na pale watakapokuwawamepisha Serikali kupitia Wizara ya Maji itakuwa tayarikuwapa ufundi na kutoa fedha kwa kujenga mabwawahayo.

(b) Kuhusu suala la matatizo ya maji katika MakaoMakuu ya Wilaya ni kweli tunayo miji ya Makao Makuu yaWilaya ipo mingi kwa Wilaya zote 136, na Miji mikubwa namidogo kwa kasi ina matatizo ya maji. Serikali ina mpangona imeanza mwaka huu kuainisha baadhi ya Miji kuipatiamaji na baadae itaenda Mji baada Mji kuhakikisha kuwawananchi wanapata maji ya kutosha.

Page 5: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

5

12 APRILI, 2013

MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Spika, vijijivilivyo karibu na bomba vitapatiwa maji, sasa mpango huuwa maji unategemea kupelekwa mpaka Jimbo la Igungaambalo ni kame. Lakini Jimbo la Igunga linapakana na vijijikaribu kabisa vilivyo na ukame mkubwa kama Kizonzo, Msekona Malendi.

Je, Serikali inaweza kuviunganisha na vyenyewekatika huo mpango?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: MheshimiwaSpika,tunachosema ni kwamba Serikali itakuwa tayarikupeleka maji katika vijiji vyote ambavyo viko umbali wakilomita 12 umbali wa bomba kuu maana awali ilikuwa nikilomita 5.

Lakini cha pili ni kwamba ili tuvipelekee vijiji hivyo nilazima sasa bomba linalotoka Ziwa Victoria tupime kuwausanifu unafanyika na ukishafanyika utaonyesha kuwabomba litapita katika njia ipi.

Mheshimiwa Spika, sasa kama litapita kwenye njiaambazo vijiji hivyo vipo ni dhahiri kabisa kuwa vitapewa maji.

MHE.MCH LUCKSON.N. MWANJALE: Mheshimiwa Spika,tataizo la usambazaji maji vijijini ni tatizo kubwa kwa nchinzima na kwangu kule pia kuna vijiji ambalo miradi ilitakiwakutekelezwa lakini imeshindikana.

Je, Serikali imetenga fedha za kutosha mwaja huukuhakikisha kuwa vijiji hivi vinapata maji?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kwelikuwa lipo tatizo la maji nchi nzima na hasa maji vijijini naSerikali kupitia Wizara ya Maji iliweka Sera na kuweka programya utekelezaji wa miradi hii ambayo tulianza kwa vijijikumikumi katika kila Halmashauri.

Page 6: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

6

12 APRILI, 2013

Kwa hiyo nimuombe Mheshimiwa Mbunge kuwa ilitupate fedha za kutosha yeye ni mmoja wa watakao pitishabajeti yetu kuiwezesha iweze kutekeleza miradi hiyo ya majikatika vijiji vingi.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, mradi wamaji bomba kutoka Ziwa Victoria umeonyesha mafanikiomakubwa sana Mikoa ya Kanda ya Ziwa, na kwasababu hiyokwa vile sasa maeneo ya Wilaya za Mbozi, Mwomba na Ilejena hasa Miji ya Tunduma kuna shida kubwa ya maji.

Serikali haioni kuwa sasa kuiga mtindo wa kuchukuamaji kutoka Ziwa Victoria ikaenda sasa kuchukua maji kutokaZiwa Rukwa kwa ajili ya kuondoa tatizo na kero kubwa katikamaeneo hayo?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, niseme tukuwa wazo lake ni zuri wao vilevile wana nafasi ya kulifanyiawazo hili katika vikao vyao vya RCC ambavyo vikitoka palevinakuja kwetu linakuwa ni wazi la pamoja na hii inawezakufanyika baada ya kuona kwamba hakuna njia zinginembadala za kiteknolojia mbadala katika yale maeneokwamba hawataweza kupata maji kwa urahisi zaidi tutafikiahiyo ya kutumia Ziwa Rukwa.

SPIKA: Kwa dakika tano tumekuwa na maswali yanyongeza manne kwa sababu ni mafupi na majibu ni mafupindivyo inavyotakiwa Swali linalofuata ni Mheshimiwa SilvetryFrancis Koka.

Na. 27

Tatizo la Maji Kibaha- Mjini

MHE. SILVESTRY F.KOKA aliuliza:-

Halmashauri ya Mji wa Kibaha ina ardhi yenyemiamba isiyofaa kwa upatikanaji wa maji ya visima na hatayakipatikana ni machache na yana chumvi nyingi hivyokuifanya Halmsahuri kutofaidika na miradi ya visima:-

Page 7: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

7

12 APRILI, 2013

Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kuipatiabomba kubwa la peke yake Mamlaka ya Maji ya Halmashauriya Kibaha kama njia mbadala ya kutatua tatizo la maji katikajimbo hili.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Majininaomba kujibu swali la Mheshimiwa Silvestry Francis Koka,Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa Mji wa Kibaha unashida kubwa ya maji. Kwa kiasi kikubwa Mji wa Kibahaunategemea maji yanayotoka Mtambo wa Ruvu Juuunaoendeshwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar essalaam (DAWASCO).

Chanzo hicho cha Ruvu juu kinahudumia pia Mjimdogo wa Mlandizi pamoja na vijiji vya Visiga, Misugusugu,Kongowe, Soga, Kwa mfipa, Simbani, Mwendapole, KwaMathias, Msangani na Picha ya Ndege, ambavyo vikokandokando ya mabomba makuu yanayotoka Ruvu juukwenda kwenye matanki ya Kimara – Dar es salaam. Sababukubwa ya kutotosheleza kwa huduma ya maji kwenye eneolote linalohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu ni uwezomdogo wa uzalishaji pamoja na upotevu mkubwa wa maji.Mtambo huu ulijengwa mwaka 1956 na ulilenga kuhudumiawatu laki nane (800,000) lakini kwa sasa unahudumia watutakribani milioni mbili.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali inakamilishataratibu za zabuni kwa ajili ya upanuzi wa mtambo wa RuvuJuu ili kuongeza uwezo wake kutoka kuzalisha wa lita milioni82 kwa siku za sasa hadi lita milioni 196 kwa siku. Upanuzihuo utahusisha ujenzi wa kitekeo cha maji kipya (intake) naulazaji wa bomba jipya kutoka Mlandizi hadi Dar es salaam.

Mabomba mawili yaliyopo sasa yatafanyiwaukarabati na yatatumika kusambaza maji kwenye vijiji vyakandokando ya bomba kuu na maeneo mengine ikiwemo

Page 8: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

8

12 APRILI, 2013

Mji wa Kibaha. Bada ya upanuzi huo kukamilika, Mji waKibaha utapata huduma za maji kwa masaa 24 kwa siku.

MHE. SILVESTRY F.KOKA: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu mazuri ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili yanyongeza:-

(a) Mheshimiwa Spika, ningependa Serikali iwezekuwapa majibu wananchi wa Kibaha sasa ni lini huu mradiwa maji utakamilika na ni lini sasa Mheshimiwa Waziri yukotayari kutembelea Jimbo la Kibaha na kujionea adha yahuduma ya maji wanayopata wananchi.

(b) Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kibahawamekuwa wakipata adha kubwa katika huduma hata yahaya machache yaliyopo na wakionekana kuwa ni ombaomba na kwamba hii huduma kwao siyo stahili.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuisaidia Halmashauriya Mji wa Kibaha ili iweze kupata Mamlaka yake ya Maji nakuweza kutoa huduma hii kwa ufasaha katika Mji wa KibahaMjini?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, swalikwamba ni lini sasa wananchi watapata maji na lini mradihuu utakamilika. La msingi ni kuwa mchakato ulishaanza hivininavyoongea tayari makampuni yameshapendekezwa,yale ambayo yanashindania katika ujenzi wa chanzo kuleRuvu Juu na Makampuni mengine yameshaorodheshwayanayoshindania ulazaji wa bomba toka Ruvu Juu mpakaMjini na kazi watakazofanya kwa sasa hivi ni kushindaniakuandaa mapendekezo ya kifedha na kiufundi ili apatikanemmoja na ambaye anatakiwa kuanza kazi ya ujenzi wa mradihuu mwezi wa nane 2015 mwanzoni.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo wananchiwatapata maji, kuhusu wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjinikwamba sasa wapate uwakilishi kwamba wapate Mamlakayao ya Maji nilishawahi kujibu swali kama hili hapa Bungeni,kwamba hatuwezi kuwa na Mamlaka mbili kwenye chanzo

Page 9: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

9

12 APRILI, 2013

kimoja tunachoweza kufanya ni kuhakikisha kuwa Kibaha naBagamoyo wanakuwa na uwakil ishi katika Bodi yaDAWASCO.

Bodi iliyoko sasa hivi inamaliza muda wake mwezi wanane tutamshauri Waziri ili kuwe na uwakilishi wa Kibaha naBagamoyo katika Bodi mpya itakayoundwa.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaSpika, kwa kuwa suala la maji limekuwa ni tatizo kubwa ndaniya nchi yetu, mwaka jana wakati ninahoji suala hili la majinchini na nikatoa ushauri wa kutumia maji ya bahari kwa ajiliya kuyageuza na kuwa maji ya kawaida, Waziri aliniambiakuwa tayari kuna timu ambayo inafanyia utafiti suala hilo,sasa ninataka kujua.

Je, utafiti ule umefikia wapi ili kuondokana namatatizo haya ambayo sehemu kubwa ya nchi yetuinakabiliwa na tataizo kubwa la maji?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kwelikuwa iko njia mbadala ya kuwapatia wananchi maji kupitiamaji ya bahari ambayo yanapitia process desalination,tunachosema ni kwamba sehemu hii kwa sasa hivi Serikaliimeruhusu sekta binafsi kujihusisha katika eneo hili ili kuwezakuyatengeneza hayo maji kwa kupitia njia ya desalination iliiweze kuwasaidia wananchi.

Lakini sisi kama Serikali kwa sasa hivi tutajitahidikutumia teknolojia zilizopo bila kutumia maji ya bahari kwamiundombinu iliyopo na maji yaliyopo aihitaji hiyo processlakini hatujazuia kwa makapuni binafsi kufanya process hiyo.

Mheshimiwa Spika, la pili ni kuwa teknolojia hiyo nighali sana na nchi za waarabu ambazo zinatumia teknolojiazinatumia umeme mwingi sana kwenye ku- process maji. Kwahiyo, tusingependa twende huko tuanze kwanza kwa hiziambazo tunazo tuone kama tunaweza kuwasaidia wananchiwetu kwa teknolojia iliyopo sasa hivi.

Page 10: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

10

12 APRILI, 2013

SPIKA: Tunaendelea na Wizara ya Ujenzi MheshimiwaDkt. Augustine Lyatonga Mrema.

Na. 28

Ujenzi wa Barabara ya Lami Kutoka Marangu-Kilema

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA aliuliza:-

Ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Marangu- KilemaSokoni umeanza rasmi.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga upyamadaraja matano ya zamani katika barabara hiyo?

(b) Je, Serikali itatoa lini kibali cha Mkandarasikuchukua moram katika Mlima wa Ngangu ili kuharakishamradi huo?

(c) Je, ni kweli Serikali ina mpango wa kubomoa jengola Hotel ya Kibo iliyoko kwenye Hifadhi ya Barabara na fidiakiasi gani itatolewa?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema, Mbunge waVunjo, lenye sehemu (a) na (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, wakati Mkandarasiakiendelea na ujenzi wa barabara Kawawa Nduoni - Kilemahadi Marangu Mtoni, ilibainika kuwa madaraja manne yaMbonjo, Ruwa, Makoa na Whona yanastahili kufanyiwamatengenezo. Ili kubaini matengenezo yanayohitajikakufanyika katika madaraja hayo, Mhandisi mshauri anafanyauchunguzi wa kitaalam. Uamuzi wa nini kifanyike kwenyemadaraja hayo utatolewa baada ya tathmini ya MhandisiMshauri.

Page 11: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

11

12 APRILI, 2013

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali ilishatoa kibali kwaMkandarasi kuchukua changarawe kutoka chanzo kinginekaribu na Kilacha baada ya Mmiliki wa eneo la awali lililopokaribu na mlima Ngangu kutoridhia eneo lake kutumika kwaajili ya kuchimba changarawe. Kwa sasa upatikanaji wachangarawe siyo tatizo.

(c) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa nyaraka zausanifu wa michoro iliyoandaliwa na Mhandisi Mshauri,Barabara ya Marangu Mtoni - Kilema itajengwa bila kuathirijengo la Hoteli ya Kibo.

Aidha, Serikali haiwalipi fidia wamiliki wa mali zilizomondani ya hifadhi ya eneo la barabara kwa kuwa hawastahilifidia kwa mujibu wa Sheria iliyopitishwa na Bunge Na.13 yamwaka 2007.

MHE. DKT. AUGUSTINO L. MREMA: Mheshimiwa Spika,naomba nimshukuru sana Waziri kwa majibu yake mazuri, ninamaswali mawili nyongeza.

(a) Kwa kuwa Serikali imeshindwa kuvunja lilejengo la Kibo na wakakubali barabara ijengwe kama ilivyo,ni kwanini barabara kutoka Marangu Mtoni kwenda KINAPAnyumba zilizopo karibu na barabara ile ikizingatiwa kulehakuna ardhi, zimewekewa alama ya kuvunjwa. Kwaninihamkuzingatia sera hiyo kama mlivyofanya kuruhusu jengola Kibo Hotel liendelee kuwepo na barabara iendeleekuwepo.

(b) Hii barabara ya Marangu Mtoni kwendaKilema Sokoni ni barabara pacha ya barabara ya Kawawakwenda Nduoni Kirua Vunjo Magharibi, sasa barabara ileimejengwa lakini sasa hivi mvua zimenyesha na wananchiwanalalamika labda wanaweza kuachiwa barabarailiyochakachuliwa. Unasemaje kuhusu hiyo barabara yaMarangu Mtoni kwenda Kilema pamoja na hiyo ya Kawawakwenda Nduoni?

Page 12: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

12

12 APRILI, 2013

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakama nilivyosema kwenye jibu la msingi kwamba ujenziunaoendelea kwa sasa hivi hautaathiri ubomoaji, lakini hotelihiyo iko ndani ya barabara.

Sasa hivi tulikuwa tumeelekezwa kwamba tuangaliemaeneo yale ambayo, maana barabara ileinayozungumzwa ipo mlimani. Sasa kuna maeneo menginekupata ile hifadhi ya barabara iliyopo kwenye sheria kidogoimekuwa na ngumu tunataka tufanyie mapitio, yale maeneoambayo ni vigumu kupata hiyo road reserve ndiyo maanahiyo imebaki. Lakini muda ukifika kwamba sasa tu-clear roadreserve basi itahusika na sheria hiyo.

(b) Kwenye barabara ambayo unasemailishatengenezwa lakini mvua zimeharibu tutazingatia kuwezakuirekebisha katika matengenezo kwa kutumia hela ya mfukowa barabara. (Makofi)

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spikaahsante, nina swali moja la nyongeza.

Kwa sababu imeonesha dalili ya ufa katika darajaambalo linaunganisha Kenya na Tanzania lililopo katika MtoMara pale Kirume.

Je, Serikali ina mpango gani kuimarisha au kujengaupya?

SPIKA: Mheshimiwa Nasari naomba urudi ulipotoka.Endelea Mheshimiwa.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,naomba nianze upya. Daraja ambalo lipo mto Mara,barabara ya lami ambayo inaunganisha Tanzania na Kenyani hatari na kwa usalama wa abiria,

Je, Serikali ina mpango gani, kujenga upya daraja lamto Mara eneo la Marasomoche kwa ajili ya kuimarishadaraja hilo?

Page 13: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

13

12 APRILI, 2013

SPIKA: Ni swali jipya hilo, ila kwa sababu ni darajakubwa naomba ujibu kama unaweza.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI Mheshimiwa Spika, naombaswali lake la daraja la Kirume tulifanyie kazi ili tuweze kumpamajibu sahihi na wananchi wa Mara waweze kusikia.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Spika ahsantesana. Mara nyingi makandarasi wanaopewa kazi ya kujengabarabara huchimba mashimo ili kuchukua moram kwa ajiliya ujenzi, lakini huacha mashimo hayo makubwa marawanapomaliza kazi zao na kuathiri mazingira ya maeneohayo.

Je, Serikali inachukua hatua gani ili kuhakikishakwamba Makandarasi wanapomaliza kazi wanayafukia yalemashimo ili kutoathiri mazingira.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakwenye mikataba ya ujenzi wa barabara tumeweka kifunguambacho mkandarasi anapomaliza kazi, ni lazima yale ma-blow pit ambapo alikuwa anachukua changaraweayatengeneze na ayaache katika mazingira ambayoynakubalika kulingana na mkataba ule. Endapo kunamkandarasi ambaye ameacha ovyo, huyu atakuwaamevunja sheria kwa kufanya hivyo.

Kwenye mikataba mingi huwa tunakuwa na kipindicha maangalizo kwa hiyo kipindi hicho ndiyo tunaangaliakama kuna mkandarasi ambaye hajatekeleza hili basitunatoa tozo na kumkata kwenye fedha zake za malipo yamwisho.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kuniona. Kwa kuwa ujenzi wa barabara inayotokaDodoma kwenda Iringa inapita katikati ya Mji wa Iringa.

Je Serikali imeweka mkakati gani kuchepusha ilebarabara, mradi ule utakapokamilika kusiwepomsongamano wa magari katikati ya Mji?

Page 14: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

14

12 APRILI, 2013

SPIKA: Maswali mapya, mnatakiwa kuuliza maswaliya kiujumla. Kwa sababu mkiwa mkoa mmoja labdaanaweza kujibu, Waziri jibu kama unataka.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kwelibarabara ya kutoka Dodoma-Iringa tunaanza kuijenga nabarabara ile ni kwamba itapita katikati ya Mji wa Manispaaya Iringa na ni kweli kwamba kutakuwa na msongamano.Suala hili tumeshaliona tunalifanyia kazi ili tupate barabaraya mchepuo, yale magari ambayo hayana sababu ya kupitakatikati ya Mji yaweze kupita pembeni ili kupunguzamsongamano wa magari katikati ya Mji. Kwa hiyo suala hilotunalifanyia kazi. (Makofi)

SPIKA: Ahsante tunaendelea na Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwaanapaswa kuuliza swali hilo, kwa niaba yake MheshimiwaJoshua Nassari.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika, kwanzanikuombe radhi nilikuwa nakwenda kwa sababu ya swali laMheshimiwa Msigwa ndiyo sababu nilikuwa nakwendakwenye dawati lake.

SPIKA: Endelea tu.

Na. 29

Ahadi ya Kufunguliwa kwa Kiwanda cha ChaiNjombe

MHE. JOSHUA S. NASSARI (K.n.y. MHE. MCH. PETER S.MSIGWA aliuliza:-

Zao la Chai limekuwa ndio tegemeo kubwa la uchumiwa wananchi Njombe Kaskazini, hususani Tarafa yaLupembe, lakini uchumi wa Chai maeneo hayo umedororakwa sasa kutokana na mgogoro kati ya Mwekezaji nawananchi ambapo Kiwanda cha Chai hakifanyi kazi kwatakribani miaka nane sasa:-

Page 15: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

15

12 APRILI, 2013

Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi ya Mheshimiwa Raisaliyoitoa tarehe 22 Septemba, 2010 ya kuhakikisha kwambaKiwanda cha Chai kinafunguliwa na kuanza kazi haraka?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, napenda kujibu swali la MheshimiwaMchungaji Peter Simon Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mgogoro wa Kiwanda cha ChaiLupembe ulianza mwezi Julai, 2008 kati ya wanahisa ambaoni Mwekezaji M/S Dhow Merchantile EA Limited na Muunganowa Vyama vya Ushirika Lupembe (MUVYULU) ambapo M/SDhow Merchantile anamiliki asilimia 70 na MUVYULU anamilikiasilimia 30.

Kiwango hiki cha umiliki kilifikiwa baada ya Serikalikuuza hisa zake zote asilimia 25.76 na MUVYULU kuuza hisazake asilimia 44.24 kati ya asilimia 74.24 ilizokuwa inamiliki nakubakiwa na asilimia 30. Mwezi Julai, 2008 MUVYULU walifikiahatua ya kufunga kiwanda hicho na kupeleka suala hiloMahakamani baada ya kutokea kutokuelewana kati yao naMwekezaji mwenza M/S Dhow Merchantile (EA) Limited.

Mheshimiwa Spika, wakati Mheshimiwa Raisalipokuwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka2010, alifikishiwa kadhia hii na wananchi wa Lupembe nakuahidi kushughulikia mgogoro wa Kiwanda cha Chai chaLupembe. Pamoja na kuweka angalizo kwamba suala hili likoMahakamani. Aidha, Serikali kupitia uongozi wa Wilaya naMkoa wa Iringa pamoja na Wizara yangu imefanya jitihadambalimbali kwa nyakati tofauti za kushawishi pande husikakumaliza mgogoro huo nje ya Mahakama bila mafanikio.Hata hivyo, kesi hii bado inaendelea Mahakamani na nimatarajio yetu kwamba kesi hii itamalizika.

Page 16: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

16

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa uchumi wawakulima na wananchi wa Tarafa ya Lupembe hauathirikina kufungwa kwa kiwanda hicho wakati wa kusubiri maamuziya Mahakama, Serikali imehamasisha wawekezaji kujengakiwanda mbadala katika Tarafa ya Lupembe ili wakulimawauze majani ya chai kiwandani hapo.

Kutokana na uhamasishaji huo, Kampuni ya Chai naKahawa ya Mufindi Mufindi (Tea and Coffee Company (MTC)Wamejenga Kiwanda katika Tarafa ya Lupembe kwa ubiana wakulima ambapo kampuni ya MTC inamiliki asilimia 75na wakulima asilimia 25. Aidha, ili kuhakikisha kiwanda hichokinafanya kazi kwa ufanisi, wabia hao wameunda Kampuniya uendeshaji wa kiwanda hicho (Ikanga Tea Company Ltd.)ili kuendesha kiwanda hicho na kwa sasa kimeanza kusindikamajani ya chai katika Tarafa ya Lupembe tangu tarehe 1Novemba, 2012.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, ukienda maeneo mengi katikanchi yetu kila eneo lina zao lake kubwa la uchumi na kamaswali la awali lililokuwa linaulizwa ni zao la chai. Ukiendamaeneo mengine.

Kwa mfano, kule kwetu Arumeru ilikuwa ni kahawaambayo ilikuwa chini ya Wizara hii ya Kilimo, Chakula naUshirika, lakini miaka ya nyuma zao la kahawa lilikuwa ndiyozao kuu la uchumi, wananchi walikatwa pesa kwenye mfukomaalum kupitia zao la kahawa, lakini leo tunazungumzamiaka 20 baadaye zaidi ya shilingi milioni mia sita mpaka leoile fedha ya mfuko maalum wananchi hawajarudishiwa navyama vya ushirika havifanyi tena kazi.

Ningependa kujua Wizara hii ya Kilimo, Chakula naushirika ina mpango gani ili kuhakikisha kwamba walewananchi ambao walikatwa fedha kwenye zao la kahawakwenye mfuko maalum wanarudishiwa fedha zao?

Page 17: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

17

12 APRILI, 2013

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini swali hilo ndiyokabisa liko nje, unajua lile lingine ni kesi ya Mahakamakwamba kiwanda kimefungwa, hili lingine halihusiki. Naombatuendelee na Mheshimiwa Kigola.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spikanashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, zao la chai ni zao mojawapo linalochangiakatika uchumi wa Taifa na Chai inalimwa Njombe – Mbeya,wakulima wana tatizo kubwa sana kupata mbolea ya ruzuku.

Je, Serikali ina mkakati gani kutoa mbolea ya ruzukukwa wakulima hawa ambao wanasaidia kuinua pato laTaifa?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mufindi ndiyo mzalishajimkuu wa chai nchini lakini zipo Wilaya kama Rungwe, Lushoto,lakini kwa kuhakikisha kwamba wakulima wadogo ambaokwa sasa hivi wanalima wastani kama wa kilo 1000 ya majanimakavu ya chai, wanaweza kufikia wastani wa kilo elfu mbilikwa majani ya chai.

Kwa hiyo, ili tufikie hatua hiyo na kwa sababu chai hiiya wakulima wadogo inaonekana ikifika hata kwenyemnada wa soko Mombasa ni chai ambayo inapendwa sana.

Mheshimiwa Spika, Serikali imejipanga na kwenyemkutano wa wadau wa chai ambapo tulikutana naoMorogoro tulitoa ahadi kwamba tutakutana na umoja wawakulima wadogo TASHTIDA wa chai, wakala wao, ili kupataufumbuzi ya namna ambavyo wao watatoka kuongeza tijakutoka kilo 1000 za majani makavu kwenda kilo 2000.

Kwa hiyo, naomba niwaahidi wakulima wetu wa chaikatika Wilaya hizi, Mheshimiwa Profesa Mwakyusa,Mheshimiwa Msolla na wengine kwamba suala hil ilinafanyiwa kazi kwa karibu na tutawashirikisha Wabungewanaotoka kwenye sehemu zinazolima chai.

Page 18: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

18

12 APRILI, 2013

SPIKA: Ahsante sana, tunaendelea na swalilinalofuata, Mheshimiwa Moshi Kakoso atauliza swali hilo.

Na. 30

Ruzuku kwa Zao la Tumbaku

MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza:-

Tumbaku ni zao linaloliingizia Taifa fedha nyingi zakigeni na hivyo kuinua pato la Taifa:-

(a) Je, ni lini zao hilo litaingizwa kwenye ruzuku yaSerikali ili kuweza kupunguza gharama za pembejeo kwawakulima wa zao hili?

(b) Serikali iliahidi asilimia mbili (2%) ya ushuru lakinihaijatekelezwa. Je, Serikali itakamilisha lini ahadi hiyo?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, naomba kujibu swali la MheshimiwaSelemani Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, lenye sehemu(a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, azma ya Serikali ni kutoaruzuku ya pembejeo kwa muda utakaoruhusu kulingana namazingira ya kiuchumi na na kijamii kwa mazao yote yachakula na biashara ili kujenga uzoefu wa matumizi yapembejeo hususani mbolea na mbegu bora.

Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa Bajeti kwa sasaruzuku inatolewa kwa baadhi ya mazao kama vile chai,pamba, kahawa, korosho, alizeti, mtama mahindi nampunga.

Page 19: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

19

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, zao la tumbaku ni miongoni mwamazao makuu ya kilimo nchini ambayo kwa sasa hayapatiruzuku ya pembejeo kutokana na ufinyu wa Bajeti pamojana uwezo wa zao lenyewe kujihami kutokana na mazingiranafuu ya bei na soko la tumbaku ukilinganisha na mazaomengine kama pamba na korosho. Aidha, mkakati waSerikali ni kutoa ruzuku kwenye mazao mengine kadiri yaupatikanaji wa rasilimali fedha utakavyoongezeka.

(b) Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katikaswali Na. 112 na Mheshimwa Victor Mwambalaswa Mbungewa Lupa na swali Na. 113 la Mheshimiwa Said Juma Nkumba,Mbunge wa Sikonge, katika Mkutano wa Tisa tarehe 9/11/2012 ni kuwa uamuzi wa kufanya mgawanyo wa ushuru wamazao wa asilimia 5 kwa kuwapatia wakulima wa tumbakuasilimia mbili (2) ya ushuru huo ulifanyika wakati sheria yaFedha ya mwaka 2011(The Finance Act 2011) ilishapitishwana Bunge na hivyo kutokufanyika kwa marekebisho katikaSheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa (The Local GovernmentFinance Act, 1982) ambayo ingeruhusu mgawanyo huo kwawakulima wa tumbaku.

Mheshimiwa Spika, ahadi hiyo ya Serikali ilitokana nana kushuka kwa bei ya tumbaku ambayo kwa sasa imeanzakuimarika hadi kufikia Dola za Kimarekani 1.82 kwa kilo msimuwa 2012/13 kutoka dola za kimarekani 1.4 msimu wa 2010/2011.

Aidha, katika kukabiliana na kubadilika mara kwamara bei za mazao, Serikali kwa kushirikiana na wadau ipokatika mchakato wa kuanzisha mfuko maalum wa kufidia beiza mazao kwa wakulima pale zao linaposhuka (PriceStabilization Fund) kwa lengo la kuwawezesha wakulimakupata bei nzuri na kuwaepusha na hasara kubwainayotokana na kushuka bei za mazao katika masoko yakimataifa hapo inapotokea.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa majibu ya Serikali lakini nina maswlai mawili ya nyongeza.

Page 20: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

20

12 APRILI, 2013

Kwa kuwa, zao hili limekuwa likizalishwa katika mikoatisa na zaidi ya Wilaya ishirini zinazalisha zao hili, ni sababuzipi zinazofanya isione umuhimu wa zao hili kuwapa ruzukuya Serikali ili waweze kuzalisha kwa wingi na kuwapa nafuuwakulima ambao wanazalisha katika nchi hii?

Swali la Pili, kwa kuwa, Serikali iliahidi ndani ya Bungelako Tukufu na kupewa uzito na Waziri Mkuu kwambawakulima wangepewa fedha zile za kuwasaidia kwa sababuya mdororo wa kiuchumi. Ni kwanini Serikali mpaka sasa badohaijatekeleza na haioni umuhimu sasa wa kuwapa fidia walewakulima ambao walipata mdororo wa kiuchumi katikamsimu uliopita na kuwafanya waweze kupata kifutajasho?

SPIKA: Ahsante sana, majibu Naibu Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie MheshimiwaKakoso na kwa bahati yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimona haya masuala tumeyazungumza hata kwenye Kamati juzi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaona ni muhimu sanawa kushughulikia zao la tumbaku. Zao la tumbaku kimsingindilo zao linaloleta pesa nyingi sana za kigeni kuliko zaolingine lolote katika mazao yote ya biashara yanayouzwahapa nchini.

Kwa hiyo, zao la Tumbaku ni zao kubwa sanaTanzania na Serikali tunalifuatilia kwa karibu na tunafanyakazi kwa karibu sana na Bodi ya tumbaku, na tunasema siyokatika masuala haya tu ya mbolea tu na ruzuku yapo masualamengi sana ya usimamizi wa zao lote hil i ambalotunafanyakazi na bodi ya Tumbaku kwa karibu sana na lengoni kuongeza tija katika zao la tumbaku na kuongezaupatikanaji wa masoko ili wakulima wa Tanzania watokekwenye kupata dola milioni mia mbili na sitini kwenda mpakamilioni mia nne ambayo ndiyo lengo la export earnings.

Mheshimiwa Spika, swali la pili wakulima wangepewafedha za mdororo, mdororo wa kiuchumi haukugonga zao

Page 21: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

21

12 APRILI, 2013

la tumbaku tu uligonga mazao mengi. Kusema kweli kwenyeile Stabilization Capacity ya Serikali inategemea na uwezowa Serikali. Uwezo wa Serikali kama wote tunavyofahamuhaukuwa mkubwa kiasi hicho.

Kwa hiyo, siyo zao la tumbaku tu lakini nadhani zaola kahawa pia lina mgogoro huo kwa Mzee Dkt. AugustineLyatonga Mrema na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, lakini tunajipanga ili huko mbeletunapokwenda haya mazao yawe na tija zaidi na manufaazaidi na mapato zaidi kwa wakulima wa Tanzania. (Makofi)

MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Katika Wilaya ya Kasulu,wapo wakulima ambao tangu mwaka jana tumbaku yaoimerundikwa stoo, hawajaweza kupata soko la kuuzatumbaku hiyo. Wakulima hao wameendelea kuwa masikinikwa sababu, walitegemea kupata kipato kutokana natumbaku yao.

Mheshimiwa Spika, wakulima hao ni wa vijiji vyaNyumbigwa, Rungwe Mpya na Ahsante Nyerere.

Je, Serikali, inawaambia nini wakulima hao ambaompaka sasa hawajaweza kuuza tumbaku yao?

SPIKA: Ah, haya. Sijui, atakumbuka?

Haya, Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kifupi sana. Niswali jipya pia.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Chakulana Ushirika, naomba nijibu maswali ya nyongeza yaMheshimiwa Josephine Ngenzabuke, Mbunge wa VitiMaalum, Mkoa wa Kigoma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hili suala la wakulima hawa waWilaya ya Kasulu, zao la tumbaku ni zao ambalo linakwenda

Page 22: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

22

12 APRILI, 2013

mpaka kwenye Wilaya nyingine mpya nyingi. Kwa hiyo,ninaomba nimsihi tusubiri kwani suala hili linaghughulikiwana Bodi, tujue tatizo ni nini na twende tukaangalie,inawezekana tatizo ni wale classifiers au matatizo mengine.Inaweza ikawa matatizo yako katika sura mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nikutane naBodi na wawakilishi wa Bodi, Viongozi wao, ili tujue suala hililina sura gani na tulipatie ufumbuzi wa namna gani. (Makofi)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, tumbakuinaleta madhara sana katika nchi yetu, magonjwa ya kansana inapigwa vita dunia nzima. Kwa hiyo, kwa nini, Serikali,isiwe na mpango wa kuwahamasisha wakulima wetu walimebangi, isindikwe, iuzwe nchi za nje, tupate hela ya kigeni?(Kicheko)

SPIKA: Badala ya tumbaku, waweke bangi? Haya.(Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Waziri, labda mmefanya utafiti.(Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Chakulana Ushirika, naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Mbunge wa Nkasi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba tu niseme, hii hali yakujaribu kupingana na uzalishaji wa zao la tumbaku kwa sasahivi, haina tija kwa sababu, nchi nyingi sana dunianizinaendelea kuwa na mahitaji makubwa ya zao la tumbaku.

Kwa bahati nzuri tumbaku ya Tanzania, inakubalikasana kwenye masoko hayo makuu ya dunia. Hivi karibunitumeingia kwenye soko la China, wametukubalia.

SPIKA: Muda, muda, muda. Msianze kujiremba hapa.(Makofi)

Page 23: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

23

12 APRILI, 2013

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, samahani, wanataka kujua.

MBUNGE FULANI: Bangi?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, zao la bangi bado halijawa zao labiashara ya kilimo. Lakini kuna nchi nyingine Ulaya ambazowameruhusu zao hilo la bangi. Sasa Mheshimiwa Esta,anatikisa kichwa pale. Mimi nadhani hapo itakapofikia bangikuruhusiwa au likikubalika zao hili litumike na likapata uhalaliwa matumizi kwenye maeneo mbalimbali duniani, basi nijambo ambalo linaweza kufikiriwa. (Makofi)

SPIKA: Jamani, sasa inabidi niendelee tu. Maananaona sasa tutaingia kwenye mabalaa bure. (Kicheko)

Wizara ya Katiba na Sheria. Mheshimiwa LeticiaNyerere, atauliza Swali linalofuata.

Na. 31

VITENDO VYA KINYAMA KWA OMBAOMBA

MHE. LETICIA M. NYERERE aliuliza:-

Kuna taarifa kuwa baadhi ya wanaumewanawapatia mimba wasichana walemavu wanao-ombaomba, kitendo ambacho ni cha kinyama:-

(a) Je, Serikali, ina mkakati gani kuhakikisha kuwavitendo hivyo vya kinyama vinakoma?

(b) Je, ipo tayari kufanya marekebisho katikaSheria ya Kujamiiana, ili kuongeza adhabu kwa watuhumiwa?

Page 24: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

24

12 APRILI, 2013

WAZIRI NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katibana Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa LeticiaMageni Nyerere, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu(a) na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, naomba nikubaliane naMheshimiwa Mbunge, kwamba ni kweli kwamba, wapobaadhi ya wanaume wanaowarubuni wasichana walemavuna wale wanao omba omba mitaani. Vitendo hivi ni kinyumena Sheria ya Makosa ya KujamiIana, yaani The SexualOffences (Special Provisions) Act, 1998. Sheria hiyo ni mojaya Mikakati iliyochukuliwa kupambana na uhalifu huu wakinyama.

Aidha, mkakati mwingine ni kuweka adhabu zakuogopesha (Deterrence). Adhabu ya kosa hilo ni kifungocha miaka 30, pamoja na viboko na faini. Sheria inatambuakwamba, wasichana wa aina hii hawana uwezo wa kiakilina utashi wa kutoa ridhaa ya kujamiiana. Hivyo, utetezi wamhalifu kwamba, msichana alitoa ridhaa ya kujamiianahaukubaliki Mahakamani.

Mheshimiwa Spika, aidha, hatua na mkakatimwingine wa Kisheria ni ambapo msichana aliyedhalilishwaana umri wa miaka 10 au chini yake, mhalifu atapewaadhabu ya kutumikia kifungo cha maisha Gerezani.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutumia nafasi hiikuwahamasisha wanawake wote, wanaume wote, wenyemapenzi mema kwa haki za watoto, walemavu na watuwote, wanapoona vitendo hivyo vya kudhalilisha wataoetaarifa kwenye vyombo vya dola, ili hatua stahiki zichukuliwena kuwafikisha Mahakamani.

(b) Mheshimiwa Spika, adhabu zilizoainishwa katika Sheriaya Kujamiina ni kubwa na zinatosheleza. Hata hivyo, kazi yakutunga na kurekebisha Sheria kwa kuongeza adhabu ni kazi

Page 25: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

25

12 APRILI, 2013

ya Bunge hili. Serikali, inaridhia kwamba, adhabu hii inakidhiviwango vya adhabu vilivyopendekezwa katika Mikataba yaHaki za Binadamu na katika masharti ya Ibara ya 13 (b) (e),ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika, kwakuwa, wanaume wengi wanaovizia walemavu, ama wanamatatizo ya ubongo, hawajiamini na vile vile hawana uwezowa kushawishi wanawake.

Je, Serikali, haioni kwamba, kuna haja sasa yakuanzisha Kituo cha kuwafundisha wanaume hawa jinsi ganiwataweza kuachana na ngono ya dezo? (Kicheko/Makofi)

(Hapa, Waheshimiwa Wabunge, walitoa sauti zavicheko)

SPIKA: Naomba uendelee, muda wangu unaisha.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika, swali lapili. Kwa kuwa, kuna baadhi ya nchi duniani wanatumiaadhabu ya kuhasi; yaani permanent disfiguration of genitalparts.

Je, Serikali, haioni kwamba, kuna umuhimu wakutazama kama adhabu hii iweze kutumika, hatimaye Taifaletu liwanusuru watoto wa kike na wanawake kwa ujumla?

WAZIRI NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napendakujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Leticia Nyerere, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuanzisha Kituo Maalumcha kufundishia. Mimi hili ninaliona kwamba, zamani katikamila na desturi kwa baadhi ya makabila walikuwawanafanya hivyo kwa watoto wa kiume wanapoenda jando,wanawafundisha baadhi ya vitu vya namna hiyo.

Page 26: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

26

12 APRILI, 2013

Lakini kwa Serikali, sasa kuanzisha Kituo Maalum, hiyohaiwezekani. Hilo ni jambo binafsi na sio kwamba, walewanakuwa na matatizo, baadhi yao hawana matatizokabisa, ni watu wazima, wana akili zao; ni kwamba, basi tuwana tamaa za kijinga.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli, mimi kama mama, kwakweli, nahuzunishwa na vitendo vya wanaume kuchukuawalemavu, mlemavu wa ubongo, unaenda kufanyanayemapenzi. Unamchukua kiwete unaenda kufanyanaemapenzi; kwa kweli, sio jambo la busara.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, adhabu ya kuhasi. Kwakweli, katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(Hapa, Waheshimiwa Wabunge, walipaza sauti yakicheko)

SPIKA: Naomba tusikilize majibu.

WAZIRI NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) MheshimiwaSpika, nimesema kwamba, katika Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Kifungu cha 13 (e), ni marufuku kwamtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabuzinazomtweza au kumdhalilisha mtu. Sasa kuhasi ni adhabuya kutweza. (Makofi)

SPIKA: Haya, tunaendelea. Leo maswali ya ajabuajabu tu, tunaendelea. Kama mengine yatakuwa ya nguonihapa.

Tuendelee Wizara ya Maliasili na Utalii. MheshimiwaFaith Mohamed Mitambo?

Page 27: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

27

12 APRILI, 2013

Na. 32

Mgogoro wa Mpaka Kijiji cha KikulyungunaPori la Akiba la Selous

MHE. FAITH M. MITAMBO aliuliza:-

Mgogoro wa mipaka kati ya Kijiji cha Kikulyungu naPori la Akiba Selous, umekuwepo kwa muda wa zaidi yamiaka kumi (10) sasa:-

(a) Je, Serikali, itamaliza lini mgogoro huo?

(b) Je, Serikali, itahakiki lini huo mpaka kamaulivyo kwenye tangazo la Serikali, la mwaka 1974?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasilina Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Faith MohamedMitambo, Mbunge wa Liwale, lenye sehemu (a) na (b), kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, mgogoro kati ya Kijiji chaKikulyungu na Pori la Akiba la Selous, ulishughulikiwa na Wizarayangu mwaka 2010 kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Halmashauriya Wilaya ya Liwale na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamaporiya Magingo.

(b) Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010, Wizarayangu ilihakiki mpaka kati ya Pori la Akiba la Selous na Vijijivinavyounda WMA ya Liwale, kwa kuzingatia maelezo yaTangazo la Serikali, Namba 275 la mwaka 1974. Uhakiki huoulibaini kuwepo maeneo yaliyokuwa yameingizwa kimakosakwenye Pori la Akiba la Selous na maeneo mengineyaliyokuwa yameingizwa kimakosa kwenye ardhi ya Vijiji,ikiwemo sehemu ya Kijiji cha Kikulyungu.

Page 28: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

28

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ilirejesha kwawananchi maeneo yaliyokuwa yameingizwa ndani ya Porila Akiba la Selous, hivyo mpaka unaotenganisha Pori la Akibala Selous na Kijiji cha Kikulyungu uliopo sasa, ni mpaka halali.Hali kadhalika unazingatia Tangazo la Serikali la mwaka 1974.

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Kwa kuwa, uhakiki uliofanywa na Wizara ya Maliasili naUtalii mwaka 2010, ulikwepesha kusudi kwa makusudi kabisampaka halali ambao ulikuwa umetolewa kwenye Tangazola Serikali la mwaka 1972 na kusogeza mpaka huo kutokaMto Matandu mpaka kuingia eneo la Kijiji cha Kikulyungu.

Mheshimiwa Spika, na kwa kuwa, wananchihawakuridhika na uhakiki ambao ulifanywa mwaka 2010.

Je, Wizara ya Maliasili, iko tayari sasa turudi tena katikaKijiji cha Kikulyungu, tuweze kuuhakiki mpaka huu upya?

Mheshimiwa Spika kijiji cha Kikulyungu, kilitolewakatika umoja wa hifadhi ya Magingo, kwa sababu yamgogoro huu wa mpaka. Wizara ya Maliasili, inaweza kusemasasa iko tayari kukirudisha Kijiji hiki katika Jumuiya ile yaMagingo? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba nijibumaswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Faith MohamedMitambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Maliasili na Utalii,inatambua jitihada hizi ambazo Mheshimiwa Faith, amekuwaakizifanya. Ninapenda niseme yafuatayo; moja ni Serikali naWizara, iko tayari kwa kuzingatia umuhimu wa kuwepo amani,mshikamano na wananchi ambao kwa kweli, wao ndiowahifadhi. Wao ndio ambao wanahifadhi hili eneo la pori laakiba la Selous, miaka yote.

Page 29: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

29

12 APRILI, 2013

Serikali hatuna ugomvi wa mipaka kama upo, hatabaada ya kurekebishwa mwaka 2010, Wizara, itakuwa tayarikurejea tena kwenye mazungumzo haya, ili tuwezekuhakikisha kwamba, mipaka iko wazi kati ya hifadhi nawananchi. Migogoro kama ipo, inatatuliwa mara moja.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema mwanzo katikajibu langu la msingi; WMA, ambayo ilifanya hiki Kijiji chaMagingo kiondolewe kutokana na mgogoro wa ardhi.Wataweza kurejesha katika mfumo huu wa WMA marabaada ya kuhakikisha kwamba, tunaumaliza mgogoro huo.Ningependa kuahidi hapa kwamba, tutafanya kilaiwezekanavyo haraka turejee yale makubaliano natuhakikishe kwamba, amani inapatikana katika eneo letu.(Makofi)

MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Kwa sababu Swali la msingi na mazingira yake yanafananana hali iliyopo katika Kata ya Kania na Kijiji cha Kania naMpago, Jimbo la Biharamulo Magharibi. Ambapo wananchiwameishi zaidi ya miaka 50 na Profesa Kulikoyela Kahigi, nimzaliwa wa pale, leo hii wanaambiwa wanaishi kwenyehifadhi.

Je, Wizara iko tayari kwenda kuangalia mipaka upyana kuwarejeshea amani wananchi wale?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba nijibuswali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali, imeunda Tume ya Kitaifa,ambayo inajumuisha wadau mbalimbali na pia sektambalimbali katika Wizara mbalimbali nchini, kwa ajili yakupitia migogoro katika maeneo yetu ya hifadhi na mipakaya wananchi nchi nzima.

Page 30: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

30

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba nilitaarifu Bunge lakoTukufu, kwamba, Tume ile tayari imemaliza kazi yake naimeleta taarifa kwa Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utaliina Taarifa hiyo, inaendelea kuchambuliwa. Naomba tunimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba, hiki Kijiji chaKaniha na Mihango, pale Biharamulo Magharibi, ambapohivi karibuni Mheshimiwa Waziri, alinituma na nilifikakutembelea hilo Pori la Biharamulo, itakuwa ni sehemu yamaeneo ambayo tutayaangalia na tutayatolea majibu yapamoja. (Makofi)

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa,tatizo la mipaka na suala zima la miundombinu hasa yabarabara inayopatikana katika maeneo ya Selous, ambapomara nyingi sana wananchi wanapotumia huwa wanapatamatatizo. Kwa mfano, watu wa Mloka, kule Rufiji, wanapopitakatika maeneo haya, huwa wanabambikiwa kesi za ujangili.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa kadhia hii yawananchi wetu katika maeneo yanayozunguka eneo laSelous?

SPIKA: Migogoro ya mipaka, tena mmeshaingiakwenye migogoro ya...

Mheshimiwa, kama unaweza kujibu? Lakini kwa kifupisana, dakika moja.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii,nijibu tu kwa kifupi swali la nyongeza la Mheshimiwa Jafo,ambalo pia linazungumzia maeneo haya haya ya mipakana maeneo haya haya yanayohusiana na mahusiano katiya wananchi na wa hifadhi. Niseme katika mchakato ambaotunaupitia unaosimamiwa na Mheshimiwa Waziri,tunahakikisha kwamba, tunarekebisha migogoro iliyopokatika maeneo yetu ya hifadhi na wananchi, nchi nzima.

Page 31: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

31

12 APRILI, 2013

Lakini pili tunaangalia upya kuhakikisha kwamba,mahusiano mazuri kati ya hifadhi na wananchiwanaozunguka maeneo yetu yanaimarishwa na kunakuwana ushirikiano kamili.

Na. 33

Wawekezaji Katika Mbuga ya Serengeti

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE aliuliza:-

(a) Je, kuna wawekezaji wangapi kwamchanganuo?

(b) Je, wawekezaji hao wanasaidiaje katikakuchangia maendeleo ya Wilaya ya Serengeti? Na kwamiaka mitatu iliyopita, wamesaidia kuchangia maendeleokwa fedha jumla ya kiasi gani?

(c) Je, kuna watumishi wangapi kwa ujumla? Katiya hao ni wangapi wanatoka Wilaya ya Serengeti?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasilina Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. KebweStephen Kebwe, Mbunge wa Serengeti, swali lenye sehemu(a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, kwa takwimu zilizopo,hifadhi ya Taifa ya Serengeti ina wawekezaji 18 kwamchanganuo ufuatao:-

(i) Kuna Loji tano ambazo ni Serengeti SopaLodge, Serengeti Seronera Wildlife Lodge, Serengeti SerenaLodge, Four Season Safari (Bilila) Lodge na Lobo WildlifeLodge.

Page 32: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

32

12 APRILI, 2013

(ii) Makambi ya kudumu (Permanent TentedCamps) ya kulaza wageni 13, ambayo ni Kusini SanctuaryCamp, Serengeti Soroi Camp, Grumet River Camp,Mbalangeti Tented Camp, Mbuzi Mawe Camp, MigrationCamp, Lamai Camp, Sayari Camp, Singita Mara River Camp,Serengeti Bushtops Camp, Serengeti Pioneer Camp, KirawiraLuxury Camp na Serengeti Balloons Safaris Camp.

Mheshimiwa Spika, wawekezaji hao wanasaidiakuchangia maendeleo ya Wilaya ya Serengeti kupitia tozombalimbali wanazotozwa na shirika. Hifadhi ya Taifa yaSerengeti hukusanya tozo kwa wawekezaji waliopo ndani yahifadhi ya Taifa ya Serengeti na sehemu ya fedha hizohutolewa kwa wananchi wa Serengeti kupitia mpango waujirani mwema ili kuchangia maendeleo ya wananchi katikamaeneo yaliyo jirani na hifadhi ikiwemo Wilaya ya Serengeti.

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha miaka mitatuHifadhi ya Serengeti imechangia miradi mbalimbali yamaendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 97, 431, 51kwamchanganuo ufuatao;

Mheshimiwa Spika, 2010/2011 shilingi milioni 44.1, 2011/2012 shilingi milioni 40, 2012/2013 kwa maneno mengine hadihapa tulipo shilingi miloni 13.

Mheshimiwa Spika, miradi hiyo ni pamoja na ununuziwa thamani katika shule ya Sekondari ya wasichana yaMama Maria Nyerere, Ujenzi wa choo katika zahanati ya BohuSedeko, ujenzi wa mabweni ya wasichana kwenye eneo lakisangula, nata, machochweni na Isenya.

Mheshimiwa Spika, mwisho lodge na kambi za kulazawageni zilizopo katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti zinawafanya kazi 1056 na kati yao wafanyakazi 156 wanatokakatika Wilaya ya Serengeti.

MHE. DR. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri, lakini ni ushauri wabure wafanye utafiti upya kwa ajili ya update ya takwimu

Page 33: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

33

12 APRILI, 2013

walizonazo. Ni masikitiko makubwa hata lodge ambayo nimaarufu duniani na imeshinda zawadi mara mbili mfululizomwaka juzi na mwaka jana sasa kwa lodge wengi wanaitaVIP lodge haiko kwenye orodha hii.

Mheshimiwa Spika, wawekezaji kwa takwimu wakatinimeleta swali hili kwa niaba ya wana Serengeti ziko campna lodge hizi zipatazo 47. Kwa hiyo, naomba wa updatetakwimu hizo.

Mheshimiwa Spika, swali (a) Serikali kupitia Wizara yaMaliasili na Utalii na Wizara ya kazi na Serikali kwa ujumla wakotayari kushirikiana na Wilaya ya Serengeti na Mbunge? Ilikusudi hawa wawekezaji waweze kutoa mchango waokatika taifa na kwa Wilaya ya Serengeti?

Mheshimiwa Spika, (b) kwa kawaida inatakiwa 75%ya waajiriwa katika maeneo ya uwekezaji watoke kwenyeeneo husika, lakini takwimu hizi ni asilimia 14.7 hali hii nikuwaonea wana Serengeti. Serikali iko tayari kwa makusudikabisa kufanya operation maalum kuweka usawia?Mheshimiwa Spika, naomba nipatiwe majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii naomba nijibumaswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Dkt. Kebwe S.Kebwe, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, moja niseme tu kwamba takwimuambazo Wizara imezitoa hapa Bungeni zilikuwa zinahusuuwekezaji ulio ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nanakubaliana kabisa na Mheshimiwa Dkt. Kebwe S. Kebwe,kwamba kuna lodge, kuna tented Camps, kuna MobileCamps nyingi ambazo hazijahusishwa katika takwimu hiziambazo tumezitoa na zipo katika maeneo mbalimbaliyanayozunguka hifadhi ya taifa ya Serengeti na ikiwemoWilaya ya Serengeti na niseme vilevile kwamba VIP Lodgeambayo katika miaka miwili mfululizo sasa imeshinda nafasiya kwanza kuwa lodge yenye sifa na ubora ulitukuka dunianiipo katika Wilaya ya Serengeti lakini bado ipo nje ya hifadhi

Page 34: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

34

12 APRILI, 2013

ya Taifa ya Serengeti.

Mheshimiwa Spika, la pili la Mheshimiwa Mbungekwamba Wizara tutafanya kila jitihada za makusudikushirikiana na Wilaya ya Serengeti, moja ni suala zima lautambuzi wa uwekezaji ambao kwanza tunauhitaji uliopokatika maeneo yanayozunguka hifadhi ya Taifa kwa sababuwote wanaowekeza ni kwa sababu waweze kuingia katikahifadhi zetu.

Mheshimiwa Spika, lakini pili uwekezaji huu uwezekuwa na tija moja kwenye ajira za watu wetu na pili katikamaslahi mengine ikiwa ni mapato kwa Halmashauri asante.

SPIKA: Ahsante sana waheshimiwa tunaenda kwamuda matangazo ya kazi. Mheshimiwa Mwenyekiti wa umojawa Wabunge wanawake naomba nianze zile kazi za Bungekwanza. Wajumbe wa kamati ya kilimo, mifugo na majiProfesa Peter Msolwa naomba niwatangazie wajumbe waKamati yake kwamba leo saa saba mchana kutakuwa nakikao katika ukumbi wa Namba 231 hii Kamati ya kilimo,mifugo na maji.

Halafu Mwenyekiti wa Umoja wa Wabungewanawake TWPG Mheshimiwa Anna Abdallah anaombaniwatangazie Waheshimiwa Wabunge wanawake wotekuwa tarehe 13 na tarehe 14 Aprili, 2013 kutakuwa navikao vya mafunzo Chuo kikuu Dodoma (UDOM)yaliyoandaliwa na Shirika la Oxfarm kikao kitaanza saa nneasubuhi yaani kule UDOM kuna mafunzo yanaendelea juuya wanawake. Kwa hiyo, tarehe 13 na tarehe 14 Aprili,2013 mnaruhusiwa takribani wanawake 300 kutoka mikoayote Tanzania.

Masuala yatokayojadiliwa pamoja na unyanyasaji wawanawake violence against women ya pili uwezeshajiwanawake kiuchumi (Women Economic Empowerment),halafu na nyingine umilikishwaji wa rasilimali ownership ofresources. (Makofi)

Page 35: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

35

12 APRILI, 2013

Waheshimiwa Wabunge wanawake wotewanaombwa kuhudhuria mafunzo hayo muhimu kwaniitakuwa fursa nzuri kwao kubadilishana uzoefu na wanawakewengine kutoka katika maeneo yao.

Tangazo la mwisho ni la Mwenyekiti wa APNAC Dkt.Mary Mwanjelwa anaomba niwatangazie wajumbe waAPNAC kuwa leo kutakuwa na kikao chumba Namba 227katika jengo la utawala hawajataja chumba lakini mtajuawenyewe mpo wachache jengo la utawala kikao chaKamati Kuu siyo wabunge wote.

Nani alisema Mwongozo dakika mbili maana yaketunaenda kwa utaratibu.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, nashukurunasimama kwa Kanuni ya 68(7) hali kadhalika Mbungeanaweza kusimama wakati wowote ambapo hakunaMbunge mwingine anayesema na kuomba mwongozo waSpika. Kwa ajili ya muda naomba nisimalizie yaliyopo hapa.

Lakini ninakwenda kwenye wakati wa swali Namba31 linajibiwa kuanzia aliyeliuliza na aliyekuwa akilijibu pichailiyopo ni kwamba mwanaume anayefanya urafiki aumapenzi na kiwete ni udhalilishaji mimi ninavyofahamu.

SPIKA: Hoja ni nini sasa.

MHE.ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, hoja nikwamba wananchi huko nje wataelewa kwamba kuoa aukutembea na kiwete ni makosa. Mheshimiwa Spika nilitakamwongozo wako.

Je, ndivyo wananchi waelewe hivyo?

WAZIRI YA NCHI,OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA): Mheshimiwa Spika, naomba kufafanuakama ifuatavyo:-

Page 36: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

36

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, mimi kama mama nimeguswa nawale wanaume ambao wanafanya mapenzi na walemavukama vile viwete halafu wanawatelekeza baada yakuwazalisha.

Mheshimiwa Spika, huo ni udhalilishaji wa hali ya juusana. Unamzalisha mlemavu halafu unamtelekeza jamani,kweli, huo ni ubinadamu kweli! Wanaume. (Makofi)

SPIKA: Haya tumeelewa, nadhani ilitakiwa ielewekekwamba unakwenda kumwona maskini huyu dada au mtotohuyu unamfanyia vitendo vibaya halafu unaenda zako.Unaenda zako wala hujulikani kufanya mapenzi ni hata nahao kama kweli wewe ukaonana na ndugu zake, ukafanyanini na kwamba utamtunza, kwa hali yake yote ile hakunaanayekataa.

Nadhani tulielewa hivyo. Naona wengine speed yamuda hawajapata tuna Makamu Mwenyekitiu wa Kamatiya Bunge ya Katiba na Sheria na Utawala anaombaniwatangazie wajumbe kwamba saa saba mchanawatakutana kwenye ukumbi wa Msekwa C. Katibutuendelee.

Waheshimiwa Wabunge kwa utaratibi tuliojipangiaasubuhi hii tutakuwa na wazungumzaji 18, jioni tutakuwa nawazungumzaji 17 tunakwenda kwa mujibu wa saa. Kwa hiyo,tuendelee kama jana msipoteze muda mzungumze kwenyepoint na mjiandae vizuri. Kwa hiyo msemaji wangu wakwanza leo atakuwa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba,atafuatiwa na Mheshimiwa Mariam Kasembe, atafuatiwa naMheshimiwa Felister A. Bura.

Page 37: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

37

12 APRILI, 2013

MHE. MWIGULU N. MADELU: Mheshimiwa Spika,ahsante sana na mimi nilikuwa JKT Msangi kule alikuwepoAfande Mbweya na Shigongo na nilihitimu AG 0593.

Sasa nianzie kwenye suala la elimu jambo la elimuna hususani kwenye elimu ya Sekondari kufuatia matokeoyaliyojitokeza, napenda nitoe mchango na naombaWaheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania mnisikilizekwa makini sana.

Mheshimiwa Spika, katika elimu ya Sekondari nchiyetu inapita katika kipindi cha mpito. Ikumbukwe kwambatangu uhuru, tangu Serikali ilipotaifisha shule za Sekondarji zaMisheni kila mmoja aangalie kwenye mkoa wake Serikalihaikuwahi kujenga shule nyingi za Sekondari kama ilivyojengakatika awamu hii kwenye shule za kata na kufuatia ujenzi washule nyingi kwa aina hiyo kwa ghafla na kufuatana namahitaji kwamba wanafunzi wengi sana walihitajika kwendani lazima upungufu wa aina nyingi wa mahitaji yanayotakiwashuleni ungejitokeza.

Mheshimiwa Spika, moja ya kitu ambachokimejitokeza ni kwamba shule nyingi sana zimejengwa kwamara ya kwanza tangu uhuru imekuja kutokea kwambaWalimu wakakosekana kabisa kabisa. Yaani Serikali hainamahali pa kutoa walimu wote wanaotoka mashuleniwanapelekwa moja kwa moja kwenda kufundisha na hililimejitokeza na Serikali ikachukua jitihada za kupandishabaadhi ya vyuo na kupanua vyuo vya walimu.

Sasa kufuatia rai ya Waziri Mkuu mimi ningeombaWabunge tuielewe hiyo kwamba hili si la kunyoshea mtukidole kwa sababu hamna yoyote yule ambaye anawezaakasema kwamba Serikali ingetoa wapi Walimu.

Page 38: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

38

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, nimeangalia hata kwenye hikikitabu, niliona tu kuanzia nje walikimbilia tu kusema Waziriwa Elimu ajiuzulu hivi akishajiuzulu ndiyo anaenda kufundishakwa sababu la kwanza tungesema hivi Walimu hawapo hatakutoka nje ya nchi. Sasa nilitegemea waje na mawazo mapyakwamba kufuatana na kwamba hakuna walimu kabisakabisa sisi maoni yetu ni haya badala yake.

Kurasa 70 zinakuja zote zinalalamika. Wananchiwanalalamika na viongozi wanalalamika huku wanasemawanatamani nchi. Mnatamani mkafanye nini wakati hatamawazo mbadala hamna. Hivi hamjawahi kujua kwambahuwa hamchaguliwi kwa sababu hamna mawazo mbadalamnalalamika, mnalalamika page 70 hivi hii ni maoni ya kambiya upinzani au malalamiko ya kambi ya upinzani what isthis?

Mheshimiwa Spika, sasa mimi ili nisilalamike naombanijikite kwenye ushauri wangu, Mheshimiwa Waziri Mkuu kwakuwa Serikali imemaliza kabisa kabisa walimu kwambainasubiria tu wale wakimaliza ndiyo iwapangie na shuletumejenga zinakuwa na walimu wawili wengine watatu,hakuna pa kuwatoa walimu.

Lakini hapa hapa nchini tuna wataalam wetu ambaowamemaliza vyuo, wapo wa vyuo vingine ma-engineer,wanasheria wapo kila mtaa hawana kazi. Mimi naombaSerikali pamoja na Bunge tufanye mambo mawili.

Kwanza tubadilishe sheria inayosema mwanafunzi waSekondari anatakiwa afundishwe na mwalimu tusememwanafunzi wa Sekondari atafundishwa na lecturer, lecturerwa Sekondari halafu tukishasema atafundishwa na lecturertuwachukue wa-engineer popote pale walipo wajiandikishewakafundishe. Mimi siamini kama engineer wa chuo kikuucha Dar es Salaam atashindwa kufundisha mwanafunzi waForm two.

Page 39: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

39

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, siamini kama Mwanasheriaatashindwa kufundisha language ya form one tuwachukuehalafu tuwalipe kama engineer anayelipwa aliyeko Wizaranihalafu wapande na cheo senior one, senior two kama aliyekoWizarani.

Kwa nini tuna wataalam waliosoma kwa fedha zaSerikali wapo hawana kazi halafu tuna form one hanamwalimu. Mbona wanafunzi anafudishwa na form six.Ukikuta shule ya kata imefaulisha kidogo ujue wale form sixwamejitolea tolea kufundisha ndiyo wale wakafanya vile.lakini tuna wahandisi, tuna wachumi, hilo ni la kwanza.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la pili tubadilishe utaratibuwa malipo kule jeshini kuna maafande, kuna maaskari nakuna maofisa tuwalipe kama wale wanavyolipa mawizarani,kwa hiyo, hilo litafanyika.

Lakini jambo la pili tatizo la mambo yote kwenye elimuni suala la kibajeti, ni suala la kibajeti na Waziri Mkuuutagombana sana na walimu lakini kama hatutabadilishauwekezaji kwenye elimu utagombana mpaka mwisho.Jambo la kufanya hapa tuongeze fedha zilizotengwa kwaajili ya walimu, tuwalipe tumalizane nao, kwa sababu kamaBajeti inaendelea kama ile ile ya wakati shule ziko chache,walimu wameongezeka, shule zimeongezeka, fedha yavitabu itatoka wapi?

Mheshimiwa Spika, sasa kwa kuwa kengele ya kwanzaimeshagongwa nihamie kwenye jambo lingine. Lakini jambola pili ninalotaka kufafanua na hili nawaomba Watanzaniamsikil ize kwa umakini sana. Kuna jambo la kigaidilimeandikwa hapa page karibu nne.

Page 40: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

40

12 APRILI, 2013

Kwa masikitiko makubwa mnapotosha mpakamambo yanayohusu maisha ya watu, mnapotosha etiUsalama wa Taifa, eti Polisi wala msihangaike na kwenyejambo hili nasema wala msihangaike na Usalama wa taifa,wala polisi jambo la ugaidi ni jambo la mkanda, aliyerekodiule mkanda yupo tayari kusema popote, aliyeniletea yupotayari kusema popote na mimi niko tayari kusema mahalipopote.

Mheshimiwa Spika, Chadema walipanga kuteka nakuua, walipanga yule kijana wa Igunga walipanga kumwuana huyu mwandishi waliyekuwa wanamwongelea walipangakumwua halafu wanadhania eti picha imetengenezwa. Sasakwa taarifa zenu hata pale walipokuwa wanaongea yulealiyekuwa anaongea alikuwa anaandika mpaka na ilekaratasi aliyekuwa anaandika hii hapa finger print ya kwake,mwandiko wa kwake na hivi vyote vimeshafanyiwa kazivimepatikana ni yeye na pale palipo fanyikia ni kwakealiyekuwa anarekodi amekubali amesema atatoa huoushahidi, aliyeniletea atatoa na mimi nitatoa popotemahakamani, polisi, Bungeni na hata mbinguni nitasema.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapanga kuua na unapangakwamba kiasi gani tutatengeneza isionekane Chademandiyo imefanya haya na lile mnalosema ipendekezwe tumependekezeni kwa sababu si viongozi wote wa Chademawanapenda yale mauaji kwa sababu hata lile lililofanyikamajibu wanayo eti kiongozi anaandika kwambaanayewasiliana na gaidi naye aunganishwe na ugaidi.

Hivi eti anasema viongozi wa CCM lakini hebu fikirieniyule aliyekuwa anapanga yale mauaji ni Mkurugenzi wa Ulinzina Usalama wa Chadema inamaana anawasiliana naviongozi gani kama siyo wale wakubwa zake na ndiyowanaomwagiza apange yale.

Page 41: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

41

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, jitihada za kumtetea mtu kablahata haijafika mahakamani inadhihirisha ule ulikuwa nimpango wa chama na kwa kauli hii hapa ambayoameandika kiongozi wa kambi ya upinzani ukurasa wa 31kwamba viongozi hawa wanao wasiliana nao wawajibishwekwa maana hiyo Jeshi la Polisi kuanzia leo hii nashukuruMbowe hayupo hapa. Kwa hiyo, ndiyo inawezekanawameshamkamata kwa sababu yeye ndiyo anayewasilianazaidi na Lwakatare, Katibu Mku wake naye ameshamteteanaye aunganishwe kwa sababu ameandika mwenyewekwamba kwa mujibu wa Sheria ya Ugaidi mtu yoyoteanayefanya mawasiliano na gaidi au magaidi yeye piaanahamasisha ugaidi na yeye anastahili kuunganishwa natuhuma hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kiongozi ambaye ndiyoMwenyekiti na Katibu wa Chama kile yule aliyekuwaanapanga ni subordinate wao na fedha walizokuwawanatumia kuwalipa wale vijana zilikuwa za Chama chao.Kwa hiyo, waunganishwe, Polisi mnasubiri nini watuwameshaomba wenyewe waunganishwe?

Sasa mnakuja na mlolongo wa malalamiko oooh! Zeronyingi! zero nyingi! Tukiulizana hapa hivi zero zimeanza leoungekuwepo Mbowe ningekuuliza wewe ulipata ninimnachochea vijana wa watu wakasirike huku mnapangakuua halafu mkishapanga mnawahi kama mchawianayeloga, halafu anawahi yeye kwenda kulia nakugaragara msibani.

Mheshimiwa Spika, kwenye suala hili la mauajiChadema nawaomba mfanye vitu viwili kwanza kimbieniharaka sana kwenye kanisa lililo karibu au msikiti ulio karibumkatubu dhambi ya kupanga kuwaua watu wasio na hatiamkishamaliza hilo mrudi mkaombe radhi kwa Watanzania youlook merciless, shameless unatafuta uongozi huku unauawatu, look at you.

Mheshimiwa Spika baada ya hapo naomba kuungamkono hoja. (Makofi)

Page 42: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

42

12 APRILI, 2013

SPIKA: Mheshimiwa Mustapha Akunaay, time, timeplease!

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika,mzungumzaji aliyepita, kwa kanuni ya 68(2), amezungumziakitu ambacho ni sub-judice, kitendo ambacho kikoMahakamani hakiwezi kuruhusiwa kuzungumziwa Bungeni.

Pil i, Mbunge haruhusiwi kuzungumza mamboyanayomhusu Mbunge mwingine moja kwa moja. Naombaaondoe hiyo kwa kuzingatia kanuni hiyo.

SPIKA: Sawa nakubali na ni vizuri wote mkaheshimukanuni hizo.

Tunaendelea! Mchangiaji wangu wa pil i, niMheshimiwa Mariam Kasembe.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mwongozo wa Spika!

SPIKA: Tumemaliza hilo, kwa sababu unajuaninachosema, wote mnatakiwa ku-observe rules, siyo mkukikwa nguruwe kwa mmoja na mwingine siyo mkuki, siyo sahihi!Tunaendelea! (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!

SPIKA: Tunaendelea Mheshimiwa Kasembe!

MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba yaWaziri Mkuu. Katika hotuba hii nitajaribu kuchangia katikaeneo la utawala, mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa nanikipata nafasi na masuala ya nishati.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la utawala ukurasawa 70, Serikali imeelezea jinsi ambavyo imejitahidi kuanzishaHalmashauri 31 ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Page 43: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

43

12 APRILI, 2013

Lengo kubwa la Serikali kusogeza huduma hizi karibu nawananchi ni kuharakisha maendeleo. Nilivyokuwa napitiakatika ukurasa huu, niliona Mheshimiwa Waziri Mkuuameelezea jinsi atakavyojitahidi kugawa rasilimali watu,vitendea kazi kwa uwiano ili kuharakisha maendeleo katikaHalmashauri hizo.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo binafsi limenipawasiwasi, nilivyokuwa naangalia fedha zilizotengwa katikaHalmashauri ya Wilaya ya Masasi na Halmashauri ya Mji,ukilinganisha na matatizo yaliyojitokeza katika Wilaya yaMasasi, maafa yaliyojitokeza katika Halmashauri ya Wilayaya Masasi na Halmashauri ya Mji, sasa hivi Halmashauri zotembili, hazina vitendea kazi vya kutosha na hazina ofisi nazimepoteza mali nyingi, kwa mfano, magari na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa naangaliakatika fedha zilizotengwa, nikawa najiuliza, je, fedha hizizitaweza kutosheleza kutatua tatizo lile kubwa ambalolimejitokeza katika Halmashauri hizi mbili? Au je, Serikali inampango wowote au kuna fedha zozote zilizotengwa kwa ajiliya kwenda kutatua matatizo haya yaliyojitokeza huko.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba MheshimiwaWaziri Mkuu atakapokuwa anatoa majumuisho, atoeufafanuzi kama wataweza kusaidia katika yale yaliyojitokezakwenye Halmashauri zote mbili.

Mheshimiwa Spika, vile vile kwenye suala la mafunzoya kijeshi, imeelezwa kwamba, Serikali imeendeleza jitihadaza kuchukua vijana kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi, lakini vilevile wamewachukua vijana wetu hawa form six ambaowanaendelea kwa mujibu wa sheria. Naombaniwazungumzie wale vijana wanaokwenda kwa ajili yakujitolea.

Mheshimiwa Spika, vijana hawa ni wengi, wanafanyakazi nzuri, ni wakakamavu na wamepata mafunzo ya kutosha.Inasikitisha sana vijana hawa wanakaa kambini mwaka

Page 44: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

44

12 APRILI, 2013

mzima, wanafanya kazi za kujenga nchi, lakini baadayewanakuja kukosa nafasi za kuajiriwa, inabidi warudimajumbani.

Mheshimiwa Spika, ombi langu kwa Serikali,tumekuwa tukitoa nafasi za ajira huku nje, kwa mfano, nafasiza Polisi, Jeshi, Magereza na Uhamiaji. Naiomba Serikali, sasahivi tungefuta kabisa utaratibu wa kutangaza nafasi hizi nje;lakini tukaenda moja kwa moja kwenye Jeshi la Kujenga Taifana kuwachukua vijana ambao tayari wamekwishapatamafunzo. Vijana hao ndiyo wawe wanachukuliwa nakupelekwa kwenye Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Uhamiajipamoja na Jeshi la Wananchi ili kuwasaidia vijana hawa,kwa sababu vijana hawa wana elimu ya kutosha, wapovijana wa form four, form six na vyuo, lakini vile vile wapovijana wa darasa la saba ambao wamekuwa wakifanya kazinzuri sana.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali ichukue ushauriwangu huu. Haina maana yoyote tunatangaza nafasi hizihuku nje, tunachukua vijana walioko mitaani, wakati kwenyeJeshi la Kujenga Taifa wapo vijana ambao wako tayari nawangeweza kuwa askari wazuri katika nchi hii.

Mheshimiwa Spika, vile vile naomba niungane mkonona Mheshimiwa mwenzangu ambaye jana alizungumziasuala la kupeleka mafunzo ya ufundi katika Jeshi la KujengaTaifa. Vijana wetu walioko katika Jeshi la Kujenga Taifa niwengi, kama tungekuwa tumeanzisha Vyuo vya VETA katikamakambi haya, nafikiri vijana wetu wangeweza kunufaikazaidi, ili wale ambao watakuwa wanakosa nafasi za ajira,Serikali iwaandalie vitendea kazi, wanapomaliza wakirudimajumbani waweze kujiajiri wao wenyewe.

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie suala lanishati. Serikali imekuwa ikiendeleza jitihada za kusambazaumeme vijijini, nilipokuwa naangalia hotuba ya Waziri Mkuu,nimeona katika Mikoa ambayo itanufaika na mpango huuwa kusambaza umeme vijini kwa awamu hii ya kwanza, Mikoaya Mtwara na Lindi ipo.

Page 45: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

45

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini ninachotaka kuzungumziahapa ni kwamba, Mheshimiwa Naibu Waziri alitembeleakatika Mikoa hii, alielezea viji j i ambavyo vinatakiwakusambaziwa umeme kwa awamu ya kwanza na awamuya pili. Nataka niambie Serikali kazi hii inakwenda taratibumno na imeshaanza kuwakatisha tamaa wananchi, kwasababu nguzo zimesambazwa na hakuna kazi yoyoteinayoendelea.

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nafuatilia niliambiwakwamba, vitendea kazi hawana. Naiomba Serikali, kamakweli tumekusudia kusambaza umeme vijijini na kama kwelituna nia ya kuwasaidia wananchi wapate umeme, naombaijitahidi sana kupeleka vifaa vya kutosha ili kazi hii iwezekuendelea. Kwa sababu kama hii awamu ya kwanza, walewaliopangiwa kupata umeme hawataweza kupata kwawakati, ina maana kazi ya kusambaza umeme vijijiniitachukua muda mrefu sana.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, wananchi waMkoa wa Mtwara na Lindi walipata punguzo la bei ilikuwasaidia kunufaika na nishati hii ya gesi. Bei iliyokuwaimepangwa ilikuwa ni shilingi 99,000/, lakini naomba niambieSerikali kwamba bei hii haikuwa wazi. Kwa hiyo, wananchiwengine wamekuwa hawaitambui, tumefanya kazi ya ziadaya kuwaelimsha, lakini wanapokwenda TANESCO imekuwani kama favour, wengine wanaambiwa kwamba ni 99,000/=na wengine wanaambia bei nyingine. Naomba Serikali irejeetena kutamka hii bei iliyopangwa.

Mheshimiwa Spika, vile vile muda ulikuwaumepangwa kwa bei hii. Naiomba Serikali ule mudauliopangwa hautawanufaisha wananchi kwa sababu mudaule ni mfupi na ukizingatia kwa mfano, wananchi wa Mkoawa Mtwara na Lindi, mwaka huu wameyumba sana katikakuuza korosho. Kwa hiyo, wananchi wengi wameshindwakujiandaa katika kufanya wiring katika nyumba zao. NaiombaSerikali irejeshe tena suala hil i la punguzo, tuweze

Page 46: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

46

12 APRILI, 2013

kuongezewa muda, ikiwezekana mngetuwekea muda wamiaka mitatu mpaka pale tutakapohakikisha kwamba,umeme vijijini umeweza kusambaa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombanisipoteze muda sana, naomba yale ambayo nimeyaombakwa Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anajumuisha, hasakwenye eneo la utawala yaweze kuzingatiwa.

Mheshimiwa Spika, vile vile sisi watu wa Mkoa waMtwara, Ruvuma na Lindi, tuliomba mgawanyo wa Mkoa,lakini Mikoa ilipotangazwa tulipigwa na butwaa kuonakwamba sisi hatumo. Sasa namwomba Mheshimiwa WaziriMkuu, atuambie, hili ombi la Mikoa ya Kusini linakwama nini?Rais alipokuja kuomba kura, wananchi walimwelezakwamba, tunayo mahitaji ya kutaka Mkoa. Rais aliahidi kuwa,kabla hajamaliza kipindi chake, ataweza kulitekeleza hilo.Sasa miaka inakwenda, namwomba Mheshimiwa WaziriMkuu atakapokuwa anajumuisha atuambie, wapi tunakoseana nini tunatakiwa kufanya kwa sababu bado tunahitajikupata Mkoa wa Kusini, unaojumuisha Wilaya ya Masasi,Nanyumbu, Tunduru pamoja na Nachingwea.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Aliko Kibona, atafuatiwana Mheshimiwa Charles Mwijage!

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Niende moja kwa moja katikakuchangia hoja iliyo mbele yetu, nikianza na elimu.

Mheshimiwa Spika, naomba nitoe pole kwa vijanawote waliofanya mtihani mwaka uliopita na wamefeli na pianitoe pole kwa wazazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo…

SPIKA: Ndiyo umechangia hivyo!

Page 47: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

47

12 APRILI, 2013

MHE. ALIKO N. KIBONA: Wazee wetu Tanzania nzimawaliwekeza katika elimu kwa ajili ya watoto wao, kuanziakidato cha kwanza mpaka kidato cha nne. Wengine waliuzamashamba, wengine waliuza mifugo. Matokeo yaliyokujaimekuwa ni masikitiko.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa ushauri, tusije namajibu mepesi katika jambo hili gumu, Mimi kule Mbeya nimdau wa shule moja ya Sekondari inaitwa Lutengano. Shuleile ina Walimu wa kutosha, lakini watoto wamefeli. Shule iletunawalipa Walimu wale vizuri lakini watoto wamefeli, shuleile watoto hawaendi na simu shuleni, lakini watoto wamefeli.Naomba tusubiri majibu ya Tume ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,tuone itatuletea nini.

Mheshimiwa Spika, lakini mimi ningependa kushaurihata kabla Tume haijaja, ili kuwaondolea kero na masikitikomakubwa wazazi wote waliopo katika nchi hii, watoto wetu,tuchukue sasa matokeo ya Mock na maendeleo ya mtotokuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne. Hayoyatumike katika maamuzi ya ama huyu mtoto amefauluaweze kuendelea na kidato cha tano au aweze kupewadaraja sawasawa na alivyopata katika mitihani ya Mock.

Mheshimiwa Spika, isipokuwa kama tu, Waziriatasema mitihani ya Mock ni geresha, basi tutakuwa nasababu ya kusema hawa watoto wameingia hasara kwamatokeo yaliyotoka. Kwenye eneo la elimu wazazi huko vijijiniwanalalamika kwa kitu kinaitwa ada au malipo ya kulipiamtihani. Malipo kwa ajili ya mitihani ni kero, naomba Wizaraiangalie jambo hili.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu Tume ya Waziri Mkuuinaendelea na kazi, nisingependa kusema mengi juu yaupande wa elimu.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kidogo kuhusuafya. Nawapongeza wenzetu wa Wizara ya Afya kwa kazinzuri, lakini niende kwenye kipengele kimoja ambachokanalalamikiwa na wananchi ambacho ni Vyuo. Hospitali

Page 48: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

48

12 APRILI, 2013

zetu nyingi vijijini hazina wataalam, vituo vya afya havinawataalam, zahanati hazina wataalam, Serikali imeendeleakufanya juhudi kuongeza idadi ya wataalam, lakinikilichotupata tulio wadau kwenye Vyuo mbalimbali vya Afyani kiwango au qualification zinazotakiwa kwa mtoto kuingiakwenye Vyuo vya Afya. Eti tunaambiwa mtoto awe amepataC tatu na hizo C zitokane na masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, naomba wataalam waliangalievizuri hili, limekuwa ni kero. Kuna manung’uniko huko nje,kwamba vyuo vingi ni vya mission, kama Mnero, kamaBumbuli, Nkasi kule na sehemu nyingine, KCMC. Uongouliojitokeza sasa ni kwamba, kule Wizarani kuna mkakati wakuhakikisha hivi vyuo havisajili, haviingizi watoto wengi kwaajili ya kusoma masomo ya afya. Naomba wahusikawaliangalie hili ili kukomesha uongo huu. Turudishe sifa zile zakwanza ili tuweze kupata wataalam wengi katika vyuo vyetu.

Mheshimiwa Spika, Kasi ya ujenzi wa Zahanati nindogo mno. Tulipokuwa tunaomba kura kwa ajili ya uchaguziuliopita, akinamama wengi vijijini na wananchi walitupa kurakwa sababu tulionesha kwamba Chama cha Mapinduzikitajenga Zahanati katika kila kijiji. Kasi ni ndogo, naombaWaziri Mkuu, naomba wahusika tafadhali na wadau wote,hil i jambo tuliangalie kwa sababu mwisho wa sikututaonekana waongo.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumzie kidogokuhusu ulinzi. Hali ya usalama katika nchi yetu, nawezakusema ni tofauti na nilivyosoma kitabu cha MheshimiwaWaziri Mkuu. Tangu nimezaliwa ni muda mrefu sasa, nilikotokani mbali kuliko ninakokwenda, sijawahi kusikia RPC anauawa,sijawahi kusikia Kituo cha Polisi kinakwenda kuzingirwa nawananchi wanaoitwa kwa msamiati wa sasa hivi, wananchiwenye hasira kali. Sijawahi kusikia Traffic anapigwa makofina dereva, sijawahi kusikia ni katika kipindi hiki ambachotumeingiza dhana inaitwa ulinzi shirikishi, Polisi Jamii.

Mheshimiwa Spika, hiki kitu binafsi nakilaani, wenzetukule Malawi walijaribu wakasema tuanzishe kitu kinaitwa

Page 49: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

49

12 APRILI, 2013

Police Service wakashindwa, wakarudi kwenye Police Force.Wataalam wastaafu ukiongea nao wale wazee wetuwaliokuwa kwenye Jeshi la Polisi, hiki kitu kinaitwa Polisi Jamiiwanasema, tuliposikia nchi inapokea kitu kinaitwa Polisi Jamii,tukajua mambo yameharibika na kweli mamboyameharibika. Ndiyo sasa tunaona hata RPC anauwawa.Nafikiri tufanye tathmini, jambo lolote ukiona hali ni mbaya,Polisi wanapigwa, Vituo vya Polisi vinavamiwa na kuchomwamoto.

Zamani tulikuwa tukisikia Polisi tulikuwa tunaheshimukama dola, sidhani kama tunakokwenda Polisi tena inaonekani chombo cha dola, kitaonekana ni chombo cha mitaani.Wananchi hawajaelewa maana ya Ulinzi Shirikishi au PolisiJamii, naomba wahusika walichukue hilo na tathimini iwezekufanyika.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kidogo kuhusuviwanda. Nasikitika katika Mkutano uliopita niliwahi kuulizaswali kuhusu uwezekano wa kufufua Kiwanda cha Zana zaKilimo pale Mbeya. Majibu mepesi yalipatikana, tukaambiwakwamba, aliyekuwa ameomba kuendeleza kiwanda kilehawezi kufanya kazi ile. Amefanya tathmini upya, ataingiahasara, kwa hiyo, anabadilisha, kitakuwa sehemu yakutengenezea bia, kutunzia makreti ya bia, vitu kama hivyo.Wananchi wanalalamika, wanasema, kama yeyeameshindwa, ni vizuri tenda ingetangazwa upya. Lengo letusisi tupate vifaa kwa ajili ya kilimo vikiwa jirani na nafuu.

Mheshimiwa Spika, naomba hilo lichukuliwe naliangaliwe upya, kama kwa kiwanda hiki haitawezekana,uwekezaji mwingine utakaokuja baada ya huu kushindakana,ni vizuri tukawa waangalifu kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Spika, sasa nizungumzie maji; nashukurukwamba Serikali imeendelea kufanya juhudi kwa ajili yakuwaletea maji wananchi wa vijijini. Lakini kule kwangunaendelea kulia, Mji wa Isongole naweza kusema unaongozakwa shida ya maji katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu alitazame hilo aweze

Page 50: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

50

12 APRILI, 2013

kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Ileje, sehemu zilezinazoitwa Isongole na Itumba.

Mheshimiwa Spika, wapo wenzetu pale Tunduma…

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Haya ahsante!

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa ajili ya nafasi hii, lakini Tunduma pia wapewe maji.(Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa atafuata Mheshimiwa Mwijage!

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mwongozo wa Spika.

SPIKA Tutumie muda mfupi jamani. Enhe!

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, natumiaKanuni ya 68(7). Naomba Mwongozo wako kuhusu Kanuniya 64(c) na (f) iliyovunjwa na mzungumzaji, MheshimiwaMwigulu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Akunaay aliombakuhusu utaratibu. Kwa kawaida, kikanuni ulitakiwa umkalisheMheshimiwa Mwigulu akae chini, halafu afute kauli yake, lakinikiti kikamlinda.

Mheshimiwa Spika, umesema Wabunge wenginewasiendelee kuvunja hiyo Kanuni. Naomba Mwongozo wako,tutafuataje hii Kanuni wakati kiti kimemlinda MheshimiwaMwigulu mpaka amemaliza, anatukana na hakufuatakanuni? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge nasema hivi, wotetushikilie taratibu hizi. Jana tumeacha hotuba nzimaimesomwa mpaka ikamalizika. Ndiyo maana nasema kuanzia

Page 51: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

51

12 APRILI, 2013

sasa, wote mu-observe, jana yalizungumzwa, hotuba nzimailisomwa tukanyamaza, kwa hiyo sasa nasema tu- observekanuni zetu.

Tuendelee na mchangiaji anayefuata, MheshimiwaMwijage, atafuatiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia bajeti hiiya Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nisije nikapanda preshanikasahau, naunga mkono bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina tatizo na takwimu, sina tatizona maelezo, nimekuja hapa kuendelea kushauri. Nimekujakushauri, sisi Wabunge tumefanya kazi, tulipokuwa Majimbonitumefanya kazi, kama unasema kazi haijafanyika ina maanamiaka miwili na nusu imepotea bure. Tumefanya kazi kweli,tumejenga madarasa, madaraja na barabara. Nimekujahapa kushauri, na zaidi nimekuja hapa kuomba il iwaniongezee. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na suala la chakula nanjaa. Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia alivyosambazachakula takribani tani 69,000, hiki ni kiasi kikubwa sana chachakula. Tungeelezwa gharama za kusafirisha, tungegunduani fedha kiasi gani imetumika.

Naishauri Serikali yangu kwamba, pamoja na jitihadahizi Serikali isaidie hali ya hewa waweze kuwasaidia wananchikutabiri ni msimu gani wa kulima. Wananchi wa mikoa yakati ambao hali ya hewa imewachenga, mazao yaoyameharibika. Laiti kama tungekuwa na hali ya hewa yenyemamlaka, yenye uwezo, watu hawa wangeambiwa wakatigani wafanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa Tanzania nzima nashauri Ofisiya Waziri Mkuu hatuna haja ya kuvumbua kitu kipya, turudikwenye misaafu yetu ya zamani, tufanye kazi kwa operesheni.Operesheni kama Kilimo cha Kufa na Kupona, zimekwisha,hazisikiki. Kumbe basi wananchi wetu wanapaswa

Page 52: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

52

12 APRILI, 2013

kukumbushwa, ni wakati gani wa kulima na wakati gani wakupanda na ukitilia maanani tatizo la chenga za hali yahewa,naendelea kushauri.

Mheshimiwa Spika, Serikali imejikita kulima maeneoambayo yanaonesha tija kubwa kwenye mazao ya nafaka,SAGCOT, mambo ya Sumbawanga, Peramiho na sehemukama hizo. Lakini ukitathmini tani 69,000 zilizosambazwautakuja kugundua kwamba pamoja na uzuri wa mpango huoiko busara na maeneo ya Kanda ya Kaskazini, upande waKanda ya Ziwa kuna haja ya kuanzisha mashamba makubwa.

Mheshimiwa Spika, unapokuwa unajadili bajetiunajiandaa kwa ajili ya bajeti ijayo. Bajeti ijayo naishauriSerikali yangu, mjiandae kusudi muweze kutumia bonde laMto Ngono, kwetu kuna bonde kubwa linaitwa Mto Ngono.Lazima tuzalishe kwa wingi katika bonge lile, tuzalishe nafaka,tuzalishe mpunga, kusudi tuweze kutumia pale, lakini zaidituokoe gharama za Serikali kusafirisha chakula kutokaPeramiho mpaka Bukoba. (Makofi)

Mtu anayejua economics, hawezi kusafirisha chakulakutoka Peramiho kupeleka Bukoba wakati Bukoba kunamilimita za mvua 1100. Lakini tija nyingine ni kwamba watuwa Mahalia watapata fursa ya kushughulika katika shughulizile. Lakini faida nyingine ya ziada, Kagera au Bukoba kamaanavyosema Mzee Mulokozi, Mkuu wa Mkoa wa Kageraanaitwa Mzee Mulokozi, anasema Kagera ndiyo hurb ofCentral Africa, The great central Africa, kwa hiyo, kamamkizalisha pale chakula kitatoka Bukoba kwenye bonde laMto Ngono na kwenda kuuzwa Sudani na Kongo – DRC.

Mheshimiwa Spika, naisaidia Serikali yangu na hasabwana Mipango afikirie, chukueni takwimu za chakulakilichopita bandari ya Dar es Salaam kikienda DRC – Congona Burundi, massive. Tunaweza kuwekeza katika kuzalishachakula kwa kuzilenga nchi jirani, tukapata fedha nyingi nakama alivyosema rafiki yangu Mheshimiwa Keissytukaepukana na bajeti tegemezi. Mchango wangu kuhusuchakula ni huo.

Page 53: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

53

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, nizungumzie maisha ya visiwani nashughuli za uvuvi. Najua kuna watu wengine hawaelewi, mtuwa Kerebe na wa Bumbile, yeye uvuvi ndiyo shughuli yakealiyozaliwa nayo. Kwa hiyo, naishauri Serikali yangu pamojana jitihada za kupambana na uvuvi haramu, nashauri walewatu wa mahali asil ia, wazaliwa wa sehemu zile,wawezeshwe kwa nguvu waweze kukabili haya maingiliomapya, hawa watu wenye mitaji mikubwa na teknolojia,kinyume cha hapo tutaendelea kushuhudia uvuvi haramuna samaki wa Ziwa Viktoria ambao watu wote mnawapendawatatoweka. Ndiyo njia rahisi, wale watu wa mahali asiliandiyo watakaokuwa walinzi na hakuna mtu atakayeharibuZiwa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende kwenye elimu.Wamezungumza mengi na wameandika mengi kuhusu elimu.Niwaambie kitu kimoja, mimi nimesoma decision making.Katika decision making kuna kitu kinaitwa inquiry au probeteam ambayo Watanzania wengi nimeshuhudia hatakwenye magazeti na hata kwenye taarifa za watu wenginehawaelewi kwa nini tunaanzisha Tume.

Mheshimiwa Spika, mojawapo ya sababu zakuanzisha Tume ni kuthibitisha kwamba kile tunachokijua kwelindivyo kilivyo, yaani unaanzisha Tume kuthibitisha kwambamtoto amefeli kwa sababu amekwenda shuleni bila kulachakula, unajua amekwenda bila kula chakula na unaundaTume. Sasa inakusaidia nini? Baadaye kwa pamoja baadaya Tume, mnakubaliana kwamba hili ndiyo hili.

Mtulie taarifa itoke, Tume ya Waziri Mkuu ije ituelezetujue. Wengine wanaolalamika tangu wamalize shule kwenyeshule aliyosomea hajawahi kupeleka hata penseli, unasemanini wewe? Unawajua Walimu wako waliokufundisha?Unasema nini? Naogopa majibu ya Ofisi ya Waziri Mkuuyanaweza kutufanya sisi ni watuhumiwa na tukafungwa,Mungu apishie mbali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumze jambo lingine. Miminimetembelea Jimbo langu, kuna tatizo nimeliona sijui kama

Page 54: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

54

12 APRILI, 2013

Tume italiona. Mafanikio ya Chama changu katika kuzuia vifovya watoto wadogo wa umri wa miaka sifuri mpaka mitano(0- 5) kumepelekea changamoto ya watoto wengi kuingiashuleni. Ni changamoto, tumefanikiwa kuzuia vifo, watotowako wengi shuleni. Shule moja yenye vyumba saba inawatoto 700. Ndugu zangu, viongozi wenzangu, WaheshimiwaWabunge tusife moyo. Kwa hiyo, changamoto tunaitatuakwa kujenga madara zaidi.

Tulichaguliwa kuwa viongozi, kiongozi ni kama kijikocha jikoni, hakiogopi moto. Tujenge madarasa mengine,tujenge vyoo vingine, lakini Serikali mhahakishe, mtu yeyotemwenye certificate ya ualimu, mtangaze tunapomalizaBunge hili aende aajiriwe. (Makofi)

Kuna Walimu wengine hawajapata ajira, kunawengine wameamua sasa kwenda kwenye ualimu waambiehata waliomaliza mwaka 2003 kama wana sifa za kwendachuoni, waende kwa sababu kipaumbele cha kwanza nielimu, kipaumbele cha pili ni elimu na atakayeikomboa nchihii anaitwa elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumze tatizo la Walimu.Walimu pamoja na matatizo yao kuna mtu anakula fedhazao. Kuna makundi ya Taasisi za Microfinance, zinakula fedhaza Walimu. Naiomba Serikali yangu isaidie Chama chaWalimu kuanzisha microfinance kusudi Walimu wakopeshanewao kwa wao kwa riba ndogo. Tatizo la Walimu ni mishaharamidogo. Tatizo la Walimu ni riba kubwa wanazopigwa nahaya makampuni ambayo hayastahili hata kusemwamdomoni mwangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende kwenye miundombinu.Nimesema nimekuja kuomba na Mheshimiwa Waziri Mkuuunajua. Naomba unitengenezee daraja la Kishara liishe.Daraja la Kishara wakulima wa kwangu ndiko wanakopitakwenda visiwani, ndiko wanakoboresha uchumi wao,wananchi wataweza kusembura na kulima sehemuzinazowezekana, lakini kwenye sehemu za matingatingatunahitaji mkono wa Serikali.

Page 55: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

55

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo languwamefanya kazi kweli, wamechimba barabara, Rwanganiwanachimba barabara, Buyanja wanachimba barabara,sehemu za Rugenge wanachimba barabara, lakini sehemuza madaraja na nimeomba daraja moja tu la Kishara,litengenezwe, roho yangu iridhike.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hojamara tano. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Tundu Lissu atafuatiwa naMheshimiwa Felister Bura na baadaye atafuata MheshimiwaBeatrice Shellukindo. Mheshimiwa Tundu Lissu!

MHE. TUNDU A.M LISSU: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi. Naomba mara moja niseme kwamba,nataka nichangie jambo la kwanza masuala ya elimu yasekondari. Jambo la pili, nitachangia sehemu inayohusu ulinzina usalama hapa nchini na jambo la tatu, kama kutakuwana muda, nitazungumzia masuala ya mchakato wa Katibampya.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tuliletewa kitabu chatakwimu muhimu za elimu kwa Tanzania. Kinaitwa basiceducation statistics in Tanzania (BEST) kuanzia mwaka 2007 –2011. Takwimu hizi ziliandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzoya Ufundi.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa mujibu wa takwimu hizimambo yanayoonekana ya kimsingi kabisa ni kwamba, elimuya sekondari katika nchi yetu imekuwa ikiporomoka kwa kiasikikubwa kuanzia mwaka 2006, Serikali ya Awamu ya Nneilipoingia madarakani. Takwimu hizi zinaonesha kwamba,katika miaka mitano ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Tatuya Rais Mkapa, ufaulu wa wanafunzi ulikuwa unapanda.Ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne umeanza kushukakuanzia mwaka 2006 mpaka hapa tulipofikia leo.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kwa mujibu watakwimu hizi waliopata daraja la kwanza kwa wastani kati

Page 56: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

56

12 APRILI, 2013

ya mwaka 2000 mpaka 2005 walikuwa asilimia 5.4 yawanafunzi wote; waliopata daraja la pili katika kipindi hichohicho walikuwa asilimi 7.0, waliopata daraja la tatu katikakipindi hicho walikuwa asilimia 21 na waliopata daraja la nnewalikuwa ni asilimia 52.

Mheshimiwa Spika, hii ndiyo kusema kwamba kwawastani wa kufaulu katika miaka mitano ya utawala wa RaisMkapa wanafunzi walifaulu kwa kiwango cha asilimia 84.5.Waliofeli katika kipindi hicho kwa wastani walikuwa ni asilimia14.8, waliopata daraja la sifuri.

Mheshimiwa Spika, baada ya Rais Kikwete kuingiamadarakani daraja la kwanza mwaka 2006 walishuka kutokaasilimia 5.4 ya wakati wa Mkapa mpaka mpaka asilimia 3.3,waliopata daraja la pili walishuka kutoka asilimi 7.0 mpakaasilimia 5.8, waliopata daraja la tatu walishuka kutoka asilimia21 mpaka asilimia 16.3, waliopata daraja la nne katika kipindihicho walishuka kutoka asilimia 52 mpaka asilimia 51.7 nawaliopata daraja la sifuri waliongezeka kutoka asilimia 14.8mpaka kufikia asilimia 22.8, hii ni kwa takwimu za mpakamwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, wastani wa kufaulu katika miakamitano ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Nne ulikuwa niasilimia 77.2 kutoka asilimia 85.4 za wakati wa Rais Mkapa.

Mheshimiwa Spika, sasa ukiangalia kwa kila mwaka,takwimu hizi zinaonesha vitu vya ajabu. Wanafunzi waliopatadaraja la kwanza mwaka 2006 ambao ni mwaka wa kwanzawa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne walikuwa ni asilimia4.9 kama sikosei, by mwaka 2010 walikuwa wamefikia asilimia2.8, kutoka asilimia 4.9 mpaka asilimia 2.8! Miaka yote yautawala wa Rais Mkapa wanafunzi waliokuwa wanapatadaraja la kwanza, la pili, la tatu na la nne walikuwawanaongezeka. Katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Nneidadi ya waliofaulu imekuwa inakwenda chini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni sahihi kusema kwamba, Serikaliya Awamu ya Nne ni janga la elimu la Taifa la Tanzania. Ni

Page 57: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

57

12 APRILI, 2013

sahihi kusema kwa, takwimu hizi, Serikali ya Chama chaMapinduzi ni janga la elimu kwa Tanzania na hizi takwimu niza Serikali yenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Waziri Mkuu ameunda Tumebaada ya matokeo ya mwaka jana kuchunguza kwa niniwanafunzi wamefeli. Mwaka 2010, baada ya wanafunzi kufelikufikia asilimia 50 Serikali iliunda Tume kuchunguza kwa niniwatoto wa kidato cha nne walikuwa wanafeli.

Mheshimiwa Spika, ripoti yenyewe hii hapa, inaitwataarifa ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha kufaulumtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2010. Taarifaimeandaliwa na Wizara ya Elimu, taarifa hii imeandaliwa naMaafisa Waandamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Waziri wa Elimuanafahamu na Waziri Mkuu anafahamu. Taarifa hii haijawahikutolewa hadharani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa jana kwenye hotuba yakeMheshimiwa Waziri Mkuu amesema kwamba, huu si wakatiwa kulaumiana na kutafuta mchawi. Nakubaliana naye, huusi wakati wa kulaumiana na kutafuta mchawi, huu ni wakatiwa kuwajibishana. Huu ni wakati wa walioshindwa kazikuwajibishwa. Waziri wa Elimu ameshindwa kazi, amekataakujiuzulu anatakiwa afukuzwe kazi. Ni janga la elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu ameshindwa kazianatakiwa ajizulu, kama hajiuzulu apigiwe kura na Bunge hiliya kutokuwa na imani. Wakati huu kinachotakiwa ni watukuwajibika kwa kushindwa kazi, si wakati wa kulea uovu nauchafu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nizungumziemasuala ya ulinzi na usalama. Ripoti iliyoandikwa kwenyegazeti la The African la siku ya Jumatatu ya wiki hii inasema,Jeshi la Polisi la nchi hii linaongoza kwa uonevu, kwa kutungakesi za uongo, kwa kushtaki watu kwa makosa makubwa yauongo ambayo kisheria hayana dhamana; makosa ya

Page 58: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

58

12 APRILI, 2013

mauaji, makosa ya wizi wa kutumia nguvu, makosa ya ugaidi.Ripoti inasema Jeshi la Polisi linahitaji kusafishwa, limekuwa nijeshi la kihalifu. Ni ripoti ya The African.

Mheshimiwa Spika, hii ripoti inakwenda sambambana ripoti nyingi ambazo zimeandikwa juu ya criminality ndaniya Jeshi la Polisi. Umekuwa ni utamaduni wa kihalifu. Jeshi hililinatungia watu vitu vya ajabu kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna watu kwa kushirikiana naPolisi, wanapigiana simu, wanalipana fedha, halafu wanakujawanafungua kesi za ugaidi. Kuna mtu amewasiliana na hawawanaoitwa magaidi kwa miezi miwili, amepigiana simu kulikoalivyompigia mke wake. Halafu leo anasema huyo aliyekuwaanapigiana naye simu ni gaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mtu amemlipa huyoanayeitwa gaidi fedha baada ya huyu mtu kufanya ugaidi,leo anasimama na kusema sisi ni magaidi. Sheria ya ugaidiinasema, anayelipa fedha kwa magaidi ni gaidi anatakiwaakamatwe na afungwe. Anayeshirikiana na magaidi,anayewasiliana nao…

SPIKA: Mheshimiwa Tundu Lissu ndiyo nilivyosemakwamba tumalize.

WABUNGE FULANI: Ahaaa!

SPIKA: Jamani tuelewane kwa utaratibu. Nimesemajana kulisemwa, leo kumesemwa, tukasema tuishie hapo,lakini kama mnataka semeni na ila mjue na wenginewatasema. Endelea Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Spika, ahsante.Natumai muda wangu umelindwa wakati nimekaa.

SPIKA: Umelindwa.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Spika, sikuambayo mkutano wa kigaidi unafanyika, Mheshimiwa humu

Page 59: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

59

12 APRILI, 2013

ndani amezungumza na mmoja wa hao magaidi, wiki mbilibaadaye akamlipa fedha, huyu ni gaidi anatakiwaakamatwe. Habari ya ugaidi ni mambo ya kutunga ya Jeshila Polisi na baadhi ya watu walioko humu ndani. Kamawanafikiri hakuna ushahidi watashangaa. (Makofi)

KUHUSU UTARATIBU

MHE. ANNA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,ninatumia Kanuni ya 64: “Kwamba Mbunge hatatoa ndaniya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli”. Sasa namwombahayo anayoyasema kwamba kuna watu wamelipwa humundani, baada ya muda wamepigiana simu. Kwa sababufedha amezitamka na amesema kwa uhakika hebu atoe huouthibitisho humu ndani ya Bunge. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwanza Kamati yaKanuni itabidi tukutane, kwa sababu tumekubalianawenyewe kwamba tufike mahali tuwe tunashauriana. Hizokesi zote mnazozungumza zipo Mahakamani. Sasaninachokisema, naomba msikilize, tatizo lenu ni kulalamika,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani akiwa kiongozi mkubwa sana,sikutaka kuingil ia hotuba yake na wengine wotewalinyamaza. Katika dunia everybody has got the right toreply.

Sasa tunachokisema, hii ndiyo anayosema mamaAnna Abdalla, mengine yapo Mahakamani kwa ninihatupendi kuheshimu mambo ya Mahakamani. Nimesematuishie hapo, tuzungumze yetu. Sasa mkitimua hapa kunaripoti nzima hapa, mta-defend nini na mimi nilimpa heshimaMheshimiwa, nilimpa heshima kwa sababu ni kiongozi wenu.Kwa hiyo, naomba tuheshimiana, tuanze kuzungumza vituambavyo vipo katika mazungumzo yetu. Mheshimiwa TunduLissu naomba uendelee.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Spika, ahsante,naomba muda wangu ulindwe. Hotuba ya Kiongozi waKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatakiwa ijibiwe na WaziriMkuu na siyo mtu mwingine.

Page 60: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

60

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, sasa naomba niendelee.

SPIKA: Endelea lakini tutunze heshima ya Mahakama.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Spika, sijatajachochote kinachohusu Mahakama, nimesema mamboyanayofanywa na Polisi na marafiki zao na watu wenginewaliomo humu ndani, hayo mambo hayako Mahakamani.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushahidi upo kama MheshimiwaAnna Abdalla anautaka wa malipo yaliyofanywa tarehe 14Januari, mwaka huu kwa mmoja wa magaidi. Mawasilianoyaliyofanyika tarehe 28 Desemba na mmoja wa magaidi namarafiki zake walioko humu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumze masuala yaKatiba. Mchakato wa kutengeneza Katiba mpya umetekwanyara na unachafuliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba naSerikali. Mwenyekiti wetu na Kiongozi wa Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni alizungumza jana. Msimamo wetu nikwamba, kwa vile Tume inachakachua utaratibu wa kupataKatiba Mpya, CHADEMA hatupo, siyo tu kwambatutanyamaza, hatutanyamaza, tutatembea nchi nzimakuwaambia wananchi kwamba huu mchakato siyo waKatiba Mpya, huu ni mchakato wa Katiba ya CCM.

Mheshimiwa Spika, tutawambia wananchi wetukwamba, kwa sababu huu ni mchakato wa Katiba ya CCMya mambo yale yale, ya watu wale wale na ya chama kilekile, kura ya maoni itakapofika hiyo Katiba ikataliwe naWatanzania. Hatuwezi tukakubali Tume ikatumia fedha zaumma, ikaharibu utaratibu wa kupata Katiba, ukaingiza nchihii kwenye machafuko.

Mheshimiwa Spika, uchakachuaji wa mfumo wakatiwa utaratibu wa kupata Katiba mpya kwa umeiingiza Kenyakwenye maafa mwaka 2008, uchakachuaji wa utaratibu wakupata Katiba Mpya umeiingiza Zimbabwe kwenyemachafuko makubwa kwa miaka 15, mpaka juzi walipofanya

Page 61: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

61

12 APRILI, 2013

maridhiano kila mtu akakubali, wakatengeneza Katiba mpyaambayo kila mtu anaikubali. Utaratibu unaofanywa na Tumeya Mabadiliko ya Katiba wa kuchakachua Katiba utaingizanchi hii kwenye machafuko. Nilishasema kwenye Kamatinasema mbele ya Bunge Mungu atusaidie, lakini hatuwezitukakubali Tume ikaharibu mchakato wa Katiba. (Makofi)

SPIKA: Kengele ya pili, Mheshimiwa Tundu.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Eeh!

SPIKA: Kengele ya pili.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Kengele ya pili?

SPIKA: Tunaendelea Mheshimiwa Felister Buraatafuatiwa na Mheshimiwa Beatrice Shellukindo naMheshimiwa Salum Barwany ajiandae.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika,nimeshangaa msemaji aliyepita alivyotumia muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwaaliyemaliza kuongea kwamba, ametambua kazi kubwailiyofanywa na Chama cha Mapinduzi katika suala la elimuna watoto wake na yeye mwenyewe amesoma katika shulehizo ambazo zimejengwa na Chama cha Mapinduzi.Amesahau kwamba kipindi kilichopita, shule hazikuwa nyingikama sasa hivi. Kwa hiyo, takwimu zake alizotoa naombaazirekebishe kwa sababu katika kipindi cha nyuma shulehazikuwa nyingi kama sasa hivi, kama kipindi cha mwaka2005 na kipindi hiki. Naomba arekebishe takwimu zake.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Serikali yaChama cha Mapinduzi kwa mambo makubwa ambayoimefanya katika kipindi cha utawala wake. Tumejengabarabara nyingi na tumefanya mambo mengi, lakini kunajambo moja tu limeshindikana katika Serikali hii, jambo hilo nikuhamisha Serikali kuja katika Makao Makuu ya Chama cha

Page 62: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

62

12 APRILI, 2013

Mapinduzi au Makao Makuu ya nchi ambayo ni Mkoa waDodoma.

Mheshimiwa Spika, tumekwishasubiri kwa muda mrefuna kila mwaka tunaliongelea hili kwamba, Serikali inatakiwakuhamia Dodoma na kama hawataki basi hili suala la kusemakwamba ndiyo Makao Makuu lifike mwisho sasa.

Mheshimiwa Spika, CDA kwa mwaka huuwametengewa shilingi milioni 500, milioni 500 hawezi kufanyakazi yoyote. Wamepima viwanja hawana fedha za kulipafidia kwa wananchi, viwanja vipo, wananchi hawawezikugawiwa viwanja, Wabunge wanataka viwanja, wananchiwanataka viwanja kwa ajili ya kuendeleza Mji wa Dodoma,lakini CDA hawana fedha za kulipa fidia. Mwaka huuwamepewa shilingi milioni 500. Bajeti iliyopita mwaka janawaliambiwa kwamba watapima Mji Mkuu wa Serikali katikatiya Manispaa Dodoma na Wilaya ya Chamwino, hizo fedhahazijatoka mpaka leo.

Mheshimiwa Spika, CDA hawawezi kupima Mji Mkuuwa Serikali kwa sababu hawana pesa. Naiomba Serikaliizingatie hilo kwamba, ifikapo mwaka 2015 tuone juhudiambazo zimefanywa na Serikali katika kuhamia MkoaDodoma au Mji wa Dodoma. Bado tunashuhudia majengomakubwa ya Serikali yakijengwa Dar es Salaam, badotunashuhudia miundombinu mingi ikifanyika Dar es Salaamlakini Dodoma bado.

Mheshimiwa Spika, tunashukuru tumejengewabarabara, barabara zimetengenezwa. Kwa hiyo,miundombinu ya barabara ipo safi kabisa, lakini bado Serikalihaijafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuhamia Dodoma.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tulikwenda naMheshimiwa Waziri katika maporomoko ya Ntomoko kuleKondoa na Waziri Mkuu akaahidi kutafuta fedha kwa ajili yamatengenezo ya miundombinu ya maporomoko yaNtomoko.

Page 63: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

63

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini mpaka leo ninavyoongea,hakuna kila kitu kinachoendelea katika maporomoko yalena tulimweleza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwambamporomoko yale yanahudumia maji vijiji 17. Lakini mpakaleo ninavyoongea hata kwenye bajeti ya Serikali hakunafedha zilizotengewa kwa ajili ya miundombinu ya Ntomoko.Namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu hii ilikuwa ahadi yaketangu mwaka jana hebu alifikirie na litimie sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumze suala la fedha zaMiradi ya Maendeleo. Fedha za miradi ya maendeleozinachelewa sana. Mwaka huu katika Mkoa wa DodomaWilaya ya Bahi mpaka mwezi Machi, walipata asilimia 12 tu,Wilaya ya Kongwa walipata asilimia 15.3, Wilaya ya Kondoawalipata asilimia 11. Kwa hali hiyo, hatuwezi kufika mbalikatika miradi yetu ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, tuna Hospitali ya Mkoa hapaambayo inajenga wodi ya watoto na wodi ya wazazi, lakinimiaka tano sasa wodi ile haijakamilika. Mwaka 2008 tulikuwatunahitaji bilioni 1.5, mpaka sasa nadhani tunahitaji fedhanyingi kutokana na ule mradi kusimama. Serikali hebu iangaliehilo. Miradi ambayo imeshaanza ni bora ikakamilishwa kulikokuanza miradi mingine.

Mheshimiwa Spika, tuna jengo la Ofisi ya Mkuu waMkoa, mpaka leo Mkuu wa Mkoa anakaa ofisi ya ajabu sanahapa Dodoma. Nadhani Wabunge hamjawahikumtembelea, anakaa ofisi ya ajabu sana na hapa ndiyoMakao Makuu ya Serikali na Bunge linakutana hapa na kunaugeni mwingi tu hapa, lakini Mkuu wa Mkoa wa Dodomahana ofisi. Majengo ambayo hayajakamilika ya Serikali,Serikali ingeweka utaratibu wa kuyakamilisha ili value formoney ionekane.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo la ajira kwa kada zachini katika Halmashauri zetu, Watendaji wa Vijiji, Wahudumu,Madereva kwamba kada hizo zote lazima waajiriwe na Tumeya Utumishi. Siyo jambo la haki kabisa. Halmashauri nyinginehazina Wahudumu, hazina Watendaji wa Vijiji kwa sababu

Page 64: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

64

12 APRILI, 2013

lazima ajira itoke Dar es Salaam. Naomba suala hili litazamweupya ili watendaji hawa wa kada za chini waajiriwe mojakwa moja na Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka jana tulipangafedha kwa ajili ya bwawa eneo la Farukwa na bwawa hililingewahudumia wananchi Wilaya ya Chemba na wananchiwa Wilaya ya Bahi, mpaka leo hakuna kinachoendelea katikaeneo lile. Wakulima wa Chemba na wakulima wa Bahiwanasubiri bwawa hili kwa hamu zaidi kwa ajili ya kilimo chaumwagiliaji cha mpunga, lakini mpaka leo hakunakinachoendelea.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2010 tuliapa hapaWabunge wote tukiwa sana na tukiwa na wadhifa sana, lakinikitu ambacho tunaona kama tumetengewa na Serikali yetu,ni kuhusu fedha za kuchochea maendeleo katika maeneoyetu, Wabunge wa Viti Maalum. Hatujaona mkakati wa dhatiambao Serikali inafanya kutusaidia Wabunge wa Viti Maalumkatika hili. Naomba hili pia lifikiriwe na Serikali kuwakumbukaWabunge wa Viti Maalum kwa nini katika hilo tunatengwa?

Mheshimiwa Spika, nizungumze sasa kuhusu NIDAShirika la Vitambulisho la Taifa. Nawapongeza sanawafanyakazi wa NIDA kwa sababu ni miaka 50 sasaWatanzania hatuna vitambulisho. Lakini kwa mwaka huuNIDA wameweza kutoa vitambulisho kwa ajili ya Watanzania.Lakini tatizo walilonalo watu wa NIDA hawana fedha zakutosha. Bajeti iliyopita waliomba shilingi bilioni 150, lakiniwalipata bilioni 10 tu. Hawawezi kufanya jambo lolote mpaka2015 kutoa vitambulisho kama tunavyodhani.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kama kweliwanataka Watanzania wapate vitambulisho, kwa mwaka2015 kila Mtanzania awe na kitambulisho cha Taifa wapewefedha za kutosha kwa ajili ya kufanya kazi ya kutoavitambulisho kwa Watanzania, bila hivyo hawataweza kufikiamalengo kama tunavyotarajia.

Page 65: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

65

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kuna asilimia 20 ya ruzuku ya fidiaya vyanzo vya mapato ambavyo vilifutwa na hii asilimia 20inatoka Serikali kuu.

Mheshimiwa Spika, huwezi kuamini mwaka wa fedhaunakwisha Halmashauri hazijapokea hizo fedha na kamawamepokea, wamepokea asilimia ndogo sana, kwa hiyo,shughuli za maendeleo katika vijiji vyetu haziendi, zinasimamakwa sababu fedha hazileti kwa wakati muafaka na Wizaraya Fedha. Naiomba Serikali yetu kwamba, ifike wakati sasafedha zifike kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tusichezee amani ya Tanzania.Wale viongozi wa dini, nawaomba sana Watanzaniawenzangu...

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, ahsantena naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nitawaita Mheshimiwa BeatriceShellukindo, Mheshimiwa Salum Barwany, Mheshimiwa IgnasMalocha, Mheshimiwa Dkt. Kebwe Kebwe, MheshimiwaPauline Gekul na Mheshimiwa Vicent Nyerere.

Mheshimiwa Beatrice Shellukindo!

MHE. SALUM KHALFAN BARWANY: Mheshimiwa Spika,ahsante.

SPIKA: Ahh! Nimemwita Mheshimiwa BeatriceShellukindo.

WABUNGE FULANI: Hayupo.

SPIKA: Aaa, hayupo, haya endelea MheshimiwaBarwany!

Page 66: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

66

12 APRILI, 2013

MHE. SALUM KHALFAN BARWANY: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi ili niweze kujadili hotubahii ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge langu la tatu la bajetitangu tuingie kwenye Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hoja yangu ya kwanza marabaada ya kuchaguliwa kwangu, nilizungumzia suala zima lamgawanyo wa rasilimali katika nchi. Nilitahadharisha nchi nanikatahadharisha Wabunge wenzangu kwamba, iwapotutafanya mchezo, tukafanya masihara juu ya mgawanyowa rasilimali katika Taifa letu, nchi yetu tutaiingiza katika jangakubwa na maafa makubwa ya mgogoro wa vita yawenyewe kwa wenyewe.

Mheshimiwa Spika, hii imetokea katika nchi nyingiduniani hata katika Bara letu la Afrika. Leo Sudan kunamgogoro mkubwa na nchi nyingine katika Afrika kwa sababuya mgawanyo mbovu wa rasilimali katika nchi na hililinanyemelea sasa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, mgawanyo mbaya wa rasilimaliunapelekea wananchi katika maeneo mengi kulalamikiamgawanyo huu. Matokeo mabaya ya Mikoa ya Lindi naMtwara juu ya suala nzima la gesi, ni matokeo ya mgogorowa kutokugawana vizuri rasilimali. Kwa nini leo watu waKusini wanalalamika kwamba, ni katika maeneo ambayoyapo nyuma kimaendeleo, wananchi wa Kusini ni wazalishajiwakubwa wa korosho, lakini wakati huo huo wananchi waKusini tayari wamepata eneo ambalo gesi inatoka. Serikaliya Chama cha Mapinduzi inajisifu sasa, umaskini wa Taifaletu unaondoka, lakini ilikuwa muhimu watu wa Kusini sasa,kujua maslahi yao ambayo yanatokana na gesi ambayo ipokatika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kumuua paka wako, basiunamtafutia jina mbaya. Huu ni utaratibu wa watu woteambao hawawatakii mema wenzao, mgogoro wa watu wa

Page 67: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

67

12 APRILI, 2013

Kusini ulikuwa ni Serikali kukaa na watu wa Kusini kutaka kujuanini wanachokihitaji katika maendeleo yao. Kwa muda mrefukabisa, imefikia mahali leo, wanapotoshwa watu wa Kusini,wanapotoshwa Watanzania wakiambiwa kwamba watu waKusini hawataki gesi yao itoke kusini, si kweli. Wananchi waMikoa ya Kusini wanataka Serikali ilete sera kuonesha ninamna gani Watanzania watanufaika juu ya rasilimali hii.

Mheshimiwa Spika, gesi ni utajiri mkubwa na Mataifamengi duniani yametajirika kupitia mafuta na gesi. Lakinikatika Taifa letu tumedai mara nyingi katika Bunge hili, hebutuleteni mikataba, leo mikataba inasainiwa na Makampunimbalimbali ya Kimataifa juu ya uchimbaji wa gesi katikaMikoa Kusini, lakini wanasaini mikataba hiyo kwa sera gani,kwa mwongozo upi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni watu wachache wanakaa nakufanya maamuzi juu ya rasilimali za Watanzania, gesi ni utajirimkubwa. Tunataka Serikali ilete sera Bungeni, sisi kamawawakilishi wa wananchi tuweze kueleza wananchi wetukwamba, mpango wa Serikali ni huu. Leo sisi Wabunge waKusini ni mabubu, tunashindwa kuwaeleza wananchi wetukwamba, mpango wa Serikali juu ya gesi ukoje, hakunaMbunge ambaye anaweza kutwambia hapa mkakati waSerikali juu ya utajiri huu uko wapi?

Mheshimiwa Spika, hili limeleta mkanganyiko naisifikiriwe kwamba, watu wa Kusini wamenyamaza leohapana, bado watu wa Kusini msimamo wao upo pale pale,wanaitaka Serikali ieleze, Ilani ya Chama cha Mapinduzikatika Awamu ya Nne ilisema, itaweka kinu cha kuchambuagesi Mtwara kwa megawati 300, umeme utapatikanaMtwara utapelekwa Dar es Salaam, siyo gesi kutoka Mtwarakwenda Dar es Salaam. Leo tunaambiwa kwamba gesiinatoka Mtwara kupitia bomba kwenda Dar es Salaam,wananchi wa Lindi na Mtwara wanataka waelezwe.

Mheshimiwa Spika, miaka 20 iliyopita wananchi waKusini waliambiwa kwamba gesi ya Kilwa Songo Songoitapelekwa Dar es Salaam na gesi ya Mtwara Mnazi Bay

Page 68: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

68

12 APRILI, 2013

itanufaisha watu wa Kusini na kutakuwa na gridi ya Taifa,mpaka leo gesi ya Kusini inatoka, lakini gridi ya Taifa katikaMikoa ya Lindi na Mtwara haipo. Huo ndiyo mgawanyombaya wa rasilimali katika nchi na ndiyo unaweza kuletamigogoro na watu wakaingia katika machafuko makubwakatika Taifa lao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la stakabadhighalani. Huu ni mwezi wa sita tangu wakulima wa koroshowavune, lakini mpaka leo mkulima bado hajauza koroshozake, anataka awapeleke shuleni watoto wake, anatakakuandaa mashamba yake kwa kilimo kipya, lakini mpaka leowananchi wetu wamekatishwa tamaa.

Mheshimiwa Spika, tunaambiwa hapa na viongozi waSerikali tu, kwamba stakabadhi ghalani imewanufaishawakulima, lakini wakulima wenyewe bado hawajasemakwamba, wamenufaishwa vipi na stakabadhi ghalani.

Mheshimiwa Spika, leo tunazungumzia soko la duniala korosho limeanguka, lakini ni korosho gani, ni korosho ghafi.Lakini leo tuna Viwanda 12 vya Korosho katika Mikoa ya Kusiniambao ni mkopo katika mabenki ya dunia. Viwanda vilevyote wamechukua viongozi wa Chama cha Mapinduzi nandio wanavimiliki viwanda vile leo. Ni mali yao, wanatumiakufanya maghala, baada ya kufanyia process korosho,tukauza korosho ambazo tayari zimetengenezwa, tukapatasoko zuri katika soko la dunia, lakini mpaka leo tunauzakorosho ghafi.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana tunapozungumziasuala la korosho, wananchi wa kusini bado hawajaielewaSerikali za CCM wanavyoing’ang’ania stakabadhi ghalanihata kama bado haijawanufaisha wananchi wao katika zaohilo.

Mheshimiwa Spika, imezungumzwa katika miaka yanyuma kwamba, msimu wa korosho unapofika, wananchiwote wananafsika na zao lile. Lakini leo msimu wa koroshounafika, huwezi kujua kwamba huu ni msimu wa korosho

Page 69: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

69

12 APRILI, 2013

katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kuna umaskini uliokithirikatika mikoa ile kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.Tunaitaka Serikali itazame upya mfumo wa stakabadhighalani, unawanufaisha vipi wakulima wa Mikoa ya Kusini,Lindi na Mtwara.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nizungumzie habari yaHalmashauri yangu. Mwaka 2010 Manispaa ya Lindiimetangazwa kama ni Manispaa kutoka katika Halmashauriya Mji wa Lindi. Lakini bado wananchi wa Lindi hawajaonaumuhimu wa kuwa na Manispaa hiyo. Ruzuku inayotolewana Serikali ni ile ile ya Halmashauri ya Mji na hii nimeizungumzamara nyingi hapa, ni shilingi bilioni nane, lakini tumeongezewatena mzigo wa Kata tano kutoka Halmashauri ya Wilaya.

Mheshimiwa Spika, tunaambiwa kwamba maslahi yaManispaa ni zaidi ya Mji. Lakini bado Serikali haijaoneshaumuhimu wa Manispaa ya Lindi kwa kuongeza ruzuku yamaendeleo. Hili nimelizungumza sana, nimelipigia kelele, lakiniSerikali imekuwa kiziwi na pofu juu ya hoja hii ya wananchiwa Lindi. Tumeongezewa shule, dispensari, barabara lakinibado ruzuku inayopatikana katika Manispaa ya Lindi ni ile ileiliyokuwa ikitolewa kwa Halmashauri ya Mji wa Lindi katikamiaka 10 iliyopita.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la Bandari yaLindi na ndio kilio cha wananchi wa Lindi na ni ahadi ya Raishiyo. Ahadi ya Rais ni kitu chenye kuheshimiwa. MheshimiwaRais ameahidi katika mambo ambayo atayashughulikia, nikuhakikisha kwamba kutakuwa na Bandari ya Lindi, leo katikabajeti tunaambiwa kwamba kuna Bandari ya Bagamoyo. Hivikuna haja gani katika nchi yetu kujenga Bandari nyingine.Tuna Bandari Mtwara haijakidhi vigezo vya matumizi yaBandari na pia bandari ya Tanga ambayo nayo badohaijakidhi mahitaji ya bandari.

Mheshimiwa Spika, tuna bandari nyingi katika nchiyetu, kwa nini leo tutumie mabilioni ya fedha, tutumie mikopoya Kimataifa, kujenga bandari wakati bandari zetu ambazotunazo, bado hazijafikia kiwango cha mahitaji ya bandari

Page 70: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

70

12 APRILI, 2013

zile. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali. Hivyotunaomba kwamba, ahadi za Mheshimiwa Rais ambazohuwa zinatolewa kwa wananchi, wananchi wanatoa kurazao kwa mujibu wa sera na Ilani unapochaguliwa kuwakiongozi na hutekelezi ahadi yako, unatapeli kura zawananchi wale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunataka wananchi wahakikishekwamba kura zao zinakidhi haja ya Ilani ya Uchaguzi yaVyama vya Siasa. Hivyo, mwaka 2010 Chama cha Mapinduzikilipata ridhaa Lindi kuliko wagombea wote wa Urais, kwamujibu wa mahitaji ya watu wa Lindi, waliahidiwa kwambabandari yenu itajengwa na itafanya kazi, leo tumeshafikamiaka saba, Bandari ya Lindi bado haijafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina zaidi ya hapa, lakinimgawanyo wa rasilimali ni muhimu katika Taifa. Ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Barwany. Sasa namwitaMheshimiwa Malocha na Mheshimiwa Dkt. Kebwe Kebweatafuatia.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kupata nafasi hii ili na mimi niweze kuchangiajuu ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Katika hotubayangu, naomba nianze na migogoro ya ardhi iliyopo nchini.

Mheshimiwa Spika, utakubaliana nami kwamba nchihii sasa hivi kila kona ina migogoro ya ardhi na ni ukweliusiopingika, ukienda Kilosa migogoro ipo, Babati na maeneomengine. Migogoro hii inatokana na Serikali kutochukuahatua za haraka za utatuzi, Serikali inachukua hatua wakatitayari uvunjifu wa amani umeshatokea kwa sehemu kubwa.

Mheshimiwa Spika, nimeona nizungumzie hili kwasababu hata kwenye eneo langu, Wilaya ya Sumbawangakuna mgogoro mkubwa ambao sasa hivi unahatarisha amanikubwa sana. Umekosesha amani wananchi na hatamwekezaji mwenyewe amekosa amani. Mgogoro huo ni wa

Page 71: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

71

12 APRILI, 2013

muda mrefu, lakini Serikali haijatoa utatuzi na matokeo yakehivi sasa ni uvunjifu wa amani, watu kuuawa, mali yamwekezaji kuharibiwa, wananchi kunyanyaswa, kukatwamasikio, kuchomwa moto na vyuma vyenye ncha kali,wananchi kuwa maskini, wananchi kutangatanga na kukosamahali pa kulima.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali ya Mkoakufanya jitihada za kuunda Tume, kuangalia chanzo chamgogoro huo na kubaini chanzo ni kwamba, vij i j ivinavyozunguka shamba la Malonje vyenye mgogoro huo,vilipimiwa ardhi hiyo toka mwaka 1974 na mwekezaji amekujakupewa nyuma. Kwa hiyo, mchonganishi mkubwa wamgogoro huu ni Serikali yenyewe. Serikali inagonganisha katiya wananchi na mwekezaji, matokeo yake wananchi namwekezaji wanaumizana.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali ya Mkoaimeliona hilo na imeijulisha Serikali Kuu. Nashangaa kwa niniSerikali inachelea kuchukua maamuzi. Bunge lililopitanilimwona Waziri wa Ardhi nikamweleza, akasema mgogorohuu ameshamwandikia Waziri Mkuu, anasubiri utetezi. Sasanashindwa kuelewa, kwa nini Serikali inachelewa wakatiwananchi wanaumia, kuna muujiza gani juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Spika, kama kuna viongozi ambaowalitumia nafasi zao kukiuka utaratibu, kumpa mwekezajikinyume na utaratibu, kwa nini hatua zisichukuliwe na kwanini Serikali isichukue hatua za makusudi kunusuru mgogorohuu. Matokeo yake kunatokea uvunjivu wa amani. Kwa hiyo,naishauri Serikali, katika mgogoro huu ichukue hatua zaharaka ili kurejesha amani katika maeneo yale.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mgogoro huu nakwa sababu ya nchi yetu imeshaingiliana na mambo yakisiasa, unakuta mtu mwingine anazusha, Mbungeumekwenda kusalimia, kuona wananchi, mtu mwingineanazusha kwamba, Mbunge amechochea, wakatiwananchi wametoa malalamiko na wewe umewaambiautayafikisha Serikalini, wanasema Mbunge anachochea.

Page 72: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

72

12 APRILI, 2013

Naomba kabisa kukanusha utaratibu huu na Serikali ichukuehatua juu ya jambo hili na ikitaka kupata ukweli itume Tumeiende ikaangalie, itaona mateso ambayo wananchiwanayapata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, l ingine ambalo nimeonanizungumzie ni suala la kilimo. Kumekuwa na tatizo kubwa laukosefu wa soko la zao la mpunga, soko lisiloeleweka.Nashangaa kwa nini Serikali inafikia hatua ya kuingiza mchelekutoka nje, wakati ndani ya nchi bado tunao mchele mwingiambao hauna soko. Mchele unaoingizwa nchini, ni mcheleambao hauna hata ladha na wala hatujui umezalishwakutumia kemikali za aina gani. Matokeo yake tunaachamchele ambao umezalishwa na wakulima wetu, wenyeladha nzuri, tunaingiza mchele mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, juzi wakati nakuja Bungeninimepitia maeneo ya Sumbawanga, mchele umejaa, ukijapale Tunduma, mchele umejaa, ukija Mbeya, mcheleumejaa, ukija Morogoro, mchele umejaa, hawana kwa kuuzana cha ajabu sasa hivi wameshaanza mavuno ya msimu huu,wananchi hawajui mpunga ule watauza wapi.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itafute utaratibuwa kununua mpunga kama inavyofanya kwenye mahindina kukusanya kutunza kwenye maghala, kama inatokea kunamaeneo yanakosa mchele, basi Serikali iweze kuwashawishiwafanyabiashara waweze kutawanya katika maeneo yale,kuliko kuingiza mchele nchini, wakati upo mchele mwinginemwingi ambao unazalishwa na wakulima na Serikali yenyeweinahimiza kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo natakanilizungumzie, ni juu ya Serikali kuangalia namna ya kutoaposho angalau kwa kiwango kidogo kwa Wenyeviti wa Vijiji,Wenyeviti wa Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji. Lazimatukubaliane kuwa, dunia ya leo hakuna mtu anayefanya kaziya kujitolea. Unakuta hata vifaa vyenyewe vya ujenzivinashushwa mtu anadai hela, sembuse huyu kiongozi

Page 73: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

73

12 APRILI, 2013

ambaye amechaguliwa na wananchi, muda woteanatumikia umma kuanzia asubuhi hadi usiku na anakosamuda kabisa wa kufanya shughuli zake za kusaidia familia.

Mheshimiwa Spika, anahamasisha wananchi katikashughuli za maendeleo, anapokea viongozi, anasuluhishamigogoro, anashiriki katika misiba mbalimbali kama kiongozindani ya kijiji, lakini mtu huyu Serikali haijamwangalia.Naishauri Serikali, kama kweli tuna dhamira njema kwamba,binadamu wote ni sawa na tunataka Serikali yetu ifanye kazikwa pamoja, naomba Serikali hata kwa kiasi kidogo iwezekuwaangalia viongozi hawa.

Mheshimiwa Spika, l ingine ambalo natakanilizungumzie ni suala la kushuka kwa kiwango cha elimunchini. Katika kipengele hiki, naomba nizungumzie kwa sualala Wakaguzi wa shule za msingi na sekondari. Nimejioneamwenyewe kutoka kwenye Mkoa wangu wa Rukwa.Ukiangalia Wakaguzi waliopo pale mkoani wana upungufumkubwa wa vyombo vya kufanyia kazi, hata ofisi wanayokaani kama wanafanya mkutano kila siku, hawana ofisi maalum.Wanakaa kwenye ofisi ambayo ukienda, utadhani ofisi ileinaendesha mikutano kila siku maana wanarundikana.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba Serikali ijaribukutazama kada hii na iwasaidie maana hawana nyenzo zakufanyia kazi na maeneo mengine ambayo wamepewamagari, hawajapewa fedha za kuendesha vile vyombo. Kwahiyo, unakuta magari yale yanatumiwa na Halmashauri, yeyehana mamlaka na madereva hawana.

Mheshimiwa Spika, ukiacha hilo, mtu anayemkaguamwenzake anapaswa athaminiwe na Serikali imwangaliekatika suala zima la uwezeshi i l i aweze kujiamini naanapokwenda kukagua awe anajiamini. Lakiniusipomwezesha mtu huyu na anakwenda kumkagua mtuambaye wakati mwingine anamzidi hata mshahara, unyongeni mkubwa sana na hawezi kufanya kazi kama ilivyo.

Page 74: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

74

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kutokana na kutowajali watuhawa wamekata tamaa, wengine wanatamani hata warudimadarasani wakafundishe, kwa sababu wanaona kuwaMkaguzi tu kwa jina tu, cheo kikubwa, lakini maslahi hakuna,ni kama nafasi ya mateso. Kwa hiyo, naomba Serikali hii ijaribukuwaangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, halafu vile vile chombo ambachokingekuwa karibu na wao ni TSD. TSD iko Dar es Salaam sijuiTemeke au Ilala. Ningeomba Serikali irudishe mfumo wa kuwana TSD kwenye Wilaya mbalimbali ili chombo hiki kiweze kuwakaribu na Wakaguzi hawa na kiwe ni chombo vile vile chakuwasaidia katika kutatua matatizo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo natakakulizungumzia, ni Bodi katika shule zetu za Sekondari.Naiomba sheria ibadilishwe...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita Mheshimiwa Dkt.Kebwe Kebwe, atafuatiwa na Mheshimiwa Pauline Gekul.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia. Nasemahivi, msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Taarifa hii yakiuchochezi, utafute utaratibu wa kutozikubali. Taarifa ya KUB(Kiongozi wa Upinzani Bungeni) ambaye mimi namwita niKiongozi wa Uchochezi Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilishangaa Mheshimiwa WaziriMkuu anapewa mambo mazito kwa kweli ya kumdhalilisha,lakini ukweli ni kwamba, mbona baada ya kutoka Bungenihapo nje, anakwenda anasema Mheshimiwa Waziri Mkuunaomba barabara pale kwangu Hai. Kwa ushahidi ambaoMheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea

Page 75: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

75

12 APRILI, 2013

Wilaya ya Hai, KUB alitamka wazi kwamba, mnyonge,mnyongeni haki yake mpeni, mbona hayo hajasema Bungenihapa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Kampeni za Uchaguzi Mkuumwaka 2010, wenzetu walisema jamani tupeni Serikali naWatanzania nao wanajua, tupeni Serikali sisi, baada ya hapo,siku 100 Katiba iko mezani, sasa mchakato wa Katibaunaendelea, wanasema hawataki Katiba. Naiomba Serikalishupavu ya Chama cha Mapinduzi sasa ifanye kazi kamaSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri ni kwamba, wenzetuwanavyosema wanakwenda mitaani kuchocheaWatanzania waandamane kwa sababu ya Katiba, hili sualasi dogo, suala hili ni la kuchukulia hatua. Serikali ijipange kwasababu kazi ya Serikali sio kuongoza, kazi ya Serikali nikutawala, kwa hiyo, Serikali itawale.

Mheshimiwa Spika, naomba nikumbushe yaliyotajwakatika hotuba ya Waziri Mkuu katika hii sehemu ya CDA. CDAwamepangiwa shilingi bilioni 4.4 kwa ajili ya mishahara. Lakinikama hiyo mishahara mikubwa kiasi hicho hata matumizimengineyo ingekuwepo lakini sifuri. Lakini hiyo imechukuakaribu asilimia 50 ya mishahara ambayo iko katika Ofisi yaWaziri Mkuu, kama ni kosa la uchapishaji ijulikane, lakini kamani hela zimechomekwa pale Serikali ilifanyie kazi suala hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala zima la MakaoMakuu kuhamia Dodoma. Hivi kweli kuna utashi wa kuhamiaDodoma? Sisi enzi yetu tukiwa wadogo, magazeti yalikuwamachache sana nchini, kulikuwa na gazeti moja linaitwaTaifa. Mzee wetu marehemu Mwenyezi Mungu amrehemu,Mzee Kawawa alionesha ishara ya Serikali kuhamia Dodomaakipanda treni. Sasa kama ishara hiyo ya kuhamia Dodomampaka leo hii mwaka wa 36, Serikali haihamii Dodoma.

Mheshimiwa Spika, hivi kweli kuna utashi wa Serikali?Mbona tunaona majengo mengi mapya ya Wizara

Page 76: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

76

12 APRILI, 2013

mbalimbali yanajengwa Dar es Salaam ndani ya kipindi hiki,ikiwemo Wizara kwa mfano, ya Maliasili, Utumishi, Maendeleoya Jamii, Jinsia na Watoto na Wizara zingine, majengo mapya,maghorofa makubwa, hayo kwa nini hayakujengwaDodoma? Suala hili si la kufanyia utani, kuwe na utashi kabisadhahiri kama ilivyokuwa Chuo Kikuu cha Dodoma. Utashiulivyokuja mbona kimejengwa chuo kikubwa kuliko vyuovingine vyote katika Afrika Mashariki na Kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzetu wa Malawi na Nigeriawalikuja kusoma mfumo wa CDA. Lagos kuhamia Abujaimewachukua miaka 10 mpaka 15 na leo wako pale. Sasainakuwaje wale wamekuja, ni wanafunzi wetu, halafuwamepiga hatua kuliko sisi. Kwa hiyo, suala hili naomba bajetiinayokuja mwakani panapo majaliwa, tusiunge mkono kamahakuna maelezo dhahiri ya Serikali kuhusu kuhamia Dodoma.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika taarifa ya Waziri waTAMISEMI, ukurasa wa 30, kuna suala limezungumziwa la ulinzishirikishi wa misitu na maeneo oevu. Ukiangalia Mto Maraunazidi kwisha kwa sababu ya hali halisi ya ulinzi na ushirikishiwa jamii ni mdogo. Ukijaribu kuangalia Sheria namba 5 yaVijiji ya mwaka 1999 haiwezi kusaidia vijiji hivi ilinde hifadhi yaule msitu.

Mheshimiwa Spika, ombi langu, Serikali ichukue msituule uwe chini ya Serikali, chini ya Maliasili. Kwa sababu katikamsitu ule kuna miti mizuri, kuna miti haipatikani sehemuzingine, wako viboko, kuna mamba katika mto ule. Sasa kwanini maliasili isichukue eneo lile kwa ajili ya kuimarisha sualala ulinzi. Suala ambalo bajeti imetengwa shilingi bilioni 4.3katika bajeti ya mwaka huu, inashangaza kwamba hadi sasani shilingi 671,000,000 zimekwenda. Je, katika mazingira hayaje tutaweza kulinda mito hii na maeneo oevu?

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala zima la maslahiya Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji. Mwenyekiti wewe huwezikwenda kufanya kazi ya kijamii wakati unaacha utapiamlounaota nyumbani kwako. Haiwezekani Diwani, mshahara

Page 77: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

77

12 APRILI, 2013

kidogo kwa maana ya posho na Wenyeviti wa Vijiji ambaohawana chochote, wasimamie shughuli za maendeleo ukitiliamaanani kwamba Diwani kwa mfano, ndio Mwenyekiti waKamati ya Maendeleo ya Kata, hawezi akasimamia hayamaendeleo wakati yeye mwenyewe anaishi kwakuombaomba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kuhusu suala la Jeshila Kujenga Taifa. Nashauri kwanza muda ambaoumepangwa, kwa hawa wenzetu Waheshimiwa Wabungewaliokwenda, wengine watu wazima kama mimi, ndugu yetuMheshimiwa Yahya akiwa ni mfano. Hili nililichangia katikabajeti ya Ulinzi mwaka jana, tubadilike tusifanye mambo kwamazoea, Serikali ilitazame upya suala hili, tunapata watuwengi kutoka nchi za nje, wanakuja kujitolea Tanzania. Kipindihiki cha mwaka mmoja, hatutarajii kuna vita ambayotunahitaji kupeleka Watanzania wote kupigana vita.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri mwaka mmoja ule wakujitolea wengi wanataaluma mbalimbali, hatuna sababuya kulia kilio cha Walimu wakati tunaweza kuwapeleka JKTkwa njia ya kujitolea, waende katika mashule mbalimbalinchini, wako wataalam wa afya, wa kilimo, waende vijijiniwakafanye kazi kwa njia ya kujitolea ikiwa ni sehemu ya JKT.Kwa sababu hata tukiangalia matrekta ambayo tuliambiwayamepelekwa katika kambi tano katika nchi hii hatujapewautaratibu kwamba yamewezaje kuzalisha katika maeneo yaJKT.

Mheshimiwa Spika, suala zima la makusanyo, ni kiliokikubwa kwa nchi nzima katika Halmashauri zetu, Tawala zaMikoa na maeneo mengine ya Serikali Kuu. Suala hililitazamwe upya ili tuache na kuombaomba katika bajeti hasaya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukijaribu kuangalia taarifailiyotolewa na Waziri Mkuu, ni asilimia 32 ya makadirio ambayoyameshapelekwa katika maeneo yote nchi nzima. Pia kuna

Page 78: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

78

12 APRILI, 2013

Sheria Ndogo ambapo inaonekana kuna ucheleweshaji waSerikali kujibu Halmashauri, ndio majibu ambayo tumekutananayo katika Kamati ya TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, lakini pia suala linguine, ni uleuwezo wa kutambua vyanzo na kusimamia, yako maeneomengine kuna udhaifu mkubwa kabisa wa usimamizi wamasuala ya makusanyo. Mara nyingine unakuta mtumishi niwa ngazi ya chini ni mkusanya ushuru lakini ana hekalu,jumba, ana magari kwa sababu hela zile zinakwenda mfukonina ushahidi upo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la kulipa vyanzo vya maeneoyale ambayo ilionekana ni kodi za kero. Serikali ikaanzishautaratibu wanaouita General Purpose Grant (GPG).Haiwezekani imekuwa ni kiwango hicho tangu utaratibu huuumeanza mpaka leo hii. Haiendani na hali halisi ya mahitajina ukiangalia eneo lile lilikuwa limekadiriwa tu, hapakuwana scientific data ambazo zilikuwa zimechambuliwa. Mahitajiyanatofautiana katika Wilaya mbalimbali na hata kama niWilaya moja hiyo, haiwezekani mahitaji ya wakati huo ndiyompaka leo hii uwe unapewa kiwango hicho hicho cha fedha.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukijaribu kuangalia katika Bajetiya Ofisi ya Waziri Mkuu inasikitisha na kwa kweli ni fedhehakubwa sana...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa wanaofuata ni MheshimiwaPauline Gekul na Mheshimiwa Vincent Nyerere.

Ngoja nifafanue; uongozi wa CHADEMAwamekubaliana na Wabunge wao kwamba, watagawanadakika katika kuchangia katika Wizara mbalimbali. Kwa hiyo,

Page 79: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

79

12 APRILI, 2013

hapa nitampa Mheshimiwa Paulina Gekul dakika tano naMheshimiwa Vicent Nyerere nitampa dakika tano. Kwa hiyo,kengele ya kwanza itagonga baada ya dakika tatu nanyingine baada ya dakika mbili.

Baadaye atafuata Mheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Nitajitahidi ili nitumie dakika hizi tano. Kuna usemiwa Kiswahili unasema kwamba, ukiona unaoga bafuni halafukichaa akapita akachukua nguo zako usikimbizane nae.Naomba niende moja kwa moja kwenye masuala ya msingiya wananchi nisikimbizane na wale wanaotukana, wananchiwatapima wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la kwanza kabisa kuhusu Bajeti yaOfisi ya Waziri Mkuu, bajeti nzima ya matumizi ni shilingi trilioni4.2/-, lakini Bajeti ya Maendeleo ni shilingi bilioni 639/-.Ukiangalia fedha za ndani tulizotenga ni shilingi bilioni 270/-tu kati ya shilingi trilioni 4.2/- tunazokwenda kuzitumia, this isshame. Ninasema hivi kwa sababu huko chini, wazazi wetu,ndugu zetu akinamama wanaolala hospitalini, wanakwendakujifungua wanalala chini lakini Wabunge tunapitisha helaza kula, za mafuta, za per diem shilingi trilioni 4.2/-, bilioni 270/- fedha za maendeleo. Lakini za nje bilioni 369/- na jumla yafedha ni bilioni 639/- hizi za wafadhili hazitolewi. NaombaSerikali ibadilishe mtazamo wa kibajeti. Hii haikubaliki hatakidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano mzuri ku-justify haya;ukarabati wa jengo hili tumejitengea shilingi bilioni sita,ukarabati tu wa hapa panapovuja. Bilioni sita tumejitengeakukarabati jengo la Bunge, lakini ukiangalia Hospitali za Rufaana za Mikoa zilizojengwa sasa hivi tulitembelea Hospitali yaSingida, hata ya Mkoa wangu wa Manyara wanaomba bilionimbili hawazipati. Sisi kukarabati tu jengo la Bungepanapovuja bilioni sita inawezekana wapi? Nafikiri hizi fedhaza ukarabati zibakishwe milioni 500/- zingine tupeleke hukoMikoani kwenye elimu na afya ziende zikafanye kazi. (Makofi)

Page 80: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

80

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa sababu nina dakika tano,sasa nizungumzie Mabaraza ya Katiba. Kwa kweli huuutaratibu kwa kweli ni utaratibu mbovu sana uliofanyika katikaWard C. Imagine watu hawajajieleza, Wenyeviti wamekaana Madiwani wao, wanajuaje wajumbe wanne wa Mtaa waOysterbay kama yeye ni wa Mtaa wa Ngarenaro.Wanakwenda pale hawajielezi, mwongozo unasemakwamba watachaguliwa kwa wao kujieleza, lakini kwenyeWard C kilichofanyika hawakujieleza.

Mheshimiwa Spika, watu wanasema hapawatashangaa kama wananchi wataandamana, siowanachama wa CHADEMA watakaokwenda kuandamana.Kinachosikitisha hata kwenye mitaa inayoongozwa naWenyeviti wa CHADEMA, viongozi wa CCM wale wanaokaakwenye mitaa ile inayoongozwa na CHADEMA walikatwamajina yao kwa kisingizio kwamba wanatoka kwenye mitaaya CHADEMA.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano katika Mkoa wanguwa Manyara. Babati pale Mtaa wa Sawe, viongozi wa CCM,wao ambao walikuwa wanafikiri kuwa wanakipigania hichochama wamekiona hiki chama hakifai, kwa sababu hatawao viongozi wanaokaa kwenye mitaa inayoongozwa naCHADEMA, majina yao yanakatwa.

Mheshimiwa Spika, huu utaratibu umevurugwa vyakutosha. Hebu sikilizeni kilio cha Watanzania na kweli kamahamtabadilisha watakaoandamana si wanachama waCHADEMA. Wataandamana Watanzania ambao wanaonautaratibu huu wa kikatiba umekwenda kuchukuliwa naChama cha Mapinduzi na wanataka kuufanya uwe wakwao.

Mheshimiwa Spika, muda hauniruhusu, naombanizungumzie suala zima linalowakabili wananchi wangu waMkoa wa Manyara. Mheshimiwa Waziri kipindi hiki alitoamahindi kwa ajili ya kupunguza makali ya njaa. Katika Wilayayangu ya Babati, katika Jimbo la Babati Mjini, mahindihayakwenda.

Page 81: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

81

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, cha kusikitisha, Mkuu wa Wilayaanakataza akinamama wanaotegemea uvuvi wa samakikuendesha maisha yao na kusomesha watoto wao, kuvuaMaziwa yote ya Mkoa wa Manyara; Ziwa Burunge, ZiwaBabati mpaka kule Basutu, Maziwa yamefungwa, mahindiya njaa hayajapelekwa. Kama sio kukomoa Watanzania waMkoa wa Manyara ni nini? Nafikiri kama hamkupelekamahindi mkafungue yale Maziwa, wale wananchi wakavuewavue samaki wasomeshe watoto wao, wale akinamamatuwanusuru waweze kuendesha maisha yao.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nimekuwa na tatizo ukurasa wa 26 na 27 aya ya 37.Tumetenga shilingi bilioni 440/- kwa ajili ya kunusuru kayamaskini zilizo katika mazingira hatarishi. Mpango huuunalenga kuwezesha kaya maskini kupata chakula,kuziongezea kipato kwa kuzipatia fedha ili kumudu mahitajiya msingi kama vile lishe bora, huduma za afya na elimu.Mpango huu unatekelezwa kwa awamu katika Halmashaurizote Tanzania bara na Zanzibar na umeanza na utambuziwa kaya maskini katika vijiji 20 vya Halmashauri ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Spika, kwa takwimu zilizopo, Wilayamaskini kabisa nchini, ni Wilaya ya Bunda. Lakini inanipawasiwasi kuona katika utekelezaji tunataka kuanza na Wilayaya Bagamoyo. Huu ni mgawanyiko ambao siukubali. Hapatunaanza kutengeneza ukabila. Nadhani hizi bilioni 440/-,tungeziacha kwanza tukafanya tathmini ya Wilaya zote,tukaenda kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kufanya Wilayanyingine ziwe mwanzo, halafu na nyingine ziwe mwisho,matatizo hayawezi kusubiri. Wilaya ambazo zitasubiri kupewafedha hizi sidhani kama wataridhika. Nadhani, yawezekanania ni nzuri, lakini utaratibu ni mbaya. Ninyi wenyewe nimashahidi, mmeangalia kilichotokea kule Mtwara baada yapropaganda ya kwamba gesi inakwenda Bagamoyo, ninikilitokea.

Page 82: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

82

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, nadhani yawezekana nia ni nzurisana, lakini mpango huu sidhani kama ni mzuri sana, tuangalieni namna gani ya kupeleka fedha hizi kwenye Wilaya zotekwa pamoja kuliko kuanza na Wilaya ya Bagamoyo. Tafsiriyake itakuwa kwamba ni kwa sababu Rais anatokaBagamoyo, ndiyo maana fedha hizi wamepeleka mwanzo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuko katika kipindi cha Bajeti,kipindi ambacho Wabunge wapo hapa kwa ajil i yakuwasaidia wananchi wao. Yawezekana lugha ikawa mbayaau ngumu, lakini ijulikane Serikali ni chombo cha mabavu,ndiyo kawaida na Mbunge alivyokuja hapa wananchi wakewalimwambia katutetee, kuwatetea ina maana kuwanusuruna chombo cha mabavu. Nadhani Wabunge wenzangu,tungejitahidi sana kujikita kuangalia namna gani Serikaliitapunguza mabavu kuwasaidia wanachi kuliko kutupianamaneno yasiyofaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nadhani Wabunge waliopo hapa,ni muda wao wa kutathmini maisha ya watu wao huko walikona wananchi wanasubiri kuangalia aidha, katika kipindi hikicha bajeti, maisha yanakuwa magumu, yanakuwa rahisi auyanakuwa vile vile yalivyo.

Mheshimiwa Spika, napenda sana niwaase Wabungewenzangu, tuangalie ni namna gani ya kuwasaidia wananchiwetu kwa sababu wana tabu. Hii tabia ya kusema, kunawananchi wanaishi katika mazingira hatarishi wengine; niuongo. Watanzania wote wanaishi kwenye mazingirahatarishi. Kama kuna utekelezaji, naomba sana uanze kwapamoja.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaSerukamba na Mheshimiwa Vita Kawawa ajiandae. HalafuMheshimiwa Dkt. Mrema pia ajiandae.

Page 83: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

83

12 APRILI, 2013

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri,lakini nina maeneo machache ambayo ningependakuchangia. Kwanza ni hili la mfumko wa bei. Mfumko wa beiumekwenda chini, ni jambo jema, lakini nilikuwa najiuliza, hivimfumko wa bei wa Kalinzi na wa Dar es Salaam ni sawa?Mfumko wa bei wa Morogoro na Nkasi ni sawa? Mfuko wabei wa Sikonge na Dodoma ni sawa? Mfumko wa bei waMkigo na Mwanza ni sawa? Mfumko wa bei wa Mlele Katavini sawa na wa Kinondoni? Mfumko wa bei wa Masasi naArusha ni sawa, Ilala na Ngara ni sawa?

Mheshimiwa Spika, haya ni maswali ambayowachumi lazima watujibu. Kwa hapa ninachokiona,tunaendesha chumi mbili kama nchi. Ili tuweze kuzi-mergechumi hizi, lazima suala la miundombinu liwe la kipaumbeleya hali ya juu na hasa miundombinu ya reli.

Mheshimiwa Spika, njia pekee ya kuweza kusafirishamizigo kwa bei rahisi ni kupitia reli wala sio kitu kingine nanchi zote wamefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la reli na bandari ndiyo kitupekee ambacho kitatusaidia kwanza katika biashara yatransit trade, kupunguza mfumko wa bei, kupunguza ugumuwa maisha na usafiri kuwa wa bei nafuu. Lakini kwenye relitunafanya nini? Ukienda kwenye bajeti yetu pamoja nakwamba ni tumesema uchukuzi kwa maana ya reli nikipaumbele, lakini si kwenye fedha.

Mheshimiwa Spika, lakini tulifanya feasibility study yakutoka Dar es Salaam mpaka Isaka – Isaka mpaka Kezakwenda mpaka Rwanda na kwenda Msongati. Feasibilitystudy hii imekwisha mwezi Desemba, 2009. Leo ni Aprili, 2013,bado hatuna project yoyote kubwa ya reli. Tunachofanya niyaleyale ya kawaida. Nadhani wakati umefika, reli hiituliyonayo ilijengwa miaka mia moja iliyopita. umefika wakatisasa niiombe Serikali, tufumbe macho, tuhakikishe tunajengana sisi reli itakayoishi miaka mingine mia moja.?

Page 84: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

84

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, tukifanya hivyo, ukijenga reli yastandard gauge, kitakachotokea ni nini? Hata gharama yakusafirisha kwa tani inapungua kuliko reli ya leo. Reli ya leo nikaribu dola nane lakini ukiweka standard gauge itakuwa 1.5dollar. Hizi ni economics tu. Kwa hiyo, ningeomba wenzetu,miaka minne tumemaliza feasibility study, bado hatujajengareli. Tukipata fedha leo maana yake ni nini, itabidi tu-updatefeasibility maana yake ni 2015 imefika. Kwa hiyo, niwaombewatu wa Serikali, Mheshimiwa Waziri Mkuu jambo hili tulifanyeharaka.

Mheshimiwa Spika, wenzetu Wakenya, leotunavyoongea wameanza kujenga standard gauge kutokabandari ya Mombasa wanakuja Nairobi wanakwendaUganda, wakifika Uganda watakwenda Rwanda.Tunachohangaikia hatuwezi kukipata, mwisho wa siku hapatunakimbizana tupate mizigo. 2015 wale watu wa Burundiwatakuwa na tani karibu milioni tatu za nickel, tunazifikishajebandarini?

Mheshimiwa Spika, lakini kuna suala la bandari tokamwaka 2008 tumesema tutajenga gati ya 13 na 14 mpakaleo tunaongea. Wakati tulivyokwenda China kutafuta mkopotulikwenda na Wakenya, wenzetu wamemaliza kujenga. Sasakama hatufanyi maamuzi huu urasimu hauwezi kutupelekapopote. Mipango yetu ni mizuri sana, lakini anatekeleza nani?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kuongelea suala linginela vision 2025. Nataka Waziri Mkuu aniambie vision 2025 nafive years plan tumefika wapi? Kama ingekuwa ni safari yaDar es Salaam kuja Dodoma sasa tumefika Morogoro,Chalinze au wapi? Akisema tulipofika na wote tukubali kwelitumefika hapo na vigezo vipo. Tuulizane GDP gross per USDni ngapi? GDP per capita income as per USD, tumefika wapi?Exports zetu tumefika? Still consumption kwa ajili ya viwanda,tumefika wapi? Power consumption, tumefika wapi? Humandevelopment industries, tumefika wapi? Maana haiwezekanikila siku tunaimba, tuna five years plan, tuna vision 2025 miakainakwenda, lakini basi tupeane na evaluation tumefika wapi

Page 85: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

85

12 APRILI, 2013

ili tuweze kujua hapa tumerudi nyuma twende kwa kasi zaidi.Tusipofanya hivyo, tutafika miaka hiyo bado hatujafanya kazivizuri.

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la udini. Nimesikiarafiki zangu wa upinzani wanasema udini umeletwa na CCM,hapana. Suala la udini, viongozi tusiogope kuchukuaresponsibility. Hili ni suala la sisi viongozi wote regardless ofour parties, lazima tulisimamie, tulinde nchi yetu. Nchi hiitumeirithi ikiwa na amani, haiwezekani leo tumeanza kufikatunachaguana kwa kuangalia dini zetu, hili ni la hatari. Hiinchi tunaihitaji wote, tukianza kutupiana lawama, hatuwezikuisaidia nchi hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe, sisi viongozituchunge ndimi zetu, sisi viongozi tuwe wa kwanza kwendakutafuta solution ya matatizo yetu. Leo tunataka kuuanakwa ajili ya kuchinja. Wakati Wakenya wanaongea mwakakesho kumpa kila mtoto laptop, sisi tunahangaika na kuchinja.Kweli jamani hii ndiyo Tanzania tunayoitaka? Jamani tusemehapana, tushirikiane viongozi wote kusema hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nampongezaMheshimiwa Waziri Mkuu kwenye speech yake anasemawameanza Presidential Delivery Bureau. Ni jambo jema sana.Lakini naomba niseme yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, ukisikiliza na hizo labs, veryfascinating, lakini je, tuko tayari kubadili culture yetu? Je,culture yetu ya urasimu tuko tayari ku-deal nayo? Je, tukotayari kuanza kuaminiana? Nchi hii hatuaminiani. Viongoziwakifanya maamuzi tunawaita mafisadi, viongozi magazetiyakiandika tunaacha kufanya maamuzi. Tutatekelezajehaya? Hakuna mtu mwenye fedha zake anataka kujakuwekeza Tanzania aingie kwenye urasimu, wakati akiendaRwanda leo anapokelewa, akienda Kenya anapokelewa,sisi hata kujibu barua ni miezi mitano, mwaka mmoja, hatuwezikuendelea. (Makofi)

Page 86: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

86

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nasema naombaniwe devil advocate kwamba jamani, kama kweli tunaletajambo hili jema, lakini na culture yetu tuwe tayari kuibadilisha,tuwe tayari kufanya kazi kwa bidii, lakini pia tuwe tayarikuchukua maamuzi. Maamuzi nchi hii yanachelewa sana.Unaweza ukaandika barua leo Wizarani, ukajibiwa baadaya mwaka mmoja, ama usijibiwe kabisa. What kind of aculture?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe sana,Tunaanzisha vitu vizuri vingi, lakini tuwe tayari kubadilishaculture yetu ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, la mwisho kama muda utaniruhusuni suala mabadiliko ya Katiba. Nimemsikiliza sana janaKiongozi wa Kambi ya Upinzani, anasema Mabaraza yaKatiba yote yanakuwa ya watu wa CCM. Hivi nataka niulizewenye hati milki ya Katiba hii ni ambao sio wana-CCM? Hiviwana-CCM sisi hatuna nafasi ya kujadili mambo haya?Kwamba kwa sababu mimi ni CCM, nimeingia kwenye Barazala Katiba na-loose monopoly ya Katiba? Lakini hawawezikuepuka sisi ni wengi, tumewashinda. Sisi ni wengi kwa maanaya Madiwani, ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, kwaWabunge na sisi ndiyo wenye Serikali. Kwa hiyo kamamnaamua kwenye jambo hili, haya lazima myakubali, hayahayakwepeki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana kamatunasema kuna Mabaraza ya Katiba, lazima tutarajie…

TAARIFA

SPIKA: Jamani nimesema, muda utakwisha. Hayataarifa ya nini Mheshimiwa Tundu Lissu?

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, naombanimpe taarifa mzungumzaji kwamba, kwa mujibu wa Sheriaya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyofanyiwa marekebisho,hakuna mahali popote ambapo Sheria hiyo imesemakwamba, Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya

Page 87: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

87

12 APRILI, 2013

watakwenda kuchujwa na Ward C, hakuna mahali popoteambako imesema hivyo. Huo ni utaratibu wa Tume, utaratibuambao tumesema haufai kwa sababu hauko kwenye Sheria.

SPIKA: Endelea Mheshimiwa Serukamba na mudawake mpeni.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, kwanzanaikataa hiyo taarifa. Narudia tenda, nimesema kama Taifalazima tuanze kuaminiana. Tumeipa Tume mandate, inafanyakazi yake, hatuwezi kuja hapa Bungeni kuanza kui-criticizena nasema Serikali kama hawa watu wanasema waowanajitoa kwenye mchakato, let them go na hii biasharatuiache. Tunayo Katiba ambayo ni nzuri, tuendelee kuongozanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali tusiingie kwenyehuu mtego wa hawa watu watatutishia kwamba,tutakwenda kuwaambia wananchi wasiipigie kura Katiba letthem go. Halafu tunaacha mchakato, Katiba ipo, Serikaliinaendelea, tunaendelea kuongoza nchi. What is a problem?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumekaa hapa wakati tunapitishaKatiba tumekubaliana, wenzetu wakatoka nje, wakaendakuomba Ikulu, tumewasikiliza, tumebadilisha, tumeya-incorporate yote haya mliyajua, leo mnataka nini?Tusiwavuruge Watanzania, hii nchi ni yetu wote, naomba sanaviongozi tuwe makini, hii nchi ni yetu wote, at the end of theday, we have nowhere to go as a country hatuna pa kwenda.This is the best country for us. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuiache Tume ifanye majukumuyake na kwa kweli ni aibu kwa Serikali na kwa Wabunge leotunaanza ku-question credibility ya Tume ambayo ina Vyamavyote, hiki ni kitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja hii.(Makofi)

Page 88: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

127

12 APRILI, 2013

Wananchi wanasema tumefyatua matofali nakujenga mpaka ngazi ya renter lakini Halmashauri hazijafanyafinishing. Hii ni kwa sababu fedha zinakuwa hazitoshi,makusanyo yanapotea hayasimamiwi vizuri. Kwa hiyo, natoaushauri tu kwamba, makusanyo yanapofanyika, Viongozi wangazi ya Mkoa na Wilaya, wasimamie vizuri makusanyo iliyapatikane kwa uhalali; fedha nyingi sana zinapotea.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo ningependakuliongelea ni la ulinzi na usalama. Kule katika Wilaya yaKalambo kuna vituo vya mpakani. Kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri Mkuu, ukurasa wa nane amezungumziausalama mipakani. Katika Kata ya Katete, Wilaya yaKalambo, kuna Kituo cha Kasesha, Mwimbi kuna Kituo chaMosi na Kasanga pia kuna kituo; utakuta askari walioko kulehawana hata silaha na immigration officers hawana hatausafiri. Sasa unashangaa mahali kama pale Kasesha, ukiingiang’ambo ya Zambia askari wana silaha, ukija upande waTanzania askari hawana hata rungu! Kwa hiyo, ina maanahata ujambazi ukifanyika upande wa pili wakikurupushwawakifika Tanzania watapumzika tu maana wanajua hakunalolote. Naiomba Serikali iwape wale vijana silaha, otherwise,maisha yao yapo hatarini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata wageni haramu kwenyeMwambao wa Ziwa Tanganyika wanaingia kiholela, tena kulekumekuwa ndiyo njia ya kuingilia na kwenda Malawi mpakaAfrika Kusini, sasa hivi wanapitia Ziwa Tanganyika. Naombausalama na ulinzi uimarishwe kwenye hivyo vituo vyampakani, lakini pia uimarishwe kwenye Ziwa la Tanganyika.

Mheshimiwa Spika, nikiongelea kuhusu afya, nikwamba, zahanati na vituo vya afya vinajengwa, lakiniwatumishi waliopo kule ni wahudumu, hakuna watumishiambao ni wataalam na tunajua kabisa shughuli za afya siyoza kubahatisha. Watumishi wa afya hawafanyi kazi na mafaili,wanafanya kazi na binadamu na kwa binadamu ukifanyakosa kidogo tu hata kama ni aspirin au panadol, ukikoseakidogo tu basi umeshaua. Kwa hiyo, nilikuwa naomba Serikaliiangalie tena hivi vituo, kwa Mpango wa MMAM vituo

Page 89: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

128

12 APRILI, 2013

vifurikishwe watumishi walio na utaalamu, lakini pia na dawana vifaa tiba.

Mheshimiwa Spika, kwa leo sina mengi, muda huunilioutumia unatosha na niliyochangia yanatosha. Ninaungamkono hoja kwa asilimia mia kwa mia. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Nilisema Mheshimiwa Eng. Mnyaa,atafuatiwa na Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa, halafuatafuatiwa na Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo.

MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA:Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kwa kuanza utangulizi, janaMheshimiwa Kayombo, alinukuu Dira ya Taifa 2020. Kwaumuhimu wa nukuu ile, napenda niirejee tena kwa hayaninayotaka kuyaongea leo.

Mheshimiwa Spika, amani, utulivu na usalama wa raiana mali zao ni mazingira ya lazima kabisa ya msingi kwamaendeleo. Hiyo aliisema jana na ni vizuri iingie kwenyemasikio ya Serikali, kwenye masikio yetu Wabunge na iingiekwenye masikio ya Wananchi. Dira hiyo hiyo ya Taifailiendelea ikasema, kimsingi maendeleo ya Taifa hayana budiyamlenge binadamu, yatokane na ukuaji endelevu wauchumi, yahusishwe na watu wote.

Mheshimiwa Spika, baada ya nukuu hiyo nisemekwamba, kuna matatizo Loliondo, kuna matatizo Mtwara,kuna matatizo Kondoa katika Kata ya Kinyasi, kuna migogoroya kidini, maendeleo yatakuwa ni shida, ikiwa hali iko hivinchini na kwenye maeneo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la ajabu ni kwamba, tunajifunzakitu cha ajabu sasa hivi kwamba, mgogoro wa Loliondo,Madiwani wa CCM wanakwenda Dar es Salaam kwenyevyombo vya habari tunawaangalia kwenye runinga, Waziriwa CCM anakwenda kwenye vyombo vya habaritunaangalia runinga. Hii njia ya kutatua migogoro kwakwenda kwenye vyombo vya habari, sawa, Wananchitumeshajua ndiyo njia sahihi? (Makofi)

Page 90: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

129

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kubwa zaidi ni kwamba, KatibuMkuu wa CCM akaunda Kamati yake iliyokuwa inaongozwana Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, nayo kutafuta suluhu yamgogoro huu, fine, lakini tuelewe kwamba, hizi suluhu zamigogoro ya Wananchi, kuna Wananchi wa kila chama, lakiniuzoefu unaonesha kwamba, kuna Kamati ya SMT na SMZambayo kwa muda wa miaka 48 inatatua migogoro yaMuungano haijamalizika. (Makofi)

Ukurasa wa 14 wa Hotuba hii ya Mheshimiwa WaziriMkuu, ameeleza wamekutana tena hivi karibuni, akaelezamambo mengi lakini hatukujua mpaka leo yaliyotatuliwa niyapi na yapi. Je, Kamati za Vyama zinaweza zikatatuamigogoro hii? Ikiwa Serikali iliyoko madarakani ni ya CCM, je,CCM nao hawaiamini tena Serikali yao? Pana question markhapa! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije suala la Mtwara; mimimwenyewe nilileta ombi la watu wa Mtwara, lakini tikitakailiyofanyika, na wala siwezi kupingana na kiti, naistahimilia.Niliistahimilia hasa pale nilipoona Mheshimiwa Waziri Mkuuamekwenda Mtwara na aliporudi alitupa briefing Wabunge,tulipata matumaini kwamba, mgogoro umekwisha, bahatimbaya kumbe kunafukuta zaidi. Ndipo nikaona ile haja yakuwasilisha ombi la watu wa Mtwara, nikaliwasilisha, bahatimbaya yakatokea yaliyotokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme Bunge lako lina haki yakuingilia kati migogoro hii kwamba, sisi kama wawakilishi waWananchi, tunayo haki ya Kikatiba na ndiyo maana ikawemokwenye Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganokwamba Serikali inaweza ikafanya kosa na Serikali inawezaikaharibu, Mungu wangu! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niseme kwamba, kilio chawatu wa Mtwara kina misingi mine; leo niitaje ili chanzo hasakijulikane kwamba wanachotaka ni nini: Megawatt 300 zaumeme zizalishwe Mtwara. Wanachotaka Lindi na Mtwaraiunganishwe na Gridi ya Taifa. Ikiwa haya mambo mawiliyatafanyika, Bandari ya Mtwara itafunguka, ajira zitafunguka,

Page 91: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

130

12 APRILI, 2013

viwanda vitafunguka. La nne ni kwamba, hayo yakitendekaile dhana ambayo naamini Mkuu wa Mkoa wa Mtwara yupoananisikia ya Mtwara Corridor, aliyoishughulikia kwa jitihadazake zote nayo itafunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yote haya ni mambo ambayowatu wa Mtwara wameahidiwa zaidi ya miaka 16. Mambohaya yapo kwenye Project iliyoitwa Power Six ya miaka yatisini. Mambo haya yapo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM yaMwaka 2005 na 2010, Ibara ya 63, kifungu (j) na (k). (Makofi)

Mambo haya yapo katika Hotuba ya Rais aliyoitoatarehe 10 Juni, 2009 hapa Dodoma. Mambo haya yapokatika Hotuba ya Rais ya tarehe 25 Julai, katika kilele chaSiku ya Mashujaa aliyoitoa Mtwara. Mambo haya yamokatika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ikulutarehe 12 Oktoba, 2011. Yote haya yamo, kilichobadilishanini? Hapa ndipo kwenye kitendawili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuangalie gharama za Mradi; watuwa Mtwara hawapingani na hoja ya gesi kutumika Dar esSalaam, wanapingana na hoja ya kwamba, mambo hayaya kubadilisha yameanza muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, leo niruhusu na nawaombaWabunge, waende wakatafute Hansard ya tarehe 31Januari, 1997, sitaisoma yote, lakini naomba ninukuuvipengele hivi: Mbunge wa wakati huo, Mheshimiwa AbdillahiNamkulala, aliuliza swali la nyongeza, la msingi mtalitafuta;akauliza akasema, Mheshimiwa Waziri amesema kwamba,Benki ya Dunia imekubali tena kuufadhili Mradi huu; je,anaweza kuwahakikishia watu wa Mtwara kwamba,hatachukua tena fedha hizo kwa manufaa ya mkoamwingine kama alivyofanya hizi? Makofi yakapigwa. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri anajibu kwamba, ni kweli kabisakwamba, sasa hivi fedha ambazo tutazipata kutoka Benkiya Dunia, kiasi cha dola milioni 300, sehemu ya fedha hizozitatumika kwa ajili ya kupeleka na kutoa umeme kwa Miji yaMtwara na Lindi na pia kuwezesha Kanda hiyo ya Kusini

Page 92: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

131

12 APRILI, 2013

kuunganishwa na Gridi ya Taifa. Sasa haya masuala nikwamba, wanachofanya ni ahadi za miaka mingi.

Mheshimiwa Spika, naomba na ninatangaza niayangu, kipindi hiki cha miezi minne; Aprili, Mei, Juni na Julai,Serikali au Bunge lako litafute hatua mahususi kumaliza sualahili. Vinginevyo, kwenye Mkutano wa Kumi na Mbili nitaletatena ile hoja au petition, ombi la watu wa Mtwara ikiwa sualahili halijapatiwa ufumbuzi.

(Hapa kengele il i l ia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA:Mheshimiwa Spika, katika suala la migogoro, lalala, ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita MheshimiwaMahmoud Mgimwa, atafuatiwa na Mheshimiwa AbdallahNjwayo na Mheshimiwa Kafulila ajiandae.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba hii yaWaziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, nitaanza na suala la maji. Maji niuhai, lakini kwa masikitiko makubwa, ni takriban miaka 51kuna baadhi ya vijiji katika Jimbo la Mufindi Kaskazini havinamaji. Kuna Kata ya Ihano yenye vijiji sita, hakuna kisima hatakimoja, Mnabulo yenye vijiji vitano hakuna kisima hata kimoja,Ikoya yenye vijiji vinne hamna kisima hata kimoja, Sadaniyenye vijiji sita hamna kisima hata kimoja.

Mheshimiwa Spika, juzi tulipata Mradi wa Maji katikaKata ya Mdabulo katika vijiji vyote vitano, wametokeawafadhili ambao wamekubali kutusaidia katika huo Mradiwa Maji, lakini kwa masikitiko makubwa tulipokuwa tunaendakutafuta vifaa likajitokeza suala la VAT. Tumewaombawenzetu wa Serikali kwa maana ya Wizara ya Fedha, VATilikuwa ina amount ya milioni 90, wale wafadhili wamesema

Page 93: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

132

12 APRILI, 2013

hatuko tayari kutoa milioni 90 kwa ajili ya kuchangia Mradihuu, fedha tulizozitoa zaidi ya bilioni moja na nusu zinatosha.Cha kusikitisha, mpaka leo hii Wizara ya Fedha hawatakikutusaidia kutoa exemption ya milioni 90 ambayo ingesaidiazaidi ya vijiji vitano kupata maji. Namwomba MheshimiwaWaziri Mkuu, aliingilie suala hili kati kusudi tuweze kupataexemption hiyo ya milioni 90.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo napendakulizungumzia ni suala la maslahi ya Wenyeviti wa Vitongoji,Vijiji na Serikali za Mitaa. Katika utaratibu wa utawala,Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Serikali za Mitaa ndiyo wenyewatu, Madiwani hawana watu, Wabunge hawana watu,wala Rais hana watu. Kazi za msingi zinafanyika katikamaeneo yale, lakini Serikali haiangalii maslahi ya wale watukule chini. Wanachangia kwa kiasi kikubwa katika utendajikatika nchi hii lakini hatuwaangalii. Wengine wanafikia hatuawanakufa hata Serikali inashindwa kuwasaidia kwa njia mojaau nyingine katika mazishi yao. Namwomba MheshimiwaWaziri Mkuu, aliangalie jambo hili kusudi watu wetu hawawaangaliwe kwa macho mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambaloningependa kuchangia ni suala la Watendaji wa Vijiji pamojana wa Kata. Wengi wanakaimu na wanakaimu kwa mudamrefu, kwa hiyo, utendaji wao wa kazi umekuwa wamashaka. Nilikuwa namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu,aziruhusu Halmashauri ziajiri kwenye maeneo haya kwasababu ukiulizia wanasema tutatoa ajira kesho na keshokutwa, kwa hiyo, ufanisi wa kutosha katika maeneo hayahaupatikani. Kwa hiyo, naomba tuliangalie kwa machomawili jambo hili.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo napendakuchangia ni suala la ajira. Kuna tatizo kubwa la ajira katikanchi hii. Kama Serikali inataka kutatua tatizo hili kwa dhatikabisa, ningeomba tujielekeze sana katika eneo la SIDO,tuwasaidie wapate mtaji wa kutosha ambao wanawezakuwafikia Wananchi walio wengi na vilevile tuisaidie Serikali

Page 94: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

133

12 APRILI, 2013

ifufue viwanda vingi vya nguo ambavyo huwa vinatoa ajiranyingi.

Mheshimiwa Spika, ukienda Cambodia ni nchi ndogo,lakini viwanda vya textile vinaajiri zaidi ya watu milioni tatu.Sisi kama tukijika katika eneo hili hata tatizo la uuzaji wapamba katika nchi yetu lisingekuwepo.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa WaziriMkuu, ambaye ameamua kwa dhati kuusaidia Mradi waNyuki. Mradi wa Nyuki hauna gharama, kama kweli ataamuakujikita na kujielekeza kwa nguvu zake zote katika eneo hili,nina hakika kabisa vijana wengi watapata ajira ya kutoshakatika maeneo haya. Nawaomba Baraza la UwezeshajiWananchi Kiuchumi (NEC) waende kwenye maeneo yote,wasichague baadhi ya maeneo. Kule Mufundi nina taasisiyangu inaitwa ASHITEK, ambayo inashughulikia suala laufugaji wa nyuki. Taasisi hii tumeshasogea hadi Mikoa yaNjombe na Mbeya, tunaendelea kutoa huduma hii. Kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, aongeze nguvu zake.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo natakakulizungumzia ni suala la kilimo hasa cha Chai. Sisi watu waMufindi tunalima Chai, watu wa Njombe na Rungwewanalima Chai, lakini cha kusikitisha, soko na mnada mkuuwa Chai uko Mombasa. Kwa hiyo, Chai yote inayolimwakatika maeneo haya inaonekana inatoka Kenya haitokiTanzania. Sasa Serikali inatakiwa ifanye juhudi za kutoshaianzishe soko na mnada wa Chai ndani ya nchi yetu kusudiChai inayotoka Tanzania ionekane kweli inatoka Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kule Mufindi tuna Mufindi PaperMills (MPM), wanazalisha karatasi, lakini cha kushangazahawana kiwanda cha kutengeneza mifuko, mifukoinatengenezwa na kiwanda ambacho kiko Kenya. Ile mifukondiyo inafanya packaging ya Chai, ikija Tanzania inauzwakwa dola 100. Namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu hasaWizara ya Ubinafsishaji na Uwekezaji, walianglie jambo hili;

Page 95: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

134

12 APRILI, 2013

hata mifuko Tanzania tunashindwa kutengeneza, hii ni aibuna inasikitisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninalopendakuchangia ni suala la nguzo za umeme. Wilaya ya Mufinditunazalisha nguzo za umeme za kutosha, lakini cha kusikitishani kwamba, bei ya nguzo katika Wilaya ya Mufindihaitofautiani na bei ya nguzo zinazouzwa Dar es Salaam naMwanza. Naomba waiangalie Mufindi kwa macho tofauti,pale zinapotoka nguzo, especially Mufindi, bei ya nguzo iwerahisi ukilinganisha na maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, suala langu la mwisho ninalotakakulizungumzia hapa ni hospitali. Katika hospitali natakanizungumzie maeneo mawili; kwanza ni tiba kwa wazee.Serikali haijajipanga kuhakikisha inawahudumia wazeekupata tiba zao za uhakika. Wazee hawapati dawa, kwahiyo, wamekuwa wanataabika. Serikali inatakiwa iliangaliesuala hili kusudi wazee waweze kupata tiba ya uhakika.(Makofi)

Wananchi wametumia nguvu kubwa sanakutengeneza zahanati. Katika Wilaya ya Mufindi, Jimbo laMufindi Kaskazini tumejenga Zahanati za Ikwea, Itona, Ifupila,Lulanda, Igeleke, Maduma, Kikombo na Vikula, lakini mpakaleo hii zahanati hizi hazijafunguliwa, hazijapelekewa dawawala hazijapelekewa waganga.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa mwisho nikuhusu Hati Chafu. Kuna statement inasemekana hapakwamba, wilaya inayopata Hati Chafu haitakiwi kusaidiwa.

Mheshimiwa Spika, Wananchi hawatakiwikuhukumiwa kwa sababu ya uzembe wa wafanyakazi. Kamakuna mfanyakazi amefanya vibaya, ahukumiwe kwa nafasiya ufanyakazi wake. Hawa ndiyo wanatuletea matatizokatika nchi hii, unakuta mfanyakazi amefanya jambo bayaanaondolewa kutoka kwenye wilaya moja anapelekwakwenye wilaya nyingine, hapo hatuwasaidii, matokeo yaketunahukumu wananchi ambao hawana hatia yoyote.

Page 96: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

135

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, baada ya mchango huo, naungamkono hoja. (Makofi)

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi jioni hii ili niungane na Wabunge wenzangukuchangia hoja iliyoko mbele yetu. Kwanza kabisa, naungamkono hoja kwa sababu nataka nipate fedha kwenyemaeneo yetu ili zifanye mambo ya maendeleo. Kwa hiyo,sioni sababu ya kukataa kuunga mkono hoja maananikikataa nitazipataje hizo fedha kwa ajili ya maendeleo yaWananchi wetu. (Makofi)

Pamoja na kuunga mkono hoja, nina mambombalimbali ya kuishauri Serikali. La kwanza, naomba Serikaliiisimamie TCRA, Mamlaka inayodhibiti Mawasiliano Tanzania,kwa sababu kama inavyokumbukwa ni karibu miaka miwilinyuma sasa ilianzisha mchakato wa usajili wa simu hapanchini na tulielezwa kwamba, baada ya usajili ule kupita sasamtu asingeweza kupiga simu bila kusajiliwa. Kilichopo sasani tofauti na mambo tuliyoelezwa; watu wamekuwa wakipigasimu zisizosajiliwa na zimekuwa zinatumika simu hizo kutukana,kufanya mambo ya ovyo na mfumo mzima wa mawasilianoumekuwa na matatizo, hata Wananchi wanaibiwa pesa zaokwenye ATM kutokana na usimamizi mbovu ulioko kwenyeeneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Ofisi ya Waziri iwasimamieTCRA na Wizara husika, Wizara Mama ya Mawasilianoiwasimamie TCRA ili jambo hili lisiendelee tena kuleta kerokwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, naomba pia kutoa ushauri kwaSerikali, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukisikia taarifakwamba, Serikali imekuwa ikipata mapato makubwa sanayanayokusanywa na TRA, lakini katika matumizi tumekuwatunawasikia Mawaziri wakilalamika kutokuwepo na fedha zakutosha wakati tumeshaambiwa TRA imekuwa ikikusanya.

Mheshimiwa Spika, mimi ninaomba tuwe tunaelezwaukweli kwa nini maeneo ya kukusanya fedha ni mengi lakini

Page 97: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

136

12 APRILI, 2013

matumizi yanakuwa na hitilafu. Kwa maana hiyo basi,naomba kuishauri Serikali labda iongeze vyanzo vyake vyakukusanya mapato ya Watanzania, tuanzishe Bandari Kavunyingi na za kutosha ili zisaidie kuongeza pesa.

Vilevile Taasisi ambazo ni chanzo kizuri cha kupatapesa, zitengenezewe utaratibu mzuri wa kuboreshwa ili ziwezekusimamia upatikanaji wa fedha. Kwa mfano, tunayoMamlaka inayosimamia Madini nchini (TMAA); ina matatizomakubwa kweli kwenye vifaa na hata mapato yao kamamamlaka. Watu hawa miezi mitano iliyopita, Airport zetuzilizopo nchini zimeweza kukusanya bilioni 13 katika muda wamiezi mitano. Maana yake nini? Watu hawatukiwatengenezea mazingira mazuri, wanaweza wakapatapesa nyingi za kutosha zikapunguza ukwasi uliopo kwenyebajeti yetu ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda nirudi nyumbani Mtwarakidogo; Mkoa wa Mtwara au Kanda ya Kusini ndiyo maeneoambayo hayana Hospitali ya Rufaa. Hivi leo mtu waTandahimba au Nanyamba akipatwa ndwele, akipataugonjwa analazimika kwenda Dar es Salaam ambako nimbali na mnajua tena wakati mwingine unapata ugonjwaukiwa haukukaa vizuri kiuchumi. Sasa hii shughuli ya kupatarufaa ya kwenda Dar es Salaam tumechoka Wanamtwara.Ningeiomba Serikali, iamue kwa makusudi sasa katika hiimiaka miwili tuijenge hospitali yetu ya rufaa pale Mtwara.Natambua kuna ujenzi wa fence pale ambao unapendezalakini haina maana kuwepo fence tu kuwepo kwa maeneo,tunachotaka hapa kutengwe fedha za kutosha ili tuwaokoeWatanzania walioko kule.

Mheshimiwa Spika, shilingi bilioni 70 ndiyo gharamaza Mradi uliopo. Ningependa tunapomaliza general budgetile, tupate angalau bilioni 35 za kuanza pale na awamunyingine tumalizie bilioni 35 tuepukane na hii adha ya kwendaDar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, naomba pia kuchangia Barabaraya Mtwara – Tandahimba – Newala hadi Masasi. Mkoa wetu

Page 98: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

137

12 APRILI, 2013

wa Mtwara unaunganishwa na barabara hii, lakini barabarahii ndiyo ya uchumi, ndiyo inayoleta mapato mengi ya Mkoawa Mtwara na nchi. Inachangia kwa kiasi kikubwa kwasababu asilimia 60 ya korosho zote za Tanzania zinatokaMtwara na hasa Wilaya za Tandahimba, Newala, Masasi naMtwara Vijijini. Tukiiboresha barabara hii itakuwa chanzo kizuricha uchumi. Natambua kwamba, tarehe 28 Machi, 2013kumetangazwa tender ya kuifanyia upembuzi yakinifubarabara hii. Ningeomba tuongeze kasi au speed ya jambohili ili katika muda mfupi ujao tusiendelee kupata adha tenahuku tukitilia maanani kwamba, barabara hiyo ipo kwenyeIlani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina matatizo makubwasana ya soko la mazao ya kilimo; ukisikia pamba ni tatizo,korosho ni tatizo, chai ni tatizo, tumbaku ni tatizo na hii kwakweli inatokana na kwamba, hatuna mpango mkakati wakutafuta masoko ya uhakika ya mazao yetu. Leo hapa kwamuda mrefu Serikali imekuwa haina mpango wakuyaongezea thamani mazao yetu, badala yake inapelekamazao yetu kwenye raw form, jambo ambalo watu inakuwavigumu sana kuchangamkia manunuzi ya namna hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, natoa rai kwa Serikali,tuamue kwa dhati kabisa sasa kuwekeza kwenye uongezajiwa thamani ya mazao yetu na hii itatusaidia sana kupatasoko la uhakika.

Mheshimiwa Spika, kwenye Bajeti ya MheshimiwaWaziri Mkuu, nimeona ukurasa wa 31 mpaka wa 37, amejaribuku-introduce price stabilization fund, jambo ambalo litasaidiakwa namna moja au nyingine, bei itakapokuwa inashuka basikutakuwa na compensation kwa wakulima. Ninachosema,kwa uzoefu nilionao, jambo hili litakuwa bure kwa sababutuna changamoto nyingi. Moja ya changamoto niwafanyabiashara wanao-curtail kuhakikisha kwambawanawadhulumu wakulima, kwa hiyo, Serikali lazima ianze

Page 99: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

138

12 APRILI, 2013

kwanza kuwabana hao maana hata tukileta huu mfumo wastabilization fund …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Njwayo, ahsante. Sasa namwitaMheshimiwa David Kafulila, atafuatiwa na MheshimiwaSelemani Zedi na Mheshimiwa Kakoso ajiandae.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika, kwasababu ya muda kuwa mfupi, nianze moja kwa moja nadhana nzima ya umaskini.

Mheshimiwa Spika, hili Taifa ni miongoni mwa Mataifatajiri sana Duniani, lakini kwa miaka mingi kwa sababu yakukosa uongozi sahihi na thabiti, tumeendelea kuwafanyaWatanzania kuwa maskini pasipo sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka huu Taifa la Tanzanialimetajwa kuwa ni la pili kwa vyanzo asilia vya utalii Dunianibaada ya Brazili. Ukitaka kujua ni kiasi gani tunapata kwenyeutalii, ni chini ya asilimia kumi ya kile ambacho tunastahilikukipata kwa sababu hatujajiandaa katika utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni nchi ya 11 kwa mitomingi Duniani, lakini zaidi inao utajiri wa Ziwa Tanganyika. ZiwaTanganyika ni Ziwa ambalo linachangia asilimia 17 ya freshwater Duniani. Maji yote duniani ni kama bilioni 1.4 kilomitaza ujazo, lakini maji ambayo yanafaa kunywewa Duniani nikama kilomita za ujazo milioni 35, Ziwa Tanganyika kati yamilioni 35 kilomita za ujazo, ina-contribute asilimia 17.

Mheshimiwa Spika, lakini ni huzuni kwamba, watu waKigoma, wanaokaa mita 100 kutoka usawa wa Ziwa, hakunamaji ya uhakika. Mlitaka Mwenyezi Mungu aisaidie Kigomakiasi gani ili isiwe na kero ya maji? Utafiti umefanywa naSENOBET, Kampuni ambayo ni miongoni mwa Makampuni

Page 100: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

139

12 APRILI, 2013

makubwa kwa ku-collect opinions Duniani. Kero ya majiTanzania ndiyo kero namba moja; yaani kama kunahitajikakuweka stimulus package tungeweka kwenye maji. Akinamama wanaumia, maji ni kero na Serikali hii nikiiangalia sionimatumaini. Sioni matumaini ya kwamba, kuna Serikaliambayo ipo serious na tatizo la maji. Watu wanaumia natatizo la maji. Serikali kila siku inapanga bajeti kidogo kwasababu uwezo wake wa kukusanya ni mdogo. Nchi inavyanzo vingi, lakini uwezo mdogo wa watawala, matokeoyake akina mama wanaumia kwa kufuata maji kilomitanzima; haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii Tanzania ina kila aina ya utajiri,tuna hii Coastal Zone, tuna karibu kilomita 1,424 za CoastalZone Bandari ya Hindi. Namibia wana kama kilomita 1,500za Coastal Zone. Namibia export peke yake ni milioni 340kwa mwaka. Tanzania ni vitu vya aibu, kila kitu cha utajiritunacho, tunashindwa nini kuwatajirisha Wananchi hawa?

Mheshimiwa Spika, leo tunalia na tatizo la ajira, lakinimoja ya maeneo ambayo yanatengeneza ajira nyingiDuniani ni processing na manufacturing industries. Mkijengaviwanda vya ku-process bidhaa, mkijenga viwanda vyakuzalisha mnaweza mkatatua tatizo la ajira. Hamuwezikuwadanganya Wananchi hapa kwamba, kuna Serikaliitakayoajiri Wananchi wote wanaohitaji ajira; haipo, lakini niwajibu wa Serikali kutengeneza misingi ambayo itasababishawatu wapate ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunasafirisha pamba zaidi yamagunia 400,000 kwenda nje; ni mambo ya aibu; tunapelekaajira Ulaya, India na Marekani wakati Tanzania kuna tatizo laajira. Tungeweza kutengeneza base ya viwanda vyamanufacturing tungetatua tatizo la ajira.

Mheshimiwa Spika, kabla muda haujakwisha,nisingependa kumaliza kuzungumza kabla sijagusia tatizo laardhi. Moja ya mambo ambayo leo hii Duniani naMheshimiwa Spika wewe ni shahidi maana unakwendakwenye vikao vikubwa Duniani, ni tatizo kubwa la land

Page 101: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

140

12 APRILI, 2013

grabbing. Kule Kigoma Uvinza amekuja mwekezaji, ambayekuna kila dalili kwamba, huyu ni tapeli, anapewa ardhi yaMakao Makuu ya Wilaya hekta 10,000. Muda siyo mrefu,taarifa zimetangazwa Duniani, mshirika wake ambayo ni LawUniversity, amejitoa kwa sababu hamwamini yule mwekezaji.Lakini Serikali yetu haishtuki kwamba huyu ni tapeli, hatukataiuwekezaji, lakini lazima tuwe na genuine investors, tuwe nawawekezaji ambao ni sahihi. Humu ndani wapo watu ambaowakiwezeshwa mitaji ya kutosha wanaweza wakawekezawakatengeneza ajira. Kenya wanafanya nini na sisitunashindwa nini?

Mheshimiwa Spika, yapo mambo ambayo tunahitajiSerikali ibadilike kufikiri na hii fikra ya Serikali inaanzia kwetusisi Wabunge. Ningependa kabla sijamaliza, nisasahau tatizoambalo tulilipitisha kwenye Bunge lililopita, tulipitisha Sheriahapa ya kwamba, CAG atakapoleta taarifa Bungeni hapohapo na Serikali itenge taarifa yake. Leo Mawaziri hawa hapatangu jana mmewaagiza; taarifa ipo wapi hapa? Tunapitishasheria za ndiyo matokeo yake tunasababisha crisis hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatuhitaji Bunge limalizike hapabila taarifa ya Serikali kuletwa. Watuambie taarifa hiyoimekaguliwa lini na CAG. Kwa utaratibu wa kawaida, CAGakishafanya uchunguzi wake anaipa Serikali, Serikali inajibu,ikishajibu hiyo ndiyo inakuwa taarifa sahihi ya Serikali. Kwasababu CAG ameonekana kwamba ni msaada kwaWatanzania, anatoa vitu ambavyo vinasababisha kui-shapeSerikali iende Wananchi wanavyohitaji, akaonekana ni tatizomnaanza kutunga sheria za kufinya kushoto, mnafinya kulia;kwa maslahi ya nani? Halafu mnawalazimisha Watanzaniawaseme hakuna haja ya kuzozana, ni nchi yetu sote; yetusote mnakula wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunasema hapa kwamba, sungurani mdogo, lakini siyo kweli kwamba sungura ni mdogo. Katikamaeneo ambayo ni tatizo katika Serikali hii ni manunuzi natunajua zaidi ya asilimia 60 ya fedha za Serikali inakwendakwenye manunuzi. CAG jana alizungumza hapa kwamba,

Page 102: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

141

12 APRILI, 2013

michakato mizima ya manunuzi, bei huwa ni mara mbili yabei ya kawaida. Hii ni kwa sababu Watendaji wa Serikali siyowaaminifu. Kuna gharama za safari, Mheshimiwa Waziri Mkuu,kimsingi, namheshimu sana na amekuwa akisema kwambaatajitahidi, lakini mpaka sasa bado kuna tatizo la matumiziya safari za Viongozi na hasa Viongozi Wakuu. Kiongozianasafiri misafara mikubwa na watu wengine hawana hatakazi, lakini traveller agents wale ambao Serikali inawatumiawana-charge fee kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuna haja ya Serikalikufanya uchunguzi kuhusu masuala ya safari. Kuna gharamakubwa sana ambazo tunazipoteza, kuna gharama kubwasana ambazo Serikali inazipoteza kutokana na mfumo mbovuwa manunuzi.

Mheshimiwa Spika, nimezungumza hapa kwamba,huwezi ukajenga uchumi kama hujajenga reli imara, kamahujawa na usafiri wa meli wa uhakika. Mwaka wa 1990, Reliya Kati ilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani 1,400 kwa mwaka,leo inasafirisha chini ya tani 400 kwa mwaka. Serikali ikianzakujitahidi kidogo wanasema kwa nini hamuisifu CCM; tuisifuimebomoa yenyewe halafu irudishe kidogo ipate sifa!(Makofi)

Mheshimiwa Spika, reli aliyoiacha Mkoloni ilikuwa borakuliko ya leo, mkirekebisha kidogo mnaomba sifa; sifa ipi?(Makofi)

SPIKA: Ahsante. Namwita Mheshimiwa Selemani Zedi,atafuatiwa na Mheshimiwa Kakoso, atafuatiwa naMheshimiwa Joseph Mbilinyi, atafuatiwa na MheshimiwaMchungaji Natse.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kupata fursa hii ili na mimi kwa niaba ya Wananchi waBukene, niweze kuchangia Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya WaziriMkuu. (Makofi)

Page 103: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

142

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, mimi nitaanza na suala la maji.Maji bado ni tatizo katika maeneo mengi ikiwemo na ndaniya Jimboni langu la Bukene.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais, alitoa ahadiambayo ni ya faraja sana kwetu sisi Wanamkoa wa Taborakwa ujumla, ya kufikisha maji ya Ziwa Victoria kutoka Kahamayafike Tabora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hofu yangu katika hili ni kasi yautekelezaji wa ahadi hii ya Rais. Ahadi hii ya Rais inatimeframe; Mheshimiwa Rais aliahidi kwamba, kabla yamwaka 2015, kabla hajamaliza muda wake wa Uongozi waAwamu ya Nne, maji ya Ziwa Victoria yatafika Tabora kutokeaKahama.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tupo mwaka 2013, badokama miaka mawili na Mradi mkubwa kama huu wa kutoamaji Kahama kuyafikisha Tabora hauwezi kutekelezwa kwamiezi mitatu, miezi sita, ni mradi ambao angalau unahitajimiaka miwili na kitu kuutekeleza. Sasa hivi tumebakiza miakamiwili kufika mwaka 2015, kwa hiyo, kwa kasi tunayoendanayo, nina hofu kwamba kama hatutaongeza speed basiinawezekana ahadi ya Rais isitekelezeke, jambo ambaloWanatabora hatutaki litokee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahadi hii ikitekelezeka, Wananchiwengi sana watafaidika na maji safi na salama kutoka ZiwaVictoria. Katika Jimbo langu la Bukene, Wananchi wa Igusule,Nawa, Wamara, Lubumbu, Itobo na Busasi, watafaidika nakupata maji haya. Wananchi wa Nzega Mjini vilevile na waIgunga na maeneo yote ambayo yapo barabarani katikanjia ya Nzega – Tabora, watafaidika na maji haya ya kutokaZiwa Victoria. Kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri wakatianafanya majumuisho, atoe maelezo ili tujue status yautekelezaji wa Mradi huu iko vipi, Serikali imejipanga vipi,upembuzi yakinifu utaisha lini, fedha zitapatikana vipi, ni zandani au ni za nje; kwa sababu hatutaki ifike mwaka 2015ahadi ya Rais iwe haijatekelezeka. (Makofi)

Page 104: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

143

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, ukurasa 30 wa Hotuba ya Bajetiya Waziri Mkuu, umezungumzia masuala ya umwagiliaji.Nimeona kwamba, Serikali imejipanga kujenga mabwawamapya ya umwagiliaji. Sipingi dhana ya kujenga mabwawamapya, lakini naishauri Serikali kwamba ni jambo jema piakuhakikisha mabwawa na skimu za umwagiliaji ambazozimeanza kujengwa zinakamilika zinafika mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu kwangukatika Jimbo la Bukene, nina bwawa kubwa la KahamaYaharanga, ambalo lina uwezo wa kumwagilizia hekta 500.Serikali karibu imetumia milioni 900 miaka minne, mitano,nyuma kulijenga kwa maana ya tuta. Bwawa hili halijawezakuanza kufanya kazi iliyokusudiwa kwa sababu miundombinuya mifereji ambayo itatoa maji kwenye bwawa kupelekakwenye hizo hekta 500 haijajengwa hadi leo.

Mwaka jana nilimwuliza Waziri mhusika, alinijibukwamba, wamefanikiwa kupata shilingi 200,000,000 kutokaMfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya ambazo zingetumikakujenga hiyo mifereji, lakini mpaka leo hakuna chochoteambacho kimefanyika. Kwa hiyo, hofu yangu ni kwamba,Serikali tumetumia shilingi 900,000,000, fedha nyingi kujengatuta kwa maana ya bwawa na mvua zimenyesha, bwawalimejaa lakini maji hayatumiki kwa sababu mifereji yakupeleka maji kwenye hizo hekta 500 haipo. Kwa hiyo,naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakati anatoa maelezo,tuelezwe kwamba, Serikali imejipanga vipi kuhakikishamiundombinu ya mifereji ili sasa shilingi 900,000,000 zilizotumikakujenga bwawa ziwe na faida, ziwe na tija, kwa sababuotherwise tutakuwa tumetumia shilingi 900,000,000 bila yafaida, ambapo ni hasara na ni jambo ambalo halina tija.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lipo katika ukurasawa 70 kuhusu ugawaji wa maeneo mapya ya utawala.Wilaya ya Nzega ni moja kati ya Wilaya kubwa sana hapanchini. Kwa mujibu wa sensa iliyopita, Wilaya ya Nzega sasahivi inakaribia kuwa na watu 600,000 na ina Kata 37 ambayonadhani ni ya pili kwa wingi wa Kata baada ya Wilaya ya

Page 105: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

144

12 APRILI, 2013

Kahama. Sasa sisi ndani ya Wilaya ya Nzega, kwa kutumiataratibu zilizopo tumeshaanza michakato ya kuwashirikishaWananchi, kushirikisha vikao halali, ili kupendekeza sasatusogeze huduma za kiutawala, huduma za kiuchumi na zakijamii karibu na Wananchi kwa kupendekeza kuimegaWilaya ya Nzega na kuunda Wilaya mpya ya Bukene.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Bukene ni kubwa, linaKata 16, zaidi ya kilomita za mraba 3000 na tuna uwezo wakukusanya mapato ya ndani karibu nusu bilioni kutokana napamba, tumbaku na mazao mengine ambayo tunalima.Kwa hiyo, imefika wakati kwamba, sasa tusogeze hudumaza kiutawala, huduma za kiuchumi na za kijamii karibu naWananchi kwa kuwa sasa na Halmashauri na Wilaya mpyaya Bukene. Tunaomba mapendekezo yetu yatakapofikangazi za TAMISEMI, ngazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yazingatiweili katika Wilaya na Halmashauri mpya zijazo, pengine mwakaujao, basi Halmashauri na Wilaya mpya ya Bukene, iwe nimojawapo kati ya Halmashauri ambazo zitazingatiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 71 wa Hotuba yaMheshimiwa Waziri Mkuu, imezungumzia maafa. Maafa nijambo ambalo mtu halitegemei, linakuja bila ya mtu kutarajia.Ni rai yangu kwamba, Mfuko huu uimarishwe kwa maana yakuongezewa fedha, kwa maana ya kuongezewa ustadi navifaa ambavyo vinahitajika, lakini uwezo huu ushuke katikangazi za Wilaya na ngazi za Halmashauri. Katika ngazi zaWilaya huko kuna Kamati za Maafa zinazoongozwa na Wakuuwa Wilaya, lakini changamoto kubwa unakuta hawako vizurikiuwezo, kiuwezeshaji, kwa hiyo, unakuta maafa yanatokeawatu wanakimbia na kuhangaika tu lakini waliokumbwa namaafa hawasaidiwi. Juzi na jana kwangu kule Jimbo laBukene, mvua kubwa zimenyesha, mafuriko yametokea nazaidi ya nyumba karibu 200 zimeanguka. Namshukuru Mkuuwa Wilaya na Kamati yake ya Maafa ya Wilaya ya Nzega,wanahangaika wanajitahidi, lakini wawezeshwe. Nawapapole Wananchi wa Bukene, ambao nyumba zao zimeathirika.

Page 106: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

145

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hojakwa asilimia mia moja. (Makofi)

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia katika Hotubahii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Nianze na suala la miundombinu. Mkoa wa Katavi nimpya na mkoa ambao uko pembezoni unahitaji zaidi kupatahuduma ya miundombinu. Serikali ilipokuwa imetoa mpangomkakati wa kuiwezesha mikoa iliyo pembezoni kupewahuduma za barabara, Wananchi tulifurahi sana, lakini bahatimbaya mpaka sasa barabara ya Mpanda - Sumbawangabado ujenzi wake unaenda kwa kusuasua. Nilikuwa naiombasana Serikali iharakishe kumalizia barabara inayotokaSumbawanga kuja Mpanda kupitia Kibaoni ikamilikemapema. Kuna barabara ya kutoka Mpanda kwendaKigoma, ni muhimu sana na ni kiunganishi kati ya Wananchiwa Mpanda na Mkoa wa Kigoma. Barabara hii iliahidiwa naSerikali ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, bahatimbaya mpaka sasa bado wala dalili zile za kuanza kwa ujenzihazijafanyika. Naiomba Serikali iharakishe mchakato wabarabara hii ili ujenzi uanze, uweze kuleta maendeleo mazurikwa Wananchi wa Mikoa hii miwili; Mkoa wa Katavi na Mkoawa Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ipo barabara muhimu sana;barabara ya Mpanda kupitia Inyonga Wilaya mpya ya Mlelekwenda Tabora. Barabara hii ni kiunganishi kwa Wananchiwalio wengi, hasa wa Kanda ya Ziwa. Barabara hii inatumiwana watu wengi kuanzia Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Taborana Mkoa wa Kagera. Ni kiunganishi kinachowasaidiaWananchi walio wengi kupata huduma ya barabara,ambayo ndiyo inayowaunganisha kupata chakula kutokakatika Mikoa ya Rukwa na Katavi. Naiomba Serikali iharakisheupembuzi yakinifu uliokuwa umelengwa ili iweze kujengwakwa kiwango cha lami. Itawasaidia sana Wananchi nakukuza uchumi katika maeneo ya mikoa hii kwa maana yaMkoa wa Katavi, Tabora na kurahisisha huduma nzuri katikaMikoa ya Shinyanga, Mwanza na mingineyo.

Page 107: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

146

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini bado kuna barabara ndogozinazounganisha Wilaya. Tunayo barabara ya Karema –Mpanda, inahitaji iboreshwe na kujengwa kwa kiwango chalami, kwa sababu eneo hili ni eneo linalounganisha mpakakati ya nchi ya DRC Congo na nchi yetu ya Tanzania. Nivizuri katika maeneo haya hasa ya kiusalama yakaboreshwana ukiangalia ni sambamba na ujenzi unaoendelea waBandari kule Ziwa Tanganyika ili tuweze kuwaunganishaWananchi wa maeneo haya waweze kukuza uchumi wao.Haitakuwa vizuri na wala haitapendeza kama tutajengabandari wakati barabara inayounganisha hapa ni yaudongo. Nilikuwa naiomba Serikali ijielekeze huko.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ninalopendakulichangia ni la huduma ya maji. Maji ni tatizo katika mikoaya pembezoni. Wananchi walio wengi katika vijiji vingihawana huduma ya maji. Tuna Vijiji vya Igagala, Vikonge,Katuma na Kasekese ambavyo havina huduma ya majiambayo toka kuanza kwa nchi hii au kupata kwa uhuru,hawajawahi kupata huduma ya maji. Naiomba Serikaliiongeze bajeti ya maji kwani maji ni tatizo na maji ni uhai namaji ndiyo yanayotegemea Wananchi walio wengi wawezekupata huduma huko vijijini. Nitawashangaa sana paletunapoelekeza nguvu kubwa sana kupeleka maji maeneoya mijini wakati kwenye matatizo mengi zaidi ni vijijini kwaniWananchi wanapoteza muda mwingi sana kutafuta majibadala ya kufanya shughuli za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni suala la kilimo;naiomba Serikali iongeze nguvu kuhakikisha wanaiwezeshaNFRA kupewa fedha za kutosha kwa ajili ya ununuzi wamazao. Wananchi walio wengi wanajitokeza wanalima lakinimazao yao hayapati soko; naiomba Serikali iliwezeshe Shirikahili lipewe fedha za kutosha ili waweze kununua mazao kwawakati mwafaka na kuweka vya kutosha na hii itawasaidiasana wakulima kuwa na jitihada za kuzalisha kwa nguvu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuzungumzia suala laelimu. Katika maeneo ya Jimbo langu tuna tatizo kubwasana la walimu hasa wa shule za sekondari. Tunaiomba

Page 108: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

147

12 APRILI, 2013

Serikali iongeze walimu. Tuna Shule ya Ikola ina walimu wawilitu na Shule ya Katuma nayo ina walimu wawili, lakini karibuJimbo zima shule hizo zina walimu wachache sana.Tunapotaka kuboresha elimu lazima tuwape walimu wakutosha sambamba na kuboresha mazingira ya walimu.Walimu walio wengi wanaishi katika mazingira mabaya,wana nyumba ambazo siyo stahili, kwa hiyo, tunaombatuwawezeshe waweze kupata nyumba nzuri na kuwafanyawapate motisha na kuboresha mishahara yao; hii itasaidiakukuza elimu katika maeneo yote hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, nimalizie na suala la migogoro yaardhi. Tuna migogoro mingi sana ya ardhi katika maeneo yaWilaya ya Mpanda hasa kuongezwa kwa mipaka katikamaeneo ambayo wanapakana na Hifadhi za Mapori naHifadhi za Taifa. Naishauri Serikali, tutumie busaratunapokuwa tunapanua maeneo haya, tuwashirikisheWananchi ili waweze kuelewa maeneo halisi na kuwapamipaka ambayo itawasaidia kuondoa migogoro.Kinachofanyika ni tofauti kabisa, Serikali inaweza ikaja tuikafika ikapanga na kuonesha mipaka ambayohaijawashirikisha Wananchi. Naiomba Serikali ikae vizuri naiwashirikishe Wananchi kwani tunapokuwa na mipangoshirikishi haiwezi ikaleta migogoro. Migogoro ya ardhi nimikubwa sana katika nchi hii, itakayochangia uvunjifu waamani. Naomba eneo hili tulipe uzito na tuhakikishetunawasaidia Wananchi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Mbilinyi dakika tano naMheshimiwa Natse dakika tano.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana. Leo naomba nianze kwa kunukuu manenomachache ya kwenye Biblia. Biblia inasema: “Mwanamkempumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yakemwenyewe.” Vivyo hivyo, Serikali pumbavu hulibomoa Taifalake kwa mikono yake yenyewe ambalo ni Baraza laMawaziri.

Page 109: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

148

12 APRILI, 2013

SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi!

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, sasasipendi tufike huko.

SPIKA: Serikali pumbavu ni pamoja na wewe.Naomba ujadili hoja yako vizuri tu. (Kicheko)

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, mimisiyo Serikali.

Bunge hili ni sehemu ya kujadili maslahi ya Taifa, lakinihawa watu wamekuwa wanatumia wingi wao katikakukwamisha masuala muhimu ya Wananchi. Juzi, Bungelililopita hapa tulikuwa na hoja ya mitaala ya MheshimiwaMbatia, mkatumia wingi wenu mkaizuia mkamnyanyapaaMheshimiwa Mbatia kwa Ubunge wake wa Kuteuliwamkidhani kwamba mnamdhalilisha yeye bila ya kujuakwamba, mnamdhalilisha mtu aliyemteua. MkamnyanyapaaMheshimiwa Mbatia, mkajaribu kuficha ugonjwa maradhiyamewaumbua, matokeo ya Kidato cha Nne mmeonakilichotokea. (Makofi)

Mimi nasema hivi: “Mlificha maradhi msibahumwumbua.” Mnakuja mnasema kwamba tunafanya kazi,sijui ooh Wanamapinduzi wale wengine akina MheshimiwaMwigulu kule wanakaa humu ndani wanaongea vitu gani,wanaongea vitu, wanataja watu majina, wanataja eeh; hiiyote ni nini? Hatuwezi kuwa na elimu wakati Wazirianayehusika na elimu, elimu yake ni ya kuungaunga na hilinitoe lawama moja kwa moja kwa Usalama wa Taifa, kwasababu Usalama wa Taifa wakati Mheshimiwa Rais anateuaMawaziri; kwa nini wasimwambie bwana tunalo faili la mtufulani huyu ni chenga, huyu ni boya usimuweke atakuumbua!Angalia sasa Mheshimiwa Rais hana la kufanya, amemteuamtu, magazeti yanaandika na hakuna mtu yeyote anayejibu.Usalama wa Taifa umekalia kufuatilia masuala ya CHADEMAtu na kung’oa watu kucha, kung’oa watu meno, hizo ndiyokazi wanazofanya badala ya kulisaidia Taifa na kumsaidiaMheshimiwa Rais kufanya vitu vilivyo sahihi.

Page 110: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

149

12 APRILI, 2013

Sasa nasema hivi, nakataa kuwa sehemu ya hii naniseme wazi, mimi Joseph Mbilinyi, kwa unyenyekevu mkubwaninayo heshima kwa Wanambeya walionichaguakuwawakilisha katika masuala yao, lakini nikikaa nikiangaliasijisikii fahari sana kuwa sehemu hii. Kuwa sehemu na watukama akina Mheshimiwa Mwigulu. Wanakuja hapa, nimpumbavu kwa sababu wewe utafanyaje dili halafuunatuma hela kwa M-Pesa!

SPIKA: Naomba ukae chini, naomba ukae chini.Lugha zingine zinaudhi na hazina sababu. Ukitaka kujengahoja yako unaweza, neno mpumbavu huwezi kulitumia katikaBunge hili. Nakwambia sasa nitawataja majina, Kanuniinaniruhusu mimi kuwataja watu majina na nikiwatajamnachukuliwa na Polisi. Endelea Mheshimiwa Mbilinyi, dakikazako zilizobaki.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, naombaTaifa linielewe kwamba, mpumbavu siyo tusi na ndiyo maanaBiblia imetumia. Upumbavu ni stupidity na stupidity is lack ofknowledge and understanding, ambapo Mawaziri wengihumu ndani wana-lack of knowledge and understanding nandiyo wanasababisha Taifa hili liwe hivi na hatutaendeleaku-take hiyo kitu kabisa. (Makofi)

SPIKA: Tunaomba tumalize, Mheshimiwa MchungajiNatse.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

SPIKA: Hakuna taarifa tunaendelea, nimesemaMheshimiwa Natse, hakuna mtu anayetoa taarifa.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba kuchangiakuhusu suala la udini. Suala la udini ni very sensitive. Migogoroimekuwepo na watu wameendelea kuifumbia macho.Kipekee niseme, Serikali iliyoko madarakani imeshindwakuchukua hatua kufanya maamuzi, ina power na authorityimenyamaza. Nakumbuka Awamu ya Pili ya Mzee Mwinyi,

Page 111: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

150

12 APRILI, 2013

matatizo yalipoanza ya mabucha ya Kitimoto alitamka tuna mambo yakaisha.

Mheshimiwa Spika, ninauliza; if you have clean heartwhy worry ya kutokufanya maamuzi? We have very poordecision making katika Serikali yetu. Niombe hilo lifanyike,hatuwezi kuvumilia kuona nchi hii inaingia katika majanga,maasi na mauaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, kwa takriban miakamiwili sasa kuhusu ugatuaji wa madaraka, Kij i j i chaChemchemi katika Halmashauri ya Karatu hakina uongozi,baada ya Wananchi kuiondoa Serikali yao. NimwombeMheshimiwa Waziri Mkuu, aki-wind up aniambie ni liniWananchi wa Kijiji cha Chemchemi watapata Serikali yao?

Mheshimiwa Spika, mwisho, Mheshimiwa Mbunge waLongido, alisema hivi kuhusu Longido na Ngorongoro,niwaambie Wananchi wa Ngorongoro na Loliondo, semeni,teteeni haki yenu. Alisema, akina mama wamenituma,Wananchi wa Dubai wanaendelea.

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kukaribiakwisha)

SPIKA: Ahsante. Okay, endelea ya kwanza.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika, dakikazangu zilichukuliwa kidogo tu. Akina mama wamemtumawanasema kwamba, watoto wa Dubai wananeemeka, waLoliondo na Ngorongoro wanateseka. Hii inadhihirisha wazikwamba, Serikali haiwajali ninyi wa Loliondo na Ngorongoro;teteeni haki yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Ukienda kwenyeTaifa la watu makini, Taifa la watu wenye akili, huwezi kukutawanapuuzia mambo muhimu kama mchakato wa Katiba

Page 112: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

151

12 APRILI, 2013

katika nchi yao. Ukienda katika Taifa la watu makini huwezikukuta watu wakipuuzia mambo ambayo ni muhimu kwamustakabali wa Taifa kama vile amani, umoja, upendo namshikamano wa Kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mambo haya yanakata crossparty lines, yanakwenda mbele zaidi ya misimamo namitazamo ya kiitikadi za vyama vya kisiasa; ni mambo yaKitaifa, ni mambo ambayo ni roho ya ustawi wa nchi yoyotekatika Dunia hii. Katika Taifa letu, kwa sababu ya upuuzitunajikuta tunadharau mambo kama haya na matokeo yaketunaacha watu wanayachezeachezea, tunaacha watuwanatuvuruga ilihali tukijua kabisa wanachezea Ikulu. Nafikirininaeleweka nikisema Ikulu? Hata siku moja huwezi kukutamzee akamruhusu mjukuu wake achezee Ikulu hata kamaanampenda namna gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sisi tunaruhusu watuwanapiga Ikulu, wanachezea mchakato wa kuleta Katibampya, wanachezea mchakato ambao utatupelekeakufanya mabadiliko ya mustakabali mzima wa kimfumo wakuongoza nchi yetu, tunawaacha wanachezea; ni upuuzi natutahukumiwa kwa upuuzi huu. Leo hii tunawaacha watuwanafanya matukio mbalimbali ya kuvunja amani katika nchiyetu, wanafanya maandamano kucha kutwa, wanatekawatu nyara, wanawaadhibu, vyombo vya ulinzi na usalamavipo, Serikali inasingiziwa imenyamaza tu! Haya mamboyanajulikana, ushahidi upo wazi na sisi tumenyamaza tutunaacha tunasema tunalinda Umoja wa Kitaifa.

Tunaleta mustakabali wa pamoja, uongozi wapamoja, inclusive leadership; hakuna inclusive leadership bilakuwa na utawala bora wa kisheria. Lazima kwanza watuwaheshimu Sheria na Taratibu zilizowekwa ili tuweze kuonasasa kuna amani. Leo hii anasimama Kiongozi Mwandamiziwa Chama cha Siasa kwenye majukwaa na hata ndani yaBunge, anasema hadharani kabisa kwamba, nchihaitatawalika na anaachwa tu. Huo wote ni upuuzi na huuupuuzi unasababishwa na wale wenzetu waliokaa kwenyeSerikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Page 113: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

152

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, sasa nawaomba hapa leo hii,muanze kuchukua hatua, watakapoingilia huu mchakato waKatiba ambao tumeupitisha hapa Bungeni tukakubalianawote hakuna aliyepinga, sasa leo hii wakatoka huko njewakafanya mambo ya kipuuzi wakaachwa tutasema sasana Serikali nayo inalea upuuzi. Basi sasa sisi tutashindwakuwaelewa wengine, ndani yetu tutaamua kuchukua hatua.Kwa mfano, wakijaribu kufika Nzega, ninaahidi ndani yaBunge hili Tukufu, nitawahamasisha Wananchi wa Nzegawatawakamata kuanzia viongozi wao hadi wafuasi wao nanitawashughulikia mimi binafsi kama Serikali itashindwakuwashughulikia. Hatuwezi kukubali upuuzi wa namna hiiukiendelea na sisi wengine tumenyamaza na Serikaliimenyamaza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ni kiongozi mpuuzi tu,anayeweza kuona hoja imeletwa kwenye Bunge imejadiliwawakatoka nje ya mchakato, sasa baadaye wanarudikinyumenyume wanapitia mlango wa uani wanaendakuongea na Mheshimiwa Rais Ikulu, Mhashimiwa Raisanawakubalia tu kwa wema kabisa twendeni na yalemnayoyataka, inatengenezwa Tume ya Katiba ambayo inaWajumbe miongoni mwao ni washauri wao kama ProfesaMwesiga Baregu, ni mshauri wao mkubwa na ni msomimkubwa katika nchi hii, yumo ndani ya Tume. Leo hii Kiongoziwa Kambi ya Upinzani Bungeni anachangia anasema, Katibahaina weledi. Katiba haina weledi wakati ndani yake kunawatu wazito kama Profesa Mwesiga Baregu, ambaye niMshauri Mkuu wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo; anasema hakuna dhamira kwamba, Tumeina upungufu ndani na nje. Sasa huu upungufu unatoka wapiwakati mchakato wa kutengeneza Tume mlishirikishwa naninyi ni sehemu ya uamuzi huo wa kutengeneza hiyo Tume.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kiongozi wa namna hiyo apuuzwena Watanzania, apuuzwe yeye na Chama chake naWatanzania wakiwaona wasiwaunge mkono wawakataekwa sababu hizo za upuuzi wao. Zaidi ya yote, Watanzaniawasikubali kuburuzwa na Viongozi wa aina hii. Watanzania

Page 114: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

153

12 APRILI, 2013

nawasihi mwangalie matukio ya uvunjifu wa amaniyanatokana na nini. Mojawapo kubwa ni kauli za Viongoziambao ni wapuuzi wanapuuza mhimili wa amani,mshikamano na umoja wa Kitanzania. Wanatoa kauli yakusema nchi haitatawalika, wanasema kila kitu waowanapinga tu, falsafa inayowaongoza ni oppose everythingpropose nothing. Hawana wanacho-propose, wao nikupinga kila kitu na ni kupinga kila siku, matokeo yakehawana hata kitu kimoja wanacholeta cha maendeleo kwaWatanzania. Watu wa namna hii ndugu zangu Watanzaniani wa kuwaogopa na kuwakataa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba sasa nijielekeze kwenyejambo moja tu ambalo ni la muhimu kwa wapigakura waJimbo la Nzega na hili ni la maji ya kutoka Ziwa Victoria kujaMkoani Tabora. Hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, ninaombaSerikali ya Chama cha Mapinduzi, isipuuze ahadi yaMheshimiwa Rais, itekeleze Mradi huu kadiri ilivyokuwaimeahidiwa ndani ya muda ili mwaka 2015 tuwe nalo lakusema kwenye majukwaa ya kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bila kusahau, naunga mkono hoja.Mwisho, nimalizie kwa kusema, wanaozomea wote ni wapuuzina niwataarifu tu kwamba, upuuzi wa namna hii hauwezikuwasaidia kuchukua nchi, upuuzi wa namna hii hauwezikuwasaidia kuwapa umaarufu, upuuzi wa namna hii hauwezikuwafikisha popote. Jifunzeni kuwa na leadership, jifunzenikuongoza na siyo kufanya harakati na kutukana na kufanyavurugu na Watanzania watawaelewa, lakini mkiendeleanamna hiyo, ninawahakikishia chama chenu kitakufa kablahatujafika mwaka 2015. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.(Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Ngenzabuke,atafuatiwa na Mheshimiwa Masele.

MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia

Page 115: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

154

12 APRILI, 2013

Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Naomba uniruhusuniendelee kuishukuru Serikali inayoongozwa na Chama chaMapinduzi, kwa kuendelea kufanya kazi ya kuunganisha nchikwa ujenzi wa barabara, madaraja, kuunganisha nchi mikoana vijij i. Nitakuwa mnyimi wa fadhila nisipomshukuruMheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuupendaMkoa wa Kigoma. Namshukuru sana na naomba niendeleekusema ahsante kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa waKigoma. Barabara zinaendelea kufunguka na tayari Darajala Mto Malagarasi limeshakamilika kwa asilimia 85. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba sasa barabarailiyobakia ya Kigoma - Nyakanazi nayo iweze kufikiriwahatimaye iweze kujengwa kwa sababu barabara ile ndiyomkombozi wa Wananchi wa Kigoma kwa wakati huuambapo usafiri wa reli haujakamilika. Naomba barabara ileiangaliwe iweze kujengwa mapema iwezekanavyo.Tunafahamu kwamba, tayari mpango wa ujenzi wa barabaraile unaendelea, lakini tunaomba uwekwe mpango mkakatiwa kuhakikisha barabara ile inakamilika kwa sababubarabara ile ndiyo inayosambaza pembejeo katika Wilayazote za Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, Serikali inayoongozwa na CCMkwa kushirikiana na Wananchi, imeweza kujenga vituo vyaafya, imeweza kujenga zanahati na sasa inaendelea na kazihiyo, lakini kuna haja sasa ya kuboresha huduma kwakuhakikisha kuwa waganga na wauguzi pamoja na vifaa tibavinapatikana. Nafahamu Serikali yetu ni sikivu na ina mpangowa makusudi wa kuhakikisha vitu hivyo vinapatikana kwasababu imejiwekea mipango mizuri ndiyo maana imeanzakujenga vituo na imejenga zahanati. Nafahamu kabisakwamba, waganga na wauguzi wanaendelea kusomeshwa,kwa hiyo, naomba watakaomaliza shule waletwe katikaMkoa wetu wa Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Wilaya ya Kasulu inamadaktari japokuwa siyo wengi lakini wapo, lakini hawanawasaidizi kwa maana ya waganga na wauguzi. NiiombeSerikali itusaidie kuwaleta waganga na wauguzi katika

Page 116: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

155

12 APRILI, 2013

Hospitali hiyo. Hospitali hiyo vilevile haina gari la kubebeawagonjwa (ambulance), naomba Serikali itusaidie kutuleteagari la kubebea wagonjwa. Vipo vituo vya afya, kwa mfano,Kituo cha Nyakintonto, Kituo cha Lusesa, navyo pia havinamagari ya kubebea wagonjwa. Wapo Madaktari ambaohawana kazi wamebaki kama wahudumu kwa sababuhawana vyumba vya kufanyia upasuaji. Naiomba Serikaliitusaidie kupeleka pesa ili tuweze kujenga vyumba kwa ajiliya upasuaji kusudi Wananchi waendelee kupata hudumahiyo katika vijiji hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu elimu ya msingi nasekondari; elimu ya msingi, walimu wapo lakini hawatoshi.Mara nyingi tunapofanya ziara vijijini, kilio cha Wananchi niwalimu katika shule za msingi na hasa katika shule zasekondari hakuna walimu, shule za msingi vyoo ni tatizo;naomba Serikali iliangalie hili. Vilevile ninawaombea walimuwapate stahiki zao ili wasivunjike moyo. Nami ni mwalimu,ninawapenda walimu wenzangu na nisipowasemeanitakuwa sijipendi mimi mwenyewe, naomba waangaliwe iliwaweze kufanya kazi yao vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na matatizoyanayojitokeza kwa watoto kutokufanya vizuri, naombaniwaambie Watanzania wenzangu na watoto wetu wa sikuhizi siyo wazuri, muda mwingi wanatumia kucheza na internet,muda mwingi wanatumiana message, ukienda muda wa jionisiku hizi watoto hawana tabia ya kujisomea. Sasa mtoto kamahataki kujisomea; hii nayo ni Serikali inayofanya mtoto afeli?Pamoja na matatizo hayo, watoto nao wajenge tabia yakujisomea ili waweze kufanya vizuri wanapokuwa wanafanyamitihani yao.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo la umeme katikaWilaya ya Kasulu, jenereta zil i letwa, umeme kidogoulipatikana lakini baadhi ya watu hawajaweza kupatiwaumeme kwa sababu ya baadhi ya watendaji ambaohawatekelezi maagizo wanayopewa na Viongozi wao.Wizara inaagiza lakini watendaji wa kule wilayanihawatekelezi maagizo waliyopewa na Viongozi wao.

Page 117: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

156

12 APRILI, 2013

Ninaomba nyaya zipelekwe sambamba na nguzo il iWananchi ambao hawajapatiwa umeme wawezekusambaziwa umeme.

Mheshimiwa Spika, pembejeo bado ni tatizo hazitoshi.Ruzuku ya pembejeo vilevile nayo ni tatizo. Pembejeozinapelekwa kule lakini Wananchi bado wana malalamiko,naiomba Serikali iliangalie hili. Naomba Serikali iliangalie hili.

Mheshimiwa Spika, kabla sijamaliza, naombaniwaombe Watanzania wenzangu kudumisha amani,upendo utulivu na mshikamano. Tunapoendakuwahamasisha kuanzisha vikundi kama hakuna upendo namshikamano na tukianza kubaguana kwa maana ya dini hiina dini hii, hata vile vikundi tunavyoenda kuvianzishahatutaweza kufaulu kwa sababu wataanza kubaguana walewatu tunaowafuata kule. Nawaomba Watanzaniawenzangu na hasa akina mama, tuuenzi utamaduni wetuwa kudumisha amani, upendo na mshikamano, kwa sababutukichezea amani sisi akina mama ndiyo tutakaoathirika. Sisindiyo tutakaokimbia na watoto, sisi ndiyo tutakaohangaikana watoto, wakati mwingine akina baba vita ikimkuta yukombali anachukua begi lake anakimbia anakuacha mamana watoto watano unahangaika. Nawaomba wanawakewenzangu tusisikie mambo ya kuambiwa, akili za kuambiwachanganya na za kwako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba, Serikaliya Chama cha Mapinduzi, Wabunge wa Chama chaMapinduzi, tusione haya kusema mazuri yaliyofanywa nachama chetu. Tutembee kifua mbele kuisemea Serikali yetu,hakuna mtu mwingine atakayekwenda kusema kama siyosisi tunaosema. Watu tuliozaliwa miaka ya 1960 kama mimina wazazi wetu, wanafahamu tumetoka wapi natunakwenda wapi. Watoto waliozaliwa siku hizi ndiyo haowanaodanganywa, hawaelewi barabara zamani zilikuwaje.Leo ukitoka Kasulu kwenda Kigoma Mjini, zamani ulikuwaunatoka saa kumi na mbili unafika saa nane mchana, leoukitoka Kigoma saa mbili, saa nne unaingia Kasulu na

Page 118: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

157

12 APRILI, 2013

unakwenda na kurudi. Serikali ya Chama cha Mapinduziimefanya mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba nikushukuru kwa kunipanafasi, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Namwita Mheshimiwa Masele,atafuatiwa na Mheshimiwa Batenga.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili na mimi niwezekuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ambayondiyo inaweka msingi mahususi wa mijadala yote ambayoitaendelea kuwepo hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, napenda kusemakwamba, naunga mkono hoja ya kwamba Bajeti yaMheshimiwa Waziri Mkuu ipite. Nchi hii imetoka mbali, nchihii inapitia katika vipindi mbalimbali, tumepata uhuru, tukawana mfumo wa chama kimoja, hivi sasa tupo kwenye Mfumowa Vyama Vingi, ni Watanzania hawahawa tunaelekeasehemu ya kukomaza demokrasia. Demokrasia siyo fujo.(Makofi)

Ndugu zangu Watanzania, niseme jambo moja tu;nchi hii inafanana na ziwa la maji au bahari, ndani yake kunaviumbe mbalimbali. Ziwani kuna viboko, kuna mamba, wotewanategemea maji yaleyale. Mamba atatoka atasemabwana wee kiboko toka, kiboko atatoka, baadaye jualikiwaka anarudi majini tena. Maji yakiendelea kuvurugikawote wataathirika. Kwa maana hiyo, nataka niseme hivi;Vyama vya Siasa tujifunze kufanya siasa za kistaarabu, kwasababu tunakwenda kuzungumza na Watanzania wenyeuelewa tofauti tofauti. Kwa maana hiyo, tunapokuwakwenye demokrasia changa kama hivi, tunatakiwa sasa sisiambao tunaelewa namna ya kufanya siasa tuwaelekezewafuasi wetu njia mwafaka ya kufikia yale malengo ambayotunakusudia. Vinginevyo, tutajikuta tunaivunja nchi hii nakufanana na nchi kama ya Somalia, ambayo ilikuwa naamani baadaye ikaipoteza na imewachukua zaidi ya miaka

Page 119: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

158

12 APRILI, 2013

20 kurejea katika hali ya utulivu, lakini napo mpakawanasaidiwa na watu wengine; tusifike huko.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombanijielekeze kwenye Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.Kwanza kabisa, nampongeza Mheshimiwa Rais, pamoja naMheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuamua kutenga maeneomapya ya utawala, mikoa na wilaya zake. Kwa maana hiyo,niombe sasa, kwa sababu tumeanzisha maeneo mapya yautawala ni sawasawa na mtoto anapozaliwa; mtotoanapozaliwa anahitaji msaada wa wale waliomtangulia nawazazi wake. Kwa hiyo, mimi naishauri Serikali sasa iwe najicho la huruma kwenye maeneo haya mapya ya utawala.Mikoa mipya ipewe upendeleo ili iweze kusimama nayo iwezekuchukua hatua za maendeleo kwa haraka kama Mikoamingine iliyotangulia.

Mheshimiwa Spika, tunapopitisha bajeti ni kitu kimojana utekelezaji ni kitu kingine. Kumekuwa na matatizo yamtiririko wa utoaji wa pesa kutoka Hazina kuja kwenyeHalmashauri zetu. Kutokana na hali hiyo, kama utaratibu huuutaendelea wa kuchelewesha pesa kuja kwenye maeneoya Halmshauri zetu ambako ndiko kwenye watendaji wengina Wananchi wengi, tutakwaza shughuli za maendeleokatika maeneo yetu. Kwa maana hiyo, ninaishauri Serikalikwamba, tutakapokuwa tumemaliza mjadala wetu twendemoja kwa moja kuhakikisha kwamba, yale ambayotunakubaliana tuyatekeleze kama yalivyo.

Mheshimiwa Spika, tunakwenda katika kipindi champito, tumejikuta katika wakati mmoja mgumu wa kutokuwana umeme wa uhakika; lakini naishukuru Serikali kwa sababuimeendelea kuchukua hatua za kuuendeleza Mradi wakuchukua gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ilituweze kuzalisha umeme wa bei nafuu na tuwe na umemeunaokidhi haja. Niombe tu hali iliyojitokeza Mtwara tuidhibitiili kuleta umoja wa nchi hii, maana tukianza kugawanamaeneo nchi hii haitakwenda. (Makofi)

Page 120: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

159

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kila mmoja akitaka ziwa Victoria;watu wa Mwanza, Geita, Bukoba liwe la kwao na maliasilizote zilizoko huko na watu wa Dar es Salaam nao wakabakipeke yao, nchi hii tutakuwa katika mazingira magumu sana.Kwa maana hiyo, niombe kuwa Serikali ya Chama chaMapinduzi kama ambavyo imekuwa sikivu, inasimamia Miradiyake ya Maendeleo vizuri, imejenga barabara za kutoshana sasa inaenda kuendelea na mpango wake wa kuwa nachanzo cha kueleweka cha umeme, ninaamini ya kwambatutafika salama.

Mheshimiwa Spika, tusipokuwa na nguvu za umemewa uhakika, uwekezaji hautakuwepo, wawekezajihawataweza kuja kuwekeza viwanda vikubwa ambavyovinaweza kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa kwa bei nafuuhapa nchini na kutoa ajira kwa vijana wetu ambao mpakasasa wanapokosa ajira wanajiunga katika makundi yakuandamana na kuipinga Serikali.

Mheshimiwa Spika, nije katika suala la ongezeko lawatu; Tanzania inaonekana kuwa watu wanaendelea kuwawengi, ardhi inakuwa ni shida na kuongezeka kwetu kamakutaendelea kama kulivyo, ina maana kuwa mbele ya safarituna hatari ya kudumaza uchumi wetu kwani tutajikutatunazozana na kuanza mapigano, kwa mfano, wanyamawanahitaji chakula, Wananchi pia wanahitaji chakula.

Mheshimiwa Spika, matokeo yake, kama kutakuwana tatizo la malisho kwa maana ya kuwa Wananchiwameongezeka na wanahitaji chakula, inakuwa ni kwambasisi sote tutakuwa tukigombea ardhi moja ambayo ni ndogo.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Batenga, atafuatiwana Mheshimiwa Mchungaji Mwanjale.

MHE. ELIZABETH N. BATENGA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia manenomachache katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Page 121: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

160

12 APRILI, 2013

Ukurasa wa 12 wa Kitabu cha Maelezo ya Mheshimiwa Waziriwa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, imeeleza namna Wananchiwatakavyoadhibiwa kwa kunyimwa fedha za maendeleo.Mimi nimeshangaa sana na kuumia sana kuamua kutotoafedha za maendeleo kwenye Halmashauri ambazo zitapataHati Chafu; ninajiulliza hivi Wananchi ndiyo wanaandikavitabu vya mahesabu? Hao wataalamu waliofundishwa nawakapewa kazi hiyo ya kutunza hesabu kwa nini waowasiadhibiwe badala yake mnawaadhibu Wananchi?

Mheshimiwa Spika, hii haikubaliki na wala haielewekina hii imeendelea kwa muda mrefu na Bunge limekemeakwa muda mrefu. Ningeshauri tufike mahali tuone kuwaunapozuia fedha za maendeleo ina maana Wananchi ndiyowalioadhibiwa, lakini Watendaji wao wanakaa wanatingishamiguu. Pia unakuwa unawadhalilisha sana Madiwani na miminikiwemo, tunapokaa katika vikao vya Halmashauri katikakusimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri, kwasababu wewe na Wananchi wako mnakuwa mmeadhibiwakwa kukosa zile fedha za maendeleo kutokana na Hati Chafu.

Pamoja na hayo, Hati Chafu na Hati Safi, ningependazote zioneshe thamani ya fedha zilizotumika katika Miradimbalimbali, kwa sababu inaweza kuwa Hati Safi lakinikiutekelezaji, Miradi iliyotekelezwa wala hailingani na fedhailiyotumika. Naiomba sana Serikali ilione hili, kutopeleka fedhaza maendeleo au kupunguza, unawaadhibu Wananchi. Sasatunapenda ile adhabu badala ya kupewa Wananchiwapewe Watendaji waliovurunda kazi zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependakulizungumzia ni posho kwa ajili wa Wenyeviti wa Vitongoji,Vijiji na Mitaa. Hawa watu ni Viongozi ambao wanaongozaSerikali ngazi za msingi, ngazi za chini walipo Wananchi, wanamajukumu mazito sana, wanasimamia Ulinzi na Usalamakatika maeneo yao, wanasuluhisha ugomvi na migogoromidogomidogo inayojitokeza, kama siyo wao penginekwenye mahakama na polisi kungekuwa hakupitiki, watuwangekuwa wanapeleka migogoro mingi kule.Wanasimamia shughuli za maendeleo, lakini pia wana

Page 122: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

161

12 APRILI, 2013

majukumu ya kutambua wakazi wa eneo lao nakuwatambulisha katika sehemu mbalimbali ambapomwananchi anahitaji utambulisho kama Benki, Polisi naMahakamani. Kwa hiyo, kwa majukumu hayo, Kiongozi huyuhapati muda mzuri wa kufanya shughuli zake binafsi zakumletea maendeleo au mahitaji yake na familia yake. Kwahiyo, ninaiomba Serikali ifikirie kuweka kiwango cha posho iliiweze kuwasaidia.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, napenda Serikaliiangalie namna nzuri ya kugawa rasilimali za Taifa na kwakutumia takwimu. Sasa, mimi huwa sielewi kama Mikoa iliyopembezoni huwa inajulikana kuwa nayo ingepaswa kupewarasilimali zaidi kwa ajili ya kuzingatia umbali huo. Kwa sababuya usafiri na usafirishaji, bidhaa nyingi katika Mikoa ile ya mbalihasa Mkoa wa Kagera na Wilaya zake, gharama ni kubwasana, lakini zinapotolewa fedha za Miradi wanahesabukwamba bei ya bati Dar es Salaam na Ngara vinalingana aukatika Wilaya zingine za Mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Hata Wakuu wa Mikoa wetu wako hapa, gharamaza usafiri za Mkuu wa Mkoa kutoka Kagera kuja hapa siyosawa na kutoka Morogoro kuja hapa. Kwa hiyo, hayo yoteyawe yanazingatiwa wakati wa kugawa fedha zamaendeleo na hata fedha za matumizi ya kawaida.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na mambo mafupi hayo,nina uhakika kuwa yameeleweka na ninaomba yazingatiwe.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na ninaungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ashsante. Mheshimiwa Mwanjale, atafuatiwana Mheshimiwa Mansoor Hiran.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, nami nikushukuru kwa nafasi hii, lakini ninataka nianzemoja kwa moja na Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.Ukurasa wa 31 ameelezea kwa kina kuhusu mwenendo wabei za mazao makuu hasa ya biashara, korosho na pareto.

Page 123: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

162

12 APRILI, 2013

Kwa upande wangu ninaomba kuzungumzia kidogo kuhusumambo ya pareto. Zao la pareto ni zao ambalo linalimwakatika maeneo mengi ya Jimbo langu la Mbeya Vijijini hasaTarafa ya Isangati, Tarafa ya Itembela, Makete, Njombe naIleje na huko Arusha. Tatizo la zao hili ni bei na ununuzilimesumbua sana. Mwaka jana alichaguliwa mnunuzi mmojakwamba anunue zao la pareto, lakini kwa bahati mbaya beiyake ikawa ni ndogo sana kwa Wananchi.

Kwa hiyo, Wananchi waligoma na baadayewakaingizwa wanunuzi wengine wa zao hili. Leo hii nilikuwaninapigiwa simu kuwa bado kuna mnunuzi mmojaameruhusiwa kununua pareto, inayolimwa katika maeneoniliyoyataja, lakini bei kateremsha tena na amewekamabango kila sehemu, akielezea bei ya pareto itakuwashilingi 1,800 badala ya shilingi elfu mbili na kitu ambayoilikuwepo wakati ule. Kwa hiyo, ninaiomba Serikali iwaruhusuwanunuzi wengine binafsi ambao hawana viwanda nahawawezi kununua viwanda kwa sababu ni watu ambaowanataka kujipatia biashara. Tukisema mnunuzi mmoja wakiwanda anunue pareto, bei yake inakuwa ya chini sana kiasiambacho hata Wananchi wamethubutu kusema kama huyundiye atakuwa peke yake ananunua pareto, basi paretohaina haja ya kulimwa tena.

Mheshimiwa Spika, maana yake ni kwamba, wakotayari kung’oa pareto kuliko mtu mmoja anunue. NinaombaSerikali iruhusu wanunuzi wawe wengi maana ni soko huria.Kwa nini mtu mmoja aruhusiwe kununua pareto na hawezikulipa bei nzuri? Ninaomba sana hili lisikilizwe hawa watuwaruhusiwe na waanze kununua pareto hiyo ambayoinalimwa na Wananchi hao. Ninafikiri Jimbo langu ni lakwanza kulima pareto kwa wingi katika nchi hii na ni zaopekee la biashara katika maeneo ambayo nimeyataja, kunasehemu zingine wanalima kahawa lakini kwenye maeneohayo pareto ndiyo zao la biashara na viazi.

Nil ikuwa ninaomba hawa wanunuzi binafsiwaruhusiwe kununua pareto hiyo ili kuwavuta Wananchi

Page 124: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

163

12 APRILI, 2013

waweze kulima pareto kwa wingi, kama kweli tuna dhamiranzuri ya kutaka kuboresha au kulikuza zao la pareto.

La pili, katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,ukurasa wa 40 ameeleza anasema, Serikali imeandaampango mkakati wa kuifanya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi,Mtwara na Tanga, kuwa ndiyo Mikoa yenye Utalii wa Fukwe.Ninaomba niseme neno hili kuwa, Mbeya ndiyo kiwanja chandege kimeisha na kimekwisha maana ndege zimeanzakutua na tuna maeneo mengi ambayo tungewezakuyaboresha au kuya-promote kuwa maeneo ya utalii; kwamfano, ukienda Kitulo, ukatengeneza barabara nzuri kutokaIsinje kwenda Kitulo, bila shaka utapata watalii wengiwatakaokwenda pale. Ukichukulia eneo la kutoka Kyela Mjiniukapeleka mpaka Matema, ni eneo ambalo watu wengiwanapenda kutembelea kule lakini barabara zake ni mbaya.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, watalii hao ambao tunategemeakwamba wakija Mbeya watatua na ndege waende hukowakapumzike, hakuna barabara. Serikali inasema nini juu yasuala hili, maana Dar es Salaam utalii umeanza miaka mingi,watu wanaenda huko lakini maeneo haya ambayo unawezakusema kuwa kwa Kusini nako huku sasa kungekuwa namaeneo ya utalii na yapo maeneo ambayo yameainishwa.Ninaiomba Serikali ijaribu kutafakari na kuifanya Mbeya naKusini yawe ni maeneo ya utalii. Kwa sababu fukwe zipo,maeneo yapo, kuna Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, ni maeneoambayo ni very potential kwa shughuli za utalii, ninaombamiundombinu yake iboreshwe ili tuweze kupata watalii nahasa wasafiri watakaotua katika Uwanja wa Ndege waKimataifa wa Mbeya. Kwa hiyo, tuboreshewe Barabara yaMatema na Barabara ya kwenda Makete.

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 64 mpaka wa66, Mheshimiwa Waziri Mkuu pia ameelezea kwa kina kuhusumambo ya Ukimwi kwamba kwa sasa maambukizi ya Ukimwiyamepungua. Juzi tumetembelea katika Kituo cha Chalinzena tukaona kituo kile kimejengwa lakini tulipofika paletukaelezwa kuwa, vituo hivyo viko sehemu nyingi; Mwanza

Page 125: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

164

12 APRILI, 2013

kipo, Mbeya kipo, Tunduma kipo na Makambako kipo.Ukiangalia hivyo vituo, sisi Wabunge tulioko hapainawezekana hatufahamu; kwa nini hivi vituo haviboreshwivikajengwa vizuri zaidi ili hawa wenye magari makubwawanaosababisha wakati mwingine hata kuleta maambukizikwa wingi, waweze kwenda pale na kujipatia huduma zaaina mbalimbali kama tulivyoelezwa wakati ule. Kwa hiyo,ninaomba vituo hivi vitangazwe na viboreshwe, vijengwekisasa zaidi ili watu waende na kupata huduma katika vituohivi na kwa kufanya hivyo maana yake hata maambukiziyatapungua.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa maambukiziyamepungua, lakini bado tunahitaji bidii zaidi ili maambukiziyaweze kupungua zaidi.

Lingine, katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuuilikuwa ni Mpango wa MMEM (III), ambao unakusudiakuboresha elimu nchini, hii ikiwa na maana ya kuongeza idadiya walimu nchini, kuongeza idadi ya vitabu vya kiada naziada, vifaa vya kujifunzia na kadhalika. Mimi nilikuwaninafikiria kwa msingi huo basi hata madarasa na shuletukienda huko vijijini ukaangalia ...

(Hapa kengele il i l ia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

SPIKA: Ahsante.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja. Nilitaka kumalizia hilo lakini basi.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mansoor, atafuatiwa naMheshimiwa Ngoye na Mheshimiwa Jafo ajiandae.

MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Spika,ninashukuru na mimi kwa kupata nafasi ya kuchangia Hotubaya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwanza, ninaunga mkono miakwa mia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Page 126: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

165

12 APRILI, 2013

Ninaomba nitoe pole kwa Wananchi wangu waJimbo langu la Kwimba, kwa mafuriko makubwa yaliyotokeajana katika Tarafa ya Mwamashimba, Kata ya Kikubiji na Kataya Shirembo, zimeathirika vibaya sana hususan Vijiji vyaMwamitinje, Mwabhayanda, Shilembo na Manganga.Wananchi zaidi ya 500 wamehifadhiwa kwenye zahanati nashule za msingi na nyumba zaidi ya 300 zimebomoka namashamba yameharibika.

Mheshimiwa Spika, mimi pamoja na Mbungemwenzangu wa Wilaya ya Kwimba, Mheshimiwa Ndassa, kwakushirikiana na Mheshimiwa DC na Wananchi wa Ngudu Mjini,leo tumetoa mchango na kupeleka msaada wa dharura kwaWananchi hawa ambao wameathirika. Pia barabara yakutoka Mabuki kwenda Jojiro na kufika Ngudu Mjiniimeharibika, daraja limebomoka na kusombwa na maji,Wananchi wa Ngudu Mjini wanazungukia Magu kwendaMwanza Mjini, hiyo njia ni ndefu sana kwao. Pamoja nakupeleka misaada ambayo tumepeleka leo, ninaombaMheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kutumia Mfuko wake waMaafa, atuletee msaada haraka iwezekanavyo, kwaniWananchi wameathirika. Katika Kata ya Kikubiji na Kata yaShirembo, maji yamejaa, Wananchi wako kwenye zahanati,hakuna madawa, chakula hawana, tunaomba wapelekewemablanketi na mahema ili wasipate matatizo zaidi.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hilda Ngoye, atafuatiwa naMheshimiwa Kandege.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa,ninaomba niunge mkono Hotuba hii ya Mheshimiwa WaziriMkuu kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, pili, katika kuzungumzia Hotubahii, naomba nigusie maeneo mawili, matatu, ambayo nafikirilabda yananikera sana ninapokuwa nikifanya kazi. Kwanzani suala la kilimo. Mimi napenda niwapongeze sana wakulima

Page 127: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

166

12 APRILI, 2013

wa nchi hii, kwa jitihada kubwa wanayofanya katikakushughulikia mazao mbalimbali na wanatufanya tuwe haikwa sababu wanatulisha kwa juhudi zao. Hii inaendana najuhudi za Serikali katika kuhimiza KILIMO KWANZA, juhudi hiyonaona ni kubwa lakini ina matatizo yake makubwa kamayalivyozungumziwa katika Hotuba ya Mheshimiwa WaziriMkuu.

Mheshimiwa Spika, suala la bei ya mazao ni gumu naWananchi wetu wanapata matatizo makubwa. Suala la beiya mazao limekuwa likizungumziwa kila mara na mazaoninayozungumzia ni mazao yote ya biashara na ya chakula.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa nikimwangalia mkulimawa ndizi wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya na mkulimawa viazi huko huko Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, mkulimawa mahindi wa Mbozi, Ileje pamoja na Mbeya Vijijini,wakulima hawa wamekuwa wakilima miaka nenda rudi lakinihawabadiliki kabisa kiuchumi, hawabadiliki kabisa kimaslahi,kwa sababu bei ya mazao ni ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakubaliana na suala la kuundachombo hiki ambacho Serikali itajaribu ku-regulate masualaya bei wakati bei inapokuwa inashuka, lakini najua pamojana kwamba wata-regulate bei, haitatosheleza kabisamchango wa mkulima anaotumia anapoandaa shambampaka anapotoa mavuno yake. Hamna namna yoyotehapa nchini tutakayomsaidia mkulima aweze kupata beinzuri, ni kuanzisha viwanda vitakavyoongeza thamani yamazao. Ukiongeza thamani ya mazao katika maeneoambayo watu wanalima mazao mbalimbali tutakuwatumemfanyia mkulima jitihada kubwa sana ili aweze kutajirika.

Mheshimiwa Spika, ninapozungumzia viwandavidogovidogo, nazungumzia vile vile viwanda vya kati; kunaviwanda ambavyo sasa hivi vinafanya kazi lakini ni vyakubabaisha babaisha tu; hakuna mtu anayefuatilia kutokaSerikalini kuona kama viwanda hivyo kweli vinafanya kazi kwastandard inayotakiwa, ndiyo maana tunapata mazaoambayo hayana thamani kubwa.

Page 128: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

167

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, napenda pia nipongeze juhudi zaSIDO; wanajitahidi kuelimisha wajasiriamali ili wawezekuzalisha vizuri, waweze kuweka viwanda. Hii haitoshi,nasisitiza Serikali ihimize kwa nguvu zake zote uanzishwaji waviwanda katika maeneo ya wakulima kulingana na mazaowanayolima.

Mheshimiwa Spika, suala la pili ni kwamba, nilipokuwanapitia Kitabu hiki cha Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,sikuona mahali popote ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu auTAMISEMI, wameliwekea mkazo mkubwa suala la uharibifuwa mazingira hapa nchini, halipo. Pia sikuona jinsi ambavyoOfisi ya Makamu wa Rais wanajipanga katika kuangaliauharibifu wa mazingira na kuiwekea mipango yake. Hilolimekuwa skipped sijaliona na nimewasiliana na Mawaziriwanaohusika nao wananishangaa. Kwa hiyo, nataka tunisisitize hapa, mpaka sasa nchi yetu ipo hatarini kuwajangwa, kwa sababu uelewa wa Wananchi katika suala zimala mazingira ni mdogo sana. Vile vile ukienda kuangalia waleambao wanatakiwa kusimamia masuala haya ya mazingiraambayo ni Serikali za Mitaa, jamani hawajachukua hatuakubwa ambazo zinaonesha kuna juhudi yoyote ya kusimamiasuala la mazingira.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba sana, nchihii tunazungumzia masuala ya mabadiliko ya tabianchi kilasiku na athari zake kwa kilimo, lakini kila wakati tumekazanakuzungumzia suala la kilimo cha umwagiliaji, suala la kilimocha mvua, lakini hatuangalii huko tuendako; je, haya mamboya kilimo yatakuwa endelevu kama masuala ya mazingirahatujayatilia mkazo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba sana tena sana, Serikaliiingie kwa nguvu katika kulisimamia suala la mazingira nahotuba za Viongozi mbalimbali zijikite huko ili Wananchi naowashtuke waone kweli kuna umuhimu wa kusimamia masualaya mazingira hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa taarifa kuwa,hatujakuletea lakini hapa baadhi ya Wabunge tumeanzisha

Page 129: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

168

12 APRILI, 2013

Umoja wa Marafiki wa Mazingira, ambao tunataka tuendeleekupiga kelele kuhusu suala la mazingira hapa nchini, kwasababu ya hali ilivyo na inavyokwenda ni mbaya sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ninalotakakulizungumzia ni kuhusu utawala wa mikoa. Nimefanya kazikatika nafasi hii ya utawala wa mikoa kwa miaka kama ishirinihivi katika uongozi kama Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa.Mimi nashangaa kidogo, kwa wale wanaosema watu hawahawana kazi, ninashangaa sana kwa sababu hakuna kitukinachokwenda huko mikoani kama hakuna msukumo waMkuu wa Mkoa wala msukumo wa Mkuu wa Wilaya! Mamboyanasimama vilevile ni mpaka Mkuu wa Mkoa au Mkuu waWilaya aingilie kati. Kama ni ulinzi wa amani ni Mkuu waMkoa, tunakaa kwa amani hapa na utulivu ni kwa sababuWakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanadhibiti masualaya ulinzi na usalama wa nchi hii, lakini na masuala yamaendeleo vilevile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, law and order has to be there.Lazima iendelee kuwepo na hawa watu, lazima waendeleekuwepo. Ila jambo ambalo ningetazamia watu waseme nikuwatetea watu hawa jinsi wanavyofanya kazi katikamazingira magumu; hawana fedha, hakuna bajeti yakutosha, lakini majukumu anayopewa kwamba nenda pale,nenda kulia, kushoto, katikati na hakuna fedha! Sasa mtummoja sijui ni nani; …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Haaa! (Kicheko)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Sasa namwita Mheshimiwa Jafo.

Page 130: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

169

12 APRILI, 2013

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, awali yayote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, ambayeamenipa fursa jioni hii ya leo kuongea, lakini nakushukuru nawewe kwa kunipa nafasi jioni hii.

Mheshimiwa Spika, kwanza, naomba niwasihi sanandugu zangu Watanzania, suala zima la amani halinambadala, tuzungumze mambo yote kama Viongozi wa nchi,lakini suala zima la amani halina mbadala. Mara nyingi hatavitabu vya dini vimesema kwamba, kuna sifa maalum ya mtuanayeitwa mnafiki, mnafiki hata ukimwamini yeye anafanyahiyana na anapozungumza ni lazima atasema uwongo naakiweka ahadi basi hatimizi! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulipitisha mchakato mzima katikaajenda ya kwanza katika Sheria ya Mchakato wa Katiba,kuna watu walitoka humu ndani, bahati mbaya wakaendakwa Mheshimiwa Rais kwa mlango wa nyuma, MheshimiwaRais akawakubalia, chai ikaanza. Ninakuomba MheshimiwaWaziri unayehusiana na mambo ya uhusiano, ikiwezekanahata staftahi nyingine wekeni pilipili siku hizi. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea maslahi ya nchi,suala zima la Katiba siyo suala la Chama fulani, ni mustakabaliwa Taifa la Tanzania. Leo hii tumekubaliana kwa pamoja,mchakato unakwenda wewe unasema hapana; nini niayako? Nia yako maana yake una ajenda nyingine nyuma yamlango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba ndugu zanguWatanzania wote, katika Vyama vyetu tulikemee hili, ni lazimatushikamane kwa mustakabali wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hilo, kamakifungua kinywa cha hotuba yangu hapa au mchangowangu, naomba kujikita sasa katika Hotuba ya MheshimiwaWaziri Mkuu. Kubwa zaidi, juzi tumeona jinsi gani Watanzaniawanalalamikia kupanda kwa nauli, lakini kupanda kwa naulimaana yake nyuma kuna hoja nyingine inayofuata,purchasing power ya Watanzania ipo chini sana.

Page 131: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

170

12 APRILI, 2013

MBUNGE FULANI: Kiswahili!

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, uwezo wakwenda dukani kununua mahitaji, hii ni changamoto kubwasana. Tatizo kubwa ni nini? Nashukuru sana Serikali imejitahidikupandisha mishahara katika vipindi mbalimbali, lakini nduguzangu naiomba Serikali, Mheshimiwa Waziri Mkuu naombaunisikilize, bahati nzuri bajeti ya Waziri wa Fedha itakujamwishoni, naomba tuangalie suala zima la makato ya kodikwa wafanyakazi wote. Makato ya kodi ni makubwa hatamshahara ukipanda, kodi inayokatwa ni kubzwa zaidi.

Kwa mtu wa kima cha chini anakatwa asilimia 14 nawale wa juu anayepata mshahara mkubwa zaidi anakatwashilingi laki moja na ishirini plus asilimia 20 ya ongezeko lashilingi laki saba na ishirini, kiasi kwamba, hata mtu akipatashilingi milioni tano, kadiri unavyokatwa maana yake mwishowa siku anarudi nyumbani akiwa hana kitu.

Mheshimiwa Spika, naiomba sana Serikali iangaliekwa kina jinsi gani itafanya, kuboresha maisha ya wafanyakaziwote na hii tuangalie jinsi gani ya kuboresha suala zima katikapay as you earn. Katika Taifa letu tunajua jinsi ganiwafanyakazi katika pay as you earn; kwa mfano, katikatakwimu za mwaka 2010/11, ni sehemu peke yake ambayoimeongoza kuliko hata corporate tax. Michango ilikuwakaribu bilioni 934, asilimia 17 ya Pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iangalie ni jinsigani itaangalia kwa kina kulipa kodi vizuri katika sehemumbalimbali zisizokusanya kodi na ninyi mnajua ni mashahidi,kulikuwa na sakata kubwa sana la jinsi gani vilabu vya mipirahapa nchini vilikuwa havilipi kodi mpaka klabu yetu na kakayangu Ismail Aden Rage na Yanga, vilikuwa havilipi kodi. Inamaana kwamba, ukusanyaji wa kodi bado ni tatizo katikanchi yetu. Naiomba Serikali iangalie ni jinsi gani tutakusanyakodi ilimradi kuhakikisha tuna-compensate katika suala zimala kupunguza kodi kwa wafanyakazi. (Makofi)

Page 132: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

171

12 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini kama nchi inaamini sasa hivituna vijana wetu wengi wapo mitaani hawana kazi,walioajiriwa ni wachache sana. Kuporomoka kwa suala zimala viwanda nchini kunasababisha janga kubwa la vijana wetuwaliomaliza Vyuo Vikuu na wa kada mbalimbali wakakosakazi. Naomba sana Serikali yetu ijielekeze zaidi katika sualazima la ufufuaji wa viwanda na kuhakikisha tunaboresha sualazima la ujenzi wa viwanda vipya, bila hivyo suala la ajiratutakuwa tunazungumza kila siku.

Mheshimiwa Spika, tulitembelea pale Mtwara, karibuviwanda vyote vya Korosho vimekufa, bila kurekebisha hilotutakuja kupata matatizo makubwa. Kwa mfano, mimikwangu Kisarawe kuna Kiwanda cha STAMICO kilibinafsishwatoka mwaka 2006, yule mwekezaji mpaka leo anahangaikakatika Ofisi ya Waziri wa Ardhi kuweza kupata hati na jinsigani aweze kuungana na wadau mbalimbali kuboresha kilekiwanda na vijana wangu wa Kisarawe wapate ajira.Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, ulisimamie hili kwakaribu zaidi kwa ajili ya kuboresha maisha ya vijana wetu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninalotakakulizungumzia ni suala zima la ajira. Toka mwaka janatumepiga kelele sana, utaratibu wa Sekretarieti ya Ajira kuajirimpaka Mtendaji wa Kijiji, jambo hili sisi haturidhiki nalo.Ukienda sehemu mbalimbali vijijini hakuna hata watendajiwa vijiji, hakuna watendaji wa kata, sababu kubwa ajira zotezifanywe na Sekretarieti ya Tume ya Ajira. Jambo hilihaliwezekani. Kwa nini Halmashauri zisiajiri tuna vijana wengikatika Halmashauri zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii inawezekana Mkuu waMkoa mpya ameajiriwa na dereva mpya ameajiriwa,wanaulizana wakipangiwa safari hata sehemu ya kwendahawajui, dereva mpya hajui maeneo yenyewe. Tungepelekaajira katika Halmashauri zetu, inawezekana ajira hizi zingetokakatika baadhi ya Halmashauri ambazo vijana wametokamaeneo yale. Naiomba Serikali iharakishe mchakato huumaana kila siku tutafanya kesho, kesho kutwa, tunawakera

Page 133: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

172

12 APRILI, 2013

Wananchi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili Waziri Mkuu lipo kwako halipokwa mtu mwingine yeyote. Ninaamini katika kuhitimishahotuba yako hii, nakuomba ikiwezekana tusikie Watanzaniakwamba mchakato huu sasa unarudi katika Halmashauri zetuilimradi vijana wetu wapate ajira katika maeneo yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana MheshimiwaWaziri Mkuu, pale kwangu Hospitali yetu ya Wilaya inamatatizo makubwa sana, lakini ofisi yako imetuma wadaumbalimbali hasa katika ofisi yako, Naibu Katibu Mkuu amefikapale. Ninakumbuka kwa sababu mwaka jana niliuliza swalila msingi mwezi wa sita na bahati nzuri mmetuahidi kutufanyiaukarabati katika Hospitali yetu ya Wilaya pamoja nakuitengeneza mortuary. Nakushukuru sana, lakini naaminibajeti hii itasaidia kuleta mchakato mzuri ili Wilaya ya Kisarawetuwe katika mazingira mazuri na kama mnavyojua, Kisaraweina-accommodate baadhi ya wagonjwa wengi kutoka Dares Salaam. Kiujumla, nikizungumzia hata Mkoa wetu waPwani pale Hospitali yetu ya Tumbi ni sehemu kubwa ambayoinapokea wagonjwa wengi hasa majeruhi. Hospitali hiitumeipandisha sasa hivi, watu wote pale Kibaha kwa nduguyangu Mheshimiwa Koka, wanapata huduma katika Kituocha Afya cha Mkoani, hakiwezi ku-accommodate akinamama ambao wanafika pale, akina mama wanadhalilika.

Mheshimiwa Spika, tunaomba ofisi yako yenye jukumuhili iangalie jinsi gani itaboresha Kituo cha Afya cha Mkoanipale Kibaha, ambapo mimi ni Mjumbe katika Kamati yetuya Mkoa, tunahudhuria Vikao vya RCC, naomba MheshimiwaWaziri Mkuu uangalie jinsi gani utatusaidia Mkoa wa Pwani.

Mheshimiwa Spika, tumeshuhudia sasa hivi Tanzania,juzi juzi nilienda kutembelea Mkoa wa Kigoma, watuwasiokuwa na shukrani ni lazima wazungumze; miundombinuya barabara hivi sasa imeboreka. Tanzania yetu hii siyo yasiku za nyuma, sasa hivi hata watu wengine

Page 134: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

173

12 APRILI, 2013

wanaohalabwanya humu ndani, kwao kuna barabara yalami wanakanyaga! (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa WaziriMkuu, aingalie Kisarawe, ile barabara yetu ya kilomita 54mwaka huu bahati nzuri imefanyiwa upembuzi yakinifu,tunaomba sasa tabaka la lami liweze kuja hapa. SikuMheshimiwa Magufuli atakapokuja hapa, nataka nione nijinsi gani Kisarawe inaguswa katika suala zima la ujenzi wabarabara ya lami.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yake MheshimiwaWaziri Mkuu amesema kwamba, Kisarawe kutatengenezwadry port, kituo cha kuwekea mizigo inapotoka bandarini, nivyema nakushukuru sana na ninaishukuru Serikali.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja,ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, naombaniseme kwamba, huyu ndiye msemaji wetu wa mwisho nautaratibu wetu bado umekwenda vizuri sana, jioni hii tulikuwatumejipangia watu 17 lakini wamefika 22, nadhani tunaendavizuri. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nina matangazomachache; kwanza, nakumbushia ile semina ambayoitatupa sisi uelewa wa wenzetu wenye ugonjwa wa ngozi namahitaji yao ya msingi na tabu waliyonayo. Semina hiyoitaanza saa tatu pale Ukumbi wa Msekwa, ni kwa Wabungewote. Najua mnataka kupumzika lakini mjitahidi kuwahi,inapendeza watu mkianza wengi na mgeni wetu rasmiatakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu; tunamshukuru kwakukubali hilo.

Waheshimiwa Wabunge, tangazo la pili sasa sijui hatanisemeje, zi le fomu za kuomba namna unavyotakakuchangia kuanzia sasa mpaka mwisho, kuna wenzetukadhaa hapa wameandika lakini wakasahau kuandika

Page 135: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

174

12 APRILI, 2013

majina sasa tunafanyaje. Mimi hata sijui nisemeje maanahata kusema nimwite nani sijui! (Kicheko)

Kuna Waheshimiwa Wabunge watano, sasa naombayule anayejifikiria kwamba labda alisahau apite pale ofisinikwetu akacheki kujua hali yake ni hiyo hiyo maana ni vigumukabisa kujua. Mwingine amepiga tick kama kura za uchaguzi;tulisema muweke priority ya kwanza, ya pili, ya tatu, sasawewe umepiga tu kama unapiga kura. Kwa hiyo, tuna watuwatano na wengine kama mna mashaka na fomu mlijazavipi tafadhali piteni pale ofisini watawasaidia.

Waheshimiwa Wabunge, jambo linguine ambaloningependa kusema ni kwamba, jana kulikuwa namwongozo ulioombwa na Waziri wa Nchi kuhusu manenoaliyozungumza Mheshimiwa Lugola, tukasema tusubiriHansard. Baada ya kutafuta na kuangalia Sheria ama Kanuniyetu, Kanuni ya 63(2) inasema: “Mbunge yeyote anapokuwaakisema Bungeni, hatachukuliwa kuwa anasema uwongoiwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo fulanilililotangazwa au lililoandikwa na Vyombo vya Habari.”

Waheshimiwa Wabunge, Hansard ya MheshimiwaLugola jana inasema katikati kwamba, nilisoma kwenyegazeti moja, Kamishna wa Tume ya Udhibiti wa Madawa yaKulevya, Ndugu Christopher Kyondo anasema,wanawafahamu kwa majina wanaohusika na madawa yakulevya, lakini wameshindwa kuwakamata kwa sababu yambinu walizonazo. Hiyo ndiyo aliyosoma kwenye magazeti.Sasa yeye anaendelea anasema maana yake ni nini? Maanayake ni, kama siyo rushwa zinazosababishwa na Watendajiwa Serikali au hata wakiwemo baadhi ya Mawaziri ndiyowanahusika na madawa ya kulevya.

Waheshimiwa Wabunge, sasa nasema kwamba,alisoma kwenye gazeti, naomba hili liishe hakuna sababu yakuthibitisha kwa mujibu wa Kanuni zetu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hivyo,nawaomba mwende kwenye semina kesho na akina mama

Page 136: 12 APRILI, 2013 MREMA 1parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461846739-HS-11-4-2013.pdf2 12 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU) alijibu:-Kwa upande

175

12 APRILI, 2013

kuna mkutano mkubwa sana wa akina mama kule juu UDOM,ni wa akina mama wa vyama vyote, kuna Mkutanounaendelea kule mkiweza kufika pia itakuwa vizuri, ni tarehe13 na tarehe 14.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, nawashukuru sanakwa weekend hii, ilikuwa weekend ya majaribu, tulikuwa tupokwenye mchakato hata wa kuangalia tunakwendaje, lakininawashukuru mmeshiriki toka kila hatua na hili ni jambo jema.Nasi tutakuwa tunaendelea kushauriana mara kwa mara ilitujaribu kurudisha hali ya kuwa pamoja wakati wote kulikokuparaganyika. Taarifa tulizonazo kutoka kwa Wananchi nikwamba, wamefurahi sana mnavyochangia, maanamnachangia habari zao. Kwa hiyo, nawashukuru sana,niwatakie weekend njema na yenye manufaa na mshirikiinavyopaswa. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naahirisha mpaka Siku yaJumatatu, saa tatu asubuhi. (Makofi)

(Saa 1. 40 jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya JumatatuTarehe 15 Aprili, 2013 Saa Tatu Asubuhi)