24 aprili, 2013 mrema 1 -...

242
24 APRILI, 2013 1 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 24 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. AMINA N. MAKILAGI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Upload: others

Post on 30-Aug-2019

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

1

BUNGE LA TANZANIA_______________

MAJADILIANO YA BUNGE_______________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 24 Aprili, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MAJI:

Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji kwa Mwaka waFedha 2013/2014.

MHE. AMINA N. MAKILAGI (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):-

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugona Maji Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Majikwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na maoni ya KamatiKuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyokwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

2

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Makilagiambaye pia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Kinamama waCCM Tanzania. Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani.Namwona Mheshimiwa Cecilia Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAJI):-

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani waWizara ya Maji Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MASWALI NA MAJIBU

Na. 95

Serikali Kushindwa Kulipa Madai Mbalimbali yaWafanyakazi

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA (K.n.y. MHE. DAVID E.SILINDE) aliuliza:-

Miongoni mwa malalamiko makubwa yawafanyakazi kwa Serikali ni kushindwa kulipa malimbikizo yaoya mishahara, likizo pamoja na makato mengine.

(a) Je, ni lini Serikali itayashughulikia matatizo hayana kuwalipa wafanyakazi stahili zao?

(b) Je, kwa nini Serikali imekuwa ikipuuzamalalamiko ya wafanyakazi hao na kuyafanya yaonekanesio ya msingi?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA aljibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa David E. Silinde, Mbunge wa Mbozi Magharibi,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 3: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

3

(a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo yamshahara ya watumishi wa Umma kulingana na uwezo wakeambapo katika mwaka wa fedha 2011/2012, Serikali ililipamadai ya malimbikizo ya mshahara kwa watumishi 54,010yenye jumla ya shilingi 72,351,994,390.92/-.

Aidha katika mwaka wa fedha 2012/2013 Serikaliimeendelea kulipa madai ya malimbikizo ya mishahara yawatumishi wa umma hadi kufikia Machi, 2013 jumla ya madaiya watumishi wa umma 11,820 kati ya watumishi 52,039wamelipwa malimbikizo ya mishahara na kiasi cha shilingi12,603,190,834/- kimetumika.

Malipo ya malimbikizo ya watumishi 27,245 yenyethamani ya shil ingi 16,089,986,605/- yalikuwayameshahakikiwa na yanasubiri kufanyiwa malipokutegemeana na upatikanaji wa fedha. Madai yamalimbikizo ya mishahara ya watumishi 12,974 lenye thamaniya shilingi 12,588,847,207/- yalikuwa kwenye hatua ya uhakikikabla ya kuingizwa kwenye mfumo.

Mheshimiwa Naibu Spika, il i kuepuka tatizo lamalimbikizo ya mshahara vilevile Serikali inatekeleza mikakatimbalimbali iliyojiwekea kama ifuatavyo:-

(i) Serikali imeanza kutumia Mfumo wa Taarifa zaKiutumishi na Mshahara (Human Capital ManagementInformation System (HCMIS) katika kushughulikia mishaharaya watumishi wa umma pale mwajiri alipo ili kuepukaucheleweshaji.

(ii) Kutekelezwa kwa Waraka wa Katibu MkuuKiongozi Na.1 wa mwaka 2009 kuhusu udhibiti na ongozekola madeni ya Serikali kwa watumishi wa Umma, Waraka waKatibu Mkuu Kiongozi Na.1 wa mwaka 2010 kuhusu uwajibikajikatika kusimamia rasilimali watu Waraka wa Katibu MkuuUtumishi Na. 1 wa mwaka 2011 kuhusu kuimarisha usimamiziwa rasilimali watu Waraka wa Hazina Na. 2 wa mwaka 2010kuhusu uwajibikaji na udhibiti katika usimamizi wa malipo yamishahara.

Page 4: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

4

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hatuahizi nilizozitaja hapo juu sio kweli kwamba Serikali imekuwaikipuuza malalamiko ya wafanyakazi kwa kuwa kwa nyakatimbalimbali ikipokea, huhakiki na kulipa madai ya malimbikizoya mshahara na matumizi mengineyo. (Makofi)

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swalila kwanza, kwa kuwa Serikali imekiri kwamba imeanza kulipamadeni ya wafanyakazi wakiwemo walimu kuanzia mwaka2011/2012 lakini kutokana na taarifa tulizo nazo ni kwelikwamba kuanzia mwaka 2011 kushuka chini bado kunawatumishi hususan walimu ambao wana malimbikizo yamishahara yao na stahili zao hususan Chama cha Walimuambacho kimetoa taarifa kwamba mpaka sasa hivi kinaidaiSerikali jumla ya shilingi bilioni 27.

Je, ni lini Serikali italipa malimbikizo ya watumishi hawahususan walimu ili elimu yetu iendelee kuwa endelevu nabora?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika Bajeti yamwaka jana tulipitisha hapa fedha za kuwalipa walimuambao watafanya kazi katika mazingira magumu jumla yashilingi 500,000/-. Lakini mpaka sasa hivi kuna malalamikomakubwa ya walimu hususan ni vijijini wanaofanya kazi katikamazingira hayo magumu kwamba zile fedha hazijalipwampaka sasa hivi na kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba zilefedha zilitoka kwa wafadhili na Wizara imetumia katikashughuli nyingine.

Je, ni utaratibu gani uliotumika kwa Wizara kubadilishamatumizi ya fedha hizo bila kwanza kuleta hapa Bungeni?Ahsante sana.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA ELIMU: MheshimiwaNaibu Spika, moja ni kwamba Julai, 2011 wakati Chama chaWalimu kilipotangaza kwamba kinaidai Serikali shilingi bilioni29, ilikuwa inajumuisha malimbikizo ya madeni yote mpakakipindi hicho.

Page 5: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

5

Lakini Serikali ilifanya hatua ya kukaa nao pamojabaada ya kutangaza hivyo, ikaamua kuhakiki pamoja naCWT na ikagundulika kwamba sio bilioni 29, waliyokuwawanasema bali ni shilingi bilioni 52. Serikali ikatenga fedhahizo ikaanza kuzilipa awamu kwa awamu lakini kwa njiauharaka kwa sababu ilipangwa mishahara ilipwe na Hazinana fedha zisizokuwa za mishahara italipwa na TAMISEMIpamoja na Wizara ya Elimu. Mpaka Januari mwaka huu2013 deni lile la bilioni 52 pesa zote zimekwishalipwa nahakuna pesa ambayo haijalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina hakika kwambakuanzia pale tulipokubaliana hivyo madeni yaliendeleakujijenga lakini tuko katika mkakati kama alivyosema,alitangulia kujibu swali hili kwamba tuko katika mkakati wakuhakikisha kwamba tunadhibiti na haturudii tenakurundikana na madeni hayo kwa miaka ijayo il ituwaondoshee adha walimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hili la pili linalohusushilingi 500,000/- zile za mazingira magumu ambazotumepewa na wahisani; tulipewa fedha hizo kwa mwakammoja na kwa walimu tu. Wakati zinaandaliwa kulipwaikazuka mgogoro kwamba wale wanaoripoti mwaka juzi ulendiyo wanalipwa posho zile za kuingia katika mazingiramagumu.

Lakini Walimu waliokuwepo nao wakadai kwambasisi je, ambao tupo tayari hapa posho zetu ziko wapi. Lakinikatika mazingira tuliyonayo kuna watumishi wengi tu kwenyeWilaya hizo kama waganga na kadhalika ambao wakajajuu nao.

Serikali ikalazimika ku-hold na kuzungumza na mhisaniili zitumike zile pesa kwa namna nyingine ya kuwafaa walimuhawa kuliko kuwapa posho ambayo tayari imeshaingia katikamgogoro. (Makofi)

Page 6: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

6

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.Kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 20 (1) na (4) suala lawafanyakazi kuwa wanachama wa chama chochote chawafanyakazi ni suala la hiari. Sasa hivi karibuni kuna kesi mojapale manispaa ya Kigoma Ujiji ya walimu kuendelea kukatwaasilimia mbili na Chama cha Walimu.

Tatizo lililopo ni mwajiri kukataa kuondoa yale makatona kesi ilishaisha Mahakamani. Suala hili halipo Mahakamanikama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyoeleza.

Je, Waziri yupo tayari kuweza kusimamia suala hili ilikuhakikisha kwamba walimu wa Manispaa ya Kigoma Ujijiambao wameshaomba kujiondoa na shauri lilishakwishaMahakamani ili makato yao haya ya asilimia mbili yawezekusimama mara moja ili wizi huu au tatizo hili la Chama chaWalimu kuendelea kuwakata pesa zao ambazo wao hawakohiari iweze kukoma?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Machali, swali la msingil inahusu malimbikizo ya mishahara lakini namwonaMheshimiwa Waziri Kazi na Ajira.

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika,ni kweli Chama cha Wafanyakazi ni chama cha hiari natunaomba wafanyakazi wote wajue hivyo. Kwa hiyo, walimokama wafanyakazi wengine kuingia CWT lazima waingie kwahiari kwa kujaza fomu na kwa kujaza fomu nyingine ambayoinaruhusu makato.

Lakini tatizo la walimu ni kwamba katika Sheria hiyowanapokuwa wafanyakazi wanapoingia kwenye chama nani zaidi ya asilimia 50 kuna kitu kinaitwa Wakala wa kusaidiamazungumzo na mwajiri kwa chama husika. Kwa hiyo, walimukinachowakumba ni hicho.

Page 7: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

7

Lakini tumeshaagiza vyama vyote vituletee taarifa niwafanyakazi wangapi wanaowakata na ni wafanyakaziwangapi wanaokatwa hiyo ada ya uwakala. Chama chaWalimu wametuambia by June, 2013 watakuwawametuletea hiyo taarifa na tumewaagiza pia watoe elimukwa wafanyakazi wao kabla hawajawakata hiyo ada yauwakala.

Na. 96

Tatizo la Ulipaji wa Mafao ya Wastaafu

MHE. SAID AMOUR ARFI aliuliza:-

Kumekuwepo na tatizo sugu la kulipa mafao yawastaafu na mirathi kwa waliokuwa watumishi wa umma.

Je, ni sababu zipi zinazopelekea Serikali isilipe stahikihizo?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM)alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waFedha napenda kujibu swali la Mheshimiwa Said Amour Arfi,Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo:-

Mhehsimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa inalipastahiki za wastaafu na warithi wa mirathi kwa wakati palenyaraka na kumbukumbu kamilifu zinapofikishwa Hazina.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu kubwainayosababisha malipo tajwa kuchelewa ni baadhi ya waajirikutokamilisha taarifa za waajiriwa wao na kuziwasilisha Hazinandani ya majalada husika kwa wakati ili Hazina wawezekulipa madai husika.

Aidha, taratibu zinamtaka kila mstaafu au mrithikuhakiki taarifa zao kwenye mifuko ya pensheni kila baadaya miezi sita (6) na asiyehakiki malipo yake husitishwa hadiatakapofika kuhakiki.

Page 8: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

8

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastaafu ambaowalilipwa kwa mkupua huko nyuma na kurejeshwa kwenyepayroll ya Serikali hivi karibuni, ucheleweshaji umekuwaunatokana kwa wastaafu hao kutokamilisha nyaraka nakuziwasilisha Hazina kwa wakati.

Aidha, kwa upande wa malipo ya mirathikumekuwepo na matatizo kwa baadhi ya warithi/wasimamiziwa mirathi ama kutoelewa taratibu au migongano ndani yafamilia hali inayosababisha malipo kuchelewa. Mfano kunamadai yalifikishwa Hazina baada ya miaka saba tangu kifocha mtumishi kutokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Fedha kwakutambua tatizo hili imekuwa ikitoa elimu kwa wadau nawaajiri kwa njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya redio, runingana semina mbalimbali za kikanda. Aidha, Hazina kupitiamaonyesho ya sabasaba, nane nane na wiki ya Utumishiwa Umma imekuwa ikitoa elimu hii kwenye mabanda yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inapenda kutoa witokwa wastaafu na wasimamizi/warithi wa mirathi kuhakikishawanahakiki taarifa zao kila baada ya miezi sita ili kuepushatatizo la kufutwa/kuchelewesha malipo yap.

Aidha Ofisi za Hazina Ndogo zilizopo kila Mkoa zinaAfisa anayeratibu masuala ya wastaafu na mirathi, hivyo nivema wananchi wakazitumia ofisi hizi badala ya kusafiri hadiDar es Salaam. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. SAID AMOUR ARFI: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na maelezo marefu sana ya Mheshimiwa NaibuWaziri, lakini kimsingi anasema kwamba wastaafu na waarithiwa mirathi wanalipwa kwa wakati. Naomba tu unisaidieMheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba nimeandikiwa SMS nayatima wanasema kwamba watanikumbuka kwakutokuwasimamia kulipwa mafao yao ya mirathi yamarehemu Peter Mtindo aliyefariki tangu mwaka 2003 naakawasilisha nyaraka zake mwaka 2005 na akafuatilia ofisi

Page 9: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

9

ya TDS mwaka 2009 akakuta jarada limepotea, likatumwatemporally file mwaka 2010 na mpaka leo mwaka 2013hawajaliwa na wewe unasema wanalipwa kwa wakati.Kama mnawadhulumu watu hawa mseme na kama Serikaliitakuwa tayari kuwalipa sasa pamoja na riba kutokana nakuwacheleweshea malipo yao. Hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili wastaafu wengihawalipwi fedha zao kwa wakati na hasa mfuko wa PSPFunachelewesha kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati, aidhakwa sababu ya ukata ulioko PSPF.

Je, Serikali imeshalipa madeni inayodaiwa kwenyemifuko hii ya hifadhi ya Jamii?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kukuhakikishiawewe pamoja na Wabunge wote kwamba Serikali amaHazina inapopata nyaraka zote halali kwa wakati, basi withinseven days tunalipa mafao hayo. Sikatai that is the policythat we have, sikatai kuna mtatizo baadhi ya communicationflow baina ya wale wanaofanya hiyo kazi na walewanaokwenda kudai mafao yao, sikatai hiyo ipo kwa sababuwale wote ni binadamu lakini ni policy yetu kulipa within sevendays.

Mheshimiwa Arfi umesema hiyo special case lakinininaomba mimi kama Naibu Waziri nipatie hizo nyarakanizifuatilie na ninakuhakikishia kuwa kama hakuna matatizoyoyote basi huyo ama hao mayatima watalipwa mali yaokama kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haioko hapakumdhulumu mtu yoyote. Lakini suala la pili kuhusiana namifuko ninadhani hiyo ni ripoti ya CAG imetokana na ripotiya CAG definitely tutakuja kujibu, tutatoa maelezo kutokanana majibu ambayo sisi kama Serikali tutalipa ku- respond hiyoripiti ya CAG. Suala la mwanzo ninamwomba MheshimiwaArfi nipatie hizo document na tutakwenda kuzifuatilia, tatizohasa liko wapi ahsante sana.

Page 10: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

10

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa kuwa wapo walimu wastaafu wa Singida Mjini ambaowalifanya kazi kwa Mkataba kwa miaka miwili na ambaonimepiga kelele sana hapa Bungeni, sasa hivi wamelipwawalimu saba kati ya nane amebakia Mwalimu ManaseMboga.

Je, huyu mwalimu Manase Mboga atalipwa lini stahilizake maana hata afya yake imedhoofu asije akafa kamawengine walivyokufa bila kupata mafao yao?

MHE. SAADA MKUYA SALUM (NAIBU WAZIRI WA FEDHA):Mheshimiwa Naibu Spika, inawezekana kuwa labda kulikuwana matatizo ya taarifa kutokana na huyu mawalimu lakinininaomba nipatiwe hizo nyaraka again twende tukafuatilieni kwa nini hasa mwalimu huyu naye hajalipwa akamaambavyo wenzie walivyolipwa. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Ninashukuru sana, sasa tuhame hapakatika Wizara ya Fedha na mimi niwaambie tu Wizara yaFedha kuwa kila Mbunge wa Jimbo hapa ana orodha yawastaafu ambao hawajalipwa miaka. Kwa hiyo, ni jambola kulitazama kipeke yake kabisa. Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge waKibaha Mjini.

Na. 97

Gereza la Mkuza – Kibaha Mjini Kuboreshwa

MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Gereza la Mkuza lililopo Kibaha Mjini lilijengwa mwaka1995/1996 likiwa na uwezo wa kuchukua mahabusu 45 tu lakinisasa hivi linachukua mahabusu 150 likiwa na uhaba wanyumba za askari na pia hospitali iliyopo inahudumiawafanyakazi na wananchi na hivyo haitoshelezi mahitaji.

Page 11: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

11

(a) Je, Serikali haioni kuna haja ya kulifanya Gerezakuwa la Mkoa na kupewa vifaa vya kutosha?

(b) Je, ni Serikali itajenga majengo na ofisi muhimuzinazokosekana katika Gereza hilo?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mmabo ya Ndani ya Nchi ninapenda kujibu swalila Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge wa KibahaMjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a)Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote ninaombanimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kuwa katika Muundo wamagereza nchini hakuna daraja la Gereza la Mkoa.Magereza yamegawanyika katika makundi manne ambayoni Magereza ya kati (Central Prisons), Magereza makubwaya wazi (Open Farm Prisons), Magereza ya Wilaya (DistrictPrisons) na Kambi ya Magereza (Prisons Camps. Kwakuzingatia maelezo hayo ni wazi kuwa Gereza la Mkuzahaliwezi kufanywa Gereza la Mkoa.

(b)Mheshimiwa Naibu Spika, Gereza la Mkuza linakosamajengo ya msingi kama vile jengo la utawala wa Zahanatiya nje ambayo ujenzi haujakamilika. Hata hivyoSerikaliitaendelea na mpango wake wa kujenga majengo yamagereza katika Magereza yote nchini kote likiwamo Gerezala Mkuza na kutoa vifaa kadiri hali ya fedha itakavyoruhusu.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwakuwa Gereza hili linahifadhi Mahabusu na Wafungwa zaidiya mara mbili ya uwezo wake ambapo lilijengwa na kwakuwa sasa Mahabusu hawa ambao ni wananchi ambaobado hawajapatikana na hatia wanakaa katika hali ngumuna hususani wakati wa jua na mvua kama hivi sasa. Kwa kuwaGereza hili limezungushiwa miti na senyenge mithili ya bomala mbuzi au ng’ombe

Page 12: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

12

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikishaMahabusu hawa na Wafungwa hawa kwa jitihada za harakawanapata mahali salama pa kukaa ili utaratibu mzima nastahili zao zote ziweze kupatikana kwa mujibu wa Sheria?

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, pale kwenye Gereza hilikuna Zahanati ambayo kimsingi inawahudumia Wafungwa,Watumishi pamoja na Wananchi, lakini majengo ya Zahanatihii ni duni kupita kiasi na hata vifaa ni duni sana.

Je, Serikali sasa kwa utaratibu huo huo Gerezalimekwishafanya utaratibu wa kujitolea na kuanza kuandaaujenzi wa Zahanati mpya?

Je, Serikali sasa ina mpango gani wa harakakuhakikisha Zahanati hii inaboreshwa ili Wafungwa hawapamoja na wananchi wa jirani waweze kupata hudumakutoka Zahanati hiyo?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kuhusu uhifadhi waMahabusu hivi karibuni mwaka jana na mwaka huu Wizarakwa niaba ya Serikali imejenga mabweni mawili pale na kilabweni lina uwezo wa kuchukua Mahabusu 50. Mabwenihaya kilichobakia ni kazi ndogo ya kupiga plasta na kuwekameshi kwa ajili ya kuongeza usalama au uhakika wakutokutoroka kwa watu hawa. Ni lengo la Serikali na Wizarakuhakikisha kuwa kazi hii ambayo iko hatua kubwa sanainakamilika ili hawa Mahabusu wapate hifadhi stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Zahanati kwanzaninaomba niwapongeze wananchi na Mkuu wa Gereza hilikwa kujitolea siyo tu kwa ujenzi wa Zahanati lakini pia kunanyumba tunaita za ubunifu pale nyumba nne wamejitolea,na ni wajibu wetu sasa Serikali kuhakikisha kuwa tunaungananao mkono ili kuikamilisha zahanati hii haraka iwezekanavyo.Pamoja na kusema hivyo ni lazima tukiri kuwa Bajeti ni ndogona Magereza yenye matatizo ni mengi nchini lakinitutaliangalia Gereza la Mkuza kama hali ya hewaitakavyoruhusu. (Makofi)

Page 13: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

13

Na. 98

Uzalishaji wa Gesi Nchini

MHE. RITA E. KABATI aliuliza:-

Nchi yetu imeanza kuzalisha gesi kwa wingi:-

(a) Je, gesi hiyo inazalishwa kiasi gani?

(b) Je, ni kiasi gani cha gesi kinafika Ubungo kwenyemitambo kutoka huko inakozalishwa?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGEB.SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Ritta Enespher Kabati lenye sehemu (a) na (b)kama ifuatavyo:-

(a)Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya futi za ujazozipatazo milioni 105 zinazalishwa Mnazi Bay na Songosongokwa siku, ambapo futi za ujazo milioni 103 zinazalishwa KisiwaniSongo Songo na futi za ujazo milioni 2 zinazalishwa MnaziBay Mtwara.

(b)Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani futi za ujazomilioni 100 hadi 203 za gesi zinafika Ubungo kwenye kituo chakupokelea gesi (receiving station) kila siku kwa ajili yamatumizi ya kuzalisha umeme, matumizi ya viwandani,hotelini, majumbani na magari. Kati ya hizo kiasi cha futi zaujazo milioni 90 zinatumika kuzalisha umeme katika mitambona kufua umeme wa SONGAS na TANESCO iliyopo Ubungona Tegeta. Kiasi cha futi za ujazo milioni 10 hadi 13 ni kwa ajiliya matumizi mengine yaliyotajwa hapo juu.

MHE. RITA E. KABATI): Mheshimiwa Naibu Spika,ninakumbuka Kamati ya Nishati na Madini iliunda Kamatindogo kwa ajili ya kuchunguza mapunjo ya mauzo ya gesiya dola milioni 21 kutoka katika kampuni ya Pan African.

Page 14: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

14

Je, malipo hayo yalishalipwa na Serikali?

(c) Serikali imejipanga vipi kuwaelimishawananchi ili kusitokee tatizo kama lililotokea Mtwara katikamaeneo mengine ambako kumegundulika dalili ya madiniya gesi au madini mengine?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGEB.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwaKamati ilipoundwa ya Nishati na Madini ile ndogo iliwezakugundua kuwa kulikuwa na mapunjo na hivyo kuagizaSerikali iweze kuzirejesha hizi fedha. Lakini pia ni kweli kuwaPan Africa wanaidai TANESCO pesa nyingi pengine kulikohata ambazo tunawadai na katika hali hiyo tunachokifanyapale ni kama tunalipana maana tunadaiana na ile nibiashara endelevu na hivyo tunakatana humo kwa humolakini itafika wakati ambapo na sisi tutakapokuwa hatudaiwibasi deni lile litakuwa limekwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hawa ni wadauambao tunafanya nao biashara na wao wamewekauwekezaji ni lazima tuheshimu uwekezaji huku tukiamini kuwatunapaswa kulinda rasilimali za Taifa ili tusiweze kupunjwa.

Suala la elimu kwa rasilimali kama ilivyotokea kuleMtwara ni kweli kuwa Mtwara kumetokea hali ambayoilipelekea kuhitajika sana kuelimishwa kwa wananchi naniseme tu kuwa mwalimu wa kwanza katika jambo hiliamekuwa ni Mheshimiwa Rais ambaye ameweza kutoa elimukatika hotuba zake, lakini pia Makamu wa Rais amesemajambo hili, Waziri Mkuu amesema jambo hili, Waziri wanguProfessor Muhongo amesema jambo hili na mimi nimesemalakini pia viongozi mbalimbali wamelisemea jambo hili.(Makofi)

Nichukue nafasi hii kuwaomba sana wote ambaotunajua umuhimu wa ku share rasilimali za Taifa letutushirikiane katika kutoa elimu pale tunapoona kuna haja yakufanya hivyo na siyo kutumia mwanya huo pengine kwafaida binafsi na faida ya muda mfupi na hasa kwa sisi

Page 15: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

15

wanasiasa. Ninasema hivi kwa sababu kwa kiasi kikubwasasa kule Mtwara hali imetulia wananchi wameelewa basiiweb ni jukumu la wananchi wote wale tunaoelewa na hasawanasiasa kutoa elimu na siyo kusema hatujatoa elimu, sotetutoe elimu kwasababu ni jukumu letu kama viongozi.

MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwakuwa nchi yetu imepata bahati ya kupata gesi nyingi namnahiyo ambayo inaweza kutusaidia kwa uchumi wa nchi yetukama kujenga viwanda, umeme na mambo mengine mengi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutokuiuza kabisa hiigesi ili iweke reserve kama nchi za wenzetu kwa miakamingi ijayo ili tuweze kuitumia na tuuze bidhaa tutakazozipatakwa ajili ya kutumia gesi hiyo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGEB.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba yaWaziri wa Nishati na madini ninapenda kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Rita Mlaki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wake ni mzuri naunawezekana tu pale kama una resource hiyo kwa kiasikidogo lakini kiasi tulichonacho tulichogundua natunachotarajiwa kuwa nacho baada ya kujengamiundombinu ni kiasi kikubwa ambacho kw hakika tunawezakutumia kwa haya yote anayoyasema ya kuzalisha umeme,viwanda na kila kitu nab ado tukauza nje. Lakini tukubalianekuwa tunapoingia katika uzalishaji, utafiti na utafutaji warasilimali hii ziko gharama kubwa za mitaji kutoka nje ambazotunashirikiana kama wadau muhimu wa kawaida katikauchumi wa kileo wa Dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katikamakubaliano hayo kuuza nje pia ni eneo muhimu sana kwasababu na wao wanahitaji kurejesha rasilimali ile kwa uchumiwetu na kwa kiasi cha uchumi wetu hatuwezi kuwarejesheafedha ile kwa muda huo ambao tumekubaliana, nirudiekusema kuwa rasilimali hii ni nyingi na inaweza kufanya hayayote lakini pia tukaweza kuuza nje.

Page 16: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

16

Na. 99

Mradi wa Kuvuta Umeme Kutoka Manyoni Kwenda Nkonko

MHE.CAPT. JOHN Z. CHILIGATI aliuliza:-

Licha ya kazi nzuri inayofanywa na Shirika lakusambaza Umeme Vijijini (REA)bado kuna tataizo lakupeleka Umeme Vijijini katika Wilaya ya Manyoni hasa katikaTarafa ya Nkonko ambako hakuna hata kijiji kimoja chenyeumeme:-

Je, ni lini REA itaanzisha mradi wa kuvuta umemekutoka Manyoni Mjini kwenda Nkonko hadi kijiji cha Sanza?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGEB. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Nishati na Madini ninapenda kujibu swali laMheshimiwa Capt. John Zefania Chiligati, Kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa kuvuta umemekutoka Manyoni Mjini kwenda Nkonko hadi Kijiji cha Sanzapamoja na vijiji vya Chikola,Chidamsulu, Heka,Mwitikiala,Sasilo, Chikombo, Mpola, Ntumbi, Iseke, Igwamadete naNtope umejumuishwa katika Mpango kabambe wakiusambaza umeme vijijini Awamu ya pili chini ya uwezeshajiwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Zabuni ya kuwapatawakandarasi wa kazi hizi ilitangazwa mwezi Desemba, 2012na kufunguliwa mwezi Machi, 2013 na wakati wowoteatateuliwa Mkandarasi wa kujenga mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi za mradi huuzitajumuisha: (i) Ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kv33 yenye urefu wa Km 156,(ii) Ujenzi wa njia ya umeme yamsongo wa Volti 400 yenye urefu wa Km 26,(iii) Ufungaji watransfoma tano(5) za KvA 25; sita (6) za kVA 50 na moja (1) yakVA100,na (iv)Kuunganisha wateja wa awali wapatao 650.

Page 17: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

17

Gharama za kazi hizi ni shil ingi bil ioni 6.1 nazinatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha2013/2014.

MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwamajibu mazuri na yanayotia moyo wananchi wa Tarafa yaNkonko lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwanza, katika orodha ya vijiji vitakavyonufaika namradi huu Kijiji cha Itetema hakimo na nguzo zinapita hapohapo katika Kijiji hicho lakini vilevile umeme ukishafika paleSanza ambako ndiko Makao Makuu ya Kata na Vijiji viwilivya Kata hiyo Kijiji cha Kiteho na Ikasi viko kilomita kama nanekutoka Makao Makuu ya Kata navyo havimo.

Je, Waziri anasemaje kuhusu Vijiji hivi?

Hivi sasa REA wanamalizia mradi wa kusambazaumeme kutoka Manyoni Mjini mpaka Kijiji cha Kintingu Vijijivingi katika mradi huo umeme umekwisha waka lakini nguzokatika vijiji hivyohivyo hazijasambazwa kulingana na Mkatabajinsi ulivyo, na wananchi ambapo nguzo hazijafikawameshalipia REA wanasema wameishiwa na fedha.

Kwa hiyo, wametukatisha tamaa ninaomba Waziri auWizara inasemaje kuhusu vile vijiji ambavyo nguzo hazijafikana wananchi wameshalipa lakini umeme hawajapatiwa?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katikaorodha niliyoitaja na pengine katika orodha zingine zozotezile za miradi iliyoko katika Majimbo ya WaheshimiwaWabunge, inawezekana tukataja kijiji cha mbele hapa vyakatikati tusivitaje. Ninataka kuwahakikishia kuwa hilo siyotatizo hata kidogo kwa sababu kama tulivyosema formulayetu kuu ni kwamba umeme hauruki kijiji sasa. Lakini paleambapo umeme umepita juu tunakuja na mradi kwa ajili yakushusha ambao utakuwa unahusisha transforma naelectrification kidogo.

Page 18: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

18

Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwakama kijiji hiki cha Itetema kiko katikati formula yetu inasemahaturuki.

Hili suala la maana ni kama masuala matatu kunasuala la Sanza ambalo anasema ni kilomita nane kutokamradi unapoishia, inapotokea kuwa ni kilomita nane napakawa kiuchumi tunapaona panafaa na kwamba mradiule umeishia nyuma kidogo hapa kuna ni tatizo. Kwa sababuni ama unasema unaongeza kazi ya ziada ama inakuwavinginevyo vyo vyote vile.

Lakini miradi hii tumejaribu kuweka provision katikamikataba yetu na wakandarasi kwamba tutahakikisha kuwatuna renegotiate kila mara kulingana na hali ya mazingirainavyokwenda. Kwa hiyo, katika Sheria yetu ya manunuzipia kuna allowance ya 15% ya extension. Kwa hiyo, wecan play within tukaona tunaweza tukafanya nini lakini hiisiyo fomula kuu, formula inasema ni ile inasema kijiji kiwekatikati.

Lakini la pili ni lile la mradi wa Manyoni - Kitinkuambapo umeme umewaka lakini bado maeneo menginehayajafikiwa, tutawasiliana na Mbunge tuone namna boraya kufanya jambo hilo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto usubiri kidogotumalizane na Manyoni, Mheshimiwa Lwanji swali fupi sanana Mheshimiwa Zitto utafuata.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Naibu Spikaahsante sana. Ili kutoa umeme kutoka Manyoni Mjini kwendaChikola au Nkonko kuna vijiji njiani, kijiji cha Kashangu, Kijijicha Idondyandole na Kijiji cha Jeje ambavyo havikutajwakatika orodha ya hivyo vijiji ambavyo umeme unapita. Je,Serikali inasemaje kuhusu hili?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, kamanilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba kama vijiji

Page 19: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

19

hivyo vipo katikati na kinachotajwa kupelekewa umeme kipomwisho na umeme utatokea Manyoni, ni dhahiri kwambaformula tuliyoiweka ni kwamba haturuki nitafanya kazi, kwahivyo nimwondoe wasiwasi Mbunge kwamba kijiji chaKashangu, Idodyandole na Jeje vitakuwa katikati kwa hivyohavitarukwa na vyenyewe vitapewa umeme.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, tokamwaka 2011 Serikali imekuwa ikipanga bajeti kwa ajili yamradi wa umeme vijijini, vijiji 16 katika Jimbo la KigomaKaskazini lakini mpaka sasa miradi hiyo bado haijafanyika.

Lakini hali ni hiyo hiyo kwa Majimbo mengi sana yauchaguzi. Hali halisi ya miradi ya umeme Vijijini (REA) ikojempaka hivi sasa, ili tuweze kupata uhakika ni namna ganitunaweza kwenda kuwaambia wananchi, kwa sababu kilawakati tunaenda kuwaambia wananchi kuhusu miradi nahaitekelezwi, hali ikoje kihalisia kwa miradi yote ya REA hapanchini.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tangumwaka 2011 tumekuwa na miradi ya REA na hapa tulikuwana REA Phase I na tumetekeleza katika baadhi ya maeneo,lakini kwa sasa tumekuja na mpango mkubwa ambaotumeukuza kutokana na Bajeti yetu ya mwaka jana tulipitishavijiji vile. Niseme tu tuna vijiji vya Mheshimiwa MbungeKaskazini vipo na tuna orodha kubwa sana ya vijiji vingi zaidiya 1200 kwa nchi nzima. Vijiji hivi dhamira ya Serikali ya Chamacha Mapinduzi ni kuhakikisha kwamba inapeleka umemekatika vijiji vyote hivi vikiwemo vijiji 16 vya MheshimiwaMbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningemwomba Mbungesiyo tu nikuletee pia na wewe uje tuweze ku-share kwasababu tumefikia hatua ya mbele sana ambayo bado ziledocuments bado zipo kwenye process ya procurement. Kwahiyo, nikuhakikishie kwamba tukionana utaweza kuviona nanitakuonesha usiwe na mashaka. (Makofi)

Page 20: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

20

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge natambuamna maswali mengi sana kwenye eneo hili la umeme, lakinituendelee na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Na. 100

Uwiano wa Mitaala ya Tanzania Zanzibarna Tanzania Bara

MHE. YAHYA KASSIM ISSA aliuliza:-

Wanafunzi wa Tanzania Zanzibar hufanya mtihani waKidato cha Nne ulio sawa na ule wa Tanzania Bara lichatofauti ya baadhi ya sehemu ya mitaala iliyopo baina yasehemu hizo mbili za Muungano:-

(a) Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu uwiano naushirikiano wa mitaala hiyo?

(b) Je, Serikali haioni kuwa ndiyo utofauti wamitaala hiyo unawaathiri sana wanafunzi wa TanzaniaZanzibar na kuwa ndiyo sababu ya kufeli katika mitihani yao?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu na Mafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Yahya Kassim Issa, Mbunge wa Chwaka, lenyesehemu a na b kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa, hakuna tofauti ya mtaala wa elimu ya sekondarikati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, kwa msingi huu,kwa kuwa, mtaala ni mmoja wanafunzi wa elimu ya sekondariwa pande hizi mbili za Muungano hufanya mtihani wa kidatocha Nne ulio sawa.

Page 21: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

21

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la ushirikianoBaraza la Mitihani Tanzania limekuwa likiwahusisha walimuwa sekondari wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muunganokatika masuala ya kutunga mitihani, kufanya moderation,kusahihisha mitihani na kuwianisha alama za ufaulu(standardization).

Aidha, Baraza la Mitihani limekuwa likishirikiana naTaasisi ya elimu Tanzania Bara pamoja na taasisi ya elimuTanzania Zanzibar katika shughuli zote za uandaaji nauboreshaji wa mitaala kama vile kushiriki katika kuboreshamihtasari ya masomo (syllabus) na mikutano mbalimbali yapaneli za masomo mbalimbali ya sekondari.

MHE. YAHYA KASSIM ISSA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa kuwa, taarifa iliyopo ya uhakika ni kwamba baada yawalimu wa Zanzibar kusahihisha mitihani na kumaliza hurejeanyumbani, na sehemu iliyosalia hadi matokeo hushirikishwasehemu moja ya Muungano ikiwa kama wapo watu pale nikama ajira. Je, hili utathibitishia vipi wananchi wa Zanzibarkuhusu taarifa hii.

Kama hili ulilolieleza ni kweli Je, ni kwa kiwango ganiushirikishi wa watu wa Zanzibar?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, si kweli kwamba baada yakusahihisha mitihani walimu wa Zanzibar wanaondoka wotekurudi majumbani na baadaye upande mmoja ndiyowanashiriki katika kumalizia kazi ile. Kwa sababu hata katikaBodi ya Baraza la Mitihani ambapo Kamishana wa Zanzibarni Mjumbe, Mkurugenzi wa Mitihani Zanzibar ni Mjumbe,Mkurugenzi wa Mitaala na mwakilishi kutoka huo Kikuu ChaSerikali ya Zanzibar vile vile ni mjumbe. Hawa wote huwawanakuwepo kuanzia mwanzo wa kazi mpaka mwisho wakazi. Ndiyo maana tunasema Baraza la Mitihani lina Bodi nahao ndiyo huwa wanatangaza hata matokeo. Kwa hiyoushirikishwaji ni kwa pande zote mbili kwa pamoja.

Page 22: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

22

NAIBU SPIKA: Swali hili linaendelea kututhibitishiakwamba mitaala ipo, Mheshimiwa Ndugulile swali la mwishola nyongeza.

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa NaibuSpika nashukuru kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa, mitaala huanzia katika sera ya elimu nakwa muda mrefu Wizara ya Elimu imekuwa inalifanyia kazisuala la sera ya elimu.

Je, ni lini sera hii ya elimu itawekwa hadharani nakuanza kutumika nchini?

Swali la Pili;..

NAIBU SPIKA: Ni swali moja tu Mheshimiwa. Waziri waElimu kwa kifupi sana.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa sababu suala la elimuni suala muhimu sana na ni la uhai wa Taifa, Serikaliimechukua muda mrefu kulifanyia kazi kwa umakini sana.Imeshaletwa Bungeni mara mbili na hivi sasa Bunge lakolimepanga kufanya mapitio ya Sera hiyo mpya tarehe 19 Mei,2013 ndiyo tarehe ambayo tumepewa.

Kwa hiyo tutakuja tena mara ya tatu katika Bungehili Tukufu, kwa njia ya semina ili baada ya hapo ipelekwekwenye Baraza la Mwaziri iweze kuwa Sera rasmi na tutaanzakuandaa mitaala mipya badala ya ile ya 2005.

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Lakini kabla sijauliza swali langu hilisisi wengine ni waumini wa utulivu naomba Serikali yetu iwemakini na mambo yanayoendelea huko Liwale ili isije ikawachachu ya kutuletea vurugu kama iliyotokea Mtwara.(Makofi)

Page 23: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

23

Na. 101

Nafasi za Masomo Nje ya Nchi kwa Vijana

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA aliuliza:-

Kwa miaka mingi vijana wa Tanzania wamekuwawakipata nafasi za masomo nje ya nchi:-

(a) Je, ni vijana wangapi wamepata nafasi zamasomo nje ya nchi kuanzia mwaka 2010-2012?

(b) Je, ni vijana wangapi kutoka TanzaniaZanzibar wamepata elimu hiyo kwa kipindi hicho?

(c) Je, ni nchi ngani vijana hao walienda kusoma?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu na Mafunzo ya Ufundi naomba kujibu swali laMhehsimiwa Khalifa Suleiman Kahalifa Mbunge wa Gando,lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya mwaka 2010hadi mwaka 2012 vijana wa Kitanzania waliopata nafasi yamasomo nje ya nchi ni 342.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, scholarshipzinazotolewa na nchi rafiki zinashindaniwa kwa kutumiavigezo vya kitaaluma, umri na uraia wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Kwa vile kinachozingatiwa zaidi ni kigezo chakitaaluma, mwombaji yeyote anayetimiza kigezo hichoanayo haki ya kunufaika na scholarship bila kujali anatokeasehemu gani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 24: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

24

Aidha, kutokana na mwingiliano wa wananchi wapande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakuwavigumu kutofautisha sehemu ya Jamhuri alipotokeamwombaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusisitiza kuwa,nafasi za masomo zinazotolewa kwa ajili ya wananchi waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wotewanashindanishwa kwa vigezo vya kitaaluma na sivinginevyo.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi chamwaka 2010 hadi mwaka 2012, nchi ambazo zimekuwazikitupatia nafasi za masomo nje ya nchi ni Cuba, Algeria,Urusi, Msumbiji, Serbia, Uingereza, Misri, Korea Kusini,Macedonia, Uturuki, China, Ujerumani na Oman. (Makofi)

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru na nimeyasikia vizuri majibu ya NaibuWaziri.

Kwa kadiri ya ufahamu wangu component hii ya elimuya juu ni issue ya Muungano na ni utamaduni wetu tokeatumeanzisha Muungano katika masuala mazito kama hayaZanzibar huwa inatengewa asilimia fulani katika masuala yascholarship na hili si jambo geni. Sasa nashtuka ninaposikiahii au kwa sababu upande wa pili watu wamesoma sana?

Kwanza; nataka kujua ni sababu ipi iliyopelekea ulempango wa zamani wa kuweka asilimi fulani kutoka Zanzibarukaondoshwa?

Kwa sababu hali hii inaweza ikapelekea watu waupande mmoja tu wakapata nafasi zote hizo wakaenda. Jeikitokea hali kama hii kama mwanafunzi hata mmojahakupata fursa kama hii, upande wa pili wa Jamhuri yaMuungano inawapa raha jambo kama hili? Kama haliwapiraha.

Je, ni lini watarekebisha basi hali hii?

Page 25: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

25

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, moja kuhusu kutengewa nafasi kwaajili ya wananchi wa Tanzania Zanzibar. Hatujawa nautaratibu huo wa tengeo kwa nafasi za scholarship kwa vijanawa Tanzania Zanzibar na wale wa Bara, tuna tengeo katikamaeneo mengine kwa mfano ajira katika sekta zile zakimuungano lakini kwenye elimu hasa scholarship hatujawahikufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye scholarship kunaKamati maalum ambayo kila zinapokuja scholarship Kamatihii ambayo inajumuisha Maafisa wa Bara na Maafisa waZanzibar kuweza kukaa pamoja na kuamua nani aende.Lakini pia nafasi hizo wakati mwingine hatuzipati zote.

Kwa mfano Commonwealth imetoa nafasi 12 mwakajuzi wamekwenda sita tu kwa sababu inaenda kwa vigezo.Mnapowapeleka wale watu mnasema hawa ndiyo watuwetu tunataka wapewe scholarship kama hawatimizi vigezovile vya kimataifa wanaweza wasiwachukue wote.

Kwa hivyo siyo suala la tengeo ni suala la qualification.Kwamba kama ana-qualify anaenda, ni kitu ambachokinatuuma lakini hatuna uwezo nacho kwa sababu hili nijambo ambalo linatoka kwa wahisani na wana vigezo vyaovya kuchukua wanafunzi ambao wanawachukua hatunajambo jingine. Lile ambalo litakuwa la mkururo tutakuwatunahakikisha kwamba Kamati hii ambayo inahusu Zanzibarpamoja na Tanzania Bara ndiyo inafanya maamuzi siyoTanzania Bara peke yake inafanya maamuzi ya scholarshiphiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kama wanafunzi waZanzibar wote watakosa nafasi ya scholarshipinawapendezesha hili upande wa Bara, nasema hapana. Sisihatufurahi kama vile ambavyo Watanzania wote hawaweziwakafurahi kama itatokea katika scholarship wanafunzi waZanzibar hawakupata nafasi.

Page 26: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

26

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, kwa sababu ya mudaWaheshimiwa Wabunge mtaona muda wetu ni mdogo nanina maswali matatu, naomba tuhamie Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika, swali la Mheshimiwa Godfrey WestonZambi.

Na. 102

Vyama vya Ushirika Mbeya

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE (K.n.y. MHE.GODFREY W. ZAMBI) aliuliza:-

Vyama vya Ushirika vya MBOCU, KYERUCU na MICUvilivyoko katika Mkoa wa Mbeya vimekufa na vinginehavifanyi kazi sawa sawa:-

(a) Je, Vyama hivyo vilikuwa na madeni kiasi ganiambayo vililipiwa na Serikali?

(b) Je, mali za Vyama hivyo kama maghala, samani nakadhalika, zinamilikiwa na nani?

NAIBU WAZIRI, KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niba ya Waziri waKilimo, Chakula na Ushirika kabla ya kujibu swali laMheshimiwa Godfrey Weston Zambi, Mbunge wa MboziMashariki, lenye sehemu (a) na (b) napenda kutoa maelezoyafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Vyama vya Ushirika vyaMBOCU, KYERUCU na MICU vilivyoko katika Mkoa wa Mbeyahavijafa, vinafanya kazi japokuwa baadhi ni dhaifu kutokanana kujigawa kiwilaya na hivyo kupunguza nguvu za umojawao. Chama cha Ushirika cha KYERUCU kilijigawa nakuanzishwa vyama viwili vya KYECU Wilaya ya Kyela na RUCUWilaya ya Rungwe.

Page 27: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

27

Mkoa wa Mbeya kwa sasa una Vyama Vikuu vyaUshirika sita ambavyo ni Mbeya Ileje Cooperative Union(MICU) cha Wilaya za Mbeya na Ileje, Isanza IyulaCooperative Union (ISAYULA) na Mbozi Cooperative Union(MBOCU) vya Wilaya ya Mbozi, Rungwe Cooperative Union(RUCU) cha Wilaya ya Rungwe, Kyela Cooperative Union(KYECU) cha Wilaya ya Kyela na Chunya, Tobacco GrowersCooperative Union (CHUTCU) cha Wilaya ya Chunya. Vyamavya MICU, MBOCU, ISAYULA, RUCU na KYECU ni miongonimwa Vyama vya ushirika 38 vilivyohakikiwa na Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Serikali na kuonekana vilikuwa na madeniya msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya,sasa naomba kujibu swali kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Vyama vya MICU, MBOCU,ISAYULA, RUCU na KYECU vilikuwa na madeni ya shilingi886,048,314 yaliyohakikiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu waSerikali CAG na kati ya madeni hayo yaliyolipwa mpaka sasani shilingi 714,005,044 na madeni ya shilingi 172,043,270hayajalipwa. Ulipaji wa madeni yaliyobaki utafanyikakulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha. Mchanganuowa madeni hayo ni kama ifuatavyo.

MICU deni lake lilikuwa 349,417,595 limelipwa lote,MBOCU deni lake lilikuwa milioni 50.6 kiasi kilicholipwa ni milioni8.9 kimebaki shilingi 41,660,039, ISAYULA deni lilikuwa shilingimilioni 36 zimelipwa milioni 32. RUCU deni milioni 245 zimelipwamilioni 178 imebaki milioni 67 na KYECU deni ni milioni 204imelipwa milioni 144 limebaki milioni 59.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vyama hivyobado vinafanya kazi na mali za vyama hivyo badozinamilikiwa na wanaushirika wenyewe. (Makofi)

Page 28: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

28

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaNaibu Spika ahsante sana. Kwa kuwa Vyama au Ushirikaimara ndiyo njia pekee ya kuweza kumkomboa mwananchikutokana na kunyonywa, na kwa kuwa Ilani ya Chama chaMapinduzi ya Uchaguzi inasisitiza kuimarisha vyama vyaushirika.

Je, Serikali ina makakati gani wa dhati kuhakikishakwamba vyama hivi vya ushirika vinaimarishwa kwa manufaaya wanaushirika wenyewe na wananchi kwa ujumla?

Pamoja na kwamba Naibu Waziri amejibu swali hilikwamba vyama vinafanyakazi lakini ukweli havifanyi kazi.

Je, ni vipi vyama hivi vitafufuliwa ili viweze kufanyakazi yake vizuri?

NAIBU SPIKA: Majibu mafupi sana Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba ushirika ni nguzomuhimu sana ya ukombozi wa mkulima pale unapofanyakazivizuri. Nguzo kuu ya ushirika ni uzalishaji ndiyo pale vyamahivi vinapopata nguvu kadiri vinavyozalisha kwa wingi navyenyewe vinakuwa na nguvu zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo jambo la kwanzaambalo tutafanya ni kuhakikisha kwamba kwa yale mazaoambayo ushirika ule umejikita Serikali itatoa msukumo zaidi ilivyama vile viwe na uzalishaji mkubwa zaidi.

Lakini kwa upande wa pili kama tulivyosema janawakati wa kuhitimisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika ni lazima sheria mpya inayokuja ya Ushirika iwe namifumo mikali zaidi ya usimamizi na adhabu kali ili kuondoamatatizo ya wizi na ubadhilifu ndani ya vyama vya ushirika.(Makofi)

Page 29: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

29

MHE. ZAINAB R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Napenda kwanza, kutoamasikitiko yangu juu ya tukio lililotokea usiku wa jana katikaWilaya ya Liwale, Wakulima wa korosho wameghadhabikasana. Kulikuwa kuna mapambano makali kati yao na Askarina hatimaye wameweza kuchoma baadhi ya nyumba zaViongozi, moto.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sababu hii inatokanana ukweli kwamba, waliahidiwa wangelipwa mauzo yakorosho kiasi cha 1,200/=.

Awamu ya kwanza wakalipwa 600/=, lakini awamuya pili wamelipwa kiasi cha 200/=, kwa maana hiyo jumlawamelipwa kiasi cha 800/=. Sasa wakulima hawa wanadaiile tofauti ya kiasi cha 400/=.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimezungumza naMheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, amenieleza kwamba,bei ya korosho imekuwa ikienda ikibadilika. Sasa ninaombaSerikali, inipatie majibu ni namna gani inaweza ikafidia hikikiasi cha 400/=, ili mkulima aweze kulipwa kile kiasi chakecha 1,200/=? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, naomba nijibu swali la MheshimiwaZainab Kawawa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tukio la Liwale jana nitukio la kusikitisha sana. Kwa sababu, kusema kweli, hii tabiaya wananchi kuchukua Sheria mkononi na kwenda kuchomanyumba za viongozi ni lazima tukubaliane kuna vituvimejificha humo ambavyo sio tatizo la zao la korosho. Kwasababu, Serikali, imeshatoa tamko kwamba, tunakwendatukibaini matatizo ya korosho yaliyotokea kwa misimu miwili.(Makofi)

Page 30: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

30

Mheshimiwa Naibu Spika, na ni lazima nikwambie,kote ambako tunalima korosho pamoja na Jimbo langu laMkuranga, matatizo yaliyosababisha korosho kutokuuzwayanatofautiana. Kuna kwingine kuna matatizo ya Vyama vyaUshirika, kwingine kuna matatizo ya wanunuzi.

Kwa hiyo, tumesema kwamba, Serikali, tutakwendakote ambako kuna zao la korosho na kuna matatizo, tutapitia,tutakutana na wananchi na tutajua tatizo ni nini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo menginetatizo limetokana na huko huko kwenye vyama vya ushirika.Sasa inawezekana hao hao Viongozi wa Vyama vya Ushirikandio wanahimiza watu kuchoma nyumba, ili kufunikamadhambi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nasema kwa kuwa,sitaki kuweka dhana hiyo ya tatizo ni nini, nimesema Serikali,itakwenda huko kubaini tatizo ni nini na italipatia ufumbuzitatizo hili.

Sasa kwa hawa waliochoma nyumba, basiwataonana na Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi, maana sasahili ni tatizo lingine sio tatizo la Wizara ya Kilimo. (Makofi)

Na. 103

Tatizo la Ukame na Fursa za Umwagiliaji KatikaWilaya ya Bahi

MHE. MWIGULU L. M. MADELU (K.n.y. MHE. OMARY A.BADWELL) aliuliza:-

Wilaya ya Bahi, yenye ukame mkubwa imekuwaikilazimika kuomba chakula Serikali Kuu kila mwaka, ili kukidhimahitaji ya wananchi. Zipo fursa nyingi zitakazowezeshakilimo cha umwagiliaji katika Wilaya hiyo na kutoa tija kwawananchi.

Page 31: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

31

Je, Serikali iko tayari kufanya utafiti katika Wilaya hiyo,ili kubaini sababu za ukame na pia kuzibaini fursa zilizopokatika sekta ya umwagiliaji ili kuondoa tatizo la njaa katikaWilaya hiyo?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKAalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, Chakula na Ushirika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Omary Ahmad Badwell, Mbunge wa Bahi, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali, inatambua kuwaWilaya ya Bahi, ipo katika ukanda wa maeneo kame,ambapo tabia ya maeneo hayo ni pamoja na kuwa na mvuakubwa za muda mfupi na zenye mtawanyiko usioaminika,unpredictable. Wastani wa mvua katika Wilaya ni milimeta600 kwa mwaka, kiwango ambacho kwa ujumla hakikidhimahitaji ya maji kuzalisha aina nyingi za mazao, isipokuwayale yanayostahimili ukame.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watafiti wengi, kikiwemoChuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kupitia Taasisi yake ya Tathminiya Rasilimali (Institute of Resource Assessment – (IRA),walifanya uchambuzi wa kitaalam kuhusu mwenendo wamvua unavyoathiri kilimo katika maeneo kame, ikiwemo yaMkoa wa Dodoma kwa kipindi kati ya miaka ya 1980 – 1997.Utafiti huo ulibaini kuwa, katika maeneo haya, ukame wasiku 10 hadi 40 mfululizo ndani ya msimu wa mvua ni halitarajiwa. Aidha, mabadiliko ya Tabianchi yamesababishatatizo la ukame na mafuriko kuwa kubwa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya hii ina historia yakukumbwa na uhaba wa chakula karibu kila mwaka na hivyo,kulazimika kuomba msaada wa chakula. Hii ni kutokana nakiwango cha ukame katika Wilaya hii, kama nilivyosema. Halihii inaonesha wazi umuhimu wa kuwa na mikakati yakuwawezesha wakulima kuzalisha katika mazingira haya yaukame.

Page 32: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

32

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali, imeanza kutumiafursa zilizopo ambazo ni pamoja na kuvuna maji ya mvuakwa hizi siku 40 zinazonyesha na ya mafuriko, ili kuimarishauzalishaji wa mazao ya chakula katika Wilaya ya Bahi, kupitiaProgramu ya Kuendeleza Kilimo katika Maeneo Kame(Special Development Programme for Marginal Areas –SDPMA).

Aidha, kupitia Programu ya ASDP, hususan Mfuko waUendelezaji Kilimo cha Umwagiliaji Ngazi ya Wilaya, (DIDF),Serikali, ilitoa jumla ya shilingi bilioni 3.2 ambazo zimetumikakuboresha mifumo ya umwagiliaji ya Skimu za Mtitaa,Chikopelo, Chali, Bahi Sokoni, Bahi Makulu, Mtazamo, Matajirana Kongogo. Uboreshaji huu uliwezesha kuongeza tija ya zaola mpunga kufikia tani 6 kwa hekta katika baadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakushirikiana na wananchi wa Wilaya ya Bahi, kutenga fedhakadiri Bajeti itakavyoruhusu, il i kukamilisha miradi yaumwagiliaji, kujenga miundombinu ya kuvuna maji na yakutumia maji ya ardhini. Hivyo kuimarisha uzalishaji wa chakulakatika Wilaya hiyo. (Makofi)

MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana namshukuru Naibu Waziri kwa majibumazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la mafuriko na kuvunamaji ni zaidi ya kuvuna maji tu kwa ajili ya umwagiliaji, balimaji yale yakitawanyika husababisha mimea pamoja namashamba yote kupelekwa na mafuriko. Maeneo mengineyanayofanana na hili yako mengi tu kama ilivyo kwa Igunga,Kidaru, Ndago na Mtoa.

Je, Serikali, inaweza ikasema sasa kwamba, italiondoasuala hili la mabwawa kutoka Halmashauri ambazo haziwezizikachimba mabwawa na badala yake wakaweka Wizaraniambako kuna fedha, ili kuweza kuvuna maji maeneo hayoambayo yana mafuriko na kuepusha mimea kuharibiwa namafuriko?

Page 33: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

33

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Afande Mwigulu Mchemba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tatizo la kuvuna maji namafuriko, Serikali, inapeleka pesa kwenye Wilaya, kwenyeHalmashauri, kwa ajili ya kuboresha miundombinu yaumwagiliaji kama tulivyosema kupitia DIDF.

Ni utaratibu ambao kupitia mfumo wa kupeleka pesakwenye ngazi ya chini D – by – D, tumeuanza katika ngazinyingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kupeleka pesa,tunapeleka na taaluma. Kwa hiyo, mimi nadhani tatizo hapahaliko zaidi sana kwenye suala la fedha kuwa kwenye CentralGovernment kwa sababu, pesa nyingi iko huko huko chini.Tatizo nakubaliana na Mheshimiwa Mwigulu Mchembakwamba, kwenye maeneo ambayo kuna mafurikotutengeneze miundombinu ya umwagiliaji ambayo,inakabiliana na mafuriko hayo kuweza kufanya waterharvesting kwa mana ya kuvuna maji hayo na kuyahifadhikwa ajili, ya matumizi ya wakulima pale ambapo yatahitajikamsimu wa mvua ukimalizika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimekubali ushauriwake, tutalifanyia kazi.

Na. 104

Usafirishaji wa Mazao ya Samaki(Mwaka 2005 – 2012)

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR (K.n.y. MHE. HAMADRASHID MOHAMED) aliuliza:-

(a) Je, katika kipindi cha mwaka 2005 – 2012,Tanzania imesafirisha tani ngapi za mazao ya samaki kutokaBahari Kuu na Maji Baridi (Maziwa)?

Page 34: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

34

(b) Je, ni meli ngapi za uvuvi wa Bahari Kuu,zilipewa leseni na zilisafirisha tani ngapi za samaki kwathamani ya kiasi gani?

(c) Je, Serikali, imepata mapato kiasi gani na kwakutoza kodi za aina gani?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVIalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Hamad Rashid Mohammed, Mbunge wa Wawi,lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi chamwaka 2005 – 2012, Tanzania imesafirisha jumla ya tani371,317.8 za samaki na mazao ya uvuvi ambapo tani 17,954.5ni kutoka maji chumvi na tani 353,362.7 kutoka maji baridi.

Ziwa Viktoria likiwa limetoa tani 339,893.1, ZiwaTanganyika tani 11,418.8, Ziwa Nyasa tani 110.9 na maeneoya maji madogo tani 1,939.9 pamoja na samaki hai 301,839.Jumla ya fedha iliyopatikana kutokana na ushuru kwa mauzoni 54,495,683,615.73/=. Kati ya hizo 5,528,438,590.96/= kutokamaji chumvi na 48,967,245,025.77/= kutoka maji baridi.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya mwaka2009, wakati Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu (Deep Sea FishingAuthority) kuanzishwa, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar,zilikuwa zinatoa leseni kila mmoja kwa ajili ya uvuvi katikaBahari Kuu.

Kati ya mwaka 2005 – 2009, Tanzania Bara ilitoa jumlaya leseni 274 kwa ajili ya uvuvi katika Bahari Kuu. Baada yakuanzishwa Mamlaka hiyo, kati ya mwaka 2010 – 2012 jumlaya leseni 124 zilitolewa. Hivyo kwa kipindi cha mwaka 2005 –2012 jumla ya meli 398 zilipewa leseni za uvuvi wa Bahari Kuu.(Makofi)

Page 35: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

35

Aidha, meli zote 398 zilizopewa leseni zilivua jumla yatani 40,081.8 za samaki ambazo zilisafirishwa na kuuzwa njeya nchi. Thamani ya samaki waliosafirishwa ni vigumukufahamika, kwani bei ya samaki hutegemea aina ya samaki,uchakataji wake, aina ya uhifadhi wake na nchi walikouzwa;taarifa ambayo hatunazo kama Wizara.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi chamwaka 2005 – 2012 Serikali, imepata jumla ya Dola zaKimarekani 7,780,908 kutokana na ada ya leseni sawa na12,605,070,960/=, kwa rate ya sasa. Ada hizi zilizotozwa kwaviwango vya dola za Marekani 35,000 kwa mwaka kwa PurseSeine na dola 32,000 kwa Longline kwa mwaka.

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Waziri, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa,kuna tofauti kubwa ya mapato baina ya uvuvi wa maji baridina uvuvi wa maji bahari, yaani bilioni 49 na bilioni 5.

Je, Serikali, iko tayari kuboresha sekta ya uvuvi wa majiya bahari? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Je,Serikali, ina mikakati gani ya kuwawezesha wavuviwadogowadogo kwa kuwapatia zana za kisasa, ili wawezekwenda kwa wakati, japokuwa kwa njia ya mkopo nafuu?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleoya Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu maswali mawili yaMheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Page 36: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

36

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana nayeye kwamba, tofauti ya mapato ni kubwa. Ukiona katikaZiwa Viktoria tu lenyewe, zaidi ya 70% ya mapato yoteimetoka Ziwa Viktoria na hii ni kwa sababu, miundombinuiliwezekana kuboreshwa katika eneo hilo na soko la uhakikala Ulaya limekuwepo.

Tutaboresha na tayari mikakati imeanza kuhakikishakwamba, miundombinu hasa ya bandari ya uvuvi pia,itajengwa katika eneo la Bahari Kuu, ili meli zinapokuja ziwena mahali pa kutua, kuweka nanga, kupewa leseni na baadaya uvuvi ziweze pia kurudi na kuhakikiwa kuhakikishakwamba, wanachovua ni halisi. Ni kiasi ambachowameidhinishiwa kuvua. Na kwa njia hii nina uhakikakwamba, mapato yatakuwa na yataongezeka kwa sababu,Bahari kuu ndio ina uwezo zaidi kiuvuvi kuliko maji ya baridi.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie tuMheshimiwa Mbunge kwamba, tayari tumejipanga kamaSerikali, na kama nilivyosema mara nyingine tena hapa, tayariBenki ya Rasilimali, imeweka dirisha la mkopo ambalolimeanza kukopesha wavuvi. Wengine wamekopeshwa zana,wengine mitaji, ili waweze kuwa na uwezo na kuongezauwezo waweze kuvuna kwa ufanisi zaidi na kujinufaishawenyewe na kutunufaisha sisi kama nchi kwa kuongezewauwezo. (Makofi)

MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nina swali moja dogo la nyongeza. Ni kwa nini, tunawaachiawenzetu wa Malawi wanavua uvuvi wa kisasa na sisitunawaangalia tu? Au kwa vile lile Ziwa si letu, kama Malawiwanavyodai? (Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Hiyo sehemu ya mwisho nimeifuta kabisa,Ziwa ni letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

Page 37: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

37

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleoya Mifugo na Uvuvi, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Capt.Damian Komba, kama ifuatavyo:-

(i) Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kupitiaBunge lako Tukufu, naomba tu niseme kwa uhakika kwamba,Ziwa Nyasa ni ziwa tunaloshirikiana na nchi ya Malawi.Sehemu ya Tanzania ambayo ipo kwenye ziwa hilo ni yakwetu na itaendelea kuwa ya kwetu daima. (Makofi)

(ii)Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Wamalawiwanavua kwa kutumia vyombo vya kisasa; nadhani nisemetu kwamba, jibu linafanana na nililotoa katika jibu langu lamsingi kwamba, tutajaribu kuwajengea watu wetu uwezo.Naomba Mheshimiwa Capt. Damian Komba atuvumilie.

Lakini pia nitumie Bunge lako Tukufu, kuwambiawenzetu wanaokaa kando ya ziwa hilo na wao wajikusanye,waanzishe SACCOS, waweze kupata mikopo na kwa njia yamikopo hiyo, kwa uhakika na wao watakuwa na vyombovya kisasa na teknolojia ya kisasa itakayowawezesha kuvuavizuri zaidi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswaliyameisha na muda wetu kwa kweli, umepita. Niwashauri tuWaheshimiwa Mawaziri, majibu ya maandishi kwa baadhi yaWizara yanakuwa ni marefu sana. Tujitahidi kuyaangalia, uleutangulizi sio wa lazima sana, ili kupunguza, kuufanya mudawetu uweze kutosha.

Naomba nimtangaze mgeni ambaye yuko kwenyeGallery ya Spika na yeye ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mheshimiwa Frederick Sumaye. Karibu sana MheshimiwaSumaye, kwa niaba ya Bunge hili, tunaomba tukukaribishetena katika eneo hili ambalo umekuwa Mbunge mwenzetukwa miaka mingi. Tutakukumbuka sana kwa ajili ya ujenzi waUkumbi huu, ambao tunautumia sasa kama Bunge, pamojana mambo mengine mengi. (Makofi)

Page 38: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

38

Matangazo mawili, la Mheshimiwa Zitto Kabwe,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu zaSerikali, (PAC) anawaomba Wajumbe wa Kamati hiyowakutane Ukumbi Namba 231, Jengo la Utawala, saa 5.00.Kamati ya Hesabu za Serikali saa 5.00 wakutane Jengo laUtwala kwa kikao maalum.

Mheshimiwa Anna Magreth Abdallah, Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, anawaombaWajumbe wa Kamati hiyo, wakutane Ukumbi wa Msekwa C,Saa 7.00 mchana. Kamati ya Ulinzi na Usalama, ikutaneMsekwa C, na tangazo hili limeletwa na Mheshimiwa AnnaMagreth Abdallah, Ukumbi wa Msekwa.

Baada ya Matangazo hayo, Katibu?

MHE. MOSES J. MACHALI: Mwongozo wa Spika.

NAIBU SPIKA: Liko tangazo la tatu, nimelipata sasahivi.Mheshimiwa Idd Azzan, Mwenyekiti wa Bunge Sports Club,anaomba niwatangazie Waheshimiwa Wabungemnaopenda kushiriki mchezo wa Kikapu (Basket Ball),mnatakiwa kuanza mazoezi kesho tarehe 25 Aprili, katikaUwanja wa Jamhuri kuanzia saa 12.00 asubuhi.

Mazoezi haya ni kwa ajili ya kujiandaa kwa mechizijazo, chini ya Kocha Mheshimiwa Injinia Ramo Makani; walewanaopenda Basket Ball. (Makofi)

Mwongozo? Mko wangapi? Wawili eeh?Asiongezeke mtu sasa hapo. Mheshimiwa Capt. JohnKomba pia? Ok, Mheshimiwa Machali. Ok, anza MheshimiwaMachali.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Ninasimama kuomba Mwongozo wako KuhusuUtaratibu, kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (1) pamoja na ile ya68 (7).

Page 39: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

39

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati nimeuliza swali lanyongeza, alisimama Mheshimiwa sana Mama yangu Waziriwa Kazi na Ajira na kulieleza Bunge lako kwamba Walimuwanakatwa ile 2% hata wale ambao siyo wanachama kwasababu ya Sheria ya The Employment and Labour RelationsAct ya 2004. Naomba niweke record kwamba ni kwa mujibuwa Sheria ya The Trade Union Act ya mwaka 1998, kifungukile cha 55 pamoja na kifungu cha 56(1),(2),(3). Vifungu vyotehivi ukiangalia vinakiuka Katiba yetu ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ambayo ndiyo sheria mama, kifungukidogo cha kwanza na kifungu kidogo cha nne.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda,naomba nisinukuu, niishauri Serikali iende ikarejee Sheria hiina vifungu hivi ambavyo vinakiuka huu utaratibu na maramoja waweze kuhakikisha kwamba wanawasaidia Walimuwa Manispaa ya Kigoma UJiji ambao wameomba kujitoakwenye Chama cha Walimu na wameweza kushinda kesiyao ili kusudi suala hili liweze kuharakishwa kwa sababukuwakata fedha ni kinyume cha Katiba yetu kama ambavyonimeeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMwongozo wako kuhusiana na taarifa ambayo ilitolewa naMheshimiwa Waziri ambayo inakiuka matakwa ya Katibayetu kama ambavyo nimefafanua nini kifanyike.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Machali, kwakweli ulichofanya ni kutimiza wajibu wako wa Kikatiba wakuishauri Serikali na umefanya hivyo, umetoa ushauri mzuritu kwa Serikali. Kwa hiyo, Serikali imepokea ushauri huoitautazama na kwa sababu hizi Wizara zinakuja huko mbele,tutafikia mahali pa kulijadili jambo hilo vizuri, MheshimiwaMpina!

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Naibu Spika,katika kipindi cha Maswali na Majibu tarehe 16 April, 2013hapa Bungeni wakati nikiuliza swali la nyongeza katika swali

Page 40: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

40

namba 47 la Mheshimiwa Thuwayba Idrisa Muhamed kuhusuDeni la Taifa, nilieleza kuwa moja ya sababu ambayoinasababisha Deni la Taifa kuongezeka ni pamoja na Serikalikuwa na matumizi makubwa kuliko uwezo wa mapato yetuya ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Fedha wakati akijibu swali langu alisema, kwa namnayoyote ile hatukopi fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida,tunakopa fedha kwa ajili ya kulipia miradi ya maendeleo naakanitaka mimi nihakikishe takwimu zangu kama ziposawasawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kukuhakikishiakwamba takwimu zangu zipo sawasawa na leo nimekujana kitabu cha hotuba ya Waziri wa Fedha cha mwaka 2012/2013 ambapo mapato yetu ya ndani yalikuwa shilingi trilioni9.1 wakati matumizi yetu ya kawaida yalikuwa shilingi trilioni10.6 na hapo kulikuwa na gape la shilingi trilioni 1.5. Misaadakama misaada tuliyopata ilikuwa ni shilingi bilioni 878.4 tu.Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba gap lililobaki lilifidiwa na fedhaza mikopo na kwamba hata hiyo shilingi trilioni 9.1, shilingitrilioni 2.2 nazo tulizipeleka kwenye maendeleo kwa hiyoukitoa pale unaweza ukaona gap la matumizi ya kawaidakulipiwa na mapato ya ndani inaongezeka kuwa kubwazaidi. Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba matumizi yetu ya kawaidani makubwa kuliko hata uwezo wa mapato yetu ya ndani.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi naombaMwongozo wako kama majibu ya Naibu Waziri wa Fedha,Mheshimiwa Saada M. Salum aliyoyatoa siku hiyo yanakidhimasharti yaliyowekwa na Kanuni ya 46(1). Ahsante.

NAIBU SPIKA: Nakushukuru Mheshimiwa Mpina,nipokee Mwongozo huo, nitatoa maelezo yangu baadaye,naomba tuendelee.

Page 41: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

41

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2013/2014 - Wizara ya Maji

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatiataarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo naMaji iliyowasilishwa hapa Bungeni kuhusu Wizara ya Maji,naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee,lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi yaKawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Maji kwa mwaka2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa shukranizangu za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Profesa PeterMahamudu Msolla, Mbunge wa Kilolo, kwa kupokea nakuchambua Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2012/2013 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangukwa mwaka 2013/2014, kisha kutoa maoni na ushauri muhimuuliozingatiwa wakati wa utayarishaji wa Bajeti ya Wizarayangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hii,kuwapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wapya waKamati mbalimbali za Kudumu za Bunge walioteuliwa hivikaribuni. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiananao katika kutekeleza majukumu yetu kwa maendeleo yaTaifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru nakumpongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda,Waziri Mkuu, kwa hotuba yake ambayo imetoa mwelekeowa utekelezaji wa bajeti na kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014. Nawapongeza pia, Mawaziri wenzangu wotewalionitangulia kuwasilisha hoja za Wizara zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu ilipokea kwamshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha MheshimiwaSalim Hemed Khamis, Mbunge wa Chambani kilichotokea

Page 42: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

42

wakati wa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge. Nachukuanafasi hii kutoa pole kwako wewe Mheshimiwa Naibu Spika,Bunge lako Tukufu, familia ya marehemu, ndugu na wananchiwa Jimbo la Chambani kwa msiba huo mkubwa. MwenyeziMungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.Amin.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya sekta ya maji nchini.Wizara yangu katika kutekeleza majukumu yake, inazingatiamaelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza UmasikiniTanzania Awamu ya Pili (MKUKUTA II), Malengo ya Milenia,Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Diraya Taifa ya Maendeleo 2025 na ahadi za Serikali. Katika mwaka2013/2014, Wizara yangu itaendelea kutekeleza majukumuyake kulingana na Sera ya Maji ya mwaka 2002; Mkakati waMaendeleo ya Sekta ya Maji; Sheria za Maji na Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP).

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu inasimamiaSekta ya Maji ambayo imegawanywa katika sekta ndogokuu tatu, ambazo ni Rasilimali za Maji, Huduma ya Maji naUsafi wa Mazingira Vijijini na Huduma ya Maji na Usafi waMazingira Miji ni. Hadi sasa hali halisi ya Sekta ya Maji ni kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, rasilimali za maji.Nchi yetu inakadiriwa kuwa na rasilimali za maji juu ya ardhizinazofaa kutumika kwa matumizi mbalimbali (annualrenewable surface water resources) ya kiasi cha wastani wakilomita za ujazo 89 kwa mwaka. Aidha, inakadiriwa kuwahifadhi ya rasilimali za maji chini ya ardhi ni kilomita za ujazo40. Hata hivyo, kutokana na tofauti ya hali ya hewa na jiolojia;mtawanyiko na upatikanaji wa rasilimali hizo nchini haukosawa katika maeneo yote. Kiasi cha maji kilichopo kwa sasakwa kila mtu ni wastani wa lita milioni 2.02 kwa mwaka lakinikutokana na ongezeko la watu, ifikapo mwaka 2025 kiwangohicho kinatarajiwa kupungua hadi lita milioni 1.5. Hivyo,inatulazimu kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi majikatika maeneo mbalimbali ya nchi na kuboresha matumiziyake.

Page 43: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

43

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi ya nchi yetuyameendelea kuwa na uhaba wa maji kwa matumiziyaliyokusudiwa kutokana na maji hayo kutokuwa na uboraunaokubalika, uharibifu wa mazingira na athari za mabadilikoya tabianchi. Sababu nyingine ni pamoja na gharama kubwaza ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi rasilimali za maji,matumizi ya maji yasiyozingatia ufanisi, uchafuzi wa vyanzovya maji unaosababishwa na shughuli za kibinadamu na kasikubwa ya ongezeko la watu. Hivyo, ni muhimu tuchukuehatua za kuhifadhi vyanzo vyetu vya maji ili kunusuru rasilimalihiyo. Jukumu hili ni letu sote kuanzia ngazi za jamii, Wilaya,Mkoa na Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Februari mwaka2013, hali ya upatikanaji wa maji haikuwa nzuri kutokana nauhaba wa mvua za vuli katika maeneo mengi nchini. Kwaujumla, hali hiyo ilisababisha kiasi cha maji katika mabwawa,mito na Maziwa kupungua ikilinganishwa na mwaka uliopita.Katika Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, kiasi cha mvuakatika kipindi hicho kilikuwa ni milimita 550 kwa upande wamagharibi wa bonde (Songea) na kwa upande wa masharikiwa bonde (Mtwara) ni milimita 800; ikilinganishwa na kiasicha mvua cha kawaida cha milimita 1,000. Aidha, hali yamaji katika Bonde la Mto Pangani kwa ujumla haikuwa nzurikutokana na mvua kunyesha chini ya wastani. Hadi kufikiatarehe 10 April, 2013 kina cha maji katika bwawa la Nyumbaya Mungu kilikuwa mita 682.53 juu ya usawa wa bahari.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa majikatika Bonde la Mto Rufiji kwa mwaka 2012/2013 haikuwa yakuridhisha. Hadi kufikia tarehe 14 Machi, 2013 kina cha majikatika Bwawa la Mtera kilikuwa mita 688.66 juu ya usawawa bahari. Aidha, hali ya maji katika mabwawa yaliyopokatika Bonde la Ziwa Tanganyika hadi Februari 2013 haikuwaya kuridhisha ambapo kumekuwa na kushuka kwa kina chamaji katika mabwawa ya Kazima na Igombeyanayohudumia Manispaa ya Tabora.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji majikatika mito ya Bonde la Wami/Ruvu imeendelea kupungua

Page 44: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

44

kutokana na mvua kunyesha chini ya wastani. Hadi kufikiamwezi Februari 2013, wingi wa maji katika mito mingiulipungua ikil inganishwa na mwaka 2012. Hali hiyoilisababisha kina cha maji katika Bwawa la Mindu kupunguana kuathiri upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Morogoro.Bonde pekee ambalo kwa ujumla wingi wa maji uliongezekani Bonde la Ziwa Victoria. Hata hivyo, katika baadhi yamaeneo kwenye Bonde hilo kulikuwa na upungufu. Hadikufikia mwezi Februari 2013, kiasi cha maji kwenye Mto Kagerakiliendelea kupungua lakini hali ilikuwa tofauti kwa Mto Marana Mto Simiyu ambapo kulikuwa na ongezeko la maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mvua za masika zilizoanzakunyesha mwezi Machi, 2013 katika maeneo mengi nchinizinaelekea kuleta ahueni ya hali ya upatikanaji wa majiiwapo zitaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Mei kamailivyo kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, huduma za maji Vijijini.Sera ya Maji ya mwaka 2002 inalenga katika kuhakikishakuwa, wananchi Vijijini wanapata huduma ya maji safi nasalama umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.Katika kufikia lengo hilo la Sera, Serikali kwa kushirikiana naWashirika wa Maendeleo, Serikali za Mitaa, Wananchi nawadau wengine inaendelea kuboresha huduma za maji Vijijinikwa kujenga miradi mipya, kupanua na kukarabatimiundombinu ya maji. Miradi ya maji Vijijini hutekelezwa naHalmashauri kwa kuwashirikisha wananchi wa Vijiji husika nasekta binafsi. Sekretariati za Mikoa husimamia na kutoaushauri wa kiufundi. Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI huratibuutekelezaji ambapo Wizara ya Maji hutafuta fedha nakuandaa miongozo ya utekelzaji na kutoa ushauri wakitaalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za utekelezaji wamiradi ya maji Vijijini kutoka Serikali Kuu hutumwa kwenyeHalmashauri kwa kutumia fomula inayozingatia kigezo chakiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji, wingi wa watuna aina ya teknolojia inayotumika katika Halmashauri hizo.Halmashauri zenye kiwango kidogo cha huduma ya maji

Page 45: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

45

Vijijini hupatiwa fedha nyingi zaidi kuliko zile zenye kiwangokikubwa. Lengo ni kuondoa tofauti ya viwango vyaupatikanaji wa huduma ya maji Vijijini miongoni mwaHalmashauri (equity).

Mheshimiwa Naibu Spika, jitihada zinazofanyika katikauboreshaji wa miradi ya maji kupitia vyanzo hivyo vya fedhazimeongeza huduma ya maji kwa wananchi waishio Vijijinikutoka watu milioni 16.3 mwezi Desemba 2005 hadi kufikiawatu milioni 20.6 mwezi Desemba 2012.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, huduma ya maji Mijini inasimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka za majisafi nausafi mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa, Mamlaka katikangazi za Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa ya Maji.Katika kuimarisha usimamizi, Mamlaka hizo zimegawanywakatika Madaraja ya A, B na C kulingana na uwezo wa kilaMamlaka kujitegemea. Mamlaka za Miji Mikuu ya Mikoazimegawanyika kama ifuatavyo; Mamlaka 13 za Arusha,Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza,Shinyanga, Tabora, Tanga, Songea na Musoma zipo daraja‘A’. Katika daraja hilo, Mamlaka zina uwezo wa kulipiagharama zote za uendeshaji na matengenezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka za daraja ‘B’ ziponne, ambazo ni Bukoba, Kigoma, Singida na Sumbawanga.Mamlaka hizo zinapata ruzuku ya kulipia asilimia 50 yagharama za umeme wa kuendesha mitambo. Mamlaka zilizokwenye daraja ‘C’ ni Babati na Lindi ambazo bado zinapataruzuku ya mishahara ya wafanyakazi wake pamoja na kulipiagharama za umeme wa kuendesha mitambo. Serikaliimekamilisha kuunda Bodi za Mamlaka za Miji Mikuu ya Mikoamipya. Miji hiyo ni Mpanda, Njombe, Geita na Bariadiambayo kwa kuanzia itakuwa daraja C.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Mamlaka zote zangazi ya Wilaya, Miji Midogo na miradi saba ya kitaifa nazozipo katika daraja C. Wizara imeendelea kuzijengea uwezoMamlaka hizo i l i ziweze kujiendesha kibiashara nakuwahudumia wateja wake kwa ufanisi. Katika kuboresha

Page 46: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

46

huduma za majisafi na usafi wa mazingira Miji ni, Serikaliimeendelea na ujenzi, ukarabati na upanuzi wamiundombinu ya majisafi katika Miji Mikuu ya Mikoa, MijiMikuu Ya Wilaya, Miji Midogo na miradi ya kitaifa ya maji.Kwa wastani, hali ya huduma ya maji katika Miji Mikuu yaMikoa, Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na maeneoyanayohudumiwa na miradi ya kitaifa ya maji imeendeleakuimarika mwaka 2012/2013 kulinganisha na miaka yanyuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya Majisafi katikaMiji Mikuu ya Mikoa hali ya utoaji wa huduma ya majisafikwa wakazi wa Miji Mikuu ya Mikoa kwa Mamlaka za darajaA isipokuwa Jiji la Dar es Salaam ni asilimia 89 hadi Desemba2012 na kwa Mamlaka za daraja B na C wastani wa maeneoyanayopata maji ni asilimia 83. Iliyokuwa Miji Mikuu ya Wilayaza Njombe, Mpanda, Geita na Bariadi kwa sasa ni Miji Mikuuya Mikoa. Hivyo, hali ya upatikanaji maji katika Miji hiyo niwastani wa asilimia 53.

Mheshimiwa Naibu Spika, uzalishaji wa majisafi kwaMamlaka zote 19 za Miji Mikuu ya Mikoa uliongezeka kutokawastani wa lita milioni 330.99 kwa siku kwa mwezi Machi2012 hadi kufikia wastani wa lita milioni 341.77 kwa siku mweziMachi 2013. Ongezeko hili limetokana na ukarabati wamiundombinu ya maji iliyokamilika na inayoendelea katikaMiji Mikuu ya Mikoa mbalimbali nchini, hususan Miji ya Mbeyana Iringa. Ufungaji wa dira za maji kwenye Miji Mikuu yaMikoa 19 umeongezeka kutoka dira 264,090 mwezi Machi2012 hadi kufikia dira 280,832 mwezi Machi 2013. Ongezekohilo limefanya idadi ya wateja waliofungiwa dira katika Mijihiyo kufika wastani wa asilimia 93. Aidha, upotevu wa majiumepungua na kufikia wastani wa asilimia 36. Lengo nikupunguza upotevu huo hadi kufikia wastani wa asilimia 20(kiwango kinachokubalika kimataifa) ifikapo mwaka 2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, makusanyo ya maduhuliyatokanayo na mauzo ya maji katika Mamlaka za Miji Mikuuya Mikoa 19 kwa mwezi yameongezeka kutoka shilingi bilioni4.45 mwezi Machi, 2012 hadi kufikia shilingi bilioni 5.53 mwezi

Page 47: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

47

Machi, 2013, sawa na ongezeko la asilimia 24. Kuongezekakwa maduhuli kunaziwezesha Mamlaka za Maji kuboreshahuduma zinazotolewa ikiwa ni pamoja na kuwekeza katikamiundombinu mipya kwenye maeneo ambayo hayajafikiwana mitandao ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma za majisafi katikaMiji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na miradi ya Kitaifa. Hali yaupatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Miji Mikuuya Wilaya na Miji Midogo ilikuwa asilimia 53 katika mwaka2011/2012. Katika Miji hiyo kuna wateja 97,718 na asilimia 57ya wateja hao wamefungiwa dira za maji. Kwa miradi yakitaifa wateja ni 11,405 na kati yao asilimia 54 wamefungiwadira za maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma za majisafi katikaJiji la Dar es Salaam. Kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam naMiji ya Kibaha na Bagamoyo, huduma ya maji hutolewa naShirika la Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO).Huduma ya maji katika Jiji hilo, inatolewa kwa mgawokutokana na uwezo wa mitambo iliyopo na ongezeko kubwala wakazi katika Jiji. Idadi ya wakazi wanaopata hudumaya maji katika Jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo niasilimia 68. Kati ya hao, asilimia 55 wanapata huduma yamaji kutoka kwenye mtandao wa mabomba na wanaobakiwanapata huduma ya maji kutoka kwenye visima, magatina huduma ya magari (water bowsers).

Mheshimiwa Naibu Spika, uwezo uliopo wa mitamboya kuzalisha maji kwa Jiji la Dar es Salaam ni lita milioni 300kwa siku. Hadi kufikia mwezi Desemba, 2012, uzalishaji wamaji ulikuwa ni wastani wa lita milioni 260 kwa siku. Upungufuhuu unatokana na tatizo la kukatika mara kwa mara kwaumeme kwenye mitambo ya kuzalisha maji pamoja namatengenezo ya mitambo na mabomba yanayovujakutokana na uchakavu. Mahitaji ya maji kwa Jiji la Dar esSalaam hivi sasa ni lita milioni 450 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, upotevu wa maji badoumekuwa ni changamoto kubwa kutokana na uvujaji,

Page 48: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

48

uchakavu wa miundombinu, wizi wa maji na uharibifuwakati wa ukarabati wa barabara na kusababisha kuharibumiundombinu ya maji. Hadi mwezi Desemba 2012, upotevuwa maji ulikuwa ni asilimia 53.75. Lengo ni kufikia asilimia 30ifikapo mwezi Juni 2014. Kati ya mwezi Machi na Aprili 2013,jumla ya watu 94 wamekamatwa kwa kujihusisha na wiziwa maji; na kesi 82 za matukio ya wizi wa maji zimefunguliwaMahakamani. DAWASCO imeanza kusaji l i magariyanayosambaza maji kwa lengo la kutekeleza kanuni zaudhibiti wa biashara ya maji yanayosambazwa na magarina visima. Hatua hiyo itasaidia kudhibiti wizi wa maji,usalama wa maji na bei za maji yanayosambazwa kwamagari hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya uondoaji waMajitaka Mijini. Idadi ya wakazi wa Miji ni wanaopata hudumaya mfumo wa uondoaji majitaka ni ndogo ukilinganisha namahitaji, hivyo mifumo hiyo inahitaji kupanuliwa. Mamlakaza Majisafi na Usafi wa Mazingira ambazo zina mifumo yamajitaka ni za Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa,Mbeya, Morogoro, Moshi, Mwanza, Tabora, Tanga na Songea.Serikali ina mpango wa kuweka miundombinu ya uondoajiwa majitaka kwa Miji ya Musoma na Bukoba. Katika Mijimingine ambayo haina mitandao ya majitaka, mfumounaotumika kuhifadhi majitaka ni makaro yaliyokomajumbani na magari yanayobeba majitaka nakuyamwaga katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajiliya kuhifadhi na kutibu majitaka. Kukosekana kwa mitandaoya mabomba ya majitaka katika Miji hiyo kumetokana nakutokuwa na uwekezaji mpya katika kipindi hicho. Uwekezajiwa miundombinu ya majitaka utaanza katika awamu yapili ya Programu ya Maendeleo ya Maji inayotarajiwa kuanzamwaka 2014/2015. Hadi kufikia mwezi Desemba 2012, jumlaya wateja wa majitaka Miji ni wamefikia 21,680 kutoka wateja20,773 mwezi Machi 2012.

Mheshimwa Naibu Spika, mapitio ya utekelezaji wabajeti ya 2012/2013 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2013/2014. Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2012/2013 na malengo ya mwaka 2013/2014 kwa Sekta ya Maji

Page 49: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

49

katika maeneo ya rasilimali za maji, huduma ya maji na usafiwa mazingira Vijijini, huduma ya maji na usafi wa mazingiraMiji ni na masuala mtambuka umeainishwa kama ifuatavyo:-

Mheshimwa Naibu Spika, kwanza, rasilimali za maji.Majukumu ya Wizara yangu katika kusimamia na kuendelezarasilimali za maji ni pamoja na kuchunguza na kutathminirasilimali za maji nchini; kuimarisha usimamizi wa rasilimaliza maji; kuimarisha Bodi za Maji za Mabonde ili zisimamiekikamilifu rasilimali hizo. Kazi nyingine ni kuandaa mipangoshirikishi ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nakuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kipaumbele,yakiwemo mabwawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, usimamizi na uendelezajiwa rasilimali za maji. Katika kusimamia mwenendo warasilimali za maji nchini, Wizara yangu imeendelea kuimarishavituo vya kufuatilia wingi na ubora wa rasilimali za maji juuna chini ya ardhi ili kuboresha upatikanaji wa takwimu nataarifa sahihi na kwa wakati. Takwimu na taarifa hizi husaidiakutambua hali ya maji kwa nyakati tofauti kwenye maeneombalimbali hapa nchini, hivyo kuwezesha kufanyika kwamaamuzi sahihi ya ugawaji wa Rasilimali za Maji kwamatumizi mbalimbali. Takwimu na taarifa hizo, pia hutumikawakati wa usanifu na ujenzi wa miundombinu ya skimu zamaji, mabwawa na madaraja. Hadi kufikia Februari 2013,jumla ya vituo 120 vya kupima mtiririko wa maji mitoni(hydrometric stations) na vituo 45 vya hali ya hewa(meteorological/weather stations) vilijengwa, ikiwa ni pamojana kufunga vifaa vya kupima mvua katika vituo 17 kotenchini. Ukarabati ulifanyika kwa vituo 43 vya kupima mtiririkowa maji mitoni. Katika mwaka 2013/2014, Wizara yanguitaendelea na ujenzi na ukarabati wa vituo 338 pamoja nakukusanya takwimu kwenye mabonde yote nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, uhifadhi wa mazingirana vyanzo vya maji. Wizara yangu imeendelea kutekelezamikakati ya kuhifadhi vyanzo muhimu vya maji kwakuviwekea mipaka na kuvitangaza kuwa maeneo tengefu.Katika mwaka wa fedha 2012/2013, jumla ya vyanzo 60

Page 50: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

50

vilibainishwa kwa ajili ya kuanza utaratibu wa kuvitenga ilikuvikinga dhidi ya uchafuzi wa mazingira kwa mujibu waSheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009 naSheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004. Aidha,chanzo cha maji cha Makutupora (Well-field) ambacho nichanzo kikuu cha maji kwa mji wa Dodoma na bwawa laKawa lililoko Rukwa vilitangazwa kuwa maeneo tengefu.Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu kwa kushirikiana naBaraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) itaendeleakuhakikisha kwamba vyanzo vya maji vinatunzwa nakulindwa. Vilevile, Wizara itaendelea kubaini maeneoyanayofaa kutengwa ili kuyakinga dhidi ya uharibifu wamazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini ya athari zaMazingira ya Miradi saba ya Maji katika Miji ya Musoma,Mwanza, Bukoba, Morogoro, Iringa, Mbeya na Masasi(Mchema Dam Water Supply) imekamilika na kuwasilishwaNEMC ili ihakikiwe. Aidha, miradi mingine ya maji katika Mijiya Babati, Lindi, Mtwara, Sumbawanga, Kigoma na Taboraimefanyiwa tathmini ya awali (Screening) na mapungufukadhaa yamegundulika. Mamlaka husika zimeagizwakurekebisha kasoro zilizobainika kabla ya kupeleka NEMC kwahatua zinazofuata. Mkataba kwa ajili ya kufanya Tathminiya Athari za Mazingira ya mabwawa matano ya Itobo,Uchama, NkiniZiwa, Leken na Enguikument umesainiwa natathmini zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradimingine mitano ya (Same –Mwanga -Korogwe; Nzega -Igunga -Tabora; Hai, Masasi – Nachingwea na Chalinze) ipokatika hatua mbalimbali za uandaaji wa hadidu za rejea iliiweze kufanyiwa Tathmini ya athari za Mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, kudhibiti uchafuzi wavyanzo vya maji. Katika kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vyamaji, Wizara yangu katika mwaka wa fedha 2012/2013ilikagua viwanda, migodi, vituo vya mafuta na hoteli nakutoa maelekezo. Jumla ya viwanda 41 vilikaguliwa katikaMabonde ya Ziwa Victoria (18) Bonde la Pangani (19), Bondela Rufiji (3) na Bonde la Ziwa Rukwa (1). Jumla ya vibali vinnevya kutiririsha majitaka yanayokidhi viwango kwenye vyanzo

Page 51: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

51

vya maji vilitolewa na Bodi za Maji za Mabonde ya ZiwaRukwa (1) na Rufiji (3) ambapo uongozi wa viwanda hiviuliagizwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye mipango yaoya usimamizi wa mazingira (Environmental ManagementPlan). Majitaka kutoka kwenye viwanda 37 vilivyopo kwenyeMabonde ya Ziwa Victoria (18) na Pangani (19) hayakuwayanakidhi viwango vya ubora vinavyohitajika ili yawezekutiririshwa kwenye mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, uongozi wa viwanda hiviuliagizwa kufanya Tathmini ya Athari ya Mazingira kwa mujibuwa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, kuwa na mifumomadhubuti ya kusafisha majitaka, kufanya ufuatiliaji wandani wa ubora wa majitaka yanayotoka katika viwandavyao na kuhakikisha kwamba majitaka yatokanayo nashughuli za viwanda yanakidhi viwango kabla ya kumwagwakwenye mazingira. Jumla ya migodi 5 ilikaguliwa katikaMabonde ya Ziwa Victoria (4) na Ziwa Rukwa (1).

Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo ya ukaguzi naubora wa majitaka katika migodi ya Geita, Bulyanhulu naBuzwagi yalikidhi viwango ambapo uongozi wa migodi hiiuliagizwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye mipango yaoya usimamizi wa mazingira (Environmental ManagementPlan). Matokeo ya ukaguzi na ubora wa majitaka katikamigodi ya North Mara na Shanta Gold Mining Companyhayakukidhi viwango. Wizara iliuagiza uongozi wa migodihii kufanya ufuatiliaji wa ndani wa ubora wa majitaka nakuhakikisha kwamba majitaka yatokanayo na shughuli zamigodi yanakidhi viwango kabla ya kumwagwa kwenyemazingira. Wizara pia iliuagiza uongozi wa mgodi wa NorthMara kudhibiti uvujaji wa maji kutoka kwenye bwawa lakuhifadhia tope (Tailings Storage Facility - TSF). Wizarainaendelea kufuatilia ubora wa majitaka kutoka kwenyemgodi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne, utafutaji wa vyanzovipya vya maji. Maji chini ya ardhi ni moja ya vyanzo vyamaji vinavyotumika hapa nchini hasa katika maeneo kame.Katika mwaka 2012/2013, utafiti wa kubaini maeneo

Page 52: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

52

yanayofaa kuchimba visima vya maji uliendelea katikamaeneo 189 katika Mabonde ya Ziwa Tanganyika (15), Rufiji(4), Pangani (46), Ziwa Victoria (7), Ziwa Rukwa (10), Ruvuma(49), Ziwa Nyasa (3), Wami-Ruvu (17) na Bonde la Kati (38).Katika mwaka 2013/2014, Wizara itachunguza maeneoyanayofaa kuchimba visima virefu vya maji na kusimamiauchimbaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba yangu yamwaka jana, nililiarifu Bunge lako Tukufu juu ya maandaliziya mradi wa uchimbaji wa visima katika maeneo kame kwakushirikiana na Serikali ya Misri. Mnamo tarehe 17 Januari 2013,Wizara yangu ilifanya uzinduzi wa visima 30 vilivyochimbwakwa ufadhili wa Serikali ya Misri katika Wilaya za Maswa,Same, Bunda, Magu, Tarime na Kiteto. Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu itaendelea na uchimbaji wa visimavingine 70 vya awamu ya pili ya mradi huo ambavyovitachimbwa katika maeneo kame ya Wilaya za Maswa,Bariadi, Magu, Tarime, Same, Rorya, Bunda na Kiteto.Utekelezaji wa mradi huo utaenda sambamba na utoaji wamafunzo kwa wataalam wa Sekta ya Maji katika fanimbalimbali. Wizara yangu pia, itachimba visima 55 kwakushirikiana na Serikali ya Watu wa China. Visima hivyovitachimbwa katika Wilaya za Kilosa na Kisarawe katikabonde la Wami/Ruvu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu ina jukumula kuratibu uchimbaji wa visima vya maji nchini. Uratibu huounalenga kuhakikisha kwamba taratibu za kitaalamzinafuatwa ili kuhakikisha visima vina ubora kwa matumiziendelevu. Kwa mwaka 2012/2013, Wizara ilihakiki na kusajilikampuni tano za kuchimba visima na kuwa na idadi yakampuni binafsi 131 hadi kufikia mwezi Machi 2013. Jumla yavisima 420 vilichimbwa na kati ya hivyo, 162 vilichimbwa naWakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa na258 vilichimbwa na kampuni binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za ujenzi waBwawa la Farkwa kwenye Mto Bubu, Wilaya ya Kondoakatika Bonde la Kati unaendelea. Bwawa hilo litakuwa ni

Page 53: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

53

chanzo cha maji kwa Manispaa ya Dodoma na Miji ya Wilayaza Kondoa, Chamwino na Bahi. Katika mwaka 2012/2013,Mtaalam mshauri anayefanya upembuzi yakinifu, usanifu wakina, kuandaa vitabu vya zabuni ameajiriwa na ameanzakazi na taarifa ya awali imewasilishwa. Mkataba wakutathmini athari za mazingira umesainiwa Septemba 2012na taarifa ya awali imewasilishwa. Kazi hiyo inatarajiwakukamilika katika mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeendelea namaandalizi ya ujenzi wa Bwawa la Ndembera katika Bondela Rufiji litakalotumika kudhibiti mwenendo na mtiririko wamaji katika kipindi cha mwaka mzima kwenye mto RuahaMkuu. Matumizi mengine ya bwawa hilo ni pamoja na kilimocha umwagiliaji na kuzalisha umeme. Katika mwaka 2012/2013, Mtaalam mshauri kwa ajili ya upembuzi yakinifu, usanifuna kuandaa vitabu vya zabuni ameajiriwa na ameanza kazi.Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu itakamilisha usanifuna maandalizi ya vitabu vya zabuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, tano, matumizi bora yarasilimali za maji. katika mwaka 2012/2013, Wizara yanguimeendelea kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali zamaji nchini; kwa kuhakikisha kuwa rasil imali hizozinagawanywa kwa uwiano kulingana na mahitaji ya sektambalimbali za kiuchumi na kijamii na kufanya ukaguzi wamatumizi bora ya maji. Jumla ya vibali vya kutumia maji 196katika mabonde ya Ziwa Victoria (15), Rufiji (87) na Ruvumana Pwani ya Kusini (94) vilitolewa; na vibali sita vya kutupamajitaka vilitolewa katika bonde la Ziwa Victoria. Vilevile,matoleo 562 ya maji kwenye miradi ya umwagiliaji,yalikaguliwa na kusajiliwa katika mabonde ya Ziwa Victoria(5), Ziwa Rukwa (30) Rufiji (31), Ruvuma na Pwani ya Kusini(496).

Mheshimiwa Naibu Spika, ukaguzi huo ulibaini sababuza ubovu wa mabanio unaosababisha upotevu wa majikutoka katika vyanzo, uchepushaji wa maji usiozingatia sheriana uchafu wa matoleo na mifereji ya maji. Wahusikawalielekezwa kukarabati mabanio na kusafisha mifereji na

Page 54: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

54

kuzingatia masharti ya vibali vya kutumia maji. Katika mwaka2013/2014, Wizara yangu kupitia Bodi za Maji za Mabondeitaendelea kutoa elimu kwa wadau juu ya umuhimu wakuwa na vibali vya kutumia maji na kusimamia matumiziendelevu ya rasilimali za maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sita, mipango shirikishi yausimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji. Katika mwaka2012/2013, Wizara yangu iliendelea na utayarishaji waMipango Shirikishi ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimaliza Maji katika mabonde yote tisa. Kazi zilizofanyika ni pamojana kutathmini wingi na ubora wa rasilimali za maji, kuainishamahitaji ya maji ya sekta mbalimbali katika muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu. Wataalam washauri kwaMabonde ya Rufij i, Wami/Ruvu na Bonde la Katiwamewasilisha taarifa za utayarishaji (interim and draft finalreports) wa mipango hiyo na kwa mabonde ya Ruvuma naPwani ya Kusini, Pangani, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, ZiwaVictoria na Ziwa Tanganyika, taarifa za awali (InceptionReports) zimewasilishwa. Katika mwaka 2013/2014, Wizarayangu itakamilisha utayarishaji wa mipango hiyo katikaMabonde ya Rufiji, Ruvuma na Pwani ya Kusini, Pangani,Wami/Ruvu, Bonde la Kati, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa na ZiwaTanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, saba, kuimarisha Bodi za Majiza Mabonde. Wizara yangu imeendelea kuzijengea uwezoBodi za Maji za Mabonde kwa kutoa mafunzo kwa watumishi,ujenzi wa ofisi na ununuzi wa vitendea kazi. Katika mwaka2012/2013, jumla ya wataalam 210 walipata mafunzo yamuda mfupi katika fani za usimamizi shirikishi wa rasilimali zamaji, usimamizi wa takwimu, matumizi ya vifaa vya utafitiwa maji chini ya ardhi, kujenga na kutumia vituo vya hali yahewa na vya kupimia maji mitoni na kwenye Maziwa,pamoja na mafunzo ya namna ya kutatua migogoroitokanayo na matumizi ya rasilimali za maji. Vilevile, watumishiwapatao 22 wanaendelea na masomo ya fani mbalimbalikatika ngazi ya Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili.Mafunzo hayo yatawezesha watumishi kuongeza ufanisi natija katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Page 55: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

55

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mafunzo kwawatumishi yaliyoainishwa hapo juu, Wizara imeendeleakuimarisha Bodi za Maji za Mabonde kwa kuzijengea majengoya ofisi na maabara na kuzipatia vitendea kazi. Kwa mwaka2012/2013 ujenzi wa jengo la ofisi ya Bonde la Ziwa Nyasakatika mji wa Tukuyu umeendelea, kwa sasa umefikia hatuaza mwisho na jengo litakamilika mwaka huu wa fedha.Aidha, taratibu za kuwapata wakandarasi wa kukarabatina kujenga Ofisi za Bodi za Maji za mabonde ya Ziwa Victoria,Ziwa Tanganyika na Bonde la Kati zinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, nane, makusanyo yamaduhuli. Moja ya majukumu ya Bodi za Maji za Mabonde nikuandaa na kutekeleza mikakati ya ukusanyaji wa maduhuliyatokanayo na ada za matumizi ya maji ili kufanikishausimamizi, utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji. Katikamwaka 2012/2013, jumla ya shilingi 658,692,000 zilikusanywahadi kufikia mwezi Machi 2013. Makusanyo hayo ni sawa naasilimia 51 ya lengo la shilingi 1,300,000,000 zilizopangwakukusanywa ifikapo tarehe 30 Juni, 2013. Katika mwaka 2013/2014, Bodi za Maji za Mabonde zinakadiria kukusanya kiasicha shilingi 1,768,887,000 kutokana na vyanzo mbalimbali vyamapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, tisa, kudhibiti migogoromiongoni mwa watumiaji wa maji. Bodi za Maji za Mabondezimeendelea kusuluhisha migogoro katika matumizi ya majikwa kushirikiana na Jumuiya za Watumiaji Maji na paleinapobidi, vyombo vya kisheria vimekuwa vikitumika kutatuamigogoro inayojitokeza. Katika mwaka 2012/2013, jumla yamigogoro 19 ya watumiaji maji ilijitokeza. Kati ya hiyo,migogoro saba ilipatiwa suluhisho katika Mabonde ya Majiya Pangani (2), Wami/Ruvu (2), Ziwa Rukwa (1) na Rufiji (2).Katika mwaka 2013/2014, Serikali itaendelea kusuluhishamigogoro ya watumiaji maji iliyopo na kutoa elimu yaugawanaji na utunzaji wa rasilimali za maji ili kudhibitimigogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, usimamizi wa rasilimali zamajishiriki. Nchi yetu ina mabonde tisa ya maji. Kati ya hayo,

Page 56: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

56

mabonde saba yanavuka mipaka ya nchi yetu ambapotunalazimika kushirikiana na nchi nyingine 17 ambazo niAngola, Botswana, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi,Msumbiji, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri,Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Uganda naEritrea. Wizara yangu imeendelea kushirikiana na nchi hizokwa kuunda vyombo vya pamoja na kuimarisha vilivyopo ilikusimamia matumizi endelevu ya rasilimali hizo. Ushirikianokatika mabonde hayo upo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Bonde la Mto Nile kwa sasalinajumuisha nchi 11 za Burundi, Eritrea, Ethiopia, Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Kenya, Misri, Rwanda, Sudan, SudanKusini, Tanzania na Uganda. Nchi ya Eritrea ni mtazamaji(observer) katika jumuiya hiyo. Nchi hizo zinashirikiana kupitiachombo cha mpito cha usimamizi wa rasilimali hiyokinachojulikana kama Ushirikiano wa Nchi za Bonde la MtoNile (Nile Basin Initiative - NBI). Madhumuni ya ushirikiano huoni kuhifadhi, kuendeleza na kutumia kwa njia endelevurasilimali za maji za Bonde hilo. Hadi sasa, nchi za Burundi,Ethiopia, Tanzania, Uganda, Rwanda na Kenya zimesainiMkataba wa Kudumu wa Ushirikiano wa Nchi za Bonde hiloutakaoanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Nile. Nchi za Misri,Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hazijasainiMkataba huo. Kwa mujibu wa Mkataba, nchi wanachamazinatakiwa kuanza hatua za kuuridhia Mkataba baada yanchi sita kusaini. Katika mwaka 2013/2014, Tanzania na nchinyingine zilizosaini Mkataba huo zitaendelea na juhudi zakuuridhia kwa kuzingatia sheria za nchi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa hifadhi yamazingira ya Ziwa Victoria. Awamu ya pili ya Mradi waUsimamizi na Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP II)ilianza rasmi mwezi Agosti 2009. Nchi zinazotekeleza mradihuo ni pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda. Madhumuniya mradi ni kuimarisha usimamizi wa pamoja wa rasilimaliza Bonde la Ziwa Victoria kwa kudhibiti uharibifu wamazingira katika Ziwa hilo. Kwa upande wa Tanzania, mradiunalenga kuimarisha taasisi zinazohusika na hifadhi ya majina samaki; ukarabati wa mifumo ya kusafisha majitaka

Page 57: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

57

katika Miji ya Mwanza, Musoma na Bukoba ambayo ipokando kando ya Ziwa. Walengwa wengine ni Halmashauriza Wilaya ya Maswa, Bariadi, Magu, Meatu na Kwimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya miradi midogo 126ya kijamii yenye thamani ya Dola za Marekani 2,819,886inatekelezwa. Vilevile, miradi tisa mikubwa ya kijamii(Co –Management Interventions) yenye thamani ya Dola zaKimarekani 2,067,563.44 imeanzishwa katika Wilaya zaMusoma Mjini, Maswa, Bariadi, Kwimba, Magu, Meatu na Jijila Mwanza. Katika mwaka 2013/2014, Wizara itasimamiautekelezaji wa miradi hiyo pamoja na kufuatilia ukamilishajiwa kazi zinazofanywa na wataalam washauri kuhusuuboreshaji wa Sera, Sheria, Kanuni na viwango vya utupajimajitaka katika Ziwa Victoria, mito na vyanzo vingine vyamaji katika bonde la Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu ilishirikikikamilifu katika kuhakikisha kwamba Sera mpya ya Matumiziya Maji ya Ziwa Victoria imepitishwa na Mkutano wa 26 waBaraza la Mawaziri la nchi za Jumuiya ya Afrika ya Masharikiuliofanyika mwezi Novemba, 2012. Kupitishwa kwa Sera hiyokutasaidia kuunda chombo huru chenye wajumbe kutokakila nchi husika ambacho kitafanya kazi ya ufuatiliaji nauperembaji wa matumizi ya maji ya Ziwa Victoria. Katikamwaka 2013/2014, Wizara yangu itaendelea kushirikiana nanchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutekeleza sera hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, bonde la mto Zambezi.Tarehe 8 Februari 2010, Bunge lako Tukufu liliridhia Mkatabawa kuanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (ZambeziWatercourse Commission-ZAMCOM). Mkataba huo umeanzakutumika rasmi kisheria tarehe 26 Juni, 2011 baada ya nchisita, ambazo ni theluthi mbili kuridhia. Sekretarieti ya muda(Interim ZAMCOM Secretariat) inayoratibu shughuli zaZAMCOM, ilianza kazi rasmi tarehe 6 Mei, 2011. Sekretarietihiyo imeongezewa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe1 Januari hadi 31 Desemba, 2013 ikiwa na jukumu lakushirikiana na nchi wanachama kukamilisha uundaji wachombo cha kudumu. Jukumu jingine ni kuandaa mikakati

Page 58: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

58

na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya usimamizi nauendelezaji wa rasilimali za maji za Bonde la Mto Zambeziiliyokubaliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Majiwa SADC vilivyopita. Katika mwaka 2013/2014, Wizara yanguitaendelea kushirikiana na Sekretarieti ya ZAMCOM katikakuratibu kazi za Kamisheni hiyo hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bonde la Mto Ruvuma naPwani ya Kusini kupitia Mradi wa Majishiriki unaoratibiwa naSADC, lilitengewa jumla ya Dola za Kimarekani 800,000mwaka 2012 kwa ajili ya kutekeleza miradi sita ya kijamii.Utekelezaji wa miradi hiyo ulianza mwezi Desemba, 2012 nautakamilika mwezi Juni 2013. Miradi hiyo inatekelezwa katikaWilaya tano za Mikoa ya Mtwara na Ruvuma ambazo niSongea Vijijini, Tunduru, Tandahimba, Nanyumbu na Mbinga.Fedha za kutekeleza miradi hiyo ni msaada kutoka Benki yaMaendeleo ya Afrika kupitia Sekretarieti ya SADC.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,miradi miwili ya kijamii imeendelea kutekelezwa katika Wilayaya Tunduru ambapo jumla ya miche ya miti 3,844 imepandwakatika Vijiji vya Daraja Mbili, Nandembo, Lelolelo na Majimajikwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kutunza vyanzovya maji. Vilevile, katika skimu ya umwagiliaji ya Namatuhiiliyoko Wilaya ya Songea Vijijini, ujenzi wa miundombinu yaumwagiliaji ikiwa ni pamoja na mfereji wenye urefu wa mita2,000 imekamilika. Aidha, uchimbaji wa kisima kirefu cha mita150 kwa ajili mradi wa usambazaji wa maji katika kijiji chaMihambwe, Wilaya ya Tandahimba unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, kisima chenye urefuwa mita 60 kimechimbwa kwa ajili ya mradi wa kusambazamaji katika mji wa Mangaka ambao ni makao makuu yaWilaya ya Nanyumbu. Utekelezaji wa mradi wa kusambazamaji katika kijiji cha Mahande, Wilaya ya Mbinga umefikiaasilimia 18. Kazi zilizofanyika ni ujenzi wa matanki mawili yamaji yenye lita 10,000 kila moja; matanki mengine mawiliyenye lita 25,000 kila moja na vituo 18 vya kuchotea maji.Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu itaendelea

Page 59: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

59

kushirikiana na SADC pamoja na Serikali ya Msumbijikukamilisha miradi ya pamoja katika Bonde hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, bonde la Mto Songwe.Serikali za Tanzania na Malawi zinatekeleza kwa pamojaProgramu ya Kuendeleza Rasilimali za Bonde la Mto Songwe.Utekelezaji wa Programu hiyo upo katika awamu tatu.Awamu ya kwanza ilihusu upembuzi yakinifu na ilikamilikamwaka 2003. Hivi sasa, utekelezaji wa awamu ya pili yaProgramu hiyo unaendelea, ambayo ni usanifu wa kina wamiundombinu ya rasilimali za maji itakayojengwa kwa ajiliya kuzalisha umeme, kilimo cha umwagiliaji na kuzuiamafuriko.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,Wizara yangu imeendelea na shughuli za kuratibu utekelezajiwa awamu ya pili ya Mradi, pamoja na kutekeleza majukumuya Tanzania kama yalivyo kwenye Hati za Makubaliano katiya Tanzania na Malawi. Wizara yangu imemwajiri Mratibu waMradi (National Project Coordinator) kutoka Tanzaniaambaye atasimamia maslahi ya Tanzania kwenye Mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, wataalam wenginewa kada tofauti wamepelekwa kwenye mradi. Mtaalammshauri ameanza kazi mwezi Machi, 2013. Kazizitakazofanyika ni pamoja na kuandaa dira ya maendeleoya programu katika bonde kati ya sasa na mwaka 2050;usanifu wa kina wa miradi ya kipaumbele katika bonde;kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii kuhusumiradi itakayosanifiwa; kuandaa mpango wa kuanzishaKamisheni ya pamoja ya kusimamia programu na kujengauwezo kwa watekelezaji wa programu katika ngazi yahalmashauri hadi Taifa. Katika mwaka 2013/2014, Wizarayangu itaendelea kushirikiana na nchi ya Malawi kuratibuutekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo. Vilevile, Wizaraitaongeza wataalam wengine kutoka Wizara zinazohusikana mradi ili kuweza kushiriki tangu hatua ya awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ziwa Tanganyika. Serikaliya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilimwajiri mshauri

Page 60: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

60

mwelekezi mwaka 2011 ili afanye tafiti ya athari za kijamii namazingira (Environmental and Social Impact Assessment), tafitiya kihaidrolojia (Hydrology Study) na usanifu wa michoro yakihandisi (Engineering Designs) ili kujenga banio la Mto Lukugaambalo lilikuwa limebomoka. Mshauri mwelekezi aliwasilishataarifa za awali za utafiti huo katika kikao cha wataalamkutoka nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika mweziNovemba 2011, na alitarajiwa kuikamilisha kazi hiyo mweziNovemba, 2012. Wizara yangu inaendelea kuwasiliana naSerikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kupata rasimuya mwisho ya taarifa ya Mshauri mwelekezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya ZiwaTanganyika, nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo na Zambia pamoja na Washirika wa Maendeleo ilikuendeleza juhudi za hifadhi ya Bonde la Maji la ZiwaTanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ziwa Chala, Ziwa Jipe naMto Umba. Serikali za Tanzania na Kenya zimesaini Hati yaMakubaliano (MoU) tarehe 14 Februari, 2013 kuhusu utunzajina uendelezaji wa ikolojia ya Maziwa ya Chala na Jipe; naMto Umba. Hati hiyo imeweka misingi ya ushirikiano katikakusimamia na kuendeleza rasilimali zilizopo katika maeneohayo ili matumizi yake yawe endelevu ikiwa ni pamoja nakulinda mifumo ya ikolojia. Chini ya makubaliano hayo, Bodiya Maji ya Bonde la Pangani, Halmashauri husika, jumuiya zawatumiaji maji, na taasisi zisizo za Kiserikali zilizopo katikabonde hilo zitaimarishwa na taasisi mpya zitaanzishwakulingana na mahitaji. Nchi hizo kwa kushirikiana naKamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria zimeandaa andiko lamradi kuhusu athari za uharibifu wa mazingira ya Bonde laZiwa Chala na Jipe pamoja na Mto Umba na jinsi ya kuzitatua.Andiko hilo pia linaelezea mfumo wa uongozi wa pamojawa kusimamia rasil imali hizo. Baadhi ya maeneoyaliyoainishwa katika andiko na ambayo yataanzakutekelezwa katika mwaka 2013/2014 ni pamoja na uondoajiwa magugu maji ambayo yamekithiri hasa katika Ziwa Jipena ufuatiliaji wa wingi na ubora wa maji.

Page 61: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

61

Mheshimiwa Naibu Spika, ubora na usafi wa maji.Mojawapo ya majukumu ya Wizara yangu ni kuhakiki uborana usafi wa maji katika vyanzo vya maji kwa lengo la kulindaafya za wananchi. Katika kutekeleza jukumu hilo, maabaraza maji zimeimarishwa kwa kupatiwa vifaa na madawa yauchunguzi wa ubora wa maji. Vifaa na madawa hayoyameongeza tija ya upatikanaji wa takwimu za ubora wamaji kwa ajili ya kutoa maamuzi sahihi ya kujenga nakuendeleza miradi ya maji. Katika mwaka 2012/2013, Wizarailipanga kukagua vyanzo vya maji kwa kuchunguza sampuli8,000 za maji ili kuhakiki ubora wake na sampuli 1,000 zamajitaka zilipangwa kuchunguzwa ubora wake ili kudhibitiuchafuzi wa vyanzo vya maji, kupunguza gharama zakusafisha na kutibu maji kwa matumizi mbalimbali pamojana kuhifadhi mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Machi,2013, sampuli 3,957 kati ya sampuli 8,000 zilikusanywa kutokakatika visima, mitandao ya usambazaji maji na udhibiti wavyanzo vya maji na kuhakikiwa ubora wake. Kati ya hizo,sampuli 1,861 sawa na asilimia 91.5 ya sampuli 2,034 kutokakwenye visima, zilionesha kuwa maji yake yanakidhi viwangovinavyokubalika kitaifa. Sampuli 173 maji yake hayakukidhiviwango kwa sababu ya kuwa na chumvi, wingi wa madiniya Nitrate na Fluoride. Ushauri ulitolewa kutafuta vyanzombadala kukidhi mahitaji na kutumia teknolojia ya mifupaya ngombe ili kuondoa madini ya fluoride kwenye maji yakunywa na kupikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji yanayosambazwa Mijiniyalihakikiwa ubora wake kwa kukusanya sampuli 1,666kutoka kwenye mtandao wa kusambaza maji kwenye Mijiya Tanga, Mbeya, Mwanza, Babati, Mbinga, Iringa, Shinyanga,Singida, Musoma, Sumbawanga, Dodoma, Bukoba, Lindi,Mtwara, Nzega na Katesh na kufanyiwa uchunguzi wakemikali na uwepo wa vimelea vya vijidudu. Kati ya hizo,sampuli 1,626, sawa na asilimia 97.6, maji yake yalikidhiviwango na sampuli 40 maji yake yalionesha uwepo wavimelea vya vijidudu. Hivyo, Mamlaka za Maji Miji nizilielekezwa kukagua mitambo ya kusafisha maji mara kwa

Page 62: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

62

mara na kuweka kiwango sahihi cha dawa ya kutibu majikabla ya kuyasambaza kwa watumiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sampuli 178 za majiyanayotumika kusindika minofu ya samaki viwandani katikaMiji ya Mwanza, Bukoba, Dar es Salaam na Musomazilifanyiwa uchunguzi wa uwepo wa vimelea vya vijidudu.Matokeo yalionesha maji hayo yanakidhi viwangovinavyokubalika kimataifa na samaki wanakuwa na uborawa kusafirishwa nchi za nje. Aidha, sampuli 79, kutoka kwenyemito na Maziwa katika mabonde ya Ziwa Victoria,Tanganyika, Wami/Ruvu, Rufiji na Ruvuma zilikusanywa nakuchunguzwa ubora wake. Matokeo yalionesha maji hayokuwa na ubora unaokubalika na takwimu hizo zinatumikawakati wa kutoa vibali vya kutumia maji na kusimamiautunzaji wa vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kudhibiti Uchafuzi waMazingira. Sampuli 410 za majitaka kutoka viwandani namabwawa ya majitaka kwenye Miji ya Dodoma, Morogoro,Mwanza, Dar es Salaam, Tanga, Musoma, Bukoba na Iringazilikusanywa na kuchunguzwa ubora wake. Kati ya hizo,sampuli 320, sawa na asilimia 81.7, zilikidhi viwango vyamajitaka kumwagwa kwenye mazingira na sampuli 70hazikukidhi viwango; hivyo ushauri ulitolewa kuboreshamabwawa au mitambo ya kusafisha majitaka ili yafikieviwango vinavyokubalika kabla ya kurudishwa kwenyemazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara yangu itaimarisha usimamizi wa utekelezaji washughuli za ubora wa maji kwa kuratibu ubora kwenye vyanzovinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani, viwanda, kilimona mazingira; ambapo sampuli 8,000 za maji na sampuli 1,000za majitaka zitakusanywa na kuchunguzwa. Usimamizi huoni pamoja na kutekeleza Mkakati wa Kusimamia Ubora waMaji na Kudhibiti Uchafuzi wa Maji (Water QualityManagement and Pollution Control Strategy) unaoelekezakuratibu madini tembo (heavy metals) aina ya Zebaki(Mercury), Arsenic, Urani (Uranium) na Cyanide katika vyanzo

Page 63: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

63

vya maji kwenye maeneo yenye shughuli za migodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ubora wa Madawa yaKusafisha na Kutibu Maji. Maji yanayosambazwa kwawananchi yanapaswa kusafishwa na kutibiwa ili yawe katikaviwango vinavyokubalika, hivyo madawa yanayotumikayanatakiwa kuhakikiwa ubora wake. Katika mwaka 2012/2013, jumla ya sampuli 50 za madawa ya kusafisha na kutibumaji kutoka DAWASCO, Mamlaka za Maji za Iringa, Morogoro,Tanga na kampuni binafsi zilihakikiwa ubora wake. Kati yasampuli hizo, 14 ni shabu (Aluminium Sulphate), 14Polyaluminium Chloride ambazo hutumika kusafisha maji; na22 Calcium Hypochlorite ambayo hutumika kuua vijidudu.Matokeo yalionesha kuwa madawa hayo yalikuwa naviwango vinavyokubalika na ushauri wa kitaalam ulitolewakuhusu matumizi yake sahihi. Katika mwaka 2013/2014,utaratibu wa kuhakiki madawa utaendelea ambapo sampuli60 za madawa ya kusafisha na kutibu maji zitahakikiwa, ikiwani pamoja na kukagua mitambo ya kusafisha na kutibu majikatika Mamlaka za Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, uondoaji wa Madini yaFluoride katika Maji. Serikali imeandaa mkakati wakusambaza teknolojia ya kutumia mkaa wa mifupa yang’ombe (bone char) kuondoa madini ya fluoride katika majiya kunywa na kupikia. Mkakati huo utaanza kutekelezwamwaka 2013/2014 na kazi zitakazofanyika ni pamoja nakuainisha mbinu za usambazaji wa teknolojia hiyo katikaukanda wa Bonde la Ufa na kutayarisha ramani (fluoridemapping) inayoonesha maeneo yenye kiwango kikubwa chafluoride katika maji ambayo itasaidia kuyatambua maeneohayo wakati wa kuainisha miradi ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Maabara za Maji kupataIthibati (Accreditation). Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufukwamba, mnamo mwezi Julai 2012, Maabara za Iringa,Mwanza na Maabara Kuu zilishiriki katika zoezi la kujipimauwezo chini ya mpango wa Southern Africa DevelopmentCommunity Measurement Traceability (SADCMET) ambalohuratibiwa na Shirika la Maji la Namibia (NAMWATER).

Page 64: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

64

Matokeo ya zoezi hilo, yaliyotolewa mwezi Oktoba, 2012yalionesha kuwa Maabara hizo zimeongeza uwezo wakekutoka asilimia 68 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 70.Kwa hatua hiyo, maabara hizo zinaweza kujisajili kwa taasisiinayotoa ithibati (SADCAS) kwa ajili ya kukamilisha taratibuza kupata ithibati.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkataba wa kutoa ushauriwa kiufundi kuhusu namna ya kuboresha maabara za majiili kupata ithibati, ambao utadumu kwa mwaka mmoja,ulisainiwa tarehe 19/09/2012. Hadi sasa, Mtaalam Mshauriamekagua maabara za Mwanza, Musoma, Bukoba,Shinyanga, Morogoro, Dodoma, Singida na Maabara Kuuiliyopo makao makuu ya Wizara kwa kuainisha mahitaji yampango mzima wa kupata ithibati. Mtaalam mshaurianaendelea kuandaa mwongozo wa ubora (QualityManual) na makabrasha mengine kulingana na viwangovya kimataifa katika upimaji wa kimaabara. Katika mwaka2013/2014, maabara ya Mwanza itapata ithibati; MaabaraKuu, Maabara za Iringa na Mbeya zitajisajili na kukaguliwakwa ajil i ya kukamilisha taratibu za kupata ithibati.Kupatikana kwa ithibati kwa Maabara hizo kutaziwezeshakutekeleza majukumu yake kwa kufuata kiwango chautendaji cha kimataifa (ISO 17025), hivyo takwimu na taarifaza ubora wa maji zitakuwa za kuaminika na kukubalika, naendapo kuna mivutano ya kisheria zitatumika kutatuamigogoro. Aidha, Maabara kupata ithibati ni matakwa yaSheria ya Rasilimali za Maji ya mwaka 2009 na ya Mazingiraya mwaka 2004.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara yangu itakarabati Maabara Kuu na za Mikoa pamojana kupanua ofisi ili kuweka mazingira mazuri ya kazi nakukidhi matakwa ya kupata ithibati ambapo tathminihuanzia kwenye majengo. Aidha, Maabara zitaimarishwana kujengewa uwezo kwa kununua samani, vifaa vyamaabara na madawa na watumishi kupatiwa mafunzo ilikuongeza ufanisi na tija katika usimamizi wa ubora wa maji.Vilevile ili kusogeza huduma za ubora wa maji karibu najamii mahitaji ya ujenzi wa maabara kwenye Mikoa ambayohaina huduma hiyo yataainishwa.

Page 65: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

65

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya maji na usafiwa mazingira Vijijini. Katika mwaka 2012/2013, Wizara yangukwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMItunasimamia utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi waMazingira Vijijini kulingana na mipango na vipaumbele vyakila Halmashauri. Programu inahusu kujenga miradi ya majikwenye Vijiji 10 kwa kila Halmashauri, kukarabati na kupanuamiradi ya maji, kujenga uwezo wa watekelezaji waprogramu, kuhamasisha wananchi kuhusu usafi binafsi nausafi wa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, uboreshaji wa Huduma zaMaji Vij i j ini. Mradi wa maji kwenye Vij i j i 10 kwa kilaHalmashauri. Katika mwaka 2012/2013, Serikali imezipatiaHalmashauri shilingi bilioni 98.4 kwa ajili ya kutekeleza miradiya maji kwenye Vijiji 10 kwa kila Halmashauri. Pia, shilingimilioni 279.6 zilitumwa kwenye Sekretarieti za Mikoa kwa ajiliya kufuatilia utekelezaji na kutoa ushauri wa kitaalam kwaHalmashauri. Aidha, shilingi bilioni 9.85 za Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji zimetumwa kwa Watekelezajiwa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Utekelezaji waMiradi ya Maji katika Vijiji 10 kwa kila Halmashauri. Katikamwaka 2012/2013 jumla ya Vij i j i 682 vinajengewamiundombinu ya kusambaza maji, hii ikiwa ni wastani waVijiji vitano kati ya Vijiji kumi vilivyopangwa kujengewamiundombinu ya maji kwa kila Halmashauri. Ujenzi wa miradiya maji katika Vijiji hivyo kwa kutumia fedha zilizotumwa naSerikali kwenye Halmashauri katika kipindi cha 2012/2013unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2013, ambapojumla ya wananchi milioni 1.7 wanaoishi Vijijini watafaidikana huduma hiyo ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nililieleza Bunge lako Tukufukatika kuomba fedha za mwaka 2012/2013 kuwa, miradi hiyoingekamilika ifikapo mwezi Juni 2013. Hata hivyo, kukamilikakwa miradi hiyo ya kwanza ya Vijiji vitano kumechelewakutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa fedha. Hadikufikia mwezi Machi 2013 fedha za ndani zil izokuwa

Page 66: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

66

zimetolewa ni shilingi bilioni 29 kati ya shilingi bilioni 140zilizokasimiwa katika wizara katika mwaka 2012/2013 sawana asilimia 20.7 tu. Kwa upande wa fedha za nje, shilingibilioni 55.4 zilipatikana na kutumwa kwenye Halmashaurimwezi Desemba 2012 lakini zilipokelewa mwezi Machi 2013.Kutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa fedha hizo,Halmashauri nyingi zimechukuwa muda kuwekeana saini nawakandarasi hata pale ambapo vibali vyotevimekwishatolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutekeleza Programu ya Maji na Usafi waMazingira Vijijini ambapo jumla ya shilingi bilioni 184.05zimetengwa. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 105.2zitatumiwa na Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa miradi yamaji kwenye Vijiji 480 kwa lengo la kukamilisha wastani waVijiji vitatu kwa kila Halmashauri ambapo wananchi milioni1.2 watapata huduma ya maji. Naomba kutumia nafasi hiikuzihimiza Halmashauri kusimamia kwa karibu Wakandarasina Wataalam washauri wanaojenga na kusimamia ujenziwa miradi hiyo ili kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwakwa wakati na kwa ubora unaotakiwa “Value for money”.Aidha, shilingi bilioni 75.45 zimekasimiwa katika Fungu laWizara ya Maji kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji Vijijini,ujenzi wa mabwawa, uchimbaji wa visima na kujenga uwezokatika ngazi zote za utekelezaji. Shilingi bilioni 108.6zimekasimiwa kupitia mafungu ya Mikoa kwa ajili yaHalmashauri, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na Wizarazinazoshiriki katika kutekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Usafi waMazingira Vijijini. Kati ya hizo, kiasi cha shilingi milioni 300zitatumiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kwa ajili ya uratibuna ufuatiliaji, shilingi bilioni 1.2 zitatumiwa na ofisi zaSekretarieti za Mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji na tathmini, shilingibilioni 12.208 zitatumika kwenye utekelezaji wa Kampeni yaKitaifa ya Usafi wa Mazingira kupitia Wizara ya Afya na Ustawiwa Jamii na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa lengo la kuepukamigogoro ya kimikataba na kuharakisha utekelezaji wamiradi ya maji katika Vijiji 5 kwa kila Halmashauri, Halmashauri

Page 67: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

67

zote zimetengewa fedha za utekelezaji wa miradi ya majikwenye Halmashauri zao ikiwa ni pamoja na miradi iliyopokwenye Halmashauri zilizoanzishwa hivi karibuni. Hii ni kwasababu Halmashauri hizo zina mikataba na WataalamWashauri na Wakandarasi wanaojenga miradi hiyo. Hatahivyo, Halmashauri mpya zitawezeshwa katika ufuatiliaji wautekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao. Kwa miradi yamaji ambayo haijaanza kujengwa na ipo kwenyeHalmashauri mpya zilizoanzishwa, fedha za utekelezaji wamiradi hiyo zitatumwa kwenye Halmashauri mpya.Halmashauri hizo zitaingia mikataba na wakandarasiwatakaoteuliwa kutekeleza miradi hiyo. Halmashauri mpyazitapatiwa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji kuanziamwaka 2013/2014. Wizara itaendelea kushirikiana na Ofisi yaWaziri Mkuu-TAMISEMI katika kujenga uwezo wa Halmashaurina Sekretarieti za Mikoa ili kuharakisha utekelezaji waProgramu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu iliendeleakushirikiana na Halmashauri kwa kuzipatia fedha na kutoaushauri wa kiufundi kwa ajili ya utekelezaji wa miradimbalimbali ya maji Vijijini. Katika mwaka wa 2013/2014,Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Halmashauri husikakwa kuzipatia fedha na ushauri wa kiufundi katika kutekelezamiradi ya maji. Wananchi 563,679 watanufaika na hudumaya maji miradi hiyo itakapokamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Wilayaza Moshi Vijijini na Hai. Mradi wa maji katika Wilaya ya MoshiVijijini unahusisha miradi ya maji ya Kirua-Kahe na Mji Mdogowa Himo. Mradi wa Kirua-Kahe ulianza kutekelezwa mweziAprili 2007 ukiwa na lengo la kuwahudumia wakazi 110,000katika Vijiji 32. Mradi huu umekamilika mwezi Desemba, 2012.Katika Mji Mdogo wa Himo, ukarabati wa matanki mawiliya maji unaendelea na ufungaji wa mabomba yenye urefuwa mita 684 umefanyika. Mradi utakamilika mwaka 2013/2014 baada ya kukamilisha ujenzi wa mtandao wakusambaza maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,

Page 68: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

68

Wizara yangu kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo yaUjerumani (KfW) na Umoja wa Ulaya (EU) iliendelea nautekelezaji wa Mradi wa maji katika Wilaya za Hai na Siha.Ujenzi wa mradi huo umekamilika mwezi Desemba, 2012baada ya kukamilisha skimu ya North West Kilimanjaro.Wananchi wapatao 5,000 wanapata huduma ya maji kutokaskimu hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Masoko.Mradi wa Maji Masoko katika Wilaya ya Rungwe ulianzakujengwa mwezi Septemba 2010. Lengo la mradi lilikuwa nikujenga banio (intake) la maji la Mbaka na Kigange, kujengachujio eneo la Kigange, kujenga matanki matatu ya kuhifadhimaji, kujenga beseni la kuchuja maji (sedimentation tank),kujenga chujio kubwa la maji (treatment plant), kujenga tankila maji yanayorudi (backwater tank), ununuzi na ufungaji wamabomba na ujenzi wa vituo 122 vya kuchotea maji. Mradiukikamilika utanufaisha wakazi wa Vijiji 15.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Machi 2013,ujenzi wa mabanio (intakes) ya maji ya Mbaka na Kigangeulikuwa umekamilika, uchimbaji wa mtaro kutoka kwenyebanio la Kigange kwenda kwenye tanki la kutuamisha topekwenye maji (sedimentation tank) umekamilika na mabombatayari yamelazwa na msingi wa chujio la maji (treatmentplant) umechimbwa. Ujenzi wa matanki manne katika Vijijivya Masoko, Lufumbi, Bulongwe na Kigange yako katikahatua mbalimbali ya utekelezaji. Halmashauri imevunjamkataba na mkandarasi baada ya Mkandarasi kujengabaadhi ya miundombinu ya maji chini ya kiwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji katika Chuocha Nelson Mandela. Mradi wa maji katika Chuo cha NelsonMandela uliopo Wilaya ya Arumeru ulianza kutekelezwamwaka 2009. Lengo la mradi ilikuwa ni kuchimba visimaviwili, kujenga nyumba ya mitambo na kulaza mabombakatika maeneo ya chuo hicho. Hadi kufikia Machi 2013 visimaviwili vimechimbwa na matanki mawili yamejengwa. Katikamwaka wa 2013/2014 nyumba ya mtambo wa kusukumiamaji utajengwa, mabomba yatalazwa na mradiutakamilishwa.

Page 69: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

69

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Kidete. Mradiwa maji Kidete uliopo katika Wilaya ya Kilosa ulianzakujengwa mwezi Septemba 2010. Kazi zi l izopangwakutekelezwa katika mradi huo unaohusu ujenzi wa bwawani uchimbaji wa utoro wa maji, uchimbaji wa msingi wa tuta,kulaza na kushindilia udongo kwenye msingi wa tuta, ujenziwa miundombinu ya kutolea maji kwenye bwawa, ujenzi wacrest weir kwenye utoro wa maji na upangaji wa mawekwenye upande wa ndani wa tuta.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Machi 2013,utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 75, ambapokazi ya kuhamasisha wananchi imefanyika, ujenzi wa tuta labwawa umekamilika. Mradi unatarajia kuhudumia wananchiwapatao 15,000 katika Vijiji vitano. Katika kipindi cha mwaka2013/2014, kazi zitakazofanyika ni kukamilisha ujenzi wabwawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Same –Mwanga – Korogwe. Mradi wa Same-Mwanga-Korogweulibuniwa mwaka 2006/2007 ukiwa na lengo la kupeleka majikatika Miji ya Same na Mwanga ambayo ina shida kubwasana ya maji. Aidha, katika mwaka 2012/2013, Serikali kwakushirikiana na BADEA na OFID inaendelea na maandalizi yamradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe. MtaalamMshauri amekamilisha kupitia usanifu wa mradi kuanziachanzo cha maji hadi katika tanki kuu la kuhifadhia maji.Hivi sasa anaendelea kusanifu mfumo wa kutoa maji kutokatanki kuu hadi Miji ya Same na Mwanga. Mradiutakapokamilika utahudumia wananchi 122,000 kwenye Vijiji38 vilivyoko katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwepamoja na Miji ya Same na Mwanga. Ujenzi wa mradiutaanza mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Bungu. Mradiwa maji Bungu upo katika Wilaya ya Korogwe. Mradi huuunalenga kuhudumia Vijiji saba ambavyo ni Bungu, BunguMsiga, Kwamshai, Ngulu, Mlungui, Msasa na Manka. Kaziambazo zimepangwa kufanyika ni ukarabati ambapo ulazajiwa bomba kilomita 1.5, ujenzi wa matanki mawili kila moja

Page 70: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

70

lenye lita 90,000, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 54 naulazaji wa bomba za usambaji urefu wa kilomita 26.8utafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi Machi 2013, kazizilizofanyika ni ujenzi wa mtandao wa maji wenye urefu wamita 5,994, vituo vya kuchotea maji 15 umekamilika, tanki lakuhifadhi maji lenye lita 90,000 umekamilika katika kitongojicha Gare. Mradi utakapokamilia wananchi 2,883 watapatahuduma ya maji. Katika kipindi cha mwaka 2013/2014 kazizilizobaki za ujenzi wa mradi zitakamilishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Vijijini katikaMkoa wa Tabora. Wizara yangu kwa kushirikiana na Serikaliya Japan inatekeleza mradi wa maji Vijijini katika Mkoa waTabora. Mradi huo ulilenga kuwapatia huduma ya majiwananchi wapatao 41,744 katika Vijiji 20 vya Mkoa huo.Kutokana na maafa ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japanmwezi Machi, 2011, utekelezaji wa mradi ulisimama kwamuda. Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa mweziFebruari, 2013, Serikali ya Japan iliridhia kuendelea nautekelezaji wa mradi huo. Katika mwaka 2013/2014, utafitina usanifu wa kina katika maeneo yaliyoonesha kuwa namaji ya kutosha utafanyika na ujenzi utaanza. Utekelezajiunatarajiwa kuchukua miaka mitatu. Vijiji vilivyolengwakupata maji kupitia mradi huo ni Busomeke na Kalemela(Igunga); Isanga, Kitangili, Makomelo na Wela (Nzega);Kasandalala, Usunga na Mpombwe (Sikonge); Mabama,Ufuluma na Mpumbuli (Tabora/Uyui); Kakola, Misha na Uyui(Manispaa ya Tabora) na Imalamakoye, Kalembela, Kilolelina Nsungwa (Urambo).

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji kwa Vijiji 100kando ya Bomba Kuu la Ziwa Victoria. Katika mwaka 2013/2014, Wizara itaanza maandalizi na utekelezaji wa kuvipatiahuduma ya maji Vijiji 100 vilivyo kandokando ya bomba kuula mradi wa Kahama Shinyanga ndani ya kilomita 12 katikaWilaya za Mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Lengo ni kuongezaidadi ya wananchi wa kunufaika na mradi huo. Mradi huoutatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani. Ili kuharakisha

Page 71: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

71

utekelezaji, kazi ya kusanifu miundombinu ya kusambaza majikatika Vijiji itatekelezwa na Wataalam wa Halmashauri zaWilaya husika na kuratibiwa na Wizara kwa kushirikiana naMamlaka ya Maji Kahama/Shinyanga (Kahama ShinyangaWater Supply Authority) KASHWASA. Ujenzi utatekelezwa nawakandarasi watakaoajiriwa na Mamlaka ya Maji ya Mradiwa Kahama na Shinyanga (KASHWASA). Katika kipindi chamwaka 2013/2014, usanifu wa miradi utafanyika katikaHalmashauri husika na ujenzi utaanza. Vijiji vitakavyohusikana mradi huo viko katika Jedwali Na. 15.1. Mradi huoutakapokamilika utawanufaisha wananchi zaidi ya 308,738.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Miradi Mingine yaMaji Vijijini. Katika mwaka 2012/2013, Serikali imeendeleakushirikiana na taasisi mbalimbali kujenga miradi ya majiVijijini kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ambavyo havipokatika bajeti ya Wizara yangu. Juhudi hizo zinachangia kwakiasi kikubwa katika kuinua kiwango cha upatikanaji wahuduma ya maji Vijijini. Katika mwaka 2013/2014, Serikaliitaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali katika ujenziwa miradi ya maji Vijijini ili kuongeza upatikanaji wa hudumahiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uvunaji wa Maji ya Mvua.Serikali inaendelea kuhamasisha na kuhimiza jamii kuhusuuvunaji wa maji ya mvua kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamojana kila Halmashauri za Wilaya kuandaa mpango wa miakamitano. Halmashauri zote zimeagizwa kutunga sheria ndogozinazohakikisha kuwa michoro ya nyumba zote zinazojengwazinajumuisha mifumo ya miundombinu ya kuvuna maji ya mvuakabla ya kuidhinishwa ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ambazozimetekeleza agizo hilo ni Jiji la Tanga, Manispaa za Iringa,Arusha, Tabora, Halmashauri za Monduli, Meru, Moshi, Mtwara,Newala, Nanyumbu, Tandahimba, Rombo, Hai na Siha. Katikamwaka 2013/2014, kupitia mradi wa Vijiji 10 kwa kilaHalmashauri, matanki na mifumo ya kuvuna maji ya mvuakupitia mapaa ya nyumba yataendelea kujengwa katika Vijijiviwili kwa kila Halmashauri husika ili wananchi waone na

Page 72: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

72

kujifunza. Mafunzo pia yatatolewa kwa mafundi katika kila kijiji.Aidha, taasisi za umma na binafsi zimejenga matanki ya kuvunamaji ya mvua kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini. Takwimukuhusu idadi ya matanki ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwakwa kila Mkoa na Halmashauri zinakusanywa ili kuwezeshakufuatilia utekelezaji wa sheria iliyowekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Kuainisha Vituo vyaKuchotea Maji. Wizara yangu imeendelea na mradi wakuainisha vituo vya kuchotea maji Vijijini kwa lengo la kupatatakwimu sahihi zinazohusiana na huduma ya maji Vijijini kwakutumia mfumo wa kompyuta. Taarifa zitakazopatikana naufahamu wa mtandao wa vituo vya kuchotea majizitawezesha Halmashauri kufahamu upatikanaji wa majikatika Vijiji na kata, pia kuwezesha kupanga vipaumbele.Taarifa hizo pia zitasaidia katika ufuatiliaji wa uendelevu wamiradi ya maji nchini. Hadi kufikia mwezi Februari, 2013takwimu za vituo 65,421 vya kuchotea maji katikaHalmashauri 143 zimekusanywa. Kazi hiyo itakamilishwa katikamwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uundaji na Usajili wa Vyombovya Watumiaji Maji. Uundaji na usajili wa vyombo vyawatumiaji maji ni mkakati wa kuisaidia miradi ya maji kuwaendelevu. Hadi kufikia mwezi Machi 2013, idadi ya vyombovya watumiaji maji vilivyoundwa na kusajiliwa kwa Sheriaya Maji na Usafi wa Mazingira Namba 12 ya mwaka 2009jumla yake ni 147 kwa mchanganuo ufuatao kiMkoa: Arusha(4), Iringa (3), Mbeya (4), Dodoma (2), Ruvuma (3), Kilimanjaro(28), Kagera (45), Lindi (10), Morogoro (7), Singida (11), Kigoma(10), Mwanza (15) na Rukwa (4). Aidha, Halmashauri zilizonyingi ziko katika hatua mbalimbali za maandalizi ya usajiriwa vyombo vya watumiaji maji kwa kutumia Sheria ya Majina Usafi wa Mazingira Namba 12 ya mwaka 2009.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2010/2011,Wizara yangu ilitoa mwongozo wa uundaji na usajili wavyombo vya watumiaji maji, kwa mujibu wa kanuniinayohusu Usajili wa Vyombo vya Watumiaji Maji [The WaterSupply and Sanitation (Registration of Community Owned

Page 73: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

73

Water Supply Organisations) Regulations, 2009, GN. No. 21 of22/01/2010]. Hadi sasa Halmashauri zote zimeteua Wasajiliwa vyombo vya watumiaji maji. Napenda kuchukua fursahii kuwaomba Wasajili kuharakisha zoezi la uundaji na usajiliwa vyombo huru vya kuendesha na kusimamia miradi yamaji. Hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuifanya miradiya maji kuwa endelevu kwa kuwa itasimamiwa nakuendeshwa na wananchi wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ujenzi wa Mabwawa. Katikamwaka 2012/2013, Wizara yangu ilipanga kukamilisha ujenziwa mabwawa matano ya Kawa (Nkasi), Sasaji la(Chamwino), Mwanjoro (Meatu), Iguluba (Iringa Vijijini) naIngondin (Longido). Ujenzi wa bwawa la Ingondinumekamilika kwa asilimia 100 baada ya kuimarisha utoro wamaji uliokuwa umeathiriwa na mvua. Ujenzi wa bwawa laIguluba umekamilika kwa asil imia 75, mkandarasianaendelea kukamilisha kazi zilizobaki kwenye utoro wa majina makinga mchanga. Matarajio ya Wizara ni kuwamabwawa hayo yatakamilika katika kipindi kilichobaki chamwaka 2012/2013 isipokuwa kwa bwawa la Sasajila ambalohalina mkandarasi kwa sasa baada ya mkandarasialiyekuwepo kushindwa kukamilisha kazi. Wizara inategemeakusaini mkataba na Mkandarasi mwingine baada yakukamilisha taratibu za manunuzi ya mkandarasi huyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara iliendelea kuratibuupatikanaji wa fedha za ujenzi wa bwawa la Kidetelinalosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambaloujenzi wake umefikia asilimia 75. Katika mwaka 2013/2014,ujenzi wa mabwawa ya Seke Ididi (Kishapu), Habiya (Bariadi)na Matwiga (Chunya) ambao ulisimama kutokana nawakandarasi wake kushindwa kazi na kuondoka maeneoya kazi, utaendelea kwa kutumia wakandarasi wapya nakwa kadri fedha zitakavyopatikana. Kufuatia tathminiiliyofanywa na Wizara ya Maji, marekebisho yatafanywakwenye Bwawa la Wegero ili kudhibiti utoro wa maji nakuongeza wingi wa maji. Ujenzi wa mabwawa madogoutatekelezwa na Halmashauri kulingana na vipaumbelevyake, ambapo Wizara yangu itatoa ushauri wa kiufundiutakaohitajika katika ujenzi huo.

Page 74: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

74

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango Maalum wa KuletaMatokeo ya Haraka. Serikali imechagua Sekta 6 za awaliambazo zitaanza utekelezaji wa mpango maalumulioandaliwa wa “Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa”(Big Results Now Program). Mpango huo utatekelezwa kwakipindi cha miaka mitatu kuanzia 2013/2014-2015/2016, Sektaya Maji ni miongoni mwa sekta hizo zilizopewa kipaumbeleambapo mpango huo unalenga kuongeza upatikanaji wahuduma ya maji maeneo ya Vijijini. Hii ni kutokana na ukwelikwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanaoishi Vijijinihawapati huduma ya maji ipasavyo kutokana na miradimingi i l iyopo kuchakaa, usimamizi duni, wananchikutokuchangia gharama za uendeshaji ipasavyo, ukosefu wavipuli na uwekezaji mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi zilizoainishwa ambazozimepangwa kutekelezwa ni pamoja na:-

(a) Kuongeza idadi ya vituo vya kuchotea majikwa kupanua miundombinu iliyopo, kukarabati na kujengamiradi mipya. Jumla ya Miradi 1,810 inatarajiwa kutekelezwa;

(b) Kuboresha usimamizi wa miradi ya maji ngaziya jamii kwa kuunda na kuimarisha vyombo vya watumiamaji na kuweka mazingira mazuri ya uwajibikaji na usimamizi;na

(c) Kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vipulina kuweka utaratibu wenye ufanisi wa matengenezo yamiradi ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango huu utahitaji kiasi chashilingi Trilion 1.45 na utakapokamilika kutakua na ongezekola wananchi milioni 15.4 waishio Vijijini watakaopata hudumaya maji na hivyo kuongeza idadi ya wananchi wanaopatahuduma hiyo kutoka asilimia 57 za sasa hadi asilimia 75 ifikapomwaka 2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, Huduma ya Majisafi na Usafiwa Mazingira Mijini. Katika mwaka 2012/2013, Wizara kupitia

Page 75: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

75

Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini imeimarishautoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira. Kazizilizofanyika ni kukarabati, kujenga na kupanua mifumo yamajisafi na majitaka pamoja na kuzijengea uwezo mamlakaza maji za Dar es Salaam, Miji Mikuu ya Mikoa, Miji Mikuu yaWilaya, Miji Midogo na miradi ya kitaifa ya maji ili kuwapatiawananchi wengi zaidi huduma ya majisafi na usafi wamazingira katika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uboreshaji wa Huduma yaMajisafi na Usafi wa Mazingira Mijini. Miradi ya Maji KukidhiMahitaji ya Muda Mfupi. Katika mwaka 2012/2013, Serikaliilitekeleza mpango wa kukidhi mahitaji ya maji ya mudamfupi hadi 2015, kwa kujenga, kukarabati na kupanua vyanzovya maji; kuchimba visima, kupanua mitandao ya usambazajimaji; na kujenga matanki ya maji katika Miji ya Babati, Lindi,Sumbawanga na Mtwara. Wizara yangu ilikamilisha ujenzina kuzindua miradi ya maji katika Miji ya Babati mweziNovemba 2012 na Lindi mwezi Machi 2013. Miradi hiyoilizinduliwa na Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, hadi Machi2013, ujenzi katika mji wa Mtwara umefikia asilimia 98 naSumbawanga asilimia 80. Miradi hiyo itakapokamilika itakidhimahitaji ya muda mfupi kwa asilimia; Babati (85%), Lindi (80%),Mtwara (100%) na Sumbawanga (80%).

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi ya Maji Kukidhi Mahitajiya Muda wa Kati katika Miji Saba. Katika mwaka 2012/2013,Wizara yangu kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo laUfaransa (AFD); imeanza ujenzi wa miradi ili kukidhi mahitajiya maji ya muda wa kati katika Miji ya Bukoba na Musomakwa gharama ya shilingi bilioni 68.2. Kazi zitakazofanyika nikujenga mitambo ya kusafisha maji, mitambo ya kusukumamaji na kulaza mabomba ya maji katika Miji hiyo. Pia, Serikalikwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulayaimeanza utekelezaji wa miradi katika Miji ya Lindi, Kigomana Sumbawanga yenye gharama ya Euro milioni 62.59.Wakandarasi wameanza hatua za awali za ujenzi wa miradihiyo na wanatazamiwa kukamilisha kazi mwezi Aprili 2015.Vilevile, Serikali ya Ujerumani kupitia KfW itatoa Euro milioni

Page 76: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

76

8.72 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa majisafi na usafi wamazingira Babati na Mtwara chini ya programu ya MilleniumDevelopment Goal Initiative (MDGI-EU). Katika mwaka 2013/2014, utekelezaji wa miradi katika Miji hiyo utaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Tabora. Katikamwaka 2012/2013, Wizara yangu kwa kushirikiana na Serikaliya Uswisi kupitia Shirika lake la Maendeleo (SECO), iliendeleakutekeleza mradi wa kupanua na kukarabati mifumo yamajisafi katikati ya mji wa Tabora. Uboreshaji wamiundombinu ya uzalishaji katika bwawa la Igombe naupanuzi wa mfumo wa usambazaji majisafi umefikia asilimia80 na unatazamiwa kukamilika mwezi Juni 2013. Aidha,upanuzi wa chujio la maji katika bwawa hilo umeanza mweziMachi 2013 na utaendelea kutekelezwa katika mwaka 2013/2014, kwa kujenga mitambo ya kusafisha maji na kusukumamaji. Kukamilika kwa kazi hizo kutaongeza uzalishaji wa majikutoka lita milioni 15 hadi kufikia lita milioni 30 kwa siku,wakati mahitaji kwa sasa ni lita milioni 24.97 kwa siku; naitagharimu shilingi bilioni 7.5. Hatua hiyo itakidhi mahitaji yamaji katika Mji wa Tabora kwa asilimia 100 mpaka mwaka2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Mjini Dodoma.Katika mwaka 2012/2013, Serikali ilianza kutekeleza mradi wakuboresha huduma ya majisafi na majitaka ili kukidhi mahitajikatika Chuo Kikuu cha Dodoma; Mradi huo utajenga mfumowa uondoaji majitaka unaojumuisha mtandao wa kukusanyamajitaka wenye urefu wa kilomita 32 na mabwawa ya kutibiamajitaka. Kwa upande wa majisafi mradi utajenga kituo chakusukuma maji na matanki makubwa ya maji yenye ujazowa lita milioni 12 katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Kazizinazotekelezwa ni ulazaji wa bomba kuu la majisafi kilomita15.5, ulazaji wa mabomba ya kusambaza majisafi kilomita7.5. Gharama ya mradi huo ni shilingi bilioni 27.7. Katikamwaka 2013/2014, utekelezaji wa mradi huo utakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Tanzania kwakushirikiana na Serikali ya Korea Kusini inatekeleza mradi Seraya wa maji katika mji wa Dodoma utakaogharimu shilingi

Page 77: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

77

bilioni 49.62 ili kukidhi mahitaji ya muda wa kati. Mradi huoulianza kujengwa tarehe 15 Januari 2013 kwa kukarabativisima 21 na kuchimba visima vipya vitatu katika eneo laMzakwe. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wamtandao wa mabomba wenye urefu wa kilomita 6.5, ujenziwa barabara za visimani zenye urefu wa kilomita 5, ulazajiwa bomba jipya lenye kipenyo cha milimita 600 kutokaMzakwe hadi Mjini lenye urefu wa kilomita 31.2, ujenzi wamatanki mawili na ukarabati wa mitambo ya kusukumamaji. Vilevile, mradi huo utajenga booster station mpya eneola Mailimbili na kununua mitambo ya kisasa ya kutibu majipamoja na kujenga maabara ya kisasa ya kupima uborawa majisafi na majitaka. Mradi huo utatekelezwa katikakipindi cha miezi 24, hivyo unatazamiwa kukamilika mweziJanuari 2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na ongezekola kasi la watu katika mji wa Dodoma, Serikali imeanzausanifu wa Bwawa la Farkwa. Bwawa hilo litakuwa chanzocha maji kwa Manispaa ya Dodoma na Miji ya Kondoa,Chamwino na Bahi ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya majikatika Miji hiyo. Gharama za usanifu wa bwawa hilo ni Euro627,930 na shilingi 219,385,000. Usanifu huo utakaokamilikaAgosti 2013 utaonesha gharama halisi za ujenzi wa bwawahilo pamoja na kiwango cha maji kitakachopatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Mjini Singida.Katika mwaka 2012/2013, Serikali kwa kushirikiana na Benkiya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA) pamoja na Mfuko waMaendeleo wa Nchi Zinazozalisha Mafuta (OPEC Fund forInternational Development-OFID) iliendelea na ujenzi wamradi wa uboreshaji wa miundombinu ya majisafi mjiniSingida. Ujenzi huo unahusu uchimbaji wa visima virefu 10vya kuzalisha maji katika eneo la Mwankoko na Irao na ujenziwa miundombinu ya maji. Utekelezaji wa mradi umefikiaasilimia 98. Ujenzi wa matanki mawili katika maeneo yaAirport na kulaza bomba umekamilika na maji yamesukumwahadi kwenye matanki na kwenye mtandao wa maji kwaeneo la Mandewa. Mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 32.53,uliwekwa jiwe la msingi na Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho

Page 78: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

78

Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mweziNovemba 2012. Kukamilika kwa mradi huo kutaongezauzalishaji wa maji kufikia lita milioni 17.76 kwa siku na utakidhimahitaji ya mji huo kwa zaidi asilimia 100 kwa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji MorogoroMjini. Katika mwaka 2012/2013, Serikali kwa kushirikiana naShirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC),iliendelea na utekelezaji wa mradi wa kupanua na kuboreshaupatikanaji wa maji safi katika Manispaa ya Morogoro kwakukarabati matanki matatu na ulazaji wa bomba kuu la majila urefu wa kilomita 1.8 pamoja na kupanua chujio la majila Mafiga na kujenga mtambo wa kusafisha maji waMambogo. Gharama za utekelezaji wa mradi huo ni shilingibilioni 10. Utekelezaji hadi Machi 2013 umefikia asilimia 60.Ujenzi ukikamilika uzalishaji wa maji utaongezeka kutoka litamilioni 23 kwa siku hadi lita milioni 33 kwa siku na kuboreshaubora wa maji hivyo kupunguza mlipuko ya magonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji katika Jiji laMbeya. Katika mwaka 2012/2013, Wizara yangu kwakushirikiana na KfW na EU ilikamilisha kutekeleza awamu yapili ya Programu ya majisafi na majitaka katika Jiji la Mbeyakwa gharama ya Euro milioni 32.52. Mradi huo ulikamilikatarehe 21/12/2011 na kuzinduliwa na Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniamwezi Julai 2012. Kwa ujumla, mradi huo umeongeza haliya upatikanaji wa majisafi katika Jiji la Mbeya kutoka asilimia80 ya mwaka 2007 hadi asilimia 95.5 kwa sasa. Mradi huouna uwezo wa kutoa huduma ya majisafi kwa wakaziwapatao 490,000 na una uwezo wa kuzalisha maji kiasi chalita milioni 49 kwa siku. Aidha, maboresho yaliyofanyikakwenye Mradi wa majitaka yatawezesha kutoa huduma kwawakazi 57,000 kutoka wakazi 26,514 wa awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji katikaManispaa ya Iringa. Katika mwaka 2012/2013, Wizara yangukwa kushirikiana na KfW na EU ilikamilisha kutekeleza awamuya pili ya Programu ya majisafi na majitaka katika Manispaaya Iringa kwa gharama ya Euro milioni 23.2. Mradi huo

Page 79: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

79

unakidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wapatao 300,000.Kiwango cha upatikanaji maji kimeongezeka kutoka asilimia68 mwaka 2007 hadi asilimia 85 kwa sasa. Idadi ya watejawapya 1,760 waliunganishwa katika mtandao wa majisafina wateja 150 waliunganishwa katika mtandao wa majitaka.Changamoto iliyojitokeza baada ya kukamilika kwa mradihuo ni upotevu mkubwa wa maji kutokana na kuongezekakwa wingi wa maji katika mfumo wa usambazaji maji wazamani uliochakaa. Kazi za kukarabati mfumo wausambazaji maji wa zamani imefanyika ili kupunguza upotevuwa maji kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia 35 kwa sasa.Katika mwaka 2013/2014, Mamlaka itaendelea na jitihadaza kupunguza upotevu wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Songea Mjini.Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu itakarabati chanzocha mto Ruhira Mjini Songea kwa kujenga banio la maji (weir)ili kukabiliana na upungufu wa maji wakati wa kiangazi mjiniSongea. Lengo ni kutega maji na hivyo kuboresha upatikanajiwa maji katika mto huo. Matokeo ya kazi hiyo yataongezauhifadhi wa maji kutoka lita milioni 15 za sasa hadi kufikialita bilioni moja. Kazi hiyo itagharimu shilingi bilioni 2.6,ambapo mwaka 2013/2014, Serikali imetenga shilingi milioni400.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji katika Miji yaGeita, Sengerema na Nansio. Katika mwaka 2012/2013,Wizara iliendelea na awamu ya pili ya Mradi wa Maji na Usafiwa Mazingira wa Ziwa Victoria (LVWATSAN II). Mradi huounatekelezwa kwa pamoja na nchi za Jumuiya ya AfrikaMashariki kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB). Utekelezaji wa Programu hiyo kwa upande wa nchiyetu ni pamoja na kuboresha huduma ya maji na usafi wamazingira katika Miji ya Geita, Sengerema na Nansioambapo msimamizi wa Programu hiyo ni Mamlaka ya Majisafina Usafi wa Mazingira Mwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mhandisi Mshauri wa kusanifuna kusimamia kazi za ujenzi wa mradi huo alisaini mkatabamwezi Februari 2013. Usanifu utazingatia uwekezaji wa muda

Page 80: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

80

mfupi na muda mrefu ili kukidhi mahitaji ya maji katika Mijihiyo. Mradi wa maji Geita ukikamilika utahudumia wakazi68,500, sawa na asilimia 40. Kazi zitakazotekelezwa ni kulazamabomba ya usambazaji, kuunganisha umeme kwenyechanzo na kufunga dira za maji. Kazi hiyo itagharimu Dolaza Marekani milioni 4.2. Aidha, katika mwaka 2012/2013,Halmashauri ya mji wa Geita kwa kushirikiana na mgodi wamadini wa Geita (Geita Gold Mine – GGM) imekamilisha kaziya ujenzi wa chanzo, chujio la maji, bomba kuu na tankimoja. Mradi unatarajiwa kuzalisha lita milioni 4.8 za maji kwasiku, hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutokaasilimia 3.5 hadi asilimia 40; ambapo mahitaji ni lita milioni11.9 kwa siku. Katika mwaka 2013/2014, ujenzi wamiundombinu ya maji itakayoleta matokeo ya muda mfupiutaanza pamoja na usanifu wa uwekezaji wa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Sengerema,kazi zilizopangwa ni kujenga chanzo, mitambo ya kusafishamaji, mtandao wa kusambaza maji kilomita 25 na matankiya maji. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 14.Katika mji wa Nansio, kazi zilizopangwa ni kujenga mitamboya kusafisha maji, mtandao wa kusambaza maji kilomita 14na matanki ya maji saba ya ujazo mbalimbali. Gharama zamradi ni dola za Marekani milioni 6.9.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana naUN-HABITAT ilitekeleza programu ya LVWATSAN iliyohusishamiradi ya kuboresha huduma za maji na usafi wa mazingirakwa Miji ya Muleba, Mutukula na Chato. Mradi huo ambaoumegharimu dola za Marekani milioni 5, upo katika hatuaza mwisho za utekelezaji. Katika mwaka 2013/2014, Wizarayangu itachangia shilingi milioni 700 ili kukamilisha mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi Mipya katika eneo laZiwa Victoria. Katika mwaka 2013/2014, Serikali kwakushirikiana na AFD na European Investment Bank (EIB) itaanzautekelezaji wa miradi ya majisafi na usafi wa mazingira katikaJiji la Mwanza; vilevile, mradi huo utahusu uondoaji wamajitaka katika Manispaa za Bukoba na Musoma, pamojana mradi wa majisafi na usafi wa mazingira katika Miji ya

Page 81: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

81

Lamadi, Misungwi na Magu. Miradi hiyo itaongezaupatikanaji wa maji kutoka asilimia 35 hadi asilimia 90 kwamji wa Magu; kutoka asilimia 5 hadi asilimia 90 kwa Mji waLamadi na kutoka asilimia 45 hadi asilimia 90 kwa Mji waMisungwi. Mradi wa kuboresha usafi wa mazingira kwa Jiji laMwanza utahusisha kupanua mtandao wa majitaka kutokaasilimia 13 hadi asilimia 30; kuwa na vyoo bora kwa shulezote za Jiji na masoko; kuwa na mfumo mzuri wa uondoshajimajitaka ya wakazi wa milimani. Mradi wa majitaka kwamji wa Bukoba utahudumia asilimia 15; na mji wa Musomani asilimia 20 ya wakazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi ya Majisafi na Usafiwa Mazingira katika Miji inayozunguka Ziwa Tanganyika.Katika mwaka 2013/2014, Serikali kupitia Shirika la Umoja waMataifa la Makazi (UN-HABITAT) itaanza utekelezaji wa miradiya pamoja ya kuboresha huduma ya majisafi na usafi wamazingira katika Miji iliyopo kandokando ya Ziwa Tanganyika.Miji hiyo ni Kigoma, Kasulu, Mpanda na Namanyere. Fedhaza kutekeleza mpango huo ambao utaanza utekelezaji wakekatika mwaka 2013/2014 zinatoka COMESA na Jumuia yaAfrica Mashariki (EAC). Mpango huo utatekelezwa katika nchiza Kongo (DRC), Burundi, Rwanda, Zambia na Tanzania. Kazizitakazotekelezwa ni pamoja na kuboresha huduma yamajisafi na usafi wa mazingira, taka ngumu, kujenga uwezotaasisi na walengwa wa mradi. Gharama ya utekelezaji wamradi huo kwa mji wa Kigoma Dola za Marekani milioni 4.6;Kasulu Dola za Marekani milioni 2,3; Mpanda Dola za Marekanimilioni 3.1 na Namanyere Dola za Marekani milioni 1.9. Aidha,katika kupunguza kero ya maji katika mji wa Namanyere,katika mwaka 2012/2013, Serikali imetuma shilingi milioni 100kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa dharura wa kuboreshahuduma ya maji katika mji huo. Kazi zilizofanyika ni kulazabomba la urefu wa mita 3,960 kununua pampu, jenereta nadira za maji 103.

Mheshimiwa Naibu Spika, uboreshaji wa Huduma yaMaji katika Miji Mikuu ya Mikoa Mipya. Katika mwaka 2013/2014, Serikali itaboresha huduma ya majisafi katika Miji Mikuuya Mikoa mipya ya Mpanda, Njombe na Bariadi. Kazizitakazofanyika katika Miji hiyo ni:-

Page 82: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

82

(1) Mpanda, ni kujenga tanki la maji, mtambowa kutibu maji, chanzo cha maji cha Manga na kupanuamtandao wa majisafi mjini Mpanda, Kununua pampu zakusukuma maji bwawa la Milala na dira za maji 1,500. Kazihizo zikikamilika zitaongeza wingi wa maji kutoka lita milioni2.8 za maji sasa hadi kufikia lita milioni 6.1 na upotevu wamaji utapungua kutoka asilimia 59 sasa hadi asilimia 35. Kazihizo zitagharimu shilingi bilioni 1.5.

(2) Katika mji wa Njombe, kazi zitakazofanyikani kujenga chanzo cha Wikichi, kulaza mabomba kutokakwenye chanzo mpaka mjini, kukarabati mfumo wa majimjini Njombe na kununua dira za maji 1,000. Matokeo ya kazihii ni kuongezeka kwa wingi wa maji kiasi cha lita 604,000kwa siku na ufungaji wa dira za maji utasaidia kupunguzakiasi cha maji yanayopotea kutoka asilimia 50 za sasa hadiasilimia 38. Wananchi zaidi 12,000 watapata huduma nakukidhi mahitaji ya maji kwa asil imia 62. Mradi huoutagharimu shilingi milioni 800.

(3) Katika mji wa Bariadi, kazi zilizopangwa nikuchimba visima sita na kufunga pampu, kujenga tanki lamaji, kupanua mtandao wa maji, kukarabati tanki laSomanda na kujenga ofisi ya Mamlaka ya maji. Mradi huoutagharimu shilingi bilioni 2. Aidha, katika mwaka 2012/2013,Serikali imetuma shilingi milioni 150 kwa ajili ya utekelezajiwa mradi wa dharura majisafi mjini Bariadi. Kazi zilizofanyikani ukarabati wa pampu na mota kwa ajili ya chujio la maji,tanki la maji Somanda, ujenzi wa nyumba ya mitambo nabomba kwa ajili ya visima vya Somanda, Sanungu na Isanzu.Kazi zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa mtandao wakusambaza maji Kidinda pamoja na ujenzi wa vioski vinnena kuunganisha umeme kwa ajili ya visima vya Somanda,Sanungu, Isanzu na Kidinda. Mradi huu ukikamilika, kiasi chamaji kitaongezeka kutoka lita 861,000 hadi 1,560,000 kwa sikuna huduma itaboreka kutoka asilimia 17 hadi 30.

Mheshimiwa Naibu Spika, Usanifu wa Miradi ya Majisafina Majitaka. Katika mwaka 2013/2014, Serikali itafanyausanifu wa kina na kuandaa vitabu vya zabuni kwa miradi

Page 83: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

83

ya maji katika Miji Midogo na Miji Mikuu ya Wilaya yaBiharamulo, Muleba, Ngara, Karagwe, Chato na Bunazi(Kagera); Kakonko (Kigoma); Namanyere, Chala na Laela(Rukwa); Manyoni na Kiomboi (Singida), na Mombo, Songe,Lushoto, Kasela, Korogwe na HTM (Tanga) pamoja na miradiya majitaka mjini Bukoba na Singida ili kukidhi mahitaji yamuda wa kati. Vilevile, Serikali itafanya usanifu na kuandaavitabu vya zabuni kwa mradi wa kutoa maji Mto Ugala hadiMiji ya Urambo na Kaliua ili kuboresha huduma ya maji katikaMiji hiyo. Taratibu za kuwapata wahandisi washauri wakufanya usanifu huo zimeanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji kutoka ZiwaVictoria hadi Tabora, Igunga, Nzega, Kagongwa, Isaka naTinde. Taratibu za kuwapata Wahandisi Washauri wa kufanyausanifu na uandaaji wa makabrasha ya zabuni ya ujenzi wamradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Miji ya Nzega,Igunga na Tabora pamoja na mradi wa kupeleka maji katikaMiji Midogo ya Kagongwa, Isaka hadi Tinde zinaendelea.Kazi zitakazotekelezwa 2013/2014, ni kufanya usanifu nakuandaa vitabu vya zabuni na itaanza mwezi Julai, 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji kutoka ZiwaVictoria hadi Bariadi, Mwanhuzi, Magu na Ngudu. Katikamwaka 2012/2013, taratibu za kumpata Mtaalam Mshauriatakayefanya upembuzi yakinifu, usanifu na uandaaji wamakabrasha ya zabuni kwa mradi wa kutoa maji kutoka ZiwaVictoria hadi Miji ya Bariadi, Mwanhuzi, Lagangabilili, Maguna Ngudu zinaendelea. Katika mwaka 2013/2014, upembuziyakinifu, usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwaajili ya kutoa maji kutoka Ziwa Victoria na kuyafikisha katikaMiji hiyo na Vijiji vilivyo jirani na bomba kuu utafanyika. Kazihiyo itaanza mwezi Julai, 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Chalinze.Katika mwaka 2012/2013, Serikali imeendelea na utekelezajiwa awamu ya pili ya mradi wa maji Chalinze, unaojumuishausambazaji wa majisafi katika Vijiji 48 vilivyogawanywa katikamakundi tisa ya utekelezaji. Mradi huo utakaonufaisha Wilayatatu za Bagamoyo, Kibaha na Morogoro unatekelezwa na

Page 84: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

84

Serikali kwa kushirikiana na BADEA, Serikali ya Jamhuri ya Watuwa China na Mfuko wa Pamoja wa Sekta ya Maji. Mradi huoutahudumia wakazi 109,648 katika Vijiji hivyo. Katika mwaka2013/2014, Wizara yangu itaendelea kutekeleza awamu hiyoya mradi na utakamilika mwezi Agosti, 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya India itaanza utekelezajiwa awamu ya tatu ya mradi Maji Chalinze. Kazizitakazotekelezwa ni pamoja na kupitia usanifu na kuanzaujenzi wa kuboresha chanzo cha maji kilichopo Mto Wami,upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji, upanuzi wamtandao wa majisafi na ujenzi wa matanki. Katika awamuya pili, mradi utagharimu shilingi bilioni 51.3 na awamu yatatu Dola za Marekani milioni 48.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Dharura kwaJiji la Dar es Salaam. Katika mwaka 2012/2013, Serikaliiliendelea kutekeleza Mpango wa Dharura wa KuboreshaHuduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibahana Bagamoyo. Madhumuni ya Mpango huo ni kuboreshahuduma kwa kuongeza wingi wa maji kutoka lita milioni 300za sasa hadi lita milioni 756 kwa siku, kuboresha usambazajiwa maji, kupunguza upotevu wa maji yasiyolipiwa, kuboreshautendaji wa DAWASA na DAWASCO kuongeza maduhuli;na kuongeza uwezo wa uondoshaji wa majitaka kutokaasilimia 10 za sasa hadi asilimia 30. Utekelezaji wa Mpangohuo unalenga kukabiliana na changamoto zinazolikabili Jijila Dar es Salaam zikiwa ni pamoja na uchakavu wamiundombinu ya majisafi na majitaka; kupungua kwa majiya Mto Ruvu, hasa wakati wa kiangazi; ongezeko kubwa laidadi ya watu la asilimia 6 kwa mwaka ikilinganishwa naongezeko la asilimia 4.5 Miji ni kitaifa; ongezeko la makazimapya katika maeneo yasiyopimwa; na ongezeko lashughuli za kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbaliiliyopangwa katika mpango huo ulioanza rasmi mweziFebruari, 2011 na umepangwa kukamilika mwezi Desemba,2014. Hadi sasa, miradi inayotekelezwa ni kama ifuatavyo:-

Page 85: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

85

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Bwawa la Kidunda.Bwawa la Kidunda linatarajiwa kujengwa ili kuhakikishakwamba maji katika mto Ruvu yanakuwepo kipindi chotecha mwaka na kuzalisha umeme wa megawati 20. Usanifuwa Bwawa umekamilika na vitabu vya zabuni viko tayarikwa ajili ya matangazo ya kumpata mkandarasi. Uendeshajiwa kituo cha umeme na usambazaji wake utatekelezwa naTANESCO chini ya makubaliano (MoU) yaliyosainiwa kati yaDAWASA na TANESCO tarehe 10/11/2012. Aidha, usanifu wabarabara ya kuingilia eneo la bwawa umekamilika kamaulivyopangwa na mtaalamu wa kufanya tathmini ya athariza kimazingira na kijamii (ESIA) amepatikana. Aidha,wananchi watakaohamishwa kutoka maeneo yao ili kupishaujenzi wa bwawa hilo watalipwa mwezi Mei 2013. Katikamwaka 2013/2014, ujenzi utaanza baada ya kulipa fidiapamoja na ujenzi wa barabara kwenda kwenye eneo laujenzi wa bwawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, visima virefu vya Kimbiji naMpera. Katika mwaka 2012/2013, mkandarasi wa kuchimbavisima 20 katika maeneo ya Kimbiji na Mpera amepatikanana kazi ya uchimbaji itaanza mwezi Julai 2013 na itakamilikamwezi Julai 2014. Taarifa ya tathmini ya athari za kimazingirana kijamii (ESIA) iko katika hatua za mwisho. Uthamini wamaeneo yote ya mradi yenye ekari 7,300 umefikia shilingi bilioni27. Aidha mkandarasi wa uchimbaji wa visima virefu vinanevya kukamilisha tathmini ya mwenendo wa maji ardhinialipatikana mwezi Septemba 2012. Uchimbaji umeanzamwezi huu wa Aprili 2013 na unatarajia kukamilika mweziDesemba 2013. Makisio ya awali ni kupata maji lita milioni260 kwa siku kutoka katika visima hivyo ifikapo mwaka 2014.Katika mwaka 2013/2014, Serikali itaendelea na uchimbajiwa visima 20, kazi ya kutathmini mwenendo wa maji ardhinina kulipa fidia kwa wananchi watakaoathirika na ujenzi wamradi katika eneo la Kimbiji na Mpera.

Mheshimiwa Naibu Spika, upanuzi wa Mtambo waRuvu Juu. Usanifu wa mtambo wa Ruvu Juu na bomba kuula kutoka mtamboni hadi Kibamba, pamoja na tenki jipyala Kibamba ulikamilika Novemba 2012. Taratibu za kumpata

Page 86: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

86

msimamizi na mkandarasi wa ujenzi zitakamilika Juni 2013na ujenzi utaanza Julai 2013. Upanuzi wa mtambo wa RuvuJuu utaongeza uwezo wa mtambo kutoka lita milioni 82 kwasiku mpaka lita milioni 196 kwa siku ili kukabiliana nachangamoto ya ukuaji wa kasi wa Miji ya Mlandizi, Kibahana Jiji la Dar es Salaam. Katika mwaka 2013/2014, ujenzi wamradi huo utaanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, upanuzi wa Mradi wa Majiwa Ruvu Chini. Katika mwaka 2012/2013, Serikali kwakushirikiana na MCC, iliendelea na upanuzi wa mradi wamaji wa Ruvu Chini. Hadi mwezi Machi 2013, utekelezajiumefikia asilimia 85 na utakamilika Julai 2013. Ujenzi wabomba kuu la kusafirisha maji yatakayoongezeka kutokanana upanuzi wa mtambo Ruvu Chini hadi Jijini Dar es Salaamumeanza. Katika mwaka 2013/2014 ujenzi wa bomba kuukutoka Ruvu chini utaendelea, lengo ni kukamilisha kazi hiyomwezi Februari 2014. Aidha, kazi ya ujenzi wa kingo za mtoRuvu katika eneo la Kidogozero unaendelea; hadi Machi 2013kazi iliyokamilika ni asilimia 75, kazi hii itakamilika Agosti 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati na upanuzi waMfumo wa Kusambaza Majisafi. Katika mwaka 2013/2014,Serikali itaanza kutekeleza mradi wa kujenga mfumo wakusambaza maji katika maeneo ya Tegeta - Mpiji na Mpijihadi Bagamoyo. Mradi huu ukikamilika jumla ya kilomita 732za mabomba ya kusambaza maji yatalazwa, wateja 3,400wataunganishwa na vioski 30 vitajengwa kati ya Bagamoyona Tegeta. Vilevile, Serikali itaanza ujenzi wa mabomba nakuunganisha wateja maeneo ya Mbezi hadi Kiluvya. Mradihuo ukikamilika jumla ya kilomita 300 za mabomba yakusambaza maji yatalazwa, wateja 10,000 wataunganishwana vioski 30 vitajengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingine yaKuboresha Huduma ya Maji Jijini Dar es Salaam. Katika mwaka2012/2013, Wizara yangu kwa kushirikiana na Shirika laMaendeleo la Ubelgiji (BTC) na Umoja wa Nchi za Ulayailiendelea na utekelezaji wa mradi wa kuboresha upatikanajiwa majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo ya

Page 87: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

87

Kibondemaji B, Mtoni Kijichi Misheni, Mbagala Kuu, Mgeninani,Mwanamtoti, Yombo-Dovya Msakala, Tandale, Kwembe,Tabata Darajani Kisiwani, Kinyerezi, Minazi mirefu, Hondogo,Gongolamboto,Guluku Kwalala -Ulongoni, Kingugi,Mburahati- Barafu na Ugombolwa yaliyoko katika Manispaaza Temeke, Ilala na Kinondoni Jijini Dar es Salaam; kwakujenga mifumo ya usambazaji maji kwenye maeneoyaliyochimbwa visima, vituo vya kuchotea maji na matankiya kuhifadhia maji. Utekelezaji wa kazi ya kuboresha hudumaya maji umefikia asilimia 60 na ujenzi wa vyoo vya mfanokatika maeneo ya shule, zahanati na masoko umefikiaasilimia 85. Mradi huu umepangwa kukamilika ifikapo mweziJuni 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia ziara yaMheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania mwezi Mei 2010 alipotembeleamaeneo yenye kero ya huduma ya maji Jijini Dar es Salaam,aliagiza kuchimba visima virefu 27 ili kupunguza adha yaupatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo hayo. Hadikufikia mwezi Machi 2013, DAWASA imechimba visima virefu33 (zaidi ya lengo la awali la visima 27) ambapo 15 vipokatika maeneo ya Mburahati National Housing, Shule ya MsingiMuungano, Kwa Shebe, Mavurunza, Malamba Mawili,Saranga, King’ongo na Kilungule katika Manispaa yaKinondoni. Visima 14 vipo katika maeneo ya KekoMagurumbasi, Chang’ombe, Chang’ombe Toroli, Sandali,Sandali Mpogo, Sandali Mwembeladu, Mtoni, Mbagala,Kigamboni katika Manispaa ya Temeke. Visima vinne vipokatika maeneo ya Mongo la Ndege, Kipunguni, Mbondelena Mvuti katika Manispaa ya Ilala. Uchimbaji huo unaendasambamba na utekelezaji wa Mpango wa dharura wakuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dares Salaam. Katika mwaka 2013/2014, Wizara itaendeleakutekeleza miradi ya namna hiyo ili kupunguza kero ya majiwakati wa kusubiri utekelezaji wa miradi mikubwa. Maeneoyatakayochimbwa visima hivyo ni Temeke, Kigamboni,Kiwalani, Vingunguti, Segerea, Kinyerezi, Goba, King’ongo,Msumi, Mbezi, Kerege, Kibaha na maeneo ya Kisarawe yaKwala, Mtunani, Chole – Samvula na Yombo Lukinga.

Page 88: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

88

Mheshimiwa Naibu Spika, Huduma ya Maji katika MijiMikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa. Miradi yaMaji katika Miji ya Ikwiriri, Kibaigwa, Kilosa, Turiani, Mvomero,Kibiti, Gairo na Kisarawe. Katika mwaka 2012/2013, Wizarayangu imeendelea na ujenzi wa miradi ya maji katika Mijisita ya Ikwiriri, Kibaigwa, Kilosa, Turiani, Mvomero na Gairo ilikukidhi mahitaji ya wakazi wa Miji hiyo. Hadi kufikia mweziMachi 2013, ujenzi wa miradi ya maji katika Miji hiyo upokatika hatua zifuatazo; Ikwiriri (95%), Kibiti (100%), Kibaigwa(85%), Gairo (86%), Turiani (77%), Kilosa (79%) na Mvomero(81%). Miradi hii inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha2013/2014. Katika Mji wa Kisarawe, mabomba ya kusambazamaji yamelazwa na uchimbaji wa visima virefu utaanzamwezi Mei 2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi ya Maji Masasi/Nachingwea na Bunda. Katika mwaka 2012/2013, miradi yakuboresha huduma za maji katika Miji ya Masasi, Nachingweaimetekelezwa. Utekelezaji huo umefikia asilimia 97. Katikamwaka 2013/2014, kazi ya kuunganisha Vijiji vinne vyaLikwachu, Chinongwe, Litama na Chiumbati Shuleni katikaWilaya ya Nachingwea itafanyika. Katika mji wa Bunda, kaziya kulaza bomba lenye urefu wa kilomita 23.5 kutoka kwenyechanzo hadi kwenye matanki iliendelea katika mwaka 2012/2013. Katika mwaka 2013/2014, Serikali imetenga shilingimilioni 800 ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Orkesumet.Katika mwaka 2012/2013, utekelezaji wa mradi wa dharuramjini Orkesumet umekamilika, ambako kwa hivi sasa uzalishajini lita 144,000 kwa siku. Vilevile, vituo 13 vya kuchotea majivilijengwa. Mahitaji kwa mji huo hivi sasa inakadiriwa kuwalita 720,000 kwa siku. Ili kukabiliana na upungufu wa majiuliopo, Serikali imetafuta fedha kugharamia mradi katika mjihuo. Mradi wa kukidhi mahitaji ya muda mrefu ya wakaziwa mji wa Orkesumet utatekelezwa kwa ushirikiano waSerikali, BADEA na OFID. Mtaalam Mshauri atakayesanifu nakuandaa makabrasha ya zabuni ataanza kazi mwezi Mei2013. Kazi ya kupitia usanifu wa mradi (review) itaanza baadaya BADEA kutoa kibali na itakamilika kwa kipindi cha miezi

Page 89: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

89

mitatu. Wizara yangu itatangaza zabuni ya awali (prequalification notice) ya kupata wazabuni wa ujenzi wenyeuwezo pindi mkataba wa fedha utakaposainiwa kati yaSerikali na BADEA/OFID. Katika mwaka 2013/2014, ujenzi wamradi huo utaanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Uboreshaji waHuduma ya Majisafi Muheza. Katika mwaka 2012/2013, Serikaliimetuma shilingi milioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa mradiwa dharura wa maji katika mji wa Muheza. Kazi zilizopangwani ununuzi wa pampu na matanki mawili ya lita 10,000 kilamoja, ulazaji wa bomba la urefu mita 150, kujenga nyumbaya mtambo na kuunganisha umeme kwenye chanzo. Kazizilizofanyika hadi Machi 2013 ni ujenzi wa nyumba yamtambo, ununuzi wa pampu na kuifunga, ufungaji waumeme jua, kulaza bomba kuu, kununua na kufunga matankimawili kila moja lita 10,000 pamoja na kuchimba mtaro waurefu wa mita 400. Kazi zitakazofanyika katika mwaka 2013/2014 ni kujenga mtandao wa kusambaza maji na vioski vyakuchotea maji. Kiasi cha shilingi milioni 300 zimetengwa kwaajili ya mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Uboreshaji waHuduma ya Majisafi Karatu. Katika mwaka 2012/2013, Serikaliimetenga shilingi milioni 495 kwa ajili ya kuboresha hudumaya maji katika mji wa Karatu kama hatua za kutekeleza mradiwa dharura. Tayari kisima kirefu chenye kina cha mita 188 nauwezo wa kutoa maji lita 45,000 kwa saa kimechimbwa kwagharama ya shilingi milioni 55. Serikali imejiandaa kuchimbavisima vingine viwili, kujenga matanki ya kuhifadhi maji,kununua pampu na kujenga vioski kumi kwa ajil i yakupunguza kero ya maji katika mji huo. Kazi hiyo ikikamilikaitaongeza upatikanaji wa maji kutoka lita 840,000 hadi lita3,000,000 kwa siku, na kuboresha huduma ya maji kutokaasilimia 20 hadi asilimia 71.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakuboresha huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Wilaya naMiji Midogo kwa kukarabati na kupanua mifumo ya majikatika Miji hiyo. Katika mwaka 2013/2014, Serikali imetenga

Page 90: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

90

fedha kiasi cha shilingi bilioni 4.0 ili kuongeza upatikanaji wamaji kwa Miji ya Korogwe, Mafinga, Mwanga, Chunya,Karagwe, Makambako, Kibondo, Makete, Mahenge, KilwaMasoko, Mvomero/Dakawa, Urambo, Nzega, Pangani,Sikonge, Kibaya, Ifakara, Ruangwa, Tunduma, Ilula, Kateshna Loliondo ikiwa ni hatua ya dharura ili kukamilisha miradiinayoendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi ya Maji ya Kitaifa.Katika mwaka 2013/2014, Serikali kwa kushirikiana na Benkiya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko waMaendeleo wa Saudia (Saudi Fund for Development - SFD)itaanza utekelezaji wa mradi wa majisafi wa Mugango/Kiabakari/Butiama. Mradi huo utagharimu Dola za Marekanimilioni 30.69. Mradi huo utanufaisha wananchi 80,000 na kazizitakazotekelezwa zitahusu ujenzi wa chanzo, ujenzi wamtambo wa kusafisha na kusukuma maji, kujenga matankimatatu, kulaza mabomba kutoka Mugango, Kiabakari, hadiButiama urefu wa kilomita 32, kukarabati mitambo yakusukuma maji ya Kiabakari na kulaza mabomba yamtandao wa usambazaji maji Butiama hadi Bisalye. Usanifuutaanza Agosti, 2013 na ujenzi utaanza Machi, 2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na upungufuwa maji katika mradi wa kitaifa HTM; katika mwaka 2012/2013, Serikali imetuma shilingi milioni 73 kwa ajili ya ukarabatiwa kituo cha kusukuma maji Segera; kununua na kufungapampu katika kituo hicho. Ufungaji wa pampu hizoumeboresha upatikanaji wa maji kutoka saa sita mpaka saanane kwa siku. Maeneo yatakayofaidika na uboreshaji huoni Segera, Kabuku, Mgambo JKT, Mkata na Handeni mjini.Katika mwaka 2013/2014, Serikali itakarabati mifumo ya majikatika miradi ya kitaifa ya Wanging’ombe, Maswa, HandeniTrunk Main na Makonde. Kiasi cha shilingi milioni 400kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuzijengea uwezo Mamlakaza Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini. Katika mwaka 2012/2013, Wizara yangu iliendelea kuzijengea uwezo Mamlakaza maji za Miji Mikuu ya Mikoa, Miji Mikuu ya Wilaya, Miji

Page 91: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

91

Midogo na miradi ya kitaifa ili ziongeze ufanisi katika utoajiwa huduma kwenye maeneo yao. Kazi zilizotekelezwa nipamoja na kuendelea na ujenzi wa ofisi ya Mamlaka yaMajisafi na Usafi wa Mazingira mjini Babati ambao umefikiaasilimia 65 mwezi Machi 2013. Kuanza ujenzi wa ofisi katikaMiji ya Wilaya ya Utete, Mpwapwa na mji mdogo waTunduma. Wizara yangu itaendelea kuziimarisha mamlakaza ngazi ya Mikoa, Wilaya, Miji Midogo na miradi ya kitaifakwa kuzitengenezea mazingira mazuri ya kazi, katika kipindicha mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Februari2013, Wizara yangu ilikuwa imechangia jumla ya shilingi milioni500 katika gharama za uendeshaji wa miradi ya kitaifa kwakulipia sehemu ya ankara za umeme wa mitambo yakuzalisha maji. Katika mwaka 2013/2014, Wizara yanguitaendelea kuijengea uwezo miradi ya kitaifa na Mamlakaza daraja B na C ili hatimaye ziweze kujiendesha zenyewe nahivyo kuipunguzia Serikali mzigo wa kuchangia gharama zauendeshaji kwenye mamlaka zikiwemo gharama za umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya majina kuzijengea uwezo Mamlaka za maji za ngazi ya Wilaya.Miji Midogo na miradi ya kitaifa ili kuongeza upatikanaji wahuduma ya majisafi katika maeneo ya Mamlaka hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Taasisi chini ya Wizara yaMaji. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji.Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)inatekeleza majukumu ya kudhibiti utoaji wa huduma kwenyesekta za umeme, mafuta ya petroli, gesi asilia, majisafi namajitaka nchini ikiwa chini ya Wizara yangu. Majukumu hayoni pamoja na kutoa leseni, kusimamia utekelezaji wa mashartiya leseni, kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma,kutathmini na kupitisha bei za huduma na kutatua migogoro.Kwa upande wa Sekta ya Maji, EWURA imeendelea na udhibitiwa huduma za maji zinazotolewa na Mamlaka za Maji 130nchini. Kati ya Mamlaka hizo, 19 ni za Miji Mikuu ya Mikoa,102 za Miji Mikuu ya Wilaya na Miji Midogo, DAWASA,DAWASCO na miradi saba ya kitaifa ya maji.

Page 92: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

92

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,EWURA ilichambua maombi ya leseni na kuzipatia leseni zakudumu Mamlaka za Maji 84 za Miji Mikuu ya Wilaya, MijiMidogo na miradi ya kitaifa kwa ajili ya kutoa huduma yamajisafi na majitaka kama inavyoonekana katika JedwaliNa. 17. Mamlaka hizo zilipatiwa leseni za daraja la C. Katikauchambuzi wa maombi ya leseni, imeonekana kuwamamlaka nyingi za Miji ya Wilaya, Miji Midogo na miradi yakitaifa zimeshindwa kupata leseni za daraja la B au Akutokana na kutokidhi vigezo vya kupanda daraja. Lesenizilizotolewa zitakuwa halali kwa kipindi cha miaka 10 na kwamujibu wa leseni hizo, kila Mamlaka ya Maji inatakiwaiboreshe huduma zake ili ipande daraja ndani ya kipindi hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,EWURA ilifanya mapitio ya mipango ya kibiashara (BusinessPlans) ya miaka mitatu iliyoandaliwa na Mamlaka za Maji.Mipango ya kibiashara iliyopitiwa ni ya mamlaka za maji zaMiji ya Mbeya, Arusha, Iringa, Singida, Tabora, Moshi, Tanga,Dodoma, Mwanza na Musoma. Mapitio ya mipango yakibiashara ya Mamlaka hizo yamefanyika kwa kuzingatiamwongozo wa EWURA wa kutengeneza mipango yakibiashara wa mwaka 2011. Mwongozo huo unalengakuzifanya Mamlaka za maji ziwe endelevu kwa kutoamwelekeo kwa kila Mamlaka ya Maji kuweza kukidhigharama zote za uendeshaji na uwekezaji. Aidha, EWURAiliidhinisha bei mpya za maji kwa Mamlaka za Maji 8, ambazoni Arusha, Tanga, Mbeya, Mtwara, Lindi, Mafinga, HandeniTrunk Main (HTM) na DAWASA. Bei zilizoidhinishwa zimelengakuziwezesha Mamlaka hizo kutekeleza mipango yao yakibiashara na kutoa huduma iliyo bora zaidi na endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka2012/2013, EWURA kwa ikishirikiana na Shirika la Maendeleola Ujerumani (GIZ) iliboresha mfumo wa kompyuta wa taarifaza kila mwezi za utendaji wa mamlaka za maji nchini uitwaoWater Utilities Information System (MajIs). Mfumo huouliboreshwa ili ufanye kazi kwa kutumia tekinolojia yamtandao, yaani Web Based. Maboresho yaliyofanyikayameufanya mfumo huo kuwa salama zaidi kwa kupunguza

Page 93: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

93

hatari ya kushambuliwa na virusi, kuwezesha kutumiwa nawatumiaji wengi ndani ya Mamlaka moja na rahisi zaidikutumia katika kuingiza takwimu na kuandaa taarifa.Mamlaka za maji za Miji ya Mikoa, DAWASA, DAWASCO .nabaadhi ya Mamlaka za Miji ya Wilaya, Miji Midogo na Miradiya Kitaifa ya Mikumi, Kilosa, Gairo, HTM, Mugango-Kiabakari,Kibondo, Maswa, Ilula, Makambako, Mafinga, Kilolo, Tukuyu,Mbalizi, Chunya, Ilege, Namtumbo, Mbulu, Orkesumet,Magugu, Same, Dereda, Gapapo, Bashmet, Kibaya, Katesh,Loliondo na Usa River.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kusimamia utendajiwa Mamlaka za maji, EWURA ilikagua miundombinu nauendeshaji wa Mamlaka za maji 22 katika kipindi cha mwaka2012/2013. Katika ukaguzi huo, EWURA ilifanya uhakiki wataarifa na takwimu za utendaji zilizowasilishwa na Mamlakahizo. Uhakiki huo ulihusu viwango vya uzalishaji maji kwakukagua dira kubwa za maji, takwimu za ubora wa maji,taratibu za kushughulikia malalamiko ya wateja na utekelezajiwa maagizo ya EWURA. Mamlaka zilizokaguliwa ni Singida,Tabora, Shinyanga, Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma,Tanga, Babati, Moshi, Mbulu, Same, DAWASA, Chalinze, Iringa,Mbeya, Sumbawanga, Morogoro, Dodoma, Lindi, Mtwarana Songea.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,EWURA ilitathmini utendaji kazi wa Mamlaka za Maji zotenchini kwa kipindi cha mwaka 2011/2012. Tathmini hiyo ilibainikuwa Mamlaka za Maji zimekuwa na mafanikio katikakuongeza kiwango cha uzalishaji maji, ufungaji wa dira zamaji, idadi ya wateja wa majisafi na majitaka, ukusanyajiwa mapato na kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimaliwatu. Pamoja na mafanikio hayo, imebainika kuwaongezeko la kiasi cha maji yanayozalishwa ni kidogoukil inganisha na ongezeko la mahitaji ya majiyaliyosababishwa na ongezeko la idadi ya watu na shughulinyingine za kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini hiyo pia ilibainikuendelea kuwepo kwa upotevu wa maji unaozidi kiwango

Page 94: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

94

kinachokubalika kitaifa cha kutozidi asilimia 20, kupunguakwa saa za upatikanaji wa maji, uchakavu wa miundombinuna upungufu wa watumishi wenye sifa hasa kwa mamlakaza maji zinazotoa huduma katika Miji ya Wilaya, Miji Midogona miradi ya kitaifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,EWURA iliandaa Mwongozo wa Udhibiti wa Uendeshaji waVisima Binafsi vya Maji na Mwongozo wa Udhibiti wa Biasharaya Maji kwa kutumia Magari Binafsi (Water Tankers) katikaeneo linalosimamiwa na DAWASA kwa lengo la kudhibitiubora na bei ya huduma ya maji inayotolewa na sektabinafsi. Miongozo hii imetayarishwa ili kuelekeza, kusimamiana kudhibiti shughuli za uendeshaji wa visima binafsi namagari binafsi katika eneo hilo ambapo huduma ya majiitolewayo na DAWASCO haikidhi mahitaji au haijafika. Aidha,rasimu ya kanuni zitakazotumika kudhibiti huduma hizozitolewazo na sekta binafsi kwa ajili ya Dar es Salaam nakwa ajili ya mamlaka zote za maji zimeandaliwa. Aidha,matayarisho kwa ajili ya kudhibiti sekta binafsi ya maji kwaJiji la Dar es Salaam yameshaanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,EWURA iliendelea kupokea, kusikiliza na kutatua malalamikoya wateja wa mamlaka za maji walioyawasilisha EWURA.Malalamiko yaliyowasilishwa yanahusu ankara za majisafi namajitaka zisizo sahihi, ukosefu wa maji, kukatiwa hudumaya maji kimakosa na udhaifu wa huduma kwa wateja.Katika kipindi hicho jumla ya malalamiko 19 yaliwasilishwaEWURA ambapo kati ya hayo malalamiko manneyamepatiwa ufumbuzi wakati malalamiko 15 yaliyobaki yakokatika hatua tofauti za utatuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,EWURA itaendelea kuimarisha udhibiti wa huduma ya majiitolewayo na mamlaka za maji hapa nchini kwa kuzingatiavipaumbele muhimu kama ifuatavyo:-

(i) Kufuatilia utendaji wa mamlaka za maji nchinikwa kuchambua na kuhakiki taarifa za utendaji na kufanyaukaguzi wa miundombinu na utendaji wa mamlaka za maji;

Page 95: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

95

(ii) Kuhakikisha kuwa mamlaka za majizinaandaa na kutekeleza mipango yao ya kibiashara (BusinessPlans) kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na EWURA;

(iii) Kuendeleza uwekezaji katika sekta ya majikwa kuziwezesha mamlaka za maji kupata fedha kwa ajiliya kujenga miradi mipya, kuibua vyanzo vipya vya maji nakukarabati miundombinu iliyopo;

(iv) Kufuatil ia udhibiti wa huduma za majizinazotolewa na sekta binafsi kupitia visima na magari binafsikwa Jiji la Dar es Salaam na Mikoa mingine;

(v) Kutoa elimu kwa umma kuhusu haki nawajibu wao katika kufanikisha utoaji bora wa huduma yamaji; na

(vi) Kuhimiza mamlaka za maji kuboreshaukusanyaji wa mapato yatokanayo na ankara za maji;kubainisha na kutatua sababu za upotevu wa maji, kuanzishana kupanua mifumo ya majitaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo cha Maendeleo naUsimamizi wa Maji. Chuo cha Maendeleo na Usimamizi waMaji, kiliendelea na jukumu lake la kujenga uwezo wakitaalam wa fani za ufundi zinazohitajika katika utoaji wahuduma za maji na usimamizi wa rasilimali za maji. Katikamwaka 2012/2013 chuo kilidahili wanafunzi 358 na kukifanyakuwa na jumla ya wanafunzi 757 wa stashahada (watertechnicians). Jumla ya wanafunzi 91 walihitimu mafunzo yaokatika fani mbalimbali kama ifuatavyo: katika fani ya uhandisiwa mifumo ya ugavi wa maji safi na usafi wa mazingira(water supply and sanitation) (47), utafutaji wa maji ardhinina uchimbaji wa visima vya maji (hydrogeology and waterwell drilling) (13), Haidrolojia (2), na Teknolojia ya maabaraza uchunguzi wa ubora wa maji (water quality laboratorytechnology) (29). Aidha, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)ilifadhili wanafunzi wa kike (34) katika kozi ya kuwawezeshakujiunga na masomo ya stashahada (Access Course). Hiiimewezesha kuongeza udahili wa wanafunzi wa kike kutoka

Page 96: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

96

29 mwaka 2011/2012 hadi 67 katika mwaka 2012/2013. Vilevilewashiriki 136 walipewa mafunzo ya muda mfupi katika fanimbalimbali zinazohusu sekta ya maji. Ushauri juu ya uborawa maji kwa wateja 54 waliowasilisha sampuli zao ulitolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha utoaji waelimu chuoni, Wizara yangu ilikamilisha mchakato waupatikanaji wa ithibati (accreditation) na Baraza la Taifa laElimu ya Ufundi (NACTE) lilitoa ithibati hiyo tarehe 01 Oktoba,2012. Ithibati hiyo inakiwezesha chuo kuanza kutoa mafunzoya shahada ya kwanza ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji naUmwagiliaji (Bachelor of Engineering in Water Resources andIrrigation). Pamoja na uboreshaji huo, Serikali kwa kushirikianana GIZ imeandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwaajili ya upanuzi wa Chuo (Land Use Master Plan). Katikakukabiliana na upungufu wa watumishi, Chuo kiliajiriwatumishi 17.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha utoaji wahuduma, Chuo kilifanya ukarabati wa darasa la kompyutana ofisi (5). Pia, ununuzi wa samani mbalimbali za ofisi,maabara, zahanati, na madarasa ulifanyika. Vilevile, ununuziwa fax machine (1), kompyuta (100), Photocopier (2), printer(2), projector (3), vitanda (122), magodoro (60), madawati(191) na jenereta moja ya KVA 250 ulifanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Chuo kitatoa mafunzo katika ngazi ya stashahada (WaterTechnician) kwa wanafunzi 1,056, sambamba na kuanzishamafunzo ngazi ya shahada kwa wanafunzi 40. Mafunzo yamuda mfupi kwa washiriki 500 yatatolewa. Pia ujenzi wajengo la ghorofa sita lenye madarasa, maabara, kumbi zamikutano na maktaba, pamoja na ukarabati wa majengoya chuo utafanyika. Chuo kitanunua vifaa vya Haidrolojia,Upimaji wa maji ardhini na uchimbaji visima, upimaji waudongo, uchunguzi wa ubora wa maji, na hali ya hewa.Katika kuboresha utoaji wa elimu, Chuo kitaajiri watumishi26 wa kada mbalimbali na kuwaendeleza watumishiwaliopo kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi.

Page 97: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

97

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Uchimbaji waVisima na Ujenzi wa Mabwawa. Katika mwaka 2012/2013,Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa(DDCA) ulichimba visima virefu 162 hadi Machi 2013 na visima300 vinatarajiwa kuchimbwa nchini kote ifikapo Juni 2013.Wakala umekamilisha ujenzi wa Bwawa la Misozwe lililopokatika Wilaya ya Muheza. Aidha, uchunguzi wa maji chini yaardhi kwa ajili ya uchimbaji visima virefu umefanyika katikamaeneo 185 na ifikapo Juni 2013 maeneo 265 yatakuwayamechunguzwa. Vilevile, ujenzi wa mabwawa matatu yaMwavi (Bagamoyo), Norband na Maole (Mkomazi- Same)umekamilika. Katika kuendelea kuujengea uwezo Wakala,Serikali imeupatia mitambo minane kwa ajili ya shughuli zauchimbaji visima.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala ulifanya uchunguziwa udongo katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sementiLindi. Aidha, Wakala umejenga matanki ya kuhifadhi majina kuweka pampu za kusukuma maji katika Hospitali ya St.Francis iliyopo Ifakara, Morogoro. Ifikapo Juni 2013, Wakalautakamilisha ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji NHC - KibadaKigamboni na kukarabati mabwawa matatu katika Wilayaya Monduli.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana wakatinawasilisha makadirio ya Wizara yangu nililiarifu Bunge lakoTukufu kuwa Wakala ingenunua mitambo minne na vifaavyake (Drilling rigs and accessories) kwa ajili ya uchimbaji wavisima na uchunguzi wa maji chini ya ardhi. Vifaa hivyohavikununuliwa kutokana na kuchelewa kusainiwa kwamkataba wa fedha kati ya Serikali ya Tanzania na NORAD.Katika mwaka 2013/2014 Wakala utanunua vifaa hivyobaada ya taratibu hizo kukamilika. Vifaa hivyo vikipatikanaWakala utakuwa na uwezo wa kuchimba visima virefu 450kwa mwaka. Vilevile, Wakala itakuwa na uwezo wa kufanyautafiti wa maji katika maeneo 300, kujenga bwawa moja,usanifu wa maeneo manne kwa ajili ya ujenzi wa mabwawana uchunguzi wa udongo kwa shughuli mbalimbali. Serikalikwa kushirikiana na JICA itaujengea uwezo Wakala ili uwezekuboresha utoaji wa huduma.

Page 98: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

98

Mheshimiwa Naibu Spika, Bohari Kuu ya Maji. Katikamwaka 2012/2013, Bohari Kuu ya Maji iliendelea kutekelezamajukumu yake ya kununua, kuhifadhi na kusambaza vifaana dawa za kusafisha na kutibu maji pamoja na kuendeleana taratibu za kuibadili Bohari hiyo kuwa Wakala wa Serikali.Bohari Kuu ya Maji imeweza kusambaza vifaa mbalimbalivya maji ikiwa ni pamoja na pampu za maji na viungio vyamabomba katika Halmashauri na Mamlaka za majimbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara yangu itaendelea na taratibu za kuibadili Bohari hiyokuwa Wakala wa Serikali. Lengo ni kuiboresha ili iweze kutoamchango mkubwa zaidi katika upatikanaji na usambazajiwa vifaa vya miradi ya maji. Aidha, Bohari itakamilisha ujenziwa uzio na itaanza ukarabati wa baadhi ya maghala(godowns).

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala mtambuka. Sheria.Katika mwaka 2012/2013, Wizara iliendelea kutoa elimu naushauri wa kisheria kuhusu utekelezaji wa sheria na hatua zakuchukua dhidi ya ukiukwaji wa Sheria za Maji. Elimu naushauri umetolewa kwenye Halmashauri, Ofisi za Maji zaMabonde, Mamlaka za maji na wadau wengine wa sektaya maji pamoja na jamii kwa ujumla kupitia warsha,mikutano, makongamano na mafunzo maalum. Aidha,nakala 840 za Sheria za Maji na Kanuni zake zimesambazwakwa wadau. Vilevile kazi ya kutafsiri Sheria za Maji kwa lughaya Kiswahili inaendelea ambapo maoni ya wadauyamekusanywa na maboresho yanaendelea kufanyika kablaya kuwasilishwa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwa ajili ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi nyingine zilizofanyikakatika mwaka 2012/2013 ni pamoja na kukamilisha kanunisaba, oda na notisi nne za kisheria ambazo kwa sasa zipokatika hatua ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Kanunihizo ni:-

(i) Oda ya kutangaza Bonde la Makutupora

Page 99: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

99

(Dodoma) kuwa eneo tengefu la hifadhi ya maji (Declarationof Makutupora groundwater controlled area) Order, 2012;

(ii) Oda ya kutangaza Bwawa la Kawa (Nkasi)kuwa eneo la hifadhi ya vyanzo vya maji (Prohibition ofHuman activities beyond sixty metres at Kawa Dam) Order,2012;

(iii) Notisi ya kutangaza wajumbe watatu waBodi ya Maji ya Taifa (Appointment the National Water BoardMembers) Notice, 2012;

(iv) Kanuni za Usimamizi wa Maji chini ya Ardhi(Ground Water (Exploration and Drilling) Licensing Regulations2013);

(v) Kanuni za Mfuko wa Uwekezaji wa Maji waTaifa (The National Water Investment Fund) Regulations 2013;

(vi) Kanuni za Usalama wa Mabwawa (DamSafety) Regulation, 2013;

(vii) Kanuni ya Usambazaji wa Maji (The WaterSupply) Regulations, 2013;

(viii) Kanuni za Uteuzi na Ukomo wa Wajumbe waBaraza la Ushauri la Watumiaji. Ewura (Appointment andTenure of EWURA CCC Members) Regulations 2013;

(ix) Kanuni za Uteuzi na Sifa za Wajumbe wa Bodiya Ewura. Ewura (Appointment and Qualifications of BoardMembers) Regulations, 2013;

(x) Kanuni za Uteuzi na Ukomo wa Wajumbe waBaraza la Ushauri wa Serikali. Ewura (Appointment and Tenureof GCC Members) Regulations 2013; na

(xi) Notisi ya kutangaza Mamlaka ya Maji na Usafiwa Mazingira ya Masasi-Nachingwea (Masasi-NachingweaWater Supply and Sanitation Authority) Notice, 2013.

Page 100: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

100

Mheshimiwa Naibu Spika, rasimu ya marekebisho(amendment) ya Sheria ya Huduma za Maji na Usafi waMazingira Dar es Salaam (DAWASA) Na. 20 ya mwaka 2001ilitayarishwa na maoni ya wadau yalikusanywa na kufanyiwakazi na sasa iko kwenye hatua ya kuwasilishwa kwenyeBaraza la Mawaziri kabla ya kuwasilishwa Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutoa ushauri wa kisheria kuhusu utekelezajiwa sheria za maji na kuendelea kutayarisha kanuni nne zasheria za maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Maji. Wakatinikihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka2012/2013, nilieleza mpango wa Serikali wa kuanzisha Mfukowa Maji ili kuongeza fedha za uwekezaji katika Sekta ya Maji.Sheria Namba 12 ya mwaka 2009 ya Huduma ya Maji na Usafiwa Mazingira, imetamka uanzishaji wa Mfuko wa Taifa waUwekezaji wa Maji (National Water Investment Fund) nakubaini vyanzo vya mapato ikiwa ni mchango wa SerikaliKuu na Washirika wa Maendeleo. Aidha, Serikali itaendeleakuutunisha Mfuko huo kwa kubaini vyanzo vingine vyamapato ikiwa ni pamoja na ada na tozo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufikia azma hiyo,Wizara yangu imeandaa Kanuni za uendeshaji wa Mfuko waMaji (National Water Investment Fund Regulations, 2013)ambazo ziko mbioni kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikalina kuanza kutumika. Katika bajeti ya mwaka 2013/2014shilingi 100,000,000 zimetengwa kama kianzio (seed money)cha Mfuko huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Habari, Elimu naMawasiliano. Katika mwaka 2012/2013, Wizara iliendeleakutoa elimu na taarifa mbalimbali kwa wananchi kupitiatovuti na vyombo mbalimbali vya habari. Wizara yanguilishiriki kikamilifu katika maonesho ya Kilimo ya Nanenanemwaka 2012 yaliyofanyika Nzuguni Mjini Dodoma ambapojumla ya vipeperushi 4,000 vilivyohusu hatua mbalimbali namafanikio yaliyopatikana katika kuwapatia wananchihuduma ya maji vilitolewa.

Page 101: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

101

Mheshimiwa Naibu Spika, machapisho 3,000 na vipindisita vya redio na televisheni vilitolewa katika maadhimishoya Wiki ya Maji ambayo kwa mwaka huu yalifanyika kitaifaMkoani Lindi, vipindi hivyo vililenga katika kufafanua nakuelimisha masuala mbalimbali ya Sekta ya Maji. Makala yafilamu (documentary film) ya mafanikio ya Sekta ya Maji katikakipindi cha miaka mitano ya awamu ya nne iliandaliwa nakurushwa. Kwa ujumla, makala 15 ziliandikwa na kutolewamagazetini na kwenye mitandao ya kijamii ya mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,Wizara yangu itaendelea kuelimisha wananchi na kutoataarifa mbalimbali zinazohusu Sekta ya Maji kwa kufufuaJarida la Maji Yetu; kuandaa na kutangaza vipindi katikaluninga na redio na kuboresha tovuti ya Wizara ili wananchiwengi zaidi waitumie.

Mheshimiwa Naibu Spika, Teknolojia ya Habari naMawasiliano. Wizara yangu imeendelea kuboresha mfumowake wa utendaji na utoaji wa huduma kwa kutumiaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Katika mwaka2012/2013, upatikanaji wa taarifa na takwimu za utekelezajiwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa njia yamfumo wa kielektroniki (Water Sector ManagementInformation System) umeboreshwa. Vilevile, Wizara imejengauwezo wa matumizi ya mfumo huo ambapo hivi sasa taarifaza utekelezaji wa mikataba na matumizi ya fedha zaProgramu zinatumwa Wizarani kutoka kwa watekelezajikupitia mfumo wa kieletroniki. Jumla ya watumishi 525walipata mafunzo kuhusu mfumo huo katika ngazi zote.Aidha, watumishi watano wa Wizara walipata mafunzo yakitaalam kuhusu TEHAMA.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaboreshamtandao wa mawasiliano katika Ofisi zake za Makao MakuuUbungo kwa kuunganishwa na Mkongo wa Taifa waMawasiliano (National Fibre Optic Cable). Aidha, kazi nyingineinayofanyika katika kipindi hiki ni uchambuzi wa kina,kutathmini hali halisi ya upatikanaji wa maji Vijijini baada yakazi ya ukusanyaji wa takwimu na utayarishaji wa ramani za

Page 102: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

102

vituo vya kuchotea maji (Water Point Mapping) kwa kutumiateknolojia ya habari na mawasiliano inayojulikana kama“Geography Information System – GIS” kukamilika katikaHalmashauri zote nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2013/2014,kazi zifuatazo zitatekelezwa:-

(i) Kupanua mfumo wa kielektroniki wa takwimuna taarifa ili kusaidia masuala ya ufuatiliaji na tathmini yautekelezaji wa mipango na miradi kwenye sekta ya maji(scaling up/out MIS to cover other M&E functions – physicalaspects). Mafunzo yatatolewa kwa watumiaji;

(ii) Utekelezaji wa Mfumo wa kielektroniki wautunzaji na menejimenti ya nyaraka na kumbukumbu(electronic documents & records management system);

(iii) Utekelezaji wa matumizi ya mfumo wakielektroniki wa ukusanyaji wa takwimu na utayarishaji waramani za vituo vya kuchotea maji Vijijini. Vifaa vya kisasavitanunuliwa na mafunzo yatatolewa; na

(iv) Kuendeleza juhudi za Serikali za utekelezaji waSerikali Mtandao (e-Government) kwa kushirikiana na Wakalaya Serikali Mtandao (e-Government Agency). Hii itahusishakujenga uwezo wa Wizara na Taasisi katika matumizi yaSerikali Mtandao ili kuboresha huduma ndani ya Sekta ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jinsia. Wizara yanguimeendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002na Sheria za Maji za mwaka 2009 kwa kuhamasisha uwepowa uwiano wa kijinsia baina ya wanawake na wanaumekwenye vyombo vya kusimamia Sekta ya Maji. Vyombo hivyovina maamuzi makubwa katika usimamizi na matumizi yamaji katika maeneo yao. Asilimia ya wanawake katikavyombo hivyo ni kama ifuatavyo: Wizara (asilimia 33), Bodiya Taifa ya Maji (asilimia 33), Bodi za Mabonde ya Maji (asilimia35), Bodi za Mamlaka za Maji (asilimia 33) na Bodi za Wakala(asilimia 50). Katika mwaka 2013/2014, Wizara yangu

Page 103: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

103

itaendelea kutoa fursa za uwiano kwa jinsia zote katika ngaziza maamuzi na uongozi. Aidha, jamii itaendeleakuhamasishwa kusajili jumuiya za watumiaji maji na kupewamafunzo ya usimamizi wa utekelezaji wa Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji, ambayo yatawashirikishawanaume na wanawake katika jumuiya zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Vita Dhidi ya Rushwa. Katikamwaka 2012/2013, Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi yaRais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilitoamafunzo ya maadili kwa maafisa wakuu wa Wizarayaliyolenga kusisitiza umuhimu wa watumishi kuzingatiamaadili. Katika mwaka 2013/2014, Wizara kwa kushirikianana Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Ummaitatoa mafunzo ya maadili kwa watumishi wengine waWizara yatakayolenga kusisitiza umuhimu wa watumishikuzingatia maadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,Wizara yangu imeendelea na Mpango wa kutekeleza shughulizake kwa uwazi (Open Government Partnership – OGP) kwakuweka taarifa ya mpango wa kati wa mapato na matumizi(MTEF) na taarifa ya fedha ya mwaka 2012/2013 kwenye tovutiya wizara, kuboresha mfumo wa upokeaji malalamikokutoka kwa wadau wa sekta ya maji kwenye tovuti ya Wizara.Watumishi wa Ofisi ya Bonde la Wami – Ruvu na MaafisaMahusiano wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira Miji niwamepatiwa mafunzo juu ya utendaji na utekelezaji waOGP. Katika mwaka 2013/2014, Wizara itaendelea na utoajiwa elimu juu ya OGP katika Ofisi za Mabonde.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu imefunguaDawati la Malalamiko linaloshughulikia malalamiko yawadau mbalimbali wa Sekta ya Maji na ya watumishi. Kwamwaka 2012/2013, Dawati hili limeshughulikia malalamikoyapatayo 59 na kuyapatia ufumbuzi. Malalamiko hayoyalihusu utoaji wa huduma za maji kwa wananchi. Dawatilitaendelea kupokea na kujibu hoja na malalamiko ya wadaukadri yatakavyojitokeza.

Page 104: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

104

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma itaendeleakutoa mafunzo kwa watumishi wa ngazi zote wa Wizarakuhusu namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwenye ofisiya malalamiko iliyoanzishwa na Wizara. Wizara itaendeleakuwakumbusha watendaji na watumishi wote kwa ujumlakufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia Sheria, Kanuni naTaratibu za kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, UKIMWI. Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeendelea kuwapa elimu ya kujikinga dhidi yaVirusi Vya Ukimwi kwa watumishi wa Sekta ya Maji kwa njiambalimbali ikiwa ni pamoja na vipeperushi na machapisho.Aidha, Wizara yangu imeendelea kugharamia lishe kwawatumishi tisa walijiweka wazi kwa mwajiri kuwa wanaishina VVU. Kwa sasa Wizara ipo kwenye maandalizi ya kufanyatathmini ya masuala ya Ukimwi kwa Watumishi wote katikaSekta ya Maji (Situation Analysis). Tathmini hiyo, itatumikakuandaa mpango mkakati (Strategic Action Plan) ambaoutatokana na mapendekezo yaliyojitokeza na hali halisikama ambavyo tathimini itabainisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Maendeleo ya Watumishi.Wizara yangu imeendelea na jitihada za kuboresha mazingiraya kazi kwa watumishi kwa lengo la kuongeza ufanisi nausimamizi wa mipango ya kisekta. Watumishi 100 wa kadambalimbali wanatarajiwa kupandishwa vyeo katika nafasimbalimbali. Katika mwaka 2012/2013, Wizara imepewa kibalicha kuajiri watumishi 63 na ajira mbadala 33 za wataalamwa kada mbalimbali. Hadi kufikia mwezi Machi 2013, Wizaraimepokea watumishi 12 kutoka Sekretarieti ya Ajira. Kati yahao, wahaidrojiolojia wawili, wahandisi wawili, mchumimmoja, afisa maendeleo ya jamii mmoja, maafisa habariwatatu, mhasibu mmoja, opareta wa kompyuta mmoja namkaguzi wa ndani mmoja. Wizara bado inaendeleakufuatilia upatikanaji wa wataalam 63 wa ajira mpyawatakaojaza nafasi za Kada mbalimbali na nafasi 21 za ajirambadala kwa ajili ya kujaza nafasi wazi za kada mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2012/2013,

Page 105: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

105

Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazotekeleza Programuya Maendeleo ya Sekta ya Maji, inaendelea kutekelezampango wa kuwajengea uwezo watumishi (capacitydevelopment plan). Hadi sasa, watumishi 47 wamepatiwamafunzo ya muda mrefu na 389 wamepatiwa mafunzo yamuda mfupi. Katika mwaka 2013/2014, Wizara yanguitaendelea kutekeleza mpango wa kuwapatia watumishimafunzo ambapo watumishi 20 watapatiwa mafunzo yashahada/stashahada ya uzamili yatakayowawezesha kukidhisifa za miundo ya kada mbalimbali za utumishi. Aidhawatumishi 150 watapatiwa mafunzo ya muda mfupiyatakayohusu, huduma bora kwa mteja, stadi zamawasiliano, matumizi sahihi ya teknolojia ya habari namawasiliano pamoja na mfumo wa kupima utendaji kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi wa kujengauwezo wa sekta unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikianana JICA; Jumla ya watumishi 26 walipatiwa mafunzo ya ainambalimbali. Watumishi 19 kutoka Bodi za Maji za Mabondeya Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Rukwa na Bonde la Kati;pamoja na watumishi saba kutoka katika Timu za Maji naUsafi wa Mazingira katika Halmashauri za Singida, Mwanzana Tabora. Kwa mwaka 2013/2014, Wizara itaendeleakuwapatia mafunzo watumishi na wadau wengi zaidi katikakutekeleza mpango wa kuwajengea uwezo watumishi(Capacity Development Plans).

Mheshimiwa Naibu Spika, Uratibu wa Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji. Katika kutekeleza Sera ya Majiya mwaka 2002, Serikali inatekeleza Programu ya Maendeleoya Sekta ya Maji (Water Sector Development Programme 2006- 2025). Programu hiyo ina programu ndogo nne ambazo ni:Programu ya kusimamia na kuendeleza rasilimali za majiinayotekelezwa katika mabonde tisa ya maji nchini;Programu ya maji na usafi wa mazingira Vijijini inayotekelezwakatika halmashauri zote nchini; Programu ya majisafi nauondoshaji wa majitaka Miji ni inayotekelezwa katikaMamlaka za Maji za Miji Mikuu ya Mikoa 19, DAWASA,Mamlaka 109 za Miji Mikuu ya Wilaya na Miji Midogo namiradi ya maji ya kitaifa; na Programu ya kujenga uwezo

Page 106: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

106

kiutendaji na kuimarisha taasisi za sekta ya maji. Programuhiyo inatekelezwa kwa awamu za miaka mitano mitanokuanzia mwaka 2007/2008. Awamu ya kwanza ya miakamitano ya utekelezaji ilianza mwezi Julai, 2007 na ilipangwakukamilika mwezi Juni 2012. Ili kukamilisha miradi mingi,Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo iliamuakuongeza muda wa utekelezaji wa awamu ya kwanzakutoka Juni, 2012 hadi Juni, 2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwa na utekelezajiwenye ufanisi wa Programu, Wizara yangu imekuwa inaratibumikutano ya majadiliano kati ya Serikali, Washirika waMaendeleo na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayohusianana Sekta ya Maji. Lengo la mikutano hiyo ni kupitia,kukubaliana na kutolea maamuzi masuala mbalimbaliyanayohusu utekelezaji wa Programu kama vile, mipangoya upatikanaji wa fedha na bajeti za miradi ya maji na usafiwa mazingira; na kuzijadili changamoto mbalimbalizinazoikabili Programu na kuzitafutia suluhisho. Katika mwaka2013/2014, Wizara itaweka juhudi katika majadiliano hayo iliyawe na matokeo chanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Maandalizi ya Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Pili. Mtaalam Mshaurianayetathmini utekelezaji wa awamu ya kwanza,anaendelea na kazi ambapo tathmini hiyo itahusisha wadauwote wa sekta ya maji ambao watatoa maoni na ushauriwao utakaotumika kuboresha utekelezaji wa awamu ya piliya Programu. Matayarisho ya awamu ya pili yanaendeleaambapo mapendekezo ya muundo wa awamu hiyoyatakamilika mwezi Juni, 2013. Katika awamu hiyo, Serikaliitaweka kipaumbele katika maeneo mbalimbali ikiwa nipamoja na:-

(i) Kukamilisha miradi iliyoanza kutekelezwakatika awamu ya kwanza ikiwemo, miradi ya majisafi na usafiwa mazingira unao tekelezwa na kila Halmashauri na kubainiVijiji vya ziada ili vipatiwe maji;

(ii) Kukamilisha Mpango wa dharura wa maji

Page 107: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

107

katika Jiji la Dar es Salaam, kuendelea kutafuta vyanzo vipyavya maji kukidhi mahitaji makubwa ya maji na kuboreshahuduma za majitaka Jijini;

(iii) Ujenzi wa miradi ya maji Miji Mikuu ya Wilayana Miji Midogo na kuendelea kuboresha huduma za majikatika Miji Mikuu ya Mikoa kukidhi mahitaji yanayoongezekakwa haraka; na

(iv) Kuanza utekelezaji wa mipango shirikishi yausimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji na ujenzi wamabwawa makubwa na uchimbaji wa visima katika kukidhimahitaji ya maji kwa sekta mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza bajeti ya2012/2013, Wizara ilikabiliana na changamoto mbalimbaliwakati wa utekelezaji. Changamoto zilizojitokeza na hatuazinazochukuliwa kuzikabili kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuongezeka kwa idadi yawatu na shughuli za kiuchumi na kijamii. Utoaji wa hudumaya maji unakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwaidadi ya watu kusikoendana na uwekezaji. Hali hiyo ni dhahirikatika maeneo ya Miji ni ambapo kiwango cha ongezekowatu kwa mwaka ni asilimia 4.5 tofauti na maeneo ya Vijijiniambapo wastani wa ongezeko la watu kwa mwaka kitaifani asilimia 2.3. Mathalan, Jiji la Dar es Salaam linakabiliwa nauhaba mkubwa wa maji kutokana na ongezeko kubwa lawatu la asilimia 5.5 kwa mwaka tofauti na wastani kitaifawa asilimia 4.5. Ongezeko jingine ni kukua kwa shughuli zakiuchumi ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la viwandana kupanuka kwa ujenzi wa makazi. Kutokana na ukuaji huowa kasi, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbaliikiwa ni pamoja na:-

(i) Kushirikisha wananchi hususan katika maeneoya Vijijini katika hatua zote za miradi ikiwa ni pamoja nakubuni, kujenga, kusimamia, kuendesha na kuchangiagharama za uendeshaji; na

Page 108: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

108

(ii) Kukarabati na kujenga miradi ya kipaumbeleambayo inatoa huduma kwa wananchi wengi zaidi ikiwa nipamoja na ujenzi wa mradi wa maji wa Vijiji 10 kwa kilaHalmashauri; Mradi wa dharura wa kuboresha huduma zamaji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga bwawala Kidunda na kuchimba visima vya maji vya Mpera na Kimbiji,kujenga Mradi wa Maji wa Mwanga-Same-Korogwe, kujengaBwawa la Farkwa kwa ajili ya mji wa Dodoma na kutekelezamradi wa maji wa Masasi-Nachingwea.

Mheshimiwa Naibu Spika, hujuma kwenyemiundombinu ya maji. Biashara ya vyuma chakavuimechangia kwa kiasi kikubwa uharibufu kwenyemiundombinu ya maji hali inayoathiri upatikanaji wa hudumaya majisafi na uondoaji wa majitaka kwa jamii. Serikaliimekuwa ikitoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa ulinzishirikishi katika kulinda miundombinu ya maji kupitiamaonesho na shehere mbalimbali za kitaifa kupitia Wiki yaMaji na maigizo kwenye luninga na redio pamoja nausambazaji wa vipeperushi. Aidha, Mamlaka za Majisafi Mijini zimeendelea kushirikiana na Uongozi wa Mikoa, Jeshi laPolisi na Wananchi ili kubaini wanaojihusisha na hujuma hizoikiwa ni pamoja na kutoa Zawadi ya fedha kwa watoataarifa. Vilevile, Wizara imetoa Waraka kwa Mamlaka zotenchini kutokununua vifaa vya maji vilivyotumika kama vilemita za maji, mabomba na vipuli vya mitambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya tabianchi.Mabadiliko ya tabianchi yanasababisha kutokutabirika kwamsimu na mtawanyiko wa mvua, ukame wa muda mrefu,mafuriko ya mara kwa mara hali inayoathiri ujenzi wamiundombinu ya maji na upatikanaji wa rasilimali za maji.Hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto hiyo nipamoja na:-

(i) Kujenga mabwawa madogo na makubwakwa ajili ya hifadhi ya maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali;

(ii) Kuimarisha ukusanyaji wa takwimu zinazohusurasilimali za maji na mabadiliko ya tabianchi;

Page 109: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

109

(iii) Kutoa mafunzo kwa wataalam na kuelimishaumma ili kuongeza weledi kuhusu mabadiliko ya tabianchi;

(iv) Kutumia utaalam asil ia ( Indigenousknowledge) katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi;

(v) Kushirikisha wadau mbalimbali katika kutunzavyanzo vya maji kwa kuvitambua na kuviwekea mipaka,kupanda miti, kuzuia shughuli za kiuchumi na kijamii katikamaeneo oevu, maeneo ya milimani na katika chemchem,kudhibiti matumizi holela ya maji kwa kutoa kibali chakutumia maji na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji nauharibifu wa mazingira kwa kutumia Sheria za Maji, Mazingirana Sheria ya Misitu pia kwa kutumia sheria ndogo ngazi zahalmashauri;

(vi) Kuendeleza matumizi ya teknolojia sahihi zaumwagiliaji zinazotumia maji kwa ufanisi; na

(vii) Kushirikiana na taasisi za kiserikali na zisizo zakiserikali zinazofanya utafiti kuhusu mabadiliko ya tabianchikwa lengo la kufanya utafiti wa pamoja na kutathminimatokeo ya tafiti mbalimbali ili kukabiliana na mabadilikoya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupungua kwa rasilimali zamaji. Pamoja na nchi yetu kuwa na maji mengiyanayopatikana kwenye mito, Maziwa, chini ya ardhi namaeneo oevu, baadhi ya maeneo hukumbwa na uhaba wamaji kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Vilevile, majiyanayofaa kwa matumizi mbalimbali yanaendelea kupunguamwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la watu,ongezeko la uzalishaji mali katika sekta mbalimbali ikiwa nipamoja na uzalishaji wa umeme, kilimo cha umwagiliaji, namatumizi ya viwandani na majumbani. Aidha, uharibifu wamazingira na ukataji ovyo wa misitu na uharibifu wa maeneooevu hupunguza sana rasilimali za maji. Katika kukabilianana changamoto hiyo Serikali inaendelea kusimamia nakuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa dhidi ya uharibifuna uchafuzi na kuhakikisha maji yanatumika kwa njia

Page 110: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

110

endelevu kwa kutumia sheria za maji na kanuni zake nakuzihimiza Halmashauri kutunga sheria ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati mwingine wakukabiliana na uhaba wa maji ni kuweka muundo bora wakitaasisi kwa ajili ya usimamizi endelevu wa raslimali za majikatika mabonde ya maji kwa kuhakikisha uwepo wamgawanyo yakinifu na matumizi bora ya maji kwa ajili yamahitaji ya kijamii na kiuchumi. Vilevile, Serikali itaendeleakusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 11 ya mwaka 2009 yaUsimamizi wa Rasilimali za Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji Kidogo waFedha kwa Sekta ya Maji. Changamoto nyingine inayoikabiliWizara yangu kwa kipindi kirefu sasa ni kuendelea kupatabajeti kidogo ya fedha za matumizi mengineyo (OC) na fedhaza ndani za kutekeleza miradi ya maendeleo. Viwangovinavyokasimiwa na kutolewa kwa Sekta ya Maji, huwapungufu ya kiwango kinachoidhinishwa na kutolewa kwakila mwaka. Mathalani, Fedha za ndani zilizoidhinishwa kwamwaka 2012/2013 ni shilingi bilioni 140.016 hadi kufikia mweziMachi, 2013 jumla ya shilingi bilioni 29.000 zilizotolewa sawana asilimia 20.7 ya fedha zilizokasimiwa. Fedha za matumizimengine (OC) zilizoidhinishwa katika mwaka mwaka 2012/2013 ni Shilingi bilioni 3.8 hii ikiwa ni asilimia 23 ya Shilingi bilioni16.5 zilizoombwa kukidhi mahitaji ya msingi ya kuiwezeshaWizara ya Maji kujiendesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hali hiyo,Wizara imekuwa na malimbikizo makubwa ya madeniyanayofikia Shilingi bilioni 10.2. Mchanganuo wa madenihayo ni pamoja na malimbikizo ya madeni ya watumishiilkiwa ni stahili zao za ajira, Shiling bilioni 2.8, malimbikizo yamadeni ya wazabuni watoa huduma Wizarani Shilingi bilioni2.2 na malimbikizo ya ankara za umeme za mamlaka darajaB na C na miradi ya kitaifa Shilingi bilioni 5.2. Malimbikizo yamadeni ya wakandarasi wanaotekeleza miradi yamaendeleo yaliyofikia Shilingi bilioni 19. Kiwango cha fedhaza maendeleo kilichokasimiwa na kutolewa kuanzia mwaka2006/2007 hadi mwezi Machi, 2013 ni kama ifuatavyo:

Page 111: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

111

Kiwango cha fedha za ndani za maendeleokilichokasimiwa na kutolewa kwa Wizara ya Maji

kuanzia 2006/2007 hadi 2011/2012

Na. Mwaka Kiasi kili- Kiasi kilicho- chokasimiwa tolewa

1 2006/2007 77,864,997,000 53,570,000,0002 2007/2008 70,754,004,000 55,193,116,2363 2008/2009 46,463,379,000 36,463,379,0004 2009/2010 50,463,379,000 15,847,952,3755 2010/2011 30,721,712,000 25,004,329,0716 2011/2012 41,565,045,000 24,746,549,5227 2012/2013 140,015,967,000 29,000,000,000*

*Kiwango cha fedha kilichotolewa Robo ya kwanza naya pili 2012/2013

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha fedhazilizoidhinishwa kwa ajil i ya utekelezaji wa miradi yaMaendeleo zinatolewa kwa wakati na kwa kiwango chakuridhisha, Wizara imeimarisha mawasiliano na wadauhususan Wizara ya Fedha na Washirika wa Maendeleo kwakuchukua hatua zafuatazo:-

(i) Kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Fedha(HAZINA) na Washirika wa Maendeleo katika hatua zote zakuandaa bajeti ya mwaka ya Wizara ili kupanga vipaumbelevya kutekeleza kulingana na fedha za ndani ambazo tunauhakika wa kuzipata;

(ii) Kuandaa na kuwasilisha kwa wakati MpangoKazi (Action Plan) wa kutekeleza bajeti ya mwaka pamojana mahitaji ya fedha kwa kila kipindi cha Robo mwakaWizara ya Fedha na Tume ya Mipango. Mpango kazi huondiyo unaotumika katika utoaji wa fedha kwa upande waSerikali na Washirika wa Maendeleo;

(iii) Kuandaa na kuwasilisha kwa wakati taarifaza utekelezaji wa miradi Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango

Page 112: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

112

na kwa Washirika wa Maendeleo kwa lengo la kupatiwafedha kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa kwa ajiliya utekelezaji katika kipindi cha Robo mwaka inayofuatia;na

(iv) Kufanya majadiliano na Washirika waMaendeleo (Wahisani) juu ya utoaji na matumizi ya fedha zaWSDP. Majadiliano hayo yamewezesha kukubaliana kuanzautoaji wa fedha kwa kipindi cha miezi sita sita badala yautaratibu wa kutoa fedha kidogo kidogo kulipa madeni yawakandarasi. Hatua ya kuanza kutoa fedha za miezi sitakuanzia robo ya pili ya 2012/2013 ni baada ya Wizarakuboresha mfumo wake wa utunzaji wa taarifa za fedha nakuimarisha mfumo wa usimamizi kutekeleza miradi ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa Wataalamwa Maji. Sekta ya Maji nchini inakabiliwa na upungufumkubwa wa wataalam kutokana na serikali kutoajiri kwamuda mrefu, kustaafu kwa wataalam wa maji, watumishiwapya kuacha kazi na ikama mpya ya Muundo waSektretariati za Mikoa ambayo imeifanya Sekta ya Maji kuwaidara kamili. Mahitaji ya wataalam ni kama ifuatavyo:-

(i) Watumishi wa wizara wanaotakiwa ni 1,801waliopo ni 1,558;

(ii) Wahandisi wanaotakiwa kwenye Sekretariatiza Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara ni 100 lakini waliopo ni 24tu, Wahaidrojiolojia wanapaswa kuwa 25 waliopo ni 3,wataalam hawa watasaidia kufanya utafiti wa maeneoyanayofaa kuchimbwa visima;

(iii) Wahandisi wa Maji wanaotakiwa kwenyeHalmashauri zote ni 760 waliopo ni 147 Mafundi Sanifuwanaotakiwa kwenye Halmashauri ni 1,672 waliopo ni 182,wanahitajika kwenye ujenzi, uendeshaji na kufanyamatengenezo ya miradi ya maji;

(iv) Mafundi Sanifu Wasaidizi wanaotakiwa ni2,880 lakini waliopo ni 329, wanahitajika kuwasaidia mafundi

Page 113: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

113

Sanifu kufanya kazi za mikono na kiufundi kwenye Miradi yaMaji inayotekelezwa nchini na kufanya matengenezo yamiradi ya maji Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na upungufuwa watumishi, Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma imewahamishia kwenyehalmashauri mafundi sanifu 39 waliokuwa kwenye ofisizilizokuwa za Wahandisi wa Maji wa Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda sasa kutumia fursahii kuwashukuru wale wote waliochangia kuiwezesha Wizarayangu kufanikisha majukumu yake. Nakiri kwamba mafanikioyaliyopatikana katika mwaka 2012/2013 ni kutokana najitihada za pamoja, ushirikiano na misaada ya kifedha nakitaalam kutoka kwa washirika wa maendeleo, ikiwa nipamoja na nchi wahisani, mashirika ya misaada ya kimataifa,taasisi zisizo za kiserikali, mashirika ya kidini na taasisi zakifedha. Napenda kuzishukuru Serikali za Ujerumani, Uholanzi,Uingereza, Marekani, Japan, Ufaransa, China, Uswisi, Ubeligiji,Ireland, Korea ya Kusini, Sweden, Denmark, Norway, India naMisri.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, napenda kutoashukrani kwa taasisi za fedha za kimataifa ikiwa ni pamojana Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), Benki ya Maendeleoya Ufaransa (AFD), Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya(EIB), Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (BADEA), Mfukowa Maendeleo wa Nchi Zinazozalisha Mafuta (OPEC Fundfor International Development-OFID), Mfuko wa Maendeleowa Saudi (SFD) Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Marekani laChangamoto za Milenia (MCC), Shirika la Misaada yaMaendeleo la Norway (NORAD), Taasisi ya Maendeleo yaUingereza (DFID), Shirika la Kiufundi la Ujerumani (GIZ), Mpangowa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNDP), Shirika laUshirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), Mpango wa Umojawa Mataifa wa Makazi Duniani (UN Habitat), Shirika la Umojawa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Misaadaya Maendeleo la Sweden (SIDA), Shirika la Misaada ya

Page 114: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

114

Maendeleo la Canada (CIDA), Shirika la Misaada yaMaendeleo la Denmark (DANIDA), na Shirika la Misaada laMarekani (USAID) kwa misaada ya fedha na michango yaoya kitaalam katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu namalengo ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nayashukuru pia, mashirikaya kidini ya World Islamic League, Shirika la Ahmadiya MuslimJamaat Tanzania, Islamic Foundation, Kanisa la Kiinjili laKilutheri Tanzania, Kanisa la Kilutheri la Ujerumani, Baraza Kuula Waislam Tanzania, Kanisa Katoliki Tanzania, Kanisa laKianglikana Tanzania, Catholic Agency for Overseas Aid andDevelopment (CARITAS), Adventist Development Relief Agency(ADRA), Norwegian Church Aid na Livingwater International.Nashukuru pia, taasisi zisizo za kiserikali za Tanzania Waterand Sanitation Network (TAWASANET), Wahamasishaji wa Maji,Maendeleo na Afya (WAMMA), Southern HighlandsParticipatory Organizasition (SHIPO), WaterAid, World Vision,Plan International, Concern Worldwide, NetherlandsVolunteers Services (SNV), Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Uasilina Mali Asili (IUCN), , World Wide Fund for Nature (WWF), AfricanMedical Research Foundation (AMREF), Clinton HIV AidsInitiative (CHAI) na Bill and Melinda Gates Foundation, nawale wote ambao kwa njia moja au nyingine wameendeleakuisaidia Sekta ya Maji kufanikisha malengo yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hiikutoa shukurani zangu za dhati kwa Mheshimiwa MhandisiDr. Binilith Satano Mahenge (Mb), Naibu Waziri wa Maji, kwamsaada na ushirikiano anaonipatia katika kuiongoza Wizaraya Maji. Naomba pia, nitoe shukurani zangu kwa MhandisiChristopher Nestory Sayi, Katibu Mkuu, Mhandisi Bashir JumaMrindoko, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi wote na Wakuuwa Vitengo, Maafisa na Watendaji Wakuu wa Mashirika,Wakala na Taasisi zilizo chini ya Wizara yangu, wataalam nawatumishi wote kwa kujituma katika kusimamia utekelezajiwa majukumu tuliyopewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuishukuru familiayangu kwa upendo na kunipa kila msaada ili niweze kumudu

Page 115: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

115

majukumu yangu. Mke wangu Kudula Maghembe yuko hapa,kwenye gallary. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa kutoa hojakwamba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya shilingi398,395,874,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara yangu kwamwaka 2013/2014, ili Wizara iweze kutekeleza majukumu namalengo yaliyoelezwa katika hotuba hii. Kati ya fedha hizo,Matumizi ya Kawaida ni shilingi 18,952,654,000 ambapo shilingi13,319,877,000 ni Mishahara ya Watumishi (PE), na shilingi5,632,777,000 ni fedha za Matumizi Mengine (OC). Jumla yaBajeti ya Maendeleo ni shilingi 379,443,220,000 ambapo katiya fedha hizo shilingi 138,266,164,000 ni fedha za ndani nashilingi 241,177,056,000 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tena nitoeshukurani zangu za dhati kwako wewe mwenyewe na kwaWaheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii piainapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Maji kwa anwani:www.maji.go.tz.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa Hoja.(Makofi)

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa ProfesaMaghembe kwa hotuba yako na hoja imetolewa naimeungwa mkono. Tunakushukuru sana kwa kutusomeahotuba nzuri sana. Kwa niaba ya Waheshimiwa Wabungenimshukuru Mama Kudula Maghembe kuwepo maanamambo haya pressure inaweza ikapanda, ikashuka, sasaangalau mama anakuwa karibu kidogo. (Makofi/Kicheko)

Mwenyekiti wa Kamati!

Page 116: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

116

MHE. SAIDI J. NKUMBA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATIYA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwamujibu wa Kanuni ya 99 (7) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007,kwa niaba ya Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilishataarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo naMaji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maji kwamwaka wa fedha 2012/2013 na makadirio ya mapato namatumizi kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ni hitaji la msingi lamaisha na uhai wa viumbe vyote. Aidha, shuguli mbalimbaliza maendeleo ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa umeme nabidhaa za viwandani, matumizi ya majumbani na usafi wamazingira zinategemea uwepo wa maji ya kutosha. KatikaNchi yetu huduma ya maji bado haijatosheleza mahitaji hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wamajukumu yake, Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji ilikutana na Wizara ya Maji tarehe 26-27 Machi,2013 katika Ofisi ndogo ya Bunge ya Dar es Salaam na tarehe17 April, Bungeni Dodoma, ili kuchambua taarifa yautekelezaji wa Bajeti, utekelezaji wa maoni ya Kamati,changamoto zilizojitokeza kwa mwaka 2012/2013 nakuchambua makadirio ya mapato na matumizi ya Wizarakwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa kupitia nakuchambua taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwamwaka 2012/2013, Kamati ilitoa maoni na ushauri kwaSerikali. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, kwa kiasikikubwa Serikali imeyafanyia kazi maoni na ushauri waKamati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla Kamatiimeridhika na utendaji wa Wizara isipokuwa kwa maeneoambayo utekelezaji wake ulikwamishwa na upungufu naucheleweshwaji wa fedha pamoja na sababu mbalimbaliza kiutendaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada kubwa

Page 117: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

117

zinazofanywa na Wizara katika kutekeleza majukumu yake,Wizara inakumbana na changamoto mbalimbali ambazozimekuwa ni kikwazo katika kufikia malengo iliyojiwekea.Baadhi ya changamoto hizo ni:-

(a) Kiasi kidogo cha fedha zinazotengwa naucheleweshwaji wa utoaji wa fedha za maendeleo na hivyokuathiri kasi ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ya Wizara;

(b) Hujuma kwenye miundombinu ya maji,ambapo biashara ya chuma chakavu imechangia kwa kiasikikubwa uharibifu wa miundombinu ya maji. Hali hii inaathiriupatikanaji wa huduma ya maji safi na uondoaji wa majitaka kwa jamii;

(c) Kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuliza kiuchumi na kijamii nchini. Kwa mfano katika maeneo yaMiji ni miundombinu ya maji ni ya zamani na chakavu hivyokusababisha wananchi wengi kutofikiwa na huduma ya maji;

(d) Mabadiliko ya tabianchi yamesababishakutotabirika kwa msimu na mtawanyiko wa mvua. Hiiimesababisha ukame wa muda mrefu na kukauka kwavyanzo vya maji kwa baadhi ya maeneo. Maeneo mengineyamekumbwa na mafuriko;

(e) Uchafuzi wa vyanzo vya maji kutokana namatumizi ya kemikali katika maeneo ya uchimbaji wamadini; na

(f) Kutopatikana kwa wakati takwimu sahihi nataarifa za utekelezaji wa programu kushirikisha taasisimbalimbali ambazo Wizara ya Maji haina mamlaka nazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, maombi ya fedha namalengo ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha2013/2014, Wizara ya Maji chini ya Fungu 49 inaomba jumlaya shilingi 398,333,474,000/=. Kati ya fedha hizo, shilingi18,890,254,000/= ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi

Page 118: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

118

379,443,220,000/= ni kwa ajili ya Miradi ya maendeleo. Kati yafedha za maendeleo, shilingi 138,266,164,000/= ni fedha zandani na shilingi 241,177,056,000/= ni fedha kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi zinazoombwahazikidhi kabisa mahitaji ya msingi ya Wizara ambayo ni kutoahuduma ya maji kwa makundi mbalimbali ya jamii. Kamatiimepitia kwa undani taarifa ya bajeti na kugundua kuwaWizara ya Maji kwa kipindi kirefu imekuwa ikipata bajetindogo kutoka fedha za ndani kutekeleza miradi yamaendeleo na fedha za matumizi mengine. Aidha, fedhazinazoidhinishwa na Bunge hazitolewi zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile Kamati ilibaini kuwamakubaliano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleowanaogharamia kutekeleza Programu ya Maendeleo yaSekta ya Maji (WSDP) ni kuwa Serikali itachangia Shilingi bilioni75 kila mwaka katika awamu ya Kwanza (2007/2008 – 2013/2014). Hata hivyo, kiwango hicho hakijawahi kufikiwa kamainavyoonyeshwa katika jedwali Na. 1

Jedwali Na.1 Mtiririko wa fedha za maendeleounaotolewa na Serikali

Na. Mwaka Kiasi kilicho- Kiasi kilicho- Kiwango kasimiwa tolewa kilichoto- lewa dhidi ya Ahadi ya Serikali ya Shs. Bilioni 75

1 2006/2007 77,864,997,000 53,570,000,000 71%2 2007/2008 70,754,004,000 55,193,116,236 74%3 2008/2009 46,463,379,000 36,463,379,000 49%4 2009/2010 50,463,379,000 15,847,952,375 21%5 2010/2011 30,721,712,000 25,004,329,071 33%6 2011/2012 41,565,045,000 24,746,549,522 33%7 2012/2013 140,015,967,000 29,000,000,000* 39%

*Kiwango cha fedha kilichotolewa hadi mwezi Machi,2013

Page 119: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

119

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuongezekakwa mahitaji ya usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wamiradi ya maji inayotekelezwa nchi nzima,kiasi cha fedhazinazotengwa kwa matumizi ya kawaida (OC) zimekuwazikipungua mwaka hadi mwaka kama ilivyoonyeshwa katikajedwali Na.2

Jedwali Na.2 Mtiririko wa fedha za matumizimengine zinazotolewa na Serikali:

Mwaka Kiasi (Tsh).

2006/2007 Bilioni 16.82007/2008 Bilioni 8.72008/2009 Bilioni 9.52009/2010 Bilioni 9.52010/2011 Bilioni 6.62011/2012 Bilioni 4.32012/2013 Bilioni 3.8

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za ndani za miradiya maendeleo ziliendelea kushuka wakati mahitaji yautekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan ngazi zaHalmashauri, Mij i ya Wilaya na Miji Midogo. Hali hiiinasababisha miradi ya maji katika ngazi hizo kutekelezwakwa kasi ndogo na kusababisha miradi kutokukamilika kwawakati au kutotekelezwa kabisa kutokana na ukosefu wafedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwenendo huu wauchangiaji mdogo wa Serikali katika ujenzi wa miradiunawakatisha tamaa Washirika wa Maendeleowanaochangia katika Programu ya Maji. Hali hii inawezakuwa tatizo katika uchangiaji wa Washirika hao waMaendeleo katika Awamu ya Pili ya miaka mitano yaProgramu itakayoanza kutekelezwa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni na ushauri waKamati kwa Wizara kwa mwaka wa fedha 2013/2014.Nyongeza ya fedha. Kamati hairidhishwi na kitendo cha

Page 120: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

120

Serikali kupunguza bajeti ya maji ambayo mahitaji yakeyanaongezeka kwa kasi mwaka hadi mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mtirir ikoulivyoonyeshwa katika Jedwali na 1 & 2, Kamati inaishauriSerikali ione umuhimu wa kutoa fedha zote na kwa wakatizinazoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huu,Kamati inaiomba Serikali kuiongezea fedha Wizara hii ili iwezekutekeleza majukumu yake ya msingi na kupunguza tatizola maji hasa maeneo ya Vijijini ambako tatizo ni kubwa zaidi.(Makofi)

Kamati inaishauri Serikali kuiongezea Wizara kiasi chashilingi bilioni 184.5 za ziada kwa matumizi yafuatayo:-

(a) Kuendeleza utekelezaji wa Programu yaupelekaji maji Vijiji katika kumi, kwa kuongeza Vijiji viwili auvitatu katika kila Halmashauri kwa gharama ya shilingi bilioni65. Hatua hii itaongeza huduma ya maji kwa wananchiwapatao 980,000 hadi Juni, 2014. (Makofi)

(b) Kujenga miundombinu ya kuwasambaziamaji wananchi kutoka katika mabwawa kumi yaliyojengwakatika Wilaya kame kwa gharama ya shilingi bilioni 13. Hatuahii itawapatia huduma ya maji safi na salama wananchiwapatao 480,000 pamoja na mifugo yao ifikapo Juni, 2014.

(c) Kujenga miundombinu ya pampu namabomba ya kuwasambazia maji wananchi kutoka katikavisima virefu vya maji vilivyochimbwa katika maeneombalimbali nchini. Gharama za kutekeleza kazi hiyo ni shilingibilioni 11.2 na utawapatia huduma ya maji safi na salamawananchi wapatao 640,000 pamoja na mifugo yao ifikapoJuni, 2014.

(d) Kupanua, kukarabati na kujengamiundombinu kwenye miradi katika Wilaya mbalimbali

Page 121: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

121

ambayo kwa sasa haitoi huduma ipasavyo kutokana nauchakavu kwa gharama ya shilingi bilioni 10.8. Wananchiwapatao 440,000 watanufaika ifikapo Juni, 2014.

(e) Kujenga miundombinu ya kusambaza majikwa wananchi kutoka katika miradi mikubwa ambayousanifu umekamilika na miradi mikubwa inayohitajiukarabati. Miradi hii itahitaji jumla ya shilingi bilioni 8.

(f) Kufanya usanifu na ujenzi wa mradi wa Ugala,Urambo na Kaliua – Mkoa wa Tabora. Mradi huu utagharimushilingi bilioni 12.1.

(g) Miradi mingine iliyoainishwa kwenye taarifa yaWaziri itakayoleta matokeo ya haraka itagharimu shilingibilioni 53.568. Miradi hiyo itahudumia watu 614,780.

Mheshimiwa Naibu Spika, kodi za madawa ya maji.Kamati inaipongeza Serikali kwa kupunguza Kodi zaOngezeko la Thamani (VAT) kwenye madawa ya kutibia majikutoka 18% hadi 9.9%. Hata hivyo, Kamati inaendeleakuisisitiza Serikali kuiondoa kabisa kodi hii na kuwa 0% (zerorated) ili gharama za maji zipungue. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mgawanyo wa bajeti. Kamatiimebaini kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya bajetiinayotengwa kwa ajili ya maji Mijini na Vijijini. Matokeo yakeni kwamba, watu wanaopata maji safi na salama Mijini niasilimia 86 na Vijijini ni asilimia 58.6 tu ikizingatiwa kwambaasilimia 80 ya Watanzania wanaishi Vijijini. Kamati inaishauriSerikali kuongeza bajeti ya maji Vijijini ili kupunguza tatizokubwa la maji linalokabili maeneo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vyanzo vya maji. Kwa kuwamahitaji ya maji yanaongezeka siku hadi siku kutokana naongezeko la watu, mifugo pamoja na shughuli za kiuchumina kijamii, vyanzo vingi vya maji nchini vimeanza kukauka.Kamati inaishauri Serikali pamoja na wananchi kutunzavyanzo vyake vya maji.

Page 122: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

122

Mheshimiwa Naibu Spika, uvunaji wa maji. Kwa kuwauhaba wa maji ni tatizo kubwa kwa nchi yetu, Kamatiinaishauri Serikali iendelee kuhimiza na kuhamasisha jamii kwakutoa elimu ya utaratibu wa uvunaji wa maji ya mvua kwakutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wamabwawa, malambo na uvunaji wa maji ya paa. Aidha,Serikali ihimize Halmashauri kutunga sheria ndogo ili kuwepona utaratibu wa uvunaji wa maji ya mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Mradi wa Majikatika Vijiji Kumi. Mradi huu ulipoanzishwa ulionekana wenyetija na kwamba ungepunguza tatizo la maji Vijijini kwakiwango kikubwa. Aidha, visima vinavyochimbwa nivichache na baadhi havitoi maji na vingine hutoa maji kwamuda mfupi. Kamati inasisitiza Serikali kufanya yafuatayo:-

(a) Serikali ione umuhimu wa kuongeza fedha zandani ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huu.

(b) Serikali iangalie namna ya kupunguzagharama kwa kuipa kampuni moja kufanya kazi ya upimajina uchimbaji. Utaratibu huu utarahisisha uwajibikaji iwapomaji hayatapatikana na hata gharama zitapungua. (Makofi)

(c) Serikali ipitie upya Sheria ya Manunuzi(PPRA,2004) ili kupunguza gharama za miradi na urasimu.

(d) Kwa kadri inavyowezekana, Serikaliinashauriwa kutumia Wataalam Waelekezi wetu badala yakutumia wataalam toka nje kwa nia ya kupunguza gharama.(Makofi)

(e) Maeneo yenye madini kama chumvi nafluoride, yaangaliwe namna ya kupata maji kwa njia nyinginekama mabwawa ili kupunguza athari zinazoweza kutokanana matumizi ya maji hayo.

(f) Serikali iendelee kutoa elimu kwa wananchikuhusu ubora na utunzaji wa pampu za maji ili kuepukauharibifu unaotokana na matumizi yasiyo sahihi.

Page 123: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

123

Mheshimiwa Naibu Spika, uharibifu wa Miundombinuya Maji. Kamati imebaini kuwa maeneo mengi ambayomiundombinu yake imeharibiwa ni kwa sababu pamoja namambo mengine ya biashara ya chuma chakavu ambapowananchi wahalifu wanabomoa miundombinu ya maji.Kamati inashauri Serikali kuangalia uwezekano wa kujengamiundombinu isiyotumia chuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, miundombinu chakavu. Kamatiimebaini kuwa maji mengi hupotelea njiani kabla ya kumfikiamtumiaji kwa sababu ya miundombinu chakavu. Kamatiinaishauri Serikali kufanya ukarabati wa miundombinu hiyona kudhibiti wizi wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho. Napenda kukushukurukwa kunipa nafasi ya kuwasilisha Taarifa hii. Aidha, natoashukrani zangu za dhati kwa wajumbe wa Kamati kwaushirikiano na kazi nzuri wanayofanya. Wajumbe wa Kamatini hawa wafuatao:-

Mheshimiwa Prof. Peter Mahamudu Msolla-Mwenyekiti,Mheshimiwa Said J. Nkumba-Makamu Mwenyekiti,Mheshimiwa Prof. David Homeli Mwakyusa, MheshimiwaSubira Mgalu, Mheshimiwa Asaa Othman Hamad,Mheshimiwa Abdusalaam S. Ameir, Mheshimiwa AbdallaHaji Ali, Mheshimiwa Namelok E. M. Sokoine, MheshimiwaDkt. Christine G. Ishengoma, Mheshimiwa Sylvestry FrancisKoka, Mheshimiwa Moshi S. Kakoso, Mheshimiwa Kheri KhatibAmeir, Mheshimiwa Meshack Jeremia Opulukwa, MheshimiwaPhilemon Kiwelu Ndesamburo, Mheshimiwa Sadifa JumaKhamis, Mheshimiwa Mch. Peter Simon Msigwa, MheshimiwaAmina Nassoro Makilagi, Mheshimiwa Donald Kelvin Max,Mheshimiwa Magdalena Hamisi Sakaya, Mheshimiwa HajiJuma Sereweji, Mheshimiwa Jitu Vrajlal Soni, Mheshimiwa Dkt.Lucy Sawere Nkya na Mheshimiwa Lolesia Masele Bukwimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo,sasa naliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinishamakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji Fungu49 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 jumla ya shilingi

Page 124: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

124

398,333,474,000/= na nyongeza inayoombwa ya shilingi bilioni184.5. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Said Nkumbakwa maoni hayo ya Kamati ambayo ni mazuri sana. Sasanaomba kumwita Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusuWizara hii ya Maji, naye ni Mheshimiwa Cecilia Pareso.

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI YA UPINZANI WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Msemaji wa KambiRasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha hotuba kuhusumakadirio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Maji kwamwaka wa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la upatikanaji wa majisafi na kuweza kushughulikia majitaka ni sehemu yamakubaliano ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhiakuingia mathalani Malengo ya Milenia (MDGs); lengo nambasaba (7) shabaha 10; la kupunguza nusu ya watu waoishibila maji safi na salama ya kunywa na usafi wa msingi katikamazingira wanayoishi. Hatua za haraka za kuboreshaupatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka nimuhimu kama sehemu ya haki za binadamu. Jambo hili linatija pia katika uzalishaji mali na uchumi wa nchi kwa kuwatafiti zinaonyesha kwamba kudumu kwa matatizo hayokunazigharimu nchi za Afrika, Tanzania ikiwemo wastani waasilimia sita (6) ya pato la taifa (Gross Domestic Product).

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti uliofanywa naStockholm Environment Institute kwa kushirikiana na Benkiya Maendeleo Afrika mwaka 2006 kuhusu uhusiano kati yamaji na umaskini Afrika kwa kutumia mfano wa nchi yetu(Water and Poverty Linkages in Africa: Tanzania Case Study)umebainisha wazi kwa vielelezo namna ilivyo vigumu kupima

Page 125: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

125

Tanzania inavyosonga mbele katika utekelezaji wa malengoya maendeleo ya milenia yanayohusu maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, utafiti huo umeelezanamna ambavyo bila kushughulikia kwa haraka matatizoya maji j it ihada za kupambana na kupunguza nakutokomeza umaskini zitakuwa ni ndoto kwani hatutawezakupiga hatua ya maana katika mapambano hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kwa kadiri yaTathmini ya Hali ya Watu na Afya ya mwaka 2010(Demographic and Health Survey, 2010); ni asilimia 4.8 tu yakaya zilizopo Vijijini ndiyo zinazopata maji katika eneo lao lakaya (water on premises) wakati ni asilimia 19.4 tu ya kayakwa Mijini ndizo zenye maji katika kaya zao. Hivyo kaya nyingiza Tanzania zinawekwa katika mazingira hatarishi kwamagonjwa ya mlipuko na mengine ambayo si ya mlipukokutokana na uhaba wa maji, ambapo inaelezwa kuwa halini tete zaidi katika maeneo yasiyopimwa yenyemsongamano mkubwa wa watu katika maeneo ya Majijina Miji mbalimbali (slums) hapa nchini mwetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la maji ni kubwa kulikotunavyofikiria na hasa Vijijini. Vijiji vingi havina huduma yamaji ya uhakika na hii inatokana na sababu nyingi. Vipo Vijijiambayo miundombinu ya maji ilijengwa zaidi ya miaka 30iliyopita na kwa kuwa haukuwepo mfumo endelevu wakuikarabati, sehemu kubwa imekuwa ni chakavu na majimengi kupotea, vyanzo vya maji vingi kupungua maji navingine kukauka kabisa kutokana na madhara yamabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa idadi ya watukulinganisha na wakati vyanzo na miundombinu hiyoilipokuwa inawekwa. Hivyo basi, ni bora ufanyike ukaguzihakiki (inventory) upya wa miundombinu na vyanzo vya majikwa kila kijiji ili kujua ni Vijiji vingapi na watu wangapiwanapata huduma ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali hii ya ukosefu wa maji

Page 126: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

126

safi na salama kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetuimeathiri sana uzalishaji mali kwani imesababisha nguvu kazikubwa kupotea kutokana na muda mwingi kutumika katikakufuatilia maji muda wa uzalishaji na hata kinamama wengiambao ndio nguzo muhimu ya uzalishaji, wamejikutahawana muda wa kutosha kwenye shughuli za uzalishajikutokana na kutumia muda mwingi kufuatilia maji maeneoya mbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani,inashangazwa na Serikali hii ya CCM pamoja na tatizo kubwala maji nchini bado leo Serikali inaleta bajeti ya maji ya shilingibilioni 397.4 ambayo ni 2% tu ya bajeti nzima ya nchi kwamwaka huu wa fedha wa 2013/2014. Wakati Mpango waMendeleo wa miaka mitano kwa mwaka huu unaonyeshakuwa Serikali ilitakiwa kutenga shilingi bilioni 529.032 kwa ajiliya miradi ya maendeleo kwenye sekta ya maji. Kambi Rasmiya Upinzani inaitaka Serikali kutoa ufafanuzi, je Mpango waMaendeleo wa Miaka mitano unazingatiwa kwa kiasi gani?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya Taifa katikaupatikanaji wa maji. Majwedwali yafuatayo hapo chiniyanaonyesha mwenendo wa hali yetu kama taifa naupatikanaji wa maji Vijijini na Miji ni kwa vipindi tofautikuanzia mwaka 1995 hadi 2010 na jinsi hali inavyozidi kuwambaya kadiri muda unavyokwenda mbele

Maji Mijini-Makadirio kwa Matumizi kwa Mwaka 2012

Mwaka %Jumla %Maji ya %Vyanzo %Vyanzo %Maji–maji safi Bomba vingine vingine ya juu

salama visivyosalama

1990 94 35 59 3 31995 90 31 59 7 32000 86 28 58 11 32005 83 25 58 14 32010 79 22 57 18 3

Page 127: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

127

Maji Vijijini Makadirio kwa Mwaka 2012

Mwaka %Jumla %Maji ya %Vyanzo %Vyanzo %Maji–maji safi Bomba vingine vingine ya juu

salama visivyosalama

1990 46 1 45 29 251995 46 1 45 30 242000 45 2 43 32 232005 45 3 42 34 212010 44 3 41 36 20

Jumla ya Makadirio ya Upatikanajiwa Maji Safi na Salama

Mwaka %Jumla %Maji ya %Vyanzo %Vyanzo %Maji–maji safi Bomba vingine vingine ya juu

salama visivyosalama

1990 55 7 48 24 211995 55 7 48 25 202000 54 8 46 27 192005 54 8 46 29 172010 53 8 45 31 16

Chanzo cha takwimu: WHO / UNICEF, Joint MonitoringProgramme for Water Supply and Sanitation. Estimates for theuse of Improved Drinking-Water Sources, Updated March 2012,United Republic of Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa takwimuhizo zinaonyesha kuwa matatizo ya maji nchi hii yamezidikuwa makubwa kila baada ya kipindi cha utawala mmojakwenda mwingine. Kama ilivyojitokeza kwenye sekta yaelimu, vivyo hivyo utawala wa Serikali ya Awamu ya Nnechini ya CCM, umesababisha huduma ya maji kuendeleakuwa mbaya nchini kwetu kwa kushindwa kusimamiautekelezaji wa Sera ya Maji ya Taifa.

Page 128: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

128

Mheshimiwa Naibu Spika, mgawanyo wa fedha zamaendeleo katika miradi ya maji kwa mwaka 2013/2014.Katika hali ya kushangaza na kusikitisha ni kuwa Wizarahaionyeshi italishughulikiaje tatizo la maji katika nchi yetukwani kwa mujibu wa randama ya Wizara hii, nitaelezeamgawanyo wa fedha hizi katika maeneo mbalimbali nchinina udhaifu wa mgawanyo huo kimradi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Programu ya maji na usafiwa mazingira Vijijini. Mradi Na.3216, kupanua na kukarabatimiradi ya maji Vijijini ambayo inaendelea, zimetengwa shilingi15,014,211,000, fedha hizi ni kwa ajili ya miradi ya Vijiji vyoteambavyo vina miradi ya maji kwa nchi nzima. Kambi yaUpinzani inahoji, hivi kwa nchi yenye Vijiji vyote hivi vyenyematatizo ya maji kwa mgawanyo huu, lini tutawezakuwapatia maji wananchi wote wa Vijijini?

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi Na.3223, uchimbaji wavisima na ujenzi wa mabwawa Vijijini zimetengwa shilingibilioni 6.0. Kambi ya Upinzani inahoji fedha hizi ni kwa ajili yaVijiji vingapi vya nchi hii? Au tunawahadaa Watanzaniawaishio Vijijini kuhusiana na suala la kuweza kupata majikwenye Vijiji vyao? Kwa mujibu wa taarifa ya Tume yaMipango iliyowasilishwa na Mheshimiwa Wassira ilionyeshakuwa tangu Disemba 2005 hadi Disemba 2012, ni ongezekola asilimia la aslimia 2.83 tu ya wananchi wapya wa Vijijiniwalioweza kupata maji kwa kipindi chote cha miaka nane.Kwa mwendo huu wa kinyonga, ni lini tutawafikia wananchiwetu wanaohangaika kupata maji kwa ajili ya uhai na afyabora?

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi Na.3341 kuboreshahuduma ya maji katika Miji ya Same –Mwanga. Mradi huuumetengewa kiasi cha shilingi bilioni 32.0 na kati ya fedhahizo, kiasi cha shilingi bilioni 20.6 ni fedha za ndani na katikamiradi yote ya maendeleo ya mwaka huu katika miradi yamaji, hakuna mradi mwingine wowote ambao umetengewakiasi kikubwa hivyo cha fedha za ndani, isipokuwa mradiwa kuboresha huduma za maji katika Jiji la Dar Es Salaamuliotengewa bilioni 43 za ndani. (Makofi)

Page 129: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

129

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kwa mujibu wa maelezoya Serikali yaliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge naWaziri wa Maji (Taarifa ya Wizara kwa Kamati kuhusuutekelezaji wa mpango na bajeti 201/2013 uk.81), alisemakuwa mradi huu unalenga kuhudumia Vijiji 38 na unategemeakugharimu shilingi bilioni 147, na kuwa Wizara ilisaini mkatabana Mtaalamu Mshauri wa kufanya usanifu, kuandaamakabrasha ya zabuni na makadirio ya ujenzi kwa awamuya kwanza na ya pili na kazi ilitegemewa kukamilika mweziMachi 2013 na awamu ya kwanza ya ujenzi ilitegemewakuanza mwezi Mei 2013 na kukamilika mwezi Disemba 2014na makisio ya gharama yake ni shilingi bilioni 56.1 na kuwatayari OPEC watachangia dola milioni 12 na BADEA dolamilioni 10 na kilichobaki kitatolewa na Serikali kwa awamuhii ya kwanza ya ujenzi wa mradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mradi huu ujenzi wakewa awamu ya kwanza ni shilingi bilioni 56.1 na tayari kunawafadhili ambao wameshakubali kutoa zaidi ya shilingi bilioni35 (OPEC & BADEA) na kwa mwaka huu wa fedhazimetengwa shilingi bilioni 20.6 za ndani, maana yake ni kuwamradi huu umetengewa fedha zote asilimia 100 kwa mwakawa kwanza wa fedha kabla hata tathimini ya gharama zaujenzi kwa awamu ya kwanza hazijajulikana kwani ripoti yaMshauri anayefanya tathimini ya upembuzi yakinifu ilikuwahaijatolewa bado.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani, inatakakupata maelezo ya kina kama fedha zinaweza kutolewawakati upembuzi yakinifu haujatolewa kwa mradi husika. Je,ni kwanini maeneno mengine yanashindwa kupatiwa fedhakwa kigezo kuwa upembuzi yakinifu bado? Tathmini yaupembuzi yakinifu imekwamisha miradi mingi ya maji hapanchini. Hali hii inapaswa kutolewa maelezo ya kina ilikuondoa manung’uniko ya dhana ya upendeleo katikamiradi ya maji na hasa huu ambao upo kwenye Wilayaanayotoka Waziri wa Maji wa sasa ya fedha kutolewa kablaya tathmini ya upembuzi yakinifu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili ni la hatari sana nahasa ikizingatiwa kuwa mradi huu haukuwa kwenye mpango

Page 130: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

130

wa bajeti wa mwaka 2012/2013, sasa leo fedhazinaondolewa kwenye miradi mingine na kurundikwa kwenyeWilaya anayotoka Waziri wa Maji au ni nini kilipelekeamgawanyo huo wa fedha? Hasa ikizingatiwa kuwa fedhazilizotengwa kwa ajili ya uchangiaji wa miradi ya maji yaVijiji 10 kwa Halmashauri zote nchini mwaka huu wa fedha2013/2014 zimetengwa shilingi bilioni 12.3 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya maji kwa ajili ya Mikoayote mipya imetengewa shilingi bilioni 4.3, miradi ya maji kwaajili ya Miji ya Masasi na Nachingwea imetengewa shilingimilioni 750, mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Miji yaNzega, Igunga na Tabora ikiwa imetengewa shilingi milioni450, pamoja na miradi mingine mingi imetengewa kiasikidogo sana cha fedha za ndani. Kambi ya Upinzani,haikubaliani na mgawanyo huu wa rasilimali za Taifa na hasakwenye sekta ya maji na ndio maana moja ya mapendekezoyetu kwenye Katiba Mpya ni kuachana kabisa mfumo huuwa Mawaziri kutokana na Wabunge, huu ni mfanommojawapo wa madhara yatokanayo na mfumo huumbovu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Programu ya Majisafi naMajitaka Mijini. Katika eneo hili jumla ya fedha za ndanizilizotegwa kwa ajili ya kutatua matatizo ya maji kwenyeMiji na Majiji yetu mwaka huu wa fedha ni shilingi bilioni74.712 na hizi ni kwa ajili ya miradi mikubwa kama yakuboresha huduma za maji Masasi na Nachingwea, miradiya kutoa maji toka Ziwa Victoria hadi Miji ya Kahama/Shinyanga, kuboresha huduma za maji Jiji la Dar Es Salaam,ujenzi wa Bwawa la Kidunda, mradi wa maji wa Kimbiji naMpera na kujengea uwezo Wizara pamoja na mamlaka zamaji Mijini ili kutekeleza WSDP. Kambi ya upinzani, inatakakujua Serikali ina mpango gani madhubuti na wa kujitegemeakatika kuwapatia wananchi wake maji safi na salama najinsi inavyoshughulikia tatizo la maji taka katika Miji yetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ndogo ya sekta ya majina utegemezi wa fedha kutoka nje. Tunategemea wafadhilina misaada kutoka nje kwa ajili ya kugharamia miradi hiikiasi cha shilingi bilioni 179.383 kwa mwaka huu wa 2013/

Page 131: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

131

2014, utegemezi wa wahisani kutoka nje ni mkubwa kwakiwango cha kuathiri miradi mbalimbali ya maji pamoja naupatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Hii ni kinyume na makubaliano yetu hapa Bungeni pamojana agizo la Kamati ya Bunge mwaka jana kuwa tupunguzeutegemezi wa fedha za maji kutoka kwa wafadhili nawahisani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Haliya Umaskini na Maendeleo ya Watu mwaka 20112 (PHDR),fedha za ndani za kutekeleza bajeti ya Sekta ya Maji imekuwaikishuka mwaka hadi mwaka toka 57% katika mwaka wafedha 2005/2006 hadi 10% kwa mwaka wa fedha 2011/2012.Hali hii imesabababisha kukithiri kwa utegemezi katika vyanzovya mapato toka nje na kwa wabia wa maendeleokuwezesha miradi ya maji; fedha ambazo hazipatikani kwawakati na kwa kiwango kinachokidhi mahitaji.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 tumeshuhudiakutokutimizwa kwa azimio la Serikali la kutenga kiasi chaDola za Kimarekani 128 milioni kutekeleza Programu yaKuendeleza Sekta ya Maji (WSDP) huku bajeti pangwa ikiwani dola za kimarekani 28 milioni tu kwa mwaka huo 2011/2012.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa bajeti ya mwaka2012/2013 umeendelea kuonesha upungufu katika utoaji wafedha za miradi ya maendeleo katika sekta ya maji, taarifazinaonyesha kwamba katika kipindi cha miezi sita ya kwanzaJumla ya shilingi bilioni 29 tu ndizo zilitolewa ikiwa ni sawana asilimia 36 katika fedha za ndani. Kiwango hiki ni kidogoikizingatiwa kuwa kiwango kilichoidhinishwa na tume yamipango kilikuwa ni shilingi 48,326,792,184 kwa kipindi charobo ya kwanza pekee.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa yamatumizi ya Serikali kwa sekta ya maji (Public ExpenditureReview of water sector Report) ya mwaka 2009 inaonyeshakuwa sehemu kubwa ya fedha za bajeti za maendeleokwenye sekta ya maji zinapelekewa kwenye Mamlaka za maji

Page 132: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

132

Miji ni na Mamlaka za Mabonde badala ya kuzipeleka kwenyeutekelezaji wa miradi inayosimamiwa na Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya mfumo wakuifanya Wizara kuwa mwezeshaji badala ya kuwamtekelezaji, hadi mabadiliko ya mfumo huu mpya yaelewekena kukubalika na watendaji inaweza chukua muda kidogokwani ni ukweli uliowazi kuwa uwezo wa watendaji kuwezakuhimili utawala wa fedha bado ni mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa (Public ExpenditureReview of water sector Report) ya mapitio ya matumizi yaSerikali kwenye sekta ya maji ya mwaka 2009 inasemakwamba ili kutoa huduma kwa kiwango cha kukidhimalengo ya Millenia inatubidi kila mwaka sekta ya maji itumiedola za Marekani milioni 567.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ili kukidhi kwa kiwangocha juu cha malengo ya milenia katika utoaji wa hudumainatakiwa Serikali itumie jumla ya dola za Marekani bilioni1.1 kila mwaka. Hivyo basi, kutokana na gharama za utoajihuduma hiyo kati ya Mijini na Vijijini kuwa tofauti, ile jamiiinayotumia huduma bora zaidi za maji katika maeneo hayoinatakiwa kuchangia zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kigezo hiki hapa kwetu nikinyume kabisa kwani wale wanaopata huduma bora zamaji ndiyo wanaolipa fedha kidogo za matumizi na walewanaopatiwa huduma ya chini ndio wanaolipa fedha nyingisana. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuliangaliasuala hili kwa makini kwani linazidi kuwa kubwa sana nahivyo kusababisha kutokea kwa matabaka katika nchi yetu,hasa katika huduma muhimu kama hii kwa ajili ya uhai wabinadamu yeyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu unaojitokeza katikautekelezaji wa mipango ya Serikali hususani katika ugawajiwa rasilimali fedha ambazo zimeidhinishwa na Bunge katikahuduma muhimu za jamii kama maji, matokeo yake ni kuwana huduma mbovu, ni dhahiri kwamba kupungua huku kwakiwango cha bajeti katika sekta ya maji kunapingana hata

Page 133: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

133

na Azimio la Sharm el Sheikh la nchi za Umoja wa Afrika lamwaka 2008 la kutaka dhamira na azma ya kuongezakipaumbele cha kisiasa katika utengwaji na kuwekwa wazikwa bajeti kwa ajili ya sekta ya maji safi na maji taka. KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuichukulia sekta ya majikama sekta kichocheo cha maendeleo ya uchumi na hivyobajeti yake inatakiwa kuongezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa programu yamaji na usafi wa mazingira vijijini. Tangu mwaka 2000 Bungehili limekuwa likipewa ahadi za utekelezaji wa Programu yaMaji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP). Wakati maelezoya kuanza kwa mpango huo yalipoletwa Bungeni mwaka2003, wakati huo ukiitwa mpango wa Vijiji kumi (quick wins),yapo maeneo katika Jiji la Dar es salaam ambayo yalikuwana Vijiji na yaliingizwa katika mpango huo. Hata hivyo,mpaka leo miaka takribani kumi baadaye mwaka 2013maeneo hayo yakiwa yameshapanda hadhi na kuwa mitaamiradi hiyo haijatekelezwa kwa ukamilifu wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Programu hii ya Maji na Usafiwa Mazingira Vijijini ilipaswa kutekelezwa kwa awamu nne,ambapo utekelezaji wa awamu ya kwanza baada yakucheleweshwa toka mwaka 2003 ulipaswa kuanza mwaka2005/2006 na kukamilika mwaka 2010/2011. Kwa manenorahisi ni kwamba hadi kufikia hivi sasa ilipaswa tayari majiyawe yameshapatikana katika Vijiji kumi vya kila Halmashaurinchini, hata hivyo ukomo wa muda wa awali ukiwaumeshapita kwa zaidi ya mwaka mmoja; utekelezaji katikamaeneo mbalimbali nchini haukufanyika hata robo. Mfanoni katika Wilaya ya Karatu ambapo kati ya Vijiji kumivilivyoahidiwa, ni kijiji kimoja tu mradi umeanza kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali iko hivyo, wakati ambapofedha zimetumika bila maji kupatikana; katika hatua hiyoya kwanza jumla ya shilingi bilioni 96.4 zimetumika kwenye“quick wins” hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2012 ilhalimaji katika maeneo mengi hakuna hadi sasa; hali ambayoni matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Page 134: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

134

Mheshimiwa Naibu Spika, Ripoti ya Tathmini (AppraisalReport) ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RuralWater Supply and Sanitation Program) ya mwaka 2010inaonyesha namna ambavyo awamu ya kwanza kati yamwaka 2007 mpaka 2010 ilivyoshindwa kutekelezwa kwaufanisi. Kambi ya Upinzani Bungeni inataka uwepo usimamiziwa kutosha wa Kibunge kuhakikisha awamu ya pili (RSSWPPhase II), ambayo awali ilipangwa ifanyike kuanzia mwaka2011 mpaka 2014, inafanyika kwa kuanza na ukaguzi waawamu iliyopita.

Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba iliyotolewa Bungenina Mheshimiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji mwezi waFebruari, 2011, ikiwa ni Kauli ya Serikali Kuhusu Utekelezaji waProgrammu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini; ukiangaliataarifa hiyo jedwali la 4 linalosema “Visima vilivyochimbwakatika Halmashauri ya Hanang’ ni 25”. Taarifa inaonyeshaHanang vilichimbwa Visima 15 na visima vyenye maji ni 8.Katika wilaya ya Karatu mradi huo wa vijiji kumi ni kijiji kimojatu ndipo mradi umeanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa iliyotolewa naHalmashauri ya Wilaya ya Hanang tarehe 25.02.2011 ikiwa nibaada ya Mheshimiwa Waziri wa Maji kutoa kauli ya Serikalikuhusu utekelezaji wa Programu ya Maji inaonyesha kuwamradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) katikavij i j i 10 (Hirbadaw, Wandela, Gawawja, Galangal,Darajameda, Ishponga, Simbay, Gidagarbu, Getasam naNg’aida) hakuna kazi yoyote iliyofanyika, bali hadi kipindihicho usanifu mitandao na uandaaji wa nyaraka za zabunindio uliofanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kutoa maelezo ya usahihi wa takwimu zakekuhusiana na miradi hiyo ya maji kwenye Wilaya ya Hanang’na kwingineko nchini. Vilevile, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina yenye usahihi watakwimu zake kuhusiana na program ya maji na usafi wamazingira Vijijini katika Wilaya mbalimbali hapa nchini.

Page 135: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

135

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Serikali kutoataarifa juu ya matumizi ya shilingi bilioni 96.4 za mradi wamaji safi na mazingira Vijijini katika Jiji la Dar es Salaam naHalmashauri zote nchini ili kasoro hizo zisijirudie katika awamuya pili ya programu hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi Junimwaka 2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabonde ya usimamizi warasilimali za maji. Nchi ya Tanzania imejaliwa kuwa na vyanzovya aina mbalimbali vya maji. Vyanzo hivyo ni mito, maziwa,ardhi oevu na maji chini ya ardhi. Wizara ya Maji naUmwagiliaji imeweka utaratibu wa usimamizi wa rasilimaliza maji katika ngazi za mabonde ili kuweza kuleta usimamiziendelevu wa rasilimali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na vyanzo vingivya maji, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka Serikalikutoa maelezo ya kina, je, Mamlaka ya Usimamizi yaMabonde ya Maji inavitumiaje vyanzo hivyo kwa uzalishajiendelevu na hivyo kuondokana na tatizo la upungufu wachakula unaolikabili taifa letu mara kwa mara? Aidha,tunaitaka Serikali itoe takwimu ni jinsi gani mabonde hayoyanavyoweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutokaSerikalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwekezaji katika miradi yamaji. Ripoti ya karibuni kabisa mwaka 2012 ya Shirika laKimataifa la Water Aid juu ya utafiti uliofanywa ukihusishawataalamu kutoka Overseas Development Institute na Chuokimoja cha nchini Uingereza (SOAS) iliyofuatilia uwekezaji wamiradi ya maji Miji ni katika nchi za Ghana, Burkina fasso naTanzania (Stregthening pro poor targeting of investments byAfrican utilities in urban water and Sanitation) ikiwemonamna miradi mbalimbali ya maji, ilivyoshindwa kuwajalimaskini na maeneo mengine kiwango cha hali ya maji safina salama kutokupatikana kwa urahisi kinyume na malengoyaliyowekwa wakati wa kuanza kwa mradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kulieleza Bunge ni mkakati gani wa makusudi

Page 136: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

136

wa kuhakikisha wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoniau wenye kipato cha chini wanapata huduma ya maji kwagharama/bei nafuu kulinganisha na wanavyolipa sasa.Mfano gari la lita elfu kumi, maji ya yanauzwa kuanziatakribani shilingi 100,000/- hadi 170,000/- kulingana na umbalikutoka kwenye vioski. Lakini watu wenye vipato vikubwawanapata maji kwa gharama za chini sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, matatizo ya kuwa namabomba yasiyotoa maji hayapo tu katika mabombawaliyofungiwa wananchi majumbani bali pia kwenye visimana ‘vioski’/maghati ya jumuiya. Kuna udhaifu wa kuanzishamiradi ya jamii na kuacha kusimamia uendelevu(sustainability) wake na hatimaye baada ya muda mfupimiradi hiyo iliyotumia fedha za umma inabaki kuwa ‘miradihewa’.

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti wa vituo vya majiuliofanywa June 2009 na Overseas Development Institute (ODI)chini ya udhamini wa Shirika la Water Aid hapa nchiniulibainisha ni asilimia 54 tu ya vituo vya maji vilivyopo ndivyovinatumika kwa kutoa huduma ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo kwa wastani baadaya miaka miwili tu ya kujengwa karibu nusu ya visima navioski huwa haviendelei tena kufanya kazi. Utaratibu wakukimbilia kutumia fedha za miradi ya maji kwa mwaka wakibajeti mpya bila kuzingatia taarifa za utekelezaji naufuatiliaji wa miradi ya nyuma ni hatari kwa uendelevu wakuwepo kwa huduma ya maji kwa siku zijazo kama hatuaza haraka hazitachukuliwa kuzingatia matatizo yaliyojitokezakatika miradi iliyopita na kuzingatia ubora na ufanisi katikamiradi ya maji nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, kweli kwa mtindo huu,Tanzania tunaweza kufikia malengo ya Milenia ambayoyanataka ifikapo mwaka 2015 nusu ya watanzania iliyokuwahaipati maji iwe inapata maji safi na salama?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini utafiti uliotolewa

Page 137: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

137

mwaka 2011 wa Water and Sanitation Programme (WSP),unaonyesha kuwa kwa sasa uwekezaji katika sekta hii ni chiniya asilimia 0.1 ya pato la Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinahoji kuwa ikiwa asilimia hiyo ya chini ya 0.1 nayoinategemea kutoka kwa wafadhili, je ni kweli hapa kunania na umakini wa dhati wa serikali kujali (uhai) wananchiwake?

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti uliofanywa naEconomic and Social Research Foundation, umebaini utofautiwa utekelezaji wa miradi ya Serikali na mashirika binafsikatika kuhakiki ubora wa matumizi ya fedha na huduma kwajamii. Utafiti ulibaini kuwa katika miradi iliyofadhiliwa namashirika ya maendeleo, wastani wa asilimia 67 ya vioskivil ionekana kufanya kazi; wakati miradi ambayoimefadhiliwa na Serikali ni wastani wa asilimia 45 ya vioskivya maji vilikuwa vikifanya kazi katika maeneo hayo hayo.Utafiti huo ulihusu Mikoa ya Singida na Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ni mbaya zaidi kwaupande wa Dar es Salaam ambapo kwa mujibu wa utafitimwingine wa Shirika la Water Aid uliobainisha kuwa asilimia85 ya vioski vilivyounganishwa Jijini Dar es Salaam havitoimaji, asilimia 10 vinatoa maji kwa kusuasua na asilimia tanotu ndivyo ambavyo vinatoa maji kwa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti hiyo ya miradiinayofadhiliwa na fedha za walipa kodi inaonyesha wizi naubadhirifu mkubwa na ndio sababu Waziri Kivuli, Ofisi yaWaziri Mkuu-TAMISEMI aliitaka Serikali kuingia ubia na Asasi zaKiraia kufuatilia utendaji wa miradi inayotumia fedha zawalipakodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kasoro katika utendaji nauwajibikaji wa mamlaka na vyombo vinavyohusika na utoajina udhibiti wa huduma ya maji. Majukumu ya utoaji wahuduma ya maji Jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneoya Kibaha na Bagamoyo yanafanywa na Mamlaka ya Majisafina Majitaka (DAWASA) ambayo ni mmiliki, mkodishaji na

Page 138: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

138

msimamizi wa utoaji wa huduma ya majisafi na maji takana ina wajibu wa kupanga na kugharamia utekelezaji wamiradi ya miundombinu, kuiendeleza na kugharamiamatengenezo ya dharura na makubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, muundo wa kimajukumuwa DAWASA hauna tofauti na miundo na majukumu yamashirika ya maji ya DUWASA-DODOMA, BUWASA-BUKOBA,MOROWASA-MOROGORO, MUWASA-MWANZA, AUWASA-ARUSHA, na kadhalika hivyo basi matatizo ya kiuendeshajina ubadhirifu yanayoikabili DAWASA yanarandana kabisa namashirika mengine ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005, DAWASAiliingia mkataba wa miaka kumi (10) wa uendeshaji na Shirikala Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO). Chini yamkataba huo majumu ya DAWASCO ni kuendesha mitambo,kusimamia usambazaji wa maji na uondoshaji wa maji taka,kuuza maji kwa wateja, kutoa ankara kwa wateja,kukusanya maduhuli, kulipia gharama za uendeshaji,kutekeleza matengenezo makubwa yanayogharamiwa naDAWASA na kutekeleza uunganishaji wa maji kwa watejawapya kwa kutumia mfuko wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kisheria na kimkatabaDAWASA ina wajibu wa kuisimamia DAWASCO iliyoingia nayomkataba; hata hivyo kwa kuwa yote ni taasisi na mashirikaya umma ambayo bodi zake na watendaji wake wakuuhuteuliwa na mamlaka zile zile na kuripoti kwa watu walewale, hali hii imekuwa na athari kubwa kwenye utendaji nauwajibikaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hauwezi ukazungumziaupatikanaji wa maji safi na na utoaji/udhibiti wa maji takakatika Jiji la Dar es Salaam bila kutaja DAWASCO (Dar essalaam Water Supply and Sewerage Company) ambayoimepewa mkataba na Mamlaka ya Maji Safi na Maji takaDar es Salaam na DAWASA (Dar es Salaam Water Supply andSewerage Authority). Mkataba huu wa miaka kumi ambaoDAWASA imeingia na DAWASCO unazidi kutia shaka

Page 139: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

139

wananchi wa Dar es Salaam hasa ukiangalia hali halisi yaupatikanaji wa maji safi na udhibiti wa maji taka katika Jijila Dar es Salaam ambao hauridhishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, madhara yaliyotokana nautendaji usioridhishwa wa DAWASCO umeelezwa vizuri sanakwenye Hoja Binafsi aliyowasilisha Mbunge wa Jimbo laUchaguzi Ubungo Mheshimiwa John J. Mnyika katika kikaocha Bunge lililopita. Hoja hiyo ilipendekeza mkataba huoambao DAWASA iliingia kufanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokamilika kwa miradimingi ya maji ambayo tayari ilishatengewa fedha, kutokutoamaji kwa miradi mingi il iyokamilika mfano mradi wakusambaza mabomba maarufu kama ‘mabomba yamchina’ na baadhi ya visima vilivyo chimbwa na kuzagaakwa maji taka katika sehemu mbalimbali ya jiji la Dar esSalaam hasa kipindi cha mvua ni ushaidi tosha DAWASCOkama kampuni lililopewa kazi ya kushughulikia tatizo iliimeshindwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati umefika sasa wamkataba huo kati ya DAWASA na DAWASCO kuwekwa wazikwa umma; kufanyiwa tathmini ya miaka zaidi ya mitanoiliyopita ya utekelezaji; kufanyiwa marekebisho kwa ajili yakipindi kilichobaki na kuanza maandalizi ya mfumo boraunaopaswa kuandaliwa baada ya kuisha kwa mkataba huomwaka 2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, EWURA na majukumu yakuthibiti bei ya maji. Utoaji wa huduma ya maji unamhusupia mdhibiti ambaye ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma yaNishati na Maji (EWURA) yenye mamlaka ya kudhibiti utoajiwa huduma, kuidhinisha bei ya huduma ya maji safi nauondoaji wa maji taka pamoja na kutoa leseni za uendeshaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, EWURA imekuwaikitoa kipaumbele zaidi kwenye kutumia mamlaka yakekudhibiti kwa karibu sekta ya nishati, huku udhibiti kwenyesekta muhimu ya maji hususan kwa upande wa watoahuduma binafsi ukiachwa uwe katika mfumo wa soko holela

Page 140: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

140

na kuchangia katika ongezeko la bei ya maji pamoja naubovu wa huduma. Huu ni udhaifu mkubwa kwa upandewa EWURA ambayo kimsingi iko chini ya Wizara ya Maji naUmwagiliaji lakini utaona kazi zao (za udhibiti) kubwazinafanyika kwenye Wizara ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya The Energy andWater Utilities Regulatory Authority Act (Sura ya 414), kifungucha 6 ambacho kinaelekeza bayana kwamba wajibu waEWURA ni pamoja na kulinda maslahi ya walaji nakuhamasisha upatikanaji wa huduma inazozidhibiti ikiwemomaji wa watumiaji wakiwemo wa kipato cha chini na waliopembezoni au katika mazingira magumu (low income anddisadvantaged consumers). Aidha, kwa mujibu wa kifungucha 7 cha sheria hiyo majukumu ya EWURA ni pamoja nakupanga viwango cha ubora, viwango vya ugavi, kufuatiliautendaji ikiwemo uwekezaji na upatikanaji, kudhibiti bei natozo na kushughulikia malalamiko na migogoro. KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwaeleza Watanzaniaambao kwa kiasi kikubwa wanatumia huduma ya majiinayotolewa na mamlaka za maji nchi nzima kuwa, chombocha kuangalia na kudhibiti ubora na viwango vya majikimeshindwa ila kimejikita kwenye udhibiti wa mafuta yapetrol na dizeli, hivyo wao watafute njia mbadala yakuwawajibisha watoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango maaalum wakutatua tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam. Mradi wavisima virefu Kimbiji na Mpera. Moja ya mikakati ambayoWaziri alilieleza Bunge wakati wa kutoa Kauli ya Serikali kuhusumpango wa kutatua tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaammnamo 7 Novemba, 2012 ni uchimbaji wa visima ishirini (20)katika maeneo ya Kimbiji na Mpera na kujenga bomba lakusafirishia maji kutoka maeneo hayo mpaka Jijini Dar esSalaam ambapo pia matanki ya kuhifadhia majiyanategemewa kujengwa. Mradi huu unategemewakuongeza kiwango cha maji yanayo ingia Dar es Salaam kwalita milioni 260 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa ahadi yaWaziri wa Maji ni kuwa Visima vya Kimbiji na Mpera

Page 141: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

141

vilitegemewa kuanza kuchimbwa mwezi Januari, 2013 nakukamilika mwezi Juni, 2015. Hadi sasa uchimbaji wa visimahivi haujaanza na adha ya upatikanaji wa majisafi katika Jijila Dar es Salaam imezidi kuongezeka badala ya kupunguakama serikali ilivyo ahidi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kueleza kwa nini mradi huu umechelewakuanza tofauti na ahadi iliyo tolewa na Serikali kuhusu kuanzakwa mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Bwawa laKidunda. Mpango wa kujenga bwawa la Kidunda ambalopia ni sehemu ya kuokoa Jiji la Dar es Salaam katika uhabawa maji uliokithiri bado unasuasua. Serikali iliahidi kulipa fidiakwa wananchi watakaopisha mradi huo katika mwaka wafedha 2012/2013 ili kuwezesha mradi huo kuanza katikamwaka wa fedha 2013/2014. Hata hivyo, mradi huu ambaoulikadiriwa kugharimu bilioni 175 hadi sasa hata fidia kwawananchi watakaopisha mradi hazijalipwa na kwa mwakawa fedha 2013/2014 ambapo mradi huu ulitegemewa kuanzaumetengewa shilingi bilioni tatu (3) tu nazo ni kwa ajili yakulipa fidia na si kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa bwawahili lililoelezwa kuanza kujengwa katika mwaka huu wafedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kasi ya utekelezaji wa miradiya Ruvu juu na Ruvu chini ambayo ndio kitovu chaupatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na mpangowa kukarabati miundombinu ya maji katika Jiji la Dar esSalaam hauridhishi. Ikumbukwe kuwa ahadi ya Serikali yakumaliza tatizo la majisafi katika Jiji la Dar es Salaam kufikia2013 lilikwama kutokana na Serikali kuwa na mipango mingikwenye karatasi na isiyotekelezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali kuchukua hatua za haraka zaidikuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati uliopangwa.Pia miradi hii lazima iendane na kasi ya usambazaji wamabomba ya maji katika kaya za wananchi ambazohazijafikiwa na mabomba ya maji katika maeneo mbalimbaliya Jiji.

Page 142: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

142

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za maisha yawakazi wa Dar es Salaam zimepanda mno, huku tatizo laupatikanaji wa maji likiwa moja ya chanzo cha kupandakwa maisha. Kwa sasa maji lita 20 yanauzwa kuanzia shilingi300 na 700 katika maeneo mbalimbali katika Jiji hilo. Hiiinasababisha maisha ya watu wa kipato cha chini kuwamagumu na kupelekea hatari ya kukumbwa na magonjwaya mlipuko kutokana na mazingira wanayoishi kutokuwa safikwa sababu ya kukosa maji safi na salama kwa ajili yamatumizi mbalimbali. Serikali hii, sikivu, kama inavyopendatuamini inabidi iangalie suala hili la upatikanaji wa maji katikaMiji mbalimbali nchini na Jiji la Dar Es Salaam ikiwa sehemumojawapo ili kuokoa muda ambao wananchi wana utumiakutafuta maji na kuboresha maisha ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufisadi katika miradi ya majinchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu waKumbukumbu Rasmi za Bunge, alipokuwa anachangiaMbunge wa Bukombe, Mheshimiwa Prof.Kahigi alisemananukuu:-

“Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya bajeti,Bukombe imetajwa kuhusiana na miradi ya Maji ya Benki yaDunia. Bukombe imetajwa katika jedwali Na.12 ukurasa 98.Wilaya ilipokea Sh. 2,902,990,461 kati ya mwaka 2007 - 2012kwa ajili ya miundombinu na Sh.144,266,260 kwa ajili yakujenga uwezo. Swali ninalotaka nijibiwe ni je, fedha hizi zotezilitumika katika miradi ipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya bajeti,Bukombe pia imetajwa kwamba ilichimba visima 16 navyenye maji ni 15. Je, Waziri anaweza kuniambia visima hivyo16 au 15 viko wapi ?” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana namatumizi ya fedha hizo alizohoji mwakilishi wa wananchikatika Jimbo hilo kwani hayajawahi kutolewa majibukuhusiana na fedha hizo na miradi ambayo ilitajwa katika

Page 143: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

143

maelezo hayo ya Mbunge, kama ambavyo awali ilikuwaimesomwa kwenye Kauli ya Serikali Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mfululizo huo huo,Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi MheshimiwaProf.Kapuya naye alihoji kama ifuatavyo, nanukuu:-

“Kuhusu vijiji vya Kaliua Mashariki, Kaliua Magharibina Ushokola ambavyo kwa ujumla wao ndiyo vinaundaMakao Makuu ya Wilaya, vilikuwa miongoni mwa vijiji hivyo.Wananchi tulichangisha na tukatimiza hizo milioni tano kwakila kijiji jumla shilingi milioni 15 ili tupate shilingi milioni 600toka Benki ya Dunia. Tulipata surveyor wa maji toka MkoaniTabora akaja kupima na kuelekeza mahali ambapo majiyatapatikana. Kampuni ya kuchimba visima ikaja kuchimba,kwa bahati mbaya visima tisa kati ya 12 vilivyochimbwavilikuwa havina maji katika vijiji hivi. Kwa Vijiji vya KaliuaMashariki, Kaliua Magharibi na Ushokola ni kisima kimoja tundiyo kilipatikana na maji. Kwa hiyo, vijiji hivi havina majimpaka leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanaulizamaswali yafuatayo:-

(a) Katika hali kama hii mwenye kosa ni nani? Wao siWataalam wa Maji, wameambiwa wachangewamechanga tena kwa shida sana. Leowanaambulia mashimo tu.(b) Hasara hii aibebe nani?(c) Lini watapata maji?(d) Je, fedha yao watarudishiwa?” Mwisho wa

kunukuu

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri alijibu:-

“Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini imetokea matatizo;watu wamelipwa fedha, wamechimba visima vile vyauchunguzi havina maji, wakaenda hatua mpaka ya kujengamiundombinu wakati wanajua maji hayapo! Nisemekwamba, hili ni tatizo la utekelezaji, ambalo sisi kama Wizaratumelichukua na tunaendelea kulifuatilia”

Page 144: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

144

Mheshimiwa Naibu Spika, huu ni utapeli uliofanywana makampuni hayo, tunataka Serikali itoe taarifa ni kesingapi za makampuni mangapi ya kitapeli kama haya, zikoMahakamani hadi sasa? Utapeli wa namna hii unaofanywana wakandarasi kwa kushirikiana na watendaji wa Serikaliumeenea sana maeneo mengi ya nchi hii. Jambo hili kwakiasi kikubwa limepelekea wananchi waendelee kupatataabu ya maji. Tunataka kujua hatua gani za kisheriazimechuliwa kwa wakandarasi hao waliohusika pamoja nawengine wengi ambao wamefanya hivyo kwenye maeneomengi katika nchi yetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la ufisadi mkubwana wa kutisha katika miradi mbalimbali ya maji hapa nchinindio jambo ambalo limepelekea wananchi wengi kutesekakutokana na kukosa maji safi na salama na hivyo kujikutawakikumbwa na magonjwa mbalimbali ya milipuko katikamaeneo mengi nchini. Hapa Kambi Rasmi ya Upinzani itatajabaadhi ya miradi ambayo kutokana na ufisadi wananchiwamekoseshwa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mabomba ya ‘Mchina’yamekuwa bila maji na miradi hewa katika maeneo yawananchi wa kipato cha chini Jijini Dar es Salaam. Kati yamwaka 2003 mpaka 2010, Serikali ilitekeleza Mradi waUkarabati na Upanuzi wa Miundombinu ya Majisafi naMajitaka Jijini Dar es Salaam na maeneo ya Bagamoyo naKibaha (Dar es Salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP). Mradi huo uliotumia dola milioni 164.6. Hata hivyo,hadi sasa katika maeneo mengi, mtandao wake maarufukama mabomba ya ‘Wachina’ hautoi maji huku kukiwa naupungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji,udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katikamatumizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naombakuwasilisha. (Makofi)

Page 145: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

145

24 APRILI, 2013

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Cecilia Paresso,kwa usomaji wako kwa niaba ya Kambi ya Upinzani.Nakushukuru pia kwa sababu ya kutumia muda vizuri; ahsantesana.

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Sasa namwita Mheshimiwa KangiLugola.

MHE. ALPHAXARD K. LUGOLA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba mwongozo wako, ukurasa wa 61 kwenyeHotuba ya Mheshimiwa Waziri. Naomba kwa ruhusa yakonisome maneno haya anasema: “Katika Mji wa Bunda kaziya kulaza bomba lenye urefu wa kilomita 23.5 kutoka kwenyechanzo hadi kwenye matanki iliendelea katika mwaka 2012/2013.”

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona niombemwongozo wako, Wananchi wa Bunda wanaomsikilizaMheshimiwa Waziri wameshangazwa sana na kauli hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasaninavyozungumza, hakuna bomba hata moja ambalolimelazwa kwenye Mradi huo wa Maji wa Bunda na Bundawana tatizo la maji la muda mrefu. Kitendo cha kuwapakaasali kwenye mdomo Wananchi wa Bunda kwa kauli hii,nimesikitika sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamwomba MheshimiwaWaziri na nipo tayari kuweka rehani Ubunge wangu, mimi nimdau mkubwa wa maji haya, atuthibitishie hii kauli kaitoawapi na hata mitalo yenyewe kuchimbwa haijakamilika.Wizara haitaki kupeleka pesa watalaza mabomba ganiwatalaza miti.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba MheshimiwaWaziri ama afute kauli yake hii, kwa sababu siyo ya kweli nakwenye suala la maji Wananchi wa Bunda hatutacheka na

Page 146: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

146

24 APRILI, 2013

mtu, hatutamwangalia Waziri usoni. Leo tunataka kujuaukweli juu ya kauli hii ameitoa wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wakotutachukua hatua gani kwa kauli kama hii kwa Waziri kwakuwamaanisha Wananchi wa Bunda kwamba mabombayanalazwa ilhali hakuna cha mabomba; tutachukua hatuagani kwa Mheshimiwa Waziri huyu? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kangi Lugola, nakushukurukwa ushauri ulioutoa kwa Kiti na Serikali. Ujumbe wakoumefika. Ushauri wangu ni kwamba, kwa sababu tunaanzamjadala wa mambo haya, Mheshimiwa Waziri atakapokuwaanahitimisha hoja yake ni moja ya mambo ambayoatayafafanua vizuri tu.

Sasa wachangiaji wangu ni wengi, naomba tuokoemuda twende moja kwa moja. Wachangiaji wangu wakwanza watatu watakuwa Mheshimiwa Esther LukagoMidimu, Mheshimiwa Amina Amour ajiandae na MheshimiwaSusan Lyimo atafuatia. Mheshimiwa Esther Lukago.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Majini uhai, maji ni afya. Mwaka 2011 nilisimama hapa nikaombamaji na leo nimesimama tena naomba maji Mkoa wa Simiyu.Mwaka 2011 niliiomba Wizara ipeleke maji Simiyu, lakinimpaka sasa hatuoni kitu chochote kinachoendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu tumejaliwakuwa na vyanzo vya maji, tuna Mto Simiyu, tuna Mto Dumana tuna Mto Manonga na pia tupo jirani na Ziwa Victoria.Tunaiomba Serikali ifikirie sasa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoriakuleta kwenye Wilaya zetu; Wilaya ya Bariadi na Wilaya yaMaswa, Wilaya ya Meatu na Wilaya ya Busega. Huo ndiyoutakuwa Mradi pekee wa kuweza kusuluhisha tatizo la majiMkoa wa Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ipelekemaji Wilaya ya Busega katika Kijiji cha Chingara, Mwasamba

Page 147: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

147

24 APRILI, 2013

na Sanga. Wanawake wa Wilaya ya Busega wanahangaikasana na maji, kiasi kwamba wameshindwa kufanya shughulizingine za maendeleo kutwa nzima wanatafuta maji.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanatembea zaidi yakilomita 16 kutafuta maji, hata wanafunzi wa shule ya msingiwanaotoka katika vijiji hivyo, naomba uamini wanaendashuleni bila kuoga, kwa sababu ya uhaba wa maji. NaiombaSerikali bwawa lililopo Mwanjoro, Wilaya ya Meatu, limalizikeili liweze kusaidia Wananchi wa Wilaya ya Meatu. Wananchiwa Wilaya ya Meatu wanateseka na maji, wanachimba majichini lakini pia wanavuna maji ya mvua kwenye mapipa;inasikitisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ilifufueBawawa la Bariadi ili Wananchi wa Bariadi tuweze kupatamaji mapema iwezekanavyo. Wananchi wa Mkoa wa Simiyusiyo wavivu, tunaweza kufanya kazi, tuleteeni maji tulimekilimo cha umwagiliaji ili tuweze kujikomboa na umaskini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, Bwawa la Kijijicha Habia limeanza kuchimbwa mwaka 2009 mpaka leohalijakamilika. Wananchi walinyang’anywa mashambawakitegemea kwamba watapata maji, mpaka leo hakunamaji wala hakuna mashamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ichimbevisima kwenye shule za sekondari, wanafunzi wanahangaikakuchota maji wakitoka shuleni jioni, matokeo yake asubuhiwanashindwa kusoma na hata kumsikiliza mwalimu hawawezikwa sababu ya kusinzia. Naomba Serikali ifanye hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa EstherMidimu, kwa uchangiaji wako mzuri sana na kwa kweliumeutumia muda vizuri sana; nakupongeza.

Page 148: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

148

24 APRILI, 2013

Sasa ni zamu ya Mheshimiwa Amina Amour,atafuatiwa na Mheshimiwa Susan Lyimo. Mheshimiwa AminaAmour.

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Nitajikita kuchangia mambo mawili tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na suala lauchimbaji wa visima. Pamoja na Serikali kujikita kuchimbavisima vingi, lakini utafiti haufanyiki ipasavyo na hiiinadhihirisha pale ambapo kisima kimeshachimbwa mpakamwishoni maji hayatoki na kwa nini hiki kisima kiwekimeshafanyiwa utafiti halafu maji yasitoke. Hilo ni sualakubwa na mimi sijawahi kuliona. Kule kwetu Zanzibarnil ivyozoea na ninavyoona ni kwamba, mahalipakishafanyiwa utafiti lazima maji yatoke.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naishauri Serikaliiende kule Zanzibar ikajifunze na ikatafute wataalamwanaochimba visima. Fedha nyingi za Serikali zinapotea kwasababu ya utafiti na matokeo yake kwa kila visima kumi, vitatuhavitoi maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nami siungi mkono hoja hiimpaka Mheshimiwa Waziri aniambie kuwa atakwendaZanzibar kufanya utafiti. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, hii bajeti nindogo sana. Kwa kweli Serikali haiko serious kutatua tatizo lamaji, hii ni bajeti ndogo mno. Naiomba Serikali vyovyoteiwavyo, waende wakakope, bila ya kukopa tukapata fedhaza kutosha, itakuwa kila siku tunaendelea kupeleka Sekta yaMaji lakini tatizo lipo hapo hapo. Sasa naiuliza Serikali kwanini inafanya kigugumizi kwenye kukopa? Tatizo wanasemadeni kubwa! Deni kubwa lisiwashughulisheni, ninyi mnajiamini,lazima mfanye maamuzi magumu.

Kwa nini msiamue tukaenda kukopa fedha hizitukapeleka kwenye maendeleo? Ingekuwa fedha zilezinapelekwa kwa mambo mengine lakini maendeleo

Page 149: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

149

24 APRILI, 2013

yatapatikana; kwa nini hamji na maamuzi magumu mkaendamkakopa mkamaliza tatizo la maji lote kwa mwaka huu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikiendelea tena kuhusuwizi wa maji Dar es Salaam ni mkubwa mno. Tunasomakwenye magazeti wanakamatwa hawa, naomba DAWASCOwafuatilie kila nyumba wapatikane watu wanaoiba hayamaji kwa wingi halafu wanakaa wanayauza kwa fedha nyingina Serikali inapata hasara. Pia kuna wengi wanakosa majikutokana na watu wengine wanachukua maji kwa wingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne,nitazungumzia kidogo kuhusu hawa wenye makampunimakubwa. Kuna makampuni makubwa yanatumia majikama Azam, kuna Tanzania Breweries na makampunimengine. Pamoja na kwamba, yanalipa lakini ipo haja yaSerikali kuyafuata makampuni haya ikayaambia yachangiemaji. Wajikite wote wachangie Sekta ya Maji na hizo fedhazikipatikana zitaweza kuisaidia Sekta ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu bajeti kuwa ndogo,nimeiomba Serikali iende ikakope, isiwe na kigugumizi, bilakukopa tatizo la maji litaendelea na ufumbuzi hautopatikana.Tayari tunaweka vipaumbele vingi, kwa nini tuwekevipaumbele vingi tusiweke viwili tu tukimaliza mwakamwingine tufanye vingine viwili? Safari hii tujikite kwenye majina elimu na tukishamaliza tatizo la maji na elimu, bajetiinayokuja tutakuja na mambo mengine, japokuwa tunampango wa mwaka huu lakini tufumbe macho kwa yalemengine tumalize tatizo la maji na tatizo la elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Amina Amour, nakushukurusana. Mheshimiwa Suzana Lyimo, atafuatiwa na MheshimiwaSaleh Pamba.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ili na mimi niweze

Page 150: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

150

24 APRILI, 2013

kuchangia katika Sekta hii muhimu ya Maji, kama ambavyowenzangu wamesema na inajulikana kwamba maji ni uhaina maji ni kila kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze na bajeti.Kama kweli maji ni uhai, lakini tumeshuhudia ni jinsi gani bajetiya maji inaendelea kuwa finyu mwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia bajeti ya mwakajana ya maendeleo, ilikuwa shilingi 465,756,000,000, wakatibajeti ya mwaka huu ya maendeleo ni shilingi 379,000,000,000;hii ikiwa na maana kwamba, tuna upungufu wa shilingi zaidibil ioni 86 huku tukitaka kusema kwamba, tunatakakuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na salama.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wote tunatambuakwamba, Tanzania zaidi ya nusu ya wagonjwa, watoto wachini ya miaka tano, kila zaidi ya watoto 20,000 wanafarikikwa sababu ya magonjwa yanayotokana na maji machafu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa takwimu hizi ni wazikwamba, tunapoteza nguvu kazi na vilevile ni wazi kwamba,bado Serikali haijalipatia ufumbuzi wa kina tatizo la maji hapanchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia takwimuzinaonesha wazi kwamba, huduma za maji vijijini na mijinifedha zake zimekuwa zikipungua. Jambo la kushangaza nahapa nikubaliane na Mheshimiwa aliyesoma Hotuba yaKambi ya Upinzani na Kamati inayoshughulikia Wizara hii.Pamoja na kwamba, Wananchi zaidi ya asilimia 75 wanaishivijijini lakini fedha iliyotengwa kwa ajili ya vijijini mwaka hadimwaka, kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 75 wakati ile ya mijinini shilingi bilioni 254 na wakati huohuo mijini tuna watu asilimia25 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni wazi kwamba, Wananchiwa Vijijini ndiyo wazalishaji wakubwa, lakini athari zake ni nini?

Page 151: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

151

24 APRILI, 2013

Takwimu zinaonesha na ni wazi kwamba, akina mama nawatoto wanatembea zaidi ya kilomita kumi, wanatumia zaidiya saa mbili mpaka saba kila siku kwa ajili ya kwenda kutekamaji na maji hayo ni ndoo moja tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii inaonesha ni jinsi ganisasa akina mama hawa na watoto hawa wanashindwakuzalisha au kufanya kazi nyingine za maendeleo katika Taifahili huku wakitafuta maji tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la elimu,tumeona ni jinsi gani baadhi ya shule zimefungwa kwasababu ya ukosefu wa vyoo. Vilevile hawana umeme kwasababu ya maji. Haya ni matatizo makubwa na kama kweliSerikali haitalipa kipaumbele suala la maji, tunaendakupoteza nguvu kazi ya Taifa hili na tunapoteza vijana.Tumeona jinsi gani wanafunzi wanatumia kigezo chakutokuwa na maji katika utoro. Tumeona jinsi gani watotowanatoroka mashuleni kwa sababu wanakwenda kutafutamaji na watoto wa kike wakipata mimba kutokana na hayahaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ihakikishetatizo la maji linapatiwa ufumbuzi wa kina.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwa kweli nchi yetuimejaliwa vyanzo vingi sana vya maji, maji yaliyopo kwenyesurface lakini vilevile maji ya underground.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba, sisitunawazidi Wakenya kwa maji mara tatu na Waganda kwaasilimia 37, lakini bado takriban nusu ya Watanzania hawapatimaji safi na salama; hii ni aibu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwenyezi Munguametujalia vyanzo vya maji; kwa mfano, tuna mito mikubwa,achilia hii midogo midogo, mito mikubwa 11 hapa nchini nalabda niitaje; kuna Ruaha, Kagera, Kalambo, Malangarasi,Mara, Rufiji, Ruvuma, Rufirozo, Thibitihuba na Wami, lakinibado vyanzo hivi havitumiki vizuri. Vilevile tuna Maziwa Makuu

Page 152: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

152

24 APRILI, 2013

ambayo sitaki kuyataja, bado Serikali haijafanya kazi yakeya kuhakikisha Wananchi wanapata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani mtuanazunguka Ziwa Victoria halafu hapati maji. Haiwezekanimtu yupo karibu na mto hapati maji. Kwa nini hatupati maji,maji yetu yote yanaenda mpaka Misri lakini wale waliopopale wanakosa maji! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ihakikisheinalipatia ufumbuzi wa kina.

Mheshimiwa Naibu Spika, nije katika maeneo yanguna niseme tu, nimefurahishwa sana na naomba Wananchiwa kule Moshi Vijijini wafurahie; nimesoma ukurasa wa 145na ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wakati uleMheshimiwa Christopher Chiza, tulienda naye Moshi akaonamatatizo na leo hii naomba niseme kwamba, Wananchiwangu wa kule Kolini Kusini na Kolini Kaskazini wafurahiekwamba Mradi wa Maji utakuwa tayari mwaka huu naniwapongeze sana Wananchi hao kwa juhudi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na chanzo hichocha maji, Wananchi wa Kijiji cha Kolini Kusini waliamuakuchanga fedha kwa ajili ya kuweza kupata maji katikachanzo kingine cha Chemchemi ya Mangi pale Rahu.Wamejitahidi sana kwa nguvu zao, lakini bado wanahitajiSerikali iweze kuwasaidia na ninaamini kabisa Serikaliitawasaidia ili Wananchi hawa wasitegemee chanzo kimojatu, kwa sababu watu wa Kilimanjaro pamoja na kwambakuna ukame, lakini pale ambapo kuna maeneo yenye vyanzovya maji, Wananchi wanaomba juhudi ya kuchangishana,basi Serikali iweze kuwasaidia na waweze kupata maji safina salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mimi kamamwanamke, naomba niseme tu kwamba ni wazi pamoja nakwamba wanawake wanafanya kazi kubwa sana, lakini wotetunajua kwamba tuna tatizo kubwa la UKIMWI nchini na walewagonjwa wa UKIMWI mara zote akina mama ndiyo

Page 153: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

153

24 APRILI, 2013

wanakuwa wanawasaidia. Tunatambua kwamba,wagonjwa wanapofikia zile stages za mwisho wanahitaji majimengi sana na hawa akina mama wanachukua muda mrefusana kwenda kuchota ndoo moja. Kwa hiyo, ninaomba sanaSerikali ihakikishe inawekeza vijijini kwa sababu kule vijijini kunamatatizo makubwa sana ya maji kuliko hata mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, niseme kwa Dares Salaam nimepata taarifa, ni wazi kwamba,tumelizungumza suala la wizi wa maji, lakini naambiwakwamba sasa hivi kumekuwa na operesheni kubwa sana yakukamata watu hawa. Mimi nakubaliana na Serikali, lakininaambiwa zoezi lile limechukua sura mpya kwamba, sasawanakamata watu ambao hata hawahusiki na vilevilewamekuwa wakichukua rushwa kwa Wananchi hao. Kwahiyo, ninaomba Serikali ihakikishe zoezi hili linaleta manufaana kuhakikisha hawawatendei vibaya Wananchi ambaohawana hatia. Wale wenye hatia wakamatwe lakini wasiona hatia, ninaiomba sana Serikali iliangalie jambo hili kwakina.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie vilevile kwakusema, suala la Bwawa la Kidunda Dar es Salaam ni wazikatika hotuba ya mwaka jana, Mheshimiwa Waziri alisemakwamba, fedha zimeshatengwa kwa ajili ya fidia, lakinimpaka leo hawajapata.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Susan Lyimo,Mheshimiwa Saleh Pamba, atafuatiwa na MheshimiwaMchungaji Getrude Rwakatare.

MHE. SALEHE A. PAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niungane nawenzangu katika kuchangia Hotuba ya Wizara ya Maji.Kwanza, napenda niseme kwamba, naunga mkono Hotubahii asilimia mia kwa mia. (Makofi)

Page 154: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

154

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Chama chaMapinduzi kilipoenda kutafuta kura kwa Wananchi tuliahidikatika Ilani yetu ya Uchaguzi kwamba, tutaondoa tatizo lamaji vijijini kwa asilimia 65 na tutaondoa tatizo la maji mijinikwa asilimia 90. Hadi sasa kufuatana na Hotuba yaMheshimiwa Waziri, tumefikia asilimia 57 vijijini na tumefikiaasilimia 75 mijini. Hiyo ni hatua kubwa sana na lazimatuipongeze Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Kwa sababukatika miaka miwili iliyobaki kwa upande wa vijijini nina hakikakabisa kwa Miradi ambayo imetajwa na Mheshimiwa Wazirikatika Hotuba hii, ina-cover nchi nzima pamoja na Mji waKaratu kwamba tutafikia asilimia 90 na asilimia 65 kwawananchi wetu walio vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nizungumziemasuala matatu makubwa ambayo yametajwa kwenyeHotuba ya Mheshimiwa Waziri. Suala la kwanza linahusuumuhimu wa kutunza vyanzo vya maji. Nimepitia katikataarifa mbalimbali hasa Taarifa ya Water Aid na Taarifa yaBenki ya Dunia ya mwaka jana. Katika Taarifa hizo mbiliwanasema nini kuhusu Tanzania kuhusu hali ya maji.Wanasema kwamba, kutokana na tatizo kubwa la ongezekola watu (population growth), pamoja na masuala mengineya kuharibu vyanzo vya maji katika miaka mitano ijayo,itakapofika mwaka 2020, Tanzania tutakuwa na kituambacho kinaitwa water stress, tutakuwa na tatizo kubwasana la maji. Kwa hiyo, ninachoiomba Serikali ni kwamba,iendelee kutenga fedha za kutosha hasa katika kuhifadhivyanzo vya maji.

Hivi sasa tumetenga asilimia 8.5, ambalo ni jambozuri sana, lakini Kimataifa wanasema kwamba, lazimatutenge angalau asilimia kumi ya bajeti ya maji kwa ajili yakuhifadhi water resources. Naiomba Serikali yangu kwamba,tumetenga fedha safari hii shilingi bilioni 19.7, natumaini katikabajeti i jayo na hasa kutokana na matatizo hayayanayotokana na uharibifu wa vyanzo vya maji, basitutatenga bajeti ya kutosha ili tusipate tatizo hili ambalo Benkiya Dunia inazungumzia juu ya suala la water stress.

Page 155: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

155

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili ambalo natakakulizungumzia ni la jumla na limezungumzwa na Mwenyekitiwa Kamati ya Kilimo na Mifugo na limezungumzwa naWabunge waliotangulia, nalo ni suala la bajeti ndogo ya maji.Bajeti hii kwa sasa hivi tunaiona ndogo, lakini kihistoria bajetihii imeendelea kukua mpaka kufikia shilingi bilioni 380. Tatizokubwa tunalolipata katika bajeti hii ni uwiano mdogo uliopokati ya bajeti hii hasa kwa maji mijini na maji vijijini. Lazimatufike mahali ambapo tunabadilisha mwelekeo huu tupelekenguvu zetu za maji hasa kule vijijini ambapo Watanzaniaasilimia 80 wanaishi. Kwa mfano, katika bajeti ya shilingi bilioni380 ambayo tutaipitisha baadaye, ni asilimia 30 tu ya bajetihiyo tunaipeleka vijijini. Lazima trend hii tuibadilishe ili tuwezekuhakikisha kwamba, vijijini nako wanapata maji na tukipatamaji vijijini, yatatusaidia katika maeneo mawili makubwa sanakwa upande wa Serikali na kwa upande wa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, tukipeleka majisafi na salama vijijini tunapunguza magonjwa, tunapunguzamaradhi yanayotokana na maji au wanaita waterbornediseases na tunapunguza gharama zetu za kununuamadawa katika zahanati. Fedha ambazo tutazi-savetutazitumia katika maendeleo mengine katika nchi yetukama kilimo, elimu na kadhalika. Kwa hiyo, naomba Serikaliihakikishe tunabadilisha mfumo huu wa bajeti. La pili nikwamba, ukiangalia katika bajeti hii ya maji, sehemu kubwasana ya fedha ambazo tumezitenga ni za wafadhili. Kwahiyo, tunatakiwa tubadilishe hiyo trend ili tuingize fedha zetuwenyewe kama tulivyofanya katika barabara, kamatulivyojenga barabara kwa fedha zetu wenyewe tuendeleehivyo hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, napenda kutoashukrani zangu kwa Wizara ya Maji hasa kwa Jimbo langu laPangani. Mheshimiwa Waziri na Wizara yake, imenipatiashilingi 260,000,000 kwa ajili ya kukarabati maji kwa Mji waPangani; nasema ahsanteni sana. Kwa sababu kwa vyovyotevile Halmashauri ambayo inapata shilingi 10,000,000 kwamwezi haiwezi ikatengeneza Mradi kama huu, hii ni hatuakubwa sana. Tunayo mipango ya maji viji j ini, tayari

Page 156: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

156

24 APRILI, 2013

tumekwishawaletea proposal zetu, tumeshachaguamkandarasi kwa vijiji vitatu ili tuweze kukamilisha Mradi huo.Kwa hiyo, ninaomba Wizara iharakishe tupate no objectionkusudi tuendelee, tuhakikishe kwamba katika vijiji vile, katikazile kata tatu ambazo tumeziombea maji, Kata ya Bweni naKikumbwi zipate no objection na Miradi iweze kuendelea kwaharaka zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,napenda nirudie tena kusema kwamba, hatua hii ni nzuri nanina imani tutakapofika mwaka 2015 tutakaporudi kwaWananchi tena, tutakuwa tumefikia zile asilimia ambazotumezisema katika Ilani yetu ya Uchaguzi. Tumeahidi na ninauhakika kwamba, tutakuwa tumetekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naungamkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Saleh Pamba, kwauchangiaji wako. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Kamishna.

Mheshimiwa Dkt. Getrude Rwakatare, atafuatiwa naMheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE P. RWAKATARE: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante. Awali ya yote, naomba nichukue nafasihii, kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kwendaBukoba katika Kijiji cha Igwilibi, kumzika mume wanguKenneth Rwakatare, ambaye ametangulia mbele za hakitarehe 9 Aprili, 2013. Mungu ailaze roho yake mahali pemapeponi. Mungu alitupa na Bwana ametwaa jina la Bwanalibarikiwe; Amin.

Pili, napenda kulishukuru Kanisa langu la MlimwamotoAssemblies of God Mikocheni, Viongozi, Wazee wa Kanisana Waumini wote. Vilevile nawashukuru Wabunge wenzanguwaliosikia jambo hili wakanitumia pole hata kwa simu,wengine walinipigia, walinitumia message na wenginewalikuja nyumbani. Ningependa kusema ahsante kwamchango wenu wa kunifariji kwa hali na mali. Mungu

Page 157: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

157

24 APRILI, 2013

awabariki na ninyi mpate kuvuna, leo mimi kesho wewe, sisini ndugu. Amin.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nijikite katikakuchangia Hotuba hii ya Wizara ya Maji. Kwa masikitikomakubwa, mwanzo kabisa naunga mkono hoja hii mia kwamia. Wanasema “Mvumilivu hula mbivu”, lakini mimi naonauvumilivu wangu umezidi na sasa utanishinda. Kwa sababuhuu ni muhula wangu wa pili Bungeni na ni mara yangu yanne kusimama kuchangia bajeti ya Wizara ya Maji nikisemahabari ya Wilaya ya Kilombero na hasa Miji ya Ifakara na Mjiwa Mlimba.

Wakazi wa Kilombero hasa Wanawake na Watoto,wamenituma nimwulize Mheshimiwa Waziri; je, lini Kilomberoau Miji ile mikubwa ya Ifakara na Mlimba tutapata maji safina salama? Maana mara nne kusimama na kuongea jambomoja watu wanasema utu uzima dawa, pamoja na utu uzimawangu lakini ninaona jibu hili halipatikani; inasikitisha.Ninaomba jamani mlifanyie kazi ili watu hawa wawezekupata maji. Jambo la kusikitisha lingine ni kwamba, Wilayaya Kilombero ina mito 38; mito 38 ni vyanzo vizuri kabisa vyamaji, lakini hatupati maji ya kudumu, maji safi na maji salamana tukipata tunapata kwa msimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilikuwa naombamwangalie kama kuna vyanzo vya maji mito 38 bado sehemuhiyo inakuwa na uhaba wa maji, inakuwa maji ndiyo tatizosugu na kubwa kweli tunamaanisha kuwasaidia watu hawa.Kila aliyekuwa Waziri wa Maji, nilimwendea na Mradi wetutukapeleka lakini sioni majibu. Naomba safari hiihatutavumilia, kama sioni mabadiliko nakwenda kumchukuaWaziri na Naibu wake, twende Ifakara na Kilombero mkaonetabu wanayoipata ya wanawake na wakazi wa kule japotuna vyanzo vya maji.

Watu wanaweza kupata maji kutoka Ziwa Victoriayakaenda mbali lakini sisi maji yako palepale kuyapata nimbinde, tunaishi kwa maji ya visima vya mdundiko ambavyovyenyewe pia ni vya muda; inasikitisha sana. Naomba

Page 158: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

158

24 APRILI, 2013

tushughulike, kwa sababu kitu tunachoambulia Kilomberounakuta ni mafuriko au kitoweo cha samaki, lakini majikwenye majumba yetu hamna. Hili ni jambo la kusitikishasana, mpaka twende tukachote na ndoo na vilevile wakatiwa kiangazi maji hamna watu wanahangaika, hayamahangaiko yataisha lini? Namwuliza Mheshimiwa Waziri waMaji. Kwa mfano, Mji wa Ifakara ni Mji ambao miundombinuyake ya maji ni ile ya miaka 1970 au 1980, michakavu, mizee,ya siku nyingi wakati huo wakazi walikuwa 7,000 tu.

Sasa hivi tuna wakazi karibu laki moja, sasa kweli hiimiundombinu ya miaka 1980 itatosha; ndiyo maana unaonakuna mahangaiko mengi na masikitiko mengi. Tunaombamlifanyie kazi sasa hivi Ifakara umekuwa mji mkubwa,umekua, umepanuka; una wakazi wengi na vilevile kunataasisi nyingi, kuna Chuo Kikuu cha Madaktari, kuna vyuokaribu 18, kuna mashule mengi, kuna shule za international,shule za kawaida, kuna hospitali, kuna vituo vya afya, kunakaya nyingi lakini zote hizi maji ni matatizo. Sasa mnaposemamaji ni uhai, maji ni afya; je, sisi watu wa Kilombero hamtutakiikuwa na afya njema tuugue? Hiyo inasikitisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ifakara mjini kwenyewe, mjiule mdogo umezungukwa na mito miwili mikubwa; Mto waKilombero na Mto Lumemo, lakini pamoja na kwamba kunamito hii mikubwa bado maji ni matatizo kuyapata. Jamaninaomba tatizo hili sugu la muda mrefu liondoke tusikae tenakuchangia tukiomba maji kwa ajili ya wakazi wa Kilombero,kwa sababu hakuna sababu ya kutokuwapa maji safi wakativyanzo vyote vya maji vipo. Jamani, sitaki nionekane kamavile ni mtu mbishi, lakini ninaomba tusaidiane hili ili tatizo liwezekuondoka.

Ahadi ya Rais, katika mwaka 2005, 2010 alituambiaahadi yenu nawaahidi daraja, maji tunashukuru Mungudaraja limeanza, matayarisho yake ya ujenzi, pia tunashukurulakini Wizara hii ya Maji bado haijatimiza ahadi hiyo. Sasa hilijambo sielewi tatizo ni nini; ni pesa au nini? Shilingi bilioni 395,mnashindwa kutoa hela kidogo tu kwa ajili ya Wilaya mojajamani au sisi siyo watu wa thamani, kama ni watu wa

Page 159: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

159

24 APRILI, 2013

thamani, naomba safari hii ombi hili ambalo kwa sasa ni maraya nne nasimama mbele ya Bunge hili kuliomba na vilevilekulitafakari na kuwaambia vyanzo vyote vya maji, ninaombasasa lipate majibu ya kudumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mradi wa Maji yakutega, huu Mradi wa Kiburugutu. Mradi huu nimewapelekeaMawaziri waliokuwepo, ambao thamani yake ni shilingi bilionimbili. Huu Mradi ni wa kudumu siyo wa kurudiarudia, lakiniwanasema Mradi wa shilingi bilioni mbili ni mkubwa mno, ninyingi mno. Shilingi bilioni mbili jamani miaka yote kumi yaRais Kikwete ni nyingi kwa ajili ya Kilombero badala yakewanawapa visima, wanachimba visima vya mdunduko,visima vitatu au visima vitano kila mwaka. Sasa hapo kweliunaondoa tatizo si bado unaendeleza hili tatizo liendeleewakati ungetoa hela mara moja. Fumba macho toa helamara moja shilingi bilioni mbili puu, tengeneza miundombinuya maji pale Ifakara ili vyuo viweze kufanya vizuri, vyuo vikuuvifanye vizuri na wakazi wa pale waweze kufaidika na majihayo.

Ninaamini ya kwamba, safari hii MheshimiwaMaghembe, Waziri wa Maji, hili jambo litatimia na tutafurahina wakati wa kufungua hakika itakuwa ni sherehe nashangwe.

Tatizo la maji katika Mji Mdogo ule wa Mlimba. Mlimbanao ni mji, ipo Stesheni ya Tazara kubwa na vilevile kimjikikubwa kilichochangamka lakini tatizo kubwa ni maji. WorldBank walichimba pale, kuna Mradi pale wa visima unatumiaumeme na umeme ni wa msimu. Leo kuna umeme keshohamna, kwa hiyo, wakati mwingine inabidi watu kwendakutafuta maji na ndoo kwenda mbali.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa MchungajiRwakatare, kwa kuwasemea Wananchi wa Kilombero hasaMji wa Ifakara. Kwa niaba ya Waheshimiwa Wabunge,ambao hawakuwa wamefahamu kuhusu msiba mkubwauliokupata wa kuondokewa na mzazi mwenzako, naomba

Page 160: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

160

24 APRILI, 2013

tukupe faraja kwa kusema pole sana; “Bwana alitoa, Bwanaametwaa, jina la Bwana Lihimidiwe.”

Baada ya Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya,atakayefuata ni Mheshimiwa Dkt. Cyril Chami.

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi nitoe mchangowangu kidogo katika Sekta hii muhimu ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kusema kwamba,kwanza, maji ni muhimu na maji ni uhai. Maji yanahitajikamajumbani, mahali pa kazi, mashuleni, viwandani, maeneoya sokoni na sehemu mbalimbali katika kilimo na mifugo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna vyanzo vingi sana vyamaji, lakini nasikitika kusema kwamba, Serikali imeshindwakutupatia maji safi na salama na kila anayesimama hapanafikiri wewe mwenyewe unasikia jinsi wanavyotoa kilio chamaji na kweli maji ni shida Tanzania. Mfano, tukiangalia trendya bajeti inavyokwenda; mimi sitaki kwenda kwenye BajetiKuu, nataka tuangalie subvote 3001 kwenye Kitabu chaMaendeleo, ukurasa wa 81, utaona kabisa jinsitunavyotegemea wafadhili katika Miradi yetu mbalimbali yaMaji. Hii inasikitisha. Ukiangalia katika rehabilitation andexpansion of urban water supply katika miaka ya 2012/2013na 2013/2014 jinsi trend inavyokwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa bajetiuliopita tuliona kwamba, tunategemea wafadhili kwa shilingibilioni 135.8 wakati fedha za ndani tulikuwa tumetenga shilingibilioni mbili. Mwaka huu wa 2013/2014 pia tunaonatumetenga pesa za ndani shil ingi bil ioni 4.8 wakatitunategemea wafadhili kwa shilingi bilioni 49.2; kwa kwelisidhani kama tunaweza tukatatua matatizo yetu kwakutegemea wafadhili kwa kiasi hiki. Naomba kuuliza kwa niniSerikali isiamue suala la kushughulikia maji liwe la kwake; kwasababu tatizo la maji ni kubwa mno na ione kwamba nimuhimu na ni wajibu wake kwa Wananchi wake kuhakikishakwamba maji yanapatikana bila kutegemea wafadhili?

Page 161: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

161

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakubaliana na wale wotewaliosema kwamba, kuna haja Serikali ione umuhimu wakuanzisha Mfuko wa Maji kama tulivyo na Mfuko wa Barabara.Hii itasaidia kupunguza utegemezi kibajeti. Tarehe 17 Aprilinilikuwa najibiwa hapa swali kuhusu matatizo ya maji.Nakumbuka Waziri wa Mazingira akasimama akasema kuwa,tatizo la maji ni la kidunia na ni kutokana na mabadiliko yatabia nchi. Nakubaliana naye lakini pia nitakataa; tunamatatizo ya maji kwa kipindi kirefu lakini vilevile tuna vyanzovingi vya maji. Hayo matatizo ya mabadiliko ya tabia nchihayakuanza miaka mingi sana, yameanza hapa nyuma. Chamsingi ni kuhakikisha tunalinda vyanzo vyote vya maji ilituweze kuvitumia vizuri. Kwa hiyo, Serikali iache visingizioitekeleze wajibu wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, Kigoma tunashida sana ya maji; ukienda Kibondo, Kankoko, Muhambwe,Kasulu, kila sehemu tuna shida sana ya maji lakini tuna ZiwaTanganyika. Nikianza na Kigoma Manispaa, baadhi yamaeneo tunapata maji mara moja kwa wiki, eneo laMwanga, Katubuka, Majengo, Ujiji, Mlole, Vamia kote ni viliovya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, toka Bunge la Tisa miminakumbuka tuliuliza maswali mengi ya maji. Nakumbukavilevile katika michango mbalimbali niliyokuwa nikitoa, majibuambayo Serikali ilikuwa ikijibu ni kwamba, hakuna umemekwa hiyo pampu inashindwa kusambaza maji. Sasa hiviumeme tunao, lakini kwa nini hatuna maji?

Vilevile walikuwa wanasema kwamba, mabomba nichakavu, yaliwekwa muda mrefu, miundombinu inafanyiwamarekebisho. Mpaka sasa kimya maji bado ni tatizo. Hebutunaomba Serikali itupe majibu fasaha ni nini tatizo. Vileviletunaongeza umaskini kwa Watanzania kwa sababu sasa hivitunategemea maji yanachotwa wapi; wananunua galoni lamaji kwa shilingi 500 mpaka 1000, maisha ni magumu sanatunaongeza umaskini kwa Watanzania. (Maskini)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia Kigoma Vijijini,

Page 162: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

162

24 APRILI, 2013

tatizo ndiyo kubwa zaidi, kuna Mji Mdogo unaitwa Mwandigani kijiji ambacho kinakua haraka, kipo karibu kabisa na mjini,pale maji ni shida mno. Mimi nashauri mtandao wa KUWASAungeibeba na hii Mwandiga kwa sababu siyo mbali sana naeneo la Mjini. Vilevile Mji wa Kuzulamimba unakua mno, kwahiyo, maji yaliyopo hayatoshi. Ninaomba Serikali iangalieuwezekano wa kuwapatia maji lakini vijiji kumi vya mradi pianavyo vinasuasua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na mudanitaongea kidogo kuhusu suala la Kasulu. Kuna Mradi waRuhita wa 2011/2012, ambapo mzabuni alipewa kazi lakiniinaonekana engineer wa eneo lile hafanyi kazi yake vizuri.Wananchi walichangia shilingi milioni 30, mabombayaliyonunuliwa kwa kweli yalikuwa substandard, yalikuwayakivunjika wakati wanatandaza mabomba chini. Mtandaowa maji Heru Juu na maeneo ya Kahunga na Muhunga, kunautaratibu wa kubadilisha mabomba yaliyopo ambayoyalifungwa tangu miaka ya 1970. Sasa pesa zilizotolewa nikidogo sana, inahitajika kama shilingi milioni 300, lakiniwametengewa shilingi milioni 80 na ni Mradi ambao ulitakiwautekelezwe ndani ya miezi sita ila mpaka sasa badounasuasua na vijiji vingine vya Nyoshe, Mruti, Kidya, Kigondo,Msambala kote maji ni shida wanahitaji maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesekia kuna sloganinayosema “Big Result Now” siamini kama itafikiwa na hiyoresult tutaipata haraka kulingana na trend ya Bajeti jinsi ilivyo.

Nikiangalia ukurasa wa 119, kifungu kidogo cha 87(a)cha Ilani ya CCM ya mwaka 2010, kinasema kwamba,kutakuwa na kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi nasalama kufikia mwaka 2015, vijijini asilimia 75, mijini asilimia95. Nasema kwamba, sidhani kama tutafikia kulingana nahali halisi kwamba sasa hivi tuko asilimia 57 vijijini na 75 mijinina hali yenyewe ya kibajeti jinsi ilivyo. Vilevile sera ya majiinasema, maji yapatikane umbali wa mita 400. Sasa hivi watuwanatembea muda mrefu sana; ni lini Mwananchi atatafutamaji umbali wa mita 400 tu?

Page 163: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

163

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshasema mengi sana,tunaomba Serikali ituambie ina mikakati gani inayohakikishakwamba Mtanzania anapata maji na malalamiko yaWabunge yanakwisha? Nashukuru kwa kunipa nafasi.Ahsante. (Makofi)

MHE. DKT. CYRIL A. CHAMI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Bajeti hii yaWizara ya Maji. Naanza kwa kusema kwamba, naungamkono bajeti hii, lakini nachukua fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri wa Maji na Naibu Waziri wake na KatibuMkuu - Engineer Sai, kwa kazi kubwa wanayoifanya katikanchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, natumia fursa hii kuwapapole, nawapa pole kwa sababu mzigo tuliowapa ni mkubwa,lakini rasilimali za kufanyia kazi ni ndogo na kilio cha Wabungewote walioko hapa, hakuna Mbunge mwenye Jimboanayeweza kusimama hapa akasema Jimboni kwake nisalama, kwa maana ya maji, salama kwa watu wote; amaatasema kwamba Jimbo lake lote lina shida ya maji auatasema kwamba sehemu fulani ya Jimbo lina tatizo. Kwamaana hiyo, nataka niwasihi Wabunge wenzangu, badalaya kuelekeza shutuma kwa Waziri na Watendaji, tukae kamaBunge tuishauri Serikali namna gani ya kupata vyanzo vyafedha vya kuondokana na tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Maji na Wasaidiziwake wanahitaji kusaidiwa na Bunge hili na siyo kutuhumiwawala kulaumiwa. Hakuna Waziri hata mmoja ambayeangekaa kwenye nafasi ya Mheshimiwa Profesa Maghembepale, ambaye leo Waheshimiwa Wabungewasingemlalamikia. Waheshimiwa Wabunge tunapolalamikatuna haki kwa sababu na sisi tunalalamikiwa katika Majimboyetu. Kwa hiyo, tuache kulalamika, tukae chini tutafakari namimi nachukua fursa hii kumnukuu Kiongozi mmoja wa nchiyetu, huwa anasema tufanye maamuzi magumu. Tufanyemaamuzi magumu tuseme kwamba suala la maji tulitafutieufumbuzi. Kama alivyosema msemaji aliyepita, kwa hakikamiundombinu mingi, iwe ya kiuchumi, iwe ya afya, haiwezi

Page 164: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

164

24 APRILI, 2013

kufanikiwa kama hakuna maji, maji ndiyo muundombinuambao kila mahali unahitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa Serikali yangu yaChama cha Mapinduzi, jambo litakalotutoa 2015 nikuhakikisha kwamba nchi hii inapata maji kila Wilaya, kilaKata na kila Kijiji. Tukifanya maamuzi magumu, Chamachangu cha Mapinduzi kitashinda kwa kishindo 2015. Natakaniombe kabisa Wabunge ambao wengi ni wa CCM tuliomohumu na Serikali yenyewe ambayo ni ya CCM, tufanyemaamuzi haya magumu kwa sababu utatuzi wa shida hii yamaji ndiyo ambao utawafanya Watanzania wote waonekwamba, maisha bora yaliyoahidiwa kweli wameyapata.

Zipo tuhuma zimetolewa hapa kuhusu Waziri wa Majikwamba, amechukua fedha nyingi akapeleka Jimbonikwake. Naomba nisimame hapa nitoe ushuhuda kwamba,mwaka 2005 wakati Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCMambaye sasa hivi ni Rais wetu, Mheshimiwa Jakaya MrishoKikwete, alipotembelea Kilimanjaro, Wananchi wa Mwanga,Same, walimlilia sana kuhusu suala la maji. Sisi kule Hai naMoshi Vijijini na Vunjo na Rombo, tukamlilia kuhusu barabaraza lami. Leo hii fedha zimekwenda Hai kujenga barabara zalami hakuna mtu analalamika. Fedha zimekuja Moshi Vijijinibarabara za lami zinajengwa, mimi siye Waziri waMiundombinu, hakuna anayesema nimetembelewa. Fedhazimekwenda Rombo Jimbo la Upinzani, barabara ya lamiimejengwa pale, fedha ambazo Serikali ya CCM imetoa,hakuna mtu analalamika. Kwa nini fedha zikienda Mwangana Same kujenga Mradi wa Maji ambao Mheshimiwa Raisaliahidi tunakuwa na malalamiko? (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwombeMheshimiwa Waziri akaze buti, asikatishwe tamaa, hii siyoahadi ya Mheshimiwa Maghembe ni ahadi ambayoMheshimiwa Rais aliitoa mwaka 2005, 2010 ameirudia tenana kila mara anapokuja Kilimanjaro huwa anakumbushaahadi hii. Haiwezekani; Mheshimiwa Maghembe, kama Mradihuu hautakamilika mwaka 2015, CCM haitavuna kitu paleMwanga na kule Same, Lushoto na Korogwe. Kwa maana

Page 165: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

165

24 APRILI, 2013

hiyo, wale wote wanaosema Mradi huu usipewe fedha ninjama ya kufanya CCM ishindwe katika maeneo hayo namimi nataka niiombe Serikali kwa ujumla kwa kweli iangalie.Mimi sina wasiwasi kwamba kuna maeneo mengine ambayokilio cha maji kipo kama ambavyo wamesema.

Inategemea maji yameahidiwa lini. Kama mtuameahidiwa miaka miwili iliyopita na haya ya miaka minane,lazima yapate kipaumbele. Sasa Waziri huyu ambayeamechukua Wizara ambayo imeshaongozwa na Mawaziriwengine, anapokuja kupitisha fedha ambayo imeshapitishwahuko nyuma, mimi naomba kabisa jamani tusimlaumu, tumtiemoyo. Mheshimiwa Maghembe, unapohangaika na Mradiwa Masasi, Nachingwea, Mradi wa Handeni, Lake Victoria,Shinyanga, Tabora, Lamadi, Meatu, Farqwa Kondoa, kujahapa Dodoma na Miradi mingine ile ambayo umeitajaukurasa wa 31 mpaka ukurasa wa 40, nakusihi sana usisahauMradi huu wa Mwanga, Same na Korogwe, kwa sababu tuya kelele za watu ambao wanapenda kutafuta jambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye Jimbo langu laMoshi Vijijini. Namshukuru sana Mheshimiwa Susan Lyimo,amesema vizuri kuhusu Kolini Kusini na akasema ni watu wakekwa sababu amezaliwa Kolini Kusini, lakini mimi ndiyo Mbungewao. Pale kuna Mradi ambao unashughulikia vijiji viwili; KoliniJuu ambayo hakuitaja na Kolini Kusini. Naishukuru Serikali yaChama cha Mapinduzi pale tumepokea shilingi bilioni 1.027na hivi sasa mkandarasi yuko kwenye site, Mradi umekamilikakwa asilimia 20. Wananchi wa Kolini Juu na Kolini Kusiniwanashukuru sana na mara ya mwisho kutembelea palewanategemea uanze kama alivyosema Mheshimiwa Lyimomwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Chemchemi yaMangi ambao amesema unaongozwa na Prof. Elisante waChuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni kweli wananchiwamechangia lakini Mheshimiwa Lyimo akasahau kusemakwamba na Mbunge naye alikuwepo naye akachangiashilingi milioni tano. Unajua mambo haya ya siasa, lakininamshukuru sana Mheshimiwa Waziri, kwa sababu Mradi wa

Page 166: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

166

24 APRILI, 2013

Kilema Juu, Kilema Kati na Kilema Boro, ambao ni wa takribanshilingi bilioni mbili, nafurashi kusema fedha zimekwenda naMkataba umeshaandaliwa. Jana nimeongea na Mkurugenzikwa maelekezo kutoka Wizarani, nimewaruhusu wasaini ulemkataba, fedha ifike kazi ianze kwa vijiji hivyo. Vilevile kwamwaka unaokuja Wananchi wa Mande Tela watapata fedhapale shilingi milioni 824 kwa ajili ya kijiji chao.

Mheshimiwa Naibu Spika, shida ya maji iko kila mahaliTanzania. Kwa upande wa Moshi Vijijini kuna Kijiji cha MwasiKaskazini na Mwasi Kusini, hivi viko Uru Mashariki, bado kabisapale suala la maji ni tatizo. Kuna kijiji cha Ungoma na Njari,Kata ya Uru Kaskazini, bado tatizo la maji liko palepale. Halafukuna vijiji ambavyo havijatajwa mahali popote, maana hivinilivyovitaja angalau vimetajwatajwa katika Hotuba yaMheshimiwa Waziri. Kwa mfano, eneo la Mabogini, eneo laTTC, eneo la Kindi na vilevile maeneo mengine ya UruMashariki na Uru Kusini, maeneo ya Kitandu, Longuo naKariwa, hakuna maji. Sasa mimi siko hapa kulalamika, kwasababu tukilalamika kwa nini hakuna maji, tutakuwa kamahatuelewi hali halisi. Mimi nataka nishauri mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza, ambaloMheshimiwa Waziri amelisemea vizuri, nataka niwashauriWatanzania wote, bila kujali itikadi zao, bila kujali kwambawako Serikalini au wako nje ya Serikali, kwa kweli tuikumbatieteknolojia ya kuvuna maji ya mvua. Tuanze kuvuna maji yamvua kwa namna yoyote ile, katika ngazi ya kaya, katikangazi ya kijiji na ikiwezekana katika ngazi ya Kata. Natakaniziombe kabisa Taasisi za Dini, kwenye misikiti na makanisa,waanze kuonesha mifano na taasisi za elimu katika mashuleyetu yote ya Primary na Secondary, tuanze kuhakikishakwamba, tunavuna maji ya mvua ambayo yanapotea bure.Tukisubiri Serikali imalize tatizo hili itachukua muda mrefu sana.Tutamtesa Waziri na Naibu wake pale, ambaye anahangaikasana, hatutafanikiwa. (Makofi)

Tufanye kama tunavyochangia fedha za harusi nasend off na zinafanikiwa. Nataka niwaombe Watanzaniawote tuamue kila mahala tulipo tujichangishe kwa ajili ya

Page 167: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

167

24 APRILI, 2013

kuvuna maji ya mvua. Nataka nimshauri Mheshimiwa Waziriwa Maji, ashirikiane na Waziri wa Viwanda na Biashara, kunaKituo cha CAMARTEC, kina utaalam wa jinsi ya kuvuna majikatika ngazi ya kaya na katika ngazi za juu zaidi kwa maanaya maji ya vijijini, kata na kadhalika. Hilo ni moja ambalonataka niwaombe Watanzania wote, tuweke itikadi kando,tuweke siasa kando, kila mtu hata ikiwezekana katika kaya,ajitahidi kufanya jambo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo natakanilishauri Bunge lako Tukufu na niishauri Serikali, narudia;tufanye maamuzi magumu kama ambavyo tumewekakipaumbele kwenye miundombinu ya barabara na tumeonamatunda yake na kama ambavyo tunapiganiamiundombinu ya reli, tuweze kuwa na reli na bandari; natakanipendekeze Serikali na Wabunge tuamue tutenge hiyoshilingi trilioni 1.8, ambayo inatakiwa kwa miaka mitatu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru naungamkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Cyril Chamikwa mchango wako, ndiyo utakuwa mchangiaji wetu wamwisho kwa asubuhi ya leo na kwa kweli nikushukuru sana.Kwa sababu kama Wabunge hilo ndilo jukumu letu kufikirikwa pamoja katika matatizo mazito yanayowagusawananchi wetu namna gani tunavyoweza kuja na majibuya kuweza kutatua matatizo badala ya kufikiri kwamba akiwafulani pale basi ni kurusha mawe tu, haisaidii sana.Nakushukuru mno kwa kutusaidia kutuwekea mwelekeo huo.Jioni tutaendelea na uchangiaji orodha imejaa kabisanaomba mtu asiniletee karatasi yoyote ataanza MheshimiwaDunstan Kitandula, Mheshimiwa Innocent Kalogeris naMheshimiwa Zabein Muhita.

Waheshimiwa Wabunge, naomba kusitisha shughuliza Bunge hadi saa kumi na moja jioni.

(Saa 7.00 mchana Bunge lilifungwa mpaka saa 11.00 jioni)

Page 168: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

168

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

Hapa Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, majadilianoyanaendelea kuhusiana na hoja ya Serikali ambayoimewasilishwa na Mheshimiwa Waziri wa Maji asubuhi ya leokwamba, Bunge sasa likubali kujadili na kupitisha Matumiziya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Tukokatika hatua ya uchangiaji, na kama nilivyosema kipindi chaasubuhi mchangiaji wetu wa kwanza ni Mheshimiwa niMheshimiwa Dunstan Kitandula na Mheshimiwa InnocentKalogeris ajiandae na Mheshimiwa Zabein Mhita aendeleekujiandaa. Mheshimiwa Dunstan!

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa NaibuSpika, ninakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi nichangiekwenye hotuba ya Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nimshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye kila uchaoanazidi kutupa baraka zake. Nitumie fursa hii kuipongeza nakuishukuru Serikali, tarehe 13 mwezi huu wa Aprili, MheshimiwaRais alifanya ziara katika Mkoa wa Tanga, alifika Mkingakufungua barabara ya Tanga-Horohoro. Tunaipongeza nakuishukuru sana Serikali kwa kukamilisha barabara hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Mheshimiwa Raisakiwa pale alisikia kilio cha watu wa Mkinga kwamba Makaoyetu Makuu hayana maji na alituahidi Shilingi milioni 200 kwaajili ya ufumbuzi wa haraka wa tatizo lile. Tunamshukuru sanaMheshimiwa Rais na Serikali. (Makofi)

Vile vile naishukuru Serikali kwa ajili ya kukamilika kwaMradi wa maji wa Daluni wananchi wa Daluni Kibaoni, BomboMtoni na Ng’ombeni wanapata huduma ya maji kwa uhakikaninawashukuru sana. Tunatarajia sasa mradi mradi ulemwingine wa mapatano uanze. Mradi ule sisi wa Wilaya yaMkinga tumekamilisha kila kinachohitajika, tunachosubiri ni

Page 169: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

169

wenzetu wa Wizarani m-push ili tuweze kupata ile no objectiontuweze kuanza mradi ule. (Makofi)

Ikumbukwe kwamba hiki kitakuwa ni kijiji cha pili katikavile vijiji10 vya utekelezaji wa vijiji 10 vya Mradi wa Benki yaDunia. Kwa hiyo, tunaomba Wizara ifanye jitihada mradi huuuanze kwa haraka kwa maana mradi huu unatakiwa kuanzakwenye financial year hii. Mradi ule ukianza, tunaamini kuwawatu wa Machimboni, Kongena, Bantu na hata watu waMienzani wataweza kufaidika kwa kupata huduma ya majisafi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi kuona kwambabaada ya kupiga kelele kwa muda mrefu, sasa mradi waKasera umeingizwa kwenye bajeti hii. Naishukuru sana Serikali.Kuweka mradi ule kwenye mpango wa mwaka huu ni jambomoja, lakini utekelezaji ni jambo muhimu zaidi. TunaiombaSerikali fedha za mradi ule zije kwa haraka, upembuzi ufanyikeili watu wa Mkinga waondokane na adha ya maji. Mradi uletunategemea ukiweza kufanikiwa basi maeneo ya BambaMavengero, Bamba Mwarongo, Doda, Barungu Kasera naMakao Makuu yetu ya Wilaya ya Kasera watapata maji kwauhakika. (Makofi)

Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu maendeleoya Mkinga yanategemea sana Makao Makuu ya Wilayayawe yametulia. Tunaomba mtusaidie tuweze kujenga Mjiule ili maendeleo yaweze kupatikana katika Wilaya yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,sasa nizungumze kwa ujumla kuhusu sekta ya maji.Waliotangulia kusema wamesema hapa kwamba maji niuhai, nami niongeze kwamba maji ni ustaarabu, maji ni isharaya binadamu kustaarabika. Bila maji, hakuna ustaarabu. Sasakatika nchi yetu tuna tatizo kubwa la maji na tatizo hililinatuondolea utu wetu. Heshima ya utu wetu inaondoka.Haingii akilini mpaka leo Watanzania tunagombea maji yakunywa, maji ya matumizi na mifugo. Hili siyo jambo zuri,linatuondolea utu wetu na hadhi yetu ya ubinadamu.

Page 170: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

170

Hatujafanya vizuri katika sekta hii. Naiomba Serikali iongezejitihada ili tuondoe kero hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi kuona kwambasasa tunaanzisha Mfuko wa Maji, lakini fedha zilizoko pale nikidogo. Lazima kama Taifa tupanue uwigo wa mfuko ule. Nilazima tubuni vyanzo vipya vya kukuza mfuko ule. Ukiangaliakatika taarifa mbalimbali za kibenki, wanasema mabenki yetusasa hivi yanapata faida kubwa. Tuna uwezo wa kukaa namabenki tukazungumza nao wachangie angalau asilimiamoja ya pre tax profit ya mfuko huu. Kama Benki inapatafaida ya Shilingi bilioni 80 CRDB, NMB Shilingi bilioni 103 naMabenki mengine hivyo hivyo haituzuii kukaa nao meza moja,wao kama watu wanaofaidika na huduma za kijamii katikanchi yetu wakachangia kwenye mfuko huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile wakatiWatanzania wanaendelea kufa kwa madhila ya matatizoya maji, siyo vibaya kama viongozi tukaonyesha njia,tukafunga mkanda. Kuna jambo limekuwa likipigiwa kelelemuda mrefu ya OC. Naamini OC inafanya mambo mengilakini kuna kile kipengele cha chai kinapigiwa kelele. Hebutuamue na kusema kuwa tunaacha mwaka huu kunywa chaina fedha yote ile au hata 5% ya kifungu hicho ielekezwekwenye mfuko huo ili tuwaokoe watu wetu na tatizo hili lamaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninashauri vilevile tuangaliekuwa na tax exempt bond ambayo tukizi-float hizi tunawezakupata source nyingine. Watanzania wanaathirika na tatizola maji. Nilisema kipindi kilichopita kwamba hii itakuwa ni hojaya uchaguzi mwaka 2015. Ushahidi umejionyesha dhahirikuwa kila Mbunge aliyesimama alipiga kelele kuhusu tatizola maji. Ifike mahali sasa tuone uwezekano wa kuhakikishakwamba bajeti ya maji inaongezeka. Haiingii akilini hatakidogo kwamba 75% ya Watanzania wako vijijini, lakini fedhatunazoelekeza kwenye Sekta ya Maji Vij i j ini ni 30%.Haiwezekani, haikubaliki! Hata hiyo 30% tunayoisema miminimepitia haya ma-book kuitafuta hiyo 30% siioni. (Makofi)

Page 171: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

171

Mheshimiwa Naibu Spika, naisihi sana Serikali yanguifanye kila linalowezekana tuifungue bajeti hii tuuiongezeefedha za kutosha ili tuondokane na tatizo hili la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, nakushukuru sanaMheshimiwa Dunstan Kitandula. Sasa kama nilivyosema, nizamu ya Mheshimiwa Innocent Kalogeris, atafuatiwa naMheshimiwa Zabein Mhita.

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa NaibuSpika, nami nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia bajetiya Wizara ya Maji ambayo iko mbele yetu. Maji ni Uhai lakinipia ni hitaji la msingi la maisha kwa viumbe vyote duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hotuba nzuri nayenye matumaini ambayo imetolewa na Mheshimiwa Waziri,lakini bado mpangilio wa bajeti haukidhi mahitaji halisi yawatu, hasa Vijijini kama mchangiaji aliyepita MheshimiwaKitandula alivyosema kwamba upendeleo mkubwaunaonekana uko katika maeneo ya Mjini na Vijijini bado nimatatizo. Mfano halisi tu, Halmashauri yangu ya Wilaya yaMorogoro Vijijini mwaka 2012 tulipata Shilingi milioni 11 tukutoka Wizarani, mwaka huu tumeomba Shilingi milioni 484lakini tumepata Shilingi milioni 267, angalau tunashukuru, lakininadhani bado hazitoshi kukidhi mahitaji ya maji Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mfumo wauendashaji wa Wizara yenyewe, kusimamia miradi lakinivilevile Wizara kupeleka miradi katika Mamlaka za Maji zaMiji, Majiji na baadhi ya Halmashauri, ni dhahiri kwambadhamira ya Serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi yaChama chetu cha Mapinduzi haitaweza kukamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 80 ya Watanzaniawanaishi vijijini na wanahitaji huduma hii ya maji. NadhaniWizara inahitaji kuwa na kiungo kati ya Wizara, Mkoa naHalmashauri katika kutekeleza majukumu yake. Hil i

Page 172: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

172

nililizungumza katika Bunge la Bajeti lililopita, niliomba Wizaraianzishe utaratibu kama wa Wizara ya Ujenzi kuanzishaWakala wa Maji nchini na ninakumbuka Mheshimiwa Waziriwakati anafanya majumuisho, alisema hili ni jambo jema naaliahidi kuleta Muswada wa kuanzisha Wakala wa Maji nchini.

Nashukuru katika bajeti ya mwaka huu tunaonyeshakuna Mfuko, lakini nadhani lile ombi langu lilikuwa bora Wizaraikalifanya. Kwasababu kuwa na Mfuko wa Maji bila kuwa naWakala wa Maji na kuwa na Bodi ya Maji itakuwa ni hadithitu. Kwa maana huu Mfuko wa Maji utakuwa unatoa fedhana kupeleka kwenye Mamlaka za Maji za Mjini na watu waVijijini wataendelea kutopata huduma za maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wazo la kuwa na Wakalawa Maji wa Taifa na Bodi ya Maji ya Taifa ninadhani ndiyosuluhisho la kudumu. Tunasema kuwa Mfuko wa Majiutachangiwa, namshukuru ndugu yangu MheshimiwaKitandula ambaye amemaliza kuongea sasa hivi ametoahata maelekezo. Mimi nadhani Bodi ya Maji ya Taifatukiwanayo kama Bodi ya Barabara, inaweza kukopa fedhaBenki kwasababu biashara ya maji ni biashara. Maji siyohuduma ambayo inakwenda kavukavu, maji ni biashara yahuduma ambayo inakwenda kibiashara, inaweza kukopaBenki na inaweza kutusaidia kuendesha miradi yote ambayotunayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu bado kwaWizara ya Maji, wakati Mheshimiwa Waziri anatoamajumuisho angetuambia ni sababu zipi za msingi siku ilealikubali, lakini amekuja na wazo lingine, hatuoni hili wazo lakuanzisha Mamlaka za Maji, lakini pia hatukuona ile Sheriaambayo pengine ingefanya sasa tukawa na Mamlaka zaMaji. Tukiendelea katika style hii mimi naomba niseme tukwamba Ilani yetu ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzimwaka 2015 tutakapokwenda kwa wananchi, tutakwama.

Mimi ninajua Ilani yetu ilikuwa inalenga siyo kwa ajiliya kushinda uchaguzi, ila kuwatumikia wananchi. Ombi langukwa Wizara, tafadhalini, tusaidieni katika hilo. Njooni katika

Page 173: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

173

style ambayo itatufanya wote kwa pamoja Watanzaniatunapata huduma za maji. Mimi katika Halmashauri yangusina la kusema lolote. Hakuna visima, mradi wa vijiji 10haujatekelezeka kwasababu hakuna mawasiliano kati yaHalmashauri na Wizara, sasa naweza kusema kwambatumeshindwa katika miradi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ninachotakakuzungumzia ni suala la kuwa Bodi ya Maji, suala la kuwa naWakala wa Maji Kitaifa litataufanya Wabunge katika Mikoayetu kuweza kufanya mapambano au kuweza kuchanganyaau kujadiliana kwa kina kwasababua pale kutakuwa naRegional Manager wa Maji na katika Bodi ya Maji Mkuu waMkoa ndio anakuwa Mwenyekiti wa Bodi kama vile kwenyebarabara. Lakini Wabunge tutakuwa ni Wawakilishi wawananchi, kutakuwepo na Wenyeviti wa Halmashauri,Watakuwepo ma-Meya wa Miji, na katika kikao kileyatakayofanyika yatasaidia badala ya kusubiri WaheshimiwaWabunge hapa kupambana na Wizara katika Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sana kakayangu Profesa Maghembe na ndugu yangu BwanaMahenge, Naibu wake, kuna mmoja alisema mchana katikauchangiaji wake, nadhani wakati wa kufanya maamuzimagumu, nami naomba, huu ni wakati wa kufanya maamuzimagumu wa kuwa na Wakala wa Maji Tanzania na kuwa naBodi ya Maji Tanzania kwa ajili ya kupata huduma kwawananchi. Naamini ukifanya hivyo, kaka yangu Professorutaondoka kwenye Wizara hiyo, Watanzaniawatakukumbuka na ninaamini kuwa suluhisho la kero ya majikwa Vijijini na hata Mijini litakuwa limekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nitumie nafasi hiikupongeza Wizara, nimeona mwaka huu kwenye Bwawa laKidunda mmetenga fedha kwa ajili ya kuliendeleza lakinivilevile umetueleza katika kitabu chako cha hotuba ya bajetikwamba mmetenga fedha kwa ajili ya kulipa wananchi fidiamwezi wa Tano. Huu ni mwezi wa Nne ninataka kukwambiakuwa ahadi ni deni, na kwa mwanadamu ukiahidi ni lazimautekeleze. Tuliwaahidi wananchi wa Kata ya Serimbala,

Page 174: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

174

wananchi wa Kata ya Mkulazi mwaka 2012 kwambatutawapatia fidia yao lakini vilevile tutawapatia viwanja,tutawajengea miundombinu na wahame wapishe ujenzi waBwawa la Kidunda.

Kwa ahadi yako hii, nakuomba malipo hayo mweziwa Tano yaende sambamba na kulipa Halmashauri yaMorogoro Vijijini kiasi cha karibu Shilingi bilioni 1.2 ambapoShilingi milioni 970 kwa ajili ya kujenga miundombinu, lakinivilevile Shilingi milioni 185 kwa ajili ya kupima viwanja iliwananchi hawa wakipata fedha hizi za fidia waende kwenyemakazi ambayo tayari yameshaandaliwa, waendewakatumie pesa zao kwa shughuli ya kujenga. Kwa maanakama utampa mtu pesa kabla hujampa kiwanja, kamamakubaliano yetu tulivyokubaliana, kabla hujatujengeahuduma zetu za Msingi, Shule, Zahanati na nyumba za ibada,ni kielelezo tosha kwamba watachukua fedha hizi na baadaya muda pesa zile zitakwisha na hawataweza kujenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile namwombaMheshimiwa Waziri wakati anafanya majumuisho ikiwezekanamradi huu, juzi kulikuwa na mafuriko katika Kata ile, Kata nzimailizama, nikielelezo tosha kwamba tukijenga bwawatukawalipa wengine wakaondoka na wengine wakabaki,mafuriko mengine yakitokea yanaweza kuleta athari kubwakwa wananchi na huko tunaweza kusababisha maafamakubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani kuna kilasababu ya kuangalia upya mradi huu kwa wale ambaohawapo kwenye Kata ile wakaingizwa ili tukiondoa tuwezekuwasalimisha wananchi wote wa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia, nimwombetu Mheshimiwa Waziri kuwa mwaka huu mmetupa Shilingimilioni 267, basi pamoja na mahitaji yetu yalikuwa karibuShilingi milioni 500 tupate pesa hizo zote kwa pamoja autuzipate zote bajeti katika 100% ili kusudi tuweze kukamilishahuduma za msingi. (Makofi)

Page 175: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

175

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba vilevile katikamradi wa vijiji 10, mtie msukumo ili uanze katika mwaka huuwa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja nikiamini kwamba fedha ikipatikana,haya yote niliyoyaomba yatatekelezeka.

NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa InnocentKalogeresi. Mheshimiwa Zabein Mhita, Mbunge wa Kondoaatafuatiwa na Mheshimiwa Agness Hokororo.

MHE. ZABEIN M. MHITA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili kwa niaba ya wananchiwa Jimbo la Kondoa Kaskazini nami niweze kuchangia hojailiyopo mbele yetu. Aidha, namshukuru Allah Sub-hanah-Wataallah kwa kunipa uwezo na afya kuweza kusimamambele yako.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naombanichukue nafasi hii kushukuru Serikali yetu kwa ajili ya fedhaya Mfuko wa Maji zilizotengwa katika Halmashauri ya Kondoakiasi cha Shilingi bilioni 1.7. Naiomba Serikali itoe hizo fedhamapema ili ziweze kufanya kazi ambayo imekusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wastani waupatikanaji maji Vijijini katika nchi yetu ni asilimia 58 lakinikatika Jimbo la Kondoa Kaskazini upatikanaji wa maji hayoni asilimia 30 tu. Asilimia hiyo 30 maji hayo yote siyo safi walasiyo salama. Kwa hiyo, inaonesha jinsi ambavyo tatizo hili lilivyokubwa na lilivyo sugu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vingi havina maji kabisakatika Wilaya ya Kondoa. Naomba nitaje vichache tu kwaleo kutokana na muda. Vijiji vya Chubi, Hachwi, Salanka,Isongolo, Ikengwa, Humai, Chandimo, Kilele cha Ng’ombe,Makirinya, Mwembeni, Majengo, Matangalimo, Gaara,Thawi, na Mauno. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata katika Mji wa Kondoaambao ni Mji Mkuu wa Wilaya bado kuna maeneo ambayo

Page 176: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

176

hayana maji. Mfano Tura, Bicha, Kwapakacha, Bamai na WisiKwantisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa kutoa uwianosawa wa miradi ya maji kwa Wilaya zote uangaliwe upyakwani kuna Wilaya ambazo zinapata asilimia mpaka sabinimpaka themanini wakati Wilaya nyingine mfano Kondoa niasilimia 30.

Mheshimiwa Naibu Spika, nioneshe masikitiko yangumakubwa. Wanawake na wasichana ndio wana jukumu lakutafuta maji, na kwa kusema kweli wanakwenda masafamarefu wanatumia masaa mengi, na kwa kweli wanaathirikasana kwa sababu huko wanapokwenda kuchota majikwenye makorongo, kwenye mito, ndiko ambako vile vilewanyama wakali wanakwenda kunywa maji.

Wapo wanawake wengi wamekwishapoteza baadhiya viungo vya miil i yao na kuna wengine ambaowamepoteza maisha yao kabisa kwa ajili ya kushambuliwana hawa wanyama wakali.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunalo bwawa la Itaswi,bwawa hili lilijengwa mwaka 1958. Wiki mbili zilizopitakumekuwa na mafuriko makubwa sana kwenye bwawa hilina lipo katika hatari ya kutoweka kabisa. Bwawa hililinahudumia vijiji na vitongoji saba. Hata hivyo, naombaniwashukuru watalaam kutoka Wizara ya Maji na kutokaBonde la Maji la Kati ambao wamefika kwa wakati nawanafanya tathmini na watatoa taarifa na nitaomba taarifahiyo tuipeleke Wizarani ili hatua za haraka na za makusudikabisa ziweze kuchukuliwa ili kunusuru bwawa hili, vinginevyowananchi wa hivi vijiji saba wataathirika sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Wizara kwakuweka vijiji vilivyoko katika mtaro wa Ntomoko katikampango wa kukarabatiwa katika mwaka 2013/2014, kwasababu mtaro huu wa Ntomoko ni mkombozi mkubwa lakinihata hivyo, ninaomba Kijiji cha Ntomoko ambacho ni chanzocha mtaro huo nacho kipatiwe maji. (Makofi)

Page 177: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

177

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu haiingii akilinina haieleweki wakati wananchi ambao wanatunza nakuhifadhi chanzo hiki cha maji wao hawana maji kabisa.Wananchi hawa wamekuwa wavumilivu kwa miaka mingi.Waswahili wanasema, mvumilivu hula mbivu, lakini mudaukiwa mrefu, mvumilivu hula mbovu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri Mkuu alipofikaNtomoko kukagua mradi huo aliahidi kuwa kijiji hicho chaNtomoko kitapatiwa maji. Hivyo naomba ahadi ya WaziriMkuu iweze kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu wamaji na kama tunavyoelewa kwamba maji ni uhai, naiombaSerikali basi iongeze fedha kwa ajili ya miradi ya maji ili Wilayaambazo zina matatizo makubwa mfano wa Kondoa nazoziweze kuhudumiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya miradi ya maji nindogo sana, kwa maana kwamba hata Mheshimiwa Waziriangekuwa na utalaam gani, hawezi kufanya chochote!Atashindwa! Kwa hiyo, naomba hiyo bajeti iweze kuongezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba MheshimiwaWaziri, kaka yangu, Rumburya, utakapokuwa unahitimishahotuba yako uwaeleze basi wananchi wa Jimbo la KondoaKaskazini ni hatua gani na za haraka zitakazochukuliwa naWizara yako ili kuweza kuwanusuru. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi pamoja na wananchiwa Jimbo la Kondoa Kaskazini tunayo matumaini makubwasana na Waziri wa Maji pamoja na Naibu wake. Hivyo basi,nikiwa na matumaini makubwa pamoja na wananchi,tunaamini kwamba Jimbo letu la Kondoa Kaskazini litapewakipaumbele katika upatikanaji huu wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sina sababu yoyote yakutounga mkono bajeti hii. Naiunga mkono kwa asilimia miamoja. Ahsanteni sana. (Makofi)

Page 178: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

178

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Zabein Mhitakwa matumizi mazuri ya muda. Sasa namwita MheshimiwaAgness Elias Hokororo atafuatiwa na Mheshimiwa FreemanMbowe na Mheshimiwa Stella Manyanya ajiandaye.

MHE. AGNESS E. HOKORORO: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi na mimi niwezekuchangia hoja iliyopo Mezani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikijitahidikutafuta ufumbuzi wa upungufu wa huduma ya maji kwawananchi wake katika kipindi hiki hasa katika Serikali hii yaAwamu ya Nne.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili linadhihirika wazi,tukiangalia hata katika vitabu ambavyo tumepata katikamwaka 2006 watu milioni 16.3 ndiyo walikuwa wanapatahuduma ya maji, na ilipofika mwaka 2012 ni takribani watumilioni 20.6. Kwa hiyo kuna ongezeko.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ongezeko hilokubwa, lakini bado pia Serikali yangu imeendelea kutambuakuwa upatikanaji wa maji Mij ini na Vij i j ini bado inachangamoto kubwa ambayo inahitaji kufanyiwa kazi kwaumakini na kwa mapana zaidi. Ndiyo maana pia kupitia ilaniyake ya CCM Serikali imejipangia kuwa ifikapo mwaka 2015tunatakiwa tufikie kwa maji Mijini upatikanji wake ufikie asilimia95 na kwa Vijijini asilimia 65. Hiyo ni nia nzuri na njema kwaSerikali. Naipongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kwa kuwa Sektahii ya Maji ni muhimu na kila Mbunge hapa amekuwa akisemamaji ni uhai, nami natambua kuwa maji ni uhai, badonaishauri Serikali na Wizara kuongeza kasi na kutafuta mbinumpya zaidi katika kuhakikisha upungufu huu ambaoWaheshimiwa Wabunge hapa tumekuwa tukiulalamikiaunaondoka kwa kasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, athari za upungufu wa majizinakwenda moja kwa moja kwa akina mama, ninamaanisha

Page 179: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

179

wanawake. Katika maeneo mengi ya Tanzania wanawakendio wasaka maji na wamekuwa wakitembea umbali mrefu,wamekuwa wakitumia muda mwingi na kwa masikitiko katikamaeneo mengine kama kule Kilwa, hata vitendo vyaudhalilishaji vinafanyika, wanawake wakiwa katika harakatiza kusaka maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali yangu piakuendelea kuongeza kasi ya kupunguza vikwazovinavyokwamisha wanawake katika shughuli zao zakimaendeleo. Ni dhahiri pia kwamba wakati wanawakehawa wanaendelea kutafuta maji kwa masaa mengi,wanakuwa pia hawawezi kushughulika katika shughuli zakimaendeleo. Hizo athari zote nilizozitoa hapo zinawaumizaakina mama kijamii kwa maana ya kisaikolojia, kiafya nakimaendeleo pia kwa sababu ule muda ambao walipaswakwenda shambani kwenye Sekta ya Kilimo, wao wamekuwawanatumia muda mwingi kutafuta maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu SPika, kwenye maeneo ya kwetuMkoa wa Mtwara pia tatizo hizo bado lipo. Kwa mfano, Kijijicha Nanjota wanawake wanatumia karibu masaa 24. Inamaana mchana mmoja na usiku mmoja, kwa hiyo, utaonadhahiri ni kwa namna gani wanawake tunashindwa kushirikimoja kwa moja kwenye shughuli za uzalishaji na hivyotunaendelea kudorora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani katika Mikoaya Kusini pia kwa upande huu wa Sekta ya Maji bado tuponyuma. Kwa mfano, katika Mkoa wa Mtwara, wastani wamaji Mijini na hapa ninamaanisha Makao Makuu ya Wilaya,tunapata kwa asilimia 58 na Vijijini tunapata kwa asilimia 42.5.Hivyo hivyo kwa Mkoa wa Lindi Makao Makuu ya Wilayatunapata kwa asilimia 57.2 na Vijijini kwa asilimia 39.Ukiangalia, bado huduma hii kwa Mikoa hiyo iko nyuma.Pamoja na kazi nzuri na jitihada kubwa iliyofanywa na Serikaliyangu kwa mradi wa Mbwinji ambao utatoa huduma ya majikatika Miji ya Masasi na Nachingwea na Mradi wa Makondeambao unatoa maji kwa Wilaya za Newala, Tandahimba,na Mtwara Vijijini, lakini naiomba Serikali kuhakikisha kwamba

Page 180: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

180

ile mipango mizuri iliyoweka kwa mfano kwenye Mradi waMakonde, ule mradi wa kuongeza watumiaji wa maji kwenyevijiji ambavyo mradi huo unapita, ni vyema ikaongeza kasina kwa sababu upembuzi yakinifu ulishakamilika, basi Wizaraihakikishe zile fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi huozinakwenda ili wananchi katika Wilaya za Tandahimba,Newala na Mtwara Vijijini waweze kufikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo litawezesha piakupunguza gharama za utengenezaji wa miundombinu kwasababu kwenye maeneo mengine ambapo maji yamekuwayakipita tu wananchi wakati mwingine wanakuwawakiiharibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya za Masasi naNanyumbu bado pia tuna upungufu mkubwa. Pamoja nahuo mradi mkubwa wa Mbwinji, lakini kwenye Wilaya hizi majiyake hata kwenye visima ambavyo vimechimbwa, badoyanakuwa hayapatikani. Kwa mfano, katika mradi wa ujiranimwema kisima cha Mangaka kilichochimbwa kati yaMsumbiji na Tanzania, kisima cha kwanza kilipatikana lita 400tu kwa saa na kisima cha pili lita 1,500 na lengo ni kupata lita15,000 kwa saa. Kwa hiyo, utaona kabisa bado hatunavyanzo vya uhakika vya maji. (Makofi)

Ninaishauri Wizara kama ambavyo kwenye hotubaya Mheshimiwa Waziri Mkuu amesisitiza kwamba ipo haja sasaya kutumia mbinu mpya. Naiomba sana Wizara kuangaliasasa mbinu mpya. Hapa ninashauri, kwenye maeneo hayaWilaya hizi za Masasi na Nanyumbu ni vyema sasa tukatumiamaji ya mto Ruvuma ili kuweza kuondoa tatizo hili na iwe nihistoria kwa upande wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suluhisho lingine ni lile lakuchimba mabwawa. Katika maeneo ya vijijini Wilaya yaMasasi kama vile Nambawala, Mpanyani, Mraushi na Nanjotahuko kuna kiu, yaani tatizo la maji kwa kiasi kikubwa. Ndiyomaana hata hili jina la Nanjota yaani kumekuwa hakuna majikabisa. Kwa hiyo, huko kunahitajika pia ufumbuzi wa harakaharaka wananchi wapatiwe mabwawa. (Makofi)

Page 181: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

181

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Wizara kuonanamna ya kuondoa wananchi katika maneo haya hasawanawake ili wasiwe wanalala huko visimani usiku namchana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya Benki ya Duniaipo, lakini miradi hii inakwenda taratibu sana, haiendi kwakasi. Hii nikiangalia inatokana pia na zile hatua zake zautekelezaji kwa mfano, ukimaliza hatua moja unatakiwakupeleka taarifa hiyo Wizarani. Kwa mfano, katika Wilaya zaMasasi na Ruangwa tangu mwezi wa Desemba kaziimetangazwa, mzabuni amepatikana, lakini mpaka sasatunasubiri kibali kutoka Wizarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiwa tunatumia miezimitano au miezi mine, ni dhahiri kwamba utekelezaji wamiradi hii haitakamilika kwa wakati. Hii inatoa malalamikomengi sana kwa wananchi lakini na Watendaji piawamekuwa wakilalamikiwa kwamba hawatimizi wajibu wao.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Wizara ya Majiiangalie namna bora zaidi ya kuona ufuatiliaji na utekelezajiwa miradi ya Benki ya Dunia unafanyika kwa wepesi kulikoilivyo sasa, kila hatua Watendaji wanatoka kwenye maeneowanakwenda Makao Makuu na hivyo kuwasababishia sasakutokufanya kazi nyingine na kuchelewesha hatua zautekelezaji hata ya miradi hiyo ambayo wamekuwawakiifuatilia Wizarani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye kitabu hiki pia,pamoja na hizo jitihada nzuri za Serikali, kwenye Mradi waVijiji 10, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, ni vijijivinane tu ndiyo vilivyoorodheshwa.

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wamzungumzaji kwisha)

MHE. AGNESS E. HOKORORO: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

Page 182: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

182

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa AgnessHokororo. Namwita Mheshimwia Freeman Mbowe,atafuatiwa na Mheshimiwa Amina Makilagi.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kunipa nafasi ya kuwa mchangiaji katikaWizara hii muhimu sana ya maji.

Kwanza nachukua nafasi hii kumpa Waziri na Naibuwake pole sana kwa sababu kwa umuhimu wa Wizara hii nakwa idadi ya fedha ambayo Wizara hii imepangiwa katikabajeti ya mwaka huu, ni dhahiri kwamba Watanzaniawataendelea kulia kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nami nakubaliana naMheshimiwa Waziri kwamba alivyozungumza katika hotubayake mwenyewe na kukiri kwamba kuna changamotokubwa ya upatikanaji wa fedha au upatikanaji wa fedhapungufu ya zile zinazopangwa katika Wizara hii. Nichangamoto kubwa ambayo kwa kweli kama Taifa, kamahatutatambua umuhimu wa maji na ulazima wa kugawafungu la kutosha kwenye Idara ya Maji ama kwenye Wizaraya Maji, bado tutakuwa hatujaweza kuthamini kwamba majisiyo tu kwamba ni uhai, lakini vile vile maji ni utajiri mkubwakwa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea mbelezaidi, nishukuru vile vile kwamba katika hotuba ya Waziriametambua tatizo kubwa sana la maji ambalo lipo katikaWilaya ya Hai hasa katika upande wa tambarare wa Wilayaya Hai.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la tambararela Wilaya ya Hai kuna vijiji ambavyo vina tatizo kubwa sanala maji. Inaweza ikawa siyo rahisi kwa watu wengi kuaminikwamba katika Mlima Kilimanjaro kuna vijiji vina tatizo kubwasana la maji, lakini ni ukweli kwamba katika eneo latambarare ambapo kina Kata za KIA, Kata ya MasamaRundugai na Kata za Machame Weruweru katika Vijiji vyaSanya Station, maeneo ya Matakuja, maeneo ya Vijiji vya

Page 183: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

183

Tindigani kuna tatizo kubwa sana la maji. Tatizo kubwa zaidila maji katika vijiji hivi ni kwamba maji ya gravity yanayotokakatika Mlima Kilimanjaro hayajafika kwenye vijiji hivi, lakini vilevile uchimbaji wa maji katika maeneo haya umeshindikanakwa sababu maji yaliyoko katika eneo lote hilo yana levelkubwa sana ya floride.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri amekiri katika ukurasawa 116 wa hotuba yake ametambua kwamba, utafitiuliofanywa katika maeneo ya Zarau, Sanya Station, Mtakuja,KIA Village, Mkoraya, Bomang’ombe na Majengo Kati, kunatatizo kubwa la floride ambapo kiwango cha kawaidakinachokubalika cha floride ni 4.0, lakini katika maneo hayokuna from 9.2 mpaka 39 ya level ya floride ambayo ni kubwasana, haifai kwa matumizi ya binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba sanaMheshimiwa Waziri katika majumuisho yake, aniambiekwamba, pamoja na kwamba, vijiji hivi vimetajwa katikampango wetu wa Serikali wa mwaka huu wa fedha namwaka ujao wa fedha kwamba, mwaka huu wa fedha Kijijicha Mbatakero, Ngosero, Sanya Station na Mtakuja pamojana Chenka, vitapatiwa maji, lakini ukweli ni kwamba, mpakadakika hii ni Kijiji kimoja tu cha Mbatakero na Ngosero, ambaoangalao mradi wa maji umeanza kwa mbali. Lakini vilevilebado havijapata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile katika mwakaujao wa fedha kimewekwa kijiji cha Tindigani, Kwa-Sadala,Kimashuku na Bomang’ombe. Ni kweli Bomang’ombe kunamaji, lakini maji yamepungua sana kutokana na kukua kwaMji wa Bomang’ombe. Kwa bahati mbaya sana katikamaeneo haya haitawezekana kuchimba maji ya ardhini kwasababu ya floride level iko juu sana. Kwa hiyo, wananchihawa wanateseka sana na nitashukuru sana katikamajumuisho kama Mheshimiwa Waziri ataweza kusemachochote kuhusu uwezekano wa kuhakikisha kwamba majikatika vijiji yanapatikana na yanakuwa ni maji ya gravityambayo yanatoka katika scheme za maji katika Mlima waKilimanjaro. (Makofi)

Page 184: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

184

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo ni la kwanza la msingiambalo ningependa nilizungumze kwa niaba ya wananchiwangu wa Hai. Sasa niingie katika suala la water as a naturalresource na water management.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi hii ina policy ya maji.Nimeisoma sana policy ya maji ya mwaka 2012. Pamoja nakwamba ina miaka 10, lakini bado ina mambo ya msingi sanaambayo kama yangezingatiwa na yakafanyiwa kazi nayakapewa resources, tuna Sera ya Maji ambayo ni Sera nzuriambayo inahitaji tu kuipatia fedha. Ikitekelezeka hakika majiyatakuwa ni utajiri mkubwa kwa Taifa hili. Lakini kwa bahatimbaya sana ukiangalia maji yetu katika Taifa hil iyanasimamiwa na mabonde tisa ya maji, kwa maana yaBonde la Pangani, kuna Bonde la Ruvu pamoja na Wami,kuna Bonde la Lake Victoria, kuna Lake Tanganyika, kunaLake Rukwa, kuna Ruvuma pamoja na Southern Coast, kunaEyasi Basin. Ziko basin kama tisa. Lakini ukiangalia idadi yafedha ambazo Basins hizi zimepewa ili ziweze kusimamia majiau resource ya maji kwa nchi nzima ni fedha kidogo sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka huu wa fedha,bajeti ya mwaka huu, pesa pekee ambayo imetolewa kwaajili ya reserve zote hizi ni Shilingi bilioni 1.8 ambayo ndiyofedha za ndani. Hizi fedha ni kwa ajili ya kulipa mishahara tu.Kwa hiyo, programme nyingi za kuendeleza mabonde hayahazina fedha za ndani. Hizi ni fedha za kulipa mishahara nacapacity building kwa ajili ya watumishi wachache. Lakinifedha nyingine zote ambazo zinategemewa ambazo ni Sh.17,487,000,000/= ni fedha kutoka kwa wafadhili. Ina maanawasipotoa wale wafadhili, hatuna mkakati wowote wa ndaniwa kuweza kusimamia rasilimali maji, ambayo ni muhimu sanakwa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tusiyaangalie tu maji kamakitu cha kunywa ama kutumia kwa matumizi ya kibinadamuya kawaida. Ni kweli hiyo ndio priority namba one. Lakini majivilevile yanaweza yakawa ni source kubwa sana ya kuondoaumasikini katika maeneo yetu ya vijijini. Kwanza maji katikahatua yua kwanza ni lazima yatumike kama maji ya kutumiwa

Page 185: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

185

na binadamu, lakini katika hatua ya pili maji yaonekane kamarasilimali muhimu mno, kwamba, huwezi kuzungumzakuondoa umasikini kwa wananchi 80% wanaoishi vijijini kamahuna mkakati na programu ya kusimamia na ku-manage yalemaji yako yaweze kutumika kwa ajil i ya shughuli zamaendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa haya mabonde yetusita ambayo ndiyo yanasimamia rasilimali maji katika Taifa,ukiangalia idadi ya fedha ambazo tumegawia hizi Mamlakani fedha kidogo sana. Nichukue kwa mfano Bonde laPangani, ambalo linasimamia karibu wakazi milioni nne.Bonde la Pangani imeandikwa ripoti moja nzuri sana,wamefanya situational analysis ya Bonde la Pangani,wameeleza crisis ambayo ni imminent, ambayo ni lazimaitajitokeza katika Bonde la Pangani kama hatua za makusudihazikuchukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanapigania maji katiya Wakulima na Wafugaji. Kuna kupigania maji kati ya Wildlifepamoja na matumizi mengine ya Hydro-Power. Kama hakunamanagement ya mambo yote haya, ni lazima patatokeacrisis kama ambayo tunaona katika maeneo mengi wafugajina wakulima wanapigana kwa sababu ya maeneo yakulisha, sasa itakuwa ni kwa sababu ya maeneo ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile niseme tujambo moja kwa niaba ya Mkoa wa Kilimanjaro, maji mengiyanatoka katika Mlima Kilimanjaro yanakwenda katika lowerbasin, ambako yanatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbaliza kimaendeleo na za kijamii. Lakini vilevile tumekuwa hatunasera maalum ya uvunaji wa maji ya mvua. Nimesikia baadhiya Wabunge wengi hapa wamechangia, hatuna mkakatiwa makusudi wa kuvuna maji ya mvua. Kuvuna maji ya mvuasiyo tu kwa sababu ya matumizi ya nyumbani, ni hata kwamatumizi mengine ya kiuchumi katika matumizi mengine yaumwagiliaji maji. Hatuwezi kuzungumzia suala la food securitykama hatuna mpango wa kuvuna maji. Yale machacheyanayochuruzika kutoka mlimani, tukisema tuyatumie kwaajili ya irrigation, watu katika ukanda wa tambarare watakosa

Page 186: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

186

maji. Lakini maji ni mengi. Mvua zinanyesha, wakati wakunyesha mvua zinanyesha mvua kubwa, kuna mabondemakubwa ambayo yangekuwa ni rahisi sana kujenga dikes.Tunajenga dikes tunatengeneza dam, tuna-reserve maji kwaajili ya matumizi ya mwaka mzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, idadi ya rainfallinayonyesha Tanzania ukilinganisha na rainfall inayoangukaBotswana, tusingestahili kulalamika tatizo la chakula. SisiKilimanjaro tumechoka kuomba chakula kwa MheshimiwaLukuvi, tunaomba tafadhali sana Serikali iweke mpangomakini kupitia Pangani Water Basin wa kujenga reserve yamaji katika mabonde ya Mlima Kilimanjaro. Kwanza nigharama nyepesi mno, kwa sababu kuna mabondemakubwa ambayo ni natural, unajenga tu dikes kidogounazuia maji. Unaweza ukazuia maji mengi sana nayakatumika throughout the year bila kutegemea kupewachakula cha msaada na Mheshimiwa Lukuvi, ambayo nifedheha sana kuomba chakula cha misaada. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niseme katikamabonde haya, Bonde la Mto Kikavu, Bonde la MtoWeruweru, kuna Bonde la Mto Makoa, kuna Bonde la MtoSemira, yako mabonde mengi ambayo yanawezayakahifadhi maji mengi mno ambayo yanaweza yakatumikamwaka mzima. Maji hayo yanaweza yakapatikana wakatiwa mvua kwa sababu wakati huo kuna mvua nyingi sana.Hatuwezi kutegemea yale maji yanayochuruzika kutokavyanzo vingine vya maji, tutumie haya maji ya mvua, tuya-reserve haya maji. Haya maji yatatumika kwa ajili ya gravityirrigation katika maeneo ya chini na nina uhakika kwautaratibu huo tutakuwa tuna food security ambayo ni yauhakika kuliko hali ilivyo sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali hiyo vilevile inakwendakatika Majimbo ya Moshi Vijijini, Jimbo la Siha, Jimbo la Vunjona hata Jimbo la Rombo. Yako mabonde mengi makubwaambayo yangejengewa dikes ndogo tu, wala siyo miradimikubwa ya kutisha, ila ni miradi ile ambayo inahitaji uthubutuku-preserve yale maji, yangeweza kutumika katika ukanda

Page 187: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

187

mzima wa tambarare wa Mlima wa Kilimanjaro na watuwakapata chakula bila kuwa na tatizo lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima sasa Serikali yetuione maji kama inavyoyaona madini. Tusiyaone maji kamajambo la kunywa tu, tuone maji kama fedha. Tunaporuhusumvua zinyeshe halafu maji yote yanakimbilia baharini, halafuwiki ijayo tunalalamika mvua, tukikosa maji kwa msimu mmojatu tunalalamika chakula. Hatuwezi kuendelea kama Taifakama tunashindwa ku-control maji ambayo tunapewa naMungu halafu tunalalamika. Tunalalamika nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli, ni lazima uwepompango wa makusudi tena mpango wa ndani wa kuhifadhimaji yetu ya mvua. Mikoa yote inanyesha mvua, kila maeneonchi hii inanyesha mvua. Zinanyesha mvua nyingi tu, mvuazinanyesha nyingi, maji yanakwenda baharini, yanapotea,halafu tunalalamika tena hatuna chakula. Umekuwa niutaratibu wa kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Sera yetu ya Maji yaMwaka 2002, katika ukurasa wa 17 wa Sera ile MheshimiwaWaziri angalia; hatujatoa priority katika uvunaji wa maji yamvua. Priority yetu katika Sera yetu ya Maji inazungumzia yalemaji ambayo ni naturaly available. Lakini harvesting ya majiya mvua hatujaiona ni priority, hatujaitambua katika Serayetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naombakuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Nakushukuru MheshimiwaFreeman Mbowe. Sasa namwita Mheshimiwa Makilagiatafuatiwa na Mheshimia Dkt. Pudenciana Kikwembe.

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kutoamchango wangu mdogo katika sekta hii muhimu sana kwamaendeleo ya Taifa.

Page 188: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

188

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwakusema kwamba, maji ni uhai na kwa kweli, maji ndiyo kilakitu. Bila maji hakuna kilimo, bila maji hakuna afya, bila majihakuna uchumi wa Taifa letu la Tanzania. Lakiniunapozungumzia maji, unamzungumzia huyu mwanamkeambaye kwa kweli ndiye tunamtegemea katika uzalishaji wauchumi wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze moja kwamoja kuunga mkono bajeti hii kwa sababu, kwanza mimimwenyewe ni mdau wa maji, lakini vilevile niko katika Kamatiya Maji, lakini vilevile naunga bajeti hii mkono kwa sababu,kwanza, Wizara imejiandaa vizuri sana safari hii. Hata ukisomakitabu chenyewe kimesheheni, bango kitita hili linatupa sisiWabunge fursa ya kujua kila kitu kilichopangwa kufanywana Serikali na hata kilichofanyika. Kwa kweli, naombanimpongeze sana Waziri na timu yake yote kwa kazi nzuri sanawaliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono bajeti hiikwa sababu, Chama cha Mapinduzi, kama tulivyoahidikwenye Ilani kwamba, tutajitahidi kufikisha maji katika Miji naVijijini kwa kweli, ukipitia kitabu hiki kazi imefanyika sana.Nilikuwa nasoma, naona sasa suala la upatikanaji wa majiMijini tumeshafikia 86%, ni ukombozi kusema ukweli. Lakini siyokuishia 86% peke yake, ukisoma kitabu hiki utaona hatamipango sasa ya kufanya Miji yetu ya Tanzania yote sasainapata maji kwa kiwango cha asilimia cha ya juu zaidi.Naomba nipongeze sana mpango huu na ninaiomba Serikali,iendelee, ikaze buti i l i Mij i yetu yote ipate maji.Nimefurahishwa sana kusikia sasa hata Jiji la Dar es Salaamambalo mwaka 2012 nilisimama hapa nikasema kamahamtatenga fedha za kutosha mwaka huu sitaunga mkono,nimefurahi sasa fedha za ndani zimetengwa karibu zaidi yaShilingi bilioni 40. Naomba niipongeze sana Serikali yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimefurahishwa nampango sasa, Serikali yetu sasa imewasikiliza wananchi waSame kilio chao, kule Mwanga na maeneo mengine, Serikali

Page 189: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

189

inakuja na mpango makakati wa kuhakikisha wananchi walewaliopiga kelele kwa muda mrefu sasa wanapata maji safina salama. Siyo pale tu, maeneo mbalimbali ya nchi yetu,kwa kweli, kitabu hiki kimenifurahisha na ndiyo maananaunga mkono asilimia mia kwa mia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuunga mkono,sasa naomba nilete kilio cha wanawake wa Tanzania na kwakweli, natoa pia kilio cha wananchi wa Tanzania. MimiUbunge wangu ni wa Tanzania nzima kwa mujibu wa Sheria.Kwa bahati njema kabla sijaja hapa Bungeni, huwa nafanyaziara nakutana na wananchi na huwa sifanyi maandamano.Huwa nafanya Mikutano ya Hadhara, naongea nawanawake, naongea na wananchi wote. Katika Mikutanoyangu, huwa nawapa nafasi wananchi waulize maswalibaada ya mimi kuongea na wao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia Mikutano ilenimeshakwenda Mikoa mbalimbali kule Lindi, Morogoro,Pwani, Mtwara, kila mahali nimefika. NimeshatembeleaMikoa 10 kabla sijaja hapa. Katika ile Mikutano nimejaribukuuliza maswali, katika wananchi 10 waliopata fursa yakuongea na katika maswali waliyoniuliza na katika mambowaliyonituma niyalete hapa Bungeni, wale wote nilioongeanao, katika watu 10 walioniuliza maswali, watu nane waliliakilio cha maji; na watu wawili waliobaki ndio waliozungumziamahitaji mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata Wabunge humu ndani,nilipotoka huko ziara nimejaribu kuongea na Wabunge,nimeshaongea na Wabunge zaidi ya 200 na hata wa Upinzaniwakiwemo, asilimia ya Wabunge wote wanasema kilio chamaji ndiyo kipaumbele namba moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaniwasilishe kilio hicho kabisa kwa heshima kubwa naunyenyekevu, tuiombe Serikali yetu ambayo ni sikivu, safarihii ifanye maajabu. Kama walivyosema Wabunge wenzangu,bajeti imekuja, naomba kabisa tuungane na maoni yaKamati. Kama yalivyoelezwa vizuri kuanzia ukurasa wa tano

Page 190: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

190

mpaka ukurasa wa saba, Serikali itafute fedha za ziada Shilingibil ioni zaidi ya 100 tuweze kutekeleza miradi kamailivyooneshwa kwenye kitabu hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababukusema ukweli, watu wanahangaika sana. Ninapozungumzahivi akina baba walio wengi wanajua; kazi yao huwa nikusema nataka maji ya kuoga, nataka maji ya kunywa,nataka maji ya kufua, nataka niwe msafi. Wanaohangaikana kutembea tangu asubuhi mpaka saa 12 wanahangaikani wanawake ambao kusema ukweli ndiyo nguvu kazi yaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, najua chini ya Kamati yaMzee Chenge, kwa sababu pia ni Kamati makini sana, chiniya Serikali yetu madhubuti, nina imani Kamati ya Bajeti, itasikiakilio cha Kamati ya Fedha, chini ya Uongozi wa Mwenyekitiwetu Mzee Msolwa na watathubutu na watafanya uamuziwa busara kutenga fedha kabisa za kutosha kupeleka katikaSekta ya Maji kwa manufaa ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huonina imani mmenisikia, na kusema ukweli mimi ninasemaninaunga mkono. Nami ninavyoona, Waswahili wanasemadalili njema huanza asubuhi. Nimeona Kamati ya Bajeti kilawakati inakutana, na Serikali wakati wote inaangalia, ninaimani jambo hili kabla ya kuhitimisha bajeti hii na penginemara baada ya kukamilisha mjadala huu na hata baada yakumaliza Bunge, tutapata majibu namna ya kuongezewafedha ili kazi ziende zikafanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hilo, naombasasa niende moja kwa moja kuzungumzia matatizo ya dawaya maji. Kwa mujibu wa taarifa tuliyopokea hapa na Kamatiimeunga mkono, kwamba kodi ya dawa ya majiimepunguzwa. Naomba niungane na maoni ya Kamatikwamba, badala ya kupunguzwa, tunaomba iondolewekabisa. Kwa sababu Mamlaka za Maji hapa nchinizinaendesha maji kama huduma. Kusema ukweli gharamaza maji huko Vijijini ndoo inauzwa Sh. 20,000/=, Sh. 10,000/=

Page 191: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

191

kwa ndoo. Suala la maji ni huduma, sio biashara. Ninaombahii kodi ya madawa ya maji iondolewe kabisa, siokupunguzwa ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nilete kilio sasa chawale wananchi wanaoishi katika mazingira makame nawananchi wanaoishi katika mazingira ambayo wakichimbamaji hawayapati. Hata wakiyapata, wakati mwingineyanahamahama, mfano Mkoa wa Mtwara, Wilaya yaNanyumbu. Nanyumbu wakichimba maji wanayakuta, lakiniyana chumvi, lakini baada ya muda mfupi yanahama. KunaMiji kama ya Kisarawe kule Vikumburu, kuna Miji kama yaLongido kule Ngorongoro, kuna kule Nzega, kuna kule Igungana maeneo mengine. Wana hali ngumu sana, hakuna mito,hakuna nini, tulikuwa tunaomba sana maeneo haya yapewekipaumbele katika mpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahishwa sana kupitiakitabu hiki kimetuonesha kabisa, jinsi ambavyo Serikaliimejipanga kupeleka maji katika kila Halmashauri. Tumeonampaka fedha zilizopelekwa kwa kila Halmashauri, zinajielezakabisa na kwa kweli tumefurahi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mimi naomba nisemekwamba pamoja na mipango hii bado hivi vijiji vilivyoainishwahapa havitoshi. Kilio cha maji ni kikubwa sana, tunaombakabisa fedha zitakapopatikana tuongeze miradi zaidi kwaajili ya kuimarisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nizungumzie upotevuwa maji. Serikali inafanya kazi nzuri, tunajenga miundombinu,lakini baadhi ya maji yanapotelea barabarani. Naomba sasaSerikali, kupitia Taasisi zetu za Mamlaka za Maji Nchini nakupitia Bodi zote za Mamlaka za Maji zidhibiti na ziwekemkakati maalum kama walivyofanya Bodi ya Maji DAWASA.Tujitahidi kuwabaini wale wote wanaofanya hujuma katikamiradi hii. Tujitahidi kabisa kwa sababu wapo watuwanafanya hujuma humu barabarani, wanapitawanachukua vyuma vichakavu, wanapita wengine

Page 192: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

192

wanajiunganishia mabomba, wanapita wengine wanafungamita zisizofaa, wale wote tuwadhibiti na hata Watendaji wetupia wasiokuwa waaminifu. Anapewa kazi ya kwendakununua mita ya Sh. 10,000/= yeye anachukua fedha nyingineanaweka mfukoni, anakwenda kununua mita ambayo ni yachini ya kiwango. Anapewa fedha akanunue bomba la maji,anakwenda kununua bomba chini ya kiwango na fedhanyingine anaweka mfukoni. Wote hao tuwabaini na Serikaliichukue hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata Serikali ingefanyanamna gani, lazima tushirikiane na wananchi kuhakikishasuala la maji linatatulika. Naiomba niimbe Serikali na kwasababu Sera ya Maji imetamka kabisa na kwa sababuMiongozo ilishatoka na hata katika Bunge lililopita Kamati yaMaji tulisema kwamba hebu tusaidie kuhamasisha wananchiwaanzishe utaratibu wa kuvuna maji kwa kutumia nyumbatunazozijenga. Serikali hapa il ituahidi kwamba sasainakwenda kuelekeza Halmashauri zote nchini kutunga Sheriaitakayofanya sasa kila nyumba inayojengwa hapa Tanzania,angalau inakuwa na michoro ya kuvunia maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipokuwa kwenye Kamatina taarifa hapa inaonyesha kwamba tangu agizo lilelimetoka mpaka leo tunavyozungumza ni Halmashauri mbilitu ndiyo zimetekeleza agizo hili. Naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuwa ana-wind up atuambie sasa Serikali inasemanini na inawaagiza nini Halmashauri katika suala zima lakuhakikisha inatunga Sheria kwa ajili ya uvunaji wa maji kwaukombozi wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa mchoyo wafadhila kama sitazungumzia Mkoa wa Mara ambao ndioninatoka. Pamoja na kwamba Ubunge wangu ni Tanzanianzima, lakini na mimi nina nyumbani na nyumbani ni Mkoawa Mara. Nimefurahishwa sana kuona mipango iliyowekwahapa ya kuimarisha Mkoa wa Mara na wenyewe sasaunapata maji safi na salama kama Mikoa mingine.Nimefurahishwa sana na Mpango wa Serikali wa kutupelekeamaji Musoma Mjini kutoka 86% mpaka karibu 95%. Naomba

Page 193: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

193

niupongeze sana mpango huo. Naomba mpango huu sasauende mpaka Wilaya nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naunga mkonohoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa AminaMakilagi. Sasa namwita Mheshimiwa Pudenciana Kikwembeatafuatiwa na Mheshimiwa Moses Machali.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi na miminiweze kuchangia katika hoja hii iliyoko mbele yetu. Miminaomba niende moja kwa moja kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri katika ukurasa wa 52, sehemu yauboreshaji wa huduma ya maji katika Miji Mikuu ya MikoaMipya. Lakini nitajikita moja kwa moja katika Mkoa wangumpya wa Katavi, Wilaya ya Mpanda Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maelezo yaMheshimiwa Waziri, inaonesha kwamba, huu mpango wakujenga tanki la maji Mjini Mpanda, mtambo wa kutibu majikutoka katika chanzo cha Mto Manga; hii imeelezwa tukwamba ni mpango ambao unaonekana kama vile nimpango wa baadaye. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababuhakuna mahali panapoonesha huu mpango unaanza lini?Utakamilika lini? Upembuzi yakinifu umefanyika amahaujafanyika? Tofauti na miradi mingine ambayoimeorodheshwa humu ndani, kwa mfano miradi ya Ruvu,Kimbiji, imeoneshwa inaanza lini mpaka lini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Waziriatakapokuwa anafanya majumuisho awaambie Wananchiwa Mpanda kwa sababu mpaka sasa hivi ninavyoongeapamoja na kwamba mvua zinanyesha, wanatumia maji yamvua, hawana maji kwenye mabomba. Huu mradi ndiyomradi ambao ni tegemezi kwa Mkoa wa Katavi Wilaya yaMpanda. Kwa hiyo, tunaomba tupatiwe majibu mradi huuutaanza lini? Utakamilika lini? Mchakato wake ukoje? (Makofi)

Page 194: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

194

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na hayonakwenda pia moja kwa moja kwenye mgawanyo wa bajeti.Katika mgawanyo huu wa bajeti, bajeti hii ukiisoma vizuri naukichanganua pesa za maendeleo, nyingi zinakwenda Mijini.Je, wananchi wa Vijijini hawana haki ya kupata huduma hiiya maji? Nami pia natoka Kijijini, najua taabu ya majiwananchi wanayopata Vijijini. Pamoja na mradi wa hivi visimakumi kwa kila Halmashauri mnavyosema lakini badohavijaweza kutatua tatizo la maji Vijijini. (Makofi)

Mhehimiwa Naibu Spika, Vijijini ndiko kwenye watuwengi, ndiko kwenye wakulima, ndiko kwenye wakulima wamboga na matunda, ndiko kwenye umwagiliaji, sasatusipopeleka pesa za kutosha kwenye hii miradi ya vijijini: Je,tunategemea kweli tutaondokana na umaskini? KilimoKwanza tutakifanyaje bila kuwepo na upatikanaji wa maji?Maana yake tunatoka sasa kwenye awamu ya mvua sasahivi tunaingia kwenye kiangazi. Kwenye kiangazi ndipotutakapoweza kuanza kulima bustani za mboga mboga namatunda na vitu vinginevyo ambavyo vinahitaji umwagiliaji.Vinginevyo, mtu akishavuna, akiuza mazao yake atakaaanasubiri tena msimu ujao which means kuanzia mwezi waSita mpaka mwezi wa Kumi na Moja mwananchi wa Kijijiniatakuwa amekaa bure kusubiri msimu wa mvua unaokujakwa sababu hiki kipindi hana uwezo wa kuweza kulimabustani za mboga ama za matunda kwa sababu hanamiundombinu ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri atakapokuwa anafanya hayamajumuisho, azingatie sana maoni ya Kamati iliyowaombaSerikali kuongeza karibu Shilingi bilioni 185 katika bajeti hii nawala siyo ijayo, ili wananchi wa Vijijini hasa akina mamawapate maji. Haya mambo ya kusema hela hii tunapelekasasa Ruvu chini tunasahau Katavi, tunasahau Rukwa,tunasahau Songea Vijijini, tunasahau Kyerwa huko, kwa nini?Wananchi wa Vijijini tumekosa nini? Maendeleo yoteyanaelekezwa Mjini: Je, tutapunguza hili wimbi la kusemakwamba wananchi wanahama kutoka Vijijini kwenda Mijini?Hatuwezi kuipunguza rural urban migration kama hatutaweza

Page 195: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

195

kuangalia disparity i l iyopo kati ya rural and urbandevelopment. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naipongezaSerikali kwa juhudi zake zote zinazofanya lakini naomba sanatena sana kwa niaba ya Wana-Katavi na Wana-Rukwawenzangu na Watanzania wote hasa tunaoishi Vijijini, hii pesaSerikali ifikirie katika bajeti hii kuitoa ili iweze kuongezeka katikahii bajeti iliyopo hapa, wananchi tuweze kupata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengi wamekwishasemahapa kwamba maji ni uhai, maji ni usafi, maji ni afya, ni ukweliusiopingika, bila maji hatutapunguza maradhi, bila majihatutapunguza umaskini. Kwa hiyo, mimi naomba mipangoni mizuri sana iliyowekwa humu umwagiliaji maji, sijui vitu gani,lelele, vipo vingi sana! Ni vizuri, lakini vitafanyika vipi? Kamahii bajeti imejielekeza zaidi Mijini kuliko Vijijini, hawa wananchiwa Vijijini wana makosa gani? Kosa ni kukaa Vijijini? Siyo kosana wakulima wengi tunajua wako Vijijini. Asilimia 85 niwakulima na ndiyo wananchi wanaokaa Vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sanaSerikali isikilize na kwa kweli nawaomba Wabunge wenzanguhakuna ambaye amesimama hapa hajasema suala la maji.Naomba kabisa tukubaliane na tuishinikize Serikali iongezehiyo hela katika bajeti hii na wala siyo ya mwaka kesho, kwamaana ya kwamba hata kwa mwaka kesho napo iongezeke,bajeti iwe inaongezeka kwa kuangalia vyanzo vya mapatovya ndani na siyo tu kutegemea pesa za kutoka nje. Hizi pesaza kutoka nje zinakuja kujazia tu. Wakizitoa hata ukiangaliakwenye haya ma-book, utasoma kwenye hii vote, hela nyingiiko Mjini. Iko Ruvu, Dar es Salaam, Kimbiji sijui wapi, hakunaVijij ini humu hela. Sasa tunafanyaje kazi? Wananchitunawaambiaje kule Vijijini? Tunawaambia nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii katika kata yaMamba maji ndoo moja ni Sh. 1,000/=. Nimeambiwa naPeramiho, ndoo moja Sh. 1,000/=. Mwananchi kule hanauwezo. Sasa hivi ndiyo anaanza kuvuna mazao. Muhula washule ujao unakuja, anatakiwa kutoa ada, ana familia

Page 196: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

196

nyumbani ya watu siyo chini ya 12. Atatumia ndoo ngapi kwasiku? Shilingi ngapi kwa siku ata-spend kwenye maji? (Makofi)

Nimeongelea mwaka jana kwenye bajeti, vyanzo vyamaji Mkoa wa Katavi na Rukwa tunavyo vingi. Wizara ya Majina Katibu wake niliongea naye mwaka 2012 akaniahidiataleta timu ya wataalam kuja kuchambua na kuchukuasample ya maji yanayotoka kule, yanatiririka kati ya Kata yaMuze pamoja na Kasanza na Mamba. Tuna vyanzo vizuri sanana picha nilimletea yule Katibu. Hakuna kilichofanyika hatakimoja! Tukisema, mnasema wanasiasa wanapiga kelele. Hizisiyo kelele, haya ni matatizo ya wananchi, ni matatizo yakina mama, ni matatizo ya wananchi Watanzania hasawanaoishi Vijijini. Wataalam wamekuwa na tabia kwambamkiongea wanakwambia kelele za wanasiasa hizo. Achaneninao! Hatuwezi kufanya kazi kwa mtindo huu! Hatuwezi kufika,katika malengo tuliyojiwekea ya maendeleo. Lazima tuwena commitment, tufanye kazi wananchi wanatakamaendeleo, wananchi hawataki porojo, wananchi hawatakimaneno, wananchi wanataka vitendo ambavyo vitawaleteamaendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sana,mimi nakaa Kijijini kama nilivyokueleza kuwa hiyo adha zaVijijini, nazijua tofauti na wengine wanaotoka Mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maji katika kilaVijiji kumi, kwa namna ambavyo kama tutaufanyia tathminiinaonekana kama tumeshindwa. Sasa tunafanyaje?Naomba Wizara iangalie tunafanyaje ili kuhakikisha mradi huotunauendeleza na tunaumaliza na tunaendelea na mambomengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,napenda kuongelea uhifadhi wa vyanzo vya maji hasamabonde ya maji, kwa mfano, Ziwa Rukwa. Mwaka 2012nimeongelea sana kuhusu Ziwa Rukwa, nimewaambia Wizaraya Maji kwa kushirikiana na Wizara ya Mazingira wakaewaangalie, lile Ziwa lipo hatarini kupotea. Kwa nini lipo hatarinikupotea? Sasa hivi mvua zikinyesha, maporomoko yale ya

Page 197: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

197

udongo yanakuja kufukia Ziwa. Ziwa limehama nanilimwomba Mheshimiwa Waziri wa Maji pamoja na Waziriwa Mazingira na wataaalam wake waende kwenye lile ZiwaRukwa wakaliangalie, lakini hakuna mpaka leo. MheshimiwaMalocha Mbunge wa kule ni shahidi yangu, kamawalikwenda, aseme hapa. Naamini hakwenda mtu yeyotekwa mwaka 2012 wote mpaka leo hii. Kisa, tupo Vijijini. Sasawote tutahamia Mijini, hii Miji itatosha kweli? Maana yakendiyo tutahama sasa tufuate maendeleo Mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana, wananchiwa Vijijini wana mchango mkubwa sana katika maendeleoya Taifa hili. Naomba katika bajeti hii, Kamati imetoamapendekezo ya kuongezewa angalau Shilingi bilioni 185,zitafutwe na ninajua Serikali ina uwezo wa kufanya hivyo. Kwahiyo, itafute hizo pesa iongeze kwenye hii bajeti, wananchiwa Vijijini nao wanufaike na mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja lakinikwa msisitizo hizo hela zitafutwe. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt.Pudenciana Kimwembe. Sasa namwita MheshimiwaMachali, atafuatiwa na Mheshimiwa Salome Mwambu.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru nami kwa kunipa fursa nichangie hoja ya maji.Naomba nianze kwa kujielekeza ukurasa wa 184 na ukurasawa 192.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ridhaa yako naombaninukuu Mheshimiwa Waziri hapa amejibu hapa katikaukurasa wa 184 mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Maji kwakila Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Naomba ni-appreciate mmtenga pesa japo pesa nikidogo, lakini masikitiko yangu yanajielekeza kwenye ukurasawa 192, kuna sehemu moja linatolewa angalizo, naombaninukuu: “Halmashauri mpya za Mijini hazikupata fedha kwasababu hazina miradi ya maji ya Vijijini.” Halmashauri hizo

Page 198: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

198

zimetajwa ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Naambiwakwamba na Tarime Mbunge wa Tarime anaeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitendo cha kuonekanakwamba baadhi ya Halmashauri za Miji ikiwemo Halmashauriya Mji wa Kasulu ambayo ina Vijiji vingi ambavyo vina tatizola maji, jambo hili ni kutokuwatendea haki wananchi waHalmashauri ya Mji wa Kasulu ambayo ni Halmashauri mpyahasa wananchi wa Vijiji kama vya Erujuu, kule Mhunga,Kalunga, Kidiama, Kigondo na maeneo mengine. Sasaningeomba Serikali mkae mliangalie hili kwamba huu niuzembe wa Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya yaKasulu kwa kutokuona umuhimu wa kuomba fedha kwa ajiliya miradi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa kweli Waziriaangalie na bahati nzuri tumekuwa tunawasiliana. Nimepatakumweleza kwa mfano Mradi wa Maji wa Erujuu kwamba nimuhimu sana tangu mwaka 2012 na this time hakuna fedhana hivi ndivyo Vijiji miongoni mwa Vijiji ambavyo vina tatizosugu la maji kwa Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Nitaombawakati Mheshimiwa Waziri anafanya majumuisho angalauatafute fedha kidogo. Kwa mfano, hii Kata moja ya Muhungaambayo ina Vijiji vya Erujuu, Kalunga pamoja na Muhungawanahitaji takribani Shil ingi milioni kama 300, majiyakipatikana, na pale kuna miundombinu ya maji ni mradiuli jengwa toka miaka ya 1970 kwa kuwa haukuwaunafanyiwa rehabilitation, matokeo yake mradi ulikufa.Wanachi wanataabika, wanakosa maji. Miundombinubaadhi kama matenki, kuna tenki kubwa sana limekaa palelimechakaa, fedha hazikutengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa kweli katikasuala hili Mheshimiwa Waziri ili kusudi niweze kuunga hoja,wakati anapo-wind up angalau aseme chochote juu yamradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukiangalia katika kitabuchetu hapa juu ya miradi ambayo inatekelezwa mwaka huu,upo mradi mmoja wa maji ambao unafadhiliwa kwa hii miradi

Page 199: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

199

ya World Bank, unatekelezwa katika Kijiji cha Nyumbigwakatika Halmashauri ya Mji wa Kasulu hali kadhalika. Mradihuu umegubikwa na utata, ulipaswa ukamilike ndani ya miezisita. Mradi umeanza kujengwa tangu mwaka 2012 mwezi waNovemba, Desemba lakini maajabu Mkandarasi aliyepewakazi hakuweza kujenga, mradi ule alianza kwa kujenga tenkilimeishia kwenye foundation stage. Tuhesabu miezi kuanziaNovemba hadi leo hii mwezi huu unakwenda kwisha, miezisita imekwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni wazi kabisa kwambaSerikali imeweza kumpatia Mkandarasi zabuni ya kuwezakutekeleza mradi huu, mtu asiyekuwa na uwezo wa kufanyakazi. Naomba yule mtu afukuzwe mara moja kwa sababuanachokifanya pale ni danganya toto.

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu pia jambo linginewakati ndiyo wameanza kujenga, nilikwenda pale nikakutakuna mchanga wa ovyo, nikasema mkijenga mtabomoa. Hiini kutokana na ushauri wa Mhandisi wa Ujenzi ambayeameshatoa ushauri kwamba mchanga fulani usitumike, nikama vile ni udongo.

Sasa ningeomba kwa kweli wakati Mheshimiwa Waziriana-wind up, huyu Mkandarasi ambaye anatokea Mbeya,jina la Kampuni yake hapa linatajwa kuwa ni ConsultantEngineers Research Associates Limited ya Dar es Salaam naowanaonekana tu wako pale hawawezi kuishauri Serikali vizurina ndiyo maana unaweza kuona kwa kipindi cha miezi sitawamejenga tenki limeishia kwenye foundation stage. Hiihaikubaliki! Contractor ni M/S Earth Plan Contractors Limitedya kutoka Mbeya. Mambo gani haya wanakuja kutuchezeaakili? Mheshimiwa Waziri naomba kwa kweli katika hili uwezekuangalia kwamba watu hawa wanafanya nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tunaona kwambavimetajwa baadhi ya Vij i j i ambavyo pia vitawezakutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Nilikuwanawasiliana hapa na Mheshimiwa Mbunge wa ArumeruMashariki, kuna baadhi ya Vijiji mmeandika kwamba mradi

Page 200: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

200

unatekelezwa, havipo katika maeneo haya. Kwa hiyo,takwimu ambazo mnapewa Waheshimiwa Mawaziri,mmpewa takwimu ambazo ni feki kwa mujibu waMheshimiwa Mbunge. Kwa mfano, Kijiji cha Kasanumba kuleMeru Mheshimiwa Mbunge anasema hakuna Kijiji hichoambacho miradi ya World Bank inatekelezwa.

Sasa nafikiri hebu mjaribu kwenda ku-deal na watuwenu ambao wako kule kwenye Halmashauri, kwa niniwanawapa taarifa za uongo ambazo mnazileta hapaBungeni? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kule Nkasi ukurasa wa 52mmeonyesha kwamba Serikali kuna miradi ambayomnatekeleza katika Halmashauri za Wilaya ya Kasulu, kuleNkasi hali kadhalika kwa Mheshimiwa Ally Kessy ambayeanasema mara nyingi huwa anaoga akiwa hapa Bungenikwamba akiwa huko huwa haogi kwa sababu ya shida yamaji.

Hebu tuombe basi haya maeneo kama katikaHalmashauri za Wilaya ya Kasulu, huko Nkasi, Namanyere,hizi fedha ambazo tumesema ni kwa ajili ya maji safi pamojana usafi wa mazingira, zipelekwe na miradi tuone ikitekelezwaisije tu kuwa kwamba ni suala la kuandika kwamba mnamipango mizuri lakini utekelezaji wake ni kidogo, itakuwahaitusaidii.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, hebu niombemtufafanulie vizuri, maana yake kwa mfano nimeona katikaHalmashauri ya Wilaya ya Kasulu mmesema kwamba kiasicha takribani dola 2,300,000 zitatumika kwa ajili ya programya usafi pamoja na maji safi, mnakwenda kutekeleza kwamaana ya kujenga miradi? Maana yake hii bado ni kauliambayo ni tata.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kupata ufafanuzikatika hili. Mnapozungumzia program ya maji safi pamojana usafi wa mazingira, mnamaanisha nini? Mtawezakuchimba mitaro na tuone sasa kwamba mabomba

Page 201: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

201

yanaunganishwa kwenda kwenye Vijiji mbalimbali auinakuwaje? Hili jambo bado halijakaa vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningependaWizara kwa kweli hizi fedha japokuwa bado ni kidogo lakinituone zikitumika vizuri.

Tatizo kubwa ambalo linajitokeza ni usimamizi mbovuhuko katika Halmashauri zetu, ndiyo maana unakuta, mfanomradi huu nimewaambia, miezi sita inakwisha tenki bado likokwenye foundation stage.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni tatizo. Ni wazi kwambaMhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasuluameshindwa kusimamia mradi huu. Nitawashangaa sanakama miezi sita, huyu anapaswa kuwa sample tu pamoja nahuyo Mkandarasi ambaye mmempatia kazi. Miezi sitawamejenga tenki ambalo tukiangalia kipenyo chakeambacho ni kidogo sana, miezi sita wameishia kwenyefoundation stage halafu tunamwacha kwamba huyuMkandarasi anaendelea kufanya kazi na Mhandisi yuko pale!

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa na mashaka,nitaanza kuhoji wakati mwingine sasa pengine uwajibikajiwenu nyinyi kama Mawaziri angalieni isije kuwa miongonimwa Waheshimiwa Wabunge ambao huwa wanasemaMawaziri mwajibike kwa sababu mmeshindwa kufanya kaziyenu vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sisemi sasa hivi, lakinikama mtamwacha Mhandisi huyu ambaye anashindwakusimamia kazi yake vizuri na mtamwacha huyu Mkandarasiambaye kwa kipindi cha miezi sita mradi ambao ni mkubwaunaogharimu zaidi ya Shilingi milioni 850 amefanya kazi kwakuweza kujenga foundation halafu ameacha leo

Page 202: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

24 APRILI, 2013

202

anakwenda kudai malipo alipe, nimemwambia Mkurugenziukimlipa fedha, huyu Mkandarasi hizo pesa zitawagharimunyinyi pamoja na Mkurugenzi wenu. Tutaanza hapa hapa!

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishie hapa,nitahitaji ufafanuzi katika maeneo hayo ambayo nimeya-address Bungeni. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa MosesMachali. Sasa ni zamu ya Mheshimiwa Salome Mwambu,atafuatiwa na Mheshimiwa Blandes na Mheshimiwa Ole-Sendeka ajiandae.

MHE. SALOME D. MWAMBU: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza kabisa kipekee naomba nitoe shukurani zangu. Najuashukurani zimesitishwa, lakini kwa unyeti wa jambo lililonipatanaomba niwashukuru wananchi.

Kwanza kabisa, nawashukuru Madaktari na Manesiwalionihudumia wakiniombea mpaka sasa hivi nipo hapa naMwenyezi Mungu akasikia sala zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kweli nilipatwa na haliambayo kila mtu hakutegemea kuwa mimi ningewezakusimama tena hapa, lakini kwa ajili ya uwezo wa MwenyeziMungu akanisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote waliokuwa wananiombea,wengine walikuwa wanatuma message kwenye simu,wengine Makanisani na Misikitini, dua hizo Mwenyezi Munguakazisikia. (Makofi)

Page 203: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

203

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, sina budi kuwashukuruwananchi wa Jimbo langu la Iramba Mashariki, Wilaya mpyaya Mkalama, kwa utulivu na kunivumilia ule muda wotenil iokuwa naumwa, lakini hawakusita kuendeleakujishughulisha na shughuli zao za maendeleo. Wakati huohuo wakiniombea.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijikite katikamambo mawili au matatu tu. Kwanza kabisa, kuhusu maji;maji limekuwa tatizo la Kitaifa. Kila mahali kama Waheshimiwawaliotangulia walivyoongea, tatizo kubwa ni maji. Hili tatizolinaathiri watu wachache. Sana sana ni wanawake nawatoto na wanafunzi wanachelewa kwenda mashuleni kwaajili ya kutafuta maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Serikaliiongeze bajeti angalau hili tatizo la maji tulimalize. Ni tatizoambalo kwa kweli sasa hivi, mpaka imekuwa aibu kuliongeleakila wakati. Tunaongea kila wakati tunashida ya maji, tunahiki, tuna hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo ambayo majihayapatikani. Mfano, katika Wilaya yangu ya IrambaMashariki, Kijiji cha Matongo, mwamba ni mgumu ambaohauwezi ukapasuliwa wala kutobolewa. Kwa hiyo, wananchihao tangu uhuru wana shida, hawajaona maji safi na salama.Naomba Mheshimiwa Waziri atamke kitu atakapokuwaanafanya majumuisho, kuhusu hawa wananchi wa Kata yaMatongo, wana shida sana na maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nashauri Serikaliiangalie huo msimamo il ioweka wa wananchi wotekuchangia miundombinu ya maji hasa kwenye ukarabati.Kuna mahali pengine wanashindwa, kwa hiyo, linakuwa nitatizo. Tukiangalia wananchi wana mambo mengi yakuchangia. Wachangie mashule, wachangie vituo vya Afya,Zahanati na kadhalika. Hili suala la maji bajeti ya Serikaliingeongezwa ili wananchi wachangie mambo mengine,lakini siyo miundombinu ya maji inapokuwa imeharibika.(Makofi)

Page 204: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

204

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhilinisipoipongeza Serikali ya CCM kwa jitihada zake inazojitahidikuhakikisha maji yanafika vijijini. Katika phase ya kwanzakwenye Wilaya yangu ya Mkalama, kuna visima 10nilivyopatiwa. Nimepatiwa visima vya Uguguno, Isene,Nyahaa, Bumanga, Kikonda, Mitala, Ndukuti, Kidarasa nakadhalika, hivi visima kweli vimetobolewa maji yapo, lakinivimekuwa kama pambo, kwa sababu viko ndani ya mradiwa Benki ya Dunia. Imekuwa muda tangu maji yatobolewe,lakini miundombinu ya kusambaza inasuasua kuwafikia walajiau watumiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vile vile Serikalina Wizara ihakikishe basi na yenyewe inaweka mkono wakemahali ambapo tunajua fedha za wafadhili zinachelewa kujaau wanatoa wenyewe wanapoamua, kwa Serikali kuwekafedha zake ili iongezee hapo kwenye hizo fedha, tusitegemeewafadhili tu. Ninachokiomba ni hicho, Serikali isikie kwasababu ni kilio kikubwa cha wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hii awamu ya pili,tumeomba visima 30 katika Wilaya ya Mkalama, hivyo visimavitekelezwe kwa sababu sisi ni wamojawapo ambao tupokwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya kudumu vyamaji. Ili kulipunguza tatizo hili, basi Serikali na Wizara iangalienamna gani iongeze matenki ya kuvuna maji ya mvua.Pamoja na maeneo ambayo yanafaa kujengwa mabwawaangalau kwa matumizi ya mifugo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iliangaliehilo, bajeti iongezwe kwa kweli. mifugo inakuwa haina majikiangazi kinapoanza. Waziri anayehusika na hii Wizara,natumaini atakuwa amesikia hili, basi atusaidie kwani sisi niWilaya mpya. Sasa hata ule ujenzi wa Wilaya mpyatutaufanyaje kama hakuna maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ni muhimu, tunaombaSerikali itupe kipaumbele, maji yapatikane katika Wilaya yaMkalama, ili na sisi tuweze kuishi maisha kama wanavyoishikatika Wilaya nyingine, siyo kila siku usiku watu wanapishana

Page 205: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

205

24 APRILI, 2013

na ndoo wanaondoka kwenda kutafuta maji. Kwa hiyo,naomba sana tuchimbiwe visima vingi ili tuweze kujenga hiyoWilaya mpya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengi sanatunayakosa kwa ajili ya kukosa maji. Kwa hiyo, ninachoombaWizara na Serikali isikie na hizi Wilaya zijitegemee kamazilivyotangazwa. Sasa hivi tumeshakuwa Halmashauri yaWilaya ya Mkalama, Halmashauri haina maji, makao makuuyake hayana hata visima vya kuweza kusambaza maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hao watumishi wataishijekwenye Halmashauri ya Mkalama. Watumishi wa Serikaliwanaoletwa, watafikia shida ya maji, basi haitachukua mudawataanza kuomba uhamisho na kuondoka. Naomba Serikaliiliangalie hilo na ilitupie macho mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya,nazidi kuwatangazia wananchi wangu wa Iramba Masharikikuwa Mungu anazidi kuniimarisha kiafya kwani afya yanguimekuwa nzuri, kwa hiyo tupo pamoja. Mbunge nipo,waliokuwa wanasema Mbunge hayupo, Mbunge nipo,naendelea kuijenga Wilaya yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mwalimu SalomeMwambu, kwa kweli na mimi nashuhudia kwa wana IrambaMashariki kwamba, Mbunge yupo! (Kicheko)

Mheshimiwa Gosbert B. Blandes atafuatiwa naMheshimiwa Christopher Ole–Sendeka, Mheshimiwa Lugolana Mheshimiwa Clara Mwatuka wajiandae.

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kupata nafasi hii. Nimejaribu kusoma hotubaya Mheshimiwa Waziri kwa umakini sana kuanzia ukurasa wakwanza mpaka wa mwisho. Kwenye ukurasa mmojawapo,Mheshimiwa Waziri ametukumbusha kwamba mwaka 2009

Page 206: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

206

24 APRILI, 2013

tulitunga Sheria hapa Bungeni ya kuanzisha Mfuko wa Maji.Ni miaka mitano iliyopita kwa sababu ni Sheria ya mwaka2009 nami pia nilishiriki kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa,hadi leo hii miaka mitano imepita, Mheshimiwa Waziri anakujaBungeni kutwambia kwamba sheria hii haijaanza kufanyakazi. Hili ndiyo chimbuko la mgogoro wa maji katika nchi yetukwa sababu Mfuko huu ungekuwepo tusingekuwa leotunalumbana. Nimtake Mheshimiwa Waziri na timu yake,wafanye haraka Mfuko huu uanze kazi, ili wananchi waTanzania wapate maji ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze MheshimiwaWaziri kwa kupata mradi wa maji katika eneo lake la Samena Mwanga. Wengi wamezungumzia suala hili, lakini nakujakatika mtazamo tofauti. Hapa Mheshimiwa Waziriametuambia kwamba, ahadi hii ni ya Mheshimiwa Rais yamwaka 2005, ni sawa na nakubali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Raisalitoa ahadi sehemu mbalimbali ikiwa pamoja na Jimbo laKaragwe mwaka 2005. Nimengalia kwa makini, kwenye eneola Mheshimiwa Waziri la Same na Mwanga kuna bilioni 30zimetengwa, ahadi ya Karagwe ya mwaka 2005 haihitaji hatabilioni moja, yenyewe inahitaji angalau shilingi milioni 400 au500, lakini sijaona ahadi hii ya Rais ikikumbukwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wanasheria tuna usemimmoja, tunasema kwamba, haki siyo kwamba itendeke tu,lakini haki lazima ionekane inatendeka. Pengine na miminingekuwa Waziri wa Maji, ahadi yangu ya Mheshimiwa Raisingeonekana hapa na ningesema Mheshimiwa Rais aliahidindiyo maana iko hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefuatilia sana ahadi yaMheshimiwa Rais kwenye ofisi ya Waziri wa Maji, nimekwenda,nimeandika barua mbalimbali kwa Waziri, kwa Naibu Waziri,kwa Katibu Mkuu, mpaka leo sijajibiwa. Sasa sijui ahadi yaMheshimiwa Rais ya Karagwe aliyoifanya, aliyoitoa

Page 207: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

207

24 APRILI, 2013

kuwapatia maji wananchi wa Karagwe sijui imesahaulika auimetupwa kapuni. Nataka Mheshimiwa Waziri wakatianajumuisha anifahamishe ni kwa nini Mji wa Omurushaka,Mji wa Kayanga, Vij i j i vya Kishao, Lukole, Bugene,Nyakahanga na sehemu nyingine hazina maji. wakatiMheshimiwa Rais aliahidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo Karagwe tu peke yake,zipo ahadi mbalimbali, Tarime kwa mfano, kwa mtani wanguMheshimiwa Nyangwine. Kuna ahadi ananikumbushakuanzia enzi za Mzee Mwinyi, enzi za Mzee Mkapa, enzi zaMzee Kikwete, anakumbusha ahadi hizo na wananchi waTarime wanamshangaa anakaa hapa anaunga mkonohotuba hii, wakati hizo ahadi hazijatekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na Ngara kwaMzee Ntukamazina na Kyerwa kwa Mzee Katagira, ahadi zetusisi Mkoa wa Kagera, leo nil ikuwa nasoma hapa,tumeambiwa kwenye ukurasa wa 54, kwenye bajeti hiiutafanyika usanifu wa miradi ya maji safi na maji taka tu. Huuni usanifu, hakuna hela ambazo zimetegwa kwa ajili yakutupatia maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri awe muungwana katika bajeti hii, nchi hii ni ya kwetuwote, naomba sana, maji ya Karagwe pale ninapozungumzaKaragwe Mjini na Omurushaka ni kilometa nne kutokaambako chanzo cha maji kipo, hela inayotakiwa siyo zaidiya shilingi milioni 500. Katika bilioni 30 ambazo zimetengwakwenda Same na Mwanga, naomba amege shilingi milioni500 tu ili wananchi wangu wa Karagwe wajue kwamba nchiyao inawajali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani wengi mnafahamujiografia ya Mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kagera MwenyeziMungu ametujalia tumekuwa na vyanzo vingi vya maji. TunaZiwa Victoria, tuna Mto Kagera, Tuna Mto Ngono, tuna MtoLubuvu .

MBUNGE FULANI: Mto Ngono!

Page 208: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

208

24 APRILI, 2013

MHE. GOSBERT B. BLANDES Eeh, ndiyo kuna Mto Ngonona kuna maziwa mbalimbali. Hata hivyo, kwa masikitikomakubwa Mkoa wa Kagera pamoja na Mara na Mwanzandiyo Mikoa inayoongoza kwa ukame wa maji. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Blandes, tunatoa wito jinahilo libadilishwe, litafutwe jina mbadala. (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Haiwezekani!

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Blandes endeleakuchangia!

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Naibu Spika,namwomba sana Mheshimiwa Waziri, aweke mpangomkakati, badala ya kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Mikoamingine, sisi ambao tumezungukwa na hilo Ziwa natunalitunza, lakini tunabaki kuwa waangaliaji ni kwa nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye mgawanyo wafedha za maji katika Halmashauri zetu za Wilaya. NimeonaKondoa wamepata bilioni 1.7, Geita bilioni 1.8, Kigoma bilioni1.3, Rombo 1.1, Karagwe ambayo ina Wilaya mbili Karagwena Kyerwa imetengewa shilingi milioni 912. Kwa maana hiyoitapata shilingi milioni 456 tu. Mheshimiwa Waziri naombauiangalie Karagwe kwa jicho la huruma tafadhali sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri na Kamatiimeshauri hapa, bajeti ya maji iongezewe shilingi bilioni 181,nadhani hilo halina mjadala, Serikali ijipange vizuri ili tupatemaji. Pia, napendekeza kama tulivyoanzisha TANROAD,ambayo iko kila Mkoa, kwa nini tusianzishe kitu kinachoitwaTANWATER, tukawa nacho, tukajipanga vizuri kwa ajili yakupeleka maji kwa watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, namwombasana Mheshimiwa Waziri yeye na timu yake, waangalie kwamakini Wilaya ya Karagwe. Sisi tuko mjini lakini Mji wangu waKaragwe unapata maji asil imia sifuri (0%), sasa sijui

Page 209: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

209

24 APRILI, 2013

wanatutenga kwa sababu sisi tuko pembezoni huko, hataNgara sijaona kwa Mzee Ntukamazina na kwa Mzee Katagirakule Kyerwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tafadhali Serikaliij itahidi katika bajeti hii, sisi hatutaki kusubiri, wakatimnajumuisha mtuambie Mkoa wetu wa Kagera katika Jimbolangu la Karagwe kwa Blandes mmenitengea shilingi ngapi,ambazo na mimi nikiondoka hapa niende kifua mbele kamaambavyo Mheshimiwa Waziri atafanya atakapokwendaJimboni kwani na yeye ni Mbunge kama mimi. Naomba hilikwa sababu nitakosa mambo ya kusema pale Jimbonikwangu, wataniuliza umetuwakilisha nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Mheshimiwa Waziriamenisikia na Naibu wake na timu yake. Naomba maji katikaWilaya yangu na Jimbo langu la Karagwe. Ahsante sana.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ole-Sendeka atafuatiwa na Mheshimiwa Lugola na MheshimiwaClara Mwatuka ajiandae.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangiaWizara hii muhimu kwa mustakabali wa maisha yaWatanzania. Nianze kwanza kabisa kuwakumbusha kwamba,sisi wa Chama kinachotawala, katika Ilani yetu ya uchaguzi,tulieleza nia yetu ya kuwatoa Watanzania kutoka uchumi ulionyuma na tegemezi na kuwaelekeza katika uchumi wa kisasawa Taifa linalojitegemea.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi kufikia malengohayo kama huna miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji,miundombinu ambayo unakinga maji na kuyavuna, iliwakulima waweze kuwa na uhakika wa kilimo waondokanena kilimo cha kutegemea mvua ili waweze kuongeza tijakatika kilimo chao. Pia, huwezi kuleta mapinduzi hayo ya

Page 210: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

210

24 APRILI, 2013

kuwatoa wafugaji kutoka uchumi ulio nyuma na tegemezina kuwapeleka katika uchumi wa kisasa, wenye tija na ufugajiwa kisasa, kama mifugo yenyewe haina uhakika wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni rai yangu basi niunganena Waheshimiwa Wabunge wenzangu kuomba Serikali yetusikivu iongeze fedha katika miradi ya maji, ili wengine kamarafiki yangu Blandes waweze kurudi Majimboni wakifurahibadala ya kuondoka wamenuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema nianze hivyo,lakini pia naomba tukumbushane sisi sote ni Wabunge, hataMawaziri ni Wabunge, kwa hiyo, tunapojenga hojazinazoelekea kuwalaumu hata pale ambapo hawanamakosa, tunakuwa hatuwatendei haki wao na wapiga kurawaliowaleta katika Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu,Mradi wa Mwanga, Same, Korogwe ulibuniwa na kutengewafedha za usanifu pamoja na Mradi wangu wa Maji waOrkesmet kutoka Mto Ruvu, na ulitengewa jumla ya shilingibilioni moja ambayo tuligawana milioni 500 kila upande nabaadaye Serikali ilitafuta fedha kutoka BADEA na OPEC Fund.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tumesikia kwamba,kuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi hiyo miwili. Natakaniwambie wakati haya yakifanyika kama alivyosema ProfesaMwandosya wala Profesa Jumanne Maghembe wakati huohakuwa Waziri katika Wizara hiyo, alikuwa kwenye Wizaranyingine. Kwa hiyo, nataka niseme wazi kabisa kwamba,katika hili wala Mheshimiwa Maghembe hakujipendeleakama ambavyo baadhi ya watu walitaka tuamini hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, natakaniwaambie Mradi wa Maji wa Olokesmeti ambao leoumetamka kutengewa shilingi bilioni 15.5 siyo mradi wa leo.Mwaka 1974 wakati hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawaakizindua Wilaya ya Kiteto wakati tunatengana na Wilayaya Monduli, aliyekuwa Mbunge wetu wa pamoja

Page 211: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

211

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa hayati Edward Moringe Sokoine, alieleza nia yaSerikali ya kuvuta maji kutoka Mto Ruvu kuja Makao Makuuya Wilaya iliyokuwa imeamuliwa kwamba ni Orkesmet.

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo ni wazo la mwaka 74na leo baada ya miaka, kwa wanaojua mahesabu wanajuakabisa huu siyo mradi uliobuniwa juzi, ni mradi uliobuniwatangu mwaka 74. Kwa hiyo, kutengewa bilioni 15.5 natakanimwambie Waziri wa Maji, Waziri Mkuu na Rais Jakaya MrishoKikwete mmeandika historia na wananchi wa Simanjirokamwe hawatawasahau, kwamba jambo hili sasa mkilitekezalitakuwa ni jambo jema.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nasema hilo siyoupendeleo kwetu, ukienda kwenye Randama ya Waziri,ukurasa wa 78 wa Randama hiyo, Wilaya ya Hai iliwahikutengewa euro milioni 55 ambayo ni sawasawa na zaidi yashilingi bilioni 100 kwa sasa kwa exchange ya leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mradi huo pia, miakahiyo hiyo, Wilaya ya Moshi Vijijini ilitengewa euro milioni 9.6.Hii yote ni katika kuhakikisha kwamba tunawasaidiaWatanzania ili waondokane na tatizo la maji na wakati huowala Majimbo haya hayakuwa yanawakilishwa na Mawaziriwa Maji. Kwa hiyo, nataka niwaambie kwamba hii ni nianjema tu ya Serikali ya CCM ya kuendelea kuwahudumiaWatanzania bila upendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Simanjiro ikomiongoni mwa Wilaya zilizoko kwenye ukame, mwaka huupeke yake, Wilaya ya Simanjiro Mabwawa karibu manneyamebomolewa na maji ya mvua iliyonyesha miezi miwiliiliyopita. Bwawa la Nalakawe limebomoka, la Lengai, laLengumumwe, na Mabwawa mengine ya Leberela katikaKata ya Ruvu Remiti. Naiomba Serikali ilitupie macho jambohili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtakumbuka kwamba,Bunge hili lilipitisha shilingi bilioni 1.8 kufuatia ahadi ya Rais ya

Page 212: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

212

24 APRILI, 2013

kupunguza makali ya maji katika Wilaya ya Simanjiro, katikaBajeti ya 2010/2011, lakini hadi sasa hatujapata hata shilingimoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sanaMheshimiwa Profesa Maghembe atakapokuwa anafanyamajumuisho yake, awaeleze wananchi wa Simanjiro hiyobilioni 1.8 ya Mradi wa dharura ambao utawazuia wananchiwa Simanjiro kuhamia Kilindi wakati wa kiangazi itapatikanalini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niwakumbushe piakama alivyosema rafiki yangu Mheshimiwa Freeman Mboweambaye tumepakana, maeneo ya Mtakuja na maeneo yaMererani, ni ukanda mmoja, pamoja na Kata ya Naisinyai,ya Indiamtu na ya Shambalai. Maeneo yote hayo maji yakeyana fluoride kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo, wananchi nawatoto wanapata matatizo ya fluoride na watotowanapinda miguu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambieni,ukanda wote huu unaopakana na Kilimanjaro InternationalAirport, unafanana. Kwa hiyo, rai yangu bado ni kwamba,Serikali ione uwezekano wa kuvuta maji kutoka Mlima Meruau Mlima Kilimanjaro na kuweza kuupatia maji Mji waMererani na Kata yote ya Indiamtu, ya Shambalai na yaNaisinyei.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, bado ni rai yangukwamba, Wizara ione uwezekano wa kuwasaidia watoto waMererani, watoto wa Kata ya Naisinyei, ya Shambalai ambaowanapinda miguu. Nilitaka niwaletee picha ya watotowaliopinda miguu, lakini nilishawaleteeni, lakini nikasemamadhali Serikali hii nilishaionesha, naamini itakuwa sikivu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tuna maji ambayoyanamwagika kutoka Mlima Meru ambayo yanapitia kwenyeJimbo la rafiki yangu, mdogo wangu wa Chama chaDemokrasia na Maendeleo, Mheshimiwa Nasari, ambayo leo

Page 213: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

213

24 APRILI, 2013

yameleta maafa makubwa katika Kata ya Shambalai,kwenye Vijiji vya Oldiri, Kilombero na Shambalai yenyewe nakuathiri baadhi ya maeneo ya Mererani na Naisinyai.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji yale yangevunwa,wananchi wa ukanda huo wa Tarafa ya Mbuguni kwaupande wa Arumeru na Tarafa ya Shambalai, Tarafa yaMwaipo, wote tungeondokana na kupiga simu kila siku, kwaMheshimiwa Lukuvi kuomba chakula.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni rai yangu pia kwa Serikalikwamba, sasa hivi tunatambua Serikali yetu imeweka kodikwenye mabomba ya maji. Nashauri kodi hiyo ifutwe ili miradiyote ya maji iweze kuwa ya bei ndogo au ya gharama ndogona wananchi waweze kupata huduma hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaja mabwawa ambayoyalivunjika, lakini nilitaja maeneo ambayo vijiji vyake kufikiamwezi wa saba wananchi wanahama na Walimuwanakwenda zaidi ya kilometa 30 kufuata maji na wakatimwingine wanasubiri maji ya punda kama matrektahayajapatikana. Maeneo hayo ni Lerumo, Lendanai, Okutu,Rorbene, Orjohonyori, Lengumumwa, Namarulu, Lengai,Rekuid, Elinorili pamoja na maeneo mengine ya Kata yaLosnyei. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niiambie Serikali, hiini aibu sana, ninyi mnazungumza habari ya kufuata maji yakunywa umbali wa mita 400, kutoka Lerumo kwendaRuvulemiti ni kilometa 32, kutoka Langai kwenda maeneoambayo kuna maji ni kilomita 25 kwenda na kurudi ni kilomita50. Hiyo ndiyo hali ya Simanjiro tunayowaambieni,hatuzungumzi habari ya maji ya kufuata kilomita 10, achenimita 400 ambayo ni hadithi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu Serikali hii iamue, kwawananchi wa Simanjiro na Watanzania, itenge fedha kwaajili ya kusaidia miradi ya maji. Maana mkizungumza hatamradi kabambe wa maji Orkesmet, unazungumza Simanjiro

Page 214: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

214

24 APRILI, 2013

ambayo ina kilometa za mraba elfu 20, sawasawa na Mkoamzima wa Kilimanjaro, karibu sawasawa na Mkoa wa Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, unaposemakwamba, unasaidia Wilaya ya Rombo, eti utegemee nawananchi wa Same wakanywe maji Rombo, hiyohaiwezekani! Nataka niwaambieni tu kwamba, umbali ndiokama huo niwaowaelezeni, ni sawasawa na kuwa na majiKilindi, utegemee na wananchi wa Muheza wakanywe majiya Kilindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitaiunga mkonoBajeti hii bila kigugumizi, nikiamini kwamba, ahadi ya RaisKikwete ya bilioni 1.8 itafika Simanjiro, nikiamini kwamba mradikabambe hautakuwa wa maneno utatekelezwa, lakininikiamini pia kwamba Wizara itaongeza fedha katika Bajetihii ili Wilaya zingine katika nchi yetu iweze kupunguza matatizoya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naungana naWaheshimiwa Wabunge waliopendekeza kama ikibidikufunga mikanda, tufunge mikanda na ikibidi hata kuanziakwenye Bunge hili, tutoe baadhi ya fedha ambazo zinatumikahata katika vinywaji vyetu, soda au kitu chochote, tuelekezehuko na baadhi ya posho zielekee kwenye miradi ya maji.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukianza kuonesha mfanosisi Wabunge, Watanzania watatuelewa. Naiomba Serikaliitusaidie katika mradi huo wa Mererani, kulikuwa na fedhaza Société Générale ambapo Benki ya Ufaransa walioneshania ya kusaidia Mradi wa Maji wa Orkesmet, tusaidieni. Fedhahizo za Société Générale zinaweza zikatatua tatizo la maji laWilaya ya Hai kwa upande wa Bomang’ombe, Mtakuja. Piaitasaidia Arumeru kwa Tarafa ya Mbuguni, itasaidia Simanjirokwa Kata za Naisinyai, Mererani na Shambalai.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ikiamua kuchukuafedha hizo zichukueni, riba yake ni ndogo, inaweza kumalizatatizo hilo. Dola milioni 40 inaweza kutatua tatizo hilo kwa

Page 215: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

215

24 APRILI, 2013

kiasi kikubwa na wananchi wa ukanda huo, na ukanda watambarare wa Meru na ukanda wa tambarare wa Hai naukanda huo wa Mererani na Naisinyei na Lengai City,watakuwa wametatuliwa tatizo lao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Ole-Sendeka kwa mchango wako.

Sasa namwita Mheshimiwa Lugola, atafuatiwa naMheshimiwa Clara Mwatuka.

MHE. ALPHAXARD K.N. LUGOLA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza kabisa naomba, ewe Mwenyezi Mungu,epusha Bunge hili na ushabiki wa Vyama katika suala la maji.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kweli kila mmojaanasema maji ni uhai, hainiingii akilini kuunga mkono hojahii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, Bajeti hiiimesheheni miradi mingi, lakini imesheheni miradi yaupendeleo katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, imesheheni miradiisiyotekelezeka katika nchi yetu. Kwa nini nasema hivyo, Bajetihii ni mchezo wa karata tatu, hapA Waheshimiwa Wabungetunaliwa kekundu.

WABUNGE FULANI: Ni kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu mwaka 2007, tulipatamradi wa Vijiji 10; Kijiji cha Karukekere, hadi ninavyozungumza,mradi huu hausongi mbele, wananchi hawapati maji. Mwaka2007 tuliunga mkono, mpaka 2012 tuliendelea kuunga mkono,nina sababu gani ya kuunga mkono kwenye mwaka wa nanejuu ya miradi isiyotekelezeka? (Makofi)

Page 216: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

216

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, pale Buramba, mpaka leohakuna mradi unaotekelezeka. Tuliendelea kuunga mkonomiaka sita yote Bajeti hii ipite, hainishawishi leo mwaka wanane, kuendelea kuunga mkono bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2007 tulikuwa namradi wa maji Kibara, hadi leo, hakuna fedha inayopelekwa.Tumeunga mkono miaka sita, leo mwaka wa saba, itakuwajeniunge mkono bajeti hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa Bunda,Mheshimiwa Waziri amelidanganya Taifa, amewadanganyawana Bunda na wana Mwibara ambako maji yanaanzia.Hadi ninavyozungumza, hakuna cha mabombayanayolazwa, kinachoendelea pale, ni kuchimba mitaro,mitaro ambayo haijafika hata kilomita 10 ndani ya kilomita23.5. Nina sababu gani ya kuunga mkono bajeti hii,nitawaambia nini wana Mwibara, nitaingia nyumba ya nanikatika Jimbo la Mwibara!

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtu mmoja anaitwaMusa, kwenye Biblia, aliwaongoza wana wa Israel kutoka nchiya Misiri kule utumwani, kwenda nchi ya ahadi ya Kanani.Walisafiri muda mrefu sana, walipata matatizo mengi najangwani walianza kuumwa na nyoka, wakawa wanakufa,lakini Mungu akasema na Musa, akamwambia, tengenezanyoka wa shaba, halafu umtundike hapo. Kila atakayekuwaanang’atwa na nyoka, amtazame nyoka wa shaba atakuwamzima, na yule ambaye hatatazama pale, hakika atakufa.Sasa leo nimekuja na nyoka wa shaba na nitaomba upokeepicha hizi za akinamama, ambazo zinaonesha kero ya majikatika nchi yetu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kisima cha maji mamaana pampu hakitoi maji, kuna akinamama wawili wana ndoowanagombea maji, kuna akinamama wengine wameshikamashavu, wanasikitika, lini watapata maji katika nchi yao!(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naomba niwape ushauri wa

Page 217: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

217

24 APRILI, 2013

bure na Mheshimiwa Naibu Spika naomba uniruhusu nitundikepicha hii ya akinamama ili kila Mbunge atakayekuwaanachangia hapa, awe anatazama picha hii, kama nyokawa shaba. Vinginevyo nawaambieni, msipotazama picha hiikama nyoka wa shamba, hakika Majimboni mwenuakinamama hawatawarudisha ndani ya jengo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, najua utasema Kanunihaziruhusu, naomba utumie Kanuni ya 5, pale ambapohakuna Mwongozo unaosema kwenye Kanuni, uniruhusuSeargent at Arms na wahudumu, watundike picha hii ya keroya maji katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaiwasilisha kwako, olewenu Waheshimiwa Wabunge msitazame nyoka wa shaba,akinamama, hawatawarudisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, akinamama wanatembeaumbali mrefu, kuanzia saa kumi wanarudi saa tano. Rafikiyangu Hokororo amesema akinamama wanadhalilishwa.Katika mazingira ambayo akinamama wanadhalilishwa, kwanini Kange Lugola nipitishe bajeti hii kwa mama aliyenizaakutoka tumboni mwake akiwa anadhalilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kule kwetu, kutokana naakinamama kutumia muda mrefu kutafuta maji, wakoakinababa ambao wana upendo uliopindukia, nadhani ninyimnaita wivu, wanakwenda kuthibitisha huko kwenye majikama kweli wake zao wako kule.

Wengine wakifika kule wanapanda juu ya miti mirefuili waweze kuona kama wake zao wako kwenye visima vyamaji. Hakika nawaambieni, yamewatokea wale ambaomacho yao hayakuona vizuri, wakadhani wake zao hawapo,walidondoka chini ya miti na wengine ni vilema. (Kicheko)

Hakika nawaambieni na natoa ushauri wa bure…

NAIBU SPIKA: Hawa watu wa Mwibara wana wivukweli hawa. (Vicheko)

Page 218: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

218

24 APRILI, 2013

MHE. ALPHAXARD K.N. LUGOLA: Mheshimiwa NaibuSpika, maneno ya suala la maji katika nchi yetu yamekuwani ya muda mrefu, ya miaka mingi, tumeunga mikono,tumeunga, tumeunga, Waheshimiwa Wabunge, tutaungaunga mikono mpaka lini? Wakati maji hayapatikani!

Leo ni muda mzuri Waheshimiwa Wabunge, nawaonamna nyuso za kuwahurumia akinamama na kila mmojaanayetazama kulia, kushoto, nyuma na huku mbele, naonawote mnaamini mmezaliwa na mwanamke, tuwahurumieakinamama, leo tutumie Bunge hili kutatua kero ya maji katikanchi hii. Hakika nawaambieni, tukiwaunga mkono,wataendelea kuja na Bajeti ambazo hazitekelezeki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ole-Sendekani rafiki yangu wa siku nyingi, kuniambia kwamba,Mheshimiwa Maghembe ni mgeni kwenye Wizara hii, hivyohakujipangia fedha kwa sababu hakuwepo, nakubaliana nawewe, lakini kuna upendeleo miongoni mwa Mawaziri,wanapendelea Mawaziri wenzao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapa wosia na ushauriwa bure kwa Waheshimiwa Mawaziri kwamba,wapendeleeni na Wabunge, na wao wanahitaji maji kwenyeMajimbo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Ziwa Victoria, Kijiji chaMwibara ni cha mwisho, kiko kilomita nane kutoka upandewowote wa Ziwa. Hivyo, hainiingii akilini, kila siku mnatafutavisima vya kudanganya watu na hakuna maji, mnakula fedhawakati maji yako kilomita sita. Kuna Mlima Nyamitweibiri pale,mkiweka matenki na kuna miundombinu tayari ya pampuya maji, vijiji vyote vya Mwibara, hakika nawaambieni,vitapata maji kutoka ndani ya Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya mambo ya kutuleteavisima, sijui Wakandarasi, Watafiti, visiwa havitoi maji, hii nimiradi ya ulaji. Mwibara hatutaki miradi ya ulaji, majitunayaona, weka pampu kule, sisi tupate maji.

Page 219: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

219

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, wakati naelekeakukabidhi nyoka wa shaba, ambao ni akinamamawanaopata adha ya maji, naomba niwakumbusheWaheshimiwa Wabunge, mwaka jana, bajeti hii ilikuwa namatatizo mengi, tulitoa ushauri mwingi. Nashangaa leoKamati ya Maji, inakuja hapa inashawishi Bunge hili kwamba,Wizara ya Maji imefanya mambo vya kutosha, wakati mambotuliyoelekeza hayakufanyika na bado kuna tatizo la maji nahasa ukifika kwenye Miji mikubwa kama Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikienda pale nina chumbakimoja cha kupanga pale, nil iwahi kusema, hatanilipokwenda Ludewa kwa rafiki yangu Deo Filikunjombe,nilipotaka kuoga asubuhi, hakika nilikosa maji ya kuoga mwilimzima! Nilinunua chupa ndogo ya maji ili niweze kuogaangalau sehemu nyeti. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakwenda wapi? Wizarahii wanazo siku zile ambazo wanakwenda kutafuta pesa,wanazo siku za kujadiliana na Kamati ya Bajeti, katafutenifedha, halafu mje mtuambie. Mheshimiwa Chenge kamaMwenyekiti, nitaiomba picha hii kutoka kwa MheshimiwaNaibu Spika akuazime, wakati mnajadili suala la maji, muwemnaangalia nyoka wa shaba, ambaye ni akinamama,muwaonee huruma, ndugu zangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa, uniruhusunikabidhi nyoka wa shaba ili Waheshimiwa Wabungewatakaoendelea kuchangia wawe wanatazama nyoka washaba. Wasipotazama adha ya akinamama kama nyoka washaba, akinamama hawatawarudisha humu ndani. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikae ili mudawangu uliobaki nianze kushuhudia Waheshimiwa Wabungewanachangia kwa kutazama nyoka wa shaba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Kangi Lugola.

Page 220: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

220

24 APRILI, 2013

Baada ya matazamio hayo, Mheshimiwa ClaraMwatuka wewe ndiyo mtihani wa kwanza. (Makofi/Kicheko)

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Kwanza, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakunipatia afya njema kufika siku hii ya leo na kuwezakusimama hapa kuchangia Bajeti hii ya Maji. Pia nikushukuruwewe kwa kunipa nafasi hii. Mheshimiwa Lugola, nitaangalia,baadaye lakini. (Vicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingikakwamba nchi nzima ya Tanzania kero ya maji ni kubwa mno.Karibu kila mahali, kama kuna sehemu ambapo wanakunywamaji ya bure ni chache sana, lakini maeneo mengi maji ni yakununua. Hata humo mijini wanamosema yanapatikana kwaurahisi, au Bajeti inapelekwa ya kutosha, napo wananunuavile vile. Nakaa mjini pale nina kibanda changu, majinanunua, sasa, ni suala ambalo kila mahali linalalamikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule kwetu Mikoa ya Kusinini miongoni mwa maeneo ambayo yana shida sana ya maji.Kuanzia Mkoa mzima wa Mtwara, Mkoa wa Lindi na hatawa Ruvuma, maji ni shida. Kuna sehemu zingine ambazo kunavyanzo vya maji lakini, bado havijafanyiwa kazi vilivyo yakuweza kusambaza hata katika maeneo ambayo hakunavyanzo karibu ili yaweze kufika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo ningeiomba Serikaliiangalie sasa maeneo yale ambayo yana vyanzo vizuri vyakudumu, basi wategeshe pale maji, yasambazwe katikamaeneo yale mengine ambayo hayana maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianzia na Wilaya yaNewala, hakika Wilaya hii ni ya kuisikitikia, kama hivyoalivyosema Mheshimiwa Lugola kwamba, Mawaziriwanapendeleana, basi niombe Waziri wa Maji ampendeleendugu yetu, Mheshimiwa Waziri kaka Mkuchika, Wilaya yaNewala anahitaji upendeleo wa hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda Newala bahati

Page 221: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

221

24 APRILI, 2013

nzuri kwamba hivi sasa yanatumika maji ya viwandani, mkifikawageni mnapewa maji yale, lakini laiti mngekuwa mnapewamaji wanayokunywa wananchi wa Wilaya ya Newala,msingekunywa na msingeamini kama kweli maji hayawanakunywa watu. Kwa hiyo, ule usemi wa kwamba,Mwafrika hafi uchafu ni kweli kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Newala maji yaowanayapata kwa kutengeneza kishimo uwanjani, wakati huuwa mvua ndiyo wanachota maji pale. Sasa angalia maji navumbi zile yanakuwa ni maji ya namna gani? Yanakuwamazito kama uniform za wahudumu wetu wa ndani. Sasahali kama ile ni ngumu! (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba basi Serikalipamoja na kwamba, uwezekano wa kungoja kuletewa majimazuri ambayo tunahitaji wayapate, basi wapelekewe dawaza kusafisha maji hayo il i yaonekane mazuri kulikoyanavyotumika, hali ni mbaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, wale wanaojiwezeawakachimba visima vyao na kuvijenga kwa cement,wanategesha hivyo hivyo maji hayo hayo ya mvua ambayosiyo mazuri, ni machafu, wengine ambao hawana uwezo,nyumba nyingi kule kwa sababu zao la biashara kule nimashaka, kilimo chao cha mhogo ambacho hakina sokowanashindwa kupata bati, angalau waweze kupata maji yakutoka kwenye bati siku za mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wanachofanyani kukinga maji kwenye nyumba zile za nyasi, maji yanayotokamle ni kama chai ya rangi. Sasa fikiria maji yale upewe wewekunywa, kwa kweli huwezi kutamani. Naomba sana Waziriachukue hatua za upendeleo ili wawapatie maji wananchiwa Newala. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikienda Wilaya nyinginekama Masasi, kule mradi huu wa visima kumi vilipatikana,lakini visima vile havitoi maji. Nashangaa, visima vipo lakinimaji hakuna kwa nini, hatujui! Lakini vijana wanachimba

Page 222: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

222

24 APRILI, 2013

visima na maji yanapatikana, wanachota kwa karibu tu kwamakopo, wanafunga kamba kopo wanatumbukiza nakuchota maji. Sasa nashangaa visima vinachimbwa namashine lakino vinakosekanaje maji? Naomba MheshimiwaWaziri afuatilie hilo, waone kwa nini visima vile havitoi maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na michangokatika vijiji kwamba, walitakiwa wachangie shilingi milioni sitaau sijui tatu, kitu kama hicho, nimesahau kidogo na Serikaliisaidie. Watu walikuwa wanachangia na mwisho wakulimawalikuwa wanakatwa kwenye mazao kwa ajili ya maji hayo,lakini mpaka hivi sasa baadhi ya maeneo utaratibu huohaujafikia mwisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, sijui zile pesa kama zilikuwazinawekwa mpaka lini sijui na ufuatiliaji wake nani afuatilie,wananchi mnafahamu kwamba wengi wanashindwa kuuliziaau kutafuta haki, wanaogopa maana ndiyo sera yaWatanzania, woga vijijini. Kwa hiyo, naomba MheshimiwaWaziri, afuatilie hili katika vile vijiji ambavyo walichangishwapesa zao kwa ajili ya maji na mpaka leo hawajapata.Naomba sana kwani akinamama wanalala visimani yaani niMkoa mzima wa Mtwara uko hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda Nanyumbu vile vilehali ni hiyo hiyo, lakini kuna mkombozi ambao ni Mto Ruvumaupo karibu. Naomba ule mto utumike, maji yasambazwekatika Wilaya zile za Mikoa yote miwili kwa maana naRuvuma, mto huu unapita kwao, hivyo wasaidiwe ili majiyapatikane. Haiwezekani akinamama wawe daimawanakesha visimani, wakiondoka asubuhi wanawaachawatoto wao, wengine hata jinsi ya kwenda shule hawanakwa sababu hakuna hata maji ya kunawa uso. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tufanye kilalinalowezekana, kwanza niiombe tu Serikali ituongezee bajeti,hiyo iliyopewa Wizara ni ndogo, haitoshi kwa tatizo lililoponchini. Kwa hiyo, iongezewe na kila sehemu iongezwe ili

Page 223: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

223

24 APRILI, 2013

mambo haya yawe sawa. Ukweli maji ni mama, sasainapofikia kila sehemu wanalia kwa ajili ya maji, kwa kwelihali ni mbaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo naomba sana hasaNewala ndugu zangu tuwahurumie, wananchi wale wanaishisiyo Tanzania hii ya leo bali ni ile ya mwaka 47. Sasa imekuwaKusini ni kusini kweli kwa kila kitu? Naomba mtuonee hurumaangalau kitu kimoja kipungue, tuseme kwamba, Kusini kwahili aah, ni nafuu. Isiwe kila kitu ni tabu; mazao tabu, sokohakuna, mbegu za kisasa kule tunasikia tu kwa wenzetu, sasana maji haya iwe hivyohivyo jamani? Naomba sanatutazamwe kwa macho manne, mawili tuliyopewa na Munguna mengine sisi tuongezee ili yawe manne. Hiki ni kilio chaWatanzania katika kila sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kule hali ni ngumu, Masasina sehemu karibu zote za Kusini tunapata maji ya kununua,vijana ndiyo mradi wao na wengine wanajenga majumba,plastiki moja sh. 1,000/=, sasa fikiria kwa matumizi yanyumbani, familia wanatumia ndoo ngapi kwa siku? Sasa kilasiku awe na pesa za kununua wakati soko la mazao ndiyokama mnavyosikia korosho ndiyo hizo. pesa hatupati, sasatunafanyaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mtuonee huruma Kusini!Tupieni macho Kusini, pamoja na kwamba ni kwa muda, sasageuza angalau kusogee kuwe kunakwenda juu kuliko kubakiKusini, Kusini tu daima. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nafikiri mwakawa kuwa kila sehemu maji yanapatikana kwa urahisi, furahaitakayokuwepo kule, uchaguzi utakapofika CCM mtaokotatu, mtaokota tu kwa sababu ni kero kubwa. Kwa hiyo,watasema tumepatiwa maji basi hata Mpinzani akisimamawataona aah hakuna kitu, tunakimbilia wapi, CCM! Lakinimkiwanyima maji mnawaongezea adhabu, akinamamawatasema hapana, mbona mambo yanakwenda hivi hatuipikura.

Page 224: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

224

24 APRILI, 2013

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. CLARA D. MWATUKA: Ah! ni kengele ya ngapihiyo?

WABUNGE FULANI: Ya pili!

MHE. CLARA D. MWATUKA: Lah!

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa ClaraMwatuka, maneno ya mtu mzima.

Mheshimiwa Laizer atafuatiwa na Mheshimiwa MaribaChacha Nyangwine.

MHE. LEKULE M. LAIZER: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi nichangie bajetiya maji. Nizungumzie hali ya maji Wilaya ya Longido. Pamojana sera ya Serikali kwamba, inatakiwa kila Mtanzania achotemaji umbali wa mita 400, nadhani kwangu hii itakuwa nihadithi ambayo haitatekelezwa hata siku moja. Nasema hivikwa sababu Wilaya ya Longido ina matatizo ya maji karnena karne na hakuna sera au utaratibu uliopangwa kuondoamatatizo ya maji katika Mji wa Longido pamoja na Wilayanzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kusemakwamba, Mji wa Longido kila siku hapa Bungeni nasema, unamatatizo kuliko Wilaya nyingine, kwa sababu Mji wa Longidoni Makao Makuu ya Wilaya na ni Wilaya ambayo wananchiwanajitahidi kujenga sana, lakini tatizo la maji limekwamishamaendeleo yote ya Longido. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Longido wananunua majishilingi 1,500/= kwa debe. Kwa hiyo, hata maisha ya pale nimagumu kuliko maisha ya eneo lingine, maisha bora kwakila Mtanzania ni vigumu kufikiwa na wananchi wa Longido

Page 225: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

225

24 APRILI, 2013

kwa sababu ya matatizo ya maji. Huwezi kuamini kwambafamilia wanapokezana kuoga, yaani wanaoga kwa zamu,baba akioga leo, mama hawezi kuoga siku hiyo na watotohawaogi. Kwa hiyo, sidhani kama kuna Wilaya nyingineTanzania ambayo baba na mama wanapanga zamu yakuoga. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali inisikilizekwa sababu nimekaa muda mrefu hapa Bungeni napigakelele kwamba Longido wana matatizo ya maji. NaombaMheshimiwa Waziri kama kuna safari au ziara za watendajiwa Wizara hii kwenda nje, basi hizo fedha zielekezwe Longidoili waondokane na tatizo hili la maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Longidounategemea maji ya Mlima Meru, inahitaji zaidi ya shilingibilioni sita kuleta maji kutoka Mlima Meru na kuyafikisha katikaMji wa Longido na kama ni ahadi za Rais, hata Raisamekwenda Longido na ametoa ahadi na amesemakwamba, atamwambia Mheshimiwa Waziri wa Maji, hiyo niahadi Mheshimiwa Rais amefikisha kwake, kwambaatekeleze, lakini bahati mbaya sikuona katika bajeti hii kamakuna mradi wowote wa Longido.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lingine katika Mji waLongido, kasehemu kadogo wanashirikiana maji wananchina mifugo. Naomba mifugo inayozunguka mji wa Longidowajengewe mabwawa ili ipunguze kasi ya wananchi Longidokung’ang’ania sehemu moja ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kijiji cha Orbomba,Ortevesi na Ranchi, kila kijiji kikipata bwawa itapunguzamatatizo ya maji katika Mji wa Longido. Nashangaa sananikiona mmeandika kwamba, Halmashauri za Vijijini au Vijijiniwanapata maji kwa zaidi ya 50% ambayo Wilaya ya Longidotunapata maji kwa 15% tu. Kwa hiyo, maeneo mengi kamaGlailumbwa kule hawana maji, akinamama wanakeshaporini na kurudi baadaye bila hata maji, tatizo ni kubwa katikaeneo hilo.

Page 226: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

226

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme kamawalivyosema wenzangu na naomba Serikali isikilize naitekeleze, tuwe na Mfuko wa Maji kama ulivyo Mfuko waBarabara na Mfuko wa Umeme Vijijini (REA) na Mfuko huuunahitajika haraka sana kwa sababu hali ni mbaya. Jamanitukifika mwaka 2015 kama hakuna maji nchi hii sijui kitatokeanini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Vijiji Kumi umefeli,tuufute kabisa Mradi wa World Bank, wala tusiwape tenawananchi matumaini, Serikali ichukue jukumu hilo, itafutefedha kwa ajili ya Vijiji Kumi hata visima vilivyochimbwaambavyo vina maji Serikali sasa ianze kutekeleza nakuwapatia wananchi maji, kwa sababu kuna baadhi yavisima ambavyo vina maji. Kwangu wamechimba visima 12lakini visima nane havina maji na sita vina maji. Naomba hivyovisima sita ambavyo vina maji viendelezwe ili wananchiwapate maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho ni mgawowa fedha. Kama wenzangu wanavyosema kwamba, kwakweli kuhusu mgawo wa fedha, kila mtu anasikitika.Tunaomba mwongeze hizo fedha kwa sababu hali ni mbaya,sizungumzii fedha zilizokwenda Jimbo au Wilaya yoyote balinaomba fedha za maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Wizara hii auSerikali imetusikiliza na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajetinaomba awasikilize Wabunge ambao wamesema kwamba,tunataka fedha ziongezwe katika Wizara ya Maji. Kwa hiyo,Kamati wakutane, wafikirie jambo hilo kwani ni kilio chaWabunge wote ili fedha ziongezwe katika mradi huu, msijemkasema kwamba tumepitisha baadaye bajeti, mkaendakunyamaza kwa sababu bajeti imepita, tunaomba fedhaziongezwe. Kesho Kamati ikae na kutafuta namna, punguzeniposho na safari za nje pia punguzeni ili fedha zote ziingiekwenye maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. (Makofi)

Page 227: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

227

24 APRILI, 2013

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Lekule Laizer.Tumekusikia kwamba kuoga kwa zamu.

Mheshimiwa Nyambari Chacha Mariba Nyangwineatafuatiwa na Mheshimiwa Ahmed Shabiby.

MHE. NYAMBARI C.M. NYANGWINE: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante. Kwanza nianze kwa kusema kwamba,sitaunga mkono hii bajeti kamwe kwa sababu, baadhi yaWabunge wenzangu wamesema kwamba, wananchi waowanaoga kwa zamu, lakini kwangu hawaogi kabisa hatakidogo. Kwa hiyo, naunga mkono nyoka wa shaba. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni aibu katika nchi kamaya Tanzania ambayo tuna mito na maziwa mengi nakadhalika, lakini tunakaa tunalalamikia maji, na ni aibu kwaWabunge wenzangu tunalalamika maji, maji, maji lakinitunasema kwamba tunaunga mkono hoja. Kwa kwelinawashauri Wabunge wenzangu tusiunge mkono hoja hii.Naomba Waziri Mkuu atusikilize, leo usiku atafute fedha kamani bilioni 200 azilete, kesho tutaunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni aibu kabisakwamba tulalamika, tunalalamika na bado tunasemakwamba tunaunga mkono hoja. Tusiunge mkono hoja kwasababu tunajua kabisa kwamba ndani ya Majimbo yetu kunaahadi nyingi zilitolewa. Kwa mfano kwenye Jimbo la Tarime,Rais Mwinyi alitoa ahadi kwamba Mji wa Tarime utakuwa naneema ya maji, akaingia Mkapa, mwisho Rais Kikweteamesema mara mbili, lakini ni aibu mpaka sasa hivi hakunautekelezaji wowote ule ambao umetekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda nchi jirani ya Kenya,maji yanamwagika yanakuja mpaka Tanzania, yaani kwakweli ni aibu Mheshimiwa Waziri nimwambie kabisa hilo.Mwaka jana katika bajeti naomba ninukuu, mlinijibu kwamba:“Serikali imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrashaya zabuni kwa ajili ya mradi wa maji safi kwa Mji wa Tarime.Chanzo cha maji kwa Mji huo ni Mto Mori, Serikali inaendeleakutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo”.

Page 228: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

228

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua haiingii akilinikwamba, makabrasha yameshatengenezwa ndio mnatafutafedha, kwa nini hizo fedha mlizochukua mkapeleka sehemunyingine, msikumbuke kwamba kuna Tarime? MheshimiwaNaibu Waziri alitembelea Tarime, alikwenda akaangalia nawananchi wakamweleza, sasa sijui amemshauri nini Wazirikuhusu maji ya Tarime. Mheshimiwa Waziri Mkuu alikwendaTarime, wananchi wakamlilia na kumwambia, lakini sijuiamemshauri nini Rais kuhusu maji Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nasema ni aibuna sitaunga mkono hoja hii, hata kama kesho nitakuwanimeondoka, nasema sitaunga mkono hoja hii kwa sababuwananchi wa Tarime...

MBUNGE FULANI: Hawaogi!

MHE. NYAMBARI C.M. NYANGWINE: Hawaogi,wanaoga siku ya nini, Blandes anasema yeye kwao wanaogasiku ya Pasaka, Christmas na Eid, kule kwangu wanaoga sikuwanayonyeshewa na mvua, ni aibu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nasema ukweli,Mheshimiwa Waziri naomba asikilize, nimekwenda kwakenikamweleza, sitaki kwenda kumpigia magoti kwa sababuni haki yake atekeleze. Narudia tena kwamba hakuna Wazirinitakayekwenda kumpigia magoti kwamba afanyemaendeleo Tarime. Kama kuna upendeleo mnajipendeleawenyewe, kwa kweli nasema kwamba mtaalaniwa hapaduniani na mMbinguni mtalaaniwa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mto Mara unawezaukatatua tatizo la maji katika Mkoa wa Mara. Mto Maraunazunguka Wilaya ya Serengeti, Rorya, Tarime na Musomana wakati huo huo tuna Ziwa Victoria, Mto Mara unapelekamaji katika Ziwa Victoria, hivi siku Wakurya wakaamuawakaziba ule Mto Mara usipeleke maji Ziwa Victoria hayomaji mtayatoa wapi ya Ziwa Victoria au Mto Simiyu naKagera.

Page 229: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

229

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli utaona kabisakuwa, hii Serikali sasa hivi haiitendei haki Kanda ya Ziwa.Kanda ya Ziwa hatutendewi haki, lazima tuseme ukweli,mmeelewa? Tunakaa tunalalamika maji na mwaka janatulisema na kulalamika kwamba, Mto Mara uko karibudistance zero kutoka Wilaya ya Tarime, Ziwa Victoria lipo zerodistance kutoka Wilaya ya Musoma, Rorya na Musoma Vijijinilakini ukienda kila kitu ni kilio, kilio ni kilio. Kwa nini msiwekama Baba wa Taifa, mbona Baba wa Taifa yeye mpakasasa Butiama hakukuwa na maji ndiyo mmemkumbuka sasahivi? Ninyi mnapeleka kwenu tu huko huko. Ni aibu kwa kwelina nasema hebu tutafakari upya tunapolipeleka hili Taifa letula Tanzania.

MBUNGE FULANI: Safi!

MHE. NYAMBARI C.M. NYANGWINE: MheshimiwaNaibu Spika, naomba majibu ya uhakika kuhusu mgawanyowa rasilimali katika nchi yetu, maana kwa kweli inaonekanadhahiri ukiangalia mgawanyo unavyokwenda, unapokuwaWaziri au Mbunge ukienda kujikomba kwa Waziri ndiyo Wazirianaangalia. Sasa nasema kwamba, wengine hatukuzaliwakujikomba. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, muangalie na mtekeleze.Wananchi wa Tarime wameniambia kwamba usijikombe.Sasa sitajikomba, ila mtekeleze na kama msipotekelezasiwahitaji Tarime. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata Waziri Mkuu aliwaahidiwananchi wa Tarime, asipotekeleza nay eye simhitaji Tarime.Maana nitawaambia wananchi wa Tarime kwamba nilisema.Profesa Mwandosya alipokuwa Waziri wa Maji aliwaahidiwananchi kabisa kwamba, upembuzi yakinifu umekamilika,maji yatakwenda, lakini mpaka sasa hivi, naona leo mmetoabajeti mnasema kwamba, Mji wa Tarime hauna bajeti ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hakuna bajeti ya maji,hawa wananchi wa Tarime watakunywa nini, wataoga nini,watafanya nini jamani? Hebu muihurumie Tarime, au twende

Page 230: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

230

24 APRILI, 2013

Kenya, si ndiyo? Niwaambie wananchi wa Tarime waendeKenya, kwa sababu Wakurya na Wajaluo wako Kenya? Kwakweli ukiangalia kule Kenya maji yapo kila sehemu, lakiniTarime ni aibu kabisa. Hata Mbunge wa Kenya akinitembeleakule, anashangaa kwamba kuna nini hapa? Ni nini hicho?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli, naitaka Serikalina narudia kusema, siwezi kujikomba, ni wajibu wenumtekeleze, kama hamwezi mpishe. Nitamwandikia hata Raisbarua nimwambie kwamba, kama ahadi aliyotoahaitekelezeki na Mawaziri mliokuja mkatoa ahadihamtekelezi, kwa kweli hatutaelewana na patachimbika.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwakusema kwamba, Naibu Waziri alikuja Tarime na wale watuwa Tarime walimweleza tatizo lililopo Tarime na yeyemwenyewe alishuhudia. Hata kama viongozi wa Serikaliwalijitahidi sana kumpamba kwa kumpatia maji safi yakununua ya kwenye chupa, Tarime maji ya kunywa ni tatizo.Ukinywa maji ya Tarime utafikiri yamechanganywa na ugoroau ni juisi. Kwa kweli ni maji machafu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikwenda ofisini kwaMheshimiwa Waziri, tukakutana akaniambia kwamba,amekumbuka Tarime, lakini nimekwenda kusoma hotubayake anasema kabisa kwamba, miji ambayo imekuwaHalmashauri haikutengewa fedha. Sasa kama haikutengewafedha na wakati Julai, 2012 aliahidi katika kitabu chakemwenyewe, nami nikaenda nikawaambia wananchi waTarime, lakini hakuna utekelezaji wowote ule, leo hiinitakwenda kuwaambiaje? Naomba kwa kweli wananchi waTarime hilo walisikie na walielewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu naomba tuangalienamna ya kutumia rasilimali tulizonazo bila upendeleo kwasehemu yoyote ile. Labda kwa sababu wengine tuna natureya kutojikomba ndiyo maana hatutekelezewi. Nasema

Page 231: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

231

24 APRILI, 2013

kwamba, hatujikombi, lakini lazima kieleweke. Narudia kwakumwambia Mheshimiwa Waziri kwamba ni lazima wajitahidikuleta hayo maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba kuuliza,kwa nini Kanda ya Ziwa tuna mito mikubwa: Mto Kagera ukoKaragwe kwa jirani yangu, Mto Simiyu, Mto Mara, ambayo nimito mikubwa kabisa, lakini hatunufaiki nayo hata kidogo.Tuna Ziwa kubwa lakini hatunufaiki nalo hata kidogo.Wanachukua maji kutoka Ziwa Victoria wanapeleka Tabora,sawa kupeleka Tabora siyo tatizo, lakini sasa waleunaowaacha pale siyo binadamu? Au ni Wakenya? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo naomba wakaewalitafakari. Nasema ukweli kwamba, nitaondoa shilingi nasitaunga mkono hoja, daima. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Asante sana, nakushukuru MheshimiwaChacha Mariba Nyangwine. Huyo ni Mura, anasema fita nifita tu hata fya maji. Mheshimiwa Shabiby.

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa hii nafasi. Mimi labda tu nitachangiamachache sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia katika ukurasawa 61 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri ameitaja Gairo namwaka jana aliitaja tena Gairo. Kuna baadhi ya Wabungewengi tu hasa ndugu yangu Ngeleja akawa ananipahongera kwamba, sasa Gairo shida ya maji imekwisha. Lakinini kwa vile haelewi tu. Mwaka jana sikuunga hii hoja mkonona siungi tena mpaka maji yatoke Gairo. Siyo kwamba tunaogopa sijui nyoka wa shaba, hata aje nyoka wa chumahapa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi kweli nitaeleweka katikasehemu ambayo watu wananunua ndoo moja ya maji shilingi2,000/=, halafu ninakaa hapa nasema naunga mkono hoja?Naunga mkono hoja ipi sasa? (Makofi)

Page 232: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

232

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu amesemamradi wa umefikia asilimia 86 na utakamilika mwaka 2013/2014. Mwaka jana alizungumza hivyo hivyo tu, alitaja sijuiasilimia 50 au 60. Sasa toka mwaka jana mpaka mwaka huunilichoona kilichoendelea kwenye ule mradi ni kupalilia yalematanki. Sasa kusafisha matanki nje pale kumeshafikishatayari asilimia 36, hata mimi sielewi tunaelekea wapi kuhusuhabari ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli sielewi nasitaunga hoja mkono na nitakuja na hoja binafsi sasa. Siyokwamba wajiuzulu tu, wataalam na wao wanahusika, kwasababu hapa tuna kazi ya kupiga makofi, tunagombanawenyewe kwa wenyewe na wenyewe wanakaawanashangilia pale. Wakipata viposho kwa kuja Dodoma,hawana chochote wanachokifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitakuja na hojabinafsi tuhakikishe kwamba, Wizara ya Maji wataalam wotehawapo, watafutwe wapya kwani hawana faida yoyote.(Makofi)

Naibu Spika, ukiangalia hapa Wabunge wengiwameshazungumza ile miradi ya Vijiji 10 vya World Bank.Jamani toka mwaka 2003 mpaka leo, kila siku mradiunatekelezwa. Kwenye Wilaya ya Kilosa, Jimbo langu la Gaironilipata vijiji vya Chakwale na Kibedya, mpaka leo hakunamaji. Zinaletwa fedha, ukiangalia katika ukurasa huu wa 123,Wilaya ya Kilosa imepata milioni 281, Gairo hata senti mojahaijafika, fedha zote zinaishia Kilosa wanakula, nainavyoonekana kabisa wanakula pamoja na Wataalam waWizarani. Ndiyo maana hata ukiangalia visimavilivyochimbwa viko wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi mnatoa fedha halafuhamwendi kuchunguza huko kwenye Wilaya kwamba,tumewapa hizi fedha za kuchimba visima kwa mgawanyowa fedha wa kila Halmashauri, mnakwenda kusimamia,kuangalia zinafanya kazi? Hakuna! Kuna visima wanachimbahapa futi nne nne tu, maji hata ng’ombe hanywi. Halafu

Page 233: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

233

24 APRILI, 2013

watu wamekaa Wizarani huko, wana kazi ya kusemaWabunge tumewapelekeeni huko huko nyie na Madiwanimjipangie. Sasa sisi ni wataalam wa maji? Halafu unangojaMbunge yuko hapa kule Halmashauri wanaitisha kikao.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda hapa,mazungumzo ni hayo hayo tu kwamba, ninyi mmeshapitishakwenye Halmashauri, iko wapi? Mwaka huu Wilaya ya Kilosaimepewa zaidi ya milioni 1,900, lakini lazima mjue kwambaimegawanyika katika Wilaya mbili; Wilaya ya Gairo na Kilosa.Wilaya ya Gairo kijiografia ni kame kabisa kuliko eneo lolotekatika mkoa mzima wa Morogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa mzima waMorogoro, Wilaya ya Gairo ndiyo iko sehemu kame kamaMkoa wa Dodoma, lakini hakuna chochote. Toka niingiekatika Ubunge, sijawahi kuona hata kisima cha hand pumppale, ukikiona ujue nimetoa mwenyewe Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba kwenyemgao wa mwaka huu wa fedha 2013/2014, fedha za Gairoziletwe Gairo na siyo zipitie Kilosa. Kilosa wao wabaki na kiasifulani tu, lakini nyingi zije kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia Gairo majihayatoki, lakini hapa tunasifiwa. Katika ukurasa wa 206,EWURA imetoa leseni kwa Mamlaka ya Maji Gairo. Sasa hiyoleseni inauza hewa au nini kama maji hayatoki yaani unajuavitu vingine hata havieleweki! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimuunge mkonoMheshimiwa ole- Sendeka. Mheshimiwa Ole-Sendeka naWabunge wengi tu wamesema kwamba, tukitaka tupatemaji, lazima tuwe na Mfuko wa Maji. Nasema Serikalihaijathubutu kuondoa tatizo la maji, wako watu walithubutuhapa kwenye nchi hii na wakafanikiwa. Kama MheshimiwaLowassa alithubutu kwenye mradi wa Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulitumia fedha zetu za

Page 234: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

234

24 APRILI, 2013

ndani shilingi bilioni 273, lakini sasa hivi kila kitu mkopo, sijuiBenki ya Dunia, sijui nani aje atoe msaada. Hivi sisi hatuwezikujifunga mkanda kama alivyosema Mheshimiwa Ole-Sendeka hapa?

Mheshimiwa Naibu Spika, nilipochangia hotuba yaMheshimiwa Mkuu nilijaribu kutoa tu mawazo ya namna yakupata fedha angalau tuongeze Mfuko huu. Lakini hatatukizungumza, tutaongeza Mfuko, tutapiga kelele, mapatoni yale yale. Tutaongeza bajeti ya Maji, fedha tutapunguzakwenye Wizara ya Elimu. Tuweke Mfuko kama ilivyo kwaWizara ya Ujenzi, Wizara ya Ujenzi ina Mfuko wake ambaokila lita moja ya mafuta inakatwa sh. 200/= na ndiyo maanabarabara nyingi zinatengenezwa. Wizara ina Mfuko maalum.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunasema maji ni uhai,maji ni uhai, tunajali kweli? Tunajali kama maji ni uhai kweli?Sasa tuweke Mfuko maalum kama ulivyo ule wa kwenyeWizara ya Ujenzi, Mfuko wa Barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina mapendekezo yangu,kwenye simu, watumiaji wa simu tuko zaidi ya milioni 20Tanzania. Wengi wao hapa wanaitana, mtu mzee kamaMheshimiwa Komba au Mheshimiwa Kapuya utasikia anaitwababy, baby, eeh, watumiaji wengi wa simu ndiyo kauli zaohizo na hazina kodi ya aina yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hicho lazima tukubalikwamba, hapa kwenye simu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MBUNGE FULANI: Mwongezee muda kidogo bwana!(Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Shabiby.Sasa mchangiaji wetu wa mwisho.

Page 235: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

235

24 APRILI, 2013

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

NAIBU SPIKA: Samahani kidogo Mheshimiwa.Mchangiaji wetu wa mwisho kwa dakika chache sana,naomba radhi sana. Mheshimiwa Nimrod Mkono kwa dakikatano. Jitahidi zisizidi dakika tano.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ndogo sana ili nami niwezekuchangia hoja hii muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusema, siungihoja hii kabisa, kabisa. Siungi hoja hii kwa sababu kubwamoja, waasisi wa Taifa hili katika Jimbo la Musoma Vijijiniwaliweka bayana misingi bora ya kuwapatia maji wananchina wakazi wa Musoma Vijijini. Katika hatua hiyo walibunimiradi ya trunk route four, trunk three, kwamba itasambazamaji kutoka Ziwa Victoria kwenda Butiama mpaka Buhemba.Trunk route three kutoka Mto Mara kwenda Buhemba nasehemu jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahadi hiyo ya mwaka 1974mpaka leo haijatekelezwa. Mwaka 1974 na mimi kwa miaka12 nimekuwa Mbunge hapa, nasimama kila siku nazungumziajuu ya trunk route four bila mafanikio. Kwa nini sasa niungemkono hoja hii iliyoko mbele yetu? Sioni sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maji yanayopatikanaButiama ni yale niliyochimba, lakini maji kutoka Mugangohakuna yanayofika pale. Mradi wa Mugango ulikuwa ukidhimahitaji ya vijiji mbalimbali vikiwemo Kyabakari, Kwitururu,Mugango, Kiriba mpaka kufikia sehemu nyingine za karibuna Ikizu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo trunk route fourimesahaulika kabisa, mabomba yake yameng’olewa,mabomba ya kuhifadhi maji hakuna, lakini kila wakatianakuja Waziri, anapita pale anampa mkono Mama Maria,anamsalimu halafu anaondoka akisema nitaleta maji, lakinimpaka sasa hakuna maji. Kwa nini niunge mkono hoja? Watu

Page 236: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

236

24 APRILI, 2013

wa Musoma Vijijini watadhani mimi ni mwehu. Mkono ninaolakini siyo wa kuunga hoja ambayo haina msingi. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Namna hiyo.

NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Naibu Spika,nazungumzia sehemu ya Kyagata. Kyagata Mto Maraunakwenda, unatoka Kenya unaingia Ziwa Viktoria. Mto huukila mwaka unapofurika maji yanaenea katika maeneo yaWegero, Kongoto, Buswahili, lakini wakati wa kiangazi hakunamaji na wananchi wote wa Kyagata hawapati maji. Kwa nininiunge mkono hoja hii kama wananchi wangu wanalia miaka12 nikiwa Mbunge wao na kwenye Chama cha Mapinduziambacho nakiendesha pale? Sioni kwa nini niunge mkonohoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mto Mara una matatizomakubwa kwa wananchi wa Musoma Vijijini. Mwezi uliopitaulifurika ukaziba hata lambo ambalo tulipewa na Wizara hiiya Maji. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji alitembelea eneohilo akakuta bwawa la Wegero limepasuka na maji hakuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, akaenda pale sehemumoja ya Mugango ambayo ndiyo chanzo cha trunk routefour kwenda Butiama, wananchi wanaohudumia mradi huohawajapewa mishahara yao kwa miezi 20 sasa. Miezi 20wafanyakazi hawajapewa mishahara, lakini Mawaziriwanakwenda pale wanaongea nao wanasema watawapafedha, lakini hawajalipwa mpaka leo. Kwa nini niunge mkonohoja hii iliyoko mbele yako?

Mheshimiwa Spika, sina mengi ya kusema, nashukurusana kwa kunisikiliza. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa NimrodMkono.

Nawaona Waheshimiwa wawili wamesimama. Kwadakika moja moja, Mheshimiwa Aliko na Mheshimiwa

Page 237: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

237

24 APRILI, 2013

Serukamba, nendeni moja kwa moja kwenye sualamnalotaka kusimamia.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Naibu Spika,nasimama kwa Kanuni ya 68(7) “Hali kadhalika Mbungeanaweza kusimama…”

NAIBU SPIKA: Ahsante. Endelea kwa ajili ya kuokoamuda.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Ahsante sana. Kwa kuokoamuda naomba niseme hivi, mjadala ulioko mbele yetuumevuta hisia za Watanzania wengi na humu Bungenitungetazamia kwamba, Mheshimiwa Waziri Mkuu angekuwaana-pay attention kwa ajili ya jambo hili. Lakini nasikitikakwamba kuna Mbunge mwenzetu amekaa na MheshimiwaWaziri Mkuu kwa zaidi ya nusu saa bila kumruhusu Waziri Mkuuku-pay attention katika mambo haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiti chako kiliwahi kutoamsimamo na kutuonya sisi Wabunge tumuache Waziri Mkuua- concetrate na mijada inayoendelea Bungeni. NaombaMwongozo wako jambo hili linaruhusiwa? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Serukamba kwa kifupi sana.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,baada ya kusikiliza mjadala huu toka asubuhi unaona tatizokubwa ni fedha. Nataka kupata Mwongozo wako, ukiangaliabajeti ya Serikali ya mwaka huu OC (Other Charges)zinakaribia trilioni Nne (4,000,000,000,000/=). Nataka niliombeBunge lako na Wabunge wenzangu tufanye maamuzi,kwenye zile trilioni nne tupunguze asilimia 15 tu prorata kwawote, tutapata shilingi bilioni 600. Shilingi bilioni 600 tuzipelekekwenye miradi ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, toka nimeingia Bunge hilimwaka wa Nane, tunaongea matatizo ya maji. Nadhani

Page 238: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

238

24 APRILI, 2013

wakati umefika sasa tuamue tujifunge mikanda, kamaningesafiri mara tano kwenda nje ya nchi, niende mara tatu,lakini tutatue tatizo la maji kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMwongozo wako kama inawezekana tunazo trilioni nnekwenye Other Charges (OC) across the board, tupunguzeasilimia 15 tu. Nadhani hawawezi kushindwa kufanya kazi ilifedha itakayopatikana tuipeleke kwenye miradi ya maji.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Sasa WaheshimiwaWabunge nina miongozi mitatu ya kushughulika nayo kwamuda mchache sana uliobaki. Mheshimiwa Waziri wa Nchi,naona unataka kusimama, karibu!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kidogo nisemehili jambo ambalo linajirudia sana juu ya Waziri Mkuu kukaaanasikil iza humu Bungeni. Kuna maelekezo kweli yaMheshimiwa Spika, kwamba, Waziri Mkuu asiguswe,asitembelewe, asifanywe nini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu niseme kwamba,Waziri Mkuu ni kiongozi, lakini kama mnavyojua ni Kiongoziwa shughuli za Serikali Bungeni, Serikali iko hapa, siyo WaziriMkuu. Serikali siyo huyu Pinda, Serikali ni hawa wote. Wakatimwingine kwa sababu yanayoendelea Kiti au wenginehawajui, Waziri Mkuu anawaita hapa. Kiongozi wa shughuliza Serikali anaendesha Serikali hata hapa alipo. (Makofi)

Kwa hiyo, msijenge notion hii wananchi wakamuonahuyu Waziri Mkuu siyo msikivu sana, hatii amri ya Kiti,anakaribisha watu. Yuko kazini hapa, watu wana shida zao.Nataka ieleweke kwamba, Serikali siyo Pinda, siyo Waziri Mkuu,

Page 239: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

239

24 APRILI, 2013

huyu ni kiongozi wa shughuli za Serikali. Serikali ni sisi sote hapana hata waliopo nje wanafanya kazi, wanatuletea majibu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pamoja naMwongozo wako, nataka kidogo umuonee hurumaMheshimiwa Waziri Mkuu, kwa sababu vinginevyo mtasemaasitoke kabisa hata ndani ya Bunge, asije akatoka hapa. Sasakama yupo hapa anatatua migogoro ya WaheshimiwaWabunge kama jukumu lake la Kiserikali analaumiwa, akitokahuko sasa si mtamfanyia na maandamano kabisa! (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, ahsante,nakushukuru sana.

Sasa Mheshimiwa Saada Mkuya Salum, hapo hapoulipo, kwa ule mwongozo wa asubuhi wa Mheshimiwa Mpina,ikiwezekana usizidishe dakika tatu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Naibu Spika, asante. Naomba kutoa maelezokidogo kutokana na Mwongozo wa Mheshimiwa Mpina.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo nililoliona kwaMheshimiwa Mpina ni ufahamu wake wa recurrentexpenditure vis-a- vis development expenditure. Siku ilewakati tumejibu lile swali alikuja hapa, nikamfahamisha kwakadri ya uwezo wangu na nilitumaini sana kwamba,angekuwa amefahamu, lakini ndiyo hivyo hakufahamu.Labda probably hii sehemu aliyokuwa amekaa ilikuwa kidogoinampa shida au pengine sauti yangu by then ilikuwa ikimpashida, lakini niko tayari kumpa extra tuition.

Mheshimiwa Naibu Spika, niko tayari kumpa extratuition, kumfahamisha vizuri what real means developmentand expenditure. Anachoongea yeye ni kwamba, matumiziya kawaida, yaani other charges or recurrent expenditureyanafikia 10.6 trillion lakini bado kuna mapato yetu ya ndaniya 9.1 trillion.

Page 240: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

240

24 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumwambiaMheshimiwa Mpina pamoja na Waheshimiwa Wabungekwamba, 10.6 trillion ambayo iko kwenye bajeti does not only,haina maana kwamba ni mishahara, ni matumizi mengine.Ndani yake mna a big chunk ya development expenditure.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu nimpe mfanokidogo, nilimwambia aende akafanye analysis aweke hesabuzake vizuri. Akienda akachambua mle ndani atakutaexpenditure ya 1.6 trillion peke yake imekwenda kwa ajili yahuman capital investment. Hiyo peke yake ni development.Yeye alisema tuna gap ya 1.5, lakini namwambia kuna 1.6trillion kwa ajili ya human capital development.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini akumbuke ndani yahiyo recurrent or OC ndani yake mna Deni la Taifa. Maanayake nini? Deni la Taifa tunakopa fedha kwa ajili ya miradiya maendeleo, lakini ile fedha ambayo tunairejeshatunakwenda kufidia kule, definitely that is development.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa muda wenyeweni mchache na hatuna maelezo mengi, lakini kunacomponents nyingi ambazo ziko katika recurrent expenditureambazo anavyoona yeye ni kwamba, sisi tunafidia kutokanana mikopo. Naomba kama hajaridhika nitaendeleakumwelimisha, kumwelimisha na kumwelimisha. I hope oneday in life atakuwa amefahamu.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Naibu Waziri wa Wizaraya Fedha, Mheshimiwa Saada Mkuya Salum.

Miongozo iliyobakia miwili midogo, ni ya MheshimiwaAliko Kibona kuhusiana na Wabunge wanaokwendakumwona Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Namshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,

Page 241: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

241

24 APRILI, 2013

Uratibu na Bunge) amesaidia kufafanua. Lakini niongezee tukwa kweli kwa Mheshimiwa Mbunge ambaye suala lako siyomuhimu hivyo, ni vizuri kumpa nafasi Mheshimiwa Waziri Mkuuili apate kuwasikiliza Waheshimiwa Wabunge. Kwa waleambao haliwezi kusubiri, basi itakuwa hivyo. Vilevile waleambao wanakwenda kumwona kwa mambo fulani fulani,basi tuwe na summary. Unapokaa nusu saa unamhutubiaWaziri Mkuu jambo gani? (Makofi)

Kama dakika 10 unaweza ukahutubia Bunge la Taifa,kwa nini usiongee na Waziri Mkuu kwa dakika tano, halafuukamucha asikilize mambo mengine? Kwa hiyo, tunatoa witosana kujaribu kumpa nafasi Mheshimiwa Waziri Mkuu. Lakinipale ambapo inabidi kama alivyosema Mheshimiwa Lukuvi,basi hilo liweze kuendelea.

Mheshimiwa Serukamba ametoa pendekezo,pendekezo hilo kwa kweli tunayo Kamati ya Bajeti ambayomuda wote inakutana na Serikali. Tunawaomba walitazamekama moja ya mapendekezo ambayo nina hakikawanayafanyia kazi. Kwa kufuatilia kinachoendelea humundani, ukisikiliza upepo wa humu ndani message ni moja tukwamba, jambo fulani lifanyike katika bajeti hii na wala siyonyingine ili kuona namna gani tunatatua tatizo la maji ambaloni kero kubwa nchini kote kwa ajili ya wananchi wetu na hasaakinamama. (Makofi)

Wako wachangiaji wengi ambao walikuwawameomba kuchangia, wenginje tutaendelea kesho nauchangiaji. Msiwe na wasiwasi, wale wote ambao mliombamajina yenu yako salama kwa Makatibu hapa.

Kwa suala hili la maji ni ajabu sana, kuna baadhi yawapiga kura wa Waheshimiwa Wabunge wamekuwawakiniandia moja kwa moja wakiwaombea Wabunge wao,kwa nini Mbunge wetu hatumsikii kwenye maji, mpeni nafasi.Kwa hiyo, mjue tu ni suala ambalo linawagusa watu wengisana.

Mwisho kabisa, baadhi ya Wabunge wengi sana

Page 242: 24 APRILI, 2013 MREMA 1 - parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461851204-HS-11-12-2013.pdf · 24 APRILI, 2013 3 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo

242

24 APRILI, 2013

wameniandikia karatasi nyingi kweli hapa, wanasema, aah,Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini siku tano hizi zimekuwa nautulivu mzuri, watu wamechangia kwa utulivu sana nakumekuwa na amani kubwa? Wengine wakasema kuhusuile Kanuni ya Tano ambayo wengi huwa hawaisomi, kwa hiyo,wanakwenda kwenye vyombo vya habari wanasema NaibuSpika ametumia Kanuni gani? Hawajasoma Kanuni ya Tanoinayonipa mamlaka ya ziada kidogo.

Wabunge wengi walikuwa wanapendekeza kwautulivu huu, adhabu iongezeke iendelee kidogo. Naombaniwakatilie, niwaombe tu kwamba, adhabu ndogo ndogohizi ni kukumbushana tu kurudi kwenye mstari, wala hazinania mbaya. (Makofi/Kicheko)

Kwa kweli huu ndiyo utulivu uliokuwa kwenye Bungela Tisa kwa wale ambao hawafahamu. Ndiyo maana Bungela Tisa lilisifiwa sana, sana. Ni kwa sababu ya utulivu wa ainahii, kwamba kila Mbunge anachangia, anasikilizwa, ikibiditaarifa ni wakati ambao inabidi, siyo kuvurugana kwa taratibuambazo hazina kichwa wala miguu.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya maelezo hayo,naomba niwashukuruni sana kwa ushirikiano wenu. Siku yaleo imekuwa nzuri sana. Kwa hiyo, naomba kuahirisha shughuliza Bunge hadi kesho Saa Tatu asubuhi.

(Saa 1.45 usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaAlhamisi, Tarehe 25 Aprili, 2013 Saa Tatu Asubuhi)