31875247 kwaheri ukoloni kwaheri uhuru

485
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Harith Ghassany [email protected] SOMA HAPA KWANZA Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani. Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo: Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi binafsi ya kitabu Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo wa kitabu Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://creativecommons.org/licenses/ by-nc-nd/3.0/us/ Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi. Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu. Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao.

Upload: abdulbasit-almauly

Post on 20-Feb-2015

2.573 views

Category:

Documents


316 download

TRANSCRIPT

Page 1: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!Harith Ghassany

[email protected]

SOMA HAPA KWANZA

Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani. Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:

Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi •binafsi ya kitabuKutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo •wa kitabuKutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi•

Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi. Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu. Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao.

Page 2: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, http://kwaherikwaheri.com, au moja kwa moja kutoka http://lulu.com na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu http://kwaherikwaheri.com ikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao. Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao. Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake. Mnakaribishwa nyote—walio karibu na walioko mbali.

Page 3: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni,Kwaheri Uhuru!

Page 4: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru
Page 5: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni,Kwaheri Uhuru!

Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia

Page 6: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Copyright 1431 Anno Hegirae / 2010 Anno Domini by Harith Ghassany

Library of Congress Cataloging-in-Publication Data

Mapinduzi ya Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ukweli na Mapatano, Zanzibar na Oman, Afrabia, Masomo ya Afrabia.

English translation of title:Goodbye Colonialism, Goodbye Freedom! Zanzibar and the Afrabia Revolution

Keywords: Zanzibar Revolution, Union of the Republic of Tanzania, Truth and

Reconciliation, Zanzibar and Oman, Afrabia Studies.

Printed in the United States of America

Page 7: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Na mtaujuwa ukweli na ukweli utawaweka huru.

Biblia Yohane 8:32

Na sema: Ewe Mola wangu! Nipitishe kunako mlango wa ukweli na hishima, na nitowe kupitiya mlango wa ukweli na hishima. Na unipe nguvu kutoka kwako

zenye ushindi zinisaidie.

Qur’ani 17:80

Page 8: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ujasiri mkubwa wa uongozi hufanywa na viongozi wenye kusukumwa na fikra zenye kuungwa mkono na nguvu na hisia za umoja wa kijamii katika kilele kipya cha kihistoria. Historia mpya ya kiutawala ilianza katika nchi ya Zanzibar na shujaa mwenye dhamana ya uongozi wa utawala, Rais Amani Abeid Karume, alipokutana na shujaa Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu ya Zanzibar, tarehe 5 Novemba 2009. Picha kutoka kwenye mtandao.

Page 9: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tabaruku

Kwa wananchi wote wa Zanzibar, kwa Wazanzibari na marafiki wa Zanzibar popote pale walipo duniani, ili watoke katika kiza totoro cha upotoshaji wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, mojawapo ya matukio makubwa kutendeka katika nchi yao, Afrika Mashariki na Kati, na kusudi waelekee kwenye mwangaza wa kudumu utakaoyaimarisha na kuyangarisha maridhiyano yao na kufunguwa kitabu kipya cha kujijuwa na kujitambuwa. Kwa Alhajj Rais Amani Abeid Karume kutokana na hikima, busara na ustahamilivu wa kibinaadamu na wa kisiasa anaouonyesha kwenye medani za Utawala wa leo Zanzibar, kuanzia kutochukuwa hatua ya kuyarejesha yaliyopita hadi kifo cha baba yake aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar baada ya mapinduzi, na kwa kujitahidi kwake kupatanisha kambi zilizofarakana kwa nusu karne, ni ushahidi unaotosha wa dhamira ya kuelekeya kwenye Zanzibar Mpya inayotamaniwa na kila mwananchi wake na kila mpenda amani duniani. Ni majuzi tu ambapo katika historia ya nchi ya Zanzibar, Alhajj Rais Amani Abeid Karume na Alhajj Maalim Seif Sharif Hamad wameitekeleza ahadi waliyoitowa mbele ya ulimwengu ya kuyaweka maslahi ya nchi na utaifa wa Zanzibar mbele kuliko utashi wa kisiasa. Ahadi hiyo imepata baraka kamili za Baraza la Wawakilishi kutafuta suluhu ya kudumu itakayoungwa mkono na nguvu za wananchi wote ili kuumaliza mpasuko na mnaso wa kisiasa Zanzibar. Kwa ajili ya ndugu zetu wa iliyokuwa Tanganyika, leo Tanzania Bara, ili kiwafunguwe minyororo ya utumwa wa nafsi iliyowafanya wawaone ndugu zao wa Zanzibar kuwa ni mahasimu zao wanaopaswa kuendeleya kudhibitiwa kwa nguvu zote. Hii leo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya utawala wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, imepata Raisi ambaye anapopata nafasi hupenda kukumbusha namna viongozi wa Kizanzibari walivyompaliliya na leo hii ni mmoja kati ya Marais vijana wenye utawala mzuri na umaarufu barani Afrika. Furaha yangu ilifikiya kilele pale Rais Kikwete alipoizuru 1600 Pennsylvania

Page 10: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tabarukuviii

Avenue, Washington DC, kama Rais wa Kiafrika wa kwanza kuonana na Rais Barrack Obama wa Marekani, ambaye mwenyewe ana asili ya jirani zetu wa Kenya. Inafahamika kuwa babu yake Rais Obama amewahi kuishi Zanzibar na kusoma ilimu ya dini ya Kiislam. Kwa ajili ya Wazanzibari na Watanganyika kwa ujumla wao ili kitabu hichi kiwawezeshe kuzibadilisha nafsi zao. Waweze kuona fursa za mapenzi na neema zilizopo kwao wao na kwa ndugu na majirani zao wa jadi, na kisha wafanye kazi kwa pamoja katika kujenga Muungano Mpya na uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia—utakaosimama juu ya ukweli na hivyo kuimaliza kabisa mitikisiko na misukosuko ya muda mrefu. Sina jengine la kuwatunukiya Watanzania Wazanzibari, Watanzania Bara, Waomani na Watanzania, Waafrika na Waarabu (Waafrabia) isipokuwa kitabu hichi ambacho ni tunda la fursa nyingi za ilimu ya bure ya msingi na ya sekondari niliyotunukiwa na Dola ya Zanzibar, pamoja na fursa za ilimu ya juu nilizotunukiwa na Dola ya Oman. Namshukuru Mungu Muweza kwa wema na ukarimu nnaotunukiwa katika maisha yangu na ya aila yangu na kufaidika nao kutoka Serikali ya Sultan Qaboos bin Said Al Said kiongozi ambaye anautambuwa na kuuhishimu wajibu wa Oman na taarikh zetu kwa Zanzibar. Sultan Qaboos bin Said Al Said anasifika duniani kwa kujitenga na mizozano na kwa siasa yake ya urafiki na kila nchi, na amekuwa tegemeo la kimataifa katika jitihada za kuleta mapatano ya kudumu katika migogoro mikubwa ya kimataifa na kwa kulinda amani duniani. Kwa unyenyekevu mkubwa nauomba uongozi na viongozi wetu adhiim wa pande mbili za Muungano na za uhusiyano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia, hadi raia kwa jumla, wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo, vijana wa leo hadi Taifa letu la kesho, mkipokee kitabu chenu hichi kama ni kielelezo cha uzito wa nchi adhiim tuipendayo kwa dhati ya Zanzibar. Kwa wote hao, na kwa yote hayo natabaruku. Nawaomba tusome kwa pamoja kutoka historia ya Zanzibar ya nusu karne iliyopita juu ya umuhimu wa kuishi na kuongeza mapenzi baina ya watu wa Tanzania Zanzibar, Tanzania Bara, Oman na Khaleej, na Afrika Mashariki na Kati. Muhimu katika kufanikiwa katika kheri ni kujipa nguvu za kuweza kutazama mbele na kusamehe juu ya kuwepo uwezo wa kulipa kisasi. Tusiuwachiye uchungu wa mitihani iliyotukumba kuzigeuza shingo zetu kuangaliya nyuma tulikotoka.Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Page 11: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Yaliyomo

Kutanabahisha xi

Utangulizi xviii

Siri Nzito 1. 1

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 2. 11

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! 3. 31

Tupendane Waafrika 4. 40

Sakura: Sadaka ya Tanganyika 5. 54

Victor Mkello na Chama cha Wafanyakazi 6. 73

Ali Muhsin na Nduguze 7. 87

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 8. 99

John Okello – Kuibuka na Kuzama 9. 120

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 10. 142

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 11. 154

Waafrika, Waarabu na Ukombozi wa Afrika 12. 184

Misha Finsilber na Mapinduzi 13. 216

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 14. 224

Page 12: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Yaliyomox

Fikra za Kuunda Shirikisho 15. 242

Wagawe, Wasahaulishe, Watawale 16. 249

Hayeshi Majuto Yao 17. 259

Kosa la Mzee Nyerere 18. 281

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 19. 289

Mapinduzi Ndani na Nje 20. 323

Nyumba ya Afrabia 21. 348

Mapitio kwa Jumla 355

Viambatanisho 409

Marejeo 421

Faharisi 431

Shukurani 445

Mkusanyiko wa Picha 453

Mwandishi 497

Page 13: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahisha

Fikra na maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hichi hazina uhusiano wa aina yoyote ile na Serikali, misimamo au sera za vyama vya siasa. Ni kitabu chenye kukusanya simulizi za wazee zenye kuungwa mkono na ushahidi kutoka nyaraka za kimataifa wenye kuufunuwa upotoshaji na kuukombowa utumwa wa kiakili ambao umekuwa ukitumika kwa nusu karne nzima kuipumbazisha na kuinyima usingizi na utulivu Zanzibar na Tanganyika—Tanzania. Kudhihirika kwa ilimu iliyofichwa huenda ikawa sababu ya kuwaingiza wengi kati ya wasomaji katika harakati mpya na kubwa zaidi kutoka historia na siasa kuelekeya kunako ilimu ya maadili (ethics) na kutoka kwenye nafsi iliyotupwa gizani kuelekeya kunako nafsi iliyo huru, itakayoongeza nuru na utulivu Afrika Mashariki na Kati. Si lengo la kitabu kukusanya yote yenye kujulikana au yasiyojulikana kuhusu mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na kuusimamisha “ukweli halisi” wa tukio hilo. Kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kuusimamisha “ukweli” mpaka atakapotokeya mtafiti mwengine atakayekusanya taarifa nyingi zaidi na kutunga “ukweli halisi mpya” mwengine wa mapinduzi.1 Yaliyomo ndani ya kitabu hichi ni asilimia ndogo sana ya yale ambayo yanaweza kutolewa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na muungano na Tanganyika ndani ya wakati tulionawo. Lengo la kitabu ni kukusanya maelezo na tafsiri mbalimbali za mapinduzi ya Zanzibar na vipi yanavyotumika hii leo, kwa kufahamu au kwa kutokufahamu, katika kuinyima Zanzibar na Tanganyika milango na madirisha ya kutoka ndani ya mnaso ambao unaonekana kuhatarisha mustakbal wa nyumba ya Tanzania. Kwa hiyo na kwa upande muhimu, maudhui ya kitabu si upotoshaji wa historia ya mapinduzi ya 64 bali vipi upotoshaji wa historia hiyo unavyotumika ndani ya mkwamo wa wakati tuliyonao hivi sasa na vipi maelezo na tafsiri mpya ya tukio hilo itaweza kutusaidiya kutuongoza nje ya matatizo ya Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika. Mtizamo wa kitabu ni tafauti na mitizamo ya maandishi mingi sana yaliyoandikwa kabla kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Msomaji hatojikuta amenasishwa kutokeya mwanzo ndani ya mtego wa gurudumu la historia lenye

Page 14: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahishaxii

kuiweka mbele na kuisukuma biashara ya utumwa kama ndiyo sababu kuu ya mapinduzi ya Zanzibar. Lengo ni kuyapiga tochi mapinduzi ya Zanzibar ndani ya pango la upotoshaji kwa kuizingatiya mipango na sababu halisi za mapinduzi badala ya kuzidhoofisha nguvu za akili za wasomaji kwa kuwapumbaza kwa visingiziyo na ubunifu wa sababu za mapinduzi. Ni vyema msomaji akayaweka kando mifuniko ya macho ya historia kabla ya mapinduzi na kujaribu kuyafahamu mapinduzi kwa mujibu wa mazingira na vikomo vyake wenyewe. Ni kweli kuwa historia ya kabla ya mapinduzi itakuwa ina mchango fulani lakini tathmini hiyo ni ya kuja baada ya kukusanya maalumati na tafsiri sahihi kutoka kwa wahusika sahihi wa mapinduzi hayo. Kwa kifupi na kwa kukariri, msomaji anatakiwa auweke kando uzowefu wenye kuihusisha biashara ovu ya utumwa na matabaka ya kiuchumi kama ni bashraf ya taarab ya mapinduzi ya Zanzibar. Maelezo yasiyokuwa na uthibitisho wa kiutafiti na yenye kuongozwa na chuki dhidi ya watu fulani na wenye kufuata dini fulani, huwa yamesimama juu ya msingi wa nadhariya ya uchokozi (provocation thesis) ambayo lengo na udhaifu wake mkubwa ni kuvidharau vitendo vya wahusika halisi wa mapinduzi ambao wanatoka kunako dini zote. Lengo la kitabu ni ushindi dhidi ya ukataaji wa kuyafahamu mapinduzi kwa mujibu wa vitendo na sababu halisi za tukio lenyewe. Kila taifa lina fitina yake na fitina ya Dola ya Zanzibar ni utumwa. Fitina hizo ambazo wahubiri wake wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini, wanasiasa wa Kiisilamu wa jeshi na vikosi vya Zanzibar, au majumba ya makumbusho ya kitaifa yaliyopo Dar es Salaam, au Bagamoyo, huwa haziichafulii tu jina zuri la Zanzibar peke yake bali zaidi huichafuliya jina la dini aliyokuja nayo Kristo Issa (Yesu) mtoto wa Bibi Maryam, na Mtume Muhammad, sala na salamu za Mwenye Enzi Mungu ziwashukiye. Wahubiri hao wanakunywa maji kutoka kisima cha fitina na ufisadi ambacho hakikaukwi na sauti isiyosita yenye kusema kuwa Waarabu wameleta vitu viwili vibaya Afrika: Uislam na utumwa. Chimbuko la fitina hizo kwanza lilitoka nchi za Ulaya na zinatokana na mrengo maalumu wenye chuki dhidi ya Uislamu na sio ule ambao unaoitambuwa na kuihishimu dini hiyo ambao upo lakini si wenye kujulikana na kupendwa na vyombo vya habari na wasomi.2 Mfano mzuri ni ule wenye kuupa utumwa wa Afrika Magharibi jina la bahari ya Atlantic na ukajulikana duniani kote kwa jina la Atlantic Slave Trade (Utumwa wa Bahari ya Atlantic), na si utumwa wa Wazungu Wakristo. Kinyume chake, utumwa wa Afrika Mashariki haukupewa jina la Indian Ocean Slave Trade (Utumwa wa Bahari ya Hindi) na badala yake na mara nyingi hubatizwa jina la “Utumwa wa Waarabu/Waislam.” Fitina ya utumwa juu ya nchi ya Zanzibar si jambo ambalo linahusishwa na Dola ya Zanzibar iliyopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 peke yake. Fitina ya utumwa ni moja kati ya visingiziyo vya ukoloni wa mtawala mweusi kutoka

Page 15: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahisha xiii

Tanganyika kuiondoleya Zanzibar kiti chake Umoja wa Mataifa na bega la kuliliya duniani. Na si kweli kuwa kiundani suala la “utumwa wa Uislam au wa Waarabu” ni suala linalotokana na dini ya Ukristo au ujumbe wa Mtume Issa, mtoto wa Bibi Maryam. Ukristo na Uislam wa Mabwana Issa na Muhammad unasingizwa na unatupiwa lawama chafu kutokana na vitendo vya watu wenye chuki binafsi na wenye kuupenda utukufu wa kidunia. Suala la utumwa wa Waarabu Waislam limebuniwa na kuvikwa guo la Ukristo na watu ambao lengo lao khasa ni kulinda maslahi yao ya kiuchumi na ya kisiasa kwa kuwafitinisha Waafrika Waislam na Waafrika Wakristo. Lengo lao jengine ni kuhalalisha unyama waliowafanyiya Waafrika kwa kujifanya kuwa wao ndio wakombozi wa Waafrika na wapingaji wakubwa wa utumwa ambao wao au mabwana zao walikuwa ndiyo washiriki wakuu na makatili wakubwa. Kwa wale ambao wako tayari kujihangaisha na kulifahamu suala la utumwa watafahamu kuwa kuingiya kwa mapinduzi ya viwanda au Industrial Revolution utumwa ulikuwa hauna tena faida duniani kwa sababu ya mfumo mpya wa kibepari ambao ukitegemeya malipo bila ya kuwalisha na kuwahudumiya watumwa. Wazungu hawakuusitisha utumwa duniani kwa sababu waliwapenda Waafrika. Katika kuusitiri ubaya wao na kuyaendeleza maslahi yao ya kiuchumi wakaufanya utumwa wa Afrika Mashariki kuwa ni suala la kurusha nambari yoyote ile ya idadi ya Waafrika waliyotiwa utumwani almuradi ipatikane idadi kubwa ya “biashara ya utumwa wa Uislam”, waufunike ubaya wao, na waendelee na maslahi mapya ya kiuchumi.3

Ilikuwa ni njia ya kuwaondoleya wahusika khasa wa biashara hiyo hisiya ya uovu wa waliowafanyiya mamilioni ya Waafrika ambao ushahidi wa kizazi chao na maovu waliyowafanyia ni jambo ambalo lina ushahidi mzito na wala si wa kubuni. Ili kuugubika uovu wao wamejifanya kuwa wao ndiyo watetezi wakubwa wa Kristo na kuwatupiya Waislam zigo la lawama na fitina za chuki ambazo athari zake ni mauwaji ya halaiki na mateso makubwa na maovu zaidi hata kuliko yale waliyokusudiya kumtendeya Kristo. Kwa nini ikawa hivyo wakati Ukristo ulianza miaka mia sita kabla ya Uislamu na wakati Qur’an ina aya nyingi sana ambazo zinawaamrisha waumini wa Uislam kuwakombowa watumwa? Kwa nini wafuasi wa dini ya Mitume Issa na Muhammad wafitinishwe wakati ujumbe wao ni kutoka kwa Mungu mmoja na si ujumbe wa wafuasi wa dini fulani dhidi ya wafuasi wa dini nyngine? Hili wasomaji wa Kiislam na wa Kikristo wanatakiwa walizingatiye sana wasije wakaingizwa na wakaingiya ndani ya mtego wa kuendeleya kuchukiyana. Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa na kufanywa na Wakristo na Waislam waliyotekwa akili na propaganda chafu iliyokilenga Chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kuwa ni chama cha Waarabu wenye kutaka kuurudisha utumwa Zanzibar. Chama cha ZNP kilichukiwa na kuwatisha Waingereza

Page 16: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahishaxiv

kwa sababu kilikuwa kikisema wazi kuwa mkoloni Afrika Mashariki aliingiya kupitiya Zanzibar na atatoka kupitiya Zanzibar na Uislam utaruka kuingiya Afrika Mashariki na Kati kupitiya Zanzibar.4

Kitabu hichi hakina niya ya kukisaidiya au kukiharibiya chama chochote kile cha kisiasa kwa sababu mwandishi haungi mkono chama chochote cha kisiasa au wanasiasa wasiotaka kuutizama na kuongozwa na ukweli. Hichi ni kitabu cha wenye kuomba kuongozwa na ukweli utakaoilinda hishma ya Zanzibar na ya Tanganyika (Tanzania) bila ya lengo la kupata mavuno binafsi ya kisiasa. Kwa hiyo si lengo la kitabu hichi kuwaharibiya wazalendo waaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) au wa Chama cha Wananchi (CUF), au vyama vyengine vya kisiasa, ambao wameshatambuwa kuwa Zanzibar imeingizwa ndani ya makucha ya vyama vingi na chui yuleyule ambaye aliingizwa ndani ya zizi la ngombe la Tanganyika kwanza na baadaye la Zanzibar. Ni moja wapo wa fitina na mkakati mkubwa na wa zamani wa kuwatenganisha Wazanzibari walio wengi. Hapana shaka wapo wanasiasa wahafidhina ndani ya vyama vikubwa vya kisiasa wenye kufaidika na hali ilivyo Zanzibar na wako tayari kuendeleya na hali hiyo midam matakwa na mapato yao yataendeleya kuhifadhiwa. Kwa mujibu wa hali inavyokwenda Zanzibar na duniani, wanasiasa wenye kuyalinda maslaha yao ya kibinafsi na kuizuwiya Zanzibar kufikiya umoja, huenda wakajajikuta wameondolewa ngazi na kuanguka ndani ya pango la ujanja, ugonganishaji vichwa, na upotoshaji wa maadili ya ukweli na kuaminiyana. Kutofahamika kwa mapinduzi ya 1964 na kubomolewa kwa Dola ya Zanzibar kumesababisha Zanzibar kukosa kuungwa mkono na vyombo vya habari pamoja na mataifa yenye kuunga mkono demokrasia ya kweli duniani. Hii ni sababu moja kubwa Zanzibar kukosa bega la kuliliya duniani kutokea 1964 mpaka hii leo. Kukosa kuilimika kwa vyombo vya habari, walimu na wanafunzi, na mataifa jirani na mataifa makubwa na madogo duniani, kumeendeleza kwa muda mrefu sana kukosa kuifahamu Zanzibar na kuisababisha kusota kwa muda mrefu. Kukosekana kwa ilimu iliyofichwa kunaleta hatari ya kuwapa uwanja wanasiasa waliokata tamaa kusababisha vurugu za makusudi ambazo huenda zikatowa kisingiziyo chengine cha kuvamiwa upya Zanzibar kwa kutangaziwa hali ya hatari, almuradi ubinafsi wao uendelee kunenepa. Kwa upande wa lugha, kitabu hichi kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili watumiaji wa lugha hiyo waweze kufahamu namna gani historia ya Zanzibar ilivyopotoshwa na wachangiye kujenga harakati mpya itakayounawirisha umoja baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika na Waarabu kwa ujumla. Tafsiri ya maandishi ambayo marejeo yake ni ya lugha ya Kiingereza au ya Kiarabu imefanywa na mwandishi wa kitabu hichi isipokuwa hotuba ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume ya kuukaribisha uhuru wa Zanzibar (kiambatanisho A).

Page 17: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahisha xv

Maandishi ya baadhi ya maneno yaliyomo ndani ya kitabu yameandikwa kufuatana na matamshi ya wazungumzaji waliyonukuliwa. Kwa mfano neno “ndio” limeandikwa “ndo” kama lilivotamkwa na mzungumzaji aliyenukuliwa, lakini alipoliandika mwandishi mwenyewe ametumia neno “ndiyo.” Neno “siku” limeandikwa “sku” kwa mujibu wa matamshi ya mzungumzaji, na kadhalika. Neno “mapinduzi” limetumika namna mbili tafauti. Namna ya kwanza ni ile inayotumiwa na wanamapinduzi wenyewe, yaani washiriki wakuu wa mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964. Wanamapinduzi wamelitumiya neno “mapinduzi” kumahanisha kuanguka kwa serikali ambayo kwa ufahamu wao haikuwa ikisimamiya haki za Waafrika wa Zanzibar. Mapinduzi hayo yalikuwa mapinduzi ya kutumiya nguvu na ya kumwaga damu—kuuwa. Wengi waliyomo ndani ya kundi hili, na ni kundi ambalo wamo viongozi na wafuasi wa vyama tafauti vya kisiasa, wanaona kuwa muungano ndio wenye kuwafarikisha na kuwafukarisha Wazanzibari na si mapinduzi yaliyouzaa muungano. Wengi pia wanasononeshwa zaidi na dhiki za muungano kuliko upotoshaji wa mapinduzi. Wako watakaojitiya wenyewe kunako mtego ya ima kwa kujaribu kuyapinga maelezo ya wazee wa mapinduzi yaliyomo kwenye kitabu hichi au kuyanyamaziya kimya na kuyatumiya kuyaonyesha maovu ya muungano. Na wako watakaokuwa kama dagaa kwenye ubavu wa papa. Hata hivyo, baadhi ya waliyomo ndani ya kundi hili wanaamini kuwa muungano ndiwo wenye kuyalinda mapinduzi ya 1964 na si upotoshaji wa mapinduzi wenye kuulinda muungano wenye kutawaliwa na Tanganyika. Kundi hili la kwanza ni kundi muhimu ingawa duara lenye kuyaunganisha matukiyo mawili ya Mapinduzi na Muungano bado halijafunga ndani ya akili zao. Matumizi ya pili ya neno “mapinduzi” yanatokana na ufahamu mwengine wa tukio la tarehe 12 Januari 1964. Kwa kundi hili, mapinduzi ni tukio la kuvamiwa Zanzibar kutoka nje na kumezwa na Tanganyika tarehe 26 Aprili 1964. Maana ya mapinduzi kwa kundi hili la pili ni namna wanavyotafautisha baina ya Uzanzibari wa waliopinduwa na Uzanzibari wa waliyopinduliwa. Suala kubwa linalolifarikisha kundi hili na lile kundi la mwanzo ni suala la uhalali wa mapinduzi katika kuipinduwa dola halali ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964. Kundi hili halina uwelewa kuwa hata viongozi waliyoitawala Zanzibar baada ya mapinduzi ya 1964 mpaka hii leo wamekuwa wakikabiliwa na suala la kuiteteya Zanzibar na walilikabili bila ya kutetereka na liliwagharimu kwa hata kupoteza maisha yao, uongozi, au afya zao. Kwa ujumla, Wazanzibari waliyo wengi bado neno “mapinduzi” halina utata kama ulivyo mfumo wa muungano. Hii inatokana na kukosekana kwa ilimu iliyofichwa ambayo ndiyo yenye kukiweka kiungo baina ya mapinduzi na muungano. Kutangaziwa Zanzibar si nchi na kuibuka kwa suala la mafuta

Page 18: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahishaxvi

kumewaamsha Wazanzibari wengi hata kuliko huko kunyimwa ilimu juu ya historia ya mapinduzi na mahusiyano yake na mapinduzi, na hata kuliko machachari yote ya vyama vya upinzani. Tanganyika iliupata uhuru wake kutoka kwa Mngereza mwaka 1961 kwa njia ya salama kabisa, na kwa hiyo lazima iweko sababu ya chama cha siasa chenye chimbuko Tanzania Bara kubeba jina la “mapinduzi”. Jee, ingelikuwa si Tanganyika mapinduzi yangelipatikana Zanzibar na baadaye kupatikana Chama cha Mapinduzi Tanzania? Nguvu za mapinduzi ya Zanzibar zilizotokana na mrengo uliyoasi ndani ya ASP na TANU kwa kupitiya Chama cha Wafanyakazi na ndipo kilipokuja kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).5 Inavyoaminika ni kuwa kuundwa kwa CCM kulitokana na niya ya kuzifuta tafauti zilokuwepo huko nyuma baina ya ASP na TANU na kuanzisha mapinduzi yatakayowafanya watu wasimame juu ya kitu kimoja. Ilikuwa ni fikra yenye lengo zuri ingawa lengo lilificha mapinduzi ambayo usiri wake uliwanyima walengwa mapinduzi yaliokusudiwa kufanyika. Mwalimu Julius Nyerere piya alikuwa na fikra ya mapinduzi dhidi ya uhafidhina ndani ya Ukristo na alikuwa akiufuata mrengo wa kiukombozi wa Kikristo ambao una chimbuko lake Marekani ya Kusini wenye kujulikana kwa jina la “liberation theology” (theolojia ya kikristo ya ukombozi). Kwa hiyo neno “mapinduzi” linaongeza maana zaidi kuliko zile mbili zilizotajwa hapo juu. Na kitabu hichi piya ni aina ya chimbuko jipya la mapinduzi na ni kazi ya mtafiti mwenye niya ya kuusimamisha baadhi ya ukweli ili Zanzibar na Tanganyika, Waafrika na Waarabu, Waislam na Wakristo, wapate kupiga hatuwa zitakazowazidishiya masikilizano, amani na neema kwao na kwa vizazi vya mustakbal wa mbali. Haikuwa jambo rahisi kuyakusanya, kuyaandika, na zaidi, kuyatowa hadharani maelezo ya kitabu hichi bila ya kuzingatiya kwa kina kikubwa faida na khasara zake. Kuna sababu kadhaa zilizonifanya nikiandike kitabu hichi. Moja wapo ni hamu ya muda mrefu ya Wazanzibari wengi wenye kuipenda Zanzibar na wenye kuitakiya umoja na mema. Kuna mengi zaidi ambayo watakuja watu baadaye kuyaeleza na kwa ufasaha mkubwa zaidi. La msingi ni kutambuwa vipi tafsiri tafauti za mapinduzi za miaka arubaini na sita nyuma zimeweza kutumika kuwaweka Wazanzibari katika hali ya kushindwa kukaa kwa kusafiyana niya kunako meza moja ya umoja na kutambuwa kuwa adui yao mkubwa ni fitina. Adui mkubwa wa Wazanzibari si Tanganyika, wala si Muafrika au Mwarabu, bali ni adui aliyeweza kujificha nyuma ya akili na nafsi za Wazanzibari, Watanganyika, Waafrika na Waarabu. Adui hayuko nje na adui mbaya zaidi ni yule aliyejificha au kufichwa ndani ya nafsi ya binaadamu bila ya mwenyewe kutambuwa na kukubali. La mwisho na la muhimu la kumtanabahisha msomaji ni kuwa kitabu hichi si cha Wazanzibari dhidi ya Watanganyika bali ni cha Wazanzibari na Watanganyika ambao kwa pamoja waliwekwa ndani ya pango la upotoshaji

Page 19: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kutanabahisha xvii

wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar. Hili linafaa likafahamika kwa lengo la kuzidhibiti tuhuma za watakaotaka kujenga chuki binafsi dhidi ya Watanganyika wananchi au hata wanasiasa wasiokuwa na hatiya. Ni muhimu kutafautisha baina ya mtawala na watawala wa Zanzibar na wa Tanganyika waliohusika na maafa ya Zanzibar na ya Tanganyika na wananchi na wanasiasa ambao hawana ilimu au mafunzo kutokana na historia ambayo wengi wao hawaijuwi. Kitabu kitasomwa na kuchipuwa kaumu za aina mbili. Moja itakuwa ni sawa na ile kaumu ya zama za Nabii Musa na kisa cha ngombe. Watauliza masuala na watapewa jawabu na watauliza masuala zaidi na watajiweka mbali na kila ushahidi utakaowadhihirikiya mbele ya macho yao hata kama baadhi yao pembeni watakiri kuwa yanayozungumzwa yana ukweli ndani yake. Kihistoria kundi hili ni la zamani sana na likiamuwa kuendeleya na fitina na vitendo vya kuwagawa Wazanzibari na kuwagawa Wazanzibari na Watanganyika, watajijengeya mazingira ya kuwajibika na kuwajibishwa na sheria za Zanzibar na/au za Tanganyika au za Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, International Criminal Court (ICC). Kaumu ya pili itakuwa ni ndogo kwa idadi ya watu kuliko ile ya kwanza, na haitopendeleya kuuona Muungano unavunjika na piya haitopendeleya kuuona ukitawaliwa kwa hoja na vitendo vya kikoloni ikiwa ni kutoka kwa wahafidhina wa upande wa Zanzibar, wa Tanganyika, au wa nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Ni matumaini yangu kuwa baada ya kukisoma kitabu hichi Wazanzibari na Watanganyika watachukuwa hatuwa ya kujenga maridhiyano mapya ya kisheriya na ya kikatiba yatakayoujenga msingi mpya na kuuimarisha mustakbal mwema baina ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Harith Ghassany Washington DC

Page 20: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi

Kutoka nusu ya pili ya karne ya ishirini mpaka kuingiya karne ya ishirini na moja, Zanzibar imekuwa ikisifika kwa mambo matatu yenye umuhimu mkubwa wa kijamii na wa kisiasa: kupatikana kwa uhuru wa Zanzibar tarehe 10 Disemba 1963, kupinduliwa dola huru ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964, na kuungana na Tanganyika tarehe 26 Aprili 1964. Kitabu hichi kinasajili majadiliyano ambayo hayajapata kutolewa, kwa njia rasmi au zisizokuwa rasmi, na kikundi maalumu cha wazee waliyokuwa wanachama wa Afro-Shirazi Party (ASP) na wa Tanganyika African National Union (TANU) katika kuyafanikisha yale yenye kujulikana rasmi kama ni Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964. Kitabu piya kinatumiya marejeo ya daraja la kwanza ya kihistoria ambayo ni maandishi ya nyaraka za kitaifa za maofisa waliyoyashuhudiya mapinduzi au waliokuwa karibu sana na waliyoyashuhudiya. Kushuhudiya jambo kuna daraja. Mchango wa wazee khasa waliyohusika na waliyokuwa mstari wa mbele kwenye Mapinduzi kunaziba pengo kubwa la kihistoria na ni dira na ramani mpya kwa wananchi wa Zanzibar na wa Tanganyika, kwa Wazanzibari waliyoko ughaibuni, na kwa wenye kufuatiliya masuala ya umoja na muungano wa nchi za Kiafrika. Piya ni mchango muhimu baina ya uhusiyano wa Waafrika na Waarabu ambao mwaka 1990 Profesa Ali A. Mazrui aliubatiza jina la Afrabia akimaanisha uhusiyano mkongwe na maalumu baina ya Waafrika na Waarabu na kubashiriya makundi mawili ambayo yamo katika safari ya mfungamano wa kuwa kitu kimoja.6

Zanzibar na Tanganyika, Tanzania, ziko kwenye njiya panda kuelekeya kunako mfungamano na zimekabiliwa na uamuzi mkubwa na wa haraka wa ya imma kuifuwata njiya ya amani na neema au kuifuata njiya ya ghadhabu na yenye kupoteza dira. Usomaji wa maneno, udadisi wa maana, na uwelekezaji wake kwenye daraja za juu za ufahamu ndizo pekee zenye uwezo wa kutowa makusudiyo na maana ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Zanzibar, kwa Tanganyika, na kwa mustakbal wa

Page 21: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xix

Zanzibar na Tanganyika—Muungano. Tatizo la Zanzibar, Unguja na Pemba, au la Waafrika Waislam, ni tatizo ambalo lina picha ndogo na picha kubwa. Picha kubwa ni ustaarabu na khasa wa Dola ya Zanzibar ambao ni tishio kwa wale ambao bila ya kutambuwa wamefundishwa na kuamini kuwa wao wana haki zaidi Zanzibar kuliko hata Wazanzibari ambao hawana kwao kwengine isipokuwa Zanzibar. Na kwanini tatizo likawa na Zanzibar, na si na Tanga, au Mafia, au Kilwa, au Lamu, lakini likawa na Zanzibar na Mwambao wa Kenya? Sababu ni Dola ya Zanzibar ndiyo dola pekee iliyo kongwe (mbali na Ethiopia) kuliko zote Afrika chini ya jangwa la Sahara ambayo iliupata uhuru wake tarehe 10 Disemba 1963. Kuukataa uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Muingereza ni kukataa kuwepo kwa Dola ya Zanzibar na ustaarabu wa Waafrika Waislam wa karne juu ya karne. Na ni kuyakataa piya Mapinduzi ya 1964. Mapinduzi yangelikuja kama si uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963? Jan P van Bergen wa Uholanzi ameelezeya kwa ufasaha kuwa “Kutokeya ulipoanza, Ukristo umekuwepo kwenye bara la Afrika, Masri, Libya, na Afrika ya Kaskazini, na labda Ethiopia. Lakini hakuna kumbukumbu yoyote katika Zama za Giza (Dark Ages) ya kuingiya kwa Ukristo sehemu za kusini, si kwa kupitiya njiya ya baharini au ya barani. Kuingiya kwa Ukristo Tanzania ni jambo la miaka ya karibuni.”7

Ukifananisha na Afrika Magharibi, kufaulu kwa uenezaji wa Ukristo Afrika Mashariki kulisababishwa na “uhaba wa nguvu za Uislamu, uhaba wa Dola zenye nguvu na zilizojiandaa kuuzuwiya Ukristo, na rukhsa aliyoitowa Sayyid Said wa Zanzibar kwa mamishionari kuanza kufanya kazi zao, ambazo ni kinyume na imani yake ya Kiislamu, na upeo wa kipropaganda wa Livingstone Uingereza na nchi za Ulaya.” 8

Tukirudi nyuma zaidi na katika mwaka kama wa 975, anaelezeya mtafiti Bergen, “wakimbizi wa kidini na wa kisiasa kutokeya Persia na Arabia walianzisha miji midogo katika pwani ya Afrika Mashariki. Miji hiyo baadaye ilikuwa na kuwa miji mikubwa ya kibiashara, na dini kubwa ya ukanda wa pwani ikawa dini ya Kiislam…Kuowana kwa Waarabu, Wafarsi, Washirazi na Waafrika kukazaa kabila la mchanganyiko la Waswahili, na ustaarabu wa Kiafrika wa Kiislam.”9

Vipi udugu wa mtiririko wa zaidi ya karne kumi za ustaarabu, mila, na dini moja, utaweza kuvunjwa na miaka isiyozidi khamsini ya fitina zinazotokana na hadithi za kubuni za dhiki na dhuluma za utumwa? Juu ya yote yaliyotokeya na kufanyika ndani ya fitina za miaka michache, Wazanzibari wengi sana wamekuwa wakisononeshwa na kuwaombeya dua watu wa Zanzibar watuliye nafsi zao na Zanzibar ijirejeshee hishma na hadhi yake. Haya ya Zanzibar ni mfano wa yale aliyoyaelezeya msomi Eqbal Ahmad kuhusu mpasuko wa India:

Haiwezekani kukosa njia za kujiepusha na kufarikiyana kwa jamii mbili zinapoishi

Page 22: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizixx

pamoja kwa miaka mia saba. Sifahamu kwa nini uongozi wa India, wa Kiislam na wa Kihindu, pamoja na Gandhi, wakashindwa kuhakikisha uendelezaji wa mtitiriko wa jamii mbili, moja ya Kihindu ya pili ya Kiislam, kuweza kuishi kwa pamoja. Kulikuwa na mivutano katika mahusiano yao kama kunavyokuwepo mivutano kwenye mahusiano yoyote yale. Muhimu zaidi ni makundi mawili haya yameishi kwa kutegemeyana na ndani yake kumezaliwa mambo mengi sana. Ustaarabu mpya umezaliwa. Lugha mpya ya Urdu imechomoza kutokana na mchanganyiko wa nini Waislam wameleta na walichokikuta Bara Hindi…Kutengana kungeliweza kuepukika kama alivyotabiri mshairi na mwandishi mkubwa Rabindranath Tagore ingelikuwa harakati za India zilizo dhidi ya ubeberu zingeliutambuwa umuhimu wa kujitenga na ideolojiya ya uzalendo (nationalism). Tuliupinga ubeberu wa Magharibi lakini katika kufanya hivyo tukaukumbatiya uzalendo wa Magharibi mzima mzima.10

Uongozi wa Zanzibar na wa Tanganyika, pamoja na Mwalimu Nyerere, ungeliweza kuhakikisha uendelezaji wa mtiririko wa makarne ya jamii mbili zilizouzaa ustaarabu wa Waafrika Waislam, lugha ya Kiswahili, na mengi mengineyo. Mtengano ulioletwa kwa makusudi na mapinduzi ya 1964 ulisababishwa na mrengo wa kisiasa wa kizalendo wa Pan-Africanism ambao chimbuko lake limetokana na Waafrika waliyosoma na kulelewa Ulaya. Matatizo pia yaliletwa na khofu ya mrengo wa kizalendo wa Pan-Africanism kuja kutawaliwa na mrengo wa Pan-Arabism ambao ulikuwa ndiyo mrengo wa Masri ya Rais Gamal Abdel Nasser, rafiki wa chama cha Zanzibar Nationalist Party kilichokuwa kikiongozwa na Zaim (kiongozi) Sheikh Ali Muhsin. Ni jambo la kushangaza vipi mirengo ya kizalendo ya viongozi wakubwa wa Afrika, Julius Kambarage Nyerere na Gamal Abdel Nasser imalizikiye na mauwaji ya halaiki na kuguswa na sumu ya fitina za utumwa. Mara nyingi Zanzibar imejaribu kujipatiya utulivu na haikuweza kufaulu. Haya yalitokeya kabla ya Mapinduzi na yakajaribiwa tena baada ya Mapinduzi na zaidi kwenye Miafaka ya hivi karibuni. Wakati wa Mwenye Enzi Mungu kutaka ulikuwa bado haukufika na pia kwa sababu ya mashindano ya kisiasa baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe yanayotokana na tabia ya kutoaminiyana. Miaka arubaini na sita yameutiya umoja wa umma wa Kizanzibari wenye dini, mila, na kuingiliyana kwa kuowana, ndani ya mtego wa upotoshaji wa historia ya nchi ya Zanzibar. Kwa mujibu wa Bwana Abdulshakur:

Ukweli ni uvamizi ulikuwa ni tukio tu lakini yaliyofuata mavamizi hayo ulikuwa ni mlolongo maalum uliojengwa kiitikadi katika kumpotosha Mzanzibari na utambulisho (identity) wake. Mipango ya kumgeuza na kumpotosha Mzanzibari [mweusi na mweupe] ilianza kwa bahati tukiwa wadogo maskulini. Mengi yalitupata na mengi tukayashuhudia lakini kama watoto, mengi tuliyaona kwa jicho la kitoto pia.Tukitafakari leo kwa kutizama nyuma tulikotoka tunaweza kuona kuwa yote hiyo ilikuwa ni mipango yenye nia na madhumuni maalumu.11

Page 23: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xxi

Lililotoswa na kuzoweleka ndani ya akili za wengi ni kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuja kuondowa dhiki na dhuluma za kikundi cha mabwanyenye wa Kiarabu wachache dhidi ya Waafrika walalahoi waliyo wengi. Kitabu hichi kinahoji kwa ushahidi kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na lengo la kuubomowa uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu na kuuweka uhusiano huo chini ya udhibiti wa nguvu za kiutawala za Tanganyika. Kama alivyosema Eqbal Ahmad, hakuna uhusiano usiokuwa na matatizo yake na uhusiano wa zaidi ya miaka elfu mbili baina ya Waafrika na Waarabu uliyozaa ustaarabu, lugha, na dini ya Kiislam ilyozikaribisha na kuzihishimu dini nyengine Zanzibar, ushindwe kuundeleza mtiririko wa jamii hizo mbili kuweza kuishi kwa udugu na ujirani mwema. Kwa mujibu wa mchoraji maarufu na bingwa wa lugha ya Kiswahili na habari za Waswahili, Profesa Ibrahim Noor Shariff:

Hakuna mgongano wowote wa mtu kuwa Mwarabu na wakati huohuo akawa Mwafrika kama vile hakuna mgongano wowote wa mtu kuwa Mbantu au Mmasai akawa pia ni Mwafrika.12

Wakati akizungumziya mapinduzi ya Zanzibar, Profesa Ali A. Mazrui aliandika:

Kwa maana ya uzalendo wa Kizanzibari, Jamshid bin Abdalla na Ali Muhsin walikuwa Wazanzibari zaidi kuliko John Okello lakini kwa maana ya uzalendo wa Kiafrika, John Okello alikuwa Muafrika zaidi kuliko Jamshid bin Abdalla na Ali Muhsin.13

Jambo lilokuwapo wakati ule wa nyuma ni kuwa Zanzibar si nchi ya Kiafrika kwa sababu ilikuwa na utawala wa Kisultani ambao ni wa asili ya Kiarabu na wa Kiislam. Na si hivyo tu ulikuwa utawala uliotanguliwa na tawala nyengine kongwe za Kiislam katika Pwani ya Afrika Mashariki na ushawishi mkubwa ndani ya bara la Afrika Mashariki na Kati ambazo pia zilikuwa zina asili ya mchanganyiko wa Kiarabu na wa Kiafrika. Hilo halikuwa jambo geni kwa Afrika Mashariki na Kati ziliyoko chini ya Jangwa la Sahara. Tatizo lilikuja pale wakoloni wa Kizungu walipoona wazi kuwa kuna mahusiyano mazuri na makubwa baina ya Zanzibar yenye ushawishi Afrika Mashariki na Kati na nchi za Kiarabu za Kaskazini ya Afrika ambazo zilikuwa dhidi ya Wakoloni wa Kizungu. Inafaa ikakumbukwa kuwa “nchi kumi (10) za Kiarabu ziko ndani ya bara la Afrika, na thuluthi moja ya umma wa Kiarabu inaishi Afrika, na aslimia 72% ya ardhi za nchi za Kiarabu ziko Afrika na kuwa dini ya Kiislam ni dini iliyotapakaa katika bara la Afrika kuliko dini yoyote nyengine.”14

Wapenzi wa matumizi ya neno “Muafrika” katika Afrika Mashariki hawana

Page 24: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizixxii

budi kuuzingatiya ushahidi wa kihistoria au ushahidi wa viini vya DNA vya miaka ya hivi karibuni wenye kuthibitisha kuwa Waafrika Wakristo na Waislam walikuwa kitu kimoja kwenye kuupendeleya mrengo wa uzalendo wa Kiafrika uliyotokana na Waafrika ambao waliishi nchi za Ulaya wakati Afrika ilipokuwa ikitawaliwa na Wakoloni wa Kizungu. Na hata baadhi ya Waarabu pia walitumbukiya ndani ya mrengo huo. Lakini haina maana kuwa hisiya za kidini zilikuwa hazipo. Ukristo ambao ulikuwa ndiyo dini ya Wakoloni wa Kizungu ulikuja kufananishwa na sifa zote za Muafrika Mkristo aliyeonewa na aliyekosewa na dhuluma za kihistoria, na Waarabu Waislam wakapewa sifa zote mbovu kuwa wao ndiwo waliyoleta uovu wa biashara ya utumwa Afrika. Uchafu wote ukapelekwa Bagamoyo kwenye Uislam na usafi wote ukapelekwa Arusha kwenye Ukristo. Tanganyika ikageuzwa kuwa ndiyo msalaba wa kuisulubu Dola ya Zanzibar bila ya kujali hali ya mchanganyiko wa kidamu baina ya watu wa pande hizo mbili. Yaleti siku ifike Katiba ya Zanzibar na ya Tanganyika zikapinga kwa maneno na kwa vitendo ubaguzi wa binaadamu yoyote yule kwa misingi ya kikabila, asili, au dini na kuwalinda na kuwapa zawadi watu binafsi au taasisi zitakazowaanika na kuwawajibisha bila ya kuwaoneya haya mafisadi wa kiasili, kidini na wa kiuchumi. Yasije yakawa yale ya Tom Mboya alipomuambiya Sheikh Abdillahi Nasser wa Kenya “rudi kwenu Oman!” na Sheikh Abdillahi akamjibu Mboya “na wewe rudi kwenu Sudan!” Mboya akajibu “angalau Sudan iko Afrika!” na Sheikh Abdillahi akamjibu “hata hivyo. Sudan bado ni memba wa Arab League! ( Jumuiya ya Waarabu).” 15

Suala la ubaguzi Afrika limedharauliwa sana kutokana na imani kuwa mtu mweusi hawezi kuwa mbaguzi au kaburu kwa sababu ya historia ndefu ya kubaguliwa, kuuzwa, na kutumbikizwa ndani ya ukoloni. Chembelecho Mwalimu Nyerere, mbaguzi ni mbaguzi tu hata akiwa ni Muafrika mweusi.16 Muhimu binaadamu kujitambuwa na kushikiliya kutambuliwa kuwa ni binaadamu bila ya kuwaoneya haya wabaguzi wa Kiafrika kwa sababu ni weusi.

Nadhariya ya Kitunguu na Mlango Uliyofungwa

Nilifanya mahojiano mengi na kuzisajili sauti za wazee wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini baadaye nikaamuwa nisizitumiye kwenye kitabu hichi kwa sababu niligunduwa kuwa nimekamata ganda kavu la kitunguu lililo karibu na nje. Nadhariya ya kitunguu imenisaidiya kufahamu kuwa kitunguu cha mapinduzi ya Zanzibar kina tabaka maalumu na chache mno. Mikono ya Mapinduzi huenda ikawa mingi lakini vichwa vya mapinduzi ni vichache sana. Hilo ni jambo la kawaida. Hakuna nafasi ya watu wengi kwenye jambo la siri kama la kupanga mapinduzi.

Page 25: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xxiii

Mapinduzi ya Zanzibar yana tabaka au vikundi tafauti vya kijamii na vya kisiasa ndani ya Zanzibar, Tanganyika, na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Kuna maelezo ya dhahiri kukhusu Mapinduzi na piya yaliyojificha juu ya tukiyo hilo hilo. Maelezo ya dhahiri ni kuyaweka Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya mabano ya visiwa na kutamka kuwa hakukuwa na mkono wa nje kwenye kuyafanikisha mapinduzi hayo. Maelezo yaliyojificha ambayo ni muhimu zaidi kwa mustakbal wa Zanzibar yanakubali kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na wenyewe, na wenyewe hao walikuwa vichwa vya juu vya Mapinduzi na hawakuwa wanakindakindaki wa Kizanzibari. Wazanzibari wenyeji ambao hawakushirikiyana na vichwa vya mapinduzi kutoka nje hawakuaminiwa kupewa siri ya mipango ya mapinduzi na siri hiyo haikuwa kuingiya Bomani, au Ziwani kwenye vituo vya polisi na silaha. Majiko ya Mapinduzi yalikuwa machache lakini nguvu zake ambazo ndizo zilokuja kuamuwa wapi Zanzibar ielekee hazikuwa nguvu za Wazanzibari wenyeji. Kwa vile majiko yalikuja kupinduwana msomaji anatakiwa awe makini kuelewa wapi kuna migongano ya maelezo na wapi kuna migongano ya majiko. Jiko asiliya la ndani la Mapinduzi ya Zanzibar lilipinduliwa siku tatu tu baada ya Mapinduzi kutokeya baada ya mikono ya mapinduzi ambayo kisiasa ilikuwa ikicheza mchezo baina ya jiko asiliya la Mapinduzi na baadaye kumkabidhi uongozi Mzee Karume. Kitabu pia kinahoji kuwa hakukuwa na Kamati ya Watu 14 kabla ya tarehe 12 Januari 1964 iliyokaa kitako peke yao na Mzee Karume kupanga mipango ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kamati hiyo iliundwa na kupewa jina hilo baada ya kupinduliwa jiko la kwanza la akina marehemu Abdalla Kassim Hanga, Saleh Saadalla Akida, na Abdulaziz Twala. Waliyojiita baadaye kuwa ni Kamati ya Watu 14 walikuwa ni vijana wa Afro-Shirazi Party Youth League (ASPYL) ambao wakichukuwa miongozo yao kutoka kwa akina Saleh Saadalla. Lakini kwa sababu Hanga, Saadalla, na Twala walikuwa ni viongozi wasomi na wakiupinga uongozi wa Mzee Karume, vijana wa ASPYL ambao takriban wote hawakusoma walikuwa karibu zaidi na Mzee Karume. Mapinduzi yalipofaulu vijana wakamkabidhi uongozi Mzee Karume siku chache tu baada ya mapinduzi ya akina Hanga kufanikiwa. Kuna sababu tafauti zilizowafanya wazee waamue kusimuliya kwa undani simulizi za Mapinduzi ya Zanzibar. Kuna waliyotaka kuisajili historia inayo-poteya. Kuna waliyotanabahi kuwa Mapinduzi hayakuwaleteya faida walizo- kuwa wakizitarajiya. Wapo wenye hisia kuwa wakati umefika wa kubadilisha serikali kwa njia ya kura za wananchi badala ya kutumiya mtutu wa bunduki. Kuna wanaohisi wamedhulumiwa na wametupwa wao na kizazi chao baada ya kazi kubwa waliyoifanya katika Mapinduzi. Ni dalili ya msemo maarufu wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani [mabadiliko] khasa Tanzania yatatoka ndani ya chama hichihichi na uongozi huuhuu wa CCM na si nje yake kwa sababu

Page 26: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizixxiv

hakuna njiya ya kuyafahamu Mapinduzi na Muungano nje ya ASP, TANU na CCM. Na piya katika wazee wapo ambao wanataka kuiona Zanzibar na Tanganyika zinazoheshimu historia itakayomtowa binaadamu kutoka jela ya yaliopita na yasiyojulikana, na kuelekeya kunako Zanzibar na Tanganyika zenye mapenzi, umoja, na neema za maisha mazuri kwa kila mwananchi. Zaidi ya yote ni kugu-bikwa na kusahaulika kwa kumbukumbu za Mapinduzi ambazo kukosekana kwake kwa nusu karne kumezipotezeya Zanzibar na Tanganyika nafasi za kujikwamuwa.

Mfumo wa Kitabu

Muundo wa kitabu hichi ni wa simulizi kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Asilimiya kubwa sana ya kitabu ni simulizi za wazee waliyoshiriki au walioyashuhudiya Mapinduzi kwa undani wake. Kiwakati asilimiya kubwa ya mahojiano ya simulizi ziliyomo ndani ya kitabu yalifanyika kuanziya katikati ya mwaka 2004 na mwisho wa mwaka 2009. Usajili wa mahojiyano ya muda mrefu ya awali ambayo hayamo ndani ya

kitabu yalikuwa na akina marehemu Ali Omar (Lumumba), Othman “Bapa”, na wenginewo ambao hawakutaka majina yao kutajwa. Kutokana na nadhariya ya kitunguu nilikuja kuamuwa kuwa mahojiyano ya baada ya mwaka 2004 na kuendeleya yalikuwa yana umuhimu mkubwa zaidi katika kuisajili na kuiweka sawa historia ya mapinduzi ya Zanzibar kuliko ya kabla yake. Ni vigumu kuyatoleya tarehe mahojiano niliyoyafanya ndani ya nyakati tafauti

na ambayo nimeyapanga chini ya mtiririko wa maudhui na milango tafauti. Na kwa vile baadhi ya wazungumzaji hujitokeza kwenye mlango zaidi ya mmoja nimeona hakuna haja ya kumjuulisha tena msomaji ni nani anayezungumza endapo wasifu wake ulikwisha kutolewa huko nyuma. Kuna sehemu chache sana ambazo mahojiyano yalifanywa na zaidi ya mtu mmoja ndani ya wakati mmoja. Kwa kifupi kitabu kinaanza na maelezo na simulizi ya vipi ndoto ya uhuru wa

Zanzibar ilivyozimwa kwa siri nzito ya Mapinduzi na kinamalizikiya na tafsiri ya nyumba ya Afrabia ambayo inatowa picha ya mustakbal mwema wa Zanzibar na wa Tanganyika. Huenda msomaji kutoka Zanzibar, Tanganyika, na kokote kule duniani, aliyekuwa akisononeshwa na suala la Zanzibar akaweza kuuona mwangaza nje ya pango la upotoshaji wa historia. Msomaji wa aina hiyo ni sawa na yule mama aliyotoka ndani ya pango lenye giza huku amebeba ndoo ya maji ya hikma juu ya kichwa chake. Hapana shaka uamuzi wa mwisho na muhimu utakuwa ni wako msomaji. Kitabu hichi kina mfumo wa binaadamu mwenye hamu na kiu ya kuisaidiya

Zanzibar, ikiwa yuko ndani au nje ya Zanzibar, lakini hawezi kufanya hivyo bila ya kwanza kuandaliwa mazingira ya kikatiba na ya kimaisha ambayo yatamvutiya

Page 27: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xxv

kuweza kufanya hivyo. Hichi si kitabu cha siasa ingawa kwa mtizamo wa kijuujuu kinaweza kuonekana kuwa ni kitabu cha kisiasa na cha wanasiasa. Ni kitabu cha wenye dira na ushujaa wa kumchaguwa kiongozi na uongozi ambao utakuwa na sifa na uwezo wa kuituliza Zanzibar na Tanganyika kwa kuufuta upotoshaji wa fitina ya historia ambayo ndiyo mzizi wa shari ya chini kwa chini ndani ya muungano. Muhimu zipatikane nguvu kazi za Wazanzibari na Watanganyika waliyozagaa duniani ili wasaidiye kuutekeleza mkakati wa kuuinuwa uchumi wa Zanzibar na Tanganyika na kuziweka nchi zao kwenye daraja bora zaidi. Baina ya milango mitatu ya mwanzo na mitatu ya mwisho, katikati kuna

milango kumi na tano iliyokusanya simulizi za wazee kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Asilimia kubwa sana ya simulizi hizo zinatoka kwa wazee waliyopinduwa na simulizi mbili kutoka kwa marehemu Sheikh Ali Muhsin juu ya Mapinduzi ya 1964 na Shirikisho la Afrika Mashariki. Kivitendo, mchango wangu katika kazi hii ni kuandaa minhaji ya utafiti

(methodology); kuwasaka na kuwapata wazee; kuisajili na kuiweka sawa historia ya Mapinduzi na kuwakumbusha wazee dhamana zao za kukisaidiya kizazi kipya kufahamu na kuyaondowa matatizo ya Zanzibar, baina ya Zanzibar na Tanganyika na baina ya Waafrika na Waarabu; kuandaa masuala yaliyomuongoza mtafiti ndani ya midani ya utafiti na nyaraka za kitaifa; kukaa na wazee kwa muda mrefu; kuwafanyiya mahojiyano na kuyasajili katika vilimbo vya kunasiya sauti; kuyaandaa majadiliyano katika milango na kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyotumiwa na wazee wengi; kuwapiga picha baadhi ya wazee kwa rukhsa yao na kuzipiga picha sehemu muhimu za midani ya utafiti; pamoja na uchapishaji wa kitabu hichi. Niliweza kuwachaguwa wazee niliyowahoji kwa kuzifuatiliya dalili tafauti

kutoka midani ya utafiti na nyaraka za kitaifa za Kiingereza na za Kimarekani na muhimu zaidi kutoka kwa wazee wenyewe kunijuulisha na wanamapinduzi wenzao. Msomaji ataweza kuwatambuwa baadhi ya wazee wanaozungumza na wanaozungumzwa baina ya maelezo yao ya ndani ya kitabu. Kuna baadhi ya wazee nimewagubika wasijulikane kwa sababu hawakutaka kujulikana kwa hivi sasa. Wako wazee muhimu ambao wanayajuwa mengi zaidi kuliko yaliyomo ndani ya kitabu lakini sikuwafuatiliya kwa sababu nilifahamu kuwa walikuwa na uzito wa kuzungumza kwa sababu wanazozijuwa wao wenyewe.

Masuala ya Kujiuliza

Wazee wengi wenye kusimuliya simulizi za Mapinduzi ya Zanzibar ni wazee ambao wamebobea kwenye historia ya Mapinduzi. Ni wazee waliyokaa kitako mara nyingi na kukongeshwa kwenye viti vyao kwa fikra na mawazo ya muda mrefu ambayo hawajawahi kuwakabidhi watoto na wajukuu zao. Kitabu kinauliza masuala matatu ya msingi. Jawabu za masuala hayo zilimezwa

Page 28: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizixxvi

na nyangumi aliyeamuwa kuzamiya au aliyezamishwa kwa makusudi kwenye bahari ya historia kwa zaidi ya miaka 46. Masuala ambayo msomaji wa kitabu hichi anafaa kuyazingatiya kwa umakini mkubwa ni haya yafuatayo:

1) Ufunuo wa Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya kipindi cha maridhiyano baina ya Wazanzibari utaweza kuisaidiya Tanganyika kuisitisha mivutano iliyojitokeza kwa kuukaribisha mfungamano ndani ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya pili ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar?

2) Umoja wa maridhiyano baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika Weusi na Waarabu Waafrika, utakuwa na faida gani kubwa za kisiasa na za kiuchumi kwa wananchi walio wengi wa Afrika Mashariki na Kati?

3) Madola makubwa ya Magharibi yalishiriki katika upangaji na utekelezaji wa Mapinduzi au waliyasaidiya kwa kuzidharau kwa makusudi taarifa za kiusalama walizokuwa nazo kwa sababu Mapinduzi na Muungano ilikuwa ni mihimili miwili yenye maslahi na wao zaidi kuliko maslahi ya Wazanzibari, ya Wazanzibari na Watanganyika, na ya Waafrika na Waarabu?

Yapo masuala mengi yaliyo muhimu ambayo hayakupewa haki yake na kitabu hichi. Kwa mfano, nini chanzo cha fedha zilizotumika kuyagharimiya Mapinduzi ya Zanzibar? Inatosha kumnukuu Bwana Godfrey Mwakikagile ambaye kwenye kitabu chake Nyerere and Africa: End of an Era anakiri kuwa katika mada alizozungumza kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na mtoto mkubwa wa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyerere, moja wapo ni “viongozi kama Mfalme Haile Selassie, Dk. Kwame Nkrumah waliyagharimiya kifedha Mapinduzi ya Zanzibar.”17 Ufuatiliyaji wa chanzo cha fedha zilizotumika katika kuyagharimiya mapinduzi ya Zanzibar unahitajiya kufanyika ikiwa chanzo chenyewe ni serikali ya Tanganyika, au Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) au vyanzo vyenginevyo. Iko haja ya kujiuliza kama kuna ushahidi wowote Msalaba Mwekundu kuwaondosha Waarabu ilikuwa kwa ajili ya kuyasaidiya Mapinduzi au la. Kwa mujibu wa Frieder Ludwig, mwandishi wa kitabu Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994 “Mapinduzi ya Zanzibar yalipokelewa vizuri na Wakristo waliyokuwa wakiishi Zanzibar.” Ludwig amemnakili Mmishionari mmoja aliyemnakili mama mmoja mtu mzima aki sema “Nilishindwa kujizuwiya kukumbuka vipi Bwana wetu alisema ‘Nimeyaona mateso ya watu wangu—na nikampeleka Musa kuwakombowa’—na sasa amemleta John Okello kutukombowa…Si Kamishna wa Polisi [Edington Kisasi] peke yake, bali

Page 29: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xxvii

Makamishna wa Gereza na Kazi ni wanachama wenye bidii katika kikundi cha dini yetu”.18 Suala la kujiuliza, ni jee, Kanisa lilimuunga mkono Mwalimu Nyerere katika kuipinduwa Zanzibar? Misikiti pia ilishiriki? Na viongozi wa Kiislamu wa TANU walikuwa na mchango gani katika kuipinduwa Zanzibar?19 Wazee wengi waliyohojiwa na mwandishi wa kitabu hichi ni Waislam, ingawa uongozi mkubwa ulikuwa kwa mwenyewe Nyerere na madola makubwa yaliyomuunga mkono. Lakini hata akina Oscar Kambona pia walikuja kuangushwa na Mwalimu Nyerere ingawa alikuwa Mkristo Muanglikani. Kuna masuala ya msingi kuhusu mchango wa Mzee Abeid Amani Karume katika Mapinduzi ya 1964 na Muungano ambayo ni muhimu sana kuwekwa sawa kwa faida ya historia na zaidi kwa faida ya Zanzibar. Kwa mfano msomi maarufu Tanzania, Profesa Issa G. Shivji ameandika juu ya mahusiyano ya Mzee Karume na Muungano:

Maelezo rasmi yanarudia ….kuwa Karume alikuwa ni mwenye shauku kubwa juu ya Muungano. Hivyo ni mbali na ukweli ulivyo. Kama kuna kitu ambacho Wazanzibari wanamtukuza Karume nacho, mbali ya utawala wake wa kidikteta, ni Uzanzibari wake na upinzani usiyotetereka wa kukataa kuingizwa ndani ya Muungano na kuipoteza haki ya Zanzibar ya kujiamuliya mambo yake wenyewe. Kwa mfano, Smith, ambaye alikuwa hana kizuizi cha kumfikiya Nyerere na maofisa wengine wakati wa utafiti wake, anataja kuwa tishiyo la Nyerere la kuwaondowa askari wa polisi wa Tanganyika visiwani ndiyo lililomfanya Karume aukubali Muungano. Lakini alikuwa anasitasita mpaka dakika ya mwisho.20

Au angaliya namna R. K. Mwanjisi, ambaye aliwahi kuwa Seketeri wa Bunge, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanganyika, kwenye kitabu chake kiitwacho Abeid Amani Karume anavyoelezeya matukio ya “Siri za Mapinduzi”. Kati ya nukta 46 za matukio ya Mapinduzi, Mwanjisi anaelezeya kunako nukta ya kwanza kuwa “Mwishoni mwa mwaka mwaka 1963 au mwanzoni mwa mwaka 1964 iliundwa ‘Kamati ya Mapinduzi ya watu 14’. Nukta 14 inaelezeya kwa ‘Sultani akaelea baharini siku nzima ya tarehe 12 na kesho yake. Meli yake ikakataliwa kutua Mombasa. Ndipo iliporuhusiwa kuingia Dar es Salaam na Serikali ya Tanganyika baada ya kuombwa na Mwingereza.’ Nukta ya 15 inasema: ‘Tarehe 12 Mwalimu Nyerere na Bwana Kambona waambiwa mambo yaliyotokea Unguja [Zanzibar].’ ”21

Kwa hiyo Mwalimu Nyerere na Oscar Kambona hawakujuwa kitu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar mpaka pale yalipotokeya. Ina maana walikuwa hawana taarifa yoyote kabla ya siku hiyo. Piya hakuna popote pale ambapo Mwanjisi anaelezeya na kwa ushahidi kuwa Mzee Karume alihusika na upangaji wa Mapinduzi ya 1964. Maelezo rasmi juu ya wahusika wakuu wa Mapinduzi ni Kamati ya Watu 14 ambayo ni ya viongozi ambao hawaonekani kuwa walikuwa na kiongozi.

Page 30: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizixxviii

Jambo moja muhimu ambalo Mwanjisi aliligusiya ni pale alipoandika:

Madola ya Magharibi yanaamini kwamba ati Mapinduzi ya Unguja na Pemba yameendeshwa na Wakomunisti, hii ni dharau ile ile ya kusema kuwa Mwafrika hawezi kutenda kitu cho chote chenye maana! Pia ni kuwapa Wakoministi sifa wasiyostahili kupata.22

Wakati umefika wa kukaa na kujiuliza masuali mazito ya nafsi zetu na wapi tunataka kwenda. Hukumu ni ya wasomaji wenye kuyapima mambo kwa kutumiya vipaji vyao na uhuru wao wa kufikiri bila ya kupendeleya hata kama ukweli utakuwa unawagusa wale ambao wanawapenda. Bado kuna kuingiya ndani ya nyumba, vyumba na vipembe. Mwenzangu una akili na moyo wako mwenyewe. Jiulize mwenyewe. Jijibu mwenyewe. Wazee wameshatusaidiya mpaka hapa. Sasa tujisaidiye wenyewe palipobakiya kwa kujihami kidini, kihaki, kiakili, kukilinda kizazi kipya na kuilinda Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) pamoja na kuutengeneza upya uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu kwa kuwaleteya maisha mazuri zaidi wananchi wa pande mbili za Muungano. Lakini lengo muhimu na kubwa zaidi liwe lenye kutizama mbele. Hilo ndilo la muhimu zaidi. Lengo ni kuufuta ujinga wa kuidanganya dunia na kuinyang’anya Zanzibar sifa zake kama ni nchi. Kama tutakavyoona huko mbele, Mzee Karume hakushiriki katika mipango ya Mapinduzi na wala hakuupenda Muungano kama ukweli unavyopotoshwa na wenye kutaka kuupa uhalali kwa kumtumiliya kisiasa baada ya kufa kwake. Kama tutakavyokuja kuona baadae piya, alijaribu kuirudishiya Zanzibar sifa zake kama ni nchi na matokeo yake alijibiwa “wakati wake bado haujafika” na baada ya miezi michache akauliwa. Mzee Jumbe na Maraisi waliyofuatiliya wa Zanzibar pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi, Maalim Seif Sharif Hamad, piya walijaribu kwa njia zao kuirudishiya Zanzibar sifa zake kama ni nchi na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuzidisha muamko wa Wazanzibari katika kuiteteya nchi yao na katika kuiteteya na kuinusuru Zanzibar ndipo itakaponusurika Tanzania. Tukitaka kurudishana nyuma hatutokosa la kulitafuta na kuwapata wa kuturudisha nyuma, na khasa kikundi kidogo cha wahafidhina wa Kizanzibari pamoja na wahafidhina wenziwao kutoka Tanganyika watakaotaka kumrudisha chui ndani ya zizi la ng’ombe badala ya kumtimuwa. Upinzani mkubwa wa kitabu hichi utatoka kwenye jumuiya zisizo za kiserikali kama pale Zanzibar au Tanzania zinapotaka kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC). Jumuiya hizo hazimo ndani ya mikono ya Waislam na zinamiliki zaidi ya asilimia 95% ya vyombo vya habari pamoja na bodi za wahariri wa magazeti, televisheni na vituo vya redio. Vyombo hivyo vya habari vitauelekeza umma na madola makubwa duniani kwenye khofu zisizo kuwa na msingi kwa kusema kuwa Zanzibar sasa inataka kugeuzwa kuwa Dola ya Kiislam. Niya na

Page 31: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Utangulizi xxix

lengo litakuwa ni kuwatiya khofu za chini kwa chini na za wazi wazi wananchi na madola makubwa kuwa kuja juu kwa Zanzibar ni kuja juu kwa ugaidi. Au wataamuwa kukaa kimya na kuzipa kasi fitina za miaka 46 katika jamii na taifa na watapima muamko wa kijamii kabla kutekeleza mipango yao ya muda mrefu kwa Zanzibar na Tanganyika. Tutarajiye kupaliliwa ngojera za “biashara ya utumwa wa Waarabu” na kuiunganisha fikra ya Afrabia na kuvunjika kwa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Upande wa umma ambao ungelipendeleya kuiunga mkono fikra ya mfungamano wa Afrabia utakabiliwa na hatari mpya kwa sababu ungali dhaifu kiuchumi, kisiasa, na haumiliki vyombo vingi vya habari, au kupeyana khabari kwa njiya na mikakati mipya.23 Inatosha neno “Arabia” ndani ya neno “Afrabia” (Afrika na Arabia) likafyatuwa upinzani mkali kama ule uliyoonekana dhidi ya OIC. Inatosha pia kwa baadhi ya watu kuchagazwa na jina na asili ya mwandishi ambaye ana damu za makabila mengi tu yakiwemo makabila kadhaa ya Kiarabu, ya Kimanyema na ya Kimwera, nk. Inatosha pia kutowa mfano wa tukiyo liliyotokeya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2001 wakati mwanafunzi wa ilimu ya Sayansi ya Jamii alipokuwa anatowa hoja ndani ya semina ya darasa. Mwanafunzi huyo alikuwa akinukuu sentensi kutoka kipindi cha Profesa Ali Mazrui cha The Africans: A Triple Heritage. Wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akimnukuu Profesa Mazrui, Profesa mmoja Mkristo wa ilimu ya sayansi ya jamii ambaye alikuwa mwalimu wa hiyo semina alikurupuka kwa hamaki na kusema “…kwa nini unamnukuu Ali Mazrui…yeye hata si Muafrika. Ni Mwarabu!”24

Kitabu hichi ni cha kuwailimisha wale ambao wamejazwa khofu dhidi ya Waarabu na Waislam au dhidi ya Waafrika na Wakristo. Lengo ni kuwa, hatimaye kitabu kituletee mapatano ya haraka na mashirikiyano baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika na Waarabu. Wenye kuogopa mfungamano wa Wazanzibari na wa Waafrika na Waarabu hawana uwezo wa kuuzuwiya kwa sababu kipindi cha uhusiano mkongwe wa zaidi ya miaka elfu mbili ni kirefu sana kuliko huu muda mfupi wa miaka arubaini na sita uliyogubikwa na guo la khadaa. Kwa hakika kwa hali ya leo ya Zanzibar na ya Tanganyika, kitabu hichi ni bishara njema. Kwa mujibu wa mwandishi Bwana Mohamed Said “mazungumzo ya wazee yaliyomo ndani ya kitabu ni kama watu wanaotubu ili wapate msamaha. Jinsi wanavyozungumza utadhani wametiwa kitu waseme yote wautue mzigo.” Na wewe msomaji, popote ulipo, huenda ukautuwa mzigo wako pia na ukawa na moyo uliyotuliya na wenye matumaini makubwa katika mustakbal mzuri wa Zanzibar, Tanganyika, na wa Afrika Mashariki na Kati.

Page 32: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru
Page 33: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa KwanzaSiri Nzito

Mtawaliwa siku zote anataka kumuigiza mtawala katika maumbile yake, mavazi yake, kazi zake na yote yanayokhusiana na hali yake na dasturi zake. —Ibn Khaldun

Mapinduzi Tanganyika na Kenya

Picha kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 haiwezi kufahamika bila ya kuyafahamu ijapokuwa kwa mukhtasari mfupi mapinduzi ya kabla yake yaliofanyika Tanganyika, na baadaye Kenya. Mapinduzi ya Tanganyika, ya Zanzibar, na ya Mwambao wa Kenya ni mifano ya mapinduzi ya kalamu na ya umwagaji damu. Tanganyika iliupata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 na Waislam wa Tanganyika walikuwa na mchango mkubwa sana katika kuupiganiya uhuru huo. Hayati Julius Kambarage Nyerere alitowa mchango mkubwa na yeye mwenyewe alikiri hivyo kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee aliyoitowa Dar es Salaam katika mwezi wa Novemba mwaka 1985. Kwa mara ya kwanza Mwalimu alie­lezeya namna alivyopokelewa, kujuulishwa na kusaidiwa sana na wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam. Kwenye shughuli za TANU yeye alikuwa ni Mkristo peke yake na mara nyingine alikuwepo John Rupia. Muhimu pia na kwa mara ya kwanza Mwalimu alisikika akisema kwenye hotuba hiyo kuwa hata jina la Tanganyika African National Union (TANU) lilifikiriwa na kuundwa na akina marehemu Abdulwahid Sykes walipokuwa askari Burma katika vita vya pili vya dunia.1

Historia iliyofichwa ya mchango wa Waislam katika kuupiganiya uhuru wa Tanganyika imeandikwa na kuelezwa kwa ufasaha mkubwa na mwandishi maarufu wa Tanzania Bwana Mohamed Said kwenye kitabu chake kwa lugha ya Kiingereza, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968), na kwa Kiswahili Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu

Page 34: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kwanza2

Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Kitabu hicho ni muhimu sana kwa wanaotaka kufahamu vipi Waislam waliupiganiya uhuru wa Tanganyika na namna walivyopinduliwa kwa mapinduzi baridi kwanza kabla ya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964. Kilele cha mapinduzi ya Tanganyika ni kudhoofishwa nguvu za umma wa Kiislamu pale ilipovunjwa East African Welfare Muslim Society (EAMWS) na zilipozimwa juhudi za kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislam mwaka 1964.2 Bwana Mohamed Said pia amefafanuwa katika kitabu chake Uamuzi wa busara wa Tabora namna gani uongozi wa Waislam kutokeya African Association mpaka kuundwa kwa TANU walivyopinduliwa kwa mapinduzi ya kalamu. Baraza la Wazee la TANU ambalo Mwenyekiti wake alikuwa marehemu Mzee Suleiman Takadiri lilipinduliwa chali kwa kazi iliofanywa na kiongozi na viongozi wa Kiislam waliouweka mbele uzalendo wa Kiafrika kuliko mafundisho ya dini yao. Chanzo cha mapinduzi hayo yalikuwa masharti matatu yalioikabili TANU katika kushiriki uchaguzi wa kwanza wa Tanganyika wa kulichaguwa Baraza la Kutunga Sheria. Mkutano wa TANU wa Tabora wa tarehe 21–26 Januari 1958 uliamua kuingiya uchaguzi wa kibaguzi wa kura tatu ambao ulikuwa na masharti matatu magumu:

1) Ili Mwafrika aweze kupiga kura alitakiwa awe na kipato cha pauni mia nne za Kiingereza kwa mwaka.

2) Awe na kiwango cha elimu ya darasa la kumi na mbili.3) Na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.3

Uamuzi wa busara wa Tabora haukuwanasa Waingereza kama ulivyowanasa Waislam wa Tanganyika ambao wengi wao hawakuweza kuwachaguwa viongozi wao kwa sababu uchaguzi wa kura tatu “ulikuwa ukizuia uongozi wa kuchaguliwa kuingia kwenye madaraka.”4

Kwa upande mwengine, Kenya kabla ya kupata uhuru wake tarehe 12 Disemba 1963, siku mbili baada ya uhuru wa Zanzibar, ilikuwa imegawanyika sehemu mbili: Koloni la Kenya, au bara, na Himaya ya Kenya, au Mwambao. Sheikh Abdillahi Nassir ni mmoja kati ya viongozi wa Mwambao ambaye alihudhuriya mkutano wa Mwambao uliofanyika Lancaster House, London, baina ya tarehe 8–12 Machi mwaka 1962. Anaelezeya Sheikh Abdillahi kwenye kanda iitwayo “Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki,” kuwa Himaya ya Kenya ilikuwa ni nchi kabla ya Koloni la Kenya kuwa ni nchi kwa miaka isiyopunguwa 1,300, na namna chuki za uzalendo wa Kiafrika zilivyowaathiri Waislam na khasa chuki za kikabila na propaganda ya utumwa na Uarabu.5

Sehemu hizo mbili za Kenya, Koloni la Kenya na Himaya ya Kenya au Mwambao, zikawa ni nchi moja ya Kenya kwa makubaliyano ya mabadilishano ya barua baina ya Waziri Mkuu wa Kenya, Mzee Jomo Kenyata na Waziri Mkuu

Page 35: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Siri Nzito 3

wa Zanzibar Bwana Mohammed Shamte walizoandikiyana London tarehe 5 Oktoba 1963. Barua zote mbili zilikubaliyana juu ya mambo matano yafuatayo:

1) Uhuru wa kuabudu wa watu wa dini zote katika sehemu hiyo utalindwa kwa mujibu wa dini zao; na khasa wale raia wa Sultani na vizazi vyao, ambao ni wa dini ya Kiislamu, watahakikishiwa uhuru wao wa kuabudu katika nyakati zote na hifadhi za nyumba na sehemu zote za dini yao.

2) Uwezo wa Kadhi Mkuu na Makadhi wengine wote kuhukumu kwa sharia ya Kiislamu utahifadhiwa kufuatana na sharia ya Kiislamu katika kesi zote za ndoa, talaka na mirathi.

3) Katika zile sehemu ambazo wakaazi wake wengi ni Waislamu, watawekwa, kila inapowezekana, Maafisa Utawala (Mabwana Shauri) Waislamu.

4) Watoto wa Kiislamu, kwa kadri inavyowezekana watasomeshwa lugha ya Kiarabu katika kudumisha dini yao ya Kiislamu kwa vile lugha hii ndiyo lugha ya dini yao. Ule msaada wa fedha unaotolewa kuzisaidia skuli za msingi za Kiislamu katika hilo jimbo la Mkoa wa Pwani utaendelea. Hautakatwa.

5) Umilikaji wa ardhi kutokana na mikataba iliyokwisha kusajiliwa utatambu­likana na kukubalika wakati wote. Mwenendo huohuo utaendelea na kuhi­fadhiwa katika kusajili mikataba mipya ya kumiliki ardhi isipokuwa tu pale itakapokuwa ni lazima kuchukua ardhi kwa masilahi na faida ya umma; lakini papo hapo wale wenye ardhi zao watabidi kulipwa fedha.6

Kwa mujibu wa Sheikh Abdillahi, makubaliano hayo baina ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Kenya hayakutimizwa na amethibitisha namna nguvu za umma zilivyoporwa na umuhimu wa kujenga muamko wa kuelewa badala ya muamko wa hamasa. Mfano mkubwa ambao ameutowa Sheikh Abdillahi am­bao ni kinyume na makubaliano waliyotiya sahihi Mawaziri Wakuu wa Zanzibar na wa Kenya, ni kunyanganywa Waislam, wa makabila yote, Taasisi muhimu sana ambayo ikijulikana kwa jina maarufu la Mombasa Insititute of Muslim Education (MIOME) ambayo ilikuwa ni:

baraka kubwa kwa Waislam wa Afrika Mashariki. Hapa ndipo mustakbal wa vizazi vya Waislam vinapewa mafundisho katika masomo ya ufundi chini ya Maprofesa mabingwa ambao wameajiriwa na Serikali kutoka Ulaya. Sir Phillip Mitchell ambaye alikuwa ni Gavana na sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Waendeshaji wa Taasisi alikuwa ndiyo nguvu ya usukumaji wa Taasisi [MIOME]. Mtukufu Sultan wa Zanzibar alitowa mchango wa Shs. 2,000,000/­ kutoka mfuko wa Colonial Welfare Fund, Mtukufu Aga Khan alichangiya Shs. 2,000,000/­: Mtukufu Sheikh Mkuu wa jamii ya Kibohora amechangiya Shs. 1,000,000/­; na Sheikh Khamis Mohammed bin Juma [El Mutwaji] amekodisha ekari 34 na nusu za ardhi nzuri na kwa muda mrefu kwa matumizi ya Taasisi, na kwa bei khafifu kwa kila mwaka.7

Mbali ya Muslim Teachers’ Training College iliyokuwepo Kibuli, Kampala, Uganda, Khamisi Sekondari ya Mombasa, Muslim School ya Soroti, ya Jinja, na kadhalika. Iliyovunja rekodi zote na ambayo marehemu Sheikh Ali Muhsin akiamini kuwa ndiyo moja kati ya sababu za kupinduliwa Zanzibar, ilikuwa ni fikra na mipango

Page 36: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kwanza4

ya kuanzisha Chuo Kikuu Cha Kiislam cha Afrika Mashariki na Kati. Kwa mujibu wa Sheikh Ali Muhsin, Chuo hicho kilikuwa na lengo la kuwafundisha Waislam kutoka sehemu zote za Afrika Mashariki na Kati. Mwandishi wa ramani wa Chuo hicho alikuwepo Zanzibar mapinduzi yalipotokeya na alisaidiwa kuondoka na Bwana Ahmed Omar Jahadhmy. Wamasri waliishauri serikali ya Zanzibar wasubiri mpaka watakapokuwa na wanafunzi wa kutosha ambao wataweza kufundishwa kwenye Chuo hicho. Fikra iliyoona mbali kwa wakati huo ni hii ambayo leo inaitwa Open University. Redio na televisheni vilikuwa viwe ndiyo vyombo viwiili vikubwa vya kufundishiya kote Afrika Mashariki na Kati. Majaribio ya kwanza yalifanywa kabla ya mapinduzi lakini yalifeli.8

Baada ya kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society ambazo khabari zake zinapatikana kwa urefu kwenye kitabu cha Kiswahili cha Bwana Mohamed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes, taasisi na mali zake zote zikataifishwa na badala yake pakaundwa BAKWATA Tanzania, SUPKEM Kenya na UMSC Uganda. Hali ya Waislam chini ya utawala wa Kiingereza ilikuwa ni ya kuridhisha zaidi kuliko hali waliyokuwa nayo baada ya kupatikana uhuru Tanganyika, Kenya na hata Uganda.

Waingereza Walijuwa Nini Kuhusu Mapinduzi?

Ukiangaliya kwa makini utakuja kuona kuwa walikuwepo Waingereza na mamishionari ambao walikuwa hawana chuki dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu lakini kwa bahati mbaya sauti zao sio zilizokuwa zikisikilizwa na kupewa nafasi. Kwa mfano alikuwepo Dk. Gerald Broomfield ambaye alikuwa ni mmishionari wa Kianglikani aliyekuwa na uzowefu mkubwa Zanzibar. Dk. Broomfield alinukuliwa na Arab Association ya Zanzibar kutoka kitabu chake Colour Conflict in Africa kwa maneno yake yafuatayo:

Afrika iliyobakiya ina jambo la kujifunza kutoka Zanzibar…Zanzibar inaonyesha uwezekano wa kuwepo amani na kuhishimiana baina ya makabila. Huenda likawa ni jambo zuri kwa roho zetu kukumbuka [Zanzibar] inafanya hivyo kwa sababu Sultan wa Kiarabu ndiye mkubwa wa Dola.9

Hilo halistaajabishi kwa sababu Ukristo uliingiya Zanzibar na bara kwa kupewa hishma na Masultani waliokuwa ni Waarabu na Waislamu. Lakini Muingereza mtawala alipoona kuwa Ufalme umegeuka na kuiunga mkono siasa ya kizalendo ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) ambayo ilikuwa karibu sana na siasa ya uzalendo wa Kiarabu (Pan­Arabism au Arab Nationalism) wa Gamal Abdel Nasser wa Misri, akaamua kuwatupa mkono ZNP­ZPPP na kuubwaga uhuru wa Zanzibar ambao ulikuwa hauna salama kwa Waingereza au kwa Mwalimu Nyerere kwa sababu, na kama alivyoelezeya Sheikh Abdillahi:

Page 37: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Siri Nzito 5

Zanzibar ilikuwa ni nchi pekee katika Afrika nzima ambayo isingelihitajiya Mzungu hata mmoja. Zanzibar ilikuwa ina watu wa kuendesha nchi na kuwaazima majirani kuendesha nchi zao.10

Sababu kubwa ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu kuwageuka watawala wa Kiingereza na watawala hao kupanga kuwakomowa Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu, kulianza kwa kupigwa mabomu Misri na Muingereza mwaka 1956.11 Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu walihisi kuwa Uingereza haiaminiki na kuwa ilikuwa dhidi ya Waarabu. Hisia hii ilisababisha kudai uhuru kamili bila ya kungojea maendeleo zaidi ya baadae. Mwisho wa mivutano Muingereza alikataa kuisaidiya serikali ya Zanzibar ilipopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 na sababu kubwa iliyowafanya kukataa ni imani yao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni suala la ndani ya Zanzibar na kuwa hakukuwa na mkono au uvamizi kutoka nje ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanganyika Muingereza aliamuwa kuzuwiya fujo na kumrejesha kitini Mwalimu Nyerere pale jeshi la Tanganyika lilipoasi tarehe 20 Januari 1964 na Nyerere akakimbilia mafichoni siku tisa tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.12 Viongozi wa Serikali ya Tanganyika haraka walikwenda kuomba msaada kutoka kwa wakubwa wa Kiingereza. Anaelezeya Brigadier Douglas:

Kambona, akifuatana na [Paul] Bomani, Waziri wa Fedha, akionekana ana jambo ameficha, na ana khofu zaidi kuliko kabla, walikuja nyumbani kwangu na barua kutoka kwa Naibu Raisi Kawawa ilosema: Nimeelekezwa na Raisi wa Jamhuri ya Tanganyika kuiletea ombi la msaada wa kijeshi serikali ya Kiingereza ili utuwezeshe kuweka sheria na amani ndani ya nchi.13

Mara nyingi uasi wa jeshi la Tanganyika umekuwa ukihusishwa na mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa wanajeshi wa Tanganyika, Kenya na Uganda waliingiwa moyo wa kuasi kutokana na kufaulu kwa Mapinduzi ya Zanzibar ingawa hakukuwa na uhusiano wowote baina ya matukio hayo mawili. Uamuzi huu unatokana na kukosekana kuyafahamu Mapinduzi ya Zanzibar kwanza, na pili, kukosekana huko kufahamika kwa mapinduzi ya Zanzibar kumeondowa hoja ya kufanywa utafiti wa mahusiano baina ya mapinduzi na uasi wa kijeshi wa Tanganyika. Suala moja muhimu ambalo linavutiya hoja ya uhusiano baina ya mapinduzi ya Zanzibar na uasi wa kijeshi wa Afrika Mashariki ni suala la kukamatwa kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi baada ya kutokeya uasi huo Tanganyika. Tarehe 29 Januari 1964 Balozi wa Kiingereza kwa niaba, alipeleka ujumbe wa telegram kwa Commonwealth Relations Office, London, uliopitiya Ubalozi wa Kiingereza Kampala, Nairobi, Aden na Washington:

Matokeo ya kuasi kwa jeshi la Tanganyika ni kundi kubwa la viongozi wa vyama vya wafanyakazi kukamatwa Jumapili usiku Tanganyika nzima pamoja na

Page 38: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kwanza6

takriban viongozi wote wa chama cha Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanganyika (Tanganyika Federation of Labour). Wote walipelekwa kwenye vituo vya polisi kwa kuhojiwa na baadhi yao baadaye waliwachiwa huru. Rais [Nyerere] kwenye hotuba yake ya redio ya jana usiku aliligusiya suala hili na aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Wilaya mmoja pia amekamatwa. Nyerere alitamka kwenye hotuba hiyo ya redio kuwa watu hawa, wa vyama vya wafanyakazi, walikuwa wamekula njama na viongozi wa uasi wa kijeshi “kusababisha mtafuruku zaidi.” Kulikuwa na uvumi mwingi wiki iliyopita kuwa vyama vya wafanyakazi vilikuwa vinapanga mgomo wa jumla au angalau mgomo wa wafanyakazi wa gatini na wa reli. Pia inaaminiwa kuwa viongozi kadhaa wa vyama vya wafanyakazi walikuwa wakipitisha wakati wao mwingi kwenye kambi ya kijeshi ya Colito.14

Msomaji anaombwa baadaye aunganishe mchango wa vyama vya wafanyakazi katika mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na uasi wa jeshi la Tanganyika wa tarehe 20 Januari 1964. Waingereza hawakuwacha kuuhusisha uasi wa jeshi la Tanganyika na mchango wa Oscar Kambona ambaye wakati huo alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi. Walimuandikiya makala kwenye ukurasa wa nyuma wa gazeti la Daily Telegraph la tarehe 22 Januari 1964 ambayo ilimuudhi sana Kambona. Balozi wa Kiiengereza aliyekuwepo Dar es Salaam alielezeya kwenye barua yake aliyompelekea Bwana W.G. Lamarque wa Commonwealth Relations Office, Downing Street, London, kuwa “Stephen Miles alipokutana na Rais [Nyerere] wiki iliyopita waligusiya kuwa Kambona alikuwa kiongozi wa uasi wa kijeshi, na Rais, kama unavyojuwa, alimwambiya Oscar kuwa ‘Masikini Oscar, maisha yeye ndiye mwenye kulaumiwa.’ Kwa kusema kweli, Oscar alikasirishwa sana alipozisikiya habari hizo na akaanguwa kilio na ikabidi apewe siku moja nzima ya mapumziko.”15 Waingereza walimtiliya shaka sana Kambona kuwa alikuwa amehusika na uasi wa jeshi la Tanganyika kwa kuzingatiya kuwa katika siku mbili za kwanza za uasi, Kambona alikuwa akitangaza kwenye redio kila baada ya nusu saa na kuwa alikuwa tayari achukuwe khatamu za serikali na ajitangaze kuwa ni Rais lakini aliogopa dakika za mwisho. Pia walilalama kwa kusema “Lazima iulizwe kwanini ulinzi wa ndani wa Tanganyika dhidi ya tukio kama la uasi wa jeshi ukawa dhaifu namna hii. Hapana shaka kukosekana kwa taarifa kutoka vyombo vya usalama kuipa serikali kumetokana na Kambona na [ Job] Lusinde kulibomowa Tawi la Usalama na badala yake kuwaweka watu wa T.A.N.U. aliowachaguwa Kambona.”16 Licha ya kuwa hawakuwa na taarifa za kiusalama watawala wa Kiingereza waliamuwa kupeleka jeshi la Makamandoo kurudisha amani na utulivu Tanganyika na kumrudisha kitini Mwalimu Nyerere. Na Zanzibar ikapinduliwa, mauwaji ya halaiki yakafanywa, na Bwana Adrian Forsyth­Thompson aliyekuwa Permanent Secretary katika ofisi ya Waziri Mkuu

Page 39: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Siri Nzito 7

Bwana Mohammed Shamte akaondoka Zanzibar tarehe 8 Februari 1964, na alitarajiwa kuondoka Nairobi kuelekeya Cape Town, Afrika Kusini, tarehe 11 Februari 1964. Baba yake Adrian alikuwa ni ofisa katika serikali ya kikoloni ya Kiingereza na alistaafu Cape Town. Adrian aliondoka Cape Town tarehe 18 Machi kwenda kwenye kazi yake mpya katika visiwa vya Seychelles. Forsyth­Thompson alikuwa ni ofisa wa usalama kwenye ofisi ya Balozi wa Kiingereza Zanzibar na punde tu kabla ya mapinduzi alikabidhiwa kazi na Katibu Mkuu wa Kiingereza, Bwana Mervyn Vice Smithyman, katika ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Mohammed Shamte kuleta mabadiliko katika vyombo vya usalama vya Zanzibar. Alipokuwapo Nairobi na tayari kuondoka kwenda Cape Town, Forsyth­Thompson alitowa ripoti muhimu ambayo ilipelekwa Commonwealth Relations Office, London kwa njia ya telegram na kopi zikapelekwa ubalozi wa Kiingereza Dar es Salaam, Aden, Kampala, Washington na Cape Town. Ujumbe huo ulikuwa ni mfupi ukiufananisha na ripoti yake yenye kurasa nane aliyoiandika alipokuwa Nairobi tarehe 10 Februari 1964. Kwenye ripoti fupi aliyoitowa Nairobi na iliyopelekwa London na Washington, Forsyth­Thompson aliziwasilisha nukta tano lakini hapa tutainukuu nukta ya kwanza na nukta ya nne:

1) Hakuna (rudia hakuna) ushahidi wa mkono kutoka nje katika mapinduzi ambayo yalikuwa ni mapinduzi ya Afro­Shirazi Youth League dhidi ya siasa ya Kiarabu ya Serikali iliyokuwepo, na mapinduzi yalifanywa katika kipindi ambacho viongozi wa ASYL na washabiki wao wakiamini patatokeya ukamataji wa viongozi wakati wowote. Babu alichupiya, na Karume (? Alichaguliwa) na wanamapinduzi kuwa ndiye kiongozi anayejulikana na Okello alichomoza tu.

4) Kwa mtizamo wa mbali mustakbal wa Zanzibar umo katika uhusiano wa karibu na maeneo ya bara ikiwa ndani ya Shirikisho au kuunganishwa na Tanganyika. Hili litafanyika kwa urahisi ikiwa Tanganyika au Kenya watakuwa tayari kupeleka vikosi vya polisi (kwa mfano kikosi cha huduma) kutokana na ombi la Karume ambaye atakubali kutokana na hali ya mambo ilivyo ikiwa Watanganyika na Wakenya watampa ishara kuwa wako tayari.17

Kwenye ripoti yake ya kurasa nane, Forsyth­Thompson anaelezeya kuwa:

Umma Party na viongozi wa ASP wenye mitizamo isiyo mikali hawakujuwa chochote [kuhusu mapinduzi]. Saleh Saadalla labda akijuwa…Alkhamisi tarehe 9 [ASYL] walisikiya kuwa mzigo wa meli wa silaha kutoka Algeria ulikuwa utaletwa na Serikali…Hadithi za silaha kutoka Algeria zilikuwa zimezagaa kwenye wiki baada ya mapinduzi: na kwa hakika ulikuwa ni upuuzi mtupu.18

Kuhusu mapinduzi yenyewe, anaelezeya Forsyth­Thompson, “yalipangwa na kutekelezwa ndani ya muda mfupi na hii ni dalili ya kukosekana kabisa taarifa

Page 40: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kwanza8

zozote kutoka kitengo cha usalama (Special Branch) kuwa kulikuwa na mpango. Kwa muda mrefu kulikuwa na mazungumzo ya kufanya fujo, lakini hakukuwa na pendekezo la mpango wa kuipinduwa Serikali kwa kutumiya nguvu.”19

Kamati ya Ukombozi wa Afrika

Mkutano wa nchi huru za Kiafrika uliofanyika Addis Ababa mwezi wa Mei 1963 uliunda Kamati ya Ukombozi wa nchi tisa yenye makao makuu Dar es Salaam. Nchi zilizounda kamati hiyo zilikuwa Tanganyika, Nigeria, Uganda, Algeria, Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu (U.A.R.), Guinea, Senegal, Ethiopia na Kongo. Ghana haikuwemo. Nyerere hakupendeleya makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ichukuliwe na Ghana, U.A.R. au Algeria. “Alikhofiya kuwa kati ya nchi hizo Kamati ingelitumiliwa na Rais wa Dola kujijengeya sifa, na mtizamo wa kamati ungelikuwa juu ya utumiaji nguvu badala ya shinikizo la amani.”20

Baada ya uchaguzi wa mwisho wa Zanzibar wa kabla ya mapinduzi wa tarehe 8 Julai 1963, Mwalimu Nyerere alifanya ziara ya Marekani na alionana na Rais John F. Kennedy, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant. Pia aliitembeleya nchi ya Canada kwa muda mfupi na alikuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bwana Lester Pearson. Tarehe 21–25 Julai alikuwa mgeni wa Serikali ya Uingereza. Mwalimu na ujumbe wake uliondoka London siku ya Alkhamisi tarehe 25 Julai kuelekeya Algiers, mji mkuu wa Algeria. Katika msafara wa Rais Nyerere walikuwemo:

Rais NyerereBwana Oscar Kambona, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na UlinziBwana I. M. Bhoke Munanka (Waziri Mdogo, Ofisi ya Makamo wa Rais)Bwana A. B. C. Danieli (Katibu Msaidizi, Mambo ya Nje)Bwana G. Rockey (Katibu wa Habari)Bwana F. Sangu (A.D.C.)Bwana P. Mwinbo (Mkuu wa Maofisa Wafanyakazi)Bwana J. M. Simba (Katibu Khasa wa Rais)Bwana U. Nyondo (Ofisa Mfanyakazi wa Rais)Bwana K. Kondo (Ofisa Mfanyakazi wa Bwana Kambona)

Ziara rasmi ya Rais Nyerere na msafara wake nchini Algeria ilikuwa kuanziya tarehe 25 mpaka tarehe 28 Julai. Inavyoonesha Ubalozi wa Kiingereza mjini Algiers hakuambuliya kitu chochote cha maana kati ya mazungumzo ya Rais Nyerere na Ahmed Ben Bella, Waziri Mkuu wa Algeria na baadaye Rais wa nchi hiyo. Katika mwezi huohuo wa Julai 1963 Waingereza walikuwa wameshazipata

Page 41: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Siri Nzito 9

habari kutoka jeshi la Tanganyika kuwa kulikuwa na silaha zikitarajiwa kutoka Algeria. Baina ya mwezi wa Agosti na Septemba 1963 listi ya silaha ilionekana Wizara ya Ulinzi. Halafu kimya mpaka wiki ya kwanza ya Januari 1964.21 Tarehe 2 Januari 1964, meli iliyopewa jina la mwanafalsa maarufu duniani wa historia, MV Ibn Khaldun kutoka nchi ya Kiarabu ya Afrika ya Kaskazini ya Algeria, ilitia nanga Dar es Salaam huku ikibeba shehena ya silaha zilokusudiwa kupelekwa Msumbiji na kwa ajili ya mapinduzi ya Zanzibar. MV Ibn Khaldun haikuwa Sultana iliotiya nanga New York Alkhamisi, tarehe 30 Aprili mwaka 1840 na iliyobeba ujumbe wa amani na biashara kutoka Zanzibar kwa Sultan Sayyid Said bin Sultan. Meli ya MV Ibn Khaldun ilikuwepo Dar es Salaam kwa siku nane, kuanziya tarehe 2 Januari 1964 na iliondoka tarehe 9 Januari 1964. Ilipowasili mara ya kwanza meli hiyo “ilikaa nje ya bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa masaa arubaini na nane. Kutokana na kuhojiwa kwa maofisa wa Kiafrika waliohusika na upakuwaji wa mizigo ya meli ilikuwa dhahiri baadhi ya mizigo iliondolewa na inawezekana sana kuwa baadhi yake iliondolewa kabla ya meli kufunga gati.”22 Rais Nyerere aliongozana na Bwana Djoudi aliyekuwa Charge d’Affaires katika Ubalozi wa Algeria Tanganyika katika kuikaguwa meli hiyo. Djoudi pia alikuwa mhusika wa mafunzo ya kijeshi wa Kamati ya Ukombozi wa nchi tisa za Kiafrika. Kijana mdogo mwenye umri wa miaka 24 aitwaye Racchid Ben­Yelles alikuwa Kepteni wa meli hiyo ya MV Ibn Khaldun. Kepteni Ben­Yelles alitowa maelezo kuwa meli hiyo ambayo alichukuwa dhamana ya kuiyendesha miezi mitatu nyuma ilikuwa kwa kawaida yake ikifanya kazi kwenye Bahari ya Mediterranean. Mzigo wa kawaida wa meli hiyo ulikuwa ni ulevi wa zabibu na meli hiyo ambayo ikimilikiwa na Serikali ilikuwa na matenki yenye uwezo wa kubeba tani 2,000. Meli ilipoondoka, Rais Nyerere aliwapungiya mkono kepteni na wafanyakazi wake na kuwaombeya safari njema. Wakati inaondoka meli hiyo ilikuwa imebeba shehena ya tani 80 za kahawa na tani 100 za mbao kutoka Tanganyika na ilielekeya Tanga kuongeza mizigo zaidi.23

Kwa mujibu wa ripoti ambayo haiyoneshi imetoka kwa nani na inakwenda kwa nani, Serikali ya Tanganyika iliwalipa Waalgeria “thamani ya pauni za Kiingereza 260,000 za kahawa na bidhaa nyengine.”24 Wapi pesa hizo zilitoka bado ni suala la michirizi yake kufuatiliwa. La muhimu ni kahawa na mbao yalikuwa ni malipo kwa ajili ya silaha zilizoletwa kutoka Algeria na meli ya Ibn Khaldun. Kwa amri ya Oscar Kambona, kazi ya upakuwaji wa mizigo ya silaha hizo alipewa Kepteni Nyerenda na aliamrishwa mzigo wote wa silaha auweke kunako ghala za P.W.D. (Public Works Department).25

Huo ulikuwa ni wakati wa uanzishaji wa harakati za ukombozi wa Msumbiji na baadaye kuanzishwa kambi za kuwapa mafunzo wapiganiya uhuru wa Msumbiji Tanganyika. Oscar Kambona aliwababaisha waandishi wa habari kwa kuwaambiya kuwa silaha kutoka Algeria zilikuwa kwa ajili ya Tanganyika

Page 42: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kwanza10

Rifles lakini Waingereza walipotaka taarifa zaidi kutoka kwake aliwajibu kuwa “…ni za Tanganyika Rifles isipokuwa maboxi yaliopigwa krosi nyeusi. Maboxi haya yanatakiwa yawekwe karibu na mlango wa ghala ili yaweze kuondolewa kwa haraka. Pia alisema kuwa maboxi hayo yasifunguliwe. Tuliyafunguwa baadhi yake…Zanzibar ilitokeya Jumapili iliyofuatiliya, tarehe 12 Januari na maboxi yale bado yalikuwepo kunako ghala. Baada ya hapo yakawa hayana umuhimu wowote.”26

Page 43: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa PiliMirengo ya Kizalendo na Mapinduzi

Mapinduzi yalikuwa, kwa kiasi fulani ni kisasi dhidi ya utumwa, yaliofanywa na watu na kufanyiwa watu ambao hawahusiki na utumwa. —Yasmin Alibhai-Brown

Fikra ya uzalendo ya Pan­Africanism ambayo ilikuwa ikiongozwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa kila asiye “Muafrika” ni mgeni Afrika na kwa hiyo asiyekuwa na asili yenye kutoka bara la Afrika basi ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu ndani ya nchi hiyo. Na aliyekuwa ana asili ya Kiafrika na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuitawala Zanzibar kwa sababu ni “Muafrika.” Neno “Afrika” linatokana na neno Ifriqiya, ambayo kihistoria ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo leo inajulikana kwa jina la Tunisia. Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociology) aliyeishi miaka 676 nyuma, anamtaja katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus b. Qays b. Sayfi, ambaye “aliishi wakati wa [Nabii] Musa au labda kidogo kabla yake” na kuwa wanahistoria wanajisemea kuwa ndie alieivamia “Ifriqiyah”.1 Ibn Khaldun hakuwa anashuku kuwepo kwa mfalme kutoka Yemen ambaye akijulikana kwa jina la “Afriqus” ambalo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina la “Afrika.” Wako wenye kusema neno “Afrika” linatokana na lugha ya kienyeji ya Afrika ya Kaskazini iitwayo “Berber.”2 Lini bara la Afrika lilianza kujulikana kwa jina la “Afrika” ni jambo liloanzishwa na wakoloni wa kizungu na ni suala linahohitajia kuthibitishwa kwa ushahidi wa kiutafiti. Fikra zilizozagaa ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa daraja nyingi. Fikra hii inatokana na fikra nyengine iliyokalishwa kwenye fikra za wengi yakuwa “Bara la Waafrika” ni Bara la watu weusi tu, na

Page 44: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili12

labda tuseme la Mungu Mweusi. Na watu weusi wenyewe ni wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu wenyewe wawe hawana asili au uhusiano wa karibu na Waarabu. Na mizizi ya “Waafrika ni Wabantu peke yao” inalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Afrika ya Kaskazani, Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea, Mauri­tius, wazungu wa Afrika Kusini, au Zimbabwe, Kenya, pamoja na Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya kibinaadamu ambayo yana chimbuko lao Afrika. Hapana shaka yoyote kuwa Afrika imedhulumiwa na Waafrika weusi bado hawajachukuwa dhamana ya kushiriki kwa machifu na makabila yaliyoshiriki kuwatia utumwani Waafrika wenzao. Haya yameelezwa kwa ufasaha ndani ya kitabu Zanzibar: Kinyang’ayiro na Utumwa na mwaka 2009 kimetoka kitabu muhimu chenye kichwa cha maneno It’s Our Turn to Eat (Sasa ni Zamu Yetu Kula) ambacho kinaelezea kwa undani namna ufisadi ulivyokumbatiana na ukabila nchini Kenya.3

Historia yote na kharita (ramani) zenye kulionyesha bara la Afrika kabla halikupewa jina la “Afrika” huonekana kuwa haina maana. Kwa hiyo kharita za miaka ya 1860 na za nyuma sana kabla ya hapo, zenye kuonyesha eneo la Afrika Mashariki kuwa likijulikana kama ni “Ethiopia” au mwambao wa “Azania” au “Sudan” au “Zinjibar” huonekana ni dalili tosha za ushahidi wa ubeberu kabla ya “Waafrika” kujitawala baada ya Wazungu kulipa bara lote jina la “Afrika.” Tawi la uafrika ni mtu mweusi lina mzizi mrefu katika kuyakana makabila mengine ya Kiafrika ambayo yaliwasili mwambao wa Afrika hata kabla ya kuwasili Wabantu Pwani ya Afrika ya Mashariki. Anaelezea Profesa Ibrahim Noor Shariff:

Kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa “Waafrika” wote ni “Wabantu” na kuwa kila asiyekuwa Mbantu ni mgeni Afrika Mashariki. Ukweli ni kuwa “Wabantu” ndio katika waliofika Afrika Mashariki, khasa sehemu za Pwani karibuni kabisa. Kwa mfano, “Wabantu” Wagiriama wamewasili “Giriama” Kenya kama miaka mia tatu iliyopita. (Soma kitabu cha chifu wao R. G. Ngala kiitwacho “Nchi na Desturi za Wagiriama.” E. A Literature Bureau. 1949. Ukurasa wa 2).4

`Mohamed Said ni msomi wa kwanza kabisa aliyeweza kuweka mkono wake juu ya mpigo wa moyo wa propaganda ya TANU kuhusu suala la Ubantu na wasio Wabantu, yaani, Waislamu. Kwa mujibu wa Mohamed Said:

Katika mwaka 1955, kikundi cha TANU Bantu kiliundwa makhsusi kukabiliana na tatizo la udini kutokana na hisia za baadhi ya Waislam ndani ya TANU. Tangu kuundwa kwa TANU, kulikuwa na hisia ya kupinga Ukristo ndani ya chama. Tatizo hili la udini lilikuwa likichemka pole pole na chini kwa chini ndani ya TANU. Ilikuwa kazi ya kikundi cha TANU Bantu kuwafichua na kuwapiga vita wana­chama wa TANU waliokuwa na hisia kama hizo. Bantu ilifanikiwa sana ka tika

Page 45: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 13

hili hadi kudiriki kupiga marufuku mamkuzi ya Waislam ya “Asalaam Alaikum” (Amani iwe juu yako) baina ya Waislam kwa msingi kuwa ilikuwa inawabagua Wakristo na hivyo inawatenga…Mamkuzi yale ya Kiislam yalionekana kama yanakwenda kinyume na imani ya TANU na ilishauriwa kuwa “salaam aleikum” ipigwe marufuku isitumike. Ikiwa mathalan kwa kusahau Muislam mmoja atatoa salaam kwa Muislam mwenzake, kwa kawaida angejibiwa “Alaikum salaam” maana yake “Amani iwe juu yako pia.” Badala ya majibu haya mazuri, majibu yaliyobuniwa na Bantu yalikuwa—“Ahlan tabu” maana yake—“ah tabu tu!”5

Lengo la Bantu Pan­Africanism si kuutumikiya uhakika wa historia au kuwapenda Waafrika na kuwachukiya Waarabu, bali ni kulipuuza suala zima la makabila, tamaduni, na staarabu na dini ya Kiisilamu zilizokuwepo Afrika ya Mashariki kabla ya kuwasili kwa Wabantu na khasa kwa Ukristo kutoka Ulaya. Mgeni mmoja kutoka Umoja wa Mataifa aliyekwenda kuitembeleya taasisi ya kihistoria ya kitaifa iliopo Dar es Salaam, alisikitishwa sana kuona historia ya Waarabu Tanzania imeshirikishwa na kitu kimoja tu: utumwa. Wanahistoria na wataalamu wa ilimu ya athari (archaeology) wanashindana na kuukiuka au kuuficha ukweli wowote ule wenye kuonyesha kuwa hakujakuwepo makabila yasiyo ya Kibantu Afrika ya Mashariki kabla ya kuwasili kwa Wabantu. Ile historia ndefu ya Bahari ya Hindi yenye kuiunganisha Afrika ya Mashariki na ya Kati na Bara Arabu, Uajemi, Bara Hindi, Uchina, Misri, n.k, huwa inaonekana haina maana kwa sababu haikidhi haja na hoja za kisiasa. Au kama itatambulikana itakuwa kujengea hoja kuwa ilikuwa historia ya kibeberu iliyokuwa na kituo chake Zanzibar. Marejeo ya historia ya Afrika ya Mashariki yaliyoandikwa na akina Ibn Battuta, au Muruj al-Dhahab wa Ma’adin al Jawhar cha Al­Masudi, au Kilwa Chronicles iliopo jumba la makumbusho la Uingereza, hayapitiwi na wasomi wengi wa Tanganyika waliojazwa na kujaa chuki dhidi ya makabila mengine yasiyo ya Kibantu ya Afrika ya Mashariki. Katika utangulizi wa kitabu chao Mapambano ya Ukombozi Zanzibar, B.F. Mrina na W.T. Matokke wa Chuo Kikuu cha Chama, Kivukoni, wanafafanuwa kuwa: “Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kujaribu kukusanya pamoja data kwa ajili ya kuweza kufundishia. Jitihada zilizofanywa zilikuwa na lengo la kupata maandishi ambayo yanaweza kutumiwa na walimu na wanafunzi katika Vyuo vya Chama Cha Mapinduzi.”6

Pia katika sifa iliyopewa kitabu na kampuni ya uchapaji, Tanzania Publishing House, ni hii propaganda bila ya kizoro ambayo nainukuu kwa urefu:

Historia ya Afrika ni hadithi ndefu ya mapambano ya wananchi wake dhidi ya ubeberu ili waishi katika ardhi yao kwa amani na ustawi. Visiwa vya Unguja na Pemba havikukwepa adha ya kuwa sehemu ya uwanja wa mapambano hayo na kwa vizazi vingi vimekuwamo katika harakati moja baada ya nyingine hadi Mapinduzi ya 1964 yaliyokatilia mbali minyonyoro ya ukoloni mkongwe na kuashiria maisha mapya.

Page 46: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili14

Mapambano ya Ukombozi Zanzibar ni kitabu cha kwanza kuchapishwa kinachofuatilia kwa undani safari ndefu ya wananchi wa Zanzibar kuelekea ukombozi tangu majilio ya kwanza ya wageni kwenye pwani ya Afrika Mashariki yapata miaka 2000 sasa….Ndugu Mrina na Ndugu Matokke wamefanya utafiti wa hali ya juu uliowawezesha kutalii sehemu nyingi za historia ya Zanzibar ambazo hazijaguswa na mwandishi mwingine yeyote. Matokeo yake ni kitabu cha lazima kwa wanafunzi wa historia na siasa katika ngazi zote.7

Bila ya kutowa ushahidi wa marejeo yoyote yale, Mrina na Matokke wanakiri kuwa “Pwani ya Afrika Mashariki ilikuwa imefikiwa na wageni kutoka sehemu za mashariki ya mbali yapata miaka 500 kabla ya kuzaliwa Kristo.”8 Katika safari yao ndefu ya “utafiti wa hali ya juu” Mrina na Matokke hawakutaka kujuwa nini kimeandikwa katika kitabu maarufu duniani The Periplus of the Erythrean Sea kilichoandikwa miaka 2000 iliyopita kuwepo kwenye pwani ya Afrika Mashariki kwa karne nyingi tawala za kifalme za Arabuni ya Kusini na kuwa Waarabu “walikuwa wameingiliana na kuowana na wenyeji na wakiifahamu pwani nzima na lugha zilizokuwa zikizungumzwa.”9

Mrina na Matokke hawakujali kuyapitia matokeo ya utafiti makini wa wanahistoria na mabingwa wa ilimu ya athari (archaeology) au hata Biblia yenye kumtaja Kush na watu wa kutoka ustaarabu wa Kikushi ambao wanaiunganisha Afrika Mashariki na Somalia, Ethiopia na Bara Arabu. Lakini hilo halikuwa lengo lao na ndio maana safari yao haikuwapeleka huko. Lengo lao lilikuwa kupiga siasa na kuziharibu akili za walimu na wanafunzi kutoka Zanzibar na Tanganyika.

Misafara ya masomo ya dhiki na dhuluma

Hadithi dhidi ya Waswahili na Waarabu ambazo hazitegemei aina yoyote ile ya ushahidi zimekithiri kama uyoga kunako vichwa na nyoyo zenye kuipa jina baya Dola ya Zanzibar ili ipatikane sababu ya kuiangusha au kuizuwia isije juu. Yako mambo mtu akisema hapohapo hutakiwa ushahidi na hoja mpaka msikilizaji aridhike na kuna mambo hayahitajii hata chembe moja ya ushahidi midamu makapi ya hoja yanaonekana. Kwa mfano, R. K. Mwanjisi kwenye kijitabu chake Abeid Amani Karume utakuta ameandika kuwa:

Kuna mambo mengi sana ambayo yalitendeka nchini Unguja na Pemba na ambayo hayana budi yathibitishwe kwa ushahidi kamili, na kuandikwa kwa makini. Kuna nyumba Unguja iitwayo “Mambo Msiige” ambayo baada ya kumalizika kujengwa wale Waafrika walioijenga waliuwawa wote ili wasiige maarifa ya ujenzi wa nyumba kama ile. Yasemekana pia kuwa wake za Waarabu siku hiyo wakifurahi huwaambia mabwana zao “mie sijapata kuona mtoto anavyokaa tumboni mwa mwanamke,

Page 47: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 15

nataka kuona hivi leo.” Basi bwana wa Kiarabu hutuma watumwa wake wamlete mama wa Kiafrika mja mzito na akapasuliwa tumbo kumwonyesha bibi mkubwa jinsi mtoto anavyokaa tumboni! Kisha maiti ya yule mjakazi wa Kiafrika ikatupwa shimoni! Yasemekana kuwa wakati huo Mwarabu akitaka kuhakikisha ikiwa gobori lake lina nguvu humwambia mmoja wa watumishi wake apande mnazi. Akiisha fika juu yule “Bwana” alifyatua gobori lake, kisha “Mtumwa” akalia “Yallah” akaanguka chini na kufa. Kiisha yule Mwarabu akaja na kuipiga teke ile maiti na kusema “Ama, hivi kafa huyu!” Inasemekana kuwa kuna Mwarabu mmoja alizaa mtoto na mtumwa wake Mwafrika. Jambo hili lilipojulikana yule Mwarabu akachukua kisu akamwua yule kijakazi wake na kumtumbukiza chooni!10

Hizo ni sumu kali ndani ya kijitabu ambacho lengo lake ni kuzielezeya habari za maisha ya Mzee Abeid Amani Karume kwa wasomaji ambao wanatakiwa wafahamu kuwa:

Unguja na Pemba imepita katika tanuri la moto wa utumwa, udanganyifu wa wafanya biashara na washika misahafu, utawala wa kigeni, ubaguzi wa rangi, utetezi, juhudi za uhuru, mapinduzi na ujamaa.11

Cha Mwanjisi ni kijitabu kidogo kilichotungwa kwa ajili ya wasomaji wa kawaida. Mambo yalizidi kuwa hatari wakati kasumba kama za Mwanjisi zilipoingizwa ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Zanzibar. Na hayo yalifanywa na Wazanzibari Waafrika Waislamu ambao walitekwa akili na hadithi za utumwa zisizokuwa na hata chembe moja ya uthibitisho. Angalau Mwanjisi alitahadharisha kuwa hadithi zake kuhusu ushenzi na mambo maovu kabisa ya Waarabu waliyowafanyiya Waafrika “hayana budi yathibitishwe kwa ushahidi kamili, na kuandikwa kwa makini.” Akina Luteni Kanali Musa Maisara Kheri, mkuu wa uandishi na muandikaji wa utangulizi, Maalim Ubwa Mamboya Ismail, Mwenyekiti wa halmshauri ya uandishi wa kitabu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania, 1964–1974, Zanzibar na ndugu zao wengine wa Kiislamu walioshiriki kwenye uandishi wa kitabu hicho, hawakuiyona haja wala madhara ya kuitumiya sumu ya hadithi zisizo na uthi­bitisho wowote midam sumu hiyo iliwapa uhai wenye utukufu wa kidunia. Mafunzo ya dini ya Kiislamu na ule msemo wa Imam Ali usemao “Utukufu hupatikana kwa kumtumikia Muumba na mwenye kuutafuta kwa viumbe hatoupata” haukuwa na maana yoyote kwao. Jambo la kupendeza lilikuwa kwamba mpaka mwaka 1974 kulikuwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Zanzibar. Zanzibar ikijilinda wenyewe. Mambo makubwa zaidi ni yale yenye kuwasononesha wale waliohusika katika kushiriki kuwauwa ndugu zao ambao leo wameshakuwa watu wazima na kesho kuna kukutana na Muumba wao. Kitabu hicho kiliandikwa chini ya uwenyekiti wa

Page 48: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili16

halmashauri ya uandishi wa kitabu chini ya uongozi wa Kanali Seif Bakari Omari, na Luteni Kanali Musa Maisara Kheri akiwa Mkuu wa Uandishi na muandikaji wa Utangulizi. Propaganda ya “misafara ya dhiki na dhuluma” inasema:

Vikosi vya jeshi la wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kazi yake ya siasa hufanya misafara kila mwaka mara mbili kwa kuvizuru vituo vyote ambamo wakiteswa Waafrika katika zama za utawala wa kifalme na vibaraka vyao ili kuelewa wanakotoka kwa makusudi ya kunyanyua juu nguvu za kimapigano na kuwa na chuki kwa matendo hayo waloyofanyiwa wafanyakazi na wakulima. Halmashauri ya siasa baada ya kukaa na kuzingatia ilitoa mpango maalumu kwa vikosi vyote kupita sehemu zote ambazo masalio ya baadhi ya vitu ambavyo Waafrika wakiteswa…Vituo hivyo ni:—

1. Mkunazini – U.M.C.A. 2. Tumekuja 3. Maruhubi 4. Kijichi 5. Dunga jumba la mawe

BEIT – El AJAB [Beit alajaib – jumba la maajabu]

Hapo Forodhani Unguja lipo jumba kubwa la ghorofa tatu lililojengwa na mflame Baraghashi katika mwaka wa 1883 na mpaka hivi leo lipo bado. Ujenzi wa jumba hili ulipoteza roho chungu nzima za Waafrika wasio na hatia. Ilikuwa ni desturi kwa mujibu wa itikadi za kiarabu—kuchinja kinyama kama mbuzi, au ngombe ili awe kinga kwa kila baya. Watawala wa kiarabu badala ya kuchinja vinyama wao waliwachinja Binadamu badala yake! Dhulma ilioje!!! Katika sehemu zote hizo zilizokwisha elezwa ndio sehemu muhimu kwa historia ya Waafrika walimoteswa na ndizo sehemu muhimu. Kwa hivi sasa zinazo pitiwa na wanajeshi na kufahamishwa hali ya tawala za kisultani na vibaraka vyao walivyo watesa kikatili Waafrika katika nchi hii. Ili kuwafanya wanajeshi wa kimapinduzi wawe na chuki kubwa mioyoni mwao kwa wapinga maendeleo ya kimapinduzi.12

Kuwatia chuki wasomaji na wanajeshi kwa kutoa mifano ya unyama wa Waarabu dhidi ya Waafrika ambayo imetumiwa na Mwanjisi hata baada ya kutanabahisha kuwa “hayana budi yathibitishwe kwa ushahidi kamili, na kuandikwa kwa makini” ni kushiriki katika uovu wa kimsingi ambao unaonekana katika mifano yote ya mauwaji ya halaiki ya viwiliwili na ya saikolojiya baada ya kuwanyima watuhumiwa haki yao ya kuishi na kuishi bila ya khofu au huzuni. Misafara ya dhiki na dhuluma ambayo tunayazungumziya hayana nguvu kwenye Zanzibar ya leo kama ilivyokuwa kwenye miaka iliyopita ingawa juhudi ya kuvipiga marufuku vitabu au vijitabu vyenye kuwatia sumu Waafrika dhidi ya Waarabu au Waarabu dhidi ya Waafrika bado haijafanyika kama inavyopasa kufanywa. Ipo haja kubwa ya kuandikwa vitabu na vijitabu vipya na vyombo vya habari kutoa ilimu yenye kusimama juu ya ushahidi wa hadithi za utumwa walioufanya Waarabu, Waafrika, Wazungu na Wahindi.

Page 49: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 17

Hii leo, hamira za fitina za kubuni na zisokuwa na ushahidi wowote za utumwa wa Waarabu na ukombozi ulioletwa na Ukristo kuwaokoa Waafrika zinaendeleya kuwalisha na kuwakogesha watalii wanaolizuru Kanisa la Anglikan Mkunazini Zanzibar. Kwa shilingi elfu 3,500 (au dola 3 za Kimarekani) watembezaji watalii hao ambao wengi wao si Wazanzibari, hutowa darasa kwa kila mtalii anayefika hapo kuwa Waarabu wameleta vitu viwili vibaya Afrika: Uislamu na Utumwa. Kilele cha darasa hufikiwa pale mtalii anapoongozwa na kuonyeshwa alama ya duara dogo jeupe la jiwe la marmar liliopo ndani ya kanisa ambalo linamahanisha alama mbele ya meza panapotolewa dhabihu au kafara (altar) na panaposemekana kuwa ndipo palipokuwa pamesimama mti wa Mkunazi ambao Waarabu wakiwafunga watumwa wa biashara yao na kuwapiga viboko. Kwa mujibu wa mwalimu wa watalii wa msafara wa dhiki na dhuluma, duara hilo jeupe limezungukwa na jiwe refu jengine la marmar lenye rangi nyekundu­nyekundu ambayo ni alama ya damu ya Waafrika iliyokuwa ikichururuzika kutoka na mipasuko ya viboko vya Waarabu (Waisilamu). Kinachosafirishwa kwenye akili ya mtalii ni namna gani wafuasi wa Nabii Issa (sala na salamu za Mwenye Enzi Mungu zimfikie) wamekuja kusimama kunako alama iliyokuja kuwakombowa Waafrika kutokana na biashara ya utumwa wa Waarabu (Waislamu) na kuupa kasi ufalme wa Yesu Afrika. Watu wenye akili za kibiashara wametambuwa kuwa fitina za utumwa zinaweza kufanyiwa biashara juu ya migongo ya Waarabu na Waislamu na pengine hata bila ya kutambuwa kuwa kunajenga mazingira mapya ya chuki dhidi ya Waislamu wa Zanzibar na wa Tanganyika. Mkutano wa kimataifa ambao umeandaliwa na taasisi ya African Diaspora Heritage Trail ya Marekani, ulitangaziwa kufanyika Dar es Salaam na Zanzibar baina ya tarehe 25–30 Oktoba mwaka 2009. Anwani iliyotumiliwa kuutangaza mkutano huo ilikuwa ni “Utumwa wa Waarabu Afrika Mashariki” na sambamba na mkutano huo ni zinduo la “Msafara wa Pembe za Ndovu na Utumwa” ambao utaihusisha miji kadhaa na mwahala munamohusika na utumwa na ubakaji wa Waafrika weusi milioni tano! Upande mmoja mkutano huo umejihalalisha kwa kushirikiana na Mradi wa Biashara ya Utumwa (Slave Trade Project) wa shirika la Umoja wa Mataifa (UN) UNESCO. Mradi huo una kitengo cha utumwa katika nchi za Kiarabu na za Kiislamu. Kwa upande mwengine, madhumuni khasa ya mkutano huo ni kukuza biashara ya utalii kwa kuihusisha na urathi au turathi ya utumwa. Mashirika ya utalii na usafiri yameangaza na yamegunduwa kuwa kuna mijipesa inasubiri kuokotwa kwenye njia ya misafara ya dhiki na dhuluma. Walichokisahau ambacho hakimo kwenye hisabu yao ni umuhimu wa kuweka misingi ya maadili (ethics) kwenye kulifanyiya biashara suala kama hili ambalo limeamuwa kwenye anwani ya mkutano kuwabebesha Waarabu na watalii mizigo ya hadithi za utumwa ambazo hazina uthibitisho wala mashiko ya kitaaluma. Mkutano uliwalenga Waarabu dhidi ya Waafrika milioni tano na si kuhusu

Page 50: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili18

utumwa wa Afrika Mashariki au wa Bahari ya Hindi ambao utawahusisha baadhi ya Waarabu, baadhi ya makabila ya Kiafrika, Wazungu na Wahindi. Walitokeya wapi hao Waafrika milioni tano na walimalizikiya wapi na walinunuliwa na kupelekwa na nani na ndani ya vyombo vya nani si suala ambalo limo katika matangazo ya mkutano huo. Wako wanaoamini kuwa mkutano kama huo ni wa kupuuzwa kwa sababu wenye kuuandaa si watu wazito sana duniani. Wanachokoseya ni kuwa mambo ya biashara za kipropaganda hayahitaji wataalamu au utaalamu mkubwa. Mikutano kama hii ndiyo yenye kuivumbika sumu ya chuki dhidi ya kikundi fulani cha watu ambayo mwisho wake hugeuka kuwa ni biashara mbovu kwa alotaka kufanya pesa na zaidi juu ya waliolengwa kufitinishwa, kuuliwa, na kufanyiwa faida juu ya migongo ya mauti yao.13

Mrengo wa Umoja wa Kiafrika—Pan-Africanism

Kwa Zanzibar, siasa ya Pan-Africanism au Pan-Arabism ni mfano wa globu za taa ambazo hazina budi kuzimika kwa sababu ni taa za siasa zenye kuumurika upande mmoja wa jamii na kuuwacha upande wa pili ndani ya giza. Zanzibar ni jamii ya mchanganyiko kwa hiyo mirengo ya kisiasa yenye kuiwacha nje nusu ya jamii na matokeo yake ni kuraruka kwa jamii ambayo ilitakiwa kwa pamoja ilikamate guo la kuwapamba na kuwasitiri. Siasa ya Pan-Arabism na Uislamu inakuja kuikusanya nusu ya pili ya jamii ya Zanzibar ambayo iliongozwa na chama cha “Hizbu” (Zanzibar Nationalist Party, ZNP) ambalo ni neno la Kiarabu lenye maana ya “chama” kwa Kiswahili. Mchango wa Chama Cha Wafanyakazi cha Tanganyika, Tanganyika Federation of Labour (TFL), ni sehemu muhimu ya historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndiyo chombo kikuu kilichoendesha Mapinduzi kutoka Tanganyika kwa kushirikiyana na TANU na wafuasi wa Chama cha Wafanyakazi cha Afro­Shirazi (Zanzibar and Pemba Federation of Labour (ZPFL)). Pan­Africanism kama alivyoichambuwa Dkt. Saleh Al­Miskry katika tasnifu yake ya shahada ya udaktari wa falsafa Pan-Africanism and Nyerere in Tanzania ni harakati yenye kuungwa mkono na kikundi cha watu na si na nguvu za umma. Sababu kubwa anayoitowa Al­Miskry ni ule ukaribu uliopo baina ya thakafa, dini, na mila baina ya viongozi wa Pan­Africanism na thakafa, dini, na mila za Ulaya. Anaendelea Al­Miskry, “…pan­Africanists na mabeberu kutoka Ulaya walifanya kazi kwa pamoja wakati wa ukombozi dhidi ya ukoloni.”14

Hoja ya kibaguzi iliyotumika ni kuwa Waarabu kutoka kokote kule ni wageni Zanzibar na Mwambao wa Afrika Mashariki. Na si Waarabu peke yao, bali hata Washirazi pia. Ubaguzi huu unaonekana waziwazi katika barua ya Jumuiya ya Waafrika /African Association ya 1949 waliyomuwandikia Balozi wa Kiingereza Zanzibar na kwa Waziri wa Makoloni wa Uingereza isemayo:

Page 51: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 19

Tunasikitika sana kuona kwamba Serikali imemteuwa Mshirazi, Mwasia kwa ajili ya kumtumiliya, badala ya Waafrika wa Zanzibar. Inaeleweka wazi kwamba Mshirazi ni Mwasia katika rekodi za Serikali ya Zanzibar. Tunaelewa kwamba tunanyimwa haki zetu za uraia na hii imewabakiza Waafrika katika hali ya kukata tamaa. Kwa jina la Demokrasi, Ukristo, na usawa wa Binadamu, tunapinga vikali hatua ya Serikali na tunaomba ufikirie na kutizama upya mwenendo huu wa ubaguzi, ukandamizaji, kunyimwa haki na kunyanyaswa katika nchi yetu.15

Hii ni ajabu kubwa sana kuwa Wakristo, wageni kutoka bara ndiyo wenye kudai haki kwa fujo kwa kumpinga mwenyeji Mshirazi na Muislamu mwenye mizizi Zanzibar kwa kutumia garasa la “Uafrika”! Tatizo kubwa la Zanzibar ni mavuno ya mti wa udanganyifu na wa mrengo maalum wa kisiasa wenye kuongozwa na kikundi kidogo chenye kuiamini itikadi maalumu ya uzalendo wa Kiafrika (Pan­Africanism) ambayo inasisitiza kuwa Waarabu/Washirazi/Waswahili/Waislamu chini ya Jangwa la Sahara ni wageni na kuwa Zanzibar ni mlango mkongwe uliyouingiza ubeberu Afrika Mashariki na Kati na Ukristo ndiyo muokozi wake. Kwa nchi kama Zanzibar ambayo ina mchanganyiko mkubwa wa watu wa kila asili, fikra ya umoja wa watu weusi peke yao ni fitina iliyovaa guo la udugu wa kibaguzi dhidi ya Waafrika wa makabila mengine. Fikra ya mrengo huu iko kinyume na ilimu ya asili ya binaadamu ambayo inatuonyesha wazi kuwa binaadamu wote wametoka Afrika kwenda majuu katika nyakati tafauti. Dalili ni kuna watu ambao wamelelewa na fitina maalum na ambao wamewatiya chuki za kidini na za kikabila wenziwao bila ya hata kuona kama iko haja ya kuupima ushahidi wa ukweli au uongo unaotapakazwa au kutafuta juhudi za kuuondowa kwa faida ya makabila na dini nyenginezo. Kwa mujibu wa falsafa hiyo ya mrengo huo wenye kuweza kutafakhari kuwa “Afrika Kwetu” au “Tupendane Waafrika” ni wale Waafrika wenye asili ya kibara tu peke yao na wakati huohuo kuuficha ukweli kuwa hayati Mwalimu Nyerere asingeliweza kuwa kiongozi wa Tanganyika African Association (TAA), na baadaye wa Tanganyika African National Union (TANU) bila ya kwanza kuungwa mkono na wazee mashuhuri wa Dar es Salaam, wakiwemo wenye asili na makabila tafauti, yakiwemo ndani yake makabila ya Kibantu wenye kuifuata dini ya Kiislamu. Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi wa Kiafrika mwenye sifa kubwa duniani na kupendwa sana Tanganyika. Mwalimu alijaaliwa kufanya kazi moja kubwa katika maisha yake, nayo ni kuupiganiya na kuupata uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Muingereza. Na katika hilo aliwasahau majasiri wa Kiislam ambao ndio chimbuko la harakati za kupiganiya uhuru Tanganyika na waliyoianzisha TANU hata kabla ya yeye kukaribishwa Dar es Salaam na wazee wanaharakati wa uhuru wa Tanganyika. Waislamu ndio waliokuwa wakiumizwa zaidi na ukoloni kuliko kundi au kikundi chengine chochote kile cha kidini Tanganyika.

Page 52: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili20

Waislamu wa Tanganyika walijipinduwa na wakapinduliwa kwa mapinduzi baridi ya mwaka 1954 baada ya kwa makusudi kumuachiya kwa makusudi, Mwalimu Nyerere achaguliwe kuwa kiongozi wa TANU.16

Miaka kumi baada ya hapo, 1964, ikawa zamu ya kupinduliwa Zanzibar kwa mapinduzi ya kumwaga damu. Ndipo ilipoandikwa makala mwezi wa Juni 1964 katika jarida maarufu la The Economist yenye kichwa cha maneno “Mashaka ya Nyerere” kuwa Mwalimu Nyerere “ameweza kuifanya nusu ya kazi ya chatu. Ameimeza Zanzibar sawa, lakini hakuziuwa nguvu zake za kujiteteya kwanza. Mnyama ambaye yungali hai anaendeleya kukila chakula chake, na mateke yake yanaendeleya kumuumiza [chatu] kwa maumivu makubwa, na pengine hata kuyahatarisha maisha yake, ndani huko kunako mwili wa kisiasa wa Tanganyika.”17

Katika hotuba yake muhimu kuliko zote aliyoitowa kwenye hoteli ya Kilimanjaro siku ya Jumaane, tarehe 15 Machi 1995, Mwalimu alianza kwa kuuzungumzia ufa mkubwa uliyoipasuwa nyumba ya Tanzania ni ufa mkubwa wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Mwalimu alitabiri kuwa ama mtikisiko utakwisha na nyumba ya Tanzania itakuwa imara, au utaendeleya na nyumba itabomoka hata ikiwa imara. Alisema lengo liwe mtikisiko usiendelee. Katika kuhamasika na kipaji cha kuzungumza alichojaaliwa Mwalimu Nyerere, kuna Mchungaji ameandika kunako blogi moja: “Hakika alikuwa nabii, zile nyufa alizoona ziliendelea na sasa naona zimekuwa mianya mikubwa kwenye kuta. Kama hatutaangalia, nyumba yetu itabomoka na kuanguka…” Mwalimu kweli alikuwa “nabii” kwa maana aliweza kuzitabiri nyufa na mianya mikubwa inayoukabili Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ufa mkubwa kati ya nyufa zote alizozizungumzia Mwalimu ni ufa wa muungano ambao aliongeza kwa kusema kuwa uko katika “hatari ya kuvunjika [na] wala haijesha.” Mwalimu pia alisema “ningependa mjadala wa sasa” uwe kuhusu kueleweka nyufa ziliopo na “tupate uongozi unaoelewa hivyo.” Ombi la Mwalimu haliku­jibiwa ipasavyo na wenye kutaka kuinusuru nyumba ya Tanzania kubomoka ingawa ndani na nje ya nchi tayari wapo watu na mataifa yenye kuanza kukubali kuwa pengine hilo ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Bahati mbaya Mwalimu alitaka mjadala uendelee bila ya kutoa sababu za chanzo au mzizi wa mtikisiko. Hilo asingeliweza kulifanya kwa sababu lilikuwa ni gumu sana kwake, maana kama angelizieleza sababu halisi za mtikisiko basi zingelimuondolea sifa ya kuwa kiongozi pekee katika bara la Afrika ambaye aliweza kuziunganisha kwa hiari nchi mbili huru za Kiafrika. Tukirudi nyuma kwenye mizizi ya mitikisiko, na kwa mujibu wa ripoti ya mazungumzo ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Sir N. Pritchard yaliyofanyika Dar es Salaam tarehe 27 Februari 1963, Mwalimu Nyerere alisema:

Page 53: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 21

Peke yao Wazanzibari hawatojaribu kufanya kitu dhidi ya Tanganyika lakini wanaweza wakawaleta marafiki ambao wataweza kuwafanya wawe wakorofi. Zanzibar ilikuwa ni kituo cha kwanza cha ubeberu Afrika Mashariki. Uingereza ilichukuwa jukumu la kuulinda utawala huu [wa Zanzibar] na mantiki inasema kuwa baada ya Uingereza kuondolewa Tanganyika, Waafrika wa Zanzibar huenda wakauondowa utawala wa Kisultani.18

Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 27 Februari 1963 chini ya mwaka mmoja kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nia ya Mwalimu Nyerere ya kuipinduwa Zan zi­bar ilikuwa imeshadhihirika kabla ya hapo lakini hilo lilikuwa kama tamko rasmi kwa Waingereza ambao hawakuonyesha kushituka au kukerwa na kauli hiyo. Jambo ambalo tutakuja kulieleza baadae kuwa ingawa Muingereza alichukuwa jukumu la kuilinda Zanzibar kabla ya uhuru alikataa kuilinda Zanzibar iliyopata uhuru na alipendekeza imezwe na Tanganyika ili awakomowe Wazanzibari wali oupiganiya uhuru wao kwa kuungana na harakati za kikombozi dhidi ya Waingereza katika bara la Afrika.19

Upotoshaji mwengine mkubwa wa kihistoria ni kuwafanya watu waamini kuwa Waingereza, chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP), na Sultan Jamshid walikuwa kitu kimoja na walipinduliwa pamoja tarehe 12 Januari 1964. Msomaji anafaa pia akagutuka tena juu ya utumiaji wa neno “Muafrika” au “raia” na kadhalika, na ujasiri wa kujipa haki wageni katika nchi ya Zanzibar isiyokuwa yao na utumiaji wa neno “Muafrika” kuhalalisha haki za wageni Zan­zibar na kuwaharimisha wenyeji. Utumiaji wa neno “Mwafrika” ni kiini hai ndani ya simulizi nyingi za wazee ambazo utakuja kuzisoma huko mbele kuwa Mapin­duzi ya Zanzibar hayakuwashirikisha wenyeji wa Zanzibar ambao si “Waafrika wa Zanzibar” kwa matumizi ya Mwalimu Nyerere ingawa katika hotuba ya Mwalimu ya 1995 aliweka wazi kuwa “hatuwezi kuwahishimu makaburu hapa [Tanzania] kwa sababu ni weusi tu.” Zaidi ya nusu ya jamii ya Zanzibar iliyokuja kuvipigiya kura vyama va Zanzibar Nationalist Party na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZNP na ZPPP) na kushinda kwa asilimia 46 ya kura na wingi wa viti 18 kati ya 31 katika uchaguzi wa Zanzibar wa Julai 1963 hawakuwa “Waafrika wa Zanzibar” kwa maana walikuwa ni Wazanzibari wa mchanganyiko wa damu na thakafa za Kiafrika na za Kiarabu na kwa mantiki hiyo haikutosha tu “Waafrika wa Zanzibar huenda wakauondowa utawala wa Kisultani” bali kuwauwa wale waliyoonekana kuwa si “Waafrika wa Zanzibar” yaani, Waarabu, Washirazi, nk. Mazungumzo ya Mwalimu Nyerere na Sir Pritchard yalikuwa tarehe 27 Februari 1963 na Mapinduzi yalifanyika tarehe 12 Januari 1964, yaani miezi sita kabla ya uchaguzi wa Zanzibar wa Julai 1963 na takriban mwaka mmoja kabla ya mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964. Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad anaelezeya kunako kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake:

Page 54: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili22

Julius Nyerere, Rais wa Tanganyika, ana sehemu ya lawama kwa mapinduzi ya Zanzibar. Aliamini kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika na alianza kuyaingilia mambo ya Zanzibar mapema kuanzia katika miaka ya 1950…Mpaka sasa hivi, hadithi iliopo ni kuwa watu wa Zanzibar ndio walioyapanga mapinduzi, lakini kuna ushahidi kuwa Tanganyika ilihusika tena sana. Wengine wanaamini kuwa askari kutoka Tanganyika ndio waliyoyaongoza mapinduzi. Kwa kutumia ujanja, Watanganyika waliyagubika mavamizi kwa kuyafanya yaonekane ni mapinduzi, na ndio mwanzo wa matatizo ya Zanzibar kama ni dola. Hisia yangu ni Nyerere alikuwa ndio kichwa nyuma ya mapinduzi. Ni vigumu kuziamini hadithi zenye kusema kuwa mwanzoni wanamapinduzi waliipinduwa serikali kwa mapanga tu; silaha walizozitumia zilitoka bara. Nyerere anabeba lawama pamoja na wanasiasa wa Kizanzibari kutoka pande zote mbili…Wanasiasa wetu wenyewe walimpa Nyerere fursa kuyaingilia mambo ya Zanzibar.20

Hisia za Maalim Seif zinalingana na matokeo ya utafiti na ushahidi kutoka kwa wazee wa ASP, TANU na CCM, kutoka Zanzibar na Tanganyika, waliohojiwa na mwandishi huyu na wenye kuufahamu uhakika wa mapinduzi ya Zanzibar. Hii ni dalili tosha kuwa uongozi na viongozi wa Kizanzibari na wa Kitanganyika ni kitu kimoja katika muelekeo na ufahamu wao wa kitendawili cha jinamizi lenye kuurusha usingizi Zanzibar kwa miaka arubaini na sita. Tafauti kubwa iko baina ya hisiya za Maalim Seif na “ushahidi” kutoka wazee wa ASP, TANU na CCM. Kuanziya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar; kudanganywa kwa marehemu Mzee Abeid Amani Karume na kutopewa fursa ya kushauriana na Wazanzibari wenzake kuhusu Hati za muungano; kujiuzulu kwa Mzee Aboud Jumbe; kuundwa kwa katiba ya CCM na kutiwa mnofu wa kisheria na Ilangwa Shahidi bila ya kuwashirikisha Wazanzibari; kufitinishwa marehemu Mzee Idris Abdulwakil na Maalim Seif Sharif Hamad; uingiaji madarakani wa Mzee Ali Hassan Mwinyi na kuondolewa kwa Idara ya Usalama ya Zanzibar wakati wa Urais wake; kuakhirishwa kwa Zanzibar kujiunga na OIC wakati wa uraisi wa Mwinyi na Dk Salmin Amour Juma; kugonganishwa Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kupitiya vyama vya siasa ambavyo vimewekewa sheria za kutoweza kuihoji mihimili ya Dola—Mapinduzi na Muungano; kuzama kwa mkono wa Bara ndani ya mambo ya Zanzibar halafu waowao kuombwa na baadhi ya viongozi wa Zanzibar wawe wasuluhishaji; mpaka kufikia Uraisi wa Dkt. Amani Abeid Karume na utetezi wa kuirudishiya Zanzibar haki zake za kinchi; ni mtiririko wa matokeo ya uvamizi wa Zanzibar ambao kwa mujibu wa maadili ya Nuremberg “ni kikomo cha jinai ya kimataifa kwa sababu unakusanya maovu yote yanayofuatiya.” Zanzibar ya leo imeshaelekeya kuwa kitu kimoja na ni hikma na uwezo wa Mwenye Enzi Mungu ndio uliowafanya wazee wa Mapinduzi wazungumze na kuielekeza Zanzibar izungumze kwa sauti moja ndipo mtikisiko aliokuwa akiukhofiya Mwalimu Nyerere utakaposita na umoja wa Waafrika wenye asili na dini mbali mbali ndipo utakapoimarika na neema ya utajiri wa bara la Afrika

Page 55: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 23

kuwafikiya watu wake. Kila wakati wa binaadamu unakwenda kwa dhamira yake na wakati tulionao ni wa kujikombowa kutokana na upotoshaji wa ukweli wa historia ya Zanzibar baada ya kuvifahamu vyanzo nyake.

Mapinduzi Ndani na Nje ya Afro-Shirazi Party

Sheria mbili kati ya saba za chama cha Afro­Shirazi zinasema:

1. Kutafuta uhuru na utawala kamili utaokuwa miongoni mwa Dola zilizomo katika Shirikisho la Udugu na Dola ya Kiingereza… 2. Kuifanya na kuiamirisha Serikali ya Kidimokrasi katika visiwa vya Unguja na Pemba chini ya utawala na utii kwa Bwana Seyyid Mtukufu.21

Maneno yenye kuongoza kunako sheria mbili za chama cha Afro­Shirazi ni maneno “Shirikisho” na “utii kwa Bwana Seyyid Mtukufu.” Hizo zilikuwa ni sheria rasmi za chama cha ASP ambazo zilikubaliwa na viongozi wake na kukubalika kwa mujibu wa sheria za wakati ule. Msomaji anatakiwa awe makini kabisa na hata kabla hajaendeleya kusoma inampasa afahamu kuwa viongozi wakubwa wa chama cha Afro­Shirazi, kama marehemu Mzee Abeid Amani Karume, na marehemu Mzee Thabit Kombo Jecha, au Sheikh Aboud Jumbe, hawakushiriki katika mipango halisi ya mapinduzi ya Zanzibar. Amekiri Mzee Jumbe katika kitabu chake The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union: 30 Turbulent Years pale alipoandika kwenye kurasa 9–10 kuwa “ijapokuwa nilikuwa Katibu wa Mipango wa chama cha Afro­Shirazi, sikujuwa vizuri [kuhusu Mapinduzi] asubuhi ya tarehe 12 Januari 1964. Ilikuwa ni siri iliyohifadhiwa vizuri ambayo ilifahamika na uongozi wake [Karume] tu. Mpaka hii leo hadithi kamili imefungwa ndani ya nyoyo na kumbukumbu zao.”22 Mzee Jumbe amemuingiza marehemu Mzee Karume katika uongozi wa mapinduzi bila ya kutowa dalili au ufafanuzi wa aina yoyote. Marehemu Mzee Thabit Kombo ambaye alikuwa chini ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume pia ndani ya kitabu Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha kilichoandikwa na Minael­Hosanna O. Mdundo na chenye Utangulizi aliouandika Mwalimu J.K. Nyerere, amekiri kwa maneno yafuatayo:

Usiniulize vijana wetu walioendesha mapinduzi walipata wapi mafunzo, au nani hasa alivamia mahali gani; mimi sijui. Nasikia hadithi tu kila mmoja akijinasibu baada ya kushinda, mengi ya kweli na mengine ya uwongo mtupu.23

Mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wowote, mbali ya ule wa kinaga ubaga ambao unaweza kuthibitisha kuwa marehemu Mzee Abeid Amani Karume alikuwa jemedari wa Mapinduzi ya Zanzibar kama ilivyofanywa iaminike na kusadikiwa na wengi. Mara utasikia jemedari alikuwa Mzee Karume, na mara nyingine utasikia jemedari mkuu alikuwa ni “Field Marshall” John Okello. Mara

Page 56: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili24

nyingine utasikia mpishi mkuu alikuwa marehemu Abdulrahman Mohammed Babu na nadhariya iliozamishwa ndani ya bongo za kila Mzanzibari na asiyekuwa Mzanzibari ni Mapinduzi yaliongozwa na Kamati ya Watu 14 au 13 + 1. Hili ni jambo muhimu kuweza kuufahamu undani wake kwa sababu hapa ndipo kwenye kizungumkuti cha Mapinduzi ya Zanzibar. Hapa ndipo penye guo zito ambalo linatakiwa angalau ligeuzwe liwe chandarua. Kuanguka kwa Kamati ya Watu 14 kwenye chati ya Mapinduzi ya Zanzibar ni njia pekee ya kulivuwa guo la khadaa na kuirudishiya jamii nzima ya Kizanzibari na ya Kitanganyika nuru ya kufahamu inakotoka na kujipangiya inakotaka kwenda na kufika. Suala ni jee, Kamati ya Watu 14 walikuwa ndio viongozi wa mapinduzi ya Zanzibar au walikuwa ni walinzi wa kulilinda paziya la uongozi khasa wa mapinduzi? Kati ya memba wa Kamati ya Watu 14 waliokuwa hai na wenye siha ya kuzungumza ni wazee Hamid Ameir na Abdalla Saidi Natepe. Katika mahojiano ambayo alifanyiwa Mzee Hamid Ameir katika gazeti la Mwananchi la tarehe 11 Januari 2008, mwandishi Salma Said alimuuliza “ni kwa nini wewe uko kimya kiasi hicho na hadi vizazi vya sasa haviutambui mchango wako?” Alijibu Mzee Hamid Ameir, memba wa Kamati ya Watu 14 kwa kusema:

Mimi sipendi kujitokeza kwa sababu kuna vitabu vingi sana tayari vimeshaandikwa kuhusu historia ya Sultani na kufanyika kwa Mapinduzi lakini cha muhimu zaidi ni kuwa unapojitokeza na kuzungumza wanatokea watu wanajibu hoja ulizozungumza na kuweka listi kubwa ya watu waliofanya Mapinduzi, nami kwa kuwa sipendi mabishano na kwa kuwa nafahamu kwamba kuna mtu siku moja ataandika historia ya kweli, hivyo mimi nimeamua kukaa kimyaa.24

Tarehe 8 Septemba 2002, alizungumza marehemu Mzee Khamis Daruweshi, memba mwengine wa Kamati ya Watu 14, na gazeti la Johari ya Mwananchi katika habari yenye kichwa cha maneno “Hamis Daruweshi afichua siri ya Mapinduzi Zanzibar”. Katika sababu alizozitowa Mzee Daruweshi za kufanyika mapinduzi Zanzibar ni kuwa watu wa Zanzibar “walikuwa hawataki kujinasibu kama Waafrika. Hawapendi kuunga mkono Waafrika na walikuwa wakiwaita wakata maji.” Daruweshi pia alielezea kuwa:

Huyu Okello alikuwa miongoni mwa Afro Shirazi [Youth] League. Tulimchukua Pemba alikokuwa akichonga mawe ili kutoa matufali. Tulimchukua kwa kazi maalum kwa sababu baada ya mapinduzi, tulijua tulihitaji mtu ambaye atatangaza mapinduzi hayo kwa lafudhi ambayo ni tofauti kabisa na ya wenyeji wa Zanzibar.25

Mzee Daruweshi alijifahamisha kuwa:

Mimi ni Myao, mtu wa Ruvuma, Tunduru, kijiji cha Masuguru, kata ya Malumba. Lakini hapa Zanzibar nimekuja zamani kidogo tangu mwaka 1941, niko hapa

Page 57: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 25

‘nimenationalize’ uraia wa Zanzibar. Nilipiga kura katika uchaguzi wa mwaka 1957. Lakini uchaguzi wa pili ikaja pingamizi kwamba wote waliozaliwa Bara ha wa tapiga kura. Ukijipanga kwenye mstari, wanakuja wakikuuliza, katika mstari walikuwapo mawakala wa Hizbu na wa ASP. Unaulizwa utamke ‘halua’, wengine hawawezi wanasema ‘haarua’ kwa hiyo wanakutimua kwenye mstari kwa kuwa wanajua kwamba wewe siyo Mzanzibari na kwa hiyo tuliotoka Bara wengi tukashindwa kupiga kura. Kwa hiyo nikaomba uraia wa Zanzibar Aprili 19 mwaka 1960 na kupewa kadi nambari 2020.26

La msingi katika mazungumzo ya Daruweshi ni kule kuelezea kwake bila ya kuweka ushahidi au vielelezo vyovyote vile kuwa: “Labda ni vyema ikajulikana tangu mwanzo kwamba kamati iliyoundwa na Karume ya kuongoza mapinduzi hayo, ilikuwa na jumla ya watu 14.”27

Walipotembeleya Cuba katika mwezi wa Mei 1964, Shirika la Habari la Cuba liliwafanyiya mahojiano memba wawili wa Kamati ya watu 14, Ramadhani Haji na Saidi Idi Bavuai yenye kutowa mwangaza mzuri juu ya maandalizi ya Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya kutowa historia fupi ya Afro­Shirazi kutokeya mwaka 1957 walielezeya matukio yaliofikiya kupinduliwa kwa Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah:

Uchaguzi ulipofanyika mwaka 1963 chini ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza, chama cha Afro­Shirazi kilishindwa na kiliunda kamati ya kufanya mapinduzi. Baada ya uchaguzi kikundi kidogo cha chama cha Afro­Shirazi kiliungana na Chama cha Kizalendo (Nationalist Party). Haya mapinduzi ya watu 14 hayakuungana wakati wowote ule na chama chochote chengine kikiwemo chama cha Afro­Shirazi…hata chama cha Afro­Shirazi chenyewe kilikuwa hakielewi kinachoendelea.28

Inaendelea ripoti ya Kiingereza juu ya ziara ya Bavuai na Haji:

Mchango wa kimapinduzi wa John Okello ulidharauliwa na Iddi na Haji na walisema kuwa mashirika ya habari yalikosea kumhusisha yeye kama ni kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar…Waliwaeleza Rais Karume na Waziri wa Mambo ya Nje Babu kuwa ni watu ambao hawakushiriki moja kwa moja katika harakati za mapinduzi, lakini hata hivyo, wanastahiki vyeo walivyokuwa navyo. Inavyoonyesha, memba hao wawili wa Baraza la Mawaziri walishtukiwa na muungano wa Zanzibar na Tanganyika, na waliona haya kutamka chochote kuhusu maendeleo hayo huku wakieleza kuwa [muungano] umefanyika wakati wao wako nje ya Zanzibar.29

Mara nyingi imekuwa ikisikika kuwa Mzee Abdalla Saidi Natepe ameandika kitabu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar lakini hakitotolewa mpaka kufariki kwake. Hapa panaonekana kuna dalili kuwa mwanamapinduzi Mzee Natepe amekosa ushujaa wa kuandika kuhusu mapinduzi ya Zanzibar katika uhai wake na kuweza kuingiya katika midani ya mazungumzo wakati yungali hai.

Page 58: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili26

Fikra iliyozoweleka na kushindiliwa ndani ya bongo za Wazanzibari na wasiokuwa Wazanzibari ni kuwa Kamati ya watu 14 ndiyo kamati iliyokabidhiwa kazi ya kuyapanga mipango ya mapinduzi na Mzee Karume. Hapana shaka memba wa kamati hiyo walihusika na mapinduzi na kama alivyosema marehemu Mzee Thabit Kombo “Usiniulize vijana wetu walioendesha mapinduzi walipata wapi mafunzo, au nani hasa alivamia mahali gani; mimi sijui. Nasikia hadithi tu kila mmoja akijinasibu baada ya kushinda, mengi ya kweli na mengine ya uwongo mtupu.”30

Sasa inawezekana kuwa Mzee Karume alikuwa jemedari wa Mapinduzi na msaidizi wake Mzee Thabit Kombo asiwajuwe vijana wa mapinduzi na awe amesikia hadithi tu. Lakini hili la “uwongo mtupu” ndilo linalofaa kutushughu­lisha. Ni uwongo gani huo wenye kuupotosha ukweli wa Mapinduzi ya Zanzibar? Uwezekano unaoingiya akilini na msomaji akawa ana uhuru wa kupima baada ya kumaliza kukisoma kitabu ni mambo mawili. La kwanza ni kuna utata wa idadi na majina ya memba wa hiyo Kamati ya Watu 14. Pili, na muhimu zaidi, inamkinika sana kuwa Kamati ya watu 14 iliundwa na kukwezwa baada ya Mapinduzi kwa lengo la kuufunika ukweli wa chimbuko la Mapinduzi yenyewe. Tukirudi kunako kitabu maarufu na muhimu cha Mzee Aboud Jumbe The Partner-ship utakuta anwani yenye kusema “siasa za Zanzibar kabla ya muungano.” Mzee Jumbe anaelezeya kuwa:

Hata kabla ya Mapinduzi, Uongozi wa Siasa [wa ASP] ulikuwa haujaungana sawasawa. Kulikuwa na mvutano wenye kukuwa, kati ya wale, nikiwemo mimi mwenyewe, tuliomuunga mkono Karume, na baadae tukapewa jina la “Karume­Yeka”; na wale waliokuwa wakimpinga; na waliobakia waliojaribu kuyakubali makundi yote mawili. Mpasuko huu nusura ukivunje chama mwaka 1961 kwenye mkutano mkuu wa chama uliofanyika Municipal Hall, Mji Mkongwe.31

Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu The Zanzibar Revolution and Its Aftermath, Anthony Clayton, “tarehe 2 Januari [1964] mivutano ndani ya A.S.P. ilikamilika pale walipojiuzulu Othman Sharif, Hasnu Makame, Idris Wakyl na Saleh Saadalla.”32

Bwana George Mooring, katika barua yake ya tarehe 29 Agosti, 1963, kwa W. B. L. Monson wa Ofisi ya Makoloni, London, ameandika kuwa:

Imeripotiwa kuwa Moshe Feinsilber, Yahudi mwenye kuendesha biashara ya samaki hapa [Zanzibar], amejishughulisha na siasa kwa kuiunga mkono A.S.P. na yumo kujaribu kuwavutia viongozi wakubwa wa chama waachane na Abeid Karume na waungane na Othman Shariff katika jitihada zake za kuungana na Z.P.P.P. Ijapokuwa kikawaida maoni yake huwa yana uzito ndani ya chama, yeye [Finsilber] pia ameshindwa kukipeleka chama kwa Othman Shariff. Wakati huu viongozi wa A.S.P. wamekuwa wakitembelea Dar es Salaam mara kwa mara kwa kupata ushauri, ambapo imeripotiwa kuwa washauri wao wakubwa ni Kawawa na Kambona. Inasemekana kuwa Watanganyika wameshinikiza kuwa

Page 59: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 27

endapo Z.P.P.P. itakataa kujiengua kutoka Z.N.P. na kujiunga na A.S.P. basi A.S.P. iwe chama cha upinzani na isikubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na vyama vingine viwili [Z.P.P.P. au Z.N.P.]. Bahati mbaya ushauri huu umekubaliwa na A.S.P.; kwa vyovyote vile uwezekano wa kuundwa Serikali ya vyama vyote ya Umoja wa Kitaifa, umepotea. Hapana shaka A.S.P. wameridhika kuwa mwisho wake, uzito wa kuungwa mkono na bara ndio utakaowaweka madarakani Zanzibar, na inawezekana ni imani hiyo kuliko kitu chengine chochote inayotuweka kwenye hali tuliyo nayo.33

Ripoti ya siri na kielelezo cha mukhtasari cha kitengo cha usalama cha Zanzibar cha tarehe 31 Julai–28 Agosti, 1963 kinamuelezeya:

MOSHE FINSILBER, mtu wa Israel Zanzibar, ambaye ni memba kamili wa A.S.P. Katika mikakati ilioelezewa katika kifungu kilichopita, [Finsilber] dhahiri amekuwa akimuunga mkono OTHMAN SHARIFF MUSA katika mkakati wake wa kuungana na Z.P.P.P. na amejaribu kwa uwezo wake wote kumvuta SALEH SAADALLA AKIDA na ABOUD JUMBE MWINYI kuachana na ABEID AMANI KARUME na kujiunga na OTHMAN SHARIFF MUSA. Lengo la FINSILBER, ni bila shaka, ni kukingowa chama cha Z.N.P. chenye kuongozwa na Waarabu ili kisiungwe mkono na walio wengi. Anatumia ushawishi wake mkubwa ndani ya chama [A.S.P.] kuondowa ushirikiano wowote ule wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itaihusisha Z.N.P.34

Ni dhahiri baada ya kukamata khatamu za serikali marehemu Mzee Karume aliwabadilishia kibao Maisraeli kwa kule kuwaunga mkono makhasimu wake ndani ya A.S.P. Anaandika William Edgett Smith kwenye kitabu chake Nyerere of Tanzania:

Israel, kwa mfano, ilikuwa iwe rafiki wa kwanza na wa karibu wa serikali mpya, kwa sababu Maisraeli walikuwa wachangiaji wakubwa wa chama cha Afro­Shirazi katika miaka kabla ya uhuru. Lakini, baada ya mapinduzi, Maisraeli walipojaribu kuanzisha mahusiano na serikali ya Karume, walikutana na upinzani mkubwa usiofahamika.35

Kwa upande wake, Mzee Jumbe ameonyesha kuwa mvutano ulikuwa baina ya ujumbe kutoka Pemba ambao ulishikiliya kuwa Othman Shariff awe Waziri Mkuu baada ya uchaguzi mkuu wa kabla ya uhuru wa Zanzibar. Mvutano huo, anaendeleya kuelezeya Mzee Jumbe, uliendeleya kufukuta na ulijitokeza kwa nguvu katika mkutano wa pili wa kikatiba uliofanyika jijini London. Anaandika Mzee Jumbe:

Karume alikuja kujuwa kuwa baadhi ya wajumbe wa ujumbe wake walikuwa wanataka kufanya urafiki na ujumbe wa serikali kwa lengo la kutaka kujuwa wangeliweza kupewa nafasi gani za uongozi wakiamuwa kutoka kwenye chama cha upinzani [ASP]…Karume alifupisha mazungumzo ya London na akaweza kuuondowa uwezekano wa mpasuko ndani ya safu ya chama.36

Page 60: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili28

Mpasuko ndani ya ASP ambao Mzee Jumbe amejaribu kuuonesha ni mpasuko baina ya ujumbe wa ASP kutoka Pemba na ule uliokuwa chini ya uongozi wa Mzee Karume. Hakuna mahala ambapo Mzee Jumbe ameutaja upinzani wa marehemu Abdalla Kassim Hanga, Abdulaziz Twala au Saleh Saadalla Akida dhidi ya uongozi wa Mzee Karume. Wala hakutowa maelezo yoyote kuhusu TANU kama ilikuwa ikimuunga mkono Mzee Karume au kundi lipi lililokuwa dhidi ya uongozi wake ndani ya ASP. Kwa mujibu wa Mzee Abbasi, “TANU ilikuwa imeshachoka na hayati Mzee Karume na khasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Julai 1963.”37

Katika kuthibitisha kutoelewana Mzee Karume na Mwalimu Nyerere, anaelezeya Profesa Issa G. Shivji, kuwa Mzee Aboud Jumbe anaelezeya kuwa baada ya daktari wa Kichina kumuambiya kuwa Mzee Karume alikufa palepale alipopigwa makao makuu ya A.S.P. Kisiwandui, Mzee Jumbe moja kwa moja alimpigiya simu Mwalimu Nyerere na kumwambiya:

Huku jambo kubwa limetokea. Yeye [Nyerere] akaniambia “Karume?” Nikasema “ndio.” Akasema “basi nitaitisha Baraza la Mawaziri.” …Sauti ya maelezo ya Mzee Jumbe ilitowa ujumbe kuwa Mwalimu Nyerere alikwishajuwa kuwa Karume ameshauawa Zanzibar kabla ya kuarifiwa na Mzee Jumbe.38

Kipindi cha kabla ya kuuliwa kwa Mzee Karume hali ya uhusiano baina yake na Mwalimu Nyerere ilikuwa mbaya kuliko wakati mwengine wowote ule. Anaelezeya Shivji:

Kwa mujibu wa Jumbe [Karume na Nyerere] walikuwa hawazungumzi kwa mwaka mzima au kama hivyo kabla ya kuuliwa. Bhoke Munanka kwa upande wa Nyerere, na Jumbe kwa upande wa Karume, walikuwa wajumbe wa kupeleka na kurudisha habari. Salim Rashid amemuambia mwandishi [Shivji] kuwa alipokwenda kumuaga Karume baada ya kuwacha kazi serikalini siku moja kabla ya kuuliwa, Karume alimshauri kuwa asiwache kazi kwa sababu alikuwa anataka kuuvunja Muungano.39

Undani wa kuuwawa kwa marehemu Mzee Karume umeficha Mapinduzi kama kuundwa kwa Kamati ya Watu 14 kulivyolifunika kombe mwanaharamu apite. Nadhariya iliyopo ni kuwa waliyopanga kumuuwa marehemu Mzee Karume walikuwa wanafanya kazi ndani ya mpango ambao hawakuutambuwa undani wake. Maalim Seid Sharif Hamad ameandika kuwa “Baadhi ya watu wanafikiria kuwa Nyerere alimtumilia Babu na chama cha Umma kumuuwa Karume kwa sababu ikijulikana vizuri kuwa yeye [Nyerere] na Karume walikuwa hawana masikilizano mazuri.”40

Alipohojiwa Babu na mwandishi wa televisheni wa Kiingereza alikiri kuwa Balozi wa Cuba aliyekuwepo Dar es Salaam alikuwa hajui chochote kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kama alivyokuwa hakuyajuwa yeye. Babu aliyarudiya

Page 61: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 29

maneno ya John Okello kwa kusema kuwa hakusaidiwa na nchi za kikoministi katika kuyapanga mapinduzi ya Zanzibar bali alisaidiwa na “Mungu wa Waafrika.” Jee, Waingereza hawakumuona “Mungu wa Waafrika” alipokuwa akiandaa kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar na badala yake waliamua kuwanyosheya kidole wana­Umma Party kutokana na imani yao kuwa ASP haikuwa na uwezo wa kufanya Mapinduzi bila ya Tanganyika? Na si hivyo tu, Mzee Karume, Babu na viongozi wengi wengine wakaipokeya sifa ya kuyaongoza mapinduzi na kumfunikia kombe “Mungu wa Waafrika?” Kama John Okello alikuwa ni mtu aliyekuwa na nyota mbaya iliyochomoza na kuanguka papohapo, na marehemu Babu na Karume walikuwa hawayajuwi mapinduzi lakini walijaaliwa kupata vyeo, watakuwa wamebakiya nani na kwa ushahidi gani ambao walikuwa viongozi wa mapinduzi ya Zanzibar? Ni Waafrika waliowapinduwa Waarabu Zanzibar au ni Waafrika waliowapinduwa Wazanzibari?

Takwimu za Kikabila Zanzibar

Ukiiweka kando propaganda inayolinganisha Ubantu peke yake na Uafrika utakuta Marais wakubwa wa Kiarabu wa Kaskazini ya Afrika, marehemu Gamal Abdel Nasser, na Ahmed Ben Bella ambaye yuhai, walikuwa upande wa ASP na TANU katika kuyafanikisha mapinduzi ambayo kijuujuu yamekuwa yamefahamishwa na kufahamika kuwa yalikuwa mapinduzi ya “Waafrika” wanyonge dhidi ya “Waarabu” mabepari wa Zanzibar. Kana kwamba hao Wa arabu wote wa Zanzibar walikuwa matajiri na mabepari. Akitumiya takwimu za Michael Lofchie, Profesa Issa G. Shivji ameeleza

yakuwa asilimia moja (1) tu ya jamii ya Kiarabu ilokuwa ikiishi Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa katika tabaka la juu la kijamii, na asilimia 76 ya Waarabu walikuwa katika tabaka la chini. Kwa mujibu wa takwimu za kikabila za 1948 Waafrika Asilia (Washirazi) walikuwa asilimia 56.2, Waafrika kutoka bara walikuwa na asilimia 19.4, Waarabu asilimia 16.9, Wahindi asilimia 5.8, na Wangazija asilimia 1.2.41

La msingi si kutafautisha baina ya tabaka za Waarabu baina ya asilimia 1 na 76, bali kufahamu kuwa hawa Waarabu masikini za Mungu wa asilimia 76 waliokuwa wakiishi mashamba ndio walioubeba mzigo wa kifo na maangamizi katika mapinduzi ya 1964.42 Na hao hao Waarabu wa kawaida wa Kizanzibari waliokuwa wakulima, wavunjaji mbata na wazegazega hubebeshwa tuhuma za utumwa. Na katika hiyo asilimia 1 ya tabaka la juu na la kati la Kiarabu ipo haja pia ya kujiuliza Waarabu wa Zanzibar wakijiona kama raia au watawala? Kama watawala mbona hawajazijaza skuli za Kiarabu nchini? Mbona wengi wao walikuwa hawaijuwi lugha ya Kiarabu? Na nini mchango wa Waarabu katika kuijenga Zanzibar?

Page 62: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Pili30

Leo Mji Mkongwe wa Zanzibar una heshima ya Kimataifa (World Heritage Site) uliopewa na shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa (UN). Wakfu wa mwanzo wa maji ya mji wa Zanzibar ulianzishwa na Sayyid Barghash bin Said bin Sultan. Mchango wa Wahindi hauelezwi vya kutosha na khasa katika kuigharimiya misafara ya utumwa, au kuipa misaada ya kifedha chama cha Afro­Shirazi, au hata mchango katika kazi za udobi, ukataji nywele, au kuuza vifuu. Na huenda sababu ikawa kutaka kuonyesha pengo la kibaguzi baina ya Waafrika kutoka bara (asilimia 19.4) na Waarabu (asilimia 16.9). Takwimu hazisemi asilimia ngapi kati ya Waafrika kutoka Bara na Waarabu walikuwa Wazanzibari kisheria au kinyume na sheria.

Page 63: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa TatuKwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!

Mmoja wa maofisa mcheshi wa polisi wa Kiingereza alipokuwa anaondoka Zanzibar nilikwenda kumuaga na nikamshika mkono na kumuambiya “Kwaheri Ukoloni!” Aliupokeya mkono wangu na kuniambiya “Kwaheri Uhuru”! —Marehemu Suleiman Behlani, alokuwa ofisa wa polisi (CID) Zanzibar

Waingereza na Siasa ya Kuikataliya Uhuru Zanzibar

Utawala wa Kikoloni wa Kiingereza ulikuwa na sera maalum juu ya Zanzibar ambayo waliita sera au mkakati wa kuikataliya Zanzibar (strategic denial) isije ikachukuliwa na nchi yenye uadui na Muingereza. Uingereza hakuitaka Zanzibar kwa kuwa ilikuwa muhimu kiuchumi au kibiashara. Kilichoaminiwa wakati ule ni kuwa Zanzibar ni mlango wa asili wa kuingiliya bara la Afrika na mwenye kuitawala basi amekuwa na uwezo wa kukitawala kinachoingiya na kutoka Afrika ya Mashariki na Kati. Siasa ya Kiingereza juu ya Zanzibar ya karibuni ambayo ipo kutokeya mwezi wa Mei 1957 ni “haja ya kuvikataliya visiwa hivi visiingiye ndani ya mikono ya dola adui” na kwa mintarafu ya umuhimu wa kistratijia wa eneo lote la Afrika ya Mashariki.1 Ingelikuwa Zanzibar haikusimama kama ni Dola kwenye kizingiti cha Afrika Mashariki na Kati, Waingereza na wafuasi wake wasingejali kuhusu umuhimu wake. Visiwa vya Zanzibar vimetakiwa viwe kama visiwa vya Ukerewe na Nabuyondo ambavyo havina sifa ya kuwa ni dola. Siasa ya Muingereza juu ya Zanzibar ilirithiwa na Tanganyika baada ya kupata uhuru wake mwaka 1961. William Edgett Smith ni mwanahabari na mwandishi wa jarida la Times la Kimarekani kwa muda wa miaka 35. Alizifuatiliya habari za hayati Mwalimu Nyerere kwa karibu na ameandika kuwa “marafiki wa Julius Nyerere wanakumbuka kuwa kwa muda mrefu alikuwa ana wasiwasi juu ya ukaribu wa Zanzibar na bara ya Tanganyika” na miaka michache kabla Nyerere

Page 64: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tatu32

alisema kuwa “Kama ningeliweza kukiburuta kisiwa kile nikakitupa katikakati ya Bahari ya Hindi, basi ningefanya hivyo.”2

Katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanywa Dar es Salaam, mwaka mmoja au miwili kabla ya uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere alisema kuwa anafikiriya kuwa tatizo kubwa litakaloikabili Tanganyika katika miaka ya baadaye itakuwa Zanzibar. “Hapana, sifanyi utani” alisema Mwalimu. “Ufalme wa kigeni, na watoto wenye kucheza na siasa. [Zanzibar] iko wazi kushawishika kutoka nje. Nakhofiya itakuja kutuumisha kichwa sana.”3 Kwa kurudia, mkutano wa tarehe 27 Februari 1963, ambao alihudhuria Makamo wa Rais Rashid Kawawa, chini ya mwaka mmoja kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwalimu Nyerere aliulizwa na Commonwealth Secretary Sir N. Pritchard kama Zanzibar itaachiwa kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki. Nyerere alijibu:

…ndiyo na itakuwa bora ikiwa Zanzibar itafungwa na mapema ndani ya Afrika Mashariki. Kinyume chake kuna hatari ya Zanzibar kugeuka Cuba na kuipa Afrika Mashariki tatizo lake la kwanza la kimataifa. Peke yao, Wazanzibari hawatojaribu kufanya kitu chochote dhidi ya Tanganyika lakini wanaweza wakawaleta marafiki zao ambao watawafanya wawe wakorofi. Zanzibar ilikuwa ni kituo cha kwanza cha ubeberu Afrika Mashariki. Uingereza iliuhifadhi utawala huu [wa Zanzibar] na ni jambo la kimantiki kuwa baada ya Uingereza kuondolewa Tanganyika Waafrika wa Zanzibar huenda wakaungowa Usultani.4

Kuitaja Cuba ilikuwa ni kumshituwa Sir N. Pritchard kwa kumtajiya Ukoministi lakini ni wazi alichokikusudiya Nyerere si Ukoministi bali ni uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu ambao akipenda sana kuwavunja maadui zake kwa kuwaita “Masultani” wakati “Sultan” ni neno la Kiarabu lenye maana ya nguvu au mamlaka. Kutokeya tarehe 1 Disemba 1961, siku nane kabla ya Tanganyika kupata uhuru, tayari Balozi wa Kiingereza wa Zanzibar kwa niaba, alikwishapendekeza kwa The Secretary of State for the Colonies kuwa Zanzibar ni ndogo mno kuwa ni nchi ingawa aliupendekeza mfumo wa Shirikisho ambao ungelikubalika Zanzibar. Hapo tayari siasa ya kuinyima Zanzibar uhuru wake ili isianguke ndani ya mikono ya nchi adui bado inafanya kazi. Anaandika Balozi:

[Zanzibar] ni ndogo sana na haina umuhimu (uhusiano wake na shirikisho utakuwa sawa na kitongoji kimoja cha Kiiengereza kwa Uingereza (England) nzima), haitowezekana sauti yake kusikika katika mabaraza ya Bunge la Shirikisho; na ikiwa shirikisho ni la kubana, na lenye nguvu kubwa ukilifananisha na nchi zilizoshirikiyana, hapana shaka [Zanzibar] itaonewa na washiriki wengine ndani ya shirikisho na itapoteza utambulisho wake. Wakati sehemu ya jamii ya kutoka “bara” iliyopo hapa hawatojali sana ikiwa hili litafanyika, hakuna shaka kuwa Wazanzibari wa kweli, ambao ndiwo walio wengi, wataupinga mfumo huo, hata kama utawaleteya faida za kiuchumi. Kuulinda utambulisho wa kitaifa na uhuru

Page 65: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! 33

wa kitaifa ni mambo ambayo yanatizamwa kwa hamasa na si kwa mantiki, na wanayatabiri kuwa ni mambo yenye umuhimu sana kwao. Aina ya shirikisho lenye kutowa nafasi, lenye nguvu za Serikali ya Shirikisho zilizobanwa kwenye maeneo maalumu ya kiutendaji, na nguvu zilizobakiya zikabakishwa kwenye serikali za nchi [za shirikisho], ndilo aina ya shirikisho litakalowavutiwa walio wengi Zanzibar. Kunako shirikisho la aina hiyo kila eneo la nchi linaweza kujiwekeya serikali yake ya kitaifa, na huku likinufaika na faida za nguvu na ulinzi ambao unaweza kupatikana kwa kushirikiyana na mataifa makubwa, yenye utajiri na watu wengi zaidi.5

Hapana shaka yoyote shirikisho la aina hiyo lingelitegemeya kuwapo chini ya udhamini na ulinzi wa Muingereza au wa Tanganyika ili kulinda isitokee Zanzibar kuingiya ndani ya mikono na makucha ya nchi “adui” au ya “kibeberu.” Hapana shaka pia Nyerere akifahamu vizuri kuwa Oman ndiyo iliyoungowa ukoloni wa Kireno Afrika Mashariki baada ya kuushinda huko Oman na khasa ukatili waliouonyesha Wareno kwa wenyeji wa miji ya Qalhat na Quriyat na Hormuz. Anaandika Profesa E. Harper Johnson:

Wenyeji waliokandamizwa walihisi hawawezi kustahamili zaidi dhiki na udhalimu waliogubikwa nao na wakaamua kutafuta kujikomboa. Kulifikia lengo hili waliupeleka ujumbe wa siri Oman. Walipofika walitoa malalamiko yao kwa Imam juu ya unyama na udhalimu wa Kireno, na mabaya yote yaliyofanywa dhidi yao. Zaidi ya wananchi mia mbili walikatwa vichwa au kuuliwa kwa panga kwa jina la Mungu. Wareno waliwaingiliya kwenye nyumba zao, na kuwafukuza wenyewe na kuwanajisi wanawake wao. Wale waliokwenda kuomba msaada kabla walihukumiwa kifo.6

Oman ilikuwa ni dola ya kwanza ya Mashariki kuishinda dola kubwa ya kibeberu kutoka Magharibi. Ilifanikiwa kuwaondowa Wareno kutoka Mutrah baada ya Sultan bin Saif Al­Ya’rubi (1649–1668) kupewa taarifa muhimu na Muhindi aliyekuwa na Wareno lakini akiiunga mkono kadhia ya Waomani na “Baada ya Wareno kufukuzwa kutoka fukwe za Oman…walilipiza kisasi kwa kuwaadhibu Waswahili na Waarabu wa Kiomani wa Mombasa na sehemu nyengine za Afrika Mashariki kwa ukali mkubwa zaidi.”7 Dola ya Zanzibar ilikuwa imetanda Afrika Mashariki na Kati kabla ya kuingiya wakoloni wa Kizungu ambao walianza kunyanganyiana mpaka mwisho wake vikabakiya visiwa vya Unguja na Pemba. Pamoja na kuwa ilipofikiya Agosti 1961 iliamuliwa kuwa tarehe ya uhuru wa Zanzibar “isingeliwezekana kuwa kabla sana au baada sana ya [uhuru] wa Kenya na sababu kubwa ya hili ni mara Kenya itakapopata uhuru, uwezo wa ufalme wa Kiingereza wa kuilinda Zanzibar kwa nguvu za kijeshi utapunguwa kwa kiasi kikubwa sana.”8

Dhihaka ya kihistoria ni Zanzibar pamoja na historia ya Waarabu wa Kiomani waliyopigana na kuwashinda wakoloni wa Kireno kupotoshwa kutoka mtazamo wa kiukombozi na kuangaliwa kipropaganda kuwa ilikuwa ni kiti cha mwanzo

Page 66: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tatu34

cha ubeberu Afrika Mashariki. Nyerere alikuwa ameshatiya niya ya kuindowa Dola ya Zanzibar kwa kukitumiya kisingiziyo cha ubeberu na aliiyona fursa ya kuweza kufanya hivyo baada ya Tanganyika kupata uhuru na kwa kukosekana kwa uwezo wa Kiingereza wa kuilinda Zanzibar kwa nguvu za kijeshi kutoka Kenya. Na serikali ya ZNP­ZPPP ilimpa Nyerere fursa aliyokuwa akiisubiri ilipotaradadi baina ya kuipeleka Zanzibar kwenye njia ya siasa kali ya kizalendo ya Kiarabu ya Raisi Gamal Abdel Nasser, na kuwaomba Waingereza wabaki kuisaidiya Zanzibar kiulinzi baada ya uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963. Matokeo yake ulinzi wa dola na uhuru wa Zanzibar ukapoteya.9

Tarehe 21 Novemba 1963, Balozi wa Kiingereza wa Zanzibar, Sir George Mooring alipeleka barua kwa Secretary of State for the Colonies yenye kusema:

Waziri Mkuu amenijiya na ombi la kutaka kutimiza Mkataba wa Kijeshi baina ya Zanzibar na Serikali ya Malkiya (H.M.G.). Serikali ya Zanzibar makhsusi inaomba kuwa Serikali ya Malkiya iombwe ikubali kutowa nguvu kwa ajili ya usalama wa ndani na wanataka kujuwa kama vikosi vya Kiingereza vitaweza kupatikana vyenye nguvu za kijeshi. Makadiriyo ya Serikali ya Zanzibar ni kuwa kutakuwa na tishio la usalama wakati na mara tu baada ya Siku ya Uhuru. Nitashukuru kama nitaelekezwa nitowe majibu gani, na kama Gavana wa Kenya ambaye namnukuu ujumbe huu atashauri kama Serikali ya Kenya itakuwa na upinzani wowote wa kuvitumiya vikosi vya Kiingereza viliyoko Kenya kwa ajili ya kuweka usalama Zanzibar ikiwa itahitajikana.10

Ujumbe wa hapo juu wa Sir George Mooring ulipelekwa kwa Secretary of State for the Colonies tarehe 21 Novemba 1963 saa kumi na mbili na nusu za magharibi. Siku hiyohiyo na wakati huohuo Sir George Mooring alimpelekeya Secretary of the Colonies ujumbe mwengine ambao uliongezewa hadhi ya kuwa ni siri na wa binafsi (secret and personal):

Suala hili [la mkataba wa ulinzi] limejadiliwa na Mawaziri pamoja na mimi mara nyingi hivi karibuni lakini kwa njia zisofahamika vizuri. Mpaka tarehe 20 Novemba sikuweza kupata makusudiyo au maelekezo ya niya kutoka kwao. Kwa hakika kama ripoti zinavyoeleza walikuwa wanalizungumza suala hili na Misri na nilifikiriya kuwa suala hili [la ulinzi] limeshamalizika. Upinzani kutoka A.S.P. kuwa na mahusiano na Misri pamoja na matatizo ya kujaribu kutafuta msaada kutoka kwengine kokote kule mbali na Uingereza ndiko kulikosababisha mabadiliko ya mtizamo wao wa hivi karibuni. Unafahamu kutokana na ripoti zetu za usalama za mwezi wa Oktoba kuwa ziko sababu za kufikiri kuwa kipindi cha mara tu baada ya uhuru kinaweza kikawa kigumu. Hali ya kijuujuu inaonekana kuwa imekuwa afadhali lakini chama cha U.M.M.A. bado ni tishio kubwa. Hili si tishio la kupuuzwa kwa sababu ingawa ni chama kidogo na hakina uwakilishi katika Baraza la Kitaifa, lakini kimekusanya takriban [wanasiasa] wote wenye misimamo mikali kutoka pande zote na kina uwezo wa kujenga mstari wa umoja wa wanafunzi, wafanyakazi na A.S.P. dhidi ya Serikali.11

Page 67: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! 35

Haistaajabishi kuwa majibu aliyoyapokea Balozi wa Kiingereza, Sir George Mooring, kutoka Secretary of State for the Colonies, tarehe 9 Disemba 1963 hayakuwa ya kuridhisha:

Kwa hisani yako muarifu Waziri Mkuu kuwa Serikali ya Kiingereza imeyapitiya kwa kina maombi yake ya kutaka mkataba wa kijeshi baina ya Uingereza na Zanzibar. Iwapo patatokeya hatari ya kuvamiwa Zanzibar kutoka nje, hapana shaka kutakuwa na mashauriyano ya hapo kwa hapo baina ya Serikali ya Uingereza na ya Zanzibar kama ni wanachama pamoja wa Commonwealth na msaada gani utahitajika kutolewa.12

Tangu hapo na kutokeya tarehe 2 Novemba 1963, Sayyid Jamshid bin Abdullah, Sultan wa Zanzibar alikuwa ameshamuandikiya barua fupi Sir George Mooring iliyoiyondoleya dhamana Serikali ya Kiingereza juu ya Zanzibar:

Mheshimiwa, Nina hishma ya kuuhusisha Mkataba baina ya Sultan wa Zanzibar na Kanali Euan­Smith, Wakala wa Mtukufu Malkiya na Konseli­Mkuu, kuiweka Zanzibar chini ya himaya ya Kiingereza, ambao ulitiwa sahihi tarehe 14 Juni, 1890. Ili Zanzibar iweze kuelekeya kunako uhuru tarehe 10 Disemba, 1963, hapana budi Mkataba ufutwe juu ya mamlaka yangu ambayo hayamo kwenye Mkataba nilioutiya sahihi tarehe 8 Oktoba, 1963, ambao unahusiyana na Himaya ya Kenya. Kwa hiyo nina hishma ya kupendekeza kuwa mkataba wa 1890 uamuwe, kwa kuhusiyana na mamlaka yangu yasiyojumuuisha Himaya ya Kenya, kuanziya tarehe 10 Disemba, 1963.

Jamshid bin Abdullah bin Khalifa Sultan wa Zanzibar13

Baada ya siku kumi, tarehe 12 Novemba 1963 yakaja majibu ya Balozi wa Kiingereza wa Zanzibar, Sir George Mooring:

Mtukufu, Nina hishma ya kukuhusisha na barua yako Mtukufu ya tarehe 2 Novemba, 1963, kuhusu Mkataba wenye kuiweka Zanzibar chini ya himaya ya Kiingereza, ambao ulitiwa sahihi Zanzibar tarehe 14 Juni, 1890. Nimeamrishwa na Mtukufu Malkiya kuwa makubaliyano Yake na Wewe Mtukufu kuhusu Mkataba utashika kuanziya tarehe 10 Disemba, 1963, wenye kuhusiyana na mamlaka Yako Mtukufu ambayo hayamo ndani ya Himaya ya Kenya.

A. G. R. Mooring Balozi14

Kwa kifupi, siku Zanzibar ilipopata uhuru wake ilikuwa haina ulinzi wa aina

Page 68: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tatu36

yoyote na ilipovamiwa kutoka nje Waingereza walikataa kuipa msaada Dola ya Zanzibar na hawakutaka tena kujihusisha nayo na badala yake mkubwa wa usalama, Forsyth­Thompson akashauri imezwe na Tanganyika. Askari wa jeshi la polisi kutoka Bara na baadhi ya maofisa wa polisi wa Kiingereza walikuwa wameshatakiwa kuondoka nchini. Kulikuwa hakuna mkataba wa kijeshi na Uingereza wala Misri. Mshauri wa mambo ya Afrika wa Gamal Abdel Nasser, Mohammed Faiq alimwambia mwandishi wa kitabu hichi kuwa hapajakuwa na mkataba wowote wa kijeshi baina ya Zanzibar na Misri na suala hilo lisingeliwezekana.15

Kwa upande wa usalama, Mervyn Vice Smithyman, aliyekuwa Katibu Mkuu katika ofisi ya Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Sheikh Mohammed Shamte, anakiri kuwa mbali ya serikali kuwa macho tangu ghasia za Zanzibar za Juni 1961, hakukuwa na “onyo la wazi la kabla [kuhusu mapinduzi], isipokuwa ripoti ya Abeid KARUME kwa Alan Bott wa kitengo cha Usalama” na kuwa kulikuwa na “operesheni kamili iliopangwa na iliowahusisha mamia ya watu pamoja na wale waliokuwa nje ya Zanzibar.”16 Kwa mujibu wa Smithyman, usalama wa Zanzibar wakati wa uhuru ulikuwa na miundo minne: Baraza la Usalama, Kamati ya Usalama ambayo ilikuwa chini ya uwenyekiti wa Smithyman, na Kamati ya Usalama kwa ajili ya visiwa vya Unguja na Pemba, na Kamati ya Uchunguzi ambayo Smithyman pia alikuwa ni memba. Muundo muhimu wa Usalama ulikuwa ni Baraza la Usalama ambalo memba wake walikuwa “Waziri Mkuu, Mawaziri wakubwa mmoja au wawili, Kamishna wa Polisi, Makatibu Wakuu wawili wenye kuhusika, na Tawi Maalum la Usalama (Special Branch).”17

Mfumo wa Usalama ambao sera zake zilikuwa zinashughulikiwa na Baraza la Usalama “ziliandikwa upya na Bwana Forsyth­Thompson. Bw. Forsyth­Thompson kwa miaka mingi sana alikuwa ni Mtumishi wa ngazi za juu wa Serikali ambaye alikuwa amehusika na masuala ya Amani na Usalama katika Ofisi ya Balozi wa Kiingereza. Siku kumi kabla ya Uhuru, Baraza la Mawaziri lilipanguliwa na mimi [Smithyman] nikampangia [Forsyth­Thompson] awekwe kwenye kazi maalum ya kuhakikisha kwamba kazi za Usalama zinawekwa katika hali ya juu ya kuweza kufanya kazi vizuri kabisa kabla ya kuondoka kwake katika mwezi wa Februari [1964].”18

Kwa mujibu wa Forsyth­Thompson “hakuna ushahidi wa kuwepo kwa mkono wa nje katika mapinduzi bali mapinduzi yalianzishwa na kikundi cha Afro­Shirazi Youth League chenye msimamo mkali. Si Umma Party wala si viongozi wa ASP wenye siasa wastani waliojuwa chochote kuhusu mapinduzi. Inawezekana Saleh Saadalla alikuwa anajuwa.” Ameelezea kabla kuwa Alkhamisi tarehe 9 Januari 1964, wanamapinduzi “walisikia ya kuwa Serikali inateremsha silaha kutoka Algeria…Hadithi ya silaha za Algeria zilivuma sana katika wiki baada ya Mapinduzi: kwa hakika ilikuwa ni upuuzi mtupu.”19

Page 69: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! 37

Bwana Forsyth­Thompson kwenye ile ripoti yake juu ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyoiandika Nairobi tarehe 10 Februari 1964 anatowa ushauri kuwa “Ufumbuzi bora wa Zanzibar wa mustakbali ni kumezwa (absorbed) na Tanganyika; ima kumezwa moja kwa moja, au bora, kuwekwa ndani ya mfumo wa Shirikisho wa karibu. Haiwezi [Zanzibar] kumiliki jeshi, wala shughuli za Mambo ya Nje, wala Serikali kamili yenye Mawaziri… kwa kuondolewa Mfalme na kuwekwa sawa kwa wenye kuutetea Uarabu, kikwazo kikubwa kimeondoka.”20

Kwa upande wa jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi wa Kiingereza, Bwana Sullivan hakukubaliyana na Waziri Mkuu Bwana Mohammed Shamte kuhusu kutolewa watu wa Bara kutoka jeshi la polisi la Zanzibar. Kwenye ripoti Kamishna Sullivan alimuandikiya Waziri Mkuu na kupeleka nakala kwa Balozi wa Kiingereza kwamba ikiwa polisi wa kutoka bara waliokuwa wanafanya kazi polisi Zanzibar watatolewa:

…uti wa mgongo mzima wa nguvu za polisi utapotea…idadi ya polisi 270 na katika hao, 90 ni Watanganyika, wengi waliobakia ni Wakenya, na kidogo kutoka Rhodesia, Zululand, Swaziland, Nyasaland na Uganda…Baadae nikamuonesha barua yangu John Harrison wa Usalama na alifadhaishwa vipi Serikali yoyote ile itaweza kufanya kitendo kama hicho. Alikwenda [Harrison] kumuona Waziri Mkuu.21

Kamishna Sullivan anamaliziya kwa kusema “Yote haya yalikuwa na athari mbaya juu ya jeshi la polisi, na ingawa hazikuonekana dalili za kukosa utiifu…haikufikiriwa kuwa hali ilioko haikuwapa askari moyo wa kupigana au kutoa taarifa za Usalama kwa Serikali, ambayo askari walihisi kuwa haiwaamini.”22

Kuna tafauti kubwa katika ripoti ya Kamishna Sullivan kuhusu upangaji na uendesheaji wa Mapinduzi ya Zanzibar na ripoti ya Bwana Forsyth­Thompson ambaye kama tulivyoona huko nyuma alihusika na kurekebisha mambo ya usalama kabla ya kuondoka kwake mwezi wa Februari 1964. Ripoti ya Kamishna Sullivan ilianza na safari za vijana wa Kizanzibari waliopelekwa nchi za Kikoministi na inamalizikia kwa maneno yafuatayo:

Mpaka hapa inaonekana kwamba operesheni iliendeshwa kwa mujibu wa mipango mizuri na watu ambao walikuwa wameidhibiti hali na wenye ujuzi wa kutosha wa mikakati ya kivita ambayo ilikuja kufuatiliwa katika matukio ya baadae kwa karibu na kile nilichokisoma kuhusu mbinu za kuipindua serikali ndani ya kitabu cha Babu chenye kumbukumbu zake za mambo ya kila siku (diary).23

Makomred na Kivuli cha Mapinduzi

Ripoti za awali za Waingereza zilikuwa kimya kuhusu mkono wa Tanganyika ndani ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata baada ya kutambuwa, Uingereza haikuweza

Page 70: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tatu38

kubadilisha mawazo yake juu ya Zanzibar na waliendeleya kutizama maslahi yao na kumuunga mkono Mwalimu Nyerere katika jitihada zake mpya za kuimeza Zanzibar. Kisingiziyo kipya kilikuwa ni Ukoministi hata kama alifahamu kuwa Makomred walikuwa ni “kikundi cha watu wachache [Waarabu?] na kibanzi cha wachache.”24

Kwenye mahojiano mbele ya televisheni aliyofanyiwa marehemu Mzee Karume, John Okello, na Abdulrahman Babu, na mwandishi wa habari wa Kiingereza, Babu alitamka wazi kuwa yeye na kikundi chake hawakusaidiwa na nchi za Kikoministi katika kufanikisha Mapinduzi na kuwa Balozi wa Cuba aliyekuwepo Dar es Salaam alikuwa hajui kitu kuhusu Mapinduzi kama alivyokuwa yeye hakujuwa chochote kuhusu mipango ya Mapinduzi ya Zanzibar. Okello alisema kuwa alisaidiwa na “Mungu wa Waafrika” kuyafanikisha Mapinduzi hayo Zanzibar na Babu aliyarudia kikasuku maneno ya Okello kwa kusema “tulisaidiwa na Mungu wa Waafrika.” Mara tu baada ya kutokea Mapinduzi ya Zanzibar, “Jorge Serguera Balozi wa Cuba nchini Algeria aliruka kwa ndege kwenda Zanzibar kuitathmini hali ilivyokuwa. Baada ya siku chache aliruka akenda Moscow kuonana na Fidel Castro ambaye alikuwa anautembelea Muungano wa Kisovieti kuanzia Januari 13 mpaka 23. Castro alifadhaishwa kabisa na habari za Mapinduzi [ya Zanzibar]. ‘Fidel aliniuliza,’ anakumbuka Serguera, ‘Ni kweli [viongozi wa Mapinduzi Zanzibar] wanazungumza Kispaniola?’ Nikasema: ‘Ni kweli Fidel.’ Halafu akauliza: ‘Ni kweli wanasema “Patria o muerte. Venceremos!” ’ Nikasema: ‘ni kweli Fidel.’ Halafu akauliza: ‘Ni kweli tuliwapa mafunzo [ya kijeshi]?’ Nikasema: ‘Ni kweli, Fidel.’ Akasema: ‘Nilifikiri ni propaganda ya Kimarekani!’ ”25

Ingawa Babu na Makomred walikuwa na mipango yao ambayo ikiongozwa na fikra za kisoshalisti na zaidi za Mao Tse­Tung, isingeliwezekana kuungwa mkono na Cuba kwa wakati ule kufanya mapinduzi Zanzibar wakati Cuba ilikuwa na uhusiano mzuri na Urusi na ilikuwa haisikilizani na Uchina. Pia, ilikuwa ni kwa faida ya wahusika khasa wa Mapinduzi ya Zanzibar kuwatupiya mpira Makomred au Kamati ya Watu 14 kwa sababu kwa kufanya hivyo walikuwa wanajipa himaya ya bure. Waliokuwa hawakijuwi kiini cha Mapinduzi wakipita wakitamba kuwa wao ndio wao wanamapinduzi wenyewe! Na ndio maana mpaka hii leo hakuna maelezo kutoka kwa Komred yoyote aliye hai au aliyekufa yenye kuthibitisha mchango wao kabla ya Jumapili tarehe 12 Januari 1964. Walikubali kuyatumiya na kutumiliwa na Mapinduzi kama walivyokubali wengineo katika chama cha Afro­Shirazi wakati Babu alitambuwa kuwa:

Waingereza waliiendeleza hii sera ya kuigawa Afrika Mashariki na Kati kutoka Afrika ya Kaskazini kwa nguvu ambazo hazijapata kuonekana. Walifikia kupandikiza chuki za migongano ya kikabila baina ya “Waarabu” na “Waafrika”

Page 71: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! 39

Sudan na Zanzibar, na kwengineko Afrika Mashariki.26 Mtizamo wa kisoshalisti ulimpa Babu na wafuasi wake mgando wa ajabu wa kiitikadi na kuwafanya wadharau hisia za uzalendo za uzawa na ukabila wa mrengo wa Mwalimu Nyerere na wanamapinduzi wenzake.

Ali Sultan Issa kwenye kitabu cha kumbukumbu za maisha yake ameandika kuwa “Kulikuwa hakuna shaka kuwa Zanzibar ilielekea kunako njia ya mgongano na majirani zake, na sisi tulikuwa tuko tayari kuutumilia mgongano huo wakati utakapowadia.”27 Juu ya kutambuwa kwa Babu kuwa Waingereza walikuwa na sera ya wagawe uwatawale, Ali Sultan na Babu wakaona wataweza kuutumilia mgongano/mwanya huo na kuipenyeza itikadi yao ya kisoshalisti kutoka China.

Kigogo kimoja cha CCM, jina nalihifadhi, ameyaita Mapinduzi ya Zanzibar kuwa yalikuwa ni ya bahati “lucky affair.” Zanzibar iliupiganiya uhuru wake na ikaupata lakini haikujuwa namna ya kuulinda kwa sababu iliidharau sumu ya fitina za utumwa na stratijiya ya kutojiwachiya Zanzibar kuingiya ndani ya mikono na makucha ya “maadui” wawili, Muingereza na Mwalimu Nyerere.

Page 72: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa NneTupendane Waafrika

Ilivyoelekea mbiu ya “Zanzibar ni ya Wazanzibari” ni yenye kukubalika kwa kila mtu kuliko ile ya “Zanzibar ni ya Waafrika kutoka Bara.” —Ofisa wa Kikoloni wa Kiingereza

Mzee Issa Kibwana alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa juu wa kikundi cha Tupendane na alikuwa memba wa chama cha kisiasa cha Afro-Shirazi. Katika mapinduzi ya Zanzibar alikuwa ni katika watu wa mwanzo kuingiya kambi ya jeshi la polisi ya Mtoni na baada ya mapinduzi alijiunga na Jeshi la Wananchi la Tanzania Zanzibar ( JWTZ).

Mie ndo mwenyewe. Mimi ndo kiongozi wa Tupendane. Hapoo Miembeni. Mimi ndo mwenyewe kigogo wa Tupendane. Nadhani ukintizama sana hata ninge kwenda utaona bega langu moja limekwenda upande. Kiini cha Tupendane…hawa Tupendane ni kama kitu kilijichomoza tu hapo Miembeni. Hakina msingi hakina chochote. Watu walianza tu, tupendane, tupendane. Sasa ikawa chama kikubwa Tupendane. Sasa kilipopata nguvu alipoamuru Sultani kuwakamata wale viongozi wa Tupendane kuwapeleka Bungi meli nane kwenda kuwatupa usiku. Na mimi nikawa nimo ndani ya kundi. Sababu tunaharibu nchi kwa makosa kwamba kwanza mwendo wetu hatujui shabaha yetu nini kwenda mwendo kama ule. Halafu hatujuwi haya masuruali kuyashona yakawa namna hii. Hatujui mnataka kutia nini huko chini. Kwa vile hili neno lilimkera Sultani. Huu mwendo ulitokezea uwanjani pale palikuwa na ngoma moja iko pembeni yetu ikiitwa Ndala Ndala. Wale Ndala Ndala na Tupendane waliweka mpaka hapa katikati. Ndala Ndala wako kule Tupendane wako huku. Sasa hawa Tupendane wakenda hivi wanakwenda wachokoza wale Ndala Ndala katika banda lao kule. Na wao watainuka “mnakuja tuchokoza!” Zikaanguka ngumi. Vikaanza vigongo vitupuu. Miembeni hapo. Vigongo vitupu. Sasa Sultani alikuwa na njia

Page 73: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 41

yake, akipita lazma msimame. Sasa hawa Tupendane walianza kuvunja adabu kwamba hawamjui Sultani tena. Wakimuona yule, kama wako wawili basi utaona wameongoza hivi, hata hawasimami. Yule mtu anaona “mbona hawa watu wananringia? Bwana we! Chukueni kikundi hiki kakitupeni Bungi.” Basi tukenda tukatupwa huko bwana. Usiku. Lakini hatukukaa huko. Kwa mwendo wetu ule tumerudi. Wanachama wetu wakatufata Kidongo Chekundu. Wanatufuata sie tunarudi. Bwana tunakufuateni, sisi tunawaambia bwana tunarudi twendeni. Ndo umesimama mdundiko mkubwa kweli kweli, Ndala Ndala na Tupendane. Yamezidi mambo. Makubwa. Hapiti mtu yoyote! Kuingia kule [kwenye ghasia za Juni 1961],1 yule bwana mkubwa, Mzee Karume, alikuja Miembeni akakuta hizo ngoma mbili, Tupendane na Ndala Ndala. Sasa alisimama katikati. Wengi wao waliona yule mtu kaingia kundi la wahuni huenda wakampiga yule, lakini hataa. Walimshangiria uzuri sana yule bwana mkubwa pale. Mpaka akaamuru kwamba nyinyi wenye suruali nyeupe mwende kwenye duka moja pale la Afro­Shirazi, Mlandege pale, sasa hivi wanauza nondo, lililoelekea Bwawani kule. Pale kulikuwa na duka la vitambaa la Afro­Shirazi. “Nendeni mkapime hizo suruali za derei.” Suruali zao ni za derei, nyeupe tupu. Tukenda pima suruali za derei pale! Sasa yule bwana mkubwa akaja pale, pesa kalipa mwenyewe. Sisi tumepoa tu nguo kuvaa. Basi akifika pale, Miembeni, hakuna mtu yoyote anozungumza. Atazungumza pale eshe, amalize, anakwenda zake, haya. Hutoa pesa pale. “Haya vijana wangu, tumieni, tumieni, lakini eh, mti na macho!” Sasa huyu bwana “mti na macho” nini, tunatafuta jina hilo. Sasa mle mna wataalamu, tusishirikiane na wale watu wabaya. Sisi tuingie kundi letu la peke yetu. Kashika Tupendane. Inamla roho Sultani. Manake hata kama alikuwa anakwenda sawasawa hivi akiona gari ya Sultani basi utaona kageuka. Yule mtu alokuja pale kutufanyia siasa zile kwenda kutupima zile nguo ndo alotuteka. Na lengo lake lilikuwa hawa watu niwapate kwa sababu hawa watu hawakimbii kitu. Hata! Walikuwa Tupendane hawamkimbii mtu yoyote. Anochotaka kufanya saa yoyote, wakati wowote, anafanya palepale. Na mfano alionyesha Juni 1961. Sasa ikawa Tupendane wamo kwenye mkono wa Mzee Karume. Mzee Karume anatoka huko anakuja zake Miembeni, “leo mna chakula gani hapo?” “Ah, leo hakuna chakula.” Basi utaona anateremsha ngombe, anateremsha mchele. Wahuni wanakula hapo hapo. Sasa imekuwa kiteko cha kumpenda Mzee Karume wahuni wote. Wote wanakuja ndani ya kikundi kwa hii, “kula.” Mtego wake alotega Mzee Karume hata akatunasa pale. Wale viongozi wanohusika na Tupendane ndo waloanza kuambatana na Karume, ndo waloanza kushirikishana na Mzee Karume. Kwa vile walikuwa wapenzi wa Mzee Karume. Hata tukatiwa ndani ya uongozi wa kundi hilo la wakubwa na sie. Wakatupakaza pale, kwamba hawa Tupendane tuwachukuwe wale viongozi wao tuwatie ndani ya kundi. Sasa ukizungumza kule wanakwambia, bwana we, kunakuja kitu hivi hivi hivi, watu wenu wafanye hivi. Ikaenea mpaka

Page 74: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne42

mashamba Tupendane. Nguvu zikagawika mpaka mashamba. Leo naweza ku­kwa mbia twende Mkwajuni nakwambia tawi letu la asubuhi la Tupendane hili hapa. Tumefanywa kushirikishwa na wale askari wa kichama. Mlikuwa na zile shughuli za fete. Sasa wale Tupendane ndo walokuwa walinzi wa milangoni. Hata kwenye fete ya mapinduzi wao ndo walokuwa walinzi wa milangoni na wakifa­hamu kinachoendelea. Juni, ugomvi ulisimama hapo, banda la Ng’ombe hapo. Kulikuwa jamaa mmoja anaitwa Vuai, yeye yumo katika kundi letu la Tupendane. Sasa yule bwana alikuwa na ngombe wake hawa—watatu. Sasa ugomvi wamechukuwa ngombe wa yule bwana kutiwa ndani ya kundi la ngombe kwenda kukoshwa na yule bwana hataki. Sasa kilio chake akaja kulia Miembeni “jamani e, ngombe wangu mimi sitaki wakakoshwe wamekwenda chukuliwa.” Tupendane hawana sheria. Wakachukuwa vigongo. Sasa pale ndo ukasimama muungano baina ya Tupendane na Ndala Ndala kumfuata Mzee Vuai. Hawakumuuliza mtu. Kufika pale wakamuuliza yule bwana hebu tuonyeshe ngombe wako wako wapi? Tizama basi, mambo yenyewe shetani au bilisi tu. Wale ngombe si kwamba wanakwenda chinjwa. Wale ngombe wanakwenda koshwa dawa. Sasa madhumuni yule bwana hataki ngombe wake kwenda tiwa dawa kule. Huenda dawa ile ya kuuwa. Ana wasiwasi. Tupendane na Ndala Ndala, wanafika Kiinua Miguu pale, ndo ilipodata bunduki. Mpaka kesho nikitazama lile guzo lilopigwa hukaa peke yangu nikacheka. Vita vimesimama hapo bwana. Tupendane, Ndala Ndala na hao kushirikishwa ndani ya kundi lile. Sasa yule bwana, Mzee Karume, akajuwa mimi nna wanaume. Sasa safari zake zote ana watu wake ana nini mtego wake kashika Tupendane ndo watu anowapenda. Kula anomotembea anajuwa mwahala fulani pana kikosi changu fulani hata saa sita za usiku. Tulikuwa na Mshihiri mmoja alikuwa na kondoo wengi sana na mbuzi basi kenda kuambiwa yule Mshihiri “wewe Mshihiri wewe hawa watu kama wamepata chakula hawana kitoweo wape kondoo mmoja au wape mbuzi mmoja halafu njoo sema tukupe pesa.” Basi tukiwa kitoweo hatuna tunakwenda, “e bwana tunataka kondoo.” Tunachukuwa kondoo tunakwenda chinja. Ndo shirika, Karume na Tupendane, hapo. Juni ndo iloshiriki hasa Tupendane na Ndala Ndala pamoja. Wakashirikiana. Ilikuwa wameshiriki vizuri sanaa Juni! Kuliko kundi jingine lolote! Kila lilipojengwa tawi la Afro­Shirazi Tupendane wapo. Walifanya kuwashirikisha kwenye jeshi la umoja wa vijana. Sasa ikawa wale kiungo sasa. Sehemu ya Darajani katika vita va Juni, wao ndo waliofunga mpaka ati. Kwamba anayetoka ndani majumba makubwa hawezi kuvuka akaingia Mtendeni. Manake mwisho ilikuwa ni ile barabara tu ya Darajani. Wa kule wa kule. Wa huku wa huku. Kazi zao wale walikuwa hawana kazi maalum. Wakwezi wamo, wa punda wamo, wa virongwe wamo, kuokota nazi na nini. Mchango wao pesa nne nne. Kuna watu makusudi hununuwa vyakula wakenda pika pale Miembeni. Hawana

Page 75: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 43

kazi maalum. Tupendane khasa walikuwa zaidi kwenye punda kuokota nazi. Ndo wakawajuwa heshma za Wamanga. Tupendane kamjuwa Mmanga kwa nazi. Ile kwenda kuokota. Anamjuwa Mmanga huyu yuko hapa yuko sehemu gani. Sasa hata yalipoingia mapinduzi haraka kwenda kuuliwa yule mtu. Kwa sababu anamjuwa khulka yake. Na Tupendane walikuwa wengi. Wengi sanaa. [Tupendane walikuwa wanavaa nguo] nyeupe. Shati jeupe, suruali nyeupe. Dereli ikiitwa. Viatu vikiitwa “kunguru wa shamba” rangi mbili, wekundu na weupe. Hakuna tai. Bega la kulia linaangushwa. Umenikumbusha mbali sana. Miembeni ndo makao makuu yao. Shamba walikuwa wako Potowa. Potowa lilikuwa tawi letu moja. Halafu unakuja zako Tunguu. Lilikuwa liko tawi letu moja. Halafu unakwenda njia hii, namba saba, pale wapi pale, walipotaka kuchimba saruji—Kisakasaka. Upite kidogo Kisakasaka. Lilikuwepo tawi letu moja. Sasa lile la karibu na Kisakasaka likishughulika na ngombe. Sasa Karume akisema “jamani e, watu wengi leo hawana nyama” wale kule wanatuletea. Sasa iko wale wanojuwa “huyu alikuwa Tupendane huyu.” Wale wanojuwa wale, wazee, wazee. Wanawake hamna. Wanaume watupu. Kwa sababu wale watu walikuwa wa shari. Ushari mtupu wale. Wale hawakusikilizana na Ndala Ndala kwa kupigana. Vigongo! Mikunguni tu. Hapana mambo ya ngumi. Mambo ya ngumi kampige mkeo huko. Utamkuta mtu ana kirungu bichwa lake linafika hivi kachomeka hapa basi anakwenda tu. Hujui kakitowa vipi mgongoni huko. Ilikuwa kazi yao hiyo. Hata kama watu kumi utafikiri wanakwenda paredi. Wamenyoosha lakini anajuwa sasa hivi tuko kushoto, anajuwa sasa hivi tuko kulia. Kiongozi tu, akisimama mwenyewe anajuwa sasa hivi wote wamesimama. Anageuka anazungumza na jamaa zake. “Tukamkere nani?” Ndo ilokuwa kazi yao. “Nani bedui tukamkere sasa hivi? Si fulani bwana kamkamata jamaa yetu kamwambia mwizi kamuibia nazi. Twendeni tumfuate. Halali bwana. Haki ya Mungu halali.” Moja kwa moja na si kwamba anakwenda kwa kujificha. “Hodi! Hayumo kenda wapi? Kenda mahala fulani. Atarejea saa ngapi?” “Ah sijui,” watu watatu mgonjeeni, sisi tunakwenda zetu. Tuhakikishe tumeshatenda kitendo. Kama yuko ndani anakwenda darini. Wao kazi yao ilikuwa hivo tu. Karume hukaa zake pale Mnazi Moja pale. “Hebu niitieni wale, wale viongozi Tupendane wale.” Basi huja jamaa, “Mzee Karume yuko pale anaita.” Wewe watazame sasa. Wanakwenda mstari mmoja, wakianguka, “wu!” Wote unaona wamegeuka. Wanamtizama. Basi jibu lake “askari wangu mmeiva, hahahaa haaa! Oooo! Askari wangu mmeiva! Leo vipi kwenu kuna mboga, au kuna chakula?” “Ah, tunacho chakula, mboga tunayo.” “Hahahahaaa! Lakini nasikia nyinyi mnalewa nyinyi. Mnakula gongo nyinyi. Bwana siku za kazi hizi, msilewe gongo!” “Wamo wanokunywa Mzee, wengine hatunywi.” “Haya, mh (pesa), nendeni zenuni.” Hakuna anaeificha pesa ile mpaka uwanjani pale. Jamani Mzee Karume katupa pesa hizi. Lakini si za kulewa. Tununuwe ugari. Hiyo ilikuwa kazi yao Tupendane. Shabaha yake

Page 76: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne44

utakuta nywele zao hawanyoi. Hazikatwi. Kazi yao utamkuta anapokaa anafanya hivi tu, anazisokota sokota. Kama siku hizi tunaita Marasta [nywele za Rastafari], na wao zilikuwa vilevile lakini zao hazianguki. Mtindo huu wa masuruali mapana kayaleta Mnyamwezi. Wacheza Beni Bati. Wale walikuwa Wanyamwezi, walikuwepo nao Miembeni pale, na Beni Bati. Sasa wao hutandika mablangeti namna hii, sasa wale wakubwa wakubwa wanojipenda wale, kila mmoja amesimama kwenye blanketi lake. Masuruali yao mapana mtu anaingia. Vilevile dereli. Shati jeupe, suruali nyeupe. Sasa wao walikuwa na nguo kama kitenge au kikoi au nini anafanya hivi. Aliposimama ndo hapo hapo mwenyewe anajitikisa tu. Kuna watu wakasoma pale. Hii nini hii? Hii ngoma ya utamaduni. Ikaanza kuchipuwa ile ngoma ya Beni Bati mpaka mashamba. Walipo Wanyamwezi ipo. Mashamba mle utakuta leo kuna Beni Bati mahala fulani, utawakuta Wanyamwezi wa wapi wa wapi wa wapi, wote wanakutana huko huko. Utakuta wote uwanja mzima nguo zao nyeupe. Sasa wale ndo walokuwa wameshirikiana na akina mama, wamo “Wangaruka wala. Rimo rimo rimaio. He, he, he he!” Wanashangiria. Ngoma zile zimekufa baada ya mapinduzi. Hizi ngoma zetu zikafilia mbali. Manake katika mapinduzi ngoma zote zilishiriki katika mapinduzi. Beni Bati imeshiriki, Ndala Ndala imeshiriki, Tupendane kashiriki. Wale wote walishiriki ndani ya mapinduzi. Ndo wale wale utakuta “Ah! Huyu bwana alikuwa…si mcheza Beni Bati we? Sasa hivi umekuwa kanali wa jeshi? Ama kweli Karume katuweka mambo!” Ilikuwa namna hiyo. Viongozi wa Tupendane walikuwa na mitaa.2 Lakini viongozi wote walikuwa wako mjini tu. Sasa mle mashamba yanakwenda matawimatawi tu. Mwenyewe aloanzisha ngoma ile ya Tupendane, mwenyewe akiitwa Saidi Omari Saidi. Ali­kuwa akikaa wapi? Alikuwa akikaa Mahonda meli kumi na nne hasa! Kibaoni pale. Huyu ndo mwenye kuanzisha ngoma hii ya Tupendane. Kwamba ndani ya siasa yake ile Tupendane, tupendane jamani tuwe pamoja, lakini aliitia kama iko katika ubaguzi. Maana alitaka wale watu wa bara watupu. Lakini kukosa vile na kutaka kujificha akaona wote tuwe pamoja, Zanzibar, nani nani, lakini wote tuwe katika Tupendane. Tupendane kwa sababu usoni kwetu kuna hatari. Ndo manake ile Tupendane ikaja hivo. Naye yule aloanzisha, kwisha mapinduzi tu wakamsafirisha. Serikali ikamsafirisha. Yeye pamoja na nani, pamoja na Mfaranyaki, wote wamesafirishwa. Kwamba hawa kama tutawaweka hapa, itakuwa hatari hawa. Wakasafirishwa. [Mafaranyaki] alikuwa mshiriki mkuu wa mapinduzi. Ni mshiriki mkuu. Na kama unasikia alikuwa Mzee Hamid Ameri wa Donge, yule kapewa lakini mwenyewe hasa alikuwa huyu Mzee Saidi Omari Saidi wa Tupendane. Hamid Ameri siku ya mapinduzi alipoambiwa alisema “mimi staki kuuwa.” [Mzee Saidi] alikuwa mtu wa Tanganyika lakini alikuwa kahusika Mnyakyusa, watu wa Mbeya, lakini kaja zamani hapa. Ndo hao walokuja wakati wa mfalme

Page 77: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 45

anapigisha kuchimba mashimo. Saidi alikuwa msimamizi mkubwa wa bwana Yahaya wa Pongwe. Maana watu wengine ndo wanasema kulikuwa na watu wameletwa walokuwa sijui Manamba, na nini, kumbe sivo hivi. Hawakuja kwa ajili ya kushiriki mapinduzi. Wale walikuja kwa ajili ya MaSultani wale watu kuja habari ya mikarafuu kulimia. Sasa mapinduzi yamekuja yamewakuta. Sasa tusiseme wametoka watu bara kuja fanya mapinduzi Zanzibar. Kuna walokuweko hapahapa tele kama kina sisi. Maana na mie nimo msintoe. Alikuwapo mmoja Mikidadi wa Tanga. Alikuwa huyu mdogo wake Khamisi Hemedi, Athmani Hemedi. Halafu alikuwepo shemegi yake Sefu Bakari, Ali, yule alokuwa akikaa Kwahani. Ali, hata akaingia usalama. Mpaka sasa hivi kafa yeye watoto zake bado wamo katika kazi ya usalama. Manake, viongozi wa Tupendane, tulikuwa sisi kama watu saba hivi. Hawa ndo wenye kundi hili. Lakini kiongozi wa kundi mwenyewe ni mie. Kwa sababu sasa hivi tu mimi nimeregea. Nilikuwa simkimbii mtu yoyote. Hata kama angelikuwa kama mbuyu. Na mshipa nlikuwa nao. Simuogopi mtu. Haki ya Mungu. Simuogopi mtu. Hata kidogo. Tena si kama unazungumza mimi nakutetemekea. Hata! Kwanza huyo Sultani mwenyewe tulikuwa hatusikilizani ajabu. Ugomvi wetu, nilimpiga nani yule…tausi teke pale Kibweni. Pale mimi nnatoka Mahonda nikiingia ndani ya gari. Sasa yule mnyama alikuwa ana ila. Hukaa katikati ya njia pale. Hafungwi ati. Sasa yule akija pale hukaa katikati ya njia akajitikisa halafu hulia “hyeee!” Anainama anaokotaokota pale. Sasa tunatoka shamba sie na gari letu asubuhi tunapeleka ndizi marikiti. Kufika pale yule mnyama katoka porini kakaa katikati ya njia wala hupiti huku wala huku. Yuko katikati ya njia. Mkewe kasimama huku yeye yuko katikati ya njia. Akaanza kuchanuwa akapiga “kukukukuu, hyeee!” Tumesimama bwana, tunamsubiri mpaka aondoke. Tupite wapi? Mkipita mtafatiwa na walinzi wa Sultani. Nkamuliza “we dereva we, vipi bwana?” Akasema “Sultani yuko usoni kwangu hapa bwana we.” Mimi nikatoka nyuma huko. “Huyu ndo Sultani?” Nikampigilia mbali teke! Likaanguka huko, puu! Nikaingia ndani ya gari dereva akatia jembe! Sasa si wanakuja nitaja wenzangu wa ndani ya gari kwamba alopiga huyu. Wote ndani. Bwana alopiga huyu. Nimekwenda hapo Kiinua Miguu. Nimechezea miezi sita. Kahama yule tausi. Mimi nilikuwa namtafuta nimuuwe lakini sikumpatia tu. Kwenda kuniweka bure ndani miezi sita kuwa nimempiga tausi! Mimi mpaka sasa hivi ilikuwa kama wanatambua siri yangu na Mzee Karume nisingekuwa hivi halo. Wallahi laadhim nisingekuwa hivi. Na maisha namtafuta Karume mdogo nimpate ili nimpe siri yangu hii. Tulivo mimi na yule Mzee Karume. Bado sijampata. Karume mimi nilikuwa kama ndugu yake, ndugu baba mmoja mama mmoja. Hataki afanye jambo mimi nisilijuwe kwa ile shabaha alompa hayati Yusuf Himidi kwa mie wakati alipokwenda kunitambulisha. Bwana huyu mtu yuko hivi hivi hivi hivi. Basi yule mtu alikuwa saa ishirini na nne mimi nakwenda Ikulu wala habari sina,

Page 78: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne46

wala siulizwi na mtu. “Assalam Alaykum.” “Alaykum Salaam.” “Mimi bwana leo sina pesa.” “Wewe hwishi kutumia pesa kama Banyani. Haya nenda zako. Au una shida zaidi?” “Hata.” Huyo nakwenda zangu. [Zilipotokea ghasia za June 1961] Mzee Karume kaja zake mpaka msikiti mdogo Mwembe Rikunda hapo kampata alie wake kamwita upesiupesi. Njoo, vipi huko? Akasema, huku mpaka sasa hivi kumetulizana kimyaa! Hawa maasikari wanatafuta watu waliopigana ni watu gani? Akamwambia, wewe sasa nnakutuma, nenda hapo, usipige tarumbeta. Mkamate mmojammoja, pita kidookidogoo, wanongoneze wote muwe mulivo hivi hivo, pastokezee fujo tena. Mimi nakwenda zangu. Yule bwana alotumwa akatimiza ile ahadi. Sasa hawajuwi wale [askari] shina lake nini. Hivo ndivo ilivo. Hawajuwi kabisa shina lake nini. Lakini ilikuwa makusudio yao [askari] pale wapate njia ya kuwakamata wale watu [waliofanya fujo]. [Mpaka leo] wapo walojuwa lakini hawawezi kuzungumza kitu hicho. Siri yao wanaijuwa wenyewe. Ni siri tu. Hiyo moja kwa moja. Ukiizungumza anakwambia “aaahh! Huko usende huko. Huko usende hakukufai kwenda.” Kwa sababu hiki kitu kishaambiwa kisizungumzwe hasa! Huyo anokijuwa asikizungumze. Unajuwa kama tunakwenda mambo ya Kingereza, Mngereza mpaka sasa hivi suala hilo [la ghasia za Juni 1961] bado analitafuta hapa. Saana analitafuta hapa. Alikuja mwanamke mmoja wa Kiingereza tena alipanga nyumba hii ya Michenzani, namba moja hii, yaani kwa kutafuta kitu hicho. Kuna watu nyumba hiyo, kulikuwa na mtu mmoja jina lake la kwangu mie, akamwambia yule bibi, ukitaka kitu hichi nenda kwa fulani. Kaja hapohapo. Akachekacheka pale, kunchekesha, ananiuliza, nikamwambia mie mgeni hapa. Mie mgeni sijui hayo. Hawapo. Na khasa wanaohusika hawapo zaidi. Sasa kula likiwa hivo ndo vizuri zaidi. Maana watakujaingia watu walokuwa siwo kwa vile bora ife hivohivo. Midamu wenyewe hawakutambuwa chanzo chake nini na kiini chake nini, bora iwe hivohivo.3

Walifanya sivyo. Wamefanya kinyume ya mambo yanavotakiwa kufanywa. Sasa likitokezea jambo lile likiwa na nguvu zaidi itaonekana aibu kwao. Bora lilivokufa life tu. Kula mmoja anaomba dua life hivohivo na Mwenyezi Mungu kalijaalia life hivohivo. Anolijuwa, ukilizungumza, kwanza nakutizama macho hasa. Jibu lake rohoni mwake atasema “yule kuuliza jambo lile lina miaka fulani kakusudia nini huyu?” Midam jambo limepita, wenyewe hawakujulikana, basi, halina lazma. Utamtaja wapi, Mzee Issa ameshakufa zamani. Karibu miaka kumi. Hata ukimtaja si bure. Kumtaja kwako kunafaa nini? Wanajuwa wengi lakini ile hadithi yake ngumu Ndo ikafa hivohivo. Hadithi yake ngumu ikafa hivohivo.4

Tupendane na Ghasia za Juni 1961—Mzee Selemani

Suala la Juni, ukisikia hao “Tupendane” masuruali mapana, Waruguru, Waza ramo,

Page 79: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 47

pale Kizota [Darajani] palikuwa na bekari ya kuni za mikate pale, Tupendane pale wakaanza kufanya machafuko bwana wewe, piga mtu, pale pale. Piga mtu. Huku wamekwenda Malindi na huku wamekwenda Kisiwandui. Wakasema kinachotoka huku kuingia huku halali yetu. Sasa vurumai lile likaja likaingia moja kwa moja mpaka Ngambo kote huko, Ngambo unajuwa zamani Wamanga wapo, Washihiri wapo, vikaja vifo vya ghaflaghafla tu. Kitu alichoamuwa Mfalme ni kutaka askari kutoka Kenya kulinda ule usalama wa hapa. Walipokuja wale askari, walichokifanya, hawakulinda majumba makubwa. Wao wamekuja kuingia nyumba za Ngambo. Ikawa wanalinda raia wa huku Ng’ambo huku. Lakini juu ya hivyo, Tupendane kazi waliokuwa wakiifanya, askari wale wanakwenda zao huku, wakizunguka round [mzunguko] kuja zao huku, kuja kuingia tena, wanakuta maiti mmoja, wawili, pale. Hapo ndipo ikaonekana sifa ya Tupendane. Ikaonekana kwamba hawa Tupendane bwana machafuko. Na kuna baadhi yao walishiriki kwenye mapinduzi. Wale Tupendane mwananchi hawezi kufanya kitu pasi kuwa kiongozi wa nchi anajuwa. Hiyo, kwanza huyu Kisasi alishauriwa, bwana we, hapa pataingia vurumai, sijui wewe utatowa mchango gani. Yeye nafsi yake akasema, kweli mimi nna cheo, lakini utakuja kukuta siwezi leo kufanya mapambano kuingilia kati wakati mimi ni mfanyakazi, lakini langu la kufanya, nyinyi mnaweza kufanya tendo, mimi nikakuteteeni, itakapokuja kesi. Mzee Karume alikuja sema “lazima mshituko wa nchi, kujuwa na sisi tuko wengi, lazima ishtuliwe.” Kwa hivihivi tu mambo yatakwenda hivihivi, tutakuwa hatuhishimiki. Aboud Jumbe akatoa kauli kuwa hakuna la msingi la kufanya isipokuwa ni kupigana tu. Wao Tupendane walikuja kwa muundo wa majahazi, wanatoka kule [bara] wanakuja hapa, wanafanya biashara, wanaondoka, wanarudi, wakiingia wakitoka. Zamani kulikuwa na vibali vidogovidogo hivi. Ukitoka kule unaingia hapa. Mambo yalikuwa yakenda hivo. Lilivomalizika hili suala likatulia kabisa, kwamba zile chaguzi kila wakati tunapata lakini tunaambiwa hapana, tunapata tunaambiwa hapana, ndo akina Kassim Hanga sasa hapo walipokaa ushauri, jamani e, hapa bwana hapapatikani nchi, na akina Ali Muhsin ndo nanga kama hii, na uchaguzi unaokuja karibu bendera zitapandishwa. Kwa hiyo bwana la kufanya tukaeni kikao cha kujadili tufanye nini. Suala la Tupendane bwana…Tupendane lilikuwa na mambo makubwa na mwenyekiti wake ni mwenyewe Mzee Karume. Yeye ndo mwenyekiti aliyefanya mpango wa kuwatafuta vijana wa Tupendane, vijana wa kibara. Tupendane, kijana wa Kizanzibari hayupo. Pahala popote, mtu yoyote mkatalie. Mwambie kwamba Tupendane kijana wa Kizanzibari hakuwepo. Tupendane walikuwepo kwanza Wazaramo, Wandegereko, Wayao, Wamwera, Waruguru…hawa ndiwo waliefanya mpango wa kulizuwa Tupendane.5 Ni vijana wa kibara waliotambuwana. Mzee Karume aliwakusanya pahali pamoja akawaambia “skilizeni, mimi staki kujitokeza ila nyinyi vijana nnataka mnifanyie kazi yangu. Kwanza Hizbu lazma wataulizana kutokana na haya mavazi yenu na jina lenu litakuwa Tupendane.” Na kwa kweli

Page 80: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne48

walikuja wakaulizana “mambo haya vipi, hawa vijana namna gani?” Mpaka Wahindi walibidi kila wanapotokea wale vijana ikiwa wawili ikiwa watatu ule mwenendo wanaokwenda “Tupendane e, Tupendane.” Ikawa kama msemo tena ndani ya mji. Lakini halafu kumbe Mzee Karume alikuwa na lengo lake suala la Tupendane. Aliwakusanya wale akawaita, akawaambia njoni. Baada ya kuwakusanyaa, kilichotendeka akiwepo mwenyewe Mzee Karume, akiwepo Sefu Bakari, akiwepo Natepe, unaona bwana, akiwepo na Antoni Kisasi, halafu alikuwepo nani? Mzee Adamu, alikuwepo Kamishna wa Magereza. Huyu Mzee wa Kiyao huyu. Walikuwa watu kiasi wanane hivi. Wakawaambia, “skilizeni vijana, tunachokwambieni, sisi hapa Afro­Shirazi ni wapinzani, sasa tunachokwambieni, kura kila ikipigwa tunakosa na sisi ni wengi kuliko wao. Sasa tunachotaka siku zile tutakaposema sasa tunachaguwa, uchaguzi, kazi ya Tupendane ni kufanya kurpushani.” “Kurpushani vipi?” Akasema, “eheeeeee, kurpushani yenyewe wakati mnajuwa jimbo fulani panaingia uchaguzi. Mmeshachaguwa. Mnatoka. Shati ulilolivaa wakati ulipokuja kupiga uchaguzi, si utakalokujia tena.” Mpango ule ikabidi ukapangwa, halafu hapo ndipo alipotoka Yusuf Himidi, akasema “skiliza Mzee Karume, kazi ya Tupendane kubwa nnayoiona mimi ni hii moja, hayo yote sawa, Jee, wale wanaejiita Wangazija, wanaejiita Waarabu, wanaejiita Wamanga, na Waswahili, kuna Uwarabu wa kununuwa, kuna Umanga wa kununuwa, kuna Uswahili wa kununuwa, ni katika sie Waafrika wenziwao. Nnachosema mimi Mzee Karume nakwambiaje? Tupendane wale ndio wakuwa cover [wakuwafuatilia] kwelikweli. Kwa sababu mambo yoote sisi wale ndio wanaotuharibia.6 Kila tunalolifanya wale wako mstari wa mbele. Sasa huku sisi kila tukisema tufanye hivi tufanye hivi limeshafika. Kwa sababu nini, ni Waswahili wenzetu, kabila imekuwa ya kununuwa. Sasa badili ya kabila ya kununuwa ni kujipendekeza. Sasa ikiwa ni kujipendekeza bwana kazi ya Tupendane ni mtu akifanya…[upuuzi] rohoni! Hapana kumstahi. Rohoni!” Mwanya ule Sefu [Bakari] ndo aliposema “sasa sisi mtu harakati kwa masuala kama haya ambaye anaweza kuifanyia harakati hii timu hii basi tumpate Ibrahim Makungu, tumpate Hassan Mandera, kwa sababu yeye ndo atakuwa benet benet [bega kwa bega] na hawa.” Kwanza, Sefu Mdengereko, ni ndugu zake hawa [Tupendane]. Mimi Yusuf nikijitia katika kundi hili, wengi watasangalia. Huyu Yusuf ana nini? Huyu Yusuf khasa, Yusuf Himidi, ana nini? Lakini Sefu hawamsangalii, watajuwa kwamba “si jamaa zake, wote hawa wabara watupu.” Mzee Karume akaja akasema “sawasawa hiyo.” [Ibrahim] Makungu sifa yake yeye ni kuuza tende [ulevi]. Kivutio. Kazi ile walimpa maksudi. Kwamba wewe ni kivutio. Akija mtu pale yale anayeyazungumza si akili yake. Huyu Mandera kazi yake yeye kama unavojuwa kazi yake ni kunyakuwa tu. Gari ya Kipanga ilikuwa inakwenda kwa siiri “bwana we, kuna mtu keshaanguka kwa Makungu na aliyetueleza haya,

Page 81: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 49

haya, haya, haya.” Sasa Tupendane mnasemaje? Haya chukuwa! Anachukuliwa. Ngazi Mia unakujuwa? Anapelekwa Ngazi Mia. Akipelekwa Ngazi Mia tena wao kule la kumfanya wanalijuwa wao. Sasa watu wanashtukiwa tu “Ah! E bwana we. Kuna mtu kule alilewa lakini tena mabiruko yameshambirukia.” Hakijulikani kitu gani. Kumbe Tupendane hao. Sasa imekwenda kwenda, imekwenda kwenda, imekwenda kwenda, imekwenda kwenda, Mzee Karume dakika ya mwisho… Kazi ya Musa Maisara haijafika. Musa kazi yake itafika. Lakini hii kwanza wende watu wawili hawa. Makungu na Mandera. Wewe Sefu kazi yako, wana­pokuja unaposhona vifungo, Tupendane wao wanazungumza na wewe kuwaficha hawa watu hawa. Makungu na Mandera. Suala lile lilikwenda, lilikwenda, lilikwenda, hatma yake Mzee Karume akaja kuita tena kikao. Na kikao hicho kilikuwa na watu wangapi? Baada ya Sefu, Kisasi, pamoja na huyu, Makungu, na Mandera, na yeye Mzee Karume akiwa ni mtu wa tano. Akaanza kuwauliza “jamani eee, sasa, hakika sasa tunaamini kwamba Tupendane kazi wanazozifanya ni nzuri sana. Jee, tunafikiri nini, mfumo wa baadae? Hawa si watakuja julikana? Si watakuja julikana hawa? Wakija julikana sisi roho zao tutaziweka wapi? Au tutawafanyaje vijana hawa?” Nakumbuka mjadala huu ulikwenda wakafikia mahala pa kusema “saasa, la kufanya, hawa tuwafanye kama vijana wa Youth League.” Tuwafanye vijana wa Youth League. Sasa vijana wa Youth League itaonekana tu “hawa Youth League bwanaa.” Sefu yeye ndo mwenyekiti pale. Sasa ina maana hii timu tulioipanga hii, itafanya vipi? Timu tulioipanga itabidi ikae kitako. Makutano ya hawa kwa wakati wake. Tupendane mmoja atowe ripoti zake kwa Tupendane kwa jumla. Sio kundi. Sasa ikabidi hapo sasa wakatumia njama hizo zimekwenda, Mzee Karume akaja akasema “hapana.” Michenzani pale palikuwepo chama cha densi. Akasema “hawa waingie kwenye muziki.” Lakini siri hasa kubwa zaidi ndo hapo alipokwambia Mzee Issa “bwana wee, haya mambo haya kweli wengine wameshakufa lakini sasa kuna wawili wahaiii! Wawili wahai.” Sasa wawili hawa wakija kuupata mnongono huu kamba hukatikia pabaya. Atajulikana ni yeye [Mzee Issa]. Wawili wako hai. Viongozi. Wanaelielewa suala hili shina. Na siri hii wameificha siri kabisa! Kwa sababu mpaka chama cha upinzani hakijuwi kwamba Tupendane hawa hasa walikuwa na shughuli gani? Unaona bwana? Sasa walio hai. Natepe yuhai, Hamid Ameri yuhai, katika memba wa Baraza la Mapinduzi hao. Sasa na hawa wanajuwa hili suala hili. Wamelifunika, manake wamechukuwa chungu wakakifunikiza “jibuuu.” Ndo maana Mzee Issa akakwambia “bwana we, hilo suala zito kwa sababu hawa watu hawa wahai, sasa wakija sikia Issa Kibwana katowa hadisi hii kwa urefu, bwana itakuwa mimi, serikali itaniandama. Itaniandama vibaya vibaya!” Wakintia mkononi itabidi waniulize. “Bwana we, ilikuwaje? Haya mambo haya. Woote wapinzani hawajuwi. Wewe umelitowa. Haya vipii? Kwa madhumuni gani?

Page 82: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne50

Ilianzia nini?” Nitakuwa la kusema sina. Ndo ukamuona Issa kila ukimbumbukiza anakwambia “Mmmmhh, bwana we, hebu tulia” kwa kuogopa watu hao wawili ambao walio hai wanaolijuwa suala hili. Waliobakia wote unaowaona maofisini hawaelewi nini maana ya Tupendane. Hawajuwi kabsaa! Sasa utakuja kuta kwamba baada ya hapo, Mzee Karume sasa akaanza sasa kurpushani zake kwamba hawa Tupendane, wewe utakwenda sehemu za Ndagaa, huko utahudumiwa na chama, wewe utakwenda Mkokotoni. Sasa ripoti za mule moootee mule wanakuja mjini hapa anapewa mtu huyu mmoja. Akipewa huyu mtu yeye hasimami, moja kwa moja anakwenda kwa Kisasi, kwa sababu Kisasi yeye mkubwa wa polisi. Sasa baada ya yeye anamuwakilisha Mzee Karume. Bwana kesi nilioipata kwa Tupendane hii, hii, hii. Wakati huo huyo mtu anakuwa havai nguo za Tupendane na Kisasi havai nguo za kipolisi. Anaweza kwenda nyumbani kwake tu, halafu yeye yule anatoka Kisasi anamuendea Mzee Karume “bwana, iko hivi, iko hivi, iko hivi.” Mzee Issa nakumbuka randa yake akitoka Kisiwandui pale, huyooo, anaelekea Malindi anaichunguza, jee huko kazi zinafanywa vipi? Zinafanywa hivi. Hayaa. Anatoka hapo Kinazini, vipi kazi inakwendaje huku? Inaendelea. Za Tupendane. Huyoo, Kikwajuni. Kazi inaendelaje huku? Inaendelea. Walichokifanya Tupendane, ile Kwahani ile, walikuwepo Washihiri, na ndo hao Wangazija Wangazija, sehemu za Michenzani humu, yaani wale walionunuwa kabila wale. Sasa askari wa Kenya wanapita huku, wanakwenda hivi, Tupendane, wanapita huku. Hawa wanakuja huku wanakuta maiti watatu wanne wamelazwa. Mpaka askari wa Kenya wakauliza “jamani, haya mambo vipi? Tumepita sasa hivi hapa hapana maiti. Huyu mtu keshauliwa huyu hapa.” Mpaka askari wa Kenya wakaingiwa na wasiwasi, kuwa juu ya bunduki zetu tunaweza kuvamiwa wakati wowote. Hawa lazima wanatumia dawa hawa kama wanazotumia sisi kwetu Kenya Mau Mau. Iko dawa wanaitumia hawa. Haiwezi kuwa. Wakaanza msako nyumba hata nyumba. Wanawakuta watu wamekaa wametulia. Jamani vipi? Kila wakimtizama mtu wanamuona wa kawaida. Kumbe, Tupendane huyo! Tupendane huyo bwana. Wazungu walikuja kulijuwa lile suala, wakamwita Karume. Karume akajibu watu wangu hawana matatizo isipokuwa wanachokozwa. Wazungu waliona kuwa Waswahili ni wengi na wana nguvu kuliko Waarabu. Wazungu waliongeza vikosi na Karume akawabonyeza Tupendane na kuwaambia “tulieni” kwa sababu sisi hatuna ugomvi na Mngereza. Huyu akipeleka simu tu Uingereza kitakuja kikosi hapa sisi hakuna tutachofanikiwa. Muwe shwaariii! Kweli watu wakawa shwaari kabisa. Sasa watu walipoona hawa watu wametulia na haya mambo yamekwisha, ikabidi wale waondoke, waende zao, nyuma kukawa na utulivu. Karume kama anaitaka serikali Juni alipinduwa lakini alimuogopa Mngereza. Sasa Ali Mushin alitaka Mngereza aondoke kwa kuwa yeye ndie anaetuharibia. Sisi wenyewe kwa

Page 83: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 51

wenyewe tutaelewana. Karume alimcheka. Akamuuliza “umefikiri” Ali Muhsin akajibu “nimefikiri.” “Umefikirii?” “Nimefikirii.” Ali Muhsin akasema sisi kwa sisi hatugombani. Wakatiliana mkataba. [Kina Hanga] hawakuwa na Tupendane. Tupendane wa mwenyewe Karume tu. Peke yake, na vikosi vake ambavyo alivokuwa ameviteuwa. Shughulikieni suala hili. Kwanza, Mzee Issa. Halafu kaja huyu nnokwambia, Mohamed “Mkunjeke.” Mdengereko huyu, anatokea Rufiji. Akaruka, Mfaranyaki, yaani Mfaranyaki ni Mngoni. Hawa watu watatu hawa. [Mfaranyaki] alikuwa Tupendane. Lakini Tupendane yenyewe alikuwa chini ya Mzee Karume. Ripoti za kukutana na Kisasi, na nani, nani…yeye anakwenda anawakilisha moja kwa moja. Kama Mfaranyaki hayuko, Mkunjeke anaingia, au Issa anaingia. Watu hawa watatu. Mfaranyaki alikuwa karibu sana na Mzee Karume baadae alirejeshwa Songea. Saidi Washoto alitaka kuingia katika Tupendane. Mzee Karume akamwambia, “aa, hapana.” Kwa sababu alimuona huyu ni Myamwezi, hana ukweli. Kaujore kaja kuingia mwisho Tupendane. Mwisho. Sasa hawezi kuvaa suruali buga mtu mzima. Tupendane akijua tu nini kinatendeka. Hamid Ameir alijuwa tu kwamba wako Tupendane na mwenyekiti mwenyewe ni Karume. Waliokuwemo Tupendane, Ibrahim Makungu, Musa Maisara, Antoni Kisasi, Yusuf Himidi, Sefu Bakari. Hawa watu watano hawa. Bwana wewe Yusuf Himidi aligeuka moja kwa moja. Kwani hizi silaha akileta nani? Yeye alikuwa dereva publiki. Kuna wale chipukizi wanovaa mabuga majiani. Wale mbali wale. Kuna magwiji. Hawakutaka wao kuvaa maguo yale. Hata siku moja. Kwenye mapinduzi ya Zanzibar, mzalia wa Zanzibar, hakuaminika. Kabisaaa! Kwa sababu. Mzee Karume alisema, damu nzito kuliko maji! Mapinduzi yanataka kufanywa, wakishiriki watu Wazanzibari itavuja. Na sababu? Kuwadondowa watu wa bara. Alijuwa tu, hawa wakisema tufanye, watafanya. Mzanzibari akisema tufanye, atarudi nyuma. Na mfano mmoja ulionyesha. Hamid Ameir alisema, Muislamu kuuwa haramuu! Watu wakastaajabu. Muislamu huyu leo akaja kuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi (MBM). Imekuwa vipi? Sasa hii pesa anayokula si haramu? Kumbe ilikuwa nini? Moga. Mikidadi ni mtu wa Tanga. Songorokirangwe ni mtu wa Donge, lakini ana asili ya kibara. Mzee Karume akisema, Wazanzibari waliokuwa hawaaminiki sio nlokuwa nao mimi mikokoni mwangu. Mizizi yao ya karibu si ya hapa Zanzibar. Inatoka bara. Hafidh Suleman Mdigo yule. Bavuai yule ni mtu wa hapa, kazaliwa hapa, kama si baba yake, basi babu yake si mtu wa hapa…Hawakuaminika watu wa kusini. Makunduchi. Na Pemba ndo kabisaa! Kwenye listi ya wazee wa mapinduzi, Mmakunduchi mle hayumo. Huyu Ibrahim Amani katiwa tu. Hakushiriki mapinduzi. Kabisaa! Bambi wako wapinduzi. Bambi hiyo, Kinyasini, Mkwajuni palikuwa na wasiwasi, wakadokolewa kidugu Kidoti, wakaja kudokolewa kidugu,

Page 84: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nne52

wapi? Donge. Wakadokolewa kidugu Mfenesini. Wakaja dokolewa kidugu jimbo la kati hilo hapo, Dole hii mpaka kuja kufikia wapi? Bumbwi Sudi, mpaka Ndagaa. Kwa sababu kule ni mchanganyiko wa watu wa bara. Jimbo la Kati hilo. Sasa Wazanzibari watakuja itazama historia ya Ikulu. Kwa sababu zile picha zote zile wanajuwa huyu ni mtu wa wapi, huyu ni mtu wa wapi. Lakini wengi wao memba wa Baraza la Mapinduzi ni wabara. Mzee Thabit mapinduzi hakushiriki lakini kujuwa anajuwa. Lakini yeye huyu hakuwa memba wa Baraza la Mapinduzi. Sasa pale pameshajitenga. Sasa historia, chanzo chake, hawa kindakindaki [kutoka bara] ndo walolianza suala hili. Wazanzibari, kuwakera kitawakera lakini hilo suala limeshatendeka na wao hawakushiriki. Ndo ukweli wenyewe. Kwa sababu mgelikuwa mmeshiriki ndio. Mbona walioshiriki hawakutengwa? Ehe! Sasa watakuwa na masuala wengine watakuja kuuliza. Kama hukushiriki humo lakini mapinduzi ni yetu sote. Hukuaminika kiromoromo. Na madhehebu ya Kiunguja tunajuwana. Unamuangusha. Wengi wao watakaokuja ujuwa ukweli wataupenda, kwa sababu kuupenda kwenyewe kwa sababu nini, khasa kwa upande waliokuwa wamedhulumiwa wazee wao [wanamapinduzi]. Watasema nyinyi mnayetembea na mabenzi nyinyi bwana, baba zenu si waliofanya kazi hizo bwana! Waliofanya kazi hizo ni baba zetu sisi, lakini nyinyi mmevamia tu. Nyinyi virukia! Nyinyi bwana virukia. Sasa wale watachukia. Kwa sababu nini? Ureda. Wa bure. Sasa hawa wenye uchungu ndio watakaofurahia. Hatukufikiria sisi yatakuja kufunguka haya. Bora yalivofunguka bwana. Wanatutambia hawa bwana! Ukweli wa mambo si huu bwana. Sasa utakuja kukuta wengi wao, khasa, khususan mashamba, wengi wao, basi watafurahia. Kwa sababu humo ndimo walikotoka watu ambao walioifanya kazi hii. Mashamba. Kwa sababu hata hao watu wa bara nnaokwambia wametoka mashamba ati. Hakuna mtu wa bara aliyekaa hapa mjini. Wote wameelekea sehemu za mashamba mashamba huko. Sasa, mule wamezaliana na watoto wao. Ndo mana Joseph Bhalo akasema “nchi hii mtihani.” Kwa nini Joseph? Anasema ehe! Mmakonde songa mbele, kumalizika mapinduzi, Mmakonde kaa pembeni. Hufai. Na leo utakuja kukuta Mmakunduchi hawezi leo kujitamba kama si Mzaramu. Si kweli. Wamakunduchi wote Wazaramu. Kunduchi hii ndo walikotokea. Hii mambo Shirazi haya, Shirazi Persia…Aliomo hatoki, na asiyekuwemo haingii. Serikali watakipokea kitabu kwa mikono miwili. Watakisoma. Japo kidogo watakuja kusema “Mmhh! Hii sasaa funika kombe mwanaharamu apite, hii sasa imeshakuwa ngoma ndo hii.” Wataisoma ile historiaaa, watajuwa tu, hii ndio historia ya mapinduzi. Wanyonge kitabu kitawasaidia lakini iliokuwa mijoga na misomi watasema “mmh! Huyu sasa, bwana sasa, kula yetu sasa inafichuka sasa hapa. Hii kula sasa inafichuka hii. Tutakuja kuonekana sisi virukia sasa.” Sasa kitu kimeshatoka hakuna wa kukizuwia. Labda serikali iseme “hiki kitabu hivi kwanza bwana hapa, aa, ngojeni kwanza bwana.” Lakini sasa kikiziwiwa hapa, huko nje jee? Watu watataka kujuwa. Mbona hiki kitabu kinazuwiwa? Kwa nini? Kina nini

Page 85: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Tupendane Waafrika 53

ndani? Watakitafuta. Ikiwa watakipata Kenya, watakipata Uganda, watakipata bara. Sasa watakisoma wale. “Aaaa, serikali ya mapinduzi ndo maana ikazuwia kwa sababu kumbe haki za unyonyaji hizi kumbe hazikuanza leo bwana. Unaona watu walivowanyonya hawa? Kumbe huko nyuma kuna haki zao wameshindwa kuwapa.” Suala hilo usiwe na wasiwasi nalo. Tuliokuambia si wendawazimu. Watu na akili zetu timamu. Na hiki kitu tumekifanya. Mtu aliyefanya haogopi kusema. Anasema hivi hivi. Hiki nimefanya. Aa, hiki sikufanya. Sasa mimi ntakuficha wewe. Mwenyezi Mungu anafichika? Watu wanakufa midomo wazi. Wanasema “Ah! Mimi mpinduzi nakufa nawaacha watoto wangu maskini?” Huku walioikombowa nchi wanakula majani! Hawako radhi. Tukamate mavi kwa mkono na njia tunaiona? Hakuna hiyo. Hamna, hamna. Madam njia wazi bwana, twende njia ilionyooka, sio tupinde pinde krosi. Hamna! Watu watajiweka sawa. Ndo watakapojuwa ‘Doo! Kweli ndo hii hapa.’ Sasa hivi jamani tujirekebisheni. Haya mambo yetu tujirekebishe. Waliokueleza si wendawazimu. Watu na akili zao! Wameishi na wakayaona yale mambo yaliotendwa. Wamefanya. Madhara yake, raha yake, tabu yake…Sisi tunapokufa Wallahi tunazikana wenyewe kwa wenyewe. Sisi wenyewe tunaingia vichochoroni “bwana we, fulani keshakufa.” Tunakamatana mashati. Tukope, tunyanganye tutalipa sisi lakini yule mtu tumzike. Wakati mwengine tunakwenda kuazima sanda msikitini! Halafu tunamzika mwenzetu, halafu tunarudi tunailipa ile sanda.

Page 86: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa TanoSakura, Sadaka ya Tanganyika

Hayo ndio maumbile ya uhuru; lazima upiganiwe na ulindwe na wenye hamu nao. Uhuru wenye kupiganiwa na watu wa nje unakwenda kwa watu wa nje. —Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Mzee Mohammed Omar ambaye amehusiana na Chief Mkwawa pia anajulikana kwa jina la “Mzee Mkwawa”. Mzee Mkwawa alikuwa karibu sana na hayati Oscar Kambona na alikuwa mhusika mkuu wa kuwakusanya watu kutoka Mkoa wa Tanga kuwapeleka Zanzibar kupiga kura kabla ya mapinduzi ya 1964 na kuwapeleka wafanyakazi kutoka mashamba ya mkonge ya Tanga kushiriki katika Mapinduzi ya Zanzibar.

Madhumuni yetu ni kutafuta historia yetu ya Kiafrika matokeo yalotokea baina ya Visiwani [Zanzibar] na Tanganyika. Mwaka wa 1960 kwenye mwezi wa tisa [Septemba] kama hivi, walitolewa vijana wawili kati ya Zuberi Mtemvu na Chipaka, kuja eneo la Wete, Pemba, kuja kufanya kampeni. Hawa walichukuliwa na chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kuja kufanya kampeni ili kuonekana chama cha TANU kibaya. Zuberi Mtemvu alisema mnachokifata si chama cha haki, mnafikiri ule msikiti mkubwa ulojengwa Tanga msikiti, lakini si msikiti ule wanasali Waislamu na Wakristo. Kwa hivyo kama mnafuata TANU mmepotea ndugu zetuni, wa visiwani. Nyinyi ni Washirazi, waumini, leo mnaweza kuungana na chama dhaifu kama TANU ambapo kiongozi wao hana maadili ya Kiislamu. Kwa hivyo nyinyi ule sio msikiti na kama yupo ambaye anaweza kuhakikisha kuwa ule ni msikiti kwa hivyo ajitokeze. Kwa hivyo mimi nikaona nijitokeze. Nikasema mimi nauwelewa sana, nawaelewa watu walokuwa wameshuhudia kuwa ule ni msikiti wakaukubali. Wa kwanza ni Sultan mwenyewe Abdalla bin Khalifa ni mmoja aloalikwa kuufunguwa huo msikiti. Msikiti mkuu wa Ijumaa wa Tanga. Kwa hivyo mimi nikaeleza Seyyid Abdalla alikuwepo, Sheikh Abdalla Saleh Farsi alikuwepo, Kabaka kutoka Uganda

Page 87: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 55

alikuwepo. Naskitika kusikia ati ule si msikiti. Kwa hivyo kama sku hiyo ndipo nliposema kama ni hivyo watu hawa watatu walitanassar wakafata dini ya Kikristo. Kwa sababu wamemfata kiongozi wa TANU wa Kikristo. Kwa hivyo hapo niliona uchungu. Nikakata kadi ya Afro­Shirazi sku hiyo nikawa mwanachama rasmi. Kwa hivyo hata shughuli zangu, mimi nilikuwa ni mjenzi…kama sub­contractor nikichukuwa majumba kujengesha, nilinyimwa. Nilinyanganywa kabisa shughuli zote. Nikafutiwa. Sasa kwa Zuberi kusema hivyo alikuwa kanunuliwa. Akaona awafurahishe mabwana lakini ana hakika kuwa yeye Zuberi ule ni msikiti. Lakini kwa sababu ya mambo ya kampeni ilibidi azungumze hivyo apate haja yake. Baada ya hapo mkutano ukafungwa, watu wakarudi, na mimi nikawekwa kituoni Wete, nikahojiwa umetuharibia kampeni yetu wewe, hufai. Nikaandikwa. Nikatiwa katika Tanganyika Standard ili nisafirishwe, wakati niliishi katika hapo mahala si chini ya miaka kumi na tano niko hapo. Hapo Pemba. Kwa hivyo nilipokuwa nimenyimwa kula kitu, hata nikenda dukani kutaka kitu japo kipo naambiwa hakipo. Nikawa nadhilika, nikatafuta mashuwa, nikapanda nikarejea Tanga. Ile kurejea Tanga nikafika ndani ya mikono ya serikali, nikahojiwa, nikakamatwa immigration paspoti sina, wakati ule mkubwa wa immigration wa kwanza alikuwa Alkabeza wa Mkoa wa Tanga. Myamwezi huyu. Kwa bahati asubuhi nikawachiwa nikaja zangu nyumbani. Kufika nyumbani si nikakaa kiasi ya wiki moja ya mapumziko, nikafatwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na wazee wa TANU, nikachukuliwa ofisini, kwa Mkuu wa Mkoa, marehemu Bwana Jumanne Abdalla. Akanambia “tulikuwa tunataka mtu anaweza kuijuwa Unguja na Pemba vizuri kwa hivyo tumefurahi kukuona wewe.” Kwa hivyo mzazi wangu akanambia “utatumikia”. Kwa vile unaelewa utatumika kwenda, lolote la kule la kulielewa tukalipata sisi hapa. Kwa hivyo alikuwa mzee wangu hasa alonizaa mwenyewe, Mzee Omari, na jamaa yangu Mwalimu Mlimhere, na wengineo, kina Abdalla Rashid Sembe, kina Kisenge, waziri huyu alikuwa. Kwa hivyo nilishughulika nikaambiwa nirejee Unguja. Kwa hivyo nikakubali kutumika. Nikaambiwa utakwenda Unguja pamoja na vitu vetu, kama barua hivi, security inaweza kujuwa hizi siri, kwa sababu security ina vyombo vya mivuke, barua inachanuka wenyewe, ikasomwa halafu ikarudishwa ikafika mahala. Tunazungumzia mwaka 62. Kwa hivyo nikaanza kushughulika kwenda kule nikapeleka barua kule kama kutambulisha huyu kuwa ndiye atakayekuwa anawasiliana. Na nilifika ofisi Kijangwani. Na nikapokewa vizuri sana na wahe­shimiwa kina Aboud Jumbe, kina Saleh Saadalla, wengi tu.1

Barua zinatoka huku. Na mwenzetu, mkuu wetu wa safari alikuwa ni Master Oscar Kambona, ambaye alinichaguwa mimi na marehemu Issa Mtambo. Lakini ilikuwa lazma tukutane kule [Zanzibar]. Kwa hivyo mimi nikaambiwa nikutane na Issa na naweza mpa maelezo yangu niliyoyagunduwa mimi kule ayapeleke moja kwa moja kwa Oscar. Hata ndipo nliporudi tena ndo tukaanza kampeni ya

Page 88: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano56

kuona katika uchunguzi wetu kuiona hali ya Unguja na Pemba kwenye uchaguzi umeingiliana na Sultani kauvalia njuga. Kwa hivyo tulipata ari tukaona lazima tutetee Uafrika. Itabidi mimi nijitolee hali mali, kwa hivyo nikarudi Tanga nika­wa ambia hali ya huko ni ngumu kwa sababu Ufalme umeingilia kati. Hili suala ni gumu. Sasa lazma haya yetu tuchukuwe ziada. Kukaa kuendelea kiasi ya miezi miwili, uchaguzi karibu karibu, ZNP wakaanza kuchukuwa watu kujaza majimbo kutoka Kenya kuwatia Zanzibar. Kwa hivyo tukashtuka na sisi tukaanza kuomba misaada Tanganyika kupata watu wa kuweza kuwachukuwa na kuweza kupiga kura. Kwa hivyo tukaweza kuchukuwa watu kutoka Tanga, vijiji vyote vya Tanga, wanaojuwa lugha, lafidhi nzuri ya Kiswahili inofanana na Unguja. Kwa hivyo tukafanya hivyo. Tukachukuwa wake, waume, vijana, wavulana wanojiweza. Kwa hivyo tukapeleka Pemba na Unguja. Vijiji vya Mkoa wa Pwani wote. Mikoa ya pwani na walokuwa lugha zao mbaya tulikuwa tukishawatia Unguja tunawatia chuoni mule ndani ya nyumba tunamowaweka. Na tulikuwa tunatumia kuwapa kila mtu mwana wa Afro­Shirazi kumpa watu watano alale nao, kumi, na wanafundishwa Kiswahili safi, na kijezo kilokuwa cha madhumuni, kilikuwa ni kijezo cha kuweza kutaja “halwa”, kutaja “binzari”, “tangawizi”. Kwa hivyo walikuwa wana uhakika hawa watu wa Unguja, kuwa watu wa bara hawawezi kutamka Kiswahili kama hicho. Kwa hivyo, tulifuzu katika watu tulokwenda nao wakaweza kutumia lugha vizuri, walipita. Ilikuwa sentensi yako kabla hukiingia katika kuandika kutaka kwenda kupewa cheti, tiket ya kwenda kuvoti unaambiwa “taja suala hili, hii nini, inaitwa nini?” Majina yameandikwa. Hii taja, hii ni halwa, tangawizi, binzari. Kwa hivyo walipita. Kwa sababu tuliwafundisha si chini ya miezi mitano, sita. Tumo ndani ya kuwafundisha lugha ile mpaka wakaelewa kuwaita watu kwa lafidhi za Kiunguja, japo wengine walikuwa wakijikwara, lakini ilikuwa si rahisi kumtambuwa. Kwa hivyo tulifuzu, tukaanza kuingia. Tukakaa kitako. Sasa kabla ya kura, tulipoona kuwa sasa vipi tutapata wanachama wengi katika upande wa Pemba, ikabidi tuwalishe yamini kwa sababu wote Pemba walijihisi ni Hizbul Watan (ZNP). Wote. Kwa hivyo pamoja na ZPPP, wakijifanya wao ni Washirazi, si Waafrika.2 Kwa hivyo sasa mtu alipokuwa akitaka aingie chama, tukifanya kampeni aingie cha Afro­Shirazi, tunampiga kampeni, tunampa msahafu, aape “Wallahi Billahi Tallahi mimi nitaipigia kura Afro­Shirazi hapo kama kuna sadaka ya kumhangaisha tunampatia. Na awe ana wazimu akiiunga mkono Hizbu. Awe akili zake si timamu.” Wengine walitupigia, wengine waliona haiwezekani. Kwa hivyo tulifaulu sana, hata vijiji vilokuwa vigumu, kijiji kimoja cha Ole na Kangagani, kilikuwa kigumu sana, kwa hivyo nilikwenda mimi pale nikaitwa “Tindo.” Nikaipauwa, nikajenga shule ya pale. Pale nilifanya vituko vangu, pesa ya pale yote nikaiwacha pale. Nikawanunulia wanawake pale nguo. Nikaweza kupata wanachama pale na ilikuwa hakuna, kwa hivyo tukamwita Mzee hayati Karume, akaweza kuingia Kangagae na kufanya mkutano mkuu. Tukaipata Ole. Baada ya

Page 89: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 57

kufanya hivyo wakajuwa ni mimi nlofanya hivyo, hakuna alofanya isipokuwa yule fundi aloletwa. Kwa hivyo ikabidi mimi nitoke, nikaja kijiji cha Ole, Dodo. Pale usiku wa saa saba, nikatoka ili kufanya kampeni zangu, nikakamatwa kijiji cha Macho Mane, njia ya kwenda uwanja wa kutua ndege Vitongoji. Nikakamatwa hapo. Nikakamatwa na gari la Mohamed [Ahmed] Nassor Mazrui, ndo lilikuwa ni gari lake, na vijana kina Mtendeni, kina…wengi tu, kina Mkomi, kina Hatibu. Nikakamatwa, nikarudishwa Ole usiku huohuo. Nikatiwa kula rangi, nikapigiwa beni, nikaitwa “Kitimbakwiri cha Tanganyika”. Kwa hivyo nikakokotwa, nika­pigwa sana, na nikatiwa pilipili lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na Inspekta wa Kingazija, aitwa, kama Khamisi hivi, kile kifupi, pamoja na chini yake Master Benecto. Pilipili nilipakwa mwilini. Kwa hivyo, kupelekwa Ole, nyumbani kwa candidate [mgombea] mwenyewe anayesimamia uchaguzi, yule ndiye atakayechaguliwa, Sheikh Rashid Hamadi. Wakaanza kupiga kelele wakamwita kwa jina lao la kichama “Ya Zaim!” Wakapiga kelele “Hayyen na Mkashkash!” Kwa hivyo tumekikamata hichi kitimbakwiri. Mimi nikatamka, nikamwambia “nakusikitia Sheikh Rashid hujapata kutawala unaanza kuuwa. Ukitawala utakuwaje? Wewe unaamrisha kikundi hiki kinikamate na kunitesa.” Kabla ya hapo, baada kumaliza hapo, wakaingia yule Inspekta pamoja na wa chini yake, Master Benecto, wakamwambia “unafahamu suala, kitendo kinopita kisheria unawezekana kuwa kesho usisimame kwenye uchaguzi? Kwa hivyo hichi kitendo kiondoke.” Kwa hivyo Sheikh Rashid akatowa amri palepale “mwachilieni! Mimi wala sikuwatuma nyie. Mmejifanyia kwa hamasa zenu na ari zenu za siasa tu, lakini mimi siwezi kuamrisha kitendo kama hicho cha haramu.” Kwa hivyo nikaachiwa, nikarudi, nikapelekwa hospitali Chake Chake, nikahudumiwa na kijana, huyu alikuwa ni dresser msaidizi wa daktari, anaitwa Hassan Al Maardhi, wa Mtambwe kwao. Kwa bahati palikuwa na daktari mmoja wa Kiarabu, Dr Mahfudh, kwa hivyo alisaidia sana, nashkuru. Nikatiwa malhamu, nikatoka malengelenge, majimaji kwa lile joto la pilipili, na mpaka leo mbavu, hivi nnavozungumza hapa, mpaka leo mbavu huwa zanibana bana, kwa sababu zisizokuwa za kawaida—pilipili. Kwa hivyo nikaachiwa. Kuwachiwa, sasa mimi wakanitia moto zaidi. Hapo nikapamba moto. Nikachukuwa hatua kubwa sana ya kuigombania Afro­Shirazi kuliko hapo. Ndipo nilipoweza kuja huku, nikarudi Tanganyika, nikaanza kuchukuwa watu kwenda fanya kampeni, nawaorganise [nawapanga] watu…nikisha waorganise nawachukuwa nawapakia ndani ya magari, watu wa town [mjini] pale, na branch [tawi] yangu ilikuwa ni ile ya chama cha Wazungu, Magiriki, barabara ya kumi na nne.3

Kwa hivyo nikashirikiana na Chama cha Wafanyakazi [Tanganyika Federation of Labor] kiongozi, Bwana Victor Mkello. Kaweza kunikusanyia watu kufanya kampeni na kuweza kupata watu nikawa napakia hapa nenda nao kutoka [barabara ya] kumi na nne Head Quarters [makao makuu] nenda nao moja kwa

Page 90: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano58

moja napita njia ya Pangani, kijiji cha Kipumbwi.4 Nilikuwa nikipakia ndani ya mabasi yanoelekea njia ile ya Pangani na kutoka mashamba ya mkonge. Mabasi kutoka Tanga yalikuwa ni gari ya Abdalla Saidi, marehemu sasa, magari yakina Hashu Sleman, mabasi ndo yalokuwa wakati huo yapo. Na magari mengini yoyote, yoyote yale, yanoelekea njia hiyo walikuwa watu wanarukia. Hata magari ya mizigo. Sio lazima basi. Kwa hivyo nikatia watu kwenda kuandikisha na kuwarudisha na kuwapeleka tena, kutegemea chaguzi. Tulifanikiwa, na kuwatia watu kama walivofanikiwa wao Hizbu. Kwa bahati tukafuzu. Tukapata viti va kutosha. Ikawa viti vilivotuangusha ni viti va Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP), viti sita. Tukasema, tutafanikisha. Tukamfata mwenzetu Mohamed Shamte, tukamvika buibui, tukaja naye YASU, mpaka kwa mkwewe Othman Sharifu. Akatujibu kuwa “hata mkinipa utume sitaweza kuwa pamoja na nyinyi.” Maneno hayo aliyasema nyumbani kwa mkwewe, Othman Sharifu. Na juhudi hizo zote alizifanya Othman Sharifu. Kumchukuwa mkwewe, akashirikana na wenzake kina Mdungi Usi, kina Saleh Saadalla. Karume akajitolea kuwa uongozi wote nitakupa wewe, mimi niwe chini yako, au niwache kamwe, niwe mtu wa kawaida lakini serikali iongozwe na Waafrika. Shamte akakataa. “Hata mkanipa utume,” nasema tena.5

Shamte alisema sitaki tu kuungana na watwana kama nyie. Sababu zake hatukuzielewa.6 Lakini mwanawe Baraka tulikuwa naye ndani ya chama. Katika watoto wa Shamte wote walokuwa mstari wa mbele ni Baraka Shamte. Ndipo ilipofanywa “coalition” [kuungana] ya kuunga chama chao, iwe siku hiyo ndo walete taarab kutoka Cairo, na wageni mbalimbali wa Kiarabu, na Waarabu wengine wa Pangani, na Ithnaasheri wengine wa Pangani. Walihudhuria. Mimi nlisema, hapa niliwaokoa hawa watu, nikawatetea kwa vile hawajitambuwi, nikawaona kama wapumbavu tu kujitia ndani ya mambo yale, kwa vile nawajuwa ni watu wa huku Tanga, niliwatowa Raha Leo. Nikalala nao kama wiki mbili tatu hivi nikawasafirisha wakarudi Tanga. Kwa hivyo niliwasaidia. Na niliporudi Tanga walinishukuru kwa kuwasaidia kuwatowa katika nakama kama hiyo. Na huku tulikwisha unda huku nyuma tukishindwa tufanye nini. Kwa bahati mbaya walieka kuwa, tarehe kadha walipanga ndo waanze kusheherekea hivo vitu. Kwa hivyo Afro­Shirazi ikajiandaa. Lolote litakalotokea, lakini serikali tuchukuwe. Kwa hivyo ndo vijana wakajitolea, kuvamia serikali wakaingia Ziwani, wakaingia Mtoni, Magereza, Raha Leo. Tukakaa ndani ya muwafaka wetu tukafikiri, katika huo muafaka, tukafikiri nani atakoweza kuleta tishio, ndio tukamchaguwa John Okello, kwa sauti yake ya kibara mbaya, ya kutisha, hajuwi kusema vizuri, itawatisha Wazanzibari. Huyu John Okello akifanya kazi kwa Ahmed Nassor Mazrui. Na alikuwa ni mgeni kutoka Uganda. Baada ya mapinduzi, kupinduwa, kufanikiwa kwa magongo yetu, tulipanga askari wa polisi, magereza, tulikuwa na vijana mule ndani, tuliwachomeka wajifanye ni ZPPP wapate kazi, ili tupate usiri wa ndani. Kwa hivyo walitusaidia

Page 91: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 59

sana. Wakati hawa wanakwenda kufurahikia furaha yao huku nyuma tulikuwa tuna mabaruti yetu, tukayatia katika mageti. Muafaka wetu ulikuwa ni usiku wa manane. Tukafyatuwa, tukawasha, boma la Mtoni, likaripuka, vijana maskini walokuwa wamewekwa na Hizbu, vijana wadogowadogo. Wakashtuka, vijana wa Afro­Shirazi wakaingia ndani wakavamia wakachukuwa silaha wakaanza kuteremka kwenye starehe. Tukateka. Kwanza ilianguka Mtoni.7 Yale mabomu zilikuwa ni tambi za kuvunjia mawe majabali ndo zilochomwa katika mageti. Tambi zimechukuliwa kutoka Tanganyika. Tukazipeleka. Kisiri chetu, bila ya serikali kuelewa. Mkono ni Tanga, mapitio ni Tanga. Na wengine kutoka Bwagamoyo, akawa ni Abdalla Kheri, kijana wa Unguja. Abdalla Kheri alikuwa akipeleka watu. Alikuwa mfanya kazi bandari Dar es Salaam. Lakini kwa hamasa ya uchungu wa kampeni kwa kuwa ni mwananchi alijitolea. Alikuwa anachukuwa watu kutoka bandarini, vijana wa Kiunguja, na vijana walio bandarini Dar es Salam, na vijana wa ki­Dareslam, wanaojuwa lafdhi nzuri. Akawapeleka Unguja na akawatafutia malazi pale mpaka siku za uchaguzi, mpaka mapinduzi. Basi kwa hivyo tukafanikiwa kupata serikali. La ukweli, utaweza kuona kuwa wengine hawaelewi, wakaona ramda Waunguja ndio msaada wamejitegemea wao peke yao kwenye mapinduzi. Lakini utakuta si kweli kwa sababu kama ni WaUnguja wenyewe hawawezi kitu. Kwa sababu kwanza ni waoga. Hawakuzowea mambo ya harakati. Kwa hivyo ilikuwa kama ni wao ilikuwa haina maana kwenda kusaidiwa kuandikisha kura, wala kusaidiwa Wamakonde kujitia, vijana kupinduwa, wakashirikiana.8

Kuna Wamakonde walokuweko kule, kuna Wamakonde walotoka Tanganyika. Na walikuwa wanatoka sehemu za Sakura, wanatoka Ruwazi, Amboni, makabila mengi tu.9 Kulikuwa na Wamakonde, Wangindo, Wayao, Wamwera, Wahehe, na Wanyamwezi wengine, wengi tu. Kama akina Khamis Darweshi ni Myao, Mohamed Kaujore, Mohammed Mfaume, Mmakonde, watu wa Mtwara. Kwa hivyo hao wote Mungu aliwajaalia mapinduzi walipata nafasi ya kupata vyeo. Technique [mbinu] za Afro­Shirazi ziliwafanya wote wapewe uwenyeji, uzalia, wawe ni wenyeji. Wanapewa mababu, wanafundishwa kupewa babu, na kumtambuwa Sheha wa zamani. Yule Sheha aliopo sasa, apewa Sheha wa zamanii asema “wewe ni mwenyeji.” Haya yalikuwa ni mahoji ya katika kupiga kura, kufanywa mtu mwenyeji. Unaambiwa “Sheha wako nani.” Fulani, Magaramwadi aliyemzaa fulani ndio babu yake fulani. Yule Sheha aliopo akitajiwa yule anaunganisha. Hawezi kuhoji. Katajiwa babu yake. Kwa kuona Tanganyika, visiwani, wote wanodai uhuru ni Waafrika, kwa hivyo walikaa viongozi wakawa wanakutana. Tutashinda au tutashindwa. Tukishindwa tufanyeje. Ndipo wazee wakakaa kitako wakaziba macho yao, na mashikio, wakaweza kuwaachia vijana walio na ari kuingia. Wakati huo kulikuwa hakuna serikali ya Tanganyika. Kulikuwa na serikali ya kikoloni, haijahama. Mwaka 61

Page 92: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano60

Tanganyika inapata uhuru wake, kwa hivyo ikafumba jicho, ikawaachia uhuru bahari ile, vinavyokwenda, madhali vinakwenda upande wa Afro­Shirazi watu wazibe macho wasione, wala nini. Ili kuwapisha Waafrika wapate hatuwa ya kujitawala. Kwa hivyo, vijana waliingia, na shauri walikaa kitako, tukishindwa walikaa pamoja kupeana mawazo. Tufanyeje mpaka tushinde? Hakuna. Waka­amua hakuna. Kama hakuna tukiwavamia WaUnguja wana kitu gani? Basi, kikatokea kikundi, kikakaa kitako, cha Makomred na Youth League. Vijana wa Youth League ni vijana wa Afro­Shirazi. Wakaamuwa twajitolea, hali, mali. Nafsi zetu. Kwa hivyo wakaanza, ndipo kilichopangwa, hapo tena, kikundi cha kuingia watakuwa hivi, hawa watakwenda Bomani, hawa watakaa boma hili. Ikapangwa, ikaenea. Sasa ikawa watu wanakula doria katika sehemu zile kutizama utaratibu. Wakati huu vipi, kuna nani, kuna walinzi gani? Kwa hivyo wakapata fursa. Wakajuwa kumbe tukija hivi tufanye hivi, tutafanikiwa. Lakini humo ndani tuna watu pia, wanojuwa hilo litakalotokea, katika hiyo hiyo serikali ya Mfalme, kuwa kuna watu wetu. Kina marehemu kina Sheikh Daud Mahmud, kwao Kilwa, ni katika hao. Watu wengi karibu Unguja wamechangia suala hilo. Vimezikwa vitu tu mpaka njia za panda. Katikati. Watu wamepiga makafara ya kuwashona paka macho. Nia kubwa Waarabu wapumbaye serikali. Wasiwaze kabisa. Wadharau kila kitu. Hilo ndo lilofanikisha. Hakuna kitu kengine. Kikao kikuu cha kuweza vijana kuchukuwa mazowezi, wa kibara na wa kisiwani [Zanzibar], pamoja, yalifanyika mbuga ya Sakura. Tukichukuwa askari waliowacha vita, walostaafu, tukawapa bunduki, nne, tano, huku na kule, kufundisha namna ya kufetuwa bunduki. Japo ilikuwa hatuna bunduki lakini ilikuwa hayo mazoezi yalifanyika, pamoja na kina Jimmy Ringo [ Juma Maulidi Juma]10 wakishaona kuwa hatuna vitu va kuvipata, ndo tulipoamuwa, tutakapovamia, tunapopata bunduki, iwe wawili watatu, wanaweza kuzitumia. Walikuwapo watu kama watu mia na hamsini kwenye mbuga. Walikuwa wanakwenda kikundi cha watu kumi, wanarudi, wanakwenda wingine, wanarudi, sio wote kwa pamoja wanashughulika hizo habari. Waloonekana wameshajuwa wanakwenda zao. Wanavushwa wana­kwenda zao. Walozowea wanavushwa wanakwenda zao. Hawana silaha, hawana chochote. Kitu kilichotumika kupinduwa serikali ni mapanga, shoka, misharee! Na pinde hizi. Na hivo vimetoka ndani ya Zanzibar na Tanganyika. Vimenunuliwa na wakapewa watu. Walikuwepo kina Jimmy Ringo, akina Khamisi Hemedi, na vijana wengine. Viongozi wakubwa ni hao. Tulikuwa katika mwaka 1962, Jimmy Ringo alikuwa yuko Tanga barabara ya kumi na tatu kwa Fundi Kidere, halafu akarejea kisiwani Zanzibar. Ndani ya kufanya organisation [mipango] ya mapinduzi ikabidi yeye achaguliwe awe Sakura, yaani kuwashughulikia vijana watakaokwenda kupinduwa serikali ya Zanzibar, kwa hali na mali, wakiwa hawana silaha yoyote isipokuwa mapanga, marungu, mashoka, pamoja na wenzake kina Musa Maisara

Page 93: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 61

na Abdalla Kheri. Musa Maisara alikuwa ni kiongozi mkuu, wa pili ni Jimmy Ringo. Abdalla alikuwa akitokea katika safari zake Dar es Salaam anakuja Tanga, anafika Sakura, halafu yeye alikuwa ni msafirishaji pia vijana kutoka Bagamoyo kupitia Fumba, akaingiza mjini Zanzibar. Usaidizi wa kuweza kupinduwa serikali. Alipokuja Jimmy Ringo Tanga pale mwanzo mbuga ya Sakura ilikuwa haijaanza kufanya kazi ya maandalizi ya mapinduzi. YASU [Young African Social Union] ilikuja Tanga 1962 ili kuisadia Afro­Shirazi kupata pesa kwa ajili ya matumizi ya kampeni ya uchaguzi, badala kuwa kama tutashindwa ndio tukakaa kitako kikundi maalum, halafu ndipo tulipoamua tufanye hivo vitu. Uamuzi wa kuijenga kambi ya Sakura tuliufanya kiwiziwizi tu kwanza bila ya kufahamika, baada ya kufahamika sawasawa ni kwenye 1962 mwishoni. Kufikia 1963 watu walikaa wako tayari. Palikuwa na historia. Ile historia ilihusikana na kina Jumaane Abdalla, Regional Commissioner wa hapa, kuamua kuweka Sakura kwa kuwa ni karibu na Kipumbwi, pa kuvukia kwenda Zanzibar. Watu wakitoka pale waingie mojamoja kwenda zao, bila ya kuingia mjini tena. Kuhusu Sakura nilikuwa nikifahamu, kwa sababu nimefahamu kutoka kwa Jimmy Ringo na Musa Maisara, na kujuwa pia kwa kamati nzima kuwa [mimi] ni mbebaji wa watu kuwapeleka na kuwarudisha Zanzibar. Uamuzi mkubwa ulikuwa na kina Jumaanne Abdalla, mimi pia mawazo ya kupatia pesa, nauli, na nini, nachukuwa kwake. Hayo yalikuwa na watu wenyewe wa Jamhuri. Yako juu hayo. Vitu vote ni ngazi za juu kuanzia marehemu Nyerere, Kawawa, Kambona, Serkali nzima inajuwa hapo Sakura, na inajuwa, kwa sababu ilikuwa ni intelligence [usalama] ni siri kabisa. Kwa hivyo hivi vitu vinajulikana juu. Kwa sababu wasingeliweza kuwepo pale bila ya ngazi hizo hazielewi. Na sisi tunaelewa, mimi naelewa, kwa sababu ndizo ngazi zilikuwa lazima nizipitie. Kambona ndo alokuwa kiongozi wangu. Kwa sibabu yeye alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani. Ndo aloweza kutoa authority [amri] ya hii bahari kuitumia. Na nikapewa kiwango nikifika Chumbe pale mpakani basi huko litakalonikuta ni langu mwenyewe. Lakini huku nna hifadhi ya kupewa, wakati kule bado hakukuwa tayari na utawala. Mara ya mwanzo kusikia habari ya kambi ya Sakura ilikuwa kutoka kwa Maulidi Sheni na yule Mzee, Victor Mkello. Kwa sababu pale ndo ilokuwa kambi kuu. Pale ndo wafanyakazi wa mashamba ya mkonge walikuwa wakipelekwa. Kwa sababu pale ndo ilikuwa kambi kuu. Matajiri wa mashamba ya mkonge walikuwa ni Magirigi na Wahindi walikuwepo, akina Karimjee hawa. Kazi ya Chama cha Kazi kilikuwa kinakwenda kuchukuwa watu, watu wawili watatu, lakini wasikatwe mishahara yao. Katika wafanyakazi wa mashamba ya mkonge walokwenda Zanzibar walitokea sehemu za Tanganyika zaidi ni Wamakonde, Wangoni, Wahehe, Muha, Wahyao, Wahaya, ni mchanganyiko wa makabila. Walikuwa wanachukuliwa hawa watu

Page 94: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano62

ikiwa wao wenyewe matajiri pia hawajuwi, walikuwa ni wasimamizi tu. [Matajiri] hawajuwi. Kwa sababu yeye achukuliwa mfanya kazi, yeye ajuwa mtu fulani hakuja kazini, ndani ya master roll [daftari la kuhudhuria kazi] wamejazwa. Tajiri yeye hawezi kujuwa. Hawajuwi matajiri. Lakini makarani wale wakubwa, kama mameneja, wakielewa. Kwa sababu msiwakate hawa, wanakwenda saidia umma. Maulidi Sheni khasa yeye ni mtu wa Unguja. Kwao ni Mlandege na nyumbani kwao palepale. Huu mti, ule Mlandege wenyewe uko chini ya nyumba yao. Kwa upande wa mama, nafikiri ni mtu wa Uzini. Yeye msomi. Yeye kenda mpaka Ujerumani bwana. Huyu alikuwa kwenye utawala. Utawala ndo usomi wake. Si alikuwa ni katibu huyu, wa Victor Mkello. Wenzake Maulidi Sheni mmoja ni bwana mmoja kwao Pongwe, ya hapa Tanga, lakini yuko Dar es Salaam. Alikuwa chini ya Maulidi Sheni. Huyu yuhai. Anakaa mtaa wa Magomeni pale. Tukimpata huyu atatwambia katika lile tawi lao. Wote ni wa Chama cha Wafanyakazi na wao ndio wakusanyaji. Victor Mkello alikuwa na Kambona, na mwengine marehemu ameshakufa, ni Issa Mtambo, wa hapa huyu, kwao ni Korogwe. Na huyu ni mmoja alohusika hapo. Ndo alokuwa akigawa mambo ya pesa. Akichukuwa kwa Kambona. Nyerere ilikuwa si rahisi yeye kuja kwenye mambo kama haya. Wengine waliowahi kufika Sakura ni akina [Mustafa] Songambele, kina Mzee Jangukire, John Rupia, walikuwa mstari wa mbele hao. Wao ndo walokuwa mstari wa mbele wanopanga. Songambele, alikuwa ni Area Commissioner wa Dar es Salaam. John Rupia ndo mwenyewe, ndo alokuwa tajiri kwa wakati ule, kifedha. Alokuwa IGP, Mzee Hamza Aziz, akijuwa. [Kwa upande wa Zanzibar] Kinyasini kuna ithbati ya makabila. Wanyamwezi walikuwepo pale wengi, sasa na wale wanokuja ile siri itakuwa imefichika. Kwa sababu wote walikuwa ni vijana wa Afro­Shirazi. Kulikuwa hakuna tafauti. Ukiingia ulikuwa unajulikana kuwa huyu si wetu. Ndo walokokuwa akina Saidi Washoto, na nani, na nani. Kifikra na kikubwa ilikuwa, kikambi pale [Sakura] watu walipokuwa wamekaa, tunapoingia, Mungu katusaidia tumeweza, tunapovamia, kwa sababu Waarabu wametuuwa, ili ndipo tulivoweza kupata kutawala pale, kwa sababu wametutia minyororo, wametupofowa macho, wametufanya ngombe kututoa khaswa, wanaake zetu kupasuliwa mimba kuonyeshwa watoto, kwa hivyo na sisi nasi tuwafanye hivyo, waone uchungu.11

Wakiona wale watoto wamepasuliwa, mke kapasuliwa na tunamwita mtoto wa Kiafrika, yamefanyika hayo, yamefanyika hayo Unguja, yamefanywa. Kuwa bibi njoo hapa uone mtoto anavokaa ndani ya tumbo. Nani asojuwa Unguja. Walofanya wamefanya. Kwenye vikao vyote walikuwa hisia hiyo wanayo. Ipo tayari. Hiyo ipo. Kusimama [mapinduzi] lililetwa kundi kutoka Tanganyika, la Field Force. Likasimamisha vile vita. Matatizo kutuliza. Hilo ndilo lililotuliza na kuondoa

Page 95: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 63

wakabaki memba tu wa Baraza la Mapinduzi, kuna chuki sasa za moyo, wakiwaona watu wamekaa au wanasali kuwapiga risasi bure. Yaani ni uwehu tu. Ufahari wao wenyewe, mwenye akili chafu, kutumia vile vitendo. John Okello ni mtu alochomozwa lakini hakuwa kiongozi. Ni jumla ya hiyo akili chafu. Kwa sababu mtu mmoja huwezi kupinduwa serikali. Pasipokuwa aliona katika yale mapenzi anopendwa, akajiamini, lolote anaweza kufanya na akaskizwa. Hatukutaraji kuwa atakuwa hivyo. Ni mtu aloletwa tu. Okello hakufika Sakura. Alikuwa hajuwi. Kama aliambiwa aliambiwa tu watu walivokuwa wanakutana katika vikao. Hakufika hapa kwa sababu namuelewa alipokuwa Vitongoji, Pemba, kwa Ahmed Nassor Mazrui. Na kazi yake alikuwa akisonga matumbawe ya matofali, lile kulichonga likaelekea. Ukweli alikuwepo Vitongoji. Yule Okello alikuwa ni fundi wa matofali wa Ahmed Mazrui. Nafikiri Ahmed Nassor kapata tabu sana. Kafungwafungwa sana mpaka ukiwa na imani yako unamuonea imani. Sasa sijui alikuwa naye ana siri gani baina ya Afro­Shirazi na Hizbu. Kwa sababu baada ya serikali kawekwa mstari wa mbele kapewa contracts za Zanzibar yote. Mashule yote anajenga yeye. Toka ukoloni ajenga hayo na hii kapewa, bila ya bughdha. Lakini ikitokea struggle [mapambano] atiwa ndani. Kapata tabu sana yule. Kama ni mchoraji unaichora ile kambi ya Sakura, watu walikutana hapa kisirisiri, wakawa wanakaa sirisiri, sehemu ya mazoezi kwenye msitu huu, kulikokuwa wazi, hapa ndo walikuwa wanapata chai (mkahawa), wanachomoka mmojammoja wanaingia baharini, mpaka wamalizika, waingia ndani ya vyombo hivyo, wanakwenda. Usiku mnalala kujifichaficha, kuziba siri zenu zisitangae. Lakini fununufununu, serikali yenyewe ilikuwa haijatimia hivyo. Je, Muengereza keshatoweka kabisa? Lawama, kuwa hawa wanakwenda ingia nchi ya watu.12 Nafkiri nlikwambia unapopewa barua hapa kupeleka Zanzibar, waambiwa, ukikamatwa wewe ukubali kufa, hii izamishe, isipatikane. Barua zilikuwa ni za mazungumzo na mipangilio. Zinatoka serikalini huku. Kutoka kwa Oscar na yeye inatoka kwa mwenyewe kinara, inakwenda kwa kinara cha kule. Hizi si za chama. Ukifika moja kwa moja unampa Aboud Jumbe au Hasnu Makame. Mipangilio ile ya huku na huku. Mimi nilikuwa sielewi ndani mna nini. Mimi kazi yangu kufikisha mzigo. Nyengine ni fedha. Kuwasaidia wale viongozi wanapotaka kusimamia kura. Zamani pesa zilikuwa zikitiwa kwenye ile mifuko ya kuvuta ya nguo. Barua za Abdalla Kheri zinatoka Dar es Salaam. Na yeye alikuweko katika Chama cha Kazi, pia huyo. Chama cha Kazi ndo kimefanya kazi kubwa! Chama cha Wafanyakazi ndo mstari wa mbele. Mkubwa wao yule pale Victor Mkello. Na yule kapata cheo cha kuwa Regional Commissioner, kama si Regional Commissioner…kwa sababu ya chama, kwa sababu ya wale wafanyakazi wa mkonge walokwenda pinduwa Zanzibar, akapewa uwezo na madaraka. Akazidi kupanda hadhi. Uongozi wote unatoka kwenye Chama cha Wafanyakazi, pande zote mbili. Si ndo walokuwa

Page 96: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano64

wakichanga pesa wakikamuliwa. Mkello akafungwa. Inasemekana alihusika. Ndo maana akafungwa ati. Sasa tumpate kijana wa Pongwe, mimi nimuone Makalo nimuulize, alochaguliwa katika Bunge wa kuteuliwa na Nyerere wakati ule. Sasa nimuulize yule bwana alokuwa katika chama cha kazi, Abdulrahman nafikiria hivi, yuko Dar es Salaam au yuko Mazazara, Pongwe? Wako wengi tu walokuwa kwenye chama cha kazi wenye kumbukumbu ya mapinduzi ya Zanzibar.13 Wafanyaji kazi wa mashamba ya mkonge hawakupelekwa Zanzibar kama ni Manamba. Wamenyokolewa tu kwenye mashamba ya mikonge tafauti, wawili watatu, wamekubaliana, nikawatia katika chombo mpaka Zanzibar. Ndivo ilivokuwa. Baadhi yao ni hao hao Wamakonde wanaokataa. Mwisho wengine waliozwa watoto wa kike wa Kiarabu wakaja nao ndani ya meli hapa katika kile kipindi kilichovusha Waarabu wengine wakarudi Oman, wengine katika hao Manamba wakateremka hapa wakenda mwakwao. Sasa unakuta wale walipokwenda, sasa wale wengine walibaki wakaoa. Mmoja tulikuja nae mpaka hapa na mkewe, Mmakonde, wakenda zao. Baadhi ya hao Wamakonde na makabila mengine yalokwenda wapo hapa Tanga. Wamakonde waliokuwa wakiishi Zanzibar nawajuwa na kweli walikuwepo. Wale walikuja zamani. Walikuweko. Walokwenda walikamatwa kwenye ma­shamba ya Mkonge. Hawakwenda kwa ajili ya kufanya kazi za Manamba Zanzibar. Walikuwa Manamba huku. Zanzibar walichukuliwa kwa kwenda kusaidia mapinduzi tu. Hakukuwa na utaratibu wa Manamba Zanzibar. Ukenda ukawauliza watu wa Mwera ya hapa Tanga utapata habari zao na utawapata. Hapa ukimpata yule Mmakonde alotiwa upande wa jeshi akaowa mke wa Kiarabu na marafiki zetu wa Kimakonde, na makabila mengine, walioko huku wanayafahamu haya. Walioko Unguja wanaweza kukataa kwa sababu hakuna alochukuliwa pale. Lazma wakatae. Kwanza walikuwa woga. Walishiriki wengine lakini ki organization [kimipango] walikuwa hawamo. Kwa sababu walikuwa walinzi katika mashamba ya Waarabu. Wataunga vipi? Victor Mkello ni mzuri sana kwa habari hizi lakini na yeye ndo vile, sijui ana woga gani. Alitiwa ndani yule ndo mana. Ana woga yule. Ukenda kuwauliza wenyeji wa pale pale Kipumbwi karibu na shamba la mkonge la Sakura, wangesema kweli watu waliondokea hapa. Pale pale. Leo mwana TANU wa hapa hawezi kusema hajui suala hilo. Wanaweza wengine wakawa woga lakini wapo wanaosema. Ningekueleza Unguja au Dar es Salaam mbele ya [Shaaban] Mloo basi Mloo angekuambia kuwa ni kweli. Angelikuambia kuwa huyu ndie alokuwa akiwasafirisha. Manake walikuwa wanapigwa kampeni, ewe bwana tuna kazi yetu twende Unguja ukatusaidie. Kulisha na mpaka kula na gharama kila kitu zilikuwa zinatowa TANU. Marehemu Jumaane Abdalla alokuwa Regional Commissioner [Mkuu wa Mkoa] hapa ndo alokuwa anotukusanyia hapa halafu tunakwenda. Na yule alokuwa Area Commissioner, Issa Mtambo, naye amekufa. Yule alitolewa kama security [usalama] akakaa mtaa wa Malindi, akawa anasali

Page 97: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 65

msikiti wa Malindi, kuchunguza wanazungumza nini. Alikuwa karibu na Sheikh Abdalla Saleh Farsy, kasoma vizuri, kajitia imamu kuchunguza. Ukweli ni huo.

Wafungwa wa Siri Nzito ya Historia

Nyerere ndie alokuwa akifanya organisation [mipango] yote na kuweza kuwafanya watu wapinduwe serikali ya Zanzibar. Yeye Nyerere. Sasa yeye akaona akifanya historia, kumbukumbu, anaogopa Umoja wa Mataifa wa ulimwengu wakamuelewa kuwa yeye ni kitimbakwiri…Ile ni siri yake. Hakutaka siri itoke. Ingekuwa aibu kwake. Anasikia lawama litamfika kubwa. Kwa sababu halafu si unamuona ataka utawala uje kwake. Yeye ndo awe leader [kiongozi]. Yeye si ndo alotaka Regional Commissioner [Mkuu wa Mkoa] wa Zanzibar aje Tanzania, Regional Commissioner [Mkuu wa Mkoa] wa Pemba aje mkoa wa Tanga. Yaani aichukuwe Zanzibar kimaarifa. Alikuwa keshaanza zamani sana, baada ya mapinduzi tu. Akakataa marehemu Karume. Akatia guu. Akasema, “mimi nikiingia Zanzibar, ni Rais kamili,” kaannounce [akatangaza] hasa mwenyewe kwenye mkutano: “Nikishafika Chumbe, nikipita ninakuwa ni Makamo wa Raisi. Na yeye Nyerere akiingia Zanzibar lazma aniskize mimi huku kwa sababu mimi ndo Rais wa Zanzibar. Na sina haja ya uchaguzi kama anavotaka Nyerere. Au mnasema nini wananchi? Muangalieni yule mtoto Nyerere, anataka uchaguzi ati, Zanzibar. Mimi nimeshachaguwa Januari. Mnakubali wananchi au mnakataa?” “Ndiooo!” Sasa alikuwa ana maana gani? Mie hasa usinikumbushe mambo ya Nyerere. Akaingilia Uganda. Uganda rafiki yake Obote kwa kuwa ni Mroma mwenzake na yule Idi Amini ni Islamu, akaona ampe uwezo na awauwe watoto wetu hapa kuwapeleka Uganda, hakuna maana yoyote aloyafanya. Wale pale wako. Hawana macho, masura mabaya, wazazi hawakupewa single penny [hata pesa moja] kwa mchango wao walioutowa. Hawa wasojuwa ndo wanamuona Nyerere ni binaadamu. Sasa watu wamepata maradhi yale, wote wanakuwa waoga. Wanaiona serikali hii ya Tanzania tukifanya historia tutaingizwa ndani, tutapoteza maisha yetu. Ndo woga wote wa kina Mkello. Kwani watu hawajuwi? Hakuna hata kimoja kisichojulikana. Sasa ile kutishwa. Unajuwa unapopelekwa ndani ya nakama, ukitolewa, una hofu. Sasa ukitupwa namna ile alivotupwa Mkello, ukirudi, unakuwa umefungwa. Yeye yule hayuko huru pale. Anamuogopa huyu alorithi [Benjamin Mkapa] mwanawe Nyerere. Akili zao si moja tu. Nini maana ya kumchaguwa lazima achaguliwe Mkapa? Si kampigia kampeni yeye? Njia yao moja. So Mroma mwenzake? Nakwambia, kamlea mwenyewe. Watu wengi wanasema. Huko uliko hujajuwa kuwa Nyerere anaikwamisha hii nchi? Nyerere alichukia baada ya kuokolewa na Kambona nchi ilipochukuliwa na

Page 98: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano66

jeshi. Alikuwa amekwisha Nyerere. Alikwisha! Yule akalituliza lile jeshi. Sasa Nyerere akaona doo! Hivi mimi si lolote, si chochote, mbele ya huyu? Wakati wowote, mimi nimeshindwa kulisimamisha. Huyu kasimamisha kama kunusa? Akapata nafasi ya kukimbia akenda akakaa kando!14 Nyerere akaona huyu, bila ya kumtia query [kumdhania dhana mbovu], bila shaka walikuwa pamoja. Kambona akaona anusuru roho yake akapotoka. Na wengine wale waliotaka kumpinduwa Nyerere 1964 wajomba zangu. Mpaka leo mjomba wangu yuko. Huyo alotaka kupinduwa. Utapata tabu sana kuyapata yaliyotokea. Yataka kula mmoja umtekenye, atowe kidogo. Wengi walioshiriki katika mapinduzi si Wazanzibari. Kwa mfano, Khamisi Hemedi Nyuni kwao hapo Kivumbitini [Tanga]. Si ndo mana nikakuuliza wepi? Yusuf Himidi yule ni mbara lakini kazaliwa kule. Ni mtu wa Pemba. Wengi wao ni wabara. Mbona unajuwa ulimwengu mzima, mapinduzi ya Zanzibar headquarter [makao makuu] ni Tanga? Wengi wanajuwa Unguja. Si unawaona viongozi wa CUF? Juma Ngwali, anajuwa. Mzee [Shaaban] Mloo, anajuwa. Ni mmoja katika chama cha kazi huyo. Kwanza Mloo mimi nikimpata aweza kuntosha. Nitamwambia “komredi wewe umeshakuwa mzee, ukifa kufa, na mimi ndo hivo hivo. Kwa nini tunaitupa historia?” Katika CUF wako wengi tu. Yuko yule bwana wa Donge yule alokuwa polisi [Machano Khamis Ali], yule alokuwa mwanasheria, Ali Haji Pandu, anajuwa. Na ni wenzangu hao.15

Serikali yenyewe ndo ilogoma kuweza kupata lawama. Kuambiwa ni chanzo cha vita, uchochezi.16 Linoogopwa hilo tu. Hakuna jingine. Sasa imewabana watu kuwa ukiitowa siri hii basi mawili yatakukuta: kifungo cha maisha au kunyongwa. Sasa hivi haidhuru. Ilikuwa ikitisha kwa Nyerere tu alikuwa haitaki. Wote wasomi sasa hivi. Sasa hivi watu wote wasomi. Ni kumbukumbu za hawa wanosoma. Hawa watoto wanosoma hawa. Jimmy Ringo alikuwa mtundu bwana. Alikuwa ni mtu matata. Katili. Kulikuwa na bwana mmoja, Abdi Tarazo, alikuwa akitia tarazo. Huyu aliwahi kusafirishwa. Badala ya kupatikana serikali alitiliwatiliwa maneno kwenda kinyume na serikali, Zanzibar, hiihii Afro­Shirazi, wakamsafirisha, wakamrudisha kwao Morogoro. Alikuwa ni kijana wa mapinduzi. Alishiriki kwenye mapinduzi vizuri tu. Aliku­wepo Sakura. [Kama nilivoelezea kabla] mimi niliporudi kuchukia kisiwani, nirudi niondoke kisiwani Pemba, nikaja zangu Tanga, nilipofika Tanga, nikakaa, ndipo nilipopewa uwezo wa kuweza kuwapeleka watu Unguja na Pemba, halafu, nilipowapeleka huko, nikapewa, kuwa unapokutwa ndani ya chombo hichi, basi kama una barua ya kuipeleka huko, basi bora ufe kuliko kukamatwa na hii. Kwa hivyo utakubaliana na kifo? Wewe uwe kama sadaka ya Tanganyika. Kwa hivyo nikajitolea nikawa kweli ni sadaka ya Tanganyika. Nikakubali kifo, nikakubali kusalimika, na nikapewa gharama ya kuwa uwezo nlopewa ni kutoka bahari yetu ya Hindi hii mwisho ni Chumbe, mpaka wa bahari ya Tanzania Bara,Tanganyika, na Zanzibar.

Page 99: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 67

Lakini hii ya Tanganyika nimeitawala. Nikiingia tu, naingia bahari ya Zanzibar litakalonikuta, nimeuliwa, nimepona, basi yote yawe ni sawa. Lakini isiwe nije nimeshikwa nijieleze. Ah! Mimi nimetolewa Tanganyika. Hapana. Niwe niko serious [madhubuti] na kuokoa Zanzibar. Kwa vile nikakubali kwa moyo mmoja wa kufanya hayo kwa sibabu tunataka kuukomboa Uafrika. Kwa hivyo na mie ni Muafrika, na ni asili yangu pia. Na Zanzibar, mimi nilikuwa nalala chugachuga. Leo nikilala nyumba hii, nikae sku mbili, nikishaona hawa watu wameshaanza kunitambua naondoka, nakwenda mahala kwengine. Ni mtu wa kushtukiza. Sku nyingine kwa Mdungi Usi, sku nyingine Mosi Jecha Pili, sku nyingine YASU na sana nililala YASU pamoja na Swanzi. Ilikuwa wakati nikifika na watu Kipumbwi, ninagawa mashuwa. Napeleka watano, kumi. Hawa nawapeleka waingie pale saa nane, wengine waingia alfajiri, wengine saa kumi, mashuwa mbalimbali. Kusudi nisishtuwe kuingiza kwa kikundi moja kwa moja. Wakifika pale Muwanda, kituo cha Muwanda, Zanzibar, wanapata mtu anawashindikiza mpaka barabara kubwa. Kwanza wanakwenda kwa chairman [mwenyekiti] wa Afro­Shirazi, nyumba yake iko ufukweni, unai­ona bahari ile pale. Na ilikuwa nkitia watu, wakati wavuvi wanatoka baharini na wale nawatia waonekane ni wavuvi. Na tunavua tunateremka na mashazi yetu ya samaki. Baharini kunaweza kuwa na vyombo kama kumi na tano, kumi. Manake vinakwenda mbalimbali tafauti. Kula mmoja na mivuvi yake. Mwengine enda mbali zaidi, mwengine enda karibu. Kwa hivyo sisi tunaanzia Tanga kuvuwa, Kipumbwi. Tunavuwa tukenda, huku tunakwenda tunavuwa mishipi. Tunachukuwa samaki tunatia tunatunga ndani ya mashazi. Na nguo zetu safi tumevuwa tuna nguo za kivuvi. Suruali kipande au mashuka machafuchafu. Kofia tunavaa za makindu. Tukifika pale twatoa begi zetu zatangulizwa barabarani. Kijangwani ilikuwa tunaingia saa mbili usiku. Hatujapanda gari mchana, ila mimi peke yangu. Wanajulikana wageni kadhaa wameingia. Tukifika Kijangwani tunasajili watu wangapi wameingia. Hasnu Makame ndo alokuwa akiwasajili, ndo bwana fedha ati. Hatoi fedha. Anajuwa wakati wa asubuhi posho itahitajika ya watu wangapi. Kula mtu na wageni wake atakaekuwa nao apewa hela awapikie huko. Pale Kipumbwi wanalala usiku majumbani, pale nje kwenye branch ile hoteli nlokuonesha. Ile ilikuwa ikilala watu. Chai, mbaazi, mikate, kila kitu hapo. Halafu kisha pale mmeshiba tena, kula unakwenda kula Unguja huko. Tunatoka alfajiri wakati wa umande tunaingia mapema kule, saa nne, tano. Twateremka, Ya Allah! Sasa tutafute mahala watu wanapumzika, mpaka wakati utakapofika. Walikuwa wanalala chumba watu watano, watu kumi, kumi na tano. Hawatoki. Watakuwa wanasoma Kiswahili humo. Watoto wa kike wana­wasomesha, wa Kiunguja. Manake ukitaka lafdhi nzuri ni mtoto wa kike. Sasa wale watu walikuwa hawana cha mafao. Pesa walikuwa wakipewa kama

Page 100: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano68

pocket money [pesa kidogo za kutumia] za sigara. Bas. Baada ya mapinduzi wamerudi wenyewe. Wote. Wamerudi. Walotaka kukaa wapo, wamekaa. Wako wengine walibaki. Wale walokuwa hawana kazi huku. Wengi wao waliokuwepo walirudi wote. Baada ya mapinduzi wakaanza kuwakataa watu wa Tanganyika, Kenya. Fitna. Wakaingiwa na moyo wa choyo. Vijana wa Kizanzibari. Kutakuwa hawawapendi watu wa Tanganyika. Wakawa wanawafitinifitini. Maneno ya uongo yasofaa na Mzee [Karume] akawa anayakubali, mengine hayakubali, manake wanatisha. Na mtu ukipinduwa ukitishwa watishika. Japo lisiwe la ukweli lakini ukiambiwa kuwa wale wataka pinduwa, wamekaa tumewakuta, kumbe hawana lolote, wewe utatishika kwa sababu unafahamu ukidharau itakuwa umejidharau. Sasa lazima ulibane, halafu ulichunguze. Ni kweli? Wako watu waliwekwa namna hiyo halafu walitolewa jela. Ikaonekana si kweli. Matarajio ya muungano ulivokuwa, ilikuwa muungano ni wa misaada inavo­tokea harakati mbaya wasaidiane, lakini kula mmoja na mambo yake ya nchi, ya ndani. Na ilikuwa ni ten years [miaka kumi], tulivofahamu wote Wazanzibar ni ten years [miaka kumi], na kwa bahati Mzee [Karume] hakufika miaka kumi, amechelea kwenye miaka minane. Mazungumzo ukweli ya mwenyewe marehemu Mzee Karume ilikuwa “tukiona muungano wetu wahitajika kuwa tuuendeleze tutakaa kitako tuuendeleze. Tukiona tutauwacha utabaki urafiki mwema.” Na kuitengeza Zanzibar iwe ni huru ni nchi ilokuwa haitaki ghasia, iwe kama Paris. Hizo ndo fikra nilizokuwa nikizipata kwake. Na ndivyo, kwa sababu alikuwa keshaanza kujenga mambo ya starehe. Majumba, mtu huwa hachajiwi [halipishwi] achajiwa umeme tu. Hata kisiwani kule alitaka kufanya kiwe kisiwa cha starehe. Na dalili ni ile alojenga Bwawani. Alikuwa akiendelea. Kwa hivyo alikuwa hana lengo baya Mzee Karume. Akizijuwa hizi habari lakini jemedari wa mambo bwana [Abdalla Kassim] Hanga. Nyerere aliyasema maneno kwenye radio kuwa leo Wazanzibari mnajuwa hakiii? Sasa sisi tunofahamu tulibaki kucheka. Tukafasiri kama leo Wazanzibari mwataka haki, mwaijuwa haki, ni kusema, wakati ule mbona mlikataa msiungane mkawa wamoja, ikawa hawa ZPPP, hawa ZNP, hawa nini, leo badala ya sisi kuwasaidia mwaidai haki kwetu. Vipi? Kwa sisi tunojuwa namna gani Tanganyika ilivoisaidia Zanzibar, mimi haikunipa tabu. Nilifikiri haraka sana. Na nikacheka sana. Kwa hivyo aliwatukana. Hawa watu kwa kuwa utawala kwao ni mgeni, utawala ni mgeni kwao wote, basi ilikuwa wajuwa nikifanya historia labda ntateswa, eh, rabda nikisema hivi ntatengwa, ntaonekana sifai, na hususan hasa ntafichwa, ntafungwa, au ntauliwa kwa mateso. Mara nyingi ukweli Tanganyika na Tanzania nzima, ukweli ndo hawautaki. Kula unaposema ukweli, wewe ni mbaya sana. Ndo mana hawathaminiani. Ukiwa na wazo lako zuri basi Mtanganyika halitaki. Kwa sababu

Page 101: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 69

Mtanzania anajitaka yeye mwenyewe manfaa yeye mwenyewe tu. Ashapata mahala pazuri basi yuko tayari kukukandamiza wewe usende. Historia si hiyo imeshapotea! Hii ya Zanzibar ni filam kali sana. Hata ya Uganda ni historia kali sana. Wameipoteza pia. Iko wapi? Mimi nimekwisha andika historia na kitabu cha babu yangu marehemu Mzee Mkwawa. Nnayo historia yetu ya Wahehe. Tumeanza kutoka mlimani kule mpaka tukaja makaburi ya Nyondo, Ibamba, Ikwatwiru. Chifu Adam Sapi ni mjomba wangu. Mkono wa Nazi ni mjomba wangu. Gaugen Marangarira ni kakangu. Kamati ya Ukombozi ilikuwepo. Msaada wa kuweza kuzikombowa nchi zilizokuwa na matatizo kuzisaidia kisiasa. Ndani ya TANU. Mpaka sasa zinaendelea. Baada ya Zanzibar ikaja Uganda. Kabaka halafu Amin. Ikaja Sychelles, Komoro. Kamati ya Ukombozi ilikuwa ikiongozwa na Oscar pamoja na Mzee, kina Kawawa hao. Hao ndo wenyewe. [Na kama nilivokwishaeleza] Issa Mtambo alikuwa anatumwa na Oscar Kambona, ndo alokuwa moja kwa moja na upande wa Kambona na Usalama wa Taifa. Sasa Issa alikwenda upande ule kuweza kujuwa mazungumzo ya Waarabu wanasema nini katika nchi. Ni rafki zake, aswali nao, kawa shekhe mkubwa, alikuwa kasoma uzuri, na anafaham dini. Sasa akawa yuko kule. Akiyapata yale, na nafkiri alikuwa ana chombo cha kurikodia maneno, sasa unakuta Issa, yaani yeye alikuwa akikutana na viongozi hao. Na halafu akajikubalisha kama yuko upande wao. Wanamuona ni mwenzao. Sasa akawa anapata sehemu mbalimbali. Akitoka pale sasa ndo anakwenda kukutana na akina Mzee Karume, pale pale Zanzibar. Si anapachuka. Ana safari zake. Anaonana na wale, anaeleza, anazungumza. Rafiki zake wakubwa zaidi mimi nilikuwa siwezi kujuwa kwa sababu yeye alikuwa akifatilizia kule moja kwa moja. Akitoka huku, Tanzania Bara, alikuwa anakwenda moja kwa moja kule Zanzibar. Mwenyeji wake alikuwa yule Kadhi, Sheikh Abdalla Saleh Farsy, ndo alokuwa mwenyeji wake. Alikuwa anajitia kama anasoma ilimu. Alikuwa yuko mjini Zanzibar. Anapiga kanzu yake, akaa kule, taratibu, dini na yeye na mkeka, bas. Hata mimi nikiwa nimeishiwa na pesa Zanzibar nikiambiwa nionane na yeye Issa Mtambo. Akaja YASU pale tukaku­tana, akanipatia hela ya matumizi, mimi nikarudi huku. Kwa hivyo yeye alikuwa kule, mimi nilikuwa katika Uafrika, na yeye alikuwa upande wa Waarabu. Abdalla Kheri yeye kazi zake kama za Issa lakini anapeleka watu kule, na wakati ule wa organisation [mipango] ya mapinduzi, yeye alishiriki pia, kuwaleta watu kwa kupitia Bweleo. Ni ndo njia mbili tu hizo, Bweleo na Muwanda. Hakuna njia nyengine ilokuwa ikitumika. Hii ya Pemba hii sio sana. Ilitumika, lakini ilitumika wakati wa kura tu. Halafu huyu Abdalla Kheri alikuwa ni mstari wa mbele. Kwa sababu alikuwa ni mkakamavu sana. Ndivo alivokuwa. Mimi ni grupu la akina Maulidi Sheni. Sikuwa na wasaidizi. Mimi nlichaguliwa peke yangu kwa sababu nilikuwa kama ni amiri jeshi kuwakuta wale kwenda

Page 102: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano70

nao, na kuwahifadhi na kuwarudisha. Usalama wao wote upitie kwangu. Na alonchaguwa mimi ni Kambona mwenyewe pamoja na Jumaanne Abdalla hapa, marehemu. Tulikaa pamoja. Hadithi ni ukombozi. 62 hiyo mwishoni mpaka 63. Na ndio tumo kwenye kazi sasa hiyo 63. Tulikuwa hatujuwani isipokuwa tulikuwa tukikutana Kijangwani, Zanzibar. Lazim kule tutakutana. Huku kula mmoja ana njia yake. Kula mmoja alikuwa akikutana na Kambona kivyake. Haijapata kutokea kukutana kwa pamoja na Kambona. Haijatokea. Hata mara moja. Kiunganisho kilikuwa ni Ungujaa! Kule ndo twafahamiana sasa. Mimi nilikuwa nakutana…tulokuwa tunakutana tulikuwa ni Jumaanne Abdalla pamoja na Kambona hapa, Ikulu hapa Tanga, si Dar es Salaam. Yeye alikuwa akija hapa. Kawawa alikuwa akija hapahapa Tanga. Kwa hivyo ilikuwa haina haja mimi kwenda kule, kwa sababu hapa naweza kutoa ripoti zote kwa Regional Commissioner [Mkuu wa Mkoa]. Anaweza kuzitekeleza OK, hawezi anampigia simu Kambona. Sijapata kukaa na Nyerere hata mara moja. Yeye akikaa na Kambona, Jumaanne Abdalla. Pale juu. Na halafu yeye alikuwa anajuwa yote, si kwa sababu alikuwa akielezwa. Kuonana naye lazma utaonana naye. Kusudi si atambue. Alikuwa hawezi kujitambulisha kwa sababu alikuwa si mtendaji.17 Si katika sheria mtendaji ni Katibu Mkuu [wa TANU], Kambona na wenzake? Nyerere alikuwa ana wasiwasi kwa kwamba hili suala halitofaulu kwa sababu walikuwa hawana silaha. Sasa wewe uwe utakwenda kichwa kichwa itakuwa vipi? Na sasa yale nlokwambia walitiwa bumbuwazi wadharau. Habari za silaha kutoka Algeria mimi sina. Si angelinambia Issa kwa sababu alikuwa karibu sana na mie kwa sababu tunatoka mji mmoja. Yeye si Mzigua anatoka hapo Korogwe. Kwa sababu mengi tukiambizana sisi. Tulijuwa kuwa tungefeli tungelitawaliwa vibaya. Sasa hilo tuwe nalo. Tusilie. Lakini tulipima tuliona hawa lazima tutawaweza. Kwa sababu, kwanza walikuwa na jeshi la kipumbavu, la kitoto. Watoto watupu. Uimara wa moyo walikuwa hawana. Mie pia nlikaa nikawa najiuliza “hizi silaha walizonazo kweli watawezekana watu kama hawa?” Haya tuyitazame. Mimi bwana nilikuwa mtu nikiishi kule toka 1949. Ofisini mwake Jumanne Abdalla akanambia “tunashukuru kukuona kwa sababu tulikuwa na shida na mtu anayeijuwa Unguja na Pemba vizuri.” Mzee wangu alikuwa mstari wa mbele katika TANU. Yeye Jumanne Abdalla akanijuulisha kwa Kambona. Walichaguliwa vijana watatu wakakataa. Ukikamatwa itakuwa wewe umeshiriki kutia vita kule kwa sababu si nchi yako.18 Akampigia simu Kambona akaja tukakaa watatu. Tulipokaa ndipo waliponambia kuwa wewe utashughulika kupeleka barua zetu kwa sababu zinafunguliwa kwa posta. Pia nilikuwa napewa maagizo ya mdomo na kikaratasi cha idadi ya watu. Basi imekwisha. Nikiwasilisha tu, zinasomwa, zinapigwa moto. Huwezi kuweka kitu

Page 103: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Sakura, Sadaka ya Tanganyika 71

kama hicho. Mambo yote Kijangwani ndo headquarter [makao makuu]. Pesa za kampeni pia ndo nlokuwa nikipita nazo. Walikuwa hawana lolote. Afro­Shirazi ilikuwa haina hela bwana. Haina kabisa. Pesa zikitoka Tanzania Bara, Tanganyika. Hapa hapa tu. Ndo maana sku ile, Sefu [Sharifu] adai serikali tatu, Nyerere akamwambia “leo hii. Mnaweza kufika mkajuwa haki yenu? Nawashangaa sana.” Mimi nkacheka sana. Nyerere awatukana hawa. Kwa Kiswahili unawatukana. Awafanya hawa walikuwa ha­wajuwi, msingetaka msaada mgelijikombowa wenyewe. Manake ni hiyo. Wasinge­liweza kujikombowa wenyewe bila ya msaada wetu. Hawawezi. Iangalie Pemba na Unguja ilivyo. Bila ya hapa ilikuwa hawawezi. Kwa sababu angalia wakati wa uchaguzi wa Julai 1963. Umma Party usiwatowe.19 Wao ndo walokuwa na harakati zote za kupinduwa. Uongozi na kitendo mambo mbalimbali. Uongozi wa kujuwa namna mambo ya mapinduzi yakoje, na kujuwa kutumia silaha ni Umma Party. Huku imeshirikiana kiwatu na kipesa. Lakini watendaji, tukiingia, tukifanya hivi, hapa patabomolewa hivi, Umma Party. Na kamando si anopiga. Ni mwekelezaji. Wao ndo waloelekeza. Badala ya kushika serikali wao ndo wakawa wasimamizi wakuu. Fanyeni hivi, wakatiwa utomvu wa mafenesi, ukangandishwa, imetokana na wao, sio hawa. Majani unaona kama yanapepea, yamo kwenye migongo ya watu. Kazi yao. Si Babu huyo? Alikuwa keshaweka watu wake sawasawa halafu huyo akaondoka zake. Akajiweka Dar es Salaam. Na Ali Mahfudh ndo mwanajeshi mkuu khasa wa Umma Party ndo alotowa vitu kwenye mapinduzi. Halafu anakataa nani? Ali Nyau aweza juwa kwa sababu ni mmoja mstari wa mbele. Wale ndo walokuwa wameshika mstari mbele. Tanganyika walikwenda kupeleka watu, kama jeshi, na wote alama zao wavae mapakacha, ili wajulikane kuwa ni wenzetu. Hata bila ya Umma Party mapinduzi Zanzibar yangelitokea. Yangelitokea. Kama ndo wamekwisha funguka. Kwa sababu, hata hiyo Afro­Shirazi haikuandaa kuwa ati wasaidiwe na Umma Party. Pasipokuwa, baada ya kukaa, kuwa wana­chama walojiunga pamoja, ndo wakafanya kikao cha pamoja tutashirikiana juu ya hili suala, na sisi kulielewa na kivita, na kutoka hapo uelewe, kuwa Abrahman Babu anaelewa muongozo wa kivita, kwa sababu ni Mkoministi. Na ni kweli kutoka siasa yeye alikuwa na Ma China, wakatia silaha, magari, sijui nini. Makomred usiwatowe kabisa. Kwa sababu ni watu wanojulikana… Kabla ya yote ni kuweza kukaa kukusudia kwenda Zanzibar kwa kufanya mapinduzi ilibidi tufanye mambo ya jadi ya kuweza kula amini kiapo kikubwa ambapo ukiweza kukikosea kiweze kukudhuru. Kwa hivyo tulifanya kiapo kwa kukubaliana atakayevujisha siri basi ina maana aone nyungu impige, kiapo cha nyungu, cha jadi ya mila ya Kidigo, ya Kisambaa, ya Kiziguwa. Kwa hivyo tukafanya kiapo hicho kwa pamoja na kikundi chote kiliopo pale mstari wa mbele kwenye mbuga ya Sakura. Kwa hivyo hakuthubutu mtu yoyote kuweza kujuwa.

Page 104: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tano72

Nyungu inakuwa hichi chungu cha kupikia, lakini kinakuwa bado hakijapikiwa, safi, hakina kitu ndani, pasipokuwa ni kunuwia, kinakamatwa na watu wawili, watatu, wane, kwa sauti moja, kwa yule mwenzake huyu amkamata huyu amkamata huyu, basi inakuwa kashiriki pale, kwa hivyo hiyo siri imefanyika bila kutangaa. Halafu kinaangushwa chini. Kikivunjika bas, kinaokotwa vigae vile kinatupwa. Ukivujisha, ukiumwa, safari tu unakwenda. Ukiumwa kidole unakwenda, uki­umwa kichwa unakwenda, ukiumwa tumbo unakwenda. Ilimradi kitakachokuuma ndio mauti yako. Nyungu kazi yake. Nayo inaeleweka. Watu sita pamoja na wengine kushika mashati na nini, ili wote ni kama wamekishika. Wote jumla kama ni ishirini.

Page 105: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa SitaVictor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi

Victor Mkello wa Tanganyika Federation of Labour [Chama cha Wafanyakazi cha Tanganyika], akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Pemba, aliushambulia ukoloni “chini ya bendera mbili—bendera ya Union Jack [ya Kiengereza] na bendera nyekundu (ya Usultani). Akaendelea kusema kuwa bendera zote mbili lazima ziondolewe…Kwa kuzingatia kuwa hakukuwa na tamko la ndani [kutoka upande wa Zanzibar] au juu ya uhusiano wa Mkello na Mawaziri wa Tanganyika, sishadidii sana ichukuliwe hatua yoyote, na nitakuwachiya wewe uamuwe kama kutapatikana faida yoyote kuifikisha taarifa hii kwa Serikali ya Tanganyika.” Barua kutoka kwa George Mooring (Balozi wa Uingereza Zanzibar) kwa F. S. Miles (Balozi wa Uingereza wa Tanganyika), tarehe 26 June 1963. CO 822/3204 116805

Mzee Victor Mkello

Kwa nini huku visiwani hakutulii kama tulivokusudia sisi? Inaonekana kuna maneno, maneno, maneno…Tulidhani sisi muungano huu umekubalika pande zote mbili bila ya tatizo lolote. Mimi hili suala tulitaka kujuwana wakati ule tuna msimamo wa namna gani ambao tungekubaliana nao. Mimi nikianzisha wangu nnaoujuwa na wewe wako unaoujuwa…Tulidhani kule kwenu Zanzibar juu ya vikundi vote vilokuwa mbali mbali hatimaye tutakuwa kikundi hiki “kimoja.” Bas! Tunajenga nchi yetu. Aliekufa, aliepona, bahati yetu, kazi ya Mungu. Lakini sasa tunachotaka sisi ni kitu kimoja. Asiingie mtu mwengine akasema mimi naleta Uarabu, mimi naleta…ah, ah! Hakuna. Tukae, tuzungumze, tukubaliane, kwamba sasa kama ikiwa kuna haja ya kujenga nchi yetu tukae basi tuijenge. Palikuwa na vuruguvurugu nyingi. Kuwa kitu kimoja ingekuwa jambo rahisi na mimi nasema kilichovuruga, watu walidhani tukimtia yule Shekhe Karume atatupa uwezo zaidi wa kuongoza mambo yetu na tukafanikiwa. Lakini halafu yakatokwa manenomaneno ya akina Abdalla Kassim Hanga alienyongwa.

Page 106: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita74

Maneno haya ya akina Hanga ndo yaloleta chuki. Wengine walisema Hanga ameonewa. Hata kama angekuja juu namna gani sisi kama tungesema tunasimama imara pamoja na Hanga asingeweza kutufanya kitu. Asingeweza. Sasa kikapita kipindi ikaonekana kama ni jambo la hatari kuwa naye huyu. Mojawapo ilikuwa ni kuwaogopa wasomi. Sasa, kinachotakikana, labda, ni tutafute njia ya kuwaweka watu wetu hao katika hali ya kuelewa mambo. Kuelewa mambo katika line [mstari] hii tunayoitaka sisi, na ya line tuliokuwa nayo zamani. Jee, tukiziunganisha line zetu kutakuwa na mushkel kwa upande wetu? Labda kuna wengine hawatoridhika kama hawatopata ukubwa. Mimi nilifikiria tulipokuwa na skukuu ya miaka 43 ya mapinduzi, labda katika sikukuu hii, yatatobolewa mambo mengi, yakatupwa nje yasiotufaa, yanayotufaa tukawa tunayo. Niliona dalili kwamba watu waliokuwa waogawaoga hivi…wakati wa ku­nyongana watu walinyongana. Sasa mambo yamekwisha. Ilobaki sasa ni kama unavosema, tusameh mambo yote na tutafute tusimame juu ya nini. Hili ni jambo la watu wote sasa. Dunia inavosema jambo kubwa kama hivi halitokufa tu hata kama tunataka sisi life.1 Litakwenda linachomokachomoka tu. Mwisho watu watakuja tambua mambo yalivyokwenda lakini hii Zanzibar mpaka hivi leo hawa waliokuwa wakubwa wenzetu pia hawajakubaliana kwamba uongozi wao ulikuwa ni thabiti kabisa. Bado kuna wasiwasi. Hawa viongozi wa Zanzibar, ikiwa nia zao haziko pamoja na sisi [viongozi wa Tanganyika] na kama hatuwezi kuziunganisha tukawa sote pahali pamoja wanachotaka ni nini? Manamba Zanzibar walikuwepo. Kuna mambo mengi tuliyafanya kwa kutu­mia Manamba. Kwenye Zanzibar. Watu walikuwa wanakutana bwana lakini kuna wengine hawataki lijulikane hilo kuwa fulani na fulani aliwaongoza. Sasa hapo ndipo vurugu hiyo. Sasa hapo panakuja ukubwa na uongozi. Hapo panakuja ukubwa sasa na uongozi.2 Basi akitajika Mkello, ni mtu mkubwa huyu, lazma apate heshma huyu kwa sababu ameshiriki. Sasa kama hatukumtaja Mkello, hatukumtaja mtu mwengine, akina Kassim Hanga, tutaonekana hatuko pamoja. Tukikataa tunanusurisha mgawanyiko. Tukikataa tunanusurisha mgawanyiko. Tukisema tuunganike pamoja wote itakuwa ni kitu kizuri kwa upande mmoja, lakini kuna watu wengine kwa ukubwa hasa hawa vijana wetu wa Unguja walopata Uraisi. Sasa watu wa namna hiyo wanataka mambo yao yaende katika msingi huo. Ujulikane kama huo ndo msingi uliofanya mambo yote hayo. Ambapo kuna upande huu unaosema wewe hawataki, wanasema Manamba “si kweli.” Hawa walioko sasa wanataka wajulikane kwamba wao ndo wao! Wao ndio wao na ndo waliokuwa wakiyafanya baba zao. Sasa panapotakiwa kutobolewa ile siri kama haikuwa hivo. Mlikuwemo lakini sio katika uongozi mkubwa kiasi hivo. Hawajakuwepo katika shina. Inategemea kule kutoboa kwenyewe kutatobelewa katika picha gani.3 Kuna wanaosema hamna faida yoyote. Sisi tulichotaka ni Mwarabu aondoke

Page 107: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 75

na ameshaondoka. Tunatakia nini kuingia mambo haya hayana faida yoyote. Tunataka kujenga nchi. Bas! Wengine wanasema, hapana, lazma tujenge nchi kwa kupenyeza uongozi mkubwa kwa watu flani flani. Wakati huo Mwalimu Nyerere akijuwa na mengine akiyasogezasogeza yeye. Kwa mfano niliwahi kutumwa kwenda Moshi usiku wa manane. Nakwenda Moshi kwenda kupanga mipango hayohayo ya mapinduzi. Kushika chaji ya mambo yetu haya ya Zanzibar kuogopa kwamba kama tukichelewa watu wa Zanzibar…manake Zanzibar yenyewe nayo imekuwa headache [inaumisha kichwa]. Watu wawili Zanzibar. Kuna Waarabu na wasiokuwa Waarabu. Sasa kuna watu ambao wanataka, hawatakiwi wajitokeze katika unasaba wao na Uarabu. Hawatakiwi wajitokeze kwa ajili ya Uarabu wao. Hapana, hawa si watu wa upande wetu. Sasa tuwachujeje hawa mpaka wawe hawako upande wetu. Kazi kubwa! Maana watu tunao lakini hawa hawapendwi na kundi lingine. Kwa hiyo kazi hii ni kubwa sana.4

Moshi nilitumwa na Nyerere kwenda kuweka mambo sawa. Wakati huo Katibu Mkuu alikuwa ni Kambona na alikuwa katika kazi maalumu huko Moshi na ilikuwa lazma apatikane basi ikaonekana utoke ujumbe makao makuu umfate ndo nikachaguliwa mimi. Nyerere akilifahamu kwa sababu watu fulani akiwatuma katika jambo flani itakuwa hivi, itakua hivi, itakua hivi. Tena saa nane ya usiku natafutwa na magari ya polisi. Uingie ndani ya gari hii. Barua hii mpelekee Oscar. Nakwenda…nafika Morogoro nakutana na Kawawa naye ana kalendrova chake kadogo. Naye pia ametimuliwa. Sasa haya yote ulikuwa bado ujenzi, utafutaji wa kipi kinatafutwa. Wakati ule tulikuwa na wasiwasi. Tulitaka nchi yetu ya Zanzibar tuigomboe.5 Vilizuka vyama kule na walipozusha vyama hawakuzusha kwa amani na mapenzi. Wasiwasi wako mkubwa ni kwa nini jambo hili halishi. Hapo katikati hapo pakatoka vikundi venye kurusha maneno maneno hivi na kutupeleka mbali. Makabila yote yalikwenda Zanzibar kushiriki katika mapinduzi. Wamakonde, Wabena, Warundi, Wanyamanga, wakina nani…Mahali mambo yakitaka kuharibika! Yanaharibika tu. Wote walikwenda. Sasa wao wanakataa tu huo ushahidi. Lakini watu wengi wamekuja. Wote ni woga tu. Unajuwa tulianza vibaya, kugongana kule, watu kuuwana kule. Sasa hao wenye kusema kuwa Manamba hawakwenda Zanzibar kwa kushiriki katika mapinduzi na watueleze ilikuwaje. Wakati wa Abedi Karume akina Kassim Hanga hao, ukizungusha nyuma hivi, bas, hurudi salama. Sasa kitu gani kinachoharibika hapa, kinachovurugika…ni kutaka Uarabu mbali, sijui unani sijui mbali. Ni nini kinachotuogopesha tusiungane pamoja tukafikia kwenye point unayoitaka weye? Machano na Makame [Wazanzibari wenyeji] hawajakuwemo kwenye mapinduzi ya Zanzibar. Neno lenyewe hilo unalolisema si la uongo kwa sababu ya uhusiano wa kindowa, basi kabla ya hayo yakatokea mauwaji yale, sasa hapo wameingia woga. Wameowana hawa.6

Page 108: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita76

Kielimu mimi sikwenda mbali. Sikwenda mbali. Tumesoma haya madarasa ya shule haya, shule za Anglican. Top kabisa wakati huo Anglican ilikuwa Kiwanda na Minaki. Hizo ndo shule ambazo mimi nilipata bahati ya kutafuta mitihani yao na nikakubalika. Baada ya shule ya Kiwanda kuvunjika ikapelekwa moja kwa moja yote Minaki. Kiwanda ilikuwepo hapo Muheza. Kutoka Muheza ikapelekwa Minaki. Baada ya hapo sasa ikasemwa watapunguzwa watu kwenda kusoma Minaki ambayo iko juu zaidi. Tukakubali. Sisi wengine tukasema turudi kwenye mkonge. Si kazi tunayo! Kwa hivyo hatukuendelea na masomo. Kurudi nyuma kwetu sisi ndo ikatokea uingiaji wa vyama va wafanyakazi. Hivi vyama va wafanyakazi, sisi Watanzania tulivipata kutoka Kenya kwa Tom Mboya. Tom Mboya yeye ndo alokuwa mwenzetu, halafu katika nafasi zao akapewa amri au order ya kuunganisha East Africa [Afrika Mashariki] kama ataweza kuipata katika vyama. Sasa katika kufanya hivyo ikaonekana kwamba tuanze kazi. Tukapatikana pale na baada ya kupatikana sisi pale tukafanya uchaguzi, baada ya kufanya uchaguzi na nini, mimi nikawa kiongozi mkubwa wa Tanganyika Federation of Labor (TFL). Kwanza walianza huyu Kawawa,7 Kamaliza, halafu mimi Mkello, katika huuhuu upresident wa TFL. Baada ya hapo tulizuwia, ngoma ilichezeka sasa hapo. Mimi sikulaza usingizi, bibi huyu hapa hakulala usingizi, kwa sababu sasa ni vita. Wazungu wa mkonge wamesimama imara kupinga movement [harakati] yetu ya haki za wafanyakazi na walinikuta mimi kama nilikozaliwa kwenye kupingana! (vicheko). Wamesikitika sana, na walijaribu hata kumuomba Mwalimu kama huyu kwa nini ukampa nafasi ile, Mwalimu [Nyerere] akawaambia “huyu si mtu wetu, huyu ni mtu wa labor [wafanyakazi] huyu. Mkimgonga huyo kesho watu wote asubuhi hakuna kazi.” Wakawa wananitizama kwa jicho baya lakini hawana la kufanya. Basi sasa baada ya kuwa wameshindwa kunifanya lolote sasa wakatumia ujanja mmoja. Wakamtumia huyuhuyu Mwalimu, basi wakamtumia kumuambia, huyu matata huyu bwana, kidogo migomo, kidogo migomo, kama unaweza kumbanabana hivi. “Kumbana naweza kwa sababu ya u­President wa serikali naweza kumbana kwani kama sikuweza kumbana hii nchi si itaharibika? Sasa ngoja nitafute nafasi ya kumbana huyu ili isiwe mnagombana naye, ili naye akubali kama kuna mambo mengine si lazima sana maana yake hii nchi bado ni changa.” Basi, ikawa sisi tumekubali hilo na mimi wakanihishimu na security wao [watu wao wa usalama] wakajuwa habari zile Mzee amekubali kunibana na wao wakapata nguvu. Sasa kazi ikawaka moto ikawa na wao sasa wakashindwa kunitupa kando ikawa kila kitu kinachotokea katika mkonge nikawa mimi nilihusika. Mwalimu ana washauri privately [pembeni], na wakimuambia kuwa huyo alipokuwa shule alikuwa mkorofi. Kwa hakika hapo mtakuwa mmemvisha kofia ambayo alokuwa anaitaka yeye. Basi, mimi nimekaa hapa na jamaa wa mkonge moja kwa moja, tuko pamoja. Na Central Sisal Council, hiki ni section [sehemu] ya cha chama cha mkonge,

Page 109: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 77

lakini kilikuwa na uzito wake kwa sababu chairman [mwenyekiti] wake alikuwa anatoka London! Eeeh! Mwenyekiti wetu alikuwa Mzee Fek yeye alikuwa ni interpreter [mtarjumani] na mimi chairman wa TFL. Basi mzee akija, ananipigia simu kutoka London kupanga tarehe ya kukutana. Huko Uiengereza yeye alikuwa ni ex­judge [kadhi aliyestaafu] na kwenye mkonge alikuwa ni chairman kabisa. Akaambiwa huyu mtu [Mkello] tunayekupa kidogo hana adabu lakini tunakuomba ujaribu u­create friendship [ujenge urafiki] naye. Usimuone hivyo huyo, akikasirika hata mbele za watu atakutukana huyo! Mzee akaona mmhhh! Nitapata kazi kubwa. Basi mzee yule ikawa hatwendi mbali. Kidogo ikawa “Mzee yule anakwita.” Mtu mzima, amenishinda mie. Basi, tukawa tumeshughulika wote pamoja na ikaleak [ikavuja] kuwa amepata warning [onyo] ya kuniheshimu. Basi hatukuhitalifiana sana isipokuwa mkonge wenyewe mambo yao kidunia yakawa si mazuri kwenye biashara ya mkonge. Basi mimi nilikwenda nao hawa jamaa mpaka hapa katikati hapa ikatokea nikosane na President [Nyerere]. Sasa hapa ule mwiko unavunjika sasa. Nikakosana na President na nikapelekwa Sumbawanga. Lakini kule sikukaa sana. Tulikaa miezi mitatu pamoja na assistant [msaidizi] wangu [Shehe Amiri ambaye alikuwa Seketeri wa Oganizesheni wa Tanganyika Workers Union]. Ni kifungo ambacho ni cha ajabu manake, mimi sijapata kukiona. Tuko Sumbawanga, bwana mkubwa wetu wa Sumbawanga, afisa mkubwa yule wa kazi anaeshughulika na sisi, kila siku ya jumatatu tunapita kwake anatupa pesa, shilingi miamoja, mia moja. Kila jumaatatu. “Jamani ndo sheria!” Detention [kizuizini] unalipwa! Zingelinifika mpaka hii leo ingelikuwa ni vizuri. Mama Mkello atakuwa hana taabu ya mafuta ya taa tena. Basi bwana, mambo yakenda tukarudi baada ya miezi mitatu. Mwalimu nae tukagombana tena. Nilikuwa na Regional Commissioner [Mkuu wa Mkoa] kule Sumbawanga na akanambia wewe kaa hapo nitazungumza na mzee kuhusu habari zako. Kaa hapo usikilize. Commissioner akanambia “unataka mke wako aje hapa?” Nikamwambia “ndio nataka mke wangu aje hapa kwa ndege, manake mimi nimekuja hapa kwa ndege.” Lo! Kumbe hilo limemuudhi Mwalimu. Kwa nini nimesema nimeletwa hapa kwa ndege na mke wangu aletwe kwa ndege. Baada ya Sumbawanga kikaja kifungo cha miaka miwili na nusu. Tulifungwa huko Kilwa Kivinje. Mapinduzi Zanzibar yameshatokea. Sasa hapo tulikuja kusikilizana kwa masuali ya Zanzibar kwa sababu vijana ilionekana wana interest [hamu] sasa kwa Zanzibar hawa kuingia katika movement [harakati] yetu ya labor [chama cha wafanyakazi]. Wameona ina nguvu na ikitoa sauti inasikilizwa nchi nzima. Kama akina Adam Mwakanjuki hawa mara wakawa wenzetu, wanatuonea huruma na nini. Tukawa tuna solidarity [mshikamano]. Safari moja nilisafiri na mama Mkello hapa, kwa air [kwa ndege] lakini, nilipewa ndege na Raisi tukaruka hapa mpaka Zanzibar halafu tukenda Dar es Salaam. Hakunisahau Mwalimu. Baada ya kifungo cha Kilwa alinita ofisini

Page 110: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita78

kwake anipe kazi. Kwanza, alikuja Tanga kwenye ziara yake ya kawaida ya Mkoa wa Tanga na wakati ule Area Commissioner [Mkuu wa Wilaya] alikuwa Rajabu Kundya. Basi akamwambia Rajabu Kundya anitafute, nilikuwa nalima shamba baada ya kurudi Kilwa. Rajabu akanitumia salamu naitwa na Mzee. Nikashtuka. Mwalimu ni rafiki yangu lakini tulikaliana kiujanjaujanja. Nikasema nishavuruga nini tena? Nikaonana na Mwalimu. Akanambia kwanza, mimi nafikiri mambo yame­kwisha, “serikali ni serikali bwana, inawezekana tumekosea, au inawezekana imekwenda vizuri, lakini tumetekeleza kama tulivoelewa sisi. Sasa wewe huwezi kukaa hivihivi tuu, hapana. Sasa nitakupa kazi ambayo msimamizi wake nitakuwa mimi mwenyewe kwa sababu watu wengi ni maadui zako, sasa itabidi nikulinde. Sitaki watu wanatungatunga habari zao wananiletea mie. Akiniletea mtu habari na mimi nitakwita hapahapa. Watajuwa mmh…!” Nikamwambia mimi nakushukuru. Ilikuwa anipeleke Moshi kuwa Katibu wa chama wa Mkoa wa Moshi, halafu Kawawa akabadilisha, akaweka Dodoma. Kutoka Dodoma nikapata transfer [uhamisho] nikapelekwa Morogoro, lakini habari zangu zinajulikana wazi kabisa kwamba mbele ya Victor Mkello huwezi kuleta mchezo. Kutoka Morogoro akanipa u Area Commissioner [Ukuu wa Wilaya] akanipeleka Njombe. Nikamwambia “sawa, lakini ninachokuomba mimi ni binaadamu, ukiniona nateterekatetereka unite unieleze, sio kuntumia asikari.” Basi akafurahi, akacheka kabisa! Akasema, “unaogopa askari eh?” Nikamwambia “askari si mchezo bwana, wale ukishawaambia neno basi.” Baada ya hapo nikahamishwa tena nikapelekwa Mkoa wa Tabora. U­Area Commissioner huohuo. Halafu nikapelekwa Area Commsioner Same, halafu Wilaya ya Bagamoyo ndipo nilipomalizia u­Area Commissioner wangu nikarudi Muheza nikawa Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM. Ndo mwisho wangu na sasa niko kitandani. Ndo mwisho wangu wa u­Area Commissioner wangu huo. Lakini hakunisahau Mwalimu. Hakunisahau hata kidogo. Hakunisahau hata kidogo. Huo ndo mukhtasari wa elimu yangu na majukumu niliopewa. Wengi hapa wananifata kuniuliza kuhusu mashamba ya mkonge na Manamba waliingia kipivi, si kama ni wewe peke yako. Suala la mapinduzi ya Zanzibar hilo hawakulitaja. Hilo hawalijui na ni tafauti ya hayo mengine. Jambo la labor movement [harakati za wafanyakazi] ni kitu ambacho kilianza kwa undani sana. Ya Zanzibar na hata hii ya huku. Yaani, hawakuwa na uhusiano mzuri wa kushirikiana katika mambo…wenzetu Zanzibar kidogo walikuwa wakijitengatenga kwenye mambo ya labor movement. Wakijitengatenga. Hakujakuwa na mawasiliano mazuri. Labor [chama cha wafanyakazi] ya Afro­Shirazi tulikuwa tumeshirikiana sana. Hata Nyerere mwenyewe alikuwa anapenda hiyo kuona kwamba sisi vijana tunashikana kuleta ile labor movement yetu na kusiwe na mtu wa kutuingilia. Manake walikwishaona vinenovineno va kutaka wenzetu hawa wa Kenya, hawa

Page 111: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 79

wa Zanzibar. Akasema hapana. Nilitiwa kwenye suala hilo mara tu baada ya kutoka Pemba…hapana…wapi hapa?…tuliporudi mara ya pili…Kilwa…tukapata habari kwamba….tuliporudi kutoka Sumbawanga palitokea mgogoro ambao haukuwa na sababu yoyote ya maana sana ilionekana kana kwamba ni mgogoro wa kugawana, kwamba wenzetu wa Zanzibar na sie tuweke mambo yetu kando…hakuna atakayefuatilia la mwenzie katika mambo ya labor kwa sababu ile ni nchi kamili.8 Basi yalikwenda hivo. Vineno vidogovidogo, kina Adam Mwakanjuki hawa…tulikwenda nao vizuri. Mambo sasa yalikuja haribika lakini hivi vinenovineno vilipoungwa mkono na vyama va siasa hivi…jambo hili baya, jambo hili zuri, basi kidogo…. Sisi tulikuwa tukiitwa katika mambo mengi…Watu wetu, wao wenzetu walikuwa na nia hiyo ya kutaka kuungana. Sisi tuwe kitu kimoja lakini sasa kule kwetu, sio sisi sasa, kule Zanzibar huko, kule jamaa wakaanza kama kuwa na wasiwasi kwamba tunataka kunyang’anywa madaraka. Tunataka kunyanganywa madaraka manake Tanganyika…tena hivi hivi hivi…Oh, sasa hapa kidogo ikawa ule urafiki wetu uliingia maji. Kumbe hawa wanaletwa wanakuja…wanataka kuwa wakubwa nao ndani ya nchi yetu.9 Lakini halikuwa jambo baya saana. Ah, ah. Ilikuwa maneno ya uvumi wa watu tu lakini hatukuwa na kitu ambacho kinashamiri kabisa kama kuna vita. Aa. Isipokuwa kuna arguments [mabishano]. Tukikutana katika vikao tu, imekuwaje tena akina Mkello kutuingilia…yalikuwa maneno kama hayo. Wenzetu wa Zanzibar walikuwa wakilalamika. Kulikuwa na vikundi va watu lakini havikutueffect [havikutuathiri] sisi na shughuli zetu. Hakukuwa na kitu cha kubishana mpaka ikawafanya watu…hakuna. Maneno maneno yalikuwepo. Mchango wa mashirikiano baina yetu na wenzetu kule, huyo Kassim Hanga tulikuwa naye, na huyu kijana mwengine wa Songea…Hassan Nassor Moyo, tulikuwa naye, na mwengine, Mustafa Songambele kutoka Songea. Hawa ni wenzetu ambao kama kuna jambo kuweza kuleta umoja, tulizungumze kwa umoja basi mara moja tunakubaliana, kuitana na kuzungumza. Mapinduzi [ya Zanzibar] yana chombo chake na chombo chake ni vyama va wafanyakazi. Mada ni nzito na uzito wenyewe ni vitu viwili vimekuja kama pamoja—serikali na vyama va wafanyakazi—labor. Sasa, mambo tulifunzana, kama mambo ya serikali tuiwachie serikali, yana sheria zake na nini na nini. Kama kuna mambo ya raia ya kiserikali kama yanataka yazungumzwe kwenye labor basi tuwe na vikao vingine.10 Tusichanganye mambo. Tutakuja zungumza vitu ambavyo havimo kwenye mandate [mamlaka] yetu. Suala kama kuna watu walidokolewa mle kutoka kila shamba la mkonge kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mapinduzi mimi sidhani kama hili suala lili­kuwa la wazi. Halikuwa suala la wazi. Hawajalijuwa. Hawajalijuwa kabisaa, kama watu wetu wanadokolewa. Katika kuwaorganize [kuwaandaa] wale watu sisi hatukushauriwa. Walishauriana wale watu na Mameneja. Kama wangelijuwa

Page 112: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita80

wao wasingelithubutu bila ya mimi. Lakini kuna wazungu wengine wana hamu, wakina David Leed, huyu wa hapa Mazimbe hapa. Mtoto yule kigego yule. Hashikiki kabisa. Yeye anaweza kufahamu manake ni mpekepeke sana au anaweza kufanya kitokee kitu fulani. Kama hakikufanywa akishtukia tu kimefanywa au yeye anaweza kukipekenyuapekenyua. “Basi huyu Bwana Mkello anafanya hivi anafanya hivi.” Ndo kazi kubwa alokuwa anafanya yeye. Ugumu wa Mwalimu, kuna mambo yanapoingia kwa Mwalimu, na yeye anakubali kuyatoa nje kwenye vikao vake vile. Anayazungumza. Lakini kuna mengine yakimwendea basi anachukuwa kitu kama kutokuwa na hamu ya kutowa kitu hiki, hiki, hiki, labda kijulikane na kina Mkello kitaweza kuleta maneno. Maneno hayo tumeyapata. Kama kuna mambo mengine Mwalimu amekuwa na wasiwasi kwamba tukiambiwa sisi tunaweza kuyatowa. Mie nasema watu tulokuwa tukifuatana nao ni hao niliokutajia, Hanga, Adam Mwakanjuki. Moyo na mimi tukinongona sana. Mwalimu [Nyerere] alikuwa hapendelei sisi tuwe vianzo va matatizo ya Zanzibar.11 Khasa kama kuna jambo tunakaa kwenye ofisi yake anazungumza, “jamani, tumesikia nani hapa, kuna hivi, kuna hivi.” Sasa hapo kila mtu anajitetea lakini hilo mimi silikumbuki sana. Nataka ijulikane kama hatukuwahi kukaa na Mwalimu kuzungumza suala hilo la mapinduzi ya Zanzibar. Kawawa tulionana Morogoro. Mimi nakwenda Dar es Salaam narudi, yeye anakwenda Moshi. Huko Moshi kuna Kambona huko. Mwalimu [Nyerere] ndo alokuwa akitoa miongozo (sauti ya chini). Mwalimu alikuwa muongozo wake mkubwa hataki itokee fujo ionekane kwamba hawa Wazungu walitaka ku create [kujenga] kama Tanganyika Federation of Labor, ndio wanaovuruga hii nchi. Mwalimu hakutaka mtu abuni maneno yasiokuwa na msingi halafu afanye labor movement [harakati za wafanyakazi] kuwa inahusika. Mimi nakataa kwa sababu mikutano yote nilioitisha mimi na wenzangu hamna tabu. Kama kuna kitu chengine chairman si lazima awepo pale all the time [kila wakati]. Chairman wa chama cha wafanyakazi anakuwa na majukumu mengi lakini nikirudi lazma niambiwe. Mimi sikuhusika na ukusanyaji wa watu kwenda kufanya mapinduzi Zanzibar, lakini mimi nimehusika na mikutano yote ya wafanyakazi, karibu yote nimehudhuria mimi. Sasa ufahamu kama ni Zanzibar, mimi sikuwa kiongozi wa Zanzibar. Kama wenzangu wa Zanzibar wameitisha mikutano yao wakafanya bila ya mimi kuwepo hawawezi kunitaja kwamba na Mkello alikuwepo. Manake vitu vengine mimi sikuwepo. Kama ni jambo hilo la Mkello, na Nyerere, na Kawawa, na kina Hanga, si mambo mageni hayo, wala si mambo yanayofichwa na mtu yoyote yule. Tunapokosana ni pale “Mkello ulikuwepo.” Mimi vema, mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi, pengine mkutano unaitwa mimi siko Tanga, lakini nasikia kuna mkutano huko. “Haya fanyeni.” Hata Nyerere

Page 113: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 81

mwenyewe, vikao vengine alikuwa hayupo tunakaa na Kawawa. Mimi ninavyokumbuka siku ya mapinduzi, wenzangu wa Zanzibar, au tuseme wenzetu, tunavosema sisi wengi kutoka Tanga, wenzetu wa Zanzibar kutoka Tanga kwenda kwenye hiyo siku kuu ya mapinduzi, hakuna anaweza kukataa, na wengi wanaweza kuona kama ni fahari. Lakini mimi kama nilikuweko wakati huo… Unajuwa kama kuna siri moja inayotokana na suala lile la mapinduzi kwamba yasingetangazwa na mtu mwengine yoyote kwa sababu ni vitu va hatari. Hatukutaka vijulikane kabla. Iwe siri ya hali ya juu. Nilikuwepo Tanga. Kama hunioni Zanzibar niko Tanga. Watu Tanga walikuwa wanayasubiri. Hiyo, tena…nyinyi mnafanya mchezo. Tanga tulikuwa tunayasubiri kwamba leo ni mapinduzi. Leo tunapinduwa leo. Lakini mpaka nimekwambia hivo nimekutizama mara mbili mara tatu uso wako kama wewe ni mtu wa sawasawa au…Siku ile ya mapinduzi hakuna mtu alielala Tanga katika sisi. Hakunaaa! Sisi tuko huku tunawaunga wenzetu walioko Zanzibar kwenye muungano [mapinduzi ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika]. Sisi tulikuwa tunataka Mwarabu aondoke. Hanga alikuwa anakuja Tanga lakini hakuwa na uhusiano wa karibu na mimi. Hanga alikuwa anakuja Tanga, alikuwa anakuja kwenye vikao va Tanga, lakini alikuwa haji kuniona mimi. Mimi sikuwa na urafiki na mtu yoyote ambaye ni zaidi ya Adam Mwakanjuki. Huyu manake tunaelewana. Kiuongozi alikuwa mdogo lakini unajuwa katika mikutano watu wadogo huwa ndo wakubwa kwa sababu huwa wanaandika andika minutes [mukhtasari wa maneno yaliozungumzwa kwenye mkutano] kumpelekea huyu na yeye mlemle kimsimamo anakuwa anatia hivihivi. Hapa tulipo tunaozungumza wewe na mimi. Tunaisemaje Zanzibar? Iwe tumeshinda katika nia yetu ya kujenga Zanzibar mpya au hatukushinda? Hakuna kwamba tumefaulu Mwarabu hayupo na nini, na nini? Mbona yeye Mwarabu hakubali kuiacha Zanzibar? Na haitaki vipi na yeye ameshindwa? Zanzibar sio nchi ya mwanzo duniani kupinduliwa. Nchi nyingi zimepindu­liwa lakini nyingi zimeokoka vilevile. Zanzibar wasingeweza kupinduwa bila ya msaada wetu. Sasa hawa wanaolalamika Zanzibar kuhusu mapinduzi ni akina nani basi kumbe mambo yamekwenda vizuri namna hiyo na Mwarabu kaondoka? Mtu ambaye anaweza kujulikana kama ni Victor Mkello ni huyu John Okello. Mimi nakumbuka waliokuwepo pamoja na akina Mkello, ni mimi mwenyewe, na wengine nimeshakutajia. Na mimi nilikuwemo katika huo muungano wa tarehe 12 January 1964. Muungano [mapinduzi ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika] waingia sisi tuko hapa Tanga tumeusubiri. Sisi tulikuwa tunasubiri katika ofisi yetu ya TANU. Tulikuwa watu wengi ambao tuna kazi mbalimbali.

Page 114: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita82

Mzee Maulidi Sheni alikuwa kati ya viongozi wa Chama cha Wafanyakazi Tanganyika na msaidizi wa Mzee Victor Mkello.

Mzee Maulidi Sheni

Alikuwepo bwana mmoja alikuwa akiitwa Abdalla Mwinyi alikuwa ana chongo jicho lake moja. Yeye alikuwa ni kiungo baina ya TANU huku bara na Afro­Shirazi, Zanzibar. Kuna kitu kinakuja kutoka Dar es Salaam analeta mtu mpaka Mkwaja, kutoka Mkwaja mpaka Muwanda. Abdalla Mwinyi alikuwepo Dar es Salaam. Mimi nilikuwepo Tanga. Nikenda Zanzibar nikikaa siku moja mbili, nakula vitu pale halafu huyo nakwenda zangu. Najuwa mpango wote wa pale. Tulikuwa na kina Moyo, kina Mwakanjuki hawa, kina Khamis Masudi, kina Ahmed Diria, Shaabani Mloo, Twala. Juni 1961 tukijuwa kila kitu. Nikalipeleka gari la Land Rover Zanzibar likasaidiye. Itakuwa haina maana wafanyakazi wasiwasaidiye wafanyakazi wenzao walioko Zanzibar. Watu tulikuwa tukiwapeleka sisi Waunguja. Tukiwachukuwa watu kimyakimya. Kama Tanga tuliiba. Wasambaa hawa, wadude gani. Bado wiki moja. Wiki moja kabla. Kwanza tulikuwa na yule kijana, “Jimmy Ringo”, Maulidi Juma. Aliuwawa yule. Yule alikuja mapema Tanga, alikimbia kukamatwa kule Unguja. Siku ile ya mapinduzi niko Unguja. Nalikuja siku ile. Nikaambiwa mimi kazi yangu ku­patrol, kupiga doria. Kila mti unaoujuwa wewe uliokuwa pale Kiinua Miguu ulikuwa una watu. Mimi nilikuwa nikizunguka kwa baiskeli lakini. Unapita chini ya mti unasimama mtu anakutokelea. Nimetaka kujuwa tu kama upo. Sote tuko hapa. Nimezunguka nimezunguka mpaka juu kule Mwembe Matarumbeta. Nyerere akamwambia Karume kuwa asikubali Hanga awe Waziri Mkuu na yeye asiwe na kitu. Lazima serikali ukaivunje, wewe uwe Rais na Hanga awe Makamo wa Rais. Kwa siku tatu serikali ilikuwa chini ya Hanga. Nyerere ana hadhar. Hakuitowa serikali kumpa mtu ovyoovyo. Alikuwa tayari akupe ukubwa wa majeshi lakini Nyerere alikuwa mgumu sana wa Ikulu. Ulipoundwa Muungano Hanga akaletwa huku [Tanganyika]. Mkello na Shehe Amiri walipopelekwa kizuwizini mimi tu nalibaki nje nikawa mimi naliongoza jahazi. Watu tuliowapeleka Zanzibar kwa ajili ya mapinduzi wengi walitoka Tanga na Dar es Salaam. Wengi. Watu wa Unguja walitutaka tuwapelekee watu wende wakapige kura kwa sababu baadhi ya majimbo yao yalikuwa na upungufu wa watu. Hao walikuwa kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi. Hatukuwapeleka wote kwa pamoja. Tuliwapeleka kidogokidogo. Mohammed Mkwawa na Haruna ndiwo waliokuwa wakiwapeleka watu Unguja kutoka Tanga. Haruna kaka yake Abasi. Haruna amefariki. Chama cha Wafanyakazi kilinipa magari kutumia kupeleka watu Kipumbwi, Mshongwe na Mkwaja. Na chakula cha kuwapa wale watu wenye kupiga kura.

Page 115: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 83

Mkello alikuwa kucheza wazi hawezi. Alikuwa akinikubalia tu yangu. Ile active participation ilikuwa yangu mimi peke yangu. Si Muunguja! Waunguja wengine walikuwa pwani. Wengi walikuwa pwani. Wengi! Ndo kina Abasi hao, kina Haruna. Mtu na ndugu yake, baba mmoja mama mmoja. Wakifanya kazi Tanga. Kutoka Unguja kuja Tanga, alikuja Natepe, alikuja kutaka Jimmy Ringo arudi Unguja. Natepe alikuja Tanga wiki mbili kabla ya mapinduzi. Akatwambia kuna shida ya mapanga na watu. Tukamwambia atakuja nao Jimmy Ringo. Ndo tukatia watu kupitia Kipumbwi watu ishirini na tano na mapanga mia mbili. Tukapeleka. Wakapelekwa wakatupwa Mkokotoni. Siku tatu kabla ya mapinduzi, mimi Abasi na Mohamed Mkwawa tukenda. Tukashukia Bumbwini. Wale kina Abasi kwao Bumbwini tukaja zetu mpaka mjini. Hatujuwani kila mmoja ana kwake. Mkutano Kijangwani. Mimi nilijishirikisha mwenyewe huku bara. Nafanya mambo yangu, napeleka. Suala hili limegubikwa kwa sababu Serikali haitaki kujijuulisha na walikuja waandishi wengine wakaandikaandika maneno yao…Watu wengi wameandika ati na baadhi ya mambo yameoneka lakini yameonekana mengine ni uwongo. Mengi uwongo, maana yake sivo yalivokuwa. Kwanza wengi waliokuwa wakiulizwa sio wenye kuhusika! Unakwenda kumuuliza mtu wa Dar es Salaam katoka bara kaja hapa Dar es Salaam kwa kazi tu, kaletwa kwa kazi, unamuuliza mambo ya mapinduzi atajuwa? Yale sharti umpate mtu wa Unguja anacheza kati ya Unguja na huku. Yule ndo anajuwa. Wanasema Wazanzibari upole wao hawawezi kufanya vitu kama vile [va mapinduzi], sasa hawa lazima watu wamekuwa imported from mainland, [wameletwa kutoka bara]. Maana yake hapakuwa na mtu aliyeletwa kutoka mainland isipokuwa wale watu kama mia mbili, mia tatu, sisi Tanga tumeleta kama mia mbili, hapa Dar es Salaam wameleta kama mia tatu, ambao wengi wao ni Waunguja wenyewe waliokuwemo humu wakifanya kazi. Na Waunguja wote waliokubali kwenda kufanya kazi ile ni wale waliokuwa pwani [bandarini], makuli. Wewe utamchukuwa Muunguja aliyokuwa ofisini karani ende akapigane? Atakubali? Nyerere akijuwa na hata Mgereza alikuwa anajuwa na angetaka kuzuwia angezuwia. Mgereza aliiunga mkono ile na angetaka kuzuwia angezuwia. Babu alikuwemo kweli katika mipango lakini zile siri za ndani kabisa hakuwemo. Kuna mipango ile ya kwamba leo tutafanya, tena na kuna watu walijuwa toka mwanzo, na kuna watu walikuja kujuwa dakika ya mwisho. Tunapigana siku fulani. Makomred walijua, walijua hapa baadae tena kama sasa watu wanaeka na wanatafuta siku ya kupigana, sasa tutafuteni silaha na silaha kutafuta kazi. Kama Algeria ilileta silaha basi hiyo ilikuwa siri kali sana! Ambayo hata mimi sikuijua, ilikuwa siri kali sana hiyo. Baada ya mapinduzi tu mimi niliingia serikalini, nikakaa serikalini [Ikulu] pale Unguja. Hapana hata mmoja katika sisi tulotoka Tanga hasa aliyepata kazi

Page 116: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita84

nzuri. Labda mimi. Wengine hawakupata chochote…Baada ya mapinduzi kwisha ikabakia kazi ya kukamatana wenyewe kwa wenyewe. Nani alikuwa nini. Tukawa tunawaendea watu. Majeshi yakagawanyika mapande mawili. Kuna jeshi likawa la kwenda kwa wanawake, kuwalala wanawake wa maadui zetu, kuna jeshi likawa linakwenda kwiba, mali zote unozojiuwa wewe za matajiri wa Unguja zilichukuliwa, na kuwakamata wale maadui zetu wale, kuwakamata na kuwapeleka vituoni. Mtu anaambiwa, “lala chini, lala!” Mama wa Kihindi anasema “baba, hii bado toto dogo, hii haiwezi baba, kuja hapa.” Mambo yalipotulia walihama wote wakaja zao Dar es Salaam. Wale wanawake walokuwa wakifanywa hivo ni wale Hizbu matusi. Wale walifanyiwa vurugu. Mzanzibari nyama we! Kama yule alokuwa polisi Mwarabu wa Kimombasa yule. Sketty. Yeye alimpiga mtu risasi pale kwa Ali Msha na yeye alirushiwa shoka likamshinda kukwepa likamuingia. Shoka, mkuki? Alirushiwa mkuki…Watoto wa kwa Ali Msha. Tena pale Ngambo polisi pale. Watu wa Unguja nyama we. Upole wao, uungwana wao, ustahmilivu wao, uwongo mtupu! Kumbe upole ule wakati kuna usalama tu. Basi ikishakuwa kuna matatizo basi mbaya. Kina Rashidi Kawawa wao wakijuwa tu, tena tunapokuja huku [bara] wanatupa hongera. Mimi nikikaa na Mkello na Regional Commissioner wetu, Jumaanne Abdalla. Area Commissioner wa Tanga mjini alikuwa Ali Mwinyi Tambwe. “Hongera, hongera, hongera!” Mimi sikwenda Dar es Salaam. Mimi nalikwenda special kwa Regional Commissioner wa Tanga, Jumaanne Abdalla. Tulikwenda watu watatu. Mimi, Abasi na Haruna. Wakati ule natoka kupigana. Akanambia, nieleze. Nikamueleza mapambano yalivokuwa na kila kitu. Akanambia, “hongera sana bwana.” Nikamuambia nitarudi tena Zanzibar, wamenita wale. Sisi sote tutarudi tena Unguja. Jumaane akaniambia, haya, lakini mimi naona nyie msifanye haraka ya kwenda kule. Wale watu sku nyingi wamekaa wamebanwa wale. Hawakupata fursa ya kuitumikia serikali yao. Sasa waacheni wao wafanye nyinyi mbaki na kazi zenu. Sasa na sisi tukawa na hamu ya kukaa Zanzibar. Tuna hamu ya Zanzibar. Nilikaa kwangu Tanga. Baada ya kukaa Unguja siku kumi hali ishatulia nikenda kwangu Tanga. Wakanambia usikawie urudi. Nikarudi Tanga nikakaa kitako kazini kwangu kama kawaida, kama miezi mitatu. Nikarudi Unguja. Niliporudi Unguja nkakaa nkahisi nahangaishwa. Nikawaambia kama mimi tabu kufanya kazi basi nitarudi Dar es Salaam. Hanga akanambia hapana bwana. Usiondoke bwana. Nisiondoke na mie sina kazi? Akatia mkono mfukoni akanipa pesa za kutumia, akanipa na barua kama huyu bwana hamna haja naye basi mwambieni arudi Tanga. Arudi kwake. Aboud Jumbe akaniambia usirudi, mimi kwangu nahitaji mtu. Akanambia, kwanza twende kwa Mzee. Karume akanambia nenda hukohuko ofisini kwa Hanga. Hanga akanambia meza ile pale kakae. Haya meza hii inataka kufanywa

Page 117: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi 85

nini? Akaniambia utakiona hapohapo juu ya meza. Nikenda nkakaa juu ya meza hiyo nikakuta ma file. E jamani, haya ma file niyaingilie? Wakanambia “ingia, yafanye.” Nikafanya. Anakuja huku [bara], Hanga, Aboud [ Jumbe] na Babu. Wanakuja katika mambo ya Muungano sasa. Mara Oscar [Kambona] anakwenda Zanzibar, hawa wanakuja huku. Alimuradi ikawa fujo. Wakija huku mimi nakaa kule [Zanzibar] peke yangu, mimi na nani? Yule kijana yule, Ali Mohamed Ali Omar, yule jaji. Nikakaa pale. Na siri kubwa ya security yote iko pale. Huku kwangu mie kulikuwa hakuna kitu. Alipoondoka Ali Mohamed Ali akaja Rajab Saleh. Hakukaa hata miezi miwili akafukuzwa. Alitoa uamuzi mbaya. Badili ya kuiwachia serikali kutoa uamuzi alitoa uamuzi yeye. Wakamuhamisha. Sasa mimi nikakaa pale, nikawa mimi na Makame Mzee. Makame Mzee hamna chochote. Hata kuandika hajui lakini Karume kataka basi. Akenda kule katika Baraza [la Mapinduzi] anaandika, minutes zikawa hazieleweki. Kina Badawi na Ali Sultani wakaleta fujo katika Baraza, Kwanini asipewe Maulidi “Mgazija” akaandika? Nikaitwa horofa ya pili. Minutes zikitoka tu Barazani asizitowe mpaka kwanza zipite kwako. Thinian Mohamed Suleiman, kijana wa Kipemba pia alikuwemo mle na yeye pia alikuwa hazioni minutes. Yule Makame aliyachukuwa mambo ya Baraza kwa siri kubwa kwamba mtu yoyote asijuwe isipokuwa yeye. Kazi ikawa haifanyiki. Kaibana sana…Nikafukuzwa kazi. Nikarudi hapa nikapata kazi TANCOT, Tanganyika Cotton Company. Sikukaa hata miezi mitatu, nikapata habari mamangu anaumwa Zanzibar. Nikaondoka nkenda. Na ilikuwa mwezi wa Ramadhani. Nimefika nimekaa sku moja pale, baada ya Magharibi kumalizika, tushafturu, nimekaa karibu na msikiti. Nimekaa tunazungumza zungumza na jamaa tunangoja sala ya Isha ifike tuingie, Mandera akanjia akanchukuwa palepale. Sikuibuka mpaka jela. Na skuibuka tena mpaka baada ya miaka mitano. Hata sikuambiwa sababu. Nimekaa miaka miwili detention [kizuwizini], miaka mitatu nkenda jela hasa. Nilikuwa na mtoto mmoja wa Simba Makwega, ndugu yake huyu Sophia Makwega huyu. Sophia Simba Waziri huyu. Akanambia, mzee, wewe umefanya nini? Nikamwambia, shika adabu yako wewe mtoto. Unauliza unataka umbeya. Ma file unayo huko ndani, hebu soma hayo ma file. Akanambia, e bwana we, mie nshasoma hamna kitu. Nikamwambia, hata! Akanambia, basi kesho mimi nitayatizama halafu ntakiona, nkiiona ntakwita wewe uje uone hapo ilipoandikwa. Haya vyema. Kweli siku ya pili yake saa kumi akanifungulia huko chumbani kwangu nilikolala. We mzee twende ukanifagilie, ofisi chafu bwana watwana asubuhi wamekaa hawakuisafisha. Tukenda mpaka huko ndani. Akanambia file hili soma. Maulidi Sheni mkaazi wa Mlandege kakamatwa siku fulani na kaekwa ndani, Sababu hamna. Akanambia, sasa unaona? Akanambia, wazee wenzio hawa. Haya basi. Nikamvizia Mandera. Kila nikimuona, bwana sina nafasi bwana, sina nafasi bwana. Huna nafasi nini wewe? Mimi nataka

Page 118: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Sita86

nikuulize. Sina nafasi bwana! Sina nafasi. Kwani unataka nini? Nataka kujuwa nimefanya nini? Sina nafasi bwana, kweli bwana, sina nafasi bwana. Nimekaa miaka miwili. Mandera alikuwa akipiga sana watu lakini mimi hajawahi kunipiga hata siku moja. Wala sikuulizwa. Nimekaa miaka miwili yote Wallahi Laadhim sijaulizwa, hata kutukaniwa mamangu sijapata. Mwisho nikaanza kunenepa. Nimeshaondosha hofu. Si nakula bure. Nalala tu. Nakula nikiamka, nakula nikiamka. Kabla ya hapo, niko jela nshafungwa. Ile siku ya kwanza nimekwenda jela, sku ya pili, ya tatu, Hassan Ali, yule alokuwa Kamishna wa jela, yule Ithnaashir yule. Yule tulifanya kazi pamoja. Akanita. Aliwaambia, huyu msimpeleke shamba kwanza mpaka nionane naye. Siku ile nkaitwa. Maulidi, njoo bwana. Haya nkenda. Akanambia, umefanya nini wewe. Nikamwambia, hata sijui. Kama kujuwa wewe unajuwa. File hili halina kitu. Hapa inasema umefungwa miaka kumi. Bas! Miaka kumi e? Haya. Sasa? Nakuuliza wewe mwenyewe, umefanya nini? Tunatafuta sote kujuwa sababu wewe kwanini umekamatwa, hatujui. Nikamwambia, hata msitafute, mimi nimeshafungwa basi, na nyie msije mkajifungisha ndugu zangu…Tukatolewa kwa kuwaambiwa kuwa sisi wezi wa karafuu, sasa kwa hivo tunaachiwa kwa sababu tunaowapelekea zile karafuu hawapatikani. Kwa hiyo sisi upande wa serikali inaona kama inatuonea kutufunga sisi wakati wezi wenzetu hawapatikani! Ndo tukafunguliwa. Nilipotoka jela nikamwendea Kawawa kumuomba kazi. Zanzibar wame sign ile agreement [Articles of Union] unknowingly, bila ya kujijuwa. Alokuwa akiijuwa ile agreement ni Nyerere. Karume alifinyangwa na Nyerere. Hakumuachia kukaa na watu wake. Nyerere alikuwa ana akili zaidi. Hakumuachia Karume akae na watu wake kuijadili ile agreement. Imefanywa kati ya Karume na Nyerere na Nyerere alikuwa akimfahamisha Karume yale tu ambayo akitaka ayafahamu lakini mengine alikuwa hayajui. Sasa kukwambia yote ndugu yangu siwezi lakini mustakbal wa Zanzibar na Tanganyika sioni bright future. Naona kama mwisho tutagombana tu. Naona tutagombana tu mwisho. Uwongo, hakuna mwisho mwema. Manake hawa [Tanganyika] kuregeza kamba hawatoregeza, na wale [Zanzibar] watakaza kamba zaidi. Na kila kinachokuja, hawa wanasema, hata, haiko hivi, na hawa wanasema…kwa sababu kile kitu kiko ndani ya maandishi na yamefinyangwa kiasi ya vile wanavotaka wenyewe. Patakuwa na usalama hapo? Leo ikiwa Zanzibar CCM itashindwa atakamata Sefu, Sefu hatokubali hayo. Hii party ya Sefu [CUF] haitokubali hayo. Itataka lazma Articles of Union ibadilike, Hawa watakataa! Hapo pana usalama tena hapo? Kwa hiyo mimi sina tamaa ya…kwaherini jamani.

Page 119: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa SabaAli Muhsin na Nduguze

“Hawa watu hawatoyawacha makoloni yao bila ya kukusababishieni matatizo makubwa tena ya muda mrefu.” Wakati ule nikifikiri yule bibi masikini alikuwa hakijuwi anachokisema lakini kumbe nilikoseya. —Sheikh Ali Muhsin

Mzee Selemani ni mmoja kati ya wazee ambaye hakupendelea jina lake kutajwa ndani ya kitabu hichi.

Kabla ya kuendelea na suala la Manamba ni vema tukaizungumzia Mikindani ilioko Lindi kusini mwa Tanzania Bara. Kutoka sehemu ya Rasi ya Lamu, kwenda Tanga, Saadani hiyo, imekuja Bagamoyo, ukanda mzima huu, mpaka umefika Lindi, mpaka umefika Mikindani, hii jamii, ilikuwa koloni la Kiarabu kupita sehemu hiyo.1 Sasa katika koloni hizo zilikuwepo sehemu Waarabu walikuwa wameweka kama makao yao makuu. Mikindani, sababu ya kuingiliana Wamakonde, wale wa akina Ali Muhsin, MaBarwani kule ina maana walikuwa ni watu walioimarisha. Kuimarisha kwao, walichokifanya, wamemuoa mtoto wa Kimakonde. Kumuowa mtoto wa Kimakonde, sio Mmakonde machale, wa maraba wale, ni Waisilamu hao, wamesoma kweli kweli hao. Baada ya Waarabu kuwaowa wale Wamakonde, imekuja wamezaliwa watoto. Kuzaliwa watoto, kabila si wanafata upande wa baba, wanakuwa MaBarwani? Sasa utakuja kukuta Natepe yeye hakubahatika. Kaolewa baba Mmakonde, mama Mmakonde. Lakini ni ndugu. Ndo maana aliposikia Ali Muhsin amefariki akasema “lo, jamaa yangu keshakufa.” Kwa kujuwa yule Ali Muhsin ni Mmakonde mwenzangu mimi, kwa upande mmoja wa bibi zake wa upande wa mama. Sasa Ali Muhsin kwa kwetu kule sisi tunaweza kusema ndugu yetu.2

Mchanganyiko wa Kiarabu na Kimakonde, haujaweza kusaidia katika siasa za kuleta amani Zanzibar. Unajuwa, kitu kinachotufanya hivo ni ubinafsi. Ubinafsi umejenga ubinafsi. Na ubinafsi huu kukatika kwake ni muda mrefu sana. Kwa

Page 120: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba88

nini nikakwambia ubinafsi umetujenga? Mtu wa Chwaka si anasema “mimi si ndo kindakindaki Chwaka?” Sasa mtu wa Kidombo anasema “ebo! Itakuwaje? Tumbatu yote yangu mie. Asili ya kutoka huko na huko sie tumefikia Tumbatu. Sasa tukasambaa, ndo tumekuja Kidombo, tumefanya hivi, kwa hivo mpaka hivi sisi hasa watu wa Mkwajuni ndo kiboko yao!” Wa Kusini pia wanakuja kusema hivohivo. Mwarabu pia alikuwa haolewi na Muafrika au na Besar. Mwarabu akiweza kumuoa Muafrika, lakini Muafrika alikuwa hawezi kumuoa Mwarabu hata kama ni Muisilamu. Sasa hii haiwezi masuala kama haya jamii ikawa kitu kimoja, kutafuta maslahi ya nchi. Mshirazi hakubali kirahisi kuolewa na mtu wa bara. Unajuwa sasa hivi, Wapemba bara hawakuchukiza. Ni watu waliopendwa sana. Tizama Dar es Salaam mpaka kuendelea kufika huko Msumbiji, biashara zao kubwa sana. Kubwa sana. Kiasilimia Zanzibar, Mpemba ndo anayeongoza kibiashara. Mpaka leo. Kwa sababu Wapemba wana kitu kimoja. Huna kitu, nakuuliza “bwana we? Haya maisha unayoishi, vipi?” “Aa, mimi naishi mpaka sasa hivi hali yangu iko ovyo tu mpaka sasa hivi.” “Hapana. Sitaki uishi namna hiyo. Kamata hiki. Funguwa biashara hapo.” MuUnguja mpango huo hana. Ubinafsi zaidi. Nimsaidie fulani? Atanifanyia nini? Mwache akae hivohivo. Bora akucheke kuliko kule kumwambia, mimi nnakunyanyuwa. Sisi hapa hatuwezi kusonga mbele bila ya kwanza kuondosha ubinafsi wa mtu, wa kijamii, na wa kimajimbo.3 Tusijikatae, lakini tusijipe umbele wenye kulirudisha nyuma taifa. Pili, tuundoshe huu U­CUF na U­CCM na tuliweke mbele taifa la Zanzibar.4

Lakini hayo mengine. Tukirudi kwenye mada yetu [Manamba], kwa mfano, utakuta Amboni Matias ambaye ni Mmakonde kaandika Manamba kutoka Mtwara, kaja zake mpaka Tanga. Kufika Tanga, pahala pa kwanza alipofikia, alifikia shamba la Girigi. Kufikia shamba la Girigi, kakaa shamba la Girigi, ndo akahama, kuhama na akahamia shamba la Baniyani Mbezi. Mbezi ndipo walipokutana na Victor Mkello. Mkello akaja akawaeleza, skilizeni, kuna kazi yangu inataka kufanyika Zanzibar. Sasa kitu tunachotaka, yaani katika nyinyi Wamakonde, nyinyi Manamba nyinyi, mkutanike, mimi kazi yangu kukutana na nyie, nipate kiasi ya kiongozi mmoja au wawili wa kuweza kulizungumza hilo nnalolikusudia. Wakati huo wameshakutana na Abdalla Kassim Hanga, Musa Maisara, na Victor Mkello. Wamekaa pamoja kulijadili suala kama lile. Mkello, akasema, mimi nnachotaka kufanya, ni kuwashawishi hawa Wama­konde waliekuja Manamba. Nnapowapata hawa, ntawarubuni, kusudi kuja kukusaidieni kazi yenu lakini nnachokuulizeni, mnajuwa wanakokuja kuna kifo, familia yao itatizamwa na nani? Au wao wakisha fanikisha, watatizamwa na nani? Wakakubaliana viongozi watatu tu kwanza. Hanga, Musa Maisara pamoja na Victor Mkello. Hili suala tunaweza kukatibiana kwamba sisi hawa maisha yao, na atakayekufa, kizazi chake maisha yake, kwa hiyo mkataba huo ukapita. Alichofanya Mkello kuwashawishi akina Amboni. Akina Amboni

Page 121: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ali Muhsin na Nduguze 89

wamekaa kigengi chao pamoja. Jamani, kuna kazi hivi, hivi, hivi. Sasa vipi hili suala? Wakakubaliana wote kwa sauti moja. Sasa siri ile sio alikuwa anapita akisema tu. Anachukuwa kigengi cha wakubwa. Sasa wenyewe kwa wenyewe wanajuwana. Ikabidi lilivokamilika lile suala kwamba wale kukubaliana, wakati wa kuondoka, hawakutumia kuchukuwa likizo. Hawakusema sisi tunakwenda likizo pahala, au tunataka likizo. Aa! Victor Mkello alichofanya, kuwatilia right [tiki] kuwa hawa wapo wakati wakiwa hawapo. Wakubwa, matajiri wa yale mashamba siri hiyo hawakuijuwa. Kwa sababu na yeye alizungumza kwamba hii isijulikane. Kwa sababu ikija ikijulikana itabidi hawa wataulizwa tu kama wametoroka au wamekwenda wapi? Mkello itabidi aulizwe kwa sababu yeye ndo alokuwa mdhamini mkuu wa wale wafanyakazi. Kwa sababu kwanza alikuwa anatetea haki za wafanyakazi wa mkonge wote, yule, Mkello. Shamba fulani kadhulumiwa mtu yule anaingia, e bwana, e mbona hivi, mbona hivi, mbona hivi? Sasa uwezo huo ndo maana akawa all round [kahusika na kote] yeye. Mashamba. Akaweza akawafikia hawa Wamakonde hawa kuwaeleza suala, kama lile, manake wanajuwa kwamba huyu ni mtetezi wetu mkubwa huyu. Wamakonde hawa walikuwa wa mwanzo. Kwanza, Wangoni wamo, mpaka Wanyasa waliokuwa walowezi wa Tanganyika, wapo walikuwemo. Wahyao, walikuwemo. WaMwera walikuwemo. Wamakonde wa Lindi, walikuwemo, pia walikuwemo. Kina Amboni wao ni Wamakonde wa Msumbiji. Wamakonde wa Lindi mbali, Wamakonde wa Msumbiji mbali. Hii ni jamii imetiwa pamoja tu, kwamba jina ni Wamakonde. Kwa sababu bara hakukuchuliwa kwamba jamii ya Kimakonde peke yake ndo ilochukuliwa. Hapana. Yamechukuliwa makabila tafauti. Na wali­ochukuliwa zaidizaidi ni wale walokwenda vita vikuu vya pili va dunia. Ndo wale waliochukuliwa kwa sababu walijuwa kulenga risasi. Na usifikirie na hawa Wamakonde na hawa, kwamba wamechukuliwa bila ya fani za kivita walizokuwa nazo. Mkuki huu hapa, mpinde huu hapa, panga hili hapa. Mimi najuwa bunduki, bunduki. Sasa ikawa kutokana na wale nnaokutajia kama Wangoni, Wahyao, Wama­kuwa, wao wamechaguliwa kutokana na Mkello. Yeye aliwataka wale watu hasa waliekwenda vita vikuu kupigana, yaani wakati huo wakiita KAR [King African Rifles]. Aliwapata wale. Wakaingia. Kuingia, kilichofanyika, kuficha ile siri, kwenye mashamba, ondoka yao kutoka Kipumbwi kufikia Muwanda. Muwanda walivofika, hawakusambaa kwa kuja mjini. Wamepitia huko kwa huko, wanaefika Ndagaa, wanaefika Ghana, Dole, Ndunduke, hili Jimbo la Kati tu. Wao walikuwa wamo katika sehemu hizo. Kitu kikubwa walichokifanya, kufika kuchukuwa panga mahala wanalima. Huku shughuli zinaendelea. Mpaka kuna baadhi ya vikao misituni, hapa, kama va Masingini, shamba la Ndagaa lile, walikuwa wanashirikishwa, lakini nakumbuka kushirikishwa kwao katika sehemu ya Wamakonde, [Fundi] Tajiri peke yake ndo aliekuwa akishiriki vikao hivyo.

Page 122: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba90

Wengine hawajenda. Yeye akirudi anawaita wale kibusara. Kikao cha leo hivi hivi hivi…Kuchukuwa kigengi cha Wamakonde kuwapeleka sehemu za misituni kwenda kufanya mkutano siri itakuwa itatoka manake watu wataona “mbona hawa Wamakonde hawa wanaingia sana kwenye misitu. Kuna nini?” Tajiri alikuwa Mmakonde wa Msumbiji. Tena machale hasa. Pwani hapo, custom [sehemu ya mizigo bandarini] nakumbuka kawahi kufanya kazi miaka mingi. Kwa hiyo utakuja kukuta alikuwa ni mtu mzowefu, mpaka Waarabu walimzowea, kuona kwamba huyu mfanyakazi mzuri, mtaratibu, kwa vile hawakuwa na shaka. Lakini kumbe ulikuwa moto wa kumbi. Unamungunya chini kwa chini. Baada ya kukamilika jamaa, Mkello kaja Unguja, akakutana pamoja na Kassim Hanga. Baada ya kukutana na Hanga, Hanga akasema, sasa hii kazi imeshakamilika. Sasa madam imekuwa imeshakamilika sasa tumwite Yusuf Himidi kwa sababu Yusuf Himidi ni mkubwa wa ukusanyaji silaha. Hili suala la Manamba na yeye alielewe. Alikuwa halijuwi. Alipoitwa Yusuf Himidi, Yusuf Himid na yeye akasema “hata!, nisiwe peke yangu.” Nendeni Mikunguni kamwiteni Mfaranyaki, alikuwa anachonga Mikunguni. Kamwiteni Mfaranyaki. Wakakutana Mkello, Twala, Hanga, Yusuf Himidi, na Mfaranyaki. Wakawa watu watano. Yusuf Himidi kumpenda Mfaranyaki ilikuwa kwa sababu Mfaranyaki kenda vita vikuu, na anajuwa nini vita. Baada ya kufanikiwa yale mauwaji yalikuwa makubwa sana. Hii ilikuwa kutokana na Wamakonde [na makabila mengine kutoka bara] walikuwa wageni. Wanaona, mpaka sasa hivi huyu ndiye, huyu ndiye. Kumbe sio. Afro­Shirazi wangapi waliuliwa. Kuna Afro­Shirazi tulikuwa nao Waarabu, Washihiri, Wamanga. Wapo. Kwa vile Wamakonde waliingia kama ni wageni wasiejuwa kitu. Ndio Mzee Karume akasema “hapana, ho!” Anayekamatwa aletwe Raha Leo. Na wale [Wamakonde na makabila mingine] wakaambiwa, kilichobakia, wapi? Moja kwa moja Miti Ulaya. Wakaletwa Miti Ulaya, Miti Ulaya pale tena ikabidi wakapolea, walivoambiwa “kazi yetu tuliokusudia imekwisha! Sasa murudi kwanza majumbani mwenu, mtulie, tupange serikali, tupoze haya mapinduzi yetu, halafu tukae pamoja tulijadili suala lenu nyie na sie.” Kila waziri wa wakati ule baada ya kuchaguliwa waliwekewa Wamakonde kuwalinda kama ni walinzi. Ilikuwa mwanzo tu. Manake na suala hilo halikufika hata mwezi. Lilifanyika mwanzomwanzo. Mwanzomwanzo tu. Baada ya kuchaguwa mawaziri wakasema, sasa hawa washirikiane na watu kulinda, kutafuta nini, kwamba wale mtu anavotokezea akimkuta Mmakonde machale kama yule anasema “huyu bwana, aa! Hana stahmali huyu.” Lakini mwezi haukufika ikaondoka ile halafu wakawekwa polisi tu. Mwanzo mwanzo ule. Joto joto lile. Baina ya kufikiwa Manamba na mapinduzi hii bwana ilichukuwa chini ya miaka miwili. Chini ya miaka miwili ilitokea hiyo. Hii ilifika miaka miwili, inakwenda tu, inakwenda tu. Kwa sababu nini kufanya hivo? Lile suala halikuwa la vu! vu! vu! tu. Ni suala la kuwatongoza wale. Sasa Mkello alochukuwa dhamana

Page 123: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ali Muhsin na Nduguze 91

akasema hii kazi niwachieni mimi. Ndipo alipofanya utaratibu. Mkello kazi ile alipewa na Hanga. Na Hanga katoka hapa kampata yule baada ya kusema kwamba…Hanga alichotumia, Oscar Kambona kamwambia, weye kama unataka ufanikiwe uwapate watu wa Tanganyika. Kwa sababu watu wa visiwani wanajuwana, na halafu wamezaliana.5 Utamuona huyo Mswahili wa Tumbatu, lakini Mwarabu kamuoa dada yake au mama yake. Sasa kwa vyoyote utavofanya wewe, ukimpiga Mwarabu, yule pale aliyemzalia dada yake, basi ni lazima ataona uchungu, mtapigana. Sasa na siri hii, usiitumie kuisambaza kwanza Zanzibar. Hapana. Itumie kwanza kuisambaza kule bara.6 Hapo utapata mafanikio. Ndio ikabidi Oscar wakati ule Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje akija hapa, na alikuwa kuja kwake kama kupitia, anakwenda safari zake, ah! Ntateremka Zanzibar. Anateremka hapa, anaonana na Mzee Karume, lile suala sasa, Mzee Karume hamzungumzii, anamzungumzia Hanga. Siri yao. Ndo akamwambia, unataka Wamakonde machale, yuko mkuu wa Manamba, umpate huyu. Mimi ntampataje huyu, mbona simjui? Njoo Dar es Salaam. Akenda Dar es Salaam. Kilichotendeka, Oscar akamwita Mkello. Wakakutana sasa watu watatu. Bwana nilokwitia huyu hapa, mimi nishazungumza yangu kwamba kuna mtu atakutana na weye. Bwana, yule mtu niliyekwambia ni huyu. Sasa tufanye nini? Akasema la kufanya bwana hivi sasa hivi tunataka hivi: tunataka Manamba wako. Tuna kazi yetu tunataka kuwatumilia. Je, bwana msaada huu utatusaidia? Mimi ntakuwa tayari lakini kutokana na utaratibu wa hao watu… Si kazi yako hiyo. Wewe utufanyie kazi hiyo tu. Kazi ya hao watu tunayo sie. Sawa! Unajuwa tena na yeye yule lazima kutoka pale, anaambiwa motisha yako hiyo hapo kwa hiyo kazi unotaka kuifanya. Mkello akashughulikia mpaka akafika kuhitimisha. Baada ya kuhitimisha, Oscar alipoona imekamilika, akamdokolea Mwalimu. “Mwalimu eh! Tunakaa, lakini Zanzibar Afro­Shirazi wakati wowote wanaweza kuipinduwa ile serikali.” Mwalimu akasema “eh, vipi?” Akamwambia “wanaweza kuipinduwa wale. Lakini siri hii, wewe na mimi, na Mkello, lakini Karume usimwambie.” “Nisimwambie vipi Karume?” “Hii siri anayeijuwa, mimi, Musa Maisara, Hanga, Yusuf Himidi, na Jimmy Ringo. Hii siri ndo wanayoijuwa pamoja na Mfaranyaki. Ndio waliokuja kunieleza mie kisiri. Lakini njia watakayoitumia, watawatumilia Manamba.” Mwalimu alimwita Hanga. “Njoo. Kuna mnongono kidogo nimeupata.” “Umeupata vipi mnongono huo?” “Kuna mambo kidogo ya chinichini lakini hii ni siri kubwa. Kweli Unguja nyie mnaweza kupinduwa hii serikali, kweli?” Akamwambia “tunaweza.” “Sasa kwangu mnataka msaada gani?” Utusaidie, wakati utakaposikia nchi wameshaanza kupambana nao wale basi utuletee jeshi lako kwa siri. Pasi kujuwa. Kwa sababu wakijuwa watu, ile nchi tukishapinduwa itabidi sasa kabla hatujakaa miaka mitano, au miaka kumi, kwanza hapa itabidi wewe na sisi kwanza tuwe “benet, benet! [bega kwa bega]” Tukiwa sisi tu, wakati wowote tutaweza kupinduliwa. Mwalimu pale akaingia top [tele].

Page 124: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba92

Akasema “sasa hii, Zanzibar ntaipata!” Hapo ndipo palipojengeka…lakini akasisitiza, akamwambia “Oscar njoo, na wewe Hanga, hebu njoo!” Bwana wewe sisi tunakusisitiza, kuna siri nyuma ilitendeka hii ikavuja. Jamali Nasibu aliivujisha. Karume kidogo tu auliwe. Sasa, sasa hivi tumegeuza mbinu. Sasa hii bwana, usije ukamwambia Karume kwa sababu Karume alisema “Wacheni kabisa! Wacheni!” Huyu sasa sisi itabidi tumwambie siku ya mwisho. Sawa sawa. Wakakubaliana. Mwalimu unajuwa tena mtu wenyewe, “mimi nimeshalizuwia hili, lakini nyie kuna Mfalme kule, na kuna Mngereza. Bwana mkija mkaanza vurugu hiyo msije mkampiga Mngereza! Hamfanikiwi. Mkija mkimgusa Mngereza bwana nchi mtaiona chungu kwa sababu yule Mfalme analindwa na Mngereza. Jamani msije mkafanya hivo?” Tumekubali. Sawa. Na kwa kweli yaleyale aliyeyazungumza Mwalimu ndo yalofatwa. Mngereza hakuguswa. Mngereza hapa nakumbuka yule wa jela aliuwa lakini jamaa wakasema “jamani msimdase huyo!” Manamba walipomaliza mapinduzi wengi walikuwepo hapa, wengi walifanya kuselelea, wameselelea wengi tu. Wao na familia zao,7 walokufa wamekufa, waliobakia akina Amboni hao ndo wapo. Kama Tajiri alijiajiri kazi hapa. Alivotoka Manamba yeye kuja hapa, akajiajiri kazi, kwa sababu ukitazama utaona Tajiri alikuwa hadharani, na tizama basi Mwenye Enzi Mungu alivomjaalia, aliweka videvu, ndevu zake zilijaa zikawa nyeupee! Waarabu walimpenda sana. Kutokana na rangi yake ile na zile chale hazikuwa za kuonekana sana. Basi mjini utamkuta kakaa kitako barazani anazungumza na Waarabu. Wakisema “huyu Umakonde kapitia tu lakini huyu hasa baba yake huyu Mreno safi huyu.” Kachanganya yeye basi alikuwa ni mtu waliyempenda. Kustaafu kazi akenda zake Mfenesini. Khamisi Hemedi mbele ya Tajiri alikuwa hafui dafu hivo? Hasemi kitu. Hasemi chochote. Ndo mambo yalivokuwa yamekwenda. Manamba waliokuja hapa viongozi wao walikuwepo hawa watatu. Baada ya Tajiri, alikuwepo mmoja Thomas, alikuwepo mmoja tukimwita “Kangaroo”. Walikuwa watatu hawa. Hawa ndo walokuwa mstari wa mbele wa kuwaongoza wale Wamakonde. Kwa sababu mara nyingi sana walikuwa wanatumia kilugha. Halafu wanasemeshana kilugha. Mpaka listi Mzee Karume anayo ya hawa watatu. Watu watatu hawa walikuwa watu madhubuti. Hawatetereki. Na kiapo chao waliapishana, wenyewe Wamakonde kwa Wamakonde. Bwana kama tutafeli, ukija ukikamatwa, bora ukatwe kichwa, usiseme. Kazi ya Manamba ilikuwa zaidi katika kuyavamia maboma. Mtoni alikuwepo Tajiri. Hawa wawili, Thomas na “Kangaroo” walikuwa Bomani. Katika hawa watatu Tajiri tu peke yake ndo alokuwa Mtoni. Kwa sababu Mtoni Tajiri alisema “askari walioko Mtoni vitoto vidogo. Hawawezi kuhimili vishindo wale. Watakimbia wale. Lakini kambi kubwa Ziwani. Watu walokwenda mpakani wapo pale.” Akina Anthony Musa, wale wamekwenda vita vikuu na ndo walokuwa wakifundisha kule. Sasa operation ya mwisho wa kuwapanga wale, Anthony Kisasi ndo aliekuwa kapanga. Walikuweko na wengine. Weye uwende kule, nyie

Page 125: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ali Muhsin na Nduguze 93

mushirikiane na hawa jamaa. Mwende Bomani, mwende Mtoni. Bila ya Manamba mapinduzi ingekuwa si rahisi kufanyika. Si rahisi. Kwa sababu yenyewe, nnavokwambia. Moja tumelizungumza kwamba, sisi tunajuwana. Na mauwaji yalikuwa kwa wingi kwa sababu tulikuwa na wageni hawawajuwi wenyeji.8 Wamakonde, na makabila mengineyo kutoka bara, walikuwa wageni.9

Kutoka Bomani, boma limeshapinduliwa, pale pamebaki, askari wa Afro­Shirazi wapo pale, na wapinduzi wa Afro­Shirazi wapo pale, mchanganyiko pale wa Wamakonde…nakumbuka Ziwani watano, Mtoni watano, Malindi watano, wangapi hao? Kumi na tano. Waliobakia kumi na tano. Kumi na tano wanaingia kwenye magari ya patrol [kuranda doria]. Zilikuwepo gari za patrol kama sita hivi. Hizo gari zilikuwa zinafatana na mwenyewe John Okello. Wana round sasa, Unguja na mashamba. Unajuwa ndani ya kundi, kuna watu wana chuki binafsi. “Mwarabu huyu hapa!” Sasa unajuwa “Mwarabu huyu hapa” hapohapo Wamakonde watatu, wanne, watano. Nyote mnashuka pale. Sasa unajuwa, ukatili wa yule, yeye anakwenda tu anaingia tu mle ndani. Hamshauri mtu. Tena ikiwa panga, panga tu anaelekeza. Nyie sasa watu hapa mnaejuwa mnasema “aaa! Sivo hivyo.” Halafu yeye anarudi anakwambia “njomba, wewe mbona umekuwa una huruma, hawa wamekutawala, leo wewe unafanya huruma.” Sasa mtu kama yule sisi tulikuwa tunatahadhari sana nao wale. Ndo ikabidi ripoti sasa. Kwanza alielezwa Mfaranyaki, “Mfaranyaki eh! Sasa mauwaji yamekuwa makubwaa.” Sisi kazi yetu sasa hivi ni kuwachukuwa watu kuwapeleka Raha Leo, sio kufika leo ikawa mtu anauwa. Sivyo namna hii. Mfaranyaki alichofanya yeye, kamueleza Okello kwa Mzee Karume. Mzee Karume “zuwia sasa mambo ya mauwaji, kwa sababu sasa yamekuwa makubwa.” Sasa katika 10,000 aliowataja Okello, walouwa wengi wao wakiwa mchanganyiko, wengi wako wale wabara nlokutajia. Hili gurupu nnalokutajia mimi ni la Wamakonde tu. Makabila mengine waliuwa, na Wazanzibari pia, lakini hawakufika kiwango cha Wamakonde. Tuligutuka sisi, tukiwaogopa wenzetu. Ndo ikaamulika “hapana, na wakusanywe! Wapelekeni Miti Ulaya.” Wakaambiwa kaeni hapo. Kazi imekwisha, sasa kaeni hapo. Sisi tunabakia tukipita tukiwachukuwa watu tunawaleta Raha Leo. Mimi nakumbuka nilikuwa 64 [jina la mtaa] hapo. Kuna Mwarabu alikuwa anatukana ile mbaya, lakini nyumba hii kwa hii. Sasa mimi nilivoona nikasema sasa huyu watamuuwa. Mbona nilichomoka na bunduki zangu mbili, nikaja zangu mpaka pale, nikamgongea mlango “pa, pa, pa, pa.” Akasema “ah, …anakuja kuniuwa.” Nkamwambia “funguwa wewe!” Namwambia “funguwaa!” Akafunguwa, nkamwambia toka huko ndani, njoo kwangu. Nikamtowa yeye, mkewe, watoto wake. Nikampeleka kwangu, nkamwambia, bwana nakukomelea, chakula hicho hapo, stover [jiko la mafuta ya taa] hio hapo, hakuna raha hapa. Pika ule, choo ndo hicho. Usije ukafunguwa mlango mpaka ukasikia mimi nnagonga. Sijaondoka mimi ile nyumba yake wamekwenda kuivamia watu ati. “Vunja, vunja! Vunja, vunja!” Kukukuu, kuingia ndani wanakuta hakuna mtu.

Page 126: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba94

“Mwanaharamu, kakimbia huyu!” “Keshakimbia huyu mwanaharamu.” Mwarabu huyo nnakuhakikishia mpaka leo, Maskati aliko huko hukaa akasema “mimi namshukuru Selemani” Mimi nikaona “hmm!” Mimi yule sku moja alintukana matusi ya nguoni lakini mimi siyajali yale matusi. Mimi nijali roho yake. Nikenda nikamtowa bwana. Nikamtia mwangu ndani. Nikamueleza palepale Mzee Saidi Kibiriti nikamwambia “nyumba yangu ile pale asije akagonga mtu. Uwe mkali sana.” Kufika Maskati mwanawe mmoja huwa anakuja. Anapokuja anakuja mpaka nyumbani. Halafu hivi karibuni nlipata habari alikuwa ana safari ya kuja huku lakini bahati mbaya alipatwa na accident [ajali] ya gari. Sasa tulivoona sasa Okello hili blanket [guo] anataka kulitumia vibaya, akaambiwa, hebu nenda ukakaguwe Pemba. Mimi nimeshuhudia yangu katika hizo safari za Okello na Wamakonde. Nakumbuka, najuwa, kutoka kwa Ali Natu [jina la mtaa]. Tumekwenda kwa miguu, moja kwa moja tumekuja zetu, tumekuja pinda Raha Leo, tumeingia kwa Haji Tumbo [jina la mtaa]. Kwa Haji Tumbo tulipofika, Mshihiri alikuwa hana habari kumbe serikali imepinduka. Kafunguwa hoteli yake, maharagwe yanapwaga, sasa, Okello akamuuliza “Mwarabu eh! Umefunguwa hoteli, usalama gani wewe uliokuwa nao.” “Ah, karibu bwana, karibu.” “Aa! Umefunguwa hoteli leo, usalama gani unao weye?” “Kwa nini basi jamani. Hebu nielezeni.” Wewe huna habari kama serikali imepinduka. Imepinduliwa serikali. Basi Mshihiri pale pale alipinduka “tu!” Sasa tizama Mmakonde hatari alokuwa akitaka kuifanya. Aipuwe maharagwe kwenye sufuriya amwagie! Akitaka kumwagia. Ikasukumiliwa mbali huko na Okello. Akamuuliza “we! Sasa huyu mateka unataka kumwagia maharagwe sufuria zima, unajuwa hii sufuria nzima unauwa? Unauwa!” Sasa Okello, alichofanya kutokana na yeye ilimjia hisia kwamba sasa mbona kunatumika ukatili. Pale pale, alimwambia “wewe utafatana na mie.” Mshihiri, sisi na familia yake akatwambia “mpelekeni Raha Leo.” Mimi nafsi yangu tukamchukuwa mpaka Raha Leo. Tukamuweka tukarudi tena. Sasa Okello alichofanya yule Mmakonde kamchukuwa moja kwa moja mpaka kwa Yusuf Himidi. Anasema “huyu si mzuri kwa vile adabu yake huyu apelekwe moja kwa moja Kiinua Miguu, jela, afungiwe, mpaka tumalize haya mapinduzi hapa haya kwanza. Huyu damu imeshamlevya huyu.” Yusuf Himidi akamweka ndani kama hifadhi ya kumuweka atulie. Kweli wewe mtu leo, mie umenikuta umeniuliza kitu, sasa katika ile kuniuliza nimefanya msangao wangu, roho imenishtuka, nimeanguka, uchukuwe kisu tena unipige? Unguja hii Wamakonde wameshindwa kwa Sayyid Sudi [Sayyid Soud bin Ali bin Humud] peke yake. Kwa Seyyid Sudi peke yake ndo walokoshindwa Wamakonde. Lakini kwa suala la kimapinduzi, madam wale tuliwachukuwa ni Manamba, lazima watumie uwezo wa aina namna hiyo. Manamba, walikuwepo viongozi. Viongozi hawa ndio waliokuwa wameshirikiana kwanza hapa. Mmoja akiwa Hanga, akina Juma Maneno hao, akina Jimmy Ringo hao. Mpaka yuko yule

Page 127: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ali Muhsin na Nduguze 95

jamaa wa Tanga, Victor Mkello, ndio alipitia kwa sehemu ya Chama Cha Wafanyakazi. Katika kifungu cha wafanyakazi, wao wa bara ndo wakaweza kutowa ufumbuzi wa kujuwa kuwa sasa hivi bwana tufanye utaratibu wa kukutana na wenzetu bara, kule bara tutumie njia ya kupitia upande wa jamaa wa Chama Cha Wafanyakazi. Walimpata Victor Mkello wakakaa pamoja kulijadili suala hili. Hili kwanza ilikuwa kwa kuelezwa na mzee Abdalla Kassim Hanga, pamoja na Juma Maneno, halafu na huyu Jimmy Ringo, na huyu Musa Maisara, mpaka Natepe pia alikuwepo, akina Sefu Bakari hao, walikuwepo kulijadili hilo suala. Halafu, kinyume chake, Natepe na Sefu kwanza waliwekwa pembeni. Hanga ndo alokuwa hili suala alikuwa kalizamia mbizi. Kulifanyia utafiti, njia gani nipite kusudi hili suala isijulikane nnafanya nini. Hata nnafikiria hata baada ya kukutana na hawa, mkuu wa Wafanyakazi wa Tanganyika, Victor Mkello, ambaye kuona kwamba Manamba hawa ntawatumilia kwa kuwapeleka Zanzibar kwa kushirikiana na wale wenzi wao. Hapo baada ya kupata usahihi huu walifanya safari Hanga na Hasnu Makame wakenda bara kukutana na Mkello. Walipokutana na Mkello, wakapanga ushauri, kwamba sasa bwana utaratibu wa kuikombowa Zanzibar ni lazima tushirikiane baina ya nyinyi na sisi, nyinyi mutupe msaada. Tupate kujikombowa. Kule walikotoka Tanga kwenye mashamba ya mkonge, Manamba walikuwa wakiishi ndani ya jamii za makabila yao. Jamii ya KiMakonde, ya Kingoni….Hapa Zanzibar Wahyao kiongozi wao Mohamed Kaujore. Yeye mwenyewe Mhyao. WaNgoni, Mfaranyaki. Wanyamwezi, hawakupewa siri. Wanyasa walikuwemo lakini Wanyasa walijiunga na Wangoni, kwa sababu hawakuwa na kiongozi wao hapa. Walikuwa na Mfaranyaki. Na jamii kuu ya kibara, baada ya Mohamed Kaujore na Mfaranyaki, hao ndio waliokwenda nao sambamba jamii ya kibara. Hao wawili hao. Ndo viungo vikubwa hivyo. Na hata katika utendaji wa mikutano ya siri, ya ndani kwa ndani, wao ndio waliokuwa wanahudhuria kwenye vikao vile, kwa niaba ya jamii zao. Sasa wanapotoka kule, wanakuja kuwatizama wafuasi wanaowajuwa, huyu anafaa kumueleza suala hili, huyu hafai. Wanaelezwa. Jamani tumekutana kwenye kikao, majadiliano tumefanya hivi hivi hivi. Sasa wale unakuwa mnongononongono kwa wale walioaminiana. Jamani, Kaujore leo na Mfaranyaki wamekutana mashimoni huko, kitu walichozungumza, suala linaendelea, hivi sasa hivi nakumbuka, mishale pamoja na mikuki inatengenezwa shamba kisirisiri. Halafu nani mchukuwaji? Mchukuwaji Yusuf Himidi, kwa sababu yeye alikuwa PWD [Public Works Department] akiendesha gari. Viongozi wa Manamba waliokuja Zanzibar ni hao wawili, Kaujore na Mfaranyaki, lakini kiudokozi, kutokana na Victor Mkello, nakumbuka Mrangi alikuwemo, Warangi walishiriki, Wadigo walishiriki, mpaka hawa Waziguwa walishiriki. Ilikuwa si grupu, lakini ilikuwa wanachukuliwa watu kama watatu, wanne, watano, sita, kwa kila kambi, lakini wale walikuwa chini ya udhamini wa viongozi wawili hao. Hapa sio kama walikuja Wamakuwa tu, au Wahyao tu,

Page 128: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba96

au Wanyasa tu. Walichukuliwa makabila tafautitafauti waliokuwa wameshiriki. Fundi Tajiri yeye alikuwa mkubwa wa Wamakonde machale. Angelikuwa yuhai, yeye alikuwa ameweka ndevu. Wakimwita “Mwarab, Mwarab.” Manake ndevu zake zilikuwa nyeupeee, na halafu kutokana na ile rangi yake alikuwa mwekundu, sasa yeye ndo alokuwa kiungo cha Wamakonde. Na sehemu zake yeye alizokuwa akiwekea mikutano yake ya siri, Mfenesini. Kaujore yeye mikutano yake pamoja na Mfaranyaki, Shauri Moyo. Kutoka Shauri Moyo, Masingini, msitu wa serikali, kwamba hapa bwana kidogo pana dosari. Wakati huo Shauri Moyo ilikuwa ni pori lakini wakaona juu ya hivyo bora tuendelee tukazamie ndani huko Masingini. Watu wawili hao walikuwa wanashiriki sehemu kama hizo. Kwenda kwenda, sasa hapo ndipo walipokuja kuja kuchukuliwa akina Sefu Bakari, akina Abdalla Saidi Natepe hao, wakafikishwa mahali kama kule, jamani kinachoendelea, hiki hiki hiki hiki. Kwa kuarifiwa sasa. Kushirikishwa kwa sababu wao wako kwenye Umoja wa Vijana, ASPYL. Kwamba kama hatukuweza kuwashirikisha hawa, kidogo hapa mambo yanaweza kwenda kombo. Lakini hawa ni lazima tuwashirikishe na ushauri huu alitowa Hanga na Hasnu Makame.10 Jamani hili suala tukitaka tufanikiwe na hawa tuwaweke katika kundi hili, tuwavute kwetu, kwa sababu hawa ni Umoja wa Vijana. Hatuwezi kuwaacha mkono, Umoja wa Vijana utakuja kukuta utakuwa na nguvu. Kina Sefu Bakari na Natepe kwanza walizibwa midomo. Wakaambiwa, bwana eh, kikao hiki hakielezwi kiongozi. Haelezwi kiongozi, alisema Kassim Hanga. Kikao hiki tunakutana sisi tu. Kiongozi anapewa top [siri] ya mwisho, lakini suala la huku linakuwa limekwisha malizika. Tunalimaliza sisi. Baada ya vikao vile vyote kumalizika, ndipo Kassim akenda kama kumdokolea Mzee Karume. Hapa pana mpango tunataka kufanya hivi. Japo aligutuka “vipi?” Sisi tunataka kufanya hivi. Jamani hili suala mtakuwa hamuwezi. Tutateketeza umma hapa. Akamwambia, hiyo si kazi yako. Sisi tunakueleza kama kukupa ushauri tu, lakini kazi hiyo sio yako. Na wewe Juni 1961 uliwahi kusema kwenye Baraza la Kutunga Sheria, kwamba vijana Tupendane walifanya fujo hapa, watu wakasema Karume anataka kupinduwa serikali. Wewe ndo ukakanusha kwamba, hakuna mu Afro­Shirazi wa kupinduwa serikali. Sasa tatizo hili sisi, hili sasa, hatukubambiki wewe. Mkello aliwahi kufika Zanzibar. Yeye sio kuja mara kwa mara. Mimi kufahamu kwangu kaja hapa safari zake hizi mbili. Katika safari mbili hizi, Hasnu Makame ndiye aliyekuwa anakwenda naye bega kwa bega, kwenye mambo yao, kwa sababu inaonekana huyu yuko katika kazi na hapa pana chama cha wafanyakazi. Sasa inajulikana vyama va wafanyakazi ni lazima wanafanyiana ziara, kupeana utaratibu wa kikazi. Sasa kwa vile ikawa lile suala likafanya kufichika kidogo. Kurudi na kuja kwa Mkello kwa mara ya pili ndipo mpango sasa ulipokuwa umejengeka. Hii nakumbuka ilichukuwa mwaka kabla. Alikuja Mkello kabla ya mapinduzi. Kwa sababu hili suala lilipangwa mipango muda. Nakumbuka mwaka mzima kabla ya 1963, tuseme 1962, miaka miwili kabla, alikuja akajitokeza Mkello.

Page 129: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Ali Muhsin na Nduguze 97

Hata Hanga akawa anatoka hapa anakwenda kule, inakuwa yeye wanamuona yuko katika chama cha Afro­Shirazi, Afro­Shirazi na TANU ilikuwa ni moja. Na nnakumbuka baada ya kuja Mkello, Mwalimu alikuja akaja akafikia kwa Ali Natu, kuja, ilikuwa safari ile anakwenda zake Uingereza. Kupita, wakakutana na Mzee Karume, Thabit Kombo, na wazee wengine. Nyerere alikuwa yeye, John Rupia, na mtu mwengine nimemsahau. Nyerere akasema “hapa mpaka hivi mtapiga kura mpaka mnyonyoke mvi, mimi siwezi kukuambieni fanyeni hivi, kauli hiyo sitowi, lakini nnachosema mimi, nyinyi jisaidieni, msaada wa kichinichini mimi ntautowa.” Sasa msaada wa kichinichini alieutumia yeye kuwa address [kuwazungumza] Manamba na mkuu wao. Hiyo chamber [kikao cha siri] sasa kwa bara huko. Bwana wewe, hapa hakuna njia ya kufanya mpaka wasaidiwe Zanzibar. Kwa Wazanzibari tu peke yao hawatafanya kitu.11 Hawafanyi chochote. Kwa sababu kwa kukwambia hivo, ujuwe jamii ile imekuwa na mchanganyiko.12 Mwarabu kamuowa Mswahili, kamzaa Mwarabu. Mswahili ndie anayeshindwa kumuowa Mwarabu, lakini Waarabu wamewaowa Waswahili. Na jamii zaidi khasa ya Kimanyema imetokana huku bara, sasa utararatibu wa kufanya ni lazima wale, mara linapozungumzwa suala kama lile siri inatoka mara moja. Wamanyema wameingiliana na wamezaa na Waarabu.13 Lakufanya sasa hivi msaada utoke Tanganyika. Anaambiwa Victor Mkello kule na mwenyewe Nyerere. Mkello jawabu alilomjibu, kwa kauli ya Kassim Hanga hiyo, akasema, tumekutana na Hasnu Makame na Kassim Hanga, tumelizungumza hili suala, na hivi sasa hivi, kuendeleza kujuwa tutawapata vipi sisi hawa Manamba. Wakapewa muongozo. Hakuna njia ya kufanya, mchukuwe Wamakonde na tabaka za makabila. Isiwe mnawachaguwa Wamakonde tu. Siyo. Mnachukuwa kabila hili, hili, hili, hili. Muwachanganye. Na wanapofika Zanzibar wao muwatumbukize sehemu za mashamba. Wasilete mshtuko. Walitumia njia ya kutoroka. Wanatoroka kwenye mashamba ya mkonge. Kwenye shamba la mkonge Wahindi waliokuwemo mule, walikuwa wao wanajuwa tu “ah! Mbona fulani hayupo? Kila wakiita fulani hayupo. Kishashindwa kazi huyo. Kishatoroka huyo.” Sasa matoroshaji ya kule yalikuwa ya siri sana. Sasa mkuu wa wafanyakazi, Mkello, ndiye aliefanya usajili wa kuwafanyia utaratibu wale watu wake aliewajuwa kwamba hawa sasa hivi walitoroka hapa, wamekwenda kule, wamefanikisha, sasa serikali ilipopatikana, Karume na Mwalimu iko fidia fulani walipewa wale.14 Walipewa wale fidia fulani, kutokana na tumekuvunjieni kazi yenu na mmekuja kutusadia. Tunakwiteni ni wakombozi mliekuja kuikombowa nchi. Lakini la kufanya, kwa kuficha hii siri, kumficha huyu…Mwalimu atakapojulikana na Waingereza kwamba kashiriki mapinduzi itakuwa makosa hiyo, ikijulikana. Sasa la kufanya wale, mkuu wa Manamba, bwana eh, wewe kwanza tunakufunika blangeti, sisi na huku tunajifunika blangeti. Hawa watu tumewatowa sisi hapa tumewapeleka kule, sasa lawama hatutaki na Waingereza, sio na Sultani. Hatutaki lawama na Mngereza.15

Page 130: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Saba98

Na juu ya kulifunika blangeti huko lilijulikana. Kumfunika kwenyewe wale waliowachukuwa hesabu yao inaonekana kama hawa wametoroka, wameshindwa kazi. Kwa sababu unajuwa bara siku za nyuma Manamba walikuwa wanatoroka toroka sana. Na kule akitoroka mtu hafatiliwi tena. Anaetoroka hafatiliwi. Kwa sababu mimi nafsi yangu niliwahi kufanya kazi katika shamba la mkonge. Sasa nikaja nikaona hii! Hii kazi mbona ngumu. Ya mkonge. Kukata mkonge nikaona hapa bwana hapafanyiki kazi. Hii kazi itatuumiza sisi. Tukirudi kazini mikono imechanika chanika namna hii! Hii kazi ngumu hii. Tustahmili kwanza mwezi mmoja au miwili, tutapenya. Basi tuliondoka pale tukenda Dar es Salaam mafichoni. Hakuna alietufata. Manamba kwa kutoroka ni suala la kawaida. Na usajili wa Manamba wao walikuwa wanatoka wanakwenda Lindi, Mtwara huko ndo wanakwenda kuwasajili. Na sehemu nyengine tafauti. Baada ya kuwasajili na kukabidhiwa mwenyewe Muhindi, au Mgiriki, wakitoroka tena wao hawana jukumu tena. Wale wasajili wa kule hawana jukumu. Wale matajiri wenyewe wa mashamba ya mkonge walikuwa hawalijuwi suala lile. Kwamba hawa wametoroka kwa sababu ya kwenda kupinduwa Zanzibar, hawalijuwi. Ila mkuu wa wafanyakazi analijuwa. Wale wanaotoroshwa kisirisiri kutoka Kipumbwi. Nendeni Zanzibar. Wa kwanza nlokuwa nikimtambuwa ni huyu Mkello alokuwa akiungana na Hasnu Makame. Kwamba yeye ni fawahisha hapa. Tumemuona kwa macho yetu. Nakumbuka katika speech [khutba] yake ya mwisho alikuja kutueleza Shauri Moyo, jamani kuna ndugu zenu ntawaleta, Manamba, watakuja kukusaidieni kazi yenu, lakini muwe kitu hiki kimoja, kitu ubinafsi kiondoweni. Mkijenga ubinafsi hiki kitu hamfanikiwi. Alisema Mkello kauli hiyo. Alikuja alihutubia. Hasnu Makame yupo, Kaujore yupo, Juma Maneno yupo, Mfaranyaki yupo, Musa Maisara yupo, mpaka Kassim Hanga alikuwepo. Shauri Moyo. Likajadiliwa hilo suala kwa pamoja. Kumalizika suala lile Mkello akaondoka hakuja tena mpaka kumalizika kwa mapinduzi. Kufanyika mapinduzi alikuja kwa kifua kipana. Akaja hapa, nakumbuka alikumbatiana na Mzee Karume. Hapa sasa ndo alipoanza kujuwa Mzee Karume. Mapinduzi yameshapindu­liwa, serikali imeshaundwa, Mkello akafanya ziara ya kuja hapa Zanzibar. Alipofika, kampokea Kassim Hanga, Kassim Hanga akenda kumjuulisha na Mzee Karume, “huyu bwana kampeni zote tulizokuwa tukizifanya, Manamba katuleteya huyu hapa.” Mzee Karume aliinuka kwenye kiti akamkumbatia Mkello. Mambo hayo Ikulu. Nnakushukuru kwa msaada wako na sitokusahau maisha yangu, kwa sababu msaada ulionifanyia wewe, Kassim Hanga, Hasnu Makame, akina Mfaranyaki, nyote nnakushukuruni, lakini shukurani hiyo John Okello hakuwepo. Wakati huo keshawekwa kwamba yeye ndo “Field Marshall” mwenyewe na anashughulika na mambo yale, lakini siri ya ndani hasa ya kujuwa kwamba huu U John Okello nimepewa, napewa vipi? John Okello hapo hapakuelewa. Yeye aliona tu kaebuka “mimi John Okello!”, anatamba.

Page 131: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa NaneMusa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar

Mzee Jonas Joseph Mchingama ni katika vijana waliopelekwa Shimo la Mungu na Chama cha Afro-Shirazi na kusomea masomo ya siasa na mafunzo ya kijeshi. Baada ya mapinduzi alijiunga na Jeshi la Watu wa Zanzibar na kufundisha somo la siasa. Hivi sasa anajishughulisha na shughuli za Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na Msumbiji—Tanzania-Mozambique Friendship Association (TAMOFA).

Asili ya Wamakonde—J. J. Mchingama

Mimi kwa jina naitwa Jonas Joseph Mchingama. Sasa hivi nasema ni mzee wa Kimakonde kulingana na umri wangu nilizaliwa tarehe 6 Julai 1944. Katika kisiwa cha Unguja nlifika kwanza mapema mwaka 1953. Nimefika hapa kukiweko utawala wa kikoloni wa KiSultani na Mngereza. Mwaka 1956 nilichukuliwa na hayati Mtoro Rehani Kingo ambaye baadae alikuwa Meya wa Zanzibar. Yeye huko nyuma alikuwa na mashine yake ya kuchapisha magazeti. Gazeti lake likiitwa Afrika Kwetu.1 Basi yeye akawa ananilea. Alikuwa hana mke na mara zote nilikuwa nakula nyumbani kwa hayati Abeid Amani Karume. Mpaka mwaka 1957 ndipo ulipotokea muungano wa African Association na Shirazi Association. Huo ni mukhtasari wangu wa kwanza. Pili, Mmakonde, asili yake ni Msumbiji, Mkoa wa Kaskazini kabisa wa Msumbiji unaitwa Cape Delgado. Ndiko walokotokea Wamakonde. Katika kuzaliana wengine wakavuka wakaja Mtwara. Hawa wakaitwa “Wamakonde wa maraba.” Kwa nini wakaitwa Wamakonde wa maraba? Kwa kuwa huku Tanzania wanatumia sana “shikamoo, marahaba, shikamoo marahaba.” Sasa wa kule na wa huku wamekuwa wajukuu na vitukuu wamezaliana basi wale wa kule Msumbiji wanasema “Wamakonde wale Wamakonde wa maraba wale.” Hata sasa hivi ukenda Mtwara sehemu za Newala mpaka Mtwara mjini kuna watu wanalima Msumbiji. Ni kwao wanadhani hii ni koo imetoka kule Msumbiji lakini yeye

Page 132: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane100

kazaliwa huku Tanzania. Na mimi nimezaliwa Tanzania [Morogoro] lakini asili yangu nimetoka Msumbiji. Kwa hivo hiyo ndo ikawa wale Wamakonde wa Mtwara wanaitwa wa “maraba” na wale kwa kuwatania wale wanasema “Wamahiwa hao” kwa sababu mara nyingi walifikia hapo kwenye kijiji cha Mahiwa. Lakini wote ni watu wamoja. Na hii kuita “Wamakonde machale” ni kwa sababu ile ya kuchanja. Na sio wote wenye kuchanja. Lakini zamani ilikuwa ni utamaduni wa kabila lenyewe la Wamakonde. Pengine unaweza ukamkosa mchumba kama hukuchanja. Ni kama sifa fulani ya ushujaa. Kwamba mtu anaweza kustahmili maumivu yale ya kuchanjwa. Kuna Wamakonde waliletwa hapa Zanzibar mwaka 1953 kulima na kuchuma karafuu. Shida iliokuwa ikiwakuta wanyonge wa Afrika wa nchi hii ilikuwa ikiwakumba na wao. Na hasa ilipokuja harakati ya kisiasa za kudai uhuru wa nchi hii.2 Chama kikubwa kilokuwa kinawatenga watu hasa wanyonge wakulima na wafanyakazi ni chama cha Hizbu. Hiki kilikuwa kabisa hakitaki kuwaona Waafrika wanatawala. Kama ndo sera yao. Na kulikuwa na mfumo maalum mtu mweusi kuonekana majumba ya mawe labda awe na kazi maalum, boi au katumwa mchukuzi kupeleka mizigo. Lakini si mtu wa kutembea kule. Anaweza kutangazwa akaambiwa mwizi au akasingiziwa jambo lolote. Huo ni mfumo. Kwa hivyo tayari ukatokea ubaguzi, wale wanyonge wakaonekana kwamba wananyanyasika, na wao wakajenga chuki kwa wale ambao wanajifanya waungwana. Zanzibar Nationalist Party (ZNP) walikuwa wamegunduwa kuwa watu wa kutoka bara wana support [wanaunga mkono] zaidi Afro­Shirazi Party (ASP). Kwa hivyo tufanye njia ya kuwaondosha watu wa bara. Ukiacha jeshi la polisi, lakini hata raia walianza kufukuzwa kwenye mashamba, wengine zikatolewa meli bure, kama tripu nne au tano zilitolewa hapa na utawala huo kwamba watu wa bara warudi kwao. Hapa si kwao.3 Tendo hili iliifanya ASP iitumie nafasi hiyo nayo kuwachukuwa vijana wake kuwapeleka nje kujifunza mambo ya kisiasa. Mimi mmoja wapo nilokuwa nimetumiwa nafasi hiyo nikaelekea Mtwara kwenda kujifunza mambo ya siasa na mambo ya kivitavita. Lakini niliondoka hapa kama kwenda kujifunza mambo ya siasa tu. Ilikuwa ni siri ya mwenyewe Mzee Karume. “Nyinyi mnakwenda kwa sababu nyinyi mnategemewa kuwa viongozi wa kesho.” Sasa nafasi ya meli ya bure ya kuwarudisha watu wa bara kwao, na sisi tukaingia pale. Tukenda zetu kule tukawa tumechukuwa mafunzo ya siasa kweli pamoja na mafunzo mengine.

Shimo la Mungu

Safari yetu ya kwenda kusoma sisi tulikuwa watu kama 58. Lakini baadae

Page 133: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 101

1963 tukarudi lakini huku mambo yalikwisha kuanza kuwiva mno. Mambo ya mapinduzi. Yamewiva mno. Siri zake hatuzielewi vizuri lakini nataka kusema kwamba Mzee Abedi Amani Karume alikuwa anajuwa viini vote.4 Na tishio kubwa lilikuwa ni kwa Mngereza kwa sababu ndo alokuwa mdhamini wa nchi hii katika utawala wa Sultani. Ndipo baada alipokwenda kufunga mkataba wa kuondoka Mngereza hapa, kule Lancaster House [Uingereza], wakenda kufunga mkataba Muingereza aiwachie Zanzibar. Yaliyobakia tutamalizana wenyewe. Kwa lugha hii nataka kusema kuwa Mzee Karume alikuwa anajuwa habari za mapinduzi. Inakuja automatic kama kumalizana huku kama watakuwa wa­kaidi tutafanya mapinduzi. Na jengine ni baada ya kupatikana kwa uhuru 1963 mimi nilikuwepo pale Coopers pale bendera ya Muingereza inashushwa na ya Zanzibar inapanda, ya nyekundu na karafuu. Niko pale. Wengi walimlaumu sana Karume kaiuza nchi na katika kundi hilo tuloliongelea hapa la wasomi. Walimlaumu. Karume kauza nchi, kenda huko katia saini mkataba kwamba nchi ile basi tupate uhuru basi sisi tuendelee kutawaliwa tu. Walimlaumu sana Karume. Kauza nchi huyu. Hapa si kwao.5 Yeye [Karume] Mnyasa. Anajuwaje mambo ya hapa. Wakamlaumu lakini uhuru ukapitakana. Ikaandaliwa fete lakini maandalizi ya fete hii yanajulikana, tunafanya fete hii kwa madhumuni gani. Mkutano ukafanyika mkubwa, nakumbuka mpaka leo maneno ya Karume akasema “Wananchi tunatakiwa sisi WaAfro­Shirazi tusherehekee uhuru huu uliopatikana Zanzibar. Lazma tuusherehekee huu uhuru. Nchi yetu sasa iko huru. Yaliobakia tutasawazisha.” Bado anasisitiza lugha ile ile ya mapinduzi. Yaliobakia tutasawazisha wenyewe lakini Muingereza akishaondoka kwa sababu kizingiti kikubwa Muingereza. Hatumtaki Muingereza. Watu wakashangiria. Fete ika­andaliwa usiku kwamba sherehe za kusherehekea uhuru wa Zanzibar. Lakini uhuru huo huo ndo utakaopinduliwa siku hiyo hiyo! Ulisheherekewa kwanza.6

Na taarifa hizo za kwamba alikwenda kuzungumzwa yule Kamishina wa Polisi, yule Mzungu, ilikuwa moja ya mbinu za kivita. Nafikiri Mzee Karume si msomi lakini alikuwa ana akili ya mbinu za kivita. Ile ilikuwa ni triki ya kuwavuta askari kutoka makambini wakati mnahitaji kambi kuvamiwa. Wakiwepo wengi kutakuwa na upinzani mkali. Ni kuwavuta wawe nje. Yule Mzungu akaona Karume amefanya jambo la busara. Anataka nchi iwe na amani. Kumbe kambi tayari zilikuwa ziko wazi. Wanamapinduzi usiku ulipofika ilikuwa si ngumu kwao kuingia katika kambi na kuteka kwa haraka. Na siku ile nakumbuka tulikwishaambiwa, kwamba vijana wote turudi sehemu zetu za majumbani kwa wazee. Kusiweko mtoto yoyote anafanya kazi kwa Wahindi na nani. Wote warudi majumbani. Lakini hatujui ile siri yenyewe iko vipi. Tulikuwa hatujui. Hapana. Na kweli wakatokea wazee wa kabila langu la Kimakonde, na wao wakati ule kulikuwa na viongozi wao. Chama cha FRELIMO kilikuwa tayari kishakuweko. Kulikuwa na branch [tawi] hapa Zanzibar, Dar es Salaam, Tanga,

Page 134: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane102

na Mtwara. Sasa wale viongozi wa FRELIMO tayari walikwishakuwa wamepata hizo habari. Kwa hivyo wakusanywe vijana watakaoshiriki katika mapinduzi lakini iwe ni siri. Asitiwe mtu yoyote. Na wakakabidhiwa watu maalum. Mfano watu wa Kitope kiongozi wao ni fulani. Watu wa Mfenesini kiongozi wao ni fulani. Watu wa wapi, mtu fulani. Lakini silaha zao zote zilipakiwa mapema kwenye magari kuletwa mjini. Mjini zikapelekwa porini Mtoni pale, nyengine zikafichwa hapa. Kwa hivyo zilipofika time za usiku wazee wale waliondoka tu kuingia katika kambi. Na silaha wakazikuta huko huko. Baadhi ya viongozi wenzake, kwa sababu ya hitilafu zilokuwa zimejitokeza baina yao wakati huo walikuwa si rahisi kuzipata habari za Karume moja kwa moja. Na huu utata wa kwamba walikuwa wamekusudia kumuuwa ni kweli, walikusudia kumuuwa, lakini kwa sababu yeye ni kamanda alikuwa ana kitu kinaitwa RV, sehemu yake ya kutolea amri ya maficho.7 Badala mnamjuwa kuwa Kamanda wetu yuko mahala fulani lakini yeye yuko sehemu flani. Wanajuwa watu wachache tu. Pindi ikitokea mkinihitaji nitakuwa niko wapi. Ndani ya kundi hilo hilo la mapinduzi wako walokuwa wakimsaka. Wale walikuwa wanamtafuta Karume si kwa nia njema, kwa nia wamuuwe. Wamakonde kutoka Msumbiji wameshiriki mapinduzi kikamilifu. Walikuwa watu wa kwanza kweli kuunga mkono mapinduzi. Na waliambizana, na wakapanga mission zao kwa Kimakondemakonde, wakaweka ngoma zao na wao. Moja ilikuweko Jumbi, moja ilikuweko Dunga, kwa niaba ya kuwakusanya wanawake na watoto tu kwenye kundi lakini wanaume wote wakaja kushiriki katika mapinduzi.8 Hizo mbinu walizifanya, waliunga mkono vizuri, na hapo Ziwani, Mzee Joseph Balo alokwenda vunja kwa shoka ghala ya silaha. Na wengine ni akina Mzee Ngamia, Tajiri Fundi, Mzee Tomeo, Namina. Katika nnaowatambua hao. Walikuwepo hapahapa. Kwa hivo Wamakonde mapinduzi ya Unguja walishiriki vizuri kwa kuwaunga mkono wenzao ambao wote walinyanyaswa pamoja katika serikali hiyo ya mkoloni. Zanzibar FRELIMO iliundwa baada ya kutoka katika chama cha Mozambique African National Union (MANU). Na kulikuweko na chama chingine kikiitwa ODENAMO. Vyama hivi kwa pamoja vilikuwa vikidai uhuru Msumbiji lakini vikawa vinabaguana. MANU ilikuwa inataka uhuru wa Msumbiji upatikane kwa mkoa mmoja tu wa Msumbiji, yaani Cape Delgado. Wanokoishi Wamakonde na Wamakua. Na RENAMO yenyewe ilikuwa ni ya wasomi. Wao walikuwa wanataka wale wasomi na wana maarifa tu wajitawale wao wapate hadhi katika serikali ya ukoloni wa Kireno. Lakini Dr. Eduardo Chiwambo Mondlane yeye kwa kuombwa na hayati Mwalimu Nyerere, wakati yuko Amerika, kuna wananchi wenzako wa Mozambique wako kule Tanganyika, wanataka chombo lakini wamefarakana katika mfumo wa vyama vingi. Unaonaje ukenda wasaidia? Ndipo akaja Dar es Salaam akaunganisha vyama hivi kikawa chama kimoja cha FRELIMO, mwaka 1962 tarehe 25 June. Ikaundwa hiyo FRELIMO (Front

Page 135: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 103

Liberation Le Mozambique). Sasa kuunganika huko, wana Msumbiji walioko Zanzibar wakawa na makao makuu yao pale Makadara baada ya kuvunjwa hiyo MANU ambayo ilikuwa makao makuu yake pale Msikiti wa Bi Zeredi. Wakiita “klabu ya Wamakonde, klabu ya Wamakonde.” Kama unaelekea kwa Haji Tumbo. Kiongozi wa kwanza alikuwa Mzee Mtalama Likolo, halafu baada ya yeye akafatia Mzee Jabir Mpinyeke, sasa hivi ni marehemu, amezikwa hapo Dunga. Hawa ndo walokuwa waanzilishi na wazee wengine wapo hapa Zanzibar. Wakawa wanahamasisha vijana lakini pia walikuwa chini ya msaada wa Afro­Shirazi Party. ASP ikawa inawaunga mkono katika harakati hizi za ukombozi wa Msumbiji. 1964 ulipopatikana ukombozi wa Zanzibar FRELIMO nayo ikawa ina vijana wanahitaji kwenda ikombowa Msumbiji. Lakini vijana hao ikumbukwe kwamba pia walishiriki katika mapinduzi ya Zanzibar. Sasa wale FRELIMO wakahitaji msaada wa Afro­Shirazi kwa sababu wameshajikombowa, kuwasafirisha vijana wake waende Algeria kwenye mafunzo ya kijeshi baadae waende Msumbiji. Hayati Abedi Amani Karume akasema “Hapana. Ni gharama kubwa mwanafunzi mmoja kumlipia katika nchi katika mambo ya masomo ya kijeshi. Lakini kwa kuwa sie hapa tushafanya mapinduzi, vijana wote wataingia katika jeshi la Zanzibar, watapata mafunzo hapa, baadae tutawasafirisha kuwapeleka nyumbani.” Ndipo likatengwa hilo eneo la Dunga, jumba la mawe, kuwakushanya vijana wote walokuwa tayari kwa ajili ya ukombozi. Pale ikawa wanapata mafunzo ya kwanza ya kijeshi kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Zanzibar. Nakumbuka wanafunzi wake mmoja alikuwa Muharam Mohamed Dosi na Musa Maisara hao. Muharam alikuwa sana akishughulikia mambo ya afya. Maana alikuwa ni daktari. Lakini kina Musa Maisara, kina mzee Issa Kibwana, wao ndo walokuwa wakienda kutoa mafunzo ya awali na ili kuwaandaa hao vijana. Wanapokuwa tayari wanasafirishwa pale, wanapelekwa Nachingwea ndo kwenye kambi kubwa ya wapigania uhuru wote. Wanachukuwa mafunzo tena pale ya mwisho, baadaye wanapelekwa nyumbani. Wakati wanafunzi 58 tulipopelekwa Shimo la Mungu kiongozi wa FRELIMO Zanzibar alikuwa Mzee Mueba Mfaume. Viongozi wa FRELIMO walikuwa wakikutana na viongozi wa Afro­Shirazi hasa na Mzee Karume. Wanaporudi wanatuhamasisha sisi kwamba lazima tuwe kitu kimoja na Afro­Shirazi na hawa ni ndugu zetu, kwa hivo lazma kitu chetu kiwe hiki: kimoja.9 Lolote mtakalokuwa mmetumwa na Afro­Shirazi Party lazima mulitumikie. Na kutoka hapo vijana wengi ndo tukaingia katika Afro­Shirazi Youth League, huku tukiwa ni wanachama wa FRELIMO lakini wakati huohuo ni Afro­Shirazi Youth League. Lakini kwenye mapinduzi sisi 58 hatukuingia. Viongozi wa zamani wanaijuwa historia ya FRELIMO na Afro­Shirazi Party inafahamika hapa Zanzibar lakini hawa wa sasa hivi hawaijui.

Page 136: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane104

Mzee Selemani

Unajuwa mpaka sasa hivi nchi hii kama walivofanya Msumbiji na nchi nyengine kwamba kuna sehemu ya mashujaa. Zanzibar hakuna sehemu ya mashujaa. Hakuna! Na sisi tunawaambia kwamba Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu] kenda kujenga mwahala kwenye kaburi la mkusanyiko wa wanamapinduzi!10 Sasa tizama basi. Pana nini pale? Palifaa pawekwe nini? Pawekwe mnara wa kumbukumbu kuwa mashujaa wako hapa! Mimi siku moja nilimwambia ati Mzee Ali Hassan Mwinyi. Nikamwambia “Mheshimiwa, unakuja kutujengea juu ya migongo? Au ndo kwa sababu hatuna maana tena kwa sababu tumekufa?” Basi aliinama chini hivi akasema “Ah!”

Mzee Issa Kibwana

Pale napafahamu uzuri saana. Huwenda katika hao wanozungumza kwa ajili ya mahala pale mimi mmoja wapo, lakini hakuna anonisikiliza. Kisa, sijui kwa nini hawanisikilizi, lakini napigia ngoma saana. Nadhani mtu mmoja angelikuwa huyu yuhai pale mahala pangelifanikishwa. Mzee Kaujore, au Idi Bavuai. Kwa sababu wale wana idili ya mambo ya kumbukumbu.11

J. J. Mchingama

Walikwenda Shimo la Mungu na walikutana na vijana kutoka Msumbiji akiwemo marehemu Samora Moses Machel, alokuwa Raisi wa Msumbiji. Wakati huo hajawa kiongozi, hajawa chochote. Na yeye safari yake ya mwanzo anaenda kuchukuwa mafunzo ya kijeshi. Mpigania uhuru tu wa kawaida. Wanakwenda Algeria kusomea mambo ya kijeshi lakini itabidi wapitie hapo Shimo la Mungu kwa kuchukuwa hayo mafunzo. Na vijana hao waliotoka Zanzibar wakenda wakachanganywa pamoja pale. Sasa wakati wa kuondoka pale wale wanakwenda Algeria kuchukuwa mafunzo ya awali ya kijeshi, hawa wakarudi Unguja. Wale wa Msumbiji hawakuja Unguja. Wa Msumbiji walikwenda zao Algeria kwa ajili ya kuchukuwa mafunzo zaidi na Samora Moses Machel na wale wa Unguja wakafaulu wakarudi huku. Tulokwenda pamoja Shimo la Mungu kuna George Jua Kali. Yuhai sasa hivi anaishi Mwakaje hapa hapa Zanzibar. Nnaye ndugu yangu mwengine Lucas Anthony, yuko Koani, yuhai. Nnaye mwenzangu mwengine anaitwa John Mango, yupo hapa Unguja, yuko Ziwani. Kwa bahati mbaya kuna wenzangu wengine wamefariki. Michael Sakoma amefariki. Kafia Uganda katika vita va Uganda. Kuna mwengine Mohamed Ali Mzee, naye bahati mbaya amefariki alikuwa akiishi hapa hapa Bububu ninapoishi. Lakini hao watu wapo ni wazima na afya. Kama utawafatilia hao watu ukawapata basi ni rahisi sana wakakueleza kwamba

Page 137: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 105

kweli tulikuwepo. Kama si wewe basi hao watakaohoji au kutaka kufuatilia. Kwa sababu ni muda mrefu wengine watakuwa hatujawasiliana hadi sasa na wengine wamekufakufa. Sisi tulipoondoka hapa kwanza tulikusanya vijana kutoka sehemu mbalimbali. Tukakutanika Miti Ulaya ndo palipokuwa Afro­Shirazi Youth League [ASPYL]. Tukaambiwa kama wako wenye kutaka kwenda kusoma masomo ya siasa nje wajitokeze. Tukajitokeza sisi. Wengine walikuwa waoga pale. Ah! Huko tutapelekwa sisi, nchi za watu, tutakwenda kuchinjwa, na nini. Lakini watu wengine tukawa kama tumekufa wadudu. Tukanyosha vidole. Huo ulikuwa mwaka 1962. Tukajiandikisha pale nendeni, basi siku fulani muje mtakutana na wazee mpangiwe safari yenu. Kweli ikafika siku hiyo tukenda pale tukakutana na Mzee Karume, Sefu Bakari, Khamisi Hemedi, Hafidh Suleman. “Nyinyi vijana mmejikubalisha safari sio?” Msemo wake [Mzee Karume] ulikuwa wa kutishatisha. “Mmekubali safari? Mnajuwa mnakokwenda? Basi mtakutana na wenzenu kwenda hiyo safari huko. Mkajifunze siasa ya nchi. Namna gani kujitawala. Nyinyi. Kwa hiyo hapana kufanya mchezo mnakokwenda. Watengezee safari.” Kina Rajabu Kheri walikuweko pale. Mtu wa bara anaetaka kwenda kwao meli bure! Mpaka Dar es Salaam. Tulipofika kule tukapokelewa na TANU Youth League. Tukafikia kwenye kambi ya TANUYL, tukaondoshwa pale Dar es Salaam moja kwa moja mpaka Mtwara. Tuliondoka kwa magari ya malori. Tukenda zetu mpaka Mtwara tukafikia kambi sasa hivi ni makao makuu ya Tanzania­Mozambique Friendship Association (TAMOFA). Chama cha urafiki. Ndo tukafikia pale. Tukafika pale tukalala, asubuhi yake tukapelekwa huko kwenye kambi yetu Shimo la Mungu. Tukaanza kupangiwa pale kwa section [kikundi] na tena tukagawanywa. Hatukuwa Wazanzibari watupu pahala pamoja.12 Tukachanganywa katika vikundi. Wabara na wa visiwani [Zanzibar] tukachanganywa kando. Hii platoon number 1,2, hii namba 3…Tunakutana kwenye madarasa kwenye masomo na wakati wa chakula, na wakati wa michezo. Kwa bahati wenzetu bara walikuwako na wasichana. Kwanza kulikuwa na vijana wa TANU Youth League baadae kulikuwa na wataalamu hawa wa Kichina na baadae kutoka Kanada. Walikuwepo pale wakifunza lakini kwa siri kabisa. Na nafikiri harakati hizi alokuwa akizijuwa ni Mwalimu Nyerere na Karume. Pia kulikuwa na kambi ya Bagamoyo ya wapigania uhuru wa Msumbiji, FRELIMO. Kukawa na kambi ya Mazimbo, ni jirani ya Ngerengere. Kwanza ilikuwa ya FRELIMO halafu wakaachiwa hawa ZIPA, nafikiri wa Afrika ya Kusini. Kuna kambi ya FRELIMO ilokuwepo Kongwa, Dodoma kule. Kambi ya Nachingwea ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuja baadae. Lakini hiyo ninayoinzungumzia ya Shimo la Mungu ni ya TANU Youth League na Afro­Shiraz. Ya Mtwara. Njia za kurudia [Zanzibar] walizozitumia zilikuwa njia za ngarawa. Wengine walikuwa wakivukia Mtoni hapo, au Mangapwani, au Bweleo, na moja ya

Page 138: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane106

Kizimkazi. Kulikuwa na nahodha mmoja sana ndo alokuwa akiwachukuwa akiitwa Mzee Kopa. Huyu ndo alokuwa akitumiwa sana kuvusha watu kwa njia ya magendo. Alikuwa akikaa Makadara hapo, Msikiti Zabibu. Walikuwa manahodha kama watatu lakini mimi namkumbuka huyo. Ilikuwa si rahisi wakati wao wameshawaondowa watu wa bara kurudi kule halafu wapite tena njia za meli kurudi huku. Ilibidi warudi njia za panya. Wakifika Dar es Salaam wanatawanisha. Nyie mtaondoka leo, wengine mtaondoka kesho, lakini pengine siku ile ile mtaondoka makundi mawili. Lakini hamuwezi kujuwa. Nyinyi mnaondoka kwa njia ya Kunduchi, wengine wanaondoshwa kwa njia nyingine. Mnakutana mshafika huku.

Manamba Hakuna

Kwa uzushi wa watu wanaweza kusema kuwa wameletwa watu kutoka mashamba ya mkonge ya Tanga kuja kupinduwa Zanzibar. Hio si kweli. Mfano John Okello, wanasema John Okello ni Mau Mau alieletwa makusudi kwa ajili ya revolution [mapinduzi] ya Zanzibar. Si kweli. Kwa kuona ile lugha alokuwa akitumia. Lafidhi yake. Wameona, kweli Mau Mau wameingia hapa. Unajuwa kwenye vita kuna vita va kipropaganda. Wanaweza kusema watu hivo lakini kuletwa watu kwa ajili ya mapinduzi hakuna. Hakuna kabisa nakataa…Kwa sababu kama itatokea Manamba watakuwa Wamakonde, Warundi, ndo watu walokuwa wakiishi kwenye mashamba ya mikonge. Wanyamwezi kiasi tu, si wengi sana. Wanyachusa. Na hao hakuna Unguja waliokuja kwa njia hiyo. Hakuna. Walikuwa hakuna Wajaluo wengi ambao walikuwa wakishiriki kwenye mambo hayo ya mikonge. Wajaluo walikuwa wachache. Torozima Luich, na Thomas Pet alikuwa jeshi la polisi. Kwa hiyo suala hilo kabisa mimi naona, sio naona, nakuhakikishia kuwa hakuna mtu alieletwa kwa njia hiyo. Si kweli kabisa! Ni uzushi na propaganda. Lakini ukinambia mkataba wa kuchuma karafuu, au watu waliokuja wenyewe binafsi, hiyo nakubali. Ndo mana pale Kinazini. Unajuwa mfumo wa Unguja wakati ule, mtu yoyote akionekana akionekana Mnyamwezi tu. Akiwa Mgogo, Mnyamwezi. Kwa hivo pale Kinazini unasikia “Banda la Wanyamwezi.” Pale inapojengwa ile benki mpya, palikuwa na banda la Wanyamwezi. Wakitoka huko wanafikia pale, Waarabu wanawachukuwa watu pale kuwapeleka mashambani mwao. Mkubwa wao alikuwa nani? Abdalla Kututu. Ndo akipokea jamaa pale yeye anawauza. Kwa upande mmoja mimi naipongeza sana serikali kujenga benki pale. Badala ya kuwa benki ya watu sasa wameweka benki ya kuhifadhi fedha. Mimi nimefurahia sana kile kitendo na amefikiri sana Raisi. Kwa sababu ilikuwa ni benki ya watu. “Wanyamwezi” walikuwa wanakuja kuchukuliwa pale na matajiri. Sasa imekuwa benki ya kisasa. Mimi napongeza sana kitendo hichi. Vijana wa kisaivi wanajuwa Kinazini lakini mtu mzima yoyote mwambie “banda la Wanyamwezi.” Na mimi mwaka 1953

Page 139: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 107

nilifikia pale nikiwa na umri wa miaka minane, na babangu na mamangu. Tulifikia pale. Akaja Mwarabu, Yahya wa Pongwe. Akaja kutuchukuwa pale! Baada ya kufika pale siku mbili kuna jamaa yetu, ndo huyo wa Tunguu kapata habari tumefika pale akaona “Lo! Pabaya hapa.” Akaja akatuhamisha usiku kwa kututorosha! Tukendahamia Tunguu nyumbani kwake. Ukenda Pongwe huvuki. Si kweli. Si kweli kabisa. Musa Maisara ni mtu wa Kitundu. Hayati babake akiitwa Maisara Kapungu, ana rungu lina meno saba! Akijiita “Mungu mtu.” Ule utundu wote alokuwa nao Musa Maisara kampeleka [kaupata kutoka kwa] babake. “Jimmy Ringo” [ Juma Maulidi Juma] namfahamu wakati wa siasa yeye kwenye mkutano alikuwa anahutubia, neno lake la kwanza anasema “chama kimeniruhusu niseme ninachokitaka. Nikichelea nitachelea mimi lakini chama changu imara.” Ndo anaanza kufunguwa mkutano “Jimmy Ringo.” Kuwa yeye na Musa Maisara wakisimamia kambi kwenye mashamba ya mkonge hizo ni propaganda. Au mtu alikuwa anataka kufurahisha hizi taarifa zinoge zaidi lakini sio kweli. Omari Kopa ndo alokuwa nahodha mkubwa wa kuvusha watu kutoka Tanga kuja hapa. Magendo. Kwa hiari zao wenyewe watu. Yeye anasema “ukitaka kuta­jirika nenda Unguja. Pesa mara moja. Unachuma karafuu ukimaliza wewe una pesa.” “Njia gani? Omari Kopa yupo. Anavusha watu.” Anakwenda mtu binafsi anakwenda pale anapatana na Omari Kopa. Ningepata ushahidi kwanza huyo mtu anaejuwa hivo akatueleza hao watu alokuwa akiwakusanya walikuwa kambi fulani. Akatupatia japo mmoja wawili wakatwambia kuwa wao walikuja kwa njia hiyo.13 Akiri yeye mwenyewe kuwa mimi nilikuja kwa njia hiyo ya Manamba. Na kambi yako ilikuwepo pale. Nafikiri ingetusaidia zaidi. Mtu atafikiri mwenyewe. Mimi mmoja wapo nilishiriki. Ndo mmoja nilikuwepo kambi hiyo. Lakini kama atazungumza mtu akasema mimi ni mmoja wapo nilikuwa kiongozi nilikuwa nikiwasimamia, anaweza kuwa anajipamba ili na yeye apate sifa fulani. Nijipambie sifa. Anaweza kufanya hivyo. Kama tutampata mwenyewe muhusika…basi sio wote wamekufa, watakuwa wapo watu. Watakuwa wapo na yeye atakuwa anawajuwa. Katika kukaa nao katika kambi hakosi mtu mmoja wawili walokuwa wa karibu. Suala la Manamba linawezekana lakini mimi siwezi kulijibu hili suala lakini nnachokifahamu mimi ni kweli watu wengi kutoka Msumbiji walikwenda kuchukuliwa Manamba. Wanakuja Mtwara wanasafirishwa wanapelekwa Tanga, Morogoro, wapi, kabla wakati huo Chama cha Wafanyakazi hakijaundwa wala TANU. Nyuma kabisa huko! Ambapo mimi babangu alichukuliwa Manamba na mjomba wake kutoka Msumbiji. Mjomba twende huku kuna kazi, na nini, na nini. Akamchukuwa mpaka Mtwara, Mtwara akamsafirisha mpaka Morogoro. Morogoro yapo mashamba ya mkonge. Kuna shamba la Mazimbo, Kilosa, Kinguruwira, Ngerengere. Yote mashamba ya mkonge. Si Tanga peke yake. Mashamba ya mkonge yapo Tanga na Morogoro. Babangu alipofika

Page 140: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane108

Morogoro kwa bahati yuleyule mjomba wake akamkabidhi cheo cha unyapara kwa kuwasimamia Manamba wenziwe. Mimi nikazaliwa mwaka 1944 kwenye shamba la mkonge. 1953 ndo tukaondoka Morogoro kuja Dar es Salaam babangu kuja fuata karafuu. Kwamba Unguja wakati ule karafuu ilikuwa ni mali sana. Pishi unachuma kidogo tu una mapesa mengi sana. Ukenda kulima kibarua hapa na pale ushapata pesa nyingi sana. Kweli anakwenda mtu mwezi mmoja miwili anarudi nyumbani. Babangu akashawishika akaja hapa Zanzibar. Sasa kama Chama cha Wafanyakazi kilifanya organization [mipango] hizo kwa sehemu ya Tanga, kwa sababu ya urahisi, karibu na Zanzibar, kwa hiyo inawezekana kama kulikuwa na organization hizo za kuwashirikisha watu kutoka huko. Itakuwa hiyo ni high level [daraja ya juu kiongozi] ambako pengine sisi hatujuwi kama walikuja watu wa aina hiyo. Lakini suala la vijana waliokuwa wamekuja au wamekwenda huko Shimo la Mungu…njia zake walikuwa wanaandaliwa kiuongozi, kisiasa na hata kijeshi kidogo. Walikuwa wanaandaliwa hivo. Karume alikuwa ameipata mapema kwamba lazima niwe na vijana niliowaandaa katika misingi ya Afro­Shirazi Party kuliko hawa wasomi ambao tumekutana katika chombo cha Afro­Shirazi Party. Ndo hao akina Abdalla Kassim Hanga, na Twala, na yeye mwenyewe akawagunduwa kama hawa watakuwa kidogo si wenzangu hawa. Sasa lazma mimi niandae kikosi changu. Vijana wangu ambao wataondokea katika migongo ya chama cha Afro­Shirazi Party. Kwa hivo tukapelekwa kule Shimo la Mungu. Zaidi tukawa tunafanya siasa. Namna gani kuutumikia umma wa watu. Namna gani kuijenga nchi. Namna gani kulinda nchi. Hiyo kweli tulikuwa tumefanya. Nilikaa na Mzee Karume tukazungumza haya masuala kuhusu kupelekwa mafunzoni. Nilikuwa mimi, Kali Haji, Juma Haji, tulikuwa tunakwenda sana kula pale kwake. Tunakula, yeye anatwambia “nyinyi vijana fanyeni hiyo kazi lakini pia nyinyi mnatakiwa msome mjifundishe, hali ya nchi yenu muijuwe, kwa sababu nyinyi kesho mtatakiwa kuwa viongozi wa nchi hii. Sisi tunafanya kazi kumsaidiyeni nyinyi ili muweze kukaa vizuri ndani ya nchi yenu.” Katika mwezi wa Aprili au Mei hivi 1963 tulirudi Zanzibar kutoka Shimo la Mungu. Kwa sababu ule uhuru ulipatikana mwisho wa mwaka 1963 sote tuko. Tuko pamoja. Tunakutana Youth League pale Miti Ulaya. Tunaonana wote. Mzee mwenyewe anakuja pale anasema “nyie tulieni tu. Msiwe na wasiwasi. Haya mambo yamekwisha haya.”

Mapinduzi Si Kuuwa

Tuliporudi Zanzibar tulitakiwa na Mzee Sefu Bakari tuwafunze wenzetu masomo ya siasa na baada ya mapinduzi nikawa mwalimu wa siasa katika kikosi nilichopewa. Katika somo fulani la kisiasa wakati ule Sefu Bakari alitusomesha, kwamba katika Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Kenya inatakiwa ilete mjumbe

Page 141: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 109

mmoja katika kikao kinapokutana. Lakini Kenya hawashiriki kwa vile kila wakati kiti kile kinakuwa kiko wazi.14 Kwa sababu gani? Kenya ilichangia mapinduzi ya Zanzibar baada ya kumkataa Sultani kushuka katika bandari ya Mombasa. Kwa sababu kama angeshuka bandari ya Mombasa, Mombasa kihistoria ni sehemu ya Zanzibar. Kwa vile alikuwa na haki kuomba msaada pale wakati wowote ulimwenguni. Kwa sababu bado yumo ndani ya nchi. Lakini kitendo cha Jomo Kenyata kusema “aa, huku mimi staki fujo” ikabaki aelee baharini. Kitendo hicho tayari alikwisha shiriki kuyaunga mkono mapinduzi. Kwa hivo [Kenya] ikapewa heshma iwe na kiti chake kwenye Baraza. Lakini kwa bahati mjumbe wa kule akawa haji na hakufahamu maana zake kile kiti kikawa kiko wazi kila Baraza linavokutana. Na hivi sasa Baraza la Mapinduzi linakufa taratibu na nafasi yake inachukuliwa na Baraza la Wawakilishi ambalo kikatiba halina nguvu mbele ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.15 Neno hili “Baraza la Mapinduzi” na kwa sababu lilokotokea, limefanya mambo makubwa. Limetaifisha mali, mashamba, majumba, limefunga watu, pengine limenyonga watu. Leo ukilizungumza watu wanatishika. Wanaona “Lo! Unakuja mfumo ule ule.” Lakini ndani ya Baraza la Mapinduzi kulikuwa na vipengele ambavo walivipanga. Tunataka mapinduzi ya kilimo, mapinduzi ya elimu, mapinduzi ya afya. Ni neno “mapinduzi.” Mapinduzi si kuuwa. Si kutisha. Si kunyonga. Hapana. Mapinduzi ni kukigeuza kitu fulani kukifanya kitu fulani. Mapinduzi ni ya maendeleo. Kama ni hivo basi, lile Baraza la Mapinduzi, na still [bado] wangetafuta vipengele fulani, vitakavoungana baina ya Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi katika miswada pengine inayopitishwa au vikao fulani wanavokaa. Wakajadili kitu fulani na Baraza la Mapinduzi. Kinyume cha hivo, kuwepo basi Baraza la Mapinduzi hakuna maana kwake. Na hao vijana wetu ambao tayari wameshakuwa memba wa Baraza la Mapinduzi wakati hawayajuwi hayo mapinduzi yenyewe, wakati pengine hawakuona kumbukumbu yoyote kwenye maandishi nini na nini, wataendelea kubaki tu, mimi nina nafasi ya rank [cheo] cha memba wa Baraza la Mapinduzi. Lakini mapinduzi yenyewe siyajui. Sasa vipi mimi nitakuwa memba wa Baraza la Mapinduzi wakati mapinduzi yenyewe siyajui? Kwa hivyo huu utata huu nafikiri upo. Kuna watu wengine wanafurahi kwa kutokuwepo kwa jina hili la “Baraza la Mapinduzi” kwa sababu wameathirika wakati wa mapinduzi yenyewe. Hata katika sherehe zenyewe hizi unapowakumbusha kuna watu wanaathirika. Kuna watu muungano [na Tanganyika] hawaupendi. Kwa sababu zao tu na malengo yao. Hawapendi kwa sababu labda wengine wamehusika kwa kupinduliwa. Hawapendi kwa sababu pamoja na kwamba ni kupinduliwa ingelikuwa ni rahisi wangeomba msaada kurudisha tena (counterrevolution), lakini wanashindwa kwa sababu wakiigusa Zanzibar tayari wameigusa Tanzania nzima. Kwa hivo muungano hapo hapo unalinda mapinduzi.16 Kwa sababu sasa hivi

Page 142: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane110

ukiichokoza Zanzibar umeichokoza Tanzania nzima. Ukiichokoza Tanzania nzima watakuuliza sababu wewe kwanini unaivamia Tanzania. Hawasemi unaivamia Zanzibar. Kwa hivo hapo kuna mtu anasema mimi staki muungano. Tukae wenyewe hivi hivi. Wengine wanasema mimi staki mapinduzi kwa sababu wameathirika na mapinduzi. Hataki kusahau yale yaliopita kwamba yale yamepita sasa tuendelee na kujenga nchi yetu. Ni wachache wanaofikiria hivo. Lakini hii kama itatoka kwa vovote vile itakuwa inatuletea usahihi hata kama umeupata kasorobo, sio kamili, kasorobo sio kamili, itakuwa imesaidia pakubwa sana.17 Kwa mtu mwenye akili ataanza kufikiri hapa panazungumwa ukweli ulikuwa huu, huu. Hivo sasa mimi nakwenda wapi? Kwanini tusikae pamoja tukajenga hii nchi?

Mauwaji ya Mashamba

Kwanza walianza Hizbu kuwafukuza wanachama wa Afro­Shirazi Party kwenye mashamba yao. Kama hutaki kuwa Hizbu ondoka. Na wakati ule mashamba mengi yalikuwa yamemilikiwa na matajiri wao. Mimi nafsi yangu nilikuwa Cheju tuliondokea pale kuja mjini. Kulikuwa na bwana mmoja Mwarabu akiitwa Sleman bin Hemedi. Mjomba wake yuko mpaka sasa. Yeye nilimlipiza kisasi kwa mambo mawili. Jambo la kwanza lilokuwa limeniuma ni nilipokuja hapo 1953 niliwakuta wazee wawili wa Kinyasa. Ni watu wazima. Na mmoja ana mshipa. Walikuwa watumwa wa baba yake huyo Mwarabu. Lakini wameshakuwa wazee sana. Wazee wale wakawa wanapewa kazi ya kila siku, hiyo ni daily routine [utaratibu wa kila siku]. Ajaze makalbi mawili yule bwana maji. Kisha apasuwe kuni vigogo va mkarafuu. Akangowe muhogo au akate ndizi, aweke pale. Hizo ni kazi za asubuhi. Afue nazi, aweke pale. Yule mwanamke, kazi yake ya kwanza amenye ndizi na muhogo, akune nazi lakini lile tuwi asilikamue yeye. Tui atakujakamua bibie. Wakati wa kula wao hawaruhusiwi kupewa kula. Watakaa wangojee, wao wakishamaliza halafu yale makombo wapewe. Sasa mzee yule sku moja akawa amepindwa na ule mshipa wa ngiri, usiku. Akawa anapiga kelele babangu akatoka kwenda kumsikiliza akamwambia wewe umepindwa na ngiri. Sasa hawana la kufanya. Ikabidi walale mpaka asubuhi. Asubuhi yule bwana Mwarabu anamwambia kwa nini hukwenda kuchota maji? “Mimi nnaumwa.” “Ebo, unaumwa? Sisi hatuna maji unatwambia wewe unaumwa?” Babangu akamwambia yule Mwarabu “huyu mtu mgonjwa atachotaje maji?” “Wewe inakuhusu nini? Wewe umekuja hapa kufata kazi si kuulizia mambo ya watu.” Hakujibu kitu. Ikabidi yule bibi afanye kazi mbili, yake na yule bwana yule. Zote mbili. Mimi nna miaka kama kumi mpaka kumi na mbili. Hilo kidogo mimi nikahisi unyonge na baba alivokuwa akinungunika na mamangu nikajuwa hili jambo limewauma sana. Halafu jengine, huyu bwana Mwarabu huyu, alichonikera ni kuwa tunatozwa kodi tunalima katika bonde la mpunga lile, lile shamba anasema ni ardhi yake.

Page 143: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 111

Kila mwaka ukilima mpunga utowe pishi tano, kama umepata kama hukupata, lakini umlipe pishi tano za ardhi yake. Sasa mwaka ule hatukuvuna mpunga, hatukupata. Akasema mimi sijui habari hizo. Mimi nataka unletee pishi zangu tano. Ikabidi babangu na mamangu wende wakaombe kwa jirani ambaye amelima pishi tano akakope kule aje amlipe huyu bwana. Kwa hivo siku ile ya mapinduzi baada ya kutulizana mmoja katika mlipa kisasi nlikuwa mie. Nilikwenda hukohuko kwake. Kwa bahati walikuwa hawajakamatwa bado…Kitendo kile nilichofanya wale wenzangu wengine walosikia vile wakasema “ala! Kwanini mmemuacha.” Wao wakenda mchukuwa wakamleta Raha Leo. Imekuwa kama mimi nimechangia sasa kisasi kile. Kwa sababu kama sio mimi kuelezea na kufanya vile pengine angenusurika yule. Nimewatia mori wale. Hivo kisasi kitapanda zaidi. Kwa hivo inawezekana kuwa na wenzangu wamefanya zaidi ya hivo kulingana na jinsi walivyo. Lakini mimi nimeshiriki kwa sababu ya kuona uchungu wa yale nilokuwa nimeyaona. Halafu siku moja yuko mjomba wake Saidi mpaka leo tunakwenda kuwinda usiku paa. Mimi nabeba bunduki, napiga paa, wawili watatu. Tukirudi anakata ile miguu ndo ananipa mimi nikafanye kitoweo. Paa yule, matumbo, kila kitu anachukuwa yeye, mimi nikale ile miguu. Babangu anasema “wewe mwanangu umemuendesha usiku kucha halafu unakwenda kumpa miguu. Kuanzia leo sitaki tena umchukuwe mwana wangu. Na wewe nikikuona unafuatana na yule hapa pangu uhame.” Kuna watu walifanya chaka la watu wa bara. Yule kanifanyia hiki na hiki lakini nikijitokeza mimi ni jirani atakuja kunilaumu. Nitamtizama vipi. Kwa hivo anamtumia mtu wa bara. “Unamuwacha yule vipi bwana?” Yule hivi na hivi na hivi. Sasa mtu wa bara anajitokeza anafanya kitendo kile. Anapata lawama yeye. Yule anakwenda kulekule. “Binaadamu hawa hawasikii.” Kumbe yeye ndo aliyemtuma. Aliyetomeza. Imetokezea mifano mingi sana ya namna hiyo. Wazanzibari walishiriki kwenye Mapinduzi ya Zanzibar. Wamo. Si Pili Khamisi, Hafidh Suleman “Sancho”, Ramadhani Haji? Wapo lakini wengi inawezekana kwamba katika ku advance [kusonga mbele] wakawa nyuma. Hawakuwa mstari wa mbele. Baada ya kufanikisha ndie anakuwa mstari wa mbele. Sasa kapata nguvu. Imekua hivi eh! “Sasa tufanye hivi, tufanye hivi, njoo hapa.” Sasa wewe ndo umekuwa leader [kiongozi]. Lakini wakati ule wa kukitafuta kitendo chenyewe anakuwa nyuma nyuma. Ni wachache walokuwa wamesonga mbele. Kabla ya mapinduzi ilipotea bunduki Ziwani. Bunduki hii ilikuwa ikichukuwa mafunzo sehemu zote nyingi. Kwa Hani imekaa hapo watu wanachukuwa ma­funzo. Lakini walikuwa wanachukuliwa watu maalumu. Ilipogunduliwa kwamba iko Kwa Hani ikahama. Ikenda mpaka Kiwengwa huko. Bunduki hiyohiyo moja. Watu wanachukulia mafunzo. Huku inatafutwa huku watu wanajifundisha. Mpaka ilipofikia tarehe watu wakagawiwa. Sasa Wamakonde hawa. Wamakonde

Page 144: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane112

tabia yao mara zote watakuwa ni wapole lakini ukimchokoza akishasema “see!” basi hapo hakuna utakachomfanya. Anakuwa mbogombogo. Chinja! Chinja! Hiyo tabia wanayo. Lakini kwa kawaida utawaona kimya. Ushahidi huo ntakupa kuwa hata ukiangalia ukombozi wa Msumbiji wenye asili ya Wamakonde ndio walioikombowa hiyo nchi. Kutoka Cape Delgado kuelekea huko, hawa wana jadi ya vita. Mbali ukimuongezea mafunzo. Na Wamakonde hapa walikuwa hawachanganyiki. Shamba wanokaa, maalum kwa sehemu ya kwetu hii, Kitope. Walikuwa Kitope pale watupu! Sasa wenyeji wa pale Kitope wazaliwa wa hapo wakisema “hapo wako Wamakonde ukenda unaliwa! Wamakonde wanakula watu!” Sasa ile khofu imewapa wale jamaa msisimko. Tunaogopwa, bora tuzidishe! Ndo wakazidi kuwa wakali. Kitu hicho tuliwapa sie. Kwa kilimo huwagusi! Kumbe sivo. Wapole sana. Na wasafi sana. Ukenda kondeni utamkuta yuko kazini lakini ukirudi nyumbani tafauti. Nyumba ya nyasi lakini safii! Ukiambiwa sufuria hii inapikiwa utakataa. Inasuguliwa safi. Sahani inaanikwa kwenye jua ikauke! Hata alokuwa mkubwa wa Hizbu, Ali Muhsin, wazee wake kwa upande wa bibi zake wana asili ya Kimakonde kutoka Lindi.

Waafrika wa Zanzibar na wa Msumbiji

Kihistoria sisi binaadamu wananchi ni wamoja. Pemba Kaskazini sana wametokea Tanga. Wadigo na sehemu za Lamu, huku Mombasa huku. Ukija kusini yake wengi wametokea Msumbiji. Ukenda kisiwa Panza pale ukiwakuta wazee wenye umri mkubwa ukimuuliza asili ya kabila yake atakwambia Mmakonde, Mmakua. Waliletwa na Mreno. Unguja hii Matemwe ni watu wenye asili ya Pemba Bay. Kuna kisiwa pale kinaitwa “Matemo” ndiko walikotokea. Ukifika Pemba Bay mjini pale ukiuliza “Matemo” utaambiwa kisiwa kile pale wanatoka hapa na ni Wamakua. Kivazi, tabia zao zote, vyakula wanavyotumia Matemwe ndivo wanavotumia wale kule. Uwele, mtama, mhogo mkavu ule. Chaani. Asili yake ni Wamakonde wa Mtwara. “Chaani mwepo.” Wawili wale walikuwa wanagombana. Sasa yule watatu akauliza “Chaani mwepo. Simgombana?” Nini nyinyi mnachogombana? Ndo neno “Chaani.” “Chaani mwepo champatana.” Akiwauliza wale hawataki kujibizana wanagombana tu “e, nipamuwanda.” Ndo ikawepo Donge Muwanda sijui na Chaani. “Muwanda” maana yake “mimi nenda zangu” hamnisikii, hamnijibu, mimi naondoka. Asili yao Wamakonde. Na ukienda pale Chaani masingini uliza maana ya “Chaani” kwa wazee watakwambia. Asili yao ni Wamakonde. Sasa wote sisi ni ndugu. Leo tuwe katika mfumo huo wa mapinduzi yalotokea, tunatafuta historia ya mapinduzi, tujenge tujijuwe kwamba wote tuwa moja. Halafu mwengine awe anabeza aone kuwa historia hii si nzuri. Ni historia nzuri. Kwa sababu kwa vizazi vijavo tutakuwa na historia ya changamoto kubwa

Page 145: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 113

ya kuwafundisha vizazi vyetu “Ah! Kumbe mapinduzi yalitokea hivi na hivi na hivi.” Unajitowa muhanga, unawacha shughuli zako muhimu. Sasa hiyo si kazi rahisi. Historia itakuwa ya vizazi vijavo wa pande zote, ziwe za Kiarabu, ziwe za Kiswahili, wote wanaingia. Utakapotoa historia hii itakuwa “Ah! Kumbe makosa yalikuwa upande huu. Kumbe makosa yalikuwa yetu sisi.” Na sasa hivi kinachotakiwa tufanyeje sote tujenge nchi [ya Zanzibar] kwa pamoja. Lakini hatuwezi kujenga nchi kama tunakotoka hatukujuwi. Tukirudi kwenye mapinduzi yenyewe sisi hatukupangwa na wala hatukuingia mabomani. Aloingia bomani aliingia kwa mpango wake. Na wengi sisi vijana hatukuingia mule. Ilikuwa siri ya wenyewe watu wa mapinduzi. Kwa kwenda kuiba na kuvunja maduka huko tulishiriki. Hiyo ukweli wa mambo. Wengine tulikuwa tunakutana “Vipi? Nimeshachukuwa vitambaa. Nimeshachukuwa baiskeli.” Wengi wetu tulitokea mashamba. Mimi branch yangu ilikuwa Chuini. Mwengine Mwakaje. Mjini walikuweko wachache tu. Mapinduzi Jumapili. Alkhamisi watu wakaitwa kujiandikishi jeshi. Sisi tulipelekwa makambini. Mimi nilipelekwa Mtoni. Wengine walipelekwa makamisaa. Kilimo sijui. Vitu kama hivo. Basi, nikabaki mie jeshini. Nilipostaafu nikarudi kwenye mambo ya FRELIMO ya ukombozi wa Msumbiji. Mmoja alikuwa Mchunga Mitama, yeye aliondoka akenda nyumbani kwenye ukombozi. Huyo mmoja tu. Suala la nguvu za ukombozi wa Msumbiji kutoka kwa Mreno hilo ni suala la jeshi la Tanzania lote kwa jumla limeshiriki. Pamoja na huyu Ali Mahfoudhi alikuwa akiongoza mkanda mzima wa kusini. Vikosi vote vile vilokuwa kusini yeye ndo akivishughulikia.

Ali Mahfudhi na Msumbiji

Kwa kweli aliisaidia Msumbiji kwa kiasi kikubwa sana. Kutoa ushauri kuhusu ulinzi wa kijeshi. Wakati wa ukombozi wa Msumbiji yeye ndo alokuwa mtu wa kwanza kusaidia suala la ukombozi. Na alikuwa ni mpelelezi mkali sana wakupeleleza kambi za Msumbiji, hasa zilioko mipakani mwa Tanzania na Msumbiji. Moja wapo ikiwa kambi ya Nangade. Albarto Sipande na Raymundu Pasinuwapa, hao ni majemedari wa Msumbiji. Hawa ndo majemedari wakuu wa Mkoa huu wa Cape Delgado. Wote wahai. Na ndo walokuwa wanakwenda sambamba kabisa na Ali Mahfudh. Hiyo, yeye alikuwa amekwenda kule kwa mda wa siku tatu nzima akiifanyia upelelezi na alipokamilisha upelelezi wake ndipo sasa akatowa ushauri wake wa kuvamiwa kambi ile na kuipiga kambi ile ya Wareno ilioko Nangade. Ikawaka moto muda wa siku saba! Wakati huo yeye akifanya tena upelelezi wa kambi nyengine, Shaishai. Iko mbele zaidi. Nayo pia ikashambuliwa. Kwa hivo Wareno wakaona huku ni kwahala hakukaliki tena. Mipakani. Ikawa Wareno sasa wanatumia kuleta ndege za kivita, kupiga mabomu, wanaondoka. Wakawa

Page 146: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane114

ndugu zetu wengi wa Mtwara wakaathirika kwa makombora ya ndege za Kireno, mabomu ya kutegwa, walikuwa wanakuja wanatega huku kusudi kuona watu wa Mtwara wanawakaribisha watu wa Msumbiji kuja kujihifadhi huku. Lakini Ali Mahfudhi alijitahid sana kufanya kazi hiyo na walikuwa sambamba kabisa na Rais Samora Machel. Hasa juzijuzi tu katika kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Samora, pia na yeye Ali Mahfudh ametajwa katika mdahalo wake kwamba ni mmoja alisaidia sana ukombozi wa Msumbiji. Mpaka Msumbiji kupatikana kwa uhuru yeye bado alikuwa anaendelea kusaidia. Ali Mahfudhi akifahamu Kireno. Wareno na Kispaniola wanaelewana. Na habari nyingi tulikuwa tunazipata, zilikuwa zinapatikana Msumbiji kwa yeye baada ya kuwakamata na kuwatesa na kuwahoji, ndo zikawa zinapatikana habari kwa wingi. Alikuwa hodari wa kufanya interrogation [mahojiano ya nguvu yenye lengo la kupata habari]. Sana, sana! Mwisho alichukuwa uraia wa Msumbiji. Ndo maana maiti yake imezikwa kule. Alipokufa ililetewa taarifa kwa family na serikali hapa [Zanzibar] ikaomba mwili wake uje uzikwe hapa. Lakini serikali ya Msumbiji ikasema, hapana. Tutamzika sisi kwa sababu huyu alikuwa tayari ni raia wetu. Lakini tunaruhusu family yote ije kwa mazishi. Na kwa bahati yuko kakaake kule. Ni Dokta na ndo alokuwa akishughulika kumtibu wakati wote alipokuwa anaumwa. Kaka yake anafanya kazi hospitali ya Beira, Msumbiji. Kwa hivo family hapa ikaondoka ikenda kule. Kazikwa kwa heshma zote kwa kweli. Amepewa heshima zote za kitaifa. Sijui, mambo ya tamaa tamaa haya. Alikuwa mtu amependeza sana katika jeshi la Tanzania. Majeshi wakimpenda sana. Lakini kumbe mambo yao, alikuwa against [dhidi] na matakwa. Akaingia kesi ya uhaini. Lakini sasa kuna ushahidi ambao ulionekana katika kifo cha Karume. Yeye ndo aliefanya movement [harakati] ya kwanza, ya kuzunguka jumba lile kama kufanya inspection [uchunguzi]. Wakati Mzee Karume anaingia pale kwenye jumba yeye kapita kaangalia alivokaa, karudi, kapita tena. Ndipo kikaja kile kikundi kuja kumuuwa. Halafu la pili, wakati Karume keshapigwa risasi, yeye akawa wa kwanza kutokea katika tukio. Na baada ya kutokea, kufika pale kwenye tukio, badala ya kumhami Mzee Karume kumpeleka hospitali, alimkimbilia muuwaji wa Karume kwamba akimbizwe hospitali. Yaani kamuona yule Karume sio muhimu kuliko huyu Humudi ambaye amemuuwa Karume. Inasadikika kwamba Ali Mahfudhi anahusika. Kwanza, yeye alikuwa Chief of Staff, Makao Makuu ya Jeshi, Dar es Salaam. Baadae akapata uhamisho wa kuja Zanzibar kuwa Operations Commander, Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita, Chief of Operations wanaita wenyewe au kitu kama hicho. Wakati huo kukawa na fununufununu ya upotevu wa silaha katika kambi za jeshi hasa kambi ya Idi Bavuai pale Migombani. Pakawa na upotevupotevu wa silaha. Palikuwa na vikosi vingi. Ahmada alikuweko pale. Humudi alikuweko pale. Ahmada alikuwa akishughulikia mambo ya michezo (sports) katika jeshi. Alikuwa na kikosi chake

Page 147: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 115

pale lakini wakati huohuo akawa anashughulikia michezo. Kwa hivo mara nyingi alikuwa kwenye sports lakini kwenye kikosi chake kukawa na huyu Humudi, ambacho kikosi hicho kilikuwa kikenda mara kwa mara Mtwara kufanya ulinzi wa mipaka kati ya Msumbiji na Tanzania. [Kikosi] hicho cha Humudi mara nyingi kilikuwa kinakwenda huko. Na yeye Humudi alikuwa akienda. Lakini mwezi wa Aprili 1972 kikosi kikapewa likizo askari wake wote.18 Akabakishwa askari mmoja tu wa kutunza silaha pale, ghala ya silaha. Ni huyo Saidi Sindano. Wengine wote likizo. Ila yeye Saidi Sindano akaendelea kubaki pale kutunza ghala ya silaha mpaka watakaporudi wenzake ndipo yeye atatoka ataenda likizo. Lakini ile ilikuwa pia ni ujanja wa kumfanya, kwa sababu yeye alikuwa ni mtu wao [Makomred], kuwa yeye atakapobaki pale kikosi kimekwenda likizo hakuna atakayeshughulika pale, yeye itakuwa ni urahisi kutowa silaha kuzipeleka nje. Alipangiwa hivo. Na akafanya kazi hiyo. Ikawa kila siku anapotoka kidogo kwenda nje anaondoka na silaha moja. Anaifunguwa, anaitia kwenye mfuko, anatoka nayo. Na kulikuwa hakuna mtu wa kumsachi [kumpekuwa], wa kumuuliza anatoka na nini. Lakini zikapatikana fununu hizo kwanza kuna upotevu huo wa silaha. Ikaenda fununu hiyo mpaka ikabainika kwamba kuna kitendo cha uhaini kinataka kufanyika kwa kupinduwa serikali. Kukawa kuna habari hizo, kuna mpango unafanywa nje ya kambi za jeshi kwa kutaka kupinduwa serikali. Kwa sababu ripoti ilikuwa inapatikana huko nje. Na mikutano ilokuwa ikifanywa huko nje ilikuwa ikiwataja kina Ali Mahfoudh, Babu, wako katika mpango huu wa kutaka kupinduwa serikali. Sasa wakawa wanafatiliwa katika nyendo zao, taratibu na vikosi va usalama, kutaka kujuwa. Hata mwisho ndo inafika tarehe hiyo, 7 Aprili 1972, wakajikuta wale kumbe siri zetu zimeshajulikana. Sasa tufanye mpango gani? Mpango hakuna, japokuwa tumejulikana, na sisi tulipe kisasi japo kidogo. Ndipo njama za kumuuwa Karume zikabainika. Na siku ile Karume anauliwa, tayari habari zishamfika yeye mwenyewe. Kwamba leo wewe usiondoke, usitoke nyumbani kwako. Aliambiwa hivyo na Kanali Sefu Bakari na Yusuf Himidi, na huyo kijana ambaye alizipokea hizo habari. Kijana mmoja wa Kiarabu. Jina lake simjui lakini najuwa alikuwa kijana wa Kiarabu alopeleka habari hizo kwa Sefu Bakari. Bwana, kuna hiki, na hiki, na hiki, kitafanyika. Mimi kwa uchungu naona zitateketea roho za watu bure. Hakuna maana. Na kijana huyo alikuwa anaripotiwa tokea nyuma kwamba anazipokea hizo habari, nafikiri alikuwa akiwasiliana na watu wa Usalama wa Taifa. Akizipeleka huko. Wanasema alikuwa akiuza kahawa sehemu za Raha Leo pale. Alikuwa muuzauza kahawa hivi. Sasa siku ile anaripotiwa Karume habari hizi kachukuliwa na yule kijana wa Kiarabu. Msikilize mwenyewe huyu kijana anachokizingumza. Nyumbani kwake pale Maisara. Siku ile ndo atakuja kuuliwa. Akaambiwa, Mheshimiwa masuala kama umeyasikia ni kweli leo usitoke. Wana njama za kutaka kukuuwa. Habari

Page 148: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane116

ziko hivi na hivi na hivi, wakahadithia picha yote, lakini mwisho wameshindwa, njama yao ni kukuuwa wewe. Usitoke. Jibu alolijibu pale Karume ni kwamba nimekusikia, fiamanillah! Nendeni. Wakaondoka.19 Sasa kitendo cha kutoka yeye ni ule ukaidi wake, au ndo wito umeshamfika wa kifo, akaondoka. Akaanza kutembea, na yeye alikuwa na tabia lazima akitoka jioni atembee mpaka sehemu za Kianga hapo kwa rafki yake mmoja wazungumze. Akirudi lazima afike Sebleni majumba ya wazee awasalimie wazee pale, japo kwa kuzunguka na gari, halafu ndo anaongoza anakwenda zake Makao Makuu [ya ASP] Kisiwandui, anacheza pale dhumna. Ulikuwa mchezo wake akiupenda sana. Basi akafanya hivo. Ali Mahfoudh alikuwa kwa Khamis Machungwa. Ali­poona msururu wa magari unaingia, ndipo yeye mtu wa kwanza kupita kwenda kuangalia. Lakini wale walinzi pale hawakuwa na khofu naye kwa sababu wanamjuwa huyu ni mkubwa katika jeshi, anapita njia zake. Punde kidogo aka­pita na huyu Humudi na yeye akapita. Wakati huo alikuwa na cheo cha Kepteni. Na wale walinzi wa usalama hawakumtilia mashaka kwa sababu ni kiongozi wa jeshi. Kapita akarudi. Halafu Ali Mahfoudh alipita, akarudi. Ikaja gari pale ikapiga risasi za harassing [za kuudhi mazingira], wale walinzi walipolala chini ndipo Humudi akatoka akamshoot [akampiga risasi] Karume na yeye alikuwa amepiga goti, akapigwa risasi pale pale na wale walinzi na amekufa akiwa na bunduki yake. Ahmada ndio waliotoroka. Kuna ripoti za Humudi tangu yuko Urusi kuwa atalipa kisasi cha babake na ripoti hizo zilikuwa zikiripotiwa wakati yuko na wanafunzi wenzake hukohuko. Inasemekana kabla hajashoot [hajapiga risasi], sauti ilitoka kwa Karume “Humudi unafanya nini?” Sauti ilisikika “Humudi unafanya nini?” Ilisikika hiyo. Kwa sababu pale waliokuweko kina Thabiti Kombo hao walikuweko, na mmoja katika waliojeruhiwa. Kabla hajapiga risasi, keshashuka ndani ya gari, kapinda goti, ndipo Karume akasema “Humudi unafanya nini?” Unafanya nini, risasi zikatoka. Zikampiga yeye na kuwajeruhi wengine. Isipokuwa Mtoro Rehani Kingo tu, alikuwa hayuko, yuko chooni. Kwa hiyo aliposikia mlio wa risasi na yeye akabana huku huko! (anacheka). Akangojea mpaka mambo yametulia, akaja kugongewa ndo akatoka. Siku ile jioni nilikuwa uwanja wa Mao Tse Tung tukifundisha hawa Valantia mambo ya gwaridegwaride. Tunaanza kufundisha tu, ndo ikatoka amri, akaja Sefu Bakari, akasema leo zoezi vunjeni askari wote warudi makambini. Hatujaambiwa sababu. Kwa vile mimi nilikuwa nimetoka nyumbani kwangu, siko kwenye zamu kambini, ilikuwa niende nikafundishe nirudi nyumbani kwangu Sebleni. Lakini si dakika kumi, kumi na tano, ndo nikasikia mayoo yanapigwa sasa, “vita, vita!” Magari, watu wananinginia kwenye magari wanakimbilia mashamba. Mwenye kwao anarudi kwao. “Kuna nini?” “Kuna vita mjini.” Wengine wana­sema kumesikika risasi Kisiwandui. Nikaona hali hii mimi kama ni askari nikimbilie kambini. Kwa hivo nikapita kwa njia za ndani kwa ndani mpaka nikatokezea kiwanda cha viatu cha Mwendo, Maruhubi. Pale nikakutana na Yusuf Himidi anafanya mazoezi kwa sababu wakati ule karibu amerudi Ujerumani

Page 149: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 117

kufanyiwa operation fulani na akaambiwa moja wapo afanye mazoezi. Anatroti kwa miguu. Nkamsimamisha nafsi yangu, nikamwambia “Mheshimiwa, kuna suala limetokea huko mjini.” Akasimama “Suala gani?” “Kuna mayowe mingi kuna vita Kisiwandui.” Kwa hivo pale pale aligeuza na nnafikiri kina Ahmada hawakumtambuwa Yusuf Himidi pale. Kuna gari ilitupita pale na wangelimjuwa kama ni yeye wangelimshoot. Lakini hawakumjuwa kutokana na zile nguo alizovaa za kisports, za kiraia tu. Yusuf Himidi akasimamisha gari akarudi kwake Sharifu Msa. Palepale akarudi moja kwa moja kuelekea makao makuu [ya jeshi]. Tayari Ali Mahfudhi keshafika makao makuu. Yeye keshaanza kutangaza katika vyombo va habari va kijeshi, hali ya hatari kwa sababu yeye ndo Kamanda wa Mafunzo na Utendaji wa Kivita. Keshatangaza vikosi vote hali ya hatari, standby, na wakati huo kutaka serikali nzima ya Zanzibar iwepo makao makuu ya jeshi. Na wakati huohuo katika opereshen yake yeye akatangaza kwamba popote mtakapomkuta Ahmada na Saidi Sindano, wapigwe risasi. Wauliwe moja kwa moja! Sio wakamatwe. Hapana. Popote atakapopatikana Ahmada na Saidi Sindano wauliwe na tayari akaandaa kikosi cha kumsaka Ahmada na Saidi Sindano. Kina Chwaya hatujawajuwa hawa. Hao wawili. Timu haijajulikana hapo. Kwa hivo kikosi kilipoondoka kumsaka Saidi Sindano na yeye Ali Mahfudhi akawa yumo ndani ya gari. Wakaelekea, sijui, Unguja Ukuu, akawa hayupo, lakini ndani anazungumza kwenye army radio [redio ya jeshi] huku anakwenda, “popote pale mtakapomkuta Ahmada auliwe.”20

Huku viongozi wote wa serikali, viongozi wote wa kijeshi wako makao makuu ya jeshi, Migombani except [isipokuwa] yeye tu kajitia yuko nje katika harakati! Ndo walipoulizana ndani. Mimi nimetolewa kwenye kikosi changu Mtoni kwenda makao makuu kuwalinda viongozi wote wa serikali walioko pale. Ndo tukawa tuko mlangoni. Anayeingia hana ruksa kuingia na silaha. Haidhuru ni viongozi. Kwa sababu pale haijulikani nani ni nani! Suala hilo tunaambiwa na Sefu Bakari kwamba viongozi wote watakaoingia silaha zote waziweke nje kwa sababu hatujuwani katika sisi ni nani mkweli nani nini. Ni suala kubwa. Yasije yakatokea mengine ndani. Mimi nayasikia hayo. “Itakuwaje huyu Operations Kamanda ndiyo, lakini vikosi vyote vina makamanda. Yeye hawaamini hao kwamba wanaweza kumpata.” Anazungumza Khamisi Hemedi kwa sababu ndo alokuwa mkubwa wa usalama wa jeshi. Sasa nafikiri yeye anachambuwa katika mambo yake ya kisecurity [kiusalama]. Itakuwaje huyu mtu mzima, kamanda mkubwa asiwaamini makamanda wake wadogo aende yeye? Na wakati katika ripoti zake za mikutano ya nje huyu yumo! Leo inatokea anajitowa yeye hapa anakwenda nje kwenye operation na ananganganiza lazma hawa watu wauliwe. Kwa nini? Kuna maana gani? Aitwe! Akaitwa. Huko nje aliko huko. Akaambiwa, wewe bwana, hupaswi sasa hivi kuwa nje kufata kikosi kumfata askari mmoja au wawili. Kama itatokea vurumai kubwa zaidi, nani ataongoza operation ya vikosi vote? Wewe unapaswa ubaki hapa makao makuu ili likitokea kubwa wewe uweze kuongoza vikosi vote! Anaelezwa

Page 150: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Nane118

na Khamisi Hemedi, Yusuf Himidi na Sefu Bakari. Ndipo akabaki yeye pale, Migombani. Sasa hapo ndo ikabidi wakamatwe watu walokuwa wakituhumiwa katika ripoti za usalama za nyuma. Huku watu wanaendelea kusakwa. Ikenda hali hiyo mpaka Ahmada akakamatwa, akajeruhiwa sehemu za Mangapwani. Hajafa bado. Lakini baada ya kuripoti wale vikosi kwamba tumeshawapata hawa watu, tumepambana nao, tumeshawajeruhi, yeye, nafkiri kama skosei na huyu Chwaya. Tunawaleta. “Mnawapeleka wapi?” Anajibu kwenye radio. “Nimesema kwamba Ahmada mkimuona popote auliwe! Kwanini mnamleta. Mpige risasi. Askari akapokea amri, akapigwa risasi.” Wameuliwa Mtoni. Huko wametoka wakiwa hai. Basi, maiti zao zikapelekwa hospitali. Lakini ripoti huku za usalama zinaripoti Ali Mahfudhi anahusika, lakini nani atayemkamata pale ufike kumtia ndani? Kwa sababu the most senior [mwenye cheo kikubwa] alikuwa ni yeye katika rank zote [vyeo vyote] zilioko pale. Wote pale. Yeye alikuwa full Kanali. Sefu Bakari ni Luteni Kanali. Ni mdogo mbele yake. Anaweza akamwambia tu “mguu sawa! Geuka!” na yeye akafata amri. Sasa ifanyike triki gani? Ndipo ripoti zile zikaripotiwa Dar es Salaam, kwamba kati ya watuhumiwa yumo na fulani lakini tunashindwa kumkamata. Ndipo ikatoka ndege na message [ujumbe] ikatumwa. Sefu Bakari, Natepe, na Ali Mahfudhi, mnatakiwa muje katika Kikao Maalum cha Ulinzi (KMU). Na ndege inakuja kumchukuweni. Kwa hivo wakaondoka hapa kama wao wanafuata kwenda kwenye Kikao Maalumu cha Ulinzi. Watatu hao. Natepe alikuwa vilevile Luteni Kanali, kama Sefu Bakari. Wakaingia ndani ya ndege mpaka Dar es Salaam. Kufika Dar es Salaam, pale tena, kuna wakubwa mbalimbali, wenye vyeo vikubwa, wamefika pale, ndipo alipokuja mkuu wa majeshi, akasema, “kikao cha leo sio kikubwa sana. Wewe na wewe na wewe, mko chini ya ulinzi kuanzia sasa hivi.” Vua viatu, vua mkanda, vua rank! Na ma MP [Military Police] wameshazunguka. Ikabidi Ali Mahfudhi akatoa kitabu chake cha check (check book) aka sign cheki zake kwa familia yake. Jambo ambalo ni la ujasiri. Na akaona sasa nimeshanaswa. Nimeshaingia kwenye mtego. Anatengeneza mipango sasa. Kaandika cheki zake za miezi sita kwa ajili ya familia yake nyumbani. Hizi nipelekeeni nyumbani. Twendeni. Katulia, hata wasiwasi hana. Wakachukuliwa wote watatu wakapelekwa mpaka Ukonga. Kufika Ukonga, wakaingizwa ndani, wakagawiwa vyumba, wale wengine wakatolewa mlango wa pili wakatoka. Alokusudiwa ndo keshapatikana. Wale wakapanda ndege jioni wakarudi Zanzibar. Lakini bado katika kesi ilipokuwa ikiendeshwa, Ali Mahfudhi alikuwa anatakiwa, Babu alikuwa anatakiwa. Waje Zanzibar lakini Mwalimu Nyerere akawa mgumu kuwatowa kwa sababu alijuwa kwamba wakifika huku hakuna chengine kitakachotokea isipokuwa ni kuuliwa. Na nafikiri labda Mwalimu Nyerere alikuwa hapendi sana masuala haya ya kuuwauwa. Ikawa wanazuwiliwa mpaka ikabidi mahakama iwahukumu wale kifo lakini wakiwa nje ya Zanzibar.

Page 151: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar 119

Sasa iwe mfano kama wameshaondoka nchini, Tanzania kwa jumla, akienda Umarekani pengine, kama iko tuhuma hio, au akenda nchi nyengine, anaweza kufanya vurugu kubwa zaidi dhidi ya Zanzibar. Kwa hivo ikafanyika triki tena ya Samora Moses Machel wa Msumbiji amfanye Ali Mahfudh awe mshauri wa kijeshi lakini tayari wakati huo atakuwa katika detention [kifungo]. Anaangaliwa. Anachunguzwa. Na yeye alikuwa anajuwa. Anajuwa kuwa mimi nimeletwa nchi hii nikiwa chini ya ulinzi. Lakini yeye haijamshughulisha. Hicho kitu naweza kusifu alijitahidi. Na amekaa kule mpaka vilipotokea vita va Uganda. Ali Mahfudh aliomba akiwa Msumbiji, kwamba mimi nataka kwenda Uganda nikapigane kwa sababu nchi yangu imeingia mapiganoni. Kwa hivo mimi popote nlipo lazima niende. Akakataliwa. Msumbiji ilitowa ushauri, Mwalimu Nyerere akasema “hapana. Huyu asije hapa. Abakie hukohuko.” Wao walikuwa tayari wamtowe lakini Tanzania ikakataa kwa sababu vikosi vinavopigana ni pamoja na va Zanzibar. Pengine watakuwa bado wana uchungu wa kuuliwa kwa Karume, wanaweza wakamlipa kisasi huyu vitani. Akabakia Ali Mahfudh Msumbiji mpaka kifo chake. Lakini kule aliunda shirika la ujasusi la upelelezi wa nchi za Kiafrika. Kama nchi fulani inataka kuvamiwa, kijeshi au kisiasa, yeye akipokea anazipelekea nchi hizo. Bwana, nchi yako inataka kufanyiwa kadhaa, kadhaa, kadhaa. Alikuwa analipwa na ile nchi pengine. Makaburu Afrika Kusini, wakagunduwa habari zetu za Msumbiji zina vuja kutokana na huyu Ali Mahfudhi. Wakamtumia majasusi kutaka kumshambulia kwenye nyumba yake alokuwa akilala. Lakini kwa sababu na yeye watu wake alikuwa nao, walikuwa very sharp [wako macho]. Wakazipata zile habari. Leo nyumbani kwako utakuja kushambuliwa. Kwa hivo siku ile Ali Mahfudhi hakulala nyumbani kwake. Kenda kulala hoteli. Wale wakaishambulia nyumba yake kwa mabomu. Yeye kumbe hayumo. Na wakatangaza Afrika ya Kusini, yule jasusi mkubwa anayepeleleza basi ameshauliwa—Ali Mahfudhi. Wanatangaza radio ya Afrika ya Kusini. Tushampata tayari. Asubuhi Ali Mahfudhi amekutikana mitaani Maputo anatembea. Na yeye akasema, bado. Ali Mahfudhi huyo sie! Mie bado nipo. Basi akaendelea kubaki kule na mwisho akaamua kuchukuwa uraia wa Msumbiji. Na yeye wakati wote yuko full uniform. Hata siku moja humkuti amevaa kiraia Ali Mahfudhi. Yeye yuko katika combat. Kama amepumzika avue viatu. Na mkewe ilikuwa hivohivo. Alikuwa amechukuwa mafunzo. Hata haya mambo ya Judo, Karate, yule mama usimchezee. Kabisa, kabisa. Ali Mahfudhi akijuwa mambo haya ya Judo. Amejiandaa vizuri sana. Cuba ndo alikosoma sana. Siku moja nakumbuka katika mambo ya kawaida, mkewe alikuja sokoni pale, akawa amechukuwa pesa mkononi, sasa kuna jamaa fulani anamfahamu akamwambia. “Wewe mama utanyanganywa pesa zako.” Akasema “kwa vijana hawa walioko hapa wote hakuna hata mmoja. Waje kumi hawazichukuwi hizi pesa. Na kama husadiki atokee mmoja ajaribu. Nitaondoka nazo hivihivi.” Ni kweli.

Page 152: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa TisaJohn Okello—Kuibuka na Kuzama

Mzee Selemani

John Okello, hapa nakumbuka walitoka watu, wametoka watu hapa wakenda Pemba. Kwa hali ya kiuchunguzi. Je, Pemba tunaweza kuwapata wenzetu tukaja kusaidiana hapa? Wakatupa motisha? Kule nakumbuka mtu wa mwanzo aliekwenda kule alikuwa Ibrahim Makungu. Alikwenda na Jaha Ubwa, Mdungi Usi. Watu watatu hao. Sasa walipokwenda kule, sasa wale Ma Afro­Shirazi magogo wa kule Pemba, wakawauliza, jamani e, vipi tunaweza kumpata kijana mshupavu huku wa kutusaidia hii kazi yetu sisi, au vijana washupavu hivi tunaweza kuwapata? Sasa alikuwepo mzee mmoja Mkoani. Huyu akasema jamani mnajuwa nyinyi? Hapa yuko Mganda mmoja anachonga mawe huko. Huyu kijana naona kachangamka sana. Kachangamka sana! Sasa hatujuwi utaratibu wake hatuujuwi vipi. Sasa hapo mtu kama huyo sio anaingiwa tu ovyo ovyo. Panataka mbinu. Wakarudi wale kwanza. Kufika huku Mfaranyaki na Washoto wakasema “twende tukachonge mawe.” Wakenda Pemba. Kufika Pemba, wakaanza shughuli ya kuchonga mawe, sasa yule akiwa kama ni fundi wao. Wamechonga mawe pale, wamechonga, wamechonga, ile data wakamuelezea yule. Hii kazi gani hii? Utumwa gani huu? Pangelikuwa na wanaume wa kuipinduwa hii nchi…1

Lengo walilolikusudia ni kumvisha blangeti Okello kwa sababu yeye ni mgeni. Si mwenyeji. Sasa sisi tukitaka kutafuta sababu ya kujifunika tumvishe huyu. Huyu si Mtanganyika huyu. Ni Mganda! Mbali huko. Kwasababu leo Mtanganyika hapa akilizuwa balaa hili lazima atajulikana “Oh! Mwalimu umefanya chokochoko.” Lakini huyu, huyu anatoka Uganda huyu. Sasa watu watakuja kumuuliza Obote “vipi mambo haya?” Wewe Obote vipi mtu wako anakuja kufanya machafuko nchini kwetu. Sultani sasa atakuwa atapambana na Obote. Sio na Tanganyika.2

Bwana yule [Okello] kumueleza vile akasema “nyinyi wapumbavu, sisi tunazo dawa tunaweza kwenda kuzichukuwa hapo kwa Mau Mau, tukafanya mambo hapa yakajulikana yakawa kweli.” “Ah ewe bwana huwezi bwana. Mambo gani hayo? Unatufanyia kitu masihara tu bwana.” Akasema “bwana e hayo mambo

Page 153: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 121

yapo, tunaweza kuyafanya.” “Kweli?” “Kweli.” “Hebu fanya.” Akatoka Okello, akenda Nairobi. Kufika Nairobi akakutana na Mau Mau, wakampa dawa. Bwana eh, mnaweza kulifanya hili nyie lakini dawa hizi shote wote watakaoshiriki kwenye mapinduzi dawa hii sote mmoja mmoja uwapake. Unavowapaka dawa hizi, ina maana nyinyi mnawapumbaza wale watu wasijuwe. Japo kama watajuwa watadharau. Watadharau dharau. Okello akarudi Pemba. Kurudi Pemba kamkuta Washoto kaja Unguja. Kule kamkuta Mfaranyaki, vipi? Nimeleta. Umeleta nini? Hizi hapa. Dawa. Akamwambia sasa bwana wewe inabidi sasa tuondoke mimi na wewe twende Unguja. Wakaondoka, wakaja zao hapa. Okello akakaa na mzee mmmoja sehemu za Bambi huku, pamoja na dawa zake. Kutwa nzima humkuti na mazungumzo na watu. Imekwenda kwenda ikabidi, akina Sefu Bakari, akina Natepe, akina Ingine, ndio wakaanza kusema, unajuwa nyie, sisi tumeshapata mtu wa kumfunika blangeti bwanaa! Vipi? Huyu hapa. Tumpeni cheo huyu. Tukimpa cheo huyu kwani iwe nini? Mambo yetu yakikaa sawa si basi! Si tunamwambia “chukua chako hichi, kwaheri.” Okello sogea, vipi bwana wewe, masuala ya huyu Washoto na huyu Mfaranyaki. Mmekubaliana vipi nyie? Nimewaambia hakuna uzito. Lakini mimi nimewaambia, ngojeni mimi nikachukuwe dawa. Mimi nimechukuwa dawa. Zipo. Dawa hizi masharti yake? Akasema hizi dawa bwana, hizi dawa zinako­ rogwa kwenye maji, wale watu siku ile khasa ya mapambano, wanamwagiwa mwagiwa hawa, wanajipakaa pakaa, tayari, halafu kuna dawa moja watu wanakunywa, wakishakunywa hiyo, suala limekwisha. Watu wanaondoka wanakwenda kwenye mapambano. Washakingika. Lakini shoti mfanye ngoma. Ngoma tunaweza kufanya fete, kubabaisha. Watakapokuja watu mjini kutoka mashamba watakuwa hawajulikani. Watakuwa wanaonekana wanakwenda kwenye sherehe, starehe na furaha. Baada ya kupitishwa watu kuja kunako fete, hapo sasa ndo Kisasi na Okello, Mfaranyaki, huyu Kassim Hanga pamoja na Hasnu Makame waliambiwa “kaeni pembeni kabisa! Pembeni kabisa nyinyi. Msiingie huku, tuwachieni sisi kwa sababu nyinyi ndo chimbuko.” Suala hili aliyekuwa akilishughulikia Kaujore. Kumalizika “jamani tume­shamaliza.” Sasa katika hao mmoja ile dawa akawa hakuipata, kama utaskia habari za chinichini, yuko mmoja alitoka Bomani akakimbia moja kwa moja mpaka Ndagaa akenda akasema “jamani huko mjini serikali imekwisha pinduliwa.” Ile dawa kwa sababu hakuipata. Lakini aliepata dawa bwana, hakupepesa hapa na pale. Hakupepesa hapa na pale. Khofu hamna. Mtakuwa khofu hamna. Hamuogopi kitu chochote. Hamuogopi kitu chochote. Na kwa kweli bwana. Leo we ufikirie, kweli tizama, mtu kuvunja mlango wa nyuma wa Bomani. Yule Kamanda yuko pale, watu wanapita pale, Kamanda yuko pale, hakuna anayemuona, mpaka kuja kumkabili sentry [askari wa zamu]. Si mchezo. Hapa kiinimacho hiki kilipita kikubwa sana. Hata ikabidi mambo yakaja yakaingia sura. [Kwa upande wa Umma Party] Hanga ilikuwa kama ni kitu geresha kwa

Page 154: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa122

Abrahmani Babu. Siasa za Babu zilikuwa za Kikoministi za Kichina. Juu ya kuwa Mkoministi na siasa zake za Kichina, Hanga alisema, huyu vyovote itakavokuwa, wale ni wenzake. Kwa vyovyote itakavokuwa, damu nzito kuliko maji.3 Alisema hivo. Usifikiriye kama leo huyu Babu apigwe, Waarabu hawakubali. Hawato­kubali, kwa sababu itakuwa aibu kwao. Watasema “ala! kwanini Mwarabu apigwe? Kaasi tu huyu chama cha Hizbu, anapigiwa kwanini. Hapana.” Hilo suala kwanza ndoto ya kumueleza Babu hamna. Asielezwe kwanza huyu. Babu, Ali Mahfudhi, na wenzao, hakuna suala namna hilo. Hii yote mambo ya Manamba, walikuwa hawayaelewi. Katika vikao vyote vilivopita hakuna mmoja aloshiriki katika Makomred. Hata sku moja. Kwa sababu Komred siku ya Jumapili ndipo alivochukuwa bunduki kuumiza wenzake kujificha macho. Kujionyesha yeye kwa Mzee Karume au kwa Afro­Shirazi, yeye yuko bega kwa bega na Afro­Shirazi. Kujiaminisha. Kujikubalisha. Kwamba mimi hawa Waarabu sina imani nao. Na aliwaumiza kweli Babu. Jumapili bwana ndipo wale walipojuwa, mimi nikifanya hivi madam ile serikali imeshapinduka, wadhifa ntapewa na mzee Karume. Huyu anafaa kupewa posti [cheo] kwa sababu aligombana na Hizbu na ataweza kutumika kuwazuwia kina Hanga na Othman Sharifu. Kilichokuwa kinatendeka mpaka Jumamosi usiku walikuwa hawakijuwi. Kabisa. Komred hakijuwi kabisa kwa sababu Hanga alizungumza “bwana, mtu damu nzito kuliko maji.” Sasa ukija ukitizama, Babu, Ali Mahfudhi, Badawi, nk, hawa wamezaliwa mshipa wa Kiarabu. Wazee wao Waarabu. Sasa leo mkija kuwazungumzia watakuwa na fikra hawa wawaze “je, wanotaka kupinduliwa hawa Waarabu. Sasa vita vikitokezea vitakuwa va Waarabu. Je, sisi tutanusurika?” Ikabidi pakafunikwa hapo. Wasiambiwe. Jumapili, kweli Komred walikuja Raha Leo kifua mbele.

Okello na watu wa Mkello

Family za Manamba wao wanajuwa. Lakini kwa sasa hivi wengi Wazanzibari wanajuwa kwamba Wamakonde bwana wameshiriki mapinduzi hapa. Wana­fahamu kwamba wameshiriki na ndo watendaji wakuu hawa. Sasa familia ya Kimakonde au familia ya Kizanzibari, nadhani kiungo hiki madamu kinajulikana, sifikirii kwamba leo Mmakonde ataambiwa “wewe ndo muuwaji.” Au sifikirii atoke Mmakonde kumwambia Mzanzibari kwamba “wewe ndio muuwaji.” Sifikirii. Manake akisema kwamba “wewe ndio muuwaji” Mmakonde na yeye atasema “skiliza, mimi unaniambia muuwaji, huwezi kupewa cheo cha MBM [Memba wa Baraza la Mapinduzi], wewe lazima ulishiriki, sasa baba yako? Si alishiriki? Sasa ikiwa kama baba yako alishiriki basi na mimi baba yangu alishiriki, wewe na mimi basi jungu letu moja.” Kwa sababu nini, wazee wetu ndo waliokombowa kitu hiki. Sisi watoto haikutuhusu kitu. Ukinisema hivo, na mimi ntakwambia “na wewe!” Utata huu hapa itabidi utaondoka kwa sababu wote hawa wanajuwa. Hii

Page 155: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 123

hapa patakuwa hapana ngonjera. Hilo ndo liliopo. Shina ndo lilotufanya sisi kutukusanya mahala pamoja. Baada ya hilo shina lenyewe kutueleza kwamba, jamanii, wasaidieni wenzenu kule hawawezi kufanya kitu. Kwanini wasifanye kitu? Akauliza yule bwana, Victor Mkello. Kwanini wasifanye kitu? Ndio. Kwa sababu ni jamaa ni watu walokuwa wanaelewana. Jamii moja hii. Mimi nilitembelea, nikaitazama Zanzibar nikenda nikaona, ndio Wazanzibari hawa, hawa Waswahili, na hawa Waarabu, lao moja Kwa sababu jamii hii, itikadi zao ni moja, mila yao ni moja, tafauti labda itakuwa ni kiutawala.4 Lakini ni watu waliokuwa wameingiliana. Akasema, nimetembea mjini na mashamba. Shamba ndo ndiko nlokofaidi. Nikaja nkaona “hawa wamekuwa ni kitu kimoja.” Sasa ndivo nilivoamua baada ya kukutana na mashina wenzangu. Suala lile nikaona mimi niamue nikuiteni nyie. Anasema Mkello maneno hayo. Khamsini hatukufika. Sasa baada ya [Victor Mkello] kutuita akatupa ushauri “jamani kuna ndugu zenu nataka mkawasaidie. Wenyewe hawawezi.” “Hawa­wezi?” Hawawezi. Kwa nini hawawezi? Kwa sababu ile ni jamii ya mchanganyiko. Madam mchanganyiko itakuwa si siri. Lazima itatoka nje. Huyu ataweka siri, huyu atasema. Itakuwa hakuna mafanikio. Nyie mwende mkawasaidie ndugu zenu. Kukubali kwetu, suala tuloliuliza. Sisi tuna familia, halafu sisi wenyewe. Hili suala kama tunafanikisha tuna hongo gani? Tunalipwa vipi? Mimi [Mkello] sasa hivi siwezi kukujibuni. Lazima nende nikakutane na mashina yale kule. Tushauriane. Bahati nzuri, hata wiki mbili hazijafika, tukenda kule. Mashina ya huku yamentuma nende nikakutane na shina lile kule. Manamba wamekubali kushiriki lakini suala waloniuliza nimeshindwa kulijibu. Hawa wanaweza kujiunga na suala hilo lakini watakuwa wapi? Na wakati wana familia zao nyuma? Kuna kupona, kuna kufa. Je hizi familia huku zitatizamwa na nani? Jimmy Ringo [ Juma Maulidi Juma] alikata mkato moja kwa moja. Kwa sababu yeye anatoka kwenye shina. Akajibu moja kwa moja: “watahifadhiwa, na iko haki itatolewa. Haki zao zitatolewa wakifanikisha tu. Haki yake atapewa na familia yake itatizamwa. Heshima zenu zipo, hamtatupwa. Atakayekufa aelewe kuwa familia yake itatizamwa maisha.” Jimmy Ringo anasema. “Mmesikia?” “Tumesikia.” Je, tamko hili mnalikubali au mnalikataa? Tukajibu kwamba ukituuliza “mmelikubali, mmelikataa” ina maana hapa unatwambia sisi tunaweza tukatae. Anasema, sasa niulize vipi? Mnavoona nyinyi, nikuulizeni vipi? Wewe lako la kufanya, jee kazi jee mmeikubali? Sisi wajibu wetu tukwambie tumeikubali. Je, huu mkataba mmeukubali? Sisi tumeukubali. Akasema hapo siwezi kurudia tena, kwa sababu nini, lile suala umenipa halafu limekurudia. Akasema aa! Uliza. Kwa sababu kila unapouliza ndipo unapopata maana. Jamani, ndugu zenu ndo hawa, mmoja ni huyu hapa Jimmy Ringo. Je, hili suala, mmekubali kwenda kuwasaidia hawa ndugu zenu? Tumekubali, sawa. Je, hizi haki alizozizungumza huyu hizi, mmezikubali au na nyinyi mna masharti? Akasema, ehe! Sisi itabidi lazima tutowe masharti yetu. Waswahili hawa, sisi Wamakonde

Page 156: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa124

tunachanja uso, hawa hawachanji uso. Sisi wachanja uso wakati tunaposema “huyu anakwenda, anakwenda.” Lakini Waswahili watasema “yakhe, yakhe, yakhe.” Hafanyi kitu. Kwa hivyo tukubaliane hivi. Yule wa kule [Mkello] akasema sawasawa. Nyinyi mnakwenda vitani ati, makubaliano ni lazima yawepo. Familia yako, mkataba huu lazima uwepo. Yule kule akachukuwa karatasi akatuandika majina tulokuwepo pale. Akatuandika majina. Alipokwisha, kilichofanyika, Jimmy Ringo, kila mmoja katika sie alitupa ngapi, shilingi ishirini, ishirini. Katoa katika wale. Tena siku hizo ishirini nyingi. Jimmy Ringo akazungumza kuwaeleza wale, “nitakuwa na imani kubwa sana, au tutakuwa na imani kubwa sana, tulioko Zanzibar, kuja kwenu sisi ndo itakuwa mafanikio yetu.” Na wale wakasema, “wakati wowote, saa yoyote, hata leo utatwambia twende, sisi tuko tayari.” Akasema Jimmy Ringo “tunakwenda kumalizia mipango, tukishamalizia mipango, ntakuja mimi, au atakuja mwenzangu mimi, au tutamuarifu huyu bwana [Victor Mkello].” Sisi tulokuja huku Zanzibar tulikaa tukashauriana. Tulishauriana hivi. E bwana we, wale ndugu zetu wa Zanzibar, kila wakipiga kura wanakosa, kila wakipiga kura wanakosa. Wameamuwa kufanya mapinduzi. Maana ya mapinduzi tunayajuwa? “Si ndo yale yalioko Msumbiji? Sisi na Wareno? Hata tukaingia msituni? Si ndo haya? Si ndo wamekusudia hawa? Ehee! Tujuwe hivo. Manake msije mkafikiria kwamba kule tunakwenda kupiga miraba. Aa! Hatwendi kupiga miraba ya matuta. Kule tunakwenda, tukifika, tutakapoambiwa, kitanda hiki ingia ulale, au nyumba hii ingia ulale, bwana leo unakula muhogo, leo unakula sembe, shote tufahamu, suala litakuwa hilo. Na ahadi ndo imeshakuwa imekamilika hiyo. Tunakubaliana hivo? Tunakubaliana. Sote kwa pamoja.” Mimi na yuko mwenzangu mmoja, tuliliendea lile shina letu, lile la kule Tanga. Tukamuuliza, “bwana we, mkataba umeshafungwa, kila kitu kimeshatengenezwa, umeandika majina, umefanya kila kitu. Barabara. Wewe, saini yako umetia?” Akasema “sijatia.” Tukasema “kama hujatia sisi hatwendi.” Akasema hakuna tatizo. Akachukuwa karatasi akatia. Baada ya kutia saini tumekaa, tumeendelea na shughuli zetu za kukata mikonge. Lakini huko jungu linatokota. Jungu linatokota. Siku moja alikuja kutuaga huyu [Mkello]. “Mimi nakwenda Zanzibar. Nakwenda Zanzibar kukutana na wenzangu wamenita.” Akaja Zanzibar. Kufika Zanzibar wakakutana na mashina ya ndani kabisa. Wakazungumza, na yeye kule alichofanya, alikutana na watu hawa, Wamakonde watano tu, viongozi, sio wote, na akawaambia kwanini nakutana na nyinyi watu watano. Siri mliyopewa ni kubwa mno. Anasema, “mnaweza kuzungumza kilugha, lakini kuna wenzenu wengine wasiokuwepo katika gurupu hilo wanaweza kusikia lakini hatutaki yatoke nje. Na kama wanakuulizeni wenzenu, suala la kusema, kuna mipango kule inapangwa, lakini nnachokwambieni, baada ya wiki moja safari tayari. Mtakwenda nyie kule.” Katika hao watano mmoja, Naruka, Tajiri, alikuwa akifanya kazi custom

Page 157: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 125

Zanzibar, Joseph Bhalo, Shindano, na mimi mwenyewe. Watano. Shindano kweli uhakika, kwa sababu alipigwa risasi jela, ubongo ukachanika huu. Mzee Karume akasema, hapana, huyu apelekwe Nairobi kwa matibabu. Sisi watano tukahamia Unguja. Nakumbuka Amboni alikuwepo Ndagaa, Joseph alikuwepo Ndagaa, yule wa custom [Tajiri] alikuwepo Mfenesini. Ina maana tulisambazwa sambazwa. Sasa, Tajiri wakakutana na Khamisi Hemedi. Mimi nimeshachoka kulima. Je, pale pwani siwezi kupata kazi? Ngojea tufanye mipango. Kumfanyia mpango bahati nzuri akabahatika yule, ndo akenda pwani. Sasa yule wa Tanga [Mkello] alikuja kulisifu shina la hapa kuwa limefanya kitu busara. Kumchukuwa mmoja kumuweka custom atakuwa ni mpokezi wa hawa walioko Tanga. Kwa njia ya custom. Atakuwa anawapokea. Wageni wale wanafika pale anawapokea. Yeye anajuulishwa tu “ndugu zako hawa.” Tumekaa hapa hata yalivokuwa mambo yanakaribia ikabidi wanakuja mmoja mmoja, kila anayekuja hapa, mbebaji ungo, Wamakonde hao, wamekuja kushughulika mambo ya miraba. Wanakwenda mashamba. Lakini shina la hapa linajuwa kinachotokea. Siku moja tulikuja kukutana na Jimmy Ringo, Kilombero. Siku hiyo ndo nilimuona Kaujore, Hanga, siku hiyo ndo nilimuona Twala. Walikuja viongozi kama wanne hivi, kuja kutuona na kutuambia “tulieni msiwe na wasi wasi.” Sasa walipotueleza akina Hanga pale, kidogo sisi tukatulia. Hanga alichofanya, anasema “mko pamoja au mko mbalimbali?” Tukasema “tuko mbalimbali.” Kama mko mbalimbali wewe itabidi uje Kijangwani. Ziko pesa ntakupeni, kiasi ishirini ishirini za chakula, kuendesha maisha, na kila kitakachopunguwa huyu itabidi aje pale, ndo kiungo. Huyu ndo kiungo wenu. Mmemkubali, tumemkubali. Bas. Kutoka siku hiyo viongozi wale mimi sikuwaona mpaka serikali inapinduka. Sisi tunaendelea na shughuli zetu lakini mimi nakwenda kule. Nikifika kule nikitokewa na shida napewa pesa. Kwa maana kitu kikubwa nikifika kule ninachokionyesha ni kadi ya Afro­Shirazi tu. Huyo, Chairman [Mwenyekiti] wa Ndagaa huyo amekwenda kujenga taifa mahala fulani. Mpeni kiasi fulani huyo. Anapewa. Shina lilijenga huyu apitiye kwa njia hii. Blanketi sasa. Kafunikwa. Siku ilivodhihiri, tulikutana mmoja juu ya mmoja. Kikao cha tano kilichofanywa kwenye msitu wa Ndagaa ule, lakini uamuzi wa pamoja tuliamuwa na Victor Mkello alikuwepo kuja kuthibitisha na kuhakikisha, wamekamilika? Manamba wa Tanga hapa wamekamilika? Tulokuwa tumekuja sisi hapa tulikuwa ishirini na mbili. Wenzenu wako njiani wanakuja [anasema Mkello]. Ishirini na mbili tulitoka kule. Kuna baadhi ya wenzetu kidogo waliingia mitini. Wakasema “njomba, kifo hicho!” Idadi yoteyote ni arubaini na nane. Ya Manamba waloingia hapa. Jimmy Ringo akasema “sasa hawa itatosha.” Mkello akauliza “wanatosha”. Tusiwafunguwe watu macho, “mbona Wamakonde siku hizi wanaingia sana hapa?” Tumekaa hapa tunalima. Tumejenga vibanda vetu va migongo. Tunaishi, bila ya wasiwasi. Hakuna mtu anatuuliza au kututuhumu. Manake watu wanajuwa kazi zetu sisi ni kulima. Na wengi wao kwa

Page 158: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa126

upande wa Waafrika walijuwa, hawa wamekuja kwa lengo kadhaa. Lakini sasa tuwaache kama walivyo. Wale walimaji tu wale. Sasa, hata siku inawadia, kwamba bado wiki hii, moja, hili suala litendeke, palivuja siri, kuvuja siri Manamba hawakutajwa. Manamba hawakutajwa. Isipokuwa yule alievujisha siri Jamali Nasibu, kasema Afro­Shirazi inataka kufanya mapinduzi. Sasa siri ile ilikwenda kwenda mpaka ikaja kuonekana kama ni uwongo. Watu wakaingia kazini. Kwa sababu ndani ya polisi mle Afro­Shirazi wamo. Wakenda kucheketa. Ikabidi hapo Jamali hakuulizwa kitu. Akawa ni wa kutengwa tu kwenye mashughuli. Ikabidi watu wakafanya shughuli zao, hata zilipokuja kukamilika, tukapokewa mjini kutoka Ndagaa, tukapelekwa kwa Yusuf Himidi. Hata Yusuf Himidi akatuonyesha, hapo kuna magari mabovu hapo, hebu waficheni waficheni kwenye hayo magari mabovu. Baada ya nyumba moja ya Mgoni huyo, kujaa hiyo nyumba. Suala linalonisikitisha mie, na wenzangu wengi wamekufa, familia zao hazi­julikani. Kinachonisikitisha nini? Mimi huku ndo nimepinduwa, bendera ile pale inapepea, nimepata nini? Eh! Karume katoa shilingi arubaini na nane, zilikuwa khamsini, mbili za risiti, nikipata arubaini na nane. Ndo nikaona hakuna faida ya kuandika historia. Mimi nitapata nini? Mimi kazi yangu itakuwa ni ileile kazi ya zeze. Nitapata faida gani? Lakini leo imebidi nikueleze ukweli kwa sababu iliniuma nikueleze ukweli baada ya kukukimbia. Suala la Manamba hilo hapa. Idadi yote ni tisini na mbili. Kutoka Manamba mpaka hawa wa hapa. Jeshi lenyewe. Tisini na mbili. Katika hawa tisini na mbili, Mfaranyaki na Okello, walikuwa ndani ya gari ya polisi, kawapa Antoni Kisasi, na ndani yake akiwemo askari. Wanazunguka. Sasa askari wao kama wanajuwa tu alikuwemo askari, na ndani wamo askari wawili. Okello na Mfaranyaki, wao wanafanya patrol. Ulipofika wakati yule askari alivuwa gwanda akavaa nguo zake za kawaida. Okello alifahamu sana kuhusu Manamba. Sana. Mwisho lakini baada ya tukio. Okello kwa BiKazija hakufikishwa. Kwa sababu huyu ni Mganda. Tunamuamini kweli lakini sasa kumuamini kwetu tunamuamini vipi?5 Haiwezekani hiyo! Lakini kina Kaujore, Saidi Washoto, Sefu Bakari, Ingine, wakijuwa kuwa Manamba walikuwa wameingia. Ni ndugu zenu. Jamani Manamba wameingia. Wako mashamba huko wanalima. Ndo hapo ndipo utakapoona, Wamakunduchi walishindwa kushirikishwa kwa sababu Ameir Tajo kuwa bega na bega na Mfalme. Wakasema hapana. Huyu atasema huyu. Kwa sababu huyu Shekhe. Anapewa kilemba kikubwa sana. Kusini suala hili lisizungumzwe.

Kiini cha John Okello—J. J. Mchingama

Walompa Okello ile hadhi ni kina Sefu Bakari, Natepe, akisaidiwa na akina Kaujore, Saidi Washoto. Sefu na Natepe ndo walomkabidhi. Sasa zilipomalizika zile shughuli ikawa moja kwa moja na yeye akajivika kile kilemba kwa sababu

Page 159: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 127

alipewa basi ni changu kwelikweli. Anataka kuingilia sasa amri zote za serikali. Mpaka zipitie kwake. Ikabidi apewe masaa ishirini na nne Zanzibar kuondoka. Akaondoka akenda zake Kenya. Kenya akafuatwa na waandishi wa habari wanataka kujuwa habari za mapinduzi yalitokea vipi. Hakuwa anaeleza misingi. Akasema tu, tulikusanyika na mapanga na marungu basi tukaingia bomani. Ndio. Lakini source, chimbuko nini? Hakueleza. Hata kwenye magazeti mengi tu. Jambo hilo hawakulipata. Akaenda Uganda ambako ndo asili yake. Kwao. Ni mu Acholi huyu. Kabila la Acholi la Uganda. Alipokwenda kule, kabla hajafanya lolote, akakutana na waandishi wa habari wengi. Wakimhoji lakini hakutowa cha msingi. Nakumbuka gazeti fulani nililisoma, anatembelea shule, yeye huyo, baada ya kutimuliwa hapa [Zanzibar]. Anatembelea hospitali, wagonjwa. Uganda huko. Pale, inasemekana serikali ikaanza kushtuka. Huyu mtu kaingia karudi kwao, lakini mbona anaanza kujiweka ufahari namna hii? Kuna nini hapa? Unaona hiyo? Sasa ikawa hakuna njia isipokuwa wamvute sasa. Wamvute karibu (vicheko). Wakamwambia bwana wewe huko ulishiriki mapinduzi na nini. Akasema “ndio.” “Sasa kule wewe kama uliongoza mambo haya ulifikia cheo gani?” Akasema “Field Marshall.” Wenzetu wanajuwa kuna taratibu. Ufield Marshall huwezi kuufikia kama hujapigana na taifa. Ukashinda taifa. Mfano kama Samora Moses Machel. Amepata Ufield Marshall baada ya kulishinda taifa la Kireno. Kwa sababu alikuwa anapigana na taifa. Hukipati kienyeji, kiholela. Hapana, hapana. Lazima umefikia level [mustawa] ya kupigana na taifa ukalishinda. Sasa huyu bwana wakaona, basi kama ulikuwa Field Marshall itabidi uingie jeshini. Wakamuingiza jeshini. Huko habari nilizokuwa nimezipokea alikuwa ni platoon commander. Kamanda alikuwa akiongoza platoon moja, ya watu tha­lathini labda kitu kama hivi. Sasa pale yule akaona mimi nimetoka rank [cheo] ya “Field Marshall” Zanzibar leo nakuja kupewa platoon commander ndo manake nini? Akadanganywa. Palikuwa na udanganyifu fulani wa kumpozapoza. Baadae akaambiwa wewe nenda, kasomee kulinda mpaka wa Kenya na Uganda. Kape­ lekwa sehemu inaitwa Busia. Mji wake unaitwa Mbale. Basi alipofika kule wakafanya mbinu wakamuuwa. Akafa. Wakamzika hukohuko. Wala hawa­kumrudisha kwao Acholi ambako kwenye asili ya kabila lake. Baada ya kumuuwa wakamzika hukohuko na hazikutangazwa habari zake. Zikawa kimya moja kwa moja. Mpaka hii leo. Okello alikuwa halijuwi chimbuko. Pengine angelikuweko katika kamati ile ya mapinduzi yenyewe akajulikana muandalizaji nani kwa uandalizi wote wa mapinduzi yenyewe, akamjuwa fulani na fulani ndo wenzangu. Hiki kitu alikuwa hakijuwi. Waliopika mpango huu walipanga wao wenyewe lakini kwa kutumia mbinu wakasema “wewe bwana njoo! Unajuwa kuna kitu fulani hichi kafanye hivi.” Kama kungetokea jambo lolote pale la kufichuka hao wote wangeliruka wangelimuachia mpira yeye na asingekijuwa cha kueleza nani alikutuma, nani

Page 160: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa128

mulipanga nae. Asingejuwa. Na ndio maana aliendelea kutokujuwa chimbuko hasa, nani na nani waliopanga huu mpango. Yeye alikuwa ni kama mtu aliekuwa ameokotwa tu akapewa ule umbele na yeye akaupokea. Kwa kuona Waswahili wenzangu hawa wameniambia hivi akaupokea. Lakini kiini, nani na nani walioandaa, hakujuwa. Kiini, ni kuna watu katika jeshi la polisi wakijuwa hizi habari. Bahati mbaya sasa hivi wameshatangulia mbele ya haki. Kwa mfano mzee mmoja wa Kijaluo akiitwa Thomas Tete. Alikuwa akijuwa mpango huu. Kuna mzee mmoja wa Kimwera akiitwa Anthon Musa Shamwingo, alikuwa katika jeshi la polisi, alikuwa akijuwa. Kuna Juma Maneno [Muheza]. Kuna Edington Kisasi, alikuwa anajuwa hizi habari kwa upande wa jeshi la polisi. Ambao wao walikuwa wakiungana moja kwa moja na akina Sefu Bakari, Kaujore, na Natepe. Hawa ndo walokuwa wana siri hizo. Na wao ndo walikuwa wakisema, nani na nani tutawapata wa karibu wa kuweza kuungana nao. Mngereza nahisi alikuwa halijuwi kwa sababu kujuwa kwake angelilipata kutoka kwa hawa ambao walikuwa katika jeshi la polisi na ndio wakubwa. Lakini hawa walimficha Mgereza. Hawajamwambia Muingereza. Kufahamu kwangu mimi hivo. Walikuwa hawakumwambia Muiengereza. Wakumwambia Mueingereza ni Edington Kisasi, Anthon Musa, na Thomas Tete. Hawa ndo walokuwa wamelishikilia wakati ule jeshi la polisi.6 Hawa ndo walokuwa wepesi wa kumwambia lakini hawa kwa vile walikuwa wameungana na huku hawakuweza kumwambia na kama walikuwa wanamwambia ilikuwa ni udanganyifu, sio ule uhakika. Pengine kumwambia kama kuna rumours [uvumi] hivi, labda, tuweke standby [tahadhari]. Kuna wasiwasi hali lazima tuweke standby. Vitu kama hivi. Lakini kiini kuwa kutafanyika hivi alikuwa hajuwi.7

Unajuwa wakati mwengine nahisi kwamba mara nyingi Afro­Shirazi ikitaka kufanya jambo lake walikuwa wakiwatumia sana Youth League. Kama ni suala likitokea jambo lolote kwamba ni vijana hao wamefanya fujo na vijana kimataifa hukumu zao zinakuwa tafauti. Wakiwatupia vijana. Hata kama lile jambo wata­kuwa wamelifanya watawatupia wale vijana waonekane Youth League. Wanajitowa wao. Nasema hivo kwa sababu kulikuwa na maktaba ya Mmarekani ilikuwepo hapo Kikwajuni ile nyumba ya Ubalozi wa Msumbiji sasa. Lakini kutoka na michezo walokuwa wakionesha pale, wao kina Sefu Bakari ndo walokuwa wakiwatuma vijana kwenda kutupa mawe pale, kwenda kufanya fujo pale. Yule Mmarekani akalalamika kwamba mimi naonyesha filamu hizi kufanya burudani kwa vijana hasa pale kipindi cha Apollo 11. Akasema “wewe si unajuwa vijana tabia zao? Kwenu si mnao vijana?” Mpaka mwisho ikaamuliwa kwamba bora wahame pale, watakufanyieni fujo. Akahamishwa pale akapelekwa Mji Mkongwe. Kwa hivo walikuwa wanatumia trick [ujanja] hizo kutumia Youth League kwamba vijana mara nyingi ni ulimwengu mzima wanaeleta fujo sana. Kina Babu, mapinduzi, nnavofahamu mimi, wamefahamu alfajiri yake, ila

Page 161: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 129

wao walikuwa na maandalizi ya kufanya mapinduzi kwa njia zao wenyewe. Kwa sababu walipofukuzwa kutoka ZNP wakaunda chama cha Umma Party na walikuwa na wanafunzi wao ambao walikuwa wamechukuwa mafunzo ya kijeshi. Bila ya shaka walikuwa na maandalizi yao lakini maandalizi haya wamekuja kushtukizia asubuhi. Wakaona na sisi tukitaka hichohicho ili kitokee. Madam yameshatokea mapinduzi ambayo sisi tulikuwa tumeshajiandaa, basi tujiunge moja kwa moja. Wakaunga mkono moja kwa moja. Lakini kiini cha kabla hawakushirikishwa. Lakini baada ya kuwa wameunga mkono na kweli ule udhalilishaji wa ZNP dhidi ya kina Abdurahman Babu, wakawa wao kama kundi moja na ASP. Na wao wakawachukuwa moja kwa moja wakawapokea. Ndo maana baadhi yao wakapata nafasi ya kuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi (MBM) kwa kutokana na kuunga kwao mkono. Hawakuwa katika kiini. Kiini kilikuwa watu separate [mbali] na wao kabisa. Mimi suala hili la mchujo kwa kweli nafahamu kwamba wao walitaka Waafrika wenye asili ya kutoka bara walijuwe suala hili peke yao bila ya kumshirikisha mtu yoyote wa Zanzibar. Mzaliwa wa Zanzibar. Hilo kwanza. Na ndio mana utakuta pale kuna Saidi Washoto Myamwezi. Umeona hivo. Kuna Kaujore ni mtu wa wapi, Tunduru pale. Sefu Bakari Mdengereko. Hafidh Suleiman ni wa hapa lakini nafikiri katika masuala hayo hakuingizwa zaidi. Kina Ibrahim Makungu hawa wamekuja mwishonimwishoni lakini kiini cha siri ya mwisho ilikuwa hivo. Nafikiria hivo, sina hakika ya kutosha. Lakini mchujo ulikuwa uko wazi. Kwa sababu tukiwaambia hawa wengine wameowana na kuzaliana na Waarabu.8

Hatokubali shemegi yake au mwanawe akauliwe. Ataona uchungu japo kuwa hakubaliani na matendo yale lakini hatokubaliana kuona family yake inakufa. Kwa sababu vitendo vina mauwaji. Haya ashtukie yametokea bas. Asijuwe mapema. Hiyo ilikuwepo. Ndo mchujo nnaoufahamu mimi, kwa ufahamu wangu mimi. Kwa kabila letu sisi Wamakonde tuna mambo ya kuigiza sana. Ukenda mahakamani kuna mtu anaitwa Bwana Shauri anaeshauri mahakama, basi mama wa Kimakonde anajiita mimi Bwana Shauri. Pesa shilingi mia, basi mwanamke anasema mimi “bwana mia.” Ni watu wenye kuigiza sana majina. Wepesi wa kuchukuwa majina. Akikuta kitu cha ajabu tu hivi kinatajwatajwa sana yeye yuko tayari akichukuwe. Anabadili jina lake la asili sasa hivi, akirudi kwao anasema jina lile nimeliacha naitwa fulani. Hii ni tabia ya Wamakonde. Kwa hivo Mzee Amboni Matias anaweza kuwa ameitwa kwa hivo tu. Amboni kweli ni mji, kuna yale mapanga pia, Amboni. Yalikuwa yakitolewa kwa ajilii ya shamba lile la Amboni. Yanaitwa mapanga ya Amboni kwa shughuli za kukata mkonge. Kwa sababu yale mapanga ni makali basi na yeye atajita “Amboni.” Ni sifa ile. Mie ni “Amboni.” Huyo Tajiri pengine nyumbani alikotoka jina lake si tajiri. Lakini kufika hapa, bwana kuna tajiri mmoja pale, alaa, kumbe yule tajiri, manake ni mwenye pesa. Basi na yeye anajita “Tajiri” ili apendwe na wasichana. Amboni, mkali, Tajiri ni mapesa japo hana.

Page 162: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa130

Turudi kulekule kwenye mazungumzo yetu, kama kulikuwa na plani [mipango] hizo mimi kwa kweli sizielewi hili suala na halimo katika kichwa changu na wala katika historia. Mimi nakubali kwa sababu hata siku hiyo, nakumbuka, kulikuwa na tetesi tetesi lakini si za uhakika. Lakini saa kama hizi za jioni tukiwa pale Makadara. Tuliitwa vijana wote wa Kimakonde tulokuwa tukifanya kazi kwa Wahindi humu majumbani, kukosha vyombo, kulea watoto, sijui nini, wote tuliitwa Makadara kwenye ofisi ya FRELIMO. Wao wanajuwa hicho kitu, kwa muda mrefu, na siku ile kwa kutwa nzima wanazo hizo habari lakini hawakutaka kulitowa. Wa kike na wa kiume. Hata wale wanofanya kazi za dangurodanguro wakaitwa. Tukaambiwa bwana, kuanzia sasa hivi vijana nyote hamna ruhusa kulala peke yenu. Mtalala jengo hili. Kwa sababu hali ya nchi leo si nzuri. Mmesikia, tumesikia. Tunakwambieni msiondoke. Mimi nakumbuka nilikuwa napenda kukaa palepale Mwembeladu palikuwa na duka moja la Muhindi. Huyu Muhindi alikuwa akijifanya yeye ana asili ya Msumbiji. Kwa hivo Wamakonde wengi walikuwa wanakwenda pale, nafikiri ulikuwa ni mvuto wake. Kwa hivo mimi nilikuwa napenda sana kwenda pale. Sijui kwa njia gani au vipi alikuja akapata fununu huyu Muhindi. Akaniuliza kama nimesikia kutakuwa na fujo. Nikamwambia mimi sijui. Basi nikarudi. Saa kama hizi akaja babangu akanambia nimekuja kukwita twende nyumbani kwa sababu wenzako kuku wanakula kule wanamaliza. Kamchukuwe kuku wako umle. Kumbe yeye anajuwa anataka kuniondowa kiu­janja. Siku ile kukawa na ngoma nzuri sana ya Kimakonde sehemu za Jumbi. Siku ile ya mapinduzi. Na mimi na appointment [miadi] zangu za ujana kule kwenye ngoma. Nikamwambia baba leo siji huyo kuku nitakuja mla Jumapili kwa sababu leo nataka kwenda ngomani. Akasema leo usende ngomani. Wenzako kule kuku kaka zako wanamaliza. Juzi yule kala wawili, yule mmoja jana kachinjwa, huyu nikasema hata, huyu muachieni mwenzenu kwa hivo twende. Nikamwambia mimi leo hapana. Akaniona mgumu. Akaniita pembeni. Sikiliza. Ninachokwambia leo hali ya nchi hii si nzuri. Huenda vikatokea vita. Mimi nilivokuja nimekuja kamili. Amevaa shuka na hilo panga la Amboni amelichomeka kwa ndani. Akakunja shuka akanionyesha panga. Kalinowa sawasawa. Unaliona panga hili? Mimi sirudi tena nyumbani ila wewe rudi nyumbani, mimi nimepona sawa, nimekufa utaongozana na wazee wako. Kama ananiaga. Nikamwambia baba, mimi mwanamme. Kwenda kuniungamanisha mimi na wanawake nikakae niwachunge wanawake wewe unakwenda kufa mimi sikubali. Utakapo kufa wewe ndo nitakapokufa mimi. Kwa hivo mimi sikubali. Tufatane wote. Yule baba akaona hapa amefanya makosa kuitoa hii siri. Kumbe sasa imekuwa ni kero kwake. Kwa hivo yeye akasema kama ni hivo nisubiri nende kwa Haji Tumbo nikanunuwe kiteweo ili tuje tuambatane tuondoke. Nikamwambia kiteweo cha nini na nyumbani kuna kuku? Nimembana zaidi pale! Kidogo nilijitahid machachari. Akasema aa, yule kuku wa kwako wewe lakini huyu

Page 163: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 131

samaki nakwenda kununuwa sisi tule. Yule wa kwako. Nikamwambia haya nenda. Nakusubiri basi. Hakurudi tena yule. Ikawa sasa mambo yangu nimeshayapata mara tatu. Kutoka kwa baba yangu, Makadara ofisi ya FRELIMO na kwa yule Mhindi. Kumbe ile ngoma inayofanywa Jumbi nayo ni mkusanyiko wa kuwakusanya wanawake na watoto tu lakini wanaume watu wazima wote wanakuja zao kwenye kazi. Mimi mshipa umenishika. Lazma niende kule. Wikiendi [mwisho wa wiki] itanipita! Sasa na wenzangu fulani wakawa wamejitokeza. Twendeni bwana, si tutarudi? Ah! Twende, twende. Tulikuwa watu watano. Wakati huo baiskeli zinakodishwa. Shilingi mbili mpaka kesho asubuhi. Tukenda kukodi baiskeli zetu. Safari, Jumbi! Kufika kule ngoma wanawake wengi lakini wanaume hamna! Wanaume ndo tumekwenda sie tu pale. Kufika saa sita tukaona upuuzi huu. Bora turudi zetu. Tukarudi. Tunafika Fuoni polisi, saa nane za usiku, tukakuta road block [kizuwizi cha njia]. Mnakwenda wapi? Tunakwenda mjini. Kufanya nini? Sisi tunafanya kazi kwa Wahindi. Huku mnatoka wapi? Tunatoka kwenye ngoma. Hiyo ngoma inamuhusuni nini? Sisi watoto wa Kimakonde. Mmoja akasema tuwekwe ndani, tuzuwiliwe. Mmoja akasema hapana, waachie. Watakaloliona watakuja kutwambia kuliko kuwazuwia hapa linalotendeka huko hatulijuwi. Road block [kizuwizi cha njia] imeshafungwa pale. Kuna gari moja inatoka shamba inakuja spidi kali sana. Ilipofika pale kumurika ikakuta kile kizuizi haikujali, ikavunja poo! Ikapita tu. Kwa sababu yule askari alikuwa na tochi, akamurika ndani ya gari na kutaka kuisoma ile namba. Kwa jicho langu niliwaona watu waliokuwemo mle, wamevaa weusi mtupu na hata miili yao wamejisinga weusi mtupu. Gari ikaondoka! Lakini wako kimya. Basi tukaja zetu mpaka meli tano Fuoni. Kufika Fuoni, ndo tunasikia sasa risasi zinalia. Jamani turudini. Tumeambiwa na wale askari wale. Aah! Turudi vipi bwana. Twendeeni! Tukafika Mwembe Njugu. Tunafika Mwembe Njugu saa kumi na moja za alfajiri ndo kinachukuliwa kituo cha Ngambo police station. Hapapitiki. Risasi mtawalio mmoja. Ikabidi tena tukimbilie Mwembe Matarumbeta. Mwembe Matarumbeta ni opposite [inakabiliana] na Ziwani barracks [kambi ya jeshi la polisi]. Nako kule kuna marisasi yanaangukia hapa. Na la mgambo likatoka pale, mwanamme nje, mwanamke ndani. Ndo tuko nje. Ikabidi sisi tuwache baiskeli ndani ili kumfata mzee wetu pale. Tukawacha baiskeli, sisi tukarudi tuka join [tukajiunga] kuelekea Raha Leo. Tayari nayo Ziwani ishachukuliwa. Pale tunakutana na John OKello. Asubuhi hiyo. Mapema! Ukifika hapo “unajuwa bunduki?” “Najuwa au sijuwi.” Basi kama hujuwi shika “kama unakuta Mwarabu piga yeye.” Okello anasema. Kilugha chenyewe cha Kigandaganda cha kuvunjavunja tu. Sasa likatokea lorry moja. Lina mapanga, lina mamishare, mapinde. Nikaona ile ndo jadi yangu. Mimi nikawacha bunduki nikenda kuchukuwa upinde nikaona ni silaha naiamini kuliko bunduki. Tukajiunga pale, tunapakiwa wapi, mahala flani kuna Mwarabu anafanya fujo.

Page 164: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa132

Tunakwenda. Pengine tunakutana nao, pengine tayari tumeshamuuwa au tushamchukuwa. Tunarudi wapi, twende Kipange, mara twende huku. Hivyo, ikawa vurugu. Kwa hivo inawezekana kwamba kama kuliweko vitu hivyo, nataka kukubaliana kwamba hili gari nloliona alfajiri linapita pale Fuoni, usiku ule wa saa nane, inawezekana pengine katika hawa watu waliokuja kuandaliwa kutoka huko Tanga. Sijui. Inawezekana hivo.9 Lakini kwa ufasaha hasa kusema kwamba kuna watu walitoka sehemu nje ya Zanzibar kuja kufanya hivo ndo itakuwa mara yangu ya kwanza kuisikia. Watu wengi hawaijui. Inawezekana ilikuwa high level [inajulikana na daraja la juu la uongozi]. Mimi najuwa katika kambi za mkonge makabila yalokuwa yameshamiri: Warundi, Wamakonde, nk. Wananyaruwanda ndo walokuwa sana katika kambi za mkonge. Myamwezi alikuwa sio fani yake. Mmasai alikuwa sio fani yake. Ila wako wale Wakwami walikuwa wanashiriki lakini sio sana. Kama nilivosema siku ile. Haya mambo yanakwenda kwa level [kwa daraja ya cheo]. Wewe unaweza kupewa kitu ufahamu hichi. Usitake kukijuwa kengine. Na yule na ajuwe pale, asitake kujuwa kwengine. Huwezi kuyajuwa yote. Mimi kwa level [daraja] hizo na miaka hiyo sijui. Kwa sababu huyu Tajiri Fundi kwa upande mmoja mimi alikuwa ni mzee wangu wa karibu kifamilia. Na wanawe wapo ambao wao mimi ni ndugu zangu. Wapo hapohapo Shakani. Tulikuwa tunaongea sana hata katika Jumuiya ya Wanamsumbiji sikukumbuka katika historia yake alikotokea. Na sisi nakumbuka tulimkuta na yeye Fundi Tajiri na alikuwa mpinzani wa FRELIMO hata kwenye shughuli za jadi, kama jando, yeye alikataa akaamuwa kuwachezea watoto wake kwa mila za Kizanzibari. Kawapigia beni na tarab kwa kupingana na FRELIMO. Mpaka 1975 ulipopatikana uhuru wa Msumbiji ndo akasurrender [akasalimu amri], akaja upande wetu. Kuna Mzee Thomas ambaye bahati mbaya alifariki hivi karibuni alitokea Tanga vilevile lakini hakuja kwa njia hizo naye pia alikuwa against na FRELIMO, na watu walokuwa wakisupport ASP ni chama cha FRELIMO. Hao wengine kwanza walikiita chama chao Afro­Shirazi Makonde. Michango yao wakiwapa Mzee Thabit Kombo na Mtoro Rehani Kingo. Na FRELIMO iliposhamiri wakawaruka [wakawalia pesa zao]. “Wafateni wenzenu. Kwa nini msiwe na wenzenu?” Ndo hao kina Tajiri Fundi, kina Thomas Kalawone, na wengi wengine tu. Lakini kama Mzee Amboni alikuwa FRELIMO. Joseph Bhalo FRELIMO na mwaka 1974 alienda Msumbiji baada ya FRELIMO kupata madaraka, bado uhuru kamili, ndo alipoondoka Joseph Bhalo kwenda Msumbiji kwa kuitwa na viongozi wa kule ili kwenda kuangalia hali ya madaraka inavopatikana.

Kuibuka kwa Mzee Karume—Mzee Issa Kibwana

Mzee Karume alikuwa na mawasiliano na watu watatu katika jeshi la mkoloni. Alikuwa na mawasiliano kwanza na Edington Kisasi. Alikuwa na mawasiliano na

Page 165: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 133

Anthon Musa. Alikuwa ana mawasiliano na Juma Maneno. Huenda wakawemo na wengine lakini mie nisitambuwe. Nazungumza kile kitu nnachokitambua. Sasa wale walikuwa maisha siri ya yale maboma wanampa yule. Halafu akaweka, kwamba wale watu wake wa kuwatumia, siri zake ndani ya maboma yale. Nadhani hata tulipoingia katika boma la Mtoni mtu wa kwanza wa kumtafuta Anthon Musa kwa sababu ule ufunguo wa armoury [ghala ya silaha] alikuwa nao yeye. Mawasiliano yalikuwa mnakwenda mahala fulani mkishamaliza vilevile vidogovidogo huku mlangoni mpenye mumtafute fulani ndo mwenye ufunguo wa silaha. Tunakwenda pale kwa kujuwa kuwa fulani ndo mwenye ufunguo. Na wanokwenda Bomani wanajuwa nani mwenye ufunguo. Hawa watu [akina Hanga] walikuwa wasomi. Karume si msomi. Karume kasoma umaarufu wake ndani ya vyombo tu baharini. Lakini usomi wa ndani ya vibuku, vitabu hivi, hayumo. Sasa Karume kichwa chake kilikuwa kinafanya kazi akili ya kuzaliwa. Anajuwa kitu kinachokuja usoni kwake ni kibaya na anajuwa kitu kinachokuja usoni kwake ni kizuri. Sasa wale japo kama walishiriki ndani ya mapinduzi yale lakini alitambuwa kabisa hawa kuja ndo maji yangu mie.10

Nasema kwa kujuwa ndo nkakwambia kuwa mie nlikuwa karibu naye mtu yule. Alijuwa kabisa. Maana kuna saa ingine huita hasa. Humwita Idi Bavuai, humwita Juma Maneno, humwita Sefu Bakari, kina Kisasi, wote huwaita pale. Huwaambia hasa “mnajuwa nyie, kula mkikaa kuna watu wengine mkizungumza mambo ya masilaha yenu watu wengine msiwaambie. Au kunakuja chombo chenye silaha watu wengine msiwaambie. Muwe na akili. Kwa sibabu bado maadui tunao hapa. Kama si wewe mie, kama si huyu, huyu. Huja tukapoteza maisha yetu kabla hatujajuwa ulimwengu uko vipi.” Sasa mtu wa kwanza wa kutambua lile suala analolizungumza Mzee Karume, Waziri Kiongozi wa kwanza—Ramadhani Haji. Ramadhani Haji haraka aliijuwa siri ya Mzee Karume. Jibu lake anamwambia “hakika na mie natambua. Kuna kitu kwanza huyu Hanga anakuja vibaya sana kwa sababu wewe hujui kusoma kwanini ukawa kiongozi. Hujui kusoma utakuwa vipi kiongozi. Umtizame sana mtu huyu. Halafu kuna mtu wewe unampendelea saana mambo yako kumpa. Huyu kwako wewe si mzuri. Kuna kitu anataka kwako wewe. Sisi tunavoona. Au tuwachie sisi tufanye shughuli zetu.” Jibu lake “ntakupangeni. Mimi mwenyewe ntakupangeni halafu ntakupeni kazi.” Wakachaguliwa watu ishirini na tano, wakapelekwa wapi? Hapoo, pakiitwa Kambi ya Jitegemee. Kambi ile wamechaguliwa watu ishirini na tano makusudi wana kazi yao maalum huja nayo Mzee Karume akaja akawapa, ikiwa usiku ikiwa mchana waifanye. Jambo la kwanza kabisa kabisa kabisa kabisa akawaambia mtizameni Hanga. Akawaambia “mtizameni mtu huyu. Huyu mtu mbaya sana. Mbaya sana. Mtizameni sana mtu huyu.” Wakamwambia “basi nyamaza.” Hakujulikana kapelekwa wapi. Wao wanapeleka ripoti, “bwana kazi yako tumeshamaliza hii.” Kule wale viongozi wabaya wabaya wale wanasema “Mzee Karume anauwa.” Sasa na kwa kujuwa na mwenyewe ile wanavokwenda kula masaa wale watatu

Page 166: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa134

hawabaguani: Abdalla Kassim Hanga, Abdul Aziz Twala, na Saleh Saadalla. Na Othman Sharifu. Ramadhani Haji anamwambia “watu hawa watizame sana.” Jibu “nyota yangu, uso wangu, maelekezo yangu weye, weye pamoja na [Saidi] Idi Bavuai. Nilindeni.” Wewe utakuwa sehemu ya jeshi, Bavuai atakuwa sehemu ya usalama, akisaidiana na Ibrahim Makungu. Kawaambia “hiyo kazi yenu nyie. Kama kuniua nyie, kama kunilinda nyie.” Wote hao wacha kidogo pembeni lakini Idi Bavuai yuko mbele. Halafu baadae akaitwa “Sancho,” Hafidh Selemani. Yeye huyu ndo akimwambia “Mzee wewe, tizama bwana weye, usiweke watu wabaya wako matakoni mwako. Wacha tukulinde. Usitwambie sisi wapumbavu. Hata!” Ndo akapewa jina hilo “hili Sancho hili.” Kitu kibaya chochote, haraka wanakwenda kumuambia Mzee na yeye anawaambia “nakuwachieni wenyewe.” Jibu lake “nakuwachieni wenyewe.” Basi wale wanatimiza. “Sancho” kuwa karibu na Mzee Karume, “Sancho” ni mtu mkweli. “Sancho” ni mtu shujaa! “Sancho” ni mtu asieogopa mtu. Hata kama mrefu kama mbuyu, midam anataka kuzungumza kitu cha halali anamzungumza. Hamuwekei mtu kinyongo. Anamwambia hapo masuala yake alonayo, akimaliza hapo basi. Hamuwekei kitu hapa (moyoni). Sasa Karume kile kitu alikuwa ndo ugonjwa wake. Hiyo ndo sifa alokuwa nayo “Sancho” na Karume kuwa jirani yake. “Sancho” akizungumza kitu, Karume anakaa nacho siku tatu, ya nne anamwita. “Umefikiri siku ngapi kitu hiki?” “Ah, kimentokezea tu kwa vile nataka mawazo.” “Haya tukaye tufanye uta­fiti mimi na weye, au tumdokezee mtu atusaidie mawazo.” Anamuuliza. Madokozi yake anakwenda kwa Ramadhani Haji, au anakwenda kwa Saidi Idi Bavuai, au kwa Saidi Washoto. Kutafuta mawazo. “Sancho” mchango wake wa mapinduzi, yule alikuwa ni mwanaharakati mkubwa katika sehemu ya mapinduzi. Ni mwanaharakati mkubwa kama tulivorudi kwa yule,Tete. Anakaba kitu. Hakitoki nje. Kwa vile mchango ule wa mapinduzi, ikizungumzwa ndani ya baraza lake yule Mzee Karume, yule mmezaji sana siri ile. Haitoki. Pia alikuwa dereva mzuri sana wa Afro­Shirazi. Halafu Ibrahim Makungu. Kawekwa na Karume awe mkubwa wa usalama, Unguja na Pemba. Unampelekea kitu Ibrahimu, “bwana kuna suala hivi hivi hivi.” Anakuuliza “umeliona weye au umesikia na mtu?” Sasa umpe ukweli. Nimesikia na mtu au nimeliona mwenyewe. Anakwambia “niachie.” Hakuulizi umesikia kwa nani. Aa. Niachie, hiyo kazi yangu mie mwenyewe. Ibrahim Makungu hendi mahala popoote anakwenda bar kwenda kunywa. Nyie mnaweza kumaliza chupa kumikumi yeye chupa moja ile hajaisha. Kumbe kuna mzigo wake anautafuta pale. Kama kweli neno ulilolisema anakwenda mdokolea mtu pale. Anajuwa hicho kitu changu kinakuja. Sasa analipeleka kwa yule mzee la uhakika. Mzee naye yumo kwenye uchunguzi wake. Mzee hakusoma lakini kama tulivosema, kichwa chake kinafanya kazi kweli. Hawezi kumbana mtu kama kile kitu si sahihi. Kwa vile kipenzi chake kwa yule bwana kwa kazi zake. Anazozifanya anazifanya kwa uhakika. Analomwambia ni kweli.

Page 167: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 135

Ibrahimu alikuwa ana mchango mzuri kwenye mapinduzi. Kwa sababu Ibrahimu kwenye mchango wake wa usalama alitafuta vitu vizuri saana ndani ya usalama katika mabaraza yale kwa ajili kwamba kuna kitu kinatakiwa. Sasa yeye yumo ndani ya mabaraza yale. Kutafuta. Hiki kitu kimevuja au hakijavuja. Na kama kimevuja ntakipata wapi. Kama hakikuvuja ntakipata wapi. Na kazi yake kubwa kukaanga samaki na kuuza gongo sasa pale alikuwa anayapata mengi sana. Pale alikuwa anayapata mengi. Basi ilikuwa hiyo. Mchango ule anaoupata pale anautuwa. Sasa kuutuwa kule yule Mzee haufanyii kazi. Kwanza yumo kwenye mapekuzi. Alikuwa na mchango mzuri sana. Saidi Idi Bavuai alikuwa yule mkulima. Yule mpanda bangi. Shambani kwake kulikuwa na bangi tupu. Sasa anamwita “Bavuai e, mbona shambani kwako watu hawafiki kuna nini? Wewe shambani kwako umefuga majibwa tu, majibwa tu.” Kwani majibwa ya Sultani aliyachukuwa yeye ati. Anasema Bavuai “sikiliza Mzee Karume. Mimi bwanaa, mimi mpendaje mzuri sana kwako wewe. Mimi walinzi wangu wauza bangi na mimi napanda bangi. Nyumbani kwangu kote imeenea bangi. Mikarafuu kidogo kuliko bangi. Na ndizi. Kula penye mgomba pana mche wa mbangi. Sasa ukitaka kujuwa ulimwengu ulivo kamatana na watu hao. Usikutane na walevi wa pombe. Walevi wa pombe wanalewa wanaanguka hawajuwi la kusema. Lakini mlevi wa bangi anasema!” Mzee Kaujore kipenzi wa Karume tena wala usimsengenye kwa Mzee Karume! Hata! Mchango wake akikutana naye yeye kazi yake kuuwa. Mzee Kaujore. Akizungumza kitu anamwambia “ah! Sasa kama wale kina fulani ya nini kuwaweka duniani?” Halafu hutowa bunduki lake lile. Akalitizamaa! “Ah, masikini.” Basi palepale humwambia “ushakupiga mshipa wa kutaka kuuwa watu. Bwana usende kuuwa watu majiani huko. Leo wazimu wako uwache.” “Ah, Mzee hapana bwana.” Ala, mara ushasikia kapiga watu msikitini. “Mzee Kaujore keshapiga watu, mleteni mleteni. Wewe Mzee Kaujore si nlikwambia bwana! Unafanya nini? Serikali yako, unakwenda uwa raia kwa nini?” Humuonya yule mpaka anarudi. Mpaka akawa mzuriii! Kawa mzuri mwishoni lakini karibuni pale motomoto ya mapinduzi alikuwa Mzee Kaujore kama hajauwa hajafurahi. Kabisa! Hajafurahi! Washoto alikuwa yeye, hana makuu sana. Washoto ilikuwa kazi yake yeye alikuwa Shekhe. Watu wakizozanazozana wakisema twende kwa Mkuu wa Mkoa kufika pale “mnawazimu. Muozesheni huyu.” Unaozeshwa palepale. Washoto ndo ilikuwa kazi yake. Alikuwa ana maingiliano na watu. Alikuwa habaguwi huyu nani, huyu nani.

Kamati ya Watu Ishirini na Tano

Vitisho vilikuwa vikubwa baada ya mapinduzi kwa sababu wangelivamiwa. Hilo Komred walikuwa wameliweka tayari bwana. Komred alikuwa tayari

Page 168: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa136

kuipinduwa serikali. Sasa ndo utakuta baraza [la mapinduzi] lilikuwa na nguvu. Linozungumzwa harakaharaka anapewa Mzee Karume. Akipewa Mzee Karume anapeleka kule tulikozungumza. Kwa kamati yake ile. Ingelikuwa bila ya mu­ungano Komred angeliichukuwa nchi. Na asikari kutoka Mombasa wangetuvamia pia. Ndo ukaona umuhimu wa kuwa na shirikisho la Afrika ya Mashariki. Kamati ya watu ishirini na tano ikiongozwa na Kanali Tete.11 Humjui. Ali­kuwa Jaluo moja huyo sawasawa na Mzee Anthon Musa. Cheo chao walipewa siku moja katika ukoloni. Alikuwa msasi sana wa nguruwe. Huyo ndo alopewa kambi hiyo. Tete, akiitwa. Huyo ndo alokuwa kiongozi wa kundi hilo la watu ishirini na tano. Suala la mapinduzi Mzee Karume alikuwa akilijuwa lakini kulikuwa na mchezo baina yake yeye na wasomi. Sanaa! Wasomi walikuwa hawamuamini na yeye alikuwa hawaamini. Lilikuwa suala la nani atamzidi kete nani. Hicho ndo kitu chenyewe lakini Karume ndo mwenye mapinduzi khasaa. Kwa sababu shabaha zote zile za kuwafukuza Waengereza anazijuwa Karume. Wale wote wengine fikra hizo walikuwa hawanazo. Zile kaziwaza mwenyewe na kazitenda mwenyewe. Na tumepata njia ya mapinduzi kwa Karume. Sasa kama kuna mtu anasema hakushiriki mapinduzi huyo namkatalia. Moja kwa moja. Karume ndo mshiriki mkuu wa mapinduzi. Ndo mpangaji mkuu wa mapinduzi halisi. Yeye ndo alotupa mlango kuondoka Mgereza. Tusingefanikisha. Hata kidogo. Tusingefanikisha. Hiyo hakika. Ntasema mpaka kesho kutwa. Kulikuwa na kamati ya watu ishirini na tano nje ya Baraza la Mapinduzi. Baraza la Mapinduzi linajuwa kwamba kuna kamati yetu fulani ndo yenye shughuli zake. Wao wakisikia kitu wanapeleka kule. Baraza la Mapinduzi linampelekea Karume. Kuna kitu hivi, hivi, hivi. Yule ndo analijuwa Baraza lake la kulipa kazi. Asikudanganye mtu bwana. Mtu asikudanganye. Hawa wasomi, huyu si msomi, lakini huyu mwenyewe khasa wa mapinduzi. Wale wote wako nje ya Baraza la Mapinduzi. Wote! Kamati hii aliiunda mwenyewe Karume baada ya mapinduzi ilipoanza ile chokochoko.12 Hata lile Baraza la Mapinduzi kamati ile wanaiogopa. Kwa sababu wanajuwa wazi kuwa kamati hii hata sisi wanaweza kutuchukuwa. Kabisa, kabisa. Ilikuwa serious hiyo kamati. Hii ilikuwa siri ya mwenyewe kabisaa! Tena hao watu walikuwa, huyu Tete huyu, hayuko mbali. Saa ishirini na nne wako hivi (pamoja). Mzee Tete kafa. Kafa kazini. Anthony Musa kafa kastaafu kazi. Anthony alikuwemo kwenye kamati ya watu ishirini na tano. Katika wakubwa wakubwa, Tete, Anthony Musa, na Juma Maneno. Mshauri Mkuu “Sancho.” Kwa sababu yule mtu alichaguwa makatili matupu. Mtu kama Sefu Bakari anajuwa tu lakini hayumo. Kwa mambo ya chini kwa chini “Sancho” alikuwa na nguvu kuliko Sefu. “Sancho” ofisi yake ilikuwa kwa “Bwa Mkwe” [Hassan Mandera] katika Kamati hiyo ya watu ishirini na ngapi hiyo. Yeye kucheka kwake anachekea tumboni, lakini mdomo wake kuinua, “he, he, he”, hata. Akifika anakwambieni “tume­

Page 169: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 137

ambiwa kuna kazi, kazi ifanywee! Sasa mnaijuwa wenyewe. Kwaherini.” Ana­ripoti “bwana kazi yako nishatimiza huko, tena wewe tusikilize tu ulimwengu ulivo.” Memba wa Baraza la Mapinduzi wakijuwa “nikifanya kitu fulani hapa hawa watu wakiipata taarifa hii mimi naondoka. Tena kuondoka kwenyewe si kama wanantowa ndani ya baraza. Hata. Naondoka roho yangu! Kwa vile aa. Midam nataka ugari aa. Yamalizikie hapohapo.” Yule Mkenya. Kanali Tete, Mkenya. Lakini siri ya mapinduzi anaijuwa vizuri sana pamoja na huyu Anthony Musa. Tangu mwanzo inakwenda siasa wale wanaitambuwa. Aliletwa na Mgereza hapa. Tete alikuwa pamoja na Lazaro. Halafu anavoitambuwa, huyu mtu, madhubuti moyo wake kuficha siri. Hakuwa mropokwaji. Yeye ukizungumza, anakwambia kesho anakwenda saka nguruwe. Ndo kazi yake. Hujui, hujui, hujui. Utamkuta katika baraza zake, anakuja Miembeni pale, kwa ajili “jumaapili hii tunakwenda saka wapi?” Hujui! Hujui. Bwana, mazungumzo yake yeye na wasasi. Huwezi kumtilia shaka hata mara moja. Anakwambia mahala fulani pana mbwa fulani, na mbwa huyo bwana “heeee! Nikimpata mie huyo raha sana.” Hiyo ndo kazi yake. Wakitaka kufanya fujo kule Baraza la Mapinduzi basi wanaambizana “jamani ee! Lakini mnaijuwa nyie kamati ya Mzee Karume? Pengine wengine wako hapahapa!” Kamati hiyo ikikutana pahala padogo saana. Tena katikati ya mji. Polisi ya Kisima Majongoo unaijuwa? Sasa ile ilikuwa nyumba na nyumba yake [Karume] si ilikuwa pale pale? Sasa pale mazungumzo yao mle, Karume mchezaji bao. Utakuta hapa pana bao, hapa pana karata, hapa pana nini, hapa pana keram. Mle ndani mle. Kumbe wana yao wanakula. Hawamshitui mtu. Akitoka pale “je, unaona! Nimeshakufunga leo. Utafanya nini. Huna pesa wewe. Wacha nikupe pesa ukatumie kwa sababu nimekufunga sana.” “Wewe ngoja, tutaonana kesho. Mzee wewe leo unakujanifunga namna hii? Kesho tutaonana.” “Mawee! Umekwisha we! Kamata, katumie!” Yule bwana, sisi, au nikisema, mimi, ningekuwa nimetimiza miaka ishirini mpaka ishirini na tano na yule bwana, mimi nisingelifanya kazi ya mtu yoyote. Mimi namkumbuka mzee Karume, kipenzi wa watu. Hukaa nikainama hasa, kwamba, Karume ni kipenzi wa watu. Karume hakusema huyu mwanangu, huyu mjukuu wangu, huyu fulani. Aa! Karume alipenda msema kweli. Mtu yoyote anozungumza na yeye anozungumza ukweli yeye anamtambuwa, basi yule anampenda Karume. Karume hakutaka wewe ukae kitako ukambughudhi mtu au ukamsengenya mtu. Hata. Ukimsengenya mtu kesho atakuweka na yule “bwana we hebu nambie yale maneno ulosema jana. Huyo hapo. Sema yale ulosema jana.” Utaona haya. Husemi. Hivo ndo alivokuwa yule kiumbe. Anatoka hapaa, anakwenda Dar es Salaam anakwenda cheza bao na Mzee Nyerere. Sisi tunasema wanacheza bao kumbe kule wana lao wanatafuna. Akija huku humsikii. Mara anakwambia “natoka Dar es Salaam. Si bora tukaungana? Sisi wadogo hapa, watu hawa wazaliwa saa ingine ni watu wabaya. Watakuja

Page 170: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa138

kutugeuka hawa. Bora tuungane na serikali kubwa.” Akituzungumza sie. Kwa kukuogopa hapa [Zanzibar]. Aliwajuwa hawa watu eti bwana we! (anasema mbio mbio). Alijuwa. Hawa bwana, wabaya!13

Ubaya wake watageuza watu kuwa wanapendana binafsi na yeye ubinafsi alikuwa hataki. Watu wote walokuwa Zanzibar, Mnyamwezi wake, Mmakonde wake, wote walio hapa ni wake, midam wanazungumza kitu sawa. Sasa watakuja watu wabaguzi wa watu itakuwa si nchi tena. Tutaharibikiwa. Na itakuwa mapinduzi, mara tatu, mara nne. Itakuwa mara fulani, mara fulani. Bora nijitie hapa [Tanganyika]. Kakubaliana na watu hawa nnokwambia ni jirani zake. Fulani, fulani, jamaa mnaonaje tukafanya hivi? “Ah! Hivyo ndivyo.”14

Sasa wale mabotea wanotaka kufanya uharibifu hawajui washike wapi. Akiuliza mtu hapa “jamani, khasa serikali iko wapi? Atakwambia serikali iko Tanzania. Sisi hapa tawi tu hapa. Sasa wewe unayo nguvu ya kuingiliana na kule? Huwezi.” Wakaingia hao akina Makomredi kutaka ubabaifu. Karume akenda. Fulani unajuwa anafanya hivi anafanya hivi. “Ngojea, ngojea. Hapo hapo. Ngoja hapo hapo.” “Fulani we, njoo! Naona nyinyi nafasi zenu hapa kwa serikali sasa hivi ilivosimama, nafasi zenu cheo kimoja kina watu kumi, ishirini, thalathini. Hakuna anaojifaraguwa.” Siasa ya Nyerere hiyo. Tena kafurahi mwenyewe kapigwa transfer [uhamisho]! Kumbe jungu lishapita pale. Anakuja tambuwa baadae! Yuko mbali na Zanzibar, hana base [jukwaa la wafuasi]. Sina hivi sina hivi na huko nliko nna cheo lakini nafatwa. Haya, mkuu wa jeshi Tanzania Bara! “Bwana hapa vyeo vote, kula cheo kina watu kumi, kumi na tano, bara huko hakuna nafasi?” “Ah, nafasi ziko. Nani nimchukuwe?” Kwanza akaanza kuchukuliwa Yusuf Himidi akapelekwa Tabora. Kamati ya watu isihirini na tano ilikuwepo na ilikuwa na nguvu ile kwa mwenyewe, hayati Karume. Kafa yeye na ile imekufa. Kwa sababu ya yeye ilikuwa na mtetezi. Huna hata kitu kimoja cha kwenda kumgusa katika kamati yake ile. Kafa yeye hamnahamna, na kiongozi wa kamati, Tete, kafa. Na msaidizi kafa. Na wengine kwenye Baraza la Mapinduzi. Wale wote wamekufa mfululizo tu. Anakufa huyu, anakufa huyu, anakufa huyu. Likawa halina nguvu na sasa hivi ndo haliko kabisa. Wenyewe wamo humu. Tena ukikaa wanakwambia hasa “masikini, kufa kwa baba Karume, e Mungu! Mungu muweke mahala peponi.” Wanaomba dua hilo. Katuwacha maskini. Maskini. Maskini sie. Leo mie si mtu wa kusema “e bwana, hebu nigaie nauli nende zangu Mbweni hapo bwana. Hebu nigaie nauli nende zangu Mahonda. Sie. Hata! Sie kabisa!”

Mapinduzi Yasiofahamika

Sherehe za mapinduzi, ile kumbukumbu tu lakini mwenye kujuwa hasa hamna. Kwa sababu ingelikuwa wanaijuwa historia ilee, mpaka sasa hivi wanamapinduzi wamo japo kama wamebakia kidogo. Wale wangechukuliwa kama siku ile ya

Page 171: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 139

sherehe za mapinduzi wakawekwa mahala hasa. Wageni wanokuja wakaonyeshwa “jamani hawa ndo wenyewe wanamapinduzi.” Sasa hivi hawajulikani. Hata. Hawajulikani. Kitu kilichodharaulisha historia ya mapinduzi ni ubinafsi! Ubinafsi. Leo mimi mkata maji. Unanchukuwa mimi ndo nnoijuwa historia ya hapa. Leo unaweza ukansogeza hapo nikafanya historia. Nikufanyie historia wewe ulozaliwa hapa? Hatuwezi kukubaliana. Huyu ataniponda mimi ntakuwa sijulikani. Kumbe wewe ndo ungepata masilahi yako. Leo unantupa mie, utaipata wapi siri ya mapinduzi? Utaipata wapi? Alikuja jamaa mmoja kutoka Cuba tena akaja kwangu. Nimezungumza naye historia ilee, kapiga picha na nini. Alikuja kwa marehemu Athumani Bapa. Sasa Bapa hajui, ikawa kaniletea mie. Kwani [Athmani] Bapa hajui ndo akanileta kwako. [Ali Omar] Lumumba hajui ndo akakwita wewe mzee… Na wewe [mwandishi wa kitabu hiki] umenita mie hujui ndo mana ukanita mie. Na mimi siri yangu hasa, sikukupa pale. Sikutowa. Kwa sibabu wewe hutaki faida kwangu. Mimi sitaki faida kwako. Kwa sababu mimi mwenzio nimetembea nao wanamapinduzi. Kina mzee Kaujore, kina nani, huko tumekwenda kula mananasi mwitu. Na mpaka hivi nnavokwambia ukenda kulekule Ikulu kuna picha yetu maalumu ya mapinduzi. Hawataki kuitowa. Ukenda utakuta hasa. Huyu si fulani, mbona hapa kawa kizee na sasa hivi kijana huyu? Kumbe kwa ule uchungu wa kutafuta nchi. Nilikuwa na manywele shetani hafai. Mimi sina ndevu nilikuwa na ndevu. Unajuwa, utakuta watu wa mapinduzi, lao moja, lakini kuna siri. Mimi inaweza kuwa kuna baadhi ya siri sizijuwi na huyu baadhi ya siri hii haijuwi. Lakini sasa basi. Inatokana na nini? Ufuatiliaji. Hilo suala, kwa mimi, sikatai, sikubaliani nalo, kwa sababu. Sikuona, wala sikulisikia, nalisikia hapa kama kuna Wamakonde na makabila mingine kutoka bara yamekwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki katika mapinduzi. Lakini humo mote ninamotembea humo, sijalipata. Inawezekana. Kwa sababu sisi ni watu. Kwa sababu mimi baada ya mapinduzi, nimekaa miaka yangu miwili, mwaka wa tatu mimi nikatoka, niko nje tu. Urusi, China, wapi huko. Sasa matokeo ya huku nyuma, nisije nikayapinga kumbe yapo. Au nisije nikayakubali na mie sijayaona. Kwa sababu nikiyakubali mtu atanambia “hebu nihadithie.” Ntahadithia vipi? Hili suala mimi nnavolisikia Wamanamba, Manamba huchukuliwa huko kwenda kukata mkonge. Hili nasikia huko bara. Kuna Manamba wamechukuliwa mahala fulani, Kisarawe, Shimo la Mungu, nk, wamepelekwa Ngerengere kwa ajili ya kukata mkonge shamba la Mzungu fulani Mjerumani. Kuna Manamba Wanyakyusa wamechukuliwa wapi wamepelekwa Ngerengere kukata mkonge. Hili nnajuwa. Myakyusa alichukuliwa Manamba, Mmakonde alichukuliwa Manamba, lakini sio kwa sehemu za huku Zanzibar. Sehemu za bara kukata mkonge. Katika mashamba ya mkonge hili natambuwa. Wanaweza walikuwa Manamba wametoka kule wamekuja hapa kabla ya

Page 172: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Tisa140

mapinduzi. Lakini tafauti yenyewe ni kwamba nini, kukosa kuelewana kwamba hawa wamekuja hapa tunawaona tu wanalima kwenye nini… Si sawa sawa hapa tumetowa hadithi moja, Baraza la Mapinduzi, kamati ya watu ishirini na nne walikuwa hawawatambuwi. Na kama wanatambuwa, wanajuwa kama kigengi hiki ni cha nini? Ilikuwa hawakielewi. Na hili lilikuwa Baraza la Mapinduzi zima lakini kigengi hichi hawakijuwi. Na hiyo ya Manamba inawezekana au haiwezekani.

Machano, Makame, na Joseph

Hili suala sahihi kwa sababu kuwa sahihi, hivi sasa tunavozungumza kuna watu hawa wa hapa [Zanzibar] na watu wanotoka bara hawaaminiani mpaka kesho kutwa. Hata wakiwa ni Waisilamu. Chimbuko lake liko hivii. Anotoka bara la Afrika anamwambia huyu mtu wa Zanzibar “weye bwana, Mwenye Enzi Mungu kakujaalia tu ule kwenye serikali hii lakini mapinduzi yake huyajuwi. Wewe kama ulikuwa mdogo babako alijificha mvunguni. Suala hili lote waloungana ni wale wenye kulijuwa ndo walofanya kazi hii. Leo ukinambia mimi kwamba mimi ni mbara sijulikani hapa utakosea. Mimi ndo nlokupa mwega kupata serikali wewe hata ukawa mtu. Leo unanibaguwa mimi si mtu tunakubaliana. Kwa sababu wewe unasema mtoto wako waziri au babako waziri. Ndo unalinda hiyo. Mimi sina baba waziri lakini ndani ya mapinduzi mimi ndo mwenyewe. Sasa hilo suala ndo watu unaona mtu wa hapa anojuwa suala hilo anajuwa ‘alaa, huyu anaanza kuleta ubaguzi.’ Sasa utaona atakwambia ‘hapana, hebu tuliwache suala hili. Tuliwache. Tuingie kwenye chama chetu kinasema hivi, kinasema hivi.’ ” Chuki itasimama kwa hawa wenye kupata mavyeo hapa na nini, watawachukia wabara. Hiyo uhakika. Hiyo hakika kwamba haya mambo ya hawahawa wabara na kumbe wamezungumza ukweli, wao ndo wenye kufanya shughuli hizi. Hawa wa hapa watafanya chuki. Kitabu kitaleta chuki lakini hakileti chuki kwa sibabu kuna watoto wetu sisi, wajukuu zetu sisi, wanapata hii historia, sasa kitabu kile wale watasuta Wewe unajuwa nini? Hiki kitu halali. Leo hapa kinazungumza hiki. Hakuna mbara hakuna wa wapi. Wote wameshiriki kwenye shughuli hizi kwa manufaa yetu. Ngao hiyo sasa ndo itakayoweka bayana. Sasa tuungane tufanye shughuli zetu za kuijenga Zanzibar yetu. Hakuna chuki hapa. Atakaefanya organisation kwamba wewe mbara hii inaeleza hivi hivi hivi, atamwambia “Hata. Kwanini? Tazama, hapa, panaeleza hivi. Kabila hili, kabila hili, kabila hili, viongozi hawa na hawa, wa Kiafrika, mbona waliungana kwenye suala hili kwa umoja? Leo kwanini sisi tubaguwane?” Hakileti sura mbaya kitabu. Kinaleta upendo suala hili. Kwa vichwa vetu sisi wazee tunopotea kitaleta upendo kwa watoto zetu wale wasomi, kila atosoma akaona historia ilivo ataona hawa watu walishirikiana hawa. Ushirika wao mmoja, baba, mama, walikuwa pamoja hawa. Kwa vile na sisi hebu

Page 173: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

John Okello—Kuibuka na Kuzama 141

tukamatane kwenye suala hili kwa upendo. Isipokuwa Jazeera, Pemba, watakuja kujiuliza. Hakuna alieshirikishwa hasa baada ya Shamte kusema “hata mkinipa utume sitoshirikiana na nyinyi.” Wangekubali kuwa kitu kimoja Zanzibar kusingelikuwa na mapinduzi. Bwana hili lifanyie mpango litokee! Saana. Safi kabisa. Litokee! Watoto zetu ambao ni Wazanzibari watapata mbegu za kutembea. Watapata nguvu ya kuzungumza. Wanakaa wawili, wanakaa wawili. Pengine wote wako chuoni au skuli, wamesoma wakaona “Ah! Bwana we, kwanini tukaanza kuchukiana mimi na wewe? Wewe babako si huyu hapa? Mimi babangu si huyu hapa? Sasa walipokutana walikuwa wakitafuta nini? Si walitafuta serikali. Serikali si ndo hii? Mbona hawa hawakubaguwana, tubaguwane mimi na wewe? Hata! Tufuate hii bwana. Hii inatuongoza.” Hatima utakuta hii Zanzibar hakuna tena mpasuko.

Page 174: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa KumiMakomred na “Mungu wa Waafrika”

Walikuwa ni wasoshalisti wa mrengo wa kushoto, ndio, lakini kikundi kidogo na kibanzi cha kikundi kidogo. Wangeliweza kutomaza sera za mrengo wa kushoto lakini isingelisababisha Vita Baridi. Kilichofanya wajiambatanishe na Mashariki ni kule kukataa kwa nchi za Magharibi kuitambuwa Zanzibar. —Julius K. Nyerere

Mzee Ramadhani

Kwanza nilimkabili huyu Khamisi Darwish. Nilimwendea nikenda muuliza. Bwana wewe, nataka nkuulize. Hawa Komred kweli nambari moja kunako mapinduzi? Akanambia, bwana Komred si nambari moja. Nikamuuliza kwa nini wasiwe namba moja? Mbona kuna uvumi kuwa hawa ndo nambari moja? Akasema “si kweli.” Ingelikuwa namba moja hii siri ingelivuja, ingekuwa si siri tena hiyo. Isingekuwa siri tena. Mbona hili suala limeshakuwa linavuma kuwa hawa ni nambari moja? Akanambia “sikiliza e bwana wee. Mimi suala nnalokwambia, hawa ni kirukia.” Kirukia? Eeeh. Kirukia vipi? Akasema, ehee! Hawa bwana suala la Jumamosi hawalijuwi. Hawa wanalijuwa suala la Jumapili, watu wameshachukuwa hatamu. Na wao walikuwa na utaratibu wao. Siri yao wenyewe. Sisi hatujuwi, wala kikundi cha Mfalme hakijuwi. Wao walikuwa na siri yao. Na Ali Muhsin na yeye alikuwa na siri yake kwa upande wa Mfalme. Makundi matatu haya yalikuwa hayaelewani. Komred angelikuwa yuko shinani, hii serikali sasa hivi ingelikuwa ya Abrahmani Babu. Komred si mpumbavu. Na unawajuwa kama Makomred ni wasomi, kuliko huku tuliko sie? Sisi tulikuwa mabumbumbu, tumetumia kichwa mchungu, lakini wenzetu walikuwa wakitumia elimu. Komred kirukia. Jumaapili Komred ukimtaja. Sio shina. Hamna. Kamuulize Natepe atakwambia kuhusu jamaa hawa. Ma Afro­Shirazi magogo, wengine walio hai wanajuwa. Suala letu sie, hili bwana, ni akina Mdungi, akina Hanga, pamoja na akina

Page 175: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 143

Twala. Kikundi chao nakumbuka kilikuwa ni watu watano. Mwanzo. Walikaa pamoja, walijadili, hata Mzee Karume, yeye alikuwa hajuwi kwamba watu wanazungumza nini. Mzee Karume kaja kujuwa dakika ya mwisho, kuambiwa, bwana we, sasa inabidi wewe ingia botini, nenda zako nyuma ya Chumbe au Dar es Salaam. Kuna nini? Akaambiwa, aa! Wewe tulizana. Sasa leo ukisema kuwa hawa Komred ni namba moja, si kweli. Kirukia. Bahati nzuri kwa siku ya pili yake, nikamkuta Natepe sasa. Nikasema, ehe! Bwana we, hebu njoo. Kuja pale nkamuuliza. Bwana we, kidogo nna utata. Mimi naona kidogo kama limenitia uchungu. “Haya, uchungu wako nini? Komred wawe nambari moja, sisi tuwe namba mbili?” Akasema “ah! Wewe umechanganyikiwa? Darweshi, hebu ugoro wako unao?” “Nnao.” Mpe kwanza anuse huyu. Nikanusa ugoro. Akanambia, “sasa akili zako zimeshachangamka.” Sasa nnachokueleza, kama utasahau, au umesahau, wao ikiwa leo kama ni namba moja, hivi unafikiria hii serikali ingelikuwa mikononi mwetu? Kwa sababu ingekuwa wao bado sasa hivi ingekuwa wao ni President wa nchi hii. Babu ndo angelikuwa President wa nchi hii. Chupuchupu yetu sisi ingelikuwa si vile kuwa kuwazuwia wale walitaka kutupinduwa sisi. Na uelewe kwamba kwanza walikuwa na mtu, kamandoo wa hali ya juu anaejuwa vita. Sisi hatujuwi. Sisi tulikwenda kule kimabavu tukalivamia tu lile boma. Na yalikuwa kutokana na position [nafasi] tulikuwa naye Kisasi na yeye ni mkuu katika kituo cha polisi. Kila akiulizwa “hata, hapafanyiki kitu chochote. Hata, hapafanyiki kitu chochote.”

Wanawake wa Mapinduzi

Sasa, hii ukisema kuwa wao ndo namba moja, inatoka wapi namba moja hiyo? Na nani aliyekubaliana na masuala haya? Mimi ninachokueleza ukweli hasa ukitaka kujuwa ukweli, hii siri, ni kubwa mno. Na angelikuwa yule Bi Kazija yuhai basi ningelikwambia nyumba hiyo yeye alikuwa kama ni mkunga wa Wamanyema, yaani watu sasa wakiingia kule, wanazungumza…Bi Kazija alikuwa Michenzani hapa. Huyo ungelikwenda ukamuuliza, angelikwambia “mwanangu kaa kitako. Mwanzo, hawa kina Hanga, kina nani, walikuwa wanakutana humu mwangu wanazungumza.” Mimi mwisho nikalishwa kiapo, bibi alinilisha kiapo khasa, tukijakusikia umedumba, hili limevuja, tutajuwa wewe. Yamezugumzwa huko, yamepangwa, hata yalipokuja kutoka mikononi mwao, yakatufika sie, wakaingizwa kina Mfaranyaki, hata wakaingia kina Okello, hili jungu huku limeshamaliza kazi yake. Watu walikuwa wanavaa kanzu kwa sababu yule bibi alikuwa mtu wa tiba tiba, kama mganga. Wakenda kule, watu watasema “si mganga wao Wamanyema huyu?” Mtu anakwenda nampenda mwanamke huyu nipatie dawa, mtu anakuwa hashtukiwi, na mtaa wenyewe wa Ngambo. Kila mmoja ni kivyakevyake tu. Zamani mitaa yenyewe ilikuwa ni ya kuokoteaokotea tu. Sasa, Natepe akanambia,

Page 176: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi144

sahau kitu kama hicho kunambia kuwa hawa ni namba moja. Si kweli. Nakula kiapo mahala popote. Mzee Khamis Darweshi katika kutueleza, bwana, Michenzani kulikua na bibi mmoja pale wa Kimanyema. Huyu bibi tulikuwa tunakutana pale watu fulani. Mchango wake yule mama alikuwa anatupa busara tunampa busara. Lakini siri zetu yule mama alikuwa anazielewa vizuri. Tulikuwa tunazingatia mambo yetu ya mapinduzi. Yule bibi alikuwa anatowa mchango wa hali na mali katika utendaji wa masuala haya. Khasa, lengo wao walimuweka kama security [usalama] wao, kwa sababu ni aliyekuwa majumba makubwa haya alikuwa kwa yule aliyekuwa akijengesha maskuli ya serikali, Humud Said Kharusi. Alikuwa nao karibu kwa sababu nini, yeye kule kafanya kazi muda mrefu sana na wale, sasa jamii ile anaifahamu vizuri sana, na wakati wowote yeye anaweza kwenda kuzungumza nao, akataka chochote anachotaka. Wale wakijuwa huyu ni mzee wetu kwa sababu kwanza huyu mfano kama katulea. Akiuza uji. Sio kilikuwa kikao cha kila siku. Wanaweza wakaa wiki hawajukatana. Lakini kikao hicho Musa Maisara, au Yusuf Himidi, wao wanaambiwa majumbani. Manake waliwachaguwa wale wabarawabara. Wanakwenda pale kama mazungumzo ya kitani, sasa watu walikuwa hawana wasiwasi nao. Kumbe bwana moto wa kumbi unakwenda. Hapa pia palikuwa na mwanamke mmoja wa Kirundi, na wote wawili hawa wameshafariki wako mbele za haki na mumewe, Shauri Moyo, ndiko kulikokuwa na nyumba yao. Msituni. Huko kulikuwa na vikao tafautitafauti kila wakati. Na huyu mwanamke huyu katowa mchango mkubwa katika mapinduzi kuliko Bikazija wa Michenzani. Kwa sababu huyu alikuwa anajuwa nini kinatendeka. Alikuwa anajuwa nini kitatendeka na nini kinatendeka. Halafu utakuja kukuta kwamba masilaha mengi anayaficha huyu mwanamke. Masilaha ambayo kama mapanga yalinunuliwa hapa, na zengine nakumbuka, kama pinde, mishare, zile walikuwa wakitengeneza Wamakonde sehemu za sirisiri tu. Mumewe tukimwita Mohamed “Mrundi.” Alitowa mchango mkubwa na alishiriki Mtoni. Alikuwa na masharubu makubwa sana. Yeye alikuwa ni msimamazi wa publiki. Mkewe alikuwa na hali kubwa sana, tena alikuwa ni mtu alietumikia mambo haya kwa hali na mali, juu ya unyonge wake. Mimi nilikuja kusikitika niliposikia yule bibi na mumewe wamefia Welezo, kwenda kutupwa kama mbwa. Wamekufa hata yule jongoo anathamani. Wamefia Welezo. Mimi roho iliniuma sana. Kwa kukosa kutazamwa. Sisi tu ndo tulokuwa tunakwenda “vipi, vipi…” lakini mtu kama huyo ushujaa alioufanya ni wajibu ashughulikiwe. Watatu alikuwepo Kidongo Chekundu hapo. Ameshafariki pia huyo. Alikuwa Myasa huyu. Lakini katika wote hao watatu hawaingii katika huyu wa Kirundi. Kwa sababu wa Kirundi alikuwa yeye anageuka kama kiroboto. Akikwambia “baba pita ndani, toka mlango wa nyuma, nenda kiunga cha mua hicho, kakate mua” wewe unakwenda kule unasema unakwenda kukata mua, unamkuta mtu kule anakwambia, ukitokeza tu pale, anajuwa huyu ndiye wetu huyu. Na mambo

Page 177: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 145

mengi kuhusu habari ya hii serikali ya kimapinduzi alikuwa anayajuwa vizuri sana. Hili suala la Manamba akilijuwa, viongozi gani gani walivokuwa wakikutana, alikuwa anajuwa, suala zote zote. Hanga alikuwa akijuwana naye sana. Kwa sababu yeye Hanga alikuwa anakwenda kuzungumza na baba yake yule mtoto mwanamke. Akizungumza naye bukheri. Mwisho huyu babake Hanga alikuwa akimwambia yule mtoto mwanamke wewe ungelikuwa mwanamme bwana ungelikuwa kiongozi shujaa mkubwa sana wewe. Lakini lake liko hapa. Hazungumzi kwa baba yake Hanga. Lakini Hanga anamwambia. Mpaka ilibidi ujuwe kitu mpaka kufika Hanga kumuamini yule mama na kumpa maelezo ya hawa Manamba ujuwe kwamba ni mtu siri kubwa sana. Hanga anatoka saa sita za usiku, saa saba za usiku, saa nane za usiku, anakwenda Shauri Moyo anamchukuwa yule bibi anakwenda naye kwake kule kuzungumza na wakubwa wengine. Kutaka kujuwa yale yake yanayotokea upande ule. Wakishamaliza anapelekwa nyumbani yule mtoto mwanamke. Kwa sababu kwa Hanga hawezi kwenda mtoto mwanamme kule. Ndo maana ukaja ukisikia, Hanga anacheza bao hapo Mwembe Shauri, mpaka akina Sefu [Bakari] wakaja kusema “waziri mzima anakwenda kucheza bao na raia bwana, halafu anatoka kwa miguu anapita akitembea.” Watu wakamwambia “kwani si kachaguliwa na watu yule?” Sasa Sefu neno hilo ndo likamkera zaidi, “Mbona huyu ana mapenzi na watu kupita kiasi?” Na hii, pesa, Hanga alikuwa ana mwaga tu. Na alikuwa mcheshi sana. Na ni mtu mkarimu. Sasa Sefu ile ikimchukia. Natepe kahudhuria mara mbili tu kikao cha Bi Kazija, tena mwisho, sio shinani. Shina limeshamaliza, sasa makombo yakuitwa tufanye nini, tunaitwa mmojammoja. Kaitwa Sefu Bakari kwanza, kaitwa yeye Natepe, halafu akaja akaitwa Darweshi, mwishomwisho, akaja kuitwa Kisasi, kwa sababu Kisasi yeye ni mkubwa wa polisi. Bwana hapa pana ushauri. Utatusaidia vipi wewe? Polisi ndo wewe, sasa sisi tunatafuta hii nchi. Sasa wewe utatusaidia nini? Jawabu ya Kisasi, anasema, siri itazuwilika? Mimi naweza kukinga lakini jee, nyinyi wenyewe mtazuwia. Tutazuwia. Mtazuwia? Tutazuwia. Sawa. Yule sentry wa kule ni Afro­Shirazi. Kapanguwapanguwa, kawaweka wale Afro­Shirazi. Siku ile ya Jumamosi. Sefu Bakari nafsi yake hakuingia. Na Natepe pia hakuingia. Akaingia Yusuf Himidi, Mfaranyaki, Washoto, Kaujore, Okello.

Shina Lapinduliwa

Jiko lilipanga mipango yake yakakamilika. Likakabidhi mipango ile. Kwa dakika za mwisho. Baada ya kuwa mipango imeshapangika, watu wameshaingia, wameshachukuwa, wamekuja kumkabidhi Mzee Karume. Sasa utakuja kukuta Mzee Karume jiko lile kaja kulijuwa mwisho. Uwaziri Mkuu akachukuwa Hanga. Kumbe mambo haya yalivokuwa chimbuko liko kwa huku? Utakumbuka kulikuwa na vijana wa Kizaramo walikuwa wakivaa suruali

Page 178: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi146

kipande wakiitwa “Tupendane.” Ile iliwahi kumtia hatiani Mzee Karume. Aliwahi kushtakiwa Mzee Karume na akakanusha pale Victoria Gardens kwenye Baraza la Kutunga Sheria. Akasema wale Tupendane ni watu wahuni. Akanusurika hapo lakini walimkamia vibaya sana Hizbu kwa suala la Tupendane. Kutokana na suala lile ikaonekana kwamba masuala haya Mzee Karume asiambiwe. Akija kuambiwa huyu bwana atakuja sema “aa mimi sifanyi.” Watu walichoka. Kila wakipiga kura watu wananyanganywa. Kila ikipigwa kura, kushinda, watu wanachukuwa. Akaambiwa Mzee Karume. Hatufanikiwi, sasa hivi wewe una mpango gani? “Twendeni hivohivo, kuna siku Mungu atatupa.” Wakaona, huyu keshaogopa. Yalee ya Tupendane. Majungu ya Sefu [Bakari] kwa Hanga. Babu yeye alikuwa kama ni mchochezi tu hivi. Sasa na huyu Sefu alikuwa akili duni. Babu akaona sasa mimi nitafanya vipi hawa niwaparaganye? Akaona hapa sasa nipitishe chokochoko hii. Lakini wa kumtumilia huyu Sefu. Sefu anamwambia Mzee Karume, hawa bwana wanataka kukupinduwa. Akina Hanga na akina Othman Sharifu. Mzee Karume aliwahi kukataa. Asema “hata!” Akamwambia “ehee!” Bwana kama huyajuwi mimi ndo naeyajuwa. Sasa kwa mapenzi aliyokuwa akimpenda Sefu, Mzee Karume, sote tulikuwa tunasangaa. Huyu kampenda kiasi gani, hata inafika budi leo kwamba huyu uwongo umekuwa wenzake anawauza tu, anawauza tu? Kujipendekeza kwa Mzee Karume na kumwambia maneno ya unafikiunafiki na Mzee Karume hata alipokuja kushtuka, na wakati huku watu wameshakufa. Baada ya akina Saidi Idi Bavuai kumpa ule kweli kuwa maneno anokwambia huyu ni ya uwongo. Utapoteza viongozi wangapi wewe? Baadae Babu alitaka akiondoka Mzee Karume cheo akamate Sefu Bakari. Babu anamdanganya. Kwa sababu sifikirii kama kweli Mzee Karume cheo akamate Sefu iwe kikae muda wa wiki moja Babu hajachukuwa. Si kweli. Angemzidi maarifa. Lazma. Abdurahmani Babu lilikuwa Koministi la kupepea. Sio mchezo bwana. Kwanza, moja, lilikuwa somi. Msomi mzuri kwelikweli bwana. Sasa utakuta leo mtu kama Sefu kurubuniwa na Babu ni kitu rahisi. Babu masuala ya Manamba aliyajuwa kwa mshtukio tena. Nakumbuka safari moja aliwahi kusema “hi! Afro­Shirazi wana uchawi yakhe. Mpaka wamefika kuwashirikisha Wamakonde? Kwamba leo mpaka Wamakonde wamekubali kuingia kunako mapinduzi? Ama hawa Afro­Shirazi wachawi hawa.” Akina Ali Sultani hao walikuwa wanazungumza “jamani, na nyie Wamakonde nanyi mnakuja kuipinduwa nchi?” Kubakia masihara tu “mjomba, mjomba!” Kukaa kwa siku tatu yule bwana halafu akapewa Umakamo wa Raisi, jungu la Sefu Bakari. Alimuendea Mzee Karume akamwambia, huyu Waziri Mkuu. Unajuwa Waziri Mkuu ndo serikali? Ukimpa Uwaziri Mkuu huyu na huyu msomi, kuliko wewe, muda tu serikali hii atakuja iweka miguu juu matokeo yake atakuja kuwa Raisi huyu. Wewe umeipata pataje hata ukaja kuniambia hivo?

Page 179: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 147

“Kiundani, kikundi kikubwa hiki, mpaka akina Othman Sharifu wamo, katika kikundi hiki cha Hanga.” Akamwambia hawa wana vikao va siri. Cabinet [baraza] ya akina Sefu, Natepe, Hamid Ameir wa Donge, wakakutana na wakasema mtu akenda akaulizwa masuala haya na Mzee Karume sie tutayaunga mkono. Wasomi wale, sisi hatuna tulichokisoma, tunaambiwa tu ni Baraza la Mapinduzi. Lakini hawa wasomi hawa, huyu bwana huyu, atatuweka miguu juu? Sasa Mzee Karume kila anomuita anampa hadithi zilezile. Twala alisema kama tunataka kupinduwa serikali, tunataka kumpa nani? Wale walipoona Hanga amewachaguwa wasomi kuendesha nchi wale waliona vibaya. Pale ndipo alipoambiwa Mzee Karume, badilisha system haraka sana, muweke makamo wako, usimuweke Waziri Mkuu. Akaja akabadilishwa Hanga akafanywa Makamo wa Raisi. Okello kitu kilichokuwa kikimchukia, kwamba Wamanga, Mzee Thabit Kombo akenda Raha Leo, hakuna adhabu wanayoipata. Anawahifadhi. Ilimkera zaidi, Mmanga wa hapa Koani. Kateketeza watu yule Mmanga, halafu leo kakamatwa yule Mmanga. Baada ya kukamatwa kaletwa Raha Leo, hakuadhibiwa. Sasa Okello ndo akasema “Mmanga yule kauwa watu, Mzee Thabit leo kamtia kwenye chumba cha peke yake? Na hakuna adhabu yoyote.” Kila sisi tukitaka atolewe mle ndani Mzee Thabit anasema “tulieni, tulieni, huko ndani adhabu yake anaipata!” Sasa bwana huyu tumekataa nini anafanya nini. Itabidi mpaka serikali tuipinduwe. Ipinduliwe tena hii! Lakini hapo, walewale askari wake wakaja kusema “huko tunakotaka kwende siko.” Wanamwambia Okello. Kikao kilekile sasa kilibidi kizungumze katika kikao na akina Mfaranyaki. Masuala haya yakamfika Sefu, Sefu yakamfika Mzee Karume. “Mpelekeni Pemba!” Hapo utakuja kukuta, askari wake Okello hawakuwa na imani hiyo. Wakimfikiria, leo huyu Mganda, ametoka Uganda huyu, Mzee Thabit ametoka Makunduchi, sasa, kwa nini leo hawa viongozi wadhalilishwe? Okello alituita ati hapa Miti Ulaya. Ndo walewale askari walitoka wakasema mbona kunataka kuingia umwagaji wa damu wa kipumbavu? Sisi tumesema kama Karume ndio President wa nchi hii, ndo jabari wa nchi hii, na yeye huyu anataka kumuua Mzee Thabit Kombo, huyu Karume atanusurika vipi? Ndo hapo jamaa, kina Sefu, ikabidi sasa Okello apelekwe Pemba. Wewe sasa nenda kwa Wapemba ukawafanyie kazi. Kwa sababu huko nako kuna kina Mkame Ndume. Wanawaka! Kawashughulikie! Kenda Pemba, kawashughulikia kweli. Baada ya kumaliza kuwashughulikia kule, kurudi sasa, anarudi, jamani mimi nnarudi. Panda ndege uje zako. Kuja hapa moja kwa moja, uwanja wa ndege. “Bwana hii ndege ulopanda hii utaipanda hiihii.” Baada ya hapo huku usisogee tena. Kikundi hichi cha Hanga, wote wasomi. Sasa utakuja kukuta hiki kigengi hichi [cha] Hanga, kilimchafuwa roho Mzee Karume, kuona kwamba, huyu katika hili jiko hili hakushiriki! Sisi tuloshiriki, sisi kwanini tubakwe bakwe hivi tuwekwe ovyoovyo. Na hili jambo letu? Hili jiko letu sie. Sasa Karume alipokuja

Page 180: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi148

kuligundua hili jiko linataka kwenda hivyo ndo pale aliposema “wapelekeni Kama.” Likapelekwa Kama. Hukohuko Kama ndo walokopigwa marisasi na kuzikwa huko handaki moja. Liko handaki bwana tena lilichimbwa na jeshi. Huyu alokuwa anakaa Gongoni hapa, Saadalla, kwanini akapiga kelele hapo juu Kiinua Miguu, tena usiku “jamani e, nakwenda kuuliwa wee!” Alitolewa usiku hapo akapelekwa moja kwa moja Kama. Hilo ndo lilosababisha wale jamaa kupoteza maisha yao. Ingelikuwa hakuuliwa Zanzibar ingekwenda kisomi na nakumbuka huenda hata huu muungano pengine usingekuwepo. Mwalimu aliunga mkono, lakini sasa kutokana na Ukoministi wengine waliousoma, madam Mchina hapa aliingia, basi vitu vote hapa vingekwenda kwa Mchina, kwa hivyo linda hii nchi! Lakini hapo tena walipofeli, ikabidi sasa vile walivokuwa wakitaka…kwa sababu Kassim Hanga alikuwa ni Mzaramu yule. Sasa utakuja kuta, jiko lingekuwa lihai, basi Thabit Kombo na Karume wangekwama. Kabisa! Wangelikwenda mfumo wa Afro­Shirazi. Kusingelikuwa na Muungano. Wangelitafuta himaya kutoka nchi za Kisoshalisti kwa ajili ya ulinzi ingelikuwa hii nchi inataka kupinduliwa na Waarabu. Mfalme alipotoka hapa kwenda Uiengereza, mkimbizi, kwanini natawaliwa kwenye kizimbani na nyinyi mpo? George Mooring alimjibu: wewe [Ali Muhsin] na Karume muwe kitu hiki: kimoja. Msiwabaguwe. Hawa wengi kuliko nyie. Wewe ukakataa. Kukataa kwako vita vya Juni nikakwambia, kidogo tu nusra serikali yako iaunguke. Nikaleta jeshi kutoka Kenya. Hatima yake wewe si uliniondosha mimi Zanzibar? Ondoka, nenda zako. Kuondoka kwangu mimi nikafika Kenya nikamkuta balozi mwenzangu. Kitu nilichomwambia. Zanzibar mimi naondoka lakini nchi haipo mbali itapinduliwa. Sijaondoka nikaja kusikia imeshapinduliwa. Sasa leo wewe [Sheikh Ali Muhsin] unakuja kuzungumza masuala kama hayo, tukusaidie nini? Sasa hapo ndo inabidi sisi tukuhifadhi tu sisi hapa. Lakini tena Ali Muhsin yeye ikabidi akaruka na chokochoko. Waingereza ikabidi kule wakamfanyia matatizo, wakaona sasa huyu Ali Muhsin itabidi ende akaishi Dubai au Maskati. Kwa sababu hajatulia. Ilionekana wazi wale wangelifanya chini juu kuipinduwa hii. Kwa sababu mfano mmoja ntakupa. Mmarekani alipoambiwa aondowe mnara wake wa Tunguu, basi ziliwahi kuja hapa manwari mbili kwa uchungu na hasira. Lakini Mrusi alisema hapo ndipo patakuwa maziko yetu, na Mchina akasema tutazikana hapo, tutakitumbuwa maji kisiwa hicho. Lenye nguvu zaidi bwana wewe, huu upande wasio soma huu, ndo wenye wengi, na huyu, huyu Karume huyu, ndo walomtaka wenyewe. Ndo walokuwa wana mtaka wenyewe! Wana Afro­Shirazi wote. Sasa waliosoma kila wanalolizu­ngumza wanabanisha tu wenyewe kwa wenyewe tu huko. Halivuji hilo! Hilo hata mimi ukiniuliza ntakwambia, “Wallahi Laadhim,” undani hasa silijuwi. Kwa sababu ilikuwa siri yao wenyewe kabambe. Wameliweza hili jiko la mwanzo

Page 181: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 149

hili, e vipi hili jiko la pili? Kwa sababu haya yalikuwa wasomi kwa wasomi, hawakuthubutu kulileta uraini. Na wengi walokuwa wakimsapoti Mzee Karume walikuwa hawakusoma. Upande wa huku juu, wasomi wao ndio kweli, walikuwa wengi lakini walikuwa haba. Sasa wakasema hiyo hangaika yote alotuhangaikia, huyu kwanini aondoke, wakae hawa? Haiwezekani! Haya wanasema upande wa uraiani sasa. Huyu ndo alotuhangaikia. Na Sefu sasa, alikuwa upande wa huku, na watu walokuwa hawakusoma, na yeye kwa sababu hakusoma. Katika wana mapinduzi wengi walokuwa wamesoma labda Kisasi peke yake. Ndo aliyekuwa katoka kwao Moshi na cheo chake kaja hapa. Yeye ndiye aliyekuwa kasoma. Lakini waliobakia wote hao, usidanganyike, akina Mfaranyaki hao, akina Kaujore, mbumbunda, akina Saidi Washoto, mbumbunda! Wengi wengi, akina Hamid Ameri hao Kurani. Sasa utakuja kukuta wengi walikuwa hawana elimu. Huku nyuma lilikuwa lao hili, moja. Akina Hanga na Mzee Karume. Kwa sababu Afro­Shirazi ndio iliowasukuma wale masomo ya nje. Imewapeleka. Kisomo. Sasa hawakuweza kuja kukanusha ghafla tu wakati yule ndo alowapeleka kule. Hanga, nenda nje. Mdungi, nenda nje. Twala, nenda nje. Wote walipelekwa na Afro­Shirazi kwenda kusoma ili tukija kupata utawala hapa tusije tukayumba. Walisoma, walipasi, wamerudi. Sasa kuja kurudi matokeo yake, kukamata serikali, Othman Sharifu alipelekwa Marekani. Hukohuko na yeye alifanya majungu yake. Wasomi walitaka lile shina lisiwe halikusoma. Lile shina liwe na mtu kasoma. Sio mtu kama Mzee Karume. Majungu ya utawala sasa. Msomi na asiosoma pana tafauti hapo. Sasa hapo wakaona Karume akitowa command [amri] yake ndo moja kwa moja. “Tunakwenda nao tu lakini mbona mambo yanakwenda pindukapinduka hivi?” “Hakusoma huyo! Tumchukulie hivohivo.” “Tumchukulie vipi?” Sasa tutamchukuliaje hivo? Lazima pafanywe mabadiliko hapa. Sasa pakaingia kidudu sasa, kikawa kinachokowa. Kikachokowa, kikachokowa, kikachokowa. Sefu yeye ina maana anarudi upande wa Mzee Karume.1 Kwa kwamba ikiwa hutowahishimu wenye elimu matatizo. Jamii inakuwa haiwezi kwenda mbele. Na wenye elimu wakiwadharau walokuwa hawajasoma, sasa wataiendeleza vipi jamii? Mzee Karume ndo pale alipotowa elimu bure. Elimu bure, hakuna malipo. Akafunguwa maskuli. Ikawa watoto wanakwenda kusoma. Unajuwa, usifikirie kwamba hawa wasomi, jamii isiosoma, raia, wao ndio wakiwachukia. Hata. Wangeliwaelimisha, wasiwangeliwachukia. Ila tu hii ngazi ya mwanzo. Hii ngazi ya mwanzo itakaa hapa kwa muda gani na kishasema madam mimi nimekaa katika kiti hiki hakuna labda kusema mpaka mbono huyu, mpaka afe. Wewe unajuwa atakufa lini? Una taarifa zake unajuwa siku gani atakufa? Aa! Sasa? Lakufanywa lazima upatikane utaratibu wa mageuzi. Hatamu tukamate sie. Wale jamaa ndo walipojiponza hapo. Ingelikuwa hawakupanga njama hiyo wangelikuweko mpaka sasa.

Page 182: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi150

Baada ya Mzee Karume, tabaka ile ingelikuwa imeendelea. Mpaka Othman Sharifu na yeye angelikamata hatamu. Walifanya pupa. Uroho wa madaraka. Walifanya uroho. Uroho ndo uliosababisha kuwaponza. Unaona sasa. Sefu na yeye, majungu yake yote alioyafanya, matokeo yake, kufa Mzee Karume, na yeye aliangukia kilio “utawala wangu huu!” Sasa tutakuonaje weye? Unalilia utawala wako. “Utawala wako vipi? Hebu tufahamishe” aliulizwa. Kuja Aboud Jumbe akalitawanya lile Baraza la Mapinduzi. Jumbe alimwambia Mzee Thabit “mimi Baraza nalitawanya hili.” Midomomidomo haya nje. Sefu akampeleka mikoani huko. Suala hili lilipangwa na Mwalimu kule. Mlete mkuu wa mkoa. Fulani? Mlete mkuu wa wilaya huku. Lengo lake [Sefu] lilikuwa hata Jumbe atakapokufa atapata utawala. Nafasi ile alikuwa anaitaka hasa. Kila alipokuwa anawaendea akina Natepe, Natepe akisema “mmh, usitafute balaa. Cheo si unacho, si unakwenda unapotaka. Uhuru si unao bwana. Madaraka hayo unalindwa na askari. Mengine yako peke yako hayo.” Wasingelimuunga mkono.

Zanzibar Mtihani—Mzee Joseph Bhalo

Mzee Joseph Bhalo ni mmoja kati ya viongozi wakubwa wa Kimakonde ambao walishiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Wakati mashirikiano baina ya askari wa polisi na kikundi cha akina Mzee Aboud Mmasai hayajulikani, Mzee Joseph alimiminiwa sifa ya kuwa yeye ndiye aliyeivunja ghala ya silaha ya Ziwani. Wapinduzi nnaowakumbuka ni Joseph Nchelenga, alikuwepo Chefu Mawile, Joni ( John) Kawajire, Tajiri Fundi, hao ndio watu nnaowakumbuka. Na hapo yuko Koani alikuwepo Kakarange. Yule Mzaramu. Hao ndio watu nnaowakumbuka. Viongozi walikuwa John Okello, Muhammed Kaujore. Hao viongozi wali­kuwepo. Hao ndo walioshika sukani pamoja na sie watu kumi. Sasa Karume alikuwa hajuwi kama nilivokueleza. Ukisikia kama Karume alikuwa anajuwa, uongo. Atakupoteza bure. Unasikia bwana. Utapata uongo. Karume hakujuwa! Tumefanya sisi. Hakuambiwa kwa sababu yeye ni mkubwa, ni kiongozi, kiongozi wa nchi. Ukenda kumwambia itakuwa “lo! usifanye hivo. Usifanye! Usithubutu kufanya kama hivo.” Tulikuwa na wasiwasi naye atamkatazeni. Bora tusiseme tumuache hivohivo. Alikwenda kuchukuliwa. Akapelekwa Raha Leo. Pale ndo akakabidhiwa yeye [Karume] serikali. Sasa wewe kazi yako. Manamba hakuna. Karume hakuna. Mmakonde kuwa ni mwanamapinduzi mpaka leo hajulikani! Hajulikani kabisaa! Hayumoo! Nchi amaeshaichukuwa mwenyewe [Mzanzibari] ndo mwanamapinduzi. Yule hayumoo! Hayumoo kabisa! Mwenyewe ndo mwana­mapinduzi. Uwongo mwingi na yeye [Mzanzibari] hajuwi. Ameshapata sasa hivi, anasema uongo, uongo, uongo. Yeye yuko ofisini sasa. Sasa yeye hajuwi

Page 183: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 151

alofanya kazi hii. Hajuwi ni nani. Binaadamu tulivyo, tulivyo. Leo ukimwambia mwanamapinduzi Mmakonde alishiriki atakwambia “muongo huyo! Muongo huyo!” Hakushiriki chochote. Niulize mimi, yule hajuwi chochote! Unaona kazi sasa hiyo. Hajajulikana mpaka leo. Wanawatupia Wamakonde uongo mtupu. Mmakonde gani alokaa kwenye kiti? Hiyo ni chuki. Hiyo ni fitna isiokuwa na maana yoyote. Mambo yamepita basi. Mambo ya kifitina. Siku ya mapinduzi hasa ndo siku ya kumuogopa mtu. Si leo. Hayo yanayozungumwa leo yanazungumzwa kwa shibe. Sisi soote tumeuwa! Unajuwa, sote tumeuwa. Si fulani ndo alouwa. Hapana. Wote tumeuwa kwa sababu sote tulikuwa wanamapinduzi. Kwenda kwenye mapinduzi tulikwenda kwa pamoja, tukafanya kazi kwa pamoja, kwa kugombowa nchi yetu, bas! Wale walokuwa wamekalia mapinduzi, kuweka mapinduzi, kumbe sivyo! Walofanya mapinduzi wengine, anavosema yeye vingine. Mapinduzi, mapinduzi, mapinduzi, siku ileile iliopatikana serikali, siku ileile, wakati huohuo, yakawa yamekwisha! Sasa yale ya uundaji serikali, yale ni mapambo yale. Haya yalofanyika nje ndo mapinduzi. Itakapoandikwa [historia ya mapinduzi] uongo utajulikana hapohapo. Ukweli utajulikana hapohapo. Walofanya mapinduzi khasa pesa hawajapata. Wanatumia wale walokuwa hawakufanya kazi yoyote hapa. Wao ndo wenye kula matunda yale. Wale walofanya mapinduzi hakuna hata shilingi moja walopata. Upo lakini? Wale mpaka leo hata shilingi moja hawajapata. Hata kuhisabia kuwa mwanamapinduzi. Hakuna! Hakuna! Tokea ile siku ya vita imekwisha, bas! Hili neno nakwambia. Ukiwa utaandika [kitabu], itakuwa “eee! Kumbe imekwenda hivi. Huyu bwana ameandika vipi? Mbona mapinduzi namna kadhaa kadhaa kadhaa.” Itazuwa mjadala kwa watu. Eeeh! Mimi nakwambiaje? Unataka khasa historia ya mapinduzi? Hiyo mnayo­danganywa mnoipata ofisini mtu ameshapata kazi amekuwa mwanamapinduzi. Watu wanadanganywa. Hapa, mapinduzi halisi walikuwa watu wachache. Watu wachache hao wa kutoka bara. Si watu wa hapa. Watu wa hapa walifichwa. Kwa sababu ya kuwa walifichwa. Sijui namna gani. Mwenyewe Karume, msiwaambie watu wa hapa mkiwaambia watu wa hapa watahalibu. Mwenyewe Karume anasema.2 Sasa kweli imefanyika, Wandekereko, Wanyamwezi, Wamakonde, wakafanya kazi hiyo. Tulikwenda wakaanza kuwasambaza watu, msiwaambie watu. Siri! Watu wahapa. Mwenyewe Karume. Suala hili ni hatari ya nchi. Wasiambiwe watu wa hapa. Hapa tulipo tuwaambiwe watu wa bara. Tuwaambie watu wa bara watupu! John Okello anasema. Wandengereko, Wanyamwezi na Wamakonde na Warundi, Waruguru. Ilikuwa na siri hiyo. Kenya (Ndagaa) alikuwa askari Unguja, Yangeyange, Mruguru (Koani) alikuwa askari Dar es salaam, Okello wamemfata Bhalo. Tunataka mtu anaojuwa bunduki. Mmakonde alopelekwa Nairobi kutibiwa. Alikuwepo Sidimba, wengi walikuweko Wamakonde lakini hata mmoja hakutiwa katika baraza au serikalini.

Page 184: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi152

Mfaranyaki alitiwa kwa jeuri yake mwenyewe. Si kwa kumchaguwa wao. Huyu atatoboa siri bora tumtie. Bavuai alikuwa anaaminiwa kwa ushiriki wa ulevi na uvutaji bangi. Huyu angeweza kutuongoza. Akawasahau wale walomtia kwenye mapinduzi. Kule anatutizama yeye kwa moyo wake wa kutupenda sie. Manake Karume alikuwa peke yake. Si mtu wa bara! Karume mtu wa bara ati. Watu wa hapa walikuwa hawamuungi mkono yule. [Sasa] tuongoze sisi wenyewe [Wazanzibari] si wageni. Washafanya kazi imekwisha. Mtu aloshiriki hawamfuati. Wakikubali kama sisi tumeshiriki tutaonekana wakubwa. Tutaonekana watu. Madam sisi tumefanya kazi ime­patikana serikali, basi. Ndizi ile anaweza kuidai mtu akisema kama ardhi yake. Sisi tunatizama tu. Wanaleta maneno ya juujuu ya uwongouwongo. Hawajuwi chochote. Chochote hawajuwi. Wale hawakubali. Kwasababu yenyewe: siri hii wamepata wapi watu hawa? Manake washenzi hawa wameipata wapi? Tunaitwa washenzi sie. Tukiwaeleza ukweli watatuita washenzi. Hawakubali. Wanakubali uwongo. Kuniweka mimi mbele Mwanansumbiji hawataki. Kumfata Mwanansumbiji hawataki. Kitu hicho hawataki kabisaa! Lakini mambo kama haya sisi tumewachia. Tumepeleka barua yetu kwa Raisi na majina. Maraisi wote walokuja hapa. Hawakujibu. Karume angelikuweko saa hizi angelinisikiliza lakini alikuwa peke yake. Majina tumepeleka kule. Mpaka leo, kimyaa! Kesho anatoka Uraisi yule. Si basi. Imeshakwisha! Tutamwendea mwengine. Bure! Bas! Hapa alioshiriki, Raisi [Ali] Hassan Mwinyi. Basi huyo haijambo kidogo. Ilikuwa haijambo kidogo lakini na yeye akaambiwa usiwape kichwa hao. Ikesha! Nasie, tumechoka hasa kwenda [Ikulu] kila wakati. Tukafanye nini? Tumewaachia. Tunawatizama macho. Alikuweko Dadi, mtu wa hapa, kwao Mkokotoni. Alikuwa anashiriki yote. Lakini akisema yeye peke yake! Haifai kitu! Mwisho wamemwambia “wewe unatetea watu kuliko wewe mwenyewe? Watu kwao bara? Kwanini?” Ndo wanavosema. Hayaa! Wataona aibu kubwa! Kutoa siri yetu kutangazwa wataona aibu kubwa. Hatujapata mtu wa kulifanya suala kama hilo. Na mambo yatakwenda. Muda ni mrefu lakini inaweza kupasuliwa. Kumbe watu wamefichwa. Walofanya kitendo hichi kumbe hawakufanikiwa. Itakuwa aibu kwao. Kubwa! Mpaka leo serikali yetu hii ina dhambi ilofanya. Wamefanya tendo, halafu wameficha, halafu anaonekana yeye ni mtu. Siyo. Dhambi ya kuficha. Ndo mambo mengine hayaongoki. Uongozi hauongoki. Mambo hayendi. Alofanya kitendo wewe umemficha. Alokuwa hajafanya kitendo amekuwa mtu. Si dhambi hiyo? Suala kama hilo tungelimpata mtu akalitowa nje. Wasishtuke kwanini na wao wanasema uwongo? Wasishtuke kwanini? Kumbe wamegunduwa wapi? Sasa mimi ntakuwa vipi? Mimi muongo! Hana uso. Uongo! Sasa kimyakimya mambo

Page 185: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Makomred na “Mungu wa Waafrika” 153

yenu tudanganyane hapahapa. Si nje. Nje watu wanajuwa ukweli wa mambo. Tudanganyane hapahapa Unguja. Mnavofanya Unguja si halali. Watu walofanya hawakupewa kitu. Sisi tutaendelea hivihivi tutakataa. Basi Mungu yuko. Ukitaka ukweli wa mambo ya mapinduzi watu wa hapa hawajuwi kitu. Watu wanojuwa watu wa njee! Watu wa nje wale wametupwa kwa sababu si pao hapa. Wako watu wanasema petu hapa! Basi hao ndo wanoharibu wanosema “petu hapa!” Serikali ya pili [ya Tanganyika] inasema ukweli wakati mwengine. Mna dhambi. Mmekosa radhi nyie. Uongo ndo mnootegemea. Si halali. Limegundulikana, aibu itakuwepo. Halali gani itakuwa kwao wao? Itabidi waweke uhalali mpya. Wengine watakuwa nje. Haitokuwa salama. Mwanya mkubwa utakuwa kwa wanaodai serikali. Upinzani utakuwa umepata mwanya mkubwa! Kumbe wanatudanganya, uongo. Si halali. Sisi hatufanyi hivo. Unaona kazi hio? Zanzibar itapata faida gani kwa mwanya huo? Serikali itajuwa mbele baadae kipi cha kufanya. Hawa watafanya mbele hawa. Si mepesi. Makubwa! Mwizi umejificha, ukakamatwa, atakuona weye mbaya! Mwizi atakuona weye mbaya! Yeye anataka afiche siri yake mpaka afe. Ndo anavofikiria yeye afanye. Ukimgunduwa atakuona wewe mbaya. Serikali itakuona wewe mbaya! Miaka 45 haiondoki siri kama hii? Si halali. Kwa watu waliosaidia tungekuwa tunadanganywadanganywa. Leo hu­danganywi chochote. Unatupwa kama…Sisi tulofanya kile [kitendo cha ma­pinduzi] tunaombewa mabaya. Tulofanya kitendo roho iuliwe halafu leo mtu anakuficha na anakuona wewe si kitu. Si ubaya huo? Halali hiyo? Nakupa Nchumbiji. Siri ya Nchumbiji watu wanatizama mbele. Hapa hawaoni mbele. Uongo mwiingii! Mambo mabaya ya kiserikali hakuna. Yamekatika. Tuondoshe uchafu huu kwanza kwa kungudulikana kitu hicho [mapinduzi]. Watajijuwa. Lazma watajijuwa. Kwenye serikali kuu itakuwa ubaya, wataamuwa wao. Tumefanya hivi, tumefanya hivi…Si uzuri, si halali. Tufanye kitu, watu watawale, wawe radhi. Itakuwa hivo. Tukipigana wewe na mie atokee mtu atuamue. Ikitoka nje itaamuliwa. Serikali hii inavuma mapinduzi lakini sivo! Serikali inajuwa. Suala hili linajulikana wazi. Walofanya wengine walokaa watu wengine. Serikali inajuwa. Aibu. Tufanye kitu sasa. Itaamuliwa wakati huo. Lazima! Madam liko nje litafanyiwa kazi. Pana aibu gani tena. Tutaweza kwenda mbele.

Page 186: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na MojaKatibu wa Midani ya Mapinduzi

Kila mzee mtu mzima anayekufa Afrika ni sawa na maktaba nzima kuwaka moto. —Amadou Hampate Ba

Mzee Ahmed Othman Aboud, maarufu Mzee Aboud “Mmasai” kutokana na marehemu mama yake mzazi alitokana na kabila la Kimasai. Mzee Aboud alijiunga na Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) tarehe 1 July 1956. Pia alikuwa memba wa The Tanganyika Local Government Workers Union, Tanganyika African Traders Union, na National Union of Tanganyika Worker’s (NUTA). Mzee Aboud alikuwa Katibu wa Midani ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na katika siku zake za mwisho alikuwa ni memba wa Chama cha Wananchi (CUF). Katika picha ya “Wanamapinduzi wa Zanzibar II” kwenye kitabu cha Anthony Clayton “The Zanzibar Revolution and Its Aftermath,” Mzee Aboud yuko baina ya Abdalla Kassim Hanga na Abeid Karume na kwa vile mwandishi alishindwa kumtabuwa akamuandika kuwa ni “unknown”—“yaani hajulikani”. Kwenye picha hiyo Mzee Aboud anaonekana ameushika mkono wake wa kulia.

Mzee Aboud “Mmasai”

Tuanze pale baada ya uchaguzi wa Julai 1963, watu walivokuwa kama wamepata kiharusi. Nilivokuta mimi. Mimi binafsi nilikuwa mtumishi wa serikali bara, katika Baraza la Mji, Dar es Salaam katika 1950s. Ikaundwa TANU katika 1957. Mimi nilikuwa mwanachama wa TANU. Baada ya harakati za kisiasa zilokuwepo kule Tanganyika na zilokuwepo hapa Zanzibar 31 Disemba 1959 nikaacha kazi kule Dar es Salaam nikaja Unguja 1960 Januari mimi nipo Unguja. Nimekaa nikaangalia hali ya mambo nikajiunga na Afro­Shirazi Mei 27, 1960 na tawi langu lilikuwa Mwembetanga. Baada ya shughuli za kisiasa 1961 zikatokea fujo Unguja. Ilipotokea riot ya Unguja kwa hakika mimi nilikuwa siijui.

Page 187: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 155

Nilikuwa wakala katika kituo cha polisi cha Mwera, ilokuwa skuli ya Mwera na hili ni jimbo la Fuoni. Mgombea wa Afro­Shirazi alikuwa Aboud Jumbe, mgombea wa Hizbu alikuwa Maalim Hilali. Baada ya uchaguzi kufungwa, saa imekwisha, kituo kufungwa tukapata habari kuna ugomvi, fujo. Hapo tukaja sisi kuchukuliwa na gari ya polisi, ikiwa chini ya usimamizi wa Major Bott, tukapelekwa Fuoni kwenye kituo cha kuhisabia kura. Mimi nikiwa wakala katika kituo cha kupigia kura cha Mwera, halafu nikawa wakala wa kuhisabu kura katika kituo cha Fuoni. Baada ya uchaguzi kwisha, mahesabu yale ya uchaguzi kumalizika, ikawa ni usiku, tukapakiwa ndani ya gari ileile, chini ya Major Bott, mpaka Kijangwani ilipokuwa ni ofisi ya Afro­Shirazi kwa mambo ya uchaguzi. Tukatuliwa pale, akaripoti Bott kwa ofisi ile kwa watu wa jimbo la Fuoni wa Afro­Shirazi ndo hawa na watu wa Hizbu sijui kenda nao wapi, lakini sote tulipakiwa kwenye gari moja chini ya ulinzi wa polisi kwa usalama wetu. Tukaongoza, mimi nikaja zangu nyumbani nikaletwa na polisi vilevile mpaka kwangu, basi umekwisha uchaguzi ule na ghasia zile, watu wakatiwa ndani, wakafungwa, wengine wakahukumiwa miaka mingimingi, na kundi la watu likakamatwa likajaa jela tele, wakapelekwa kisiwani wengine. Kwa bahati nzuri au mbaya, lakini kwa maisha ya kisiasa kila mtu alokuwa kidogo ana muamko wa kisiasa anaweza kuona kuwa ilikuwa bahati nzuri kukamatwa kwangu nikatiwa jela. Nikakaa rumande, nikashtakiwa mahakamani kiasi ya miezi sita kama hivi, siwezi kusema miezi sita kamili. Sikuweka rikodi hiyo. Niliposhtakiwa, nilishtakiwa na mtu mmoja nilikuwa simjui ndo siku hiyo nilimjuwa, watu wawili, mimi nilikuwa mshtakiwa nambari moja, yule mwenzangu ni mshtakiwa nambari mbili. Na mashtaka yetu kwamba tumechochea, nimechochea, na nimeongoza fujo, tangu wakati wa asubuhi, kuanzia saa nne ya asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Sasa tuzungumze hiyo kesi. Sote tulikuwa na shahada za memba wa kuhisabu kura au wa kituo cha kupigia kura, ASP na Hizbu. Na kwa bahati nzuri kituo cha kupigia kura chetu ofisa wake alikuwa Maalim Ali Said Al Kharusi na mgombea alikuwa Maalim Hilali kwa ZNP. Walikuwepo polisi kulinda usalama na polisi alokuwepo pale alikuwa Inspekta Aboud Saidi na moja wa Konstebul alokuwepo nnaemkumbuka alikuwa namba PC 47. Hii namba mpaka ntakufa naikumbuka. Kwa sababu hawa wote, wagombea wa ZNP na maofisa wa polisi walikuwa ni mashahidi wangu ndani ya korti kwamba mimi sijakuwemo katika fujo za Juni na wengine polisi akiwa mmoja ni Aboud Saidi, huyu ndo alokuwa na dhamana ya eneo lile wakati ule. Na huyu askari nilokuwa naye ubavuni PC 47, na Major Bott aliyekuja kutuchukuwa, naye nilimtia katika ushahidi huo. Ijapokuwa wote niliowatia hawakuitwa mbele ya mahkama, mahkama ilitosheka kama mimi sijakuwa ndani ya fujo, nitolewe, sina makosa. Mashahidi walikubali baada ya kutowa zile saini zao nje, kama Maalim Ali Said Al Kharusi yeye alikuwa ndo ofisa msimamizi na zote saini zake, na Maalim Hilal alikubali. Hawajakataa

Page 188: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja156

kama hawanijuwi, wananijuwa kutokea utoto wangu, nilipokuwa mie niko skuli lakini habari ya uchaguzi walikuwa hawajuwi mpaka nilipotowa zile hati ambazo zina saini zao. Na ile kesi ilishikwa na mwanasharia Talati, ndo aloishika ile kesi yangu. Ikawa mimi sina kesi ya kujibu, nikawachiwa huru. Hakimu aliniambia, alinieleza ndani ya mahkama kwamba unaweza kuwashtaki hawa polisi kwamba wamekudhulumu kwa kukuweka ndani lakini kwa bahati nzuri au mbaya kushtaki kunataka pesa, kwanza, kwa sababu unataka uwende ukanunuwe hukumu halafu ina taratibu nyengine kubwa na yote inataka pesa na mimi sina pesa. Mimi nikiishi mkono kwa mdomo. Sasa nitafanyaje. Tukaacha. Nilipomaliza tumekaa tukizungumza habari ya fujo watu kwa jumla, memba wote wa Afro­Shirazi walikuwa wamevunjika moyo na tayari kufanya ugomvi wowote kama walivoanziwa, lakini matokeo yake yalikuwa si mazuri, yalikuwa mabaya kwa sababu wale watu wanoishi mashamba pande zote mbili, upande wa Afro­Shirazi na upande wa Hizbu, lakini kuna baadhi ya watu walikuwa si Hizbu wala si Afro­Shirazi lakini waliathirika katika ghasia zile kwa maumizi, wengine watu wenye mashamba yao ambao ni memba wa ZNP waliwakatiakatia migomba wakawafukuza ndani ya mashamba, matokeo yakawa si mazuri, uhusiano wa kijamii ukawa mbaya. Na jamaa waliokuwa Hizbu ambao wanakaa kule wanyonge wameishiwa wameumizwa, wamepigwa, wengi wamekufa. Haijulikani nani kafanya, na saa ngapi imetokeya, haijulikani, ni vurugu. Fujo siwezi kuzielezea lakini ukweli wa mambo uchaguzi ulikuwa na mambo ya kupenyezana watu ambao walikuwa na haki ya jimbo lile au na wengine hawana haki ya jimbo lile. Hizo ndo sababu mpaka leo watu wanagombana hapa Unguja. Imeshakuwa sugu hiyo. Inavyosemekana, ni kituo cha Gulioni kiloanza fujo ikaambukizwa na Darajani. Kituo cha kule kilianza fujo kwa sababu ya watu kutoka Funguni kuja Gulioni kupiga kura, ni karibu pale wanavuka tu. Sasa na kwa mujibu wa wakati ule watu wa Malindi walikuwa wakiogopwa kwa sababu walikuwa wana umoja, akipigwa mmoja wamepigwa wote. Hivo ndo ilikuwa watu wanawaogopa. Inavosemekana. Mimi si shahidi wa jambo hilo. Inavosemekana. Sasa ndo ikaendelea ghasia Darajani mpaka…Darajani ndo ilikuwa kubwa, kubwa sana ndo ilikuwa Darajani. Basi pale tukawa tunakaa tunafanya uchaguzi kwa kujiamini, tunajiona akilini mwetu kwamba sisi ni wababe! (Vicheko). Hata ulipofanywa uchaguzi wa mwisho, na hapa katikati ilikuwa serikali ya mpito, mpaka tulipokuja kwenye uchaguzi wa mwisho [ Julai 1963], ZNP ikapata serikali baada ya kufanywa kuunganisha viti na ZPPP. Mimi binafsi nilikuwa wakala wa kuhisabu kura, mimi na Diria, tulikuwa wawili, mimi na Mheshimiwa Ahmed Diria, Victoria Garden, ndio uchaguzi ulikohesabiwa. Tukashindwa. Wa jimbo hili la Darajani tukashindwa kwa voti mia mbili na mgombea wetu alikuwa Thabit Kombo, na mgombea wa ZNP alikuwa Ibun Saleh. Basi tukashindwa tukarudi. Mimi nilisikitika sana. Nilipotoka kule sikutoka nje kwangu kabisa.

Page 189: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 157

Nililala nyumbani nikatapika matapishi mabaya mpaka damu. Uchungu. Kwa nini tumekosa na kulikuwa hakuna sababu ya kukosa. Na tukajuwa sababu zengine za kukosea, baadae lakini. Haya, siku ile mimi nimekaa kitako, sikutoka, siku ya pili nkenda Gongoni. Hiyo hapa inaanza sasa maudhui.

Uchaguzi au Risasi?

Kujuwa chanzo cha mapinduzi, ina maana kila mtu anajuwa chanzo chake yeye kujuwa mapinduzi. Sasa kwa mfano wangu mie. Mimi nimejuwa mapinduzi kutokana na Saleh Saadalla, ndo alonambia “sasa tufanye mapinduzi.”1 Kwa kweli zile fikra yeye alizozitowa yeye kuhusu mapinduzi zimetokana na uchaguzi kwa mujibu ninavozielewa mimi. Uchaguzi ule kwamba tushashindwa lakini tuloshindwa tuna idadi kubwa ya voti kuliko waloshinda. Lakini waloshinda wana majimbo mengi zaidi kuliko sie wenye idadi kubwa. Sasa hapa hizi ndo fikra za Saleh ziloingia kwangu na mimi nkakubali tufanye. Haijawa uchaguzi wa kura kwa mtu mmoja. Uchaguzi ulokuweko ni wa viti. Mtu mmoja, voti moja, ndo ilivokuwa, lakini ushindi hauhisabiwi kwa mujibu wa idadi ya kura. Ukihisabiwa kwa idadi ya ushindi wa viti, majimbo, ndo aloshinda. Sasa ukija kuangalia idadi kubwa ya viti ilikuwa baina ya vyama viwili, mchanganyiko wa viti va chama cha Hizbu, mchanganyiko wa viti va ZPPP ilipoungana pamoja, vikawa ni vingi kuliko viti vya Afro­Shirazi. Kiti cha Mlandege wamechukuwa Hizbu. Tulipitwa kwa kura mia mbili ziada. Na zilikuwa hizi kura zilopita hapa, ni wapiga kura wa Kihindi, ambao hawakuipigia Afro­Shirazi. Waliipigia Hizbu. Ni wao walikuwa idadi yao mia nne. Wengi wao ni Wahindi wa jamatini. Sasa ukiangalia, ukichambua, kwa nini wakatupita kwa kura mia mbili? Tulikuwa sisi tumewapita Hizbu kwa kura mia mbili kabla kufanya hesabu za Wahindi ambao walikuwa ni kura mia nne. Kwa sababu walikuwa Wahindi wale kutoka Mlandege njia panda, Darajani, mpaka Mlandege, kituo cha polisi. Ilikuwa mtaa ule ni Wahindi watupu. Usione leo kuna maduka ya jamaa. Kulikuwa hakuna duka la mtu mweusi, hata moja…Kwa maoni ya kila mtu, uchaguzi mkuu wa Julai 1963 ulikuwa wa haki. 100%. Haijawa ugomvi, haijawa vita, haijawa kupandikiza watu. Haijakuweko. Tulikataa kwamba hatutaki. Kuna njia mbili, kuna karatasi na kuna risasi. Sasa unaweza kuchaguwa moja wapo katika hizo. Uchaguzi ulikuwa wa haki. Mia juu ya mia. Kwa fikira zangu. Kila mtu anaweza kusema anavotaka. Hata akisema kuwa Mngereza kahusika kugawa majimbo, alikuwa ndiye muendeshaji wa nchi hii. Kwa hivyo ni lazim atakuwa yeye amehusika na kugawa majimbo na kusimamia uchaguzi. Lazima tufike kunako ukweli. Tusijidanganye nafsi zetu. Ninavofahamu mimi, mapinduzi yalikuwa ni kwa ajili ya kufata uchaguzi namna mbili, kura au risasi, hakuna jingine. Lakini kwa kudai kulikuwa na ghilba, ni uwongo. Si kweli. Uchaguzi wa Juni uloleta fujo, tulipiga kura, kura ilikwenda safi

Page 190: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja158

kabisa. Fujo tu ndo ilitokea mjini. Tukahisabu kura akashindwa Maalim Hilal na Aboud Jumbe. Kihalali kabisa, wakapeana mikono, wakakubaliana. Ule ulikuwa uchaguzi wa kwanza ambao ungelikuwa pia ni wa mwisho. Kwa ajili ya fujo, na kwa ajili ya usawa wa viti, ambavyo ndo kitu kikubwa, ikafanywa serikali ya muungano, au ya mshikizo, ikiitwa “interim government.” Mapinduzi yamekuja kutokana na fujo za Juni. Kwa sababu viongozi maalumu wakaona kwamba sie hawa Hizbu hawatuwezi, wamepata kama majaribio. Watu wote wakisema “hawatuwezi, sie tunaweza kupigana nao”. Sasa tulipoingia katika fikra za mapinduzi tulikuwa na moyo kwamba watu wote watatuunga mkono. Hii ni fikra ya msingi nnoweza mimi kuielewa kwa kutokana na Saleh Saadalla. Tatizo la Waarabu na Waunguja halijakuwepo. Hii nakwambia kitu kweli. Hata utakuja kukuta Waarabu wengi wameuliwa mashamba, ukipeleleza, walouwa si Waunguja, lakini walokuja Unguja. Kama jamaa Wamakonde, wameuwa Waarabu wengi sana. Hii nyumba ingekuwa kuukuu ningekuonyesha risasi ya Mmakonde mmoja. Sie tumekaa barazani kapiga risasi pale. Walikuwa watu watatu wamefatana, halafu wakenda kumuuwa kijana mmoja anaitwa Mzee, kwenye kijumba cha simu. Wakamkuta. Kuna sababu gani? Wakaingia ndani kwake wakaiba. Si kuiba, kuchukuwa. Watu wa Kiunguja bwana ukitaka kumfurahisha mwite “Mwarabu”, “Mwarabu wangu hebu njoo nkwambie.” Ukitaka kumfurahisha, kumridhisha khasa. Ni upuuzi. Mambo yametengenezwa baada ya mapinduzi kuleta msuguwano katika nchi. Kuhusu Wamakonde sijuwi. Hilo jambo siwezi kukueleza kwa sababu sijakaa mie kuona wanavokuja, na kuja kwao na nini. Lakini hapa ile kuambiwa kuwa kuna chuki baina ya Waarabu na watu wa Unguja, uwongo. Kwa sababu hawa ndo wanotawala. Kumbuka Baraza la Mapinduzi lote ni watu wa Kitanganyika. Utasema nini? Mie siwezi kuelewa jambo hilo, lakini mimi ninavyoelewa, Muunguja, Mzanzibari, anaishi shamba, mjini, unakwenda kumridhisha unamwita “e Mwarabu wangu njoo nkwambie bwana.” Tizama bwana, hii baada ya mapinduzi kwisha kila kitu kinasemwa. Kuna hadithi nyingi. Si za kweli, si chochote. Karume akisema [kuhusu utumwa] kwenye mikutano mara nyingi. Ni huyo tu. Hajatokea kiongozi mwengine kusimama akasema maneno kama hayo. Hayana ushahidi wa chochote. Manake alisema yale makaburi pale wamezikwa Waafrika watumwa sijui walofanya nini. Na yale makaburi ya wagonjwa wa ndui pale. Na yakapata majina mpaka leo, Kisiwa Ndui. Lakini ndo anasema, mtu hajibiwi. Wewe utashangaa kwani. Viongozi wengi wa Afro­Shirazi ni wabara, kina Mtoro Rehani Kingo, kina nani. Unatarajia nini kutoka kwao? Wanolaumiwa ni viongozi. Na anolaumu ni mwanachama wa uongozi ule. Yule ndo anolaumu. Nimejaribu kuwalaumu waache mambo hayo. Manake hili suala ni zito, lakini kweli limesemwa. Na amesema Karume “wakimbieni wenye ilimu”.

Page 191: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 159

“Na hawa Waarabu walitufanya watumwa.” Na ni kweli, watumwa walikuwepo duniani. Si Waarabu tu walofanya. Mambo mengi sana. Wapo watumwa wa Kihindi hapa. Au hujui? Hilo ni jambo litakufa wenyewe. Unajuwa kitu kitakachouwa? Ni lazima ipatikane serikali ya kidemokrasia, kwa kura, halafu iwepo biashara huru, biashara zikipatikana, biashara nzuri, na hakuna khofu. Leo khofu tele. Kwa kuifikiri tu hivi. Zanzibar ingekuwa nzuri. Na jambo ambalo lingekuwa gumu, jambo moja lingekuwa gumu, ni ubaguzi. Ubaguzi ungelikuwapo. Ambayo sasa ni kubwa zaidi kuliko tunavofikiri ingelikuweko. Lazima ingelikuwepo. Kwa sababu kutokea hapo ulikuwapo ukabila. Hii ndo kitu kikubwa kinachojulikana. Huu sio ubaguzi. Huu ni udikteta wa moja kwa moja. Udikteta wa moja kwa moja. Iwe serikali yenye kuchaguliwa na watu, ambayo imepigiwa kura kama ilopigiwa kura hiyo ya historia [ZNP) na iwachiwe iendelee, ili upatikane utulivu. Manake sasa raia hana haki. Anakuja askari kukukamata tu saa yoyote, huna makosa, akakutia ndani. Wewe huna kosa. Lakini keshaamini yeye akukamate akutie ndani. Au kakaa Raisi, kakaa kwake huko anafikiri, fulani mtieni ndani. Huendi mahakamani, huhukumiwi, hujui umekosa nini. Kwani risasi matokeo yake ni Zanzibar tu? Imeanza Uingereza. Lakini haijawa hivyo. Haijafika hadi hii. Hivo leo daraja hii tulonayo leo, wakati huu, saa hii, tunaweza kutoa pumzi, lakini kabla ya hivi, tulikuwa hata kuongea hatuwezi (vicheko). Chombo cha Afrabia kitafanya kazi. Lakini hawa watu mafisadi huku, wote. Bara na hapa Zanzibar. Watu wamejaa ufisadi. Tena kila akiwa ana cheo kikubwa, anakuwa fisadi zaidi. Ingelikuwa hawa wafanyakazi kweli wanataka maendeleo, mambo yasingeliharibika hivi ya uchumi. Watafanya lakini hawatofanya. Afrabia itakufa njiani. Kabisaa. Chini ya mfumo wa serikali hii, itakufa. Na yasajili maneno yangu, ukumbuke jina langu. Vingapi vimekufa vilivoanzishwa vizuri? Vingapi? Sasa mimi ndo nakuwa ndo dhamana wa biashara ile. Mimi namuweka ndugu yangu, rafki yangu, jamaa yangu, ambaye tunasikilizana. Yeye ndo atakaa pale kufanya vile. Yule ndo atakuwa wakala wa kuiba vitu vetu sie. Kwa hivyo itakuwa biashara inakwenda bila ya faida. Inakwenda kwa khasara. Waarabu kule hawakubali. Ufumbuzi, tubadilishe serikali tu basi. Tupate serikali nyengine ya wapiga kura, tupige kura, tupate serikali mpya. Ile serikali mpya kwa miaka miwili, mitatu ya mwanzo, itaweza kujiamini. Haya hawa hawafanyi kitu. Hawatofanya maisha. Donda ndugu mara mbili hawa watu! Chronic, double chronic. Hawendi. Wamejaa ufisadi. Jamii inabadalika kwa sababu ya ubinafsi. Kitu kilicholeta hii ni utawala. Watu walokuwa kwenye utawala, hawako tayari kuutowa utawala kuwapa wengine kwa njia ya kura. Hawako tayari. Sio mie, ni binaadamu, yoyote, anapofanya kitu kikawa sivyo huona kwanini

Page 192: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja160

nimefanya. Hujuta. Na sio leo tu. Kutokea zamani. Watu wakijuta kwa mambo yao. Nimejuta eh! Kwa nini nisijute na hakuna kilicho chema kilichofanyika katika taifa? (anacheka). Kwa nini tusijute. Huna uwezo wa kuzuwia lisifanyike. Yale mazingira yaliokuwepo ndo yalochaguwa mawaziri. Jana nilimfikiri kijana moja, yuko Kwa Hani, akivuta kiko hivi, akifanya kazi melini. Najuwa meli aliacha zamani. Alikuwa ana mchango mkubwa katika mapinduzi. Anawajuwa watu wengi, na alikuwemo kwenye kundi letu. Karume alikuwa ana ushawishi mkubwa juu ya memba wa Afro­Shirazi. Na ungemkosa ndani ingekuwa fujo nyengine. Sasa kuzuwia fujo ile ndo akafanywa Raisi bila ya madaraka ya utekelezaji, kama Mfalme wa Kikatiba. Ndo Hanga akawa Waziri Mkuu. Kuondowa fujo. Hiyo kitu wazi kila mtu anajuwa. Kuja hawa kuja kumbadili kumfanya yeye [Karume] mtekelezaji, aaah!

Jiko la Mwanzo la Mapinduzi

Baada ya kushindwa uchaguzi wa Julai 1963 nilikwenda Gongoni, nikakutana na Mheshimiwa Saleh Saadalla, kwa matembezi. Sahib akaniuliza, “sasa tutafanya nini?” Nkamwambia “mimi sijui la kufanya, hapa sasa hivi imefika mahala la kufanya mimi sijui.” “Lakini wewe uko tayari?” Nikamwambia “lolote litakalo­kuwa limekubalika kufanyika mimi niko tayari nalo.” Akanambia “unajuwa hakuna jambo la kufanya isipokuwa mapinduzi?” Nikamwambia “niko tayari mimi kufanya mapinduzi. Niko tayari saana.” Akanambia, kamwite Hanga. Nkenda Kikwajuni, Hanga akikaa Kikwajuni maanake. Nikenda nkamwita, nikamwambia bwana, “Maalim Saleh anakwita bwana, sasa hivi wende.” “Sasa hivi, eh?” Nikamwambia “eh.” Akaingia ndani, nilimkuta amevaa nguo ya kulalia, maana hana anapokwenda. Na akaingia ndani, akavaa suruali na shati, viatu, tukaandamana. Tulipokwenda Gongoni tukamkuta Saleh kakaa anafikiri nini la kufanya au nini la kusema. Tumeingia ndani mpaka tumefika pale ukumbini kwake, hana khabari, yupo amezama kwenye fikra. Tukamwita, Hanga akamshika kichwa “unasinzia?” “Nafikiri namna ya njia ya kuyaingilia, mkabala wa mwanzo.” Tunajuwana. Tuko watu wa chama kimoja. Umefahamu. Shughuli zetu za pamoja, za kisiasa. Wakati fulani niliwahi mimi kuwa memba, mfanya kazi wa jimbo la Saleh Saadalla, nikimsaidia kama seketeri wake binafsi wakati mimi nilikuwa seketeri wa Aboud Jumbe. Tunaendeana. Sote ni memba wa chama cha ASP. Basi. Sio jambo jengine ziada. Wale viongozi na sie wafuasi. Tunapata pakuzungumza. Sijui umenielewa? Sasa Saleh akamueleza Hanga, Bwana Abdalla Kassim Hanga, akamuelezea kwamba hivi hivi…kwamba nimefikiri tufanye mpango wa mapinduzi. Hanga akasema “sawasawa”. “Wewe nenda kamwite Twala”, ili mimi. Nikenda nkamwita Twala, Miembeni katika ofisi ya chama cha wafanyakazi. Sasa sikumbuki alikuwa

Page 193: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 161

kwenye chama kipi cha wafanyakazi kwa sababu vyama vilikuwa mbalimbali. Nikamwita akaja, akaambiwa, akasema “hakuna njia nyengine, nina hakika.” “Njia ilioko tukubali kutawaliwa iwe imekwisha kesi au tuamue.” Ilivokubalika, tukasema sasa bwana, haya mapinduzi si rahisi, kumuendea mtu kumwambia “tupinduwe.” Hawatokuwa tayari ikiwa kwa kuwaambia jambo lolote, lakini kwanza tutafute watu maarufu katika vitaa vitaa vetu vidogo ambao wana msimamo madhubuti tunaowajua. Ikawa imefikiriwa hivyo. Hanga akasema, hakuna, kwanza tujuwe kama tuna watu madhubuti tunoweza kuwapata katika jeshi la polisi. Nkasema, Twala akasema, polisi wako wengi, hao wakubwa wakubwa wako upande wa huku, Kwa Hani. Ikiwa tutapata watu wa Kwa Hani yoyote mwenye ushawishi na askari yoyote tutaanza kuzungumza habari hizi. Pale nikachukuwa mie dhamana, nikamwambia mie nnaye Hamisi “Beni”, nnaye Mohammed, na wengine, tutakwenda zungumza huko. Na yuko kijana mmoja Rajab, wa bara huyu, kwao bara, Rajab nani yule? Nimemsahau, sasa ndo namkumbuka, namuona hasa. Nikenda nkazungumza na Hamis “Beni” kama ni mtu wa kwanza kabisa. Hamis “Beni” akanambia “sawa”. Hamis “Beni” alikuwa pwani kule “boat man”, baharia, alikuwa na akina Karume pamoja. Nkamwambia twende kwa Mohammed Omar, tukamuendea Mohammed Omar, Mohammed Omar kumzungumza, akiitwa maarufu Mohammed Omar “Masharubu”. Akaniambia “sikiliza bwana, mimi nauza ulevi hapa, na hapa wanakuja kulewa askari hawa, sasa tukae hapa tungoje mpaka mchana, jioni, usiondoke, tutapika chakula, tutakula hapa hapa.” Ina maana yeye kakubali mapinduzi. Akaja Sajent Ngusa. Akampampa ulevi. Kabla ya kunywa, akamwambia, mimi sikupi ulevi kwanza. Sikiliza habari zangu hizi. Akamueleza. Akamwambia, sie tuko tayari zamani watu, lakini hatujuwi tuungane na nani, tunakuogopeni watu wa Unguja. Tukaja tukaongea naye pale pamoja, akaniambia “sasa bwana wewe wapate watu wawili. Ukiwapata watu wawili hawa wakakubaliana na wewe, basi tumeshafaulu.” Namwambia “nani?” Akanambia “mmoja anaitwa Simba Ismail, Sergeant Simba Ismail. Huyu Simba Ismail ana ushawishi na nusu ya asikari wa Ziwani, kwa sababu ni Sergeant anopendeza kwa asikari.” Nikamwambia “nitampataje. Mimi hata kumjuwa kwa sura simjui.” Rahisi. Mimi kesho, wewe njoo, mimi ntakuja hapa mapema, mimi kesho sina kazi kabisaa, nitakuja. Asubuhi mie ndo nimeshakunywa chai nikapita Gongoni nikampa taarifa Saleh tulipofika, Saleh akaniambia “vizuri sana.” Nikamwambia “mimi nakwenda.” Nkenda mimi zangu kwa Mohammed. Kufika nilimkuta Ngusa na Simba tayari. Akanambia Ngusa, “huyu ndio Simba Ismail, nilokwambia.” Tukaongeaongea, akanambia “e bwana kuna mambo mawili, mimi tayari kubahatisha lakini si tayari kumuona Sergeant Saleh kumwambia maneno haya, lakini nimefikiri kuna mmoja ana ushawishi mkubwa Mtoni ntakwenda kumwambia.” Namwambia “sasa huyu ntampataje mie?” Akanambia mimi nikimpata ntamleta kwako tu

Page 194: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja162

saa yoyote. Ntakwenda mimi lakini Saleh, huyu Saleh ndo mwenye kikosi cha ulinzi. Kuna sehemu kazi yake ulinzi tu, wanakuwa katika mapalace huku, pale quarter guard, wanakuwa wao, manake wao ndo wanachukuwa ulinzi wa nchi nzima. Mtu wa Kilwa huyu kwao. Nikamwambia “ntampataje” akanambia sijui lakini huyu anasali msikiti wa Ijumaa wa Malindi kila siku, hakosi. Sasa mie ntakwenda kule ntakuonyesha tu “yulee” siku ya Ijumaa. Nkamwambia “nipeleke.” Na kwake anakaa Kikwajuni. “Ah! nende Kikwajuni, nende msikitini?” Nkasema “twende, ntakwenda mskitini.” Nikenda msikitini nkamuona Saleh nkamwamkia nkesha, nkamwambia “Saleh, mimi sikufichi bwana, sina siri ya jambo hili, nataka unifahamu. Unakujuwa kwangu?” Akanambia “sikujuwi. Kwani kuna nini?” Ndo nakwambia nlivyo mimi. Tunafanya mipango, na tuna kikosi chetu tayari kikubwa, lakini nimeona lazim nije nikuone wewe kwa sababu wewe ndo dhamana wa kikosi cha ulinzi cha Zanzibar! Na juu yako ni maofisa wengine. Umefahamu? Tunataka kupinduwa Unguja, unasemaje? Akanambia “Ah, hiyo rahisi. Tunaweza kufanya, ngoja siku ya zamu yangu, mimi ntakapokuwa mlangoni, siku ile ndo mfanye. Lakini itachukuwa kipande hapa itapindukia mwezi huu wote wa Disemba huu utakwisha huu, mie sijachukuwa, mie ntachukuwa katika Januari, katikati ya mwezi. Lakini ntakwambia rosta.” Nkamwambia “sawa.” Kuja, nika ripoti, nikamwambia “bado Juma Maneno sasa.” Tukaja tukampata Juma Maneno. Saleh akaja kunipa ripoti hapa nyumbani. Juma Maneno kaja kwangu na Simba Ismail. Juma Maneno wa Mtoni, Saleh wa Ziwani. Hawa ndo walikuwa wale wakiitwa Police Mobile Force [PMF]. Sasa huyu Juma Maneno alipokuja hapa, tukaongea akanambia “mimi nimekubali, lakini jambo moja. Tukaonane na huyo alokuwa juu yako wewe.” Nikamwambia “rahisi, twenzetu.” Nikavaa suruali hapa tukenda Gongoni nikampambanisha na Saleh. Ilikuwa Hanga kwa hali yoyote hatoonyeshwa na mtu. Walipokwenda wakaongea wakapatana wakapeana mkono tukapika chakula tukala pamoja sku moja. Sasa tunamtaka Kisasi. Mimi nkenda nyumbani kwake. Nkamwambia, e bwana Kisasi mie nimekuja unifunge au unikubalie. “Nini?” Namwambia, sie bwana tunataka kufanya mapinduzi tena kikosi kikubwa hata ukinifunga tutakuuwa. Nataka ufahamu kiasi hicho. Mimi niko jela lakini wewe utauliwa. “Nini?” Namwambia “sisi tunataka mapinduzi.” Akanambia, lakini mimi wewe peke yako bwana sikubaliani na wewe, lazim nimpate alohusika khasa mkuu. Nikamleta kwa Saleh. Kisasi akakataa kabisa mpaka akakutana na Hanga. Hanga alipokutana naye, tuifupishe hadithi…wakazungumza, akakataa kuongea mjini hapa wakenda kuongea Kitope. Kitope, kwenye nyumba ya Mwarabu fulani. Ah! Huyu Mwarabu nimemsahau jina lake, lakini siku yoyote, ngekuwa mzima mie ningekwishakwambia hata kesho ngekupeleka, maana yake yupo Kitope hapo kwake kwenye msikiti na, ule mti unonuka mavi, mdoriani. Mdoriani mkubwa, msikitini, iko nyumba pale pembeni, kubwa, ina saruji mbele ya kuanikia karafuu,

Page 195: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 163

mbata, nini. Tukenda tukakaa pale, tukapikiwa chakula tukala na wanawe na yeye. Kitope ni ngome ya Afro­Shirazi, na ni karibu, kuliko kwenda Bambi. Ilipokwisha kubalika, ikawa sasa Hamis “Beni”, Mohammed “Masharabu” wao ndo kazi yao kukusanya watu wa kufanya mambo yale, kutafuta watu kwa kuingia Ziwani. Wao ndo walokuwa mas’uli wa kutafuta watu wa kuingia ndani ya boma Ziwani. Sie huku tumebaki na uongozi wa juu. Mtoni aliwachiwa Juma Maneno, lakini hakufanya kazi nzuri. Ilibidi sie tulokuwa Ziwani twende tukasaidie.Tukenda Dar es Salaam, mie na Saleh Saadalla. Madhumuni tumuone Mwalimu Nyerere kumpa habari hizi. Kwa hivyo tukenda muona Waziri Mkuu Mheshimiwa Rashid Kawawa. Tukaongeaongea naye kutaka nafasi hizo akazungumza na Mwalimu tukashindwa kumpata. Kakataa kuonana na sie, kwa sababu anazozijuwa mwenyewe. Tukarudi mikono mitupu. Umenipata lakini. Tuliporudi mikono mitupu tukaripoti kwa mwenyekiti wa mapinduzi, Abdalla Kassim Hanga. Tulipokwisha ripoti kwake akakaa kwa muda tukafanya safari nyingine. Mimi, Hanga, Saleh, Twala. Tukenda kumuona Oscar [Kambona]. Oscar alituunga mkono mara moja. Lakini akasema mimi ni Waziri tu, lazima nipate rukhsa ya juu kwa jambo hili, lakini niwachieni mie. Pale, palikuwa, sijui, na yule, ndo Balozi, au ndo nani, wa Algeria, nadhani Balozi, maana yake kulikuwa na bendera pale. Tukenda kwake, tukaongeaongea kidogo, tukampigia simu moja kwa moja, akapiga Oscar, direct na Ben Bella, akaongea Hanga. Ben Bella akatuunga mkono na akatuletea silaha kamili, ndani ya meli. Meli imezuwiliwa na serikali ya Tanganyika, bandarini Dar es Salaam. Hatuna la kufanya. Wakati ule, tuliporudi huku, mimi na Twala tulikwenda Bweleo kwa Mzee Mwinchum kuona namna gani tukiweza kupata silaha tutaziweka. Ikawa, tukaingia baina ya Bweleo na Dimani na kuelekea pwani. Kuna mapango makubwamakubwa ya majabali. Tukenda tukalitazama pamoja watu watatu, tukakubali lile, kwamba hili na hili litafaa. Mzee Mwinchum alokuwa Mwenyekiti wa Afro­Shirazi, Bweleo. Hapo, tukarudi mjini tukaripoti. Siku ya tatu au yane, tukenda na Saleh, na Mwenyekiti tukenda naye, akatazamaa, tukakubaliana napo, kwa sababu ni pazuri, tena pako ndani ya ghuba. Ile ya kutokea kwa BiKhole, na huku Bweleo, na Fumba. Si lipo ghuba limepita. Ilikuwa pale ni mahala pazuri sana kwa sababu za usalama wa kimapinduzi. Kulikuwa na silaha kidogo kwa Oscar Kambona, hizi silaha zetu za jeshi hizi. Akatupa mukhtasari, tulikuwa mie na Twala. Tukabeba zile silaha, Msasani tumezichukuwa, kwake ndani manake karibu ya pwani. Na tulikuta zimeshafikishwa pale. Na alokuwa akibeba kutusaidia kutia alikuwa Kitwana Kondo. Huyu ndo alokuwa mlinzi wa Oscar, ambaye mpaka alifanywa akawa Meya [wa Dar es Salaam]. Yule ndo alotusaidia kubeba. Akazifikisha pwani pale ufukweni. Akazilinda, sie tulipofika, tulikuwa tunatokea Bagamoyo, kwa ngarawa. Tulitokea Bagamoyo kwa ngarawa na mshipi wa kurambaza ule. Tumekuja nao

Page 196: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja164

huku tunaonekana, pale tukakutana na boti moja ya Tanganyika police. Pana kama kichunguu hivi ukiingia hivi, kama jabali lile, visiwavisiwa vidogovidogo. Lakini walitupuuza tu. Waliona hawa wavuvi. Tumevaa matambara yale. Na chombo chetu ulikuwa upepo mzuri, mpaka tulipofika pale tukatia zile. Kuja zetu sasa. Tulikuwa na mashine ya kubandika ile. Tukabandika mashine. Tukapiga spidi kubwa. Sasa tushapita kisiwa hiki cha Chumbe, tuko ndani ya Zanzibar. Sasa tunataka kukisi kuingia ndani ya ghuba ya Fumba, na boti ya polisi inakuja, Zanzibar police. Alikuwa yule Banyani ndani, wako katika patroli, akiitwa Samra, Simri [Misra] sijuwi, tunamuona yeye, alikuwa Mshangama Masharubu, na nadhani Mohamed Ali Bahari. Lakini walikuwa watu wazuri, wengi. Wana­nyayuwa lile dude lile, lenye kupaza sauti. “Punguza spidi, simameni!” Twala akawaambia “Hatusimami, wala spidi hatupunguzi, na chochote mtakachofanya na sie tutafanya.” Twala ali kreki. Anamwambia Mzee Huseni “kaza moto, pandisha na tanga pale.” Twala akasema “unajuwa, tukifanya maskhara watatukamata, hii boti yao kubwa.” Akatoa ki bren gun cha pata hivi, kile wanaita nini? Sten gun. Ndio Sten gun. Hapana. Liko jina lake dogodogo. Wanatumia sana askari, kama bunduki. Akaitoa ile akaijaza. Akawaambia “hivi ndo tulivyo, njooni!” Hawakuja. Mambo hayo yalikuwa wiki moja, au wiki mbili kabla ya mapinduzi. Hata wiki moja bado, mbili hazijafika. Badala ya kuingia Fumba tukaingia Bweleo. Kwa sababu Bweleo ndo tulikuwa na mipango yetu. Lakini Bweleo kulikuwa ni 100% usalama juu yetu. Sasa tulipofika tu, tukamkuta, nani yule pwani pale ufukweni…tukamwambia “kamwite Mwinchumu chairman haraka kabisa mwambie tupo hapa.” “Na aje na vijana.” Usiku bwana, alfajiri kubwa. Wamekuja watu sijui, zaidi ya kumi. “Unasemaje Mzee.” “Vitu hivi, chairman.” Tukavituwa tukawa salama. Sasa tatizo lilioko polisi sasa. Sisi hatujasafiri navyo. Tumeviwacha palepale, kwa chairman Mwinchumu wa Bweleo. Asubuhi tulipoingia ndani ya mutukari, tunafika kituo cha polisi cha Kiembesamaki, wanasachiwa watu. “Ewe bwana, tokeni tusachi gari.” “Kuna nini?” Ananambia “jana kulikuwa na vishindo huku.” Sachi. Yuko askari mmoja “umelala Fumba leo” nikamwambia “kesho ntalala Makunduchi,” kwao Makunduchi (vicheko). Tukasachiwa pale. Na tumekwenda gari mbalimbali mie na Twala. Zile gari za abiria. Silaha hizi tulizokuja nazo sie, tulizozichukuwa kwa Oscar ni silaha khasa. Nipe, nkupe. Hatukuzitumia. Hatujatumia silaha ya risasi sie. Ila ikiwa kujihami. Tulikuwa nazo zile na tulizigawa kwa fulani, kwa fulani, kwa fulani. Lakini zote ziliru­dishwa. Basi, tukarudi, tukawa tunangoja. Sasa ile [silaha za Algeria kupitia Dar es Salaam] inakuwa imekawiya, tukaenda Tanga, mimi na Saleh, kutafuta njia ya pili. Wakati ule Tanga, Area Commissioner [Mkuu wa Mkoa] alikuwa Ali Mwinyi Tambwe. Tukaongeaongea kule, tukakutana na Jimmy Ringo, katika…ilikuwa sherehe fulani ya chama, usiku katika michezo ile. Tukakutana na Jimmy Ringo. “Nini Jimmy?” anasema “nakuja tu.” Nikamwambia “kuja tupu huwezi. Umekuja

Page 197: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 165

na vitu vingine lakini haizuru.” Sie tukatoka, hatujafanikiwa Tanga. Tukarudi, tukaripoti. Tukawaambia, basi tuwache, tungoje, wakati unawadia. Sasa ikija Januari, Disemba inamalizika. Tukaamua tuingie. Sasa tumuone Saleh kwanza na Ngusa. Tukarudi tukamuona Saleh tukamwambia jitihada nyengine hatuna, jitihada yetu ya kutaka kuingia tu. Akasema “sawa,” siku yoyote mtakayokuja mie ntakupeni nafasi. Nkamuona Ngusa, Ngusa akanambia “sasa sie tunataka kujuwa nini cha kufanya?” Asikari wakija wakivamia bunduki si watatuuwa tu. Sisi hatuna kitu. Akasema, tuzitowe bunduki zote zilio ndani quarter guard, bolt, spring, na magazine, tuziweke mbalimbali, vitu hivi, hata asikari akija kuchukuwa bunduki, haina kitu chochote ndani. Bolt iko mbali, magazine iko mbali, bunduki yenyewe liko mbali. Na risasi ziko mbali. Sasa hiki chumba cha risasi kiko sawasawa na pipe juu kule ile ya upepo, atatakiwa mtu apande madhubuti, ikiwa mambo yamezidi atie moto tu. Nikamwambia “sawa.” Tukafanya utaratibu ukesha. D­Day [siku ya siku] ilipofika, ilikuwa Jumamosi kuamkia Jumapili, Januari 11 usiku, ni Jumaamosi kuamkia Jumaapili. Tumeingia sie Ziwani. Mimi nimekwenda Ziwani. Mimi nimepanda juu ya quarter guard, mimi nimekosewa risasi na Major Bott, Ziwani. Sergeant Saleh kuona kikosi kile kiloingia simo mimi, akazuwia pale. Ndo tumekwenda kwa mujibu wa muongozo wake. Kwamba sku ile yeye alikuwa pale. Ndo ikawa rahisi ati. Lakini alizuwia, alizuwia kwanza, hakuniona mie, na zile alama tulopeana. Kwa bahati nzuri kutaka kupiga kengele ile, alipigwa begani hapa. Kupigwa begani Major Bott kaja kule juu tena. Kuona mtu akapiga risasi Major Bott. Risasi ya kwanza kulia ilikuwa yake yeye na nnadhani huyu alikuwa ni Major Bott kwa sababu alikuwa anaonekana wazi katika usiku ule. Lakini ukweli wa mambo ilikuwa inangojwa zamu ya Sergeant Saleh atakapokuwa kamanda wa silaha Ziwani. Ile kusema leo na kesho alikuwa Twala. Twala mwenyewe aliwahi kuitwa polisi, alihojiwa na Nassor “Mlawwaz.” Akimuhoji Twala kwa jambo hilo. Halafu akampeleka akenda kwa Kamishina mwenyewe. Akaachiwa. Akisema, na watu wakizungumza hoteli, barazani, nikawa na mimi nazungumza hivyohivyo. Ile ilikuwa kwa makusudi. Sio kitu kilotengenezwa uwongouwongo. Na ilitumiwa Twala kwa sababu ya Chama cha Wafanyakazi. Na ndo akaitwa. Lakini haijakawiya. Alipomaliza yale mazungumzo alipoondoka, siku mbili tatu, Saleh akawa yuko kazini na ikawa siku nzuri Juma­mosi, watu wakaingia. Na ule usiku wote walikuwa wako hadhiri. Hata Raha Leo siku walodhania kuwa itakuwa khasa, walipeleka jeshi kubwa pale radio. Siku ilokuwa iwe hawakupeleka. Mtu tuloweza kumsaidia ilikuwa Babu tu kwa sababu ilikuwa afungwe. Tulimsafirisha kwa amri ya Saleh Saadalla. Hata Hanga alimlaumu Saleh. “Kwanini umemsafirisha huyu?” Hanga na Babu ilikuwa ni mdomo tu, lakini kisiasa walikuwa mbalimbali. Hawafahamiani kabisa! 100%. Kuhusu uhusiano wangu na jeshi la Kiingereza, tumeondoka hapa 1942, watu sabini na tano, kutoka skuli, watu wawili kutoka jeshi la polisi. Huyu alotoka

Page 198: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja166

polisi alikuwa ni Khelef Said Rashid Al­Mauly. Na mwengine alikuwa ni Jacob Malambeka, Msukuma. Tukawa sote watu sabini na saba. Sabini na tano sote kutoka skuli. Tumefika Nairobi, katika kambi ya Karen Camp, tukawa depot pale, Karen. Katika “signal.” Ndipo tulipozinduka. Tunaingia tukakuta imeandikwa kwenye bango kubwa “ingia kujifunza wende kufa.” Sasa ile kufa imeandikwa double “a”, “kufaa.” Inamaana kama “kufaa.” Uende ukafae. Lakini haijulikani nini maana yake. Basi tukarejea depot pale, kama asikari kuruti. Tulipomaliza depot, tukenda kituo cha ufundi palepale kutufunza mambo mbalimbali. Kuna walokuwa wanajifunza dispatch radio, kuna walokuwa wanafunzwa wires, to lay down telephones, kuna tulokuwa tunafunzwa wireless and line operators. Wireless na line tukifunzwa namna ya kutandika wires, na Morse Code, na matengenezo madogomadogo ya wire sets. Sets zetu na sounders tukitumia. Kilichotendeka kwa kuondoka kwangu asubuhi ile siku ya Jumamosi tarehe 11 Januari, 1964 mpaka kuamkia Jumapili, baada ya kuamka asubuhi, kitu cha kwanza baada ya kumaliza mambo yangu na kutoka, nilikwenda kwa Saleh. Nilipokwenda kumuona Mheshimiwa Saleh Saadalla Akida, tukaongea habari hizi kwamba sasa ilobaki ni kupita kituo, na katika kituo muhimu khasa tukajuwa watu wako vipi. Sehemu zote mbili. Basi, kituo chetu muhimu cha kwanza, kwa ajili ya Ziwani ni Kwa Hani. Kwa yule Khamis “Benii”! Tukenda tukaongea, Mohamed “Masharubu” akenda Ziwani ndani, quarters, kumuona Sergeant Ngusa. Tukajuwana mipango ya pale ilivokuwa. Akamuona Sergeant Waziri, tukenda sote, sehemu zote mbili, sehemu ya juu kule ilokuwa skuli ya Aga Khani, kule, kulikuwa karibu na magari. Tukenda tukaona zile waya zilivokuwa zishakatwa kama tulivyoagiza. Zile zimekatwa Jumamosi, alfajiri ya kuamkia Jumamosi. Ijumaa mosi zimeshakatwa. Na ilivokuwa upande ule hakuna mtindo wa polisi kupita kule, mara kwa mara, wanatarajia kwamba yale magari yako depot, yako pale parking yard [panapowekwa magari] yake, wale sentry wa pale ndo wanokuwa muhimu kwa ile pale, na wakati ule alikuwa jamaa mmoja akiitwa Feruzi, siku ile, na ndo alokuwa yeye dhamana. Huyu ni Sergeant wa madereva. Sasa, tukakuta mambo yale pale yapo tayari, na tukaja huku upande wa Mwembe Matarumbeta, pana gate pale, ya sentry. Ili ku cheki police quarters, ndo pale mlango wao wa kuingilia pale. Anakaa asikari pale, akifunguwa mlango kwa magari, kwa nini, watu wanapita. Kuona kama zile bawabu za mlango zimetolewa. Si vinakuwa vyuma kama va geti zile, za kupandisha na kuteremsha. Basi tulihakikisha ile moja imetoka ile bolt yake yote, kwa hivo huwezi kufunga, unakwenda tu bila ya kizuwizi. Sasa ile imetolewa usiku wa kuamkia Jumamosi, kama ulivotolewa waya kule, usiku wa kuamkia Jumamosi. Sasa sehemu mbili ziko wazi. Kuna mtu mmoja ambaye ndo alokuwa mkuu wa kikosi kile kule Kwa Hani, akiitwa Farhani. Farhani nani huyu? Nimemsahau babake. Lakini ana jina la Kimanyemamanyema hivi. Watu wa Kimanyemamanyema. Nikamkuta. Akasema, “watu wote hata kazini hawakwenda leo. Watu

Page 199: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 167

wamekaa standby [tayari]. Wanokwenda pwani hawajenda, wanokwenda wapi hawakwenda. Wote wako tayari.” Hawa ndo wanopita kwenye geti, chini ya quarters. Nilikwambia kulikuwa na vile visilaha viwili vitatu, hawa ndo walokuwa navo, kwa kujihami ikiwa wametoka watu kule. Manake hawa ndo wanopita quarters. Tukarudi, mimi nikaripoti kwa Saleh. Nikenda kwa Twala nikaonana naye. Twala akanambia “Saleh na brother Hanga lazim waondoke leo.” He! Namwambia “sasa wataondoka na nini?” Ananiambia “wataondoka na chombo chochote.” Na nani atasafiri nao? Ikabidi Mohamed Omar “Masharubu” afatane na msafara ule. Manake ni lazim ende mtu tunomuamini, tunakuwa hatuna wasiwasi naye. Litakalotokea si atakayekwenda mbio. Lakini atakuwa na wao pamoja. Nikarudi tena Kwa Hani. Nikamtafuta Mohamed. Nikaambiwa kenda shamba, Mwera, jirani na kina Amar Salum. Yeye alikuwa ana mawasiliano na wazee wake. Ikanibidi nichukuwe gari ya Ali Saidi. Tukenda. Tukamkuta Mohamed. Nikamwambia Mohamed “utakwenda na Hanga na Saleh.” Akanambia “sawa twendezetu basi.” Tukaja akajitengeneza, saa moja ya usiku, baina ya saa moja na saa mbili ya usiku wa Jumamosi Hanga na Saleh wakaingia ndani ya ngarawa wakaondoka. Saleh alikuwa hataki kuondoka. Nikamwambia “ikiwa hutaki kuondoka utakuwa umeasi.” Kwa hivyo sisi tunataka uondoke. Kwa sababu ikiwa kutakuwa na makosa yoyote ya kuelekea kushindwa au kukamatwa au kulipiza kisasi, watakapokuja kukulipiza wewe kisasi utatuvunja sote nguvu zetu. Kwa hivyo watu washakubali wende. Akaja Simba Ismail, akasema “lazim ende. Akiwa hataki tutampakia kwa nguvu.” Akakubali, akalainika. Kama saa tatu ya usiku, mbili, tatu, akaondoka. Wakati mimi nakwenda kuhakikisha kusafiri, memba wa Umma Party, hawana hata habari. Wako hapo barazani. Hapohapo nimepita mimi, wako pale wamekaa kitako. Mimi nlikwenda mchukuwa Hanga usiku ule wa mapinduzi, mapema kidogo. Nlikwenda mie na Mohamed Omar Masharubu. Kikwajuni, kwa Ali Ngwengwe. Sasa alipokuwa anatoka Hanga akamuaga mjomba wake, mwangoni pale, akamkumbatia. Akambusu. Na mjomba akambusu Hanga. Wakabusiana. Akamwambia “mjomba Mgu akipenda tutakutana, lakini usitaharruk kwa utakayoyasikia yatakayotokea leo usiku. Mwenye Enzi Mungu akipenda tutafuzu.” Na hapo ndo mkewe Hanga, yule Bimkubwa Saidi wa Maghee, yuko ndani. Basi sijui sku zile keshamuoa au bado, Allahu Yaalam Wa Rasulu. Anakuja mwangoni kumuaga. Tukamchukuwa tukaja naye Kizingo, upande huu kuna makaburi na mikadi, pale ndipo tulipompeleka akaingia ndani ya ngarawa. Ngarawa ya nani, ya baba yake Fuko.2 Napita mimi, Imam wetu wa Msikiti ananambia “usiku huu unatoka unakwenda wapi?” Nikamwambia natoka nakwenda kumuamkia bwana mkubwa [baba yangu]. Mie lazim nende usiku, kwake, lazim, halafu ndo nakuja lala. Nikakutana na Mzee Mbaba, alokuwa Inspekta wa polisi, na baadhi ya wanawake, kakaa

Page 200: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja168

katikati na kundi la wanawake. “Wapi unakwenda usiku huu?” Nikamwambia “nakwenda nyumbani kwa babangu mie. Ndo kweli nilikuwa nakwenda kumuaga.” Huu ndo ulokuwa ukweli wa mambo. Niliporudi tena kutokea huko kama saa nne unusu ya usiku. Sasa mimi niliporudi hapa saa nne usiku nilikutana hapa nyumbani na Simba Ismail, tuko barazani, Juma Maneno, Ngusa yupo hapa barazani, Saleh hayupo. Saleh yuko kazini. “Je vipi?” Nkamwambia “kila mtu position [nafasi] yake sasa hivi ende akakae. Hakuna mchezo sasa. Wakati ukifika, hakuna kungojana, time ikifika, saa sita kasoro dakika tano, tunaingia bomani.” Isizidi. “Barabara, barabara.” “Barabara, barabara.” Kwaheri. Wakatoka wakenda zao. Saa sita kasoro dakika kumi na tano, mimi nimeshaingia ndani ya yard [eneo]. Peke yangu. Nimepita hapa chini Mwembe Matarumbeta. Kwa sababu mimi nataka kupanda juu kule, ya quarter guard. Kuna kidude kile cha kuunguzia nyumba yote iunguwe. Sasa nilipoingia mie pale nakwenda zanguu mpaka kwenye muembe mkubwa Bomani ulokuwa nyuma kule, wakichezea paredi askari. Pale mchana pana kivuli kizuurii! Pale na quarter guard ile pale. Sasa ilibidi nitambae kwa tumbo. Sasa kwa upande huu, wa magharibi, kuna taa nyingi, ndo mbele. Kule ndo kuna mahala pazuri pa kupanda. Huku hakuna lakini, nkaona sasa ntarudisha mafunzo yangu ya kijeshi. Pale ndo nkapanda kwenye bomba la maji lile. Mimi ndo mtu wa mwanzo kuingia Bomani [Ziwani]. Wa mwanzo kabisa. Mpaka dakika kumi, dakika tano nzima nimekaa kwenye nanhii, kwenye sakafu ya juu. Natazama harakati. Ndo kukatokea kidogo kutofahamiana. Kwasababu Sergeant Waziri alikuwa anantarajia ataniona mie, halafu awache wazi gate [lango]. Sasa hakuniona, kataka kuzuwia. Kutaka kuzuwia, Bott akaona kule juu. Major Bott. Sasa Major Bott alipoona, kilichomjuulisha ni ile sauti yangu juu kumwambia Sergeant Waziri “wacha!” Bott akaanza kupiga risasi kule. Na ukenda Bomani, nadhani, mpaka leo utakuta alama ya risasi alokosea Bott akapiga kwenye hii kona hapa ya jengo, mimi nkaaunga chini, au sivo angenipiga risasi ya mbavu. Sasa kuondoka mie kuanguka kwangu pale nikafika miguu yangu juu ya magunia ya mchanga yalokuwa yamewekwa pale. Kichwa kikafika kwenye saruji, kwenye lami, ile njia imetiwa lami, ndo nkaanza kupata na ugonjwa wa macho kudhihirika. Hapo ndipo mapambano yalianza. Alipigwa begani Sergeant Saleh kwa kuangusha ile firimbi ya alert. Watu wakavunja mlango, gari kule zilikwishatiwa funguo, na yule Sergeant Feruzi alokuwa dhamana pale, ilikuwa imeshatengenea. Wale walipoingia walivamia magari tu. Wale waloingiliwa kule. Wale walikuwa ni madereva. Walipoingilia kule kwenye waya ule walifikia kwenye gari. Zile gari ndo zilikuja moja ikapakia bunduki zote zilokuwa pale zikapelekwa Kijangwani. Ni kiasi ya watu ishirini tu wa Ziwani. Na hawa ni kundi lilotoka Kwa Hani. Mtoni ilikuwa ni mchangayiko. Juzi tulikutana na kijana mmoja akiitwa Hamid Ameri ambaye ndo nlokwenda kumshawishi akubali. Yeye ndo alokuwa dhamana

Page 201: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 169

wa Mtoni, chini ya Youth League. Na kina Ramadhani Haji. Wengine siwajuwi. Lakini kina Haji Mlenge, ambaye alikuwa dereva wa Waziri Mkuu Hanga, halafu akawa dereva wa Makamo wa Raisi huyohuyo baada ya mabadiliko… Sie tumekwenda, mimi nimekwenda kule [Mtoni], mambo yashawaka moto. Kufika kwangu Ramadhani [Haji] akapigwa risasi ya tumbo ile, pamoja na kikundi nlokuwa nacho. Kikundi nlokuwa nacho mimi ni wanachama wa ASP walokuwa kutokana na Kitope. Tukaingia kwa daafa moja, kwa nguvu kabisa. Na sie tuna silaha za kawaida kama za wale. Pale wakasalimu amri. Kwa nguvu hii ilotoka huku [Ziwani]. Mtoni walikuwa hawajamaliza. Wanazonganazongana tu. Wale wana silaha za bunduki, hawa hawana. Watu walitoka Kwa Hani, Kitope kidogo, halafu kwa alivokuwa Hamid [Ameir] yule ni mtu wa Donge walikuwepo, watu wa Donge walikuwepo wakaungana naye. Na Youth League, ndo akina Sefu Bakari walikuwa na hadhi, na [Abdalla Saidi] Natepe. Mimi sikuwaona kina Sefu Bakari na Natepe, lakini wanajuwa mambo. Kama Natepe, ndo alokuwa anakuja kwa mashauri mara kwa mara kwa Saleh [Saadalla]. Alikuwa kila wakati ndo anakuja kuuliza. Lakini wao walikuwa na kisehemu chao, cha Youth League, mimi siwezi kukieleza, sijui. Manake walipewa dhamana, kwa sababu itakuwa haijaelekea kutaka kumuongoza mtu ambaye ni Raisi au ni Katibu Mkuu. Manake yule Sefu alikuwa ni mkubwa wa Youth League.3 Natepe alikuwa ni Katibu Mkuu wa Youth League. Sasa wale wawili walikuwa wanakuja kufanya mashauri kwa Saleh Saadalla. Hilo jambo lilikuwa ni mafahamiano ya kwanza. Ilikuwa hatutaki kuchanganya mapinduzi na chama.4 Ni vitu tafauti. Hata wao Youth League waliripotiwa wale na akina Karume, Youth League walikuwa wanataka kufanya mapinduzi. Karume alisema “wahuni hawa wanataka kufanya nanhi.” Karume alikuwa akipinga kabisa. Ati amejikinga, anataka ale yeye tu, kuku mzuri na mbuzi. Wanaweza Youth League kutengeneza listi yao ya watu wale walokuwa kwenye matawi, kwa sababu wanajuwa hizo habari zote. Na upande huu ambao tulookuwa waasis wa mapinduzi, nchi hii, yetu, nafasi yetu haikuwa ya kawaida, maanake mara kuingia, chuki ya huyu anamchukia huyu, kama nilivokwambia mie kwanza, Raisi wa dola anawachukia raia na memba wa chama. Wewe fikiri pataandikika kitu. Wale wakipendeza kwa Raisi. Kwa hivo itakuwa listi kamili wamejaa watu wa bara watupu au wengi wao. Listi ya waasisi, mbali ya sisi viongozi, ntakwambia ni Hanga, Saleh, Twala, Khamis Beni, Mohamed Masharubu, Ngusa, Juma Maneno, Ismaili, Saleh, bas! Hawa nawakumbuka uzuri. Hata akija Munkar wa Nakiri ntajibu suala hilo. Sina tabu nalo. Khamis Beni khasa alikuwa ni raia wa kawaida, kazi yake boatman, alikuwa akisikilizana na Karume sana, lakini kaanza kuudhiana naye sana wakati wa maandalizi ya mapinduzi. Manake alikuwa hataki anamuona mtu anashughulika

Page 202: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja170

asijue anashughulikia nini. Lazma ajuwe, kama Mngu. Kwa sababu alikuwa…Mzee Karume alikuwa ni mtu mzuri, lakini alikuwa ni dikteta wa daraja la kwanza. Hataki kukosolewa. Hata ukimkosowa, akiliona ni zuri atakujalifanya mwenyewe baadae. Lakini kwa wakati ule wewe umeliongoza halitaki. Madam halikutoka kwake. Amekuwa kama Musollini wa Italy. Ile ingekuwa tumekishauri chama yasingefanyika mapinduzi. Hili jambo kabisa nakupa. Ilikuwa wale watu hatuwaamini. Tulikuwa hatuna fikra nyengine ziada. Siwezi kukudanganya. Lakini wale watu walikuwa si waaminifu. Wote walikuwa ni watu wazima, wazee, hawako tayari kupangana na chochote cha nguvunguvu. Ewe bwana wee ukumbuke miaka mingapi leo, arubaini, nilikuwa na umri gani hapo? Leo unambie mapinduzi leo, ntakubali? Sote tuloshiriki kupanga, na nini, ukiwatazama wazee wa Afro­Shirazi, wanaweza kutuzaa sote. Huna utakayemwambia akakubaliana na wewe. [Kwa upande wa Tanganyika] Kitwana Kondo alikuwa mlinzi wa Oscar Kambona. Hata tulipokwenda sie kuonana na Oscar, huyu tunaye. Tukenda Msasani kwake kule Oscar pwani majabalini huyu tunaye usiku. Sie tunaongea yeye kakaa kule. Huyu kaja Unguja, kama kesho kutwa tutaingia Ziwani. Kaja kafikia nyumbani kwa Saleh Saadalla Akida, Gongoni. Na kaja na ujumbe kutoka kwa Oscar kwa Saadalla. Ujumbe ule ulimwambia Abdalla Hanga, green light, go ahead, [endelea na mapinduzi] na siku ya mwanzo mtakapotangaza serikali yenu mie ntaleta askari kukulinda wewe. Sasa sijui alikuwa na maana gani kusema ntaleta askari nikulinde. Sasa siku ya pili, ya tatu, akaleta jeshi, jeshi aloleta ni askari wa FFU [Field Force Unit] wakiongozwa na Captain Baruti kutoka Kigoma na Inspekta Zonga kwao Tanga. Mie ndo nkenda pokea jeshi lile. Na tukawapeleka Mtoni. Hiyo ndio zawadi ya Kitwana Kondo. Pundugu alikuja, baada ya mambo kutulia, akawa polisi kama ni Naibu Kamishna kwa kuongoza kikosi cha polisi. Tulifikiria ingekuwa mapinduzi hayajafaulu tungelifanya nini na ndio maana tukawaondowa watu wawili wale [Hanga na Saadalla]. Najuwa wale kwa kuamini kwamba wale watafanya kila njia kupata msaada wa sisi hapa wa kupigana. Sisi siku ile tuloingia ndani ya mapinduzi tuliandika barua kwa President Nyerere, President Kenyata, na President Milton Obote. Tukazitia posta. “Tunataka kuondoa ukoloni wa mwisho.” Hatukusema tunataka kuondoa Waarabu. Tumesema tunataka kuondoa “last colonialism”. Ukoloni wa mwanzo wa Kiingereza uliulinda ukoloni wa Zanzibar wa Kiarabu. Kwa hivyo hii ya kwanza [ya Muingereza] tushaondoa, na hii [ya Mwarabu] tunaondoa. Tunataka mtutambuwe kwa haraka. Tuliiandika siku moja kabla. Hanga, Twala na Saadalla, na mimi, lakini mwandishi dhamana ni Twala. Timu yetu ya watu wane. Tumeandika wazi. Sie tunaingia Bomani na barua zinakwenda huku. Zimetiwa posta Dar es Salaam. Barua inasema: usiku tunachukuwa khatuwa hii, tunataka mtutambuwe. Na ndio sababu ilivoondoka meli hapa ya Unguja ilipompakia Mfalme na watu wake

Page 203: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 171

ikenda Kenya, ikakataliwa kupewa mafuta, ikakataliwa kukaa, wakakataliwa kushuka. Basi sijui kama wamepewa vyakula na vyenginevyo.5 Chini ya ushawishi wa Kiingereza, British High Commission [Balozi], na serikali ya Tanganyika, wakakubali wale kushuka [Dar es Salaam], na British High Commission ikawapokea kama ni wakimbizi, na ikawasafirisha Uingereza kwa usalama wao. Si ndo mara tu baada ya mapinduzi akaja hapa Waziri wa mwanzo wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya, tukanywa naye chai Ikulu. Jina lake linaanza na K [Mbiyu Kionange] mwembamba mwembamba hivi. Ndo alokuja hapa akaonana na Raisi na akafanyiwa party, na ndo siku alosema Karume kumwambia Jamali Ramadhani Nasibu, “hii ni nzuri kinywani lakini ikishaingia tumboni inakuwa kama farasi alokuwa hana khatamu, anakwenda mbio anakimbilia polisi tu. Basi usinywe.” Uganda hawajatujibu kheri au shari. Walikuwa kimya. Basi sijui tena baadae. Mambo ya kiserikali yanaishia kwenye cabinet ambayo mimi siyajuwi. Nyerere kaleta kikosi kile cha polisi. Barua amesaini kiongozi wa mapinduzi, Abdalla Kassim Hanga. Na yeye Hanga ndo alofanya ordha na watu wapewe medal [nishani], ya walopigana, na akampa Raisi Nyerere, kabla ya kuuliwa, kabla ya hata kufukuzwa. Basi sijui ndo hiyo ilomsababisha kufukuzwa, sijui. Tunavoamini sisi Ali Muhsin, shabaha yake yote ni kumuondowa Mfalme na kuifanya jamhuri nchi hii. Tunavoamini sisi. Pengine kweli, pengine si kweli. Kwa sababu sote tunaamini Ali Muhsin alikuwa hataki Ufalme. Sisi tunajuwa Mngereza anajuwa yote. Matokeo yake alileta manwari mbili zikasimama hapa. Moja Chumbe, moja Prison Island. Hata kama zile details [maelezo] walikuwa hawajazijuwa walijuwa mapinduzi yatatokea.6

Mimi binafsi, dadangu alikuwa ni mmoja katika viongozi wa wanawake katika ZNP. Siku ile ya mapinduzi Ali Muhsin alikuja mchana hapa na mimi nilikwenda kule kwa shangazi langu. Nkenda, nikakutana na dada, Ali Mushin kaja akanikuta mimi nyumbani. Tukaongeaongea maskharamaskhara, nikamwambia, “Sheikh Ali mimi naona kama mwisho wenu uko karibu bwana. Hamuwezi kuendesha hii serikali.” Akanambia “Mimi najuwa nyie magozi mnataka kupinduwa Unguja zamani gani.” Walikuwa wanajuwa. Dharau. Na dharau yao kubwa ni ilikuwa juu ya silaha.7 Wanaona hawa hawana hata bunduki, watapinduwa wapi. Na sie tuna jeshi kubwa huku. Hajui kwamba hili la huku lishakufa kama fimbo ya Nabii Sulemani. Kumbe imeshaliwa na mchwa imeshaanguka yote. Jeshi lilokuwa madhubuti ni Mtoni na limewahi kuzuwiliwa kabla hatukuingia mpaka likamalizika. Na lile lilikuwa jeshi kubwa, lile ndo special service, SS, wakiita Mobile Police Force. Mapinduzi, first shot round about [risasi ya mwanzo ilifyetuliwa] saa 1:30, 1: 45 alfajiri/asubuhi. Wale kuingia ndani, wale waliokuwa na Youth, wamepita kule, gari zilikwisha tiwa funguo, gari hizi za serikali, sasa wale madereva walokwisha tengenezwa kule walikuja kuvamia gari tu. Sasa zile gari ndo zilichukuliwa kubebea silaha, hizi za quarter guard huku, kwanza kupeleka Kijangwani. Halafu

Page 204: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja172

watu wametia wakipigapiga. Zikilia ovyo usiku zile. Hazina shabaha yoyote. Sasa hapa ndipo control [udhibiti] ya mapinduzi imepotea. Kwa sababu ilikuwa ni fujo tu, kila mtu akifika anapewa bunduki anapiga, akipewa bunduki anavunja nyumba ya mtu. Huo ndio mwanzo wa mapinduzi ya Unguja [Zanzibar] na ikamalizikia hapo. Sasa hapo kuna tatizo kubwa lilikuwa Mtoni. Wale waloingia Mtoni, kikosi cha polisi cha Mtoni kilipigana mpaka sisi huku [kutoka Ziwani] ikabidi tutoke twende kule. Sasa imeleta matatizo kwamba kituo cha Malindi kimesahauliwa. Kituo cha polisi cha Malindi kilivamiwa na maofisa wakubwa wa polisi kwa kuzuwia gati na upande ule wa kule wa palace [jumba la Mfalme]. Na huku ilikuwa lazim twende kwa sababu tukiwacha ile itakuwa na nguvu, na wale wana silaha nyingi kule. Tukabidi twende kule. Tukaacha kidogo huku. Kule walikufa watu wawili, wa kikwetu, lakini pia kuna askari wane watano walipoteza maisha yao vilevile na mmoja alodhurika zaidi na yuhai ni Ramadhani Haji. Alipigwa risasi na mlinzi lakini ilikuwa haikwendwa uzuri tumboni. Badili ya kuingia imepita. Kwa hivyo imemuunguza huku, matumbo yametoka, na alikuwa upande wangu, kwa hivyo alivokuwa karibu yangu lile shati langu mimi ndo nlovaa, ndo nlotowa nkamfunga mie, matumbo yalikuwa yashakuwa yako nje, akatiwa ndani ya gari na yuko kijana mmoja ambaye ni katika nduguze vilevile huyo. Huyo Ramadhani ni katika mmoja alotokea Youth League. Ziwani hakujakuwa na kazi, na ilianguka kwa urahisi, mara moja. Hakujakuwa na tatizo. Ilozuwiwa ilikuwa ndo hiyo [Mtoni] tu nlokwambia. Mtoni kulikuwa na mapigano. Sio madogo, makubwa kidogo. Kwa sababu baadhi yao wengine [wanamapinduzi] kule hawana ujuzi wa bunduki. Halafu, kulikuwa hakuna mipango mizuri. Sasa lakini sisi tulivokwenda tulikwenda kimabavu. Maanake ilikuwa hakuna njia nyengine. Tulikuwa na jamaa mmoja…akasema “jamani? Twendeni tu. Tuingie moja kwa moja pale quarter guard. Tukishaingia quarter guard, basi.” Hapa ndipo walipokufa watu wawili. Lakini tumeingia quarter guard. Tulipoingia quarter guard, likapigwa tarumbeta, tarumbeta lile lilipigwa quarter guard na ofisi kuu. Yule alopiga tarumbeta, alipigwa, amekufa yule. Sasa wale wanakuja kukusanyika kwa nguvu upande ule, sie tushachukuwa kila kitu. Iliwabidi wasalim amri. Wengi walisalim amri wakachukuliwa wakapelekwa, huku…gerezani. Wengine walikimbia. Polisi ya Ziwani, Mobile Police, walikuwa vijana wenye damu safi ya Kizanzibari. Haijakuwa nanii…chakachaka, hapana. Kwa hivo hata zile risasi zilokwenda za kuchaguwana kidogo. Ilikuwa ni damu ya Kizanzibari safi. Na ndo wengi wametolewa tolewa, nini, ah! Magereza haikuendewa. Magereza ilikwenda funguliwa tu na mob [watu]. Halafu kwa sauti ilotolewa katika redio, mahabusu wote watolewe huru, wakafunguliwa wale. Mtoni ndo kulikuwa na mapambano mazito. Na Malindi Police Station. Malindi ilikuwa chini ka Kamishna wa Polisi [Sullivan]. Palikuwa pazito mpaka akatoka Mfalme, akenda akapanda na watu wake ndani ya meli, ndo akatoka Kamishna na maofisa wake kwenda kule.

Page 205: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 173

Kuivamia Malindi hii ilipangwa Raha Leo wazi. Manake Malindi vikosi vyake vimetengenezwa va mkamatio hapa Raha Leo. Makundi tu ya Afro­Shirazi yalokuja, wewe utakuwa dhamana wa kundi hili, wewe utakuwa dhamana wa kundi hili, wewe utakuwa dhamana wa kundi hili. Baada ya vita va Malindi hata Raha Leo sikwenda tena. Baada ya kurudi kumaliza nikakaa nyumbani. Baada ya kurudi kule siku ya pili au ya tatu nkakutana na Ali Muhsin, Raha Leo. Anapanda ngazi, mie nateremka ngazi. Nilimwambia mie Ali Muhsin “umefanya makosa” Ngazini, ngazini. Manake kaja kujisalimisha mwenyewe, hajakamatwa. Kajileta mwenyewe. Halafu sikumuona tena Ali Muhsin mpaka nkaja nkamuona niko Magomeni mwezi wa Ramadhani ashafunguliwa, Dar es Salaam, msikitini tena. Yeye na Abudu, na alifikia Magomeni kwa jamaa yake fulani. Tukaongea pale. Akawa “mimi nakwenda Lindi kwa jamaa zangu.” Nkamwambia, “Ali Muhsin, mimi si mtoto. Mie najuwa unakwenda zako Arabuni na unapitia Tanga, tena sio mpakani.” “Ah! Tusiongee tena.” Nikamwambia “basi. Mie hayajanihusu. Nayajuwa. Mie tangu uko jela naijuwa njia utakayopita.” Mapinduzi tulivotaka ifanyike sivo ilivofanyika, lakini ingefanyika tulivotaka ingekuwa…tena wakati ule ilikuwa mob [kundi la watu] limeshaingia, fujo. Na ndipo alipokufa rafki yangu, Mapolo. Huyu alitoka Kitope. Huyu kafa Malindi. Yeye akiendesha gari ile, ya polisi tulochukuwa kule, akapakia watu, wakapita njia ya Hollis Road. Njia ileile tulosema isipitwe. Watu wateremkie Funguni, waje hapa kituo cha petroli, ndo inaitwaje? Auto Sale. Watokee pale, na wengine wapitie kwa Safriji, wapite Kokoni, watokee uwanjani Malindi kwa pembeni. Wengine wende mlangoni Malindi kuingia gatini. Hawakufanya vile. Wamekwenda mob mbele, wote wamekwenda Hollis Road, wale wako juu wanakupigeni wanakuoneni. Sasa Mapolo anafunguwa mlango, wale waliomo watoke, yeye kala chuma, kafa pale pale. Nimeskitika sana. Rafiki yangu mpenzi Mapolo. Myamwezi huyu wa Kitope. Mimi nilopoambiwa kuwa amekufa, nililia. Nimesema wangekufa wote wale afadhali (vicheko). Wale walikimbilia kwa kumzuwia Jamshid asipatikane. Sasa Malindi ilikuwa iwe hivi. Kaskazini ni kutoka Hollis Road kuja Malindi polisi. Hii ndo Kaskazini, isitumiwe. Watu wapite Funguni, waje Malindi, Jongeani, wakiwache Kituo cha Polisi cha Malindi, wapite katika kijia kile cha Bwawani, kwa leo, watokee Auto Sale, chini ya kituo cha polisi. Pale pana mikingo ya lile dude la barafu, ya Auto Sale, na kuna vituo va petroli. Si rahisi kupiga risasi pale. Na wengine wapite Darajani kwa Sapriji, watokee Kokoni, wapite Dega, watokee Malindi, ubavuni. Hizi ndo zilokuwa zangu mimi. Yale maagizo yote ya pale yalikuwa yangu. Hii nikimpa Ahmed Gharibu na kundi lake kubwa, ya Malindi, ya kupita Kokoni. Walikuwa wengi kwa sababu baada ya Ahmed kupitia njia ile kavuka, unaona hapa Makao Makuu ya Hizbu ilipokuwa [Darajani], akapita pale, kama Mbuyuni anakwenda, na pale palikuwa rough-rough hivi, mpaka karibu ya Kituo cha Polisi cha Malindi. Huku kaona kuzunguka. Ndo nkamwambia “Maalim namna gani?

Page 206: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja174

Umefanya makosa. Tungewakamata wote wale, manake wasingeliweza kutoroka.” Hakufuata amri. Na ndo hata wale waloingia Malindi kule akauliwa Mapolo. Walichukuwa njia ya katikati wakaacha kuchukuwa njia ya Malindi, Funguni. Ahmed Gharibu tulimwambia apite hapa Darajani police station, apite, pale kona ile inaitwaje. Dega, umefahamu, apinde kulia, anakwenda kama kwa yule Muhindi alokuwa akiuza vifuu yule, akiuza vifuu na maganda ya machungwa. Pana uchochoro wa maghala, palikuwa na maghala hivi. Njia nyembamba hivi. Mkono wa kushoto unakwenda kwa Sayyid Omar bin Smeit huku, mkono wa kulia unakwenda zako Kituo cha Polisi cha Malindi. Hapa katikati ndo kwa Omar Zahrani. Sasa ile ndo njia nyembamba ile ndo tulotaka apite ya ghala, ili atokee kwenye kile kikuta chembamba cha Malindi police station. Wakiingia mle wanavamia counter kwa mgongoni. Ile ya kupita Malindi, ilikuwa chini ya Mapolo. Kupitia Funguni, waje zao hapa. Kuna instruction [maelekezo] ambayo mimi binafsi naliongoza kikundi. Kupita Darajani police station, tukatambaa na line ileile ya njia ile, kwenye benki ile, moja kwa moja, mpaka kwenye garage ya motokari na petrol station, ambayo ndo pale polisi, hili hapa ndo jengo, hii njia unakwenda zako Malindi, Kokoni. Pale ndo zikaanza action, kuja kuandamana na nyumba zile zoote, mpaka hapa Baraza la Mji, halafu tukatokea duka la petrol station na zikiuzwa motokari. Hapa na pale. Tukitumia cover ya zile ngoeko za nyumba. Mapolo alikosea au hakufuata mipango. Wakapita Hollis Road moja kwa moja, katikati. Kwa bahati mbaya, Mapolo kufika kwenye [leo pana] traffic light, akapigwa risasi, akafa. Na pale yeye ndo alokuwa the first man to enjoy the bullet [mtu wa mwanzo kula risasi]. Wakati ule anapigwa, mimi namuona. Nalitokwa na machozi, lakini siku lose control. Nashukuru. Kwa hivyo tulikuwa na watu sita. Wawili walikuwa na machine gun, zile [kutoka Algeria] tukazipiga kwa pamoja. Wakati Ahmed Gharibu, kwa kutokea Dega, akawa anapiga yeye juu, walikokuwa wale. Kwao Ahmed Gharibu alipata risasi ya mguu. Ilikuwa kwa makosa kwenye kisigino. Kiatu (anacheka) kiliruka. Ilikuwa very nice joke [lilikuwa ni jambo la kuchekesha]. Na si rahisi kuamini. Lakini risasi ilipiga kwenye kisigino. Nilikuwa nimepanda juu. Sasa utapigaje? Sasa ungekaa chini pale wanakupiga na wewe huwaoni. Lile jengo lile, petrol station, ubavuni mwake, kuna jengo jengine, kuna ngazi, mpaka leo ziko pale. Pale ndipo unapopandia juu balcony. Juu wakikaa Wahindi, Bohora, walokuwa na biashara ile. Wasifadhaike kwa nini? Ilikuwa gari moja Simca, ndani mle, alikuwa mtoto…“kuna wezi wanataka kuiba gari chini”, anawaambia wazee wake. Kwa Kihindi mpaka Kiswahili. Yeye kila akisema wale wazee wale wanamvuta. Mie nilikuwa sina hamu hiyo [ya kuiba gari], wala sie hatujawa na hamu hiyo. Pale ndo zilipoanguka risasi. Nadhani polisi ilipiga risasi ndani mle lakini sijui kama iliuwa au haikuuwa, sina hakika. Walipiga.

Page 207: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 175

Kilikuwa ni kipindi kifupi. Kama dakika arubaini na tano au kama saa moja. Manake wale mpaka wamehakikisha Jamshid ameshaingia ndani ya meli. Mimi ndo nloongoza, na Mohamed Khatibu. Hawezi kunambia mtu jambo jengine. Na akisema atasema tu anavotaka. Mimi sipendi kuongea habari hizi. Na juu walikuwa chungu nzima na walikuwa wana risasi nyingi. Hatujapata fursa ya kukiuka kile kikuta kile, zilikuwa risasi zinakuja kama mvua pale. Yuko kijana mmoja, Khatibu Mohamed, maskini amekufa, huyu alikwenda kwa tumbo, na upande huu wa pili ambao Ahmed anakuja kwa tumbo, kwa sababu hawa wote walipata mafunzo ya kijeshi. Wote walikuwa asikari kabla. Ahmed Gharibu, na huyo Khatibu. Ahmed Gharibu alikuwa katika East Africa Education Corp, alikuwa mwalimu jeshini na aliondoka na cheo cha Sergeant-Major. Ami yake alikuwa mwalimu wa chuoni wa nyumba ile ya palace [nyumba ya mfalme]. Kazaliwa humo, kazaliwa palace, kakuwa palace, wote na wazee wake huko.8

Na Mapolo alikuwa polisi wakati ule. Sasa wanataka kuingia kwenye kile kikuta kile. Si umeona kikuta kile kimekuja nyuma hivi kifupi? Lakini kilikuwa kinatoka risasi ka mvua, hapiti mtu pale. Sasa pale ndipo zilipotumika Bren Gun (anacheka) kutoka Algeria, pale zimetumika Bren Gun, ndo hizo anozosema yule Kamishna Sullivan, hakuitambuwa sound [sauti ya bunduki] aliyoisikiya.9 Zilikuwa sita, huku na huku. Zimetumika, zilikuwa za polisi vilevile pale. Sasa upande ule mmoja, wa pili, ambao wangekuwa wamekwenda Mapolo, kuwazi. Ndio mlango mkuu wa kituo cha polisi. Kule ndo walokopita kina Sullivan na wenzake wote, na yule Banyani [Misra], nimeshawasahau kwenda kumtowa Jamshid. Sasa wale wote wakenda mwangoni kuingia gatini. Walipotoka pale sie tunafukuzia gatini. Sasa gatini ilikuwa pata nikushike. Hakuna kiongozi. Zilikuwa zinakwenda risasi kutoka Cine Afrique. Si ile alama ile ya round about, na gate ile, kwa kumzuwia Jamshid. Asitoke. Lakini kapita. Kwa sababu wale walioipanga mipango walikuwa ni maofisa wenye ujuzi. Kumbe hiki kishindo chote huku kilikuwa wao wameshamtowa na watu wake wote. Amur Dugheshi hata mapinduzi yuko? Baada ya mapinduzi ndo wamekuja wao. Musa Maisara ndo nlomuweka mie polisi. Manake yuko mtoto, huyu anoitwa Maulidi Mshangama, ndugu yake Maulidi Mshangama, Othmani. Yule alikuwa amekamatwa, sijui kwa kosa la trafik au nini. Akaekwa ndani sku moja kabla ya mapinduzi. Alikuwa Malindi kule. Mie ndo nlokwenda wafungulia. Ahmed Gharibu alikuwa Sergeant huyu katika jeshi. Alikuwa mwalimu na memba wa Action Group ya Afro­Shirazi. Sikiliza. Makao makuu ya mapinduzi ni Saleh Saadalla. Sasa kuna vikosi vilotoka mle na vinaripoti kwake. Sasa vingine wewe huvijuwi. Lakini tulikuwa na alama ya kitambaa tulifunga hapa siku ile, ndo tulijuwana, nani anaongoza wapi, nani anaongoza wapi.

Page 208: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja176

Mapinduzi na Muungano

Ama muungano hatukufikiria kabisaa. Sisi tulifikiri tuiwache iwe Jamhuri ya Zanzibar, na bendera tulitengeneza, na wimbo tukautengeneza. Alofanya habari ya wimbo, na habari ya bendera, ni Sergeant Juma. Mimi niliposikia imetangazwa Muungano kwamba Zanzibar imeungana na Tanganyika, mbona nilipata shoki ya maisha yangu. Kwa sababu mimi nimesikia asubuhi katika radio hapa alipokuwa akitengeneza kofia Mohamed Ashrak. Ushapita kwa Sapriji [Sapurji] hapa, kwenda kazini. Lakini Hanga alikuwa anajuwa habari ya muungano. Sisi tulikuwa tutaungana na nchi za Afrika ya Mashariki, East African Federation. Ilikuwa msemo upo kabla ya uhuru. Sisi tuliunga mkono hii. Saadalla ni hiyo nlokwambia, Jamhuri. Sera zetu hazikuwa zikifahamika khasa. Hakuna kikao kilokaa kupanga sera. Hata. Asikudanganye mtu bwana wee. Sie hamu…tazama kitu kilikuwa…Kutawaliwa tena tulikuwa hatutaki lile lilokuwa mbele ya macho. Hayo tuliwachia tukishinda watu wafikiri. Kutawaliwa tena iwe basi. Zanzibar lazima iwe Jamhuri. Na haijakuwa na dhamana au fikra za kusema tutauwa Ufalme, hakuna. Tutakuwa hatuutaki Ufalme. Na katika kukubaliana kwetu, jamii ya Kifalme ijengewe mahala. Tuseme kwa mfano. Kama Kizimbani, inafanywa hivi kipande cha ardhi, lakini sio Kizimbani. Hapajaamuliwa wapi watajengewa. Lakini hiyo imoo. Wasidhuriwe manake. Awekwe mahala akae na kipande chake cha shamba kujitafutia maisha yake kama watu wengine. Na sijui ilikuwa kama muda gani wa kupewa maisha ya kujitegemea. Iko hiyo. Tuliandika kibuku hichi, kijitabu kidogo, “How to deal with the royalty” [Vipi kuushughulikia ufalme]. Tukishapata serikali, hawa watu tutawafanyaje? Kwa mfano imekubaliwa Kibweni, tuseme hii nyumba ya ufalme, na kipande hiki chake cha kutumia, katika maisha yake, na muda wake, sijui mda gani, wa kuweza kupata usaidizi wa kifedha na matumizi ya kila siku, kwa ajili ya kuweza kujirekebisha. Sote watu wane. Lakini mwandishi dhamana ni Twala, “the high code com-mando.” Ewe bwana, Twala alikuwa mtu bwana! Ah! Yakhe, wamewauwawauwa hawa fitina tu, ehe. Baada ya mapinduzi ndo wameuliwa ati. Hanga, Twala, Saleh. Walouliwa pamoja ni Hanga, Twala, na Khamis Salum Beni.10 Ile kabila yake ya Kiarabu siijui, nimeisahau. Siku moja hao. Mohammed Omar “Masharabu” alitiwa ndani, lakini hakuuliwa, aliteswa kidogo tu. Mtu wa Dar es Salaam pale. Huyu alikuwa auliwe naye pamoja, yeye na Simba Ismail. Lakini hawa kwa sababu ni watu wa Tanganyika [na Uganda], walitolewa wakarudishwa kwao—Okello, Mfaranyaki, nk. Wakawachwa huru. Mohammed na Simba walinieleza namna walivouliwa Hanga, Twala na Khamis Beni. Walifungwa kamba kwenye mti mkubwa, na…[memba watatu] wa Baraza la Mapinduzi wakawa wanaivuta hivi na kuiwacha, na katikati yuko mtu na pauro akimpiga nalo kichwani Hanga

Page 209: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 177

mpaka kampasuwa.11 Kikatili kabisa wameuliwa. Wacha bwana, tusiongee habari hii. Juma Maneno tena alikuwa opportunist [mbinafsi]. Alikuwa tena hata sisi alikuwa kutuona hataki. Akatuacha mkono. Alifika kuwa Kanali na nafikiri alipigana vita va Uganda. Yakhe unajuwa. Sijui kiasi gani utaweza kukubali. [Mapinduzi] yamefanyika bila ya fedha. Lakini kuna kitu kimoja. Kwa sababu, wale watu wawili, walikuwa memba wa parliament, wakipata marupurupu. Sasa ile allowance [marupurupu] yao ndo tukigawana sisi tunokwenda mbio. Wakitoa kutoka mifukoni mwao. Hatuna pesa zozote. Si Oscar, si nani. Hakuna alotusaidia pesa “bunda hili, hii fanyeni.” Basi sijui, kama mtu kapata akiiba, haya. Lakini mie najuwa hakuna. Kwa sababu watu tulokuwa nao na watu wangepokea pesa ni watu waaminifu. Hanga na Saleh ni watu wakweli sana. Kama Twala alikuwa hana pesa. Hana allowance yoyote. Ana allowance ya trade union. Labda wakimgaia senti ishirini na tano, kumi, bas. Lakini hao watu wawili ndo walokuwa na allowance.12

Yusuf Himidi silaha kazitowa wapi? Maneno ya uongo hayo bwana. Achana nayo. Mimi habari hizo za watu kina Yusuf Himidi, mimi sizijuwi. Mimi naamka asubuhi nasikia wao waheshimiwa. Vipi, namna gani, sijuwi. Kwa hivyo kila ntakachosema ntasema uwongo. Inaweza kuwa ndiyo, inaweza kuwa siyo. Kwa sababu kuna kikundi cha Youth League, lakini kwa gari ya PWD kubebea mchanga wakati ule na akabebea silaha, ni jambo lisilowezekana kabisa. Security ilikuwa very highly tight.13

Mambo ya hao wa Chumbuni, na wapi na wapi, mimi siyaelewi. Lakini najuwa kuna section ya Youth League, ambayo wakija chukuwa ripoti kutoka kwa Saleh Saadalla, wakati wote. Hawa, wakiongozwa na Natepe na Seif Bakari. Sasa mambo yao… manaake kuna kitu kimoja utaona ajabu. Nikikwambia mie hata huyu mtu mmoja akiitwa nani?…Okello, mie simjui. Organization [mipango] iliachiwa Youth League. Twala ndo alokuwepo hapa. Na Twala alikuwa ndani ya action. Kaingia Ziwani. Saleh na Hanga tuliwaondowa. Hata Karume aliondoshwa na yeye. Jimmy Ringo ndo alomuondowa. Habari ya Nyerere mimi baada ya kiasi hicho siwezi kukwambia, kwa sababu hatujapata kukutana mimi na yeye. Baada ya siku ya pili ya mapinduzi, serikali ya Tanganyika walileta kikosi kimoja cha polisi, hawa Field Force, chini ya Captain Baruti. Mimi ndo nlokwenda ipokeya gatini. Oscar alikubaliana na sie. Oscar kakubaliana na sie. Lakini, ikiwa kashauriana yeye na Raisi wake hayo mambo mie siyajuwi. Kulikuwa hakuna kiongozi yoyote ziada ya hao nilokutajia wanojuwa mapinduzi hayo. Chama cha Afro­Shirazi hakijaingia ndani ya mapinduzi. Wanachama wa Afro­Shirazi ndo walopinduwa.14

Kina Sefu Bakari na Natepe walikuwa hawawezi kuwaambia viongozi wakubwa wa ASP, kwa sababu ni kitu cha siri. Chama cha Afro­Shirazi hakijapinduwa, hakijakaa katika kiti kuamua kupinduwa. Mapinduzi yamefanywa na wanachama

Page 210: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja178

wa Afro­Shirazi bila ya kujuwa Chama cha Afro­Shirazi. Baada ya mapinduzi wanachama wakawakabidhi chama chao. Hanga, Twala, Saadalla, hawa walikuwa viongozi wenye nguvu za utekelezaji katika chama. Hawa katika Chama cha Afro­Shirazi, ni executive [wana nguvu za utekelezaji]. Ndo mapinduzi yalivyo. Hata ukisoma historia ya Urusi Lenin hakuwa Raisi wa chama chao. Na chama chao kilikuwa hakijuwi mapinduzi. Kimefanywa na Lenin. Na ingekuwa kimeambiwa chama yasingelikuwepo mapinduzi. Hawana hamu hiyo wale watu. Watu wengine walikuwa hawataki. Sasa ungelikuwa mvutano, maneno, mpaka habari zote zikatoka nje. Babu ni Hizbu, moja kwa moja. Na akitumiwa na China. Na wakafukuzana na Ali Muhsin. Babu hakuwa mwanachama wa Afro­Shirazi. Hajapata. Saleh Saadalla ndo alomuondosha Babu, kwa kumtumia mkewe na buibui la mkewe, kwenda kumtowa kule nyumbani, akenda akavishwa. Ilikuwa akamatwe na nanhi… Basi ikiwa kuna mazungumzo ya mapinduzi, na nini, kaongewa na kina Saleh, hukohuko Dar es Salaam, lakini siyo Unguja. Kaambiwa tu, watu watapinduwa. Hanga na Saadalla wakimuamini Babu labda aslimia sifuri. Haaminiki ati Babu, tunamjuwa ni muongo kutokea mwanzo. Watu wote wanamjuwa hapa, viongozi wa Afro­Shirazi, wa Hizbu. Anajulikana Babu. Ni mtu rahisi. Ni rahisi kutumika. Kusafirishwa kwa Babu kutoka Unguja…alikuwa Ali Muhsin, au serikali ilokuwepo, ni serikali, maanake Ali Muhsin peke yake si kitu. Serikali ilikwisha pendekeza kumtia ndani Babu. Sijui kumfungulia kesi gani na gani. Ikabidi atoroke. Ile kesi ilivopatikana habari, huku upande wa Afro­Shirazi, Saleh kama ni mtu mwenye kufikiri…tumemkosa mtu mzuri sana sie Unguja, akasema “kwa nini hatumsaidii?” Ikakubalika. Akenda usiku, kama saa ngapi sijui, akapelekewa habari Babu akakubali, tukenda. Mimi, Khamis Beni, na mkewe Saleh Saadalla, Sauda bint Haydar wa Kisutu, Dar es Salaam, kwao Bagamoyo. Tukenda. Sasa sisi tulipokwenda tulikutana na asikari pale, lakini tumeteremka watu watatu na mwanamke. Tukaingia ndani, Migombani huku, buibui la Sauda akavaa Babu, sasa tunamwambia “wewe tukitoka uringeringe kidogo”. Dereva wa gari alikuwa Ali Saidi, taxi-driver, tulimchukuwa, kwa sababu yeye huyu alikuwa ni memba wa mapinduzi. Alikuwa ni mwenzetu. Tukampita asikari, akaingia ndani ya gari ile, tukatoka tukenda Kizingo. Kizingo Babake Fuko, mzazi, alikuwa na ngarawa na mwanawe mdogo, Huseni, ndo akapakiwa Babu kupelekwa…kateremkia Mlingotini. Akateremshwa pale, sie tukarudi huku. Sauda sijui karudi na chombo gani. Na ndo hivo hivo alovokwenda Mzee Karume. Hapo hapo kapakiwa ndani ya ngarawa na Jimmy Ringo, kenda Bagamoyo. Jimmy Ringo ndo alomuondowa. Jimmy Ringo akijuwa mapinduzi. Alikuwa katika group la Youth League. Tulikuwa

Page 211: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 179

tunajuwa sie. Ndo alokwenda mchukuwa kule, na alomsafirisha ni babake Fuko. Jimmy Ringo hakuingia Bomani wala Mtoni. Alikuwa na Karume pamoja huko, kakimbia na yeye. Hajakuwepo hapa. Aliondoka naye Karume yule. Mie nakwambia, silaha zilivotolewa Ziwani zikaletwa Kijangwani. Wakati jengo la radio hatujalipata! Bado! Asubuhi nimekwenda kwa Mzungu alokuwa na ufunguo wa radio. Alikuwa hukuhuku Migombani. Tukamfata. Iko nyumba moja ukishapita, hii ya Karimjee mbele ina vigae vitupu hii, basi nyumba ya pili yake ndo akikaa. Nimekwenda asubuhi mie anakula chakula cha asubuhi. Ujuwe mapinduzi yamekwisha wakati huo. Ziwani ishachukuliwa, Mtoni ishachukuliwa, pa kuweka bunduki hatuna. Bunduki zinatolewa kulekule…tukenda tukaja funguwa, tukafunguwa na mlango wa pili, ule mlango ulokuwa na dirisha kubwa linotazama uwanjani, ndio zilipotiwa silaha. Na katika silaha zile, alikuweko Sergeant Simba Ismail, dhamana wa silaha, na Sergeant Ngusa, wakitia zile bolts. Halafu akaja Abdalla Juma Bulushi wa Umma Party, akaja pale na kuwasaidia. Mzungu alikataa kwanza kutoa ufunguo, alisema ufunguo uko kwa Mmarekani kwenye ubalozi wao. Nimemkuta anakula, yeye na mkewe pamoja, na mtoto wao, apata hivi [mdogo]. Mimi binafsi, nilikwenda kule, tulifuatana, tulikwenda na gari ya Land Rover ilokuwa polisi, dereva akiendesha yuko kijana mmoja, alikuwa polisi hapa, alipewa upolisi na serikali akawa hana sehemu. Nani jina lake? Mohamed yule? Mohamed ndio. Yuko mwengine yuko Raha Leo mpaka leo yuhai, anaitwa Muadhi, aliajiriwa usalama, na yuko mmoja, huyu watatu sijui nimemsahau. Huyu Mohamed alokuwa akiendesha gari mtu wa Kilwa. Huyu Muadhi sijuwi wapi kwao, yupo Raha Leo hapo. Na huyu mmoja nimemsahau jina lake. Mie nikamwambia yule Mzungu, “Kuna moja kati ya mawili.Tupate ufunguo au niitowe roho yako!” Nimekaa tayari. Nna bunduki Mac 4 na pistol. Nna vitu hivi viwili. Akainuka akachukuwa ufunguo tukenda akafunguwa tukaingia ndani, radio ikatangaza, yale mambo yakawa yanafanya kazi. Mimi Mzungu huyu nikaja tukakutana tena Dar es Salaam, katika benki ile, inaitwa “Clock Tower Bank”. Pale ndo nilipokutana naye. Akantazamaa! Akaniambia, ndie wewe Mr.…? “Ndiye yuleyule, hakuna mabadiliko.” Tukazungumza kutaniana pale, akenda zake. Sikumuona tena mpaka leo. Ama mimi kutoka pale baada ya kazi hiyo ndo nkenda kumchukuwa Aboud Jumbe. Kwake. Tena aliponsikia sauti yangu akaingia chooni. Akafungua maji akajitia na sabuni na mwanawe mwanamke mdogo, Fatma. Ananiambia “nini?” Namwambia “hapana,” twende zetu huku, mambo tayari na wewe ndo Seketeri wa Mipango wa Chama [cha ASP]. Kituo cha polisi cha Malindi hakijakamatwa bado. Kashtuka. Mpaka aliponiona mie. Mie ndo nlokuwa seketeri wake kwenye mambo yote. Ndo mwisho alikuja kunlaumu, anasema “basi mnafanya mambo hamtwambii?” Nikamjibu “ndo mambo yenyewe yalivyo.” Akenda Raha Leo. Kikosi cha mwisho alichokipeleka kilichokwenda aliki­

Page 212: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja180

peleka yeye. Aliwaita pale watu, nani…, akampa chaji Ahmed Gharibu, kwenda. Hichi ndo kilokwenda kikamaliza, basi. Lakini zilikuwa ghasia zimemaliza. Na kule zimekwisha vilevile. Aboud Jumbe hakuambiwa na mtu. Aboud Jumbe kujuwa mapinduzi kumwendea mimi kumchukuwa. Mimi binafsi kwa mkono wangu, na kwa mguu wangu, ndo nlokwenda mchukuwa Hasnu Makame kwake, Idris Abdul Wakil, na Aboud Jumbe, kuwaleta Raha Leo. Walikuwa hawajuwi chochote. Usihangaike bwana. Hii ndo picha halisi. Na unaweza kumuuliza Aboud Jumbe. Nimemkuta chooni. Kanikimbia mimi. Kaingia chooni. Na mwenyewe kwa kauli yake, akaja akaungama mbele ya nduguye, kwamba nyinyi mnafanya mambo haya hata hamtwambii sie? Tuko Dar es Salaama! Yupo Yusuf Jumbe, yuko Aboud Mwinyi Mgeni, yuko Hamisi Mparama, yuko nani huyu? “Mmanga”, yuko Maalim Ramadhani alokuwa na nanhi pale…, yuko kijana mmoja “Mwinyi”, yuko ndugu yake Ahmed Gandhi. Pale ndo kasema. “Nyie basi mnafanya mambo hamtwambii?” Karume alikuwa hanipendi. Sijui kwa nini, akinchukia tu. Akiniona nakwenda zile safari zangu nnazoenda ni nyingi na hazijui, na za kisiasa, alichukia, alikuwa ananchukia, kweli najuwa akinchukia. Na mie nilipojuwa kuwa ananchukia baada ya mapinduzi ilipoundwa serikali, mie nlikataa. Nlikataa kabisa kwa kutafuta amani yangu. Kwa sababu mie simchukii. Serikali ya mwanzo alikuwa Karume ni Raisi bila ya nguvu za utekelezaji. Waziri Mkuu na mwenye nguvu za utekelezaji alikuwa Abdalla Kassim Hanga. Waziri wa ilimu alikuwa Othman Sharifu. Waziri wa Afya, Aboud Jumbe. Waziri wa Mawasiliano na Kazi Idris Abdul Wakil. Waziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi, nlikuwa mimi kwa siku tatu. Mambo ya Nje hakuwa Babu. Babu alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje baada ya mageuzi.15 Alikuwa mtu mmoja nimemsahau. Hasnu Makame alikuwa Waziri wa Fedha. Twala alikuwa Naibu Waziri wakati ule. Alipokuja kuwa Waziri wa muungano ndo akawa minister. Sikumbuki uzuri, ndo mpaka hapo. Sasa hao, kwanza ilotangazwa mwanzo ndo hiyo. Hii ilitangazwa bado Karume yuko bara, hajafika hapa. Bado kabisa! Na ikatangazwa, tena ilitangazwa asubuhi. Sasa nani alitangaza hii? Kuliingia matatizo mengi sana hapa baada ya kazi kumalizika. Katika kupanga vyeo uliingia ugomvi, mvutanovutano, ufisadi wote uliingia siku hiyohiyo. Mara moja, wakati mmoja. Nadhani ilichapishwa. Ilichapishwa ndio. Mmmh! Mimi sikuona gaazeti. Mimi binafsi sikuona gaazeti. Kama imechapishwa…mimi sikuona. Manake, baada ya kutangazwa tu Karume kuwa Raisi, mimi hamu yangu ilikufa kabisa. Kwa ukweli. Kwa sababu nilijuwa hakutokuwa na amani. Baada ya Karume kuwekwa Raisi, ndo akafanywa Waziri Mkuu [Hanga] kuwa ni Makamo wa Raisi. Yakhe, hilo ndo jambo limenikera mimi zaidi hata kuliko yote. Kukubali Hanga mimi kumenikera.

Page 213: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 181

[Mimi] sikutia saini document yoyote. Hata sku moja. Hata ofisini skuingia. Na karibu wote walokuwa kwanza hawajuwi lini wameingia. Mpaka alipokuja Karume akachaguliwa na nini. Sijui ile picha imekwenda wapi? Ilikuwa picha hapa kwangu ya Baraza la kwanza la Mawaziri. Hata ile picha tulopiga na kikundi cha wanamapinduzi tunatoka juu hapa, People’s Palace. Na wale watu wote ungeliwaona mle. Hata huu mkono wangu ulokuwa umeumia, ile kwenye picha ipo, na ile kitu nlotiwa hapa, ambayo ndo sababu ya maumivu yangu ya macho. Huu mkono nimeufunga hivi. Anyhow, mapinduzi yalikuwa mazuri. Yalifaulu vizuri. Viongozi walikuwa wote wasomi. 100%. Pale mambo yalipokwisha kuwa tayari asubuhi, mawasiliano yalikuwa kupitia Radio Zanzibar. Hatukuwa na njia nyingine za mawasiliano. Mimi sikwenda hata sku moja. Sijapata kuwa Memba wa Baraza. Watantia wapi na Mwenyekiti Karume? Mie nlikataa hasa kazi. Baada ya mapinduzi nlikaa kama miezi mine. Hapo, kwanza nimekaa nimetangazwa nende Kilimo. Nlikuwa ndani ya radio nimesikia, siku ripoti kokote. Nikaja nkakaa. Akanjia Hanga hapa ananambia Raisi anakupeleka uwende polisi utavaa nyota tatu, Captain, nikamwambia “mie staki.” Mie sina imani na Karume. Kwa kunchukia kwake. Na ndivo nlivyo. Maanake, hata huko kilimo nlokopelekwa na yeye Karume nikawa Assistant Secretary…kutoka hapo nikafukuzwa 1965. Haya mtu uliyeajiriwa kazi na serikali unafu­kuzwa kama mtu alochukuwa maji ya taka kama nilivotupa mie nje hivi umepata kuona wapi? Naelewa ile kazi au vipi? Sio leo unamuondosha Trimblet, Assistant Agricultural Director, unakuja kuniappoint [kunichaguwa] mie! Kuchukuwa nafasi yake. Sasa bila ya sababu, kujuwa kwa nini nimefukuzwa, nikaandikiwa, nikaambiwa, hakuna. Watu walivokuwa wabaya hawa. Kwa sababu hiyo ndo kauli mbiu ilokuwa ya Mzee Karume. Wazi, kila mtu anajuwa. Akisema hadharani “wakimbieni wenye ilimu.” Sasa yeye kapata utawala ndo wenye ilimu atawapa kazi kweli? Basi wewe utakwenda mchukuwa Sergeant-Major Saleh Saadalla Akida, the ex-military Sergeant-Major, the Sergeant-Major in the British Army, Second World War, Education Department, huyu ni mwalimu wa skuli. Nadhani alikwenda Burma, alikuwa katika Education Department. Nafasi yake inakuja kuchukuliwa na Hassan Nassor Moyo. Afadhali Moyo ni seramala. Akaja akabadilishwa akapewa Saidi Idi Bavuai! Chama cha Wafanyakazi wenyewe kilijiunga na Chama cha Afro­Shirazi. Ni Twala ndiye aliyehusika na mapinduzi. Yeye alikuwa ni seketeri wa chama cha wafanyakazi. Lakini yeye ndo alokuwa anahusika kuwashawishi wale wenzake kwenye trade union kuunga mkono. Wengi walikuwepo wengine. Siwajuwi, siwakumbuki. Wazungu ingekuwa wameshirikiana tungemkamata Jamshid ati. Nakwambia wameizuwia Malindi na upande ule ukawa safi, wakampeleka Jamshid na watu

Page 214: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Moja182

wake wanotaka wote katika meli wakaizuwia na wakaiongoza meli chini ya ulinzi, mpaka ikafika Mombasa, ikakataliwa, ikaja Dar es Salaam, Nyerere akawapokea akawafanyia safari wakenda zao England, wote. Isa Mtambo tulikuwa “signal” pamoja na hapo siku tulokwenda sisi mara ya kwanza kuweka miguu yetu kwenye ofisi ya Waziri Mkuu, yeye yuko pale, assistant secretary. Tena assistant secretary wenyewe, mapokezi, kupokea watu. Baada ya mapinduzi alipewa cheo cha Mkuu wa Mkoa, sijui Tanga, au wapi.

Kifo Bila ya Matanga—J. J. Mchingama

Katika kifo cha Abdalla Kassim Hanga na wenzake, kilipotokea, Othman Sharifu alikuwa na kaka yake ambaye ni mkuu wa mkoa Pemba akiitwa Ali Sharifu. Wakati waliponyongwa, mwaka 1967 au 1968 katikati hapa, ukatumwa ujumbe kupitia jeshini.16 Ukapitia jeshini akapelekewa Mkuu wa Mkoa ambaye ndugu yake ndio ameuliwa. Wakenda kumchukuwa Ali Sharifu kutoka ofisini kwake mpaka makao makuu ya jeshi Pemba. Kule akasomewa ujumbe kwamba imetumwa taarifa ya kuuwawa kwa ndugu yako Othman Sharifu. Baraza la Mapinduzi limeamua kuwauwa Othman Sharifu, Abdalla Kassim Hanga, na wenzake, kwa sababu walikuwa wanakwenda kinyume na matakwa ya chama na Baraza la Mapinduzi. Kwa taarifa hiyo huruhusiwi kuweka msiba wala tanga, na popote mtakapokutikana, watu wawili au watatu katika familia mmekaa, Baraza litajuwa kwamba mnafanya msiba na mtachukuliwa hatua. Baada ya kusomewa akaambiwa umefahamu, akajibu nimefahamu, lakini nataka kuuliza. Akajibiwa kwamba utaziuliza salamu? Wewe umepokea, sema nimepokea! Imekwisha! Anajibiwa na mkubwa wa kikosi pale Pemba. Mkuu wa kikosi wakati ule alikuwa akiitwa Tirace Lima kwao huko huko Pemba sehemu za Kangani, lakini sasa ni marehemu. Basi Mkuu wa Mkoa akatia saini kwamba ameiona na ameipokea hiyo message na akaondoka. Lakini bahati mzuri kutokana na mwenendo huo hayati Mwalimu Nyerere aligunduwa akampa uhamisho Ali Sharifu kutoka Mkuu wa Mkoa Pemba na kumpeleka Tanzania Bara. Huko sijui alimalizikia wapi. Hiyo ndo hali ilikuwepo hapa. Kwa hivo zile chuki na kutiliana mashaka kulikuweko ndani ya uongozi wenyewe kwa wenyewe. Vurugu gani lilitokea ndani yake hata hawa ikabidi wauliwe sikuelewa ni nini. Message ilitumwa tu hivi. Ina maana Baraza la Mapinduzi liliamua hivyo. Sasa inawezekana ni hitilafu iliotokea tokea mwanzo, kutoelewana kati ya wasomi na wasiosoma. Inawezekana ni hiyo iliendelea mpaka kufikia 1964. Kwa hiyo hali kama tutaendelea nayo kuwa tunakumbuka ya nyuma itakuwa kila siku tunaendelea kulipizana kisasi, jambo ambalo hatuwezi kujenga hii nchi. Hatuwezi kuendelea. Kilochobaki ni kusameheana yalopita. Wote tuwe kitu kimoja tuweze kuitengeneza hii nchi kwa sababu sote ni kitu kimoja. Hata kama tuna hitilafu za kirangi, kidini, hiyo isisababishe kwamba tusiwe watu wamoja. Nchi mbalimbali tunaziona zina watu

Page 215: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Katibu wa Midani ya Mapinduzi 183

wa makabila mbalimbali, matabaka mbalimbali, lakini wanajenga nchi yao. Hivi ndo navoona mimi maoni yangu. Hawakuweka msiba. Kulikuwa na vikosi maalum vikitembea kila family ilotolewa hukumu ile basi kila familia ilikuwa inafuatiliwa. Ilikuwa mimi na wewe kama ni familia moja tusikae pamoja baada ya tukio lile. Wakitukuta tumekaa pamoja wanakwenda kuripoti. Mimi nafikiri kwamba kwanza kule nyuma tulikotokea Baraza la Mapinduzi lilikuwa na nguvu na watu wengi walikuwa wanaliogopa lile baraza. Kwa hivo hata kama kuna Mwenyekiti mwenyewe lakini alikuwa anaogopa nguvu kubwa kutoka kwa wajumbe wa baraza. Kwa hivo anaweza kusema nikisema hivi baraza linaweza kunigeuka likanifahamu vibaya kwa hivo wacha nende ninavokwenda. Nafkiria kitu kama hicho. Sidhani kama serikali itajibu. Haitojibu kwa sababu yenyewe hiyo serikali yenyewe haina hata hiyo historia yenyewe au kumbukumbu yoyote ile na kama inayo basi imehifadhiwa isikumbushwe. Ukikumbusha utaleta balaa la familia la wale waliouliwa kuwa wanaweza wakafanya, pengine wakashtaki kwenye mahakama za kitaifa, wanaweza kuyalalamikia mataifa, ili wajuwe pengine kitu kama hicho. Kwa hivo wanapojaribu kufatilia wanaweza hata kushindwa kupata maelezo kamili. Wao wanahisi kwamba kutoa habari hizi kwa familia ni kuibuwa mzozo mpya. Linyamaziwe hivohivo ingawa wale wanaungulika, wanaumia, lakini bora linyamaziwe hivo hivo. Lakini sasa hatari zake kuna siku litakuja kuibuka likawa mzozo mkubwa zaidi kuliko hivi sasa pengine wangefanya likajulikana kuliko kulimezea. Kwa sababu wanasema kwamba moto unaotisha zaidi ni moto wa makumbi. Lakini hawa watu kweli wameuliwa. Wameuliwa na ni watu wa Afro­Shirazi. Lakini migongano ndani ilikuwepo. Wale [watu kumi na tisa] inasemekana waliuliwa Kibweni, KMKM [kikosi cha wanamaji na kuzuwia magendo] pale. Ndo walivonizungumzia wale [platoon yangu] mimi baada ya kurudi safari zangu kunihadithia kwamba wanatoka Kibweni walikwenda kutekeleza majukumu hayo [ya kuuwa]. Ilitangazwa hata kwenye vyombo va habari, tarehe fulani kutakuwa na mazoezi ya shabaha ya KMKM, hawaruhusiwi wavuvi kupita maeneo hayo. Kama sku tatu mfululizo iliendelea kutangazwa. Lakini watu wengi tukajuwa hivo, kuna zoezi, na pale wao wanafanya mazoezi na kumbe mazoezi yale siku ile yalikuwa na shabaha nyengine. Mambo yalikuwa makubwa sana. Manake kama hali ile tungeliendelea nayo tungekuwa katika hali mbaya sana.

Page 216: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na MbiliWaafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika

Tukimpinga yoyote yule aliyekuwa akifanya kazi kwa maslahi ya Ufaransa au Uingereza. Mpaka hii leo niko dhidi yao. —Ahmed Ben Bella

Mzee Aboud “Mmasai”

Algeria ni kitu chepesi kufahamika. Nilikwenda Algeria kabla ya mapinduzi na ipo picha nilopiga mie na Ben Bella na watu wengine. Tulikwenda mwishomwisho wa mwezi wa Novemba [mwaka 1963]. Mimi, Twala, Ali Mwinyi Tambwe, yupo kijana mmoja akiitwa Khatibu. Tuliondokea Dar es Salaam kwa ndege. Tumepitia Addis Ababa, Ethiopia, Jordan. Msafara wenyewe ulikuwa mzungukomzunguko. Hatukwenda moja kwa moja. Safari sisi tulipakiwa kama mizigo. Alotowa fikra ya kwenda Algeria kwa kweli alikuwa Oscar [Kambona]. Manake unajuwa, kitu kimoja nataka…Hanga alikuwa hawezi kufanya kitu chochote bila ya kumshauri Oscar. Alikuwa rafki yake sana. Waliishi Ulaya pamoja nasikia. Walikuwa wako karibu sana sana…Kutoka Jordan tukaja Sudan, halafu ndo tukenda Algeria. Ilikuwa ni safari ya kubabaisha. Sie tumekaa Algeria sku tatu. Hatukukaa Algiers. Tulikaa kwenye kijiji kimoja karibu ya kilima. Pale ndo tuliwekwa sie na Ben Bella alikuja kule na mara nyingi akija laasiri. Tulikuwa na mtarjumani wao. Kulikuwa na jambo moja la viongozi wa Kiaafrika. Walikuwa wanataka kufanya Umoja wa Afrika kama alivokuwa anataka Kwame Nkrumah. Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yameshafikiriwa Zanzibar, sasa watu wa Zanzibar wakitaka silaha za kuwasaidia. Ndo kitu kilichowapeleka na lengo kubwa ni sisi tumepata kura nyingi lakini tumenyimwa.1 Kuna mapendeleo baina ya Waarabu na British Resident, serikali. Iliwapendeleya hawa. Hiyo ndo sababu tulozungumzia kule kwa Ben Bella ili atusaidie kupata silaha. Kakubali baada ya maneno mengi. Halafu tukaondoka sisi hatukupata kitu. Nasikia wakenda watu wengine mimi siwajuwi.

Page 217: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 185

Nadhani hata Oscar [Kambona] alikwenda. Huku kwetu sie aliondoka Saleh [Saadalla], ndo alikuwa Mwenyekiti wetu kwenda kwa Ben Bella. Hapa Zanzibar aliondoka, Saadalla, na mie, na Twala, na Khatibu, basi. Tambwe tulikwenda naye. Si alitumwa na Oscar. Tulikuwa na mtu mmoja mwengine lakini simjui nani. Alikuwa mtu wa bara, alikuwa katika ofisi ya Mambo ya Nje lakini simjui uzuri mtu huyo. Mimi nilijuwana naye katika hiyohiyo safari. Nadhani tulikuwa tunafika watu wanane. Tukaekwa katika nyumba ya nje kilimani kule. Aloanza mazungumzo ilikuwa ni Saleh. Na ilitakiwa aanze yeye kwa sababu yeye ndio Mwenyekiti wa lile tendo lenyewe. Na ndo mwenyewe katika nchi, wale wengine ni katika msaada wa kutufikisha sisi pale, hawajuwi kitu. Na Saleh neno lake aloanza mazungumzo…Ben Bella alikuwa na watu wake pale. Sijui walikuwa wangapi. Nasikitika, ile picha ngelikuwa nayo hapa. Nilipiga na Waarabu fulani walikuwa wamevaa vilemba. Ben Bella alikuwa amevaa nguzo za kijeshi. Wale waliovaa vilemba kwenye ile picha tulopiga Algeria walikuwa ni watu wa kule kule. Sio sie. Tena ni watu wakubwa kwa sababu wale ndo walo­kuwa wanatufundisha mambo yote. Na ndo alokuja nao yeye [Ben Bella] siku ya awwal. Hawa watu watatu vigogo hivi vinaonekana. Sasa Saleh alisema hivi: sisi hatukushindwa katika uchaguzi. Uchaguzi sisi hatukushindwa. Tuna viti vingi kuliko ZNP. Sisi tuna kura nyingi kuliko kura za ZNP na ZPPP. Lakini kwa mujibu wa majimbo yalivokatwa, ndio wakaweza ZNP kupata viti viwili va kuweza kufanya muungano na ZPPP ili wapate kufuzu kuunda serikali. Na juu ya hivo, tulikwishawazidi ZNP kwa viti viwili, viti viwili au kimoja kama hivi. Lakini muungano wa ZNP na ZPPP ndio uliofanya ZNP kupata madaraka ya serikali na ndio kumuwacha Shamte mwenye viti vitatu kuchukuwa madaraka ya Uwaziri Mkuu. Haya ni maneno ambayo Saleh Saadalla Akida... [Kama nilivoelezea kabla] sisi tulikwenda kumuona Nyerere mwezi mmoja kabla ya mapinduzi, kakataa kutuona. Kakataa kabisa. Nyerere alizizuwia [silaha] khasa zisende Zanzibar.2

Hawa watu walikuwa na ugomvi, baina ya Kawawa na Oscar. Hata kwenye mikutano ya hadhara wanavutana. Kwa sababu kila mtu anamsema mwenzake kwa Nyerere. Nyerere akijitizama mwenyewe. Silaha zetu kachukuwa yeye Nyerere. Zilikuwa zetu na zilituwa Dar es Salaam kwa usalama, lakini ndo tumekosa usalama. Alokwenda kwiba ni mtu mkubwa sana—Oscar [Kambona].3 Silaha nyengine zilikuwa ni mzigo maalumu pamoja na bastola. Alituletea Oscar. Miwani zilitengenezwa Ujerumani. Manake zile bastola tulizoletewa mimi ilikuwa mara ya mwanzo kuziona. Zilikuwa kubwa, nzuri, ndogo, zina magazine [kitasa cha risasi]. Mimi sikuiona mizigo. Imezuwiliwa ndani ya meli Dar es Salaam. Hapa kilikuja kijizigo kidogo. Kina Bren gun mbili tatu. Shot gun zipo. Machine gun ipo, hand pistols zilikuwemo. Zile zilipitia Pemba kutoka Tanga. Kutoka Pemba zikashuka Forodhani, kwenye mchanga pale, saa nne ya asubuhi. Asikari wako tele pale. Na huku ni benki ya Standard Bank of South Africa.

Page 218: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili186

Pale kwenye Forodha Mchanga ndo iliposhuka. Manake ingeshuka uchocho­roni ingekamatwa. Nilikwenda na Khalid Sefu Al­Mauly. Alikuwa hajuwi kabisa kuhusu aina ya mzigo. Yeye alikuwa anafanya kazi ndani ya meli. Tukenda, nkachukuwa masanduku yangu. Ananiambia “nini”, nikamwambia “bia hizi.” Bia, brandi, manake imepangwa uzuri sana. Pombe hii, wacha tunakwenda pata chochote. Imepangwa kwenye sanduku kama hardboard laini lilikuwa na kanda za chuma. Yalikuwa masanduku matatu. Nilikuwa nalo hapa nyumbani, lilikaa likigaragara. Moja nilikuwa nalo mie. Lina kamba zile za chuma za kufungia mizigo hivi katika masanduku. Ya mistari ya rangi ilopiga hivi [kama krosi].4 Lilikuwepo hapa chumba hiki, hata nikivumbikia ndizi. Ngarawa ndo ilobeba hayo masanduku. Kuna ngarawa zinaweza kubeba hata mbuzi sita. Tulipakia ndani ya motokari ya Ali Saidi. Tumetoka pale Forodha Mchanga, tumepita Beitlajaibu, tumeingia njia ya Wizara ya Kilimo mlangoni pale, kichochoro kile kidogo, tukapita moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Darajani, tukaja zetu mpaka kwangu tukateremsha sanduku moja kwangu. Tukenda nalo mpaka Kwa Hani. Kwanza tumepita Gongoni kwa Saleh na tumeipita polisi ya Kisimamajongoo, mwangoni. Tukenda tukasimama kwa Saleh, hatujapakuwa. Tumeongea tu. Tukenda zetu Kwa Hani. Kwa Hani tukateremsha kwa Mohamed Omar “Masharubu”. Moja tukateremsha kwa Khamis Beni. Waladhaaliin. Yale ndo yalotumika Ziwani. Ni kidogo tu. Moja, mawili. Vijibastolabastola vile vilikuwepo mkononi. Alaaa. Si dhahir bwana, utakwenda bila ya kile. Nyingi sana hazijatumika. Zilotumika labda zitakuwa nne au tano kama hivi. Hazifiki. Ilikuwa haina haja. Halafu zote zilikwenda Ubago wakati Warusi wako hapa. Na Warusi ndo wakatengeneza lile handaki la kuweka [silaha]. Hakuna mtu aloleta silaha kabla ya mapinduzi isipokuwa Algeria tu peke yake. Zile zilotoka baina ya Kenya na Tanga sijui zilipita njia gani lakini zilifika Unguja. Sikuhusika nazo. Zilitokea Kenya zile. Manake Kenya kuna mahala unavuka, mimi sikujui, sijapata kwenda. Kule Mombasa kuja Tanganyika iko sehemu ina bahari unavuka, lakini ukivuka ile ukija katika Tanganyika unaweza kuja kwa miguu huku, mpaka juu, na ukenda kwa ngarawa unaweza kuvuka ukaja tokea Pemba, na wanokimbia Pemba ndimo wanakomofikia humo. Mara nyingi utasikia wamefikia humo. Sasa hizi zilifika, zimekwenda Ubago, lakini naamini zimepitia Pemba, halafu Pemba tena, baada ya mapinduzi zimebebwa polepole. Zilipitia Pemba, Mkoani, kule zimekaa, manake ndo mahala penye ngome ya Afro­Shirazi. Ile operation ilikuwa bara. Silaha zile ziloibiwa zile katika meli kwa amri ya huyu Mnyasa, Oscar Kambona. Na akapewa askari wale wawili, ndo waloteremsha na wakashindika. Mmoja Kepteni nani huyu, mtu wa Kigoma, na mmoja wa Tanga. Hawakuleta wenyewe. Hizi ilikuwa boti ya nanhii…ya wavuvi…manake misafara yote ilikuwa inafanywa na baba yake Fuko. Bagamoyo, Mlingotini, ndo kwake, na hapa Gongoni, Unguja. Jirani ya Saleh Saadallah. Kwasababu ndugu

Page 219: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 187

yake yeye babake Fuko ndo mkewe Ibrahim Saadalla, biti Huseni. Operations zile aliwachiwa babake Fuko pamoja na mtoto wake anaitwa Huseni. Manake Abdulaziz Twala alikuwa na mchango mkubwa katika mambo haya ya kuwasili kwa vitu kama silaha. Unajuwa mambo mengi unasahau. Siku nyingi. Yeye alikuwa ni wa tatu katika uongozi wa mapinduzi. Baada ya Hanga, Saleh, Twala. Mimi habari nyingi za watu wa mbalimbali sizijuwi. Kulikuwa na vikundi tafauti katika Chama cha Afro­Shirazi, lakini sio Umma Party. Mie nlozungumza wote, visa vyote va memba wa Afro­Shirazi. Lakini viongozi wa Afro­Shirazi wa akhir ya juu, kina Karume, hawahusiki. Wamekuja kufanywa tu kuwa viongozi wa mapinduzi baadae. Kwa sababu watu wengi walokuwa kwenye shughuli za mapinduzi walikuwa hawamuamini Karume. Mimi mapanga najuwa watu wote walikuwa nayo. Lakini mishare na mikuki, hayo mambo labda ya Youth League walikuwa nayo. Sisi hatujapanga kishenzi, tume organize vitu kisayansi kabisa. Ukitaka kuingia mahala lazim jeshi la polisi liwe na wewe. Ndo maana wakanitenga kina Karume kuwaambia watu, watumishi wa serikali wasiseme na mimi ati. Na asikari hasa! Hana haki ya kusema na mie. Wakaeneza picha zangu mote humu. Jabir Uki na Khamis Fadhil wanaweza kuzikumbuka tarehe. Mimi sizikumbuki. Ukweli, nilikuwa mtu wa hatari sana, na mpaka leo. Si nimekuonesha barua ya usalama ilioniondolea kizuwizi alioitia saini George Salim.

Rais Mstaafu Ahmed Ben Bella

Ni kweli [Nyerere] alikuja kututembelea na alionana na mimi na alifurahi kuniona. Nilimjuwa Nyerere wakati wa ukombozi wa kisilaha dhidi ya ukoloni uliokuwa ukiishi ndani ya nchi zetu. Hivi vilikuwa ni vita va ukombozi. Katika mabara ya Asia, Amerika ya Kusini na Afrika. Kilikuwa ni kipindi cha kihistoria. Historia inatengenezwa kwa mujibu wa vipindi, awamu. Kipindi tunachokizungumzia kilikuwa kipindi cha ukombozi wa kutumia silaha. Ukoloni ulikuwa umekwisha na tulitaka kuunda Umoja wa Afrika kupitia [Organisation of African Unity] OAU. Mimi nilikuwa mmoja wa waasisi wa OAU. Wakati huo Nyerere alikuwa akiiwakilisha Tanganyika na akiitwa “Mwalimu.” Ndani ya OAU kuna baadhi walikuwa dhidi ya Waarabu. Kwa mfano, kulikuwa na maudhui ya kuchaguwa lugha. Kiingereza na Kifaransa lakini waliikataa lugha ya Kiarabu. Gamal Abdel Nasser alikuwa na mimi na alikasirika sana. Kulikuwa na tatizo la Zanzibar. Waarabu walikuwa wameifanya Zanzibar koloni lao. Nyerere alikuwa na fikra hizo (na sisi pia) au tusingelimpokea. Ukweli mimi ni Mwarabu ndugu yangu. Wakati huo mimi nilikuwa ni Raisi na nilikuwa na thaqafa [taarifa]. Nilikuwa najuwa kuwa kulikuwa na matatizo na ndugu zetu weusi wa Kiafrika. Kulikuweko ubaguzi na Uislamu ni dhidi ya ubaguzi. Na Uislamu dhidi ya Ukristo pia si mzuri. Nyerere aliniambia “una mahusiano mazuri

Page 220: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili188

na [Gamal Abdel] Nasser na msimamo wake juu ya Zanzibar si mzuri.” Nyerere aliniambia “sikiliza, Nasser aniunge mkono…” na akaniomba nizungumze na Nasser abadilishe msimamo wake na asiwaunge mkono wabaguzi wa rangi Zanzibar ambao ni dhidi ya uzalendo wa Kiarabu na Uislamu, na nini Waarabu wanafanya dhidi ya ndugu zetu wa Kiafrika. Ni haramu katika dini ya Kiislamu. Hakuna ubora isipokuwa kwenye kumcha Mungu. Nyerere mwenyewe aliniomba hilo. Nasser alikuwa yuko pamoja na kikundi [ZNP] ambacho kilikuwa dhidi ya Nyerere.5 Na ndani ya OAU kulikuwa na vikundivikundi ambavyo vilikuwa havina mahusiano mazuri na Waarabu. Ukweli, Nyerere hakuwa mmoja wao. Yeye na Nkrumah wa Ghana, Modibo Ketia wa Mali na Sekou Toure wa Guinea. Hawa ndio walikuwa mijitu mikubwa ya Afrika. Nyerere akaniomba, baada ya ziara yake, nimuombe Nasser aizuwie sauti ya Masri ya Waarabu kuwaunga mkono Waarabu wa Zanzibar na tukaanza [kazi na] Djoudi. Namjuwa na yuhai. Anazungumza Kiingereza kizuri sana lakini sionani naye mara kwa mara. Kulikuwa na mirengo yenye kupingana ndani ya OAU na nilifaulu pamoja na Nasser kuwakinaisha wengine wenye fikra kama zetu kuianzisha Kamati ya Ukombozi wa Afrika. Na Djoudi alihusika na mafunzo ya kijeshi. Alikuwa muwakilishi wetu na mimi ndiye niliemchaguwa. Alikuwa ni Kanali katika chama cha ukombozi cha FLN na alikuwepo nchini kwenu. Alikuwa ndo dhamana wa Kamati ya Ukombozi wa Afrika.6 Viongozi wote wa ukombozi wa Afrika walikuwa hapa Algeria na mimi. Tukiwapa chakula na silaha. Siwezi kukumbuka vizuri lakini ndugu zetu walituomba silaha na meli ya Ibn Khaldun ilikuwa kwa ajili ya kubeba silaha. Kiukweli, tulikuwa pamoja na Nyerere. Hatukushajiisha ukombozi ndani ya Zanzibar. Tulimuunga mkono [Nyerere] na kazi yake na nilimtetea kilillahi. Nyerere ni Mkristo lakini tukimuhishimu. Sikiliza ndugu yangu. Kitu chochote ambacho Waafrika walikubaliana nacho sisi tulikiunga mkono. Mrengo wowote ule ambao ukiungwa mkono na nchi za Magharibi tulikuwa dhidi yake. Yoyote yule ambaye alikuwa akifanya kazi kwa maslahi ya Ufaransa, au Uingereza, sisi tulikuwa tuko dhidi yake. Mpaka hii leo nitakuwa dhidi yake. Wamemchukuwa ndugu yetu mweusi kutoka Afrika wamempeleka Marekani kufanya kazi katika mashamba ya pamba. Huu ndio ustaarabu wa nchi za Magharibi. Mimi si mbaguzi lakini ni dhidi ya ukoloni. Sisi tuliona ni jambo takatifu kuwaunga mkono Waafrika ambao walikuwa wakifanya kazi ya kuzigomboa nchi zao. Akinijia Muafrika, au Mhindi Mwekundu [wa Marekani], na anataka kuigombowa nchi yake, kwangu mimi huo ni wajibu uliotakasika. Na hatuwaungi mkono kwa maneno matupu. Tunawaunga mkono kwa silaha. Tunawaunga mkono kwa pesa. Kwa kuwatengenezea nyaraka na pasipoti. Mpaka hii leo. Fidel Castro na Che Guevara walikuwa wanafahamu kuhusu Zanzibar lakini kijuujuu. Si kwa undani. Walikuwa hawaruhusiwi kufanya jambo lolote.7 Che

Page 221: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 189

Guevera alikuwa mtu asie na majigambo na alikuwa mtu wa Magharibi! Nini nchi za Magharibi zimeifanyia Afrika ni kitu kisichoweza kukubalika. Ni dhambi. Nilitowa silaha, na leo na kesho nitafanya hivohivo. Tulimuunga mkono Nyerere [pale alipopinduliwa] ili aweze kujirudishia nguvu za utawala. Ndani ya mwaka mmoja yalifanyika mapinduzi ya kijeshi isihirini na mbili baada ya yetu Algeria. Nchi za Magharibi ndio chanzo. Viongozi wetu, mpaka hii leo, wana vitu viwili tu. Bendera na wimbo wa taifa. Hatuna ilimu yenye kutuunganishia mambo. Tuna ilimu ya vipandevipande. Tuna OAU au AU ambayo haifanyi kitu. Haitangulizi kitu, wala haibadilishi kitu. Hata ndani ya OAU Nkrumah alikuwa ana nguvu kuliko Nyerere. Katika kazi khasa ya ukombozi dhidi ya nchi za Magharibi Nkrumah alikuwa ana nguvu zaidi kuliko Nyerere.8 Tuliwaunga mkono wale ambao waliokuwa dhidi ya maadui zetu—nchi za Magharibi. Jana na leo. Ndugu yangu, sikubali kuwa Nyerere alikuwa ni haini. Hii siwezi kukubali. Alikuwa dhaifu. Namfahamu vizuri. Nilionana naye, nikazungumza naye na akaja kwetu na tulikuwa pamoja ndani ya OAU tukipigana myereka na wale ambao walikuwa si dhidi ya ukoloni. Na mpaka leo OAU/AU inaumwa gonjwa hili. Tulikuwa nchi kumi na mbili, pamoja na Nyerere, ambazo ziliusimamia ukombozi wa Afrika. Djoudi tulikuwa naye katika jeshi la ukombozi na alizisimamia nchi tisa za Kamati ya Ukombozi wa Afrika, na akizungumza Kifaransa na Kiingereza kizuri alichojifundisha Yujbara, moja katika miji ya Algeria. Kamati ya Ukombozi wa Afrika ilikubaliana kwa pamoja au bila ya pamoja kuunga mkono kila harakati za ukombozi za Afrika. Ni lazima wajuwe kila kitu kiliopo kuhusu ukombozi. Tulikuwa pamoja dhidi ya wengine. Nkrumah, Modibo Keita, Sekou Toure, Nasser na mimi mwenyewe. Wengi walikuwa wako dhidi yetu. Kwa ukweli Nyerere alikuwa pamoja na sisi. Haile Sellasie hakusema kitu chochote dhidi ya njia tuliokuwa tunakwenda juu yake. Lakini kwa ukweli nilikuwa sina raha na siasa zake za Ethiopia. Sikuwa na raha kama nilivokuwa na raha na misimamo ya Sekou Toure na Nkrumah. Hao wawili walikuwa dhidi ya ukoloni.

Balozi Noureddin Djoudi na Kamati ya Ukombozi ya OAU

Nilizungumza na Rais [Ben Bella] jana. Kama unavojuwa anaamini sana mashirikiano baina ya Waafrika na Waarabu. Unajuwa kuna mengi sana ya kusema ambayo hayajapata kuzungumzwa si kwa njia za rasmi au zisizo rasmi. Wakati ule [wa mapinduzi ya Zanzibar] Maisraili walikuwa wana ndege zao pale, na kile walichokiita kuwa ni programu ya mafunzo. Nilizungumza na Kambona na Nyerere na tukaweza kuwatowa [Maisraili] na pia walikuwa na mpango wa kijeshi Uganda. Kwa hiyo kuna mahusiano baina ya kuwepo wao Afrika Mashariki na mambo mengi yaliotokea. Kwa hakika, mapinduzi yalipotokea

Page 222: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili190

Zanzibar, niliwasiliana na Abdurahman Babu na Nyerere. Nikasema kuwa kama mna mahusiano mazuri na Rais Ben Bella basi sidhani kama atakuwa na furaha na yanayotokea. Munaweza kufanya ukombozi lakini si mauwaji ya halaiki. Na kuwepo kwa Okello ni jambo lisilofahamika. Hakuhusika kabisa na Zanzibar. Unajuwa hata watu kama Abdurahman Babu walipumbazwa na tukio la mapinduzi. Nakusudia hawakuwa na mahusiano ya moja kwa moja nayo. Si rahisi kuelezea na maelezo yake kidogo ni marefu. Kuna masuala mengi, na maelezo mengi ambayo hayawezi kufahamishwa kiurahisi na unajuwa mahusiano baina ya viongozi wa Zanzibar hayakuwa mazuri. Habari ya [meli] MV Ibn Khaldun hiyo ni hadithi nyingine kwa sababu Ibn Khaldun ilipeleka msaada Tanganyika na tulikuwa na baadhi ya silaha kwa ajili ya FRELIMO, Msumbiji, lakini baada ya kushindwa kwa maasi ya kijeshi Tanga­nyika ya mwezi wa Januari [1964] niligunduwa kuwa walipaingilia [Waingereza] mahala tulipozificha silaha na pakategwa mtego wa bomu. Ungelitokea mripuko mkubwa ambao ungeiangukia Algeria lakini tuliutambuwa na mapema. Na hapo pia yapo mengi ya kusemwa. Baadhi ya silaha zilipotea, nyengine ziliharibiwa. Kilikuwa ni kipindi muhimu kwa sababu FRELIMO ilikuwa inaandaa ukombozi wake. Hata suala la utumwa ni lazima liulizwe kwa njia ya maana ya utumwa. Nakusudia, kuna utumwa wa kuwekwa nyumbani. Na kuna kuwakamata na kuwauza watumwa na kuwapeleka Marekani ya kaskazini na ya kusini na kwengineko. Sasa wamejaribu kuficha nini Wazungu wamefanya, kama ni Waingereza, Wafaransa, au Wareno, na kuzitupa lawama juu ya migongo ya Waarabu wakati kihistoria Waarabu hawajaingia ndani ya bara la Afrika kukamata watumwa.9 Watumwa walisalimishwa kwa Waarabu ya imma kutoka kwa Wareno au mara nyingine kutoka kwa machifu wa Kiafrika wenyewe. Na zaidi, kuna sharia ndani ya Qur’an inayowalazimisha Waarabu/Waislamu wanapomiliki watumwa. Mtumwa anatakiwa ale chakula kilekile anachokula bwana wake, anatakiwa achukuliwe kama ni memba wa familia, na zaidi ya yote, watu wanasahau kuwa kitendo cha kwanza dhidi ya utumwa katika Uislamu ni pale Mtume Muhammad (Salaa na salamu za Allah zimshukie) alipomnunua mtumwa wake na akampa uhuru hapohapo. Kwa hakika Uislamu ulikuwa ni wa mwanzo kupinga utumwa na maamuzi ya Wazungu ya kupinga utumwa yalikuja mwisho wa karne ya kumi na tisa, na mwanzo wa karne ya ishirini. Nilipokuwepo Angola niliona na Wanaangola watakwambia, kuwa walipokuwa wanachukuliwa watumwa kupelekwa Brazil, Kanisa liliibariki biashara ya utumwa kwa kusema kuwa imehalalishwa kidini kwa sababu mtu mweusi alikuwa hana roho! Haya ni mambo ambayo yanafaa kuonyeshwa tena hadharani. Nafikiri pia Waarabu wamefanya makosa mingi kwa kutokwenda Afrika na kujionea wenyewe hali halisi ya mambo yalivyo kwa kutumia angalau pesa zao kidogo. Siku za harakati za ukombozi, nani alisimama na Waafrika? Walikuwa

Page 223: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 191

ni Waarabu peke yao! Afrika kulikuwa na watu kama Mobutu ambaye aliiunga mkono siasa ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini. Ni lazima tuyafahamu vizuri yaliopita nyuma kwanza.

Kwenda Somalia Kuisaidia Zanzibar—Balozi Mbarak Khalfan

Jina langu Mbarak Khalfan Al Sabahi, nimezaliwa Zanzibar siku kama leo, na nimesomeshwa Zanzibar katika skuli za serikali mpaka standard 8, baada ya standard 8, nikafanyiwa varangevarange na Wazungu ikabidi kugombana ugomvi mkubwa ukafika mpaka Jumuiya ya Wazee. Muhimu nikasoma kidogo miezi sita katika Muslim Academy, Al Maahad Al Islami, baadae ilipofika mwezi wa June mwaka 1956 nikaondoka Zanzibar kuelekea Masri kwenda kusoma. Na tangu miaka hiyo tena nlosoma Masri…ilipotokea mapinduzi ikabidi tena kuondoka Masri. Kwanza tulitiwa jela. Nimetiwa jela kwa sababu nilikuwa President wa Zanzibar Youth and Students Union ambayo ilikuwa ikiwakilisha All Zanzibar Students Union. Ilikuwa mwezi wa June 1965 vilevile baada ya kumaliza mtihani siku ile ile wamekuja maaskari kanzu wakanambia tuna haja na wewe mara moja. Sababu yao ni kuwa Karume kataka nirudishwe. Kulikuwa na mzozano mkubwa. Walitakiwa watoto kwanza, wale walokuja 1958 wote, wadogowadogo wale, wote warejeshwe sasa kila wakija kuwachukuwa hawaonekani. Walikuwa hawawapati. Sasa Hija Saleh akasema huyu ndo yuko nyuma ya mambo yote. Kulikuwa na vijana wengi kwa hakika na kila mmoja alikuwa ana mchango wake lakini yule bwana akashikilia kuwa mimi ndo nilokuwa ukubwa nimeukamata mie kwa hio ni lazim mie wa ilhali wakati ule mie, tulikuwa sisi tumeshawaachia wengine kuiongoza Zanzibar Youth Union na sisi tulikuwa tuko nje. Mimi, Maalim Ahmed Humud, Mohammed Abdalla Gharib, Nassor Mohammed Nassor, vijana wengi…Maryam bin Breik, vijana wengine tulokuwa katika kamati. Tumekata shauri kwamba tuwaachie watu wa nje tu. Basi, wakaniweka ndani mwezi na kitu, mimi na Mohammed Abdalla Mohammed Gharibu Al­Oufy. Vijana hawakunyamaza alhamdulilllahi. Walipiga mbio huku na huku wakapeleka ma telegrams katika students unions zote za dunia ikawa telegrams zinakwenda kwa Gamal Abdel Nasser, na bakhti nzuri kulikuwa na mkutano wa Arab League. Tena kule wakatokea wale ma leaders [viongozi] wa Arab League, King Hussein, Abdel Salaam Aarif, hawa wamesema kwamba OK, usiwarudishe hawa, sisi tutawachukuwa. Bakhti nzuri yule Abdel Salaam Aarif kamleta tena Waziri Mkuu wake kutaka twende Baghdad. Tukatolewa pale, tukapelekwa Baghdad.10

Wallahi kwa wakati ule tunavojuwa sisi kwamba wote walikuwa wana sympathize [wanatuonea huruma] kwa sababu yale mapinduzi yalivotolewa, lile tangazo lake, kwamba Waarabu wamewakandamiza Waafrika wamepinduliwa.

Page 224: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili192

Ilivotoka duniani. Sasa Cairo wao hawakutaka kufahamisha, au sio hawakutaka, manake, sikusikia mimi kitu chochote kinachofahamisha kwamba hii kinyume na hivo, na ilhali hakuna katika Dola ya Kiarabu yoyote inayoijuwa Zanzibar na kifaah [mapambano] ya Zanzibar, zaidi kuliko Masri hakuna. Nakupa mfano tu. Ilifika hadi Karume katika mkutano wa kisiasa, uhuru wetu sisi hautotoka Cairo wala Accra. Kwa sababu kulikuwa na mahusiano mazuri na ZNP (Zanzibar Nationalist Party) na nchi zote nyingine za Kiarabu, na za Kiafrika zinazopigania uhuru. Na Afro­Shirazi hawakuwa nayo hiyo. Na Cairo ndo ilokuwa inasaidia nchi nyingine zote wakati ule kupata uhuru wao. Sasa sisi ilikuwa Wamasri au serikali ya Masri ilikuwa alal akal [angalau] iwafahamishe watu wengine hii serikali ya Zanzibar si serikali ya Waarabu, ni serikali ya wananchi wa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wako hivi hivi hivi. Mimi nahisi kwanza, kuna mfano wa Kiarabu, ngombe akishaanguka visu vinakuwa vingi. Kwanza upande mmoja ZNP ilikuwa haipo tena. Wamehakikisha kwamba wameshaondoka, hawa jamaa wameshaidhibiti hali kisawasawa, mawaziri wametiwa ndani, Mfalme kaondoshwa, na hakuna ispokuwa hawa [ASP] kushirikiana nao. Najua kwamba Iraq walikuwa wanafahamu kwa sababu wale vijana wetu, wanafunzi waliokuwa wanasoma Iraq waliwafahamisha vizuuri na bakhti nzuri waliifahamu kwa sababu tangu hapo wao wanao mchango katika watu wao, Waarabu wa Kiiraqi walokuwako Zanzibar. Walikuwa wanafuatilia vizuri sana. Kwa hivo naona Iraq waliwahi hata kutaka kuleta jeshi lakini hapakuwa na mawasiliano. Wale National Guards wenyewe walijitolea as volunteers valantia. Unajuwa wakati ule magaazeti yote ya Magharibi na ya Mashariki yalikuwa yakiunga mkono mapinduzi. Manake wale Makomred walikuwa wakiungwa mkono na nchi za Mashariki, na hawa wengine huku [ASP], wamekuwa wakiungwa mkono na Wazungu. Na magazeti ya Kiarabu ya wakati ule yalikuwa mara nyingi yananakili kila kitu. Maana yake, chochote ulichokuwa unakisoma wakati ule katika habari za Kiarabu zilikuwa zikinakiliwa kutoka kwenye magazeti yaliotoka Ulaya, makala za zamani sana. Nasser yeye alikuwa anayo idhaa lakini magazeti wana copy kutoka Associated Press (AP), lao walikuwa nalo moja ambalo halifanyi chochote. Hakukuwa na mkataba wa kijeshi lakini kulikuwa, mimi sikuhudhuria katika mikutano yao ya siri, lakini nilikuwa nikiona wanaletwa vijana wa Kizanzibari kuchukuwa mafunzo kwenye mambo ya kijeshi. Na vilevile kulikuwa, na baada ya uhuru, kulikuwa na mipango imefanywa, kuja vijana kutoka Zanzibar kusoma fani za kijeshi za kila aina. Moja katika hizo ni jeshi la anga, navy, majeshi ya ardhi, na mimi mmoja katika hao nlikuwa nishapasi kwenda zangu Chuo Kikuu nikaambiwa la, wewe bwana serikali ya Zanzibar imekuteua kuwa wewe ndo utokuwa kiongozi wa jeshi la anga la Zanzibar kwa hio wewe jina lako namba one, tulizana kwanza, usende popote, ngojea mpaka itakapokuja listi kaamil, kopi ya list imeshaletwa, mpaka itakapokuwa tayari utaungana na wenzio, wewe

Page 225: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 193

utakwenda Jeshi la Anga. Kwa hivo Mohammed Faiq hakusema kweli au kakupa nusu habari. Na kabla Waengereza kukataa kuwapa himaya Wazanzibari ilikuwa huku chini kwa chini ZNP ilikuwa inao muelekeo namna huo. Mambo kama hayo alikuwa [anayo] mwenyewe Sheikh Ali Muhsin. Yeye mwenyewe binafsi. Maana yake ndo alokuwa akija sana huku [Masri]. Na mambo mengine ya ZNP yalikuwa hayapitishwi penye ofisi yake Cairo kwa sababu ilikuja kujulikana kwamba baadhi ya vijana wepya wepya pale, wanakuja pale kufanya ujasusi na kuwapelekea habari. Kumbe wanajia yao. Tuliwahi kuwakamata watoto wawili watatu. Waliwahi kukamatwa namna hiyo na wengine wahai mpaka leo. Lakini katika gurupu lilokuja mwaka 1958 kumekuja watoto wa scholarship tu. Na group moja watu wazee wenyewe na pesa zao wamewaleta watoto wao wamefuatana nao watizamwe wakae katika nyumba wanaotizamwa Wazanzibari lakini masomo yao wazee wao watalipa wenyewe. Alikuwepo Ibrahim Omar, Masoud Makua, Usi Khamis ambaye yuhai mpaka leo, Ibrahim Omar nasikia tu yupo yuhai, mbali kuna Daulat Khamisi, mtoto wa Maalim Khamis Mandoa, hao wote si Waarabu hao, na wengineo na wengineo chungu nzima. Hakuna Mwarabu na imefanywa kusudi kwa sababu huyu Ahmed Rashad alisema “unaona hizo [nafasi za kwende kusoma], basi utaona watakuja watoto wa Kiarabu watupu!” Alisema kabla yake. Na baadae alivowaona kina Yusuf Bahurmuz na nani na kina Thani wale watoto wa Kikumbaro akasema “sikukwambia unaona hao!” Akaambiwa hawa bwana wamekuja kwa pesa zao. Hiyo argument [hoja] inakuwa baina ya Ahmed Rashad na Seleman Malik. Seleman Malik ndo alokuwa rais wa maktab (ofisi) ya Zanzibar pale Cairo. Sasa ndo anatueleza, “huyu yakhe mtu hatari sana huyu!” Nilijuwa kuhusu mapinduzi through BBC ya Kizungu na ya Kiarabu. Asubuhi na mapema. Kwamba kuna ghasia za mapinduzi Zanzibar na serikali imeshapinduliwa na hakuna upinzani Zanzibar nzima ispokuwa Malindi na Mfalme anatarajiwa kuondoka wakati wowote Zanzibar. Basi tena ndo tukaitana sisi, wale viongozi wakubwa wa umoja wa wanafunzi wa Kizanzibari. Baada ya hapo ndo tukaitana sote mkutano tukakata shauri twende kwa Sheikh Ahmed Lemky. Nnaoweza kuwakumbuka ni Maalim Ahmed Humud Al­Maamiri, Mungu amrahamu, na Mohammed Abdalla Mohammed Gharib, Nassor Mohammed Nassor Al­Hadhrami, Mohammed Ali Muhsin, Mariam bin Breik, Salha Al­Mugheiri, Maalim Harith bin Khelef, ambaye sasa ndio Mufti wa Zanzibar, Masoud Rashid Al­Gheithi, Ahmed Sleman al­Gheithi. Tukakutana sote, tukakata shauri kwamba sote tukakutane na Balozi wa Zanzibar, Masri, Ahmed Lemky. Balozi alikuwa bado hata hana nyumba yuko katika hoteli. Tukenda hoteli, tukakutana. Bwana Ali Khamisi [ Jaribu] alokuwa Naibu Balozi na baadae Spika [wa pili]

Page 226: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili194

wa Baraza la Wakilishi (BLW) alikuwepo.11 Basi tukazungumza pale tukasema sasa tuyatizame nini la kufanya. Halafu usiku yeye [Ahmed Lemky] akatuchaguwa mimi na Maalim Ahmed Humud, na baadhi ya vijana, Muhammed Gharib, kwamba nyie njoni tukutaneni siri. Pale ndo tukapanga tena kwamba tujaribu kukutana na Mfalme, Sayyid Jamshid, na jamaa kuwa na mawasiliano na ndani. Jamshid alikuwa ndani ya meli, inakwenda ikirudi. Tena pale tukatafuta kila njia.12

Asirande tu ndani ya meli, wende Pemba aiuzulu ile serikali yake na afanye serikali ya Kipindi cha Hatari (Emergency Government) kwa mujibu wa nguvu za kikatiba alizokuwa nazo. Na kwa sababu Pemba ni 100% majority ni wafuasi wa ZNP na ZPPP kwa hivo, wafanye hivo. Tukatoka na mie nimepelekwa Mogadishu. Alopelekwa Mombasa ni Muhammed Abdalla Muhammed Gharibu. Tukenda. Ikiwa Mfalme kafika Somalia niiombe serikali ya Somalia aje zake pale nionane naye mie nimpe fikra ile. Na alokwenda Mombasa Muhammed Gharibu anajuwana na watu chungu nzima kule jamaa zake wapo, wamfanyie mpango ende akaonane naye amwambie sisi tumetumwa na Ahmed Lemky na tunashauri hivi hivi hivi hivi. Somalia mimi nilikuwa na rafiki zangu wengi sana wamo katika jeshi. Tulikuwa nao skuli ya sekondari nimesoma nao Helwan [Masri]. Kwa hivo ilikuwa rahisi kwangu mimi kuwa na mawasiliano nao. Nimetoka Cairo halafu Aden mpaka Mogadishu. Nilikwenda kwa ndege. Nimefika Mogadishu siku ileile nimeanza mawasiliano na nikawapata siku ya pili au siku ya tatu yake. Wamefurahi sana. Nakumbuka wao wakaniambia sisi tumeshasikia, sisi tuna wakubwa zetu, wakati wowote tunaweza kuja kukuchukua ukaonane na General Siad Barre. Basi wakanijia asubuhi siku hiyo wakaniambia haya yallah! Kavae upesi upesi twende zetu. Nilikuwa nakunywa chai wakaniambia wacha twende zetu. Wakanitia pale ndani ya gari moja kwa moja mpaka makao makuu ya jeshi. Nikawekwa ukumbini pale nikaitwa nikamkuta. Anasema Kiswahili kama mimi na wewe. Siad Barre. Akanambia yote unotaka kusema nshajuwa lakini ilobakia sasa hivi wewe unambie wewe tu. Akasema sisi kwa moyo wetu watu wa Somalia na hakuna wanayofahamu haya zaidi kuliko sisi. Kwa hivyo sisi tayari kwa lolote nambie nini nyinyi mnataka tu. Nikamwambia tunataka mutusaidie turudishe nchi. Kwa kifupi hivo. Vipi? Twende tukapinduwe! Mnao watu? Nikamwambia wapo vijana na ndani tuna watu wetu vilevile. Akasema basi, kwanza, mimi sitoweza rasmi kufanza hivo. Ikiwa tutafanya tutafanya kifichoficho na wapo vijana telee hapa askari wanasema Kiswahili kama mimi au zaidi kuliko mie. Tutakupeni hao. Hatupeleki mtu ambaye hajui Kiswahili lakini usafiri kutoka hapa kwenda Zanzibar hatuwezi kutowa sisi kwa vile Serikali haina njia nyingine. Lakini juu ya hivo ntakupa fikra toka wewe hapa nenda zako mpaka Kismayu. Kismayu watu wote wanasema Kiswahili na kuna watu wana alaka nzuri na Sultan na wanampenda Sultan wenu kama sisi, na kaonane nao. Nani huyu bwana?

Page 227: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 195

Unamjuwa Seif Rizeiki? Baba yake! [Akanambia] akini usije ukataja kuwa una alaka na mie kwa mtu yoyote ispokuwa huyu bwana. Peke yake. Mwambie kuwa mimi nimekutuma. Mueleze hiyo kadhia yenyewe asijuwe mtu yoyote mwengine. Nikamwambia hakuna tatizo. Nikatoka mie nikenda. Sasa katika kuulizauliza kumbe mimi nafatwa na watu wa usalama wa Kisomali. Na bahati mbaya siku ile zilikuja ndege za Kikenya kupiga mipakani mwa Somalia. Sasa nyuso ngeni pale ni mimi nilioingia. Usiku akaja Seif huyu akanchukua akanipeleleka kwa Babake tukafuturu palepale Kismayu. Baada ya kufuturu akakaa pembeni, haya sasa nambie. Umejia nini? Nikamuelezea ile yoote kadhia tangu mwanzo mpaka mwisho. Akanambia kwanza nionyeshe kitambulisho chako. Nikamuonyesha. Nilikuwa na barua mimi kutoka kwa Ahmed Lemky akiwa ni Balozi wa Zanzibar yenye kusema: “Huyu ni mjumbe wangu mimi kwa yoyote atakayehusika na naomba apewe msaada wowote.” Basi akanambia sisi tayari na tunaijuwa Unguja na Pemba yake vizuuri na wapi pakushuka tunajuwa. Mimi nna watu wangu wanaweza kukushusheni kama mnataka Pemba, mnataka Unguja, popote pale. Na mimi nnazo jahazi kiasi 10 au 12 kanambia. Na zote ntakupeni. Nendeni mkafanye mipango mkiwa tayari nipeni habari tu. Basi, nikarudi mie , siku ya pili asubuhi, nataka kwenda kupanda gari kurejea Mogadishu, nikakamatwa! Akanikamata yule askari kanzu, akanambia wewe jasusi. Nikatiwa ndani pale, ghasia moja kwa moja, nkamwambia mimi namtaka mkubwa wenu. Basi akaja mkubwa pale akanambia hapana, hakuna mmoja ataweza kukusikiliza hapa, atakayeweza kukutowa wewe, labda muhaafidh [Mkuu wa Mkoa] mwenyewe wa Mogadishu. Nikamwambia nnaomba basi kupelekwa. Yule ofisa aliniona mtu maakul kidogo akanipeleka mpaka kwa muhaafidh. Nikamwambia muhaafidh skiliza, mie nimekuja hapa kuzuru jamaa imetokea bakhti mbaya, basi akanambia basi sasa hivi toka nenda zako. Nikamwambia hakuna basi sasa hivi au gari. Akanifanyia nikapanda lori la polisi. Kunipeleka pale, mpaka Barawa, Barawa nipande gari mpaka Mogadishu. Nikarudi pale nkamwambia Siad Barre huyu mtu hivi hivi hivi. Akanambia sasa nendeni mkatayarishe, silaha tutakupeni sisi. Mufanye tektiki zenu mkiwa tayari nambieni. Sasa Sheikh Ahmed Lemky, kanipa code barua kwa maneno mengine kumbe unakusudia mengine. Kanambia hii ndo ya kutumilia. Akanambia ukitaka kuwasiliana na mimi barua zako zipeleke Ubalozi wa Masri pale Mogadishu. Kumbe yakhe yule Balozi barua zangu zote alikuwa hakuzipeleka. Ama balozi au kule zilokokwenda hazikumfika Sheikh Ahmed. Alivonambia Sheikh Ahmed. Yeye kakaa ananlaumu mimi katika mkutano kwamba huyu bwana tumempeleka kule ameshapata watoto wanawake wa Kisomali kule wameshamrusha roho, hatuulizi kheri wala shari. Nimekaa mwezi mzima mimi. Ramadhani nzima nimemaliza kule. Nangojea jawabu. Kila nkenda kwa nanhi anasema hakuna jawabu, hakuna hivi, hakuna hivi. Mwisho nikaamua niondoke. Nikamwambia mie naondoka nakwenda Masri. Nikenda Masri.

Page 228: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili196

Kwenda Masri, jamaa wakanambia wewe yakhe namna gani? Haikufika hata barua moja? Hata barua moja haikufika! Haiwezi kuwa. Basi twendeni sasa hivi. Ilikuwa usiku. Nikatoka palepale usiku nakwenda nikamkuta Ahmed Lemky na mkewe, na mtoto wa dada yake, wanatoka wanakwenda sinema. Nikamwambia Ahmed kwa hiasni yako bwana, mara moja. Akasema aa! Njoo kesho asubuhi maana yake nitawavunjia, unawajuwa wanawake. Njoo kesho asubuhi. Ukinambia sasa hivi na ukinambia asubuhi sawasawa. Kwa hiyo njoo asubuhi. Basi, mimi jamaa huku wakanambia, yakhe huyu bwana sie yule wa mwanzo, hakuna zile hamasa, na anasema umekwenda huko na sasa hivi sidhani kama ataukubali ushauri wako. Mimi nikasisitiza lazima nikutane nae. Basi nkakutana naye nkamueleza yoote yale yamefika wapi, akanambia, lakini Mbarak hukutwambia chochote! Nkamwambia mie nimeleta, akasema, wapi bwana we! Unajuwa akaanza kufanya maskharamaskhara pale. Kunistihizai yaani. Mie nikasema maneno alonambia kina Maalim Ahmed kweli. Akasema basi si lazima sasa hivii. Huu si wakati munasib. Tena basi tukaishia pale, huu si wakati munasib, na bora tuanze tena, haidhuru japo ikichukuwa miaka khamsini. Katika maneno yalonivunja moyo ya Ahmed Lemky ni hiyo. Inahitajia mipango mipya…hakuwa na zile hamasa za mwanzo na kwa hivo mie, Maalim Ahmed akasema, haya, tufanye harakati ya ukombozi wa Zanzibar. Namwambia, kwanini hatuwi na contact [mawasiliano] na Ahmed Seif Kharusi na Sultan? Siku hizo bado hawajagombana bado. Basi tukafanya contact sisi na Ahmed Seif. Na tukawaita walewale vijana wale, wenye msimamo mkali wale, nkafahamisha sasa hivi ndo kama hivi, sisi hatuna mawasiliano na ndani, itabidi tufanye mawasiliano na ndani, nchi ziko tayari za kutusaidia. Kwa ukweli vijana wa Eritrea yakhe walikuja, wale wa harakati za ukombozi wa Eritrea, walikuja, wale tangu siku za marehemu Seleman Malik, alikuwa ni rafiki wa karibu wa Idris Kalaidos, amekufa maskini, mmoja katika viongozi wakubwa wa ukombozi wa Eritrea. Wao walikuwa tayari. Wanasema uhuru wa Zanzibar ni uhuru wa Eritrea vilevile, kama walivosema Wasomali. Kwa hivo tukaanza tena upya. Tulipokuja kukutana tukasema lazima tuwe na kiongozi wetu hapa, mimi na wewe na nanhi, hapana anotujuwa sisi. Ndani ya Zanzibar wala duniani. Kwa hivo tutafute mtu wa kutuwakilisha, ama Mfalme, au Ahmed Lemky, au Ahmed Seif Kharusi tukakata shauri pale tumwendee Ahmed Lemky, tumwambie yeye atuongoze.13 Wakati huo ameshahama katika hoteli yuko kwenye fleti chini Midan Tahrir. Tukamwendea bwana. Tukamwambia yote hayo. Hayaa. Maalim katunga kijitabu kidogo kizuri kinachoelezea ile nukta tuliozungumza na wewe sasa hivi, ya kufahamisha, nini ZNP, na kuwa ZNP­ Hizbu, si chama cha siasa. Ni harakati ya umma. Kwa hivo tukafanya hiyo, tukampelekea Sheikh Ahmed, kafurahi sana Sheikh Ahmed Kharusi, aka­kichapisha yeye, halafu baadae kitabu kilekile Ahmed Lemky kakifasiri akatia jina lake yeye kwamba yeye ndo mwandishi wa kile kitabu. Kakitafsiri kwa Kiarabu

Page 229: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 197

lakini. Kile cha kizungu cha Maalim Ahmed hakutia jina lake lakini kiliandikwa vizuri sana.

UAE Yawapokea Wazanzibari—Sheikh Mohammed Abdulmuttalib (Mutta)

Kwa hakika mimi mwanzo nilielewa hili suala la kuletwa silaha Dar es Salaam. Nililifahamu kama lilivokuwa likisemwa kwamba Ben Bella ameleta silaha kusaidia harakati za ukombozi pale Dar es Salaam, kwa sababu kilikuwa kituo cha harakati za ukombozi wa Afrika. Kwa vile kulikuwa na makao makuu ya harakati za ukombozi zilikuwa zikisimamiwa na Nyerere na Kambona, ambao wote wamefariki hao. Mimi nafahamu kwamba ile meli, MV Ibn Khaldun, ilifika Dar es Salaam tarehe 6 Januari 1964. Nilifahamu hivo. Linonifanya kufahamu zaidi ni maneno ya Ben Bella mwenyewe kutoka kwenye mdomo wake. Ilifika meli ya Algeria MV Ibn Khaldun imebeba silaha, ikasemekana kwamba ni mchango wa Ben Bella katika harakati za ukombozi. Sasa nakuja kuelewa Ben Bella zile silaha kazileta kwa lengo la uvamizi wa Zanzibar unotusikitisha ulotokea 1964. Katika vitabu fulani fulani. Na miongoni ni kitabu nilichokisoma Al Hakika Al Zinjibar—Ukweli wa Zanzibar alikiandika marehemu Ahmed Lemky. Nikazidi kufahamu kumbe silaha lengo lake lilikuwa kusaidia harakati za ukombozi. Nyerere kazitumia, ambapo katika kitabu cha Bwana Ahmed Lemky amesema, silaha hizo zilipakiwa katika mashua ya shirika la uvuvi lilokuwa mwenyewe Myahudi maarufu akiitwa Frans Misha [Misha Finsilber]. Zikavushwa, ndo zilotumika katika mauwaji na uvamizi ulofanyika Zanzibar. Na hizo silaha kumbe zilikuwa Ben Bella kwa kukubali mwenyewe katika mahojiano ya magazeti baada ya kutoka jela, kumbe mwenyewe kasema kwamba kazileta kwa lengo la kumsaidia Nyerere katika kuondosha, kupinduwa, kumuondosha Sultan, anamwita Sultan Jair, yaani Sultan dhalim wa Zanzibar. Ben Bella mahojiano hayo aliyafanya alipokuja hapa Emirates. Sasa kutoka jela, Sheikh Sultan, hakimu wa Sharjah, alimualika. Kamualika aje hapa kutembea kama ni mmoja wa viongozi wa Afrika, maarufu duniani, na maarufu kwa sote. Na sisi Wazanzibari nataka kusema, katika wakati wa mapinduzi ya watu mashahidi milioni ya Algeria, kumpinga mkoloni wa Kifaransa, katika nchi za Kiafrika, sisi, Zanzibar, ndo tulokuwa katika nafasi ya mbele katika kuunga mkono kadhia hiyo, kumuunga mkono Ben Bella na wenzake katika kugomboa nchi yao.14 Tulifanya maandamano, tukamlaani mkoloni wa Kifaransa, ndio nguvu tuliokuwa nazo wakati huo wa ukoloni Zanzibar. Tungelikuwa na uwezo zaidi tungelifanya. Imani yetu ilikuwa kubwa, na kadhalika napenda kurudi nyuma. Katika wakati ilipokuwa imehujumiwa Masri, 1956, Wazanzibari ni sisi tulokuwa katika watu wa mwanzo kufanya maandamano, na vikafungwa vitambaa veusi na kuonyesha msimamo wetu kuiunga mkono Masri, kwa mujibu wa mambo nilioyasoma katika taarikh/historia ya Zanzibar. Inasemekana pia marehemu Suleiman Badar,

Page 230: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili198

marehemu Muhsin Badar, na wengineo, walijitolea kwenda kupigana kuitetea Masri. Kinyume na tulivofanya sisi, yeye Ben Bella anatafakhari kwamba anakuja kuleta silaha, kusaidia kuuliwa watu kama sisi tulosimama na yeye. Aliulizwa katika magaezeti suala hili la silaha. Akajibu akasema “naam nimefanya.” Alihojiwa na majarida kama skukosea, hili Al Khaleej lilioko hapa au kabla halikubadilishwa jina likiitwa Aazimiya Al Arabiyya, nafikiri mimi. Lakini muhimu alihojiwa. Akaulizwa suala hili khassa, akajibu, naam, nimefanya. Kwa nini? “Nimemsaidia Msoshalisti mwenzangu Nyerere.” Hivi ndo alivojibu. Akaambiwa, unajuwa kama waliouliwa ni watu na wengi ni Waislamu? Akasema “haijanikhusu, mimi nilikuwa namuondosha Sultan Al Jairu,” yaani, Sultani alokuwa dhalimu. Yeye Ben Bella kasema. Zikafanywa mbinu za kutaka sisi tuonane na yeye, yeye mwenyewe akakwepa, akakataa. Wakati ule wanasiasa wa zamani wa Kizanzibari walikuwa wapo hapa. Alikuwepo Dr. Ahmed Idarus Baalawi, alikuwepo Bwana Amani Thani. Sina hakika kama marehemu Sheikh Ali Muhsin alikuwa ameshatoka jela au bado kwa sababu nimesahau kidogo. Almuhimu, alikwepa manake na mimi niliambiwa nende, almuradi alikwepa, alikataa kuonana na sisi. Ilikua twende Sharjah, Emirates, ilikuwa nchi ya mwanzo iliomualika, Sheikh Sultan, alimuhishimu lakini kwa hakika halafu alimvunja moyo kila mtu. Kisha akenda zake Kuwait akaulizwa suala hilohilo akajibu vilvile katika jarida la Al Mujtamaa Al Balaagh la Kuwait, mhariri wake Abdurrahman Wilaayati. Jarida maarufu hilo. Jawabu alojibu huku [Emirates] akajibu kule [Kuwait] vilevile. Zaidi alosema wazi ni Ahmed Khalifa Suwedi alokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa United Arab Emirates (UAE). Katika kuzungumza naye jambo hili sku hiyo, alikuweko marehemu Hammuda bin Ali, Assistant Minister of State for UAE, alikuweko na Khilaf Said Al­Dhahiri, mkubwa wa uhamiaji wa UAE yotee. Siku hiyo tulikwenda kuzungumza matatizo ya Wazanzibari kuhusu sisi ukaazi wetu, hilo ndilo lengo tulioliendea. Tulionana nao hapo Sharjah. Ahmed Khalifa akasema, kwa hakika yalipotokea mambo ya Zanzibar nilikuwa mwanafunzi Cairo, ambaye sasa Ahmed Khalifa Suwedi ndo mumathil khaassa, mjumbe khassa wa Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al­Nahyan. Na ambaye kabla huyu huyu alikuwa ana wadhifa huo kwa Sheikh Zayed bin Sultan. Mmoja katika mtu shupavu, na alikuwa ni mtu mmakinifu, na ana sifa nyingi nzuri Ahmed Khalifa Suwedi. Sisi tulikuwa tukililia suala la ukaazi wetu kwa vile tulikwenda pale kwa kuwa sisi watu wa Zanzibar, Jumuiya ya Kizanzibari. Sasa katika kuzungumza alisema kuwa, mimi nilikuwa mwanafunzi wakti ule. Abdel Nasser ndo alotupoteza katika kadhia hii, alitupoteza katika hii kadhia. Katueleza vengine kumbe tumekuja kuona mambo vengine, sivo vile tulivokuwa tumeelezwa na Wamasri. Hii ni kauli kaisema mbele yangu mie na Bwana Amani Thani yupo. Hii ilikuwa katika mazungumzo. Hakukuwa na mazungumzo kuhusu politics [siasa] za Zanzibar au

Page 231: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 199

haikuwa kuzungumza juu ya mpango wowote juu ya Zanzibar. Wakimbizi wa Zanzibar walioko UAE, nini khatima yao juu ya suala la uraia? Kwa sababu yeye ndo alikuwa ni mtu mwenye khatamu nyingi na mkubwa wa uhamiaji, alikuwepo na pia Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwapo, marehemu Hammuda bin Ali. Katika mazungumzo, baada ya kumuuliza na kumueleza, na kama kususuika kwa msimamo wao, akasema, sisi msitulaumu, mimi nilikuwa mwanafunzi, tulikuwa hatujuwi, na akendelea kusema, sisi wengi mawazo yetu tulikuwa tukiiangalia Masri. Haya ndo maneno alokuwa amezungumza Ahmed Khalifa Suwedi. Sasa tukirudi nyuma huku sijui kama umeisoma ile ripoti ya shirika la kijasusi la Kimarekani CIA inayotoka kila baada ya miaka fulani. Na mimi naongeza vile kusema pia nimesoma, wavamizi wa kuivamia Zanzibar, wewe mwenyewe umeona. Na nafikiri umesoma kitabu alichokiandika mwenyewe John Okello Revolution in Zanzibar, kwa kuwa wao jumla walovamia, sote hatukuwa Wazanzibari.15

Nakumbuka kama skukosea, hotuba yake ilonukuliwa katika majarida [magazeti] ya Kenya yote, alipokuwa anarudi Korea, Moi Raisi wa Kenya. Palipokuwa na mgogoro baina ya yeye na Kanali Udongo, kwa vile Kanali Udongo yeye kabila yake ni Mjaluo. Aliporudi Moi Korea, kama sijakosea, 1992 au 1993, alimwambia, nyinyi ndugu zangu akina Kanali Udongo, mnapenda kujiingiza katika mambo, kila kitu mnajiingiza. Nyinyi mmejiingiza mambo ya South Sudan, nyinyi mmejiingiza mambo ya Uganda kumuweka Museveni, nyinyi mmehusika na njama za lile jaribio la kutaka kupindua Kenya, kisha akamwambia, na nyinyi ndo mlotumiliwa katika kuipinduwa Serikali ya Zanzibar! Haya maneno kayasema Daniel Arap Moi. Hakusema Mutta au mtu mwengine. Mchango wa nje ndio ulioleta kuja kuiondosha serikali yetu ya Zanzibar. Imezinduliwa kihalali tarehe 10 Disemba 1963. Dola ya Zanzibar. Haya yote nanukuu kauli mbalimbali. Na alokuja akasema zaidi tulipokaa nae ni Oscar Kambona. Kambona kaeleza yoote, mipango yote ilofanyika. Kakubali yeye mwenyewe mbele yangu. Kakubali mbele ya Sheikh Ali Muhsin. Kakubali mbele ya Amani Thani. Kakubali mbele ya jumla ya watu. Hatukukusudia sisi tudhukuru majina ya watu woote. Tunataka ule ushahidi tu. Waloipinduwa nchi ni wageni. Kwamba na mimi pia, Kambona, naskitika sana nilikuwa na mchango wangu. Lakini sisi ndo tulopanga yale mambo, pamoja na Nyerere, na walokuja kuvamia nchi yenu ni watu wengine. Haya ndo maneno alosema hayati Oscar Kambona. Na nafikiri inafahamika kasema mara nyingi, kasema wazi na katika kuzungumza na watu. Yote ukiangalia utaona inaskitisha, si fikra tulizokuwa nazo. Tulikuwa tukiona imetokea mapinduzi, kumbe kumetokea uvamizi. Khasa kwa vile sisi wengine tulikuwa wadogo, kama unavojuwa. Tumeona yale mambo, kwa hakika tumeona watu, lakini tulikuwa sisi kwa wakti ule ah! mbona huyu anasema Kiswahili chake cha kibara. Mbona hatumjui. Anatoka nchi gani huyu? Watu wageniwageni tumeona. Hata wengine wametuulia wazee wetu. Alokuja akamuuwa baba yangu mimi, kama unavojuwa, ni Kaujore ambaye kwamba si Mzanzibari. Alikwenda

Page 232: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili200

wazi kuwauwa watu watano msikitini buree! Mambo haya yanaonekana kwa ushahidi wa CIA, kwa kitabu cha John Okello, kwa ushahidi wa President Daniel Arap Moi. Ushahidi anosema mwenyewe Ben Bella na Kambona. Hawa ndo watu muhimu sana walotoa ushahidi kuonyesha kwamba yalotokea Zanzibar wao wametoa michango na zote zilikuwa kwa nguvu za kigeni. Mwenye hoja yoyote ataweza kuzielezea anavotaka yeye mwenyewe, azizungumze kama anaweza kuzungumza kinyume cha hivo. Raisi Boumedienne katika utawala, unajuwa utawala wake ulikuwa kipindi halafu yake akafariki. Lakini kuhusu suala letu sisi, tulimuona Balozi wa Algeria kwa masikitiko makubwa, na nikamulezea vipi Zanzibar msimamo wetu na wao, na khatima waliotufanyia wao Algeria, na hii ndo hali yetu unatuona hii. Anaitwa, familia yao namkumbuka, Al Masoudi au Al Masoud, nafikiri karibu kafariki huyu bwana. Balozi wa mwanzo wa Algeria UAE. Ipo katika munasaba fulani fulani ilitokea katika pirikapirika inatokea siku ya kusheherekea kupata uhuru, mara itatokea kwenda kuwaamkia Mashekehe katika munaasabat fulani fulani, huwa tunazungumza nae sisi akavutika na mazungumzo, akasema, njooni tuzungumze ofisini. Tukenda tukazungumza ofisini kwake tukamuelezea yote. Akakaa kimya sku hiyo akatwita. Akatwambia skilizeni, haya tunazungumza baina ya sisi na nyie, yametokea hayo yametuskitisha sana na Boumedienne anayajuwa na ni jambo linalomtia uchungu juu ya msimamo kwenda kututia sisi katika taarikh, historia, chafu kama hiyo. Haya maneno namnukuu Balozi wa Algeria alotwambia maneno kutoka kwa Boumedienne. Msimamo alofanya sisi tunaujuwa na hata akatumia Boumedienne kama ni moja katika sababu ya kujiingiza mambo huyu Ben Bella yalokuwa hastahiki, ndio moja katika sababu sisi tumempindua. Kwa hiyo Boumedienne alilielewa sana suala la Zanzibar. Boumedienne alikuwa ana hamu na suala la Zanzibar na alipata kuwajuwa watu mbalimbali wanaouhisika na suala la Zanzibar. Tukamwambia, mmoja anohusika bwana, na alotwambia sisi maneno ya ushahidi huo ni hayati Oscar Kambona. Huyo ndo atakupeni yeye maneno zaidi kafanya nini Ben Bella. Kambona akatakiwa aitwe, tukawapa njia wakamwita Kambona wakaonana naye. Akenda Kambona akaona nao wanohusika. Na katika jambo ambalo huyu Balozi akiskitika, akisema huyu Boutaflika anamtetea sana huyu Nyerere kwa sababu huyu ni katika watu alokuwa pamoja na Ben Bella. Ni jambo ambalo sisi tukiona unyonge. Hatufurahiki na msimamo wake huyu Boutaflika. Kambona walikutana na Boumedienne tena wakenda kivyao wenyewe. Mimi nimekuja hapa Dubai 1966. Nimeondoka Zanzibar baada ya matokeo ya kuskitisha yalotokea na kadhalika matokeo ya kuuliwa babangu miezi minane baada ya kutokea matokeo ya kuskitisha ya 1964. Nimekuja kwa kuondoka kama ni mkimbizi. Kwa sababu baada ya kutokea mambo yale, ya kuuliwa mzee wetu sisi, Mwenye Enzi Mungu amrahamu, miezi minane au saba baada ya mapinduzi, uvamizi, mimi nliondoka nikenda zangu bara. Nikenda zangu bara kwa sababu

Page 233: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 201

mimi mama zangu watu wa bara. Mamangu mimi mama zake, wazee wake ni watu wa bara, Kilosa, Usagara. Ndo nikenda kwa wajomba zangu nikakaa nao watu wa kule, halafu yake, ikanibidi mimi lazma niondoke nikatafute mustakbal, Zanzibar ilikuwa hapakaliki sku zile. Nikaja zangu Zanzibar, nimefika Zanzibar sikukaa, muda mchache mara siku hiyo saa nane ya usiku, ilikuwa nimekaa barazani kwetu nyumbani, nafikiri kama tunavokaa majumbani pale barazani tunazungumza tunapiga masoga, nakumbuka kama nilikuwa na kijana mmoja, sahiba yetu jirani akiitwa Ali Nassor Falahi, nafikiri unamjuwa yuko Maskati, ndugu yake Muhammed Nassor Falahi and Ahmed Nassor Falahi. Tumekaa tunazungumza pale, mara akatokea mtu mimi nilikuwa sikumjuwa kavaa nguo za kiraia nikamjuwa kakake pale, nikamjuwa anaitwa Sergeant Kongo (CID) mimi mwanafunzi 1966 nna miaka kama kumi na tano kumi na sita. Kaja pale akankuta nimekaa, nilikuwa na kijichuma mkononi, akaja akanikamata na wenzake wawili, Sergeant Kongo, maarufu alikuwa. Akaingia ndani nyumbani kwetu na kunisachi mimi mwilini huku akinichochachocha kwa bastola na ilhali yeye alikuwa kalewa! Nini? Kwamba wamekuja kunkamata mimi wamesikia mtoto wa miaka kumi na tano nataka kulipa kisasi cha babangu. Ndo kosa langu na hata kama nilikuwa nataka kufanya kweli. Ndo nnakuja habari ya Dubai nakuelezea hapo yangu mwenyewe. Nikaja nkachukuliwa pale nikapelekwa Malindi Police Station, nikakamatwa nikaambiwa huyu bwana tumemkamata, yaani mimi mtoto wa miaka kumi na tano, kumi na sita, tumemkuta kakaa barazani, tena tumepata ripoti kwamba anataka kulipa kisasi cha babake, manake babangu mie kauliwa na Muhammed Abdalla Kaujore, memba wa Baraza la Mapinduzi, ambaye anatoka bara. Hii haikuwa ghasia huyu ni memba wa Baraza la Mapinduzi, ni mtu wa serikali, ni kama Waziri. Kaja kufanya kitendo hicho. Hakikufanywa na watu wahuni tu. Mimi nikistaajabu yale mambo, manake yale mambo yenyewe sielewi. Tangu hapo sijifahamu katika hali ya mambo yalotokea Zanzibar yale, halafu kuuliwa babangu. Manake hatujijuwi tumetawanyika. Halafu tena kinatokea kitu kama kile. Naona jambo kubwa saana. Hatari kubwa hii! Watakuja kuniua maana yake kazi yao ilikuwa kuuwa tu. Sasa pale baada ya kukamatwa, wakawa wanaandikaandika wale polisi wakawa wanazungumza, wanasema “Kama huyu, huyu mtoto mdogo, kuna ushahidi gani?” Wenyewe kwa wenyewe. Wakasema tufanyeni hatutaki balaa. Tutamngoja bwana mkubwa asubuhi, yaani siku zile usiku wa manane ni usiku mkubwa Zanzibar. Nkakaa pale nkawekwa kituo cha Malindi mpaka asubuhi, kesha nkapelekwa, kuna mahkama. Ilikuwa mahkama hiyo ilikuwa primary court ikiitwa. Ilikuwa korti yenyewe waliiweka pale ilipokuwa ofisi ya Bwana Soud Ahmed Busaidi. Pale ilikuwa imewekwa mahali ilikuwa imefanywa kama mahkama hivi. Basi asubuhi mimi napelekwa kwenda kushtakiwa kwamba nataka kulipa kisasi cha babangu alouliwa buree! Watu watano na mtoto mdogo

Page 234: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili202

waliuliwa msikitini Zanzibar. Katika hao na watu wawili walijeruhiwa. Siku nlopelekwa mimi nikamkuta na marehemu Maalim Juma Himidi wa Darajani School. Tulikuwa pamoja na wengine siwakumbuki. Na alikuwa jaji wakti ule yule jamaa akiitwa Haji, sijui nani, ni mtu wa Kizanzibari, mamake alikuwa Hizbu mmoja mkubwa, lakini huyu alikuwa Afro­Shirazi mkubwa. Akaitwa Maalim Juma Himidi, alianza kabla yangu mimi au baada yangu mimi, almuhimu mimi nikaitwa. Yule bwana Haji akaulizana na wenzake. Ndo mambo gani vipi hivi? Alishangaa yeye kuona mambo yale. “Toka nenda zako nyumbani. Mbio!” Na mimi nyumbani ndo palepale. Nkazidi kuingiliwa na vitisho. Nkaona bora niondoke haraka. Sasa mimi ndo nnasafiri kutoka Zanzibar. Mimi nikaondoka Zanzibar baada ya matokeo yale, nikasafiri nafikiri tarehe naikumbuka. Nimeondoka Zanzibar katika tarehe 19 Julai 1966 kwa meli ya Karfuyes. Tulikuwa majmua ya watu. Kundi letu sisi alikuwako Sheikhuna, bila ya shaka unamjuwa, alikuweko Muhammed Seif Barwani, Ahmed Ishti, Said Seif Riyami ambaye yeye ni mmoja katika wakuu wa Polisi Oman, unamjuwa wewe mwenyewe, ndugu yake Abii Seif. Khalfan Hilali. Yaani jamaa wengi sana waliingia ndani ya meli hiyo. Wengine Zanzibar, wengine wakapandia Mombasa iliposimama. Ilikuwa kitu maarufu wakti ule watu kufahamu maudhui yetu. Wakawa wanatuonea huruma. Wengine hujificha chini ya pango chini. Kuna wengine kama unavojuwa taabu walioipata. Waliingia kwenye mavi ya ngombe. Wengine wakafa njiani. Tuliingia kwa njia ya bandarini. Tuliogopa zaidi tusije tukakamatwa na askari wale wa Karume pale. Wale waliokuwa katika meli wakituonea huruma kusema kweli. Kuna wengine waliingia walikata tiket mpaka Mombasa. Sisi nafikiri tulikuwa hatupungui ishirini. Muhimu chombo kikenda na muhimu tumefika Dubai. Mwezi huo huo wa Julai 1966 tulifika Dubai. Tukafika Dubai. Kufika bandari. Kwa hakika si bandarini. Kulikuwa hakuna bandari wakti ule 1966. Tumefika tumesimama mbali sana hata Dubai hatukuoni manake Dubai bado ilikuwa hakuna maendeleo ya leo. Mbali sana hata hatukuoni. Tukakaa zaidi ya saa moja. Mara ikaja boti. Kwa mbali tunaiona inakuja hiyo, hiyo, hiyo, hiyo. Katika boti akateremka mtu Mwarabu, nimekuja kumjua baadae, tumejuwana, akiitwa Rashid Matrushi, mmoja katika maofisa wa Idara, nafikiri ilikuwa ya bandari au idara ya paspoti. Akapanda ndani ya meli na maaskari walikuwepo pale wa Kidubai. Akasema Wazanzibari wasimame upande mmoja. Tukasimama. Akasema hawa kwa amri ya Sheikh Rashid na bila ya kikwazo chochote wateremke nchini. Huo ulikuwa ni ujumbe kaleta mwenyewe marehemu Sheikh Rashid bin Said Al­Maktoum, Mungu amrehemu na amuweke pahala pema. Sie tukateremka rasmi. Tukashuka nchini kila mmoja tena akatafuta njia yake. Dubai muhimu nilipofika mimi nimekuta jamaa wameshasimama, wameshaunda jumuiya ya kusaidiana. Nimeyakuta tayari kabisa. Ishaundwa Association. Na hapa nna barua ambayo kwamba alipelekewa Sheikh Rashid ya tarehe 13 July

Page 235: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 203

1964 ilotiwa saini na Bwana Ali Masoud Thani ndo aloanzisha jumuiya wakati ule ndo aloandika barua. Mwanawe yule alokuwa Cairo, Masoud Ali Masoud Thani. Marehemu babake ndo alotia saini barua hii akampelekea Sheikh Rashid, baada ya kumuamkia kumwambia nakuletea hii barua kwa niaba ya Wazanzibari walokimbia baada ya kile kinachoitwa mapinduzi ya kibaguzi. Tunakuja kwako kutaka himaya na kutaka msaada. Nia yetu ni kuasisi sisi jumuiya ya khairiya chini ya uangalizi wako ili kusaidia wale watoto walobaki kule watakapokuja huku. Hatuwezi sisi hii jumuiya kuiunda bila ya kutaka muwafaka wako. Na napenda kukujuulisha tunataka utupe muwafaka wako ili tuweze kuiasisi jumuiya hii ya khairiya. Na kadhalika anamwambia katika barua hiyo, British Resident [Balozi wa Kiingereza], anajuwa hayo na yeye hana kizuizi chochote kuundwa jumuiya hii. Tunaomba utupe rukhsa ili jumuiya hii iwe inasema kwa niaba ya Wazanzibari wote. Hii ndo barua. Sheikh Rashid barua hii hii akaandika “La mania ladayna.” Sina pingamizi kuunda Jumuiya ya Wazanzibari. Jumuiya hii iliundwa. Ilikuwa na Katiba yake na vipengele va Katiba viko vingi lakini katika lengo kuu ilikuwa ni kuwapokea katika makaazi mepya Wazanzibari hapa katika nchi walotuchangilia hapa Dubai. Na katika mwaka 1965 alikuja Mtukufu Mfalme wetu Sayyid Jamshid bin Abdullah, pamoja na marehemu Bwana Ahmed Seif Kharusi. Kaja Mfalme wetu kuja kumshukuru Sheikh Rashid kwa mapokezi ya kuwapokea wakimbizi wa Kizanzibari. Katika kumshukuru, pia kumuomba, na kumtafadhilisha, awe raia zake ni kama amana, yeye awatabir kama ni raia zake. Awachukulie kama ni raia zake. Sheikh Rashid Mungu amrehemu, alilipokea suala hili kwa furaha kubwa sana na akakubali kama sisi ni amana kwake. Na ndo mpaka leo hii ndo sisi tumekaa hapa. Sasa Mwenye Enzi Mungu, Sayyid Jamshid, Mungu ampe umri mrefu Mfalme wetu nasema tena, na namshukuru na namuombea dua daima Sheikh Rashid Al­Maktoum, na wanawe watukufu, ambao hatuna fadhila za kuwalipa. Baada ya sisi kuwa tumetoka kwetu, tumenyanyaswa nchi yetu wenyewe! Tumefukuzwa, tumenajisiwa, tumenyanganywa kila kitu. Kwetuu! Tumekuja kwa watu wageni wasotujuwa wametupokea, alhamdulillah Mungu awajazi kheri. Baada ya hapo mimi niko hapa nikendazangu kusoma Qatar, na 1966 mwaka huo huo nkenda zangu kusoma Kuwait na Kuwait wakitoa scholarships [nafasi za kusoma] khasa kuwasaidia wakimbizi wa Kizanzibari. Alofanya jambo hili, alolisimamisha Mungu amrehemu na amlaze mahali pema, ambaye hatuna fadhila za kumlipa, Bwana Ahmed Lemky. Yeye ndo alokuwa balozi wetu wa kwanza kuteuliwa baada ya kupata uhuru wetu Zanzibar, wa halali, tarehe 10 Disemba 1963. Alikuwa Balozi huko Masri. Na kama unavojuwa, Zanzibar ilipopata uhuru ilijiunga na Umoja wa Mataifa kuwa ni Dola kamili na tulikuwa na ofisi kama unavujuwa, na vilevile na Cairo, na ilikuwa Zanzibar inaendelea kufungua ubalozi Indonesia ambako aliyekuwa Rais Ali Hassan Mwinyi ndie angelikuwa Balozi wetu Jakarta, lakini bahati mbaya Dola ya Zanzibar ikaanguka.

Page 236: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili204

Na kadhalika vilevile Qatar ilitowa scholarships kwa njia ya huyu huyu Bwana Ahmed Lemky. Baadae nikashika mimi nafasi ile kuhusu scholarships za Qatar. Na Bahrain, Arabian Gulf University ilichukuwa watoto wetu wa Kizanzibari, mbali kutoka Zanzibar Association. Na kadhalika hatuitoi kwenye shukurani serikali na watu wa Iraq ya wakati ule. Walitusaidia sana. Tulikuwa na wanafunzi mimi nafikri wanafika mia tatu! Kuwaonea huruma kwa kibinaadamu watoto wetu wakasomeshwa. Tunashukuru sanaa! Tunazishukuru pia nchi mbalimbali zilizosimama na sisi. Saudia Arabia pia ilitusaidia kwa upande wa kibinaadamu vilevile. Sasa kuna kitu muhimu sana baada ya hiyo Association yetu kuundwa Dubai. Jumuiya hii ilitambulikana na United Nations High Commission for Refugees (UNHCR) ambayo ilisimama na sisi na kutusaidia sana! Hata ndio msingi wa kusi mamishwa majengo ya Kizanzibari ya hapa Rashidiya, Dubai. Iliasisiwa kha sa fikra hii, kweli walitoa Zanzibar Association, lakini ilikuwa UNHCR, alikuwepo muwakilishi Bwana Gubia, aki deal [akiwasiliana] na sisi. Yeye nafi­kiri ndo alokuwa mjumbe wa UNHRC, nafikiri katika Mashariki ya Kati, kwa wakimbizi wa Kifalastini na sisi Wazanzibari nafikiri. Na Bwana Gubia kwa upande wake United Nations ikawa tukapata scholarships sisi watu wetu wakasoma Libnani, Lebanon. Njia ya huyu UNHCR. Baada ya Gubia wakaja watu wengine tena wanohusika, tukaendelea nao. Na kadhalika vilevile mimi vile msimamo wangu walivoniona jamaa wa kuwasaidia wenzangu na kujuwana na watu kidogokidogo wakapendelea mimi niingie katika Jumuiya ya Kizanzibari. Nilikuwa mgumu sana, sikukubali kuingia kwa sababu ni kitu kipya kwangu mimi. Kuna kazi ngumu. Basi mwisho wakamtumilia marehemu ndugu yangu Hashim ambaye yeye ndo alonchukuwa mimi toka udogoni kuja hapa. Kama babangu alikuwa. Akanilazimisha mie nikaingia Kamati ya Jumuiya kama ni memba. Ndo nlivoanza. Haukufika muda mkubwa nikachaguliwa Raisi wa Jumuiya ya Kizanzibari na nikazidi kufunguwa mawasiliano sehemu mbalimbali. Tulilazimika kwa vile Wazanzibari walikuwa wametawanyika kwenye nchi zote za jirani ya Dubai. Bila ya shaka msimamo wa viongozi wengine wa UAE, Mfalme wa Sharjah, Mfalme wa Ummu Qulwein, kote, tunashukuru. Abu Dhabi. Kote tunashukuru. Hii Zanzibar Association baada ya kuingia mimi tukazidi kutafuta sehemu za kuweza kusaidia watu wetu, na katika Al Aalam Al-Islami, ulimwengu wa Kiislamu. Tumejaribu zaidi sisi kutafuta njia katika jumuiya za kibinaadamu na nyingine zilikuwa zina nguvu za kututetea na kutusemea. Sisi tukawa tunafanya kazi na Zanzibar Organisation ambayo ilikuwa ni organization ya kisiasa. Sisi kwa upande wa kibinaadamu tumeshirikiana nao khususan wale watu wetu walokuwa wakionewa bure na hawajulikani kama ni hai au maiti. Tukawa vilevile tuna deal na Amnesty International, shirika maarufu la kupigania haki za binaadamu duniani na kuwa tunashirikiana na Human Rights Association Organisation. Na

Page 237: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 205

kadhalika vilevile Zanzibar Association ilitambuliwa rasmi na World Muslim League ya Saudi Arabia. Kudhulumiwa watu wetu wa Zanzibar bure, walikuwa wakifungwa na dhulma zilozokuwa zikipitikana, kama zile ndoa za nguvu, za kuuliwa watu kiholela, au kunajisiwa watu kwa nguvu. Haya yote yalipita na yalifanywa na watu wenye nyadhifa zao. Ni mambo ya kuskitisha. Walishirikiana wote pamoja na Nyerere vilevile. Na Nyerere angeliweza yeye kumwambia Karume alipolizuwia gazeti la Uhuru Zanzibar, haya maneno sasa namnukuu Oscar Kambona, narudi nyuma samahani…Kambona anasema Othman Sharifu alipokuwa Ubalozi wa Tanzania Washington, D.C. na Hanga alikuwa kama Balozi kule Guinea. Karume kawataka hawa na lengo lake lilikuwa anataka kuwauwa kwa sababu Karume walikuwa maadui zake hawa walokuwa wale Afro­Shirazi wazalendo. Mimi nikamuuliza Kambona, kwani Afro­Shirazi wazalendo ni nini? Namuuliza Kambona katika mazungumzo., anatuzungumzia sisi. Anasema Afro­Shirazi wazalendo ni wale walokuwa Wazanzibari wenyeji. Anasema, samahani leo nakwambia hivi. Anamuogopa Othman Sharifu, anamuogopa Hanga, wale walokuwa wasomi. Ndo maana alitangulia kuwamaliza kina Twala, Saleh Saadalla Akida, Mdungi Usi. Hawa walikuwa tishio kwake na khususan kuwa wamesoma na wana msimamo. Alipowaita akina Hanga ilikuwa ni katika mpango wa kutaka kuwauwa. Hanga alivoitwa, anasema Kambona, alimwendea Ahmed Sekou Toure, akamwambia naitwa na mimi nachelea nikiitwa ntakwenda kukamatwa niuwawe wakati mimi ni Balozi. Akasema, hakukasir Sekou Toure, almuradi akampigia simu Nyerere na akaandika barua, kuwa huyu anakuja, chukuwa dhamana kama kuna wasiwasi wowote wa kuuliwa na kama anakosa ahukumiwe kwenye vyombo va kisheria. Nyerere akamjibu kwa barua, kuwa dhamana mimi, basi aje Hanga na sitompeleka Zanzibar. Hatouwawa. Kadhalika Othman Sharifu. Wao wakaja zao, Kambona akapata habari. Anasema yeye alikuwa hayupo, alikuwa Mwanza au sijui wapi, lakini tena Othman Sharifu keshavishwa nguo za jela na kanyolewa kipara na ndege ishaletwa kutoka Zanzibar. Anasema, nkatoka nkenda kwa Nyeyere. Nkamwambia, Mwalimu, kama unataka kumkamata huyu, kwanza ujuwe huyu ni Balozi, aachishwe wadhifa huyu kwanza. Akamjibu kwamba mimi siwezi, Karume kamtaka. Akamwambia Karume kamtaka huyu na Hanga lakini wewe si ulimuahidi Sekou Toure hutawapeleka Zanzibar? Akamwambia, lakini Mwalimu, Karume ulipoandika makala na haikumpendeza alisema Karume kuwa yeye atavunja Muungano ikiwa utataka gazeti la Uhuru litaingia Zanzibar, itakuwa gazeti bora kuliko roho ya mtu? Kambona anasema haikuwa lolote isipokuwa aliwapeleka Zanzibar. Hiyo ndio hali ilivokuwa. Sasa mimi nimezungumza kirefu kwa bahati mbaya lakini kuna mambo na nimerukia hili, lakini Zanzibar Association ilikuwa ikiendelea. Iikuwa ikifanya kazi zake za kibinaadamu. Ilikuwa ikisimamia watu kupata scholarships kwenda kusoma. Ilikuwa na haiba na heshma yake sehemu za

Page 238: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili206

Gulf. Pakitokea popote matatizo ya Wazanzibari ilikuwa mie nakwenda kwa vile mie nilikuwa Raisi wa Jumuiya, naonana na authorities [wakubwa], wanatusaidia wakubwa wa nchi, wafalme. Kote huko, Saudi Arabia mpaka Bahrain. Kwa mfano kadhia moja inanikumbusha msimamo wa Bahrain. Nasrin unamjuwa katika wale walioolewa kwa nguvu. Baada ya kuwachiwa, bila ya shaka baada ya pressure [shinikizo] kubwa alofanyiwa Nyerere. Wakafunguliwa, wakatoroshwa. Nasrin maskini alikuwa hajui afanye nini. Kaja zake Dubai, hana visa, hawamjui airport, mimi nilikuwa nimesafiri, ikabidi ende Bahrain. Bahrain marehemu Bwana Salim Slim, Mungu amrehemu, akawaelezea kuhusu mtoto wa kike kuwa hana visa tumteremshe hapa, ikaelezewa kadhia yake. Watawala wa Bahrain kwa ubinaadamu wa Al Khalifa, Mungu amuhifadhi, walisimama wakamsaidia mtoto. Mimi nilipofika nikasikia. Kupata habari yake nikachukuwa nyaraka zote na magazeti na kila kitu nkenda kwa Sheikh Rashid Mungu amrehemu. Nikamwambia Sheikh Rashid nimekuja kwa kadhia hii. Akanambia nenda kwa Sheikh Muhammed bin Rashid ambaye ni Ruler wa leo wa Dubai. Sheikh Muhammed akasema nipitie usiku. Nikampitia usiku nikamuelezea, hakukassir, hapohapo akatoa amri akifika ateremke kwa amri yake. Jinsi walivokuwa na huruma watu hawa. Huko kwetu viongozi wetu wanatuuwa, wanatunyanyasa, hawa wametuonea huruma jamani. Nasrin unajuwa, mtoto wa miaka kumi na tatu, kaozeshwa kwa nguvu kwa bunduki! Haya, akaletwa Nasrin, nikapelekwa mimi mpaka kwenye mlango wa ndege kwa amri ya Sheikh, nikamteremsha akapata fursa kukaa nchini. Hii ni kadhia moja tu katika kadhia nyingi za kibinaadamu ambazo Association ilikuwa ikipigania kuwapigania watu wetu katika nchi hii. Hapa kwa hakika hadithi ya Zanzibar Association ni hadithi ndefu sana kama unavojuwa. Hadithi ndefu sana. Kuna mengi yamefanyika katika Association ya kibinaadamu, na misimamo mingi ya kiungwana imesimama, inajulikana. Association ilikuwa ni kitu muhimu sana kwa Wazanzibari, la ingelikuwa hakuna Association Wazanzibari wangelikuwa wamesambaratika. Mimi naeleza Zanzibar Association ilikuweko, bila ya shaka ilikuwa ni kitu, sijui wanakiona vipi Watanzania, walikuwa wakifasiri Serikali kama ni tishio kwao ilhali sisi mambo yetu yote yalikuwa ni ya kibinaadamu tu. Ilikuwa wanaona kuwa ni aibu kwamba kuna Association ilotambuliwa na United Nations High Commission for Refugees. Jambo hili lilikuwa likiwauma saana! Wakiona ni matusi kwa Dola yao. Kama ni aibu kufedheheshwa, kutoka aibu zao mambo waliotufanyia. Dhulma waliotufanyia wakti ule. Zanzibar Association kwa hakika sasa haiko tena. Kutokuweko kwake hakuna alaka na kuweko kwa Tanzania Association. Ni vitu viwili mbalimbali nnataka kukueleza ufahamu. Baada ya kufa kwa Jumuiya ya Kizanzibari ikafunguliwa hiyo Jumuiya ya Watanzania, ukafunguliwa sasa na ubalozi Abu Dhabi. Ilifunguliwa Tanzania Association si kwa kuwa kuja kuichukuwa Zanzibar Association. Zanzibar

Page 239: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 207

Association ilikuwa imeshakufa. Ishauliwa! Tanzania Association inakuja kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na Katiba yao. Juzi Tanzania Association wamefanya futari, wametualika sote, bahati mbaya mimi sikupata gari lakini nilialikwa. Kenya Friendship Association tunaalikwa tunakwenda. Mpaka sasa hivi hakuna mgogoro khassa. Imefika wakati hakuna mgogoro kwa sababu upande wa pili [Zanzibar] hakuna tena. Zanzibar Association haiko tena lakini nataka kukwambia kitu kimoja. Sisi tulipokuwa na Association, tulikuwa sisi hapana haja ya kufanya ugomvi kwa sababu tukiwachukuwa ndugu zetu, kutoka Tanzania, madam ndugu zetu kutoka Dar es Salaam au kutoka Kenya ilikuwa sisi tukiwasaidia na wanajuwa wenyewe. Tulikuwa na memba sisi wa aina hiyo tena wengi na si wa kutoka Zanzibar tu. Na katika Katiba ya Association Coastal Strip [Mwambao] imo lakini sisi tukazidi kuomba zaidi tukakubaliwa tukawatia hao wenzetu kutoka Dar es Salaam na nini na nini. Si sisi kwa sisi? Sisi ndugu ati. Sote sisi ni ndugu. Kisiasa kitu kingine, wendawazimu wa kisiasa na wazimu wao, walokuwa na akili wataendesha vizuri. Ikiwa wendawazimu wataendesha mambo kiwazimu. Sisi yapo mahusiano. Saudia imeshafungua Ubalozi Dar es Salaam, na Tanzania imefunguwa Ubalozi Saudia. UAE ina Ubalozi Dar es Salaam, Dar es Salaam ina ubalozi huku [Abu Dhabi] vilevile kama unavojuwa. Msimamo wa Omani kama unavojuwa masala ya Wazanzibari kwa jumla, sasa mimi nam quote Mfalme Mtukufu wa Oman, Sultan Qaboos bin Said. Alipoanza kuja katika utawala na khatamu za utawala, alifanyiwa mahojiano, kama sijakosea lile jarida zamani likiitwa Al Hawadith, alifanyiwa mahojiano ilikuwa makala jarida lote Qaboos tu anaelezea. Lote! Nakumbuka kile kifungu alichoulizwa nini maoni yako juu ya kadhia ya Wazanzibari na kadhia ya Zanzibar? Nakumbuka hivii. Sultan akajibu kwamba hii ni kadhia ya kibinaadamu, si jukumu linalotukhusu sisi Oman, bali linakhusu ulimwengu mzima na nchi za Kiarabu zote. Hii ndo jawabu alojibu Sultan Qaboos bin Said. Sayyid Khalifa bin Haroub akizungumzia katika miaka ya 1920 au 30 kuhusu ndoto yake ya kutaka kuona nchi za East Africa zinaungana kama United States of America. Kama kawaida yake Sayyid Khalifa, ulikuwa utawala wake, sio kama wanavosingizia watu, sisi ndo tulikuwa wa mwanzo tulosema juu ya masuala ya muungano. Wala isimpitikie mtu kama labda sisi Wazanzibari tunaupinga muungano. La hakuna anayekataa Muungano. Nani anakataa Muungano? Lakini mambo yende kwa kidesturi, kuheshimiana, si kukandamizana na kunyanyasana. La. Na haya mambo ya kufanya East African Community, mchango wa watu wa mwanzo toka wakati wa vuguvugu la ukombozi walisimama kina marehemu Sheikh Ali Muhsin na wengineo, walikuwa akina Tom Mboya. Wazanzibari ndo walokuwa katika mstari wa mwanzo. Hakuna mtu alopinga. Kinachopingwa ni unyanyasaji. Kama kwamba sisi tumekutekeni! Kutufanyia kejeli. Ndo jambo lisilotakiwa. Sisi si tanguwapo tumeungana? Si mimi nimekwambia mamangu Msagara? Na wangapi na wangapi walikuwa wengine wazee wao

Page 240: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili208

Wanyamwezi, Wazaramu, tumechanganya damu sote. Na hili suala la kutia fitna, sijui utumwa, sijui kitu gani. Hili suala bwana limefanywa na kabila moja tu? Walikuwa Waafrika wakiuzana. Iwe kosa wamefanya watu walokuwa Waislamu tu? Ndo iwe kosa. Uchafu wote walofanya wengine walokuwa si Waislamu wamechukuliwa wametupwa na kusahaulia na wamekumbukwa Waislamu tu. Makabila yanajulikana ya kibara, wa kabila fulani walikuwa watumwa wao fulani, na kabila fulani walikuwa watumwa wao fulani. Yote yanajulikana hayo. Waafrika kwa Waafrika. Mie ntakuelezea kisa. Nilipokwenda zangu bara mimi huo mwaka 1966, nilipofika mimi nkawaona wazee wangu, mjomba wangu Habibu nikamuona, nkawaona bibi zangu kina Biti Kinyamare, Biti Farahani, wazee wetu wengine kina Mjomba Kibwana, na hao wengine tulikhusiana nao kina Mwinyi Kondo, na nani, kwenye ukoo wa mama yetu. Kina Khamisi Mrisho. Sasa siku hiyo nkaambiwa nitapelekwa kwenda kumsalimia bibi yetu. Anakuwa upande wa babake bibi yetu Biti Kinyamare na Biti Hogore katika daraja ya wazee. Nikatoka mimi nikapelekwa siku hiyo. Biti Hogore siku hizo alikuwa ana uwezo. Biti Hogore alikuwa mtu mzima nilipomkuta wakti ule. Ameshafika 70 na kitu. Nikenda zangu, kumsalimia. Nyumba yake ina uwa mkubwa. Kakaa kwenye kiti, kashika bakora, na mapete ya dhahabu kwenye vidole, na kajifunika kanga. “Karibu mjukuu wangu.” Nikenda kumbusu mkono, nikamsalimia. Nilikwenda mimi na mjomba wangu Habibu, na Bibi Kitimare, ndugu wa mama yangu marehemu. Hapa nataka kukueleza kitu. Akatokea bibi mmoja sikumbuki kama nimekosea jina, kama akiitwa Biti Nyama. Huyo bibi mkubwa kuliko Biti Hogore. Huyo bibi mimi nasema alikuwa thamanini na kitu. Anakuja pale. Mimi nainuka kwenda kumsalimia yule Bibi, Biti Nyama. Tabia yetu Wazanzibari, tunamsalimia mtu yoyote. Hakuna ubaguzi. Nikazuwiliwa “kaa kitako!” Nikashtuka. Nikakaa kitako mie. Yule bibi akaulizwa, “unamjuwa huyu?” Akatizama, “huyu kama sura za Biti Muhamedi naona.” Nikaulizwa, “unamjuwa huyu bibi?” Nikasema “bibi ni bibi.” “Huyu ni mtumwa wenu!” Msagara, hawa ni Wasagara. Waafrika kwao Kilosa. Wasagara na Waruguru ni bin ami lazima ujuwe. Mimi bwana nkwambie nilishtuka kwa sababu kule Zanzibar nasikia utumwa lakini hatujauona utumwa wanaousema. Huyo mwenye kuusema hajauona. Utumwa, sijui nini, Waarabu! Sasa mimi nnasema, bibi zangu mimi, hawa si Waafrika? Mbona yule mtumwa wao? Nikamuuliza mjomba wangu Habibu. Kwani bibi zetu Waarabu? Akanambia hata. Waafrika, Wasagara. Ndo nkaanza kufahamu sasa. Wana watumwa hawa Wasagara Waafrika nao huku Nyerere akituambia “Waarabu!” Karume akituambia “Waarabu!” Kumbe watumwa wako Waafrika kwa Waafrika, sisi wenyewe upande wa mama yangu Wasagara, mimi bibi zangu Wasagara. Bibi zetu wenyewe ndo hao Waafrika. Hadithi yangu mwenyewe. Tunasikia mvutano uliokuweko huko kwetu sasa hivi juu ya suala la Zanzibar,

Page 241: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 209

na jambo ninaloliomba wakae chini wazungumze. Fujo haitoleta kheri. Wakae chini wazungumze, wahafamiane namna watakavotekeleza. Haiwezekani kwani ni kweli Zanzibar ilikuwa ni Dola. Ilipata uhuru tarehe 10 Disemba 1963. Ilikuwa memba katika Umoja wa Mataifa. Ni jambo ambalo haikutangaza Umoja wa Mataifa wala haikuandikwa barua itolewe na mpaka leo haikutolewa. Yamefanywa mambo kiholela tu. Walivoingia Muungano, kila mtu anaulezea, mimi nasema si wa halali. Almuhimu ni kwamba huu si wakati wa kuendeleza migogoro. Huu ni wakti wa kusikilizana. Tusitafute mambo ikawa kama Ruwanda, ikawa nchi yetu kama Iraqi, ikawa nchi yetu kama Afghanistani, kama Somalia, tukawapa fursa madola. Leo madola yamekaa yanangojea tu wapi pakwenda kushika watakwenda kushika. Tukianza kugombana wataanza kuingia hawa. Tizama leo Pakistani inavoingia katika matatizo kwa kutofahamiana. Itakuja kuwa kama Iraqi na Afghanistan. Bahati mbaya. Au kama Somalia. Ni jambo la kuskitisha. Waangalie watu watizame mbele. Mahatma Gandhi kasema kama macho yetu yako mbele hayako nyuma, tutizame mbele. Nchi isitiwe katika fujo labda iwe hapana budi na kwa nini iwe hapana budi wakati watu wana akili zao. Hayo yalopita tunajuwa, ni madola makubwa. Tutasamehe lakini hatutosahau. Bila ya shaka yaliotufika wewe unayajuwa unakumbuka yanaumiza sana. Mtu umekaa anakuja kumchukuwa binti yako, anakwenda mtu fulani amchukuwe akamnajis tu. Ilikuwa hamna usalama katika nchi. Unaweza ukakaa ukaambiwa nyumba toka kaitamani Saidi Washoto, kaitamani nani. Haya mambo yalifanyika kwetu sisi. Nani asojuwa? Kuna watu waliouliwa wazee wao wakaona machoni mwao. Haya mambo jamani ni mambo mingine. Hawa wanazungumza vitu vengine. Haya mambo yanaumiza. Au kama mimi aliuliwa babangu buree! Kaambiwa Karume akasema “mwendawazimu yule” ndo ilokuwa jawabu yake. Mwendawazimu yule Kaujore. Haya. Nyerere wala hakushituka! Nyerere hakushituka wala hakujali! Anasema siku Kambona alokwenda kumwambia Nyerere habari ya kuuliwa watu msikitini, akamwambia “unaona mambo haya?” Maana Kambona akijaribu baadae akiyaona yale makosa. Akasema nimemwendea Nyerere, hakunambia “ndio” hakunambia “sio.” Kanitizama tu hivi akageuza uso. Hakunambia “sio” wala “ndio.” Kimya! “Asukuut alamatu ridhaa.” Kunyamaza ni dalili ya kukubali jambo. Anasema Kambona, Nyerere hakunambia “fyoko!” Hii ndo hali. Utaona mambo mengine haya watu wameyafanya kama mali yao. Hii nchi (Zanzibar) kama mali yao. Walobaki wote si mali yao. Ndo haya masala yanayozungumzwa juu ya Zanzibar na Tanganyika. Maana mimi sizungumzii masala ya kijamii. Masala ya kijamii sisi hatuwezi kukosana sisi watu wa Zanzibar na watu wa bara. Ni ndugu kama ninavofahamu mie. Lakini anaelezea Kambona anasema, wakati ilipokuwa kunazungumzwa juu ya jina, jinsi wengine walivokuwa wana hamu ya kulifuta hili jina la Zanzibar, walipozungumza kutafuta jina la muungano wa Zanzibar na Tangayika

Page 242: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili210

upewe jina gani? Yakatoka majina matatu: Tanzibar, Tangabar, nimelisahau la mwisho. Muhimu, Nyerere katoka na jina jipya. Akasema “Tanzania.”16 Jamaa wakasataajabu, hii “Tanzania” ina alaka gani? Nyerere akasema nataka “Tanzania” kwa sababu hili jina la “Azania” ndilo jina la Bahari ya Hindi mpaka Afrika ya Kusini ikiitwa hivooo! Huyu Nyerere anasema. Sasa ndo kuna “Azania Street” kule bara Tanganyika, na kama unakumbuka Afrika ya Kusini ikiitwa “Azania.” Harakati za mwanzo za Afrika ya Kusini zikiitwa harakati za “Azania.” Anaelezea Mahmud Ismail katika kitabu cha taarikh ya Tanzania, kitabu kinaitwa Tanzania, Tanganyika na Zanzibar, ni majina mawili yameunganishwa. “Tan” ni Tanganyika, na “Zania” ni “Azania.” Azania ulikuwa ni utawala miaka elfu kabla hajaziliwa Yesu, ulikuwa ufalme wa kipagani, inajulikana. Kulikuwa mwanzo na “Osanik” halafu ikaja “Azania” Empire. Kote huku, inaingia mpaka Indian Ocean, mwanzo ikiitwa “Osanik” kasha ikaja kuitwa “Azania.” Kama alivosema Nyerere, Afrika ya Kusini kulikuwa na pahali pakiitwa “Azania” ni kweli. “Tanzania” haina uhusiano wowote na Tanganyika na Zanzibar! Ni Tanganyika na Azania! Tukiambiwa siku zote, unaona majina mawili, Tanganyika na Zanzibar! Imekhusu nini “Azania?” Zanzibar wapi? Kitendawili hicho kakifichuwa Oscar Kambona. Kambona ni kiungo muhimu kwa matokeo ya Zanzibar. Bila ya kiasi. Kwanza, yeye alikiri rasmi kwetu sisi, mbele ya Sheikh Ali Muhsin, mbele ya Bwana Amani Thani, na mimi nlikuweko. Alikiri rasmi kama zile njama zilifanywa kule (Tanganyika). Hilo alikiri rasmi. Na alikiri rasmi kwamba ulikuwa uvamizi na kama hivo unavosikia wewe. Hilo kakiri rasmi. Pia alitaja vitu vingine ambavo nilivihakikisha kutoka kwa watu wengine. Jambo moja ni kuna nyimbo kubwa inayoimbwa Tanzania juu ya ujamaa, yaani “African socialism.” Sasa Kambona alituelezea ambavo sivyo tulivodhania. Baada ya ukombozi katika Afrika chini ya Jangwa la Sahara kulikuwa na wasiwasi wa nchi kuja kuifuata njia ya Ukoministi zile siku za Vita Baridi (Cold War). Vitu kama usoshalisti na ideology kama hizo zilikuwa zikiwatia khofu sana Wazungu. Kwa hivo kitu cha kuwatowa watu kutoka kwenye “usoshalisti wa kisayansi” na Marxism, ndipo walipokaa, anasema Kambona, Mmarekani ilifika hadi kumpa onyo Nyerere la saa 24. Wamarekani pia walimwambia Mngereza kuwa huyu mtu wenu huyu tunampa masaa 24 kama hamtochukuwa action yoyote kuhusu kusambaa kwa ukoministi na usoshalisti, sisi tutamuondosha katika utawala. Haya maneno Kambona kasema. Kesha kasema, Waengereza, wakamtumainisha, wakampa matumaini Mmarekani kwamba usijali “Nyerere is our post-office in Africa.” [Nyerere ni sanduku letu la barua Afrika]. Sasa nini wakafanya Waingereza? Wakakaa wakafikirii, sasa sikiliza hapa ndo muhimu. Wakaitunga wao hii ideology ya “African socialism” wakakaa chini na Nyerere. Wakampa mwanamke anaitwa Joan Wickens, akawa analipwa mshahara kukaa na Nyerere. Joan Wickens ni British Jew, ni memba,

Page 243: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 211

anatuelezea Kambona, katika British House of Commons, akachaguliwa rasmi na kulipwa mshahara na serikali ya Kiingereza, kumfahamisha Nyerere hiyo walomtegenezea wao Waengereza “African socialism” ambao ndio huo ujamaa.17 Kwanini? Kwa sababu kuwa divert attention Waafrika wasiifate socialism ya ki Marxism-Leninism. Ujamaa, kwa alivosema Kambona ulitengenezwa na Waingereza na ulipangwa na Waingereza. Nyerere alikuwa kama ni chombo, anatuelezea Kambona, kuweko kwake pale, ile Sekretariat ya Kamati ya OAU ya Ukombozi wa Afrika, Nyerere awe ni kama chungio. Wanaomtaka nchi za Magharibi, yeye Nyerere ndo ampeleke mbele. Asotakikana, amkwamize, huku akijivika pazia la kisoshalisti. Huyu [Robert] Mugabe wakati ule, alituambia Kambona, kwamba alichaguliwa na Waingereza kuliko Joshua Nkomo, kwa sababu zao wenyewe, mafalio yao wenyewe. Waingereza hawakumtaka Nkomo. Halafu katika baadhi ya maneno aliyotueleza Kambona, na hizi ni fursa mbali mbali. Wakati mmoja Nyerere aliwaita hawa wenye vyama va kupigania uhuru chini ya Jangwa la Sahara. Anakusudia watu kama Joshua Nkomo, watu kama Samora Machel, kina Kapwepwe, na nani. Anasema Kambona, siku moja Nyerere aliwaita hao viongozi na katika jumla ya maneno alowaambia, nakutahadharisheni sana na Waafrika weupe walokuweko Kaskazini ya Afrika. Hawa ni hatari zaidi kuliko Waafrika weupe walioko kusini ya Afrika. Katika kusema maneno yale, katika mtu aliyetatizana na Nyerere, ambaye tangu wapo walikuwa hawapatani vizuri, aliyetatizana naye sana na kujibizana naye ni Nkomo. Akajibizana naye sana Nkomo juu ya masala haya. Kabla ya ukombozi wa Zimbabwe kwa siku chache, nilikwenda kutembelea Libya, palikuwa na mkutano wa kama sherehe ya vijana wa Kiarabu. Mimi nikapata bahati Balozi hapa katika watu aliowaalika hapa Imarat (Dubai) na mimi nikapata kupachikwa nkenda. Kule Libya hoteli (Funduk Al Shaati) nlokaa nlikaa na huyu Nkomo. Tukakaa tukazungumza nkampa salamu za Sheikh Ali Muhsin akaniuliza vipi hali yake, akaskitika sana mambo alofanyiwa Sheikh Ali na Nyerere, mtu barabara na nini. Katika kukaa siku mbili tatu mimi nikamuuliza na nikam quote [nikamnukuu] Kambona hasa. Nikamwambia Kambona kasema kadhaa, kadhaa, kadhaa. Nini fikra yako? Akanijibu Nkomo mwenyewe kuniambia, hayo ni kweli na huyu Nyerere ana mambo ya ubaguzi wa kidini na kikabila. Vipi itakuwa leo atatufarikisha sisi na Waafrika weupe wa kaskazini? Hawa walitusaidia katika ukombozi wetu. Huyu Nkomo alinambia. Sasa, baada ya kugomboka Zimbabwe, kulikuwa na maonyesho fulani, nikenda mimi nikafuatana na watu wa Imarati (Emirates), katika niliofuatana nao Issa Al Ghureri, na watu wawili wengine. Sote watu wane kutoka huku. Tulifuatana tukenda. Kulikuwa na kama chakula cha usiku kidogo hivi alifanya Mugabe kwa wageni walokuja kutoka nje. Nkamuona Nkomo nkamfatia, tukasalimiana,

Page 244: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili212

tukakumbatiana na ghasia, tukakaa tukazungumza. Tukayarudia tena mazu­ngumzo yale na huku Zimbabwe imeshagomboka. Akazidi kuyahakikisha yale maneno kuhusu Nyerere na akanitajia mengi zaidi juu ya ubaguzi wa mtu huyu. Sasa mimi nimepata kwa Kambona, nimepata kwa Nkomo. Na kuna maneno ambayo aliwahi kutuambia huyuhuyu Kambona kwamba yule Mondlane wa FRELIMO wa mwanzo, alituelezea kisa chake. Mimi nilikuwa nkijuwa kuwa Mondlane alipokea parcel [kifurushi] Dar es Salaam kutoka kwa Wareno na alipoifunguwa ilimripukia akafa kwa sababu Wareno ndo alokuwa akipigana nao yeye. Kambona ananieleza na kuniambia, sikiliza Mutta, wewe huyajuwi haya mambo. Haya mambo usitake kutafuta mambo. Haya mambo alifanya Nyerere kwa kutumwa. Aliyefanya ni yeye huyu. Kafanya kwa njia maalumu kwa sababu Mondlane alikuwa hajapendeza kwa bwana zake Nyerere. Na kweli alikuwa na msimamo tafauti na kwa hakika nilipata habari zaidi kutokana na wenyewe watu wa Msumbiji. Basi sisi Wazanzibari tunasingiziwa uwongo mwingi bila ya kiasi na Nyerere na watu wake. Wametusingizia uwongo mwingi hasa sisi Wazanzibari. Hata ikafika hadi Kambona akatueleza siku moja na alisema maneno makubwa sana. Alisema nataka nikuelezeni. Mnakumbuka kile kisa cha Katanga? Mimi wakati ule nilikuwa mdogo. Anasema Kambona, kulikuwa na mkutano, ambao Nyerere alikuwako kwenye mkutano huo. Wakakubailiana Nyerere, Gamal Abdel Nasser, Bourguiba, nk. Walikubaliana kwamba hawa jamaa wapatiwe silaha wasije wakazidiwa kwenye ukombozi wa Kongo. Silaha zikitoka nchi za kisoshalist na zinapita Tanganyika kwa kuwasaidia wale wenye kupigana. Sasa kwa ajili mapigano makali Kongo wakati ule, katika harakati za Lumumba kama unakumbuka, kulikuwa na vita vikali sehemu ya Katanga. Wale wakombozi walipigana washafika sasa kufaulu lakini katikati hapa ilikuja misaada kutoka madola ikabidi sasa wakombozi wanahitaji misaada kwa haraka.18

Anasema Kambona, kwa vile mimi ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi wa Afrika ya OAU, na wakati Nyerere ni mkubwa wangu, nikapeleka salamu kwenye zile nchi ambazo zina kawaida ya kusaidia. Hawakurudi nyuma. Egypt Air ikaja imebeba shehena kamili ya silaha kusaidia ili wakombozi wasishindwe kule wanopigana Kongo watu wa Lumumba.19 Nimekaa kule mimi, niko Mwanza, anasema Kambona nangoja silaha zije. Mara huku amenijia Regional Commissioner anantafuta. Nini? Akanambia unaitwa Dar es Salaam. Nikapewa simu nizungumze na mtu alokuwa responsible [dhamana] pale Dar es Salaam alikuwa mkubwa wa polisi au kitu kama hivi. Nikenda Dar es Salaam, anasema Kambona. Kufika Dar es Salaam nikamuuliza kwanini umefanya hivi? Akasema nilipata amri mie. Nani? Mwalimu kanipa amri hiyo. Anasema, nikatoka mimi nikamwendea Mwalimu. Mwalimu namna gani kule watu wanauwawa bwana? Wameelemewa, wanangojea silaha kwa haraka na zimeletwa kwa emergency. Anasema Mwalimu akasema, mimi sizipeleki silaha kule. Kwanini? Wale ni

Page 245: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 213

Wakominist. Anasema katika kujibizana pale Nyerere akamwambia kwani mimi kanijia balozi wa Kimarekani kaja hapa analia. Anasema unawasaidia Makominist wewe? Mimi siwezi kuwasaidia Makominist. Anasema Kambona, kwisha ndo ukaona ule ukombozi ukabinywa ndo ikapelekea mchango mkubwa alioufanya Nyerere kurahisisha kuuwawa Patrice Lumumba ambaye baadae akajifanya yeye ni kama mmoja aliyeskitika sana kumsemea Patrice Lumumba. Haya maneno kanielezea Oscar Kambona kwa mdomo wake. Mimi haya nilikuwa sikuyasikia. Nikiona mie kinyume cha huyu Nyerere mimi sikufichi, kama unavojuwa wewe. Huyu bwana, upande mwengine kumbe akitumika kwa faida nyingine. Tukiona hivi, tukiona vile, haya ndio mambo ambayo yalitendeka. Na nakumbuka kijana mmoja katika watu walokuwa muhimu katika struggle [harakati] ya FRELIMO. Katika jumla ya mazungumzo ananambia, wakati Zanzibar ilipopinduliwa, sote tulitiwa sumu kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Mapinduzi ya Afrika, Waarabu wachache, na ghasia. Anasema huyu kijana, mimi nikifuatana sana na Mzee Mondlane kabla hajauwawa. Kwenye mkutano wa Zanzibar sote tukenda. Karume anatowa hotuba. Mondlane alisikitishwa sana na ile hotuba. Anasema kama naweza kufanya ningeliondoka. Anasema katika hotuba yake Karume, nakwambieni, na nyinyi mnaokaa na Wazungu, nyie wengine, hata nyinyi watu wa Mozambique nyinyi, msikae mkanywa chai nao hawa mashombe walochanganya na Wareno hawa. Pia wao wachinjwe tu kama sisi tulivochinja Zanzibar. Huyu ndo mkombozi anasema maneno kama haya, alisema Eduardo Mondlane. Nikamuuliza yule kijana kwanini wewe ulishtushwa na haya maneno? Akanambia sikiliza bwana. Sisi Mozambique tuko wenye asili mbalimbali. Wengine ni weupee lakini wazee wetu ni Waafrika. Na kwani Wareno wote walikuwa wabaya? Akawataja wakubwa waliokuwa weupe ndani ya FRELIMO. Kama fulani, tukamuuwe yule. Kama fulani tukamuuwe yule. Basi anasema Mondlane alikasirika sana hata akamtoa maana mchonga meno Nyerere kwa kumsikia Karume kusema maneno kama yale. Kambona akisema wazi kuwa yeye mwenyewe alishiriki katika kuivamia Zanzibar. Anakubali yeye. Anasema kwanza Nyerere alikuwa hataki kusikia neno “Uislamu.” Pili, anasema, ile Nyerere kutaifisha haya majumba na vidu­kaviduka Tanzania nzima unajuwa maana yake nini? Yeye sasa anatuuliza sisi Kambona. Nikamwambia kwa ajili ya huo Ujamaa wake alionao. Akasema hapana! Kwa sababu wakati ule Dar es Salaam, not less [si chini ya] 80–85% wa wamiliki walikuwa ni Waislamu Waswahili. Kwa sababu mazingira ya Dar es Salaam yalikuwa ya Kiisilamu na unajuwa Tanzania ni nchi ya Kiisilamu. Sasa Nyerere kuupiga vita Uislamu na kuipiga vita East African Muslim Welfare Society (EAMWS) akazitaifisha mali za Waislamu ili wasiweze kutowa mchango kwa harakati za kimaendeleo za Waislamu. Halafu Kambona akasema, kwa mfano wale waliokuwa si Waislamu, kwa mfano mzee wangu mimi mwenyewe mtu mzima, John Rupia [Nyerere] aliitaifisha mali yake lakini alimrudishia baada

Page 246: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Mbili214

yake. Lakini wale walokuwa Waislamu Nyerere hakuwarejeshea kwa sababu ni Waislamu. Mpaka wakfu na misikiti na kila kitu kikataifishwa. Mwisho tukashtuka sisi. Tukaona eh! Kila kitu cha Waislamu kimechukuliwa! Nyerere alitaka kuwalemaza Waislamu. Na Nyerere na Kambona hawakusikilizana kwa sababu alikuwa hataki mtu yoyote awe juu yake. Ndo ukaona hata vijanavijana waliosoma huwavunja moyo. Wewe nini wewe, si umesomea mambo ya umeme? Ngoja ngoja! Atapiga simu Nyerere, fulani mchukuweni ende akalemazwe huko. Utaona mtu kama Kawawa ndo kamuweka karibu na chini yake. Kwanza hakusoma. Pili, ni mtu heewallah bwana! Wale walosoma aliwaweka halafu akawanyanyapaa akawaweka mbali hukooo. Wengine akawaondowa akawapeleka Mabalozi. Kambona alisema hajakubaliana na Nyerere kuhusu Ujamaa kwa sababu akijuwa kuwa ni mambo ya uwongo. Mimi, anasema Kambona, sijakubaliana kuwachukuwa watu kwenda kuwatupa katika vijiji maporini wakenda kuliwa na simba. Vijiji vinachukuwa miaka mingapi kuvitengeneza? Mambo aliyokuwa akifanya Karume anavotaka pia Kambona alikuwa akipingapinga. Nyerere akimuona Kambona kuwa alikuwa ana tamaa ya kutawala lakini Kambona akisema kama alikuwa ana tamaa asingelimuokoa Nyerere pale alipopinduliwa tarehe 20 Januari 1964 wakati jeshi la Tanganyika lilipoasi. Nani asojuwa kuwa jeshi lilimtaka Kambona aishike nchi? Akenda kumtafuta Nyerere mafichoni yakaletwa majeshi ya Kiingereza kumrudisha Nyerere madarakani. Alikuwa akisema, mimi hamu yangu nitoke nikishafaulu nikalivunje lile sanamu la Karume, nikishalivunja, basi tena nakuwachieni wenyewe mwende upande gani. Na baina ya sisi Tanganyika na nyinyi Zanzibar itakuwa ni shauri la kulirekibisha suala la muungano ikiwa Wazanzibari na Watanganyika wanataka au hawataki. Alikusudia mambo yende kwa mafahamiano na si kwa mabavu. Jambo muhimu ambalo Kambona alituhadithia ni kwamba wakati alivokuwa Nyerere bado yuko katika utawala mchango mkubwa katowa juu ya haya mambo yanayotokea mauwaji yalofanyika Ruwanda na Burundi. Tukamuuliza kwanini? Akasema kulikuwa na kambi, kama sikukosea, ikiitwa “sabasaba” kule Tabora au Dodoma. Anasema kwenye kambi hii walikuwa wakifunzwa Wahutu ili wende wakawapige Watutsi. Nyerere akiwafunza Wahutu wende wakawauwe Watutsi kwenye hiyo kambi ya “sabasaba” huko Tanzania, anasema Kambona. Na utakuja kuona baada ya matokeo yaliotokea ya mauwaji Watutsi walisema mchango mkubwa kautowa Nyerere katika mauwaji ya wenyewe kwa wenyewe hapa. Kwa hiyo alipochaguliwa Nyerere kama ni mpatanishaji Watutsi walikataa. Huyu ndo sababu kubwa ya mauwaji yaliotokea kwetu. Mimi nikayakumbuka maneno ya Kambona kumbe hawa walikuwa wana kambi ya Wahutu wakipewa mafunzo wawauwe Watutsi. Mpaka mwisho [Benjamin] Mkapa akipata tabu kuamiliana na hawa Watutsi kwa sababu wale bado wanaona hawa Watanzania wanawasaidia tu hawa Wahutu. Nyerere akiwapa training [mafunzo] na mimi

Page 247: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika 215

nafikiri hakuna tatizo katika Afrika Nyerere hakuwa na mkono wake. Utakumbuka Biafra. Hakuna tatizo mtu huyu hakuna mkono wake. Mpaka makanisa East Timor akaingia na akakorofisha karafuu za Zanzibar zisinunuliwe na Indonesia. Na alisema kama ataweza kukichukuwa kisiwa cha Zanzibar mpaka katikati ya Bahari ya Hindi akakizamisha basi nitafanya kwa sababu kisiwa hichi kina “foreign influence” [ushawishi kutoka nje] nao ni Uwarabu, nao ni Uislamu. Na neno “Mwarabu” nini maana yake nataka kukwambia hapa anapokusudia mtu kama Nyerere. Maneno aliyoyasema mwana historia maarufu Basil Davidson anasema alokuwa Muisilamu ni Mwarabu hata akiwa na kabila gani kwa sababu Afrika linatakiwa liwe bara la Wakristo. Niliwahi kumwambia Dokta Salmin [Amour] maneno haya zamani alipokuwa President wa Zanzibar. Anaposema Mwarabu hakusudii Mwarabu damu, anakusudia Mwarabu dini! Ndo pale Nyerere aliposema Waafrika weupe wa Kusini hawana hatari kubwa kwetu sisi kama Waafrika weupe wa Kaskasini ya Afrika kwa sababu wale ni Waisilamu. Kina Masri, kina Sudan, kina Tunisia, wale ndo Waarabu! Sio wao tu bali hata Wanyamwezi waliokuwa Waislamu kwa nadharia yao hawa kina Nyerere yule ni Mwarabu. Madam ni Muislamu, Msagara, Mzigua, Mruguru, Mzaramu, madhal ni Muislamu ndio ile “Mwaarabuu!” anamkusudia Muislamu. Kwa hivo Mwarabu hapigwi vita, Muislamu ndo anopigwa vita. Ndo ukaona vile vinyago mpaka leo kaviwacha kila siku ya ukumbusho Mwarabu anapigwa mapanga na mashoka, maana yake ndo wanampiga Muislamu. Hio ndo nadharia yao waliokuwa nayo wao wenyewe. Nambie tatizo gani katika Afrika ambalo haumo mkono wa Nyerere? Lipi? Hakuna tatizo ambalo hayumo. Kila pahala penye ugomvi, kila pahala penye vita kachochea. Kaingilia Uganda. Si kwa sababu yoyote. Kwa sababu nini? Idi Amin ni Mwarabu kwa sababu ni Muislamu. Yamefanywa maovu mangapi mbona hakuingilia. Mimi baba yangu kauliwa msikitini na Baraza la Mapinduzi wakati yeye anaweza kumfunga, mbona kawafunga wengine akawaachia wengine? Lakini si kwa maslahi yake. Haya ni mambo ya chuki wakati sisi Waislamu wa Afrika ya Mashariki hatuna mambo ya chuki za kidini. Bila ya shaka kuna mengi zaidi watu hawajuwi na watakayoyasoma watafunguwa macho. Walikuwa hawayajuwi. Maana haya ni maalumati tunayanukuu. Watu bila ya shaka wataerevuka. Anapofahamu mtu “Kwani sawa wenye kujuwa na wasiojuwa?” Na kama mtu umemtia ujingani ukaweza ukamfanya hivo basi jinga likierevuka mwerevu yuko mashakani.

Page 248: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na TatuMisha Finsilber na Mapinduzi

Hakuna aliyetokwa na machozi Israel kwa kuondoka kwa Sultan [wa Zanzibar]. Ngome nyengine ya Kiarabu ya Afrika imeanguka, na dola nyengine imeufungulia ushawishi Israel. Dave Kimche “alisadifia” kuwepo Zanzibar siku ya mapinduzi. Kuwepo kwake kuliiongezea sifa Mossad kwa wanadiplomasia wa nchi za Magharaibi na wachambuzi wa kiusalama, kuwa [Israel] ina uwezo wa kufanya jambo lolote. —Every Spy a Prince

Mzee Ahmed Ali Ghulam Hussein, maarufu “Shebe”

Nimejuwana naye Misha Finsilber katika mwaka 1955, 1956.1 Nikimfikiria kama Girigigirigi. Tukikutana Zanzibar Hotel na alikuweko Girigi mmoja akiitwa Kilosa, na kwa vile alikuwa sana na Kilosa nikamhisi na yeye Girigi vile vile. 1958 aliponiajiri ndo nlijuwa kama yeye ni Myahudi. Yeye amechanganya, nafikiri German Jew. Baba yake ni Mjerumani. Kazi yake yeye ni bingwa wa kupasua mabomu. Kaanza wakati wanatengeneza barabara ya Njombe sijui, Mbeya kule, yeye kazi yake ilikuwa kwenda kuvunja milima ile. Kabla hakuja Zanzibar. Hapa kaja baada miaka chungu nzima keshakaa Tanganyika. Miaka mingi kafanya kazi kubwa. Misha ni mtu mfupi, mpana, ana kifua hivi. Sasa hivi anaweza kufika hata [miaka] thamanini na. Mara ya mwisho nilisikia alianguka chooni kavunjika bega sijui na mguu, akaja kuchukuliwa hapa. Daktari katoka huko, Israel, amekuja kumtowa [hospitali ya] Aga Khan, wamempeleka Israel. Anaonyesha mtu muhimu kweli. Sasa huko kakaa muda mrefu sana. Mimi nimekaa pale miezi miwili na nikiwaona watoto wa ndugu yake wakinambia, yuko huko anatibiwa. Hakuwa mtu wa utaniutani. Mazungumzo yake hayana mzaha. Mpaka kaondoka Zan zibar biashara aliyobaki nayo ni uchimbaji wa maadini hii. Yuko Arusha kwenye madini. Hata mara ya mwisho mimi nimefanya kazi kwake kaja nchukuwa Tanga tukenda kwenye migodi huko, nisimamie zile machine za

Page 249: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Misha Finsilber na Mapinduzi 217

compressor. Si wanachimba kwa manyundo yale. Kulikuwa na compressor tatu kwenye migodi mbalimbali. Sisi tulikuwa sehemu za Mito Mingi, kutoka Tanga njia ya kuendea Mombasa lakini ndani kwenye milimamilima kule. Anakubali tabu. Manake yakhe kwenda kukaa wiki mbili ndani ya hema? Mashida shida yalikuwa hayamshughulishi. Hiyo ya huko mie kanambia “sikiliza Shebe. Sisi tunakwenda porini bwana. Porini tunakaa wiki mbili. Weekend ya baada ya wiki mbili ndo tunakuja mjini.” Ndani ya hema. Pahala hapana mfereji wa mvua, hapana nini. Anajuwa kutafuta pesa bwana. Alikuwa maarufu kwa kuwapa watu vyombo va kuvulia. Mashua ni yake, bunduki ni zake, masks na nini na kila kitu, kwa wale wanojuwa kuogelea. Nini yeye akitaka, mumpelekee kamba, lakini samaki uzeni wenyewe. Akiwasafirisha nje. Hapa Unguja wakati ule hakuna aliyekuwa hamjui Misha. Kila penye bahari basi yule mtu anajulikana. Unguja tu. Hii habari ya kuvuwa huwezi kuwa na vyombo kila pahala namna hiyo. Kwa sababu uvuvi wa kuzamia kuna siku za kusi, huwezi kuvua bahari za kusini, bahari inachafuka, vumbi tupu. Siku za kusi watu wa kusini wanakwenda kupiga dago kule kulotulia. Akijuwana sana na mzee moja wa Nungwi akiitwa Mzee Haji. Huyu alikuwa mtu mzima sana na Misha alikuwa yupo karibu nae sana. Alikuwa hawezi kazi nyingine yoyote kwa sababu mkono wake mmoja umelemaa, na Nungwi alikuwa ni mtu akihishimika sana. Yeye ndo nkimuona akijakija sana pale. Na Uroa rafiki yake alikuwa Muhsin. Alikuwa mzamiaji mzuri. Muhsin alikuwa ndo kiongozi wa wavuvi wa kuzamia kwa upande wa Uroa. Kama Fumba si pahala palikuwa pakipatakana vitu hivo sana. Inatokea tu. Khasa mavuvi yanakuwa Kizimkazi, Uroa, Nungwi ndo khasa, Mkokotoni. Kaskazini yote kule ndo kwenye bahari kubwa kuliko huku kusini. Na biashara yake nyengine ilikuwa chokaa ambayo akisafirisha kupeleka Dar es Salaam. Kila baada ya siku moja akipeleka tani kumi na moja za chokaa Dar es Salaam. Kulikuwa na boti moja hapa ikiitwa “Cheetah” ambayo kabla ya mie kuwa na yeye, mimi nilikuwa engineer mle ndani. Aliikodi yeye kuwa usiku inaondoka hapa na tani kumi inafika kule, wanapata mzigo, wakirudi hapa, hapa hapakii kitu chengine ila chokaa na passenger [abiria]. Pale Dar es Salaam kulikuwa na Mhindi mmoja ana duka la zana, Ithnaasher nafikiri yule, yule ndo anaichukuwa kwa wingi. Hapa Misha alijenga ile tanuri ya chokaa mbali anonunuwa kutoka kwa wenyeji. Chokaa yake yeye inatoka saa ishirini na nne. Inawaka tu moja kwa moja miezi mitatu. Alikuwa na tanuri hapa, Dunga. Mnatia vifuu, mnatia mawe, inawaka tu, na huku chini ikishakuwa jivu, inadondoka mnatowa. Mwaka 1999 walikuja hapa Zanzibar wachomaji wa kienyeji wa chokaa kutoka Ulaya walifanya semina hapa kuwaeleza wachomaji chokaa, namna nzuri ya kuchoma chokaa kwa kiln [tanuri]. Na katika kutembezwa walitembezwa kuwa hapa hichi si kitu kipya. Tukenda kule Dunga. Majenzi ndo walofanya semina ile na Ahmed Sheikh ndo alokuwa Mkurugenzi wa Majenzi wakati ule.

Page 250: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tatu218

Katika viongozi wa Afro­Shirazi waliokuwa wakija kwenye ofisi ya Misha, ya Zanzibar Sea Products, pale karibu na Bwawani, walikuwa marehemu Mzee Thabit Kombo na Mzee Mtoro Rehani [Kingo]. Kwanza wakija milango inakuwa imefungwa, ofisini kwake Misha kuna air conditioner, kuna vioo, mapazia yanafungwa. Kwa hiyo hata ile kumuona mtu mdomo kuwa anasema humuoni. Mara nyingi wakija walikuwa wanakuja wao. Niliwahi kumwambia Misha, kama kighadhabu tu mara moja, kwenye uchaguzi wa pili wakaja kufanya mashirikiano baina ya ZNP na ZPPP. Usiku wa kuamkia kesho uchaguzi, mimi na Misha siku zote ilikuwa kwenye saa mbili ya usiku lazima tunakutana Zanzibar Hotel. Tunakaa palee, kwa kungojea abiria wa hiyo boti nilioifanya, glass boat, na wakati ule kuna kituo cha Kimarekani Tunguu, Project Mercury. Sasa tulikuwa na bodi letu pale Zanzibar Hotel. Mtu anotaka kwenda anaandika jina lake pale. Sie tunaandika time, boti itaondoka saa fulani, maji yanapokupwa, tunawatembeza kwenye miamba wapate kuona samaki, majani, halafu tunawatoza pesa. Sasa ikawa siku zote lazim mie nende Zanzibar Hotel kujuwa kesho tuna abiria wangapi, na saa ngapi tutaondoka. Halafu ananrudisha nyumbani. Sasa kesho sie tunaamkia uchaguzi amenleta nyumbani Kikwajuni. Basi tuko juu pale kabla ya kushuka akataka fikra yangu mimi, akanambia “Shebe unaonaje huu uchaguzi wa kesho.” Nkamwambia “hakuna wasiwasi wowote ZNP watashinda.” “Unafikiri hivo?” Nkamwambia “nna uhakika.” “Kwanini?” Nkamwambia “kwa sababu chama kile wamejipanga vizuri, watu wamefahamu nini wanaambiwa. Kwa hiyo nna imani na watu wengi wanojuwa mambo hayo wana confidence kama hawa watashinda.” Akanambia “lakini unajuwa kama wengi wa watu walioko hapa ni Waafrika.” Nkamwambia “hata hivyo.” “Unajuwa kuwa nchi zote za Kiafrika zinawasaidia hawa Afro­Shirazi?” Nkamwambia “nnajuwa, wanawasaidia kimapesa. Hawatoweza kuwasaidia kwa kupiga kura. Watawasaidia fedha, wao wenyewe wanagombana kwa mapesa. Kwa hiyo hawatashinda. Na nyie Mayahudi mnawasaidia pia.” Alikasirika sana. Inafika wiki hatujasema mie na yeye, na ndo tunafanya kazi. Siku ya pili yake ile baada ya kutoka matokeo ya uchaguzi, na wakashinda ZNP­ZPPP, ah!, alishindwa hata kuntizama macho hivi. Kwa kuwa mie nilimwambia kabla aliona haya hata ile kuntizama. Na hasa ile kumwambia, najuwa kuwa nchi zote za Kiafrika zinawasaidia pamoja na nyie Mayahudi, Israel. Alinyamaza kimya. Na ndo ikawa mwisho wa hadithi nkashuka ndani ya gari. Kuhusu safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar baada ya mapinduzi, mimi nilijuwa asubuhi ya Jumapili. Kwa sababu Jumaamosi usiku nilikuwa Anatoglo na Director-General wa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC), Mikimdowe. Alikuwa kamualika lecturer mmoja wa chuo kikuu ende kula chakula cha mchana kwake. Sasa tulivokutana usiku mimi na rafki yangu Mustafa akasema napenda muje muwe na mimi, nna mgeni na hivi, mtakuja kuzungumza nyumbani. Mimi Misha aliniweka Excellssier Hotel, pale Clock Tower. Asubuhi hatuna mpango wa kwenda baharini, Jumapili manake. Kwa hiyo Mustafa rafki

Page 251: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Misha Finsilber na Mapinduzi 219

yangu akanambia “basi mie ntakupitia hotelini kwako asubuhi kama saa nne, Jumapili.” Basi kaja Mustafa Jumapili, “unayo habari ya Unguja?” Nkamwambia “sina.” Tumetoka moja kwa moja mpaka kule kwa Mikimdowe. Tunafika anasema “unayo habari ya kwenu weye?” Kuna mapinduzi na Sultani ameshakimbia…Mimi nimetaka kwenda Unguja sasa hivi lakini hakuna ruhusa, hakuna chombo kwenda…wala…yupo pale Director-General wa TBC, na makanda yake pale. Anasema mimi nimeanza kuskiliza BBC [British Broadcasting Corporation]. Basi tukashinda pale, manyimbo hayoo, mpaka mchana ndo inaanza kutangazwa, mapinduzi yamefanikiwa, anatakiwa Mzee Abedi Amani Karume popote alipo aje, na hivi. Basi, tumeondoka kama saa nane pale. Mustafa kanrudisha hotelini kwangu, nkasikia “kaja hapa yule tajiri wako anakutafuta, na anasema ukija usiondoke.” Nkaona sawa, basi akija mie nipo hapa, hoteli ya pili. Akaja kama kwenye saa moja hivi ya usiku, Jumaapili. “Una habari Shebe?” Eh, mie nimesikia kule kwa Mikimdowe, nilialikwa chakula mchana na yeye ndo kanambia mapinduzi, na hivi… Akanambia “huyu Abdul Faraji kantafuta sana, mpaka kaja kaniona nimechelewa anataka tuwapeleke watu hawa Unguja.” Nikamwambia “sawa.” Haya twende chumbani kwako. Nkenda chumbani kwangu, nataka kuchukwa begi ananambia “ewe bwana unakwenda wapi? Hili begi unataka kwenda tembea huko? Vaa hivohivo.” Basi nikachukuwa nguo nzito, tukatoka pale usiku moja kwa moja mpaka huko tulokoweka boti Kunduchi. Kabla ya kufika Kunduchi kwanza, akasema “twende tukachukuwe mafuta Agip Petrol Station pale new post office [posta mpya] pale.” Tumekwenda pale tukachukuwa drum moja la petroli, na geloni kama nne za mafuta, zikapakiwa kwenye Land Rover, ikawa tunasubiri pale. Misha akitumia Land Rover ya “Mwananchi.” Abdul Faraji wakati huo alikuwa ndo General Manager wa “Mwananchi Trading” ya TANU. Basi tumeondoka pale tumekwenda zetu sisi mpaka Kunduchi. Zikaja gari kama tatu, Mercedes, lakini ilivokuwa usiku tena, huoni kitu, hujui nani, wala vipi. Hizo Mercedes zilikuja Kunduchi. Sie tunatowa engine ndani ya store ili tupeleke pwani, basi nkaona hivo, lakini sikujuwa nani. Akanambia, sasa tunakwenda Unguja, na tunakwenda Kizimkazi. Nkamwambia sawa. Mie najuwa compass ya kwenda Kizimkazi. Ni masaa mawili tu mpaka Kizimkazi. Tukaingia ndani ya boti kama saa sita ya usiku hivi, sijuwi nani aliomo ndani ya boti wakati ule, mpaka alfajiri tena. Tungefika usiku lakini engine moja iliharibika njiani, ikawa tunakwenda na moja.2

Tumeingia alfajiri Kizimkazi, kama kwenye saa kumi na mbili alfajiri hivi. Kunaanza kupambazuka tena ndo nakuja kuona nani na nani wamo kwenye boti. Kwa sauti nlikuwa najuwa kama Babu nlikuwa nikimsikia sauti yake alipokuwa akizungumza. Na Colonel Ali Mahfudh. Hao ni watu ambao mara nyingi tunakuwa pamoja kwenye kunywa, kwenye nini, kwa hiyo hawanpotei. Wengine sikuwaelewa lakini nlikuwa nnajuwa hao wamo ndani ya boti. Na ndivo ilivokuwa. Kulipopambazuka ndo nimekuja kujuwa alikuweko Mzee Karume, alikuweko

Page 252: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tatu220

Abdalla Kassim Hanga, Babu, Ali Mahfoudh, Ali “Nyau,” Jimmy Ringo, na watu wa usalama wawili wa Dar es Salaam, nimewasahau majina yao kwa walikuwa si watu close na mie, mmoja anaitwa “Makenzi,” kwa jina la kiutani, wa pili simjui kabisa jina lake, si la kimasihara wala hivi, kisura tu nikimjuwa. Fuko alikuweko. Jimmy Ringo, Fuko, na Ali Nyau ni watu wa hapa, pamoja na hao nlokwambia. Ile boti ilikuwa futi thalathini na mbili, ilikuwa life boat ya katika meli. Imetupwa na maji, imeokotwa, akauziwa Misha. Misha ndo akanambia “mie nlivotoka huku Port Sudan safari hii nimeona boti imetiwa kioo chini. Shebe unaweza kufanya?” Nkamwambia “hapa sijapata kufanya lakini kwa kiasi ya kimaarifa ntaweza kufanya.” Mie alonfundisha kazi kanambia “usiseme huwezi kufanya kitu. Jaribu.” Sasa kama unataka tujaribu nitajaribu. Ndo tukafanya tukafaulu. Sasa namna nlivoifanya, matengenezo yenyewe, mimi kama ntakaa kwenye usukani huku nyuma huku, humuoni mtu alioko pale, labda akae mbele kabisa, nimejengea ninhii hivi, na wao ndo wako chini huko, isipokuwa uinuke khasa kwa kutizama hivi ndo utaona. Sasa hata wakati nnawatembeza watalii kwa kuona chini [ya maji], mie nakuwa siwezi kukaa kwenye kiti changu, itakuwa lazima nisimame na mie nione pale kwenye kioo, kama ndo pana mawe hivi, hapa pana hivi. Tukafika mpaka Kizimkazi. Tumeshuka Kizimkazi pale, watu tele wamejaa pale pwani, na katika walokuweko mtu nnomjuwa Maalim Ubwa Mamboya, yeye ndo alokuwa Mwalimu Mkuu wa skuli pale Kizimkazi. Hakuna mawasiliano, simu zimekatwa. Akatoka Jimmy Ringo na Ali Nyau, kama kwenye saa mojamoja [za asubuhi] tena hiyo, wakapewa gari ya Maalim Ubwa Mamboya, Standa, wamekuja zao mjini halafu walivorudi wamekuja na Land Rover tatu. Ndo tukaingia Land Rover moja mimi, Misha, Mzee Karume, na Ali Mahfudhi nnafkiri, wao wamekaa mbele kwenye Land Rover, sisi tumekaa huku nyuma. Gari ingine ndo wameingia walobaki, lakini tumefika Raha Leo ndo tunaona hali hiyo. Watu na mabunduki. Njiani peke yake huko Fuoni, wapi wapi, maiti ziko njiani. Hiyo Jumatatu hiyo asubuhi. Jumapili ndo watu wamefuswa kwelikweli. Hakuna mazungumzo. Kimya! Sie tulikuwa na Jimmy Ringo anasema “hii tangu jana bwana. Leo asubuhi sisi tunatoka kule kuja huku, lo! Ndo tumeyaona hapa, sijui watu gani walokujia upande huu.” Kufika Raha Leo, tumeshuka pale, ndo wanakuja mawaziri kuja kujisalimisha. Kwanza kaja Amirali Abdulrasuli, kapokelewa vizuri. Halafu kaja Ibuni Saleh kaja Idarus [Dr. Ahmed Idarus Baalawy]. Sasa anakuja Ali Muhsin. Kushuka pale akapigwa pale pale nje kwanza. Jamaa gani sijui kampiga kigongo hapa, kamchana, anapanda ngazi ile, nakumbuka kavaa shati jeupe la nylon, limerowa damu. Basi, walioko juu wakakasirika sana. Hasa mtu sauti hasa aliotowa Mtoro Rehani “nani kafanya mambo kama haya bwana. Nyie mnafanya mambo ya kishenzi, na hivi…” Sasa sie tulioko juu habari imekuja kuwa yule mtu alompiga

Page 253: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Misha Finsilber na Mapinduzi 221

Ali Muhsin na yeye kapigwa, kauliwa palepale. Nkichungulia uwani huku, namuona Nassor “Mlawwaz” anasema mimi sikubali, lazima mtanipeleka kwangu. Tunamsikia hasa. “Nataka munipeleke kwangu, Sijui hali ya watoto wangu ikoje. Haiwezi kuwa kabisa.” Misha alikuwa na Mzee Karume most of the time. Anazungumza na Karume, anazungumza na Mtoro Rehani. Akipiga simu Mzee Karume “tusaidieni dawa na silaha.” Mimi nkawa nnacheka. Hivo vitu mbona havifuatani? Anasema na simu na Dar es Salaam. Akizungumza na Mwalimu. Anataka dawa na risasi! Sasa sie tulivopanga pale na Misha akasema leo tutalala kwa Erickson [Erick Steven] Administrator General, manywele. Lakini baada ya kufika saa nane Misha akasema, Shebe hapalaliki hapa. Tusilale kabisa. Manake hapana usalama wowote. Watu wamemahanika. Hanga yeye ndo mtu alokaa kimya sana. Hanga ndo mtu katika walokaa kimya sana yeye. Hakuwa akitembea sana kuwa kama ndo kasheherekea na nini lakini wengine harakati zao unahisi wanasheherekea hasa. Ilipofika saa nane, Misha akasema bora twende zetu Kizimkazi. Tukapewa Land Rover pale, na walinzi, tukatoka moja kwa moja, tukenda mpaka Mtoni kwenda kuchukuwa petroli. Hali wakati huo hapana mtu anayetembea. Anotembea mtu ana mrao, ana bunduki. Na wengi utamkuta mtu keshalewa, ana bunduki na mabostala kavaa huku, almuradi, tukasema hapa hapakaliki. Na sisi ilikuwa twende kwa Erick Steven ili tuazime mashine yake moja. Ile moja imeshaharibika, halafu turudi na moja tu. Erik alikuwa ni mtu anayependa sana mambo ya baharibahari tu. Jambo kama lile mtu kukupa kitu chake itakuwa si tabu. Tukenda Mtoni tukachukuwa petroli, tukasema tusiondoke hii jioni bwana madam tuna mashine moja. Tulale hapa hapa Kizimkazi asubuhi tutaondoka Kizimkazi tutakwenda zetu Kunduchi. Tukalala Kizimkazi, Jumatatu. Tukaondoka Kizimkazi asubuhi Jumanne kwenda Dar es Salaam na mashine hiyohiyo moja. Mimi, na Misha, na baharia wetu mmoja, kijana mmoja mdogo wa Kimakonde, ambaye alikuwa akikaa palepale. Na hiyo usiku na yeye alikwenda kuamshwa hivohivo hajuwi hata anakwenda wapi. Tulivoondoka Dar es Salaam kuja Zanzibar. Tukafika Dar es Salaam kama saa nne hivi asubuhi. Tulipofika Dar es Salaam, siku ya tatu yake Misha akaondoka kwa ndege kutoka Dar es Salaam kuja Unguja. Sijui ilikuwa ni ndege ya kukodi au ndege maalumu? Ijumaa nafikiri alikuwa kaondoka kuja huku Unguja. Mie nkabaki kule. Mie nkawa kazi za pale si lazim yeye aweko. Watu wanakuja wanasajili na mapema, ewe bwana tuko watu kumi tunataka kwenda nje saa tisa. Watu wanopenda mambo kama yale anajuwa ile jaduweli ya kujaa na kukupwa maji. Maji yanajaa saa ngapi, yanakupwa saa ngapi kwa hiyo time nzuri ipi ya kwenda pahala. Halafu kutoka hapo ikawa Misha kila wiki anakuja Unguja. Anaondoka Dar es Salaam Jumanne, anarudi Alkhamis au Ijumaa, kila wiki. Manake anakuja huku kunako kazi zake za chokaa zile vilevile. Sisi, mimi na Misha, tuliondoka Zanzibar

Page 254: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tatu222

1963. Manake nakumbuka Babu mara moja alisema, hapahapa kwenye mkutano, hapa Weles tena ilikuwa, mwezi wa Ramadhani, akasema “sisi tunawajuwa watu wanaowasaidia hawa, na tukipata uhuru watu wa mwanzo tutowaondowa hawa Mayahudi walioko hapa.” Yeye si akiona watu wa Afro­Shirazi wakenda kwa Misha pale. Moshe Dayan aliwahi kuja Zanzibar baada ya fujo [za June 1961]. Alikuja peke yake. Misha alinambia kesho asubuhi kwenye saa mbili nna mgeni nataka kumtembeza tutakwenda Kizimkazi. Haya. Akawaambia na mabaharia na hivo. Tukatayarisha boti, asubuhi, kaja yule bwana, ambapo siku ile walikwenda familia yote, alikwenda Misha, alikwenda shemegi yake Abraham na mkewe ndugu yake Misha mwanamke alokuweko hapa. Abraham sasa alivokuja hapa, mbali ya hiyo biashara ya kamba, na kutia katika mifuko na nini, ikawa anaagiza mboga kutoka Nairobi. Wiki mara mbili kwa ndege zinakuja hapa Zanzibar. Vitu visopatikana hapa, lettuce, beetroot, cabbage, cauliflower, spinach, spring chickens. Na customers [wateja] wake wengi walikuwa wale watu wa Project Mercury ile. Wamarekani wa ile tracking station [kituo cha uchunguzi wa anga] walikuwa wateja wake wakubwa. Wakikaa Mazizini nyumba ya hayati Rashid Mohamed bin Mbaruk. Wote watatu wakikaa pamoja. Wao ndugu wanaume watatu, mwanamke mmoja. Ndugu mmoja mwanamme alikuwepo Dar es Salaam, mdogo kabisa wa mwisho wao. Akiondoka Misha kwenda Israel yeye huondoka Arusha akaja Dar es Salaam. Wanasema Kiswahili kama kawaida na ni raia [wa Tanzania]. Basi tukatoka na yule bwana moja kwa moja mpaka Kizimkazi, hatukusimama pahala kuwa labda tuzamie tupige samaki. Si kawaida, tukitoka lazma tutasimama pahala kwenye mwamba tupige samaki, tupige hivi, lakini sku ile haikuwa hivo. Wameshuka, wakasema sasa nyinyi rudini kama mnataka kupiga samaki au nini. Wao wote wakashuka. Gari zao zinawangojea pale. Wakaja kwa njia ya juu, mimi nikarudi na mabaharia wangu na boti. Tukarudi. Halafu ndo tena akanambia “yule ni mtu mkubwa sana kwetu.” Ah! baadae sana tena ndo nakuja kuona mapicha “Moshe Dayan, Moshe Dayan.” “Huyu mtu si alikuja huyu Unguja, tumekuwa hivi hivi…?” Nimekuja kujuwa baadae kabisa. Misha alianza kuondoka kabla ya mapinduzi kwa usemi wa Babu kuwa tukipata nanhii [uhuru] watu wa mwanzo watakaoondoka watakuwa wao. Kwa hiyo kaondoka mapema yeye. Kaisikia, na yale mambo aliyaona kweli. Babu siku zile akikaa Funguni kule karibu na Ali Mdogo, ilikuwa lazima apite pale kwenye ofisi ya Misha. Anaona kila kitu. Kwa hiyo sie tumeondoka hapa 1963, mwaka mzima kabla ya mapinduzi. Maisraeli wakaja wakafunguwa ubalozi hapa. Kampuni ya Misha haikutaifishwa. Walimwambia aiendeshe yeye, iwe ya serikali. Akafanya hivo, senti moja hajalipwa. Yeye mwenyewe akawa taabani na hawa watu. Gharama zake za ndege, kwenda na kurudi, akija hapa ndo anakaa Zanzibar Hotel, production [uzalishaji] inakwenda kule, pesa zinaingia huku kwenye mfuko wa Afro­Shirazi. Senti moja hakupata. Mambo hayo alimwachia

Page 255: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Misha Finsilber na Mapinduzi 223

Hanga, Hanga tena wakamtenga akawa hajuwi ashike wapi. Hanga kawekwa ndani, ikawa yeye sasa na Saleh Saadalla, Saadalla na yeye kawekwa ndani. Saleh Saadalla akiingiliana sana na Misha. Hata hiyo baada ya mapinduzi, Saleh Saadalla alikuwa kila vinapofanywa vikao va serikali Dar es Salaam, anakuja na mkewe anakaa hotelini kwa Misha, siku tano, sita, wiki. Misha si alikuwa na hoteli “Silver Sands?” Akija Dar es Salaam akikaa kwa Misha khasa pale hotelini. Hanga sijapata kumuona hata sku moja. Hanga alikuwa si mtu wa raha namna hiyo. Mambo yake peke yake peke yake tu. Mara nyingi. Abdul Faraj kwenye fishing survey yetu ya prawns, kwenye hiyo Mwananchi Ocean Products, tulipokuwa Mafia alikuwa akija Mafia. Kuna Mwananchi Trading, kuna Mwananchi nini…Na Abdul Faraji alikuwa General Manager wa zote hizo. Faraji alikuwa mwezi mara moja anakuja kule Mafia. Misha alikuwa kama treni. Ana njia maalum. Akitoka huku Mazizini anakuweko pale ofisini. Alipokuwa akikaa Mwera pale, baada ya kilima cha Koani, mkono wa kushoto, nyumba ilokuwa ya ukoo wa kifalme wa Zanzibar. Akitoka pale nyumbani kwake akenda Dunga kwenye biashara yake ya tanuri ya chokaa. Misha alikuwa ana mabaharia wengine. Watu waliobakia na chombo wakati wote ni mimi peke yangu, kwa kuwa ni kepteni, lakini wengine akipata kazi nyengine bora anawachilia mbali. Kwa hiyo alikuwa nao wengi. Ikiwa kwa vyombo vidogovidogo sijui vinatokea wapi…kulikuwa na harakati kubwa Bagamoyo na Kunduchi, hizo ndio bandari za magendo toka zamani. Kule Kunduchi kuna watu wamejenga nyumba maji yakijaa wewe unaweka boti anaingia mlango wa nyuma kwake. Hutaki kubeba mzigo kuupeleka wapi sijui. Watu maarufu wako kule. Akina Mzee Masanga, Bwana Khamisi, Mzee Kibosha. Mzee Masanga na Bwana Kibosha watu maarufu sana hao. Watoto wa mdogo wake [Misha], mmoja anaitwa Victor. Wewe ukenda Rungwe Oceanic Hotel nyumba yao iko hapohapo, na Silver Sands haipo mbali. Hao wamezaliwa hapahapa. Wana duka Oysterbay la milango na madirisha ya aluminium. Ndugu yake mwengine yuko Arusha.

Page 256: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na NneKuanguka kwa Ngome ya Kusini

Mshikamano wa kijamii unapobomoka, kabila linakuwa halina tena uwezo wa kujihami, mbali ya kuweza kutanguliza madai yoyote. Lifikapo hapo litamezwa na mataifa mingine. —Ibn Khaldun

Mahojiano yafuatayo yamesajiliwa Cairo mwaka 1975 na hayakufanywa na mwandishi wa kitabu hichi. Marehemu Sheikh Ali Muhsin wa mwaka 1975 pale ndo kwanza alipotoka jela ni tafauti na Sheikh Ali Muhsin wa siasa za baadae za Zanzibar katika kipindi cha siasa za vyama vingi.1

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini

Hivi karibuni jamaa mmoja katika ndugu zetu ambaye nna yakini naye kuwa ni mukhlis wetu na ana imani na sisi, katuunga mkono tangu mwanzo wa juhudi zetu na jihadi zetu, na akapata misukosuko, akafungwa, pamoja na sisi, akatolewa kabla yetu sisi, lakini amepata taabu, amenyanganywa yake, ameuliwa watu wake, alikuwa anazungumza na mimi kuniuliza mambo yalotokea. Akanambia, kwanini hamkufanya hivi, kwa nini ilikuwa hivi? Siku ya mapinduzi na kabla ya mapinduzi. Kwanini msifanye hivi, nasikia mmefanya hivi, mmedharau hivi, mmekataa msaada hivi. Nkastaajabu. Nkamwambia “fulani wewe? Kwani hukuwapo?” Ah, nlikuwepo. Vipi, hata ukawa na mawazo hayo? Sasa nieleze, manake utansameh, manake kwa hakika sijui, mimi ninavofikiri ni hivi na watu ndo wanavosema. Nikamueleza ilivokuwa akastaajabu sana. Akasema, basi hakika nataka uwaeleze watu wajuwe upesi. Nataka muandike upesi. Nikamwambia kwa hakika tutayaandika lakini uandishi unachukuwa siku kutengenezwa, mpaka upigwe chapa, lakini kama hata watu kama wewe wana mawazo kama hayo, mimi nilifikiri walokuwa hawayajui walokuwa mbali au wana chuki tu. Lakini ikawa hata wewe ulokuwapo? Na wewe ni mukhlis, tangu mwanzo na mpaka sasa. Si mnafik wala si chochote, wala huna makusudio kwa kuwa…imani yako haikurega

Page 257: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 225

kwa sababu unaamin tu habari unazosikia au unavofikiri ndio ndizo, basi naona yafaa kwa hakika jambo hilo ni la haraka kueleza kwa sababu huenda watu wa karibu na sisi sana hawayajuwi, wanasema maneno. Basi kwa hivo nikaona rai nisajil upesiupesi maneno nieleze kwa mukhtasar yale yalokuwa siku zile za mapinduzi, au siku za kushambuliwa na watu wa nje. Watu wapate kujuwa hakika ya mambo yalivokwenda ili walau jamaa huko mliko Dubai mpate kujuwa na wengine watayasikia na wengine wanaotaka watapata kusajili kukopi maneno haya wayatangaze, lakini wenzetu wapate kuyajuwa walokuwa hawayajuwi. Siku ile ya Aljumaa, mapinduzi kama mnavojuwa yalitokea Jumaapili, alfajiri Jumaapili. Siku ya Aljumaa Sheikh Muhammed Shamte alinipigia simu nyumbani kunita nende kwake. Jioni. Kwenda akanambia kuwa nimepata habari yakini kwa kuwa siku ya Jumaamosi kuamkia Jumaapili watapofanya fete Afro­Shirazi pale Kisiwandui watafanya ghasia. Watatafuta fursa ile ya fete kufanya ghasia. Ghasia zenyewe kwa hakika hatujuwi namna gani na Sheikh Muhammed aliniambia kuwa watafanya ghasia na mimi nimeshachukuwa khatwa, nishamwita Kamishina wa Polisi na nimeshampa amri askari wawe tayari, kwa hivo sina khofu wala wasiwasi kwa hapa mjini lakini nnakhofia hawa watu wa kihizbu walioko shamba, watu wetu walotupikatupika, tengeneza wewe kwa mpango wako waambie watoto wa Hizbu wapeleke habari waondoke kama mipango yetu tulivyo, waondoke kule katika vijijivijiji walioko mbalimbali wakae mwahali kwenye dhamana. Pale pale nkatoka. Natoka kwa Sheikh Muhammed nkaonana na mtoto wangu Muhsin Muhammed nikamuagizia ende amwite Muhammed Abudu Mkandaa. Mimi nkenda zangu nyumbani. Muhammed Abudu mara akatokea nikamuagizia, nikamuagizia kuwa afanye na watu wake kama desturi yetu kwa kuwapelekea habari watu. Hizbu tulikuwa na majlis, baraza, Kamiti ya Usalama. Yakitokea mambo namna hiyo waweze watu kupashwa habari upesi. Na yeye Muhammed Abudu ni mmoja kati ya watu wenyewe waliokuwako. Bas. Muhammed Abudu kutoka pale akatengeneza na jamaa alokwenda nao kina Muhsin Badar, Mngu amrehemu, na nafkiri Muhammed Noor na jamaa wengine, Abdalla Bachu sijui, na jamaa wengine, lakini jamaa jamaa walokuwa na gari. Wakatawanyika palepale. Mimi alfajiri, siku ileile Aljumaa, tena kuamkia Jumaamosi, Muhammed Aboud akanle­tea habari kwa kuwa wamekwenda koote, tangu Nungwi mpaka Makunduchi, watu wote wameshapata habari. Yaani, mipango yetu ilikuwa tunajuwa wapi nyumba zenye usalama katika nchi yote. Tunajuwa wapi kwenye bunduki, bunduki zao wenyewe watu waliokuwa nazo zenye license [leseni] na zisizokuwa na license [leseni], za magendo tunajuwa, wenye bastola tunajuwa, na za halali tunajuwa. Walotengenza wenyewe tunajuwa. Wote wanajulikana na listi yao inajulikana na walokuwa vijiji mbalimbali katika baraza ya usalama. Mimi sikuwa memba wa Kamati ya Usalama. Napata ripoti yao wanapotengeneza kama tunavopata watu wengine wakubwa. Najuwa katika mipango yao ikiwa jambo la

Page 258: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne226

hatari kama vile ilivotokea mwezi wa June 1961 zamani na kama itakavotokea basi kwa kuwa watu walotupikatupika wende kwenye nyumba ambazo zenye bunduki na zinaweza kulindika. Nyumba yenyewe madhubuti, nyumba ya mawe na bati haina hatari ya kutiwa moto wala nini, au kushambuliwa mara moja ikahujumiwa. Bas. Wende wakusanye watoto na wanawake wakae katika pahala pa salama na bunduki zikae madhubuti waweko watu na ulinzi. Hata alfajiri na ndo kama nnavosema, gari zimejaa umande, Muhammed Abudu kaja kanipa ripoti, timam, tumekwenda kote. Mimi nimekwenda ofisini kazini katika wizara, nimerudi mchana kuja kula, Sheikh Amour Ali Ameir kaja akanita hata sijawahi kula. Akaja nyumbani akanita pembeni kuniambia nimepata habari kwa wanangu jinsi kadhaa kadhaa kadhaa. Nikamwambia sisi tumeshapata habari na tumeshachukuwa khatwa kadhaa kadhaa. “Oh! Basi vizuri. Basi kama polisi imeshapata khabari basi na wafanye!” Na mimi namwambia, natamani wafanye jinsi tulivokuwa tayari. Isitoshe vile, mimi nikaondoka nikenda shamba kucheck mashamba kule. Na kabla ya hapo…Kamishna wa Polisi alikuwa Sullivan, Mzungu, na naibu wake wake alikuwa Sheikh Seleman Said Kharusi, na chini yake alikuwa marehemu Sketty. Waziri Mkuu ndo alokuwa mas­ul wa usalama na yeye keshamuendea Commissioner wa polisi. Hayo yanatosha lakini sisi wenyewe kwa kienyeji kutengeneza kuambizana na wenzetu kina Sheikh Seleman na jamaa wengine wanofanya kazi polisi tunaowajuwa. Pale mimi nikajaribu kuttasil nao wote, Sheikh Seleman na Sketty. Nikipiga simu kwao siwapati. Tukawatuma jamaa kwenda kuwatafuta. Kila mtu kwa upande wake. Muhammed Aboud anakwenda kuwatafuta. Haji Husseni anakwenda kuwatafuta. Seleman hayupo, Sketty hayupo. Kila pahali tunakokwenda tunasikia wamekwenda shamba piknik. Hilo moja katika lilotupa moyo sisi. Tukaona labda huu ni uvumi manake kama jambo kama hili limeenea Unguja na sisi sote tumejuwa, na mimi kabla ya Muhammed Shamte nimeusikia uvumi huo. Tumesikia na ulikuwa umeenea kwa kuwa watataka kufanya ghasia. Lakini tulipojuwa Sheikh Seleman na Sketty, marehemu, wameondoka wamekwenda mashamba tukaona kuwa pengine si kweli manake haiwezi kuwa wao wasijuwe na Unguja nzima wanajuwa. Na vilevile, Kamishna keshaambiwa na yeye tena awape ruhsa wende zao kutembea shamba basi imeelekea kwa kuwa hapana jambo hapa. Lakini mimi baada ya kwisha kula pale mchana nikachukuwa gari nikenda, nafsi yangu, nikenda mashamba kucheki. Nimekwenda Mwera, Kiongoni. Nimepita Dunga, Kiboje, Ndijani. Yaani, kutizama kule kama kila nikipita katika branch pale naonana na watu, nauliza, napita kote jamaa wameshafika. Nikajuwa kuwa huku kwa hakika wamefika jamaa na watu wamepata habari. Wengine wakanambia, kwani tuna khofu nini? Nikawaambia, la, pengine huu ni uvumi lakini mara tisa utisiini inaweza kuwa ni uvumi wa uongo na mara nyingi yametokeya mambo kama hayo ya uvumi haikuwa kweli. Lakini huenda mara ya

Page 259: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 227

mia ikawa ndio basi mwanamme hata akikaa huchutama. Hakai na kulala. Basi tuwe hadhar [macho]. Bas. Huku kurudi, mimi sku ile sikulala. Vile vile nimepeleka jamaa zangu wa kupeleleza na nini, kunipa habari. Wakawa wanapeleleza na walikuwa wanaitizama ile hali inavokwenda na nikakaa ila mnamo saa saba za usiku nimekuja kupata ripoti kuwa mambo salama, fete imekwisha na mambo kimya, na walokwenda kutizama mpaka sehemu za mashamba, mpaka pande za Maruhubi na Bububu, wanaona jamaa vijana wa Kihindi wengine wanatoka katika mandal zao, wanaimba njiani wanarudi na maaccordian. Hapana kitu. Salama. Pale ndo nikasinzia. Haikufika mda, saa hivi na nini, nikasikia simu na huku nnasikia bunduki. Mambo yamechafuka. Mle nilivosikia vile kwanza niliona ni kwa kuwa hawa zitakuwa ghasia kama za June labda kwa kuwa watakuja na mapanga na mimi nyumbani nilikuwa na bunduki ya .22 na bastola. Nikaona hawa jamaa wakija hapa na mie nnaye Sheikh Hilal Muhammed, bin ammi yangu, na shemegi zangu wengine, nna vijana hapa watu madhubuti, wakija hapa na waje, lakini nikapata habari Smithyman kanipigia simu kwa kuwa Ziwani imeshaanguka. Smithyman alikuwa ni Katibu wa Sheikh Muhammed Shamte. Mzungu yeye. Akanipigia simu kuwa Ziwani imechukuliwa. Na Mtoni imechukuliwa. Imebaki Malindi Station tu. Bunduki nazisikia jela pale ambapo ni kama khatua mia mbili kutoka kwangu. Nazisikia karibu pale. Sasa nikaona khatari sasa. Nikamwambia Abdalla Sudi uchukuwe ndugu zako na wanao hawa mwende mjini. Kwa mkwe wangu mjini. “Wewe mwenyewe?” Nikamwambia ukiweza kuja nchukuwa njoo. Hukuweza basi. Muda si muda akenda Abdalla Sudi akanipigia simu yuko hospitali anasema baina yangu mimi hapa hospitali na kwako, katika njia ya mivinje pale, gari ya 99 imepindiluwa na askari hatujuwi wamekwenda wapi.2 Wameshambuliwa. Kama wameuliwa au wamekimbia, hatujuwi. Basi hapapitiki. Nikamwambia usije. Mimi nitatafuta njia mwenyewe. Muda si muda, Abdalla Sudi jabbari, naona kapita katika minazi, kazima taa gari yake, kaja pale tukapanda sie tukenda zetu mjini. Kufika mjini… Nimesahau kitu kimoja kwanza. Nililetewa askari. Alikuja Misra kunambia kuwa tumepata habari kuwa kumefanywa nini na nini…askari wenyewe na marungu na ngao za majani za mabuwa. Tumesikia kuwa wewe ni katika mtu anayetakiwa kuuliwa. Mimi nkacheka. Nikamwambia “haya.” Sikumwambia kuwa mimi nategemea bunduki yangu mwenyewe na bastola na imani za wenzangu nlonao kuliko hao askari. Nkaona ndo ulinzi wenyewe ndo huu? Askari wale wakabaki. Nkenda zangu mjini, watoto walikuwa wameshatangulia, na wenzangu wale tukenda nao kwenye gari ile. Tukenda mpaka nyumbani kwa Sheikh Muhammed Shamte. Tukasikia kuwa yuko katika nyumba ya pili kule Shangani. Tukenda Shangani kule tukawakuta jamaa wengine, tukawakuta Mawaziri wengine wamekuja, halafu tukafanya mkutano katika nyumba ya Sheikh Amour Ali

Page 260: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne228

Marhubi karibu pale. Halafu tukaondoka, mimi na Sheikh Muhammed Shamte, nafikiri na Sheikh Hilali nadhani, sijui na Sheikh Juma [Aley] tulikuwa pamoja…tukenda Malindi police station. Kwenda kule tukaona pale ndo kuna ulinzi na nini. Tukamkuta Kamishna wa Polisi na akasema kuwa hali mbaya lakini piteni…kabla ya hivo tukataka kuttasil [kuwasiliana]…tunajuwa wako askari wa Kiengereza Kenya. Wa jeshi la Kiingereza. Na desturi yetu mambo yakitokea, na sisi ni memba wa Commonwealth [ Jumuiya ya Madola], japokuwa tumepata uhuru wa mwezi mmoja, lakini ni memba wa Commonwealth, na tumesimama katika miguu yetu, ni wajibu wetu kusaidiana katika jambo linolotokea katika mji. Fujo na ghasia zinafanywa katika mji. Manake kuna sheria zimevunjwa na watu wasojulikana manake mpaka wakati ule hakuna kitu chochote rasmi kama ni Afro­Shirazi, nani, na nini. Lakini fujo katika mji tu. Si askari. Ni watu tu wanafanya ghasia. Sasa, tukataka msaada ule wa askari wa Kiingereza. High Commissioner, Balozi wa Kiingereza alokuwako pale, alisema askari wa Kiingereza hawawezi kuja hapa ila wapewe rukhsa na Serikali ya Kenya, wao ndo wenyeji wao. Sheikh Muhammed Shamte akapiga simu Nairobi. Kule asimpate Kenyatta lakini akampata Makamo wa Raisi naye alikuwa Joseph Murumbi. Joseph Murumbi akasema Raisi yuko shamba sasa hivi lakini nna yakini atakubali kuwaruhusu. Kuona taathira ile, tukamwambia tutachelewa ikiwa mpaka asubuhi Kenyatta aje na nini, tukaona kwa kuwa tuwasiliane na Tanganyika japo kuwa hatuna maskilizano mema na Nyerere, lakini rasmi hatuna ugomvi. Kwa pale kwa hakika hatuna maskilizano mema lakini kiserikali tulikuwa tukisaidiana kila likitokea jambo Tanganyika au Kenya au Uganda wanatusaidia, na Tanganyika likitokea jambo Zanzibar inaisaidia vilevile. Tunapelekeana askari na nini. Hili ni jambo la siku zote. Tukaona ni mazoea yale ya ujirani mwema tulokuwa nao tokea wakti wa Mgereza basi sisi wenyewe tuendelee nao. Sheikh Muhammed Shamte akampigia simu Nyerere kutaka kusema naye. Akaambiwa bwana kalala. Mwamshe mwambie mimi ni Prime Minister [Waziri Mkuu] wa Zanzibar nataka kusema nae. Akasema hatuwezi kumwamsha. Saa kumi ya alfajiri. Hapo tuliona japokuwa hatusikilizani mtu akikosa ziwa la mama hata la mbwa hunyonya basi na tuombe msaada wa Tanganyika lakini tukaambiwa bwana hatuwezi kumuamsha! Tizama uwongo huo? Na hali wakti huo Karume, Babu, Ali Mahfudhi, Saleh Saadalla, wote wako pale, na bwana kalala ati hajuwi! Sisi hapohapo, tukamwambia yule Balozi wa Kiengereza, basi wako askari wa Kiengereza Aden itachukuwa saa tatu nne hata kufika hapa kwa aeroplane au zaidi, lakini haizidi kuliko hivo.3 Wataweza kufika. Akasema jeshi la Kiengereza haliwezi kuja hapa bila ya rukhsa ya serikali London Tukamwambia, basi taka rukhsa huko! Akasema leo weekend, weekend Jumaamosi na Jumaapili, hapana mtu. Hebu serikali ya Kiengereza hulala weekend! Sijapata kusikia serikali ya Kiengereza kulala au serikali yoyote. Ina weekend kuwa haiwezi kupatikana watu kufanya kazi. Waziri popote pale alipo anapatikana hata akiwa wapi. Hata

Page 261: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 229

akiwa wa upelelezi. Akasema, tena akaongeza hivi. Ala kulli hali, mimi siwezi kupendekeza, siwezi kupendekeza, kupendelea, kuwa nyinyi mpokee msaada, serikali ya Kiengereza iingilie mambo ya ndani ya Zanzibar yanotokea, na ya pili kwa kuwa nyinyi ni serikali ya watu wachache.4 Nikamwambia sikiliza bwana we: si serikali ya wachache. Sisi tulikuwa na viti 18 dhidi ya viti 13 va wapinzani tunaambiwa ni serikali ya wachache iloshinda kwa uchaguzi wa halali kwa mujibu wa katiba na sheria zote zilokuwa duniani. Anatwambia ni serikali ya watu wachache. Lakini ukishashindwa huna lakusema. Huyo mtu ndo hataki. Ndo tumeshindwa hivo. Mimi nafsi yangu nikapiga simu Dar es Salaam kumpigia simu na Balozi wa Misri, El Isawi, ili kumtaka msaada wa Misri ije kutusaidia. Hiyo tena yane. Ya kwanza Kenya, ya pili Tanganyika, ya tatu Waengereza, yane Ubalozi wa Misri. El Isawi, Balozi, ananjibu boi, boi wa Kiswahili, wa Kiafrika, ananjibu kwa kuwa bwana hayupo. Sasa, hatuna la kufanya. Tuko kwa Balozi wa Kiengereza tunashindana nae, nikapata mimi simu kutoka kwa Inspekta General wa Polisi (Hamza Aziz), mkubwa wa polisi wa Tanganyika. Ananambia mimi “kumetokea nini huko?” Nikamueleza kwa kuwa kumetokea fujo na nini. Akaniambia je wanapigana Waarabu na Waafrika? Nikamwambia si masala ya Waarabu na Waafrika. Katika hao wanofanya kazi wamo Waarabu na Waafrika. Lakini ni watu tusiowajuwa kama ni wahuni tu. Hawakujitambulisha kuwa wao ni nani. Ni watu wanafanya ghasia, wanauwa watu, wanawake. Manake akasema Raisi anataka kujuwa. Baada ya muda Nyerere akapiga simu. Tena mchana mnamo saa tatu kama hivi. Nyerere akapiga simu kusema na Sheikh Muhammed Shamte. Akamwambia kumetokea kadhaakadhaa, nilipotaka kusema na wewe alfajiri nilitaka msaada wa askari. Sasa, sisi mambo yamesha­haribika na sisi tutayari kujiuzulu. Wao wanataka kuendesha serikali na waendeshe serikali. Tunataka hapa Waengereza wawete, wao waendeshe serikali lakini wasiuwe wanawake na watoto wasiokuwa na makosa. Sisi Mawaziri mbali lakini raia wasiwaguse na sasa tutawapa serikali. Hawataki hata kuja kusema na Balozi wala kusema na sisi, basi sasa tunaomba aje Waziri kutoka kwako huko watamsikiliza. “E bwana mimi nnaambiwa…” Raisi Nyerere anavosema. “Mimi nnaambiwa siku zote naingiliaingilia lakini naapa kwa haki ya Mungu, mimi siyaingilii mambo…siyajuwi mambo hayo hata kidogo. Siku zote naambiwa naingilia mambo…hata. Sina habari nayo wala siyajuwi.” Akamwambia, wacha hayo bwana. Watu wanakufa bwana na watoto na mambo yote, wanauliwa bure, si watu wa siyasa, wala nini, wanauliwa bure. Si watu wa siasa. Kuna mauwaji, tunataka mtu aje, ataskilizwa tu. Akasema, haya ntafanya shauri. Hakuja mtu yoyote! Watu wakaendelea kuuliwa wiki nzima! Na Nyerere hakumleta mtu kuja kuzuwia mauwaji. Wakti huo tena, hapana la kufanya. Hapana la kufanya ila kila mtu alokuwepo pale…mimi nkenda kwa wakwe zangu pale kwa miguu. Sheikh Juma [Aley]

Page 262: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne230

akenda kupanda motokari na Muhammed Shamte, Abdalla Sudi akawachukuwa. Mie nkashuka salama pale, risasi zimo mote majiani mle lakini na mimi nilikuwa na bastola. Sikufa lakini nisingekufa peke yangu. Nkenda mpaka nyumbani halafu nikasikia, Jumaatatu jioni, wakati nasinzia, siku ngapi skulala, mke wangu akanambia kuwa wamesema katika radio Mawaziri wende….Kwa hakika, sisi tulitengeneza palepale Mawaziri tulipokuwa kwa Sheikh Amour Ali Ameir, tangu niko Malindi, nikampeleka Haji Hussein nafkiri ende akamwambie Sayyid Jamshid aoondoke yeye asafiri. Akasema Sayyid Jamshid sendi mie ntakufa na wanangu. Ntakufa na watu wangu. Nikampeleka Sheikh Hilal [Barwani], nkamwambia lazma aondoke. Kama anataka salama, hata salama ya watu wake ni bora yeye aondoke. Tukatengenezewa meli pale, ikaagiziwa. Dr. Baalawy nadhani ndo alokuwa amehusika. Akatengeneza meli ikawachukuwa yeye pamoja na jamaa…na kabla ya hivo, Malindi pale, Kamishna wa Polisi, akawaambia waje jamaa, kila mtu mwenye bunduki, hata wenye bunduki za shotgun zile za kupigia ndege za mchezo. Tukawapelekea habari jamaa, alhamdulillah walokuja wamekuja. Wengine wamekaa, hawakuja. Wengine wamekuja katika sahib zetu. Kina Said Badr, Salum Ahmed, na kadhaa kadhaa watu wengine, Muhammed Msellem, wamekuja Malindi pale, wakawa wanajibizana risasi zile, nipe nikupe, wao na watu wa upande wa pili kule. Sasa wale walokuwa Malindi ndo waloweza kusaidia hata Sayyid Jamshid na wengineo wakaweza kusafiri na kwenda na meli kuondoka. Wao ndo walokuwa walinzi wa mwisho Malindi pale.5

Kutoka hapo sisi tukenda kupanda gari na Abdalla Sudi akanchukuwa kwenye gari ya Sheikh Ali Masoud Riyami, kuukuu, ndogo, mpaka Makao Makuu ya Polisi juu ya jela. Nkenda kule, nikatoka mimi katika upande mmoja wa gari, na Abdalla Sudi akatoka hivi, mikono juu kama “hands up” hivi. Kule juu katika roshan ya ofisi, si mbali, haifiki, haizidi kuliko futi thalathini kutoka nlipo pale, kuna watu wawili, mmoja ana machine gun na mmoja ana bastola, wanapiga mfululizo. Wananipiga mimi na Abdalla Sudi lakini hazilii. Wameshika wamekazana lakini Mungu kajaalia hawajui kufungua safety pin nafikiri. Hawajuwi. Wote walokuwepo pale, wanapata watu sita, saba, wanane. Watu wachafuwachafu hivi na nini. Mmoja akatoka ananijuwa akanita “Sheikh Ali.” Wale wengine hawanijuwi. Wale ni dhahir si watu wa Unguja kwa sababu hakuna mtu wa Unguja asonjuwa. Nikamwambia tumepata radio kwamba nije huku, tuje huku. Akasema “si huku bwana. Raha Leo.” Wakanchukuwa katika gari ya 99 [ya polisi] imevunjikavunjika. Tuko njiani ndani ya gari moja katika alochukuwa bastola katika wao…kwa hakika pale sina woga, sina ushujaa. Manake sikuogopa. Nnaona kiama kimefika, watu wanakufa na mimi mmoja katika wao. Nimeona maiti njiani kadhaakadhaa na watu walivouliwa. Sioni athari yenyewe kitu nini kile. Sioni kitu. Njiani ikawa watu wengine wanapiga kelele. Mkungu Malofa kule “huyu Zaimu, huyu Zaimu. Zaimu huyu.” Mimi nkawaambia, jamaa wako

Page 263: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 231

kule wanataka wakapelekewe gari. Wakasema “sisi tunakutaka wewe, hatuwataki wao.” Gari ya Abdalla Sudi tukaiwacha pale pale. Tukenda mpaka Raha Leo. Wasinteremshe mlangoni khasa. Watu wamejaa mamia kwa mamia. Marisasi yanalia, maghasia, harufu ya bangi na tende tu basi. Tumeshuka kidogo khatua kidogo nyuma hivi kabla ya ule mlango mkubwa wa Raha Leo, ikawa tunakwenda kwa miguu, mimi niko mbele na huku nyuma nafatwa na mabunduki na masilaha na mabastola. Nakwenda juu. Akaja mtu nyuma akanipiga rungu la kichwa. Sikugeuka mimi kutizama. Nimepasuka, madamu yanamwaika. Sikugeuka. Naomba. Kufa siogopi lakini kupondwa hivi hivi mbele za watu naona fedheha. Basi nilikuwa naomba nisianguke. Nisianguke. Nikawa natizama mbele tu. Hata sikumtizama nani aliyenipiga. Kwenda, naingia mlangoni, namuona Babu, namuona nani sijui, Khamis Abdalla Ameri na bunduki yake, nikacheka nao hivi, kama kutabbasam hivi, manake mashujaa, mmefanya kazi yenu barabara. “Haya” katika akili yangu. Mmefanya. Ndio, haya. Bas. Nikapanda juu. Kupanda juu, Karume kuingia kuona damu ile. “Ah! Nani huyo?” Nikamwambia basi jamaa wengine wako kule, wako Shangani wanangojea English Club chini. Wakawachukuwe, manake yatawapata kama yalonipata mie. Kwenda juu, watu walonpokea, ni Karume, amezaliwa Kongo, John Okello, ambaye hata Kiswahili hakijuwi, Mcholi kabila ya Obote, na Misha, Yahudi Muisraili, aliyekuwa na kampuni ya samaki pale Malindi. Yeye Misha ndo akanipa sigireti. Nikamwambia sivuti. Pale nalomkuta alikuwa Amir Ali Abdulrasuli (cabinet minister), Mungu amrehemu. Akatoka John Okello akawa yuko mtu anatulinda pale na ana bunduki. Sisi tumekaa na yule mtu amekaa na heshma yake kwa hakika, mchafu na miguu chini na bunduki na nini, lakini kakaaa kwa utulivu. Hakutufanyia utovu wa adabu wowote. Akatoka John Okello akamwambia atampa bastola mbili, moja ya Ali Muhsin, moja ya Amir Ali. Wakifanya vyovyote vile wapige risasi. Sijui kwa nini sharti bastola mbili sijui. Lakini hakumpa. Basi ikawa hivo halafu ndo akaja Karume akaja kututaka, na walikuwa wamekuja jamaa wengine tena, wamekwenda kuchukuliwa. Karume kapeleka gari kuwachukuwa. Halafu Karume akatutaka na Shamte kutuliza watu. Haya mambo ndo yameshatokea, na nini na nini, yasizidi watu wasifanye upinzani. Sisi tukaona hapana maana. Kweli, sisi tunataka liliopo jambo kubwa ni kuokoa roho za watu. Tukasema nao katika radio, Sheikh Muhammed Shamte akasema, na halafu nikasema na mie, kuwatuliza watu wasifanye papara, watizame kama haya ni majaaliwa ya Mwenye Enzi Mgu, zaidi baada ya haya Mwenye Enzi Mgu ndo mwenye kujuwa. Lakini iliopo, kwa sababu ya kuokoa roho za watu zisitilifu zaidi zilivotilifu, watu wasifanye upinzani, waitii hiyo serikali mpya, utawala mpya, kwa maslaha ya nchi yote na wao wenyewe. Hayo basi kwa mukhtasari ndio yaliotokea siku ile. Sasa kuna lawama kadhaa kadhaa kadhaa. Kuna watu wanalaumu kwa kuwa sisi tulikuwa waregevu. Kwa kuwa hatukuchukuwa khatuwa za kutosha za ulinzi kabla yake. Kwanza watu

Page 264: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne232

wafahamu kwa kuwa ni mwezi mmoja tangu sisi kushika ulinzi wa Zanzibar. Kabla yake ulikuwa ulinzi uko katika mikono ya serikali ya Kingereza kamili. Sisi kwa mwezi mmoja tu tumepewa mambo hayo na mwezi mmoja ndo mambo yametokea. Kama lawama ya kujenga uaskari au nini au nini lawama hiyo ni ya Mngereza, si yetu sisi. Lakini juu ya hivo, tuliokuwa tukiyafanya wakati wa Mngereza ni ya kudai na kuomba na kudai, nguvu za kutekeleza hazikuwa katika mikono yetu.6 Jambo lolote lilohusu ulinzi halikuwa katika mikono yetu ya Hizbu au ZPPP. Ilikuwa katika mikono ya serikali ya Wangereza. Na juu ya hivo, ilipotokea yale machafuko ya mwezi wa June mwaka 1961 sehemu ya askari wa Kizanzibari katika polisi ilikuwa thuluthi moja tu. Thuluthi mbili zilikuwa ni wageni. Na kabla ya hivo ilikuwa hapana kabisaa! Yalianza hayo kwa hakika, siwezi kukumbuka katika mwaka gani, mwaka 1950 au kabla yake, nimo katika Majlis Tashrii [Baraza la Kutunga Sharia], tulidai habari hiyohiyo, tuko Majlis Tashrii tukiteuliwa na serikali ya Kingereza, jina ni Sayyid [Mfalme] lakini hakika ni Resident ndo alokuwa na nguvu japokuwa kama tulikuwa tukipendekezwa na jamiiyati zilokuwako. Mimi na wenzangu katika gazeti la Mwongozi tulikuwa tukidai habari ya polisi waingizwe Wazanzibari. Ilikuwa daima serikali ya Kingereza ilikuwa ikitaka kuandikisha watu inakwenda Dar es Salaam na Mombasa kuandikisha watu wa bara, sio watu wa Zanzibar. Na huo ndo mtindo wao wakoloni, si hapa tu. Tanganyika walikuwa wanachukuliwa askari kutoka Kenya, Kenya wanachukuliwa askari kutoka Tanganyika, mpaka Sudani na nini. Uganda wanachukuliwa askari kutoka Sudani, au Malawi, na Malawi wanachukuwa watu wa Tanganyika. Manake Wangereza walikuwa hawaamini askari wa kienyeji. Basi sisi ndo walikuwa kabisaa hawatuchukuwi. Tulipodai saana nikapinga katika kamiti ya pesa, ikawa mimi khasa nafsi yangu nikachukuliwa kwa Kamishna wa Polisi akasema hatuwezi kuwatia watu wa Zanzibar kuwaandikisha kwa kuwa mishahara iko chini, nyumba za kukaa ziko chini. Nikachukuliwa mimi nikaonyeshwa Bomani kule, nikaona kweli kwa hakika nyumba zilikuwa za mabati na kuta zake ni mabati, hapana chochote, hapana njia kufikiri kwamba mtu wa Zanzibar ataweza kuishi katika maisha yale. Tukakubali sisi serikali itumie mapesa zaidi kutengeneza hali za askari wa polisi.7 Ndio zikajengwa hizi nyumba za polisi, mishahara ikaongezwa, wakapata viatu, ndo wa Zanzibar wakaanza kuvutika kuingia chumba cha nane, watu waliosoma, basi hapa Zanzibar wakaanza kuandikisha. Hata tulipofika mwezi wa June 1961 ilipotokea machafuko yale wakauliwa watu wetu wanafika 64 walivouliwa na Afro­Shirazi ilikuwa jeshi la polisi thuluthi moja watu wa Zanzibar, thuluthi mbili za wageni. Hivohivo, tukashika sisi serikali ya madaraka, hatuna nguvu kamili lakini tunadai na kusema na Wangereza, tukaandikisha watu askari mpaka tukaongeza tukafika thuluthi mbili. Kuja mapinduzi thuluthi mbili

Page 265: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 233

za jeshi la polisi walikuwa ni watu wa Zanzibar na thuluthi moja walikuwa watu wageni. Na hawa watu wageni tulikuwa tushafanya mipango kuwabadilisha na askari wetu wa Zanzibar walioko Kenya, Tanganyika na Uganda waje huku na sisi tutawapelekea wao. Kama hatukupata nafasi. Ilikuwa ameshakwenda Seleman Said [Kharusi] kusema na serkali na polisi za kule habari za kubadilishana watu. Na haya nahakika ndio yaliotokea hata kwao Kenya wakafanya na nchi nyengine za Afrika Mashariki. Kila nchi inataka kuwa na polisi wake na jeshi lake liwe la wananchi wake. Lakini ilikuwa wakti hatujamaliza ikawa thuluthi moja watu wa bara, au watu wa nje, na thuluthi mbili wenyeji. Watu wengine wanasema vilevile kwa kuwa kwa sababu hatukuwa na jeshi, hatukuunda jeshi. Kama ni kuunda jeshi ni baada ya uhuru manake kabla ya uhuru kama tunavosema ni serikali ya Kingereza ilokuwapo na serikali ya Kingereza hakuna jeshi. Na vilevile, jeshi sio linolinda mapinduzi ya nchi. Jeshi linahami kwa mambo yanotokea nje. Pengine hilohilo jeshi ndo linoweza kupinduwa. Kama jeshi linalinda lingemzuwia Nkrumah asipinduliwe, lingemzuwia Ben Bella asipinduliwe. Nchi ishirini na mbili zimepinduliwa baada yetu sisi Zanzibar katika Afrika tu. Majeshi yangeweza kuwazuwia hao watu zenye serkali hizo zilokuwa zenye majeshi makubwa. Alakulli hali ilikuwa polisi kazi yake ya ulinzi wa nchi na ndo kazi yake ya upelelezi na kutafuta usalama wa nchi. Lakin jambo moja nitaeleza kuwa, nimepata habari baada yake, kwa kuwa Kamishna wa Polisi Sullivan baada ya kupewa amri na Sheikh Muhammed Shamte kuwa aweke askari tayari, kaitikia naam, hewalla bwana, na Sheikh Muhammed Shamte wakati ule keshatekeleza wajibu wake wa kuwa yeye ndie aliyekuwa mkubwa wa usalama, si Ali Muhsin, wala si Juma Aley, wala si Amir Ali, wala si Rashid Hamadi, wala si Maulidi Mshangama, wala si Baalawy, wala si yoyote katika sisi, bali hata si Salum Kombo aliyekuwa ndie Waziri wa Mambo ya Ndani. Manake Waziri wa Mambo ya Ndani ndiyo kazi yake habari ya amani lakini, kabla ya hivo, mimi nalikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika wakti wa Serkali ya Utawala wa Ndani wa madaraka na nalikuwa na nufudhi za mambo ya ndani. Lakini tulipokuja kupata uhuru mimi nkashika Wizara Kharijiya, mambo ya nje, na Salum Kombo akashika Wizara ya Mambo ya Ndani, lakini khasa mambo ya amri ya polisi na mambo ya security yalikuwa katika mikono ya Waziri Mkuu mwenyewe. Sheikh Salum Kombo alikuwa ni Idara tu habari ya mishahara yao, kutizama hali zao na nini, hakuwa na nufudhi na amri ya polisi. Sheikh Muhammed Shamte, na mkubwa wa serikali popote pale ndie mwenye amri ya mwisho katika mambo ya usalama wa nchi. Hata huyo Waziri wa Mambo ya Ndani hana nguvu ila kwa amri ya Waziri Mkuu. Na Waziri Mkuu ndiye aliyemwita Kamishna wa polisi ambaye ndiye executive, mtu wa kutekeleza amri. Akamwita Kamishna wa polisi akamuamrisha nini la kufanya. Ndiye kama commander-in-chief kama tungekuwa tuna jeshi. Sasa naye vilevile akamuitikia hewalla. Kazi ya kisiasa, kazi ya uwaziri, kazi ya utawala,

Page 266: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne234

pale imekwisha. Yeye ni kazi yake kuamrisha keshaamrisha. Bado ingehitajia kwa kuwa yeye khabari ile badala ya kuwa Sheikh Muhammed Shamte kaipata mbele yeye, yeye ndo kawaambia polisi. Inataka polisi, sehemu ya “special branch” [usalama] tulokuwa nayo, ndo sehemu ya upelelezi, itupe khabari, impe khabari Commissioner of Police atwambie sisi, amwambie Sheikh Muhammed Shamte, ampe khabari ya kuwa kuna khatari hivi na nini na nini atowe mapendekezo yake, nini anataka tufanye. Lakini polisi haikufanya hivo. Badala yake sisi, sisi wanasiasa ndio tuliopata khabari kwa njia ya vyama na njia nyengine tulizonazo, ndo tukapata khabari. Sisi si polisi, si serikali. Sisi ndio tulopata khabari, Sheikh Muhammed Shamte, ndiye yeye akamwambia Kamishna wa polisi na Kamishna wa polisi katoka pale, hakutekeleza amri aliyopewa. Badala yake, ninavosikia, Speight alokuwa ndio mkubwa wa “special branch” alipoelezewa na Kamishna akasema “a, huu uzushi, Hizbu kazi yao kuwazushia Afro­Shirazi.”8 Fikra zake zile zile za kizamani, ilipokuwa Afro­Shirazi ndio kipenzi cha serikali ya Kiingereza na sisi ndo maadui, ndo tunotaka kupinduwa serikali ya Kiingereza. Basi yeye hajuwi sasa sisi ndo tumekuwa serikali na wajibu wake afate. Lakini waongo hao. Wametengeneza, wanajuwa! Maana yake ingelikuwa hawakuamini kwa kujuwa hivo wasingeondowa family zao, family zao na watoto wao, kuwatowa Ziwani kule na wapi na nini, wakawaleta mjini kwa usalama. Wakaachilia ndugu zetu, askari wale, wakiuliwa vitandani, bila ya bunduki bila ya chochote, wamepewa marungu tu basi. Basi hali ni hivo, hakuchukuwa khatuwa yoyote Sullivan.9 Wamekwenda wamewaachilia wale ikawa watu wale waharibifu walokwenda kushambulia wakachukuwa armoury [ghala ya silaha] kwa mipango yao, silaha zile za Bomani na nini. Kitu kinafaa mtu kushukuru vilevile kwa kuwa polisi yetu haikuwa khain. Wachache kama Edington Kisasi na wengine, lakini wengi wao walikuwa ni watu madhubuti hata hawa watu wa bara. Watu kama Kilonzi, mtu wa Kenya, yeye ndo maana wakamfukuza mwisho. Mmoja kabila yake mwenyewe Nyerere! Prison yote ilikuwa ni tiifu, wamepigana mpaka mwisho. Mmoja chief officer wa Kitende, kabila yake Nyerere, Langoni. Kafa huku kwa kuhami na kukataa kuwatii hao waasi.10 Sasa tizama mambo yalivokuwa. Ingelikuwa si Mgereza kujuwa mambo haya na kutengeneza mbele na kujuwa, kwanini Sullivan kafanya vile na wakakataa kutii amri ya Prime Minister kuchukuwa hadhar, hawakuchukuwa hadhar, hadhar yenyewe ilikuwa kama kuna mechi ya mpira au nini. Lakini hapana khatwa yoyote ilochukuliwa ya ulinzi kamili. Kina Seleman Said na Sketty walipotaka rukhsa kwenda shamba wakaambiwa mnayo rukhsa kwenda shamba, hapana chochote, iko fete tu basi hiyo. Almuradi imekuwa katika hali ya kutojiaandaa na kuwa hapana chochote. Ndo Sketty maskini ya Mgu akaja akauliwa anatoka shamba hana habari, hajuwi lolote linalotokea. Sasa kama nnavosema kuwa ni wajib wa polisi na security kuwaambia wakubwa wa siasa, yaani Mawaziri, kuiambia serikali ambayo ndo Mawaziri, nini

Page 267: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 235

kinachotaka kutokea, na watoe pendekezo nini lifanywe, khatwa gani ichukuwe. Tena Mawaziri wale, au serikali ile, ndo inatowa amri kuwaambia wale polisi nini cha kufanya. Hapa kinyume chake. Kinyume chake kabisa. Sisi ndo tulojuwa. Serikali ndo ilojuwa. Wanasiasa ndo walopata khabari. Wakawaambia polisi na wakawaamrisha, naam, polisi hawakufanya kazi. Na polisi yenyewe ni kwa sababu ni mkubwa wa polisi alikuwa huyo Sullivan ambaye hakutii amri aliyopewa. Sasa watu wengine watasema kwa nini mkawaachia Wangereza? Wako wengine wanasema hivo. Kwa nini mkawaachia Wangereza mpaka mkapata uhuru. Kinyume chake, watu wengine wanasema, mmewatoa Wangereza upesi ndo mana ikaleta haya. Hakika basi, ukifanya hivi utalaumiwa, ukifanya hivi utalaumiwa. Jambo likishatokea, kila mtu anakuwa na akili kuliko mwenziwe. Kila mtu anaweza kutowa habari kwanini ikawa. Kwanini msingefanya hivi? Kwanini msingefanya hivi. Limeshatokea. Kabla yake hapana mtu anoweza kukupa busara ikawa na kila mtu atasema lake. Haya ni hadithi kama yule mtu, mzee yule, na mwanawe, na punda. Kila analofanya, wakipanda wote wawili, lawama, akimpandisha mtoto, lawama, akipanda mzee, lawama, mwisho wake wakaangukia labda tumbebe punda huyu, nayo pia lawama. Au wote kutokumpanda. Pia lawama. Binaadam hana atendalo, kila analotenda ndo lawama. Sisi tumelaumiwa, kuna wengine wanalaumu kuwa, kwa sababu mmewatowa Wangereza upesi, na hakika sisi katika nchi zote za kikoloni, ndo tulowatoa sana Wangereza upesi. Na tuna sababu. Tuna maendeleo, tulikuwa tunastahiki kutawala nchi yetu zamani kwa sababu nchi yetu kutokea hapo huru. Mipango yetu tulioitengeneza, alhamdulillahi, tumeyatengeneza, tumesomesha watu wetu, tumewafundisha mbele. Tumepigania ilmu kwanza, kwa kuwaweka tayari watu wetu. Na ilikuwa mwaka uleule, 1963 Disemba, katika mwaka 1964 kiasi katika mwezi wa September, hatokuwapo Mzungu hata mmoja katika polisi. Na nyadhifa chungu nzima zitakuwa hapana. Hata madaktari wengi isipokuwa ma specialist officers tutakuwa nao wenyewe wa kutosha. Kila kazi tena. Jeshi ilikuwa sisi tunaliunda baada ya uhuru manake tulikuwa hatuna nufudhi za kujenga jeshi. Mngereza hakutuwachia jeshi. Kaachia jeshi Tanganyika, kaachia jeshi Kenya, na nini, Zanzibar kaiacha hivihivi. Kwa sababu Zanzibar alikuwa makusudio yake, plani ya Mgereza sku zote ni itekwe na nchi hizi ambazo walizitengeneza wao ndio watoto wake mwenyewe. Huu ni mpango. Katika jela nimesoma buku moja la mwandishi mmoja Towards the African Unity anasema kuwa si jambo la kuwa ni bakhti nasibu tu kuwa nchi nyingi za katika Afrika kuwa hata zenye kuwa na Waislamu wengi zinatawaliwa na watu Wakristo walofundishwa na mamishionari. Huu ni mpango ulotengenezwa tangu mwanzo kwa sababu kwa kuwa hata bendera itakapoondoshwa lakini nguvu za ukoloni zibakie katika nchi ile. Basi ilikuwa sisi, kwetu sisi hawezi kumweka mission [Mkristo], na sisi ndo tulokuwa mbele kushika serikali. Sasa iliokuwapo ni kuondowa nguvu zetu sisi ni kuiondowa ili Zanzibar yote

Page 268: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne236

imezwee! Imezwe. Kule wameshajenga wenyewe bwana Nyerere alofundishwa katika skuli zake za mission, na nini, kalelewa kwa kuwa atabaki vovote vile. Zanzibar ilokuwa imeendelea kuliko nchi zote katika East Africa lakini imebaki ndo ya mwisho ya kupata uhuru kwa sababu kwa kuwa isiwe na nufudh na hatuna jeshi, hatuna njia yoyote. Mngereza katoka, bas! Kawacha mikono yake hakutengeneza kitu. Liliopo sisi kujenga, lakini sisi, vovote tulivokuwa tunafikiri hatukuwa na, kweli tunajuwa, tumechukuwa khatwa, tumechukuwa khatwa za kutaka kujenga jeshi letu, ulinzi wetu. Tulikuwa tumeshasema na nchi za kuweza, za kirafiki, za kuweza kutusaidia sisi kujenga jeshi letu. Mngereza katuwacha mkono, lakini nchi nyengine zilikuwa tayari kwa kuja kutusaidia, za urafiki, lakini lazim tupate uhuru mwanzo. Hatuwezi kumuingiza, kuwa na alaka na mtu mwingine na Mngereza yuko ndani na ambaye hataki. Kwa sababu wameogopa. Moja katika jambo lilotuletea khasama kubwa sisi ni siasa yetu ya kupinga ukoloni kwa kupinga Uzayoni na mambo ya Mayahudi na kuunga mkono nchi za Kiislamu na za Kiarabu katika siasa zao za kupata uhuru wa nafsi zao. Hii alaka zetu na wao ndo zilotuletea khasama sisi na haya hayakuanza sasa. Yameanza zamani! Na ni siasa yao wanatuona sisi ni hatari. Ni hatari kwa sababu inakuwa ni kinyume na siasa yao. Inakuwa ni kama mwiba katika nyama. Sasa, kama nnavosema, ilikuwa September 1964 polisi yetu ingekuwa yote Wazanzibari na Slemani Saidi atakuwa Kamishna. Ukitizama nchi nyingine zimeendelea miezi, bali miaka na Waengereza na wakoloni wako. Na ziko mpaka sasa bado zinaendeshwa na wao, na nini. Hayo hayakuwa kwetu sisi kwa sababu siasa yetu ilikuwa siasa ya uhuru. Lakini watu wengine wanasema kuwa kwanini mkawaweka Wangereza? Hatukuwaweka ila kwa kiasi ya kuwa sisi tulifika katika hali ya wasat, hali ya katikati. Hatukuwatowa kabisa kabla ya uhuru, na hatukuwa na mipango ya kuwaachilia kuendelea kwa muda mrefu. Tulikuwa katika hali ya wasat nayo haikutufaa. Hatukwenda extreme [taraf ] ya huku wala extreme [taraf ] ya huku. Sasa sijui tungefanya nini. Tungefanya hivi ingekuwa watu wana haki ya kutulaumu, ingekuwa tumefanya hivi ingekuwa watu wanatulaumu. Imekuwa hali ya kati nayo bado watu wanatulaumu. Lakini haya ndio lazim yatokee na katika watu, haya hayakutupata sisi tu, yamempata hata Mtume Muhammad (SAW). Ameambiwa hivohivo na wanafik. In tusibhum hasanatun yakulu hadha min indi Allah, wa intusibhum sayiatin yakulu hiya min indak. Kul kullu min indi Allah. Fa ma lihaulail qawm la yataduna la yafkahuna hadeeth, “likiwapata jema wanasema limetoka kwa Myezimgu, likiwapata ovu wanasema limetoka kwako wewe Muhammad, sema yote yanatokana na Myezimgu.” Watu hawa. Watu hawa wana nini? Hata hawakaribii kujuwa kuzungumza! Mazungumzo hawajuwi. Jambo jingine kuwa inaonyesha kwa kuwa mipango hii wao wameyapanga wakubwa wakoloni wenyewe. Balozi wa Kingereza amesema mimi siwezi kupendekeza kwa kuwa waje Wangereza waingilie kati katika mambo ya ndani

Page 269: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 237

haya na nyinyi ni serikali ya wachache. Huku wiki moja baada ya pale, yametokea maasi Tanganyika ya jeshi! Si wahuni kama hawa wetu. Ni jeshi! Discipline force [nguvu yenye kufuata nidhamu]. Ambapo likiasi jeshi basi kweli ni waasi. Manake inakuwa ni watu wa mwisho kuasi manake jeshi ndo linofata amri sio wahuni ambao hawana pesa, hawana chakula, hawana chochote, wana dhiki. Ni jeshi lilofunzwa kulinda serikali, likaasi. Sisi alhamdulillah, halikuasi jeshi letu. Jeshi la Tanganyika liliasi wakampinduwa Nyerere hajulikani yuko wapi. Ingelikuwa si Kambona, wote wamekimbia, Mawaziri wote wamejificha, na Nyerere pia. Oscar Kambona ndo alobaki akawaokowa. Wakaja Wangereza wakateremka kwa nguvu. Wakapiga mizinga. Wakateka. Wakawanyanganya silaha askari wa Tanganyika, wakamrejesha Nyerere katika kiti chake. Halafu likaletwa jeshi kutoka Nigeria.11 Likaja likashika uangalizi mpaka wakajenga jeshi jipya la Tanganyika. Basi Mngereza huyuhuyu aliokataa, na Kenya ilitokea uasi akatumia, Uganda vilevile, akatumia. Lakini khasa Tanganyika kwa sababu kwa kuwa yeye ndiye anapendelea utawala ule wa Nyerere uendelee. Sisi ilikuwa tuondoke. Wiki moja tu khitilafu baina yetu! Mbona kule kaweza kuingia? Kaweza kuingia kule katika Tanganyika akaja akamrudisha Nyerere ambapo serikali yake Tanganyika ya Nyerere ilikuwa imechaguliwa kwa 9% ya voti bas! Watu walopiga voti, walopiga kura, hata Nyerere akapata serikali yake ya TANU ikapata, ni chini kuliko tisa katika mia! Sisi zaidi ya 33% watu walopiga voti hata tukachaguliwa sisi kuchukuwa serkali. Sasa wepi walokuwa wachache? Walopigiwa voti na watu 33% ya jumla ya population [idadi ya watu ndani ya nchi] au 9% ilokuwa chini kuliko ushur [1/10] au walokuwa thuluth [1/3]? Lakini wanalolitaka ndo liwe. Jengine linaonyesha, palepale Mngereza manwari yake Mngereza ipo, manwari yake Mmarekani ipo imekuja kuchukuwa raia zake na watu wake. Na tizama, katika watu wote waliouliwa, kila kabila limeuliwa, kila watu wameadhibiwa na nini, kila kabila. Waarabu, Waswahili, Washirazi, Waafrika, Wangazija, Wahindi, wote wameuliwa. Ila Mngereza, Mzungu hata mmoja hakuguswa! Licha kuuliwa. Hata kupigwa. Hapana Mzungu hata mmoja alopata masaib yoyote. Hili ni jambo la ajabu. Katika fujo lote lilotokea Mzungu hata mmoja hakuguswa. Basi haya watu na wayapime wenyewe katika akili zao. Katika watu waliouliwa maalafu ya watu, maalafu katika watu, wenyewe wanavosema zaidi ya 11,000 elfu, anosema mwenyewe.12 Basi katika watu hao hakutokea Mzungu hata mmoja aliyekatwa ukucha. Au aliyefinywa? Hili ni jambo la kupima watu wajuwe. Na vilevile manwari za Mngereza na Kimarekani zimetokea wapi pale pale? Mara! Na hali zilikuwa haziwezi kutuletea sisi msaada? Walikuwa wanajuwa yepi yatakayotokea na wakawapo.13

Basi sisi jamaa yakuwa mambo wanayafanya ni madogo haya yaliotokea Zanzibar. Kwa sababu wanasema kwa nini hamkufanya hivi, kwa nini hamkufanya hivi? Kwanza unataraji Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, mimi nilikuwa Waziri wa Kharijiya, mambo yangu ni mambo ya nje, sikuwa hata

Page 270: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne238

Waziri wa Ndani. Waziri wa Mambo ya Nje, mimi niwe dhamana wa usalama wa nchi, hili ni jambo la ajabu. Kutarajiwa kuwa mimi, amani ya nchi niwe nayo mimi. Sijui jeshi, sikufundishwa jeshi. Mimi si polisi, si askari jeshi, wala si Waziri wa Mambo ya Ndani, wala si Waziri Mkuu. Mas­uliya yote yaniangukie mimi, nakubali yaniangukie mimi mas­uliya, kwa sababu mimi siogopi mas­uliya, lakini kweli lazma isemwe. Hapana nchi ambayo Waziri Kharijiya anakuwa responsible [dhamana] for security, anakuwa yeye ndo jukumu yake habari ya amani. Si kazi yake. Pili, yakwakuwa, aa, kwa sababu ni kiongozi wa Hizbu. Kiongozi wa Hizbu au si wa chama chochote, Wilson, England, sio anayehusika kwa kuwa yeye ni mkubwa wa chama, au Mrs Hat wakuwa ni mkubwa wa chama cha Conservative kwa hivo ndo mkubwa wa security au Wilson. Licha hivyo, mtu serikali kama hii—President Saadat, ni mwanajeshi, ni Rais, ni mwanajeshi na rais wa kwelikweli. Naye ni mkubwa wa majeshi. Leo waliadh billahi, akipinduliwa Anwar Sadaat au kama alivopinduliwa Ben Bella, lawama si ya Ben Bella alopinduliwa, wala si ya Nkrumah aliyepinduliwa, ila ikiwa siasa yake ni mbaya, unamlaumu kuwa siasa yake ndo ilopelekea mapinduzi. Lakini kwa sababu ya kupinduliwa tu si mas­ul yeye. Hata Saadat akitaka kupinduliwa, waliadh billah, sio masul. Lawama ya polisi ambayo haikulinda serikali ya Saadat. Lawama ni ya usalama haikujuwa mapinduzi mbele si lawama yake.14 Yeye kazi yake ni kulindwa na serikali, Mawaziri na nini, kazi yao ni kulindwa na security, polisi, ndio kazi yake ulinzi, ilinde serikali. Halipwi mshahara Waziri, Waziri mkuu, au Waziri wa Mambo ya Ndani, au Waziri wa Mambo ya Nje, wote Mawaziri, hawalipwi kwa sababu wao ndo walinde usalama wa nchi. Wao wanafanya mipango ya siasa ya kuendesha nchi. Polisi kazi yake wanalipwa, sasa, ikiwa wale hawakufanya kazi yao sawa ndio walaumiwe.15 Sasa sisi tunatarajiwa kwa kuwa kama lawama basi sisi tulikuwa na security [usalama] mbovu, tulikuwa na polisi mbovu, lini tulipata nafasi ya kuijenga hiyo polisi mpya au security mbovu? Mwezi mmoja? Haya ni mambo basi watu wapime wenyewe kwa nafsi yao. Na mengi yako ya kueleza lakini naona kwa kuwa sina wakti na sasa kwa hakika nna haraka ya kuiwahi hii tepu apate kuchukuwa Sayyid Muhammed Abdul Muttalib (Mutta) anataka kukimbilia mambo ya tarawehe na nini, naye pia anaondoka kesho asubuhi, basi siwezi kuendelea zaidi. Nna mengi, mengi, mengi sana ya kueleza na Inshaalla itafika wakti watu watakuja kusoma wenyewe kwa utulivu watapoyajuwa na tutapoyasema. Lakini moja ni kwakuwa watu likisha, wanasema Wapemba “lishawavusha ni gogo.” Mkishavuka, mkavuka kwa dau mkenda upande wa pili, hamneni tena kuwa hilo ni dau. Hilo ni gogo! Basi waliovuka wakapata uhuru wao, wakamtowa Mngereza na nini, wakavuka na nini, sasa lilobaki ni gogo tu, tulitukane tu manake kwa kuwa ndo basi, tambara bovu tena limekuwa. Lakini Inshaalla kweli itakuja kudhihiri, watu watakuja kuisikia, watakuja kuifahamu, na wataelewa itakapokuja wakti wake, watakapoona ukweli, na leo ni hivi kesho ni hivi.

Page 271: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 239

Na haqqi al haqq yaalu wala yuula alayhi. Na haki maisha inakuja juu wala haijiwi juu. Itakuja itadhihiri itadhihiri mpaka watu watafahamu. Na hao wanozuwa na kutafuta fursa kuleta fitna na nini tokeapo wao wako walokuwa wamepandia katika Hizbu kwa makusudi yao wapate malengo yao. Walipokuwa hawajayapata maarib yao basi wamevunjika moyo lakini watu wakweli wenye moyo wao watu wanostahmili tabu, na hii ni mitihani tunopata, na hii ni mitihani. Hakupewa mtu kwa kuwa kupata adhabu hizi, taabu hizi, ila kwa sababu kwa kuwa tumtahiniwe ili Myezimgu apate kujuwa wepi waliobora. Liyaalamu Allah aladhina aamanu walladhina minkum almunaafiqin. Myezimgu apate kuwajuwa wepi walioamini kweli na wepi wanafik. Wepi makhain, wepi wanafik, wepi wanoregarega, wepi wakweli. Na hii ni mitihani na ni sunna ya Myezimgu. Wa min qariyaatin ila nahnu muhlikuha wa nuadhibuha kabla yawmil qiyama. Hapana mji ila utahilikishwa, utaadhibiwa kabla ya qiyama na hii tumepata adhabu hii Myezimgu iwe ndo ya mwisho ya kutuonyesha sisi katika nchi yetu na Inshaalla baada ya hapo itakuwa ni faraj na faraj iko karibu. Inna fatahna laka fathan mubiinan yaghfir laka Allah ma taqaddamma min dhambika wa ma taakhara [Hakika tumekufungulia ushindi wa dhaahiri Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyo tangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyo nyooka (Qur’ani 48:1–2)] Inshaalla itakuwa karibu al fath wal nasr minal Allah wa fathin karib. Inna aaidun! Tutarudi! Labda kosa letu sisi mawaziri kosa moja. Nao kuwa hatukutoroka hapo mbele tukawawacha watu wetu katika hilaki, peke yao. Ilitolewa shauri hiyo, tuondoke pamoja na Sayyid Jamshid katika meli.16 Mimi nikakataa na Mawaziri wote kwa umoja wao wote walikataa kuondoka. Tukataka sisi tukae. Vipi tutatoka sisi na watu wetu bado wanauliwa? Tukimbize nafsi zetu sisi, au sisi na aila zetu, tuwawache watu wanauliwa. Itakuwa namna gani? Sisi tukae mpaka tulete salama katika nchi ndo tukakaa pale tunafanya juhudi ya kutaka kusema na Nyerere na nini, alete Mawaziri na nini, wakutane na wale maasi, wanaofanya ghasia zile, ili waje tukutane nao tuwakabidhi serikali, wasite kuuwa watu tu. Sisi watufanye wanavotaka. Na hii tumekaa sisi tubaki mwisho. Sisi tunafata mwendo aliotuachia Mtume Muhammad (SAW). Hata katika Hijra, ilikuwa yeye ndo wa mwisho.17

Kwanza kawasalimisha watu wake halafu ndo kakimbia yeye mwenyewe na Sayyidna Abu Bakar na Seyyidna Ali. Lakini yeye kwa kuwa akimbie yeye Mtume kwanza awaache watu wake nyuma. Vipi? Na sisi tumeambiwa tuna kiigizo kizuri katika Mtume wa Myezimgu. Je tumeambiwa na Myezimgu hivo leo twende mwendo mwengine sisi tuondoke sisi mbele tuwaache watu wetu nyuma. Tukaona la, hapa sivyo. Inaweza kuwa tumekosa, inaweza kuwa ni khataa katika mambo ya siasa, au vyovote vile, lakini kwa njia, basi kama tumekosa tumekosa kwa njia safi. Hilo ndo kosa letu kwa kuwa hatukukimbia wenyewe, tukaawacha watu wetu. Na tukakaa tunaadhibika mpaka mwisho, tukawa ndo wa mwisho kutoka. Wallahi nakwambia. Nlikuwa naomba, jela, mimi niwe wa

Page 272: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nne240

mwisho kutolewa. Na kila waziri alokuja. Kaja Twala, wamekuja kina Karume…waachieni wana makosa gani. Tuwekeni sisi mawaziri tulofanya mambo haya. Tumeweka rekodi, tumetoka sisi watatu wa mwisho ni Rehma ya Myezimgu. Tunaona ni fakhri na ni wajibu wetu kukaa namna hii. Tumefanya jitihada yetu kama tulivoweza, tumeshindwa katika hayo lakini kushindwa kwetu namna hii sio kwa kuwa kushindwa. Hii ni Uhud hii.18 Hii ni Uhud. Vita va mwisho bado havijaja. Na iwe Uhud…lakini vita va mwisho havijesha bado. Vitakuja na vitakuwa, Inshaalla, vitakuwa upande wa hakki. Watu wasighurike, wasivunjike moyo, kwa sababu ya…sisi tulikuwa na amana ya kuweka kule ikhlas, kuweka Uislamu, kuweka ustaarabu. Sisi ni ngome ya kusini. Sisi na visiwa va Ngazija ndio ngome ya kusini ya kuweka Uislamu, Ustaarabu. Miaka kadhaa wa kadhaa wamejaribu watu kutuvunja. Kwa karne kadhaa kadhaa. Wamejaribu Wareno miaka 200 wamepigana. Wamekuja Wangereza na Majermani na Wafaransa, na sasa na wao wafurahi kidogo hivi. Falyafrahu qalilan wa yabku kathiran [Wache wafurahi kidogo lakini watakuja kulia sana]. Itakuja siku yao ya kulia. Itakuja siku yao, lakini mwenge wa Uisilamu utaendelea na ustaarabu utaendelea. Watu wanokaa yakatokea haya halafu wengine wakafurahi wakakimbia upesi, kukimbia ni kukimbia, walokimbia kule wakenda kwengine wajuwe kwa kuwa wanakimbia, lakini kuna lazma warejee huko walokokwenda…siku moja lazima warejee. Na waondoke na wakimbie, wakimbie wao kuwa wamekimbia tumeshindwa, wakti wenyewe mdogo, lakini ni kwa sababu ya kwa kuwa, zile nguvu zimekuwa nyingi kweli. Nguvu, si mapinduzi hayakutokea Zanzibar, ni wazi kuwa ni maadui wakubwa kuliko Afro­Shirazi. Afro­Shirazi ni alama tu, ni chambo tu kimetumiwa, lakini adui zetu ni wakubwa zaidi. Adui zetu ni wakubwa zaidi. Ni ubeberu, imperialism, na uzayoni, Zion­ism. Yamejikusanya pamoja! Hizi ndo zilokuja kutaka kuvunja Uislamu ulojengwa kwa juu ya miaka elfu sasa. Juu ya miaka elfu Uislamu uko katika visiwa vetu va Zanzibar na Afrika Mashariki. Mimi siku zote nnasema kuwa Uislamu umekuja Afrika Mashariki mbele kuliko kufika Madina kwa sababu ya Hijra walokuja wakaja Ethiopia ambayo Ethiopia ni sehemu ya Afrika Mashariki na khasa ilikuwa imeeenea mpaka katika Kilimanjaro na zaidi. Habash ya zamani, manake kote huku kukiitwa Habash. Hivi karibuni Dr. Mustafa Mu’min, ametoka kutoka mkutano wa Muslim Student Association ya America, United States na Canada. Amekuja Profesa wa Kimarekani mwenye asli ya kipalestina, Muislamu, alikuja kutowa khutba katika mkutano ule, amethibitisha kwa ithbati za kisayansi na nyaraka, wathaiq amekuja nazo, kwa kuwa amethibitisha kwa kuwa Uislamu umeingilia Zanzibar, umeingilia Zanzibar kuingia East Africa, kabla kwenda Madina, kabla ya kufika Ethiopia. Sijaipata khutba hiyo mwenyewe nikaisoma lakini nimesimliwa na Dr. Mustafa Mu’min. Alakullihal, sisi ni Waislamu wa zamani na tulikuwa sisi ndo muraabitin kule, tunashika ngao, ngome. Kutoka kule, nguvu hizi tulizokuwa

Page 273: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kuanguka kwa Ngome ya Kusini 241

nazo za miaka elfu na zaidi. Si nguvu bali kwa kuwa sisi tulikuwa ndo askari wa kule wa kushika ulinzi. Ni wajib wetu kuendeleza Uislamu wende mbele. Sio kuwa sisi ndo tuutupe kwa sababu ya hayo mapinduzi ya saa chache yalotokea. Tuseme tujifakhari kwa kuwa sisi basi yamekwisha leo. Tusahau. La, siyo. Inna aidun, Inna aidun—Inshaalla. Tutarudi, tutarudi—Mungu Akipenda. Alikubali Mtume (SAW) na masahaba kurudi baada ya sulhi ya Hudaybiya.19 Kurudi Madina bila ya kuingia Makka haikuwa pale kwa kuwa ni kushindwa. Waislamu wengi, masahaba wengi wakubwawakubwa waliona tumeshindwa jama na wakaona haya kubwa na wakawa wanawachukia lakini Myezimgu akamjuvya Mtume wake “Inna Fatahna Laka Fathan Mubina Liyaghfiraqa Allah ma takaddma min dhambika wa ma taakhara.” Haya siyasahau, na hata nlipokuwa Morocco baada ya kushindwa mazungumzo yetu ya katiba ya mwanzo. Nikenda Morocco nikaonana na Malik Hassan nikamwambia ya kuwa mkitwachia tukashindwa sisi katika mambo haya, sisi tukashindwa, basi nakwambia taarikh ya Al Andalus [Spain] itaandikwa tena. Zanzibar ukiondoka Uislamu basi Uislamu ndo kurudi tena nyuma. Akanambia, “usinkumbushe hayo na Inshaalla hayatatokea. Na sisi tunaona uchungu haya ya Andalus.” Siku zilezile, niko kulekule, nalionyeshwa nyumba ya mayatima, mayatima wa mashahidi walookufa katika kupigania uhuru wa nchi yao (Moroko) dhidi ya Mfaransa. Nyumba ya mayatima. Basi nikalala sku moja. Huku niko jela Tanganyika. Nimelala nikaota nyumba ileile, ile ya mashahidi imeandikwa kwa khati kubwa! Ukuta mzima! Mbele pale. Inna fatahna laka fathan mubina liyaghfira laka Allah ma takaddama min dhambika wa ma taakhara. Basi Inshaalla itakuwa kheri. Assalam Alaykum wa rahmatu Allah wabarakatuh.

Page 274: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na TanoFikra za Kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki

Oscar Kambona alifafanuwa kuwa fikra ya Shirikisho la Afrika Mashariki linalotawaliwa na Tanzania sio fikra ya Nyerere bali ni fikra ya Muingereza na ililengwa kuwadhibiti Mau Mau wa Kenya. Ilipokuwa Kenya si tishio tena kwa maslahi ya Magharibi, anahoji Kambona, fikra ya Shirikisho ikatupiliwa mbali.

Sheikh Ali Muhsin

Hizi fikra za kutaka kufanya Shirikisho la Afrika ya Mashariki hazikuanza leo. Kwa hakika tokea zamani Afrika Mashariki ilikuwa kitu kimoja. Hata pale ilipokuwa watawala ni maimamu wa Omani waliowatangulia Wafalme wa ukoo wa sasa, Afrika Mashariki ilikuwa ni moja. Lakini aliyeifanya khasa kuwa ni moja ni Sayyid Said bin Sultan, wa ukoo huu unaotawala hivi sasa Oman. Seyyid Said bin Sultan ndie aliyekuja, kwa kutumia lugha ya kizungu—kui “consolidate the whole of East Africa” [kuileta pamoja Afrika Mashariki yote]. Na akafanya makao yake makuu Zanzibar na Unguja ndio ikawa makao yake makuu. Akayahamisha Maskati akayaleta Unguja, na mwenyewe akawa anakwenda huku na huku (mara Maskati mara Zanzibar) na mwisho wake akafia Zanzibar. Japo kama alizaliwa Omani, lakini alifia Zanzibar. Nchi zote za Afrika ya Mashariki zilikuwa moja na kitu kimoja. Watu wakiendeana, wakifanya biashara na kila kitu kwa pamoja na kwa maelewano. Ni Wazungu, walipoingia na kufanya kinyanganyiro, kama ilivyoelezewa katika kitabu cha bwana Issa Nasser Al­Ismaily [Kinyang’anyiro na Utumwa] baada ya kukutana huko ulaya na kugawana Afrika yote kwa kuifanya kinyang’anyiro—“The Scramble of Africa”. Kabla ya kinyanganyiro hicho, katika nchi zote hizi ilikuwa hakuna mambo ya Kenya, Tanganyika, Uganda, wala Zanzibar kuwa mbalimbali. Zilikuwa pamoja mpaka Kongo—zote zilikuwa nchi moja. Baada ya kuingia ukoloni wa wazungu

Page 275: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Fikra za Kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki 243

kukaanzishwa majina mapya. Tanganyika akaichukua Jerumani, na Rwanda na Burundi na Kongo wakazichukuwa Belgium, Kenya akaichukuwa Mngereza, Uganda ikafanywa Mahamia ya Mngereza, na halafu yake hata hiyo Zanzibar yenyewe ambayo ilibakia visiwa viwili tu vya Unguja na Pemba na Mwambao wa Kenya, lakini hata hivyo, mwisho wake vilichukuliwa na Waingereza katika mwaka 1890. Hivyo basi Afrika ya Mashariki kuwa nchi moja ndio maumbile yake na ndio asili yenyewe. Kugawanyika kwake ni mamboleo tu yaliyoletwa na wakoloni. Kwa hivyo hizi fikra za kutaka kufanya Shirikisho la Afrika ya Mashariki ni kujaribu kurejea kwenye uasili na pia hazikuanza leo na jana kama tutavyoona. Nakumbuka, kama sikosei, walialikwa katika mwaka 1957, viongozi wa siasa wa Kiafrika na Kwame Nkrumah aliyekuwa Rais wa Ghana baada ya Ghana kupata uhuru wake kwa mwaka wa pili yake. Alitualika viongozi wote kutoka katika nchi zilizokuwa zinatawaliwa na wakoloni wakati huo. Katika hao walioalikwa baadhi yetu tulikuwa viongozi wa vyama vya kisiasa na wengine wa vyama vya Trade Union [wafanyakazi] na Cooperatives [vyama va ushirika] za nchi mbalimbali. Alitualika kusheherekea mwaka wa kwanza wa kupata uhuru wa Ghana. Mimi ndie niliealikwa kutoka Zanzibar. Kule nikawakuta wenzangu wengine kutoka Afrika Mashariki kama vile Julius Nyerere kutoka Tanganyika, Joseph Murumbi na Peter Kaunange kutoka Kenya, na Mudira kutoka Uganda. Nkrumah, baada ya kwisha zile sherehe alituita nyumbani kwake ambako vilevile tulimkutia George Padmore ambaye alikuwa mshauri wake juu ya mambo ya Afrika. George Padmore ni mtu mweusi kutoka Trinidad, West Indies. Ni mtu aliekuwa mjuzi kwelikweli wa nchi za Kiafrika zilokuwa chini ya ukoloni. Yeye alikuwa amehamishwa kutoka nchi yake iliyokuwa inatawaliwa na Muingereza na akawa hana ruhusa ya kwenda nchi nyingine; na akawa anakaa England. Ilipopata uhuru wake Ghana, Nkrumah ambaye alikuwa ni rafiki yake akamleta Ghana na kumfanya mshauri wake. Wote wawili, Nkrumah na Padmore, walitoa shauri kuwa ufanywe mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika na wakutane Ghana watengeneze mipango ya namna ya Ki­Ghandi iliyokuwa ikiitwa “Passive Resistance” na ambayo aliifanya yeye [Mahatma] Ghandi kule India katika kupi­gana na kupambana na ukoloni kwa njia ya kisalama.1 Tufanye mipango hiyo ili kuokoa nchi zote za Kiafrika kutoka na ukoloni. Mazungumzo haya yalikuwa katika mwezi wa March na mkutano huo wa kufanya mipango hiyo ya ukombozi wa kutoka na ukoloni ulikuwa ufanywe katika mwezi wa December. Mimi niliwapa shauri wenzangu wa Afrika Mashariki kwamba kabla ya sisi kwenda Ghana sisi wenyewe kwanza tutengeneze kukutana nyumbani Afrika ya Mashariki ili tuwe shauri moja na tujuwane na tufahamiane kabla ya kurejea Ghana. Wenzangu wote waliwafiki sana shauri hiyo na hapo tena nikatoa shauri kwamba niwaalike Unguja [Zanzibar] kwa ajili ya mkutano huo. Nikawaarifu ya kwamba nilikuwa safarini nakwenda Egypt, lakini wenzangu huko

Page 276: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tano244

Zanzibar watatengeneza kila matarayisho yanayohitajika kwa ajili ya mkutano huo. Haitadhurisha kitu mimi mmoja ikiwa sipo. Safari yangu ya Egypt ilinichukua miezi mingi kukaa huko. Na kwa kutokana na taakhira hiyo huku nyuma Nyerere akauteka nyara ule mkutano. Badala ya kufanywa Unguja, Zanzibar, akaufanya Mwanza, Tanganyika, na hapo ikapatikana sura katika ulimwengu kuwa Nyerere ndie alieanzisha kuundwa kwa PAFMECA. Lakini ukweli ulikuwa ni Zanzibar ndio iliyoanzisha fikra ile ya ule mkutano wa mashirikiano na ulikuwa ufanywe Zanzibar. Mimi kule Misri nilichelewa sana kupata fursa ya kuonana na Gamal Abdel Nasser aliyekuwa Rais wa Misri. Nilipata taabu sana ya kupata fursa ya kuonana naye. Nafikiri ilipita kiasi ya miezi mine nimo kusubiri tu kupata miadi ya kumuona, lakini nilipopata kumuona njia zote zilifunguka kwa upesi na wepesi. Wakati niko chumba cha wageni nangojea zamu yangu ya kuingia ofisini mwake kumuona, seketeri wake aliniambia unazo dakika kumi na tano tu za kuonana nae kwa sababu memba wa Baraza la Mawaziri wanangojea kufanya mkutano nae. Na ni kweli—maana nilipokua naingia kuonana nae nimewaona wako katika chumba kingine wamekaa. Ilipofika dakika kumi na tano alikuja yule seketeri kumkumbusha Abdel Nasser kuwa wakati wake umefika wa kuonana na Mawaziri ambao walikuwa wakingojea. Gamal Abdel Nasser akamjibu awambie wangojee zaidi. Watafurahi kuyasikia haya anayoyasema ndugu yako hapa. Mazungumzo yetu yalimchukuwa mbali kabisa katika mawazo mpaka nikamuona machozi yanataka kumtoka. Kabla ya kumalizika mkutano akanambia atanipa scholarship [nafasi za masomo] kwa vile nimekwenda kuwaombea watoto wetu fursa ya masomo. Sikwendea jambo jengine lolote. Zanzibar kulikuwa hakuna nafasi za kutosha za masomo ya juu. Secondary schools zenyewe zilikuwa hazitoshi Zanzibar na baada ya masomo ya secondary school kulikuwa hakuna masomo ya juu zaidi Zanzibar katika wakati ule. Tulikuwa tukiokoteza misaada ya udohoudoho kutoka nchi zingine. Pale pale akanambia, atanipa scholarship arubaini za wanafunzi kwenda kusoma Egypt na watawalipia gharama zote, chakula, nguo na gharama zinginezo. Watasoma mpaka wachoke wenyewe. Vilevile akanambia atanipa idadi ninayotaka ya walimu wa kwenda kusomesha Zanzibar na pia watawalipa wao mishahara yao lakini sisi tuwape makaazi—yaani nyumba za kukaa. Kwa hivyo alinitaka nikashauriane na wenzangu jinsi ya kutayarisha nyumba za walimu. Ama kuhusu zile scholarship arubaini za wanafunzi kwenda kusoma Egypt, pale pale mimi nilimwambia Abdel Nasser kama sisi Afrika Mashariki tuna desturi ya kufanya mambo yetu pamoja, pamoja na wenzangu kwa hivyo, nakuomba uniruhusu katika hizi scholarship arubaini, tuwagaie Tanganyika na Kenya. Sikuitaja Uganda kwa vile wao walikwisha kuwa na wanafunzi ishirini na tano tayari wanasoma kule Misri. Jibu lake lilikuwa nimekupa wewe hizi scholarships basi wewe na wenzio fanyeni mnavyotaka. Mazungumzo yetu yote yalituchukuwa dakika sitini, na dakika kumi zingine za

Page 277: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Fikra za Kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki 245

kuagana na kupiga picha. Niliporejea Zanzibar niliwakabidhi scholarships hizo Parents Association [ Jumuiya ya Wazazi] wazigawe kama wanavyoona inafaa kwa maslaha ya nchi zetu, Zanzibar, Tanganyika na Kenya. Wakatangaza kutaka watu kutoka Kenya na Tanganyika wanaotaka kusoma. Watu walitaka, lakini kwa kinyume cha chini­kwa­chini alizuka Kenya mtu mmoja aliekuwa akiitwa Francis Khamisi ambaye alikuwa mwanasiasa wa Mombasa, na Nyerere nae kwa upande wake (vilevile chini kwa chini) wakawa wanaziambia serikali zao kwamba hatari sasa imekuja hii. Watu watakwenda Misri na wanafunzi hao watakaporejea watakuwa wanawapendelea Waarabu. Nchi zetu zitachukuliwa na Waarabu. Hivyo basi serikali ya Tanganyika, serikali ya Kenya, za Waingereza, sio za wananchi katika wakati ule, zikatoa marufuku hapana rukhsa kwenda mtu Misri. Zanzibar serikali haikuweza kufanya hivyo kwa sababu ya makhusiano ya asili na asili na Misri. Hawangaliweza kufanya hivyo kwa sababu ya makhusiano ya asili na jadi na Misri, tangu zama za zamani za Uislamu na Al­Azhar walipokuwa watu wanakwenda na kurudi baina ya Zanzibar na Misri, bila ya pingamizi ya aina yoyote. Baada ya kwenda watoto na kusoma Cairo, ikawa Misri itayari kujenga University [Chuo Kikuu]. Na University tuliotaka sisi kujengwa Zanzibar ilikuwa ni ya Waislamu wa Afrika ya Mashariki na ya Kati.2 Hatukutaka kuifanya kuwa ya Zanzibar tu. Misri ilikuwa tayari kusaidia na pia hata America alikuwa tayari kuchangiya kusaidia Teachers Training katika University hiyohiyo iliokuwa iwe ya wanafunzi wanaume na wanawake. Lakini mara tu baada ya kupata uhuru wetu tukapinduliwa baada ya mwezi mmoja. La kwanza walilolifanya Nyerere na Karume ni kwenda Misri wao wenyewe na kudai kwa Abdel Nasser avunje misaada yote aliotuahidi sisi na si kama aliahidi misaada ile kwa serikali ile tu, bali alikuwa tayari kuitoa hata kwa serikali yao lakini wao hawakutaka kuwa na mahusiano yoyote na Misri. Walilolitaka ni kwamba wanafunzi walioko Cairo warudishwe. Wakati Abdel Nasser akitoa scholarships vilevile akaweka nyumba ya wanafunzi wa East Africa na ndio ikawa sababu ya nyumba ile aliyoitoa kufanywa bweni la kukaa wanafunzi wakaiita “East Africa House”, kwa madhumuni ya kwamba msaada huo wa nyumba utawafaa watu wote wa Afrika ya Mashariki siyo Zanzibar peke yake. Lakini kama walivyotaka Nyerere na Karume, wanafunzi waliokwishakuwa tayari wanakaa katika nyumba ile, wakakamatwa kwa nguvu na kurudishwa makwao na nyumba ile ikafungwa na mpango wote ukafisidika. Sijui namna gani, Nyerere alikuwa anacheza mchezo huku na huku, bila ya kumtambua. Huku kwa dhahir alipigania kuwepo East African Federation. Tukakutana Dar es Salaam. Wakati huo sisi hatujapata uhuru wetu lakini Tanganyika ilikuwa wapo katika Serikali ya ndani. Basi tukakutana Dar es Salaam. Kutoka Zanzibar nilikuwa mimi na Dr. Baalawy na Attorney General wetu, Australian, Mr. Rumble aliekuwa mshauri wetu wa mambo ya sheria. Na chairman alikuwa Oscar Kambona ambaye siku zile alikuwa bado hajagombana

Page 278: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tano246

na Nyerere. Yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanganyika. Na mshauri wake [Nyerere] ndie alotengeneza kila kitu, George Brown, Mngereza. Sisi tulikuwa tumelikubali lile shirikisho lakini katiba walioitaka wao iwe tuliiona haifai kwa sababu nguvu zote zilikuwa zinampa mtu mmoja au nchi moja na ilikuwa dhahir kwa kuwa itapata Tanganyika na Raisi wake Nyerere. Sisi tulolipinga siyo Shirikisho lakini hilo la nguvu zote kupewa nchi au mtu mmoja. Hili ndilo tulokuwa tunapinga. Zanzibar na Uganda ndio waliokuwa wakipinga. Kenya ikawa wamekaa kimya, wanaachilia tu. Hata, Charles Njonjo aliekuwa Attorney General wa Kenya, alikuwa takriban anasinzia tu, hashughulikii. Na Kenyatta alisema baada yake, sisi hatutaki Shirikisho, hatutaki chochote, tulikuwa tunawahadaa tu. Nyeyere aliposhindwa kupata ukubwa kwa nafsi yake kwa njia ile alioshauri katika katiba ndio akatumia mabavu. Uganda, alikuwepo Godfrey bin Issa, kama Attorney General na mwengine Kioni alikuwa bin ami yake Obote lakini yeye Muislamu shadid, kakaa pale na translation [tafsiri]ya msahafu (Qur’ani). Wao walikuwa shadid sawasawa na sisi. Walikuwa hawataki nchi moja iwe na nguvu za utawala peke yake kuliko wengine. Lakini baada yake ikaonekana kuwa ndio sisi wapingaji. Sijui kama hii ni moja ya sababu hiyo au sababu nyengine zipo lakini tukajapinduliwa. Serikali yetu ikapindiluwa na wale wapinzani wetu wakatumiwa wakawa ndio serikali mpya ya mapinduzi ambayo ilioachilia kuundwa Tanzania. Na Zanzibar nchi ilokuwa huru na Tanganyika ilokuwa huru zikawa zimekwisha ikaundwa Tanzania. Sisi tuliosoma Uganda tulipokuwa ndani gerezani Dar es Salaam pale Keko, mimi, na Dr. Baalawy, na Maulidi Mshangama, na Seleman Said, tulisema yoyote atakaetoka hapa gerezani mwanzo ende haraka Uganda akawatahadharishe wao watakuwa wa pili, maana yake inaonekana kwamba sisi hatutakiwi kwa sababu nchi yetu ina mfalme na kwa hiyo ndio imezwe, na wa pili itakuja kuwa Uganda. Hatukuwahi kufunguliwa yoyote katika sisi, mara ikawa Kabaka kule akapinduliwa na Uganda yenyewe ikapinduliwa yote na wafalme wote wakawa si kitu, si chochote si lolote na akasimamishwa Obote. Kabla ya hii fikra ya kuundwa Shirikisho la East Africa, kulikuwapo na “East African Common Service Organisation”. Nchi zote za East Africa zilikuwa pamoja katika mambo ya kibiashara. Sarafu ni moja, postal service [huduma ya posta] ni moja, isipokuwa Zanzibar ilikuwa haimo bado katika huduma ya posta. Na custom [mizigo] ni moja lakini Unguja [Zanzibar] ilikuwa forodha yake bado haijaingia. Lakini zilobaki mambo mengi ya siha, ya afya, ya research [utafiti], na railway [reli], na aeroplanes [ndege] yalikuwa pamoja. Ilikuwa ndege za East Africa Airways zikenda East Africa kote, hata Zanzibar. Na sarafu, shilingi ya East Africa ilikuwa na nguvu. Shilingi ishirini za East Africa kwa pound moja sterling [ya Kiingereza]. Ghafla, katika mkutano wa Mawaziri wa fedha uliokuwapo Zanzibar, Waziri wa Tanganyika akawaambia wenziwe wa nchi nyengine za Kenya

Page 279: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Fikra za Kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki 247

na Uganda na Zanzibar, kwa sababu sisi tunakwenda mwendo wa Kisoshalisti, wa kijamaa (wanavoita wenyewe), na nyinyi mnakwenda kibepari, basi hatuwezi kuwa pamoja kwenye mambo ya sarafu. Sisi tunatoka katika sarafu tuwe na sarafu yetu wenyewe. Walipata mtikiso mkubwa wale Mawaziri wa East Africa. Hawakutarajia yale. Hapa ndipo ilipovunjika East African Currency Board pamoja na kuanguka shilingi ya Tanganyika na khasa ikaanguka zaidi kwa sababu wao ndio waliokuwa maskini zaidi. Wao wanaojigamba kujenga, wakati mwengine wao ndio huwa wavunjaji—mjengaji ndie mvunjaji. Lakini sasa alhamdulillah inaonekana hapana viongozi wenye tamaa ya ubinafsi ya kutaka kutawala East Africa nzima au Afrika nzima mtu mmoja. Hapana katika East Africa, la Tanganyika, wala Kenya, wala Uganda, wala Zanzibar, mtu wa namna hiyo. Hao walokuwa wenye tamaa hizo wamejifia. Kwa hivyo, tunaweza kufikiri tena upya juu ya muundo wa Shirikisho na mustakbali wake. Mimi na wenzangu wengine vilevile, tunaona kuwa Shirikisho linaweza kuwa na maslaha sana sasa kwa sababu tumeona mifano ya nchi sehemu mbili kubwa zilofanya mambo ya namna ya Shirikisho, na namna ya Muungano. Na moja ni huu wa Ghuba [Gulf ] nchi za Khaleej zimekusanyika pamoja, zimefanya umoja wao na wamekaa kwa uzuri. Europe, nchi kadhaa wa kadhaa na zinakuwa kila siku, na mamilioni ya watu wamekusanyika pamoja vilevile. Wameweza kufanya namna ya Shirikisho. Na ziko nyengine. Bara Hindi [India] tokea hapo mwanzoni ni Shirikisho kwa hakika. States zao kadhaa wa kadhaa zina serikali zake zimo ndani ya muungano wa India. America ni mfano vilevile wa Shirikisho. Basi tunaweza kuona mifano hiyo ya watu wakakusanyika wakasikilizana East Africa. Kenya na Uganda, na Tanganyika na Zanzibar (nchi zilizokuwa zimetawaliwa na Wangereza kwa miaka) zikawa moja. Mwendo wao wa Kiingereza na lugha yao ya Kiswahili, imeenea na inaweza kuendelea zaidi. Imeanza pwani ya Afrika ya Mashariki na imeenea, na Tanganyika inaweza kusaidia sana kueneza zaidi uswahili wake. Na jambo moja jingine ambalo Tanganyika imeweza kufanya na inafaa ishukuruwe nikuondoa kutojuwa kusoma, kwa kufundisha kusoma watu wazima. Watu wengi sana sasa Tanganyika wanajuwa kusoma Kiswahili. Hata ukabila katika Tanganyika ni mchache kuliko kwengineko. Kenya, imeonyesha uhodari wake na uzuri wake wa ujirani mwema. Imeweza kutumia uwezo wake kusuluhisha ugomvi wa Sudan na Somalia. Haujesha kabisa lakini wamo katika kusuluhisha. Wamefanya kazi kubwa sana na wanafaa kushukuriwa. Hawakufanya wao kama alivyofanya Nyerere, watu wa Zanzibar hawapatani basi dawa yake ya kuwafanya wamoja ni kuwaua wengine. Kwa kufanya mapinduzi, na natija ya mapinduzi, ndio Zanzibar imedorora mpaka sasa haina kheri yoyote inayotengenea. Watu wakafukuzwa, wengine wakafungwa. Mimi ndio katika hao tuliofungwa gerezani zaidi ya miaka kumi bila ya kuhukumiwa. Wengi wengine wakauliwa kwa maelfu. Watu wakanyanganywa mali zao. Hapana hukumu, hapana chochote.

Page 280: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tano248

Lakini Kenya mpaka leo iko serikali na inayo mahakama zenye sheria. Kumiliki mali binafsi (private property) kunaheshimiwa. Vilevile, Uganda, Museveni baada ya kushinda amewaalika Wahindi wale waliofukuzwa na Idi Amin warudi na wakarudishiwa na mali zao. Wafalme walofukuzwa, kina Kabaka, na wafalme wengine wa Uganda, Bunyoro, Toro na Busoga wakarudishwa. Museveni akasema hawa si watu wa siasa. Hawa, ni mila yetu, ni mila yetu asli. Wakae, siasa zimo katika watu watakaochaguliwa katika serikali lakini hawa wafalme ni mila yetu na tuiheshimu. Kwa hivyo wamerejeshwa na heshma zao. Basi kila mmoja inayo jambo la kuleta faida. Sisi Zanzibar tuna nini cha kuleta? Sisi Zanzibar tunayo faida ikiwa tutapata uhuru wetu kamili na kuingia katika Shirikisho kwa kuwa ni nchi yenye kutambulika. Tukiingia kama ni nchi yenye kutambulika, kama Tanganyika, kama Kenya, kama Uganda, kwanza tutaipa nguvu hiyo Tanganyika yenyewe vilevile. Itakuwa sisi ni wawili badala ya kuwa mmoja, kuliko sisi kuwa ni mkia tu au tumemezwa na Tanganyika. Tunaburutwa tu. Kwanza itakuwa hapana imani ya Shirikisho lenyewe, tutakuwa kila siku tunataka kujitoa. Hivi sasa watu wengi hawataki kuendelea na huu muungano wa Tanzania kwa namna ulivyo kwa kutokana na vituko vya kumezwa na aibu zake. Basi ilioko khasa Zanzibar irejeshewe uhuru wake kwa sababu imepigania uhuru wake mbali na iliupata. Muingereza katoka na Zanzibar ikawa huru na pia ikawa nchi yenye kutambulikana katika Umoja wa Mataifa na ikawa na kiti chake na bendera yake huko. Ijapokuwa uhuru huo ulidumu kwa mwezi mmoja tu kabla ya kupinduliwa, lakini vilevile inajulikana wazi kwamba mapinduzi hayo hayakuwa ya halali na kwamba Zanzibar, kwa dahari na dahari ilikuwa ni nchi huru. Haikupatapo kutawaliwa katika taarikhi yake yote. Sasa Zanzibar ikiwa kama ni mkia wa Tanzania haitoleta faida yoyote. Lakini ikiwa huru inaweza kuleta faida nyingi na kubwa. Hii ni kwa sababu Zanzibar inayo mahusiano ya asili­na­asili na nchi nyingi nyingine. Inayo mahusiano na Oman, Yemen, Misri, India, Pakistani, Sri Lanka, Indonesia, Iran, na nchi nyingi nyingine. Kwa mahusiano haya ya wema baina ya watu wa Zanzibar na watu wa nchi nyingine; na Zanzibar ikaja ikapata nafasi yake kuingia katika Shirikisho hilo ikiwa kama nchi huru yenye kutambulikana, basi inaweza kuleta faida nyingi na kubwakubwa katika kuineemesha Afrika ya Mashariki kiuchumi na kisiasa na hata ikawa ndio chanzo cha kuleta Shirikisho la Afrika yote kwa kutokana na mahusiano mema ya watu wa Zanzibar na ulimwengu wote kwa jumla. Itakumbukwa kwamba katika miaka arubaini hii ya tangu mapinduzi Wazanzibari wengi wamezagaa ulimwenguni. Na wengi wamesoma na wana ilimu za juu mbali ya wale ambao wamekwisha tajirika. Wapo vilevile wenye experience [ujuzi] za kazi kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu. Wote hawa watakuwa tayari kuchangia katika hilo Shirikisho la Afrika ya Mashariki kama tu itaonekana ipo insafu na itatenda haki kwa Zanzibar.

Page 281: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na SitaWagawe, Wasahaulishe, Watawale

Historia ya Algeria inaendelea kufunguka: kila rika ni lazima lianze tena upya kubuni kila kitu, kwa sababu tabaka ya watawala inachukuwa sura tafauti lakini bado haioneshi sura ya kubadilika, na haijali kuwacha kumbukumbu yoyote ya mpito wake, kama kwamba lengo lake la msingi la kisiasa ni kuwa ni rahisi kuwatawala watu waliopoteza sahau. —Ghania Mouffok

Mzee Issa Kibwana

Hawa wana ila moja. Hawasomi historia. Wale wanajuwa mwanawe yumo mle anasoma alif, be, te, basi, kamaliza. Lakini hawasomi historia. Mawaziri wetu wote! Wawakilishi, wabunge. Hawasomi kitu hicho. Hata! Kwamba hawaki­pendi. Hawapendi kumbukumbu. Nadhani zilikuwepo kumkukumbu nyingi pale. Wengi wao waliamua zikachomwe moto. Kwa jicho langu hili na mashikio yangu haya. Wenyewe hawataki. Kabisa! Hiyo kitu kweli. Hawataki. Mtu yoyote unomsikia huyu mbunge, huyu muwakilishi, ukimuuliza suala kama hili mwishoni atakwambia “kwani nishughulike nalo lina mana gani na mimi?” Hilo ndo jibu atakalokujibu. Lina mana gani na mimi? Sina mana nalo mie kwa vile hana haja nalo kulishughulikia. Linataka mtu anojuwa hatma kunakuja nini? Kizazi changu kitapata nini? Yule ndo atoshughulika na jambo hilo. Yeye kapata nyumba zake mbili tatu, anajuwa watoto zangu washarithi basi. Hana haja ya kumbukumbu. Kwa vile bwana kumbukumbu hizo pana watu wanazijuwa na pana watu hawazitaki kuzijuwa! Sasa utakuta wengi hawazitaki. Kidogo wanazitaka.

Mzee Mchingama

Nataka niongezee. Labda kasumba hii pia ilitokea katika kipindi, sisemi kwa nia mbaya, kwa vile tuko katika mfumo wa vyama vingi na wewe humo katika mambo haya, lakini alokuwa Waziri Kiongozi huyu Maalim Sefu, alichochea kufutwa

Page 282: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Sita250

kwa historia. Kwa sababu mashuleni pia ilikuwa imetolewa historia, Maalim Sefu alipokuwa Waziri wa Elimu. Kwamba alifuta kwamba lisikuwemo somo la historia. Alifuta. Kwa mana hiyo bila shaka alikuwa na lengo maalum kwa sababu watu wakijuwa historia wanokotokea inaweza kuleta muamko fulani.1 Kwa hivyo ikabidi imezama kabisa historia ya Zanzibar haikupatikana. Moja ilochangia hiyo. Ikawa somo la historia halijapewa umuhimu. Na kwa hivo hao viongozi walioko sasa hivi na wamekulia katika masomo hayo hawawezi kuelewa historia yoyote kwa sababu historia hiyo ilikwisha futwa. Lakini sasa hivi nashukuru kama hivo nyinyi vijana mmepata muamko wa kutaka kutafuta historia chimbuko. Mmefanya jambo la busara kuwawahi hawa wazee kabla hawajaondoka, hawa­jamalizika. Kwa hapa nafikiria tumpate huyu Mheshimiwa Ramadhani Haji, Mzee Natepe, akina Amboni Matias, Joseph Bhalo. Hawa nafikiria watakuwa wanazifahamu vizuri tu kwa sababu ni washiriki.

Mzee Isa Kibwana

Nawaambia ilokuwa ofisi ya Afro­Shirazi pale Kijangwani tuifanye makumbusho au tuifanye tawi la CCM. Jibu: ah! Hili bwana, jumba hili, labda sasa hivi tuwaambie hawa jamaa kwa sababu eneo hili lote limechukuliwa na posta. Ndo jibu nnopewa. Na kumbe posta haihusiki na jumba lile! Lakini wao wanakwambia linahusika eneo lote hili la posta. Ndo jibu wanokujibu. Lile chimbuko la historia safi kabisa! Ndo shina hasa!

J. J. Mchingama

Mawazo yao yako wapi wakati wanakuja watalii wanawapeleka kwenye makumbusho mengi ya zamani. Historia ya utumwa, au historia gani…mbona wanawapeleka!? Kwanini basi pale wasipelekwe watalii wakaonyeshwa kwamba hapa ni pahala penye chimbuko la ASP? Lakini ni watu kufanya ubadhirifu, ni kupuuzia jambo ambalo kwa kweli kwa wakereketwa khasa linaskitisha. Lile jengo lisingekuwa la kuweza kuvunjika. Nafikiria kwamba labda vijana hawachukulii umuhimu wa haya masuala. Wanataka kuongozwa. Labda mwenye kuwaongoza, mwenye nguvu zaidi hayuko na hao walioko wakitoa ushauri hawendi mbali. Wanaona kama huyu analeta kitu cha upuuzi. Lakini ukweli ni kuna mambo mengi ya historia ya Zanzibar yanayohusu ukombozi wa nchi hii, mapinduzi ya nchi hii, yanatupwa na yanakufa. Yanakufa kabisa. Jambo ambalo linaskitisha. Unapofanya ukumbusho au kuchukuwa historia hatuna mana kulipa visasi. Tuna maana kuvikumbusha vizazi vijavo wajuwe asili yake alipotokea na nchi hii. Ndo shabaha kubwa. Lakini sasa watu hawajali hivo madhali anapata maslahi yake basi. Inatosha. Hayo mengine wanaona kwamba yataleta uchochezi, yataleta

Page 283: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Wagawe, Wasahaulishe, Watawale 251

vurugu, labda mawazo yao yako hivo, jambo ambalo linawafanya waone bora mambo yaachiwe hivihivi.

Mzee Isa Kibwana

Mashamba yote hapa Unguja yalikuwa ya Waarabu. Mashamba yote ya Wamanga.2 Sasa unakwenda lima weye kwa hii hekaheka ya mambo ya kisiasa ikabidi tuanze kuchukiana. Wenye mashamba na mkaazi alokuwa kwenye shamba lile. Unachokipanda huitwa watu wanaitwa “Maburuki.” Huambiwa “kangowe mhogo ule, tupa! Kangowe mpunga ule, tupa!” Unangolewa, una­ tupwa. Asubuhi unakwenda unakuta peupe, ardhi mtupu. Wapi utakwenda sema. Huna. Ndo ngoma yenyewe ilipoanza. Huna mahala pa kulia. Kulia kwako utamtafuta Mzee Karume yuko wapi. Kwa sababu ndo mkuu wa chama chetu. Utakwenda utakutana nae uzuri sana na atakujibu maneno mazuri sana. Atakwambia hivi: kama wewe unanifuata mie, mimi hayo yananipata lakini nastahmili, na wewe ustahmili. Allah mwenyewe anajuwa. Iko siku hamaki zako, wahka wako na nini, utapoa. Endelea kustahmili. Kwa vile tunaendelea, 55, mpaka 56, 57, 58. Tumo katika shughuli hizo. Hapa Unguja yote. Hakuna shamba hata moja wasiofanya vituko hivo. Zaidi ilikuwa hasa, zaidi zaidi, kutoka Kinduni, Donge, Muwanda, mpaka unakwenda Potowa yote ile, unakwenda zako Kilombero alikotununulia shamba Mzee Karume. Ile yote ilikuwa kazi yake ni hiyo. Kwa ile watu wanavomwendea yule bwana ikabidi afanye kula njia apate shamba la kuwapa wanachama wake. Kwa vile alifanikisha mwaka 1959 kununuwa shamba hilo la Kilombero. Mwaka 59 ule baada ya kulipata lile shamba aliweka mkutano mzuri sana hapa Maisara. “Jamani wanachama wangu nimenunua shamba. Kwa vile mtu yoyote anoona mambo yamemzidi pale anapokaa wako wasimamizi kule Kilombero, aende atafutiwe mahala pa kulima. Hakuna kodi. Kodi yako jembe lako ulime mwenyewe.” Kwa vile jamaa wengi wakahamia kule kwa kulimalima. Kwa vile mie nilikabidhiwa kwa yule bwana na sina kazi hata moja akaniita “njoo.” Chukuwa basikeli hii, lakini baiskeli yenyewe ilikuwa dungudungu. Mimi mdogo kuliko ile basikeli. Wewe utakwenda Umoja wa Vijana kazi yako kuchukuwa magazeti wende unauza hukohuko mtaani kwenu. Nikawa mimi muuza magazeti. Lakini magazeti yangu yale yana tija kwa mie. Yana kujuwana na watu wa mitaani kote. Gazeti lilikuwa la “Kipanga”. Nikatembea nalo gazeti la Kipanga kama miezi mitatu. Likaja gazeti jingine kubwa. Linaitwa nani? “Tai.” Ni mnyama mmoja ana mdomo mkubwa kama kasuku hivi kakamata jiwe anaruka nalo. “Sasa wewe muuza magazeti ujuwe tafsiri hii manake nini.” Nikawekwa mie kitako. “Unajuwa fasiri yake hii nini?” “Karume anangowa serikali ya Kiarabu. Ndo huyu. Hili jiwe serikali, huyu kipanga ndo Mzee Karume anaondoka nae kwenda mtupa baharini.” Sasa imekuwa mie hadithi yangu “kipanga sasa

Page 284: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Sita252

anawachukuwa watu anakwenda kuwatosa baharini. Litazamane gazeti la Tai na Kipanga!” Sasa wengi walio vijana… e bwana nletee…Tena bei yake senti kumi. Halafu nna umaarufu kwa Wamanga. Wamanga umaarufu wangu umekuja vipi. Mimi nilikuwa na nguvu nyingi. Basi tulikwa na Mmanga mmoja Kitope pale, anaitwa Abdul Salaam Yusuf. Yule kazi yake kukodi karafuu. Sasa mahala popote alipokodi karafuu lazma aje anchukuwe mie. Muanikaji mie na mimi ndo mbebaji magunia ya karafuu kwenda kuuzwa. Alikuwa ananiamini uzuri sana. Lakini alikuwa ananambia “wewe bwana, mtu wa Karume lakini nakuona mie mtu wangu. Panapo kazi yangu na mie nsaidie.” Namwambia “nakusaidia.” Kumbe Mwenye Enzi Mungu yote anasema “hii ndo inokupa umaarufu kwa huyu Mmanga huja ukapata kitu kwake.” Ikiwa inakuja habari ya karafuu mimi nlikuwa nakwendachukuwa magazeti. Sasa pale kambini watu wananyambuwa karafuu mimi nauza magazeti. Nauza magazeti, nachambuwa karafuu, nauza karafuu. Tunaendelea. Karafuu zimekwisha. Sasa jamani eh! Mambo yamekuja sawa. Huyu bwana keshapasi kupata serikali. Bendera yake ishapasi. Sasa nnachokuombeni, ile nnokwambieni mstahmili ndo ileile. “Sasa mhakikishe tunapata serikali.” Mpinzani wetu Mzee Yusuf Himidi yupo pale. “A! Sasa tuta pata vipi?” Mzee Karume akamjibu: “Kitu kinakujia miguuni kwako bado tena unataka kukisoma!” “Hapana Mzee, tunaiyona hali yenyewe…haya bwana twendeni.” Wamekwenda kwenye Baraza la Kutunga Sheria baada ya kumaliza lile baraza lao, anakuja Karume anasema “imepasi Ali Muhsin tarehe 9 Disemba anapewa serikali yake. Bendera yake tarehe 10 inapanda. Sasa mfanye mipango hii serkali isitoke nje watu wakaijuwa. Ife kabisa. Mimi naanza kuiuwa hukohuko Ulaya.” Sisi, Mzee Kaujore, Yusuf Himidi, na wengineo, sasa tuko Upenja msituni kule. Humu midomo yetu yote imeoza. Chakula chetu mananasi mwitu. Au wale wanavijiji wa Upenja kwa vile wanafahamu shabaha ile wakituletea vyakula kule msituni lakini vyakula vyenyewe si vyakula. Tumejikalia kule tunafanya mazoezi yetu. Taarifa Mzee Karume alivokwenda kule Ulaya akauliza. Mwenye kupewa serikali kuna serikali nyengine inamuongoza? Hakuna. Sasa pale pana Sultani na pana serikali ya Kiengereza. Hizi serikali zote zinakuwa wapi? Jibu, hizi serikali zote madam zinatiwa saini hapa, hizi serikali zote hazipo. Itakuwa hiyo ya Ali Mushin peke yake. Ali Mushin akasema Sultani ntamuhifadhi, Mngereza ende kwao. Karume anasema: “Kuanzia leo tunatia saini Mngereza umetowa mkono wako Zanzibar. Humo tena. Chochote kitakachotokezea humo. Tukubaliane.” “Karume maneno yako sahihi. Kuanzia hivi sasa tukitia saini Balozi anakwenda zake Zanzibar anakwenda zake hamisha vitu vake,” anasema Ali Muhsin. Yule bwana alipiga makofi makubwa sana pale. Karume alipiga makofi makubwa sana. Hawajui shabaha ya yule bwana shabaha gani. Kumbe yule bwana si msomi lakini

Page 285: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Wagawe, Wasahaulishe, Watawale 253

kasoma kweli, kichwa chake. “Sasa nyinyi mipango yetu vipi serikali tutaipata hii.” “Kitu rahisi. Sie tu­mejiandaa. Sisi tuko wengi. Hatuna tatizo kuchukuwa serikali. Dakika tano tu tunachukuwa serikali.” “Haya fanyeni kazi yenu.” Makunduchi haimo. Mikoa miwili tu: Mjini Magharibi na Kaskazini. Hawa watu ndo wanojuwa mambo ya mapinduzi. Ndo watu washiriki wa mambo ya mapinduzi. Japokuwa huko Makunduchi wamo lakini nadhani utampata wa kuokotea. Mwalimu Hanga asubuhi walikuwa na msimamo wao kama mpinzani, wanapinga pinga ile. Wanampinga yule bwana—Mzee Karume. Kwa ukaribu sana hawakuwa naye. Walikuwa naye tu. Lakini msimamo wao ulikuwa wa peke yao. Hanga, Othman Sharifu…wamo tu kama bendera. Mzee Karume muongozi wa mapinduzi. Huyo anaozungumza kuwa mzee Karume hayumo ni muongo. Hao ndo hao walokuja katikati yake wakaanza kuligawa jeshi la kimapinduzi mafungu matatu. Kuna fungu moja lilikuwa Mchangani alikuwa nalo Mfaranyaki. Kulikuwa fungu moja liko Pemba. Ali­kuwa nalo nani? Alikuwa nalo Okello. Kulikuwa fungu moja lipo hapa Mtoni. Hilo ndo lilikuwa fungu la Mzee mwenyewe Karume. Hilo ndo lenye kujuwa mambo hayo. Mfaranyaki alikuwa ameshajitenga. Yuko Chwaka na kikosi chake kamili. Anasema askari wangu yoyote alokuwa yuko kwenye kambi yangu hana haki kwenda mjini. Akitaka bibi mnao humuhumu ndani ya kambi yetu. Mimi nilikuwa niko Pemba. John Okello kakalia kisima cha pesa. Tena wapi? Mkanjuni, nyumba ya kasuku, kwamba yeye mpinduzi mkubwa! Ndo aloyapanga mapinduzi hasa! Mfaranyaki anazungumza Chwaka. Anasema: “watu wanasema tu kwamba Karume ndo anojuwa mapinduzi, ndo muongozi wa mapinduzi. Mapinduzi yangu! Kundi langu! Kwa vile sasa hivi najiandaa kuingia ndani ya mji.” Vile vitatange, kwenye kundi lake vimo, kundi la Pemba vimo. Haraka vinamletea ripoti huyu bwana—Karume. “Bwana, Chwaka kuna jambo kadhaa, kadhaa, kadhaa. Jambo hili unalijuwa?” Anasema “silijuwi.” “Siku mbili tatu huja ukasikia yameanguka mapinduzi mengine tena hapa. Kwa vile tufanye utaratibu.” Ndo hao unaowasema, kwamba kuna watu wanazungumza hiki kikao Karume kaweka wapi? Watu wenyewe nshakutajia. Mmoja Chwaka, mmoja Pemba. Unguja yuko mwenyewe. Sasa harakati za kwanza tumchukuwe huyu alokuwa karibu—Chwaka. Katumwa Khamisi Daruweshi, Saidi Washoto, Idi Bavuai, Yusuf Himidi, Sefu Bakari, na Makomred. Mfanye kula njia. Huyu mtu [Mfaranyaki] ana silaha kule. Mfanye kula njia mumkamate. Atatuharibia huyu. Mchango wake Mzee Karume wa kwanza kwamba yeye ndo alokuwa akitumia ndani ya Baraza la Majlis Tashrii. Halafu mtu mmoja yule katika kisiasa chake baada ya kuamkia kwamba sasa serikali ishapatikana kwa hawa jamaa, yeye ndo alotowa mchango mkubwa kwa kumfukuza Mngereza na serikali ya Sultani. Kama si Mzee Karume kwenda Ulaya na Ali Musini nadhani pangelikuwa na kazi hapa!

Page 286: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Sita254

Serikali isingepinduka. Mchango wake kwanza mkubwa yeye ndo alokwenda muondowa Mngereza. Karume. Kumbe tunakubaliana mimi mpinduzi Karume lakini serikali hii ya Kiengereza ianze kuhama. Isiwepo pale. Ili tupate nafasi huyu bwana kutandika serikali yake. Mie Karume mpinzani. Mngereza ndo nguzo yake atamlinda mtu huyu. Sasa suala lile kalikubali na Ali Musin kwamba kweli maneno unosema. Huu mchango mkubwa. Tuliuamini sisi sote tuloshiriki kwenye mambo ya kisiasa na mapinduzi. Hili suala tulikubali. Angekosea yule bwana (Karume) mapinduzi yasingekuja. Yasingekuja. Yasingekuja kabisaa! Bwana, mimi nilikuwa, hao watoto hawatambui…lakini mimi nadhani nilikuwa begani kwa Mzee Karume. Yanazungumzwa na mimi niko begani kwa Mzee Karume. Wanapeana picha. Mzee Kaujore ndo alokuwa mshirika wake hasa! Idi Bavuai ndo alokuwa mshirika wake hasa! Saidi Washoto ndo mshirika wake hasa! Ramadhani Haji. Hawa watu maisha kundi lao ni moja. Bwana mimi nakataa kutupiwa watu wa bara. Mapinduzi ya Zanzibar hayana mmoja. Kila mwanachama wa Afro­Shirazi Party ni mpinduzi wa Zanzibar. Hakutoka mtu nje kuja kupinduwa serikali ya Zanzibar. Kama nnavokwambia, sisi wengine wote tumetoka huko nje. Na ukiizungumza sana, hata hao wote walokuwa wakiitwa Memba wa Baraza la Mapinduzi (MBM) hakuna hata mmoja anojuwa kwamba ametoka bara. Wote ni watu wa hapahapa, ambao hakika, jadi yake yote iko bara, lakini yeye mwenyewe ni mtu wa hapa. Hakuna mtu alotoka bara kujapinduwa serikali. Hakuna. Hakuna. Bwana, hapa palikuwa na miji miwili, hii miji ndo ilokuwa inatisha, inampa nguvu Sultani. Mji wa kwanza Bomani hapo. Mji wa pili Mtoni. Ambapo silaha zote zile ziko sehemu hizo mbili. Mtoni na Bomani. Washiriki, mkusanyiko wa washiriki—Chumbuni. Kama nilivozungumza mwanzo, Kusini hawajuwi. Mjini Magharibi, Kaskazini. Hao ndo watu wanojuwa. Mapinduzi hasa ni ya watu hao. Na wapinduzi hao hakuna Mmakonde, hakuna Mmanyema, hakuna Mturuki, hakuna nani. Yoyote anokubali kwamba kuna madhila ya Mmanga, kashiriki mapinduzi. Hakuna Mmakonde alotoka huko, au Mruguru alotoka huko kwamba nakwenda Zanzibar kushiriki kwenye mapinduzi. Yaliomkuta hapa kashiriki. Mzalia alokuwa tatizo hilo analo kwamba hili dhila tulonalo, kashiriki. Wako wengine majina siwataji. Tumewafuata milangoni mwao na kuwaambia na wakasema “mimi Muisilamu siuwi”.3 Wapo hapa na ndo wazalendo wa hapahapa. “Siuwi tena mkome kunijia kwangu.” Anaingia mvunguni. Wapo hapa. Baada ya kumalizika suala hilo yeye ndo wa kwanza kupata jina la “MBM.” Wengi tukakaa tukacheka hasa. Tena humwambia hivihivi. “Wewe jina hili umelipata wapi? Wewe si ulisema wewe kwamba hutaki kuuwa? Leo umelipata wapi jina hili. Lakini haya na tuendelee. Tunakwenda naye.” Kwa vile bwana mtu anokwambia kwamba wametoka Wamakonde kuja kupinduwa serikali Zanzibar, hiyo mimi nakataa mpaka mwisho wangu. Baada ya kupinduwa Mtoni na Bomani, watu wote mkusanyiko ulikuwa Raha

Page 287: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Wagawe, Wasahaulishe, Watawale 255

Leo. Raha Leo walikuweko watu wa sehemu zote za Unguja hii na wanatambua kwamba mahala fulani pana watu flani, hawa wapinzani wetu wakubwa. Siku ile bunduki zilikuwa hazizuiliki pale ndani. Na mfundishaji yuko mlangoni. Mfundishaji nani? Juma Maneno, Anthon Musa, na Natepe. Wale wako pale, kazi yao wanachukuwa bunduki ndani unaambiwa “Fanya hivi. Risasi tia hapa. Haya piga. Piga juu, piga juu. Buuu! Ushajuwa. Haya, nenda!” Sasa unakwenda weye unamfuata fulani, huyu ndo akiniadhibu mimi kwenye shamba lake. Sasa atakiona huyu! Anakuona wewe, bunduki lako umelitia ndani ya kanzu au shati. Hajui. Mauwaji yakaingia sasa. Mji mzima utasikia hapa wamekufa watano, hapa wangapi. Wale wale wenyewe wanotoka mashambani mle. Wenye hamaki vyakula vyao vilikuwa vikingolewa. Hawa ndo waloleta mauwaji hayo ya kulipiza kisasi. Mpaka akaja mwenyewe Karume akapanda juu Raha Leo. “Jamani basi, serikali tushapata, msiuwe watu mashamba humo! Basi, basi, basi. Bunduki haraka zirudishwe. Mnohusika mchukuwe watu wenu mrudishe bunduki.” Ikasimama sasa, cabinet [kikundi] nyengine mpya ya kwenda Pemba. Wanatakiwa watu kwenda Pemba kwa sababu Pemba msukosuko watu wanasikia tu lakini haujaingia. Wakachukuliwa jamaa hapa. Haraka nendeni zenu Pemba. Karume anazungumza. Hakuna kuuwa mtu. Nendeni kwenye mapolisi mle kwa sababu polisi wamo watu wasije wakatuuwauwa. Kwa vile kachukuweni zile bunduki. Mzee Kaujore, Yusuf Himidi, Sefu Bakari, Mzee Natepe, chaguweni watu wa kwenda Pemba. Wakachaguliwa watu. Kiongozi wao nani? Anthony Musa. Miji mingapi kule? Miji mitatu. Kombo Juma Kombo, simama hapo kwa Mzee Anthony. Isa Kibwana Sanze, simama hapo kwa Mzee Anthony. Feruzi Kayanga, simama hapo kwa Mzee Anthony. Mzee Anthony watu hawa tunakupa na tutakupa na askari. Kugawa kwako unajuwa mwenyewe huko unakokwenda. Miji mitatu tumekupa viongozi watatu. Meli iko pwani. Makofia tunaazimiwa, yale makofia ya chuma kwamba tujulikane asikari. Utakuta suruali ya asikari, shari la kiraia. Au utakuta shati la kiraia, suruali ya polisi. Tukatiwa ndani ya meli. Tukafika Pemba. Tumefika Pemba saa ngapi? Saa saba ya usiku. Lakini bahati mazungumzo tumewakuta watu maalumu wanatungoja. Tumewakuta watu wanasema hao watu wanokuja wasikae katika mji hapa. Wapelekwe wapi? Kigomasha! Mnarani, msituni, mpaka amri ije kutoka Zanzibar ya kuingia ndani ya mji. Kama mizigo bwana, valantia wamekusanywa pale chakula kinapikwa Wete tunapelekewa kule tuliko. Nadhani kama sikosei, tuko watu wa ngapi? Hamsini. Tukaaga. Kufika kule Mzee Anthony akagawa. Gora Kombo, Wete. Isa Kibwana, Chake Chake, Feruzi Kayanga, Mkoani. Gari tumechukuwa gari za wapi? Gari za publiki. Gari za njia. Lakini kuna watu special wanojuwa kitu kile kinafanyika vipi. Wale ndo wapokezi wenyewe na wale ndo wenye kutafuta gari hizo. Mimi siwajuwi. Wewe ingia gari hii dereva yumo, wewe ingia gari hii dereva yumo. Tukaondoka tukafuata saa yetu ya Zanzibar kwamba mimi jukumu langu

Page 288: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Sita256

naikamata Madungu. Gora Kombo jukumu lake anaikamata Wete. Polisi tu. Feruzi jukumu lake anaikamata Mkoani. Lakini saa yetu iwe hii, kama ilivokuwa Unguja. Kiongozi wetu kaipanga safari ile ile na saa ile ile. Bwana we, saa tisa ya usiku tufanye kazi hiyo. Wale jamaa wasiopenda mabadiliko ya nchi washaanza kunongona mle kwenye vituo va polisi. “Leo mtakuja kamatwa hapa. Jana jeshi limekuja. Liko Kigomasha msituni! Miadi yao leo. Kula boma litakamatwa leo.” Polisi wamekaa standby. Pale Chake Chake ndo alipo Inspekta Mkuu akiitwa Harry, Inspekta Harry, Banyani. Mkorofi kafiri huyo! Basi tumetoka kama kawaida, saa ile tunajuwa saa yetu. Wale wanapiga hodi polisi, wale wanapiga hodi polisi. Hakuna zogo. Hodi, karibu. Bwana wewe, silaha zote tunazitaka hapa. Kwa vile wale polisi walivokuwa washapata ile fununu kwamba hiki kitu kipo tutakuja uliwa, wenyewe wamezileta. Hata ukaidi hakuna. Anatokea Inspekta mmoja huyo nlokwambia anatoka Kibirinzi. Moto mkali anakuja, kuja kuihami polisi. Sisi tuko Chake Chake hasa pana jumba moja linaitwa la maaskari ndo jumba moja lilikuwa kubwa la tajiri mkubwa wa karafuu. Pale ndo kambi yetu sie watu wa Chake Chake. Kuna jamaa mmoja anatwambia “jamani eee, huyo Inspekta anakuja na ana hatari na ana bunduki mfukoni mwake.” Kulikuwa kijana mmoja nilikuwa namwita mpaka leo “Humudi” lakini siye Humudi aliemuuwa Mzee [Karume]. Humudi mwengine. Basi ile anafika pale kakuta watu wamesimama pale. Yule Banyani akashuka pale na bastola yake “nini, nini hapa.” Aaah! Hakuwahi hata kupiga alishtukia tu anaanguka. Pemba nzima wamekufa watu wawili tu. Jicho langu ukilitaka la Unguja nadhani nilikwisha kupa kitu. Unguja kulikuwa wako viongozi. Mfaranyaki Zanzibar, Kaujore Zanzibar, Yusuf Himidi Zanzibar, Sefu Bakari Zanzibar, Natepe Zanzibar, Idi Bavuai Zanzibar, Ramadhani Haji, Washoto, Rajabu Kheri, Zanzibar. Katika vituo viwili, mgawanyiko ulogawanyika kutoka Chumbuni. Kikundi kinokwenda Bomani kinaongozwa na Yusuf Himidi akisaidiwa na Idi Bavuai akisaidiwa na Saidi Washoto. Kikundi kilokwenda Mtoni kikiongozwa na mzee Kaujore, Mfaranyaki, Juma Maneno, na wengine wadogo wadogo kama sie. Lakini uingiaji katika boma la Mtoni kaingia Mzee Kaujore na Isa Kibwana. Hao ndo watu wa kwanza kuingia kwenye nyumba hiyo. Viongozi wengine wako watatu pale lakini wamezuwia kundi la watu lisije likaingia ndani kabla hatujafanikisha lile lengo lilokuwa mle. Bora watolewe watu kama wanosema hawa wanatolewa muhanga. Sisi ndo tuliyojitolea muhanga tupate zile silaha ziliopo pale kwa sababu picha tushapata. Picha ile ya kwenda mashamba haina kiongozi. Mimi nakaa Donge, kuna Wadonge wengi wanankera au kuna Wamanga fulanifulani wanankera sasa nimeshapata silaha mimi nakwenda Donge. Nikifika siwasalimu, mimi nawauwa wale. La mashamba halina kiongozi. Ni mripuko tu. Maana utamsikia mtu hasa atakuona na silaha “mahala fulani pana Wamanga bwana pale wamekaa kitako.” Unakwenda. Ukifika huulizi. Kwamba wale basi. Kwa mashamba Komredi

Page 289: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Wagawe, Wasahaulishe, Watawale 257

hakuingia. Manake shabaha yetu sisi, tulipomaliza Malindi tukatawanyika. Watu wa mashamba tukarudi kwetu mashamba. Mimi kwa safari ya Pemba nilikujachukuliwa Mkokotoni lakini tumo kwenye kazi hiyo hiyo. “Hapa wali­kuwa watatu wakitukera hapa. Tunajuwa bonde la Mnyimbi hapa tukilimalima si Mmanga fulani akitufanyia.” Ah! Mnajuwa nyie, wamo wamejifungia ndani humo. Leteni petroli. Piga dirisha rusha ndani. Piga, tupa bomu, buuu! Mabomu ya chupa za petroli. Hii kazi ilifanyika. Haina kiongozi. Mtu akikwambia ina kiongozi, aa. Hivo ndo ndivo ilivo. Wamanga waliuliwa lakini wenyewe wahusika wale hawakuuliwa. Wengi wao walihifadhiwa kwa sauti ya mwenyewe Mzee Karume, kwamba midam mtu ameshafika miguuni kwangu hamna amri. Kazi yenu mgeifanya huko huko lakini hapa basi. Idadi ya watu waliouliwa hasa kimapinduzi, ningekupa hasa waliouliwa kimapinduzi ntakosea. Ntakupa watu walouliwa kwa njaa. Kwa sababu kuna watu wameuwana wenyewe kwa wenyewe. Sehemu ya kwanza pale Mlandege kituo cha mafuta. Wamekufa watu wengi saana. Kwa nini? Kwa kutaka mle ndani mna pesa. Unaona bwana. Halafu tukatoka pale tunakwenda duka la Malindi, duka la ubavuni pale, watu wanatafuta ngawira. Wamekufa watu wengi sana. Utazunguka utakwenda zako Darajani, ukifika Darajani utamkuta mtu kaanguka na gunia limemlalia. Huyo alikusudia kupora gunia anataka kwenda nalo kwao akapigwa risasi. Hii ilikuwa kubwa kuliko ile siku yenyewe ya mapinduzi. Kwenye yale mapinduzi yenyewe yakuingia ndani ya maboma hata watu waliouliwa kumi hawakufika. Ukizungumza sana kifo zaidi kimekwenda mashamba kuliko mjini. Kwa sababu kule mashamba wale watu walikuwa na vitu vao viwili. Kwanza, tunasema mkono wa mzee Karume ulikuwa unalia kuuwa watu kwa sababu wakingolewa vyakula vyao. Sasa kile kisasi cha kungowa chakula na kuzuwiliwa visima kuteka maji ndo wakaanza kuuliwa Wamanga wa mashamba.4 Wewe kama hukuambatana na Mmanga yoyote shamba au mjini huli. Kuna kitu ilikuwa nguvu iko kwa Wamanga. Sasa suala lile watu wanaojuwa historia kwamba hii si nchi ya Wamanga. Hii nchi ya Waefrika. Kwanini hawa wanazidi kutuonea sie? Hii ukitizama wanojuwa historia ndo asili ya kuja mapinduzi haya. Mmanga umeletwa weye kuja kumuondowa Mreno sisi wengine tulikuwa tuko nje bado huko.5 Lakini wenyewe wanajuwa kuwa Mmanga kaletwa kuwakombowa Waswahili hapa kutoka kwa Mreno halafu akageuka kuwa Mmanga. Ilitakiwa iwe anolizungumza Mswahili Mwarabu alikubali midamu ni la uhakika na analolizungumza Mwarabu Mswahili alikubali midam ni la uhakika. Mambo ya mazogomazogo, ya mdomomdomo, ndo ya kukataliwa. Na waliku­ weko Waarabu wa namna hiyo ambao hawakuguswa na tukawekwa sisi tunayalinda magari na mali zao. Manake walikuwa hawamo kwenye mambo ya vyama na mdomo mdomo. Vyama hawataki na mambo ya maneno maneno haya ya kisiasa walikuwa hawayataki.

Page 290: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Sita258

Komredi alikuwa hayumo. Kachupia. Na kuchupia kwao kwa kujipendekeza. Ali Sultani huyu huwa anawaambia CUF “Hata mkifanya vipi, tulishindwa sisi mtakuja kuwaweza nyinyi hawa?” Ali Sultani alianza zamani yule kujitowa kwenye kundi la Waarabu. Yule kajitowa mapema sana. Mwenyewe alikuwa ana mawazo anasema “karne inokuja Mswahili atajitawala, si karne ya Mwarabu tena, kwa hivo mimi somo naanza kujitowa nakwenda Uswahilini.6 Kajitowa mapema bwana. Kabisaa. Babu alikuwa mwanasiasa mkubwa sana na kwa kupendelea kuwa kuna kitu anataka. Alomgamua Babu ni hayati Saidi Idi Bavuai ndo akamwendea hayati Karume kwamba kila ukikaa umtizame mtu huyu. Yule mtu bwana alikuwa kama tukizungumza sana, ana kitu kinamjia, na kikimjia ndicho. Usisikie kwamba kuna watu wamenyongwa, kuna watu Karume kawauwa, kuna watu kawafanyaje. Hata. Nia zao na nyoyo zao zilivyo kwa sababu wengi wao walikuwa hawampendi yule bwana. Wengi walikuwa hawampendi mzee Karume kwa sababu mzee Karume alikuwa na uamuzi wa uhakika. Hakumchukia mtu. Karume alikuwa kula mtu wake lakini tukaanza kubaguana. Sasa wale wanojidai kwamba wao wazaliwa mara tatu mpaka mara nne Zanzibar, wale walikuwa ni Wazanzibari wenyewe. Sasa sisi tulozaliwa mara moja Zanzibar watu wa bara. Hatufai kukaa hapa. Suala hilo likaanza kuingia hapa. Mpaka sasa hivi hilo suala liko.

Page 291: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na SabaHayeshi Majuto Yao

Jambo la ajabu ni kuwa Kambarage akipenda sana kuwatolea Watanganyika wenziwe hadithi isemayo kama haya: Miti midogo ilikuwa ikipiga kelele kuwaambia miti mikubwa:

Jamani wanakuja hao!Miti mikubwa ilijibu: Vipi mwenzetu yumo?Hayumo.Basi hamna matatizo. Waachie, waachie waje.

Mara nyingine tena miti midogo ilinadi: Jamani wanakuja tena haoo!Nani?Mashoka!Mwenzetu yumo?Wamo tele!Ah, basi tumekwisha! —Ibrahim Noor Shariff

Mzee Aboud “Mmasai”

Khiyana imekuwa kubwa, kubwa sana. Na hii yote, kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza, ni ujinga wa Karume. Yeye alikuwa na khofu na watu walokuwa na ilimu, hata mapinduzi bado. Aliwahi hata kuhutubia kusema “wakimbieni wenye ilimu.” Na sababu hizo ndo akenda kujiunga moja kwa moja na Nyerere bila ya kumshauri mtu kwamba asipinduliwe na hawa halafu wataleta Waarabu. Mimi nilikuwa sijui habari za muungano. Pia Babu alikuwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na yeye alikuwa hajuwi habari hio. Mimi nilikuwa nakwenda kazini, nafika kwa Sapriji, mbele si kuna duka la yule Muhindi anatengeneza radio anaitwa Dawud, nimesikia radio pale inasema juu, habari za muungano. Babu akasema yeye hajuwi habari hizo na yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Na Nyerere kakubali kwa makusudi kuitawala Zanzibar. Hichi ndicho

Page 292: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba260

ninachokiamini. Sababu moja ni hiyo ya Karume, ya pili ya Nyerere kukubali bila ya kuwashauri wananchi. Halafu Karume Mawaziri wote walosoma kawapeleka bara. Kina Babu, kina Idris, Hasnu Makame. Wote wamepelekwa bara wakawa wanacheza ngoma huko. Na ndivo inavotawaliwa Zanzibar, manake mpaka leo hakuna Bunge la Muungano. Kuna Bunge la Tanganyika. Lina watu mia sita na ngapi, na watu wa Zanzibar wametiwa ndani watu khamsini, watafanya nini ndani yake? Kinacho tawaliwa kwenye muungano si idadi ya watu, bali ni mambo ya nchi za nje na ulinzi.1 Zanzibar ina nguvu yake kama Tanganyika hata kama Tanganyika ina mamilioni ya watu zaidi. Zanzibar ni nchi huru kama weye wa Tanganyika. Ningelikuwa mimi ni mtu wa kisiasa sitokubali. Namshukuru Mungu nalisema, mara tu baada ya kutangazwa muungano ikiwa kuwa hatuna Bunge la Muungano, tena mbele ya Bhoke Munanka, alikuwa ofisi yake Beitlajaibu, Waziri wa Mambo ya Muungano “ikiwa hatuna Union Parliament, Bunge la Muungano hatuwezi kulichukuwa Bunge la Tanganyia tukalifanya ni Bunge la Muungano.” Udhaifu wa watu wetu wote hawaitetei hii Zanzibar. Nadhani kama Hanga alikuwa akiitetea ilikuwa ndo sababu ya kuuliwa. Mimi sikusikia kama aliwahi kuitetea Zanzibar. Hanga alitaka kufanyisha nishani kwa walioshiriki kwenye mapinduzi kwa sababu ni kujionyesha na kujiaminisha kwa watu. Na watu walopigana wawe na furaha. Mwalimu akamkubalia halafu akamuuwa.

Ubaguzi kwa Risasi: Karume “Afro”—Kombo “Shirazi”

Mzee Muhammed Baramia alikuwa memba wa Chama cha Umma na alihusika katika kesi ya mauwaji ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Hivi sasa ni memba wa Chama cha Wananchi (CUF) na ni Imamu wa Msikiti.

Halikuwa jaribio la kwanza. La 1972 tulipanga tangu 1968. Madhumuni khasa ilikuwa kukamata serikali ya Zanzibar. 1968 tulijiona kidogo. Sababu ni tuliona kuna mabadiliko against [dhidi] yetu. Upepo ulikwisha anza kutugeukia. Karume kaifanyia hii nchi kama moja kwa moja yake, hasikilizi mtu, anafanya anavotaka. Mwisho wake ilikuwa baada ya wale kina Hanga, kina Twala, kina Saleh Saadalla, nani…, sasa alikuwa anamtaka Babu. Ndo akasema hasa, “lipo Hizbu kubwa huko Dar es Salaam, tunalitaka hapa.” Kwenye mkutano wa hadhara. Kweli Babu ali­kuwa Katibu Mkuu wa Hizbu na ndo maana Karume akasema “Hizbu kubwa.” Sasa anaanza kumtia hewani, kumuandama. Anamtaka yeye kwa kuwa aje au atavunja muungano. Alimwambia Nyerere hivo. Akiogopa kwa sababu wataalamu wote yeye hawataki. Kina Twala, kina Hanga…Yeye na Sefu Bakari kuwa waendeshe nchi wanavotaka, wafanye wanavotaka, hivo ndo ilivokuwa. Baada ya kutangaza hivo sisi tukaitana, hapa Zanzibar na Dar es Salaam, mikutano ilikuwa mingi. Hata mie nafsi yangu nilimwambia Sefu Bakari “mbona upepo

Page 293: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 261

unatubadilikia?” Akanyamaza kimya. Nilimkumbusha wakati wa interrogation [kuhojiwa]. Umesahau? Manake alinihujumu “hata wewe, wewe ulikuwa Afro­Shirazi na ghasia?” Nkamwambia “mmetugeukia.” Tukaendelea mpaka tuka­ panga mipango. Kila nkiwatia kwenye line hawaingii, kina Natepe, kina nani, lakini Sefu Bakari sikuweza hata kujaribu kwa sababu alikuwa pro­Karume [akimuunga mkono] bila ya kiasi, Ali Mahfoudh alikuwa pro-Karume, akisikia chochote vilevile hatari. Wengi katika Baraza la Mapinduzi walikuwa pro- Karume. Hata Khamis Abdalla Ameir, Ali Sultani, tuliwaogopa. Badawi [Quallatein] baada ya kuhujumiwa Pemba, yeye alikuwa Waziri Mdogo, kahu­jumiwa na Karume, akageuka. Akabadilika akawa pamoja na sisi. Babu akitushtakia sisi kuhusu Khamis Abdalla Ameir. Ilikuwa linakuja jambo mbele ya Baraza la Mapinduzi dhidi ya Babu, basi Khamis akinyamaza kimya na wala hakuripoti kwa Babu kwa kuwa iko hivi hivi hivi. [Saidi] Bavuai ndo alokuwa anamwambia Babu, mambo yako hivi hivi hivi. Ukisemwa hivi hivi hivi. Basi tukenda tukafanya mkutano mpaka karibu ya mwisho tena sasa tayari mambo lakini sasa sie watu wenyewe kidogo. Mimi nafsi yangu nimewaambia Hizbu, nimewaambia wale walokuwa Mobile Force wale, Afro­Shirazi nno­waweza wale, nimewaambia. Madhumuni ilikuwa tupinduwe kijeshi. Ikafeli kwa sababu walewale tulowaambia waje, kina [Amour] Dugheshi, kina nani, wote wamefanya woga. Ila yeye Babu ndo amesema kaja mpaka pwani hapo, akarudi. Kina Tahir Ali, wamepanda boti hasa waje. Walipopanda wakaona mambo yameshavuja wakarudi. Mambo hayo lini. Alkhamisi tuliwaambia watu wote waje, tuliagana Youth Tournament inakuja hiyo, kwa kuwa na nyie kabisa, Alkhamisi tuwe tayari. Lakini alokuja mmoja tu. Hashil Seif. Bas. Ndo baada ya kuona tumefeli ndo akapanda Cariboo bado hajajulikana, akarudi Dar es Salaam akakamatiwa hukohuko. Na wengine wengi wamekuja lakini tulikataa kuwataja majina. Babu ilikuwa aongoze ile coup d’état [mapinduzi ya kijeshi]. Viongozi wangelikamatwa, akamatwe Karume akatangaze kwenye radio, aseme kuwa ameshindwa, na nini. Tulikuwa tuna wenzetu ndani ya jeshi. Walipoona tumefeli wakapinda wote. Sasa wakajifanya wao shrewd against [mahodari dhidi] yetu. Hao wanajeshi waliofanyiwa kampeni na Ahmada, Humudi, etc. Sisi tumepanga wiki moja ya kule store [ghala] ya silaha ni yetu sisi, na wiki moja yao wao, Afro­Shirazi. Wale walioko zamuni, wote wale wetu sisi. Kina Sindano, hao walokufa. Na wiki ya pili wanakuwa wao. Sasa sisi tulianza tangu Jumatatu kutowa silaha. Zikakaa kwa Humudi, kiasi mia, silaha mbalimbali, bastola, bunduki, machine gun. Aliziweka kwake. Humudi alimtowa mkewe akenda zake Dar es Salaam, ukumbi mzima zikawekwa silaha. Tungeweka kwa Ahmada ingelikuwa hatari. Niliwaambia tukiziweka kwa Ahmada na yeye Captain in charge wa mambo ya silaha atasachiwa. Na kweli, walishughulika juu ya Ahmada hawakumgusa Humudi. Mpaka saa tisa za jioni silaha hazijajulikana ziko wapi.

Page 294: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba262

Mpaka saa kumi. Mpaka magharibi sisi tunaripuwa hazijajulikana zile silaha ziko wapi. Siku ile walipokamata wale ma­ASP ilipojulikana silaha zimeshaibiwa siku ya Ijumaa, manake wiki nzima zimekaa, siku ya Ijumaa zilipohisabiwa hakuna, kina Ali Mahfoudh wakataka kutupiga curfew ile Ijumaa usiku, sisi tukasema hatuwahi. Humudi ndo alipata ripoti hiyo saa nne asubuhi ndo akatuletea. Kuwa tuka­matwe sote siku ileile ijumaa. Saa tisa tumekutana kwa Humudi ndo tukaamuwa. Hapo alikuweko Miraji, Chwaya, Harakati, Humudi, Ahmada, kina Falahy walikuwa chumba cha pili, hawajajuwa tunazungumza nini. Ishajulikana, hapana njia isipokuwa tumpige Karume na Sefu. Kwa sababu wale hawakuja, tutafeli, kina Amari Kuku, Ali Mshamgama, wogawoga, hawakuja kwenye mkutano saa tisa. Wote hawakuja. Potelea mbali. Wale wengine, khasa Saidi [Sindano] alokamata store silaha alikwishasema “tumeshakufa.” Kwa sababu Sindano keshakimbia tangu saa nne ilipojulikana, anatafutwa. Sasa watu wetu tena wakaanza khofu. Kupatikana gari ndo Harakati akenda kuazima kwa Khamis Abdalla Ameir, manake ndo dereva wake. Nna safari yangu nataka kwenda. Sasa Khamis hajuwi anataka gari kwa sababu gani. Hajui, kampa, haya nenda. Chwaya kachukuwa gari ya People’s Bank yeye ndo dhamana. Tena kina Ahmada wakaingia katika gari ya Chwaya, pamoja na…Gari ya Khamisi, Harakati, Saidi alouliwa Vuga. Na Rashid Falahy akaingia palepale Makao Makuu [ya Afro­Shirazi]. Sasa kumi na moja unusu tuseme wametoka, kumi na mbili wameshafika pale, wakaripuwa. Gari ya Chwaya, rangi ya bluu bluu ilitokea Malindi, ya manjano, ya Khamis, ina kipande cha MBM (Memba wa Baraza la Mapinduzi) kimeandikwa, ikapitia njia ya Majestic Cinema. Iliamuliwa kuwa tumuuwe Karume, tusimuuwe Thabit Kombo. Tumtishe tu basi. Kwa sababu kuweka mgawanyiko, iweko ubaguzi, Karume na Kombo. Wote tungewaweza ati pale lakini tumefanya makusudi tuweze kubaguwa. Afro na Shirazi labda italeta mgongano. Manake Karume ndo “Afro”, yule Thabit Kombo “Shirazi.” Alomuuwa Karume ni Ahmada. Lakini ile Humudi tumemtaja kwa kisiasa. Tangu mwanzo ndo alisema hasa kuwa yeye ndo atofanya.Tumehakikisha kwa sababu Falahy ndo alokuwepo pale, akaona. Hivo ndo ilivyo.Humudi ali­zubaa kule akawa anapiga ovyo. Watu wanaondoka wanakimbia, yeye kapiga tu lile hall zima juujuu kule, kutisha, watu washaondoka na gari. Sasa kutoka yeye, sasa hapa kuna kauli mbili. Moja kapigwa kwenye bustani na alikuwepo mtu akampiga, moja inasema alivoona vile hakuna mtu kajipiga mwenyewe.2

Nafikiri walikunywa kidogo. Walipofika Makao Makuu [ya ASP] mimi naona. Nipo pale ice cream club. Naona gari zinavoingia. Walipita pale Ahmada akaninyoshea mkono kuwa tunaingia. Nikawaambia haya kwa ishara ya kidole juu. Nikawaambia, haya! Manake kumpiga yule [Karume] faida itakuwepo. Asaa wale wenyewe wataweza kutanabahi…Iko siku karibu tena korti tunapelekwa,

Page 295: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 263

tushapigwa, tushafuswa sote, tukachukuliwa mpaka Migombani. Baada ya korti kwenda wamekubali watu tisa, walobaki wote wamekataa. Sasa wale tisa sote tulikuwa tupangwe tuseme vipi kule korti. Na Dourado alikuwepo, Mandera. Kama mtu kama Nourbhai alikuwa matusi sana kule korti mtajeni manake hakutajwa na mtu. Sasa akalazimishwa Miraji. Kwa sababu mlikuwa China pamoja basi sema wewe ninhi…hakumtaja. Mie nililazimishwa nimtaje Saidi “Tumbo.” Hakujuwa ati, sasa mimi nimtaje nini. Manake yeye hakutajwa vile vile. Lakini kapigwa wee basi kenda katowa statement wiki nzima anataja, mimi hivi nilikuwa hivi. Na hayumo. [Kutoa amri Karume auliwe] mimi ndo ino ni haunt [inanipa jinamizi]. Inani haunt Naona nimefanya, kiama huko kuna dhambi, au vipi? Naona kama dhambi. Hiyo kusema, tumpige, tumuuwe. Japokuwa yeye kauwa watu wengi lakini. Mara nyengine nahisi, e bwana we, madam kauwa watu wengi na nini, nimesema auliwe, basi, potelea mbali. Lakini wakti mwengine Islamu mwenzio kumtia kwa kuwa auliwe si uzuri. Nna khofu ndani yake mbele ya kiyama. Khofu iko. Inanjia. Babangu alikuwa Hizbu. Ananambia tia tu hapo picha ya Ali Muhsin hata kama humpendi. Namwambia “sitii” na yeye akinfata mie kwa sababu mimi skuzile ndo nkiiendesha nyumba. Basi sijuwi tuko wapi. Hata sijuwi. Ah, watu wanapinga sana. “Nyie ndo mlotutakia haya.” Hawajuwi madhumuni yake kwa nini tukaingia Afro­Shirazi. Kwa sababu chama chetu kilifungwa na Hizbu. Kulikuwa hakuna njia nyingine. Kilipigwa marufuku chama chetu tukaona sasa tunaninginia. Tena tukaingia Afro­Shirazi. Tukiwaponda Afro­Shirazi kwenye Hizbu tangu mwanzo. Kwa sababu tumefunguwa huku, huku hawatutaki. Tumefunguwa chetu hawataki. Twende wapi? Haikuwa makosa Babu kutoka Hizbu. Makosa wao waloyafanya kumtowa. Manake kapeleka pendekezo wamelikataa. Basi kama mnalikataa mie natoka. Haya toka. Na wao wakitafuta hiyo. Wakitafuta atoke ili wapate uhuru. Kawaambia Mngereza, yule Koministi na ghasia, na ile wao ikawajaa tele. Mkimtowa sisi tutakupeni uhuru. Na yeye Babu hajajisema kama ni Mkominist. Hata sku moja. Lakini alikuwa na falsafa zake basi Mngereza akasema huyu ni mtu hatari. Sasa mkimtowa tutakupeni uhuru. Siku hiyo ndo alokuja Sefu, watu tisa tulipokutana. Ndo anaulizwa mmojammoja. Wewe utafanya hivi, wewe hivi. Sasa nilipofika mie akanambia “hata wewe umeshiriki kwenye mambo haya?” Manake mimi kina Natepe wamenitetea kulekule kwenye Baraza la Mapinduzi, kwa kuwa hayumo haiwezi kuwa. Haiwezi kuwa yumo, mtu tunaye tunanhii… Ikasemwa imeamuliwa Makomred wote wakamatwe, tena ndo nkakamatwa. “Mimi si nlikwambia wewe kuwa mbona upepo unatubadilikia?” Kanyamaza kimya [Sefu Bakari]. Ndo Mandera nlipotoka tunarejeshwa gerezani tena, alinambia “unamjibu yule vile ufidhuli angelitwambia pale tukuuwe tungekuuwa tu.”

Page 296: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba264

Sijaogopa chochote. Hata. Haijanijia hasa ile hisia kuwa niogope. Naona nimesema tu kama ilivo kwelikweli. Na ni kweli ati. Na nlikuwa naye kutwa Sefu ati. Aliponiuliza nikamwambia hivo ndivo ilivokuwa. Tena nifiche nini tena pale. Kufa na kupona. Bora mara kumi Natepe kwa fikra zake za kisiasa. Nikimsafiria sana Natepe kuliko Sefu. Tukizungumza manake. “Huyu Karume katuteka kila kitu anafikiri yeye tena, bora huo ufalme.” Tulikuwa tuna jina letu tunamwita Karume, “scandal bag.” Mie, Rajabu Kheri, Khatibu Hassan. Ukisema “scandal bag” manake Karume. Nimewacha mambo ya dini na ghasia nimekwenda kwenye siasa. Hiyo ndo nnajilaumu. Akili inakujia ati. Wewe binaadamu ati. Na mimi Msikiti Baraza nilikuwa pamoja na huyu alokufa juzi, Zagar. Tumesoma pamoja. Kilochonifanya khasa kuingia siasa baada ya nilipomaliza skuli nilitafuta kazi kote lakini skupata. Tena Mr. Davis akanipeleka pwani, gatini. Naona kila nkenda kufanyiwa mahojiano naambiwa “wewe unaweza wapi kuchukuwa file huku ukaweka huku.” Rohoni mwangu nasema, siku hiyo nanyenyekea ati, lakini ngekuwa najibu ngemwambia “kwani skuli mabuku ukinchukulia weye?” Ingekuwa sasa, ah, ningemjibu hivo. Manake file tu yakhe kuweka huku na huku unanambia siwezi. Na kote nlipokwenda, ustawi wa jamii nlikwenda, afya nlikwenda, wapi, wote, wananijibu “tunasikitika kukuarifu…” Babu naona ni mtu wa siasa tu. Mie kanivutia maneno yake, u­peasant na working class [wakulima na wafanyakazi]. Naona loh! Mimi tanguwapo nilikuwa trade unionist mwanzo, na nlikuwa 1956 nliingia Dock Workers na nlikuwa General Secretary wa Dock Workers, na Ismaili ndio President. Babu angeweza kuchukuwa serikali angelikuwa kiongozi mzuri. Mpaka leo naamini hivo, lakini hakubahatika, na kuna uwezekano wa Mwenyezi Mugu hapo tena, au vipi? Alikuwa mtu mfanyakazi wa kwelikweli, masaa ishirini na nne ukimwendea anafanya kazi. Baada ya Natepe nnomjuwa mie basi. Kina Twala mimi sikuwa na uhusiano nao sana. Kassim Hanga na kina Babu, na Hassan Nassor Moyo.

Wasia wa Zanzibar wa Hayati Rais Samora Machel—J. J. Mchingama

Marehemu Samora Machel wakati alipokuwa karibu na kupata uhuru alitembelea Zanzibar mwaka 1972 kabla kidogo tu kabla ya kuuwawa Karume. Alikuja juulisha kwamba sisi karibu na ukombozi wetu, karibu tutapata uhuru, na kwamba ukoloni umeshaanza kufikia ngazi ya kushindwa. Tayari wanafanya mazungumzo ya kumaliza vita baina ya Mreno na wananchi wa Msumbiji. Pale alielezea, alikuwa anaongea na Makamanda wa kijeshi Migombani kwamba sisi Mozambique ukombozi tunaoufanya tunatafautiana na ukombozi mlioufanya nyinyi Zanzibar. Nyinyi mmekombowa Zanzibar kuondowa utawala lakini bado wananchi hamjawakombowa kifikra. Sisi Mozambique tunajikombowa kuondowa utawala na kumkombowa mwananchi kifikra bila ya kujali ukabila, rangi, dini,

Page 297: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 265

au asili ya mtu, au jinsia. Hapana. Tunasema wote ni watu wa Mozambique. Awe Mmakuwa, au Mmakonde, awe Mwarabu, awe Mreno. Mreno mwenyewe akikubali kwamba mimi ni mwana Mozambique na nakubaliana na matakwa ya FRELIMO, huyu ni mwenzetu. Hatumkatai kwa sababu alitawala. Lakini nyinyi Zanzibar, bado watu wamekuwa na fikra finyu. Bado watu mnayo matabaka. Bado watu mnajaliana sana asili, kabila, rangi, jambo ambalo si ubinaadamu. Nitamleteeni matatizo siku za baadae. Wakati anazungumza Ali Mahfudh alikuwa amefatana nae. Ali Mahfudh huyu anajuwa ukombozi wa Mozambique ulivofanywa na anaona tunavofanya mpaka sasa. Kweli mnajitawala. Bendera mnayo, utawala mnao, lakini watu bado wana fikra zile zile za kumuangalia mtu huyu ni fulani, huyu ni fulani. Huo si ukombozi. Akaondoka Samora. Haikuchukuwa muda, kama wiki mbili tu, tukasikia kwamba Abedi Amani Karume ameshauwawa. [Wengine] wakasema bila shaka Samora alikuwa akisema vile kumbe alikuwa anajuwa huu mpango! Zile zikawa fikira finyu. Yeye alizungumza kama kiongozi jinsi alivoona upeo wake. Mimi kukaa na wewe sasa hivi basi kama atapita mtu mwengine ataona, unajuwa bwana, tumemkuta Mchingama JJ amekaa sijui wanaongea nini na yule Mwarabu? Sijui niongee nini wakati wewe ni binaadamu mwenzangu? Na mtu mwengine atasema. Yule Mwarabu kimempeleka nini kwenye kituo cha FRELIMO? Vipi yule, kakaa na Wamakonde anazungumza nao. Hawawezi kufahamu. Hicho ndo kiliopo hapa Zanzibar. Bado ukombozi wa fikra.

Abdalla Kassim Hanga: Wasia wa Mwisho—Mzee Salum

Kwanza ningelipenda tuzungumze kutoka mwaka 1963 na 1964. Kwa sababu huo ndo wakti muhimu kwa mambo yale ya Unguja na haya tunayotafuta. Na vile vile muhimu kwangu mimi kuwa mimi nilikuwa nimeshaondoka Zanzibar 1963, niko Nairobi na nilivofika kule nikaombwa na umoja wa mapinduzi ya Ngazija kuwa niwe Katibu Mkuu wa MOLINACO. Nikaifufuwa MOLINACO Nairobi na nikabadilisha mikakati yake. Kabla ya hapo Katibu Mkuu wake alikuwa ni mwalimu Zanzibar na wengine wawili walikuwa wakitia vifungo kwa Bwana Ali Barwani. Ni harakati ya kiukombozi ya Comoro ili kumtowa Mfaransa. Na nilikubali na katika watu ambao walikuwa mbele katika hiyo kamati ya ukombozi ya MOLINACO, Nairobi, alikuwa kijana mmoja Ahmed Abdalla Mbamba ambaye yeye ni mmoja katika walorejea Ngazija na wakawa wakubwa wa mapinduzi ya Ngazija na yeye aliuliwa pamoja na Rais Ali Saleh walivoingia hawa Wazungu kutoka South Africa. Mwengine kijana akiitwa Kenya, jina lake silikumbuki. Sasa wakati mimi niko pale kama ni Secretary General nilikwenda mbele kufanya usajili wa kukubaliwa na Organisation of African Unity (OAU) kuwa MOLINACO ikubaliwe. Ilikuwa imeshakubalika kwa Dar es Salaam lakini hichi

Page 298: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba266

kipande cha Kenya na Uganda kilikuwa ni chengine. Uongozi ni wangu mimi na sio ule wa Dar es Salaam. Wakati ule nikaweza kujuwana na viongozi wengi wa serikali mpya ya Kenya, mfano, Mzee Mdiu Kaunange ambaye ndo alokuwa wa pili baada ya Kenyatta. Alikuwapo Tom Mboya ambaye ndo kila mtu akimjuwa, akimuelewa, alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Biashara na Viwanda. Oginga Odinga alikuwa ndo Waziri wa Mambo ya Ndani na ni mtu mzito vilevile kwa pale, anakubalika Kenya na wengi nao ambao walikuwa pale, walinikubali mie kuwa huyu ni kijana ambaye anapigania uhuru wa Comoro. Ama Oscar Kambona tumeweza kujuwana kwa yeye alivokuwa akija Nairobi. Nimejuwana naye kwa kujuulishwa na Tom Mboya na alipokwishajuwa kuwa mimi ndo nnaendesha MOLINACO pale, nasimamia MOLINACO, akafurahi kuwa ni Mzanzibari anoshughulikia mambo hayo. Kwa hivo jambo lile lilimfurahisha na akanambia kuwa hata nikihitajia msaada wowote, tangu wa pesa na venginevo yeye atakuwa nao uwezo wa kunisaidia kwa sababu yeye wakati ule ndo alokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukombozi (ALC) ya OAU. Hapo ndiyo nilipojuwana naye Kambona. Sasa wakati ule yeye ndo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanganyika, au Tanzania kwa sasa. Ilikuwa wakati ule bado 1963. Muungano haujakuwa bado. Kwa vile yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje akija sana Nairobi na kurudi, na kila akija ikiwa Tom Mboya kapata habari hunipigia simu na kuniuliza kama mzee yuko hapa ukiwa utataka kuonana naye basi kama kuna jambo lolote mie nlikuwa nakwenda kumuona. Niliwahi kuonana naye kama mara mbili tatu pale Nairobi. Sijaonana naye tena kwa sababu niliondoka Nairobi Septemba 1964 kwenda Ungereza kusoma. Na nlikuweko kule Ungereza kutoka 1964 mpaka 1969. Kabla ya hapo mnamo mwezi wa October/November 1963, nilionana supermarket in Nairobi na Chief Clerk wa City Council of Nairobi ambaye alikuwa chini ya Meya wa Nairobi. Akanambia “Iko wapi wewe Mswahili? Nasikia iko matata Zanzibar. Sisi tunapata uhuru na jirani yetu anatawaliwa na Mwarabu, tena Muislamu.3 Hii Aibu kubwa! Unapata uhuru halafu unatawaliwa! Kweli itakuwa hii? Ipo karibu sana.” Nikampa barua mbili [jina nimelihifadhi]. Moja ampe mke wangu, ya pili ampelekee Zaim (Sheikh Ali Muhsin). Marehemu Sheikh Yahya Alawi aliwahi kuniambia “wameendesha serikali gani hawa (ZNP) hata ukawavulia kofia?” Wakati ule Idhaa ya Zanzibar ilikuwa imetawaliwa na utamaduni wa Kiarabu dhidi ya bara. Mimi niliiunga mkono ZNP kwa sababu mbili: moja ni shetani unayemjuwa, na pili, chama kilikuwa na ilani ambayo ilitayarishwa na Babu. Baada ya mapinduzi Babu alimchaguwa jamaa yake Omar Zahran mwenye asili ya kutoka Yemen awe Rais wa Zanzibar chini ya utawala wa Chama cha Umma. Jumaatatu tarehe 13 Januari Mboya akaniambia kuwa Oscar Kambona yupo Nairobi na anahitajiya msaada. Nyerere alimtuma amtake Mzee Kenyatta atumie

Page 299: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 267

ushawishi wake awazuwie Waingereza wasiingilie Zanzibar. Nyerere pia alimtaka Kambona aziombe Kenya, Uganda, na Tanganyika waitambuwe Serikali ya Zanzibar na pia kuziomba serikali za hizo nchi tatu wasaidie kijeshi au kwa njia yoyote ile nyengine. Akanambia Mboya kuwa ujumbe kutoka Uganda ulikuwa uwasili siku ya pili na mkutano ulifanyika kwenye uwanja wa ndege wa Nairobi tarehe 14 Januari. Hakukuwa na waandishi wa habari, hakuna ruhusa kupiga picha na wala kuweka rekodi zozote zile. Tanganyika iliwakilishwa na Oscar Kambona. Kutoka Uganda alikuja Milton Obote na Mawaziri wake wawili. Inawezekana ikawa nachanganya majina. Mmoja alikuwa Lulee aliyewahi kumuowa Mjapani, wa pili, ni Godfrey Binaisa ambaye ni bingwa wa sheria na aliwahi kusema kuwa Othman Sharif hatopumzika mpaka aupate Uraisi wa Zanzibar. Kutoka Kenya alikuwepo Tom Mboya na Joseph Murumbi. Obote alikuwa akipinga moja kwa moja mipango ya Tanganyika. Alisema “Hatuwezi kukubali kupeleka silaha kwa nchi jirani. Hawa ni watu wamoja. Tuwaachiye wayatatuwe matatizo yao wenyewe kwa wenyewe.” Abubakar Mayanja alikuwa Minister of Education ilikuwa aje kwenye mkutano wa uwanja wa ndege wa Nairobi lakini hakuweza kuja. Mboya aliniambia kaa kimya uyasikilize mambo ya kwenu [Zanzibar]. Kambona aliendelea kusisitiza kuwa serikali mpya ya Zanzibar inahitajiya kutambuliwa, silaha, na pesa. Kwa upande wa Tanganyika msukuma gurudumu mkubwa alikuwa ni Katibu Mkuu na Mshauri wa Nyerere na Kawawa na rafiki wa karibu sana wa Nyerere, Bhoke Munanka. Paul Sozigwa, aliwahikuwa mtangazaji na mwenzake David Wakati, alikuwa ni Katibu Mwenezi wakati wa mapinduzi. Kulikuwa na Wazanzibari ambao walijiunga na TANU kama Shaaban Ame, Rajab Saleh na David Wakati ambaye alikuwa Katibu Ofisi ya Rais na mtangazi mkuu wa Idhaa ya Tanganyika. Rajab Saleh alikuwa Katibu Mkuu wa pili wa Baraza la Mapinduzi baada ya Salum Said Rashid. Unafikiri kwa nini? Mwaka ule wa 1968 au 1969 ndo tukajuwa kwamba Oscar Kambona kaja [London] na nkawahi kuonana naye, ndo sku hiyo akatuletea habari kuwa anataka kuonana na sisi. Na alokuja kutupokea station [kituo] ya treni alikuwa ni huyu bwana, Kasembe. Na nilikuwa mimi na Ahmed Rajab. Ikawa Muhammed Nura maskini hajaja. Tukenda mpaka nyumbani kwake Oscar Kambona, tulipofika kupiga kengele alofunguwa mlango ni yeye. Ni fleti first floor [ghorofa ya kwanza]. Tumeingia akatuvuta upande. Sasa tulivokuwa London yeye [Ahmed Rajab] kataja watu watatu tu. Kasema namtaka Ahmed Rajab wa BBC, na namtaka huyu kijana Muhammed Nura, ambaye ni kijana wa Kizanzibari ambaye alikuwa keshamaliza Masters yake pale na nnaskitika kusema Muhammed Nura hajaja katika mkutano huo na sasa amefariki, hayuko hai. Yeye si mtu wa BBC. Na yeye Oscar Kambona alimtuma kijana mmoja wa BBC, Kasembe anaitwa. Mtangazaji maarufu yeye tangu Tanganyika, Tanzania kwa sasa, na BBC katangaza sku nyingi sana. Baadae

Page 300: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba268

alirudi nilionana naye Arusha alifanya kazi East African Community na alikuweko katika ofisi of the agent wa public trustee [wakala wa amana ya umma] wa East African Community Arusha. Yeye ndo alokuwa in charge [mhusika] pale Arusha. Nnavokumbuka mimi Oscar akatwambia sikilizeni bwana. Mimi nimekwiteni hapa mje mseme na ndugu yenu na mzee wenu huyu, Abdalla Kassim Hanga amekuja hapa na anataka kurudi nyumbani. Hajataja pahala. Na mimi nimemkataza. Nimemwambia huu si wakti mzuri ni bora yeye asiende. Ama angelibaki huko huko West Africa anokotoka kwa mkewe, au abaki hapa London lakini kakataa, anataka lazma arudi. Na mie na hofu maisha yake kuwa akifika kule hatoweza kupata salama. Kwanza kuwa yeye amefikia kwangu, anajulikana yeye na mimi ni rafiki, Nyerere atajuwa zaidi/uzuri hayo kuwa mimi tangu tuko kule tunasikilizana mimi na ndugu huyu Abdalla. Kwa hali hiyo mimi namwambia. Na yeye Abdalla anasema hana ugomvi na Nyerere. Sasa mimi nimekwiteni mzungumze naye, mseme naye. Akatuchukuwa akatupeleka kwenye chumba akasema “Abdalla, hebu zungumza nao hawa jamaa wamekuja kukuamkia.” Tukaingia sie chumbani akatuacha mimi na Ahmed [Rajab] na Abdalla. Peke yetu watu watatu. Ndivo navokumbuka mie na ndivo anavokumbuka Ahmed [Rajab]. Mimi sikumbuki ile nilikwenda railway station. Kile mimi sijakumbuka. Kama ulivosema, mimi nyumba nilikuwa naijuwa, sina haja ya Kasembe kunpeleka. Lakini inaweza kuwa nimekwenda mimi na Kasembe kumpokea Ahmed Rajab. Yeye Ahmed kafkiri tu na mie ni mgeni. Hajajuwa kuwa mimi na Kambona tunajuwana na jirani, na nyumba yangu mie na yake si mbali. Ahmed Rajab ndo anosema, tumefika alofunguwa mlango ni Oscar Kambona, na akatuonyesha chumba. Hajaeleza nini Kambona katwambia. Lakini mimi nakumbuka Kambona katwambia kwanza, “semeni naye.” Yeye kazungumza moja kwa moja, sisi tumekaribishwa tumekwenda kwa Abdalla. Yeye Ahmed amekumbuka mambo mimi sijayakumbuka. Kwa sababu, kasema tulipofika Abdalla Hanga katwambia skizeni: nyinyi ni vijana, watoto kwa sasa, lakini kesho nyie ndo mtakuwa viongozi. Nna maneno nnataka kukwambieni. Tukawa sasa tumekaa tunamsikiliza nini atasema. Anasema nataka kukwambieni juu ya habari ya mapinduzi yetu ya Zanzibar. Kuna mabaya ambayo tuliyafanya na kabla sijasema lolote nnakutakeni jambo moja muhimu mlikumbuke. Msije mkakubali kufata siasa za ukabila.4 Siasa za ukabila ndizo zinotuletea matatizo na ndizo zitozidi kutuletea matatizo. Hilo ni jambo la mwanzo ambaye yeye Hanga katwambia. Akasema mimi (Hanga) nilivoondoka Zanzibar kupelekwa Dar es Salaam, kuwa Waziri wa kule, badili ya kuwa Vice-President [Makamo wa Rais] huku na Mzee Karume, alivopelekwa bara, anasema jambo moja katika mambo aloyafanya ni kuwasaidia Wazanzibari walokimbia kutoka Zanzibar wakakaa pale, wale ambao wataalamu, kuwatafutia kazi. Akataja majina. Akamtaja Maalim Salim Sanura, na akawataja wengine,

Page 301: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 269

mimi siwakumbuki. Kuwatafutia kazi na wakapewa kazi serkalini. Hata ikafika akaanza kusemwa, akalaumiwa, kuwa Abdalla, mbona unakwenda kinyume sasa? Hawa si ndo tuliowapinduwa, mbona wewe sasa hapa unawasaidia? Unawapokea? Akasema bwana, hapa mimi naona ni Mzanzibari tu hapa. Hawa wote ni Wazanzibari bwana. Na hawako nchi nyengine. Wako na sisi pamoja hapa. Kwa hali hiyo yeye anasema ule ndo uzi anataka sisi tuufate. Tusibaguwane. Jambo la pili akasema, sisi Mungu atusamehe, tumefanya mambo mengi ambayo mabaya, tumedhulumu, tumechukuwa watoto na wake za watu, na Mwenye Enzi Mungu ndiye anojuwa. Basi mimi namuomba Mweye Enzi Mungu anisamehe na ninajuta kwa haya nlioyafanya. Ahmed Rajab akamuuliza suala. Akamwambia, mzee, lakini wewe na Janab [Babu] mnaskizana vipi kisiasa? Akamwambia, mimi na Babu sote wawili ni Marxists lakini Babu si tishio kwa Karume. Mimi ndo tishio. Mimi ndo ni tishio juu ya Karume, lakini Babu is not [si tishio]. Hiyo tafauti yangu mimi na Babu, anasema. Kwa Unguja. Sasa ndio tukamuuliza, Vipi ikawa wewe ndo tishio? Yeye Ahmed Rajab ndo anamuuliza. Rome ilijaribu kuingia kati katika ugomvi wa Oscar na Nyerere na ilishindwa. Kambona alinieleza. Hata makanisa yamejaribu. Ugomvi ulikuwa mkubwa na hiyo akijuwa yeye zaidi Kambona ndo mana akahofu Abdalla asirudi. Ile imani yake ilikuwa kubwa kuwa Nyerere hatomdhuru. Na yeye akiona watu wangapi wamepotea lakini hajafikiria atakuja kuwa yeye. Tukasema naye tukamwambia kweli hayo maneno anayoyasema Oscar inaonyesha ni bora usirudi kwa sasa. Akasema hapa kuna mambo mawili. Moja, kuna kutosikilizana baina ya Oscar Kambona na Mheshimiwa Nyerere, Raisi Nyerere. Sasa huyu bwana akisema mimi nisirudi anazungumzia kule kutosikilizana baina yake yeye na Raisi Nyerere. Sasa anahisi mie nikirudi labda kwa sababu mimi nimefikia kwake au ni rafki yake Nyerere anaweza akachukuwa hatuwa. Mimi nimeshafanya kazi na Nyerere na namjuwa uzuri mzee Nyerere, mimi na yeye hatuna ugomvi wowote. Abdalla Kassim Hanga anasema kuwa yeye na Nyerere hawana ugomvi. Na yeye ikiwa anarudi harejei kwa Zanzibar. Atarudi anakwenda zake akakae nyumbani Dar es Salaam. La pili alisema, kuna ukweli wa kuwa mimi na Mzee Abedi Amani Karume kuwa hatuskizani na kusema kweli si makosa yangu. Akasema Abdalla, jambo dogo sana limemfanya Mzee Abedi anichukie mimi hata ikawa mimi nikienda Zanzibar sasa siwezi kukaa nikalala Zanzibar. Lazima siku ileile nirudi Dar es Salaam. Na hili jambo anasema, mimi nilivokuwa niko Tanzania Bara na Dar es Salaam ni mmoja katika Mawaziri, nilikuwa nnakwenda Zanzibar mara kwa mara. Na nikenda nikifia katika nyumba ilioko Migombani ambayo niliwahi kukaa nilivokuwa Makamo wa Raisi. Wakati mmoja nafikiri baada ya mapinduzi, President wa Zanzibar alikuwa ni Karume na Makamo alikuwa Hanga. Sasa ile nyumba ya Migombani ikawa yeye bado Hanga hajairejesha serikalini kila akienda Zanzibar anafikia pale. Siku katika siku alizokuweko pale anasema yeye

Page 302: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba270

kaja kafikia nyumbani pale Migombani na kila akenda watu wakipata habari kuwa Abdalla kaja, watu, jamaa, ndugu na marafiki, walikuwa wanakwenda kumuona na kuzungumza naye, na wengineo wanakuwa nayo mahitajio yao wanakwenda kumuomba awasaidie. Sasa sku moja hiyo Mzee Karume anatokea njia ya uwanja wa ndege kwenda zake mjini akapita pale Migombani akaona magari, akauliza. Kuna nini hapa, mbona magari mengi? Akaambiwa basi lazim Mzee Abdalla Kassim Hanga kaja. “Ala, sasa yeye kila akija lazma iwe namna hii?” Akaambiwa, yeye akija watu wanakuja hapa kumuamkia na kuonana naye. Basi jambo hilo anavosema Abdalla Kassim Hanga ndilo liloanzisha ugomvi baina yake na Mzee Karume. Karume akawa hataki tena na ikawa na yeye Abdalla akenda Zanzibar hafikii tena katika nyumba ile. Akakataa kabisa.5

Lakini inaskitisha kuwa tangu wakati ule yeye yupo pale London habari zishafika Cairo. Walioko Cairo maambassador wa pale wameshapeleka habari Tanzania kwa Mzee Nyerere. Ikawa serikali ninavosikia wamekaa wakimgojea arejee tu. Yeye Hanga hajajuwa, wala sisi hatujajuwa.

Tupendane na Vifo va Kina Hanga—Mzee Selemani

Tupendane wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wameshahifadhika. Sasa kurupushani waliokuja kuifanya Tupendane, ndo tukasema, bwana hadithi zao kuzieleza hakika tishio, tunaogopa. Manake kuogopa kwenyewe kwa kwamba vipi? Unajuwa Tupendane baada ya kuja mapinduzi hapa, Tupendane wapo, lakini chini kabisa huko! Chini kabsaaa! Huwaoni. Wala zile suruwali hawavai tena. Lakini Tupendane ilikuwa iko pale pale baada ya mapinduzi. Karume alikuja kuwaita “njoni nyote.” Wakaja. Bwana we, mapinduzi haya tayari lakini kazi nnayokupeni, watatu nyinyi ntakupeni kazi. Wachunguzeni hawa. Kikosi hiki hiki, kichunguzeni. Kuja chunguzwa kile kikosi, matokeo yake, ikaonekana Othmani Sharifu kutoka Mrekani alikokuweko Ubalozi kufika hapa alimfata Twala, alimfata Hanga, alimfata nani huyu… Saadalla. Wakaambizana, huyu mtwana wa Mungu huyu katoka Nyasaland huko kaja hapa, leo sisi atutawale, lakini Hanga alisema. Jee, ikiwa huyu katoka Nyasaland, haya mimi Mzaramu niliotoka huku [Tanganyika] mnanihisabu kundi gani? Itakuwa ina maana kwamba hata huyu akafa leo mimi sina thamani. Othmani akamwambia hapana. Wewe ndie sisi tunayetaka kukuvisha kilemba cha nchi hii kwa sababu wewe msomi ati. Wewe Makamo unawawakilisha watu Uingereza, Marekani, wapi, nchi zote. Huyu [Karume] wapi alikokwenda? Hakupoo. Bwana yule kaingia tele. Kuingia tele, matokeo yake, hawakujuwa kwamba kikao kile walichokutana kilikuwa kama Mungu kawalani. Alikuwepo Ramadhani Juma, Mzaramu huyo, halafu akawepo Mohamed tukimwita Mohamed “Mkunjeke” kafariki mwaka jana, huyu mtu wa Rufiji huyo,

Page 303: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 271

alikuwepo Ramadhani Asumani Bakari. Huyu ni mtu wa Masasi. Watu watatu hao. Kikazi watu watatu hao walikuweko “Health Office.” Wote hao kazi yao ilikuwa “afya”—health office. Kuja mapinduzi Mohamed “Mkunjeke” kapelekwa kwa “Bwamkwe” [Hassan Mandera]. Usalama. Halafu mmoja, akapelekwa wapi? Pwani. Huyu Ramadhani huyu. Tupendane hao. Kumbe siku ile kunaamulia mambo kama yale, kumbe, huyu nani… Musa Maisara kakaa chonjo pale, anaskiliza tu. Hasemi wala hanyanyuwi mdomo wake. Akatoka. Akakutana na nani? Akakutana na Mohamed “Mkunjeke.” Mohamed, hebu njooo. Yaliopo unayajuwa? Siyajuwi. Bwana we, hawa wanakusudia wamuuwe huyu Mzee Karume lakini kilemba hichi, nafasi hii, wanataka kumpa Hanga. Hanga anasema ikiwa nyinyi mnamsema huyu leo Mnyasa, mimi Mzaramu, vipi, inaa maana hata mimi vilevile ntakuwa uhai wangu haupo. Huyo alosema Hanga atakuwa mtawala wa nchi hii kauli hiyo aliitamka nani? Akasema Othman Sharifu ndie aliezungumza maneno kama hayo. Ikachukuliwa ripoti ile moja kwa moja mpaka kwa mzee Karume akenda akaambiwa. Kuambiwa, akasema hapana. Nimeshayasikia, lakini nnachotaka nipatafute pahala wanapokutana hawa. Wakikutana kina Othman Sharifu, akina Jaha Ubwa, Mdungi Usi hao, wanakutana. Hata siku hiyo akawaambia ngojea. Ikachukuliwa tepu ikenda kuwekwa chini ya meza. Ikafungiwa kule. Yoote yale, yalipomalizika kanda akapelekewa Mzee Karume. Akaisikilizaa, akawaambia, alaa, kumbe masuala yenyewe ndo kama hivi? Hapo nnakumbuka sasa, Mohamed “Mkunjeke” akiwa yeye ni Tupendane, akatoka akamwambia Mzee Karume, sasa wewe una utaratibu gani? Kwa sababu ajiziajizi matokeo yao huwa ndio. Sasa una mawazo gani. Aaa, wewe mfate Kisasi, na mfate Yusuf Himidi. Wakafatwa wale, kuja pale, likajadiliwa lile sualaa. Yusufu unajuwa alikuwa ni mtu mapresha. Anamwambia, bwana, unaweza kufilia mbali weye. Hawa watu hawa, ni wasomi hawa. Wana mipango ya kila aina hawa. Kwahivo watu kama hawa uwaondowe na mapema hawa. Hawa uwaachishe kazi na mapema hawa. Mzee Karume akamwita Kisasi. Kisasi njoo. Nnachokwambia, hawa watu hawa, wafanyie kazi, lakini usiwapeleke kwenye upelelezi uwemo u CID ikajulikana. Wafanyie kazi. Nakukabidhi Tupendane hawa. Ikabidi ile kazi inakwenda chini kwa chini. Chini kwa chini. Mzee kuja kuita mkutano People’s Palace, hapo sasa ndo palipokuwa pametoka kizaazaa cha Saadalla katowa bastola mfukoni kutaka kum shoot Mzee Karume. Siku ile ikabidi kamatakamata. Yeye, akina Jaha Ubwa hao, ndo mwanzo wa kuchukuliwa kundi la akina Othmani Sharifu, akina Hanga, akina nani, kuchukuliwachukuliwa. Kiinuwa Miguu. Kupelekwa kwa “Bwamkwe.” Matokeo yakee, akawaambia, kumbe fadhila ya punda mashuzi. Mimi nimewaweka mistari wa mbele vyeo vikubwavikubwa, leo matokeo yake wanataka kunigeuzia mimi, basi nawaanza wao mie hawa. Wakaitwa Tupendane wote wakaambiwa, wale kaburi lao likachimbwe Kama. Kachimbeni Kama.

Page 304: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba272

Limechimbwa handaki na Tupendane bwana. Likachimbwa lile handaki. Moja tu. Hayakuchimbwa mawili bwana. Moja tu. Akawaambia, haya. Kuchukuliwa wale jamaa, walivopelekwa kule, kila mmoja, tupwa mle, tupwa mle, sasa kila anayetupwa, chuma! Kila anayetupwa, chuma! Haya. Mchezo ukamalizika, wakafukia jamaa pale. Kurudi. Mohammed “Mkunjeke” nafsi yake mwenyewe ananihadisia. “Selemani, mambo mazito sasa hapa nchini.” Vipi? Ananiambia, “bwana we, kina Othmani Sharifu wanaambiwa wamesafirishwa wamepelekwa bara, si kweli.” Nikamwambia ilio kweli ni ipi? Akasema tumekwenda kuwazika Kama. Nikamwambia “muwongo wewe.” Akanamibia alaa! Tafuta siku wewee, tafuta baskeli, mimi yangu nnayo. Kweli, tukapanda baskeli mpaka Kama. Akanambia jitie kama unakwenda chooni. Hapa tulipofika hapa. Jitie kama unakwenda chooni. Utalikuta kaburi hapo chini ya midodo. Chini ya midodo. Nakwenda kweli nakuta kaburi moja, ah! Nikatazama. Pale pale, mimi nkatoka nkajifanya kama nachuchumaa pahala hivi. Kwasabu mimi isije ikawa kama mtu ananiona kama nimekuja kutazama tu pale. Unaona? Nikajitia kama kuchuchumaa pahala hivi halafu nikatoka pale, huyo nikamwambia “nimeona” akasema “basi hapo.” “Lakini wewe, wewe, wewe…” Kurudi kule ananiambia Hanga yuko pale, Othmani [Sharifu] yuko pale, Jaha Ubwa yuko pale, Mdungi Usi yuko pale. Anasema sisi tulikuwa ndani ya gari kama ni wachukuzi tumewafunga vitambaa veusi, sisi ndio tuliofukia. Baraza la Mapinduzi ndilo lilouwa. Lakini sasa bunduki walikuwa nazo askari. Ni haohao wanajeshi hawa. Walitolewa watatu, na bunduki zao. Watatu tu. Haina haja ya kwenda mkururo kule ati. Watatu tu. Anaangushwa chuma kinapigwa. Anaangushwa chuma kinapigwa. Mpaka wamemalizika. Karume alikuwepo. Yumo uchungu kwa namna alivomfikiria yule mtu alivomuweka. Kassim, hata weye? Hata weye unathubutu weye? Alikuwepo mwenyewee, Karume. Ndo mwenye kichwa cha Tupendane ati. Wale majeshi waliambiwa ”tusikie hadithi tu basi na nyie mtakuja hapa!” Kimyaa! Sasa kimya kile kimekwenda sa babu, imekuja vipi, kwamba kati ya hao wanajeshi mmoja akiwepo huyu Issa Kibwana! Katika hao watatu, mmoja ni huyu Issa Kibwana. Ehee, wakati huo yuko jeshini yule ati. Kugeuka utakuja kukuta baada ya jeshi na huku Tupendane! Unasikia hapo sasa? Ndo ukaja ukamuona Issa anakwambia “leo nikajiseme, mimi ndie niliofanya tendo hili. Pagumu?” Yeye kachukuliwa jeshini kwa kazi ile. Kufika pale, hakuna cha kusaidiwa. Mzee Karume anasema “piga sasa. Piga!” Kulikuwa na askari wengine wawili, mmoja alikuwa Mkamba, lakini Mkamba mwenyewe huyu, baadae, baada ya kustaafu kazi aliondoka akenda kwao Mombasa, Kenya. Mmoja huyu tukimwita Benedicto, kijana mmoja wa Kingoni. Benedicto baada ya kustaafu akakaa hapa akafikwa na maradhi, tumekwenda kumzika Kwerekwe. Kafia hapahapa. Watatu hao. Mkamba, Mzee Issa, Mruguru, na Benedicto. Mimi hayo nisingeyajuwa isipokuwa Mohamed “Mkunjeke.” Hii siri ni kubwa mno kwa sababu utakuja kukuta chairman [mwenyekiti] [Karume]

Page 305: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 273

mwenyewe kashiriki. “Mkunjeke” alipelekwa kwa “Bwamkwe” ili wale wakorofi wakorofi wale watakutana na “Mkunjeke.” “Mkunjeke” hana mswalie. Hana msalie. Akikwambia bwana vua nguo, vua nguo. Tumbukia karo hili, weka! Mtumbukizeni huko kwenye karo, funga karo! Unataka kubughudhi hapa? “Mkunjeke” Mkunjeke kweli! Alikuwa Mkunjeke kweli. Namba kumi na moja huyo bwana. Mdengereko so anachanja humu? Hataki masihara bwana. Hataki masihara huyo. Ukatili wake na wa Sefu [Bakari] sawasawa. Tupendane, historia zao, na kutokana na yale walioyafanya, ikaonekana, hawa bwana, Tupendane, hawasifikani tu lakini mambo walioyafanya Tupendane makubwa.

Mwalimu Nyerere na Visiwa va Ngazija—Mzee Salum

Mzee Nyerere, baada ya ule muungano na Zanzibar, fikra zangu ni kuwa ali­shindwa kuunganisha Uganda na Kenya wakawa kitu kimoja. Ile ndo ikawa ishavunjika. Basi akabadili mawazo yake. Akaona bora aendelee na ule ule mpango wake, kama alivofanya Zanzibar, aviunganishe vile visiwa. Visiwa va Komoro na visiwa va Seychelles vikaingia ndani ya plani. Ikawa yeye akapeleka majeshi Seychelles kumsaidia yule President alioko pale katika uchaguzi na nini, na akaleta na Komoro vilevile. Kwa wakati huo alikuwa Ali Saleh, ndo huyo kishapinduwa kamuondowa Mfaransa. Kina Ali Saleh wakatowa maneno bora Mfaransa aondolewe moja kwa moja. Sasa kina Ali Saleh yeye alikuwa Waziri tu wa Ulinzi lakini alikuwa ana nguvu na Raisi alikuwa akiitwa Said Ibrahim wakati huo. Wakapasisha kunako Bunge lao la Ngazija kuwa Mfaransa hatumtaki hapa kabisa sasa. Hatutaki ulinzi wao, na wala hatutaki wakamate mambo yetu na nchi za nje. Hii ilikuwa 1975–76. Ilivokuwa wao kisharia wameshapasisha pale Wafaransa wakahamaki sana, basi wakatoa na wao kuwa masaa arubaini na nane wataondoka Ngazija. Masaa arubaini na nane. Kwa sababu walijuwa Ngazija haitoweza kusimama bila ya wao.6 Sisi tunatoka, hakuna mambo tunakubaliana mkataba wa miaka miwili au mitatu au nini. Hamtutaki sisi tunaondoka kesho! Madege yakaanza kuja, na nini. Serious! Na wakafanya sabotage nyingi. Magari yao walijuwa hawachukuwi basi wakayatia chumvi, na nini, kunako petroli. Hapati mtu kitu! Kwa sababu walihamaki sasa. Wakatangaza, Komoro ikatangaza, kama sasa wanahitaji msaada na nini. Hawawezi kuiendesha nchi. Hawana maengineer wa uwanja wa ndege, hawana maengineer wa kituo cha matangazo—redio. Mimi nikajitolea. Nikaawaambia kazini kwangu kule East African Community nina ujuzi wa radio. Nilifanya kazi Radio Uganda, Radio Zanzibar kabla, na sasa niko na East African Community, nikisimamia Civil Aviation Engineering. Nilipata mafunzo kutoka Board of Trade in England kwa muda wa miaka mitano, ambayo nafikiri ilikuwa Wizara ya Ulinzi. Sasa mkinipa ruhusa nitakwenda

Page 306: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba274

kufanya uchunguzi Ngazija na wanahitajia kitu gani. Wakati huo niko Nairobi. Nilikuwa mkubwa engineer, mkubwa wa operations, wakati huohuo nilikuwa Chief Instructor wa East African School of Aviation. Wakakubali nende Ngazija. Na hii ilitoka juu kabisa kwa sababu tulipewa ruhusa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa kifupi niliruhusiwa kwenda Komoro. Nilikwenda na nikakaa wiki moja au mbili. Nilionana na Mawaziri wa pale, mmoja wao alikuwa Ali Saleh ambaye baadae akawa Raisi na tukazungumza kuhusu njia ya kuchukuwa katika kuisadia Ngazija. Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kusaidia, nchi za Afrika ya Mashariki zitaweza kusaidia. Basi nilikwenda tukafanya vile. Mimi niliona kuwa hawana engineers na ndio kwanza wamemaliza kuujenga uwanja wa kutuwa ndege. Airport nzuri yenye vyombo vipya. Kuna transmitters na nini…ukiwa ni kisiwa na unataka kuwasiliana na ndege inayoondoka kuulekea Afrika ya Kusini kwa mfano,, au Dar es Salaam, kabla hujaondoka ni lazima uiarifu nchi unokwenda, sasa zile transmitters zilikuwa zina nguvu na ya imma hazikumalizika au ziliharibiwa kwa makusudi. Nikarudi huku (Nairobi), mimi nikaambiwa na mabosi, wewe mwenyewe uko tayari kwenda? Nikawaambia, niko tayari. Unaona. Na wakati ule tangu wapo tulikuwa tuna problem Kilimanjaro na rada system, nilikuwa nakwenda kuwasaidia jamaa kuwa train, engineers wetu local, wakaniambia umeshakuwapo hapa kwa muda mrefu unaweza kwenda. Ndo yeye Nyerere, hao ndo watu wake bwana! Lakini hatukujuwa wakati ule. Sisi hatujui. Sisi tunaona tunasaidia tu. Nimeanza kujuwa nshafika Ngazija. Nimeshafika kule. Mimi nilikaa mwaka na miezi mitatu sio? Ndo nikajuwa kwa sababu kaanzisha, kaleta jeshi la kuwafundisha wananchi wa Komoro wenyewe. Alikuja mmoja akiitwa Major Idi, baadae Kanal na nini, kijana wa Arusha, ndo alokuwa mkubwa wa Jeshi la Tanzania, Komoro. Wakawa tayari wao kufanya biashara ya kuleta ngombe. Ngazija ilikuwa haina pesa. Ilijitangaza muflis kwa kufuata ushauri wa Umoja wa Mataifa (UN), au kitu kama hivo. Iliwabidi ili wapate misaada yaani. Na hiyo ilikuwa tamu kwa Nyerere. Mwanya! (Anacheka). Yeye analeta ngombe, analeta michele, kutoka Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje akawa anakuja pale, wa Ulinzi, wanakuja Komoro wakiondoka. Ali Saleh alisaidiwa na Nyerere kuja madarakani. Ile ilikuwa wakati wa biashara, sasa Ali Saleh yeye ana matatizo yake za kiserikali na Wafaransa na nini. Sasa hawajamuwacha sasa. Wamemsakama kwa sababu wameshaona kaingia Tanzania pale. Akitaka mashine, vitabu, kila kitu kwa Kifaransa. Kama sisi tulosoma kwa Kiingereza tulikua hatuwezi kusoma, tulikuwa hatuwezi kufanya kitu. Hatukuweza kusaidia. Wale watu wa biashara wakawa wao wameambiwa ziko cooperatives [vyama va ushirika] hapa. Sasa serikali ilipokuja ya Tanzania pale kutaka kufanya biashara, Ali Saleh kawaambia, sisi serikali, hatuhusiki na mambo ya biashara. Ziko cooperatives, nyinyi fanyeni mikataba yenu na wao. Sasa

Page 307: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 275

Tanzania wakawaalika wale Dar es Salaam, wakawachukuwa mabara, wakasain mkataba. Ikawa kila meli inokuja inaleta ngombe, inaleta michele, inaleta nini. Sasa muda ukapita, miezi mitatu, sita, wale wanangojea pesa, huku bara. Pesa hazendi. Hawa jamaa washakula na hawalipi. Sasa ikalazim aje Waziri kutoka Dar es Salaam, akaja Waziri wa kwanza, akazungumzaa, akarudi. Baada ya muda akaja Malecela nafikiri, na babake Ahmed Rajab, Mzee “Makopo”. Basi yeye aliletwa, angalau Mngazija, atafahamiana. Akapata tabu yule Waziri peke yake kuonana na Raisi. Kila akitaka amuone anaambiwa azungumze na Waziri wa Mambo ya Nje, azungumze na nani, na nini, mzee kashughulika sana, hawezi. Na yeye hawezi kurudi sasa. Anataka lazim apate jawabu kwenda kumwambia Mzee Nyerere. Sasa ule mpango wa biashara ndo Wangazija walopiga kelele kwa sababu wao Wangazija wanasema ikiwa umetupa sisi chakula, kama hiyo michele, unga, tumeshasain sisi tutakuwa tunawalipa. Lakini wao wanasisitiza kuwa sisi tuwalipe kwa karafuu, na nazi, cacao, langilangi, mali asili ya nchi. Wao wamezitaka hizo. Uwe mpango wa kubadilishana vitu kwa vitu na si vitu kwa pesa. Sasa hapo ndo ikawa ni mushkila. Wale Wangazija wakasema aaaa, hii haiwezekani. Mpango huo hakuna bwana. Vipi nyie mtatupa mavi sisi tukupeni dhahabu bwana! Anasema, wakawa wananishambulia mie sasa. Manake mimi ndo Mtanzania pale. Wananambia wewe ni mmoja katika hao. Wewe umeletwa hapa lakini sisi tunakwambia, kwanza sisi hatulewi, sisi Waislamu, vipi mnaleta nyinyi meli mmejaza ma whisky, manini, kutoka Tanzania. (Anacheka). Hatujaagizia sisi! Mnaleta sigireti, mmeleta masigara, hatuna watu wengi wa kuvuta sigara hapa. Wanovuta watu kidogo. Sasa hizi cooperatives haziwezi kuuza, zimejaa huko maghalani. Sasa wale jamaa walikuja kutoka Dar ikawa wamevunjika moyo sana. Wakafanyiwa mpango wakamuona Raisi, Ali Saleh, na Ali Saleh akawaambia, tizama skilizeni, e bwana, sisi kiserikali hatuwezi kuwaingilia hawa cooperatives kwa sababu hawa ni huru na nyie mmezungumza nao hawahawa, wamekuja Dar es Salaam, mmetia saini zenu, sisi hatumo! Lakini tunaweza kukusaidieni ili wakulipeni kidogokidogo, na hizi biashara ambazo wamelalamika kuwa wao hawataki, mchukuwe wenyewe mali yenu. Masigireti, ma whisky. (Anacheka). Lakini sasa wao walikuwa wanaiuzia serikali vitu va jeshi. Wakileta matandiko, magodoro na vitanda va vyuma, vinaletwa kwa meli kutoka Dar es Salaam, bunduki, umeona? Jeshi ndo wao kina Major Idi. Major Idi ndo in charge [dhamana]. Anaagizia lakini yote ile inatozwa serkali ya Komoro. Nafikiri mimi Komoro ilitia wasiwasi, hii itatufunga sisi kibiashara. Wanatutia kamba hapa kibiashara, baade tutaingizwa kwenye siasa zao za Tanzania, ambazo hatuzitaki. Waligutuka! Nakwambia wasiwasi walokuwa nao pale, ni kuwa hiyo wanaona hii, sisi tumemtowa Mfaransa, sasa hawa Waafrika wanatufunga sisi kibiashara. Wanatufunga kibiashara na vilevile, jeshi wameshalichukuwa wao, sasa la pili litakuwa bendera tuambiwe basi. Na yeye Mzee Nyerere akiwasabilia Komoro

Page 308: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba276

na Seycheles kuwasaidia kwa hali na mali. Malecela tulimuonea huruma. Sisi tulokuwa Watanzania, manake hajafaulu. Wale cooperatives walikuwa wagumu na serkali ilikataa kuingilia kati. Ikawa ni makosa ya wao serkali ya Tanzania kwanini wao hawajawaachia watu wa biashara. Ingekuwa wamewaachia watu wa biashara wa Tanzania pale isingekuwa tatizo. Baina ya watu wenyewe kwa wenyewe bila ya mkono. Wao wamefanya vengine. Yeye [Ali Saleh] hata siku moja hajawahi kumzuru [Nyeyere] lakini mashirikiano yalikuwepo. Ali Saleh alikuwa msoshalisti na aliuliwa walipoingia mamluki wa Kifaransa. Wakati fulani alifanya jambo ambalo alijuta. Alikwenda kunako radio akajiuzulu. Akasema tangu leo mimi nakuwachieni wenyewe Wangazija wa Komoro mchaguwe mtu wa kuiendesha hii nchi, na Major Idi atakamata jeshi mpaka mtakapochaguwa. Watu wote wa serikali, anatangaza kunako radio, watu wote wa serikali, kila mmoja arejee kwao kwa mamake akanyonye! Na nnakusikitikieni wenye mama vizee ambao maziwa yao yameshakauka. Kafika kumuachia nchi Major Idi na akamuamini! Lakini baada ya siku tatu, nne, tano, ikafanywa ghasia kama vile Egypt vile [wakati wa Gamal Abdel Nasser], “tunamtaka Raisi wetu arejee”. Akarudi, akachukuwa tena. Na ile Major Idi ilikuwa ni jina tu, jeshi atakuwa yeye huku, lakini vijana wake Ali Saleh ndo walokuwa wamelimiliki jeshi la nchi. Ikiitwa Komanda Muwasi. Vijana wetu hawa kina Ahmed Abdalla Mbamba, ambao wamesoma Unguja hao wote, na yeye mmoja alikuwa memba katika hiyo MOLINACO, mimi nnaye, tulikuwa pamoja Nairobi. Waziri wa Mambo ya Ndani, Salim Himidi, anatoka Zanzibar. Yuko Paris sasa. Amin Ali Mvuani alikuwa United Nations [Umoja wa Mataifa]. Wote hao wamemaliza pamoja Cambridge Unguja. Amin kasoma Kuwait baadae, baadae kenda Sorbonne na akenda special courses za foreign affairs [kozi maalumu za mambo ya nchi za nje] Ufaransa. Yuhai, yeye yuko United Nations mpaka leo. Sasa mfanyaji kazi Congo. United Nations Representative. Anakuja hapa. Si tunakwenda kwenye mikutano yetu ya ITU hii ya Telecoms ya United Nations, tunakuwa na jamaa hapa, mimi nime represent Kenya, au nime represent Komoro, in Geneva, tunawakuta jamaa kutoka Zanzibar au kutoka Oman, from Zanzibar, ni members wetu. Tunawakuta jamaa wengine kutoka nchi nyengine, wote walewale. Abdurahman Babu hakuwa na mahusiano ya karibu hali kwao pale Ngazija. Hata ule wakati wa Ali Saleh utafikiria yeye kama ni Msoshalisti atajaribu kuja Ngazija. Hakufanya hivo. Lakini jina la “Comrades” lilikuwa baya Comoro. Kwa sababu ya Karume kuwarejesha Wangazija wa Zanzibar [waliokuwa raia wa Mfaransa], akawatangazia wafanye tajnisi, na wengine wale ambao hawajafanya wakarejeshwa, ilimfanya kila Mzanzibari pale anokuja mpya anaitwa “Comrade.” “Wewe Komred wewe, mtu mbaya wewe.” Sidhani kama Babu angeweza ku survive. Propaganda ilikuwa mbaya dhidi ya Makomred. Imeiharibu ile alaka

Page 309: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 277

[na Zanzibar] kabisa, nzuri ilokuweko, baina ya miaka na makarne. Ile kusema tu Karume hawa Wangazija si wananchi wa hapa, basi ile ilikoroga mambo yote. Mpaka wengine mimi niliwaona Ngazija ambao sijajuwa mie kama wale walikuwa nayo asli au hawana. Mmoja nimemkuta kule, Ali Sugu. Alitoka Unguja, yeye ni Muunguja, bila shaka. Lakini nimemkuta katika watu walorejeshwa. Yeye Ali Sugu, na wale wazee wa kiserikali walokuwa maofisa wa polisi na nini, wale wote walichukuliwa kumlinda Raisi wa Ngazija kule. Aliwafanya ndo aide-de-camp [msaidizi wa Rais], kama huyu Ahmed Darwesh, ambaye alikuweko Zanzibar lakini alikuwa yeye ni Inspekta wa Polisi Dar es Salaam. Bwana Aboud Said alikuwa Inspekta Aboud Said Zanzibar, katika watu waloondolewa. Bwana Hassan Muhammed Mshangama, Inspekta Hassan Mshangama. Kama Hassan Mshangama alikuwa ndo mkubwa wa uhamiaji pamoja na Darwesh, na wakati huohuo ni aide-de-camp wa Raisi, wanamtizama Raisi. Wakati huo alikuwa President 1970 ile, Said Muhammed bin Sheikh. Ndo alokuwa President. Sasa yeye alivofanya Said Mohammed bin Sheikh, yeye alihudhuria uhuru wa Zanzibar, ile Disemba 10, 1963. Kanambia mwenyewe kuwa mimi na Naibu wangu Prince Said Ibrahim, sote tulialikwa, tulikwenda tulikuweko Mnazi Moja. Sasa kuna uzuri, jambo moja ambalo Wazanzibari Mwenye Enzi Mungu awabarik, wana umoja. Kuwa hata wakiwa wana ugomvi wao wa ndani kwa ndani Zanzibar lakini wakikutana nje yale yote yanasahauliwa. Utaona wanakuwa pamoja na nini. Sasa yale mambo yalivotokea Zanzibar, kama Wazanzibari wengine wakarejeshwa Komoro, serikali ya Komoro ikawapokea lakini hata na wananchi wa Komoro wao wenyewe wanazo alaka zile za miaka, wakawachukuwa watu, wakawapa viwanja, na serkali vilevile ya Komoro ikawa inawa interview [hoji]. Watu wanakuwa wanahojiwa na kamati. Walifanya kamati ya kuwapokea na kuwauliza vitu gani wanataka. Ikiwa wewe unataka kulima, mkulima, basi serikali ilikuwa imetenga ardhi kwa alotoka Zanzibar. Kama eka sijui ngapi wakipewa. Mmoja ni yeye Ali Sugu na jamaa wengine. Wamepewa ardhi. Walokuwa wamesoma, kapenta kama wajomba zetu na nini, au engineers, wakachukuliwa na Public Works Department au Vava Publik wenyewe wanaita, au hiyo polisi. Lakini Nairobi, kulikuwa na watu, vijana ambao wamejitolea na wao. Watu wanokimbia, kwa sababu ilikuwa wasiwasi ukikimbia wewe kutoka Zanzibar, unakimbilia Dar es Salaam pale halafu ukipata njia unaingia Mombasa. Sasa mpaka Mombasa watu hawana salama. Kuna watu wengine, muhimu wale, wakawa wanakimbia wanakuja zao Nairobi. Kama kaja nakumbuka Salum Hakim Khuseibi, yeye nafikiri alipokimbia akenda Dar es Salaam, kutoka Dar es Salaam akenda upande wa Kongo, kutokea Kongo ndo akarejea kwa Nairobi. Sasa yeye Salim akachukuliwa. Kuna mwengine Nassor Muhammed Miskiri, huyu alokuwa Cairo sasa yuko hapa alikuwa akifanya kazi Gulf Air. Ahmed Nassor Riyami, huyu wa hapa wa msikiti hapa. Mara nyingine tukipigiwa simu mtu yuko Dar es Salaam bado, bwana mimi nakuja kwa basi fulani, nipokee bwana kwa

Page 310: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba278

hisani yako, mimi sina pakwenda bwana. Wengine walikuwa wapita njia, akina Daudi Muhammed huyu, anaitwa Babuchi. Anapita yeye tunakwenda kumpokea halafu siku ya pili yake au ya tatu anapanda ndege anakwenda zake Uingereza. Anakuwa keshafanya mipango yake. Yeye transit. Wengine wanakaa mpaka mezi sita. Wengine wanatafuta kazi tena palepale. Lakini ile mimi nasema kuwa bado ule utu wetu ule wa Kizanzibari Mwenye Enzi Mungu auendeleze, watu hawajatupana yaani. Na ndo nimeuona Ngazija, nimeuona huku Nairobi, Mombasa, wengine wakati tuko Uganda. Wanakuja Uganda jamaa, jee una­kwenda wapi? Bwana mimi nataka kwenda Ulaya bwana. Sasa mbona umekuja Uganda? Ndo nnafanya kazi hapa kiasi mwaka mmoja miwili nkipata pesa ntakata tikti ntafika Sudani halafu Cairo, ntakwenda mpaka ntafika. Njia sku hizo ilikuwa tabu. Mimi mwenyewe nimewahi kupokea watu nkakaa nao miaka miwili Kampala. Wametafuta kazi, wafanye pesa, wakate tikiti, wende zao mbele. Wengine wamekwenda Europe, wengine wametafuta ma scholarship kwenda kusoma.

Bwana Amani Thani Fairoz alikuwa Katibu Mkuu wa pili wa Chama cha Zanzibar Nationalist Party baada ya Abdulrahman Mohammed Babu.

Bwana Amani Thani Fairoz

Oscar Kambona namna alivonihadithia mwenyewe mambo ya mapinduzi ya Zanzibar kwamba hili jambo walikuwa nalo baina ya, khasa, yeye Kambona, Nyerere na Kawawa kwa muda mrefu sana. Waliona wao kwamba kwa mwendo huu wa uchaguzi Afro­Shirazi haitoweza kushinda. Na ikiwa haitoweza kushinda wao hawatoweza kuwa na mamlaka yoyote juu ya Zanzibar. Kwa hivyo wao waliweka mipango hii zamani wafanye lazima waipinduwe serikali yoyote itayakuwa sio ya Afro­Shirazi. Haya ni maneno ya Kambona mwenyewe. Sasa siku ile ya mapinduzi, yalipotokeya yale, ikawa mawaziri wanakwenda mbio kutaka msaada khasa kwa Balozi wa Kiingereza alokuwepo Zanzibar, anaitwa Crosswaith. Walikwenda kutaka msaada kwake. Sasa ilipofika habari kuwa msaada huu uko Kenya, askari wa Kiingereza wako Kenya, hapana shaka huyu Crosswaith alipeleka habari kwamba hawa mawaziri wanataka msaada kutoka Kenya. Kwa hivo Nyerere alimtoa Kambona kwenda kuonana na Jomo Kenyatta ili kuzuwia lisije jeshi lolote la kutoka kule. Jeshi haliwezi kuondoka mpaka kwa rukhsa ya nchi ile. Kwa hivo Kambona alikwenda kule lakini Jomo Kenyatta alikuwa hayuko mjini akaonana na Odinga. Akamwambia kama kuna mpango wa kutakiwa jeshi la Kiingereza lende likazuwie mapinduzi, na haya mapinduzi ni Waafrika walofanya kwa hivo likipelekwa jeshi hili basi itakuwa linakwenda

Page 311: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Hayeshi Majuto Yao 279

kuwauwa ndugu zao. Na nyie mna nguvu la kulizuwia kwa hiyo tunaomba, Mwalimu Nyerere anaomba kwamba msifanye kitendo hicho. Hayo maneno ya mwenyewe Kambona. Wakawa wamefunga njia kulizuwia jeshi la Kiingereza lisende Zanzibar. Kwa hakika jeshi lilikuwa limeshakuwepo uwanja wa ndege. Liko tayari kuondoka. Kambona kwa nafsi yake ndo alopelekwa na Nyerere. Kanambia mwenyewe hayo. Pia alisema Kambona, kuwa, wacha mambo ya kupinduwa, tangu ilipokuwa mambo ya uchaguzi, anasema ilikuwepo kamati maalumu ya kupeleka watu Zanzibar, toka wakti wa uchaguzi mpaka katika masala ya mapinduzi. Kanielezea kuwa walipeleka watu wengi kutoka bara, kutoka Tanganyika. Aliniambia watu wametoka kwetu. Alitumia neno hilo. Alisema madam Zanzibar Serikali atakuwa yuko Mfalme ndani yake wanaona kwao wao hautokuwa mlingano mzuri baina ya jirani kwa jirani. Mimi nikamwambia kwamba, hilo tu au kuna suala la dini limo ndani yake? Hiyo khabari ya ufalme tu au na dini ilikuwa ndani yake Nyerere anayo? Akanambia Kambona kuwa Nyerere alisema tujaribu kama tutakavoweza kupunguza nguvu za Uislamu katika Zanzibar. Na ikiwa hatutokuwa na serikali Zanzibar hatutomudu kulifanya hilo. Yeye akanijibu, na dini ipo ndani yake. Hilo ndo jibu lake yeye. Hilo pia kanizungumzia. Katika hizo plan zao. Kambona alinihadithia mengi. Alisema, Mwalimu unavomuona vile sivo alivo. Nikamuuliza nini khasa ugomvi wenu, wewe Kambona na Nyerere? Anavosema yeye tangu yalipotokea majaribio ya mapinduzi tarehe 20 Januari 1964. Wale majeshi wakamuendea yeye Kambona na kumtaka achukuwe nafasi ya Nyerere. Anasema mimi nilikataa na mimi ndo niliowabembeleza hao majeshi. Tangu pale alimuona Mwalimu kama ana wasiwasi na mimi. Na ilipotokea Hanga kutofahamiana na Karume na yeye Kambona anafahamiana na Hanga kwa mengi na wako pamoja kila mara ikawa Nyerere kaweka askari wa siri kuwatizama mwendo wao, nini wanafanya, nani wanaonana nao, wanakwenda wapi. Nyerere kafanya hayo. Akasema kwa bahati nzuri wale watu aliowaekea Nyerere walikuwemo ndani yake watu ambao walikuwa wasikilizana sana na Kambona. Wakamwambia tahadhar bwana, Mwalimu ana wasiwasi sana juu yako hasa kuhusu wewe na huyu rafiki yako Hanga kwa hiyo tumepewa kazi kulitizama kila jambo lako unalolifanya. Na hilo ndilo lilomfanya Kambona awe na wasiwasi kwa vile anavomjuwa yeye Nyerere akishaanza mambo kama hayo mara hutumia njia zake za kumpoteza mtu. Amesema Nyerere kawapoteza watu wengi usione hivi. Na ndo sababu ya Kambona kuondoka katika nchi. Tulipoonana naye sisi Kambona alikuwa kabadilika hali. Yeye alikuwa anasema kwamba Muungano umefanywa kwa njia si za barabara. Yeye akiwafika kuwepo Muungano. Si kwa sababu ya Zanzibar na Tanganyika tu, lakini yeye fikra zake Muungano uwepo Afrika Mashariki lakini kwa njia za matengenezo si za kwa njia hizo zilizokwenda ambazo Nyerere katumia kama kumzidi nguvu tu Karume.

Page 312: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Saba280

Lakini haukuwa mwendo barabara. Muungano haukufanywa kwa mujibu wa maadili ya kuungana. Kwa hivo yeye anasema kwamba hata ikiwa tutaigombowa Zanzibar itakuwa uzuri sana ikiwa tutakuwa sote pamoja na ndio maana akataka kushirikiana na sisi katika kuigomboa Tanzania. Kitwana Kondo alikuwa katika watu ambao walikuwa karibu sana na Kambona. Saidi Tewa pia alikuwa yuko karibu naye sana. Kama Fundikira ameshafariki. Alikuwa akiwasiliana naye. Aliwahi kuwa karibu na Chipaka lakini naona kama waliwachana baadae. Khasa alikuwa amekamatana sana na Kitwana Kondo. Kondo alikuwa trade unionist huyu. Very powerful wakati wake. Na huyu [Kitwana Kondo] alikamatana naye mpaka kufa Kambona. Kambona alikuwa na imani na alikuwa akitaassaf [akiona vibaya] sana juu yetu kwa mambo yaliopitikana kwetu Zanzibar. Alipokwenda kuonana na Sheikh Ali Muhsin Cairo alisema nilikuwa naona tabu kumkabil mtu kama yule kwa ubaya tuliokuwa tumeufanya sisi. Alikuwa na Bwana Ahmed Seif Kharusi [London] kabla ya Sheikh Ali kutoka jela. Alipotoka akamwambia Bwana Ahmed kwamba sasa midam mzee katoka nataka kwenda kuonana naye kwa hiyo nitengezee nikaonane naye. Bwana Ahmed akazungumza na Sheikh Ali na Sheikh Ali akasema yeye tayari na wakti wowote aje. Kambona akafanya safari kutoka Uingereza kwenda Cairo. Yeye Kambona alinihadithia kwa urefu mambo ya Hanga tangu kuondoka, kukamatwa, mpaka alipokwenda Guinea akaonana na Rais Ahmed Sekou Toure, akenda kwake Uingereza akaonana naye, yeye akamshauri Hanga asirejee Tanzania. Akamwambia huu si wakati wa kurejea Tanzania. Wewe humjui Mwalimu kama ninavomjuwa mie. Mimi namjua zaidi. Hatojali ahadi yoyote atakapotaka kulifanya jambo lake. Usende sasa. Lakini Waswahili wanasema shikio la kufa halisikii dawa.

Page 313: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na NaneKosa la Mzee Nyerere

Sisi Wazanaki tuna sifa mbili kwa majirani zetu…Kwanza, ni wajanja, na sifa ya pili ambayo inaifuata sifa ya kwanza, ni kuwa si waaminifu. Watu husema ‘Rafiki wa Kizanaki atakuuwa’ ambayo si kweli. Sijui vipi tumeipata sifa hiyo… —Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ningekuwa na uwezo, ningevikokota visiwa va Zanzibar nikavitupilia mbali katikati ya Bahari ya Hindi. —William Edgett Smith

Wanayaita mapinduzi, lakini sisi tunasema mavamizi. —Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah

Mzee Faraji

Nilipata kusikia kutoka kwa mmoja wa Marais wa zamani wa Zanzibar, kuwa manunguniko na madai ya Wazanzibari yaliyoanza katika miaka ya 70; kuhusu kuvunjwa mkataba wa 1964, kwa manufaa ya Tanganyika; madai hayo yalikuwa yakiwaudhi sana viongozi wa Tanganyika. Hivyo siku moja Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, akamwambia Raisi wa Muungano (wakati huo) Mwalimu Nyerere, kwamba kwanini hawavunji mbali muungano ili wapumzike na “kelele” za Wazanzibari? Inasemekana Mwalimu Nyerere alimjibu kwa kumkatalia kwa kusema mengi pamoja na “…tukiwaachia tu, utaona jinsi mapesa ya Waislamu na Waarabu yatakavyo miminika Zanzibar…hapana, hatuwaachii.” Laiti shida ya Mwalimu Nyerere ingelikuwa nae anazitaka pesa hizo kwa ajili ya Tanganyika, kisa kifuatacho kisingelitokea. Kwa mujibu wa kisa hiki kama kilivyosimuliwa na Rais huyo wa zamani [wa Zanzibar], Mwalimu Nyerere, wakati huo akiwa ameshastaafu, alipita akiwa safarini, katika uwanja wa ndege Jeddah, Saudi Arabia. Balozi wa Tanzania aliyekuwepo Saudi Arabia ilimlazimu ki­protokoli, kwenda uwanja wa ndege kuzungumza nae katika muda wa transit. Pamoja na mambo mengine, Balozi huyo alimwambia Mwalimu Nyerere

Page 314: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nane282

“…katika nchi hizi kuna mapesa mengi, na jamaa yaelekea wapo tayari kutusaidia mipango yetu mingi ya maendeleo, ilimradi tu, tuwaombe.” Nasikia Mwalimu alimjibu kwa mkato na kwa kiasi cha kuonekana kakasirishwa: “Hapana. Acha kabisa!”1

Ni dhahiri, mpishi wa mapinduzi na muungano, Mwalimu Nyerere, alikuwa ameacha “grand design” [mpango mkubwa] katika kuipata Zanzibar, bila shaka si kwa manufaa ya nchi (Tanganyika na Zanzibar), bali kwa manufaa ya wale wasiowatakia mema Waislam (pamoja na Waarabu ambao wengi wao ni Waislam). Niliwahi kumuuliza mmoja wa Maraisi waliopita wa Zanzibar kama aliwahi kuuona waraka asilia [wa Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika] uliotiwa saini tarehe 26 April 1964, akaniambia hapana, hajawahi kuuona. Nikamuuliza tena, je, yule uliyemuachia nafasi yako unaweza kumuuliza kama kawahi kuuona? Akanijibu: “hapana haja ya kumuuliza, kwa sababu nafahamu kuwa nae pia hajauona.” Kwa kawaida nchi inapotaka kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN), hutowa taarifa ya mwezi mmoja na kisha kuwasilisha maelezo/vielelezo na vithibitisho kuwa ni nchi (yenye sifa ya kuwa na Utaifa), inayostahili heshma ya uwanachama huo. Nchi zilizokuwa zinapata uhuru wake toka ukoloni zilitoa taarifa ambayo tarehe yake ya mwisho ilisadifia na tarehe ya kupandisha bendera mpya. Hivyo nchi iliyojisajili UN na kupewa kiti, bila shaka ilipobadili nafasi iliyoiondosha uwananchi wake, haikuondoka katika umoja huo bila ya taarifa yoyote. Bila shaka patakuwepo maelezo na vielelezo vilivyokubalika kiti chake kurudishwa, bendera yake kushushwa katika mlingoti wa UN, na majukumu yake kame vile michango n.k., kufutwa. Vipi leo nchi kama hiyo isiwe na hati halisi ya makubaliano ya muungano ambayo wananchi waliona Sheikh Karume na Mwalimu Nyerere wakisaini na kupeana April 26, 1964? Na vipi nchi isiwe hata na zile nakala halisi za vielelezo japo vile vilivyopelekwa UN kuhusu suala zito la utaifa wake? Au hata ushahidi wa kisheria kuwa hakuna nchi inayoitwa “Tanganyika” au yakuwapi maelezo/vielelezo kuhusu kuongezeka kwa mambo ya muungano na nani alotia saini kwa niaba ya Zanzibar? Ni saini yake au ni ya nani na kwa ushahidi gani wa kisheria? Wenye kuumizwa na yote hayo khasa ni Wazanzibari na si Watanganyika. Mapinduzi ndo yalioipinduwa nusu ya jamii ya Zanzibar ilioshinda uchaguzi [wa Julai 1963]. Mapinduzi ndo yaloleta muungano na kuyapinduwa makubaliano ya mwanzo ya muungano. Mapinduzi ndo yaliokifuta kiti cha Zanzibar UN kwa nia ambazo Wazanzibari bado hawajazitambuwa. Mapinduzi ndio yaliomuondowa Al Hajj Aboud Jumbe madarakani, na kilichomponza khasa Mzee Jumbe ni pale alipolianzisha Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA); yakamtia ndani Maalim Seif Sharif Hamad; na ndiyo yaliyopelekea Dk. Salmin Amour akataliwe kuiingiza Zanzibar/Tanzania katika OIC na kuiakhirishia Zanzibar kutojiunga na taasisi hiyo. Ndiyo yaliyoifanya Katiba ya nchi itamke kuwa Raisi wa Zanzibar

Page 315: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kosa la Mzee Nyerere 283

siyo tena Makamo wa Kwanza wa Rais wa muungano, kama ilivotamkwa 1964. Na ndiyo yaliyo “thibitisha” kuwa nchi ya Zanzibar sasa ni Mkoa kama mkoa wowote Tanzania. Na kubwa zaidi, hayo ndiyo yaliyofanywa kuwaonesha rasmi Wazanzibari kuwa hata ndani ya chama kilichoundwa kwa kuunganisha ASP na TANU, TANU, CCM Bara, ndiyo itakayoamua nani atagombea Uraisi Zanzibar. Hivi sasa hakuna udhibiti kwa watu kutoka bara kuingia na kuishi Zanzibar. Lengo ni kubadilisha “demographic situation in favor” [hali ya wingi wa watu] ya bara katika miaka michache ijayo. Na hiyo population [idadi ya watu] mpya inaandaliwa kuwa “superior” katika uchumi, ilimu na ushawishi wa kisiasa. Wapemba kuunga mkono chama kinachoongozwa na Maalim Seif Sharifu, Mpemba, university graduate [mhitimu wa Chuo Kikuu] na mzoefu katika serikali na siasa; mtu ambae alikhitalifiana na Mwalimu Nyerere inakaa vizuri katika “grand design” [mkakati mkubwa] ya Mwalimu ya kuwatenga Waunguja. Nyerere alipoenda Zanzibar kueleza kwa nini CCM iliwafukuza Seif na wenzake, alimtaja Seif kama watu “…tuliokuwa tukiwapokea katika chama pasipo kuwachunguza kwa undani ili kujua asili yao na huko watokako…” Mbali ya maneno hayo, Nyerere pia alianzisha propaganda za kwamba watu wenye rangi ya kuchovya kama ya Seif, japo si Waarabu, alitaka watazamwe kama Waarabu. Siasa zao zitakuwa za kutaka kumrudisha Mwarabu Zanzibar. Nyerere pia alianzisha lugha ya kampeni ya “kuwanasihi” watu wa bara (Tanganyika), kama moja ya propaganda zake za kujenga hoja ya kujitetea pale itakapoonekana kuwa bara inatumia nguvu kulazimisha muungano. Ikawa akisema mara kwa mara kuwa “…hawa wanataka kuuvunja muungano, mkiwaachia, watauana ovyo…sasa wameshaanza kugawanyika na kubaguana, kati ya Wazanzibari na Wazanzibara…Wapemba na Waunguja…” Ingawa hoja hiyo inakusudiwa kuwaomba Watanganyika “kuwanusuru” Wazanzibari ili wasi­ jeuana, haikumpitikia Mwalimu wala wengineo kuhoji; kama Wazanzibari wame gawika kiasi hicho, msimamo wa uhalali wa muungano ukoje hivi sasa? Tanganyika hivi sasa imeungana na nani; Wapemba, Waunguja, Wazanzibari au Wazanzibara? Siri ya mapinduzi ya wazee inatowa jawabu lililo safi; Tanganyika iliungana na Waafrika kutoka bara kuwapinduwa Wapemba na Waunguja—Wazanzibari. Katika mambo ya kudhulumiana nchi, wajanja hufanya kila njia kuepuka masuala ya mfumo. Watakupelekeni kwenye utendaji kazi. Huko mtazungumza na wale waliopewa kazi ya ku “run” government [kuendesha serikali]. Hamtokutana tena na wale wanao “rule” [wanaotawala]. Sioni sahihi kuutegemea Muwafaka badala ya Mkataba wa Muungano na Katiba na sheria za nchi, kutupa muelekeo wa kule tunakostahili kwenda. Hivyo hivyo, siamini kuwa mtu atayewekwa na madhalim katika madaraka ya nchi, ana uwezo wa kujua na kuipeleka nchi hiyo pahali pasipokuwa pale panapo takiwa na madhalim hao. Kwa vyoyote vile, endapo tutatanabahi, tukatambua kuwa nguvu za wananchi

Page 316: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nane284

ni muhimu kuliko chochote, na kwamba nguvu hizo hazipatikani ila kwa kuwatoa katika umasikini wa kiza cha ujinga wa ilimu duni; tunakoelekea si kubaya. Kuwatowa wananchi kunako giza la tunakotoka na Zanzibar kujiwakilisha nchi za nje, kuujenga na kuulinda uchumi wake, pamoja na kulindwa na Wazanzibari, ni kuzuri, na huko ndiko kwa kuanzia.

Mzee Ayubu

Kisera Mzanzibari mwenyeji hakushirikishwa kunako mapinduzi. Na ndo mpango ulivokuwa! We ndugu yangu na ukisikia nimekufa leo lazima ufike. Ukitoka leo mimi nijuwe. Ndo alivotuwacha mzee hapa. Mimi nilipewa kazi na Afro­Shirazi. Nakumbukia mimi niko mle nakwenda na yale. Karibu yangu akawa huyu marehemu Hafidh Suleiman alokuwa memba wa Baraza la Mapinduzi. Huyu mtu wa Tanga lakini ndo katika hawa waliozaliwa hapa. Mdigo. Wazee wake walipofika walifikia wapi…Kinduni na ndo alipokwendazikwa alipokufa. Lakini wakahamahama ndo wakaja pale Kizimbani kwa wajomba zake kina Mbaruku Juma. Saidi Bavuai ni watu wa Mlingotini, hapa Bagamoyo. Kwani ukafata sana, watu walopinduwa ni kutoka nje. Daislama, Tanga. Wengi na ndo wamezalika hapa, kwa muda mrefu wamekulia hapa. Nilipoingia hasa nikawa nayapata ya juu kidogo, nadokolewa. Ya chini ndo nilikuwa nayo yote! Ya juu yakidondoka nilikuwa napewa. Sasa kuhusu kuitowa siri ya mapinduzi, ujumbe huo sasa hivi utoke kwa vijana bila ya kuogopa lakini kuwe na watu wenye historia nzuri ye kuweza kuwaeleza vijana. Sasa ni kuanza upya kuwaekea sawa na kuendelea na umoja wetu. Kwanza. Mpaka hali ya Unguja yenyewe, sisi tulioko hapa, tukubaliane. Hiyo ije iwe ni nafasi ya pili sasa ya kutaka kuja kupafatuwa, tushikamane. Kwa sababu sisi wenyewe hapa bado kuna kundi liko tayari kutuangusha. La kwanza tuondoshe haya yaliopo hapa tukamatane. Tuondoe mfarakano uliopo hapa…Sikiliza. Tuondoshe la Upemba na Uunguja maana lipo na lina nguvu. Sasa itakuwa watu wakeshatambua kama hivi watu wanabaguwana, huyu ndie, huyu sie, kiini hawakijuwi. Hao walopinduwa inasemekana ni watu wa nje. Si Wazanzibari. Ufasaha na hivo ilivokuwa hapaelezwi. Sasa kueleza ni hawa walohusika, ni vipi? Hawa walikuja ni kama mafundi tu lakini wenyewe waloifanya hii asili zao na walivo ni hivii! Mfaranyaki alikuwepo Songea. Akenga akachukuliwa John Okello. John Okello ndo alokuwepo hapa. Wakapewa maelekezo kwa dhamana ya kwamba mnakuja kufanya haya lakini si kwakua mtakuwa watawala. Nyie mtapata malipo mpaka kufa kwenu. Watu watatu wale [Okello, Ingine na Mfaranyaki]. Sasa vipi itakavokuwa? Hawa watu watatu ndo watakuwa viongozi. Lakini wapatikane vilevile watu watakaokuwa wanakutana na hawa. Nguvu kazi. Ndo wakachuku­

Page 317: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kosa la Mzee Nyerere 285

liwa waliokubali maana baadhi ya wengine sikudanganyi kwenye plani ya hayo mambo hawakuwemo. Kama Aboud Jumbe. Kuna watu wengi hawajahusishwa makusudi. Aboud Jumbe hajakuwemo makusudi. Pakapimwaaa, pakaonekana wapatikane watu sasa na ikafatwa asili. Hayo nokwambia ni ya hakika hayo. Asili zao! Hao wote asili zao bara. Mizizi yao ya karibuni. Hao wote Kamati ya Watu 14 asili zao bara lakini wako walozaliwa Zanzibar. Ibrahim Makungu pia. Kwao Bweleo hapo na walitokea Kunduchi. Sasa wakatafutwa asili, wazee wao. Hiyo nakwambia nakupa ya uhakika. Wakadurusiwa wote hawa asili zao. Wengine wametokea Mafia na Kilwa huko. Wandengereko, Wayao. Wana asili zao. Na wanaeleweka. Wanatambulikana. Hawa asili wataweza kuizuwia mpaka tutafikia tutakapopafikia. Hiyo ndo ikaitwa klabu ya mapinduzi ya watu wenye kukamata siri mpaka tufanikiwe. Isivuje! Katika shughuli za ku mobile [kusu­kuma] wakapatikana wawili, yuko kijana mmoja anaitwa Agostino Mikaili, yuko Chuini, na mimi mmoja. Vijana! Ndo tukaja tukaelezwa na Hafidh Sulemani na Saidi Washoto. Tukajakufanya kikao mwenyekiti alikuwa Aboud Jumbe, Mwembe Makumbi. Hiyo ilikuwa ni final [ya mwisho] sasa lakini hii siri [ Jumbe] haijuwi. Siri haijui yule. Atakuja kuupiga mtindi atasema. Ikawa sisi tunafundisha yale mafundisho sasa. Wafundishaji ni walewale kina John Okello. Dakika 15 tunatoa maelekezo. Sisi tulikuwa Kichwele, na Jozani, na Masingini, wanakuja kutoa yale maelekezo. Yusuf Himidi alihusika na ubebaji wa silaha za mashoka na mapanga. Wakati ule anafanya kazi PWD (Public Works Department). Ana yale magari ya malori. Silaha liziwekwa kwa Mzee Mwinkondo, mtu mzima, keshafariki zamani. Mfaranyaki, Ingine na Okello walikuwa wanapita siku maalum katika wiki wanatoa mafundisho silaha na mbinu za kivitavita. Sasa bado. Kama bado iwe vipi? Mimi na huyo nlokutajia (Agostino Mikaili) ndo tukapata kazi ya kuingia Mtoni. Nani atamuingia Juma Maneno Muheza? Yeye alikuwa msaidizi wa kituo cha Police Mobile Force (PMF). Wa kumuingia alikuwa Saidi Washoto, Myamwezi mwenzake. Siku ikifika atuwekee watu wenye kulifahamu lengo letu. Wakatafutwa akina Kisasi. Akafungashwa Kisasi na watu. Mzee Adam wa Magereza na yeye akafungashwa na watu. Akapigwa msasaa, akakaa sawa! Wazungu hawakulijuwa. Hawakujuwa na wangejuwa pangelikuwa na standby [tahadhari] kubwa. Kulikuwa na mazungumzo ya blah blah [ya kubabaisha] tu. Kwa sababu walikuwa ni watu ambao hawako karibu na watu wengi kuweza kujuwa mambo. Kwa hiyo mtu wake Mzungu wa kumsogelea ni wale waliokuwa karibu naye tu na si askari wadogowadogo. Si rahisi. Ilipobadilika Magereza, Ziwani na Mtoni, ikawa rahisi. Tengenezeni mchezo. Ikatayarishwa Fete na pakatayarishwa na madansa hapa Raha Leo. Siri ya mapinduzi imefichika kwa sababu ilikuwa kwenye vikao vikuu vijana walikuwa hawakuelezwa! Hii nokwambia mie ni kubwa sana hii. Wataelezwa

Page 318: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nane286

vipi na hao nnaokuambia [Wazanzibari] pengine hawaaminiki? Kina mzee Mloo wanajuwa! Viongozi wale watu wazima ndani ya CUF wote wanaujuwa undani wa mapinduzi. Kuna suala la yule Sayyid [ Jamshid] kule alikuwa anadai kuwa hajapinduliwa na Wazanzibari, nimepinduliwa na watu kutoka njee! Kabisaa! Aliitoa hiyo Jamshid alipokuwa Ulaya na ikitisha ndani ya Zanzibar. Alisema eti. Mimi sikupinduliwa na Wazanzibari. Mimi nimepinduliwa na watu kutoka nje! Ikiogopwa hiyo! Hiyo ndo point [nukta] nakupa mimi. Point [nukta] hiyo! Uingereza katika kuhojiwa hilo alilijibu. Watu wakaona sasa hatari. Sasa ikabidi wazee walinganganie hilo kutolitowa. Kwa sababu ilikuwa yule asipate pakushika. Angeipata hiyo angelifanya uchunguzi wa hali ya juu. Uhalali wa mapinduzi ya nchi ya Zanzibar! Na sasa wale ilijulikana wazi kuwa ni watu kutoka nje. Sasa ikaogopwa moja kwa moja hiyo! Na wakati huu, nakwambia, bado wengi hawawezi kuitoa na wengi hawapewi na wanaiosoma tu ndani ya history. Blah blah [babaisha] tupu kuisoma kwao. Sasa wataificha mpaka lini? Sasa hiyo ndo question mark [suala la kujiuliza] ya kuikalia na kuiweka sawa. Kwa sababu pasipoeleweka pakawekwa sawa bado itakuwa inakwenda na huko mbele itakuja na kutokea hatari kubwa zaidi. Sasa hapo hawa waliopo hivi sasa hivi midam ndio watu wa bara waliifanya hiyo kazi na wamezaa watoto wao na ndo hawa walionao. Sasa hapo ndo pakuzingatia. Wakubalike.2 Kweli waloifanya kazi hiyo wazee wao walikuwa wametoka bara, si Wazanzibari. Waloifanya kazi hiyo si Wazanzibari, walitoka bara lakini hivi sasa watoto na wajukuu zao ni Wazanzibari kutoka hapa. Lakini Wazanzibari wa hapa watakubali? Hapo! Ndo hio iliomfanya kukataa moja kwa moja Nyerere ni hiyo. Manake hapa tatizo hilo alilisababisha Mwalimu Nyerere. Ehe! Alipokwenda [Karume] yule kule kwa agizo la Baraza la Mapinduzi, ukifika kule unapanda mti huu nchi moja, serikali moja, Nyerere Raisi. Nyerere akakataa. Alipokataa alitia sababu zake pale. Manake tukiungana moja kwa moja watoto watakujakosa historia ya nchi yao. Kwa hivo wacha tuwawache itakuja kuwa nchi moja, Serikali moja, automatically [wenyewe]. Si tatizo kwa sababu watakujakukubaliana wenyewe baina ya wa bara na wa visiwani. Nyerere aliparoweka hapo na ndipo palipoharibika. Akaona asubiri. Kumbe kuna watu sasa watakuja kupafatilia na kupakumbusha. Mimi hilo hata viongozi wenzangu nnaowafahamu hukaa tukazungumza “makosa yetu.” Kama Zanzibar itakujafika pahala kwenye mfarakano wa kuumia yakuwa ni makosa yetu lakini aliyesababisha mzee wetu Mzee Nyerere. Kulikataa hili la nchi moja, serikali moja! Alilikataaa kwa kuliogopa lakini hapo ndipo alipoliharibu. Wakati huo kulikuwa pana khofu kwa watu, akaona aliwache. Yeye matumaini yake kwa namna tulivokwenda na jazba na namna wale watu tulivoshikana,

Page 319: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kosa la Mzee Nyerere 287

akaona hili halitokujaleta uchunguzi kuona huyu wa hivi, huyu wa hivi. Huyu mzalia, huyu mgeni. Litakufa wenyewe. Alitaraji hivo Nyerere lakini Karume yeye alijuwa litakuwa gumu. Ndo ukaona wakaingia khofu kwa sababu tangu mapema ilivokuwa watu kimya na watu hawana la kusema, kuelemishwa kila wakati, sasa lina kazi kubwa! Wazanzibari hawakuridhika. Wana kazi kubwa kuridhika. Wanataka nchi yao! Bila ya kuwachukulia kidogokidogo na kuwachukulia hadhari wale ambao wenye majority [wengi wape] na watu kuzungumza nao kwa uhakika kutaka mawazo yao na kupima faida na hasara. Tupate watu kama hao. Bado umoja tuuweke sawa wa sisi tuliokuwepo hapa. Tujitizame sisi wenyewe kwa wenyewe hapa tunavokwenda. Hapo patakaponogea ule ukaribu wetu sasa unaanza na wale watu wenye fahamu. Lakini pia patakuwa bado hapana muamko wa ukweli wa mapinduzi. Sasa hilo walokuwa CCM wakilikataa zamani sasa ndo wanalolitaka sasa. Lile walokuwa wakilitaka Chama cha Hizbu. Wametumbukia huku sasa, wako against [dhidi]. Wametumbukia Hizbu. Mfano hai Mohammed Gharibu Bilali hakupita, alipita [Amani] Karume. Mimi nikikutizama wewe ni wangu na nakupa la uhakika kabisa. Huko unakokwenda unajua, mzee, ndugu yangu, kaka, kanambia hapa. Kufika kule ikakubalika kuwa huyu (Bilali) akipata anatupeleka siko! Atatupeleka kwenye Hizbu! Mwengine asikudanganye. Na alifahamika hivo. Huyu Bilali yuko mwenziwe [Dkt. Salmin Amour] huyu na atakapofanikiwa huyu atatupeleka siko. Kinachoogopewa atakujaleta sura ya kudai anataka serikali ya nchi ya Zanzibar, na Raisi wake, na mambo yake. Na huko mwanzo nimekuambia, Zanzibar ni koloni la Tanzania (Tanganyika). Nilikwambia mapema hivo. Ukimpa mwanya atafundisha na ataleta tabu ya kuondosha azma yetu ya serikali moja, nchi moja manake mpaka sasa hivi kule [Tanganyika] ndo lilioko. Mambo ya haki za binaadamu na hii sheria ilioletwa ya demokrasia si kweli. Hii (demokrasia) iko kwenye mabano hata huko kwa wakubwa. Kwetu sisi imewekwa uwatawanye uwatawale. Hivi tumo katika kutawanywa tuendelee kutawaliwa. Mwananchi kachagua anachokitaka. Alokuwepo pale anasema hapana! Tanzania Bara itaendelea sana kuleta majeshi Zanzibar kila wakati wa uchaguzi kwa sababu ule muelekeo wa madukuduku ya kusema Zanzibar na wao wanataka pao, wanataka kuwa na nchi yao na sio lengo! Lengo tuna sera au tuna utaratibu wa mda mrefu wa kufikia serikali moja. Nyerere mpaka amefariki dunia hakufaulu kwa sababu hakupata watu wakumuunga mkono huku Zanzibar kuiendeleza ile sera. Hakupatikana kiongozi. Hakupata kwa sababu wote wale aloungana nao wamepotea, wamekwisha ati na ikaifanya nchi kwenda hivo. Wenzake kama hao kina Karume na wenzake wakubwa na wale wazee ambao walikuwa na Karume, baadae waliogopa kufata utaratibu wa yanaozungumzwa na vijana ya kuwa na nchi yetu na iwe na msimamo

Page 320: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Nane288

wake, mpaka Uingereza Jumuiya ya Madola inajulikana, nchi yetu inasagwa wazee, tutafikia wapi…sisi mnatuelewa vipi, sasa ikawa hawasemi ukweli. Waki­fika kule wanakaa pembeni, wakija huku wanasema vipembeni. Alikosa watu wa kumfuata huku. Amekosa watu wa kumfata huku. Wale wazee wakawa wazito wa kuliendeleza shauri zito! Hapa hapana serikali, pana mgawano tu. Huyu awepo pale aendeshe shughuli za Zanzibar na watu wake. Maamuzi ya kitu na uzito hakuna! Yako kule! Ushindi hapa Zanzibar shabaha yake ilikuwa hakika. CCM watu walikuwa wamekwisha choka nayo. Walikuwa Wazanzibari wote wanataka mabadiliko. Ndo hali halisi. Lakini sasa, kuna kitu tayari, na wakulaumiwa zaidi ni nyinyi vijana mnokwenda kule mkalishwa kuku wa kukaanga, mkapigwa moto wa kibara kule, mkawekwa lodging kule mkakaa, mkanywa soda, mkalala, mkaamka, na vitumbo vinashuka, mkaja hapa mkapewa nafasi “Mheshimiwa”, nani, mkababaika. Mkafika kule ukweli mkashindwa kuu­sema. Wakifika kule watu wa Zanzibar kwenye Kamati ya Chama [cha CCM], wacha Bunge, katika Wazanzibari hakuna wanaozungumza kuhusu Zanzibar! Na atakayejitokeza hivo ataanzwa kuchujwa tangu huku, asifike kusema kule. Sasa kule kujitokeza mtu namna ile anashindwa. Bilali alifanya hivo alipompinga Karume kipindi cha pili. Akajaza fomu kupeleka kule. Akaambiwa wewe huna akili? Tanzania bara umepata kumuona mtu akampinga Raisi anapoingia kipindi cha pili? “Lakini katiba.” Akaambiwa “hapana Katiba. Utaratibu.” (Vicheko). Akazungumzwa mle. Akaambiwa sasa unatupeleka wapi? Subiri amalize. Akimaliza tunaweza tukakupa kama alivofanya Kikwete kwa Mkapa. Anaweza kuwekwa lakini yuko ndani ya mtihani hapo. Hivi unavomuona yule anapokwenda msalani usalama wanataka wapajuwe. Anozungumza naye. Kabisa! Ikiwezekana hata mkewe, hivi sasa hivi nnavokwambia ana usalama unamfuata. Na ndugu zake watamfuata kupata mawazo yake, fikra zake. Kabisa! Hata ndugu zake wa karibu wana usalama. Wanazungumza nini watu wakapeleke. Sasa akivuka anaweza akapenya. Akapigiwa debe kule wakampa support [wakamuunga mkono] akapewa kule. Lakini wakapata dosari kidogo tu atajaza fomu atapeleka kule wale watatawanya akivuka malengo. Hayo ndo yalioasisiwa. Nchi moja, serikali moja na bado Zanzibar ni Mkoa na itaendelea kuwa Mkoa. Na aneyezungumza hapo hapataki basi hata uongozi wa Uraisi kwa hapa Zanzibar hapati! Anokwenda kwa msimamo kuwa akipata Zanzibar anataka kuiweka kwenye utawala wa serikali na nchi yake hapati! Labda anyamaze kimya mpaka akae juu ya kiti na ikijulikana basi anaweza hata akauliwa kwa kusingiziwa ajali ya gari! Huo ndo ukweli ulivyo.

Page 321: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na TisaKwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru!

Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu nchi shiriki itapoamua kujitenga. —Mwalimu Nyerere

Dharau za Uwakilishi wa Nguvu za Umma

Kosa walilolifanya akina marehemu Abdalla Kassim Hanga ni lile ambalo limeelezwa kwa ufasaha na Ibn Khaldun ambalo ni “kudharau umuhimu wa nguvu za kijamii, za umma, katika kufaulu kwenye mambo kama haya. Ikiwa khadaa imetumika, ni vizuri kwa mtu kama huyo asifaulu na alipishwe kwa makosa yake.” Kwa daraja la kwanza mapinduzi ya Zanzibar ni mapinduzi dhidi ya Wazanzibari waliyoipigiya kura serikali ya ZNP­ZPPP, na kwa daraja la pili yalikuwa dhidi ya Mzee Karume ambaye alikuwa ameukamata uongozi wa nusu ya pili ya jamii ya Kizanzibari. Khadaa kubwa ni mapinduzi ya Hanga na Kambona yaliyopewa nguvu na Dola ya Tanganyika na kupuuzwa na watawala wa Kiingereza kwa sababu chaguo lao la uongozi lilikuwa ni Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, na si Kambona na Hanga. Kilichoiparaganya mipango ya mapinduzi ya Hanga na Oscar ni khadaa yao ilipokutana na khiyana ya Sefu Bakari na Abdalla Said Natepe pale alipochomozeshwa John Okello ambaye hawakumjuwa na mapema mbali ya kuwa hawakumtarajiya kuwa atakuja kuwa mbele ya mapinduzi ambayo Kambona na Oscar walikuwa ndiyo wapishi wakuu. Kutokuwemo kwa Mzee Karume na Chama cha Afro­Shirazi ndani ya mipango ya mapinduzi yaliyoandaliwa na Hanga pamoja na wenzake ndani ya ASP, kuliweka pengo ambalo lilikuja kuzibwa na Okello. Kama Mzee Karume alikuwa anajuwa kuhusu mapinduzi basi ilikuwa ni kwa kuambiwa na bado hakujatolewa ushahidi wa kinagaubaga kuwa yeye ndiye aliyekuwa na mipango ya kufanya mapinduzi Zanzibar.

Page 322: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa290

Tatizo jingine ni Hanga hakuwa na kiongozi mwenye sifa za kuwaongoza wanamapinduzi wenye silaha kama alivyokuwa nazo John Okello. Kwa Hanga kumkosa mtu kama Okello kulisababishwa na kukosa kuwa nao karibu sana watu kama Sefu Bakari na Abdalla Said Natepe. Siasa za kutoaminiyana hazina mwisho mwema. Mwanzoni viongozi hao wawili walikuwa na Hanga na Saleh Saadalla katika kuyapanga mapinduzi lakini baadaye wakawageukiya na kumuunga mkono na kumpa madaraka khasimu wa Hanga na Saadalla—Mzee Karume. Anthony Clayton ameandika kuwa:

Ingelikuwa mipango ya Hanga imefaulu basi angelikuwa yeye ndiye angelikuwa kiongozi khasa wa Zanzibar, na si Karume. Tamaa hii ya Hanga ikijulikana na Okello ambaye alimuona Karume, katika nafasi yake kama ni kiongozi wa A.S.P., kuwa ndiye kiongozi halali wa serikali ya baada ya mapinduzi; Okello alimtizama Hanga kuwa ni kiongozi mwenye uchu wa kujitwaliya madaraka, ambaye ameungamana sana na siasa za Tanganyika, wakati Okello mwenyewe alipendeleya uwepo uhusiyano na Kenya. Kwa kweli, Kassim Hanga alikuwemo kwenye listi ya Okello ya watu aliyotaka wauliwe na wakati wa Mapinduzi Okello alimtangaziya ajisalimishe.1

Upinzani ndani ya Afro­Shirazi baina ya kundi lililokuwa likimuunga mkono Mzee Karume (Karume Yeka) na waliyokuwa wakimpinga uliingiya moja kwa moja katika ushikaji wa madaraka mara tu baada ya mapinduzi kufaulu. Ugomvi baina ya viongozi wa ndani ya chama cha ASP ulikuwa haujulikani na wafuasi nje ya chama kwa hiyo suala la uongozi wa mara tu baada ya mapinduzi lilipochomoza, viongozi waliyoyapanga mapinduzi kwa siri bila ya kumshirikisha Mzee Karume walijikuta wako katika hali mbaya na ya hatari mbele ya wafuasi wa chama cha ASP. Hawakuwa na njia isipokuwa kuukubali uongozi wa Karume na wao kupoteza nafasi zao na hata maisha yao. Tutakumbuka na kurudiya kuwa kina Sefu Bakari na Abdalla Said Natepe walikuwa wakenda kuripoti Gongoni kwa Saleh Saadalla Akida. Hapo piya panaonyesha kuwa utiifu wao haukuwa moja kwa moja kwa Mzee Karume peke yake. Baada ya serikali kupatikana baada ya mapinduzi kina Sefu Bakari na Abdalla Said Natepe walikuwa katika upangaji mikakati ya kuwamaliza wapishi wakuu wa mapinduzi, Abdalla Kassim Hanga na wenzake. Mchango wao wa kushirikiyana na Saadalla na Hanga ukafunikika na utiifu wao ukarudi kwa Mzee Karume mpaka alipokuja kuuliwa kwa kukosa kuwekewa mipango yoyote ile ya ulinzi mkali wakati kina Sefu Bakari na Mzee Natepe wakijuwa kuwa kuna mipango ya kuipinduwa serikali.

Mkataba wa Maofisa wa Umma wa Kiingereza

C. L. R. James, mwandishi maarufu kutoka kisiwa cha Trinidad, ameandika

Page 323: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 291

kuwa katika riwaya ya daraja la kwanza ya mwandishi wa Kimarekani Herman Melville iitwayo Moby­Dick, kuwa kuna sifa mbili za binaadamu wawili ndani ya kitabu hicho. Mmoja ni Ishmael, na wa pili Ahab. Ishmael ni msomi lakini hana msimamo wala hana dira—anayumba:

Ishmael anauwona wazimu wa Ahab, anakumbwa nao, ana akili za kutosha za kuupinga; lakini kama Melville mwenyewe, hana mtu mbadala, wala nguvu za kumpinga nahodha mwendawazimu. Usiku ule Ishmael alikuwa kwenye usukani na hakuona kitu mbele yake isipokuwa maafa. Melville aliona na kutokana na uzowefu wake kuwa hakukuwa na dawa; lakini inaonekana kuwa huyu Mmarekani, ambaye ni tunda la kujivuniya la uhuru wa nafsi wa miaka 1776 mpaka 1850 alikuwa hana imani na usomi au uokovu wa kukimbiya au wa aina yoyote ile. Jamii ilikuwa imeshaangamiya na akaisukuma kunako maangamizi yake. Ahab alijuwa nini anataka; na Melville sio tu kuwa anamuhusudu Ahab, bali hana isipokuwa dharau kwa msomi asiyekuwa na msimamo.2

Tutamuachiya msomaji kuamuwa nani ni Ishmael, nani Ahab, na nani Melville, katika historia ya uongozi ndani ya bahari ya Zanzibar na ya Tanganyika ya kabla na ya baada ya mapinduzi. Ushahidi wa Kiingereza unaonyesha kuwa sababu kubwa ilioifanya serikali ya ZNP­ZPPP kuyumba katika kuchukuwa maamuzi ya kuulinda uhuru wa Zanzibar ni kuikumbatiya siasa ya kutokufungamana na upande wowote (Non-alignment). Anaelezeya Kamishna Sullivan:

…niliakabili Serikali wiki iliyopita juu ya suala lenye unyeti ya hali ya juu wa kutafuta mipango ya msaada wa kijeshi kutoka nje, suala ambalo Serikali ilikuwa ikilikwepa bila ya kiasi kwa inavyoonyesha walikuwa wanasumbuliwa na suala la kufungamana ikiwa watafunga mkataba wa kijeshi na nchi moja wapo kati ya madola makubwa. Waziri Mkuu alinihakikishiya kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendeleya lakini hakunipa dalili yoyote yalikuwa na nani.3

Wakati wa Mkutano wa Uhuru wa Zanzibar, Zanzibar Independence Conference uliofanyika tarehe 31 Agosti mwaka 1963, Mawaziri wa Zanzibar waliombwa: “…kufikiriya kama watapenda kuzungumza kuhusu Mkataba wa Kijeshi na Uingereza na kama watataka wampe maoni na mahitajiyo yao Mheshimiwa [Mwenyekiti wa mkutano], ili amuarifu Secretary of State…”4

Waingereza waliona kuwa Mawaziri walikuwa wanafikiriya kutafuta Mikataba ya Kijeshi na Misri, Tunisia au Algeria na walieleza wazi ugumu wa kuwa na mkataba wa kijeshi na nchi zilizokuwa ziko mbali sana na Zanzibar kwa sababu za upelekaji wa vifaa, na kadhalika. Katibu Mkuu wa Waziri Mkuu Bwana Mohammed Shamte, Bwana Mervyn Vice Smithyman alilalamika kwa kusema:

Tena, baada ya Uhuru, nilizungumza na Waziri Mkuu mara sita tafauti kumuelezeya kuwa vikosi viliyopo havitoshi ikiwa kutatokeya ghasiya kubwa na ashauriyane na

Page 324: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa292

Serikali ya Kiingereza au Serikali ya Kenya, kujaribu kupata Mkataba au kufanya mipango ya kuongeza nguvu za aina yoyote ile. Baada ya kumkumbusha kwa mara ya sita ndipo alipofanya mpango wa mazungumzo yaliyofanyika na Balozi wa Kiingereza pamoja na Sheikh Ali MUHSIN juu ya maudhui hiyo. Mawasiliyano yalipelekwa kwa Serikali ya Kiingereza lakini kwa bahati mbaya ilijibu kuwa haiwezi kukubaliyana kufunga mkataba wa aina hiyo. Waziri Mkuu, mbali ya shinikizo langu, alikuwa hayuko tayari kuruka kwenda Nairobi kwa mazungumzo na Jomo KENYATTA juu ya maudhui hii. Wakati huo alikuwa ana mahusiyano mazuri na Jomo KENYATTA kwa sababu ya mazungumzo ya Mwambao, bado ingeliwezekana kwa wakati ule kwa Jomo KENYATTA kukubali kuitowa G.S.U. au vikosi na kama angeliombwa vingelikuwa tayari viko visiwani kabla ya maamuzi kufanyika katika mustawa wa kisiasa.5

Mwandishi wa Kiomani Nassir bin Abdulla Al­Riyami katika kitabu chake kwa lugha ya Kiarabu Zinjibar: Shakhsiyyat wa Ahdaath ameelezeya juu ya suala la ulinzi wa Zanzibar kabla ya Mapinduzi. Pia ameelezeya namna Naibu Kamishna wa Polisi wa Kizanzibari, marehemu Sheikh Suleiman Said Al­Kharusi, alivyowaomba Mawaziri wa serikali iliyopinduliwa kuukubali ushauri wa Bwana Biles kuwaomba Waingereza kwa njiya iliyokuwa rasmi wakibakishe kikosi cha Gordon Highlanders ambacho kilikuwepo Zanzibar wakati wa sherehe za uhuru. Waziri wa Fedha, marehemu Sheikh Juma Alley Al­Abrawi alifanya istihzai na kusema “Unafikiriya serikali ni kombe cha chai kinaweza kupinduliwa kiurahisi!” Anaelezeya Nassir Al­Riyami kuwa mjumbe mwengine wa Baraza la Mawaziri, Bwana Maulidi Mshangama ambaye alikuwa Waziri wa Ilimu na Ustawi wa Jamii alimjibu Al­Kharusi kuwa:

Ikiwa tutalikubali pendekezo hili hatutakuwa popote pale karibu na uhuru na anaona ni bora kuondoka kwa kikosi cha kijeshi cha Kiingereza kusadifiye na kuondoka kwa ukoloni wa Kiingereza nchini. Na hivi ndivyo alivyoonesha Al­Kharusi namna gani Baraza la Mawaziri lilikataa kuzikubali nasaha za Polisi kwa umakini na badala yake wakaziyona kuwa ni kejeli juu ya kejeli, mbali ya Al­Kharusi kushikiliya kuwa hali ya usalama wa nchi iko katika hali ya hatari na kuwa nchi itakuja kushuhudiya ghasiya kubwa zaidi kuliko zile zilizoonekana mwaka 1961.6

Hakuna kati ya wanasiasa wa Zanzibar wa wakati huo, ambaye aliiyona hatari kubwa ya Muingereza kuiwacha Zanzibar bila ya ulinzi ndani ya kipindi baina ya kuondokana na utawala wa kikoloni na kuingiya ndani ya uhuru. Baadhi yao walifikiriya kuwa aliyepinduliwa ni Muingereza pamoja na utawala wa Kikatiba wa Sultan Jamshid kama vile alivyo Mfalme wa Uingereza. Wengine wakiwemo Waingereza wenyewe, waliyaweka macho yao yote juu ya chama cha Umma na kuudharau mvutano uliyokuwepo ndani ya ASP. Wakati ule Ufalme ulikuwa na jina baya duniani hata kama ulikuwa si mbaya, na Jamhuri ilikuwa pepo ya siasa na ya wanasiasa hata kama mlikuwa na hilaki. Mfalme wa Zanzibar alikuwa hana madaraka ya kuingiliya kati taasisi za kisiasa

Page 325: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 293

na za kisheria za serikali isipokuwa tu pale anapotakiwa kufanya hivyo. Mambo yote ya kiutawala yalikuwa mikononi mwa Waingereza yaani British Resident na Chief Secretary wake. Ilitosha Ufalme kuchukiza kwa sababu Mfalme aliyekuwa akitawala Afrika Mashariki alikuwa ana asili ya Kiarabu na Muislam. Ethiopia mambo yalikuwa vyengine na Mfalme Haile Selassie alikuwa kati ya viongozi wa mwanzo kwenda Zanzibar kuwapongeza wanajamhuri kwa kumpinduwa Mfalme mwenzake. Picha kubwa inaonyesha kuwa lengo la Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa kuupinduwa uzalendo wa Kizanzibari ambao ulikuwa ukiipinga siasa ya Kiingereza na ya Tanganyika chini ya Mwalimu Nyerere. Kwa mtizamo wa Waingereza wa wakati ule, Zanzibar ilikuwa imeshaingiya ndani ya mikono ya nchi adui ambayo ni Misri chini ya uongozi wa Gamal Abdel Nassir, ambaye angelikuja kuyahatarisha maslahi ya Uingereza na vibaraka vyake vya Afrika Mashariki. Sheikh Ali Muhsin alilifahamu hilo na ndiyo maana pale alipokuwa anapelekwa gerezani haraka alimtuma mtu akampe salamu seketeri wake wa Kigoa auchane muswada wa waraka ambao alikuwa anautayarisha kuupeleka kunako Baraza la Mawaziri baada ya kurudi safari kutoka nchi ya Misri. Kusitasita kwa uongozi wa ZNP­ZPP kwenye suala la ulinzi wa Zanzibar baina ya kuwategemeya Wamisri na kuwarudiya Waingereza ambao hawakutaka kuamini kuwa Zanzibar itaweza kuvamiwa na Tanganyika, ndiko kulikoiyangusha Dola ya Zanzibar na kuzuwiwa kuinuka mpaka hii leo. Si ajabu pia kwa Maofisa wa polisi wa Kiingereza, kama Kamishna Sullivan na wenzake ambao wakilipwa mishahara mikubwa kutaka uwepo mpasuko baina ya Wazanzibari wenye asili zinazotoka bara la Asia na bara la Afrika ili pasikuwepo na masikilizano Zanzibar na Afrika Mashariki ambayo yatawaharibiya mambo yao. Ikumbukwe kuwa Kamishna J. M. Sullivan alikuwa ameshapewa barua ya kuwachishwa kazi tarehe 15 mwezi wa Novemba 1963. Naibu Kamishna wa Kizanzibari, Bwana Suleiman Said Al­Kharusi alipotakiwa awe Kamishna wa Polisi, aliomba awachiwe mpaka mwezi wa Septemba 1964 baada ya kuzielezeya “…hadhari zake za kufanya haraka kushika nyadhifa katika polisi, alisisitiza haja ya kupewa miezi michache kabla ya yeye kuchukuwa wadhifa wa Mkuu wa Polisi, alitaka aendelee Mkuu wa Polisi, Sullivan katika wadhifa wake.”7

Wakati wa Mkutano wa Katiba wa Zanzibar uliofanyika mwaka 1962 kulikuwa na makubaliyano uwepo Mkataba wa Maofisa wa Umma (Public Officers Agreement, POA), baina ya Serikali ya Malkiya na Serikali ya Sultan wakati Zanzibar itakapopata uhuru.8 Kwa kawaida Mkataba huo huwa unasimamiwa siku ya uhuru katika hafla ndogo na unatiwa saini na Balozi wa Kiingereza (High Commissioner) kwa niaba ya serikali ya Kiingereza. Kulikuwepo na Mkataba wa aina hiyo ambao:

uliwahusisha maofisa wa Kiingereza 60 wa mkataba na maofisa 70 wa kudumu na

Page 326: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa294

wanaofaa kupewa mafao baada ya kumaliza kazi…Ina maana wakati mishahara yao inakadiriwa na Serikali ya Kiingereza hakuna malipo yoyote yanayofanywa na Serikali ya Kiingereza kwa ofisa yoyote yule. Tunachokifanya ni malipo ya jumla kwa mujibu wa makubaliyano ya makadiriyo ya mwaka kwa Serikali ya Zanzibar kufidiya gharama za maslahi waliyowapa maofisa waliyokuwa chini ya Utaratibu huo.9

Mkataba wa Public Oficers Agreement uliipa dhamana ya moja kwa moja Serikali ya Kiingereza juu ya Maofisa wake kuliweka jeshi la polisi (na usalama) la Zanzibar chini ya Maofisa wa Kiingereza.10

Mshahara wa Kamishna Sullivan ulikuwa pesa za Kiingereza za wakati huo pauni 3,125 (Shilingi za Tanzania milioni 6,572,967.40 za leo). A. B. P. J. Derham, Superintendent, akilipwa pauni 1,956 kwa mwezi (Shilingi za Tanzania milioni 4,114,151.75 za leo). Wa chini yake kwa niaba, R. M. Misra akilipwa pauni 1,128 (Shilingi za Tanzania milioni 2,372,578.30 za leo) na Assistant Superintendent, T. Waring, akilipwa pauni 1,425 (Shilingi za Tanzania milioni 2,997,273.15 za leo). Cha kuzingatiya pia ni Kamishna Sullivan aliwahi kutumika Palestine baina ya mwaka 1936 na 1945. Mbali ya Cyprus, Kamishna wa kabla yake, R. H. V. Biles alitumika Palestine baina ya mwaka 1937 na 1946. British Resident mpya, Sir George Mooring alitarajiwa kufika Zanzibar kuanza kazi mwezi wa Januari 1960. Katika kikao cha mkutano uliofanyika London tarehe 11 Julai 1961 Bwana Mooring, baada ya fujo za Juni za 1961, alifahamisha kwamba ni:

…wazi kama mivutano iliyopo [Zanzibar] itaendeleya basi kuondoka kwa Muingereza itakuwa ni operesheni sawa na ile iliyofanyika Palestine. Na Bwana Morgan alisema kuwa inawezekana Kamati ya Uchunguzi ikatowa picha safi ya Zanzibar iliyogawanyika baina ya makundi mawili ya kikabila na itakuwa wazi kwa kila mtu kuwa kutakuwa na hatari nyingi ndani ya harakati kuelekeya kwenye uhuru. Utaratibu kama wa Palestine au Cyprus itabidi ufikiwe. Naye Bwana Mooring alisema kuwa anafikiriya kuwa suluhu baina ya makundi mawili inaweza ikapatikana kwa njiya ya:

a) katiba maalumub) kuunda Shirikisho la nchi za Afrika Mashariki [na Zanzibar ilindwe ndani

ya mfumo wa Shirikisho]c) kwa kuhakikisha kuwa hakutofanyika maendeleo mengine yoyote ya kikatiba

mpaka uchaguzi mwengine utakapofanyika.11

Yote matatu hayakufanywa kwa sababu picha iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi wa fujo na mauwaji ya Juni haikukiangaliya kiini cha matatizo ambacho kilikuwa ni wageni waliyokuwepo Zanzibar na waliyoletwa kutoka nje, kuamini kuwa wana haki zaidi Zanzibar kwa sababu ya Uafrika wao kuliko Wazanzibari na Uzanzibari wao. Ingawa vikosi vya askari (1,000) vililetwa ku­

Page 327: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 295

toka Kenya kutuliza hali, vyombo vya usalama havikuingiya na kuzama ndani ya jamii za wageni na za wenyeji na kuuchunguza kwa kina mtandao wa viongozi wa mipango ya maafa ya Juni 1961. Kufikiya tukio la Januari 1964, usalama chini ya uongozi wa Kiingereza ukafeli tena kuutambuwa na kuuingiya mtandao wa vichwa na mikono ya Mapinduzi. Wakati wa mapinduzi marehemu Bwana Nassor Abdulla Nassor Al Shihemy, maarufu “Mlawwaz”, alikuwa ofisa wa tatu katika jeshi la Polisi la Zanzibar katika kitengo cha Criminal Investigation Department. Marehemu Iddi Mjasiri alikuwa ofisa wa tatu katika Special Branch pamoja na marehemu Inspekta Marjebi. Kwa mujibu wa Nassor “Mlawwaz”, Harub Said Busaidy, ambaye akikaa kwa marehemu Bwana Ali Ahmed Riyamy, aliwahi kumpelekeya taarifa kuhusu Mapinduzi na akampeleka kutowa statement na ikatiwa saini lakini Waingereza hawakuchukuwa khatuwa yoyote ile. Ni jambo linalowezekana kabisa kuwa watumishi wachache wa Kizungu wa serikali ya Zanzibar waliyopewa muda wa mwisho wa kazi zao na waliyokuwa na chuki na tamaa zao walishiriki kichinichini katika Mapinduzi ili wapate kubakiya katika kazi zao na khasa wale wa polisi. ASP walipewa muongozo na Nyerere wasiwaudhi Waingereza na sera yao ilikuwa hatukusoma kwa hivyo tutakuhitajini. ZNP ilikuwa itawaweka Wazanzibari wengi sana katika kazi nyingi ambazo zilikuwa zimeshikwa na Waingereza ambao walijuwa kuwa ikipata ZNP wengi wao hawatokaa na ikipata ASP itabidi waombwe wakae kwa sababu ASP walikuwa hawana watu kama ZNP na ASP ilikuwa haina wasomi kama ZNP.12

Hapa kuna suala la wazi la kisheria kwa upande wa Uingereza kushindwa kuweka amani na utulivu Zanzibar, na kuzuwiya mauwaji ya halaiki, pamoja na kushauri Zanzibar itawaliwe na Tanganyika ili kukamilisha siasa yake ya kuikataliya uhuru Zanzibar, na kurithiwa kwa siasa hiyo na Dola ya Tanganyika ili Zanzibar isiingiye ndani ya mikono ya “adui” yao. Kilichokusudiwa khasa ni propaganda ileile yenye kutamka kuwa Zanzibar ilikuwa kituo cha mwanzo cha ubeberu Afrika Mashariki na cha “utumwa wa Waarabu.” Kinyume kabisa na ukweli wa kihistoria ulivyosajili, Zanzibar na sehemu kubwa ya Afrika Mashariki ilikuwa ikijulikana kwa jina la Ethiopia au Wamisri wa kale wakilifahamu eneo hilo kwa jina la Punt.13 Katika karne ya kumi na saba nchi ya Oman ilisaidiya kwa hali ya juu ukombozi wa Afrika ya Mashariki kupata uhuru wake kutoka ubeberu wa Kireno, kutangaza maadili yake ya kiutamaduni na akhlaki njema, pamoja na kuwacha mchango mkubwa wa kijamii na wa kiuchumi. Wangapi leo wanayajuwa au wanayaona kwenye nyumba za kumbukumbu za kitaifa za Afrika Mashariki majina ya wakombozi mashujaa wenye asili ya Kiarabu ya Kiomani kama Muhammad bin Khalfan Al­Barwani, maarufu

Page 328: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa296

“Rumaliza” aliyepiga risasi kwenye tundu na kumuuwa askari wa Kijerumani aliyekuwa akiwamaliza Wahehe kwa marisasi Tanganyika? Au Bushir bin Salim Al­Harthi aliyekamatwa na kunyongwa Pangani baada ya vita vyake vya kuwatowa Wajerumani Tanganyika? Au Kanali Ali Mahfudh aliyepigana na majemedari wa Msumbiji Albarto Sipande na Raymundu Pasinuwapa katika ukombozi wa nchi hiyo kutoka kwa ukoloni wa Kireno? Au mchango wa chama cha ZNP katika kuupiganiya uhuru wa Zanzibar na kuupata, au wa Misri katika Sudan, Somalia, Kenya, Algeria, Zambia, Kongo, Uganda, Burundi, Mali, Eritrea, FRELIMO, ANC, MPLA, nk?14

Kinachopigiwa debe na kuitwa “kituo cha ubeberu” ni uhusiano mkongwe duniani wa binaadamu wenye asili zenye kutoka mabara ya Afrika na Asia. Ubeberu wa Kiingereza kuiwachiya Tanganyika kuibomowa Dola ya Zanzibar umefichwa na kupuuzwa kwa makusudi ili uhusiano mkongwe wa Afrabia usipate fursa ya kuendeleya na kuwanufaisha washiriki wake.

ZNP Ikiota Watu Wanateremka Zanzibar

Kamishna Sullivan na Katibu Mkuu wa Waziri Mkuu Mohammed Shamte, Bwana Mervyn Vice Smithyman, walitambuwa kuwa kulikuwa na upungufu mkubwa wa tahadhari za kiusalama na za kiulinzi katika kuulinda uhuru wa Zanzibar. Bwana Smiythman amekiri kuwa kulikuwa na ripoti nyingi kuhusu fujo zilizokuwa zikitarajiwa usiku wa tarehe 11 Januari 1964 na:

…ingelikuwa ripoti zote hizi zingelifika zinakofaa kufika, basi japo tahadhari ndogo zaidi zingelichukuliwa…na somo liliopo ni hizi ripoti zingelifikishwa kwa polisi na tathmini zake wangeliwachiwa wale ambao wamo katika nafasi ya dhamana na wenye ujuzi wa kuzifanyia kazi. Hapa polisi wanaweza kuwa walikuwa wana makosa.15

Bwana Smithyman amekaribiya kukiri baada ya kutokeya Mapinduzi kuwa Zanzibar haikupinduliwa na Wazanzibari lakini kufahamu huko hakukuibadi­lisha sera ya Uingereza juu ya kudhibitiwa Zanzibar na Tanganyika:

…ukweli ni kuwa sasa tunajuwa kuwa watu waliletwa kutoka nje ya nchi na kutowa mchango mkubwa katika mapinduzi. Historia ya jambo hili ni muhimu. Suala la uhamiaji usio wa kisheria lilichomoza wakati wa uchunguzi wa machafuko ya Juni 1961, na chama cha Z.N.P. na Sheikh Ali MUHSIN, walishadidiya kwa nguvu kuwa wengi kati ya waliyokuwa wakifanya fujo na waliyoanzisha machafuko ya Juni 1961 walikuwa ni wabara ambao ni wageni Zanzibar na walitambulikana kuwa ni watu kutoka nje ya nchi. [Suala] hili lilikataliwa kwa nguvu sana na vyombo vya usalama vilivyokuwepo, polisi, na wote waliokuwa na madaraka, kwa sababu haukupatikana ushahidi wa hilo. Kutokeya wakati huo, na miaka miwili sasa, kumekuwa na ripoti zenye kujirudiya kuhusu watu kuingiya kutoka bara kwa njiya za magendo…Nafikiri ni uadilifu kusema kuwa imani ya wengi ndani ya

Page 329: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 297

vyombo vya usalama, makao makuu ya Polisi, na ofisi ya British Resident [Balozi wa Kiingereza] ni kuwa Sheikh Ali MUHSIN na Z.N.P. walikuwa wakiota watu wanaingiya [Zanzibar] wakati haikuwa kweli.16

Assistant Sperintendent Thomas Waring naye ameandika kwenye ripoti yake ya tarehe 16 Januari 1964 juu ya Mapinduzi ya Zanzibar:

Wakati niko Zanzibar, na hivi sasa ni miaka miwili na nusu, nimekuwa nikiambiwa mara kwa mara kutoka kwa Waarabu kuwa wanakhofu ya kuvamiwa kwa silaha kutoka Tanganyika. Wakati nafanya kazi ndani ya Himaya [ya Zanzibar] nilifanya kazi Zanzibar [Unguja] na Pemba. Daima nikisikiya uvumi, ambao kama utakuwa ni kweli, basi matokeyo yake yatakuwa na athari za kutisha. Chache kati ya maneno yaliyokuwa yakivuma yalikuwa na msingi. Nilijifunza kuzipuuza hadithi za uvumi.17

Pia anaripoti Waring kuwa:

Waziri bila ya Wizara, Ibuni SALEH, wa serikali ya zamani aliniambiya kuwa anaingaliya Police Mobile Force kuwa ni kiini cha Jeshi jipya la Zanzibar. Ameniambiya nifanye mipango ya kuliongeza jeshi na nianze kuwaandikisha askari. Ameniambiya kuwa anaona umuhimu wa hili, na kikundi changu kiongezeke mpaka kifikiye watu 500. Amesema kuwa hili ni muhimu kwa sababu kuna uwezekano huenda Tanganyika ikaivamiya Zanzibar.18

Mwisho wa ripoti za Kamishna Sullivan na Bwana Smithyman ni masomo ya kuzingatiya kwa yaliojiri katika Mapinduzi ya Zanzibar. Khitimisho la Kamishna Sullivan lilikuwa kama ifuatavyo:

1. Si ushauri mzuri kwa nchi ambazo zina ufukwe wa bahari kuwa hazina mfumo wa vikosi vya wanamaji vya sawasawa.

2. Si ushauri mzuri kwa nchi ndogo kama Zanzibar, Mauritius, Seychelles, kuziweka silaha nyingi kwenye ghala moja au mbili, ingawa kuzigawa pia kunaweza kuleta matatizo mengi ya kiusalama.

3. Katika nchi ndogo usalama wa nchi unakuwa imara ikiwa kila sehemu ndogo ya idadi ya watu ina polisi mmoja.

4. Kama inavyoonekana ni kuwa operesheni nzima ilikuwa imepangwa vizuri sana na kwa nidhamu na watu wenye kuyadhibiti mambo ambao walikuwa na ujuzi wa kutosha wa mbinu za kivita na waliyofuata, katika matukiyo yaliofuatiliya, ni kwa karibu sana kile nilichokisoma kuhusu mbinu za kupinduwa serikali kutoka kitabu cha kumbukumbu (diary) cha BABU.19

Mwisho wa ripoti ya Smithyman ni mukhtasari wa masomo matano kutokatukiyo la Mapinduzi ya Zanzibar:

a) Taarifa za Usalama

Wakati wa kuzitathmini ripoti ni lazima tuuweke akilini mgogoro baina ya

Page 330: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa298

Mashariki na Magharibi [Vita Baridi]. Katika mazingira ya Afrika ina maana kuwa kuna mpango wa siri wa kuzipinduwa serikali zote za kidemokrasia. Kwa hivyo ripoti zozote zile za usalama ambazo zinaonekana kuashiriya mpango maalumu wa siri zisidharauliwe kiurahisi.

b) Wafanyakazi wa Polisi

Mchujo wa wafanyakazi wote wa polisi na Usalama uwe ni wa kila wakati na kusiwe na huruma kuwafukuza au kuwapa uhamisho.

c) Vyombo vya Usalama

Baraza la Mawaziri lazima likubali kuwa vikosi vya usalama lazima vipewe nafasi ya juu ya kifedha. Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar ya zamani ambao leo wamenyongoyeya jela watalikubali hili kwa moyo mkunjufu.

d) Ghala za Silaha

Zanzibar inaonyesha kuwa kuna uwezekano wa uvamizi wa ghafla kutokeya kwa hiyo uchoraji wa ghala za silaha ni lazima ziwe ndani ya mikono ya polisi hata kama zitavamiwa na mamia ya watu.

e) Uhuru wa Kujieleza na wa Kutembeya

Ili kuzuwiya kufanyika mazingira ambayo yataleta hali tete ya kiusalama, dola lazima itafute njiya ya suala la uhuru wa kuzungumza na kutembeya. Kwa Zanzibar mizani iliangukiya upande wa uhuru wa kuzungumza na uhaba wa usalama wa dola.20

Utumwa, Ukristo, Uislam, na Mapinduzi

Sababu ya zamani ya kuangushwa kwa Dola ya Zanzibar ni Uislam wa Afrika Mashariki:

Kwa namna ulivyokuwa na uadui na Ukristo una ‘uwezo mkubwa wa kuendeleya kunako muelekeyo wa ustaarabu wa kileo’, na kwa hiyo serikali uutumiliye, kama wanavyofanya Ufaransa, Uingereza, na Uholanzi, kama ni chombo cha kuwailimisha wenyeji, na uwepo mtizamo wa usiokuwa na nguvu juu yake. Wakati huohuo…Uislamu wenye nguvu usiwemo kwenye Makoloni ya Kijerumani, na njiya pekee ya kuuzuwiya ni kujenga vituo vya Kikristo vyenye nguvu, kama ilivyokusudiwa na Misheni.21

Ushahidi wa malengo haya unaonekana wazi kwenye vitabu vya Jan P van Bergen Development and Religion in Tanzania: Sociological soundings on Christian participation in rural transformation, John C. Sivalon Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, Frieder Ludwig Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994. Uchunguzi wa vitabu hivyo pamoja na vya Bwana Mohamed Said na Dkt. Hamza Njozi unaonyesha vipi Kanisa lilivyoitumiya Dola ya Tanganyika na baadaye ya Tanzania kujiimarisha ndani ya nchi kwa kuwazuwiya Waislam wasipige hatua za kimaendeleo zitakazoweza

Page 331: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 299

kuwapita Wakristo. Tafauti na Waislam, wakala za kujitoleya na taasisi za Kikristo zinatowa mchango mkubwa katika huduma za kiafya na za kiilimu Tanzania. Huduma nyingi za kiafya katika sehemu za vijijini huwa zinatolewa na taasisi hizo ambazo zinapata misaada kutoka kwa wafadhili wa taasisi za kimataifa. Inakuwa ni vigumu kwa Waislam kupata misaada kutoka nchi za Kiislam na taasisi za kimataifa. Upande mmoja wameelemewa na vita vya kipropaganda dhidi ya Waarabu Waislam na utumwa wa Waislam ambavyo vinawaghadhibisha na kuwakimbiza wafadhili Waislam na taasisi za Kiislam. Au zitatafutwa taasisi za Waislam ambazo zimejaa ufisadi na kuwafanya wafadhili Waislam na taasisi za Kiislam zikataye kuwasaidiya Waislam kwa kupitiya taasisi hizo. Baina ya mifarakano yote hiyo Wakristo wanaongeza na wanaongezewa nguvu na waumini wenzao kutoka nchi za Magharibi. Tarehe 21 Februari mwaka 1992, Baraza la Kikristo Tanzania na Baraza la Maaskofu Katoliki walitiya saini Mkataba wa Maridhiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliyoandaliwa na Profesa, Dokta, C. R. Mahalu wa Kitengo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kutiwa saini na Edward Ngoyai Lowassa kwa niaba ya Serikali, Elinaza Sendoro kwa niaba ya Baraza la Kikristo Tanzania, na Josephat Lebulu, kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki. Mkataba wa Maridhiano una lengo zuri la kuendeleza huduma za afya na ilimu katika jamii na unaikalifisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania:

…itajitahidi kujumuisha misaada ya kifedha kwa ajili ya huduma za jamii zinazomilikiwa na ‘Makanisa’ itakapokuwa katika mazungumzo ya kuomba misaada husuusan mazungumzo yake na Jamhuri ya Kifedirali ya Ujerumani. Uwezekano kama huo uangaliwe pia itakapokuwa na mazungumzo na wafadhili wengine.22

Wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na shirika la Kiislam la Organization of Islamic Conference (OIC), Askofu E. Sendoro wa Mkataba wa Maridhiano alitahadharisha juu ya uamuzi wa kitendo hicho kwa kusema: “Zanzibar ikiwa ni Dola ya Kiislamu, itaendeleya kuwa sehemu ya Muungano? Bunge la Muungano litakuwa na dhamana juu ya Zanzibar au lipo kwa ajili ya Tanzania Bara?”23

Askofu Sendoro kalikozesha suala la Zanzibar kutaka kujiunga na OIC na kulifanya ni suala la Zanzibar kutaka kuwa Dola ya Kiislam. Kwani Mkataba wa Maridhiano ambao lengo lake kubwa ni kuendeleza huduma za kijamii za Kanisa katika sekta za ilimu na afya ulikuwa na lengo la kuifanya Tanzania kuwa Dola ya Kikristo? Kwa vile Mkataba wa Maridhiano ni mkataba baina ya Taasisi zisizo za kiserikali na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jee, ulipata baraka za Baraza la Wawakilishi la nchi ya Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano au ilionekana kuwa hakuna haja ya kufanya hivyo? Mambo hayajaanziya hapo.

Page 332: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa300

Mwaka 1970 shule zote za msingi, sekondari na za kuwafundisha walimu zilitaifishwa. Hali iliporuhusu Kanisa likaanza tena kujenga shule na Waislam walikuwa wamelala mpaka mwaka 1982 ilipojengwa Morogoro Shule ya Sekon­dari ya Jabal Hira. Mwaka 1991 Kanisa lilikuwa na shule 413 za chekecheya, skuli za sekondari 82 pamoja na seminari, skuli 73 za ufundi, vituo 48 vya kazi za kisanii kwa wanawake, college mbili za kuwafundisha walimu, na shule 6 kwa ajili ya wanafunzi walemavu.24

Kufikiya mwaka 2008 shule hizo zimekuwa za daraja la juu katika mashindano ya kitaifa. Shule za Sekondari 10 bora katika matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne ni seminari za Kikristo na tano za chini katika mashindano ni za Kiislam kwa sababu ya mazingira mabovu, walimu wasiyokuwa na ujuzi na kukosa misaada ya kifedha kutoka taasisi na nchi za Kiislam. Bado hujahisabu vyuo vikuu, vyombo vya habari yakiwemo magazeti, televisheni na redio. Mwaka 2005, Waislam walitunukiwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, majengo ya iliyokuwa Taasisi ya TANESCO ya Morogoro kwa lengo la kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislam. Hata hivyo, Waislam wa Tanzania bado hawana Taasisi zisizo za kiserkali zenye nguvu ya kufunga Mkataba wa Maridhiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Watakapojijengeya nguvu za kisiasa na za kiuchumi ndipo watakapoweza kuwa na ubavu wa kuingiya kwenye Mkataba na Serikali na kuweza kusaidiwa na waumini wenzao kati ya Waafrika Waislam, Waarabu Waislam milioni 200, na Waasia Waislam bilioni 1, na kuweza kufunga Mikataba ya kibiashara na ndugu zao wa Kikristo na majirani zao. Miradi ya kheri kama ule wa Loliondo wa Dubai au wa Qatar wa kuendeleza kilimo cha chakula Kenya, itaendeleya kupigwa vita vya chini kwa chini mpaka Waarabu na Waislam watakapokuja na sera moja yenye: “Kushadidiya hoja ambazo zitawapa tabu viongozi wa kisiasa na wenye kasumba ya kutangaza habari ambazo hazikufanyiwa uchunguzi wa kina na zenye uwezo wa kuzichafuwa akili za binaadamu wa kawaida kwa kuwakosesha ustahmilivu na kuwatiya chuki.”25

Makosa yaliyofanywa na wanasiasa wengi wa Kizanzibari pamoja na viongozi wa Kiislam wa Tanganyika ni kuona haya kuzipiga vita hadithi chafu za “utumwa wa Waarabu” ili wasije wakatupiwa doo la matope kwa kuitwa “Waarabu” au “Mahizbu” au “Masultani”; majina matatu ambayo yamekuwa yakitumika kwa muda mrefu kuwanyamazisha watu au mijadala yenye nguvu za hoja. Kwanza, akili inachafuliwa kwa kulishwa uzushi wa historia iliyopotoshwa kwa makusudi, halafu mwenye kutaka kufikiri na kujiteteya kwa hoja hutupiwa kombora jingine linalomfanya ashindwe kujiteteya kwa sababu tayari ameshaitwa “Hizbu”, “Mwarabu” au “Sultani.” Lengo ni kuwatisha waliyoko ndani na nje ya nchi wasishikamane na kusaidiyana. Chanzo kinasema kuwa mradi wa Loliondo umejenga visima, unawalipiya wanafunzi kusoma shule na vyuo vikuu, na kila mwaka unatowa zaidi ya shilingi

Page 333: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 301

milioni 50 kwa kila kijiji. Juu ya yote hayo uvumi unaendelezwa kwa makusudi kuwa Waarabu wanawachukuwa wanyama wa pori nchini kwao kinyume na sheria au wanawauwa bure katika kipindi cha uwindaji wakati wanajuwa fika kuwa wanyama ambao wametolewa ruhusa na wenye kulipiwa kuwindwa ni wachache sana kuliko wenye kuuliwa. Wenye kuyajuwa mambo wanakiri kuwa Dubai ikiuondowa mradi wake Loliondo basi Wamasai wa sehemu yote watakhasirika bila ya kiasi. Ndugu yetu mmoja wa Kichaga alisema “tungeliweza kumpata Sheikh wa Dubai basi uchagani kote kungelingara.” Matunda ya chuki na fitina za muda mrefu zimewafanya Waislam na Wakristo kutopendana na hata Waislam wenyewe kwa wenyewe kuchukiyana, kutooneyana huruma, na kutoaminiyana. Ukirudi nyuma zaidi mwaka 1904 utakuta tayari J. J. Willis wa Usalama wa Ujumbe wa Kanisa (Church Mission Intelligencer) ameandika kuhusu “Ukristo au Uislam katika Jimbo la Askofu wa Uganda”:

Ikiwa uwezekano wa Uislam kuingiya kutoka Kaskazini [Sudan na Misri] ni tukio ambalo halina budi kutarajiwa, basi hatari kubwa zaidi na yenye kutisha itatokeya Mashariki. Kuwa karibu na pwani, ambako zamani mtu alikuwa akifika [Uganda] kwa miezi, sasa anaweza kufika kwa masiku. Jambo ambalo lisingeliweza kuzuwilika ni kuingiya kwa mkumbo wa Waswahili watakaoletwa kwa treni [Afrika Mashariki]; na lisiloweza kuzuwilika ni uzowefu wao [Waswahili] mrefu wa ustaarabu ambao utakuwa na ushawishi mkubwa juu ya makabila ya Afrika Mashariki ambayo bado ni wanagenzi.26

Ni muhimu kutoyachukuwa maelezo ya kitengo cha usalama wa Kanisa na kuyaunganisha moja kwa moja na Mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja wenye kuonyesha mchango wa Kanisa katika Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini tunawaeza kusema kuwa kutokana na fikra ya Mwalimu Nyerere ambayo ilipokelewa na viongozi Waislam wa TANU na wa ASP ni kuitazama Zanzibar kwa mtizamo wa ubeberu wa Kiarabu na Usultani na kuongozwa na hamasa za kizalendo ambazo undani na upeo wa athari zake haukutambulikana na kuzingatiwa ipasavyo na wanasiasa wa zamani, Waislam na Wakristo. John Okello kwenye kitabu chake Revolution in Zanzibar ametumiya lugha ya maamrisho ya Ukristo na chanzo kinasema kuwa mmoja kati ya Marais wa Zanzibar amesema kuwa Mwalimu Nyerere aliamuwa kumuondowa Okello Zanzibar kwa sababu alikuwa ameingiliwa sana na hamasa za dini ya Kikristo. Okello ameandika waziwazi kuwa washiriki wa Mapinduzi walichujwa kisawasawa na kati ya watu 4,000 walichaguliwa askari 270 na 245 kati ya hao “walitoka nje ya Zanzibar (Kenya, Uganda, Tanganyika, Msumbiji, Malawi, Congo na Zimbabwe, wote waliwakilishwa).”27 Si muhimu kuwa Okello hakututajiya wangapi kati ya hao walikuwa Waislam na wangapi Wakristo kwa sababu sumu ya fitina dhidi

Page 334: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa302

ya Waarabu Waislam iliwakumba Wakristo na Waislam pamoja. Wengi wao walikuwa tayari wameshamezeshwa sumu ya biashara ya utumwa wa Waarabu pale John Okello alipowahutubiya wanamapinduzi kwa kuwaambiya:

Wapenzi ndugu zangu. Nimesimama mbele yenu na naapa kwa mchana na kwa usiku kuwa niko tayari kuwaonyesha vipi tutaweza kujitawala. Mababu zenu, baba zenu na sasa nyinyi wenyewe mmeteseka na ukandamizaji wa Waarabu kwe­nye Kisiwa hichi. Mnajuwa kuwa matumbo ya mama zenu yalifunguliwa ili mabibi wa Kiarabu wapate kuona namna ya mtoto anavyokaa ndani? Mnajuwa kuwa babu zenu walichinjwa chini ya miti hii ili mabibi wa Kiarabu wapate kuona namna binaadamu waliokufa wanavyoanguka? Si mahala hapahapa walipokandamizwa mababa zenu? Nikaendeleya kuwakumbusha kuwa masoko ya utumwa pamoja na vyuma na minyororo waliyokuwa wakifungiwa ndugu zenu bado inaonekana Kisiwani, pamoja na makaburi ya halaiki walimozikwa Waafrika waliouliwa; wao wenyewe wameyaonyesha mapango mengine ambayo damu ya Waafrika ilimwagika juu ya ardhi. Damu ya mababu zenu ilimwagika chini ya utawala wa Kiarabu; mnataka kuona damu za watoto wenu zikimwagika pia? Nani ataweza kuniambiya vipi Waarabu waliingiya kunako Kisiwa hichi na vipi walivyokitawala?28

John Okello alikuwa hazungumzi na Wazanzibari bali alikuwa akizungumza na watu ambao wengi wao, tena kwa sana, walitoka nje ya Zanzibar kwa sababu hakuwaamini Wazanzibari:

Nilihisi wengi kati ya Waafrika wa Zanzibar walikuwa hawaaminiki, kwa sababu walikuwa na uhusiano mkubwa na Waarabu wa Kisiwani, na wangeliweza kuwa ni majasusi na wangelizitobowa siri zetu ili wapewe vyeo kutoka maofisa wakubwa wa Kiarabu. Waafrika kutoka bara wasingeliweza kuwa na tamaa hiyo, na kwa kweli baadhi yao walikuwa wameshafukuzwa kutoka kwenye jeshi la polisi ambalo walikuwa wanaingizwa Waarabu kwa nguvu.29

Mpaka binaadamu akaamuwa kumdhuru binaadamu mwenzake na bila ya sababu basi huwa imepita fitina kubwa na fitina ya “utumwa wa Waarabu” na si “utumwa wa Afrika Mashariki” au “utumwa wa Bahari ya Hindi” ni fitina/propaganda kubwa Zanzibar ambayo iliuondowa utumwa mwaka 1897 wakati utumwa uliendeleya Tanganyika mpaka mwaka 1920. Oscar Kambona alimuelezeya Sheikh Ali Muhsin kwamba: “ilikuwa ni kawaida kwa baadhi ya makabila ya Kiafrika huko Tanganyika ya kwamba chifu akifa huzikwa pamoja nae kundi la watumwa wake (wahai) wakiwa wamebeba maiti ya bwana wao…mtindo huu ulisita pale tu ulipoingia Uislamu na Ukristo huko Tanganyika.”30 Ameelezeya Kambona mwenyewe kuwa “Babu yangu alikuwa ni chifu na mamishionari walipoomba wapewe mtoto wamsomeshe, babu yangu akawapelekeya mtumwa tu.”31

Kanisa la Anglikan la Zanzibar lilijengwa mwaka 1905 miaka 32 baada ya soko la utumwa kuondolewa na miaka 8 baada ya kuondolewa utumwa Zanzibar.

Page 335: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 303

Kwa mujibu wa mtafiti wa Kimarekani, Profesa Jonathon Glassman:

Jengo lenye mahandaki ya watumwa lilijengwa kama ni hospitali na mamishionari wenyewe, miaka ishirini baada ya soko la watumwa kufungwa. Mabaraza ya saruji kwenye ghorofa ya chini ya nyumba yanatambulikana wazi kama ni sehemu ambayo haifai kuingia maji, na hapana shaka ilikusudiwa kwa ajili ya kuwekea madawa.32

Lengo si kuufuta au kuingiza siasa ndani ya Ukristo Zanzibar lakini ni kuuingiza ukweli ndani ya uwongo ambao wenye kuuendeleza hawana hoja wala ushahidi wa kuziteteya na badala yake huamuwa kuwarushiya matope wale ambao hawawezi kusimama nao kwa hoja. Mwenye kurusha matope maisha hupata ushindi wa muda mfupi kwa sababu mwenye kurushiwa huwa hana njiya ya kujiteteya bila ya kurushiwa matope zaidi. Wakati umefika wa kufanya utafiti wa kina juu ya masoko ya utumwa yaliyokuwapo sehemu nyingi za Tanganyika, za pwani na za bara, makabila yaliyokuwa yakinunuwa watumwa, na makabila yaliyokuwa yakiwauza watumwa, na kazi ambazo watumwa walikuwa wakifanyishwa na Waafrika wenzao ili ipatikane ilimu yenye uthibitisho juu ya suala muhimu kama hili. Na pia ipo haja na hoja kubwa ya kuonyesha kwa ushahidi, kuwepo na kutokuwepo kwa mchanganyiko wenye kuhishimiwa baina ya watumwa waliyokuwa ndani ya mikono ya Waarabu na watumwa waliyokuwemo ndani ya mikono ya Wazungu. Nchi za Magharibi hazijapatapo kuuhishimu au kuupa madaraka ya kiutawala mchanganyiko wa mabwana na watumwa zao wakati Wafalme, na majemedari wengi wa Kiislam walikuwa wamezaliwa na mama weusi. Lakini nyuma ya tuhuma zote dhidi ya Waarabu na Waislam kuna khofu za kisiasa na za kiuchumi na ni jukumu la Waislam na Wakristo kuzitambuwa na kuja na mfumo wa mashirikiyano ambao utakuwa na manufaa ya haraka kwa waumini wa dini zote mbili. Si ubeberu wa Kiarabu/Kiislamu, “utumwa wa Waarabu”, wala kunyanganywa ushindi kwenye chaguzi, ndizo sababu kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vyote hivyo ni visingiziyo vya kumpa mbwa jina baya halafu ukamuuwa. Kama ni ubeberu ilikuwaje Waarabu waliokwenda Afrika Mashariki wakaisahau lugha yao ya Kiarabu na badala yake wakawa wanasema lugha ya Kiswahili? Kama Zanzibar ilikuwa ni kiti cha kwanza cha ubeberu Afrika Mashiriki basi mbona Zanzibar imeendeleya kudhibitiwa na watawala wa Tanganyika hata baada ya kupinduliwa “uhuru wa Waarabu?” Washirazi na Waarabu hawakuaminiwa kushirikishwa katika Mapinduzi kwa sababu wameingiliyana na kuchanganya damu na Waarabu. Na zaidi ya hilo ni kuwa Washirazi, kama Waarabu, wana asili yenye kutoka bara la Asia kwa hiyo wameonekana kuwa hawana haki ndani ya bara la Afrika. Marekani ni mfano adhimu wa watu waliyohamiya kutoka sehemu mbalimbali za dunia na katika

Page 336: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa304

vipindi tafauti. Hivi juzi tu Rais Barack Obama ambaye baba yake mzazi ametoka Kenya na aliyezaliwa na mama mweupe amevunja rekodi zote kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi katika nchi ya watu weupe na yenye nguvu kuliko zote duniani. Vipi leo wenye historia ya zaidi ya miaka elfu mbili wawe wageni Zanzibar au Afrika Mashariki au aliyekuja jana Zanzibar na kuishi kinyume na sharia awe ana haki zaidi ya wenyeji kwa sababu ni “Muafrika?” Basi kwanini asende Uganda au Nigeria akadai kuwa ana haki kuliko wenyeji wa huko na waliyojaribu kufanya hivyo walifikwa na nini? Hata Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW) wametokeya bara la Asia. Basi wafuasi wao wasizifuate dini zao kwa sababu si Waafrika na ni Waasia? Zanzibar imefika mahala kuwa haitawaliki isipokuwa kwa chama kimoja cha jamii ya watu wenye mchanganyiko wa karne nyingi na ndani ya mchanganyiko huo imezaliwa lugha ya Kiswahili, dini ya Kiislam, dini ya Kikristo na dini nyenginezo na wasiokuwa na dini, musiki, vyakula, na mavazi tafauti na mambo mengineyo ya kimaisha. Mwalimu Nyerere aliiogopa Zanzibar na akatanguliza dhambi ya ubaguzi wa kuwabaguwa Wazanzibari wenyeji kuwa Zanzibar si kwao bali ni ya Waafrika Wabantu kutoka bara. Sasa dhambi hiyo inaiandama na kuifisidi Tanganyika na Muungano wake na Zanzibar. Mwalimu Nyerere aliifanya Zanzibar kama haina wenyewe na kuitendeya mambo kama yaliyotokeya katika nchi ya Kusadikika. Matokeo yake Dola ya Tanganyika iliivamiya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 na badala yake tatizo la Zanzibar limekuja kufanywa kuwa ni tatizo baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na Tanganyika kuwa mpatanishaji na muweka amani. Wazanzibari ambao walionekana kuwa hawana matatizo na ndio maana hawakuweza kuami­niwa kuivamiya nchi yao wamegeuzwa kuwa wakiwachiwa watakuja kuuwana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo kweli Wazanzibari wanaweza kulaumiyana kwa mambo waliyofanyiyana wakati chanzo cha fitina walikuwa hawakijuwi? Sera, agenda, ya “strategic denial” ya Kiingereza ya kuizuwiya Zanzibar isiingiye ndani ya mikono ya maadui wa Uingereza ilirithiwa na kuendelezwa na Dola na Serikali ya Tanganyika kwa kwanza kuibomowa Dola ya Zanzibar iliyobakia, na baada ya muda wa siku 100 kuinyanganya Zanzibar uhuru wake wa kujilinda na kujiamuliya mambo yake ya nje baada ya kuwa na kiti chake Umoja wa Mataifa (UNO) na Jumuiya ya nchi za Commonwealth. Kwa kifupi Zanzibar ilitoka kwenye mikono ya ukoloni wa Kiingereza ikaingizwa ndani ya ukoloni wa Tanganyika. Utumwa ukawa ni kisingizyo. Uislam ukafanywa ndiyo sababu, na Ukristo ukatangazwa kuwa ndiyo muwokozi wa Muafrika aliyetiwa utumwani na Mwarabu Muislam. Zanzibar ikageuzwa kuwa ni kituo cha kale na cha mwanzo cha ubeberu Afrika Mashariki. Mwalimu Nyerere akapata nafasi aliyokuwa akiitafuta kwa muda mrefu.

Page 337: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 305

Ripoti ya CIA na Mapinduzi ya Zanzibar

Ametahadharisha mwandishi Anthony Clayton katika kifungu cha kwanza cha utangulizi wa kitabu chake juu ya Mapinduzi ya Zanzibar cha mwaka 1981 kwa maneno yafuatayo: “Matukio khasa ya Zanzibar ya mwaka 1964 na baada yake hayakupewa umuhimu unaopaswa kutolewa, zaidi kwa sababu ya kukosekana utafiti wa midani visiwani.”33 Tumekwisha kuelezeya kuwa utafiti wa midani ndani ya Zanzibar una faida na khasara zake kutokana na nani mwenye kuhojiwa na kahusika vipi na chimbuko la Mapinduzi. Kuna mikono na vichwa vya Mapinduzi na asilimia kubwa sana ya utafiti wa Mapinduzi umetokana na mikono yake na kama alivyosema marehemu Mzee Thabit Kombo “na mengine ya uwongo mtupu.” Alinihakikishiya aliyekuwa mkubwa wa jeshi la polisi la Tanganyika wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Mzee Hamza Aziz, kuwa ripoti ya Shirika la Kijasusi la Kimarekani (CIA) ina maelezo mazuri juu ya kuhusika kwa Tanganyika katika mapinduzi ya Zanzibar. Kwa wakati ule hata kama ningelikuwa ninayo ripoti hiyo isingeliweza kunisaidiya sana bila ya utafiti wa midani na utafiti wa midani usingeliweza kunisaidiya kama si kuongozwa na dalili na alama kutoka nyaraka za kitaifa za Uingereza na za Kimarekani.34

Helen­Louise Hunter, mtafiti na mtaalamu wa kiuchumi na kisiasa alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Kijasusi la Kimarekani (CIA) kwa zaidi ya miaka ishirini na ni mwandishi wa ripoti ya CIA aliyonigutuwa marehemu Mzee Hamza Aziz. Kwa ripoti iliyoandikwa miaka arubaini na tatu nyuma Hunter alifanya kazi nzuri sana. Kukosekana kwa utafiti wa midani kumemfanya mchambuzi huyo kuufikiya uamuzi ufuatao: “Ingawa viongozi fulani wa ASP, na mwenye kujulikana zaidi ni Hanga, walikuwa wapangaji wa mikakati ya mapinduzi, hawaonekani kama wao ndiyo walioyaanzisha Mapinduzi usiku wa tarehe 11–12 Januari.”35

Hata hivyo Hunter ameandika kuwa: “Mnamo katikati ya mwaka 1963, mara tu baada ya uchaguzi wa Juni [ Julai], kikundi cha viongozi wa ASP, akiwemo Hanga, walikwenda Tanganyika kuomba msaada wa pesa na silaha kwa kuunga mkono mpango wao wa mapinduzi.” “Ni dhahiri”, anaandika Hunter, kuwa Mwalimu Nyerere “alijuwa na aliunga mkono jumla ya mpango wa mapinduzi. Inavyoonekana, mapinduzi yalikuwa yamepangwa yafanyike mwezi wa Machi au Aprili 1964.”36

Baada ya kuonyesha kidole lilipo chimbuko la Mapinduzi ya Zanzibar, Hunter ameandika kuwa katika kitu kilichochangiya kuupotosha ukweli wa Mapinduzi hayo ni ile: “Fikra kuwa kufungiwa kwa chama cha Umma Party kiliwaongoza Babu na wafuasi wake kuasi kwa kutumia silaha huenda ikawa ndio kosa kubwa la kutoyafahamu Mapinduzi ya Zanzibar.”37

Msomaji atakumbuka kuwa hata ripoti ya Kamishina Sullivan wa jeshi la polisi la Zanzibar ilianza na kumalizika kwa kumtwisha marehemu Babu na wafuasi

Page 338: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa306

wake dhamana kubwa ya kuyaandaa Mapinduzi ya Zanzibar. Khitimisho la CIA kuhusu Babu ni: “…alikuwa ni mtu wa wazi wa kutuhumiwa katika upangaji wa kuipinduwa serikali lakini hakuna ushahidi wa kukinaisha kuwa alikuwa na mchango wa maana kwenye Mapinduzi.”38

Hata baada ya Mapinduzi ripoti ya CIA pia inaelezeya kuwa: “Inavyoonyesha kwa makusudi Rais wa Tanganyika [Nyerere] aliziongezeya chumvi khofu zake kuwa Zanzibar itaingiya ndani ya mikono ya Makoministi; hii ilikuwa hoja ambayo aliweza kuitumiya na kuziridhisha nchi za Magharibi ili kupata kuungwa mkono katika njama zake za kuimeza Zanzibar ndani ya Tanganyika.”39

Mapengo makubwa ya ripoti ya CIA yanatokana na nadhariya kuwa kulikuwa na mipango mingi ya kupinduwa Zanzibar na ule wa Hanga, Kambona na Nyerere, sio uliyotekelezwa tarehe 12 Januari 1964. Kuna sehemu ya ripoti imeandika kwa njiya ya kukhitimisha kuwa “Kiongozi muhimu kuliko wote katika njama [za kupinduwa] alikuwa ni Hanga” na kuendeleya kuwa:

Karume alifadhaishwa bila ya kiasi na mauwaji ya kishenzi na kuibiwa Waarabu na Waafrika katika siku za baada ya mapinduzi lakini alikuwa hakuweza kufanya kitu. Vikundi vyake vya kuweka usalama vilikuwa havifuwi dafu na vikosi vyenye silaha ambavyo vikijinadi kuwa ni wafuasi wa Okello aliyekuwa akiranda sehemu za mashamba, akiuwa na kupora.40

Ripoti inakariri tena na kwa uwazi zaidi kuwa

Inaonyesha kuwa kiongozi muhimu katika mipango ya ASP ya kupanga mapinduzi, alikuwa Hanga ambaye alisaidiwa na memba wa mrengo mkali wa ASP, na khasa watu fulani kutoka vyama vya wafanya kazi na khasa Hassan Nassor Moyo, Katibu Mkuu wa ZPFL na kiongozi ndani ya ASP, alikuwa katika upangaji [wa mapinduzi]. Karume binafsi hakuhusika kabisa; Karume binafsi alikuwa hajahusika kabisa; inawezekana O. [Othman] Shariff na Aboud Jumbo [e] walikuwa hawana habari na mpango [wa mapinduzi].41

Hakuna popote pale ndani ya ripoti ya Hunter ambapo inatajwa Kamati ya Watu 14 chini ya uongozi wa Mzee Karume kuwa ndiyo iliyokuwa imeyaandaa na kuyashika mambo ya Mapinduzi. Hakuna. Majina yanayojichomoza sana ni ya Hanga na Kambona. Kwenye masuala kama haya ni vigumu kuthibitisha kinagaubaga mchango wa Rais au kiongozi wa juu kabisa wa nchi. Daima kiongozi wa juu wa nchi anakuwa na viongozi watekelezaji wa sera waliyokubaliyana pamoja. Kilicho muhimu ni hakuna mgongano wa aina yoyote baina ya simulizi za wazee wa Mapinduzi na marejeo ya nyaraka za Kitaifa za Kiingereza au za Kimarekani. Hata hivyo kushiriki kwa Mwalimu Nyerere kunathibitishwa zaidi na dondoo zifuatazo:

Page 339: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 307

Katikati ya mwaka 1963 pale Hanga na viongozi fulani wa ASP walipomuendeya [Mwalimu Nyerere] kumuomba msaada wa silaha na kifedha, inasemekana Rais wa Tanganyika aliwakataliya kwa sababu hakufikiri kuwa mpango wao wa kufanya mapinduzi ungelifaulu.42

Ingawa ni dhahiri Nyerere alijuwa na aliuwafik mpango wa mapinduzi kwa jumla, inawezekana Kambona hakumuarifu Rais [Nyerere] mambo madogomadogo. Ipo sababu ya kuamini kuwa [Nyerere] hakuarifiwa kuhusu silaha ambazo Kambona aliwapa ASP.43

Katikati ya mwaka 1963 inasemekana Kambona alimpa Hanga na wafuasi wake bunduki 2 za machine gun na bunduki 10 za aina ya rifle kwa njia ya siri. Kambona pia aliandaa baadhi ya mzigo mwengine wa silaha kutoka Algeria kwenda Tanganyika ambao huenda uliwafikia wanamapinduzi wa Zanzibar, ingawa labda sehemu kubwa ya hizo silaha walikusudiwa wapigania uhuru wa Msumbiji.44

Mzee Aboud “Mmasai” amesimuliya namna yeye na Twala walivyokwenda kuchukuwa silaha nyumbani kwa Kambona na walivyoziingiza Zanzibar kupitiya Bweleo. Suala linalojitokeza ni kuwa Mwalimu Nyerere aliijuwa mipango ya mapinduzi lakini alikuwa ana wasiwasi huenda yasifaulu. Sababu za kuwa na wasiwasi zinaweza kuwa ni kwa sababu ya kumuogopa Muingereza na Gamal Abdel Nasser lakini kutokana na kuwa hao wawili walikuwa ni maadui kulimpa Nyerere mwanya wa kucheza nao kuyafanya Mapinduzi yaliyokuwa na bahati na­ye kwa sababu Wazanzibari na Watanganyika wengi hawakuzijuwa sababu zake. Tumeona pia kwenye simulizi za Mzee Aboud “Mmasai” kuwa waliwapelekeya barua viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kuwaarifu kuhusu Mapinduzi kabla ya kuingiya mabomani. Hapana shaka barua hizo zilipata muongozo wa wapi pa kuzipeleka kutoka kwa Oscar Kambona. Maelezo yanazidi kuweka mambo sawa: “Kwa mujibu wa ripoti moja, Rais Kenyatta aliarifiwa kuhusu mipango ya mapinduzi lakini alikuwa hakupewa tarehe maalumu lini yatafanyika. Inaonyesha alikubali asilipeleke jeshi la Kenya ikiwa serikali ya Zanzibar itaomba msaada kutoka nje dhidi ya waasi.”45

Mashirikiyano baina ya Hanga na Kambona ni jambo ambalo limethibitishwa mara nyingi na maandishi na watu tafauti na kitabu cha Hunter kinayaunga mkono mashirikiyano hayo:

Ushirika wa Tanganyika na viongozi wa ASP waliyokuwa wakiyapanga mapinduzi ni jambo ambalo limethibitishwa ipasavyo. Hanga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika, Kambona, ni marafiki wa zamani, na waliishi chumba kimoja London. Kwa kuwa [Kambona] alikuwa anataka Waafrika wauchukuwe utawala kutoka kikundi cha Waarabu, alikuwa muda wote anaijuwa mipango ya kupinduwa; aliyaunga mkono mapinduzi kwa silaha na pesa…46

Juu ya umuhimu wa ripoti ya Hunter, bado katika khitimisho lake kuna

Page 340: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa308

mgongano baina ya maelezo na tafsiri zisizolingana kama alivyoandika:

Kwa mukhtasari, ingawa kulikuwa na mpango wa mapinduzi zaidi ya mmoja Zanzibar, mapinduzi yaliyofanyika tarehe 12 Januari hayakuwa yale yaliyopangwa na ima Babu na chama chake cha Umma Party, au Hanga na kikundi chake cha ASP. Yalikuwa ni mapinduzi yalozuka tu.47

Sababu ya kuufikiya uamuzi huu wa haraka baada ya kukusanya ushahidi unaweza kuwa umetokana na ugumu wa kupima bila ya ushahidi wa utafiti wa midani baina ya uongozi na viongozi gani khasa walioyapanga Mapinduzi na uongozi na viongozi wengine waliokuja kuchomoza na kuwa wakubwa na majemedari wa Mapinduzi ambao hawakuwa viongozi wa juu ndani ya jiko la Mapinduzi. Na zaidi kuloleta migongano ya nadhariya na tafsiri zenye kugongana ni kuchomoza kwa John Okello ambaye ripoti ya CIA imemueleza kuwa ni “bahati nasibu ya kihistoria.”

Odinga Oginga na Mapinduzi ya Zanzibar

Juu ya kuwa majina ya Hanga na Kambona yamekuwa yakitajwa kwa pamoja, kuna majina mengine pia ambayo bado hayakufanyiwa utafiti wa midani na kuthibitishwa. Kwa upande wa viongozi wa Serikali ya Kenya “Ilikuwa ni dhahir kwao kuwa oganaizisheni yenye uwezo mkubwa zaidi kuliko Sheikh Karume ndiyo iliyokuwa na uwezo wa kuyaongoza mapinduzi.”48 Jina la Oginga Odinga ni moja wapo wa majina ambayo yananasibishwa na majina ya Hanga na Kambona na ripoti ya Hunter inamtaja kwa kusema kuwa:

Kumekuwepo ripoti zenye kusema kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Oginga Odinga alikuwa pamoja na Hanga na Kambona katika kuyapanga mapinduzi…ametamka kuwa [Odinga] amehusika sana [katika mapinduzi] kama alivyohusika Kambona. Kama alivyo na Kambona, Hanga alikuwa ana mahusiano binafsi na Odinga, ambaye alimsaidiya kumpeleka nje kusoma…Kwa hiyo, kuna hisia ya kijumla kwamba huenda Odinga alikuwa ana mkono katika matukio ya Zanzibar ingawa kuhusika kwake kwenye mapinduzi hakujapata kuthibitishwa.49

Jeshi la Kenya lilipoasi tarehe 23 Januari 1963 viongozi wa Uganda waliwasiliyana moja kwa moja na Serikali ya Kiingereza na kuomba msaada na bila ya kuwaarifu au kuwashauri Wakenya.50 Bwana Odinga:

aliposikiya kuwa majeshi ya Kiingereza yako tayari kuondoka kwenda Uganda akasababisha viongozi wakubwa wa Wizara [ya Ndani] kupiga simu Uwanja wa ndege na kuzuwiya ndege isiruke. Kwa bahati nzuri walipiga simu uwanja wa ndege sio. Inawezekana kuwa wakati huu Bwana Odinga alikuwa hajuwi kuwa tumeshaijibu Serikali ya Kenya kuhusu ombi lao la msaada.51

Page 341: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 309

Kwa mujibu wa mwenyewe Bwana Odinga:

Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa na viongozi wake wenyewe na si na mtu mwengine—si na mimi wala Castro au Cuba au yoyote popote pale—pale katiba ilipotengenezwa kuwazuwia Waafrika walio wengi kuweza kuungoa utawala wa Kiarabu kwa njia ya sanduku la kura.52

Odinga hakueleza ni nani kati ya viongozi wa Zanzibar waliyoyapanga Mapinduzi na nini ulikuwa uhusiyano wake na viongozi hao. Kitu kimoja Odinga ametuhakikishiya nacho ni suala la mchango wa Babu kwenye mapinduzi:

Mara moja Babu alikuja Nairobi na akakaa nyumbani kwangu. Nilijuwa kuwa alikuwa ndio nguvu nyuma ya chama cha Umma na nilikuwa nafahamu kuwa yeye na wenzake walikuwa wanapanga mapinduzi wakati ule lakini sikuwa na hakika ya chochote, na sikuambiwa chochote, na kama ingelitokea kuulizwa rai yangu basi ningelimwambia Babu kuwa ningelipendeleya kumuona ndani ya uongozi wa chama cha Afro­Shirazi. Ni kinyume na vyombo vya habari vyenye kuandika kuwa nilikuwa nyuma ya Babu ambaye alikuwa nyuma ya mapinduzi ya Zanzibar.53

Babu asingeliweza hata siku moja kuingizwa ndani ya uongozi wa Afro­Shirazi kwa kupewa cheo cha Ukatibu Mkuu ambacho kilikamatwa na Mzee Thabit Kombo ambaye alikuwa ni alama ya nguvu za Washirazi ndani ya ASP. Odinga, Kambona na Nyerere wakisumbuliwa na siasa ya kufarakanisha ya Pan­Africanism yenye kuwabaguwa Wazanzibari wenye asili ya Kishirazi na ya Kiarabu ikiwa walikuwa ni wapenda au wapinga maendeleo. Kichekesho cha historia ni kuwa ubaguzi wa kuwabaguwa Wazanzibari kuwa si Waafrika kwa maana wanayoitaka wao, ndiwo uloipa Tanganyika hadhi ya uongozi katika suala la Umoja wa Afrika! Maneno ya Odinga yamefika ulingoni:

Hapana shaka yoyote kuwa mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 ni tukio kubwa la Afrika Mashariki. Huu ulikuwa mwanzo wa tishio kubwa la vita baridi Afrika Mashariki. Athari juu ya Tanganyika na Kenya kutokana na matukio ya Zanzibar baadae yalikuwa yenye msisimko wenye kutafautiana: Tanganyika ikaelekeya kunako sera za Umoja wa Waafrika zenye msimamo mkali zaidi; Kenya ikachukuwa mkato mwengine kuelekeya kwenye siasa za kihafidhina.54

Zanzibar iliyovamiwa ikawa ni sababu ya sera tafauti baina ya Tanganyika na Kenya. Kenya ilibidi ichukuwe siasa za kihafidhina kwa sababu ikitambuwa Tanganyika iliifanyiya nini Zanzibar. Kichekesho kikubwa zaidi ni vipi dola za Mashariki, Urusi na Uchina zilirukiya kuyasaidiya Mapinduzi ambayo yaliungwa mkono na wakoloni wa Kiingereza. Na ikiwa wazungu wakiujuwa msimamo wa Babu na Makomred na kuwaogopa, kwanini waliachiliya maingiliyano na ASP na Mapinduzi? Kwanini Umma Party walihitajika? Kuufunika mkono wa Tanganyika na kuiwachiya Zanzibar imezwe na Tanganyika kwa kisingizyo cha

Page 342: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa310

kuwaogopa Makomred? Inaonyesha hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kuwaweka mbele na kuwatumiliya Makomred. Viongozi wa Kiafrika, wa Kiarabu na wa Kiyahudi, Waislamu na Wakristo, Waafrika na Waarabu, pamoja na wanamapinduzi wenyewe, wote na bila ya kujuwana walikuwa ndani ya kambi moja katika kuipinduwa Dola ya Zanzibar. Katika vurugumechi ya Zanzibar ni Tanganyika peke yake iliyoweza kuibuka mshindi kwa kuungwa mkono na Dola ya Uingereza kwa kumuokowa Nyerere na kumrudisha madarakani baada ya uasi wa kijeshi na kumuachiya aidhibiti Zanzibar hata baada ya kuwa na hakika Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa Tanganyika. Nchi za Magharibi zilikawiya kuitambuwa Zanzibar ya Mapinduzi kwa sababu ya kuchomoza John Okello ambaye alikuwa hajulikani na mtu. Nyerere pia alikawiya kuitambuwa serikali mpya ya Zanzibar kwa sababu hali ya uongozi uliyochomoza na Okello, na khasa wa Babu, ulikuwa ni tishio kwa siasa ya kizalendo ya Kiafrika ambayo ilimuona Babu na wafuasi wake kama ni Wazanzibari Waarabu hata kama walikuwa na siasa za kimaendeleo. Tarehe 17 Januari 1964 Mwalimu alipeleka Zanzibar askari 100 kutoka Tanganyika. Tarehe 20 Januari yeye mwenyewe akapinduliwa na jeshi la Tanganyika pamoja na vyama vya wafanyakazi. Tarehe 13 Januari Kenya iliyokubaliwa uwanachama wake siku moja na wa Zanzibar iliitambuwa serikali mpya ya Zanzibar Jumatatu tarehe 13 Januari 1964. Nyerere hakuitambuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mpaka tarehe 23 Januari 1964 baada ya kuokolewa na Waingereza. Muingereza alisubiri na hakuitambuwa serikali mpya ya Zanzibar mpaka tarehe 23 Februari. Alikuwa akiidurusu hali ya kisiasa kutoka kwa Nyerere na kumuunga mkono Karume dhidi ya wanamapinduzi waliyokuwa na misimamo mikali dhidi ya nchi za Magharibi. Nchi za mirengo ya siasa za mkono wa kushoto ambazo hazikuwa na mchango wowote katika mapinduzi ya Zanzibar zikawa ndiyo za kwanza kuitambuwa serikali mpya ya Zanzibar.

Ubeberu wa Nyerere na Mapinduzi ya Tanganyika

Wakati Mapinduzi yameshamalizika na siku sita kabla ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, J. D. B. Shaw wa Commonwealth Relations Office, Downing Street, alimuandikiya barua Naibu Balozi wa Kiingereza wa Tanganyika, Stephen Miles, kutaka kujuwa kama: “…mtizamo wa Serikali ya Tanganyika kwa vikundi vya wapiganiya uhuru tafauti walivyovikaribisha katika eneo lake umeathiriwa na kufuzu kwa Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yamepangwa (mounted) kutoka Tanganyika.”55

Kupinduliwa kwa Zanzibar kulikokuwa hakujulikani na waliyo wengi, kulimpatiya sifa kubwa Nyerere na kuiweka Tanzania katika mstari wa mbele wa ukombozi wa Afrika. Maafa ya Zanzibar yaligeuka na kuwa ni neema kwa jina la

Page 343: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 311

Nyerere na la Tanzania. Waingereza walitaka:

…maamuzi yote muhimu ya kuulinda muungano yafanyike Dar es Salaam. Rais Nyerere amejitahidi sana kuuonyesha umuhimu kwake wa hii khatuwa ya kwanza kuelekeya Umoja wa Afrika. Kushindwa kuulinda Muungano kutamvunjiya sana hishima yake.56

Wakati Tanganyika, na baadaye, Tanzania, ikijivuniya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwalimu Nyerere kumnukuu Mzee Aboud Jumbe waziwazi kuhusu sababu zilizowafanya Wazanzibari kukamata mapanga kumwaga damu yao wenyewe na ya wenziwao ili waepukane na Usultani, na kushadidiya kuwa Tanganyika haikushika mapanga bali iliupata uhuru wake kwa njiya ya amani, nchi na jina la Zanzibar liliendeleya kudidimiya na kufifiya na la Tanzania kupanda chati duniani. Lakini bado kulikuwa kuna wasiwasi wa kumaliza kazi. Kuimaliza kazi na kuweza kuidhibiti Zanzibar ipasavyo kulihitajiya kufanyike mambo matatu muhimu. La kwanza, ambalo liliungwa mkono na Uingereza, lilikuwa ni kuifanya Zanzibar iwe na sifa ya Mkoa. P. A. Carter wa Commonwealth Relations Office ameweka wazi:

Tumekubaliyana na mtizamo wa jumla kuwa inawezekana kuiendesha Zanzibar chini ya mfumo wa idara wa jimbo. Nakumbuka Kambona aliwahi kunitajiya zamani kidogo alipokuwa akinungunika kuhusu mtizamo wa serikali ya zamani ya Zanzibar kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki kuwa Zanzibar itizamwe na iendeshwe kama jimbo lolote lile la Tanganyika. Mafia ni sawasawa na ukubwa wa Pemba na inaendeshwa na Mkuu wa Wilaya chini ya Mkuu wa Mkoa uliyopo Dar es Salaam. Namnukuliya barua hii Le Bretom ambaye anaweza, kutokana na uzowefu wake wa Zanzibar na ilimu yake ya mfumo wa majimbo ya Tanganyika, akupe fikra zaidi kuhusu njiya muruwa ya kuiweka Zanzibar.57

Jambo la pili ambalo Kambona alilisimamiya kwa nguvu ni kuzishusha hadhi Balozi zilizokuwepo Zanzibar na kuziweka kunako mustawa wa Consulates. Ubalozi wa Uingereza uliyokuwapo Dar es Salaam umesajili:

Katika mazungumzo mafupi ambayo Balozi wa Kimarekani na mimi tulokuwa nayo na yeye [Kambona] tarehe 11 Juni wakati wa kuondoka Rais [William] Tubman, tulimhimiza atupe taarifa ya tarehe ya kuziteremsha balozi zote. Ameahidi atafanya hivyo na siku ya pili alipokuwa Nairobi alinukuliwa katika magazeti akisema kuwa ameshachaguwa tarehe ya kufanya hivyo. Tunaisubiri taarifa.58

Kuziteremsha Balozi ziliyopo Zanzibar na kuzifanya ziwe Consulates kulikwenda sambamba na kukifuta kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa. Hili tutalizungumza kunako mlango ujao katika safari yetu iliyotubakiliya. Jambo la tatu (na mengineyo) ambalo lilikuja kufanyika baadaye ni kulidhibiti jeshi la Zanzibar ambalo “Nyerere amekiri kuwa linamtiya wasiwasi mkubwa.”59

Page 344: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa312

Juu ya mambo yote hayo bado Waingereza na Nyerere walikuwa wana wasiwasi kwa sababu:

Midam Zanzibar inaendeleya kujiendesha kama ni Nchi Huru, Muugano baina ya Tanganyika na Zanzibar utakuwa hauna nguvu. Rais Nyerere kama ni Mkubwa wa Muungano anajaribu kuwavuta Mawaziri wa Zanzibar waulinde Muungano. Kuna wakati utafika itambidi ama akubali kuuvunja Muungano au aombe msaada kutoka nje umsaidiye kuutekeleza.60

Waingereza walimtathmini Mwalimu kuwa “Kisaikolojiya hapendi kuchukuwa maamuzi yasiyofurahisha na yenye msimamo mkali.”61

Huko nyuma Tanganyika, na baadae Tanzania Bara, hazijawahi hata mara moja kukiri kuwa zilihusika katika mipango ya kuipinduwa Dola ya Zanzibar na Muungano uliyofuatiliya. Wako watakaofanywa waseme kuwa Tanganyika ilitowa msaada tu kwenye Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 kwa kushirikiyana na watu wa Bara lakini siyo iliyoipinduwa na yenye kuendeleya kuidhibiti Dola ya Zanzibar isinyanyuke tena. Hoja itazungumza: kwani akina Hanga, Saadalla, Twala, Mmasai na wengineo hawakuwa Wazanzibari? Hoja itasahau kuuliza: kwani utawala wa Zanzibar ulirudi kwao? Wapangaji mikakati wa hoja wasisahau kuwa kuna mgongano mkubwa baina ya kusema kuwa Mapinduzi ya 1964 ya Zanzibar yalipangwa na Wazanzibari wenyewe halafu ukautaja mchango wa Dola ya Tanganyika! Hoja huvunjwa na hoja. Hoja kuwa Zanzibar ilisaidiwa tu kwenye mapinduzi huenda ikapewa sauti mpya na kupokelewa na baadhi ya waandishi wa habari ili kipatikane kikundi au hata chama cha kisiasa kipya bara na chenye nguvu Zanzibar ambacho kitakuja kuzipinga juhudi za Wazanzibari kuwa kitu kimoja. Ripoti ya shirika la ujasusi la Kimarekani, CIA, imeandika bila ya kumumunya au kutafuna maneno:

Kwa miaka mingi, Watanganyika, akiwemo Nyerere, walikuwa na fikra kuwa Zanzibar ni hakika sehemu ya Tanganyika. Walikuwa wanaingojeya siku serikali ya Kiafrika itakapokamata utawala Zanzibar ili waziunganishe nchi mbili. Inaweza kuwa ni hamu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kulikomfanya Nyerere ajiingize ndani ya siasa za Zanzibar kutokeya mwanzo, kuanziya mwaka 1956. Ingawa [Nyerere] hatokiri kuwa maamuzi yake juu ya Zanzibar ni ya kibeberu, inaweza hili likawa ndio motisha yake kuutaka muungano. Ni wazi hivi sasa, na kama si zaidi huko nyuma, kuwa muungano uliokuwa kichwani mwa Nyerere ulikuwa ni ule ambao yeye na Watanganyika watautawala. Kwa sababu zilizo wazi, hakumuarifu Karume kuhusu masala hayo kabla ya muungano. Karume hakuwa na fikra iliyo wazi kuhusu aina ya mahusiyano yaliyokusudiwa na hakuna shaka yoyote kuwa hakutarajiya muungano wa mkazo kama alivyofikiriya Nyerere.62

Odinga Oginga wa Kenya pia anathibitisha kuwa:

Page 345: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 313

Tanganyika ambayo maisha ilikuwa ikiteteya umoja baina ya kisiwa [Zanzibar] na bara [Tanganyika]—na ilivyo, TANU, ilichukuwa hatua zilizomalizikiya kuundwa kwa nguvu za Afro­Shirazi—ilikuja kuisaidiya Zanzibar na kuuteteya sio uhuru wake kamili, bali kuipa nguvu Tanganyika kujiamuliya sera zake zilizo huru na bila ya kushawishiwa na upinzani wa kibeberu wa mabadiliko yaliyotokeya Zanzibar.63

Sio tu kuwa Mzee Karume hakuukubali Muungano utakaoifuta Zanzibar, bali hata hakushirikishwa katika Mapinduzi yaliyokuja kuibomowa na kuifuta katika ramani ya dunia Dola ya Zanzibar. Hata kama kisiasa alikubali kuupokeya ukubwa kuwa yeye ndiye alikuwa Jemedari wa Mapinduzi ya Zanzibar, ni wazi kuwa waliyompa cheo hicho walimpa kwa sababu zao na yeye alikipokeya kwa sababu zake. Ukweli ni kuwa:

Karume katamka kwa kujiamini kuwa tafsiri ya muungano na Tanganyika siyo aliyokuwa nayo yeye. Yeye [Karume] na viongozi wengine wa Zanzibar sasa wameweka wazi kuwa wameazimiya kuwa wao na nchi yao hawatojidhalilisha kwa Tanganyika. Hata Hanga, ambaye anauunga mkono sana muungano katika Wazanzibari, ambaye anadai kuwa ni mpishi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Kambona kutokeya walipokuwa wanafunzi London, amesema kuwa Watanganyika ni wajinga kama wanafikiriya kuwa watautawala muungano; wanapoteza wakati wao kuja Zanzibar kujaribu kutuambiya kipi cha kufanya. Karume hatokubali hata siku moja kuchukuwa amri kutoka kwao.64

Lakini hizo hazikuwa fikra za Nyerere na wenzake wa Tanganyika. Kuonyesha hamu ya kuwa na muungano watakaoutawala wao: “Nyerere na Kambona na viongozi wengine wa Tanganyika wamesema kuwa hawatokubali, chini ya dhurufu zozote zile, kuvunjika kwa Muungano, na kuwa wako tayari kuulinda kwa thamani yoyote ile hata ikibidi kuingiliya kijeshi…”65

Tanganyika inaweza kuingiliya kijeshi kwa kukitumiliya kipengele cha Katiba kwa ajili ya kuilinda hali ya amani na utulivu Zanzibar. Wazanzibari wachache wenye kupendeleya fujo kwa kujipatiya mavuno ya kisiasa ndiwo wa kutahadhari kutowapa viongozi wa Tanganyika wasiyoitakiya mema Zanzibar kuivamiya tena kwa mantiki ileile ya 1964 na Mapinduzi mengine yaliyofuatiliya. Waingereza ambao walikataa kuingiliya kuzuwia mauwaji ya halaiki punde baada ya Mapinduzi ya 1964 kwa kusema kuwa matatizo ya Zanzibar yalikuwa ni ya baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na hayakutoka nje, walitambuwa kuwa kulikuwa na mchango kutoka Tanganyika. Chenye kustaajabisha ni Kamishna Sullivan hakuyataja hayo kwenye ripoti yake juu ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyoiandika tarehe 17 January 1964. Kutokeya mstari wa kwanza mpaka mstari wa mwisho wa maelezo yake aliukamata uzi ule ule kuwa Ma­kominist [Makomred] ndio waliofanya Mapinduzi wakati ripoti nyengine ya Kiingereza imeandika kuwa:

Page 346: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa314

Tunaendelea kupokeya ushahidi wa mchango fulani wa Tanganyika katika mapinduzi kutoka kwa vyanzo tafauti wakiwepo maofisa wanne wa Kiingereza kutoka Zanzibar ambao hivi sasa wako Dar es Salaam, nao ni Sullivan (Kamishna wa Polisi), Waring, Derham na Misra.66

Isitoshe, kulikuwa na ripoti nyengine ambayo inashuhudiya kuwa watu kutoka Tanganyika walikwenda Zanzibar kushiriki katika Mapinduzi na ushahidi wa silaha za jeshi la polisi la Zanzibar ambazo zilikamatwa Tanganyika:

Inaaminika kuwa Waafrika kutoka Tanganyika wamekwenda Zanzibar kushiriki katika mapinduzi. Inajulikana kuwa baadhi ya Waafrika walobeba silaha wamerudi Tanganyika kwa njiya ya bahari Jumapili usiku baada ya mapinduzi na silaha zao zikakamatwa na askari wa Tanganyika. Ofisa wa Kiingereza aliyekuwepo Dar es Salaam amemuonyesha Waring orodha ya silaha zilizokusanywa na Waring aliitambuwa nambari ya bunduki aina ya Sterling ambayo ilikuwepo Zanzibar ndani ya ghala la silaha la [PMF].67

Mbali ya ushahidi wa bunduki moja iliyokamatwa Tanganyika ambayo ilikuwepo Zanzibar “ndani ya ghala la silaha la [PMF]” kuna watu walionekana kuondoka Zanzibar asubuhi baada ya kuimaliza kazi waliokwenda kuifanya usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili tarehe 12 Januari 1964:

Kiasi ya saa 5:45 za Jumapili asubuhi, Waring aliiyona meli ndogo yenye uwezo wa kubeba watu 100 ikiondoka kwenye gati ya Zanzibar. Mkuu wa Idara wa Zanzibar Steven (ambaye bado yuko Zanzibar) amesema kuwa [meli] ilikuwa ikipeperusha bendera ya Tanganyika. Uwezekano uliopo ni meli hii ilikuwa inawarudisha wanamapinduzi wa Kitanganyika Tanganyika.68

Waingereza pia walijuwa kuwa silaha kutoka Algeria alipelekewa Nyerere na zilipelekwa Zanzibar na kutumika katika Mapinduzi. Hii ni kinyume kabisa na maelezo ya miaka yenye kusema kuwa wanamapinduzi walitumiya mapanga na mashoka peke yake pale walipoyavamiya maboma ya jeshi la polisi ya Ziwani na Mtoni:

Maofisa wa polisi wa Kiingereza wanakisiya baina ya watu 200 na 300 waliyashambuliya makaazi ya askari polisi wa Ziwani, na kiasi ya idadi hiyohiyo ilikishambuliya kituo cha [PMF]. Sullivan anasema kuwa wapinduzi walikuwa tayari wana silaha na wakizipiga silaha za automatic kabla ya kuingiya ghala ya silaha na kuziiba silaha za polisi. Silaha kutoka Algeria zinatiliwa shaka kutumika.69

Na pia:

Tumeripoti kabla kuwasili Tanganyika katika miezi ya karibuni shehena ya ndege mbili ziloleta silaha kutoka Algeria na meli kutoka Algeria iliyokuwepo hapa wiki iliyopita. Inaaminiwa kuwa silaha zote kutoka kwenye meli zimefungiwa na kikosi cha Tanganyika Rifles. Djoudi, kiungo cha ubalozi wa Algeria Dar es

Page 347: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 315

Salaam alikuwepo Zanzibar kabla ya mapinduzi, na aliondoka Zanzibar kurudi Dar usiku wa Jumamosi. Lakini aliona haya sana na inawezekana sana kuweko kwake Zanzibar wakati ule ilikuwa ni sudfa tu. Hisiya yetu siku zote ilikuwa silaha za Algeria zilikuwa kwa ajili ya wapiganiya uhuru wa Mozambique, na kama kuna silaha zozote walipelekewa wapinduzi wa Zanzibar, basi ilifanyika bila ya Waingereza kujuwa.70

Chanzo kinasema kuwa kulikuwa na harakati kubwa za kijeshi Bagamoyo katika siku za kukaribiya Mapinduzi ya Zanzibar. J. J. Mchingama alituelezeya kuhusu gari lililopita kwa kasi kubwa kituo cha polisi cha Fuoni na nyuma yake aliwaona watu waliovaa nguo nyeusi na kujipaka rangi nyeusi. Uthibitisho wa kupelekwa maofisa fulani kutoka jeshi la Tanganyika Zanzibar umo kwenye maelezo yafuatayo:

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Tanganyika waliwaambiya maofisa fulani wa Kiafrika na N.C.Os wa Tanganyika Rifles Ijumaa tarehe 10 kuwa huenda wakahitajika kwa operesheni maalumu nje ya Tanganyika. Ushahidi huu na mwengineo unaitiliya nguvu fikra kuwa Kambona alihusika kwenye mpango [wa mapinduzi]. Kwa kweli tuna habari kutoka kwa ofisa mmoja wa Kiingereza aliyoko wizarani kuwa Kambona amejuwa kinachoendeleya siku ya Jumamosi. Waziri wa Mambo ya Ndani Lusinde hakika atakuwa amehusika. Katika miezi ya karibuni alimsaidiya Babu na marafiki wengine kutumiya vyombo vya polisi kuwapeleka baina ya Zanzibar na Tanganyika na kuwapa pasi za kusafiriya nje. Hakuna (hakuna) ushahidi mpaka sasa hivi kama Nyerere na mawaziri wengine wamehusika. Labda Odinga ambaye yuko karibu sana na Kambona atakuwa amehusika kwa upande wa Kenya, lakini pia hakuna ushahidi madhubuti.71

Huu wote ni ushahidi kuwa Tanganyika ilihusika kikamilifu katika kuipinduwa Dola ya Zanzibar, na kama alivyosema Mzee Aboud “Mmasai”, kuwa hata kama Muingereza hakuijuwa mipango ya Mapinduzi kwa tafsili zake basi alijuwa kuwa yatatokeya, na hakuchukuwa hatuwa yoyote ya kuyazuwia au kuyazuwiya mauwaji ya halaiki. Muingereza hakushiriki katika kuipinduwa Dola ya Zanzibar bali alishiriki kwa kujuwa kinachoendeleya na kuamua kutofanya kitu kwa sababu Uingereza ilikwishaamua kuutowa mkono wake Zanzibar na kuiwachiya Zanzibar itawaliwe na Tanganyika. Ni sawa na watu wazima waliyokaa kitako karibu ya hodhi la maji na waka­muona mtoto mchanga anatambaa kuelekeya kwenye hodhi na wakaamua kutizama upande wa pili. Ushahidi wa kushiriki kwa Muingereza kwenye Mapinduzi ya Zanzibar ni ushahidi wa uamuzi wa kutochukuwa hatua ya kukizuwiya kile ambacho wakijuwa kitatokeya ambacho walitaka kitokee kwa sababu walijuwa kitamalizikiya wapi, kwa nani, na kwa nini. Kwa mujibu wa marehemu Nassor Abdalla “Mlawwaz” zilikuwepo taarifa zilotiwa saini kuwa Edington Kisasi na memba wa jeshi la polisi walikuwa wakifanya mikutano lakini hakukuchukuliwa hatuwa yoyote.72

Page 348: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa316

Inavyoonyesha kitengo cha Usalama cha Jeshi la Polisi la Zanzibar kilikuwa kimekufa au kimeuliwa kwa makusudi. Kwa mujibu wa Mzee ambaye hakuta jina lake lijulikane, Mkurugenzi wa Usalama wa Tanganyika, Emil Mzena alikuwepo Zanzibar wakati wa mapinduzi. Regional Police Commander wa Dar es Salaam, Samuel Pundugu pia alikuwepo Zanzibar na alikuwa ameshukiya kwa Omar Hassan. Mzee mwenyewe alishukiya kwa Rajabu Suwedi. Saleh Saadalla, kiongozi mtendaji wa mapinduzi aliwahi kufanya mikutano Dar es Salaam katika nyakati tafauti na Hanga, Pili Khamis, Muhiddin Ali Omar, Seif Bakari, Saidi Idi Bavuai, nk. Ilokuja baadaye kujipa na kujulikana kwa jina la Kamati ya Watu 14 ilikuwa bega kwa bega na Saleh Saadalla, Abdalla Kassim Hanga na Abdulaziz Twala. Mapinduzi yanatokeya Mzee Abeid Amani Karume alikuwepo nyumbani kwa Mzee Abbas Sykes ambaye wakati huo alikuwa ni Regional Commissioner wa Dar es Salaam.

TANU Hawakutaka Kujulikana—Mzee Ally Sykes

TANU ilimsaidiya sana Karume katika mambo ya siasa za Zanzibar. Kambona alikuwa anataka kuchukuwa utawala wa nchi hii na Nyerere aliona kama Kambona anaweza akamuweka pembeni. Kambona alisahau kuwa ni mimi na kaka yangu Bwana Abdulwahid Sykes na Bwana Dossa Aziz tulomsaidiya kupata kazi katika TANU. Na wakati huo Kambona alikuwa bado anafanya kazi Dodoma na Nyerere alikuwa akifanya kazi St. Francis, Pugu, hapa Dar es Salaam. Wakati ule TANU haikutaka kuonyesha kwamba wao ndiwo walofanya njama za kupinduwa Zanzibar. Hawakutaka kujulikana wanafanya kitu gani. Ilikuwa kama ni kitu cha siri maana yake. Tulikuwa sisi wote hapa. Nyerere asingeliweza kufanya kitu peke yake bila ya kuwa sisi hapa. Alikuwa hawezi kufanya kitu peke yake. Manake yeye kaletwa hapa na sisi ndiyo tulomsaidiya mpaka akafika pale alipo. Asingeliweza kufanya kitu chochote bila ya sisi kumsaidiya, marehemu Bwana Abdul Sykes, mimi, Dosa Aziz, John Rupia, Bwana Bakari wa Tanga. Baada ya kupatikana Zanzibar, yale mapinduzi tulivyoyapata, tuliposhinda, sasa ilikuwa hawa kina Nyerere na wenzake walichukuwa kiti cha mbele zaidi kuonyesha kwamba wao walifanya peke yao. Kwa hiyo Bwana Abdu hakupendeleya kujionyesha kwamba kulikuwa na kitu gani. Na hakupenda yatokee mambo ya kutofahamiyana. Bwana Abdu aliyaunga mkono mapinduzi ya Zanzibar. Aliyaunga mkono sana kupita kiasi. Pia nataka ufahamu kuwa Karume asingeliweza kumpata Nyerere bila ya Bwana Abdu kwa sababu Bwana Abdu ndo alokuwa karibu kidogo na Karume kwa sababu Bwana Abdu alikuwa na sauti kubwa katika TANU. Afro­Shirazi isingeliweza kuendeleya na siasa zake Zanzibar bila ya msaada kutoka Tanganyika. Alipokuwa anakuja Dar es Salaam Karume alikuwa akishukiya kwa Bwana Abbas Sykes. Karume akijitiya tu kama

Page 349: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 317

alihusika na mapinduzi lakini zaidi aliyekuwa akiyafanya mambo hayo ni akina Babu ambaye alihusika kidogo. Babu alikuwa ni mwanasiasa na aliona kuwa Wazanzibari wengi waliwekwa nje na Waarabu. Hakupendeleya hivyo.73

Msituonee—Mzee Badawi Qullatein

Tulikuwa wakweli kwa kile tulichokiamini nacho ni Usoshalisti. Mtuhukumu kwa hilo na msituonee kwa kusema kuwa tulikuwa waongo au wanafik. Kama kuna kosa basi iwe kwa kuutizama Usoshalisti kama ni idiolojiya na baadaye sisi. Hanga alileta Warusi kuandika Katiba na Twala aliwaambiya kuwa Zanzibar iwe na uhuru wa kujiamuliwa (autonomous). Wakamwambiya Hanga na Hanga akamwambiya Twala “Brother Twala kwani wewe huungi mkono muungano?” Wachina hawakuunga mkono muungano. Warusi waliuunga mkono. Chou En Lai alimshauri Karume asikubali muungano. Alimuambiwa ajenge strong base ndani ya Zanzibar. Piya alimuambiya asiunganishe vyama. Alipokuwa Waziri, Twala aliomba nafasi ya kwenda kusoma nchi za Mashariki na za Magharibi. Haikuwa siri lakini walikwenda kuziiba fomu zake za kuombeya nafasi ya kusoma na kumuonyesha Ali Mahfoudh na baadaye Karume. Hanga alikuwa myenyekevu sana kwa Oscar Kambona kwa sababu Oscar akimfadhili sana na kumlipiya kukaa Rex Hotel Dar es Salaam na mambo mengineyo. Hanga alikuwa hana maana. Akikopi na alikuwa hawezi kuwasilisha hoja. Oscar alikuwa ni mbaguzi na opportunist [mbinafsi]. Hakuwa Msoshalisti wala mpenda maendeleo. Alikuwa anataka ulwa tu. Niliishi na Twala na kulikuwa hakuna vizingiti baina yetu. Nilimpa baadhi ya makabrasha yenye kufundisha namna ya kutengeneza mabomu. Amur Dugheshi alimfundisha namna ya kutumiya silaha ingawa alikuwa amepata mafunzo kutoka sehemu nyengine pia. Kuna vijana wenye kusema kuwa mapinduzi yasingeliweza kufanyika bila yetu. Tarehe za mapinduzi zilikuwa zikibadilika kila siku. Tulimpelekeya salamu Babu alipokuwa Dar es Salaam. Sisi hatukuitegemea Umma Party baada ya mapinduzi. Ali Mahfoudh aliona keshafika na sisi tuliamini kuwa bado. Tulijuwa kuwa hatutokwenda naye Karume mpaka mwisho. Asingelikubali Babu awe Katibu Mkuu wa ASP. Akimtaka Thabit Kombo kwa sababu akikubalika kwa Washirazi. Akijuwa kuwa Washirazi waliyosoma walikuwa hawamtaki. Siku ya mapinduzi Aboud Jumbe alikuwa anasitasita kuunda serikali na alisema “tuwangojee wenyewe.” Mimi ndiye niliyeandika majina ya Baraza la Mawaziri. Alikuwepo Twala, Okello, na Jumbe. Watu wa Saleh Saadalla waliingiya mabomani na akina Bavuai na wengineo ambao walikuwa Wazanzibari.

Page 350: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa318

Babu alipewa Uwaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwa sababu kilikuwa cheo cha Ali Muhsin. Khamis Abdalla Ameir alipewa cheo kwa sababu ya Chama cha Wafanyakai (FPTU), na Mohamed Mfaume pia.74

Sultan Jamshid kutupwa Uingereza

Mervyn Vice Smithyman aliwasili kwenye meli ndogo ya “Salama” saa tatu na robo za asubuhi na akamkuta Sultan Jamshid ameshafika “lakini wakubwa wa Serikali walikuwa hawapo. Kutofika kwao ulikuwa ni mwisho wa tamaa zote za kuirejesha Serikali halali.”75

A. W. Hawker alikuwa ni Katibu Mkuu wa Fedha katika serikali iliyopinduliwa ya ZNP­ZPPP na Smithyman alikubaliyana na Hawker kuwa akishindwa kufika kwenye meli ya “Salama” achukuwe nafasi yake kwa niaba. Wakati huo Mawaziri wote walikuwa wako nyumbani kwa Smithyman. Hawker ndiye aliyemuarifu T. S. Crosthwait wa Ubalozi wa Kiingereza uliyokuwepo Vuga, Zanzibar, kuhusu mripuko wa Mapinduzi. Hawker baada ya Mapinduzi akawa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais. Kuhusu Mawaziri kwenda kwenye meli na kuungana na Sultan Jamshid, Hawker ameandika hivi:

Kiasi ya [ Jumapili] saa tisa za mchana Kamishna wa Polisi aliniambiya kuwa atamalizikiwa na risasi baada ya dakika 10 na baada ya hapo anapendekeza kuondoka Malindi na kwenda kupanda meli ya ‘Salama.’ Nikautuma ujumbe huu kwa Waziri Mkuu ambaye aliutaka ushauri wangu. Nilimuuliza nini ilikuwa tathmini yake na kama anafikiriya kama Serikali yake itaweza tena kutawala Zanzibar. Akasema kuwa anafikiriya kuwa hawatoweza; lakini kama yeye na Mawaziri wawili wataweza kuungana na Sultan na Smithyman kwenye meli ya ‘Salama’ bado watakuwa ni serikali yenye kutambulikana na wataweza kufanya kazi mbali ya Kisiwa cha Zanzibar. Nikamshauri Waziri Mkuu kuwa sifikirii tena kama hilo litawezekana kutokana na suala la usalama wao. Nikamshauri zaidi kuwa ikiwa ni fikra ya Waziri Mkuu na viongozi wenzake wakubwa, wenye wafuasi kidogo, kuwa hawatoweza kutawala tena Zanzibar, basi kwa nini asifikiriye kujiuzulu rasmi ili mapigano yasite na kuokowa maisha ya watu na mali. Waziri Mkuu akashauriyana na wenzake na akanambiya kama hakuna uwezekano wa kupanda meli ya ‘Salama’ basi atajiuzulu, ikiwa atahakikishiwa usalama wake na wa wenzake na familia zao. Akaniomba niufikishe ujumbe wake upande wa pili [wa ASP]. Akaniambiya pia nimuarifu Sultan kuhusu niya yake na nimshauri aendelee katika moja ya meli za Serikali katika moja wapo ya bandari za bara.76

Saa tisa kasorobo za jioni ulipokelewa ujumbe ndani ya meli ya Salama kutoka kwa Hawker kwenye Ubalozi wa Kiingereza wa Zanzibar wenye kusema “Tunatarajiya mazungumzo na Abeid Karume, na pia tuna mawasiliyano na Mawaziri. Kwa hisani yako musipeleke, narudiya, musipeleke ujumbe wowote kutoka ‘Salama’ kuomba msaada kutoka nje Mwisho.”77

Maandishi na kauli nyingi sana zinajirudiya kwa kusema kuwa Mapinduzi ya

Page 351: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 319

Zanzibar yalikuja kuungowa Usultani ambao ulikuwa ukilindwa na Muingereza. Hata kabla ya akina Sheikh Ali Muhsin kungiya siasa za kupiganiya uhuru wa Zanzibar, Waingereza walikuwa wameshagutuka kuwa utawala wa Kifalme wa Zanzibar ulikuwa umeshaingiwa na hamasa za kizalendo za kudai uhuru. Ukweli huu unaonekana wazi kutokeya mwaka wa 1950 wakati wa uongozi wa Sayyid Seif bin Hamoud bin Feisal na kuendeleya. Dalili zilizo wazi za Waingereza kutompenda Sultan Jamshid ni nyingi. Moja wapo ni pale walipomuombeya kwa Mwalimu Nyerere ampokee Dar es Salaam baada ya kukataliwa na Odinga Oginga kushuka Mombasa kwa khofu ya kuzusha maandamano ya kumuunga mkono kutoka kwa waliyokuwa raia zake. Angaliya namna Muingereza alivyokuwa akimzungumza Sultan ambaye anaambiwa alikuwa akimlinda:

Nina hakika kikundi cha [mfalme na watu wake] wanataka waondoke [Dar es Salaam] haraka. Wao hawataki kubakia na ni fedheha kwa Watanganyika na kwetu sisi.78

Nimezungumza na makamo wa Raisi [Kawawa] ambaye anatutizama sisi tupange safari ya [Sultan na watu wake] nje ya Tanganyika bila ya kuichelewesha. Kuweka uhusiano mzuri na mashirikiano na Serikali ambayo imeonyesha ubinaadamu ambao tunajuwa ni vigumu kwao naona ni muhimu sana sisi tuwafanyie mipango ya kuondoka.79

Si kuwa Uingereza haikutaka tena kuendeleya na utawala wa Sultan wa Zanzibar bali haikutaka kuwalinda Wazanzibari wakati ilipokuwa ipo haja kubwa ya kufanya hivyo. Manwari za Kiingereza zilipewa maagizo maalumu ya kwenda Zanzibar kuwanusuru raia zake tu ambalo ni jambo lenye kukubalika kwenye kanuni ya kimataifa. Lakini wale aliyokuwa ana dhamana ya kuwalinda na mishahara yao ikilipwa na nchi yao ya Zanzibar hawakuwa na thamani yoyote kwao. Baada ya kuwasili Sultan Jamshid Uingereza, tarehe 7 Mei, 1964, Serikali ya Kiingereza kupitiya Commonwealth Relations Office (CRO) ilimtumiya salamu zifuatazo Balozi wa Uingereza kwa niaba aliyekuwepo Dar es Salaam za kumtuliza Mwalimu Nyerere:

Mfahamishe Nyerere kuwa Sultan alikaribishwa Uingereza si kama mkimbizi wa kisiasa bali kama ni raia wa Zanzibar ambaye anaruhusika kukaa hapa kama raia yoyote yule wa Commonwealth. Ikiwa Nyerere atauliza yoyote kati ya haya yafuatayo unaweza kumjibu hivi:

a) Hatuna ushahidi kuwa Sultan amejihusisha na mipango dhidi ya kuipinduwa Zanzibar kwa msaada wa Waarabu waliyojitoleya…na tunafikiri kuwa mpango kama huo utakuwa hauna mashiko na hautozaa matunda mazuri.

b) Muda kidogo tuliona makabrasha ya kisiasa ambayo yakitolewa na oganaizesheni

Page 352: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa320

yenye kujiita Organisation of Zanzibar in the United Kingdom. Oganaizesheni hii inaonekana sasa kuwa haifanyi kazi na pengine hata haipo tena. Haikupata wafuasi au kuungwa mkono hapa. Tulimuonya Sultan wakati huo asimruhusu memba yoyote wa nyumba yake kujihusisha na oganaizesheni hii.80

Hayo yalikuwa ni maagizo ya tarehe 7 Mei, 1964 ambayo yanazidi kudhihirisha kuwa kinyume kabisa na kauli zenye kusema kuwa Muingereza alikuwa akimuunga mkono Sultan wa Zanzibar kwa hakika alikuwa dhidi yake na alikuwa yuko pamoja na Nyerere na Mapinduzi yake. Kinyume na magwiji wa kupanga mikakati ya kisiasa walivyotarajiya, tatizo la Zanzibar halikutoka ndani ya Zanzibar kama walivyokuwa wanaogopa Waingereza na baadae Tanganyika na Tanzania Bara. Tatizo la Zanzibar limetoka Tanganyika na limeshakuwa ni tatizo kubwa la Tanzania Bara (Tanganyika) na la Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavoonyesha, bado haijawadhihirikiya watawala wa Tanganyika kuwa baada ya miaka 50 kuwa ipo haja kubwa kwa Tanganyika kuubadilisha mtizamo wake juu ya Zanzibar na kuupinduwa msimamo mkongwe wa kuinyanganya na kuinyima Zanzibar haki zake kwa kukhofia kuwa ikiwachiwa huru Zanzibar itakuwa ni tatizo la kimataifa kwa Tanganyika. Au Zanzibar itakuja kutumiliwa au kutumika kama ni mlango wa kuuingiza ubeberu wa Kiarabu na wa Kiislamu Tanganyika na Afrika ya Mashariki na Kati. Wako wengi wenye kuhadaika na udogo wa Zanzibar ingawa athari zake wanaziona lakini wameamuwa kuukataa ukweli huo. Anasema Jalaluddin Rumi “Yatizame macho yako. Ni madogo lakini yana uwezo wa kuyaona mambo makubwa.”

Waliyokuwa Karibu Machozi Yao Baridi

Suala la watu wangapi wameuliwa Zanzibar kwenye Mapinduzi ni suala ambalo kutoondoka kwake kunaviondoleya baraka visiwa ambavyo ni pepo katika dunia. Na kuondoka kwake ni kutokeya kiongozi na uongozi utakaokiri kuwa mauwaji hayo yalitendeka na nchi nzima kusoma dua na kumuomba Mwenye­Enzi­Mungu istighfari na kuendeleya kumshukuru kwa neema na njia yake iliyonyooka. Takwimu zinatafautiyana kuhusu binaadamu waliyouliwa katika mapinduzi ya Zanzibar kuanziya watu 5,000 mpaka 18,000.81 Ingelisaidiya sana kama serikali ingewaomba watu waripoti juu ya watu wao waliouwawa ili lithibitike jambo hili. Ile filam ya Kitaliana Africa Addio, imezidisha kuthibitisha kutendeka kwa mauwaji ya halaiki katika Mapinduzi. Idadi ya watu waliouliwa haiwezi kufikiwa kwa sababu wapo watakaotaka idadi iwe ndogo sana ili wajikoshe na wapo ambao watakaotaka idadi iwe kubwa kwa sababu wanawajuwa watu katika kila familia waliyopoteza mtu au watu wao. Pia kuna kauli nyingi juu ya sehemu tafauti zenye makaburi ya halaiki Zanzibar

Page 353: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 321

zikiwemo sehemu kama maeneo ya Kibanda Maiti ambazo zimekujajengwa nyumba juu ya watu waliyouliwa katika Mapinduzi. Pia kuna ambao hawakuzikwa bali wametupwa baharini kama anavyoelezeya mpiga picha mashuhuri duniani kutoka Kenya, marehemu Mohamed Amin (Mo):

Mo alipiga picha za mwanzo za wanamapinduzi, na aliombwa kufanya hivyo na Abdulrahman Mohamed Babu, mtu wa mwanzo alomshituwa kuwa kutakuwa na mapinduzi na ambaye alikuja kuchaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Alichukuwa filam za wageni wakiyakimbia maafa, makaburi ya halaiki, na maziko ya majahazi yalokuwa yakitupa mizigo yao ya maiti baharini na bila ya maandalizi yoyote huku ikifatiliwa na mkururo wa mapapa waliokuwa wakiisubiri kwa hamu.82

La msingi ni kwa mujibu wa idadi ya watu waliyokuwepo Zanzibar wakati ule, idadi ya watu waliyouliwa walikuwa ni watu wengi sana. Zaidi ya idadi, tendo lenyewe lilikuwa ni kubwa bila ya kiasi kwa sababu Zanzibar haikupata kuwa na utamaduni wa watu kuuliwa au kuuwana namna ile. Idadi ya watu waliyouliwa Zanzibar ni jinamizi la kitaifa na haiwezekani kwa njia yoyote ile kuondowa mifarakano Zanzibar bila ya suala hili kukabiliwa na kuyakubali matokeo yake ili kufikiya kusameheyana na kusikilizana. Maelfu ya Wazanzibari wa asili tafauti waliuliwa na maelfu ya Waomani walisaidiwa na shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kurudi Oman kwa kutumia majahazi kutoka nchi za Kifalme za Ghuba, kwa mfano, Hari Sagar, Nasrul Mulk, Samhan, Salaam, Badry, nk, na manwari ya Kidachi, Van Riebeeck.83

Katika makala ya tatu na ya mwisho yenye kichwa cha maneno “Kumbukumbu na Sheikh Abdulla Al­Khalili”, mwandishi wa Kiomani Ahmad Al­Fallahi ameandika kuwa mshairi maarufu wa Kiomani, Sheikh Abdulla Al­Khalili alitunga kasida yenye kichwa cha maneno “Watu Waliokuwa Karibu Macho Yao Yabaridi” akikusudiya:

…mauwaji makubwa ambayo waliteketeya ndani yake maelfu ya Waomani kutoka wanawake, wanaume, watoto, Mashekhe, vijana ambao wakiishi [Zanzibar] na nyoyo za Waomani siku hiyo zilijaa uchungu na mzigo wa huzuni…waliyo karibu na watu wa Oman hawakuathirishwa wala hawakuhuzunika na aliukusudiya umma wa Kiarabu kutokeya Misri kuelekeya Shaam, Iraq, nchi za Afrika Kaskazini na siku hizo hisiya za kizalendo zilikuwa zimetanda na kuzitawala akili, lakini maneno yake (Sheikh Al­Khalili] yalimuathiri Sultan Sayyid Said bin Taimur wa Oman na akamuamrisha Sayyid Hamed bin Humud ambaye alikuwa ni Waziri wake wa karibu na akamtuma ampelekee salamu Sheikh Abdullah [Al­Khalili] kupinga kuwa macho yake ambayo yako karibu hayana ‘machozi baridi’ kutokana na msiba wa damu uliyotokeya Zanzibar.84

Kuna Wazanzibari wengi ambao wanaishi na majeraha na makovu ya mavamizi ya Zanzibar. Wengi wao wamekuwa wakisononeka na kulaumiyana

Page 354: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Kumi na Tisa322

kwa yaliyotokeya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964. Ukweli ni hawakuwa na umoja au uwezo wa kuyazuwia isipokuwa kwa kupambana na vifo na mateso makubwa zaidi. Ni hikma ya Mwenye Enzi Mungu kuwaweka hai ili kizazi kipya kipate kujiilimisha kutoka kwao na wao wapate kupona na maradhi ya kujilaumu na kuwalaumu wenziwao. Inshaalla kitabu hichi kitakuwa kipoza moyo na kuwapa nguvu za kuwasaidiya kuujenga mustakbal mpya wa Zanzibar na uhusiano mkongwe baina ya Zanzibar na Tanganyika, na baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia.

Page 355: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa IshiriniMapinduzi Ndani na Nje

Kwahivyo, kuanzisha vita vya uonevu vya kuishambuliya nchi nyingine si jari­ma la kimataifa tu, bali ni upeo wa jarima la kimataifa ambalo linatafautiyana na jarima nyinginezo za vita kwa vile katika vita vya uonevu hutendwa jumla ya matendo maovu yote ya jarima. —Robert H. Jackson, Muendesha mashtaka wa Kimarekani katika kesi za Nuremberg

Profesa Ali A. Mazrui ametowa mifano miwili mikubwa ya mapatano duniani. Mfano wa kwanza ni mapatano baina ya Waingereza na Wamarekani ambao waliwahi kuwa maadui wa muda mrefu na hivi sasa ni marafiki wakubwa duniani. Mfano wake wa pili ni mapatano baina ya Japan na Marekani baada ya kuwa maadui na hivi sasa kuwa marafiki wakubwa duniani. Profesa Mazrui ameandika:

Kusameheyana baina ya Waarabu na Waafrika huenda kukawa baina ya mfumo wa Kimarekani­Kiingereza (wa mwendo mdogo lakini imara) na wa Kimarekani­Kijapani (wa haraka lakini wa kijuujuu)…Mapatano baina ya Waarabu na Waafrika yanakusanya si kumbukumbu za mapinduzi ya Zanzibar peke yake, bali kimsingi zaidi, kumbukumbu za kuhusika kwa Waarabu na biashara ya utumwa Afrika.1

Tumeshaona kuwa ni mara nyingi sana suala la mapinduzi ya Zanzibar limekuwa likihusishwa na “utumwa wa Waarabu.” Chimbuko la itikadi hii limetokana na kutojulikana kwa chimbuko halisi la mapinduzi yenyewe. Tatizo kubwa lilikuwa ni kuyatizama mapinduzi ya Zanzibar kuwa ilibidi yatokee kwa sababu ya unaosemekana kuwa ulikuwa ni utawala wa kimabavu wa Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu. Mavamizi ya Zanzibar hayakuwa ni kitu ambacho lazima ilibidi kitokee. Ulikuwa ni mpango maalumu wa nchi moja kuivamiya ya pili na kuificha siri nzito ambayo umekijenga kimya kilichoikosesha usingizi Zanzibar kwa muda wa miaka arubaini na sita. Kwa miaka zaidi ya khamsini Wazanzibari wamekuwa wakiendeshwa na

Page 356: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini324

upotoshaji wa kihistoria ambao umechangiya kwa njia kubwa katika mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyowaondoleya utulivu wa kujipa maendeleo na neema kubwa zaidi wanazostahiki kuwa nazo. Vitabu vingi kuhusu historia ya Zanzibar havikuandikwa na Wazanzibari na vimejaa fitina za upotoshaji zenye kuwagawa Wazanzibari katika misingi ya Uafrika na Uwarabu na khasa kushadidiya uovu wa Waarabu bila ya kudaiwa ushahidi wa tuhuma zao. Haitoshi kuitambuwa hakika ya yale yaliyoisibu Zanzibar katika mapinduzi na muungano na Tanganyika bila ya Wazanzibari wenyewe kukiri kuwa mifarakano yao wenyewe kwa wenyewe ndiyo iliyowapa wengine mwanya wa kuwaingiliya na kuwaondoleya masikilizano na neema za kuungana. Kurekebishika kwa mapinduzi na muungano kutatokana na mapinduzi ya kifikra na muungano wa Wazanzibari ndani ya Zanzibar kwanza. Hakuna nchi, au kiongozi, au taasisi ambazo zitaweza kuwapatanisha Wazanzibari kabla ya wenyewe kulivuwa jumba la buibui liloendeleya kuwapotosha na kuwanyima njiya ya kutokeya. Watu wenye kupatana ni wale wenye nia ya kupatana na wakawalazimisha viongozi wao kwenda na uwamuzi wao. Penye jahazi lenye kuzama watu huwa hawamtafuti nahodha mweusi au nahodha mweupe na ubaguzi huchukuwa likizo la moja kwa moja. Kwa mujibu wa matokeyo ya utafiti huu, Zanzibar haina budi kwanza kuamuwa kujikombowa kutokana na mzimu wa kihistoria uloziiba nyoyo na akili za Wazanzibari na za Watanganyika kwanza na kuendeleya kuiandika na kuisomesha historia ambayo haikupotoshwa na kuitiya jamii nzima ndani ya upofu. Mtoto wa tembo anapolelewa kutokeya mdogo huwa anafungwa myororo wa mguu kunako chuma basi hata anapolifikiya tambo la kuwa tembo mkubwa bado huendelea kuamini kuwa hana nguvu za kuuvunja myororo wa chuma ambacho hakina nguvu za kumzuwiya ikiwa ataamuwa kuukata. Ukombozi wa Wazanzibari wa kwanza ni ukombozi wa nguvu za akili ambazo zinafikiri nje ya gofu/sanduku la kihistoria. La pili ambalo haliwezi kupatikana bila ya ukombozi wa kifikra ni uchapaji kazi kwa kuwasomesha watu wake na uongozi mpya wa mustakbal wenye kuwatiya tamaa kubwa ya kimaisha kizazi kipya, na kuchachamaa kujirejesheya utambulisho wake badala ya kupoteza nguvu kwenye makosa ya wanasiasa waliyopita na siasa za kulaumiyana na kutoaminiyana. Tabia ya kumgojeya kiongozi mmoja kuja kuikowa jamii ni tabia yenye kuwapa viongozi wachache mwanya wa kuitumiliya jamii kuendeleza maslahi yao ya kisiasa na ya kibinafsi. Jamii inapoamuwa kumuwachiya kila kitu kiongozi mmoja peke yake huwa imeamuwa kuwa nchi ikifaulu husifiwa kiongozi na inaposhindwa kufaulu pia hulaumiwa kiongozi. Jukumu la kijamii hubakishwa katika kutiya kura kila baada ya kipindi maalumu na kupumzika mpaka baada ya kipindi chengine kuwadiya. Kwa upande mwengine wa dunia, Europe iliyopondwapondwa kwa vita, na

Page 357: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 325

Japan iliyoangamizwa ziliamuwa kujirudishiya tena uhai. Japan haikupoteza wakati kuilaumu Marekani kwa kuipiga mabomu na Ujerumani iliamua kuungana na maadui zake baada ya kujengwa upya kwa Mpango wa Marshall. Hivi karibuni Ujerumani imeamua kujenga mapatano na nchi ambayo ilikuwa ikiiandama kuivuruga ambayo ni Urusi. Nchi ambazo zilikuwa maadui zimeamuwa kwa utulivu na kwa akili kufuata maslahi yao. Jee, Zanzibar na Tanganyika zinahitajiya Mpango wa Afrabia kama Europe ilipojengwa upya kwa Mpango wa Marshall? Kuna maslahi gani baada ya kuufahamu uhalisia wa mapinduzi, kuendeleya kuyakumbatia yaliyopita badala ya kuyafukuziya na kuyatiya mkononi ya mustakbal? Wazanzibari watatizama nyuma ambako kamwe hawatoweza kurudi au wataelekeya mbele kunakowakabili? Tanganyika haina haja kuendeleya kuji­tisha au kutishwa na umoja wa Wazanzibari bali iyakaribishe mabadiliko Zanzibar kwa faida za pande mbili. Tanganyika na Zanzibar zilizo huru zina nafasi kubwa zaidi ya kulijenga Shirikisho la Afrika Mashariki na Kati na kujinyankuliya nguvu za kiuchumi na za kisiasa bila ya kujitafutiya uhalali wa kuunganganiya muungano wenye kutawaliwa na Tanganyika. Lakini Mwalimu Nyerere akisisitiza kila alipopata fursa baada ya kufariki duniya Mzee Karume kwa kusema kuwa kiongozi huyo wa Zanzibar alikuwa ana hamasa kubwa juu ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa mujibu wa Profesa Issa Shivji na kwa kurudiya:

Hakuna kitu kilicho mbali na ukweli kama hicho. Kama kuna kitu kimoja ambacho Wazanzibari wanamuadhimisha Karume nacho, mbali ya utawala wake wenye kutumiya nguvu, ni Uzanzibari wa Karume na ukaidi wake usiotetereka kukataa kumezwa ndani ya Muungano utakaoipotezeya Zanzibar uhuru na haki yake ya kujitawala. Smith, ambaye alikuwa ana nafasi ya kuonana na Nyerere anapotaka na maofisa wengine alipokuwa akifanya utafiti wake, kwa mfano, alisema kuwa ilikuwa tishio la Nyerere kuwaondowa askari wa Kitanganyika visiwani ndiko kulomfanya Karume mwisho kuukubali Muungano. Lakini alikuwa anayumba mpaka dakika ya mwisho. ‘Hata alitishiya kutohudhuriya sherehe zilizofanywa Dar es Salaam pale hati za Muungano zilipokuwa tayari kubadilishana…’ Kama tulivokwisha kuona, Karume aliitawala Zanzibar bila ya kuzijali hati za Muungano wakati Nyerere aliendeleya kuitumiya sheria kuzidi kuimeza Zanzibar ndani ya Muungano.2

Mapinduzi ya tarehe 7 Aprili 1972

Mzee Abeid Amani Karume aliingiwa na wasiwasi mkubwa kutoka kwa akina Abdalla Kassim Hanga na wenzake. Kama Hanga aliweza kuyapanga Mapinduzi kwa msaada mkubwa kutoka Tanganyika na kuipinduwa serikali ya Zanzibar bila ya kumshirikisha basi na yeye pia anaweza kupinduliwa. Kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya Mzee Karume na Mwalimu Nyerere baina ya mwisho wa mwaka 1971 na mwanzoni mwa mwaka 1972. Kwa mujibu

Page 358: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini326

wa vyanzo vyenye kuaminika Mzee Aboud Jumbe aliandika barua na kuipeleka Bara yenye lengo la kutaka mambo kadhaa yarejeshewe serikali ya Zanzibar. Kuna mengi kabla ya hapo ambayo Bara iliikataliya Zanzibar na khasa yale yaliyoonekana kuyaingiliya madaraka ya Zanzibar. Chanzo kinasema kuwa Mzee Karume akisema kuwa Nyerere “keshatuowa sote sasa na anajifanya kama mume ndani ya nyumba.” Karume na wenzake walikuwa washamgunduwa nini Nyerere anafanya ndani ya jamii na akiwafanyiya wao nini. Mwanzo na kwenye huo mkutano muhimu baina ya Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri wa Bara Nyerere aliwafurusha wajumbe wa Zanzibar kama watoto wadogo na ikabidi zitafutwe mbinu nyingine za kupambana naye. Hapo ndipo baina ya mwisho wa mwaka 1971 na mwanzoni mwa mwaka 1972 Mzee Karume aliondoka Zanzibar pamoja na memba wa Baraza la Mapinduzi kwenda kuonana na Nyerere pamoja na Baraza lake la Mawaziri. Mzee Karume alikwenda Dar es Salaam akiwa na ile barua iliyoandikwa na kutiwa saini na Mzee Aboud Jumbe kwa sifa yake kama ni Waziri wa Nchi kuhusu Mambo ya Muungano. Walipofika kwenye kikao Mwalimu Nyerere aliliuliza BLM: “Haya yaliyomo ndani ya hii barua ndiyo mnayoyataka?” Mzee Karume alimjibu kwa kumwambiya “waulize wanaume”. Walipoulizwa wote walijibu “ndiyo” mara tatu. Nyerere alikasirika sana na akaomba makaratasi yote yaliyokuwapo pale yakusanywe na akasema “wakati wake bado haujafika!” Mzee Karume akamjibu: “kaa nayo hayo makaratasi na wakati utakapofika utatwita!” Mzee Karume akainuka, akavunja kikao, akarudi kwake Zanzibar. Mzee Karume alikwenda Dar es Salaam na ujumbe mzito wenye mambo mane ambayo yalikuwa na niya ya kuirudishiya Zanzibar sifa zake kama ni nchi. Barua iliyotiwa saini na Mzee Jumbe ilitaka Zanzibar iwe na polisi wake wenyewe, igawane na Tanganyika asilimia 50­50 ya nafasi zote za Balozi za Tanzania duniani, uwepo uraia wa Zanzibar, na Zanzibar iwe na sarafu yake wenyewe. Maalim Seif Sharif Hamad amesajiliwa kwenye kitabu kuhusu maisha yake akisema kuwa “Karume pia alikuwa anapanga awe na sarafu yake mwenyewe tafauti na ya bara. Maandalizi yalikuwa yamefika mbali na yalikuwa yakifanyika kwa siri kubwa. Kulikuwapo na Kaunsela katika Kamisheni ya Juu ya Tanzania ya London kwa jina la Omar Zahran ambaye alikuwa ni mtu wa kutoka Zanzibar na ndiye aliyepewa kazi maalumu ya kutengeneza sarafu mpya. Kwa hiyo ni jambo ambalo linajulikana kuwa viongozi hao wawili walikuwa hawasikilizani na Karume alikuwa akitiliwa shaka kuwa alikuwa akijiandaa kuuvunja muungano —ndipo nadharia ya Nyerere kuwatumiliya Makomred wa Umma kumuuwa Karume.”3

Mwalimu Nyerere alipinga Mzee Aboud Jumbe asiwe Rais wa Zanzibar baada ya kuuliwa Mzee Abeid Amani Karume lakini jawabu ya viongozi wa Zanzibar ilikuwa “sisi tushamtangaza.” Baada ya tarehe 7 Aprili 1972 Mzee Jumbe akaanza kuyapitiya yote yale yaliyokuwa yakiibana Zanzibar na akaamuwa

Page 359: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 327

kwenda kinyume na wenzake wote na kuitathmini upya na hadharani kesi ya uhaini ambayo baadhi ya vikao vyake vilikuwa vikisikilizwa hadharani jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa ni la nadra ulimwenguni. Mzee Jumbe alifahamu kuwa kesi ile ilikuwa na utata mkubwa katika masuala ya uadilifu na mwisho wake akawasamehe wote waliyokuwa wametuhumiwa. Baada ya kesi hiyo ambayo ilikuwa maarufu sana Zanzibar ndipo Mzee Aboud Jumbe alipoamuwa kutafuta njiya ya kuilinda Zanzibar kwa kuifunguwa milango ya kidemokrasiya na kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi. Alitambuwa kuwa hakukuwa na niya safi baina ya viongozi wa Zanzibar na wa Tanzania Bara. Wakati viongozi wa Zanzibar walikuwa wanataka kuuimarisha udugu na ujirani mwema kumbe wenzao wa Tanganyika walikuwa wana lao la kuitawala Zanzibar na kuwa lengo hilo bado limo ndani ya nyoyo zao. Na kwa kuwa viongozi wa bara walitambuwa kuwa viongozi wa Zanzibar walikuwa wanataka kuirejesheya Zanzibar sifa zake kama ni nchi, viongozi wa bara maisha wakiwarudisha kwenye Katiba ile ambayo iliwapa ukubwa wa utawala juu ya Zanzibar. Ikumbukwe kwamba baada ya kuuliwa Mzee Abeid Amani Karume na yaliyotokeya hakukuingiya tena katika jeshi, polisi au usalama Zanzibar, Muhindi, Mwarabu au Mgazija.

Mapinduzi Dhidi ya Mzee Aboud Jumbe

Mzee Aboud Jumbe ameiweka sawa rekodi ya historiya ya kujiuzulu kwake khasa kwa wale wenye kusema au kuandika kuwa aliamuwa kuzikoroga hisia za uzalendo Zanzibar baada ya kuukosa Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kipindi cha uongozi wa Mwalimu Nyerere. Piya ameweka sawa kuwa aliamuwa kujiuzulu kwa khiyari yake nafasi zote alizokuwa akizishikiliya. Kumbukumbu za mkutano maalum wa Halmashauri Kuu ya Taifa uliofanyika Dodoma tarehe 24–30, Januari, 1984 umenukuu:

Endapo mkutano utaamini au hata kuwa na mashaka kwamba yeye au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanahusika na tuhuma hizi, mkutano umpe hisani ya kumruhusu avue wadhifa aliopewa. Kwa kuzingatia maneno haya, mkutano haukuwa na mashaka yeyote kwamba mambo haya yalitendeka mbele yake na chini ya uongozi wake, hivyo Mkutano ulimpa Makamu hisani hiyo. Naye Makamu Ndugu Aboud Jumbe akaipokea hiyo hisani na kwa moyo mkunjufu alisimama na kuiambia Halmashauri Kuu ya Taifa kwamba anajiuzulu katika nafasi zake zote za uongozi. Kikao kilikubali kauli hii bila ya kutokea wa kuipinga. Makamu alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza kuwa sababu ya msingi ya ombi lake imesimama juu ya msingi wa kuaminika; ikiwa haaminiwi, basi hana haki ya kuendelea kwenye siasa au kuutumikia umma.4

Mzee Jumbe alitaka kurudi Zanzibar moja kwa moja kwa ndege yake lakini rubani wake aliamuwa kuumwa siku ile.5 Maelezo ya Katibu Mkuu Mzee

Page 360: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini328

Rashidi Kawawa yalielezeya juu ya “hali mbaya ya vurugu ya kisiasa nchini” na Mwenyekiti [Mwalimu Nyerere] alitowa “ufafanuzi kuhusu maadui wa maendeleo ya Zanzibar” ambao adui wa kwanza aliyemtaja alikuwa ni:

a) Hizbu—Hawa ni wapinzani wa siku nyingi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano. Wanaona Muungano unawapunguzia uwezo wa kufanya fujo Visiwani. Hawa wanajulikana tangu zamani. Lakini siku hizi hawana nguvu. Na upinzani wao hauhitaji kuzungumzwa na kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa.6

Si hivyo tu, Mwenyekiti alisisitiza kuwa: “Kosa la uhaini wa kuvunja nchi ni kubwa na ni tofauti kabisa na uhaini wa aina nyingine. Kuvunja nchi maana yake ni kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Afadhali kosa la kuiondowa Serikali kuliko hili la kuvunja nchi.”7

Kama ni kosa basi ni kosa la jinai la kimataifa kwa Dola ya Tanganyika chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere kuivamiya na kuimeza dola ya Zanzibar na si kwa Mzee Aboud Jumbe ambaye hata hajahusika na mapinduzi ya Zanzibar awe dhambi yake ni kusema kuwa Tanzania kuna Serikali Tatu, na kuomba ijadiliwe upya hati ya Muungano, na “kuhusu maandalizi ya kesi ya SMZ dhidi ya serikali ya Muungano” ambayo Mwenyekiti “alitoa hadharani mpango mkubwa na wa siri sana wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuishtaki Serikali ya Muungano katika Mahakama ya Katiba kwa madhumuni ya kuleta mzozo wa kisheria na hatimaye kuvunja Muungano.”8

Chanzo kinaelezeya kuwa tarehe 20 Disemba 1983 Mzee Aboud Jumbe alimuandikiya barua (yenye saini yake) Mwalimu Nyerere kumuelezeya masikitiko yake juu ya kudhoofishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hatuwa za kuchukuliwa za kuirejesheya Zanzibar hishma yake. Pia alielezeya Mzee Jumbe kuhusu suala la muungano na khasa kuhusu Mkataba wa Muungano ambao ulikuwa uundiwe Kamati ya pamoja kabla haukupitishwa na kuwa kitendo hicho hakikufanyika na Mkataba wa Muungano ukachukuliwa kuwa ni Mkataba wa kudumu kinyume na makubaliyano. Pia alitaka paundwe Baraza la Rais na Korti ya Rufaa juu ya mambo yanayohusiyana na muungano. Alielezeya pia katika mambo ambayo yasingepasa kuwemo ndani ya

muungano ni Polisi, Uhamiaji, Mikopo ya Biashara na mashirikiano na nchi za nje, aina tafauti za Kodi, Bandari, Mabenki, Mafuta na Gesi, nk. Mzee Jumbe aliongeza kuwa yuko tayari kuonana na Mwenyekiti wa CCM na kuyafahamisha zaidi maudhui ya barua yake ikiwa kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Tarehe 22 Disemba 1983 Mzee Jumbe alipokeya majibu ya barua yenye saini ya Mwalimu ikielezeya kuwa ni vizuri hayo masuala yakajadiliwa ndani ya Zanzibar (Baraza la Wakilishi) kabla ya kulifikisha kunako Halmashauri Kuu ya CCM. Matokeo yake Mzee Jumbe akakatwa kichwa na anaishi mpaka leo wakati

Page 361: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 329

matokeo ya Mzee Karume yalimsafirisha kutoka dunia hii kuelekeya ya pili.

Mapinduzi Dhidi ya Dokta Salmin Amour na OIC

Dokta Salmin Amour atakumbukwa milele kwa msimamo wake juu ya kujaribu kuiingiza Zanzibar ndani ya taasisi ya Kiisilamu ya OIC na kutokubali kuburuzwa na hayati Mwalimu Nyerere. Aliona mbele mtego wa kuingizwa kwenye Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hakupata kuwa na tamaa ya kuishika nafasi hiyo kwa kufahamu kuwa haikuwa na maslahi kwa Zanzibar. Tatizo la uongozi wake ni alilotaka kulifanya katika kuikwamuwa Zanzibar kutoka makucha ya Tanganyika halikupata kuungwa mkono na muamko wa Wazanzibari waliyo wengi. Dkt. Salmin alijaribu “Kuondoa kikomo cha vipindi viwili vya miaka mitano mitano kwa mtu yeyote ambaye ni Rais wa Zanzibar.” Mwalimu Nyerere hakujiwekea muda wakati wa uraisi wake ili apate muda wa kuyakamilisha malengo yake lakini alipoamua kungatuka aliweka vikwazo vya muda kwa maraisi waliofuatilia wa Zanzibar na Tanganyika.9

Kamati Kuu ya CCM ilimkataliya Rais Mstaafu Dk. Salmin Amour na Rais yoyote yule atakayekuja baadaye Zanzibar kwa kusema: “…inapendekeza na kuishauri Halmashauri Kuu ya Taifa, kwamba suala la kujadili ukomo wa vipindi viwili vya Urais wa Zanzibar liahirishiwe hadi wakati mwengine muafaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2000.”10

Mapinduzi Dhidi ya Maalim Seif Sharif Hamad

Mzee Aboud Jumbe aliomba kustaafu tarehe 28 Januari 1984 baada ya kupinduliwa kwa mapinduzi baridi. Katika uchaguzi wa uteuzi wa “Mgombea pekee katika Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” uliofanyika tarehe 14 Agosti 1985, mapinduzi mengine yalikuwa yanamsubiri Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake. Idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu waliopiga kura walikuwa 163. Seif Sharif Hamad alipata kura 78 na Idris Abdul Wakil alipata kura 85 na hakukuwa na kura zilizoharibika. Mzee Idris alipata kura 7 zaidi kuliko Maalim Seif. Amir Jamal, aliyekuwa Waziri wa Fedha bara, alilalamika baada ya mkutano, “Hii nchi inakwenda wapi? Tumemuacha huyu kijana [Maalim Seif ] mwenye nguvu, na tumemchagua huyu mzee.”11

Mwalimu Nyerere aliwataka viongozi wote akiwemo Maalim Seif wamuunge mkono na wamsaidiye Mzee Idris Abdul Wakil kuwa Rais wa Zanzibar ingawa kwenye kampeni za CCM Pemba alikuwa anapingwa waziwazi. Kwa mujibu wa Maalim Seif, Nyerere aliamuwa kwenda Pemba na kila alipokuwa analitaja jina la Mzee Idris alikuwa anazomewa na kila alipokuwa analitaja jina la Maalim Seif alikuwa anapigiwa vifijo.12 Alisema Mwalimu kuwa “anafahamu shauku ya

Page 362: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini330

Wapemba kuwa Idris ni Raisi wa nne wa Zanzibar ambaye hatoki Pemba” kwa hiyo “naahidi kuwa mara ijayo nitayachukuwa maoni yenu na nitayafanyiya kazi.” Siku ya pili, anaendelea kuelezeya Maalim Seif, Mwalimu Nyerere alihutubiya Unguja na waziwazi alitumiya siasa za wagawe uwatawale. Alisema “Watizameni hawa Wapemba. Wanamtaka Raisi wao wenyewe, na ikiwa na nyinyi mtamtaka Raisi wenu wenyewe, basi vipi tutaiendesha nchi hii?” Aliwaaambiya “Idris ni mtu wenu, ikiwa Wapemba wanampenda au hawampendi, wamuunge mkono.”13

Maalim Seif anamsifu Mzee Idris kuwa alikuwa ni “mtu asiyejiona, mkweli, na mtu wa dini…Alikuwa anaipenda Zanzibar na alikuwa akiwachukiya wanasiasa mafisadi lakini alikuwa hana uamuzi mkubwa wa uongozi…Kabla hajafariki alimtuma rafiki yake mkubwa, marehemu Mzee Ali Muhammed aje anione. Alisema alikuwa na ujumbe kutoka kwa Sheikh Idris wa kuniomba msamaha kwa mambo yalionifika…nikamwambia mwambie nimemsamehe kwa lolote lile alilonifanyia duniani na akhera.”14

Tarehe 11–13 Mei 1988 kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilifanya mkutano wa tatu Dodoma na Halmashauri ilipokeya na kujadili taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa Chama, Mzee Rashid Mfaume Kawawa uliyofanyika mwezi Aprili 1988 “kukagua uhai wa chama.” Katika jumla ya sababu ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa Unguja na hasa Mikoa ya Kaskazini na Kusini zilikuwa hujuma dhidi ya Chama, Chama kuingiliwa na Maadui, na Kampeni Dhidi ya waasisi wa Chama. “Wazee wa Mikoa ya Pemba walimwarifu Katibu Mkuu kwamba Pemba Chama hakipo, ipo Serikali tu.” Kampeni dhidi ya waasisi wa Chama “imekuwa ikiambatana na kebehi ya mapinduzi ya mwaka 1964, mapinduzi ambayo yaliungoa utawala dhalimu wa sultani, na kurejesha uhuru na heshima ya Wazanzibar.” Halmashauri Kuu ya Taifa

iliwaona watuhumiwa wafuatao ni wasaliti wa Chama, hivyo kwa kauli moja iliamua kuwafukuza kutoka katika Chama Cha Mapinduzi.

1. Ndugu Seif Shariff Hamad 2. Ndugu Suleiman Seif Hamad 3. Ndugu Hamad Rashid Mohamed 4. Ndugu Soud Yussuf Mgeni 5. Ndugu Khatib Hassan Khatib 6. Ndugu Shaaban Khamis Mloo 7. Ndugu Ali Haji Pandu …Tume ya Udhibiti na Nidhamu ifanye kazi ya kuwadhibiti Juma Ngwali, Masoud Omar, Maulidi Makame, Juma Othman Juma, Makame Ussi Machano, na Asha Bakari… Vile vile Kikao kilisisitiza kuwa wanachama washirikishwe kupitia vikao vyao matawini kuwafichua wale wote waliohusika katika kuvuruga hali ya utulivu wa kisiasa Zanzibar.15

Page 363: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 331

Mapinduzi Umoja wa Mataifa (UN)

Tanganyika ilipoupata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 na ilipotaka kujiunga na Umoja wa Mataifa, Mwalimu Nyerere kwa sifa yake kama ni Waziri Mkuu alipeleka ombi kwa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Bwana U Thant, na alipeleka barua tarehe 9 Disemba 1962 ya kukubali uwanachama na masharti yake kwa mujibu wa Katiba ya jumuiya hiyo. Zanzibar piya ilifanya hivyohivyo. Waziri Mkuu, Bwana Muhammed Shamte, alimpelekeya barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuomba uwanachama na kumhakikishiya kuwa Zanzibar imeyakubali masharti ya uwanachama wa jumuiya. Zanzibar ilipoupata uhuru wake tarehe 10 Disemba 1963, miaka mitatu baada ya uhuru wa Tanganyika, Waziri Mkuu wake, Sheikh Muhammed Shamte, alipeleka barua ya ombi la kutaka kujiunga na Umoja wa Mataifa na Zanzibar ilipokubaliwa uwanachama Bwana Shamte alimpelekeya barua Katibu Mkuu kukubali kuyatimiza masharti ya Katiba ya Umoja wa Mataifa (Angaliya kiambatanisho B).16

Tarehe hiyohiyo ya 10 Disemba 1963, Sultan wa Kikatiba wa Zanzibar, Sayyid Jamshid bin Abdulla bin Khalifa alimpelekeya barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumjuulisha kuwa Waziri Mkuu Sheikh Muhammed Shamte Hamadi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Biashara, Sheikh Ali Muhsin, wataiwakilisha Zanzibar katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati ombi la uwanachama wa Zanzibar litakapowasilishwa (Angaliya kiambatanisho C).17 Zanzibar ikawa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa tarehe 16 Disemba 1963 na Dola ya Zanzibar ikapinduliwa tarehe 12 Januari 1964. Tarehe 27 Aprili 1964 Umoja wa Mataifa ulipata taarifa kutoka vyombo vya habari kuwa Tanganyika na Zanzibar ambazo kabla zilikuwa ni memba tafauti wa umoja huo kuwa zimekuwa ni Nchi moja yenye uwakilishi wa nchi za nje mmoja. Bwana C.A. Stavropoulos, Katibu Mkuu wa Ushauri wa Sheria wa Umoja wa Mataifa, alimuandikiya barua Katibu Mkuu U Thant, kupitiya kwa Bwana Jose Rolz­Bennett (Deputy Chef de Cabinet), kuwa Umoja wa Mataifa bado haijaarifiwa rasmi kuhusu kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Barua imeanza kwa kusema:

Kukosekana kwa waraka [wa makubaliyano ya muungano] ni vigumu kuamuwa kwamba Dola mbili za Tanganyika na Zanzibar zimeungana kuunda Dola mpya kabisa, au Zanzibar imejiunga na Tanganyika (ambayo ni kubwa sana kwa eneo na kwa idadi ya watu), na huku Tanganyika ikiendeleya kuwepo chini ya jina jipya na eneo na idadi ya watu kubwa zaidi. Kuna mifumo tafauti ndani ya sheria ya kimataifa, na mifano ya mifumo tafauti ipo katika uwanachama na uendeshaji wa Umoja wa Mataifa.18

Barua inaendeleya kufahamisha kuwa muungano wa Misri na Syria wa kuunda Nchi moja ya Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu [UAR] ulifanyika mwaka

Page 364: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini332

1958. Serikali ya UAR ilimuarifu rasmi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumuomba awaarifu rasmi wanachama wa umoja huo na mashirika yake. Tarehe 24 Februari 1958 Ujumbe wa Kudumu wa Misri wa Umoja wa Mataifa uliuarifu kwa barua Umoja huo kuwa:

Maoni ya wananchi wa Misri na Syria yaliyokusanywa tarehe 21 Februari 1958 yameonyesha wazi khiyari ya watu wa Misri na Syria kuziunganisha nchi zao mbili na kuunda Nchi moja, na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu ana hishima ya kumuarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuundwa kwa Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu, na Cairo mji mkuu wake, na kuchaguliwa kwenye kura hiyohiyo ya maoni, kuwa Rais Gamal Abdel Nasser atakuwa ni Rais wa Jamhuri mpya.19

C. A. Stavropoulos hakuwa na hakika Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa na sura gani na alimuarifu U Thant kuwa “iko wazi kuwa Katibu Mkuu atakuwa ana mamlaka ya kubainisha hali na kutokana na msingi huo afanye mipango ya kuwaweka wawakilishi wa Jamhuri ya Muungano badala ya wale wa Tanganyika na Zanzibar na kuchukuwa hatuwa nyingine kuhusu kubadilisha jina, bendera, nk.”18 Badala ya kuwasiliyana na serikali mpya ya nchi ya Zanzibar ambayo ilikuwa na uwanachama wa Umoja wa Mataifa, Stavropoulos aliomba mawasiliano na muwakilishi wa Tanganyika tu na kuwa “aarifiwe kuhusu umuhimu wa kupata tamko kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa Katibu Mkuu kwa ajili ya kusambazwa kwa mashirika husika juu ya kuundwa kwa Jamhuri, na kuzileta sifa za uwakilishi mmoja wa Jamhuri.”20

Mei 6 1964 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kutoka Dar es Salaam ilimpe­lekeya barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumuarifu kuwa

Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar umetiwa saini tarehe 22 Aprili 1964 na kuwa Mkataba huo ulipitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zimeungana na kuwa Nchi moja tarehe 26 Aprili 1964, chini ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na chini ya Uraisi wa Mwalimu Julius K. Nyerere. Kopi ya Mkataba wa Muungano imeambatanishwa na barua hii.21

Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambalo lilipelekwa Umoja wa Mataifa kutoka Dar es Salaam kwenye barua ambayo haina nembo, wala jina la mhusika aliyetiya saini, halikukaa zaidi ya miezi sita (Angaliya viambatanisho mwisho wa kitabu).22 Tarehe 2 Novemba 1964 barua kutoka Ujumbe wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliyopo New York, na yenye mhuri wa Tanganyika, na ambayo haina jina au saini ya mtu yoyote, ilimuarifu Katibu Mkuu kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kuanziya sasa, itajulikana kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” (Angaliya viambatanisho D, E, F, G, H, I).

Page 365: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 333

Barua muhimu ya kuuarifu Umoja wa Mataifa kuhusu kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na miezi sita baada ya hapo kubadilishwa jina na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilikosa jina la mtu na cheo chake na saini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Dar es Salaam. Barua ya ujumbe mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na jina na saini ya Oscar S. Kambona, Waziri wa Mambo ya Nje. Barua haikusema ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na watu 16. Kati ya hao watatu (3) walitoka Zanzibar:

1. Mheshimiwa Abdulrahman Babu, Waziri wa Biashara na Mashirika.2. Mheshimiwa Othman Sharif, Balozi wa Tanzania Marekani. 3. Bwana Adam Mwakanjuki, Ofisa wa Mambo ya Nchi za Nje.

Wajumbe kumi na tatu (13) waliyotoka Tanganyika ni:

1. Mheshimiwa Oscar S. Kambona, Waziri wa Mambo ya Nje, na Mwenyekiti wa Ujumbe.

2. Bwana John Malecela, Mjumbe wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

3. Bwana E.E. Seaton, Mkurugenzi wa Utafiti, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.

4. Bwana G.S.Magombe, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.

5. Bwana Benjamin Mkapa, Naibu Katibu, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.

6. Bwana A. B. C. Danieli, Konsela, Ujumbe wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa.

7. Bwana W. Ramsay, Ofisa wa Utafiti, Ujumbe wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa.

8. Bwana D. Phombeah, Ubalozi wa Tanzania, London (Mshauri).9. Bibi Martha Bulengo, Naibu Seketeri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii

na Utamaduni wa Taifa (Mshauri).10. Bwana P. C. Bakilana, Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Uadilifu

(Mshauri). 11. Bibi E. Malecela (Mshauri).23

Mbali ya kuzidiwa kwa idadi, waheshimiwa waliochaguliwa kuiwakilisha Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakukuwa na hata mmoja ambaye alikuwa ana mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya Zanzibar. Babu alikuwa si tena Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Othman Sharif hakuwa

Page 366: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini334

karibu au akipatana na uongozi wa Mzee Karume uliyokuwemo ndani ya Zanzibar. Adam Mwakanjuki alikuwa mpinduzi lakini alikuwa ni ofisa baina ya waheshimiwa wawili kutoka Zanzibar ambao kisheria hawakuwa wakiwakilisha mamlaka ya nchi ya Zanzibar ambayo ilikuwa imeshafutwa kwenye barua kutoka Wizara ya Nje ya Dar es Salaam kwenda Umoja wa Mataifa. Nyuma kidogo, tarehe 14 Mei 1964 C. A. Stavropoulos alimuandikiya tena barua Jose Rolz­Bennett juu ya maudhui ya kuusajili Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu 102 cha Katiba ya Umoja wa Mataifa. Alimuarifu kuwa “Kifungu hichohicho kinatowa maelezo kuwa mikataba ambayo haikusajiliwa haiwezi kutajwa mbele ya shirika lolote lile la Umoja wa Mataifa.”24 Stavropoulos akapendekeza kwa Rolz­Bennett apeleke barua ya simu kwa muwakilishi wao aliyekuwepo Dar es Salaam ili aufikishe ujumbe ufuatao Serikalini:

Kwa hisani yako iarifu Serikali kuhusu maelezo yaliyomo kwenye kifungu 102 cha Katiba ambacho kinawataka memba wa Umoja wa Mataifa waisajili kwa haraka mikataba ambayo wameifunga, na sharti hili linatumika kwa Mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Taratibu za kukipa nguvu kifungu 102 cha Katiba kinahitajiya Serikali inayosajili kuipa Seketeriet kopi moja ya Mkataba ambayo imeshuhudiwa kuwa ni ya kweli na kopi kamili ambayo itakuwa na maelezo ya kutoridhika yatakayofanywa na pande husika, na kopi mbili zaidi za Mkataba, na kauli kuhusu tarehe na mpango wa kuanza uwanachama.25

La msingi ni kwa vile Zanzibar na Tanganyika zilikuwa nchi mbili ambazo zilikuwa ni wanachama wa Umoja wa Mataifa suala la uwanachama wa Nchi moja haukupelekwa kujadiliwa kwenye Kamati ya Usalama ya Umoja huo. Kulikuwa na taarifa tu kutoka kwa Katibu Mkuu kwenda Baraza Kuu kuutambuwa uwanachama mpya wa nchi mbili kuwa moja kwa mujibu wa barua iliyotoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Dar es Salaam ya tarehe 6 May, 1964.26

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliridhika na barua hiyo na ule ushauri aliopewa na C.C. Stavropoulos wa kutaka Mkataba wa Muungano usajiliwe kwa mujibu wa kifungu 102 cha Katiba ya Umoja wa Mataifa ukawachwa kwa sababu zisojulikana. Hapa tena inawezekana kuwa wasiwasi usiokuwa na msingi aliyowatiya Nyerere Wamarekani kuhusu Vita Baridi na kuingiya Ukoministi ulitowa tija ya kumsaidiya Mwalimu akae na uwanachama wa Nchi moja ndani ya Umoja wa Mataifa bila ya kuulizwa au kuhojiwa zaidi. Ukweli unabakiya kuwa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar haukuwahi kusajiliwa katika Seketeriet ya Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa Andrei Kolomoets wa Ofisi ya Mambo ya Kisheria ua Umoja wa Mataifa “Kama ulisajiliwa basi kungelikuwepo rekodi katika Data Base na shahada ya usajili ingelikuwepo. Nimecheki, haipo.”27

Page 367: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 335

Zanzibar, Ezekieli, na Jangwa la Mifupa Mikavu

Wazanzibari na Watanganyika wamechotwa akili na wapishi wachache sana waliyoamuwa kujificha nyuma ya paziya la mapinduzi na la muungano kwa miaka arubaini na sita. Mwalimu Nyerere alisema kuwa “nyumba ya Tanzania imetikisika” ingawa hakuweza kutupa sababu halisi za mtikisiko huo ingawa alitaka mjadala wake uendelee. Kuendeleya kulaumiyana hakutoleta faida yoyote ila kulizidisha joto la malumbano lisilotowa mwangaza. Mapinduzi yamejitandiya nyumba ya buibui na yameweka bawaba zenye kutu kwenye mlango wa Muungano. “Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.”28 Kabla ya kufariki kwake, hayati Mwalimu Nyerere alikwishatowa ishara ya kuanguka kwa jumba la buibui kwa sababu, kama mjenzi mahiri, alikuwa akiufahamu upya, uimara, na hatima wa nyumba aliyoijenga. Utabiri wa kuanguka kwa jumba la buibui utatimiya pale patakapopatikana uongozi ambao umeamuwa kuendeleya kuyafumba macho na kukataa kuziyona nyufa za misingi ya Mapinduzi na Muungano. Watawala wasiotaka kuziyona nyufa za misingi ni mfano wa ile mifupa mikavu iliyokata tamaa na kushindwa kuamini kuwa itaweza kuitomeya na kuinusuru nyumba na maendeleo ya wananchi wao. Kwa kumaliziya, Nabii Ezekieli aliombwa atowe habari nzuri juu ya mifupa iliyojaa kunako bonde. Pakatokeya kishindo kikubwa “na mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe…lakini haikuwamo pumzi ndani yake.” Mifupa iliweza kuzungumzishana lakini ilishindwa kuungana. Ndivyo jamii mbili za Kizanzibari, ile yenye mizizi mirefu, na ile yenye mizizi mifupi Zanzibar, kukatishwa tamaa na mirengo yenye kuwafarikisha na kushindwa kuishi pamoja na kuijenga Zanzibar. Mifupa yao imekauka na imetawanyika na haiko pamoja ndani ya kiwiliwili cha Zanzibar. Aliposhindwa Nabii Ezekieli kuisemesha mifupa ndipo alipoambiwa: “Tabiri utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana Mungu anasema hivi: njoo kutoka pande za upepo nne. E pumzi ukawapuzie [puliziye] hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivoniamuru, pumzi ikawaingia, wakaishi wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.”29

Viongozi wa Zanzibari wameisemesha mifupa ya Kizanzibari na inaitikiya na inahudhuria mikutano na vikao lakini haikuamuwa kusimama kuiteteya na kuidai haki ya Zanzibar kwa sauti moja kwa sababu uongozi bado ulikuwa haujaamuwa. Umma huamka wakati wa uchaguzi na kurudi kunako bonde la mifupa uchaguzi unapomalizika. Kitabu hichi huenda kikawa ni upepo wa kuiondowa khofu ili Wazanzibari na Watanganyika kwanza waweze kuukubali ukweli na baadaye kukaa na kuzugumza kama ni watu walio sawa na wenye kuishi ndani ya wakati mmoja na kuamuwa namna ya kuitengeneza upya misingi ya Mapinduzi na Muungano. Upepo huu utategemea kuwepo kwa mazingira matatu muhimu:

Page 368: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini336

1. Ushirikiyano wa makundi makubwa wenye kuongozwa na Uzanzibari, na wenye kuongozwa na ilimu iliyokomboka, vyombo vya habari vyenye kufuata maadili na uchunguzi wa kina, na raia wenye ukakamavu katika kila jimbo, mtaa, na viyambo.

2. Kutowachiya kuyafahamu makisiyo ya ukweli wa historiya kuninginiya juu ya maslahi ya vyama vya siasa vinavyopingana juu ya utaifa na dola ya Zanzibar, ikiwa tawala au vya upinzani, ambavyo bado vina viongozi na wafuasi wengi ambao wamo ndani ya jumba la buibui la mapinduzi na muungano.

3. Kuuilimisha umma kuhusu mapinduzi mapya ya kifikra na kuupiga fundo mtutu wa bunduki wenye kuilinda dhambi ya Tanganyika ya kuivamiya nchi ya Zanzibar, ni njia pekee ya kuzuwiya kuendeleya kuitesa Zanzibar na kuirejesheya kiti chake katika Umoja wa Mataifa.

Oscar Kambona na Afrabia

Katika mwanasiasa muhimu sana wa Tanganyika na Tanzania muhimu sana ambaye hakubahatika kuandika au kuandikiwa kumbukumbu juu ya maisha yake ni hayati Oscar S. Kambona na khasa juu ya undani wa ugomvi na mivutano baina yake, Mwalimu Nyerere na Mzee Rashidi Kawawa. Hadithi ya Kambona na uhusiyano wake na mapinduzi na muungano wa Zanzibar ni ndefu kuliko ilivyogusiwa ndani ya kitabu hichi na sidhani kama kuna mtu mbali ya hayati Mwalimu Nyerere ambaye angelikuwa ana uwezo wa kuiyandika kwa tafasili zake. Kabla ya kufariki duniya Oscar alikuwa ni mtu aliyevunjika kabisa na hayati Mwalimu Nyerere alipozipata habari za kifo chake kutoka Balozi wa Tanzania London, kauli yake ya kwanza ilikuwa “Oh, poor fellow!” Watu waliogopa hata kwenda mazikoni kwake alipozikwa Dar es Salaam kwa kumuogopa Mwalimu. Kambona alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU na baada ya uhuru wa Tanganyika aliwahi kuzishika Wizara za Ulinzi, Mambo ya Nchi za Nje, Ilimu na Mambo ya Ndani. Mwaka 1967 alikosana na Mwalimu Nyerere na alikimbiya na kwenda zake uhamishoni London alikoishi miaka 25. Kwa mujibu wa mdogo wake, Andrew Kambona, Oscar alirudi Tanzania wakati wa kuanzishwa vyama vingi akiwa katika hali mbaya ya kinafsi na kiuchumi.30 Alianzisha chama cha kisiasa The Tanzania Democratic Alliance Party (TDAP). Katika barua ya tarehe 15 Oktoba, 1993, Oscar Kambona alimuandikiya barua kiongozi mmoja wa nchi za Kiarabu za Ghuba ambayo kwa mujibu wa Andrew Kambona haikumfikiya. Aliandika Oscar: “Moja katika hamu yetu ni kuujenga upya uhusiano maalumu uliyokuwepo baina ya nchi zetu kutoka zama za kale na tunachukuwa fursa hii kuelezeya shauku yetu kuwa baada ya kuunda Serikali ijayo tungelipendeleya utupe hishma ya kuwa wa mwanzo wa kuipa

Page 369: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 337

nchi yetu Ziara ya Kitaifa….Na mwisho tutapenda kukuhakikishiya niya yetu ya kuuimarisha uhusiano maalumu na wa kihistoria baina ya nchi zetu mbili ambao tunautizamiya kuwa nje ya itibari za kisiasa.”31

Hayo ni maneno ndani ya barua iliyotiwa saini na Oscar S. Kambona baada ya kuyasimamiya mapinduzi yaliyokuwa na lengo la kukimaliza kiti cha ubeberu mkongwe Afrika Mashariki na Kati. Barua haina dalili ya kujuta kwa yaliyotokeya kunako mapinduzi lakini ni ishara tosha kuwa hata kinara cha utekelezaji wa mapinduzi ya Zanzibar kilifika mahala na kuziyona faida za uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia. Hiyo ndiyo kazi ambayo inangojewa kufanywa na uongozi ambao unaona ipo haja ya kuusitisha mtikisiko aliyouzungumziya Mwalimu Nyerere usiendelee pale aliposema:

Tunachotaka ni kwamba nyufa hizo zieleweke na tukubaliane kwamba kazi yetu ni kuziziba na tupate uongozi unaoelewa hivo. Kwamba kazi ni kuziba nyufa tulizoziona katika taifa letu. Kazi si kuendelea kulitikisa taifa hili. Litabomoka. Halitabaki.32

Pambazuko jipya la kheri limejichomoza katika siku za karibuni Zanzibar. Tumeshuhudia viongozi wa kambi mbili za siasa, CCM na CUF, wakiweka kando tafauti zao za itikadi na wakiwaongoza Wazanzibari kwenye umoja na utengamano. Kinachowaunganisha ni kuzisimamiya kidete haki za Zanzibar. Hizi ni dalili njema zinazopaswa kupongezwa na kila mwenye kuitakiya kheri Zanzibar. Viongozi wakuu wa vyama viwili vya siasa Zanzibar, Mheshimiwa Rais Dkt. Amani Abeid Karume wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maalim Seif Sharif Hamad wa Chama Cha Wananchi (CUF) wamejitokeza kuwaunganisha Wazanzibari kuulinda utambulisho wao na kuzihami rasilimali zao. Kati ya wawili hawa, mwenye kustahiki pongezi za aina ya pekee ni Mheshimiwa Rais Amani Abeid Karume kwa sababu yeye ndiye mwenye dhamana ya uongozi. Asingetowa nafasi ya kujengeka umoja huu, jitihada za wengine zisingefuwa dafu. Katika kipindi cha takriban miaka miwili sasa, ameonyesha ushujaa wa hali ya juu kwa kuongoza Serikali ambayo imeweka rekodi ya kutoogopa katika kupiganiya maslahi ya Zanzibar, tena kwa uwazi na kwa hoja. Hapana shaka yoyote historia itamuandika vyema katika hili na bado ana nafasi ya pekee ya kuwaongoza Wazanzibari siyo tu kufunguwa ukurasa mpya bali kuandika kitabu kipya kabisa katika mahusiyano yao yatakayotowa nafasi ya ujenzi wa mustakbali mwema kwao na kwa vizazi vyao. Katika hili, Rais Karume ana nafasi pekee kwani yeye na familia yake ni mfano mwema wa mjengeko wa jamii ya Kizanzibari uliyotokana na mchanganyiko wa damu wa aina yake, mchanganyiko wa Afrabia. Wazanzibari wote wamepitiwa na dunia vichwani na miguuni mwao kwa yaliyotendeka huko nyuma na wakati umefika kwa Rais Karume kuwaonyesha

Page 370: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini338

na kuwaachiya Wazanzibari njia za kutokeya, za nje na za ndani, ili Zanzibar ijirudishiye utulivu na maendeleo ya kudumu. Maalim Seif naye anapaswa kuendeleza mkabala mpya wa kisiasa aliyojitambulisha nao katika miaka ya karibuni ili pamoja na Rais Karume wakumbukwe kwa kuitendeya kheri Zanzibar. Historia iko upande wao.

Nguzo Saba za Hikma na Mapinduzi ya Afrabia

Kwenye kitabu chenye kuchemsha bongo kiitwacho The New Asian Hemisphere: The Irressistible Shift of Global Power to the East Profesa Kishore Mahbubani amezitaja “nguzo saba za hikma za Magharibi” zilizochangiya kulirudishiya bara la Asia hadhi na mchango wake duniani: Soko Huriya, Sayansi na Teknolojiya, Ustahiki (meritocracy), Kutoongozwa na Mirengo ya Kiaidiolojiya (pragmatism), Thakafa ya Amani, Utawala wa Sheria, na Ilimu.33 Zanzibar imepita ndani ya nusu karne ambayo ingeliweza kupiga hatuwa kubwa zaidi ingelikuwa imepata nafasi ya kuziiga nguzo saba za hikma kutoka Magharibi:

1. Kutoongozwa na Mirengo ya Kiaidiolojiya: Mapinduzi ya Zanzibar na muungano yaliongozwa na mrengo wa kisiasa wa Pan­Africanism ambao umewafitinisha Waafrika na Waarabu. Mrengo wa Pan­Africanism umeshindwa kuwailimisha Wazanzibari au Watanganyika kuhusu historia ya mchango wa Tanganyika katika mapinduzi ya Zanzibar na muungano wake na Tanganyika. Kutokana na historia ndefu ya mchanganyiko mkubwa wa Kiafrika na wa Kiarabu, Zanzibar inahitajiya kuongozwa na mrengo wa kisiasa wa Afrabia ambao unautukuza uhusiyano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu badala ya kuudhoofisha na ndiyo msingi uliyoijenga Organisation of African Unity (OAU) na hivi sasa African Union (AU).

2. Thakafa ya Amani: Mavamizi ya Zanzibar kutoka Tanganyika yaliofanywa na makhasimu wa Mzee Karume na mauwaji ya halaiki na vitisho vilivyofuatiliya baada ya Mapinduzi, kumewafanya Wazanzibari waliyopita wasiaminiyane wenyewe kwa wenyewe na wasiwaamini ndugu na jirani zao wa Tanganyika. Hishima ya maisha ya binaadamu ilivurugwa kwa kiasi kikubwa na haki za binaadamu zilidharauliwa sana huko nyuma. Hadithi za kubuni za “utumwa wa Waarabu” zimesababisha kukosekana kuuhishimu mchanganyiko maalumu wa kikabila na wa kiasili wa Kizanzibari na ukaongeza chuki na kutoelewana baina ya vyama vya kisiasa. Zanzibar ya leo imepiga hatuwa kubwa sana kwa kutoruhusu usambazaji wa habari zisizo na uthibitisho au zenye kuongeza mifarakano ndani ya jamii ya Kizanzibari.

Page 371: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 339

3. Utawala wa Sheria: Ulitoweka kwa muda mrefu kwa sababu roho ya kupinduwana iliendeleya kwa kipindi kirefu na ikawa vigumu kurudi kunako utulivu na amani kwa sababu vyombo vya sheria vilikosa misingi ya kuwajibika. Hali ilianza kurudi katika kipindi cha utawala wa Mzee Aboud Jumbe na khasa pale alipolianzisha Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Hali ya kisheriya ya hivi sasa Zanzibar ni yenye kutowa matumaini makubwa na mustakbal mzuri. Kizazi cha leo cha Zanzibar hakina kumbukumbu ya mapinduzi ya Zanzibar na kwa hiyo kina uwezo mkubwa zaidi wa kusonga mbele kuliko kile kilichokuwa karibu na mapinduzi.

4. Ustahiki: Fikra ya Uafrika kuutawala Ushirazi, Uwarabu, Uhindi, nk, ni athari za mrengo wa kisiasa wa Pan­Africanism katika mazingira ya Zanzibar ya mchanganyiko wa watu. Kuuliwa kwa marehemu Mzee Abeid Amani Karume kulisababisha makabila fulani yasikuwemo ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi au kutopewa nafasi za kuendeleya na masomo. Msingi wa baadhi ya Wazanzibari kuonekana kuwa ni wa daraja la pili au umuhimu wao kuwemo zaidi kwenye biashara na si utawala pia unatokana na mrengo wa kisiasa uliyokuwa ukishadidiya nani ana haki zaidi Zanzibar, mgeni au mwenyeji na tafisiri ya ugeni au uwenyeji ulitegemeya kigezo cha kuwa na asili ya kutoka bara la Afrika au bara la Asia. Zanzibar ya leo inaelekeya kuwashirikisha Wazanzibari wa kila kabila na asili katika maamuzi muhimu ya mustakbal wake.

5. Ilimu: Wazanzibari wengi sana wenye ilimu na ujuzi wa kimataifa wameweza kutowa mchango mkubwa sana kwenye nchi zilizowakari­bisha na tayari Wazanzibari wamejiandaa na kujielekeza kuuvuna utajiri huo kwa maslaha ya Zanzibar. Kukiwezesha kizazi kipya na taasisi za kijamii, walimu na wanafaunzi kuufahamu ukweli wa mapinduzi ya Zanzibar na muungano wake kutawajengeya Wazanzibari ari na utambulisho mpya ndani na nje ya nchi yao. Zanzibar inaweza kuwaandaa wanafunzi wake na kuwaombeya misaada ya nafasi nyingi za kusoma kwenye vyuo vikuu vyenye kuhishimika vya nchi za Magharibi. Wakati hali ya kiuchumi ya Zanzibar inakuwa wanafunzi wengi au wote watakaopatiwa nafasi za kwenda kusoma masomo ya juu nchi za Magharibi wataweza kurudi kuitumikiya Zanzibar.

6. Sayansi na Teknolojiya: Hili limekuwa gumu kupiga hatuwa kwa sababu ya utajiri wa Zanzibar ambao ni watu wake wenye ilimu na ujuzi kuwepo nje ya Zanzibar na kukosekana mbinu za kuwavutiya

Page 372: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini340

kurudi ikiwa moja kwa moja, kuazimwa na kulipwa na nchi husika kuja kuisaidiya Zanzibar, au kwa kujitoleya.

7. Soko Huriya: Linategemeya jamii ambayo imewekeza kwa hali ya juu kwenye sekta ya ilimu kutoka chekecheya mpaka chuo kikuu na kuitumiya ilimu kwenye sekta za sayansi na teknolojiya katika miradi ya kiuchumi ambayo itawainuwa Wazanzibari walio wengi kutoka hali duni za kiilimu na kiuchumi na kuwaweka kunako tabaka lenye nguvu za kiuchumi na lenye kulinda amani. Miradi ya kiuchumi ya Zanzibar itaweza kutekelezeka kwa ufanisi mkubwa iwapo itaendeshwa na Wazanzibari wenye kila aina ya ujuzi na ilimu na katika sekta ambazo Zanzibar itaweza kujiimarisha kutokana na sifa zake za kiilimu, kiuchumi, na za kihsitoria.

Eqbal Ahmad alikuwa na fikra ya kufunguwa Pakistani Chuo Kikuu cha Ibn Khaldun ambacho kilikuwa kiwe na minhaji ya masomo yenye mfungamano baina ya masomo ya kisasa ya kidunia na tamaduni za turathi za zamani. Hoja ya Ahmad ilikuwa

hatutoweza kupigana na misimamo mikali ya kidini mpaka tutakapoweza kulizalisha tabaka lenye masomo ya kileo la wapenda maendeleo ambao pia wana ilimu ya turathi zilizopita na wenye kuweza kuchaguwa yale yaliyo mazuri.34

Zanzibar inaweza kufikiriya mifumo tafauti ya Chuo cha Afrabia ikiwa kwa njiya ya mitandao au teknolojiya mpya za mawasiliyano, au kwa kuudurusu mfumo wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, au kwa kuuchanganya mfumo wa kwanza na wa pili, au kuzipeleka mbele programu za Afrabia katika vyuo vikuu vya kawaida.35 Lengo ni kuwaleta pamoja wanafunzi na wasomi wa Kiafrika na wa Kiarabu na kukiandaa kizazi kipya ambacho kitapatiwa nafasi za kusoma za makusudi kunako vyuo vyenye hadhi duniani. Lengo la mwisho si kuukuza Uafrika au Uwarabu au kukwama ndani ya uzalendo wa Afrabia. Hapo itakuwa tumeipanda ngazi halafu tumetumbikiya ndani ya pango jingine na jumba jipya la buibui. Siku zote, lengo liwe kuondowa umasikini unaoletwa na ujinga na upotoshaji wa binaadamu kwa ujumla. Na ujinga na upotoshaji unaletwa na fitina zenye kuichafuwa na kuiiba akili ya binaadamu kujitegemea mwenyewe na kumuomba Muumba wake ampe na amuongezee ilimu ili atoke kunako giza aelekee kunako zuka la ukweli na ukombozi. Mapinduzi ya kuziondowa fitina ni mapinduzi yatakayoleta thakafa na utamaduni wa amani Zanzibar na Afrika Mashariki yake. Hili litawezekana ikiwa litaongozwa kwa kuvifufuwa vituo vikongwe na kuvijenga vituo vipya vya ilimu vya Waafrika na vya Waarabu, vya Waislam na

Page 373: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 341

vya Wakristo. Kucha za chuki na fitina hazitamuwacha binaadamu peke yake kama hajapigana kujenga mfungamano baina ya binaadamu wenye kuongozwa na mwangaza wa dini na ilimu za kidunia zisoweka mipaka, mirengo, au madhehebu. Utekelezaji wa nguzo saba za hikma kutoka ustaarabu wa Magharibi ambazo ni chachu ya muinuko wa bara la Asia unahitajiya kufungamana na turathi za dini ya Kiislam na mijadala ya amani na dini nyenginezo ili msukumo wa maendeleo ya kiilimu na kiuchumi uweze kusimama juu ya mafundisho ya kidini yenye kuzingatiya mahitajiyo ya kidunia, na kitengo cha akhlaki cha shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO.36 Zanzibar iliyopitiya misukosuko mikubwa mikubwa katika historiya yake ya karibuni ina nafasi kubwa ya kutowa mfano wa uongozi kwa nchi jirani na za mbali. Kwa hakika katika ufunuo wa uvamizi wa Zanzibar wa tarehe 12 Januari 1964 limo zingatiyo kwa wenye kiu ya kuipatiya Zanzibar njiya mpya na muelekeyo mpya wa mustakbal wake. Ndoto ya Mwalimu Nyerere ya kuitupa Zanzibar katikati ya kisima cha Bahari ya Hindi imekuwa ni neema kwa Yusuf wa Zanzibar. Mapatano ya Wazanzibari ndani na nje ya Zanzibar ni jambo ambalo haliwezi kuzuwilika endapo wataliweka kando suala la uzawa kutoka mabara ya Afrika na Asia au visiwa vya Unguja na Pemba. Mchango wa wazee wa mapinduzi ni changamoto nzito kwa uongozi na viongozi wa Tanganyika usiojali kujipa madaraka na ukubwa kwa kuitawala Zanzibar. Mapinduzi ya Afrabia ni mapinduzi ya kukataa kubaguliwa kwa misingi ya kutoka bara la Afrika au la Asia, Pemba au Unguja na ndiyo msingi pekee wa mashirikiyano ambao utaweza kuijenga Zanzibar ikawa almasi ndani ya taji la Afrabia. Wenye kuyachezeya mapinduzi yenye kuwaunganisha na kukataa kubaguliwa kwa mujibu wa mabara ya Afrika au Asia na badala yake kuenziwa kwa mujibu wa mchango na utu na uraia wao wanazichezeya nguvu za uwakilishi wa umma ambazo hawana nguvu za kuzizuwiya. Hakuna tamaa kuwa maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hichi yatayabadilisha mawazo ya wale waliojazwa na kujaa chuki dhidi ya Zanzibar au wale ambao hawako tayari kusamehe hata kama wako tayari kusahau. Max Planck alisema: “ukweli mpya wa kisayansi haushindi kwa kuwaridhisha wapinzani na kuwafanya wauone mwangaza, bali kwa sababu mwishowe wapinzani wake hujifiya, na kizazi kipya huinukiya na uzowefu wa ukweli mpya.”37

Na kizazi kipya chenye uwezo mkubwa wa kiilimu na upungufu wa ubinafsi kinahitajiya kuuonyesha umma faida zitakazoweza kupatikana kwa kuifuata njia mpya na mustakbal ambao hakuna atakayewajengeya isipokuwa wao wenyewe. Ikiwa mfumo wa njiya mpya ni wa kushinda katika mapinduzi mapya ya Zanzibar “idadi na nguvu ya hoja zenye kukinaisha na zitazouunga mkono mfumo huo utaongezeka.”38 Hoja moja ya kitabu kama hichi siyo itakayoweza

Page 374: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini342

kuleta mapinduzi mapya ya kifikra Zanzibar au kuukaribisha mustakbal mpya wa Waafrika na Waarabu. Mapinduzi yatakayoongozwa na walimu, wanasharia, wafanyabiashara, viongozi wa kidini, na mabingwa wa fani mbalimbali, ndiyo yatakayoweza kuleta mabadiliko yenye kuongozwa na hisia ya jamii moja ya Uzanzibari ambayo ina nguvu zaidi kuliko Uunguja, Upemba, Uafrika, Uwarabu, Ushirazi, Ukaskazini, Umakunduchi, na si mapinduzi ya mtu au kikundi cha watu au ya chama kimoja cha siasa. Baada ya kupatikana mapinduzi yatakayowaunganisha Wazanzibari badala ya kuwagawa ndipo hatuwa ya pili ya kuendeleya kuujenga na kuulinda umoja na uhuru wa Zanzibar kwa kuziinua hali ngumu za kiuchumi za Wazanzibari wa makundi yote yenye utiifu kwa Zanzibar itakapofuatiliya. Na kufaulu kwa hatuwa ya pili hapana budi kuzitumiya ilimu za Wazanzibari waliyoko ndani na nje ili kuijenga nchi ya Zanzibar—almasi ya Afrika na ya dunia ndani ya taji la uhusiano mkongwe wa Waafrika na Waarabu. Fikra ya Afrabia imesimama juu ya ukweli na ushahidi wa uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu ambao umeunganishwa na dini na thakafa ya Kiislamu. Afrabia inaondowa haja ya kuindeleza dhambi ya kuukaba uhuru wa Zanzibar na umoja wa Afrika. Ina uwezo wa kujenga mazingira mapya ya mustakbal wa Waislam Waafrika na Waislam wa Asia kwa kuutumiya umahiri wenye kujenga amani na neema kwa Waislam na kwa Wakristo. Afrabia itaweza kuwa mradi wenye kufaulu iwapo itaziunganisha nguvu za kifedha za Waarabu, rasilimali za watu na maliasili ya Afrika, na kuzitekeleza nguzo saba za hikma kutoka ustaarabu wa Magharibi. Zanzibar ina kila sifa za kujiandaa na kuweza kuutekeleza mkusanyiko wa fedha, rasilimali, na maadili na kuwa mfano wa kujivuniya wa Afrika Mashariki na nchi za Kiarabu. Lakini hayo hayatokuja iwapo kuchezewa na kuchafuliwa kwa historia ya Zanzibar kutaendeleya kulifanya suala la muungano wenye kuyalinda mapinduzi ya Tanganyika ndiyo suala lenye kuwagawa Wazanzibari zaidi kuliko mapinduzi yenyewe yenye mkono mkubwa wa Tanganyika. Miafaka mitatu ilifeli kutokana na Wazanzibari kutoaminiyana wenyewe kwa wenyewe na kutokana na waasisi na warithi wa Tanganyika ambayo ilikuwa mshiriki mkuu wa mapinduzi na muungano wenye kuyalinda mapinduzi kuwa mpatanishaji mkuu. Katika historia ya miaka 50 iliyopita hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuwapatanisha Wazanzibari isipokuwa Wazanzibari wenye niya na vitendo vya kuaminiyana na kupendana. Mwenye Enzi Mungu amesema kuwa “Hatabadilisha hali ya watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yaliomo ndani ya nafsi zao.”39 Na wa kubadilika si Waafrika tu bali na Waarabu wa bara la Afrika na la Asia pia wanatakiwa kuibadilisha mitizamo yao juu ya mapinduzi ya Zanzibar kutokana na upotoshaji uliyowakumba na wao piya. Waarabu wa Afrika na Waarabu wa Asia watakuwa na mchango mkubwa iwapo watavichanganya vitu viwili kwa faida yao ya leo na ya baadaye.

Page 375: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 343

Jambo la kwanza ni mchango wa kiuwanachama wa Waarabu wa Afrika katika Jumuiya ya Afrika (Africa Union) na mchango wa kifedha kutoka Waarabu wa Asia katika kuigharimiya miradi itakayokuwa na faida kubwa na za muda mrefu kwa Waarabu na kwa Waafrika.40 Afrika ni bara lenye neema kuliko mabara yote duniani na linaweza kujileteya maendeleo makubwa sana bila ya kutegemeya siasa ya ombaomba na kuingiliwa kuendesha mambo yake kwa kulifuata zumari la kisiasa linalopigwa kutoka nje ya Afrika. Jambo la pili ni kulichangamsha Gwaride la Zama Hizi (March to Modernity) ambalo msomi kutoka kisiwa cha Singapore, Profesa Kishore Mahbubani, amefahamisha kwa kuandika: “Hakuna njiya yoyote ile ya Gwaride la Zama Hizi litaweza kulifagiya Bara la Asia bila ya kuwaathiri Waasia bilioni moja ambao ni Waislam (Waislam milioni mbili tu ndiwo wenye kuishi Afrika Kaskazini na Ulaya).”41

Mahbubani hakuuweka mkazo wa Gwaride la Zama Hizi lenye chimbuko lake kutoka nchi za Magharibi kupitiya Japan, Korea ya Kusini, Singapore, Malaysia, India, Uchina, na Indonesia, kwa kulifananisha na majumba marefu yaliyojengwa Dubai peke yake. Anaendeleya Mahbubani na maneno haya:

Hadithi kubwa zaidi ni gwaride la zama hizi ni la ndani ya nafsi. Viongozi wakuu wenye kuiongoza Dubai ni viongozi wa kileo na waliyobobeya kama wengine wowote wale wa miji ya kimataifa. Lengo lao ni kuifanya Dubai na miji mengine ya Ghuba kuwa ni ya kileo. Ikiwa Dubai itafaulu, basi inaweza ikatowa mwangaza mpya wa tamaa katika ulimwengu wa Kiislam. Inaweza nchi za Magharibi wakayaunga mkono maendeleo ya namna hiyo—na wanaweza wasiyaunge mkono!42

Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani kinatiliya mkazo na kuringiya mahusiyano yake na Uchina ambayo yanarudi nyuma mwaka 1854 alipokhitimu Yung Wing kutoka chuo hicho.43 Wakati wa utawala wa Sayyid Said bin Sultan, Zanzibar na Oman ziliandaa safari ya meli ya Sultana iliyopakiya mizigo ya zawadi kutoka Maskati na kuongeza mengine zaidi kutoka Zanzibar na kuwasili New York Alkhamisi tarehe 30 Aprili 1840.44

Wachina waliijuwa Afrika Mashariki na sehemu nyenginezo kutoka Waomani. Mwaka 1050 A.D. Sheikh Abdullah Al­Omani aliuingiya mdomo wa mto Pearl na akatupa nanga Whampoa na akaendeleya mpaka akafika Guangzhou. Anauliza Bingwa, Profesa E. Harper Johnson:

Nini ingelikuwa khatima ya Oman na mataifa mengine yaliyowekwa chini ya utawala wa Kireno na nchi nyengine zenye nguvu za Magharibi kama Uchina ingeliungana na Oman na nchi nyengine za Afrika na Mashariki ya Kati kwa lengo la kuitawala Ulaya? Hichi ni kitendawili kilichofunikwa ndani ya siri kwa vizazi vitakavyokuja baadaye kukiteguwa.45

Page 376: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini344

Kizazi cha leo kutoka Zanzibar, Tanganyika, nchi nane zinazopakana na Tanzania, nchi za Magharibi na za Kiarabu, kina nafasi kubwa ya kuiongoza njiya iliyopitwa na safari ya meli ya Sultana ya Marekani au ya kabla yake ya Sheikh Abdulla Al­Omani ya Uchina, kulizinduwa Gwaride jipya la ilimu na la kiuchumi la Zama Hizi. Njia nzuri na yenye tija la muda mrefu ni kuwachaguwa na kuwaanda vijana wa Kiafrika na wa Kiarabu watakaoweza kupata nafasi za kusoma kwenye ngazi zote za vyuo vikuu vyenye sifa Ulaya na Marekani. Hawa ndiwo vijana watakaoweza kuzivunja kuta baina ya Waislam na Wakristo na baina ya Waafrika na Waarabu alizozizungumziya Rais Barack Obama wa Marekani na Profesa Ali A. Mazrui. Kuta ndefu zenye kuwagawa Waafrika na Waarabu, Waislam na Wakristo, zinapaswa kuvunjwa kwa kuanzisha mfumo wa ilimu utakaowafundisha wanafunzi tamaduni za Kikristo zenye kutowa ilimu nzuri kuhusu Uislam kama zile za akina Johann Wolfgang von Goethe wa Ujerumani, Ralph Waldo Emerson wa Marekani, na Alexander Pushkin wa Urusi, nk.46 Pia wanafunzi wataweza kusoma kuhusu daraja kubwa anayopewa Yesu Kristo (Issa mtoto wa Bibi Maryam) katika Qur’an na historia ya mchango wa kiilimu katika Ustaarabu wa Kikristo wa nchi za Magharibi.Uhuru utakaoweza kuletwa na ilimu ya juu hauna budi uanze kuzipanda ngazi kutokeya ilimu ya chekecheya, ya chuoni, ya msingi, na ya sekondari. Ni mapinduzii ya ilimu peke yake yenye uwezo wa kumkombowa Muafrika na Mwarabu, Muislam na Mkristo, na kuwatowa kunako kwenye giza la upotoshaji na khadaa la mapinduzi ya Zanzibar na sababu zake. Ufunguo wa historia iliyofichwa huenda pia ikautikisa msingi wa iliyokuwa Tanganyika, marafiki na majirani zake, na kwa karibu zaidi waasisi wakongwe wa vyama vya kisiasa wenye kuujuwa ukweli uliyofichwa ambao umeendeleya kuwanufaisha wao na warithi wao. Kizazi kipya, na wengi kati ya wazee, kimegubikwa na guo la khadaa na upotoshaji wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo kufunguliwa kwake huenda kukatowa mwangaza utakaoimurika njia mpya ya Shirikisho.

Maudhui na Mazingatio

Mpaka hapa tulipofika, na kutoka na simulizi za wazee za kabla yake, inadhihirika kwamba Wazanzibari kwa ujumla walipandiya tu kwa kujigamba kama wali­kuwemo katika mapinduzi wakati hawakuwemo ndani ya jiko la mapinduzi au ndani ya usiku wa mapinduzi. Hata Mzee Karume alishirikishwa kwa sababu alikuwa ni kiongozi mwenye kuungwa mkono na wafuasi wengi wa ASP lakini si kama alikuwa Jemedari wa mapinduzi ya Zanzibar kama inavyotangaziwa. Na wengine kutoka pande zote za ASP na Makomred ingawaje baadhi yao walishirikishwa kijuujuu tu bila kuujuwa undani wa matayarisho ya mapinduzi yenyewe. Na khasa wale wenye asili ya Kizanzibari yenye kwenda nyuma kwa

Page 377: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 345

daraja nyingi ndiyo kabisa waliwekwa kando. Kwa ufupi, mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na wageni kwa lengo la kuwadhibiti wenyeji (Wazanzibari) pamoja na nchi yao. Hii inauthibitisha ule msemo wa Nyerere “Hayo ndio maumbile ya uhuru; lazima upiganiwe na ulindwe na wenye hamu nao. Uhuru wenye kupiganiwa na watu wa nje unakwenda kwa watu wa nje.” Kutokana na maelezo yote yaliyopita ionekanavyo humu kitabuni, ingefaa viongozi wa aina zote na wasomi wa kitabu wakajiuliza masuala matatu yafuatayo ili kusawazisha hali ya mambo kutokana na khadaa zilizotendeka ili papatikane kuaminiyana tena baina ya Wazanzibari na baina ya Wazanzibari na Watanganyika kwa maslahi ya nchi na vizazi vijavyo.

1. Siasa ya Pan­Africanism yenye kusema kuwa Zanzibar ni ya Waafrika wenye asili ya kutoka bara la Afrika peke yake na si ya Wazanzibari kutoka mabara mengine ni siasa ya kibaguzi na kikaburu yenye kuongozwa na kikundi cha viongozi wachache waasisi na wafuasi wao.

2. Wakati umefika kwa Tanganyika na dunia kuukubali ukweli kuwa Zanzibar ni ya Wazanzibari wote na si mali asili ya Tanganyika na kutambuwa kuwa Umoja wa Afrika hautoweza kufikiwa ikiwa Muungano pekee barani Afrika baina ya Tanganyika na Zanzibar hautopata suluhisho la kudumu.

3. Licha ya mahitajio ya kuufahamu ukweli wa “Mapinduzi”, Wazanzibari walionyanganywa nchi yao na waliodhulumiwa kwa hali, mali au mali asili, au kifo, watakuwa na madai gani ya kikanuni za kimataifa dhidi ya kikundi cha watu wachache na ushawishi wao mkubwa ndani ya taasisi wanazozimiliki na kuziongoza?

Mabadiliko ya mfumo uliozoweleka kwa muda mrefu kunaweza kusambaza khofu kongwe ya kuiona Zanzibar ikiinuka. Tutarajiye sana upinzani mkali kutoka Tanganyika na khasa kutoka kwa jumuiya zisizo za Kiserikali (NGOs) ambazo zimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda chafu dhidi ya Wazanzibari na Waarabu—Waislamu kwa jumla. Kwa mujibu wa mwandishi Mohammed Ghassany “Watafanya kila hila na kila mbinu. Watatupa tabu sana na njia pekee ni kuuilimisha umma na wale ambao wameshatiwa sumu dhidi ya Waarabu na biashara ya utumwa peke yao.”47

Wajanja na wenye kukhadaa wanapenda sana kutumiya mbinu za kuhamakisha, kutiya hisiya ya kudhulumu, kuonyesha hatari kubwa itakayowakabili wasiyotaka kuwafuata, na hujivalisha guo la utukufu, ili kuulinda ujanja na khofu zao. Kwa vile ni binaadamu wenye khofu ya kuogopa kujulikana huanza kuwatiya khofu na kuwaondoleya hoja wale wenye kutaka kuwadhibiti na kuwatawala kimawazo na kimabavu. Wanaposhindwa kupata muradi wao hujaribu kujifanya wamehamaki

Page 378: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini346

na wamekereka. Wakishindwa hubabaika na wakawa hawana raha na kuanza kutishiya. Wanapoona tayari kushindwa huanza kukata tamaa na kuingiwa na dhiki ya moyo. Saikolojiya yao inafuata mwenendo na vituo maalumu.48

Faida za Mapinduzi ya Afrabia

Nchi ya Oman inajenga bandari ambayo ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inaweza ikaingiya ubia na bandari mpya yenye sifa ya kimataifa ya Zanzibar au bandari mpya za Tanganyika. Watalii wanaotembeleya Oman au UAE, au sehemu nyengine za Asia wanaweza kuendeleya na safari zao na kuzizuru mbuga za wanyama za Tanganyika, Kenya, nk. Katika faida nyenginezo, hakuna watu wengi wenye kusema lugha ya Kiswahili nje ya Tanzania kama nchi ya Oman na hakuna watu wengi wenye asili ya Kiomani nje ya Oman kama Afrika Mashariki. Wananchi wa Oman kwa upande wao wanaweza kuleta mabadiliko kwa kutoogopa kuutumiya Uswahili au Uafrika wao. Vipindi va televisheni vya Kiomani juu ya Afrika Mashariki vimeleta muamko mkubwa kwa Waomani ambao wakiisikiya tu Afrika Mashariki. Waomani wengi wa Oman ya leo huenda wakawa wameyasikiya mapinduzi ya Zanzibar au wamezisoma habari zake lakini hawakuyashuhudiya mapinduzi au athari zake. Kwa hiyo uwezekano mkubwa wa kuyaondowa machungu na khasara upo. Ndani ya muda mfupi Zanzibar na Tanganyika pamoja na Msumbiji na Oman, na UAE, au Qatar, zinaweza zikapiga hatuwa kubwa kwa kutumiya rasilmali kidogo za kifedha. Fikiriya utajiri wa mahusiyano ya kihistoria, kithakafa, na kilugha baina ya sehemu mbili hizi za duniya. Fikiriya Zanzibar na Tanganyika zisinunuwe kutoka nchi nyingine yoyote ile duniani nini Oman na UAE zinaweza kuuza, na Oman na UAE zisinunuwe kutoka nchi yoyote nyengine nini Zanzibar na Tanganyika zinaweza kuuza. Fikiriya mashindano ya mpira wa miguu yenye kujenga urafiki na udugu baina ya vijana waliyo chini ya umri wa miaka 15 baina ya pande mbili za uhusiyano mkongwe wa Afrabia. Zanzibar na Tanganyika zinaweza kununuwa mafuta ya petroli, kubadilishana utaalamu na Oman na UAE kuendeleza viwanda vyake vya petroli na gesi. Oman au UAE zinaweza zikafunguwa vituo vya petroli Zanzibar na Tanganyika kwa kushirikiyana na wafanyabiashara wenzao. Zanzibar na Tanganyika zinaweza zikamiliki pamoja na Oman au UAE meli na ndege kubwa za kubebeya mizigo ambazo zinaweza kufika mpaka Kongo. Oman na/au UAE inaweza ikazinunuwa karafuu za Zanzibar na kuzisafirisha ndani ya vyombo vya bahari vinavomilikiwa na Wazanzibari na Waomani. Inasemekena marehemu Abdulrahman Babu alikuwa na miradi mitatu ambayo alivinjari kuiweka sawa lakini Nyerere aliikataa. Mradi wa kwanza ulikuwa ni mradi wa kiwanda cha mafuta ya chikichi (palm oil) alichotaka

Page 379: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapinduzi Ndani na Nje 347

kukianzisha Kigoma ambapo Majapani walikuwa waugeuze ukanda wote wa eneo lenye kulizunguka Ziwa Tanganyika kuwa ni la chikichi na viwanda vya mafuta. Wajapani wangelijenga njiya za mabomba mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya kuyasafirisha mafuta. Mradi wa pili wa Babu ulikuwa ni kujenga miji midogomidogo ambayo ndiyo ingelikuwa ni vituo vya kibiashara khususan kutoka vijijini ambapo WaCuba walikwishatuma hata watu wao kwa matayarisho ya uchoraji na usanifu wake. Mradi mwengine na wa tatu ulikuwa Rufiji Basin Development wa kilimo na khasa cha mpunga. Alikwisha kagua nyumba ya kununuwa ambayo ndiyo ilikuwa ikiendeleya kujengwa, lengo lake likiwa ni kufunguwa ofisi (NGO) ya masuala ya kijamii lakini akafariki dunia mwaka 1996. Ni vigumu kuweza kutoka kwenye mapinduzi ya kuumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar kuelekeya kunako mapinduzi ya kiuchumi wakati jina la “Serikali ya Mapinduzi” haliashirii utulivu na usalama wa nchi au rasilmali za wawekezaji khasa kwa uchumi ambao hautegemei sana sekta ya utalii. Dunia nzima hakuna nchi yenye kuitwa “Serikali ya Mapinduzi.” Wasiwasi wa mwandishi huyu ni kuwa wenye kufaidika khasa na jina hilo ni wale waliyohusika na mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu kisaikolojiya Zanzibar maisha inakuwemo kunako hali ya kupinduwana na kuwapoteza waekezaji makini. Zanzibar kabla na baada ya uvamizi wa Tanganyika ilikuwa na jina ambalo ndilo jina la nchi kama ilivyokuwa ikijulikana Umoja wa Mataifa.

Page 380: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini na MojaNyumba ya Afrabia

…Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. —Qur’ani 2:216

Tanzania haiwezi kwenda na wakati na Tanganyika isiende na wakati huo huo pia. —Julius K. Nyerere

Hakuna asiyefahamu kuwa Wazanzibari ni watu waliochanganya damu sana na wanatoka kwenye makabila yenye asili tafauti ima kwa uzawa au kwa ndoa, kabla na baada ya mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964. Ni bahati mbaya kwamba kuchanganya damu kwao huko hakukuwasaidiya pale walipoingiliwa na kuchanganywa na siasa za kuupinga ukoloni na kudai uhuru wao, na matokeo yake wakaathiriwa na fitina na chuki za kikabila zilizojengwa na kushamiri khasa ndani ya kipindi cha ukoloni kutoka madola makubwa ya Magharibi. Waafrika na Waarabu, wakiungwa mkono na Wazanzibari wa makabila mengi ne wakiwemo Washirazi ambao ndiyo waliyo wengi Zanzibar, wote, walitawaliwa na mirengo ya kizalendo iliyoshadidiya kwa siri au kwa dhahiri misingi ya kikabila ambayo iliwagawa badala ya kuwaunganisha. Hata Uislam, dini ya takriban asilimia 99% ya Wazanzibari, ambao hautambuwi mipaka ya uzawa wala ya ukabila haukuweza kuwasaidiya Waislamu waliotawaliwa na kuzongwa kifikra na siasa chafu ya wakoloni ya “Wagawe Uwatawale”. Lakini ukichunguza kwa undani utakuta ni wachache tu kati ya watu wa koo zilizochanganya damu Zanzibar waliyomo katika vurugu za hapa na pale katika siasa mambo leo. Ukipeleleza utawakuta wengi wanaoendeleza malumbano ya siasa za chuki na khasama hawana mchanganyiko huu wa damu na wa ndoa baina ya watu wenye asili za Kiafrika na Kiarabu. Tukifanya uchunguzi mdogo tu wa familia moja moja utakuta Zanzibar ya jana si ya leo. Kukhasimiyana na kuuwana Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe

Page 381: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Nyumba ya Afrabia 349

wakati kila mmoja takriban amemhusu mwengine au ameowana naye ni jambo lisiloelezeka kirahisi bila ya kuufahamu upotoshaji wa ukweli wa mapinduzi ya Zanzibar. Mlolongo ni mrefu na hautokwisha tukiuendeleza ndani ya kitabu hichi na itabidi kikosee kwa kutowataja wengine ambao watahisi nimewadharau au sikuwajali uzawa wao kabla na baada ya mapinduzi. Mfano mmoja ninaoutowa utosheleze kuthibitisha hoja ninayoijenga. Saeed Al Battashy amezaliwa karibuni na ana umri mdogo wa miaka minne leo na ni mzaliwa wa Uingereza sehemu za East London. Mtoto mdogo huyu pia ni Banyani na kizazi chake wameishi na kutumika kwenye kasri ya Sultan wa Zanzibar kabla ya mapinduzi.1 Wengi katika ukoo wa kifalme wa Zanzibar wana asili za Kiomani, Kitumbatu, Kiganda, Kinyasa, Kingazija, Kiethiopia, Kimsumbiji na makabila mengi mengineyo ya Kiafrika kutoka bara ambayo ni vigumu kuyajuwa. Babu yake Saeed Al Battashy amewahi kuwa Rais wa Zanzibar kwa miaka mingi baada ya mapinduzi. Kati ya mengi, mjukuu huyu ana babu aliyewahi kushtakiwa kwa kosa la kumuuwa marehemu Rais Abeid Amani Karume mwaka 1972 na akahukumiwa kifo. Kama ilivyo kwa Saeed Al Battashy aliyeko Uingereza hivi leo, ndivyo walivyo babu zake wote hawa, Mungu awarehemu waliokufa na awape umri mrefu walio hai. Hivi karibuni tu babu yake mmoja alizinduwa kitabu Zanzibar kuhusu maisha yake na siasa za Zanzibar kiitwacho Ukabila, Mapinduzi, na Harakati za Kupiganiya Haki za Binaadamu Zanzibar: Kumbukumbu za Maisha ya Ali Sultan Issa na Seif Sharif Hamad. Watoto wa khaloo yake (mama mdogo) Saeed Al Battashy ni wajukuu wa Rais Karume kutoka mmoja kati ya watoto wa marehemu Rais Abeid Amani Karume. Mzee Karume alishazaa watoto wawili wa kiume ambao wana damu za mchanganyiko kabla ya tarehe 12 Januari, 1964. Nimemchagua kijana huyu Saeed Al Battashy kama ni kigezo cha mahusiyano ya Afrabia yalivyo kwa nchi ndogo kieneo na masikini kiuchumi lakini kubwa kisiasa na tajiri kwa historia na uzawa wa raia zake. Leo hii watoto, wala si wajukuu, wa marehemu Brigedia Yusuf Himid, mwanamapinduzi aliyetajwa sana ndani ya kitabu hichi ni Waafrabia na ni wajukuu wa marehemu Sheikh Ali Muhsin Al­Barwani, kupitiya muasisi wa siasa ya uzalendo wa Kizanzibari, marehemu Bwana Mohamed Salim “Jinja” ambaye alisoma Chuo Kikuu cha Oxford (1944–48). Watoto wa marehemu Mzee Yusuf Himid wana damu za ki­Al­Busaidi na wametokana na ukoo wa Awlad Hemed bin Said ambao ndiyo wafalme wa karne na karne na watawala wa eneo lote kuanziya pwani ya Somalia kushuka chini kwenye ukanda wa Pwani wa Afrika Mashariki. Rais wa hivi sasa wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Amani Abeid Karume ana damu ya Kihindi kabla hata ya Mapinduzi ya 1964 na watoto wake wote aliyozaa wana damu ya Kisomali na Kiarabu tena wakiwa katika mizizi ya utawala tokea enzi na enzi za nchi ya Zanzibar. Hii ndiyo Afrabia. Ni wajukuu wa mwanzilishi

Page 382: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini na Moja350

wa vuguvugu la siasa za kizalendo za kujigombowa kutokana na fedheha ya kutawaliwa na kudai uhuru, na msomi wa kusifika na mwandishi wa kutajika, marehemu Sheikh Mohamed Salim Al­Barwani (maarufu “Jinja”). Hawa ndio watoto wa Rais Amani Abeid Karume. Mmoja wa Manaibu Waziri katika Serikali ya sasa Zanzibar anafuata madhehebu ya Kiismailiya yanayoongozwa na Aga Khan. Daktari mmoja maarufu nchini Oman ana mtoto wa kuzaa na marehemu Mzee Abeid Amani Karume na kati ya ndugu zake kwa baba, mmoja ameolewa na aliyepata kuwa mgombea nafasi ya makamo wa Rais kupitiya chama cha upinzani cha CUF ambaye ana asili ya Kishirazi (Kiirani). Kabla mapinduzi ya 1964 kufanyika Rais Aboud Jumbe Mwinyi watoto wake aliwazaa na bibi wa kabila ya Al­Kindy ambaye mwaka huu amefariki akiwa na umri wa miaka 103. Watoto wake wakubwa kabla mapinduzi ya 1964 wote wana babu mzaa mama akiwa ni Sheikh Abdullah Al­Kindy. Bibi Moza bint Khalfan Al­Barwani, bibi yake aliyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP au “Hizbu”, neno la Kiarabu ambalo maana yake kwa Kiswahili ni “Chama”), marehemu Sheikh Ali Muhsin, amekhusiana na Wamakonde. Babu wa Kimakonde wa babu yake Sheikh Ali Muhsin wa upande wa kwa mama, Sheikh Nassor bin Issa Al­Barwani, ambaye ni Chifu Mwanya wa Wamakonde ndiye aliyeitowa ardhi ya mji wa Mgao Mwanya ambayo ndiyo iliyouasisi mji wa Lindi.2 Tukichunguza tutakuta ni watu wachache sana waliyoko Zanzibar ambao hawana mtiririko wa aina hii kati ya watawala, wanasiasa na hata raia wa leo au kabla ya mapinduzi. Itakubidi uchambuwe koo nyingi na historia za mtiririko wake, utafute nani hawakukhusiyana toka ntoke na watu wa asili za makabila tafauti iwe kwa uzawa au ndoa. Na hili si la baada ya mapinduzi bali ni la kutokeya karne na karne, dahari na miaka. Koo hizi ukizifuatiliya utazikuta damu zilizojikita khasa ni za Kiarabu na za Kiafrika na haya hayakuanziya hivi karibuni bali ni muendelezo wa maingiliyano ya jamii mbali mbali karne kwa karne. Hakuna buku kubwa kama buku lililoandikwa na viini vya uzazi vya DNA ambavyo vimo ndani ya kila kiwiliwili cha binaadamu. Mimi ni Muafrabia wa uzawa, ndowa, thakafa na imani. Baba yangu mzazi, marehemu Bwana Mohammed Abdalla Mohamed Ghassany (maarufu “Bingwa”) amezaliwa na baba mwenye kabila ya Kiarabu ya Al Ghassani na mama yake ni Bibi Sarah bint Ahmed bin Muhammed Al Barwani Awlad Hijji ambaye alizaliwa Kongo, Kisangani. Bibi yake marehemu baba yangu mzaa baba, Bibi Zuhura bint Mfaume, ni Mwera wa Lindi, kusini ya Tanzania. Bibi yake baba yangu mzaa baba ni Bibi Mwajuwaye bint Tambwe Waminakule, kutoka kabila la Kimanyema la Wabwuywe. Marehemu mama yangu, Bibi Asya bint Abdalla Al­Jahdhami na bibi yangu mzaa mama ni Bibi Neyu bint Hemed bin Muhammed bin Hemed bin Said Al­Busaidi (Awlad Hemed).

Page 383: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Nyumba ya Afrabia 351

Matokeo ya vipimo va DNA vinathibitisha kuwa upande wangu wa baba unatokana na Haplogroup J1e (+L147). Kundi hili linarudi nyuma miaka 10,000 kwenye historia ya viini vya Y­chromosome na asili ya kundi hili inatokana na sehemu ambayo leo inajulikana kuwa ni Iraq au ile sehemu baina ya mito miwili ya Tigris na Euphrates. Kabla ya hapo kundi la M267 liliondokeya kaskazini ya Afrika Mashariki kiasi ya miaka 60,000 nyuma. Kundi la J1 M267 ni kundi liloanzisha mapinduzi ya kilimo katika kipindi kinachojulikana kwa jina la “Neolithic.” Kuna waliyoelekeya Afrika ya Kaskazini, na wapo waliyoelekeya Arabuni na Ethiopia. Wengine wakaelekeya sehemu ya Bahari ya Mediterranean na walomalizikiya Europe wengi wao ni Mayahudi wa Ashkenaz. Kutokana na matokeyo ya utafiti wa mtDNA, kundi la upande wa marehemu mama yangu, Haplogroup L3, liliondoka Afrika inapata miaka 80,000 elfu nyuma kuliko kundi la marehemu baba yangu. Haya yote yanathibitisha kitu kimoja nacho ni kama tunavyofahamishwa na dini zote kuwa binaadamu wote asili zao ni moja na wote wanatokana na Adam na Hawa na asili ya binaadamu wote ni Afrika. Ametuambiya Bwana Mtume Muhammad (SAW) kuwa hakuna aliye bora baina ya Mwarabu na Muajemi. Ametufundisha Nabii Issa (Sala na salamu za Mwenye Enzi Mungu zimteremkiye), kuwa wafanyie watu yale ambayo wewe utapenda wakufanyie. Zanzibar ni mfano mzuri wa kuzitambuwa, kuziheshimu na kuzisherehekeya asili za binaadamu wote na zuka la mustakbali wake litaletwa na watu wa kawaida waliyotoka nje ya pango la upotoshaji na kupitiya wao kupatikana uongozi unaotokana na mchanganyiko wa uzawa ambao una nguvu zaidi kuliko zile za Kiafrika au za Kiarabu—nguvu za umoja, nguvu za Afrabia. Mfano mzuri wakati wa Mapinduzi ni ule wa urafiki na ubinaadamu baina ya Mmakonde Bwana Yohana (Sadiki) Ntanga na Bwana Abdallah Majid Al­Siyabi, Mzanzibari mwenye asili ya Kiarabu kutoka Nizwa, Oman. Watu hawa wawili waliishi kwa urafiki na mafahamiyano mazuri kabla ya mapinduzi na wakati wa mapinduzi Bwana Yohana alimchukuwa na kwenda kumficha rafiki yake Bwana Abdalla ambaye alikuwa akitafutwa na wanamapinduzi. Inasemekana kuwa wakati wa siasa za chuki baadhi wafuasi wa ZNP waliwazuwiliya wafuasi wa ASP kulima au kuteka maji kwenye visima vyao, lakini Bwana Abdalla hakufanya hivyo na alimuachiya Bwana Yohana kufanya shughuli zake kama kawaida. Ulipofika wakati wa Mapinduzi Bwana Yohana akamchukuwa Bwana Abdalla na kwenda kumficha uwandani sehemu za Tunguu. Bwana Abdalla alikuwa ameficha fedha zake mahala fulani na akamuelekeza Bwana Yohana wapi zilipo mpaka hali ilipotuliya. Alipoondoka kwenda Oman, Bwana Abdalla alimkabidhi Bwana Yohana kwa maandishi na mbele ya viongozi wa serikali vikataa vya shamba la minazi pamoja na nyumba mpaka atakaporudi mwenyewe kutoka Oman. Mwaka 1999 Sheha kwa ushirikiyano na Polisi wa Fuoni na Katibu wa Wilaya ya Kati walitaka kumnyanganya Bwana Ntanga hivyo vikataa na nyumba.

Page 384: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini na Moja352

Kwa kifupi, marafiki wawili hawa walisimama pamoja na Bwana Abdalla akampelekeya mualiko Bwana Yohana ende Oman akatembee lakini safari hiyo haikujaaliwa kuwa.3

Kwa upande mwengine, utakuta pia kuna familia zenye majina nusu ya Kikristo na Kiislamu na hili kwa Zanzibar halishangazi hata kidogo. Hivi leo ukenda sehemu za Kisauni kuelekeya barabara mpya ya Fumba pana sehemu inaitwa “Msikiti na Kanisa” na tayari limeshakuwa jina la mtaa huo. Sababu yake ni msikiti uliyopo ukuta kwa ukuta na kanisa na mote humo mnasaliwa wala waumini hawagombani. Ni pa kutolewa mfano lakini hukutii vyombo vya habari vya Zanzibar kulikuza hili kwani kwa Zanzibar ni jambo la kawaida tu. Ndivyo historia ilivyoijenga Zanzibar na ndivyo ilivyo hadi leo. Na mfano mwengine wa kale ni ile minara miwili, wa kanisa na wa msikiti iliyopo Mkunazini katika kisiwa cha Unguja. Kujenga mshikamano madhubuti baina ya Waislamu wa Afrika Mashariki na Kati utategemeya kuwakusanya na kuzinyanyuwa hali za Waislam kiilimu, kiuchumi na kijamii katika kupiganiya haki zao sawasawa na raia wengine katika nchi hizo. Ni muhimu pia kwa Waislam kuwa na mahusiano mazuri na waumini wa dini nyingine na kuondowa chanzo kikubwa cha fitina na uadui ambacho ni suala la utumwa lililojengwa juu ya misingi ya ujinga bila ya uthibitisho wenye kulindwa na ushahidi madhubuti. Kosa kubwa la Zanzibar ilipokuwa inadai uhuru wake na wakati inadai haki zake kama ni nchi ni kulipuuza suala la utumwa ambalo ndilo lililowafitinisha na linalotumiwa kama ni kisingiziyo kikubwa cha kubomolewa Dola ya Zanzibar na kuogopwa kurejea tena. Mtizamo uliyojikombowa kutokana na upotoshaji wa suala la utumwa wa Afrika Mashariki una uwezo wa kuwaondoleya ukhasama Waislam na Wakristo. Nchi za Kikristo na za Kiisilamu zina nafasi ya kufanya ukarimu wa kuwaleteya Waafrika Wakristo na Waislam maendeleo yatayojengeka juu ya msingi wa kuhishimiana na wa kutafuta maslahi ya pamoja. Kuwatakiya maendeleo waumini wa dini fulani na kuwazuwiliya waumini wa dini nyengine maendeleo si dalili ya kumtakiya mwenziyo mema unayojitakiya mwenyewe. Ukombozi wa Zanzibar haumo kwenye kujenga hamaki dhidi ya mazingira ya khadaa, njama na hila, bali umo ndani ya umoja unaosimama baada ya kulivuwa guo la buibui lililolifunika pango la upotoshaji wa historia. Tuondoe mabuibui tuukumbatiye umoja. Jambo muhimu na la kwanza kuliko yote ni kuusimamisha msamaha ndani ya jamii ya Kizanzibari kupitiya ukweli na pengine hata kusoma dua nchi nzima kuiombeya Zanzibar na Tanganyika maghfira na mazingira ya haraka ya mustakbal mwema. Msamaha kupitiya ukweli haina maana ya kufukuwa majeraha ya historia. Maafa yaliyoikumba Zanzibar si ya kubuni bali ni mambo ambayo yametokeya na yameshuhudiwa. Utumwa ulifanyika Zanzibar, Tanganyika, na kote Afrika Mashariki na Kati, na hakuna haja ya kujiroweka ndani ya uwongo wa hadithi

Page 385: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Nyumba ya Afrabia 353

za kubuni za utumwa na kuwa uokovu wa Yesu Kristo ndiwo uliyomkomboa mwana wa Afrika kutoka uovu wa utumwa wa “wageni” wakikusudiwa Waarabu na Waislam. Waliyoipinduwa Zanzibar hawakuwa vijukuu wala virembwe vya watumwa na hakuna ushahidi wowote ule kuwa wapinduzi na wapinduliwa walikuwa na uhusiano wowote ule na utumwa uliofanyika Zanzibar. Ukweli ni kuwa nyuma ya propaganda hakuna kuwachukiya Waarabu au kuwapenda Waafrika bali kuna maslaha ya kisiasa na ya kiuchumi yenye mtizamo na upeo wenye kuona mbali sana. Kwa hiyo si lengo la kitabu hichi kutonesha vidonda na kufukuwa majeraha ya historia. Wala si lengo lake kuamsha hisia za chuki na khasama kati ya watenda na watendewa. Maana tukiichunguza kwa makini historia ya Zanzibar, sote ni watenda na watendewa kwa nyakati tafauti. Tulipoacha kuukubali na kuusherehekeya mchanganyiko wa kipekee unaounda jamii yetu, sote tulikosa. Huu si wakati wa kutazama nyuma. Tuangaze mbele kwenye mustakbal unaotuunganisha tena na kwa pamoja tusimamiye maslahi ya nchi tuipendayo—Zanzibar na Tanganyika. Tukiwa na mtazamo wa aina hiyo, tutangunduwa kuwa hakuna haja ya kukataana na kutaka kutimuwana, tutagunduwa kuwa pamoja na udogo wake kieneo, Zanzibar ina nafasi ya kutosha kutuingiza sote. Kama ilivyokuwa hakuna haja ya watawala wa Watanganyika kuwa na khofu juu ya Zanzibar na Wazanzibari hawana haja ya kuhuzunika kwa yaliowafika. Zanzibar ina kila sababu ya kuziteteya haki zake ndani ya muungano bila ya Tanganyika kuhamaki na kuwaona Wazanzibari kuwa ni watu matata. Zanzibar inahitajiya mtizamo na mfumo mpya kabisa wa mahusiano yake na Tanganyika lakini usiwe mfumo uliojengwa na uadui au khofu ya Zanzibar kuuvunja Muungano unaotawaliwa na Tanganyika. Wakati umefika wa kuanza kuzijenga fikra mpya Zanzibar na Tanganyika. Kwa mfano, pafanyike mabadiliko ya Katiba ili Urais wa Muungano uwe kwa mzunguko kikatiba baina ya nchi shiriki za Tanganyika na Zanzibar badala ya kufuata utaratibu usiyokuwa na dhamana au unaotegemeya dhana ya “wengi wape.” Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Muungano anaweza akawa Kikatiba anatoka Zanzibar. Jeshi linaweza likawa ni la Muungano lakini ulinzi wa ndani wa Zanzibar ukawa ni wa Wazanzibari. Zanzibar inaweza ikajiunga na Taasisi za Kimataifa ambazo zitakuwa na maslahi makubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar na Tanganyika, na kadhalika. Juhudi maalumu zinaweza zikachukuliwa kuvifuta vitabu vyenye kuendeleza chuki na fitina baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waislamu na Wakristo, kwa kutunga vitabu na vipindi vya redio na televisheni ambavyo vitaielekeza jamii kunako ukweli na msamaha. Dola ya Zanzibar inaweza ikaanzisha mfuko maalumu utakaochangiwa na jamii ya kimataifa na utakaokuwa na lengo la kuzipoza nyoyo za Wazanzibari waliofikwa na maafa tafauti. Zanzibar ni lulu ndani ya taji la Afrabia juu ya kichwa cha bara tajiri kuliko yote na la mwangaza—Afrika.

Page 386: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mlango wa Ishirini na Moja354

Ametahadharisha Bwana Muyaka bin Haji Al­Ghassani pale aliposema:

Kimya kina mshindo mkuu, ndivyo wambavyo wavyeleKimya chataka k’umbuu, viunoni mtatileKimya msikidharau, nami sikidharawileKimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya

Kimya ni kinga kizushi, kuzukiya walewaleKimya kitazua moshi, mato musiyafumbuleKimya kina mshawishi, kwa daima na mileleKimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya

Kimya vuani maozi, vuani mato muoleKimya kitangusha mwazi, mwendako msijikuleKimya chatunda p’umzi, kiumbizi kiumbileKimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya

Na amesema mpigania haki za watu weusi Marekani, Dk. Martin Luther King Jr.: “Si mabavu ya wachache yenye kunitisha mimi, bali ukimya wa walio wengi.” Ewe Mola Wetu! Tuingize kunako mlango wa ukweli wenye kuiwekeya Zan­zibar na Tanganyika hishima duniani na tutowe kunako pango la upotoshaji wa historia kupitiya mlango wa ukweli na hishima. Tupandishe ngazi itakayotuzi­dishiya ilimu na kutuondoleya umasikini wa ujinga na ujinga wa umasikini na tupe uwezo wa kuzitambuwa dhamira za maisha yetu duniani zitakazokuridhisha Wewe na utupe furaha za kuzikamilisha. Wewe Ndiye Mwenye Kutulinda na Wewe Ndiye Mwenye Majeshi Yasiyoshindwa! Mungu Ibariki:

Zanzibar Mpya Tanzania Mpya Afrabia Mpya

AMIN

Page 387: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla

Kurasa za Mwanzo

Profesa David Cohen wa Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor, alitushauri mimi na 1. Profesa Kelly Askew tulipokutana naye Ann Arbor kwenye mkahawa wa Blue Nile, tarehe 5 Oktoba 2004. Pia alishauri kuwa ni muhimu muswada wa kitabu ukasomwa na wadau wenye mirengo tafauti kuhusu mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kukichapisha na kukitowa kitabu.

Minou Reeves, 2. Muhammad in Europe: A Thousand Years of Western Myth-Making, New York University Press, 2000, uk. 300 unatowa majina ya wasomi wa Kizungu na Kikristo ambao umewacha utamaduni mkubwa na mtizamo mzuri “wenye kutafuta kufahamu kadhiya ya Muhammad, ujumbe wake, mabadiliko yake ya kijamii na ya kisiasa, akhlaki na tabiya yake kwa mujibu wa mazingira ya wakati wake na kwa mtizamo usiyokuwa na vizingiti vya chuki.” Majina yenye kutajwa ya wale wenye utamaduni mzuri juu ya Mtume Muhammad ni ya Roger Bacon, John wa Segovia, Lessing, Goethe alipokuwa kijana, Boulainvilliers, Bolingbroke, Caryle, Dawson, Reland, Rilke, Paret, Sprenger, Tor Andrae, Bodley, Montgomery Watt, Rodinson na Annemarie Schimmel.

Abdul Sheriff, 3. Slaves, Spices & Ivory in Zanzibar, James Currey, 1987, uk. 34.Abdilahi Nassir, Kanda, 4. Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki, (Hamna

tarehe). Kwa mujibu wa marehemu Sheikh Ali Muhsin “Nyerere alitaka tupelekwe mahakamani 5.

na alitaka tukae ndani mpaka avunje ASP na TANU afanye CCM.” Mazungumzo na mwandishi, May 5, 1999. Pia kulikuwa na fikra ya “Kuwahamisha mawaziri wa serikali iliyopinduliwa kuwapeleka Dar es Salaam tarehe 28 Juni [1964] inavyosemekana kutokana na ombi la Mfalme Haile Selassie, ambaye angeliwatizama [mawaziri] watakapopelekwa Addis Ababa kabla ya maamuzi kufanywa,” The National Archives, DO 185/60.

Ali Mazrui, “Pan­Africanism and the Intellectuals: Rise, Decline and Revival,” 6. Keynote address for CODESRIA’S 30th Anniversary on the General Theme, “Intellectuals, Nationalism and the Pan­African Ideal,” Grand Finale Conference, December 10–12, 2003, Dakar, Senegal.

Jan P. van Bergen, 7. Development and Religion in Tanzania: Sociological Soundings on Christian Participation in Rural Transformation, 1981, Leiden, the Netherlands, published jointly by The Christian Literature Society, Madras and The Interuniversity Institute for Missiological and Ecumenical Research Department of Missiology, uk. 40.

Ibid., uk. 8. 47.Ibid., uk. 9. 40.Eqbal Ahmad, 10. Confronting Empire: Interviews with David Barsamian, South End

Press, 2000, uk. 2.

Page 388: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla356

Abdul Shakur (Zimbabwe), mawasiliyano kupitiya mtandao wa 11. Zanzinet, 30 Aprili, 2007.

Ibrahim Noor Shariff, mawasiliyano kupitiya mtandao wa 12. Zanzinet, 22 Mei, 2009.Ali A. Mazrui and Michael Tidy, 13. Nationalism and the New States in Africa: From

About 1935 to the Present, London: Heinemann Educational Books, 1984, pp. 224–225.Mohamed Faiq, 14. Abdel Nasir wa a-Thawra Al-Afriqiyya [Abdel Nasser and the African

Revolution), Dar el Mustakbal Al­Arabi, 2002, uk. 14.Abdilahi Nassir, “Kenyan Muslims and the Righting of Historical Injustices: The 15.

Case of Mwambao,” Zentrum Moderner Orient (ZMO). Taasisi ya Utafiti ya Kijerumani, 10 Julai, 2008.

Hotuba ya Rais Mstaafu Mwalimu Julius K. Nyerere kwa waandishi wa habari 16. aliyoitowa Kilimanjaro Hotel (sasa Kempinski), Jumanne, tarehe 14 Machi 1995. Hii ni katika hotuba muhimu sana za Mwalimu Nyerere kwa sababu inazungumziya kuhusu mtikisiko na nyufa muhimu zilizojitokeza katika nyumba ya Tanzania.

Godfrey Mwakikagile, 17. Nyerere and Africa: End of An Era, Protea Publishing, 2005, uk. 5.

Frieder Ludwig, 18. Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994, Brill, 1999, uk. 69.

Kwa mujibu wa Mzee Ally Sykes, Nyerere asingeliweza kufanya kitu chochote 19. Zanzibar bila ya kuwashirikisha wao kwa sababu walikuwa na nguvu Dar es Salaam na katika kukianzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU) na hata kabla ya kuanzishwa TANU. Kaka yake Mzee Ally, marehemu Abdulwahid Sykes aliyaunga mkono mapinduzi ya Zanzibar bila ya kiasi. Mazungumzo kwa njia ya simu na mwandishi, tarehe 18 Aprili, 2009.

Issa G. Shivji, 20. Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union, Mkuki na Nyota Publishers, 2008, uk. 123–124.

R. K. Mwanjisi, 21. Abeid Amani Karume, East African Publishing House, 1967, uk. 55.

Ibid., uk. 22. 58. Bishop E. Sendoro amenukuliwa wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na Shirika la 23.

Organisation of Islamic Conference (OIC) wakati wa utawala wa Dk. Salmin Amour: “Ikiwa Zanzibar itakuwa ni Dola ya Kiislam, itaendelea kuwa sehemu ya Muungano? Bunge la Muungano litakuwa na dhamana yoyote juu ya Zanzibar au lipo kwa ajili ya Tanzania Bara tu?” Frieder Ludwig, p. 213.

Mawasiliyano kwa njia ya barua pepe na “Baba Salim,” 24. 2001.

Mlango wa Kwanza

Hii pia ni katika hotuba muhimu sana ya Mwalimu Julius K. Nyerere aliyoitowa 1. tarehe 5 Novemba 1985 kwa ajili ya kuliaga na kulishukuru Baraza la Wazee wa TANU, Dar es Salaam, kabla ya kustaafu urais wa Tanzania, kwa sababu kwa mara ya kwanza alizungumziya mchango wa wazee wa Kiislam katika harakati za kwanza za kupiganiya uhuru Tanganyika. Kwenye hotuba hiyo Mwalimu kwa mara ya kwanza alizungumziya namna alivyopokelewa Dar es Salaam na wazee wa Kiislam ambao ndiyo waliyokuwa na zile harakati za mwanzo za kupiganyia uhuru Tanganyika. Anaelezeya namna Kasella Bantu alivyomjuulisha na marehemu Abdulwahid Sykes na vipi alikuwa Mkristo peke yake, na mara nyengine na John Rupia, katika mikutano ya wazee wa TANU Dar es Salaam na Bagamoyo. Mwalimu pia amezungumziya kuwa jina la Tanganyika African National Union (TANU) lilibuniwa na akina Abdulwahid Sykes walipokuwa askari Burma katika vita vya

Page 389: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 357

pili vya dunia. Tizama Mohamed Said Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika, Nairobi 2002, Phoenix Publishers.

Ibid., uk. 2. 313–316.Mohamed Said, 3. Uamuzi wa busara wa Tabora, Dar es Salaam 2009, Abantu

Publications, uk. 16.Mohamed Said, 4. 2002, uk. 266.Abdilahi Nassir “Kenyan Muslims and the Righting of Historical Injustices: The Case 5.

of Mwambao.” Muhadhara aliyoutowa kunako Taasisi ya Utafiti ya Kijerumani (Zentrum Moderner Orient), Berlin, tarehe 10 Julai 2008.

Issa bin Nasser Al­Ismaily, 6. Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa, 1999, uk. 94–95. 7. Souvenir of the East African Muslim Welfare Society, uk. 43. Sheikh Ali Muhsin kwa mwandishi, tarehe 8. 8 Machi 1999, Maskati, Oman.National Archives, “National Statement of Policy on Constitutional Reform Prepared 9.

by the Arab Association Zanzibar,” June 1955, uk. 5, CO 822/913. Pia waandishi kama J. M. Gray walionesha uadilifu kuliko akina Sir Reginald Coupland na Ralph A Austen ambao wamechambuliwa vizuri na mwanahistoria mashuhuri kutoka Zanzibar, Profesa Abdul Sherif katika kitabu chake Slaves, Spices and Ivory in Zanzibar.

Abdilahi Nassir “Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki.” Kanda.10. Public Record Office, Outward Telegram from the Secretary of State for the 11.

Colonies, CO 822/825, 16th August, 1956. Ofisa wa serikali ya Kiingereza, W. A. C. Mathieson ameandika kwenye barua yake ya tarehe 8 Januari 1957: “siku za kumchaguwa kwa urahisi Sultan tumtakaye kutoka ukoo wa Kifalme na tukambandikiza juu ya Zanzibar kama tulivyofanya na Sultan wa hivi sasa mwaka 1911, zimekwisha…Nafahamu kuwa Jamshid amekasirishwa sana na sera ya Kiingereza ya Mashariki ya Kati na kitu chochote ambacho Waziri atakachokisema kitasaidiya kumfahamisha kuwa kitendo chetu [cha kuivamiya Masri] hakikushawishiwa na hisiya dhidi ya Waarabu au Uislam.” Kufikiya tarehe 11 Julai 1963, Balozi wa Kiingereza, Zanzibar, Sir George Mooring alitowa utabiri wake juu ya Sultan Jamshid na Ufalme Zanzibar: “Wazalendo watamuunga mkono kwa mujibu wa sera zao za kichama [ZNP]; Afro­Shirazi wanatumiya sera ya ‘kungoja na kutazama,’ kwa matarajiyo kuwa karibuni atawapa silaha zote wanazozihitajiya kuushambuliya ufalme. Ikiwa tabia yake haitobadilika basi kupoteya kwa ufalme ni suala la wakati tu: lakini ikiwa atazitumiya fursa zake vizuri basi ataweza kufanya mengi kuirudishiya hishima serikali ya Sultan.” The National Archives, CO 822/3014. Alilokuwa hakulijuwa au hakulisema Sir George Mooring ni nguvu kutoka nje ndizo khasa zilizokuja kuumaliza, sio ufalme wa Zanzibar tu, bali kuimeza na kuidhibiti kwa muda mrefu baadaye Zanzibar yenyewe kama ni nchi kamili. Baadaye Waingereza walitambuwa kuwa Kambona na Lusinde walikibomowa Kitengo cha Usalama cha Tanganyika na kuwaweka watu wa Kambona kutoka TANU. Pia wanakiri Waingereza kuhusu misukosuko ya Afrika Mashariki ya 1964: “Hapana shaka yoyote kuwa upelelezi wetu wa Kiingereza juu ya hali ilivyo ulikuwa haupo kabisa, na sababu ni kwa makusudi tulijiondowa katika ukusanyaji wa kivitendo wa habari katika Tanganyika.” The National Archives, “Oscar Kambona and the East African crisis,” DO 213/236. Maelezo haya ni dalili kuwa Waingereza walikuwa hawana wasiwasi kabisa na Tanganyika na ndiyo maana hawakujali kabisa kuyadhibiti mapinduzi Zanzibar ingawa walifanya haraka sana kuudhibiti uasi wa jeshi Tanganyika. Lakini hata walipokuja kujuwa kilichotendeka Zanzibar imani yao ilikuwa kumuunga mkono Nyerere moja kwa moja kuimeza Zanzibar na kuwa dhidi ya Sultan mzalendo ambaye alikuwa si yule Sultan kibaraka ambaye Muingereza alizoweya kumchaguwa na kumfinyanga anavyotaka yeye. Kinyume na inavyoaminiwa na wengi, ufalme uliyopinduliwa Zanzibar ulikuwa ni ufalme wenye hisia kali ya kizalendo na haukupendwa na haukupendeza kwa Muingereza na kwa hiyo

Page 390: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla358

hakutaka tena kuuhami kabla na baada ya kupinduliwa. Pia inaonyesha kuwa Waingereza walimpenda sana Nyerere lakini ikiwatiliya shaka baadhi ya mawaziri wake kama Kambona na hata waliamuwa kumuarifu Nyerere awachukuliye hatuwa na awang’owe kutoka kwenye madaraka wale ambao walihusika na kuubomowa utulivu wa ndani wa nchi yake wakati wa uasi wa jeshi la Tanganyika katika Januari 1964, DO 213/236. Sayyid Jamshid akapokelewa Uingereza na baadaye Oscar Kambona akenda uhamishoni Uingereza na wakawa wote wawili wako chini ya macho ya Muingereza.

Kwa mujibu wa Sheikh Ali Muhsin12. , “Tulitaka kutokeya mwanzo tujihusishe na Masri peke yake chini ya Gamal Abdel Nasser kwa sababu tulikuwa na vitu vitatu vya kutuunganisha: Uwarabu, Uislamu na dhidi ya Ubeberu. Hawatotubadilisha kwenye kitu chochote chengine kipya. Masri walikuwa watupe ndege zao za ‘Al­Qahira’ ambazo zilibuniwa na mbunifu wa ndege wa Hitler ambaye alikwenda Masri baada ya kuanguka kwa utawala wa Kinazi. Uwanja wa ndege ulikuwa upanuliwe na Sadat alisema mbele ya Gamal kuwa hatuna ulinzi na pakitokeya kitu chochote ndege zao hazitoweza kutuwa moja kwa moja Zanzibar na itabidi zende Nairobi au Dar es Salaam. Kuhusu hali ya kijeshi Gamal alitwambiya kuwa kutakuwa na mkutano Alexandria, Masri Januari 13, 1964 na baada ya mkutano Mohamed Faiq atakuwa ana nafasi ya kuitembeleya Zanzibar kuja kuzungumza juu ya suala la ulinzi.” Mazungumzo na mwandishi, tarehe 8 Machi, 1999. Kwa mujibu wa ripoti ya “The Tanganyika Mutiny” iliyoandikwa na Balozi wa Kiingereza, Dar es Salaam, F. S. Miles:

Kitu cha kusikitisha ni kimya kizito cha Rais Nyerere kwa siku moja na nusu. Alijikomeya mafichoni pamoja na Makamo wa Rais Kawawa. (Kumbe walikuwapo kwenye kibanda cha Ikulu ya Rais baharini maili sita kutoka mjini na upande wa pili wa kambi ya jeshi la polisi). Tunajuwa kuwa Nyerere alitikiswa sana na muawaji ya Rais Olympia wa Togo, na huenda alihisi katika hali kama ile alikuwa ana jukumu la kuinusuru nafsi yake. Lakini ukweli unabaki kuwa wakati wa msukosuko Baba wa Taifa (kama anavyopenda kujiita) alikimbiya. Mpaka jioni ya tarehe 21 ndipo alipoweza kulihutubiya taifa, na hiyo ilikuwa katika hali dhaifu na sauti iliyofifiya hata watu wengi waliamini kuwa si yeye au alikuwa akizungumza katika hali ya kutishwa. Kabla ya hapo, Kambona alikuwa waziri peke yake ambaye alizungumza kupitiya njia ya redio. Kuingiya Jumanne, rais na mawaziri, ambao wengi wao walijificha siku ya uasi, waliweza kujizowazowa na kuwa na moyo wa kurudi kwenye meza zao. Lakini ile siku ya Jumatatu, mawaziri ambao walikuwa wakifanya kazi walikuwa Kambona, Lusinde na Bhoke Munanka. Kinyume ya mambo, walikuwa wakionekana walikuwa ni wenye misimamo mikali na ni wanachama ambao walikuwa dhidi ya Waingereza…Mwanzo Nyerere alifahamisha kuwa matatizo yaliyopo ni mgomo wa askari. Na akasema kuwa ana silaha moja tu ambayo anaweza kuitumiya kwa askari—silaha ya kisiasa ya kufanya mazungumzo nao. Tulimfahamisha kuwa huu si mgomo bali ni uasi na adhabu yake chini ya Sharia ya Kijeshi ya Tanganyika ni kifo, na kuwa serikali ya Tanganyika itahukumiwa kwa mujibu wa namna itakavyorudisha mapigo dhidi ya uasi na si kwa mujibu wa kutokeya kitendo cha uasi ndani ya ardhi yake. (Nyerere sasa katika matamshi yake ya hadharani anauita uasi). Tulipendekeza kuwa madam wameweza kukipata walichotaka kwa mtutu wa bunduki basi lazima watarudi tena na kutaka zaidi, na serikali haitopata salama; baada ya kuonja madaraka mara moja, mara nyengine askari huenda wakaamuwa kuanzisha udikteta wa kijeshi. Zaidi, nikampa ushauri wa Brigadier Douglas, ambaye, pamoja na maofisa watatu wa kijeshi wa Kiingereza, waliwatoroka waasi na wako wamejificha nyumbani kwangu: na ushauri huu ulikuwa, ikiwa Nyerere ataomba msaada wa majeshi ya Kiingereza,

Page 391: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 359

waasi wataondoka hata bila ya kupigana. Matukio ya baadaye yalihakikisha kuwa [Brigadier Douglas] hakukoseya…Tukakutana na Brigadier Douglas na maofisa wake chumbani kwao. Douglas akasema kuwa lazima apande juu ya meli yenye kubeba ndege H.M.S. Centaur asubuhi ileile ya uasi wa jeshi la Tanganyika, chini ya uongozi wa Kepten O. H. M. St. J. Steiner, R.N. ilikuwa imeshafika pwani ya Tanganyika na majeshi ya makomando 45 na ndege za helikopta. Kambona akakubali kuwa Douglas ambaye ataindesha operesheni pia awe Kamanda wa Tanganyika Rifles, na atakapofika kwenye kambi ya jeshi, Douglas azungumze na waasi na awaombe wasalimu amri. Kambona akaandika ujumbe kwa Kiswahili ili Douglas ausome kupitiya kipaza sauti. Mawasiliyano yalifanywa na H.M.S. Centaur (kwenye chombo cha mawasiliyano Ubalozi wa Marekani), na saa 1:30 asubuhi ya Jumamosi asubuhi, Brigadier Douglas na Major Marciandi, baada ya masaa mawili ya kusubiri ufukweni ambapo tochi ilimurikwa kuwavutiya wapiganaji wa navy ambao walichukuliwa kwa siri kutoka sehemu karibu na bandari na wakapandishwa juu ya chombo chenye kubebeya ndege. Uamuzi wa haraka (ambao sote tulishukuru bila ya kiasi) ulichukuliwa London ili operesheni ifanye kazi. Baada ya usiku mgumu wa kusubiri, H.M.S. Cambria ambayo ilikuwa imefatana na Centaur ikapiga mizinga yake ya 4­in. saa 6:20 za asubuhi na kuuamsha mji wa Dar es Salaam ili kuwatikisa askari waliyoasi. Brigadier Douglas pamoja na makomando walokuwa wakiongozwa na Liutenant­Colonel T. P. Stevens, M.C., wakaruka maili mbili kwa helikopta mpaka kambi ya Colito na wakatuwa ndani ya kambi. Kihoro kikawaingiya askari wa Tanganyika; walikuwa hawana maofisa na hawakujiandaa; na baada ya saa moja kambi ikatekwa. Hakuna askari wa Kiingereza aliyeumiya; ingawa waasi watano walipoteza maisha walipotaka kupigana. Ingawa wengi wao walikimbiya, takriban wote walikamatwa ndani ya saa 24 na viongozi wao wakakamatwa…Bado limebakiya suala lenye kutatanisha kama uasi ulipangwa na Kambona mwenyewe ili aweze kushika madaraka; au pengine hata aliuanzisha lakini baadaye akaogopa na akapigana kuirudisha hali The National Archives, “The Tanganyika Mutiny,” 18th March, 1964, DO 185/47.

Msomaji anafaa afananishe namna ya Muingereza alivyofanya Zanzibar yalipotokeya mapinduzi na alivyofanya Tanganyika ulipotokeya uasi halafu ajiamuliye mwenyewe. Pia inampasa msomaji kuunganisha mchango wa Oscar Kambona katika mapinduzi ya Zanzibar na uasi wa jeshi la Tanganyika na kuhusika kwa vyama vya wafanyakazi katika matukio yote mawaili. Kulikuwa na mahusiyano gani baina ya maofisa waliyoasi, kina Francis Hingo Ilogi, Elisha Kavana, nk, na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambao wameripotiwa wakiingiya na kuzungumza na askari katika kambi ya Colito?

The National Archives, Telegram kutoka Balozi kwa niaba wa Kiingereza Dar es 13. Salaam kuelekeya kwa Commonwealth Relations Office London, LAB13/1958 116923, tarehe 29 Januari, 1964.

The National Archives, British High Commission, Dar es Salaam kwa W. G. 14. Lamarque, Esq., M.B.E., Commonwealth Relations Office, Downing Street, London, S.W.1. DO 213/236, 30 January 1964.

The National Archives, “Oscar Kambona and the East African Crisis,” from T. D. 15. O’Leary to Mr. Costley­White, copies to Mr. Aspin, Mr. Payne (Cork Street) and Mr. Lamarque, DO 213/236.

The National Archives, Inward Telegram to Commonwealth Relations Office from 16. Nairobi, “Zanzibar” CAB 21/5524.

The National Archives, “Zanzibar Revolution” A report by Mr. A. A. E. Forsyth­17.

Page 392: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla360

Thompson, Ex­Permanent Secretary, P.M’s Dept., Zanzibar, DO 185/59 116805, Nairobi, 10th February 1964.

Ibid.18. The National Archives, “Tanganyika and the Liberation of Africa,” from Acting 19.

British High Commissioner in Tanganyika to the Secretary of State for Commonwealth Relations, DO 216/41, tarehe 5 December, 1963.

The National Archives, “Tanganyika—Arms Supplies from Algeria” Headquarters, 20. British Land Forces Kenya, British Forces Post Office 10. From Major General, General Officer Commanding, to the Under Secretary of State, the War Office, London, British High Commission, Nairobi, DO 185/48 116923.

The National Archives, “Tanganyika—Arms Supplies from Algeria.”21. 22. Tanganyika Standard, 9 January 1964. The National Archives “Algerian Arms” DO 23. 185/48 116923The National Archives, “Arms from Algeria” From P. A. Carter to G. J. Price­Jones, 24.

Esq., Commonwealth Relations Office, London. DO 185/48 116923, 4th January, 1964.The National Archives, “Algerian Arms” DO 25. 185/48 116923.

Mlango wa Pili

N. J. Dawood, ed. 1. The Muqaddimah An Introduction to History, Princeton: Princeton University Press, 1981, uk. 14. Kwa mujibu wa Profesa Benjamin W. Fortson, bingwa wa lugha za Kigiriki na Kilatino, fasihi na historia ya masomo ya lugha, Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor:

Mwanzoni Warumi hawakulitumiya neno “Afrika” kwa maana ya bara zima. Neno “Afrika” kwanza lilitumika kuashiriya sehemu ya pwani ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Masri. Sehemu ya eneo hili likaja kuwa ni jimbo la Kirumi baada ya Warumi kuishinda Carthage katika Vita vya Tatu vya Punic (vilimalizika mwaka 146 kabla ya kuzaliwa Kristo). Jimbo hilo lilikuwepo kwenye nchi za leo za Tunisia na Algeria. Ilimu za wataalamu juu ya jimbo ilivyoongezeka, na jimbo ambalo lilijulikana kwa jina la “Afrika” likaongezeka, mpaka mwisho (muda mrefu baada ya nyakati za Warumi kumalizika) likaja kujulikana kwa hili jina ambalo hii leo linatumika kwa bara zima—lakini hata wakati wa Warumi lilikuwa likijulikana kuwa ni zaidi ya jimbo na maeneo yaliyolizunguka ya karibu. (Ilitokeya hivyohivyo na utumiaji wa neno “Asia”, ambalo mwanzoni lilikuwa ni jimbo dogo la Kirumi ambalo liko katika nchi ya leo ya Uturuki). Nina hakika, Scipio Africanus, aliyemshinda Hannibal na Carthaginians katika Vita vya Pili vya Punic (vilimalizika mwaka 202 kabla ya kuzaliwa Kristo), alipewa jina lake la uchokozi (“Africanus”) kutoka jimbo na si kutoka jina la bara zima. Neno “Ifrikiya” (Nafikiriya uandikaji sahihi utakuwa ni “Ifriqiya”) ni kutoka lugha ya Kiarabu na lilikuja baadaye sana; lazima liliazimwa kutoka neno la Kilatini na si kinyume chake. Inawezekana sana neno “Afrika” limetokana na neno “Afri” ingawa hatujuwi walikuwa ni watu gani na jiografiya na ilimu ya makabila ya Warumi haikuwa yenye sifa kubwa. Inawezekana kuwa jina la “Afri” likitumika kwa watu kadhaa waliokuwa wakiishi katika jimbo liloizunguka Carthage. Hakuna maana ya maana ya asili ya neno “Afrika” ingawa kuna madai ambayo (kwa bahati mbaya) hayana ushahidi. Libya ina historia ya zamani zaidi, kwa sababu jina la “Libya” linajitokeza kwenye nyaraka za kale za Kimasri. Walibya walikuwa wanaishi Magharibi ya Mto Nile, na Wagiriki walilichukuwa jina la “Libya” na wakilitumiya kwa kulikusudiya eneo hilo na Afrika ya Kaskazini kwa

Page 393: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 361

ujumla. Majina kama “Afrika” “Libya” na “Ethiopia” yalikuwa yakitumika kwa pamoja kama ni majina ya kijumla ya bara la Afrika (au angalau kwa kile ambacho kilikuwa kikijulikana kuwa ni bara kwa wakati huo ambayo ilikuwa ni sehemu ya Bahari ya Mediterranean na sehemu ya Masri na Nubia). Hii iliendelea kutumika kwa muda fulani katika matumizi ya fasihi ya Kiingereza katika msemo “Chui anaweza kubadilisha madoto yake au Muithiopia rangi yake?” Mawasiliano kwa njia ya barua pepe na Profesa Benjamin Fortson, tarehe 6 Julai 2009.

Ali A. Mazrui “AFRABIA: Africa and the Arabs in the New World Order.” 2. UFAHAMU: The Journal of the African Activist Association XX no. 3. 1992, uk. 53.

Michela Wrong, 3. It’s Our Turn To Eat: The Story of a Kenyan Whistle-Blower. Harper, 2009.

Mawasiliano kwa njia ya barua pepe na Profesa Ibrahim Noor Shariff, tarehe 4. 5 Januari 2008.

Mohamed Said, 5. 2002, uk. 205–206. B. F. Mrina na W. T. Matokke, 6. Mapambano ya Ukombozi Zanzibar, Dar es Salaam:

Tanzania Publishing House, 1980, uk. vi. Ibid., gamba la nyuma la kitabu.7. Ibid., uk. 8. 14. Zanzibar Nationalist Party, 9. Whither Zanzibar? Growth and Policy of Zanzibar

Nationalism, Cairo: Printed by The National Publications House Press, no date, uk. 9. R. K. Mwanjisi. 10. ABEID AMANI KARUME, Nairobi: East African Publishing

House, 1967, uk. 50. Ibid. uk. 11. 7. Afro­Shirazi Party, 12. Jeshi la Wananchi wa Tanzania, 1964–1974. Zanzibar, Printed

by Printpak Tanzania Limited, 1974, uk. 9–10, pia kuna waraka wenye kurasa 11 uitwao “Historia ya Dhiki na Dhuluma Walizotendewa Wazee Wetu Zanzibar Kabla ya Mapinduzi ya tarehe 12­1­1964” ambao ulitolewa na Luteni Kanali M. M. Haji kwa ajili ya Semina ya Jumuiya ya Wazazi, Jimbo la Jan’gombe, mwaka 2004.

“Historic slave trade summit could reopen old wounds.” 13. The East African, September 7, 2009.

Saleh S. I. Al Miskry, 14. 1994, “Pan­Africanism and Nyerere in Tanzania”. PhD Thesis in International Relations, University of Salford, uk. 42.

B. F. Mrina na W. T. Matokke, 15. Mapambano ya Ukombozi Zanzibar. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House, 1980, uk. 51–52.

Mohamed Said, op. cit., 16. 2002, uk. 121. William Edgett Smith. 17. 1981. Nyerere of Tanzania, Harare: Zimbabwe Publishing

House, 1981, uk. 130. The National Archives, “Note of a Meeting between the Commonwealth Secretary 18.

and the President of Tanganyika,” Dar es Salaam, 27th February 1963. DO 121/237. Anaelezeya Sheikh Ali Muhsin: “James Callaghan (baadae akawa Waziri Mkuu 19.

wa Uingereza) wakati alipokuwa ni Waziri Kivuli wa Fedha siku moja alikula chakula cha mchana nyumbani kwangu. Katika mazungumzo alinambia ya kwamba Zanzibar musitarajie hata mara moja kuwa ni dola huru. Mustakbali wake, alisema, uko katika kuunganishwa na Tanganyika. Zanzibar peke yake haiwezi kuishi. Alikuwa mkweli hakuficha dhamiri zao. Wengine, ambao walikuwa wamebobea katika mbinu zao za ufisadi wa kikoloni huona bora wakupe kwa mkono wa kulia kile ambacho wataweza kukunyang’anya kwa mkono wa kushoto. Hivyo ndivyo walivyofanya. Ikiwa Tanganyika mikononi mwao chini ya mtu wao—Nyerere—walikuwa na hakika ya kuendelea hukumu yao. Wakati ule hawakumtambua balaa na ufisadi ambao mtu wao huyo ataufanya. Hawakutambua uwezo wake mkubwa

Page 394: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla362

wa kuvunja kila kile ambacho watu wengine walikijenga kwa taabu na juhudi. Wakati huo ilikuwa bado hajaingia kuivunja ‘Kilimanjaro Cooperative Union’, ‘Bukoba Robusta Coffee Growers’, ‘Sukuma Cotton Growers Cooperative’, ‘Tanganyika Sisal Estate’, zote hizi zilikuwa ndio mishipa ya damu ya uchumi Tanganyika. Pia aliingia kuzivunja serikali za mitaa na mipango yake yote ambayo ilikuwa ikifanyakazi zake uzuri kabisa. Vilevile akaingia kuivunja (East African Common Service Organization), na kwa kumaliza, akaivunja (East African Currency), Sarafu ya Pamoja ya Afrika Mashariki, ambayo ilikuwa inakwenda sambamba thamani yake na pauni ya Kiingereza. Kwa hakika bwana huyu alivunja na kufisidi kila kitu ambacho hao wafadhili wake walikijenga katika miaka sabiini waliotawala na baadae kumkabidhi yeye nchi katika kisahani cha fedha, yaani bila ya kuhangaikia. Hao ndio wakoloni wa Kiingereza na mtu wao Nyerere. Zaidi ya yote haya ilikuwa ni kuivunja Dola ya kale, Zanzibar, nchi ambayo hakuweza hapo awali kuiburura katika Bahari Hindi kama mara nyingi alivyokuwa akisema kuwa hio ndio haja yake kubwa. Hawa ndio wale Mola wetu Mlezi aliotueleza kuwa tusiwafanye kuwa ni wenzetu kutokana na vile vitimbi vyao dhidi yetu: ‘Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.’ ” (Al­‘Imraan: 118. Uk. 229.)

G. Thomas Burgess, 20. Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad, Athens: Ohio University Press, 2009, uk. 190–191.

Afro­Shirazi Party, “Zanzibar and Pemba. Sheria.” Hamna tarehe, uk. 21. 1. Aboud Jumbe, The22. Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30 Turbulent years,

Dar es Salaam: Amana Publishers, 1994, uk. 9–10. Minael­Hosanna O. Mdundo, 23. Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha, Dare es

Salaam University Press, 1996, uk. 132. Hamid Ameir, “Shabaha ya Mapinduzi haijatekelezwa.” 24. Mwananchi, Toleo Maalumu,

Miaka 44 ya Mapinduzi Januari 11, 2008, uk. 13. “Hamis Daruweshi afichua siri ya mapinduzi Zanzibar,” 25. Mwananchi, Septemba 8,

2002, uk.10. Ibid., uk. 26. 11. Ibid., uk. 27. 10. Public Record Office, “Visit of Zanzibar Officials” FO 28. 371/174035. Ibid., pp. 29. 1–2. Minael­Hosanna O. Mdundo, op. cit. 30. Aboud Jumbe, op. cit., uk. 31. 10. Anthony Clayton, 32. The Zanzibar Revolution and Its Aftermath, Hamden, Connecticut:

Archon Books, 1981, uk. 65. Public Record Office, 33. 29 August, 1963, CO822/3126. Public Records Office, “Supplementary to Zanzibar Special Branch Intelligence 34.

Summary for 31st July–28th August, 1963,” CO 822/3063. William Edgett Smith, 35. Nyerere of Tanzania, Harare: Zimbabwe Publishing House,

1981, uk. 125. Aboud Jumbe, op. cit., uk. 36. 11. “Mzee Abbasi,” Dar es Salaam, 37. 2004. Issa G. Shivji,38. Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar

Union, Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers, 2008, uk. 121. Ibid., uk. 39. 123. G. Thomas Burgess, op. cit., uk. 40. 211.

Page 395: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 363

Issa G. Shivji, op. cit., uk. 41. 11. Tarehe 42. 23 mwezi wa Novemba mwaka 1998, Sheikh Ali Muhsin alinielezeya

kuhusu mkutano uliofanyika Tumbatu. Watumbatu walitaka kuonana na yeye peke yake lakini alikwenda na Muhsin Abeid. Walikuwepo kiasi watu 15 na mmoja wao akiitwa “Matambuu” alimuuliza Sheikh Ali. “Waarabu wametupa ahadi gani tukishinda?” Sheikh Ali alikasirika na akawauliza: “Sultan ni nani? Mwarabu. Nani aliwaomba Waarabu waje hapa? Watumbatu. Voti moja mtu mmoja. Waarabu watapata voti mbili kwa mtu mmoja? Nani atakuwa ana voti nyingi zaidi? Waarabu au Watumbatu? Kwa hiyo nani anahitajiya ahadi, Waarabu au Watumbatu?”

Mlango wa Tatu

The National Archives, “Maslahi pekee ya kistratijiya ya Kiingereza juu ya Zanzibar 1. ambayo imeweza kuoneka katika mwezi wa Mei 1957 wakati ‘Mustakbal wa maendeleo ya kikatiba’ ulipoandikwa ni kuwa kuna haja ya kuvinyima visiwa visiingiye ndani ya mikono ya dola adui.” CO 822/2335. Uingereza haikuwa na maslahi ya kiuchumi au ya kibiashara na Zanzibar bali ilikuwa na khofu.

William Edgett Smith, 2. Nyerere of Tanzania, Harare: Zimbabwe Publishing House, 1981, uk. 90.

Ibid., uk. 3. 90.The National Archives, “Note of a meeting between the Commonwealth Secretary 4.

and the President of Tanganyika” The National Archives, 27 February 1963, DO 121/237 116923.

The National Archives, From the Acting British Resident, Zanzibar, to the Secretary 5. for the Colonies. 1 December 1961. CO 822/2731.

E. Harper Johnson. 6. OMAN A Pictorial Resuscitation, Sultanate of Oman: Ministry of Information, 1999, p. 94.

Ibid.7. The National Archives, Telegram from Sir George Mooring to the Secretary for the 8.

Colonies, “Defense Agreement,” CAB 21/5524, 21 November 1963. The National Archives, Commissioner J. M. Sullivan, DO 9. 185/59 116805.The National Archives, Inward telegram from the British Resident, Zanzibar, to the 10.

Secretary of the Colonies, 21st November 1963, CAB 21/5524.The National Archives, Inward telegram from the British Resident, Sir G. Mooring, 11.

to the Secretary of State for the Colonies, 21st November 1963 CAB 21/5524.The National Archives, Outward telegram from the Secretary of State for the 12.

Colonies to British Resident, Sir George Mooring, Zanzibar, 9th December 1963 CAB 21/5524.

The National Archives DO 13. 118/295. Ibid.14. Mazungumzo baina ya Bwana Mohamed Faiq, Mshauri wa Rais Gamal Abdel 15.

Nasser kuhusu mambo ya Afrika, na mwandishi nyumbani kwake Cairo, tarehe 6 Oktoba, 2006.

The National Archives, “Report by Mervyn Vice Smithyman, Permanent Secretary 16. to late Prime Minister of Zanzibar, dictated on Thursday, the 16th January 1961” DO 185/59 116805, uk. 1.

Ibid. uk. 17. 1.Ibid. uk. 18. 1.

Page 396: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla364

The National Archives, “Zanzibar Revolution: A Report by A. A. E. Forsyth­19. Thompson, Ex­Permanent Secretary, PM’s Dept., Zanzibar,” 10th February 1964, 185/59 116805, uk. 2.

Ibid. uk. 20. 2. Ibid. uk. 21. 8.The National Archives, “Notes made by the late Commissioner of Police, Zanzibar 22.

­ J. M. Sullivan,” 17th January 1964, DO 185/59 116805. uk. 3. Ibid. uk. 23. 4. William Edgett Smith, op. cit., uk. 24. 126. Piero Gleijeses. 25. Conflicting Missions Havana, Washington, and Africa, 1959–1976,

University of North Carolina Press, 2002, uk. 59–60. A. M. Babu 26. African Socialism or Socialist Africa (London: Zed Press), uk. 121.

Marehemu Ali Nabwa alimuambiya mwandishi wa kitabu hichi katika siku za mwisho wa uhai wake pale kwake Kisiwandui, Zanzibar, kuwa walipokuwa gerezani Dar es Salaam alimuomba Babu aandike kitabu kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na akakubali lakini badala yake akaandika African Socialism or Socialist Africa. Hata kwenye mpango wa maandishi ya kumbukumbu ya maisha yake, Babu alitaja tu kuwa “tarehe 12 Januari 1961, kulitokeya Mapinduzi Zanzibar ambayo yalisababisha nichaguliwe Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Biashara wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.” Tizama “Memoirs: An Outline” ndani ya kitabu Babu I saw the Future and It Works: Essays Celebrating the Life of Comrade Abdulrahman Mohamed Babu 1924–1996, kilichohaririwa na marehemu Profesa Haroub Othman. Pia inasemekana kuwa Babu aliwahi kualikwa ende Harare, Zimbabwe kwa madhumuni ya kuandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar. Aliwekewa vitendeya kazi ili kufanikisha uandikaji lakini hakuwahi kwenda na akafariki dunia.

Thomas Burgess. 27. Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad, Athens: Ohio University Press, 2009, uk. 81.

Mlango wa Nne

“Baada ya uchaguzi wa 1. 1957 joto la kisiasa lilipanda kwa kasi kubwa na matokeo yake ni kufungwa kwa kugomewa maduka mengi sana ya Waarabu na kufukuzwa kwa wakulima wa Kiafrika kutoka mashamba yenye kumilikiwa na Waarabu, kuyagomea mabasi yenye kumilikiwa na memba wa vyama vyenye kupingana, na wafanyakazi wa chama cha Zanzibar Nationalist kuwaondowa wafanya kazi wa zamani wa gatini ambao ni memba wa Afro­Shirazi.” Report of a Commission of Inquiry into Disturbances in Zanzibar during June 1961, London: Her Majesty’s Stationary, 1961, uk. . 2–3. Ripoti hiyo hiyo imesajili kuwa “Katika ghasia za Juni na baina ya tarehe 1–8 waliuliwa Waafrika 3, Waarabu 64, na mtu mmoja asiyejulikana kabila yake. Majeruhi waliotibiwa hospitali walikuwa Waafrika 144, Waarabu 137, na wengineo 9. Waliojeruhiwa na kulazwa hospitali walikuwa Waafrika 39, Waarabu 51, na mwengine mmoja asiyejulikana kabila yake,” uk. 12.

“Ghasia za Juni hazikuwa kabisa matokeo ya mpango wa makusudi wa mtu mmoja au 2. kikundi cha watu, au chama cha kisiasa.” Report of a Commission of Inquiry into Disturbances in Zanzibar during June 1961, London: Her Majesty’s Stationary, 1961, uk. 26.

Kwa mujibu wa kitabu cha Helen­Louise Hunter wa shirika la ujasusi la CIA: 3. “Imeripotiwa kuwa viongozi wa TANU wameipa pesa na ushauri ASP kwa ajili ya uchaguzi. Makundi ya watu yalipelekwa [Zanzibar] kwa ngarawa kutoka Tanganyika kushiriki katika ghasia za uchaguzi [wa 1961]” Zanzibar: The Hundred Days’ Revolution, 2010, uk. 19.

Page 397: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 365

Suala muhimu ambalo Mzee Issa Kibwana alilizungumza kuwa wengi wao walioshiriki 4. katika ghasia na mauwaji ya Juni 1961 kwamba wana afadhali, wanaomba Mwenye­enzi Mungu awaletee mauti kuliko hili suala kuja kutolewa na wataalamu. Maana yake wengi wao wanaona kuwa lilikuwa ni kosa kubwa sana, dhulma, na aibu kubwa. Kwa hiyo wote kwa ujumla ni kama watu walokuwa wamechukuwa kiapo na yoyote yule aliyeonekana kalizungumza hili suala, si muda mrefu baada ya kulizungumza, walijihisi hawako sawasawa na wengine hata kuonekana kwamba ilikuwa ni sababu ya mauti yao. Sasa kwa hivo liliamuliwa hili suala kabisa, bora wafe wote na hili suala lenyewe life kuliko kuzungumzwa kutokana na aibu kubwa ambalo suala hilo limewaachia watu ambao walishiriki katika mauwaji ya Juni 1961. Pia alisema Mzee Issa kuwa ule haukuwa wakati munasib wa kufanya suala lile, labda hakukuwa na sababu ya kufanya suala lile, lakini mauwaji yalifanyika, roho za watu nyingi zilipoteya, na ilikuwa ni dhulma. Lilikuwa ni kosa kubwa, dhulma, na suala la aibu kwa Zanzibar.

Ripoti ya Waingereza 5. Report of a Commission of Inquiry into Disturbances in Zanzibar during June 1961 iliochunguza ghasia na mauwaji ya Juni inawataja Wazanzibari asilia na Wamakonde kutoka Msumbiji na Tanganyika ambao walifanya fujo na kuuwa sehemu za Chwaka, Bambi, Tunguu, Kazole, na Ndagaa. Hakukuwa na haja ya kuuchunguza undani wa ghasia na mauwaji kwa sababu ripoti ya Waingereza imekhitimisha kuwa tukio la Juni 1961 lilikuwa tukio liliojichomoza wenyewe na halikupangwa na kiongozi, viongozi au chama cha kisiasa.

“Bwana M. V. Smithyman, O.B.E. ametowa maelezo ambayo tunayakubali, kuwa 6. hisia ya uungaji mkono wa Waafrika, khasa wale walioko sehemu za mashamba, kwa Mtukufu Sultani, inawezekena ikawa ina nguvu zaidi Zanzibar kuliko kivutio cha msemo wa ‘Afrika ni ya Waafrika’ ambao kiwakati si wa zamani sana. Kwa kuwa ukweli uko hivyo, tunafikiri kuwa asilimia 70 ya voti zilizokipigia kura chama cha Zanzibar Nationalist Party lazima zilikuwa za Waafrika. Fikra ya utiifu kwa Mtukufu Sultani ni ya muda mrefu sana, na tunahisi kuwa inaelekea kuamini kuwa utumiaji wa Zanzibar Nationalist Party wa fikra kuwa chao ni chama tiifu ndio sababu iliowavutia wapiga kura wa Kiafrika.” Report of a Commission of Inquiry into Disturbances in Zanzibar during June 1961, London: Her Majesty’s Stationary, 1961, uk. 15.

Mlango wa Tano

Hapa inafaa kuzingatia kuwa Mzee Mkwawa alihusika kuwapeleka watu Zanzibar 1. kutoka Tanganyika wakati wa chaguzi za kabla ya mapinduzi ya 1964 na kwa hiyo kwenda kwake Kijangwani kulikuwa kwa ajili ya kuwasilisha lengo hilo. Ulipofika wakati wa kuwapeleka wafanyakazi kutoka mashamba ya mkonge na wa bandari ya Dar es Salaam, nk, siasa za mivutano ndani ya ASP zilikuwa kali na uongozi wa chama uligawika baina ya makundi ya Mzee Karume na makhasimu wake waliokuwa wameshajipanga kuuchukuwa uongozi kutoka kwake. Kabla ya uchaguzi mkuu wa Julai 1963 uongozi wa ASP ulifanya kikao kizito kwanza pale iliopo leo Karume House (ikiitwa “Khalifa Hall” kabla ya mapinduzi) na baada ya muda wa kikao kwisha na kwa kuwa hawakuwa na pesa za kuendelea kuilipia sehemu ya kufanyia mkutano, jioni yake kikao kikahamia Miembeni kwenye jengo la YASU. Suala la mkutano lilikuwa ni nani atakayeiongoza serikali ikiwa ASP itashinda uchaguzi na nani atakayeiongoza kambi ya upinzani ikiwa ASP itashindwa? Jawabu iliotakiwa na makhasimu wa Mzee Karume ilikuwa apatikane kiongozi mwengine kwa sababu yeye hakusoma. Mwenzake (jina nimelihifadhi) marehemu Balozi Ahmed Diria Hassan alijibu kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa siasa za Commonwealth kiongozi

Page 398: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla366

mkuu wa chama ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa serikali ikiwa chama chake kimeshinda na huwa kiongozi wa upinzani ikiwa chama chake kimeshindwa.

Huu ni mrengo wa kisiasa na wa kidini ambao unarudi nyuma kwenye zile fikra 2. ziliomo ndani ya barua iliyomo kunako kitabu cha Mrina na Matoke Mapambano ya Ukombozi Zanzibar iliyoandikwa na memba wa Kikristo wa Jumuiya ya Waafrika ya tarehe 9 Julai, 1949, waliyompelekea Balozi mtawala wa Kiingereza, Zanzibar, kupinga uteuzi wa Sheikh Ameir Tajo kuwawakilisha Wazanzibari katika Baraza la Kutunga Sheria. Mzizi wa udini na wa kikoloni uliojificha ndiwo wenye kutamka kuwa Washirazi wa Zanzibar si Waafrika, au Wazanzibari wenye mizizi mirefu Zanzibar si Waafrika, unatokana na tafsiri kuwa mwenye haki ya utawala kwenye Bara la Afrika ni Mwafrika mweusi ambaye pia ni Mkristo. Waislamu wengi wametumbukia kunako mtego huu wa ukoloni uliovaa kizoro cha udini uliojificha bila ya kuitambuwa nia na makusudio ya tafsiri ya mrengo wenye kutamka hadharani au kwa siri kuwa Wazanzibari si Waafrika au hakuna watu wenye sifa za kuitwa Waswahili. Jawabu inapokuja kuwa Wazanzibari si Waafrika au hakuna watu wenye kuitwa Waswahili basi hupatikana mwanya wa kutowa uhalali wa kuwabaguwa na kuwapora haki zao. Tizama hoja ya kitabu cha Alamin M. Mazrui na Ibrahim Noor Shariff THE SWAHILI: Idiom and Identity of an African People, Africa World Press, 1994.

Kwa mujibu wa mwandishi Mohamed Said kwenye kitabu chake 3. Uamuzi wa Busara wa Tabora chama cha United Tanganyika (UTP) kiliundwa na Wazungu mwaka 1955 kwa lengo la kujaribu kuivunja nguvu TANU. Baada ya kushindwa walivunja chama na jengo lake lilokuwepo barabara ya kumi na nne likawa tawi la TANU la Tanga mjini.

Zifuatazo ni mchanganyiko wa dondoo muhimu kutoka “Moments and Processes: 4. Redefining the Building of ‘A New Society’ in Tanzania,” risala ya shahada ya udaktari, PhD, Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Baltimore, Maryland, June 2000: “Mwaka wa 1936 shamba la mkonge la Sakura lilokuwa likimilikiwa na kampuni ya Kijerumani iitwayo Sakura Estates Ltd iliomba kuitenga sehemu ya ukubwa wa ekari moja ambayo inaitwa Kipumbwi. Wenyeji 10 wenye kumiliki minazi 59 walikuwa wanaishi kwenye ardhi hiyo. Wakaazi [wa Kipumbwi] walikubali kutengwa kwa sehemu hiyo kwa misingi ya kuwa ardhi itakodishwa na haitouzwa na muda wa kuikodisha hautopindukia miaka 33. Mwaka wa 1951 kampuni ya Amboni ilipewa mkataba wa miaka 99,” uk. 495.

Sababu ya [wafanyaji kazi wa mashamba ya mkonge] kuitwa “Manamba” ni walikuwa wakiajiriwa wakati mmoja na pahala pamoja kigengi cha watu 5–20 na wakipewa mkataba mmoja wenye namba moja. “Manamba” ikaja kuondolewa na mfumo mwengine wa “Wakalenda” ukaanzishwa katika mwaka 1963. Katika mwaka 1963/64 kima cha uzalishaji mkonge kilifika tani 230,000 ambazo zilikuwa sawa na asilimia 37 ya uzalishaji wa mkonge duniani. Jambo la kushangaza ni shirika la Amboni la mkonge halikutaifishwa wakati wa kutaifisha mali Tanzania. Sababu zinazotolewa za kutotaifishwa ni kuwa kampuni ilisajiliwa Switzerland na ikipepea bendera ya Switzerland, na kuwa Mwalimu Nyerere alitaka Amboni itoe muongozo na mfano mzuri wa kampuni za kibinafsi zilizofaulu, na kuwa Amboni ilikuwa na mahusiano mazuri na Serikali na ilikuwa ni vizuri kwa sote kuendelea na shughuli zetu. Kambi za wafanyakazi wa mkonge zikiitwa SILABU (Sisal Labor Bureau). Mara wanaotaka kuajiriwa kwenye mashamba ya mkonge wanapofika SILABU walikuwa wakipokelewa kwa njia isio na adabu na safari yao kuelekea pwani kwenye mashamba ya mkonge ilikuwa yenye kutia kihoro na kuchukia kuhama makwao. Mwaka 1993 Sabea alionana na Don, ofisa wa Kitanzania katika Ofisi ya Benki ya Dunia, Dar es Salaam na Don alitamka kuwa suala la kufufua ufanyaji kazi katika mashamba ya mkonge ni suala la: “Hadhi. Manamba ni aibu ya kijamii. Ni ukoloni. Wakataji mkonge ni manamba. Wana tabaka na utamaduni wao wenyewe. Kazi

Page 399: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 367

yao inategemea umahiri maalum lakini pia ni kundi la watu wahuni (immoral lot). Maisha utawakuta wamelewa na wako karibu na malaya. Ni watu ambao wanaelea, wakuja na wa kwenda. Ni wageni, hawana mizizi, na ni watu wasiokuwa na adabu.” Meneja mmoja wa shamba la mkonge alohojiwa na Sabea mwaka 1995 anasema: “Kuwa Manamba maana yake ni kuwa mbali, mwituni, mbali na njia kuu, mbali na watu na mbali na ilimu. Kutokujuwa mengi ni hatua ya mwanzo ya kuwadhibiti wafanyaji kazi [wa mkonge]. Kila wafanyaji kazi wakiwa wametengwa inakuwa ni rahisi kuwadhibiti.” “Mapanga ya wafanyaji kazi katika mashamba ya mkonge lazima yawe makali sana na ukataji lazima uchukuwe angle maalum ili decortication ifanyike bila ya matatizo.” [Suala la umahiri wa matumizi maaulum ya ukataji mkonge kwa mapanga linaweza kutumika katika ilimu ya uchunguzi ya forensic science na kufananisha alama za mabaki ya ukataji wa mifupa ya watu waliouliwa katika mapinduzi na ukataji wa mkonge. Mashamba ya mkonge yalikuwa tisa kwa jumla. Tanga kulikuwa na Amboni, Pongwe, na Kigombe. Pangani kulikuwa na Kilimwangwido, Mwera, Sakura, Kwamdulu (njia ya Muheza­Arusha), Kwaraguru (magharibi ya Kilimangwido), Magrotto (baina ya Kwamdulu na shamba la Pongwe, njia ya Tanga­Arusha)]. Anaendelea Sabea: “Muhimu zaidi, ilikuwa uhusiano baina ya harakati za umoja wa wafanyakazi uliokuwa ukiwakilishwa na Chama Cha Wafanyakazi (Tanganyika Federation of Labor), TANU (Tanganyika African National Union) na wafanyakazi wa mashamba ya mkonge. Kama Friedland, W. anavyoonyesha katika kitabu chake Vuta Kamba: The Development of Trade Unions in Tanganyika, Stanford: Hoover Institution Press, 1969, kazi ya Plantations Workers Union ilikuwa ni muhimu katika kusambaza matawi ya TANU katika maeneo ya mashamba [ya mkonge].”

Kwa mujibu wa mwandishi Sheikh Issa bin Nasser Al­Ismaily: “mimi sikupata 5. kuisikia la kutoka kwa mwenyewe Sheikh Mohamed Shamte au hata Sheikh Ali Muhsin au Sheikh Rashid Hamadi ambao wote nilikuwa nao karibu. Kwa kadri ninavyomjua Sheikh Mohamed, adabu zake, hishma zake na upole wake, sidhani kama angeliweza kutamka utovu wa adabu kama huo,” Maskati, 2007.

Inasemekana kuwa marehemu bwana Mohamed Shamte alipata kutoa hotuba 6. ambayo ndani yake alipinga aina zote za ukoloni, ukoloni wa mtu mweupe na ukoloni wa mtu mweusi. Shamte alitambuwa kuwa hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ana nia ya kuimeza Zanzibar na ndiyo maana hakutaka kushirikiana na viongozi wa ASP waliokuwa tayari kushirikiana na Mwalimu katika kulifanikisha lengo lake.

Kwanza ilianguka kambi ya jeshi la polisi la Ziwani na waliotoka Ziwani walikwenda 7. kambi ya Mtoni ambako kikosi cha jeshi la polisi wa Kizanzibari, Police Mobile Force (PMF) kilipigana kabla ya kuzidiwa nguvu kwa kukosa uongozi na msaada.

Hii fikra kuwa Waunguja hawawezi kitu imekuwa ikipewa tafsiri tafauti kwa 8. kutegemea kitu gani kinazungumzwa na nani anazungumza. Kwa mfano, inasemekana kuwa kiongozi wa chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP), marehemu Sheikh Ali Muhsin aliamini kuwa kwa mujibu wa tabia na silka za Wazanzibari ni vigumu au hata tuseme haiwezekani Mzanzibari kumuuwa Mzanzibari mwenzake kirahisi. Viongozi wakubwa wa chama cha ZNP (Hizbu) walikuwa ni Wazanzibari kindakindaki, kwa mfano, marehemu Sheikh Vuai Kitoweo ni mtu wa Jambiani na alikuwa Rais wa Chama cha ZNP kutokeya mwaka 1955–1964. Sheikh Haji Hussein kwao Mbuzini na baba yake, Sheikh Hussein “Lemba” alikuwa mkubwa wa Tariqa ya Kisufi na alisoma kwa Sheikh Muhsin bin Ali, baba yake Sheikh Ali Muhsin. Maalim Zaidi Mbaruk alikuwa Makamo Rais wa ZNP baada ya kufa Sheikh Miraji Shaalab. Mzee Haji Hussein na Miraj Shaalab hawakuwemo kwenye kundi la wazee wa Kiembe Samaki kama alivyodai Abdulrahman Babu katika

Page 400: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla368

maandishi yake. Wazee wote hawa ni Wazanzibari wa toka ntoke na ni sehemu ya jamii ambayo haina sifa ya kupigana. Jambo kubwa kwa jamii ya Kizanzibari ya miaka hiyo ilikuwa kuvunjiana hishma barazani. Utafiti wa ripoti na rikodi za polisi za Zanzibar na za mahkama ndiyo pekee zenye uwezo wa kuthibitisha aina ya mauwaji Zanzibar kabla ya kuingiya mauwaji makubwa yaliyosababishwa na khasama za kisiasa. Mzee wangu mmoja kutoka Tanganyika amenielezea kuwa zamani ilikuwa si rahisi kwa Mzanzibari kuuwa au kuiba lakini hivi sasa anauwa na anaiba. Ni khulka njema kuwa si rahisi kwa binaadamu kumuuwa binaadamu mwenzake ingawa kwa upande mwengine mwenye kutaka kumuuwa Mzanzibari au Wazanzibari huwa anafahamu kuwa Mzanzibari anaweza kudhulumiwa na kutokana na tabia yake hatoweza kufanya kitu. Saikolojia ya mwanaadamu huwa inabadilika kwa mujibu wa mazingira na mafundisho anayoyapata na si jambo la kuzaliwa peke yake au la kudumu. Wazanzibari walipopata mafunzo ya kuuwana na kutesana walifanya hivyo na wako walioweza kuuwa bila ya wasiwasi wowote ingawa jamii ya Kizanzibari kwa ujumla si yenye sifa ya kuwa ni jamii ya kivita. Albert Einstien alimuuliza Sigmund Freud katika mawasiliano yao ya mwaka 1932: “Inakuwaje hichi kikundi kidogo cha watu kikenda kinyume na matakwa ya walio wengi, ambao ndiwo wenye kukhasirika na kuumizwa na vita ambavyo vinautumikia ubinafsi wa kikundi kidogo?” (Tizama “Violence and Human Nature” iliyoandikwa na Howard Zinn kwenye kitabu chake Declarations of Independence Cross-Examing American Ideology, Harper Perennial, 1990). Fikra ya kuwa Waunguja, au Wazanzibari, hawawezi kitu inatokana na historia yao kupotoshwa na kuwaweka kizani. Nguvu ya Zanzibar imo kwenye kummeza kila ajae Zanzibar na kumfanya awe Mzanzibari. Ni nguvu laini (soft power) ya watu wenye asili zenye kutoka sehemu zote za dunia ambayo inasubiri maendeleo ya kiilimu na kiuchumi kwa Wazanzibari walio wengi ambayo, ukiondowa upotoshaji wa historia, ndiyo peke yake yenye uwezo wa kuzizima siasa za chuki na fitina. Uraia wa Zanzibar ukiwa na nguvu basi itakuwa ni rahisi piya kuzisheherekeya tamaduni, asili, na dini zote za Zanzibar na bila ya kuipa nguvu jamii moja kuliko nyengine.

Hanan Hosni Sabea ambaye tumeshamtaja, ametuarifu kwa kulikuwa na mashamba 9. tisa ya mkonge. Mashamba ya Amboni, Pongwe na Kigombe yalikuwepo Tanga na mashamba ya Kilimagwido, Mwera, Sakura, Kwandulu (njia ya Muheza­Arusha), Kwaraguru (magharibi ya Kilimangwido), na Magrotto (baina ya mashamba ya Kwamdulu na Pongwe, njia ya Tanga­Arusha) yalikuwepo Pangani. Kwa mujibu wa Sabea katika mwaka 1995 daftari la wafanyakazi wa mashamba 4 ya Amboni yameonyesha kuwepo makabila 67 tafauti wakati makabila ya Tanzania yalikuwa 123. “Kila kambi ya wafanyaji kazi ilikuwa na jina maalumu na wakikaa makundi ya kikabila tafauti; kulikuwa na kambi ya Warundi, kambi ya Wamakonde, nk.,” uk. 609.

Alikuwa mwanasiasa Idara ya Urithi na alikuwemo katika kikundi cha tano (kati ya 10. vikundi tisa) kilichokamatwa mwisho wa mwaka 1967 na kuuwawa. Wengine waliokuwemo kwenye kikundi cha Juma Maulidi Juma ambao wametajwa kwenye kitabu kilichoandikwa chini ya uwenyekiti wa Kanali Seif Bakari Omari, ni pamoja na Jaha Ubwa Jaha, Msaidizi wa Katibu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Mdungi Usi Mcha, Karani Mkuu wa Municipal, Khamis Masoud Khamis, Idara ya Hazina, Abdul­Aziz Khamis Twala, Waziri wa Fedha, Aboud Nadhif, Katibu wa Biashara na Viwanda, Saleh Saadalla Akida, Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme, na Abdalla Kassim Hanga, Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar baada ya mapinduzi na baadae Makamo wa Rais na Waziri wa Muungano. “Madhumuni ya kikundi hichi ilikuwa ni kufanya mapinduzi kwa kutumia njia ya kuharibu siasa ya chama ili kudhoofisha uchumi, maana wote hao walikuwa watu wenye madaraka katika Serikali.” Jeshi la Wananchi wa Tanzania 1964–1974 Zanzibar, uk. 30.

Fitina zilizoelekezwa dhidi ya Zanzibar juu ya suala zima la biashara ya utumwa ndio 11. kiini cha chuki na mifarakano isiokwisha. Sheikh Ali Muhsin walipokuwa wanaupiganiya

Page 401: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 369

uhuru wa Zanzibar hawakuutathmini vya kutosha ukweli na uwongo wa muda mrefu sana kuhusu suala zima la utumwa. Suala la vitendo viovu walivyokuwa wakifanyiwa watumwa Zanzibar si suala ambalo wenye kuliamini wanalidaiya hoja ya ushahidi. Mbali ya hivyo, suala zima la utumwa ambalo ukifanywa Tanganyika na kwengineko Afrika Mashariki na Kati halijafanyiwa utafiti wa midani ambao utawahusisha wote waliyohusika na biashara ovu ya utumwa badala ya kuwafanya Waafrika Waislam na wasiokuwa Waislam “wawe na chuki kubwa mioyoni mwao” dhidi ya Waarabu ambao wengi wao ni Waislam. Kila taifa limepewa mtihani na mtihani wa Zanzibar ni fitina ya utumwa. Wazanzibari ambao wengi wao ni Waislam na Wazanzibari ambao ni Wakristo wanaishi maisha yao ya kila siku nje na ndani ya misikiti na makanisa ndani ya mtego wa fitina ya utumwa ambayo mamishionari wa Kizungu wameipeleka Afrika sumu yao dhidi ya Uislam ili kuhakikisha kuwa hakutakuwa na maelewano baina ya Waislam na waumini wa dini ya Kikristo. Kwa ufafanuzi zaidi pitia makala ya “Slavers and Saviours: Images of Arabs and Englishmen in Uhuru wa Watumwa,” Bashiru: Journal of African Languages and Literature, Vol. 13, No. 1, Spring 1987 na khasa kitabu kilichoandikwa na Minou Reeves Muhammad in Europe: A Thousand Years of Western Myth-making, New York University Press, 2000.

Fikra ya Tanganyika kwenda kuivamia Zanzibar na khofu ya matokeo ya uvunjaji 12. sheria ya kimataifa ya nchi moja kuivamiya ya pili inajitokeza waziwazi.

Kwa mujibu wa Sabea, wazee ambao walikuwa wafanyakazi wa mashamba ya 13. mkonge ya Tanga ambao hawakurudi makwao wanaishi Majengo Destitute Camp [Kambi ya Mjengo ya Mafukara] ambayo iko kilomita 10 nje ya mji wa Tanga.

Anaelezeya mwandishi Mohamed Said: “Kwa kiasi cha siku mbili Nyerere alikuwa 14. hafahamiki yuko wapi. Wanajeshi walikuwa wakiwasiliana na Oscar Kambona kujaribu kutatua mgogoro uliokuwepo. Dossa Aziz ndiye aliyemtorosha Nyerere kutoka Ikulu akapita nae lango kuu Nyerere akiwa amejificha katika gari la taka chini ya takataka. Dossa akiwa na bunduki yake alienda na Nyerere hadi Kigamboni kwenye nyumba iliyokuwa ufukweni pwani ambayo ilikuwa ikitumiwa na Gavana kama mahali pa kupumzika. Baadae Rashid Kawawa aliyekuwa makamu wa rais alikwenda pale na wakawa pamoja na Kambona ambae alikuwa kiungo kati ya serikali na wanajeshi walioasi. Nyerere mwenyewe hajakieleza kisa hiki kwa yoyote. Baada ya kujitokeza waandishi wa habari walimuuliza alikuwa wapi wakati wote wa uasi wa wanajeshi. Nyerere kwa ukweli kabisa alijibu, ‘Nilikuwa Dar es Salaam’.” Kutoka Mohamed Said Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002, uk. 307.

Shaaban Mloo na Ali Haji Pandu ni kati ya viongozi saba waliofukuzwa kutoka 15. chama cha CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, mkutano wa tatu uliofanyika Dodoma tarehe 11–13 Mei 1988. Shaaban Mloo alituhumiwa kuwa “Ni miongoni mwa Viongozi ambao kwa kauli na vitendo vyao wanaendesha uchochezi na vurugu dhidi ya Chama na Muungano, hivyo amechangia katika kuchafua hali ya kisiasa Zanzibar.” Ali Haji Pandu alituhumiwa kuwa “Amehusika na usambazaji wa maneno ya uchochezi dhidi ya Chama na Muungano.” Juma Ngwali alyekuwa mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa alionekana kuwa ni mmoja aliyekuwa akishirikiyana na watu saba waliofukuzwa kutoka CCM. Juma Ngwali, Shaaban Mloo, Machano Khamis Ali na Ali Haji Pandu ni viongozi wa ngazi za juu wa Civic United Front, CUF. Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Tatu Uliofanyika Dodoma tarehe 11–13 Mei 1988.

Maadili ya Nuremberg yalio washitaki na kuwahukumu viongozi wa ngazi za juu wa 16. serikali ya Kinazi ya Adolf Hitler kwa kuzivamia nchi nyengine na kusababisha mauwaji ya halaiki, yaliingizwa katika hati ya Umoja wa Mataifa na kipengele muhimu ni kile chenye kusema kuwa “Uvamizi ndiyo kilele cha jinai la kimataifa kwa sababu unakusanya

Page 402: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla370

maovu yote yaliofuatiliya.” Ingawa Zanzibar haijapata kuidhuru nchi nyingine na daima imedhuriwa, serikali zote kuanzia 1964 zilikabiliwa na hatari ya kumezwa na/au kuweza kuvamiwa wakati wowote ule kutoka Tanganyika.

Ripoti ya shirika la ujajusi la Kimarekani (CIA) inaielezeya kuwa “Kukosekana 17. kwa shura juu ya tabia ya Nyerere kunatokana kwa kiasi kikubwa na mbinu anazozitumia. Anapendelea kujiepusha na vikao visivyofurahisha au migongano ya aina yoyote ile, na mara nyingi hupenda kuwaambiya wasikilizaji wake yale wanayopenda kuyasikia; akibanwa atowe maelezo, humalizikia kutowa kauli zenye nusu ya ukweli au kukwepa.” Central Intelligence Agency Office of National Estimates, Special Memorandum No. 17­65, “A Reassessment of Julius Nyerere,” 10 June 1965. Lyndon Baines Johnson Library.

Kauli ya tatu yenye kuthibitisha khofu na wasiwasi wa kupeleka vita ndani ya nchi 18. ya watu.

Kwa mujibu wa Mzee Ali Yusuf, “Tumeshatubu na tunaona haya na ndiyo hatutaki 19. kuzungumza kuhusu mapinduzi. Mauwaji yalikuwa makubwa na hakuna cha kujivunia. Hatukuingia mabomani lakini tulijuwa wiki moja kabla kuwa mapinduzi yatafanyika. Babu hakuwa mastermind (mpangaji mkuu) wa mapinduzi kwa sababu mapinduzi hayafanywi na mtu mmoja. Alitowa mchango mkubwa wa kifikra na namna ya kuyafanikisha. Siwezi kukwambiya alichangia kwenye kesi gani lakini alichangia. Pistols zilitoka Somalia na Badawi alikwenda zichukuwa. Bastola yangu ilitoka Cuba na sijuwi chochote kuhusu Ben Bella na mapinduzi ya Zanzibar. Tulokuwa pamoja ni Sharifu [Badawi?], Ali Mahfudhi, Babu, Dugheshi, na mimi mwenyewe. Babu hakufaulu kwa sababu alikuwa hana mass support [hakuungwa mkono na umma], sumu dhidi yake na wafuasi wake ilikuwa kubwa, muda ulikuwa mdogo sana, hakukuwa na vyombo vya kujibu. Makomred walionekana watu si wazuri. Ilibidi watu waufahamu na waukubali Ukoministi kwanza lakini ilikuwa tabu kwa sababu watu wa Zanzibar wanafuata dini zaidi kuliko siasa. Hapo ndipo alipofeli Babu. Wanataka kuonyesha kuwa mapinduzi yalikuwa ya Waswahili. Wakitukubali itabidi wawakubali Waarabu, Wangazija, nk. Sisi si wapumbavu kushindana nao. Wache wajisifu na watutowe. Bora kwetu.” Mazungumzo na mwandishi, Zanzibar, tarehe 10 Juni, 2006.

Mlango wa Sita

Haliwezi kufa mpaka Wazanzibari na Watanganyika watakapoliyayusha na kuliaga 1. barafu la huzuni isiyokwisha kwa kuundowa ujinga waliyogubikwa nao kwa makusudi ili wenye khofu zao wapate kujilinda na waliowatiya kwenye ujinga wa makusudi wapate ilimu itakayowaondoleya asili ya shari wasiyoifahamu na chimbuko la kila madhara kwa jamii na taifa la Zanzibar na la Tanganyika.

Muhimu na kubwa zaidi kuliko uongozi unaoangaliya maslahi ya kisiasa na ubinafsi 2. ni kuuzingatiya mustakbal wa Zanzibar na wa Tanganyika wenye kuufahamu ukweli wa historia zake ili nchi mbili hizi zipate kuujenga msingi mpya wa masikilizano na mashirikiyano. Tatizo kubwa katika historia ya Zanzibar ni kuchomoza kwa vitambakwiri vinavyoungwa mkono kwa hali na mali na makundi maalumu kutoka Tanganyika au kwengineko na kujijengeya kundi la wahafidhina ili kuwapiganiya waingiye Ikulu. Hili la viongozi machachari wenye lengo la kuukamata uongozi wa Zanzibar bila ya kuungwa mkono na Wazanzibari walio wengi limeonekana Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi. Tafauti ndani ya tabia hii ya viongozi wa Kizanzibari iko katika kuungozwa na ideolojiya, uroho au ulafi, badala ya kukidhi haja na matakwa ya Wazanzibari walio wengi. Ibn Khaldun pia ameizungumziya tabia hii na mwisho mbaya wa viongozi wa namna hii kwa sababu wanakuwa na ujasiri wa kuyaanzisha mambo ambayo athari zake za baadaye wanakuwa hawazioni na wanapokuja kuziona hukosa ujasiri wa kujiwajibisha na hutaka kuwapotezeya

Page 403: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 371

wengine wakati kukaa na kuyashughulikiya matatizo yao ambayo huwa hawana nia ya kuyatatua. Watu wa namna hii huwa hawana lengo maalumu na mifano yao imetajwa ndani ya aya kumi za mwanzo katika Sura ya Baqarah na katika Sura Al­Munafikun katika Qur’an Tukufu au katika tabia ya Iago katika mchezo wa mwandishi maarufu William Shakespeare, Othello. Pia binaadamu hawezi kwenda mbele bila ya ilimu ya kuufahamu ukweli wa janga lilomsibu. Taifa au mataifa pia yanahitajiya kufika mahala pa kuomboleza na kuyaaga maafa yaliyopita. Kama alivosema Khalifa wa Waislam Othman bin Affan. “kila kitu kina maafa yake na maafa ya ilimu ni kusahauliwa.” Tizama kitabu kiitwacho Ambigious Loss: Learning to Live with Unresolved Grief, Harvard University Press, 1999, kilichoandikwa na Pauline Boss ujionee faida na khasara za kuyafahamu au kutoyafahamu maafa yanayowakumba kila aina ya binaadamu au hata mataifa.

Hili ni suala muhimu bila ya kiasi. Kuliweka hadharani suala la siri nzito ya mapinduzi 3. ya Zanzibar au siri yoyote ile ni suala ambalo linahitajiya uangalifu mkubwa na mtizamo ambao utahikikisha kuwa lengo, chemebelecho Mwalimu Nyerere, ni kuuzuwia mtikisiko wa taifa la Tanzania na si kuundeleza. Binafsi nimepigana sana na nafsi yangu juu ya faida na khasara za kukiandika kitabu hichi na niliweza kufanya uamuzi wa kukitowa hadharani pale nilipoamini kuwa lengo langu si kuvirudia vita vya jana na kuzichimbuwa khasama zilozokwisha pita na wahusika wake, bali kujaribu kwa kadri nitakavoweza kulifanya lengo la kitabu liwe kuwafanya Wazanzibari wakaribiane badala ya kuendeleya kulaumiana na kuumizana wao wenyewe kwa wenyewe na baina yao na ndugu zao wa Tanganyika.

Kuwachuja Wazanzibari katika chungio ya kikabila ili wapatikane “Waarabu” na 4. wabakishwe nje, au wapatikane Waafrika na watupwe nje ya uhusiyano wa kijadi na Bara la Asia ya Magharibi, ndiwo msiba wa mtihani na fitina iliyotiwa Zanzibar. Ni Mzanzibari gani aliye kindakindaki ambaye hatokuwa na damu ya Kimakonde, Kindengereko, Kimanyema, Kihindi au ya Kiarabu? Wote ni Wazanzibari kwanza halafu ndo inakuja asili ya mtu, na kwenye mtiririko wa kuipenda nchi kwanza halafu kabila ndipo penye amani na mustakbal mwema kwa Wazanzibari wote.

Zanzibar haijapatapo kuwa sehemu ya nchi ya Tanganyika ambayo umri wake kabla 5. yakupata uhuru haukupindukiya miaka 70. Ukweli wa historia unatuambiya kuwa nchi ya Tanganyika ni nchi changa sana ukiifanananisha na ukongwe wa Dola ya Zanzibar. Baada ya fitina ya utumwa, jambo la pili lenye kuiondoleya amani Zanzibar ni hii imani dhaifu yenye kuamini kuwa Zanzibar ni “yao” Tanganyika na kujitia khofu na huzuni Zanzibar isiwatoke, liwe litakalokuwa.

Watu walioowana na wenye uhusiano wa kindowa hawahitajii kufanyiwa mchujo na 6. kurudishwa kwenye hali ya kuwatenganisha. Hiyo ni sawa na kuipa talaka jamii nzima iliyoowana na kuzaliana. Athari yake ni kuiondoleya jamii ya Kizanzibari uwezo wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika mustawa wa nchi na taifa la Zanzibar.

“Viongozi wa wakati ule, Nyerere na Kawawa walikuwa wakitutembelea na 7. kutusomesha…(Tanganyika Federation of Labor) iliisaidia TANU kwa sababu ilikuwa na dhamana ya kukusanya michango,” Angalia Hanan Hosni Sabea, uk. 624.

Mkello anakubali kuwa Zanzibar, “Ni nchi kamili” na wakati huohuo alisema kuwa, 8. “Tulitaka nchi yetu ya Zanzibar tuigomboe.” Kauli ya “Zanzibar si nchi” ni fikra iliyomo ndani ya vichwa vya kikundi maalumu cha wanasiasa wa Tanganyika ambao wanafahamu kuwa Zanzibar ni nchi kamili lakini wameamuwa kuwa si nchi kwa sababu wanaamini ndani ya nyoyo zao kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika hata kabla ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kubadilishwa jina na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tangu huko nyuma wazalendo wa chama cha Afro­Shirazi ambao pia walikuwa 9. wanachama wa chama cha wafanyakazi walitambuwa kuwa Zanzibar ni nchi na ndiyo maana Mkello hapa analalamika.

Page 404: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla372

Kutochanganya Chama cha Wafanyakazi na Serikali ni njia moja ya Serikali 10. kujiwekeya kinga iwapo ingelaumiwa ingeliweza kujitowa kwa kukitowa muhanga Chama cha Wafanyakazi au kusema kuwa kilopinduwa Zanzibar ni Chama cha Wafanyakazi na si Serikali ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa akitambuwa alichokuwa anakifanya na ndiyo maana alikuwa 11. akichukuwa tahadhari ya hali ya juu asije akaonekana anaisaliti Zanzibar.

Mlango wa Saba

Utumiaji wa neno “koloni la Kiarabu” ni upuuzaji wa ushahidi wa magofu na 1. maandishi juu historia ya Waarabu katika Pwani ya Afrika Mashariki. Fikra ya kuwafanya Waarabu ni wageni Afrika Mashariki ingali ikiwasumbuwa wazee.

Tizama kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Al Barwani 2. Kujenga na Kubomolewa Zanzibar (Kumbukumbu) kuhusu babu yake, ambaye ni mjomba wa mama yake, Chifu Mwanya wa Makonde aliyetowa ardhi ya “…asili ulioasisiwa huo mji wa Lindi,” uk. 51.

Ubinafsi wa mtu, wa kijamii, au wa kimajimbo hauwezi kuondoka isipokuwa kwa 3. kuvunjwa na imani ya dini inayotoka ndani ya nafsi ya binaadamu mwenyewe na bila ya kulazimishwa kutoka nje ya nafsi yake, au kwa kidunia na kwa kuiweka mbele ilimu na maana ya uraia.

U­CUF na U­CCM ni matokeo ya kugawiwa Wazanzibari na viongozi vitimbakwiri 4. na wahafidhina na kuuendeleza mpasuko ambao chanzo chake huko nyuma kilikuwa ni nani ana haki zaidi Zanzibar, Mzanzibari au Muafrika kutoka bara? Kitakachosaidiya ni mapinduzi ya wananchi yanayotokana na maridhiyano ya mustakbal mwema baina ya vyama vyote viwili kuwa ni chama kimoja cha mapinduzi mapya ya Wazanzibari yenye lengo la kuziinuwa hali za kiilimu na za kiuchumi za wananchi walio wengi.

Hapa ndipo penye chimbuko la matatizo yote ya Zanzibar. Huku kutambuwa kuwa 5. Wazanzibari wanajuwana halafu wamezaliyana halafu kuwaoneya choyo wasikamatane na wasiwe na mafahamiyano.

Kuisambaza kwanza bara siri ya kuwapinduwa Wazanzibari ni kuonyesha wazi kuwa 6. fikra hiyo isingeliweza kukubaliwa na Wazanzibari na kukubalika Zanzibar. Kheri hutoka ndani ya tumbo la shari na leo hii vyama vya kisiasa ndani ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar vina nguvu na ushawishi mkubwa Zanzibar na Tanganyika.

Katika mahojiano ambayo aliwahi kufanyiwa Joseph Bhalo na Palmira Velasco, 7. Zanzibar, Velasco aliandika kuwa familia za Wanamsumbiji zina idadi kubwa ya watu na jamii ya Wanamsumbiji iliyoko Zanzibar inafika watu 4,000.

Tatizo la wageni kutowajuwa wenyeji ni moja wapo ya mbinu za kale za kuweza 8. kuwatala watu duniani kwa sababu panapokosekana nguvu za kijamii zinazotokana na kushirikiyana au kuowana inakuwa ni rahisi watu kufanyiana mabaya pale niya zinapokuwa si safi.

Baadhi ya Wazanzibari piya walishiriki kuwauwa Wazanzibari wenziwao. Wazanzibari, 9. kama walivyo Wamakonde, ni watu wapole lakini ushahidi unathibitisha wanaweza kute­ sana na hata kuuwana lakini lazima piya papatikane kikundi cha watu wenye kuwa­chocheya.

Utafiti wa ndani zaidi wa vyama vya wafanyakazi Zanzibar unahitajiwa kufanywa ili 10. mchango wa viongozi waliyotanguliya kama marehemu Mzee Mohamed Mfaume, Hasnu Makame na wengineo ukatambulikana kwa ufasaha zaidi.

Hii fikra inasema kuwa Wazanzibari ni watu ambao wanapenda kujipendekeza kwa 11. watu na ndio maana ni watu wa kuogopwa kwa sababu ni watu ambao ni rahisi kuchochewa

Page 405: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 373

au kutumiliwa. Mwalimu Nyerere ameieleza fikra hiyo katika kitabu cha William Edgett Smith Nyerere of Tanzania, uk. 90. Kinachosahauliwa ni kuwa mengi ya uwongo yamesemwa na kuandikwa dhidi ya Wazanzibari na kukosa kwao bega la kuliliya huwafanya watafute mashirikiyano na yoyote yule ambaye atakuwa tayari kuwasaidiya ili waondokane na hali ya kunyanyaswa na kudharauliwa.

Huku ni kukiri tena kuwa jaamii ya Kizanzibari ni jamii ya mchanganyiko. Cha 12. kustaajabisha ni kule kutiwa na kutiya chuki kwa sababu Waafrika wameingiliyana na wamechanganya sana damu na Waarabu.

Katika makabila ya Kiafrika ambayo yamezaa sana na Waarabu ni kabila la 13. Kimanyema ambao wengi wao ni Waislam. Katika makala muhimu iitwayo “Fashioning Sexuality: Desire, Manyema Ethnicity and the Creation of the Kanga, c 1880–1900,” katika jarida la International Journal of African Historical Studies, 39, 3: 441–469, Dkt Sheryl A. McCurdy anaelezeya jinsi ya asili ya kanga inavyotokana na wanawake wa Kimanyema. Wazee wengi wa Kiarabu walipendeleya zaidi kuwaowa wanawake wa Kiafrika hata kuliko kuwaowa wanawake zao wa Kiarabu. Hii si dalili kuwa waliwapenda Waafrika kwa sababu waliwafanya watumwa bali kinyume chake ni kuwa hawakuwa na ubaguzi wa kukataa kuchanganya damu na Waafrika. Sasa tizama hali ya maingiliyano baina ya watu weupe na weusi kutoka nchi za Magharibi na khasa wakati wa utumwa wa mtu mweusi na kama waliowana nao au kukikubali na kukihishimu kizazi chao.

Bwana Joseph A. Rimmer na mkewe ni Waingereza waliyoishi Zanzibar kuanziya 14. Mei 1955 mpaka Aprili 1964, na mtoto wake Michael alizaliwa Zanzibar, walikuwa wanaishi Beit­el­Ras yalipotokea mapinduzi. Kwenye barua yake kwa mwandishi huyu, Rimmer ameandika kwa lugha ya Kiingereza maneno yenye tafsiri ifuatayo: “ ‘Wapiganiya uhuru’ kutoka bara (baadhi yao katika muigizo wa Kimau­Mau) waliahidiwa ngawira nzuri iwapo watajiunga katika kuvishambuliya vikosi vya polisi ya Zanzibar mapema katika Januari 1964. Wanamapinduzi wa Kizanzibari piya walipewa ahadi kama hizo.” Kwa mujibu wa Bwana Rimmer majina ya maofisa wastaafu ambao bado wahai wanaweza kupatikana kwenye orodha mpya ya Overseas Pensioners Association ya Uingereza. Barua kwa mwandishi, tarehe 12 Julai 2000.

Kwanini waogope lawama na Mgereza? Ni kipi ambacho kikimuunganisha Mkoloni 15. wa Kiingereza na Muafrika aliyetawaliwa na Muingereza? Mwalimu Nyerere amelijibu suala hilo kwenye kitabu cha William Edgett Smith uk. wa 22 kwa maneno yafuatayo: “Kitu kimoja ambacho ninacho sawa na Magharibi ni Ukristo. Mimi ni Mkristo…Ukristo ni imani ya kimapinduzi, lakini kuna kitu mahali fulani hakijenda sawa.” Na kabla ya hapo kwenye uk. 18 wa kitabu hichohicho anasema Mwalimu Nyerere: “Nimeishi miaka sita hapa [Tabora] kama ni mwanafunzi wa shule, na mitatu kama ni mwalimu. Lakini Tabora ni tatizo. Unajuwa, iko kwenye njiya ya zamani ya msafara wa watumwa hapa. Watu wake ni watoto wa wauza watumwa. Wanapenda sana kubishana.”

Mlango wa Nane

Kulikuwa na mahusiano ya karibu baina ya gazeti la 1. Afrika Kwetu na Indian Association ya Zanzibar na hata baadhi ya makala za magazeti zikitoka kwa Wahindi wa Nairobi.

Mzee J. J. Mchingama hakuzaliwa Zanzibar na hakutaja kama alichukuwa uraia wa 2. Zanzibar lakini anazungumza kwa uhalali wa Uafrika wake na si kwa mujibu wa sharia za uraia wa Zanzibar.

Hili la “hapa watu wa bara si kwao” lilipewa nguvu na baadhi ya wahafidhina wa 3. chama cha Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) na khasa pale walipoanza kuwafukuza

Page 406: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla374

wafuasi wa ASP kutoka kwenye mashamba yao na kubwa zaidi pale walipowafukuza askari wenye asili za kutoka bara badala ya kuwapa uraia na kuwafanya ni sehemu muhimu ya jamii ya Kizanzibari na ya jeshi la polisi.

Uwezekano wa Mzee Karume kuvijuwa viini vyote upo lakini haina maana kuwa 4. alivichaguwa na kuviongoza yeye. Maelezo ya baadhi ya wazee wa mapinduzi yanaonyesha kuwa Mzee Karume akivijuwa viini kwa kuzijuwa habari zake na si kwa kuviongoza.

Wazee wazito wa Kiarabu wa Mwera waliyoapa kuwa Mzee Karume alizaliwa Zanzibar 5. walikuwa ni wazee waliyoona mbali kwa sababu hata kama angelikuwa hakuzaliwa Zanzibar wazee wake walitokeya sehemu ambayo ilikuwa ina ukaribu mkubwa na Zanzibar. Mbali ya kuwa dini ya Kiislam haitambuwi mipaka ya uraia kama inavyotambulikana na itikadi za kizalendo ya nchi za Kimagharibi iliyorithiwa na Waislam pamoja na Wakristo. Inasemekana kuwa Hizbu ilimuomba radhi Mzee Karume kwa kumfunguliya kesi dhidi ya uzawa wake lakini tayari watu wa bara walikuwa wameshatambuwa kuwa hawatakiwi Zanzibar na huo mwanya ukajakutumiliwa na Mwalimu Nyerere kwa maslahi yake ya kisiasa. Kukataliwa Mzee Karume kuwa hajazaliwa Zanzibar au kung’olewa mimeya wafuasi wa ASP hakuko sawa na mauwaji ya 1961 au mauwaji ya halaika yaliyofanywa baada ya kuanguka Serikali ya ZNP­ZPPP, na mateso ya kuipoteza Dola ya Zanzibar na yaliyowafika Wazanzibari. Mwenye Enzi Mungu amewalipa Wazanzibari wadhulumiwa kwa kuwapa subra na nguvu za kuendeleya kuiteteya nchi ya Zanzibar na watu wake na pia kwa kuwapa kheri nyingi na kubwa zaidi ambazo kuna siku zitaweza kusaidiya katika kuijenga Zanzibar Mpya. Kupotoshwa kwa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na uhusiyano wake na muungano kumesababisha kwa kiasi kikubwa kadhiya ya Zanzibar kukosa kuungwa mkono duniani na Zanzibar kuchelewa kujenga mazingira ya kuwarudisha Wazanzibari waliyotapakaa ulimwenguni kurudi kuisadiya Zanzibar kwa ziara za matembezi na kazi, au kwa kuazimwa kutoka nchi ambazo wanaishi ndani yake, au kwa wenyewe kuamuwa kustaafu na kurudi Zanzibar.

Mzee Karume aliukaribisha uhuru wa Zanzibar kwenye hotuba yake ya wakati wa 6. kuupokeya uhuru (Angaliya kiambatanisho A) na mmoja kati ya viongozi wakubwa wa TANU ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kwa mwandishi wa kitabu hichi kuwa TANU ilikuwa imeshachoshwa na Mzee Karume kwa sababu alikuwa ameshakubali kuwa kiongozi wa upinzani ndani ya Baraza la Kutunga Sheria na ilionekana wazi kuwa Zanzibar haitoweza kupatikana kwa njia za amani na za kisiasa na ndipo mpango wa kuipinduwa Zanzibar ulipopewa nguvu na kasi. Pia ameelezeya mzee huyo kuwa TANU ilipoteza fedha nyingi kuisadiya Zanzibar kwenye uchaguzi na bila ya kupata mafanikio. Kwa kejeli, mzee huyo alinielezeya kuwa viongozi wa ASP walikuwa wakenda Dar es Salaam kuomba kama mafakiri. Walikuwa hawana kitu.

Hakuna hata mmoja kati ya wazee wanamapinduzi waliyohojiwa ambaye ameweza 7. kuthibitisha Mzee Karume alikuwepo wapi siku ya mapinduzi. Taarifa za kuthibitika zinaelezeya kuwa Mzee Karume alikuwapo Dar es Salaam kwa Mzee Abbas Sykes. Kwa mujibu wa marehemu Mzee Aboud Mmasai baada ya kuanguka Ziwani kilikwenda kikundi cha watu ndani ya Land Rover kumfuata Mzee Karume nyumbani kwake Kisiwandui kwa lengo la kutaka kumuuwa kwa sababu alikwenda polisi, yeye na Mzee Jumbe, kuiarifu Serikali kuhusu fujo zilizokuwa zinataka kufanywa na wahuni wa ASP ambao yeye hahusiki nao, lakini hawakumkuta.

Njiya moja nzuri ya kuyathibitisha haya ni kufanya utafiti wa ziada juu ya vikundi vya 8. ngoma tafauti zilizoshiriki kwenye kuwakusanya wanawake wa kibara siku ya mapinduzi. FRELIMO ilipokuwa inafanya maandalizi ya vita iliwaandaa vijana wenye kukusanya michango, chakula, nguo, na misaada mbali mbali. Mzee J. J. aliongezeya: “Na wananchi wa Zanzibar pia kwa kusaidia ukombozi wa Mozambique walichangia vifaa kama hivo na zaidi ya hivo pia walichangia punda. Kama punda 32 waliwatowa kwa ajili ya kusaidia

Page 407: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 375

kuchukuwa zana nzito za kivita kutoka mto Ruvuma kuingia nazo ndani Msumbiji kuwasaidia wapiganaji wa ukombozi. Kwa sababu ilikuwa haziwezi kubebwa na watu kwa kutumia nguvu zao, zana nyengine inabidi zichukuliwe kwa magari na badala ya magari ilibidi watumiwe punda. Kwa wataalam wale wa Kichina waligunduwa kwamba kinachomfanya punda apige kelele kuna mishipa fulani inakuwa kama ina washawasha ndo inamfanya punda analia. Akilia ndio anatulia. Kwa hivo walifanya operation ya kuwafanyia operation wale punda wote wale kusudi ile sound ya kulia itoke kwa vile wanakwenda kimya kimya, kuficha zile siri za wapiganaji mule wanamotembea. Baadhi ya hao punda au kizazi chao wapo bado Maputo kama ni kumbukumbu ya historia ya misaada tulioipata kwa wananchi wa Tanzania na Zanzibar kwa jumla. Wako katika National Museum Maputo. Mimi mwaka 1989 nilikwenda nikawakuta. Punda hao walinunuliwa na chama cha FRELIMO na wengine walitolewa bure na wananchi wa Zanzibar kusaidia ukombozi kama mchango wao.”

Hii ni dalili kuwa utambulisho wa kikabila na khasa uzalendo wa Kiafrika ulikuwa 9. una nguvu sana Zanzibar hata kuliko utambulisho wa kidini.

Karibuni palifukuliwa maiti pale Kiinua Miguu kwenye barabara pembezoni mwa 10. nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Kauli na tafsiri tafauti zilitoka Zanzibar isipokuwa hii ya kaburi la halaiki ilikuwa haijulikani.

Sidhani kama hili lingeliweza kufanywa kirahisi na marehemu Mzee Mohamed 11. Kaujore au Saidi Idi Bavuai kwa sababu lingelizuwa utata mkubwa wa nani atiwe katika listi ya mnara wa mashujaa wa mapinduzi na nani awachwe. Au ingelibidi iamuliwe yawekwe majina ya Kamati ya Watu 14 ambayo yalikuwa yameshazoweleka, na hilo pia lingekuja kuleta utata na mzozo baadaye.

Akina Mzee J. J. walijitambulisha na kujiona kuwa ni Wazanzibari lakini wakati 12. huohuo walikuwa wakiwatizama Wazanzibari kwa jicho la kuwa si Waafrika.

Hakuna aliyepelekwa au kwenda Zanzibar kwa kufanya kazi ya Manamba kwa 13. maana ya kuajiriwa kigengi cha wafanyakazi Zanzibar wakati mmoja na kupewa mkataba mmoja wenye namba moja. Hilo halikuwepo Zanzibar na kweli halikufanyika.

Hoja ya mustakbal ni kiti cha Kenya katika Baraza la Mapinduzi au kiti cha Zanzibar 14. katika Bunge la Kenya?

15. Katiba ya Zanzibar ya 1984, Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza, Kifungu Nambari 4 kinasema: “Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yo yote inatafautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itakayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.” Kifungu kinasema hivi: (1) “Kwa masharti ya kifungu hiki Baraza la Wawakilishi linaweza kubadilisha kifungu cho chote katika Katiba hii. (2) Muswada wa Baraza la Wawakilishi wa kubadilisha Katiba hii hautopitishwa na Baraza isipokuwa uwe umeungwa mkono kwa mara ya kwanza na mara ya pili katika kusomwa kwa kura si chini ya theluthi mbili ya kura zote za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.” Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inakubali kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mahakama ya Zanzibar, na Baraza la Wawakilishi, mbali ya kutamka kuwa Rais wa Zanzibar anakula kiapo cha kuwa Rais wa Zanzibar mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar, na mambo mengi mengineyo ambayo yanaipa nguvu Zanzibar ikiwemo Katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Kinachotawaliwa ndani ya Muungano ni Mambo ya Nchi za Nje, Jeshi, Uraia na Sarafu, na yote hayo yanaipa nguvu Tanganyika na kuidhoofisha Zanzibar, ambayo mengi yamo kwenye yale mambo 11 ya awali ambayo ndiyo uti wa mgongo wa kila yenye kuitwa nchi au taifa duniani.

Muungano unalinda Mapinduzi na Mapinduzi ndio msingi wa Muungano. 16. Kama tulivyotanabahisha mwanzoni si lengo la kitabu hichi kuukusanya “ukweli 17.

wote” au “ukweli mmoja” au hata “ukweli huu” kwa sababu hilo jambo haliwezi kufanyika.

Page 408: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla376

Kikosi kupewa likizo askari wote wakati kikitiliwa shaka kutaka kuipinduwa serikali 18. ni jambo ambalo si rahisi kuingiya akilini bila ya kujiuliza “ilikuwaje?”

Walichukuwa hatuwa gani za kumlinda Raisi baada ya kumpa taarifa muhimu 19. kama hizo na kwa nini isiundwe tume ya kuchunguza mauwaji ya Rais wa Zanzibar na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni suala ambalo jawabu yake isingelikuwa nyepesi. Chanzo ambacho hakikupendeleya kutajwa kilimshauri Mzee Aboud Jumbe bora pasiundwe Tume ya Uchunguzi.

Hakuna uthibitisho kwanini Kanali Ali Mahfoudh atowe amri ya kuuliwa Ahmada 20. na wenzake mbali ya kutaka kuonyesha kuwa alikuwa amehusika na mpango wa kumuuwa Mzee Karume kwa sababu alikuwa Mwarabu. Pia wako wenye kuamini kuwa kulikuwa na mpango mkubwa zaidi katika kuuliwa Mzee Abeid Amani Karume ambao uko juu ya mipango ya Makomred na huenda mpango huo ukawa umewahusisha baadhi ya memba wa Kamati ya 14.

Mlango wa Tisa

Hii hadithi haingii akilini kiurahisi. Filamu yenye jina “Power Play” inafahamisha 1. uwezekano wa mtu kama John Okello kuibuka ndani ya mazingira kama ya mapinduzi ya Zanzibar. Filamu hiyo ilifanywa kwa kukitegemea kitabu cha Edawrk Luttwak kiitwacho Coup D’Etat: A Practical Handbook. John Okello amenukuliwa akisema kwa uchungu: “Sultan amepokelewa vizuri Uingereza na ndugu zangu wenyewe wamenifukuza. Nimesababisha Sultan apoteze utawala wake, lakini mwisho wangu mimi ni mbaya zaidi kuliko wake,” kutoka William Edgett Smith, Nyerere of Tanzania, uk. 123. A. H. Hawker, Ofisa wa Kiingereza ambaye alibakiya Zanzibar baada ya mapinduzi na alifanya kazi ya Permanent Secretary katika Ofisi ya Rais, aliombwa na Baraza la Mawaziri atowe ruhusa ya malipo ya shilingi 10,000 kwa Okello ikifikiriwa kuwa ni malipo kwa mchango wake katika kuyaongoza mapinduzi, The National Archives, WO 276/541.

Njama na ujanja wa kuogopa kujulikana kwa sababu ni kosa la jinai kuivamiya nchi 2. nyengine ambayo haikutangaza vita na nchi jirani.

Juu ya Makomred kulidharau suala la ukabila na kuiangaliya dunia kwa miwani ya 3. matabaka ya kiuchumi, watu kama Hanga ambaye akiihisabiwa kuwa alikuwa ni Muislam na Marxist aliwatizama Marxists na Waislam wenzake kwa jicho la kikabila. Fikra za Hanga kabla ya kuuliwa zinatowa mwanga zaidi wa nafsi yake ilivyokuja kuyaona mambo baada ya mambo kudhihirika.

Dalili nyingine iliyo wazi kuwa Wazanzibari walikuwa ni watu ambao wakiishi kwa 4. mashirikiyano na mafahamiyano kabla ya zama za fitina (siasa) kuanza.

Kama Muafrika kutoka Uganda ilikuwa ni vigumu kuaminiwa na Muafrika kutoka 5. Tanganyika basi ni dhahiri kilichokuwa na nguvu zaidi si Uafrika peke yake bali Uafrika na fikra ya kuwa Zanzibar ni mtoto wa Tanganyika na si wa Uganda au Kenya kwa hiyo nchi mbili hizo hazitokuwa na haki sawa juu ya Zanzibar kama ilivyo Tanganyika. La msingi ni kizingiti cha Zanzibar kwenye mlango wa Tanganyika.

Ingawa Muingereza hakuijuwa mipango ya ndani kabisa lakini kama asingelitaka basi 6. mapinduzi yasingelifanyika na kama yangelifanyika bila ya yeye kutaka basi yasingelifaulu, na kama yangelifanyika na alikuwa hakuyaunga mkono basi angeliweza kuyadhibiti na kuyazuwiya mauwaji ya halaiki.

Ripoti za kitaifa za Kiingereza zinaonyesha kuwa maofisa wa usalama na wa polisi 7. waliyokuwepo Zanzibar hawakuipenda Serikali ya ZNP­ZPPP na walitaka Serikali ya Zanzibar ianguke kwa sababu ya mahusiyano yake na Rais Gamal Abdel Nasser wa Masri. Walipoufahamu mpango walihakikisha kwanza kutoitambuwa serikali mpya mpaka iwe

Page 409: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 377

imeongozwa na ASP na Mzee Karume na iko ndani ya utawala wa Nyerere. Tena kuowana na kuzaliyana Waarabu na Waafrika lilionekana kuwa ni tatizo na 8.

badala ya kuleta mfungamano na maridhiyano baina ya pande mbili ikaonekana bora uletwe mpasuko wa kijamii kukidhi malengo ya kikundi kidogo cha wanasiasa.

Uwezekano ni kuwa watu hao walitokeya Bagamoyo na si Tanga kwa sababu kulikuwa 9. na harakati kubwa za kijeshi Bagamoyo wakati wa mapinduzi ya Zanzibar ambazo hazikukuwapo Tanga.

Ni dhahiri kutokuaminiyana na uadui baina ya akina Hanga na Mzee Karume 10. uliharakisha majungu ya kupikuwana na khasara kwa pande zote mbili zenye kukhasimiyana. Ndo ule msemo “ugomvi hauna biashara.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Superintendent Derham, Thomas Tete alikuwa ni 11. Inspekta wa Kijaluo na mhusika mkuu wa kuweka nidhamu kwenye kambi ya jeshi la polisi ya Ziwani. Usiku wa mapinduzi Tete alikuwa amelewa na alijaribu kumtuliza Derham kuwa asiwe na wasiwasi hakutotokeya matatizo usiku ule wa mapinduzi. Kutoka The National Archives “Statement of Superintendent Derham” Dar es Salaam, 16 January 1964, DO 185/59 116805, p. 3.

Kulikuwa na mivutano mikubwa baina ya makundi ya kisiasa ndani na nje ya 12. ASP na baina ya mirengo tafauti na madola makubwa kuwalipa watu wao ili wakifaulu wawatumiye kufanikisha malengo yao. Uzuri au ubaya wa mambo ni kuwa wachezaji wote huja kujulikana baada ya nyaraka za siri baina ya mabalozi wa nchi za Magharibi na nchi zao zinapokuja kuwekwa wazi kila baada ya muda wa miaka fulani kupita.

Mzee Issa alitambuwa kuwa Wazanzibari ni watu wenye ari na hawakubali 13. kutawaliwa ndani ya nchi yao.

Mzee Issa hakuelezeya kuwa Mzee Karume alikubali kujiunga na Tanganyika baada 14. ya kutishwa na Mwalimu Nyerere kuwa kama hakujiunga na Tanganyika basi ataliondowa jeshi lake la polisi Zanzibar. Tizama Helen­Louise Hunter, 2010, uk. 99.

Mlango wa Kumi

Seif Bakari na wenzake walikuwa upande wa Mzee Karume na wakati huohuo 1. walikuwa upande wa kina Saleh Saadalla na Abdalla Kassim Hanga ambao walikuwa dhidi ya Mzee Karume.

Mzee Joseph Bhalo ametowa kauli mbili ambazo zinaonekana zinagongana. Upande 2. mmoja anasema Mzee Karume alikuwa hajuwi kuhusu mapinduzi na upande wa pili alijuwa na aliwaambiya wasiwaambiye Wazanzibari kuhusu mapinduzi. Kiini cha mazungumzo kimo kwenye neno “kujuwa.” Kujuwa kinachoendeleya au kujuwa kuwa Mzee Karume ndiye aliyekuwa na ile mipango ya mapinduzi?

Mlango wa Kumi na Moja

Inavyoonyesha na ilivyoelekeya ni tayari kulikuwa na mazungumzo kuhusu mapinduzi 1. baina ya Hanga, Saadalla na hata na Twala. Si rahisi ghafla tu likazuka suala la kufanya mapinduzi na watu wakaitana na wakakubaliyana hapohapo.

“Fuko” ni jina la uchokozi la marehemu Mzee Mwinyi Chande Chambuso ambaye 2. alikuwa mkubwa wa usalama Zanzibar na aliwahi kupata mafunzo Israel.

Rais wa Youth League wa kwanza alikuwa Mzee Hassan Nassor Moyo na chanzo 3. kinasema kuwa baada ya kuuliwa kwa Mzee Karume, marehemu Saidi Washoto alimpendekeza Mzee Moyo awe Rais mpya wa Zanzibar lakini Mzee Natepe alipinga na

Page 410: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla378

ndiyo badala yake akapendekezwa Mzee Aboud Jumbe. Chanzo pia kinasema kuwa baada ya Uraisi wa marehemu Mzee Idris Abdul Wakil, Mzee Moyo alipendekezwa awe Rais Kiongozi wa Zanzibar lakini Mzee Natepe akashauri bora apewe Maalim Seif Sharif kwa sababu anatoka Pemba.

Hili suala la kutochanganya mapinduzi na chama ni muhimu sana katika kuweka 4. sawa historia kwa sababu daima mapinduzi ya Zanzibar yananasibishwa na chama cha Afro­Shirazi wakati walofanya mapinduzi ni wanachama ambao hawakutaka kukishirikisha chama cha ASP.

Chanzo kinasema kuwa marehemu Bibi Freya Mbarak Al­Hinai ndiye aliyefanya 5. mpango na kuweza kuwafikishiya maji ya kunywa na vitu vya kula abiriya wa meli ya Sultan Jamshid bin Abdullah na wasafiri wenzange pale ilipofika Mombasa na kukataliwa Sultan Jamshid asishuke. Nyerere akakubali Sultan na watu wake washuke Dar es Salaam na wakaandaliwa safari na Waingereza kwenda Uingereza.

Kwa hiyo si kweli kuwa Waingereza walikuwa wakimuunga mkono Sultan wa 6. Zanzibar na Serikali ya ZNP­ZPPP.

Haikuwa dharau juu ya silaha kwa sababu walikwisha waonya maofisa wa Kiingereza 7. kuhusu uwezekano wa Zanzibar kuvamiwa na Tanganyika. Ilikuwa ni tabia piya kuwa iwe itakavyokuwa haitowezakana Wazanzibari kupinduwana na kuuwana wenyewe kwa wenyewe na kweli hilo silo lililotokeya.

Ahmed Gharibu alikuwa ni mtu wa kutoka Zanzibar na baba yake, Mzee Gharibu 8. alikuwa na ndugu wawili wa kike, Menkaliya na Kujuwa Kwangu. Bi Menkaliya alichukuliwa Maskati na akaolewa huko na Bwana Almasi na wakazaa mtoto akiitwa Masoud ambaye alifariki msikitini Maskati. Marehemu Mzee Gharibu na Mzee Abasi walikuwa wakifanya kazi kwenye majahazi ya matanga kama ni maofisa wa afya. Mzee Gharibu alikuwa yuko karibu sana na nyumba ya Serikali (palace) ya wakati huo.

Ameripoti Kamishna Sullivan wa jeshi la polisi la Zanzibar la kabla ya mapinduzi 9. kuwa “bunduki za aina ya Sterling zilitumika katika mashambulizi haya na kulikuwa na silaha ambayo sauti yake sikuweza kuitambuwa iliyokuwa ikitowa sauti kali, na yenye sauti ya kukera ya mpasukopasuko, ambayo ikipigwa kusini kwangu kutoka juu ya mapaa.” The National Archives, “Notes made by the late Commissioner of Police, Zanzibar – J. M. Sullivan,” 17th January 1964, DO 185/59 116805, uk. 8.

Khamis Salum Beni alikamatwa na kuuliwa pamoja na akina Abdalla Kassim 10. Hanga.

Ni vigumu kuwazungumziya wahusika na kitendo cha kikatili kama hichi bila ya 11. uhakika unaotokana na ushahidi usiokuwa na shaka ndani yake, ingawa baadhi ya memba wa Kamati ya Watu 14 wanatajwa.

Mwandishi Godfrey Mwakikagile wa kitabu 12. Nyerere and Africa: End of an Era ameandika kwenye ukurasa wa tano wa kitabu kuwa alizungumza mengi na Andrew Nyerere, mtoto mkubwa wa Mwalimu Nyerere, na kati ya hayo vipi “viongozi kama Mfalme Haile Selassie na Dkt Kwame Nkrumah walivyosaidiya kuyagharimiya mapinduzi ya Zanzibar.” Mwakikagile hakutowa ufafanuzi wa zaidi fedha hizo zilitolewa vipi, au kupitiya chombo gani, au kwa ajili ya kulipiya kitu gani.

Mtaona vipi Mzee Aboud aliweza kuteremsha silaha Forodha Mchanga siku chache 13. kabla ya mapinduzi na security ya nchi ilikuwa iko very tight.

Suala la ASP haikupinduwa amelitaja tena Mzee Aboud kuonyesha namna mambo 14. yalivyokwenda kinyume yanavyofahamika na watafiti wa pande zote mbili za Muungano au hata waliyoko nje.

Inasemekana kuwa Babu alipewa cheo cha Uwaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwa 15. sababu kilikuwa cheo cha Sheikh Ali Mushin kabla ya mapinduzi.

Othman Sharif Mussa alikamatwa katika mwezi wa Agosti na inasemekana aliuliwa 16.

Page 411: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 379

pamoja na Abdalla Kassim Hanga katika mwezi wa Novemba mwaka 1969, Nyerere of Tanzania, uk. 134. Kitabu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 1964–1974 Zanzibar kimeandika na kutaja majina ya vikundi 9 ambavyo vilituhumiwa kutaka kuipinduwa serikali ya Zanzibar baina ya 1964 na 1974. Kitabu hakitowi maelezo juu ya wako wapi watu wenye majina yaliyotajwa katika “Vikundi vya kiadui vilivyo fichuliwa kutoka mwaka 1964–1974.”

Mlango wa Kumi na Mbili

Mzee Aboud ameelezeya kwa maneno yake mwenyewe kuwa uchaguzi wa Julai 1. 1963 na wa mwisho wa Zanzibar kabla ya mapinduzi ulikuwa huru na haukuwa na kuibiyana kura. Kwa Saleh Saadalla kumwambiya Rais Ahmed Ben Bella kuwa ASP ilishinda na wakanyimwa serikali ilikuwa ni njama tu ya kutaka kuungwa mkono kuipinduwa Serikali ya ZNP­ZPPPP.

Katika sababu za Mwalimu kuzizuwiya silaha za Algeria zisende Zanzibar inaweza 2. kuwa bado hakuwa akijiamini kuwa utumiaji nguvu katika kuipinduwa serikali ya nchi jirani unaweza ukafaulu; Waingereza walikuwa bado wako Zanzibar, na Gamal Abdel Nasser alikuwa bado ana mahusiyano mazuri na chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP).

Oscar Kambona wakati huo alikuwa ni Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nchi za 3. Nje wa Tanganyika na piya alikuwa Mwenyekiti wa African Liberation Committee (ALC) ya Organisation of African Unity (OAU). Wanachama wa mwanzo tisa wa Kamati ya Ukombozi wa Afrika walikuwa Tanganyika, Uganda, Nigeria, Ethiopia, Algeria, U.A.R., Guinea, Congo (Leopoldville), na Senegal. Ushindi wa mwanzo wa Kamati ya Ukombozi ulitokana na kupinduliwa kwa Serikali na Dola ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964. Baada ya hapo Kamati iliingiwa na mori mkubwa na Dar es Salaam ikageuka kuwa Makka ya wakombozi na wapiganiya uhuru wa Afrika kuliko ilivyokuwa kabla ya kupinduliwa Zanzibar. Ilipofika Machi 1964 wanachama waliongezeka na kufikiya 23 (na baadaye 24) na Kamati ilikuwa ina mchango wa kifedha ambao Waingereza walikisiya kufikiya pauni 494,000 za Kiingereza. Wachangiaji wakubwa walikuwa Algeria, Ethiopia, Guinea, Libya, Mali, Nigeria, Tanganyika na U.A.R., The National Archives, “Liberation Fund: Round­up” DO 216/41. Ndani ya TANU Oscar Kambona na baadhi ya wenzake walikuwa wana msimamo mkali wa kisiasa ambao hata Waingereza walikuwa hawaupendi na walimuonya Mwalimu Nyerere atahadhari naye na khasa mahusiyano yake na nchi za Mashariki. Kambona na Hanga walikuwa marafiki wakubwa na waliwahi kuishi kwenye fleti moja walipokuwepo London. Kambona na Nyerere walikuwa wakipokezana mchezo wa kujifanya kuwa walikuwa hawahusiki na mambo ya Zanzibar. Baada ya mapinduzi kutokeya Zanzibar Kambona alisema “Mapinduzi yenyewe hatukuyatarajiya kabisa; nafikiri hata Wazanzibari wengi hawakuyatarajiya” (uk. 102). Baada ya miaka, Hanga “…alisisitiza kuwa Watanganyika waliyajuwa mapinduzi kabla” (uk. 106) na akasema kuwa “yeye na mwana Afro­Shirazi mwengine, Abdul Twala walikuwepo Tanganyika kwa miezi miwili mwisho wa 1963 wakichukuwa mafunzo ya utumiaji wa silaha kutoka kwa askari polisi wa Kitanganyika” (uk. 106). Miaka miwili baada ya mapinduzi, Mwalimu Nyerere alisema: “Kilichotokeya ni kile ambacho dunia nzima ilipasa wakifahamu…lakini Magharibi wakatangaza kuwa Ukoministi umefanya mapinduzi! Upuuzi! Kwa miaka tumekuwa tukizungumza kuhusu hatari ya kutokeya mapinduzi. Hawa jamaa wenye pinde, mishale na mapanga wamechukuwa. Lakini nchi za Magharibi zimesema, ‘Ni Ukoministi!’ ” (uk. 125). “Kutotaka au labda kutoweza kuyamaliza matatizo ya Zanzibar kama hata kwa kutumiya nguvu, Nyerere amekuwa na mtizamo wenye kukata tamaa kuhusu uwezekano wa

Page 412: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla380

Muungano kufaulu.” “Naamini kuhusu umoja wa Afrika,” alisema mwishoni mwa mwaka 1969, “Lakini hii mipaka ya nchi si kitu kitukufu cha kidini. Ilitengenezwa na mabeberu. Watu wa Afrika ni watukufu zaidi kuliko hii mipaka. Nina vipande viwili va muungano. Hata kama Wazanzibari hawajakataliwa na Tanganyika, ikiwa watahisi tu kama Muungano hauna faida kwao, na wakajitenga, na ikiwa ni hisia ya kweli ya Wazanzibari, basi sitoweza kuwauwa Wazanzibari. Kama walijiunga wakiwa huru, basi wataondoka wakiwa huru. Hatukuitawala Zanzibar. Na wakibakiya, huu utakuwa ni uamuzi wao wenyewe. Huu ni msingi wa peke yake wa kulijenga taifa. Ufalme unauangusha kwa kulipanuwa jeshi. Taifa unaliweka pamoja kwa kuupa nguvu uwamuzi wa ndani wa umoja” (134–135). Dondoo zote zinatoka kwenye kitabu cha William Wdgett Smith Nyerere of Tanzania.

“Mara ya kwanza kutajwa kwa silaha kutoka Algeria ilijulikana katika Jeshi la 4. Tanganyika katika mwezi wa Julai 1963. Katika mwezi wa Agosti–Septemba 1963 listi ilionekana Wizara ya Ulinzi…na ilikuwa imeandikwa kwa lugha ya Kifaransa…meli ilikaa nje ya Dar es Salaam (bila ya kuonekana) kwa masaa kama 48 kabla ya kutiya nanga. Kutokana na kuwauliza maofisa wa Kiafrika waliyokuwa wanahusika na upakuwaji wa meli, ilikuwa wazi kuwa baadhi ya mzigo uliondolewa na inawezekana sana ulitolewa kutoka kwenye meli wakati meli bado iko nje….Kuna maboxi fulani ya silaha na risasi yalikuwa yametiwa rangi chafuchafu ya krosi nyeusi. Hizi ziliwekwa mbali na inavyoonyesha zilikuwa na umuhimu maalumu. Kepteni Dillon alipomuarifu Kamanda TMP (Brigadier Douglas) kuwa moja au mawili katika maboxi hayo yalifunguliwa aliamrishwa kuwa maboxi yenye michoro hii isifunguliwe kabisa…Kutokana na ushahidi wa karibuni ni wazi kuwa siku za mbele Jeshi la Tanganyika lina nia ya kusaidia kuwafunza na kuwaunga mkono wapiganiya uhuru wa Mozambique na nchi nyengine za Kiafrika ambazo bado hazikupata uhuru. Kwa hiyo inaonyesha kwamba silaha zote ziliyoko Tanganyika ikiwa zimepelekewa Jeshi au halikupelekwa zitizamwe kuwa ni za kutumiliwa kwa mujibu wa maelekezo ya ‘Kamati ya Nchi Tisa’,” The National Archives “Tanganyika—Arms Supplies from Algeria” DO 185/48 116923. Anaelezeya ofisa mwengine wa Kiingereza kuwa “Jumanne tarehe 7 Januari, nilionana na Kambona na nikamuuliza kama silaha zote hizi ni kwa ajili yetu au kwa ajili ya mtu mwengine. Alinijibu kuwa ni kwa ajili ya Tanganyika Rifle isipokuwa maboxi yaliyotiwa alama ya krosi nyeusi. Maboxi haya yanatakiwa yapangwe karibu ya mlango wa ghala ili yaweze kuchukuliwa kwa haraka. Alisema kuwa maboxi haya hayafai kufunguliwa. Lakini tuliyafunguwa baadhi yake na tuliona zimo bunduki za Kiingereza za Mark IV, Bren guns, magazines, 303 ammunition na aina ya Molotov Cocktail. Zanzibar ikatokeya Jumapili iliyofuatiliya, yaani, tarehe 12 Januari na maboxi bado yalikuwepo kwenye ghala. Baada ya tarehe hii umuhimu wake ukapoteya,” The National Archives, “Algerian Arms” DO 185/48 116923.

Chama cha ZNP hakikuwa dhidi ya Nyerere bali kilikuwa dhidi ya njama zake za 5. kutaka kuitawala Zanzibar kwa kupitiya Katiba ya Shirikisho la Afrika ya Mashariki na kukhofiya kuwa Tanganyika ilikuwa iko tayari wakati wowote ule kuivamiya Zanzibar na baada ya Zanzibar, Uganda.

Balozi Noureddine Djoudi alikuwa Balozi wa Algeria Dar es Salaam. Alipopinduliwa 6. Rais Ahmed Ben Bella, “Wachina waliamuwa kuiunga mkono serikali mpya ya Algeria na Nyerere alisema ‘Hawafahamu nini maana ya urafiki? Urafiki hauna maana kuwa rafiki yako akipinduliwa unamsahau. Sasa wananitaka nende Algeria wakati Ben Bella yuko gerezani. Inanishangaza kuwa marafiki zangu hawawezi kulifahamu hili, na inawastaajabisha wao kuwa mimi linanistaajabisha.’ Nyerere alichukuwa msimamo kuwa hatokwenda Algeria isipokuwa kama Ben Bella ataachiliwa huru, au atashtakiwa na mashtaka yakathibitishwa. Siku chache baadaye, Nyerere alistaajabishwa wakati balozi wa Algeria Tanzania [Djoudi], ambaye kabla alikuwa akimuunga mkono sana Ben Bella, aliporudi kutoka Algeria baada ya

Page 413: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 381

coup [19 June 1965], na wakati yupo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, alimponda Ben Bella kuwa alikuwa ni mtu ‘aliyemgonganisha Mualgeria dhidi ya Mualgeria mwenzake’ ili ajikweze kama ni dikteta. ‘Kila kitu kiko sawa na ndani ya mikono mizuri,’ alisema balozi. Nyerere hakumpokeya tena Ikulu,” William Edgett Smith Nyerere of Tanzania, uk. 161–162. Mwalimu hakuweza kuuelezeya mchango wa Rais Ahmed Ben Bella katika Mapinduzi ya Zanzibar uliyompa nguvu kuujenga msingi wa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Ahmed Ben Bella amethibitisha kwa kuandika “Kwa vile Cuba ilikuwa chini ya 7. uchunguzi wa karibu, kulikuwa hakuna uwezekano wa kupanga mipango ya kupeleka silaha na makada waliopewa mafunzo Cuba kwenda nchi nyengine za Amerika ya Kusini.” Kutoka “Che as I knew him” Le Monde Diplomatique, October 1997. Mwaka 1963 “meli yenye kupeperusha bendera ya Cuba ilitupa nanga kwenye bandari ya Oran [ya Algeria]. Pamoja na shehena ya sukari ambayo tuliahidiwa, tulishangaa kugunduwa baadhi ya matenki na mamia ya askari wa Kicuba kuja kutusaidiya…Dhahiri hatukuweza kuiwachiya meli ikaondoka tupu. Tukaijaza mazao ya Algeria na kutokana na ushauri aliotupa Balozi Jorge Serguera, tukaongezeya farasi wa Kiberber.” Maelezo ya Rais Ahmed Ben Bella yanatowa mwangaza juu ya mambo mawili muhimu. La kwanza ni kuwa kwa vile Cuba ilikuwa ipo chini ya macho ya Kimarekani isingeliweza kuwasaidiya Makomred wa Zanzibar kupinduwa serikali tarehe 12 Januari 1964. Pili, mpango wa mashirikiyano wa kupelekeyana silaha na bidhaa ulianza kabla ya meli ya Algeria Ibn Khaldun kupeleka silaha Dar es Salaam kwa ajili ya wapiganiya uhuru wa Msumbiji na mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mfano Waingereza na Wamarekani walimpenda zaidi Nyerere na walimuogopa 8. sana Nkrumah. Tathmini ya CIA ya tarehe 10 Juni 1965 ina maelezo yafuatayo kuhusu Nyerere: “Inavyoonyesha ni kuwa Nyerere anaitegemeya shakhsiya yake ya ucheshi na anavyopendwa na nchi za Magharibi kutowa picha kuwa bado ni ‘mtu wa Magharibi.’ Wachunguzi wengi wa Magharibi wanaendeleya kumtizama kwa jicho hilo. Wengine wanamuona kuwa ni dhaifu na anayumba, mara nyingi hupumbazwa na hughumiya na matukio ambayo hawezi kuyadhibiti na ambayo hayafahamu kiukamilifu…. Anapendeleya kujiepusha asiingiye kwenye hali zisofurahisha au migongano ya aina yoyote ile, na mara nyingi huwaambiya watu yale ambayo wanapenda kuyasikiya; na akibanwa atowe maelezo, basi husema nusu ya ukweli au hukwepa…Ukimfananisha na viongozi wa ulimwengu wa Afro­Asian ambao wameamuwa kuegemeya upande wa Makoministi, basi hana msukumo wala umoja wa dhamiri wa Nkrumah, au uwanamapinduzi wa Ben Bella au Nasser. Nyerere ni mdogo zaidi, na anapenda kuyachangamkiya malengo makubwa kuliko kuwa na mipango, na pengine bila ya msimamo imara au ushujaa wa kuidhibiti hali wakati wa misukosuko.” CIA, “A reassessment of Julius Nyerere,” Office of National Estimates, 10 June 1965, Lyndon Baines Johnson Library.

Kwa mujibu wa mwandishi mashhuri wa fasihi ya Kiswahili, Shaaban Robert “…9. Mswahili alituhumiwa kuwa ni mchuuzi wa biashara ya utumwa na lugha yake ni chombo cha kufanyia biashara hiyo. Marafiki zangu, hakuna jambo lenye makosa kama maneno haya. Makundi madogo ya Waswahili ambayo yalisafiri hadi ndani mabarani hayangeweza kwa vyovyote vile kuwafanya wenyeji mashujaa na wenye nguvu kuwauza ndugu zao utumwani. Watu walifanywa mfano wa vitu vya biashara kwa sababu ya (a) dasturi za watu majahili, ambao inafaa tushukuru, walikuwa na idadi ndogo tu, na (b) haki ya kiushindi ambayo iliwafanya walioshindwa na mateka kupata shida. Tukitoa mfano, Waswahili hawakuruka kwenda mabarani. Walisafiri kwa miguu kupitia nchi za Wazaramo, Wagogo, Wanyamwezi na kwingineko ambako soko za utumwa hazikuweko, hadi kufikilia kule kwenye soko hizo.” Imenukuliwa kwenye kitabu cha Ibrahim Noor Shariff Tungo Zetu: Msingi wa Mashairi na Tungo Nyinginezo, uk. 22–23.

Page 414: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla382

Kwa mujibu wa Helen­Louise Hunter “Syria, Iraq, na Jordan waliyaita mapinduzi 10. ya Zanzibar ni ‘bloody massacre’ [mauwaji ya halaiki] na waliitisha aina tafauti za harakati za kimataifa.” Helen­Louise Hunter, 2010, uk. 76.

Bwana Ali Khamis Jaribu ni kiongozi pekee ambaye yuko hai kati ya viongozi 11. waasisi wa chama cha Afro­Shirazi.

Walikuwa hawakujuwa kuwa huo mpango usingeliweza kufanyika kwa sababu 12. Waingereza walikwishaamuwa kuwa pasiweko na mawasiliano yoyote baina ya Sultan aliyekuwemo melini na nje.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa Kiomani, Nassir bin Abdalla Al­Riyami 13. kwenye kitabu chake kwa lugha ya Kiarabu, Balozi wa Zanzibar aliyokuwepo Cairo, Bwana Ahmed Lemky alimuendeya Al­Shaarawi saa nane za usiku na ombi la haraka la kutaka kuonana na Rais Gamal Abdel Nasser kusaidiya kuiokowa serikali ya Zanzibar isianguke. Al Shaarawi akamchukuwa Ahmed Lemky mpaka nyumbani kwa Mohammed Faiq na Lemky alikuja na fikra ya kuviomba baadhi ya vikosi vya Masri vilivyokuwepo Yemen vyende Zanzibar lakini Faiq akaona kuwa hakuna uwezekano wa kuitekeleza fikra hiyo kwa sababu taasisi zote muhimu kama uwanja wa ndege tayari zilikuwa ndani ya mikono ya wanamapinduzi. Pia Faiq alisema kuwa Nasser aliona kuwa kwa Masri kuyatambuwa mapinduzi ya Zanzibar kwa haraka kungelisaidiya kusimamisha mauwaji. Nasir Abdullah Al­Riyami. 2009. Zinjibar: Shakhsiyyaat wa Ahdaath: 1827–1972, London: Dar Alhikma, 2009, uk. 447. Ikiwa kutoingiliya Masri watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa kwa mujibu wa hisabu ya John Okello, basi uamuzi wa busara wa Nasser ungelikuwa kuingiliya au angalau kuonyesha kuwa wako tayari kuzitumiya nguvu zao na huenda mauwaji yasingelikuwa makubwa kama yalivyotokeya. Tatizo kubwa lilikuwa Nasser na Ben Bella walikuwa hawana ufahamu wa yaliokuwa yakitendeka Zanzibar na wakiwategemeya watu kuwapa habari ambao hawakuvijuwa viini vya mapinduzi. Kwa mujibu wa Mohammed Faiq, nyumba ya mwanzo kutaifishwa Zanzibar ni nyumba ya Karimjee ambayo ilitaifishwa na kufanywa ni makaazi yake alipoitembeleya Zanzibar mara tu baada ya mapinduzi ya 1964.

Miaka michache iliyopita Ubalozi wa Algeria uliyopo Dar es Salaam ulitowa nishani 14. maalumu kwa Khamis Abdalla Ameir, Kingunge Ngombale Mwiru, Ali Sultani Issa, na watu wengine wawili. Makomred hawakujuwa wala hawakushirikishwa kwenye suala la silaha kutoka Algeria kwa ajili ya Mapinduzi ya Zanzibar na haiwezi kuwa walipewa nishani hizo kwa kutambuliwa mchango wao kwenye jambo ambalo hawakulijuwa. Inawezekana sana kuwa walitunukiwa nishani hizo kama ni utambulisho wa mchango wao pale chama cha ZNP kilipokuwa kikiyaunga mkono mapinduzi ya Algeria dhidi ya Mkoloni wa Kifaransa pamoja na harakati zote za ukombozi wa Afrika.

Okello amekiri wazi kwenye uk. 15. 119 na uk. 130–131 wa kitabu chake Revolution in Zanzibar kuwa hakuwaamini Wazanzibari na wengi wa wanamapinduzi walitoka nje ya Zanzibar.

“Katika mwezi wa Agosti serikali ilialika mapendekezo kwa ajili ya jina jipya la 16. Jamhuri ya Muungano ‘ambalo litatowa maana ya kuungana na liwe rahisi kutamkwa. Zawadi kwa pendekezo litakalokubalika zitakuwa pauni kumi.’ Miezi miwili baadaye, Nyerere akatangaza jina liloshinda: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashindano yaliwavutia watu 1,534 kutoka nchi zaidi ya arubaini. Majina yaliyopendekezwa, mbali ya Tanzania, yalikuwa Tanzan na Tangibar. Siku tatu zilipita kabla ya serikali, katikati ya hali isiyojulikana, ikatowa taarifa fupi: tamko rasmi litakuwa ni Tan­za­ni­a.” Nyerere of Tanzania, uk. 130.

Mwana blogi kwenye blogi ya Issa Michuzi ameandika: “Mama Joan Wickens pia 17. alitaka kupewa heshima ya Lady eti kwa kulinda masilahi ya Uingereza nchini Tanzania! Lakini kakataa kwa sababu ingekuwa skandali kubwa kwa serikali…alikuwa one of the private secretaries wa Mwalimu!” Wickens alisomeya siasa, falsafa na uchumi kutoka Chuo

Page 415: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 383

Kikuu cha Oxford na alikuwa ni Msoshalisti aliyepelekwa Tanzania na chama cha Labour Party cha Uingereza na alifanya kazi kubwa katika kukusanya michango ya kukijenga Chuo cha Ideolojiya cha Kivukoni, Dar es Salaam, na alimsadiya Mwalimu Nyerere kuianzisha The South Foundation pamoja na Nyerere Foundation. Kwa mujibu wa Attorney­General wa Tanzania (1961–1965) Ronald Brown “…Joan alikuwa ni ‘kiyoo cha akili ya Julius Nyerere’ na katika kujihusisha na mawasiliyano yake, alikuwa ana kipaji cha ajabu cha kumuandikiya mambo ambayo yalionekana kama yeye [Mwalimu]. Aliandika muswada wa barua nyingi kwa viongozi wengine wa nchi pamoja na hotuba zake nyingi kutokana na mazungumzo mafupi naye” Wickens alifariki tarehe 5 Disemba 2004. Tizama http://www.tzaffairs.org/2005/01/joan­wicken/ Maandishi ya mwishoni ya Abdulrahman Mohammed Babu yanatowa mwanga mkubwa wa kifikra na sera za mapinduzi ya kiuchumi Tanzania na mifano mikubwa ya mageuzi ya kiuchumi ambayo Bara la Afrika linaweza kujifunza kutoka Uchina. Bahati mbaya maandishi yake hayamo kwenye lugha ya Kiswahili na hayajulikani kama ipasavyo na pande mbili za Muungano wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika.

Maelezo zaidi kuhusu mchango wa Masri katika Afrika na khasa Kongo unapatikana 18. ndani ya kitabu kwa lugha ya Kiarabu cha Mohamed Faiq ambacho kinaelezeya kwa urefu mchango wa Rais Gamal Abdel Nasser katika mapinduzi ya bara la Afrika. Faiq ana mlango kamili juu ya Abdel Nasser na mgogoro wa Kongo na vipi alivyotaka kumsaidiya na kumuokowa Patrice Lumumba na alishindwa isipokuwa aliweza kuwatoleya paspoti za Misri familia ya Lumumba kwa kuwafanya ni watoto wa mwanadiplomasiya Abdelaziz Ishaq. Tizama Mohammed Faiq, Abdel Nasir wa Thawra Al-Afriqiyya [Abdel Nasser and the African Revolution). Dar el Mustakbal Al­Arabi, Fourth Edition. 2002.

Mlango wa Kumi na Tatu

Fikra ya kabla ilikuwa Zanzibar ni mahala pa amani na ilikuja kubadilika pale chama 1. cha ZNP kilipochukuwa msimamo wa kumkumbatiya Rais Gamal Abdel Nasser na siasa zake za kibabe dihidi ya ukoloni na ubeberu na hilo ndilo lilomleta Misha Zanzibar. Miaka mitatu tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar Gamal Abdel Nasser alifanya uzembe ambao ulisababisha jeshi lake kuvurugwa na Israel na ramani nzima ya Mashariki ya Kati kubadilika. Tizama kiungo cha youtube: http://www.youtube.com/watch?v=zoTtGXkZuhY Mwezi wa Julai 2009 lobby mpya iitwayo A New Policy PAC ilianzishwa Marekani kwa madhumuni ya kuwaunga mkono na kuwapatiya pesa kwa ajili ya uchaguzi wanachama wa Congress ya Kimarekani ambao wataunga mkono sera ya dola mbili, ya Israel na ya Palestina Mashariki ya Kati. Lobby hiyo mpya imepokelewa kwa msisimko mkubwa na Wamarekani ambao wamechoshwa na mgogoro wa Mashariki ya Kati ambao umeyatiya sumu mahusiyano baina ya Waislam na nchi za Magharibi. Ni raia wa Kimarekani tu au wale wenye kumiliki “green card” ndiyo wenye haki ya kutoa mchango wa pesa kwa lobby hii mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na kuanzishwa na Mkurungenzi Mtendaji Sama Adnan. Tizama https://www.newpolicy.org/home.html Wazanzibari hawana haja ya kujiingiza kwenye migogoro mikubwa ya mafahali wa dunia. Nchi ndogo kama Zanzibar haina haja ya kujiingiza kwenye mgogoro mkubwa kama wa Mashariki ya Kati na kwa kuelemeya upande mmoja. Zanzibar itaweza kujisaidiya zaidi kwa kuzingatiya kujijenga upya kama ni kituo cha ilimu na cha uchumi baina ya Afrika Mashariki na Kati na Bara la Asia. Tizama kiungo kifuatacho cha maelezo muhimu ya Profesa Kishore Mahbubani cha youtube: http://www.youtube.com/watch?v=zIaVB­k7QlY

Page 416: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla384

Mlango wa Kumi na Nne

Moja katika athari kubwa za ukoloni wa nchi za Mgharibi juu ya Waislam ni utukufu 1. wa uzalendo (nationalism) wenye kuweka mipaka baina ya nchi na watu kuliko utukufu wa binaadamu mwenye kumcha Mwenye Enzi Mungu ambalo ndiyo fundisho sahihi la risala ya Uislam ambayo Waislam wameitupa baada ya kuufuata mwenendo mpya kutoka Magharibi ambao unadhoofisha udugu na mapenzi baina yao. Pia kikundi kidogo cha Waislam kimekuja na tafsiri mpya na kali ya Uislam ambayo ilikuja kuungwa mkono na kupewa kipaumbele na tafsiri nyengine kali kutoka Marekani kama inavyoonekana kwenye kiungo http://www.informationclearinghouse.info/video1037.htm Lengo kubwa lilikuwa la kuuzuwiya na kuushinda ushawishi wa Kikoministi katika nchi kadhaa za Kiislam na mwisho wake nguvu mbili hizo ziliungana kuipiga vita dola ya Kisovieti kupitiya Afghanistan na kwa kumtiya moto na mori Andrei Gorbachev kuubadilisha mfumo wa kisiasa wa Kisovieti badala ya kuubadilisha mfumo wa kiuchumi kama ilivyofanya Uchina. Kabla kuingiliwa Uislam wa Afrika Mashariki na tafsiri kali ya Uislam, Waislam walikuwa wakiishi kwa masikilizano na mapenzi na Waislam wenzao wa madhehebu tafauti na pia wakati huohuo waliwafanya wasiri wao viongozi ambao hawakuwa Waislam kuwaongoza katika kupiganiya uhuru wa nchi zao. Matokeo yake Waislam wa Tanganyika na wa Mwambao wa Kenya wakaja kugeukiwa na Nyerere na Kenyatta. La msingi ni Uislam baina ya Mogadisho na Kismayu, Zanzibar, Tanganyika, Mwambao wa Kenya, Uganda, Ngazija, nk, ulikuwa ni Uislam wenye kuongozwa na upole na hikma na ndivyo ulivyo mpaka hii leo kwa Waislam wengi wa Afrika Mashariki na Kati. Kupingwa kwa Mzee Karume kwa misingi ya kizalendo peke yake ndiko kulompa umaarufu Tanganyika na kuipa nguvu Tanganyika kuyaingiliya mambo ya Zanzibar.

Wakati wa mapinduzi “Hoodhood” alikuwa ni askari katika kikosi cha Police Mobile 2. Force (PMF) cha Dola ya Zanzibar na ametowa kwa mukhtasari maelezo muhimu juu ya kilichotendeka kabla na wakati wa mapinduzi ya 1964:

Miezi miwili kabla ya uhuru, Mngereza alileta manuwari za askari wake. Mojawapo ya manuwari hizo ilikuwa bandarini, na ndio ambayo ilimchukuwa George Mooring (Gavana wa mwisho). Kuwepo kwa manuwari hizo ni kisingizio cha kushiriki katika sherehe za uhuru. British Marines walifanya Mock Training mara tatu kwa kuivamia Kambi ya Mtoni na Ziwani. Huko ilikuwa ni kujaribu uwezo wa kambi hizo kuweza kujihami patokeapo uvamizi. Mara zote tatu kambi zote zilishindwa kujitetea katika uvamizi uliojaribiwa na British Marines. Hilo lilikuwa funzo zuri sana kwa adui kuweza kujuwa nguvu na uwezo wa kujilinda. Siajabu Mngereza alijuwa kuwa hatuwezi kujilinda patokeapo uvamizi kama ule aliofanya yeye na kuwaonesha maadui njia. Lakini serikali yetu, hawakujuwa…Na baada ya mapinduzi ni hao Marines ndio waliokuwa wakituhudumia sisi melini kwa chakula na venginevyo. Ni uhakika kuwa wao hawakuondoka katika eneo la Zanzibar bila serikali yetu kujuwa…Ni wao ambao (marines) waliotushawishi sisi kuweka silaha chini na wakatutengezea barua za ahadi ya usalama wetu hata kama sisi silaha tulizitupa baharini mbele yao. Siajabu kuwa Serikali yetu walikuwa hawana habari patokeapo uvamizi Mtoni na Ziwani nguvu za kujilinda na mavamizi zilikuwa ndogo sana.

Mimi binafsi “Hoodhood” pamoja na marehemu (mashahidi) Salim Nassor, Ishak Haji, Salim Muhamed, Hassan Hija, Abdullah Khamis, tulikwenda kumueleza Ali Muhsin akiwa pamoja na Dr. Ahmed Abdulrahman Baalawy (Waziri wa Afya) nyumbani kwake, ukumbini peke yetu, yale tuliokua tunayajua, na yale tuliokua tunayasikia, offers tulizopewa; vitisho vya maisha yetu, na ahadi za vifo tulivyo

Page 417: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 385

ahidiwa. Jibu lake kama kawaida na kama alivyokua akiwajibu wengine, eti kwani ni kikaango cha mboga. Majina ya wale waliokua wamepewa dhamana ya mipango ya kuivamia kambi ya Mtoni (PMF) na ambayo tulimpa ZAIM ni: Juma Maneno, zamani alikua Sajent, Khamis Microson, zamani alikuwa Koplo na baadae body guard wa A. A. Karume, Sajent Efedha, huyu alifariki katika daraja la Piki wakati yumo katika shughuli za kugawa mishahara ya wanajeshi Pemba, Antoni Mussa, huyu alikua Inspekta mshupavu sana.

Sgt Crispin nae alikufa Pemba katika ajali ya gari. Mimi na niliowataja ni watu wa mwanzo kufika Ziwani Police Barracks, hiyo siku ya siku. Tulitoka Malindi Police Station wakati tukijua kwa ukamilifu nini kinatokea. Tulifika hapo [Ziwani] wakati ghala ya silaha imo katika heka heka ya kuvunjwa…Mimi ujana wangu niliahidiwa execution [kuuwawa] kwa vile nilikataa kushirikiana nao. Walijua tulikwenda kumueleza Ali Muhsin. Sgt. Juma Mneno alinambia “Wewe Mpemba wewe, I will pull the trigger on your head.” …vilevile kwa mara ya kwanza naeleza…kua hichi kikundi ambacho kilikabidhiwa uvamizi wa kambi ya Mtoni…ni watu ambao tulikua tunafanya nao kazi wengine walikua walimu wetu, wengine walikua ni marafki zetu nao walikua wanatafuta support katika baadhi yetu, hivyo tukaweza kujumlisha na yale mambo mengine ambayo yalikua yako wazi mji mzima.

Mimi nimeingia Ziwani Barracks baada ya kupata habari ya kuanza machafuko nikiwa standby hapo Malindi Police Station. Nilifika Ziwani…nikiwa na Land Rover nne wala sio sita. Wakati huo bado ghala za silaha zinavunjwa. Ni alfajiri kizaa, hakuna alieweza kumuona mwenziwe. Nilipewa amri kutoka Malindi nitoke hapo Ziwani. Hali ya hewa ilikuwa imeharibiwa kwa tear gas. Gas masks zetu hazikusaidia ila kuhatarisha maisha zaidi. Kutoka kwetu hapo Ziwani tulipitia huko Maisara kuelekea Palace na njiani kupata ajali ya gari ya Abdul (Kumbaro)…hapo ndio tukabidi kubakia Mnazi Mmoja Hospital kwa ajili ya wale walio jeruhika. Tulipata orders kurudi Malindi kwa kupitia Saateni na Msikiti Mabuluu, na yaliotokea njiani ni hadithi ndefu mpaka kuweza kujiunga tena na wenzetu hapo Malindi Police Station. Inawezekana kulikua na wakubwa wa jeshi la polisi kule kwenye kijighorofa cha juu, orders nilizopata baada ya kufika hapo ”Take Position”…kilichokua kinatakikana, mobilisation, regrouping of others from PMF na Ziwani barracks pamoja na shaab [umma] ambao wengi sana walikuwa tayari lakini wanasubiri orders kutoka kwa wakubwa waliokuepo…ndani ya meli askari walikuwa wanapiga kelele tupelekwe Pemba. Hakuna aliekubaliana na hilo. Amri iliotoka ni kupigana na jamaa waliokuwa wakija. Tukiwa kama vijana wadogo sana, tukiwa na mafunzo finyu sana, tukiwa wengi wa wenzetu hawajapatapo kuona maiti ziliokufa kwa risasi, tukiwa wengi wetu waliojeruhiwa hapo Malindi, tukiwa wengi wao kosa kosa za risasi za Okello bado zinawajia ndani ya mawazo yao! Kitu chochote ambacho kimeandaliwa vizuri hufanyika vizuri. Kwa upande wetu hakuna kilichoandaliwa na viongozi wetu.

Alisikika mtangazaji kwenye Radio. Hapana shaka ilikua Sauti ya Unguja. Mara “Mimi ni John Okello ninawatangazia wale askari wote walioko pale Malindi kuweka silaha zao zote chini na haraka sana kujisalimisha kwa John Okello kiongozi wa mapinduzi na kama hawakufanya hivyo mpaka saa kumi na mbili jioni leo hii kituo cha Malindi hatuna budi kukipiga mabomu. Marehemu Juma Bukhety ambae alikua kidogo mbali na mimi pale chini ya daraja karibu ya Msikiti Mabuluu alikuja haraka sana pumzi juu juu, ‘Jamani mumesikia tangazo la Okello?’ Kabla ya kumjibu basi alijijibu mwenyewe ‘Loo, kumbe hapa Unguja wavutaji bangi tuko wengi. Sikiliza Hassan Hija mimi nina sigara moja ya mwisho, huyo sala tano (mimi) huwezi kuvuta mbele yake nifuate nikamalize risasi zangu.’ ” Baada ya kurushiana risasi kwa hali ya juu sana, maana baada ya tangazo lile uwanja

Page 418: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla386

wa mapambano ulibadilika. Okello alimimina wachafuzi kama vile alikua hana kheri nao; Walikua wanakuja pale eneo la Malindi kama vile wamefunga macho. Tulikubaliana na wenzangu kwamba hawa ni insurgents [waasi]. Bahati ile team ya sharp shooters wote walikua wamejipanga katika eneo moja na kila mmoja alikua karibu sana kuwasiliana na mwenziwe…Subhana Allah, kwenye shari Mola nae huteremsha kheri zake. Ile neighbourhood ya Malindi yote kila nyumba ziliteremka sahani za kila aina ya chakula na tukaweza kustirika kwa hio riski Mola alio tuteremshia bila ya tegemeo. Hali ilipozidi kua mbaya nilishauriana na jamaa baada ya kuwaacha kuvuta sigara zao, kua ni bora kwenda juu ofisini mmoja wetu na kuona kama kuna lolote jipya. Ali Abdulrahman (Uthant) akajitolea kwenda kuonana na wakubwa na kusikiliza kama kuna lolote jipya na kweli aliporudi alielezwa kwamba tutayarishe askari wa kwenda kuongeza ulinzi hapo Palace. Wakati hali hio inazidi kutukera kwa wingi wakutupiana risasi, tulifikiria kwenda kumuona Dr Ahmed Abdulrahman Baalawy pamoja na marehemu Ustaadh Abadhar Juma. Hao walikua ni Mawaziri ambao tulikua nao sana katika enzi za kheri…Salim Muhamed (Mabavu), Ishak Haji, Hassan Hija, Ali Rukun, na wengine walipoteza maisha yao; kwa kukosa busara…na ukosefu wa ushauri.

Tuliamrishwa kwenda bandarini bila kujua nini kinachoendelea. Mwenzangu Abdullah Khamis (Tembo) aliniuliza “Hivi ndio biashara imemalizika hapa?” Nilimjibu bila kufikiri, “Mimi sijui.” Kulikua na meli mbili bandarini: MV Khalifa na MV Salama. Lile kundi langu tuliambiwa kuingia MV Salama na wengine waliingia ile meli ya pili. Sijui ilikwisha pangwa au ilisadifia. Sihaba vijana wangu wote nilikua nao katika meli ile MV Salama. Usiku ule ule tulivamiwa tena. John Okello na watu wake walitufuata mpaka melini. Ajabu, meli ilibakia katika eneo hilo hilo hapo bandarini. Karibu boti nne ndogo ndogo ziliizunguka meli yetu na huku risasi zikaanza tena upya. Mara left handed, sharp shooter Tembo akaanza “Nilisema mimi biashara bado haijamalizika.” Sikuuliza zile boti zilirudi au ziliishia wapi. Leo miaka 43 namtafuta Tembo anieleze kisa cha boti zile namna zilivomezwa. Alfajiri ya siku ya pili meli yetu ilikua kidogo nje ya bandari karibu na Mtoni bali kabla kufika Beit Ras hapo iliwekwa nanga na mara tulipandiwa na Royal Marines nao walitoka katika manuwari HMS Messina ambayo haikua mbali na bahari ya Zanzibar siajabu wiki nzima kabla ya machafuzi…tuliletewa breakfast nzuri sana. Meli nyengine ambayo hapana shaka Jamshid na aliokua nao walikua katika meli hio walikua hawapo katika eneo la Zanzibar. Wakuu wa Polisi na wakuu wa serikali Wallahi sikumbuki kumuona yeyote ukiwaacha hao tuliowaacha nyuma…tuliokua katika meli hio wale wale vijana ambao walikua tokea juzi alfajiri tuliokua tukirushiana risasi na akina Eddington Kisasi; Juma Maneno, John Okello, Macomrades na watu kama hao ambao kila mmoja wetu alikua anataka kumtoa mwenzake roho tena kwa risasi (jamani kiumbe mzito). Meli MV Salama ikiwa katika matayarisho ya kusogea gatini, maofisa wa Royal Marines wakiwa pamoja na kundi la wachafuzi wamesimama mbele yetu, amri ilitoka kwamba baada ya kupata barua zetu za kutuhakikishia usalama wetu sasa ni kusalimisha silaha zetu. Kabla kuteremka melini, hapo niliona mabadiliko ya nyuso za jamaa na haraka sana nili nusa matatizo na hasa wasi wasi wangu ulikua juu ya Ahmed Guliva na Abdullah Khamis (Tembo) hawa walikua watu wa sigara kubwa na mara walikua tayari kufanya mambo ya ajabu. Na kweli mara nilimsikia Guliva akiwa ana sigara yake ya biri mdomoni akisema “mimi sitowi silaha yangu.” Hapo nikajiuliza nakuwa tayari kwa mripuko. Mohamed Juma (Mawingu) naye akasema “na mimi yangu sitowi.” Watu hawa ilikuwa hakuna anayeweza kusema nao. Wakiamua, wameamua. Guliva bila hili wala lile alifungua magazine yake akatoa risasi zote na kuzitupa ndani ya

Page 419: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 387

maji huku akifuatiwa na Tembo na bunduki zao zote kuzitosa baharini. Mawingu naye kwa sauti ya kutisha alisema, “Munangoja nini?” Wakati haya yanaendelea kila mmoja kwenye meli amenyamaza kimya wakiangalia actions za vijana wetu mmoja baada mmoja vijana wanavyofanya. Baada ya wote kutosa baharini silaha zetu na hakuna aliesubutu kuzuwia kitendo hicho, Muhamed Mawingu alisimama na kupiga kigelegele “PMF Hurray,” “PMF Hurray,” “PMF Hurray.” Royal Marines labda walifahamu maana ya kitendo kile kwani walijibu kwa kupiga makofi kama kwamba na wao wanasherehekea. Tuliteremshwa melini kama ngombe wa bara bila silaha bila nyuso za kuitizama Unguja. Hapo bandarini kulikua na ulinzi wa hali ya juu. Hapakua na dalili ya raia bali ni wanajeshi watupu waliokuepo hapo na mji mzima yaonekana ulikua na ulinzi wa hali ya juu kwani hata ile siku alionyongwa Saddam Hussein, Baghdad, haikua na ulinzi kama ulinzi tuliouona siku ile. Tulipakiwa ndani ya malori na tukatupwa Ziwani Barracks na siku ya tatu yake tukenda kuonana na His Excellency A. A. Karume (the father), Ikulu. Chini ya ulinzi mkali sana baada ya kufika tu Mheshimiwa alitoa hotuba kali sana ya kututukana sisi wote na baadae akatwambia “Nani kasema kua nyie mutafanya kazi jeshini? Alaa! Kazi zimejaa tele kila pahali lazima jeshini?” Mpaka leo ndio ukaona bado kuna ndugu zetu wanazeekea Shirika la Umeme, Said Abdullah Tumbo, Sharrif Muhamed Shehe, Saleh Muhamed. Leo miaka 43 bado wanasugua na Shirika la Umeme mshahara shilingi 20,000. Baada ya hapo wengi wetu His Excellency alitupeleka jela. (Kutoka kwa “Hoodhood” kupitiya mtandao wa Zanzinet, Septemba 2007.)

Maelezo ya Ali Khamis Musa (Baucha):

Sasa Hassan Mandera na Det Sgt Bison, haijakuwa kama ni coincidence kuwepo hapo Malindi Station usiku ule.Walichaguwa zamu/Roster makusudi ili wao wawepo hapo, na waweze ku influence the events as they happen. Ilikuwa imeshapangwa lakini hawajafikiriya kama sisi tutafika hapo mapema sana, na tutafika well armed. Hawaja expect reaction na swift reaction time. Kilichowazuiya wao ku implement ile plan yao ni sisi tuliokuwepo ndani na pale juu kwenye ghorofa Malindi Station. Syd Majid Barghash, Sh. Salim Ahmed Busaidy, Sh. Mohammed Said Riyami, Sh. Ahmed Seif Kharusi, Sh. Hilal Mohammed wa Bububu baba yake Hemed Hilal, Sh. Said Badar, Sh. Mohammed Msellem, Sh. Salim Humoud Kharusi na mimi Al Fakir [Ali Baucha]. Sisi ndio tuliye kuwa ndani na juu kwenye zile parappets, na kuona mbali zaidi.

Sasa sisi tuli wa out number hao akina Hassan Mandera. Ilikuwa baada ya muda tu na wao wachukuwe khatwa kabla Commissioner au Prime Minister hawajawahi kuji—establish pale Malindi. Walipoona mambo kidogo yamebadilika wakaakhirisha zile plans zao, au Malindi station ingekwenda kama kambi nyenginezo. Mandera ingekuwa wanataka kuwapiga hao waliopo hapo nje ingekuwa mara moja kuwamaliza. Wangengojea attack ije kutoka Raha Leo, kwa upande mmoja, na wao kwa upande wa pili, pale juu wakawapiga hao kina “Hoodhood” na Sh Salim Ahmed, wao wakajifanya kama wanawapiga hao watu wa Raha Leo, kumbe huku wanawapiga watu wetu. Nani angejuwa katika zahma zile? Kila mmoja anapiga risasi, noise and confusion.

Sh. Salim Ahmed na Sh. Mohammed Said Riyami, asubuhi 0700 hrs walishuka chini na wakakaa pale Hollis Bridge khasa. Mwanzo wa bridge, wameelekeya Mlandege na Mchangani. Na kupambana na magari yaliokuwa yanataka kuja hapo Malindi.

Ya kisha pita ile nyumba sasa ya Bakhresa na kuanza lile jaa kushoto. Hapo

Page 420: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla388

ilikuwa ndio front line. Ama wasimame au wanasimamishwa kwa nguvu, na hao wawili kwanza. Ikiwa wameweza kuwapenya zaidi hawamalizi ile bridge mpaka kwenye junction [njia panda]. Tunawasimamisha sisi…na wanaotokeya Darajani? Area of operation na front line ilikuwa Hollis Bridge kuelekeya Msikiti Mabuluu, na Hollis Bridge kuelekeya Darajani. Gari za wanamapinduzi, black police mini bus za kuchukuliya askari kama kuwapeleka pale palace kwa ajili ya zamu au kuwapeleka band stand Forodhani. Zilipita Msikiti Mabuluu mpaka Hollis bridge pale kwa Bakhresa halafu sisi tukazisimamisha. Hawamalizi kwa Kapadia Motors, kama ile gari ya marehemu Superitendant Sketty. Sh Said Nassor Al Oufy ambae akifanya kazi pale fisheries plant. Alikuja na Sh Ahmed Seif na Sh. Mohammed Msellem. Sijui bunduki aliipata wapi lakini alikuwa nayo. Sh. Juma Hemed Jabir Al Farsy alikuwa Sub Inspector of Police akafukuzwa kazini pale Ng’ambo Station, kabla ya Mapinduzi. Alikuja asubuhi sana at 0700 hrs mikono juu na hata yeye Mandera alitaka kumpiga. Tukamwambiya angojee kidogo maana tunamjuwa na mikono yake ipo juu. Mandera mimi alitaka kunipiga mara mbili lakini Sh. Mohammed Msellem na Sh. Said Badar walimzuiya. Mimi nilikuwa paa la chini karibu na ile bank, wao wapo juu paa la pili. Juma, nadhani akarejeshwa on duty na akawa promoted on the spot to full Inspector of Police. Na nadhani Sh. Salim Hakim, akawa promoted to Superitendant on the spot. Inaweza kuwa nimekoseya.

Superitendant Sh. Salim Hemed Al­Barwani alifanya kazi kwelikweli pale. Sh. Abdullah Soud Bin Ali Al­Busaidy kutoka Mombasa alifanya kazi kweli kweli lakini hajaweza kukaa pale Malindi kwa sababu ya Sh. Ali Muhsin. Alikuwa akimlinda na yupo ubavuni kwake all the times. Abdullah Soud, yeye ndiye aliyekuja nyumbani kwetu Malindi na kunizinduwa, kama sasa hivi, hii ni for REAL, na nichukuwe vitu vyote nilivyokuwa navyo na niende Malindi Police Station. Order and request from Sh. Ali Muhsin. Abdullah kaniambiya, sasa hivi hakuna tena kama ni halali au si halali kuhusu weapons [silaha], na kila weapon kwa sasa hivi halali, hivi ndio Sh. Ali alivyosema pale alfajiri 0300 hrs au just before maybe 0230 hrs. Time siikumbuki vizuri. Sh. Said Kharusi alikuja Malindi lakini hajakaa sana na akaondoka na kurudi Mnazi Mmoja pale nyumbani kwa Bw Abdullah Mzungu, next house to Sh Ahmed Seif Kharusi. Nadhani baada mambo yalivyokuwa makubwa waliondoka hapo Mnazi Mmoja au Kikwajuni, na kwenda nyumbani kwa Said pale Soko Muhogo, ubavuni kwa Bw Khamis Mayai.

Tulipotoka Malindi Police Station kwanza tulipanda MV Salama pale gatini. Na tukaingojeya MV Khalifa irudi kutoka Mombasa. Ilipofika MV Khalifa tukabadilisha meli na tukapanda Khalifa. Akina “Hoodhood” na Supt Sh Salim Hemed wakabakiya kwenye Salama. Ilipokuwa wale jamaa [wanamapinduzi] wakaanza kujiamini na kuweza kupenya mjini na kufikiya Forodhani siku ya pili hiyo. Captain na Mr Sullivan wakashauri tusogee mbele au turudi nyuma kidogo karibu na kule bahari kubwa baina ya Chumbe na kile kisiwa chenginecho sio Prison Island. Halafu ikaja shauri kama twende Mombasa. Lakini majority katika sisi vijana, hatukuwafik hayo. Tukasema tuende Pemba. Kwa sababu Pemba bado na kwa sababu Pemba majority ni ZPPP na ZNP.

Idea na fikra yetu ikatupwa na wakubwa na wakaamua tuende Mombasa. Royals na wengineo walifikiri labda Kenyatta au wengineo watatupa msaada. Tulipofika bandari ya Mombasa hatukupewa ruhusa mtu yeyote yule kushuka. Meli ikazungukwa gatini na GSU na kwa baharini na boti za navy. Aliachiwa mtu mmoja tu kupanda na kuja juu, kuonana na HM Sultan. Huyu ni yule kijana aliyekuwa UN Ambassador wa Oman ndugu yake Fakhri na Fahad al Hinai mtoto wa Liwali wa Mombasa wa wakati huo. Alituleteya chakula, mbatata na maji na mayai. Tukala mayai na chips.

Page 421: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 389

Maana chakula kilianza kupunguwa melini.Seyyid Mohammed, alitustajabisha, alisema: “Alaa? Mimi nilidhani Kenyatta

atafanya Uislamu na atatuachiya tushuke?” Juma Hemed akashtuka kusikiya maneno haya. Alaa! Nyinyi mulidhani nini? Huyu Muafrika Kenyatta atukupeni msaada au atakuwa na huruma kwetu? Muulize Juma mpaka kesho atakueleza. Lakini Juma ni pro royalist, lakini alishtushwa alivyosikiya yale maneno. Maana sisi sote vijana melini tulikuwa tayari tuichukuwe meli kwa nguvu na tuipeleke Pemba na halafu Somalia tuchukuwe silaha na turudi tena Pemba. Muulize Captain Shillingi ata confirm haya. [“Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Joseph Murumbi alikataa Sultan kushuka Mombasa kwa kuogopa kuchocheya maandamano ambayo yangelifanywa na jamii kubwa ya Kiarabu na maandamano dhidi yao ambayo yangeliifanya hali kuwa ngumu,” The National Archives, DO 185/59 116805].

Basi tulipoondoka Mombasa tukarudi tena Zanzibar na pale bandarini lakini sasa tukakaa mbali zaidi. Ilipofika usiku tukaelekea Kaskazini tena na Nungwi. Tukazunguka halafu tukaelekeya Kusini kwenda Kiwengwa, Makunduchi, Kizimkazi, na baadae Dar es Salaam. Wakati wote huu communications zilikuwepo baina ya meli na Royal Navy na British High Commissioner Zanzibar, Dar es Salaam na Nairobi.

Kabla hatujaingiya bandari ya Dar es Salaam, Commissioner na wakubwa wa Polisi walitupigisha foleni na parade. Wenye uniforms upande wa kuliya na wasiyo na uniforms na civilian dress upande wa kushoto na tuka March mpaka strong room ya meli, na tukaambiwa tu hand in all our weapons for safekeeping. Zitakapo hitajiwa tutarejeshewa. Tukafuata amri na tuka surrender zote na bullets zote. Lakini ndio tungelifanya nini Mzungu kavaa pistol kiunoni. Na hakuja local officer wetu kusema no! Do not hand in your weapons. Wote walikaa kimya. Salim Hakim na Mohammed Issa Mugheiry. Basi bora tungemfuata “Hoodhood” na tukazitosa silaha zote baharini na wasingezipata tena.

Tulipofika gatini Dar es Salaam wakapanda police officers na FFU na wakatu search sote mmoja mmoja kabla kushuka ngazi melini na kuteremka gatini. Sote tulisachiwa. Body search. Baadae British High Commissioner reps wakaja na wakatuchukuwa huko Oyster Bay Govt Houses. Tukakaa hapo sote pamoja, Lakini HM alikuwa nadhani pale juu. Baada ya siku tatu au nne usiku wakaja reps wa British High Comission na wakatuambiya tufunge funge virago vyetu na huenda tukasafiri. Jee wapi mutataka kwenda? Zanzibar au UK au wapi? Nikaona hili ni trick question. Niseme Zanzibar na watanirudisha Zanzibar au jela? Sote tukasema anakokwenda HM na sisi tutakwenda huko huko. Juma pia alisema hivyo hivyo. Alfajiri zikaja gari za British officers na police na zikatuchukuwa mpaka Dar Airport, na moja kwa moja to the plane. Kumbe wakati ule ndio KAR mutiny ipo in full swing, sisi hatujajuwa wakati ule. Tuliondoka asubuhi na mapema jua ndio kwanza linachomoza tukatiwa ndani ya landrovers kama 10, mini bus na gari moja ndogo kuelekeya airport.

Tukaruka alfajiri, na tuka stop Nairobi, hapo wakaja family ya HM na family ya kina Seyyid Jeiffar bin Seif, actually Bi Shuruq na family yake, ambao hawajawahi kuondoka kwa meli, maana meli ilirudi Zanzibar kwa haraka. Baada ya kuruka Nairobi tuka re fuel Khartoum au Aswan, na moja kwa moja mpaka Manchester Airport. Maana London Heathrow kulikuwa na fog [umande] kubwa sana.

Alikuja hotelini Sh. Ahmed Sharrif Al Bakry na akakaa na sisi mpaka tulipoondoka Manchester kwenda zetu London. Kutoka Manchester tukachukuwa train mpaka London tukakaa Buckingham Gate Hotel kwa wiki moja karibu na Scotland Yard Headquarters na wengine Ambassador Hotel karibu na Earlscourt. (Mawasiliano na mwandishi, 3 Novemba, 2008 na January 2010.)

Page 422: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla390

Naibu Balozi wa Kiingereza, Dar es Salaam ameandika kwenye telegram yake kwenda Commonwealth Relations Office kuwa:

Mpaka sasa hivi Watanganyika wamemtizama Sultan na watu wake kwa vizuri na kwa hishma. Kundi la watu lilikusanyika bandarini na kuna waliyozomeya pale msafara wa magari ulipoondoka. Kulikuwa na jeshi la polisi lenye nguvu na hakukutokeya kitu. Lusinde aliwakera waandishi wa habari na maripota wa Televisheni kwa kukataza wasichukue picha au kufanya mahojiano. Carter na mimi tuliwashindikiza kwenye nyumba na katika mazungumzo ya mwanzo na Sultan na ndugu yake Prince Mohammed na watu wao tuliwaona kuwa walikuwa wameghumiwa kabisa. Walihisi kuwa mahala pekee ambapo wangeliweza kwenda ni Uingereza na kila ikiwa mapema basi ndo vizuri. Wote wanataka kwenda Uingereza—na wanasema hawana pesa na wao au kokote nje ya Zanzibar. Smithyman, Katibu Mkuu katika ofisi ya Waziri Mkuu Zanzibar ambaye kwa sasa yuko Dar es Salaam amehakikisha kuwa ni kweli. Lusinde sasa anazungumza na Kawawa kuhusu hatua ijayo. Wakati tunasubiri nashauri njia nzuri ni kuwasafirisha watu wote 43 [wakiwemo watoto 18] wende Uingereza kwa ndege ya kukodi. Tatizo nani atalipa. Sitarajii Watanganyika watajitoleya na sihisi kama tunaweza kuwaomba. Wanaweza wakahoji kuwa hii ni zawadi duni kwa kutukubaliya kumpa Sultan uhamisho na njia za muda za kusafiriya wakati Kenya waliokataa kumpa himaya hawalipi kitu. Nataraji utanikubaliya kwa haraka kuilipiya ndege ya kuwachukuwa. Ni bora wakaondoka mapema iwezekanavyo. Sultan na watu wake waliwekwa kunako nyumba mbili za Serikali, kulishwa, na kupewa ulinzi na Serikali ya Tanganyika. Wao wenyewe hawataki kukaa na ni fedheha kwa Watanganyika na sisi. (HO 344/309, 15th January 1964.)

Ndege (GAOVM, Flight No. 3376) ililipiwa pauni 11,000. Walipofika uwanja wa ndege wa Manchester Ofisi ya Mambo ya Ndani ilitowa amri kuondowa taratibu za mambo ya uhamiaji na ya afya. Watu wawili tu ndiyo waliyokuwa na pasipoti lakini hawakuombwa kuzitowa. Sultan na familia yake wakapelekwa kwenye ukumbi wa V.I.P. na maofisa wa Manchester Corporation. Walikuwa hawana nguo zaidi ya za mwilini na khasa kwa ajili ya baridi. Salvation Army ilitowa msaada wa nguo. HO 344/309.

Haya yameandikwa kwenye kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Al Barwani 3. Kujenga na Kubomolewa Zanzibar (Kumbukumbu), uk. 245.

“Mambo ya ndani” na “serikali ya wacahache” zilikuwa ni sera mbili ambazo 4. Muingereza alizing’ang’aniya katika kukataa kuinusuru Zanzibar kutokana na maafa ambayo wangeliweza kuyazuwiya. Pili, ilikuwa ni kujenga boma la hoja kuwa hakukupelekwa watu kutoka nje ya Zanzibar wakati ushahidi wao wenyewe unaonyesha kuwa walijuwa lakini walitaka kuilinda Serikali ya Tanganyika ya Julius K. Nyerere. Pia wakitambuwa kuwa Washirazi ambao ndio wengi Unguja na Pemba, walivipigiya voti vyama vya ZNP na ZPPP lakini Waingereza walipendeleya kuwaona kuwa ni wageni na kuwatizama wageni kutoka Tanganyika kuwa ni wenyeji Waafrika ambao ndio wenye haki zaidi juu ya Zanzibar.

Waliyotajwa ndani ya kitabu cha Sheikh Ali Mushin ni hawa wafuatao: Ahmed Seif 5. Kharusi, Muhammad Said Kassim, Salim Ahmed Busaidi, Muhammed Msellem Rawahi, Ali Khamis Musa (Baucha), Said Badar, na Hilal Muhammad (wa Bububu), Ali Muhsin Al Barwani, Kujenga na Kubomolewa Zanzibar (Kumbukumbu), uk. 248.

Ripoti za maofisa wa Kiingereza waliyokuwapo Zanzibar wakati wa mapinduzi 6. wanailaumu Serikali ya ZNP­ZPPP kwa kutolizingatiya ipasavyo suala la usalama na ulinzi wa dola pamoja na kukiri kuwa waliyadharau mambo mengi ambayo walikuwa wakiambiwa na kuombwa na serikali iliyopinduliwa. Mengi kuhusu suala hili muhimu yataelezewa kwa upana mkubwa zaidi katika milango ya baadaye.

Page 423: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 391

Katibu Mkuu katika ofisi ya Waziri Mkuu Mohammed Shamte, Mervyn Vice 7. Smithyman, ameandika kwenye ripoti yake juu ya mapinduzi ya Zanzibar: “Wiki chache tu zilizopita, Kamishna wa Polisi aliandika barua kuomba fedha kujenga ghala ya silaha ya kisawasawa kwa sababu ghala iliyopo kwenye makao makuu ya polisi ilikuwa katika nyumba kongwe ambayo ilifanyiwa marekebisho kidogo. Kwa shida niliweza kupata ruhusa ya kupewa fedha kwa mradi nyeti kama huu, ina maana katika matawi mengine ya Serikali kulikuwa hakuna muamko juu ya umuhimu wa suala la usalama wa nchi. Tena, tulikuwa tukifikiriya kwa muda mrefu nguvu za jeshi la polisi na Jumatatu tarehe 13 Waziri Mkuu alikuwa aonane na baadhi ya wenzake, mimi na watu wa fedha kujadili mfuko wa fedha kwa lengo la kuliongezea nguvu jeshi la kawaida la polisi, ‘special constables’ na ‘police mobile force’ [PMF]. Kitengo cha fedha kilikuwa kimeshaweka kwenye kumbukumbu za mkutano [minutes] kuwa hakutotolewa fedha kwa lengo hili. Tena, baada ya uhuru, nilizungumza mara sita na Waziri Mkuu kwa kumfahamisha kuwa vikosi vyetu havitotosha iwapo patatokeya fujo kubwa na kumnasih aishauri Serikali ya Kiingerea, au Serikali ya Kenya, kujaribu kufunga mkataba au maandalizi ya aina yoyote ya kuongeza nguvu. Baada ya kumkumbusha kwa mara ya sita ndipo alipofanya mpango wa mazungumzo na Balozi wa Kiingerza na Ali Muhsin na mimi juu ya maudhui hiyo. Barua ilipelekwa kwenye Serikali ya Kiingereza. Bahati mbaya, Serikali ya Kiingereza ilijibu kuwa hawatoweza kuukubali mkataba wa aina hiyo. Waziri Mkuu, juu ya kumshinikiza kwangu, alikuwa hayuko tayari kuruka kwenda Nairobi kuzungumza na Jomo Kenyatta juu ya suala hili.” “Report by Mervin Vice Smithyman, Permanent Secretary to late Prime Minister Zanzibar, dictated on Thursday, the 16th January 1964,” DO 185/59 116805, uk. 5.

The National Archives, “Abdulla Kassim Hanga” CO 8. 822/3232. Ripoti ya R. L. Speight, Head of Special Branch, Zanzibar Police Headquarters ya tarehe 12 Septemba, 1963, haina taarifa yoyote muhimu juu ya Hanga na kuhusika kwake na upangaji wa mapinduzi yaliyofuatiliya miezi michache baada ya kuandikwa kwa ripoti hiyo. Ripoti ya Hanga inaelezeya kuwa tarehe 23 Novemba mwaka 1959 polisi ya Zanzibar katika upekuzi wake iliikamata barua ambayo iliandikwa na Hanga: “Nukta yangu ya pili ni kukuarifu kuwa nitakuwa mtu wa kwanza kumfukuza Chifu Khalifa bin Harub, yule mbwa mwenye ndevu. Hii leo, Urusi haitoogopwa na hawa wizi wa haki za uzawa za Waafrika, wamwagaji damu za Waafrika, madhalim wa Waafrika, wauwaji wa Waafrika, ingelikuwa hawajaung’owa ufalme nchini kwao. Ni jukumu langu kuwa wakati ukifika lazima niuongowe ufalme kutoka Zanzibar. Hakuna sababu ya ufalme kuwepo Zanzibar wakati mwanzoni wazee wetu wa kale wakiishi kwa ‘usoshalisti’ na ‘ukoministi’ na kwa sababu hiyo sioni sababu ya kuwepo ufalme Zanzibar. Katika jambo hilo kumbuka kuwa ukinipa nguvu kitendo changu cha kwanza kitakuwa kuung’owa ufalme. Sioni jambo moja la kheri ambalo Sultan wako, Khalifa bin Harub aliloifanyia Zanzibar au Pemba. Ni mtu ambaye hajaleleka, anakula na kunya bila ya kufanya kazi yoyote ile. Anaishi katika palace bila ya sababu yoyote. Anapewa mshahara mkubwa na hafanyi kazi, anafanya […neno chafu] na yule […neno chafu] na anakula vyakula vizuri wakati Waafrika wanakufa na njaa. Nambie nini faida ya mtu kama huyu kwa nchi? Mimi ni…(neno chafu) kama sitoung’owa ufalme utakaponipa madaraka. Mshenzi aliyekuja kutoka Maskati,……..(neno chafu) amekuja kuishi kwa raha Zanzibar wakati Waafrika tele wamekumbwa na njaa na hawana pa kulala.” Kubwa walilolifanya Waingereza ni kumnyang’anya Hanga pasipoti katika mwezi wa Januari 1963 baada ya kusema maneno ambayo alikuwa hapaswi kuyasema alipokuwa nje ya Zanzibar.

Assistant Inspector Pandi, an Indian expatriate and very anti­Arab uhuru ulipokuja 9. alistaafu na akanipa anwani yake na kuniambiya: “Niandikiye barua baada ya mwezi mmoja.” Ofisa wa polisi wa Kizanzibari (jina nimelihifadhi).

Ilibidi askari wa polisi kutoka Kenya (Albert Kadenge and Joseph Peter) waondolewe 10.

Page 424: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla392

Zanzibar kwa sababu waliwauwa watu wengi katika kuihami kambi ya jeshi la polisi la Ziwani. Ofisa wa polisi wa Kizanzibari (jina nimelihifadhi).

Baada ya kupinduliwa Nyerere katika Januari 11. 1964, Balozi Msaidizi wa Kiingereza, Dar es Salaam alimuuliza Kambona kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Nje na Ulinzi wa Kiafrika, ambao ulipangwa ufanyike Dar es Salaam. Ameandika Naibu Balozi wa Kiingereza kuwa Kambona:

Alisema kuwa sababu kubwa ni kumfunga kinywa Nkrumah ambaye angeliyatumiliya machafuko ya Afrika Mashariki kwa maslaha yake. Alikuwa amejaribu kila awezavyo kuivuruga mipango ya Shirikisho la Afrika Mashariki na Watanganyika wakiogopa kuwa sasa atajaribu kuonyesha kuwa kitendo cha Serikali za Afrika Mashariki kuyaita majeshi ya Kiingereza inaonyesha kuwa zimo ndani ya mfuko wa Waingereza. Kwa hiyo Watanganyika wanataka kuungwa mkono na Serikali za Kiafrika kwa uamuzi wao wa kuyaita majeshi ya Kiingereza. [Serikali ya Tanganyika pia iliwaarifu maofisa wa Kiingereza kupitiya Kambona kuwa haina nia ya kuyaalika majeshi ya Kiafrika kutoka Ghana au Algeria kusaidiya kuweka usalama na kulijenga upya jeshi la Tanganyika na wataliomba jeshi la Nigeria.] The National Archives, “Inward Telegram to Commonwealth Relations Office” DO 216/47, 30th January 1964. [Balaozi wa Kiingereza, Dar es Salaam alipeleka telegram Uingereza iliyomaliziya kwa kusema]: “Akaongeza [Kambona] na kwa ukali kuwa ana hakika kuwa hataki majeshi kutoka Ghana,” The National Archives, tarehe 5 Februari 1964, DO 213/236.

John Okello ametoa idadi ya watu 12. 11,995 ambao waliuwawa kwenye mapinduzi ya Zanzibar. Okello alikuwa ni mtu wa kutia chumvi na inafaa ikumbukwe kuwa kitabu chake kiliandikwa baada ya kufukuzwa kwake Zanzibar na aliona iko haja ya kuonyesha ushujaa wake na umwagaji damu uliyofanyika mpaka ilipopatikana serikali ya kimapinduzi. Kudhulumiwa roho ya binaadamu mmoja bila ya haki ni dhambi kubwa kwenye dini ya Kiislam na ya Kikristo lakini inavyoonesha Okello alikusudiya kusema kuwa watu wengi waliuwawa kwenye mapinduzi na hakuna ushahidi wowote wa kwanini au vipi aliweza kuifikiya na kuitangaza idadi hiyo. Ni vigumu sana kupata idadi sahihi ya watu waliouwawa katika mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Mazingira ya kuandikwa kwa kitabu cha Okello yanahitajiya utafiti zaidi na khasa mchango wa Cylde Sanger ambaye ni mwandishi wa utangulizi wa kitabu cha Okello ambacho ni kwa lugha ya Kiingereza. Okello aliandika dibaji ya hicho kitabu katika mwezi wa Juni 1966 wakati yuko Jela ya Kamati, Kenya. Ilikuwaje mpaka akaweza kupewa nyenzo zote hizo? Kuipotosha historia ya Zanzibar kwa kutowa kitabu cha kwanza kuhusu mapinduzi ambacho kimeandikwa na “Field Marshall” wa mapinduzi ya Zanzibar?

Meli ya H.M.S Owen imeweka kumbukumbu kamili ya matukio ya mapinduzi 13. na imesajili kuwa “Saa tatu za asubuhi siku ya Jumapili, tarehe 12 Januari 1964, meli ya H.M.S. Owen ilitiya nanga nje ya Malindi kwa mapumziko mafupi ya mwisho wa wiki ilipopata taarifa wende kwa haraka Zanzibar na kuwa kundi la watu wameishikiliya Makao Makuu ya Polisi pamoja na silaha na risasi. Kazi yetu ilikuwa tuwahifadhi—na tuwaondowe ikiwezekana—raia wa Kiingereza waliyoko Zanzibar na tusiingilie kwa njia yoyote ile. Wakati iko njiani na meli 8 kutoka Zanzibar, OWEN ilikutana na meli ya Sultan iitwayo SEYYID KHALIFA; baada ya mazungumzo juu ya meli hiyo baina ya Kamanda D. W. Haslam, Royal Navy, na Kamishna wa Polisi wa Sultan, ilifahamika kuwa Sultan na ndugu zake wawili wa kiume na wake zao na watoto 20 wa Sultan walikuwemo ndani ya meli, pamoja na abiria 300 wengine na nusu ya jeshi la polisi waliyokuwa watiifu. Meli iliondoka baada ya kupokeya taarifa ya ghafla wakati Sultan walipokimbiya katikati ya risasi kiasi ya

Page 425: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 393

saa tisa za mchana; inapokuwa haitumiliwi na Sultan, meli ya SEYYID KHALIFA kwa kawaida hutumika kama ni meli ya mizigo na abiria na imeondoka bandarini na mahitajiyo kidogo kwa sababu ilikuwa ndio kwanza imemaliza safari ya Tanga na iliondoka mara tu baada ya kuzipata taarifa kuhusu mapinduzi.” “Diary of Events in Zanzibar 12th 17th January as Recorded on Board H.M.S. Owen Zanzibar Revolution” DO 185/59 116805, uk. 1.

Hili baadaye atakuja kulihakikisha Mervin Vice Smithyman.14. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu H.M.S. Owen ilikuwa imeshapewa amri 15.

isiingiliye kurudisha utulivu Zanzibar na Kamanda Haslam na Kamishna Sullivan wa jeshi la polisi la Zanzibar walikwisha onana kwenye meli aliyokuwemo Sultan Jamshid.

Fikra hii piya ilipingwa na Balozi wa Kiingereza Hawker na alipeleka ujumbe wa 16. simu kwenye meli ya MV Seyyid Khalifa wa kuwataka maofisa wa Kiingereza waliyokuwemo ndani ya meli wasiombe msaada kutoka chanzo chochote kile. Ushahidi wa haya uko kunako mlango wa huko mbele.

Hijra ni safari aliyoifanya Mtume Muhammad (sala na salamu za Mwenye Enzi 17. Mungu zimteremkiye) pale alipoondoka Makka kwenda Madina mwaka 622 AD pamoja na Khalifa Abubakar Al­Siddiq baada ya kupata fununu za mpango wa kumuuwa na ndiyo mwanzo wa kalenda ya Kiislam.

Vita vya Uhud vilipiganwa mwaka 18. 625 AD na karibu ya kupata ushindi kikundi cha wapigaji mishale waliziacha sehemu ambazo Mtume Muhammad aliwausiya wasiziwache kwa namna yoyote ile. Kwa maelezo zaidi ya vita hivyo na vyenginevyo soma The Sword of Allah: Khalid bin Al-Waleed, His Life and Campaigns kilichoandikwa na Lt. General A. I. Akram.

Mlango wa Kumi na Tano

“Kwa ushawishi wa Frantz Fanon (mwanamapinduzi wa Algeria aliyeandika 1. The Wretched of the Earth) na ujumbe wa Algeria, ambao kwa wakati huo walikuwa wakipiganiya uhuru kutoka Ufaransa, maudhui ya mkutano [wa Accra] yalibadilishwa kutoka harakati za mapambano ya kiukombozi bila ya kutumiya nguvu kuelekeya kwenye ‘mapambano kwa njia yoyote ile, ikiwemo utumiaji wa nguvu.’ Hii ilikuwa ni mbali kabisa na mkutano wa Manchester wa mwaka 1945 ambao ulipendekeza mikakati ya kutotumiya nguvu ya Ghandi na upinzani wa kipole dhidi ya ukoloni.” The Future That Works: Selected Writings of A. M. Babu, edited by Salma Babu & Amrit Wilson, uk. 102. Dkt. Saleh Al Miskry amemnukuu Joseph S. Nye, mwandishi wa kitabu Pan-Africanism and East African Integration kuwa “Oscar Kambona alibainisha kuwa fikra ya shirikisho lenye kutawaliwa na Tanzania haikuwa fikra ya Nyerere bali ilikuwa fikra ya Muingereza na ililengwa kuwadhibiti Mau Mau Kenya. Wakati Kenya ilipokuwa si tishio tena kwa maslaha ya nchi za Magharibi, anahoji Kambona, mpango wa shrikisho ukatupiliwa mbali,” kutoka Saleh S. I. Al Miskry “Pan­Africanism and Nyerere in Tanzania,” PhD Thesis in International Relations, University of Salford, uk. 155.

“Mwezi Aprili 2. 1964 ujumbe wa hali ya juu wa EAMWS [East African Muslim Welfare Society] ndani yake wakiwemo Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omar Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS Abdul­Aziz Khaki na wazee wa TANU—Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi waliondoka kwenda ziara ya nchi za Kiislam kutafuta msaada wa kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam na kuanzisha uhusiano na nchi za Kiislam. Gamal Abdel Nasser alifurahishwa sana na ujumbe wa Tanganyika kiasi kwamba ingawa alikuwa katika matayarisho ya mapokezi

Page 426: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla394

ya Waziri Mkuu wa Urusi Nikita Kruschev, na ingawa ujumbe wa EAMWS ulikuwa wa kidini zaidi kuliko wa kiserikali, alikutana na ujumbe ule akaupatia ofisi, huduma za simu, na makatibu muhtasi ili waweze kutayarisha mipango yao kwa serikali ya Misri bila ya shida. Halikadhalika alimuagiza makamu wake Sharbasy afanye makubaliano na mikataba na EAMWS kwa niaba yake. Serikali ya Misri ilikubali kugharamia ujenzi wa chuo hicho. Mkataba wa makubaliano ukatiwa sahihi mjini Cairo kati ya Tewa Said Tewa kwa niaba ya EAMWS na Makamu wa Rais wa Misri, Sharbasy kwa niaba ya serikali yake. Serikali ya Misri iliahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam ambacho kitamilikiwa na kuendeshwa na EAMWS. Gharama ya mradi mzima ulikuwa pauni milioni hamsini na tano za KiMisri. Baada ya kukamilisha kazi ile ujumbe ule uliondoka Cairo kuelekea Makka kufanya ibada ya hija. Baada ya kumaliza hija wajumbe wane walirudi nyumbani. Tewa, Aziz Khaki na Sayyid Omar Abdallah wakaendelea na safari kwenda Aman, Jordan ambako walifanya mazungumzo na Mufti na Waziri wa Aukaf. Kutokea hapo ujumbe ulikwenda Kuwait ambako walikutana na Sheikh wa Kuwait kisha wakaenda Bhaghdad, Iraq na kukutana na rais wake, Abdisalama Arifek [Abdul Salaam Arif ]. Kutoka hapo ujumbe ulielekea Beirut, Lebanon, ambako ulifanya mazungumzo na viongozi wa harakati za Kiislam…Mara baada ya ujumbe wa EAMWS kurudi kutoka ziara yake, Nyerere alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na Tewa Said Tewa, Mwenyekiti wa EAMWS upande wa Tanzania akajikuta nje ya serikali. Nyerere akamteua Tewa balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Watu wa China. Mwezi Januari, 1965 Tewa alikwenda China kwenda kuanza kazi yake mpya. Inasemekana uteuzi wa Tewa kwenda China ulisababishwa na juhudi zake za kutaka kuwaunganisha Waislam kuwa kitu kimoja chini ya jumuiya moja yenye nguvu.” Mohamed Said, Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika, uk. 313–314.

Mlango wa Kumi na Sita

Ni kweli Maalim Seif Sharif Hamad alilifuta somo la historia alipokuwa Waziri 1. wa Ilimu wa Zanzibar baada ya kuuona upotoshaji wake na namna historia ilivyokuwa ikisomeshwa na kuendeshwa kupitiya hadithi za kubuni za chuki na fitina za kina Sefu Bakari kuhusu dhiki na dhuluma walizofanyiwa Waafrika “katika zama za utawala wa kifalme na vibaraka vyao.” Historia ya Zanzibar aliyoisoma Maalim Seif alipokuwa mwanafunzi Beit Ras ni ya akina W. H. Ingrams Zanzibar: Its History and Its People na ya W. H. Ingrams na L. W. Hollingsworth A School History of Zanzibar, na nyenginezo. Mawasiliyano baina ya mwandishi na Maalim Seif kupitiya Ismail Jussa, Januari 2009.

Mwanahistoria maarufu wa Zanzibar Profesa Abdul Sheriff ameonyesha kuwa 2. Michael Lofchie alikuwa msomi wa kwanza aliyoelezeya mfungamano baina ya kabila na matabaka ya kiuchumi ya Zanzibar kutoka ripoti rasmi ya 1932 ambayo ilikhusiyana na kisiwa cha Unguja peke yake. Alichokifanya Lofchie na baadaye kuja kuigwa na Mrina na Matokke na Omar R. Mapuri ni kuyafanya maelezo ya kisiwa cha Unguja kuielezeya Zanzibar nzima wakati asilimiya 80 ya chumo la karafuu linatoka kisiwa cha Pemba. Katika miaka ya mwisho ya 90 kitabu cha Omar R. Mapuri Zanzibar the 1964 Revolution: Achievements and Prospects kiliuweka uhusiyano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu katika sura mbaya kwa namna ya kilivyoupa kasi upotoshaji wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuuonyesha ubaya wa Waarabu na khasa Waomani Zanzibar. Maelezo ya Profesa Sheriff aliyatowa tarehe 5 Februari 1999 juu ya mada “The Zanzibar Revolution at 35: Dreams & Nightmares.”

3. Qurani Takatifu, sura ya Al­Maida, aya ya 32, kwa tafsiri ya Al­Marhum Shekh Abdullah Saleh, inasema: “…atakayemuuwa mtu bila ya yeye kuua mtu, au bila ya

Page 427: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 395

kufanya ufisadi katika nchi, basi ni kama ameua watu wote; na mwenye kumwacha mtu hai (kumsaidia kuishi) ni kama amewaacha hai watu wote. Na bila shaka Mitume wetu waliwafikia na hoja zilizo wazi; kisha wengi katika wao baada ya haya walikuwa waharibifu sana katika nchi.”

Kumzuwiya binaadamu mwenzako kuteka maji si jambo lenye kujenga mapenzi 4. na mashirikiyano baina ya watu lakini kumuuwa binaadamu mwenzako kwa sababu kakuzuwiya kuteka maji ni kuvuka mipaka ya kulipiza kisasi. Kuna daraja nne katika akhlaki za kujihami katika vita. Kuna mtu hata bila ya kuchokozwa na kwa uamuzi wake mwenyewe anamshambuliya mtu mwengine na kumuuwa. Daraja ya pili ni kumchokoza mtu kwa makusudi halafu ukamuuwa. Daraja la tatu ni mtu aliyeshambuliwa na akajihami na mtu wa pili akauliwa au akajeruhiwa vibaya. Na kuna daraja ya nne ya mtu mwenye nia ya kujihami bila ya kumuumiza mtu aliyemchokoza au kumshabuliya. Hili ni daraja la juu kabisa ambalo linahitajiya maandalizi ya hali ya juu kama inavoonekana katika fani ya kujihami ya Aikido ambayo inatowa mfano mzuri wa kumaliza migogoro bila ya kumuumiza au kumuuwa mtu wa pili. Ni fani ya hali ya juu kutoka Japan na ni maarufu duniani na hutumiwa sana na hata na vikosi vya polisi na vya ulinzi. Fani nyengine ambayo ina faida kubwa katika kutowa mwangaza na namna ya kumaliza migogoro (conflicts) ambayo mara nyengine hufananishwa na Aikido, ni Ba Gua Zhang kutoka Uchina. Tizama Aikido and the Dynamic Sphere: An Illustrated Introduction, by A. Westbrook and O. Ratti, illustrations by O. Ratti na Nei Jia Quan: Internal Martial Arts, edited by Jess O’Brien. Polisi wa nchi nyingi duniani na walinzi wa viongozi wakubwa huwa wanaandaliwa katika fani mbili hizi za Aikido au Ba Gua Zhang kwa sababu zinamaliza migogoro mara moja na kwa ima kumshinda adui bila ya kumuumiza au katika fani ya Ba Gua Zhang kwa kumdhibiti adui kwa njia fupi na za haraka.

Hapa Mzee Issa anaidhukuru historia ya kweli ya kuja Waomani Zanzibar kama 5. ni wakombozi waliyoalikwa na kushirikiyana na wenyeji wakati kizazi chake yeye bado kilikuwa hakikufika Zanzibar.

Kama Ali Sultani alijitowa kutoka Uarabu na kwenda kwenye Uswahili au Uafrika basi 6. ilikuwa kwa kufuata nadhariya ya kisoshalisti ya matabaka ya kiuchumi na si kwa kufuata ukabila na juu ya kujikaribisha na kuuweka pande ukabila wa Kiarabu, Abdulrahman Babu na wenzake waliendeleya kuoneka kuwa ni Waarabu tu hata kama walikuwa hawana imani ya kikabila.

Mlango wa Kumi na Saba

Mambo ya nje na ulinzi ni mambo mawili makubwa ambayo yametumika kuidhibiti 1. Zanzibar kiuchumi na kiuslama na ndio vyanzo vya migogoro isiyokwisha. Ni jambo la mantiki kuwa baada ya maridhiyano mapya baina ya Wazanzibari litakalofuatiliya litakuwa ni suala la kuijenga nchi kwa kuutumiya ujuzi wa Wazanzibari waliyoko Zanzibar na waliyotapakaa duniani, na kuwa na mahusiyano ya kiuchumi na ya kibiashara na nchi za nje. Kama Zanzibar imeweza kuondowa ukhasama baina ya wafuasi wa vyama vikubwa vya kisiasa vya CCM na CUF, kuliondowa suala la mafuta katika mambo ya Muungano, basi pia ina uwezo wa kuanzisha Wizara ya Mambo ya Nje au kuendeleya na makhusiyano na nchi za nje ambazo zina nia ya kikwelikweli ya kuisaidiya na kushirikiyana na Zanzibar bila ya kuiyogopa Tanganyika. Pia, Tanganyika isiyokuwa na nia ya kuendeleya na urathi wa viongozi wenye hamu au khofu ya kuidhibiti Zanzibar inaweza kuanzisha utaratibu wa Kikatiba utakaokwenda sambambamba na kuyakaribisha matakwa ya kikatiba ya nchi ya Zanzibar.

Ahmada alimuelezeya Rashid Falahy walipokuwa pamoja Mangapwani kuwa alimpiga 2.

Page 428: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla396

risasi Humudi kimakosa. Rashid Falahy alikuwa na akina Ahmada walipokwenda Kambi ya Jeshi ya Migombani baada ya kutoka Makao Makuu ya Afro­Shirazi na alipokwenda nao mbele ya Mangwapani. Walipofika Mangapwani walimpelekea salamu mwenziwao aliyekuwa akiishi kule awapelekee chombo cha kuwavusha kuwapeleka Mombasa lakini mwenziwao hakufanya hivyo. Mwisho wake Ahmada na Chwaya wakaamuwa kuwa watabakia hapohapo na watapigana mpaka kufa. Rashid Falahy akaamuwa kuondoka kwa miguu kwa kupitia sehemu za mashamba mpaka akafika nyumbani kwa Pili Khamisi ambaye mkewe alikuwa jamaa yake. Hapo aliwakuta watoto wa kike wa Kizanzibari wenye asili ya Kiirani. Kutokea hapo alikwenda moja kwa moja na kujisalimisha kunakohusika. Maelezo haya nimeyapata kutoka kanda aliyonisikilizisha Professor Ibrahim Noor Shariff.

Kenya ilipata uhuru wake tarehe 3. 12 Disemba 1963, siku tatu baada Zanzibar kuupata uhuru wake. Marehemu Sheikh Ibuni Saleh alihudhuria sherehe za uhuru wa Kenya kwa niaba ya Zanzibar kwa sifa yake kama ni Waziri bila ya Wizara pamoja na marehemu Sheikh Hilal Barwani ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wake.

Suala la nguvu za ukabila na nguvu za mrengo wa kushoto ni suala muhimu katika 4. kuifahamu misimamo ya viongozi wa Zanzibar. Ukabila ulikuwa na nguvu zaidi kuliko mirengo mengineyo ya kisiasa katika Zanzibar iliyochanganyika sana kikabila. Umuhimu wa kuzitambuwa kabila kwa lengo la kujuwana na kuuweka uraia mbele kuliko ukabila ni suala ambalo hivi karibuni tu limeweza kujengewa mazingira ya ufumbuzi na viongozi majasiri wa Zanzibar. Bado kuna suala juu ya vipi mfumo wa kikabila uliyozoweleka kwa zaidi ya nusu karne utaweza kuondolewa ghafla bila ya mkakati wa ilimu kubwa ya uraia kutokeya chekecheya mpaka vyuo vikuu.

Hanga hakuweza kuwaeleza ukweli kina Mzee Salum na Ahmed Rajab kuhusu kiini 5. cha ugomvi wake na Mzee Karume kwa sababu kufanya hivo ingelibidi awaelezee mengi kuhusu kupigania uongozi ndani ya ASP na mipango ya mapinduzi ambayo iliipinduwa serikali ya ZNP­ZPPP na uongozi wa Mzee Karume ndani ya ASP. Anaelezeya mwandishi, Bwana Mohamed Said wa kitabu maarufu cha maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes:

Mimi nikiishi na baba yangu mtaa wa Somali, namba 22. Klabu ya mwanzo maarufu ya Kilwa Jazz Band ilikuwa kwenye nyumba ya mama yake Abdu Kigunya. Mbele ya nyumba yao ikifika kama saa tisa, kumi, laasiri, wazee walikuwa wanaweka jamvi pale, wanacheza bao. Sasa hivi ukenda pamejengwa majumba ya maghorofa. Hanga akija pale mtaa wa Gogo, kona na Mtaa wa Mchikichi, nyumba ya kona barazani wazee wametandika majamvi wanacheza bao. Mimi nilimjuwa Hanga kwa sababu nikimuona kwenye magazeti. Na wakati ule mawaziri wakitembeya na yale magari meusi yakiitwa “Humber.” Sikumbuki kumuona Hanga kuja pale na gari. Basi ikapita, mapinduzi Unguja yakatokeya sisi wadogo, hatujui nini kinachotokea. Mwaka 67 nadhani, pale Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Anatoglou Hall, tukicheza mpira wa miguu pale. Mambo yalianza Mnazi Mmoja katika mkutano wa hadhara. Hanga katolewa jela Ukonga kaletwa pale kuadhiriwa na Nyerere. Sisi ni watoto, mambo yale na nyimbo zile lazima tujumuike. Hanga akaletwa pale. Namuona Hanga mimi kwa macho yangu ya kitoto na miwani yake ile. Hanga alikuwa mwembamba na mrefu na alikuwa na thick hair. Alikuwa mtu mwenye kupendeza. Kaja pale na uso ulionyongonyeya. Lakini sisi hatujui kinachotendeka. Watoto wa Kiswahili miaka 14, 15, 16, ni wadogo. Hatujui kinatendeka nini. Lakini mimi najua kuwa yule pale Hanga namuona kuwa ni mfungwa. Hanga miwani iko puani uso umemparama kama jiwe la kiama, madevu yamemjaa. Anaadhiriwa! Jua la saa sita mchana linampiga vizuri. Kwa pale kukaa na kajiinamia nilijuwa kuwa mambo si mazuri. Nyerere pale anazungumza na wote wanasikiliza. Nyerere unajua. Nyerere alikuwa ni orator. Na kuna kumuuwa mtu kiungwana. Nakumbuka incident moja

Page 429: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 397

anamuonyesha kidole anasema “hili, hili, hili. Hana lolote. Hakuna lolote anaweza kufanya huyu. Afadhali huyu mwanzake [Babu].” Ukitizama kwenye Tanganyika Standard, wakati ule bado halikuchukuliwa na serikali, wakati ule editor ni yule Muingereza, Brandon Grimshaw. Utakuta full page. Mimi kwa jicho langu nimeona kwa sababu baba yangu mimi akinunua lile gazeti. Picha ya Hanga iko mbele na madevu na miwani yake ile. Si mimi tu, watu wengi wanakumbuka hiki kisa. Mimi baba yangu rafiki zake walikuwa Jaha Ubwa, Twala…Wakitembeleyana zamani wakati wa Easter…baba yangu alikuwa memba wa band ya Black Birds ya Bwana Ally Sykes. Nadhani kule ndo walikofanya urafiki na hawa jamaa wa Zanzibar. Picha yangu mimi ya Mzanzibari, wakija kule nyumbani, unamuamkia na suala lilikuwa “wewe umeshahitimu wewe.” Na ile sophistication za wake zao wakija nao pale, yale mavazi, mabuibui, uturi ule, vile vyakula wakiandaa nyumbani pale. Hi ndo picha yangu ya Mzanzibari. Palikuwa na picha pale ukutani ya marahemu father wangu na kina Jaha Ubwa. Ile picha ikapotea pale ukutani. Ikawa haionekani tena. Lakini palikuwa mzee akizungumza habari za akina Twala alikuwa akinong’ona. Nahisi mzee alikuwa ana khofu. Ile ni dalili ya woga. Kitu kibaya kimetendeka. Lakini lazima aulize. Vipi mkewe. Watoto vipi? Lakini hawezi kusema kwa sauti. Siku nilipokuja kukutana na Ali Nabwa aliponielezeya habari za Zanzibar, nikamwambia mimi baba yangu alikuwa ana masikilizano na akina Twala na yeye akaanza ku open up sasa. Nikasema duu! Alipotoka jela Ali Nabwa alikuja pale mtaa wa Narungombe na Skukuu. Pale palikuwa na baraza maarufu sana ya Saigon Football Club. Nabwa alikuwa anakuja pale. Tukitoka tukikaa pembeni tukizungumza chamber. Nilijua baadaye sana kuwa kumbe alikuwa ametoka jela. Pale ndo nilipoanza kuwaona Wazanzibari kwa sura nyingine sasa. Kumbe zile bashasha zinadanganya? Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa mauti yaliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho na kutangulia mbele ya haki yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma na kuhangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa miujiza ya aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kwa mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo. Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa hao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi? Fikra za Hanga zilikuwaje pale alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikimpitikia katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali akijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah na Masultani wengine waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu, au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde wakata mkonge kutoka Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti? Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyaasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano

Page 430: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla398

wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere, ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume. Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, “Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliyopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong’ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ya kifo haimuhusu.” Maelezo kwa njia ya barua pepe kutoka kwa Mohamed Said kwenda kwa mwandishi, terehe 10 Februari, 2010.

Kwa mujibu wa kigogo kimoja (jina nimelihifadhi) kutoka Tanganyika (Tanzania 6. Bara), Zanzibar haitoweza kusimama juu ya miguu yake wenyewe kwa sababu haina vitu vitatu muhimu: utajiri wa watu kutoka Zanzibar (human resources) uko nje ya Zanzibar; ikiwa nchi kama Oman haikuisaidiya Zanzibar na kuziomba nchi za Ghuba kuekeza Zanzibar na Tanganyika; hata kama Zanzibar itaweza kupata misaada kutoka nje hakuna miundo mbinu kama uwanja wa ndege wa kimatiafa au bandari kwa ajili ya kupokeya abiriya au mizigo mikubwa. Hayo yote yasingeliweza kuwazwa licha ya kufanyika bila ya kwanza kuwepo maridhiyano ya mfungamano wa ndani baina ya Wazanzibari.

Mlango wa Kumi na Nane

Kwa mujibu wa hoja ya Uislamu, Imam Ghazzali aliyezaliwa Iran mwaka 1. 1058 na kufariki dunia mwaka 1111, ameelezea katika kitabu chake Ihya Ulum-Iddin yakuwa hasad ziko za aina na daraja nyingi. Sheikh Rashid bin Ali bin Rashid Al­Khanbshy wa Oman ameelezea katika kitabu chake Niombeni Nikupeni yakuwa hasad ziko za namna tatu. Ya kwanza, “Anapotamani hasidi neema imuondokee ndugu yake ili aipate yeye.” Ya pili, “Anapotamani hasidi neema imuondokee ndugu yake hata ikiwa yeye hatoipata,” na ya tatu “Anapotamani hasidi neema imuondokee ndugu yake kwa kutumia njia na mbinu za kuiondowa kwa kuharibu, au kumdhuru yule anayemhusudu. Na hasadi hii ndio hatari zaidi kuliko zote.” Nilipomuuliza Mzee Ally Sykes, ambaye ni katika waasisi wa TANU, pale ofisini kwake Mtaa wa Indira Gandhi, Dar es Salaam, anipe sifa moja ya Mwalimu Nyerere, alinijibu kwa kuniambia kuwa sifa yake kubwa ilikuwa ni hasad na maneno ya Bwana Ally Sykes yanathibitisha kuwa hasad ya Nyerere kwa Zanzibar ilikuwa ni ya hatari kuliko zote.

Bado kuna khofu ya watu wa bara kujihisi kuwa hawajakubalika Zanzibar na khofu 2. hiyo haitowatoka iwapo wataendeleya kujiona si Wazanzibari na utiifu wao hauko kwa Zanzibar.

Mlango wa Kumi na Tisa

Anthony Clayton, 1. The Zanzibar Revolution and Its Aftermath, Archon Books: Hamden, Connecticut, 1981, uk. 69.

Page 431: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 399

Anna Grimshaw, ed. “Whitman and Melville” in 2. The C. L. R. James Reader, Blackwell Publishers, 1999, uk. 218.

Notes made by the late Commissioner Sullivan, p. 3. 1. The National Archives, Zanzibar Independence Conference, “Extracts from Cabinet 4.

Minutes on Papers Considered up to and including Saturday,” 31st August 1963, p. 4. CO 822/3148 116805.

The National Archives, “Report by Mervyn Vice Smithyman, Permanent Secretary to 5. late Prime Minister of Zanzibar, dictated on Thursday, the 16th January 1961” DO 185/59 116805, p. 5

Nassir Abdulla Al­Riyamy 6. Zinjibar: Shakhsiyyat wa Ahdaath. Dar Al­Hikma, London, 2009, uk. 396.

Ali Muhsin Al Barwani, 7. Kujenga na Kubomolewa Zanzibar (Kumbukumbu), uk. 246–247.

The National Archives, Acting British Resident to Colonial Office, DO 8. 166/79 116843, 20 September 1963.

The National Archives, “Letter from the Department of Technical Co­operation, 9. London, to W. G. Lamarque of the Commonwealth Relations Office, 13th January, 1964,” DO 214/79.

The National Archives, “Public Officers Agreement Between Her Majesty’s 10. Government in the United Kingdom and the Government of Zanzibar,” DO 166/79 116843.

The National Archives, ”Note of a meeting in Mr. Morgan’s room on Tuesday, 11. 11th July, 1961,” C0 822/3002 116805, p. 3.

Mazungumzo baina ya mwandishi na Bwana Nassor Abdulla Nassor (Mlawwaz), 12. tarehe 7 Novemba, 1998.

Tizama William Leo Hansberry, Pillars in 13. Ethiopian History: The William Leo Hansberry African History Notebook, Volume I, edited by Joseph E. Harris, Howard University Press, 1974) na William Leo Hansberry, Africa and Africans as Seen by Classical Writers: The William Leo Hansberry History Notebook, Volume II, edited by Joseph E. Harris, Howard University Press, 1977.

Tizama Mohammed Faiq, 14. Abdel Nasir wa a-Thawra Al-Afriqiyya [Abdel Nasser and the African Revolution), Dar el Mustakbal Al­Arabi, Fourth Edition, 2002.

Smithyman, uk. 15. 8.Ibid., uk. 16. 8The National Archives, “Statement of Assistant Superintendent Thomas Waring, 17.

Dar es Salaam, 16 January 1964,” DO 185/59 116805.Ibid., uk. 18. 6. The National Archives, “Notes made by the late Commissioner of Police, Zanzibar 19.

– J. M. Sullivan, 17th January 1964,” DO 185/59 116805, uk. 13.The National Archives, “Report by Mervyn Vice Smithyman, Permanent Secretary 20.

to the late Prime Minister Zanzibar, 16th January 1964,” DO 185/59 116805, uk. 14.Ibrahim El Zein Soghayroun, “The Arabs in East Africa: Results of Colonial 21.

Administration as Viewed by Missionary Circles” Islam, Christian Missions and the Colonial Administration in East Africa, International Printing Press, Ruwi, Oman, 1992, uk. 117.

22. Memorandum of Understanding Between Christian Council of Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and The United Republic of Tanzania, Drawn by Prof. Dr. C. R. Mahalu, Faculty of Law, University of Dar es Salaam, 21 February, 1992.

Frider Luwig 23. Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994, uk. 213.

Kutoka waraka ambao haukuchapishwa uitwao “Christian Schools and Health 24.

Page 432: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla400

Centers” na katika sehemu yake ya mwisho una “Jeduweli ya Semina za Shule za Sekondari” zenye kutoa majina ya shule 104 zilioko Tanganyika (Tanzania Bara) zikiwemo za Kikristo na za Kiislam.

United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO), 25. Division of Ethics of Science and Technology, COMEST The Teaching of Ethics, Paris, 26th January 2003, Oslo, 10th–12th May 2003, uk. 11.

Ibrahim El Zein Soghayroun, op. cit., uk. 26. 118.John Okello, uk. 27. 131.Ibid. uk. 28. 108.Ibid. uk. 29. 119.Ali Muhsin Al Barwani, op. cit., uk . 30. 289–290.William Edgett Smith 31. Nyerere of Tanzania, uk. 60Jonathon Glassman, “Racial Violence, Universal History and Echoes of Abolition 32.

in Twentieth­century Zanzibar” In Abolition and Imperialism in Britain, Africa, and the Atlantic, edited by Derek R. Peterson, Ohio University Press, 2010, uk. 178–179. Tarehe 25 Septemba 2009 gazeti la Nipashe liliandika makala yenye kichwa cha maneno “Wanafunzi Arusha wakoshwa na Zanzibar.” Mwanafunzi Cero Marcy kati ya wanafunzi 46 kutoka Shule ya Kimataifa ya Shalom ya Arusha waliyopelekwa Zanzibar amenukuliwa akisema “Tumejifunza mambo mengi, lakini historia ya biashara ya utumwa imetugusa kutokana na mazingira mabaya waliyokuwa wakihifadhiwa binadamu wenzetu.” Marcy aliendeleya kusema kuwa “…vyumba walivyokuwa wakihifadhiwa watumwa huwezi kuamini kwamba chumba kimoja kilikuwa kikihifadhiwa watu 75, kikiwa katika mazingira ya giza na hewa ndogo inayoingia ndani kupitia kwenye matundu madogo.” Wakati Zanzibar haina tena misafara ya dhiki na dhuluma ya kuwatiya chuki wanajeshi na wafanyakazi wa vyombo vya usalama, tayari watoto wadogo kutoka Tanganyika wanaandaliwa misafara mipya ya dhiki na dhuluma na watu wazima. Gazeti la Nipashe limeandika: “Mkuu wa msafara huo, Afisa Tawala wa IPP Media, Joachim Kajembe, alisema ziara hiyo kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo, ni utekelezaji wa ahadi ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliyoitoa Septemba 12 wakati wa maadhimisho ya shule hiyo kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwake.” Amezidi kufafanuwa kwenye kielelezo cha 9 cha chini ya mlango wa maandishi ya Profesa Jonathon Glassman:

Dhana yangu ni kuwa haya mashubaka, na ghorofa ya ardhini ya hospitali kwa jumla, yalizinyakuwa khayali za wenyeji kwa sababu majengo ya Kizanzibari hayana ghorofa za chini ya ardhi. Kwa maelezo kuhusu Mtakatifu Monica na eneo la Kimishionari la Mkunazini tizama Anderson­Morshead, Universities’ Mission; “The New Hospital at Zanzibar,” Central Africa 9 (1891): 133–36; barua kutoka kwa J. S. Wimbush na C. A. Smythies, Central Africa 11 (1893): 65, 70; Universities’ Mission to Central Africa, East Africa in Picture (London: UMCA, 1900) 15–16. Prita Meier kwa hisani yake amenitanabahisha kuhusu rejeo kutoka mwaka 1902 ambalo linaunganisha ndani ya khayali za wenyeji vyumba vya chini ya ardhi na utumwa: Sorabji Manekji Darookhanawala, “Africa in Darkness,” katika Two Indian Travellers: East Africa 1902–1905, ed. Cynthia Salvadori (Mombasa: Friends of Jesus, 1997), 180.

Anthony Clayton, uk. xv.33. Ripoti ya CIA ambayo imetungiwa kitabu hivi karibuni na Helen­Louise Hunter 34.

ina masuala mengi zaidi kuliko jawabu na ina migongano ya kitafsiri na inakhitimisha kwa maneno yafuatayo: “Sasa, kiasi ya miaka 50 baadaye, inawezekana kuyatizama Mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni sahihisho la tukio lililokirudishiya kisiwa kidogo kiliyoko nje ambacho kilikuwa kinageuka kuelekeya kunako njia mpya chini ya ushawishi wa Makoministi wa

Page 433: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 401

Kiarabu na kukirudisha kunako utamaduni wa turathi ya Kiafrika uliyosambamba na bara na wenye uwiyano na Magharibi.” Helen­Louise Hunter, ZANZIBAR: The Hundred Days Revolution, Praeger Security International, 2010, uk. 111.

Kutoka ripoti asilia ya CIA ya mwaka 35. 1966 iliyoandikwa na Helen­Louise Hunter Zanzibar: The Hundred Days’ Revolution, 1966 uk. 41.

Hunter, 36. 2010, uk. 5. Ibid., uk. 37. 7. Ibid., uk. 38. 7.Ibid., uk. 39. 97.Ibid., uk. 40. 48.Ibid., uk. 41. 42. Ibid., uk. 42. 41.Ibid., uk. 43. 41.Ibid., uk. 44. 40–41. Ibid., uk. 45. 42.Ibid., uk. 46. 40.Hunter, 47. 1966, uk. 2.The National Archives, “Revolution and Mutiny in East Africa, 48. 26th February,

1964,” DO 185/59 116805, uk. 2.Hunter, 49. 2010, uk. 41.The National Archives, “Revolution and Mutiny in East Africa, 50. 26th February,

1964,” DO 185/59 116805, uk. 8.Ibid., uk. 51. 8–9.Oginga Odinga, 52. Not Yet Uhuru (Heinemann, 1967), uk. 280.Ibid., uk. 53. 279. Ibid., uk. 54. 279. The National Archives, J. D. B. Shaw to F. S. Miles, Dar es Salaam, 55. 20th April, 1964,

DO 216/41.The National Archives, J. Bourn, 56. 23th September, 1964, DO 185/51 116937.The National Archives, P. A. Carter, Commonwealth Relations Office, 57. 1st August

1964, DO 185/51 116937.The National Archives, 58. 14th June, 1964, DO 185/51 116937.The National Archives, British High Commission, Dar es Salaam, to C.R.O, 59.

25.5.1964, DO 185/51 116937.The National Archives, Joint Staff Intelligence, HG Middle East Command, June 60.

1964, DO 185/51 116937.The National Archives, J. Bourn, 61. 23rd Sepetember, 1964, DO 185/51 116937.Hunter, 62. 1966, pp. 121–122. Ripoti ya CIA iitwayo Zanzibar: The Hundred Days’

Revolution iliyoandikwa na Helen­Louisie Hunter mwaka 1966 hailingani sawasawa na kitabu cha Helen­Louise Hunter Zanzibar: The Hundred Days Revolution kilichochapishwa mwaka 2010 na Preager Security International. Kwa mfano, haya maelezo ya ubeberu wa Nyerere yamo kwenye maelezo ya ripoti ya CIA ya mwaka 1966 lakini hayamo kwenye kitabu cha 2010. Hunter amezifahamisha baadhi ya sababu za kufanyika Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa mfano, moja katika sababu za Nyerere kuungana na Zanzibar ambayo imo ndani ya ripoti na kitabu ni “Inaweza kuwa kulikuwa na sababu nyengine ya shinikizo la haraka la Nyerere kuufanya Muungano ambayo hakuwatajiya Wazanzibari. Namna alivyolikabili suala la uasi wa jeshi la Tanganyika katika mwezi wa Januari, na khasa kuwaomba msaada Waingereza, haikuisadiya hishma yake au hishma ya bara. Muungano na Zanzibar ulikuwa ni ushindi wa kishindo ambao aliuhitajiya ili kuweza kujiimarisha. Kama Rais Kenyatta alivyosema: ‘Nyerere alikuwa anajaribu kuweka mambo

Page 434: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla402

sawa baada ya tabia yake ya kijoga wakati wa uasi wa jeshi la Tanganyika.’ ” Maelezo ambayo yamo kwenye maelezo ya chini ya ripoti (footnotes) ambayo yamo ndani ya maandishi ya kitabu ni pia kuhusu suala la muungano ambalo Nyerere alilielezeya (ukurasa 121) kwa njia ya siri: “Nilikabiliwa na mashaka ya ima kutumiya nguvu, au bora, kuifuata njia ya salama. Kutumiya nguvu baada ya mkutano wa Addis Ababa kungelileta upinzani mkubwa usiyohitajika kutoka nchi nyingi za Afrika. Tulipokuwa Addis Ababa ilikubalika kuwa hakutokuwa na kuingiliya mambo ya ndani ya nchi nyengine za Kiafrika. Kwa hiyo nikachaguya kutumiya mbinu nyengine na nilikuwa niko tayari kuigharimiya. Nilifanya hivyo kwa kutowa nyadhifa tano za uwaziri na kumfanya Karume awe Makamo wa Rais. Kwa mfano, wilaya ya Moshi (ya Tanganyika) ina watu wengi zaidi kuliko Zanzibar na Pemba na haiwezi kufahamu kwanini Zanzibar iwe na watu wengi zaidi kwenye Baraza la Mawaziri.” Na anaelezeya Hunter kwenye maelezo ya chini ya ukurasa (121) ya ripoti ya CIA kuwa “Mbali ya Nyerere, Waziri wa Ulinzi Kambona anatajwa kuwa kwa muda mrefu alikuwa anaamini kuwa Tanganyika iimeze Zanzibar. Ingawa muungano unaelezewa kuwa ulianzishwa na Nyerere na Nyerere alikuwa ameyadhibiti majadaliyano yake, hii ni sehemu moja ambayo Kambona alikubaliyana kabisa na Nyerere.” Pia anaelezeya Hunter kwenye ukurasa 120–121 wa ripoti kuwa “Uwezekano wa Babu na wafuasi wake wa Kiarabu kuihodhi Serikali ya Zanzibar lilikuwa ni mwiko; kwa Nyerere ingelikuwa ni kuyakebehi mapinduzi ya Zanzibar. Ilipofika mwisho wa Machi au mapema Aprili, Babu alikuwa ameshajijenga na uwezekano wa Waarabu kuchukuwa nchi ulikuwa tayari wakati wowote. Nyerere ni wa kutarajiwa kufanya jambo lolote lile na kila kitu ndani ya nguvu yake kuzuwiya uwezekano kama huo kutokeya. Na njia bora ya kuhakikisha kuwa mapinduzi ya Zanzibar ya Waafrika yanadhibitiwa, akaamuwa kuufanya muungano baina ya nchi mbili ambao Waarabu watamezwa na Waafrika walio wengi.” Pia ameandika kwenye ripoti maelezo ambayo hayamo ndani ya kitabu: “Nyerere na Watangayika wana wasiwasi kuwa Wazanzibari wana dhana kuwa Tanganyika ina mikakati ya kivamizi juu ya Zanzibar. Katika mwezi wa Disemba 1964, Tambwe, mmoja kati ya maofisa wachache wa Tanganyika ambaye anaishi Zanzibar baada ya muungano, kamwambiya Balozi wa Kimarekani kuwa baada ya muda mrefu Watanganyika wameweza kuwakinaisha Wazanzibari kuwa Tanganyika haina ‘mikakati ya kivamizi.’ Inawezekana sana kuwa Tambwe mwenyewe hakuyaamini maneno aliyomuambiya Carlucci; kwenye nafsi yake, aliyaona zaidi kuliko watu wengi matatizo ambayo Watanganyika walikuwa wakiyapata kuhusu muungano. Baada ya kuvunjika moyo sana na kutafishiwa na mgomo wa Zanzibar dhidi ya bidii za Tanganyika kuziunganisha nchi mbili, karibuni Tambwe alistaafu kazi na kurudi Dar es Salaam.” (uk. 122 kwenye ripoti ya CIA).

Odinga Oginga, uk. 63. 280.Hunter, 64. 1966, uk. 130.Ibid., uk. 65. 136.The National Archives, “Outward Telegram [No. 66. 43] from British High Commission,

Dar es Salaam” telegram ya siri kuelekeya Commonwealth Relations Office (London), U.K. Rep, Nairobi, U.K. Rep, Kampala, POMEC, Aden, Washington, na Zanzibar. DO 185/59, haina tarehe.

Ibid.67. Ibid.68. Ibid.69. Ibid.70. Ibid.71. Mazungumzo baina ya mwandishi na Bwana Nassor Abdalla Nassor [Mlawwaz], 72.

Maskat, Oman, tarehe 7 Novemba, 1998.Mazungumzo kwa njia ya simu na Bwana Ally Sykes, Aprili 73. 18, 2009.

Page 435: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 403

Mazungumzo baina ya mwandishi na Mzee Ahmed Badawi Qullatein, Malindi, 74. Zanzibar, tarehe 26 Julai 2005.

Report by Mervyn Vice Smithyman, Permanent Secretary to the late Prime Minister 75. Zanzibar, 16th January 1964, p. 12, The National Archives, Do 185/59 116805.

Outline of Events, 76. 12th January, 1964., by A. H. Hawker, Permanent Secretary, Office of the President, 19th Januari, 1964, p. 2, The National Archives, DO 185/59 116805. Sultan Jamshid na familiya yake waliosafiri naye kwenda Uingereza walikuwa watu 22. Wenginewo waliopanda naye meli lakini hawakwenda naye Uingereza walikuwa watu 50 wakiwemo maofisa wa polisi wa ngazi tafauti na baadhi ya askari wa bandarini. Kati ya hawa walikuwepo maofisa wa polis wa Kizanzibari kama Salum Hakim Al­Khusebi na baadhi ya askari wa forodha na wafanyakazi waliweza kushuka Dar es Salaam. Wengine waliendeleya na safari na wengine walirudi Zanzibar. Katika waliorudi Zanzibar ni Harub Sheikhan ambaye alikuwa akifanya kazi bandarini Zanzibar. Walioendeleya na Sultan Jamshid mpaka Uingereza ni Sultan Jamshid mwenyewe pamoja na aila (familiya) yake waliyokuwepo Mombasa kwa matembezi wakati yalipotokeya mapinduzi na wakaungana naye Nairobi na wakaendeleya naye katika safari. Waliosafiri na Sultan Jamshid baada ya kupigana vita vya Malindi mpaka Mfalme akaingiya melini na umri wao baina ya mabaniyo ni kati ya hawa wafuatawo: na Ahmed Seif Kharusi (52), Salim Humoud Kharusi (25), Mohammed Said Riyami (50), Said Badar Barwani (44), Hilal Mohammed Barwani (54), Salim Ahmed Seif (39), Suleiman Ahmed Riyami (21), Mohammed Msellem Ruwehi (47), Mohammed Rahid Busaidi (57), Said Nassor Al­Oufy (40), Ali Abbas Ali (25), Ali Khamis Musa (Baucha) (21), Juma Hamad Jabir (22), Mzee Juma, Maria bint Kassim (16), Mize Shafi (13), Khamis Juma (12), Leila Salum (7) na Asha Kimbo (9). Ndege haikuweza kushuka London kutoka na umande mwingi na badala yake ikashuka uwanja wa ndege wa Manchester.

Mervyn Vice Smithyman, uk. 77. 12–13.The National Archives, Inward Telegram to Commonwealth Relations Office, 78.

“Sultan of Zanzibar,” 15th January 1964. Ibid. 79. The National Archives, From Commonwealth Relations Office (C.R.O.) to Acting 80.

British Hisgh Commissioner Dar es Salaam, 7th May, 1964, DO 213/251Bob Smith with Salim Amin. 81. The Man Who Moved the World: The Life and Work of

Mohamed Amin, Camerapix Publishers International, 1998), uk. 53.Hapana shaka idadi ya watu waliouwawa Zanzibar katika mapinduzi ya tarehe 82. 12

Januari 1964 ilikuwa ni kubwa sana kutokana na idadi ya watu waliyokuwa wakiishi katika kisiwa cha Unguja wakati huo. Na wengi waliyouliwa walikuwa ni Waomani wenye kuitwa “Wamanga” ambao wengi wao walikuwa wakiishi sehemu za mshamba. Pia Wazanzibari wengi waliuwawa ambao si Waarabu waliyokuwa wakiviunga mkono vyama vya ZNP na ZPPP ambao ni Washirazi na inavyoonesha wengi wao wanaonekana kwenye filam ya Africa Addio na kitabu cha Africa Addio. Kwa mujibu wa Mohammed Said Harib Al Mahruqy, “Ukichukuliya idadi ya watu wote kutoka visiwa vya Unguja na Pemba ya wakati huo kuwa ilikuwa ni 400,000 na idadi ya Waarabu peke yao ilikuwa ni 50,000 (asilimiya 12 ya idadi ya watu wote), kuna wenye kukisiya, kwa mfano Naibu Balozi wa Kimarekani, Zanzibar, Don Petterson, kuwa Waarabu waliouliwa au waliobidi kukimbiya ni mmoja kati ya wawili. Ameandika Petterson kuwa ‘Nusu ya idadi ya Waarabu 50,000 wa kabla ya mapinduzi imefutwa.’ Hata kama nambari ya waliofutwa maisha yao au kuondoka nchi itakuwa ni 1 kati ya 5 basi idadi pia itakuwa kubwa na kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, yataitwa mauwaji ya halaiki (genocide). Kuifahamu hii idadi ya mtu 1 kati ya 2 kwa mujibu wa idadi ya watu wa Zanzibar ya wakati huo ambayo ni 400,000, ni sawa na kuwauwa au kuwafukuza hii leo Wamarekani milioni 19, au Waingereza milioni 3.75, au Watanzania

Page 436: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla404

milioni 2.5. Na kama tutaiweka idadi ya waliyouliwa au kufukuzwa ni 1:5 badala ya 1:2 basi idadi ya waliyouliwa au kufukuzwa bado itakuwa yenye kutisha na itakuwa sawa na kuwauwa au kuwafukuza Wamarekani milioni 7.6, Waingereza 1.5, au Watanzania milioni 1. Hapo bado hakuna idadi ya wafuasi wa ZNP na ZPPP waliouwawa ambao kiidadi ndio wengi zaidi na ambao si Waarabu ingawa wameingiliyana sana na Waarabu. Kama haya si mauwaji ya halaiki basi ni kitu gani?” Mawasiliyano na mwandishi kwa njia ya barua pepe, tarehe 9 Aprili, 2009. Matukio yamoto Afrika Mashariki yalikuwa baina ya tarehe 12 Januari 1964 na tarehe 18 Januari 1964. Tarehe 17 Januari 1964 “Bwana Stanley alipigiwa simu na Katibu wa Baraza la Mawaziri la Kenya Ndegwa yenye kusema ‘telegram 2 kutoka Karume kwenda Serikali ya Kenya zikisema kuwa Zanzibar inavamiwa na kuiomba Kenya kupeleka majeshi.’ Majaribio ya Serikali ya Kenya kuwasiliyana na Zanzibar yameshindikana. Labda ujumbe ulikuwa si wa kweli. Bwana Stanley katuomba tuwasiliyane na Aden na London.” Tarehe 18 Januari 1964 meli za HMS Owen na Hebe ziliwasili Mombasa saa 0930 za asubuhi. Saa 1610 za jioni Wazungu waliyokuwepo Pemba wameondolewa. Saa 1800 za Magharibi asikari 150 wa jeshi la polisi kutoka Tanganyika waliwasili Zanzibar na kupelekwa kambi ya Mtoni. Tarehe 19 Januari 1964 Zanzibar imeripotiwa kuwa kila kitu kimetuliya na kimya. The National Archives, “An Outline History of Events in East Africa during the period 12th to the 26th January, 1964” WO 276/373 na The National Archives, “LOG SHEET” WO 276/373.

Majahazi 83. An’Nasser na Al-Qahira yalikuwa yamejaa watu na kubwa lao lilikuwa na watu 500. Kwa mujibu wa Kepten H. F. G. Leftwich wa tanker Southern Venture alikutana na hayo majahazi katikati ya bahari yakielekeya Aden na akawapa maji ya kujaza matenki yao, maboxi mawili ya unga wa maziwa ya kuganda kwa ajili ya watoto na nyama za kibati. Anasema Kepten Leftwich “Walishukuru sana na tulipokuwa tunaondoka tulimuona nahodha wa jahazi akitowa msala wa kusaliya. Jahazi dogo la pili walitaka kutupa samaki kama malipo lakini tulikataa.” The National Archives, kutoka gazeti la East African Stan-dard, tarehe 3 Juni 1964, DO 185/60.

Ahmad Al­Falahi “Dhikriyyat maa Al­Shiekh Abdullah Al­Khalili” 84. Iilaaf: Awal Jarida Yawmiyya Ilektroniyya, 18 November, 2007.

Mlango wa Ishirini

Ali Mazrui Mazrui, “AFRABIA: Africa and the Arabs in the New World Order.” 1. UFAHAMU: The Journal of the African Activist Association XX no. 3. 1992, uk, 52. Wakati kitabu hichi kinakwenda kuchapishwa, Zanzibar kumetokeya mapinduzi ya maridhiyano au ya mfungamano ambayo yalikuwa yanataka kufanywa kwa kutumiya mbinu na njia tafauti, na vyama vya ASP, Umma, na ZNP­ZPPP kabla ya mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964 na kabla hayakutekwa nyara na Nyerere na Dola ya Tanganyika. Sharia rasmi ya chama cha Afro­Shirazi ililenga “kufanya bidii ya kuondoa katika taifa letu kila namna ya upembuzi wa ukabila na ubaguzi wa makabila.” Katika barua yake ya tarehe 29 Agosti, 1963 kwa Ofisi ya Makoloni London, Balozi wa Kiingereza Zanzibar, Sir George Mooring aliandika kuwa “Katika kipindi chote hichi viongozi wa A.S.P. wamekuwa wakiitembeleya sana Dar es Salaam kwa ushauri, na imeripotiwa kuwa washauri wao wakubwa wawili ni Kawawa na Kambona. Inasemekana kuwa Watanganyika wamekuwa wakishadidiya kuwa iwapo ZPPP haijawachana na ZNP na ikashirikiyana na ASP basi ASP iingiye kwenye upinzani na isikubali kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na vyama hivyo viwili. Bahati mbaya, ushauri huu unaonyesha umekubaliwa na ASP; kwa vyovyote uwezekano wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya vyama vyote hakika umepoteya.” The National Archives, CO 822/3058. Daima Zanzibar imekuwa ikiyatafuta mapinduzi ya Afrabia, na chanzo

Page 437: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 405

kinasema kuwa hayakutokeya mpaka mashujaa wachache walipoamuwa kufanya mapinduzi ya maridhiyano nje ya vyama vya CUF na CCM na baadaye kuvihusisha vyama hivyo. Mapinduzi ya maridhiyano na mfungamano ni mapinduzi ya amani na hayakugharimu chochote isipokuwa imani na kuaminiyana baina ya wanamapinduzi ambao historia yao itakapokuja kuandikwa itakuwa kubwa zaidi kwa mustakbal wa Zanzibar kuliko hii iliyomo ndani ya kitabu hichi ambayo ilitokeya miaka 46 iliyopita. Mapinduzi ya maridhiyano ni mapinduzi ya mfungamano baina ya Wazanzibari ambao kwa muda mrefu walifanywa na wakakubali kufarikishwa juu ya misingi ya Uafrika na Uarabu na kuungana kwao na kufuta kisheria ubaguzi wa kikabila ni njia moja kubwa ya kuundeleza mfungamano baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia. Cha msingi ni mapinduzi ya maridhiyano na mfungamano mapya ya Zanzibar kutojiingiza kunako migogoro na nchi kubwa zenye nguvu kwa sababu nguvu kwa nguvu wenye nchi jirani na nyenginezo zilizo kubwa ulimwenguni zina nguvu na kubwa zaidi kuliko Zanzibar. Zanzibar ni nchi inayohitajiya kuongozwa kwa hikima na busara na si kwa kujitumbukiza kwenye siasa za kibabe au za kichokozi. Mapinduzi ya Afrabia yatategemeya pia mabadiliko kutoka upande wa nchi za Kiarabu na za Kiislam na khasa zile ambazo zimeshaanza kukumbwa au zitakuja kukumbwa na wimbi la maendeleo kutoka Bara la Asia na ambazo zina makhusiyano mazuri na ya karibu sana na vyuo vikuu vikubwa kutoka nchi za Magharibi. Kwa upande wa Afrika Mashariki na Kati, na khasa Zanzibar, Afrabia haitoweza kujengwa upya iwapo barafu la mfumo wa upotoshaji wa suala la utumwa na wa miaka 46 wa mapinduzi ya Zanzibar, ambao ni mtaji mkubwa wa wahafidhina na vitimbakwiri, halijayayushwa na umotoumoto wa ilimu ya historia mpya kwa kizazi kipya.

Issa G. Shivji, 2. Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union, Mkuki na Nyota Publishers, 2008, uk. 123–124.

Gary Thomas Burgess,. 3. 2009, Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad, Ohio University Press, 2009, uk. 211–212.

Jumbe, Aboud. 4. Conjecture vs Truth. 1964, uk. 6.Gary Thomas Burgess, op. cit., uk. 5. 235.Chama Cha Mapinduzi, “Kumbukumbu za Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa, 6.

Mkutano Maalum Uliofanyika tarehe 24–30/1/84,” Dodoma, uk. 25.Ibid., uk. 7. 28. Ibid., uk. 8. 29.Chama cha Mapinduzi, “Taarifa Maalumu ya Kamati Kuu kwa Halmashauri Kuu ya 9.

Taifa,” 14­12­1999, uk. 1. Ibid., uk. 10. 3.Gary Thomas Burgess, op. cit., uk. 11. 247–248.Ibid., uk. 12. 248.Ibid. uk. 13. 248.Ibid. uk. 14. 250–251.CCM, 15. 1988, uk. 12–13. 16. United Nations, UN Archives and Records Management Section, New York, S­0446­

0018­201(1). Baada ya mapinduzi Jamhuri ya Watu wa Zanzibar haikukifuta kiti chake cha Umoja wa Mataifa bali iliendeleya na uwanachama wake kwa kushirikiyana na Tanganyika chini ya jina la Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hakuna ushahidi wenye kuonyesha kuwa serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliiandikiya Umoja wa Matiafa kukifuta kiti chake Umoja wa Mataifa au hata kuonyesha iko radhi kuwa na kiti kimoja Umoja wa Matiafa na Jamhuri ya Tanganyika. Hakuna. Kilichotokeya ni ujumbe wa Dola ya Zanzibar baada ya uhuru wa tarehe 10 Disemba 1963 kwenye Umoja wa Mataifa ulikuwa haupo kwa sababu Serikali ya ZNP­ZPPP ilikuwa imepinduliwa. Ujumbe wa Jamhuri ya Tanganyika ndiyo uliyokuwepo Umoja wa Mataifa.

Page 438: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla406

Kituo cha Nyaraka za Kimataifa (Archives) cha Umoja wa Mataifa (United Nations), UN Archives and Records Management Section (ARMS) kiliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, kina zaidi ya maboksi 60 yenye maelfu ya nyaraka kuhusu historia na hali halisi ya hivi karibuni ya mawasiliyano baina ya Wizara ya Nchi za Nje ya Tanganyika (Tanzania Bara) na Umoja wa Mataifa bila ya kuihusisha nchi ya Zanzibar ambayo ni nchi shiriki kwenye Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kwa wenye kutaka kufanya utafiti zaidi na maalumu juu ya suala hili muhimu juu ya uwakilishaji wa Zanzibar ambayo ilikuwa ina kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa wanaweza kuwasiliyana na mtandao wa ARMS: http://archives.un.org/unarms/­

Ibid., S­17. 0446­0134.421.2(1­1).Ibid., S­18. 0285­0002­38[1].Ibid.19. Ibid.20. Ibid.21. Ibid., S­22. 0446­0138.S­23. 0083­0003­08[1].Ibid., S­24. 0083­0003­08[1].Ibid.25. Ibid., S­26. 0285­0002­38. United Nations General Assembly, Nineteenth Session,

“Note Verbale dated 14th May 1964 from the Secretary­General to the Representatives of Member States,” 18 May 1964. Kwa vile nchi zote mbili, Zanzibar na Tanganyika zilikuwa tayari ni wanachama wa Umoja wa Mataifa suala la Jamhuri mpya halikupelekwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliliandikiya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuliarifu huhusu mabadiliko ya mfumo mpya. Syria ilipotaka kukirudisha kiti chake Umoja wa Mataifa baada ya muungano (UAR) wake na Masri, Dr. Maamoun Kouzbari, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria alipeleka barua Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama. Kulikuwa na mjadala mmoja tu kwenye Baraza Kuu. Rais wa Baraza Kuu aliwauliza wanachama kama kuna yoyote ambaye anapinga Syria irudi kwenye kiti chake. Kwa vile hakukuwa na aliyepinga, Rais wa Baraza Kuu na mjumbe wa Syria wakatowa kauli zao.

Mawasiliyano kwa barua pepe na Andrei Kolomoets, Machi 27. 2 Legal Information Officer, Treaty Section, Office of Legal Affairs United Nations, New York 5, 2009.

28. Qur’an: Al A’nkabut 20:41. 29. Biblia: Ezekieli 37:1–14.Mazungumo baina ya mwandishi na Andrew Kambona, London, tarehe 30. 27 Agosti

2002.Barua ya Kambona yenye kichwa cha maneno “Tanzania Democratic Alliance Party 31.

(TDAP), P.O. Box 33599, Buguruni, Malapa, Dar es Salaam, Tanzania, 15 Oktoba, 1993.”Hotuba ya Rais Mstaafu Mwalimu Julius K. Nyerere kwa waandishi wa habari 32.

aliyoitowa Kilimanjaro Hotel (sasa Kempinski), Jumanne, tarehe 14 Machi 1995.Kishore Mahbubani, 33. The New Asian Hemisphere: The Irresistible Shift of Global Power

to the East, Public Affairs, 2009, uk. 52. Eqbal Ahmad, 34. Confronting Empire, Interviews with David Barsamian. (South End

Press, 2000), uk. 22Fikra ya kuanzisha jumuiya ya Afrabia isiyo ya Kiserikali (NGO) ilikuja baada ya 35.

mawasiliyano baina Waafrabia wa Afrika Mashariki na wa Ghuba na kwa kushirikiyana na Profesa Ali A. Mazrui pamoja na mwandishi wa kitabu hichi. Lengo la Afrabia ni kuongeza mafahamiyano na mashirikiyano baina ya staarabu za Kiafrika na za Kiarabu na watu wake kwa maslaha ya pande mbili na kwa ajili ya kudumisha amani duniani. Misheni ya Afrabia ni kutambuwa, kutafakhari, na kuiendeleza turathi ya Afrabia kwa kujenga mahusiyano

Page 439: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla 407

yenye faida kwa pande mbili za Afrika na Arabuni na kwa orodha ya vitendo kupitiya ilimu na kuujenga uwezo wa kijamii. Fikra ya jumuiya ya Afrabia inategemeya kujihusisha na masuala muhimu yafuatayo: ilimu; maendeleo ya jamii na ya kiuchumi; makhusiyano ya kisasa na ya kihistoria; utamaduni, sanaa na turathi; na habari.

United Nations, Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO), 36. Division of Ethics of Science and Technology Social and Human Sciences Sector, ETHICS EDUCATION PROGRAMME Bioethics Core Curriculum Proposal.

Thomas S. Kuhn, 37. The Structure of Scientific Revolutions, The University of Chicago Press, 1996, uk. 151.

Ibid., uk. 38. 159. 39. Quran, 13:11.Ali Mazrui “AFRABIA: Africa and the Arabs in the New World Order.” 40.

UFAHAMU: Journal of the African Activist Association. Vol. XX, no. 3. 1992, uk. 61.Kishore Mahbubani, 41. 2009, p. 163.Ibid. uk. 42. 164.Ibid., uk. 43. 95.E. Harper Johnson, 44. Oman: 1999, uk. 114. Ibid. uk. 45. 60. Minou Reeves, 46. 2000, Pia tizama George Makdisi The Rise of Humanism in Classical

Islam and the Christian West.Kwa mujibu wa Mohamed Ghassany “Matokeo ya mapinduzi yetu ni matatu 47.

makubwa: Kwanza ni paradigm shift. Tumeanza, kwa hakika, kuiangalia upya misimamo yetu hasa hasa kuelekea nani adui halisi wa Zanzibar. Huo ndio mwangwi wa sauti kutoka mikusanyiko ya hadhara na jahara nyumbani au baina ya Wazanzibari walio nje ya Zanzibar. Tunabadilisha mtazamo wetu mkongwe wa kuangaliana sisi kwa sisi kama maadui na sasa tunamuangalia adui hasa machoni mwake. Pili, mapinduzi yetu yanaweza kusambaza khofu kongwe ya kuiona Zanzibar ikiinuka. Natarajia sana upinzani mkali kutoka Tanganyika. Watafanya kila hila na kila mbinu, maana paradigm shift niliyoisema hapo juu, kwa hakika, inatokezea ndani ya jamii ya Wazanzibari tu na sio ndani ya nyoyo za Watanganyika watawala. Tatu, majirani wa Zanzibar, ukiacha Tanganyika ambayo kama nilivyosema itaendelea kuleta tabu yake kwa Zanzibar, Wakenya na Waganda wanaonekana kubadilisha sana muelekeo wa siasa zao kuelekea Zanzibar na kwa hivyo, wanaweza kutokushughulika nayo sana. Matatizo ya ndani ya nchi hizo hivi sasa ni makubwa na kujihusisha na suala la Zanzibar hakuna faida sana kwao, hasa kwa kuwa wanaona kuwa tayari Zanzibar ilishamilikiwa na Tanganyika kitambo. Na pia ushawishi wa kiongozi wa sasa wa Tanganyika, Rais Kikwete, si mkubwa kwao. Nyerere alikuwa anawatumikia mabwana wa Magharibi lakini alikuwa mjanja wa kuficha utumishi wake na hivyo akatumia Ukritso wake kama bango mbele ya Obote na Kenyatta. Sivyo ilivyo sasa.” Mawasiliano ya barua pepe baina ya Mohammed Ghassany na mwandishi, 21 Oktoba, 2008.

Hii ni mikakati ya binaadamu ambao wanaongozwa na khofu na maslahi yao 48. yanategemeya kuwadhibiti binaadamu wenziwao na wanapoyakosa humalizikiya kwenye huzuni na lawama juu ya yule ambaye wanamuoneya choyo. Utasikiya kila siku kuwa Zanzibar ni mzigo na haina faida kwa Tanganyika na itapata tabu bila ya Tanganyika lakini hupewi jawabu kwanini basi hawataki kuiwachiya?

Mlango wa Ishirini na Moja

1. Ramesh M. Misra alizaa watoto watatu wa kike na mmoja mwanamume. Alikuwa ni

Page 440: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mapitiyo kwa Jumla408

mmoja kati ya maofisa wa Kiingereza waliowasili Dar es Salaam pamoja na Sultan Jamshid bin Abdullah katika meli ya Sayyid Khalifa. “Mbali ya kuwa alipigana vita vya Kituo cha Polisi cha Malindi, katika jukumu lake alipokuwa ana dhamana ya Mjini Magharibi alifanya upekuzi wa makao makuu ya chama cha Umma tarehe 4 Januari na kutafuta silaha tarehe 10 Januari, na anajulikana kuwa alikuwa ofisa aliyekuwa akiwasaka wafanyaji fujo wa Afro­Shirazi katika fujo za 1961 na alimkamata mmoja wa wanasiasa ambaye alikuwa na umuhimu fulani na akanyongwa.” The National Archives DO 214/79. Letter from the British High Commission, Dar es Salaam to the Department of Technical Co­operation, London, 18th January, 1964. 2. Sheikh Ali Muhsin, uk. 51. 3. Kesi hiyo ilipelekwa Ubalozi Mdogo wa Msumbiji Zanzibar na ilisimamiwa na Bwana Gabriel I. Magoma. Nchi ya Oman haina sifa ya kujitambulisha inapofanya wema lakini jambo la kufurahisha ni kuwa wakati wa mafuriko yaliyotokeya Msumbiji mwaka 2000 nchi hiyo ilitowa msaada wa dola za Kimarekani milioni moja, na mwaka 2001 yalipotokeya tena mafuriko kwenye nchi hiyohiyo Oman ilitowa tena msaada wa dola milioni moja za Kimarekani. Inasemekana kuwa Rais Mstaafu wa Msumbiji aliwahi kumuambiya ofisa wa Kiomani kuwa nchi yake Mozambique (Msumbiji) ilipewa jina hilo kutokana na Chifu wa Kiomani aliyekuwa akiitwa Musa bin Bek. Balozi wa Ubalozi Mdogo wa Msumbiji aliyoko Zanzibar aliwahi kufanya kazi Dubai. Mifano ya Mabwana Yohana na Abdalla, na baina ya Msumbiji na Oman ni mifano mizuri ya daraja la Afrabia lenye kuwaunganisha Waafrika na Waarabu kwa maslahi ya pande zote mbili. Pia kuna kwenye gazeti la East African Standard la tarehe 6 Februari 1964 lenye kichwa cha maneno “Brutality Alleged by Arab Refugees” ambayo inaelezeya vipi “Bibi Sleyum Said Shariff alivyoyakimbiya mauti chupuchupu mapema kwenye mapinduzi. ‘Mpiganiya uhuru,’ kutoka kabila la Kimakonde kutoka Tanganyika alikuwa tayari kumuuwa mtoto, akatokeya jirani ambaye ni mwanachama wa ASP na kuingiliya. Mtoto wake wa kike baadaye alipigwa na alipigwa vibao na matokeyo yake anaamka katikati ya usiku anapiga makelele ya jinamizi. Mumewe alitaka kuuwawa aliporushiwa mkuki. Mrushaji alikuwa si hodari na ukamchuna kwenye kifua. Aliwaona watoto wa kike wadogo wakiingiliwa katika kambi ya kizuwizi ya Raha Leo.” The National Archives DO 185/60.

Page 441: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho

A. Hotuba ya Mzee Abeid Amani Karume kuukaribisha Uhuru wa Dola ya Zanzibar ya tarehe 10 Disemba, 1963.

Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru. Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola za Commonwealth. Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi hii ni huru chini ya mpango wa Sirikali ambayo msingi wake umejengwa juu ya kuendelea kwa ridhaa ya wananchi. Ili kufikilia matarajio yetu hayo tunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliyohusika na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siasa na uhuru wa dola yoyote nyengine. Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila ya kujali fikra zetu za siasa au madaraka yetu kusaidia kweli kweli Katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru. Tulioyapata leo mwezi 10 Disemba ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu nao ni ujinga, umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa adawa ipo, na kuleta mapenzi mahala ambapo pana chuki, ili dola yetu mpya ichomoze katika neema, umoja na furaha. Kwa hivyo katika hii siku ya leo na tumwombe Mwenye Enzi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala, atuweke tuifanye na tuitimilize kazi kubwa ya kujenga taifa letu ili dola yetu mpya ya ZANZIBAR ipate baraka ya matunda mema ya kazi zetu. Uhuru na Umoja, Uhuru na Kazi!

Page 442: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho410

B. S­0446­0018­201 [1]

Page 443: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho 411

C. S­0446­0134.421.2 [1­1]

Page 444: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho412

D. S­0083­0003­08 [1]

Page 445: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho 413

E. S­0083­003.08 [1]

Page 446: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho414

F. S­0285­0002­38 [1]

Page 447: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho 415

Page 448: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho416

Page 449: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho 417

G. S­0083­0003­08 [1]

Page 450: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho418

H. S­0285­0002­38 [1]

Page 451: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho 419

I. S­0285­0002 38

Page 452: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Viambatanisho420

Page 453: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo

Wingi wa vitabu vinavyoandikwa juu ya mada ni kizuizi katika kubobea kuitawala mada. —Ibn Khaldun

Nyaraka za Kitaifa

The National Archives (Public Record Office) Kew, Surrey:

CAB 21/5524CO 822/825CO 822/2335CO 822/2731CO 822/3014CO 822/3063CO 822/3126CO 822/3148 116805DO 118/295DO 185/59DO 185/60DO 166/79 116843DO 213/236DO 213/251DO 216/41DO 185/47DO 185/48 116923DO 185/59 116805FO 37/174035HO 344/309WO 276/541WO 276/373

Page 454: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo422

The United Nations, UN Archives and Records Management Section, New York:

S­0083­003­08S­0285­0002­38S­0446­0138S­0446­01342.2 (1­1)

Kituo cha Nyaraka za Kimataifa (Archives) cha Umoja wa Mataifa (United Nations), UN Archives and Records Management Section (ARMS) kiliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, kina zaidi ya maboxi 60 yenye maelfu ya nyaraka kuhusu historia na hali halisi ya hivi karibuni ya mawasiliyano baina ya Wizara ya Nchi za Nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Umoja wa Mataifa. Kwa wenye kutaka kufanya utafiti zaidi na maalumu juu ya suala hili muhimu juu ya uwakilishaji wa Zanzibar ambayo ilikuwa ina kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa wanaweza kuwasiliyana na mtandao http://archives.un.org/unarms/­ Kitengo hichi cha Umoja wa Mataifa kina nyaraka kamili juu ya historia ya viti vya Zanzibar na Tanganyika katika Umoja wa Mataifa, na kwa vile hakina wafanyakazi wa kutosha na nyaraka nyingi sana na bado hazijawekwa kunako mtandao, iko haja ya kufanya miadi kabla ya kwenda kufanya utafiti.

Mapitio yaliochapishwa na yasiochapishwa

Afro­Shirazi Party. Hamna tarehe. “Zanzibar and Pemba. Sheria.” ———. 1974a. The Afro-Shirazi Party Revolution, 1964–1974. Printpak Tanzania

Limited.———. 1974b. Jeshi la Wananchi wa Tanzania, 1964–1974, Zanzibar. Printpak

Tanzania Limited.Ahmad, Eqbal. 2000. Confronting Empire. Interviews with David Barsamian.

South End Press.Al Barwani, Ali Muhsin. 2003. Kujenga na Kubomolewa Zanzibar

(Kumbukumbu). ———. 2000. Tarjama ya “Al Muntakhab” Katika Tafsiri ya Qur’ani Tukufu. Daar

Al­Fajr Al­Islami, Damascus. Tarjuma ya Qur’an Tukufu ya al­marhum Sheikh Ali Muhsin kwa lugha ya Kiswahili inapatikana hapa: http://www.iiu.edu.my/deed/quran/swahili/index.html

al­Barwânî, Sauda, R. Feindt, L. Gerhardt, L. Harding and L. Wimmelbücker, eds. 2003. Unser Leben vor der Revolution und danach – Maisha yetu kabla ya mapinduzi na baadaye. Hamburg.

Al­Ismaily, Issa bin Nasser. 1999. ZANZIBAR Kinyang’anyiro Na Utumwa.

Page 455: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo 423

al­Maamiry, Ahmad Hamoud. 1988. Omani Sultans in Zanzibar (1832–1964). New Delhi.

Al Miskry, Saleh S. I. 1994. “Pan­Africanism and Nyerere in Tanzania.” Ph.D. diss., University of Salford.

Al­Riyamy, Nasir Abdullah. 2009. Zinjibar: Shakhsiyyaat wa Ahdaath: 1827–1972. Dar Alhikma, London.

Ameir, Hamid. 2008. “Shabaha ya Mapinduzi haijatekelezwa.” Mwananchi. Toleo Maalumu. Miaka 44 ya Mapinduzi. Januari 11, 2008.

Askew, Kelly. 2002. Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. University of Chicago Press.

Attwood, William. 1967. The Reds and the Blacks: A Personal Adventure. Harper & Row.

Axel, Brian Keith. ed. 2002. From the Margins: Historical Anthropology and Its Futures. Duke University Press.

Baalawy, A. E. No date. Nyerere and Muslim Tanzania. The Zanzibar Organisation.

Babu, A. M. 2002. The Future That Works: Selected Writings of A.M. Babu. Edited by Salma Babu and Amrit Wilson. Africa World Press.

———. 2001. “Wanted: A Third Force in Zanzibar.” I Saw The Future and It Works: Essays Celebrating the Life of Comrade Abdulrahman Mohamed Babu, 1924–1996. Ed. Haroub Othman.

———. 1981. African Socialism or Socialist Africa. Zed Press.Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). 2009. Mpango wa Kuhamasisha

Huduma ya Kiunchungaji Katika Jamii Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010. Bengelsoorf, Carollee, Margaret Cerullo, and Yogesh Chandrani, eds. 2006. The

Selected Writings of Eqbal Ahmad. Foreword by Noam Chomsky. Columbia University Press.

Bergen, Jan P. van. 1981. Development and Religion in Tanzania: Sociological Soundings on Christian Participation in Rural Transformation. Published jointly by The Christian Literature Society, Madras and The Interuniversity Institute for Missiological and Ecumenical Research, Department of Missiology, Leiden.

Biblia Takatifu: Agano la Kale. 1985. Chama cha Biblia, Dodoma.Bogdanovich, Peter. 1997. Who the Devil Made It: Conversations with Legendary

Film Directors. Ballantine Books.Boss, Pauline. 2000. Ambiguous Loss: Learning to Live with Unresolved Grief.

Harvard University Press.Boullata, Issa J. 1990. Trends and Issues in Contemporary Arab Thought. State

University of New York Press. Burgess, G. Thomas. 2009. Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in

Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad. Ohio University Press.

Page 456: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo424

———. 2002. “Youth and the Revolution: Mobility and Discipline in Zanzibar, 1950–80.” Ph.D. diss., Indiana University.

Central Intelligence Agency (CIA). 1966. “Zanzibar: The Hundred Days’ Revolution.” Written by Helen­Louise Hunter.

Chama cha Mapinduzi. 1999. “Taarifa Maalumu ya Kamati Kuu kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.” Tarehe 14­1212/1999.

———. 1988. Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Tatu Ulio­fanyika Dodoma tarehe 11–13 Mei 1988.

———. 1985. “Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Kumi na Mbili (Mkutano Maalum) Uliofanyika Dar es Salaam tarehe 14 Agosti 1985.”

———. 1984. “Kumbukumbu za Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano Maalum Uliofanyika tarehe 24–30/1/84.” Dodoma.

Chaudhuri, K. N. 1985. Trade and Civilisation in the Indian Ocean: An Economic History from the Rise of Islam to 1750. Cambridge University Press.

Clarence­Smith, William. 2006. Islam and the Abolition of Slavery. Oxford University Press.

Clayton, Anthony. 1981. The Zanzibar Revolution and Its Aftermath. Archon Books.

Cohen, David William. 1994. The Combing of History. The University of Chicago Press.

Daruweshi, Khamis. 2002. “Hamis Daruweshi afichua siri ya mapinduzi Zanzibar.” Mwananchi. Septemba 8, 2002.

Davidson, Basil. 1992. The Black Man’s Burden: Africa and the Curse of the Nation-State. Times Books.

Dawood, N. J., ed. 1981.The Muqaddimah: An Introduction to History. Translated from the Arabic by Franz Rosenthal. Bollingen Series/Princeton.

Donham, Donald L. 1999. Marxist Modern: An Ethnographic History of the Ethiopian Revolution. University of California Press and James Currey.

Duggan, W. R. and J. R. Civille. 1976. Tanzania and Nyerere. Orbis Books.Eaton, Gai. 1997. Islam and the Destiny of Man. The Islamic Texts Society.Faiq, Mohammed. 2002. Abdel Nasir wa a-Thawra Al-Afriqiyya (Abdel Nasser and

the African Revolution). Dar el Mustakbal Al­Arabi, Fourth Edition.Fanon, Frantz. 1963. The Wretched of the Earth. Grove Weidenfeld. Friedland, W. 1969. Vuta Kamba: The Development of Trade Unions in Tanganyika.

Hoover Institution Press.Gordon, Colin, ed. 1980. Power/Knowledge: Selected Interviews and Other Writings,

1971–1977, by Michel Foucault. Pantheon Books.Glassman, Jonathon. 2010. “Racial violence, universal history and echoes of

abolition in twentieth­century Zanzibar.” In Abolition and Imperialism in

Page 457: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo 425

Britain, Africa, and the Atlantic, edited by Derek R. Peterson. Ohio University Press.

———. 1995. Feasts and Riots: Revelry, Rebellion and Popular Consciousness on the Swahili Coast, 1856–1888. Portsmouth.

Gleijeses, Piero. 2002. Conflicting Missions Havana, Washington, and Africa, 1959–1976. The University of North Carolina Press.

Grimshaw, Anna, ed. 1999. “Whitman and Melville.” The C. L. R. James Reader. Blackwell Publishers.

Hall, Richard. 1996. Empires of the Monsoon: A History of the Indian Ocean and Its Invaders. Harper Collins Publishers.

Harding, Leonhard. 2003. “Nyerere in neuem Licht. Interpretationen in den Lebensgeschichten von Sansibaris” [Nyerere in a New Light. Interpretations in the Life­Histories of Zanzibaris]. Unser Leben vor der Revolution und danach - Maisha yetu kabla ya mapinduzi na baadaye, eds. Sauda A. Barwani, Regina Feindt, Ludwig Gerhardt, Leonhard Harding, and Ludger Wimmelbücker. Rüdiger Köppe.

Hansberry, William Leo.1977. Africa and Africans as Seen by Classical Writers: The William Leo Hansberry History Notebook, Volume II, edited by Joseph E. Harris. Howard University Press.

———. 1974. Pillars in Ethiopian History: The William Leo Hansberry African History Notebook, Volume I, edited by Joseph E. Harris, Howard University Press (Washington).

———. 1972. Africa at Nsukka: Inagural Address Delivered at The Hansberry College of African Studies Nsukka, Eastern Nigeria, September 22, 1963. Howard University, Washignton, D.C.

Hennelly, Alfred T., ed. 1990 Liberation Theology: A Documentary History. Orbis Books, Maryknoll.

Her Majesty’s Stationery Office. 1962. Report of the Kenya Coastal Strip Conference, 1962. Presented to Parliament by the Secretary of State for the Colonies by Command of Her Majesty.

———. 1961. Report of a Commission of Inquiry into Disturbances in Zanzibar during June 1961. London.

Hinton, Alexander Laban. ed. 2002. Genocide: An Anthropological Reader. Blackwell Publishers.

Hourani, Albert. 2004. Arabic Thought in the Liberal Age 1798-1939. Cambridge University Press.

Hunter, Helen­Louise. 2010. Zanzibar: The Hundred Days Revolution. PSI Reports, Praeger Security International.

Ingrams, W.H. 2007. Zanzibar: Its History and Its People. Stacey International.Iqbal, Azal. 1983. The Life and Work of Jalaluddin RUMI. The Octagon Press,

London.

Page 458: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo426

Jacopetti, Gualtiero and Franco Prosperi. 1966. Africa Addio: Africa Aflame – The Book of the Sensational Documentary Film by the Makers of “Mondo Cane.” Ballantine Books, New York.

Johnson, E. Harper. 1999. Oman: A Pictorial Resuscitation. Ministry of Information, Sultanate of Oman.

Jumbe, Aboud. 2004. Conjecture vs Truth.———. 1994. The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30 Turbulent years.

Amana Publishers, Dar es Salaam.Khamis, K. S. and H. H. Omar, eds. 1994. Historia Fupi ya Zanzibar, Idara Ya

Nyaraka, Makumbusho na Mambo ya Kale. Zanzibar. Kharusi, Ahmed Seif. 1971. Letters Smuggled Out of Zanzibar. Portsmouth

Printers Ltd. Kimche, David. 1973. The Afro-Asian Movement: Ideology and Foreign Policy of the

Third World. Israel Universities Press.Kritman, Lawrence D., ed. 1988. Michel Foucault: Politics, Philosophy, Culture:

Interviews and Other Writings 1977-1984. Routledge.Kuhn, Thomas S. 1996. The Structure of Scientific Revolutions. The University of

Chicago Press. Ladhu, Ismail Jussa. 1999. “Treating the disease not the symptoms: The case of

Zanzibar’s opt out from the United Republic of Tanzania.” LLB (Hons.) diss., University of Hull.

Las Casas, Bartolome de. 1999. Short Account of the Destruction of the Indies.Penguin Classics.

Laurence, Tony. 2007. The Dar Mutiny of 1964, and the Armed Intervention That Ended It. Book Guild Publishing.

Lemarchand, Rene. 2009. The Dynamics of Violence in East Africa (National and Ethnic Conflict in the 21st Century). University of Pennsylvania Press.

Lofchie, Michael. 1965. Zanzibar: Background to Revolution. Oxfrod University Press.

Loimeier, Roman. 2009. Between Social Skills and Marketable Skills: The Politics of Islamic Education in 20th century Zanzibar. Brill.

———. 2008. “The Baraza in Zanzibar: Local Sitting and Transnational Thinking in a Cosmopolitan Setting.” In A. Adogame, Magnus Echtler and Ulf Vierke (eds.), Unpacking the New: Critical Perspectives on Cultural Syncretization in Africa and Beyond. Hamburg, 143–174.

———. 2006. Memories of Revolution: Zur Deutungsgeschichte einer Revolution (Sansibar 1964), in: Afrika Sepectrum, 41, 2, 175–197.

Ludwig, Frieder. 1999. Church and State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994. Brill.

Mahbubani, Kishore. 2009. The New Asian Hemisphere: The Irresistible Shift of Global Power to the East. Public Affairs.

Page 459: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo 427

Makdisi, George. 1990. The Rise of Humanism in Classical Islam and the Christian West. Edinburgh University Press.

Mamdani, Mahmood. 2001. When Victims Become Killers: Colonialism, Nativism and Genocide in Rwanda. Princeton University Press, Princeton; David Phillip, Cape Town; Fountain, Kampala; and James Currey, London.

———. 1996. Citizen and Subject: Contemporary Africa and the Legacy of Late Colonialism Princeton University Press, Princeton; David Phillip, Cape Town; Fountain, Kampala; and James Currey, London.

Marshall, Peter. 1992. Demanding the Impossible: A History of Anarchism. Harper Collins Publishers.

Mazrui, Alamin M. and Ibrahim Noor Shariff. 1994. The Swahili: Idiom and Identity of an African People. Africa World Press.

Mazrui, Ali A. 2008. Euro-Jews and Afro-Arabs: The Great Semitic Divergence in World History. Edited by Seifudein Adem. University Press of America, Inc.

———. 1992. “Afrabia: Africa and the Arabs in the New World Order.” UFAHAMU: The Journal of the African Activist Association 20 no. 3.

Mazrui, Ali A. and Michael Tidy. 1984 Nationalism and the New States in Africa: From about 1935 to the Present. Heinemann Educational Books.

Mbotela, James. 1934. Uhuru wa Watumwa. Sheldon Press.Mdundo, Minael­Hosanna O. 1996. Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha.

Kimechapishwa na DUP. LTD, Dar es Salaam. Memorandum of Understanding Between Christian Council of Tanzania and

Tanzania Episcopal Conference And The United Republic of Tanzania. Drawn by Prof. Dr. C. R. Mahalu, Faculty of Law, University of Dar es Salaam, 21 February, 1992.

Mouffok, Ghania. 2000. “Remembering a Forgotten History: Amnesia in Algeria.” Le Monde diplomatique, June 2000.

Mpiga chapa Mkuu wa Serikali Zanzibar. 2002. Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 1995.

Mrina, B. F. and W. T. Matokke. 1980. Mapambano ya Ukombozi Zanzibar. Tanzania Publishing House.

Mudimbe. V. Y. 1988. The Invention of Africa: Gnosis, Philosophy, and the Order of Knowledge. Indiana University Press and James Currey.

Mwakikagile, Godfrey. 2005. Nyerere and Africa: End of An Era. Protea Publishing.

Mwanjisi, R.K. 1967. ABEID AMANI KARUME. East African Publishing House.

Njozi, Hamza Mustafa. 2000. Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania. Globalink Communications.

Nye, Joseph S. 1986. Pan-Africanism and East African Integration. Harvard University Press.

Page 460: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo428

Nyerere, Julius K. 1966. “The Race Problem in East Africa.” In Freedom and Unity: A Selection from Writings and Speeches 1952–1965. Dar es Salaam: Oxford University Press.

Obama, Barack. 2006. The Audacity of Hope: Thoughts on Reclaiming the American Dream. Three Rivers Press.

———. 2004. Dreams from My Father: A Story of Race and Inheritance. Three Rivers Press.

Oded, Arye. 2000. Islam and Politics in Kenya. Lynne Rienner Publishers.Oginga Odinga. 1967. Not Yet Uhuru. Heinemann.Philipson, Robert. 1987. “Slavers and Savious: Images of Arabs and Englishmen

in Uhuru wa Watumwa.” Ba Shiru Journal of African Languages and Literature, Spring, 13, no. 1.

Prunier, Gerard. 2008. Africa’s World War: Congo, the Rwandan Genocide, and the Making of a Continental Catastrophe. Oxford University Press.

Rabinow, Paul, ed. 1984. The Foucault Reader. Pantheon Books.Raviv, Dan and Yossi Melman. 1990. Every Spy a Prince: The Complete History of

Israel ’s Intelligence Community. Houghton Mifflin Company.Reeves, Minou. 2000. Muhammad in Europe A Thousand Years of Western Myth-

Making. New York University Press.Rocker, Rudolf. 1998. Nationalism and Culture. Black Rose Books Ltd.Rodney, Walter. 1982. How Europe Under Developed Africa. Howard University

Press.Rosenthal, Frantz, trans. 1967. The Muqaddimah: An Introduction to History.

Princeton University Press.Roth, Michael S. and Charles G. Salas, eds. 2001. Disturbing Remains: Memory,

History, and Crisis in the Twentieth Century. Getty Research Insitute. Rumi, Jalaluddin. 2007. The Masnavi. Book 2, translated by Jawid Mojaddedi.

Oxford University Press.———. 2004. The Masnavi. Book 1, translated by Jawid Mojaddedi. Oxford

University Press. Sabea, Hanan Hosni. 2000. “Moments and Processes: Redefining the Building of

‘A New Society’ in Tanzania.” Ph.D. diss., Johns Hopkins University.Said, Mohamed. 2009. Uamuzi wa busara wa Tabora. Abantu.———. 2002. Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia

Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Kimefasiriwa na Ali Salum Mkangwa. Phoenix Publishers, Nairobi.

———. 1998. The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. Minerva Press.

Page 461: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo 429

Shariff, Ibrahim Noor. 1988. TUNGO ZETU Msingi wa Mashairi na Tungo Nyinginezo. The Red Sea Press.

Scheper­Hughes, Nancy and Philippe Bougois, eds. 2004. Violence in War and Peace: An Anthology. Blackwell Publishing.

Sheriff, Abdul. 2001. “Race and Class in the Politics of Zanzibar.” Afrika Spectrum 3, 301–18.

———. 1987. Slaves, Spices and Ivory in Zanzibar. James Currey.Sheriff, Abdul and Ed Ferguson, eds. 1991. Zanzibar under Colonial Rule. James

Currey.Shivji, Issa G. 2008. Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-

Zanzibar Union. Mkuki na Nyota Publishers.———. 2006. Let the People Speak: Tanzania Down the Road to Neo-Liberalism.

Codesria.———. 1986. Law, State and the Working Class in Tanzania. James Currey.Sider, Gerald and Gavin Smith, eds. Between History and Histories: The Making of

Silences and Commemorations. University of Toronto Press.Sivalon, J. C. 1992. Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985.

Peramiho. Smith, Bob, with Salim Amin. 1998. The Man Who Moved the World: The Life and

Work of Mohamed Amin. Camerapix Publishers International. Smith, William Edgett. 1981. Nyerere of Tanzania. Zimbabwe Publishing

House. Soghyroun, Ibrahim El Zein. 1992. Islam, Christian Missions and Colonial

Administraion in East Africa. Tagore, Rabindranath. 1917. Nationalism. The Macmillan Company.Tanpinar, Ahmed Hamdi. 2002. The Time Regulation Institute.Turko­Tatar Press.Tanzania People’s Defence Forces. 1993. Tanganyika Rifles Mutiny January 1964.

Dar es Salaam University Press.The Supreme Council, The East African Muslim Welfare Society. 1954. Souvenir

of the East African Muslim Welfare Society. Haderbhoy Building, Fort Jesus Road, Mombasa.

Tiberondwa, Ado K. 1998. Missionary Teachers as Agents of Colonialism in Uganda: A Study of Their Activities in Uganda, 1877–1925. Fountain Publishers.

Tolstoy, Leo. 1984. The Kingdom of God Is Within You: Christianity Not as a Mystic Religion but as a New Theory of Life. University of Nebraska Press.

———. 1983. Confessions. Norton.Truffaut, Francois. 1983. Hitchcock: The Definitive Study. Simon & Schuster.Turner, Thomas. 2007. The Congo Wars: Conflict, Myth and Reality. Zed Press.United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO),

Division of Ethics of Science and Technology, COMEST The Teaching of Ethics. Paris, 26th January 2003, Oslo, 10th–12th May 2003.

Page 462: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Marejeo430

Vidyarthi, Shravan. The African Lens: The Story of Priya Ramrakh. A documentary film screened at the Zanzibar International Film Festival, July 14th, 2008.

Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT). 2009. Ilani: Mapendekezo Yetu ya Vipaumbele Vya Kitaifa.

Wheatcroft, Andrew. 1983. The World Atlas of Revolutions: The Antecedents, Character and History of the Revolutions of the Modern Age from the American Revolution to the Revolutionary Violence of the 1980s. Simon and Schuster.

Williams, Eric. 2007. Capitalism And Slavery. Williams Press.Wrong, Michela. 2009. It’s Our Turn To Eat: The Story of a Kenyan Whistle-Blower.

Harper.Young, Robert J. C. 2001. Postcolonialism: An Historical Introduction. Blackwell

Publishing. Zanzibar Nationalist Party. No date. Whither Zanzibar? Growth and Policy of

Zanzibar Nationalism. The National Publications House Press, Cairo. Zanzibar Protectore. 1960. Staff List (As at 1st January 1960). Government

Printer. Zeleza, Paul Tiyambe. 2003. Manufacturing African Studies and Crises. Codesria

Book Series.Zinn, Howard. 1990. Declarations of Independence Cross-Examining American

Ideology. Harper Perennial.Zwanenberg, R. M. A. 1975. “Anti­slavery, the ideology of the 19th century

imperialism in East Africa.” In HADITH 5 Economic and Social History of East Africa. East Africa Literature Bureau.

Page 463: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Abdalla, Jumaanne, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, 55; uteuzi wa Kambi ya Sakura, 61; kuwakusanya watu kwenda Zanzibar, 64; kamchaguwa Mohammed Omar Mkwawa, 70; kumjuulisha na Oscar Kambona, 70.

Abdel Salaam Aarif, Rais wa Iraq (1963–1966), 191.

Abdulshakur, kumpotosha Mzanzibari, xx.Affan, Khalifa Othman ibn, maafa ya ilimu,

371n.Afrabia, jina lililobuniwa na Profesa Ali A.

Mazrui, xviii; Aboud Mmasai, 159; 296; 322; na Kambona, 336; faida za, 337; kukwama ndani ya uzalendo wa, 340; mapinduzi, 341; fikra, 342; na thakafa ya Kiislamu, 342; 346; 349, 351.

Afri, watu ambao bado hawajulikani na wakiishi Afrika ya Kaskazini, 360n.

Africa Addio, 320; hakika ya tukio, 404–405n.

Africa Diaspora Heritage Trail, mkutano Dar es Salaam na Zanzibar, 17.

African Association, barua kwa Balozi wa Kiingereza, 18.

African Socialism (Ujamaa), utengenezaji, 210.

Afrika, asili ya jina, 12; 360–361n. Afriqus b. Qays b. Sayfi, Mfalme wa Yemen,

11.Afro­Shirazi Makonde, 132.Afro­Shirazi Party (ASP), Shirikisho na

Ufalme, 23; duka na Tupendane, 41; maamuzi ya mapinduzi, 177; TANU na kuundwa kwa, 313.

Afro­Shirazi Party Youth League (ASPYL), na Saleh Saadalla, 169; na Tupendane, 49; vijana wa Kimakonde kujiunga na, 103.

Ahmad, Eqbal, mpasuko wa India, xx; na Chuo Kikuu cha Ibn Khaldun, 340.

Ahmada, kifo cha Karume, 114.Aikido, 395n.Al­Barwani, Ali Muhsin, moja katika

sababu kubwa za mapinduzi, 3; kuondoka Mngereza, 50; Wamakonde, 87; mawasiliano na Smithyman, 227; na Khamis Abdalla Ameir Raha Leo, 232; kuhusu Kamishna Sullivan, Salum Kombo, 233; Uzayoni, 236; Ubeberu na Uzayoni, Ethiopia, 240; King Hassan, 241; Shirikisho la Afrika Mashariki, 242; Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Joseph Murumbi, Peter Koinange, George Padmore, Mahatma Ghandhi, 243; PAFMECA, 244; Gamal Abdel Nasser, 244; 349; 358n, kwa nini kujikaribisha na Gamal Abdel Nasser, ndege za “Al­Qahira”, 358n; James Callaghan juu ya Zanzibar kuwa ni dola huru, 361n; mkutano uliofanyika Tumbatu, 363n.

Al­Barwani, Mohamed Salim ( Jinja), 350.Al­Barwani, Moza bint Khalfan, na

Wamakonde, 350.Al­Barwani, Muhammad bin Khalfan

(Rumaliza), 295–296.Algeria, Nyerere na Makao Makuu ya

Kamati ya Ukombozi, 8, 9; silaha, 36; kwenda kusoma wapigania uhuru wa Mozambique, 103; silaha zilizotumika

Faharisi

Page 464: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi432

kwenye vita vya Malindi, 174; Aboud Mmasai, Twala , Ali Mwinyi Tambwe, Saadalla, Khatibu, 184; silaha, 380n.

Al­Ghassani, Muyaka bin Haji, 354.Algiers, 8.Al­Harthi, Bushiri bin Salim, 296. Ali, Machano Khamisi, kujuwa kuhusu

mapinduzi, 66.Al­Ismaily, Issa Nasser, 242; juu ya tabia ya

Sheikh Mohammed Shamte, 367n.Alkabeza, mkubwa wa uhamiaji, Tanga, 55.Al­Khalili, Sheikh Abdulla, athari ya

mapinduzi juu ya Oman, 321.Al­Khanbshy, Rashid bin Ali bin Rashid,

aina za hasad, 398n.Al­Kharusi, Seleman Said, 226; na msaada

wa kijeshi, 292; kukataa kuchukua nafasi ya Kamishna wa Jeshi la Polisi la Zanzibar, 293.

Al­Maamari, Ahmed Humud, 191; Al-Hakika Al Zinjibar – Ukweli wa Zanzibar, 196.

Al­Maktoum, Sheikh Mohammed bin Rashid, 206.

Al­Maktoum, Sheikh Rashid bin Said, kupokewa kwa Wazanzibari Dubai, 202, 203.

Al Masoudi, Balozi wa Algeria UAE, 200.Al­Mauly, Khelef Said Rashid, 166.Al­Miskry, Saleh, 18.Al­Qasimi, Sultan bin Mohammed,

kumualika Ben Bella Sharjah, 197, 198.Al­Riyami, Nasser Abdulla, 292. Al­Sabahi, Mbarak bin Khalfan, 191. Al­Ya’rubi, Sultan bin Saif, kuwaondowa

Wareno Oman, 33.Amani, Ibrahim, na mapinduzi, 51.Amboni, shamba la mkonge, 59.Ameir, Hamid, mahojiano kuhusu

mapinduzi, 24; na Saidi Omari Saidi, 44; na habari za Tupendane, 49, 51.

Amin, Idi, na Nyerere, 65, 215. Amin, Mohamed (Mo), maziko ya majahazi,

321. Amnesty International, 204.Amour, Salmin (Rais Mstaafu), OIC, 22,

282, 329; na Mohammed Gharibu Bilal, 287.

Anthony, Lucas, mwanafunzi wa Shimo la Mungu, 104.

Arabian Gulf University, 203.Arusha, usafi wa Ukristo, xxii.Askew, Kelly, 355n.Awlad Hemed, 349.Azania, 12.Aziz, Dossa, 316.Aziz, Hamza, na mapinduzi, 62; siku ya

mapinduzi, 230; na ripoti ya CIA, 305.Babu, Abdulrahman Mohammed, jemedari

wa mapinduzi, 23; Balozi wa Cuba na mapinduzi, “Mungu wa Waafrika” 28, 38; mikakati ya kupindua, 71; kuyafahamu mapinduzi, 128; kusafirishwa na Saadalla, 178; ndani ya boti ya Misha, 220; Ngazija, 276; diary, 297; miradi mitatu, 346–347; Ali Nabwa juu ya kuandika kitabu kuhusu mapinduzi, 364n.

Bagamoyo, uchafu wa Uislam, xxii; harakati kubwa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar, 223.

Baghdad, 191. Ba Gua Zhang, 395n.Bahari ya Hindi, kuunganisha mabara, 13. Bakari, Sefu,15; na Tupendane, 51; siri

ya mapinduzi, 128, 169; vikundi tisa vilivotuhumiwa kutaka kufanya mapinduzi, 368n.

Balozi Abdul Faraji, 219, 223. Bambi, wanamapinduzi, 51.Bantu Pan­Africanism, dhidi ya wasiokuwa

Wabantu, 13. Bapa, Othman, mahojiyano, xxiv;

kutoyafahamu mapinduzi, 139. Baramia, Muhammed, alomuuwa Abeid

Amani Karume, 262; jinamizi la kuuliwa Karume, 263.

Barawa, 195.Baraza Kuu la Waislam Tanzania

(BAKWATA), baada ya kuvunjwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS), 4.

Baraza la Mapinduzi (MBM), na Hamid Ameir, 51; na kiti cha Kenya, 108–109.

Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA), na Aboud Jumbe, 282.

Baraza la Wawakilishi, nguvu mbele ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 109; kuanzishwa, 327; jawabu ya barua ya Nyerere kwa Jumbe, 328.

Page 465: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 433

Barghash, Sultan, wakfu wa maji, 30.Barua kwa Nyerere, Kenyatta na Obote,

170, 176. Bavuai, Saidi Idi, mahojiani Cuba, 24. Ben Bella, Ahmed, mazungumzo na

Nyerere, 8; kufanikisha mapinduzi, 29; na Nyerere, 187; Gamal Abdel Nasser na Zanzibar, 188; Modibo Keita, 188, Ahmed Sekou Toure, Nkrumah, 188, 189.

Benedicto, na vifo vya kina Hanga, nk, 272.Beni, Khamisi, 161, 163; kuonana na

Mmasai Kwa Hani, 166; kuuliwa, 176; kwenda kumsafirisha Babu, 178; kuteremshwa silaha, 186.

Beni Bati, na Tupendane, 44.Ben Yelles, Racchid, Kepteni wa MV Ibn

Khaldun, 9.Bhalo, Joseph, “nchi hii mtihani”, 52;

kuvunja ghala ya silaha, 102, 123. Biafra, 215.Bi Kazija, 126, 143, 145. Bilali, Mohammed Gharibu, kudai nchi ya

Zanzibar, 287.Boff, Leornardo, 447.Bomani, Paul, 5.Bonhoeffer, Dietrich, 447.Bott, Alan, ripoti ya Karume kuhusu

mapinduzi, 36. Boumedienne, Houari, 200. Boutaflika, Abdelaziz, 200.Broomfield, Gerald, 4.Brown, Ronald, Mwanasheria Mkuu wa

Tanganyika na baadaye Tanzania (1961–1965), juu ya Joan Wickens, 383n.

Bulushi, Abdalla Juma, 179.Bungi, 40.Bweleo, kuingizwa watu kutoka bara, 69;

njia ya magendo, 105. Cape Delgado, 99, 102, jadi ya vita, 112,

113. Cape Town, 7.Castro, Fidel, na Zanzibar, 188.Chaani, asili na maana ya jina, 112.Chama cha Mapinduzi (CCM), wazalendo

waaminifu, xiv; upinzani kutoka ndani, xxiii­xxiv; Halmashauri Kuu ya Taifa, 327, 329, 330.

Chama cha Wananchi (CUF), wazalendo waaminifu, xiv.

Chifu Mwanya, 350.Chipaka, na ZNP, 54.Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro, 300.Chumbe, mpaka na Zanzibar, 61, 65, 66.Chumbuni, mikutano ya mapinduzi, 254.Chuo cha Afrabia, 340.Chuo Kikuu cha Chama, Kivukoni, 13.Chuo Kikuu cha Kiislam cha Afrika

Mashariki na Kati, sababu ya kupinduliwa Zanzibar, 3–4; 245.

Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, 340.Clayton, Anthony, kujiuzulu kwa Othman

Sharif, Hasnu Makame, Idris Wakyl na Saleh Saadalla, 26; kukosekana kwa utafiti wa midani Zanzibar, 305.

Cohen, David, 355n.Colito, 6.Commonwealth Relations Office, na uasi

wa jeshi la Tanganyika, 5. Coopers, 101. Crosthwait, T. S., 278. Cuba, mahusiano na Urusi na Uchina, 38;

uwezo wa kusaidia kupindua Zanzibar, 381n.

Cyprus, Sir George Mooring, Zanzibar na, 294.

Daily Telegraph, na Oscar Kambona, 6. Danieli, A. B. C., safari ya Algeria, 8. Dar es Salaam, watu wa bara wanaoishi Dar

es Salaam hawajui kuhusu mapinduzi, 83.

Daruweshi, Khamis, mahojiano kuhusu mapinduzi, 24; na Makomredi, 142.

Dau, Ramadhani Kitwana, 447.Davidson, Basil, 215. Dayan, Moshe, ziara ya Zanzibar, 222.Derham, A. B. P. J., mshahara, 294.Djoudi, Noureddine, na Nyerere, 9; 188,

189; kuwepo Zanzibar, 315; 380n.DNA, viini vya, xxii. Dosi, Muharam, wanafunzi wa kituo cha

FRELIMO cha Dunga, 103.Douglas, Brigadier, na Kambona, Paul

Bomani na Rashidi Kawawa, 5. Dubai, 300.Dugheshi, Amour, na Kituo cha Polisi cha

Malindi, 175; na kumfundisha Twala kutumia silaha, 317.

Dunga, kituo cha FRELIMO, 103.Dunga, ngoma ya Kimakonde, 102.

Page 466: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi434

East African Muslim Welfare Society (EAMWS), kuvunjwa, 2; kupigwa vita na Nyerere, 213; ujumbe nchi za Kiarabu/Kiislam, 394n.

Egypt Air, 212.Emerson, Ralph Waldo, na Uislam, 344.Ethiopia, jina la eneo la Afrika, 12; mpaka

Kilimanjaro, 240; Zanzibar na Afrika Mashariki, 295.

Faiq, Mohammed, mkataba wa kijeshi baina ya Zanzibar na Masri, 36.

Fanon, Frantz, mkakati kinyume na wa Mahatma Ghandi, 393n.

Farsy, Abdalla Saleh, kwenda kusoma Isa Mtambo, 65.

Finsilber, Moshe (Misha), kumvuta Othman Shariff, 26, 27; 197; na Shebe, 216; Raha Leo, 221.

Forsyth­Thompson, Adrian, kuelekeya Cape Town na Seychelles, 6; ofisa wa usalama katika ofisi ya Sir George Mooring, mabadiliko katika vyombo vya usalama vya Zanzibar, 7; ripoti ya telegram kuhusu mapinduzi, 7; mpango wa kuipinduwa Serikali, 7–8; kushauri Zanzibar imezwe na Tanganyika, chuki dhidi ya Mfalme na Uarabu, 37.

Fortson, Benjamin W., asili ya neno “Afrika”, 360–361n.

FRELIMO, 101, 102, 103, kambi Bagamoyo, Kongwa, Mazimbo,105; habari za mapinduzi, 130; Djoudi, 190.

General Siad Barre, 194, 195. Ghana, Nyerere na Makao Makuu ya

Kamati ya Ukombozi, 8. Gharibu, Ahmed, 173, 174, 175; na uhusiano

na ukoo wa Kifalme, 378n.Ghassany, Mohammed, kuuilimisha

umma, 345, matokeo ya mapinduzi ya Wazanzibari, 408n.

Ghazzali, Imam Abu Hamid Muhammad, aina na daraja za hasad, 398n.

Glassman, Jonathon, vyumba vya kuhifadhia madawa chini ya jengo la hospitali ya mamishionari, 303, 400n.

Godfrey, Binaisa, 246; mkutano wa Nairobi, 267.

Goethe, Johann Wolfgang von, na Uislam, 344.

Gongoni, 160, 161, 162, 170; kuonana na

Saadalla na silaha, 186; 186, 290.Gordon Highlanders, 292. Guevara, Che, na Zanzibar, 188.Guiterrez, Gustavo, 447.Haile Sellasie, kuyagharimiya mapinduzi,

xxvi; kuyapongeza mapinduzi, 293; kuomba Mawaziri wa Zanzibar wapelekwe Addis Ababa, 355n.

Haji, Ramadhani, mahojiano ya Cuba, 25; siri ya Hanga, 133; mapigano ya Mtoni, 172.

Hamad, Seif Sharif, ahadi mbele ya ulimwengu, vii; Nyerere na mapinduzi, 21–22; kuuliwa kwa Karume, 28; Nyerere juu ya kuidai haki ya Zanzibar, 71; somo la historia Zanzibar, 249–250, 394n; alivokaa ndani ya mkakati wa Nyerere, 283.

Hamadi, Rashid, na Mohammed Omar Mkwawa, 57.

Hanga, Abdalla Kassim, upinzani dhidi ya Abeid Amani Karume, 28; maamuzi ya mapinduzi, 47; jemedari wa mapinduzi, 68; Mkello kuhusu Hanga, 73; mashirikiano na Victor Mkello, 79, 80; namna ya kuwapata Manamba, 97; mkutano Shauri Moyo, 98; na Manamba Kilombero, 125; na Twala, shina la mapinduzi, 142–143; kukutana na Kisasi, 162; salamu za mapinduzi kutoka kwa Kambona, 170; kuuliwa pamoja na Twala na Khamisi Beni, 176; kifo, 176–177; kufanywa Makamo wa Rais, 180; kifo, 182; ndani ya boti ya Misha, 210; kudharau nguvu za umma, 289; ripoti ya mkubwa wa Usalama, R. L. Speight, 391–392n.

Harrison, John, kutolewa kazini askari kutoka bara, 37.

Haruna na Abasi, mchango katika mapinduzi, 82, 83, 84.

Hawker, A. W., khiana dhidi ya Serikali na Mawaziri kinyume na maagizo ya Smithyman, 318; alivohamia Ofisi ya Rais, 376n.

Hemedi, Athmani, kutoka Zanzibar, 45.Hemedi, Khamisi, kutoka Zanzibar, 45;

kutoka Kivumbitini, Tanga, 66.Himaya ya Kenya, 2, Himidi, Yusuf, na Isa Kibwana, 45; na

Page 467: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 435

Tupendane, 51; siri ya Manamba, 91; kumuhifadhi Mmakonde, 94; ubebaji silaha, 95; kupelekwa Tabora, 138; kizazi cha Afrabia, 349.

Hizbu, maana ya jina, 18; kuwatenga wanyonge, 100; kuwafukuza wanachama wa ASP kutoka mashamba, 110.

H. M. S. Owen, 392–393n.Hoodhood, 384–387n.Human Rights Association Organisation,

204.Humudi, Mohammed Humud, na kifo cha

Karume, 114.Hunter, Helen­Louise, ripoti ya CIA juu

ya mapinduzi ya Zanzibar, 305; Hanga na kutohusika na mapinduzi ya tarehe 11–12 Januari 1964, 305; Nyerere na kuyaunga mkono mapinduzi ya Zanzibar, 305; Umma Party na kutofahamika mapinduzi ya Zanzibar, 305; Kamati ya Watu 14, 306; kitabu juu ya mapinduzi ya Zanzibar, 307.

Huseni (Fuko) na misafara ya mapinduzi, 187.

Husseni, Haji, 226.Ibn Batuta, historia ya Pwani ya Afrika

Mashariki, 13. Ibn Khaldun, na jina la Ifriqiya, 11. Ifriqiyah, jimbo la Afrika ya Kaskazini, 11. Ikulu, Tanga, mkutano wa Kambona,

Jumaanne Abdalla na Mohammed Omar Mkwawa, 70.

India, ideolojia ya uzalendo, xx.Inspekta Zonga, kiongozi wa jeshi la

polisi kutoka Tanganyika lilopelekwa Zanzibar, 170.

Ishmael na Ahab, kwenye Moby-Dick, 291.Ismail, Sajenti Simba, 161.Israel, 216, 218. Issa, Ali Sultan, kuutumilia mgongano wa

Zanzibar na nchi jirani, 39.Jacopetti, Gualtiero, mpiga filam na picha

wa Kitaliana, 405n.Jahadhmy, Ahmed Omar, na mwandishi wa

ramani wa Chuo Kikuu cha Waislam cha Afrika Mashariki na Kati kutoka Masri, 4.

Jamshid, Sultan, na Waingereza, 21; ende Somalia, 194; ziara ya Dubai, 203; kudai hajapinduliwa na Wazanzibari, 286;

alipokuwa Tanganyika, 390n; waliosafiri naye, 403n.

Jangukire, na Kambi ya Sakura, 62.Jangwa la Sahara, tawala kongwe za Kiislam,

chini ya, xix.Jaribu, Ali Khamis, 193.Jimbo la Kati, mchanganyiko wa watu wa

bara, 51, 89. Johnson, E. Harper, Oman na Wareno, 33;

343.Jumbe, Aboud, kutokujua kuhusu

mapinduzi, 23; kujiuzulu, 22; kuvutwa na Moshe Finsilber, 27; kutojuwa kuhusu mapinduzi, 179–180.

Jumbi, ngoma ya Kimakonde, 102.Juni, na Tupendane, 41; Karume, na

mapinduzi, 96; Kamati ya Uchunguzi, 294; ripoti ya CIA na makundi ya watu kupelekwa Zanzibar kushiriki katika ghasia, 364n.

Jussa, Ismail, 450.Kabaka, 246; baada ya kupinduliwa

Zanzibar, 69. Kakarange, 150. Kalaidos, Idris, kiongozi wa Eritrea, 196. Kali, George Jua, mwanafunzi wa Shimo la

Mungu, 104.Kamaliza, Michael, Raisi wa chama cha

wafanyakazi, 76. Kamati ya Ukombozi (OAU), wanachama

9, 8, 9, 379n; ndani ya TANU, 69; na Ben Bella, 188; Kambona na Katanga, 212; MOLINACO na Kambona, 266.

Kamati ya Watu 14, kabla ya mapinduzi, idadi halisi ya wanachama, 24; na mipango ya mapinduzi, 25–26, 26; na mapinduzi, 38; ndani ya ripoti ya CIA, 306; na Saadalla, 169, 316.

Kamati ya Watu 25, 133; kufa kwa Kamati, 138.

Kambi ya Jitegemee, 133.Kambona, Andrew, 336.Kambona, Oscar, uasi wa jeshi la Tanganyika,

kulibomowa Tawi la Usalama, 6; safari ya Algeria, 8; mizigo ya silaha, 9; na Mohamed Omar Mkwawa, 55; kumuokoa Nyerere, 65; na Kamati ya Ukombozi ya TANU, 69; kamchaguwa Mohammed Omar Mkwawa, 70; kuendewa Moshi na Mkello, 75;

Page 468: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi436

kuzichukuwa silaha kutoka MV Ibn Khaldun, 186; kuhusu Othman Shariff, Hanga, Twala, Saadalla, Mdungi Usi, Rais Ahmed Sekou Toure, 205; asili ya jina la Tanzania, 209–210; juu ya Ujamaa na Waislam, 213; kosa la Nyerere, 286; chifu kuzikwa na watumwa wake Tanganyika, 302; babu yake alikuwa na watumwa, 302; Zanzibar iendeshwe kama jimbo lolote la Tanganyika, 311; kuhusika na mapinduzi, 315; kutoyatarajia mapinduzi, 379n.

Kanga, Wamanyema na asili ya, 373n.Kangaani, na Mohammed Omar Mkwawa,

56.Kangagae, na Mohammed Omar Mkwawa,

56. Kangaroo, 92.Kanisa la Anglikan, limejengwa miaka 32

baada ya soko la utumwa kufungwa Zanzibar, 302.

Karen Camp, 166. Karume, Abeid Amani, Muungano, 22;

ushiriki katika mapinduzi, 23; njama za Moshe Finsilber, 26, 27; upinzani ndani ya ASP, 28; na Tupendane, 41; mwenyekiti wa Tupendane, 51; taarifa za kuuliwa kwake, 115; kutowaamini wasomi, 136; kukutana na Thomas Tete Kisima Majongoo, 137; ndani ya boti ya Misha, 219; kutokubali kuchukua amri kutoka Tanganyika, 313; nyumbani kwa Abbas Sykes siku ya mapinduzi, 316; kusafirishwa na Jimmy Ringo, 178; kufadhaishwa na mauwaji ya 1964, 306; wazee wa Kiarabu wa Mwera kumdhamini kazaliwa Zanzibar, 374n; hotuba ya kuukaribisha uhuru wa Zanzibar, 410.

Karume, Amani Abeid, kutoyarudisha yaliyopita, kupatanisha kambi zilizofarakana, ahadi mbele ya ulimwengu, vii; uetetezi wa Zanzibar, 22; kuwaunganisha Wazanzibari, 337.

Karume Yeka, 290.Katanga, 212.Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na

Zanzibar, 375n.Katiba ya Zanzibar, nguvu, 375n.

Kaujore, Mohamed, kiongozi wa Wayao Zanzibar, 95; mikutano Shauri Moyo, 96; siri ya mapinduzi, 128.

Kawajire, Joni, kiongozi wa Kimakonde katika mapinduzi, 150.

Kawawa, Rashidi, na Kambi ya Sakura, 61; Kamati ya Ukombozi ya TANU, 69; Raisi wa chama cha wafanyakazi, 76; hongera kwa kufaulu mapinduzi, 84.

Kayanga, Feruzi, mapinduzi na Pemba, 255.

Kenyatta, Jomo, makubaliano na Waziri Mkuu Mohammed Shamte, 2; kumkatalia Sultan Jamshid kushuka bandari ya Mombasa, 109.

Kepteni Baruti, kiongozi wa jeshi la polisi kutoka Tanganyika lilopelekwa Zanzibar, 170, 177.

Khaleej, (GCC), 247.Khamisi, Francis, 245.Kharusi, Ahmed Seif, 196. Kharusi, Humud Said, uhusiano na Bi

Kazija, 144. Khatibu, Mohamed, vita vya Malindi, 175. Kheri, Abdalla, kuwapeleka watu Zanzibar,

59; Sakura, 61; Bagamoyo, 61; kupeleka barua Zanzibar, 63; kupeleka watu Zanzibar, 69.

Kheri, Rajabu, 105.Kiapo cha nyungu, 71.Kiembesamaki, kundi la wazee kwa mujibu

wa Abdulrahman Babu, 367n.Kigomasha, jeshi la mapinduzi, 255.Kiinua Miguu, wakati wa mapinduzi, 82.Kijangwani, uchaguzi na mapinduzi, 55, 67,

71; silaha kutoka Ziwani, 171, 179; ofisi ya Afro­Shirazi, 250.

Kikwete, Jakaya Mrisho, alivyopaliliwa Zanzibar, vii; na Obama, vii­viii; amani na utulivu, 445; umoja na amani ya Wazanzibari, 446.

Kilombero, shamba la Afro­Shirazi, 251. Kilwa Chronicles, historia ya Afrika

Mashariki, 13.Kilwa Kivinje, kufungwa Victor Mkello,

77.Kinazini, Isa Kibwana wakati wa fujo za

Juni, 50; “Banda la Wanyamwezi”, 106. King Hussein, 191.

Page 469: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 437

Kingo, Mtoro Rehani, na Afrika Kwetu, 99; na Misha Finsilber, 218; kusikitika kwa kupigwa Ali Muhsin Raha Leo, 220.

Kinyasini, wanamapinduzi, 51.Koinange, Mbiu, 171.Kipumbwi, kupelekwa watu Unguja, 58; na

mapinduzi, 64, 67; kwenda Muwanda, 89; kutoroshwa Manamba kwenda Unguja, 98.

Kisasi, Edington, mwanachama wa kanisa, xxvi; na Tupendane, 51; 93; siri ya mapinduzi, 128; kuwaambia Waingereza kuhusu mapinduzi, 128; mawasiliano na Karume, 132; na Aboud Mmasai, 162.

Kisima Majongoo, mkutano, Tete na Karume, 137.

Kismayu, 194.Kiswahili, kuwafunza watu wenye kwenda

kupiga kura Zanzibar, 67.Kizimkazi, 219; boti ya Misha Finsilber na

wanamapinduzi, 220.Kizota, fujo za Juni, 47.Koloni la Kenya, 2. Komanda Muwasi, 276.Kombo, Thabit, ushiriki katika mapinduzi,

uwongo wa washiriki, 23; kukerwa Okello kwa kuwasaidia “Wamanga”, 147; na Misha Finsilber, 218.

Komoro, baada ya kupinduliwa Zanzibar na Uganda, 69.

Kondo, K., safari ya Algeria, 8; kusaidia kupakia silaha Msasani, 163; mlinzi wa Oscar Kambona, kushukia kwa Saleh Saadalla, 170; 280.

Kunduchi, 219; harakati kubwa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar, 223.

Kundya, Rajabu, Mkuu wa Wilaya, Tanga, 78.

Kush, katika Bibilia, 14.Kututu, Abdalla, mkubwa wa “Banda la

Wanyamwezi” la Kinazini, 106. Kwa Hani, waliongia Ziwani, 168;

kuteremsha silaha, 186.Lamarque, W. G., Kambona na uasi wa

kijeshi, 6.Lancaster House, mkutano wa Mwambano,

2. Las Casas, Bartolome de, 447.Lebulu, Josephat, Baraza la Maaskofu

Kataloki, 299.Lemky, Ahmed, 195, 196; Al Hakiika Al

Zinjibar, 197; na nafasi za masomo, 203; 382n.

Liberation theology (theologia ya ukombozi), xvi; 447.

Likolo, Mtalama, kiongozi wa kwanza wa MANU, 103.

Lima, Tirace, taarifa za kifo cha Othman Shariff, 182.

Livingston, David, upeo wa kipropaganda, xix.

Lofchie, Michael, takwimu za kijamii za Zanzibar, 29.

Loliondo, 300, 301. Lowassa, Edward Ngoyai, 299. Ludwig, Frieder, mapinduzi na Wakristo

wa Zanzibar, xxvi; 298.Lumumba, Ali Omar, mahojiyano, xxiv;

kutoyafahamu mapinduzi, 139.Lumumba, Patrice, 214.Lusinde, Job, kulibomowa Tawi la Usalama,

6; kuhusika na mapinduzi, 315.Luttwak, Edawrk, “Power Play” na

kuchomoza kwa John Okello, 376n.Machano na Makame, kushirikishwa

kwenye mapinduzi, 75; 140.Machel, Samora Moses, kwenda kusoma

Shimo la Mungu, 104; na Ali Mahfudh, 114; ukombozi wa kifikra bado Zanzibar, 264.

Macho Mane, na Mohammed Omar Mkwawa, 57.

Mafeje, Archie, 447.Mahakama ya Jinai ya Kimataifa,

International Criminal Court (ICC), xvii.

Mahakama ya Katiba, 328.Mahalu, C. R. na uandalizi wa Mkataba wa

Maridhiano, 299.Mahbubani, Kishore, 338, 343, 383n.Mahfudh, Ali, mikakati ya kupindua, 71;

na Albarto Sipande na Raymundu Pasinuwapa, 113; kukamatwa baada ya kifo cha Karume, 118; mshauri wa Samora Machel, 119; ndani ya boti ya Misha, 219; 296.

Mahmud, Daud, makafara ya mapinduzi, 60.

Page 470: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi438

Mahonda, na Saidi Omari Saidi, 44.Maisara, Musa,15; na Tupendane, 49, 51;

siri ya Manamba, 91; mkutano Shauri Moyo, 98; kituo cha Dunga, 103.

Majengo Destitute Camp, 369n.Major Idi, Komoro, 274, 275, 276. Makomred, na mapinduzi, 38; na Youth

League, 60; walijua baadae siku ya mapinduzi, 83; kwa nini Wazungu waliwachilia maingiliano na ASP, 309; kutumiliwa, 310.

Makungu, Ibrahim, na Tupendane, 48, 51. Malambeka, Jacob, 166.Mamboya, Ubwa, 15. Manamba, 64, Mkello juu ya Manamba,

74; miaka miwili baina ya kufikiwa Manamba na mapinduzi, 90; Hanga, Juma Maneno, Jimmy Ringo, Musa Maisara, Natepe, Sefu Bakari, 94–95; kutoroka mashamba ya mkonge, 98; utata wa suala la Manamba, 107; na kuchukuliwa Manamba, 123; kuwalipa Manamba, 124; na Mmasai Tanga, 164; sababu ya kuitwa “Manamba”, 366n.

Mandera, Hassan, na Tupendane, 48; “Ba Mkwe”, 136.

Maneno, Juma, mkutano Shauri Moyo, 98; polisi na kushiriki kuipinduwa Zanzibar, 128; mawasiliano na Karume, 133; alivogeuka, 177.

Mangapwani, njia ya magendo, 105. Mango, John, mwanfunzi wa Shimo la

Mungu, 104.Mapinduzi 7–8, ya maridhiano, 406n.Mapolo, 175.Marhubi, Amour Ali, 227–228.Masharubu, Mohamed Omar, 161; kuonana

na Sajent Ngusa Ziwani, 166; kusafiri na Hanga na Saadalla, 167; silaha kuteremshwa, 186.

Masingini, mikutano ya mapinduzi, 96.Maskati, 94.Matemo, uhusiano na Matemwe ya Unguja,

112. Matias, Amboni, kuandikisha Manamba,

88, 125. Matokke, W.T.13.Mau Mau, dawa za kienyeji, 50.Mawile, Chefu, kiongozi wa Kimakonde

katika mapinduzi, 150.

Mazrui, Ahmed Nassor, na Mohammed Omar Mkwawa, 57.

Mazrui, Ali A., mbunifu wa jina la Afrabia, xviii; maana ya uzalendo wa Kiafrika xxi; mapatano baina ya Waafrika na Waarabu, 323; baba wa Afrabia, 434.

Mboya, Tom, na Abdillahi Nasser, xxii; kuanzishwa kwa vyama vya wafanyakazi Tanzania, 76; na Ali Muhsin, 207; mkutano wa Nairobi, 267.

Mdundo, Minael­Hosanna O., 23.Meja Bott, 168. Mengi, Reginald, utekelezaji wa msafara

wa wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Shalom, Zanzibar, 400n.

Mfaranyaki, Mohamed, kusafirishwa, 44; Tupendane, 51; siri ya Manamba, 91; kiongozi wa Wangoni Zanzibar, 95; mikutano Shauri Moyo, 96, 98.

Mfaume, Mueba, kiongozi wa FRELIMO Zanzibar, 103.

Mgao Mwanya, Lindi, 350.Mikidadi, mwanamapinduzi kutoka Tanga,

45, 51. Mikindani, 87.Miles, Balozi Stephen, mapinduzi ya

Zanzibar yamepangwa Tanganyika, 310.

Misra, R. M., mshahara, 294. Miti Ulaya, mkutano kuwapoza

Wamakonde, 90; wanafunzi wa Shimo la Mungu, 105; Okello na kutaka kumuua Thabit Kombo, 147.

Mkandaa, Muhammed Abudu, 225.Mkapa, Benjamin, na Nyerere, 65; na

usuluhishaji baina ya Wahutu na Watutsi, 214; na Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro, 300.

Mkataba wa Maridhiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 299; Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, 299; Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 299.

Mkello, Victor, kuwakusanya wafanyakazi wa mashamba ya mkonge, 57; na Kambi ya Sakura, 61; mkubwa wa chama cha wafanyakazi, 63; akijulikana atapata sifa, 74; kumfuata Kambona Moshi, kuonana na Kawawa Morogoro, Manamba kwenda Zanzibar, 75; kusoma Kiwanda

Page 471: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 439

na Minaki, 76; na Adam Mwakanjuki, 77; utafiti kuhusu Manamba, 78; na Hanga, Hassan Nassor Moyo, Mustafa Songambele, 79; na Mwakanjuki na Moyo, 80; na Kawawa, Morogoro, 80; kikao na Nyerere, 80; na Kawawa, 80; urafiki na Mwakanjuki, 81; kukutana na Mkello shamba la mkonge la Mbezi, na Hanga, Musa Maisara, 88; kuwatilia tiki wafanyakazi wa mkonge, 89; kwenda Zanzibar, 90; kazi ya kukusanya watu alipewa na Hanga na Kambona, 91; kufika Zanzibar, Hasnu Makame na Mkello, 96; hotuba Shauri Moyo, 98; Ikulu na Hanga na Karume, 98.

Mkoa wa Pwani, mchango kwenye chaguzi na mapinduzi Zanzibar, 56.

Mkokotoni, na Tupendane, 50; watu kutoka Kipumbwi, 83.

Mkonge, mashamba ya Tanga, 368n.Mkunjeke, Mohamed, kiongozi wa

Tupendane, 51; 270–272.Mkwaja, mawasiliano kutoka Dar es Salaam

kwenda Muwanda, 82. Mkwajuni, wanamapinduzi, 51. Mkwawa, Mohamed Omar, mawasiliano na

Kijangwani, 55; na Oscar Kambona, 55. Mlenge, Haji, dereva wa Hanga, 169.Mlingotini, 186.Mloo, Shaaban, na Mohammed Omar

Mkwawa, 64; kujuwa kuhusu mapinduzi, 66.

Mmasai, Aboud, mkutano na Saadalla, Hanga na Twala, 160; na Saadalla Dar es Salaam, 163; kumuona Kambona, 163; na silaha pamoja na Twala, 164; kwenda Algeria, 184; na Bhoke Munanka, 260.

Mogadishu, 195.Moi, Daniel Arap Moi, Kanali Udongo na

mapinduzi ya Zanzibar, 199, 200.MOLINACO, 265. Mombasa Institute of Muslim Education

(MIOME), 3. Mondlane, Dr. Eduardo Chiwambo, 102;

Kambona juu ya kifo cha Mondlane, 212; na Karume Zanzibar, 213.

Mooring, Sir George, juu ya Moshe Finsilber, 26; na Umma Party, 34; utabiri wa mwisho wa Ufalme Zanzibar, 357n.

Moyo, Hassan Nassor, na Victor Mkello,

79, 80; Rais wa kwanza wa Afro­Shirazi Youth League, 377n.

Mozambique, na Musa bin Bek, 409n.Mozambique African National Union

(MANU), 102.Mpinyeke, Jabir, kiongozi wa pili wa

MANU, 103.Mrundi, Mohamed, 144. Mshangama, Maulidi, 292.Mshongwe, kupelekwa watu na chama cha

wafanyakazi, 82.Msikiti na Kanisa, 352.Msumbiji 9, 99. Mtambo, Issa, na Mohammed Omar

Mkwawa kwenye usalama, 55; na Kambona, 62; usalama, 64; kusoma kwa Sheikh Abdalla Saleh Farsy, 65, 69, 182.

Mtemvu, Zuberi, na ZNP, 54.Mtoni, njia ya magendo, 105. Mugheiry, Muhammad Ahmed Sultan

(Eddy Riamy), 451.Muingereza aiwachie Zanzibar, 101.Munanka, I. M. Bhoke, safari ya Algeria, 8;

na Aboud Mmasai, 260.Munkar wa Nakiri, 169. Murumbi, Joseph, 228; mkutano wa

Nairobi, 267. Musa, Ali Khamis (Baucha), 387–390n.Musa, Anthony, kushiriki katika kuipinduwa

Zanzibar, 92, 128; wa kuwaambia Waingereza kuhusu mapinduzi, 128; mawasiliano na Karume, 133; mapinduzi na Pemba, 255.

Museveni, Rais Yoweri, na Wafalme wa Uganda, 248.

Muslim Teachers’ Training College, 3.Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, sababu za kufanyika, 402n.

Muwanda, kuingiliya Unguja kutoka Kipumbwi, 67; kuingizwa watu kutoka bara, 69; asili na maana ya jina, 112.

MV Ibn Khaldun, kuwasili Dar es Salaam, upakuwaji wa mizigo, 9; na Ben Bella, 188; Djoudi, 190; 197.

Mwakanjuki, Adam, na Victor Mkello, 77, 79.

Mwakikagile, Godfrey, kuyagharimiya mapinduzi, xxvi.

Mwambao, 2.

Page 472: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi440

Mwananchi Ocean Products, 223.Mwananchi Trading TANU, 219. Mwanjisi, R. K., siri ya mapinduzi, Nyerere

na Kambona kujuwa kuhusu mapinduzi, xxvii; hadithi za utumwa; 14–15.

Mwembe Matarumbeta, 166.Mwembe Rikunda, msikiti wakati wa fujo

za Juni, 46.Mwera, Tanga, na wapinduzi, 64. Mwinbo, P., safari ya Algeria, 8.Mwinchum, Mzee, kuzipokea silaha

Bweleo, 163; 164. Mwinyi, Abdalla, kiungo baina ya TANU

na ASP, 82.Mwinyi, Ali Hassan, majengo yaliopo

kwenye kaburi la halaiki, 104; na wanamapinduzi, 152; kupelekwa Ubalozi wa Zanzibar, Jakarta, 203.

Mzee, Ali Mohamed, mwanafunzi wa Shimo la Mungu, 104.

Mzena, Emile, Mkurugenzi wa Usalama wa Tanganyika kuwapo Zanzibar siku ya mapinduzi, 316.

Namina, Mzee, 102. Nangade, kambi ya Wareno, 113.Naruka, kiongozi wa Wamakonde, 124. Nasser, Gamal Abdel, kuubwaga uhuru wa

Zanzibar, 4; kufanikisha mapinduzi, 29; uzembe ulioikoroga Mashariki ya Kati, 383n.

Nassir, Abdillahi, na Tom Mboya, kiongozi wa Mwambao 2, 3, 4.

Nassor, Nassor Abdalla (Mlawwaz), kumhoji Twala, 165; 295; taarifa juu ya Edington Kisasi, 315.

Natepe, Abdalla Saidi, kitabu kuhusu mapinduzi, 25; na habari za Tupendane, 49; kwenda Tanga, 83; siri ya mapinduzi, 128; 169.

Nchelenga, Joseph, kiongozi wa Kimakonde katika mapinduzi, 150.

Ndagaa, na Tupendane, 50.Ndala Ndala, 40.Ngamia, Mzee, 102. Ngazi Mia, na Tupendane, 49; 404–405n.Ngusa, Sajenti, 161, 179. Ngwali, Juma, kujuwa kuhusu mapinduzi,

66.Njonjo, Charles, 246. Njozi, Hamza, 298.

Nkomo, Joshua, 211.Nkrumah, Kwame, na mapinduzi ya

Zanzibar, xxvi.Ntanga, Yohana (Sadiki), 351.Nuremberg, mashtaka ya viongozi wa

serikali ya Kinazi ya Adolf Hitler, 369–370n.

Nyau, Ali, Komredi, 71; ndani ya boti ya Misha, 220.

Nyerenda, (Kepten), upakuwaji wa MV Ibn Khaldun, 9.

Nyerere, Andrew, Haile Selassie na Kwame Nkrumah kuyagharimiya mapinduzi, xxvi.

Nyerere, Julius Kambarage, uhuru wa Tanganyika 1; Pan­Africanism, 11; mtikisiko wa Tanzania, 22; Nyerere na ukorofi wa Wazanzibari, 20–21; Zanzibar kituo cha ubeberu, 32; na Kambi ya Sakura, 61; na Seif Sharif Hamad kudai haki ya Zanzibar, 71; na mchango katika mapinduzi, 75; na Eduardo Chiwambo Mondlane, 102; Jeddah, Saudi Arabia, 280; kuitambua Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, 310; ripoti ya CIA na ubeberu juu ya Zanzibar, 312; kutolewa wasiwasi na Waingereza kuhusu Sultan Jamshid bin Abdulla, 319–320; nchi za Magharibi kusema kuwa Ukoministi ndio uliopindua Zanzibar, 379n; tathmini ya CIA, 381n; kutosikilizana na Kwame Nkrumah, 392n.

Nyondo, U., safari ya Algeria, 8.Obama, Rais Barrack, na Rais Jakaya

Mrisho Kikwete, vii­viii; 304.Obote, Milton, na Nyerere, 65, 246.ODENAMO,102.Odinga, Oginga, na mapinduzi ya

Zanzibar, 308, 309: juu ya Babu, 309; athari ya mapinduzi ya Zanzibar juu ya Tanganyika na Kenya, 309; TANU na kuundwa kwa ASP, 313.

Okello, John, kufananishwa na Nabii Musa, xxvi; jemedari wa mapinduzi, 23; na “Mungu wa Waafrika”, 29, 38; kuchomozwa, 63; kufunikwa blangeti, 94; kuwa ni Mau Mau, 106; kufuatiwa Pemba, 120; kuuliwa Busia, Mbale, Uganda, 127; kuchomoza, 289, 290; lugha ya maamrisho ya Ukristo, 301;

Page 473: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 441

askari kutoka nje ya Zanzibar, 301; utumwa, 302; kutowaamini Wazanzibari, 302; bahati nasibu ya historia, 308.

Ole, na Mohammed Omar Mkwawa, 56.Oman, na ukombozi wa Afrika Mashariki,

295; bandari, 346.PAFMECA, 244.Palestine, R. H. V. Biles, 294, Sir George

Mooring, Zanzibar na Palestine, 294.Pan­Africanism, na nani Muafrika, 11; na

Zanzibar, 18; kusumbuliwa kwa Odinga, Kambona na Nyerere, 309, 345.

Pan­Arabism, mrengo wa Gamal Abdel Nasser na wa chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP), xx; na ZNP, 4; na Zanzibar, 18.

Pandu, Ali Haji, kujua kuhusu mapinduzi, 66; 369n.

Pangani, watu kupelekwa Unguja, 58.Pasinuwapa, Raymundu, jemedari wa

ukombozi wa Msumbiji, 113, 296.Pemba, kudhibitiwa Wete, Chake Chake na

Mkoani, na Isa Kibwana Sanze, Anthony Musa, Feruzi Kayanga, Kombo Juma Kombo, Gora Kombo, 255–256.

Pemba Bay, 112.Persia, wakimbizi wa kidini na wa kisiasa

kutoka, xix.Pili, Mosi Jecha, na Mohammed Omar

Mkwawa, 67.Planck, Max, 341.Public Officers Agreement (POA), 293,

294. Pundugu, Samuel, Regional Police

Commander, 170; kuwapo Zanzibar wakati wa mapinduzi, 316.

Punt, 295.Pushkin, Alexander, 344.Qaboos, Sultan, kiungo cha mapatano

duniani, viii; kadhiya ya Zanzibar, 207.Qatar, 300.Qullatein, Ahmed Badawi, Usoshalisti,

317.Raha Leo, Karume na anayekamatwa

apelekwe Raha Leo, 90; 93; na Kituo cha Polisi cha Malindi, 173; Ali Mushin, 173; kupigwa Ali Muhsin, 220; wafundishaji bunduki, 255.

Rajab, Ahmed, na Hanga, London, 268–269.

RENAMO, 102.Rimmer, Joseph, juu ya mapinduzi, 373n.Ringo, Jimmy ( Juma Maulidi Juma), kambi

ya Sakura, 60, 61; katili, 66; kwenda Tanga. 83; siri ya Manamba, 91; 107; na Manamba, 125; ndani ya boti ya Misha, 220.

Rizeiki, Seif, 195. Robert, Shaaban, Mswahili na biashara ya

utumwa, 381n.Rockey, G., safari ya Algeria, 8.Rufiji Basin Development, 347.Rumi, Jalaluddin, 320.Rupia, John, na Nyerere Dar es Salaam, 1;

na Kambi ya Sakura, 62; kutaifishwa na kurudishiwa mali, 213; na Nyerere, Wakristo peke yao na wazee wa Kiislam Dar es Salaam, 356n,.

Ruwazi, shamba la mkonge, 59. Saadalla, Saleh, kuvutwa Moshe Finsilber,

27; upinzani ndani ya ASP, 28; kujuwa kuhusu mapinduzi, 36; mkutano na Aboud Mmasai, Hanga na Twala, 160; makao makuu ya mapinduzi, 175; Burma, 181; kwenda Algeria, 185; silaha kuteremshwa Forodha Mchanga, 186; kuwa karibu na Misha Finsilber, 223.

Sabea, Hanan Hosni, 366n, 368n, 371n.Said, Mohamed, mchango wa Waislam

katika kuupigania uhuru wa Tanganyika, 1–2; TANU Bantu, 12; 298; kuokolewa na kujificha Nyerere wakati wa uasi wa jeshi la Tanganyika, 369n; ujumbe wa EAMWS nchi za Kiarabu/Kiislam, 394n; Abdalla Kassim Hanga kuadhiriwa na Nyerere, 396–398n.

Saidi, Omari Saidi, muasis wa Tupendane, 44.

Sajent Feruzi, 168. Sajent Juma, wimbo wa taifa wa Zanzibar,

176. Sajent Waziri, 166, 168. Sakura, kambi ya shamba la mkonge, 59;

mazowezi ya silaha, Jimmy Ringo, Khamisi Hemedi, Musa Maisara, 60, 61; kiapo cha nyungu, 71.

Saleh, Ibuni, Tanganyika kuivamia Zanzibar, 297.

Saleh, Rais Ali, 275.Sangu, F., safari ya Algeria, 8.

Page 474: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi442

Sayyid Khalifa bin Harib, Sultan, umoja wa Afrika Mashariki, 207.

Sayyid Seif bin Hamoud bin Feisal, 319.Sayyid Soud, bin Ali bin Humud, na

Wamakonde, 94. Sembe, Abdalla Rashid, na Mzee Mkwawa,

55.Seminari za Kikristo, 300. Sendoro, Elinaza, Baraza la Kikristo

Tanzania, 299; na OIC, 299.Serguera, Balozi Jorge, na Fidel Castro

kuhusu mapinduzi, 38.Seychelles, 7; baada ya kupinduliwa

Zanzibar na Uganda, 69.Shahidi, Ilangwa, na Katiba ya CCM, 22.Shaishai, kambi ya Wareno, 113.Shamte, Mohammed, makubaliyano na

Jomo Kenyatta, 2; 7, Shariff, Ibrahim Noor, Mwarabu na

Mwafrika, 12. Shariff, Othman, na Moshe Finsilber, 26,

27; na Uwaziri Mkuu, 27; habari za kifo kwa Ali Sharifu, 182.

Sheni, Maulidi, na Kambi ya Sakura, 61; katibu wa Victor Mkello, 62; gurupu la Mohammed Omar Mkwawa, 69; na Moyo, Mwakanjuki, Khamisi Masoud, Ahmed Diria, Shaabani Mloo, Twala, Jimmy Ringo, 82; Kiinua Miguu wakati wa mapinduzi, 82; Nyerere kumwambia Karume asikubali Hanga kuwa Waziri Mkuu, 82; Mkello na Shehe Amiri, 82; Mkwawa na Haruna, Haruna na Abasi, kupeleka watu Mshongwe, 82; kupeleka watu ishirini na tano na mapanga mia mbili Unguja kupitia Bumbwini, 83; watu wa bara waliopo Dar es Salaam hawajui kuhusu mapinduzi, 83; kukaa na Victor Mkello, Jumaane Abdalla baada ya mapinduzi, 84; na Hassan Mandera, 85–86.

Shimo la Mungu, 100, wanafunzi 58 walipelekwa kusoma, 103.

Shindano, kiongozi wa Wamakonde, 125.Shirikisho la Afrika Mashariki, Ali Muhsin,

242, 248.Shirikisho la Afrika Mashariki na Kati,

325.Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanganyika

(Tanganyika Federation of Labour),

na uasi wa jeshi la Tanganyika, 5–6; uongozi wa mapinduzi, 63.

Shivji, Issa G., Abeid Karume na Muungano, xxvii, 325; Aboud Jumbe na kifo cha Abeid Amani Karume, 28; takwimu za kijamii za Zanzibar, 29; Abeid Karume na Muungano, 325.

Simba, J. M., safari ya Algeria, 8.Sindano, Saidi, na kifo cha Karume, 115.Sindimba, 151.Sipande, Albarto, jemedari wa ukombozi

wa Msumbiji, 113, 296.Sisal Labor Bureau (SILABU), 366n.Sivalon, John C., 298.Sketty, Mohamed Salim, alivouliwa na

vijana wa kwa Ali Msha, 84, 226.Slave Trade Project, na UNESCO, 17.Smith, William Edgett, Maisraili, 27;

Nyerere na kuiburuta Zanzibar, 31–32.Smithyman, Mervyn Vice, Forsyth­

Thompson na vyombo vya usalama vya Zanzibar, 7; onyo kuhusu mapinduzi, 36; mkataba wa kijeshi, 291–292; makosa ya polisi, 296; wageni kutoka bara na fujo za Juni, 296; kumuagiziya A. W. Hawker achukue nafasi yake ikiwa hatoweza kufika kwenye meli ya “Salama”, 318; Waafrika wa mashamba na utiifu kwa Sultani, 365n; ulinzi wa Zanzibar, 391n.

Songambele, Mustafa, na Kambi ya Sakura, 62; na Victor Mkelllo, 79.

Songorokirangwe, na mapinduzi, 51.Strategic denial, 30; 304.Suleman, Hafidh, mizizi ya karibu, 51;

“Sancho”, 134.Sullivan, J.M., na kutolewa askari kutoka

bara, 37; ZNP­ZPPP na siasa ya kutokufungamana na upande wowote, 291; mshahara, 294; na silaha za Algeria Ziwani, 314.

Sultan, Sayyid Said bin, 9.Sultana, kuwasili New York, 9, 343. Sumbawanga, kufungwa Mkello na Shehe

Amiri, 77. SUPKEM Kenya, baada ya kuvunjwa East

African Muslim Welfare Society, 4.Suwedi, Ahmed Khalifa, Zanzibar na

Gamal Abdel Nasser, 198.Suwedi, Rajabu, 316.

Page 475: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi 443

Sykes, Abbas, na Abeid Amani Karume, 316.

Sykes, Abdulwahid, jina la TANU, 1, 356n; 316; na mapinduzi ya Zanzibar, 316.

Sykes, Ally, TANU hawakutaka kujulikana, Nyerere asingeliweza kufanya kitu Zanzibar bila ya wao, 316; 356n.

Tagore, Rabindranath, India na kujiepusha na kutengana, xx.

Tajiri, Fundi, na vikao vya Wamakonde, 90; mkubwa wa Wamakonde machale, mikutano Mfenesini, 96; 102, 124, 150.

Tajo, Shehe Ameir, barua ya African Association kupinga uteuzi wake kwa sababu anatoka bara la Asia na kwa hio si Muafrika, 366n.

Tambwe, Ali Mwinyi, Mkuu wa Wilaya, Tanga, 84; 164.

Tanganyika African Association (TAA), na Nyerere, 19.

Tanganyika African National Union (TANU), asili ya jina 1; na Nyerere, 19.

Tanganyika Federation of Labour (TFL), vyama vya wafanyakazi na uasi wa jeshi la Tanganyika, 6, na mapinduzi, 18.

Tanganyika Rifles, silaha kutoka Algeria, 9–10; kupelekwa Zanzibar kwenye mapinduzi, 315.

TANU Bantu, 12.Tanzania, maana na asili ya jina, 209–210;

mashindano ya kuchagua jina, 382n.Tanzania Association, 207.Tanzania­Mozambique Friendship Asso­

cia tion (TAMOFA), 105. Tarazo, Abdi, mpinduzi kutoka Morogoro,

alikuwapo Sakura, 66. Tete, Thomas, kushiriki katika kuipinduwa

Zanzibar, 128; wa kuwaambia Waingereza kuhusu mapinduzi, 128; na Lazaro, 137; kukutana na Karume Kisima Majongoo, 137; na Superintendent Derham usiku wa mapinduzi, 377n.

Thani, Ali Masoud, 203. Thani, Amani, 198.The Economist, Nyerere na chatu, 20. The Periplus of the Erythrean Sea, tawala

za Kiarabu Afrika Mashariki, 14. Thomas, 92.Tomeo, Mzee, 102. Tupendane, 40; tawi la Mkwajuni, 42;

Potowa, 43; Tunguu; Kisakasaka, 43.Twala, Abdulaziz, upinzani ndani ya ASP,

28; na Manamba Kilombero, 125. U.A.R., Nyerere na Makao Makuu ya

Kamati ya Ukombozi, 8. Uasi wa Jeshi la Tanganyika 5, 358n.U­CUF na U­CCM, 88.Ufalme, khatima kwa mujibu wa

wanamapinduzi, 176. Uganda, baada ya kupinduliwa Zanzibar,

69. Uislam, tafsiri ya upole na hikma na yenye

msimamo mkali, 384n.Umma Party, mikakati ya kupindua, 71;

kwa nini walihitajika, 309.Umoja wa Mataifa, Nyerere kuiogopa, 65;

C. A. Stavropoulos, 331, 332, 334; Jose Rolz­Bennett, 331, 334; barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Tanganyika, 332; ujumbe wa Tanzania Umoja wa Mataifa, 333; Andrei Kolomoets na usajili wa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, 334; nyaraka, 406–407n; kiti cha Zanzibar baada ya mapinduzi, 407n.

UMSC, Uganda, baada ya kuvunjwa East African Muslim Welfare Society, 4.

UNESCO, Ethics Education Programme, 408n.

United Arab Emirates (UAE), Zanzibar na Tanganyika, 346.

United Nations Commission for Refugees (UNHCR), 204.

Usi, Mdungi, na Mohammed Omar Mkwawa, 67.

U Thant, 8, 331.Utumwa, Angola, Brazil, 190. Utumwa, Bahari ya Hindi, Waarabu/

Waislam, xii; hadithi 14–15, 16; Shaaban Robert, 381n.

van Bergen, Jan P., kuingiya Ukristo Tanzania, xix.

Van Riebeeck, 321.Wabantu, 12.Wagiriama, 12.Wamanga, na Tupendane, 43.Waring, Thomas, kuvamiwa Zanzibar

kutoka Tanganyika, 297.

Page 476: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Faharisi444

Waunguja, mchango katika mapinduzi wa waliokuwa wakiishi na kufanya kazi pwani na bandarini bara, 83.

Wickens, Joan, African Socialism, Ujamaa, 210–211; Nyerere Foundation, The South Foundation, 383n; Ronald Brown juu ya, 383n.

Willis, J. J., Usalama wa Ujumbe wa Kanisa, 301.

World Heritage Site, Mji Mkongwe, 30.Yangeyange, 150. Yusuf, Mzee Ali, juu ya mapinduzi, 370n.Zahran, Omar, na Babu, 266.Zama za Giza (Dark Ages), hakuna

kuingiya Ukristo sehemu za kusini za Afrika, xix.

Zanzibar and Pemba Federation of Labour (ZPFL),18.

Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP), uchaguzi wa Julai 1963, 21.

Zanzibar Association, kuundwa, 202–203, 204, 205.

Zanzibar Independence Conference, 291.Zanzibar Nationalist Party (ZNP), propa­

ganda chafu dhidi xiii; uhusiyano na Ufalme, 4; uhusiyano na Waingereza, 21; kutambua watu wa bara wanaiunga mkono ASP, 100.

Zanzibar, na Shirikisho la Afrika Mashariki, 248; mikataba ya kijeshi na Misri, Tunisia, au Algeria, 291; kuvamiwa na Tanganyika, 297; P. A. Carter na ushauri ifanywe Mkoa wa Tanganyika, 311; Balozi kushushwa hadhi na kufanywa Consulates, 311; kujiendesha kama nchi huru, 312; kuvamiwa na Tanganyika, 314; wapinduzi kutoka bara kwenda kushiriki mapinduzi, 314; meli kuwarudisha wapinduzi, 314; Tanganyika Rifles kushiriki katika kuipindua, 315; kutoweza kusimama juu ya miguu yake, 398n.

Ziwani, kuingia Aboud Mmasai, 165. ZNP­ZPPP, kutupwa mkono na Gamal

Abdel Nasser, 4; kutaradadi juu ya msaada wa kijeshi, 43.

ZPPP, kujifanya “Washirazi”, 56.

Page 477: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani

Kwanza kabisa kuliko yote au yoyote, sina budi kumsujudiya na kumshukuru Mwenye Enzi Mungu kwa Rehma zake na kwa kunionyesha njia ndani ya midani ya utafiti ambayo haikuwa na alama rahisi za kupitwa na iliyokuwa imewekewa ngazi yenye kuelekeya kunako mlango wa jiwe uliyofungwa.

Baada ya Mwenye Enzi Mungu sina budi kuwashukuru kwa dhati kabisa wazee wote wa simulizi za Mapinduzi ya Zanzibar waliyomo ndani ya kitabu hichi. Bila ya Mungu kuwawezesha sio tu kitabu hichi kisingelikuwepo, bali mtazamo mpya wa wananchi wengi wa kawaida, wanasiasa, wasomi na watafiti wa pande zote mbili za Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na hata waliyoko nje, ungelikosekana.

Kama Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yalikuwa ni Mapinduzi ya mfarakano wa kijamii, basi nawashukuru wazee kwa kuuweka msingi wa mapinduzi ya mfungamano utakayoipa Zanzibar na Tanganyika mabega makubwa ya kusimamiya pamoja na kutambulikana na kuungwa mkono na madola yenye kupenda demokrasia na amani duniani.

Simulizi za wazee wa Mapinduzi ni mchango na changamoto muhimu sana kwa wasomi waliyobobeya wa nchi mbili za Muungano ambao wana jukumu la kuwafikishiya Wazanzibari na Watanganyika ujumbe utakaohifadhi utulivu wa kijamii na wa kisiasa ndani ya nchi mbili zilizoungana—Zanzibar na Tanganyika. Moja wapo wa ujumbe huo ni kuutambuwa na kuuhifadhi uhuru wa Zanzibar ulioupata tarehe 10 Disemba, 1963 na ndiwo uliyoipa Zanzibar nafasi ya kukubaliwa kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UNO). Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, yasingeliweza kuja bila ya Uhuru wa tarehe 10 Disemba, 1963. Kwa hilo natowa shukurani zisizokuwa na mwisho kwa wazee wa simulizi za Mapinduzi.

Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete umeweza kujenga utamaduni wa amani na utulivu kwa kutowa mvuto kwa kizazi kipya cha uongozi wa Tanzania. Ndani ya kipindi chake cha

Page 478: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani446

uongozi wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Zanzibar imekuwa shwari kwa sababu yuko upande wa umoja na amani ya Wazanzibari.

Zanzibar piya imebahatika kuwapata viongozi wawili majasiri, Mheshimiwa Rais Amani Abeid Karume na Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad ambao wameamuwa kwa pamoja kutorudi nyuma katika kazi ya kujenga mazingira ya kuizaa Zanzibar Mpya. Yote hayo yanafaa kushukuriwa na ndiyo msingi utakaokuja kuujenga Muungano imara, ilimu bora na uchumi endelevu kwa tabaka kubwa la wananchi walio wengi.

Napenda kuwashukuru kwa dhati yangu marehemu wazazi wangu wawili ambao wamenileya na kunipa furaha ya utotoni ambayo ndiyo yenye kunipa utulivu na furaha ya moyo popote pale nilipo. Nilipokuwa bado niko Cairo masomoni, marehemu mama yangu, Bibi Asya Abdalla Jahadhmy, aliniandikiya barua na kunielezeya ndoto aliyoiyota na iliyoifananisha Zanzibar na mtu aliyekuwa ndani ya pango lenye giza totoro na nje limezungukwa na mwangaza mkubwa. Mapenzi yangu ya utotoni juu ya Zanzibar na Tanga pamoja na ndoto ya marehemu mama yangu ni moja kati ya motisha kubwa kwangu katika kuufanya na kuufanikisha utafiti huu.

Marehemu baba yangu, Bwana Mohamed Abdalla Ghassany, maarufu “Bingwa” wa kilimo na ufugaji, alikuwa na mapenzi makubwa juu ya Zanzibar na aliwahishimu sana watu wake. Baina ya ndoto ya marehemu mama yangu na mapenzi ya marehemu baba yangu juu ya Zanzibar, na sababu nyenginezo, ndipo nilipoingiwa na shauku ya kuutafuta ukweli wa Mapinduzi. Kabla ya hapo nilikuwa ni mmoja wa majeruhi ya upotoshaji wa historia na niliyaamini mengi ambaye leo najuwa kuwa hayakuwa na ukweli wowote.

Sina budi kuishukuru Dola ya Zanzibar chini ya uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume, na khasa walimu wangu, kwa kunipa ilimu ya bure kutokeya ya msingi mpaka ya sekondari. Sio kuwa nilizaliwa tu na kulelewa Zanzibar bali tone la maji la Zanzibar ndilo lililonitiya kiu ya kutaka kuliangaza pango la saikolojiya ambalo limekuwa likiwanyima furaha ndugu zangu wengi kutoka Zanzibar. Hakuna ambaye hakuumiya Zanzibar na hakuna ambaye atashindwa kushukuru kwa fursa ambazo Zanzibar imetowa kwa watu wake. Msemo wa kheri imo ndani ya tumbo la shari ni msemo wenye kumgusa kila Mzanzibari na kila binaadamu aliyekuwa hai katika dunia hii.

Bado nakumbuka wakati nilipokuwa mtoto mdogo nimesimama mbele ya sinema ya Majestic iliyopo Zanzibar na kufadhaishwa na mgongano wa kiakili baina ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu waliyokuwa wamevaa nguo za kuvutiya za kijeshi, bastola kiunoni na bunduki mikononi, na mimi kuikamata kalamu na kujibu masuali kuhusu somo la utumwa wa Waarabu darasani skuli ya Tumekuja. Suala langu lilikuwa, kama Waarabu wanachukiwa na wanachukiza mbona Makomred walikuwa mstari wa mbele Zanzibar?

Napenda kutowa shukurani zangu za dhati kwa Dola ya Oman chini ya

Page 479: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani 447

uongozi wa busara wa Sultan Qaboos bin Said Al Said, kwa kukipokeya kizazi cha mashujaa wa KiOmani kilichotowa na kinachoendeleya kutowa mchango mkubwa katika kuikombowa, kuweka amani, na kuijenga Afrika Mashariki na Kati. Tumeweza chini ya uongozi wake kukutana na watu wetu na kufunguliwa milango ya kheri na fursa zisizokuwa na mwisho, na kwangu binafsi kwa kuipa familia yangu fursa zisizokuwa na idadi na watoto wenye kuinukiya ndani ya mazingira yaliyotuliya. Yote hayo yasingeliwezekana kufanyika bila ya hikma na mtazamo wenye kuona mbali wa Sultan Qaboos bin Said. Tunamuombeya dua Mwenye Enzi Mungu amzidishiye nguvu katika kuendeleya kuwaongoza watu wa Oman kwa ruu’ya yenye kuongozwa na umoja wa ndani wa nchi wa raia zake na urafiki na nchi jirani na za mbali—Amin.

Shukurani maalumu zinakwenda kwa Profesa Kelly M. Askew ambaye ni mshiriki mwenzangu katika kuandika kwa pamoja pendekezo la utafiti huu uliyoweza kutupatiya msaada wa kifedha wa awali uliyonidhihirishiya umuhimu wa kufanya utafiti mkubwa zaidi baada ya mwaka 2004. Kwa niaba ya Kelly na yangu, nalishukuru shirika la Kimarekani la Wenner-Gren Foundation for Anthropological Research liliyopo jijini New York, Marekani, kwa msaada wao muhimu na wa awali. Kelly, ahsante sana kwa urafiki na ushirikiyano wako kwenye utafiti huu na kwa kunijuulisha na mtandao wa mapinduzi ya uchapishaji wa Lulu.com. Ahsante sana sana Kelly.

Walimu wangu hayati Maprofesa Archie Mafeje na Cynthia Nelson wa Chuo Kikuu cha Kimarekani kiliyopo Cairo–Egypt, wamechangiya sehemu kubwa katika mafanikio ya masomo yangu. Hayati Profesa Roy Rappaport wa Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor, alikuwa mtu karimu na mwepesi wa kunikaribisha ofisini na nyumbani wake. Pia nilipokuwa masomoni Ann Arbor, nilibahatika kuhudhuriya mihadhara ya baba wa “theolojiya ya ukombozi ya Kikristo” Gustavo Guiterrez; na baba wa “Afrabia” Profesa Ali A. Mazrui.

Guiterrez alinifanya nimfahamu zaidi Yesu Kristo na khasa jinsi mchungaji Bartolome de Las Casas wa karne ya kumi na sita alivyopinga utesaji na mauwaji ya halaiki ya wenyeji Wahindi Wekundu uliyofanywa na wakoloni kutoka Spain. Niliwafahamu kutoka kwa Guiterrez na baadaye kutoka kwa Profesa Harvey Cox, Jr., akina Dietrich Bonhoeffer, Leonardo Boff, na wakombozi wengineo wa Kikristo kuwa ujumbe wa Kristo Yesu/Issa mtoto wa Bibi Maryam, ni ujumbe wa kiukombozi wenye lengo la kuleta amani duniani na haukubaliyani kabisa na vitendo vya utumiaji nguvu, mauwaji au ukandamizaji wa binaadamu wengine kwa jina la dini. Namshukuru sana Mzee Guiterrez kwa kunifunuwa macho na kunifanya niufahamu uwezo wa tafsiri ya kiukombozi ya Ukristo katika kumuinuwa binaadamu kutokana na ufakiri na kudumisha amani ulimwenguni.

Juu ya yote, milango ya utafiti huu kabisa isingeliweza kufunguka bila ya Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kunijuulisha na wazee ambao majina yao wameomba yahifadhiwe, pamoja na kunijuulisha na mwandishi Bwana Mohamed Said.

Page 480: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani448

Nilijuwana na Ramadhani tulipokuwa wanafunzi American University in Cairo (AUC) na sidhani kama tungeliweza kutambuwa kama kuna siku njiya zetu zitakutana na atanielekeza kwa wazee ambao ishara na mafumbo yao yalikuwa ni dira iliyoniongoza kunako njiya na matokeo ya utafiti huu.

Si Ramadhani, wala Mohamed, wala mimi mwenyewe, tungeliweza kutambuwa wakati ule kama ishara nilizopewa na wazee waliyonijuulisha nao zingeliweza kumalizikiya katika sura ya kitabu hichi. Mohamed ndiye aliyenijuulisha na Mzee Mkwawa na tulikwenda pamoja kuizuru mbuga ya Sakura na kijiji cha Kipumbwi kwa mara ya kwanza. Hiyo ilikuwa ni ishara ya pili iliyonifahamisha kuwa njiya ya Mapinduzi ya Zanzibar iko Tanganyika na kuyatafuta Mapinduzi ndani ya vichochoro vya Mji Mkongwe wa Zanzibar itakuwa ni kupotezana njia.

Ishara ya kwanza nilipewa na marehemu Mzee Hamza Azizi aliyekuwa Inspector General of Police (IGP) wa Tanganyika wakati wa mapinduzi ya Zanzibar. Mzee Aziz hakuwacha kuirudiya kauli yake ya kunipa moyo “Endelea kutafuta, usichoke; na hapa kwangu unakaribishwa tena na tena.” Piya alinidokoleya kuwa nitafaidika na ripoti ya Shirika la Ujasusi la Kimarekani (CIA) ambayo yeye alipata kuiona alipokuwa Balozi wa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Canada. Bahati nzuri au mbaya niliipata ripoti hiyo mwishoni mwa utafiti wangu. Lakini mpaka kufariki kwake dunia, Mzee Hamza Aziz alifika kukubali kuzungumza na mimi lakini kwa ishara na mafumbo, tena nje ya nyumba yake! Khofu yake ilijieleza pale aliponiambiya kuwa “sisi tulikula kiapo kuhusu hili suala la Mapinduzi na ni kikundi cha watu wachache sana wanaoufahamu undani khasa wa Mapinduzi ya Zanzibar.”

Aliponielezeya Mzee Hamza Azizi kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalizungum­zwa katika nchi fulani ya Kiarabu wakati ujumbe wa Mwalimu Nyerere ulipoizuru nchi hiyo nilimuuliza “Ni Algeria?” Mzee Hamza alinijibu “umesema wewe!” Ishara kubwa aliyonipa Mzee Hamza ni pale aliponigutuwa kimafumbo kuwa itabidi kwanza niamuwe kama Mapinduzi ya Zanzibar yaliandaliwa Zanzibar au Tanganyika.

Napenda kumshukuru Mzee Abbas ambaye alinionesha anachokijuwa kwa kunitaka nikamate simu nyengine ya nyumbani kwake ili nisikilize simulizi za kiongozi na rafiki yake mpenzi huku yeye akizungumza kwenye simu iliyoko chini ukumbini kwake. Balozi Abdul Faraji ambaye alihusika na kuandaa chombo kilichowarudisha Zanzibar baadhi ya viongozi wa Afro­Shirazi kama Mzee Abeid Amani Karume na kiongozi wa chama cha Umma marehemu Abdulrahman Babu, aliamua kunihoji mimi kwanza kabla ya kumuuliza masuala yangu. Khofu zao zilikuwa ni ishara njema kwangu, kwa Zanzibar na kwa Tanganyika. Nilifahamu moja kwa moja kuwa wazee wa TANU wa Tanganyika walikuwa wana kitu wamekificha kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu walifahamu kuwa waliivamiya nchi ya watu na waliloifanyiya Zanzibar lilikuwa ni kosa la jinai la kimataifa.

Page 481: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani 449

Nilikumbushwa na Profesa Ibrahim Noor Shariff, kuwa msomi mmoja maarufu duniani alipata kusema kuwa hayati Mwalimu Nyerere alikuwa tayari kuzipeleka nchi zote zilizoulisha raia wasiokuwa na makosa kwenye mahakama ya Arusha isipokuwa Tanganyika! Niliwahakikishiya wazee kuwa lengo langu ni kuiweka sawa historia na kuwa wana uhuru kamili wa kukubali au kukataa kuzungumza na mimi au kusajiliwa, au kuzungumza na kusajiliwa, kwa kuyataja au bila ya kuyataja majina yao ya kweli au kamili. Kwa waliyoniomba nisiyataje majina yao kwenye uhai wao nimeyahishimu matakwa yao na kwa hiyo sikuwataja. Waliyokubali nimeyataja majina yao kwa ukamilifu na wengine pamoja na picha zao.

Kuna kigogo kilosema wazi kuwa ana afadhali afe amenyooka na jeneza lake limevalishwa bendera na apigiwe wimbo wa taifa kuliko kunipa anayoyajuwa kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na khasa kwa kujuwa kuwa anayetawala sasa Zanzibar ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume. Kwa nini watu wa nchi nyingine waliogope jambo la ufakhari la kuiokombowa nchi jirani isipokuwa wanajuwa na wanaogopa kuwa hawakuitendeya haki nchi jirani?

Anaelezeya mzee mwengine ambaye jina nimelihifadhi: “Father K hakuweza kujidai kuwa anayajuwa mapinduzi na walokuwa wanayajuwa hawakuweza kujionyesha kuwa alikuwa hayajuwi. Karume alikuwa ni Mungu­mtu ambaye alifanya maamuzi yake kupitia Baraza la Mapinduzi (BLM). Alikuwa hawahe­shimu hata mmoja katika BLM na aliwafanya wajue hivo. Karume alikuwa ni bingwa wa ‘bush politics’; tafauti baina ya kuwa na akili na kuwa na maarifa. Karume alikuwa ana kipaji cha kuzaliwa cha kujuwa hatari iko wapi na hisia kali ya kujilinda.”

Bwana Said Suleiman Al­Behlani ambaye aliishi sana Bagamoyo alinielezeya nilipomtembeleya nyumbani kwake Maskati jinsi siku moja manahodha wawili, Nakoma na Buguma walivyogombana pale Bagamoyo na Nakoma akamtukana Buguma na kumwambiya kuwa “wewe mnyama vipi unakula kwa Waarabu wakati wewe ulikuwa ukinijiya usiku nipeleke silaha Zanzibar? Mimi nilikuwa nikiogopa nisiuwawe tu lakini wewe si mtu”.

Kila alokuwa ana khofu alikuwa na khofu kuwa fulani yuhai na akisikiya nimeitobowa siri ya Mapinduzi nitakuwa nimejiweka pabaya. Kinyume na Shahrazade wa kitabu maarufu cha Alfu Lela U-Lela ambaye aliendeleya kumtoleya hadithi Sultan Shaharia mpaka saa za asubuhi kukimbiya kifo, wazee wa Mapinduzi wanaangaliya nani yuhai na nani kafa kabla ya kuamuwa kuyatowa walioyavumbika kwa miaka mingi. Kila anapokufa kiongozi wa Mapinduzi ndipo wazee walio hai hutokwa na khofu ya kuueleza ukweli wa Mapinduzi.

Wazee wengi walitokwa na khofu kwa kujuwa kuwa hayati Mwalimu Nyerere hayupo tena duniani lakini wengine bado wana khofu kwa kujuwa kuna viongozi wakongwe ambao bado wako hai. Baada ya kumuambiya Mzee Victor Mkello

Page 482: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani450

kuwa wanamapinduzi wengi wameshatanguliya kwenye haki, alinikumbusha kuwa Mzee Rashidi Kawawa bado yuhai na kwa nini sijazungumza naye? Sikutaka kumpa sababu zangu lakini niliyakumbuka maneno ya marehemu Mzee Hamza Aziz kuwa “atakachokuambia Kawawa take it with a spoon of salt.” Yaani juu ya kuwa ataelezeya na yasiokuwa sahihi pia.

Kwa upande wa Zanzibar napenda kumshukuru jamaa yangu Ali Saidi Al­Kittani kwa kunijuulisha na katibu wa Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud “Mmasai.” Pia napenda kuwashukuru marehemu Ali Omar [Lumumba] wa Weles, Zanzibar, pamoja na marehemu Mzee Othman “Bapa”. Wazee wawili hawa walinisaidiya sana kwa kunijuulisha na wazee wengine ambao waliifahamu historia ya Mapinduzi ingawa kulikuwa na vipengee ambavyo hata wao walikuwa wanagenzi.

Mzee wangu na mwandishi Bwana Issa Nassor Al­Ismaili ametumiya wakati wake thamini na hikma zake za umri mrefu kunishauri nijaribu kadri nitakavyoweza niandike kwa kuungwa mkono na ushahidi na si kwa maneno yangu mwenyewe peke yake. Bwana Issa pia aliwahi kunihadithiya kuwa safari moja katika mazungumzo yeke na marehemu Abdulwahid Sykes, Bwana Abdu alipata kumuambiya kuwa “Bora tusiyazungumze mambo ya Zanzibar kwa sababu tukiyazungumza urafiki wetu utavunjika.” Kwa wengine kutoyazungumza Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ni ishara ya kuyajuwa mengi ambayo yanatowa taswira mbaya kwao.

Namshukuru sana Profesa Ibrahim Noor Shariff kwa kuniruhusu kuitumiya picha iliyoko mbele ya gamba la kitabu aliyoichora mwaka 1960 wakati bado ni mwanafunzi wa shule ya sekondari. Kitabu chake Tungo Zetu kilizidi kunifunguwa macho kuhusu khabari kutoka Uswahilini na vita dhidi ya Waswahili, Waarabu, na baadaye Washirazi kwa kutumiliwa garasa la utumwa. Profesa Ibrahim aliwahi kunipa ushauri ambao zitoweza kuusahau pale aliponiambiya kuwa utaweza kuandika kwa lugha ya Kiswahili bila ya kutumiya maneno mengi ya Kiingereza ikiwa utakumbuka namna gani utasema Kiswahili na Bibi yako asiyejuwa Kiingereza!

Napenda kuwashukuru Susan Brandt kwa kulichora gamba la kitabu, Sherif Wahdan kwa kunisikiliza na kunishauri mengi ambayo sikuwa na hakika nayo. Huwayda, mtoto wa marehemu Bwana Nassor Abdalla Al­Shahimi, maarufu “Mlawwaz” ametowa mchango wa kifikra juu ya utangazaji wa kitabu, na Profesa Benjamin W. Fortson kwa kuuandaa muswada wa kitabu na kuuweka tayari kwa uchapishaji. Pia napenda kumshukuru Aziz Al Harrasi kwa kunisaidiya kulitengeneza jopo la kitabu katika facebook na mtandao wa kukipokeya kitabu.

Nimekuwa na mawasiliyano ya miaka mingi na Ismail Jussa na hivi karibuni amekuwa akisisitiza sana juu ya umuhimu wa kupatikana uongozi mpya Zanzibar ambao unatokana na viongozi wa CUF na CCM watakaosukumwa na umma uliyozindukana kuziongoza na kuzijenga Zanzibar na Tanganyika ambazo

Page 483: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani 451

ni huru, zenye demokrasia ya kweli, ustahmilivu, na zenye amani na neema za kiuchumi kwa wote. Fikra zetu zimekuwa zikikutana kwenye imani kuwa kuusitisha mtikisiko wa nyumba ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar utategemeya sana kuunga mkono mpigo mpya wa moyo wa Zanzibar. Ahsante sana Al Habib.

Nimebahatika kukaa na kumsikiliza kwa muda marefu Muhammed Ahmed Sultan Mugheiry (Eddy Riamy). Eddy amekuwa akisisitiza tena na tena na ku­choka kunukuliwa kuwa Zanzibar inahitajiya chama kimoja tu cha kisiasa ambacho si CCM wala si CUF bali chama kimoja cha Uzanzibari na cha Wazanzibari wenye uaminifu na kuaminiyana. Amenitanabahisha juu ya umuhimu wa kujitenga na mirengo ya kisiasa ya Zanzibar na kuukamata mtitiriko wa historia ya uzalendo wa Kizanzibari. Ahsante sana Eddy kwa kuniongoza kwenye bahari ya uzalendo na matukiyo ambayo hayamo kwenye vitabu au hata katika maelezo yaliyoandikwa chini katika ukurasa.

Napenda pia kumshukuru Mohammed Khelef Ghassany, ambaye amechangiya sana katika kulijenga jukwaa la mawasiliyano kati ya Zanzibar na ulimwengu kupitiya mtazamo na msimamo wake usiyotetereka. Khalid Said Suleiman (Gwiji) maisha amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kizazi kipya kujiilimisha na kuuilimisha umma juu ya historia ya Zanzibar ambayo haikupotoshwa. Kizazi kipya cha Kizanzibari hakina kumbukumbu ya Mapinduzi na daima kimekuwa kikiomba wakati ufike wakifahamu kiini cha fitina zisizokwisha. Historia mliyokuwa mkiitafuta ndiyo hii hapa. Sasa kazi kwenu.

Undani wa Mapinduzi ya Zanzibar ulikuwa umefunikwa kwa muda mrefu na ikawa si rahisi kuufikiya kwa kukosekana utulivu na fursa za kufanya utafiti. Utulivu na fursa nilizozipata katika kufanikisha zisingelikuwepo bila ya wema mkubwa kutoka kwa upande wangu wa baba na khasa kutoka kwa marehemu Ami yangu Omar Abdalla Ghassany na mwanawe Rashid Omar Ghassany, marehemu Bwana Nassor Abdalla Nassor (maarufu “Mlawwaz”) na mke wake Anti Bishara Yahya, marehemu Ami Hamdan bin Ali Al­Abri, na ndugu zangu Abdullah Ahmed Abdullah Ghassany, Thurayya Mohammed Abdalla Ghassany, Dada Hinda Ahmed Ghassany, Ahmed Seif Msellem Al­Rawahi, Ami Harub Sheikhan Ghassany, na Shangazi langu Bibi Zayyana bint Ali Al­Abriyya na ukoo wangu wote kutoka Mwera Magayani, Zanzibar.

Kila Jumaapili jioni marehemu baba yangu alipokuwa akija kunichukuwa mimi na ndugu yangu wa kike kutoka Mwembetanga kurudi nyumbani mjini, marehemu bibi yangu mpenzi mzaa baba na mlezi wangu, Bibi Sarah bint Ahmed bin Muhammed Al Barwani Awlad Hijji alikuwa akituimbiya nyimbo ifuatayo ya kutuaga “Mbweyu mbweyu, indendi kuranga indendi mwanja, aruuu!” Sikuwa nikiifahamu maana ya nyimbo hiyo lakini nilifahamu kuwa nimezaliwa na kulelewa kuuhishimu ubora wa tamaduni za Kiarabu na za Kiafrika.

Daima nitamkumbuka marehemu bin ami yangu, Farid Ahmed Abdalla

Page 484: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Shukurani452

Ghassany ambaye tulifunga urafiki mkubwa kutokeya aliporudi kutoka msitu wa Ngezi, Pemba, alikokuwa akiishi na marehemu baba yake na ami yangu, Bwana Ahmed Abdullah Ghassany. Marahemu Farid alinifundisha kutembeya shingo juu na kutokubali kuonewa au kuanzisha ugomvi na mtu.

Sina shukurani za kutosha kwa Shangazi langu Bibi Khadija Abdalla Jahadhmy ambaye alikuwa mstari wa mbele katika maamuzi yote makubwa yaliyochangiya katika kunileteya mafanikiyo katika maisha yangu. Sina cha kuwalipa ndugu zangu Dr. Saadia Amour Sultan Al­Riyami na mumewe Sheikh Abdullah Hamoud Al­Riyami, Da Fatma Ali Jahadhmy/Trudeau, Dr. Abdullah Amour Al­Riyami, Mohammed Ali Al­Barwani, kwa kunipokeya, kunitazama, kuniongoza, na kwa kunipa msingi mzuri wa kimaisha.

Balozi Bwana Nassor Seif Al­Buali na mkewe Bibi Sharifa (Da Hobo) Mohammed Nassor Al­Lamki ni wazee ambao sitoweza kuusahau wema wao katika maisha yangu na katika uhai wangu hapa duniani. Ni Mwenye Enzi Mungu peke yake mwenye uwezo wa kuwalipa ihsani zao.

Na mwisho, napenda kumshukuru kwa dhati mke wangu, Asya Mohammed Suleiman Al­Lamki, nguzo madhubuti ya hikma na upole, kwa kusimama na mimi katika mambo yote muhimu katika maisha yangu. Asya ni shifaa na ni muongozo uliyotuliya na wenye kutuliza. Siwezi kumsahau shemegi na ndugu yangu, Fatma Mohammed Suleiman Al­Lamki kwa kusimama na familia yangu katika kila hali na kutuondoleya kila vikwazo katika maisha yetu, na mumewe, mwingi wa uungwana na ushauri wa busara, Sheikh Ali Mohammed Said Al­Busaidi.

Ni shauku na matamaniyo yangu kuwaona watoto wangu Aisha, Fatma, Ghassan, na Sarah, na kizazi kipya kilicho kama chao kwa jumla, wanayaendeleza mapenzi na wajibu wao kwa Zanzibar na Oman na kwa niya ya kudumisha amani na maendeleo, na kuzipenda lugha na turathi zao nzuri za Kiarabu na za Kiafrika, na za kutoka nchi za Magharibi. Wazee wangu, mke na watoto wangu na ndugu zangu niliyowataja hapo juu hawahusiki hata kidogo na utafiti au yaliyomo ndani ya kitabu hichi.

Piya napenda kuwashukuru wahafidhina wa Kizanzibari na wa Kitanganyika wasiopendeleya mashirikiano baina ya Wazanzibari na hata wale ambao wanataka milele Waarabu na khasa wakikusudiwa Waislam, wasisikilizane na waliyoko kusini ya Bara la Afrika, kwa kujitokeza kwa hoja na sera zao. Iwapo hoja zao ni za kitaalamu na hazina chuki basi watashukuriwa kwa kuuongoza mjadala utakaojenga usalama na mustakbal mwema kwa Wazanzibari.

La, wataendeleya kupinga kwa misingi ya khofu zinazotokana na chuki na fitina, piya wataonekana kwa niya na vitendo vyenye kupendeleya fitina na mitafaruku badala ya umoja baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika na Waarabu. Vyoyote itakavyokuwa, kheri hutoka ndani ya tumbo la shari na kheri na si shari ndiyo yenye kudumu na yenye uhakika wa kuwepo.

Page 485: 31875247 Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru

Mwandishi

Harith Ghassany ni Muafrabia kindakindaki aliyezaliwa na wazazi wa Kiarabu na mabibi wa Kiafrika kuumeni kwake kutoka kabila la Kimanyema na la Kimwera. Amekhitimu kutoka chuo cha Msikiti Baraza na Skuli ya Tumekuja (Mtakatifu Yusuf ) Zanzibar, na Shule ya Popatlal, Tanga. Alitunukiwa shahada yake ya kwanza kwa daraja ya “heshima” katika masomo ya Mashariki ya Kati kutoka Chuo Kikuu cha Kimarekani, jijini Cairo – Misri. Pia alitunukiwa shahada ya Masters mwaka 1988 kutoka Chuo Kikuu cha Kimarekani cha Michigan katika masomo ya Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Karibu, na shahada ya Masters ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani, na kumaliziya na shahada ya Udaktari wa Falsafa pia kutoka Chuo Kikuu cha Harvard katika masomo ya Ilimu ya Binaadamu (Anthropology) na ya Mashariki ya Kati. Harith Ghassany ni msomi/mtafiti huru na anaishi Marekani, Washington DC.