home | ilala municipal council - 2 m0ac2h0i...ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye...

16

Upload: others

Post on 04-Sep-2020

57 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

MACHI2020

Page 2: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

Page 3: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

ILALA TUPO VIZURI JARIDA LA MWEZI

KUHUSU HALMASHAURIYA MANISPAA YA ILALA

00

TAHARIRI01

MRADI WA UENDELEZAJI WA JJJI LADSM ‘DMDP’

02

MANISPAA YA ILALA YAPITISHABAJETI YA MWAKA WA FEDHA

2020/2021

04

HABARI PICHA06

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALAS.L.P 20950, DAR ES SALAAMSIMU: 2128800 / 2128805TOVUTI: www.ilalamc.go.tz

BARUA PEPE: [email protected]

MHARIRI: TABU F. SHAIBU

AFISA HABARI: HASHIM JUMBE

MSANIFU: FEROOZ KILLAH

SEMA ILALA

ilala_manispaa

ilala manispaa

ilala municipal

YALIYOMO

Page 4: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

ILALA TUPO VIZURI SEMA ILALA

KITENGO CHA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina Kitengo maalum chenye kushughulikia taarifa mbalimbali zinazohusu Manispaa ya Ilala ikiwa kujenga taswira nzuri na kuendeleza mahusiano bora baina ya Halmashauri na umma pamoja na wadauwake, kutoa elimu kwa umma na kutangaza kazi za Halmashauri kupitia vyombovya Habari ikiwemo mikutano na Waandishi wa Habari, na Kuandaa Majaridaambapo ndani yake utaweza kusoma Habari Mbalimbali na Matukio yaliyojilinndani ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha Mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na

utekelezaji wa Miradi ya Kimaendeleo.

DHIMA

Kujenga Jamii yenye Maisha bora, iliyopata huduma za Msingi na kuondoaumaskini ifikapo 2025

Kutumia Rasilimali zilizopo kwa kushirikisha wadau ili kujijengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa kuzingatia malengo ya kisekta.

01KUHUSU HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALAMANISPAA YA ILALA

DIRA

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ni Miongoni mwa Manispaa tano { 5 } zilizopo katikaMkoa wa Dar es salaam, Manispaa ya Ilala ilianza mnano mwaka 2000 Mwezi februariina ukubwa wa Kilomita 210 za Mraba, upande wa Kaskazini imepakana na Manispaaya Kinondoni, upande wa Magharibi imepakana na Mkoa wa Pwani, Manispaa ya Temeke

upande wa kusini na bahari ya Hindi upande wa Mashariki.

Hali ya hewa kwa Manispaa ya Ilala ni joto la wastani kiasi cha nyuzi joto 25 - 33,huhupata wastani milimita 1000 za mvua kwa Mwaka kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2002, Manispaa ya ilala ina jumla ya watu 637,537,kati yahao Wanawake ni 315,670 na Wanaume 32,903. Kiutawala Halmashauri ya Manispaaya Ilala ina Tarafa tatu ambazo ni Kariakoo, Ilala na Ukonga na ina jumla ya Kata 36

Page 5: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM_DMDP

Na: Hashim Jumbe

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2012, Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na Watu wapatao Milioni 4.3, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka hadi kufikia Watu Milioni 10 ifikapo mwaka 2030, hivyo kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kati ya Majiji yanayoongoza kwa ukubwa na makazi mengi.

Sambamba na ongezeko hilo, lakini pia Jiji la Dar es Salaam ndiyo Jiji linalochangia kwaasilimia kubwa katika ukuaji wa pato la Taifa na kuwa lango la biashara kwa Mataifa ya jirani,huku Jiji hilo likikabiliwa na changamaoto ya ubora wa Miundombinu, hivyo kuzoroteshahuku Jiji hilo likikabiliwa na changamaoto ya ubora wa Miundombinu, hivyo kuzoroteshabaadhi ya shughuli na kuwa kikwazo kwa ustawi wa Jiji na Taifa kwa ujumla.

01

01SEMA ILALA

Aidha, kasi ya ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam haikuwa ikiendana na Miundombinu iliyopokwaniinakadiriwa kuwa asilimia kati ya 70 hadi 80 ya makazi ya Jiji la Dar es Salaam hayajapimwa, hivyo kutokanana ukuaji huo na mabadiliko ya tabia nchi yanayoikabili Dunia, athari za mafurikozinatarajiwa kuongezeka katika Jiji la Dar es Salaam,kwa hali hiyo bila ya kuwana mipangobora yautoaji wa huduma, Jiji hili linaweza kutokukalika.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ndipo ilipokuja na wazo la kuwa na Mradi wa Uendelezaji wa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ndipo ilipokuja na wazo la kuwa na Mradi wa Uendelezaji wa iji la Dar es Salaam ujulikanao kama Dar es Salaam Metropolitan Development Project ‘DMDP’.

MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DSM ‘DMDP’ ULIVYOPANDISHA THAMANI YA MAISHA YA WAKAZI WA ILALA

MACHI, 2020

Page 6: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Utekelezaji wa Mradi wa DMDP kwa Manispaa ya Ilala

Manispaa ya Ilala imetengewa shilingi Bilioni 115 kwa utekelezaji wa mradi wa DMDP, na hadi sasa Manispaa ya Ilala imeingia Mikataba yenye thamani ya shilingi Bilioni 94.57 katika kujenga Kilometa 33.61 za barabara za lami, Kujenga jengo la ghorofa 1 Ofisi na Maabara ya mradi, kujenga vituo vya kukusanyia taka ngumu 24, kujenga masoko 3, kujenga maeneo ya mapumziko ‘Community parks’ 2, kujenga mifereji ya maji ya mvuakilometa 16.43 (storm drainage), kujenga na kuweka huduma za vyoo vya umma 3, kujenga vizimba vya maji safi 9 pamoja na ununuzi wa magari ya taka ngumu 5. kujenga vizimba vya maji safi 9 pamoja na ununuzi wa magari ya taka ngumu 5.

Hata hivyo, kazi za ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua ya Bonde la mto Msimbazi,Tenge, Liwiti, Yombo, Tembo mgawaza na Mto Sungura yenye urefu wa jumla ya kilometa 5.96 pamoja na bwawa la kukinga maji kwa muda (Detention pond) zilianza pia tangu tarehe 15 August, 2019 na kutegemewa kukamilika tarehe 14 Novemba, 2020.

Maandalizi ya mradi wa DMDPVigezo muhimu vilivyozingatiwa wakati wa kuchagua Miradi ni kama vifuatavyo;i) Miradi inayounganisha maeneo ya Watu wenye kipato kidogo na yaliyojengwa holelaii) Miradi inayounganisha Wilaya na Mkoaiii) Miradi inayounganisha maeneo mbalimbali na ukanda wa mabasi yaendayo haraka (BRT) ili kurahisisha usafirishaji

Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, vigezo hivyo vitatu viliibua miradi ifuatayo;i) Ujenzi wa barabara za mlisho (feeder roads) zenye urefu wa kilometa 3.695ii) Ujenzi wa mifereji ya kutiririsha maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 15.96 katikamabonde ya mto Msimbazi na Yomboiii) Kupandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela katika Kata za Gongolamboto, Minazi Mirefu, Kiwalani, na Ukonga, kuweka nyenzo za ukusanyaji wa taka ngumu, kujenga mitaro ya kutiririsha maji ya mvua, kuweka taa za barabarani, kujenga njia za watembeamitaro ya kutiririsha maji ya mvua, kuweka taa za barabarani, kujenga njia za watembeakwa miguu, ujenzi wa maeneo ya mapumziko na vituo vya mabasi, ujenzi wa vyoo vya umma na ujenzi wa maeneo ya michezo.iv) Kuandaa Mpango kabambe wa Mfumo wa Maji ya Mvua na Maji Taka (Storm Drainageand Sewerage Master plan)v) Kundaa Mpango Mkakati wa kuendeleza Ukanda wa mabasi yaendayo haraka (BRTCorridor Development Strategy). Kwa kushirikisha Sekta Binafsi; kujenga masoko ya kisasa na ya kawaida, kujenga maduka makubwa (shopping malls) na ya kawaida, kuboreshakisasa na ya kawaida, kujenga maduka makubwa (shopping malls) na ya kawaida, kuboreshamaeneo ya utalii, kujenga maeneo maalum ya maegesho, kuweka njia za waendeshabaiskeli na watembea kwa miguu n.kvi) Kufunga mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa mapato wa Halmashaurivii) Kujenga uwezo wa mwitikio wa haraka katika kukabiliana na majanga.

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM_DMDP

SEMA ILALA

MACHI, 2020

02

Page 7: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Kata ya Gongolamboto ambapo ujenzi umefanyikabkwenye barabara za Chunge iliyo na urefu wa km 1.49, Kampala km 2.06, Limbanga km 2.44, High Mount km 1.44 na Baghdad Kilometa 0.35. Aidha Kata ya Gongolamboto pia unajengwa mtaro wenye urefu wa Kilometa 1.85, vizimba 7 vya taka na kununua garimoja la kusomba taka.

Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049 zimejengwa kujengwa, barabara hizo ni Zileza Bush iliyo na urefu wa km 1.07, Gude km 1.332, Jongo km 0.587, Mbilinyi km 0.35, Pepsi km 0.59,Jamaka km 0.667, Zahanati km 1.17, Kamungu km 2.08, Mkwajuni km 1.16, Binti Musa km 2.14, Betheli km 0.315, Mnara km 0.53, Kijiwe Samli km 0.42, Bombom km 0.51.

Aidha, Kata ya Kiwalani pia itanufaika na ujenzi wa vituo vitatu vya kutolea huduma za vyoo,vizimba 8, kununua gari 1 la kusombea taka,kujenga masoko matatu, kujenga maeneo ya kupumzikia mawili na kujenga vituo vitatu vyaa kutoleaa huduma za maji safi.

Kata nyengine inayonufaika na Mradi huu wa DMDP ni Ukonga ambapo hadi sasa maeneo yaliyotekelezwa ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zanye urefu wa Kilometa 11.572 kwenye makazi yasiyopangwa ambapo zinajengwa barabara za Markaz yenye urefu wa km 1.86, Zimbili km 3.3, Dispensary yenye urefu wa km 1.06, School km 2.18 na Chacha km3.17

Ujenzi wa barabara kwenye makazi yasiyopangwa

Moja kati ya barabara za mlisho iliyojengwa Kata ya Upanga Mashariki, barabara ya Olympio inavyoonekana kwa sasa baada ya kujengwa kupitia

Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam 'DMDP'

zenye urefu wa Kilometa 3.695 ambazo ni Ndanda yenye urefu wa km 0.35, Kiunganikm 0.7, Omari Londo km 0.665, Olympio km 0.86, Mbarouk km 0.4, Kongokm 0.3, Livingstone km 0.15, Swahili km 0.2 na Nyamwezi km 0.25. Pamoja na barabara hizo, lakini pia ujenzi wa mifereji ya chini (underground storm drainage) yenye urefu wa km 2.8 imekamilika sambamba na ujenzi wa Ofisi na maabara ya kisasa.

Ujenzi wa barabara za Mlisho (feeder roads)

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM_DMDP

SEMA ILALA

MACHI, 2020

03

Page 8: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Manispaa ya Ilala yapitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 181.7 kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Katika kuandaa Mpango na Bajeti ya mwaka 2020/2021 Halmashauri ya Manispaa ya Ilalaimezingatia Mwongozo wa uandaaji wa bajeti uliotolewa na Hazina mwaka 2019, Ilani ya CCM ya mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano, hotuba ya Rais Magufuli yaNovemba 2015, Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015,Vipaumbele vya Halmashauri na Maoni ya Wadau mbalimbali.

Aidha, katika makisio ya mpango na bajeti ya mwaka 2020/2021 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imejiwekea vipaumbele kumi na moja (11) huku ikiwa na mikakati saba (7) katika kufanikisha utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2020/2021.

Na: Hashim Jumbe

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, leo limefanya kikao maalum cha mapitio ya Bajeti ya mwaka 2019/2020 na mapendekezo ya Mpango na Bajetiya mwaka wa fedha 2020/2021 wenye Jumla ya Shilingi Bilioni 181.7, ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 60 sawa na 33.02% ya Bajeti yote ni kutoka kwenye vyanzo vya Mapato ya ndani na Shilingi Bilioni 121.7 sawa na 66.9% ya Bajeti ni ruzuku kutoka Serikali Kuu.

AAidha, Bajeti ya Mapato ya ndani ya mwaka 2020/2021 imeongezeka kwa 5% ukilinganisha na Bajeti ya Shilingi Bilioni 57 ya mwaka 2019/2020,hii imetokana nakuongezeka kwa gharama za uchangiaji huduma za afya pamoja na uwepo wa hospitali mpya ya Wilaya Kivule inayotarajiwa kuanza kutoa huduma hivi punde, ambapotaongeza mapato sambamba na kituo cha afya cha Mzinga, Zahanati ya Lubakaya, Bangulo, Luhanga na Mbondole.

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

04

Page 9: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Mchanganuo wa Matumizi ya kawaida kwa fedha za ruzuku

Health sector basket fund 2,865,701,325

School meals grants 830,843,000Responsibility grants 546,600,000

School fees compensation grants 1,102,710,000Capitation Grants-Dev 1,868,149,000

Mfuko wa Jimbo 189,180,000Ujenzi wa Miradi Mkakati TSh. 2,500,000,000Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya TSh. 500,000DMDP TSh. 18,228,375,100

Matumizi mengineyo (OC) Shilingi 2,116,869,000

Mchanganuo wa fedha za Miradi ya Maendeleo kwa fedha ya ruzuku

Mishahara Shilingi 91,024,147

Matumizi ya Mapato ya ndaniHalmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka 2020/2021 kwenyeMapato yake ya ndani inatarajia kutumia fedha kiasi cha ShilingiBilioni 60 katika mchanganuo ufuatao;

Makisio ya fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu Ruzuku ya Shilingi Bilioni 12.7 kutoka Serikali imegawanywa katika maeneo mawili ambayo ni; Matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo.

Mapato ya vyanzo fungiwa Shilingi 14,014,000,000 sawa na 23.3%

Miradi ya Maendeleo Shilingi 27,591,600,000 sawa na 45.9%

Mishahara Shilingi 2,311,166,720 sawa na 3.8%

Matumizi mengineyo Shilingi 16,083,233,280 sawa na 26.8%

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

05

Page 10: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Ujenzi wa Soko la Bombom, ni Moja kati ya Masoko Matatu yanayojengwa Manispaa ya Ilala kupitia Mradi wa DMDP

Muonekano wa Barabara ya Chacha iliyopo Kata ya Ukonga

Moja kati ya Visima vya Maji Safi vilivyojengwa kupitia Mradi wa DMDP

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

06

Page 11: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo ( waliosimama mbele upande wa kulia ) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa Jengo la huduma ya haraka ( Fast track ) kwenye

Hospitali ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kivule kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ,Ndugu Jumanne K. Shauri , ( wapili kushoto ).

Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe.Mwita M. Waitara ( kushoto ) akisalimiana kwa kugongeshana miguu na

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Jumanne K. Shauri, salamu hiyo imetumika ili kukwepa kupeana mikono ili

kujiepusha na ugonjwa wa corona.

HABARI PICHA

Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga ( kushoto ) akiangalia michoro ya Mifereji inayochimbwa kata ya kiwalani kupitia Mradi wa DMDP

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

07

Page 12: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

HABARI PICHA

Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Bi.Charangwa Suleiman akipokea Mapipa ya kuhifadhia takataka kutoka kwa

Philip DeGaulle ambaye ni muwakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Omary Kumbilamoto ( kushoto ) akisaini mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya

Ulongoni-Bangulo –Kinyerezi wenye thamani ya Tshs. 17,608,000,955.08

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Ndugu Ubaya Chuma pamoja na wajumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala wakinywa maji ikiwa ni kujiridhisha aina ya maji yanayotoka kwenye moja kati ya visima vilivyochimbwa

kata ya ukonga kupitia mradi wa DMDP.

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

08

Page 13: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Ilala wakipatiwa Semina elekezi, semina hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Tambaza na ilifunguliwa na Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.Omary Kumbilamoto

HABARI PICHA

Afisa Utumishi Manispaa ya Ilala Bi.Benadeta Mwaikambo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Diamond

Mwl. Hashimu Semvua wakati wa hafla ya Tathmini ya Elimu Manispaa ya Ilala.

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

09

Page 14: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

MIEZI 18 YA MKURUGENZI SHAURI ‘Ilala tunasonga mbele’

Na: Hashim JumbeMwaka 1824 huko Huntly Scotland alizaliwa muandishi wa vitabu na mtunzi wa mashairi aliyeitwa George MacDonald, katika kipindi cha miaka 80 ya uhai wake,aliwahi kusema “to be trusted is a greater compliment than being loved” kwa tafsiri isiyo rasmi sana kwa lugha ya Kiswahili alimaanisha kuwa kuaminiwa ni bora na kunaleta maana zaidi kuliko kupendwa.

Maneno ya George MacDonald yameendelea kuishi nasi hadi sasa ikiwa imepita miaka miaka 115 baada ya kifo chake mwaka 1905, maneno yake yameendelea kuwa na maana zaidi hapa kwetu katika kipindihiki ambacho tunaongozwa na Rais Magufuli ambaye Serikali yake inazingatia uadilifu, uaminifu na uwajibikaji.

Katika mazingira hayo, makala hii itakuelezea miezi 18 ya mmoja kati ya wateule wa Rais Magufuli nanamna anavyoitafsiri kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ kuanzia tarehe 03 Septemba, 2018 alipoanza kuitumikia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa nafasi ya Ukurugenzi.Katika kipindi cha Mkurugenzi Jumanne Shauri, mambo mabalimbali ya kimaendeleo yametekelezwa ndani ya Manispaa ya Ilala, huku tukimtazama kama mtu mwenye maono katika utendaji wake, kwani ndani ya muda mfupi ameweza kufanya mambo mengi yakimaendeleo kama yafuatayo; Ujenzi wa Miradi ya Ki-mkakatiKatika uboreshaji wa huduma za kijamii na kiuchumi zinazotolewa na Manispaa ya Ilala, pamoja na kupanua wigo wa mapato ya ndani, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia Mkurugenzi Jumanne Shauri inaendelea na ujenzi wa Miradi mikubwa miwili ya Ki-Mkakati ambayo ni Ujenzi wa Soko la kisasa la Kisutu ulioanza rasmi tarehe 12 Disemba, 2018 na Ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti ulioanza tarehe 08 Julai, 2019 Utawala bora“Katika eneo la utawala bora, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala tumeendelea na uboreshaji wahuduma bora kwa Wananchi ambapo mwaka wa fedha 2019/2020 tumeanza ujenzi wa Ofisi Nne (4) mpya za Kata, ambazo ni Vingunguti, Mnyamani, Mchafukoge na Zingiziwa” alisema Mkurugenzi Shauri

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

Page 15: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

ILALA TUPO VIZURI

TOLEO MAALUM

SEMA ILALA

MACHI, 2020

Uboreshaji katika Sekta ya ElimuElimu ni nyenzo ya maendeleo kama ambavyo Serikali imekuwa ikiipatia kipaumbele kwa kuwekeza katika Sekta hii, hivyo uboreshaji wa miundombinu umekuwa ukipewa kipaumbele na Manispaa ya Ilala ili kuweka mazingira mazuri yautolewaji wa Elimu kuanzia ngazi ya Awali hadi Sekondari

.“Kwa Idara ya Elimu Msingi, hadi sasa tumejenga vyumba vya madarasa 29, Ofisi Kumi (10) za Walimu katika Shule za Msingi Yangeyange,Buyuni II, Kivule,Kimwani, Kidugalo, Zavala, Kichangani, Uamuzi, Kinyamwezi mpya na Chanika,llakini pia tunaendelea na ujenzi wa Shule mpya Tatu (3) ambazo ni Msongola Annex, Kibaden na Kivule Annex na Shule Moja (1) ya Gulukakwalala inajengwa kwa fedha kutoka Serikalini ambazo ni fidia ya eneo la reli ya mwendokasi” alisema Mkurugenzi Jumanne Shauri.

Pamoja na maboresho hayo,lakini pia kwa kipindi cha miezi 18 Halmashauri imeweza kukamilisha ujenzi wa mabomayenye vyumba 18 kutoka kwenyeShule 14, ambapo Halmashauri imeweza kutoa Shilingi Milioni 45 na Serikali Kuu imetoa Shilingi Milioni 225.Kwa upande wa Idara ya Elimu Sekondari, Mkurugenzi Shauri amesema “kwa mwaka wa fedha 20192019/2020 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala tumetenga Shilingi Bilioni 8 na hadi sasa tumeweza kujenga vyumba vya madarasa 72 na tumenunua viti 4,000, lakini sambamba na hilo tunaendelea na ujenzi wa shule mpya Tano (5)ambazo ni Zavala, Minazi Mirefu, Kinyerezi mpya,Bonyokwa, Magole pamoja ukarabati wa shule ya Buguruni Moto”

Ongezeko la mapatoKatika kipindi cha miezi 18 ya Mkurugenzi Shauri, Manispaa ya Ilala imeweza kuongeza mapato ikilinganishwa nahali ya ukusanyaji wa mapato huko nyuma, kwa mwaka wa fedha 2018/2019 makisio yalikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 56.8 na Halmashauri ilivuka lengo kwa kukusanya Shilingi Bilioni 58.1 sawa na102% ya bajeti na mwaka 2019/2020 makisio ni kukusanya Shilingi Bilioni 57 na hadi kufikia Disemba, 2019 Halmashauri ilikuwa imekusanya Shilingi Bilioni 28.9 sawa na 51% ya bajeti.

Uwezeshaji kiuchumi Wanawake, Vijana na wenye ulemavuKatika jitihada za kuwezesha Wanawake, Vijana na wenye ulemavu kiuchumi, Manispaa ya Ilala imeweza kutoa mikopo ya jumla ya Shilingi Bilioni 3.727 ambapo vikundi vya Waanawake 357 wamepata Shilingi Bilioni 1.49 na vikundi vya Vijana 134 wamepata Shilingi Bilioni 1.49 na vikundi 64 vya wenye ulemavu wamepata Shilingi Milioni 745.4

Mafanikio ni mengi na hayawezi yote kuelezeka kwa siku moja, kwa uchache nifupishe makala hii kwa maneno yaliyowahi kusemwa na Mwanamapinduzi wa Kijamaa, raia wa Argentina Daktari Ernesto “Che” Guevara aliposema ““Mashujaa ni wale wanaoacha alama zisizofutika katika njia wanazopita”

Uboreshaji wa Huduma za AfyaKatika kipindi cha miezi 18 ya Mkurugenzi Shauri, Manispaa ya Ilala imeshuhudia mapinduzi makubwa ya uboreshaji wa miundombinu katika Sekta ya Afya ambapo Hospitali ya Wilaya ya Kivule imeweza kujengwa kwa fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Magufuli, sambamba na ujenzi huo, lakini pia Manispaa ya Ilala inaendelea na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mzinga kwa mapato ya ndani na Kituo cha Afya cha Gulukakwalala kinachojengwa kwa fedha za fidia kutoka Serikalini.

Aidha, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati Nne (4) kwa mapato yakeyya ndani, ambazo ni Mbondole, Luhanga, Lubakaya na Bangulo, pamoja na ujenzi wa jengo la huduma za haraka ‘fast track’ katika Hospitali ya Kivule.

Page 16: Home | Ilala Municipal Council - 2 M0AC2H0I...Ujenzi mwengine ni kwenye barabara zilizopo kwenye makazi yasiyopangwa Kata ya Kiwalani ambapo barabara zenye urefu wa Kilometa 12.049

SIMU NA. 2128800

2128805

FAX NA. 2121486

OFISI YA MKURUGENZI1 MTAA WA MISSION

S.L.P 20950DAR ES SALAAM

Ilala MunicipalIlala MunicipalIlala_Manispaa

MAJENGO PACHA YA BENKI KUU YA TANZANIAPAMOJA NA HYATT REGENCY, KILIMANJARO HOTEL

NI MOJA YA MAJENGO YANAYOVUTIAMANISPAA YETU YA ILALA

MAJENGO PACHA YA BENKI KUU YA TANZANIAPAMOJA NA HYATT REGENCY, KILIMANJARO HOTEL

NI MOJA YA MAJENGO YANAYOVUTIAMANISPAA YETU YA ILALA

MAJENGO PACHA YA BENKI KUU YA TANZANIAPAMOJA NA HYATT REGENCY, KILIMANJARO HOTEL

NI MOJA YA MAJENGO YANAYOVUTIAMANISPAA YETU YA ILALA