tutembee kwenye website au …

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1432 DHULQAADAH 1441 , IJUMAA, JULAI 17-23, 2020 BEI TShs 1000/=, Kshs Tutembee kwenye Website www.annuurpapers.co.tz au mpaper.co.tz tunapatikana pia katika simgazeti NAMBA YA KITUO: P 5633 Mnatangaziwa nafasi za MASOMO kwa ajili ya kurudia mtihani wa kidato cha nne kuanzia tarehe 3 Februari – Septemba 2020. Gharama za masomo ni kama ifuatavyo:- 1. Ada ya masomo ni Tsh. 350,000/= 1. Ada ya bweni (HOSTEL) kwa kulipa kila mwezi ni Tsh 120,000/= na kwa kulipa kwa mkupuo wa miezi mitatu mitatu ni Tsh 300,000/=. 1. Ada ya mtihani wa taifa (NECTA) ni Tsh 50,000/= ikilipwa kipindi cha usajili wa kawaida kuanzia sasa na kabla ya tarehe 29/02/2020. Ada ya Mtihani inalipwa kupitia POSTA. 2. Ada ya kituo ni Tsh 50,000/=. Kituo kimesajiliwa na kupata namba P.5633. 1. Ada kwa mitihani ya vitendo (practicals) Physics, Chemistry na Biology ni sh 50,000/= kwa somo. Fomu zinapatikana ofisi ya Mkuu wa Shule kwa shilngi 5,000/=. Nafasi ni chache sana. Wahi kuchukua fomu mapema Wabillaah Tawfiiq MKUU WA SHULE NAFASI ZA MASOMO KWA AJILI YA KURUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE , 2020 (KUTWA NA BWENI) UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL Tuhuma za ugaidi zazidi kuliza familia Familia tatu zatoa kilio, sononeko kwa Serikali Zaeleza masaibu yaliyowakuta vijana wao Wayemen milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa MMOJA wa watoto wanaokabiliwa na njaa nchini Yemen. WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Simbachawene. EU kuiadhibu Israel Iwapo itatwaa ardhi ya Palestina Benjamin Netanyahu. Uk. 5

Upload: others

Post on 14-Nov-2021

11 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Tutembee kwenye Website  au …

ISSN 0856 - 3861 Na. 1432 DHULQAADAH 1441 , IJUMAA, JULAI 17-23, 2020 BEI TShs 1000/=, Kshs

Tutembee kwenye Website www.annuurpapers.co.tz au mpaper.co.tz tunapatikana pia katika simgazeti

NAMBA YA KITUO: P 5633

Mnatangaziwa nafasi za MASOMO kwa ajili ya kurudia mtihani wa kidato cha nne kuanzia tarehe 3 Februari – Septemba 2020.Gharama za masomo ni kama ifuatavyo:-

1. Ada ya masomo ni Tsh. 350,000/= 1. Ada ya bweni (HOSTEL) kwa kulipa kila mwezi ni Tsh 120,000/= na kwa kulipa kwa mkupuo wa miezi mitatu

mitatu ni Tsh 300,000/=.1. Ada ya mtihani wa taifa (NECTA) ni Tsh 50,000/= ikilipwa kipindi cha usajili wa kawaida kuanzia sasa na

kabla ya tarehe 29/02/2020. Ada ya Mtihani inalipwa kupitia POSTA.2. Ada ya kituo ni Tsh 50,000/=. Kituo kimesajiliwa na kupata namba P.5633.1. Ada kwa mitihani ya vitendo (practicals) Physics, Chemistry na Biology ni sh 50,000/= kwa somo.Fomu zinapatikana ofisi ya Mkuu wa Shule kwa shilngi 5,000/=.

Nafasi ni chache sana. Wahi kuchukua fomu mapemaWabillaah Tawfiiq

MKUU WA SHULE

NAFASI ZA MASOMO KWA AJILI YA KURUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE , 2020

(KUTWA NA BWENI)

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Tuhuma za ugaidi zazidi kuliza familia

Familia tatu zatoa kilio, sononeko kwa SerikaliZaeleza masaibu yaliyowakuta vijana wao

Wayemen milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa

MMOJA wa watoto wanaokabiliwa na njaa nchini Yemen.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Simbachawene.

EU kuiadhibu IsraelIwapo itatwaa ardhi ya Palestina

Benjamin Netanyahu. Uk. 5

Page 2: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR2 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Ujumbe wa Ijumaa/Habari

Na Bakari Mwakangwale

MTU kuwa na kauli (neno) nzuri kutoka katika kinywa chake ni kiashirio cha kuwa mtu mwema kwa mwenye kulisema au kulitamka, ndio maana

Uislamu ukapitisha kuwa ni sehemu ya Sadaka.Neno zuri, ni neno ambalo mtu akilitamka

hupendeza kwa watu au watu wanalipenda na kulifurahia na hapo ndipo neno zuri linaweza kuunganisha nyoyo za watu linaweza kumsogeza aliyembali, linaweza kuwa patisha waliogombana, lakini pia linaodoa hasadi katika vifua.

Miongoni mwa athari za neno zuri ni kusababisha mtu kupedwa na watu na kusikilizwa kwa makini kwa anayoyasema na hata kufanyiwa kazi maneno yake.

Neno zuri, linamsababisha mtu kufaulu siku ya Kiyama, kama ilivyo kuja kua mtu moja aliomba aambiwe kitu ambacho akikitenda basi kitapelekea yeye kuimgia peponi, Mtume (s.a.w) akamwambia adumu kusema maneno mazuri.

Neno zuri au maneno mazuri yawezekana kufuta maovu na kuamrisha mema na kuenea kheri katika jamii, mwenye maneno mazuri hukusanya ndugu jamaa marafiki, majirani na watu wote kwa ujumla kumpenda, mwenye maneno mazuri huwa na tabia nzuri, heshima, adabu kwa mwonekano wa jamii.

Sifa hii ya kuwa na neno au maneno mazuri zaidi anatakiwa aivae mlinganiaji watu katika kheri, ili Da’awa yake ifanikiwe.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur an, Suratul Ibrahim:24:

“Je, hukuona jinsi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri (ambao) mizizi yake ni imara na matawi yake yamenyoka juu.”

Allah (s.w) kapigia mfano wa neno zuri kama mti mzuri ambao mizizi yake huwa madhubuti na kama mizizi ikiwa madhubuti basi mti huwa imara matunda yatatoka mazuri na kila kitu chake kitakua kizuri kwa sababu asli ni nzuri.

Pia Allah (s.w) kamsifu mja wake kua asingekua na tabia nzuri maneno mazuri kwa watu kwa hakika Da’awa, isinge fanyika kwa sababu watu wange kua mbali na yeye, kwani angeshidwa kuwalingani.

Basi ni lazima pia sisi tufate mwenendo wa Mtume wetu ili tufanikiwe katika kuwalingani na tujizuie na kauli mbaya za ukali kwani hatutofanikiwa kabisi kuwavuta watu katika haki.

Kasema mtume (s a w) katika Khadithi: ‘Uogopeni moto hata kwa kokwa ya tende, na kama hamtoipata (hio kokwa ya tende), basi hata kwa neno zuri na neno zuri ni Sadaka na mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho (siku ya Kiyama) basi aseme kheri au anyamaze.

Allah (s.w) atujaalie tuwe na maneno mazuri kwa watu na atuepushe na maneno mabaya ili tuwe wema, wachamungu, wenye kuheshimika, wenye kupedwa na wenye kuridhiwa na watu duniani na akhera.

Neno zuri na jema ni Sadaka

Ujumbe wa Ijumaa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa

Chakula Duniani (WFP), limesema Wayemen wasiopungua milioni 10 wanakabiliwa na ubaha mkubwa wa chakula na hivyo wanahitaji misaada ya dharura ili kuzuia baa la njaa.

Katika taarifa Ijumaa iliyopita, WFP imesema linahitaji dola milioni 737 kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ili kukabiliana na baa la njaa linaloisumbua nchi hiyo ya Kiarabu.

Elisabeth Byrs, msemaji wa WFP amesema hayo katika mkutano uliofanyika mjini Geneva na kuongeza kuwa, mgogoro wa

Wayemen milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa

kibinadamu nchini humo upo katika hali ya kutisha.

Amesema dunia inapaswa kuchukua hatua za dharura haraka iwezekanavyo na kwamba, hatari ya njaa inaikabili zaidi ya asilimia 80 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo.

Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani wapiganaji waliotwaa serilai wa Houth na kumrejesha madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdrabbuh Mansour Hadi, aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kimetoa ripoti

na kutangaza kuwa, tangu muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen Machi 26, 2015 hadi sasa, watu 16, 672 wamepoteza maisha kutokana na vita hivyo na miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa kushirikiana na dola za Magharibi hasa Marekani na utawala wa Israel.Iqna

MTOTO anayekabiliwa na njaa Yemen.

Page 3: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR3 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Habari

Na Bakari Mwakangwale

TAASISI za kutetea haki za Binadamu zimetakiwa kujitokeza na

kutoa msukumo kwa Serikali izingatie haki kwa mahabusu wenye tuhuma za ugaidi watekelezewe haki zao za kisheria ili kesi zao zianze kusikilizwa.

Wito huo umetolewa na wawakilishi wa familia tatu ambao ndugu zao wapo mahabusu zaidi ya miaka miwili sasa kwa tuhuma za ugaidi katika Gereza la Lilungu Mkoani Mtwara, huku kesi yao ikitajwa kila baada ya wiki mbili na kurudishwa mahabusu, kwa maelezo kuwa upelelezi haujakamilika.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Julai 9, 2020, Magomeni Makuti Jijini Dar es Salaam, Bw. Tiba Moshi Athumani Kakoso, waliojitambulisha kwa majina ya Salum Omar Bumbo pamoja na Faizuna Juma Issa, alisema wanawakilisha kilio kutoka katika familia tatu.

Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari, alizitaja familia hizo kuwa ni familia ya Mzee Kakoso, familia ya Mzee Bumbo pamoja na familia ya Bw. Suleiman Mkaliaganda ya Mtwara, ambao kwa ujumla vijana wao walichukuliwa na watu walijitambulisha kuwa ni Usalama wa Taifa, katika mazingira tofauti.

“Tumewaita hapa kuelezea kilio, masikitiko na sononeko letu kutokana na masaibu ya wanafamilia wetu ambao ni Omar Salum Bumbo (51) Ustadh Ramadhan Moshi Kakoso (41) na Waziri Suleiman Mkaliaganda (33), wote hao wapo mahabusu katika gereza la Lilungu Mkoani Mtwara kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa.” Amesema Bw. Kakoso.

Kutokana na mwenendo wa kesi zote za ugaidi nchini, Bw. Kakosa, akazitaka Taasisi za kutetea haki za Binadamu, kuingilia kati na kuililia Serikali kukamilisiha upelelezi wa kesi hizo ili

kukamatwa kwa wawili hao zilipita wiki kadhaa bila ya kupatikana taarifa zozote za mahala walipo licha ya jitihada kubwa za familia, ndugu na marafiki kufuatilia katika vituo mbalimbali vya Polisi, Jijini Dar es Salaam, jambo lililoashiria kutokuwepo kwa nia njema kwa vyombo vya dola dhidi yao.

Alisema, baada ya siku nyingi kupita taarifa za ndugu zao hao ziliibukia Mkoani Mtwara, ambako waliunganishwa na Mwalimu Waziri Suleiman Mkaliaganda, aliye Mwalimu wa Sekondari hapo Mtwara Mjini, aliyekamatwa Oktoba 21, 2017, jirani na nyumbani kwake mtaa wa Kiyangu Mtwara mjini.

Alisema, wakati wao wanahangaika kuwatafuta Jijini Dar es Salaam, walipata taarifa kuwa walishitakiwa kimyakimya Mkoani Mtwara kwa makosa ya ugaidi Desemba 5, 2017.

Na kuanzia hapo, alisema Bw. Kakosa, kuwa ndugu zao hupelekwa Mahakama ya Wilaya ya Mtwara kila baada ya wiki mbili kwa ajili ya kutajwa kesi yao na kurudishwa Gerezani, kwa maelezo kuwa ushahidi haujakamilika.

zianze kusikilizwa.“Sisi wanafamilia wa

watuhumiwa hao watatu tunachukua fursa hii kupitia vyombo vyenu vya Habari, kupaza sauti zetu kuitaka Serikali ambayo imejipambanua kuwa inasimamia haki na kutetea wanyonge, isimamie haki kwa ndugu zetu pamoja na mahabusu wengine kama hao wanaoendelea kusota Mahabusu.”

“Watekelezewe haki zao kisheria ili kesi zao zisikilizwe kama ushahidi haujakamilika, basi wapatiwe dhamana na kama ushahidi haupo, waachiliwe huru kuliko kuendelea kuwashikilia hali inayatoa sura ya uonevu kwani uadilifu na haki huzaa furaha na utangamano, lakini dhulma na uonevu huzaa chuki na uadui.” Amesema Bw. Kakosa.

Alisema, ndugu zao walikamatwa kwa nyakati na mazingira tofauti, ambapo wawili walikamatwa Jijini Dar es Salaam, na mmoja Mjini Mtwara kisha kwa pamoja walishitakiwa kwa makosa ya ugaidi.

Akielezea mazingira ya kukamatwa kwa ndugu zao hao alisema, mashaibu yalianza kumfika Omari Salimu Bumbo, ambaye

ni fundi ujenzi na mkaazi wa Tandika Relini, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2017.

“Alinyakuliwa na kutekwa na wanaoaminika kuwa ni maafisa wa Usalama, baada ya kumpigia simu kwamba angetaka waonane ili kumpatia kazi ya ujenzi na alipofika eneo aliloahidiwa kukutana nae maeneo ya Tabata, alitekwa na kumsweka garini, na kutoweka nae kusiko julikana,” amesema Bw. Kakosa.

Alisema, siku tatu baada ya tukio la kutekwa Omar Bumbo, Oktoba 30, 2017, Ustadh Ramadhan Moshi Kakoso, ambae ni mwalimu wa dini ya Kiislamu na mfanyabiashara, alitiwa nguvuni akiwa nyumbani kwake Magomeni Makuti, Dar es Salaam, mbele ya familia yake na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa Usalama.

Katika tukio hilo, Ustadh Kakoso, na familia yake walitoa shinikizo la kuwataka watu hao kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambapo mbele ya Mwenyekiti, walitoa maelezo kuwa taarifa za Ust. Kakoso, zitapatikana katika kituo cha Polisi cha karibu yake.

Hata hivyo, alisema

Tuhuma za ugaidi zazidi kuliza familia

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Simbachawene.

Page 4: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR4 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

TAHARIRI

OKTOBA mwaka huu Watanzania wataelekea vituoni kuwachagua viongozi kwa miaka mitano ijayo.

Ni muhimu tukakumbushana kwamba Tanzania imepitia mifumo mitatu ya vyama vya siasa katika historia yake hadi sasa. Kabla na hata kipindi kifupi baada ya uhuru wa iliyokuwa Tanganyika hapo mwaka 1961 na Mapinduzi ya Januari 1964 visiwani Zanzibar, pande hizi mbili Zanzibar na Tanganyika ambazo zilikuja kuungana baadaye kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zilikuwa na mifumo ya vyama vingi vya kisiasa vilivyoshiriki kupigania uhuru kutoka kwa Muingereza.

Kwa hiyo kwa uzoefu tuliokuwa nao wa kushiriki katika uchaguzi mkuu zilizohusisha vyama vingi, hatudhani kama tunapaswa kuingia Oktoba 2020 tukiwa na hofu au shaka kuhusu kuwepo Uchaguzi Mkuu wenye heri, wa haki na uhuru kamili, katika mazingira ya amani na utulivu, Tanzania Bara na Tanzania visiwani.

Tunapaswa kujiandaa vizuri kufikia lengo hilo lenye maslahi makubwa kwa kila raia mwema.

Tunakumbuka siku za nyuma, kila unapofikia wakati wa uchaguzi, kada mbalimbali za Watanzania hujaribu kutoa yao ya moyoni kuelekea uchaguzi huo. Zilikuwepo asasi za kiraia ambazo wakati wa maandalizi ya uchaguzi, zilikuwa zikifanya semina mbalimbali na kuendesha elimu ya uraia kuhusiana na uchaguzi.

Maneno kama uhuru wa kushiriki, uwazi, haki za binadamu, mwafaka, utawala wa sheria, ukweli, utamaduni wa kuvumiliana, elimu ya mpiga kura, uadilifu, nafasi sawa nk. Yalitawala katika semina hizo. Alimradi kila asasi ikijitahidi kutoa elimu ili kuwashawishi watu wajitokeze, washiriki kupiga kura kwa maslahi na kwa mustakabali mzuri wa Taifa lao.

Lengo kubwa la asasi za kiraia na zisizo za kiserikali kutoa elimu ya uchaguzi, ni kuwafanya watu kushiriki uchaguzi wakiwa na ufahamu wa kutosha juu ya kwanini wanafanya uchaguzi, wanachagua kwa maslahi ya nani, waamchagua nani kwa maslahi ya umma.

Aidha tumezoea kuona katika chaguzi zilizopita, unapokaribia uchaguzi mkuu wanasiasa nao hutumia muda mwingi

kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi, kwa kupitia majukwaa ya kisiasa, vyombo vya habari nk hutoa hamasa kwa wananchi tangu kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Huhamasisha watu juu ya umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi. Lakini lengo kubwa kwao likiwa ni kuweka mazingira ya kupata kura zaidi kwa wagombea wa vyama vyao, na kushinda na hatimaye kutwaa madaraka, tofauti kidogo na malengo ya watu wa asasi za kiraia.

Lakini tumeshuhudia hata taasisi za kidini, nao wamekuwa wakitoa nyaraka mbalimbali za kuelekea uchaguzi mkuu, wakieleza shida zao, kero zao na wakati mwingine kutoa mwongozo, maoni na ushauri kwa waumini wao juu ya kushiriki uchaguzi.

Viongozi wa dini wamekuwa wakifanya hivyo,

ili kuwakumbusha wanasiasa kuwa wao wakiwa wanadini, nao wanaona kuna haja ya kuboreshwa mambo kadhaa yasiyokaa vizuri kiimani na jamii.

La muhimu kwa Watanzania wa leo ni sote tubakie ndugu. Udugu wetu ndio unatufanya tujione sisi sote ni binadamu sawa, wenye utu sawa, haki sawa na mahitaji ya msingi sawa.

Tumezoea utaratibu wa kuwapata viongozi wetu kwa kuchaguliwa na watu. Tuelekee kwenye uchaguzi mkuu wa nchi yetu, huku kukiwa na maridhiano baina ya watu au makundi ya watu katika jamii yetu.

Tuelekee katika uchaguzi tukiwa na fahamu kwamba ni vizuri watu wakaishi kwa upendo na umoja na kukabili matukio yoyote ndani ya Taifa letu kwa pamoja, tukijua sote ni wadau kamili wa hatma ya nchi yetu.

Tunahitaji Maridhiano kwa Amani ya nchi yetu

MWAKILISHI wa kudumu wa Misri

katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa viongozi wa baadhi ya nchi waache kupeleka majeshi mamluki katika maeneo ya machafuko, hasa wakati huu wa kuenea maambukizi ya kirusi cha corona.

Televisheni ya Rusia al Yaum imemnukuu Mohamed Edrees, akisema hayo katika kikao cha kufunga shughuli za Wiki ya Mawasiliano ya Intaneti kwa ajili ya kupambana na ugaidi zilizoendeshwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, wakati umefika kwa baadhi ya nchi kuacha vitendo vyao visivyo sahihi vya kupeleka mapiganaji wa kigeni katika maeneo ya machafuko, tena wakati huu ambao dunia

Misri yataka nchi za dunia kuacha kupeleka mamluki maeneo ya machafuko

nzima imekumbwa na ugonjwa wa COVID-19.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa aliongeza kuwa, maambukizi ya kirusi cha corona yanalifanya kuwa jambo la dharura kuongeza jitihada za kimataifa za kukabiliana na ugaidi wa aina zote kama vile ugaidi wa kibiolojia, ugaidi wa mawasiliano ya kompyuta na pia matamshi na

fikra za kibaguzi na misimamo mikali.

Aidha alisema mchakato wa kuchunguza mkakati wa kukabiliana na ugaidi kwa usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ambao umeahirishwa hadi mwakani ni fursa nzuri ya kutilia mkazo upya ahadi za kisiasa za nchi wanachama wa umoja huo, kwa ajili ya kukabiliana vilivyo na vitisho vya ugaidi kimataifa.Parstoday.

MWAKILISHI wa kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa, Mohamed Edrees.

Page 5: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR5 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Habari za Kimataifa

Umoja wa Ulaya (EU) umetahadharisha

kwamba, iwapo Israel itatekeleza uamuzi wake wa kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi, mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika umoja huo hawatafanya safari huko Israel.

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, utauadhibu utawala wa Kizayuni wa Israel kama utatekeleza uamuzi wa kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na maeneo mengine ya Palestina yaliyoghusubiwa na utawala huo.

Adhabu hiyo ni pamoja na kuwazuia mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ulaya kutembelea Israel, kutotumwa wanachuo wa Ulaya katika utawala huo na kufutwa shughuli za utafiti wa kisayansi katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).

Baadhi ya nchi za Ulaya pia zimetishia kuwa, iwapo Tel Aviv itatekeleza mpango huo zinafanya mabadiliko makubwa katika uhusiano wao na Israel.

Siku chache zilizopita Vatican pia iliwaita na kuwahoji mabalozi wa Marekani na Israel, ikipinga mpango wa Tel Aviv wa kutaka kutwaa na ardhi zaidi ya Palestina.

Utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umepanga kwamba Jumatano ya tarehe Mosi Julai, ungeanza kutekeleza mpango wake haramu wa kupora na kuunganisha asilimia 30 ya ardhi za Ukingo wa Magharibi na ardhi nyingine za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Hata hivyo umelazimika kuahirisha tarehe ya utekelezaji wa mpango huo, baada ya kushadidi mashinikizo ya upinzani ya Wapalestina na ya nchi mbalimbali duniani.

Mpango huo ni sehemu ya mapendekezo ya Rais Donald Trump wa Marekani, yaliyowekwa katika kile kinachodaiwa ni “Muamala wa Karne”. Parstoday.

Jeshi la Syria limetangaza kutekeleza oparesheni ambayo imesababisha

kukamatwa wanachama wa kundi la wapiganaji linafungamana na Marekani Mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan, Jeshi la Syria Jumanne wiki hii liliwanasa magaidi hao waliokuwa wakitoka katika kituo cha wanajeshi vamizi wa Marekani, katika eneo la Al Tanf Mashariki mwa Syria.

Magaidi hao walikamatwa karibu na mji wa Al Sakhna, katika mkoa wa Homs Mashariki mwa Syria.

EU kuiadhibu IsraelIwapo itatwaa ardhi ya Palestina

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Syria yakamata magaidi wanaofungamana na Marekani

Zindzi Mandela, mwana wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson

Mandela na Winnie Madikizela Mandela, amefariki dunia kwa mujibu wa shirika la habarila taifa hilo SABC.

Zindzi alifariki dunia jijini Johannesburg mapema Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 59.

Kifo chake kilichothibitishwa na chanzo kimoja cha familia, kilisema chombo cha habari cha SABC.

Zindzi alikuwa balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark na ameacha mume na watoto wanne.

Binti huyo wa Mandela alikuwa mwanarakati wa kisiasa na ni miongoni mwa wale waliopigana dhidi ya uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Alianza kuhudumu kama balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark mwaka 2015. Alikuwa mwana wa sita wa Nelson Mandela na wa pili kati yake na Winnie Madikizela Mandela.

Wakati alipokuwa na

Mtoto wa Mandela afariki dunia

umri wa mwaka mmoja na miezi sita, baba yake alifungwa jela. Mama yake pia alifungwa mara kwa mara wakati huo. Mwaka 1977 Madikizela Mandela, alipelekwa katika eneo la Brandfort, katika jimbo la Orange Free State na Zindzi aliandamana naye.

Baadaye alielekea nchini Swaziland na alipokamilisha shule ya upili, alijiungana na Chuo Kikuu cha Cape Town kwa shahada ya sheria.

Wakati baba yake,

Nelson Mandela, alipotoka jela mwaka 1990, mazungumzo yalianza kati ya chama cha ANC na utawala uliokuwepo kufutilia mbali mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Huku afya ya aliyekuwa rais wa ANC ikizorota , Mandela alichaguliwa kama Rais mpya wa Chama cha ANC na mgombea wa urais nchini Afrika Kusini katika uchaguzi wa mwaka 1994.Parstoday.

Zindzi Mandela.

Page 6: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR6 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Kalamu ya Ben

Na Ben Rijal

Inaendelea Uk. 9

HAKIKA yaliopo sasa duniani ni kulazimishana. Kuyataka ambayo

wengine hujiona wana nguvu za kiuchumi na kijeshi kuwalazimisha wengine kufwata matakwa yao hata yakiwa hayana mashiko kidini na kiutamaduni. Lakini wao hutaka wengine wayakubali na wanapoyakataa huwawekea vikwazo vya kiuchumi, kutotaka mashirikiano nao na hata kufikia nukta kukata mahusiano yote waliokuwa nayo na nchi ndogo ndogo ambazo zimekataa kufwata yaliokuwa ya kifirauni kutenda khasa khasa ya ubaradhuli na usagaji.

Nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu cha Aberdeen, Aberdeen University niliona ni fursa kubwa ya kukipata kitabu cha ‘’False Start in Africa na Rene Dumont’’ nilihangaika katika maduka ya vitabu wengine walifika kunambia hata kukisikia hicho kitabu hawajakisikia. Mmoja wa wauza duka akanambia kitabu hicho unaweza kukipata duka fulani liopo mtaa kadhaa. Nalifarajika siku hio baada ya masomo na kurudi kusali Adhuhuri nilifika katika duka hilo.

La ajabu nililoliona ni kuwa duka hilo lipo chini (basement) unapoingia unakaribishwa kuna wanaume waliovaa kiajabu na nyuso zao kuziremba na wanawake hivyo hivyo. Nikaaanza kujiuliza hapa ndipo nilipoelekezwa? Nikashikwa bega kwa kuulizwa kama nataka Chai au Kahawa? Nikasema laa sicho nilichokijia ila natafuta kitabu tu, wakanielekeza niteremke chini ambako ndipo penye

Mkitaka msitake, hatutaki

vitabu vikongwe (second-hand). Nilipoteremka chini ya jengo nikayaona ya ajabu, lakini langu lilikuwa ni mmoja tu, nalo kupata kitabu ‘’False Start in Africa’’.

Ajabu nilioikuta ni kuwa wanaume kwa wanaume wamekumbatiana na kupigana mabusu na kwa wanawake hayo hayo. Kisha nikajiwa na wanaume wawili na mwanamke mmoja kila mmoja ananiuliza, jee, nimekuja kujiunga na uanachama? Jee, napendelea yepi? Nikapewa kipeperushi kinachojieleza. Kukitupia jicho nakujua nimeingia pahala sipo nikasingizia saa za masomo zimefika nikimaliza masomo nitarudi tena.

Kitabu kikanitumbukia nyongo wala sijataka kujua zaidi ila nilikwenda kumuhadithia sahib yangu wa Ki-Malaysia ambaye na yeye yaliomkuta yaliomkuta ila yeye alikuwa Jabari alikaa kazungumza nao kisha akanunua vitabu alivyovitaka ambacho mathalan kitabu cha shillingi 20,000 unaweza kukipata kwa 5,000 akanifahamisha pale ni kwenye umoja wa wasagaji na mabaradhuli. Hukutana na kutambulishana

na kupigia tarumbeta, nitatumia neno hilo wala sio debe. Tarumbeta huvuma zaidi kuliko debe. Basi hapo ni pahala pa ufuska na kuna vyumba vya kufanyia huo ufuska.

Balaa hii imezagaa, kwenye Chuo hicho hicho ukiingia maktaba utakuta kuna gazeti la wiki linaitwa ‘’Pink’’ hilo linaelezea wenye amali hizo.

Leo dunia inadidimia kuingia katika dimbwi la kuhalalisha watu wenye amali hizo yaani za kufanya mapenzi ya jinsia mmoja na kutolewa msisitizo mkubwa kuwa zile nchi zisotaka kukubali hayo hawatopewa misaada.

Sasa kuna msamiati ambao ndio kiini cha makala haya nao ni: LGBT kirefu chake ni L’’ ikiwa Lesbian’’ hao ni Wasagaji, ‘’G’’ ni ‘’Gay’’ hao ni Mabaradhuli, ‘’B ’’ ni ‘’Bisexual’’ ni Mchicha mwiba yeye ni huwa Jabari na yeye hushughulikiwa na ‘’T’’ ni ‘’Transgender’’ ikiwa ni Khuntha, leo kumekuja kuwa haki watu hawa wa LGBT zitimizwe. Labda kwa Kiswahili niiweke kwa ufupisho huu MBMCK kwa maana Msagaji, Baradhuli, Mchicha mwiba Khuntha.

Kabla sijaenda kwa undani kabisa tuangalie

aya za Qur’an kwanza kisha ndio tuje na LGBT/MBMCK.

‘’Na tulimtuma Lut’, alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!’’ (Suurat Al-A’raaf 7:80)

Maelezo: ‘’Na hakika tulimtuma Nabii wa Mwenyezi Mungu, Lut’, kwa kaumu yake; awaite wafuate Tawhidi, yaani ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja. Na awazindue juu ya waajibu wa kuachana na makosa maovu kabisa waliyo kuwa wakiyafanya. Aliwaambia: Nyinyi mnakwenda kufanya jambo liliopita mpaka kwa ubaya wake, kinyume na maumbile? Mmezua uchafu huo ambao unapingana na khulka, na ambao hapana watu walio kutangulieni waliofanya hayo!’’

Aya zinaendelea kuelezea: ‘’Hivyo nyinyi

mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji!’’ (Suurat Al-A’raaf 7:81).

Maelezo: ‘’Na jambo hilo ni kuwa mnawaendea wanaume kwa kuwatamani, na mnawawacha wanawake! Nyinyi kwa jambo hili inakuwa mnafanya fujo, na mmetoka nje ya maumbile, na mmefanya kitendo asichofanya hata mnyama.’’

‘’Na haikuwa jawabu ya kaumu yake isipokuwa kuambizana: Wafukuzeni katika mji wenu, maana hao ni watu wanao jitakasa.’’ (Suurat Al-A’raaf 7:82).

Maelezo: Na haikuwa jawabu ya watu wake kwa kukatazwa hichi kitendo kiovu kisicho kuwa na mfano, ila ni kusema: Watoeni Lut’ na jamaa zake na wafuasi wake katika mji wenu! Nayo ni kwa kuwa wao wanajitahirisha na wanajitenga na hichi kitendo ambacho akili na maumbile yanakiona ni kibaya, na wao hao watu wanakioni kizuri! Hii ni kaumu ya Mtume Lut.

Aya zinaendelea kufafanua na kututaka sisi Waislamu ukiwa uma bora kufahamu na kuelewa juu ya haya machafu.

MABARADHULI wakiwa wamefunga ndoa ya jinsia moja.

Page 7: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR7 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 SHAJARA YA MWANAMZIZIMA

Inaendelea Uk. 8

Kumbukizi ya Shaaban Robert: Mwanafalsafa aliyetetea utu wa mtuNa Alhaji Abdallah

Tambaza

MAKALA hii, ni tabaruku kwa kumbukizi ya miaka 58 tangu alipofariki

mwandishi, mwanafalsafa na mshairi mashuhuri wa Afrika Mashariki, hayati Shaaban Robert. Yeye alikuwa mwandishi wa kwanza wa Tanganyika katika enzi za kikoloni kuandika kwa Kiswahili cha kisasa, sifa ambayo imemfanya aitwe “Baba wa Lugha ya Kiswahili”.

Aliweka wakfu kipaji chake cha kipekee katika kupigania heshima ya Mwafrika, kwa ajili ya utu huru katika jamii huru, ambayo inaheshimu na inalinda usawa wa watu wote— wanaume na wanawake. Katika kazi zake, aliainisha dhana yake binafsi ya uelimishaji kwa kuwafanya mashujaa wake kuwa ndio mfano chanya wa mtu mpya.

Mwelekeo wa kifalsafa- kivielelezo wa riwaya za Shaaban Robert, umekuwa na ushawishi mkubwa kwa Watanzania waandishi wa nadhari.

Jina la Shaaban Robert (1909-1962), linaambatanishwa na sifa nyingi - mtu maarufu, mashuhuri, adimu, muasisi, mtafakari, msomi, mtaalamu, mwanzilishi, mwelimishaji, baba wa lugha ya Kiswahili ...

Na huo ni ukweli kwa msanii mkubwa huyu, aliyeweka wakfu kipaji chake binafsi na cha kipekee; pamoja na kazi zake za ubunifu katika “kutumikia watu na katika mapambano endelevu dhidi ya ujinga” na pia kupigania heshima ya Mwafrika na uhuru wa mtu katika jamii huru.

Shaaban bin Robert, anayejulikana zaidi kama Shaaban Robert, alizaliwa mnamo Januari 1, 1909, katika kijiji kidogo cha Vibambani, Kusini mwa mji wa bandari wa Tanga, Tanganyika; ambayo wakati huo ilikuwa sehemu ya Koloni la Ujerumani la Afrika Mashariki.

Jina lake ni matokeo ya muunganiko wa mila mbili za kutoa majina: ya Kiislamu - Shaaban na ya Kikristo - Robert.

Robert ni jina la Mzungu, ambaye alikuwa anamiliki mashamba ambamo babu yake Shaaban alikuwa anafanya kazi; na wakati alipozaliwa baba wa Shaaban, yule Mzungu alipendekeza kwamba mtoto apewe jina lake.

Baadaye, jina hili la Robert likawa jina la ukoo. Aidha, jina la muunganiko huu baadaye zaidi lilikuja kuwa udhihirisho wa mtazamo wa kuchukuliana na pia heshima ya mwandishi huyu katika masuala ya dini.

Waswahili, kwa taratibu za mila zao, hutambulisha uhusiano wao wa kifamilia kwa kuegemea upande wa mama. Mama yake Shaaban Robert, aliwahi kuwa na ndoa tatu; na Shaaban alikuwa mtoto wa pekee katika ndoa yake ya pili. Kwa upande wa mama,

Makala hii ya kumbukizi ya miaka 58 tokea kifo cha Shaaban Robert, imetayarishwa na Dr. Nelly Gromova, Daktari wa Falsafa ya Sayansi za Lugha, Profesa, Mkuu wa Idara ya Afrika katikaTaasisi ya Nchi za Asia na Afrika, Chuo Kikuu cha Moscow, Urusi, ([email protected]) na imetafsiriwa kwa Kiswahili na Kituo cha Utamaduni wa Urusi na Tanzania, Barabara ya Sea View, Dar es Salaam. ([email protected]).

Kutokana na maombi maalumu, na kwa kuzingatia kwamba hayati Shaaban Robert, alilelewa na babu yake hapa Mzizima alikopata elimu yake katika Shule ya ‘Kitchwele African Boys Middle School’, imeonekana ni vyema ikawa sehemu ya historia hii ya Mzizima pia, kwani alishiriki kwenye harakati kadhaa za kupigania haki za wanyonge hapa nchini akisaidia kuasisi African Association (AA). Sasa endelea…….

alikuwa na kaka na dada wa kambo 13, ambao alikuwa karibu nao zaidi kuliko na ndugu zake wa upande wa baba.

Aliwatunza ndugu zake, akiwasaidia kifedha na alimlipia mmoja wa wadogo zake ada ya masomo, gharama za usafiri, nk. Shaaban mwenyewe, pia aliwahi kuwa na ndoa tatu ambazo kwazo alikuwa na watoto sita.

Mnamo mwaka 1922, baada ya kifo cha baba yake (wakati huu sasa Tanganyika ikiwa ni koloni la Uingereza), Shaaban Robert, alipelekwa kwa babu yake jijini Dar es Salaam, ambako alijiunga na shule ya msingi na akahitimu mwaka 1926, akiwa amefaulu vizuri mtihani wa Kiingereza. Alishika nafasi ya pili katika mtihani huo na akapewa cheti cha kumaliza shule. Kwa utaratibu wa kikoloni uliokuwepo nchini Tanganyika, cheti hicho cha shule kilitosha kumpatia haki ya kuajiriwa katika taasisi za utawala wa kikoloni wa Uingereza, na hivyo akawa mtumishi wa serikali Mwafrika katika makoloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki.

Shaaban Robert, alitambua mapungufu ya elimu ya msingi, na kwa hiyo aliamua kusoma

kwa njia ya posta, Uingereza na Afrika Kusini; akisoma kwa bidii vitabu muhimu vya elimu na vya sanaa.

Maisha yote ya Shaaban Robert, yalipita katika mazingira ya jamii ya ukoloni, ambamo maisha asilia ya Mwafrika yalikuwa yametengemana na utumwa wa kikoloni, ila nyakati zikawa zinaleta marekebisho yake zenyewe. Intelejensia ya Kiafrika ilikuwa inaibuka, na Shaaban Robert akiwa ishara ya kuchipuka kwa “kizazi hiki kipya”.

Akiwa amelelewa katika misingi ya maadili ya Kiswahili, ya kuwa na adabu na kuheshimu wazee, alifanya kazi zake kwa umakini na uangalifu, akitumika katika nafasi mbalimbali kama mtumishi wa serikali ya kikoloni. Kwa miaka 18, alifanya kazi katika Ofisi ya Forodha ya mji wa Bandari wa Pangani; kisha katika Idara ya Tiba ya Mifugo; baadaye katika Idara ya Usimamizi wa Ardhi na katika Serikali ya Mtaa ya Mji wa Tanga. Katika miaka 34 ya utumishi wake, alifanya kazi, siyo huko Pangani tu, bali pia katika miji ya Moshi, Arusha, Dar es Salaam, n.k.

Mnamo mwaka 1930, alianza kazi yake ya fasihi, kwa

machapisho katika jarida la kila mwezi la “Mambo Leo” (lililoanzishwa mwaka 1923). Tayari katika machapisho yake madogo madogo, aliainisha dhana yake mwenyewe ya uelimishaji. Mathalan, alitoa wito wa kuwaheshimu wanawake na pia kuheshimu taasisi ya ndoa na familia; huku akisisitiza umuhimu wa elimu kwa wote, ikiwa ni pamoja na wanawake. Alikosoa kasumba kama vile ya kuvaa hirizi, n.k.

Katika makala ya “Jogoo la shamba haliwiki mjini “ (sawa na methali ya Kirusi isemayo “Ni bora kuwa mvulana shupavu kijijini kuliko kuwa zuzu mjini)”, alitaja sifa tano ambazo Mswahili halisi anapaswa kuwa nazo: ushirikiano, umoja, uadilifu, uaminifu na uvumilivu. Kama kila mtu atakuwa na sifa hizi, basi kwa mujibu wa Shaaban Robert, jamii yote itakuwa yenye haki sawa.

Katika mashindano ya kazi za fasihi, alishinda tuzo yake ya kwanza - vitabu viwili vyenye thamani ya shilingi 5 kila kimoja.

Baadaye aliendelea kupata tuzo nyingi: alipata Tuzo ya “Margaret Wrong Memorial Prize” na Nishani ya kutambua mchango wake katika fasihi ya Kiafrika, “Order of the British Empire – M.B.E.” na Serikali ya Uingereza, pamoja na Hadhi ya “Mwandishi Bora” kutoka Wizara ya Utamaduni, n.k.

Kuanzia katikati ya miaka ya 1940, riwaya zake pamoja na machapisho madogomadogo, zilianza kuchapishwa kwa mtiririko.

Mnamo mwaka 1936, Shaaban Robert aliandika rasimu ya historia ya maisha yake “Maisha Yangu”, ambayo ilishinda nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya waandishi-chipukizi wa Afrika Mashariki; lakini rasimu hiyo ya maandishi ya kwanza ikapotea.

Aliikamilisha kazi hii ya fasihi mwaka 1946 (na ikachapishwa mwaka 1949). Baadaye, katika miaka ya 1959-1960, aliandika mwendelezo wa riwaya hiyo ya maisha “Baada ya Miaka Hamsini”, iliyochapishwa mwaka 1966. Nyuma ya simulizi ya kina juu ya maisha yake na kazi zake, kuna uchungu uliofichika ndani ya mtu ambaye, ingawa ana hadhi ya upendeleo, akilinganishwa na Waafrika wengine wasio na elimu; lakini hapo haponi raia wa “tabaka la chini”, ambaye angeweza kuhamishiwa mahali pengine pa kazi bila ridhaa yake, ambaye angeweza kutolewa nje ya gari la abiria, ili tu kupisha viti kwa ajili ya Waasia waliofika kituoni kwa kuchelewa; tena mtu ambaye ilikuwa vigumu kwake kupata nafasi katika shule ya msingi kwa ajili ya binti yake, na kadhalika.

Nyuma ya mpangilio wa maelezo mepesi juu ya matukio ya maisha ya Mwafrika mtumishi wa serikali wakati wa ukoloni, unahisiwa upinzani alionao mwandishi dhidi ya uonevu na ubaguzi wa aina zote.

MAREHEMU Shaaban Robert

Page 8: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR8 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 SHAJARA YA MWANAMZIZIMA

Inatoka Uk. 7

Inaendelea Uk. 13

Kumbukizi ya Shaaban Robert: Mwanafalsafa aliyetetea utu wa mtuMwaka 1946, ulikuwa ndio

wa mafanikio mengi katika kazi za Shaaban Robert. Alianza kuandika riwaya za kifalsafa, kama yeye mwenyewe alivyoziita, “za hadithi za kisasa.” Riwaya zake ni tungo za kipekee ambazo zinatumia sura na maudhui ya sanaa za asili ya watu wa Nchi za Mashariki (Asia). Hizi ni – utatu: “Kufikirika” (nchi ya kubuniwa, 1946), “Kusadikika” (nchi ya kuaminika muamana, 1948) na “Adili na Nduguze”

(1951).Matukio hayo, yanajiri

katika nchi za kubuni ambako, “malaika na majini wanakutana ili tu kubainisha juu ya jambo moja muhimu.” Na jambo muhimu hilo, kwa mujibu wa Shaaban Robert, ni jamii bora yenye usawa, ambamo kila mtu anafanya juhudi ya kujiboresha na kuwa mwema, na kwamba sifa hizi ndizo zitakazouokoa ulimwengu kutoka kwenye balaa la chuki, wivu na ukatili. Mwandishi anahubiri juu ya maadili mema kwa wanadamu wote na kulaani maovu.

Katika hadithi hizi anaelezea maoni yake juu ya aina bora ya jamii na muundo mzuri wa serikali, ambayo inawezekana kuwapo endapo kutakuwa na mtawala mwerevu na mwadilifu, kama ilivyotokea katika nchi ya muamana na inayoning’inia (hewani) - “Kusadikika”.

Mtawala mwenye busara wa nchi ya “Kufikirika”, anaelewa hitaji la kusonga mbele huku akihifadhi mila muhimu na kuiga mpya zilizo njema. Lakini raia wenyewe pia wanapaswa kuwa na roho adilifu, wenye subira na wapenda haki, kama mhusika mkuu katika riwaya ya “Adili na Nduguze” alivyo. Kuweni kama Adili alivyo, na msingi huu mzuri utaondoa mabaya yote katika maisha,”- mwandishi anatoa wito.

Katika riwaya ya “Utubora Mkulima”, iliyoandikwa mnamo miaka ya 1946-1947 (na kuchapishwa mwaka 1968), Shaaban Robert, anasimulia juu ya mapenzi kati ya vijana wawili ambao wanavuka vizuizi vingi vya mila za jamii ya Kiswahili - msichana kutoka familia tajiri anaolewa na kijana mkulima masikini lakini mwadilifu.

Toleo hili ni tofauti na “hadithi za vichimbakazi”, kwa sababu, hapa mwandishi anamtambulisha mhusika katika hali halisi ilivyo.

Utubora, kwa mujibu wa mwandishi, ni mtu anayefanya kazi kwa bidii, ni mtu huru na mwadilifu anayeishi kwa jasho lake.

Kwa hakika, watu kama hao ndio watakaotengeneza “uti wa mgongo” wa jamii bora ya baadaye,- ndivyo mwandishi anavyodhani.

Majina mengi ya wahusika wa riwaya za Shaaban Robert, yana maana maalumu: Utubora ni neno gumu ambalo “utu” ni “sifa za ubinadamu, asili ya binadamu, ubinadamu”; “bora” ni “nzuri

sana, njema”; kwa mfano “mtu mwenye maadili mema”.

Jina la mhusika wa riwaya ya “Kufikirika”, nalo limejengwa katika misingi hiyo hiyo: “Utubusara” (utu + busara = “hekima, maarifa”); mfano “mtu mwenye hekima na maarifa.

“Karama”- jina la muhusika wa hadithi ya “Kusadikika”, linamaanisha “Zawadi kutoka kwa Mungu, ruzuku, talanta”, Adili - mwadilifu, mkweli, mwenye heshima”.

Hata majina yenyewe aliyobuni mwandishi kwa ajili ya wahusika wa riwaya zake ni ushahidi wa falsafa yake ya utu bora na imani yake ya ki-utopia juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwenye busara, asiye na mawaa na ambaye hawezi kutishwa na majaribu yoyote maishani.

Mawazo ya kupenda-utu ya Shaaban Robert, yalishabihiana na malengo ya Chama cha Waafrika Tanganyika (“Tanganyika Africans’ Association”), ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 1929, na ambacho yeye alikuwa mwanachama wake.

Katika barua zake kwa mdogo wake-wa kambo anaandika, kwamba angetamani pia kuwa mwanachama wa “Chama cha Ushirika wa Wakulima Handeni”.

Haiwezi kunukuliwa hapa, kwamba alikuwa mwanasiasa hai, lakini alikuwa na hisia za kuunga mkono harakati za wazalendo katika kupigania haki zao na heshima yao; na kwa kauli yake, hakujiona kuwa na haki ya kukaa kando na kuwa mtazamaji tu wakati wengine wakiwa tayari wanajihusisha kikamilifu katika siasa”.

Ushiriki wake katika harakati za ukombozi, ulikuwa ni kwa kupitia kazi zake za fasihi na insha zake ambazo wahusika wa riwaya zake wanaonyesha mfano wa mtu aliyemo katika jamii mpya iliyo na usawa kwa watu wote, wanaume kwa wanawake.

Hivyo basi, mnamo mwaka 1958 aliandika hadithi fupi, “Wasifu wa Siti binti Saad, Mwimbaji wa Zanzibar”.

Kwa talanta yake na msimamo wa king’ang’anizi, msichana kutoka katika familia masikini, kinyume na mila na taratibu za jamii ya Kiislamu, aliweza kupata umaarufu; sio tu katika Afrika Mashariki, bali pia hata mbali ya mipaka yake.

Kama ilivyokuwa katika mwanzo wa kazi ya uandishi wake, Shaaban Robert anatetea usawa wa kijinsia, anasisitiza nafasi ya wanawake; sio tu katika familia, bali pia katika jamii; na anawahimiza wanawake wa Kiafrika wasivumilie manyanyaso na kwamba walenge katika kubadilisha hatma yao kuwa bora.

Mnamo miaka ya 1960-1961, wakati Tanganyika ikiwa imekwishapata uhuru (09/12/1961), mwandishi alitunga riwaya yake ya mwisho “Siku ya Watenzi Wote” (Siku ya Wafanyakazi Wote).

Shaaban Robert aliupokea kwa furaha uhuru wa nchi yake na akatunga shairi maalumu – “Istakhali ya Tanganyika (lenye maudhui ya Uhuru” katika kuenzi tukio hili lisilosahaulika.

Shairi hilo lilichapishwa katika gazeti kuu la Urusi “Pravda” tarehe 28 Januari, 1963 –

“Katika vitu vizuri hapana kama uhuru,

Ni neno lenye fahari: daraka la kuamuru,

Uhuru huja na ari, na uthabiti na nuru,

Huja na matumaini uhuru kwa kila mtu,

Uhuru sawa na Dini kwa utukufu wa watu,

Na furaha ya moyoni katika maisha yetu.

Sawasawa na laana, utumwa na upotee,

Kwenye malindi ya vina uzame usirejee

Ni jambo dhaifu sana, na uhuru uenee!.”

Katika riwaya ya “Siku ya Watenzi Wote”, mwandishi anajaribu kujibu maswali juu ya jinsi ya kuishi katika nchi huru chini ya uongozi wa Waafrika wenyewe, kanuni na misingi ipi ya kiitikadi na kiroho zinapasa kufuatwa katika kuunda jamii mpya.

Mwandishi anamuonyesha mhusika mkuu wa riwaya hiyo - Ayubu, mwakilishi wa kizazi kipya, kama mfanyakazi mwaminifu na kiongozi aliyeelimika, ambaye, chini ya uongozi wake, jamii ya wafanyikazi itakuwa huru bila ya mawaa; kama vile kukosa haki-sawa, udhalimu, umasikini, ujinga, ubaguzi; na ambamo kila mtu atafanya kazi kwa manufaa ya wote.

Mwandishi anahubiri juu ya imani mpya iliyo na misingi katika muunganiko wa maadili

ya Kiislamu na Kikristo, pamoja na ukombozi wa mwanadamu kutokana na hali duni.

Riwaya hii ya “kiutopia”, imeainisha fikra za kimaadili na za kiupenda-utu za Shaaban Robert, ambazo kwa kiasi fulani, zimeshabihiana na dhana ya “Ujamaa”-itikadi ambayo muasisi wake alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania huru, Mwl. J.K. Nyerere, ambaye siku zote alikuwa anasifia sana kazi za mwandishi huyu.

Shaaban Robert, alikuwa pia mshairi maarufu. Sambamba na riwaya zake za kwanza kwenye jarida la “Mambo Leo”, pia alichapisha mashairi, na shairi lililomletea umaarufu mkubwa zaidi ni “Utenzi wa Vita vya Uhuru”, ambalo lilichapishwa katika jarida lilo hilo karibu katika kila toleo, tangu mwaka 1942 hadi 1945.

Mshairi huyu hakuweza kujizuia kuainisha msimamo wake juu ya tukio baya lililokuwa linaathiri si Ulaya tu - Vita Kuu ya Pili ya Dunia: “Pale, ambapo mwaka 1939, Hitler (ambaye Shaaban Robert anamwita “mbwa mwitu”) alipoanzisha vita.

Ushairi wenyewe ulinilazimisha kuinuka dhidi ya matukio hayo, na sikuweza kujizuia kufanya hivyo ... nilihisi kuwa nisingeweza kukaa bila kujali— bubu na kimya— wakati vita ikiingia katika mawazo na hisia za kila mtu hapa duniani. Furaha ya watu ilikwishakuwa furaha yangu, huzuni ya watu - huzuni yangu; Ilinibidi nifanye lolote, kwa njia yoyote iliyo katika uwezo wangu, ili nihusike katika kile kilichokuwa kinatokea.

MAREHEMU Shaaban Robert.

Page 9: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR9 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Kalamu ya Ben

Inatoka Uk. 6 Mkitaka msitake, hatutaki‘’Basi tukamwokoa yeye na watu wake, isipokuwa mkewe, alikuwa miongoni mwa waliobakia nyuma.’’ (Suurat Al-A’raaf 7:83).

Maelezo: ‘’Amri ya kuadhibiwa ilikwisha thibiti. Basi Sisi tukamwokoa Lut’ na watu wake, isipo kuwa mkewe, kwani yeye alikuwa katika hao walio potea.’’

Wake wa Mitume wawili walikhalifu amri za Mitume wakiwa waume zao nao ni mke wa Mtume Nuh na Lut. Nini kilichowatokea umma huo uliogubikwa na Liwat?

‘’Na tukawamiminia mvua. Basi tazama jinsi ulivyo kuwa mwisho wa wakosefu.’’ ’’ (Suurat Al-A’raaf 7:84)

Maelezo: ‘’Basi tuliwateremshia mvua ya mawe ya kuteketeza, na ardhi ikatandazwa kwa mitetemeko ya chini yao! Basi ewe Nabii! Angalia vipi ulikuwa mwisho wa wakosefu.’’

Hali hii ya kufanya mapenzi ya wanaume kwa wanaume ina maradhi makubwa na huleta aidha dhara kubwa kwa jamii katika kupoteza nguvu kazi na inafaa kukemewa kwa kila njia. Huu huwa zaidi ya uraibu. Tuzisoma aya zinavyofahamisha watu wa Mtume Lut walivyokuwa. Madhambi ya umma mbalimbali yote yamo sasa kwenye umma wa Mtume Muhammad SAW. Inataka tujihadhari kwani umma mbalimbali ziliadhibiwa kwa yale makosa yao tu, sisi tumeyakusanya yote.

‘’Na wajumbe wetu walipokuja kwa Lut’ aliwahuzunukia na akawaonea dhiki. Akasema: Hii leo ni siku ngumu!’’ (Surat Hud 11:77)

Ujumbe ukawafikia watu hao. Maelezo: ‘’Walipokuja wajumbe wetu, hao Malaika, kwa Lut’ kwa sura ya vijana wazuri, Lut’ aliungulika na akaudhika. Alihisi unyonge hana nguvu za kuwahami na hao watu wake, akawaonea dhiki kwa kuwaogopea ufisadi wa kaumu yake! Akasema: Hii leo ni siku ya karaha kubwa na machungu!’’ Mtume Lut ugeni uliomjia hakuwa na furaha kuona kuwa ataingia taabuni na hao waliozama na vitendo hivyo vya kiharamia ndio akatoa kauli hio.

‘’Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya

haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka?’’ (Surat Hud 11:78)

Maelezo: ‘’Watu wake wakajua kuwa wamekuja wale wageni, wakamwendea mbio mbio. Na kabla ya hayo ilikuwa kazi yao kufanya huo uchafu wao na kutenda maovu! Lut’ akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, waoeni. Hao ni safi zaidi kwenu kuliko kwenda kufanya uchafu kwa wanaume! Mwogopeni Mwenyezi Mungu, na jilindeni nafsi zenu na adhabu yake; na msinifedhehi na mkanidharaulisha kwa kuwavamia wageni wangu! Basi hivyo hamna kati yenu hata mtu mmoja mwenye rai iliyo sawa, mwenye akili iliyo ongoka, akakuzuieni na maasi na akakukatazeni maovu?’’

‘’Wakasema: Bila shaka umekwishajua hatuna haki juu ya binti zako, na unayajua tunayo yataka.’’ (Surat Hud 11:79)

Maelezo: ‘’Wakasema:

Wajua vyema ewe Lut’, kuwa sisi hatuna haki ya kuwaoa binti zako, wala hatuwataki. Na wewe hapana shaka unajua tukitakacho tulipo kujia kwa haraka.’’

Maradhi yalokuwa yashawavaa kwa hio hawakutaka lolote lile, ila wawapate wageni wa Mtume Lut wafanye Liwat.

‘’Akasema: Laiti ningelikuwa na nguvu kwenu, au nategemea kwenye nguzo yenye nguvu! ‘’(Surat Hud 11:80)

Maelezo: ‘’ Lut’ akasema: Laiti ningeli kuwa nina nguvu au nina nguzo yenye nguvu ya kutegemea, msimamo wangu juu yenu ungelikuwa mwengine, na ningeliweza kuwalinda wageni wangu nikakuzueni msiwafanye mambo mabaya.’’

‘’(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut’! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Na wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipo kuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakao wafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu?’’ (Surat Hud 11:81)

Maelezo: ‘’Malaika wale wakamwambia, na wao ukweli wao ulikwisha dhihiri: Ewe Lut’! Usikhofu wala usihuzunike! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi, wala si binaadamu kama tuonekanavyo kwako na kwa hawa kaumu yako. Wala wao hawa hawatakufikishia shari yoyote ya kukuudhi au kukudhuru. Basi toka wewe na ahali zako usiku ukisha zagaa. Mtoke mji huu, wala yeyote katika nyinyi asigeuke kutazama nyuma, asije akaona vitisho vya adhabu naye akasibiwa na shari yake! Lakini mkeo ambaye amekukhuni, yeye hatokuwa pamoja na watao toka nawe. Yeye lazima yampate yatao wapata hawa watu. Na miadi ya kuangamia kwao ni asubuhi, na miadi hiyo ni karibu. Basi usitie khofu.’’

‘’Basi ilipofika amri yetu tuliigeuza nchi juu chini, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu ulio kamatana wa Motoni,’’ (Surat Hud 118:2)

Maelezo: ‘’Ulipofika wakati wa adhabu tuliyo ikadiria na tukaitolea hukumu, tuliupindua mji ule waliokuwa wakiishi ndani kaumu Lut’ juu chini. Na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo ulio okwa Motoni hata ukawa changarawe! zilizo tiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo.’’ (Surat Hud 11:83)

Maelezo: ‘’Wakawa wanaangukiwa na hayo mawe mfululizo kuwa ni adhabu inayotoka kwa Mola wako Mlezi, ewe Nabii! Na hayo si mbali kumfikilia kila mwenye kudhulumu katika kaumu yako.’’

Msomaji twende khatua kwa khatua. Tuwe pamoja katika kusema laa juu ya LGBT/MBMCK. Kwa hio tuwe pamoja wiki ijayo.

Page 10: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR10 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Kalamu ya Ben

UISLAMU umeweka wazi mengi ambayo sayansi hivi

sasa ndio wamekuja kuyaweka wazi. Na kwa hio mara zote tunasema kuwa Qur’an haipingani na uvumbuzi wa mwanadamu ila mwanadamu anajionyesha kibri kupingana na Qur’an. Aya nyingi katika Qur’an zimeweka wazi namna ardhi na mbingu zilivyoumbwa na kuja na hoja nzito ambazo hoja hizo zinasomwa ndani ya Qur’an miaka 1441 iliopita na kuendelea kusomwa hadi hio siku litapopigwa Parapanda na kuwa ndio mwisho wa maisha duniani.

Tunapozichambua mbingu tunaona mwanadamu kama miaka 200 iliopita hakuwa na maelezo yalio wazi juu ya mbingu, ikiwa Qur’an inatueleza kupita karne 14 ziliopita:

‘’Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.’’ (Sura Adh-Dhaariyaat 51:47.)

Allah anaelezea sisi Allah hana mshirika lakini katika lugha haya yanafahamika na siku za mbele tutafahamisha ikiwa ni mamoja lakini unaandika au unasema kwa kutumia wingi.

Maelezo: Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa’la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua

Hii ndio Qur’anNa Ben Rijal

katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika.

Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe.

Qur’an imetufahamisha kitu kilichokuja kueleweka kama karne chache zilizopita kuwa juwa ndio lenye nuru walakini

mwezi unapata nuru kutokana na juwa:

‘’Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng’ara.” ( 25:61).

Allah ndio aliojaalia hayo ya nuru ya juwa hakuna anayoweza kuizuia nuru ya juwa isitoke na Allah katika kutokea kimya ndio yeye atakayebadilisha mkondo wa hali ya kila siku na kulifanya jua litoke upande wa Magharibi, hali hio ikitokea ndio kusema sayari zitajigonga na nidhamu yote ya maisha itapukutika na ndipo maisha mengine ya waja kuja kulipwa. Sayansi ilipofika haithubutu wala haitothubutu kuligeuza juwa na kulileta katika nidhamu ya ubinadamu.

Usiku na mchana haupo kibahati nasibu kwani ni Allah ndio aliojaalia na kufanya uwiyano wa maisha kuweza kupatikana na kuweza kupata chakula chetu wanadamu kutokana na miti na kuujalia usiku kuwa ni mapumziko. Mwanadamu hatoweza kuugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku, ila anaweza akajipumbaza akalala mchana na usiku kufanya kazi, lakini

nidhamu alioiweka Allah itakuwepo pale pale.

‘’Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili.” (Sura Al I’mran 3:190)

‘’Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanaojua.“ (Sura Yunus 10:5)

Katika aya hii tunaona kuwa mwezi una vituo kuanza unaoozaliwa unapopotea na kurudia kuonekana na sayansi ya kujua haya Allah amemfunulia mwanadamu ila Muislamu mara nyingi anajizonga katika kuandama kwa mwezi na kuiondosha nidhamu alioiweka Allah na kuja na maelezo yake yasiokuwa na mashiko. Huko mbele nitakuja kuvielezea vyuo 5 na mwezi wa muandamo na hoja za kila mmoja.

‘’Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mungu’’ (Sura Yunus 10:6).

Kuna kuelewa huu mchana na kuna kuelewa usiku. Kuna viumbe mchana vinakuwa kwenye harakati usiku hulala (Diurnal) na kuna viumbe usiku ndio huwa kwenye harakati, ila idadi ya wenye kuwa kwenye harakati mchana ni kubwa kuliko wanaokuwa kwenye harakati usiku.

Wanataaluma wanatufahamisha hii nidhamu ya mwanadamu kuwa mchangamfu mchana anapobadilisha na kuwa usiku ndio anaingia kazini wengi waliofanya hivyo katika

Inaendelea Uk. 11

Page 11: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR11 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Kalamu ya Ben

Inatoka Uk. 10 Hii ndio Qur’anmaisha yao huja wapata maradhi kama mfumo wa hisia (Nervous breakdown). Madaktari wanayo matibabu yake lakini muathirika huwa anasumbuka sana na shindikizo na kumpelekea kuwa katika hata hali ya khofu na kutojisikia kutulia na haya wale wafanyao kazi za ulinzi kwa miaka mingi huja kupata maradhi haya na matokeo ni kule kuufanya usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.

Katika Uislamu kuna Kailula na Kailula huu ni usinguzi mfupi wa mchana wenye siha ambao unajulikana kwa jina la kigeni kama Siesta. Leo katika nchi ya Spain Siesta imekuwa muhimu na kutengwa vyumba maalumu katika maeneo ya kazi watu kupata usingizi mchache ili kuweza kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na watu wanochelewa kutoka makazini ni watu wa nchi ya Spain kwa sababu ya kuwa na Kailula/Siesta na wengine hutoka kazini na kwenda nyumbani kujilalia kidogo kisha kurudi kazini.

Mwanadamu amekuwa mahiri katika kugeuza mambo, jee sayansi inapo pahali angalau katika mji mmoja ikafanya majaribio ya kugeuza baina ya usiku na mchana? Allah ndio kazi yake na anaielezea kuwa ndio yeye mwenye uwezo na ujuzi wa kugeuza mchana na usiku wake.

‘’Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.” (Surah Faat’ir

35:13)Qur’an huwa inaitaja

Mbingu na ardhi mara zote na kila kimoja kimebeba umuhimu na mara zote hutangulizwa kutajwa mbingu kisha ikafwatiwa kutajwa ardhi.

‘’Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.” (Surah Faat’ir 35:1 )

Upepo na mawingu kisha kuja kwa mvua na ardhi kuwa tupu kisha tukaweka mbengu tukaitoa ardhi kutoka kwenye umauti na kuwa hai Qur’an haikuyaeleza juzi na jana kama mwanadamu alivyokuja kujuwa baadaye ila imeyaelezea haya kwa karne 14 kupita na kuja kuelewa kinachotokea hadi mvua kunyesha.

‘’Na Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma Pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyo kuwa kufufuliwa.’’ (Surah Faat’ir 35:9 )

Jee yupo wa kuziondoa mbingu pahali pake? Jawabu laa, hakuna

sayansi wala Uhandisi wenye elimu hii na Allah anatufahamisha kuwa ni yeye hakuna mwengine alioyafanya na kuyajaalia ardhi kubakia ilivyo na mbingu kusimama zilivyo zikiwa hata nguzo hazina.

‘’Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe. (Surah Faat’ir 35:41)

Suala la mzunguko wa maji ni unaelezwa hapa (Hydrological cycle ) unaelezwa bayana kwenye aya hii kwa mwenye kuzingatia.

‘’Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana.’’ (Surah Faat’ir 35:27).

Mchana na usiku umuhimu wake huko nyuma nishauelezea. ‘’Naye ndiye aliyefanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anayetaka kukumbuka, au anayetaka kushukuru.’’ (Sura Al - Furqan 25:62).

‘’Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu,

na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.’’ (Al - Baqara 2:29)

Suala la mbingu Saba wengine husema ni mabara hii ni mada peke yake lakini Allah ndio mjuzi wa yote.

Qur’an na Bibilia inaelezea namna Allah alivyoumba mbingu na siku alizozitumia nayo hii ni mada inayotaka kuelezewa peke yake.

‘’Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?’’ (Yunus 10:3),

‘’Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda’’ (Al -H’adiid 57:4)

‘’Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye ni Mwenye kuyajua yaliomo vifuani.’’ (Al -H’adiid 57:6),

“Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasi na ruwaza; na anapotaka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.’’ (Al - Baqara 2:117).

‘’Na kila kilichomo mbinguni na kilichomo ardhini ni cha Mwenyezi Mungu; na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu’’. (Al I’mran 3:109)

Hii ni changamoto (Challenge) Allah anatoa tukiwa wahai na hio hio itakuwa kuulizwa pale tutapomaliza maisha yetu juu ya kupinga na fikra za kuwa ni mwanadamu ndio aliofanya kila kitu.

Allah anaapa hapa kwa mbingu na zile njia zake ambazo ni yeye alizozifanya. ‘’Naapa kwa mbingu zenye njia. (Adh-Dhaariyaat 51:7).

Page 12: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR12 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Habari

Mshauri wa Rais wa Uturuki amesisitiza kuwa, Saudi

Arabia haina ustahiki wa kuendesha kesi za wauaji wa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari raia wa Saudia aliyeuliwa kinyama ndani ya ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki.

Fuat Oktay, anayemshauri Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, amekosoa jinsi maafisa wa utawala wa Riyadh walivyoshughulikia faili la mauaji ya Khashoggi na kueleza kwamba, waliohusika na jinai hiyo na watu waliowaunga mkono wangali wanaendelea kila leo kutenda jinai na kukiuka haki za binadamu ndani na nje ya Saudi Arabia.

Akizungumza sambamba na kuanza kesi ya maafisa wa Saudia wanaoshtakiwa katika mahakama ya Uturuki bila wenyewe kuwepo mahakamani kwa kuhusika na mauaji ya Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Al Saud, Oktay amekosoa vikali hatua ya maafisa wa Saudi Arabia ya kuwazuia maafisa husika wa serikali ya Uturuki wasiingie na kufanya uchunguzi katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Instanbul mara baada ya kuuliwa Khashoggi na kuongeza kuwa, hatua hiyo ya maafisa wa Saudia ilikuwa fursa muafaka iliyotumiwa na nchi hiyo kuharibu nyaraka na kufuta ushahidi wa mauaji hayo.

Mshauri huyo wa Rais wa Uturuki amemkosoa pia Mkuu wa Mashitaka wa Saudi Arabia, ambaye alifanya safari mjini Istanbul baada ya kuuliwa Khashoggi na kueleza kwamba, katika safari yake hiyo si tu, hakutoa taarifa zozote kuhusu hatima ya mwili wa Khashoggi na kuungama kwa washtakiwa wa mauaji

Saudia haistahiki kuendesha kesi ya wauaji wa Khashoggi

Fuat Oktay, Mshauri wa Rais wa Uturuki.

yake, lakini badala yake mkuu huyo wa mashtaka wa Saudia alitaka apatiwe taarifa za mazungumzo ya simu aliyofanya Jamal Khashoggi pamoja na laptop yake; tena si kwa ajili ya kuhakikisha haki na uadilifu unatendeka bali ni kwa ajili ya kuzidukua taarifa kwa manufaa wa wahalifu.

Kesi ya raia 20 wa Saudi Arabia wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Jamal Khashoggi, ilianza kusikilizwa siku ya Ijumaa iliyopita na mahakama ya Caglayan iliyoko mjini Istanbul, Uturuki bila washtakiwa wenyewe kuwepo mahakamani. Waendesha mashtaka wa Uturuki wamesema wameshatoa waranti wa kukamatwa washtakiwa hao.Parstoday.

Ukosefu wa uhuru wa waandishi wa habari

umezidi kujidhihirisha ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya waandishi 40 wa habari kufutwa kazi kwa kumkosoa Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.

Gazeti la Yedioth Ahronoth, limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Barak Ravid, mwandishi wa habari wa utawala wa Kizayuni wa habari za kidiplomasia pamoja na waandishi wengine 39, Jumapili ya wiki iliyopita walipokea barua za kuachishwa kazi na taasisi zao kutokana na kumkosoa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni,

Waandishi 40 wafukuzwa kazi kwa kumkosoa Netanyahu

Benjamin Netanyahu na masuala mengine ya kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kabla ya hapo, Netanyahu aliwahi kumlalamikia vikali Barak Ravid, na waandishi wengine kwa kumkosoa.

Ikumbukwe kuwa hivi sasa Waziri Mkuu huyo wa Israel ana kesi nne

za ufisadi na anatakiwa kuzijibu mahakamani. Ilikuwa imepangwa kuwa kesi za Netanyahu zisikilizwe mwezi Machi mwaka huu, lakini ziliahirishwa kutokana na maambukizi ya kirusi cha corona.

Kesi za ufisadi ni moja ya sababu kuu za upinzani wa makundi ya kisiasa ya Israel kwa Benjamin Netanyahu.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel.

Page 13: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR13 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Makala

Inatoka Uk. 8Hisia zilinizidi na zikafurika

katika aya kuhusu vita”. Katika shairi hili la vita,

linaloundwa na beti elfu tatu, mwandishi anaelezea kwa mtiririko matukio yote muhimu ya vita - mapigano ya Sevastopol, Kharkov, Stalingrad, anaandika kwa hisia ya kusifia ushujaa wa askari wa kiSoviet na vile vile makamanda wa jeshi - Timoshenko, Konev, Zhukov na kuyakashfu “maovu ya Wajerumani, yasiyo na mfanowe uliowahi kuwa hata katika enzi za ukatili wa kishenzi” kuwa ni ya aibu.

Shairi hilo linaishia na saluti mjini Moscow kwa heshima ya Ushindi huo mkubwa:

“Mizinga makusudiElfu mbili idadi,Ya ngurumo kama radi,Kwa nguvu ililia. Hasa mara thelathini,Ilinguruma hewaniKushangilia amaniNa kushindwa mdawa. Tangu kuumbwa dunia, Shangwe bado kutokea, La mizinga kulia,Kama hili la Russia.” Nadhari za Shaaban Robert,

nazo zimejaa vionjo vya kishairi. Hizi ni - shairi alilotabaruki kwa mke wake wa kwanza Amina, na pia mashairi mawili yenye kufundisha maadili ambayo mwandishi anaongea na binti yake pamoja na mwanawe katika hadithi ya “Maisha yangu”.

Urithi wa ushairi wa Shaaban Robert, ni vitabu zaidi ya 20, vilivyo katika muundo wa machapisho madogo-madogo, vilivyochapishwa wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake, vinaunda urithi wa ushairi wa Shaaban Robert. Mada ya kazi hizi, kimsingi ni sawa na ile iliyomo katika nathari zake – msisitizo wa maadili, usawa na furaha ya watu huru na walioelimika, ukombozi wa mwanadamu, dhamira na uchapakazi.

Hizi ni kama ile mikusanyiko ya mashairi ya “Mapenzi Bora”, 1969, “Mwafrika Aimba”, 1969, ”Almasi za Afrika”, 1960, “Insha na Mashairi”,1959 na mengine mengi.

Tafsiri zake za “Rubaiyat of Omar Khayyam” kwa Kiswahili (“Utenzi wa Omar Khayyam”, 1952), zinatambuliwa kuwa ndizo bora zaidi katika kazi za tafsiri ya Kiswahili.

Kipindi cha kuibuka kwa nathari na ushairi wa kisasa katika lugha ya Kiswahili, kinahusishwa sana na jina la Shaaban Robert.

Kazi yake ya fasihi, huku ikihifadhi mwendelezo wa mila ya uandishi wa mashairi ya Kiswahili na fasihi za kitaifa wakati huo huo, inaonyesha uwezekano wa kurekebisha, kuboresha na kubadilisha ushairi na nathari ili ziendane na lugha ya kisasa.

Haishangazi kwamba, Shaaban Robert anaitwa “baba” wa lugha ya Kiswahili cha leo, mhenga na mwanzilishi wa nathari na ushairi

Kumbukizi ya Shaaban Robert: Mwanafalsafa aliyetetea utu wa mtu

wa kisasa. Kwa muda wa miaka kadhaa,

Shaaban Robert, alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki “East African Swahili Committee”na mjumbe wa Ofisi ya Fasihi ya Afrika Mashariki “East African Literature Bureau”, iliyokuwa na jukumu la kurekebisha lugha ya Kiswahili.

Katika wasifu uliyochapishwa katika jarida la Kamati hiyo, kunatamkwa mchango mkubwa wa Shaaban Robert katika kukuza lugha ya Kiswahili na pia fadhili zake za upendo na haiba ya kiungwana.

Washairi tisa walichapisha katika toleo la jarida hilo, mashairi yao kwa kumbukumbu ya Shaaban Robert. Na humo ilichapishwa hotuba ya Shaaban Robert- “Kiswahili kama nyenzo ya kuunganisha Afrika Mashariki” aliyoitoa katika Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda) mnamo mwezi Novemba 1961, chini ya mwezi mmoja tu kabla ya kutangazwa kwa uhuru wa Tanganyika.

Kazi nyingi za fasihi za Shaaban Robert, zilikuwemo katika mitaala ya elimu ya msingi, sekondari na pia elimu ya juu nchini Tanzania, na mara kwa mara zilikuwa zikichapishwa kwa marudio.

Kazi zake kadhaa zimetafsiriwa katika lugha nyingine, ikiwamo Kirusi. Nchini Urusi machapisho mawili yalitafsiriwa kutokana na juhudi za wasomi-watafiti wa lugha ya Kiswahili, wa Urusi - (A. Zhukov, E. Myachina, G. Gotsko, A. Averyanova, N. Girenko, V. Kudryavtsev):

- La kwanza (1969)- “Shaaban Robert. Maisha yangu”(1969), ambayo ni pamoja na hadithi za “Kusadikika “,”Adili na Nduguze”, “Maisha yangu”, “Wasifu wa Siti binti Saad, Mwimbaji wa Zanzibar” na “Masomo yenye Adili”.

- La pili (1981) - “Shaaban Robert. Kazi zilizochaguliwa” zikijumuisha hadithi tatu za historia ya maisha: “Maisha yangu”, “Baada ya Miaka Hamsini”, “Wasifu wa Siti Binti Saad, Mwimbaji wa Zanzibar”, na riwaya mbili: “Siku ya

Watenzi wote” na “Utu bora”.

Machapisho yote mawili, yametanguliwa na dibaji iliyotolewa na mchambuzi maarufu wa fasihi, A.A. Zhukov, ambao pia una kumbukumbu ya kazi za Shaaban Robert pamoja na za ile enzi ya kihistoria ambamo mwandishi aliishi na kufanya kazi.

Urithi wa ubunifu wa Shaaban Robert unajulikana ulimwenguni kote; kazi zake zinasomwa katika vyuo vikuu vingi na zimetafsiriwa katika lugha mbali mbali.

Ikumbukwe kwamba ilikuwani katika lugha ya Kirusi, ambapo tafsiri za kwanza za kigeni za vitabu vya Shaaban Robert zilichapishwa.

Kwa maoni ya watafiti wa kazi zake, “Shaaban Robert ni kilele cha utamaduni asilia, ambaye, kwa umuhimu na nafasi yake katika utamaduni wa kiswahili, ndani ya utamaduni- mamboleo wa Tanzania, anaweza kulinganishwa na A. Pushkin katika utamaduni wote wa Kirusi, Shakespeare - wa Kiingereza, Goethe - wa Kijerumani ... ”.

Nchini Tanzania, watu wanamkumbuka na kumuenzi mwandishi na mshairi wao mahiri; shule na mitaa ya miji kadhaa zimepewa jina lake.

Tunakubaliana na kauli ya mshirika wa Shaaban Robert, mshairi mashuhuri wa Kitanzania Sheikh Amri Abedi, ambaye kwa namna ya pekee alitabiri hatma ya urithi wa ubunifu wa mwandishi huyu:

“Kwa mawazo yenye busara ya Shaaban njia kubwa imeandaliwa.

Hakuna udanganyifu katika mambo yake, ubeti huo ni huru na haujafunikwa.

Ana kipaji na hana dosari, ana ujuzi na elimu.

Kila mtu anapaswa kuambatana na mawazo yenye busara ya Shaaban.”

Mawazo ya kiuelimishaji na kibinadamu ya Shaaban Robert yamekuwa na mguso mkubwa katika maendeleo ya fasihi ya lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki. Waandishi wa Tanzania na Kenya, wanategemea kanuni zilizowekwa na yeye katika

kushughulikia Kiswahili cha sasa na mwelekeo kwa usomaji mpana.

Katika kipindi cha baada ya uhuru, aina mpya ya uandishi iliibuka. Katika orodha ya kazi maarufu zaidi zenye uhalisia ni riwaya za E. Kezilahabi, S. A. Mohamed, K. Valibory na wengine.

Aina ya uhalisia wa kijamaa inawakilishwa na kazi za mwandishi wa Zanzibar Adam Shafi.

Wito wa kuzingatia kanuni za kisanii za sasa na baadaye zimeainishwa katika kazi za E. Kezilahabi, S.A. Mohamed, K. Vamitila, K. Mkangi na wengine. Fasihi ya kisasa juu ya lugha ya Kiswahili ni “mfumo unaoibuka kwa kasi, na unaoendana na vumbuzi za fasihi za ulimwenguni kote, jambo ambalo linatufanya tutarajie maendeleo yake ya kasi katika karne hii”. Na hatua za kwanza katika mwelekeo huu tayari zilikwishaanzishwa na “Baba wa lugha ya Kiswahili” Shaaban Robert.

Fasihi za Marejeo:1. Gromov M.D. : Fasihi ya

Kisasa katika lugha ya Kiswahili - IMLI RAN, Moscow, 2004, k.319 (kwa Kirusi)

2. Zhukov A.A. :Kiswahili. Lugha na Fasihi. Mchapishaji - Chuo Kikuu cha St. Petersburg, 1997.k.346( kwa Kirusi.)

3. Shaaban Robert: “Maisha Yangu”. Mchapishaji -”Hudozhestvennaya Literatura”, Leningrad, 1969.k.181 (kwa Kirusi)

4. Shaaban Robert: Kazi Zilizochaguliwa. Mchapishaji “Hudozhestvennaya Literatura”, Leningrad, 1981. K.255 (kwa Kirusi).

5. Shaaban Robert: Kufikirika. Oxford University Press, 1968.

6. Mulokozi M.M.: Barua za Shaaban Robert 1931-1958. Taasisi ya Utafitiwa

Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam. 2002. k.239.

7. “KISWAHILI”. Jarida la Kamati ya Kiswahilli ya Afrika Mashariki,Toleo la 33. Dar es Salaam, Mombasa, 1962/3. uk.145.

Page 14: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR14 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Habari

Balozi mdogo wa Marekani mjini Kabul amesema kuwa majeshi ya

nchi yake yataendelea kuwepo katika ardhi ya Afganistan.

Ross Wilson, amesema wanajeshi wa Marekani hawana nia ya kuondoka Afghanistan na kwamba suala hilo, nalo halimo katika hati ya makubaliano ya amani ya Doha kati ya Washington na kundi la Taliban; hivyo wanajeshi hao wataendelea kuwepo nchini Afghanistan.

Katika makubaliano hayo yaliyotiwa saini miezi minne iliyopita mjini Doha huko Qatar, Washington iliahidi kuwa majeshi yote ya kigeni yaliyoko Afghanistan chini ya uongozi wa Marekani yataondoka katika ardhi ya Afghanistan miezi 14 baada ya kusainiwa makubaliano hayo.

Matamshi yaliyotolewa na Balozi mdogo wa Marekani mjini Kabul kuhusu kuendelea kuwepo majeshi ya nchi hiyo katika ardhi ya Afghanistan, ni katika mipango ya kimkakati inayotekelezwa na ikulu ya rais wa Marekani, White House.

Washington inaendeleza mikakati hiyo licha ya kwamba kundi la Taliban linasisitiza kuwa, litaendeleza mapambano yake nchini humo, hadi pale wanajeshi wote vamizi wa nchi za kigeni watakapoondoka kikamilifu katika ardhi ya Afghanistan.

Hata baada ya kutia saini makubaliano ya Doha tarehe 29 Februari mwaka huu, kundi hilo la Taliban halina imani na ahadi za Marekani kutokana na tabia ya nchi hiyo ya kukiuka makubaliano ya pande mbili na ya kimataifa.

Katika kipindi cha sasa serikali ya Rais Donald

Marekani yasisitiza kuendelea kuikalia Afghanistan Trump, imesitisha mipango yake ya kimataifa ikiwemo kadhia ya Afghanistan na suala la kuondoka wanajeshi wake nchini humo kutokana na kuzongwa na migogoro mingi ya ndani, kama maafa ya virusi vya corona na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga dhulma na ubaguzi wa rangi.

Msimamo wa Marekani wa kuendelea kuwepo wanajeshi wake huko Afghanistan, unaweza kukwamisha au kuvuruga kabisa jitihada zinazofanywa na viongozi wa Kabul za kuitisha mazungumzo ya amani na kundi la Taliban na kupelekea kufungwa kikamilifu njia iliyofunguliwa kwa ajili ya mazungumzo ya kisiasa baina ya makundi yote ya Afghanistan.

Marekani inadai kuwa inataka kubakisha sehemu ya wanajeshi wake nchini Afghanistan kwa ajili ya kuzuia uwezekano wowote wa kundi la Daesh kupata nguvu zaidi nchini humo.

Siku kadhaa zilizopita gazeti la Times lilifichua kwa mara ya kwanza kwamba, hati ya makubaliano ya amani baina ya Marekani na Taliban ina kipengele cha siri kinacholiruhusu jeshi la nchi hiyo kubakisha kikosi kilichodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi nchini Aghanistan. Kundi la Taliban halijatoa taarifa yoyote kuhusu madai hayo.

Inaonekana kuwa, kutokana na mikakati yake muhimu kuhusiana na eneo la Asia, Marekani haitakuwa tayari kuondoa wanajeshi wake wote huko Afghanistan, na iwapo suala hili litakuwa kweli, basi suala la kurejea amani nchini humo litaendelea kuwa ndoto kwa miaka mingine kadhaa.Parstoday.

Balozi mdogo wa Marekani mjini Kabul amesema kuwa majeshi ya nchi yake yataendelea kuwepo katika ardhi ya Afganistan, Ross Wilson.

Msomi wa Iran Dkt. Hakimeh Saghaye-

Biria, amesema taasisi za utafiti nchini Marekani zinatumiwa kupanga sera za serikali ya nchi hiyo kuhusu ulimwengu wa Kiislamu na hasa dhidi ya harakati au mapambano ya Kiislamu.

Dkt. Saghayeh-Biria ameyabainisha hayo katika kitabu chake alichokiandika chenye anuani ya “Chuki dhidi ya Kiislamu ya Kisiasa katika Taasisi za Utafiti Marekani: Kukabiliana na Nguvu za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu” (Political Islamophobia at American Institutes: Battling the Power of Islamic Resistance).

Dkt. Saghayeh-Biria ni msomi wa historia, ustaarabu wa Kiislamu

Taasisi za utafiti Marekani hupanga sera dhidi ya harakati za Kiislamu

katika Kitivo cha Fikra za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Kitabu hicho kimezinduliwa Jumatatu Julai 6 mjini Tehran katika kikao kilichofanyika katika Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa (IQNA).

Kitabu hicho chenye kurasa 210 kimechapishwa na Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu yenye makao yake London na kinaelekezea bayana kuhusu nafasi ya taasisi za kifikra za Marekani katika kueneza na kuchochea fikra za chuki dhidi ya Uislamu ndani ya serikali ya Marekani na katika uga wa kimataifa.

Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Wayne State nchini Marekani, Saeed Khan, amekitaja kitabu hicho kuwa chenye uchambuzi wa kiwango cha juu.IQNA.

Page 15: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR15 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020 Makala

Na Bint Ally Ahmed

Ukumbi wa Wanawake

KAMA mume ni mwema na anapata riziki yake

halali ambayo ameipata kutokana na kazi ngumu anayoifanya, mke anaweza kumkosha mumewe kwa kuonyesha shukrani na kufurahia mafanikio yake kwa matendo. Kufanya hivyo kunaleta hali ambayo itachangamsha mume hisia zake za ndani na kumfanya ahisi amefanikiwa.

Matendo ya ukarimu yanaweza kuwa kawaida ya mtu ambapo hujenga mazoea kutumia na kugawana kipato chake na wale wanao hitaji. Hata hivyo, kama matendo ya ukarimu yanapuuzwa na hayafurahikiwi, mhusika anaweza akapoteza utashi na msukumo wa kufanya wema.

Itakuwa ni kawaida kwa mtu kuhitimisha kwamba ilikuwa ni kutumia vibaya kutoa fedha yake aliyoipata kwa jasho ambapo hakuna shukrani inayotolewa.

Shukrani na kufurahishwa ni tabia za kuvutia akiwa nazo mke kwa mumewe na ni siri ambayo kwayo mtu anaweza kuvuta matendo ya msaada.

Hata Mwenyezi Mungu ametaja kwamba shukrani kwa neema

zake ni sharti ambalo husababisha neema zake kuendelea kutolewa kwa wanadamu:

“Na alipotangaza Mola wenu: Mkishukuru nitakuzidishieni; na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali.” (Qur’ani 14:7).

Mpendwa mke mwema! Mumeo naye pia ni binadamu kama mtu mwingine yeyote yule. Yupo tayari kusaidia familia yake na anaiona kama wajibu wa uadilifu na kisheria. Anapopewa shukrani na kufurahikiwa kwa kutekeleza kazi yake, kazi hizo haziwi tena mzigo kwake.

Wakati wowote anaponunua vitu vya nyumbani au kitu kama nguo na viatu kwa ajili yako na watoto, furahi na umshukuru yeye. Onyesha shukrani zako kwa vitu vidogo anavyofanya kama kununua bidhaa za

vyakula, kusafiri na familia na kukupa wewe fedha. Unapoonesha shukrani, unamfanya mumeo ajihisi kuwa mwema na kuzawadiwa kwa usumbufu uliompata. Uwe mwangalifu kwamba usizipuuze kazi zake na kuwa mtu asiyejali mchango wake kuhusu ustawi wa familia.

Akihisi kwamba hujali wala huridhiki na kile anachojitahidi kukifanya kukuridhisha wewe na familia, anaweza akahisi kama hakuna anayejali juhudi zake na akaanza kutumia fedha yake kwingineko au kwake yeye mwenyewe.

Ikiwa tu rafiki au ndugu amekupa zawadi ya jozi ya soksi au shada la maua, unatakiwa kumshukuru mara nyingi, hivyo ni kawaida tu na ni haki kumfurahia mumeo kwa kukupendelea na kukufikiria. Usidhani kwamba utakuwa unajidhalilisha kwa

kuonesha shukrani zako. Kinyume chake, utapendwa na kujaliwa kwa vitu vingi zaidi kwa sababu unafurahia juhudi ya mumeo, ambapo dharau na ubinafsi ni tabia ambazo zinaweza kuipeleka familia kwenye mabalaa.

Imam Sadiq (a.s) alisema: “Wanawake bora zaidi miongoni mwa wanawake wenu ni hao ambao huonesha furaha wakati waume zao huleta kitu nyumbani na hawaoneshi kutokuridhika kama hakuna kilicho letwa nyumbani.”

Alisema tena katika nukuu nyingine, “Mwanamke yeyote ambaye husema kwa mumewe kwamba hajaona vitu vyovyote vizuri kutoka kwake, basi anakuwa amekosa uaminifu na anavuruga ibada yake.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema: “Yeyote asiye washukuru watu wanaomsaidia, kwa kweli, haoneshi shukrani zake kwa Mwenyezi Mungu kwa neema zake.”islamonline

Uwe mke anayeonyesha shukrani kwa mume

Page 16: Tutembee kwenye Website  au …

AN-NUUR16 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17 - 23, 2020

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 Dar es Salaam.

16 DHULQAADAH 1441, IJUMAA JULAI 17-23, 2020

Gazeti la AN-NUUR sasa linapatikana katika website www.annuurpapers au kwenye

Mitandao kupitiampaper.co.tz, Dondosha na simgazeti.com

Usipitwe na habari na Makala za uchambuzi kila Ijumaa

katika simu yako ya mkononi au Kompyuta yako.

AN-NUUR

FAINALI za Mashindano ya Kuhifadhi Qur`an tukufu

kwa kina mama wa Ummul-Muuminina Aisha Foundation (UMAIF), mwaka huu yatafanyika Agosti 23, 2020 sawa na 1442 Hijriya mwaka mpya wa Kiislamu.

Mashindano hayo yatafanyika katika ukumbi wa City Garden Hall, Gerezani Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa UMAIF, Ustadhi Mohamed Samata, wakati alipoongea na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam Jumanne wiki.

Alisema kuwa siku za nyuma kwa kipindi cha miaka minane mfululizo mashindano hayo yalikuwa yakifanyika wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lakini mwaka huu wameamua kuanza kuyafanya mwezi wa Agosti kwa kuyanasibisha na mwaka mpya wa Kiislamu.

Mashindano hayo maarufu kwa kina mama jijini yanashirikisha watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 40 kutoka Katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Awali Mashindano hayo yalipangwa kufanyika 2, Mei 2020 sawa na mwezi 9 Ramadhani 1441h baada ya hatua ya mchujo wa pili kukamilika na kubaki mchunjo wa tatu ili kuingia fainali, lakini yaliahirishwa na Kamati ya Mashindano kutokana na janga na COVID- 19.

Mchunjo wa tatu utafanyika siku ya Jumamosi 8, Agosti

Mshindano ya Qur’an wanawake kufanyika mwaka mpya wa Kiislamu

Na Bint Ally AhmedJuzuu 1, 3, 5, 7, 10 na Juzuu 15.

Washiriki hao watapita katika michujo mikuu mitatu ambapo kuna jumla ya washiriki 54 kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii.

Ustaadh Samata amewaomba Waislamu kuwasaidia katika jambo hili la kheri, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya kuelekea fainali hizo kwa kuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya maandalizi hayo na kuwapa zawadi washindi watakao shika nafasi za juu.

Alisema ugonjwa wa Corona umeathiri maandalizi ya mashindano hayo kiuchumi na mambo mengi yalisimama na kusababisha kukwama katika maandalizi ya jambo hilo.

Hivyo amewaomba watu binafsi, wahisani, makampuni au mabenki kusadia katika kufanikisha jambo hilo la kulitangaza neno lake Allah (S.w).

Aidha Ustadh Samata ametoa wito kwa kina mama kujiunga na Madrasa za wanawake, ili kujua mambo muhimu ya Dini yao na kumudu kufanya ibada zao kwa ufasaha na kuwafanya kuwa kina mama na wake bora katika familia zao.

Alisistiza kuwa mwanamke aliyesoma dini na kuielewa, atamudu vyema kutekeleza majukumu yake katika maisha yao ya kila siku, na hawatopata shida katika malezi ya familia zao.

Madrasa ya kina mama ya Ummul Muumina Aisha Foundation, ipo Buguruni jijini Dar na inatoa mafunzo kwa kina mama watu wazima, lakini na mabinti wanaotaka kujifunza na kuijua vyema dini yao wanakaribishwa. Kwa mawasiliano zaidi wapigie namba: 0714 265 664.

WASHIRIKI wa shindano la mwaka jana.

Buguruni Makukula jijini Dar na kilele chake kitafanyika siku ya Jumapili ya Agosti 23, 2020.

Akifafanua juu ya uamuzi wa kubadili kipindi cha kufanyika mashindano hayo, alisema kuwa katika mwezi wa Ramadhani kunakuwa na shughuli nyingi za mashindano hivyo UMAIF wameona ni bora kuyahamisha mashindano hayo kutoka katika mwezi

wa Ramadhani na kuyafanya katika mwaka mpya wa Kiislam.

Ustadh Samata amesema kuwa matarajio yao mwaka huu ni kuona ongezeko kubwa la washiriki wa mashindano hayo, kutokana na mwamko wa wanawake wa Kiislamu katika kuisoma na kuhifadhi maneno ya Allah (S.w).

Aliongeza kuwa mwaka huu mashindano hayo yatashirikisha washiriki wa