idil ghadiri

80
IDIL GHADIRI (‘Iydi ‘l-Ghadiyr) Kimeandikwa na: Muhammad Ibrahim al-Muwahhid al-Qazwini Kimetarjumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page A

Upload: alitrah-foundation

Post on 09-Mar-2016

676 views

Category:

Documents


12 download

DESCRIPTION

Idi ya Ghadiri imetokana na tukio kubwa la kihistoria. Tukio hili lilitokea wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akirudi kutoka Makka ambako alikwenda kutekeleza ibada ya Hija. Hija hii ni maarufu sana na hujulikana kama Hijjatu ’l-Widaa’ (Hija ya Mwago). Ghadir ni tukio maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja tukio hili, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kulitaja tukio hili. Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir: “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...” (5:3) Aya hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (saw) pale Ghadir Khumm baada ya kumtangaza Imam Ali (as) kama Khalifa wake, kiongozi wa waumini wote na mrithi wake.

TRANSCRIPT

IDIL GHADIRI(‘Iydi ‘l-Ghadiyr)

Kimeandikwa na:Muhammad Ibrahim al-Muwahhid al-Qazwini

Kimetarjumiwa na:Abdul Karim Juma Nkusui

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page A

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 - 34 - 8

Kimeandikwa na:Muhammad Ibrahim al-Muwahid al-Qazuwiniy

Kimetarjumiwa na:Abdul Karim Juma Nkusui

Kimepangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Februari, 2011Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page B

YALIYOMOAya ya Tabligh...................................................................................2Kiapo cha utii cha chukuliwa kwa ajili ya Imam...........................10Masheikh wawili watoa kiapo cha utii.............................................11Wanawake watoa kiapo cha utii.......................................................13Mshairi wa kwanza kati ya washairi wa Ghadir...............................13Umuhimu wa tukio la Ghadir...........................................................14Ushahidi wa hadith ya Ghadir.........................................................17Rejea za tukio la Ghadir...................................................................20Kukamilika kwa dini...................................................................... 29Taji la Ukhalifa............................................................................... 31Shahada ya tatu katika adhana.........................................................33Mwenyezi Mungu na shahada ya tatu.............................................35Mtume wa Mwenyezi Mungu na shahada ya tatu...........................36Ahlul Bait na shahada ya tatu..........................................................38Fatwa za Maulamaa.........................................................................40Kisimamo pamoja na Sheikh As-Suduuq........................................42Swali na Jawabu............................................................................. 45Nembo ya Shia.................................................................................46Kombora la Mbinguni.................................................................... 46Iddi ya Al-Ghadir.............................................................................49Imam Ali na Iddi ya Ghadir..............................................................51Maimam wa Ahlul-Bait na Iddi ya Ghadir.......................................53Shia na Iddi ya Ghadir......................................................................55Iddi al-Ghadir huko mbinguni.........................................................58Masjid al-Ghadir............................................................................ 60Maelezo kuhusu ardhi ya Ghadir.....................................................62Nafasi ya washairi katika Iddi ya Al-Ghadir....................................63

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page C

NENO LA MCHAPISHAJIKitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabukiitwacho, ‘Iyd al-Ghadiyr kilichoandikwa na Muhammad Ibrahimal-Muwahhid al-Qazwini. Sisi tumekiita, Idil Ghadiri – Idi yaGhadiri.

Idi ya Ghadiri (Sikukuu ya Ghadir) imetokana na tukio kubwa lakihistoria. Tukio hili lilitokea katika jangwa la Ghadir Khumm kati-ka njia ya msafara baina ya Makka na Madina wakati MtukufuMtume alipokuwa akirudi kutoka Makka ambako alikwendakutekeleza ibada ya Hija. Hija hii ni maarufu sana na hujulikanakama Hijjatu ’l-Widaa’ (Hija ya Mwago). Ghadir ni tukio maarufusana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu yaKiislamu hata moja ambayo haikutaja tukio hili, ingawa kuna tofau-ti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo,ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamubila ya kulitaja tukio hili. Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamuulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir: “...Leo nimekukamilishienidini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeniUislamu uwe dini yenu...” (5:3)

Aya hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (saw) pale GhadirKhumm baada ya kumtangaza Imam Ali (as) kama Khalifa wake,kiongozi wa waumini wote na mrithi wake. Baada ya hapo Waislamuwaliifanya siku hii kuwa Idi (Sikukuu) kama utakavyoona maelezoyake katika kitabu hiki.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page D

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huuwa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwon-go, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayohayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu,Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabuhiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale yakuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ilikuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Abdul Karim Juma Nkusui kwakukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vileviletunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyinginehadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page E

DIBAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehemaMwenye kurehemu.

Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu, sala na salamu zimshukie bwanawetu na Nabii wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na nduguyake, msaidizi wake, wasii wake, khalifa wake na kiongozi baada yakeanayependeza mno kwake, Imam Amirul- Mu’minina Ali bin Abu Talib, nasala na salamu ziwashukie Ahlul-bait wa Mtume wa Mwenyezi Munguwateule na viongozi wema waongofu, amana ya Mwenyezi Mungu navipenzi vyake, na makhalifa wa Mtume Wake na mabwana wa mawaliiwake, na hasa mwisho wa mawalii Imam wa kumi na mbili, Al-Mahdianayesubiriwa kudhihiri, na laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie maaduizao wote kuanzia sasa hadi siku ya Kiyama.

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Siku ya Ghadir Khum ni Iddibora katika Iddi za umma wangu, nayo ni ambayo ameniamrishaMwenyezi Mungu Mtukufu kumtawaza ndugu yangu Ali bin Abu Talibkuwa ni bendera ya umma wangu, wataongoka kwayo baada yangu, nayoni siku ambayo Mwenyezi Mungu alikamilisha humo dini na kutimizahumo neema na kuwaridhia Uislaam kuwa ndio dini yao.”

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page F

i

UTANGULIZI.

IDDI AL-GHADIR NI NINI?

Hili ni swali ambalo linakaririwa sana katika vinywa vya vijana ambaowana tatizo la upungufu wa itikadi, na wanakutana na mifumo batili navikundi vilivyopotea ambavyo vinajaribu kupotosha na kutia shaka kwakutoa tuhuma baina ya watu. Wanaulizana: Iddi Al–Ghadir ni nini?Imekuja kutoka wapi? Lini na vipi?

Tulikuwa tumeeleza maudhui haya kwa ufafanuzi na uwazi zaidi katikakitabu chetu Al-Imam Aliyu Khalifatur-Rasuulillaahi, na kwa ajili yakuwarahisishia ndugu zetu vijana, basi tumeyachapisha peke yake katikakitabu hiki pamoja na baadhi ya masahihisho na nyongeza kwa kutoamchango wetu katika kueneza itikadi ya kiislamu na kuondoa shutumazenye kupotosha….. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe taufiki katikakuitumikia haki na watu wake, hakika yeye ni Mwenye kusikia dua naMwenye kutoa msaada.

Muhammad Ibrahim Al-Muwahid AL-Qazuwiniy 14/ 1/ 1401 A.H.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page i

ii

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page ii

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 1

2

Iddi al-Ghadiyr

AYA YA TABLIGHINayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wakona kama hutofanya hivyo utakuwa hujafikisha ujumbe wake naMwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu, hakika MwenyeziMungu hawaongozi watu makafiri.” (Surat al-Maidah: 67.)

Watu wa historia na watu wa hadithi wanafasiri Aya hii kwamba: Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipanga kwenda Hijja mwaka wa mwishokatika uhai wake na ambayo baadae ilijulikana kama Hijjatul-Wida’a,habari ya safari yake ikaenea na watu wakaelekea Madina na wakajiungana msafara wa Mtume hadi idadi ya waliotoka pamoja nae ikafikia lakimoja na ishirini elfu.1

Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza ibada ya Hijja aliondoka kurejea Madina.Alipowasili katika bonde la Juhfah katika ardhi ya Ghadir Khum, nayo nisehemu ambayo kuna njiapanda za kwenda Madina, Iraki, Misri naYemeni, na kuwasili kwake ilikuwa ni siku ya Alhamisi mwezi 18 Dhulhajiwakati wa dhuha.1 Riwaya zimetofautiana katika idadi ya waliokuwa wameandamana na Nabii(s.a.w.w.) isipokuwa idadi hii ndio ambayo wameitaja baadhi ya wanahistoriakama vile Ibnu Sa’ad katika Tabaqaat Juz. 3 uk. 355. Na inasemekana walikuwa124,000, na inasemekana ilikuwa ni pungufu ya hiyo, na inasemekana ilikuwa nizaidi ya hiyo.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 2

3

Iddi al-Ghadiyr

Wakati msafara mkubwa unaendelea na safari yake, aliteremka MalaikaJibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa naAya Tukufu: “Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwaMola wako na kama hutafanya hivyo basi utakuwa hujafikishaujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu,hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.” Na akamfik-ishia kwamba Mwenyezi Mungu anamwamuru amtawaze Ali ibn AbuTalib kuwa Imam kwa watu na Khalifa wake na wasii wake baada yake, naawafikishie yaliyoteremshwa humo kwake miongoni mwa uongozi nawajibu wa kila mtu kumtii.

Nabii (s.a.w.w.) akasimama na akaamuru ambao bado wako nyumawasubiriwe wafike kwake na waliotangulia warejee kwake, waislamu wotewakakusanyika kwake na wakati wa Swala ya Adhuhuri ukaingia, Mtumeakasalisha watu. Hali ya hewa ilikuwa ni ya joto kali sana, hadi mtu katiyao alikuwa anaweka baadhi ya nguo zake juu ya kichwa chake na baadhiyake chini ya miguu yake kutokana na ukali wa joto, Mtume alitengeneze-wa kivuli kutokana na miti ya Samuraat na yakawekwa matandiko yangamia baadhi juu ya mengine hadi yakawa kama mimbari.

Mtume (s.a.w.w.) akasimama juu ili kundi la watu wamuone na akapazasauti yake na akawahutubia hotuba kali na ndefu, alianza kwa kumhimdiMwenyezi Mungu na kumsifu na akatilia mkazo mazungumzo yake namaneno yake juu ya shakhisiya ya khalifa wake Imam Ali (a.s.) fadhilazake, sifa zake, msimamo wake na nafasi yake kubwa mbele ya MwenyeziMungu na Mtume Wake, na akawaamuru waislamu wamtii na kuwatiiwatu wa nyumba yake watukufu, na akahimiza kuwa wao ndio hoja zaMwenyezi Mungu na mawalii wake walio karibu, waaminifu wake katikadini yake na sheria yake, na kwamba kuwatii wao ni kumtii MwenyeziMungu na Mtume Wake, na kwamba wafuasi wake wataingia peponi nawapinzani wake wataingia motoni na mengine mengi yasiyokuwa hayo.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 3

4

Iddi al-Ghadiyr

Na kati ya aliyoyasema ilikuwa ni: “Enyi watu…. hakika mimi nahofiakuwa nitaitwa na nitaitika (wito), mimi ni mwenye kuulizwa na nyinyi niwenye kuulizwa.2 Je, mtasemaje?”

Sauti zikasikika huku na huko na wakasema: “Tunashuhudia kwambawewe umeshafikisha, umetoa nasaha na umepigana jihadi, MwenyeziMungu akulipe kheri.”

Akasema (s.a.w.w.): “Je, simnashuhudia kwamba hakuna Munguisipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake naMtume Wake, na kwamba pepo Yake ni ya kweli na moto Wake ni wakweli, na kwamba mauti ni ya kweli na kwamba Kiyama kitakuja na walahakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu atafufua walio makaburini.?”

Wakasema: “Ndio, tunashuhudia hayo.” Akasema: “Ee Mwenyezi Mungushuhudia.” Kisha akanadi: “Enyi watu: Hamsikii?” Wakasema: “Tunasikia,tunasikia.” Akasema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nitawatangulia katika biri-ka, na nyinyi mtanikuta kwenye birika, na kwamba upana wake ni kamaupana uliopo baina ya Sana’a na Busra3 humo kuna vikombe vya fedhakama vile idadi ya nyota, basi tazameni namna gani mtanifuata katika viz-ito viwili.”

Akanadi mwenye kunadi: “Ni nini vizito viwili ewe Mtume wa MwenyeziMungu?” Akasema (s.a.w.w.): “Kizito kikubwa ni Kitabu cha MwenyeziMungu ncha yake moja iko kwa Mwenyezi Mungu, na ncha nyingine iko

2 Amesema Sayyid Sharafud-Dini katika sherehe ya kitabu chake cha Al-Murajaat: Huenda kauli yake (s.a.w.w.): “Na nyinyi ni wenye kuulizwa” ni isharaya aliyoyatoa Dailamiy na Ibnu Hajar katika Sawaiqu kwamba, Nabii katika tafsiriya kauli ya Mwenyezi Mungu “Wasimamishe hakika wao ni nwenyekuulizwa,” yaani juu ya uongozi wa Ali. Na amesema Imam Al-Wahidiy:“Hakika wao ni mwenye kuulizwa juu ya uongozi wa Ali na Ahlul-baiti wake.”3 Sanaa iko Yemen na Busra iko Syria.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 4

5

Iddi al-Ghadiyr

kwenye mikono yenu basi shikamaneni nacho na wala hamtapotea. Nakizito kingine ni kidogo, kizazi changu Ahlul-bait wangu, na kwambaMwenyezi Mungu Mjuzi amenipa habari kwamba havitatengana hadivitanifikia kwenye birika, na nimemuomba Mola Wangu hilo, basi msivi-tangulie mtaangamia na wala msivipuuze mtahiliki.”

Na akasema (s.a.w.w.): “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi warehema Mwenye kurehemu: Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwakwako kutoka kwa Mola Wako na kama hutofikisha basi utakuwahujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokanana watu. Enyi watu! Sikuzembea katika kufikisha aliyoyateremsha kwan-gu na mimi ni mwenye kuwabainishia sababu ya kuteremka Aya hii.Hakika Jibril ameteremka kwangu mara tatu ameniamuru juu ya amani yaMola Wangu nisimame mahala hapa na nimfahamishe kila mtu kwambaAli ibn Abu Talib ni ndugu yangu wasii wangu, khalifa wangu na ni Imambaada yangu, na ambaye cheo chake kwangu ni kama vile cheo cha Harunkwa Musa isipokuwa hakuna Mtume baada yangu. Naye ni kiongoziwenu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake, na MwenyeziMungu ameshateremsha juu ya hilo Aya katika kitabu chake: “Hapana sijingine Kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waleambao wameamini ambao wanasimamisha Swala na wanatoa sadakahali ya kuwa wamerukuu.” Na Ali amesimamisha Swala na ametoasadaka hali ya kuwa amerukuu, anamtaka Mwenyezi Mungu katika kilahali…..”4

Kisha Mtume (s.a.w.w.) akashika mkono wa Imam Ali (a.s.) akaunyanyuahadi weupe wa kwapa zao ukaonekana, na akamfahamisha kwa watu wote.Akasema: “Enyi watu! Ni nani mwenye haki zaidi kwa waumini kulikonafsi zao?” Wakasema: “Ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Akanadi(s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu ni kiongozi wangu na, mimi ni4 Biharul-An’war Juz 37 uk. 206.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 5

6

Iddi al-Ghadiyr

kiongozi wa waumini, na mimi ni mbora zaidi kwao kuliko nafsi zao,ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni Kiongozi wake.” Na alikaririmara tatu kisha akamuuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: “EeMwenyezi Mungu mpende atakayemtawalisha, na mfanye adui atakayem-fanyia uadui, mpende atakayempenda, mchukie atakayemchukia, mnusuruatakayemnusuru, mdhalilishe atakayemdhalilisha, na izungushe hakipamoja naye popote atakapozunguka. Ee! kila aliyeko hapa amfikishie(habari hizi) asiyekuwepo.

“Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amewawekea kiongozi na Imam,ni wajibu kutiiwa na Muhajirina, Answari na watakaowafuata wao kwawema, kwa wajao na waliopo waajemi na waarabu, huru na mtumwa,mdogo na mkubwa, mweupe na mweusi na kwa kila anayemwaminiMwenyezi Mungu. Hukumu yake ni yenye kupita, kauli yake ni yenyekujuzu, amri yake ni yenye kutekelezwa. Amelaaniwa atakayemkhalifu naamehurumiwa atakayemfuata. Atakayemwamini, kumsikiliza na kumtiibasi Mwenyezi Mungu ameshamsamehe.

“Enyi watu! Hakika hiki ni kisimamo cha mwisho nasimama mahali hapa,sikilizeni na mtii na mfuate amri ya Mola Wenu kwani Mwenyezi Munguni kiongozi wenu na ni Mola Wenu, kisha baada yake ni Mtume wenuMuhammad kiongozi wenu ambaye amesimama anawahutubia, kishabaada yangu Ali ni kiongozi wenu na Imam wenu kwa amri ya MwenyeziMungu Mola Wenu, kisha uImam utakuwa katika kizazi changu, katikakizazi chake hadi siku mtakayokutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu naMtume Wake. Hakuna halali isipokuwa aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu,wala hakuna haramu isipokuwa aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu.Mwenyezi Mungu alinifahamisha halali na haramu na mimi nimemweleza(Ali) aliyonifundisha Mola Wangu kutoka katika Kitabu chake, halali yakena haramu yake.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 6

7

Iddi al-Ghadiyr

“Enyi watu! Hakuna elimu isipokuwa Mwenyezi Mungu amenifundishana kila elimu nimemfundisha Imam wa wachamungu na hakuna elimuisipokuwa nimemfundisha Ali naye ni Imam. Enyi watu! Msipotee walamsikimbie kutoka kwake wala msije mkatoka katika uongozi wake, yeyendiye anayeongoza kwenye haki na anafanya kwa haki na kuiondoa batilina kuikataza, na wala haogopi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama yamwenye kulaumu. Kisha yeye ndio wa kwanza kumwamini MwenyeziMungu na Mtume Wake na ambaye aliitoa muhanga nafsi yake kwa ajili yaMtume, ambaye alikuwa pamoja na Mtume na wala hakuna yeyoteanayemwabudu Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume Wake katikawanaume isipokuwa yeye.

“Enyi watu! Mheshimuni huyu, kwani Mwenyezi Mungu ameshamtukuzana mkubalini kwani Mwenyezi Mungu ameshamchagua. Enyi watu!Hakika yeye ni Imam kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wala MwenyeziMungu hatokubali toba ya aliyepinga uongozi wake na wala hatomsame-he. Enyi watu! Mheshimuni Ali kwani yeye ni mbora wa watu baadayangu katika wanaume na wanawake maadamu riziki inateremka namaadamu kuna viumbe.

Amelaaniwa amelaaniwa, amekasirikiwa amekasirikiwa atakayepingakauli yangu hii na wala asiikubali. Kauli yangu ni kutoka kwa Jibril kuto-ka kwa Mwenyezi Mungu, basi naitazame nafsi kitu gani inakitangulizakwa ajili ya kesho, na muogopeni Mwenyezi Mungu msije mkakhalifu basimkateleza baada ya kuthibiti, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnay-oyafanya.

“Enyi watu! Itafakarini Qur’ani na fahamuni Aya zake, angalieni Aya zili-zo wazi kati yake na wala msifuate zenye utata (mutashabihaati), Wallahihatowabainishia makemeo yake wala hatafafanua kwenu tafsiri yakeisipokuwa ambaye mimi nimeshika mkono wake na nimempandisha kwan-gu na nimeunyanyua mkono wake.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 7

8

Iddi al-Ghadiyr

“Enyi watu! Huyu ni Ali ndugu yangu, wasii wangu mtambuzi wa elimuyangu, khalifa wangu katika umma wangu na katika tafsiri ya Kitabu chaMwenyezi Mungu, mwenye kulingania Kwake mwenye kufanya kwayanayomridhisha, mwenye kukataza maasi Yake, khalifa wa Mtume Wakena Amirul-Mu’minin na Imam mwenye kuongoza, mwenye kuwapiga vitawenye kutengua ahadi, waasi na wenye kuritadi katika amri ya MwenyeziMungu.

“Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amekamilisha dini yenukwa Uimam wake basi ambaye hatakuwa chini ya uongozi wake na uon-gozi wa atakayeshika nafasi yake katika kizazi chake hadi Siku ya Kiyamana akawa kampinga Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hao amali zao zime-batilika na watakaa motoni milele, hawatapunguziwa adhabu na walahawatahurumiwa.

“Enyi watu! Huyu ni Ali aliyeninusuru zaidi kati yenu, mwenye haki zaidikwangu kati yenu, aliye karibu yangu zaidi kati yenu, mtukufu wenu zaidikwangu. Mimi na Mwenyezi Mungu tumemridhia na haikushuka Aya juuya ridhaa ila kwake, na hakuwasemesha Mwenyezi Mungu wale walioami-ni isipokuwa ameanzia kwake, na haikushuka Aya ya kusifu katikaQur’ani isipokuwa kwake, wala Mwenyezi Mungu hakushuhudia pepokatika “Je, haikupita kwa mwanadamu dahari….” isipokuwa kwake,na wala haikuteremshwa kwa asiyekuwa yeye na wala hakumsifu kwayoasiyekuwa yeye.

“Enyi watu! Yeye ni mwenye kunusuru dini, na mpiganaji wa Mtume waMwenyezi Mungu naye ni mchamungu, msafi, muongozaji mwenye kuon-goka. Nabii wenu ni mbora wa Manabii na wasii wenu ni mbora wamawasii, na watoto wake ni mawasii bora. Enyi watu! Kizazi cha kilaNabii kinatokana na mgongo wake na kizazi changu kinatoka katika mgon-go wa Ali. Enyi watu! Hakika Ibilisi amemtoa Adam peponi kwa husuda,hivyo msimfuate amali zenu zisije zikabatilika na visigino vyenuvikateleza. Ee! Hakika hamchukii Ali isipoikuwa muovu na wala hampen-

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 8

9

Iddi al-Ghadiyr

di Ali isipokuwa mchamungu na wala hamwamini isipokuwa Muuminimwenye ikhilasi.

“Enyi watu! Mwaminini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na nuru iliy-oteremshwa pamoja naye. Nuru itokayo kwa Mwenyezi Mungu iko kwan-gu kisha kwa Ali kisha katika kizazi chake hadi kwa Al-Qaimu Al-Mahdi.

“Enyi watu! Baada yangu kutakuwa na maimam watakaolingania kwenyemoto na siku ya Kiyama hawataokolewa. Hakika Mwenyezi Mungu namimi tuko mbali nao, wao na wanaowanusuru na wafuasi wao watakuwakatika tabaka la chini la moto, na wataufanya uongozi kuwa ni ufalme wakunyang’anyana.

“Enyi watu! Nimewabainishieni na nimewafahamisheni na huyu Aliatawafahamisheni baada yangu. Ee! Hakika mimi - baada ya kumalizikahotuba yangu – nawataka mnipe mkono wa kiapo cha utii katika kumtii Alina kumkubali kisha mtampa mkono wa kiapo cha utii baada yangu.

“Enyi watu! Mimi nimempa utii Mwenyezi Mungu na Ali amenipa utiimimi, na mimi namchukulia utii kwenu kutokana na niaba ya MwenyeziMungu Mtukufu na atakayetengua utii hakika anatengua kwa ajili ya nafsiyake.

“Enyi watu! Hakika fadhila za Ali ibn Abu Talib ziko kwa MwenyeziMungu na amekwisha ziteremsha katika Qur’ani na ni nyingi sana siwezikuzitaja katika hotuba moja, basi atakayekuelezeni na kukufahamishenimwaminini. Enyi watu! Atakayemtii Mwenyezi Mungu, Mtume, Ali naMaimam ambao nimewataja basi atakuwa amefaulu kufaulu kukubwa.Enyi watu! Wanaofanya haraka katika kumpa kiapo cha utii na kumfuatana kumsalimia kwa uongozi wa waumini, hao ndio wenye kufaulu katikapepo yenye neema.”

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 9

10

Iddi al-Ghadiyr

Hotuba ya Nabii ikamalizika kwa kumteua Imam Ali ibn Abu Talib kuwaAmirul-Mu’minin kwa waumini na Khalifa wa Mtume wa Mola wa wal-imwengu.5

KIAPO CHA UTII CHACHUKULIWAKWA AJILI YA IMAM

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka na akawaamu-ru waislamu wote wampe kiapo cha utii Imam Ali ibn Abu Talib (a.s.) nawamsalimie kwa kumpongeza kwa kuwa kwake kiongozi wa waumini.6

Mtume (s.a.w.w.) akakaa katika hema lake maalumu na akamuamuru khal-ifa wake akae katika hema lingine kwa ajili ya kuwapokea wanaom-pongeza. Watu wakamiminika kwanza kwa Mtume (s.a.w.w.) kwakumpongeza kwa Iddi hii tukufu na ukumbusho mtukufu nao wakawawanasema: “Ndio tumesikia na tumetii amri ya Mwenyezi Mungu naMtume Wake…...tumemwamini kwa nyoyo zetu.” Kisha wakaenda katikahema la Imam Ali Amirul-Mu’minin kumpa kiapo cha utii na kumpa5 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 204. Katika hotuba tumenukuu nukta za muhimutu, na Tabarasiy ameipokea katika kitabu cha Ihtijaji, na Allamah Al-Majlisiy kati-ka Biharul–An’war Juz. 37 uk. 204. Na katika Maulamaa wa Kisunni namasheikhe wao ameipokea: Al-Hafidh Ibnu Uqudah katika kitabu maalumu kamaalivyoitaja mwanahistoria mashuhuri Ibnu Jarir alichokiita Kitabul-Wilaayat FiTuriq Hadithi-Ghadir, na imechapishwa hotuba hii tukufu peke yake vilevile.

6 Imepokewa kwa Zayd bin Arqam kwamba Nabii (s.a.w.w.) alisema katikamwisho wa hotuba yake tukufu: “Enyi watu! Semeni tumekupa ahadi kutoka kati-ka nafsi zetu na kiapo na kukupa mkono, tunakipeleka kwa watoto wetu na ahalizetu, na familia zetu na hatutaki katika hilo badili na wewe ni shahidi juu yetu, nainatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni shahidi Ali kuwa ni Amirul-Mu’minina.Semeni tuliyowaambia na msalimieni.”

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 10

11

Iddi al-Ghadiyr

mkono huku wakisema: “Amani iwe juu yako ewe Amirul-Mu’minin.”7

Nabii (s.a.w.w.) hakuondoka katika ardhi ya Ghadir isipokuwa baada yawaislamu wote kumpa kiapo cha utii Ali (a.s.). Zayd bin Arqam amesema:“Kiapo cha utii kiliendelea kwa muda wa siku tatu.”8 Ndio kiapo cha utiikiliendelea kwa muda wa siku tatu kwa sababu ya watu na idadi kubwa,haiwezekani kumpa kiapo cha utii kwa muda wa saa moja au siku moja.

MASHEIKH WAWILI WATOAKIAPO CHA UTII

Aliondoka Abu Bakr na Umar kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) nawakamwambia: “Jambo hili ni kutoka kwako au ni kutoka kwa MwenyeziMungu?” Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Je, jambohili litakuwa limetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ndio ni jambokutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Wakasimama wakaendakwa Ali (a.s.) na wakampa kiapo cha utii cha Uimam na ukhalifa, Umarakasema na huku anatoa mkono wa kiapo cha utii kwa Ali: “Hongerahongera kwako ewe mtoto wa Abu Talib.” Na katika habari nyingine:“Pongezi kwako, umekuwa ni kiongozi wangu na kiongozi wa kilamuumini mwanaume na muumini mwanamke.”9

7 Kwa maelezo ya ziada rejea kitabu cha Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270.8 Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270.9 Kundi kubwa la maulamaa wa Kisunni na maimam wao wametaja tukio lamasheikh wawili (Abubakr na Umar) kumpongeza Imam Ali kuwa ni Amirul-Mu’minin, kati ya hao ni: Ahmad bin Hambal katika Musnad, Juz. 4 uk. 241, IbnuJarir Tabari katika Tafsiir yake Juz. 3 uk. 428, Kaadhi Abubakr Al-Baqalaniykatika kitabu At-Tamhiydu Fi Usuulud-Diyn uk. 171, Haafidh Bin SwabaghAl–Malikiy katika Al-Fusulul-Muhimmah Juz. 2 uk. 169, Fakhrur-Raziy katikaTafsir yake Juz. 3 uk. 636 na Sheikh Al-Amin katika Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270,humo ametaja masdari sitini za Hadithi ya kumpongeza.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 11

12

Iddi al-Ghadiyr

Mshangao mkubwa mno ni vipi Abu Bakr na Umar waliuliza swali hilikwa Nabii (s.a.w.w.)? Watu wote walitoa kiapo cha utii bila ya kuulizaswali na bila ya mushekili wowote, lakini vipi Masheikh wawili peke yaowaliuliza swali hili? Je hapa ni mahala pa kuuliza swali hili? Je,hawakusikia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “Hatamki kwa mata-manio isipokuwa ni wahyi unaofunuliwa.” (Suratun-Najm: 4). Je,haikuwafikia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Alichokuleteeni Mtumekichukueni.” (Surat Hashir: 7). Je, hawakusoma kauli yake (s.w.t.):“Enyi mlioamini muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.”(Surat Anfaal: 24). Na jua fika kuwa Aya hizi zilikuwa zimeshateremkakabla ya tukio tukufu la Ghadir.

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza hotuba hiiya Al-Ghadir – ghafla alionekana kwa watu mtu mmoja mzuri mwenyekunukia vizuri akasema: “Wallahi sikumuona Muhammad kama alivyohivi leo katu. Ni mkazo ulioje katika kusisitiza juu ya mtoto wa ami yakena anafunga kwake ahadi ambayo hataitengua isipokuwa aliyemkufuruMwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake Mtukufu. Maangamiomabaya ni kwa atakayetengua ahadi yake.”

Umar akageuka aliposikia maneno yake na akastaajabishwa na mandhariyake kisha akageuka kwa Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Je hukusikia aliyoy-asema huyu mtu? Amesema kadha wa kadha.” Mtume wa MwenyeziMungu akasema: “Ewe Umar unajua ni nani yule?” Akasema: “Hapana.”Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Huyu ni Jibril, ole wako usije ukatengua haki-ka ukitengua basi Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, malaika na wauminiwatakuwa mbali na wewe.”10

10 Biharul– An’war Juz. 37 uk. 219. Na Ihtijaji ya Tabarasiy.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 12

13

Iddi al-Ghadiyr

WANAWAKE WATOA KIAPO CHA UTII

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anatilia mkazo katikakuimarisha misingi ya ukhalifa na kuthibitisha misingi ya Uimam kwaukamilifu zaidi. Kwa ajili hiyo hakutosheka kwa kiapo cha wanaume tu,bali aliwaamuru wanawake na miongoni mwao ni wake zake kutoa kiapocha utii kwa Imam Ali (a.s.), lakini kiapo cha utii cha wanawake kilikuwa-je kwa Amirul-Mu’minin (a.s.)? Je, ni kwa kupeana mkono? Hali kupeanamkono mwanamke ajinabi na mwanamume ajinabi ni haramu, hivyoilikuwaje?

Jibu: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alichagua njia yaishara kwa ajili ya wanawake kutoa kiapo cha utii, aliamuru kuletwe chom-bo chenye maji na akamwamuru Ali (a.s.) aingize mkono wake upandemmoja wa chombo na wanawake waje waingize mikono yao katika upandemwingine wa chombo na wamsalimie kwa kumpongeza kwa kuwa kwakeAmirul-Mu’minin. Kwa njia hii nzuri na safi kilitimia kiapo cha utii kwaAmirul-Mu’minin kutoka kwa wanawake.

MSHAIRI WA KWANZA KATI YA WASHAIRI WA GHADIR

Kisha akasimama Hassan bin Thabit mshairi wa Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) na akasema: “Niruhusu ewe Mtume wa MwenyeziMungu nisome beti kuhusu Ali uzisikie.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambiasoma kwa baraka za Mwenyezi Mungu. Hassani akaanza kusoma:

“Anawaita siku ya Ghadir-Khum Nabii wao, na alishamjia Jibrilu kwaamri ya Mola Wao, kwamba wewe ni ma’sum hivyo usiwe mwoga, wafik-ishie aliyoteremsha Mwenyezi Mungu Mola Wao kwako, na wala usiwao-

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 13

14

Iddi al-Ghadiyr

gope maadui. Akasimama kwao hali mkono wake umenyanyua mkono waAli, hali anatangaza kwa sauti ya juu, akasema: ‘Ni nani kiongozi wenu nawalii wenu?’ Wakasema na wala hawakudhihirisha kutokujua: ‘Mola wakoni walii wetu na wewe ni walii wetu, wala hutaona katu siku moja tunaasi.’Akasema: ‘Simama ewe Ali kwani mimi nimekuridhia baada yangu uwe niImam mwenye kuongoza. Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi huyu nikiongozi wake, basi kuweni wenye kumnusuru na kumfuata kikwelikweli.’ Hapo aliomba: ‘Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayemtawal-isha na mchukie atakayemfanyia Ali uadui, Ewe Mola mnusuru atakayem-nusuru Imam wa uongofu kama vile mbalamwezi inavyoondosha giza.”’

Nabii akafurahishwa na beti hizi za kuonyesha mapenzi na utiifu, akadhi-hirisha tabasamu tukufu na akamshukuru Hasan kwa mashairi yake kwakusema: “Hutaacha kuwa ni mwenye kuungwa mkono na Malaikamaadamu utaendelea kutunusuru kwa ulimi wako.”11

UMUHIMU WA TUKIO LA GHADIR

Msomaji mtukufu, tukio hili la kudumu lililo maarufu kwa jina la Tukio laGhadir, ni miongoni mwa matukio maarufu ya kihistoria, na ni kati yamatukio makubwa katika maisha ya Nabii (s.a.w.w.) na wamelishuhudiasahaba laki na kumi elfu, ambao wao wenyewe walihudhuria, kati yao ni:

Abu Bakr bin Abi Quhaafah.Umar bin Al-Khattab.Uthman bin Afaan. Abdur-Rahman bin Auf. Saad bin Abi Waqaas.Abu Huraira.

11 Al-Ghadir Juz. 1 uk. 34. Tadhkiratul-Khawas cha Sibtu Ibnu Jauzi uk. 20,As-Suyutwiy katika Risalatul-Izdihaar. Na Al-Kunjiy katika Kifaayatu-Twalib uk.17.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 14

15

Iddi al-Ghadiyr

Abu Qudaamah Answaariy.Hudhaifah bin Al-Yaman.Abu Said Al-Khudriy.Zubair bin Al-Awaam.Twalha bin Ubaidullah.Abbas bin Abdul-Muttalib.Usamah bin Zaid.Ubayya bin Kaab.Al-Baraa bin Aazib.Anas bin Malik.Jabir bin Samrah.Hubah bin Jarir Al-Araniy.Hasan bin Thabit. Abu Ayubu Al-Answariy.Khalid bin Walid.Khuzaimah bin Thabit.Zayd bin Thabit.Sa’ad bin Ubaadah.Sahal bin Saad bin Sa’adiy.Qaisi bin Saad bin Ubaidillah.Al-Miqdad bin Amru Al-Kindiy.Abdillah bin Umar.Salman Al-Farsiy. Abu Dhar Al-Ghafaariy. Ammar bin Yaasir. Maimam wawili Hasan na Husein, mabwana wa vijana wa watu wapeponi na wengineo.12

Ama wanawake ambao walishuhudia na kuhudhuria tukio hilo ni wengipia, mashuhuri kati yao ni:Fatmah Zahraa, binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).

12 Rejea Al-Ghadir Juz. 1 uk. 41 utakuta majina kwa kirefu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 15

16

Iddi al-Ghadiyr

Ummu Salamah, mke wa Mtume.Fatmah binti Hamza bin Abdul–Muttalib. Ummu Haaniy binti Abbas bin Abu Talib. Asmau binti Umais. Aisha binti Abu Bakr na wengineo katika wanawake.

Na hukuti mwandishi au mtunzi ameandika au anaandika kuhusu maishaya Nabii au maisha ya Imam Ali isipokuwa anataja kisa hiki kwa kifupi aukwa kirefu, ila kama mwandishi au mtunzi ni mwenye kuchukia haki au niadui wa kizazi cha Muhammad au ni mamluki wa baadhi ya masultaniwaovu au mwenye kukanusha fadhila za Ahlul-bait (a.s.) au mfano wahayo, hivyo basi hujifanya kasahau au kaghafilika kutaja tukio hili lenyekudumu.

Ama tukio lenyewe hakuna nafasi ya kulikataa na kutilia shaka usahihiwake na kujadili sanadi yake, kwa sababu maulamaa wakubwa, mahafidh,muhadithina na wanahistoria wa zamani, wote wamethibitisha usahihiwake na ukweli wake na wamelitegemea hadi leo hii. Hakika tukio laGhadir sio tukio lenye kupita na jepesi hadi liweze kusahaulika bali ni laz-ima litatajwa katika nyanja mbalimbali za kielimu, kama vile lugha, histo-ria, tafsiri, hadithi, fasihi n.k.

Mtu wa lugha kama ni mwadilifu lazima aashirie kwalo anapozungumziamaana ya neno: Ghadiyru Khum. Mwanahistoria naye kama ni mwadilifuvilevile lazima ataje tukio la Ghadir angalau kwa muhtasari katika historiaya Uislamu kwa kuwa ni tukio la kiislamu, na katika historia ya Nabii waUislamu (s.a.w.w.) kwa kuwa lilitokea katika Hijja yake ya mwisho(Hijatul-Widaa) na kabla ya kufariki kwa Nabii kwa siku sabini, na katikahistoria ya Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) kwa kuwa linahusiana nayena ndiye mhusika mkuu.

Na mfasiri kama yuko huru kutokana na ushabiki (ta’asubu) lazima atata-ja tukio la Ghadir angalau kwa muhtasari wakati wa kufasiri Aya zili-

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 16

17

Iddi al-Ghadiyr

zoshuka huko mfano Aya ya Tablighi, Aya ya Kukamilisha dini, Aya yaKuteremka adhabu, na nyinginezo katika Aya nyingi zinazofungamana naukhalifa wa Imam Ali Amirul–Mu’minina (a.s.) na Uimam wake kama vileAya ya Kuonya.

Na mwanahadithi lazima alitaje katika sehemu ya kutaja hadithi tukufu zaNabii kama vile kauli yake (s.a.w.w.) kwa Ali: “Wewe kwangu ni kamaalivyokuwa Haruna kwa Musa isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.” Nakauli yake (s.a.w.w.) akiashiria kwa Ali (a.s.): “Huyu ni ndugu yangu, wasiiwangu, khalifa wangu na mrithi wangu baada yangu, msikilizeni na mtii-ni.” Na kauli yake (s.a.w.w.): “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali nikiongozi wake.” Na nyinginezo katika mamia ya hadithi sahihi zilizopoke-wa kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) juu ya ukhalifa wa Imam Ali, vivyo hivyokatika nyanja zinginezo.

USHAHIDI WA HADITHI YA GHADIR

Ewe msomaji mtukufu! Hakika ushahidi wa hadithi ya Ghadir juu yaukhalifa wa Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) na Uimam wake baada yaMtume wa Mwenyezi Mungu moja kwa moja unategemea mambo maw-ili:-

SanadHoja

Ama Sanad ya hadithi tumekwishaiashiria na kwamba iko katika daraja lajuu kabisa la usahihi na nguvu, ni hadithi mutawatir, wameipokea sahabawakubwa na watukufu wao kama tulivyotangulia kutaja.

Amesema Al-Haafidh Ibnu Hajjar Al-Hanafiy katika Swawaiqul-Muhriqahuk. 25: “Hakika hiyo ni hadithi sahihi hakuna shaka humo, na wameshaitoajamaa kama vile Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ahmad, na njia zake ni nyingi

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 17

18

Iddi al-Ghadiyr

sana, kisha wameipokea sahaba kumi na sita. Na katika riwaya ya Ahmadni kwamba wameisikia kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) sahaba thelathini nawaliitumia kutoa ushahidi kwa Ali pindi alipopokonywa ukhalifa kamailivyotangulia na itakuja baadae na sanadi zake nyingi ni sahihi na hasana,na wala hatazamwi aliyekosoa usahihi wake, wala aliyejibu kuwa Alialikuwa Yemen, kwa kuwa imethibiti kurejea kwake toka huko na kuwahiHijja pamoja na Nabii (s.a.w.w.). Na ama kauli ya baadhi yao kwambaziada ya “Ewe Allah mpende atakayemtawalisha…….” hadi mwisho niuzushi, kauli hiyo inapingwa kwani yamepokewa hayo kwa njia nyingi,kati ya hizo Adh-Dhahabiy amesema zilizo nyingi ni sahihi.”

Nasema: Insha’allah tutataja maelezo ya baadhi ya maulamaa na hufaadhkuhusu usahihi wa sanad ya hadithi ya Ghadir, wakati wa kutaja uthibitishona rejea za kihistoria.

Ama hoja, pia iko katika daraja la juu kabisa, na hasa baada ya tanbihi yaviambatanisho vya mazingira na nukuu vinavyoizunguka hadithi.

Neno Al-Maula alilolitumia katika kauli yake (s.a.w.w.): “Man kuntumaulaahu fa Aliyun maulaahu.” Maana yake ni mwenye haki zaidi najambo na kulitawalia, kwa ajili hiyo Nabii (s.a.w.w.) alisema kwanza: “Je,mimi si nina haki zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Sahaba wakewaliposema: “Ndio.” Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Ambaye mimi ni kion-gozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” Maana yake ni kwamba haki ileileniliyonayo kwenu ndio ileile aliyonayo Ali (a.s.) kwenu, na kwa sababuhiyo imekuja kwa Fau atafri’i (tawi) na akasema: “Fa Aliyun maulaahu.”Yaani “Basi Ali ni kiongozi wake.” Hili ni la kwanza.

Pili: Hakika kauli yake (s.a.w.w.): “Hakika mimi nakaribia kuitwa na kuiti-ka (anaweza kunijia malaika wa mauti) na mimi ni mwenye kuulizwa nanyinyi pia ni wenye kuulizwa.” Ni dalili ya kuwa yeye amekaribia kufa nakwamba huu ni wakati wa kuusia na kuteua Imam baada yake ili yeye aweni kigezo kwa waislamu baada yake.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 18

19

Iddi al-Ghadiyr

Tatu: Aliyoyafanya (s.a.w.w.) siku ya Ghadir Khum baada ya kuteremkaAya ya Tablighi, kwanza kushuka kwake katika ardhi kama hiyo katika juakali, kuamuru kwake kurejea waliotangulia miongoni mwa waislamu nawalio nyuma wawasili, kutoa hotuba kali, kunyanyua kwake mkono wa Ali(a.s.) kisha kuchukua kiapo cha utii kwa ajili yake kwa muda wa siku tatu,na kuteremka Aya ya kukamilika dini…… hayo yote sio kingine bali nihoja iliyo wazi kwamba Nabii (s.a.w.w.) alikuwa katika kumteua khalifabaada yake.

Nne: Hakika kauli ya Umar bin Al-Khattab kwa Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) wakati wa kutoa kiapo cha utii: “Hongera hongera ewemtoto wa Abu Talib umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa kilamuumini mwanaume na mwanamke.” Sio kingine ila ni ushahidi wakwamba alifahamu ukhalifa wa Imam Ali kwa Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w) na kwa ajili hiyo alikwenda kutoa kiapo cha utii napongezi.

Tano: Hakika kila aliyehudhuria siku ya Ghadir alifahamu kuwa Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikusudia katika “Maula” Uimam naUkhalifa, na kati yao ni Hasan bin Thabiti mshairi wa Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambapo aliiweka maana hii katika utungo washairi na akataka ruhusa kwa Nabii Mtukufu ili kusoma kaswida yakeambayo umekwishaisoma huko nyuma. Na maana hiihii ya Uimam naUkhalifa ndio waliifahamu sahaba wengine na taabiina na wakaliwekatukio la Ghadir katika tenzi nzuri za mashairi kwa muda wote wa karne navizazi.13

Maana hii hii aliifahamu Al-Haarith bin Nuuman Al-Fihriy kamautakavyosoma kisa chake katika sehemu itakayokuja. Ewe msomaji

13 Rejea kitabu cha Al-Ghadir cha Allammah Al-Amin, humo amewatajawashairi wa Ghadir kuanzia karne ya kwanza hadi karne ya nne na kuelezeamaisha yao na kaswida zao walizozitunga katika mnasaba huu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 19

20

Iddi al-Ghadiyr

mtukufu! Huu ni muhtasari wa ushahidi wa hadithi ya Ghadir, na maula-maa wamefafanua hilo katika hadithi ambapo hakuna tena ziada juu yakena kama utataka ufafanuzi zaidi rejea kitabu Al-Muraja’at cha SayyidSharafud-Din.

REJEA ZA TUKIO LA GHADIR

Ewe msomaji mtukufu! Ili uzidi kuwa na matumaini na yakini basi naku-tajia majina ya baadhi ya rejea na vitabu ambavyo vimetaja tukio hili tuku-fu angalau kwa muhtasari ili uvirejee mwenyewe kama ukitaka ili usometukio na wala usipatwe na shaka katika usahihi na ukweli wake. Kablasijataja majina ya rejea lazima nitaje vidokezo:

Kwanza: Baadhi ya vitabu na rejea hizi zimechapishwa mara nyingi nakwa ukubwa tofauti ambapo imesababisha ziada ya idadi ya kurasa zakeau kupungua kwake kwa sababu ya ukubwa wa kitabu, kwa hiyo miminasisitiza juu ya ulazima wa kutafuta maudhui katika hali ya kutopatikanakatika ukurasa uliotajwa katika kurasa zilizotangulia au zinazofuatia, nakutofanya haraka katika kutoa hukumu ya kutopatikana na kumtuhumumtunzi kwa uwongo n.k. Bali kuwa na uhakika na yakini kuwa mimi sita-ji ila rejea na vitabu maarufu na vinavyozingatiwa, na sina lengo lingineisipokuwa kubainisha ukweli na uhakika.

Pili: Kumepokewa habari kwamba chuo kikuu cha Azhar huko Kairokwa msaada wa moja kati ya nchi za kiarabu kimeunda kitengo cha sirikwa lengo la kuviangalia upya vitabu na rejea zote zinazotegemewa naSunni, na kati ya hivyo ni Sahih Bukhari.

Lengo la hayo ni kuondoa wanayotaka kuyaondoa na kupotosha ambayowanataka kuyapotosha katika hadithi zilizopokewa kuhusu fadhila zaAhlul-baiti (a.s.) katika yale ambayo Shia wanaweza kuyatolea ushahidijuu ya ukweli wa madhehebu yao. Kitengo hiki ni cha siri kimefichwa na

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 20

21

Iddi al-Ghadiyr

zimechapishwa baadhi ya rejea chapa mpya na humo baadhi ya hadithizimeondolewa au zimepotoshwa katika baadhi ya maneno yake muhimukama vile kupotosha neno “Khalifatiy” lenye maana ya khalifa wangu, nakulifanya “Khaliliy” lenye maana ya rafiki yangu.

Nimeshasoma kitabu cha mmoja wa wapotoshaji anamshambulia humoAllammah Mtafiti Sayyid Abdul Husein Sharafud-Din (r.h) na anamtuhu-mu kwa uongo eti kwa sababu ametaja katika kitabu cha Al-Murajaathadithi kutoka katika moja ya rejea maarufu, kisha mwandishi akarejea nahumo hakukuta hadithi, basi akawa anatoa uongo na uzushi wa chuki dhidiya Sayyid mtukufu.

Jua kwamba kama tukijaalia ukweli wa mwandishi huyo basi sababu inare-jea ima kwenye kuchapishwa kitabu hicho mara nyingi kamatulivyoashiria hapo nyuma, au kwa yale yanayofanywa na kitengo hichomiongoni mwa vitendo vya kuchezea hadithi. Nilikutana na maulamaawawili na kila mmoja alikuwa amehifadhi Sahih Bukhari iliyochapishwakabla ya miaka 100 huko Misri, akasema hakika katika chapa hii kunahadithi ambazo hazipo katika chapa mpya.

Alaa kulihali hakika kitengo hiki kinaleta hatari kubwa kwa Uislamu naathari zake. Je, haijatosha mustashirikina kuchezea historia yetu ya kiisla-mu na kupotosha ukweli wake hadi wakaja hawa ambao wanapotoshamaneno kutoka katika asili yake na wanafanya hiyana hii kubwa katikaathari za asili za kiislamu.

Hakika hii inaonyesha ushabiki (ta’asubu) wa upofu walionao maumalaawaovu ambapo wanaona ni bora kupotosha hadithi au kuziondoa badala yakukubali haki na kuifuata. Kwa ulimwengu wa kiislamu na kwa waislamuwote katika kila sehemu nasema: Hakika kitengo hiki kama kitaendelea nakazi yake ya uovu basi vitabu vyote na rejea za Kisuni zitakosa asili yakeya kihistoria na thamani yake ya kielimu na havitaweza kutegemewa kwasababu ya kukosekana uaminifu kwavyo, hivyo wahini kuzuia jambo hilo

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:31 PM Page 21

22

Iddi al-Ghadiyr

kabla hamjapitwa na wakati. Hakika mimi sishangai chuo kikuu cha Azharkukanusha habari hii baada ya kufichuka siri hii…. lakini tajirba ni dalilibora na chapa za zamani zimejaa katika maktaba. Msomaji mtukufu! Juakuwa tuliyoyategemea katika kutaja tukio la Ghadir na mengineyo ni rejeazilizochapishwa zamani yaani kabla ya miaka ishirini na kuendelea.

Tatu: Baadhi ya rejea hazijataja tukio la Ghadir kwa ukamilifu balivimeashiria kwa muhtasari, zimetaja sehemu na kuacha sehemu zingine,kwa ajili hiyo nimejaribu kulisoma tukio hili tukufu kwa kuchukua kuto-ka katika kitabu hiki au kile. Isipokuwa rejea na athari za kihistoriazimeafikiana juu ya tukio nayo ni kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w.) alisema wakati wa kuondoka kwake katika Hijjatul–Widaa kati-ka ardhi ya Ghadir Khum na akanyanyua mkono wa Ali (a.s.) na akasema:“Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake, eweMwenyezi Mungu mpende atakayetawalisha…” hadi mwisho, kishaakachukua kiapo cha kumtii Imam toka kwa waislamu wote. Haya ndiomakusudio na inatosha kuthibitisha ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Mu’minin baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu moja kwa moja.

Na yaha hapa ni baadhi ya majina ya vitabu vya rejea:Tafsir Asbabin-Nuzuul cha Waahidiy, anapotafsiri Aya ya Tablighi.Sahih Tirmidhiy Juz. 2 uk. 298, na amesema ni hadithi hasan sahihi.Sunnan Ibin Maajah Juz. 1 uk. 28 na 29.Sunnanul-Baghawiy Juz. 2 uk. 119.Mustadrakus-Sahihain cha Al–Haakim Juz. 3 uk. 109 na 533, ameipokeakwa njia nyingi.Al-Wilaayatu Fiy turqil-Hadithi Al-Ghadir cha mwanahisoria mashuhuriMuhammad bin Jarir At–Tabariy aliyefariki 310 A.H. Na ameipokea humohadithi ya Al–Ghadir kwa njia zaidi ya 70.

Na sababu iliyosababisha Tabariy kutunga kitabu hiki kama alivyotaja Al-Hamwainiy katika Mu’ujamul-Udabai, Juz.18 uk. 8 katika maelezo yamaisha ya Tabariy ni kwamba: Mmoja wa masheikh wa Baghdad alipinga

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 22

23

Iddi al-Ghadiyr

tukio la Ghadir na akadai kwamaba Imam Ali alikuwa Yemen wakati waHijjatul–Wida’a, basi Tabariy aliposikia hilo akatunga kitabu hiki kumjibuna kuzungumzia usahihi wa hadithi zilizopokewa kuhusu Ghadir Khum.

Ibnu Kathir katika Al-Bidayatu wan-Nihayah Juz. 5 uk. 208 amesema: “Najambo hili la Al-Ghadir amelipa kipaumbele Abu Jafar Muhammad binJarir Tabariy mwenye Tafsir na Tarikh, basi alikusanya humo mijaladimiwili na akapokea humo njia zake na matamko yake.”

Kitabu Man Rawa Hadithul-Ghadiyr Khum cha Abu Bakri Jaabiy aliye-fariki 355 A.H. Amepokea humo hadithi ya Ghadir kwa njia 125 na ameita-ja As-Sarawiy katika kitabu Al-Manaaqib Juz. 1, uk. 529.

Ad-Dirayatu Fiy Hadithil-Wilayah cha Hafidh As-Sajastaniy chenye juzuu17, humo amekusanya njia za hadithi ya Al-Ghadir kutoka kwa sahaba120.

Uddatul-Baswir Fiy Hajji Yaumul-Ghadir cha Abul-Fuutuh Al-Karaajikiy.

10. Al-Wilayatu Fiy Turuq Hadithil-Ghadir cha Haafidh Ibnu Uqudahaliyefariki 333 A.H. Amepokea humo hadithi ya Ghadir kwa njia 105.Amesema Ibnu Hajjar Al-Asqalaany katika Fatuhul-Bariy: “Ama hadithi“Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” AmeipokeaTirmidhiy na Annasaaiy na ina njia nyingi sana na ameshazikusanya IbnuUqudah katika kitabu maalumu na nyingi ya sanad zake ni sahihi na has-san.”11. Tafsiru Fakhri Ar–Raaziy Juz. 3 uk. 636.12. Tafsiru Ibnu Kathir Juz. 2 uk. 14.13. Tafsiru Anisaburiy Juz. 6 uk. 194.14. Tafsiru Durrul-Manthur ya Suyutiy Juz. 2 uk. 259.15. Tafsiru Shaukaaniy Juz. 2 uk. 57.16. Tafsiru Al-Manaar Juz. 6 uk. 464.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 23

24

Iddi al-Ghadiyr

17. Tafsiru Ruhul-Maariy ya Al-Alusiy Juz. 2 uk. 350 na 249. Na ame-sema:

“Imethibiti kwetu kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema katika haki yaAmirul-Mu’minin: (Mankuntu maulaahu fa Aliyun maulaah). “Ambayemimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”

18. Tafsiru Tabariy Juz. 3 uk. 428.19. Tafsiru Qurtubiy katika tafsiri ya Aya ya Tablighi.20. Tafsiru Abu Said.21. Tafsiru Siraajil–Muniyr cha Shiriyniy katika tafsiri ya Aya ya Tablighi.22. Yanabiul-Mawaddah cha Qanduziy Al-Hanafiy uk. 40.23. Al-Istiabu cha Ibnu Abdul-Barr Juz. 2 uk. 373.24. Dhakhairul-Uqba cha Muhibu Tabariy Ashaafiy uk. 67.25. Al-Fusulul-Muhimah cha Ibnu Swabagh Al-Maalikiy uk. 25.26. Faidhul-Qadir cha Munawiy Ashaafiy uk. 218.27. Usudul-Ghabah cha Ibnul-Athiir Juz 3 uk. 307 na Juz 5 uk. 205.28. Al-Manaqib cha Al-Khawarizimiy Al-Hanafiy uk. 130 na 35.29. Riyadhun-Nadhrah cha Muhibud-Din Tabariy Juz. 2 uk. 169.30. Kifayatut-Talib uk. 15 cha Al-Haafidh Ashaafiy Al-Kanjiy aliyefari-ki 658 A.H. Na amesema: “Hii ni hadithi mashuhuri, hasan, wameipokeawakweli, na kuziweka pamoja sanadi hizi baadhi kwa baadhi yake ni hojakatika usahihi wa nukuu.”31. Tarikhu –Khulafau cha Suyutiy uk. 114.32. Tarikh Baghdad cha Khatibul–Baghdadiy Juz. 8 uk. 290 na Juz. 7uk. 377 na Juz. 1 uk. 47.Al-Bidayatu Wan-Nihayah cha Ibnu Kathiir Juz. 5 uk. 208 na Juz. 7 uk.348.Tarikh Ibnu Assakir.Tarikh Ibnu Khuldun katika utangulizi wa kitabu chake.Hulyatul-Awliyai cha Abu Naiym Juz. 4 uk. 23.Kanzul-Ummaal Juz. 6 uk. 398 na Juz. 2 uk. 154.Tahdhibut-Tahdhib cha Hafidh Ibnu Hajar Al-Asqalaaniy Juz. 7 uk. 337.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 24

25

Iddi al-Ghadiyr

Al-Iswabah cha Ibnu Hajar Al-Asqalaany Juz. 7, uk. 780 na Juz. 6, uk.223 na Juz. 2, uk. 408.Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4, uk. 372 na Juz. 1, uk. 118.Talkhiys cha Dhahabiy Juz. 3, uk. 533 na amasemea ni sahihi.Majmauz-Zawaid cha Haithamiy Juz. 9, uk. 107.Al-Muujamul–Kabiir cha Tabaraniy.Al-Khawas Al-Alawiyah cha Hafidh Anasaiy uk. 21, na 125.As-Swaiwaqul-Muhriqah cha Ibnu Hajar uk. 25 na 75 na amesema kuwani hadithi sahihi hakuna shaka humo.Al-Mawahibu Ad-Dhuniyah cha Qastalaaniy Juz. 7, uk. 13 na amesema:“Njia za hadithi hii ni nyingi sana na sanadi nyingi ni sahihi na hasan.”Mizanul–I’itidal Juz. 2, uk. 303.Matalibus–Suul cha Ibnu Talha Ashaafiy uk. 16 amenukuu kutoka kwaTirmidhiy.Shamsul-Akhbar cha Al-Qarishiy uk. 38.Nuzulul-Abrar cha Badi Khishiy uk. 21 na amesema: “Hii ni hadithi sahi-hi mashuhuri na hakuacha kuzungumza katika usahihi wake isipkuwamwenye ushabiki (ta’asubu), na mpinzani kauli yake haizingatiwi, kwanihadithi hii ina njia nyingi sana.”Al-Imamah Was-Siyasah cha Hafidh Ibnu Qutaibah Juz. 1.Muujamul–Udabai cha Yaqut Al-Hamawiy Juz. 18, uk. 84.Al-Milali Wanahli cha Shaharistaaniy.Tadhkiratul-Hufadh cha Haafidh Dhahabiy Juz. 3, uk. 231 na amesema:“Ama hadithi (man kuntu–maulaah) “Ambaye mimi ni kiongozi wake..”ina njia nzuri na nimeandika kitabu mahsusi juu ya hilo vilevile.”Naasema: Ameshaandika Hafidh Dhahabiy kitabu maalum kuhusu tukio laGhadir tukufu na amekiita Tariyq Hadithil-Wilaayah.Nihayatul-Irbi Fiy Fununul-Adab cha Nawawiy.56.Al-Khutat cha Maqriyzi.57.Akhbar Duwal cha Qaramaniy Admishiqiy.58.Siratul-Halabiyah cha Halabiy Ashafiy Juz. 3, uk. 302.59.Musnad Abu Yaaliy Al- Muuswiliy.60.Tadhkiratul-Khawasil-Ummah cha Sibit Ibnu Jauziy Al-Hanafiy uk.18.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 25

26

Iddi al-Ghadiyr

Amesema: “Wameafikiana maulamaa wa sira kwamba kisa cha Ghadirkilikuwa ni baada ya kurejea Nabii (s.a.w.w.) kutoka Hijjatul-Wida’a tare-he 18 Dhilhaji, aliwakusanya sahaba na walikuwa mia na ishirini elfu naakasema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”Alisema Nabii (s.a.w.w.) ibara iliyo wazi bila ya kupinda wala kuashiria.”

Mushikilul-Athar Juz. 2, uk. 308 cha Haafidh At-Tahawiy aliyefarikimwaka 279 A.H.

Al-Manaaqib cha Ibnu Al-Maghaaziy Shaafiy aliyefariki 483 A.H.Amesema kutoka kwa Sheikh wake Abul-Qaasim baada ya kupokea kwakehadithi ya Al-Ghadiyr. “Hii ni hadithi sahihi kutoka kwa Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.w) na wameipokea takriban watu mia moja,kati ya hao ni watu kumi waliobashiriwa pepo, nayo ni hadithi iliyothibitisijui ubovu wake, Ali amepwekeka na fadhila hii na wala hashirikiani nayeyeyote.”

Faraidus–Simtain cha Al-Juwayny Ashaafiy.At-Tamhiid Fiy Usulid-Diin cha Baqalaamiy.Al-Mirqaatu Fiy Sharhul-Mishkaati Juz. 5, uk. 568 cha Al-Harawiy Al-Qaaniy Al-Hanafiy aliyefariki 1014 A.H. bali baadhi ya Hufaadh wameih-esabu kuwa ni mutawatir ambapo kuna riwaya ya Ahmad bin Hambal,kwamba wameisikia kutoka kwa Nabii sahaba thelathini na waliitumiakutoa ushahidi kwa Ali alipopokonywa ukhalifa wake.

Sharhul-Mawahib cha Zarwaaniy Al-Maalikiy.Al-Bayan Wataarif cha Ibnu Hamza Ad-Dimishiqiy Al-Hanafiy.Zaynul-Fataa cha Aswimy na amesema: “Hadithi hii umma umeipokea naumeikubali, nayo inaafikiana na misingi.” Kisha akaipokea kwa njia nyin-gi.

Sirul-Alamiyna uk. l9, cha Al-Ghazaliy aliyefariki 505 A.H. Amesema:“Hoja imeshinda kwa upande wake na jamhuri imeafikiana juu ya matini

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 26

27

Iddi al-Ghadiyr

(matamko) ya hadithi kutoka katika hotuba yake (s.a.w.w.) katika siku yaGhadir Khum, kwa muafaka wa wote, naye amesema: ‘Ambaye mimi nikiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”’

Al-Manaaqib cha Haafidh Abu Al-Faraj Ibnu Jauziy Al-Hanbaliy aliyefari-ki 598 A.H. Amesema: “Wameafikiana maulamaa wa sira kwamba tukio laGhadir lilikuwa baada ya kurejea Nabii (s.a.w.w.) kutoka Hijjatul-Widaa18 Dhilhaji na alikuwa pamoja na sahaba, mabedui na wanaoishi karibuna Makka na Madina, laki moja na ishirini elfu wamesikia kutoka kwakemaneno haya, na washairi ni wengi katika kuelezea tukio hilo.”

Is’afur-Raghibiina cha Swabana Ashaafiy kilichochapishwa, katika sharhuya Nurul-Abswar uk.153.

72. Al-Muutaswar Minal-Mukhtasar cha Abu Al-Mahaasim Al-Hanafiy uk.413.

73. Wasilatul-Maali Fiy Manaaqibil-Aal cha Sheikh Ahmad bin BakathyrAl-Makkiy Ashafiy.

74. Asnal-Matwalib Fiy Manaaqib Ali bin Abutwalib uk. 3, cha Al-JauziyDimishiq Ashafiy aliyefariki 833 A.H humo amepokea hadithi ya Ghadirkwa njia themanini na akasema: “……. Ni mutawatir kutoka kwa Nabii(s.a.w.w.) wameipokea kundi kubwa kutoka kwa kundi kubwa na walahazingatiwi aliyejaribu kuidhoofisha miongoni mwa asiyekuwa na ujuzi auelimu hii (yaani elimu ya hadithi).” Kisha aliyataja majina ya kundi lasahaba ambao wamepokea hadithi na katika yao ni Abu Bakr, Umar, Talha,Zubairi, Saad bin Abi Waqaasi, Abdur-Rahman bin Auf na wengineo.Kisha akasema: “Imethibiti vilevile kwamba kauli hii ilikuwa imetokakwa Nabii (s.a.w.w.) siku ya Ghadir Khum.”

75. Asnaal-Matwalib cha Al-Bairtiy Ashafiy uk. 227.76. Tashriful-Adhaana uk. 77 cha Haafidh Ali bin Muhammad bin As-

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 27

28

Iddi al-Ghadiyr

Sadiq Al-Hadharamiy na akasema: “Ama hadithi “Ambaye mimi ni kion-gozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” ni mutawatir kutoka kwa Nabii(s.a.w.w.) kutoka katika riwaya ya zaidi ya watu sitini, na kama tutatajasanadi zote tutarefusha sana.”77. Al-Uruwatul-Wuthuqah cha Sheikh Alau Diyn Asamnaniy aliyefariku736 A.H.78. Ansaabul-Ashiraf cha Baladhuriy.79. As-Swalatul-Faakhirah Bil-Ahaadithil-Mutawatir chapa ya misri uk.49 cha Mufti wa Sham Al-Haadi Al-Hanafiy.80.Tafsiru-Thaalabiy.

Msomaji mtukufu haya ni majina themanini ya vitabu na rejea zilizoandi-ka tukio la Ghadir tukufu na vyote ni vya maulamaa wa Kisunni namaimam wao na mahafidhi wao. Na jua kwamba mimi hapa sikutajavitabu vya rejea vya Shia hata kimoja ili msomaji asije akasema kuwa Shiapekee ndio waliotaja tukio la Ghadir. Hapana…. maulamaa wa Kisunnivilevile wametaja tukio hili la kihistoria. Kama ningetaka kutaja majina narejea za Kishia ambazo zinazungumzia tukio tukufu la Ghadir, idadiingekuwa kubwa mno, tukiongezea kwamba kuna rejea zingine za Kisunnihazikutajwa kabisa kwa ajili ya kufupisha kitabu, na anayetaka ziada yaufafanuzi ni juu yake kurejea juzuu ya kwanza katika kitabu cha Al-Ghadircha Sheikh Abdul-Husein Al-Amim.

Msomaji mtukufu baada ya kutaja rejea hizi na vitabu vinavyozingatiwa,je kumebakia nafasi ya kupinga uongozi wa Imam Ali ibn Abu Talib nakwamba ni yeye tu ndio Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na jeinajuzu kushikamana na asiyekuwa yeye katika ambao haikupokewakwake nasi (aya au Hadithi) wala dalili? “Ni kitu gani baada ya hakiisipokuwa ni upotovu.” “Hakika huu ni ukumbusho anayetaka afuatenjia kuelekea kwa Mola Wake.”

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 28

29

Iddi al-Ghadiyr

KUKAMILIKA KWA DINI

Tunarea tena kwenye mazungumzo kuhusu tukio la Ghadir tukufu tunase-ma: Kiapo cha utii kilipomalizika kwa Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.)na kabla watu hawajatawanyika aliteremka Jibril kwa Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) pamoja na Aya hii tukufu:

“Leo hii nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieeni neemazangu na nimekuridhieni Uislamu kuwa dini yenu.” (Surat Al-Maidah:3).

Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Allaahu Akbar kwa kukamilika dini, kutimianeema, na Mola Wangu ameridhia ujumbe wangu na uongozi wa Ali baadayangu.”

Ewe msomaji mtukufu wameafikiana wafasiri na wanahadithi wa kishiakuwa Aya hii ya kukamilika dini imeteremka siku ya Ghadir. Na wame-waunga mkono juu ya hilo kundi kubwa katika maulamaa wa Kisunni,mahafidhi wao na wanahadithi wao kati yao ni:-

Al-Haafidh mwana historia Ibnu Jarir Tabary aliyefariki 310 A.H. katikaKitabul-Wilaayah kwa sanadi yake kutoka kwa Zayd bin Arqam.

Al-Haafidh Ibnu Marduwaihi Al-Is’fahaaniy aliyefariki 410 A.H. kutokakwa Abu Said Al-Khuduriy kama ilivyo katika Tafsir Ibnu Kathir Juz. 2uk. 14.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 29

Al-Haafidh Jalaluddini As-Suyutwiy katika Tafsir yake Juz. 2, uk. 259kutoka kwa Abu Said Al-Khudiry na Abu Huraira.Al-Haafidh Abu Bakr Al-Khatib Al-Baghdadi katika Tarikh BaghdadJuz.8 uk. 290 kutoka kwa Abu Huraira.Al-Haafidh Al-Haskaaniy katika Shaawahidut-TanzilAl-Khatib Al-Khawarizimiy katika Al-Manaaqib uk. 80 na 94.Al-Juwainy Ashaafiy katika Faraid As-Samtwainy Juz.1.Al-Haafidh Ibnu Al-Maghaaziliy Ashaafiy katika Al-Manaqib, na wengi-neo.

Ewe msomaji mtukufu hakika Aya hii tukufu ya kukamilika dini inatufanyatuzinduke na kutazama baadhi ya nukta na misingi muhimu. MwenyeziMungu Mtukufu anasema: “Leo hii”: Tunaulizana ni siku gani hii, ambayoina utukfu mkubwa kiasi hiki kwa Mwenyezi Mungu hadi akamilishehumo dini?

Jawabu: Hakika ni siku ya Al-Ghadir tukufu, siku ya Ghadir yenye kudu-mu …siku ambayo alisherehekea Nabii (s.a.w.w.) kwa kumvika taji Ali ibnAbu Talib kwa taji la ukhalifa mtukufu na Uimam mkuu.

“Leo hii nimewakamilishieni dini yenu” hii ina maana kuwa dini ilikuwapungufu kabla ya siku hii, nayo ni siku ya Ghadir, siku ya kuteuliwa khal-ifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba dini imekamilika kwauongozi wa Ali na ukhalifa wake. Na maana ya hilo ni kwamba dini naimani bila ya Ali inazingatiwa kuwa ni pungufu, kama ambavyo dini naimani bila ya Mtume wa Mwenyezi Mungu inazingatiwa kuwa ni pungufuvilevile.

“Na nimewatimizieni neema Yangu.” Na neema hii ni uongofu uliokami-lika na uongozi uliokamilika ambao unapatikana kwa kumwaminiMwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola na Muhammad kuwa ndiye Nabii nakwamba Ali ndiye Imam. Na kwa maana nyingine ni kwamba uongofukamili unapatika kwa:- “La ilaaha ila llah, Muhammad Rasuulullah,

30

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 30

Aliyun Waliyullah.”

Na kana kwamba Mwenyezi Mungu anazingatia neema Zake zilizotangu-lia zilikuwa hazijakamilika kwa waja wake hadi “Siku” hiyo ambapo“Nimewatimizieni neema Zangu” kwa uongozi wa Ali ibn Abu Talib(a.s.).

“Na nimewaridhia Uislamu kuwa dini yenu” ndio ….Uislamu ambaounaotokana na Tauhid, Unabii na Uimam ndio unaoridhiwa na MwenyeziMungu Mtukufu, uislamu uliochanganywa na mapenzi ya Ahlul-bait, nakuitakidi uongozi wao na uma’sum wao.

Ama Uislamu ambao umeepukana na uongozi….umekosa kiungo chaitikadi ya Uimam wa Ahlul-baiti, na ambao umesimama katikakuwachukia Ahlul-baiti, huu unakataliwa mbele ya Mwenyezi Mungu nawala hauridhii (s.w.t.).

TAJI LA UKHALIFA.

Umeshafahamu ewe msomaji kwamba Mtume wa Mwnyezi Mungu(s.a.w.w.) alimfanya Imam Ali ibn Abu Talib kuwa khalifa wake katika sikuya Ghadir …….., ilikuwa ni ada na bado inaendelea kwa wafalme nawatawala kuwavika taji wale wanaotarajiwa kuwa watawala baada yao namakhalifa wao, kwa taji lililopambwa kwa dhahabu na kurembwa kwajohari na vito vya thamani, huwavisha siku ya kutawazwa kwao. Na kwakuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu hawadanganyiki kwa dhahabu, fedhana vinginevyo katika mapambo ya kimaada na wala hawajali mandharihaya yasiyo na thamani, pamoja na kwamba wana uwezo juu ya hayo nakutokushindwa kwao juu ya hilo....Mtume wa Mwenyezi Mungu – nayendiye bwana wa mawalii wa Mwenyezi Mungu - alikuwa ni mwenye kuya-pa mgongo mandhari haya na mwenye kupinga udanganyifu huu, nanimwenye kukubali maana ya kiroho, kwa sababu hii alimvika khalifa wake

31

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 31

kwa taji ambalo ni ghali kuliko mataji ya wafalme wote na ambalo ni borakuliko utajiri wa kilimwengu pamoja na urahisi wake…..

Alimvika kwa mikono yake mitukufu taji la ukhalifa mtukufu na uimammkuu, alimvika katika namna mahsusi kilemba chake kinachoitwa As-Sahaabah14, ikiashiria utukufu, ubora, utakatifu na haiba….. katika mku-sanyiko huo mkubwa, siku tukufu na sikukuu ya furaha. Katika sehemu hiianatusimulia Imam Ali (a.s.) juu ya kuvikwa taji hili tukufu la Nabii,anasema: “Alinivika kilemba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) sikuya Ghadir Khum kwa kilemba maalumu, akaiteremsha ncha yake kwenyebega langu na akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amenipa nguvu siku yaBadir na Hunaiyn kwa malaika wenye kuvaa kilemba hiki.”’15

Na kutoka kwake (a.s.) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)alimvika kilemba kwa mikono yake, kikaanguka nyuma na kuteremkiambele yake kisha Nabii akasema: “Geuka nyuma,” akageka kishaakamwambia: “Geuka mbele,” akageuka na akawageukia sahaba zakeakasema: “Hivi ndivyo linavyokuwa taji la Malaika.”

Ibnu Abbas anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomvika Ali (a.s)kilemba alisema: ‘Ewe Ali kilemba ni taji la Waarabu.”’16 Al-Halbiyanasema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kilemba kinachoitwa As-Sahabahalimvika Ali ibn Abu Talib, na Ali alipokuwa akitokeza kwake basi anase-ma (s.a.w.w.): ‘Amekujieni Ali akiwa ndani ya As-Sahabah.’ Yaani kilem-ba chake ambacho alimpa.”17

32

Iddi al-Ghadiyr

14 Wanahistoria wanasema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)alikipa jina mahsusi kila kitu kilichofungamana naye mfano: Kilemba chake aliki-ita As-Sahaabah, na fimbo yake aliita Mamshuq na ngamia wake alimwiita Al-Adhabau, n.k.15 Fusulul-Muhimah cha Ibnu As-Swibagha Al-Malikiy uk. 27.16 Kitabul-Ghadir Juz.1 uk. 290.17 Siratul-Halabiy Juz. 3 uk. 369.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 32

SHAHADA YA TATU KATIKA ADHANA

Baada ya tukio la Ghadir……….uliwadia wakati wa swala akasimamasahaba mtukufu Abu Dhar Al-Ghafaary au Bilal na akaadhini kwa ajili yaSwala. Na katika adhana baada ya kauli yake: “Ash’hadu annaMuhammadan Rasuulullah” akaongeza “Ash’hadu anna AliyanWaliyullah.” Wanafiki na wapinzani wakafanya haraka kwenda kwaMtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wakalalamikia waliyoyasikiakutoka kwa Abu Dhar au Bilal, na wao wakawa wanasubiri kukemewahuyu mwadhini na kumkataza kutokana na ziada hii, isipokuwa Nabii(s.a.w.w.) akaelekeza lawama na makemeo kwao akasema: “Je hamkufa-hamu hotuba yangu hii juu ya uongozi wa Ali? Je hamkusikia kauli yangukuhusu Abu Dhar kuwa: Haikufunika mbingu wala hajatembea ardhinimkweli wa kauli kuliko Abu Dhar?” Kisha akawaambia: “Hakika nyinyimtageuka baada yangu kwa visigino vyenu.”18

Na katika mjadala huu umemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)anaafiki ziada hii na anaikubali, na tambua kuwa ridhaa ya ma’sum ni hoja,na anaipitisha ili iwe ni sehemu katika adhana na itajwe kila linapotajwajina la Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kila unapokuja utajo wa Laailaaha illa llahu na Muhammad Rasuulullah.

Na kuna ihtimali kuwa Nabii mwenyewe ndiye aliyemwamuru Abu Dharau Bilal kwa ziada hii katika adhana kwa kujua kwake kuwa wanafikiwatakosoa hatua hii tukufu, na Mtume (s.a.w.w.) akajibu ukosoaji wao nakupitisha maneno ya Abu Dhari.

33

Iddi al-Ghadiyr

18 Kitabu Salaafah Fiy Amril-Khilaafah cha Sheikh Abdullaah Al-Maraaghiy.Naye ni kati ya maulamaa wa Kisunni katika karne ya saba hijiria, na amemtajaSheikh Abdul-Adhim Ar-Rabiy katika kitabu As-Siyaasatul-Hussainiyah uk. 108

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 33

Na unona jinsi Mtume wa Mwenyezi Mungu alivyotilia mkazo kuwapingawale waliokosoa na akawaambia: “Je hamkufahamu hotuba yangu hii juuya uongozi wa Ali?” Yaani nini maana ya hotuba hiyo ndefu ambayo nili-itoa kwenu katika hali ya joto kali na jangwa lenye kuwaka? Na anazidikuwapinga kwa ukali wake: “Je hamkusikia kauli yangu kuhusu Abu Dharkuwa: Haikufunika mbingu wala hajatembea ardhini mkweli wa kaulikuliko Abu Dhar?” Yaani Abu Dhar hafanyi upuuzi bali yeye ni mkwelimwaminifu hasemi isipokuwa ukweli, basi ni kwa nini mkaja kuni-lalamikia juu yake? Kisha Mtume (s.a.w.w.) akafichua kuhusu uhakika wawale wakosoaji na hatima yao kwa kauli yake: “Hakika nyinyi mtageukabaada yangu kwa visigino vyenu.” Yaani: hakika nyinyi mtapotoka baadayangu na kumwaasi khalifa wangu na mwisho wenu utakuwa mbaya, kanakwamba Mtume (s.a.w.w.) ameashiria kwa kauli yake kwenye kauli yaMwenyezi Mungu.

“Hakuwa Muhammad isipokuwa ni Mtume wameshapita kabla yakeMitume, je akifa au akiuliwa mtageuka nyuma kwa visigino vyenu, naatakaegeuka kwa visigino vyake hatomdhuru Mwenyezi Mungu cho-chote na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.” (Surat Al-Imran: 144).

Na maana ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kwam-ba Imam Ali ibn Abu Talib ni nguzo ya tatu katika dini baada ya MwenyeziMungu na Mtume Wake, na kwamba uimam ndio nguzo ya tatu ya kiisla-mu baada ya Tauhidi na Unabii. Ndugu yangu msomaji! Zaidi ya hadithiiliyotajwa kuna hadithi zingine zinaamrisha shahada ya tatu nayo ni kuse-ma: “Ash’hadu anna Aliyan Waliyullah” baada ya shahada mbili. Na kwa

34

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 34

kutazama umuhimu wa maudhui haya na wingi wa maswali juu ya hilobasi inafaa na ni dharura sana tuzungumze juu ya hili kwa ufafanuzi kishaturejee ili tuendelee na mazungumzo yanayohusiana na tukio tukufu laGhadir.

MWENYEZI MUNGU NASHAHADA YA TATU.

Hakika wa kwanza aliyeamrisha kutajwa Imam Ali baada ya shahada mbilini Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imepokewa kutoka kwa Imam As-Sadiq(a.s.) kwamba amesema: “Alipoumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhialimwamuru mwenye kunadi na akanadi: ‘Ash’hadu an laa ilaaha illallahu’ mara tatu. ‘Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah’ mara tatu. NaAsh’hadu anna Aliyan Amirul-Mu’minin haqan’ mara tatu.”19

Tunaulizana: Kwa nini Mwenyezi Mungu ameamuru miito hii mitatu kwapamoja? Na hiyo inaonyesha nini? Je, haionyeshi umuhimu wa mafunga-mano ya shahada hizi mbili na shahada ya tatu? Je, haionyeshi kwambaimani ni wajibu ikite juu ya shahada hizi tatu? – Jawabu ni ndio…. hivyondivyo.

Tunarejea ili tutilie mkazo kwamba muumini katika mantiki ya MwenyeziMungu na Mtume Wake ni yule ambaye anaamini kwa kauli na kitendoLaa ilaaha ila llahu, Muhammadu Rasulullaah, Aliyun Amirul-Mu’mininWaliyullah. Kinyume cha hivi sio muumini bali ni mwislamu, hivyo inahi-fadhiwa kwa shahada mbili damu yake tu, mali yake na heshima yake.

Aya zote za Qur’ani ambazo zinaanza kwa tamko “Enyi mlioamini” kwahakika zinawahutubia walioamini shahada hizi tatu kwa pamoja.

35

Iddi al-Ghadiyr

19 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 295. Na inayokaribiana na hiyo ni ile iliyomo kati-ka Amaal cha As-Saduuq, majlis ya 88. Kwa nyongeza, rejea Surat al-Maida, ayaya 55, kwenye sababu ya kushuka kwa aya utakudhihirikia ukweli huu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 35

Muhtasari wa mazungumzo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu haku-tosheka na shahada mbili bali aliamuru mlinganiaji wake aunganishepamoja na hizo, shahada ya Amirul-Mu’minin kwa kutangaza uongoziwake, na hii ni dalili juu ya umuhimu wa kuleta shahada ya tatu kilaunapokuja utajo wa Mwenyrezi Mungu na Mtume Wake.

MTUME WA MWENYEZI MUNGU NASHAHADA YA TATU

Ama kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), hadithi zimepokewakutoka kwake zikihusu Sunna ya kumtaja Imam Ali (a.s.) kila unapokujautajo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Katika yafuatayo tunatajamifano hiyo:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mwenye kusema:‘Laa ilaaha ila llahu’ inafunguka kwake milango ya mbingu. Na mwenyekufuatiliza kusema Muhammad Rasulullah unakunjuka uso wa haki tuku-fu20 na anafurahika kwa hilo. Na mwenye kuifuatilizia kwa Aliyun Waliyullaahi, Mwenyezi Mungu anamsamehe dhambi zake hata kama ni kamaidadi ya matone ya mvua.”

Hakika hadithi inaeleza waziwazi kujuzu kutaja jina la Imam Ali (a.s.)baada ya kumtaja Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila ya kutofautishabaina ya adhana na pinginepo bali ni kwa jumla na inahusu sehemu zote.

36

Iddi al-Ghadiyr

20 Haki hapa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu na hakuna shaka kwamba kauli yake:“unakunjuka uso wa haki” ni katika upande wa majazi na sio wa uhakika, kwasababu imeshathibiti katika nuru ya Qur’ani na akili kwamba Mwenyezi Munguhana mwili wala hana viungo, na kauli yake “unakunjuka uso wa haki” ni kinayaya ridhaa ya Mwenyezi Mungu kwa kauli hii. Nayo ni kumtaja Imam Ali baadaya kumtaja Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kauli hii. Na kuenea rehema yakeMwenyezi Mungu na maghufira yake kwa mwenye kusema hivyo. Na aina hii yamajazi ni nyingi katika Qur’ani tukufu na hadithi tukufu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 36

Bali hadithi hii inaonyesha Sunna ya utajo huu, kutajwa kwake na uborawake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa ajili hii amesemaMtume (s.a.w.w.): “Na mwenye kuifuatilizia kwa Aliyun Waliyu llaahi,Mwenyezi Mungu anamsamehe dhambi zake hata kama ni kama idadi yamatone ya mvua.”21

Je, baada ya haya; mosi tunahitaji dalili juu ya kujuzu? Pili dalili ya kuwani sunna? Je, yanafahamika maneno yaliyo dhahiri na wazi kuliko manenoya hitimisho la Manabii? Na kama sentensi hii haikuwa ni yenye kuridhi-wa kwa Mwenyezi Mungu, je Mwenyezi Mungu angesamehe madhambiya mwenye kuisema, hata kama ni kama vile idadi ya matone ya mvua?

Hakika Mwenyezi Mungu anawalingania waislamu kwa ulimi wa MtumeWake wote waseme: Aliyun Waliyullahi kila wanaposema Laa ilaaha ilallahu Muhammadu Rasulullah katika adhana na kunginepo. Na kuna ihti-mali kuwa yeye mwenyewe alimwamuru mwadhini kwa hatua hii tukufuna uwezekano huu hauko mbali kwa sababu sahaba mtukufu kama vileAbu Dhar au Bilal hawezi kufanya hivyo mwenyewe. Bali ni lazima kunamoja kati ya mawili: Ima itakuwa Nabii alimwamuru na au yeye alifahamuhivyo kutokana na hotuba ya Al-Ghadir na kisha Nabii akaipongeza naakaipitisha hatua yake na akaiafiki. Vyovyote iwavyo hata kamakusingekuwa na dalili juu ya kujuzu Sunna ya kutaja jina la Imam Ali (a.s.)katika adhana na penginepo isipokuwa ni kuwa hadithi ya Nabii iliyotan-gulia ingetosha kuwa ni dalili na hoja kwa ambaye moyo wake una marad-hi.

Ewe msomaji mtukufu, katika hadithi zilizotajwa katika maudhui haya niile ambayo imepokewa kwamba jamaa miongoni mwa waarabu, waajemi,waqibti na wahabeshi walihudhuria kwa Nabii (s.a.w.w.) na akawaambia:“Je mmekubali kushuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa MwenyeziMungu peke Yake hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake na

37

Iddi al-Ghadiyr

21 Biharul-An’war Juz. 38 uk. 318.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 37

Mtume Wake, na kwamba Ali ibn Abu Talib ni Amirul-Mu’minin na kion-gozi baada yangu?” Wakasema ndio. Mtume (s.a.w.w.) akakariri mara tatuna wao wakashuhudia hivyo.22

Kutokana na hadithi hii tunafahamu upeo wa kuuliza Nabii juu yaumuhimu wa shahada ya tatu na kwamba ndio yenye kukamilisha shahadambili. Mtume (s.a.w.w.) hakutosheka kwa kukubali kwao mara moja balialikariri mara tatu ili wafahamu vizuri kwamba imani inakita katika sha-hada hii ya tatu, na kwamba kujitenga nayo ni kama vile kujitenga na sha-hada zote, na hiyo inazingatiwa kuwa ni upotofu mkubwa. AmesemaMtume wa Mwnyezi Mungu (s.a.w.w.): “Naapa kwa aliyenituma kwa hakikuwa ni mwenye kubashiri, haikutulia Kursiyu, Arshi wala hazikuzungukasayari na wala hazikusimama mbingu na ardhi hadi Mwenyezi Mungualipoziandika Laa ilaaha ila llahu Muhammadu Rasulullah Aliyun Amirul-Mu’minin.”23

AHLUL-BAIT NA SHAHADA YA TATU

Njoo pamoja na mimi ewe msomaji kwenye historia ya Ahlul-bait ambaoMwenyezi Mungu amewahifadhi kutokana na uchafu na akawatakasakabisa …. ambapo utakuta kwamba wao walikuwa wanakariri maneno yababu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wote ni nuru moja.Huyu hapa Imam Jafar As-Sadiq mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Munguna khalifa wake wa sita wa kisheria ameamuru kumtaja Imam Ali (a.s.) kilaunapokuja utajo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Imepokewa kuto-ka kwa Qasim bin Muawiya amesema: “Nilimwambia Abu Abdillah As-Sadiq (a.s.) hawa24 wanapokea katika miraji yao kwamba Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipopelekwa miraji aliona katika arshi

38

Iddi al-Ghadiyr

22 Kitabu Al-Aamal cha As-Saduq uk. 230 majlis ya 60.23 Biharul-An’war Juz. 27 uk. 8.24 Anakusudia kwa “hawa” wapinzani wa Ahlul-bait (a.s.).

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 38

(maandishi ya) Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullah, Abubakari As-Swiddiq. Imam akasema: ‘Subhanallaah! Wamebadilisha kila kitu na hilipia?’25 Nikasema ndio.

Akasema (a.s.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoumba Arshialiandika nguzo zake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah AliyunAmirul–Mu’minina. Alipoumba Kursiyu akaandika: Laa ilaaha ila llahuMuhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba lawhu akaandika: Laa ilaaha ila llahu Muhammad RasulullaahAliyun Amirul–Mu’minina. Alipomuumba Israfiyl akaandika kwenye paji lake: Laa ilaaha ila llahuMuhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipomuumba Jibril akaandika katika ubawa wake: Laa ilaaha ila llahuMuhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba milima akaandika juu ya vilele vyake: Laa ilaaha ila llahuMuhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba jua akaandika juu yake: Laa ilaaha ila llahu MuhammadRasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba mwezi akaandika juu yake: Laa ilaaha ila llahu MuhammadRasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina.”’

Ewe msomaji! Tazama sentensi hii vizuri: “Kisha akasema (a.s.):‘Atakaposema mmoja wenu: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaahbasi aseme: Aliyun Amirul–Mu’minina Waliyu llahi.”’26

39

Iddi al-Ghadiyr

25 Sentensi hii katika maneno ya Imam As-Sadiq inatufunulia pazia la uzushimuovu ambao wameufanya wahalifu katika hadithi za Nabii kwa ajili ya kuwa-tengenezea watu wao sifa takatifu mkabala wa walizonazo Ahlul-bait katikashakhsiyah, uchamungu na utukufu waliopewa na Mwenyezi Mungu. Hivyo (a.s.)kwa mshangao akasema: “Subhanallaah wamebadilisha kila kitu hata hili pia?”Hapa unajua ukweli wa hadithi ya “watu kumi waliobashiriwa pepo” na mfanowake kuwa ni katika hadithi za uongo.26 Biharul-An’ar Juz. 27 uk. 1.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 39

Ni utukufu ulioje wa hadithi hii. Hakika ni hadithi tukufu inatubashiriaumuhimu wa kuiweka shahada ya tatu pamoja na shahada mbili katikasehemu zote. Tazama ewe msomaji jinsi Mwenyezi Mungu alivyotiliamkazo jina la Imam Ali (a.s.) kila ulipokuja utajo wake na utajo wa MtumeWake (s.a.w.w.).

Mkazo wote huu ni wa nini ? Ni wa nini msisitizo huu katika kuandika jinala Imam Ali (a.s) katika Kursiyu, Lawhu, paji la Israfyli, ubawa wa Jibrilu,ncha za mbingu, tabaka za ardhi, na vilele vya milima na kwenye jua namwezi? Je, katika haya yote sio dalili ya kutakiwa kutaja jina la Imam Ali(a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu? Kisha wewe umeona kwam-ba Imam As-Sadiq (a.s.) anaamuru kwa kuelewa somo hili kutoka kwaMwenyezi Mungu Mtukufu na kusema: “Atakaposema mmoja wenu: Laailaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah basi aseme: AliyunAmirul–Muuminina Waliyu llahi.”’27

Na amri hii ni ya jumla inahusu adhana na penginepo. Amesema Sheikhul-Islaam Al-Majlisy baada ya kuashiria hadithi hii: “Inaonyesha juu yaSunna ya hilo kwa ujumla, na adhana ni katika sehemu hizo, na imeshapi-ta mifano ya hadithi hii katika mlango wa fadhila zake (a.s.).”28

FATWA ZA MAULAMAA

Kwa kutegemea hadithi hizi tukufu na mifano ya hizo na nyinginezo kati-ka dalili, maulamaa wa dini na mafaqihi wa sheria wametoa fatwa yakujuzu kusema: “Ash’hadu anna Aliyan Amirul-Mu’minin Waliyu llah”katika adhana. Bali limetoa fatwa kundi kubwa kati yao juu ya Sunna yahilo na kupendeza kwake, na wengine wametoa fatwa ya wajibu wake kwaanuani ya hukumu ya dharura (thanawiy) katika zama hizi. Baadhi ya

40

Iddi al-Ghadiyr

27 Biharul-An’ar Juz. 27 uk. 1.28 Biharul-An’war Juz. 48 Kitabu Swalatu uk.111.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 40

maulamaa wameandika vitabu maalumu juu ya shahada hii na dalili yakujuzu kwake, kuwa kwake Sunna na kupendeza kwake.29

Amesema Sheikh Muhammad Hasan mwandishi wa kitabu Al-Jawaahirkinachohusu fiqhi na ambacho kinazingatiwa kuwa ni katika vitabu vikub-wa vya rejea vya kifiqhi na humo ndimo imo duru ya ijitihadi na istimbati,amesema katika risala ya Risalaatun-Najatil-Ibaadi anapozungumziaadhana: “Ni Sunna kumswalia Mtume na ahali zake – wakati wa kutajwajina lake - na kukamilisha shahada mbili kwa Shahada ya Ali (a.s.) kuwayeye ni walii wa Mwenyezi Mungu, na shahada ya kuwa yeye ni kiongoziwa waumini, hiyo ni katika adhana na penginepo.”

Amesema Seyyid Al-Hakim: “Hakuna ubaya kuleta Shahada ya wilayah,kwa makusudio ya Sunna isiyo na mipaka, hiyo ni kutokana na habari iliy-omo ndani ya Al-Ihtijaj: “Atakaposema mmoja wenu Laa ilaaha ila llahuMuhammad Rasulullah basi aseme: Aliyun Amirul-Mu’minin.” Bali hilo –katika zama hizi – linahesabiwa ni katika alama ya imani na nembo yaushia, hivyo kwa upande huu inakuwa ni yenye kupendeza kisheria baliwakati mwingine inakuwa ni wajibu.”30

Kwa muhtasari ni kuwa ilivyo mashuhuri kwa mafaqihi na maulamaa nikwamba Shahada ya tatu inapendeza na ni wajibu kuileta katika adhanakwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bali tumetajabaadhi ya maneno ya maulamaa (Mwenyezi Mungu awarehemu) kama

41

Iddi al-Ghadiyr

29 Katika walioandika katika maudhui haya ni Allamah As-Sayid Abdur-RazaqAl–Musawiy Al-Muqarram, ameandika kitabu maalumu kuhusu nembo hii tukufuamekiita Sirul-Imaan na ameshataja katika kitabu chake hiki majina yanayozidisabini ya mafaqihi miongoni mwa mafaqihi wa sheria na maulamaa wa dini, nawote wanatoa fatwa ya kujuzu Shahada hii au kuwa kwake Sunna, au kuwa kwakewajibu. Mwenyezi Mungu amlipe mema As-Sayid Al-Muqarram kwa ajili ya hakina watu wake. 30 Mustamsaku–Wuthqa cha Ayatullah Al-Hakim.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 41

mifano katika yaliyotoka kwao miongoni mwa fatwa kuhusu maudhuihaya.

Baada ya yote haya yaliyotangulia tunasema: Hayo ni maneno yaMwenyezi Mungu, na ni hizo hadithi za Mtume Wake, na zile ni hadhi zamaimam watukufu, na hizi ni fatwa za maulamaa, je baada ya yote hayokunabaki nafasi ya kutuhumu na kusema kuwa ni bidaa? Kwa faida zaiditumeona ni bora tunukuu baadhi ya maneno ya mtunzi wa kitabu hikikatikka utangulizi wake katika kitabu cha Sirul-Imani cha Allaamah Al-Muhaqiq Al-Kabir Seyyid Abdur-Razaq Al-Musawiy Al-Muqarram. Naifuatayo ni nukuu hiyo.

KISIMAMO PAMOJA NASHEIKH AS-SUDUUQ.

Kila aliyesimama dhidi ya Shahada ya tatu katika adhana ameathirikakutokana na maneno ya Sheikh As-Suduq katika maudhui haya, ambapoameinasibisha Shahada ya tatu katika adhana kwa Al-Mufawidhah,akawalaani na akajiweka mbali nao na akasema: “…..na Al-Mufawidhah,Mungu awalaani!! Wamezua habari na wameongeza katika adhana:“Muhammad wa Aali Muhammad Khairul-Bariyah” mara mbili. Na katikabaadhi ya riwaya zao ni kuwa baada ya: “Ash’hadu anna MuhammadanRasulullaahi” ni “Ash’hadu anna Aliyan Waliyullaah” mara mbili. Na katiyao kuna waliopokea badala ya hayo: “Ash’hadu anna Aliyan Amirul-Mu’minin haqan haqan” mara mbili ……” hadi mwisho wa manenoyake.31

Haya…… na katika kutafakari katika maneno ya Sheikhe As-Suduquyanatubainikia yafuatayo:- Kwanza: Kwa hakika kuna hadithi tukufu zilizopokewa kuhusu Shahadaya tatu katika adhana, lakini As-Suduqu amehukumu kuwa ni za uongo na

42

Iddi al-Ghadiyr

31 Man Laa Yahdhuruhu Al-Faqihi: Kitabu cha Swala, mlango wa Adhana.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 42

amekataa kutaja hadithi zake, wapokezi wake na sanadi zake. Na hii bilashaka sio njia ya istidilali wala sio mtindo wa utafiti na ijitihadi bali mtin-do unaofuatwa na maulamaa na mafaqihi ni kutaja hadithi kwa sanadi zakena wapokezi wake kwanza, kisha kuzihukumu kwa usahihi au kwa ubovu,kuzikubali au kuzipinga, pamoja na kubainisha mtazamo wao wakati wakubainisha sehemu za mushikeli na udhaifu katika sanadi au matini auhoja.

Ama kuacha kuzitaja kabisa na kuziba njia kwa wanaokuja miongoni mwamaulamaa na muhadithina ili wasizione na kutoa maoni yao kwa mnasabawa hadithi hizo, hii sio sahihi. Kwa sababu hii amesema mmoja wamaulamaa wetu naye ni Al-Faqihi Al-Kabir Sheikh Abdun-Nabiy Al-Iraqiy(Mwenyezi Mungu amrehemu)32 katika kuyaelezea maneno yaAs–Suduq: “Hakusema yeyote katika Imamiyah kwamba katika sharti lahabari kuwa hoja ni As-Suduq kuifanyia kazi au kutoipinga, hakunamafugamano ya kukataa kwake au kukubali kwake na masuala ya habariya wapokezi wachache kuwa hoja, hii ni katika mapito yao mengi. Kwaniyeye - yaani As-Suduq – anazo fatwa za ajabu nyingi hakuziafiki yeyotekati ya maulamaa, kama vile masuala ya Nabii kusahau33 na akatupahadithi ambazo zinasema haisihi Nabii (s.a.w.w.) kusahau, uwajibu waHijja kwa kila mwenye kuweza kila mwaka, kujuzu udhu na kuoga kwamaji mudhafu, utohara wa damu ikiwa ni kwa kiwango cha khumsi, utoharawa pombe, na kutonajisika maji machache kwa kukutana na najisi …..kama zitakusanya fatwa zake za ajabu zitakuwa ni kitabu kikubwa kamaambavyo tumeashiria. Kwa ajili hiyo amesema Sheikh Al- Baharain katikaAl-Hadaiq katika masuala ya maji mudhafu: ‘Hakika As-Suduq hakuwama’sum hadi kauli yake iwe ni hoja kwa asiye kuwa yeye au ilazimu kui-fuata.”’

43

Iddi al-Ghadiyr

32 Katika Risalutul-Hidayah anapozungumzia kuhusu shahada ya tatu ya uwaliikuwa ni sehemu ya adhana na iqama kama zilivyo sehemu zingine. uk. 39.

33 Maneno mazuri yalioje aliyoyasema mmoja wa Maulamaa: “Suduqu amesahaukwamba Nabii ni ma’sum hivyo hasahau.”

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 43

Pili: Hakika Sheikh As-Suduq amezinasibisha kwa mufawidhah hadithihizo ambazo zinathibitisha kuwa shahada ya tatu ni katika adhana.Tunaulizana: Al-Mufawidhah ni nani? Jawabu: Hakika Al-Mufawidhahkwa As-Suduq ni tofauti kabisa na Al-Mufawidhah waliotajwa katikavitabu, wewe ukirejea vitabu ambavyo vinawaeleza Al-Mufawidhah utaonavinasema: Al-Mufawidhah ni watu waliosema kwamba Mwenyezi Munguamemuumba Muhammad na akamwachia kuumba dunia, hivyo yeye nimuumbaji wa vilivyo humo. Na inasemekana amemwachia hilo Ali. Nakatika hadithi nyingine imekuja: “Mwenye kusema juu ya tafwidhi ame-shamtoa Mwenyezi Mungu katika mamlaka yake.”34

Hii ndio maana ya Al-Mufawidhah iliyotajwa katika vitabu, lakini SheikhAs-Suduq anasema: “….. hakika Al-Ghulat na Al-Mufawidhah MwenyeziMungu awalaani!! wanapinga kusahau kwa Nabii (s.a.w.w.) na wanasema:Kama ingejuzu kusahau katika Swala ingejuzu kusahau katika tablighi,kwa sababu Swala ni faradhi kwake kama ambavyo talibighi ni faradhikwake.”35

Inadhihirika katika maneno yake kwamba kila anayemwamini Nabii naahali zake watoharifu itikadi kamili iliyokita na sahihi kabisa basi ni kati-ka Ghulat na Mufawidhah, kwa sababu hiyo unamuona anawalaaniMufawidhah wanaoamini kutosahau kwa Nabii (s.a.w.w.). Na Shia wote -tangu siku ya kwanza - wanaitakidi kutosahau kwa Nabii na wanampingakila anayesema kuwa Nabii anasahau. Na katika maudhui haya anasemaSheikh wetu Al-Majlisiy wa kwanza, At-Taqih Al-Kabir SheikhMuhammad Taqiy: “…….ambayo yanadhihiri kwake - kama itakavyokuja– yeye (yaani As-Suduq) anasema: Kila asiyesema kuwa Nabii anasahaubasi yeye ni katika Al-Mufawidhah, kama ni hawa basi ni Shia woteisipokuwa As-Suduq na Sheikh wake, na kama sio hawa basi hatujui mad-hehebu yao hadi tuwanasibishie uzushi na laana.”36

44

Iddi al-Ghadiyr

34 Majmaul-Bahrain Juz. 223, madatu: Fawadha.35 Man Laa Yahdhuruhu Al-Faqihi Juz. 1, uk. 359.36 Raudhatul-Mutaqiyna Juz. 2 uk. 245.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 44

Tatu: Inadhihiri katika maneno ya Sheikh As-Suduqu kuhusu shahada yatatu kwamba ilikuwepo katika adhana katika zama yake, yaani katika karneya nne hijiria na Shia wakati huo walikuwa wako karibu na zama yaGhaibu fupi (Ghaibatus-Sughura) na mawakala wanne waliowekwa naImam Al-Hujjah Al-Mahdi (a.s.), hivyo kama shahada ya tatu ingekuwa nibidaa katika adhana basi lingetoka katazo juu ya hilo kutoka kwa Imam Al-Mahdi (a.s.) kama ambavyo ilikuwa ni ada iliyozoeleka kutoka makatazo,ya kujiepusha na watu waovu, bidaa na batili, kama vile As-Shalmaghaniyna mfano wake. Bali inaonyesha kwamba jambo hili lilikuwa ni lenyekuafikiwa na Shia na hapakuwa na tofauti yeyote baina yao kuhusu shaha-da ya tatu katika adhana, hadi alipokuja Sheikh As-Suduq na akanyanyuabendera ya khilafu. Na sisi wakati tunamtazama sheikh As-Suduq kwamtazamo wa heshima na utukufu hilo halituzuii sisi kujadili maoni yakeambayo ni mahsusi kwake kama ilivyo adabu ya maulamaa na mafaqihi wazamani hadi wa leo.

SWALI NA JAWABU

Muulizaji anaweza kuuliza na kusema: Tumekubali kupokewa habari nahadithi tukufu juu ya shahada ya tatu katika adhana lakini vipi tunawezakuzitegemea na kusema kuwa ni sahihi?

Jawabu: Sheikh At-Tuusiy ambaye ameitwa Sheikh madhehebuamezieleza habari hizo na hadithi hizo kuwa ni Shaadhu na maana yaShaadhu hapa ni hadithi ambayo ameipokea mpokezi mkweli na ikawainapingana na yaliyopokewa na jamhuri, na hili ni dalili kuwa hadithi hiyoni sahihi lakini mafaqihi hawakuifanyia kazi. Hivyo Sheikh At-Tuusiyamethibitisha usahihi wa hadithi hizo tukufu. Zaidi ya hapo ni ile kanuniya kuzifumbia macho (Tasaamuhu) hoja za Sunna, kanuni hii inakubalikabaina ya maulamaa na mafiqihi wa zamani na wa leo.” Mwisho wakunukuu.

45

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 45

NEMBO YA SHIA

Haya maneno: Ash’hadu anna Aliyan Waliyullahi yameshakuwa ni nemboya waislamu Mashia, wafuasi wa Ahul-bait (a.s.) wameshikamana nayokatika adhana na iqamah, na katika sehemu mbalimbali za kidini kwakumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na kwa sababu hiyo wamepa-ta upinzani na shutuma, lakini wao wamevumilia kwa ajili yake na wamek-abiliana nazo na wamezidi kuwa na imani na mshikamano na nembo hii yaMwenyezi Mungu, kwa sababu wao wanajua kuwa ni haki na hakunabaada ya haki isipokuwa upotovu, na ni juu ya kila mwislamu anayejilaz-imisha kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wakeashikamane na nembo hii na ailete katika adhana na penginepo.Tahadhari…tahadhari asije akaiacha, hivyo akawa katika wale aliowaam-bia Mtume (s.a.w.w.): “Hakika nyinyi ni wenye kugeuka nyuma baadayangu kwa visigino vyenu.”

Ewe msomaji mtukufu! Tumezungumza sana kuhusu maudhui haya kwakuangalia umuhimu wake mkubwa, na sasa tunarejea ili tuendelee namazungumzo yetu yanayohusiana na tukio la Ghadir.

KOMBORA LA MBINGUNI

Habari ya Ghadir ilisambaa katika kila pembe na yakawa ndio mazungum-zo baina ya watu na waislamu wakawa wanamwita Imam Ali (a.s.) Amirul-Mu’minin baada ya tukio hilo. Ndipo mwanaume katika mabedui mwenyehasira, jina lake ni Nu’uman bin Harith Al-Fihriy ambaye alikuwa ni aduiwa Ali (a.s.) na ni mwenye chuki na Ahlul-bait (a.s.) ikamfikia habari yaGhadir na Nabii kumteua Ali kuwa khalifa baada yake, basi hilo halikum-furahisha na ndipo munkari wa kishetani ukampanda na akaonekanakwamba chuki inamchomachoma na shari inamsukuma kwenda kwa Nabii(s.a.w.w.) ili kupinga hatua hii tukufu.

46

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 46

Jahili huyu hakujua kuwa hatua ya Mtume na maamuzi yake ni kutoka kwaMwenyezi Mungu Mtukufu, na kana kwamba amesahau au ameghafilikakwamba Nabii (s.a.w.w.) hakubali rai ya yeyote mbele ya amri yaMwenyezi Mungu. Nabii (s.a.w.w.) alikuwa anaswali katika hema na ndipoalipowasili huyu bedui mwasi na akasimamisha farasi wake mlangoni naakaingia kwa kiburi na chuki na akasimama mbele ya Nabii akisema: “EweMuhammad!” Nabii akanyanyua kichwa chake kwa huyu katili ambayeamemwita Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa jina lake. Je, MwenyeziMungu hakuwakataza waislamu kumwita Nabii kwa jina lake binafsi. Je,Mwenyezi Mungu Mtukufu hakusema: “Msimwite Mtume kama baadhiwanavyowaita baadhi yao.” Na akasema: “Lakini ni Mtume waMwenyezi Mungu na hitimisho la Manabii.”?

Nabii (s.a.w.w.) aliona kwamba ni mwanaume wa kibedui ambaye badohajawa na adabu ya kiislamu na wala bado hajawa na utamaduni wa imani,kwa sababu hiyo Mtume (s.a.w.w.) alianza kusikiliza maneno ya huyubedui: “Ewe Muhammad umetuamuru tushuhudie kwamba hakuna Munguisipokuwa Mwenyezi Mungu, tukakubali. Umetuamuru kwambatushuhudie kwamba wewe ni Mtume wa Mweneyzi Mungu tukakubali nakatika nyoyo zetu kukiwa na kitu. Umetuamrisha tutoe Zaka, tufunge natuhiji tukakubali. Hukuridhika kwa hayo hadi ukanyanyua mkono wamtoto wa ami yako na ukamfadhilisha juu yetu, na ukasema: ‘Ambayemimi ni kiongozi wake basi Ali ni Kiongozi wake.’ Je, hili ni jambo kuto-ka kwako au ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu?”

Eeh, ni uovu mbaya ulioje? Ewe mwenye ukosefu wa adabu na uchache wahaya! Je, huu ni utaratibu wa kumuuliza hitimisho la Manabii? LakiniNabii (s.a.w.w.) alimgeukia na akaanza kumsikiliza kwa upole, tabia nzurina mantiki ya hekima kwa kusema: “Ee! Naapa kwa ambaye hakunaMungu isipokuwa Yeye, hakika hili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”

Sasa itakuwaje? Je, kinachotakiwa si kutii na kusalimu amri? Je, si niwajibu kuridhia na kufuata? Lakini bedui akaondoka akielekea kwenye

47

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 47

farasi wake huku akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu kama haya anayoy-asema Muhammad ni kweli basi tuteremshie mvua ya mawe kutoka mbin-guni au tuletee adhabu kali.” Hakukamilisha dua yake hadi MwenyeziMungu akamtupia jiwe dogo kutoka mbinguni, akamwangushia juu yakichwa chake na likatokea nyuma, mwanaume mkaidi akaanguka juu yaardhi hali ya kuwa ni maiti. Na hapo wahyi ukashuka kwa Mtume waMwenyezi Mungu kwa kusema:

“Muulizaji ameuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya makafirihakuna awezaye kuizuia. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenyeutukufu wa daraja.” (Surat Al-Maa’riji: 1 - 3.)

Nabii (s.a.w.w.) akawaambia sahaba zake: “Mmeona?” Wakasema ndiotumeona. Akasema: “Mmesikia?” Wakasema ndio tumesikia. Akasema:“Ni wema kwa mwenye kumtawalisha na maangamio ni kwa mwenyekumchukia, kana kwamba namwangalia Ali na wafuasi wake wamepandakatika ngamia za peponi, vijana wamevalishwa taji wamepakwa wanjahawana hofu wala huzuni, wameridhiwa na Mwenyezi Mungu, na hiyo nikufaulu kukubwa.”37

Aya hii ilikuwa ni kombora katika uso wa wapinzani, kemeo kwa waasi,onyo kwa kila anayempiga vita Amirul-Mu’minin na kukataa tukio laGhadir Khum, onyo kwake kwa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na MtumeWake na mwisho mbaya, akhera yenye matatizo na adhabu iumizayo.

Ewe msomaji mtukufu! Ama vitabu na rejea ambazo zinazotaja tukio navinavyotaja kushuka Aya hizo juu ya hilo ni nyingi. Nakutajia baadhi yake

48

Iddi al-Ghadiyr

37 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 167.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 48

ili ujue kwamba ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Mu’minin ulithibiti mbin-guni kabla ya ardhini na katika Qur’ani kabla ya hadithi, na kwambaMwenyezi Mungu anamnusuru anayemnusuru Ali na anamdhalilishaanayemdhalilisha.

Tafsirul-Qurtubiy, katika tafsiri ya Aya husika.Tafsiru Gharibul–Qur’ani ya Haafidhul–Harawiy katika tafsiri ya Ayahusika.Tafsiru Abiy Su’ud Juz. 8, uk. 292.Tafsirus–Siraajul–Muniyr ya As-Shiriyniy Ashaafiy Juz. 2 uk. 364.Tafsirul-Manaaru, katika tafsiri ya Aya husika.Tafsiru Majmaul-Bayaan katika tafsiri ya Aya husika.Tafsirul-Mizaan ya Tabatabaiy katika tafsiri ya Aya husika.Tafsirus-Swafiy katika tafsiri ya Aya husika. Tadhkiratus-Sibtu Ibnu Jauziy Al-Hanafiy.10.Faraidu As-Simtwain ya Sheikhul-Islam Al-Hamwainiy, mlango wa 13.11. Al-Fusulul-Muhimah ya Ibnu As-Swibaagha Al-Maaliky uk. 26.12. Faidhul-Qadiyr kwenye maelezo ya Jaamius-Swaghir Juz. 6, uk.2318.13. As-Siratul-Halabiyah Juz. 3, uk. 30214. Maelezo ya Jaamius-Swaaghir ya Suyutwiy Juz. 2, uk. 378.15. Nuurul-Abswar ya Shablanjiy As-Shaafiy uk. 78

Hizi ni rejea kumi na tano kati ya makumi ya rejea ambazo zimeandikakuhusu kushuka adhabu katika tukio hili, na hii inatosha kwa anayetakakuongoka.

IDDI YA AL-GHADIR

Huenda anuani hii mwanzoni itakuwa ni ngeni kwa baadhi na hatimayewataulizana: Ni nini Iddi ya Al-Ghadir? Na nani anatambua Iddi ya Al-Ghadir kuwa ni Idd ya kiislamu? Lakini anuani hii inabadilika kwao kwaurahisi wakijua kwamba wa kwanza aliyeitambua siku ya Ghadir kuwa ni

49

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 49

Iddi ya kiislamu ni Mtume wa Uislamu Muhammad (s.a.w.w.). Nabii(s.a.w.w.) alitangaza Iddi hii katika siku hiyo hiyo ya Ghadir baada yakumteua Imam Ali ibn Abu Talib (a.s.) kuwa khalifa wake baada yake.Akasherehekea Iddi kwa kukaa katika hema lake na kuwapokeawapongezaji kwa kila furaha na moyo mkunjufu na kushirikiana nao kati-ka furaha na shamrashamra, huku naye akiwaambia: “Nipongezeninipongezeni kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amenijaalia kuwa ni mah-susi kwa Unabii na amejaalia Ahlul-baiti wangu kuwa ni mahsusi kwaUimam.”38

Hatupati katika historia ya Nabii (s.a.w.w.) na maisha yake na furaha zakesiku aliyosema humo nipongezeni.. nipongezeni…..isipokuwa siku yaGhadir. Hata siku ya kuhama kwake Makka kwenda Madina na kunusuri-ka kwake toka kwa washirikina hakusema nipongezeni. Na hata siku yakuifungua Khaibar na kunusurika waislamu hakusema nipongezeni, laki-ni katika siku hiyo ya Ghadir alikuwa anakariri kauli yake:“Nipongezeni……nipongezeni…” Kwa nini? Kwa sababu yeye (s.a.w.w.)alikuwa anafahamu kwa kina utukufu wa siku hii na alikuwa anajua utuku-fu wa kumbukumbu hii na ubora wa Iddi hii.

Kwa sababu hiyo Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Siku ya Ghadir Khum nibora zaidi kati ya Iddi za umma wangu nayo ni siku ambayo aliniamuruMwenyezi Mungu Mtukufu kumteua ndugu yangu Ali ibn Abu Talib kuwanembo (Bendera) ya umma wangu, wataongoka kwayo baada yangu, nayoni siku ambayo alikamilisha humo dini, akatimiza humo neema naakawaridhia wao dini ya Uislamu.”39

50

Iddi al-Ghadiyr

38 Kitabu Sharaful-Mustafaa cha Haafidh Abiy Said Al-Khurukushiy An-Nisaaburiy.

39 Rejea kitabu cha Al-Ghadir cha Al-Amini Juz. 1, uk. 283 na tumeshatajakwamba Aya ya kukamilisha dini imeshuka siku ya Ghadir.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 50

Na katika hadithi hii Nabii (s.a.w.w.) anaizingatia siku ya Ghadir kuwa:Kwanza ni Iddi ya kiislamu yenye kudumu miongoni mwa Iddi za kiisla-mu. Pili anaizingatia Iddi ya Ghadir Khum kuwa ni katika Iddi bora zaidiza kiislamu kuliko zingine.

IMAM ALI NA IDDI YA GHADIR.

Baada ya Nabii Mtukufu (s.a.w.w.) akaja Imam Amirul-Mu’minin Ali (a.s.)na akaifanya siku ya Ghadir kuwa ni sikukuu ya kiislamu,40 alishahutubia(a.s.) ndani ya siku hiyo mwaka ambao Iddi ya Ghadir ilikuja pamoja naIjumaa, na katika hotuba yake ni kauli yake (a.s.): “Hakika MwenyeziMungu Mtukufu amewakusanyia enyi waumini katika siku hii Iddi mbilikubwa tukufu, na wala haisimami mojawapo isipokuwa pamoja na mwen-zake ili akamilishe kwenu neema zake nzuri, akuwekeni katika njia ya uon-gofu wake na kukuwekeni katika athari za wenye kuangaziwa kwa nuru yauongofu wake … akajaalia Ijumaa kuwa ni mkusanyiko na akajaalia kuwani njia ya kutoharisha yaliyokuwa kabla yake na kusafisha ambayo kuchu-ma kumekutumbukizeni katika uovu, toka Ijumaa moja kwenda kweyemfano wake …..

Hivyo hakubali Tauhid isipokuwa kwa kumkubali Nabii wake (s.a.w.w.)kwa unabii wake na wala hakubali dini isipokuwa kwa uongozi wauliyeamriwa uongozi wake, wala hazitapatikana sababu za utii wakeisipokuwa kwa kushikamana na uma’sum wake na ma’sum wa Ahlul-baitna uongozi wake, hivyo akateremsha kwa Nabii Wake (s.a.w.w.) katikasiku ya Dauhah41 ambayo yalibainisha matakwa Yake kwa vipenzi vyakena wateule wake, na akamwamuru kutangaza na kulipuuza kundi la watuwapotovu na wanafiki na akamhakikishia ulinzi Wake dhidi yao.”

51

Iddi al-Ghadiyr

40 Siku aliyopokea uongozi baada ya kuuliwa Uthman.41 Nao ni mti mkubwa, siku ya Ghadir imeitwa hivyo kutokana na kuwepo mitimikubwa eneo hilo la ardhi ya Ghadir.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 51

Kisha Imam Ali (a.s.) akawaamuru kufanya sherehe ya Iddi katika siku hiiakasema: “Sherehekeeni Iddi Mwenyezi Mungu awarehemu baada yakumalizika mkusanyiko wenu kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenu nakuwafanyia wema ndugu zenu na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufukwa yale aliyokupeni. Na kusanyikeni Mwenyezi Mungu atakusanyajambo lenu, na fanyianeni wema Mwenyezi Mungu atabariki huruma yenu,na peaneni zawadi katika neema za Mwenyezi Mungu kama alivyokuahi-dini thawabu kwayo kwa sikukuu nyingi za Iddi kabla na baada yake ilaatatimiza mfano wake.

Na kufanya wema humo kunaongeza mali na kuzidisha umri, na kuhuru-miana humo kunaleta rehema na huruma ya Mwenyezi Mungu, na andaenikwa ajili ya ndugu zenu na familia zenu miongoni mwa fadhila zake, jitahi-dini kwa ukarimu wenu kwa kile ambacho mnakiweza na dhihirisheni fura-ha baina yenu na bashasha katika kukutana kwenu.”42

Na amesema (a.s.) katika hotuba ya Iddi ya Al-Ghadir: Hakika hii ni sikutukufu humo kumetokea faraja na kunyanyuliwa daraja, na hoja zimesihi43

nayo ni siku ya uwazi na kutangaza cheo kilicho dhahiri, siku ya kukamil-isha dini, siku ya ahadi iliyoahidiwa, siku ya mshuhudiaji na mwenyekushudiwa, siku ya kubainisha misingi kutokana na unafiki na upinzani,siku ya kubainisha ukweli wa imani, siku ya kufukuzwa shetani44 na sikuya burhani, hii ni siku ya upambanuzi ambayo mlikuwa mmeahidiwa, hii

52

Iddi al-Ghadiyr

42 Al-Ghadir Juz.1 uk. 284. Misbaahul-Mujtahidi cha Sheikh Tusiy uk. 524.43 Nayo ni dalili na hoja kwa maana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w.) ametilia mkazo katika siku ya Ghadir juu ya ukhalifa wa Imam Aminul-Muuminina (a.s.) na akahimiza zaidi kuliko wakati mwingine, hivyo hoja juu yaukhalifa wake ikawa ni yenye nguvu zaidi.44 Katika hadithi ni kwamba mashetani walipiga kelele kwa Ibilis kutokana nahotuba ya Nabii siku ya Ghadir kwa sababu haikuacha mwanya wa kupetuka juuuimam na uongozi, lakini Ibilisi akawapa habari ya njama ya Saqifah, ndipowakatulia. Rejea Biharul-An’war Juz. 37 mlango unaouhusu habari za Ghadir.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 52

ni siku ya mkusanyiko mkubwa ambao nyinyi mnaupinga, hii ni siku yauongofu na siku ya mtihani kwa waja, na siku ya hoja kwa mtetezi, hii nisiku ya kuanza kwa chuki katika nyoyo na njama za mambo, hii ni siku yamaelezo ya kisheria kwa watu mahsusi, hii ni siku ya Shaythu, hii ni sikuya Idrisi, hii ni siku ya Sham’un…….”45

Ewe msomaji mtukufu! Hakika kila sentensi katika sentensi za hadithi hiitukufu zina maana na zinaonyesha mambo na kadhia, tunaacha ufafauziwake na tutauzungumzia mahala pengine.

MAIMAM WA AHLUL-BAIT NAIDDI YA GHADIR

Na baada ya Imam Ali Amirul-Mu’minin alikuja Imam Hasan na Huseinna maimam watukufu katika kizazi chake (a.s.) wakaitukuza siku yaGhadir46 na wakaizingatia kuwa ni Iddi yao. Katika kila mwaka wanaku-sanyika humo na wanapongezana kwa furaha na kila bashasha na wana-jikurubisha kwayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kufunga, kusalina kuomba dua Kwake na wanafanya mema na ihsani sana, na wanalishachakula kwa wingi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yalealiyowaneemesha katika siku hiyo miongoni mwa Aya juu ya Amirul-Mu’minin, na walikuwa wanaunga udugu wao humo na wanawapa famil-ia zao hidaya na wanawatembelea ndugu zao na wanawaamuru wafuasiwao kufanya hivyo.47

Na hivi sasa ewe msomaji mtukufu tunakuletea hadithi tatu:Kutoka kwa Abu Hasan Al-Laithiy kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s.) ali-waambia wale waliohudhuria miongoni mwa wafuasi wake: “Je, mnajua

53

Iddi al-Ghadiyr

45 Biharul-An’war Juz. 37, uk. 164.46 Nayo ni siku ya 18 katika Dhulhaji. 47 Hizi ni dondoo kutoka katika Al-Muraja’at uk. 197.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 53

siku ambayo Mwenyezi Mungu aliupa nguvu Uislamu na akadhihirishakwayo mnara wa dini na akaifanya kuwa ni Iddi yetu na wafuasi wetu naShia wetu?” Wakasema: “Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mtoto waMtume Wake wanajua, je ni siku ya Iddi Al-Fitri ewe bwana wetu?”Akasema (a.s.): “Hapana.” Wakasema ni Iddi Al-Udhha? Akasema (a.s.):“Hapana, hizi ni siku mbili tukufu, na siku ya kinara cha dini ni bora kulikohizo, nayo ni siku ya kumi na nane Dhulhaji, na Mtume wa MwenyeziMungu aliporejea katika Hijja ya Al-Widaa alipowasili katika bonde laKhum….” Hadi mwisho wa hadithi.

Kutoka kwa Furat bin Ahnaf alimwambia Imam As-Sadiq: “MwenyeziMungu anijalie niwe fidia kwa ajili yako, je, waislamu wana Iddi borakuliko Iddi Al-Fitri na Iddi Al-Udhha, Ijumaa na Arafa?” Akasema (a.s.):“Ndiyo, bora zaidi na tukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kwa cheo, nayondiyo siku aliyoikamilisha Mwenyezi Mungu humo dini na akateremshakwa Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.): ‘Leo hii nimekukamilishieni diniyenu na nimewatimizeini neema zangu na nimemwadihieni uislamukuwa ndiyo dini yenu.’”

Nikamwambia ni siku gani? Akasema: “Hakika Manabii wa Bani Israiliwalikuwa anapotaka mmoja kati yao kuacha wasia na uongozi baada yakebasi anapofanya hivyo wanaijalia siku hiyo kuwa ni Iddi, na hakika ni sikuambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Alikwa watu kuwa kiongozi, na yakateremshwa humo yaliyoteremshwa, diniikakamilika humo, na humo zikatimia neema kwa waumini.” Nikasema:Inatupasa tufanye nini katika siku hiyo? Akasema: “Ni siku ya ibada,kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi, kufurahi kwa yale aliyowa-pa Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongozi wetu, hakika mimi napendakwenu mfunge siku hiyo.”48

54

Iddi al-Ghadiyr

48 Al-Ghadir Juz.1 uk. 285.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 54

Kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Salim kutoka kwa baba yake amesema:“Nilimuuliza Abu Abdillah As-Sadiq (a.s.): Je, waislamu wana Iddi zaidiya siku ya Ijumaa, Iddi Al-Fitri na Iddi Al-Udhha? Akasema: ‘Ndio, iliyobora na tukufu zaidi.’ Nikasema: Ni Iddi ipi hiyo Mwenyezi Mungu ani-jaalie niwe fidia kwako? Akasema (a.s.): ‘Siku ambayo Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Amirul-Mu’minin naakasema: Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.’Nikasema: Ni siku gani? Akasema (a.s.): ‘Siku utaifanyia nini? Hakikaimeshapita lakini ni siku ya kumi na nane ya Dhul-Hija.’ Nikasema:Inatupasa tufanye nini siku hiyo?’ Akasema: ‘Mtajeni Mwenyezi Munguhumo kwa kufanya ibada, kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu naahali zake, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuusia Amirul-Mu’minin kuifanya siku hiyo kuwa ni Iddi, hivyo ndivyo Manabiiwalivyokuwa wanafanya, walikuwa wanawausia mawasii wao nawanaifanya siku hiyo kuwa ni Iddi yao.”’49

SHIA NA IDDI YA GHADIR

Kutokana na hadithi hizi tukufu ambazo zinahimiza watu kuifanya siku yaGhadir kuwa ni Iddi ya kiislamu na zinawaelekeza watu kwenye ibada nawema, ndio maana unaona waislamu wa madhehebu ya Shia50 katika nchizote tangu zama za Maimam watukufu hadi leo hii wanaichukulia siku yaGhadir kuwa ni Iddi yao ya kila mwaka, wanajikurubisha kwa MwenyeziMungu kwa kufanya kumbukumbu ya mnasaba huu mtukufu kwa kusali,kusoma Qura’ni na dua zilizopokelewa kwa kumshukuru MwenyeziMungu kwa kukamilisha dini na kutimiza neema kwa uongozi wa Amirul-Mu’minin (a.s.), wanatembeleana na hali ya kuwa na furaha na bashashana wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya mema na kuwa-furahisha jamaa na majirani, mmojawapo anapokutana na mwenzake kati-ka siku hii anampa mkono na kusema: Shukurani ni kwa Mwenyezi Mungu

55

Iddi al-Ghadiyr

49 Al-Kaafiy cha Sheikh Al-Kulainy Juz. uk. 402.50 Wao ni wafuasi wa Imam Ali mbao wanamfuata kwa sababu yeye ni haki nahaki iko pamoja naye kama alivyosema Nabii (s.a.w.w.).

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 55

Mtukufuu ambaye ametujaalia kushikamana katika uongozi wa Amirul-Mu’minina na Maimam watoharifu.

Na linakusanyika kundi kubwa la Shia katika Iddi hii tukufu huko NajafTukufu ambapo kuna kaburi la Imam Amirul-Mu’minin (a.s.) na idadi yawanaokusanyika katika kaburi lake kwa ajili ya ziara ni nusu milioni51 nawanakuja kutoka katika kila sehemu ili kutia mkazo katika nafsi zao, kinacha mapenzi na umadhubuti wa itikadi kwa Imam wao wa haki Amirul-Mu’minina (a.s.), na kusajili katika nafsi zao utukufu wa kuhudhuria kati-ka kaburi lake tukufu. Hawasogei wala hawaondoki mpaka walizungukekaburi tukufu na kumzuru Imam wao, kumsalimia na kumpongeza kanakwamba yuko mbele yao.52

Na wanasoma katika kumzuru kwake hotuba iliyopokewa na baadhi yaMaimam watukufu ambayo inajumuisha ushuhuda wa kutangulia kwaAmirul-Muminina katika Uislamu, misimamo yake mitukufu, kutanguliakwake kutukufu, jihadi yake kubwa, kutaabika kwake katika kuwekamisingi ya dini, na kumhudumia kwake bwana wa Manabii naMitume……… na kwa yale aliyonayo (a.s.) kati ya fadhila na sifa ambazokwazo Nabii amemteua kuwa Khalifa siku ya Ghadir.53 Naam….. hii ni

56

Iddi al-Ghadiyr

51 Idadi hiyo ni kwa mujibu wa ripoti za hapo awali, lakini kwa hivi sasa ni zaidiya hapo - Mhariri.52 Kwa sababu Imam ni Imam akiwa hai au maiti, na kwa sababu Imam yu haianaruzukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t.):“Wala msidhani wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa niwafu bali wako hai…” Na kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t.): “Wala msisemekwa ambao wanauliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu baliwako hai…”53 Kama si ufinyu wa nafasi basi ewe msomaji ningekutajia mifano ya manenoya ziyara hiyo ili uone humo utamu, ladha ya imani , utakaso wa moyo na vugu-vugu la shauku. Ziyara hiyo imetajwa katika vitabu vya dua na ziyara hivyo rejeahuko.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 56

desturi ya waislamu wa madhehebu ya Shia kila mwaka, na makhatibu waowameendelea katika kila zama na kila mji katika kudumisha kuadhimisha,kutilia mkazo na kuzungumzia tukio la Ghadir kwa muhtasri na kwa kire-fu.54

Na inadhihirika kwa mtafiti kwamba Shia sio peke yao ndio wameifanyasiku ya Ghadir kuwa ni Idd ingawa wao ndio walioizingatia zaidi kulikowatu wengine, bali hata wasiokuwa wao katika waislamu walikuwawanazingatia kuwa ni Iddi pia…. Ametaja mtafiti mkubwa Allamah SheikhAl-Amin (r.a) katika kitabu cha Ghadir Juz. 1, uk. 267 kwamba Al-Abaiyruniy ameihesabu siku ya Ghadir kuwa ni katika sikukuu walizozi-fanya waislamu55 na kwamba Ibnu Talha Ashaafiy ameandika katikakitabu Mataalibus-Suul uk. 53 anapozungumzia Iddi ya Ghadir kwamba:“Siku ya Ghadir Khum ameitaja (yaani Amirul-Mu’minin) katika hotubayake. Na siku hiyo ikawa ni Iddi na sikukuu kwa sababu ni wakati alio-tamka humo Nabii wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) cheo hiki kitukufu naakamtukuza humo kuliko watu wote.”

Mfuasi huyo wa Shafiy ameongeza katika ukurasa wa 56 hivi: “Na kilamaana inayowezekana kuthibitishwa miogoni mwa zile zinazoonyeshwana tamko la Maula la Mtume (s.a.w.w.) basi alilijaalia kwa Ali, nacho nicheo kikubwa, nafasi ya juu, daraja la juu, na sehemu tukufu aliyompa bilaya mwinginewe. Kwa sababu hii siku hiyo imekuwa ni siku ya Iddi nasikukuu ya furaha kwa wafuasi wake.”

Amesema Sheikh wetu mtukufu Al-Amin: “Neno hili limetupa faidakwamba waislamu wote wanashirikiana katika kusherehekea siku hiyo, nisawa dhamiri iliyopo kwenye “wafuasi wake” iwe inarejea kwa Nabii(s.a.w.w.) au wasii. Ama kwa wa kwanza iko wazi na ama kwa wa pili nikuwa: Waislamu wanamfuata Amirul-Muminina ni sawa katika hilo kuna

57

Iddi al-Ghadiyr

54 Hizi ni dondoo kutoka katika Al-Muraja’at uk. 198.55 Kitabu Al-Athaarul-Baaqiyatu Fil-Quruunil-Khaaliya uk. 334.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 57

wanaomfuata kwa kuzingatia kuwa ni khalifa wa Mtume bila fasili (uten-ganisho) au anayemuona kuwa ni khalifa wa nne katika makhalifa ……Navitabu vya historia vinatueleza juu ya hili kwa kuafikiana na kukubalianaumma wote wa kiislamu Mashariki na Magharibi, na kwamba Wamisri,Wairaki na Wamoroko wanaizingatia kwa utukufu wake tangu karne zamwanzo, na kwao imekuwa ni siku iliyoshudiwa kwa Swala, dua, hotubana kusoma mashairi kama ilivyoelezwa kwa ufafanuzi katika kamusi.

IDDI AL-GHADIR HUKO MBINGUNI

Ewe msomaji wetu! Mazungumzo yetu yalikuwa hadi sasa juu ya Iddi yaGhadir na sherehe zake ardhini. Ama hivi sasa imewadia duru ya swali hili:Kitu gani kinafanyika mbinguni siku ya Iddi ya Ghadir? Swali hili halijibuyeyote isipokuwa Imam ma’sum anaekubalika kwa Mwenyezi Munguambapo elimu yake ni katika elimu ya babu yake Al-Mustafa (s.a.w.w.)Nabii mwenye mawasilano ya mbiguni, ambaye anajua na hali yeye yukoardhini yanayofanyika mbinguni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hivyonjoo pamoja na mimi hadi kwa Imam wa nane wa Ahlul-bait (a.s.) ImamAli Ar-Ridhaa (a.s.) ili atueleze yanayofanyika mbinguni siku ya Iddi yaAl-Ghadir kila mwaka.

Amesema (a.s.): “Hakika siku ya Ghadir katika mbingu ni mashuhuri zaidikuliko ardhini.56 Mwenyezi Mungu ana kasri katika Firdaus yenye tofali zafedha na tofali za dhahabu, humo kuna kuba elfu mia moja nyekundu naelfu mia moja za yakuti za kijani, udongo wake ni miski na ambari, humokuna mito minne, mto wa pombe, mto wa maji, mto wa maziwa na mto waasali, pembezoni mwake kuna miti ya matunda ya aina zote, kuna ndege

58

Iddi al-Ghadiyr

56 Huenda sababu ni kwamba walio mbinguni wote ni waumini na kwa ajili hiyowanasherehekea wote katika siku ya ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Muminina.Ama watu wa ardhini humu kuna waumini na wasiokuwa waumini, na walahawasherehekei Iddi ya Ghadir isipokuwa waumini tu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 58

miili yao ni ya lulu na mabawa yao ni ya yakuti, wanaimba kwa kila ainaya sauti. Inapofika siku ya Ghadir wanakuja kwenye kasri hiyo waliombinguni, wanamtukuza Mwenyezi Mungu, kumsabihi na kufanyatahalili, ndege hao huruka na kutua juu ya maji hayo wanajigaragaza kati-ka miski na ambari hiyo. Malaika wanapokusanyika basi wanarukaruka nakuwanyunyizia marashi hayo juu yao. Na wao katika siku hiyo wanapeanazawadi ya manukato ya Fatmah, na unapowadia mwisho wa siku hunadi-wa: Ondokeni nendeni kwenye sehemu zenu kwani mmeshanusurikakutokana na hatari na kuteleza hadi mwakani kwa utukufu wa siku hii yaleo kwa kumkirimu Muhammad na Ali….. hivyo wao wanapeana zawadihadi siku ya Kiyama.”57

Ewe msomaji mtukufu! Hakika katika jumla ya ada zinazoendelea kwawatu katika sikukuu ni watu kupeana zawadi baadhi yao kwa baadhi, kwasababu zawadi ni nembo ya upendo na alama ya urafiki. Na kwa kawaidazawadi hutofautiana kwa kutofautiana mtoa zawadi na mpewa zawadi,kuna zawadi rahisi na kuna zawadi za ghali…… Na umeshasoma katikahadithi ya Imam Ridhaa (a.s.) kwamba zawadi ya walio mbinguni katikasiku ya Iddi ya Ghadir ni manukato ya Fatmah (a.s.).

Basi ni yapi manukato ya Fatmah?

Jawabu: Amepokea As-Sufuriy Ashaafiy kutoka kwa Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba amesema: “Naapa kwa aliyenitumakwa utukufu na akanifanya mahsusi kwa ujumbe, hakika MwenyeziMungu alimuoza Fatmah kwa Ali …… kisha aliamrisha mti wa Tubaupukutishe kwao lulu mbichi pamoja na duru nyeupe, zabarjadi ya kijanipamoja na yakuti nyekundu.”58

59

Iddi al-Ghadiyr

57 Biharul-An’war Juz. 270 uk.165, vile vile ameipokea Sheikh Tusiy katikaAmaal. 58Nazahatul-Majaalis Juz. 233. Na yanayofanana na hayo yamo katika kitabuHilyatul-Awliyaai cha Abu Na’im Juz. 59, na katika Riyaadhun-Nadharah chaMuhibu Tabariy Juz. 2 uk. 184.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 59

Vile vile kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Nabii alipokuwa msiki-tini alimwambia Ali: Huyu ni Jibril amenipa habari kwamba MwenyeziMungu amekuozesha Fatmah na wameshuhudia katika kukuozesha kwakemalaika arobaini elfu, na ameufunulia (ameupa wahyi) mti wa Tuba uwa-pukutishie duri, yakuti, hulu na hulali, basi ukawapukutishia na hurlainiwakaanza kuziokota kwa sahani za duri, huli na hulali, hivyo wao wana-peana zawadi kwazo hadi siku ya Kiyama.”

MASJID AL-GHADIR

Tukio la Ghadir lilichukua nafasi muhimu katika historia ya kiislamu namaisha ya Mtume (s.a.w.w.) hivyo sehemu ambayo lilitokea tukio hiliimekuwa ni msikiti maarufu. Waislamu huenda na kusali humo na kukum-buka siku hiyo tukufu na sehemu takatifu aliyosimama humo Mtume(s.a.w.w.) kwa kumtangaza khalifa baada yake.

Imepokewa kutoka kwa Imam Jafar As-Sadiq (a.s.) kwamba amesema: “NiSunna kusali katika msikiti wa Ghadir kwa sababu Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Amirul-Mu’minin, nayo ni sehemuambayo Mwenyezi Mungu aliidhihirisha humo haki.”59

Na kutoka kwa Hasan Al-Jamaal amesema: “Nilimchukua Abu AbdillahAs-Sadiq (a.s.) kutoka Madina hadi Makka, tulipowasili katika msikiti waGhadir alitazama kushoto mwa msikiti akasema: ‘Hiyo ni sehemu yanyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambapo alisema:Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”’ Hadi mwishowa hadithi.60

60

Iddi al-Ghadiyr

59 Biharul-An’war Juz. 37 uk.173.60 Biharul-An’war Juz. 37 uk.172 na 221.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 60

Abdur-Rahmani bin Al-Hajaji alimuuliza Imam Musa bin Ja’far (a.s.)kuhusu kusali katika msikiti wa Ghadir Khum akasema (a.s.): “Sali humokwani humo kuna fadhila na baba yangu alikuwa anaamuru juu ya hilo.”61

Amesema Sheikh mwandishi wa Al-Jawaahiri: “Vilevile ni mustahabukwa anaerejea kupitia njia ya Madina kusali katika msikiti wa Ghadir nakuomba humo dua kwa wingi, nayo ni sehemu ambayo Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimteua Ali Amirul-Mu’minin.”62

Na wanatahistoria wametaja sehemu ya msikiti huu kuwa ni baina yaGhadir na chemchemu63 lakini kwa masikitiko makubwa ni kwamba haku-na athari ya msikiti huu leo kwani jengo lake limebomoka na hakuna athariyeyote, umekuwa ni habari tu baada ya kuwepo kwake, jengo lake haliku-jengwa upya hadi leo, pamoja na kwamba:

Ni nyumba katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu kutajwahumo jina lake na ni msikiti katika misikiti ya Mwenyezi Mungu ambayoameamrisha kuimarishwa.

Kama ambavyo umezingatiwa kuwa ni katika athari za kiislamu ambazo niwajibu kuzihifadhi ili kudumisha historia ya kiislamu, watu wake na atharizake.

Hakika hiyo ni kuhuisha kumbukumbu tukufu, kwani unalirejesha tukiohilo la kihistoria tukufu katika fikra, tukio ambalo linazingatiwa kuwa nialama ya imani. Na huenda hii ndio sababu ya kupuuzwa kwake na kuto-jengwa upya jengo lake. Na hata njia inayoelekea huko na ambayo ilikuwani njia ya mahujaji baina ya Madina na Makka kwa karne nyingi ime-badilishwa kwa kuwekwa njia nyingine, na hatimaye imesahaulika na

61

Iddi al-Ghadiyr

61 Wasailus-Shiah kitabu kinachohusu Swala, mlango unaohusu misikiti.62 Inklopedia ya Jawahirul-Kalaam Juz. 20 uk. 75.63 Muujamul-Buldan Juz. 2 uk. 389.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 61

athari zake zimetoweka….. Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa MwenyeziMungu Mtukufu.

MAELEZO KUHUSU ARDHI YA GHADIR

Jarida la Turaathunaa64 lilisambaza makala mazuri kuhusu ardhi yaGhadir Khum na mahala pake kijiografia na kihistoria ya Ustadh Dr.Sheikh Abdul–Haadiy Al-Fadhiliy ambaye alisafiri mara mbili kwendakatika sehemu hiyo tukufu. Hapa tunadondoa yafuatayo kutoka katika jari-da hilo:

Hakika Ghadir Khum ni sehemu ya bonde la Juhfah na iko katika mwan-zo wa bonde na mwisho wa bonde la Al-Kharaar, nayo iko umbali wakilometa nane kutoka katika kituo cha Juhfah, upande wa kushoto wa njiakwa wanaokuja kutoka Madina kwenda Makka, Kusini Mashariki mwaRabigh kwa kilometa 26 takriban.

Na bonde la Ghadir ni bonde kubwa sana, ardhi yake ni tambarare kwasababu hiyo inaweza kuingia humo idadi kubwa ya watu tofauti na ardhiya Al-Khazinah ambayo ina miinuko na vilima, ambapo hawawezi kuku-sanyika watu humo kwa upande mmoja. Hapa unafahamika uchaguzimzuri wa Mtume (s.a.w.w.) ambapo alichagua ardhi hii pana kwa ajili yakutoa hotuba na kuchukua kiapo cha utii toka kwa watu.

Na sehemu hii kwa sasa inajulikana kwa jina la Ghurubah na watuwanaishi humo kutoka mji wa Hirbu, na mwandishi alikutana na baadhiyao huko.

62

Iddi al-Ghadiyr

64 Linalotolewa na taasisi ya Ahlul–baiti (a.s.), Qum – Iran toleo No. 25.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 62

Na humo kuna chemchem ya maji kaskazini magharibi katika sehemuhiyo, na inaonyesha ilikuwepo tangu zama za Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) na bado inaendelea kuwepo hadi leo.

Kama ambavyo kuna dimbwi ambalo chemchem iliyotajwa inamwagamaji yake humo.

Na kuna idadi kubwa ya miti ya Samuru, nao ni mti wenye miba na ni mtimkubwa, na kwa ajili hiyo umeashiriwa kwa jina la Dauhah, kama ilivyokatika hadithi na mashairi. Na Dauhah ni mti mkubwa uliotawanyika nawenye matawi mengi.

NAFASI YA WASHAIRI KATIKA IDDI YA AL-GHADIR.

Washairi tangu karne ya kwanza hijiriya hadi karne hii wanashiriki katikasherehe hii ya kidini ya kila mwaka yenye kudumu, na wana nafasimuhimu ya kueleza kina cha mapenzi yao na ufuasi wao kwa Imam mtuku-fu, kupitia kaswida zilizotungwa, na beti za mashairi ambazozinazungumzia Iddi ya Ghadir na aliyevikwa taji katika Iddi ya Ghadir,naye si mwingine bali ni Amirul-Mu’minin Ali (a.s.).65

Hata wasiokuwa waislamu kuanzia Manasara na wengineo wameshirikikutunga kaswida na kueleza kuhusu ukweli wa mapenzi kwa shujaa wabinadamu na Uislamu Ali Amirul-Mu’minin (a.s.). Nakudondolea kidogotu ewe msomaji kati ya mamia ya kaswida ambazo zimetungwa katikamnasaba wa Ghadir. Beti hizi ni kutoka katika kaswida ya Ustadh PauloSalamah, mshairi wa Kinasara maarufu anasema:

63

Iddi al-Ghadiyr

65 Rejea inklopedia ya Al-Ghadir ya Sheikh Al-Amin ili uone kaswida zilizo-tungwa katika mnasaba huu wa kidini wenye kudumu.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 63

“Usiseme Shia wanampenda Ali, hakika kila mwadilifu ana wafuasi, yeyeni fahari ya kihistoria na wala sio fahari ya watu wanaemtambua na kum-fanya kuwa kiongozi. Utajo wake linapotanda giza la usiku unaangazakama mapambazuko ya asubuhi. Ewe Ali wa zama, haya ni manenoyangu, nimesikiliza humo wahyi wa Imam waziwazi. Ewe Amiri waubainifu, hii ni ahadi yangu, namshukuru Mungu kwamba nimeumbwa namtimiza ahadi. Ewe Amiri wa Uislamu yanitosha kuwa fahari, kwambamimi kwako ni mfuasi mdogo. Ilidhihiri haki kwa Nasara mpaka akah-esabika kwa wingi wa mapenzi yake kuwa ni mfuasi wa Ali. Mimi ni katiya wanaopenda ushujaa na wahyi, uadilifu na tabia nzuri, hata kama Alihakuwa Nabii, lakini tabia yake ilikuwa ya Kinabii. Ewe mbingu shuhudiana ardhi pia kubali na nyenyekea hakika mimi nimemtaja Ali.”

Na anapohamia katika kumbukumbu ya Iddi ya Al-Ghadir yenye kudumuanasema: “Alirejea kutoka Hijjatul-Wida’a tukufu, na kundi la mahujajikama vile mawimbi ya bahari. Waliwasili wenye kurejea kwenye bonde laKhum kana kwamba msafara upo katika tanuri. Waliwasili humo hali yakuwa wamechoka, hali wanaswaga ngamia wao ili watembee haraka.Ndipo Nabii alipoona jambo zito nalo kwake ni mtihani mgumu. AlikujaJibril hali akisema: ‘Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu fikisha maneno yaMola muokozi, eleza wewe uko katika ulinzi kutokana na watu, tangazahabari za mbinguni kwa watu, tangaza ujumbe wa Mwenyezi Munguwahyi wenye kudumu na hoja ya milele.’”

Mlinganiaji akawaita watu ili waje wasikilize. Watu wakarejea kwa kuiti-ka wito, wakamzunguka kama duara la mwezi ukiangazia ardhi kwa mialeyake yenye nuru. Wote wanasubiri tangazo na hakuna shaka katika jambo,kwani kauli ni muhimu mno. Nabii hakuwaita kwa jambo jepesi na ardhiya bonde inawaka kwa joto. Nabii akapanda mimbari ya Haudaji, akiyavu-tia masikio kusikiliza maneno muhimu: ‘Enyi watu hakika MwenyeziMungu ni kiongozi wenu na ni kiongozi wangu, mwenye kuninusuru namwokozi wangu, kisha mimi ni kiongozi wenu hadi mwisho wa dahari.Ewe Mola Wangu ambaye mimi ni kiongozi wake kweli, basi hatopinga

64

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 64

kuwa Ali ni kiongozi wake. Ewe Mola Wangu wapende wanaompendamtoto wa ami yangu, na mnusuru khalifa wangu mwenye kuninusuru,kuwa adui kwa mwenye kumfanyia uadui na mdhalilishe kila mpinzani namdhalilishe muovu.’

Alisema hayo hali akishika mkono wa Ali, na kunyanyua mkono waHaidar shujaa. Zikaonekana nywele za kwapa wakati wa kushikanamikono katika sehemu mashuhuri, kana kwamba Nabii ananyanyua ben-dera ya utukufu wa Iddi ya kiongozi mwenye kunusuriwa na kiongozi wazama. ‘Fadhila za Ali ziko wazi kwa wenye kuona kweli anafaa kuwamsaidizi. Haidar mume wa Fatmah na baba wa wajukuu wawili na shujaawa siku ya kukata shingo (vita), mtoto wa Mtume wa kulea na mtoto wamlezi wake aliyejitolea katika kumpunguzia ufakiri, faqihi mkubwa namwenye kupatia rai katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na kwa mwenyekutaka msaada wa uongofu. Nitakutana nanyi katika birika, ambapo Aliatawatangulia mapema, nitawauliza waumini vipi mlihifadhi Qur’ani kati-ka jambo la msaidizi wangu. Msipotee, shikamaneni na Kitabu chaMwenyezi Mungu na kizazi changu na Amiri.’

Alitamka Nabii kwa Ali maneno yaliyo wazi kama mchana bila ya sitara,majazi, kufunika wala mkanganyo ambao fahamu inaweza kufasiri,wapongezaji wengi wakamwendea, kaumu ikadhihirisha alama ya heshi-ma, wakamjia sahaba wawili mapema wakasema haraka kwa kueleza:‘Pongezi umekuwa kiongozi wa waumini kwa baraka unafaa kuwa Imam.’Wakampongeza wake wa Nabii hali ya kuwa wanasoma kaswida wakion-goza kundi kubwa: ‘Iddi yako ni Iddi ewe Ali, hata kama atanyamazahasidi au mwenye kuzuia mbaramwezi.’ Mwenyezi Mungu akateremshaAya baada ya hapo, siku ya kukamilika dini yake tukufu, siku ya furahailikuwa ni siku ya joto kali, na machweo matukufu yalikuwa ni ya siku yaGhadir”66

65

Iddi al-Ghadiyr

66 Diwani ya ‘Iydil-Ghadir cha mshairi Paulo Salamah uk.106.

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 65

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL-ITRAH FOUNDATION:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an.

66

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 66

29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka Na Aba'Khalifa37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya46. Kusujudu juu ya udongo47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)48. Tarawehe49. Malumbano baina ya Sunni na Shia50. Kupunguza Swala safarini51. Kufungua safarini52. Umaasumu wa Manabii53. Qur’an inatoa changamoto54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume

Muhammad (s)

67

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 67

61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili63. Kuzuru Makaburi64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita70. Tujifunze Misingi Ya Dini71. Sala ni Nguzo ya Dini72. Mikesha Ya Peshawar73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia

iliyonyooka75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake76. Liqaa-u-llaah77. Muhammad (s) Mtume wa Allah78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi?80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )83. Mazingira84. Utokezo (al - Badau) 85. Sadaka yenye kuendelea 86. Msahafu wa Imam Ali87. Uislamu na dhana88. Mtoto mwema89. Adabu za Sokoni90. Johari za hekima kwa vijana91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili

68

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 68

93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu94. Tawasali95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia96. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu97. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi98. Swala ya maiti na kumlilia maiti99. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)100. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu101. Hadithi ya Thaqalain102 Fatima al-Zahra103. Tabaruku104. Sunan an-Nabii105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)107. Mahdi katika sunna108. Kusalia Nabii (s.a.w)109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza110. Ujumbe - Sehemu ya Pili111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu112. Ujumbe - Sehemu ya Nne113. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa114. Iduwa ya Kumayili115. Maarifa ya Kiislamu.116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu119. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne120. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano121. Johari zenye hekima kwa vijana122. Safari ya kuifuata Nuru123. Idil Ghadiri124. Myahudi wa Kimataifa125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

69

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 69

70

Iddi al-Ghadiyr

126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza127. Visa vya kweli sehemu ya Pili128. Muhadhara wa Maulamaa129. Mwanadamu na Mustakabali wake130. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza131. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili132. Khairul Bariyyah133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi134. Vijana ni Hazina ya Uislamu.135. Yafaayo kijamii136. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu137. Taqiyya138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?140. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza141. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu145. Kuonekana kwa Allah146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt

(Sehemu ya Kwanza)147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)148. Ndugu na Jirani149. Ushia ndani ya Usunni150. Maswali na Majibu151. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu152. Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.1153. Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.2154. Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 70

BACK COVERIdi ya Ghadiri (Sikukuu ya Ghadir) imetokana na tukio kubwa la kihisto-ria. Tukio hili lilitokea katika jangwa la Ghadir Khumm katika njia ya msa-fara baina ya Makka na Madina wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akiru-di kutoka Makka ambako alikwenda kutekeleza ibada ya Hija. Hija hii nimaarufu sana na hujulikana kama Hijjatu ’l-Widaa’ (Hija ya Mwago).Ghadir ni tukio maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakunamadhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja tukio hili, ingawakuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo,ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bilaya kulitaja tukio hili. Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikami-lika baada ya tukio hili la Ghadir: “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, nakuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe diniyenu...” (5:3)

Aya hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (saw) pale Ghadir Khummbaada ya kumtangaza Imam Ali (as) kama Khalifa wake, kiongozi wawaumini wote na mrithi wake. Baada ya hapo Waislamu waliifanya siku hiikuwa Idi (Sikukuu) kama utakavyoona maelezo yake katika kitabu hiki.

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah FoundationS.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

71

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 71

72

Iddi al-Ghadiyr

IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd 7/1/2011 4:32 PM Page 72