ijumaa, januari 9, 2015 mwananchi.co.tz mwananchi … tanzania 2035.pdf · ni asilimia tano (5) tu...

4
TANZANIA YA MWAKA 2035 IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ 1 MWANANCHI Toleo hili la mustakabali wa Tanzania ni mchakato ulioanza mwezi Februari 2014 kwa kuwakusanya wasomi, wafanyakazi wa serikali, wataalam, wanafunzi na wanazuoni kujadili hali ya nchi ya sasa na ya baadaye. SID, pamoja na washiriki wake Twaweza na Foundation for Civil Society imewahoji wananchi zaidi ya 1,500 kwa njia ya simu za mkononi na katika mikutano kwenye mikoa tisa ya Tanzania. Mikoa hii ni Dar es Salaam, Arusha, Kusini Pemba (Chake Chake), Mjini Magharibi (Zanzibar-Unguja), Mbeya, Kigoma, Mtwara, Dodoma na Mwanza. SOCIETY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT (SID) Society for International Development (SID) ni mtandao wa kimataifa wa watu na taasisi zisizo za kiserikali ulioanzishwa mwaka 1957 kwa lengo la kukuza haki katika jamii naku- hamasisha ushiriki mkubwa wa watu. Kwa kupitia miradi mbali mbali, SID inaimarisha uwezo wa pamoja, kuwezesha majadiliano na kubadilisha uzoefu na maarifa miongoni mwa washirika wake. SID ina matawi zaidi ya 55 duniani kote, pamoja na taasisi 50 na wanacha- ma binasfi 3,000 kutoka nchi 125. Sekretariati ya SID ina ofisi tatu - Dar es Salaam, Nairobi, Kenya na Roma, Italia. MRADI WA TANZANIA YA KESHO Tanzania iko njia panda. Taifa letu linaonesha dalili za kuelekea pazuri ikiwa na uchumi imara na jamii yenye umoja na mshikamano. Lakini pia, kuna dalili za kutisha. Umimi, ufisadi na kutojali vinaweza kuisambaratisha nchi. Lengo la mradi huu ni kuibua na kucho- chea tafakuri, mazungumzo na mijadala miongoni mwa wananchi kuhusu mustakabali wa Tanzania katika miaka ishirini ijayo. Nia kuu ni kuhakikisha majadiliano yanaongozwa na taarifa na uchambuzi wa kina kuhusu matumaini ya watanzania, hali halisi ya jamii, siasa na uchumi wa nchi, changamoto za msingi zinazotukabili, na hatima ya taifa letu ifikapo mwaka 2035. Tanzania itakuwaje miaka ishirini baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015? Wananchi watakuwa na maisha ya hali gani?. MATUMAINI YA WANANCHI Sauti za Wananchi ya Twaweza ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi. Katika awamu ya 23 ya upigaji simu, tuli- wafikia wahojiwa 1,408 kati ya tarehe 13 na 22 Agosti 2014 kupata maoni yao juu ya mustaka- bali wa Tanzania. Matokeo muhimu ni: l Mwananchi mmoja kati ya wawili anatarajia kwamba maisha yake yatakuwa bora zaidi katika siku zijazo, na idadi kubwa zaidi wanajiona kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kustawisha maisha yao ya baadaye. l Wananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa nchi yetu itakuwa “mahali pazuri pa kuishi” ifikapo mwaka 2025. l Wananchi tisa kati ya kumi wanaona kwamba maamuzi makubwa ya kitaifa yatakuwa chini ya udhibiti wa nchi yenyewe. l Wananchi saba kati ya kumi wanaamini kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, lakini wananchi wanne tu kati ya kumi wanaamini kuwa Tan- zania itafuzu kucheza mashindano ya Kombe la Dunia. l Wananchi wameonesha kuwa vipaumbele muhimu kwa maisha ya baadaye ni kuongeza ubora wa utoaji wa huduma za kijamii, ukuaji wa uchumi na umoja wa kitaifa. HALI HALISI YA TANZANIA Uchumi unakua kwa kasi. Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kasi katika miongo miwili iliyopita na kufikia wastani wa asilimia 6 mpaka asilimia saba 7. Hakuna nchi yoyote nyingine Afrika Mashariki iliyoweza kukua kwa kasi hii na kwa muda mrefu hivi. Tanzania ni kipenzi cha wawekezaji. Mwaka 2014, Tanzania ilipokea dola bilioni 1.9 za uwekezaji, ambazo ni mara nne ya nchi jirani ya Kenya iliyopata dola milioni 514. Lakini wananchi wengi bado wana hali mbaya. Licha ya kwamba kiwango cha umasikini umekuwa ukishuka toka asilimia 39 ya Watanzana wote mwaka 1990 mpaka asilimia 28 mwaka 2012, ongezeko la idadi ya watu imeongeza idadi ya masikini kutoka watu milioni 10 mwaka 1990 mpaka watu milioni 12.6 mwaka 2012. Kwa taswira hii, Tanzania bado hai- jafanikisha vita dhidi ya umasikini! Dalili za ongezeko la mivutano ya kijamii nayo imekuwa bayana. Uvumulivu wa kidini, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiipa sifa Tan- zania toka kwa nchi nyingine kwene ukanda, vinayeyuka huku tunashuhudia kuuawa kwa viongozi wa kidini na nyumba za kuabudu zikichomwa. Ni katika muongo huu huu nchi imeshuhudia kujadiliwa na kuangaliwa upya kwa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliodumu nusu karne sasa. MKOA PATO LA MTU KWA MWAKA (TSH) PATO LA MTU KWA SIKU (TSH) Dar es Salaam 1,730,000 4,750 Iringa 1,430,000 3,920 Mbeya, Ruvuma, Arusha, Kilimanjaro 1,200,000 3,300 Tanga, Manyara 1,000,000 2,740 Moro, Lindi, Mtwara 900,000 2,465 Shinyanga 800,000 2,120 Dodoma, Singida 670,000 - 630,000 1,840 – 1,730 Kigoma 609,000 1,700 Mfumo wa uchumi unabadilika. Tanzania ni nchi yenye ardhi kubwa na sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi inaajiri watu sita kati ya kumi. Lakini mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa umeshuka kutoka asilimia 28 mwaka 2005 hadi asilimia 24 mwaka 2012. Kwa upande mwingine, mchango wasekta ya huduma (afya, elimu, fedha, mawasiliano) imeongezeka kutoka asilimia 46 hadi asilimia 49 ndani ya kipindi hicho hicho cha miaka saba. Hii inaone- sha jinsi gani sekta ya huduma inayotumia taaluma rasmi kwa kiwango kikubwa inavyokua kwa kasi na kuwanufaisha walioajiriwa humo, wakati kilimo kinachotegemea jasho la wananchi tu kinazidi kudorora. Misuli inashindwa na akili! Watoto wengi wamedumaa. Suala la lishe ni suala nyeti sana katika ukuaji na ustawi wa taifa. Lishe duni husababisha udumavu wa mwili na akili, afya mbaya na uwezo mdogo wa kujifunza na kufikiri. Mwisho wake ni uwezo mdogo wa kujipatia kipato na kurudisha nyuma maendeleo ya watu na taifa. Kitaifa hali ya udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitano imeongezeka toka asilimia 38 mwaka 2004 na kufikia asilimia 42 mwaka 2010. Kwa ujumla, watoto wanne kati ya kumi wana udumavu kitu ambacho kina athari nyingi sana hasa katika ufanyaji vyema mashuleni na katika maisha yao ya baadaye. Dodoma, ambapo watoto sita kati ya kumi wamedumaa, inaongoza katika hali ya udumavu. IJUE TANZANIA MWAKA 2035 Chanzo: Taasisi ya Takwimu ya Taifa

Upload: others

Post on 26-Sep-2019

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI … TANZANIA 2035.pdf · Ni asilimia tano (5) tu ya nguvukazi ya taifa ambayo imeajiriwa rasmi. Wengine wote wamejiajiri au wanafanya

TANZANIA YA MWAKA 2035IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ 1MWANANCHI

Toleo hili la mustakabali wa Tanzania ni mchakato ulioanza mwezi Februari 2014 kwa kuwakusanya wasomi, wafanyakazi wa serikali, wataalam, wanafunzi na wanazuoni kujadili hali ya nchi ya sasa na ya baadaye. SID, pamoja na washiriki wake Twaweza na Foundation for Civil Society imewahoji wananchi zaidi ya 1,500 kwa njia ya simu za mkononi na katika mikutano kwenye mikoa tisa ya Tanzania. Mikoa hii ni Dar es Salaam, Arusha, Kusini Pemba (Chake Chake), Mjini Magharibi (Zanzibar-Unguja), Mbeya, Kigoma, Mtwara, Dodoma na Mwanza.

Society for international Development (SiD)Society for International Development (SID) ni mtandao wa kimataifa wa watu na taasisi

zisizo za kiserikali ulioanzishwa mwaka 1957 kwa lengo la kukuza haki katika jamii naku-hamasisha ushiriki mkubwa wa watu. Kwa kupitia miradi mbali mbali, SID inaimarisha uwezo wa pamoja, kuwezesha majadiliano na kubadilisha uzoefu na maarifa miongoni mwa washirika wake. SID ina matawi zaidi ya 55 duniani kote, pamoja na taasisi 50 na wanacha-ma binasfi 3,000 kutoka nchi 125. Sekretariati ya SID ina ofisi tatu - Dar es Salaam, Nairobi, Kenya na Roma, Italia.

mraDi wa tanzania ya KeShoTanzania iko njia panda. Taifa letu linaonesha dalili za kuelekea pazuri ikiwa na uchumi

imara na jamii yenye umoja na mshikamano. Lakini pia, kuna dalili za kutisha. Umimi, ufisadi na kutojali vinaweza kuisambaratisha nchi. Lengo la mradi huu ni kuibua na kucho-chea tafakuri, mazungumzo na mijadala miongoni mwa wananchi kuhusu mustakabali wa Tanzania katika miaka ishirini ijayo. Nia kuu ni kuhakikisha majadiliano yanaongozwa na taarifa na uchambuzi wa kina kuhusu matumaini ya watanzania, hali halisi ya jamii, siasa na uchumi wa nchi, changamoto za msingi zinazotukabili, na hatima ya taifa letu ifikapo mwaka 2035. Tanzania itakuwaje miaka ishirini baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015? Wananchi watakuwa na maisha ya hali gani?.

matumaini ya wananchi Sauti za Wananchi ya Twaweza ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa

kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi. Katika awamu ya 23 ya upigaji simu, tuli-wafikia wahojiwa 1,408 kati ya tarehe 13 na 22 Agosti 2014 kupata maoni yao juu ya mustaka-bali wa Tanzania. Matokeo muhimu ni:lMwananchi mmoja kati ya wawili anatarajia kwamba maisha yake yatakuwa bora zaidi

katika siku zijazo, na idadi kubwa zaidi wanajiona kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kustawisha maisha yao ya baadaye.

lWananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa nchi yetu itakuwa “mahali pazuri pa kuishi” ifikapo mwaka 2025.

lWananchi tisa kati ya kumi wanaona kwamba maamuzi makubwa ya kitaifa yatakuwa chini ya udhibiti wa nchi yenyewe.

lWananchi saba kati ya kumi wanaamini kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, lakini wananchi wanne tu kati ya kumi wanaamini kuwa Tan-zania itafuzu kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.

lWananchi wameonesha kuwa vipaumbele muhimu kwa maisha ya baadaye ni kuongeza ubora wa utoaji wa huduma za kijamii, ukuaji wa uchumi na umoja wa kitaifa.

hali haliSi ya tanzaniaUchumi unakua kwa kasi. Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kasi katika miongo

miwili iliyopita na kufikia wastani wa asilimia 6 mpaka asilimia saba 7. Hakuna nchi yoyote nyingine Afrika Mashariki iliyoweza kukua kwa kasi hii na kwa muda mrefu hivi. Tanzania ni kipenzi cha wawekezaji. Mwaka 2014, Tanzania ilipokea dola bilioni 1.9 za uwekezaji, ambazo ni mara nne ya nchi jirani ya Kenya iliyopata dola milioni 514.

Lakini wananchi wengi bado wana hali mbaya. Licha ya kwamba kiwango cha umasikini umekuwa ukishuka toka asilimia 39 ya Watanzana wote mwaka 1990 mpaka asilimia 28 mwaka 2012, ongezeko la idadi ya watu imeongeza idadi ya masikini kutoka watu milioni 10 mwaka 1990 mpaka watu milioni 12.6 mwaka 2012. Kwa taswira hii, Tanzania bado hai-jafanikisha vita dhidi ya umasikini! Dalili za ongezeko la mivutano ya kijamii nayo imekuwa bayana. Uvumulivu wa kidini, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiipa sifa Tan-

zania toka kwa nchi nyingine kwene ukanda, vinayeyuka huku tunashuhudia kuuawa kwa viongozi wa kidini na nyumba za kuabudu zikichomwa. Ni katika muongo huu huu nchi imeshuhudia kujadiliwa na kuangaliwa upya kwa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliodumu nusu karne sasa.

mKoa pato la mtu Kwa

mwaKa (tSh)pato la mtu Kwa

SiKu (tSh)Dar es Salaam 1,730,000 4,750iringa 1,430,000 3,920mbeya, ruvuma, arusha, Kilimanjaro 1,200,000 3,300tanga, manyara 1,000,000 2,740moro, lindi, mtwara 900,000 2,465Shinyanga 800,000 2,120Dodoma, Singida 670,000 - 630,000 1,840 – 1,730Kigoma 609,000 1,700

Mfumo wa uchumi unabadilika. Tanzania ni nchi yenye ardhi kubwa na sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi inaajiri watu sita kati ya kumi. Lakini mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa umeshuka kutoka asilimia 28 mwaka 2005 hadi asilimia 24 mwaka 2012. Kwa upande mwingine, mchango wasekta ya huduma (afya, elimu, fedha, mawasiliano) imeongezeka kutoka asilimia 46 hadi asilimia 49 ndani ya kipindi hicho hicho cha miaka saba. Hii inaone-sha jinsi gani sekta ya huduma inayotumia taaluma rasmi kwa kiwango kikubwa inavyokua kwa kasi na kuwanufaisha walioajiriwa humo, wakati kilimo kinachotegemea jasho la wananchi tu kinazidi kudorora. Misuli inashindwa na akili!

Watoto wengi wamedumaa. Suala la lishe ni suala nyeti sana katika ukuaji na ustawi wa taifa. Lishe duni husababisha udumavu wa mwili na akili, afya mbaya na uwezo mdogo wa kujifunza na kufikiri. Mwisho wake ni uwezo mdogo wa kujipatia kipato na kurudisha nyuma maendeleo ya watu na taifa. Kitaifa hali ya udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitano imeongezeka toka asilimia 38 mwaka 2004 na kufikia asilimia 42 mwaka 2010. Kwa ujumla, watoto wanne kati ya kumi wana udumavu kitu ambacho kina athari nyingi sana hasa katika ufanyaji vyema mashuleni na katika maisha yao ya baadaye. Dodoma, ambapo watoto sita kati ya kumi wamedumaa, inaongoza katika hali ya udumavu.

ijue Tanzania Mwaka 2035

chanzo: taasisi ya takwimu ya taifa

Page 2: IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI … TANZANIA 2035.pdf · Ni asilimia tano (5) tu ya nguvukazi ya taifa ambayo imeajiriwa rasmi. Wengine wote wamejiajiri au wanafanya

TANZANIA YA MWAKA 2035 MWANANCHI.CO.TZ IJUMAA, JANUARI 9, 2015 2 MWANANCHI

Shule za msingi za umma zinatisha. Mwaka 2013 Benki ya Dunia kupitia ripoti yake kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki iitwayo ‘ Viashiria vya Utoaji wa Huduma za Elimu na Afya za Benki ya Dunia’ inaonyesha kinagaubaga ubora wa huduma ya elimu ya msingi nchini Tanzania, Kenya na Uganda. Kwa upande wa miundombinu, hali inaonyesha kuwa ni asilimia 2 tu ya shule za msingi za vijijini na asilimia 8 tu za shule zilizoko mijini ndizo zina umeme, maji na vyoo safi. Ikiliganishwa na Kenya katika hili, Tanzania inajikuta katika hali mbaya. Asilimia 60 ya shule za umma zote za Kenya zinapata huduma bora ya maji, vyoo safi na umeme.

Waalimu hawaingii darasani…Asilimia 68 ya waalimu wa shule za msingi za serikali mijini hawaingii darasani. Nchini Kenya, utoro wa walimu darasani kwa shule za serikali vijijini ni asilimia 50, na mijini ni asilimia 43. Nchini Uganda, utoro wa walimu ni asilimia 53. Waalimu wa Tanzania wanaongoza Afrika Mashariki kwa utoro!

…na hawafundishi kwa masaa yaliyopangwa. Kwa mujibu wa sera ya elimu, muda rasmi wa kufundisha ni masaa matano na dakika kumi na mbili kwa siku kwa Tanzania. Taarifa za kitafiti zinaonesha kuwa wanafunzi vijijini wanafundishwa kwa muda wa masaa mawili na dakika kumi na moja ambao ni asilimia 42 tu ya muda uliopangwa. Hali ni mbaya zaidi mijini ambapo wanafunzi wanafundishwa kwa muda wa lisaa limoja na dakika ishirini na nne, au asilimia 27 ya muda uliopangwa.

Watu wachache wana ajira rasmi. Ni asilimia tano (5) tu ya nguvukazi ya taifa ambayo imeajiriwa rasmi. Wengine wote wamejiajiri au wanafanya kazi ‘kimachinga.’ Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kipato cha wastani cha wafanyakazi nchini ni dola moja au Tsh 1,700 tu kwa siku. Ila katika Tanzania takwimu zinaonesha kuwa elimu inalipa kama inavyoonekana hapo chini.

KIWANGO CHA ELIMU ASILIMIA YA WANANCHI KIPATO (KWA MWAKA)

Wasio na elimu ya Msingi 18% Tsh 111,000Elimu ya msingi (Darasa la 7) 46% Tsh 404,000Elimu ya Sekondari (Form 4) 9% Tsh 1,990,000Elimu ya Juu 3% Tsh 4,667,000

Ugunduzi wa gesi umeleta matumaini makubwa. Tanzania ina hifadhi ya gesi inayokadiri-wa kufikia ujazo wa futi za mraba trilioni 56. Lakini wenzetu nao wamegundua rasilimali kama hii nyingi tu. Uganda imegundua hifadhi kubwa ya mafuta ardhini yenye uwezo wa kuzalisha mapipa 100,000 kwa siku kwa muda wa miaka 25. Nchini Kenya ugunduzi wa mafuta ni kila uchao, hasa kaskazini kwenye maeneo ya ziwa Turkana. Tafiti zinaonyesha kuwa Somalia ina hifadhi kubwa ya mapipa bilioni 110 ya mafuta.

Gesi ni mwarobaini wa umasikini? Hapa Tanzania, mitambo ikijengwa, gesi ikazalishwa na kuuzwa kwenye soko la kimataifa, imekadiriwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwamba kuanzia mwaka 2025, mapato ya gesi yatafikia dola billion 2.5 hadi bilioni 3.5 kwa mwaka mpaka mwaka 2040. Haya ni mapato makubwa yatakayotunisha pato la taifa na kuchochea ustawi, ukuaji na maendeleo. Ila tu kama mambo yataenda kama yanavyotarajiwa.

Sintofahamu! Pamoja na ugunduzi huu uliozaa matumaini, kuna mawili ambayo hatuwezi

kuwa na uhakika nayo. Suala la kwanza ni uwingi wa gesi duniani unaozidi mahitaji na matumizi. Mwaka 2013, tani milioni 286 za gesi zilizalishwa, lakini matumizi ya gesi duniani yalifika tani milioni 237 tu. Soko la gesi la China linalotegemewa na nchi kama Tanzania na Australia, limetekwa na Urusi ambayo itawauzia gesi yenye thamani ya dola bilioni 30 hadi ifikapo mwaka 2045. Bei ya gesi tangu mwaka juzi imeanza kushuka na mwenendo huo wa kushuka kwa bei unaweza kuendelea kwa muda mrefu sana.

Chanzo: World Bank Tanzania Economic Updates 2014

Page 3: IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI … TANZANIA 2035.pdf · Ni asilimia tano (5) tu ya nguvukazi ya taifa ambayo imeajiriwa rasmi. Wengine wote wamejiajiri au wanafanya

TANZANIA YA MWAKA 2035IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ 3MWANANCHI

Page 4: IJUMAA, JANUARI 9, 2015 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI … TANZANIA 2035.pdf · Ni asilimia tano (5) tu ya nguvukazi ya taifa ambayo imeajiriwa rasmi. Wengine wote wamejiajiri au wanafanya

TANZANIA YA MWAKA 2035 MWANANCHI.CO.TZ IJUMAA, JANUARI 9, 2015 4 MWANANCHI