injilikamaalivyoiandika yohanamtakatifu · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8...

60
YOHANA MTAKATIFU 1:1 1 YOHANA MTAKATIFU 1:15 INJILI KAMA ALIVYOIANDIKA YOHANA MTAKATIFU 1 Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu. 3 Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. 4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu. 5 Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. 6 Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, 7 ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini. 8 Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. 9 Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote. 10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. 13 Hawa wamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibi- nadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao. 14 Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pe- kee wa Baba; amejaa neema na ukweli. 15 Yohane ali- waambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana

Upload: others

Post on 09-Feb-2020

8 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 1:1 1 YOHANA MTAKATIFU 1:15

INJILI KAMA ALIVYOIANDIKAYOHANA MTAKATIFU

1 Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa naMungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Nenoalikuwa na Mungu. 3Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa;hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwamwanga wa watu. 5 Na mwanga huo huangaza gizani,nalo giza halikuweza kuushinda. 6Mungu alimtuma mtummoja jina lake Yohane, 7 ambaye alikuja kuwaambiawatu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wakewatu wote wapate kuamini. 8Yeye hakuwa huo mwanga,ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. 9Huundio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni,na kuwaangazia watu wote. 10 Basi, Neno alikuwakoulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa,lakini ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja katikanchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea.12 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, haoaliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. 13 Hawawamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibi-nadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenziya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao. 14 NayeNeno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuonautukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pe-kee wa Baba; amejaa neema na ukweli. 15 Yohane ali-waambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyundiye niliyemtajawakati niliposema: Anakujamtummojabaada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana

Page 2: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 1:16 2 YOHANA MTAKATIFU 1:31alikuwako kabla mimi sijazaliwa.” 16Kutokana na ukamil-ifu wake sisi tumepokea neema mfululizo. 17 MaanaMungu alitoa Sheria kwa njia ya Mose, lakini neemana kweli vimekuja kwa njia ya Kristo. 18 Hakuna mtualiyemwona Mungu wakati wowote ule. Mwana wa pekeealiye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiyealiyetujulisha habari za Mungu. 19 Huu ndio ushahidiYohane alioutoa wakati viongozi wa Wayahudi kuleYerusalemu walipowatuma makuhani wa Walawi kwakewamwulize: “Wewe u nani?” 20Yohane hakukataa kujibuswali hilo, bali alisema waziwazi, “Mimi siye Kristo.”21 Hapo wakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Je, wewe niEliya?” Yohane akajibu, “La, mimi siye.” Wakamwuliza,“Je, wewe ni yule nabii?” Yohane akawajibu, “La!” 22Naowakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Wasema nini juuyako mwenyewe? Tuambie, ili tuwapelekee jibu walewaliotutuma.” 23 Yohane akawajibu, “Mimi ndiye yuleambaye nabii Isaya alisema habari zake: Sauti ya mtuimesikika jangwani: Nyoosheni njia ya Bwana.” 24 Haowatu walikuwa wametumwa na Mafarisayo. 25 Basi,wakamwuliza Yohane, “Kama wewe si Kristo, wala Eliya,wala yule nabii, mbona wabatiza?” 26 Yohane akawajibu,“Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu,msiyemjua bado. 27 Huyo anakuja baada yangu, lakinimimi sistahili hata kumfungua kamba za viatu vyake.”28 Mambo haya yalifanyika huko Bethania, ng'ambo yamto Yordani ambako Yohane alikuwa anabatiza. 29Keshoyake, Yohane alimwona Yesu akimjia, akasema, “Huyundiye Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi yaulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyesema juu yake: Baadayangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kulikomimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa! 31 Mimimwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja kubatiza kwa

Page 3: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 1:32 3 YOHANA MTAKATIFU 1:45maji ili watu wa Israeli wapate kumjua.” 32 Huu ndioushahidi Yohane alioutoa: “Nilimwona Roho akishukakama njiwa kutoka mbinguni na kutua juu yake. 33Mimisikumjua, lakini yule aliyenituma nikabatize watu kwamaji alikuwa ameniambia: Mtu yule utakayemwona Rohoakimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyondiye anayebatiza kwa Roho Mtakatifu. 34 Mimi nime-ona na ninawaambieni kwamba huyu ndiye Mwana waMungu.” 35 Kesho yake, Yohane alikuwa tena mahalihapo pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 AlipomwonaYesu akipita akasema, “Tazameni! Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Mungu.” 37Hao wanafunzi walimsikia Yohaneakisema maneno hayo, wakamfuata Yesu. 38 Basi, Yesualigeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata,akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao wakamjibu, “Rabi(yaani Mwalimu), unakaa wapi?” 39 Yesu akawaambia,“Njoni, nanyi mtaona.” Hao wanafunzi wakamfuata,wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda nayesiku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni. 40 Andrea,nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa hao wawiliwaliokuwa wamemsikia Yohane akisema hivyo, wakam-fuata Yesu. 41 Andrea alimkuta kwanza Simoni, nduguyake, akamwambia, “Tumemwona Masiha” (maana yakeKristo). 42Kisha akampeleka Simoni kwa Yesu. Naye Yesuakamtazama Simoni akasema, “Wewe ni Simoni mwanawa Yohane. Sasa utaitwa Kefa.” (maana yake ni Petro,yaani, “Mwamba.”) 43 Kesho yake Yesu aliamua kwendaGalilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akinaAndrea na Petro. 45 Naye Filipo akamkuta Nathanieli,akamwambia, “Tumemwona yule ambaye Mose aliandikajuu yake katika kitabu cha Sheria, na ambaye manabiiwaliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu,

Page 4: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 1:46 4 YOHANA MTAKATIFU 2:10kutoka Nazareti.” 46 Naye Nathanieli akamwuliza Fil-ipo, “Je, kitu chema chaweza kutoka Nazareti?” Fil-ipo akamwambia, “Njoo uone.” 47 Yesu alipomwonaNathanieli akimjia alisema juu yake, “Tazameni! Huyoni Mwisraeli halisi: hamna hila ndani yake.” 48 NayeNathanieli akamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesuakamwambia, “Ulipokuwa chini yamtini hata kabla Filipohajakuita, nilikuona.” 49 Hapo Nathanieli akamwambia,“Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu. Wewe ni Mfalmewa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Je, umeamini kwakuwa nimekwambia kwamba nilikuona chini ya mtini?Utaona makubwa zaidi kuliko haya.” 51 Yesu akaendeleakusema, “Nawaambieni kweli, mtaona mbingu zinafun-guka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu yaMwana wa Mtu.”

21 Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani

Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, 2naye Yesu alikuwaamealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3 Divaiilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!”4 Yesu akamjibu, “Mama, usiniambie la kufanya. Saayangu bado.” 5Hapo mama yake akawaambia watumishi,“Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” 6 Hapo palikuwana mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliwezakuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwaimewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi yakutawadha. 7 Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyomaji.” Nao wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaam-bia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”9Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwayamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakiniwale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wakaramu akamwita bwana arusi, 10akamwambia, “Kilamtu

Page 5: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU2:115YOHANAMTAKATIFU2:25huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huan-daa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpakasasa!” 11 Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana,Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wakewakamwamini. 12 Baada ya hayo, Yesu alishuka pamojanamama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaendaKafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache. 13 Sikukuuya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesuakaenda Yerusalemu. 14Hekaluni aliwakutawatuwakiuzang'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwawamekaa kwenye meza zao. 15 Akatengeneza mjelediwa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja nakondoo na ng'ombewao, akazimwaga sarafu zawenye ku-vunja fedha na kupindua meza zao. 16 Akawaambia walewaliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivi hapa. Msi-ifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!” 17Wanafunziwakewakakumbuka kwambaMaandiko yasema: “Upendowangu kwa nyumba yakowaniua.” 18Baadhi yaWayahudiwakamwuliza Yesu, “Utafanya muujiza gani kuonyeshakwamba unayo haki kufanya mambo haya?” 19 Yesuakawaambia, “Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwasiku tatu.” 20 Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hilililijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je,wewe utalijenga kwa siku tatu?” 21 Lakini Yesu alikuwaanaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake. 22 Basi,alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbukakwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini MaandikoMatakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.23 Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka,watu wengi walimwamini walipoona ishara alizozifanya.24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajuawote. 25 Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu,maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni

Page 6: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 3:1 6 YOHANA MTAKATIFU 3:16mwao.

31 Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi

cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo. 2 Siku moja al-imwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajuakwambawewe nimwalimu uliyetumwanaMungu,maanahakunamtu awezaye kufanya ishara unazozifanyaMunguasipokuwa pamoja naye.” 3 Yesu akamwambia, “Kwelinakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuonaufalme wa Mungu.” 4 Nikodemo akamwuliza, “Mtu mz-ima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumbonimwa mama yake na kuzaliwa mara ya pili!” 5 Yesuakamjibu, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa majina Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalmewaMungu.6 Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huza-liwa kiroho kwa Roho. 7 Usistaajabu kwamba nimek-wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakinihujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwamtu aliyezaliwa kwa Roho.” 9 Nikodemo akamwuliza,“Mambo haya yanawezekanaje?” 10 Yesu akamjibu,“Je, wewe ni mwalimu katika Israel na huyajui mambohaya? 11 Kweli nakwambia, sisi twasema tunayoyajua nakushuhudia tuliyoyaona, lakini ninyi hamkubali ujumbewetu. 12 Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyihamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mamboya mbinguni? 13 Hakuna mtu aliyepata kwenda juumbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu ambaye ameshukakutoka mbinguni. 14 “Kama vile Mose alivyomwinuajuu nyoka wa shaba kule jangwani, naye Mwana waMtu atainuliwa juu vivyo hivyo, 15 ili kila anayemwaminiawe na uzima wa milele. 16 Maana Mungu aliupenda

Page 7: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 3:17 7 YOHANA MTAKATIFU 3:30ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ilikila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguniili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe ulimwengu.18 “Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwaminiamekwisha hukumiwa kwa sababu hakumwamini Mwanawa pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe ndiyo hii:Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapendagiza kulikomwanga, kwani matendo yao ni maovu. 20Kilamtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala hajikwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovuyamulikwe. 21 Lakini mwenye kuuzingatia ukweli hujakwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yame-tendwa kwa kumtiiMungu.” 22Baada ya hayo, Yesu alifikamkoani Yudea pamoja na wanafunzi wake. Alikaa hukopamoja nao kwa muda, akibatiza watu. 23 Yohane piaalikuwa akibatiza watu huko Ainoni, karibu na Salemu,maana huko kulikuwa na maji mengi. Watu walimwen-dea, naye akawabatiza. 24 (Wakati huo Yohane alikuwabado hajafungwa gerezani.) 25 Ubishi ulitokea kati yabaadhi ya wanafunzi wa Yohane na Myahudi mmojakuhusu desturi za kutawadha. 26 Basi, wanafunzi haowakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yulemtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani naambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, nawatu wote wanamwendea.” 27Yohane akawaambia, “Mtuhawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu. 28 Nanyiwenyewemwaweza kushuhudia kuwanilisema: Mimi siyeKristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie! 29 Bibiarusi niwake bwanaarusi, lakini rafiki yake bwana arusi, anayes-imama na kusikiliza, hufurahi sana anapomsikia bwanaarusi akisema. Ndivyo furaha yangu ilivyokamilishwa.30Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.

Page 8: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 3:31 8 YOHANA MTAKATIFU 4:1031 “Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokayeduniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia.Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.32 Yeye husema yale aliyoyaona na kuyasikia, lakinihakuna mtu anayekubali ujumbe wake. 33 Lakini mtuyeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwambaMungu ni kweli. 34 Yule aliyetumwa na Mungu husemamaneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyoRoho wake bila kipimo. 35 Baba anampenda Mwana naamemkabidhi vitu vyote. 36Anayemwamini Mwana anaouzima wamilele; asiyemtii Mwana hatakuwa na uzima wamilele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.”

41Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza

na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane. 2 (Lakiniukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunziwake.) 3 Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudiGalilaya; 4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibuna shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe,Yosefu. 6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo,naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kandoya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. 7 Basi,mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesuakamwambia, “Nipatie maji ninywe.” 8 (Wakati huowanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununuachakula.) 9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Weweni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezajekuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikianonaWasamaria katika matumizi ya vitu.) 10Yesu akamjibu,“Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayek-wambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba,

Page 9: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 4:11 9 YOHANA MTAKATIFU 4:25naye angekupa maji yaliyo hai.” 11Huyo mama akasema,“Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, na-cho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai? 12 Au,labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo?Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watotowake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki.”13 Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataonakiu tena. 14 Lakini atakayekunywa maji nitakayompamimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwandani yake chemchemi ya maji ya uzima na kumpatiauzima wa milele.” 15 Huyo mwanamke akamwambia,“Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; nisijetena mpaka hapa kuteka maji.” 16 Yesu akamwambia,“Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa.” 17 Huyomwanamke akamwambia, “Mimi sina mume.” Yesuakamwambia, “Umesema kweli, kwamba huna mume.18Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishinaye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli.” 19HuyoMwanamke akamwambia, “Mheshimiwa, naona ya kuwawewe u nabii. 20 Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu,lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabuduMungu ni kule Yerusalemu.” 21 Yesu akamwambia, “Ni-amini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Babajuu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 NinyiWasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tu-namjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu una-toka kwaWayahudi. 23 Lakini wakati unakuja, tena umek-wisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabuduBaba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyondio Baba anaotaka. 24Mungu ni Roho, na watu watawezatu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake.” 25Huyomama akamwambia, “Najua kwamba Masiha, aitwayeKristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu.”

Page 10: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 4:26 10 YOHANA MTAKATIFU 4:4326 Yesu akamwambia, “Mimi ninayesema nawe, ndiye.”27 Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sanakuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtualiyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongeana mwanamke?” 28 Huyo mama akauacha mtungi wakepale, akaenda mjini na kuwaambia watu, 29 “Njoni mkam-wone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je,yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?” 30Watu wakatokamjini, wakamwendea Yesu. 31Wakati huohuo wanafunziwakewalikuwawanamsihi Yesu: “Mwalimu, ule chakula.”32 Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msi-chokijua ninyi.” 33 Wanafunzi wake wakaulizana, “Je,kuna mtu aliyemletea chakula?” 34 Yesu akawaambia,“Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyeni-tuma na kuitimiza kazi yake. 35 Ninyi mwasema: Badomiezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakinimimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yakotayari kuvunwa. 36 Mvunaji anapata mshahara wake,na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele;hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja. 37 Kwasababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupandana mwingine huvuna. 38 Mimi nimewatuma mkavunemavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanyakazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”39 Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababuya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mamboyote niliyofanya.” 40 Wasamaria walimwendea Yesuwakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili.41Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbewake. 42 Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuaminitu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tume-sikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi waulimwengu.” 43 Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo,

Page 11: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 4:44 11 YOHANA MTAKATIFU 5:4akaenda Galilaya. 44 Maana Yesu mwenyewe alisemawaziwazi kwamba, “Nabii hapati heshima katika nchiyake.” 45 Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi wal-imkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuuya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda hukoYerusalemu wakati wa sikukuu hiyo. 46 Yesu alifika tenahukomjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuzamajikuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa namtotomgonjwa huko Kafarnaumu. 47 Basi, huyo ofisa aliposikiakuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya,alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wakealiyekuwa mgonjwa mahututi. 48 Yesu akamwambia,“Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!” 49 Huyoofisa akamwambia, “Mheshimiwa, tafadhali twende kablamwanangu hajafa.” 50 Yesu akamwambia, “Nenda tu,mwanao yu mzima.” Huyo mtu akaamini maneno yaYesu, akaenda zake. 51 Alipokuwa bado njiani, watumishiwakewalikutana naye, wakamwambia kwambamwanawealikuwa mzima. 52 Naye akawauliza saa mtoto alipopatanafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homailimwacha.” 53Huyobaba akakumbuka kwamba ilikuwanisaa ileile ambapoYesu alimwambia: “Mwanao yumzima.”Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote. 54 Hiiilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatokaYudea kwenda Galilaya.

51Baada ya hayo kulikuwana sikukuu yaWayahudi, naye

Yesu akaenda Yerusalemu. 2Huko Yerusalemu, karibu namlango uitwao Mlango wa Kondoo, kulikuwa na bwawala maji liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwana baraza tano zenyematao. 3Humo barazanimlikuwa nawagonjwawengi wamekaa: vipofu, viwete na waliopooza.Walikuwa wakingojea maji yatibuliwe, 4maana mara kwa

Page 12: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 5:5 12 YOHANA MTAKATIFU 5:18maramalaika alishukamajini nyakati fulani na kuyatibua.Mtu yeyote aliyekuwa wa kwanza kuingia majini baada yamaji kutibuliwa, alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao.5 Basi, hapo palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mgonjwakwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Nayealipomwona huyomtu amelala hapo, akatambua kwambaalikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je,wataka kupona?” 7 Naye akajibu, “Mheshimiwa, mimisina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa.Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia.”8 Yesu akamwambia, “Inuka, chukua mkeka wako utem-bee.” 9Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake,akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato. 10 Kwahiyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia huyo mtu aliye-ponywa, “Leo ni Sabato, si halali kubeba mkeka wako.”11 Lakini yeye akawaambia, “Yule mtu aliyeniponya ndiyealiyeniambia: Chukua mkeka wako, tembea.” 12 Naowakamwuliza, “Huyo mtu aliyekwambia: Chukua mkekawako, tembea, ni nani?” 13 Lakini yeye hakumjua huyomtu aliyemponya, maana Yesu alikuwa amekwisha on-doka mahali hapo, kwani palikuwa na umati mkubwawa watu. 14 Basi, baadaye Yesu alimkuta huyo aliye-ponywa Hekaluni, akamwambia, “Sasa umepona; usi-tende dhambi tena, usije ukapatwa na jambo baya zaidi.”15Huyomtu akaenda, akawaambia viongozi waWayahudikwamba Yesu ndiye aliyemponya. 16 Kwa vile Yesu al-ifanya jambo hilo siku ya Sabato, Wayahudi walianzakumdhulumu. 17 Basi, Yesu akawaambia, “Baba yanguanafanya kazi daima, nami pia nafanya kazi.” 18 Kwasababu ya maneno haya, viongozi wa Wayahudi walizidikutafuta njia ya kumwua Yesu: si kwa kuwa aliivunjaSheria ya Sabato tu, bali pia kwa kuwa alisema kwambaMungu ni Baba yake, na hivyo akajifanya sawa na Mungu.

Page 13: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 5:19 13 YOHANA MTAKATIFU 5:3219Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezikufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile ana-chomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanyaBaba, Mwana hukifanya vilevile. 20 Baba ampendaMwana, na humwonyesha kila kitu anachokifanya yeyemwenyewe, tena atamwonyesha mambo makuu kulikohaya, nanyi mtastaajabu. 21 Kama vile Baba huwafufuawafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo naye Mwana huwapauzima wale anaopenda. 22 Baba hamhukumu mtu yeyote;shughuli yote yahukumuamemkabidhiMwana, 23 ili watuwote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimuBaba. AsiyemheshimuMwana hamheshimu Baba ambayeamemtuma. 24 “Kweli nawaambieni, anayesikia nenolangu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wamilele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita ku-toka kifo na kuingia katika uzima. 25 Kweli nawaambi-eni, wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wafuwataisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia,wataishi. 26 Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyopia alivyomjalia Mwanawe kuwa asili ya uhai. 27 Tenaamempa mamlaka ya kuhukumu kwa sababu yeye niMwana wa Mtu. 28Msistaajabie jambo hili; maana wakatiunakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikiasauti yake, 29 nao watafufuka: wale waliotenda memawatafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu wata-fufuka na kuhukumiwa. 30 “Mimi siwezi kufanya kitukwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumu kamaninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu niya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe,bali apendavyo yule aliyenituma. 31Nikijishuhudia mimimwenyewe, ushahidi wangu hauwezi kukubaliwa kuwawakweli. 32Lakini yukomwingine ambayehutoaushahidijuu yangu, nami najua kwamba yote anayosema juu yangu

Page 14: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 5:33 14 YOHANA MTAKATIFU 6:1ni ya kweli. 33 Ninyi mlituma ujumbe kwa Yohane nayealiushuhudia ukweli. 34 Si kwamba mimi nautegemeaushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ilimpate kuokolewa. 35Yohane alikuwa kama taa iliyokuwaikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahiamwanga huo kwa kitambo. 36 Lakini mimi nina ushahidijuu yangu ambaonimkuu zaidi kulikoulewaYohane. Kwamaana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye,ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.37Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapatakamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake, 38 naujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwaminiyule aliyemtuma. 39 Ninyi huyachunguza MaandikoMatakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uzimawa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhu-dia! 40 Hata hivyo, ninyi hamtaki kuja kwangu ili mpateuzima. 41 “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwawatu. 42 Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendokwa Mungu haumo mioyoni mwenu. 43 Mimi nimekujakwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtumwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtam-pokea. 44 Mwawezaje kuamini, hali ninyi mnapendakupokea sifa kutoka kwenu ninyi wenyewe, wala hamta-futi sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu?45 Msifikiri kwamba mimi nitawashtaki kwa Baba. Moseambaye ninyi mmemtumainia ndiye atakayewashtaki.46 Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini namimi pia; maana Mose aliandika juu yangu. 47 Lakinihamuyaamini yale aliyoandika, mtawezaje basi, kuaminimaneno yangu?”

61 Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa

Page 15: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 6:2 15 YOHANA MTAKATIFU 6:19Tiberia). 2 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwasababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwaakifanya kwa kuwaponya wagonjwa. 3 Yesu alipandamlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. 4 Sikukuuya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia. 5 Basi,Yesu na alipotazamana kuona umatiwawatu ukija kwake,alimwambia Filipo, “Tununue wapi mikate ili watu hawawapate kula?” 6 (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo,kwani alijua mwenyewe atakalofanya.) 7 Filipo akamjibu,“Mikate ya denari mia mbili za fedha haiwatoshi watuhawa hata kama ila mmoja atapata kipande kidogo tu!”8 Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguyeSimoni Petro, akamwambia, 9 “Yupo hapa mtoto mmojaaliye namikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakinihivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?” 10 Yesuakasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi telemahali hapo. Basi, watuwakaketi, jumla yapata wanaumeelfu tano. 11 Yesu akaitwaa ile mikate, akamshukuruMungu, akawagawia watu waliokuwa wameketi; akafanyavivyo hivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadirialivyotaka. 12Watu waliposhiba Yesu akawaambia wana-funzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki visipotee.”13 Basi, wakakusanya vipande vya mikate ya shayiriwalivyobakiza wale watu waliokula, wakajaza vikapukumi na viwili. 14Watuwalipoiona ishara hiyo aliyoifanyaYesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye nabii anayekujaulimwenguni.” 15 Yesu akajua ya kuwa watu walitakakumchukua wamfanye mfalme, akaondoka tena, akaendamlimani peke yake. 16 Ilipokuwa jioni wanafunzi wakewaliteremkahadi ziwani, 17wakapandamashua ili wavukekwenda Kafarnaumu. Giza lilikuwa limeingia, na Yesualikuwa hajawafikia bado. 18 Ziwa likaanza kuchafukakwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19Wanafunzi

Page 16: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 6:20 16 YOHANA MTAKATIFU 6:33walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano ausita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribiamashua; wakaogopa sana. 20 Yesu akawaambia, “Nimimi, msiogope!” 21 Walifurahi kumchukua Yesu katikamashua; namaramashua ikawasili nchi kavu walipokuwawanakwenda. 22 Kesho yake umati wa watu walewaliobaki upandewapili wa ziwawalitambua kwamba ku-likuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katikamashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi haowalikuwawamekwenda zao peke yao. 23Mashua nyinginekutoka Tiberia zilifika mahali hapo watu walipokula ilemikate, Bwana alipokwisha mshukuru Mungu. 24 Basi,haowatuwalipogundua kwamba Yesu nawanafunzi wakehawakuwapo mahali hapo, walipanda mashua, wakaendaKafarnaumu wakimtafuta. 25 Wale watu walipomkutaYesu ng'ambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu,ulifika lini hapa?” 26 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambi-eni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwasababu mlikula ile mikate mkashiba. 27Msikishughulikiechakula kiharibikacho; kishugulikieni chakula kidumu-cho kwa ajili ya uzima wa milele. Mwana wa Mtu ambayeBaba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.” 28 Waowakamwuliza, “Tufanye nini ili tuweze kuzitenda kazi zaMungu?” 29 Yesu akawajibu, “Hii ndiyo kazi anayotakaMungumuifanye: kumwamini yule aliyemtuma.” 30Hapowakamwambia, “Utafanya ishara gani ili tuione tupatekukuamini? Utafanya kitu gani? 31Wazee wetu walikulamana kule jangwani, kama yasemavyo Maandiko: Ali-walisha mkate kutoka mbinguni.” 32 Yesu akawaambia,“Kweli nawaambieni, Mose hakuwapeni mkate kutokambinguni; Baba yangu ndiye awapaye ninyi mkate halisikutoka mbinguni. 33 Maana mkate wa Mungu ni yuleashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uz-

Page 17: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 6:34 17 YOHANA MTAKATIFU 6:51ima.” 34 Basi, wakamwambia, “Mheshimiwa, tupe daimamkate huo.” 35Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wauzima. Anayekuja kwangu hataona njaa; anayeniaminihataona kiu kamwe. 36 Lakini niliwaambieni kwambaingawa mmeniona hamniamini. 37 Wote anaonipa Babawatakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekujakwangu, 38 kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwaajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwaya yule aliyenituma. 39 Na matakwa ya yule aliyenitumandiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alion-ipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho. 40 Maana ana-chotaka Baba yangu ndicho hiki: kila amwonaye Mwanana kumwamini awe na uzima wa milele; nami nitamfu-fua Siku ya mwisho.” 41 Basi, Wayahudi wakaanza ku-nung'unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshukakutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Je, huyu si mwanawa Yosefu? Tunawajua baba yake na mama yake!Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbin-guni?” 43 Yesu akawaambia, “Acheni kunung'unika ninyikwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Babaaliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtuhuyo Siku yamwisho. 45Manabii wameandika: Watuwotewatafundishwa na Mungu. Kila mtu anayemsikia Babana kujifunza kutoka kwake, huja kwangu. 46 Hii hainamaana kwamba yupo mtu aliyemwona Baba, isipokuwayule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.47Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uzimawamilele.48Mimi ni mkate wa uzima. 49Wazee wenu walikula manakule jangwani, lakini walikufa. 50Huu ndio mkate kutokambinguni; mkate ambao anayekula hatakufa. 51Mimi nimkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akilamkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwiliwangu ninaoutoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

Page 18: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 6:52 18 YOHANA MTAKATIFU 6:6852Ndipo Wayahudi wakaanza kubishana kati yao: 53 Yesuakawaambia, “Kweli nawaambieni, msipokula mwili waMwana wa Mtu na kunywa damu yake, hamtakuwa nauzima ndani yenu. 54Anayekula mwili wangu na kunywadamu yangu anao uzima wa milele nami nitamfufuasiku ya mwisho. 55 Maana mwili wangu ni chakula chakweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulayemwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu,nami nakaa ndani yake. 57 Baba aliye hai alinituma,nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimiataishi pia kwa sababu yangu. 58 Basi, huu ndio mkateulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokulababu zetu, wakafa. Aulaye mkate huu ataishi milele.”59 Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sun-agogi kule Kafarnaumu. 60 Basi, wengi wa wafuasi wakewaliposikia hayo, wakasema, “Haya ni mambo magumu!Nani awezaye kuyasikiliza?” 61 Yesu alijua bila kuam-biwa na mtu kwamba wanafunzi wake walikuwa wana-nung'unika juu ya jambo hilo, akawauliza, “Je, jambohili linawafanya muwe na mashaka? 62 Itakuwaje basi,mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kulealikokuwa kwanza? 63Rohondiye atiaye uzima; binadamupeke yake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho, niuzima. 64 Hata hivyo, wako baadhi yenu wasioamini.”(Yesu alisema hivyo kwani alijua tangu mwanzo ni kinanani wasioamini, na pia ni nani atakayemsaliti.) 65 Kishaakasema, “Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakunaawezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba yangu.”66 Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudinyumawasiandamane naye tena. 67Basi, Yesu akawaulizawale kumi na wawili, “Je, nanyi pia mwataka kwendazenu?” 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tutakwendakwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa

Page 19: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 6:69 19 YOHANA MTAKATIFU 7:14milele. 69Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiweyule Mtakatifu wa Mungu.” 70 Yesu akawaambia, “Je,sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmojawenu ni Ibilisi!” 71 Yesu alisema hayo juu ya Yuda,mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyu alikuwa ndiyeatakayemsaliti, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi nawawili.

71 Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea katika

Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababuviongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumwua.2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.3 Basi ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uendeYudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.4 Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kuju-likana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya,basi, jidhihirishe kwa ulimwengu.” 5 (Hata ndugu zakehawakumwamini!) 6 Basi, Yesu akawaambia, “Wakatiwangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kilawakati unafaa. 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi,lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazikwambamatendo yake nimaovu. 8Ninyi nendeni kwenyesikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maanasaa yangu ifaayo haijafika.” 9 Alisema hayo kisha ak-abaki huko Galilaya. 10 Baada ya ndugu zake kwendakwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuendakwa hadhara bali kwa siri. 11 Viongozi wa Wayahudiwalikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza:“Yuko wapi?” 12 Kulikuwa na minong'ono mingi katikaumati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.”Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.” 13 Hatahivyo hakunamtu aliyethubutu kusema, habari zake had-harani kwa kuwaogopa viongozi waWayahudi. 14Sikukuu

Page 20: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 7:15 20 YOHANA MTAKATIFU 7:29hiyo ilipofikia katikati, Yesu naye alikwenda Hekaluni,akaanza kufundisha. 15 Basi, Wayahudi wakashangaana kusema “Mtu huyu amepataje elimu naye hakusomashuleni?” 16 Hapo Yesu akawajibu, “Mafundisho ninay-ofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma. 17Mtuanayependa kufanya yale anayotaka Mungu, atajua kamamafundisho yangu yametoka kwaMungu, aumimi najise-mea tu mwenyewe. 18 Yeye anayejisemea tu mwenyeweanatafuta sifa yake mwenyewe; lakini anayetafuta sifaya yule aliyemtuma, huyo ni mwaminifu, na ndani yakehamna uovu wowote. 19 Je, Mose hakuwapeni Sheria?Hata hivyo, hakuna hatammojawenu anayeishika Sheria.Kwa nini mnataka kuniua?” 20 Hapo watu wakamjibu,“Una wazimu wewe! Nani anataka kukuua?” 21 Yesuakawajibu, “Kuna jambo moja nililofanya, nanyi mnal-istaajabia. 22 Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri.(Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitokakwa mababu). Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku yaSabato. 23 Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabatokusudi Sheria ya Mose isivunjwe, mbona mnanikasirikiakwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa sikuya Sabato? 24 Msihukumu mambo kwa nje tu; toenihukumu ya haki.” 25 Baadhi ya watu wa Yerusalemuwalisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?26 Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakunamtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwaviongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?27 Kristo atakapokuja hakuna mtu atakayejua mahalialikotoka, lakini sisi tunajua alikotoka mtu huyu!” 28Basi,Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti nakusema, “Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hatahivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeyealiyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui. 29 Lakini

Page 21: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 7:30 21 YOHANA MTAKATIFU 7:43mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiyealiyenituma.” 30 Basi, watu wakataka kumtia nguvuni,lakini hakuna mtu aliyethubutu kumkamata kwa sababusaa yake ilikuwa haijafika bado. 31 Wengi katika uleumati wa watu walimwamini, wakasema, “Je, Kristo akijaatafanya ishara kubwa zaidi kuliko alizozifanya huyu?”32 Mafarisayo waliwasikia watu wakinong'ona manenohayo juu ya Yesu. Basi, wao pamoja na makuhaniwakuu wakawatuma walinzi wamtie nguvuni. 33 Yesuakasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kishanitamwendea yule aliyenituma. 34 Mtanitafuta lakinihamtaniona, maana pale nitakapokuwa ninyi hamwezikufika.” 35 Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwawao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutawezakumpata? Atakwenda kwaWayahudi waliotawanyika katiya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki? 36 Ana maanagani anaposema: Mtanitafuta lakini hamtanipata, namahali nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika?” 37 Sikuya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalum. Yesualisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiuna aje kwangu anywe. 38 Kama yasemavyo MaandikoMatakatifu: Anayeniamini mimi, mito ya maji yenye uz-ima itatiririka kutoka moyoni mwake!” 39 (Alisema hayokumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watam-pokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababuYesu alikuwa hajatukuzwa bado.) 40Baadhi yawatu katikaule umati walisikia maneno hayo, wakasema, “Kweli mtuhuyu ndiye yule nabii!” 41 Wengine wakasema, “Huyundiye Kristo!” Lakini wengine walisema, “Je, yawezekanaKristo akatoka Galilaya? 42 Maandiko Matakatifu yase-maje? Yanasema: Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi,na atazaliwa Bethlehemu, mji wa Daudi!” 43 Basi, kuka-tokea mafarakano juu yake katika ule umati wa watu.

Page 22: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 7:44 22 YOHANA MTAKATIFU 8:744Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakunaaliyejaribu kumkamata. 45 Kisha wale walinzi wakarudikwa makuhani wakuu na Mafarisayo; nao wakawauliza,“Kwanini hamkumleta?” 46Walinziwakawajibu, “Hakunamtu aliyepata kamwekusemakama asemavyomtuhuyu!”47 Mafarisayo wakawauliza, “Je, nanyi pia mmedan-ganyika? 48 Je, mmekwisha mwona hata mmoja wa vion-gozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini?49 Lakini umati huu haujui Sheria ya Mose; umelaaniwa!”50 Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awalialikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia,51 “Je, Sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikiakwanza na kujua anafanya nini?” 52 Nao wakamjibu,“Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachun-guze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilayahakutoki kamwe nabii!” 53 Basi, wote wakaondoka, kilamtu akaenda zake;

81 lakini Yesu akaenda kwenye mlima wa Mizeituni.

2 Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tenaHekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawaanawafundisha. 3 Basi, walimu wa Sheria na Mafarisayowakamletea mwanamke mmoja aliyefumaniwa katikauzinzi. Wakamsimamisha katikati yao. 4 Kishawakamwuliza Yesu, “Mwalimu! Mwanamke huyualifumaniwa katika uzinzi. 5 Katika Sheria yetu Mosealituamuru mwanamke kama huyu apigwe mawe.Basi, wewe wasemaje?” 6 Walisema hivyo kumjaribu,wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainamachini, akaandika ardhini kwa kidole. 7 Walipozidikumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiyena dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga

Page 23: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 8:8 23 YOHANA MTAKATIFU 8:22jiwe.” 8 Kisha akainama tena, akawa anaandika ardhini.9 Waliposikia hivyo, wakaanza kutoweka mmojammoja,wakitanguliwa na wazee. Yesu akabaki peke yake,na yule mwanamke amesimama palepale. 10 Yesualipoinuka akamwuliza huyo mwanamke, “Wako wapiwale watu? Je, hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”11 Huyo mwanamke akamjibu, “Mheshimiwa, hakunahata mmoja!” Naye Yesu akamwambia, “Wala mimisikuhukumu. Nenda zako; na tangu sasa usitende dhambitena.” 12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia,“Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuatamimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwangawa uzima.” 13 Basi, Mafarisayo wakamwambia, “Weweunajishuhudia mwenyewe; kwa hiyo ushahidi wako sihalali.” 14 Yesu akawajibu, “Hata kama ninajishuhudiamwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli kwa sababumiminajua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjuinilikotoka wala ninakokwenda. 15 Ninyi mnahukumukwa fikira za kibinadamu, lakini mimi simhukumu mtu.16Hata nikihukumu, hukumuyanguni ya haki kwa sababumimi siko peke yangu; Baba aliyenituma yuko pamojanami. 17 Imeandikwa katika Sheria yenu ya kwambaushahidi wa watu wawili ni halali. 18Mimi najishuhudiamwenyewe, naye Baba aliyenituma, ananishuhudiapia.” 19 Hapo wakamwuliza, “Baba yako yuko wapi?”Yesu akawajibu “Ninyi hamnijui mimi wala hamumjuiBaba. Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba yangupia.” 20 Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba chahazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Wala hakunamtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwahaijafika bado. 21 Yesu akawaambia tena, “Naenda zangunanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu.Niendako mimi, ninyi hamwezi kufika.” 22 Basi, viongozi

Page 24: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 8:23 24 YOHANA MTAKATIFU 8:38wa Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Mbona anasema:Niendako ninyi hamwezi kufika?” 23 Yesu akawaambia,“Ninyi mmetoka papa hapa chini, mimi nimetoka juu;ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwenguhuu. 24 Ndiyo maana niliwaambieni mtakufa katikadhambi zenu. Kama msipoamini kwamba Mimi ndimi,mtakufa katika dhambi zenu.” 25 Nao wakamwuliza,“Wewe ni nani?” Yesu akawajibu, “Nimewaambieni tangumwanzo! 26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juuyenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambiaulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake.”27Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu yaBaba. 28Basi, Yesu akawaambia, “MtakapokwishamwinuaMwana wa Mtu hapo ndipo mtakapojua kwamba Mimindimi, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe,ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha. 29 Yulealiyenituma yuko pamoja nami; yeye hakuniacha pekeyangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza.”30 Baada ya kusema hayo watu wengi walimwamini.31 Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini,“Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwakweli wanafunzi wangu. 32 Mtaujua ukweli, nao ukweliutawapeni uhuru.” 33 Nao wakamjibu, “Sisi ni wazawawa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wamtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: mtakuwahuru?” 34 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, kila mtuanayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35Mtumwahana makao ya kudumu nyumbani, lakini mwanaanayo makao ya kudumu. 36 Kama mwana akiwapeniuhuru mtakuwa huru kweli. 37 Najua kwamba ninyi niwazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniuakwa sababu hamuyakubali mafundisho yangu. 38 Miminasema yale aliyonionyesha Baba, lakini ninyi mwafanya

Page 25: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 8:39 25 YOHANA MTAKATIFU 8:52yale aliyowaambieni baba yenu.” 39 Wao wakamjibu,“Baba yetu ni Abrahamu!” Yesu akawaambia, “Kamaninyi mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngefanyakama alivyofanya Abrahamu, 40 Mimi nimewaambieniukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyimwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo! 41 Ninyimnafanya mambo yaleyale aliyofanya babu yenu.” Waowakamwambia, “Sisi si watoto haramu! Tunaye babammoja tu, yaani Mungu.” 42 Yesu akawaambia, “KamaMungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maanamimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikujakwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.43 Kwa nini hamwelewi hayo ninayosema? Ni kwa kuwahamwezi kuusikiliza ujumbe wangu. 44 Ninyi ni watotowa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa zababa yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hanamsimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndaniyake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na haliyake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wauongo. 45 Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana ninyihamniamini. 46 Nani kati yenu awezaye kuthibitishakuwa mimi nina dhambi? Ikiwa basi nasema ukweli,kwa nini hamniamini? 47 Aliye wa Mungu husikilizamaneno ya Mungu. Lakini ninyi hamsikilizi kwa sababuninyi si (watu wa) Mungu.” 48Wayahudi wakamwambia,“Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, natena una pepo?” 49 Yesu akajibu, “Mimi sina pepo; miminamheshimu Baba yangu, lakini ninyi hamniheshimu.50Mimi sijitafutii utukufuwangumwenyewe; yukommojamwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu. 51Kwelinawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufamilele.” 52Basi, Wayahudi wakasema, “Sasa tunajua kwelikwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na

Page 26: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 8:53 26 YOHANA MTAKATIFU 9:7manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatiaujumbe wangu hatakufa milele! 53 Je, unajifanya mkuuzaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata namanabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?” 54 Yesuakawajibu, “Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangusi kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Babayenu, ndiye anayenitukuza. 55 Ninyi hamjapata kumjua,lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwamwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika nenolake. 56 Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione sikuyangu; naye aliiona, akafurahi.” 57 Basi, Wayahudiwakamwambia, “Wewe hujatimiza miaka hamsini bado,nawe umemwona Abrahamu?” 58 Yesu akawaambia,“Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, miminiko.” 59Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesuakajificha, akatoka Hekaluni.

91Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu mmoja, kipofu

tangu kuzaliwa. 2 Basi, wanafunzi wakamwuliza, “Mwal-imu! Ni nani aliyetenda dhambi: mtu huyu, ama wazaziwake, hata akazaliwa kipofu?” 3 Yesu akajibu, “Jambohili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, waladhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvuya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake. 4 Kukiwabado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yulealiyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezikufanya kazi. 5 Wakati ningali ulimwenguni, mimi nimwanga wa ulimwengu.” 6 Baada ya kusema hayo,akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yulekipofu machoni, 7 akamwambia, “Nenda ukanawe katikabwawa la Siloamu.” (maana ya jina hili ni “aliyetumwa”).Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi

Page 27: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 9:8 27 YOHANA MTAKATIFU 9:21akiwa anaona. 8 Basi, jirani zake na wale waliokuwawanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwom-baji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwaakiketi na kuomba?” 9 Baadhi yao wakasema, “Ndiye.”Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakinihuyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!” 10 Basi,wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbu-liwa?” 11Naye akawajibu, “Yulemtu aitwayeYesu alifanyatope, akanipaka machoni na kuniambia: Nenda ukanawekatika bwawa la Siloamu. Basi, mimi nikaenda, nikanawa,nikapata kuona.” 12 Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?”Naye akawajibu, “Mimi sijui!” 13Kishawakampeleka huyomtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo. 14 Siku hiyo Yesualipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwasiku ya Sabato. 15 Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtuhuyo, “Umepataje kuona?” Naye akawaambia, “Alin-ipaka tope machoni, nami nikanawa na sasa naona.”16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hakutokakwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakiniwengine wakasema, “Mtu mwenye dhambi awezaje ku-fanya ishara za namna hii?” Kukawa na mafarakanokati yao. 17 Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwakipofu, “Maadam yeye amekufungua macho, wasemajejuu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!” 18Viongoziwa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwakipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaitawazazi wake. 19 Basi, wakawauliza hao wazazi, “Je,huyu ndiye mtoto wenu ambaye ninyi mwasema aliza-liwa kipofu? Sasa amepataje kuona?” 20 Wazazi wakewakajibu, “Tunajua kwamba huyu ni mtoto wetu, nakwamba alizaliwa kipofu. 21 Lakini amepataje kuona,hatujui; na wala hatumjui yule aliyemfumbua macho.Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima, anaweza

Page 28: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 9:22 28 YOHANA MTAKATIFU 9:38kujitetea mwenyewe.” 22 Wazazi wake walisema hivyokwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwaniviongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtuyeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwanje ya sunagogi. 23 Ndiyo maana wazazi wake walisema:“Yeyenimtumzima,mwulizeni.” 24Basi, wakamwita tenaaliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbeleya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenyedhambi.” 25 Yeye akajibu, “Kama ni mwenye dhambimimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu,na sasa naona.” 26 Basi, wakamwuliza, “Alikufanyia nini?Alikufumbuaje macho yako?” 27 Huyo mtu akawajibu,“Nimekwisha waambieni, nanyi hamkusikiliza; kwa ninimwataka kusikia tena? Je, ninyi pia mnataka kuwawafuasi wake?” 28 Lakini wao wakamtukana wakisema,“Wewe ni mfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose. 29 Sisitunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini mtuhuyu hatujui ametoka wapi!” 30 Naye akawajibu, “Hili nijambo la kushangaza! Ninyi hamjui ametoka wapi, lakiniamenifumbua macho yangu! 31 Tunajua kwamba Munguhawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyotemwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake. 32 Tangumwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameya-fumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu. 33 Kama mtuhuyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya cho-chote!” 34Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewakatika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi,wakamfukuzia mbali. 35 Yesu alisikia kwamba walikuwawamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, “Je,wewe unamwamini Mwana wa Mtu?” 36 Huyo mtuakajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipatekumwamini.” 37Yesu akamwambia, “Umekwishamwona,naye ndiye anayesema nawe sasa.” 38 Basi, huyo mtu

Page 29: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 9:39 29 YOHANA MTAKATIFU 10:12akasema, “Ninaamini Bwana!” Akamsujudia. 39 Yesuakasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu,kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawevipofu.” 40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nayewalisikia maneno hayo, wakamwuliza, “Je, sisi pia nivipofu?” 41 Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu,hamngekuwa na hatia; lakini sasa ninyi mwasema: Sisitunaona, na hiyo yaonyesha kwamba mna hatia bado.

101 Yesu alisema “Kweli nawaambieni, yeyote yule

asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni,bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo nimwizi na mnyang'anyi. 2 Lakini anayeingia kwa kupitiamlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo. 3 Mngojamlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sautiyake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jinalake na kuwaongoza nje. 4 Akisha watoa nje huwatan-gulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sautiyake. 5 Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, baliwatamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.” 6Yesu ali-waambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotakakuwaambia. 7 Basi, akasema tena, “Kweli nawaambi-eni, mimi ni mlango wa kondoo. 8 Wale wengine wotewaliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, naokondoo hawakuwasikiliza. 9Mimi ni mlango. Anayeingiakwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, nakupatamalisho. 10Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuuana kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili. 11 “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungajimwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.12Mtuwa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoosi mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha

Page 30: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 10:1330YOHANAMTAKATIFU 10:30kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamatana kuwatawanya. 13 Yeye hajali kitu juu ya kondookwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. 14 Mimi nimchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao waliowanguwananijuamimi, 15kamavile Baba anijuavyo, naminimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajiliyao. 16Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizinihumu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sautiyangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.17 “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipatekuupokea tena. 18 Hakuna mtu anayeninyang'anya uhaiwangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe.Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena.Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.” 19Kukawa tenana mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya manenohaya. 20Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwen-dawazimu! Ya nini kumsikiliza?” 21Wengine wakasema,“Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anawezakuyafumbua macho ya vipofu?” 22 Huko Yerusalemukulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwawa baridi. 23Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katikaukumbi wa Solomoni. 24 Basi, Wayahudi wakamzun-guka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpakalini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi.”25 Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki.Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinan-ishuhudia. 26 Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi sikondoo wangu. 27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu;mimi nawajua, nao hunifuata. 28 Mimi nawapa uzimawa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtuatakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. 29 Baba yanguambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, walehakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba. 30Mimi

Page 31: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 10:31 31 YOHANA MTAKATIFU 11:4na Baba, tummoja.” 31Basi, Wayahudi wakachukuamaweili wamtupie. 32 Yesu akawaambia, “Nimewaonyeshenikazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo in-ayowafanya mnipige mawe?” 33 Wayahudi wakamjibu,“Hatukupigi mawe kwa ajili ya tendo jema, ila kwa sababuya kukufuru! Maana wajifanya kuwa Mungu hali weweni binadamu tu.” 34 Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwakatika Sheria yenu: Mimi nimesema, ninyi ni miungu?35 Mungu aliwaita miungu wale waliopewa neno lake;nasi twajua kwambaMaandiko Matakatifu yasema ukwelidaima. 36 Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu nakumtuma ulimwenguni, mnamwambia: Unakufuru, etikwa sababunilisema: Mimi niMwanawaMungu? 37Kamasifanyi kazi za Baba yangu msiniamini. 38 Lakini ikiwaninazifanya, hata kamahamniamini, walau ziaminini hizokazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndaniyangu, nami niko ndani yake.” 39Wakajaribu tena kumka-mata lakini akachopokamikononi mwao. 40Yesu akaendatena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwaakibatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi walimwendeawakasema, “Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yaleyote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa.”42Watu wengi mahali hapo wakamwamini.

111 Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania,

alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa ma-hali walipokaa Maria na Martha, dada yake. 2 Mariandiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusakwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwamgonjwa.) 3 Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwaYesu: “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!” 4 Yesu aliposikiahivyo akasema, “Ugonjwa huo hautaleta kifo, ila ni kwa

Page 32: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 11:5 32 YOHANA MTAKATIFU 11:24ajili ya kumtukuza Mungu; ameugua ili kwa njia hiyoMwana waMungu atukuzwe.” 5Yesu aliwapenda Martha,dada yake na Lazaro. 6Alipopata habari kwamba Lazaro nimgonjwa, Yesu aliendelea kukaa mahali hapo alipokuwakwa sikumbili zaidi. 7Kisha akawaambiawanafunzi wake,“Twendeni tena Yudea!” 8 Wanafunzi wakamwambia,“Mwalimu! Muda mfupi tu umepita tangu Wayahudiwalipotaka kukuua kwa mawe, nawe unataka kwendahuko tena?” 9 Yesu akajibu, “Je, saa za mchana sikumi na mbili? Basi, mtu akitembea mchana hawezikujikwaa kwa kuwa anauona mwanga wa ulimwenguhuu. 10 Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maanamwanga haumo ndani yake.” 11Yesu alipomaliza kusemamaneno hayo, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala,lakinimimi nitakwenda kumwamsha.” 12Wanafunziwakewakamwambia, “Bwana, ikiwa amelala, basi atapona.”13Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulalausingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.14 Basi, Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa;15 Lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko,ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake.” 16Thoma (ait-waye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, “Twendeninasi tukafe pamoja naye!” 17 Yesu alipofika huko alikutaLazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne. 18Kijiji chaBethania kilikuwa karibu na Yerusalemu umbali upataokilomita tatu. 19Wayahudi wengi walikuwawamefika kwaMartha naMaria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao. 20Basi,Martha aliposikia kwambaYesu alikuwa anakuja, akaendakumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani. 21 Marthaakamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kakayangu hangalikufa! 22 Lakini najua kwamba hata sasachochote utakachomwomba Mungu, atakupa.” 23 Yesuakamwambia, “Kaka yako atafufuka.” 24Martha akamjibu,“Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya

Page 33: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 11:2533YOHANAMTAKATIFU 11:42mwisho.” 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo nauzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi:26 na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je,waamini hayo?” 27Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana!Naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu,yule ajaye ulimwenguni.” 28 Baada ya kusema hayo,Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwabiafaraghani, “Mwalimu yuko hapa, anakuita.” 29 Nayealiposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.30Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahalipalepale Martha alipomlaki. 31Basi, Wayahudi waliokuwanyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwonaameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walid-hani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza. 32 Basi,Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona,alipiga magoti, akamwabia, “Bwana, kama ungalikuwahapa, kaka yangu hangalikufa!” 33 Yesu alipomwonaanalia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanaliapia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni. 34 Kishaakawauliza, “Mlimweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana,njoo uone.” 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi, Wayahudiwakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda!” 37 Lakinibaadhi yao wakasema, “Je, huyu aliyemfumbua machoyule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?” 38 Basi,Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini.Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwakwa jiwe. 39 Yesu akasema, “Ondoeni hilo jiwe!” Martha,dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, “Bwana, amek-wishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!” 40 Yesuakamwambia, “Je, sikukwambia kwamba ukiamini utaonautukufu wa Mungu?” 41 Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesuakatazama juu mbinguni, akasema, “Nakushukuru Babakwa kuwa wewe wanisikiliza. 42Najua kwamba unanisik-

Page 34: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 11:4334YOHANAMTAKATIFU 11:56iliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watuhawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewendiwe uliyenituma.” 43 Alipokwisha sema hayo, akaitakwa sauti kubwa: “Lazaro! Toka nje!” 44Huyo aliyekuwaamekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu namikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia,“Mfungueni, mkamwache aende zake.” 45Basi, Wayahudiwengi waliokuwawamefika kwaMaria walipoona kitendohicho alichokifanya Yesu wakamwamini. 46 Lakini baadhiyaowalikwenda kwaMafarisayowakatoa taarifa ya jambohilo alilofanya Yesu. 47 kwa hiyo makuhani wakuu naMafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema,“Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.48Tukimwacha tu watu wote watamwamini, nao Waromawatakuja kuliharibu Hekalu letu na taifa letu!” 49 Hapo,mmoja wao aitwaye Kayafa, ambaye alikuwa KuhaniMkuu mwaka huo, akawaambia, “Ninyi hamjui kitu!50 Je, hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtu mmojaafe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zima liangamizwe?”51 Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, balikwa vile alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, alibashirikwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao; 52 na wala sikwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watotowa Mungu waliotawanyika. 53 Basi, tangu siku hiyoviongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwuaYesu. 54 Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani katiya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibuna jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa hukopamoja na wanafunzi wake. 55 Sikukuu ya Wayahudiya Pasaka ilikuwa karibu, na watu wengi walikwendaYerusalemu ili wajitakase kabla ya sikukuu hiyo. 56 Basi,wakawa wanamtafuta Yesu; nao walipokusanyika pamojaHekaluni wakaulizana, “Mwaonaje? Yaonekana kwamba

Page 35: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 11:5735YOHANAMTAKATIFU 12:13haji kabisa kwenye sikukuu, au sivyo?” 57 Makuhaniwakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwambamtu akijua mahali aliko Yesu awaarifu kusudi wamtienguvuni.

121 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika

Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amem-fufua kutoka wafu. 2 Huko walimwandalia chakula chajioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwammoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu.3 Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safiya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipan-gusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu yamarashi. 4 Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumina wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,5 “Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha di-nari mia tatu, wakapewa maskini?” 6 Alisema hivyo,si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwasababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwamwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo haz-ina. 7 Lakini Yesu akasema, “Msimsumbue huyu mama!Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.8Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa namisiku zote.” 9 Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesualikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajiliya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro am-baye Yesu alimfufua kutoka wafu. 10 Makuhani wakuuwaliamua pia kumwua Lazaro, 11 Maana kwa sababuya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao,wakamwamini Yesu. 12 Kesho yake, kundi kubwa la watuwaliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwanjiani kuja Yerusalemu. 13 Basi, wakachukua matawiya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti

Page 36: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 12:1436YOHANAMTAKATIFU 12:27wakisema: “Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina laBwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.” 14 Yesu akampatamwanapundammoja akapanda juuyake kamayasemavyoMaandiko: 15 “Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalmewako anakuja, Amepanda mwana punda.” 16Wakati huowanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesualipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwambahayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watuwalikuwa wamemtendea hivyo. 17 Kundi la watu walewaliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutokakaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.18 Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wotewalisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo.19 Basi, Mafarisayo wakaambiana, “Mnaona? Hatuwezikufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unam-fuata.” 20 Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwawatu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakatiwa sikukuu hiyo. 21 Hao walimwendea Filipo, mwenyejiwa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, “Mheshimiwa,tunataka kumwona Yesu.” 22Filipo akaenda akamwambiaAndrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu. 23 Yesuakawaambia, “Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtuimefika! 24 Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubakipunje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa.Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi. 25 Anayependamaisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yakekatika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uzima wamilele. 26 Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate,hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtu-mishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikiaBaba yangu atampa heshima. 27 “Sasa roho yangu imefad-haika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hiiinifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja—ili nipite katika

Page 37: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 12:2837YOHANAMTAKATIFU 12:44saa hii. 28 Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasemakutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”29Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikiasauti hiyo, na baadhi yao walisema, “Malaika ameongeanaye!” 30Lakini Yesu akawaambia, “Sauti hiyo haikutokeakwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu. 31 Sasa ndiowakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasamtawala waulimwengu huu atapinduliwa. 32 Nami nitakapoinuliwajuu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu.” 33 (Kwakusema hivyo alionyesha atakufa kifo gani). 34 Basi,umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetukwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusemaati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwanawa Mtu ni nani?” 35 Yesu akawaambia, “Mwanga badouko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huomwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajuiaendako. 36 Basi, wakati mnao huo mwanga uamininiili mpate kuwa watu wa mwanga.” Baada ya kusemamaneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbalinao. 37 Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbeleyao, wao hawakumwamini. 38 Hivyo maneno aliyosemanabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbewetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”39Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:40“Mungu ameyapofushamacho yao, amezipumbaza akilizao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao;wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”41 Isaya alisemamaneno haya kwa sababu aliuona utukufuwa Yesu, akasema habari zake. 42 Hata hivyo, wengi waviongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwasababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuo-gopa kwamba watatengwa na sunagogi. 43Walipendeleakusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu 44 Kisha

Page 38: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 12:45 38 YOHANA MTAKATIFU 13:9Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu aliyeniamini, ha-niamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.45 Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.46Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wotewanaoniamini wasibaki gizani. 47 Anayeyasikia manenoyangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu; maana sikujakuhukumu ulimwengu bali kuuokoa. 48Asiyeyashika ma-neno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosemani hakimu wake siku ya mwisho. 49 Mimi sikunena kwamamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiyealiyeniamuru niseme nini na niongee nini. 50Nami najuakuwa amri yake huleta uzima wa milele. Basi, miminasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme.”

131 Ilikuwa kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua

kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwendakwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daimawatu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpakamwisho! 2Basi, Yesu nawanafunzi wakewalikuwamezanikwa chakula cha jioni. Ibilisi alikwishamtia Yuda, mwanawa Simoni Iskarioti, nia ya kumsaliti Yesu. 3 Yesu alijuakwamba Baba alikuwa amemkabidhi kila kitu, na kwambaalikuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwa Mungu.4 Basi, Yesu aliondoka mezani, akaweka kando vazi lake,akachukua kitambaa na kujifunga kiunoni. 5 Kisha akatiamaji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wakemiguu na kuipangusa kwa kile kitambaa alichojifungia.6 Basi, akamfikia Simoni Petro; naye Petro akasema,“Bwana, wewe utaniosha miguu mimi?” 7Yesu akamjibu,“Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.”8 Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!”Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusianonami tena.” 9Simoni Petro akamwambia, “Bwana, nioshe,

Page 39: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 13:1039YOHANAMTAKATIFU 13:26si miguu tu, bali na mikono yangu na kichwa pia.” 10Yesuakamwambia, “Aliyekwisha oga hana lazima ya kunawaisipokuwa miguu, maana amekwisha takata mwili wote.Ninyi mmetakata, lakini si nyote.” 11 (Yesu alimjuayule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema: “Ninyimmetakata, lakini si nyote.”) 12 Alipokwisha waoshamiguu na kuvaa tena vazi lake, aliketi mezani, akawaam-bia, “Je, mmeelewa hayo niliyowatendeeni? 13 Ninyimwaniita Mwalimu na Bwana, nanyi mwasema vyema,kwa kuwa ndimi. 14 Basi, ikiwa mimi niliye Bwana naMwalimu, nimewaosha ninyi miguu, nanyi pia mnapaswakuoshana miguu. 15 Nimewapeni mfano, ili nanyi piamfanye kama nilivyowafanyieni. 16 Kweli nawaambi-eni, mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake, walamtume si mkuu zaidi kuliko yule aliyemtuma. 17 Basi,ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza.18 “Haya nisemayo hayawahusu ninyi nyote. Miminawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimieMaandikoMatakatifu yasemayo: Yule aliyeshiriki chakulachangu amegeuka kunishambulia. 19Mimi nimewaambi-enimambohaya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokeampate kuamini kuwa mimi ndimi. 20 Kweli nawaambienianayempokea yule ninayemtuma anaponipokea mimi;na anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma.”21 Alipokwisha sema hayo, Yesu alifadhaika sana ro-honi, akasema wazi, “Kweli nawaambieni, mmoja wenuatanisaliti!” 22 Wanafunzi wakatazama wasiweze kabisakujua anasema nani. 23 Mmoja wa wanafunzi, ambayeYesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibuna Yesu. 24 Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema:“Mwulize anasema juu ya nani.” 25 Mwanafunzi huyoakasogea karibu zaidi na Yesu, akamwuliza, “Bwana,ni nani?” 26 Yesu akajibu, “Yule nitakayempa kipande

Page 40: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 13:27 40 YOHANA MTAKATIFU 14:1cha mkate nilichochovya katika sahani, ndiye.” Basi,akatwaa kipande cha mkate, akakichovya katika sahani,akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti. 27 Yudaalipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia.Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanyeharaka!” 28 Lakini hakuna hata mmoja wa wale waliokaapale mezani aliyefahamu kwa nini alikuwa amemwambiahivyo. 29 Kwa kuwa Yuda alikuwa na wajibu wa kuu-tunza mfuko wa fedha, baadhi yao walidhani kwambaYesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwasikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe cho-chote kwa maskini. 30 Basi, Yuda alipokwisha twaa kilekipande cha mkate, akatoka nje mara. Na ilikuwa usiku.31 Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema, “Sasa Mwanawa Mtu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndaniyake. 32Na kama utukufu wa Mungu umefunuliwa ndaniya Mwana, basi, naye Mungu ataudhihirisha utukufu waMwana ndani yake mwenyewe, na atafanya hivyo mara.33 “Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu.Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambiaviongozi waWayahudi: Niendako ninyi hamwezi kwenda!34 Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kamanilivyowapenda ninyi. 35Mkipendana, watuwote watajuakwamba ninyi ni wanafunzi wangu.” 36 Simoni Petroakamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu,“Niendako huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baa-daye.” 37 Petro akamwambia “Bwana, kwa nini siwezikukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajili yako!” 38 Yesuakajibu, “Je, uko tayari kweli kufa kwa ajili yangu? Kwelinakwambia, kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu!”

141 Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu.

Page 41: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 14:2 41 YOHANA MTAKATIFU 14:18Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Nyumbanimwa Baba yangu mna makao mengi; la sivyo ninga-likwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieninafasi. 3Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudina kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipomimi. 4 Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda.”5 Thoma akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda,tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?” 6Yesu akamjibu, “Mimini njia, na ukweli na uzima. Hakuna awezaye kwendakwa Baba ila kwa kupitia kwangu. 7 Ikiwa mnanijua mimimnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua,tenammekwishamwona.” 8Filipo akamwambia, “Bwana,tuonyeshe Baba, nasi tutatosheka.” 9 Yesu akamwambia,“Filipo, nimekaa nanyi muda wote huu, nawe hujanijua?Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezajebasi, kusema: Tuonyeshe Baba? 10 Je, huamini kwambamimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu?Maneno ninayowaambieni nyote siyasemi kwa mam-laka yangu; Baba aliye ndani yangu anafanya kazi yake.11 Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi nikondani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo,aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya. 12 Kwelinawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninay-ofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi, maananakwenda kwa Baba. 13Na chochote mtakachoomba kwajina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.14 Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.15 “Mkinipenda mtazishika amri zangu. 16 Nami ni-tamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine,atakayekaa nanyi milele. 17 Yeye ni Roho wa kweli.Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezikumwona wala kumjua. Lakini ninyi mnamjua kwasababu anabaki nanyi na yu ndani yenu. 18 “Sitawaacha

Page 42: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 14:19 42 YOHANA MTAKATIFU 15:1ninyi yatima; nitakuja tena kwenu. 19 Bado kidogo naoulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mtaniona; nakwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai. 20 Sikuile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba,nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu. 21 Azipokeayeamri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Nayeanipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami ni-tampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 Yuda (si yuleIskarioti) akamwambia, “Bwana, itawezekanaje wewekujidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” 23 Yesuakamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, naBaba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaanaye. 24 Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Naneno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.25 “Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamojananyi 26 lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Babaatamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu nakuwakumbusheni yote niliyowaambieni. 27 “Nawaachieniamani; nawapeni amani yangu. Siwapi ninyi kama vileulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifad-haike. 28 Mlikwisha sikia nikiwaambieni: Ninakwendazangu, kisha nitarudi tena kwenu. Kama mngalinipendamngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maanayeye ni mkuu kuliko mimi. 29 Nimewaambieni hayasasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini.30 Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana mtawalawa ulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu;31 lakini ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampendaBaba, na ndiyo maana nafanya kila kitu kama Baba alivy-oniamuru. Simameni, tutoke hapa!”

151 “Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye

Page 43: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 15:2 43 YOHANA MTAKATIFU 15:17mkulima. 2Yeye huliondoa ndani yangu kila tawi lisilozaamatunda, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaazaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya uleujumbe niliowaambieni. 4Kaeni ndani yangu, nami nikaendani yenu. Tawi haliwezi peke yake kuzaa matundalisipokaa katika mzabibu hali kadhalika nanyi hamwezikuzaa matunda msipokaa ndani yangu. 5 “Mimi nimzabibu, nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu,nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi, maanabila mimi hamwezi kufanya chochote. 6 Mtu yeyoteasipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalonje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyona kulitupa motoni liungue. 7 Mkikaa ndani yangu namaneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni cho-chotemtakacho nanyimtapewa. 8Baba yangu hutukuzwakama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.9Mimi nimewapenda ninyi kama vile Baba alivyonipendamimi. Kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amrizangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivy-ozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendolake. 11 Nimewaambieni mambo haya ili furaha yanguikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike. 12 Hii ndiyoamri yangu: pendaneni; pendaneni kamanilivyowapendaninyi. 13 Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wamtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14Ninyi nirafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. 15 Ninyi siwaititena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanyabwana wake. Lakini mimi nimewaita ninyi rafiki, kwasababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutokakwa Baba yangu. 16 Ninyi hamkunichagua mimi; miminiliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda,matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi cho-chote mumwombacho kwa jina langu. 17Basi, amri yangu

Page 44: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 15:18 44 YOHANA MTAKATIFU 16:4kwenu ndiyo hii: pendaneni. 18 “Kama ulimwengu uki-wachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimikabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngalikuwa watuwa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi kamawatu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu,ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwasababu hiyo ulimwengu unawachukieni. 20 Kumbukeniniliyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwanawake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyipia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenupia. 21 Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwasababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma.22 Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa nahatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawanadhambi. 23 Anayenichukia mimi, anamchukia na Babayangu pia. 24 Kama nisingalifanya kwao mambo am-bayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasin-galikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanyawakinichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.25 Na hivi ni lazima yatimie yale yaliyoandikwa katikaSheria yao: Wamenichukia bure! 26 “Atakapokuja huyoMsaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyoRoho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudiamimi. 27 Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwanami tangu mwanzo.

161 “Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu.

2 Watu watawatenga ninyi na masunagogi yao. Tena,wakati unakuja ambapo kila atakayewaua ninyi atadhanianamhudumia Mungu. 3 Watawatendeeni mambo hayokwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi. 4 Basi,nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika

Page 45: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 16:5 45 YOHANA MTAKATIFU 16:19mkumbuke kwamba niliwaambieni. “Sikuwaambienimambo haya tangumwanzo kwa sababu nilikuwa pamojananyi. 5 Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; nahakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: Unakwendawapi? 6 Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaahuzuni mioyoni mwenu. 7 Lakini, nawaambieni ukweli:afadhali kwenumimi niende zangu, maana nisipokwendaMsaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, ni-tamtuma kwenu. 8 Naye atakapokuja atawathibitishiawalimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadil-ifu na hukumu ya Mungu. 9 Wamekosea kuhusudhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu uadilifu,kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtanionatena; 11kuhusu hukumu kwa sababumkuuwa ulimwenguhuu amekwisha hukumiwa. 12 “Ninayo bado mengiya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili.13 Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongozakwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlakayake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, naatasema mambo yatakayokuwa yanakuja. 14 Yeye atan-itukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopatakutoka kwangu. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu;ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifuatawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu. 16 “Badokitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambokidogo tena mtaniona!” 17 Hapo baadhi ya wanafunziwakewakaulizana, “Anamaana gani anapotwambia: Badokitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambokidogo tena mtaniona? Tena anasema: Kwa kuwa ni-nakwenda kwa Baba!” 18 Basi, wakawa wanaulizana, “Anamaana gani anaposema: Bado kitambo kidogo? Hat-uelewi anaongelea nini.” 19 Yesu alijua kwamba walitakakumwuliza, basi akawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yale

Page 46: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 16:2046YOHANAMTAKATIFU 16:33niliyosema: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; nabaada ya kitambo kidogo tenamtaniona? 20Nawaambienikweli, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwenguutafurahi: mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageukakuwa furaha. 21 Wakati mama anapojifungua huonahuzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akishajifungua hayakumbuki tenamaumivu hayo kwa sababu yafuraha kwamba mtu amezaliwa duniani. 22Ninyi pia mnahuzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furahamioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeion-doa kwenu. 23 Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kwelinawaambieni, chochotemtakachomwomba Baba kwa jinalangu, atawapeni. 24 Mpaka sasa hamjaomba chochotekwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenuikamilike. 25 “Nimewaambieni mambo hayo kwa ma-fumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tenananyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu yaBaba. 26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambiikwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 maanayeye mwenyewe anawapenda ninyi, kwa sababu ninyimmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwaMungu. 28Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni;na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba.” 29Basi,wanafunzi wake wakamwambia, “Ahaa! Sasa unasemawaziwazi kabisa bila kutumia mafumbo. 30 Sasa tuna-jua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja yakuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaaminikwamba umetoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Je,mnaamini sasa? 32Wakati unakuja, tena umekwisha fika,ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, naminitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko pekeyangu, maana Baba yu pamoja nami. 33 Nimewaambienimambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana

Page 47: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 17:1 47 YOHANA MTAKATIFU 17:14nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipenimoyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!”

171Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juumbinguni,

akasema, “Baba, saa imefika! Mtukuze Mwanao ili nayeMwana apate kukutukuza. 2 Maana ulimpa Mwanaomamlaka juu yawatuwote ili awape uzimawamilelewotehao uliompa. 3 Na uzima wa milele ndio huu: kukujuawewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua YesuKristo uliyemtuma. 4Mimi nimekutukuza hapa duniani;nimeikamilisha ile kazi uliyonipa nifanye. 5 Sasa, Baba,nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa naokabla ya kuumbwa ulimwengu. 6 “Nimekufanya ujulikanekwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watuwako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika nenolako. 7 Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetokakwako. 8 Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa naowameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako,na wanaamini kwamba wewe ulinituma. 9 “Nawaombeahao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea hao ulionipa,maana ni wako. 10 Yote niliyo nayo ni yako, na yakoni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao.11 Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakiniwao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvuya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawekitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja. 12 Nilipokuwanao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lakoulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmojawao aliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimika kupoteaili Maandiko Matakatifu yapate kutimia. 13 Basi, sasanaja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni,ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu. 14 Mimi

Page 48: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 17:15 48 YOHANA MTAKATIFU 18:2nimewapa neno lako, nao ulimwengu ukawachukia, kwasababu wao si wa ulimwengu kama vile nami nisivyo waulimwengu. 15 Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naombauwakinge na yule Mwovu. 16Wao si wa ulimwengu, kamavile nami nisivyo wa ulimwengu. 17 Waweke wakfu kwaukweli; neno lako ni ukweli. 18 Kama vile ulivyonitumaulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;19 na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ilinao pia wafanywe wakfu katika ukweli. 20 “Siwaombeihao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokanana ujumbe wao. 21 Naomba ili wote wawe kitu kimoja.Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyondani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimojakusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulini-tuma. 22 Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi,ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja; 23 miminiwendani yao, naweuwendani yangu; naombawakamil-ishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujuakwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda waokama unavyonipenda mimi. 24 “Baba! Nataka wao ulion-ipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufuwangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwaulimwengu. 25 Baba Mwema! Ulimwengu haukujui,lakini mimi nakujua. Hawa nao wanajua kwamba weweulinituma. 26Nimekufanya ujulikane kwaona nitaendeleakufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao,nami niwe ndani yao.”

181 Yesu alipokwisha sema hayo, alikwenda ng'ambo

ya kijito Kedroni, pamoja na wanafunzi wake. Mahalihapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingia humopamoja na wanafunzi wake. 2 Yuda, aliyemsaliti Yesu,

Page 49: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 18:3 49 YOHANA MTAKATIFU 18:17alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutanana wanafunzi wake huko. 3 Basi, Yuda alichukua kikosicha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu naMafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge nasilaha. 4 Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea,akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5Nao wakamjibu, “Yesuwa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” MsalitiYuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao. 6 Basi, Yesualipowaambia: “Mimi ndiye”, wakarudi nyuma, wakaan-guka chini. 7 Yesu akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?”Wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” 8 Yesu akawaambia,“Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi,kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.”9 (Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Waleulionipa sikumpoteza hata mmoja.”) 10 Simoni Petroalikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikiola kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyoaliitwa Malko. 11 Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudishaupanga wako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipaBaba?” 12 Kile kikosi cha askari, mkuu wake na wal-inzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga 13 nakumpeleka kwanza kwa Anasi; Anasi alikuwa baba mkwewa Kayafa ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo.14 Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudikwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa.15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine wal-imfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwaanajulikana kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamojana Yesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu. 16 LakiniPetro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi,huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwaKuhani Mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani. 17 Huyo msichana

Page 50: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 18:1850YOHANAMTAKATIFU 18:32mngojamlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia nimmojawa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Simimi!” 18 Watumishi na walinzi walikuwa wamewashamoto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawa wanaotamoto. Naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao akiotamoto. 19 Basi, Kuhani akamwuliza Yesu juu ya wanafunziwake na mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu, “Nimesemana kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundishakatika masunagogi na Hekaluni, mahali wakutanikiapoWayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.21Kwa nini waniuliza mimi? Waulize wale waliosikia nininiliwaambia. Wao wanajua nilivyosema.” 22 Alipokwishasema hayo mlinzi mmoja aliyekuwa amesimama hapoakampiga kofi akisema, “Je, ndivyo unavyomjibu KuhaniMkuu?” 23 Yesu akamjibu, “Kama nimesema vibaya,onyesha huo ubaya; lakini ikiwa nimesema vema, mbonawanipiga?” 24 Basi, Anasi akampeleka Yesu akiwa ame-fungwa, kwa Kuhani Mkuu Kayafa. 25 Petro alikuwahapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia simmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema,“Si mimi!” 26 Mmoja wa watumishi wa Kuhani Mkuu,jamaa wa yule aliyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, “Je,mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?” 27 Petroakakana tena; mara jogoo akawika. 28 Basi, walimchukuaYesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwaalfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndaniya ikulu wasije wakatiwa najisi. 29 Kwa hiyo, Pilatoaliwaendea nje, akasema, “Mna mashtaka gani juu yamtu huyu?” 30 Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwamwovu hatungalimleta kwako.” 31 Pilato akawaambia,“Haya, mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu ku-fuatana na Sheria yenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisihatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote.” 32 (Ilifanyika

Page 51: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 18:33 51 YOHANA MTAKATIFU 19:5hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonyeshaatakufa kifo gani.) 33 Pilato akaingia tena ndani yaikulu, akamwita Yesu na kumwuliza: “Ati wewe ndiyeMfalme wa Wayahudi?” 34 Yesu akamjibu, “Je, hayo nimaneno yako au wengine wamekwambia habari zangu?”35 Pilato akamjibu, “Je, ni Myahudi mimi? Taifa lakona makuhani wamekuleta kwangu. Umefanya nini?”36 Yesu akamjibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu.Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wa-tumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwaWayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa.” 37HapoPilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesuakajibu, “Wewe umesema kwambamimi ni Mfalme. Miminimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekujaulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtuwa ukweli hunisikiliza.” 38 Pilato akamwambia, “Ukwelini kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendeatenaWayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyotekwake. 39 Lakini, mnayo desturi kwamba mimi niwafun-gulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Basi, mwatakaniwafungulieniMfalmewaWayahudi?” 40Hapowakapigakelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwamnyang'anyi.

191 Basi, Pilato akaamuru Yesu achukuliwe, apigwe vi-

boko. 2 Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakam-tia kichwani, wakamvika na joho la rangi ya zambarau.3 Wakawa wanakuja mbele yake na kusema: “Shikamoo,Mfalme wa Wayahudi!” Wakampiga makofi. 4 Pilatoakatoka tena nje, akawaambia, “Tazameni, namleta njekwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyotekwake.” 5 Basi, Yesu akatoka nje amevaa taji ya miiba na

Page 52: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 19:6 52 YOHANA MTAKATIFU 19:18joho la rangi ya zambarau. Pilato akawaambia, “Taza-meni! Mtu mwenyewe ni huyo.” 6 Makuhani wakuuna walinzi walipomwona wakapaaza sauti: “Msulubishe!Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, ninyiwenyewemkamsulubishe, kwamaanamimi sikuona hatiayoyote kwake.” 7 Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayoSheria, na kufuatana na Sheria hiyo, ni lazima afe, kwasababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.” 8 Pilatoaliposikia maneno hayo akazidi kuogopa. 9 Basi, akain-gia tena ndani ya ikulu, akamwuliza Yesu, “Umetokawapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno. 10 HivyoPilato akamwambia, “Husemi nami? Je, hujui kwambaninayo mamlaka ya kukufungua na mamlaka ya kukusu-lubisha?” 11 Yesu akamjibu, “Hungekuwa na mamlakayoyote juu yangu kama hungepewa na Mungu. Kwasababu hiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambikubwa zaidi.” 12 Tangu hapo, Pilato akawa anatafutanjia ya kumwachilia, lakini Wayahudi wakapiga kelele:“Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki yake Kaisari;kila mtu anayejifanya kuwa Mfalme humpinga Kaisari!”13 Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesunje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo:“Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha). 14 Ilikuwayapata saa sita mchana, siku ya maandalio ya Pasaka.Pilato akawaambiaWayahudi, “Tazameni, Mfalmewenu!”15 Wao wakapaaza sauti: “Mwondoe! Mwondoe! Msulu-bishe!” Makuhani wakuu wakajibu, “Sisi hatuna Mfalmeisipokuwa Kaisari!” 16 Basi, hapo Pilato akamtia Yesumikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukuaYesu. 17 Naye akatoka akiwa amejichukulia msalabawake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa”, (kwaKiebrania Golgotha). 18 Hapo ndipo walipomsulubisha,na pamoja naye waliwasulubisha watu wengine wawili;

Page 53: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 19:1953YOHANAMTAKATIFU 19:30mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wakewa kushoto, naye Yesu katikati. 19 Pilato aliandika ilaniakaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi:“Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi.” 20 Wayahudiwengi waliisoma ilani hiyo, maana mahali hapo ali-posulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji. Tena ilanihiyo ilikuwa imeandikwa kwa Kiebrania, Kilatini, na Ki-giriki. 21 Basi, makuhani wakuu wakamwambia Pilato,“Usiandike: Mfalme waWayahudi, ila Yeye alisema, MiminiMfalmewaWayahudi.” 22Pilato akajibu, “Niliyoandika,nimeandika!” 23 Askari walipokwisha msulubisha Yesu,walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne,fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzuyake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimojatu, bila mshono. 24 Basi, hao askari wakashauriana:“Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwayanani.” Jambohilolilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo:“Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigiakura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari. 25 Karibuna msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamayake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, naMaria Magdalene. 26 Yesu alipomwona mama yake, nakaribu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda,akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiyemwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi:“Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ilehuyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.28 Yesu alijua kwamba yote yalikuwa yametimia; na, iliMaandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naonakiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli limejaa siki. Basi,wakachovya sifongo katika hiyo siki, wakaitia juu ya ufitowa husopo, wakamwekea mdomoni. 30 Yesu alipokwishapokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainama

Page 54: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 19:3154YOHANAMTAKATIFU 19:42kichwa, akatoa roho. 31 Ilikuwa Ijumaa, siku ya Maan-dalio. Kwa hiyo, kusudi miili isikae msalabani siku yaSabato, maana siku hiyo ya Sabato ilikuwa siku kubwa,Wayahudi walimwomba Pilato miguu ya hao waliosulu-biwa ivunjwe na miili yao iondolewe. 32 Basi, askariwalikwenda, wakaivunja miguu ya yule mtu wa kwanzana yule wa pili ambao walikuwa wamesulubiwa pamojana Yesu. 33 Lakini walipomfikia Yesu waliona kwambaalikwisha kufa, na hivyo hawakumvunja miguu. 34 Lakiniaskari mmoja alimtoboa ubavuni kwa mkuki, na maraikatoka damu na maji. 35 (Naye aliyeona tukio hiloametoa habari zake ili nanyi mpate kuamini. Na hayoaliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasemaukweli.) 36 Jambo hilo lilitendwa ili Maandiko Matakatifuyatimie: “Hapana hata mfupa wake mmoja utakaovun-jwa.” 37 Tena Maandiko mengine yanasema: “Watam-tazama yule waliyemtoboa.” 38 Baada ya hayo, Yosefu,mwenyeji wa Armathaya, alimwomba Pilato ruhusa yakuuchukua mwili wa Yesu. (Yosefu alikuwa mfuasi waYesu, lakini kwa siri, maana aliwaogopa viongozi waWayahudi). Basi, Pilato akamruhusu. Hivyo Yosefualikwenda, akauondoa mwili wa Yesu. 39Naye Nikodemoambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku,akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane naubani kiasi cha kilo thelathini. 40Basi, waliutwaamwili waYesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatanana desturi ya Wayahudi katika kuzika. 41 Mahali hapoaliposulubiwaYesu palikuwana bustani, na katika bustanihiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtuyeyote ndani yake. 42 Basi, kwa sababu ya shughuli zaWayahudi zamaandalio ya Sabato, na kwa vile kaburi hilolilikuwa karibu, wakamweka Yesu humo.

Page 55: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 20:1 55 YOHANA MTAKATIFU 20:1520

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza,Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwelimeondolewa mlangoni pa kaburi. 2 Basi, akaendambio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingineambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwon-doa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.”3 Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaendakaburini. 4 Wote wawili walikimbia lakini yule mwana-funzimwingine alikimbiambio zaidi kuliko Petro, akatan-gulia kufika kaburini. 5 Alipoinama na kuchunguliandani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani. 6 SimoniPetro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humoakaona sanda, 7 na kile kitambaa alichofungwa Yesukichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyosanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahalipeke yake. 8 Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyem-tangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona,akaaamini. 9 (Walikuwa bado hawajaelewa MaandikoMatakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufukekutoka wafu). 10 Basi, hao wanafunzi wakarudi nyum-bani. 11 Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, ak-ilia. Huku akiwa bado analia, aliinama na kuchunguliakaburini, 12 akawaona malaika wawili waliovaa mavazimeupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa ume-lazwa, mmoja kichwani na wa pili miguuni. 13 Haomalaika wakamwuliza, “Mama, kwa nini unalia?” Nayeakawaambia, “Wamemwondoa Bwana wangu, na walasijui walikomweka!” 14 Baada ya kusema hayo, aligeukanyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitam-bue ya kuwa ni Yesu. 15 Yesu akamwuliza, “Mama, kwanini unalia? Unamtafuta nani?” Maria, akidhani kwambahuyo ni mtunza bustani, akamwambia, “Mheshimiwa,

Page 56: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 20:1656YOHANAMTAKATIFU 20:27kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, naminitamchukua.” 16 Yesu akamwambia, “Maria!” NayeMaria akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, “Raboni”(yaani “Mwalimu”). 17 Yesu akamwambia, “Usinishike;sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa nduguzangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Babayenu, Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Hivyo MariaMagdalene akaenda akawapahabariwalewanafunzi kuwaamemwona Bwana, na kwamba alikuwa amemwambiahivyo. 19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wana-funzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba,na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopaviongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama katiyao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20 Alipokwisha semahayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi,hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. 21Yesuakawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivy-onituma mimi, nami nawatuma ninyi.” 22 Alipokwishasema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni RohoMtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao, wame-samehewa; msipowaondolea, hawasamehewi.” 24 Thomammoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwapamoja naowakati Yesu alipokuja. 25Basi, walewanafunziwengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thomaakawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za mis-umari, na kutia kidole changu katika kovu hizo, na ku-tia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.” 26 Basi,baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamojamle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milangoilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama katiyao, akasema, “Amani kwenu!” 27 Kisha akamwambiaThoma, “Lete kidole chako hapa uitazame mikono yangu;lete mkono wako ukautie ubavuni mwangu. Usiwe na

Page 57: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 20:28 57 YOHANA MTAKATIFU 21:8mashaka, ila amini!” 28 Thoma akamjibu, “Bwana wanguna Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Je, unaaminikwa kuwa umeniona? Heri yao wale ambao hawajaona,lakini wameamini.” 30 Yesu alifanya mbele ya wana-funzi wake ishara nyingine nyingi ambazo hazikuandikwakatika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpatekuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; nakwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa nguvu ya jinalake.

211 Baada ya hayo Yesu aliwatokea tena wanafunzi wake

kando ya ziwa Tiberia. Aliwatokea hivi: 2 Simoni Petro,Thoma (aitwaye Pacha), na Nathanieli mwenyeji waKana Galilaya, wana wawili wa Zebedayo na wanafunziwake wengine wawili, walikuwa wote pamoja. 3 SimoniPetro aliwaambia, “Nakwenda kuvua samaki.” Naowakamwambia, “Nasi tutafuatananawe.” Basi, wakaenda,wakapanda mashua, lakini usiku huo hawakupata cho-chote. 4Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kandoya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwayeye. 5 Basi, Yesu akawauliza, “Vijana, hamjapata samakiwowote sio?” Wao wakamjibu, “La! Hatujapata kitu.”6 Yesu akawaambia, “Tupeni wavu upande wa kulia wamashua nanyi mtapata samaki.” Basi, wakatupa wavulakini sasa hawakuweza kuuvuta tena kwa wingi wasamaki. 7 Hapo yule mwanafunzi aliyependwa na Yesuakamwambia Petro, “Ni Bwana!” Simoni Petro aliposikiaya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwaamelivaa), akarukia majini. 8 Lakini wale wanafunziwengine walikuja pwani kwa mashua huku wanauvutawavu uliojaa samaki; hawakuwa mbali na nchi kavu,ila walikuwa yapata mita mia moja kutoka ukingoni.

Page 58: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANA MTAKATIFU 21:9 58 YOHANA MTAKATIFU 21:209 Walipofika nchi kavu waliona moto wa makaa ume-washwana juu yake pamewekwa samaki namkate. 10Yesuakawaambia, “Leteni hapa baadhi ya samaki mliovua.”11 Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadinchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwamia moja na hamsini na watatu. Na ingawa walikuwawengi hivyo wavu haukukatika. 12 Yesu akawaambia,“Njoni mkafungue kinywa.” Hakuna hata mmoja waoaliyethubutu kumwuliza: “Weweni nani?” Maanawalijuaalikuwa Bwana. 13 Yesu akaja, akatwaa mkate akawapa;akafanya vivyo hivyo na wale samaki. 14Hii ilikuwa maraya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake baada ya kufu-fuka kutoka wafu. 15Walipokwisha kula, Yesu alimwulizaSimoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipendamimi zaidi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana;wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia,“Tunzawana kondoowangu.” 16Kisha akamwambiamaraya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?”Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba naku-penda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”17Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana wa Yohane!Je, wanipenda?” Hapo Petro akahuzunika kwa sababualimwuliza mara ya tatu: “Wanipenda?” akamwambia,“Bwana, wewe wajua yote; wewe wajua kwamba miminakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu!18 Kweli nakwambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifungamshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwamzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine ataku-funga na kukupeleka usikopenda kwenda.” 19 (Kwakusema hivyo, alionyesha jinsi Petro atakavyokufa nakumtukuza Mungu.) Kisha akamwambia, “Nifuate.”20Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi am-baye Yesu alimpenda, anafuata (Huyu mwanafunzi ndiye

Page 59: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

YOHANAMTAKATIFU 21:2159YOHANAMTAKATIFU 21:25yule ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibusananaYesuna kumwuliza: “Bwanani nani atakayekusal-iti?”) 21 Basi, Petro alipomwona huyo akamwuliza Yesu,“Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “Kama natakaabaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe ni-fuate mimi.” 23 Basi, habari hiyo ikaenea miongonimwa wale ndugu kwamba mwanafunzi huyo hafi. LakiniYesu hakumwambia kwamba mwanafunzi huyo hafi,ila, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusunini?” 24Huyo ndiye yule aliyeshuhudia mambo haya nakuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasema ni kweli.25 Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayokama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhanihata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabuambavyo vingeandikwa.

Page 60: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA YOHANAMTAKATIFU · 2019-12-13 · wambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo hu-vuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujuiunakotokawalaunakokwenda

60Biblia Takatifu

Portions of the New Testament in the Swahili Language of Kenya,Mozambique, Somalia, and Tanzania, translation by Dr. Johann

Ludvig Krapf completed in 1850Public DomainLanguage: Kiswahili (Swahili)Dialect: KimvitaTranslation by: Dr. Johann Ludvig Krapf

2014-08-25PDF generated using Haiola and XeLaTeX on 11 Jan 2020 from source files dated 30 Dec201962071dc0-70e6-5b86-b569-c1b45e7771bd