jinsi ya kuwasiliana na tume - des moines, iowa and... · nyumba kwa sababu ya hadhi inayolindwa ya...

2
Ikiwa unahisi kuwa umebaguliwa, tafadhali wasiliana nasi. Jinsi ya Kuwasiliana na Tume Jumatatu hadi Ijumaa saa 8:00 asubuhi hadi 5:00 jioni. Simu: (515) 283-4284 Faksi: (515) 237-1408 Barua pepe: [email protected] Wavuti: www.HumanRightsDSM.org DSMCivilHumanRights @YourRightsDSM Ubaguzi ni Kinyume cha Sheria! Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ni idara ya serikali inayotekeleza sheria haramu za ubaguzi katika Jiji la Des Moines. Ikiwa unadhani, au mtu unayemfahamu amebaguliwa katika jiji la Des Moines, unapaswa kuwasiliana na Tume. Tume itachunguza malalamishi yako bila malipo ili kuamua ikiwa sheria ilikiukwa. Ikiwa kuna ukiukaji, Tume inaweza kukusaidia kupata masuluhisho ya kisheria ambayo ni haki yako. Ikihitajika, Tume inaweza kufanya vikao vya kesi au kuwasilisha kesi za ubaguzi mahakamani. Ubaguzi unaweza kuwa nyeti. Mara nyingi watu wanaweza kushuku kuwa wamebaguliwa, lakini wasiwe na uhakika wa kuuthibitisha. Wasiliana na Tume ikiwa unashuku kwamba umebaguliwa. Tupo hapa ili kusaidia. Wasiliana nasi leo bila malipo na kwa usaidizi wa siri. 515-283-4284 Jua Haki Zako Ajira Nyumba Makao ya Umma Desturi za Manispaa U b a g u z i n i K i n y u m e c h a S h e ri a ! #JuaHakiZakoDSM Haki za Raia na Binadamu za Des Moines Kukuza Nafasi na Haki Kwa Wote 602 Robert D. Ray Drive Armory Building Des Moines, Iowa 50309 Wageni wanapokelewa kwa miadi au ziara za bila miadi.

Upload: others

Post on 16-Apr-2020

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Jinsi ya Kuwasiliana na Tume - Des Moines, Iowa and... · nyumba kwa sababu ya hadhi inayolindwa ya daraja la mtu. Sheria ya Haki za Binadamu inaharamisha mtu yeyote kukataa kukupangishia,

Ikiwa unahisi kuwa umebaguliwa, tafadhali wasiliana nasi.

Jinsi ya Kuwasiliana na Tume

Jumatatu hadi Ijumaa saa 8:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.

Simu: (515) 283-4284

Faksi: (515) 237-1408

Barua pepe: [email protected]

Wavuti: www.HumanRightsDSM.org

DSMCivilHumanRights

@YourRightsDSM

Ubaguzi ni Kinyume cha Sheria!

Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ni idara ya serikali inayotekeleza sheria haramu za ubaguzi katika Jiji la Des Moines.

Ikiwa unadhani, au mtu unayemfahamu amebaguliwa katika jiji la Des Moines, unapaswa kuwasiliana na Tume.

Tume itachunguza malalamishi yako bila malipo ili kuamua ikiwa sheria ilikiukwa. Ikiwa kuna ukiukaji, Tume inaweza kukusaidia kupata masuluhisho ya kisheria ambayo ni haki yako. Ikihitajika, Tume inaweza kufanya vikao vya kesi au kuwasilisha kesi za ubaguzi mahakamani.

Ubaguzi unaweza kuwa nyeti. Mara nyingi watu wanaweza kushuku kuwa wamebaguliwa, lakini wasiwe na uhakika wa kuuthibitisha. Wasiliana na Tume ikiwa unashuku kwamba umebaguliwa.

Tupo hapa ili kusaidia.

Wasiliana nasi leo bila malipo na kwa usaidizi wa siri.515-283-4284

Jua Haki Zako • Ajira • Nyumba • Makao ya Umma • Desturi za Manispaa

Ubaguzi ni Kinyume cha Sheria!

#JuaHakiZakoDSM

Haki za Raia na Binadamu za Des Moines Kukuza Nafasi na Haki Kwa Wote

602 Robert D. Ray DriveArmory Building

Des Moines, Iowa 50309

Wageni wanapokelewa kwa miadi au ziara za bila miadi.

Page 2: Jinsi ya Kuwasiliana na Tume - Des Moines, Iowa and... · nyumba kwa sababu ya hadhi inayolindwa ya daraja la mtu. Sheria ya Haki za Binadamu inaharamisha mtu yeyote kukataa kukupangishia,

Kuwasilisha malalamishi: Tume itakusaidia kutayarisha na kuwasilisha malalamishi. Lazima malalamishi liwasilishwe ndani ya siku 300 baada ya tukio la ubaguzi wa hivi majuzi.

Usuluhishi: Baada ya kuwasilisha malalamishi rasmi kwenye tume, tume itajaribu kujadiliana mapatano na kupata suluhu yako kwenye mchakato mzima wa uchunguzi.

Upatanisho: Tume itajaribu kusuluhisha malalamishi yako kabla ya uchunguzi, ikiwa pande zote mbili zitakubaliana kuhusu upatanisho.

Uchunguzi: Ikiwa upatanisho hautafaulu, Tume itafanya uchunguzi usioegemea upande wowote.

Kuenda mahakamani Ikiwa suluhisho linalofaa haliwezi kupatikana, Tume inaweza kuenda kwenye kesi ya umma au kukusaidia kupeleka kesi mahakamani.

Unapaswa Kufanya Nini Ukishughudia Ubaguzi?Wasiliana na Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ili uwasilishe malalamishi.

Chukua Hatua Haraka• Ukisubiri kwa muda mrefu sana huenda usiweze

kuwasilisha malalamishi (siku 300 za kuwasilisha malalamishi).

• Kadri unavyosubiri zaidi ndivyo vinavyokuwa vigumu zaidi kutoa ushahidi wa kesi yako. Kwa muda mrefu, mashahidi wanaweza kusahau maelezo muhimu na nyaraka nyeti zinaweza kupotea.

Weka Kumbukumbu ya Hali Yako na Uhifadhi Rekodi

• Hifadhi madokezo yenye maelezo ya kina kuhusu kila hatua hasi dhidi yako. Andika kilichosemwa na kufanywa haswa, tarehe, nyakati na watu waliohusika.

• Orodha kamilifu ya majina, anwani na nambari za simu za mashahidi wanaoweza kuunga mkono kesi yako ukiwasilisha malalamishi ya ubaguzi.

• Unda rekodi za video au sauti za vitendo hasi. Kwa mujibu wa sheria ya Iowa, huhitaji idhini ya mtu ili urekodi mazungumzo ikiwa unashiriki mazungumzo.

• Hifadhi nyaraka zote zinazohusiana na hali yako. Hizi zinaweza kuwa pamoja na barua zilizotumwa, barua pepe na ujumbe wa sauti, makubaliano ya kukodisha na hatua za ajira.

Je, Ubaguzi Ni Nini?

Ajira - Tofauti ya heshima kazini, ikiwa ni pamoja na kuajiri, kupiga kalamu, au kuadhibu kwa sababu ya mbari, umri, dini, imani, rangi, jinsia, mvuto wa jinsia, utambulisho wa jinsia, asili ya taifa, kizazi au ulemavu wa mtu. Unyanyasaji wa kingono pia ni marufuku kwa mujibu wa sheria.

Nyumba - Tofauti ya heshima katika mazingira ya nyumba kwa sababu ya hadhi inayolindwa ya daraja la mtu. Sheria ya Haki za Binadamu inaharamisha mtu yeyote kukataa kukupangishia, kukuuzia, au kukupa mikopo ya nyumba kwa sababu ya mbari, dini, imani, rangi, jinsia, mvuto wa jinsia, utambulisho wa jinsia, asili ya taifa, kizazi, ulemavu au hadhi ya familia yako.

Makao ya Umma - Tofauti ya heshima kazini kwa sababu ya mbari, dini, imani, rangi, jinsia, mvuto wa jinsia, utambulisho wa jinsia, asili ya taifa, kizazi au ulemavu. Makao ya umma ni eneo lolote ambalo lina bidhaa na huduma za umma wote kwa jumla, kama vile duka, mkahawa, hoteli au shule.

Desturi za Manispaa - Pia ni haramu kwa mwajiriwa yeyote wa Jiji la Des Moines au afisa wa kutekeleza sheria kukubagua katika mpango au huduma yoyote ya jiji kwa msingi wa umri, mbari, dini, imani, rangi, jinsia, mvuto wa jinsia, utambulisho wa jinsia, asili ya taifa, kizazi au ulemavu wa mtu.

Je, ungependa Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ikusaidie vipi?

Kulipiza kisasi dhidi ya mtu anayewasilisha malalamishi kwenye Tume ni kinyume cha sheria.