kiswahili maswali na majibu kidato cha tatuna nne...toa maana tano za neno “panda” kisha tunga...

34
Ukurasa wa 1 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507 KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE 1. (a)Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ”Fafanua. MAJIBU Lugha husemwa ni nasibu kwa sababu kuu zifuatazo: Mwanadamu huwa hazaliwi na lugha bali hukutana nayo katika mazingira yake kwa bahati tu na kujifunza. Hakuna kikao kilichowahi kukaa na kuamua juu ya kutumiwa lugha, lugha ilizuka tu. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maneno ya lugha na maumbo ya vitu halisi. Mfano: neno “maji” halina uhusiano na kile kinachoitwa kwa neno hilo bali ni mazoea tu ya watumiaji lugha. (b) Je,wanyama wana lugha? Toasababu MAJIBU Wanyama hawana lugha kwa sababu hawana sifa za kumudu lugha kama mfumo wa mawasiliano. Lugha ni mali ya mwanadamu pekee na hutawaliwa na sifa zifuatazo. a) Sauti: Lugha huambatana na sauti za binaadamu kutoka kinywani mwake. Binaadamu lazima atamke jambo kwa kutoa sauti, zinazotamkwa kwa utaratibu maalumu kutoka kwenye maumbile yaliyo ndani ya mwili wa mwanaadamu hususan kinywa, ambayo kiisimu huitwa ala za sauti. b) Lugha ni lazima imhusu MwanadamuKimsingi hakuna kiumbe kisichokuwa mwanaadamu (mtu) kinachoweza kuzungumza Lugha. Lugha ni chombo maalumu wanachokitumia binaadamu kwa lengo la mawasiliano. c) Lugha huzingatia utaratibu maalum;Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwa kwa kufuata utaratibu fulani unaokubaliwa na jamii ya watu wanaotumia lugha inayohusika. Kwa maneno mengine, si kila sauti itokayo kinywani mwa mwanaadamu kuwa ni lugha. Sauti za vilio vya watoto, hoi hoi na vigelegele vya waliofurahi, vikohozi vya wagonjwa wa pumu na vifua, vicheko na kelele nyenginezo haziwezi kuitwa lugha. Utaratibu huo maalumu unaofuatwa na lugha za wanaadamu huitwa sarufi. d) Lugha hufuata misingi ya fonimu Wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba fonimu ni sauti yenye uwezo wa kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno la lugha husika. Dhana ya fonimu inatarajiwa kuzungumziwa kwa kirefu sana katika muhadhara wa sabaa. Kwa mfano baadhi ya fonimu za Kiswahili ni . /a/, /e/, /i/, /o/, /u/, kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno yafuatayo:-/tata/~ /teta/~/tita/~/tota/~ /tuta/. /p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /k/, /g/, /s/, /z/. kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno yafuatayo:-pawa~ bawa~ tawa~ dawa~ chawa~ jawa~ kawa~ sawa~

Upload: others

Post on 25-Oct-2020

2.877 views

Category:

Documents


173 download

TRANSCRIPT

Page 1: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 1 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE

1. (a)Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ”Fafanua.

MAJIBU

Lugha husemwa ni nasibu kwa sababu kuu zifuatazo:

Mwanadamu huwa hazaliwi na lugha bali hukutana nayo katika mazingira yake kwa

bahati tu na kujifunza.

Hakuna kikao kilichowahi kukaa na kuamua juu ya kutumiwa lugha, lugha ilizuka tu.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maneno ya lugha na maumbo ya vitu

halisi. Mfano: neno “maji” halina uhusiano na kile kinachoitwa kwa neno hilo bali ni

mazoea tu ya watumiaji lugha.

(b) Je,wanyama wana lugha? Toasababu

MAJIBU

Wanyama hawana lugha kwa sababu hawana sifa za kumudu lugha kama mfumo wa

mawasiliano. Lugha ni mali ya mwanadamu pekee na hutawaliwa na sifa zifuatazo.

a) Sauti: Lugha huambatana na sauti za binaadamu kutoka kinywani mwake. Binaadamu lazima

atamke jambo kwa kutoa sauti, zinazotamkwa kwa utaratibu maalumu kutoka kwenye

maumbile yaliyo ndani ya mwili wa mwanaadamu hususan kinywa, ambayo kiisimu

huitwa ala za sauti.

b) Lugha ni lazima imhusu MwanadamuKimsingi hakuna kiumbe kisichokuwa

mwanaadamu (mtu) kinachoweza kuzungumza Lugha. Lugha ni chombo maalumu

wanachokitumia binaadamu kwa lengo la mawasiliano.

c) Lugha huzingatia utaratibu maalum;Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwa kwa

kufuata utaratibu fulani unaokubaliwa

na jamii ya watu wanaotumia lugha inayohusika. Kwa maneno mengine, si kila sauti

itokayo kinywani mwa mwanaadamu kuwa ni lugha. Sauti za vilio vya watoto, hoi

hoi na vigelegele vya waliofurahi, vikohozi vya wagonjwa wa pumu na vifua,

vicheko na kelele nyenginezo haziwezi kuitwa lugha.

Utaratibu huo maalumu unaofuatwa na lugha za wanaadamu huitwa sarufi.

d) Lugha hufuata misingi ya fonimu Wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba

fonimu ni sauti yenye uwezo wa

kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno la lugha husika. Dhana ya

fonimu inatarajiwa kuzungumziwa kwa kirefu sana katika muhadhara wa sabaa. Kwa

mfano baadhi ya fonimu za Kiswahili ni .

/a/, /e/, /i/, /o/, /u/, kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno

yafuatayo:-/tata/~ /teta/~/tita/~/tota/~ /tuta/.

/p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /k/, /g/, /s/, /z/. kama zinavyoweza kubadilisha maana

katika maneno yafuatayo:-pawa~ bawa~ tawa~ dawa~ chawa~ jawa~ kawa~ sawa~

Page 2: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 2 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

zawa, n.k

Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana Muundo wa Lugha huwa

unafuata mpangilio wa vipashio vyake maalumu na

lazima vipashio hivyo vifahamike. Mpangilio wa vipashio huo huanza na

fonimu, neno ambalo huundwa kwa mkusanyiko wa silabi au muunganiko wa

mofimu mbalimbali, kirai, kishazi na sentensi

e) Lugha inajizalishaVipashio vinavyoiunda lugha husika huwa na sifa ya kuweza

kunyumbulishwa ili

kupata maneno mapya. Kwa mfano vitenzi hunyambulishwa kwa kuongezwa

viambishi nz kwa hivyo, lugha hujiongezea maneno mapya. Kwa mfano tuangalie

mifano ifuatayo.

i) chez-a-------ku-chez-a-------ku-m-chez-a-------tu-li-m-chez-a.

ii) chez-e-a-------chez-ek-a----------chez-e-an-a-------chez-esh-a-------chez-w-a

iii) chez-esh-a- chez-esh-an-a- chez-esh-e-an-a

Lugha husharabu

Lugha husharabu kwa maana ya kwamba huchukuwa maneno kutoka lugha

nyengine ili kujiongezea msamiati wake.Tabia hii inazisaidia sana Lugha

zinazokua.

2. Kwa kutumia mifano miwili kwa kila muundo, taja miundo mine ya silabi

MAJIBU

a) Muundo wa kwanza ni ule unaojengwa na irabu peke yake.(I)

Hebu chunguza mifano ifuatayo:

silabi “a” katika neno “angalia” $a$ $nga$ $li$ $a$

silabi “u” katika neno “ugua” $u$ $gu$ $a$

silabi “I” katika neno “niite” $ni$ $i$ $te$

b) Muundo wa silabi wa Konsonanti na Irabu. (KI)

Mifano :

Zungumza =$zu$ $ngu$ $m$ $za$

Tapatapa =$ta$ $pa$ $ta$ $pa$

Maliza = $ma$ $li$ $za$

c) Muundo wa silabi wa Konsonanti, kiyeyusho na irabu (KkI)

Mifano:

Bwana =$bwa$

Fyata =$fya$

Mpya =$pya$

Upwa =$pwa$

Ukwezi =$kwe$

d) Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)

Mifano:

Mwandani =$nda$

Chongo =$cho$ $ngo$

Nguru =$ngu$

Daftari =$fta$

Boksi =$ksi$

Page 3: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 3 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Sekta = $kta$

3. Chunguza kwa makini nomino zifuatazo. Kisha kwa kuzingatia aina za nomino, tenganisha nomio hizo katika makundi yake: mbuzi, Ashura, usingizi, kijiko, Januari, jeshi, matatizo, Zanzibar, kamati, Mungu.

MAJIBU

AINA ZA NOMINO NOMINO

Nomino za Pekee Ashura, Januari, Zanzibar,

Nomino za Kawaida Mbuzi, kijiko,

Nomino za wingi Matatizo,

Nomino za Jamii Jeshi, kamati,

Nomino dhahania Usingizi, Mungu

4. Pigia mstari vitenzi katika sentensi zifuatazo na utaje ni aina gani ya kitenzi kwa kila

tungo. (a) Yeye ni mwanafunzi hodari

Aina: kitenzi kishirikishi (t)

(b) Mwalimu alikuwa anataka kwenda darasani

Aina:

- alikuwa, anataka – vitenzi visaidizi (Ts)

- kwenda – kitenzi kikuu (T)

(c) Mimi nilikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

Aina: kitenzi kishirikishi (t)

(d) Mtoto anatembea harakaharaka.

Aina: kitenzi kikuu (T)

(e) Njoo. (T)

(f) Jiko li moto. (t)

(g) Huwa halali vizuri (T)

5. Bainisha aina za maeno katika tungo zifuatazo

(a) Vizuri vimeibiwa

W T

(b) Anatembea kitoto

T E

(c) Alisoma kwa bidi ingawa hakufaulu

T E U T

Page 4: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 4 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

(d) Viatu vya baba vimepotea

N V T

(e) Maskini! Amepoteza kila kitu.

H T E

6. Taja dhima tano za viambishi awali kwa mifao.

MAJIBU

a) Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtenda/Kiima => Hutumika kuonesha aliyefanya kitendo katika neno. Kama viambishi vya Ngeli ya

Mtenda, viambishi hivi ndivyo vinavyotangulia viambishi vingine katika kitenzi.

Mfano:

NAFSI UMOJA WINGI MFANO

YA KWANZA NI TU ni-na-andik-a,

tu-li-shind-a

YA PILI U M u-me-kasir-ik-a,

m-na-pig-w-a

YA TATU A WA a-li-simam-a,

wa-ta-p-ew-a

b) Viambishi vya Nafsi ya Mtendewa/Mtendwa

=> Hutumika kuonesha nafsi ya aliyeathirika na kitendo katika neno. Kama viambishi

viwakilishi vya ngeli ya mtendewa, mara nyingi viambishi hivi huwekwa punde kabla ya

mzizi wa kitenzi.

NAFSI YA MTENDEWA KIAMBISHI MFANO

YA PILI UMOJA KU zi-me-ku-fik-i-a

YA PILI WINGI M, MU, WA ni-na-wa-tum-a

YA TATU UMOJA M ni-ta-m-tambu-a

c) Viambishi vya Wakati/hali

Hivi ni viambishi ambavyo vinapowekwa kabla ya mzizi wa kitenzi, vinatufahamisha wakati

kitendo hicho kilipofanyika.

Viambishi hivi ni:

KIAMBISHI HUWAKILISHA: MFANO

LI wakati uliopita Ki-li-chom-ek-a

Page 5: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 5 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

ME wakati timilifu (uliopita muda

mfupi)

zi-me-anguk-a

NA wakati uliopo tu-na-ku-subir-i

TA wakati ujao wa-ta-ni-ju-lish-a

HU hali ya mazoea hu-som-a

d) Viambishi vya Kukanusha Wakati

Viambishi hivi hutumika kukanusha kitenzi katika sentensi kulingana na wakati au hali

KIAMBISHI HUKANUSHA: MFANO

KU wakati uliopita Ha-ku-ingi-a

JA wakati timilifu (uliopita muda

mfupi)

si-ja-ku-uliz-i-a

-I* wakati uliopo na wa mazoea ha-som-i

TA wakati ujao ha-ki-ta-maliz-ik-a

Tanbihi: Tunapokanusha wakati uliopo, wakati wa mazoea na wakati usiodhihirika,

tunatumia kiambishi kiishio (I) badala ya kutumia kiambishi tamati. k.m:si-ku-ju-i, ha-

pat-ik-an-i

e) Viambishi vya Kukanusha Nafsi

Tunapokanusha kitenzi, kiambishi cha kwanzwa hubadilika kulingana na nafsi.

KIAMBISHI MATUMIZI MFANO

SI nafsi ya kwanza si-ku-wa-on-a

HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u

HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a

f) Viambishi Virejeshi vya Ngeli

Hurejelea ngeli ya mtendewa au mtendwa na hutumika hasa katika vishazi tegemezi (vyenye

o - rejeshi) kama vile:

wa-li-cho-nitum-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya KI-VI

ni-ta-ka-ye-m-salim-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya A-WA

u-li-ko-ji-fich-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali KU

tu-li-po-pa-safish-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali PO

7. Katika kila tungo uliyopewa tenganisha vishazi huru na vishazi tegemezi.

a) Mwalimu aliyekuja asubuhi / anafundisha Kiswahili

K/Tg K/Hr

Page 6: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 6 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

b) Watawachagua / waliohodari

K/Hr K/Tg

c) Katika msafara wa mamba / na kenge wamo

K/Tg K/Hr

8. Kwa kutumia mifano, fafanua miundo mitano ya kiima

MAJIBU

Kiima ni sehemu ya sentensi inayokaliwa na maneno yanayodokeza kuhusu mtendwa wa jambo.

Kiima kinakuwa na miundo ifuatavyo.

Nomino peke yake Mfano:

Mtoto anasoma Juma anakimbia

Kiwakilishi peke yake Mfano:

Yeye haishi hapa

Sisi tutaondoka pamoja

Yule hataki kuondoka

Wangu wanifuate

Nomino na Kivumishi Mfano:

Watoto wote wameondoka

Wasichana wazuri wamewasili

Kitabu kidogo kuliko vyote kimeuzwa

Nomino na kishazi tegemezi kivumishi Mfano:

Mtoto aliyeingia hapa amefiwa

Kisu kilichopotea kimeonekana

Kalamu iliyoisha wino imetupwa

Kitenzi jina na Kivumishi Mfano:

Kuimba kwenu kulitufurahisha

Kuja kwao kulitutia faraja

Page 7: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 7 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

9. Changanua sentensi zifuatazo kwa kutumia njia ya jedwali

(a) Mwizi aliyeiba jana amekamatwa

MAJIBU

S. Changamano

K

A

KN

KT

N

V

E

T

Mwizi aliyeiba ja

n

a

amekamatwa

(b) Alikwendasokoni

10. Taja majina/maneno mawili yanayoingia katika ngeli za nomino zifuatazo:

(a) I-ZI >>>>> nchi, nguo

(b) LI-YA >>>>> shati, gari

(c) KU >>>>> chumbani, nyumbani

(d) U-YA >>>>> ugonjwa, uovu

(e) U-ZI >>>> ukuta, ubao

11. Je, lugha yako ina maneno mapya? Kama inayo, eleza namna maneno hayo yalivyoingia katika lugha yako.(hojatano). MAJIBU

a) Kubadili mpangilio wa herufi. Mfano:

- Lima, mali, mila, lami, imla,

b) Kuambatanisha maneno. Mfano:

- Mwana+jeshi >>>> mwanajeshi - Askari+kanzu>>>>askarikanzu

Page 8: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 8 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

- Bata+mzinga >>>> batamzinga

c) Kutohoa maneno ya lugha nyingine. Mfano:

- Trekta - Baiskeli - Sketi

d) Uambishaji wa maneno.

Mfano: - Anasoma – msomi – kisomo

e) Kufananisha sauti, umbo, mlio na sura.

Mfano: - Mkono wa tembo - Kidole tumbo - Mtutu - kifaru

12.Taja njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo:

(a) Batamzinga >>>> mwambatano (c) mtutu >>>> mwigo wa sauti

(d) chaki >>>>> kutohoa

(e) sawasawa >>>>> kurudiarudia/uradidi

(f) mkeo >>>>> kusinyaza (mke wako)

13.Tumia viambishi vya o-rejeshi kuunganisha tungo zifuatazo:

(a) Mwanafunzi alichelewa.Mwanafunzi amepewa adhabu

Mwanafunzi aliyechelewa amepewa adhabu.

(b) Kitabu kinavutia. Kitabu kimenunuliwa sana

Kitabu kinachovutia kimenunuliwa sana.

(c) Godoro lilikojolewa. Godoro limeanikwa

Godoro lililokojolewa limeanikwa.

(d) Ukuta umefanya ufa.Ukuta umeangushwa

Ukuta uliofanya ufa umeangushwa

(e) Kifaranga amepotea. Kifaranga ameonekana

Kifaranga aliyepotea ameonekana

14. Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa.

Page 9: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 9 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Kwea kitu mfano mti au mlima

Ongezeka thamani au hadhi

Ingia katika chombo cha usafiri

Sia mbegu ardhini ili iote

Mgawanyiko wa kitu au njia katika mielekeo miwili

Mtanziko wa fikra, kutojua la kufanya

Sehemu ya uso ambayo iko juu ya macho

15. (a) Eleza maana ya rejesta

Rejesta ni mtindo wa lugha unaotumiwa katika mazingira maalumu yenye shughulani

mfano shuleni, mahakamani, hospitalini, sokoni.

(b) Kwa kutoa mifano, taja mambo muhimu matatu yanayomuongoza mtumiaji wa lugha katika uteuzi wa rejesta.

- Mada: mfano – mazungumzo yanayohusu mafuriko yatatawaliwa na mada husika - Uhusiano: mazungumzo huangalia pia uhusiano baina ya wazungumzaji, mfano baba

na mwanawe, bosi na mfanyakazi wake. - Muktadha: mazingira waliyopo wazungumzaji pia huweza kuathiri mazungumzo ya

wahusika kwa mfano mkiwa hospitalini mtatumia maneno yanayosadifu mazingira hayo.

16. Moja ya faida za misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mfano mmoja wa misimu

zagao iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo: (a) Miaka ya Azimio la Arusha

Kabaila

Bwanyenye

Ukupe

Mchumia tumbo

Ujamaa

Kujitegemea

(b) Njaa ya mwaka 1974/1975

Unga wa yanga

Kufunga mkanda

kumbakumba

(c) Kipindi cha mfumo wa vyama vingi

Ngangari

Wapambe

Wakereketwa

Wafurukutwa

(d) Awamu ya tano ya serikali ya Tanzania

Hapa kazi tu

Vyuma vimekaza

17. Fafanua dhana zifuatazo:

Page 10: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 10 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

(a) Kishazi – ni tungo inayotawaliwa na kitenzi chenye kutoa taarifa kamili au isiyo

kamili. Kuna aina mbili za vishazi ambazo ni kishazi huru (H/hr) na kishazi

tegemezi (K/Tg).

Mfano.

K/Hr – Mzee amelala

K/Tg – Mtoto aliyeumia………..

(b) Chagizo – ni sehemu katika sentensi inayotoa taarifa Zaidi kuhusu kitenzi.

Chagizo hujibu maswali kama wapi, lini, kwa nini, kiasi gani, au namna gani.

Mfano: Baba ameenda shambani (shambani ni chagizo)

(c) Kiarifu – ni sehemu ya sentensi inayokaliwa na maneno yanayoarifu kuhusu

tendo lililotendwa na kiima.

Mfano: Baba analima (analima ni kiarifu)

(d) Sarufi – ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazomuongoza mtumiaji wa lugha ili

aweze kuitumia lugha yake kwa usanifu na ufasaha. Sarufi inaundwa na

matawi/tanzu nne (4) ambazo ni :

- Sarufi matamshi/ fonolojia

- Sarufi maumbo/mofolojia

- Sarufi miundo/sintaksia

- Sarufi maana/semantiki

(e) Sentensi – ni tungo yenye muundo wa kiima na kiarifu na inayotoa taarifa kamili.

Mfano: Mwalimu mkuu amehutubia wanafunzi

18. Panga maneno yafuatayo kama yanavyotakiwa kuonekana katika kamusi

(a) bunge (b) bajia (c) bomba (d) biriani(e) baskeli (f) bungo (g) bendera (h) bonde

(i) birika (j) baibui

MAJIBU

(a) bajaji (b) (b) baskeli (c) bendera (d) biriani (d) birika (e) bomba (e) bonde (f)

bunge

19. Sentensi zifuatazo zina makosa, zichunguze kwa makini kisha uziandike kwa

usahihi

a) Ninyi wote mmechelewa

Sahihi: Nyinyi nyote mmechelewa

b) Wanafunzi waliyosoma wamefaulu

Sahihi: Wanafunzi waliosoma wamefaulu

c) Ngombe zake zimeuzwa

Sahihi: Ng’ombe wake wameuzwa

d) Walimu wamewakilisha michango yao

Sahihi: Walimu wamewasilisha michango yao

Page 11: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 11 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

20. Bainisha na eleza kazi za viambishi katika maneno yafuatayo.

(a) alitukimbia (b) nitakibeba (c) kitoto (d) ukila (e) kilianguka

MAJIBU

(a) a-li-tu-kimbi-a

a- nafsi ya tatu umoja

li- wakati uliopita

tu – watendwa

kimbi – mzizi

a – kiambishi tamati maana

(b) ni-ta-ki-beb-a

ni- nafsi ya kwanza umoja

ta – wakati ujao

ki – kitendwa

beb – mzizi

a- kiambishi tamati maana

(c) ki-toto

ki- umoja hali ya udogo

(d) u-ki-la

u- nafsi ya pili umoja

ki- wakati ujao hali ya masharti

la- mzizi

(e) kilianguka

21. Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo:

(a) mwalimu wetu /alitaka kufundisha wakati wa jioni

(b) huyu /si mwenzetu

(c) Wale waliotukebehi juzi / nimewaona wakitapatapanjiani

(d) kijana mrefu mwembamba /ameanguka

22. Kwa kutumia njia ya mnyumbuliko, unda nomino mbili kwa kila kitenzi kifuatacho:

(a) piga – kipigo, mpigaji

(b) cheka – kicheko, mchekaji

(c) ongoza – kiongozi, muongozo

(d) muimbaji

23. Eleza namna barua za kirafiki na za kikazi nzinaavyotofautiana

Page 12: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 12 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Anuani: barua ya kirafiki ina anuani moja lakini barua ya kikazi ina anuani zaidi

ya moja.

Kumbukumbu namba: barua ya kirafiki haina namba ya kumbukumbu lakini

barua ya kikazi huwa na kumbukumbu namba.

Kichwa cha barua: barua ya kirafiki haina kichwa cha barua lakini barua ya kikazi

ina kichwa cha barua.

Mwanzo wa barua: barua ya kirafiki huanza na salamu lakini barua ya kikazi

huanza na Ndugu,

Wadhamini: barua ya kirafiki haiwi na wadhamini lakini barua ya kikazi huwa na

wadhamini

Cheo: barua ya kirafiki haina cheo cha mwandishi lakini barua ya kikazi huwa na

cheo cha mwandishi. 24. Badilisha simu ifuatayo ya maandishi kuwa barua

HALIMA SAIDI SLP 50 LIWALE

NITAKUJA KWAKO MWEZI HUU AMINA

S.L.P 50,

LIWALE.

17/5/2020.

Mpendwa Dada,

Salamu nyingi zikufikie huko uliko, mimi kiafya ni mzima kabisa hofu ni kwako na familia

nzima.

Lengo la varua hii ni kukujulisha kuwa mara baada ya zuio la kusafiri kutokana na maambukizi

ya ugonjwa wa KORONA nitakuja kukusalimia kama tulivyokubaliana.

Naomba sana uniandalie kuku mzuri wa supu siku hiyo nitakayofika. Nitakujulisha kabla ya

kuanza safari yangu.

Kwa leo sina mengi sana wasalimie wote hapo nyumbani hasa mwanao mdogo mwambie

nampenda sana.

Wako akupendaye,

Amina.

25. Eleza maana ya dhana zifuatazo:

Page 13: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 13 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

a) Pijini – ni lugha inayozuka pindi makundi mawili ya watu wanaosema lugha tofauti

yanapokutana. Mfano ni lugha ya Kiswahili ambayo inaaminika kuzuka baada ya

kukutana kwa Waarabu na wabantu wa pwani ya Afrika mashariki.

b) Krioli – ni lugha inayoibuka kutokana na vizalia wa watoto ambao wazazi wao

huzungumza Pijini. Baadhi ya wataalamu wa lugha husema Krioli ni Pijini iliyokomaa

au lugha ya vizalia.

c) Lahaja – ni tofauti ya usemaji miongoni mwa jamii ywatu wanaosema lugha yenye asili

moja. Tofauti ya usemaji katika lahaja haipaswi kuathiri kuelewana kwa wasemaji wake.

26. Kuna tofauti gani kati ya kukua kwa lugha na kuenea kwa lugha?

MAJIBU

Kukua kwa lugha ni pale lugha inapojiongezea msamiati wake kwa kujizalisha yenyewe

kutokana na maneno yake au kuchukua maneno toka lugha nyingine.

Kuenea kwa lugha ni kuongezeka kwa eneo la uzungumzaji na wazungumzaji wenyewe wa

lugha husika. Kwa mfano Kiswahili husemwa kimeenea kutokana na kuongezeka kwa eneo

kinamozungumzwa.

27. Kiswahili ni Kiarabu kwa jina lake lakini ni kibantu kwa tabia zake. Jadili

MAJIBU

Uarabu wa lugha ya Kiswahili unatokana na kuwepo kwa nadharia tete inayodai kuwa

Kiswahili kina asili ya lugha ya kirarabu. Madai haya yanasimamiwa na hoja kuu tatu ambazo

ni:

Neno lenyewe: hoja hii inadai kuwa Kiswahili ni neno linalotokana na neno la Kiarabu “sahil”

umoja na wingi wake “sahel” kwa maana ya pwani. Hivyo kama neno ambalo ni ndilo jina la

lugha lina asili ya Kiarabu basi hata lugha yenyewe itakuwa na asili ya huko linakotoka jina

lake.

Udhaifu, mtazamo huu unakabiliwa na kasoro kwani hata watu huwa hawajipi wenyewe

majina bali hupewa na watu wengine. Lugha ya Kiarabu kutoa jina la motto wa watu wengine

haihalalishi umiliki wao kwa huyo motto. Lakini kama ingekuwa hivyo ndivyo, basi watu wote

wenye majina yenye asili ya mataifa mengine wangekuwa na haki ya kwenda huko bila

bughudha lakini sivyo.

Msamiati: inadaiwa kuwa Kiswahili kina msamiati mwingi toka lugha ya Kiarabu nah ii ni

ushahidi kuwa Kiswahili kinatokana na lugha ya Kiarabu.

Udhaifu, mtazamo huu si kweli kwa sababu lugha kuwa na maneno ya lugha nyingine ni moja

ya tabia za lugha katika kuathiriana zinapokaribiana. Hata hizo tafiti zinaonesha kuwa idadi ya

msamiati wa Kiarabu katika Kiswahili ni ndogo ikilinganishwa na msamiati toka lugha za

kibantu.

Page 14: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 14 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Dini: wataalamu wanaounga mkono mtazamo huu wanadai kuwa upo uhusiano mkubwa kati

ya lugha ya Kiswahili na dini ya kiislamu kwa msingi kwamba dini ya kiislamu ililetwa na

waislamu ambao pia walikitumia sana Kiswahili kufanya shughuli zao na wenyeji wengi wa

pwani ni waislamu na Kiswahili kilienea maeneo ya bara kutokea pwani hivyo, Kiswahili

nacho kililetwa na waarabu.

Udhaifu, mtazamo huu nao hauna mashiko kwa sababu unajikita kwenye hoja butu, kwanza

watu huanza kumudu lugha na kisha huitumia kufasili dini, hivyo hakuna uhusiano wa moja

kwa moja kati ya dini fulani na asili ya lugha fulani.

Kwa ujumla nadharia hii haina ushahidi yakinifu wa kuaminiwa hata kukubalika kwa sababu

hoja zote zitumiwazo kutetea mtazamo huu zina udhaifu mkubwa.

28. “Lugha ya Kiswahili imetokana na lahaja za kibantu” thibitisha kauli hii kwa kutoa

hoja mbili. MAJIBU

Lugha za kibantu ni lugha zinazozungumzwa kusini kwa jangwa la sahara ambazo mtu humuita bantu na wingi wake ni abhantu. Inadaiwa kuwa lugha ya Kiswahili imetokana na lugha hizo za kibantu. Madai haya yanathibitishwa kupitia nadharia inayodai kuwa Kiswahili ni kibantu na inatumia ushahidi wa aina mbili, ushahidi wa Kiisimu na ushahidi wa Kihistoria. Kwa mujibu wa swali hili nitatumia ushahidi wa kiisimu.

Utafiti wa Profesa Malcom Guthrie: huyuni mtaalamu (mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina) 2,300 imezagaa katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500 yalilingana katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia arobaini na nne (44%). Kwa utafiti huu alihitimisha wazi kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za kibantu kuliko lugha nyingine.

Kufanana kwa Msamiati Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.

Page 15: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 15 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Mfano:

Kiswahili Kindali Kizigua Kijita Kikurya Kindendeule

Mtu Umundu Mntu Omun Omontu Mundu

Maji Amashi Manzi Amanji Amanche Maache

Moto Umulilo Moto Omulilo Omoro Mwoto

Tungo (Sentesi) za Kiswahili Miundo ya tungo (sentesi) za Kiswahili inafanana sana na miundo ya tungo za ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima na kiarifu. Mfano:

Lugha za Kibantu Kiima Kiarifu

Kiswahili Juma anakula ugali.

Kizigua Juma adya ugali.

Kisukuma Juma alelya bugali

Kindali Juma akulya ubhugali.

Kijita Juma kalya ubusima.

Kindendeule Juma ilye ughale

Ngeli za Majina Wataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa: maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; na upatanisho wa kisarufi katika sentesi. Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umoja na wingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na wingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana maumbo dhahiri ya umoja na wingi.

Mfano:

Lugha za Kibantu Umoja Wingi

Kiswahili mtu mtoto

watu watoto

Kikurya omanto omona

banto (abanto) bana (abana)

Kizigua mntu mwana

bhantu

Kindali mundu mwana

bhana bhandu

Kindendeule mundu mwana

bhana βhandu

Page 16: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 16 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

βhana

Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na uwingi.

Mfano:

Lugha za Kibantu Umoja Wingi

Kiswahili Baba analima Baba wanalima

Kindali Utata akulima Abbatata bbakulima

Kikurya Tata ararema Batata(Tata)bararema

Kijita Tata kalima Batata abalima

Kindendeule Tate ilima Akatate βhilima

Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo: Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na vya tamati.

Mfano:

Kiswahili – analima a – na – lim – a Kikuyu – arerema a – re – rem – a Kindali – akulima a – ku – lim – a 1 – 2 – 3 – 4

Sherehe: 1 – Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi. 2 – Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo). 3 – Mzizi/Kiini. 4 – Kiambishi tamati maana. Mnyumbuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu. Mfano:

Kiswahili – kucheka – kuchekesha – kuchekelea. Kindali – kuseka – kusekasha – kusekelela. Kibena – kuheka – kuhekesha – kuhekelea. Kinyamwezi – kuseka – kusekasha – kusekelela. Kikagulu – kuseka – kusekesha – kusekelela

Page 17: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 17 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama ifuatavyo:

Mfano:

Kiswahili – Ni-nakwenda Kihaya – Ni-ngenda Kiyao – N–gwenda Kindendeule – Ni-yenda

Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahili huishia na irabu – a.

Mfano:

Kiswahili kukimbi-a – kuwind-a – kushuk-a Kindali kukind-a – kubhing-a – kukol-a Kisukuma kupil-a – kuhwim-a – Kutend-a Kisunza kwihuk-a – kuhig-a – kising-a Kindendeule kuβhutuk-a – kuhwim-a – kuhuk-a

Kwa ujumla miongoni mwa nadharia tete zote zinazohusu asili ya lugha ya Kiswahili ni nadharia ya Kiswahili ni kibantu ndiyo inayokubalika kutokana na kuweka bayana utafiti wa kiisimu wenye misingi ya kisayansi katika kufikia hitimisho.

29. Jadili ni kwa namna gani vyombo vya habari nchini Tanzania vinavyotumika

kukuza na kueneza Kiswahili. MAJIBU Vyombo vya habari nchini Tanzania vinatoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Mchango huo unaweza kuangaliwa katika vipengele vifuatavyo:

Utoaji wa taarifa mbalimbali kama za habari kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kwa lugha ya Kiswahili

Kuendesha vipindi maalumu vya uchambuzi na ufafanuzi wa lugha, mfano “Redio One” wana kipindi cha Kumepambazuka Kiswahilii kila simu ya jumamosi.

Vipindi vya watoto kama hadithi ambazo husimuliwa kupitia redio na televisheni ni sehemu ya mchango wa vyombo hivyo katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili.

Mashindano mbalimbali yanayowahusisha wanafunzi katika uandishi wa insha, midahalo na utunzi husaidia sana kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili

Uchambuzi wa maswali ya lugha ya Kiswahili kupitia magazeti kama Mwananchi pia ni moja ya mchango wa vyombo vya habari katika kukuza na kueneza lugha hii.

Vipindi vya somo la Kiswahili kupitia Televisheni hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa Korona nako kunachochea kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwa sababu ufundishaji hufanywa kwa lugha hii.

Page 18: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 18 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Kwa ujumla vyombo vya habari vya ndani nan je ya nchi ambavyo hutumia lugha ya Kiswahili vinatoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha hii. 30. Kwa kutumia hoja tano, onesha juhudi za waarabu katika kukuza na kueneza

Kiswahili nchini wakati wa utawala wao. MAJIBU

Pamoja na ukweli kwamba Waarabu ni wageni wa mwanzo kufika Pwani ya

Afrika Mashariki historia inaonesha wakiwa na mchango katika kukua na

kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Mchango wa Waarabu unagawanyika

katika makundi mawili ambayo ni Athari Hasi na Chanya kama

zinavyooneshwa hapa chini.

Kuongezeka kwa msamiati wa Kiswahili kutoka lugha ya Kiarabu.

Kufanana matamshi (lafudhi) kwa watu wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Katika biashara zao Waarabu walitumia Kiswahili baada ya kushindikana

kutumia Kiarabu pekee.

Waarabu walitaka watu wote wajue Kiswahili ili wawatumie katika shughuli

zao za utawala, hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi hawakukijua

Kiarabu. Kiswahili kikafanikiwa dhidi ya Kiarabu.

Waarabu ndio walioanzisha utumiaji wa Kiswahili kwa wananchi wote katika

Upwa wa Afrika Mashariki.

Pamoja na Waarabu kuwa kuchangia katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili

kwa upande mwingine walichangia sana katika kudumaza maendeleo ya lugha hii

kwa namna mbalimbali ikiwemo kukitumia Kiswahili katika biashara ya utumwa.

31. Je, fasihi simulizi ina umuhimu gani katika jamii yako? MAJIBU Fsihi simulizi inabeba ni Sanaa yenye umuhimu mkubwa sana kwa jamii, umuhimu huo ni kama ufuatao:

(i) Kuburudisha

Fasihi simulizi huweza kutumiwa kama burudani kwenye mkusanyiko wa jamii. Tanzu

kama hadithi, ushairi, semi (methali, vitendawili, nk.) aghalabu hutumiwa ili

kuwaburudisha waliokusanyika katika jamii. Kwa mfano, watoto

wanapokusanyika kucheza, aghalabu hutegeana vitendawili kama njia ya kujiburudisha.

Hadithi, ngano, hekaya au hata hurafa huweza pia kutambwa kama njia ya burudani.

Page 19: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 19 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

(ii) Kuelimisha

Kwa kutumia fasihi simulizi, wanajamii wanaweza kuzielimisha thamani za kijamii,

historia yao, utamaduni na mtazamo wao kilimwengu kutoka kizazi kimoja hadi chengine.

(iii) Kuipa Jamii Muelekeo

Kwa njia ya kuelimishana kimawazo yanayohusiana na tamaduni na desturi za jamii

husika, wanajamii wanahakikisha kwamba jamii, kwa kutumia fasihi simulizi, inapata

muelekeo utakaowabainisha wao mbali na wengine.

(iv) Kuhifadhi Historia na Utamaduni

Katika kuhifadhi amali muhimu za kijamii, fasihi simulizi inakuwa nyezo muhimu. Aidha,

wanajamii hufahamishwa kifasihi simulizi historia yao – wao ni nani na wanachimbukia

wapi. Maarifa haya ni muhimu kwa kila mwanajamii, kwani yanamsaidia sio tu kujielewa,

bali pia kujitambua.

(v) Kuunganisha Vizazi vya Jamii

Fasihi simulizi ni msingi mkubwa wa kuwaunganisha wanajamii waliopo na waliotangulia

mbele ya haki. Kwa kutambiwa hadithi, vitendawili, methali na nyimbo zao, umbali wa

kiwakati kati ya vizazi vilivyotangulia mbele ya haki, vilivyopo na vijavyo unafupishwa

kwa kiasi kikubwa sana.

(vi) Kufundisha

Jamii ina jukumu la kuwafundisha vijana wake maadili ya jamii ile ambayo yana

adili yaani funzo au ujumbe unaowaelekeza, kuwaadibu, kuwaonya na kuwaongoza

kwenye matarajio ya jamii ile. Kwa hiyo, jamii nyingi hutumia fasihi simulizi kama njia

ya kuwaelekeza na kuwafundisha vijana wake mwenendo mzuri, maadili na falsafa ifaayo

ili kutunza jina na heshima ya jamii ile. Kwa mfano, katika vita dhidi ya Nduli Iddi Amini

1978/1979 nyimbo za kwaya, nyimbo za muziki wa dansi, tenzi, mashairi n.k. zilitumika

kuongeza hamasa kwa askari wetu waliokuwa mstari wa mbele vitani kuwaongezea ari ya

kumwadhibu adui yetu. Kitendo cha kushindwa kwa Iddi Amini katika vita vile tunaweza

kusema kwamba kazi hizo za fasihi simulizi zimefaulu katika dhima yake ya kuelimisha

ili kuongeza hamasa kwa askari wetu. Umuhimu wa fasihi unaonekana katika kufaulu

kutatua matatizo yetu katika jamii.

(vii) Kuukuza Ushirikiano

Ilivyo ni kwamba fasihi simulizi ni mali ya jamii wala sio ya mtu binafsi. Hadithi

inaposimuliwa kwa hadhira kubwa, vitendawili vinapotegewa kundi pana, ni kwa sababu

kimsingi fasihi simulizi ndivyo ilivyokusudiwa itumike katika muktadha wa kuvihusisha

sio vikundi vidogo vidogo tu, bali pia, na hasa jamii nzima.kwa jumla.

(viii) Kuzikuza na Kuziendeleza Stadi za Lugha

Kwa kuwa fasihi simulizi hutegemea usemi na matamko, hatuwezi kushiriki katika

kusimulia hadithi, kutegeana vitendawili, kuimba, nk. bila ya kuongea au kutamka au

kuimba. Kwa sababu hii, fasihi simulizi ina mchango mkubwa wa kuboresha uwezo wetu

wa kuzimiliki na kuzimudu stadi za lugha. Kwa mfano, tanzu za vitanza ulimi zilisaidia

kuhakikisha kwamba utamkaji ni mzuri; utegeanaji wa vitendawili na majibu yake sahihi

Page 20: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 20 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

huukuza uwezo wa kuwaza haraka haraka na kwa usahihi. Hadithi huukuza ule uwezo wa

kukumbuka maudhui.

Umuhimu wa fasihi simulizi ni wa kudumu zama zote iwapo jamii za wanadamu zitaendelea

kuwapo katika uso wa dunia.

32. Eleza tofauti iliyopo kati ya hadhira ya fasihi simulizi na hadhira ya fasihi andishi. Hadhira ya fasihi ni wale walengwa wa kazi ya fasihi ambao hukusudiwa na mtunzi wa kazi husika ya fasihi. Hadhira ya fasihi simulizi na ile ya fasihi andishi hutofautiana kwa vigezo vifuatavyo.

HADHIRA YA FASIHI SIMULIZI HADHIRA YA FASIHI ANDISHI 1 Hadhira ya fasihi simulizi huweza

huwasiliana moja kwa moja na fanani 1 Hadhira ya fasihi andishi haiwezi

kuwasiliani moja kwa moja na mwandishi.

2 Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi kwa kuimba, kupiga makofi, kutingisha kichwa au vigelegele (hadhira tendi/hai)

2 Hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.

3 Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji

3 Hadhira ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.

4 Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.

4 Hadhira ya fasihi andishi ni ndogo kuliko ya fasihi simulizi kwani hubagua wasiojua kusoma na kuandika.

5 Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani.

5 Hadhira ya fasihi andishi si hai yaani haijulikani na mwandishi.

33. Chora mchoro unaoonesha tanzu za fasihi simulizi na vipera vyake.

Tanzu za fasihi simulizi hugawanywa katika vipera vyake kama inavyoonekana katika

mchoro hapa chini.

Page 21: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 21 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

34. .Fafanua kwa mifano dhana zifuatazo:

(a) Nahau : ni semi fupifupi zenye kutoa maana iliyokinyume kwa kutumia lugha ya picha. Mfano:

- Amevaa miwani (amelewa) - Amepata jiko (ameoa) - Kumkalia kitako (kumsema) - Kumlamba kisogo (kumsengenya)

(b) Tashihisi: ni tamathali ya semi inayovipa uwezo wa kibinadamu vitu au

viumbe visivyo na sifa ya utendaji wa kibinadamu. Mfano:

- Kaburi lilimsitiri na aibu - Mawimbi yalipiga makofi - Misitu ikatabasamu - Mawingu yakafunga kumuondolea udhia

(c) Tarihi : ni kipera cha hadithi kinachosimuliwa kuhusu matukio ya kihistoria yaliyowahi kuikumba jamii. Tarihi aghalabu kuambatana na wakati wa utokeaji wa tukio lenyewe.

(d) Mubalagha : ni tamathali ya semi inayotia chumvi mazungumzo kwa lengo la kuleta uhalisia wa tukio lenyewe.

Mfano: - Tulimlilia Nyerere tukajaza bahari ya machozi - Watu walikuwa wengi kama sisimizi - Chakula kilikuwa kingi kama mchanga

(e) Methali : ni semi zenye hekima na busara zitumikazo kuonya, kuadibu na

kuadilisha jamii. Mfano:

- Aisifuye mvua, karowa mwilini mwake - Asiyejua maana haambiwi maana, akiambiwa maana hiyo si maana.

Page 22: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 22 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

- Mwana wa muhunzi asiposana, hufukuta - Ada yam ja hunena, muungwana vitendo

35. Andika methali nyigine moja kwa kila methali yenye maana sawa na methali zifuatazo:

a) Siri ya kaburi aijuae maiti: kitanda usichokilalia, huwajui kunguni wake.

b) Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu : kidole kimoja, hakivunji chawa.

c) Subira huvuta heri : mvumilivu hula mbivu

d) Samaki mkunje angali mbichi : mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo

e) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu : ajizi, nyumba ya njaa. 36. Fafanua changamoto nne zinazoweza kujitokeza kwa kuhifadhi fasihi simulizi

katika maandishi MAJIBU

- Kupotea kwa kazi ya fasihi - Gharama za kuipata kazi ya fasihi - Fasihi hubagua wasiojua kusoma - Fasihi huwa mali ya mtunzi - Fasihi hutumia muda mwingi kuifikia hadhira kutokana na maandalizi - Uhaba wa hadhira ya fasihi - Hupungua ubora wa kifasihi - Hupunguza uhai wa kazi ya fasihi

37. Kama ungekuwa kiongozi wa nchi, ungewashauri wasanii wa kazi za fasihi

simulizi wahifadhi kazi zao kwa kutumia njia ipi? Eleza na toa sababu za jibu lako: MAJIBU Ningewashauri wasanii wahifadhi kazi zao kichwani kwa sababu zifuatazo

- Haina gharama kwa fanani au hadhira - Ni rahisi kufanya marekebisho iwapo yatahitajika - Huweza kubadilika kulingana na wakati na mazingira - Haibagui hadhira ya wasiojua kusoma na kuandika - Huwakutanisha fanani na hadhira yake

38. Jadili mambo yanayodhihirisha uhai wa fasihisi mulizi Uhai wa fasihi simulizi unadhihirishwa na mambo mbalimbali kama vile:

- Kuwepo kwa hali ya utendaji ambapo hushirikisha hadhira na fanani. - Kubadilika kulingana na wakati na mazingira. - Kuwepo kwa mtendaji ambaye ndiye mtendaji mkuu wa fasihi simulizi.

huyu ndiye anayerithisha kazi za fasihi simulizi toka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

- Kuwepo kwa hadhira tendi . - Kuwepo kwa utegemezi katika fasihi simulizi huifanya iwe hai. - Huzaliwa, hukua na mwisho hufa kulingana na maendeleo ya jamii. - Matumizi ya wahusika hai na halisi

Page 23: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 23 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

- Uwezo wa kuibua hisia wakati wa uwasilishaji

39. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne kuhusu ugonjwa wa korona Andika insha kwa kuzingatia:

- Kichwa cha insha kwa herufi kubwa, maneno yasizidi matano, na kipigiwe mstari

- Utangulizi: ufafanue kwa ufupi mada ya insha - Insha yenyewe: hoja zipangiliwe kwa mtiririko mzuri na zitolewe

mifano/ushahidi - Hitimisho: libebe maoni, mapendekezo au mtazamo wa mwandiishi.

40. “Wahusika wa kazi ya fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na

matendo yao” thibitisha kaulihii kwa kutumia hoja tatu kwa kila muhusika kati ya wahusika wawili, mmoja kutoka katika tamthiliya kati ya mbili ulizosoma. MAJIBU Ni kweli wahusika wa fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao. Ukweli huu unathibitika kupitia wahusika wa tamthiliya ya KILIO CHETU pamoja na ORODHA kama ifuatavyo. Kwa kuanza na tamthiliya ya KILIO CHETU watunzi wanathibitisha kufaa kuigwa kwa wahusika kupitia “Mjomba” kama ifuatavyo: Mzalendo, kitendo cha kutetea kwa nguvu zake zote juu ya suala la kutolewa kwa elimu ya masuala ya kijinsia kwa vijana kama “Joti” na “Suzi” ni kitendo kinachofaa kuigwa na jamii nzima. Vijana wengi wanaangamia kutokana na kukosa welewa wa madhara ya mahusiano ya kimapenzi na wazazi hawako tayari kusaidia kwenye hilo. Mshauri mzuri, kitendo cha “Mjomba” kumshauri jirani yake ambaye ni “Baba Joti” kutosikiliza ushauri wa kwenda kwa fundi (mganga) huko Luhota na badala yake wamuuguze mgonjwa kwa kufuata ushauri wa kitabibu uliotolewa na wataalamu wa afya ni kitendo cha kuigwa kwa sababu sio tu alimsaidia “Baba Joti” kuepuka hasara ya muda na mali lakini pia alizuia kuendekezwa kwa imani za kishirikina. Mwenye upendo, mhusika “Mjomba” anaonekana ni mtu mwenye upendo na huruma kwa kitendo cha kumtetea “Suzi” asiendelee kupigwa na badala yake akataka mtoto huyu apewe elimu ambayo itamsaidia na kumlinda hata awapo peke yake badala ya kutegemea hofu na vitisho pekee. Kwa upande wa tamthiliya ya ORODHA pia mwandishi ametumia wahusika wenye kufaa kuigwa na hapa anaingia “Mama Furaha”. Mlezi, mhusika huyu anafaa kuigwa kwa jinsi alivyosimama katika nafasi yake kama mama mlezi bora wa familia, siku zote alijitahidi kuhakikisha anatoa malezi bora kwa watoto wake lakini pia alisimama katika imani ya dini yake.

Page 24: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 24 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Mwenye huruma, licha ya kuonekana kama mkali lakini “Mama Furaha” ni mtu mwenye huruma sana ndio maana alijitahidi sana kumfariji binti yake kuwa atapona licha ya kujua ukweli kwamba ugonjwa alionao mwanawe hauna kinga wala tiba. Huyu ni mama anayestahili kuigwa na jamii nzima. Mkweli, katika jamii watu wengi hupenda kuficha matatizo yanayozikumba familia zao hasa magonjwa makubwa kama UKIMWI, lakini “Mama Furaha” hakutaka kuficha chochote aliweka wazi kabisa wakati wa maziko ya binti yake kuwa amekufa kwa ugonjwa wa UKIMWI na alifanya hivyo akiamini kuwa kuficha ukweli huendeleza kusambaa kwa janga husika. Huyu anafaa kuigwa katika suala hilo pia. Kwa ujumla wahusika hutumiwa kama kielelezo cha sifa, tabia na matendo ya wanajamii kwa lengo la kuweka wazi yale yote yanayotendwa na watu katika jamii ili jamii iyaone na kuyaendeleza yale mazuri na kuyaacha yale yasiyofaa.

41. “Washairi ni wataalamu wazuri waliobobea katika kutoa ujumbe kwa jamii’

Thibitisha kauli hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma ukitoa hoja tatu kila kitabu. MAJIBU Ni kweli kuwa washairi ni wataalamu waliobobea katika kutoa ujumbe kwa jamii, ukweli huu unathibitika kupitia diwani ya WASAKATONGE pamoja na diwani ya MALENGA WAPYA kama ifuatavyo: Kwa kuanza na diwani ya WASAKATONGE mtunzi anatoa ujumbe kwa jamii yake kama ifuatavyo: Maisha si lelemama, jamii inapaswa kutambua kuwa katika maisha ni lazima kupambana sana ili kufikia malengo aliyojiwekea mtu, kinyume na hayo ni kukabiliana na hali ngumu ya maisha isiyosemeka. Ukweli huu unathibitika kupitia shairi la WASAKATONGE ambapo mwandishi anaonesha jinsi watu wa tabaka la chini wanavyohangaika kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayowakabili na bila kufanya hivyo hali inazidi kuwa ngumu. Uongozi ni wito, kiongozi yeyote anapaswa kutambua kuwa kuongoza watu ni karama wala si ujanja na akili nyingi, na unaposhindwa kuongoza basi usilazimishe kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa kama inavyooneshwa kupitia shairi la NAHODHA mwandishi anaweka bayana kuwa kama mtu ameshindwa kuongoza basi ni heri akatosa nanga kuliko kulazima mambo kisha chombo kikaenda mrama. Muungano ni tunu, kila mmoja anafahamu umuhimu wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar lakini ni dhahiri kuwa muungano huu unapaswa usiwe na malalamiko baina ya pande husika. Kumekuwepo malalamiko ya muda mrefu hasa toka kwa upande wa Zanzibar juu ya kutotendewa haki na hili linaoneshwa wazi kupitia shairi la NALITOTE ambao mwandishi anaonesha kuwa wananchi wakizichoka kero hizo wanaweza kufika mahali wakaamua liwalo na liwe

Page 25: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 25 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

halikadhalika shairi la KOSA? Linahoji juu ya kwanini wao (Wazanzibar) wanabaguliwa, wanatengwa na kunyimwa haki yao hali muungano ni wa hiyari? Kwa upande wa diwani ya MALENGA WAPYA halikadhalika waandishi wanatoa ujumbe kwa jamii kama ifuatavyo: Ndoa si jambo rahisi, katika jamii kumekuwa na malalamiko mengi juu ya ndoa kuvunjika na familia kutelekezwa kutokana na baadhi ya wanaume kuendekeza uhuni. Shairi la KWA NINI? Linawahoji wanaume ambao huwaacha wake zao majumbani na kuhangaika na akina “Selume” vichochoroni. Hii si tabia njema na wala haipaswi kufumbiwa macho katika jamii. Kumthamini mkulima, katika maisha ya kawaida mkulima huonekana kama mtu mshamba asiye na thamani yoyote katika jamii lakini ukweli ni kuwa bila mkulima maisha ya mijini yangekuwa magumu sana kwani yeye ndiye huwapatia vyakula watu wa mijini ambako hakuna mashamba. Katika kusisitiza umuhimu wa mkulima shairi la MKULIMA linasema wazi kuwa “Mkulima naye mtu, yafaa kuthaminiwa” bila kumthamini mkulima hatari inaweza kuikumba jamii nzima ikiwa ni pamoja na janga la njaa. Umuhimu wa kulinda maadili, hivi sasa kumekuwa na kasi kubwa ya mmomonyoko wa maadili katika jamii kutokana na kushamiri kwa tabia za ushoga, usagaji na wanawake kujiuza kwa lengo la kupata pesa, shairi la WEWE JIKO LA SHAMBA linaweka bayana madhara ya tabia ya wanawake kujiuza na kujirahisisha kwa wanaume, wanakuwa kama majiko ya shamba yasiyochagua kuni. Kimsingi jamii isiyolinda maadili hupoteza misingi na muelekeo wake. Mapenzi hupaliliwa, ili pawepo mapenzi ya dhati katika jamii na ndoa zenye nguvu na thamani ni lazima watu waingie gharama, shairi la UA linawaasa wale wote wanaopenda vitu vizuri pasipokuingia gharama kuwa waache tabia hiyo kwani huleta kero kwa wale waliojitoa na kuingia gharama ya kujiandalia walio wao. Kwa ujumla kazi za fasihi hubeba ujumbe mwanana kwa hadhira hivyo ni jukumu la hadhira kujitathmini kupitia ujumbe unaotolewa na kufanya mabadiliko yenye tija.

42. Kutokana na mabadiliko yanayoikumba jamii, baadhi ya methali zimepitwa na wakati. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia methali tano. MAJIBU Si kweli kwamba mabadiliko yanayotokea katika jamii yanafanya baadhi ya methali kupitwa na wakati. Kazi yoyote ya fasihi ikiwemo methali huendana na mabadiliko hayo na hivyo tafsiri yake hutegemea muktadha wa matumizi yake kama inavyodhihirika kupitia methali zifuatazo:

- Harakaharaka, haina Baraka

Page 26: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 26 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Methali hii inawataka watu kuwa makini katika kutenda mambo na sio kuharakisha tu ili yakamilike. Hivyo si kweli kwamba haraka haihitajiki bali iwe haraka yenye Baraka.

- Mficha uchi, hazai

Methali hii inawaasa wanajamii kuepuka tabia ya kuficha matatizo kwani kwa kufanya hivyo hawatapata msaada kwa urahisi.

- Si kila king’aacho, dhahabu

Methali hii inatoa tahadhari kuwa watu wasivutwe na uzuri wa vitu kwa nje kwani kuna ambavyo vinavutia nje lakini sivyo kwa ndani.

- Mvumilivu, hula mbivu

Methali hii inawataka watu kuwa na uvumilivu katika mambo wanayoyafanya ili kuyakamilisha na kupata mafanikio. Kukosa uvumilivu kumewaingiza matatizoni watu wengi.

- Aliye juu, mngoje chini

Methali hii inawaasa watu kutoumizwa na mafanikio ya wengine kwani wakifanya uzembe wanaweza kurudi katika hali ya mwanzo.

43. Utamu wa maji ya dafu ni kuyanywa kwenye kifuu chake, na utamu wa shairi

ni lugha. Eleza jinsi waandishi wawili walivyotumia taswira katika kupamba mashairi yao kwa kutoa hoja tatu kwa kila diwani. MAJIBU Ni kweli waandishi wa ushairi hutumia taswira kupamba kazi zao, ukweli huu unadhihirika kupitia diwani ya WASAKATONGE pamoja na diwani ya MALENGA WAPYA kama ifuatavyo: Kwa kuanza na diwani ya WASAKATONGE mtunzi ametumia taswira mbalimbali katika kuipamba kazi yake kama ifuatavyo: Taswira ya kinyonga, huyu ni kiumbe mwenye tabia ya kujibadili rangi kila anapokuwa katika mazingira fulani tofauti. Mwandishi anamtumia kinyonga kuwakilisha watu wenye tabia ya ukigeugeu na wasio na msimamo katika maisha yao, watu hawa hugeukageuka kila mara katika mambo mbalimbali hasa ya kimakubaliano. Dhana hii inadhihirishwa na shairi la KINYONGA ambapo mwadishi anawalinganisha watu wenye tabia hiyo kuwa ni sawa na vinyonga. Katika uhalisia watu wenye tabia hizi kama za kinyonga ni pamoja na wanasaiasa ambao hujiugeuza kulingana na upepo wa kisiasa ulivyo kwa wakati husika bila kujali wanawasaliti wananchi wao. Mwandishi anaitaka jamii kujiepusha kabisa na watu wa aina hiyo. Taswira ya asali, kila mtu anafahamu kuwa asali ni kitu kitamu ambacho mtu akikipata hatamani kukiachia, utamu huu unafananishwa na madaraka ambayo mtu akiyapata hataki kuyaachia kama ambavyo tunaona katika jamii nyingi hasa Afrika viongozi wengi hawataki kuachia madaraka kwa hiyari yao kwa sababu tu ya utamu wanaoupata katika madaraka hayo. Shairi la ASALI LIPOTOJA linasadifu kabisa dhana hii. Harakati za kudai uhuru toka kwa wakoloni zilihusisha watu wote lakini baada ya kupatikana kwauhuru huo watawala weusi wakajigeuza kuwa wakoloni na kukumbatia uhuru huo na madaraka yote hali

Page 27: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 27 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

inayochochea hata machafuko kwa baadhi ya nchi. Mwandishi anaitaka jamii itambue kuwa hakuna anayeng’ang’ania madarakani kwa sababu anapenda kuwatumikia wananchi wake bali ni kwa sababu ya utamu wa madaraka tu. Hivyo, jamii iwe makini na watu wenye uchu wa madaraka wakishakabidhiwa mzinga hawatauachia kirahisi. Taswira ya bundi, inafahamika kwa jamii pana kuwa ndege aina ya bundi huwa ni kiashiria cha mikosi, laana, na madhila ya kila namna kwa jamii husika. Mwandishi anatumia taswira ya ndege huyu kuonesha jinsi watu wa tabaka la chini walivyo katika hali ngumu ya maisha kutokana na unyonyaji, ukandamizwaji na umaskini uliokithiri. Madhila yote hayo yameng’ang’ania katika jamii na hayataki kuondoka kama bundi aliyetua kwenye mti na asitake kuondoka. Uwepo wa madhila hayo unazidisha kushuka kwa maendeleo, mathalani hivi sasa jamii imevamiwa na bundi mwingine aitwaye “Corona” ametua kila kona na kuleta taharuki kwa kila mwanajamii. Kwa taswira hii mwandishi anaitaka jamii kuunganisha nguvu ili kukabiliana na madhila yote yanayoisibu jamii hiyo. Kwa upande wa diwani ya MALENGA WAPYA watunzi pia wametumia taswira kadhaa kupamba kazi yao kama ifuatavyo: Taswira ya bendera, katika jamii huwa tunaziona bendera zikipepea kufuata upepo unakoelekea, waandishi wanatumia dhana hii kuwakilisha watu wasiokuwa na msimamo katika maisha na hivyo kupelekwapelekwa na matukio wanayokutana nayo kama ilivyokuwa kwa bendera. Shairi la USIWE BENDERA linaeleza wazi na kuasa wanajamii kuacha tabia ya kufuata mikumbo na kushiriki mambo yasiyofaa wala kukubalika katika jamii kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwa kama bendera na ni kukosa msimamo. Taswira ya samaki, katika shughuli ya uvuvi samaki akishatolewa kwenye maji huwa hana nguvu tena, shairi la SAMAKI MTUNGONI linaonesha jinsi tabaka la chini lisivyokuwa na sauti wala ubavu wa kufanya chochote hata linapoonewa na tabaka la juu ambalo linawakilishwa na “Mvuvi” ambaye hutumia nguvu alizonazo kiuchumi, kimadaraka kama mtungo wa kuwatungia samaki. Kuna watu hufanya uonevu kwa tabaka la chini kutokana tu na nguvu walizonazo kiuchumi au kimadaraka. Samaki anawakilisha tabaka la chini na mvuvi anawakilisha tabaka la juu. Kupitia shairi hili watunzi wanaiasa jamii kuepuka matabaka. Taswira ya punda, huyu ni mnyama anayefanyishwa kazi nyingi na ngumu sana licha ya kupewa matunzo haba au duni sana. Waandishi wanamtumia punda kuwakilisha tabaka la chini ambalo hubebeshwa majukumu mengi lakini kipato duni, mathalani mwanamke katika familia iwe ni mama, dada wa kazi licha ya kutimiza majukumu mengi ndani ya familia lakini hapewi huduma bora na stahiki. Waandishi kupitia shairi la PUNDA wanaitaka jamii kuwa na tabia ya kuwajali na kuwathamini wale wanaofanya kazi hasa za sulubu katika jamii na kuwapa thamani. Kwa ujumla Fasihi ni kama jicho la tatu la wasanii ambalo hutumiwa kuitazama jamii na kuyabainisha yale yote yaliyomo ndani ya jamii husika ili kuisaidia jamii kuchukua hatua stahiki na kisha kupiga hatua bora za kimaendeleo.

44. Utungaji ni nini?

Utungaji ni kitendo cha kupangilia mawazo na kuyaelezea kimazungumzo au maandishi kulingana na mada husika.

Page 28: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 28 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

a) Unafikiri kwa nini tunasoma utungaji? - Kusaidia wanafunzi kuweza kujieleza kwa ufasaha kwa njia mbalimbali - Kuwezesha wanafunzi kupangilia mawazo na kuyawasilisha - Kuwezesha wanafunzi kutunga kazi mbalimbali - Kukuza uwezo wa kujenga hoja mbele ya watu - Kuchochea ari ya utafiti wa mambo

b) Taja vitu vitatu muhimu katika utungaji - Mada ya utungaji - Hadhira lengwa - Lugha inayotumika

c) Elezea kila kimoja ya hivyo vitu vitatu ulivyovitaja katika swali la tatu - Mada: utungaji lazima uwe na mada inayoongoza utungaji husika,

mwandishi anapaswa kuandika utungaji wake kwa kuzingatia mada. Mfano kama ni insha mwandishi atapaswa kuandika insha yake kwa kuzingatia mada yake.

- Hadhira: katika utungaji ni muhimu sana kuchunguza hadhira yako kama ni ya wasomi au wasiosoma, watu wazima au watoto ili kujua uzito wa mambo ya kuwaeleza.

- Lugha: ni muhimu kujua matumizi bora ya lugha utakayoitumia kwa hadhira yako ili kazi yako isiwe inakera hadhira.

45. Taja aina za insha ulizojifunza Kuna aina mbili za insha ambazo ni:

- Insha za hoja - Insha za wasifu

46. Taja na kuelezea mambo muhimu unapoandaa hotuba. Uandaaji wa hotuba unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

- Ukweli wa jambo linaloelezwa - Ufasaha wa lugha - Nidhamu ya mzungumzaji mbele ya watu - Mantiki nzuri - Sauti ya kusikika

47. Wewe ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 2020, katika Shule ya Sekondari

Dodoma. Andika barua ya kuomba kazi ya ukarani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma S.L.P 4929 Dodoma. Jina lako liwe Pondamali Kufakwaja wa S.L.P1122 Kazuramimba Kigoma.

Kazuramimba, S.L.P. 1122,

Kigoma. 20/12/2020

Mkurugenzi, Jiji la Dodoma, S.L.P 4929, Dodoma. Ndugu,

Page 29: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 29 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

YAH: OMBI LA KAZI Mada hapo juu inahusika. Ninayoheshima kuomba kazi ya ukarani katika ofisi yako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la Mchapakazi la tarehe 10/10/2020 (Uk. 2). Elimu yangu ni kidato cha nne mhitimu wa mwaka 2020 katika shule ya Sekondari Dodoma. Nina ujuzi wa kazi hiyo toka chuo cha ukarani Mpwapwa na nina uzoefu wa miaka mine (4) katika kazi hiyo. Mimi ni mtanzania mwanamke, umri wangu miaka 20, sijaolewa na ninaishi na wazazi wangu wote wawili pamoja na ndugu zangu. Ninapendelea kusoma maandiko mbalimbali yenye kuongeza ujuzi na maarifa, pia napenda kuogelea, kurambaza mitandaoni kwa ajili ya kujiongezea maarifa. Ninapenda kushirikiana na kila mtu na ninajituma sana katika kazi. Ni imani yangu kuwa iwapo nitapewa nafasi hii basi ofisi itaongeza tija katika utoaji wa huduma na kuwavutia wateja. Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litapokelewa kwa mikono miwili na moyo wa unyenyekevu ili name nioneshe ufanisi wangu.

Wako mtiifu, …………….

Pondamali Kufakwaja Mwombaji

48. Andika insha isiyozidi maneno (miambili) 200 na yasiyopungua maneno

(miamoja na hamsini) 150 kuhusu ugonjwa wa Korona.

KORONA KWAHERI TANZANIA Korona ni ugonjwa wa homa kali inayosababisha mgonjwa kukosa pumzi na akosapo huduma stahiki basi huweza kupoteza maisha. Ugonjwa huu husababishwa na virusi vijulikanavyo kama COVID-19 kifupi cha (Corona Virus Disease) na hiyo 19 ni mwaka ambao uligundulika ugonjwa huo, 2019. Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia mbalimbali kama vile, kugusana na majimaji yatokayo kwa mtu mwenye maambukizi kwa kukohoa au kupiga chafya, kugusa sehemu alizogusa mgonjwa, au kumhudumia mgonjwa mwenye maambukizi. Wataalamu wanapendekeza kuwa njia za kujikinga ni pamoja na kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono iwapo si rahisi kupata maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuepuka kujishika uso. Mpaka sasa hakuna chanjo wala tiba ya ugonjwa huu ila mtu akibainika kuwa na maambukizi hutibiwa dalili alizonazo kama kupunguza homa, mafua, kukohoa na dalili nyingine.

Page 30: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 30 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Kwa ujumla ugonjwa huu ni hatari sana kwa sababu mpaka sasa umeshaua watu wengi sana duniani na hasa katika mataifa makubwa, hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika katika kuchukua hatua stahiki na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.

49. Eleza kufanana na kutofautiana kati ya ngonjera na tenzi Kufanana

- Zote ni tungo za kishairi - Zote huwa na beti - Zote huwa na mizani - Zote hubeba maudhui yanayoihusu jamii - Zote hutumia lugha ya kishairi

Kutofautiana

- Ngonjera hutolewa kwa majibizano wakati tenzi hazitumii majibizano - Ngonjera huwa na beti chache lakini tenzi huwa na beti nyingi hata

700/800 - Ngonjera huweza kutambwa mbele ya hadhira na kuwa Sanaa za

maonesho lakini tenzi haziwezi kutambwa mbele ya hadhira - Ngonjera huwa na vipande viwili lakini tenzi huwa na kipande kimoja - Mizani ya ngonjera huzidi 12 lakini tenzi haizidi 12 - Ngonjera hutumiwa kusifia, kuonya au kuasa lakini tenzi husimulia

matukio ya kihistoria au kishujaa (tendi)

50. Fafanua tofauti kati ya fani na maudhui Fani na maudhui ni vipengele vinavyotumiwa katika uchambuzi wa kazi za fasihi. Vipengele hivi hutofautiana kwa kuangalia vijenzi vyake. Fani

- Muundo - Mtindo - Wahusika - Mandhari - Matumizi ya lugha

Maudhui

- Dhamira - Ujumbe - Migogoro - Falsafa - Mtazamo - Msimamo

51. Unafikiri kwanini watu hawafanyi kabisa matambiko siku hizi? Jadili kwa hoja

mbili tuu huku ukitoa na mifano madhubuti. - Ni kinyume na Imani za dini zao - Ni gharama kulingana na hali ya kiuchumi

Page 31: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 31 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

- Maendeleo ya utandawazi yamefanya mambo ya matambiko kuonekana kama ni ushamba

- Mwingiliano wa kijamii hufanya iwe vigumu kufanya matambiko hasa iwapo wameoana watu wa jamii tofauti

- Kuharibiwa kwa maeneo yaliyozoeleka kufanyia matambiko

52. Taja tofauti tano stahiki kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi

FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI 1 Huwasilishwa kwa mdomo 1 Huwasilishwa kwa

maandishi 2 Fanani na hadhira huonana ana

kwa ana 2 Fanani na hadhira

hawaonani 3 Haina gharama 3 Ina gharama 4 Huweza kubadilika kulingana na

wakati na mazingira 4 Haibadiliki

5 Ni mali ya jamii nzima 5 Huwa mali ya mtunzi

6 Haibagui wasiojua kusoma 6 Inabagua wasiojua kusoma

53. Kituo bahari ni nini?

- Ni mstari wa mwisho wa kila ubeti ambao hujirudia kwa kila ubeti wa shairi.

54. Nini maana ya mshororo?

- Mshororo ni mstari katika ubeti wa shairi.

55. Eleza kwa mfano maana ya mzani/mizani katika ushairi?

- Mizani katika ushairi ni idadi ya silabi katika kila mstari. Mizani ndiyo kipimo cha

urefu wa mstari na kwa mashairi ya kimapokeo mizazi aghalabu huwa 16 kwa

mgawanyo wa 8/8.

Mfano:

Rejeeni ya mwalimu, aliyosema Arusha, Viongozi wahujumu, achene kuwapitisha, Uchaguzi ukitimu, wambieni wamekwisha, Wito wake mwenyekiti, mikoani mtimize. Ubeti huo una mizani 16 kwa mgawanyo wa 8/8

56. Je, unaelewa nini kuhusu dhana ya kina?

- Kina ni silabi zinatenganisha vipande katika kila ubeti, vina hufanana kwa kushuka chini.

Mfano: Rejeeni ya mwalimu, aliyosema Arusha,

Page 32: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 32 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

Viongozi wahujumu, achene kuwapitisha, Uchaguzi ukitimu, wambieni wamekwisha, Wito wake mwenyekiti, mikoani mtimize.

Katika ubeti huo kina cha mwanzo ni (-mu-) na kina cha mwisho ni (-sha-)

57. Taja aina 5 za virai kwa mifano

- Kirai nomino mf: Baba mdogo

- Kirai kivumishi mf: Mtoto mdogo mweusi anayelia

- Kirai kitenzi mf: Anafundisha Kiswahili

- Kirai kielezi mf: anachazea uwanjani

- Kirai kihusishi mf: ameenda kwa dada

58. Kishazi ni nini?

Kishazi ni tungo inayotawaliwa na kitenzi kinachotoa taarifa kamili au isiyokamili. Kulingana na hadhi ya kitenzi cha kishazi tunapata kishazi huru au tegemezi.

59. Taja aina mbili za vishazi na elezea kila moja kwa mifano

- Kishazi huru

Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kinachotoa taarifa kamili Mfano:

Mtoto aanacheza mpira Shule imenunua gari

- Kishazi tegemezi

Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kilichoshushwa hadhi ambacho hakitoi taarifa iliyokamili. Mfano:

Shule iliyojengwa………. Mwalimu anayefundisha ……….

60. Ainisha maneno katika tungo zifuatazo;

a) Mkoba wake wa madaftari ni mdogo sana N V V t V E

b) Mwenyekiti wa kata ya mkata amchelewa kufika kazini

N V V TS T E

c) Yule ni mpole sana W t V E

d) Nani ameiba kitabu changu? W T N V

Page 33: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 33 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

61. Onesha viambishi katika maneno yafuatayo, kisha eleza kazi ya kila kiambishi a) Imb-ian-a

- Imb- mzizi -ian- kauli ya kutendeana -a- kiambishi tamati maana

b) Pig-w-a -pig- mzizi -w- kauli ya kutendwa -a – kiambishi tamati maana

a) Kimbi-a

-kimbi- mzizi

-a- kiambishi tamati maana

b) Ha-wa-pik-ik-i

Ha- ukanushi nafsi ya tatu wingi

wa- nafsi ya tatu wingi

-pik-mzizi

-ik- kauli ya kutendeka

-i- kiambishi tamani maana kanushi

c) Ogesh-w-a

-ogesh- mzizi

-s- kauli ya kutendeshwa

-a- kiambishi tamati maana

64. Badilisha vitenzi vifuatavyo kuwa nomino

c) Tuma …… mtume

d) Imba …… wimbo

e) Kimbia …….. mbio/

f) Andika ….. mwandiko

g) Jenga …. jengo 65. Je, kuna aina ngapi za makosa katika sarufi? Yataje:

- Makosa ya kimatamshi

- Makosa ya kimuundo

- Makosa ya kimsamiati

- Makosa ya kimaana

- Makosa ya tafsiri sisisi

66. Elezea namna viungo vya mwili vinavyosaidia katika uwasilishaji wa kazi za fasihi simulizi.

- Midomo: husaidia katika kusimulia tukio la kifasihi pamoja kuishirikisha hadhira kwa

kuuliza maswali na hadhira ikajibu.

- Macho: humsaidia fanani kuonana na hadhira yake na hadhira kuyaona matendo ya

fanani

- Mikono: husaidia katika utendaji na kuonesha ishara mbalimbali katika uwasilishaji

wa kazi ya fasihi. Hadhira pia hutumia mikono kupiga makofi.

- Miguu: huwezesha kujongea na kukutana, pia kutamba kwa fanani mbele ya hadhira.

Page 34: KISWAHILI MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA TATUNA NNE...Toa maana tano za neno “panda” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana utakayotoa. Ukurasa wa 9 kati ya 34 MASWALI NA MAJIBU

Ukurasa wa 34 kati ya 34

MASWALI NA MAJIBU KIDATO CHA 3 & 4 : IMEANDALIWA NA MWL. MAEDA 0717104507

- Kichwa: husaidia katika ushiriki wa hadhira, huweza kuonesha kukubaliana,

kutokubaliana,au kusikitika kwa kile kinachowasilishwa na hadhira.

67. Elezea maana ya methali zifuatazo:

a) Siku za mwizi ni arobaini

Maana yake ni kuwa kila jambo baya lina mwisho wake, anayelifanya ajue ipo siku

atakamatwa na huo ndio mwisho wake

b) Maskini akipata matako hulia mbwata

Maana yake ni kuwa mtu ambaye hajazoea jambo au kitu kama utajiri siku akipata

hushindwa kuficha, atafanya tu ili watu waone.

c) Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno

Chungu ni aina ya wadudu wadogo wanaopenda sukari na aghalabu huwakuta

wamejazana kwenye maganda ya muwa. Mtu anapofikia kutema ganda la muwa ni

ishara kwamba hakuna kitu cha thamani amemaliza sukari yote hivyo halimfai, lakini

pindi anapolitema tu hukuta chungu (wadudu) wamejaa tele wanafanya karamu. Hii ni

kusema tusidharau visivyotufaa na kuvitupa kuna wanaovihitaji na kuvithamini.

Mathalan mavazi yaliyochujuka kwako au kuwa madogo kuna watu wakiyapata hayo

huwa ya kuzaa siku ya sikukuu.

d) Baniani mbaya kiatu chake dawa

Maana yake ni kuwa kila mtu mbaya ana jambo zuri ndani yake.

e) Vyote vin’gavyo si dhahabu

Maana yake ni kuwa tusithamini vitu kwa kuvitazama uzuri wan je.

68. Maneno yafuatayo yameundwa kwa njia gani?

a) Ufagio >>>> matumizi b) Ubeberu >>>> kufananisha tabia c) Bori >>>>>>> d) Nyamafu >>>> kuhulutisha