maajabu matokeo kidato cha sita

1
HABARI JUMAPILI, JULAI 11, 2021 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI 3 Maajabu matokeo kidato cha sita Bakari Kiango, Musa Juma, Mwananchi Dar es Salaam. Ni matokeo yenye mvuto na mchuano wa aina yake kwa shule. Ndivyo unavyoweza kuy- aelezea matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotan- gazwa jana, huku yakionyesha kuongezeka kwa ufaulu kidogo wa asilimia 0.11. Akitangaza matokeo hayo mjini Unguja jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Miti- hani Tanzania, Dk Charles Msonde alisema kuwa mwaka huu ufaulu wa jumla ni asil- imia 99.62 wakati mwaka 2020 ulikuwa 99.51 “Ubora umezidi kuimari- ka kwa idadi ya watahiniwa waliofaulu vizuri katika daraja la kwanza hadi la tatu. Ume- ongezeka kwa asilimia 0.99 kutoka 97.74 mwaka 2020 hadi asilimia 97.93 mwaka huu,’’ alisema na kuongeza: “Pia ubora wa ufaulu wa wasichana kwa mwaka 2021 umezidi kidogo ule wa wavu- lana kwa asilimia 0.10.’’ Mchuano na maajabu Mvuto wa matokeo ya mwaka 2021 sio tu kwa shule za umma kuendelea kutamba kwa kushika nafasi nane kati ya kumi katika orodha ya shule kumi bora kitaifa, lakini pia rekodi ya aina yake kwa shule ya Serikali ya Kisimiri kuende- lea kushika nafasi ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2019. Mwaka 2018 shule hiyo ilishika nafasi ya pili nyuma ya Kibaha iliyopotea kwenye orodha hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu sasa. Sehemu ya mvuto huo pia ni kuendelea kwa mchuano kati ya shule hiyo iliyopo Wanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Feza Boys, Harry Mshana (kushoto) na John Bugeraha wakiwa wamebe- bwa juu na wanafunzi wenzao baada ya kufaulu matokeo ya kidato cha sita na kuing- ia orodha ya wanafunzi kumi bora katika maso- mo yao, huku shule hiyo pia ikishika nafasi sita kitaifa.Picha na Said Khamisi ELIMU mkoani Arusha na shule binafsi ya Kemebos ya mkoani Kagera ambayo kama ilivyokuwa mwaka 2020, mwaka 2021 pia imeshika nafasi ya pili. Unaweza kuita maajabu, Kemebos ambayo kwa miaka hii imekuwa ikishika nafasi ya pili, mwaka 2019 ilishika nafasi ya kumi. Imepanda kwa nafasi nane na kuendelea kushikilia rekodi yake ya kuchuana na shule za Seri- kali. Kisimiri iliyokuwa na watahini- wa 72 imeshika nafasi ya kwanza ikiziongoza jumla ya shule nane za Serikali zilizotamba katika orodha ya shule kumi bora kitaifa. Orodha hiyo ya shule kumi bora iliyotolewa na Necta, mbali ya Kisimiri na Kemebos imeju- muisha shule za Dareda, Tab- ora Girls, Tabora Boys, Feza Boys, Mwandet, Zakia Meghji, Kilosa na Mzumbe. Mvuto zaidi wa matokeo hayo ni kutupwa nje ya orodha ya kumi bora kwa shule ya Ahmes ambayo kwa miaka miwili miwili mfulu- lizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2020 ilikuwa ikishika nafasi ya tatu kitaifa nyuma ya Kisimiri na Kemebos. Aidha, shule ya sekondari Mzumbe iliyokuwa ya nne mwa- ka 2020, mwaka huu imejikuta ikitupwa hadi nafasi ya kumi iki- poromoka kwa nafasi sita katika orodha ya shule kumi zilizotamba kitaifa. Maajabu ya matokeo hayo yamejionyesha pia kwa shule ya Dareda ya mkoani Manyara ili- yopanda kwa nafasi kumi kutoka nafasi ya kumi mwaka 2020 hadi ya tatu mwaka huu. Kwa kuchambua matokeo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021, shule zilizopotea katika orodha ya shule kumi bora ni pamoja na Kibaha iliyoshika nafasi ya kwan- za mwaka 2018. Nyingine ni St Mary Mazinde Juu ya mkoani Tanga iliyshika nafasi ya nane katika matokeo yam waka 2018 na 2019. Hii hapa siri ya Shule ya Kisimiri Siri ya Shule ya Sekondari Kisi- miri kuongoza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka wa tatu mfu- lulizo, imetajwa ni mambo manne ambayo ni kuwa na mipango, mikakati, utekelezaji mikakati na usimamizi mahiri. Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa shule hiyo ya kata ili- yopo wilayani Arumeru, Valen- tine Tarimo alisema mambo hayo manne wamekuwa wakiyasimam- ia na matokeo yake yamekuwa ni kupata matokeo bora tangu mwaka 2019. Alisema ili kufikia malengo hayo, shule hiyo imeku- wa na mikakati inayoshirikisha walimu wote, wanafunzi, wazazi na majirani wa shule hiyo. “Tumekuwa tukikaa pamoja na kuweka malengo ya kufanya vizuri na kuhakikisha wote tunakuwa na lengo moja, wanafunzi kusoma sana, walimu kufundisha lakini pia wazazi na majirani wa shule kutoa ushirikiano ambao unahi- tajika na tunasimamia malengo haya”alisema. Tarimo alisema mwaka 2019 ilishika nafasi ya kwanza baada wanafunzi wote 52 kupata dara- ja la kwanza na wawili daraja la pili. Mwaka 2020 wanafunzi wote 62 walipata daraja la kwanza na mwaka huu wanafunzi wote 72 wamepata daraja hilo. WASIFU KISIMIRI Kwa mujibu wa Tarimo, Kisimiri ni shule ya kata iliyoanzishwa mwaka 2002, kwa madarasa ya kidato cha kwanza hadi cha nne. Baadaye mwaka 2006, madarasa ya kidato cha tano yalianzishwa na kwa miaka mingi imekuwa ikifanya vizuri kwa sababu ya ushirikiano kutoka kwa Serikali na wadau wengine wa elimu. Tarimo alisema hadi sasa shule hiyo ina jumla ya walimu 42 wanaofundisha kidato cha kwanza hadi cha sita, ikiwa na upungufu wa walimu 10 lakini siku za karibuni Serikali imewa- pangia mwalimu mmoja na hivyo kuendelea kupunguza tatizo la walimu. “Tunaishukuru serikali kwa jiti- hada za kusaidia shule hii lakini pia hata vijiji jirani kwa kutupa utulivu wa vijana kusoma kwa bidii na kufanya vizuri”alisema.

Upload: others

Post on 03-Oct-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Maajabu matokeo kidato cha sita

HABARIJUMAPILI, JULAI 11, 2021 MWANANCHI.CO.TZ MWANANCHI 3

Maajabu matokeo kidato cha sitaBakari Kiango, Musa Juma, Mwananchi

Dar es Salaam. Ni matokeo yenye mvuto na mchuano wa aina yake kwa shule.

Ndivyo unavyoweza kuy-aelezea matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotan-gazwa jana, huku yakionyesha kuongezeka kwa ufaulu kidogo wa asilimia 0.11.

Akitangaza matokeo hayo mjini Unguja jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Miti-hani Tanzania, Dk Charles Msonde alisema kuwa mwaka huu ufaulu wa jumla ni asil-imia 99.62 wakati mwaka 2020 ulikuwa 99.51

“Ubora umezidi kuimari-ka kwa idadi ya watahiniwa waliofaulu vizuri katika daraja la kwanza hadi la tatu. Ume-ongezeka kwa asilimia 0.99 kutoka 97.74 mwaka 2020 hadi asilimia 97.93 mwaka huu,’’ alisema na kuongeza:

“Pia ubora wa ufaulu wa wasichana kwa mwaka 2021 umezidi kidogo ule wa wavu-lana kwa asilimia 0.10.’’

Mchuano na maajabuMvuto wa matokeo ya

mwaka 2021 sio tu kwa shule za umma kuendelea kutamba kwa kushika nafasi nane kati ya kumi katika orodha ya shule kumi bora kitaifa, lakini pia rekodi ya aina yake kwa shule ya Serikali ya Kisimiri kuende-lea kushika nafasi ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2019.

Mwaka 2018 shule hiyo ilishika nafasi ya pili nyuma ya Kibaha iliyopotea kwenye orodha hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Sehemu ya mvuto huo pia ni kuendelea kwa mchuano kati ya shule hiyo iliyopo

Wanafunzi wa kidato

cha sita Shule ya Feza

Boys, Harry Mshana

(kushoto) na John

Bugeraha wakiwa

wamebe-bwa juu na wanafunzi

wenzao baada ya

kufaulu matokeo ya

kidato cha sita na kuing-

ia orodha ya wanafunzi kumi bora

katika maso-mo yao, huku

shule hiyo pia ikishika nafasi sita

kitaifa.Picha na Said

Khamisi

ELIMU

mkoani Arusha na shule binafsi ya Kemebos ya mkoani Kagera ambayo kama ilivyokuwa mwaka 2020, mwaka 2021 pia imeshika nafasi ya pili.

Unaweza kuita maajabu, Kemebos ambayo kwa miaka hii imekuwa ikishika nafasi ya pili, mwaka 2019 ilishika nafasi ya kumi. Imepanda kwa nafasi nane na kuendelea kushikilia rekodi yake ya kuchuana na shule za Seri-

kali.Kisimiri iliyokuwa na watahini-

wa 72 imeshika nafasi ya kwanza ikiziongoza jumla ya shule nane za Serikali zilizotamba katika orodha ya shule kumi bora kitaifa.

Orodha hiyo ya shule kumi bora iliyotolewa na Necta, mbali ya Kisimiri na Kemebos imeju-muisha shule za Dareda, Tab-ora Girls, Tabora Boys, Feza Boys, Mwandet, Zakia Meghji,

Kilosa na Mzumbe. Mvuto zaidi wa matokeo hayo

ni kutupwa nje ya orodha ya kumi bora kwa shule ya Ahmes ambayo kwa miaka miwili miwili mfulu-lizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2020 ilikuwa ikishika nafasi ya tatu kitaifa nyuma ya Kisimiri na Kemebos.

Aidha, shule ya sekondari Mzumbe iliyokuwa ya nne mwa-ka 2020, mwaka huu imejikuta

ikitupwa hadi nafasi ya kumi iki-poromoka kwa nafasi sita katika orodha ya shule kumi zilizotamba kitaifa.

Maajabu ya matokeo hayo yamejionyesha pia kwa shule ya Dareda ya mkoani Manyara ili-yopanda kwa nafasi kumi kutoka nafasi ya kumi mwaka 2020 hadi ya tatu mwaka huu.

Kwa kuchambua matokeo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021, shule zilizopotea katika orodha ya shule kumi bora ni pamoja na Kibaha iliyoshika nafasi ya kwan-za mwaka 2018. Nyingine ni St Mary Mazinde Juu ya mkoani Tanga iliyshika nafasi ya nane katika matokeo yam waka 2018 na 2019.

Hii hapa siri ya Shule ya Kisimiri

Siri ya Shule ya Sekondari Kisi-miri kuongoza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka wa tatu mfu-lulizo, imetajwa ni mambo manne ambayo ni kuwa na mipango, mikakati, utekelezaji mikakati na usimamizi mahiri.

Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa shule hiyo ya kata ili-yopo wilayani Arumeru, Valen-tine Tarimo alisema mambo hayo manne wamekuwa wakiyasimam-ia na matokeo yake yamekuwa ni kupata matokeo bora tangu mwaka 2019. Alisema ili kufikia malengo hayo, shule hiyo imeku-wa na mikakati inayoshirikisha walimu wote, wanafunzi, wazazi na majirani wa shule hiyo.

“Tumekuwa tukikaa pamoja na kuweka malengo ya kufanya vizuri na kuhakikisha wote tunakuwa na lengo moja, wanafunzi kusoma sana, walimu kufundisha lakini pia wazazi na majirani wa shule kutoa ushirikiano ambao unahi-tajika na tunasimamia malengo haya”alisema.

Tarimo alisema mwaka 2019 ilishika nafasi ya kwanza baada wanafunzi wote 52 kupata dara-ja la kwanza na wawili daraja la pili. Mwaka 2020 wanafunzi wote 62 walipata daraja la kwanza na mwaka huu wanafunzi wote 72 wamepata daraja hilo.

WASIFU KISIMIRI

Kwa mujibu wa Tarimo, Kisimiri ni shule ya kata iliyoanzishwa mwaka 2002, kwa madarasa ya kidato cha kwanza hadi cha nne.

Baadaye mwaka 2006, madarasa ya kidato cha tano yalianzishwa na kwa miaka mingi imekuwa ikifanya vizuri kwa sababu ya ushirikiano kutoka kwa Serikali na wadau wengine wa elimu.

Tarimo alisema hadi sasa shule hiyo ina jumla ya walimu 42 wanaofundisha kidato cha kwanza hadi cha sita, ikiwa na upungufu wa walimu 10 lakini siku za karibuni Serikali imewa-pangia mwalimu mmoja na hivyo kuendelea kupunguza tatizo la walimu.

“Tunaishukuru serikali kwa jiti-hada za kusaidia shule hii lakini pia hata vijiji jirani kwa kutupa utulivu wa vijana kusoma kwa bidii na kufanya vizuri”alisema.